data
stringlengths
23
1.23M
rejected
bool
1 class
# Extracted Content JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA KILIMO Sehemu ya Uratibu wa Mazao ya Chakula na Tahadhari ya Awali © 2021 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TANI 18,196,733 WIZARA YA KILIMO Idara ya Usalama wa Chakula Sehemu ya Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Awali TAARIFA YA TATHMINI YA MWISHO YA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA MSIMU WA 2019/2020 NA UPATIKANAJI WA CHAKULA KWA MWAKA 2020/2021 i YALIYOMO YALIYOMO ....................................................................................................................... i SURA YA KWANZA ....................................................................................................... 1 1.0 UTANGULIZI ........................................................................................................ 1 SURA YA PILI ................................................................................................................. 2 2.0 UNYESHAJI WA MVUA KATIKA MSIMU WA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA ................................................................................................................. 2 2.1 Mvua za Vuli: Oktoba – Desemba, 2019 ......................................................... 2 2.2 Unyeshaji wa mvua za Msimu: Novemba, 2019 – Aprili, 2020 .................... 3 2.3 Unyeshaji wa mvua za Masika: Machi – Mei, 2020 ....................................... 4 2.4 Ulinganifu wa Unyeshaji Mvua Msimu wa 2019/2020 na Misimu ya Nyuma 4 2.5 Matokeo ya Mvua Kwenye Shughuli za Kilimo na Uzalishaji kwa Msimu wa 2019/2020 .................................................................................................................. 5 2.6 Mwenendo wa Unyeshaji wa Mvua za Vuli na Matarajio ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula (Oktoba – Desemba, 2020) ........................................................ 6 2.6.1 Ulinganifu wa Unyeshaji wa Mvua za Vuli Msimu wa 2020/2021 na Msimu wa 2019/2020 ................................................................................................................. 6 2.6.2 Matokeo ya mvua za Vuli, 2020 kwenye shughuli za kilimo na uzalishaji . 7 2.6.3 Matarajio ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula kwa Msimu wa mvua za Vuli 2020/2021 ................................................................................................................ 8 2.7 Mwenendo wa Unyeshaji wa Mvua za Msimu wa 2020/2021 ...................... 8 SURA YA TATU ............................................................................................................ 10 3.0 LENGO LA TATHMINI ...................................................................................... 10 ii 3.1 Lengo kuu ........................................................................................................... 10 3.2 Malengo Mahsusi .............................................................................................. 10 SURA YA NNE .............................................................................................................. 11 4.0 METHODOLOJIA .............................................................................................. 11 SURA YA TANO ........................................................................................................... 13 5.0 MATOKEO YA TATHMINI ............................................................................... 13 5.1 Mchango wa Mazao Mbalimbali Katika Uzalishaji wa Chakula Kitaifa Kwa Msimu wa 2019/2020 ................................................................................................... 15 5.2 Mtiririko wa viwango vya utoshelevu Nchini .................................................. 15 5.3 Hali ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Viwango vya Utoshelevu Kimkoa ........................................................................................................................... 16 5.4 Maeneo Yenye dalili za kuwa na Upungufu wa Chakula Nchini ................ 20 SURA YA SITA ............................................................................................................. 21 6.0 MWENENDO WA BEI KWA BAADHI YA MAZAO YA CHAKULA HADI KUFIKIA TAREHE 31 DESEMBA, 2020. ................................................................. 21 SURA YA SABA ........................................................................................................... 23 7.0 UZALISHAJI NA BIASHARA YA MAZAO YA CHAKULA WAKATI WA JANGA LA COVID-19 .................................................................................................. 23 7.1 Mikakati ya Uhakika wa Usalama wa Chakula na Biashara ....................... 23 SURA YA NANE ........................................................................................................... 24 8.0 CHANGAMOTO ZA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA KATIKA MSIMU WA 2019/2020 NA UPATIKANAJI WA CHAKULA KWA MWAKA 2020/2021 ...................................................................................................................... 24 iii 8.1 Changamoto za Uzalishaji wa Mazao ya Chakula katika Msimu wa 2019/2020 ...................................................................................................................... 24 8.2 Changamoto za Ukusanyaji waTakwimu na Taarifa za Mazao ya Chakula 24 SURA YA TISA ............................................................................................................. 26 9.0 HITIMISHO NA USHAURI ............................................................................... 26 VIAMBATISHO ............................................................................................................. 28 iv ORODHA YA VIELELEZO Kielelezo Na. 1: Kiwango cha unyeshaji na mtawanyiko wa mvua kwa msimu mzima wa 2019/2020 kuanzia Tarehe 1 Septemba, 2019 – 31 Mei, 2020 ......................... 4 Kielelezo Na. 2: Viwango cha unyeshaji na mtawanyiko wa mvua kwa kipindi cha kuanzia Tarehe 01 Oktoba – 31 Desemba, 2020 ............................................................ 7 Kielelezo Na. 3 Mchango wa mazao mbalimbali katika Upatikanaji wa Chakula kwa mwaka 2019/2020 .............................................................................................................. 15 Kielelezo Na. 4: Mtiririko wa Viwango vya Utoshelevu Kuanzia Mwaka 2009/2010 hadi 2020/2021 ....................................................................................................... 16 Kielelezo Na. 5: Ramani inayoonesha Viwango vya Utoshelevu wa Mazao ya Chakula ........................................................................................................................................ 18 Kielelezo Na. 6: Mwenendo wa bei za mazao ya mahindi, mchele na maharage 2019 na 2020 .............................................................................................................................. 22 ORODHA YA JEDWALI Jedwali Na. 1: Mchango wa mvua za Vuli kwa Kawaida na Sasa ........................................ 2 Jedwali Na. 2: Mchango wa Uzalishaji wa Mazao ya Vuli Tarajiwa ..................................... 8 Jedwali Na. 3: Uzalishaji mazao ya Chakula kwa Msimu wa 2019/2020 Zao kwa zao na Mahitaji ya Chakula kwa Mwaka 2020/2021(Tani) Kwa Mlinganishao wa Nafaka (Grain Equivalent). ........................................................................................................ 14 Jedwali Na. 4: Tathmini ya Mwisho ya Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021 .................................................................................................................................... 17 Jedwali Na. 5: Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuzingatia Mkoa ulioongoza ......... 19 Jedwali Na. 6: Mikoa yenye Halmashauri zenye maeneo yenye dalili zitakazosababisha kuwepo na upungufu wa Chakula .......................................................... 20 1 SURA YA KWANZA 1.0 UTANGULIZI Idara ya Usalama wa Chakula kupitia Sehemu ya Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Awali (Crop Monitoring and Early Warning Section) hufanya shughuli za ufuatiliaji na ukusanyaji wa takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusiana na Usalama wa Chakula nchini. Takwimu na taarifa hizo ni pamoja na:- hali ya unyeshaji wa mvua, ukuaji wa mazao shambani, athari katika ukuaji wa mazao zinazoweza kusababishwa na visumbufu, mwenendo wa bei na upatikanaji wa chakula, hali ya biashara ya mazao ya chakula (export & import), akiba ya mazao (stocks) na utoaji wa taarifa za hali ya chakula nchini. Shughuli hizi hufanyika kwa kutumia Mfumo wa Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Awali (Crop Monitoring and Early Warning System – CMEWS) ambapo nyenzo (tools) mbalimbali hutumika katika ukusanyaji wa takwimu na taarifa hizo. Tathmini ya Mwisho (Final Food Crop Production Assessment) ya uzalishaji na upatikanaji wa chakula kwa kawaida hufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba kila mwaka. Mazao makuu ya chakula ambayo yanaratibiwa kwa sasa ni mahindi, mpunga, mtama, uwele, ulezi, ngano, ndizi, muhogo, viazi vitamu, viazi mviringo, maharage, mbaazi, kunde, choroko, karanga na njugumawe. Kutokana na utaratibu huu, Wataalam wa Idara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) hufanya Tathmini hiyo nchini kila msimu/mwaka. Katika msimu wa 2019/20201, Idara imefanya tathmini hii kuanzia mwezi Desemba, 2020 – Januari, 2021. Katika tathmini hiyo, takwimu na taarifa mbalimbali za uzalishaji na upatikanaji wa mazao makuu ya chakula kutoka Halmashauri zote za Tanzania Bara zilikusanywa na kufanyiwa uchambuzi wa kina na kutolewa taarifa. 1 Hapa nchini, msimu wa uzalishaji huanza kuhesabiwa kuanzia katikati ya mwezi Septemba ya mwaka husika hadi katikati ya mwezi Mei ya mwaka unaofuata (Mfano Septemba, 2020 hadi Mei, 2021), Aidha kila msimu hupitia unyeshaji wa mvua kama inavyoonesha yaani mvua za Vuli –Septemba-Desemba, Msimu –Desemba-Mei, na Masika-Machi –Mei. 2 SURA YA PILI 2.0 UNYESHAJI WA MVUA KATIKA MSIMU WA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA Unyeshaji wa mvua hapa nchini umegawanyika katika sehemu mbili ambapo kuna maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka (Msimu) na maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Vuli na Masika). 2.1 Mvua za Vuli: Oktoba – Desemba, 2019 Mvua za Vuli kwa kawaida huanza kunyesha wiki ya pili ya mwezi Oktoba na kuisha wiki ya tatu ya mwezi Desemba kila mwaka kwa maeneo yanayopata mvua hizo ambayo ni mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Pwani, Dar es Salaam na maeneo ya Kaskazini mwa mikoa ya Morogoro, Kigoma na Shinyanga. Aidha, mwenendo wa unyeshaji wa mvua hizo umekuwa ukibadilika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na hivyo kuathiri Mikoa inayopata mvua hizo kama inavyoonekana katika Jedwali Na.1. Jedwali Na. 1: Mchango wa mvua za Vuli kwa Kawaida na Sasa SN MKOA Mchango wa mvua za Vuli kawaida (normal ) Mchango wa mvua za Vuli kwa Sasa (current ) (%) 1 Arusha 20 10 2 Pwani 10 5 3 Dar es salaam 10 2 4 Geita 55 50 5 Kagera 80 75 6 Kilimanjaro 35 10 7 Mara 45 35 8 Morogoro 15 12 9 Mwanza 55 50 10 Shinyanga 7 3 11 Simiyu 7 5 12 Tanga 20 13 Chanzo: Idara ya Usalama wa Chakula-Sehemu ya Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Awali 3 Mavuno ya msimu wa Vuli huingia sokoni katikati ya msimu wa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua na hivyo kupunguza makali ya upatikanaji wa chakula kutokana na bei za vyakula kushuka. Katika kipindi cha mwaka 2019 Mvua za Vuli ziliwahi kunyesha mapema zaidi, wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba katika maeneo ya Ukanda wa ziwa Viktoria pamoja na maeneo ya Pwani ya Kaskazini, na kuendelea kunyesha kwa mtawanyiko mzuri katika maeneo hayo. Aidha, kulikuwa na matukio ya unyeshaji wa mvua kubwa kupita kiasi, hali iliyosababisha mafuriko na maji kutuama katika maeneo mengi hususan mikoa ya Morogoro na Pwani na baadhi ya maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria. Ingawa mvua zilianza kunyesha kwa kuchelewa na kwa mtawanyiko usioridhisha katika maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), ziliendelea kunyesha vizuri na kwa kiwango cha juu ya wastani kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha na Manyara. Mvua hizo ziliendelea kunyesha hadi katikati ya mwezi Februari, 2020 katika maeneo hayo. Aidha, katika baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini, mvua hizo, ziliendelea kunyesha na kuungana na mvua za Masika kwa msimu wa 2019/2020. Pamoja na changamoto za mafuriko zilizojitokeza na kuathiri uzalishaji wa baadhi ya mazao hususan maharage, kwa ujumla uzalishaji wa mazao ya chakula kwa maeneo yanayopata mvua hizo ulikuwa mzuri. 