text
stringlengths
29
186k
Moja ya mambo muhimu ya mwaka huu katika nchi Swiss alikuwa, walau, 75 maadhimisho ya uwanja wa ndege wa Meiringen.
Kama wengi wenu tayari kujua mashapo iko katika bonde nyembamba katika Canton ya Bern, karibu sana na Ziwa Brienz.
shughuli ya kwanza ya msingi ulifanyika Desemba 1, 1941. Tangu wakati huo maji mengi imeshuka kutoka Oltschibach maporomoko ya maji, unaoelekea hangar katika pango ambapo wao ni waliolazwa Tiger kwa msingi Hornet.
F 5 Tiger II ya wanamgambo Hakuna Squadron 8, i "destructors", Walifika kutoka Buochs katika 2004 wakati tarehe kutoka 2007 kuwasili kwa nguvu F / A 18 Hornet Squadron 11 "Tiger", Alihamia kutoka D bendorf.
siku kuu ya sikukuu ilikuwa sehemu uligubikwa na hali ya hewa kidogo Clement. Tayari katika siku chache kabla ya mvua imeanguka kikubwa mno na kadhaa sentimita ya matope walikuwa sasa kila mahali. proverbial Swiss shirika, hata hivyo, ina mdogo usumbufu upeo na, maegesho ya magari, shuttles uwanja wa ndege, GRELLE kwa chuma kuruhusu wageni hoja bila kuzama, kila kitu uliandaliwa na mahesabu. Lakini kwa ajili ya kitu mvua Unaweza.
Katika asubuhi jua mkali alifanya hivyo inawezekana kuchukua picha kubwa ni tuli kuonyesha kuvutia zaidi (aina ya mini Tiger Meet katika nchi Helvetic) kwamba sorties asubuhi wa majeshi.
Tayari katika mchana mapema, hata hivyo, Jupiter Pluvio alianza kulazimisha sheria yake na zenye mawingu kuwa mnene juu ya kufuatilia, mapakuzi kwa nyakati mbadala mizigo yao. utendaji wa nguvu wa' F / A 18 Hornet Solo Display, masterfully ikiendeshwa na rubani Kapteni Julien "teddy" Meister, Ni ulifanyika kabisa chini ya mvua mwanga kwamba akawa swing wakati wa utendaji wa Patrouille Suisse, kwanza muhimu ushiriki baada tu 15 siku ya tukio la Leeuwarden.
Mbali na mvua, hata hivyo, mimi alikuwa radhi ya admiring, pamoja na kuhusu 30.000 ya washiriki jumla 2 siku, utayari na uwezo wa dogo lakini fujo Helvetic Jeshi.
Hapa na Pale: Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael 'Lulu' amewaacha watu hoi baada ya kubandika picha hiyo hapo chini ikimuonyesha yeye na baba yake mzazi 'Mzee Michael' na kummwagia sifa baba yake huku akiomba dua aje kuzaa mtoto atakaye fanana na baba yake (Mzee Michael) kitendo ambacho kila shabiki yake mtandaoni alikuwa na yake ya kusema.
Ewe Mtoto Wangu WA Kiume Popote ulipo Kama tumboni Kama kwenye mayai ya Uzazi au popote Tafadhali rithi Kwa Babu yako utakapokuwa tayari kuja "-Haya ndiyo maneno aliyoandika Lulu.
DC-Ileje apiga marufuku watoto kuonekana maeneo ya vilabuni,wachungaji na machifu waunga mkono waomba sheria ya kufungua vilabu vya pombe izingatiwe waongeza wanaovaa "kata K" pia washughulikiwe.
Mteule huyo wa Rais Ndg Joseph Mkude alitoa agizo hilo wakati wa kikao na Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) kilichofanyika katika Kijiji cha Isoko Kata ya Kafule kikijumuisha viongozi wa dini machifu na wazee maarufu toka Tarafa ya Bundali ukiwa ni mwendelezo wa vikao hivyo vinavyolenga kuifanya wilaya ya Ileje kuwa makazi salama kwa wote.
"Kuanzia sasa ni marufuku kwa watoto kuonekana vilabuni,naagiza kwa watendaji wa kata,vijiji,wazazi na wananchi kwa ujumla,hata kwa watoto wanaobebwa kwani mazingira hayo si rafiki"alisisitiza kiongozi huyo.
