text
stringlengths
29
186k
Mkuu wangu JK, Meli yako inayoitwa Tanzania inaelekea iko kwenye mawimbi ya kati hadi mazito kidogo.
Kwa sisiwadau wako tunaona ni kwa sababu nahodha uliyemuachia usukani ukiwa katika ziara zako nyingi nje ya nchi naye anayumba na Meli hiyo.
Kushitakiwa Chenge imekuwa wimbo wa itakuwa au haitakuwa, Serikali haina maamuzi ya kujionyesha iko safi.
Mzee mzima Rostama kaachia ngazi, hakuna wa kucomment rasmi juu ya kuvua gamba Sie tuna uhakika Meli haizami, lakini dhoruba wananchi wanayoipata inawatia wasiwasi juu ya umahiri wa Nahodha.
Broda , kuelewa hayo uliyoainisha inataka Hikma, kitu ambacho kwa huyo * 'Meti-Onyo', yaani hamna kitu!
Anaongea BBC kuwa shida ya umeme Tz inaletwa na ukame, wakati anajua wazi watu wanahongana billions ili kuliua Taifa kupitia bajeti ya Wizara ya Nishati!
Hata akikaa nchini hana jipya. Akae huko huko ili tuparuane vizuri. Kama ni mtu wa maamuzi angeshamtimua Jairo kabla ya giza kuzama siku ile na hayo aliyoyaamua ndio angeamua hata akiwa hapa! Natamani yamkute huko wala asirudi tena!
Kuto tulia kwake nchini kuna nipa shaka kubwa kuwa anatafuta nchi ya kukimbilia maana mwenzaka Mutharika yameisha mkuta na sasa zamu yake. Cameron alirudi England after Phone Hacking ziara zote akatupa kapuni yeye kasikia wabunge wa chama chake walikuwa wanatakiwa kuhongwa alot of Millions naye wala hata kushtuka kuwa ana scandal la umeme na watu wanajifanyia watakavyo yeye kabaki S.Africa huyo ndio leo mi nijivunie ndie Rais wa BongoLand over my Dead Body heshima ya yeye kuwa Rais ina shuka every day kukicha sielewi washauri wake ni akina nani.
My Take : Mr.President doesnt give a damn at all about this TZ ameisha ichoka kabisa anajilazimisha kututalawa na sio kutuongoza na ile kasumba ya kufuata Utawala wa Sheria na Haki huku wakiipindisha sheria kwa manufaa ya wao kubaki hapo madarakani
Kwa kweli mkuu hili la David Jairo na rushwa kwa wabunge ni scandal of un-imaginable proportions.
Serikali, mhimili mmoja wa dola, inapowahonga watunga sheria -wabunge, mhimili mwingine wa dola , hapo tuna kuwa na a constututional crisis.
Je serikali hiyo hiyo ikiingia na kuhonga mhimili mwingine, mahakama , sijui nchi itaelekea wapi?
Hiyo unayoongelea sio meli ya Tanzania hiyo ni CCM na unaweza kwenda kupanda meli ingine kama hiyo unaiona haikufai.
Meli ya Tanzania ni shwari na inahimili mawimbi na dhoruba wala si kama vijahazi.Click to expand.
Chama tawala kinaunda serikali na kinaongoza nchi.Si lazima uchangie kama huna la kuchangia,unajaza post zisizo na hoja na unasababisha urefu wa thread na wengine wanaweza kukata tamaa kusoma hata kama thread ina make sense.Tulia unawashwa mno.Aagh.
jairo alikuwa anafanya kazi za CCM au kazi za serikali . Mwenzae PM wa UK issue ya gazeti imefanaya tu akatishe safari. Yeye issue ya katibu mkuu wake kutoa rushwa tena kwa wabunge anaona powaaa tu.
Kama kule South Africa anawataka wawekezaji waje kuwekeza wakati nchi yake ipo gizani!!. Hai-sense hata kidogo, mwenzake David Cameron alikatiza ziara akarudi nyumbani kushughulikia matatizo ya nchi yake.
Vita ya MAGAMBA Vs MAGAMBA. Hapa patamu sasa maana Lole kashatangaza kabisa kuwa yeye ni MAGAMBA.
''eti miye nikae nyumbani, mle mawe! Natafuta chakula na wingu kubwa nikaweke kwenye mabwawa yote yanayozalisha umeme. Tehe! Tehe! Tehe! Tehe!''
Na inasaidia nini kama boti la magamba na serikali yake vinapigwa mawimbi na mtu anachekelea na kudai kuwa unaweza panda meli nyingine kama unaona haikufai?
