content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
Shughuli hiyo imefanyika kwa lengo la kuonesha njia vijana kufikia malengo yao na kuinua jamii inayowazunguka. Bucha yake ipo katika stendi ya mabasi ya Ngerengere, Morogoro.Akizungumza wakati wa ukarabati wa bucha hiyo, Ofisa Mauzo wa Airtel, Aminata Keita alisema: “Airtel tunajali sana jamii yetu inayotuzunguka hivyo tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, ukosefu wa mtaji wa kuanzisha biashara zao na mambo mengine mengi.”Aliongeza: “Msaada wetu kama wafanyakazi wa Airtel ni kuunga mkono mpango wa kampuni yetu ya kusaidia vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel Fursa katika kusaidia vijana wetu kwa kuwaonesha njia ili waweze kuinua jamii inayowazunguka na kufikia ndoto zao.”“Leo (jana) tuna furaha kubwa kuona kwamba tumeweza kumfikia na kumwezesha kijana huyu mjasiriamali aliyewezeshwa na Airtel Fursa ambaye Airtel Fursa imebadilisha maisha yake kwa kukarabati paa la bucha yake, kutengeneza sakafu kwa kuweka marumaru za kisasa, na matengenezo mengine mengi ambayo yameipa bucha yake mtazamo mpya kabisa,” alieleza.Wiki ijayo, Airtel Fursa itamalizia kwa kumwekea vifaa vya kisasa vikiwemo vifaa vya kukatia nyama, jokofu la kisasa la kuhifadhia nyama na vifaa vingine vinavyohitajika kwa kazi za bucha. Vifaa hivyo na gharama za utengenezaji vimegharimu Sh milioni tisa.Wakati wa shughuli hiyo ya makabidhiano, wafanyakazi wa Airtel walijiunga na wakazi wa Ngerengere ambao walijitokeza kumuunga mkono Mikidadi kwa kuwa na nidhamu kwa jamii inayomzunguka akiwa ni mfano wa kuigwa na vijana wenziwe.Mikidadi alishukuru Airtel kwa kumpatia fursa hiyo kwani vijana wengi wanahitaji msaada kama huo, lakini amepata nafasi yeye. “Bila kuwasahau nawashukuru sana wafanyakazi wa Airtel kwa kusaidia ukarabati wa bucha yangu kwani mtazamo huu mpya na vifaa vya kisasa utasaidia kuhamasisha wateja wangu na wale ambao hawakuwa wateja wangu,” alisema.
uchumi
MENEJA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Kati, Stella Rutaguza ameonya kampuni zinazofanya biashara ya bima na kuzitaka kuacha tabia ya kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na Serikali.Rutaguza ametoa onyo hilo katika kikao kilichokutanisha TIRA na mameneja na wawakilishi wa kampuni, zinazofanya biashara ya bima katika mikoa ya Kanda ya Kati ambayo ni Morogoro, Singida, Tabora na Dodoma.Amesema hatua ya baadhi ya kampuni kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na serikali, kinaathari za kijamii na kiuchumi na kuwa kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya fani hiyo na pia kinyume na sheria na taratibu za bima.Rutaguza amesema mamlaka yake, imebaini baadhi ya kampuni za bima kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na serikali, ikiwa ni kuvutia wateja na kufikia malengo waliyowekewa na kusisitiza kuwa Mamlaka itachukua hatua kali kwa kampuni ambazo zitabainika kufanya hivyo kwani huo ni uhalifu.“Huwezi ku-bargain kwenye ada za bima kama vile unauza shati dukani au kwenye mitumba, kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya fani ya bima.“Suala la kutoa ada za bima chini ya kiwango, ni hatarishi kwa sababu linaathiri kampuni za bima kwani zitafika mahali ambapo zitashindwa kumudu majukumu yake ya msingi ya kulipa madai ya bima na kulipa fidia maana itakuwa na mtaji chini ya kiwango kinachotakiwa.“Mbaya zaidi ni kuwa watu walionunua bima kwenye kampuni hizi watashindwa kulipwa madai yao pindi panapotokea matatizo na hapo tatizo la kuanza kuzungushana linaibuka, suala hili linaathari za athari za kijamii na kiuchumi na ndio maana sisi kama mamlaka tunakemea tabia ya kulipa ada za bima chini ya kiwango.”amesema.Rutaguza alisema wafanyabiashara wa bima, wanapaswa kukumbuka kuwa viwango hivyo vimewekwa baada ya kufanyiwa tathimini ya tahadhari ya majanga nchini.Aidha, Rutaguza alisema katika kaguzi wanazofanya, pia wamebaini baadhi ya kampuni za bima, mawakala na madalali wa bima ambao wamekuwa wakiuza bima ambazo hazilingani na aina ya gari.“Kuna utakaowakuta wameweka stika ya binafsi kwenye gari ya biashara, kwa mfano gari ambalo linabeba abiria linatakiwa linunuliwe bima ambayo inawalinda mpaka abiria kulingana na idadi ya abiria ambapo kila abiriwa anakatiwa bima ya shilingi 30,000 kwa mwaka na si ya gari pekee.Akichangia, Charles Balisidya ambaye ni dalali wa bima katika Kampuni ya Bima ya Phonex, aliiomba TIRA kufanya ukaguzi wa kina katika ofisi za kampuni, mawakala na madalali wa bima ili kuwabaini wale wanaolipa ada za bima chini ya kiwango.“Kuna baadhi ya kampuni kwa kutaka kuvutia wateja wamekuwa wakipunguza ada za bima hata mpaka nusu ya bei halisi lakini wamekuwa wakiingiza taarifa sahihi kwenye mfumo wa TIRAMISS. Tuwaombe TIRA wafanye ukaguzi wa kina katika suala hili” alisema.
kitaifa
Katika mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Msuva alikuwa mwiba mchungu kwa Botswana na mabao yake hayo yaliipa Stars ushindi wa mabao 2-0.Kwa matokeo hayo, Stars imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kukwea kwenye viwango vya Fifa. Msuva alianza kupeleka shangwe kwa mashabiki wa soka nchini katika dakika ya sita, alipofunga bao la kuongoza akiunganisha pasi ya Mzamiru Yassin kabla ya kuujaza mpira wavuni.Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, Msuva aliiandikia Stars bao la pili katika dakika ya 62 baada ya kuunganisha vyema pasi ya kichwa kutoka kwa Shiza Kichuya. Katika mechi ya jana, timu hizo zilishambuliana kwa zamu ambapo kuna wakati Botswana walikuja kasi na nusura wapate bao mara kadhaa.Hata hivyo, Stars jana ilikuwa na nafasi ya kupata mabao zaidi, hasa dakika ya 59, mshambuliaji wake Mbwana Samatta anayecheza soka ya kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji nusura apate bao, lakini akiwa na kipa wa Botswana, Mwampule Masule shuti lake lilidakwa.
michezo
['Real Madrid inawafuatilia winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19 na mshambuliaji wa Norway wa miaka 19- Erling Braut Haaland, anayechezea Red Bull Salzburg. (El Desmarque, via Mail)', 'Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner,23 ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. (Express)', 'Manchester United inajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 19, licha ya tetesi kuwa Barcelona inamtaka. (Sun)', 'Newcastle United inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Nigeria wa miaka 20 Victor Osimhen. (Chronicle) ', 'Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka mshamsmbuliaji wa Ufaransa wa miaka 33, Olivier Giroud, ambaye hajafurahishwa na hatua ya kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza aendelee kusalia Stamford Bridge. (Telegraph)', 'Chelsea imemuongeza mchezaji wa safu ya kati wa Atalanta na Ukraine Ruslan Malinovskyi, 26, katika orodha ya wachezaji amabao huenda wakahamia klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Express) ', 'Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 28, anasema angelijiunga na Everton msimu huu lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hakuridhishwa na ofa aliotolewa na klabu hiyo. (Het Laatste Nieuws, via Mirror)', 'Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, anapanga kurejea katika ligi kuu ya ya England baada ya kupona jereha la mguu katika mechi ya klabu hiyo dhidi ya Sheffield United siku ya Jumatatu. (mail)', 'Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman angependelea kuwa msimamizi wa klabu ya Barcelona siku moja na anasema kuwa mkataba wake una kifungu cha sheria kinachomruhusu kuajiriwa na baada ya mashindano ya Ulaya mwaka 2020, amesema mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la kandanda la Uhuolanzi, Nico-Jan Hoogma.(Fox Sports, via Marca)', 'Manchester City inajiandaa kumlipa Raheem Sterling kitita cha £450,000-kwa wiki ili kukatiza azma ya Real Madrid ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza wa miaka 24. (Star)', 'Paris St-Germain itamenyana na Real Madrid kujaribu kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Mail on Sunday)']
michezo
GOLIKIPA wa Azam FC, Razak Abalora amesema anaamini siku zote kuwa yeye ni mshindi licha ya kukosa penalti ya mwisho kwenye mchezo wa jana, huku kipa wa Simba Beno Kakolanya akisema alishajiwekea uhakika kwenye penalti tano, lazima aokoe mbili au moja.Makipa hao timu zao zilikutana juzi katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Amaan Zanzibar, ambapo Simba ilifuzu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa suluhu.Akizungumza Abalora alisema anaamini yeye ni mshindi, licha ya kukosa penalti ya mwisho na kuifanya timu yake kuachia kombe, kwani ilikuwa bingwa wa msimu uliopita.“Nilikosa penalti lakini naamini mimi ni mshindi kwenye mchezo ule, kwani nilipangua penalti mbili pia,” alisema Abalora.Naye Kakolanya ambaye aliibuka shujaa kwa kufuta penalti ya golikipa mwenzake wa Azam FC alisema alijiwekea malengo ya kupangua mbili au moja na akafanikiwa.“Nilishajiwekea uhakika,kwenye penalti tano, lazima niokoe mbili au moja,” alisema Kakolanya ambaye alifanikiwa kupangua penalti moja ya kipa wa Azam FC wa kuipatia Simba ushindi.Katika mchezo huo ambao ulianza saa 2:15 juzi penalti za Simba zilifungwa na Erasto Nyoni, John Bocco na Jonas Mkude na Azam FC zilifungwa na Yakubu Mohamed na Bruce Kangwa.Waliokosa kwa Simba ni Sharaf Shiboub na kwa Azam FC walikosa ni Idd Kipagwile, Donald Ngoma na Razak Abalora. Simba fainali inakutana na Mtibwa Sugar, ambayo iliiondoa Yanga kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1, ambao unatarajiwa kuchezwa kesho.
michezo
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens, Bakari Shime amesema wanataka kuweka historia mpya katika michuano ya chalenji ya Afrika Mashariki na Kati kwa kuchukua kombe kwa mara ya tatu mfululizo.Michuano hiyo itakayoshirikisha nchi nane za Afrika Mashariki na Kati inatarajiwa kutimua vumbi kuanzia kesho kwenye viwanja vya Azam Complex Chamazi. Timu zitakazoshiriki ni Tanzania, Burundi, Djibouti, Zanzibar, Sudan Kusini ,Kenya, Uganda na Ethiopia.Michuano hiyo inasimamiwa na Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na hii ni mara ya tatu inafanyika. Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Shime alisema wamejipanga kubakisha kombe hilo walilolitwaa mara ya mwisho mjini Kigali, Rwanda na hivyokuhimiza watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwa sehemu ya historia hiyo.“Tunajua sio rahisi ila tumejipanga katika ugumu huo kuchukua kombe hilo mfululizo, kila mtanzania ajitokeze uwanjani awe sehemu ya historia tunayokwenda kuiweka katika michuano hiyo,” alisema.Alisema maandalizi yao yamemalizika na kwamba wako katika matayarisho ya mwisho kuweka miili ya wachezaji vizuri kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan Kusini utakaochezwa kesho Chamazi. Mmoja wa wachezaji wa kikosi hicho Fatma Isa ‘Fetty densa’alisema kutokana na maandalizi waliyofanya muda mrefu ana imani watafanya vizuri kwasababu wako katika morali ya hali ya juu.“Tumejiandaa vizuri, tuko katika morali ya kutosha watanzania wategemee matokeo mazuri kutoka kwetu, yeyote atakayetokea mbele yetu tuko tayari kwa mapambano, muhimu watanzania waje kutuunga mkono kama wanavyofanya kwa wanaume kwa kuwa tunaweza,” alisema.Tanzania imepangwa kundi moja na Zanzibar, Sudan Kusini, Burundi na Djibouti. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya ndani ya michuano hiyo, Athumani Nyamlani maandalizi yote yamekamilika na timu zote shiriki zimeshawasili.“Mpaka leo (jana) saa 12 jioni ndio timu ya mwisho Zanzibar imewasili, kwa hiyo maandalizi yapo vizuri na tunatarajia kuwa na mashindano mazuri na yenye msisimko,” alisema Nyamlani ambaye ni makamu wa rais wa Shirikisho la soka Tanzania, TFF.
michezo
WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema mtandao wa ufisadi kwenye miradi ya maji una mizizi mirefu kuanzia ngazi za wilaya, halmashauri, mkoa hadi wizarani, jambo linalofanya miradi ya maji kutekelezwa kwa gharama kubwa.Aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akishuhudia utiaji saini wa miradi sita ya maji kati ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na wakandarasi mbalimbali itakayogharimu jumla ya Sh bilioni 114.Amesema pia kuwa kuna miradi mingine ya maji itaanza kutekelezwa Septemba, mwaka huu katika miji 28 kwa gharama ya Sh trilioni 1.2.Miradi hiyo sita ya maji ni kwa ajili ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa majisafi na salama katika Jiji la Dar es Salaam na miji ya Mkoa wa Pwani.Kukamilika kwa miradi hiyo kutupunguza tatizo la majisafi na salama katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.Waziri Mbarawa ambaye aliongozana na Naibu Waziri wake Jumaa Aweso, amesema mtandao huo wa kifisadi ni mkubwa kwa kuwa unaanzia kwa wahandisi wa maji wa wilaya, unakuja kwenye ofisi za Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri (DED), mkoa, wizarani na hadi katika ofisi ya waziri mwenyewe.Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, ufisadi huo unafanyika kwa kuweka makadirio ya juu ya miradi ya maji ikilinganishwa na gharama halisi inayotakiwa, hivyo kumfanya kila mtendaji katika ofisi husika kuchukua kamisheni yake na matokeo yake miradi hiyo kutekelezwa kwa gharama kubwa.“Wizara ya Maji inakabiliwa na changamoto kubwa mbili, changamoto ya kwanza ni kwa wahandisi wa maji kuweka bei kubwa za miradi ya maji.Aliitaja miradi mingine ya kifisadi kuwa ni ule wa kusambaza maji Sumbawanga Vijijini kwenye vijiji 10.Alisema zabuni ya mradi huo ilipotangazwa, mkandarasi alitakiwa kuutekeleza kwa gharama ya Sh bilioni 3.9 hadi Sh bilioni 6.2 kwa kujenga matangi manane, lakini walipoupitia upya wakabaini kuwa matangi ya maji yaliyohitajika ni matano tu na sasa unatekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 2.5.Miradi mingine ni ule wa Makete ambao ulitakiwa kutekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 5.69 lakini kwa sasa unatekelezwa kwa Sh bilioni 2.5, mradi wa maji wa Tandahimba mkoani Mtwara ulitakiwa kutekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 3 lakini baada ya kupitiwa upya unatekelezwa kwa Sh bilioni 1.6.Baada ya kueleza hayo, Profesa Mbarawa aliwaonya wahindisi wa maji wanaofanya makadirio ya juu tofauti na gharama halisi ya miradi kwa kuwa hatawavumilia.Changamoto nyingine aliitaja ni kuwa Dawasa kushindwa kutekeleza baadhi ya miradi yao wenyewe na badala yake kuikabidhi kwa wakandarasi.Alisema jambo hilo linaongeza gharama kwenye miradi ya maji kwa kuwa mradi ambao Dawasa ingeutekeleza kwa Sh bilioni 3 kwa kuwatumia wataalamu wake yenyewe, inaweza kuutekeleza kwa zaidi ya Sh bilioni 5 inapoamua kumtafuta mkandarasi.Alisema miradi mitano kati ya sita iliyosainiwa jana inatekelezwa kwa fedha za ndani na mradi mmoja unatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.Mwenyekiti wa Bodi wa Dawasa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema miradi hiyo ikikamilika itaweza kuwanufaisha wananchi 1,870,000 wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, lakini pia itasaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 85 hadi asilimia 95.Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema kuwa Wizara imeanzisha huduma ya Wakala wa Maji Vijijini kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa vijijini nao wanapata maji safi na salama.Alisema wahandisi wa maji ambao katika maeneo yao hakutakuwa na maji watafute kazi zingine.
kitaifa
AFC ni moja ya timu kongwe jijini Arusha na ni moja ya timu yenye historia kubwa mkoani humo, lakini ni moja ya timu yenye kucheza Ligi Daraja la Kwanza katika mazingira magumu sana baada ya wadau na mashabiki kusuasua kuichangia timu hiyo.Timu hiyo ya Arusha ni ya wanachana na wanachama wake hawazidi 100 na ni timu pekee naweza kusema kuwa inayopendwa na wakazi wa Jiji la Arusha kuliko timu yoyote, lakini wengi wao hawana msaada kwa timu hiyo.TIMU YA KUSAIDIANAAFC ilianzishwa katika miaka ya 1990 kama timu ya starehe na baadhi ya wadau wa soka jijini Arusha na maudhui yake ni kujikusanya na kufanya mazoezi ya pamoja na kusaidiana kwa shida na raha. Maudhui hayo yalionekana kushika kasi na kufanya wadau wengi kuikubali timu hiyo na kujitokeza kujiunga nayo kutokana na malengo yake yenye tija katika jamii.Uongozi wa AFC uliijenga timu hiyo katika misingi yenye kukubalika ndani ya Mkoa wa Arusha, nje ya Mkoa na hata nje ya nchi, kwani timu hiyo ilikuwa na mahusiano mazuri ya kirafiki na timu ya Malindi ya Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na mfanyabiashara maarufu kisiwani humo, Naushad Mohamed. Mbali ya hilo AFC pia ilikuwa na uhusiano mzuri na timu ya AFC Leopard ya nchini Kenya na Agaza ya Togo, zote ziliwahi kuja Jijini Arusha kucheza michezo ya kirafiki na AFC na timu nyingine ziliandaliwa na wenyeji lengo lilikuwa kudumisha undugu na mahusiano ya dhati kwa timu hizo.Viongozi wa AFC wa kipindi hicho waliwahi kualikwa Zanzibar na mmiliki wa Malindi wa wakati huo na lengo ni kufahamiana na kuisaidia timu hiyo ilipokuwa ikishiriki mashindano ya kimataifa ikiiwakilisha Zanzibar, ambapo kambi iliwekwa Jijini Arusha chini ya uangalizi wa uongozi wa AFC. Hayo yote yalifanyika wakati huo AFC ikiwa timu ya starehe na sio timu ya ushindani wala haikuwa timu ya kushiriki ligi yoyote hapa nchini kutokana na misingi yake.Mikakati na mipango hiyo iliwakuna sana viongozi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA) kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti Alhaji Muhidini Ndolanga na wadau wengine wa soka na kuifanya timu hiyo kukubalika zaidi na wakazi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake. Nyakati hizo Arusha kulikuwa na timu moja ya Daraja la Kwanza ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Kiwanda cha Bia cha Arusha, lakini uongozi wa juu uliamuwa kuvunja timu zote nchini ilizokuwa ikiziendesha, na timu ya Arusha ilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha wa wakati huo.ARFA haikufikiria mara mbili, moja kwa moja ilikabidhi timu hiyo kwa uongozi wa AFC na kuindesha katika misingi na malengo yale yale ya awali na kukubalika zaidi mkoani Arusha na nje ya Mkoa na kufanya vema katika ligi katika muda mrefu kabla ya viongozi waliokuwa wakiiongoza kujiuzulu wote kwa sababu ambazo sihitaji kuzisema kwa sasa kwani sio malengo ya makala hii.Baada ya hapo timu ya AFC haijawahi kukaa sawa hadi leo na imekuwa timu ikiongozwa na baadhi ya viongozi wengi wababaishaji na sio watu wa mpira na wenye kujali zaidi maslahi yao na kufikia hatua timu hiyo kushuka daraja na baadae kupanda na imekuwa timu yenye kuendeshwa kwa stahili ya omba omba kila msimu bila ya kwenda na wakati uliopo. Makala haya imejaribu kuwakumbusha wadau wa soka mkoani Arusha jinsi AFC ilikotoka, ilipo na inakokwenda na tunapaswa kujiuliza kwa sasa hivi, nani ameiroga timu hiyo hadi kushindwa kukaa sawa kama ilivyoanza miaka ya nyuma na nini kifanyike ili timu hiyo ilirudi katika enzi hizo za uongozi bora na timu bora kwa faida ya wote?MFUMO MPYAKwanza kabisa ningependa kuwakumbusha na kuwashauri wanachama na mashabiki wa AFC kuwa uendeshaji wa timu za soka kwa sasa umebadilika sana, hivyo ili timu hiyo iweze kusimama na kutisha kama zamani inapaswa kuongozwa na viongozi wasioitegemea timu, kwani viongozi wa namna hiyo katika karne hii hawahitajiki kabisa. Pili, mfumo mzima wa uendeshaji timu unapaswa kubadilika na kwenda na wakati na ndio maana timu kubwa kama Simba na Yanga zinatoka katika mfumo huo na kuanza kubadilika katika uendeshaji.Tatu, hakuna timu yoyote nchini yenye wanachama inayoweza kufanikiwa kimaendeleo katika karne hii ya sayansi na teknolojia kwa kujiendesha kwa kutembeza bakuli la kuomba omba kwa malengo ya kulipia usajili wa wachezaji, kulipa mishahara, kulipia kambi na gharama nyingine za uendeshaji, hilo halipo.Wanachama wa AFC kwa kauli moja wanapaswa kuchukuwa uamuzi sahihi na kwa wakati sahihi kuondokana na hali iliyopo na kwenda na wakati ili timu hiyo iweze kusimama na kutisha kama zamani, tofauti na hapo tutakuwa tukilaumiana na kushutumiana kuisaliti timu hiyo wakati wasaliti ni wanachama wenyewe.Arusha ni Jiji la kitalii kuna kampuni nyingi za kitalii, wafanyabiashara wa madini ya aina mbalimbali hawawezi kutoa fedha zao hovyo hovyo bila ya kuwa na faida hivyo ni wakati kwa wanachama wa AFC kuamua kuiendesha timu hiyo kisasa kwa kampuni za kitalii, kampuni za madini au mtu binafsi ili waweze kuwekeza kisasa na sio ilivyo sasa.Wanachama wa AFC ndio wenye kisu kwa sasa ama kuimaliza timu hiyo au kuikomboa timu hiyo na wasitegemee miujiza katika hilo kwani soka la sasa kiuendeshaji halihitaji mjadala bali ni uamuzi wa kubadilika na kwenda kisasa zadi tofauti na zamani. Ukiachilia mbali timu za Simba na Yanga zenye wanachama wenye uwezo mkubwa kifedha lakini bado zimekuwa zikiyumba na sasa zimeamua kuondokana na uendeshaji wa kizamani wa omba omba kwa wanachama wenye uwezo kifedha kwa kuwa wameona wazi kuwa waendako wanaweza kukwama licha ya baadhi ya wanachama kupinga mfumo huo.Mwisho nawashauri viongozi na wanachama wa AFC ili timu hiyo iweze kutamba kama zamani haina budi kubadilika kuingia katika mfumo mwingine wa kiuendeshaji tofauti na hapo suala la kulaumiana na kushutumiana litakuwepo na litaendelea kuwepo. Wakati ni huu kwa AFC kuondoka na mfumo wa omba omba na kwenda katika mfumo wa kisasa ili timu hiyo iweze kuwa tishio Arusha na nchini kwa ujumla na hilo linapaswa kufanywa haraka kwa faida ya soka la Arusha na kuwakemea wale wote wanategemea timu hiyo kwa maslahi yao kwani nyakati hizo sio zao tena.