2.2 Unyeshaji wa mvua za Msimu: Novemba, 2019 – Aprili, 2020 Mvua za Msimu kwa kawaida huanza kunyesha wiki ya tatu ya mwezi Novemba na kuisha wiki ya nne ya mwezi Aprili ya mwaka unaofuata kwa maeneo yenye msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Maeneo hayo ni ya mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Morogoro Shinyanga na Kigoma. Msimu wa 2019/2020, mvua za Msimu zilianza wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2019 kwenye maeneo mengi yanayopata mvua hizo. Katika baadhi ya maeneo 4 ya mikoa ya Kigoma na Katavi, mvua hizo ziliwahi kunyesha kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2019 na ziliendelea vizuri kwa mtawanyiko wa kuridhisha katika maeneo mengi. Kwa ujumla, unyeshaji wa mvua hizo ulikuwa wa juu ya kiwango cha wastani katika maeneo yote, ambapo hata katika kipindi cha mwezi Februari, ambacho kwa kawaida huwa kinakuwa kikavu, mvua ziliendelea kunyesha. Mvua hizo ziliendelea kunyesha hadi wiki ya tatu ya mwezi Mei, 2020 katika baadhi ya maeneo. 2.3 Unyeshaji wa mvua za Masika: Machi – Mei, 2020 Mvua za Masika kwa kawaida huanza kunyesha wiki ya pili ya mwezi Machi na kuisha wiki ya tatu ya mwezi Mei kila mwaka kwa maeneo yanayopata mvua hizo ambayo pia hupata mvua za Vuli. Katika msimu wa 2019/2020, mvua za Masika zilianza mapema zaidi kuanzia wiki ya nne ya mwezi Februari, 2020 ambapo, hadi kufikia mwezi Machi, 2020 mvua hizo zilikuwa tayari zimeenea katika maeneo mengi na ziliendelea kunyesha kwa kiwango cha juu ya wastani takriban katika maeneo yote. 2.4 Ulinganifu wa Unyeshaji Mvua Msimu wa 2019/2020 na Misimu ya Nyuma Unyeshaji wa mvua kwa msimu wa 2019/ 2020 ulikuwa ni wa kipekee kwa kuwa mvua zilinyesha kwa kiwango cha juu ya wastani takriban katika maeneo yote ya nchi. Maeneo yote ya nchi yalipata zaidi ya mm 1,000 za mvua isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Manyara na Arusha, ambayo yalipata mm 600 – 1000 za mvua (Kielelezo Na. 1). Kielelezo Na. 1: Kiwango cha unyeshaji na mtawanyiko wa mvua kwa msimu mzima wa 2019/2020 kuanzia Tarehe 1 Septemba, 2019 – 31 Mei, 2020 5 Ramani inaonesha kiasi cha mvua (mm) kilichonyesha kipindi cha msimu kuanzia Septemba 2019-Mei 2020 Ramani inaonesha tofauti ya mvua (mm) iliyonyesha kipindi cha msimu kuanzia Septemba 2019-Mei 2020 ikilinganishwa na wastani Chanzo: GeoWRSI, 2020-TMA Msimu wa 2019/2020 umechukua nafasi ya nne kwa kurekodi kiasi cha mvua nyingi tangu mwaka 1970 ikilinganishwa na misimu ya nyuma. Misimu iliyokuwa na mvua nyingi zaidi tangu mwaka 1970 ni; 1982/1983, 1997/1998 na 2006/2007 ambapo mvua za msimu wa 1997/1998 ziliambatana na tukio la El- Niño. Takriban maeneo yote ya nchi yalipata mvua nyingi zaidi zenye mtawanyiko wa kuridhisha katika msimu huu ikilinganishwa na misimu mingine. 2.5 Matokeo ya Mvua Kwenye Shughuli za Kilimo na Uzalishaji kwa Msimu wa 2019/2020 Katika kipindi cha Oktoba, 2019 – Aprili, 2020 maeneo mengi ya nchi yalipata unyevunyevu wa kutosha kwenye udongo kutokana na mvua zilizonyesha kwa kiwango cha juu ya wastani. Hata hivyo, baadhi ya maeneo yalipata unyevunyevu uliokithiri na kusababisha athari katika shughuli za kilimo. Maeneo mengine yalipata mafuriko na maji kutuama, hali iliyosababisha uharibifu na upotevu wa mazao hasa katika mikoa ya Pwani, Lindi, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Mtwara, Ruvuma, Morogoro, Rukwa, Mbeya, 6 Kilimanjaro, Kagera, Songwe,Iringa na Katavi. Athari hizo zilionekana zaidi katika mazao kama vile maharage, mihogo, viazi na mahindi katika baadhi ya maeneo.Vilevile, upotevu wa mbolea ardhini (leaching), uharibifu wa miundombinu ya kilimo, wakulima kushindwa kuandaa mashamba kutokana na kutuama kwa maji, upotevu wa mali na maisha ya watu pamoja na mifugo zilijitokeza katika baadhi ya maeneo. Pamoja na athari hizo zilizojitokeza, wapo wakulima katika maeneo mengine waliotumia fursa ya unyevunyevu uliokuwepo baada ya mafuriko na kutuama kwa maji kuendelea na shughuli za kilimo baada ya msimu wa mvua kuisha na hivyo kuchangia katika uzalishaji wa mazao ya chakula. 2.6 Mwenendo wa Unyeshaji wa Mvua za Vuli na Matarajio ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula (Oktoba – Desemba, 2020) Katika msimu wa mvua za Vuli 2020/2021, mvua zilianza mapema mwezi Septemba katika maeneo ya mikoa ya Mara na Kagera, na kutawanyika katika maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa Viktoria pamoja na maeneo machache ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam katika kipindi cha mwezi Oktoba. Mvua hizi zimeendelea kunyesha kwa kiwango cha juu ya wastani katika maeneo mengi hasa ya Kanda ya Ziwa Viktoria. Katika maeneo mengine ya Pwani ya Kaskazini na Kanda ya Kaskazini Mashariki, mvua zilichelewa kuanza (Novemba) na zimeendelea kwa mtawanyiko hafifu. Mvua hizi zinatarajiwa kuendelea kunyesha hadi katika kipindi cha mwezi Januari, 2021. 2.6.1 Ulinganifu wa Unyeshaji wa Mvua za Vuli Msimu wa 2020/2021 na Msimu wa 2019/2020 Viwango vya mvua za Vuli kwa msimu wa 2020/2021 umekuwa ni wa chini ikilinganishwa na mvua za Vuli za msimu wa 2019/2020 hasa katika maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini Mashariki na mikoa ya Pwani ya Kaskazini. Hadi kufikia Desemba 31 2020, viwango vilivyopatikana ni milimita 51 – 200 kwa 7 mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, na milimita 200 – 300 katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Tanga ikilinganishwa na milimita 200 – 500 na 500 – 1000 kwa mwaka 2019 mtawalia. Viwango hivyo ni sawa na mvua za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo hayo (Kielelezo Na. 2). Kielelezo Na. 2: Viwango cha unyeshaji na mtawanyiko wa mvua kwa kipindi cha kuanzia Tarehe 01 Oktoba – 31 Desemba, 2020 Ramani inaonesha kiasi cha mvua (mm) kilichonyesha kipindi cha msimu kuanzia Oktoba -Desemba 2020 Ramani inaonesha tofauti ya mvua (mm) iliyonyesha kipindi cha msimu kuanzia Oktoba -Desemba 2020 ikilinganishwa na wastani Ramani inaonesha asilimia ya unyeshaji wa mvua kwa wastani (75%-125%) Chanzo: GeoWRSI Januari, 2021-TMA 2.6.2 Matokeo ya mvua za Vuli, 2020 kwenye shughuli za kilimo na uzalishaji Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2020 maeneo mengi yanayopata mvua za Vuli yalipata unyevunyevu mzuri kwenye udongo kutokana na mvua zilizonyesha katika kiwango cha juu ya wastani hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Viktoria. Mazao takribani yote yamestawi vizuri na mwelekeo unaonesha yatachangia upatikanaji wa chakula katika kipindi cha mwezi Februari na kuendelea kabla ya mavuno mengine kuanzia mwezi Mei, 2021 isipokuwa zao la maharage tu ambalo limepata changamoto ya mvua kuwa nyingi na hivyo kuathiri uzalishaji wa zao hilo. Aidha, katika maeneo mengine yaliyosalia yanayopata mvua hizo, mtawanyiko mbaya wa mvua unaweza kuchangia kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula. Hata hivyo, baadhi ya mikoa ya kanda ya Ziwa imeshaanza kupata mavuno ya vuli. 8 2.6.3 Matarajio ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula kwa Msimu wa mvua za Vuli 2020/2021 Kwa kipindi cha mwezi Febuari, 2021 nchi inatarajia kupata kiasi cha tani 2,166,908 cha mavuno ya vuli toka kwenye mikoa inayopata mvua za vuli Jedwali Na. 2. Jedwali Na. 2: Mchango wa Uzalishaji wa Mazao ya Vuli Tarajiwa Arusha 591,276 20 35.2 321,615 Arusha Pwani 369,451 10 16.5 73,222 Pwani Dar es salaam 37,787 10 1.8 691 Dar es salaam Geita 472,456 55 49.3 459,698 Geita Kagera 1,129,966 80 9.8 122,546 Kagera Kilimanjaro 282,448 35 45.5 235,528 Kilimanjaro Mara 1,198,717 45 12.8 175,947 Mara Morogoro 966,505 15 13.6 151,513 Morogoro Mwanza 972,176 55 16.8 196,476 Mwanza Simiyu 550,651 7 35.0 296,577 Simiyu Tanga 754,635 20 15.0 133,095 Tanga Jumla ya Uzalishaji Mikoa ya Vuli- Msimu 2019/2020 7,326,067 36 22.8 Jumla ya Chakula Tanzania 18,196,733 15 10.6 2,166,908 Matarajio ya Uzalishaji (Tani)- Vuli 2020/2021 Mchango wa Uzalishaji wa Mazao ya Vuli Tarajiwa 2020/2021 MIKOA YA VULI Uzalishaji katika (Tani) Msimu 2019/2020 Mchango wa uzalishaji wa Mazao ya Vuli kwa Kawaida (%) Mchango wa Uzalishaji wa Mazao ya Vuli kwa Sasa (%) Mchango wa Uzalishaji wa Mazao ya Vuli tarajiwa (Tani) Msimu 2020/2021 MIKOA YA VULI Matarajio ya uzalishaji wa mazao ya chakula katika Msimu wa Vuli 2020/2021 (Oktoba –Desemba, 2020) kwa mazao ya mahindi, mtama, uwele, maharage, kunde, karanga, choroko, njugu mawe, viazi vitamu na viazi mviringo 2.7 Mwenendo wa Unyeshaji wa Mvua za Msimu wa 2020/2021 Katika msimu wa 2020/2021, mvua za Msimu zilianza mapema katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2020 kwenye maeneo ya mkoa wa Kigoma na Kusini mwa mkoa wa Morogoro na kuendelea katika wiki ya pili kwenye maeneo mengine yaliyosalia isipokuwa katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara, ambapo zilianza wiki ya tatu ya mwezi Desemba. Kwa ujumla, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba, mwenendo wa unyeshaji wa mvua hizo umeendelea kwa kiwango cha juu ya wastani katika maeneo mengi, isipokuwa mikoa ya Iringa, Morogoro (Kusini), Mtwara, na baadhi ya maeneo katika mkoa wa Lindi ambapo zimenyesha kwa kiwango cha 9 chini ya wastani. Aidha, hali ya mazao shambani ni nzuri katika maeneo mengi yanayopata mvua hizo. Kwa upande wa maeneo ya Kusini mwa nchi; mvua zilichelewa kuanza hivyo kusababisha kuchelewa kwa shughuli za upandaji wa mazao ya chakula. Vilevile, hali ya malisho ya mifugo na upatikanaji wa maji umeendelea kuwa mzuri katika maeneo yote ya nchi. 10 SURA YA TATU 3.0 LENGO LA TATHMINI 3.1 Lengo kuu Lengo kuu ni kupata uzalishaji halisi wa mazao ya chakula katika msimu wa kilimo wa 2019/2020 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2020/2021 ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki za maamuzi kuhusiana na hali ya chakula nchini. 3.2 Malengo Mahsusi Malengo mahsusi ni pamoja na; 1. Kuhuisha taarifa za uzalishaji wa mazao ya chakula na hali ya chakula hadi kufikia tarehe 31 Agosti, 2020; 2. Kukusanya takwimu za malengo ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2020/2021; 3. Kukusanya takwimu za mwenendo wa uzalishaji wa mazao ya chakula kwenye maeneo yanayopata mvua za Vuli katika msimu wa 2020/2021; 4. Kufuatilia taarifa za masoko na mwenendo wa bei za mazao ya chakula na mifugo, hali ya maji na malisho na upatikanaji wa chakula katika Halmashauri zote Tanzania bara na; 5. Kufuatilia akiba ya mazao ya chakula katika maghala ya wafanya biashara na wakulima. 