input
stringlengths
5
25.1k
label
stringclasses
6 values
TANZANIA imefanya maboresho makubwa na kutengeneza mazingira rahisi ya uwekezaji kwa ajili ya mtu yeyote kuwekeza nchini bila usumbufu. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameliambia Bunge jana kwamba miongoni mwa mazingira hayo ni pamoja kuweka mfumo wa kielektroniki, unaowezesha wawekezaji kuomba leseni, ardhi na ithibati ya uwekezaji kutoka popote walipo bila kulazimika kufika nchini.Alisema hayo wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Viti Maalumu, Jasmine Tiisekwa (CCM), aliyetaka kusikia kauli ya serikali kuhusu wawekezaji wanaosumbuliwa. “Serikali ya Awamu ya Tano imejielekeza katika uchumi wa viwanda na kuweka mazingira ya uwekezaji. Hata hivyo wawekezaji wengi wanasumbuliwa. Nini kauli ya serikali kuhusu suala hilo?” Alihoji Tiisekwa.Waziri Mkuu alisema ni kweli nchi imejikita katika kuboresha uchumi wake wa viwanda, ambavyo vinatoa fursa kwa Watanzania na mtu yeyote kutoka nje kuja kuwekeza. Akielezea maboresho yaliyofanyika, alisema awali serikali ilikuwa ikitumia Kituo cha Uwekezaji (TIC), lakini Rais ameanzisha wizara maalumu ya uwekezaji na kuteua waziri na katibu mkuu kusimamia uwekezaji kwa ukaribu zaidi, kuondoa usumbufu kwa wawekezaji.Januari mwaka huu Rais John Magufuli alimteua Angellah Kairuki kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji. Majaliwa alisema wamefikia hatua nzuri kwa kutengeneza andiko maalumu linaloonesha njia rahisi za uwekezaji nchini kuondoa usumbufu. Kituo cha Uwekezaji (TIC) kimeboreshwa kwa kukaribisha wizara zote zinazoguswa na uwekezaji kwa kuwa na mtu wao kuwezesha mwekezaji anapofika kupata huduma zote karibu. Alisema zipo takribani idara 11 za kuhudumia wawekezaji. Waziri mkuu alitaka wilaya na mikoa kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
KITAIFA
NA AMON MTEGA-SONGEA JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) mkazi wa Mtaa wa Namanyigu Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Athanasi Malindisa (70) kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kidevuni na kisha kutaka kuufukia kwenye shimo alilochimba ndani ya nyumba yao. Akizungumza na MTANZANIA jana mjini hapa mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Pius Malindisa, alisema walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu saa 1:30 jioni  kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrick Malindisa. Alisema marehemu alikuwa akiishi na mtoto wake huyo ambapo baada ya kufanya mauji hayo alianza kuwaarifu ndugu kuwa amefariki kwa ugonjwa tumbo. Kutokana na taarifa hizo ndugu walikusanyika nyumbani kwa marehemu ambapo baada ya kuingia ndani walikuta akiwa amelala ndipo walipowaita viongozi wa mtaa na baada ya kufunua walibaini marehemu ameuawa kwa kupinga na kitu chenye ncha kali kichwani na kidevuni. “Baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa awali tulitoa taarifa polisi ambapo walifika na kuuchukua mwili kwa uchunguzi zaidi. Na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma huku mtoto wake akishikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi. “Tulipofika hapa tulikuta shimo limechimbwa ndani ya nyumba na inaelekea lilimshinda na kuamua kuanza kutoa taarifa kwetu ambapo alidai alikuwa anaumwa ugonjwa wa tumbo,” alisema Pius MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo kwa sasa wanamshikilia mtoto wa marehemu, Patrick Malindisa kwa uchunguzi zaidi.
KITAIFA
JANETH MUSHI-ARUSHA KIGOGO anayefanya kazi katika Taasisi ya kusimamia na kudhibiti Viuatilifu Tanzania(TPRI),Aristerico Silayo, anayedaiwa kumbaka mtoto wake amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuamuru shauri lililokuwa likimkabili lianze upya. Mahakama hiyo jana ilipanga kutoa  hukumu katika rufaa ya  kesi ya mwanafunzi wa miaka 11 anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi (Silayo). Rufaa  hiyo iliwasilishwa na upande wa Jamhuri Mahakama Kuu ya Tanzania,Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Yohane Masara, baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi. Rufaa hiyo iliyotokana na shauri namba 339,2017, ilisikilizwa katika mahakama hiyo ya chini katika kikao maalum baada ya mahakimu kupewa (extended jurisdiction),kusikiliza kesi za Rufaa zilizopangwa kusikilizwa na Mahakama Kuu, ili zitolewe uamuzi haraka. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Aziza Temu jana Jamhuri iliwakilishwa na Wakili Mweteni Azael huku mtuhumiwa huyo akiwakilishwa na Wakili John Shirima. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Aziza alisema Mahakama hiyo inatupilia mbali mwenendo wa shauri hilo lililosikilizwa awali na kuamuru lianze kusikilizwa upya kwa Hakimu mwingine ili haki ipatikane kwa pande zote mbili na kuwa shauri hilo linapaswa kusikilziwa kwa haraka kwani limekaa mahakamani muda mrefu. Alisema baada ya kupitia mwenendo wa shauri hilo, mahakama hiyo inajielekeza katika taratibu zilizotumika kuliendesha ambapo usikilizwaji wa awali ulikuwa kinyume na Sheria ya Ushahidi nchini iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2006. “Tukitazama mwenendo huo tunaona Hakimu alimuuliza mhanga maswali mengi ya kutaka kujiridhisha, nadhani alipaswa kuweka maswali machache na kumwongoza mtoto huyo kuahidi kusema ukweli. “Hakimu alipuuzia marekebisho ya sheria hiyo ambayo yanasema mtoto mdogo anaweza kutoa ushahidi bila kuchukuliwa kiapo,” “Kwa msingi wa sheria hiyo mahakama ya awali ilipaswa kumruhusu mhanga kusema ukweli mahakamani, hiyo ilisababisha kufifisha haki ya pande zote mbili,”alisema hakimu “Mahakama hii inaona nafuu pekee inayoweza kupatikana na haki ionekane bado nashawishika ili haki ionekane imetendeka kuna haja ya shauri hili kuanza kusikilizwa upya kwa hakimu mwingine, natupilia mbali mwenendo wa shauri hili na mrufani arudi mahakama ya awali kesi ianze kusikilizwa,”aliongeza. Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo, hakimu huyo alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, Jamhuri walidai ushahidi wa mhanga, daktari aliyemfanyia uchunguzi pamoja na mwalimu aliyegundua mtoto huyo alikuwa akifanyiwa ukatili huo ulikuwa ukifanana na ulikuwa unatosheleza kumtia mjibu rufaa hatiani kwani ulikuwa wazi kuwa alikuwa akimwingilia binti yake. Alisema katika mawasilisho wakili wa utetezi alidai kesi hiyo ni ya kutunga na ilikuwa akitengenezwa huku akidai kulikuwa na mkanganyiko wa baadhi mashahidi wa jamhuri. Baada ya uamuzi huo mtuhumiwa huyo alikamatwa na jeshi la polisi na kupelekwa kituo cha kikuu cha polisi mkoani hapa ambapo katika rufaa hiyo jamhuri wanapinga hukumu iliyotolewa Desemba 14 mwaka jana katika shauri namba 339 la mwaka 2017 iliyotolewa na Hakimu Mkazi Gwantwa Mwankuga. Awali Juni 27, mwaka huu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi, alisema ofisi yake inafuatilia sakata la mtoto huyo anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi, ambaye licha ya kubainika ana makosa aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
KITAIFA
DORTMUND, UJERUMANI SHABIKI wa klabu ya Borussia Dortmund, amefariki dunia juzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mainz 05, kwenye Uwanja wa Signal Park. Katika mchezo huo, Dortmund ilifanikiwa kushinda mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Marco Reus pamoja na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa, lakini hakushangilia kutokana na kifo cha shabiki huyo. Shabiki huyo alipoteza maisha katika dakika ya 30 ya mchezo huo baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo. Taarifa ya kifo cha shabiki huyo zilienea ndani ya dakika 15 ambapo idadi kubwa ya mashabiki walipata taarifa hadi kufikia wakati wa mapumziko. Kipindi cha pili kilipoanza wachezaji wote pamoja na mashabiki walisimama kwa ajili ya kufanya maombi ya kifo hicho. Hata hivyo, shabiki mwingine alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu baada ya kupoteza fahamu kutokana na mshtuko wa moyo, lakini hali yake inadaiwa kuendelea vizuri. Rais wa klabu ya Dortmund, Reinhard Rauball, kupitia mtandao wa klabu hiyo ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na mashabiki wote kwa ujumla.
MICHEZO
LONDON, ENGLAND   NYOTA wa zamani ambaye aliwika katika klabu ya Liverpool na Tottenham, Jamie Redknapp, amedai bao la mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud, bado halijafikia kuingia katika mabao 20 bora yaliyowahi kufungwa kwenye soka. Giroud amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii wiki hii baada ya kufunga bao mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Crystal Palace, huku Arsenal ikishinda mabao 2-0. Bao hilo ambalo lilipewa jina la ‘scorpion kick’, halina tofauti kubwa na lile ambalo lilifungwa na kiungo wa Man United, Henrikh Mkhitaryan, Desemba 26, mwaka jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland, tofauti ya bao hilo ni kwamba, Giroud la kwake lilianza kugonga mwamba huku Mkhitaryan likiingia moja kwa moja wavuni. Lakini kwa upande wa Redknapp, amedai kuwa bao la Giroud ni bora ila haliwezi kuingia katika orodha ya mabao 20 bora duniani ambayo yaliwahi kufungwa. “Bao la Giroud la ‘scorpion kick’ dhidi ya Crystal Palace ni bao bora ambalo sijaliona kwa hivi karibuni. Hakuna hata mmoja ambaye alidhani kama mchezaji huyo angeweza kufanya vile. “Sina tatizo lolote na Giroud, lakini ukweli ni kwamba bao hilo halinifanyi niliweke kwenye orodha ya mabao 20 bora katika michuano ya ligi kuu. Ukweli ni kwamba, Giroud alikuwa na bahati kwa kuwa hakudhani kama mpira atapigiwa kwa nyuma. “Hata kama ni bao bora lakini siwezi kulilinganisha na lile ambalo aliwahi kulifunga Thierry Henry katika mchezo dhidi ya Manchester United au bao ambalo alilifunga Wayne Rooney dhidi ya Manchester City pamoja na lile ambalo alilifunga Dele Alli mwaka jana dhidi ya Crystal Palacem pamoja na orodha kubwa ambayo ninaweza kuitaja,” alisema Redknapp. Hata hivyo, kwa upande wa Giroud mwenyewe alidai kuwa anaamini ilikuwa ni bahati kuweza kufunga bao la aina hiyo, ila anashukuru kuwa ameisaidia timu yake kujipatia alama tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini England.
MICHEZO
NA JESSCA NANGAWE WAKATI kipa wa Simba, Said Mohammed Nduda akitarajiwa kuondoka wiki ijayo kuelekea India kwa matibabu, beki wa timu hiyo, Shomary Kapombe, atarejea uwanjani kuanza mazoezi mepesi. Kapombe na Nduda ameendelea kukosa mechi za awali za Ligi Luu kutokana na kuwa majeruhi tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Simba, Haji Manara, alisema Kapombe anatarajia kuanza mazoezi wiki ijayo, baada ya kumaliza matibabu yake kutokana na majeraha aliyopata wakati akitumikia timu ya Taifa (Taifa Stars). “Kapombe anaendelea vyema na matibabu na kwa mujibu wa daktari atakuwa fiti kuanzia Jumatatu, anaweza kuanza mazoezi mepesi ili kurudi kwenye kiwango chake kama kawaida,” alisema Manara. Alisema kwa upande wa Nduda, ataelekea nchini India mara baada ya taratibu za safari na hospitali atakapofikia kukamilika. Kipa huyo bora wa michuano ya COSAFA mwaka huu nchini Afrika Kusini alisajiliwa na Simba akitokea Mtibwa, aliumia katika kambi ya Zanzibar wakati wakijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao, Yanga. Wachezaji hao tangu wasajiliwe na klabu hiyo hawajawahi kuitumikia timu hiyo katika michezo yake ya ligi, kutokana na kuwa majeruhi.  
MICHEZO
Na IBRAHIM YASSIN-NKASI MATUMAINI ya kupata mavuno mengi ya mahindi katika Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, yameanza kupotea baada ya wadudu waharibifu wa mazao aina ya viwavi jeshi kuvamia mashamba ya wakulima na kuyaharibu vibaya. Wadudu hao wamekuwa wakiharibu zaidi mazao ya mahindi kwa kula majani, kitoto cha mahindi na mbelewele kiasi cha mahindi hayo kushindwa kuzaa. Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kaimu Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya, Permin Matumizi, alisema wadudu hao wameingia wilayani Nkasi bila wakulima kugundua, wakifikiri kuwa ni wadudu aina ya zongoli na walishitushwa baada ya kuona wadudu hao hawafi kwa dawa za kawaida walizozoea kuwaulia wadudu hao. Alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa wakulima, wataalamu walibaini kuwa, wadudu hao ni viwavi jeshi ambao umbo lao ni kama la zongoli na kwa kitaalamu wanaitwa ‘maize stalkborer-heliothisspp’ na kuwa eneo lililoathirika zaidi ni katika vijiji vya Itekesya na Ntemba, vilivyoko katika Kata ya Kate. Alifafanua kuwa, wadudu hao ni hatari sana na zinahitajika juhudi za makusudi za kuhakikisha wanadhibitiwa mapema ili kuweza kuyanusuru mazao katika msimu huu wa kilimo wa 2017-18, ili baa la njaa lisije kutokea wilayani humo. Alisema mpaka sasa jitihada za Serikali zimefanyika kuhakikisha dawa za kuulia wadudu hao zinapatikana kwa wingi katika maduka yote ya pembejeo za kilimo na dawa sambamba na wakulima kushauriwa kuwatumia wataalamu wa kilimo katika kukabiliana na wadudu hao. Matumizi amewataka wakulima kushirikiana na wataalamu wa kilimo kufanya ukaguzi wa kina wa mashamba yote ili kuweza kubaini uwepo wa wadudu hao ili waweze kushirikiana katika kumaliza tatizo hilo.
KITAIFA
Timu ya JKT Tanzania imefanikiwa kuwazuia Mabingwa watetezi wa Simba kuendelea kutamba baada ya kuipachika goli moja kwa bila. Dakika ya 27 ya Mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara JKT walifanikiwa kupata goli baada ya Adam Adam kufunga goli la Kichwa. Bao la Adam Adam akiifungua milango ya Simba dakika ya 25. 55' | Simba SC 0-1 JKT Tanzania. LIVE #AzamSports2 . . #VodacomPremierLeague #LigiKuuTanzaniaBara #VPLUpdates #VPL #SimbaSC #SSC #JKTTanzania #SimbaJKT @simbasctanzania @hajismanara @baraka_mpenja A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Feb 7, 2020 at 6:18am PST Hata hivyo unaweza kusema waamzi waliongeza umakini zaidi katika mipira ya kuotea upande wa Simba jambo ambalo wengine wanasema kuna wakati ilionewa. Kwa matokeo hayo Simba ambayo leo ilicheza katika kiwango kizuri inaendelea kuwa kileleleni na alama zake 50 katika michezo 20. Je kipigo cha Simba kinahusiana na hatua ya TFF kuwaadhibu baadhi ya waamuzi kwa kuchezasha vibaya.? Tuandikie maoni yako hapo chini.
MICHEZO
KATIBU Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza ame- sema Tamasha la Utama- duni la Afrika Mashariki (JAMEFEST) limetoa elimu na kuwanufaisha watu wengi kiuchumi na kisiasa. Akizungumza na gazeti hili Mngereza alisema mbali na wajasiriamali waliotumia fursa kuuza bidhaa zao pia, kuna hoteli na watu wa usafiri na utalii lakini pia Mama Ntilie walionufaika kupitia wageni mbalimbali kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.“Wengi wamenufaika tumeona bidhaa mbalimbali, watu wameuza kupitia tamasha, kuna watu wa tax, bodaboda ambao wamepata wateja, kuna vikundi vya wasanii navyo vimetumikia jukwaa kujitangaza pia, “alisema. Mngereza alisema alichokifurahia zaidi ni kuona makundi tofauti yameshirikishwa waki- wemo watu wenye ulemavu, ambao wameonesha uwezo mkubwa katika ubunifu wa sanaa za mikono hali iliyovu- tia kununua bidhaa zao. Alisema kwa kile alichokiona anahimiza umuhimu wa jamii ku- towafungia watoto wenye ulemavu ndani badala yake wafundishwe sanaa za mikono ziwasaidie kujik- wamua kiuchumi. “Naamini kabisa wenye ulemavu kutokana na uwezo wao wakifundishwa sanaa za mikono wanaweza kufanya mambo makubwa, jambo la muhimu wasiwa- fungie watoto ndani kwa kuona aibu, wawatoe na kuwaelimisha watafanikiwa kiuchumi, “alisema. Katibu huyo alisema ku- pitia tamasha watu wameb- adilishana uzoefu, wame- jenga mtandao, wamejifunza tamaduni za kila nchi hivyo, ushirikiano huo wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki utaendelea kudumu na kuimarisha uchumi wa nchi hizo.
MICHEZO
Mkali huyo aliyetua JKT Ruvu msimu huu akitokea Azam FC, alisema ana imani kubwa na kocha mpya Abdalaah Kibadeni kutokana na uwezo wa ufundishaji aliokuwa nao, hivyo kutua kwake kutabadili mwenendo wao mbovu walioanza nao msimu huu.“Namfahamu Kibadeni ni kocha mwenye uwezo mkubwa wa kufundisha, naamini anaweza kutusaidia na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote ila kikubwa sisi wachezaji tumpe ushirikiano ili tuweze kumrahisishia kazi yake,” alisema Mwaikimba.Mshambuliaji huyo alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo hakutokani na ubovu wa kocha aliyeondolewa Fredy Minziro , bali ni hali ya kawaida ambayo inaweza kuitokea timu yoyote zikiwemo kubwa za Simba, Yanga na Azam.Alisema Minziro alikosa bahati licha ya kuijenga timu hiyo kwa kufanya usajili mzuri wa wachezaji wengi wenye umri mdogo, lakini alikosa bahati kutokana na kufanya vibaya mechi nne za mwanzo na kuamua kuachia ngazi.Mwaikimba aliwataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanajituma na kumpa ushirikiano wa kutosha kocha wao mpya Kibadeni ili kuzinduka katika usingizi mzito na kuanza kufanya vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu zinazoendelea nchini.
MICHEZO
Promosheni hiyo itakayojulikana kama ‘Pata Patia na NMB’ itadumu kwa miezi sita, ina lengo la kuhamasisha wateja kujiwekea akiba katika akaunti zao na kuweza kujishindia fedha.Kaimu Mkuu Kitengo cha wateja binafsi, Boma Raballa alisema “NMB imeanzisha promosheni hii kwa lengo maalumu la kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba katika akaunti zao”.Alisema pia wateja wapya kujiunga na NMB kwa kufungua akaunti na kuweka akiba huku wakiwa na nafasi kubwa ya kujishindia fedha.Raballa alisema mteja anatakiwa kuweka kiasi kisichopungua Sh 50,000 na kuweza kujishindia kuanzia Sh 100,000 hadi Sh milioni tatu papo hapo.“Tunatarajia kuwafikia washindi 144 kwa miezi sita na tukimpata mshindi atapigiwa simu na ataelekezwa namna ya kushiriki promosheni hiyo,” alisema.Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NMB, Rahma Mwapachu alisema “Tayari tumepata kibali kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha na tuna imani shindano hili litawanufaisha wengi na kufikia malengo yao waliyojiwekea”.
UCHUMI
WATENDAJI wa mifuko ya hifadhi ya jamii wametakiwa kuhakikisha wanatii na kutekeleza kwa ufanisi maagizo ya Rais John Magufuli aliyotoa kuhusu wastaafu.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa agizo hilo wakati alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mjini hapa.Waziri Jenista alitaja maagizo hayo kuwa ni pamoja na kuendelea kutumia vikokotoo vya zamani vya mafao kwa kila mfuko na kuhakiki kikamilifu wastaafu wote ili kujiridhisha kuwa hakuna wastaafu hewa.Akiwa katika siku yake ya kwanza kutembelea mikoa yote nchini kuona iwapo maagizo hayo ya Rais Magufuli yanatekelezwa ipasavyo, Mhagama pia ameagiza watendaji wa mifuko hiyo kuhakikisha wanaachana na miradi isiyo na tija na kuzingatia kubana matumizi yasiyo ya lazima.Alisema kuwa jukumu kuu la Wizara hiyo ni kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali ili kufikia matarajio na malengo ya Rais Magufuli huku akitoa ujumbe kwa watumishi wote wasiotaka kuendana na kasi hiyo kuondoka kwa hiyari."Tunahitaji watumishi waadilifu na walio na weledi, hivyo watumishi wanaoenda kinyume na matakwa yetu ni vizuri wakajiondoa wenyewe mapema badala ya kusubiri kuondolewa kwa aibu," alionya .Aliupongeza uongozi wa PSSSF kwa kuendesha uhakiki kwa kiwango cha hali ya juu jambo ambalo pia liliungwa mkono na wateja mbali mbali aliowakuta ofisini hapo ambao hawakuficha furaha yao kwa kitendo cha Rais Magufuli kurejesha kikokotoo cha zamani.Hata hivyo, waziri hakuridhishwa na utendaji kazi wa NSSF katika kushughulikia wateja wao, hasa kwenye suala la fao la kujitoa, ambapo mmoja wa wateja alilalamika mbele yake uwa inamchukua muda mrefu kupata malipo yake.Awali, Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa alimwambia waziri kuwa mteja wao huchukua siku 14 kupata hundi yake baada ya kutimiza masharti yote yaliyowekwa na mfuko huo.Kwa mujibu wa taarifa aliyopewa waziri, PSSSF mkoa wa Singida una wateja 122,000 wakati NSSF ina zaidi ya wateja 18,000 .
KITAIFA
  NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM MFANYABIASHARA Yusufali Manji (41), anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, amekataa mbele ya mahakama kutetewa na Wakili Peter Kibatala, kutokana na kile alichosema ni sababu za kisiasa. Manji alitoa kauli hiyo jana mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Isaya Arufani, kabla hajatoa uamuzi wa kutupilia mbali ombi la dhamana la mfanyabiashara huyo ambaye sasa inabidi akaitafute dhamana Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. “Mheshimiwa Jaji, nilipowasilisha maombi ya dhamana nilimpa maelekezo Wakili Joseph Thadayo aniwakilishe, lakini nilishangaa kesi ilipokuja kusikilizwa Wakili Kibatala alikuja kuniwakilisha. “Sitaki kuwakilishwa na Kibatala kwa sababu za kisiasa, nitakuwa nawakilishwa na Wakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Seni Malimi,” alidai Manji. Hata hivyo, Kibatala na Thadayo wanatoka katika kampuni moja ya uwakili. Pia Manji ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kupitia CCM, huku Kibatala akiwa ni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jaji Isaya akitoa uamuzi, alisema mleta maombi hatawakilishwa tena na Wakili Kibatala kwa sababu za kisiasa.   OMBI LA DHAMANA Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, alidai upande wa Jamhuri wamewasilisha hati kinzani na nia ya kuwasilisha pingamizi la kisheria kuhusu maombi hayo ya dhamana. Kadushi aliomba kabla ya kuanza kusikiliza maombi ya dhamana, mahakama ianze kusikiliza mapingamizi yao. Kwa upande wake, Wakili Mgongolwa anayemtetea Manji, alikiri kuwa maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mteja wake, yana dosari hivyo wanakubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na Jamhuri kwamba yana msingi. Wakili Kadushi aliomba mahakama kutokana na hoja za upande wa utetezi, maombi ya dhamana yatupwe. Jaji Isaya akitoa uamuzi alisema: “Mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana, hivyo maombi yaliyowasilishwa yanatupwa.”   SABABU ZA KUTUPA MAOMBI Jamhuri walikuwa na sababu tatu za kutaka maombi hayo yatupwe, ikiwa ni pamoja na kuwa Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu yanapaswa kusikilizwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Pia walidai vifungu vya sheria vilivyotumika kuwasilisha maombi si sahihi na hoja ya mwisho ni kwamba hati ya kiapo iliyoambatanishwa kuunga mkono maombi ina dosari ambazo haziwezi kurekebishika. Katika maombi yaliyotupwa, Manji aliomba mahakama imwachie kwa dhamana kwa sababu ana matatizo ya kiafya, anasumbuliwa na maradhi ya moyo. Mawakili waliwasilisha vyeti vya daktari kuthibitisha mteja wao ni mgonjwa. Manji anashtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa uhujumu uchumi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Upelelezi haujakamilika. Katika kesi hiyo, Manji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 na mihuri. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43). Kesi itatajwa Agosti 4, mwaka huu. Hati ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao inadai Juni 30, 2017 katika eneo la Chang’ombe ‘A’, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kwa pamoja walikutwa na askari polisi wakiwa na bunda 35 za vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye thamani ya Sh milioni 192.5 ambayo ni mali iliyopatikana kinyume cha sheria. Katika shtaka la pili, inadaiwa Julai mosi, 2017 Chang’ombe ‘A’, washtakiwa hao walikutwa na polisi wakiwa na mabunda manane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania yenye thamani ya Sh milioni 44 mali ambayo yalipatikana isivyo halali. Katika shtaka la tatu, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Juni 30, 2017 Chang’ombe ‘A’, walikutwa na muhuri wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wenye maandishi ‘Mkuu 121 Kikosi cha JWTZ’ bila ya kuwa na uhalali, kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi. Shtaka la nne, anadai kuwa Juni 30, 2017 kwenye eneo hilo la Chang’ombe ‘A’, Manji na wenzake hao watatu walikutwa wakiwa na mhuri wenye maandishi ‘Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma’  bila ya kuwa na uhalali, kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi. Manji na wenzake katika shtaka la tano wanadaiwa kuwa Juni 30, 2017 huko Chang’ombe ‘A’, walikutwa na mhuri wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania wenye maandishi ‘Commanding Officer 835 KJ Mgambo P.0. Box 224 Korogwe’, kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi. Katika shtaka la sita, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Julai Mosi, 2017 katika eneo hilo la Chang’ombe ‘A’, walikutwa na askari polisi wakiwa na namba ya usajili wa gari SU 383 ambayo ilipatikana kwa njia isiyo halali. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kuwa Julai Mosi, 2017 eneo la Chang’ombe ‘A’, walikutwa na askari polisi wakiwa na namba za usajili wa gari SM 8573 ambayo ilipatikana kwa njia isiyo halali.