michezo
BODI ya Michezo ya Kubahatisha imesema katika kuhakikisha inadhibiti michezo hiyo imekamata mashine 500 za kamari zilizokuwa zimefungwa maeneo yasiyoruhusiwa na kuruhusu watoto chini ya miaka 18 kucheza michezo hiyo.Aidha, kuna kitengo maalumu cha malalamiko kwa mitandao ya simu inayosumbua watumiaji wa simu kwa kutuma ujumbe maalumu wa kuhamasisha kucheza michezo hiyo ambayo ni starehe.Ofisa Mwandamizi Mkaguzi wa bodi hiyo, Humud Abdul Hussein amesema katika kudhibiti michezo hiyo wamefanya ukaguzi nchi nzima.Alisema mashine hizo zinatakiwa kuwa katika maeneo maalumu, ikiwa ni pamoja na ndani ya baa na si nje, ili kuruhusu watu wazima kushiriki lakini katika maeneo mbalimbali watu walikuwa wakifunga nje ya baa na maeneo ya wazi, hivyo watu wa rika mbalimbali kucheza.Ameitaja mikoa iliyokaguliwa na kukamata mashine hizo kuwa Arusha, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Pwani, Tabora, Kigoma, Lindi, Mtwara, Katavi katika mipaka yote ya nchi na kwingineko.Amesema maeneo ya mipakani kuna tatizo kubwa kwa wageni kufanya biashara hizo za michezo ya kubahatisha bila kufuata sheria na kuondoka katika nchi zao, lakini sasa kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamedhibiti huku wakiendelea kutumia vyombo vya habari kuelimisha umma.Aliongeza kuwa, kwa kutumia mfumo maalumu unaoangalia michezo yote ya kubahatisha wanaweza kuthibiti ikiwa inakwenda kinyume cha sheria kwa wataalamu kufuatilia mifumo hiyo mara kwa mara.Mkaguzi huyo amesema katika kampeni yao ya kuelimisha umma kuwa michezo ya kubahatisha ni burudani na siyo ajira, imesaidia kuondoa malalamiko ya wananchi kudhulumiwa fedha zao kwa kutumia fedha nyingi katika michezo hiyo.Kutokana na wimbi la vijana wengi kujihusisha na michezo ya kubahatisha na kusahau majukumu ya ujenzi wa taifa, hivi hivi karibuni Serikali ikishirikiana na Bodi hiyo imebuni na kutengeneza mfumo maalumu ambao utatumika kudhibiti uchezaji wa michezo hiyo.Pia, mfumo huo utatumika kudhibiti udanganyifu ambao unafanywa na waendeshaji wa michezo ya kubahatisha ili Serikali ipate mapato yake halali kwa kuifuatilia kwa kutumia wataalamu wa teknolojia ya mawasiliano.Ujumbe wa simu Akizungumzia usumbufu wa kutumiwa ujumbe wa simu na michezo ya bahati na simu, mwananchi anatakiwa kwenda katika bodi hiyo na kujaza fomu maalumu ya malalamiko kwa kuonesha ujumbe unaotumwa, kisha bodi hiyo kuwasiliana na kampuni husika.Alisema bodi itawasiliana na wahusika wa michezo hiyo inayosababisha usumbufu kwa wananchi hatua stahili zitachukuliwa huku akibainisha watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kujaza fomu hizo kisha hatua kuchukuliwa.Alisema mara nyingi wanaolalamika ni wale waliowahi kucheza michezo hiyo, au walioingia katika mtandao husika, lakini pia wapo wanaopata usumbufu huo bila kucheza michezo hiyo, bali kuhamasishwa kucheza.
kitaifa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Adelhelm Meru aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa hatua hiyo ni muhimu katika undelezaji wa eneo huru la bandari ya Mtwara. EPZA inaendeleza hekta 10 za eneo huru la bandari ya Mtwara.Hekta hizo ni kati ya jumla ya hekta 110 za eneo hilo huru la bandari ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali. Eneo hilo litaendelezwa kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa na kisha kugawiwa kwa kampuni za kimataifa zinazofanya kazi za kutoa huduma mbalimbali kwa kampuni zinazofanya kazi ya utafiti wa mafuta na gesi katika Mkoa wa Mtwara.Alisema kituo hicho cha huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti wa gesi na mafuta mkoani Mtwara, kitakuwa cha kipekee si kwa Tanzania pekee bali katika ukanda mzima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.“Leo tunahitimisha safari ndefu ya uanzishaji kituo kipya katika bandari huru ya Mtwara ambacho kitahudumia watafiti wa gesi na mafuta,” alisema.Alisema kampuni hizo sasa zitaenda kuanzisha karakana kubwa kwa ajili ya kuzihudumia kampuni mbalimbali zikiwemo British Gas na Start Oil zinazofanya kazi ya kutafiti gesi na mafuta katika eneo hilo.Alizitaja kampuni zilizosaini makubaliano hayo kama Slumberger Seaco Inc ya Marekani, Altus Oil Field Supplies Services ya Singapore, Tans Ocean Industries and Services LTD ya Dubai na Lenna ya Iran.Alisema kampuni hizo ni kubwa na zina uzoefu mkubwa wa shughuli hizo na zimepatiwa maeneo katika eneo la hekta 10 kuanza kujenga na kutoa huduma.“Katika eneo hili watajenga karakana kubwa kwa ajili ya kufanyia ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mafuta na gesi,” alisema.Alifafanua kuwa karakana hizo zitajengwa za kisasa na zitakuwa na uwezo pia wa kuhudumia nchi jirani kama Kenya, Msumbiji, na Afrika Kusini.Meneja Mradi Mwandamizi wa Kampuni ya Altus Oil Field Supplies Services Singapore, aliyefahamika kwa jina moja la Sankaranarayanan, alisema kampuni yake imejiandaa kuanza kufanya kazi ya kutoa huduma kwa kampuni za utafutaji gesi na mafuta.
uchumi
JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) inatarajia kurejesha Tuzo ya Meya Bora, itakayodhaminiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Aidha, ALAT imeweka mkakati wa kujenga jengo la kitega uchumi baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi ndogo eneo la Tambukareli baada ya mwisho wa mwezi huu.Mratibu wa Tuzo ya Meya, Wilman Ndile amesema jijini Dodoma kuwa, uzinduzi wa tuzo hiyo unatarajia kufanyika Juni, mwaka huu katika Jiji la Mwanza.Amesema tuzo hiyo ambayo itadhaminiwa na TSN imelenga kuhamasisha manispaa kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali.TSN ni mchapishaji wa agazeti ya Daily News, Sunday News, Habari- Leo, HabariLeo Jumapili na gazeti la michezo la SpotiLeo.Ndile amesema mchakato wa uteuzi katika mashindano utahusisha umma wa Watanzania ambao watatuma ujumbe mfupi wa simu za mikononi kuteua halmashauri bora, majaji watatembelea manispaa husika kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuchagua manispaa bora.Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulam Mkadam ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga, alisema jengo hilo la kitega uchumi wanatarajia kulijenga karibu na ofisi za ALAT Makao Makuu.Mkadam ambaye alitembelea eneo la mradi ambapo zinajengwa ofisi ndogo, aliwahimiza wanachama wa ALAT ambao ni pamoja na Halmashauri za Jiji, Wilaya na Miji kukamilisha michango yao ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya jumuiya hiyo.“Michango ndiyo itakayosaidia kukamilisha miradi yenye thamani ya Sh bilioni nane wa ujenzi wa jengo la ghorofa nane ambalo litatumika kama kitega uchumi na Makao Makuu ya ALAT,” amesema.Aidha, Mkadam alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa ahadi yake ya kuunga mkono mradi wa ujenzi
kitaifa
UKITAZAMA kwa jicho la tatu, mwenendo wa mbio za marathon za kuwania ubingwa kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Manchester City na Liverpool, ilikuwa patashika ya nguo kuchanika, kwani City ilifanikiwa kubeba ubingwa huo kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mpinzani wake Liverpool.Mfano huo unaweza kuuleta Tanzania na ‘ku-paste’ kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), kwani vigogo wa ligi hiyo, Simba na Yanga walikuwa wanafukuzana kama farasi jangwani kuwania taji hilo.Mpaka ligi inakaribia ukingoni bado kulikuwa na kitendawili juu ya nani ataibuka bingwa kutokana na hesabu zilivyokuwa zikiibeba Simba, lakini uhalisia wa soka ulikuwa umeegemea upande wa Yanga.MABINGWA SIMBA Lakini mwisho wa siku mashabiki wa soka waliishuhudia Simba ikifanikiwa kutetea taji hilo kwa shida na kulinyakua kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufikisha pointi 91, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote huku ikiwa na michezo miwili mkononi. Hiyo ni baada ya kumuacha mpinzani wake Yanga ambaye ana hazina ya pointi 86, ambaye wakati huo alikuwa amebakiwa na mchezo mmoja tu kabla ya kuhitimisha ligi hiyo iliyofikia kileleni Mei 28.Simba tunaweza kusema kilichombeba ni kuwa na viporo vingi, ambavyo pia alijitahidi kuvila vizuri kwa kuondoka na pointi tatu kila alipocheza ukiondoa sare chache na kufungwa mara chache tofauti na Yanga.Pamoja na Simba kufanikiwa kutetea taji lake, lakini vita kubwa ilikuwa kwa timu za kushuka daraja, ambazo zilipambana kufa au kupona huku zingine kama Kagera Sugar ikicheza play-off. Mwandishi wa gazeti hili anachambua mwenendo mzima wa ligi hiyo na ushindano ulivyokuwa hadi Simba kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo.AZAM ILIPEWA NAFASIKabla ya ligi hiyo kuanza timu zilizokuwa zinapewa nafasi kubwa ya kuweza kuleta ushindani mkubwa mbele ya Simba kulingana na maandalizi iliyoyafanya ni Azam pekee. Kila mmoja anafahamu fika Azam ilikuwa miongoni mwa timu zilizowekeza vya kutosha kwa kufanya usajili mzuri wa wachezaji ambao ulitegemewa kuleta ushindani mkubwa mbele ya Simba iliyojizatiti vya kutosha chini ya bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’. Licha ya Yanga kubebwa na jina lake kulingana na historia yake ya kutwaa taji hilo mara nyingi kuliko timu yoyote kwenye ligi hiyo, lakini hakuna aliyekuwa akitarajia kuona Yanga ikileta ushindani kutokana na timu hiyo kutokuwa na mfadhili wala fedha za usajili.UPINZANI WA YANGALicha ya mabingwa hao wa kihistoria kupitia kwenye kipindi kigumu ikiwemo kukosa viongozi na kushindwa kulipa stahiki za wachezaji kwa wakati, lakini walifanikiwa kuleta upinzani dhidi ya Simba na kuongoza ligi hiyo kwa muda mrefu zaidi kuliko timu nyingine 19 zilizoshiriki ligi hiyo.Ni wazi shukurani kubwa zinapaswa kupelekwa kwa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera aliyesimama bila kujali kipindi hicho cha mpito na kuwajenga kisaikolojia kuweza kupambana bila kuchoka na kufanikiwa kuleta ushindani kwa Simba, ambao walikuwa wamefanya maandalizi makubwa kwa kupanga bajeti kubwa na kusajili wachezaji wa maana.Haikuwa rahisi kuona wachezaji wa timu kama Yanga wakidai mishahara ya mpaka miezi mitatu, lakini walionesha kucheza kwa moyo na kujitolea. Hata walipofikia kukata tamaa kabisa bado Zahera alionekana kuyeyusha huzuni na kuibua furaha katikati ya mioyo yao.Mwisho ikaonekana inawezekana, Yanga ikawa tishio bila ‘meno’ na ukisogea vibaya unapigwa nyingi. Yanga haikuwa na wachezaji wengi wa hadhi yao, lakini kwa pamoja ilionesha wao ni nani na muhimu kwao ilikuwa mabao, mengine yanafuata. Kimasihara ikauweka ubingwa wa Simba rehani na kubadili mawazo ya wengi kuwa mwisho wa msimu watarajie lolote, tofauti na ilivyotarajiwa, kwamba Simba itatetea ubingwa kirahisi baada ya Azam nayo kuyumba ilipofika katikati baada ya kucheza muda mrefu bila ya kupoteza mchezo.Muvi imeisha na Yanga imemaliza kwenye nafasi ya pili ikiacha historia kwa ilichokifanya kwa Simba waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kufanikiwa kutetea ubingwa huo, kutokana na usajili wa wachezaji walioufanya na kuweka bajeti ya maana iliyokuwa inasababisha wachezaji wa kikosi hicho kucheza kwa kujiamini muda wote uwanjani. Simba walipewa kila kitu.Mshahara kwa wakati, ‘bonus’ za kutosha na waliishi katika mazingira ya juu ya kama timu kweli inayohitaji kufanya mapinduzi Afrika lakini spidi ya Yanga ilibaki kidogo iyeyushe matumaini yao ya ubingwa na kushika chati za juu kwenye msimamo. Ilifika wakati ilikuwa inaonekana ngumu kwao kuikimbiza Yanga, huku wakiwa na mtihani wa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.Wapinzani wao Yanga walijikuta wakitawala usukani wa ligi hiyo hadi wanafikia utofauti wa pointi 21. Hakika Yanga inastahili pongezi kwa ushindani walioonesha licha ya kuonekana ni timu dhaifu mbele ya Simba msimu huu.AZAM HAIKUWA MBALIUkiachilia mbali Simba, Azam ni timu ya pili iliyokuwa inapewa nafasi ya kuleta ushindani kutokana na usajili walioufanya kujiandaa katika ligi hiyo. Lakini walijikuta kikosi hicho kilishindwa kufikia malengo ya timu na kujikuta wakipoteza michezo kadhaa na kulazimisha sare zilizosababisha kukata tamaa ya ubingwa na kupelekea uongozi wa timu hiyo kuvunja benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm na kikosi hicho kukabidhiwa kwa makocha wa mpito, Abdul Mingange na msaidizi wake Iddi Cheche.Pamoja na mabadiliko hayo, walishindwa kuleta ushindani na kujikuta wakizorota kwenye zoezi la kutwaa ubingwa huo na kuishia kupigania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo ili kulinda heshima yao ambapo wamekalia nafasi ya tatu. Tumezoea kuona Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu zinazofanya vyema ukiachilia Yanga, Simba na Azam ambapo nayo inafuatia lakini wameshindwa kuonesha umwamba wao na kujikuta wakipoteza michezo mingi tofauti na hadhi yao.KMC ni timu ngeni kwenye ligi hiyo lakini imeleta ushindani mkubwa hadi imefanikiwa kushika nafasi ya nne na kujitoa kwenye hadhi ya ‘underdog’ na kuzizidi timu nyingine tano zilizopanda pamoja msimu huu. Timu hiyo sasa itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya Tanzania kupewa nafasi nne, mbili Ligi ya Mabingwa wa Afrika na idadi kama hiyo, Kombe la Shirikisho.Biashara United na JKT Tanzania zilipanda pamoja na KMC mwishoni mwa msimu uliopita, lakini zenyewe zilikuwa zinapambana na hali yao kwa muda mrefu zikigombea kutoshuka daraja. Wengine waliopanda ligi hiyo na KMC ni Coastal Union na Alliance ambao michezo yao ya mwisho ndio iliyozihakikishia timu hizo kutoshuka daraja na sasa wana uhakika wa kuendelea kuwepo katika ligi hiyo msimu ujao.Ya mwisho iliyopanda sambamba na KMC au Kino Boys ni African Lyon ambayo yenyewe ilikuwa ya kwanza kabisa kushuka daraja na sasa inajiandaa na michezo ya Ligi Daraja la Kwanza na maisha yao mengine mapya waliyoyaacha kwa takriban miezi nane tu iliyopita na sasa wanarejea tena huko walikotoka.
michezo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemtaka mwandishi wa Kampuni ya Clouds Media, Abdi Chembeya kufika mahakamani hapo Mei 14, mwaka huu kutoa ushahidi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema).Awali, Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kesi hiyo ilikuja kusikilizwa lakini Hakimu anayeisikiliza, Thomas Simba ana udhuru.Mwita amedai kuwa, shahidi wa upande wa mashitaka aliyetakiwa kutoa ushahidi yupo hivyo aliomba aje kutoa ushahidi.Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala alidai hawana pingamizi na maombi hayo.Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Shaidi alimtaka shahidi kusimama na kumuonya kufika hapo Mei 14, mwaka huu kutoa ushahidi.Hii ni mara ya pili shahidi huyo kufika mahakamani hapo lakini kesi ikashindwa kusikilizwa kwa sababu mbalimbali.Katika kesi hiyo, mashahidi watatu wa upande wa mashitaka wameshatoa ushahidi akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.Katika kesi hiyo, inadaiwa Julai 3,2017 Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli"anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki" kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu amani.Mdee alifikishwa mahakamani hapo kujibu mashitaka Julai 10, 2017.Yupo nje kwa dhamana.
kitaifa
Hayo yalisema juzi jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchumi na Nishati wa Ujerumani, Matthias Machnig wakati ujumbe wa wafanyabiashara wa Ujerumani ulipokutana na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia BRN, Omari Issa.“Ubunifu huu wa utekelezaji wa miradi kupitia BRN ni jambo ambalo hata sisi tunatamani tungekuwa nalo nchini Ujerumani,” alisema Machnig.Katika mkutano huo, wafanyabiashara hao wa Ujerumani walionesha shauku ya kuwekeza katika miradi ya ubia ya BRN ili kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha mageuzi makubwa hasa katika sekta za nishati na uchukuzi yanafanikiwa kwa mujibu wa malengo ya BRN.Akizungumzia kuhusu mfumo wa BRN, Issa aliwaeleza wageni hao kuwa Serikali ya Tanzania iliamua kuanzisha mfumo huu ili kuharakisha utekelezaji wa miradi muhimu ya kitaifa na kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka.Alisisitiza kuwa mfumo wa BRN unaamini katika kuweka vipaumbele na kisha kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake kwa kuondoa urasimu na mtindo wa kufanyakazi kwa mazoea.“Nitawapa mfano wa sekta ya kilimo katika BRN. Tunatekeleza mageuzi katika sekta ya kilimo, lakini si katika kila kitu. Tumeanza na mazao matatu tu ya mahindi, mpunga na miwa tena si nchi nzima bali sehemu tu ya nchi ndiyo tumeanza nayo. Mafanikio yatakayopatikana kupitia vipaumbele hivi yatapelekwa mikoa mingine,” alisema Issa.Aliwakaribisha wawekezaji hao kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwani tayari nchi mbalimbali zimekwishaonesha nia na zimeanza kufanya hivyo.“Treni ya mabadiliko imeanza safari ni juu ya kila mmoja wetu kuwahi ili awe sehemu ya safari hii,” alisema Issa.
uchumi
AZAM FC jana ilishindwa kutamba mbele ya Coastal Union baada ya kuachia pointi zote tatu kwa Wagosi hao kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.Ushindi wa wenyeji Union ulipatikana kupitia bao pekee lililowekwa kimiani na mchezaji wake Haji Ugando na kuinyamazisha Azam iliyoonekana kushindwa kufurukuta kwa muda wote wa mchezo huo.Ugando alifunga bao hilo dakika ya 53 kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Azam, Mwadini Ally, baada ya kutoka langoni kwa lengo la kuondosha mpira huo wa juu. Kabla ya kufunga bao hilo, Ugando alipokea pasi safi kutoka kwa Bakari Mwamnyeto na kuwazidi maarifa mabeki wa Azam.Kwa matokeo hayo, Azam inaendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20 sawa Tanzania Prisons inayoshika nafasi ya nne na Coastal Union imepanda kutoka nafasi ya 11 hadi ya tano.Mchezo huo ulinza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu zikihitaji kupata bao la mapema ili kujikusanyia nguvu na kila upande ulionekana kuwa bora kudhibiti hatari zilizokuwa zinajitokeza, matokeo yaliyowafanya hadi wanaenda mapumziko hakuna mbabe.Kipindi cha pili timu zote zilirejea uwanjani zikiwa na nguvu sawa huku zikifanya mabadiliko ya wachezaji, ambapo mchezo ulibadilika na kutawaliwa na ufundi zaidi sehemu ya kiungo kwa kila timu kujenga mashambulizi kwa kupiga mipira mirefu kutokea pembeni mwa uwanja huo.Kipigo hicho kinaifanya Azam ipoteze mechi ya tatu kwenye ligi. Mechi nyingine ilizopoteza ni dhidi ya Simba na Ruvu Shooting.
michezo
MAMA wa binti wa miaka 17 aliyeeleza jinsi alivyofanyiwa ukatili na mwajiri wake ikiwa ni pamoja na kutumbukizwa mwiko katika sehemu zake za siri, amesema kwamba maagizo wa Polisi wa Chamwino kurejea Dar es salaam, kunafanya ufuatiliaji wa shauri la mwanae kuwa gumu.“Nimefika hapa na kupelekwa Polisi , lakini wanasema nirudi tena Dar es Salaam na mimi ni maskini tu siwezi kurudi Dar es salaam” anasema Rehema Richard , mama mzazi wa binti huyo akizungumza kwa njia ya simu jana. Alisema akiwa Dar es Salaam hakupata nafasi ya kumpeleka mtoto wake hospitali, lakini aliambiwa kwamba amepelekwa na kuwa karatasi zote zinazohusu matibabu anazo mtuhumiwa Happiness Mathew. Pamoja na kwamba Happiness alikuwa mwajiri wa binti huyo, pia wana undugu wa mama mkubwa na mdogo.“Mimi sikuwa nimeajindaa kwa shauri lolote , nilipelekwa Dar es salaam kuhudhuria harusi na kukuta shauri polisi. Nikajiuliza hali ya mtoto wangu ilivyokuwa mbaya nikibaki kuhangaika na kesi si nitauawa na mtoto wangu nani atajua, nikawaambia polisi nitarejea nyumbani tutayamaliza kutoka huko” alisema na kuongeza kuwa alipofika nyumbani hali ya mtoto wake haikuwa sawa, alienda polisi.Alisema akiwa polisi aliambiwa kwamba shauri hilo kwa kuwa limeanzia Dar es salaam wao hawawezi kuendelea nalo lazima aende huko. Mama huyo alisema kwamba kutokana na tatizo la macho kuzidi juzi akisaidiwa na shemeji yake alimpeleka mtoto hospitali ya Misheni ya Mvumi ambako alifanyiwa uangalizi wa macho na kupatiwa mawani. “Tulitumia shilingi elfu 40 kwa matibabu ya macho.Lakini tatizo kubwa ni kichwa kumuuma na pia kukosekana kwa hedhi kwa muda wote huu” alisema mama wa binti huyo. Kwa mujibu wa binti huyo tangu alipowekewa mwiko sehemu za siri amekuwa haoni siku zake na hajui nini kimetokea ndani ya mwili wake. Mama huyo anasema binti yake ambaye alikuwa mrembo kwa sasa hatamaniki kwa makovu kichwani na mwilini na haelewi atasaidiwaje ili kurejea katika hali ya kawaida. Anasema yeye ni mtu maskini kwani mume wake, Musa alifariki mwaka 2017 na sasa anaishi yeye na familia yake akitegemea kilimo.Akizungumza katika kijiji cha Manchali wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma hivi karibuni binti huyo aliyemaliza darasa la saba katika shule ya msingi Manchali mwaka 2016,alisema alichukuliwa na ndugu yake, mtoto wa mama yake mkubwa, Happiness Mathew ambaye ni Mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili akafanye kazi za ndani.Alisema katika maisha yake alikuwa akikutana na vipigo vya mara kwa mara,kwani mwajiri wake huyo akimkuta mtoto analia alikuwa akimpiga. Aidha alisema kuna siku mtoto alikuwa akicheza na akaanguka, aliporudi akamsema kwamba hamuangalii mtoto kwa vile hajui uchungu wa kuzaa na atamfanyia kitu ili asikie uchungu kama huo; ndipo alipompiga na kuchukua mwiko ambao aliuingiza sehemu za siri na tangu wakati huo hajapata siku zake (hedhi) na amekuwa akipata maumivu anapoenda haja ndogo.“Sijui ule mwiko alioniingiza umeleta madhara gani katika mwili wangu naona nisaidiwe ili nifanyiwe vipimo” alisema. Alisema alivunja ungo mwaka 2014 na alikuwa akipata hedhi kawaida lakini baada ya kuingiziwa mwiko haoni kabisa hedhi. Alisema kutokana na mateso Januari 4 mwaka huu, alikimbilia Chang’ombe ambako alilalamikia mwajiri wake huyokutumia mwiko kumpiga kichwani hali ambayo imefanya kichwa kiwe na majeraha yanayofanya ashindwe kuota nywele.Binti huyo alisema alikuwa akilipwa Sh 50,000 mshahara wa mwezi na fedha hizo alikuwa akitumiwa mama yake mzazi moja kwa moja. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Dar es salaam, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Awadhi Haji amesema kwamba kadhia hiyo ya ukatili ipo katika dawati la Jinsia na kwamba wanasubiri hati ya matibabu (PF3) ili kulifikisha suala hilo mahakamani na haki itendeke.