Uchumi na Biashara : Ongezeni kasi katika Uwekezaji na Uzalishaji wa Bidhaa Zenye Ubora - Samia Suluhu - Wazalendo 25 Blog
Home BIASHARA HABARI JAMII Lifestyles MATUKIO UCHUMI Uchumi na Biashara : Ongezeni kasi katika Uwekezaji na Uzalishaji wa Bidhaa Zenye Ubora - Samia Suluhu
Uchumi na Biashara : Ongezeni kasi katika Uwekezaji na Uzalishaji wa Bidhaa Zenye Ubora - Samia Suluhu
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi. Alisema mwaka wa kwanza wa serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi. Alisema serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipohutubia wakati wa hafla ya utoaji waTuzo za Rais za Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 zilizofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Thebeauty)[/caption] Makamu wa rais ambaye katika hotuba yake alikuwa anazungumzia changamoto zinazoikumba sekta binafsi katika kutekeleza wajibu wake, amesema kwamba serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto hizo na imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba zinamalizwa. Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia kero zinazosumgua sekta ili serikali ifanye maamuzi. Kwa sasa kuna kamati inayoangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi Wizara ya Viwanda na inakaribia kumaliza kazi yake na kuikabidhi serikalini. Akizungumza kumkaribisha Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji ili amkaribishe Makamu wa Rais kuzungumza na washiriki katika hafla hiyo,Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Shabbir Zavery alitaja changamoto tisa zinazotia msukosuko ukuaji wa viwanda nchini. Moja ya changamoto hizo ni mabadiliko ya mara kwa mara na ya ghafla ya sera au sheria za kibiashara ambayo huondoa utulivu kwa wazalishaji. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akirejea kwenye meza kuu baada ya kuhutubia wageni waalikwa kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.[/caption] Zavery alisema kwamba ufanisi na utuilivu wa kufanya biashara unategemea sana kutobadilika mara kwa mara kwa sheria na sera za biashara na mwaka uliopita serikali ilichukua maamuzi kadhaa bila kuhusisha sekta binafsi na hivyo kudhoofisha ushirikiano baina ya serikali na wafanyabiashara. Pia alisema kwamba utitiri wa mamlaka za udhibiti na tozo zao mbalimbali pia kufanyakazi zinazofanana na kutembelea viwanda kwa kila mamlaka kwa wakati wake kunachangia gharama za kufanyabiashara. Akizungumzia tatizo sugu la wenye viwanda na wafanyabiashara kutorejeshewa malipo stahiki (Vat na nyinginezo) wanazodai kutoka Mamlaka ya Kodi, na kodi zinazoua ushindani,Makamu wa Rais Samia amesema kwamba serikali kwa sasa imeshatulia na kwamba itaendelea kufanya marejesho kwa mujibu wa sheria na suala la kodi limeshafanyiwa maelekezo na kwamba wahusika wanatakiwa kukutana kushughulikia tatizo hilo. Aidha ameiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha kwamba utekelezaji wa mikakati ya kupunguza kero kwa wawekezaji na wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo. "Nafahamu kuwa sekta ya viwanda imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali. Serikali tunaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha viwanda vyetu vinakuwa katika mazingira rafiki na wezeshi ili kuwaongezea ufanisi na ushindani katika masoko ya kimataifa" alifafanua Makamu wa Rais. Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa CTI, Shabbir Zavery akisoma risala ya Mwenyekiti wa CTI kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.[/caption] Makamu wa Rais alikumbushia maneno aliyotoa katika ziara zake mikoani kwa taasisi za serikali na sekta binafsi kukaa, kujadili na kuona namna ya kuondoa adha katika uwekezaji na ufanyaji biashara bila kuipotezea mapato serikali. Aidha alisema kwamba wakati serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zinazoathiri ukuaji wa sekta ya viwanda, ni muhimi pia kwa wawekezaji na wazalishaji kutambua majukumu yao katika kuchangia juhudi hizo. Alisema majukumu hayo ni pamoja na kuzalisha bidhaa nyingi, zenye ubora na zenye bei rafiki kwa mlaji. "Tusisahau kuwa sekta ya viwanda ina jumkumu kubwa sio tu la kuipatia serikali mapato; bali pia kutoa ajira kupunguza umaskini pamoja na kuijengea nchi heshima kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa kimataifa" alisema Makamu wa Rais. Aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuratibu na kukutana na wizara au taasisi za serikali na za umma nchini ili kuwahamasisha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kama ilivyoanza kwa vikosi vya usalama ambapo wanatakiwa kununua bidhaa zao hapa nchini. Pia amewataka wafanyabiashara kuingia ubia na mifuko ya jamii ili kuwa na mitaji itakayowezesha kuanzisha viwanda kwa pamoja. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga alipokuwa akiwatambulisha wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan kuzungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Nalo shirikisho hilo la viwanda limepongeza uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano kwa kufanya uwekezeji mkubwa katika sekta za kiuchumi zinazotengeneza njia kuelekea katika uchumi wa viwanda. Wametaja uwekezaji huo kuwa katika umeme, barabara,reli, maji na bandari. Katika risala ya CTI kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016, wamesema uwekezaji huo utasaidia kushuka kwa gharama za uzalishaji na hivyo kuongeza ushindani wa wazalishaji wa Tanzania katika soko la ndani na la nje. Akisoma risala hiyo kwa Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa Shabbir Zavery, alisema, pamoja na mafanikio katika miundombinu uwekezaji uliofanywa katika elimu utasaidia kutoa wataalamu wengi wenye tija katika sekta ya viwanda ambayo inategemea kukua kwa kasi katika