text
stringlengths
0
1.31k
mwisho vyombo vya habari vimechangia kutoa elimu kwa walipa kodi nchini kutokana na shughuli ya ulipaji kodi mamlaka ya mapato tanzania kufanyika kwa urahisi
hayo yalisemwa na kaimu mkurugenzi wa idara ya huduma na elimu kwa mlipakodi bwana allan kiula wakati akizungumza na majira kuhusu mlipakodi
alisema wateja wao wanalipa kodi kwa hiari na kwa wakati na kuchangia pato la taifa kuongezeka pia kuisaidia tra kufanya kazi zake kwa ufanisi
mafanikio yaliopo kwa mlipakodi kulipa kodi kwa hiari yametokana na kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya habari kwani kila mteja anajua umuhimu wa kulipa kodi hiyo alisema bwana UNK
alisema UNK analipa kwa njia ya hundi katika akaunti ya tra benki na kisha fedha hizo huenda benki kuu na wao kubaki na rekodi za malipo hayo
alisema utaratibu wa ukusanyaji kodi umekuwa ni mzuri kwa kiasi kikubwa isipokuwa mwaka wa jana uliingia dosari kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani
vodacom tanzania jana imezindua kitengo cha biashara vodacom business kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma ya mawasiliano na taarifa kwa wateja wenye kampuni kubwa na ndogo nchini
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo hicho mkuregenzi mkuu wa kitengo hicho bwana UNK lennox alisema vodacom imefikia katika hatua muhimu kwani kitengo hicho kinatokana na mahitaji makubwa ya biashara UNK kwa kasi
kitengo hichi cha kibiashara cha vodacom kinalenga kuboresha na UNK njia za mawasiliano ya wateja wetu kwa kutumia teknolojia za kisasa za mawasiliano ya ofisini kibiashara na ya binafsi kwa gharama nafuu alisema bwana lennox alisema vodacom business inalenga kutoa huduma zote zaidi ya sauti ambapo sasa UNK katika kutoa huduma za UNK huduma mbalimbali za taarifa ambazo UNK kuunganisha kampuni nchini na kampuni mama duniani
alisema ili kuhakikisha vodacom tanzania inatoa huduma za uhakika inashirikiana na kampuni ya UNK ya UNK ambayo inamilikiwa na kundi la kampuni ya vodacom
bwana lennox alisema vodacom ina mkakati wa kuboresha huduma zake na kuwa za kisasa ili kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zote kwa pamoja na kwa wakati muafaka
teknolojia inakuwa biashara tanzania inakua na vodacom tanzania kupitia vodacom business itaweza kukabiliana na mabadiliko na kuwa tegemeo la uhakika kwa watanzania wanaopenda maendeleo na ubora alisema kampuni ya uchimbaji dhahabu ya barrick UNK mining tanzania UNK mafunzo ya kilimo kwa wakulima mia tisa na sitini wilayani kahama mkoani shinyanga
akizungumza juzi na majira katika mgodi huo meneja wa maendeleo ya jamii wa barrick UNK bibi UNK UNK alisema elimu hiyo imetolewa kwa njia ya semina na katika vijiji nane vina idadi hiyo ya wakulima kutoka vijiji nane vinavyozunguka mgodi huo
hizi ni jitihada za kuunga mkono kauli mbiu ya kilimo kwanza na lengo letu ni kuhakikisha wakulima UNK kiuchumi kila kijiji UNK na wakulima mia moja na ishirini tunashirikiana nao na tayari barrick UNK kuwapa trekta alisema alisema mbali ya barrick kufanya shughuli za uchimbaji dhahabu pia imekuwa ikishirikiana na wananchi katika miradi ya maendeleo kama kilimo na elimu uchimbaji dhahabu pia imekuwa ikishirikiana na wananchi katika miradi ya maendeleo ombaomba thebathini na tisa wakiwemo watoto ishirini na tano wanashikiliwa na manispaa ya ilala kwa tuhuma za kuomba fedha na vitu mtaani katika maeneo tofauti jijini dar es salaam
akizungumza na majira dar es salaam jana ofisa uhusiano na elimu kwa umma wa manispaa ya ilala bibi tabu shaibu alisema kuwa ombaomba hao wamekamatwa jana katika oparesheni maalumu ya kuwaondoa na kuwarudisha makwao