11 SURA YA NNE 4.0 METHODOLOJIA Tathmini hii ilihusisha mapitio ya nyaraka na taarifa mbalimbali zinazohusiana na masuala ya usalama wa chakula na kufuatiwa na ukusanyaji wa takwimu na taarifa za uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka katika Mamlaka za Mikoa na ngazi ya Halmashauri (katika vijiji vya kilimo vya sampuli kama vilivyobainishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu). Jumla ya timu tisa (9) za Wataalam wa Wizara ya Kilimo, Idara ya Usalama wa Chakula - Sehemu ya Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Awali zilikutana na Wataalamu wa Mikoa miwili hadi mitatu kutoka Idara za Kilimo katika Mikoa 26 na Halmashauri 184. Timu hizo zilitumia nyenzo za ukusanyaji wa takwimu na taarifa za Mfumo wa Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Awali (CMEWS) na kupitia, kujadili na kuhuisha takwimu na taarifa za awali za hadi mwezi Mei 2020 kuhusu uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2019/2020 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2020/2021. Vilevile, ukusanyaji wa takwimu za malengo na matarajio ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwenye maeneo yanayopata mvua za Vuli kwa msimu wa 2020/2021 ili kubaini mchango wake katika upatikanaji wa chakula nchini kwa mwaka 2020/2021 ulifanyika. Uchambuzi, uchakataji na uandaaji wa taarifa ulihusisha Wataalam kutoka Idara ya Usalama wa Chakula kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Katika uchambuzi na uchakataji wa takwimu mambo muhimu yafuatayo yamezingatiwa: 1. Kigezo cha Upimaji wa Kiwango cha Utoshelevu wa Chakula (Self Sufficiency Ratio – SSR): Kigezo hiki hukokotolewa kwa kuangalia uwiano wa uzalishaji na mahitaji ambapo: Kiwango cha asilimia 0 - 99 inaashiria Upungufu wa chakula; asilimia 100 – 119 inaashiria Utoshelevu wa chakula na asilimia 120 na zaidi inaashiria Ziada ya chakula; 12 2. Ukokotoaji wa Mahitaji ya Chakula: Mahitaji ya chakula kwa mwaka hukokotolewa kwa kuzingatia idadi ya watu kwa mwaka wa chakula2 (mid-year population),3 mahitaji ya chakula (food consumption requirement) na mahitaji mengine yasiyokuwa ya chakula cha binadamu (non-food requirement) kama vile mbegu, chakula cha mifugo, biashara na upotevu wa mazao ambayo ni sehemu ya asilimia ya chakula kilichozalishwa; 3. Ukokotoaji wa Ziada/Uhaba: Ziada au Upungufu hukokotolewa kutokana na uzalishaji wa msimu husika kutoa mahitaji ya chakula ya mwaka husika (Production less Requirement) ambapo jibu linaweza kuwa chanya (+) inayoashiria ziada au hasi (-) inayoashiria upungufu kulingana na uzalishaji ulivyokuwa na 4. Taarifa mbalimbali za athari za visumbufu na unyeshaji wa mvua katika maeneo mbalimbali nchini hususan mafuriko na kutuama kwa maji. 2 Hapa nchini, mwaka wa chakula huanzia tarehe 1 Juni hadi tarehe 31 Mei ya mwaka unaofuata, mfano Juni, 2020 hadi tarehe 31 Mei, 2021 kwa msimu wa uzalishaji 2019/2020. 3 ‘Mid-Year Population’ ni Idadi wa watu watakao kuwepo katikati ya mwaka husika wa chakula. Hii hukokotolewa kwa kutumia viwango vya ukuaji wa idadi ya watu (population growth rate) kulingana na Sensa ya idadi ya watu inayotolewa na NBS. 13 SURA YA TANO 5.0 MATOKEO YA TATHMINI Matokeo yanaonesha kuwa, hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kitaifa na kimkoa katika msimu wa 2019/2020 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2020/2021 umefikia tani 18,196,733 kwa mlinganisho wa nafaka (Grain Equivalent) ambapo nafaka ni tani 10,869,596 na yasiyonafaka tani 7,327,137. Ikilinganishwa na msimu wa 2018/2019 ambapo uzalishaji ulikuwa tani 16,293,637 kumekuwa na ongezeko la uzalishaji wa tani 1, 903,096 ambalo ni sawa na asilimia 10.5. Nafaka imeongezeka kutoka tani 8,896, 830 hadi 10,869,596 sawa na asilimia 18.1 wakati uzalishaji wa yasiyonafaka umepungua kutoka tani 7,396,807 hadi tani 7,327,137 sawa na asilimia 0.9. Aidha, kwa upande wa mahindi, uzalishaji umeongezeka kutoka tani 5,652,005 hadi tani 6,711,002 na mchele kutoka tani 2,063,598 hadi tani 3,038,080 sawa na asilimia 15.8 na 32.1 mtawalia. Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2020/2021 ni tani 14,404,171 ambapo tani 9,191,116 ni za nafaka na tani 5,213,055 ni za yasiyonafaka. Mahitaji hayo yakilinganishwa na uzalishaji yanaonesha kuwa nchi imezalisha ziada ya tani 3,792,562 za chakula ambapo tani 1,678,480 ni za nafaka na tani 2,114,082 ni za yasiyonafaka Jedwali Na.3. Pamoja na kushuka kwa uzalishaji wa yasiyonafaka, nchi imeendelea kuwa na utengamano wa usalama wa chakula wa viwango tofauti kimkoa. Aidha, hali ya uwepo na upatikanaji wa chakula nchini kwa sasa ni nzuri. 14 Jedwali Na. 3: Uzalishaji mazao ya Chakula kwa Msimu wa 2019/2020 Zao kwa zao na Mahitaji ya Chakula kwa Mwaka 2020/2021(Tani) Kwa Mlinganishao wa Nafaka (Grain Equivalent). Nafaka Mahindi Mtama&Malezi Mchele Ngano Nafaka Uzalishaji 6,711,002 1,043,237.9 3,038,080 77,276 10,869,596 Mahitaji 5,790,031 2,032,437.4 1,094,119 274,529 9,191,116 Uhaba (-)/Ziada(+) 920,971 -989,200 1,943,961 -197,252 1,678,480 SSR (%) 116 51 278 28 118 Sinafaka Mikunde Ndizi Muhogo Viazi Yasiyonafaka Uzalishaji 1,895,077 1,358,083 2,427,190 1,646,788 7,327,137 Mahitaji 819,471 963,064 2,404,512 1,026,009 5,213,055 Uhaba (-)/Ziada(+) 1,075,606 395,019 22,678 620,779 2,114,082 SSR (%) 231 141 101 161 141 JUMLA Nafaka Yasiyonafaka Uzalishaji 10,869,596 7,327,137 Mahitaji 9,191,116 5,213,055 Uhaba (-)/Ziada(+) 1,678,480 2,114,082 SSR (%) 118 141 g ( q ) y ( , ) 126 JUMLA 18,196,733 14,404,171 3,792,562 Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2019/2020 na Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021. *** Chakula hiki hakikujumuisha akiba ya chakula kutoka kwa wafanyabiashara (private stocks), akiba ya NFRA na CPB (public stocks) na akiba wanayoshikilia wananchi (farm retation) kutokana na ugumu wa sekta binafsi na wananchi kutotoa ushirikiano wa kuzipata takwimu hizi. Ikilinganishwa na matokeo ya utabiri wa awali wa uzalishaji wa mazao ya Chakula (Preliminary Food Crop Production Forecast) 2019/2020, uzalishaji umeongezeka kwa tani 454,345 sawa na asilimia 2.5 (kutoka tani 17,742,388 hadi tani 18,196,733). 15 5.1 Mchango wa Mazao Mbalimbali Katika Uzalishaji wa Chakula Kitaifa Kwa Msimu wa 2019/2020 Uzalishaji katika msimu wa 2019/2020 unaonesha kuwa Kitaifa, mahindi yamechangia asilimia 36.9, mchele asilimia 16.7, muhogo asilimia 13.3, na mazao mengine ni kama inavyoonekana katika Kielelezo Na.3. Kielelezo Na. 3 Mchango wa mazao mbalimbali katika Upatikanaji wa Chakula kwa mwaka 2019/2020 Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2019/2020 na Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021 5.2 Mtiririko wa viwango vya utoshelevu Nchini Kwa kuzingatia Kigezo cha Upimaji wa Kiwango cha Utoshelevu (Self Sufficiency Ratio – SSR), matokeo yanaonesha kuwa kwa mwaka wa chakula 2020/2021, nchi imekuwa na kiwango cha Utoshelevu cha asilimia 126 ambacho ni cha juu zaidi kupatikana. Kiwango hiki kimeongezeka ikilinganishwa na mwaka wa chakula wa 2019/2020 ambapo nchi ilijitosheleza kwa asilimia 118 Kielelezo Na.4. Kulingana na vigezo vya upimaji wa kiwango cha utoshelevu, hali ya upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2020/2021 ni ya Ziada. Vilevile, tathmini imebainisha kuwa, viwango vya utoshelevu kwa mwaka wa chakula 2020/2021 ni asilimia 118 kwa mazao ya nafaka na asilimia 141 kwa mazao yasiyonafaka. 16 Kielelezo Na. 4: Mtiririko wa Viwango vya Utoshelevu Kuanzia Mwaka 2009/2010 hadi 2020/2021 Chanzo: Taarifa za Tathmini za Mwisho za Hali ya Chakula Nchini. 5.3 Hali ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Viwango vya Utoshelevu Kimkoa Kimkoa, hali ya chakula imekuwa ya kiwango cha Ziada kati ya asilimia 120 na 238 katika mikoa 14 ambayo ni Ruvuma, Rukwa, Songwe, Katavi, Njombe, Mbeya, Kigoma, Iringa, Kagera, Morogoro, Geita, Mtwara, Manyara na Simiyu; Utoshelevu kati ya asilimia 110 na 118 kwenye mikoa 11 ambayo ni Shinyanga, Singida, Dodoma, Mara, Lindi, Tabora, Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Arusha, na Mwanza; na Upungufu asilimia 2 katika mkoa wa Dar es salaam Jedwali Na.4, Kielelezo Na.5 na Kiambatisho Na. 1a na 1b. 17 Jedwali Na. 4: Tathmini ya Mwisho ya Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021 Mkoa Mavuno Mahitaji Upungufu/Zia da Kiwango cha utoshelevu (Nafaka) Mavuno Mahitaji Upungufu/ Ziada Kiwango cha utoshelevu (Yasiyonafa Mavuno Mahitaji Upungufu/Ziada Kiwang o cha Kujitos heleza 1 Ruvuma 930,204 371,943 558,261 250 337,277 159,688 177,589 211 1,267,480 531,630 735,850 238 Ruvuma 2 Rukwa 677,123 282,959 394,164 239 294,305 134,034 160,271 220 971,428 416,993 554,435 233 Rukwa 3 Songwe 561,823 259,359 302,464 217 253,357 124,883 128,473 203 815,180 384,242 430,937 212 Songwe 4 Katavi 317,977 137,718 180,259 231 119,077 69,490 49,587 171 437,055 207,208 229,846 211 Katavi 5 Njombe 355,109 162,920 192,189 218 114,731 72,966 41,765 157 469,840 235,886 233,954 199 Njombe 6 Mbeya 794,867 408,923 385,944 194 403,850 205,549 198,302 196 1,198,717 614,471 584,245 195 Mbeya 7 Kigoma 643,247 467,223 176,024 138 593,913 252,873 341,040 235 1,237,161 720,097 517,064 172 Kigoma 8 Iringa 294,687 187,907 106,780 157 177,769 105,442 72,328 169 472,456 293,348 179,108 161 Iringa 9 Kagera 179,272 481,723 -302,450 37 950,693 307,156 643,537 310 1,129,966 788,879 341,087 143 Kagera 10 Morogoro 758,613 452,334 306,279 168 207,892 254,387 -46,495 82 966,505 706,720 259,785 137 Morogoro 11 Geita 414,658 354,319 60,339 117 302,022 204,416 97,607 148 716,681 558,735 157,946 128 Geita Tanzania 10,869,596 9,191,116 1,678,480 118 7,327,137 5,213,055 2,114,082 141 18,196,733 14,404,171 3,792,562 126 Tanzania 12 Mtwara 80,725 210,934 -130,210 38 330,485 131,399 199,086 252 411,210 342,334 68,876 120 Mtwara 13 Manyara 442,091 329,673 112,418 134 175,919 185,157 -9,238 95 618,011 514,830 103,181 120 Manyara 14 Simiyu 486,259 323,453 162,806 150 107,203 172,747 -65,545 62 593,461 496,200 97,261 120 Simiyu 15 Shinyanga 393,626 295,919 97,707 133 157,025 171,757 -14,731 91 550,651 467,676 82,975 118 Shinyanga 16 Singida 428,555 287,758 140,797 149 90,616 155,157 -64,541 58 519,171 442,915 76,257 117 Singida 17 Dodoma 435,690 391,277 44,412 111 295,027 232,537 62,490 127 730,717 623,814 106,903 117 Dodoma 18 Mara 373,197 352,522 20,675 106 274,185 201,135 73,049 136 647,382 553,658 93,725 117 Mara 19 Lindi 152,449 154,915 -2,466 98 129,999 87,266 42,733 149 282,448 242,181 40,268 117 Lindi 20 Tabora 616,843 487,494 129,348 127 262,456 272,958 -10,502 96 879,298 760,452 118,846 116 Tabora 21 Tanga 457,736 422,954 34,782 108 296,899 231,595 65,304 128 754,635 654,549 100,086 115 Tanga 22 Pwani 93,934 198,629 -104,695 47 275,517 123,037 152,480 224 369,451 321,666 47,785 115 Pwani 23 Kilimanjaro 225,199 303,577 -78,378 74 331,394 182,312 149,081 182 556,592 485,889 70,703 115 Kilimanjaro 24 Arusha 296,645 335,716 -39,071 88 294,630 200,422 94,208 147 591,276 536,139 55,137 110 Arusha 25 Mwanza 453,683 549,600 -95,917 83 518,493 333,134 185,359 156 972,176 882,734 89,442 110 Mwanza 26 Dar es Salaam 5,384 979,367 -973,983 1 32,403 641,557 -609,155 5 37,787 1,620,925 -1,583,138 2 Dar es Salaam Mazao ya Nafaka (Tani) Mazao YasiyoNafaka (Tani) Jumla ya Mavuno Yote (Tani) Mkoa Na. Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2019/2020 na Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021. Ufunguo: Ziada Utoshelevu Upungufu 18 Kielelezo Na. 5: Ramani inayoonesha Viwango vya Utoshelevu wa Mazao ya Chakula Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Hali ya Uzalishaji wa mazao ya chakula Chakula kwa Mwaka 2019/2020. na Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021 Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuzingatia Mkoa ulioongoza katika uzalishaji wa mazao hayo kabla (takwimu kama zilivyowasilishwa) na baada ya uchambuzi wa takwimu Kitaifa ni kama inavyoonekana katika Jedwali Na.5. Ufunguo Ziada Utoshelevu Upungufu 19 Jedwali Na. 5: Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuzingatia Mkoa ulioongoza Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2019/2020 na Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021. 