kipindi kifupi kijacho. Aidha alisema pamoja na changamoto zinazokabili sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji taifa katika awamu ya tano imeshuhudia kukua kwa pato la taifa kwa asilimia 6.75; kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 5.6 mwaka 2015 ukilinganisha na wastani wa asilimia 5.2 mwaka 2016. Mafanikio mengine aliyoyaeleza Zavery ni kuongezeka kwa mauzo ya nje ambapo jumla ya dola za Marekani bilioni 9.38 zilipatikana ukilinganisha na dola za Kimarekani bilioni 8.92 zilizopatikana mwaka 2015.Likiwa ni ongezeko la asilimia 5.2. Aidha katika Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira Bora ya Biashara ya mwaka 2016 Tanzania ilishika nafasi ya 139 ikilinganishwa na nafasi ya 140 mwaka 2015. "Vile vile usimamizi mzuri wa mapato ya serikali umewezesha kuongezeka mapato ya serikali kila mwezi kufikia zaidi ya shilingi trilioni moja ikilinganishwa na shilingi bilioni 900 zilizokusanywa mwaka 2015" alisema. Alisema hata hivyo pamoja na mafanikio hayo ambayo yamepatikana katika kipindi kifupi, kuna changamoto ambazo kwa kiasi zinapunguza kasi ya mafanikio. Mkurugenzi wa Ishara Consultants Ltd, Isaac Saburi, akitoa maelezo mafupi ya vigezo vilivyotumika kuwapata washindi wa Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.[/caption] Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mazingira yasiyo rafiki kwa kufanyabiashara yanayochangiwa na mabadiliko ya ghafla katika sera na sheria zinazohusiana na biashara. Changamoto nyingine ni utitiri wa kodi na tozo , kutorejeshewa malipo stahiki ya kodi ya ongezeko la thamani,ushindani unaozuiwa na kodi ya VAT kwa mali ghafi, upungufu wa makaa ya mawe,vibali vya kazi na bomoa bomoa inayofanywa na kampuni ya reli isiyofuata sheria. Zavery aliomba serikali kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo ili azma ya kuwa na Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2020 inafanikiwa. Katika juhudi za kuhakikisha kwamba kero zinashughulikiwa CTI imeandika waraka ambao umewasilishwa Wizara ya Viwanda ili kurahisisha ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. Katika hafla hiyo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji , Mh. Charles Mwijage alisema kwamba wataendelea kushirikiana na CTI kuhakikisha kwamba vikwazo hivyo vinaondoka. Alisema ipo mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa utitiri wa mamlaka na kodi ili kuhakikisha kwamba viwanda vipya vinaongezeka na vile vilivyopo vinashamiri. Alisema kwa mwaka 2015 hadi 2016 viwanda zaidi ya 2000 vimesajiliwa na mamlaka mbalimbali ikiwamo EPZ, SIDO, NDC na TIC. Amesema kwamba kwa sasa wizara yake imeweka mkakati mahsusi wa kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na katika hili wamepanga kukutana wafanyabiashara mjini Dodoma kutafakari changamoto mbalimbali. Meza kuu ya kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.[/caption] Katika tuzo hizo mshindi wa kwanza wa jumla alikuwa ni Tanzania Breweries Limited, akifuatiwa na Mufindi Paper Mills Company Limited na mshindi wa tatu alikuwa Kioo Limited. Aidha kulikuwa na washindi katika viwanda vidogo vya kati na vikubwa. Mshindi katika safu ya viwanda vidogo wa kwanza alikuwa Alliance Life Assurance Limited kwenye masuala ya fedha na bima na mshindi mwingine alikuwa ni Prisons Corporation Sole katika biadhaa za ngozi na viatu. Kwa viwanda vya kati katika hafla hiyo ambayo mdhamini wake mkuu ni Bank M, mshindi katika ujenzi alikuwa Dharam Singh Hanspaul and Sons Limited; safu ya kemikali mshindi alikuwa Royal Soap and Detergent Industiries Limited; katika nishati ,umeme na elektroniks mshindi alikuwa Tanalec Limited na katika usindikaji wa chakula mshindi alikuwa Chemi Cotex industries limited. Washindi wengine viwanda vya kati walikuwa Ital Shoe Limited katika bidhaa za ngozi na viatu; Chemi Cotex Industries limited katika bidhaa za metali ;Nyanza Mines (T) Limited katika bidhaa za madini; Hanspaul Automechs Limited safu ya magari na vifaa vyake; Tanpack Tissues limited bidhaa za karatasi na makasha na DPI Simba Limited katika safu ya bidhaa za plastiki. Kwa viwanda vikubwa washindi katika nafasi mbalimbali ni Tanzania Breweries limited, Petrolube T limited, Petrofuel T Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Said Salim Bakhressa, Alaf Limited, Kioo Limited, Mufindi paper Mills Company Limited, Jambo Plastics na Nida Textile Mills T Limited. Washindi wa tuzo hizo walipatikana kwa kuzingatia ufanisi katika uzalishaji, mauzo ya nje, uwekezaji katika teknolojia ya kisasa,matumizi bora ya nishati, utunzaji wa mazingira, afya na usalama wa wafanyakazi, uwiano wa kijinsia katika uongozi, pamoja na mchango katika jamii. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi cheti kwa niaba ya ITV na RADIO One kwa kutambua mchangao wao wa kurusha LIVE matangazo ya hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimakbidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso cheti kwa kutambua mchango wao kwa kuwa mdhamini mkuu wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Jacqueline Mengi cheti kwa niaba ya magazeti ya The Guardian Limited kwa udhamini wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo hizo, Teddy Mapunda kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (wa tatu kulia) akiwa amejumuika na marafiki zake, Nancy Sumari Neghesti (kushoto), Nasreen Kareem (kulia) pamoja na Fausta Kameja (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali nchini waliohudhuria hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage walipowasili katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakielekea katika ukumbi wa Marquee kwenye hoteli ya Serena jana jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vya umeme kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi alipotembelea banda la maonesho la Kilimanjaro Cables linalomilikiwa na kampuni hiyo wakati wa kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly ndani ya banda la kampuni hiyo maarufu kwa utengenezaji wa samani za ndani kwenye kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akimsikiliza Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (aliyeketi) wakati akitoa maoni juu ya ubora wa samani hizo za ndani zinazotengenezwa na Kampuni ya Amorette Ltd inayomilikiwa na Bi. Jacqueline Mengi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga wakitia baraka kwenye banda la maonesho la Kampuni ya Amorette Ltd katika kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye banda la maonesho wakati hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh Hanspaul (kushoto) kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru. Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (kulia) akifurahi jambo na rafiki yake Fausta Kameja katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo za CTI, Teddy Mapunda (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kushoto aliyesimama) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kulia) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mshehereshaji wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Bw. Innocent Mungy (wa pili kulia aliyesimama) akifafanua jambo kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso (kulia) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (wa pili kushoto) alipotembelea banda ya kampuni hiyo inayojishughulisha na utengeneza wa samani za ndani (Furniture). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (aliyepo pembeni ya Makamu wa Rais). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi (wa pili kushoto) alipotembelea banda Kilimanjaro Cables wauzaji wa vifaa vya umeme ambao walieleza wako mbioni kufungua kiwanda cha kutengeneza Transfoma za umeme nchini na kuongeza ajira. Kushoto ni Meneja Utawala wa kampuni ya AFRiCAB Group, Kunajal Gina na Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Bodi ya CTI. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake walioshiriki kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Askofu Inacio Saure ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nampula - Radio Vatican
Papa Francisko amemteua Askofu Inacio Saure wa Jimbo Katoliki Tete kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nampula, Msumbiji. - EPA
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Inacio Saure wa Jimbo Katoliki Tete, Msumbiji kuwa Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Nampula Msumbiji. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa Padre Sandro Faedi, kuwa Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Tete, Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Saure alizaliwa kunako tarehe 2 Machi 1960 huko Balama. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa kunako tarehe 15 Mei 1998 akaweka nadhiri zake za daima kwenye Shirika la Wamissionari wa Consolata na kupadrishwa tarehe 8 Desemba 1998.
Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 12 Aprili 2011 akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Tete, Msumbiji na kukwekwa wakfu tarehe 22 Mei 2011 na akasimikwa rasmi kama Askofu wa Jimbo Katoliki la Tete tarehe 5 Juni 2011. Tarehe 11 Aprili 2017 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nampula, Msumbiji.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia walimu wawili na mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekonda Chang'ombe (Mazoezi) kwa tuhuma za kukutwa na mtihani wa kemia wa kidato cha Sita.
Kamishna wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema kuwa wiki iliyopita Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa ofisa wa Baraza la Mitihani, Aron Mweteni kuwa aliwakuta watuhumiwa wakiwa na karatasi ya maswali ya mtihani wa kemia.
Amesema kuwa baada ya kuwatilia shaka na baadae kuwatia mbaroni walifanya ufatiliaji wa awali kwa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambapo ilibainika kuwa mtihani huo ni miongoni mwa mitihani inaofanywa na kidato cha sita.
Kamanda Sirro amewataja watuhumiwa hao kuwa Musa Elius na Innocent Mrutu ambao ni walimu na Ritha Mosha ambaye ni mwanafunzi.
Pia Kamanda Sirro amesema kuwa watuhumiwa hao wanaendelea na mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kwa mujibu sheria.
CCM sasa vurugu tupu, Mukama akiri ni kama NATO na G8 JamiiForums The Home of Great Thinkers
Chama cha Mapinduzi CCM kimekiri kuwa Makundi yanakiuwa chama na ugomvi na vurugu hizo ni sawa na ugomvi wa Nato na G8 na wakati huo huo Maige kamtaja Nape kama gamba sugu linalotakiwa kung'olewa ndani ya chama na Amemtahadharisha Spika Makinda kuwa katika kikao cha Bajeti atasema madukuduku yake yote yanayomsumbua.
Nchi zinazounda G8 ni Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Russia na Uingereza ambazo pia baadhi yao, ndizo zinazounda Nato, umoja wenye wanachama 28.
Kitendo cha CCM kupoteza wanachama zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja mkoani Arusha na sehemu nyingine wanachama 3,000, kinashitua, na ilitegemewa Nape kusimama imara na kuhakikisha chama hakiendelei kupoteza wanachama wake, lakini ndio kwanza anasema hajali na eti hao ni makapi, alisema kwa kushangaa.
Jamani Nape anachokifanya sasa ndani ya chama mimi ninaweza kuamini kwamba anatumika na kukidhi matakwa ya waliomtuma na si manufaa ya chama.
Ninalolisema hapa lisitafsiriwe kwamba nalilia uwaziri, hapana, ila ni uchungu nilionao kwa chama changu kuona kila siku tunavyopoteza idadi kubwa ya wanachama, tuliyemkabidhi jukumu la uenezi anasema hajali, sasa huyu si atupishe mapema kabla mambo hayajaharibika?