bibi tabu alisema kuwa baada ya kuwakamata ombaomba hao watawapeleka katika ofisi za ustawi wa jamii kwa ajili ya kuwapa ushauri ili waache tabia ya kuombaomba na badala yake wafanye kazi mbalimbali za kujiingizia kipato
ushauri watapatiwa ili waweze kufahamu juu ya kufanya kazi na UNK na dhana ambayo UNK ya kuomba kwa watu ambapo elimu hiyo itatolewa katika ofisi za ustawi wa jamii na wakishapewa elimu hiyo kila mmoja atapelekwa sehemu aliyotoka alisema bibi UNK
alisema kuwa katika operesheni hiyo imebainika kuwa watoto ambao wapo chini ya miaka kumi na nane ndio wanaofanya kazi ya kuomba omba na wanatumiwa na walezi ama wazazi wao katika kufanya shughuli hiyo
alisema kuwa katika operesheni hiyo jumla ya wanawake kumi na tatu wamekamatwa na akiwemo mwanaume mmoja na kwa sasa wanapatiwa elimu ya ushauri
alisema kuwa operesheni hiyo itakuwa endelevu ili kuweza kuwaondoa kabisa katika maeneo ya jiji kwani tabia hiyo imekuwa kero hasa kwa majiji makubwa
upelelezi wa kesi ya kuendesha shughuli za upatu kinyume na sheria inayowakabili vigogo wa kampuni ya development entrepreneurship community initiative bado haujakamilika huku hatma ya mbegu za wanachama ikiwa UNK
hatua ya kutokamilika kwa upelelezi huo ilijulikana jana katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu dar es salaam mbele ya hakimu mkazi bibi warialwande lema wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa
wakili wa serikali bwana justus mlokozi aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa
kutokana na taarifa hiyo mahakama iliahirisha kesi hiyo mpaka oktoba kumi na mbili mwaka huu ambapo UNK
washitakiwa katika kesi hiyo ni bwana jackson mtares bwana dominick kigendi bwana timotheo ole loitg nye bwana swamel mtares na bwana arbogast kipilimba wote wakazi wa dar es dar es salaam
wote kwa pamoja wanadaiwa kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na sheria za kibenki na taasisi za fedha
walidaiwa kuwa kati ya mwaka ishirini sifuri saba na machi mwaka huu wakiwa makao makuu ya kampuni hiyo huko mabibo dar es salaam na maeneo mengine hapa nchini walikusanya fedha kutoka kwa umma kwa ahadi ya matumaini ya kuwapa fedha zaidi ambayo katika mazingira ya biashara ilikuwa ni kubwa tofauti na mradi uliokuwepo
katika makosa ya pili washitakiwa hao walidaiwa kupokea amana kutoka kwa umma kinyume na sheria ambapo kosa hilo linadaiwa kufanyika katika kipindi cha mwaka ishirini sifuri saba hadi machi mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya nchi hii walipokea amana hizo bila kuwa na leseni
kutokana na kuwepo kwa kesi hiyo hatma ya mbegu za wanachama wa kampuni hiyo haijulikani huku viongozi hao wakiwa na zuio la kuendesha mkutano wowote kuhusiana na mambo ya upatu huo mpaka kesi yao itakapomalizika
watuhumiwa wa mauaji yaliyofanyika katika benki ya UNK tawi la temeke UNK silaha kali pamoja na bomu la kurusha kwa mkono wameiomba mahakama kuwahakikishia usalama wao endapo UNK wachukuliwe na polisi kwa ajili ya hatua zingine za mahojiano
ombi hilo lilitolewa jana na washitakiwa bwana antony sokya na bwana yusuph rajab baada ya kuwasilishwa ombi la kuwataka warejeshwe mikononi mwa polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi
mheshimiwa mimi hapa sijui kusoma wala kuandika na UNK hawa polisi wanataka tukubali mambo yao wanayotaka wenyewe hivyo naogopa wasije UNK vitu vingine na UNK UNK hivyo naomba kuhakikishiwa ulinzi na mahakama yako aliomba bwana UNK
naye bwana sokya aliiomba mahakama kuwa iangalie afya walizonazo kabla ya kukabidhiwa kwa askari hao ili UNK mahakamani wawe kama UNK kwani wanahofia vipigo wakiwa mikononi mwa askari hao
