text string |
|---|
BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO
Kikao cha Tano – Tarehe 8 Aprili, 2024 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A Naibu Spika (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua NAIBU SPIKA:
BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tano – Tarehe 8 Aprili, 2024 (Bunge Lilianz... |
KABATI aliuliza:- Je, lini Barabara ya Mtandika hadi Nyanzwa - Kilolo itajengwa kwa kiwango cha lami? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TA... |
KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake. Naomba Barabara hii iweze kupitika kwa sababu hali yake ni mbaya sana. Sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Barabara ya Ilula – Image - Ibumu ni ahadi ya Serikali ya mud... |
Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuja katika Mkoa wetu wa Iringa ajionee hali mbaya ya barabara jinsi ili aweze kusaidia wananchi, nao waweze kufaidika na Serikali yao na uchumi uweze kujengeka? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, napenda kumjibu Mheshimiwa Mbunge kwamba Barabara hii ya Kitowo – Masisiwe – Mwatasi imetengewa bajeti ya shilingi milioni 36.8 katika Mwaka wa Bajeti 2023/2024 kwa ajili ya kuchonga kilomita nane za barabara na kuweka kifusi kwa kilomita mbili kwenye maeneo korofi. Mh... |
MTATURU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga madaraja kwenye Barabara za Misughaa hadi Kikio na Matongo hadi Mpetu – Singida? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa vivuko... |
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Barabara za Misughaa - Kikio na Matongo - Mpetu kuna uhitaji wa jumla ya madaraja matatu ambayo ni Daraja la Mto Matongo lenye urefu wa mita 65, Daraja la Mto Isanja lenye urefu wa mita 45 na Daraja la Mto Siuyu lenye urefu wa mita 30. Kutokana na ukubwa wa madaraja haya usanifu wa kina u... |
Swali la kwanza; kwa kuwa Bajeti ya TARURA katika Wilaya ya Ikungi ni ndogo na kwa kuwa muunganiko wa eneo na eneo umekuwa ni changamoto kwa haya madaraja. Je, ni upi mpango wa Serikali katika kujenga madaraja haya ili kuunganisha vijiji, kata pamoja na wilaya? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Mheshimiwa Mtaturu ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nijibu swali lake la kwanza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango wa kuhakikisha kwamba inajenga na inaboresha miundombinu katika maeneo yote nchi nzima. Barabara hizi za wilaya zina jumla ya urefu wa kilometa 144,429 na ni mtandao mkubwa ambao unahitaji bajeti... |
KIMEA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati mkubwa wa Hospitali kongwe ya Magunga – Korogwe? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe ilianza kutoa... |
SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri sana ya Serikali. Kwanza, tunashukuru kwa kuona umuhimu wa Hospitali hii ya Magunga. Kwa kweli ni hospitali ya kimkakati kwa sababu ipo katikati ya Mji wa Korogwe, lakini kwenye njia kubwa ya kwenda Arusha na kuja Dar es Salaam. Mheshimiwa Naibu Spika, nina sw... |
Kwa hiyo, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba, tayari tulishaainisha hospitali zote kongwe 50 kote nchini. Fedha zinaendelea kutafutwa kwa ajili ya kuzikarabati kwa awamu. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Kituo cha Afya cha Mlalo ambacho ni chakavu, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya kuma... |
DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikipandisha hadhi baadhi ya zahanati kuwa kituo cha afya. Moja ya vigezo ambavyo vinatumika ni ukubwa wa eneo ambapo zahanati ipo, kama linatosha kujenga miundombinu ya kituo cha afya, pia idadi ya wananchi wanaohudumiwa katika eneo hilo, naomba nimhakiki... |
Ahsante sana. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahadi za viongozi wetu wa Kitaifa zinapewa kipaumbele katika mipango ya utekelezaji. Naomba nimhakikishie Mbunge kwamba, hii ni ahadi ya Mheshimi... |
Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Tarafa ya Matemanga kama ambavyo baadhi ya vituo vya afya kote nchini havina miundombinu ya kutosha na hasa wodi za watoto na wodi za wanaum... |
IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kununua Jenereta katika Hospitali ya Ilongero na Vituo vya Afya Mgori, Makuro na Msange - Jimbo la Singida Kaskazini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spik... |