kitaifa
Ushindi huo umefuta ubabe wa Lipuli iliyowasumbua katika mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Dar es Salaam, ambapo walitoka sare ya bao 1-1 lakini pia, iliondoa ile dhana ya kutokufungwa kwenye Uwanja wa Samora.Mabao ya Yanga yalifungwa na Papy Kabamba Tshishimbi na Pius Buswita. Ushindi huo wa Yanga unafikisha jumla ya pointi 31, hivyo, itaendelea kubaki nafasi ya tatu iwapo kama Azam itakuwa imeshinda mchezo wake dhidi ya Ndanda uliotarajiwa kuchezwa jana jioni.Kabamba alifunga bao la uongozi dakika ya 19 akimalizia mpira wa Emmanuel Martin aliyekuwa akijaribu kufunga, lakini ulikokolewa na kipa wa Lipuli, Aghaton Anthony na kumkuta mfungaji aliuejaza wavuni.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga iliyocheza kwa kasi kubwa huku ikijiamini ilikuwa ikiongoza bao 1-0. Bao hilo la ushindi lilipatikana baada ya kuingia kipa chipukizi Ramadhan Kabwili dakika chache kufuatia kutolewa kwa kipa namba moja, Youthe Rostand aliyeumia.Kipindi cha pili licha ya Lipuli kuchangamka walishindwa kuzitumia nafasi kadhaa walizopata lakini Yanga ilitengeneza nafasi ya pili na kuitumia ipasavyo baada ya kufunga bao la pili dakika ya 55 lililofungwa na Buswita aliyepata pasi ya Obrey Chirwa.Hadi dakika 90 zinamalizika Yanga ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0. Hata hivyo, kipindi cha pili walicheza zaidi kwa kujihami huku Lipuli ikishambulia zaidi bila mafanikio.Michezo mingine iliyochezwa jana ni Singida United ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Mwadui, Tanzania Prisons ilishinda 2-0 dhidi ya Njombe Mji na Mbeya City ikishinda ugenini 2-1 dhidi ya Majimaji. Wakati huohuo, Simba leo inashuka dimbani kucheza na Ruvu Shooting jijini Dar es Salaam.
michezo
MAMLAKA ya hali ya Hewa nchini (TMA), imewatoa hofu wananchi kuhusu mvua zilizonyesha kuwa ni za kipindi kifupi zikiambatana na upepo kwa baadhi ya maeneo.Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni, jana, mvua hizo zimenyesha kwa siku moja (jana) na kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutoendelea kunyesha kwa siku zinazofuata. Alisema katika utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 kuanzia usiku wa kuamkia jana, mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara, Dar es Salaam na Pwani, Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba, kutakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.Akizungumza na gazeti hili, Monica alisema mvua zilizonyesha jana, haziko kwenye msimu na kwamba upo uwezekano wa siku ya leo mvua hizo kutokuendelea. “Hizi mvua zimenyesha tuu kawaida na TMA ilitabiri lakini hazitoendelea japo zimeambatana na upepo,” alisema Monica na kufafanua kuwa hata utabiri wa mamlaka hiyo uliopo katika tovuti, unaeleza waziwazi.Kuhusu tovuti ya mamlaka hiyo, alibainisha kuwa kwa mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe, Ruvuma, Morogoro, Lindi na Mtwara, kutakuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua. Kwa mikoa ya Shinyanga, Kagera, Geita, Mwanza Tabora, Kigoma na Katavi, Mara na Simiyu, kutakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua. Utabiri huo ulifafanua kuwa upepo wa pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 40 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa kasi ya kilometa 30 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.
kitaifa
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki.Makonda ameyasema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilometa 300, akiambatana na kundi la watu zaidi ya 600 kutoka fani tofauati wakiwemo wasanii.“Nimeridhishwa na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii,” amesema Makonda.Amesema serikali inataka kuona malengo ya Rais John Magufuli ya kutaka kuona SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.“Nimedokezwa hapa asilimia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huu ni Watanzania, hii ni fursa nzuri, wote mliambatana nami naamini mtakuwa mabalozi wazuri kuzungumzia mradi huu na miradi mingine mbali mbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano,” alisema.Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu Sh trilioni 7.1.Kadogosa alisema mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa kilometa 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu kilometa 300 na unagharimu Sh trilioni 2.7.“Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa kilometa 422 ambacho kinagharimu Sh trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora kilometa 376.5, Tabora hadi Isaka kilometa 162.5 na Isaka hadi Mwanza kilometa 311.25,” alisema Kadogosa.“Utandikaji wa reli umeshaanza hadi sasa zaidi kilomita 15 zimetandikwa. Na zoezi la utandikaji bado linaendelea.”Mhandisi wa mradi kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, Machibya Masanja alisema mradi huo utakuwa na vivuko 17 vya juu na vivuko 15 vya chini sambamba na madaraja.Alisema katika eneo la Soga Mkoa Pwani itakuwa kiungio cha reli hiyo ya umeme ambako reli ya kisasa itapita juu na ile ya kawaida itapita chini.Alisema katika kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, mbali ya kazi ya kutandika reli, kazi nyingine zinazoendelea ni ujenzi wa madaraja, makaravati, kuzalisha mataruma, ujenzi wa miundombinu ya ishara ya mawasiliano na nguzo za umeme.Kwa upande wa mataruma uzalishaji umeanza katika kiwanda kilichopo eneo la Soga mkoani Pwani na kiwanda hicho kinatarajia kuzalisha mataruma 1,200,400 kwa kipande cha Dar es Salaam – Makutupora.Kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro yatazalishwa mataruma 500,100 na kipande cha Morogoro – Makutupora mataruma 703,300.“Mataruma tunazalisha hapa nchini kwa kutumia malighafi kutoka katika viwanda vyetu. Taruma moja lina uzito wa kilo 380 hivyo tunahitaji saruji nyingi na tunapeleka mchango katika viwanda vyetu,” alisema Machibya.Katika eneo la Mzenga na Mlandizi, ujenzi wa makutano ya barabara na reli kuwezesha watu na magari kuvuka kwenda upande mwingine tayari umekamilika ambapo barabara itapita chini na treni juu.Alisema stesheni ziko sita na stesheni kubwa zitakuwa Dar es Salaam na Morogoro wakati stesheni ndogo zitakuwa Pugu, Soga, Ruvu na Ngerengere.“Stesheni zetu zimesanifiwa kwa kufuata mazingira halisi ya nchi yetu, Dar es Salaam itakuwa na umbo la Tanzanite ya Morogoro imechanganywa kwa nyumba za asili na Milima ya Uluguru,” amesema.Hata hivyo, Machibya ame  sema katika Bonde la Mto Ruvu kuna changamoto ya udongo wa mfinyanzi, hivyo wamekata kina cha mita 2.5 kwa ajili ya kuweka mawe na kuboresha udongo ili kujenga tuta imara la reli. Katika eneo hilo pia kutajengwa madaraja sita.Maeneo mengine korofi yako kwenye Milima ya Kilosa ambayo inatakiwa kupasuliwa kuwezesha treni kupita chini.Mkuu wa Kitengo cha Habari TRC, Jamila Mbarouk amesema jumla ya wafanyakazi 6,440 wameajiriwa katika mradi huo ambao Watanzania ni 6,182 sawa na asilimia 96 na wageni ni 258 sawa na asilimia 4.Amesema reli hiyo itakapokamilika itaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hasa katika sekta ya usafirishaji kwani treni moja itakuwa na uwezo kukimbia spidi 160, akitolea mfano Dar es Salaam mpaka Morogoro kufika ni dakika 90 na pia kusafirisha tani 10,000 sawa na malori 500 yenye uzito wa tani 20 kila moja.
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mkongo Heritier Makambo amesema ameamini timu hiyo ni kubwa kuliko wachezaji kutokana na kile alichokishuhudia juzi kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.Makambo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Lupopo ya DR Congo alisema tukio alilolishuhudia uwepo wa mashabiki wengi wakijitokeza kumuaga nahodha wao Nadir Haroub ‘Canavaro’ hajawahi kuona. “Timu hii ya Yanga ni kubwa kuliko sisi wachezaji, nimeshuhudia kitu ambacho sijawahi kukiona, mashabiki wa klabu hii wamenishangaza kwani ni watulivu,” aliandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Instagram.Alisema anawashukuru wote waliojitokeza kwani walichangia kuwapa nguvu na moyo wa kupambana huku akimtakia kila la heri Canavaro katika majukumu mapya. “Nenda nahodha umefanya kile kilichostahili kufanywa na mchezaji mkubwa, najua ni msimu wangu wa kwanza lakini nilichokiona natarajia nitakipata,” alisema. Mchezaji huyo ndio mara yake ya kwanza kucheza kwenye mkusanyiko wa mashabiki wa klabu hiyo tena akiifungia bao 1- 0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu inayocheza Daraja la Kwanza ya Mawenzi.Mbali ya mchezo huo, pia aliifungia timu yake katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu ya kituo cha Tanzanite cha Morogoro katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Ujio wa mchezaji huyo aliyechukua nafasi ya Donald Ngoma huenda kukarejesha matumaini katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten alisema sherehe za kumuaga Canavaro zitafanyika tena kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii ambapo Yanga itacheza mchezo wa kimataifa dhidi ya USM Alger ya Algeria.
michezo
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Ofisa Mkuu wa Biashara Airtel, Arindam Chakrabary alisema wanatoa mikopo ili mawakala wapate fursa ya kukuza biashara zao na kuongeza mitaji.Huduma hii ya mikopo kwa mawakala itawanufaisha mawakala zaidi ya 20,000 nchi nzima. Chakrabarty alikumbusha kuwa mwaka jana walizindua huduma ya Timiza kwa wateja wa kampuni hiyo kwa nchi nzima na wateja zaidi ya milioni 7 waliweza kupata mikopo ya haraka isiyo na masharti.Alisema, “Timiza Mkopo kwa Wakala” itakayotolewa kwa mawakala wa Airtel Money itawapatia uhuru wa kupata mikopo ya haraka isiyo na masharti bila kupitia njia ndefu za kupata mikopo katika mfumo wa kawaida.Msimamizi Mkuu wa Afb Tanzania, Rwebu Mutahaba, alisema mawakala watapata mikopo kulingana na matumizi yao ya simu.“Lengo kubwa ni kuwapatia watu fursa ya kupata huduma ya kisasa na kibunifu ambayoa haijawahi kutolewa kabla. Afb Tanzania tunajivunia ushirika huu na Airtel ambao umetuwezesha kutoa suluhisho kwa wateja wa Airtel, mikopo kwa mawakala ni moja ya huduma nyingi za kibunifu tulizonazo na tunazopanga kuzindua katika mienzi ijayo nchini Tanzania,” alisema Mutahaba.“Timiza Mkopo kwa Wakala” ina viwango na riba tofauti zenye marejesho ya ndani ya siku saba, wiki mbili au mwezi mmoja. Kiasi cha kukopa kitategemeana na matumizi simu ya wakala na jinsi anavyorudisha mkopo wake kwa wakati.Kwa upande wake, kwa niaba ya Katibu Mkuu Hazina, Kamishina Msaidizi Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi alisema Serikali imefurahishwa na hatua walioichukua Airtel katika kuboresha mfumo rasmi wa kifedha kupitia huduma ya Airtel Money.“Tunafurahi kuona huduma ya Airtel Money ikikua kwa haraka na kuwafaidisha Watanzania wa kawaida hususani wanaoishi katika maeneo ya pembe zoni mwa nchi. Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Airtel waendelee kuleta bidhaa na huduma za kibunifu ili kuweza kuipatia jamii huduma bora za mawasiliano na kukuza zaidi huduma za kifedha.”
uchumi
JIMBO la Ruangwa mkoani Lindi linajiandaa kupata kiwanda cha kutengeneza betri za simu.Msaidizi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye masuala ya jimbo, Fadhil Liwaka amesema, kiwanda hicho kitapata malighafi wilayani humo hivyo kushawishi uwekezaji wa viwanda vya simu.“Kwa hiyo ndio kusema kwamba kiwanda hiki cha kutengeneza betri za simu ambacho madini yake yanapatikana Ruangwa kikishaanzishwa tunakwenda kufungua sasa kwanza soko lakini la pili tunafungua viwanda vingine ambavyo sasa materials (malighafi) yake yanaendana na hizi betri zinazopatikana hapa Ruangwa” amesema Liwaka wakati akizungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).“Tumekwishakutenga maeneo ya viwanda tayari, tunakaribisha wawekezaji na kwa wale wote ambao wapo tayari waje kufanya hiyo kazi” amesema.Kwa mujibu wa Liwaka, malighafi kwa ajili ya viwanda si tatizo Ruangwa kwa sababu kuna madini mengi ikiwemo dhahabu, graphite, vito, chuma na shaba, tayari kuna migodi ya madini wilayani humo na uwekezaji kwa ujumla umefikia hatua nzuri.“Lakini pia tunalo soko la madini, soko la mkoa lipo hapa kwa hiyo huduma zote za kimasoko zinazohusu madini zinapatikana hapa. Kwa hiyo wachimbaji wetu wana uhakika wa kuuza madini yao salama kabisa na kwa bei inayoridhisha kulingana na soko linavyohitaji” amesema Liwaka.Amemshukuru Rais John Magufuli kuipa heshima Ruangwa kwa kukubali miradi mikubwa itekelezwe Ruangwa na kuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.“Hatuna cha kumlipa ila wajibu wetu sisi ni kusimama bega kwa bega na yeye, kumuombea dua usiku na mchana lakini pia kumuunga mkono kila hatua anayokwenda, tunampenda sana na tuna imani nae” amesema Liwaka.
uchumi
['Ndoto ya Watanzania kuona raia wa kwanza wa taifa hilo kucheza kwenye makundi ya michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya (Champions League) inaweza isitimie hii leo. ', 'Mshambuliaji na nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kupitia klabu yake ya Genk ya Ubelgiji amefanikiwa kufuzu kutinga hatua ya makundi, lakini hii leo anaweza kuukosa mchezo wa kwanza kutokana na majeraha aliyoyapata hivi karibuni. ', 'Mabingwa wa Ubelgiji Genk watasafiri mpaka Austira kuvaana na mabingwa wa nchi hiyo klabu ya Salzburg katika uga wa Red Bull arena usiku wa leo. ', 'Jumapili ya Septemba 8, Samatta alikuwa akiiongoza Tanzania kwenye mchezo dhidi ya Burundi wa kufuzu makundi ya kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.', 'Japo Tanzania ilishinda mchezo huo kwa mikwaju ya penati, Samatta alipata majeraha ya goti. ', ' Mazungumzo yangu na daktari baada ya vipimo Daktari na karatasi ya kipimo mkononi. daktari- ndugu samatta Mimi- ndio daktari Daktari-majibu yako yanaonesha....... anachukua miwani anavaa anaguna mh Mimi-mapigo ya moyo yanaanza kupanda, tumbo linavurugika,haja kubwa inagonga nguo ya ndani.. Daktari-una bahati sana eneo ambalo lilikuwa karibu kuumia lingekufanya ukae nje sio chini ya miez 6 lakini alijapata jeraha zaidi ya mtikisiko kwaiyo siku chache za mapumziko zitakufanya uendelee kucheza Mimi-shuuuuuuu (nashusha pumzi) sikumbuki niliibana kwa sekunde ngapi. Daktari-kwaiyo unaweza kuendelea na matibabu na mazoez Mimi-asante. So majibu- maumivu sio mkubwa sana na baada ya siku kadhaa nitakuwa tena viwanjani kupambania kombe😂 asanteni wote mliojali na wote mlionitumia meseji za pole🙏 HAINA KUFELI.', 'A post shared by Mbwana Samatta (@samagoal77) on Sep 11, 2019 at 12:46am PDT', 'Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa samagoal77', 'Mara tu baada ya kurudi Ubelgiji alienda kufanya vipimo na kubainisha kupitia ukurasa wake wa mtandao kijamii wa Instagram kuwa hakupata majeraha makubwa japo ametakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda. ', 'Hata hivyo hakubainisha ni kwa muda gani atasalia nje ya uwanja.', 'Ijumaa wiki iliyopita, KRC Genk iliingia uwanjani dhidi ya Charleroi kwenye ligi ya Ubelgiji. Samatta ambaye ni mshambuliaji tegemezi wa Genk hakucheza mchezo huo na wala hakuwepo kwenye benchi la wachezaji wa akiba. Genk ilipoteza mchezo huo kwa magoli 2-1. ', 'Hata hivyo taarifa za kutia matumaini ni kuwa Samatta tayari anafanya mazoezi, na siku mbili zilizopita ametuma video kupitia ukurasa wake wa Instagram akipanda kilima kwa kasi. ', 'Taarifa rasmi ya majina ya wachezaji watakaocheza katika mchuano huo wa leo usiku bado haijatolewa, na itakapotolewa ndipo Watanzania watahakikisha kama Samatta atashuka dimbani leo ama watasubiri mchezo ujao kumuona ndani ya Champions League. ', 'Genk na Salzburg wapo Kundi E pamoja na mabingwa Liverpool kutoka England pamoja na Napoli kutoka Italia. ', 'Takwimu zinaifanya Genk kuwa ndiyo timu isiyopewa kipaumbele kabisa kwenye kundi hilo. Timu hiyo licha ya kushiriki mashindano hayo mara mbili msimu wa 2002-03 na 2011-12 haikuweza kupata walau ushindi hata katika mechi moja kati ya 12 ilizocheza. ', 'Katika misimu yote miwili Genk ilimaliza mkiani kwenye makundi iliyopangiwa. ', ' 🏃\u200d♂️🏃\u200d♂️ 😂 @kelvin.p.john', 'A post shared by Mbwana Samatta (@samagoal77) on Sep 14, 2019 at 10:10am PDT', 'Mwisho wa ujumbe 2 wa Instagram wa samagoal77', 'Ikifanikiwa kupata ushindi leo ama katika mechi zifuatazo watakuwa wamejiandikia historia mpya.', "Kiuhalisia mchezo wa leo ndio utakuwa 'rahisi' kwa Genk, na kibarua dhidi yao kitakuwa kigumu watakapovaana na Liverpool na Napoli. ", 'Ukiachana na Salzburg dhidi ya Genk klabu nyengine zitakazochuana usiku wa leo ni: ', 'Napoli vs Liverpool', 'B Dortmund vs Barcelona', 'Chelsea vs Valencia', 'Inter Milan vs Slavia Prague', 'Lyon vs Zenit St Petersburg', 'Benfica vs RB Leipzig ', 'Ajax vs Lille']
michezo
Hali hiyo inatokana na vyama vya msingi vya mazao ambavyo ndiyo mawakala wa ukusanyaji wa korosho kukosa sifa za kukopesheka na vyombo vya fedha.Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa wilaya hiyo Chiza Marando, alimweleza mwandishi wa habari hii mjini Tunduru juzi kuwa, katika misimu miwili iliyopita wakulima wa wilaya hiyo wamekuwa wakiuza korosho zao kwa mtindo wa soko holela ambapo na msimu wa mwaka huu hali itakuwa kama hiyo kutokana na vyama vya msingi kukosa sifa za kukopa fedha benki.Mtaalamu huyo wa kilimo alisema katika msimu wa mavuno wa mwaka 2012/13 zao hilo lilikumbwa na tatizo la soko hali iliyofanya korosho za wakulima wa wilayani humo kuuzwa chini ya bei dira iliyowekwa na hivyo kupata hasara. Wakulima na vyama vya msingi vya mazao 17 vimepata hasara.Vilikopa fedha ili kutoa malipo ya awali kwa wakulima waliokuwa wamekusanya korosho zao chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani kuingia katika madeni.Alisema vyama hivyo hadi sasa vinadaiwa na benki ya NMB Sh bilioni 2.6 ikiwa ni fedha walizokopa na riba inayokuwa mwaka hadi mwaka, na kwamba kiasi hicho kingeweza kuwa zaidi ya hapo lakini serikali imeingilia kati na kuanzisha mazungumzo baina ya vyama na benki ili riba isiongezeke.Marando alisema serikali wilayani humo imeshachukua hatua kadhaa ili kuviondolea madeni vyama hivyo na hatua iliyopo sasa limefikishwa ngazi ya taifa kuona namna inavyowezekana ili kuwanusuru wakulima na kuuza korosho zao kwa bei ya chini na kwa mfumo ambao tayari ulishapigwa marufuku na serikali.Akizungumzia uzalishaji Marando alisema mwaka huu wamekadiria kuvuna zaidi ya tani 950 ikiwa ni tani 150 zaidi ya mavuno ya msimu uliopita.
uchumi
Imeelezwa kuwa watu hao huenda kinyume na taratibu za wachimbaji wadogo, katika kuchimba na kuuza madini hayo wakifanya hivyo kwa hila bila kutambuliwa rasmi.Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Madini Tanzania, Paul Masanja, ambaye aliongeza kuwa utaratibu huo unaotumiwa na wawekezaji ni wa kienyeji na unalitia Taifa hasara kubwa kutokana na madini mengi kupotea.“Pamoja na wachimbaji hawa kulaliwa na wanunuzi wajanja kutokana na kutojua bei halisi ya madini, pia wamekuwa wakisababisha upotevu mkubwa wa madini yetu, ambapo kwa upande wa dhahabu jumla ya tani 18 hupotea kutokana na utaratibu huo wa kienyeji,” alisema Masanja.Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imeanzisha utaratibu wa kuwatambua rasmi wachimbaji wadogo kwa kuwapatia ruzuku za kujiendeleza kupitia vikundi ambapo hadi sasa wachimbaji 11 wameshapatiwa ruzuku hizo takribani dola 558,000.Aidha alisema kwa sasa Serikali haiwezi kuruhusu wachimbaji hao wadogo kuuza madini kwa kutumia dola ili wapate faida kama wanavyodai kwa kuwa kitendo hicho kitaiua Shilingi ya Tanzania.“Hata hivyo, hili ni soko huria hatuwezi kupangia mtu bei ya kuuza madini kwa kuwa kwa sasa tuna soko huria lakini ili nchi yetu iwe salama, madini hayafai kuuzwa kwa dola,” alisema Masanja.Hivi karibuni akiwa wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, baadhi ya wachimbaji wadogo walimtaka Katibu Mkuu, aingilie kati na kuwasaidia watambulike rasmi katika biashara hiyo ya madini ikiwa ni pamoja na kuruhusiwa kuuza madini hayo kwa dola za Marekani ili wapate faida.