hawa askari UNK hapa ni kama rafiki zetu lakini tukiondoka hapa ni hatari tuangalie mheshimiwa tuna hali nzuri hivyo UNK tuwe hivi hivi aliomba bwana UNK
kutokana na maombi ya washitakiwa hao upande wa mashitaka uliowakilishwa na bwana shadrack kimaro ulisema kuwa una imani washitakiwa hao UNK wakiwa salama hivyo UNK askari polisi kuhakikisha wanarudi wakiwa na hali za kawaida
mbali na hayo mahakama hiyo pia UNK washitakiwa wa kesi hiyo na kufanya idadi yao kuwa kumi ambao walisomewa mashitaka upya
washitakiwa hao wanadaiwa kuwa julai thebathini na moja mwaka huu wakiwa katika benki ya nmb tawi la temeke waliwaua bwana seif mkweke na e mia tatu na ishirini na tisa cpl josephat
watuhumiwa wengine ni boniface joseph deogratius masawe mkazi wa moshi elfu hamsini na tano na mia tisa na thebathini na tano sgt mathew mwangunga ambaye ni askari wa jeshi la wananchi na mkazi wa kibaha said hamisi issack abuu mkazi wa moshi jopo salum na yusuph rajab seleman nzowa na richard lucas ambaye ni raia wa burundi
mauaji haya yalisababishwa na uporaji wa fedha katika benki hiyo ambapo silaha kali yakiwemo mabomu ya kutupa yalitumika na zaidi ya shilingi milioni sitini ziliporwa
kesi nyingine iliyohusisha washitakiwa wote ni ya uporaji wa gari aina ya prado kwa kutumia silaha ambapo mbali na gari hilo jumla ya shilingi milioni kumi na nne zilidaiwa kuporwa na washitakiwa hao ambao wanadaiwa kutenda julai thebathini mwaka huu
mwisho chama cha wananchi kimegundua mabaki ya shahada za kupigia kura ambazo zilikuwa zimechomwa moto katika bohari kuu ya kutunzia nyara za serikali iliyopo eneo la keko karibu na wizara ya maliasili na utalii jijini dar es salaam
cuf ilidai kugundua vitambulisho hivyo juzi na baada ya kukamilisha uchunguzi jana UNK waandishi wa habari na kuwapeleka eneo la tukio kwa ajili ya UNK
msafara wa waandishi wa habari ukiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho profesa ibrahimu lipumba ulifika eneo la tukio na kukuta vitambulisho hivyo ambavyo baadhi yake vilikuwa UNK kabisa huku vingine vikiwa UNK sana vikiwa katika lundo la majivu na baadhi ya UNK
akizungumza baada ya kufika eneo la tukio profesa lipumba alisema kuwa jambo hilo ni la kusitisha na linaloonesha kuwa tanzania haina demokrasia ya kweli
tunaingia katika uchaguzi gani namna hii
vitambulisho hivi zaidi ya milioni moja tumeshuhudia leo UNK moto katika bohari ya serikali na hatujui ni nani muhusika ina maana hawa watu hawataweza kupiga kura tena alisema profesa lipumba
aliongeza kuwa anashangazwa na tume ya uchaguzi na kudai kuwa hafahamu inafanya kazi gani na kudai kuwa serikali ya chama cha mapinduzi iliyopo madarakani haina misingi ya utawala bora
ina maana watu wote hawa milioni moja hawakupiga kura na UNK kura sasa tunataka serikali UNK vitambulisho hivi vinatoka wapi alisema
mbunge wa micheweni zanzibar bwana shoka khamis shoka ambaye alikuwepo katika msafara huo alisema kuwa vitambulisho hivyo ni wazi UNK kutoka kwa wananchi
mimi nilishawahi kulieleza jambo hili hapo kabla na UNK bungeni badala yake nilitakiwa kutoa maelezo huku spika akidai kuwa suala hilo halina ukweli wowote na kwamba ni madai tu lakini leo jambo hili UNK alidai bwana shoka
viongozi waandamizi wa cuf ambao pia walikuwepo katika msafara huo walichukua lundo la vitambulisho kama ushahidi kuondoka nalo
mwisho rais jakaya kikwete amewataka viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuacha kutoa nyaraka na miongozo inayolenga kuelekeza wanaumini wao namna ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao mwakani ili kuepuka madhara yanayoweza UNK taifa