Alisema kuwa ubongo wa mtoto anayeshinda maeneo ya vilabuni hauwezi kuepukana na tabia za ulevi kwa vile anaona na kushuhudia namna maisha ya kiulevi yanavyoendeshwa hali atakayoendeleza hata shuleni na hivyo kuzalisha raia wasio wema na kuwa mizigo kwa jamii.
Awali,Paroko Laymond Kapala wa Parokia ya Ipoka aliomba wazazi na walezi wasiwaogope watoto kwasababu ya viwango vyao vya elimu ikiwemo ya Chuo Kikuu.
"Ndugu zangu mmomonyoko wa maadili haujawaacha hata wasomi,sote tunaona vijana wetu wa Vyuo Vikuu wanavyoenenda hata kimavazi hakuna tofauti kati ya msomi na asiye msomi.
Alisema kuwa kamwe mtoto hakui kwa mzaziye hivyo ni jukumu la kila mwanajamii kuvaa viatu vya ulezi ili kuepukana na kupoteza maadili yetu mazuri ya Mtanzania.
Naye Mchungaji Peter Mwakamele wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Isoko aliomba serikali itoe tamko juu ya mavazi ya aibu yanayovaliwa na vijana wakiwemo watumishi wa serikali ukiwemo mtindo wa "kata K"ambao huonesha nguo za ndani kwa wanaume.
Kikao hicho kililenga kujadili kasi ya imani ya" rambaramba" ambalo limeanza kutishia hali ya usalama ya wilaya pamoja na hifadhi ya mazingira kwa serilkali na kwa kuwatumia machifu ambao zamani waliweza kufanikiwa sana.
Huo ni mwendelezo wa vikao katika kutoa elimu kwa jamii na kupata maoni namna maovu yanavyoweza kukomeshwa katika jamii ambapo Mkuu wa Wilaya alishafanya mkutano kama huu kwa Tarafa ya Bulambya ambapo viongozi wa MUJATA Wilaya ya Ileje walimweleza jinsi wanavyoshirikiana na machifu wa nchi jirani ya Malawi katika kupiga vita maovu yakiwemo mauaji ya imani za kishirikina na albino.
KINGOTANZANIA:: HABARI, PICHA NA MATANGAZO: MAUAJI YA MWANGOSI MAPYA YAIBUKA, CHADEMA WADAIWA KUHUSIKA KWA ASILIMIA 50.
Aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Njombe Magharibi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Thomas Nyimbo kudai chama chake kilishiriki mauaji hayo kwa asilimia 50 na asilimia nyingine 50 ilifanikishwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi.
Mzee Nyimbo akimnyooshea kidole mtanagazaji wa Ebony FM ya Iringa Raymond kwa kumkumbusha kuwa si tulikuwa wote wakati nazindua tawi la nyololo miezi mitatu kabla ya kuja dk slaa kuja kuzindua tena tawi hilo mimi nashangaa sana walikuja zindua nini wakati mimi nilishalizindua tawi hilo
TUKIO la kuuawa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, limeendelea kuibua mambo mapya, baada ya aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Njombe Magharibi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai chama chake kilishiriki mauaji hayo kwa asilimia 50 na asilimia nyingine 50 ilifanikishwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi.
Nyimbo alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wandishi wa Habari Jijini Mbeya katika mkutano wake aliouandaa kwa nia ya kutangaza nia yake ya kujiuzulu uanachama wa Chadema na kubakia mwanasiasa huru asiye na chama.
Alisema kuwa Chadema hawakuwa na sababu ya kwenda kuzindua tawi la chama hicho katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi kwa sababu tawi hilo alikuwa tayari alishalizindua yeye mwenyewe miezi mitatu kabla ya kutokea kwa mauaji ya marehemu Mwangosi.
"Asilimia hamsini, mauaji ya rafiki yangu Marehemu Mwangosi yalisababishwa na Chadema kwa kutotii amri ya Jeshi la Polisi na kupanga kwenda kuzindua tawi la chama ambalo mimi nikuwa tayari nimekwishalizindua miezi mitatu iliyopita kabla ya tukio lile," alisema Nyimbo.
Nyimbo alisema kuwa tabia ya viongozi wa kitaifa wa Chadema kutoka makao makuu ya Chama Jijini Dar es Salaam na kwenda mikoani kufanya mikutano ambayo huwa haijafanyiwa maandalizi yoyote na wenyeji wao, hali ambayo inawafanya walazimike kufanya maandalizi wao wenyewe, ndiyo inayosababisha migongano isiyokuwa ya lazima na Jeshi la Polisi na hatimaye kuwa chanzo cha vurugu kwenye mikutano ya chama hicho.