uchumi
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema serikali inalitambua deni la Sh milioni 241 ambalo Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vye Ndege Zanzibar na kuahidi kulilipa. Nditiye aliyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua ni lini serikali italipa deni hilo ambalo ATCL imekuwa ikidaiwa tangu mwaka 2007. “Ni kweli tunakumbuka na kutambua deni la ada ya utuaji ambayo ATCL inadaiwa, deni hilo litalipwa baada ya mamlaka ya ukaguzi ikikamilisha uhakiki, ATCL ilikuwa na madeni mengi ambayo imekuwa ikiendelea kulipa baada ya kufanyiwa uhakiki,” alisema. Aidha kabla ya swali lake la msingi, Jaku aliipongeza hatua ya serikali hususani Rais John Magufuli ya kufuta VAT kwenye umeme kwa Zanzibar. “Tunapongeza hatua ya serikali kufuta VAT kwa Zanzibar kwenye suala la umeme na hatimaye Zanzibar kupata pumzi baada ya kuwa ICU kwa muda mrefu,” alisema. Katika swali la msingi Jaku alitaka kujua ni kwa nini ATCL kila Jumatatu inapoondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma isipitie Zanzibar ili viongozi pamoja na wananchi wanaotaka kwenda Dodoma wapate huduma hiyo. Pia aliuliza, Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa safari za ATCL kutoka Dar es Salaam zipitie Zanzibar kwa Jumatatu zote kupunguza tatizo la usafiri kwa wananchi wa Zanzibar wanaotaka kwenda Dodoma kwa shughuli mbalimbali. Jaku pia aliuliza ni lini safari hizo zitaanza ili viongozi, wananchi na watalii kutoka Zanzibar waone kuwa serikali yao inawajali na inadumisha Muungano. Akijibu maswali ya nyongeza, Waziri Mditiye alisema dhumuni la serikali kupitia ATCL ni kuhakikisha wananchi wote wa bara na visiwani wanapata huduma ya usafiri wa anga kwenye kituo chochote chenye maslahi ya biashara. “Hata hivyo, ATCL inatumia kituo cha Dar es Salaam kama kitovu ili kuwa na muungano wa kupeleka abiria sehemu nyingi na kukidhi mizania ya kibiashara,” alisema. Alisema baada ya kubaini Zanzibar kuwa ni moja ya vituo ambavyo kuna maslahi ya biashara, imerekebisha ratiba ili kuhakikisha wasafiri kutoka Zanzibar wanakuwa na uwezo wa kusafiri kwenda Dodoma kupitia Dar es Salaam kwa kuwa na ndege siku ya Ijumaa na Jumapili.
kitaifa
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesitisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.Washitakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza kesi yao ya msingi ya uchochezi inayowakabili na wenzao saba. Pia, mahakama hiyo imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuendelea kuhudhuria michezo ya Afrika Mashariki nchini Burundi na pia imeruhusu Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, kumuuguza mkewe ambaye amejifungua kwa upasuaji hivi karibuni.Hatua ya Mahakama Kuu kusitisha usikilizwaji wa rufaa hiyo ni baada ya upande wa serikali kudai kuwa wana kusudio la kukata rufaa kupinga maamuzi ya Jaji Sam Rumanyika aliyesema kuwa rufaa ya kina Mbowe ipo mahakamani hapo kisheria na kwa maana hiyo, haina mamlaka ya kuendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo.Akitoa maamuzi hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Jaji Rumanyika alisema Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa na kwamba kunapokuwepo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri. Jana, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba washitakiwa Mdee na Heche hawapo mahakamani.Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa Heche alitolewa taarifa kuhusu kufanyiwa upasuaji mdogo kwa mke wake lakini afya ya mtoto si nzuri sana na kwa upande wa Mdee yupo nchini Burundi kushiriki mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki.Mdhamini wa Mdee, Fares Robinson aliieleza mahakama hiyo kuwa Mdee yupo safarini Burundi kwa safari za kibunge na kwamba Katibu wa Bunge aliandika barua kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama kumtaarifu kuwa mshitakiwa huyo atakuwa nje kwa shughuli za kibunge na kwamba atarudi Desemba 20, mwaka huu. Akijibu hoja hiyo, Wakili Nchimbi alidai walipokea hati ya mwito ikiambatanishwa na maombi ya ruhusa ya Mdee kupitia kwa Katibu wa Bunge.Alidai kwa mantiki hiyo wanaona washitakiwa wanafuata taratibu na hawana pingamizi na hilo na kuhusu Heche anayemuuguza mkewe pia hawana pingamizi ikizingatiwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa. Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri alisema kuwa walipokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge kuomba ruhusa ya Mdee kwenda Burundi kuhudhuria michezo ya EAC na kwamba pande zote za utetezi na mashitaka walikuwa Mahakama Kuu kwa kesi nyingine.“Mahakama inamruhusu mshitakiwa kuhudhuria michezo na ruhusa ya Heche ya kumuuguza mkewe imekubaliwa lakini wazingatie kuwepo mahakamani siku ya kutajwa kesi hiyo Desemba 21, mwaka huu, “ alisema Hakimu Mashauri. Hata hivyo, mahakamani hapo kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi ambapo uliwazuia baadhi ya wafuasi wa chama hicho kuingia na waliwaruhusu viongozi wa chama hicho pekee.Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu. Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, mwaka huu Dar es Salaam.
kitaifa
WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikisimama kwa wiki mbili kupisha mashindano ya kimataifa, uwepo wa ushindani mkali msimu huu tofauti na huko nyuma ni moja ya mambo yanayozungumzwa zaidi.Hadi sasa ligi hiyo ipo kwenye raundi ya 10 lakini utofauti uliopo kinara wa ligi hiyo Simba SC anayeongoza kwa pointi 22 amepishana kwa tofauti ya pointi mbili tu na Kagera Sugar iliyopo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 20. Matokeo ya kinara huyo pamoja na anayeshika nafasi ya pili bado wapo kwenye presha kubwa ya kuhitaji muendelezo wa kushinda pointi tatu ili kukaa katika nafasi nzuri, la sivyo watajikuta waondolewa.Hali hiyo ndiyo inayonogesha na kuzidisha ushindani ikiwa ni tofauti na msimu uliopita, kwani katika hatua hiyo Yanga ilikuwa inaongoza kwa pengo kubwa la idadi ya pointi nyingi ikilinganishwa na aliyekuwa anafuatia.KUSHINDA MECHIPamoja na hilo kwa msimu huu kumekuwa na wimbi kubwa la timu nyingi zinazoshiriki ligi hiyo kukusanya pointi nje ya viwanja vyao vya nyumbani ikilinganishwa na msimu uliopita, ambapo kila timu ilikuwa ikijitahidi kushinda nyumbani. Vigogo vya Simba na Yanga vyenyewe angalau pamoja na Azam vilikuwa vikijitahidi kushinda hata mechi za ugenini, tofauti na timu zingine ambazo ushindi ulikuwa nyumbani.Ni wazi ushindani huo unatokana na kila timu kujipanga mapema kutafuta pointi zitakazowahakikishia kushika nafasi za juu kwenye msimamo kuepukana na kitendo cha kujinusuru dakika za mwisho, ikiwa ni kuepukana na panga la kushuka timu nne za ligi hiyo.Hata kwenye upande wa mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwa ufungaji bora nako ushindani umetamalaki pamoja na mshambuliaji wa Simba kuendeleza moto wake wa kupachika mabao akifikisha mabao manane akipania kutetea kiatu hicho alichotwaa msimu uliopita bado anakabiliwa na ushindani mkali kwani wachezaji wazawa wanaocheza kwenye nafasi hiyo bado wanampa ushindani mkali.Wachezaji hao ni ni Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Paul Nonga (Lipuli FC), Yusuph Mhilu (Kagera Sugar ), Gerlad Mdamu (Mwadui FC), Peter Mapunda (Mbeya City), na Miraji Athuman (Simba SC) wote hao kila mmoja wao akiwa amepachika mabao manne. Pamoja na ushindani huo mkali hatuwezi kuwamwagia pongezi wachezaji peke yao bali zinapaswa kuelekezwa kwenye benchi la ufundi ambalo ndilo linakuwa na kazi kubwa ya kupanga kikosi na kuweka mipango ya ushindi. Kutokana na kazi yao kuwa ngumu makala haya yanakuletea makocha saba waliong’olewa kwenye mabenchi yao ya ufundi kwa sababu kadhaa ikiwemo timu kufanya vibaya au sa- babu zingine.MWINYI ZAHERA (YANGA)Kocha huyo raia wa DR Congo alitimuliwa baada ya kikosi hicho kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kufanya vibaya katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Zahera alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo na kibarua chake hicho kilipangwa kufikia tamati Septemba mwakani. Lakini hata hivyo ndoa hiyo imevunjika mwanzoni mwa msimu huu baada ya kocha huyo kudumu kwa kipindi cha miezi 15, huku akikiongoza kikosi hicho kwenye michezo 75 ikiwa zile za kimashindano na zile za kirafiki akishinda 45 kufungwa 17 na sare 13. Zahera amefungishwa virago baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi nne za ligi hiyo akifanikiwa kushinda mechi mbili sare moja akipoteza mmoja na kufanikiwa kufunga mabao manne.ETIENNE NDAYIRAGIJE (AZAM)Kocha huyo raia wa Burundi alijiunga na timu Azam FC akitokea timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) alijukuta akifungishwa virago baada ya kocha huyo kupata kibarua cha kukinoa kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars. Akiwa kocha na kiongozi wa benchi la ufundi ndani ya Azam alikiongoza kikosi hicho kwenye michezo mitatu akishinda yote na kufunga idadi ya mabao matano na kufungwa bao moja. AMRI SAID (BIASHARA) Said alikuwa anakinoa kikosi cha Biashara United na sababu iliyofanya kufungishwa virago ni timu hiyo kuboronga kwenye mechi za mwanzo kabisa za Ligi Kuu, ambapo kati ya mechi nne, alipoteza tatu na kufunga bao moja na kufungwa mabao matano.ATHUMANI BILALI (ALIANCE)Bilali ni kocha wa kwanza kufungishwa virago katika kikosi cha Alliance, kwani dakika 90 tu zilipomalizika na kibarua chake kilikoma hapo licha ya timu yake kuambulia pointi moja baada ya kutoka sare na Mbao FC. Aliiongoza Alliance kwenye mchezo mmoja na kufanikiwa kufunga bao moja na kufungwa moja na kupata pointi moja, lakini mabosi wake walishindwa kumvumilia na kumtupia virago.FRED MINZIRO (SINGIDA)Alifungishwa virago Singida baada ya kikosi hicho kupata matokeo mabaya ambapo alikiongoza kwenye mechi mbili hakushinda mchezo wowote na kufungwa mechi mbili na kufungwa mabao matatu.MALALE HAMSINI (NDANDA)Hamsini alitimuliwa Ndanda na mlezi wa timu hiyo, Gelasius Byakanwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara baada ya kikosi hicho kuwa na mwenendo wa kukosa matokeo chanya. Alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi sita hakushinda mchezo wowote, akiambulia sare tatu, kufungwa mechi tatu, wakati huo akifungwa mbao saba.JACKSON MAYANJA (KMC)Mayanja raia wa Uganda amejikuta akikalia kuti kavu KMC na kung’olewa baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye mechi za ligi na zile za kimataifa licha ya timu hiyo kujiwekeza vya kutosha kwenye masuala ya kiuchumi. Mayanja alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi nane, kushinda moja, sare mbili na kufungwa mabao mitano, huku akifanikiwa kufunga mabao matano na mabao ya kufungwa nane.
michezo
Huo utakuwa mchezo wa pili baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kucheza na Morocco na kushinda bao 1-0, ushindi ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Wapinzani wa Ngorongoro, Msumbiji juzi walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Uhuru na kuifunga bao 1-0.Hivyo, sio timu ya kubeza na ni kipimo kizuri kwa Ngorongoro kujiimarisha. Michezo hiyo ni maalumu kwa ajilli ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za vijana za Afrika (AFCON) zitakazochezwa Niger, Novemba mwaka huu.Ili kutafuta nafasi ya kufuzu Ngorongoro inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Condo DR Machi 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana katikati ya mwezi ujao.Michezo hiyo ya kirafiki inatoa nafasi kwa Kocha Mkuu, Ammy Ninje kupata kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu. Asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi hicho ni wale walioshiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambao wengi wana uzoefu.Aidha, kuna baadhi ya vijana wanaotoka klabu zinazocheza Ligi Kuu kama Yanga, Azam na Mtibwa waliojumuishwa wakitarajiwa kuisaidia timu hiyo kuelekea kwenye mafanikio.Baada ya mchezo wa leo huenda kocha huyo atakuwa amekijua kikosi chake na kuandaa timu bora itakayopata matokeo mazuri siku zijazo.
michezo
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliamsha shangwe za wananchi wa Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, mkoani Dodoma baada ya kuwasha umeme katika kijiji hicho. Naibu Waziri huyo, aliwasha umeme katika zahanati ya kijiji hicho pamoja na kisima cha maji ambapo kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa Backbone Transmission Investment Project (BTIP) (kv 400) ambao umesambaza umeme katika vijiji 121 vinavyopitiwa na mradi kutoka Iringa hadi Shinyanga.Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Mgalu alisema kuwashwa kwa umeme katika kijiji hicho ni muendelezo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano kufikisha umeme katika vijiji vyote nchini. Alisema, Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mwaka 2015 kulikuwa vijiji takribani 2,018 vyenye umeme na kuanzia Januari 2016, vijiji vipya vilivyoongezeka ni takribani 5,000 hivyo hadi sasa vijiji 7,290 vina umeme kati ya Vijiji 12,268. Kuhusu usambazaji umeme katika maeneo ambayo hayajapata umeme ingawa yamepitiwa na miundombinu alisema kuwa, kuna mradi wa ujazilizi, mzunguko wa pili unaolenga kuongeza wigo wa kuunganisha umeme katika vitongoji mbalimbali na Dodoma ni moja kati ya mikoa 9 itakayoguswa na mradi huo. Naibu Waziri pia amesisitiza wananchi kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ambavyo vitawawezesha kuondokana na gharama za wiring na kuwezesha kuunga wateja wengi katika mradi huo wa BTIP. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde (CCM) alishukuru serikali kwa kupeleka umeme katika kijiji hicho, hata hivyo aliomba umeme huo ufike katika maeneo muhimu kama vile shamba la umwagiliaji, nyumba za ibada, na vitongoji vya kijiji hicho.Aidha, aliipongeza serikali kwa kufanya kazi bila ubaguzi kwani idadi ya watu katika Kijiji hicho si kubwa ukiliganisha na vijiji vingine lakini serikali haikungalia idadi ya watu ili kufikisha umeme katika Kijiji hicho wala hadhi ya nyumba. Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chamwino, Baltazary Massawe alisema wilaya ya Chamwino in jumla ya vijiji 107 kati ya hivyo, vijiji 33 vimewekewa umeme kupitia miradi mbalimbali iliyopita kijijini hapo.Alisema vijiji vitakavyokidhi na umeme kupitia REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza kwa wilaya ya Chamwino ni vijiji 32 na vijiji 11 kupitia mradi wa BTIP. Aidha wilaya ya Chamwino inahudumia sehemu ya jimbo la Dodoma katika kata ya Kikombo ambapo vijiji viwili vitanufaika kwa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza na kujumuisha vijiji kuwa 45 kwa miradi inayoendelea kwenye wilaya ya Chamwino.Massawe alisema baada ya miradi hiyo kukamilika vijiji 82 kwa wilaya ya Chamwino vitakuwa vimenufaika na umeme.Alisema miradi ya umeme itawanufaisha wananchi katika mambo mbalimbali ikiwemo kusaidia watoto na walimu katika shughuli za kielimu hasa kwa kusoma na kutumia vifaa vya Tehama.Pia upatikanaji wa maji kwa urahisi kwa kuwa nishati itasaidia kuyavuta kirahisi kutoka kwenye chanzo. Aidha huduma za afya zitaboreka kwani itasaidia kurahisisha mambo mengi ambayo yalikuwa hatafanyiki kwa kukosa huduma ya nishati ya umeme na kuamsha shughuli za kiuchumi.
kitaifa
KOCHA mkuu wa timu ya Soka ya taifa ya wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens ,Bakari Shime amesema morali ya kikosi hicho ipo juu tayari kwa kuwakabili Sudan Kusini kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi A katika michuano ya kombe la Chalenji.Michuano hiyo inayofanyika chini ya usimamizi wa Baraza la vyama vya soka Afrika Madhariki na Kati, Cecafa inatarajiwa kuanza Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi ikishirikisha timu nane. Queens ambao ni mabingwa watetezi mara mbili mfululizo watakuwa na kibarua hicho mbele ya Sudan siku ya ufunguzi wa michuano hiyo na tayari kikosi hicho kipo kwenye maandalizi kabambe.Akizungumza jana Dar es Salaam Shime alisema morali ya kikosi ipo juu pamoja na kwamba mazoezi mepesi yanaendelea kutolewa kwa kikosi hicho.“Morali ya kikosi cha Queens ipo juu na kwa sasa kwa vile muda bado benchi la ufundi tunaendelea kuwapa mazoezi mepesi kuweka sawa miili yao tayari kwa mchezo wetu ambao tunahitaji zaidi ushindi kubusti malengo yetu,” alisema Shime .Alisema mazoezi anayoendelea kuwapa vijana hao ni namna ya kutoa pasi imfikie mlengwa kwa wakati pamoja na kuwaelekeza nidhamu kwa muda wote wakiwa uwanjani. Shime alisema pamoja na kwamba mechi hiyo itakuwa na upinzani bado anaamini ubora wa mchezaji mmoja mmoja unaweza kuwapa majibu sahihii hususan kwenye kuamua matokeo uwanjani.Timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo ni Tanzania Bara, Zanzibar,Burundi na Sudan zilizo kundi A na kundi B likiwa na timu za Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibouti.
michezo
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa mwaka mmoja na Ettiene Ndayiragije kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars. Kabla ya uteuzi huo uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF, Ndayiragije alikuwa kocha wa muda wa Taifa Stars akisaidiwa na mzawa Suleman Matola na Juma Mgunda. Akizungumza jana Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema uamuzi wa Kamati ya Utendaji kumpa nafasi hiyo ulizingatia mapendekezo ya Kamati ya Ufundi ya TFF ambayo ilipitia wasifu wa makocha mbalimbali walioomba nafasi hiyo. “TFF imevutiwa na kazi nzuri ya Ndayiragije wakati akiwa kocha wa muda tangu Julai mwaka huu alipoiwezesha Taifa Stars kufuzu fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) zitakazofanyika mwakani Cameroon pia aliiwezesha Taifa Stars kuingia hatua ya makundi ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia,”alisema Ndimbo. Taifa Stars ilifanikiwa kukata tiketi ya Chan baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Sudan wiki iliyopita Uwanja wa Omdurman, Mourada mjini Omdurman. Kwa matokeo hayo, Taifa Stars ikafuzu kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2, kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam. Hiyo inakuwa mara ya pili kwa Taifa Stars kufuzu fainali za michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya mwaka 2009 nchini Ivory Coast, ikiitoa Sudan pia katika raundi ya mwisho ya kufuzu. Ndairagije ameiongoza Taifa Stars katika michezo minne, ambapo mchezo dhidi ya Rwanda ulikuwa ni wa kirafiki, Kenya, Burundi na Sudan ni za kufuzu kwa Chan 2020
michezo
Alisema Benki hiyo iko kwenye mikakati ya kuanzisha mradi wa kunenepusha ng’ombe. “Tutawakopesha fedha kwa ajili ya kuuza minadani, mpango huu ulianza na mkoa wa Arusha na walifanya vizuri kwani mafanikio yalionekana” alisema Alisema jamii ya wafugaji ya kimasai wanamiliki mifugo mingi na kama benki waliona kuna umuhimu wa kuwapa elimu ili wawe na utamaduni wa kuhifadhi fedha benki kwa kunenepesha mifugo na kuiuza.Alisema wafugaji hao wakibadili mitazamo wanaweza kufanikiwa zaidi kwani elimu wanayoipata itawafanya kufanya ufugaji wenye tija. “ Masai wana fedha nyingi ila mwamko wao wa kutumia huduma za kibenki bado uko chini, sasa tunawafuata tunawapa elimu na wengi wanahamasika na kufungua akaunti” alisema Alisema katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara baada ya wafugaji hao kupata elimu, watu 50 waliamua kufungua akaunti na sasa wengine wanafika kwenye ofisi zao kwa ajili ya kufungua akaunti.“Huo ni mwamko mzuri na wataendelea kutoa elimu ili m jamii za wafugaji na wakulima waishio vijijini waone umuhimu wa kutumia huduma za kibenki. Ndyetabula alisema pia wameweza kutoa elimu kwa wakulima wanaoishi maeneo ya pembezoni ikiwemo Kibaigwa wilaya ya Kongwa na Kiteto mkoani Manyara.Alisema wameweza kuwafikia wazajasiriamali zaidi ya 3,000 mkoani Dodoma ambao wamepewa elimu na hata kukopeshwa kupitia mkopo wa mtu mmoja mmoja na ile ya vikundi Pamoja na hayo alisema katika safari ya Dodoma kuelekea makao makuu wamejipanga kufikia maeneo yote ya mkoa hasa ya pembezoni.“Tunazidi kuongeza mtaji wa kutoa elimu, kurasimisha biashara na kuweka msisitizo kwenye suala la kutoa elimu kuhakikisha huduma zinazotolewa zinatakuwa katika viwango vinavyotakiwa” alisema Pia alisema wameweza kuwakopesha zaidi ya wajasiriamali 900 walio kwenye vikundi wengi wao wakiwa kutoka maeneo ya pembezoni
uchumi
Meneja wa Posta Mkoa wa Tanga, Rehema Marijni alitoa mwito huo jana wakati akielimisha wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya Tatu ya Biashara Tanga yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako.Alisema licha ya kufikiwa kwa maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasilianob (Tehama) ambayo yamesababisha wananchi wengi kuhamia kwenye matumizi ya kompyuta na simu za mkononi, ikiwemo kutuma na kupokea barua kupitia barua pepe, sms na whatsapp, anaamini barua za kuandikwa kwa mkono bado zina umuhimu wa kipekee hasa katika utunzaji kumbukumbu.“Kimsingi napenda niwaombe wananchi waondoe hofu na wasidanganyike na dhana potofu iliyojengeka kwenye jamii kwamba kupanuka kwa matimizi ya vifaa hivyo kumemaliza kabisa umuhimu ya matumizi ya huduma mbalimbali za Posta, hilo si sahihi,” alisema.Naye Ofisa Masoko wa Posta, Mzee Omari Mzee alisema shirika hilo linaendelea kuboresha kitengo chake cha barua ambapo usambazaji na utumaji unaendelezwa kupitia mtandao wa masanduku ya barua yaliyoko mjini na vijijini ncho nzima.