akijibu maswali ya papo kwa papo kwa njia ya simu na barua pepe kupitia redio na televisheni katika kipindi maalum kiitwacho muulize rais kupitia televisheni ya taifa kilichorushwa pia na vituo vingine jana usiku rais alisema jambo hilo UNK serikali hususani wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu
alisema tabia hiyo ikiendelea itawafanya watanzania kupigakura kwa maelekezo ya dini zao jambo alilosema binafsi UNK hofu kwani tanzania si nchi ya kidini
alisema kwa kuzingatia hali hiyo kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi kilichokutana hivi karibuni mjini dodoma UNK kuwa hoja hizo na hali hiyo zikiendelea UNK utaifa wetu
alieleza kuwa hatua hiyo ina mwelekeo mbaya kwani baba wa taifa marehemu mwalimu julius nyerere alijenga taifa lenye umoja na mshikamano bila kujali rangi dini wala ukabila bali alizingatia utanzania
alisema katika kikao hicho nec iliwataka viongozi wa ccm UNK katika mambo hayo na kumwagiza rais na wakuu wenzake wa serikali kukaa pamoja na kuzungumza na viongozi wa dini kuona mwelekeo wa taifa na namna ya kuepuka hatari UNK
ni hofu ambazo na sisi tunazo UNK kukaa nao na kuona ni wapi tutafikisha suala hilo alisema rais kikwete aliwataka viongozi wa dini kutoendelea kutoa matamko tena na kuviomba vyombo vya habari UNK kuepusha jambo hilo ili UNK kuwasha moto unaweza UNK taifa na kutoa mifano ya nchi kadhaa ikiwemo UNK ambazo UNK na migogoro ya kidini
ufisadi akizungumzia suala la ufisadi na mafisadi nchini rais kikwete alisema serikali yake imechukua hatua madhubuti katika vita hiyo hasa kwa kujenga chombo cha kuratibu mapambano ya rushwa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa
alisema kuwa hilo lilikuwa moja kati ya mambo ya msingi kuchukuliwa kwa wakati huu ambalo lilihusisha kubadili sheria ya rushwa ya mwaka elfu moja na mia tisa na sabini na moja iliyokuwa na makosa machache na muundo wa takukuru kwa kweli UNK kama swali hilo la ufisadi na mafisadi UNK si kweli kuwa UNK hatua za kutosha tumefanya mambo makubwa ikiwemo kuiangalia upya ile sheria ya zamani hii ya sasa UNK tafsiri ya rushwa ambapo hata ubadhilifu wa mali ya umma ni makosa ya rushwa
tumebadili muundo wa takukuru ambapo sasa inapatikana katika kila wilaya nchini tumeongeza watumishi na kuwapatia vitendea kazi huku UNK waendelee kuwahamasisha watu UNK vitendo vya rushwa na watoe taarifa zaidi za makosa hayo alisema rais kikwete
alikiri kuwa katika vita dhidi ya ufisadi yamekuwepo UNK malalamiko kuwa watuhumiwa wakubwa wenye dhamana na majina makubwa katika jamii hawachukuliwi hatua hivyo mkono wa sheria kuwaangukia zaidi watu wadogo
alisema kuwa amekuwa akiwasihi watumishi wenzake serikalini kuwa lazima wachukue hatua dhidi ya wale wote wanaohusika na vitendo vya ufisadi na wananchi waone hatua hizo UNK
ni kweli kuwa pamoja na yote tuliyoyafanya bado UNK kusikia malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa UNK
tunachukulia hatua dagaa tu lakini papa wale samaki wakubwa wanaachwa lakini ni vyema kutambua kuwa hili lina ugumu wake watu wakubwa nao pia wana mbinu na maarifa makubwa ya UNK
lakini tumechukua hatua katika kashfa za epa minara pacha ya bot na bado takukuru wameniambia kuwa wana kesi mbili tatu UNK mahakamani hivi karibuni
kwa kweli yale UNK fanya UNK sasa yanaifanya serikali hii iwe na rekodi ya pekee ya kuthubutu kuwafikisha watu wakubwa mahakamani alisema rais kikwete
kagoda na richmond alipoulizwa juu ya tuhuma kwamba mafisadi walioshiriki katika kashfa za kagoda na richmond ni marafiki zake wa karibu ndio maana serikali yake imeshindwa kuwachukulia hatua rais kikwete alisema katika mapambano ya rushwa hakuna rafiki wala adui