Majenereta haya bado hayajaanza kutumika kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kukosekana vile vibanda vya kuweka standby generators. Je, ni lini Serikali itaweza kujenga hivyo vibanda ili haya majenereta yaweze kutumika na kule kwenye Vituo vya Afya vya Mgori na Makuro ambavyo havina? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pi... |
DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba kutumia nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwamba, Mheshimiwa Rais ameshapeleka fedha, majenereta yamenunuliwa kwa ajili ya hospitali ya wilaya na vituo vya afya. Kazi yake ni kujenga kibanda kwa ajili ya kuweka jenereta, ili wananchi wa... |
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zahor Mohammed Haji, Mbunge wa Mwera, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa kuelimisha wananchi kuhusu ... |
ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; pamoja na kwamba Serikali imeendelea kutoa taaluma au elimu kwa wananchi mbalimbali kwa vyombo mbalimbali, je, Serikali imefanya tathmini kujua ni kiasi gani elimu hiyo ... |
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la kaka yangu, Mheshimiwa Zahor, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba kuweka record sawa; kaka yangu, Mheshimiwa Zahor, ni mzoefu sana, wakati anamsaidia Makamu wa Rais wakati ule alifanya kazi ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala zima la kutoa elimu; naomba nilichukue hili kwa sababu, nina dhamana ya Muungano. Mheshimiwa Mbunge atakumbuka huwa naenda katika majimbo yao kutembelea miradi ya Mfuko wa Jimbo na mambo mengine. Hili tunalichukua, tutaona namna bora zaidi kwa kushirikiana na wenzetu wa Ofisi ya Mak... |
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mbunge wa Manyoni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, kwanza namshukuru Mheshimiwa Mbunge alikuja kunijulisha taarifa hii. Binafsi nasema kwamba, tunakiri tatizo hilo lipo, lakini kubwa zaidi s... |
Je, Serikali na Ofisi ya Waziri kwa kushirikana wananisaidiaje kupata chakula cha dharura kwa wananchi wangu wa Jimbo la Kilombero? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Comrade, Mheshimiwa Asenga, Mbunge wa Ifakara... |
(Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mchungahela. MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Vikundi vingi vya mazingira vimekuwa vikikosa motisha na uwezo. Je, Serikali inachukua hatua zipi kuvijengea uwezo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mhe... |
Mheshimiwa Twaha hayupo, kwa niaba. MHE. SUBIRA K. MGALU K.n.y. MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. NAIBU SPIKA: Ngoja basi Mheshimiwa Subira. Mheshimiwa Subira. Na. 57 Huduma za Wakala wa Forodha Bandari ya Nyamisati MHE. SUBIRA K. MGALU K.n.y. MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza:- Je, ni upi m... |
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mgalu. MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nampa pole Mheshimiwa Mbunge Twaha na wananchi wa Kibiti kwa mafuriko makubwa yanayoendelea kule, lakini pamoja na hayo, nina maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatav... |
TARIMO aliuliza:- Je, upi mpango wa kurejesha TFDA kwani imeacha masuala ya chakula na inakinzana na utaratibu wa usimamizi wa chakula na madawa duniani? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Priscus Jacob Ta... |
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kurejesha usimamizi huo kwa TMDA bado linaendelea kujadiliwa ndani ya Serikali na mara litakapokamilika mapendekezo ya utekelezaji yatawasilishwa Bungeni. Naomba kuwasilisha. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Tarimo. MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa, tayari i... |
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Moshi kwa sababu, kwa muda mrefu huko nyuma, Moshi haikuwahi kupata Mbunge mzuri kama huyu anayejua Wanamoshi wanataka nini. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake ambalo kimsingi ni swali moja la mwisho, ni kwamba, kwa sababu... |
SAPUTU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itazuia kupaki magari ya Serikali sehemu za starehe baada ya saa za kazi? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mbunge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupit... |
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa fursa hii naomba kuwakumbusha Maafisa Masuuli wote kusimamia maelekezo hayo. Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Festo. MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kwanza naishukuru Serikali kwa maelekezo. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; lich... |