KITAIFA
Simba na Yanga zinatarajiwa kumenyana Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara.Ninja, ambaye katika mechi za hivi karibuni amekuwa akicheza kwa kiwango kikubwa, aliliambia gazeti hili jana kuwa kukutana na Simba kwake si mara ya kwanza hivyo anaifahamu presha ya kucheza na timu hiyo lakini zaidi hawahofii washambuliaji tishio kwa sasa wa wapinzani wao hao na akaapa kuwadhibiti kikamilifu.“Nilishawahi kukutana na Simba mara mbili nikiwa Taifa Jang’ombe katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa hiyo si mara yangu ya kwanza kucheza na timu hiyo, nawajua vizuri lakini pia mimi siwahofii nawaona kama ni wachezaji wa timu nyingine tu.“Kweli wanaongoza kwa kufunga msimu huu, lakini mimi nimejipanga vya kutosha ukichanganya na mbinu ninazopewa na makocha wangu katika mechi hiyo naamini hawatakuwa na madhara, tusubiri tu siku ya mechi,” alisema Ninja.Upande wa Simba, Bocco mwenye mabao 14 na Okwi mwenye 19 wakiwa vinara wa kufumania nyavu mpaka sasa wanaonekana tishio kwa ukuta wa Yanga kutokana na spidi yao, lakini Simba pia watakuwa na shughuli pevu ya kuwazuia Obrey Chirwa na kinda Yusuf Mhilu anayeonekana kufanya vizuri zaidi kila anapopata nafasi katika mechi za hivi karibuni.
MICHEZO
BUNGE limepitisha azimio la kumfungia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge baada ya kukutwa na kosa la kutoa kauli aliyoithibitisha kuwa Bunge ni dhaifu.Kutokana na uamuzi huo, Lema hatashiriki Mkutano wa 15 ambao ni Mkutano wa Bajeti unaoendelea sasa, Mkutano wa 16 utakaofanyika Septemba na Mkutano wa 17 wa Novemba mwaka huu. Wakati wa kuchangia hoja ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu shauri la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), Lema alisema: “Roho ya mwenendo wa nchi inategemea uimara wa Bunge, sasa amesema Bunge ni dhaifu, ni kweli, na mimi kama mbunge wa vipindi vitatu nathibitisha hilo,” alisema. Kutokana na kauli hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliyekuwa anaongoza mjadala huo, alimtaka Lema kufika mbele ya kamati hiyo.Akisoma taarifa, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka alisema kamati ilikataa ombi la Lema la kutaka awepo wakili wake wakati wa kuhojiwa kwa kuwa kamati iliona hakuwa amepanga kuwa na wakili huyo. Kwa kuthibitisha hilo, Mwakasaka akasema: “Kamati ilipata mashaka juu ya uaminifu wa shahidi (Lema) kwani tarehe 9 Machi 2016 aliiomba kamati impe muda wa kutafuta wakili kuhusiana na tuhuma dhidi yake kwa kufanya vurugu bungeni siku ya tarehe 27 Januari 2016 siku hiyo kamati ilikubali ombi lake.“Ilimtaka afike Machi 11, 2016 kitu cha ajabu Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lema hakurejea katika kamati na wala hakutoa sababu ya kutokufika kwa hiyo kamati ilikosa imani naye na kuyakataa maombi yake,” alisema. Alisema wakati wa mahojiano, Lema alieleza kamati kwamba anaunga mkono maoni yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad pamoja na Halima Mdee ambao kamati iliwakuta na hatia ya kulidhalilisha Bunge.“Kwa hali hiyo, kamati iliona kwamba naye ametenda kosa hilo kwa mujibu wa kifungu cha 26 e cha Sheria ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge sura ya 2096 pamoja na 74 fasihi 1 A na B ya kanuni,” alisema. Mwakasaka alisema katika uchunguzi wake, kamati ilirejea Katiba, kanuni, sheria na taratibu na maamuzi mbalimbali na video iliyomrekodi Lema akizungumza na hivyo Kamati ilijiridhisha kwamba, Lema alitamka kwa makusudi maneno kuwa bunge ni dhaifu akilenga kulidhalilisha bunge. “Kamati ilitilia maanani na kufuatilia kwa kina na ushahidi wa Mheshimiwa Lema mbele ya Kamati ikiwemo kwa kukiri.Hivyo kamati iliona kwamba Lema alitenda kosa la kudharau na kudhalilisha Bunge. Kitendo alichofanya Mheshimiwa Lema ni cha kupingwa vita ili kulinda heshima ya bunge ambacho ni chombo cha kuwakilisha wananchi ambao tunawaongoza,” alieleza Mwakasaka. Akisoma mapendekezo ya Kamati, Mwakasaka alisema kwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Lema kuitwa mbele ya kamati na kutiwa hatiani ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vyote vya Mkutano wa Tatu wa Bunge kwa kuanzia 30 Machi 2019 siku ambayo azimio lilitolewa.“Na kwa kuwa akiwa mbele ya Kamati Mheshimiwa Lema hakujutia kosa lake wala kuomba radhi kitendo chake cha kudharau Bunge, bali aliendelea kusisitiza kuwa bunge hili ni dhaifu jambo ambalo linadhihirisha alidhamiria kutenda kosa hilo. “Na kwa kuwa Lema ni mbunge mkongwe kwa vipindi viwili ana uelewa mkubwa wa kuzijua kanuni za namna ya Bunge linavyoendeshwa hivyo kwa kitendo alichofanya ni ukosefu wa heshima kwa mamlaka ya Bunge na kutokuwa na uwajibikaji wa pamoja. “Hivyo basi Mheshimiwa Spika, Bunge linaazimia kwamba Mheshimiwa Lema asimamishwe kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia tarehe ya azimio hili,” alisema.Baada ya azimio hilo, Spika Ndugai alitoa fursa kwa wabunge kuchangia azimio hilo ambako Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), alitaka Bunge lisiunge mkono pendekezo hilo akidai limekiuka Kanuni za Bunge. Alisema kauli aliyoitoa Lema aliitoa akiwa bungeni na kwamba mbunge huyo analindwa kwa misingi ya kanuni, hivyo akichukuliwa hatua itakuwa ukiukwaji wa kanuni na kuminya uhuru wa mbunge. Hata hivyo, dakika chache baada ya Mnyika kuchangia taarifa ya kamati, wabunge wa chama hicho walisimama na kutoka nje.Kufuatia hatua hiyo, Spika Ndugai alisema: “Wanaotoka nje wasifanyiwe mahojaino na waandishi huko nje na mbunge anayetaka kuzungumza basi azungumze ndani ya bunge”. Akifafanua uamuzi wake wa kuwataka baadhi ya wabunge (waliotoka bungeni kutohojiwa na waandishi wa habari kwa siku ya jana, Spika Ndugai alisema: “ Huu ni mwaka wanne wa Bunge, na tunachukulia kila mbunge anajua sheria, kanuni na taratibu. Ingawa mbunge ana uhuru wa kutoka na kuingia ndani ya bunge ni matarajio kwamba watautumia uhuru huo vizuri. “Unatumwa na wananchi kuja hapa, lakini unakuwa na tabia ya kutoka nje ya bunge na hasa baada ya kuongea wewe, na tabia hii imekuwapo kwa muda mrefu, tumechoka!
KITAIFA
RAIS John Magufuli amesema serikali itaendelea kumuenzi mgunduzi wa madini ya tanzanite, Jumanne Ngoma pamoja na kazi zake nzuri na amesisitiza kuwa Mzee Ngoma ni shujaa wa taifa.Ahadi hiyo ilitolewa wakati wa maziko ya mzee huyo, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, nyumbani kwake katika kijiji cha Makanya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, Rais Magufuli aliwataka Watanzania kujenga tabia ya kuenzi ugunduzi unaofanywa na Watanzania ili kuepuka kazi nzuri hizo kuchukuliwa na watu wa nje.“Serikali inatambua na kuheshimu ugunduzi wa tanzanite uliofanya na Mzee Ngoma, ugunduzi ambao umeijengea Tanzania heshima kubwa duniani kote na kuboresha maisha ya watu wengi ndani na nje ya nchi”, alisema.Aliongeza, “Inasikitisha kuona kuna baadhi ya wenzetu ambao wana tabia ya kuenzi ugunduzi uliofanya na watu wa nje na kupuuza ule unaofanywa na Watanzania, si ajabu kusikia ya kuwa kuna Watanzania wenzetu ambao pia walipinga ugunduzi uliofanywa na Mzee Ngoma, jambo ambalo halipendezi.“Tutaendelea kumuenzi Mzee Ngoma na ugunduzi wake alioufanya na wakati huo huo kukabiliana na wale wote ambao wanalenga kudhoofisha na kuhujumu kazi nzuri aliyoifanya shujaa huyu wa Taifa letu”.Magufuli alisema kuwa serikali na wananchi wa Tanzania wamepokea habari za kifo cha Mzee Ngoma kwa masikitiko makubwa. Rais alitoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na wale wote walioguswa na msiba huo, aliosema ni wa Taifa kwa ujumla.Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alisema kuwa kwa kupigania haki yake ya kutambuliwa kama mgunduzi wa tanzanite, Mzee Ngoma amewaachia Watanzania elimu kubwa.“Mzee Ngoma aliipigania haki yake ya kutambuliwa kama mgunduzi wa tanzanite hadi alipotangazwa na Rais Magufuli wakati akizindua ukuta wa Mirerani Aprili mwaka jana, hivyo na sisi hatuna budi kuhakikisha tunapigania kazi nzuri tunazofanya ikiwemo ugunduzi mbalimbali ili tusije kuporwa kazi zetu na watu wa nje,” alisema.Ukuta wa Mirerani umejengwa kuzunguka eneo hilo, ambako madini hayo yanapatikana.Alisema wilaya ya Same inaungana na wale wote ambao wamependekeza njia mbalimbali za kumuenzi Mzee Ngoma, ikiwemo wazo la jina lake litumike kwenye moja ya barabara za wilaya ya Same, kwa heshima ya shujaa huyo.
KITAIFA
RABAT, MOROCCO UFALME wa Morocco umelaani vikali vitendo vya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma, unayeamini anahujumu maombi ya taifa hilo kurejea katika umoja huo. Mfalme Mohammed VI alitangaza rasmi nia ya Morocco kujiunga tena Umoja wa Afrika (AU) wakati akitoa hotuba nchini Rwanda Julai 17 mwaka huu. Nchi hiyo ilijitoa kutoka AU miaka 32 iliyopita kupinga kitendo cha chombo hicho kutambua harakati za uhuru wa Sahara Magharibi zinazopiganiwa na vuguvugu la Polisario. Morocco inasisitiza eneo hilo ni sehemu ya himaya yake. Ni miezi zaidi ya minne sasa tangu hotuba ya mfalme nchini Rwanda, na ijapokuwa mapema mwezi uliopita Dlamini-Zuma alimuahidi Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar kuwasilisha ombi hilo kwa nchi nyingine za AU, hakuna maendeleo yaliyopigwa hadi sasa. Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ilitoa taarifa kwamba, “baada ya ucheleweshaji usio na msingi kwa kutosambaza ombi la Morocco kwa wanachama wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma anaendelea kutuhujumu kwa kuweka masharti mapya kinyume na yale yanayofahamika ili ombi letu lisipate baraka kutoka wanachama wa AU.” “Mwenyekiti wa Tume ya AU anashangaza kwa kushindwa kufanya kazi bila kuegemea upande na kufuata sheria na kanuni za AU na matakwa ya nchi wanachama,” wizara hiyo iliongeza. “Takriban nchi 36 kati ya 54 wanachama wa AU haziitambui Sahara Magharibi kama eneo huru na ni wakati wa kufuta uamuzi huo,” ilisema taarifa hiyo.
KIMATAIFA
Mbunge wa Kahama Mjini (CCM) Jumanne Kishimba ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itoe msamaha kwa watu wenye bangi waisalimishe Polisi iuzwe huko Serikali ipate mapato.Amesema Wizara hiyo inaweza kutoa msamaha kwa miezi sita kwa bangi iliyopo kama inavyofanywa kwenye silaha ili bangi hiyo iuzwe kwa usimamizi wa Jeshi la Polisi na mapato yaingie Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wananchi wapate fedha."Ni vizuri wakati wote Mheshimiwa Spika dunia inapobadilika lazima twende haraka sana. Uganda Mheshimiwa Spika wamepewa na EU (Umoja wa Ulaya) zaidi ya Dola milioni 500 kwa ajili ya kilimo cha bangi wanatoa udongo kutoka Malasia lakini sisi bahati nzuri wakulima wetu wana utaalamu wa kulima bangi muda mrefu"amesema Kishimba bungeni jijini Dodoma.Mbunge huyo pia ameitaka Wizara kilimo itoe ufafanuzi kwamba watu wanaotaka kulima wamuone nani kwa kuwa ipo sheria iliyotungwa na Bunge inayoruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya kutengeneza dawa."Mheshimiwa Spika bei ya bangi duniani imepanda maradufu na nchi zote zinazotuzunguka zimekwisharuhusu" amesema.Kwa mujibu wa mwakilishi huyo wa wananchi wazungu walipiga marufuku kilimo cha bangi kwenye miaka ya 1940's lakini baadaye waligundua ndani ya zao hilo kuna dawa.Amesema Tanzania ni nchi ya tatu Afrika kwa kulima bangi ya magendo hivyo kama Serikali kama itaruhusu kilimo cha zao hilo inaweza kusaidia kuongeza mapato na kuondoa magendo.
KITAIFA
MWANAMITINDO mwenye jina kubwa nchini Kenya, Annabel Onyango na meneja wa kundi la muziki la Sauti Sol, Marek Fuchs, wanataraji kufunga ndoa ya kihistoria nchini hapo. Kwa mujibu wa mtandao wa Kenyamoja, wachumba hao wa muda mrefu watafunga ndoa hiyo Septemba 19 na sherehe itafanyika katika hoteli ya Great Rift Valley tofauti na inavyofikiriwa kufanyika mjini ama kijijini kwao. Wakati wote wa maandalizi ya harusi yao hiyo wapenzi hao wameweka kila kitu chao kitakachotokea kwa kila siku hadi siku ya ndoa yao kupitia mtandao wao.
BURUDANI
Msanii wa Bongofleva hapa nchini, Gigy Money, ametoa dongo kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wanamdharau na kumchukulia poa wakati anaanza kazi ya muziki. Gigy Money ameieleza EATV na EA Radio Digital, kuwa ilifika hatua watu wanamsema na kumshambulia mitandaoni pia walijaribu kumchonganisha na Serikali ili mradi wamshushe chini. “Kwa watu walioni-follow, sio kila shabiki anakupenda kuna wanaokuchukia lakini wanakushabikia vilevile, kuna watu ambao walikuwa wanasema kwamba siwezi kuimba, sina lolote na  nilee mtoto tu, kwahiyo hili dongo linaenda kwa watu wote mnaochukulia vitu virahisi rahisi, walikuwa wanapenda tu mimi kukaa vile” amesema Gigy Money. Aidha Gigy Money ameongeza kuwa, “Ilikuwa ndoto zangu kuwa maarufu, nilitaka kuwa hapa nilipo sasa hivi, watu waliniambia  kwamba nitakufa, nitaishia kuwa malaya pia walikuwa wananiua sana, walijaribu kunichonganisha mimi na Serikali ili mradi iniingilie kati inishushe chini na inifungie vitu vyangu”  ameongeza.
BURUDANI
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Khamis Ali Mzee katika hafla ya ufunguzi wa makocha wa leseni C ya wiki mbili inayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.Mzee alisema kukamilika kwa mfumo huo kutapelekea kuonesha hali ya michezo yote ya Zanzibar inavyoendelea.Alisema suala la kuandaa mfumo huo limekuwa likipigiwa kelele na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein, kutokana na kutokuwa na takwimu sahihi za michezo yote ya Zanzibar.“Tulikuwa tukipigiwa kelele sana na rais kwamba kwa kweli hakuna takwimu katika michezo, hivyo tunafanya hivyo ili kuwa na takwimu ya kuweza kujua idadi kamili,” alisema Mzee.Sambamba na hilo, aliwataka makocha kuyaona mafunzo hayo kuwa ni muhimu kwao kwani mafunzo hayo huwajengea kujiamini na ujasiri wa kile watakachokitoa kwa wachezaji.“Kusoma ni kujiongezea ujuzi na ujasiri kwani hata aya ya Kurani inasema kuwa hawawi sawa aliosoma na asiosoma,” alisema katibu huyo. Hivyo aliwataka kuwa makini na wafuatiliaji wazuri katika mafunzo hayo ili waondoke wakiwa na ujasiri na kujiamini katika ufundishaji wao.Mafunzo hayo ya wiki mbili yameandaliwa na Chama cha Makocha wa Soka Zanzibar kwa kushirikiana na ZFA Taifa na yanaendeshwa na Mkufunzi kutoka CAF, Sunday Kayuni.
MICHEZO
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara Simba wameendelea kutembeza kichapo kwa kile anayekatiza mbele yao na kuzidi kujihakikishia nafasi ya kutwaa tena ubingwa. Katika uwanja wa Taifa leo ulipigwa mchezo kati ya mabingwa hao na anayewafuata katika msimano mwaka huu Azam Fc. A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Mar 4, 2020 at 8:43am PST Katika mechi hiyo iliyopigwa katika hali ya hewa ya mvua mvua mchezo ulimalizika kwa jumla ya magoli 5 huku simba ikiibuka na pointi tatu. A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Mar 4, 2020 at 8:49am PST Magoli matatu kati ya hayo yalifungwa kipindi cha kwanza ambapo Azam ilitangulia kupata goli dakika ya 5 kupitia kwa Never Tigere lakini Erasto Nyoni wa Simba alisawazisha dakika 4 baadaye (Dakika ya 9) na dakika ya 16 Deo Kanda wa Simba akaongeza goli lingine. A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Mar 4, 2020 at 9:36am PST A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Mar 4, 2020 at 8:57am PST Mwanzoni mwa kipindi cha pili Azam walifanikiwa kupata goli la pili la kusawazisha kupitia kwa Idi Selemani lakink Meddie Kagere aliwainua Wanamsimbazi dakika ya 71 na matokeo hayo ya goli 3-2 yalidumu mpaka mwisho wa mchezo. A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Mar 4, 2020 at 10:13am PST
MICHEZO
Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru mke wa bilionea Msuya, Miriam Msuya na mwenzake, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka   (DPP) kugoma kuifanyia mabadiliko hati ya mashtaka ingawa alipewa siku tatu   kufanya hivyo. Uamuzi huo   ulitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa baada ya Jamhuri kudai   kwamba hauwezi kuibadilisha hati hiyo kwa sababu  iko sahihi. Hakimu Mwambapa aliamua kuwaachia huru Miriam na Revocatus Muyela wanaoshtakiwa kumuua kwa kukusudia dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya, Mei mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni, Dar es Salaam, kwa kuwa hakuna hati inayowafanya washikiliwe kwa sababu iliyopo imebainika kuwa ni mbovu. Wakili wa Serikali, Hellen Moshi, alidai   kesi hiyo ilikuwa inatajwa lakini mahakama ilitoa amri ya kubadilishwa   hati ya mashtaka. “Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka  (DPP), imeona hati iko sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kwa maana hiyo hatuwezi kuifanyia mabadiliko,” alisema Hellen. Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala akishirikiana na Wakili Faraja Mangula, alidai DPP ameonyesha jeuri na nguvu aliyonayo  lakini asingeweza kupinga amri ya mahakama. Kibatala alidai mahakama ilishatoa amri na kuwapa muda wa siku tatu upande wa Jamhuri kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka na kama wasingefanya hivyo hatua nyingine ingefuata. “Mheshimiwa hakimu DPP ameshindwa kueleza sababu ya kutotii amri ya mahakama. “Hivyo tunaomba washtakiwa waachiwe huru kwa sababu hakuna hati inayowashtaki. DPP ameshindwa kukata rufaa au kuomba marejeo, hivyo amepuuza amri ya mahakama,” aliomba Kibatala. Akitoa uamuzi, Hakimu Mwambapa alisema Januari 9, mwaka huu, mahakama   iliagiza hati ya mashtaka ibadilishwe kwa kuwa ni mbovu. Alisema mahakama hiyo ilitoa muda wa siku tatu kuanzia Februari 20, mwaka huu,  kwa upande wa Jamhuri kuifanyia mabadiliko hati hiyo ya mashtaka. “Pamoja na amri hiyo mpaka leo (jana) Jamhuri haijabadilisha hati ya mashtaka hivyo Mahakama inaona hakuna hati ya mashtaka halali inayowashikilia washtakiwa, hivyo inawaachia huru,” alisema Hakimu Mwambapa. Baada yaa kuachiwa huru saa 3.55 asubuhi,  nje ya mahakama kulikuwa na askari waliokuwa wamevalia nguo za raia ambao waliwachukua na kushuka nao hadi mlango wa kuingilia mahabusu ya mahakama ambako kulikuwa na gari la polisi. Miriam na wenzake walipakiwa katika gari la polisi lililokuwa na askari   na kupelekwa kituoni. Mke wa bilionea huyo, Miriam na mfanyabiashara Revocatus Muyela, wakazi wa Arusha, wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya dada wa bilionea Msuya, Aneth Msuya. Washitakiwa wanadaiwa Mei 25, mwaka jana, maeneo ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam, kwa pamoja walimuua Aneth.   Dada wa bilionea Msuya aliuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake. Miriam na mwenzake walipofikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Baada ya kusomewa  mashitaka, Wakili wao Kibatala, aliwasilisha maombi   akiiomba itupiliwe mbali hati ya mashitaka kwa kuwa ilikuwa na upungufu katika sheria. Kibatala alidai hati hiyo ya mashitaka ilikuwa haijitoshelezi kiasi cha kuwawezesha washitakiwa kuelewa kile walichoshitakiwa. Hivyo aliomba itupiliwe mbali na washitakiwa kuachiwa huru.   Akiwasilisha majibu ya upande wa Jamhuri, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo, alidai hati ya mashitaka iilikuwa inajitosheleza kumwezesha mshitakiwa kuelewa kile alichoshtakiwa nacho. Mahakama hiyo   ilikubaliana na hoja za wakili wa utetezi na kuamuru upande wa Jamhuri kufanyia mabadiliko hati hiyo. Hata hivyo, upande huo tangu ilipotolewa amri hiyo kwa mara ya kwanza haikufanya mabadiliko hayo na kutaka kuongezewa muda, hali iliyoufanya upande wa utetezi kusisitiza washitakiwa wachiwe huru. 
KITAIFA
MOSCOW, URUSI   MAANDALIZI yameanza kwa mkutano utakaowakutanisha wawakilishi kutoka Urusi na Mshauri Mkuu wa Masuala ya Usalama wa Marekani, John Bolton, ambao unatarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Geneva nchini Uswisi. Taarifa hiyo imetolewa jana mjini hapa na msemaji wa Ikulu, Dmitry Peskov. Alisema kila kitu kinaonekana kitakwenda vizuri kama walivyopanga. Taarifa hiyo imekuja baada ya juzi, Waziri wa Habari wa Ikulu ya Marekani, White House, Sarah Sanders,  kusema kuwa Bolton atakutana pia na wawakilishi kutoka Israel na Ukraine katika mkutano huo wa Geneva. “Maandalizi tayari yameshaanza na tuna matumaini kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga. “Utakuwa ni mkutano ambao utajadili masuala mbalimbali, hususan ya kiusalama baina ya mataifa haya mawili,” alisema msemaji huyo. Kabla ya kutolewa taarifa hiyo, awali Ofisi ya Baraza la Usalama ya Urusi ilitangaza kuwapo kwa mkutano huo baina ya Nikolai Patrushev na Bolton, lakini  haikueleza ni wapi na tarehe gani utafanyika. Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa ngazi ya juu katika masuala ya usalma kukutana, baada ya Julai 27, mwaka huu, Naibu Waziri wa Usalama, Yuri Averyanov kufanya mazungumzo na Bolton mjini hapa na katika kikao hicho kilichoongelewa zaidi ni ushirikiano baina ya mataifa haya mawili.  