Alisema kuwa kwa kawaida mikutano ya siasa inapaswa kuandaliwa na wenyeji kwa kuwa ndio ambao wanaofahamiana vizuri na uongozi wa Jeshi la Polisi katika eneo husika kwa kuwa wao wakikaa na kuzungumza huelewana, lakini suala hilo linapoingiliwa na wageni husababisha viongozi wa sehemu husika kuwa na wasiwasi wa usalama na hivyo kutokea migongano inayosababisha kutokea kwa vurugu.
Akizungumzia ushiriki wa Jeshi la Polisi katika mauaji ya Mwangosi, Nyimbo alisema kuwa haikuwa sahihi kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Michael Kamuhanda kuingilia kati suala hilo kwa kuwa sheria ya mikusanyiko inaeleza wazi kuwa mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Polisi wa eneo linalofanyika tukio ambaye alipaswa kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).
Alisema kuwa ikitokea OCD akazidiwa nguvu au kushindwa kutoa maamuzi kwa suala husika ndipo hulazimika kuomba msaada kwa bosi wake ambaye ni RPC ambaye naye anastahili kutoa maelekezo na sio kwenda moja kwa moja kwenye eneo la tukio kama alivyofanya Kamuhanda.
Kwa mujibu wa Nyimbo, hata tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kuchunguza chanzo cha mauaji hayo ilikuwa ni batiri kwa sababu Dk. Nchimbi ni sehemu ya watuhumiwa kwa upande wa Serikali.
Alisema kilichotakiwa kufanyika baada ya kutokea kwa tukio hilo ilikuwa ni uwakamata viongozi wote wa Chadema na viongozi wa Polisi waliokuwa eneo la tukio na kuwaweka ndani kwa muda kupisha uchunguzi wa tukio hilo na pia kuwapa fundisho wasijaribu kuchezea roho za watanzania na amani ya taifa.
Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) aliuawa kwa kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu wakati akiwa kazini katika kijiji cha Nyororo wilayani Mufindi ambako Chadema walikuwa wakizindua tawi la chama hicho kijiji hapo.
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation: Waziri Mahiga akutana na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Kaimu Balozi wa Oman nchini, Bw. Mohammed Sulaiman Alrawahi. Mazungumzo yao ambayo yalijikita zaidi katika masuala ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2016.
.Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Italia nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Kushoto) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe.Roberto Mengon ambaye alimtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Roberto kwa mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolea na Serikali ya Italia katika kusaidia Sekta ya Elimu, miundombinu na afya kwamba Tanzania itazidi kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo.
Mhe. Robert katika mazungumzo yake alieleza kuwa amefurahishwa sana na hali ya amani iliyopo nchini Tanzania kwa kuwa wananchi wa makabila na imani tofauti wameweza kuchanganyika na kuishi pamoja na kutumia lugha moja ya Kiswahili na kwamba ni mfano unaotakiwa kuigwa na mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo, Kanda ya Afrika Mashariki ya Italia iliyopo Nairobi, Kenya Bi. Teresa Savanella ambaye alifuatana na Mhe. Roberto akieleza namna ambavyo Taasisi hiyo ambayo inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Ufundi inavyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana wa Afrika Mashariki kupata elimu ya ufundi kwa ajili ya kujiajiri. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Italia nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Antony Mtafya wakifuatilia mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Meya wa Mji wa Hamilton nchini Bermuda, Mhe. Donal Smith kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri alieleza nia ya Serikali ya Tanzania katika kushirikiana na wawekezaji mbalimbali wanaotaka kuja nchini hususan katika miradi ambayo ina tija kwa Taifa na ambayo itatoa ajira kwa Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016
Mhe. Donal nae akimweleza Mhe. Waziri Mahiga kuhusu lengo la ziara yake nchini kuwa ni kuitambulisha Kampuni ya Nelson & Pade inayojishughulisha na kilimo cha kisasa cha mbogamboga na ufugaji wa samaki inayotaka kuja kuwekeza nchini. Pia alimweleza nia ya nchi yake ya kuja kuwekeza kwenye uchimbaji wa mawe aina ya lime (limestone) na matumizi yake katika ujenzi wa kisasa pamoja na kuleta wawekezaji katika viwanda vya kutengeneza madawa ya binadamu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha wakifuatilia mazungumzo.