Je, ni hatua gani zimefikiwa hadi sasa, ili kupunguza matumizi ya Serikali, kama ambavyo wametuambia? Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Sanga, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu ya... |
Kwa kuwa, Serikali imeliambia Bunge lako Tukufu kwamba, Sheria na Kanuni za kukataza matumizi ya magari baada ya muda wa kazi zipo. Je, Serikali iko tayari kutoa maelekezo au kauli kwa wanaosimamia usalama wa barabarani kuyakamata magari ambayo yanaendelea kukaidi amri hii? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI ... |
Waheshimiwa tunaendelea na Wizara ya Uchukuzi, Mheshimiwa Maimuna Pathan. Na. 60 Serikali Kulipa Fidia Wananchi wa Nachingwea MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza:- Je, ni lini wananchi wa Nachingwea ambao mashamba yao yalitwaliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege watalipwa fidia? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI ... |
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pathan. MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali kwa kuchelewa kulipa pesa ya wananchi zaidi ya miaka mitano sasa, haioni kwamba imerudisha nyuma maendeleo ya wananchi hao kwa kukosa sehe... |
Hakuna biashara inayoendelea kwa kuwa wanategemea wapate fidia ili waendelee na maisha yao. Je, ni lini sasa hawa watu watalipwa fidia ili waweze kuendelea kuondoka pale? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu madai mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Musoma n... |
Hata hivyo, kumejitokeza changamoto ndogondogo, baadhi ya wananchi kufanyiwa tathmini ndogo tofauti na hali halisi na baadhi yao kusahaulika. Changamoto hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliiagiza Wizara ya Uchukuzi iifanyie kazi. Je, ni lini sasa Serikali itamaliza changamoto hii ikiwa ni pamoja na kurudia tathmini kwa w... |
Wananchi wa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambao kwa muda mrefu waliambiwa wasiendeleze maeneo ambayo yako karibu na barabara ambazo ni Barabara kutokea Omugakorongo kwenda mpaka Murongo zikiathiri Kata za Kibale, Bugara na maeneo mengine. Je, ni lini sasa fidia hizo zitatoka ili wapishe hayo maeneo ya uendelezaji wa bara... |
Je, ni lini wananchi ambao wanapisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Manyara watalipwa fidia? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, hebu rudia tena swali lako. MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini wananchi wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Manyara watalipwa fidia? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI W... |
Ni kweli kama ulivyosema kuna fidia inadaiwa na wananchi walishapewa mwongozo huo na Serikali na ni kweli nilishafika pale. Kitu kilichofanyika ni kwamba... NAIBU SPIKA: Tulikwenda wote mimi, wewe na Mheshimiwa Mbunge Bonnah pale. WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, tulifika na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Segere... |
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kulifuatilia kwa karibu sana jambo hili na sisi Serikali tutafanya hilo kwa ajili ya kuienzi kazi yake. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, ahsante sana na nampongeza Mheshimiwa Mbunge Bonnah kwa kazi na Wabunge wote wanaofuatilia mambo ya f... |
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Jimbo la Kilindi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji Mabalanga uliopo Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga. Mradi huo unahusisha ujenzi wa tanki le... |
KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii kwanza kuipongeza Wizara ya Maji kwa kazi nzuri sana kwa sababu kata hii ilikuwa ina changamoto kubwa sana ya maji. Sasa, nina swali moja tu la nyongeza. Je, Serikali iko tayari baada ya kukamilisha mradi huu kuhakikisha kwamba wananchi ambao wako pembezoni na kata hii... |
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Omari Kigua, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa takribani shilingi bilioni 39 katika kufanya miradi 13 katika Jimbo la Kilindi. Ka... |
Tunaishukuru Serikali kwa kuchimba visima nane katika Jimbo la Mbulu Mjini na hadi sasa hakuna kisima kilicho tayari kwa ajili ya kujengewa miundombinu. Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya visima vyote nane katika Jimbo la Mbulu Mjini? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZ... |