alisema baada ya kashfa ya epa aliunda tume kusaidia kuwapata UNK pesa hizo ili UNK kabla hawajafikishwa mahakamani kuepuka uwezekano wa kukosa vyote kama wangepelekwa mahakamani na kushinda kesi
baada ya hapo UNK uchunguzi na hatimaye watuhumiwa UNK mahakamani sasa hilo la nani UNK au UNK halimo ndani ya mamlaka yangu ilikuwa kazi ya UNK
katika hilo la richmond kwa kweli nilikuwa na wasi wasi mapema na nilimwambia hilo waziri wakati wa kuitafutia dhamana kampuni hiyo kupitia hazina kuwa awe makini isije ikawa kampuni hiyo haipo nilikuwa nikiita kwa kiingereza UNK company yaani kitu ambacho hakipo kampuni ya UNK
baada ya uchunguzi wa kamati ya bunge ambayo hata hivyo haikusema wazi kama kulikuwa na rushwa sasa kuna watu UNK viongozi wa kisiasa UNK kwa nafasi zao kwa makosa yaliyofanywa na watu waliokuwa chini yao sasa wapo maofisa ambao tunasubiri taarifa yao katika bunge la novemba ambayo natumaini itakuwa nzuri
waraka mwongozo alisema waraka uliotolewa na kanisa katoliki na mwongozo uliotolewa na shura ya maimamu UNK hofu
alisema ni mambo hayo UNK kwa kuwa yametokea katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao na kueleza hofu yake kwamba watanzania wanaweza kupiga kura kutokana na maelekezo ya dini zao
rais kikwete alisema kuwa kutolewa kwa maandiko hayo kutoka kwa viongozi wa dini katika kipindi hiki UNK mgawanyiko katika jamii kwani kuna uwezekano wa kupata viongozi UNK udini badala ya UNK na kulifikisha taifa mahali pabaya
alisema kwa kuwa maandiko ya viongozi wa madhehebu ya dini wanatoa maelekezo kwa waumini wa dini tofauti jinsi ya kumchagua kiongozi yanaweza kuhatarisha amani na kusababisha kutoelewana miongoni mwao
alisema baada ya uchaguzi mkuu kuisha kuna uwezekano kutokea kwa na majigambo kati ya wanachama wanamuunga mkono aliyeshindwa na yule aliyeshindwa na kusababisha matafaruku mkubwa
aliwataka viongozi hao kuacha kuzungumzia mambo hayo kwa sasa kutoka na kuchukua sura mpya inayoashiria malumbano miongoni mwa serikali na viongozi hao wa dini alisema kwa kuwa bado kuna muda wa kutosha hadi kufikia uchaguzi mkuu wa ishirini moja sifuri anafanya UNK za kuonana na viongozi hao ili kujadili kwa kina suala hilo
tumekubaliana na katika vikao vyetu vya chama kuwa UNK suala hili waache kulizungumzia na wale mambo wako mbioni kulizungumzia pia nawaomba UNK kwani sasa nimeanza kufanya mawasiliano na viongozi wa dini ili kujadili suala hilo alisema rais kikwete
alivitaka vyombo vya habari kutambua kuwa jambo hilo ni hatari na kuvitaka kuacha UNK kwani ni hatari kubwa kwa amani ya nchi na iwapo amani itavunjika hakuna mtu UNK UNK
alisema katika kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi kilichofanyika mwishoni mwa agosti mwaka huu mjini dodoma walikubaliana kuacha UNK suala hilo hadi hapo UNK ufumbuzi
ucheleweshaji kesi rais kikwete alikiri kuwa katika mahakama nyingi nchini haki UNK kesi UNK sana na hii ni kutokana na uhaba wa majaji na mahakimu pamoja na vitendea kazi
rais kikwete alisema kuwa serikali yake katika kukabiliana na uhaba wa majaji na mahakimu iliamua kuongeza majaji ishirini na kufikia idadi ya majaji arobaini na mbili nchini kama njia ya kuboresha utendaji wa mahakama
aliongeza kuwa mbali na kuteua majaji pia serikali yake UNK vema kuongeza idadi ya mahakimu wakazi pamoja na wilaya ambapo aliteua zaidi ya mahakimu mia moja na themanini na kufikisha idadi ya mahakimu wakazi na wa wilaya mia tatu na ishirini nchini
kwa upande wa mahakimu wa mahakama za mwanzo waliteuliwa mahakimu wengi na kufikisha idadi yake kuwa sabini sifuri jambo ambalo UNK kwa kiasi fulani tatizo la uhaba wa mahakimu nchi
alisema jambo lingine linalochangia katika ucheleweshaji wa kesi ni pamoja na mahakama kutokuwa na zana bora za kufanyia kazi zikiwamo kompyuta hivyo UNK watendaji hao muda mrefu kuandaa kazi zao