Mhe. Waziri Mahiga akiangalia moja ya miradi ya kilimo inayofanywa na Kampuni ya Nelson & Pade
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), kujiunga na chama hicho kama ana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi, vinginevyo hataweza kutimiza malengo hayo akiwa ndani ya CCM.
Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti wakati wakihutubia mikutano ya hadhara ya chama hicho, iliyofanyika juzi katika vijiji vya Kilema, Marangu Mtoni, Mwika na Himo, ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya Operesheni Sangara inayoendelea mkoani hapa.
Mbowe alimtaka mbunge huyo wa Vunjo kuungana na CHADEMA katika mapambano ya kweli dhidi ya ufisadi, kwani CCM haina dhamira ya kweli wala mfumo muafaka wa kukiwezesha kupambana na mafisadi.
Kama kweli mbunge wenu, Aloyce Kimaro, ana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi wa nchi hii, basi aje CHADEMA tuunganishe nguvu. Huwezi ukasema unapambana na mafisadi halafu uko ndani ya CCM, haiwezekani. CCM ni chama cha mafisadi. Waheshimiwa wananchi wa Marangu ni bora usijue jinsi nchi hii inavyoibiwa na kutafunwa na CCM. Wizarani kote wizi, mikoani wizi, wilayani wizi, kwenye vijiji wizi, nchi hii ni wizi mtupu!
Wakati wa kampeni nilisema chini ya mfumo wa CCM, hakuna mabadiliko. Nilisema hata aje malaika kutoka mbinguni halafu apewe kazi ya kuiongoza nchi hii, hataweza. Baada ya miezi sita tu naye lazima atakuwa fisadi. Namwambia ndugu yangu Kimaro kama kweli anawapenda wananchi wa Vunjo na anauchukuia ufisadi, basi atoke CCM, vinginevyo naye atabakia kuwa fisadi tu kama walivyo wenzake na chama chake cha kifisadi, CCM, alisema Mbowe na kushangiliwa.
Mbowe aliwataka wakazi wa eneo la Marangu Mtoni, ambalo ni sehemu ya Jimbo la Vunjo, kutokubali kugawanywa katika misingi ya vyama na badala yake, waunganishe nguvu zao katika kuutafuta ukombozi wa kweli kupitia CHADEMA.
Alisema CCM ilitekeleza mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na vyama vingi vya siasa kwa lengo la kuwagawa wananchi ili iwe rahisi kwa chama hicho kuendelea kutawala.
Alisema inashangaza kuona Tanzania, nchi yenye umaskini mkubwa duniani ikiwa na vyama vya siasa 17, wakati Marekani nchi tajiri, yenye watu wengi na iliyo kubwa, ikiwa na vyama viwili tu vya siasa.
Alisisitiza kuwa utitiri wa vyama vya siasa nchini, hauna manufaa kwa Watanzania, zaidi ya kukisaidia CCM kuwagawa na kuwatala wananchi kwa maslahi ya viongozi na matajiri wachache.
CCM inatumia wingi wa vyama vya siasa kuwagawa Watanzania. Wanatekeleza sera ya mkoloni wa Kiingereza, ya wagawe uwatawale, divide and rule policy . Leo watu wa Vunjo mmegawanywa katika misingi ya vyama na kusahau kilicho muhimu kwenu. Utakuta huyu TLP, mwingine CHADEMA, CUF, sijui CUF, NCCR Mageuzi, mmegawanywa ili mtawaliwe. Mmegawanywa katika itikadi za vyama ili iwe rahisi kwa CCM kuwatawala kwa maslahi yao, alisema Mbowe.
Akitoa mfano, alisema katika uchaguzi wa ubunge wa Jimbo la Vunjo mwaka 2005, Kimaro alipata asilimia 42 ya kura, huku asilimia 58 ya kura ikiwa imekwenda kwa vyama vya upinzani.
Alisema licha ya Kimaro kupata asilimia 42 tu ya kura kulinganisha na asilimia 58 za wapinzani, bado aliweza kukinyakua kiti hicho kwa sababu kura za upinzani, zilipigwa kwa kugawanywa, huku vyama vya CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP, kila kimoja kikipata kura pungufu na zile alizopata Kimaro.
Kimaro alipata asilimia 42 ya kura, upinzani ulipata asilimia 58. Alishinda kwa sababu kura za upinzani ziligawanyika, CHADEMA ilipata kidogo, TLP ilipata kidogo, NCCR nayo hivyo hivyo, ilipata kura pungufu ya zile alizopata Kimaro. Hayo ndiyo madhara ya sera ya wagawanye uwatawale, alisema Mbowe wakati akihutubia umati wakazi wa mji mdogo wa Himo.