Je, ni lini Serikali itakamilisha Mradi wa Maji katika Kata ya Kimochi, Moshi Vijijini? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, jibu kwa kifupi sana. Muda wetu unakwenda. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nipokee changamoto h... |
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mnzava, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, juzi Mheshimiwa Waziri Jumaa Aweso alikuwepo Kilimanjaro na alikuwa kule kwa ajili ya kuhakikisha kwamba miradi ya maji iliyoko katika Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Tanga inakamilika kwa wak... |
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Massare, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Suluhu Hassan aliagiza magari ya kuchimbia visima na hii ilikuwa ni fursa kubwa sana kwa Watanza... |
Je, ni lini Serikali itatoa fedha za kutosha ili Vijiji vya Mazimbo, Mtanila, Ifuma na Lupa viweze kupata maji haya? Nashukuru. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spik... |
FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini ujenzi wa Tanki la Maji la Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe utakamilika ukizingatia tanki lile ni la muhimu sana linahudumu Kata ya Bulyaga, Makandana, Bagamoyo, Tukuyu Mjini, Kawetele na Ibighi? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Haya, Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mhes... |
MGALU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Mradi wa Building a Better Tomorrow katika Bonde la Mto Rufiji? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri. NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia Machi, 2024, jumla ya ekari 340,245.3 zimebainishwa na kupimwa afya ya udongo kwa ajili ya Prog... |
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mgalu. MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, natoa pole kwa wananchi wenzangu wa Rufiji wakiwemo wanawake na watoto kwa janga kubwa la mafuriko linaloendelea kutokana na mvua nyingi. Pia nampa pole Mheshimiwa Mbun... |
Kwa kuwa kupitia ukurasa rasmi wa Mheshimiwa Waziri Bashe amefahamisha kwamba tarehe 20 Serikali itatangaza kazi ya ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji ya Ngorongo na Umwe; na kwa kuwa, mabwawa haya yanatarajia pia kushughulikia changamoto ya mafuriko; je, Serikali haioni sasa ipo haja ya Mradi huu wa BBT kwa Bonde la Ruf... |
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili kuhusu mwongozo, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, ushauri wake tumeupokea na tutaufanyia kazi kwa sababu jukumu la Serikali ni kusikiliza wananchi wake. Ahsante.(Makofi) NAIBU SPIKA: Wizara ya Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Salim Alaudin Hasham. Na. 63 Umiliki wa Msitu wa He... |
Kwa sasa Wizara inakamilisha taratibu za kisheria za kuanzisha msitu huo ambao utakuwa chini ya umiliki wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Salim. MHE. SALIM A. HASHAM: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naipongeza Serikali kwa hatua nzuri ambazo imezichukua, je, Serikali haioni tija kuharakisha jam... |
Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ndani ya mwaka huu wa fedha jambo hili litakamilika. (Makofi) NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Kendege. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika kwamba biashara ya hewa ukaa ni biashara ambayo ni mpya kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo elimu inahitajika kutol... |
Je, Serikali italipa lini kifuta jasho na kifuta machozi kwa wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini? NAIBU SPIKA: Hebu rudia tena swali lako. MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali italipa lini kifuta jasho na kifuta machozi kwa wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini? Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa hebu rudi... |
MANYANYA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kufanya mafunzo ya mgambo kuwa sehemu ya mafunzo kwa vijana wanaokosa nafasi ya kujiunga na JKT? WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Stella Martin Manyanya, Mbunge wa Nyasa, kama ifuatavyo:- M... |
Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kupitia Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa Na.2, Sura ya 193 ya mwaka 1964 ambayo ilirejewa mwaka 2002 kwa malengo ya ulinzi wa Taifa, kujenga uzalendo na mshikamano, uzalishaji mali na kutoa elimu ya kujitegemea. Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzishwa kwa vyombo hi... |
MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hili Jeshi la Akiba (mgambo) limeonekana kuwa na hadhi tofauti kidogo ikilinganishwa na Jeshi la Kujenga Taifa na tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni kabla ya marekebisho kwamba hata ajira zikitangazwa zilikuwa zinalenga zaidi Jeshi la Kujenga Taifa katika baadhi ya maeneo.... |
Je, Serikali haioni kwamba iko haja sasa ya kuboresha haya mafunzo ya Jeshi la Mgambo ili kuwavutia vijana wengi zaidi waweze kwenda huko na kuwezesha uwiano na Jeshi la Kujenga Taifa ukizingatiwa kwamba Jeshi la Kujenga Taifa halina uwezo kwa sasa wa kuwachukua vijana wote wenye uhitaji wa kupitia huku. Ahsante sana. ... |
NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tunaendelea na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Anna Richard Lupembe. Na. 65 Ujenzi wa Minara ya Mawasiliano Litapunga – Nsimbo MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga minara ya Mawasiliano katika Kata ya Litapunga – Nsimbo? NAIBU SPIKA: Mhesh... |
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lupembe. MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili. Swali la kwanza; kwa kuwa, Kata hii ina vijiji 10 na hakuna mawasiliano kabisa na kwa wakati huu mawasiliano ni biashara na katika shughuli mbalimbali watu wanawasiliana na sasa hiv... |
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anna Lupembe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Anna Lupembe kwa kufuatilia hili na niseme tu kama yeye alivyosema ni mradi ambao sasa hivi umeshaweza ... |
Waheshimiwa Wabunge, wageni waliopo Bungeni asubuhi hii ni waliokaa jukwaa la Spika ambao ni watumishi wawili kutoka Bunge la Uganda, Ndugu Kabanekera Ruth, Msaidizi wa Mkuu wa Utawala na Ndugu Mirembe Lubega, Msaidizi Mkuu wa Utawala. Karibuni sana. (Makofi) Tunao wageni wa Waheshimiwa Wabunge ambao ni mgeni wa Mheshi... |
(Makofi) Tunao wageni watatu wa Mheshimiwa Timotheo Mnzava ambao ni rafiki zake kutoka Shirika la PETpro Tanzania linalosimamia na kutekeleza wajibu wa wazalishaji kuhakikisha ukusanyaji wa urejelezaji (recycling) wa vifungashio vyao baada ya matumizi. Karibuni. (Makofi) Tunao wageni watatu wa Mheshimiwa Zuena Bushiri ... |
(Makofi) Waheshimiwa Wabunge, Katibu wa Bunge anaomba kuwatangazia Waheshimiwa Wabunge kwamba leo tarehe 8 mara baada ya kusitisha shughuli za Bunge saa 7.00 mchana kutakuwa na zoezi la ugawaji wa mchele. Mchele huo utagawiwa katika eneo la basement karibu na geti la Waziri Mkuu, tunashauri kila Mbunge achukue mwenyewe... |
Nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuendelea kutupa afya na uhai ili tuendelee kuwatumikia wananchi waliotuchagua. Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama kuchangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu lakini kwanza ningependa kuchukua nafasi hii kuipongeza sana Serikali hasa nikianza na kinara mweny... |
Kwa kweli naweza nikasema hata sisi wengine ambao tumekaa katika uongozi kwa muda, tunatamani tungekuwa na tabia na mwenendo unaofanana na Mheshimiwa Waziri Mkuu wetu. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya hilo napenda niwapongeze Mawaziri wanaofanya kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, dada yangu Mheshimiwa Jenista Mhagam... |
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili ni kubwa napenda niendelee kuwapa pole wananchi wangu na nitumie nafasi hii kuiomba Serikali wakati inatazama maeneo mengine itazame na eneo hili. Nimemsikia dada yangu Mheshimiwa Asia Halamga wakati anashukuru ameeleza kwamba kule Hanang wamempeleka mtu anaitwa Msangi kuendelea kuang... |
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo napenda niliseme pamoja na kazi nzuri na kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali, zipo changamoto ambazo ningependa Serikali izichukue na hasa Ofisi ya Waziri Mkuu katika suala la usimamizi. Moja ni jambo ambalo halitupi furaha sisi wawakilishi wa wananchi juu ya namna ambav... |
Namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, yeye ni mtu makini, mwenye huruma na mfuatiliaji; asaidie kuhakikisha hawa wakandarasi na wazabuni wanalipwa. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo ni pale mahali ambapo Serikali imeamua kutwaa ardhi kwa maendeleo mbalimbali. Kwa mfano Mkoani kwangu Kigoma, Uwanja wa Nd... |