uchumi
Trevelport ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha kupatia mashirika ya ndege duniani mifumo ya ukataji wa tiketi.Mathew alisema kuna kodi nyingi sana zinazotozwa mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga lakini mwisho wa siku mzigo wa kodi hizo anabebeshwa Mtanzania wa kawaida anapotaka kutumia huduma hizo kama kusafiri kwa ndege.“Hii inadidimiza uchumi kwa sababu mtalii anaona heri aende Uganda ama Kenya anakotozwa kidogo wakati Tanzania ndiyo yenye vivutio vingi vya utalii kulinganisha na nchi za Afrika Mashariki, sasa hivi tena wanapendekeza VAT iwekwe kwenye usafiri wa anga, hii nayo itadhoofisha biashara katika usafiri wa anga maana hakuna nchi yoyote duniani inayotoza VAT sekta ya usafiri wa anga,” alisema Mathew.Alisema hivi sasa watumiaji wa usafiri wa anga duniani wanapata mahitaji yao kupitia mitandao ikiwemo ununuzi wa tiketi, sehemu ya kukaa kwenye ndege, chakula na hoteli wanazotaka kufikia kwenye nchi wanazokwenda hivyo kuna haja kwa kampuni zinazotoa huduma kwenye sekta hiyo kwenda na wakati.Meneja wa mtandao huo mpya wa Precise Sky, Gloria Urasa, alisema mfumo huo ni mpya nchini utasaidia mashirika madogo ya ndege kuonekana duniani kwa kuongeza sehemu za kuuzia tiketi za ndege zao hivyo kuzidi kukua kibiashara.“Mashirika madogo ya ndege yanakua kibiashara hivyo na yenyewe yanahitaji kuwa katika ushindani kama ilivyo kwa mashirika mengine ya ndege makubwa ndiyo sababu ikaonekana uanzishwe mfumo utakaozisaidia kampuni hizi ndogo kukua, hivyo mfumo huu ni maalumu kwao,” alisema.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Charles Chacha, alikiri kwamba Watanzania wengi hawatumii usafiri wa anga kutokana na kutomudu gharama za tiketi ingawa serikali inafanya jithada kubwa kurekebisha hali hiyo.Alisema moja ya jitihada zinazofanyika ni kurekebisha miundombinu ndege ziweze kutua saa 24 kwenye viwanja vya nchini na kusajili kampuni nyingi za kigeni za ndege.Alisema wingi wa kampuni zinazotoa huduma hizo utaleta ushindani hivyo kusaidia kupunguza gharama za usafiri wa anga na Watanzania wengi siku zijazo watakuwa wanatumia usafiri huo kwani kwa mipango iliyopo gharama zitapungua.
uchumi
Timu hiyo ilipata bao hilo dakika ya nne ya mchezo.Bao hilo ambalo liliongeza kasi ya ushambulizi kwa pande zote mbili liliwekwa kimiyani na mchezaji Hamad Mshamata na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo.Kurudi katika kipindi cha pili miamba hiyo iliendelea kushambuliana kwa zamu huku kila upande ukifanya mabadiliko ambayo hayakuwa na msaada kwa pande zote.Mafunzo inayofundishwa na Kocha Hemed Morocco ilifanya mabadiliko yake kwa kuwatoa nje wachezaji watatu kwa pamoja ndani ya dakika ya 65 ambao ni Shaaban Ali, Jeremia Seif na Ahmed Maulid na kuwaingiza Ali Othman Mmanga, Ali Juma na Samih Haji Nuhu.Kwa upande wa Chuoni ambao nao wanafundishwa na Kocha Suleiman Mahmoud Jabir walifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji wake Bakari Omari, Mohammed Hashim na Mohammed Salum na nafasi zao kuchukuliwa na Ali Hilai ‘Lii’, Mustafa Zakaria na Kitwana Hassan.Timu hizo ambazo zote zinafundishwa na makocha mahiri waliowahi kuifundisha timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa nyakati tofauti zilionesha ufundi wa hali ya juu.
michezo
LICHA ya kuwafunga waajiri wake wazamani Yanga, Mshambuliaji wa Azam FC , Obrey Chirwa (pichani) ameonesha kutoridhika na hali hiyo na kudai kuwa anaitaka Yanga yenyewe iliyotimia akimaanisha ile ya wakubwa.Chirwa alifunga bao la tatu katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi juzi dhidi ya Yanga, mchezo ulioisha kwa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara kupoteza kwa mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B kwenye Uwanja wa Amaan.Baada ya kufunga bao hilo, Chirwa hakutaka kushangilia kwa kiasi kikubwa, kwa madai kuwa hakuridhishwa kukifunga kikosi hicho kilichojaa wachezaji chipukizi nay eye aliitaka Yanga ya wakubwa ili adhihirishe uwezo wake. Chirwa alisema anataka kuifunga Yanga ya kikosi cha kwanza ili kuwathibitishiwa wadau wa soka kuwa bado yuko fiti kwa kiasi kikubwa ingawaje aliwapa sifa vijana wa kikosi cha pili kuwa wapo vyema.“Mimi naitaka ile Yanga ya Dar es Salaam sio hii, naitaka ilee yenyewe ili nioneshe uwezo wangu, hawa vijana wanacheza vizuri ila nimeona mchezo mwepesi naitaka ile ingine,” alisema Chirwa. Alisema baada ya kuifunga Yanga ya kikosi cha pili anajiandaa vizuri kuikabili tena katika mchezo wa Ligi Kuu na kuongeza kuwa katika mchezo huo atahakikisha anaifunga kwa mara nyingine.Nyota huyo wa Zambia aliwahi kuitumikia Yanga, kabla ya kuondoka kucheza soka la kulipwa ndani ya miezi kadhaa na baadaye kurejea tena Bara na kusajiliwa na Azam akiunga na Mzimbabwe Donald Ngoma aliyekuwa Yanga pia. Yanga imendelea kuonesha uteja dhidi ya Azam FC katika michuano hiyo tangu mwaka 2017, ambapo ilifungwa mabao 4-0, kabla ya kupata sare tena ya 1-1
kitaifa
Nuh, ambaye mara zote amekuwa akiimba nyimbo za mapenzi, amesema nyimbo zote anazoimba huwa zinaendana na historia yake ya kweli kwenye mapenzi.Akizungumza kwenye mahojiano maalumu juzi, Nuh alisema kwamba sio pamoja na uwepo wa wimbo wa Jike Shupa lakini tayari ameimba wimbo mwingine unaitwa Upofu ambao unaendana na historia yake."Sio mara ya kwanza kuimba juu ya mahusiano yangu yaliyopita ukiacha wimbo wa Jike Shupa na sasa nimeimba wimbo mwingine unaoitwa 'Upofu' ambao ndani ya wimbo huo nimeimba yaliyonitokea kwa aliyekuwa mke wangu na mama mtoto wangu Nawal,''alisema Nuh.Akifafanua zaidi Nuh alisema, yeye sio msiri na hawezi kukaa na kitu kinachomuumiza moyo, lazima akiweke wazi ili abaki na amani, lakini pia hutumia nafasi hiyo kuelimisha wale ambao wanamuangalia yeye kama mfano ili wajifunze kutoka kwake.Mkali huyo pia amewaomba mashabiki zake kuendelea kumpatia sapoti katika muziki wake na kufuatilia nyimbo zake huku akisisitiza kwamba nyimbo zake zote ameimba historia yake ya kweli na ni mambo tu ambayo yanaweza kumtokea mtu yeyote.Nuh alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na walipoachana ndipo alipomtungia wimbo wa Jike Shupa.Alipoachana na Shilole, alifunga ndoa na Nawal waliyepata naye mtoto mmoja wa kike, lakini ndoa yao imekuwa na mikwaruzano ya hapa na pale, na hivi karibuni wanadaiwa kuachana.
michezo
['Alexis Sanchez anakataa kuondoka Manchester United msimu huu, pamoja na kwamba kocha Ole Gunnar Solskjaer kutishia kumfanya kuwa mchezaji wa akiba ikiwa atasalia na timu hiyo. Roma inatafuta wachezaji wengine. (Sun)', 'Hatahivyo, timu ya Serie A, AC Milan, Juventus na Napoli bado wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Chile, 30. (Mail)', 'Real Madrid imekataa ombi la Paris St-Germain kumjumuisha Vinicius Junior,19, katika ofa ya kumnyakua mshambuliaji wa Brazil Neymar,27. (AS)', 'Mbali na Vinicius, PSG wanapendelea Real wamjumuishe kiungo wa croatia Luka Modric,33 na kiungo wa Brazil Casemiro,27, kumpata Neymar. (Marca)', 'Neymar alikuwa mazoezini mwenyewe siku ya Jumatano, ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapouzwa.(Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza bado kujiunga na PSG ikiwa hatakuwa sehemu ya ofa ya Neymar. (Goal)', 'Beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof, 25, anajiandaa kusaini mkataba mpya kwa ongezeko la mshahara mbali na pauni 75,000 alizokuwa akipata kwa wiki. (Aftonbladet - in Swedish)', 'Bayern Munich huenda wakafufua nia yao ya kumnasa winga wa Manchester City, Leroy Sane, ingawa mchezaji huyo, 23, ana jeraha la mguu, litakalo mfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba. (Bild - in German)', 'Wachezaji wa EPL wanapumzika vya kutosha?', 'Tetesi za soka Ulaya Jumatano 14.08.2019', 'Mshambuliaji wa Marseille na Italia Mario Balotelli,29, anajiandaa kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Brescia baada ya kukataa ofa ya Flamengo ya Brazil. (Guardian)', 'Flamengo bado wana matumaini ya kubadili msimamo wa Balotelli, baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kaka yake Enock kucheza katika moja kati ya timu zao nyingine (Gazzetta dello Sport - in Italian)', 'Winga wa klabu ya Everton Alex Iwobi, 23, amesema aliondoka Arsenal katika siku ya mwisho ya usajili kuthibitisha kuwa yeye si mchezaji anayechipukia tena. (Mirror)', 'Tottenham itazungumza na Christian Eriksen, 27,tena kuhusu mkataba mpya kabla kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, tarehe 2 mwezi Septemba, baada ya Real Madrid na Juventus kuonesha nia ya kumnasa kiungo huyo.(Independent)', 'Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, anaonekana kujiandaa kujiunga na timu ya Trabzonspor ya Uturuki kwa dili la pauni milioni 2.8 kwa kila msimu.(Goal)', "Monaco imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwasajili wachezaji kiungo Blaise Matuidi,32, na beki wa kati Daniele Rugani,25, kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport - in Italian)"]
michezo
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga wamehamishia nguvu zao kwa maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) dhidi ya Biashara United utakaochezwa wiki ijayo.Vijana hao wa Jangwani walitolewa mapema katika michuano ya wadhamini wao, portPesa na timu ya Kenya ya Kariobang Sharks kwa mabao 3-2 na sasa wanaendelea na maandalizi ya FA. Akizungumza na gazeti hili Mratibu wa Yanga, Hafidhi Salehe alisema wameanza mazoezi kujiandaa na mchezo huo wakijua umuhimu wa michuano hiyo.“Timu imeshaanza mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa FA utakaochezwa Januari 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, kocha anajaribu kufanya marekebisho katika mapungufu aliyoyaona katika michezo iliyopita ili kuweka mambo sawa,”alisema. Salehe alisema huenda mambo yakawa mazuri uwanjani baada ya baadhi ya wachezaji wengi waliokuwa majeruhi kurejea rasmi na kuanza mazoezi.Wachezaji waliorejea ni Thaban Kamusoko, Papy Tshishimbi walioanza kuonekana kuanzia katika mechi dhidi ya Kariobang Sharks. Wapinzani wa Yanga, Biashara tayari wapo jijini na jana walikuwa wana mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC.Yanga imetoka kufanya vibaya katika mchezo wa ligi baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Stand United kwa bao 1-0 na kuvunjiwa rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote. Lakini licha ya kupoteza, bado wanaendelea kushikilia uongoza kwa pointi 53 baada ya kucheza michezo 17, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.
kitaifa
UTALII ni sekta muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Inachangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa. Katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, sekta ya utalii ilichangia asilimia 17.5 ya pato la taifa huku ikiliingizia asilimia 25 ya fedha za kigeni.Katika kipindi hicho, ilichangia ajira 500,000 za moja kwa moja na nyingine milioni moja za watu kujiajiri kwa shughuli mbalimbali zinazoigusa sekta hiyo. Kutokana na umuhimu wa sekta hiyo, Serikali imeendelea kupanga na kutekeleza sera mbalimbali kuendelea kuiinua, ikiwa ni pamoja na kuimarisha vyuo vinavyotoa elimu na mafunzo ya utalii nchini.Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii (CBCTC) kilichopo katika kijiji cha Likuyu Sekamaganga, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma kimeendeleza juhudi hizo za serikali kwa kutoa wahitimu wenye weledi katika sekta hiyo. Hivi karibuni kimefanya mahafali ya mafunzo kwa askari wanyamapori wa vijiji (VGS) huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu.Akizungumza katika mahafali hayo, Kanyasu aliwaasa askari kulinda na kutunza rasilimali za taifa katika maeneo yao ili ziwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho. Kanyasu aliahidi kushughulikia changamoto zinazokikabili chuo hicho, ikiwamo miundombinu chakavu na kumalizia jengo la maktaba aliloweka jiwe msingi na kusema, serikali itahakikisha chuo hicho kinakuwa na sifa ya chuo cha kati.Anasema kozi ya waongoza watalii inayoanzishwa katika Chuo cha Likuyu, mtaala wake utakuwa unafanana na vyuo vingine viwili nchini vivyotoa kozi hiyo alivyovitaja kuwa ni Chuo cha Pansiansi Mwanza na Mweka, Kilimanjaro.“Serikali imejipanga kufungua utalii wa Kusini, hivyo kozi ya waongozaji watalii ni muhimu kuwa na silabasi moja ili kupata watu watakaokuwa na sifa ya kutoa huduma zinazofanana kwa watalii ili kuwafanya watalii kuendelea kufika Tanzania,’’ alisema Naibu Waziri Kanyasu.Alisema serikali inafungua utalii Nyanda za Juu Kusini na Kusini kuhakikisha utalii unakuwa zao namba moja kwa ajili ya kuongeza mapato ya fedha za kigeni na uchumi wa Tanzania kwa sababu uchumi wa utalii bado upo wazi.Alisema utalii si kuangalia wanyama na kupanda milima pekee, bali nchini Tanzania upo utalii wa aina nyingi ukiwemo wa ngoma, vyakula, nyumba za asili, zana za kilimo kama jembe la mkono linaloshangaza wageni wengi kutoka nje ya nchi. Kwa mujibu wa Kanyasu, changamoto kubwa iliyokuwa inaikabili sekta ya utalii nchini ni miundombinu hafifu.Anasema Rais John Magufuli amenunua ndege, amejenga barabara za lami na hivi sasa anaboresha na kujenga viwanja vya ndege vilivyo muhimu kwa utalii. “Kazi yetu kubwa sasa kama Wizara ni kuangalia wapi tuwekeze ili watalii waje na kutuletea fedha za kigeni hivyo kuchangia mapato na kukuza uchumi wa Taifa letu’’, amesema Kanyasu.Mkuu wa Chuo cha CBCTC, Jane Nyau anasema katika mahafali hayo kuwa, chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1995 ni pekee cha utoaji wa mafunzo ya uhifadhi wa maliasili kwa jamii barani Afrika. Anasema hapa nchini katika vyuo vya uhifadhi, hakuna chuo kinachotoa mafunzo yanayofanana na chuo hicho hali hiyo ndiyo inakifanya kuwa ni chuo cha kipekee nchini. Katika mahafali ya kozi namba 64/2019 ya askari wanyamapori wa vijiji (VGS), wanachuo 20 wamehitimu mafunzo ya askari wanyamapori wa vijiji kwa miezi mitatu.Anasema licha ya chuo hicho kutoa kozi za mafunzo hayo ya askari wanyamapori wa vijiji na mafunzo ya viongozi wa serikali na kamati za maliasili za vijiji kwa mwezi mmoja, kuanzia Julai 2019 chuo hicho kitaanza kutoa kozi ya astashahada ya awali ya waongozaji watalii kwa muda wa mwaka mmoja. “Kozi hii itatolewa kuendana na mkakati unaoendelea wa serikali wa kukuza utalii katika Ukanda wa Kusini, mtaala wa kozi hiyo umeshakamilika na tayari umeshathibitishwa na Baraza la Usimamizi wa Vyuo vya Ufundi (NACTE),” anasema Nyau.Akizungumzia mafunzo yaliyohitimishwa, Mkuu wa chuo anasema, mafunzo hayo yametolewa chini ya ufadhili wa Shirika la Wildlife Conservation Society (WCS) na askari hao wamepatiwa mafunzo kupitia utekelezaji wa mkakati mpya wa kulinda shoroba mbili zilizoko katika maeneo yao. Anazitaja shoroba hizo kuwa ni Ruaha kupitia Piti hadi Katavi na ya pili ni inayotoka Ruaha kupitia Rungwa na Ipole.Licha ya mafunzo ya VGS, Nyau anayataja mafunzo yanayoendelea ya viongozi na wajumbe wa kamati za maliasili na vijiji pamoja na baadhi ya wenyeviti na wananchi toka vijiji mbalimbali na kwamba, mafunzo hayo yanafadhiliwa na WWF yakishirikisha washiriki 40 kutoka Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori. Anazitaja jumuiya hizo kuwa ni Mbarang’andu, Kimbanda, Kisungule katika Wilaya ya Namtumbo, Chingoli na Nalika wilayani Tunduru; pamoja na baadhi ya wananchi na wenyeviti kutoka vijiji vya Likuyu, Mchomoro, Mtelemwahi, Lusewa, Likusanguse, Sasawala, Amani, Matepwende, Msisima na Ligunga.Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo huyo, mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1995 ni kutoa mafunzo kwa wananchi 4,633, kuanza ujenzi wa maktaba na chumba cha kompyuta kwa kutumia fedha za ndani. Kwa sasa zinahitajika Sh milioni 23.4 kukamilisha ujenzi huu. Mengine ni kupitia ufadhili wa USAID, chuo kimefanikiwa kuandaa mtaala wa kozi ya waongoza watalii na kudurusu mpango mkakati wa kuandaa mpango wa biashara wa chuo.Anayataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kitaaluma kwa wakufunzi na kutoa vifaa vya mafunzo na mfumo wa umeme ambavyo ni genereta moja, kompyuta mpakato, viona mbali, mahema 16 na vitabu 40 kwa ajili kozi ya waongoza watalii. Pamoja na mafanikio hayo, Nyau anazitaja changamoto zinazokikabili chuo hicho kuwa ni upungufu mkubwa wa watumishi na uchakavu wa majengo yakiwemo mabweni, uchakavu wa magari, nyumba za watumishi, jiko na bwalo la chakula.Anasema karibu majengo yote yalirithiwa kutoka kwa wakimbizi wa Msumbiji miaka ya 1980 na kwamba, tangu wakati huo hayajawahi kufanyiwa ukarabati. Mratibu wa shughuli za uhifadhi kwa jamii (WCS), Anna Kimambo anasema WCS imefadhili mafunzo hayo kutokana na changamoto ya uvamazi katika maeneo ya uhifadhi hivyo, yanalenga kutekeleza kwa vitendo kanuni ya uhifadhi ya maeneo ya shoroba iliyopitishwa mwaka 2018 ili kulinda maeneo ambayo hayajaharibiwa sana.Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori Tanzania, Canisius Karamaga, anasema CBCTC Namtumbo kimewekwa na serikali ili kutoa mafunzo kwa wahifadhi na kutoa elimu kwa askari wa wanyamapori vijijini hivyo chuo hicho kinatoa elimu katika maeneo yaliyo nje ya mfumo rasmi wa uhifadhi. Anasema chuo hicho kinasaidia hifadhi kwa jamii na shoroba ambapo maeneo hayo yote ni ardhi za vijiji kwa kuwa yanaunganisha hifadhi moja kwenda nyingine na kwamba, iwapo shoroba hizo zitafungwa, wanyama watakuwa wanazaliana ndani ya kizazi hivyo watatoweka.“Wanyama wanavyobadilishana vinasaba kati ya hifadhi na hifadhi, hapo ndipo tunapopata uhifadhi endelevu na rasilimali endelevu ndipo panapoleta umuhimu wa kuhifadhi maeneo yaliopo nje ya mfumo rasmi wa uhifadhi chini ya vijiji,’’ anasema Karamaga.Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo anasema robo tatu ya wilaya hiyo ni hifadhi ikiwemo eneo la Pori la Akiba la Selous na kwamba, katika shoroba inayounganisha Selous na Niassa Msumbiji, kuna hifadhi tatu ndani ya Wilaya ya Namtumbo ambazo ni Mbarang’andu, Kisungule na Kimbanda.Anasema Wilaya ya Namtumbo inahusika katika mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji kwa sababu Mto Luegu unaochangia asilimia 19 katika Mto Rufiji, vyanzo vya mto huo vinaanzia Selous, hivyo wilaya hiyo ina kazi kubwa ya kulinda vyanzo vya maji vya mto huo ili mradi wa umeme uwe endelevu. Mawasiliano ya Mwandishi wa makala haya ni baruapepe: albano.midelo@gmail. com. Simu 0784765917
kitaifa
ATCL itakuwa ikitumia ndege yake aina ya Bombardier Dash - 8 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 katika njia hiyo.Ikitokea Dar es Salaam kwenda Arusha, alikuwemo Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na wakati wa kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam, alipanda Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wa Serikali ya Zanzibar, Dk Mwinyihaji Haji Makame.Akizungumza mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Arusha, Nyalandu alisema kurejea kwa ndege za ATCL katika njia ya Arusha na Zanzibar, kutakuza sekta ya utalii na kurahisisha uunganishwaji wa maeneo hayo muhimu yenye vivutio vikubwa vya utalii.“Uzinduzi wa safari hii unadhihirisha kwamba sasa ushindani wa kweli katika sekta ya usafiri wa anga umeanza. ATCL inatakiwa kuhakikisha inaendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora ili iweze kurejesha imani iliyokuwanayo kwa abiria wake walio wengi,” alisema Nyalandu.Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL, Juma Boma alisema safari ya Dar es Salaam – Arusha – Zanzibar ni sehemu ya mkakati wa shirika lake kutanua huduma katika maeneo mengi iwezekanavyo.“Tunajivunia kuendelea kutekeleza dhamira yetu ya kuimarisha huduma zetu tukiwa kama kampuni ya ndege la taifa. Tukilenga kuendelea kutanua wigo wa huduma zetu ndani ya nchi na kimataifa. Lengo letu kubwa ni kuendelea kutoa huduma zenye gharama nafuu, vile vile kuongeza uwezo wa abiria kusafiri kwa wakati wao,” alisema.Alisema wameondoa adhabu kwa abiria wanaochelewa kufika uwanja wa ndege au kushindwa kufika siku ya safari na wanaobadilisha tarehe za safari zao.Waziri Makame alisema inatia moyo kuona ATCL ikirejesha safari zake Zanzibar baada ya kusitisha huduma zake katika kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka minne.Alitaka ATCL kufuata muda na kuhakikisha wanapunguza adha ya usitishaji wa safari endapo wanataka kurejesha imani miongoni mwa abiria walio wengi.Akizungumza baada ya kupokea safari hiyo ya uzinduzi katika uwanja wa ndege wa Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela alisema kuanza kwa safari katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki , kumerejesha sifa iliyokuwa nayo ndege hiyo ya taifa kipindi cha nyuma wakati wa mikutano ya kimataifa jijini Arusha.