KIMATAIFA
JOTO la wabunge wa upinzani kuvihama vyama vyao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), linazidi kuongezeka baada ya Mbunge wa Jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA,) Marwa Chacha kutangaza kukihama chake na kujiunga na chama tawala.Hatua ya Chacha inafikisha idadi ya watano wakiwemo watatu kutoka Chadema waliovihama vyama vyao siku za hivi karibuni na kujiunga na CCM kwa kauli za kutaka kuunga mkono juhudi mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli. Wabunge hao walioihama Chadema mbali na Chacha ni Julius Kalanga (Monduli), G odwin Mollel (Siha) pamoja na Mwita Waitara (Ukonga) wakati kwa upande wa CUF, Maulid Mtulia (Kinondoni) na Zuberi Kuchauka (Liwale).Juzi akizungumza wakati wa kufungua Daraja la Juu la Mfugale eneo jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema milango ya CCM iko wazi kupokea viongozi wowote wale ambao wako tayari kutua mizigo, akirejea baadhi ya maandiko ambayo yanasema, “njooni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha.”Akizungumzia uamuzi wake huo jana kwa simu, Chacha alisema kuhamia CCM kumekuja baada ya kuridhishwa na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli, hatua iliyomfanya kutoona sababu za kuendelea kumpinga kwa kubaki ndani ya Chadema. Alisema aliopoomba kuwa mwakilishi wa jimbo hilo la Serengeti, azma yake ilikuwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo, kama ambavyo Rais Magufuli anavyofanya kwa Watanzania, huku akiahidi kuendelea na mkakati huo endapo atapewa nafasi nyingine ya ubunge katika kuwatumia wananchi hao.“Nimeomba CCM wanipokee hilo ndilo jambo la msingi kwa sasa, sijui kama watanikubalia au la! Lakini endapo ikitokea wakanikubali na ikawapendeza nigombee tena kwa nafasi nyingine ya kuwawakilisha wananchi wa Serengeti nitashukuru zaidi,” alisema Chacha aliyekuwa mmoja wa wabunge machachari alipokuwa Chadema.Akizungumzia hatua ya mbunge huyo kuhamia CCM, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema chama hicho hakijashitushwa na uamuzi wa Chacha pamoja na kuwa walipata taarifa za mbunge huyo kuhama kupitia mitandaoni. “Na sisi tumezisikia taarifa za Chacha kuhama kupitia mitandao, hajatutaarifu kwa njia yoyote, lakini hata tulipofanya juhudi za kumtafuta kwa njia ya simu ili kujua undani wa taarifa hizo, hatukuweza kumpata,” alisema Mrema.Alisema hatua ya wanachama wake mbalimbali kukihama chama hicho wakiwemo wabunge na madiwani, ni kitendo cha kawaida katika siasa, na siyo habari mpya kwao kiasi cha kuwafanya washangazwe na jambo hilo. CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, ilimpongeza mbunge huyo kwa kutumia uhuru wake wa Katiba wa kujiunga na chama ambacho kimesimama kwa dhati kusukuma gurudumu la maendeleo.Polepole alisema Watanzania ni watu wanaopenda mshikamano na umoja hasa katika masuala ya ujenzi wa Taifa na kwamba kazi kubwa anayoendelea kuifanya Rais Magufuli inaonekana wazi wazi nchini kiasi cha kushuhudiwa na waungwana na wanaotambua thamani ya maendeleo ya nchi. Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya CCM imefanya na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya kimaendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu, hatua inayowafanya watu wengi kuiunga mkono CCM.Alisema CCM inawakaribisha wanachama wengine kutoka vyama mbalimbali nchini wanaotaka kujiunga na harakati za kuletea Taifa maendeleo zinazofanywa na CCM chini ya Rais Magufuli. Hivi karibuni katika ziara ya Rais Magufuli wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, mbunge huyo alipata nafasi ya kuzungumza na kutoa kero za jimbo lake, lakini baadhi ya watu walianza kumzomea na ndipo alipowanyamazisha kwa kuwaambia wanyamaze kwani kama shida ni upinzani naye anaweza kuwa CCM vilevile. Serikali yabana NGOs
KITAIFA
“HUDUMA tunazotoa ni nzuri na zina hadhi ya kimataifa. Abiria hachukui zaidi ya dakika saba kukaguliwa na abiria anayewasili anachukua dakika tatu kupata huduma za uhamiaji hadi anatoka nje ya jengo.”“Kwa Watanzania wenye pasipoti za kielektroniki, wanatumia sio zaidi ya sekunde 15 kwa sababu wanajihudumia wenyewe kupitia mageti ya kielektroniki (e-gate).” Ndivyo anavyosema Kaimu Meneja wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Barton Komba.“Huduma ya mawasiliano ya simu ndani ya jengo ni nzuri na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambao wamepewa kandarasi ya kuimarisha mawasiliano ndani ya jengo wanaendelea na kazi hiyo, ulinzi na usalama uko vizuri, huduma ya chakula ni nzuri na inatolewa na Mtanzania, kuna duka la vito nalo ni la Mtanzania, huduma ya kubadilisha fedha za kigeni nayo ipo.”Kwa kuwa huduma nzuri kwa mteja ndiyo msingi wa mafanikio ya kibiashara, Komba anasema asilimia 30 ya jengo hilo imetengwa kwa ajili ya maeneo ya biashara, hivyo watoa huduma mbalimbali wanakaribishwa kutoa huduma katika jengo hilo na wanatarajia idadi ya watoa huduma kuongezeka kadri muda unavyokwenda. Mafanikio mengine ambayo Tanzania imeanza kuyapata ni uwezo wa kupokea na kuhudumia ndege kubwa aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 350 hadi 370.Kaimu Meneja huyo wa Terminal lll anasema kuwa, kwa sasa JNIA kinaweza kupokea kwa dharura ndege nyingine kubwa kabisa aina ya Airbus 380 yenye ghorofa moja. Anasema ingawa kwa sasa hakuna miundombinu yote inayotakiwa kuihudumia ndege kama hiyo, kama ikitokea dharura, ndege kama hiyo inaweza kutua na kuhudumiwa vizuri. Anasema abiria ambao wako kwenye sakafu ya pili ya ndege hiyo wanaweza kushuka kwenye ndege kwa kupitia sakafu ya kwanza na kisha kuingia ndani ya jengo la abiria la tatu la kiwanja hicho.Mbali na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa ya aina hiyo, kiwanja hicho pia kina uwezo wa kupokea na kuhudumia kwa ufanisi ndege nyingine zote ukubwa ikiwemo Boeing 787-8 Dreamliner, Airbus A220-300 na nyingine zenye ukubwa huo au chini yake. Haya yote yanafanyika kutokana na jengo hili kuwa na mifumo ya kisasa kabisa barani Afrika.Ubora na uwezo wa jengo hilo la abiria pia umechangia kuongezeka kwa idadi ya ndege za kimataifa zinazohudumia kiwanjani hapo. Komba anabainisha kuwa , jengo la abiria namba 3 la JNIA linahudumia ndege za kimataifa kati ya 13 hadi 15 kila siku tangu lifunguliwe miezi miwili iliyopita, huku uendeshaji wake ukiwa umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ikiwemo muda mfupi zaidi unaotumika kumkagua abiria kabla hajaingia kwenye ndege.Anaongeza kuwa, JNIA inahudumia ndege 21 zinazoruka kimataifa za mashirika mbalimbali na ndege 19 kati ya hizo zimehamishiwa katika jengo hilo la tatu la abiria kutoka jengo namba mbili. Baada ya ndege 19 za kimataifa kuhudumiwa katika jengo hili, anasema kiwango cha abiria wanaowasili na kuondoka wanaohudumiwa katika jengo hilo kwa wakati mmoja wa msongamano ni abiria 1,500. Terminal lll ni kwa ajili ya kuhudumia ndege zinazofanya safari za kimataifa pekee.Anazitaja baadhi ya ndege hizo kuwa ni pamoja na zile za Shirika la Ndege la Emirates, Ethiopia, Afrika Kusini, Zimbabwe, Msumbiji, Kenya, Oman, Mauritius, Uganda, Misri na Uswisi. Komba anafafanua kuwa, ndege za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na za Shirika la Ndege la Precission hazijahamishiwa katika jengo jipya kwa sababu ndege hizi zinafanya safari za ndani na za kimataifa, hivyo zinaendelea kutoa huduma katika jengo la pili la abiria. Katika hili, anasema gharama ya kuhudumia ndege hizo ni kubwa kutokana na kuchanganya safari za ndani na za kimataifa kwa sababu zinahitaji kusogezwa kutoka jengo moja kwenda lingine, jambo linaloyafanya mashirika hayo kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.“Tumekuwa tukipokea mrejesho kutoka kwa wadau wa kiwanja hiki na kutueleza kuridhika na kusifu huduma wanazopewa ambazo wanasema kuwa zina hadhi ya kimataifa. Mpaka sasa tumefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 katika uendeshaji wa Jengo hili tangu lifunguliwe na Rais John Magufuli Agosti Mosi mwaka huu,” anaeleza Komba.Ili kuhakikisha jengo hili linavutia mashirika mengi ya kimataifa ya ndege, Komba anasema kwa sasa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) iko katika maandalizi ya kukitangaza kiwanja hicho kupitia jengo lake jipya ili kuongeza idadi ya ndege za kimataifa, kuongeza abiria na kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi.Anasema kwa sasa JNIA inashika nafasi ya tano barani Afrika kwa idadi ya abiria inaowahudumia, kwa kuhudumia abiria milioni 2.5 kwa mwaka kikitanguliwa na viwanja vingine vikiwemo vya Johannesburg na Oliver Tambo vya Afrika Kusini. Kwa mujibu wa Komba, kwa kuwa Terminal lll imejengwa kwa lengo la kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka, matangazo hayo yatasaidia kuongeza idadi ya abiria.
KITAIFA
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema haijakatazwa mtu kumiliki zaidi ya kadi moja za simu ilimradi ziwe za mitandao tofauti.“Tunatamani kila Mtanzania awe na ‘line’ moja ya simu kwa mtandao mmoja, akitaka nyingine atoe taarifa,” amesema.Nditiye ameyasema hayo bungeni wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye kikao cha Bunge la 11 kinaoendelea jijini Dodoma.Ameongeza kuwa lengo kuu ni kupunguza wingi wa kadi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia vitendo vya uhalifu wa simu ikiwa ni pamoja na wizi akitolea mfano mbinu ya “ile pesa nitumie kwa namba hii.”
KITAIFA
Na JENNIFER ULLEMBO RIADHA ni moja ya michezo inayopendwa duniani kwa asilimia kubwa, kwani mbali na kuwapa watu fedha kwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali, pia umekuwa ukisaidia kuimarisha na kutunza afya. Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) lilianzisha mpango wa kuandaa mashindano katika baadhi ya mikoa kwa kuzingatia kanda mbalimbali, ili kuleta sura ya nchi nzima katika mashindano ya Taifa. Mpango huo ulifanikiwa na ikaweza kupatikana timu ya taifa iliyoweza kuliwakilisha taifa katika Mbio za Nyika zilizofanyika Kampala, Uganda Machi 26, mwaka huu. Licha ya Tanzania kutofanya vizuri katika mashindano hayo, bado wanariadha na viongozi wa RT waliendelea kujipa moyo wa kuhakikisha mchezo huo unasonga mbele na kurudisha hadhi yake ya miaka ya nyuma. Lakini hivi sasa upepo umeonesha kubadilika kwa chama hicho kuandamwa na madeni na kujikuta kikishindwa kufanikisha baadhi ya mipango ya kuendeleza timu ya taifa. Michezo kama riadha na mingineyo midogo midogo  inashindwa kupewa uzito mkubwa kama ilivyo kwa soka, jambo ambalo kwa upande mmoja au mwingine vyama vya michezo vinajikuta vikishindwa kupiga hatua. Inaonyesha wazi nguvu za ziada zinahitajika kuiwezesha RT kufanikisha malengo iliyojiwekea kwa mwaka huu na miaka ijayo. Umoja na nguvu baina ya viongozi wa chama hicho pekee, haiwezi kuwa njia ya kuusaidia mchezo wa riadha Tanzania kuinuka. Bado wadau na wapenzi wa michezo nchini wameendelea kuweka uzito kusaidia mchezo huu kusonga mbele. Nchi yetu imebarikiwa kuwa na vipaji vya wanariadha vijana, lakini kama watakosa misingi na msimamo imara wa kuendeleza kile walichonacho, daima tutaendelea kuwa wasindikizaji katika mashindano kwa shuhudia mataifa ya wenzetu yakibeba medali na kuweka rekodi bora zaidi. Hivi sasa tunajivunia mwanariadha Felix Simbu, ila ukweli tunatakiwa kutengeneza wanariadha wengine wengi watakaoweza kupokea kijiti cha Simbu, ambaye kwa siku za karibuni ameonekana kuliwakilisha vema taifa ndani na nje ya nchi. Wadau wa michezo ungeni mkono jitihada hizi za RT kwa ajili ya kuitangaza nchi kupita mchezo huu, ambao miaka ya nyuma ulifanya vema kimataifa kupitia wanariadha Filbert Bayi na Selemani Nyambui.  
AFYA
Na ANDREW MSECHU -DAR ES SALAAM IKIWA imebaki miezi michache kuelekea Uchaguzi Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dk Ali Mohamed Shein, ametoa onyo kwa watu wanaotaka kuvuruga amani na katu serikali  hatomvulia mtu yeyote  kwa kisingizio cha kudai haki. Kutokana na hali hiyo amesema kwa sasa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), inaendelea kutekeleza wajibu wake wa maandalizi ya uchaguzi huo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha pale itakapotangazwa rasmi. Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanazibar, Dk Shein alisema tume hiyo inaendelea na maandalizi hayo ya uchaguzi mkuu katika tarehe itakayotangazwa hapo baadaye, hivyo alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi waende kujiandikisha ili siku itakapofika waweze kuchagua viongozi watakaowataka. Hata hivyo, Dk Shein ambaye hii ni mara yake ya mwisho kushiriki sherehe hizo za Mapinduzi akiwa kiongozi wa nchi, aliwaonya wale wote wanaotaka kuvuruga amani na usalama wa Zanzibar akiwaeleza kuwa Serikali inaendelea vyema na jukumu lake la ulinzi wa watu na mali zao. “Niwakumbushe tu kuwa tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa kisheria na kikatiba, kwa kulinda amani na usalama wa watu na mali zao na hatutachelea kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayejaribu kuhatarisha amani ya nchi yetu,” alisema. Alisema ni wazi kuwa hakuna mbadala wa amani katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja jamii na taifa kwa ujumla, hivyo uvunjaji wa amani huanza kwa vitendo visivyozingatia sheria za nchi, kwa hiyo wananchi wajiepushe na vitendo hivyo. Alitoa wito kwa kila mwananchi kuzingatia suala la amani na usalama kuwa ni suala la lazima na la msingi. Dk Shein alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuendelea kutunza Muungano kwa dhamira ile ile ya waasisi wa Muungano huo, ambao ni hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume, pamoja na viongozi wa Serikali za awamu zilizotangulia ili nchi iendelee kupiga hatua kubwa zaidi na kuwa ya amani na utulivu. Dk Shein alisema miongoni mwa mambo ya kujivunia katika Serikali yake ni kupitishwa kwa mabadiliko ya Sheria ya Utumishi wa Umma mwaka 2011 na marekebisho ya mishahara yaliyofanyika kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2017 kwa ajili ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma. MISHAHARA Alisema ana matumaini makubwa kuwa kutokana na hali nzuri ya makusanyo ataweza hata kuongeza mishahara ya wafanyakazi kama sehemu ya jitihada ya kuimarisha masilahi ya watumishi wa umma. Alisema ongezeko la mishahara ambalo limefanyika tangu kupitishwa kwa mabadiliko hayo limeongeza matumizi ya Serikali kwa zaidi ya mara 5.1 kutokana na kuongezea mishahara na kuongezeka pia kwa pensheni kwa watumishi wa umma. Alisema kutokana na maboresho hayo ya maslahi matumizi ya mishahara yalitoka Sh bilioni 83.1 mwaka 2011 hadi kufikia Sh bilioni 417.9 mwaka 2019 sawa na ongezeko la mara 5.1, hata hivyo kasi ya ukuaji wa uchumi imewezesha kulipa maslahi yote kwa kipindi chote hicho. Alisema mafanikio yaliyopatikana katika sekta zote za maendeleo ndani ya miaka 56 ya mapinduzi ni kutokana na kuednelea kuwepo kwa sababu za msingi za kufanyika mapinduzi hayo ya kuondoa ubaguzi na dhuluma na kujenga amani na umoja. KAULI YA JUZI Juzi wakati akipokea matembezi ya ‘amsha amsha’ yaliyowashirikisha makanda na wapiganaji wa vikosi vya ulinzi na usalama katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Unguja, Dk. Shein,  alisema kila mwananchi ana jukumu la kudumisha amani iliopo nchini pamoja na kulinda na kuyaenzi kikamilifu Mapinduzi  ya Zanzibar ya mwaka 1964. Alisema hatua ya wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama ya kuanzisha  aina hiyo ya matembezi, inafaa kupongezwa kwani inafanikisha dhamira ya kuwajengea ari wapinaji pamoja na kuwajengea matumaini wananchi ya kuendelea kuiamini Serikali yao. Alisema dhana ya kudumisha usalama wa nchi inatokana na Sera ya chama cha Afro Shirazi Party (ASP) iliyowekwa baada ya Mapinduzi ya 1964, na kusema dhana hiyo ni endelevu na haitokuwa na mbadala. Dk. Shein alisema baada ya Mapinduzi ya 1964, Zanzibar ilianzisha Jeshi la Ukombozi (JLU) na baada ya Muungano wa Tanzania, Jeshi la wananchi wa Tanzania liliundwa, lengo kuu likiwa ni kudumisha ulinzi na usalama  ndani na nje ya mipaka yake. Rais Dk. Shein alikemea tabia ya baadhi ya watu ya kujifanya wababe na kuidharau Serikali  na kusema kila jambo lina mipaka yake, akibainisha usawa uliopo kwa kila mwananchi mbele ya sheria. Alisema Serikali zote mbili za SMT na SMZ zinaendeshwa kwa misingi ya sheria, chini ya usimamizi wa vyombo vilivyowekwa ambavyo hufanyakazi kwa misingi ya katiba na sheria. Aliwataka wale wote waliojiandaa kufanya vituko kwa kisingizo cha uchaguzi mkuu mwaka huu kuacha mara moja na kubainisha kuwa Zanzibar ni nchi ya Mapinduzi iliopinduliwa ili wananchi waweze kuishi kwa amani na usalama. Alisema siasa isiwe sababu ya watu kufanya fujo na kusema uchaguzi unaendeshwa kwa misingi ya sheria, akibainisha azma ya Serikali ya kuwashughulikiya wale wote watakaojihusisha na uvunjifu wa amani. Alieleza kuwa vyombo vya ulinzi viko makini na vinajuwa wajibu wao na kufafanua kuwa hakutakuwepo na mtu atakaeonewa katika ushughulikiaji wa jambo hilo. CHANGAMOTO Rais huyo wa Awamu ya Saba wa Zanzibar, alisema katika kipindi chake cha mika tisa madarakani, miongoni mwa changamoto katika sekta ya afya ni suala la hospitali nyingi kubaini kasi ya ongezeko la maradhi yasiyo ya kuambukiza kama moyo, saratani na kisukari na kwamba anaamaini wataalamu wa afya watafanya tafiti zao kwa bidii ili serikali iendelee kuchukua hatua za haraka na salama kupunguza kasi ya ongezeko la maradhi hayo. Hata hivyo, Dk Shein aliamua kukatisha kusoma hotuba yake yote kwa kuwahurumia watu waliokwua uwanjani kutokana na jua kali na kwaomba wananchi waridhie aeleze machache na kwa kuwa vitabu vimechapishwa kuhusu hotuba hiyo watasoma kwa wakati wao. “Saa zimekwenda, jua limekuwa kali sana ninafahamu mtihani wanaopata watoto na vijana wetu na watu wengine katika uwanja huu, ningetamani nisome hotuba yangu yote lakini lazima tuwahurumie wale wanaotaabika na jua, jua jingi lina madhara sana,” alisema kihs akuhitimisha hotuba yame muda mchache baadaye. Alisema katika miaka tisa ya Serikali ya Awamu ya Saba ya Zanzinbar katika miaka tisa cha iliyopita ya uongoziw ake, Dk Shein alisema imefanya juhudi za maendeleo katika maeneo mbalimbali. Alisema Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imeweza kuvutia wawekezaji kwenye miradi 304 mtaji wa dola bilioni 3.74 imetekelezwa na kuzalisha ajira 16,866 katika miaka tisa iliyopita. Alisema sekta ya elimu imeimarishwa na kutoa elimu bure bila ubaguzi kama uilivyitangazwa na Karume, serikali imeongeza skuli, taasisi za elimu na wanafunzi katika ngazi zote kuanza skuli za maandalizi hadi vyuo vikuu, kadhalika sekta ya afya, maji na huduma nyingine za jamii. VIONGOZI WALIOHUDHURIA Katika sherehe hizo, viongozi mbalimbali wakiwamo wastaafu walihudhuria sherehe hizo akiwamo, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli wote walihudhuria sherehe hizo. Pamoja nao, alikuwepo pia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume na waliokuwa viongozi katika Serikali yake, akiwemo Shamsi Vuai Nahodha, ambaye alikuwa Waziri Kiongozi. Kwa mara ya kwanza tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Rais Dk. Shein, mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye nao walihudhuria sherehe hizo. MAONYESSHO Katika sherehe hizo, maonyesho ya makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yalitia fora, kutokana na makomandoo hao kuonyesha ujuzi ambao haikuwahi kuonyeshwa awali. Makomandoo hao waliduwaza washiriki katika sherehe hizo kwa kuonyesha mbinu mbalimbali ikiwemo kuvunja vigae kifuani, kuvunja vigae chini ya mkono kwa kutumia nyumndo, kuvunja vigae mkononi kwa kutumia nyumdo na shoka, mateka kuvutwa na gari na kisha kuhitimisha onyesho hilo. Awali, makomandoo hao walifanya onyesho la kutoa heshima kwa kupita wakiwa wamebebba mabegi yenye uzito wa kilogramu 30 za vifaa vuinavyowasaidia wakiwa kazini, kutoka kwa kikundi maalumu cha JWTZ. Katika maonyesho ya vikundi mbalimbali katika kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar, JWTZ pia ilionyesha namna ya kulinda viongozi wao na askari anavyoweza kumiliki silaha. Askari polisi waliingia na onyesho la askari wa zamani, askari tarabushi, kuonyesha kwata maalumu iliyochezwa kabla ya mapinduzi ya Zanzibara mwaka 1964. Kwata hiyo iliitwa tarabushi kutokana na na kofia waliyokuwa wakivaa, ambayo iliitwa ‘taabushi’ kwa kiarabu lakini wazanzibar wakazi walishindwa kuitamka hivyo na kuiita tarabushi.
KITAIFA
WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la Fursa za Biashara lililofanywa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika mikoa yao, limesaidia kuwajengea wananchi na wawekezaji uelewa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo.Katika Mkoa wa Geita, jukwaa hilo la fursa za biashara na uwekezaji lilifanyika mwezi Agosti 2018 wakati mkoani Tabora lilifanyika mwezi Novemba 2018.Wakizungumza na gazeti hili, wakuu wa mikoa ya Tabora, Aggrey Mwanr na wa Geita, Robert Gabriel, walisema kuwa moja ya matokeo makubwa ya jukwaa hilo ni kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu fursa za biashara zilizomo kwenye mikoa yao pamoja na uelewa kwa wawekezaji kuhusu fursa hizo.Mwanri amesema kupitia jukwaa hilo la fursa za biashara na uwekezaji, kuna kampuni moja ya Kichina imeonesha nia ya kutaka kufanya uwekezaji wa pamoja na mwananchi mmoja mzawa wa mkoa huo kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti.Amesema kiwanda hicho, kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi Aprili 2020 na kinachoendelea kwa sasa ni taratibu za kupata hati miliki.Amesema kuwa asilimia 50 ya ardhi ambayo ilikuwa hailimwi, hivi sasa imeanza kutumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali.Mkuu wa Mkoa huyo amesema baada ya jukwaa hilo, wananchi wameelewa vizuri kuhusu suala ya uwekezaji na ujasiriamali ; na ndiyo maana Tabora ilishika nafasi ya pili kitaifa katika ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu ‘machinga’.“Jukwaa limekuwa na manufaa makubwa kwa sababu limeongeza uelewa wa wananchi kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizomo ndani ya mkoa huu, nitoe wito kwa wananchi wa Tabora warudi nyumbani kufungua biashara, viwanda na kujenga shule za kisasa, watambue kwamba fursa hazitolewi bali zinachukuliwa, hivyo waje wawekeze nyumbani,” alieleza Mwanri.Alisema kutokana na jukwaa hilo, wameamua kutenga maeneo kadhaa kwa ajili ya biashara au uwekezaji fulani.Alitaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na wilaya ya Kaliua, ambako limetengwa eneo kwa ajili ya ranchi ya mifugo, viwanda vidogo vya mazao ya misitu na kiwanda cha mafuta ya karanga na alizeti.Kwa upande wa Wilaya ya Sikonge, amesema kuna eneo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha kuchakata asili na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), iko tayari kutoa mikopo kupitia kitengo chao cha uwajibikaji wa kijamii (corporate social responsibility) kwa wanaotaka kuwekeza kwenye sekta hiyo.Kwa mujibu wa Mwanri, kuna eneo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha nyama na machinjio ya kisasa Nzega, kwa kuwa mkoa huo una ng’ombe zaidi ya milioni mbili.Alisema kupitia kiwanda hicho, wataweza kuuza ndani na nje ya nchi nyama, ngozi, pembe na samadi.“Wilaya ya Urambo tumetenga eneo kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata tumbaku, Uyui kiwanda cha chakula cha mifugo, Igunga na Nzega tumetenga maeneo kwa ajili ya kuanzisha ranchi ndogo kwa ajili ya kuboresha mifugo,”alisema Mwanri.Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel, amesema Jukwaa la Fursa za Biashara limesaidia kujenga sifa nzuri ya mkoa huo kwenye suala la biashara na uwekezaji, ambapo awali ulisifika kwa matukio mabaya ya mauaji na ushirikina.Gabriel alisema uelewa wa wananchi kuhusu biashara ya madini, umeongezeka na ndiyo maana mkoa umeamua kufungua masoko mengi ya madini likiwemo Soko Kuu la Dhahabu Geita Mjini, Nyarugusu, Nyakagwe na Katoro na masoko mengine matano yalipangwa
UCHUMI
Na ASHA  BANI-DAR ES SALAAM NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema kuanzishwa kwa mradi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kutasaidia kukuza uchumi wa nchi. Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, amesema mradi huo ambao ulianzishwa na Kampuni ya Raddy Fibre Solution (LTD) unatarajiwa kutandaza mkongo wa Taifa katika wilaya 185 ikiwemo Mkuranga Akizungumza na ujumbe wa kampuni hiyo mwishoni mwa wiki wilayani Mkuranga, alisema kukamilika kwa mfumo huo kutaisadia wafanyabiashara wenye viwanda kujua hali ya masoko ya ndani na nje haraka. “Hivi sasa serikali ipo katika harakati za kukuza uchumi kupitia viwanda na kama mnavyofahamu Mkuranga ni eneo maalumu la kimkakati la viwanda ambalo linatakiwa kuwa na mawasiliano ya uhakika. “Ufungwaji wa mfumo huu Wilaya ya Mkuranga utaiunganisha wilaya yetu, wamiliki wa viwanda pamoja na wana Mkuranga,” alisema Ulega Hivi karibuni  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Mhandisi Mshamu Munde akiwa katika mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT) alisema hatua za awali za mpango huo zitakuwa na manufaa kiuchumi. Alisema mfumo huo ambao unafahamika kama e-LGA unafanana na mfumo wa Serikali Mtandao (e-Gorvement) hivyo utasaidia kufanya kazi za mawasiliano kwa urahisi zaidi. “Imefika wakati sasa kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutumia mfumo huo kwa kuwa utakuwa na manufaa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hasa kwa ngazi za halmashauri. “Pia utakuwa na manufaa zaidi hasa kusaidia kurahisisha mpango wa malipo, kuingiza taarifa za afya za wilaya na hata shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na mifugo na mifumo mingineyo “Utasaidia kuunganisha masoko kwa wafanyabiashara, wakulima wa nyanya Iringa kuweza kufanya biashara na wakulima wa mpunga Mbeya na Korosho Mkuranga kwa kuwasiliana kupitia mkongo wa mawasiliano.