20 5.4 Maeneo Yenye dalili za kuwa na Upungufu wa Chakula Nchini Kulingana na tathmini ya mwisho ya uzalishaji wa mazao ya chakula Msimu wa 2019/2020 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2020/2021; matokeo yameonesha uwepo wa maeneo (pockets) yenye upungufu wa chakula katika Mikoa 3 yenye Halmashauri 7 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 6. Jedwali Na. 6: Mikoa yenye Halmashauri zenye maeneo yenye dalili zitakazosababisha kuwepo na upungufu wa Chakula Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2019/2020 na Upatikanaji wa Chakula kwa Mwaka 2020/2021. *** Pamoja na kwamba Mkoa wa Dar es Salaam unaonesha upungufu, Halmashauri zake hazioneshwi katika jedwali hili kwa kuwa eneo lake la uzalishaji ni dogo na linaendelea kupungua kutokana na kuendelea kukua kwa Jiji. Mkoa huo unapokea vyakula kutoka katika mikoa mingine na hivyo kuufanya kuwa salama wakati wote kwa upande wa upatikanaji wa chakula. 21 SURA YA SITA 6.0 MWENENDO WA BEI KWA BAADHI YA MAZAO YA CHAKULA HADI KUFIKIA TAREHE 31 DESEMBA, 2020. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2020, upatikanaji wa chakula sokoni umeendelea kuwa mzuri ambapo bei za mazao ya chakula hususan mahindi na mchele zimeendelea kushuka ikilinganishwa na bei za mazao hayo katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2019. Bei ya mahindi kwa gunia la kilo 100 ilikuwa shilingi za Kitanzania 56,984.00 kwa mwezi Desemba 2020 ikilinganishwa na shilingi za Kitanzania 86,461.00 kwa mwezi Desemba 2019. Kwa upande wa bei za mchele kwa gunia la kilo 100 ilikuwa shilingi za Kitanzania 147,492.00 kwa mwezi Desemba 2020 ikilinganishwa na shilingi za Kitanzania 187,799.00 mwezi Desemba 2019. Wastani wa bei ya maharage kwa kipindi cha nusu mwaka (Juni-Desemba) kwa mwaka wa chakula 2020/2021 imeonekana kuwa juu ikilinganishwa na wastani wa bei ya maharage kwa mwaka wa chakula 2019/2020 kwa kipindi kama hicho. Kupanda kwa bei ya maharage kumechangiwa na uzalishaji mdogo hasa katika kipindi cha masika na msimu ambao ulisababisha maharage mengi kuozea shambani kutokana na mvua nyingi. Pamoja na hali hiyo, bei ya maharage kwa gunia la kilo 100 kwa mwezi Desemba 2020 imeonekana kushuka (Shilingi za Kitanzania 204,999.00) ikilinganishwa na bei ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2019 ambayo ilikuwa shilingi za Kitanzania 209,139.00, sawa na asilimia 2. Kushuka huku kwa bei ya maharage kwa kipindi hicho kumechangiwa na kuanza kuingia sokoni kwa maharage mapya ya msimu wa Vuli 2020/2021. Mwenendo wa bei hizo, unatarajiwa kuendelea kushuka katika kipindi cha mwezi Februari 2021 kwenye baadhi ya maeneo kutokana na matarajio ya uvunaji wa mazao ya chakula kwenye maeneo yanayopata mvua za Vuli Jedwali Na.7. 22 Jedwali Na. 7: Mwenendo wa bei za mazao ya mahindi, mchele na maharage 2019 na 2020 2019 49,341 50,812 50,016 54,769 58,985 60,675 62,573 66,458 71,923 82,206 84,956 86,461 2020 93,021 85,038 64,476 59,749 56,355 56,914 58,362 56,627 54,856 57,188 57,885 56,984 2019 159,634 167,567 166,782 167,347 167,387 163,838 162,063 162,119 171,318 182,428 185,279 187,799 2020 189,578 190,898 183,707 181,246 165,294 152,259 148,992 147,070 143,829 139,603 144,659 147,492 2019 161,850 163,204 162,922 161,931 164,200 164,587 162,746 161,881 170,229 178,786 196,527 209,139 2020 217,613 210,208 180,682 189,560 204,493 205,234 192,772 194,553 198,746 200,952 207,382 204,999 AGOSTI SEPTEMBAOKTOBA NOVEMBADESEMBA Maharage MWAKA ZAO JANUARI FEBRUARIMACHI Mwenendo wa bei za mazao ya chakula, kwa mwaka 2019 na 2020 (Bei (TSh) kwa Gunia la Kilo 100) Mahindi Mchele APRILI MEI JUNI JULAI Chanzo: Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2018 na 2019 23 SURA YA SABA 7.0 UZALISHAJI NA BIASHARA YA MAZAO YA CHAKULA WAKATI WA JANGA LA COVID-19 Ugonjwa wa COVID-19 umekuwa tishio kubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo shughuli za uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya chakula duniani. Ugonjwa huo umeleta athari katika masuala ya usalama wa chakula katika nchi mbalimbali duniani ambapo shughuli za kilimo na biashara ziliathirika kwa kiasi kikubwa. Taarifa zilizopatikana kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara zimeonesha kuwa, uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2019/2020 na upatikanaji wake kwa mwaka 2020/2021 haujaathirika na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa huo. Aidha, kwa upande wa biashara ya mazao ya chakula, athari zilionekana katika masoko ya kimataifa kutokana na zuio la kuvuka mipaka ya baadhi ya nchi na hivyo kusababisha baadhi ya bidhaa za mazao ya chakula kukwama na kuharibikia mipakani hasa mazao ya bustani. Hali hiyo iliathiri wadau wote katika mnyororo mzima wa thamani ya mazao ya chakula na bustani. 7.1 Mikakati ya Uhakika wa Usalama wa Chakula na Biashara  Kuendelea kuboresha mifumo ya uhifadhi wa mazao ya chakula katika ngazi zote;  Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazao ya chakula kuanzia ngazi ya kaya;  Kuimarisha skimu za stakabadhi za mazao ghalani ili kuongeza viwango vya mazao, kupunguza uharibifu na kuwawezesha wakulima kujikimu wakingojea bei nzuri;  Kuhamasisha kilimo cha kiangazi ili kuendelea kuongeza upatikanaji wa chakula na;  Kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ya usafirishaji wa mazao ya chakula na bidhaa zake kwenda nje ya nchi. 24 SURA YA NANE 8.0 CHANGAMOTO ZA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA KATIKA MSIMU WA 2019/2020 NA UPATIKANAJI WA CHAKULA KWA MWAKA 2020/2021 8.1 Changamoto za Uzalishaji wa Mazao ya Chakula katika Msimu wa 2019/2020 Licha ya kuwa na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula, bado wakulima na wataalam walikuwa na changamoto mbalimbali zilizosababisha kutofikiwa kwa malengo katika baadhi ya maeneo nchini. Changamoto hizi ni kama zilivyofafanuliwa hapo chini: (i) Unyeshaji wa mvua juu ya kiwango uliosababisha kutokea kwa mafuriko na kutuama kwa maji katika baadhi ya maeneo nchini hususan katika mikoa ya Morogoro, Lindi, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Singida, Katavi, Kagera, Tanga, Pwani, Songwe, Iringa, Mbeya na Rukwa. Hali hii imechangia kushuka kwa uzalishaji wa mazao hususan jamii ya mikunde na mizizi; (ii) Kupotea kwa mbolea (leaching) kulikosababishwa na unyeshaji wa mvua nyingi katika baadhi ya maeneo hususan mikoa ya Nyanda za juu Kusini hivyo kusababisha matumizi makubwa ya mbolea na kuongeza gharama za uzalishaji kwa mkulima; na (iii) Uvamizi wa visumbufu hususan Panya, Kwelea kwelea, Tembo na Nguruwe pori kwenye baadhi ya mashamba nchini 8.2 Changamoto za Ukusanyaji waTakwimu na Taarifa za Mazao ya Chakula Pamoja na kufanikiwa kwa zoezi hili la tathmini, zoezi lilikumbwa na changamoto mbalimbali katika ngazi za Mkoa na Halmashauri. Changamoto hizo ni kama; a) Ufinyu wa bajeti inayotengwa kwa ajili ya uratibu wa mazao shambani na tahadhari ya awali; b) Upungufu wa wataalamu wa kilimo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri; c) Wataalam katika ngazi hizo kubadilishwa mara kwa mara kunakosababisha kukosekana kwa uwezo wa ukusanyaji wa takwimu 25 za masuala ya usalama wa chakula kwa baadhi ya Wataalam katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri; d) Upungufu wa vitendea kazi kwa Wataalam wa kilimo kama pikipiki, kompyuta mpakato na kompyuta za mezani; na e) Kukosekana kwa mafunzo rejea ya mara kwa mara kwa Wataalam wa kilimo katika ngazi zote. 26 SURA YA TISA 9.0 HITIMISHO NA USHAURI Hali ya uzalishaji na upatikanaji wa mazao ya chakula nchini imeendelea kuwa nzuri katika kipindi cha miaka saba mfululizo (2014/2015 hadi 2020/2021) kufuatia uzalishaji mzuri wa mazao ya chakula. Katika kipindi hicho, nchi imekuwa na kiwango cha utoshelevu kuanzia asilimia 120 na zaidi ikilinganishwa na mahitaji ya chakula nchini isipokuwa kwa mwaka 2019/2020 ambapo kiwango cha utoshelevu kilikuwa asilimia 118. Katika kipindi hicho, nchi imekuwa ikizalisha ziada ya chakula kati ya tani 1, 854,292 hadi tani 3, 792,562. Kwa kipindi cha mwaka wa chakula 2020/2021, nchi imefikia kiwango cha utoshelevu cha asilimia 126. Kiwango hiki kinathibitisha kwamba, uwepo wa janga la COVID-19 haukuathiri uzalishaji wa mazao ya chakula nchini. Mafanikio haya yanatokana na sababu mbalimbali ikiwemo hali ya hewa nzuri, pamoja na usimamizi na utekelezaji mzuri wa sera na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali na Wadau wengine wa masuala ya kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji. Ili kuendelea kuimarisha masuala ya usalama wa chakula nchini, ushauri ufuatao unapendekezwa:- 1. Kuendelea kuimarisha na kuboresha Mfumo wa ukusanyaji taarifa na takwimu zinazohusu usalama wa chakula nchini kwa kuzingatia hatua za methodolojia iliyopo katika ngazi zote; 2. Mamlaka za Mikoa na Halmashauri za pembezoni mwa nchi ziendelee kuimarisha udhibiti wa utoroshaji wa chakula nje ya nchi kupitia mipaka isiyo rasmi; 3. Kuendelea kuimarisha mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo; 4. Kuendelea kuimarisha mfumo wa masoko kwa kuweka mikakati thabiti ya kutafuta masoko kwa ajili ya mazao ya chakula; 5. Kuendelea kuhamasisha Wafanyabiashara kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya chakula ili kupata bei nzuri ndani na nje ya nchi na kupunguza upotevu; 27 6. Kuongeza wataalamu wa kilimo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri; 7. Kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa kilimo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri katika masuala ya usalama wa chakula; 8. Kuendelea kuhamasisha Wadau wa sekta ya kilimo kutumia taarifa za hali ya hewa kwa usahihi ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutumia mbinu za kilimo himilivu; 9. Taasisi za utafiti ziongezewe uwezo wa kufanya tafiti na kuzalisha mbegu kinzani za mazao ya chakula. Aidha, utafiti ufanyike kurasimisha uzalishaji wa mbegu za asili za mazao ya chakula ili zisipotee. 10. Kuendelea kutoa elimu kwa umma kupitia redio, televisheni, vyombo vya usafiri, mabango na mitandao ya kijamii ili kuufahamisha umma kuhusu mafanikio katika maendeleo ya kilimo, miongozo na tahadhari mbalimbali; 11. Kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi na usimamizi wa maghala katika ngazi zote; na 12. Kuendelea kuwekeza zaidi katika kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula nchini. 