uchumi
['Miamba ya soka Uhispania klabu ya Barcelona imemsajili msahmbuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka klabu pinzani ya Atletico Madrid kwa kitita cha euro milioni 120. ', 'Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichonyakua kombe la dunia mwaka jana. ', "Griezmann ameingia mkataba wa miaka mitano na Barcelona ambao umeweka sharti la euro milioni 800 kwa klabu yeyote itakayotaka kumng'oa Nou Camp. ", 'Mshambuliaji huyo machachari alijiunga na Atletico akitokea Real Sociedad mwaka 2014 na ameifungia Atletico magoli 133 katika michezo 256.', 'Mwaka mmoja uliopita, Juni 2018, alisaini mkataba mpya na Atletico wa miaka mitano, hata hivyo ilipofika mwezi Mei mwaka huu akatangaza kuwa ataihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la majira haya ya joto. ', 'Griezmann sasa anakuwa mchezaji wa sita ghali zaidi duniani kusajiliwa nyuma ya Neymar, Kylian Mbappe, Philippe Coutinho, Joao Felix na Ousmane Dembele.', 'Ameshinda mataji kadhaa na Atletico kama Kombe la Europa, kombe la Super Cup la Uhispania, pamoja na Uefa Super Cup. ', 'Pia amekuwa kinara wa magoli wa klabu hiyo katika misimu mitano iliyopita klabuni hapo. ', 'Griezmann anakuwa mchezaji wa nne mkubwa kusajiliwa na Barcelona katika dirisha hili la usajili baada ya kiungo Frenkie de Jong kutoka Ajax, golikipa Neto kutoka Valencia na beki Emerson kutoka klabu ya Atletico-MG ya Brazil. ', 'Atletico iliiripoti Barcelona kwa kutumia njia za kinyume cha sheria kufanya mazungumzo na Griezmann kwa mara ya kwanza mwezi Disemba 2017. ', 'Griezmann baada ya hapo akaikataa ofa ya kuhamia Barcelona mwaka jana, lakini mwanzoni mwa mwezi huu Atletico ikatoa malalamiko tena juu ya jambo hilo.', 'Klabu hiyo iliishutumu Atletico na Griezman kwa utovu wa adabu kwa kuafikiana juu ya uhamisho bila kufuata njia rasmi. ', 'Griezmann ni nyota watatu kuihama Atletico msimu huu baada ya beki Lucas Hernandez kujiubga na Bayern Munich na kapteni wa muda mrefu wa klabu hiyo Diego Godin kuhamia Inter Milan baada ya kwisha kwa mkataba wake. ', 'Klabu hiyo pia imetumia kitita cha euro 126 kumnunua Felix kutoka Benfica. ', 'Atletico ilimaliza katika nafasi ya pili msimu ulipita nyuma ya Barcelona kwa alama tisa. ', "Griezmann, ambaye alikuwa wa tatu katika tuzo za Ballon d'Or kwa mwaka 2016 na 2018, anaungana na Lionel Messi, Luis Suarez na Dembele katika safu 'hatari' ya ushambuliaji ya Barcelona. "]
michezo
MWANARIADHA Joshua Cheptegei amekuwa Mganda wa kwanza kuwa bingwa wa dunia wa mbio za nyika katika historia baada ya kumshinda Mganda mwenzake Jacob Kiplimo na bingwa mtetezi mara mbili Mkenya Geoffrey Kamworor kwa muda wa 10,240.Lakini pamoja na ahadi aliyopewa katika hafla iliyofanyika Kololo miaka miwili iliyopita, `Golden Boy’ huyo hajatimiziwa ahadi zake. Cheptegei anamuomba Rais wa Uganda, Museveni kutimiza ahadi zake alizotoa kwa wachezaji wa nchi hiyo hasa wale kutoka mkoa wa Sebei. Wakati wa chakula walichoandaliwa na Ikulu ya Entebbe Aprili mwaka jana, Museveni alimuahidi Cheptegei kumjengea nyumba baada ya kushinda mbio za meta 5,000 na 10,000 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Gold Coast, Australia.“Ni mwaka mmoja sasa kutoka Gold Coast na ahadi za Rais bado hazijatekelezwa,” alifunguka Cheptegei alipozungumza na Monitor-Uganda wiki hii. Ingawa ana mambo mengi. Cheptegei ni miongoni mwa wachezaji wakubwa ambao bado malimbikizo yao hawajalipwa na Ikulu tangu mwaka 2014.Rais Museveni alianzisha utaratibu wa kuwalipa kila mwezi wachezaji wote waliopata medali katika mashindano ya kimataifa baada ya Moses Kipsiro kutwaa medali mbili katika Michezo ya Jumuiya ya Madola New Delhi, India mwaka 2010.Zawadi zenyewe ziligawanywa kama ifuatavyo, Sh milioni 1 kwa medali ya shaba, wakati mchezaji aliyepata medali ya fedha aliahidiwa kupewa Sh milioni 3 kila mwezi na medali ya dhahabu Sh milioni 5. Wachezaji wengi mara ya mwisho walilipwa posho zao mwaka 2015.
kitaifa
WATU 13 kati ya 15 waliokufa papo hapo katika ajali iliyohusisha magari mawili baada ya kugongana uso kwa uso kwenye kitongoji cha Gokora, Kata ya Komaswa tarafa ya Inano Wilaya ya Tarime mkoani Mara, watazikwa pamoja eneo hilo la ajali baada ya miili yao kuharibika vibaya.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa wa Mara ziliamua kutenga aneo hilo ilipotokea ajali ili kuhifadhi miili hiyo kwa kuwa ilishindikana kutambuliwa kutokana na kuungua vibaya baada ya magari hayo kuwaka moto.Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alitembelea eneo hilo la ajali na kuwapa pole wafiwa wa ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria lenye namba za usajili T 220 CRY iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyetambuliwa kwa jina moja la Joseph na lingine lenye namba T 996 BAM lililokuwa likiendeshwa na Wambura Amon.Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe, watu 15 walikufa papo hapo huku 13 miili yao ikiharibika vibaya kiasi cha kutotambuliwa na kubakia mafuvu huku majeruhi wakibakia 3 kati ya wanne waliopelekwa Hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza.Akizungumza na wananchi waliofika kutambua miili ya ndugu zao katika Hospitali ya Wilaya Tarime, Mkuu wa Wilaya Tarime, Glorious Luoga alitoa mwito kwa madereva kuwa makini wawapo barabarani ili kulinda uhai wa abiria wao. Kutokana na ajali hiyo, Malima alisema miili hiyo ya watu 13 ambao haikutambuliwa kutokana na kuungua vibaya itazikwa leo katika eneo hilo la ajali.Ajali hiyo mbaya ilitokea juzi jioni eneo hilo wakati magari hayo mawili, moja lililokuwa likiendeshwa na Wambura Amon likitokea Tarime kwenda Kinesi lilipogongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Joseph lililokuwa likitokea Musoma kwenda Tarime.Wakati ajali inatokea, mvua ilikuwa ikinyesha ambapo madereva wote wawili ni miongoni mwa watu waliofariki dunia. Majeruhi waliopelekwa Hospitali ya Bugando ni pamoja na Thomas Amon ambaye alikuwa kondakta wa gari la la dereva Wambura ambaye ni baba yake, Blandina Machage, Leonard Maiko na Robhi Kiginga.
kitaifa
MKOA wa Kilimanjaro umetenga ekari 4,296 kwa ajili ya shughuli za uwekezaji, katika wilaya za Moshi na Siha na kuomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa hiyo.Aidha katika utekelezaji wa agizo la Serikali la uanzishwaji wa viwanda 100 kila mkoa, tayari mkoa huo umeanzisha viwanda vipya 74 kwa kipindi cha Desemba 2017 hadi Agosti 2018 ambavyo vimezalisha ajira 787.Mkuu wa mkoa huo, Anna Mgh’wira amesema hayo katika mahojiano kuhusu maendeleo ya mkoa huo katika nyanja mbalimbali hususan ufufuaji wa viwanda.“Kati ya viwanda 74 vilivyoanzishwa hadi sasa, viwanda 48 ni vidogo sana, viwanda 23 ni vidogo, viwanda viwili ni vya kati na kiwanda kimoja ni kikubwa...tunaendelea kutekeleza mpango huu wa serikali,” amesema.Kuhusu maeneo ya uwekezaji, mkuu wa mkoa alisema wilaya ya Moshi umetenga maeneo ya Lokolova ekari 140 na ekari tisa eneo la Njia Panda wilayani hapa huku pia ekari nyingine 1,676 zikitengwa wilayani Siha.Amesema, pamoja na maeneo hayo lakini pia zipo ekari nyingine 2,471 chini ya Chama cha ushirika cha Lokolova ambazo zinafaaa kwa ajili ya uwekezaji wa aina mbalimbali.Mgh’wira alisema pamoja na kutenga maeneo hayo lakini yanakabiliwa na ukosefu wa miundombinu ya maji, umeme na barabara na kwamba yakiwekewa miundombinu hiyo itasaidia kuwavutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.Alisema katika kufufua viwanda, tayari mkoa umewasiliana na taasisi za serikali na binafsi ambapo viwanda vya Kilimanjaro Machine Tools Manufacturers Ltd, Karanga Footwear, Mamba Myamba Ginger vipo mbioni kufufuliwa kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF.Hata hivyo mkuu wa mkoa alisema kiwanda cha dawa cha Twiga na kile cha kukoboa mpunga (KPHC) vimerejeshwa kwa msajili wa hazina ili kutafuta wawekezaji wengine.Alisema viwanda vya mbao, vibiriti na cha karatasi mwekezaji wake anaviuza huku kile cha magunia kimepewa muda wa ufufuaji.
uchumi
Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa jana wakati benki hiyo ikisherehekea miaka mitatu ya utoaji wa huduma kwa wateja.Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi, Wafanyakazi na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusherehekea mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja alisema wamepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kutokana na aina ya huduma wanazotoa.Alisema hiyo ni zaidi na matarajio ya Benki Kuu ambayo iliamini benki hiyo itaanza kutengeneza faidi kuanzia miaka mitatu.Alisema kuanzia Juni mwaka jana, hadi Juni mwaka huu, pato la benki limeongezeka kutoka Sh milioni 951 hadi kufikia Sh bilioni 2.9. Faida imepanda kutoka Sh milioni tano hadi Sh bilioni 1.4. Amana ilikuwa Sh bilioni 10.2 na imefikia Sh bilioni 13.4.“Fedha za wahisani zimeongezeka kufikia Sh bilioni 2.23 licha ya mtaji huo kutumika katika uanzishaji wa benki na hasara ya Sh milioni 500 iliyopatikana katika mwaka wa kwanza wa huduma,” alisema Mwambenja.Alisema mafanikio hayo yametokana na ubora wa huduma ambazo zimebuniwa na kuwa benki ya kwanza kutoa aina ya huduma za kipekee kwa kulenga Watanzania ambao wako katika sekta zisizo rasmi.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Balozi Salome Sijaona, amempongeza Mkurugenzi na Wafanyakazi wa benki hiyo kwa kufanya kazi bila kuchoka. Alisema bodi inatambua mchango wa wafanyakazi hao na kuendelea kuboresha masilahi yao, huku akisisitiza kuwa benki itaendelea kulenga Watanzania wasio katika sekta rasmi.
uchumi
RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa Chato mkoani Geita kwa kuitikia mwito wa serikali wa kuongeza juhudi katika kazi za uzalishaji mali, hali iliyoiwezesha wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.Rais Magufuli alitoa pongezi jana wakati akiwasalimu wananchi hao katika eneo la Njiapanda, muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Chato akitokea Dar es Salaam.Alifafanua kuwa akiwa angani kabla ya kutua amefurahishwa kuona jinsi wananchi wa Chato walivyochangamka kimaendeleo kwa kujenga nyumba za kuishi za kisasa, majengo ya biashara, majengo ya huduma za jamii na mashamba ya mazao mbalimbali.“Nawapongeza sana wananchi wa Chato, mnachapa kazi kwelikweli na maendeleo yanaonekana, Chato inabadilika. Nilishasema asiyefanya kazi na asile, kwa hiyo tuendelee kushikamana kufanya kazi na kujenga nchi yetu,” alisema Dk Magufuli.Alitoa mwito kwa Watanzania wote kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kushikamana na kutobaguana ili kwa pamoja waijenge Tanzania yenye rasilimali nyingi.Kabla ya kuwasalimu wananchi wa Njiapanda, Rais Magufuli aliwasalimu na kuwashukuru wananchi wanaofanya kazi za ujenzi katika uwanja wa ndege wa Chato. Dk Magufuli aliwasili jana katika Kijiji cha Mlimani wilayani Chato kwa mapumziko.
kitaifa
Aliweka jiwe la msingi la viwanda hivyo jana akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Viwanda hivyo vinatengeneza steel wire, pipi, vifungashio aina ya viroba.“Nampongeza Lameck Airo, Mbunge wa Rorya na Mwenyekiti wa Kampuni ya Lakairo Investment kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda,” alisema Majaliwa.Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza sera ya uchumi wa viwanda na inahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda mbalimbali. Alisema serikali itamuunga mkono Airo ili viwanda hivyo vizalishe kwa mafanikio makubwa.Pia aliwataka wananchi nao wamuunge mkono mwekezaji huyo kwa sababu viwanda hivyo vinazalisha bidhaa muhimu na kutoa ajira kwa wananchi wengi.Pia aliwaagiza viongozi wa mkoa na halmashauri wahakikishe wanatoa kipaumbele kwa wawekezaji kwa kuwasogezea miundombinu ya huduma mbalimbali zikiwemo za maji na umeme ili watekeleze majukumu yao vizuri.Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Lakairo Investment, Daniel Lameck alisema mbali na ujenzi wa viwanda hivyo vinavyotarajiwa kutoa ajira 200 hadi 300, pia wanatarajia kujenga viwanda vingine vya kutengeneza mafuta ya kupaka, dawa za viatu na kusaga nafaka.Lameck alisema mbali na mafanikio wanayoyapata, pia wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji, akitolea mfano mpango wao wa kutaka kujenga viwanda vingine viwili ambao umekwama kutokana na upatikanaji wa fedha.Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali iweke mfumo rafiki kwa ajili ya kuwawezesha wawekezaji wa ndani ili viwanda wanavyovianzisha viwe endelevu na vipanuke zaidi.
uchumi
KOCHA Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema baada ya mshambuliaji wake Haritier Makambo kupata ofa katika klabu ya Horoya AC ya Guinea alimuomba amsindikize ili asitapeliwe.Zahera aliyerejea jana alfajiri na mchezaji huyo wakitokea Guinea aliweka wazi kuwa hakwenda huko kwa mapenzi yake mwenyewe bali mchezaji ndiye aliyemuomba msaada.“Makambo mwenyewe aliomba akaniambia Kocha nimepata ofa naomba unisindikize ukanisaidie nisije nikatapeliwa, nami nikaona kweli hawa vijana wadogo wanaweza kudanganyika,”amesema.Akizungumzia kama tayari ameshasaini, alisema sio kweli kwani alikwenda kufanyiwa vipimo na mazungumzo hivyo wameleta taarifa kwenye uongozi kuamua kwasababu bado ni mchezaji wa Yanga mwenye mkataba.Alisema kama Yanga wakiamua kumuuza basi fedha zitakazopatikana zitakuwa ni kwa ajili ya klabu na zitasaidia katika usajili mpya kwa kutafuta wachezaji wengine wenye uwezo huku akikanusha taarifa za kuwa mchezaji huyo alikuwa akicheza kwa mkopo akitokea Motema Pembe ya DR Congo kama zinavyozagaa mitandaoni.Alitolea ufafanuzi kuwa ikiwa mchezaji analipwa kwa mfano Sh 100 na akapata kwingine wakatoa ofa kubwa zaidi sio mbaya kwa mchezaji kilichobaki ni maamuzi ya muhusika na viongozi kuamua kwani bado wanaweza kumbakisha wakikubaliana.Hata hivyo, alikataa kutaja kiwango cha mauzo ya mchezaji huyo akisema litakuwa ni suala la uongozi wa Yanga kama litaafikiana na klabu husika na sio jukumu lake kusema.Hivi karibuni kulikuwa na taarifa juu ya mchezaji huyo kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu hiyo baada ya kuonekana picha akiwa anasaini na amevaa jezi zao.Tayari Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla aliweka wazi juzi kuwa hakuna maafikiano yoyote kwasababu alichokuwa anajua mchezaji alikwenda kufanyiwa vipimo vya afya hivyo hakukua na makubaliano yoyote mpaka mazungumzo ya pande mbili yatakapokamilika.Alisema kuna ofa nyingine mezani na kwamba wataangalia dau litakalonona ndilo watakubaliana.
michezo
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) yenye jukumu la kukadiria, kukusanya na kuhasibu mapato ya serikali, ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo mstari wa mbele kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa vitendo katika kutekeleza azma ya serikali ya kuleta maendeleo.Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitatu, imefanikiwa kuongeza makusanyo ya mapato kutoka wastani wa Sh bilioni 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa Sh trilioni 1.3 kwa mwezi kwa sasa.TRA imeendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato. Mwaka 2015/16 makusanyo yalikuwa Sh trilioni 12.5, mwaka 2016/17 yaliongezeka hadi kufikia Sh trilioni 14.4 na mwaka 2017/18 yaliongezeka hadi Sh trilioni 15.5.Mapato yote yaliyokusanywa kwa miaka mitatu mfululizo ni Sh trilioni 42.4. Taarifa ya makusanyo ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha 2018/19 kuanzia Julai hadi Septemba 2018 inaonesha TRA imekusanya Sh trilioni 3.84 ikilinganishwa na Sh trilioni 3.65 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha wa 2017/18.Ongezeko hili la ukusanyaji mapato ni hatua kubwa nchini ambalo kwa kiwango kikubwa limechangiwa na kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na umma kumwelewa Rais hivyo kujitoa kwa dhati kumuunga mkono. Uongozi thabiti wa Rais Magufuli na wasaidizi wake ndiyo umefanikisha mafanikio haya kiuchumi.Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa pamoja na viongozi wengine wa serikali wamekuwa wakishiriki mapambano dhidi ya ukwepaji kodi unaosababisha upotevu wa mapato ya nchi.Juhudi za Rais Magufuli zimeshuhudiwa akitekeleza kwa vitendo ahadi mbalimbali alizotoa ikiwamo ya wakati akifungua rasmi bunge la 11 mkoani Dodoma; Novemba 20, 2015. Aliahidi kupambana vikali na ukwepaji kodi na upotevu wa mapato ya serikali. Akifungua Bunge hilo, Rais Magufuli aliahidi kupambana na ukwepaji kodi na upotevu wa mapato ya serikali.Katika kipindi cha uongozi, ameongoza na kuhamasisha wananchi kulipa kodi kwa hiari pamoja na kukemea udanganyifu unaofanyika kwenye risiti za kielektroniki (EFD). Wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Morogoro mpaka Makutupora jijini Dodoma, Rais alisisitiza kuwa kodi husaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini na kuboresha huduma za jamii.“Napenda kuwahimiza Watanzania wote kuendelea kulipa kodi ili kutekeleza miradi ya maendeleo nchini pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii. Pamekuwepo na mtindo, mtu anapokwenda kununua bidhaa anapewa risiti ya bei ndogo badala ya risiti anayotakiwa kupewa.” “Mtoa risiti na mpokeaji wote kwa pamoja wanaiibia serikali na hivyo wanasababisha kuchelewesha maendeleo, ninawaomba Watanzania tuwe wazalendo,” alisema.Licha ya ongezeko la makusanyo, ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Magufuli, TRA imeboresha mifumo yake ya ukusanyaji mapato kumrahisishia mwananchi kulipa kodi stahiki na kwa wakati. Miongoni mwa hatua zilizofanyika ni a uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuboresha daftari la walipakodi na kuifanya itumike katika kufanya mawasiliano na TRA hususani katika huduma za kielektroniki.Katika muktadha wa kuhakikisha watu hawakwepi kulipa kodi, TRA imeendelea kudhibiti uingizaji wa bidhaa za magendo nchini kwa kuimarisha doria sehemu za mipakani na mipaka isiyo rasmi ambayo ni maarufu kwa kupitisha bidhaa za magendo.Udhibiti huu unalenga kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa nchini zinapitia njia rasmi na zinalipiwa kodi na ushuru stahiki kwa mujibu wa sheria, ikiwa pia ni njia mojawapo ya kulinda viwanda vya ndani.Aidha, TRA kupitia Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi imejikita kuhudumia na kuelimisha walipakodi na wadau mbalimbali waelewe umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kwa manufaa yao na taifa kwa jumla. Kupitia idara hiyo, mamlaka imefanikiwa kuongeza uelewa wa masuala ya kodi kwa wananchi. Hivi sasa semina, vyombo vya habari, machapisho, makongamano, tovuti, mitandao ya kijamii pamoja na kituo cha huduma kwa mteja kilichopo ndani ya TRA hutumika zaidi kufikisha ujumbe kwa walipakodi. Mafanikio mengine ni ufunguzi wa vituo vya pamoja vya huduma mipakani.Miongoni mwa vituo hivyo ni kituo cha Rusumo kilichopo mkoani Kagera kilichozinduliwa Aprili, 2016 na Rais Magufuli pamoja na na Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Kituo kingine ni cha Mtukula kilichopo mkoani Kagera kilichozinduliwa na Rais John Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni Novemba, 2017. Vituo vingine ni Holili kilichopo mkoani Kilimanjaro na Tunduma cha mkoani Songwe.Vituo hivi kwa pamoja husaidia kuharakisha utoaji wa huduma mipakani, kuokoa muda wa kushughulikia mizigo na abiria, kukuza biashara na hatimaye kuongeza ukusanyaji wa mapato baina ya nchi zinazopakana.Sambamba na hayo, serikali imeendelea kuwajali na kuimarisha uhusiano na wafanyabiashara nchini. Kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai mosi hadi 31 Desemba mwaka huu, serikali TRA imetoa msamaha maalumu wa riba na adhabu katika malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 na mwisho wa kuwasilisha maombi ya msamaha huo ni Novemba 30, 2018.Msamaha huo unalenga kutoa unafuu kwa walipakodi wenye mzigo wa malimbikizo ya madeni ya kodi kwa kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi (principal tax) baada ya kuondoa riba na adhabu kabla ya Juni 30, 2019. Hadi mwishoni mwa Oktoba mwaka huu, TRA ilipokea maombi ya kusamehe riba na adhabu kutoka kwa walipakodi 2,029 yanayofikia Sh bilioni 245.6. Baadhi ya walipakodi hao wameshapewa majibu na wengine wako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa maombi yao.
kitaifa
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amewataka watu kushiriki michezo ili kujenga afya bora zitakazowawezesha kufanya kazi kwa bidii na kuinua uchumi wa nchi.Hayo aliyasema mjini hapa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Kimataifa ya Olimpiki iliyofanyika wilayani Chato mkoani Geita na kushirikisha zaidi ya watu 700.Siku ya Olimpiki huadhimishwa Juni kila mwaka, lakini nchini imefanyika kitaifa jana kutokana na Juni 23, tarehe iliyopangwa awali kuingiliana na Michezo ya Shule za Msingi (Umitashumta) na hivyo kufanyika jana.Alisema taifa linatakiwa kuwa na watu wenye afya njema, wazee kwa vijana, ambao wataweza kulijenga taifa kwa kuchapa kazi kwa bidii bila ya kusumbuliwa na magonjwa na matatizo mengine yanayosababishwa na afya duni.Alisema kamwe huwezi kujenga nchi kama wananchi wako watakuwa na afya legelege, hivyo aliwataka kufanya mazoezi na kushiriki katika michezo ili kuwa na nguvu.“Kamwe huwezi kujenga uchumi kama watu wako watakuwa na afya legelege, hivyo jitahidini kushiriki michezo,“ alisema Kalemani wakati akizungumza na washiriki wa maadhimisho hayo ya Siku ya Olimpiki.Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, ambao ndio waandaaji wa maadhimisho hayo nchini kwa kushirikiana na mkoa husika alisema huu ni mwaka 125 tangu kuanzishwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).Aliwashukuru viongozi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na ile ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kwa kushirikiana nao vizuri hadi kufanikisha tamasha hilo la maadhimisho ya Siku ya Olimpiki.Katika maadhimisho hayo, watoto wenye umri mdogo zaidi wa kike na kiume, Lukumai Mrisho (3.5) na Gift Munawe (3) kila mmoja aliondoka na zawadi ya fedha taslimu Sh 50,000 na mwanaume na mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi, Anicet Magayane (62) na Bertha Henry (53) nao kila mmoja aliondoka na kiasi kama hicho cha fedha.Mbali na hao, pia mtoto mlemavu, Ramadhani Fredy mwenye umri wa miaka minne naye aliondoka na kitita cha Sh 50,000 baada ya kumaliza mbio za kilometa 2.5.