KITAIFA
Na Esther Mnyika, Dar es Salaam MBUNGE wa Ubungo, Saeed Kubenea (Chadema), amesema chama hicho hakitamvumilia kiongozi yeyote anayetaka kurudisha nyuma harakati za kuleta maendeleo  na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kutoa taarifa za kiongozi anayekwenda kinyume cha taratibu ili aweze kuchukuliwa hatua. Akizungumza na wananchi wa Kimara Mavurunza, Kubenea alisema chama hicho kimejipanga kuleta maendeleo katika jimbo hilo, hivyo kuna haja ya kuwa na viongozi waadilifu ili kuweza kufikia malengo. “Ndani ya jimbo hatutaki watu wanaotukwamisha, hata akiwa chama gani tutamchukulia hatua, hapa Mavurunza kama kuna matatizo na viongozi wenu naomba mtoe taarifa tuitishe kikao ili tuwachukulie hatua zinazostahili,” alisema Kubenea. Alisema kushirikiana na viongozi wa manispaa wamejipanga kupambana na wizi pamoja na ubadhirifu atakaofanya kiongozi ama mtumishi wa manispaa hiyo. Alisema wananchi wanapaswa kufuatilia mchanganuo wa fedha, yakiwamo mapato na matumizi kupitia viongozi wao wa serikali za mitaa pamoja na kuwahoji panapokuwa na upungufu ama udanganyifu. “Sisi tumekuja kuwafanyia kazi, tunataka kuleta maendeleo ambayo hayajaletwa ndani ya miaka hamsini, hatutaki ghiliba, tutapambana na wezi hata kama ni wa chama chetu tutamwajibisha, hatutamvumilia mtu asiye na huruma na wananchi,” alisema Kubenea. Kwa upande wa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, alisema kitendo cha Manispaa ya Ubungo kujitegemea kitasaidia kuleta maendeleo haraka, kwakuwa fedha zinazopatikana kupitia makusanyo ya kodi zitatumika kutengeneza miundombinu ya eneo hilo tofauti na ilivyokuwa awali. “Zamani tulikuwa tunakusanya kodi za huku  unaandikiwa kikaratasi unaambiwa upeleke fedha ukajenge barabara za Mbezi au Masaki kwa mabwanyenye na kuziacha barabara za huku zikiwa na makorongo, sasa hivi fedha zetu zitatumika kutengeneza miundombinu yetu yenyewe,” alisema Jacob. Alisema manispaa hiyo yenye kata 14, inakusanya Sh bilioni 106 kwa mwaka ambazo zikitumika vizuri zinatosha kuleta maenedeleo katika eneo hilo.
KITAIFA
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizikia Kahama Machi 28.“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri Nape, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.Pia Msama alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ni Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro ya Mwanza na Kwaya ya Wakorintho wa pili kutoka Njombe.Viingilio katika tamasha hilo ni Sh 5,000 kwa wakubwa na kwa watoto Sh 2,000. Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vema.
MICHEZO
BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) katika kujiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwakani, limewataka Waislamu nchini kama sehemu ya Watanzania, kujitokeza kwa wingi katika hatua zote za mchakato utakapoanza ikiwamo kushiriki kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura, kugombea na kuchagua.Aidha, Bakwata limewataka Waislamu kote nchini, kujitokeza kwa wingi kuomba uongozi katika baraza hilo pindi mchakato wa uchaguzi wake, utakapoanza Februari mwakani.Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma alitoa mwito huo jana, alipokuwa akihutubia mamia ya Waislamu waliojitokeza katika dua ya maadhimisho ya Siku ya Bakwata ya kufikisha miaka 51 yaliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.Mruma alisema, “Bakwata inapenda kutumia fursa hii kuwafahamisha Waislamu wote nchini kwamba kipindi cha kufanyika Uchaguzi Mkuu wa taasisi yetu umewadia. Uchaguzi unatarajiwa kuanza mapema Februari 2020 kuanzia ngazi za misikiti, kata na hatimaye ngazi zinazofuata.”Aliwataka Waislamu kote nchini mara mchakato wa Uchaguzi wa Bakwata utakapotangazwa kuanza, wajitokeze kuchukua fomu kwa nafasi watakazzona zinafaa kwao kugombea.“Aidha, baraza linawakumbusha Waislamu wote nchini kwamba, mwaka 2020 ni Uchaguzi Mkuu wa viongozi wetu wa kiserikali kuanzia madiwani, wabunge na Rais. Baraza linawahimiza Waislamu kama sehemu ya Watanzania wajitokeze kwa wiki katika hatua zote za mchakato,” alisema Mruma.Katika sherehe hizo pia, Bakwata ilifanya dua kwa ajili ya kuombea amani nchi na Rais John Magufuli. Aidha, walimuombea hekima, busara na afya njema kiongozi wa kiimani na kiroho katika dini ya Kiislamu nchini, Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Bin Ally ili aendelee kuwatumikia vyema Waislamu nchini.Bakwata ilianzishwa mwaka 1968 kikiwa ni chombo cha kudumu cha kuratibu, kusimamia na kuongoza shughuli zote za Waislamu nchini Tanzania.Tangu kuanzishwa kwake imeongozwa na mamufti watatu, ambao ni Shehe Hemed Bin Jumaa Bin Hemed kuanzia mwaka 1977 hadi 2002 alipotangulia mbele za haki, Shehe Issa Bin Shaaban Bin Simba kuanzia mwaka 2002 hadi 2015 alipofariki dunia na Shehe Mkuu wa sasa aliyeshika nafasi hiyo kuanzia mwaka 2015
KITAIFA
Hatua hiyo ya kutenga ekari 160 katika eneo la Jitegemee, upande wa barabara ya Mandela inayolenga kuongeza ufanisi wa bandari hiyo kubwa hapa nchini na kuifanya kuwa shindani.Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alitangaza hatua hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya ujumbe wa maofisa wa serikali na wafanyabiashara kutoka jimbo la Katanga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Ujumbe huo uliokuwa na lengo la kuimarisha biashara kati ya nchi hizo uliongozwa na Naibu Gavana wa jimbo hilo, Guibert Tshibal na waziri wa Uchukuzi wa jimbo hilo, Laurent Kahozi Sumba.Waziri Mwakyembe aliwaambia waandishi wa habari kuwa sehemu ya ardhi hiyo itawekwa kwa ajili ya jumuiya ya wafanyabiashara wa Kongo DRC.“Tunafanya hivi kwa nia ya kuimarisha bandari yetu na pia biashara na majirani zetu,” alisema.Mizigo ya DRC imekuwa ikiongezeka kwa asilimia takribani 24 kwa mwaka tangu mwaka 2004 ikiongezeka kutoka tani 155,611 hadi tani 1,117,249 mwaka 2013. Nchi ya DRC ni ya pili kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam.Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mizigo ya DRC inachukua asilimia 25 ya mizigo yote ya nchi jirani inayopita katika bandari hiyo. Pamoja na mambo mengine, ujumbe huo ukiwa nchini ulitembelea eneo hilo pamoja na bandari ya Dar es Salaam.Waziri Mwakyembe alisema kuwa kamati ya ufundi iliyoundwa na wajumbe wa nchi hizo imekubaliana kushughulikia kero zote zinazokwamisha biashara kati ya nchi hizo. Kwa upande wake, Kahozi Sumba alisifu juhudi za Tanzania kwa hatua inazochukua kuimarisha bandari ya Dar es Salaam.“Tutazidi maradufu kutumia bandari hii,” alisema. Alisema kuwa bandari hiyo ni njia kuu ya kupitishia mizigo kwa nchi yake hivyo kuimarishwa kwake kutaleta nafuu ya maisha katika jimbo hilo na nchi ya DRC kwa ujumla.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande alisema kamati hiyo ya ufundi imekubaliana pia kuwa na orodha ya kampuni za wakala wa kupakia na kupakua mizigo katika nchi zote ili kuepuka wizi na matatizo mengine.Pia ilikubaliwa ianzishwe bandari kavu katika eneo la mpaka wa DRC na Zambia la Kasumbalesa ili kupunguza na kuondokana na tatizo sugu la msongamano wa malori ya mizigo. Kwa upande wake, Tshibal alisifu juhudi zinazofanywa na Dk Mwakyembe na serikali nzima za kuimarisha sekta ya usafiri.“Dk Mwakyembe ni hazina kwa Tanzania...ni mtu wa vitendo,” alisema Naibu Gavana huyo. Ziara hiyo imekuja kufuatia ile iliyofanywa na wenzao wa Tanzania katika jimbo hilo mapema mwezi Mei mwaka huu ambapo TPA ilifungua ofisi yake ndogo ya mawasiliano katika mji wa Lubumbashi.
UCHUMI
Rais wa Sudan, Omar Al- Bashir anadaiwa kuwa tayari kuandaa mazungumzo ya amani kati ya mahasimu wawili wakuu wa Sudan Kusini, Rais Salva kiir na Riek Machar. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Sudan ilitangaza kwamba ilitangaza pendekezo la Rais Bashir liliwasilishwa kwa Rais Kiir na ujumbe wa Sudan uliotembelea Juba Jumanne wiki hii ikiwa ni siku chache baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio linalozipatia pande zinazogombana Sudan Kusini mwezi mmoja kufikia makubaliano ya amani au kukabiliwa na vikwazo vikali zaidi. ​Ujumbe wa Sudan uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Sudan, Al- Dierdiry Al-dhikheri. Rais Salva Kiir anaripotiwa kuthibitisha serikali yake iko tayari kushiriki kwenye mazungumzo hayo ingawa siku bado haijatajwa.  
KIMATAIFA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ukosefu wa uadilifu ni eneo ambalo lilitia doa utendaji wa sekta binafsi hususani pale ambapo ilishirikiana na Serikali.Ameyasema hayo wakati anafungua Mkutano Mkuu wa 18 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa niaba ya Rais John Magufuli.Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema, uadilifu ni changamoto kubwa inayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali na TPSF.Waziri Mkuu ameitaka TPSF ijifunze kwa wenzao walioendelea kwa kutokuwa na vitendo vya rushwa, kwa kutoa adhabu kwa wanaoenda kinyume na misingi ya uadilifu walijiwekea.Amesema kufanya hivyo watakuwa wamejiongezea nguvu yao kama taasisi lakini pia kupeleka ujumbe kwa wanachama wao kuwa wanathamini haki na kuchukia rushwa. Aliongeza kuwa shughuli za sekta binafsi zimeendelea kuongoza katika kuchangia pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.Amesema, kwa mujibu wa takwimu sekta ya utalii inachangia asilimia tisa, huduma asilimia 35, kilimo asilimia 26.6, madini asilimia 3.3 na sekta ya viwanda inachangia takribani asilimia 10.Waziri Mkuu alisema serikali kwa upande wake, itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kuboresha miundombinu, kutoa vivutio kwenye kodi, kanuni na sheria ili kukuza sekta binafsi.Hivyo, Waziri Mkuu alisema sekta binafsi nchini nayo haina budi kutumia vema fursa hiyo ya uwepo wa mazingira wezeshi na rafiki kwa kuwekeza kwenye uchumi wa nchi.Mwenyekiti wa TPSF aliyemaliza muda wake, Reginald Mengi aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa hatua mbalimbali inayozichukua ikiwemo ya kupambana na rushwa na kuboresha mazingira mazuri ya kufanya biashara.Mengi amesema, takwimu za serikali na Benki ya Dunia zinaonesha uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2018 unatarajiwa kukua kwa kwa asilimia 6.9 na pato la mtu mmoja mmoja kuwa dola za kimarekani 1,000 kwa mwaka.Mbali ya kuishukuru serikali aliipongeza pia kwa maamuzi iliyochukua ya kutoa msamaha wa riba na adhabu za malimbikizo ya kodi kwa asilimia 100, alisema na kuongeza kuwa hiyo itahamasisha ulipaji kodi na pia kuondoa mizigo ya kodi na tozo kwa wafanyabiashara.Mwakalishi wa Wadau wa Maendeleo ambaye pia ni Mkurugenzi wa USAID hapa Tanzania, Andrew Karas alipongeza kuwepo kwa chombo kinachosimamia sekta binafsi kwani kinawawakilisha watu moja kwa moja.
KITAIFA
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) linatekeleza mchakato wa marekebisho ya katiba na limetoa siku 30 kwa wadau na wanatasnia ya filamu nchini kutoa maoni yao kwa rasimu ili kuwa na katiba yenye tija kwa tasnia hiyo. Rasimu ya TAFF iliundwa na kupelekwa kwa wadau na baada ya kikao cha utendaji kazi kati ya Bodi ya Filamu Tanzania, Basata na TAFF, ikaazimiwa upatikanaji wa katiba. Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba, alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa, ukusanyaji maoni utajumuisha wadau mbalimbali na wanatasnia ili kuboresha sekta ya filamu nchini.“Nitoe mwezi mmoja tu tangu siku ya leo (jana). Rasimu itapatikana kupitia njia mbalimbali iki- wamo kwenye ukurasa maalum wa Facebook, kusambazwa kwa njia mbalimbali za mitandao,” alisema Mwakifamba. Alisema baada ya kupokea maoni, kupitia kikao cha bodi, TAFF itaitisha mkutano mkuu wa wanachama wake kwa ajili ya ajenda kuu moja kisha kuipitisha ama kuikataa rasimu ya katiba hiyo pendekezwa. Alisema TAFF inawaomba wote wenye nia njema wasisite kutoa mawazo yao ili kuujenga umoja huo wa wenye tasnia ya filamu Tanzania ili kuifanya kuwa yenye mchango katika sa- fari ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati kufikia mwaka 2025. Mbali na wadau kutakiwa kutoa maoni ya rasimu ya katiba, alisema TAFF inajivunia kuipi- gania Sera ya Filamu Tanzania tangu mwaka 2014 kwa kiasi na serikali imeshatoa ahadi kwamba kabla mwaka huu haujaisha ita- kuwa tayari imeshapatikana. Alisema pia katika sekta ya sanaa bunifu, shirikisho hilo linaendelea kufanya utafiti kuhusu sera ya miliki bunifu (IP) ambayo inalenga kuwa na maboresho makubwa katika tasnia ya filamu. Alisema shirikisho hilo lilianzishwa na wadau wa tasnia ya filamu Tanzania, kisha kupewa baraka za utendaji kazi kwa usajili namba BST 4536 wa mwaka 2010 wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) linalofanya kazi chini ya sheria ya serikali ya uendeshaji wa Tasnia ya sanaa nchini namba 4 ya mwaka 1984.
MICHEZO
OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa mashitaka mawili likiwamo la kusafi risha dawa za kulevya aina ya heroin.Mbali na Mwamgabe, mshitakiwa mwingine ni Abdulrahman Msimu (54) ambaye ni dereva na mkazi wa Yombo jijini Dar es Salaam, waliofikishwa mahakamani jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando.Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali Aldolf Lema alidai Agosti 25, mwaka jana eneo la Posta jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 124.55.Katika mashitaka ya pili, Wakili Lema alidai Agosti 25, 2018 katika eneo la Posta washitakiwa wote kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin yenye uzito wa gramu 1.55.Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa wote walikana kutenda makosa yao na upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.Hakimu Mmbando aliwataka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja kutoka ofisi za umma watakaosaini bondi ya Sh milioni tano kila mmoja.Hata hivyo, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16, mwaka huu itakapokuja tena kwa ajili ya kutajwa.
KITAIFA
Na John Dande -Dar es Salaam  WAKAZI zaidi ya 500,000 wanatarajia kulipwa fidia kupisha mradi wa ujenzi wa Mto Msimbazi ili kuepusha madhara yanayotokea wakati wa mvua. Akizungumza mjini hapa jana wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua madhara yanayotokea kwa wanaoishi pembezoni mwa mto huo pindi mvua zinaponyesha, Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CCM), alisema endapo mradi huo utafanikiwa utakuwa ni suluhisho la kudumu kwa wakazi hao. “Wizara ya Tamisemi tayari wameshatafuta suluhisho la kudumu ikiwa ni kuomba mkopo wenye masharti nafuu kwa Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya kulipa fidia,” alisema Mtulia. Alisema tayari WB imekubali na kinachosubiriwa ni Wizara ya Fedha na Mipango kuidhinisha.  “Benki ya Dunia wamekubali kutoa fedha kiasi cha dola milioni 100 na kinachosubiriwa ni Wizara ya Fedha kuidhinisha,” alisema Mtulia. Pia alisema mradi huo wa kudumu ukifanikiwa katika bonde hilo kutakuwa ni sehemu nzuri ya kupumzikia. Naye mkazi wa Kigogo, Ramadhani Yahaya, alisema mvua zimekuwa zikileta madhara makubwa ikiwamo kukosa sehemu ya kuishi. “Mvua zimekuwa zikituathiri, mwaka 2011 wakati wa mvua nyumba saba ziliondoka na maji na kwa sasa zinaponyesha tunalazimika kuhama makazi,” alisema Yahaya.
KITAIFA
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewataka viongozi na wawakilishi vya vyama vya siasa, kuhakikisha wanatoa maoni yenye tija ili kutengeneza kanuni zilizo bora, zitakazosimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.Aidha, Jafo amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika muda wote kati ya Novemba au Desemba, mwaka huu. Jafo alisema hayo wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, unajadili rasimu ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa.Alisema Tanzania inaongozwa kwa utaratibu wa demokrasia, hivyo serikali iliona ulazima wa kutengeneza jukwaa la kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya siasa ili kuwa na kanuni bora zitakazoendesha uchaguzi kwa amani na utulivu. Alisema kutokana na umuhimu wa vyama vya siasa katika uundwaji wa kanuni za uchaguzi, ofisi yake ilipeleka rasimu hiyo mapema kwa wadau ili kuweza kupata muda wa kupitia na kuja na maoni yaliyo bora.Jafo alisema kanuni hizo zina maeneo matatu ambayo ni Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa za Mwaka 2019. Alisema pia kuna Rasimu ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa, na wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka ya Miji za Mwaka 2019 na Rasimu ya Kanuni ya Uchaguzi wa Mwenyeikiti wa wa Kitongozi katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka 2019. Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda alisema watahakikisha wanatengeneza kanuni zitakazojenga taswira nzuri ya nchi kitaifa na kimataifa. Aliomba katika kikao hicho, Msajili wa Vyama vya Siasa atoe uwianishaji wa kanuni hizo na sheria mpya ya vyama vya siasa ili isijeleta msuguano wakati wa uchaguzi huo. Baadhi ya vyama vilivyotuma wawakilishi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Union for Multiparty Democracy (UMD), ACTWazalendo, NCCR-Mageuzi, National League For Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party(UPDP), National Reconstruction Alliance (NRA) na Tanzania Democratic Alliance (TADEA). Vyama vingine ni Tanzania Labour Party (TLP), United Democratic Party (UDP), Demokrasia Makini (MAKINI), Democratic Party (DP), Sauti ya Umma (SAU), Tanzania Farmers Party (AFP), Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
KITAIFA
Na Eliza Hombo, Dodoma MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema   Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuwa ikiwatesa na kuwasumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya. Lema alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akiuliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. “Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunafahamu jitihada za serikali ya awamu hii ya kupigania sera ya viwanda ambalo ni jambo jema. “Kila mwenye akili timamu analipongeza ili suala la viwanda liwe na ukweli ni lazima wawekezaji na wafanyabiashara wawe na mazingira bora. “TRA wamekuwa wakitesa na kusumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya hasa katika  mkoa ninakotoka, TRA wanatumia polisi, Takukuru na usalama wa taifa kuwatishia katika masuala ya kodi. “Ili waweze kufanya biashara zao kwa uhakika nini kauli ya serikali juu ya mfumo wa TRA?”alihoji Lema. Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema ni kweli kipo chombo kinachowajibika kukusanya kodi kutoka kwa walipa kodi wakiwamo wafanyabishara. “Ni kweli wanatambau ulipaji kodi ni wadaiwa sugu, TRA kupitia chombo chake Task Force makao makuu, ilikuwa na mkakati wa kuwapitia wadaiwa sugu. polisi, Takukuru walienda kule kuona hakuna utoaji rushwa. “Na katika msafara huo kama Arusha, polisi walikuwa wanatumia silaha na utaratibu kama fedha zinaweza kulipwa papo kwa papo na nimshukuru RC wa Arusha kwa kuwaita wafanyabishara na kuwaeleza wale polisi walikuwapo kwa ajili ya kulinda tu na alirudisha amani. “TRA inao utaratibu, wale ambao wanadhani haiwatendei haki kusikiliza kero watumie madawati hayo kupeleka malalamiko hayo. “Serikali inawaheshimu wafanyabishara na inatambua umuhimu wao wa kulipa kodi na kila mmoja  atambue wajibu wetu na waendelee kutoa ushirikiano na haiwapelekei hofu,”alisema Majaliwa. Katika swali la nyongeza  Lema aliuliza: ”Kwa sababu TRA ina sheria zake na kwa kuwa hiyo task force inahusu wadaiwa sugu, kwa nini sheria hizo zisitekelezwe kuliko kutumia hiki chombo task force ambacho kinatumia Takukuru, usalama wa taifa… kwa nini hata kama ni task force wasihusu TRA na sheria zote?” Akijibu hilo, Majaliwa alisema: ”Kama ambavyo nimesema, task force ni kwa ajili ya watu ambao kwa makusudi hawataki kutekeleza kulipa kodi kwa kuwatembelea wachache si wote, malengo hapa kila mmoja ana wajibu wake, polisi kama kulipa hadi afuate ulinzi wa fedha. “Takukuru yupo pale kulinda rushwa kila mmoja ana wajibu wake mdaiwa sugu kama hataki anapelekwa polisi. “Hakuna vitendo vya vionevu na halilengi kumtisha mfanyabishara. Pamoja na haya yote yanayoendelea task force haina nia mbaya kabisa wawe na amani”. 
KITAIFA
Lyon ilifungwa mabao 4-0 na Azam FC katika michuano hiyo Jumatatu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili, Salvatory kiungo wa zamani wa Yanga, alikiri kuzidiwa mbinu na Azam FC na kusema wanajipanga kuhakikisha wanashinda michezo yao iliyobaki ili wapande Ligi Kuu.“Tumeondolewa kwenye Kombe la Shirikisho, lakini si kwamba timu yangu ilikuwa mbaya sana, bali wachezaji walishindwa kung’amua mbinu na ujanja wa wapinzani wetu,” alisema Salvatory.Alisema kwa sasa nguvu wanazielekeza kwenye Ligi Daraja la Kwanza ili waweze kupanda japo wamezidiwa pointi mbili na Ashanti United kwenye Kundi A.Mabao ya Azam FC yalifungwa na Mudathir Yahya, Farid Mussa aliyefunga mabao mawili na Ame Ally na kuifanya Azam FC kuingia 16 bora ikiungana na Simba, Yanga, Rhino Rangers, JKT Mlale na Mwadui FC. Timu zingine ni Toto African, Ndanda FC, Panone FC, Mtibwa na Tanzania Prisons.
MICHEZO
Na Upendo Mosha, Moshi HOSPITALI za mikoa ya Kanda ya Kaskazini, zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu salama kutokana na mwamko mdogo wa wananchi kujitolea kutoa damu ili kusaidia wagonjwa wenye mahitaji. Hayo yamesemwa na Ofisa mipango wa damu salama Kanda ya Kaskazini, Faisal Abubakari, wakati wa utoaji wa damu salama kwa vijana zaidi ya 110 wa Kanisa la Adventista Wasabato waliojitokeza kujitolea kutoa damu ili kusaidia wagonjwa wenye uhitaji.  Alisema kumekuwapo na upungufu wa damu katika hospitali mbalimbali za Kanda ya Kaskazini kutokana na jamii kutokuwa na uthubutu wa kuchangia damu, jambo linalosababisha baadhi ya wagonjwa hususani wanawake wanaojifungua kufariki dunia kutokana na kukosa damu. “Kwa sasa hospitali zetu za Kanda ya Kaskazini hazina damu kwani mwamko umekuwa ni mdogo wa jamii katika kujitokeza kuchangia damu, jambo hili limekuwa ni chanzo kikubwa cha wagonjwa wengi hususani wanawake wanaojifungua kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya damu salama,” alisema.  Awali walijiwekea lengo la kukusanya damu kiasi cha lita 30,000 kwa mwaka 2016, lakini wameshindwa kufikia lengo hilo baada ya jamii kutokuwa na mwamko wa kuchangia.  Kwa upande wake, kiongozi wa vijana hao, Heriel Tumaini, alisema vijana wamehamasika kutokana na uhitaji mkubwa wa damu kwa wagonjwa  hususani akinamama wanaojifungua  na majeruhi wa ajali ambao wanakosa huduma hiyo ili kuokoa maisha yao.  “Tumeona tujitokeze sisi kama vijana kwa umoja wetu kuja kufanya matendo ya huru kwa kuwachangia wagonjwa damu, kwani naamini kuna wagonjwa wengi wanahitaji huduma hii lakini wameikosa na kusababisha vifo ambavyo si vya lazima,” alisema.  Baadhi ya vijana waliojitokeza kuchangia damu, walisema ni vema kila mtu mwenye afya njema akajitokeza kujitolea damu ili kuokoa maisha ya watu wenye matatizo ya uhitaji wa damu.  “Vijana ni vema tukajitokeza kuchangia damu kwani suala hili litasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu wengi  iwapo tutakuwa na desturi ya kuchangia damu mara kwa mara, tatizo la upungufu wa damu litakuwa ni historia katika hospitali zetu,” alisema Joel Joakim
KITAIFA
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Mwambusi alisema wanahitaji kupandisha kiwango angalau kifike kwenye asilimia 65 ili wawe katika nafasi nzuri zaidi ya ushindi.“Bado sijaridhishwa na kiwango cha wachezaji, wanatakiwa wapandishe kiwango angalau kifike asilimia 65, tunaweza kuwa katika kiwango ambacho kinatakiwa zaidi,” alisema Mwambusi.“Tulikuwa na majeruhi lakini wameanza kurudi, tunategemea watarudi zaidi kwenye mechi ya marudiano kwani watakuwa wamepona,” alisema Mwambusi.Matokeo hayo ya juzi yanaifanya Yanga kuwa makini zaidi katika mechi ya marudiano mwishoni mwa wiki ijayo ambayo wanahitaji sare yoyote ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.Pia Mwambusi alisema katika mechi hiyo walikosa utulivu ndio maana wakapoteza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kutumia faida ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani.“Wachezaji wanatakiwa kuwa watulivu wanapokaribia au kuwa eneo la goli ili waweze kufanya maamuzi sahihi, kama walivyofunga bao la kwanza, wachezaji walitulia na kucheza tukapata bao la uhakika, tunataka mabao yafungwe kwa namna hiyo,” alisema Mwambusi.Awali Yanga ilikuwa inacheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini iliangukia kwenye kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia.