Alisema baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita, yeye na viongozi wenzake walijitahidi kuunganisha vyama vya upinzani ili kuikabili CCM, lakini jitihada zao zilishindikana kwa sababu ya vyama hivyo kutofautiana na malengo na dhamira ya kuwapigania wananchi.
Mbowe ambaye katika hotuba hiyo hakupenda kuwashambulia viongozi wa vyama vya upinzani kwa majina yao, alisema baada ya kuona jitihada za kuunganisha vyama vya upinzani zinachelewa na kushindikana, CHADEMA iliamua kubuni Operesheni Sangara ili kwenda kuwaunganisha wananchi wa vyama mbalimbali katika kupambana na ufisadi na kupigania maendeleo yao.
Ndugu zangu, tulipoona jitihada za kuunganisha upinzani zinachelewa na kushindikana, tukasema kama vyama vyetu vimeshindwa kuungana basi twende tukawaunganishe Watanzania. Kwa hiyo tulibuni operesheni sangara, tulikwenda majimbo yote ya Mkoa wa Mara, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam, tumekuja Kilimanjaro, tutarudi Dar es Salaam ili kukusanya nguvu kidogo, kisha tutakwenda Kagera, Kigoma, Shinyanga, Tabora………tunatembea nchi nzima kuwaunganisha Watanzania katika harakati za kujikomboa zinazoongozwa na CHADEMA, alisema Mbowe wakati akiwahutubia wananchi wa Marangu Mtoni.
Alisema baada ya CHADEMA kujaribu kuviunganisha vyama vingine vya upinzani bila mafanikio, sasa umefika wakati kwa wananchi kupima na kukiunga chama cha upinzani chenye nguvu kuliko vingine ili iwe rahisi kuikomboa nchi kwa kukiwezesha chama hicho kuing oa CCM.
Alisema aliwaambia wakazi wa Kilema, Marangu Mtoni, Mwika, na Himo, kuwa CHADEMA ndicho chama cha upinzani chenye nguvu hivi sasa kuliko vyama vingine na hivyo ni vema wananchi wakaunganisha nguvu zao kwa CHADEMA ili iwe rahisi kuing oa CCM.
CHADEMA hivi sasa ndicho chama cha upinzani chenye nguvu kuliko vyote, uwongo? TLP haina mbunge hata mmoja, CHADEMA tuna wabunge 11, CHADEMA tunaongoza halmashauri tatu, za Kigoma, Karatu na Tarime, TLP na vyama vingine vya upinzani hakuna anayeongoza halmashauri. CHADEMA tuna madiwani zaidi ya 118, TLP wana madiwani kidogo. Ni rahisi kuwaunganisha Watanzania kupitia CHADEMA kuliko kupitia chama kingine chochote cha upinzani, alisema Mbowe wakati akiwahutubia wakazi wa Mwika.
Katika hatua nyingine, polisi waliokuwa wakilinda mkutano wa CHADEMA uliofanyika mjini Himo, walimwaamuru Mbowe kuhitimisha mkutano huo na kushuka jukwaani kwa kile walichodai kuwa muda ulikuwa umekwisha, lakini umati wa watu waliofurika ulimlazimisha mwenyekiti huyo wa CHADEMA, kuendelea na mkutano huo bila kujali amri hiyo ya polisi.
Hiyo ndiyo nguvu ya umma bwana. Ndugu yangu polisi, sisi tunajadili mambo yanayohusu maisha yako wewe, unataka tufunge mkutano! Angekuwa kiongozi wa CCM hapa angehutubia hadi usiku na wala asingeambiwa afunge mkutano, angekuwa Makamba hapa angehutubia hadi usiku. Lakini si kosa lake, najua wanasumbuliwa sana na CCM, ukiona hivyo ujue kashapigiwa simu na CCM. Sasa nilikuwa nafunga mkutano lakini kwa sababu mmeamua Mbowe niendelee, naendelea. Siogopi polisi, nawaheshimu ninyi wananchi, alisema Mbowe na wakazi hao kushangilia.
Katika mikutano hiyo, CHADEMA ilivuna mamia ya wanachama wapya, na kupokea michango ya fedha kutoka kwa wananchi wa maeneo husika, waliojitolea kwa ajili ya kugharamia mikutano mingine ya operesheni sangara inayoendelea mkoani Kilimanjaro.