michezo
WABUNGE wameonesha kukerwa na kutokamilika kwa mazungumzo na kampuni ya China inayotaka kuwekeza bandari ya Bagamoyo kwa takribani miaka saba sasa.Aidha wamesema mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa miaka saba sasa huku nchi nyingine zikikamilisha miradi kama hiyo katika muda mfupi ni dalili kwamba kundi linalofanya mazungumzo limeshindwa kutekeleza wajibu wake na kuiweka nchi katika safari nzuri ya kiuchumi.Pia wamesema kitendo cha kushindwa kukamilisha mazungumzo hayo kwa sababu zilizoelezwa kwamba ni kwa manufaa ya taifa hazina mashiko.Wakichangia katika hoja ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliyotolewa bungeni Alhamisi iliyopita wabunge waliitaka serikali kukamilisha mazungumzo hayo kwa manufaa ya taifa.Wakati wa uwasilishaji wa hoja ilielezwa kuwa mradi huo umesimama kwa kuwa masharti yaliyowekwa katika kufikia mkataba ikiwamo kuachiwa jukumu la tozo katika bandari na pia suala la uanzishwaji wa viwanda katika eneo la Bagamoyo na Tanga kuachiwa kampuni hiyo.Pamoja na kuitaka serikali kujieleza, baadhi ya wabunge wamesema kwamba Bunge liunde kamati ya kuishauri serikali na pia kuwa na nafasi kujadili uamuzi wa serikali inapoachana na miradi mikubwa ya kimkakati baada ya kutumbukiza fedha za umma hapo.Wakiungwa mkono na Spika Job Ndugai ambaye alizungumza kwa dakika moja akichangia hoja za wabunge wengine umuhimu wa mradi huo; yeye alibaki akishangaa kilichotokea mpaka serikali ikauacha.Wabunge walisema kwamba bandari ya Dar es Salaam kwa sasa pamoja na upanuzi wote, imefikia mwisho na haiwezi tena kubeba meli mpya za kizazi cha nne na kuendelea.Mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF) alisema inafaa Bunge na wananchi kuihoji serikali pindi inapoacha miradi mikubwa yenye tija kwa taifa kama mradi wa Bandari ya Bagamoyo.“Kwanini kama nchi tunaacha mradi kama huu...” alisema Ally na kuongeza mradi wa bandari haikuwa ujenzi wa bandari pekee, bali kutengeneza ukanda maalumu wa uchumi wa Bagamoyo ambao ungeleta ajira na kuifanya Dar es Salaam ipumue.Amesema kwa mujibu wa mradi huo mji wa Bagamoyo ungelikuwa wa kisasa zaidi na kutoa nafasi ya ukuaji wa nchi.Alisema bandari hiyo ambayo ingelikuwa kubwa katika Afrika na ya pili kufuatia bandari ya Rotterdam, Uholanzi ingeneemesha uchumi wa nchi kutokana na idadi za meli zilizokuwa zikitakiwa kutia nanga.Alisema wananchi wangefaidika kwa kuuza bidhaa mbalimbali ikiwamo matunda, maji na bidhaa nyingine zinazohitajika katika meli. Alisema haoni sababu ya kucheleweshwa kwa mradi huo wakati umepangwa kutekelezwa na nchi mbili rafiki za Oman na China.Spika Ndugai yeye akihoji kuna nini bandari ya Bagamoyo alisema kwa jinsi walivyopewa maelezo nchini China wakati wa moja ya ziara huko, mradi huo ni mkubwa mno na haiwezekani kuuachia hivi hivi tu.Alisema walipofanya ziara Shenzen, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwafikisha Makao Makuu ya kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali ya China Merchant na kupata maelezo.Alisema katika maelezo hayo waliambiwa kuna haja ya kuharakisha mazungumzo kwa kuwa wakuu wa Bodi wenye moyo wa dhati na Tanzania walikuwa wanakaribia kustaafu.“Sijui kuna nini... ukisikiliza presentation (maelezo) utaunga mkono,” alisema Spika Ndugai, akisisitiza kuwa haelewi nini kimekwamisha mradi huo muhimu ambao ungeitumbukizia nchi dola za Marekani bilioni 10.Aidha katika ziara hiyo ya mwaka juzi, Spika Ndugai alisema Wachina hao walisema kwamba wanashangaa kwa taifa kama Tanzania kuanza kujenga reli badala ya bandari kwani bandari ingelikuwa ya kwanza ili kupokea mizigo ya reli.Wabunge wengi waliochangia walisema kwamba ujenzi wa bandari hiyo na mji wake wa kiviwanda ungesaidia kurejesha kwa haraka gharama za ujenzi wa reli ya kisasa. Vile vile wajenzi hao walikuwa wanajenga reli ya kisasa kuanzia Bagamoyo na kuiunganisha na reli ya Tazara.Mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa (CCM) alisema mradi huo mkubwa wa kielelezi ambao ulihusisha ujenzi wa bandari, viwanda na kuwa eneo maalumu la kiuwekezaji likiwa na viwanda vikubwa 190 baada ya mazungumzo na kutia saini hati mbalimbali kushindwa kujengwa ni hasara kwa taifa.Alisema wakati Tanzania inaendelea kuzungumza katika kipindi hicho hicho cha kuanzia mwaka 2012 kampuni hiyo imejenga bandari za kisasa katika nchi za Djibouti, Togo, Nigeria na Sri Lanka.Alisema wananchi wa Bagamoyo walitoa sehemu kubwa ya ardhi wakitambua umuhimu wake, lakini ukiangalia ukubwa wa mradi na athari zake chanya katika uchumi wa nchi, serikali inawajibika kueleza kumetokea nini.Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) alitaka kujua sababu za kusimamisha mradi huo ambao ungeliingiza nchini dola za Marekani bilioni 10 na kuiweka Tanzania katika ushindani.Mbunge wa Buchosa, Charles Tizeba (CCM) alisema wakati SGR ikimalizika watanzania watakuwa kituko kwa kuwa kutakuwa hakuna bandari ya kuhudumia mizigo inayoletwa na reli hiyo na kuitaka serikali kuendelea na mradi wa bandari ya Bagamoyo.Alisema Bagamoyo ilikuwa ni jibu ya ubora wa wa reli inayojengwa ambayo inatarajiwa kuhudumia ndani na nchi za jirani.Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Magereli (Chadema) alisema kwamba tatizo linalokumba Tanzania liko katika sera na mipango na kusema taifa lazima liwe na uangalifu katika kupanga na kutekeleza maamuzi yake.Alisema kuna orodha ndefu ya mambo ambayo yanaanzishwa na kutumia fedha za walipa kodi halafu hayamalizwi na kuhoji kutotekelezwa kwa mradi wa bandari ya Bagamoyo kwa sababu za masharti yaliyotolewa na mwekezaji pamoja na hatua kubwa iliyokwishafikiwa na matumizi ya fedha za walipa kodi katika hatua hizo.Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM) alisema kama taifa lazima liwe na fikra mpya za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kukubali kuingia katika mikataba huku vihatarishi vyake vikijulikana, kwa kuzingatia maslahi mapana na thamani ya mradi wenyewe kwa umma.Alitaka timu ya mazungumzo kukwamua mazungumzo hayo na kuhakikisha kwamba nchi inasonga mbele.Wabunge wengine walioongelea bandari ya Bagamoyo ni Mbunge wa wa Rufiji Mohamed Mchengelwa (CCM) ambaye alisema ni aibu kwa wanasheria kukaa miaka saba kujadili mradi muhimu kama huo wakati nchi nyingine zinatekeleza miradi yao.Mwingine ni Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM), Mbunge wa Hanang Mary Nagu (CCM) ambaye alihusika kutia saini mradi wenyewe na mbunge wa Singida Magharibi, Elibarick Kingu (CCM) ambaye alisema kwamba wakati wa miaka 2008 na 2012 wakati wa utiaji saini naye alikuwa katika kitengo cha ushauri. Hata hivyo Waziri Kamwelwe alisema kwamba mazungumzo yanaendelea na kwamba anatarajia yatakuwa na mwisho mzuri.
uchumi
Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa na mashabiki wengi, Goms ilikuwa ya kwanza kupata bao mapema dakika ya tatu lililofungwa na Hamza Alaba.Lakini dakika ya saba Danis David aliisawazishia Itezi bao hilo na dakika ya 20 wakaongeza bao la pili lililofungwa na Salum Upuu na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa 2-1.Kipindi cha pili kila timu iliingia ikiwa na kasi na kuanza kushambuliana kwa zamu, lakini Itezi walionekana kuwa na kasi ya mchezo lakini makosa ya kufanya faulo karibu na eneo ya goli yaliwagharimu baada ya Goms kutumia faulo na kusawazisha bao lililofungwa na Chinedu Michael dakika ya 70.Bao hilo liliamsha nderemo kwa mashabiki wa Goms na kuanza kushangilia na kutoa kejeli kwa Itezi, hali iliyowapa nguvu wachezaji wao na kufanikiwa kuongeza bao la ushindi dakika ya 78 lililofungwa na Hamza Alaba.Goms ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Ndondo mkoa wa Dar es Salaam, wanasubiri mshindi kati ya Misosi ambao ni mabingwa wa Ndondo mkoa wa Dar es Salaam na Mnadani ya Mwanza kucheza fainali keshokutwa.Akizungumza baada ya mchezo kumalizika nahodha wa Itezi, Romario Albert alisema mechi ilikuwa nzuri na walitawala mchezo kwa kipindi kirefu lakini walifungwa na kuwaomba wana Mbeya kuendelea kuwasaidia.Nahodha wa Goms, Paul John alisema waliruhusu mabao mawili kipindi cha kwanza kutokana na kuidharau Itezi, hivyo kipindi cha mapumziko kocha alibadilisha mbinu na kufanikiwa kushinda.“Pia aliwataka mashabiki wa Goms kukaa mkao wa kula kwani safari hawarudii makosa kwa sababu mara ya kwanza tuliteleza lakini safari hii wapo vizuri.
michezo
['Nchini Uingereza mwezi Agosti ni wakati wa mapumziko na familia hutumia muda huo kujumuika pamoja baada ya shule kufungwa. ', 'Lakini kwa wachezaji wa ligi kuu ya England mambo ni tofauti, wachezaji wamerejea kazini huku kukiwa na hofu huenda wasipate kupumzika kwa karibu miezi 12.', 'Mchezaji wa Liverpool Sadio Mane amegusia suala hilo akisema hajapumzika vya kutosha kwa miaka saba, baada ya kutumia mwezi wote wa Julai kuisaidia Senegal katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. ', 'Wachezaji wengi wa Premier League walikuwa mapumzikoni baada ya mechi ya mwisho ya ligi hiyo Jumapili ya Mei 12. ', 'Hata hivyo baadhi yao walichelewa kwenda likizo hasa wachezaji wa Manchester City na Watford ambao walishiriki fainali ya kombe la FA wikendi iliyofuata.', 'Vikosi vya Liverpool na Tottenham pia vilishiriki fainali ya Champions League iliyochezwa mjini Madrid Juni mosi. ', 'Na hiyo ilikuwa kabla ya michuano ya Nations League, Copa America na Kombe Mataifa ya Afrika (AFCON).', 'Mane, alicheza jumla ya mechi 57 nyumbani, Ulaya na zingine za kimataifa katika kipindi cha zaidi ya miezi 11 katika msimu wa mwaka 2018-19.', 'Hii inamaanisha nyota huyo wa kimataifa wa Senegal wa miaka 27 alianza mazoezi ya msimu mpya Jumatatu ya Agosti 5- siku 17 baada ya kufanya mazoezi yaliyopita ', '"Nadhani niko tayari," alisema Mane aliyejipata katika hali kama hiyo miezi 12 iliyopita baada ya kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi.', '"Sina muda wa kupumzika. Nimekuwa nikicheza kwa muda mrefu. Sijawahi kwenda likizo kwa zaidi ya siku 20 katika kipindi cha miaka saba lakini nimezoea. Sasa niko tayari. Nipo hapa sasa twende kazi."', 'Wachezaji wenzake Mane kama vile Alisson, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Naby Keita ni baadhi ya wachezaji wa ligi ya Premia walioshiriki mashindano ya msimu wa joto hatua iliyowafanya kukatiza likizo zao kabla ya ligi mpya msimu mpya kuanza.', 'Lakini kwa wachezaji ambao hawakushiriki mashindano walitarajiwa kufanya mazoezi baada ya msimu kwisha ili kujiimarisha huku wengine wao wakilazimika kwenda na wakufunzi wa kibinafsi likizo.', 'Kandarasi ya wachezaji inasema nini kuhusu likizo?', 'Kwa mujibu wakandarasi ya Ligi ya Premia/Soka ya Ligi ya Uingereza, wachezaji wanastahili kwenda likizo ya "wiki tano ya kulipwa wakati ambao utaamuliwa na klabu- ikiwa mchezaji yuko katika kikosi cha kwanza au anahitajika kushiriki mechi ya kimataifa".', 'Mazingira ya kazi yao haiwaruhusu kusugeza mbele likizo "Klabu hata hivyo haitamzua mchezaji kuchukua angalau likizo ya wiki tatu bila msingi".', 'Hilo lingefakiwa ingelikuwa jambo la kuvutia sana kwa Mane, na mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min ambaye alicheza mechi 78 na kusafiri zaidi ya km110,000 kuiwakilisha Korea Kusini mwaka uliopita.', 'Muungano wa kimataifa ya data ya wachezaji ilionesha kuwa wachezaji mashuhuri 16 walicheza karibu mechi 80 katika msimu wa mwaka 2018-19.', 'Wachezaji wanapigika sana?', 'Likizo ya msimu wa joto huchukuliwa kama likizo ya siku kuu ya Krismasi na wachezaji Barani Ulaya, na baadhi yao hujivinjari mbali na familia na marafiki zao katika migahawa mikubwa kabla ya michezo ua siku ya kufungua zawadi. ', 'Jedwali lisilokuwa na muda wa mapumziko limekosolewa sana kocha wa Liverpool Jurgen Klopp na mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola. ', 'Klopp alisema: "Ikiwa hatutajifunza jinsi ya kuwasiliana na wachezaji kwa njia bora, wakati wa mashindano, basi huenda tukaangamiza huu mchezo mzuri. Kwa sababu bila wachezaji, hakuna litakalofanyika."', 'Guardiola anasema michezo ya wakati wa sherehe "inawamaliza" wachezaji wake japo msimu huu angalau watapumzika wikendi moja mwezi Februari, hatua ambayo Shirikisho la Soka limesema ni "muhimu".', 'Lakini kabla ya kuangazia zaidi maslahi ya wachezaji, ni vyema kutilia maanani kuna baadhi ya kazi ambazo watu wanachukua muda mrefu zaidi ofisini ikilinganishwa na mazoezi ya kandanda.']
michezo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili jijini Cairo, Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ameongozana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na maofisa wengine wa serikali.Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, katika ziara hiyo, kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa Misri, El Sisi.Aidha, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Misri, Dk Moustafa Madbuoly na baadaye kukutana na wafanyabiashara wa Misri na Watanzania waishio nchini humo.Pia Waziri Mkuu Majaliwa akiwa nchini humo, atatembelea miradi mbalimbali ya ujenzi na kilimo ili kujifunza na kuona jinsi Tanzania inavyoweza kuazima utaalamu na uzoefu.Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Mji mpya wa Serikali jijini Cairo, kilimo cha samaki, viwanda vya uchakataji ngozi, kituo cha kufundisha masuala ya Bahari.Pia atatembelea mfereji wa Suez. Aidha, atashuhudia utiwaji wa saini wa mikataba mbalimbali ukiwemo mkataba wa ushirikiano wa vyombo vya habari baina ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) na Middle East News Agency (MENA).
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 wanaotarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu.Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini mwaka huu chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China.Ametoa ahadi hiyo alipokutana na Mwenyekiti wa Touchroad Group, Liehui He na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB, Jaji mstaafu Thomas Mihayo ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa na Liehui kwamba kundi hilo la watalii likiwa Djibouti litapokelewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na likienda Zimbabwe litapokelewa na Rais wa nchi hiyo.“Tanzania imeamua kuweka mkakati wa kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza utalii kupitia vivutio vya vyakula vya asili, mavazi ya asili, wanyama, fukwe za bahari na milima.Kwa hiyo, ujio wa kundi hili kubwa, unatoa fursa mpya ya kutangaza vivutio vya nchi yetu,” alisema.“Nitoe wito kwa Watanzania wanaoishi maeneo ya jirani na vivutio vyetu, wachangamkie fursa ya ujio wa watalii hawa katika maeneo mbalimbali. Wakifika Dar es Salaam, wanaweza kwenda Kigoma kuona Ziwa Tanganyika, mbuga zilizoko Nyanda za Juu Kusini, Arusha au vivutio vya Zanzibar. Tujiandae, tuwe tayari kuwauzia bidhaa mbalimbali,” alisema.Pia alisema amefurahishwa na wazo lao la kuifanya Dar es Salaam iwe kitovu cha utalii kwa makundi ya watalii ambayo yatakuja Tanzania na baadaye kutoka Tanzania kwenda Lusaka, Harare, Johannesburg na Djibouti.Mwenyekiti huyo ambaye aliwasili nchini juzi, ameambatana na ujumbe wa watu 31 ambao unajumuisha waandishi wa habari, wasanii, wanamuziki na watu mashuhuri.Akiwa Beijing, China, wakati akishiriki Mkutano wa Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na China lililofanyika Septemba mwaka jana, Waziri Mkuu alikutana na uongozi wa Kampuni ya TouchRoad ambayo ilionesha nia ya kutangaza fursa za utalii zilizopo nchini.Ziara ya Liehui ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyoingiwa kati ya Kampuni ya TouchRoad na Bodi ya Utalii ya Tanzania, Novemba mwaka jana.Mapema, Liehui alimweleza Waziri Mkuu nia ya kampuni hiyo kutekeleza makubaliano yao ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika soko la China ili kuvutia watalii wapatao 10,000 watembelee nchini mwaka huu.“Tumepanga kuleta watalii 10,000 kwa mwaka huu wa 2019 na tumeweka lengo la kuongeza idadi hiyo kwa asilimia 20 kila mwaka kwa muda wa miaka mitano. Pia tuna lengo la kuitumia ndege ya ATCL ili ilete watalii moja kwa moja kutoka Shanghai, China,” alisema.Akielezea ujio wa kundi la kwanza la watalii, Liehui alisema kundi hilo litakaa Djibouti kwa siku moja, Tanzania siku nne (tatu za kulala) na Zimbabwe siku tatu (mbili za kulala) na kisha kurejea China.Alisema wanapanga kila mwezi wawe na kundi kubwa la watalii watakaokuwa wanafikia Tanzania na kupelekwa nchi nyingine kwa sababu Wachina wengi hupenda kufanya utalii kwa siku walau 10, lakini wapelekwe maeneo matatu au manne tofauti kuona vivutio vya aina nyingine badala ya kukaa sehemu moja kwa kipindi chote hicho.“Watalii hawa wakija kwa siku tatu au nne, wana uhakika wa kutumia dola za Marekani zaidi 2,000, wakienda eneo jingine watatumia fedha pia, namna hiyo tuna uhakika wa kuongeza Pato la Taifa, lakini pia tuna uhakika wa kutengeneza ajira kwa Watanzania,” alisema.
kitaifa
MKUU wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Frank Mwaisumbe amewataka wauza ardhi katika wilaya hiyo (madalali) wawili na kiongozi wa kijiji, kuripoti ofi sini kwake ili kuhojiwa baada ya kudaiwa kuwa wameuza ardhi mara mbili kinyume cha sheria na kuzua taharuki na mgogoro mkubwa wilayani humo.Alitoa agizo hilo baada ya kusikiliza mgogoro wa ardhi wa wakazi wa wilaya hiyo na mfanyabiashara mmarufu Arusha, Philemon Mollel na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Oriandeke, Saitoti Leketai, jana.Aliagiza mjumbe huyo ahojiwe kuhusu mgogoro huo, madalali wawili wa ardhi wilayani, Lekenywa Asamburii na Paulo Nabii kuchukuliwa maelezo juu ya mgogoro huo ofisini kwake wiki ijayo. Hatua hiyo imetokana na wakazi watatu wilayani humo, Ismail Abdi, Aisha Mkwawa na Jane Sylvester kulalamikia mbele ya DC huyo kuporwa ardhi yao na Mollel, muuza nafaka na mazao mkoani Arusha.Akizungumza katika kikao hicho, Abdi alidai mwaka 2007 alifika Ofisi ya Serikali Kijiji cha Oriandeke na kuomba eneo la ardhi kujenga maegesho ya magari makubwa, hivyo alikubaliwa kwa masharti ya kujenga darasa moja. Alisema baada ya kupatiwa eneo hilo, alilisafisha na kulipima na alipata viwanja vitatu, namba 97, 99 na 101 kitalu E, lakini wakati akitaka kujenga ghafla eneo hilo lilizungushiwa ukuta na kuwekwa nguzo. Jane alisema mwaka 2010 alipewa kiwanja namba 141 na serikali ya kijiji hicho, ambako mwaka 2010 alifanikiwa kukipima na kisha kukilipia, lakini ghafla alikuta eneo lake limezungushiwa ukuta na Mollel.Aisha alilalamika mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo kwamba ameporwa kiwanja namba 143 ambacho alikilipia kisheria na mfanyabiashara huyo huku akiiomba serikali imsaidie kupata haki yake stahiki.Mollel alipopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya kikao hicho, alipinga tuhuma za kupora viwanja hivyo na kubainisha mbele ya Mkuu huyo kwamba mwaka 2012 alikutana naa baadhi ya madalali wa ardhi wilayani humo ambao walimweleza kuna maeneo ambayo yanauzwa na serikali ya kijiji hicho. alidai alifika ofisi za kijiji hicho na kununua ardhi, ekari moja na nusu na kisha kulipia Sh milioni nane, na alipewa mkataba na kisha kuanza mchakato wa kuvipima na kufanikiwa kupata viwanja vinane. Mwaisumbe aliamuru madalali na viongozi waliohusika kuuza maeneo hayo waletwe mbele ya kikao hicho ili waeleze mchakato wa ununuzi wa maeneo hayo kabla hajatoa uamuzi wa mgogoro huo.