MICHEZO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inaweza kukusanya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi endapo itaongeza vyanzo vipya vya kodi, itadhibiti wanaoharibu mashine za kielektroniki (EDF) na itaipa kipaumbele sekta binafsi ambayo ni injini ya uchumi wa nchi.Akichangia bajeti ya Fedha na Mpango, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage alisema TRA itafanikiwa kukusanya Sh trilioni 1.7 kutoka Sh trilioni 1.3 za sasa kama itatekeleza mpango wa kuboresha biashara (blue print) kwa kuipa fursa ya kutosha sekta binafsi katika kuendesha uchumi.Alisema mpango huo (blue print) unatakiwa kusimamiwa na Rais John Magufuli kwa kuitisha mikutano na viongozi wa serikali na sekta binafsi ili kujadiliana namna ya kuufikia uchumi wa kati na misafara ya kwenda Ikulu kwa makundi mbalimbali wafanyabiashara, wachimbaji madini na wengine itamalizika.Alisema mpango huo unatakiwa kusimamiwa na Rais Mafuguli kama ambavyo India umesimamiwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi na nchini Rwanda unasimamiwa na Rais Paul Kagame na umefanikiwa nchi hizo kusonga mbele kiuchumi. Mwijage alisema mpango huo unaonesha wazi kwamba sekta binafsi ndiyo inayoendesha biashara nchini, hivyo katika kutekeleza mpango huo, serikali inatakiwa kuipa msukumo sekta hiyo ili kutoa mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa kati 2025.Mwijage alisema TRA itaweza kufikia makusanyo hayo kama sekta binafsi itapewa msukumo ili kuwa imara na yenye ushindani kwa kushawishi wafanyabiashara wengi kulipa kodi kwani ndio wanaosimamia sekta mbalimbali nchini zikiwemo za kilimo, uvuvi, mifugo, usafiri na usafirishaji na nyingine.Mbunge wa Tarime Mjini, Esta Matiko (Chadema) alisema TRA itaweza kuongeza makusanyo kama itaongeza vyanzo vya mapato hasa kuimarisha matumizi ya ufukwe wa bahari kuu kutoka Tanga hadi Mtwara ambao haujatumika vizuri hadi sasa.
KITAIFA
CARDIF, Wales BONDIA wa uzito wa juu duniani,  Anthony Joshua, leo anatarajia kupanda tena ulingoni kuzichapa na Mcameroon, Carlos  Takam, kugombea  mkanda wa IBF katika ulingo wa Principality  uliopo jijini Cardif nchini Wales. Joshua anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika pambano hilo lakini atatakiwa kuwa makini na mpinzani wake ambaye anaaminika kuwa bora na imara katika mchezo huo. Awali kila shabiki wa mchezo huo alitarajia pambano la marudio kati ya Joshua na Wladimir Klitchko Aprili 29, mwaka huu lakini baada ya raia huyo wa Ukraine kutangaza kustaafu mchezo huo ukafutwa, baada ya hatua hiyo, Joshua alitakiwa kupambana na Kubrat Pulev, iwapo alitaka kutetea mkanda wake. Ni mchezo ambao wengi walitabiri ungekuwa mkali kutokana na uimara na ubora wa mpinzani wa Joshua ambaye alidaiwa kufanana kimbinu na Klitchko. Lakini kabla ya wiki mbili ya mchezo huo, Joshua alibadilishiwa bondia wa kupambana naye badala yake alitakiwa kuzichapa na Mcameroon, Takam, baada ya mpinzani wake kuumia bega. Hata hivyo, Takam alisisitiza kwamba, anaweza kumsambaratisha mpinzani wake na kutengeneza jina lake katika uzito wa juu duniani. Promota wa mchezo huo, Eddie Hearn, alieleza kwamba, litakuwa pambano lenye msisimko mkubwa kutokana na Takam kutojulikana na watu wengi katika mchezo huo ukilinganisha na Joshua. Takam anafahamika zaidi Cameroon na Ufaransa na limekuwa jambo la ghafla kuwa mbadala na mpinzani wakati Joshua atakapojaribu kutetea mikanda yake minne ya WBA na ABF. Mcameroon huyo ambaye amepoteza michezo mitatu kati ya mapambano 39 aliyowahi kupambana, anatarajiwa kupata sapoti ya mtoto wake au mkewe atakapokuwa akizichapa leo: “Najaribu kuyafanya maisha yangu kuwa siri, lakini rafiki zangu wengi wanatarajia kuja  kushuhudia pambano hili wakitokea nchini Ufaransa. “Watu wengi kutoka Cameroon wamenieleza wanahitaji kuja kushuhudia pambano hili, hiyo ndiyo nchi yangu, kuna wakati napenda kwenda kutembelea familia yangu.” Takam ambaye anaishi Jiji la Paris,  ana uraia wa nchi ya Ufaransa, aliamua kuishi kwenye jiji hilo baada ya michuano ya Athens Olympics kumalizika. “Mimi nafahamika kwa ubora  zaidi nikiwa Ufaransa na Cameroon, lakini baada ya mzunguko wa tatu au wa nne katika pambano la leo, natarajia watu 80 ndani ya ukumbi huo watanifahamu mimi ni nani. “Waingereza wanataka kufahamu kitu baada ya kukiona, wako sawa katika hilo, nikipata nafasi ya kumdondosha Anthony, maisha yangu kwenye ngumi yatabadilika. Katika soka Cameroon tukicheza dhidi ya Nigeria ni zaidi ya mchezo maana unakuwa na upinzani mkubwa, lakini sasa tuna pambano la ngumi ambalo ni kubwa ndani ya ulingo,” alisema Takam.
MICHEZO
Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM KIWANGO cha juu kinachoonyeshwa na viungo wa Simba, Luis Miquissone, Francis Kahata, Hassan Dilunga na wengineo, kimezua hofu miongoni mwa timu pinzani za Ligi Kuu Tanzania Bara. Kahata, Dilunga, Clatous Chama wamekuwa muhimili wa Simba katika eneo la kiungo, wakiwa chachu ya mabao ya timu hiyo, huku Luis alionyesha si mtu wa mchezo mchezo. Wachezaji hao pamoja na ‘mkongwe’ Jonas Mkude, wametengeneza muunganiko mzuri unaoifanya Simba kuwa moto wa kuotea mbali. Ukiachana na uwezo wao wa kupora mipira, kupiga pasi na kuiwezesha timu yao kutawala mchezo, pia viungo hao wamekuwa wakifunga mabao ama kuwatengenezea nafasi washambuliaji wao, Meddie Kagere na John Bocco. Kiwango cha nyota hao, kimeonekana kuwagusa makocha wa timu nyingi, akiwamo wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ambaye alikiri Wekundu wa Msimbazi hao wanatisha zaidi katika safu ya kiungo. Kocha mwingine ambaye ameonekana kupatwa na hofu juu ya cheche za viungo hao wa Simba, ni Francis Baraza wa Biashara United. Baraza aliliambia MTANZANIA jana kuwa siku zote alizoshuhudia mechi za Simba, roho yao ipo katika eneo la kiungo, hivyo anatakiwa kuwa makini nayo kuelekea mechi ya kesho ya Ligi Kuu Tanzania Bara, watakayokutana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Alisema katika mchezo huo, ataingia kwa nidhamu ya hali ya juu kwa sababu anajua ubora wa Wanamsimbazi hao ulipo. “Simba ubora wake ni eneo la kiungo, tunafanya maandalizi tukijua ni wapi tunatakiwa kuwa makini napo, sio kama naogopa, ila inafahamika mpinzani wako akiwa bora ujipange vipi. “Wachezaji wangu nimekaa nao, nimewaambia hali halisi na wenyewe wameshuhudia mechi za Simba, wanajua nini cha kufanya, kikubwa ni kuzingatia nidhamu,” alisema Baraza. Alifafanua kuwa katika mchezo huo, ataingia na mbinu mbadala kuhakikisha wanapambana hadi dakika ya mwisho, wakiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi.
MICHEZO
    Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amerejea nchini jana akitokea New York nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa za kurejea kwa Kardinali Pengo zilitolewa jana na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa facebook na kuweka kichwa cha habari ‘Karibu nyumbani baba Kardinali’. Askofu Nzigilwa alisema Kardinali Pengo aliwasili jana mchana akitokea nchini Marekani na kupitia Dubai ambako alipumzika kwa siku moja kufuatia ushauri aliopewa na madaktari wake. “Baba Kardinali amerejea nyumbani akiwa mchangamfu na mwenye nguvu za kutosha. Baba Mwadhama anawashukuru waamini na watu wote wenye mapenzi mema, waliokuwa wakimuombea na kumtakia matashi mema wakati wote alipokuwa kwenye matibabu,” alisema Askofu Nzigilwa. Kardinali Pengo amekuwa nchini Marekani kwa matibabu tangu Mei 2, mwaka huu. Juzi, alionekana katika picha na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, walipokutana Dubai, ambako kiongozi huyo alikuwa safarini akielekea nchini Canada.
KITAIFA
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar as Salaam, Daniel Chongolo amezindua kampeni kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulipa kodi ya majengo na kodi ya mabango.Chongolo amesema kampeni hiyo itaenda sambamba na kampeni ya nyumba kwa nyumba ikilenga kuhakikisha wamiliki wote wanalipa kodi kwa wakati kukusanya Sh bilioni saba.Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Chongolo amesema lengo ni kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ya majengo na mabango.Amesema hatua hiyo inatokana na wananchi wengi kujitokeza siku ya mwisho kulipia kodi hizo na kusababisha msongamano, jambo ambalo halipendezi kwani linaua ufanisi wake.Chongolo amesema kufanikisha kampeni hiyo viongozi wa wilaya, wakiwamo watendaji mitaa na kata watashirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuhamasisha wananchi wajue umuhimu kulipa kodi ya majengo na mabango.“Kutakuwa na utaratibu maalumu wa kila mwenye jengo kupewa stakabadhi yake na kisha atakwenda kulipa na watendaji watakuwa wakiwaelekeza wananchi kulipa kodi yao.“Serikali kwa kuwajali wananchi wake imeamua kodi ya jengo kuwa moja ambayo ni Sh10,000 tu. Mwenye nyumba moja atalipa kiasi hicho na mbili atalipia kila moja Sh 10,000,” amesema,Amesema baada ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya majengo, yeye akishirikiana na viongozi wa kata, mitaa na maofisa wa TRA watapita nyumba hadi nyumba kukagua wasiolipa.Meneja wa TRA wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, Masota Masatu alisema wamejipanga kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na watafanya hamasa maeneo yote.
UCHUMI
Golikipa nambari moja wa klabu ya Mtibwa Sugar Shaban Kado amezitaka mamnlaka za Soka nchini kuangalia uwezekano wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye vilabu vya ligi kuu nchini Akizungmza kwenye kipindi ha Sports HQ cha Efm Kado amesema idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni inahatarisha ukuaji wa timu ya taifa “Simba iliketa kipa wa kigeni Aishi akaka nje, Yanga wakileta kipa wa kigeni Metacha naye akakaa nje na Mtibwa wakileta kipa wa kigeni mimi pia nikakaa nje unadhani timu ya taifa itatoa wapi kipa..?” Amehoji Kado “Mimi ninavyoona idadi ya sasa wachezaji 10 ni kubwa sana pengine wangepunguzwa wawe walau hata 5 hapa italeta ushindani maan 10 ni kama timu nzima tu” amesema Hii sio mara ya kwanza kwa mjadala wa wachezaji wa kigeni kuja nchini kujadiliwa ikumbukwe misimu kadhaa nyuma idadi ya wachezaji wa kigeni iliongezwa kutoka saba mpaka 10 wa sasa
MICHEZO
Mchezo huo dhidi ya Zambia ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa timu za umri huo zitakazofanyika Papua New Guinea mwaka 2016.Akizungumzia mchezo huo jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto alisema wachezaji wote wanaendelea vizuri na wako tayari kwa ajili ya mchezo huo.“Maandalizi ya Tanzanite ni mazuri na Kocha (Rogasian Kaijage) alisema wachezaji wote wako vizuri na wako tayari kwa mchezo huo,” alisema.Baada ya mchezo huo wa kwanza, mchezo wa marudiano utachezwa Julai 25 mwaka huu nchini Zambia na timu itakayoshinda itapangiwa timu nyingine kabla ya kufuzu kwa fainali hizo.Kizuguto alisema viingilio vya mchezo huo ni Sh 2,000 kwa viti vya kawaida na VIP ni Sh 3,000 na kuhimiza mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.Akizungumzia mchezo huo kocha Kaijage alisema amekiandaa kikosi chake kushindana na anatarajia kupata matokeo mazuri leo.“Tunaiheshimu Zambia, tushacheza nayo mara kadhaa, wanatufahamu tunawafahamu, naamini wachezaji wangu wameelewa yote niliyowafundisha, nataraji kupata matokeo mazuri kesho (leo), alisema.Wachezaji waliokuwa kambini kwa ajili ya mchezo huo ni Najati Abbasi, Zuwena Aziz, Sherida Boniface, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Tatu Iddy, Niwael Khalfani, Maimuna Hamis, Anastazia Anthony, Amisa Athumani, Amina Ramadhani na Neem Paulo.Wengine ni Asha Shaban, Rebeka Daniel, Brandina Wincelaus, Happines Hezroni, Jane Cloudy, Wema Richard, Gerwa Lugomba, Sadda Ramadhani, Anna Hebron, na Shehati Mohamed, Monica Henry, Tumaini Michael, Diana Msewa na Vailet Nicolaus.Mwamuzi wa mchezo huo ni Batol Mahjob akisaidiwa na Remaz Osaman na Walaa Bilal, mwamuzi wa akiba Khadmallah Elasayed wote kutoka nchini Sudan na Kamisaa wa mchezo ni Flora Roosevelt kutoka Malawi.
MICHEZO
SERIKALI imeanza kushughulikia mgogoro wa vyama vya ushirika na wawekezaji wa mazao ya kahawa na parachichi wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro na kuahidi mazingira sawa yatakayonufaisha pande zote, ikiwemo ulipaji kodi.Kikao kilichokutanisha pande zote kimefanyika wilayani hapa kuhakikisha vyama vya ushirika, wawekezaji, Mamlaka ya Mapato (TRA), Kituo cha Uwekezaji (TIC), Wilaya ya Hai na serikali wanaondoa misuguano isiyo ya lazima.Kikao kimefanyika chini ya uenyekiti wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angella Kairuki.Dk Mpango alisema kukutana kwao ni matokeo ya barua ya wawekezaji kwenda kwa Rais John Magufuli iliyokuwa na hoja sita ambazo baadhi zililalamikia mazingira ya uwekezaji wilayani humo.Alisema serikali inahitaji wawekezaji wakubwa na wadogo hususani katika kuchangamkia fursa za uzalishaji wa zao la parachichi ambalo lina soko la uhakika nje ya nchi.Katika kikao hicho, serikali inafuatilia msuguano uliopo baina ya wawekezaji Kampuni ya Tuddle na ule wa Kuza Africa ili kuona nini kinaweza kufanyika kuhakikisha kila upande unapata haki yake.“Tumesikiliza pande zote za wawekezaji na wananchi kupata ufumbuzi, mwekezaji wa kwanza aliondoka alipokuja mwingine anataka kununua mashamba, hatuwezi kuingilia kwani analipa madeni ya Tuddle pamoja na kutumia miundombinu ya shamba,” alisema.Kairuki alisema vyama vinne vya ushirika viliingia mkataba na Kampuni ya Tuddle, baadaye Kuza Africa na kuleta mgogoro na sasa serikali inavielewesha vyama hivyo ni kampuni gani wanapaswa kufanya nao kazi.Pia alisema serikali inaangalia pia kama michakato yote ilikuwa sahihi ili vyama na wawekezaji wapate haki huku serikali ikikusanya mapato yake.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Anna Mghwira alisema wamekutana kutatua mgogoro huo wa shamba la kahawa na kumebaini mwekezaji wa awali anapaswa kurejea ili kumaliza migogoro iliyopo.Hata hivyo, alisema watamtumia Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili awashauri nini cha kufanya kwa mujibu wa sheria kwani kwa sasa uzalishaji unafanyika nusu ya malengo.Awali, Mkurugezi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe alisema wamejitahidi kujua tatizo la msingi ni lipi na mmiliki wa kwanza Tuddle hakuwa na nia ya kuendeleza uwekezaji huo.Mwambe alisema walitoa hamasa kwa wananchi kutumia fursa ya kilimo cha kisasa kama chanzo cha ajira ili kupata walipa kodi wengi na chanzo cha malighafi.Mmoja wa wawekezaji, Rob Clowes alisema anamshukuru Rais Magufuli kwani ameona changamoto hiyo na kuifanyia kazi na imani yao ni kuona utatuzi utapatikana mara moja.Shamba la Kibo and Kikafu Estate linamilikiwa na vyama vinne vya ushirika ambavyo ni Modiwa Amcos, Masama Ruwa Amcos, Songira Amcos na Masama Sawe Amcos ambavyo vinajulikana kama Morososangi.
KITAIFA
Na CLARA MATIMO MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema kama   walivyotenda wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kufanya ibada na kuliombea taifa amani. Alitoa wito huo kwa waislamu hivi karibuni   katika baraza la Idd EL Fitr kwenye  msikiti wa Shia. Alisema bila amani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana  katika taifa lolote  duniani hivyo ni vema waendelee kudumisha upendo, kuheshimiana na kufanya ibada. “Mungu anasikia maombi ya waja wake mnapokutana wawili ama watatu kwa ajili ya jina lake naye anakuwa katikati yenu , hivyo nawasihi maombi mliokuwa mkiyafanya kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan  myaendeleze  taifa letu lizidi kuwa na amani. “Ombeni bila kuchoka iwe kwa Waislamu au Wakristo wote tuungane kuliombea taifa letu amani   Mungu azidi kutusaidia amani tuliyonayo idumu,”alisema Mongella. Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliwataka Waislamu waendelee kumtumikia Mungu na kufanya kazi zilizo halali kwa bidii  wajiingizie kipato kitakachowawezesha kukidhi mahitaji yao na familia zao. “Nawasihi ndugu zangu Waislamu msifungulie kila kitu endelezeni matendo mema mliyokuwa mkiyatenda kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na Mungu atawabariki. “Hatutegemei kuona muislamu ambaye amefunga mwezi mzima wa Ramadhan halafu baada ya kumaliza mfungo akakamatwa kwa    kuvunja sheria,”alisema Tesha.
KITAIFA
MOMBASA, KENYA SENETA wa Mombasa, Hassan Omar, amemshutumu Rais, Uhuru Kenyatta, kwa kupaisha umaarufu wa Gavana wa kaunti hiyo, Hassan Joho. Akizungumza na wakazi wa Changamwe kauntini hapa juzi, Omar ambaye anagombea ugavana wa Mombasa alimtaka Rais Uhuru akome kuingilia siasa za Mombasa na kwamba yeye angependa kuona akikabana koo na Joho katika kinyang’anyiro cha ugavana wa kaunti hiyo.  “Ninamtaka yule jamaa aliyepata ‘D’- awe kwenye karatasi ya kura. Nitamshinda kwa sababu hajawafanyia chochote wakazi wa Mombasa,” alisema. Kauli zake zimechochewa na masahibu ambayo yamekuwa yakimkumba Joho kutoka kwa utawala wa Serikali ya Jubilee, ambayo yalizidi kushamiri mwezi uliopita. Umaarufu wa gavana huyo umeenea kitaifa kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akipokewa katika maeneo tofautitofauti nchini tangu wiki iliyopita. Joho amekuwa akigonga vichwa vya habari kutokana na jinsi anavyoandamwa kuanzia kuhusu biashara zake hadi matokeo yake ya Mtihani wa Taifa wa Sekondari (KCSE), ambao anadaiwa alifeli lakini akaghushi cheti kumwezesha kuingia chuo kikuu. Naibu Kiongozi huyo wa Chama cha ODM amekuwa akidai masahibu yanayomwandama yametokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali na kwamba Jubilee inatafuta sababu ya kumzuia asigombee ugavana katika uchaguzi mkuu wa Agosti. Hata hivyo, Omar alisema gavana huyo hapaswi kuzuiwa kugombea wadhifa huo hata kama alishindwa  katika mtihani wa KCSE. Kwa mujibu wa Omar, Joho kwa sasa anatumia masahibu yake ili wakazi wa Mombasa wamhurumie na kumchagua tena licha ya kuwa hajawatumikia ipasavyo. “Hakuna kitu kama kura za huruma. Kama huonei huruma wakazi wa Mombasa, huruma usiitarajie kutoka kwao hapo Agosti 8,” alisema katibu huyo mkuu wa chama cha Wiper.
KIMATAIFA
Chanzo cha picha, Instagram/Justin Bieber Mwimbaji Justin Bieber amesema Imani yake kwa Yesu imemsaidia kukabiliana na matatizo ya kimatibabu yaliyomkabili hivi karibuni. Nyota huyo wa muziki alifichua wikindi iliyopita kwamba anakabiliwa na hali ya kiafya iliyomsababishia kupooza uso wake. Tangazo hilo lilifuatia kuahirishwa kwa matamasha yake matatu. "Ninafahamu dhoruba hii itapita lakini wakati huo huo Yesu yuko nami ," Bieber aliandika kwenye Instagram. Bieber mwenye umri wa miaka 28-alisema Jumamosi kwamba hali ya kupooza kwake imetokana na maradhi yanayojulikana kama Ramsay Hunt syndrome. Maradhi haya hutokea wakati vimelea wanaposhambulia neva za uso karibu na masikio ya mtu. Dalili zinaweza kuwa ni pamoja na vipele vinavyosababisha maumivu katika kuta za ndani na masikio, pamoja na kuhiusi kizunguzungu. Chanzo cha picha, Getty Images Kama ilivyo kwa Bieber, hali hiyo inaweza kusababisha kupooza upande mmoja wa uso ambao umeshambuliwa na virusi. Jumatatu, Bieber alituma kwenye ukurasa wake wa hadithi ya Instagram- Instagram story, akisema kuwa "alitaka kushirikisha umma sehemu ndogo ya jinsi amekuwa akihisi". "Kila siku imekuwa bora zaidi na katika maumivu yote haya nimepata Faraja katika yule aliyeniniumba na anayenifahamu ," aliandika Mcanada huyo. "Ninakumbushwa kuwa anajua mambo yangu mimi yote. Anajua mabaya yangu ambayo sitaki mtu yeyote ayajue na wakati wote ananikaribisha katika mikono yake ya upendo. "Mtazamo huu umenipatia amani wakati wa thruba la kutisha ninalo likabili." Wiki ililiyopita, katika video ya dakika tatu aliyoituma kwa wafuasi wake milioni 240, Bieber alitabasamu na kukonyeza macho yake kuonyesha jinsi ambavyo upande wa kulia wa uso wake usivyoweza kutingisika kutokana na kupooza. Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue Mwisho wa Instagram ujumbe, 1 Haipatikani tena Mwimbaji huyo mzaliwa wa Canada alisema kuwa amekuwa akifanya ''mazoezi ya uso''ili kurejea katika hali yake ya kawaida'', lakini akasema hajui itachukua muda gani kupona. Ramsay Hunt syndrome ni hali nadra sana ya kiafya. Kulingana Shirika la Marekani la magonjwa yasiyo ya kawaida, ni watu watano tu kwa watu 100,000 wanaokadiriwa kupatwa na hali hiyo kila mwaka. Mara nyingi, watu hupona kikamilifu katika kipindi cha siku au wiki kadhaa, ingawa baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo la kupoteza uwezo wao wa kusikia kabisa na kuharibika kwa macho.