Nasikia ccm wameshaanza kufanyia ukarabati monchwari ya muhimbili kwaajili ya kuweza kuhifadhiwa kwani mazishi ni mbali sana 2015
Nape ameahidi kubaki na gamba hata wakijivua wote, ana uchungu na chama kuliko hata waasisi wake!
Mukama na Nape ni kama misguided missiles ndani ya CCM ni kama wako pale kimakosa hawajui hata wanatakiwa wafanye nini. Ni huyu huyu Mukama alisema makundi ndani ya chama ni uhai leo anasema yanakivuruga chama. Nape naye na kauli za kwenye karatasi anatamka lolote analoona linamjia kichwani kwa furaha ya siku moja hajui kwamba matamshi yake ni ya chama si ya familia yake. In short, hawana tangible strategy yeyote ya kujenga chama kinachobomoka kama tulivyokuwa tunaona enzi za kina Makamba na Mangula.
Ni wakati muafaka saana kwa CHADEMA kujijengwa wakti huu, CCM ikiwa imesambaratika kifikra, kwani hawapo pamoja. Ktk strategic magt, unaangalia weakness za mpinzani wako na capiltalize nazo, Hivyo CHADEMA capiltalize ktk CCM kutoelewana na makundi yao, hata ikibidi penyezeeni watu huko kufuel zaidi. Naona Maige anaenda vizuri ktk hilo.
Ccm wameshindwa kuvuwana magamba sasa waanza kukandamizana masumbwi hapo sawa.kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
Nasikia ccm wameshaanza kufanyia ukarabati monchwari ya muhimbili kwaajili ya kuweza kuhifadhiwa kwani mazishi ni mbali sana 2015Click to expand.
wakiniambia nitoe hela ya ukarabati I will give them i don't want to hear more about mafisdi jamani they are killing our people.
Wakati mtendaji mkuu huyo wa chama tawala akitoa kauli hiyo, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ameibuka na kumshambulia waziwazi, Katibu wa Taifa wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akimtuhumu kukiharibu kwa utendaji mbovu, hivyo kutaka ang'olewe haraka akidai kuwa ni gamba. Nchi zinazounda G8 ni Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Russia na Uingereza ambazo pia baadhi yao, ndizo zinazounda Nato, umoja wenye wanachama 28.
"Makundi yaliyoundwa tangu 2005 na 2010 yanaendelea kukitafuna chama, wanachama wakinyimwa uongozi wanaanza uhasama, hatufiki malizeni makundi," alisema.
"Nikiwa Mkuranga nilitaarifiwa kuwa kuna makundi ya Nato na G8 na sasa nimefika Rufiji nimeyakuta makundi hayo. Jamani makundi hayo ya nini?"
Alitoa mfano wa Chama cha Democrat cha Marekani kwamba wanachama wake hawana kadi, bali mapenzi ya chama yako mioyoni mwao na wanapojiunga hawafanyi hivyo kwa lengo la kusaka madaraka. "Hii ni tofauti kubwa na nchi zetu ambako mtu akijiunga na chama kitu kwanza kufikiria ni kusaka madaraka," alisema.
"Hapana! Chama chetu hakitakubali hali hiyo. Ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu na nchi yetu," alisema na kuongeza kuwa wanachama wa kawaida wanatakiwa kugombea hata kama hawana fedha.
Yaani makundi hadii Rufiji!! Tena makundi mabaya kweli yaani G8 na NATO. Mimi nilikuwa nadhani makundi yako ngazi ya taifa tu kumbe hadi Rufiji na Mkuranga. Mukama anafanya nini sasa kuondoa hayo makundi? Kuishia kusema tu kwamba Baba wa Taifa alisema bila CCM imara nchi itayumba sijui kama kuna tija. Watu siku hizi hawaogopi hata nchi ikiyumba na si lazima iyumbe. CCM inatakiwa ijitakase na iondoe makundi vinginevyo 2015 CCM itakuwa sawa na KANU. Kwa afya na ustawi wa nchi inatakiwa CCM iwepo imara; iwe Upinzani ama Madarakani.
Duniani, maneno political migrants (wahamiaji wa kisiasa), tafsiri yake ni wanaohama nchi zao kutokana na migogoro ya kisiasa.
Inawezekana sababu ikawa vita au sera za nchi zenye kubagua wengine, kundi lenye kubaguliwa linaamua kutafuta hifadhi katika mataifa mengine.
Tafsiri hiyo katika wigo wake ni kwamba wahamiaji wa kisiasa wanaweza kutokana na upinzani wa kisiasa.
Walio madarakani wanawajengea hofu au kuwatisha wapinzani wao kiasi cha kujiona hawapo salama, hivyo kukimbia nchi ili kutafuta hifadhi.
Uhamaji wa kawaida kutoka chama kimoja kwenda kingine hautafsiriwi kuwa ni uhamiaji wa kisiasa. Bila shaka ni kwa sababu dunia haijawahi kushuhudia kokote yale yanayotokea Tanzania kwa sasa.
Ujio wa siasa mpya Tanzania, wimbi la wabunge na madiwani kuhama vyama vyao na kutimkia CCM, ni dhahiri kuwa tafsiri ya uhamiaji wa kisiasa imepanuliwa.