hukumu ya zombe kuhusu kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini wa mkoani morogoro na dereva teksi mmoja mkazi wa manzese jiji dar es salaam rais kikwete alisema serikali UNK na hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya tanzania ya UNK washitakiwa wa kesi ya mauaji ambapo imeamua kukata rufaa mahakama ya juu
alisimulia kuwa baada ya kufika dar es salaam kutoka kwenye ziara zake kikazi alipewa taarifa kuwa polisi wameua majambazi wakati UNK kwa risasi naye UNK kwa kazi nzuri kwani wakati huo wimbi la ujambazi lilikuwa limekithiri sana lakini aliposikia malalamiko yameongezeka akaunda tume kuchunguza mauaji hayo
muafaka zanzibar akijibu swali kuhusu muafaka wa hali ya kisiasa zanzibar rais kikwete alisema kuwa hata yeye hali ilivyo visiwani humo UNK kwani hakuna jambo ambalo haliwezi kuzungumzwa mezani na kushangazwa na UNK iliyopo
alisema kuwa kakika suala la muafaka linahitaji kuketi na kuzungumza badala ya kulaumiana
mimi jambo ambalo UNK kuwa ni tatizo sana kwa yale yanayozungumzwa ni kuhusu katiba ya zanzibar uendeshaji wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar lakini tumezungumza na tukafika mahali hatukuweza kumalizia alisema
mafuta zanzibar alisema suala la mafuta zanzibar awali lilikuwa la muungano lakini baada ya kuona mafuta yanaweza kupatikana zanzibar ndio likawa sio jambo la muungano
hatuna sababu za kulumbana katika suala hili kwani mimi sioni kama ni tatizo kubwa lakini kama lingekuwa suala la kuvunja muungano hapo kweli lingekuwa jambo kubwa alisema rais kikwete
makundi ndani ya ccm akijibu swali la bwana UNK UNK wa arusha aliyetaka kujua sababu za kuibuka kwa makundi mawili ndani ya chama cha mapinduzi rais kikwete alikanusha kuwepo kwa makundi ndani ya chama
rais pia alizungumzia kilichotokea katika mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya ccm mjini dodoma na kukiri kwamba chuki miongoni mwa wabunge wa ccm ilikuwa kubwa hatua iliyosababisha kuundwa kamati ya watu watatu bwana pius msekwa mzee ali hassan mwinyi na bwana abdulrahaman kinana kufuatilia mwenendo wa wabunge wa ccm hata hivyo aliwataka wabunge wa ccm kumaliza tofauti zao kupitia vikao vya chama na si kulumbana kupitia vyombo vya habari ili kulinda hadhi ya chama
akijibu UNK la bwana tido mhando kuhusu kampuni ya reli alisema serikali inaendelea kushugulikia maslahi ya wafanyakazi hao
akijibu swali lililoulizwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la utangazaji tanzani bwana tido mhando aliyetaka kujua serikali UNK vipi na changamoto za sekondari za kata rais kikwete alisema serikali imeongeza kasi ya kufundisha walimu kupita vyuo vya umma na binafsi jambo ambalo limeongeza idadi ya walimu
alisema walimu wanaohitimu wameongezeka kutoka hamsini sifuri kwa mwaka ishirini sifuri tano hadi kufikia tano mia tatu na thebathini na moja kwa mwaka ishirini sifuri tisa aliongeza kuwa serikali ina mpango wa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika bajeti ya mwaka ujao
kuhusu suala la ujenzi wa maabara alisema serikali ina mpango wa kuongeza fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara na kwamba tayari benki ya dunia imetoa kiasi cha shilingi milioni tisini kati ya milioni mia tatu na hamsini zinazohitajika
habari hii imeandikwa na peter masangwa edmund mihale elisante kitulo na tumaini makene kesi ya wizi wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya madeni ya nje inayowakabili wafanyabiashara akiwemo bwana jeetu patel na wenzake itaanza kusikilizwa upande wa mashahidi wa mashitaka septemba ishirini na tisa mwaka huu