AFYA
JIJI la Dar es Salaam jana lilizizima baada ya kuwasili kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi, ambao baada ya kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA), msafara wake ulipita katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo.Dk Mengi alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) alikougua ghafla akiwa mapumzikoni. Leo mwili wa Dk Mengi utaagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi mbalimbali watashiriki tukio hilo, na kesho mwili utasafirishwa kwenda Machame mkoani Kilimanjaro tayari kwa maziko yatakayofanyika Alhamisi.Baada ya kuwasili saa 9.45 jioni, ndugu wa marehemu na familia walijipanga ili kuupokea mwili huo baada ya kutolewa kutoka Swiss Port huku usalama ukiwa umeimarishwa kwa kiwango kikubwa. Baadaye mwili huo ulitolewa na kupakiwa kwenye gari maalumu kwa ajili yake.Viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mawaziri, Naibu Mawaziri na wabunge walikuwepo uwanjani hapo wakati mwili huo ulipowasili.Saa 10: 29 jioni, mwili wa Dk Mengi ulipakiwa katika gari maalumu na msafara wake ulianza kwa kupita katika Barabara ya Nyerere hadi Tazara na baadaye kupita Buguruni, Ilala, Kigogo, Magomeni, Kinondoni, Morocco, Makumbusho, Sayansi, ITV, Mwenge hadi katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo ambako umehifadhiwa.Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walifurika kuanzia Uwanja wa Ndege wa JNIA na kila sehemu ambako mwili huo ulipita, huku baadhi yao wakishindwa kuhimili majonzi na kujikuta wakizimia baada ya kuona jeneza la mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini.Msafara huo ulipambwa na mambo mbalimbali ikiwamo magari, pikipiki, baiskeli na baadhi ya watu ambao walilazimika kukimbia pembezoni mwa barabara sambamba na msafara huo ili kumsindikiza mkombozi huyo wa wanyonge ambaye amezimika ghafla na kuzima ndoto za Watanzania wengi wanyonge waliokuwa wakimtegemea.Kabla ya kuwasili kwa mwili wake, mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa mbalimbali ya hapa nchini waliwasili nyumbani kwa marehemu ili kutoa salamu za rambirambi na kupata wasaa wa kueleza masuala mbalimbali kuhusiana na namna walivyomfahamu Dk Mengi.Wananchi hao hawakujali mvua iliyonyesha ghafla ambako wengi waliendelea kujipanga katika maeneo yote ambayo yalipangiwa kupitisha mwili wa marehemu Mengiw akiwa wamelowana, huku vilio vikisikika kila kona.Akizungumza nyumbani hapo; Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema Dk Mengi ni mmoja wa Watanzania waliotoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania baada ya Uhuru kwa kuanzisha kampuni na viwanda vyake lakini pia kuwasaidia Watanzania wengine kufikia ndoto zao za ujasiriamali.“Tumepoteza mjasiriamali, tumepoteza mzalendo anayependa nchi yake, tumepoteza mtu anayewapenda Watanzania, alijali watu wa aina zote, alitoa misaada kwa wenye ulemavu na watu masikini.Harakati zake zililenga katika kuinua kizazi cha sasa na kijacho,” alisema Profesa Lipumba. Viongozi wengine waliotoa maelezo kama hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makala, ambaye alisema Taifa limempoteza mtu aliyejitoa kuwajenga vijana katika uongozi.Naye Kiongozi wa ACT – Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, alisema Dk Mengi ni shujaa wa Taifa kwani ametoa mchango mkubwa katika kuwainua watanzania na Taifa kwa ujumla bila kujali itikadi za kisiasa wala dini.
KITAIFA
Na Ramadhan Hassan, Dodoma Naibu Spika, Dk. Tulia Akson leo amewagomea Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwasilisha taarifa ya kudumu ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutokana na kutowasilisha taarifa yao kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni. Kwa mujibu wa waraka wa Spika, taraifa za kuwasilishwa bungeni zinatakiwa kuwasilishwa kwa Spika siku moja kabla ya siku kuisoma bungeni. Dk. Tulia amesema waraka wa Spika ulitolewa kutokana na siku za nyuma baadhi ya taarifa kusomwa bungeni wakati hazipo kwenye kiti wala wabunge hawajapatiwa. “Kutokana na hali hiyo, hotuba ambazo zimefika mezani kwa Spika ni ya Waziri Mkuu na kamati za Bunge pekee na ndiyo zitakazosomwa,” amesema Naibu Spika.
KITAIFA
NEW YORK, MAREKANI ALIYEKUWA mshindani mkubwa wa mkali wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, msanii kutoka Uganda, Eddie Kenzo, ndiye aliyeibuka mshindi katika tuzo za Nigeria Entertainment Awards 2015 (NEA) kipengele cha ‘African Artist of The Year’ walichokuwa wakishindania. Mganda huyo alishinda tuzo hiyo katika kipengele hicho maalumu kwa wasanii wasio Wanigeria, Septemba 6 huko New York, Marekani ambapo tuzo hizo zilitolewa. Licha ya Diamond kuwania kipengel hicho, wengine waliokuwa wakiwania ni Sauti Sol kutoka Kenya, Sarkodie kutoka Ghana na Stoneboy wa Ghana.
BURUDANI
NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Hans Van der Pluijm, amesema hafikirii kuwa kupata mabao mengi katika mechi ndiyo kufanya vizuri, yeye anachokiangalia na kukiamini katika kikosi chake ni ubora, hata kama  watashinda moja kila mechi. Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi uliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema furaha yake ni kuona kikosi chake kikiingia uwanjani na kufanya vizuri hata wakipata idadi ndogo ya mabao lakini kimeonyesha ubora huo ni ushindi tosha. “Ninachokipa kipaumbele kwangu ni kiwango cha soka wanachoonyesha wachezaji wangu uwanjani, sifikirii kuwa kupata mabao mengi ndiyo kufanya vizuri au kuwa na kikosi bora. “Nitafurahi kama tutashinda kila mechi, siyo lazima tupate mabao mengi ndiyo watu waone tumefanya kitu uwanjani,” alisema Pluijm. Yanga imejikita kileleni mwa ligi ikiwa na pointi sita, sawa na Azam FC, Simba, Mtibwa Sugar na Majimaji, ambapo timu hizo zinatofautiana kwa idadi ya mabao. Kikosi hicho kilianza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kwanza  msimu huu, ambapo katika mechi inayofuata itavaana na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa.
MICHEZO
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hali ya usalama katika Sikukuu ya Idd Al-Hajj, ilikuwa shwari.Mambosasa amesema kuwa hakukuwa na tukio lolote na kwamba wakazi wa jiji hilo walisherehekea kwa amani na utulivu.Amesema jeshi hilo liliweka ulinzi katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti matukio yoyote ya uvunjifu wa amani.‘’Hakuna tukio lolote lililotokea kwenye sherehe za Idd zilizosherehekewa jana (juzi), wananchi walisherehekea kwa amani na utulivu huku jeshi letu likiwa limeweka ulinzi wa kutosha,’’ amesema.Pia aliwapongeza wakazi wa jiji hilo kwa kuhakikisha wanalinda amani ya nchi na kuwataka kuendelea kutoa taarifa za matukio ya kihalifu ili kulisaidia jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama nchini.“Kazi ya kulinda amani sio ya jeshi la polisi peke yake, hivyo ni muhimu kwa wananchi kushiriki kwa kutoa taarifa za matukio ya uhalifu ili jeshi liweze kuwachukulia hatua za kisheria,’’ amesema.Katika sherehe hizo za Idd Al-Hajj, Baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika Uwanja wa Msikate Tamaa, Vingunguti jijini Dar es Salaam ambalo liliandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata).Mbali na jeshi hilo kusisitiza amani, pia viongozi mbalimbali walioshiriki katika baraza hilo waliwataka waumini wa dini ya Kiislamu nchini kulinda tunu ya amani na utulivu iliyopo.
KITAIFA
Na JANETH MUSHI -ARUSHA UAMUZI wa kusikilizwa maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema utajulikana leo mbele ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Jaji Sekela Moshi. Jaji Moshi anatarajiwa kutoa uamuzi huo baada ya  Mawakili wa Serikali kuweka pingamizi za awali wakipinga Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kusikiliza maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa mshitakiwa Alhamisi iliyopita. ,Jaji Moshi alisikiliza hoja za sheria za pande zote mbili na  baada ya  mabishano ya sheria aliahidi atatoa uamuzi wa maombi hayo leo. Uamuzi wa pingamizi hizo unatarajiwa kueleza endapo Mahakama hiyo itasikiliza maombi hayo au kuyatupilia mbali. Katika maombi hayo namba sita ya mwaka huu, Mawakili Waandamizi wa serikali,  Matenus Marandu na Paul Kadushi, waliwasilisha maombi hayo huku upande wa wajibu maombi (Lema) ukiwakilishwa na  jopo la mawakili sita wakiongozwa na Peter Kibatala, John Mallya, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, Faraji Mangula na Charles Adiel. Akiwasilisha pingamizi hizo, Wakili Kadushi, aliiomba Mahakama  kuwaruhusu kuwasilisha pingamizi moja na mahakama ikishindwa kuridhia pingamizi hiyo wawasilishe pingamizi la pili. Alidai  maombi hayo yaliyosainiwa na Wakili Kibatala,   walitumia kifungu cha 372 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambacho kinaipa Mahakama Kuu kufanya mapitio ya mashauri ya kesi za mahakama za chini. Kadushi alidai   hoja ya sheria ni kuwa baada ya mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2002 yaliondoa haki za pande zozote katika kesi za jinai kuomba rufaa au mapitio ya uamuzi mdogo uliofanywa katika mahakama zinazoongozwa na mahakimu nchini. Hoja ya pili iliyowasilishwa mahakamani hapo ni kuwa maombi ya Lema hayajakidhi matakwa yasheria kifungu cha 359(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002. Kifungu hicho kinaelekeza mtu asiporidhika na uamuzi wa mahakama ya chini, anatakiwa kukata rufaa mahakama kuu. Kwa upande wake, Kibatala ambaye alikuwa akiwawakilisha mawakili wenzake watano, alidai hoja za sheria zilizowasilishwa   na upande wa Jamhuri hazina mashiko  katika sheria na akaiomba mahakama izitupilie mbali. Aliiambia mahakama kwamba hakimu aliyeruhusu wakili wa Serikali kusimama kabla hajafikia mwisho wa uamuzi aliokuwa akiusoma ni ishara kuwa mahakama hiyo haikuongozwa vizuri jambo ambalo linaifanya Mahakama Kuu iingilie kati na kutoa maelekezo. “Hoja walizoleta Serikali hazijakidhi matakwa ya sheria, kwanza pingamizi hiyo haijasema inakuja kwetu au inaenda kwa mahakama. “Kwa sababu  sisi na Serikali tumeitwa hapa mahakamani na hii ni kama mwananchi wa kawaida kwenda kwa msajili kulalamika. Jaji akawaita pande zote mahakamani huwezi kuweka pingamizi,”alidai Wakili Kibatala. Alidai kifungu cha 373 cha Sheria hiyo ya Makosa ya Jinai kianaeleza namna gani  mahakama kuu inaweza kupata taarifa ya upungufu wa mwenendo katika mashauri yanayoendelea mahakama za chini na ina uhuru wa kuitisha majalasda na kusikiliza maombi upande wowote kati ya serikali au utetezi. “Mahakama ilijivua mamlaka ambayo inayo, ikiwa ni pamoja na kazi yake ya sheria.  Hakimu alikosea hata kumruhusu Wakili wa Serikali kusimama wakati wa uamuzi. “Nasema hivyo kwa sababu kifungu cha 148(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema Mahakama ikitoa dhamana kwa mshitakiwa ni lazima ifikie mwisho wa hatua ya uamuzi wake kwa kuweka  masharti ya dhamana. “Lakini mahakama iliishia njiani baada ya  Wakili wa Serikali kusimama, kueleza kusudio la kukata rufaa,” alidai Wakili huyo. Wakili Kibatala aliomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hizo kwa gharama na kusikiliza maombi hayo ya dhamana ya mteja wao. Katika maombi hayo, Lema kupitia mawakili wake, anaiomba mahakama hiyo  ifanye mapitio ya majalada ya kesi za jinai namba 440 na 441 mwaka huu, ambako anakabiliwa na makosa ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. Mawakili hao wa Lema wanaomba ombi hilo kwa sababu wakati Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Desderi Kamugisha akisoma uamuzi huo uliokuwa na kurasa 22 hivi karibuni, alisema Mahakama inamwachia Lema kwa dhamana kwa masharti atakayopewa na mahakama hiyo. Hata hivyo, kabla hajakamilisha uamuzi huo akiwa katika ukurasa wa 21 kati ya 22, mawakili wa serikali walisema Serikali inakusudia kukata rufaa juu ya uamuzi huo.
KITAIFA
MANCHESTER, ENGLAND KLABU ya Chelsea inadaiwa ilitoa ofa nono zaidi ya Manchester United ili kumsajili kinda Anthony Martial, taarifa kutoka Ufaransa zimeeleza juzi. Jarida la CanalPlus limesema kuwa straika huyo wa zamani wa Monaco aliipiga chini ofa ya The Blues kwa kuwa alikuwa na ndoto ya kuhamia United, ambayo ilikamilisha usajili wake kwa pauni milioni 36. “Kwa mujibu wa taarifa zetu, Chelsea ilipanga kutoa fedha nyingi zaidi ya Manchester United kwa ajili ya Anthony Martial, lakini mchezaji mwenyewe alikuwa na ndoto ya kucheza Red Devils,” lilieleza jarida hilo. Martial, aliyesajiliwa Septemba Mosi kwa ada itakayopanda na kufikia pauni milioni 58, amefanya makubwa uwanjani tangu ajiunge na miamba hiyo ya Old Trafford. Mfaransa huyo, 19, amefunga mabao manne kwenye mechi saba alizocheza kwa mashetani hao wekundu, alianza kuwavutia mashabiki dakika chache alipofunga bao katika mechi yake ya kwanza walipocheza na mahasimu wao, Liverpool. Kocha Mkuu wa United, Louis van Gaal, alipambana na matajiri hao na kumnasa Martial, licha ya rekodi zake kuonyesha alifunga mabao 13 tu Monaco.
MICHEZO
ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba (pichani) ameingia bungeni kwa mara ya kwanza tangu kuvuliwa wadhifa huo, na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kumuamini na kumpa fursa ya kutumikia wananchi.Pia, amemshukuru Spika wa Bunge na Ofisi ya Spika kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote akiwa waziri. Jumamosi iliyopita, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa baadhi ya mawaziri akiwemo Dk Tizeba ambaye nafasi yake imechukuliwa na Japhet Hasunga ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.Dk Tizeba alitoa shukurani hizo wakati wa Kipindi cha Maswali na Majibu, huku akiibua nderemo na vifijo kwa wabunge na mawaziri baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Akson kumtaja Dk Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa mkoani Mwanza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili aulize swali la nyongeza.Baada ya kulitaja jina la Dk Tizeba kumruhusu kuchangia, wabunge na mawaziri walianza kupiga makofi na kumshangilia kwa nguvu zaidi ya dakika tatu na kumfanya mwanasiasa huyo kusubiri kuuliza swali huku akicheka.Alipoanza kuuliza swali, Dk Tizeba alisema, “Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza, lakini kabla sijauliza swali hilo, niruhusu niseme maneno mawili tu.La kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, namshukuru sana kwa fursa aliyokuwa amenipa ya kulitumikia Taifa. “Lakini pia nikushukuru wewe na Mheshimiwa Spika kwa ushirikiano mlionipa wakati nikitumika serikalini na ndani ya Bunge lako.”Baada ya shukrani hizo, aliuliza swali la nyongeza, akihoji kuwa jimbo lake la Buchosa kuna visiwa zaidi ya 28, lakini kuna vivuko viwili huku kimoja kikiwa kimepitwa na wakati, jambo ambalo watu wanaogopa kukipanda.“Nina swali dogo la nyongeza, Jimbo langu la Buchosa linavyo visiwa zaidi ya 28 na katika visiwa hivyo kuna vivuko viwili kivuko kimoja kimepitwa na wakati na watu wakati mwingine wanaogopa hata kukipanda.Hivyo naiomba serikali ijenge kivuko kipya kati ya eneo la Nyakalilo na Kome ili kupunguza adha ya usafiri. “Hili jambo Mheshimiwa Naibu Waziri (Elias) Kwandikwa analifahamu vizuri ninachoomba ‘commitment’ ya kujenga kivuko kipya kati ya Nyakalilo na Kome bado ipo pale pale au la,” aliuliza Dk Tizeba.Kabla ya kutoa nafasi kwa serikali kujibu swali hilo, Naibu Spika Dk Tulia alisema, “Mheshimiwa Naibu Waziri jibu swali hili linasubiriwa na Bunge zima kwa namna ambavyo mheshimiwa alivyopokelewa humu ndani.”Akijibu, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa alisema anashukuru kupata nafasi ya kujibu swali ambalo limeshangiliwa sana na wabunge na mawaziri na kueleza Bunge kuwa serikali imeunda tume maalumu ya kushughulikia vivuko.“Nimshukuru Mungu kupata nafasi ya kujibu swali la Mheshimiwa Tizeba ambalo limepigiwa makofi mengi sana. Nimshukuru Mheshimiwa Tizeba tulitembelea jimboni kwake tulitembelea kivuko cha Nyakalilo na nilijionea jinsi wananchi wanavyopata tabu kuvuka kwenda kule kisiwani.“Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na upatikaji wa vivuko kipya katika Jimbo la Buchosa, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tumeunda timu maalumu ambayo inatembelea maeneo yote ya vivuko na itarejesha majibu namna bora ya kuendesha vivuko,” alisema Kwandikwa.Aidha, alisema alijionea jinsi ambavyo wananchi walivyokuwa wakigombea kupanda kivuko eneo la Nyakalilo. “Na tuliona katika eneo la Nyakalilo, watu kupanda kivuko mpaka wanagombana sababu ya uwezo mdogo wa kivuko.Mheshimiwa Tizeba nikuhakikishie tutabadilisha kile kivuko na nitaendelea kukupa mrejesho ili tuboreshe usafiri wa Buchosa,” alisema Naibu Waziri wa Uchukuzi.
KITAIFA
 MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imemwita Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Imni Patterson, kujieleza juu ya taarifa wanazozitoa kwenye mitandao yao ya kijamii ikiwamo maambukizi ya corona nchini.  Taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jana, ilisema lengo la kumwita balozi huyo ni kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Itakumbukwa Juni mwaka jana wizara hiyo pia ilimwita Kaimu Balozi wa Marekani nchini, kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa ambayo ubalozi huo, uliitoa juu ya angalizo la kiusalama la uwezekano wa kutokea kwa shambulio la kigaidi. Wito huo ulitokana na taarifa ya ubalozi huo juu ya angalizo la kiusalama kuhusu shambulio la kigaidi katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo eneo la Masaki. Jana taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema Dk Patterson aliitwa na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge, kwenye Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ibuge alieleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.  “Akitolea mfano Katibu Mkuu amezitaja taarifa zilizotolewa na Ubalozi huo Mei 13 mwaka huu Mei 25 kwenye ukurasa wa Twitter wa Ubalozi huo. Alisema taarifa hizo zote zilionekana kukusudiwa kutoa tahadhari kwa raia wa Marekani waliopo nchini na wanaotarajia kuja Tanzania kuwa jiji la Dar es Salaam siyo salama kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wagojwa wa COVID-19.  “Tahadhari hizo pia zimeendelea  kudai kuwa hospitali nyingi jijini Dar es Salaam (bila ya kuzitaja hospitali hizo) zimefurika wagonjwa wa COVID-19 jambo ambalo siyo kweli na linauwezekano wa kusababisha taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi ilhali hali halisi sivyo ndivyo inavyodaiwa,” ilisema taarifa ya wizara.  Ilisema Ibuge alimjulisha Dk Patterson kuhusu umuhimu wa Ubalozi kutoa taarifa zilizothibitishwa kwa sababu Serikali haina kizuizi cha aina yoyote kwa mabalozi kutafuta na kupata taarifa sahihi na zenye ukweli.  Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ibuge alimshukuru Kaimu Balozi huyo kwa ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Marekani katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama na maeneo mengine ya maendeleo.
KITAIFA
Chanzo cha picha, Getty Images Binadamu wanakabiliwa na vitisho vingi, kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa, utapiamlo hadi kupanda kwa gharama ya maisha. Je, maharage yanaweza kuwa jibu la matatizo ya kimataifa? Jamii hii ya kunde ni sehemu muhimu ya karibu kila utamaduni duniani, na kwa sababu nzuri. Maharage yakiwa na takriban aina 40,000 tofauti, hizi ni aina nyingi sana, zenye lishe, na hayana gharama na ni rafiki kwa mazingira. Chanzo cha picha, Getty Images Ikiwa hauna uhakika wa kuyala kama mboga au protini kwenye sahani yako, jibu ni kwamba maharage yanaweza kuliwa kama mboga ua protini au zote mbili. Kwa mfano, mbaazi na maharagwe ya snap huchukuliwa kuwa mboga za wanga, wakati maharagwe yenye rangi nyeusi yako katika makundi yote ya chakula kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Katika ulimwengu ambao watu bilioni 2.5 wana uzito wam wili wa kupita kiasi, wanene au wana utapiamlo, maharagwe ni chakula chenye kila aina wa lishe. Sio tu kwamba ni mbadala wa bei nafuu kwa bidhaa za wanyama, lakini pia huwa hayana mafuta na yana virutubisho vingi, pamoja na protini, chuma, zinki na nyuzi nyuzi (fibre). Zaidi ya hayo, yana kabohaidreti zisizoweza kuyeyushwa ambazo hulisha bakteria kwenye utumbo mpana, hivyo kuwafanya bakteria hawa kuwa bora kwa matumbo yetu yetu. Chanzo cha picha, Getty Images Mikunde yote ina mchanganyiko wa amino asidi muhimu, na kati yake soya hujitokeza kwa kuwa na uwiano bora kwa afya zetu. Jamii hizi nyingne za kunde huwa hazina uwiano sawa, lakini duniani kote ni jambo la jadi kuliwa na vyakula vingine ili kuifanya lishe kwenye sahani iwe kamili. Fikiria maharagwe, wali wa dengu, mbaazi na couscous na chapati. Chanzo cha picha, Getty Images Chanzo cha picha, Getty Images Wakati maharagwe yanajulikana kwa jukumu lake katika, utoaji wa gesi, yanaweza pia kufanya kinyume chake. Mimea hii ina jukumu la kipekee na muhimu katika mifumo ikolojia muhimu kama vile misitu, nyasi na ardhi yenye unyevunyevu. Bakteria walioko kwenye mizizi yake hufyonza nitrojeni kutoka angani na kuihifadhi kwenye udongo. Utaratibu huu, unaojulikana kama urekebishaji wa nitrojeni, sio tu hutoa virutubisho kwa miti na mimea mingine, lakini pia hufanya kazikama mbolea ya asili katika kilimo, kupunguza uchafuzi wa kemikali.
AFYA
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM DIRISHA la usajili limefunguliwa rasmi Juni 15 mwaka huu kwa kuziruhusu klabu kusajili, kuuza wachezaji na kuwapeleka kwa mkopo wachezaji ambao wanatakiwa kuongeza uwajibikaji katika timu ili kuakisi ubora unaotakiwa Tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara Mei 20 mwaka huu kumekuwa na harakati za usajili kwa klabu za ligi mbalimbali ili kuhakikisha zina jiimarisha katika msimu ujao. Moja ya sababu ya kufanya usajili ni kuboresha kikosi katika maeneo korofi ambayo kwa maoni ya benchi ya ufundi akiwamo kocha mkuu, yanatakiwa kufanyiwa maboresho ili kuleta uimara wa kikosi utaosababisha kuwapo kwa ushindani. Katika kutekeleza wa hilo, zipo klabu zinazotumia fedha nyingi kulingana na aina ya wachezaji wanaowataka kuwatumia katika vikosi vyao wakiamini wataleta ushindani wa hali ya juu. Baadhi ya klabu kama  za Singida United, Azam FC, Simba, Yanga, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, na Mbeya City zimeoneakana kusajili kwa ushindani kuimarisha vikosi vyao. Lakini moja ya mambo ya ajabu na aibu katika soka letu nchini ni kitendo cha klabu kununua matokeo kwa klabu nyingine, licha ya kuwapo wachezaji waliosajiliwa kwa  gharama kubwa. Mwaka jana yalikuwapo malalamiko lukuki ya upangaji matokeo yakiwamo yale yalihusisha timu za daraja la kwanza za Polisi ya Tabora na Geita Gold Sport na kusababisha kupewa adhabu ya kushushwa daraja. Katika Ligi kuu zipo taarifa za wachezai au viongozi klabu husika kupewa fedha na viongozi wa klabu pinzani ili kupooza makali ya ushindani ndani ya uwanja na kupata pointi tatu kiulaini bila ya kutoka jasho. Kutokana na sababu hiyo, kuna wakati klabu zinalazimika kubadili wachezaji wa kikosi cha kwanza kutoka na kukosa uaminifu kwa kuhusishwa na kupokea rushwa. Vitendo hivyo vinafanya klabu kulemaa na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau ambapo mwisho wa yote lawama huenda kwa Shirikisho la Soka (TFF) ambalo ndio muhimiri mkuu wa soka nchini. Nguvu hiyo ya fedha uwakumba pia waamuzi pamoja na baadhi ya viongozi wa TFF ambapo kwa nafasi zao uchangia kuvuruga kabisa mchezo wa soka na maana nzima ya kutumia fedha nyingi kwa kufanya usajili bora. Ni  Bara la Afrika tu hasa Tanzania unaweza kukuta klabu inatumia zaidi ya milioni 500 kusajili wachezaji na  kutenga shilingi milioni 100 za kuhonga timu pinzani na shilingi milioni 50  za kufanya ushirikina ili kuloga wakiamini watafanya vizuri. Kama hatutaweza kujifunza kwa wenzetu waliotupita katika mchezo huu na tukaendelea kufanya tuliyoyazoea, hakutakuwa na sababu za kufanya sajili za mbwembwe wakati tunazonjia mbadala za kupata pointi tatu. Lazima mchezo wa soka uheshimiwe na kupewa adhi yake ya kujitawala wenyewe bila ya kuingiza mambo yetu ya ajabu ambayo hayapo katika utaratibu wa mchezo huo.
MICHEZO
NEW YORK, MAREKANI MWANAMITINDO maarfu nchini Marekani, Amber Rose, ameonesha jeuri ya fedha kwa kutumia dola 55,000, zaidi ya Sh milioni 121 kumnunulia mpenzi wake saa. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33, amethibitisha kuwa kwenye uhusiano na rapa 21 Savage mwenye umri wa miaka 24. Awali rapa huyo alitumia kiasi kama hicho cha fedha na kununua zawadi ya saa kwa Amber, hivyo Amber ameamua kujibu mapigo. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Amber aliandika: “Ninamshukuru Mungu kwa kunipa mwanaume huyu ambaye ananionesha mapenzi ya kweli. Kuna wakati najikuta nadondosha machozi kutokana na upendo wake. “Sina cha kumfanyia kwa kile anachokifanya kwangu, lakini nimeamua kununua saa kama aliyonipa zawadi na mimi nimemzawadia,” aliandika Amber Rose.