Kwamba pamoja na migogoro ya kisiasa, mvuto wa kiongozi madarakani unaweza kuwa chanzo cha uhamiaji wa kisiasa.
Viongozi wenye dhamana ya wananchi, yaani wabunge na madiwani, waliochaguliwa kwa rasilimali fedha, watu, muda na kadhalika, wanaweza kuhama vyama vyao, kujiuzulu nyadhifa zao, hivyo kuliingizia taifa hasara kwa sababu ya kuvutiwa na kiongozi aliye madarakani.
Uhamiaji huo unafanyika kwenye nchi yenye changamoto lukuki. Huduma za kijamii zina utata. Mbunge ambaye jimbo lake wanafunzi wanaketi chini kwa kukosa madawati, wanafeli mitihani kwa sababu ya uhaba wa walimu na ukosefu wa vifaa vya kufundishia, anajiuzulu kuunga mkono juhudi za maendeleo yaletwayo na serikali.
Mbunge ambaye wajawazito katika jimbo lake wanajifungua katika mazingira magumu, wastani wa vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano ni mbaya, anajiuzulu ubunge, kisha anagombea tena kupitia CCM ili arudi bungeni, wakati gharama za uchaguzi zinatosha kujenga kituo bora cha afya.
Chama tawala ambacho kina mahitaji makubwa ya fedha, kinakabiliana na changamoto kubwa ya kibajeti ili kutimiza ahadi zake za uchaguzi, nacho badala ya kuogopa wimbi la wabunge na madiwani kujiuzulu na kuhama, kwamba linaongeza gharama kwa sababu fedha nyingi zinatumika kugharamia uchaguzi mdogo, ndiyo kwanza kinafurahia.
Chama tawala kinaamua kubadili mfumo wa kupata wagombea, kinawapa upendeleo wanaohama vyama ili wagombee na kutetea viti vyao walivyoviacha baada ya kujiuzulu. Chama tawala kinawapendelea wenye kuhama kuliko wanachama wake halisi kwa kuwapitisha bila kura za maoni.
Hizo ni siasa mpya Tanzania ambazo zinapaswa kuingizwa kwenye kamusi ya kisiasa ili kupanua tafsiri ya uhamiaji wa kisiasa.
Wimbi la wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani kutimkia CCM kama inavyotokea hapa nchini kwa sasa, usipoita ni uhamiaji wa kisiasa, utatumia maneno mengine yapi yenye maana mahsusi?
Wabunge na madiwani wanatangaza wanahama ili kuunga mkono juhudi za Rais kuleta maendeleo. Ni sawa na kusema wao hawajiwezi katika kuwahudumia wananchi na kuwapa maendeleo. Hivyo, wameona Rais ndiye mwenye uwezo wa kufanikisha hili.
Dhahiri wabunge hao na madiwani hawana ubunifu wala maarifa ya kutoa matokeo chanya kwa wananchi.
Wameona bora kupanda basi la Rais Magufuli ili maendeleo yakipatikana wajione ni sehemu ya waliyofanikisha. Kwa kifupi wameona bora wasafirie nyota.
CCM na Rais Magufuli wangeliona hilo vizuri wangebaini kuwa wabunge na madiwani wenye kuhama hawana kipya cha kuongeza kwenye basi la JPM la maendeleo.
Kwa hivyo wangeweza kuwapokea lakini si kuwapa nafasi ya upendeleo ili wagombee tena ili kutetea nafasi zao. Maana hawana jipya.
Upande wa pili ni kuwa wanaohama wanagharimu fedha nyingi za uchaguzi. Je, haiwezi kuwa wanaohama wanatumika kumkwamisha Rais Magufuli? Kwamba wimbi la uhamaji ni kubwa, linateketeza fedha za umma.
Hivyo basi, wanahama ili fedha ambazo zingetumika kuleta maendeleo, zigharamie uchaguzi. Hivyo uhamaji unapunguza kasi ya maendeleo.
Je, haiwezekani wanaohama shabaha yao ni kuichafua CCM ionekane inafanya siasa za dukani? Maana maneno ya wapinzani siku zote ni kwamba wabunge na madiwani wanaohama wanakuwa wamenunuliwa. Kadiri maneno yanavyotolewa ndivyo wimbi la uhamaji linavyokolea.
Je, wanaohama hawana lengo la kuivuruga CCM? Maana wanapewa nafasi ya kugombea kwa upendeleo. Je, wana CCM wazoefu wanafurahia hali hiyo?
Isije ikawa mpango wa wanaohama ni kuwafanya wana CCM wazoefu kujiona hawathaminiki, hivyo wakasirike na kukiasi chama chao.
Wanaohama wanampenda kweli Magufuli na wanaungana naye kuleta maendeleo au wanajisalimisha baada ya kuona maisha yao ya kisiasa wakiwa upinzani yamejaa giza totoro?
Wanaona Uchaguzi Mkuu 2020 hawatashinda, kwa hiyo wanaamua kudanganya kumuunga mkono JPM kumbe wanajisalimisha wapate mbeleko 2020. JPM awaze hayo, isije ikawa ni chungu iliyopakwa tamu.
Chadema imekimbiwa na wabunge saba katika majimbo ya Ukonga, Siha, Babati Mjini, Serengeti, Ukerewe, Mon-duli na Simanjiro.