28 VIAMBATISHO Tathimini ya Mwisho ya Uzalishaji (Tani) Kimkoa kwa Msimu wa Mwaka 2019/2020(Kufikia Tarehe 31/Desemba/ 2020) Eneo (Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo (Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo (Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo (Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo (Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo (Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo (Hekta) Uzalishaji (Tani) Mkoa Arusha 108,765 1.3 142,112 24,595 0.9 22,136 558 1.3 716 52,847 2.3 119,170 4,141 3.0 12,512 190,906 296,645 Arusha Pwani 29,983 1.5 45,337 4,992 0.8 3,993 31,157 1.4 44,604 66,132 93,934 Pwani Dar es Salaam 722 1.1 760 3,303 1.4 4,624 4,025 5,384 Dar es Salaam Dodoma 122,858 1.0 124,668 152,152 1.0 156,321 1,015 1.1 1,103 99,487 1.4 137,995 5,227 3.0 15,603 380,740 435,690 Dodoma Iringa 121,876 1.8 219,486 12 1.8 22 3,666 1.2 4,388 20,085 3.0 60,087 10,598 1.0 10,704 156,237 294,687 Iringa Njombe 166,989 2.0 332,457 1,156 1.0 1,158 1,540 1.2 1,814 853 1.9 1,644 10,999 1.6 18,037 181,536 355,109 Njombe Kagera 88,350 1.7 149,886 8,530 1.0 8,343 2,652 0.9 2,426 279 0.6 166 11,532 1.6 18,451 111,343 179,272 Kagera Kigoma 222,673 2.5 561,123 2,584 1.6 4,047 201 1.4 273 26,234 3.0 77,805 251,692 643,247 Kigoma Kilimanjaro 88,011 2.0 175,916 594 0.9 529 521 1.0 523 13,661 3.4 46,202 395 5.1 2,028 102,787 225,199 Kilimanjaro Lindi 96,576 1.1 106,239 37,490 0.8 31,425 24,643 0.6 14,786 158,709 152,449 Lindi Manyara 264,713 1.4 373,438 17,618 1.2 21,401 10,118 0.6 6,513 2,546 1.3 3,285 8,954 3.0 26,862 6,741 1.6 10,592 303,949 442,091 Manyara Mara 95,927 2.0 191,621 76,428 1.5 116,168 5,656 2.3 13,004 1,270 34,937 1.5 52,405 214,218 373,197 Mara Mbeya 205,300 2.6 528,128 5,621 2.4 13,590 1,169 1.0 1,226 78,464 3.1 244,800 4,102 1.7 7,122 290,554 794,867 Mbeya Songwe 179,407 2.5 448,650 18,256 1.5 27,369 6,815 1.2 8,137 426 1.5 639 24,722 3.1 76,638 391 1.0 391 230,017 561,823 Songwe Morogoro 104,610 1.5 156,788 9,621 1.4 13,304 102 1.4 145 70 0.7 49 255,795 2.3 588,328 370,196 758,613 Morogoro Mtwara 44,745 1.1 47,092 12,321 1.0 12,463 206 1.0 196 20,974 1.0 20,974 78,246 80,725 Mtwara Mwanza 91,641 1.5 136,597 12,715 1.2 14,916 16 1.1 19 2,292 107,911 2.8 302,151 214,575 453,683 Mwanza Geita 99,677 2.0 198,524 6,842 1.0 6,523 450 0.9 424 1,657 0.6 981 90,525 2.3 208,208 199,151 414,658 Geita Rukwa 229,974 2.3 539,279 8,399 2.4 20,517 15,417 1.3 19,918 1 1.0 1 40,282 2.1 84,591 6,298 2.0 12,817 300,370 677,123 Rukwa Katavi 55,910 2.1 119,807 1,647 1.3 2,124 75,402 2.6 196,046 132,959 317,977 Katavi Ruvuma 280,008 2.8 793,595 8,999 1.4 12,436 60,552 2.0 121,104 2,566 1.2 3,069 352,125 930,204 Ruvuma Shinyanga 77,705 1.1 85,981 27,678 1.4 38,579 10,106 1.1 10,909 120,073 2.2 258,157 235,562 393,626 Shinyanga Simiyu 186,055 1.4 265,967 69,100 1.1 73,818 1,626 1.1 1,789 68,898 2.1 144,685 325,678 486,259 Simiyu Singida 174,461 1.2 212,490 98,505 1.4 138,549 3,341 1.0 3,308 45,967 0.9 42,860 15,672 2.0 31,343 10 0.5 5 337,955 428,555 Singida Tabora 220,013 1.4 314,047 27,124 1.4 37,807 505 1.0 500 2,100 1.0 2,100 110,759 2.4 262,389 360,502 616,843 Tabora Tanga 278,746 1.6 441,016 302 1.0 296 5,866 2.8 16,424 284,913 457,736 Tanga Jumla 3,635,692 1.7 6,711,002 624,281 1.3 765,399 62,946 1.2 77,065 167,826 1.0 200,774 1,309,326 2.3 3,038,080 46,240 77,276 5,846,311 10,869,596 Jumla Kiambatisho Na.1a Nafaka ( Eneo (Hekta), Tija na Uzalishaji (Tani) kwa Hekta kwa Tani) Mkoa Mahindi Mtama Ulezi Uwele Mchele Ngano Jumla Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula 2019/2020 29 Tathmini ya Mwisho - Uzalishaji wa Mazao ya Chakula - Yasiyo Nafaka Msimu 2019/2020 -(Hadi Kufikia 31 Desemba, 2020) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Tija Uzalishaji (Tani) Eneo(Hekta) Uzalishaji (Tani) Arusha 22,521 1.3 29,377 19,947 1.1 21,435 755 3.1 2,335 125 0.8 95 5,351 3.5 18,699 - 1,767 1.3 2,297 45,168 4.7 212,800 2,450 1.5 3,628 3,053 1.3 3,965 101,137 294,630 292,043 591,276 Arusha Pwani 3,619 1.2 4,163 10,102 1.4 14,060 181 0.7 122 - 66,784 3.5 233,742 2,888 4.1 11,796 6,501 1.8 11,634 90,075 275,517 156,207 369,451 Pwani Dar es Salaam 2,905 1.2 3,498 - 2,929 3.0 8,787 1,172 2.9 3,384 3,415 4.9 16,734 10,421 32,403 14,446 37,787 Dar es Salaam Dodoma 11,940 0.9 10,603 23,719 1.0 22,645 17,986 2.7 48,672 90,373 1.3 120,984 2,732 1.0 2,649 21,086 1.5 32,420 13,054 2.5 32,634 - 13,506 1.8 24,312 1,076 0.1 108 195,472 295,027 576,212 730,717 Dodoma Iringa 72,887 1.2 89,145 9,584 1.8 16,974 3,336 1.1 3,624 2 1.3 3 278 3.5 970 105 4.2 445 5,718 3.1 17,557 11,133 4.4 49,051 103,043 177,769 259,280 472,456 Iringa Njombe 31,970 0.8 26,712 12 0.4 5 473 1.1 539 405 0.8 341 45 1.1 50 5,211 2.4 12,506 582 3.3 1,925 4,341 2.3 10,148 28,528 2.2 62,507 71,568 114,731 253,104 469,840 Njombe Kagera 138,619 0.6 89,627 49 0.7 33 14,554 0.9 12,478 2,451 0.5 1,192 117,573 2.3 270,417 123,460 4.2 523,864 16,644 2.2 37,381 6,634 2.4 15,702 419,984 950,693 531,326 1,129,966 Kagera Kigoma 107,395 1.0 107,288 211 1.0 210 466 1.0 468 7,453 2.2 16,259 2,411 - 150,291 2.2 330,640 27,091 3.8 104,238 10,270 3.3 33,901 330 2.8 910 305,918 593,913 557,610 1,237,161 Kigoma Kilimanjaro 42,252 1.0 44,278 499 1.8 900 358 3.3 1,177 747 0.9 640 582 2.0 1,164 - 3,695 2.0 7,485 63,401 4.1 261,962 808 2.7 2,164 3,726 3.1 11,624 116,068 331,394 218,855 556,592 Kilimanjaro Lindi 24,043 0.7 16,518 1,160 0.8 945 3,089 0.7 2,128 - 43,873 2.3 100,908 - - 4,750 2.0 9,500 - 76,915 129,999 235,624 282,448 Lindi Manyara 111,526 1.1 122,679 22,732 1.4 32,643 582 1.6 925 1,395 0.9 1,212 1,890 1.5 2,863 - 1,659 2.0 3,321 866 3.7 3,175 2,881 2.1 6,050 1,052 2.9 3,052 144,583 175,919 448,532 618,011 Manyara Mara 12,841 0.9 11,050 662 0.8 499 474 0.5 217 398 0.9 358 - 62,326 2.0 124,652 4,239 2.6 10,874 62,736 2.0 125,471 1,977 0.5 1,063 145,653 274,185 359,871 647,382 Mara Mbeya 46,616 1.4 64,043 327 1.3 434 4,011 1.0 4,153 14,162 1.2 16,822 607 1.0 583 2,903 1.3 3,818 11,488 3.0 34,463 13,860 5.3 73,337 9,397 6.2 58,694 31,053 4.8 147,504 134,423 403,850 424,977 1,198,717 Mbeya Songwe 65,224 1.3 84,583 496 1.0 492 33,926 1.3 45,741 12 0.0 1 4 0.7 3 7,968 2.5 19,921 7,832 4.3 33,612 13,089 4.6 60,838 2,604 3.1 8,166 131,155 253,357 361,171 815,180 Songwe Morogoro 21,294 0.9 19,365 8,852 1.2 10,187 9,020 1.5 13,144 1,642 1.4 2,238 244 2.0 480 - 19,003 3.3 62,710 12,752 4.4 55,840 16,980 2.6 43,476 418 1.1 453 90,205 207,892 460,401 966,505 Morogoro Mtwara 268 0.8 218 10,580 0.6 6,348 10,387 1.3 13,136 7,105 0.5 3,837 10,443 1.0 10,443 7,561 0.5 3,781 99,618 2.9 288,892 240 2.2 535 3,023 1.1 3,295 149,225 330,485 227,471 411,210 Mtwara Mwanza 22,166 1.0 21,276 7,284 1.2 8,629 6,755 0.6 4,053 10,061 1.0 9,933 2,144 1.7 3,624 66,340 2.0 132,680 732 3.8 2,806 111,831 3.0 335,492 227,312 518,493 441,888 972,176 Mwanza Geita 32,250 1.0 32,759 4,379 1.0 4,414 13,023 1.2 15,597 1,071 1.3 1,391 140 1.3 182 68,825 2.3 158,298 656 1.3 877 58,861 1.5 88,504 179,205 302,022 378,355 716,681 Geita Rukwa 122,608 1.0 121,686 370 1.5 555 - - - 17,127 1.1 18,646 114 0.8 91 - 26,674 3.7 98,694 319 2.7 866 15,770 3.0 47,654 2,699 2.3 6,113 185,680 294,305 486,049 971,428 Rukwa Katavi 6,650 1.5 9,958 47 0.6 30 1 2.1 3 19,521 1.6 31,207 12 0.7 8 15,393 3.0 46,180 52 3.3 173 11,747 2.6 31,087 130 3.3 432 53,553 119,077 186,512 437,055 Katavi Ruvuma 43,091 1.6 67,221 1,662 1.1 1,859 4,478 1.0 4,524 6,248 1.0 6,240 387 0.6 219 58 0.9 50 77,119 2.4 185,085 5,657 5.1 28,919 13,394 3.2 42,800 186 1.9 360 152,281 337,277 504,405 1,267,480 Ruvuma Shinyanga 12,515 1.0 12,472 2,664 1.1 2,827 40,745 0.9 37,698 12,049 0.5 6,024 1,635 1.2 1,954 12,906 1.3 16,777 60,125 1.3 79,273 142,638 157,025 378,200 550,651 Shinyanga Simiyu 7,473 1.2 9,289 4,250 0.9 4,006 17,003 1.3 21,301 18,059 0.7 13,471 30,831 0.5 15,416 - 8,307 1.1 8,725 33,673 1.0 34,996 119,596 107,203 445,274 593,461 Simiyu Singida 4,937 0.9 4,299 298 1.4 417 2,152 1.2 2,552 6,469 1.2 7,754 5,976 0.9 5,525 1,527 1.1 1,734 4,742 2.3 10,905 15,564 3.7 57,430 41,665 90,616 379,620 519,171 Singida Tabora 21,005 0.7 15,436 1,314 1.0 1,314 9,990 0.6 6,356 55,926 1.5 82,339 7,566 0.6 4,583 3,066 1.1 3,422 50,260 1.2 60,312 69,162 1.3 88,694 218,288 262,456 578,790 879,298 Tabora Tanga 28,333 0.9 25,579 567 0.6 341 3,793 0.7 2,605 1,031 0.6 577 1,581 0.6 885 - 67,379 2.6 175,186 11,589 2.3 26,656 8,714 1.5 13,070 20,663 2.5 52,000 143,650 296,899 428,563 754,635 Tanga Jumla 986,383 1.0 1,018,943 123,049 1.0 124,010 120,739 1.3 174,260 363,689 1.0 444,197 92,074 1.1 81,429 45,044 1.1 52,239 1,005,461 2.4 2,427,190 322,662 3.3 1,358,083 575,349 2.6 1,283,782 115,261 2.4 363,007 3,749,712 7,327,137 9,584,786 18,196,733 Jumla Kunde Uzalishaji (Tani) Yasiyonafaka Viazi Mviringo Muhogo Ndizi Njugu Mawe Njegele Karanga (Eneo (Hekta), Tija na Uzalishaji (Tani) kwa Hekta kwa Tani) Jumla Uzalishaji (Tani) MKOA Jumla Eneo(Hekta) Nafaka na Yasiyonafaka Mkoa Maharage Mbaazi Viazi Vitamu Chanzo: Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2019/2020 30 Kiambatisho Na.2: Mwenendo wa Unyeshaji mvua za Vuli (Oktoba – Desemba, 2020)
false
# Extracted Content Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 1 SHERIA YA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA YA MWAKA 2024 MPANGILIO WA VIFUNGU Kifungu Jina SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Jina na kuanza kutumika. 2. Tafsiri. SEHEMU YA PILI SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA 3. Kuendelea kutambulika kwa Shirika. 4. Majukumu na mamlaka ya Shirika. 5. Wajibu wa Shirika katika kuandaa vipindi. SEHEMU YA TATU UTAWALA NA USIMAMIZI WA SHIRIKA 6. Bodi ya Shirika. 7. Sifa za kuwa mjumbe. 8. Majukumu na mamlaka ya Bodi. 9. Mamlaka ya ukasimishaji. 10. Ada au posho za wajumbe wa Bodi. 11. Kinga kwa wajumbe wa Bodi. 12. Mkurugenzi Mkuu. 13. Majukumu ya Mkurugenzi Mkuu. 14. Watumishi wa Shirika. /ISSN 0856 – 0331X THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA No. 12 13rd August, 2024 SPECIAL BILL SUPPLEMENT To The Special Gazette of the United Republic of Tanzania No. 33 Vol. 105 Dated 13rd August, 2024 Printed by The Government Printer, Dodoma by Order of Government Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 2 SEHEMU YA NNE MIUNDOMBINU YA SHIRIKA 15. Miundombinu ya utangazaji. 16. Ulinzi na usimamizi miundombinu ya utangazaji. SEHEMU YA TANO MAKATAZO 17. Uharibifu wa mali za Shirika. 18. Kuingia kwenye eneo la Shirika. 19. Matumizi ya maudhui. SEHEMU YA SITA MASHARTI YA FEDHA 20. Vyanzo vya fedha vya Shirika. 21. Usimamizi wa fedha. 22. Makadirio ya mapato na matumizi. 23. Matumizi ya fedha. 24. Hesabu na ukaguzi. 25. Taarifa ya mwaka. SEHEMU YA SABA MASHARTI YA JUMLA 26. Udhamini wa vipindi. 27. Matengenezo au mabadiliko yanayoweza kuharibu mfumo wa matangazo. 28. Uanzishwaji wa chaneli maalumu. 29. Adhabu ya jumla. 30. Mamlaka ya Waziri kutengeneza kanuni. _________ JEDWALI _________ Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 3 ________ TAARIFA ________ Muswada huu unaokusudiwa kuwasilishwa Bungeni umechapishwa pamoja na madhumuni na sababu zake kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma. Dodoma, MOSES M. KUSILUKA, 13 Agosti, 2024 Katibu wa Baraza la Mawaziri Muswada wa Sheria kwa ajili ya kutambua mwendelezo wa uwepo wa Shirika la Utangazaji Tanzania; kubainisha wajibu, malengo, majukumu na mamlaka ya Shirika, kuweka masharti kuhusu ulinzi na usimamizi thabiti wa miundombinu ya utangazaji, na kuainisha masuala mengine yanayohusiana na hayo. IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina na kuanza kutumika 1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 na itaanza kutumika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali. Tafsiri 2. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Bodi” maana yake ni Bodi ya Wakurugenzi iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 6; “chaneli maalumu” inajumuisha chaneli, idhaa, kituo au jukwaa lililoanzishwa na Serikali kwa madhumuni mahsusi, linalosimamiwa na kuendeshwa na Shirika; Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 4 “huduma ya utangazaji ya kulipia” maana yake ni huduma ya utangazaji ambayo inaweza kupatikana kwa mtu kwa malipo ya ada; “huduma ya utangazaji wa umma” maana yake ni aina ya huduma ya utangazaji ambayo inatolewa kwa umma, inayofadhiliwa na umma na haina faida ya kibiashara; “kipindi maalumu” maana yake ni kipindi chenye maslahi ya umma ambacho kinaweza kutangazwa wakati wowote katika kutimiza wajibu wa Shirika kwa umma na bila kujali kuwa kuna vipindi vingine katika ratiba; “matukio ya kitaifa” maana yake ni ziara za Viongozi Wakuu wa Serikali, sherehe za kitaifa, maadhimisho, matukio au kumbukumbu mbalimbali za kitaifa; “miundombinu ya utangazaji” maana yake ni miundombinu ya usambazaji wa maudhui ya utangazaji na inajumuisha mifumo ya utangazaji, studio, vifaa vya kurushia matangazo, mitambo, ardhi na majengo yanayotumika kuhifadhi miundombinu hiyo; “mjumbe” maana yake ni mjumbe wa Bodi na inajumuisha Mwenyekiti; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 13; “mtumishi” maana yake ni mtumishi yeyote wa Shirika na inajumuisha Mkurugenzi Mkuu; “Shirika” maana yake ni Shirika la Utangazaji Tanzania ambalo limetambuliwa chini ya kifungu cha 3; “tangazo la biashara” maana yake ni tangazo lolote kwa umma lenye madhumuni ya kukuza uuzaji, ununuzi au ukodishaji wa bidhaa au huduma, lililotengewa muda wa kutangazwa kwa malipo ya fedha au malipo mengine lenye madhumuni ya kuhamasisha kusudi au wazo au kuleta manufaa mengine anayotamani mtoa tangazo; “udhamini” maana yake ni ushiriki wa mtu ambaye hajishughulishi katika shughuli za utangazaji au utayarishaji wa kazi za maudhui katika ufadhili wa Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 5 moja kwa moja au usio wa moja kwa moja wa vipindi kwa nia ya kukuza jina, alama ya biashara au taswira ya mtu huyo; “Viongozi Wakuu wa Serikali” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya huduma za utangazaji. SEHEMU YA PILI SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA Kuendelea kutambulika kwa Shirika 3.-(1) Kutaendelea kuwepo Shirika linalojulikana kama Shirika la Utangazaji Tanzania au “TBC”. (2) Shirika litakuwa ni shirika hodhi lenye urithishaji endelevu na lakiri yake, na kwa jina lake litakuwa na uwezo wa- (a) kushtaki au kushtakiwa; (b) kupata, kumiliki na kutoa mali zinazohamishika na zisizohamishika; (c) kukopa kiasi cha fedha ambacho kinaweza kuhitajika kwa madhumuni yake; (d) kuingia kwenye mikataba au taratibu nyingine; na (e) kutumia mamlaka na kutekeleza majukumu chini ya Sheria hii. (3) Shirika litakuwa chombo kikuu cha utangazaji cha umma kwa ajili ya kutoa habari, taarifa, elimu na burudani na, kwa kuzingatia Sheria hii, litakuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake za kila siku. Majukumu na mamlaka ya Shirika 4. Majukumu na mamlaka ya Shirika yatakuwa- (a) kutoa huduma za utangazaji wa umma zinazohabarisha, zinazoelimisha na zinazoburudisha kupitia redio, televisheni na majukwaa mengine ya mtandaoni au kielektroniki; (b) kukuza ujuzi wa watumishi wa Shirika ili kuongeza ufanisi katika utendaji kupitia Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 6 mafunzo, elimu na utafiti; (c) kumiliki na kufunga vifaa kwa ajili ya kusafirishia mawimbi kwa kutumia waya au njia nyinginezo zinazotumika katika Jamhuri ya Muungano, na kuvitumia kwa madhumuni yanayohusiana na malengo ya Shirika; (d) kuendeleza, kuongeza na kuboresha huduma za utangazaji ndani na nje ya nchi kwa njia, mbinu na namna inayokubalika na mamlaka inayohusika na utoaji leseni; (e) kutoa huduma za utangazaji, kuandaa, kujenga, na kufunga au kusimamia uwekaji wa miundombinu ya utangazaji na vifaa vingine vya kurusha na kupokea maudhui nje ya Jamhuri ya Muungano; (f) kushiriki katika matukio yote ya kitaifa yakiwemo yanayohusisha Viongozi Wakuu wa Serikali yenye maslahi ya umma ndani na nje ya nchi kwa madhumuni ya kukusanya, kuchakata, kutangaza na kuhifadhi kumbukumbu; (g) kukusanya, kupokea au kutoa maudhui kwa vyombo vingine vya ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano na kujiunga katika mashirika ya habari; (h) kukusanya, kuchakata, kuchapisha na kusambaza, kwa malipo au bila malipo, vipindi au taarifa zozote ambazo zinaweza kufaa kwa malengo ya Shirika; (i) kuanzisha maktaba na kutunza kumbukumbu zenye maudhui yanayohusiana na malengo ya Shirika; (j) kuandaa au kudhamini matamasha na burudani nyingine zinazohusiana na huduma za utangazaji au kwa madhumuni yoyote yanayohusiana na huduma za utangazaji; (k) kuzalisha, kutengeneza, kununua, kupata, kutumia, kuuza, kukodisha au kutoa filamu, rekodi na vifaa vingine vyovyote vinavyoweza kutoa picha jongefu au sauti; Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 7 (l) kuomba na kupata, kununua au kutumia kibiashara kwa namna yoyote miliki ubunifu kuhusiana na uvumbuzi wowote wenye manufaa kwa madhumuni na majukumu ya Shirika; (m) kuanzisha chaneli, vituo na majukwaa mengine ya utangazaji kama Bodi itakavyoidhinisha; (n) kufanya tafiti zinazoendana na malengo ya Shirika; (o) kutumia teknolojia mpya na zinazoibukia zinazoendana na malengo ya Shirika; (p) kuanzisha au kuwezesha uanzishwaji wa kampuni kwa ajili ya uendelezaji wa malengo ya Shirika; (q) kutekeleza majukumu mengine kwa ajili ya kufikia malengo yake. Wajibu wa Shirika katika kuandaa vipindi 5. Katika kutekeleza majukumu yake, Shirika litaandaa vipindi- (a) vinavyochangia kukuza demokrasia, maendeleo ya jamii, usawa wa kijinsia, ujenzi wa taifa, utoaji wa elimu na kuimarisha maadili ya jamii; (b) vinavyolinda, kuimarisha na kudumisha uhuru, umoja na taswira ya Jamhuri ya Muungano; (c) vinavyolinda na kuimarisha mfumo wa kiutamaduni, kisiasa, kijamii na kiuchumi; (d) vinavyoakisi mitazamo, maoni, mawazo, maadili na ubunifu wa sanaa za Kitanzania; (e) vinavyokuza vipaji vya Watanzania kupitia vipindi vya elimu na burudani; (f) vinavyoweka anuai inayojitosheleza na inayotoa mizania ya habari, elimu na burudani ili kukidhi mahitaji ya utangazaji ya Watanzania wote; (g) vinavyotoa maoni, taarifa, habari na uchambuzi wa masuala mbalimbali kwa mtazamo wa Kiafrika; na (h) vinavyoendeleza na kulinda maslahi ya taifa na usalama ndani na nje ya nchi. Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 8 SEHEMU YA TATU UTAWALA NA USIMAMIZI WA SHIRIKA Bodi ya Shirika 6.-(1) Kutakuwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika kwa ajili ya kusimamia utendaji wa Shirika. (2) Bodi ya Shirika itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Rais; na (b) wajumbe wengine nane watakaoteuliwa na Waziri wenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika tasnia ya habari, utangazaji, uhandisi, sheria, teknolojia ya habari, usimamizi, uchumi au fedha. (3) Katika kuteua wajumbe chini ya kifungu kidogo cha (2)(b), Waziri atazingatia jinsia. (4) Mkurugenzi Mkuu atakuwa Katibu wa Bodi. (5) Masuala kuhusu muda wa kukaa madarakani, akidi, vikao vya Bodi na masuala mengine yatakuwa kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali. (6) Waziri anaweza, kwa amri itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali, kurekebisha Jedwali. Sifa za kuwa mjumbe 7.-(1) Mtu atakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi iwapo mtu huyo- (a) ni raia wa Tanzania; (b) ni mkazi wa kudumu wa Tanzania; (c) si mtumishi au mwajiriwa wa chama chochote cha siasa; (d) hajatamkwa na mahakama kuwa amefilisika; (e) ana akili timamu; au (f) hajatiwa hatiani kwa kosa lolote na kuhukumiwa kifungo kisichopungua miezi sita, bila mbadala wa faini. Majukumu na mamlaka ya Bodi Sura ya 257 na 370 8.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria ya Mashirika ya Umma na Sheria ya Mamlaka na Majukumu ya Msajili wa Hazina, majukumu na mamlaka ya Bodi yatakuwa- (a) kutoa mwongozo wa kimkakati na kutengeneza sera za uendeshaji na usimamizi wa Shirika; Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 9 (b) kufanya usimamizi wa kiutawala na tathmini ya shughuli za Shirika na utendaji wa menejimenti ya Shirika; (c) kupata na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali, ikijumuisha kuidhinisha mpango kazi wa mwaka, bajeti ya mwaka na bajeti ya nyongeza; (d) kuidhinisha mipango na miongozo mbalimbali ya Shirika; (e) kutathmini utendaji wa menejimenti na kuchukua hatua muhimu; (f) kuidhinisha taarifa za utendaji wa Shirika; (g) kuteua menejimenti katika Shirika na kusimamia nidhamu yao; (h) kupitisha mabadiliko yoyote ya mishahara na masharti ya utumishi kwa watumishi; (i) kuidhinisha na kusimamia kanuni za fedha na kanuni za utumishi; (j) kuidhinisha uondoshaji wa mali za Shirika; (k) kuidhinisha pendekezo la kukopa fedha kwa madhumuni ya Shirika; (l) kuidhinisha uendelezaji wa miundombinu ya utangazaji na vifaa; (m) kupitisha mpango mkakati, muundo wa Shirika na muundo wa kiutumishi; (n) kuidhinisha sera na kanuni za ndani za utawala na uendeshaji; (o) kuidhinisha miradi, kwa kuzingatia sheria zingine kwa madhumuni ya Shirika, isiyojumuishwa ndani ya mpango au mpango kazi wa mwaka na bajeti; (p) kuidhinisha uteuzi wa watumishi wa Shirika kwa idadi na vyeo kama itakavyoona inafaa kwa ajili ya uendeshaji bora na wa ufanisi wa shughuli za Shirika; (q) kuishauri Serikali katika masuala yote yanayohusu Shirika; na (r) kutekeleza majukumu mengine kadri Bodi itakavyoona inafaa kwa ajili ya kufikia malengo ya Shirika. Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 10 (2) Waziri anaweza kutoa kwa Bodi maelekezo ya jumla au mahsusi kuhusu utendaji wa Shirika na majukumu yake chini ya Sheria hii. Mamlaka ya ukasimishaji 9.-(1) Isipokuwa kama ilivyoelezwa katika kifungu kidogo cha (3), Bodi inaweza kwa maandishi, na kwa kuzingatia masharti kadri itakavyoona inafaa, kukasimu kwa kamati au mtumishi majukumu au mamlaka yoyote chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote. (2) Bila kujali kifungu kidogo cha (1), Bodi inaweza kutekeleza majukumu iliyokasimisha. (3) Bodi haitakasimu mamlaka ya- (a) kukasimisha; (b) kuteua wajumbe wa menejimenti; (c) kuidhinisha ajira za watumishi wa Shirika; (d) kuidhinisha taarifa za fedha za mwaka, bajeti ya mwaka au bajeti ya nyongeza; (e) kuidhinisha taarifa za fedha za kila mwaka; (f) kuanisha ada na tozo mbalimbali; na (g) kukopa. Ada au posho za wajumbe wa Bodi 10. Mjumbe atalipwa na Shirika ada au posho kama itakavyoamuliwa na Bodi na kuidhinishwa na mamlaka husika. Kinga kwa wajumbe wa Bodi 11. Mjumbe wa Bodi hatachukuliwa hatua au kufunguliwa shauri kuhusiana na kitendo au jambo lolote alililotenda au kuacha kutenda kwa nia njema katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria hii. Mkurugenzi Mkuu 12.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika ambaye atateuliwa na Rais. (2) Mkurugenzi Mkuu atakuwa afisa mtendaji mkuu na afisa masuuli wa Shirika na atawajibika kwa Bodi katika usimamizi wa majukumu na shughuli za kila siku za Shirika. (3) Mtu atakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ikiwa- (a) ana angalau shahada ya uzamili kutoka chuo kikuu kinachotambulika katika fani ya Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 11 mawasiliano kwa umma, uandishi wa habari, uzalishaji wa maudhui, sheria, uhandisi wa mawasiliano, uchumi, utawala au fani nyingine inayoendana na hizo; (b) ana uzoefu wa angalau miaka kumi, miaka sita kati ya hiyo iwe katika nafasi ya uongozi; na (c) amethibitika kuwa na ujuzi wa uchambuzi na maarifa katika sekta ya utangazaji. (3) Mkurugenzi Mkuu atashika wadhifa kwa kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena. Majukumu ya Mkurugenzi Mkuu 13. Pamoja na majukumu mengine aliyopewa kwa mujibu wa Sheria hii, Mkurugenzi Mkuu atakuwa na majukumu ya- (a) kuanzisha na kudumisha mfumo wa mpango mkakati ambao unajumuisha dira na dhima ya Shirika pamoja na mpango wa utekelezaji; (b) kusimamia uandaaji, udumishaji na utekelezaji wa sera na mifumo ya utendaji inayojumuisha nyanja zote za uendeshaji wa Shirika; (c) kusimamia rasilimali za Shirika ili kukidhi mipango ya uendeshaji wa shughuli za Shirika; (d) kuhakikisha uwepo wa watumishi wenye uwezo na ari katika utekelezaji wa majukumu yao; (e) kufuatilia, kutathmini na kuchukua hatua za kurekebisha mipango kazi iliyokubaliwa katika miradi yote ya Shirika; (f) kuidhinisha matumizi ya kawaida kama itakavyoamuliwa na Bodi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo; na (g) kutekeleza majukumu mengine kama Bodi itakavyoelekeza. Watumishi wa Shirika 14.