BURUDANI
Na Kulwa Mzee-Dodoma KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema bajeti yao ya mwaka 2017/18 ni ya  historia ina kurasa 200  ikiwa na makadirio ya Sh trilioni 29.9. Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo ya bajeti ya Serikali mwaka 2017/18 iliyowasilishwa wiki na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango. “Bajeti ya kambi ya upinzani, itakuwa na kurasa nyingi kutokana na kuongezeka kwa matatizo, itawasilishwa kesho(leo) na Mbunge wa Mbozi, David Silinde ambaye ni Naibu Waziri Kivuli wa wizara hiyo, sijui kama wataweka mwongozo kuhusu mzigo huu au vipi,”alisema. “Bajeti iliyowasilishwa Juni, 8 mwaka huu ina upungufu mkubwa, imelenga kumnyonya mwananchi masikini. “Katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18, takwimu za vitabu vyake vya mapato na matumizi zinatofautiana, kitabu cha mapato kinaonyesha kwa mwaka itakusanya Sh trilioni 23.9, kitabu cha matumizi kinaonyesha inakusudia kutumia Sh trilioni 26.9, ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 3, wakati huo huo sura ya bajeti inaonyesha bajeti kwa mwaka 2017/18 ni Sh trilioni 31.7. “Kambi rasmi ya upinzani bungeni inaungana na wale waliosema bajeti hii ni ya ajabu maana haijawahi kutokea kukawa na mkanganyiko mkubwa namna hii wa takwimu katika bajeti,”alisema. Alisema makadirio ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani ni Sh trilioni 29.9 ambako vipaumbele vyao ni   sekta ya elimu iliyotengewa asilimia 20, viwanda asilimia 15, nishati asilimia 15, kilimo asilimia 10 na sekta nyingine zitapata asilimia 40 iliyobakia. Alitaja vyanzo vipya vya mapato kuwa ni mapato yanayotokana na uvuvi katika bahari kuu Sh bilioni 492.1, sekta ya madini Sh bilioni 5.59, kodi ya mrabaha na payee Sh bilioni 270, kupunguza misamaha ya kodi kuwa asilimia moja ya pato la taifa Sh bilioni 145.2 sawa na  Euro trilioni 2.2. Alisema mapato kutoka sekta ya utalii, Sh bilioni 592.7 na sekta ya michezo ya kubahatisha Sh bilioni 30 ambako jumla ya vyanzo vya mapato ya nyongeza ni Sh trilioni 3.7. “Vipaumbele hivi vikitekelezwa kwa ukamilifu Tanzania tutapunguza umasikini kwa asilimia 50 kwa kuwa ni vipaumbele vitakavyochochea ajira kwa watu wengi,” alisema. Kuhusu bajeti iliyowasilishwa na Waziri Mpango, Mdee alisema ilipotangazwa kuondolewa  kodi ya ada ya mwaka ya ‘Motor Vehicle’ magari, viongozi wengi walifurahia bungeni. “Sisi viongozi wa siasa tuna madeni mengi viporo kutokana na kuwa na magari mengi yanayodaiwa kwa sababu hatulipi.
KITAIFA
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani, watatoa tiba ya radiolojia kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 9, mwaka huu.Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha, huduma hiyo itafanyika katika kambi maalumu itakayofanyika MNH katika siku hizo.“Napenda kuwataarifu kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili itatoa huduma hiyo katika siku hizo hivyo tunaomba mtume wagonjwa, wale wa bima za matibabu waje nazo na wale ambao hawana tutawapa huduma, lakini waje na barua za rufaa,” alisema Aligaesha. Aligaesha alisema hivi karibuni MNH imeanzisha huduma za tiba ya radiolojia inayohusisha utaalamu wa kutumia vifaa vya radiolojia kama MRI, CT-Scan, Ultra-Sound na Xray kutibu moja kwa moja au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.“Tayari tumeanza kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingoni, kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya kutoa mkojo ambayo imeziba, kuzibua mirija ya nyongo iliyoziba na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba,” alisema.Tiba nyingine alitaja kuwa ni kunyonya usaha ndani ya tumbo. Matibabu na vipimo vitakavyofanyika katika kambi hiyo alisema ni uvimbe au majipu kwenye mapafu, ini na kwenye figo. Huduma nyingine mfumo wa nyongo ulioziba, mfumo wa mkojo ulioziba na uvimbe au majipu ndani ya tumbo na nyonga.
KITAIFA
Suleiman ambaye alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba katika miaka ya 1998-2000, ambako alifanya mabadiliko makubwa kiasi cha kupewa jina na aliyekuwa rais wa Urusi, Boris Yeltsin.Wenyeviti wa Simba kwa nyakati tofauti, Ismail Aden Rage na Hassan Dalali walimlilia Suleiman wakisema kuwa alikuwa kiongozi shupavu na mwenye msimamo wakati wa uongozi wake.Rage alisema Simba imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na mwanachama wake mwenye uwezo mkubwa wa uongozi aliyeipenda klabu hiyo kwa dhati na kuitumikia vizuri wakati wa uongozi wake.Alisema kiongozi huyo alikuwa mkweli na mpenda haki na mwenye msimamo wa hali ya juu katika kutetea maendeleo ya klabu hiyo na hakuwa tayari kuburuzwa na mtu yeyote.Alisema alikuwa kiboko ya makomandoo ambao wanataka kuishi kwa kuitegemea klabu badala ya klabu iwategemee wa nachama hao.Dalali akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa, Simba imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na kiongozi wao wa zamani aliyekuwa na msimamo wa hali ya juu wa kimaendeleo.Alisema Suleiman pamoja na sasa hakuwa kiongozi wa klabu hiyo, lakini bado alikuwa akisaidia kwa hali na mali ili kuhakikisha Simba inasonga mbele.Alisema kuwa Suleiman alipewa kuiongoza Simba baada ya kusimamishwa kwa viongozi kadhaa kutokana na tuhuma mbalimbali, ambapo alipoingia madarakani alifanya mabadiliko makubwa.Dalali alisema Suleiman aliongoza Simba chini ya mwenyekiti Saleh Ghullum (sasa marehemu). Nalo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana lilituma salamu za rambirambi kwa klabu hiyo kutokana na kifo hicho.Katika salamu hizo, TFF imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, ambaye aliongoza klabu ya Simba SC na kupelekea kupewa jina la utani la ‘Yelstin’ kutokana na ufanisi wake katika kazi na misimamo akifananishwa na aliyekuwa Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris Yeltsin.“TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya Suleiman Said ‘Yelstin’ ndugu, jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ya TFF iliyotolewa na msemaji wake, Baraka Kizuguto.Boris Yeltsin alikuwa rais wa Urusi aliyefanya mabadiliko yaliyojulikana kama perestroika akiwa mpinzani mkubwa wa kisiasa wa Gorbachev.
MICHEZO
Los Angeles, Marekani MNENGUAJI maarufu nchini Marekani, Black Chyna, jana alionekana jijini Los Angeles, Marekani akitembea kwa kutumia msaada maalumu wa baiskeli ya walemavu. Hata hivyo, haikuwa wazi sababu za mwanadada huyo ambaye alikuwa na uhusiano na Rob Kardashian, kuomba msaada huo ambao hutolewa kwa watu wenye matatizo maalumu. Lakini muda mfupi baada ya kupatiwa msaada huo, Black Chyna alionekana akinyanyuka na kutembea hadi lilipo gari lake, jambo ambalo liliwaacha na mashangao watu waliokuwa wakifuatilia tukio hilo. Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya mwanamitindo huyo kuweka wazi kuwa ana mipango ya kutaka kuingia kwenye muziki.
MICHEZO
Wakizungumza jana asubuhi walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutoka katika ziara hiyo ya masomo, viongozi hao walisema mafanikio ya uchumi wa gesi, yatapatikana ikiwa Watanzania watashirikiana na serikali, kuhakikisha wanafikia uchumi wa gesi asilia.Katika kushirikiana huko, viongozi hao wamewataka wananchi kuepuka migogoro isiyo na tija huku wakitumia wakati uliopo vizuri kujiandaa na uchumi huo. Lini, maandalizi?Wameeleza kuwa licha ya kuwa gesi itachukua muda mrefu kuanza uzalishaji, ni vema Watanzania wajipe muda bila kuwa waoga kukopa, kujifunza pamoja na kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi pamoja na kujiunga na vyuo vya ufundi.Makamu wa Askofu wa Kanisa la Anglikana, ambaye ni Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Newala, Mtwara, Oscar Mnung’a alisema ni lazima wananchi wakubali kupokea uchumi huo mpya kwa kujifunza, na kujiandaa kukopa ili kuwekeza katika uchumi huo.“Ili tufikie malengo, tujifunze na tusikubali migogoro isiyo na tija huku tukishirikiana na Serikali kwa kila mmoja kuwa na bidii na juhudi kwani katika nchi hiyo (Thailand), hawana rasilimali kama zilivyo nchini lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Askofu Mnung’a.Wazawa/wageni Askofu Mnung’a alitaka wananchi washirikiane na Serikali katika kutunga sera zitakazosaidia kuwezesha wageni wakati wa maandalizi, ili washiriki kusaidia nchi kufikia malengo hayo na baadaye uchumi ushikiliwe na wazawa kama walivyofanya wananchi wa Thailand.Mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Stella Maris, Padri Dk Aidan Msafiri, alisema wakiwa nchini humo wamejifunza kuwa kufikia uchumi wa gesi inachukua muda mrefu, na ni lazima gesi isafirishwe kwa kutumia mabomba jambo lililosaidia nchi ya Thailand asilimia 98 kuwa na nishati ya umeme.Shekhe wa Mkoa wa Mtwara, Nurdin Mangochi, alisema wananchi wanatakiwa kuelimishwa na kupata muda wa kujiandaa kwa kutumia vizuri rasilimali watu na ardhi.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mohamed Sinani, alisema jambo kuu lililofanikisha Thailand kupata neema ya gesi, ni kuwekeza zaidi katika amani pamoja na kupanga mipango ya maendeleo na kuitekeleza.Alisema baada ya kupata gesi, hawakubweteka bali walipanga mikakati ya kuongeza viwanda na kuzalisha zaidi pamoja na kuendelea na utafiti mbalimbali uliowasaidia kutumia upepo na vyanzo vingine kuzalisha umeme.Naye Kiongozi wa Serikali katika msafara huo, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, Abdallah Ulega, alisema wanatarajia viongozi wa dini kuwaeleza waumini wao kuwa gesi duniani kote husafirishwa kwa kutumia mabomba, husaidia kukopa fedha na kushirikisha nchi nyingine katika kupata utaalamu.Alisema wamejifunza kuwa awali Thailand walitumia wataalamu wa kigeni kutoka Ufilipino na baadaye sera yao ililazimisha wenyeji washirikishwe, baada ya kujifunza utaalamu baada ya kusisitiza kujifunza masomo ya sayansi pamoja na vijana wengi kujiunga na chuo cha ufundi.Ulega alisema ikiwa hayo yatafanikiwa Tanzania, mafanikio yatapatikana mapema kuliko ilivyokuwa kwa Thailand, kwani walianza kuona mafanikio baada ya miaka 40 tangu wagundue gesi, wakati Tanzania ugunduzi wa gesi ulikuwa 2006, lakini mafanikio tayari yameanza kuonekana, ikiwemo matumizi ya magari kwa gesi na mengineyo.
UCHUMI
Mwandishi wetu, Tanga WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Tanga, wamesema hawaoni shidakulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleoinayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kodi zao. Hayo yalizungumzwa na wafanyabiashara wakati wa kampeni ya elimukwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo ambako maafisa wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu kwa kukishirikiana namaafisa wa TRA mkoa wa Tanga. Maafisa hao waliwatembelea wafanyabiashara kwenye maduka yaoyaliyopo barabara za namba jijini Tanga kwa lengo la kuwaelimisha nakuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.Sambamba na hilo, maafisa hao pia waliweza kusikiliza kerozinazowakabili wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao kama mpango wa kutengeneza mazingira rafiki kati yao naTRA.Thabiti Salimu ambaye ni mfanyabiashara wa Ukwaju wa jumla na rejarejakatika eneo la barabara za namba amesema kuwa, atamshangaamfanyabiashara atayekwepa kulipa kodi hususani katika kipindi hikiambacho wameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa kupitia kodi zao. “Rais Magufuli anatumia kodi zetu vizuri, tunaona utekelezaji wa miradimingi ya maendeleo hivyo lazima tuendelee kulipa kodi la sivyo kazi yautekelezaji wa miradi hii itakwama,” alisema Salimu. Naye Dina Mbenu, mfanyabiashara wa vipuli vya pikipiki amesema kuwa,ikiwa wafanyabiashara watakwepa kulipa kodi watasababisha madhara yakiuchumi na kuathiri jitihada za serikali za kuboresha miundombinuikiwemo barabara. Amesema hatua ya maafisa wa TRA kuwatembelea kwenye maduka yaokwa lengo la kuwahamasisha kulipa kodi na kusikiliza kero na maoni yaoinawasaidia kutopoteza muda kwenye ofisi za TRA wakisubiri kuhudumiwa. Kwa upande wake Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Julius Mjenga amesemazoezi la kuwatembelea wafanyabiashara ni endelevu na kabla ya kufanyikaTanga, zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,Mbeya na Morogoro. Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutoa elimu ya kodi, kuwakumbushawafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kusikiliza maoni yao pamoja nachangamoto kwa ajili ya kuzitatua.Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure, aliwaombawafanyabiashara kuunga mkono zoezi linalofanywa na maafisa wa TRA lautoaji elimu ya kodi, kusikiliza maoni na changamoto zao kwa kuwa zoezi hilo linalenga kuboresha huduma kwa mlipakodi.“Niwaombe wafanyabiashara wote mkiwaona maafisa wanatembelea,msifunge maduka, wapokeeni na kuwapa ushirikiano kwa kuwa wanalengakuwaelimisha na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenyebiashara zenu ambazo kwa pamoja tunaweza kuzitafutia ufumbuzi,”alisema Owure. Amesema zoezi hilo la utoaji wa elimu ya kodi kwa wafanyabiasharamkoani humo linatarajiwa kumalizika Juni 30, 2020 na kwamba lengo likiwani kutaka kuwafikia wafanyabiashara wengi mkoani hapo.
UCHUMI
Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema itasikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 27 hadi 29, mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Devota Msoffe amesema uamuzi huo ni kutokana na kesi hiyo kuwa nje ya wakati. “Tutasikiliza kesi hii siku tatu mfululizo kwani iko nje ya wakati na natoa wito kwa mashahidi wa jamhuri kuitwa na kuwapo wakati wote wa kesi kwani tunarajia kufunga ushahidi wao Novemba 29,” amesema Hakimu huyo. Awali, akimsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo, Wakili wa Serikali Agness Hyera katika kesi hiyo namba 440 ya mwaka 2016, amedai kuwa Lema anakabiliwa na shitaka moja la uchochezi ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 22, mwaja jana katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro akiwa anahutubia mkutano wa hadhara. Miongoni mwa maneno anayodaiwa Lema kutoa ni kuwa “Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani iko siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu,…. “Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya Katiba, Rais huyo ataingiza taifa katika majanga na umwagaji damu, watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka polisi hawa wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.”  
KITAIFA
NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM TIMU ya Simba imepanga kuwatema nyota wake watatu na kusajili wachezaji wenye uzoefu ili kuimarisha kikosi hicho ambacho kinaundwa na chipukizi wengi. Simba imeanza mikakati ya usajili kwa ajili ya msimu ujao baada ya kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ikiwa nafasi ya tatu huku ubingwa ukinyakuliwa na watani wao wa jadi Yanga na Azam kushika nafasi ya pili. Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara, alisema uongozi unasubiri ripoti ya kocha wa timu hiyo Mserbia, Goran Kopunovic, ili zoezi la usajili liweze kufanyika kwa kufuata mapendekezo yake. Alisema pamoja na Simba kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu, bado wanaamini wachezaji wao wana viwango na ubora unaokubalika hivyo hawana mpango wa kufanya mabadiliko makubwa kwa ajili ya msimu ujao. Alisema ripoti ya Kopunovic inayotarajiwa kukamilika mapema wiki hii, ndiyo itatoa mwongozo kwa Kamati ya Usajili ya Simba inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Zacharia Hans Poppe kama wachezaji watakaoongezwa ni wa kulipwa au wazawa. “Wapenzi wa Simba wasitarajie mabadiliko makubwa katika usajili kwani timu hii itaendelea kuwepo na wachezaji watakaoachwa hawawezi kuzidi watatu na watakaosajiliwa itategemea mapendekezo ya kocha,” alisema. Wakati huo huo, Kopunovic alielezea kufurahishwa na ushindi walioupata wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku akidai matokeo hayo yamedhihirisha ubora wa kikosi hicho kwa msimu huu. Alisema wachezaji walicheza kwa kujituma na kumfanya ajivunie kikosi bora licha ya kuzidiwa mbinu na watani wao wa jadi, Yanga na kushindwa kutwaa ubingwa msimu huu. Simba iliyomaliza ligi kwa kujikusanyia pointi 47 imekosa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika mwakani baada ya kuzidiwa kete na Azam iliyomaliza kwenye nafasi ya pili.
MICHEZO
WIZARA, Idara zinazozjitegemea, wakala na taasisi za serikali zote na Serikali za Mitaa zimeagizwa kuhakikisha zinajiunga na mfumo wa Serikali wa Kieletroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (GePG) kabla ya Juni 30, mwaka huu.Majaliwa alitoa agizo kwenye hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 14 wa Bunge la 11 alipokuwa akizungumzia mikakati ya serikali ya kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato.“Naziagiza tena wizara, idara zinzojitegemea, mawakala na taasisi za serikali zote na serikali za mitaa kujiunga na mfumo wa Serikali Kieletroniki wa ukusanyaji mapato ifikapo Juni 30,” alisema Majaliwa.Katika miezi sita ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019, serikali imekusanya kiasi cha Sh trilioni 12.84 kati ya Sh trilioni 15.97 zilizotarajiwa kukusanywa kwa makusanyo ya ndani ambayo ni sawa na asilimia 80 ya madirio. Pia ameiagiza ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha ifikapo Februari 28, mwaka huu kila kiwanda nchini kinakuwa kimewekewa mfumo wa ukusanyaji kodi kwa kutumia stempu za kieletroniki.“Naielekeza TRA kusimamia uwekaji wa mifumo ya kukusanya kodi za vileo kwa kutimia stempu za kielektroniki kwa viwanda vinavyozalisha vinywaji, wahakikishe ifikapo Februari 28, mwaka huu kila kiwanda kiwe kimefungiwa mfumo huo,” alisema.Akizungumzia ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogowadogo, Majaliwa alisema hadi Februari 4, mwaka huu, vitambulisho 284,945 kati ya vitambulisho 675,000 vilivyotolewa awamu ya kwanza ambayo ni sawa na asilimia 42 ya vitambulisho vilivyotolewa.“Utaratibu huu wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo umeiwezesha serikali kukusanya takribani Sh bilioni 5.7,” alisema.“Nawasihi wabunge na wananchi wote kuunga mkono kjitihada hizi za serikali. Tukiwaendeleza wajasiriamlai wadogo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kujenga sekta biafsi imara ya Watanzania ambao baadaye wataweza kufanya biashara za ndani na za kimataifa kwa umahiri na ushindani mkubwa,” alisema.
KITAIFA
Kulingana na Shirikisho la Afya ya Akili Dunia (WFMH), asilimia 75 na 95 ya watu wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya kiakili katika nchi zenye mapato ya chini na zile za mapato ya wastani hawawezi kupata huduma kabisa. Hata hivyo asilimia kubwa ya vijana hawana elimu ya kutosha ya afya ya akili, Sasa kijana mmoja kutoka nchini Tanzania ameandaa tamasha linalowakutanisha vijana kutoka sehemu mbali mbali la @watukonekt ili kuzungumzia musuala ya afya ya akili. Mwandishi wa BBC @elizabethkazibure ametuandalia taarifa hii
AFYA
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema wachezaji wapya wa timu hiyo, Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang, wanahitaji muda kabla ya kuanza kuonesha ubora wao na kuisaidia timu hiyo. Wachezaji hao ambao wamesajiliwa katika dirisha dogo la Januari mwaka huu kutoka Manchester United na Borrusia Dortmund, walionekana kuwa na msaada mkubwa wakati Arsenal ikipata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Everton hivi karibuni. Matokeo mabaya baada ya mchezo huo yamemfanya Aubameyang kushindwa kuwa na msaada na kujikuta akipata bao moja katika michezo minne aliyocheza. Hali hiyo inafanana pia na Mkhitaryan ambaye ameshindwa kufanya vizuri baada ya mchezo huo. Mkhitaryan na Aubameyang pia  wameonekana kushindwa kuizuia Manchester City kutamba mbele yao baada ya Arsenal kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wao wa pili baada ya kupita siku tano walipokutana katika fainali ya Carabao na kufungwa mabao 3-0. Katika mchezo huo raia huyo wa Gabon alikosa penalti baada ya kuokolewa na kipa wa Manchester City, Ederson Moraes. Lakini Wenger anaamini Januari ni mwezi mgumu kusajili mchezaji na kufanya vizuri, hata hivyo anajipa matumaini kuwa wachezaji hao watafanya vizuri baadaye. “Wanahitaji muda wa ziada kuzoea mazingira,” alisema Wenger baada ya kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa Manchester City juzi. “Mambo yanabadilika haraka sana. Ni sehemu ya mchezo wa soka, siku hizi ukipoteza mchezo mmoja unakuwa katika presha, lakini wachezaji waliojiunga na Arsenal hivi karibuni watafanya vizuri siku zijazo,” alisema Wenger.
MICHEZO
ALIYEWAHI kuwa msimamizi wa mwonekano wa Diamond Platnumz, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi amesema alilazimika kwenda Afrika Kusini kusomea masuala ya fasheni na muziki kwa kuwa ni vitu vinavyoendana. Akizungumza na Show Biz, Q Boy alisema mwanzoni alikuwa anapenda sana muziki na alifahamu ili kuwa mwanamuziki mzuri inakupasa kuwa na mwonekano mzuri wa mavazi ili sanaa yako ipokelewa vyema na jamii. “Hapo ndiyo nikaingia ‘deep’ sana kusoma fasheni, nikasoma namna gani ya kumpendezesha mtu au msanii ili sanaa yake ipokelewe vizuri na jamii, huwezi kuutenganisha muziki na fasheni,” alisema Q Boy anayefanya vizuri na wimbo wake wa Karorero.
BURUDANI
“NAIPONGEZA timu nzima ya Mkoa wa Arusha iliyobuni mtihani wa pamoja kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa mkoani ambao sasa unasaidia wanafunzi kukuza vipaji vyao na kuwawezesha kuongeza ufaulu zaidi.”Ndivyo anavyosema Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anapozungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuboresha elimu mkoani humo, zikiwa ni juhudi za kusaidia mkoa huo kuendelea zaidi kielimu hali iliyouwezesha kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2018.Katika mpango huo uliozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za binafsi na za serikali mkoani humo, watafanya mtihani mmoja unaofanana kwa shule zote kadiri ya madarasa yao. Mpango huo ni matokeo ya juhudi za mkuu wa mkoa huo, watendaji na wadau mbalimbali wa elimu mkoani humo kushirikiana kutatua changamoto za walimu wa shule za msingi na sekondari.Katika kufikia mafanikio hayo, mara kwa mara Gambo amekuwa akifanya vikao na walimu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro pamoja na maofisa elimu na waratibu wa elimu kata. Vikao hivyo na wadau wa elimu wa Mkoa wa Arusha vimekuwa vikilenga kuhakikisha hakuna mazingira yanayokwamisha walimu kufundisha darasani au watoto kutosoma masomo yote. Uchunguzi umebaini kuwa, juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wa mkoa, ndizo zimewezesha Mkoa wa Arusha kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu.Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega anasema mpango huo umesababisha kuwapo matokeo chanya ya darasa la saba mwaka huu. Mkoa huo wenye walimu wa shule za sekondari 4,950, mwaka 2017 ulishika nafasi ya saba katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi. Mwaka 2016 ulishika nafasi ya sita. Kwitega anasema mpango ulianza kutekelezwa mwaka 2017 kwa kuanzisha mtihani wa mihula kwa shule zote za sekondari na za msingi.“Tumejifunza mambo mengi katika mpango huu wa uboreshaji wa elimu na baadhi ya masomo vijana wanafaulu vizuri huku masomo mengine wakishindwa kufaulu kutokana na walimu kutofundisha vema,” anasema. Akizindua mpango wa kuboresha elimu uliobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na wadau wa elimu wakiwemo viongozi wa dini, Waziri Jafo anaupongeza mkoaa kwa kuzindua mpango wa uboreshaji wa elimu kwa shule za msingi na sekondari.Anasema kutokana na mkoa huo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba, ameandaa vyeti maalumu kwa mikoa mitatu iliyofanya vizuri ikiwemo wa Arusha ili kuwapongeza walimu na wadau wa elimu kwa kuuwezesha kuwa mkoa wa tatu kitaifa katika masuala ya elimu. Anawataka wadau hao kujipanga vema zaidi na kuongeza juhudi kuboresha elimu ili mkoa huo ushike nafasi ya kwanza kitaifa.Anasema uzinduzi wa mpango wa elimu ni ajenda ya kumkomboa mtoto masikini kwa kuwa Rais John Magufuli amekuwa akitoa Sh bilioni 23.5 kila mwezi kwa ajili ya elimu bila malipo akilenga kuwakomboa watoto wa Kitanzania. Anasema mitambo ya kuchapia mitihani ya pamoja iliyopo mkoani hapo, pia itasaidia kuondoa kero ya walimu kuandika mitihani ubaoni. Imebaini kuwa, mpango huo pia unaondoa majigambo ya baadhi ya walimu kudai wamefaulisha vizuri wanafunzi wao, na badala yake umewezesha shule mbalimbali kufanya vema katika kukuza viwango vya ufaulu kwa wanafunzi.“Jambo hili likisimamiwa vizuri Mkoa wa Arusha utaacha mikoa mingine kwa ufaulu na nawaomba wakuu wa mikoa wengine kuiga mfano wa mkoa huu katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” anasema Waziri Jafo. Waziri anamhimiza Mkuu wa Mkoa (Gambo) kuainisha wanafunzi wanaofaulu vema sambamba walimu wanaofanya kazi vizuri ili wapewe zawadi za kiwilaya na kimkoa na kuwataka pia kuandaa siku maalumu ya elimu ili kuhamasisha elimu.Anasema walimu na madaktari ni watu muhimu katika jamii, hivyo hawana budi kupewa motisha sambamba na kuepushiwa adhabu zinazoshusha utu na ari yao ya kazi. “Mwalimu ndiye mtu anayemwandaa mtoto kiakili na anamjenga, hivyo lazima walimu wasikilizwe na wasaidiwe kutatua kero zao…” anasema. Anausisitiza Mkoa wa Arusha kubuni mkakati mwingine wa kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuandaa jukwaa maalumu la mjadala wa kimaarifa ili kushindana kihesabu, kisayansi na kihistoria, hali itakayochochea ongezeko la maarifa ya wanafunzi.Gambo anasisitiza kuwa, mpango wa kuboresha elimu mkoani Arusha umewezesha kutatuliwa changamoto za ufaulu wa mitihani, likiwamo suala la kutofundisha mada zote na kusisitiza walimu kutunga mitihani kulingana na silabasi wanazofundisha. Awali katika mitihani ya nusu muhula kwa kidato cha kwanza hadi cha tatu kila halmashauri ilionesha hakuna halmashauri iliyofikia asilimia 50 huku somo la Sayansi likiwa na wastani wa asilimia 30 na Fikizia wastani asilimia 44. Kwa somo la Hisabati kidato cha kwanza asilimia 20, kidato cha pili asilimia 13 na kidato cha kwanza asilimia 10.“Kama ungekuwa ni utafiti, tungesema wamefaulu katika utafiti, lakini kutokana na matokeo haya tunasema hapana lazima sasa tufanye jambo la kuboresha elimu kwa Mkoa wa Arusha,” anasema Gambo. Anasema siku ya Ijumaa, masomo huisha saa sita na yanapoisha, kila mwalimu mkuu na mkuu wa shule akae na walimu wa masomo yote kujua kwa nini mwalimu husika hajafundisha somo lake kama lipo. Anasema mwalimu akieleza sababu, lazima zitatuliwe ili kuboresha elimu na waratibu wa elimu kata waangalie changamoto za walimu na kuzitatua, ikiwemo kuziwasilisha kwa maofisa elimu katika halmashauri zote.“Maofisa elimu nendeni mkajue hao wengine wana changamoto gani maana kuna mahali utakuta shule haina vyoo, mazingira yake si rafiki sasa lazima uangalie tatizo lipo wapi na siyo suala la kusimamisha tu, walimu,” anasema Gambo. Anasema: “Mfano, katika Shule ya Msingi Mkonoo kulikuwa na ukosefu wa vyoo walimu walikuwa wakichangia vyoo na wanafunzi. Nilipofika pale Aprili mwaka huu kuangalia yale mazingira, nilihuzunika sana…” “Nilichofanya ni kumchukua Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni ili ajionee hali halisi ya maisha ya walimu hawa na ndipo nilipohakikisha Halmashauri ya Jiji inatenga milioni kadhaa kwa ajili ujenzi wa matundu ya vyoo zaidi ya 20 nimeongeza hapo.”Mchakato wa Mpango wa Elimu ulianza mwaka 2017 kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, hivyo badala ya kununua mashine kwa Sh milioni 20 tulinunua mashine 10 za kuchapisha mitihani kwa Sh milioni 7. Katibu Tawala wa Mkoa (Kwitega) anasema mkakati mwingine ni kuwezesha wazazi kuwa na utaratibu wa kusoma vitabu na watoto wao kwenye maktaba zilizopo mkoani humo.Theresia Mahongo kwa niaba ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, anasema awali aliona mpango huo hauwezekani, lakini kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, umefanikiwa na kuzaa matunda chanya. Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Dk Stanley Hotay anaiomba serikali kuhakikisha mitaala inayotolewa ya kuanzia elimu ya msingi na sekondari inamjenga na kumwandaa mtoto kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa. Mwalimu Ambrose Bashayija kutoka wa Shule ya Edmund Rice iliyopo katika Kata ya Sinon, anasema awali shule za binafsi zilikuwa zikikabiliwa na uhaba wa vifaa vya kuchapisha mitihani pamoja na udanganyifu wa ufaulu, lakini mpango huo utawezesha walimu kujulikana kama kweli wanafundisha vipindi vizuri darasani ama la.