Mikutano hiyo ya operesheni Sangara, leo inaingia katika Jimbo la Rombo, kabla ya kuendelea tena kesho katika maeneo ya Mwanga, Same Magharibi na Same Mashariki. Source:Tanzania Daima
Hiyo Sangara yenyewe Wizi mtupu! Haiwezekani huyo Mbowe akafanya mikutano mingi hivyo wakati hatumii helikopta
Chadema inaanza kupoteza mwelekeo taratibu na hii operasheni sangara imekuwa sehemu ya propaganda zaidi badala ya kuwaambia watanzania watawafanyia nini.Maudhui ya karibu mikutano yote yanafanana kiasi kwamba mikutano inakosa msisimko.Mwenyekiti Mbowe amenukuliwa mara kwa mara akisifia utawala wa Mzee Ruksa na kuuponda huu wa sasa.Zitto Kabwe naye alipokuwa katika jimbo la uchaguzi la mhe W Ngeleja alimwasifa kwamba ni waziri hodari sana,na akamshauri ajiunge na Chadema.Propaganda zimeamia kwa mh A Kimaro naye ajiunge na Chadema ili aweze kupambana na ufisadi ?.
Hali inaweza kuwa mbaya sana kwa vyama vya upinzani kipindi cha uchaguzi iwapo A Kimaro,W Ngeleja na wabunge wengine wa CCM wanaosifiwa na viongozi waandamizi wa Chadema wataendelea kutetea viti vyao vya ubunge kupitia CCM.Fedha na muda wanaopoteza kusifia wabunge wa CCM inaonyesha wazi Operesheni Sangara ni mkakati wa hovyo.
Bado nasisistiza bila upinzani kuungana na kuwa kitu kimoja wasitarajie wataweza kuiondosha CCM madarakani.Fedha na muda wanazotumia Chadema lazima zilenge kuondoa CCM madarakani.Nasikitika kusema kwamba Chedema na Operasheni sangara wanazidi kuwaondolea wananchi wengi tuliokuwa na matumaini ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Huo ni ushauri mzuri kwa Kimaro, Moshi hawaipendi CCM, Kimaro bila kuhama CCM atalipoteza jimbo la Vunjo. Sio kweli kuwa Chadema ndio chama kikuu cha upinzani. Chama kikuu ni CUF, Chadema ni baadhi ya maeneo bara. Lazima kiunganishe nguvu na vyama vingine kwa kutosimamisha mgombea maeneo ambayo vyama vingine vinakubalika zaidi.
CCM inatumia wingi wa vyama vya siasa kuwagawa Watanzania. Wanatekeleza sera ya mkoloni wa Kiingereza, ya wagawe uwatawale, ‘divide and rule policy'. Leo watu wa Vunjo mmegawanywa katika misingi ya vyama na kusahau kilicho muhimu kwenu. Utakuta huyu TLP, mwingine CHADEMA, CUF, sijui CUF, NCCR Mageuzi, mmegawanywa ili mtawaliwe. Mmegawanywa katika itikadi za vyama ili iwe rahisi kwa CCM kuwatawala kwa maslahi yao," alisema Mbowe.
"Kimaro alipata asilimia 42 ya kura, upinzani ulipata asilimia 58. Alishinda kwa sababu kura za upinzani ziligawanyika, CHADEMA ilipata kidogo, TLP ilipata kidogo, NCCR nayo hivyo hivyo, ilipata kura pungufu ya zile alizopata Kimaro. Hayo ndiyo madhara ya sera ya wagawanye uwatawale," alisema Mbowe wakati akihutubia umati wakazi wa mji mdogo wa Himo.Click to expand.
Kazi hii sio kosa la wananchi ila Upinzani na hakika CCM wataendelea kushinda hata kama Chadema itachukua wabunge wote wa CCM.
Ikumbukwe tu kwamba wananchi huchagua mgombea kutokana na kuwepo kwa vyama vingi na sio nani mgombea.mpenzi wa CCM, CUF, NCCR ataendelea kuchagua mgombea wake.
Chadema si chama kikuu cha upinzani wala haitakuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania hata siku moja.Viongozi wa Chadema wako tayari kusema uongo ili kutimiza malengo yao ya kifisadi.Ki msingi CCM ya kwanza na TLP ilikuwa ya pili kwa tofauti ya kura zisizozidi mia Chadema ya tatu.Ni kwanini Mbowe na Ndesamburo hawataki kuelewa TLP inakubalika zaidi Vunjo kuliko Chadema !.Badala ya kuiunga mkono TLP wanaanza kuwachanganya wananchi kwa maneno ya uongo na upuuzi.Mrema atachukua kiti cha ubunge Vunjo Chadema watake wasitake.