MACHAFUKO NCHINI KWENYA: UKABILA AU MAPAMBANO YA KITABAKA (MAKALA NDANI YA GAZETI LA MTANZANIA) ~ Kulikoni Ughaibuni
Miongoni mwa adha za kumiliki runinga hapa Uingereza ni kuilipia ada ya leseni (TV Licence Fee).Ada hiyo kwa kiasi kikubwa hutumika kuendesha BBC ambalo ni shirika la utangazaji la nchi hii.Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika kwamba baadhi ya vipindi vya BBC havina ladha inayoweza kuhalalisha shirika hilo kuendelea kupewa ruzuku inayotokana na ada ya leseni za runinga.Hata hivyo,BBC imeendelea kuwa shirika la habari maarufu na lenye mtandao mkubwa sio tu ndani ya Uingereza bali duniani kwa ujumla.Na miongoni mwa vipindi maarufu vya shirika hilo la habari ni Newsnight,kipindi kinachoonyeshwa siku za wiki kuanzia saa 4.30 usiku.
Kipindi hicho huchambua habari muhimu zilizojitokeza katika siku husika ndani na nje ya nchi hii.Hivi karibuni,Newsnight ilizungumzia machafuko yanayoendelea nchini Kenya.Kwa hakika ilikuwa inatia uchungu kuona namna watu wanavyotaabika nchini humo.Moja kati ya mambo yaliyolinisikitisha zaidi ni mahojiano mafupi kati ya mtangazaji wa BBC aliyeko nchini Kenya na mwanamama mmoja ambaye wakati wa mahojiano hayo alikuwa kamanda wa polisi wa eneo flani (jina la afande huyo na mahala alipokuwa anaongoza vimenitoka kidogo).
Kamanda huyo alianza mahojiano hayo kwa kukanusha madai kwamba jeshi la polisi la Kenya limekuwa likiuwa raia wasio na hatia katika kutekeleza sera ya "piga risasi kuua" (shoot-to-kill policy).Alidai kuwa wanachofanya wanausalama ni kudhibiti machafuko na uhalifu.Mwishoni mwa mahojiano,afande huyo alieleza uchungu alionao kuona nchi yake ikiteketea.Alisema kwamba ameshatembelea sehemu nyingi duniani na kuona watu wa nchi hizo wakiwa na fahari na nchi zao,jambo ambalo lilimwongezea mapenzi kwa nchi yake.Aliwalaumu wanasiasa wa Kenya kwa kuzorotesha jitihada za kuleta amani.
Cha kusikitisha ni kwamba kamanda huyo aliyeonekana kuguswa sana na madhila yanayowakumba Wakenya wenzie aliondolewa kwenye usimamizi wa operesheni za mitaani na kukabidhiwa majukumu ya kiofisi (desk job).Yaani aliadhibiwa kwa kusema ukweli wa moyoni mwake kuhusu namna wanasiasa wanavyoendekeza maslahi yao kuliko ya nchi na wananchi.Naamini mwanamama huyo ni mmoja tu kati ya askari wengi ambao wanalazimika kupiga na hata kuua Wakenya wenzao katika kutekeleza amri "halali" za serikali.
Ilielezwa katika kipindi hicho cha Newsnight kwamba licha ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge mwezi Desemba mwaka jana kuwa chanzo kikuu cha machafuko hayo yasiyoonyesha dalili ya kupungua,msingi wa matatizo ulijengwa miaka kadhaa iliyopita.Kwa mujibu wa uchambuzi wa wajuzi wa siasa za Kenya,kwa muda mrefu kumekuwa na manung'uniko miongoni mwa baadhi ya makabila kuhusu umiliki wa njia za uchumi ambapo inadaiwa Wakikuyu wamekuwa na upendeleo zaidi.
Tofauti za kikabila na kidini ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya machafuko sehemu mbalimbali duniani hususan barani Afrika.Lakini tofauti hizo hustawi vizuri zaidi mahala ambapo kuna manung'uniko kuhusu haki na usawa hasa katika uchumi.Ni rahisi kumshauri fukara aingie mtaani "kujikomboa" kuliko kumshawishi mtu afunge biashara zake akashiriki maandamano.Pia ni vigumu kwa watu wa makabila au dini tofauti wanaoshirikiana katika ajira na utoaji au upokeaji huduma kuanzisha vurugu ambazo kwa vyovyote zitapelekea kuathiri mahusiano yao (kwa mfano, mahusiano kati ya mfanyabiashara na mteja au mwajiri na mwajiriwa).
Tofauti na nchi kama Uingereza ambapo mvuto wa kisiasa miongoni mwa wapiga kura uko chini hasa kwa vijana,wengi wetu tulishuhudia namna kampeni za uchaguzi nchini Kenya zilivyogusa karibu kila sehemu ya maisha ya Wakenya,kama ambavyo chaguzi zetu huko nyumbani zinavyokuwa na mvuto mkubwa.Ni dhahiri kwamba amani ingeshapatikana iwapo nguvu nyingi zilizotumiwa na wanasiasa wa Kenya na vyama vyao kushawishi wapiga kura zingeelekezwa pia kwenye kutafuta mwafaka katika vurugu zinazoendelea.