KITAIFA
NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM   MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekubali kupokea ripoti za mkemia zinazothibitisha kwamba sampuli ya mkojo wa Mlimbwende wa Tanzania 2006, Wema Sepetu, imekutwa na chembechembe za bangi na majani yalibainika kuwa dawa za kulevya aina ya bangi.   Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, alikubali kupokea ripoti hizo mbili na kuzitambua kama kielelezo namba moja cha upande wa mashtaka, baada ya kutupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala.   Hakimu Simba alisema hakuna ulazima wa ripoti ya mkemia kuwasilishwa mahakamani ikiwa imeambatana na fomu ya maombi iliyotoka Polisi, ikielekeza mshtakiwa afanyiwe uchunguzi.   “Kazi ya mkemia ni kufuata maelekezo kwa kuchunguza, Jamhuri ndiyo yenye jukumu la kujua ni nani anayestahili kuitoa fomu hiyo mahakamani kama kielelezo, mahakama imepokea ripoti zote mbili kama kielelezo namba moja,” alisema Simba.   Agosti mosi mwaka huu, Mkemia Elias Mulima, akiwa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, alidai mahakamani kwamba alivyoufanyia uchunguzi mkojo alibaini mshtakiwa huyo anavuta bangi na akataka kutoa kielelezo ambacho kilipingwa na upande wa utetezi.   Wakili Peter Kibatala, anayemtetea Wema, alipinga ripoti hiyo isipokelewe kwa sababu haijakidhi kifungu cha 63 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.   Kibatala alidai kuwa, kifungu hicho kinaeleza utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kitabibu kwa mshtakiwa ambaye yupo chini ya ulinzi kuwa ni lazima Polisi awasilishe maombi mahakamani.   Kibatala aliomba ripoti hiyo ikataliwe kwa sababu hakukuwa na ombi wala amri kutoka mahakamani.   Pia alipinga ripoti hiyo kupokelewa kwa sababu haijaambatanishwa na fomu namba DCEA 001 iliyotoka Polisi kwenda kwa mkemia kuomba mteja wake afanyiwe uchunguzi.   Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, akijibu hoja hiyo, alidai fomu  yenye namba 001 inatumiwa na  Polisi wanapopeleka sampuli  na fomu namba 009 ni taarifa ya Mkemia na kwamba fomu moja haitegemei nyingine kwa kuwa zinaandaliwa na watu tofauti.   Kakula alidai kuwa, sheria haijasema muda wote ni lazima maombi yapelekwe mahakamani amri itoke ndiyo mshtakiwa afanyiwe mchunguzi wa kitabibu, ila pale ambapo mshtakiwa hataki Polisi wanaweza kufanya maombi mahakamani.   Katika ushahidi wake, Mulima alidai Februari 8, mwaka huu, alipokea sampuli ya mkojo wa Wema na Februari 6 alipokea majani ambayo aliyafanyia uchunguzi kujua kama yalikuwa dawa za kuleya ama la.   “Wema aliletwa ofisini kwa Mkemia na Inspekta Willy na WP Mary, alipofika nilimfanyia usajili na kumpa namba ya maabara 321/2017.   “Walimleta kwa sababu walitaka Wema apimwe mkojo na nilimpa kontena maalumu na kumpatia WP Mary ambaye aliongozana naye hadi kwenye vyoo akatoa sampuli ya mkojo.   “Baada ya kupatikana mkojo nilipokea sampuli hiyo na kuendelea na uchunguzi ambapo hatua ya kwanza ni kuangalia chembechembe za dawa za kulevya ndani ya mkojo wa Wema na baada ya uchunguzi nilibaini kuna dawa za kulevya aina ya bangi,” alidai.   Mulima aliendelea kudai kwamba, kitaalamu bangi inaweza kuonekana kwenye mkojo ndani ya siku 28.   Alidai baada ya kuthibitisha kwamba anatumia bangi aliandaa taarifa ya mchunguzi ambayo aliisaini yeye mwenyewe na ikathibitishwa na Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Februari 8, mwaka huu.   Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa, Februari 6 mwaka huu, akiwa ofisini kwake, alipokea kielelezo kutoka Jeshi la Polisi Tanzania kupitia kwa D/Koplo Robert, kikitakiwa kufanyiwa mchunguzi kuthibitisha ni dawa ya kulevya aina ya bangi ama la.   Alidai alikipokea kwa njia ya fomu DCEA 001, akakisajili na kukipa namba ya maabara 291/2017.   Anadai alifungua na kukuta msokoto mmoja na vipisi viwili, ndani yake kuna majani yadhaniwayo kuwa ni bangi.   “Niliyapima na kuyakuta yana uzito wa gramu 1.08, nilifanya uchunguzi kwa kutumia kemikali na kubaini ni bangi,” alidai.   Washtakiwa katika kesi hiyo ni Wema, Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas, ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.   Inadaiwa Februari 4, katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio,  washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. Kwa upande wa Wema, yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka huu, katika  eneo lisilojulikana, jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.   Hata hivyo, kesi imeahirishwa hadi Agosti 15 na 16, mwaka huu, kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.
BURUDANI
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara wamefanikia kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuwatoa Azamu kwa penati 3 kwa mbili. Katika mechi iliyopigwa usiku wa leo dakika 90 zilimalizika kwa timu zote kutokufungana na baadaye zikaingia hatua ya penati. Kwa matokeo hayo Simba itakutana fainali na Mtibwa Sugar ambayo ilifuzu jana kwa mikwaju ya penati 4 kwa 2 dhidi ya Mabigwa wa kihistoria Tanzania Yanga. Wengi wanatumai kuwa mechi ya fainali na ya mshindi wa watatu zitakuwa bora kwakuwa hata timu zilizopo katika nafasi hiyo zimeonyesha ushindani mkubwa. Wanyama hao fainali. #MapinduziCup2020 #NguvuMoja A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania) on Jan 10, 2020 at 11:24am PST Tuandikie maoni yako hapo chini kutabili nani ataibuka mshindi.
MICHEZO
Na CLARA MATIMO,  MWANZA   ASKARI mmoja wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,  amefariki ghafla akiwa eneo la kazi katika kituo cha Polisi Nyagezi, jijini Mwanza. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi,  alimtaja askari huyo kuwa ni Koplo Marco Mahona,  ambaye alifariki juzi saa saba  mchana wakati akitekeleza majukumu yake. Akielezea jinsi kifo hicho kilivyotokea, Kamanda Msangi alisema,  Koplo Mahona akiwa ndani ya ofisi iliyopo eneo la stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Nyegezi,  alisikia sauti za wananchi waliokuwa eneo hilo wakimzomea mwanamke ambaye alikuwa anapita karibu na kituo  akiwa na watoto wake ndipo alinyanyuka kuangalia ili kujua tatizo ni nini. Alisema wakati akiwa karibu na mlango wa kituo hicho akiwa na lengo la kusogea eneo ambalo wananchi wanamzomea mwanamke huyo, ghafla alianguka na  kupoteza maisha. “Kwa mujibu wa mashuhuda mwanamke huyo wakati anazomewa  huku akirusha mikono juu ikiwa ni ishara ya kuwaambia  waachane naye, sasa  kwa kuwa kazi ya askari polisi ni usalama wa raia ilimlazimu  askari wetu kutoka nje ili aweze  kujua kinachoendelea. “Lakini kwa bahati mbaya alipotoka tu nje alianguka akapoteza fahamu na baada ya kupelekwa hospitali  na kubainika  kwamba amepoteza maisha,  mwili wake upo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili tubaini sababu za kifo chake. “Lakini cha kusikitisha ni kwamba tangu  baada ya tukio hili kutokea baadhi ya wananchi wamekuwa wakisema mambo mbalimbali ambayo hayana ukweli.
KITAIFA
WACHEZAJI wa timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 12 ya Afrika itakayofanyika Rabat, Morocco kuanzia Agosti 19 hadi 31 wametakiwa kutokuwa wanyonge kutokana na idadi yao ndogo na badala yake kupambana na kuleta medali.Tanzania katika michezo hiyo inapeleka timu za michezo miwili za riadha yenye wachezaji sita, huku judo yenye wachezaji watatu, makocha wawili na meneja wa timu pamoja na viongozi kadhaa.Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Yusuph Singo akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema uchache sio hoja kinachotakiwa kwenda kufanya vizuri na kurudi na medali.“Msijisikie wanyonge kwa uchache wenu, kwani kuna nchi zinaweza kupeleka wachezaji wengi zikatoka kapa, lakini nyinyi wachache kama mtakwenda kupambana na kurudi na medali za dhahabu mtakuwa katika nafasi nzuri kuliko wale waliopeleka wachezaji wengi, “alisema Songo katika hafla hiyo. Pia aliwataka wachezaji hao kuwa wazalendo kwa kulishindania taifa lao na kuwa na nidhamu wakati wote wa michezo hiyo hiyo na kutothubutu kujaribu kutoroka. Nahodha wa timu hiyo, Gabriel Gerald akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema watahakikisha wanapambana vizuri na kurudi na medali kutoka katika michezo hiyo, ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne.Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema wenyewe wamechangia tiketi tatu katika timu hiyo ili kuhakikisha Tanzania inapeleka wanariadha hao na meneja, Donath Massawe.Mbali na Gerald wanariadha wengine katika timu hiyo ni Sarah Ramadhani, Natalia Elisante, Benjamin Kulwa, Khamis Gulam na Regina Mpikachai nakocha Mwinga Mwanjala huku wachezaji wa judo ni Anogisye Fwele, Hamis Ally na Abdulab Alawi na kocha ni Innocent Mallya.
MICHEZO
Faraja Masinde, Dar es salaam BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), limemvua nafasi zote za Uongozi aliyekuwa katibu Mkuu wake , Islamil Suleiman. Akizungumza Dar es Salaam leo Januri 25, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Nicholaus Zacharia, amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya  kikao cha dharura kilichofanyika mapema leo. Amesema hatua hiyo inatokana na matokeo ya kamati ya uchunguzi ya NaCoNGO iliyoundwa na baraza hilo Desemba 19, mwaka jana ambayo iliketi jijini Dodoma. “Baraza limefikia uamuzi huo w akumvua nafasi zote za uongozi aaliyekuwa katibu Mkuu Suleiman, kufuatia tuhuma mbalimbali dhidi yake, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za NaCoNGO karibu milioni 540. “Pamoja na kutotoa ushirikiano wakutosha kwa baraza, kamati ya uchunguzi ilimkuta, Suleiman na makosa ya kuingiza kwenye baraza wajumbe watano ambao hawakuchaguliwa kwa mujibu wa kanuni za NaCoNGO, kwa ajili ya kuwakilisha Mikoamitano,” amesema. Amewataja, wajumbe hao waliochaguliwa na, Suleiman na mikoa waliyoelezwa kutoka kuwa ni, Remmy Nemmes (Geita), George Nyanda(Simiyu), Heiman Didas(Pwani), Bakari Salum(Tanga) na Gilbert Alex(Ruvuma). Aidha, Zacharia amesema kuwa, mtuhumiwa alikuwa akiendesha akaunti mbili za benki ya CRDB za Sh na Dola bia ya kuwa na uelewa wala idhini  ya kamati tendaji au baraza . “Alikuwa amemuweka mtiasaini ambaye siyo kiongozi ndani ya baraza, pamoja na kutoa vitisho kwa wawakilishi wa NGOs waliokuwa wanadai uwazi na uwajibikaji wa fedha waliotoa kwa NaCoNGO,” amesema Zacharia. Amefafanua kuwa, kufuatiab uamuzi huo, baraza hilo limemteua, Focus Magwesela kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa NaCoNGO kuanzia jana Januri 25, hadi hapo itakapo amriwa. “Kwakuwa baadhi ya makosa aliyokutwa nayo Suleiman yana viashiria vya jinai, tunapenda kuujulisha umma mtuhumiwa siyo kiongozi katika ngazi yoyote ndani ya baraza na hatua stahiki dhidi yake zitachukuliwa,” amesema Zacharia. Mtuhumiwa Akizungumzia tuhuma hizo Suleiman anayetuhumiwa kutumia nafasi yake vibaya ambapo amekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa siyo za kweli na kwamba ni mbinu za kutaka kumchafua kwa kuwa amekuwa akihoji masuala kadhaa ndani ya baraza hilo. “Nimezipata hizi habari, lakini hizi tuhuma siyo za kweli bali kuna kitu kimefichikia kwani mimi nimekuwa nikisimama mstari wa mbele wka ajili ya kutaka sheria ya NGOs itekelezekee, lakini baadhi ya watu haiwataki kwa kuwa itabana maslahi yao, ndiyo maana wakaunda mbinu ya kutaka kuniondoa. “Haya mambo mengine wanayosema ni siasa tu kwnai hata hiyo kamati wanayosema kwamba ilikuwa inanichunguza haijawahi hata kuniita, hivyo naona walichokuwa wanataka kufanya wamekitekeleza,” aamesema Suleiman na kuongeza: “Kimsingi baraza tayari limemaliza muda wake na hivyo kiutaratibu uchanguzi ulitakuwa kuwa umefanyika tangu mwezi uliopita,” amesema.
KITAIFA
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
UCHUMI
Akitoa maelezo hayo juzi jioni bungeni, mbunge huyo alisema ametumia Kanuni ya 28 (8) ya Kanuni za Bunge za Kudumu.Alisema mashine hizo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara na bei ni kubwa, ikilinganishwa na gharama halisi na pia bado matumizi yao hayajaeleweka kwa watumiaji wengi.“Naomba Serikali isitishe uuzaji wa mashine hizo bei ni kubwa sana, itoe elimu ya kutosha kuhusu matumizi, lakini pia ipitie upya sheria zote za kodi ili kufanya marekebisho katika sheria zitakazoonekana zina upungufu,” alisema Zambi.Alisema maelezo yake hayo, msingi wake ni malalamiko ya bei kubwa za mashine hizo, ambapo awali ziliuzwa Sh milioni mbili kwa wafanyabiashara ambao mzunguko wa biashara zao unafika Sh milioni 14 kwa mwaka.Hata hivyo, wafanyabiashara walikuwa wakilalamika kuwa bei hiyo ni kubwa sana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikapunguza bei hadi Sh 800,000.Msingi wa malalamiko ni kuwa mashine hizo huko zitokako bei yao huanzia kati ya dola 60 hadi 150 sawa na Sh 75,000 hadi Sh 300,000.Alihoji uhalali wa mashine hizo kuuzwa kati ya Sh 800,000 na Sh milioni 1.5 kwani ni sawa na kuibia Watanzania.“Baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara wakiwamo wa Mbeya, nilisafiri hadi Dubai na China ambako nilikuta zinauzwa dola 60 hadi 150 kutegemeana na aina ya mashine,” alisema Zambi.
UCHUMI
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM KATI ya Novemba 25 hadi Desemba mosi, 2017 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), ilifanya upasuaji mkubwa wa moyo wa kihistoria nchini. Madaktari Bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International kutoka nchini Austraria waliwafanyia upasuaji wagonjwa 16 wenye matatizo mbalimbali ya moyo. Kati ya wagonjwa hao, tisa walikuwa watoto na saba watu wazima, ambao walifanyiwa upasuaji wa kubadilisha milango ya moyo iliyokuwa imeharibika na kuwekewa milango ya chuma. Miongoni mwa watu wazima waliofanyiwa upasuaji wapo waliopandikizwa mishipa ya damu iliyovunwa kutoka miguuni na kwenda kuzibua ile iliyokuwa imeziba. “Upasuaji huo kitaalamu unaitwa ‘bi-pass surger,’ hii si mara ya kwanza kwa taasisi yetu kufanya kwani tayari wagonjwa wapatao 30 wamefanyiwa kwa mwaka huu pekee,” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi. Anasema: “Watoto waliofanyiwa upasuaji walikuwa na umri wa kuanzia miezi minne wakiwa na uzito wa kuanzia kilo nne hadi 12, kati yao, mmoja alikuwa amezaliwa akiwa na moyo upande wa kulia.” Profesa Janabi anasema kibaiolojia moyo wa binadamu unapaswa kuwa upande wa kushoto hata hivyo, hutokea mara chache mtoto kuzaliwa moyo ukiwa upande wa kulia. Anasema hadi sasa bado haijajulikana wazi nini hasa husababisha mtoto kuzaliwa moyo ukiwa upande wa kulia. “Duniani, tafiti zinaonesha kati ya watoto 2000 wanaozaliwa basi mmoja huwa katika uwezekano wa kuzaliwa moyo wake ukiwa upande wa kulia,” anasema. Anasema hata hivyo hakuna madhara yoyote yanayoweza kumpata mtoto ambaye moyo wake umeumbwa ukiwa upande wa kulia. “Anaweza kuishi vema kabisa kama binadamu wengine ambao wameumbwa wakiwa na moyo katika upande wa kushoto,” anabainisha. Mtoto aliyefanyiwa upasuaji Profesa Janabi anasema mtoto ambaye walilazimika kumfanyia upasuaji alikuwa na matatizo makubwa mawili ya moyo. “Moyo kuumbwa upande wa kulia haikuwa tatizo kubwa kwake, isipokuwa tulibaini mishipa yake ya damu ilikuwa haifanyi kazi inavyopaswa. “Katika moyo kuna mishipa inayoingia upande wa kulia ambayo kazi yake kuu ni kubeba damu chafu yenye hewa ya kabondaioksaidi na kuna inayoingia upande wa kushoto yenyewe hubeba damu safi yenye oksijeni,” anabainisha. Anaongeza: “Huyu mishipa yake ilikuwa inachanganya damu safi na chafu kwa pamoja jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa maisha yake. “Ni kama vile uchukue maji safi na taka halafu uyachanganye kwa pamoja kisha unywe, kamwe mwili hauwezi kuhimili mchanganyiko huo. “Sasa yeye badala ya damu chafu kupita katika upande unaostahili ili ikasafishwe huchanganyika pamoja na damu safi iliyokwisha safishwa kisha iende mwilini kutumika, ni tatizo,” anasema. Anasema pamoja na tatizo hilo, tatizo jingine lilikuwa ni mapigo yake ya moyo yalikuwa chini mno kutokana na kiwango kidogo cha umeme kilichopo kwenye moyo wake. “Kutokana na hali hiyo, ilibidi tumpandikize betri ndani ya moyo wake, hii ni oparesheni ya tatu kwa watoto na sasa mapigo yake yanakwenda vema,” anasema. Anasema ilichukua takriban saa tisa kukamilisha upasuaji huo kwa sababu kwa kesi kubwa kama hiyo huwalazimu ‘kuusimamisha’ moyo wake kwa saa kadhaa. Mwili kuwa na rangi ya bluu Anasema damu safi na chafu inapochanganyika ni lazima mwili wa mgonjwa ubadilike rangi na kuwa bluu. “Kitendo cha kubadilika na kuwa rangi ya bluu maana yake ni kwamba kile kiwango cha oksjeni kinachohitajika mwilini huwa hakitoshelezi,” anabainisha. Dalili zake Anataja dalili za awali kwa mtoto aliyezaliwa na tatizo la moyo ambazo mzazi anaweza kuziona ni pamoja na kushindwa kunyonya vizuri. Anasema hii huwatokea zaidi watoto walio katika umri wa kunyonya, lakini kwa wenye umri wa kwenda shule wengi huchoka mara kwa mara. Makuzi baada ya upasuaji Anasema mtoto waliyemfanyia upasuaji ataendeelea vizuri na kwamba ataishi na kulelewa kama ilivyo kwa watoto wengine wasio na tatizo. “Kila mshipa wa damu sasa unafanya kazi yake kama inavyotakiwa na mfumo wa umeme upo sawa sawa baada ya kumpandikiza betri. “Lakini kama asingetibiwa mapema basi kidaktari naweza kusema wazi kwamba asingefika na kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa ya mwaka mmoja. “Ila kwa kuwa tumewahi kumfanyia upasuaji tunaamini Mungu akimjalia basi atasherehekea sikukuu yake ya mwaka wa kwanza na kuendelea,” anasema. Masharti Anasema mtoto huyo ambaye ni mchanga, ataishi na kula kila kitu isipokuwa amepewa masharti kadhaa. “Tumempatia kadi maalumu ya utambuzi, hatatakiwa kupita katika maeneo yenye sumaku kubwa kama vile uwanja wa ndege kwa sababu ile nguvu inaweza kukiwasha na kuyafanya mapigo ya moyo kubadilika na kwenda kasi,” anasema. Ushirikiano zaidi Mkufunzi wa Wagonjwa Mahututi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa OHI, Russel Lee anasema wataendelea kushirikiana kwa ukaribu na JKIC katika kutoa matibabu. “Kila ninapokuja Tanzania naona JKCI inazidi kufanya matibabu kwa kiwango cha juu zaidi ya awali, hili ni jambo linalotia faraja kubwa, OHI tutaendelea kushirikiana nao pia kwa kuwapatia mafunzo wataalamu wake ili wazidi kufanya vizuri zaidi,” anasema. Daktari Bingwa wa Upasuaji Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI, Godwin Sharau anasema faida kubwa wanayopata katika kambi hizo za matibabu ni kubadilishana ujuzi. “Kuna baadhi ya magonjwa ya moyo ambayo ni magumu na JKCI tunahitaji kupanda hatua kwa hatua ili tuweze kuwahudumia vizuri watoto na wakubwa wenye matatizo haya. “Tunataka twende sambamba na wenzetu katika teknolojia ya kutibu magonjwa ya moyo ili kufikia adhma ya serikali kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi,” anasema. Wito Anawasihi wazazi wanapoona dalili hizo wawahi kuwapeleka watoto wao hospitalini kwa uchunguzi zaidi. “Ukimpeleka hospitalini watabaini tatizo na kama anastahili kuletwa JKCI watampa rufaa kuja huku, kuendelea kukaa naye nyumbani kutahatarisha zaidi maisha yake hatimaye kifo. Anasema katika kipindi cha mwaka huu pekee wamewafanyia upasuaji watoto 300 wenye matatizo ya moyo, ukijumlisha na watu wazima idadi yao inazidi 600. “Watoto waliopoteza maisha ni wanne tu, hivyo wasiogope kuja kuwafanyia uchunguzi na upasuaji watoto wao,” anawasihi. Profesa Janabi anawahimiza pia wataalamu wa afya kuhakikisha wanawapa rufaa mapema kwenda JKCI watoto wanaowapokea wakiwa na dalili za maradhi makubwa ya moyo.
AFYA
README.md exists but content is empty. Use the Edit dataset card button to edit it.
Downloads last month
47
Edit dataset card