Chadema si chama kikuu cha upinzani wala haitakuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania hata siku moja.Viongozi wa Chadema wako tayari kusema uongo ili kutimiza malengo yao ya kifisadi.Ki msingi CCM ya kwanza na TLP ilikuwa ya pili kwa tofauti ya kura zisizozidi mia Chadema ya tatu.Ni kwanini Mbowe na Ndesamburo hawataki kuelewa TLP inakubalika zaidi Vunjo kuliko Chadema !.Badala ya kuiunga mkono TLP wanaanza kuwachanganya wananchi kwa maneno ya uongo na upuuzi.Mrema atachukua kiti cha ubunge Vunjo Chadema watake wasitake.Click to expand.
Wewe ndio uko tayari kusema uongo kwa malengo yako. Si kweli kwamba TLP ilikuwa ya pili kwa kura zisizozidi mia. Ilizidiwa kwa kura nyingi. Lakini alichokisema Mbowe hapo juu ni kuwa kura za upinzani zingeunganishwa, zingemishinda wa CCM.
Kwa taarifa yako, TLP imeporomoka vibaya vunjo kama ambavyo Mrema amekuwa akiporomoka. Kwa TLP ni Mrema na Mrema ndio TLP. Kumbuka kwamba matokeo ya mwaka 2000 TLP ilishinda jimbo hilo, pamoja na kuwa kulikuwa na wagombea wa vyama vingine kama CCM, CHADEMA, NCCR.
Hivyo, kushindwa mwaka 2005 ni aibu kwa TLP kwa kuwa ilishuka na kupoteza jimbo lake lililokuwa chini ya Jesse Makundi pamoja na Mrema kuweka kambi kule.
Sababu sio kugawana kura tu kwa kambi ya upinzani, kwani kama ingekuwa hiyo ndio sababu pekee TLP isingeshinda mwaka 2000. Sababu ni watu kupunguza matumaini na Makundi, Mrema na TLP ndio maana wakafikiria vyama vingine, CHADEMA na NCCR kule.
Sasa hiyo ni mwaka 2005, sasa ni 2009. Hali imebadilika zaidi, TLP imekwisha kule kabisa. Utakuja kuniambia matokeo ya mwaka 2010, TLP hata Mrema akigombea yeye mwenye akijitahidi sana anashika nafasi ya tatu.
Na hii si vunjo tu, maeneo mengi katika nchi ambapo TLP ilishika nafasi ya pili imeporomoka kabisa katika chaguzi za sasa. Mfano ni Arusha ambapo TLP ilikaribia kuing'oa CCM lakini kwenye uchaguzi wa juzi wa marudio pale Arusha kati ilipata kura moja tu! Na kushika nafasi ya nne, walishindwa hata na CUF.
Siasa za Tanzania bara zimebadilika sana, mwaka 1995 ilikuwa ni fursa ya NCCR, Mwaka 2000 TLP, mwaka 2005 ilikuwa ni CUF. Sasa upepo wa siasa uko CHADEMA. Tuombe heri upepo huu udumu na kufanikiwa kuindoa CCM madarakani. Kwa upande wa Zanzibar upepo bado ni wa CUF. Huyo Kimaro, kama bado anapenda kuongoza vunjo, asipoteze muda CCM. Atapita kwa tabu kura za maoni, na atakuja kushindwa na CHADEMA.
Ikumbukwe tu kwamba wananchi huchagua mgombea kutokana na kuwepo kwa vyama vingi na sio nani mgombea.mpenzi wa CCM, CUF, NCCR ataendelea kuchagua mgombea wake.Click to expand.
Mbona Zitto alishinda Kigoma Kaskazini pamoja na kuwa palikuwa na mgombea wa CUF? Au Mbona Dr Slaa alishinda pamoja na kuwa kulikuwa pia na wagombea wa NCCR na SAU. Mbona Ndesamburo alishinda wakati palikuwa na vyama vingi vya upinzani ikiwemo TLP?
Ukipitia matokeo ya uchaguzi mwaka 2005, ni majimbo hayafiki kumi kati ya majimbo zaidi ya mia mbili ndiyo ambayo kura za upinzani ukizijumlisha zinazidi za yule wa CCM. Kwa hiyo vyama kuungana sio sababu kuu ya kufanya upinzani ushinde.