Kwa hiyo ninachomwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kupitia Ofisi yake wahakikishe maeneo ya wananchi wanayoyatwaa kwa shughuli za maendeleo wanalipa kwa wakati ili kuruhusu wananchi hao waendelee na shughuli zingine. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka nilizungumzie ni suala la mifumo. Bahati nzuri ... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, sikatai mifumo, ninachosema tusiende speed katika jambo ambalo tunajua kabisa kwamba, hili jambo halijawafikia wananchi kwa kiasi kikubwa. Wa-introduce Mfumo wa NeST ili wakandarasi wote wanaotaka kuomba kazi waingie kwenye mfumo huu. Wakandarasi wengi wameshindwa kuomba kazi kwenye mfu... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais amekwishalisema jambo hili, lakini nimwombe Mheshimiwa Waziri Mkuu kupitia... MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa taarifa. TAARIFA MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpe taarifa mzungumzaji, anazungumza... |
Pamoja na kuanzishwa kwa mifumo hiyo, inaelekea bado kuna maeneo ambayo kuna mawasiliano duni na hili nilikuwa naomba katika usimamizi, Mheshimiwa Waziri Mkuu alichukue. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tumepitisha hapa katika Bunge hili bajeti, kodi inayoitwa hotel levy inayotozwa na halmashauri, 10% kwa kila mtu anay... |
Nampongeza na Mheshimiwa Waziri Mkuu kama msaidizi wake wa karibu kwa namna wanavyoendelea kushughulikia changamoto za wananchi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mambo na maendeleo mazuri yaliyopo, lakini zipo baadhi ya changamoto ambazo Serikali inahitaji izifanyie kazi tena kwa haraka. Kwanza naendelea kuip... |
Kwa hiyo nimwombe Mheshimiwa Waziri Mkuu aweze kuona ni kwa kiasi gani sasa vyumba vile vyote ambavyo vimechakaa vinaweza kujengwa vizuri. Hata yale maboma ambayo hayajakamilika, yakamilishwe ili watoto wote wajione katika level sawa, kuliko hii ambayo inaonekana, wengine wanasoma vizuri lakini wengine hawasomi vizuri.... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande huo, upande wa wakandarasi na wazabuni yaani inaonesha dhahiri kwamba Serikali inawapa fedha, lakini baadaye inaamua ku-drain zile fedha. Mfano pale Musoma, wapo wazabuni ambao wame-supply vyakula mashuleni, karibu miaka 10 hawajalipwa. Sasa kama huyo mtu aliona hiyo ni bi... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani hiyo siyo haki, Serikali inapaswa ilisimamie hilo na ione kwamba ni kwa kiasi gani itawasaidia watu wake kwa maana ya wakandarasi, lakini na hao wazabuni ambao wameendelea kusaidia watu wetu. Kwa hiyo nadhani katika hilo, Serikali ina kila sababu ya kulitafutia majibu na ione kw... |
Naamini kwamba kati ya jambo utakalolifanya na wananchi hasa watumishi Watanzania wakakuelewa, ni pale utakapowarudishia kile kikotoo chao cha zamani badala ya hiki cha sasa. Kwa hiyo nadhani hilo ni kati ya jambo ambalo ni suala la muhimu sana na Waziri alipe kipaumbele ili hiyo kero ya watumishi wa Tanzania iweze kwi... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwa imekisimamisha wale watu wanadai mafao yao sasa kwa miaka mingi na hadi leo hawajapewa chochote. Matokeo yake wanaendelea kupoteza maisha kwa kuwa wanategemea kwamba watalipwa lakini hawajalipwa. Sasa kwa sababu walimpa barua yao Mheshimiwa Waziri Mkuu, wanaomba safari hii... |
Bahati nzuri Mheshimiwa Waziri Ummy akalijibu vizuri, akasema hivi “anakubaliana kwamba ni changamoto na kwa sababu ni changamoto tusubiri ile Bima ya Afya.” Sasa kwa sababu Serikali imekubali kwamba hili suala sasa la matibabu bure kwa wajawazito pamoja na watoto wa chini ya miaka mitano ni changamoto, basi ni vizuri ... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, hivi tunavyoelekea kwenye bima ya afya, ushauri wangu wa bure, tuondoe kabisa Serikali kwa maana ya kuwa na vituo vya afya pamoja na zahanati na kwa sababu tutatumia bima ya afya ni vizuri hivyo vituo vya afya, zahanati na hospitali tukavipa kwanza yale Mashirika ya Kidini ili ... |
TAARIFA WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango mzuri wa Mheshimiwa Mbunge, napenda nimpe taarifa kwamba, tunavyo vituo vya kutoa huduma za afya vinavyomilikiwa na Serikali ambavyo vinatoa huduma bora kuliko huko private. Hapa nataka kusema aende Muhimbili akaone mapinduzi makubwa katika Hospitali ya ... |
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Manyinyi, kengele ya pili imeshalia. MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa. MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ndiyo maana tunasema kwamba... MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa. NAIBU SPIK... |