Ni vigumu kubashiri namna gani vurugu hizo zitadhibitiwa na kumalizwa kwa vile Kibaki na Raila wanaonekana kutokubaliana katika njia sahihi za kuleta amani.Yayumkinika kusema kwamba hakuna uwezekano wa Kibaki na serikali yake kukubali mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huo kwa vile kwa kufanya hivyo watakuwa wameongeza nguvu kwenye hoja za Raila na wafuasi wake kwamba matokeo ya uchaguzi huo ni feki.
Kwa upande mwingine,Raila anafahamu gharama kubwa ya maisha na mali wanayoipata wafuasi wake kwa kupinga matokeo ya uchaguzi huo,na kukubali kushirikiana na Kibaki pasipo makubaliano ya kutengua ushindi wa rais itakuwa ni sawa na usaliti wa daraja la kwanza.Historia nayo haitoi matumaini ya amani kwa jirani zetu wa Kenya kwani hakuna rais yeyote (hasa barani Afrika) anayeamini alishinda uchaguzi kwa njia halali aliye tayari kukubali uchaguzi urejewe kwa minajili tu ya kuridhisha wapinzani wake au kutuliza machafuko nchini mwake.
Madhara ya muda mrefu ya kinachoendelea nchini Kenya ni kuzaliwa kwa kizazi chenye kinyongo.Ni kipi kinachoweza kufuta kinyongo cha mtoto aliyepoteza wazazi wake katika machafuko hayo?Kibaya zaidi ni kwamba kadri machafuko yanavyoendelea ndivyo kizazi hicho cha kinyongo kinavyozidi kuongezeka.
Miezi michache iliyopita Watanzania walitoa maoni kuhusu wazo la kuunda muungano wa nchi za Afrika Mashariki,na wengi wao walipinga uharakishaji wa muungano huo.Ni kama walifahamu kwamba kelele za kuwa na muungano zilikuwa za kisiasa zaidi kuliko kuzingatia hali halisi ndani ya nchi husika. "Mikoa" ambayo ingeunda "nchi" hiyo (yaani sie na Uganda,na pengine Burundi na Rwanda) imeshindwa kuwa na mchango wa maana wakati "mkoa mwingine" (Kenya) unazidi kuteketea.Sijui ingekuwaje iwapo haya yangekuwa yanatokea ndani ya muungano huo!
Baadhi ya wapinzani wa muungano huo walieleza bayana kwamba japo wanafahamu umuhimu wa ushirikiano,au hata kuungana kisiasa,ukweli unabaki kwamba nchi husika zina matatizo yake lukuki ambayo yanapaswa kushughulikiwa kwanza kabla ya kuyakuza kwa kuunda "nchi" kubwa zaidi iliyojaa vipande vyenye matatizo binafsi.
Jeuri za wanasiasa wa Kenya kutosikiliza vilio vya wananchi wao na kupuuza jitihada mbalimbali zinazofanywa na wasio Wakenya ni onyo muhimu kwa wenye ndoto za ya muungano wa Afrika Mashariki kwamba kama wanashindwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na wananchi wao watajali vipi maslahi ya Watanzania au Waganda.
Kubwa la kujifunza katika sakata hili ni jinsi ilivyo amani iliyojengwa kwa miaka miongo kadhaa inavyoweza kuyeyuka ndani ya kipindi kifupi kabisa.Harakati za kumfukuza mkoloni nchini Kenya zilichukua miaka mingi na kugharimu maisha mengi.Wakenya walikuwa bado wako katika harakati za kupata uhuru wa kweli hadi wakati machafuko yanaanza nchini humo.Kinachoendelea sasa ni sawa na kusigina jitihada na damu za mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo.
Kwa Watanzania,wakati tunaendelea kuwaombea jirani zetu amani (yaelekea hakuna la ziada tunaloweza kufanya zaidi ya hilo) ni muhimu kutambua kwamba amani na utulivu tulionao unaweza kudumu milele iwapo tu jitihada za makusudi zitafanyika kuondoa umasikini,kuhakikisha pato la taifa linatumika kwa maslahi ya wote na "haki" kuwa haki ya kweli kwa kila Mtanzania bila kuangalia tabaka.Kelele dhidi ya ufisadi na mafisadi ni sehemu muhimu ya harakati za kuhakikisha amani na utulivu nchini inadumu milele.
1 Day Ago Posho za madaraka wakuu wa shule, maofisa elimu kata ziinue ubora wa
Dar es Salaam. Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amekutana na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho ya alichozungumza na Rais John Magufuli.
Haraka kulinganisha safu mbili ili kuchagua / kivuli duplicate au maadili ya kipekee katika Excel
Kwa kawaida, unaweza kutumia kazi ya kupangilia masharti ili kujua tofauti kati ya safu mbili za Excel. Lakini ni ngumu sana kutumia. Kutools kwa Excel'S Chagua Same na Masiko tofauti utumishi unaweza kukusaidia urahisi kuchagua au kivuli duplicate au maadili ya kipekee kulingana na kila safu au seli moja katika Excel.
1. Weka CTRL ufunguo wa kuchagua safu mbili ambazo unataka kulinganisha kama ifuatavyo (Ona Screenshot). Kumbuka: Huduma hii itachagua marudio katika Kipengee A. Unaweza kutaja Rangi A na Rangi B katika vitabu tofauti na vitabu vya kazi.