Hivi ni kwa nini katika siku za hivi karibuni Chadema imekuwa ikiwakaribisha sana hawa wabunge wa CCM wanaitwa kuwa ni wapambanaji dhidi ya ufisadi. juzi tulisikia wakimwita Mwakyembe aungane nao
yes, ccm si chama cha uleta mabadiliko katika hali kama hii ya matajiri tu wanatumia kisingizio cha kupambana na ufisad kwa maslahi yao na vikampuni vyao mikobani.
Asaha inamaana kuwa unaona ni jambo zuri la Mwenyekiti wenu kumkaribisha KIMARO kujiunga na CHADEMA. Hivi kweli mnakitakia mema CHADEMA na nchi yetu Tanzania? Kuna wengi wa kuwakaribisha lakini sio KIMARO ninayemjua mimi.
Bwana mzee nadhani hii ni lugha ya picha. Anaekaribishwa hapa sio Kimaro, isipokuwa wapiga kura wa Kimaro, kwani angekuwa kimaro angekuwa approached popote pale na sio jimboni kwake.
Simuungi mkono Mwenyekiti kumkaribisha Kimaro. Kwani CHADEMA ina wagombea wazuri waadilifu ikiwemo vijana wenye kuweza kugombea hilo jimbo. Lakini naamini hapo Mwenyekiti ametumia lugha ya picha kuonyesha uozo wa CCM na kuvunja kila Kimaro aliposhikilia. Hivi mnadhani ni nani anafaa kugombea hilo jimbo?
Hivi ni kwa nini katika siku za hivi karibuni Chadema imekuwa ikiwakaribisha sana hawa wabunge wa CCM wanaitwa kuwa ni wapambanaji dhidi ya ufisadi. juzi tulisikia wakimwita Mwakyembe aungane naoClick to expand.
Kwani CHADEMA hawajatoa sababu za kuwakaribisha wabunge hao wa CCM?Mbona kila siku wanazitaja sababu hizo na hata katika habari hii Mbowe ameeleza bayana kwamba ni vigumu mno kwa wabunge wanaopambana na ufisadi kufanikiwa ndani ya CCM kwa vile chama hicho kinalea mafisadi.
Wakitumia helikopta mnawaita wabadhirifu. Wakiacha kutumia helikopta mnasema wizi mtupu. Acheni wivu. Chadema kimebaki kuwa chama chenyewe kinachoweza kufanya mikutano inayovuta wananchi wengi bila kutumia mafuso au misikiti. Nenda mwenyewe ukajionee.
Zamani, Mwaka 2005, Mwenyekiti wa chadema, Mbowe alipata kura 13,812 za urais jimbo la vunjo. Mwenyekiti wa TLP, Mrema alipata kura 12,587 za urais katika jimbo hilohilo. Ndani ya Vunjo, ALIKOZALIWA MREMA, waliomkubali Mbowe walikuwa wengi kuliko waliomkubali Mrema. Sio hivyo tu, majuzi katika uchaguzi mdogo wa kijiji ALIKOZALIWA MREMA Chadema imeshinda.
Zamani, Mwaka 2005, Aloyce Kimaro wa CCM alipata kura 30,554 na Jesse Makundi wa TLP alipata kura 21,771. Tofauti hapa ni maelfu sio "zisizozidi mia" kama unavyotaka tukuingiza mjini.
Hata hivyo, takwimu za 2005 zitakusaidia ku-evaluate vyama vinavyokuwa active wakati wa uchaguzi tu - Vyama kama UPDP, NRA, NLD, Jahazi Asilia, UMD, Makini etc. Vyama ambavyo viko active vinavyojijenga kila siku takwimu hizi haziwezi kukupa picha kamili. Ukitaka kujua chama kikuu cha upinzani Tanzania bara ni kipi waulize walioko madarakani, yaani CCM. Waulize Tambwe na Makamba wanaopoteza nusu ya muda wao kufukuzana na operation sangara. Mwulize Mama Nsilo Swai anavyohaha sasa Kilimanjaro na operation nyavu. Waulize vikao vyao vya usiku visivyoisha wanamjadili nani? Simple observation - hapa JF ni vyama vipi vinavyoongelewa kupita vingine? Utake usitake chama kikuu cha upinzani bara ni Chadema, na chama kikuu cha upinzani visiwani ni CUF.
README.md exists but content is empty. Use the Edit dataset card button to edit it.
Downloads last month
1
Edit dataset card