NAIBU SPIKA: Una hoja mwandikie Mheshimiwa Waziri kwa sababu sasa unachukua muda wa mchangiaji mwingine. Tunaendelea, Mheshimiwa Gambo, ajiandae Mheshimiwa Butondo. MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kupata fursa ya kuchangia kwenye Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na nitajitahidi leo anga... |
Nashukuru Katibu Mkuu TUCTA wamekwenda mpaka kutaja kiwango. Tulikuwa kwa muda mrefu tukivutana kutoka 25 kwenda 50, lakini leo TUCTA wamesema tukutane katikati. Sasa Serikali tutakwenda kukaa katika utatu wetu au sisi na TUCTA kuangalia tunavyoweza kufanya, lakini wazo tulilokuja nalo siyo baya.” Mheshimiwa Naibu Spik... |
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nimeweza pia kupitia sheria na kanuni mbalimbali kama hii ya tarehe 20 Mei, 2022, Kanuni ya tarehe 27 Agosti, 2018, Sheria ya SSRA ya 2008, Kanuni ya SSRA ya tarehe 17 Agosti, 2018, Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya 2017 pamoja na Maoni ya Kambi ya Upinzani ya 2017. (Makofi) Mheshi... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, mtu ambaye mshahara wake ni 1,500,000 kwa kikokotoo cha kabla ya Julai, 2014 alikuwa anapata 108,500,000. Kwa kikokotoo cha sasa anapata 53,767,101 ambayo tofauti yake ni 54,732,000. Kwa yule ambaye mshahara wake kama level ya Wakurugenzi 3,720,000. Kwa kikokotoo cha kabla ya Julai, 201... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tunakuja hapa 2018 tunaweka mambo yetu, tunakwenda 2020 tumebadilisha kabisa kikokotoo chenyewe, tunakwenda kumuathiri kabisa hata mfanyakazi ambaye sheria iliyotungwa 2022, imemkuta, kitu ambacho nadhani siyo sawa. Kama kuna ulazima sana nadhani kikokotoo hiki kingeanza kwa wale waajir... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tumeelezwa pia hapa kulikuwa na changamoto ya gharama kubwa za uendeshaji. Mifuko ilikuwa mitano, kila Mfuko una bodi yake na uendeshaji wake na ofisi yake. Kwa hiyo, unagundua kwamba, kuyumba kwa Mfuko sababu yake siyo tu kikokotoo. Sababu yake kubwa ni namna ambavyo tulikuwa tunaisima... |
Ushahidi ni kwamba CAG ametuambia mara nyingi namna ambavyo hela zimechukuliwa na Serikali kwenda kufanya shughuli tofauti na shughuli zinazohusiana na watumishi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali tutenge bajeti, kwa sababu ukifanya utafiti unaona kwamba pengine kwa mwaka tunalipa approximately 1.5 trillion... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, la nne, katika ushauri wangu, ikikupendeza na Bunge lako Tukufu, tumeona Serikali wamehangaikia kwa muda mrefu sana suala hili, ni namna ambavyo Mheshimiwa Rais ameonesha nia ya kutaka kulifanyia kazi jambo hili. Bunge lako Tukufu liunde Kamati Maalum, Kamati Ndogo kwa ajili ya kwenda k... |
Katika mchango wake ni vizuri pia akumbuke na aweze kuelezea, kama ameli-study vizuri jambo hili, kuhusiana na maslahi wanayopata wale pre 99 ambao wao katika mifuko ya awali walikuwa wanapewa mafao bila hata kuchangia shilingi moja kwenye Serikali na Serikali imekuwa ikilipia. Baada ya mabadiliko ya sheria hata wale a... |
Kama una hoja unaweza kuomba taarifa. Huruhusiwi kusema unachotaka kusema ndani ya Bunge. Hii ni mara ya pili sasa unakataa maelekezo ya kiti. Nakwambia wewe, Kanuni ya 84 inaeleza vizuri sana na wewe bado mdogo, unaweza ukapotea. (Makofi/Kicheko) Mheshimiwa Gambo malizia. MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ... |
BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kadri mjadala unavyoendelea. Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba nzuri, lakini bajeti ambayo ina matumaini makubwa. Hotuba ... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kuanza kumpongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu kwa namna ambavyo anashirikiana vizuri sana na Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kuona kwamba shughuli za kimaendeleo, azma na matarajio ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na wananchi na shughuli za ... |
Kwa kweli tumeshuhudia mafanikio makubwa sana katika kipindi kifupi cha miaka mitatu ambapo Serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi imekuwa ikifanya kazi kubwa na hasa kwa maendeleo ya wananchi wetu. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, sote kila Mbunge hapa akisimama anaweza kashuhudia mambo mbalimbali ambayo yamefanyika kati... |
End of preview. Expand in Data Studio
- Downloads last month
- 114