-(1) Kwa kuzingatia sheria zinazosimamia utumishi wa umma, Shirika litaajiri watumishi kwa idadi itakayohitajika kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Shirika. (2) Shirika linaweza kuteua washauri na wataalam katika taaluma mbalimbali kwa kuzingatia vigezo na Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 12 masharti yatakayowekwa na Shirika. SEHEMU YA NNE MIUNDOMBINU YA SHIRIKA Miundombinu ya utangazaji 15.-(1) Shirika litasimamia miundombinu ya utangazaji iliyotengwa kwa ajili ya shughuli za utangazaji na litakuwa na mamlaka ya- (a) kupanga matumizi ya miundombinu hiyo; (b) kuzuia mtu yeyote kuingia au kuendeleza miundombinu ya utangazaji; na (c) kuidhinisha uwekaji wa miundombinu kwenye ardhi ya Shirika. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1), Shirika linaweza kutoa maelekezo na kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya kuhakikisha usimamizi bora wa miundombinu ya utangazaji. (3) Maelekezo ya Shirika katika kifungu hiki yanaweza kujumuisha matengenezo ya vifaa, malipo ya ada au tozo, uendeshaji wa shughuli za biashara na masuala mengine ya usimamizi wa miundombinu ya utangazaji. Ulinzi na usimamizi wa miundombinu ya utangazaji 16. Shirika litasimamia miundombinu katika namna inayohakikisha manufaa ya kiusalama, kiuchumi na kibiashara katika miundombinu ya utangazaji. SEHEMU YA TANO MAKATAZO Uharibifu wa mali za Shirika 17.-(1) Mtu hataingilia au kutumia kwa madhumuni yoyote au kushiriki katika kitendo kinachosababisha au kinachoweza kusababisha mabadiliko, uharibifu au kusababisha kuondolewa kwa au uharibifu wowote wa miundombinu ya utangazaji inayomilikiwa na Shirika. (2) Mtu anayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyozidi mara kumi ya thamani ya pato la uharibifu wowote wa miundombinu ya utangazaji, mfumo Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 13 wa utangazaji au mtambo au kifaa au kifungo kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano, au vyote. Kuingia kwenye eneo la Shirika 18. Mtu ambaye- (a) bila ruhusa au kama si mtumishi wa Shirika- (i) anakutwa katika eneo lolote linalomilikiwa na Shirika bila kibali cha maandishi cha Shirika; au (ii) anakataa kuondoka katika eneo la Shirika baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Shirika; (b) akiwa kwenye maeneo ya Shirika, anapohitajika na mtumishi kutaja jina na taarifa zake, anakataa au anatoa jina au taarifa za uongo; (c) anaharibu au bila ruhusa anaingilia mali yoyote ya Shirika; au (d) anamzuia mtumishi au wakala wa Shirika kutekeleza majukumu yake, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano au vyote. Matumizi ya maudhui 19.-(1) Mtu hatatumia maudhui ya matangazo ya Shirika kwa njia yoyote au kupitia katika chanzo chochote bila idhini ya Shirika. (2) Mtu anayekiuka masharti ya kifungu hiki anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano au vyote. SEHEMU YA SITA MASHARTI YA FEDHA Vyanzo vya fedha vya Shirika 20.-(1) Vyanzo vya fedha vya Shirika vitakuwa ni- (a) kiasi cha fedha ambacho kitatengwa na Bunge; (b) ada na tozo zitakazotozwa kwa bidhaa na Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 14 huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika; (c) ada na tozo kwenye bidhaa au huduma ambazo Serikali itaelekeza kwa ajili ya utangazaji wa umma; (d) mapato yatakayotokana na uwekezaji; (e) fedha zitakazopatikana kupitia mikopo, michango, zawadi au ruzuku kwa ajili ya Shirika; (f) fedha kutoka kwenye mfuko kama ambavyo Serikali inaweza kuanzisha kwa madhumuni ya majukumu ya Shirika; (g) fedha kutoka- (i) katika shughuli za kibiashara kama vile ushauri elekezi au kukodisha mali yoyote ya Shirika; (ii) katika ukodishaji wa vifaa vingine ambavyo picha jongefu au sauti inaweza kutengenezwa; na (h) mapato mengine yanayotokana na utendaji wa shughuli za Shirika chini ya Sheria hii. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1)(b), huduma zinazotolewa na Shirika zitajumuisha- (a) huduma za chaneli maalumu chini ya Sheria hii; (b) huduma za utangazaji za kulipia; na (c) matangazo ya biashara na udhamini wa vipindi. Usimamizi wa fedha 21. Fedha za Shirika zitasimamiwa na Bodi kwa mujibu wa sheria na kanuni za fedha na zitatumika kulipia gharama zinazohusiana na utendaji wa majukumu ya Shirika chini ya Sheria hii. Makadirio ya mapato na matumizi Sura ya 439 22.-(1) Kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti, Mkurugenzi Mkuu ataandaa makadirio ya bajeti inayojumuisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka unaofuata na kuwasilisha kwa Bodi kwa ajili ya idhini, na anaweza, wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha kuandaa na kuwasilisha kwa Bodi kwa ajili ya idhini makadirio yoyote ya nyongeza. (2) Bodi inaweza kulitaka Shirika kufanya Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 15 marekebisho ya bajeti ikiwa kwa maoni yake bajeti haiakisi makadirio sahihi na ya kuridhisha ya mapato na matumizi. Matumizi ya fedha 23.-(1) Matumizi yote ya fedha katika Shirika yataidhinishwa na Bodi katika mwaka wa fedha husika. (2) Mkurugenzi Mkuu atahakikisha kwamba malipo yote kutoka kwenye fedha za Shirika yanafanywa kwa usahihi na kuidhinishwa ipasavyo. (3) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (2), Mkurugenzi Mkuu anaweza, pale inapotokea dharura katika utendaji wa majukumu ya Shirika, kufanya matumizi ambayo hayajaidhinishwa na Bodi na Mkurugenzi Mkuu atalazimika kuomba idhini ya Bodi ndani ya miezi mitatu baada ya matumizi hayo. Hesabu na ukaguzi Sura ya 348 24.-(1) Shirika litatunza na kuhifadhi vitabu vya hesabu na kumbukumbu nyingine zinazohusiana na shughuli zake na kuandaa taarifa ya hesabu ya mwaka kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma. (2) Hesabu za Shirika zitakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa kwa ajili hiyo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Taarifa ya mwaka 25.-(1) Ndani ya miezi miwili baada ya kupokea hesabu za Shirika zilizokaguliwa, Mkurugenzi Mkuu atawasilisha kwa Waziri taarifa ya mwaka husika ikijumuisha- (a) nakala ya hesabu zilizokaguliwa za Shirika, pamoja na taarifa ya mkaguzi wa hesabu hizo; (b) taarifa ya utekelezaji wa malengo muhimu na taarifa nyingine yoyote inayohusiana na utekelezaji wa malengo hayo; (c) taarifa ya uendeshaji wa Shirika katika mwaka wa fedha husika; na (d) taarifa nyingine kadri Waziri anavyoweza kuhitaji. (2) Waziri atawasilisha Bungeni nakala ya taarifa ya mwaka ya Shirika ndani ya miezi miwili au katika Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 16 mkutano wa Bunge unaofuata. SEHEMU YA SABA MASHARTI YA JUMLA Udhamini wa vipindi 26. Kipindi chochote au kipindi maalumu kinachotangazwa na Shirika au kwa niaba ya Shirika kinaweza kudhaminiwa na kujumuisha matangazo ya biashara. Matengenezo au mabadiliko yanayoweza kuharibu mfumo wa matangazo 27. Endapo taasisi ya Serikali, mamlaka ya serikali za mitaa au mtu yeyote atafanya matengenezo au mabadiliko yoyote katika miundombinu yake yatakayohusisha kuondolewa au kuharibiwa kwa mfumo wa matangazo, kifaa au mtambo wa Shirika, atapaswa kufanya matengenezo ili kurejesha huduma za Shirika katika hali ya awali. Uanzishwaji wa chaneli maalumu 28.-(1) Waziri anaweza, kwa amri itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali, kuanzisha chaneli maalumu kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya umma. (2) Vigezo vya uanzishaji na uendeshaji wa chaneli maalumu vitaainishwa kwenye kanuni. Adhabu ya jumla 29. Mtu anayetenda kosa chini ya Sheria hii na hakuna adhabu mahsusi iliyoainishwa, akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano na isiyozidi shilingi milioni kumi au kifungo kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano au vyote. Mamlaka ya Waziri kutengeneza kanuni 30.-(1) Waziri anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya Sheria hii. (2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1), kanuni zitakazotengenezwa chini ya kifungu hiki zinaweza kuainisha- (a) vigezo vya uanzishaji na uendeshaji wa chaneli maalumu; (b) ada na tozo za bidhaa na huduma zinazotolewa Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 17 na Shirika; (c) utaratibu wa uendeshaji wa kipindi au kipindi maalumu; na (d) utaratibu wa ukusanyaji na utunzaji wa kumbukumbu za maudhui ya matukio yenye maslahi ya kitaifa. _________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 6(5)) __________ MASUALA KUHUSU BODI Muda wa kuwa madarakani 1. Mjumbe wa Bodi, isipokuwa kama uteuzi wake utatenguliwa au atakoma kuwa mjumbe kwa namna nyingine yoyote, atakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. Makamu Mwenyekiti 2. Wajumbe watachagua kutoka miongoni mwao Makamu Mwenyekiti. Kujaza nafasi iliyo wazi 3. Endapo mjumbe yeyote atakoma kuwa mjumbe kabla ya kumaliza kipindi cha ujumbe, mamlaka ya uteuzi inaweza kumteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo mpaka muda wa kuhudumu kipindi hicho utakapokwisha. Vikao vya Bodi 4.-(1) Bodi itakutana kwa kawaida kila robo ya mwaka kwa ajili ya kuendesha shughuli zake wakati na mahali kama itakavyoamuliwa. (2) Bila kujali aya ndogo ya (1), Bodi inaweza wakati wowote kuitisha kikao maalumu endapo kuna suala la dharura linalohitaji uamuzi wa Bodi. (3) Mwenyekiti ataongoza kila kikao cha Bodi au ikiwa hayupo Makamu Mwenyekiti. (4) Endapo katika kikao chochote cha Bodi Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hawapo, wajumbe waliohudhuria watamchagua mjumbe mmoja kutoka miongoni mwao kuongoza kikao hicho. (5) Bodi inaweza kumwalika mtu yeyote ambaye si mjumbe kuhudhuria na kushiriki katika majadiliano katika kikao chochote cha Bodi isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. Kamati za Bodi 5.-(1) Bodi inaweza kuunda na kuteua kamati kadri itakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu yake. (2) Kamati itakayoudwa chini ya aya ndogo ya (1)- Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 18 (a) itajumuisha wajumbe Bodi au watu wengine watakaoteuliwa na Bodi kadiri Bodi itakavyoona inafaa; na (b) itakutana kwa nyakati na mahali kama itakavyoamuliwa na Bodi. (3) Mjumbe wa kamati ambaye si mjumbe wa Bodi au mtumishi wa Shirika atalipwa na Shirika ada au posho kwa kiwango kitakachoidhinishwa na Bodi. Lakiri 7. Lakiri ya Shirika itawekwa ipasavyo katika nyaraka ikiwa imeshuhudiwa kwa saini ya Mkurugenzi Mkuu au mjumbe mwingine yeyote wa Bodi atakayeteuliwa kwa madhumuni hayo, na uwekwaji huo wa lakiri iliyosainiwa na kuthibitishwa utatambulika kisheria. Amri na maelekezo ya Bodi 8. Amri, maelekezo, notisi au nyaraka nyingine zozote zinazotolewa na Bodi au kwa niaba ya Bodi zitasainiwa na- (a) Mwenyekiti; au (b) Katibu au afisa yeyote wa Shirika aliyeidhinishwa kwa maandishi na Bodi. Mgongano wa maslahi 9.-(1) Mjumbe wa Bodi atachukuliwa kuwa na mgongano wa maslahi ikiwa anapata maslahi ya kifedha au maslahi mengine yoyote kwa madhumuni ambayo yanakinzana na utendaji bora wa majukumu au mamlaka yake kama mjumbe wa Bodi. (2) Endapo mjumbe wa Bodi ana mgongano wa maslahi kuhusiana na- (a) jambo lolote lililo mbele ya Bodi kwa ajili ya kujadiliwa au kuamuliwa; au (b) jambo lolote ambalo Bodi ingelitarajia kuja mbele yake kwa ajili ya kujadiliwa au kuamuliwa, mjumbe huyo ataweka wazi maslahi aliyo nayo na kujiepusha kushiriki au kuendelea kushiriki katika majadiliano au uamuzi wa jambo husika. Kujiuzulu au kutenguliwa kwa mjumbe 10.-(1) Mjumbe wa Bodi anaweza kujiuzulu nafasi yake wakati wowote kwa kutoa taarifa kwa mamlaka ya uteuzi kwa maandishi. (2) Mjumbe wa Bodi anaweza kuondolewa madarakani na mamlaka ya uteuzi kwa maandishi iwapo- (a) hatahudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bodi bila kibali cha Bodi; (b) atapoteza uwezo wa kutekeleza majukumu yake kutokana na ugonjwa wa muda mrefu wa kimwili au kiakili; (c) hafai kutekeleza majukumu yake kutokana na kukosa uwezo na ukosefu wa maadili; (d) atapoteza sifa ya kuteuliwa kuwa mjumbe; au (e) kwa sababu nyingine yoyote ambayo mamlaka ya uteuzi itaona inafaa. Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 19 Akidi 11. Akidi katika kikao chochote cha Bodi itakua zaidi ya nusu ya wajumbe wa Bodi. Uamuzi wa Bodi 12.-(1) Uamuzi wa Bodi katika suala lolote utafikiwa kwa wingi wa kura za wajumbe waliopo na pale ambapo kura hizo zitalingana, Mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi. (2) Bodi inaweza kufanya uamuzi bila kikao kwa kusambaza miongoni mwa wajumbe nyaraka zinazohusika na mawasilisho ya wajumbe kwa maandishi yatakuwa uamuzi wa Bodi, isipokuwa mjumbe yeyote anaweza kuomba uamuzi husika uahirishwe na suala hilo lijadiliwe katika kikao cha Bodi kitakachofuata. Muhtasari wa vikao 13. Muhtasari wa kila kikao cha Bodi utahifadhiwa na kuthibitishwa na Bodi katika kikao kitakachofuata na kusainiwa na Mwenyekiti au mjumbe aliyeongoza kikao kinachohusika na muhtasari huo pamoja na Katibu. Uhalali wa shughuli za Bodi 14. Shughuli za Bodi hazitakuwa batili kwa sababu ya kasoro yoyote katika uteuzi wa mjumbe yeyote au kwa kigezo kuwa mjumbe yeyote wakati wa uteuzi hakuwa na sifa au hakustahili kuteuliwa. Bodi kuweka taratibu za kujiendesha 15. Kwa kuzingatia masharti ya Jedwali hili, Bodi itajiwekea utaratibu wa kujiendesha. Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 20 ________________ MADHUMUNI NA SABABU ________________ Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania (Shirika) ya Mwaka 2024 kwa madhumuni ya kuweka mfumo madhubuti na thabiti wa usimamizi na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania likiwa ni chombo cha utangazaji cha umma. Pamoja na kuanzishwa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania kupitia Amri ya Uanzishwaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, 2007 (Tangazo la Serikali Na. 186 la Mwaka 2007), Shirika limepitia changamoto mbalimbali za kiuendeshaji ikiwemo kutokuwa na msingi imara wa kisheria unaohakikisha uendelevu wake. Aidha, kutokana na kuanzishwa kwa Shirika chini ya Amri ya Uanzishwaji, Waziri mwenye dhamana ya utangazaji hakupewa mamlaka ya kutengeneza kanuni kwa ajili ya kusimamia na kuendesha masuala mbalimbali muhimu yanayohusiana na utendaji bora wa Shirika ikiwemo ukusanyaji wa mapato na ulinzi wa miundombinu ya utangazaji. Vilevile, kumekuwa na changamoto ya kukusanya na kuhifadhi maudhui ya kumbukumbu za matukio yote yenye maslahi ya kitaifa kwa njia ya sauti na picha jongefu. Kutokana na changamoto hizo katika usimamizi, uendeshaji na uendelevu wa Shirika, Sheria inayopendekezwa kutungwa itajumuisha masharti mbalimbali yanayotoa ufumbuzi wa changamoto zilizobainishwa ili kuliwezesha Shirika kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ufanisi zaidi. Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Kuu Saba ambapo Sehemu ya Kwanza inaainisha masharti ya utangulizi yakijumuisha jina la Sheria, utaratibu wa kuanza kutumika kwa Sheria na tafsiri ya baadhi ya misamiati iliyotumika katika Sheria. Sehemu ya Pili ya Muswada inaweka masharti kuhusu kuendelea kulitambua Shirika, majukumu na mamlaka ya Shirika pamoja na masharti kuhusu wajibu wa Shirika. Masharti ya Sheria katika Sehemu hii yanalenga kuhakikisha muendelezo wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lililoanzishwa mwaka 2007. Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 21 Sehemu ya Tatu ya Muswada inaweka masharti kuhusu utawala na usimamizi wa Shirika ambao unajumuisha uanzishwaji wa Bodi ya Wakurugenzi, sifa za wajumbe wa Bodi, majukumu na mamlaka ya Bodi, mamlaka ya Bodi kukasimisha madaraka yake, ripoti ya mwaka ya Bodi, ada au posho za wajumbe wa Bodi, kinga kwa wajumbe wa Bodi, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu, sifa za uteuzi, majukumu ya Mkurugenzi Mkuu pamoja na masharti ya watumishi wa Shirika. Masharti haya yanalenga kuimarisha usimamizi na utekelezaji bora wa shughuli na utendaji kazi wa kila siku wa Shirika. Sehemu ya Nne ya Muswada inaweka masharti kuhusiana na miundombinu ya utangazaji na ulinzi wa maeneo ya Shirika ambapo Shirika limepewa mamlaka ya kusimamia na kulinda miundombinu ya utangazaji na mali za Shirika. Masharti ya Sehemu hii yanalenga kuhakikisha maeneo ya Shirika yanalindwa ipasavyo. Sehemu ya Tano ya Muswada inaweka masharti ya makatazo mbalimbali pamoja na adhabu. Miongoni mwa makatazo hayo ni pamoja na mtu kutokuingia katika maeneo ya Shirika, kutokufanya uharibifu wowote miundombinu ya utangazaji. Masharti ya Sehemu hii yanalenga kuhakikisha miundombinu na mali za Shirika zinalindwa kisheria pamoja na kuwezesha utii wa Sheria. Sehemu ya Sita ya Muswada inaweka masharti ya fedha ambayo ni vyanzo vya fedha vinavyojumuisha kiasi cha fedha kinachotengwa na Bunge, mapato yatokanayo na ada ya huduma za utangazaji wa umma, ada zinazotozwa kwa bidhaa na huduma zinazotolewa na Shirika ikiwemo huduma zinazotolewa na chaneli maalumu, ada ya huduma za utangazaji wa umma, usimamizi wa fedha, makadirio ya mapato na matumizi, matumizi ya fedha, hesabu na ukaguzi na taarifa ya mwaka. Sehemu hii inalenga kuliwezesha Shirika kuwa na vyanzo vya uhakika, toshelevu na endelevu vya mapato na kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika masuala ya fedha ya Shirika. Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania ya Mwaka 2024 22 Sehemu ya Saba ya Muswada inaweka masharti ya jumla yanayohusu udhamini wa vipindi, uharibifu wa mfumo wa matangazo, uanzishwaji wa chaneli maalumu, adhabu ya jumla na mamlaka ya Waziri kutengeneza kanuni. Dodoma, JERRY WILLIAM SILAA, 12 Agosti, 2024 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
false
# Extracted Content JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA Simu: +255 026 23222761-5 Fax No. +255 026 2322624 Baruapepe: cna@bunge.go.tz Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro S.L.P. 941, 40490 Tambukareli, DODOMA. TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SHUGHULI ZA KAMATI ZA BUNGE ____________ Shughuli za Kamati za Kudumu za Bunge kwa mwezi Oktoba, 2024 zitaanza tarehe 7 hadi tarehe 25 Oktoba, 2024. Shughuli hizo ni pamoja na vikao vya Kamati kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 29 Oktoba, 2024. Katika kipindi hicho, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) zitatangulia kuanza vikao tarehe 7 Oktoba, 2024. Kamati zilizosalia zitaanza vikao tarehe 15 Oktoba, 2024. Vikao vya Kamati zote vitafanyika Dodoma na vitaendelea hadi tarehe 25 Oktoba, 2024. Shughuli zitakazotekelezwa wakati wa Vikao vya Kamati za Bunge katika kipindi hicho ni kama ifuatavyo:- Kuchambua Miswada ya Sheria Shughuli hii itatekelezwa na Kamati tatu (3) za Bunge ambazo ni Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma. Kuchambua Sheria Ndogo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, itafanya Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni katika Mkutano wa Kumi na Sita. Kupokea Taarifa za Utendaji wa Serikali na Taasisi zake Kamati kumi na moja (11) za kisekta zitapokea na kujadili taarifa mbalimbali za utendaji wa Serikali na Taasisi zake. Aidha, Kamati ya Bajeti itapokea taarifa mbalimbali kutoka Serikalini kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Fedha na masuala yanayohusu vyanzo vya mapato ya Serikali. Kuchambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kamati mbili (2) zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, zitachambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu za Wizara, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa kwa Mwaka wa Fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2023. Matokeo ya uchambuzi huo yanatarajiwa kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge utakaoanza tarehe 29 Oktoba, 2024. Kuchambua Taarifa za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itapokea na kuchambua taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma ili kubaini iwapo uwekezaji huo una ufanisi na kwamba, umezingatia taratibu na miongozo mujarabu ya biashara. Ratiba ya Shughuli za Kamati inapatikana katika tovuti ya Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz Imetolewa na:- Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, DODOMA. 01 Oktoba, 2024.
false
# Extracted Content JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA Simu: +255 026 23222761-5 Fax No. +255 026 2322624 Baruapepe: cna@bunge.go.tz Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro S.L.P. 941, 40490 Tambukareli, DODOMA. TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SHUGHULI ZA KAMATI ZA BUNGE ____________ Shughuli za Kamati za Kudumu za Bunge kwa mwezi Oktoba, 2024 zitaanza tarehe 7 hadi tarehe 25 Oktoba, 2024. Shughuli hizo ni pamoja na vikao vya Kamati kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 29 Oktoba, 2024. Katika kipindi hicho, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) zitatangulia kuanza vikao tarehe 7 Oktoba, 2024. Kamati zilizosalia zitaanza vikao tarehe 15 Oktoba, 2024. Vikao vya Kamati zote vitafanyika Dodoma na vitaendelea hadi tarehe 25 Oktoba, 2024. Shughuli zitakazotekelezwa wakati wa Vikao vya Kamati za Bunge katika kipindi hicho ni kama ifuatavyo:- Kuchambua Miswada ya Sheria Shughuli hii itatekelezwa na Kamati tatu (3) za Bunge ambazo ni Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma. Kuchambua Sheria Ndogo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, itafanya Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni katika Mkutano wa Kumi na Sita. Kupokea Taarifa za Utendaji wa Serikali na Taasisi zake Kamati kumi na moja (11) za kisekta zitapokea na kujadili taarifa mbalimbali za utendaji wa Serikali na Taasisi zake. Aidha, Kamati ya Bajeti itapokea taarifa mbalimbali kutoka Serikalini kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Fedha na masuala yanayohusu vyanzo vya mapato ya Serikali. Kuchambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kamati mbili (2) zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, zitachambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu za Wizara, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa kwa Mwaka wa Fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2023. Matokeo ya uchambuzi huo yanatarajiwa kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge utakaoanza tarehe 29 Oktoba, 2024. Kuchambua Taarifa za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itapokea na kuchambua taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma ili kubaini iwapo uwekezaji huo una ufanisi na kwamba, umezingatia taratibu na miongozo mujarabu ya biashara. Ratiba ya Shughuli za Kamati inapatikana katika tovuti ya Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz Imetolewa na:- Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, DODOMA. 01 Oktoba, 2024.
false
"# Extracted Content\n\nJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA \n \n \n \nBUNGE LA TANZANIA \n \n \n \n \n (...TRUNCATED)
false
"# Extracted Content\n\nJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA \n \n \n \nBUNGE LA TANZANIA \n \n \n \n \n (...TRUNCATED)
false
"# Extracted Content\n\nJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA \nBUNGE LA TANZANIA \n \nTele: +255 026 2322(...TRUNCATED)
false
"# Extracted Content\n\nJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA \nBUNGE LA TANZANIA \n \nTele: +255 026 2322(...TRUNCATED)
false
"# Extracted Content\n\nJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA \n \n \nBUNGE LA TANZANIA \n \n \n \n \n \n (...TRUNCATED)
false
"# Extracted Content\n\nJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA \n \n \nBUNGE LA TANZANIA \n \n \n \n \n \n (...TRUNCATED)
false
README.md exists but content is empty.
Downloads last month
9