kitaifa
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kuishauri vizuri serikali juu ya utendaji wa wakala ili azma ya kuboresha mazingira ya biashara na kufi kia uchumi wa kati unaotegemea viwanda itimie.Alisema hayo akizindua bodi hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kakunda aliishauri itoe ushauri ikiwa na uhakika wa mipango na malengo ya Brela na wakati huo huo ikilinda maslahi ya taifa.“Simamieni utendaji na utekelezaji wa majukumu ya wakala na shaurini kwa kuzingatia mwelekeo wa mahitaji ya nchi katika kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda,” alisema Kakunda na kuongeza kuwa juhudi za bodi katika kusimamia Brela ilenge katika kuongeza mapato ili kuiwezesha serikali kujiendesha kwa ufanisi.Aliipongeza Brela kwa kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa njia ya mtandao, lakini ameitaka ijipange vizuri kuwahudumia wateja wake hasa katika eneo la kurasimisha biashara na viwanda kwani hivyo ndivyo vitu Tanzania inategemea kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.“Nimeambiwa kuna changamoto zinazoikabili wakala, naamini kwa kuwepo kwa bodi na ushirikiano wa menejimenti zitatatuliwa. Fuateni miongozo, sheria na kanuni za utumishi wa umma ili kufikia malengo na utendaji wenye ufanisi,” alisema.Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Emmanuel Kakwezi, aliiambia hafla hiyo kwamba mfumo wa awali wa usajili wa majina na biashara ulikamilika Mei 2, 2015, na kuongeza kuwa Brela tayari imejenga mfumo mpya wa usajili wa jumla na umeanza kutumika Februari mwaka huu.Alisema wateja wa wakala wanaweza kupata huduma popote walipo bila kufika Dar es Salaam. Alisema mradi wa Brela umeunganishwa na masijala nyingine zinazotegemeana kama vile za Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).Alisema mradi wa mfumo wa ‘national business portal’ unafanyiwa majaribio tangu Novemba Mosi, mwaka huu na Brela inatarajia kuwa dirisha la uwezeshaji biashara. Alisema Brela imepanga kufanya kampeni ya kutoa elimu kwa wananchi katika mikoa yote nchini, ingawa ina upungufu mkubwa wa wafanyakazi.Mwenyekiti wa Bodi ambayo imeundwa Juni mwaka huu, John Lyanga, alisema bodi itajitahidi kuondoa kabisa kero za wafanyabiashara wa aina zote “kwa kuwa Brela ndiyo mlango wa kwanza katika urasimishaji biashara.”
kitaifa
 JKT Queens imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara kwa kufikisha pointi 39 ikifuatiwa na Simba Queens yenye pointi 28.Baada ya zote kucheza michezo 13. JKT Queens bingwa mtetezi hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa ligi ikiwa imefikisha mzunguko wa pili ikiwa imefunga mabao 76 na Simba Queens imeshinda michezo tisa, sare moja na kufungwa mitatu.Alliance Girls ya Mwanza inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 26, ikiwa imeshinda michezo minane, sare mbili na kufungwa mmoja na Mlandizi Queens ya Pwani ina pointi 26 ikiwa imeshinda michezo minane, sare mbili na kufungwa mitatu.Panama ya Iringa inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 25 baada ya kushinda michezo minane, sare moja na kufungwa minne, Sisterz FC ya Kigoma ina pointi 24 ikiwa imeshinda michezo saba, sare tatu na imefungwa michezo mitatu .Yanga Princess ina pointi 19 ikiwa imeshinda michezo sita, sare moja na kufungwa mechi sita, Baobab ya Dodoma ina pointi 12, ikiwa imeshinda michezo mitatu, sare tatu na kufungwa michezo saba.Tanzanite ya Arusha ina pointi 10, ikiwa imeshinda michezo mitatu, sare moja na kufungwa michezo tisa, Marsh Queens ya Mwanza ina pointi saba, ikiwa imeshinda mchezo mmoja, sare nne na kufungwa michezo nane.Evergreen ya Dares Salaam ina pointi tano baada ya kushinda mchezo mmoja, sare mbili na kufungwa michezo kumi na Mapinduzi ya Njombe ina pointi mbili ikiwa na sare mbili na kufungwa michezo 11.Ligi inatarajiwa kuendelea Machi 20 ambapo Alliance Girls itaikarisha Simba Queens katika Uwanja wa Nyamagana Mwanza, Tanzanite itaialika Yanga Princess katika uwanja wa Sheikh Abeid Kaluta Arusha na Baobab itacheza na Panama FC ya Iringa katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.Mapinduzi ya Njombe itawaalika vinara JKT Queens katika Uwanja wa Sabasaba Njombe, Evergreen itacheza na Marsh Queens katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na Sisterz itaikaribisha Mlandizi Queens kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Bingwa wa msimu huu ataiwakilisha nchi katika mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
michezo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea treni ya kwanza ya mizigo kutoka Tanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa reli ya kutoka Tanga hadi Moshi huku akisisitiza kuwa ujenzi wa reli hiyo ni kwa kutumia fedha za ndani.Alipokea treni hiyo jana baada ya kuwasili saa 4:30 asubuhi kwenye stesheni ya Moshi na kukata utepe wa uzinduzi saa 4:32, kisha akapanda kwenye treni hiyo saa 4:33.Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Moshi na wengine kutoka mkoa jirani wa Tanga, Waziri Mkuu alisema amefurahi kupokea treni hiyo yenye mabehewa 20 yaliyokuwa na mzigo wa tani 800 za saruji kutoka kampuni ya Saruji ya Tanga.Alisema kukamilika kwa kipande cha reli ya Tanga - Moshi na kuanza kutoa huduma jana ni mwendelezo wa utekelezaji wa dhamira ya Serikali kuhakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inafaidika na fursa ya kijiografia iliyopo nchini kwa kutoa huduma za usafiri na uchukuzi wa reli kwa uhakika, usalama na kwa gharama nafuu.“Wataalamu wa masuala ya usafirishaji duniani wanaeleza kuwa matumizi ya reli kwa ajili ya usafirishaji wa shehena, hupunguza gharama za bidhaa kwa asilimia kati ya 30 na 40. Vilevile, matumizi ya reli huwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kutokana na ukweli kwamba, kupitia usafiri wa reli unaweza kusafirisha mizigo mingi kwa haraka na kwa wakati mmoja kwenda kwa mlaji,” alisema.Alisema kama ilivyo kwa mradi wa SGR, njia ya reli ya Tanga - Moshi yenye urefu wa kilometa 353, ukarabati wake unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umetekelezwa na wataalamu wazawa.“Kwa msingi huo, naagiza viongozi na watendaji wa mikoa na maeneo ambayo yanapitiwa na reli hii, kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania, waanze mara moja kampeni ya kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama lakini pia kuwakumbusha wananchi kuwa walinzi wa miundombinu hii muhimu ya reli,” alisema.Akitoa salamu kwa niaba ya makatibu wakuu wa vyama 19 vya siasa nchini, Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo alisema kufufuliwa kwa treni hiyo ya mizigo kutawasaidia wachimbaji wa madini walioko Makanya, Same ambao walikuwa wakipata taabu ya kukodisha malori na kusafirisha bidhaa zao hadi kiwanda cha saruji cha Tanga.Alisema reli hiyo itawanufaisha pia wachimbaji wa Kabuku, wilayani Handeni.“Wachimbaji wa madini ya chuma walioko Kabuku, walikuwa wanapata shida ya kusafirisha mizigo yao kwa barabara hadi Mtwara, gharama ziko juu mno. Lakini sasa watapata ufumbuzi baada ya reli hii kufufuliwa.”Mapema, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema makadirio ya gharama za kufufua reli hiyo kutoka Korogwe hadi Arusha yalikuwa Sh bilioni 14 lakini m
kitaifa
['Chelsea imetoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Times)', 'Babake Cavani amesema nyota huyo atajiunga na Atletico Madrid ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itaafikiana na PSG. (Guardian)', 'Tottenham wanamlenga mshambuliaji wa Real Sociedad, Mbrazil Willian Jose na kiungo huyo wa miaka 28-anatarajiwa kusafiri London kwa mazungumzo. (AS)', 'Klabu sita za ligi ya premia zinataka kumsaini beki wa Tottenham Muingereza Danny Rose, 29, mwezi huu. (Sky Sports)', 'Tottenham wanapanga kutoa ofa ya pili ya kumnunua mshambuliaji wa Fenerbahce na Kosovo Vedat Muriqi. (Aksam, via Sport Witness)', 'Beki wa Shakhtar Donetsk na Ukrain Mykola Matviyenko, 23, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Manchester City, yuko katika mazungumzo na Arsenal, ajenti wake anasema. (Football.London)', 'West Ham imeonesha nia ya kutaka kununua winga wa kimataifa wa Ukochi na Bournemouth Ryan Fraser, 25, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu wa joto. Kiungo huyo pia ananyatiwa na Arsenal na Liverpool. (Mirror)', 'Everton bado wanamtaka mshambuliaji wa Gremio Mbrazil Everton Soares, 23. (UOL, via Star)', 'Barcelona wanajitahidi kukamilisha mkataba wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 28, baada ya kumkosa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Sport)', 'Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumuuza kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, msimu wa joto, na huenda wakamnunua kipa wa Burnley Nick Pope, 27. (90Min)', 'Winga wa Uholanzi Tahith Chong, 20, yuko tayari kuondoka Manchester United mwisho wa msimu huu. (Goal.com)', 'Middlesbrough, Stoke na Derby wanasubiri kuona ikiwa Bournemouth itamruhusu beki Muingereza Jack Simpson, 23,kuondoka kwa mkopo. (Sky Sports)', ' Inter Miami imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 31, na David Silva, 34, ambao wataondoka klabu hiyo msimu wa joto. (Sun)', 'Manchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kwa mkataba wa £55m mwisho wa wiki hii baada ya kuafikiana na Sporting Lisbon. (Mirror)', 'Mkufunzi wa Barcelona Quique Setien anasema kuwa klabu hiyo inamtafuta mchezaji atakayeziba pengo lililoachwa na mshambuliaji wa Uruguay aliyeumia Luis Suarez, 32 mwezi huu. (Sport)', 'Barca inapania kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Rodrigo Moreno lakini Valencia inataka kumnunua kiungo huyo kwa euro milioni 60. (Marca)']
michezo
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga ametangaza neema kwa wakulima ya kununua mahindi baada ya kupatikana kwa soko kubwa kwenye nchi za kusini mwa Tanzania zinazohitaji tani milioni moja.Kutokana na hali hiyo, Wiki hii Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na taasisi ambayo imepewa kazi ya kupeleka mahindi Zimbabwe wataanza kununua na kukusanya mahindi kutoka kwa wakulima. Hasunga alitoa tamko hilo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu, Aida Khenani (Chadema) ambaye alihoji serikali imejipangaje mwaka huu katika ununuzi wa mahindi kwa kuwa hivi sasa ni msimu wa mavuno.Akijibu swali hilo, Hasunga alikiri kuwa kwenye msimu uliopita wa kilimo kulikuwa na changamoto ya masoko ya zao hilo lakini serikali imekuwa ikihakikisha inatafuta masoko. “Hivi sasa tumepata masoko makubwa ya mahindi nchi za kusini, Rwanda wanahitaji zaidi ya tani 100,000, Burundi wanahitaji zaidi ya tani 100,000, Zimbabwe wanahitaji tani 800,000 za mahindi na nchi nyingine nyingi zinahitaji kwa wingi,” alieleza. Hasunga alisema kwa sasa soko la mahindi ni kubwa sana na kutoa wito kwa wakulima wa mahindi kujitokeza kueleza kiasi alichonacho ili kushirikiana na serikali. “Pia taasisi nyingine ambayo imepewa jukumu kupeleka mahindi nchini Zimbabwe itaanza kununua mahindi wiki hii. Wakulima wakae mkao wa kula kwa kuwa hivi sasa ni wakati wa kula mkate mzuri,”alisema. Katika swali la msingi, Mbunge wa Namtumbo, Edward Ngonyani (CCM) alisema Mkoa wa Ruvuma umepata mnunuzi wa tumbaku ambaye amekubali kuwawezesha Chama cha Ushirika (Sonamcu) kufufua kiwanda cha kuchambua tumbaku na kugeuza Green Leaf kuwa Dry Leaf. Katika swali lake Ngonyani alitaka kuijua Serikali itasaidiaje kutatua changamoto zinazomkabili mnunuzi wa tumbaku hasa kutokana na kuwapo kwa changamoto za kodi na soko mnunuzi kutotekeleza azma yake. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa alisema kutokana na kuondoka kwa kampuni mbili za ununuzi wa zao hilo mkoani humo mwaka 2014/15 wakulima walikosa soko la uhakika na hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada za kutatua changamoto hiyo. Alisema jitihada hizo zilisaidia kupatikana kwa mnunuzi wa tumbaku ambaye ni kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) ambayo ilianza kununua kilo 250,000 na sasa imeongeza hadi kilo 1,000,000.“Serikali pia inapongeza nia ya kampuni hiyo ya kutaka kukiwezesha Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa huo cha Sonamcu kufufua kiwanda cha kuchakata tumbaku,” alisema. Bashungwa alisema kuwa Wizara ya kilimo ipo tayari kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na mwekezaji huyo kutafuta ufumbuzi wa changamoto za mnunuzi huyo ili kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inatimiza azma hiyo.
kitaifa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Tanzania haina shida ya sukari kwa sababu inayozalishwa ndani ya nchi ipo na inatosha.Majaliwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda kwenye Maonesho ya Nne ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Rais John Magufuli alizindua maonesho hayo jana.Kwa mujibu wa Majaliwa, sukari ya Tanzania inazalishwa kwenye viwanda vilivyopo Tanzania bara na Zanzibar."Tuna fursa pia ya kukaribisha viwanda kutoka nje ya nchi kuja kwekeza hapa Tanzania. Moja ya wito wetu sisi kama Serikali na sisi kama Watanzania ni ujenzi wa viwanda. Mataifa yote haya ya nje yaliyokuja hapa yameleta bidhaa zao..." tunayo fursa ya wao kuja kuzalishia hapa kwetu, kuungana na Watanzania wenye ardhi, wenye mtaji ambao wanaweza kuunganisha na mtaji wa wageni wetu wakaanzisha kiwanda na kupanua wigo" amesema.Ametoa mwito kwa Watanzania kutembelea maonesho hayo ili waweze kutambua nani anataka kuja kuwekeza Tanzania ili waunganishe nguvu wajenge kiwanda chenye mtaji mkubwa, wazalishe bidhaa na kusaidiana kupanua wigo wa masoko.Majaliwa pia ametoa mwito kwa wafanyabiashara nchini kuziuza na kuzitambulisha vizuri bidhaa zao ili zipate masoko ndani ya nchi wanachama wa SADC na kwingineko.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi wanachama SADC yamekamilika kwa kiasi kikubwa na tayari kuna ratiba ya uingiaji wageni.Ametoa mwito kwa Watanzania kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vyote vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini."Sisi Watanzania tunayo sifa na heshima ya ukarimu.Tutumie nafasi hii sasa kuonyesha kwa kuwakaribisha wageni wetu, waingie nchini, wakae katika kipindi chote na warudi wakiwa salama lakini warudi wakiwa wamerudi na ujumbe wa ukarimu ambao tunao" amesema.
uchumi
MKUU wa mkoa wa Dar es Salama ametangaza kuwa wasanii na wanamichezo watajengewa ukumbi mkubwa wa kisasa wa burudani na bwawa la kuogelea utakaogharimu Euro milioni 200 ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 500.RC Makonda amesema ukumbi huo utajengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Kifaransa, ambapo zinahitajika hekta 15 wakati Bwawa la kuogelea litajengwa na moja ya kampuni kutoka Dubai. Alisema Bwawa hilo la kuogelea litajengwa karibu na Coco beach ambapo pia kutakuwa na kiwanja cha mpira.“Watu watajifunza kuogelea humo, pia kutakuwa na kiwanja cha mpira, tayari wafadhili wameshapatikana kujenga vitu hivyo, kwa sasa tunatafuta eneo la kujenga ukumbi wa kisasa.”alisema Makonda “Ukumbi tutakaojenga utaingiza watu 20,000 kwa wakati mmoja utakuwa ni wa kimataifa zaidi.” alisema Makonda alitoboa siri hiyo jana jioni wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya wasanii za maigizo na wanamichezo mbalimbali.Aidha Makonda aliwataka makundi hayo kuchangamkia mikopo ya vijana inayotolewa katika kila manispaa na kwamba wasanii wametengewa shilingi milioni 500. “Kila Halmashauri ina bajeti ya Shilingi bilioni 2 kwa makundi ya wanawake, vijana, walemavu, wasanii nimewapambania mpaka katika hiyo bilioni 2 mtengenewa bajeti yenu ya milioni 500 lakini nasikitika mnashindwa kutumia fursa hiyo.“Andaeni mpango mkakati mzuri, nendeni mkakope fedha hizo mfanye maendeleo, hivi mnashindwa kuandika ‘proposal’ nzuri mkaenda mkapewa milioni 20 mkatengeneza movie yenye ubora? “Mnabaki mnalilia lia njaa, mmefulia, alafu hamtaki kuchangamkia fursa, mnataka kukutana na viongozi mkipata nafasi mnaacha kuongea mambo ya muhimu eti mnataka siri, siri gani? “Nina makundi mengi ya kuwasaidia, nina masuala ya barabara, elimu, na mambo mengine kibao, kama nawaelekeza fursa zilipo na mkashindwa kuzitumia basi sitaweza kuwabeba tena.”alisisitiza.
kitaifa
KOCHA wa timu ya Yanga, Charles Mkwasa amesema ushindi walioupata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons umewapa nguvu ya kujipanga kuikabili Biashara United katika mchezo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Mkwasa alitoa kauli hiyo juzi baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi kwa kuifunga Tanzania Prisons bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Samora Iringa, na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 21. Alisema wanauchukulia mchezo huo kama fainali kwa kuwa ni moja ya timu zinazoonesha ushindani mkubwa kutafuta matokeo hususani kwenye viwanja vya ugenini.“Ninawashukuru wachezaji kwa ushindi tuliopata kwani umetuongezea nguvu ya kujipanga kwenye mchezo wetu unaokuja dhidi ya Biashara United kuhakikisha tunapata matokeo kama haya kujipanga na mchezo wetu wa Januari 4 dhidi ya Simba,” alisema Mkwasa Alisema mchezo uliopita walicheza kwa kiwango cha juu kwa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza lakini wachezaji wake walikosa umakini na kushindwa kumalizia kupata mabao ambayo yangewafanya kumaliza mchezo kipindi cha Kwanza. Alisema kipindi cha pili wapinzani wao walicheza mpira wa nguvu na kupiga vikumbo kuwatoa mchezoni jambo ambalo walifanikiwa lakini alitoa maelekezo kwa wachezaji wake kurudi nyuma kulinda ushindi waliopata kipindi cha kwanza. Naye kocha wa Tanzania Prisons, Mohamed Rishaard ‘Adolf’ alikubali matokeo na kukiri kufanya makosa katika dakika za mwanzo na kufungwa bao jambo ambalo hakulitegemea.“Sina sababu ya kusema uwanja shida lakini kimsingi tulifanya makosa na kuruhusu kufungwa bao la kizamani jambo ambalo sikutegemea, nimekubali kama benchi la ufundi tunaenda kujipanga na ratiba ya mechi zinazokuja kuhakikisha tunapata ushindi” alisema Adolf Alisema matokeo hayo kwa kiasi fulani yamevuruga malengo yao kwani ilikuwa ni kulinda rekodi yao ya bila kufungwa lakini kukosa umakini dakika za mwanzo zimewafanya wafungwe.
michezo
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali itaanzisha Wakala wa Viwanja vya Ndege nchini, ili kusimamia shughuli za viwanja zikiwemo za kudhibiti viwango vya mafuta ya ndege.Waziri Kamwelwe alisema hayo jijini hapa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi (Mamlaka za Viwanja vya Ndege (TAA). Kamwelwe alisema wafanyabiashara wa mafuta ya ndege wanaendesha kazi hiyo wenyewe bila udhibiti wowote.“Katika kuboresha mamlaka hii tupo mbioni kuanzisha wakala wa ndege ambayo yatasaidia kudhibiti masuala ya uuzaji wa mafuta, na mtakuwa mnatuuzia nyie, na mimi kama nitakuwa bado nipo baada ya miezi miwili mtasikia naisoma bungeni,” alisema Kamwelwe na kuongeza: “Unakuta mfanyabiashara wa mafuta ya ndege anajiendelea tu hana udhibiti wowote, mbona kwenye huduma nyingine zinadhibitiwa, kwanini huku kwenye ndege msimamizi asiwepo?” Aidha, alisema, mamlaka hiyo inatakiwa kuhakikisha kuwa inajenga uzio katika viwanya vya ndege, ambavyo havina uzio ili kuongeza ulinzi katika viwanja hivyo.“Uzio huu unatakiwa uwepo wa nje na wa ndani kwa lengo la kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama,” alisema. Pia Kamwelwe alisema Serikali ina mpango wa kuleta ndege mbili, ambazo zitatumika kwa ajili ya mafunzo ya rubani. Kwamba Uwanja wa Ndege wa Tanga ndio utakaotumika kwa kazi hiyo ya mafunzo kwa marubani.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela aliiomba serikali kuijengea uwezo taasisi hiyo, ikiwemo kuipatia nyenzo za kufanyia kazi na kuajiri wafanyakazi. Mayongela pia aliomba wafanyakazi hao waliopo, waongezewe mishahara na marupurupu mengine.Alisema;”Usiwaone leo wamevaa suti, lakini ukiwona siku za kawaida nyuso zao zimekunjamana kwani wana njaa.” Alisema wakati mamlaka hiyo inaanzishwa mwaka 1999, ilikuwa inakusanya Sh bilioni tatu lakini makusanyao hayo yameweza kuongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo mwaka wa fedha 2017/18 walikusanya Sh bilioni 70 kwa makusanyo ya ndani.
kitaifa
SHIRIKA la Makumbusho ya Taifa linatarajia kuanzisha mazungumzo rasmi ya jinsi gani Tanzania inaweza kunufaika na mikusanyo ya mjusi wa kale, aliyehifadhiwa katika makumbusho ya Berlin nchini Ujerumani.Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho, Mawazo Jamvi amesema hayo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa mazungumzo hayo, yataweza kupata majibu kama unufaikaji huo ni wa muda mrefu ama wa muda mfupi.Alisema hatua ya kuanzisha mchakato huo, inatokana na agizo lililotolewa kwa shirika hilo na Waziri Mkuu, la kurejeshwa kwa mikusanyo hiyo iliyoko nje ya nchi ikiwemo mjusi aina ya Dinosaur.Kuhusu agizo hilo, Jamvi alisema limeingizwa katika mipango yao ili kupata taratibu kamili za namna ya kuirudisha mikusanyo hiyo.Hata hivyo, amesema utekelezaji wa agizo hilo ni moja ya changamoto inayokabili shirika hilo kutokana na ufinyu wa bajeti, ambayo hadi sasa inadaiwa zaidi ya Sh milioni 700 ikitokana na masuala mbalimbali ya uendeshaji.Kadhalika amesema ufinyu wa bajeti umesababisha kushindwa kukarabati majengo na miundombinu ya makumbusho zilizopo nchini kukosa vitendea kazi, ikiwemo kompyuta na samani mbalimbali na hata kushindwa kujenga makumbusho nyingine na kuboresha zilizopo.“Suala la kurudisha kwa mikusanyo hiyo ni kitu cha muda mrefu chenye kuhitaji mazungumzo, au kujua namna Tanzania inavyoweza kunufaika nayo kabla haijarudi au wakati wakijenga taratibu za kurudisha,” alisema.Alisema jambo la msingi ni kwanza kutambua kama ipo mikusanyiko mingine, ambayo hawaijui kwa kuwa yote ilichukuliwa wakati wa ukoloni. Jamvi alisema katika utaratibu huo, shirika litaweka utaratibu namna ya kuitambua, ipi inafaa irudishwe kwa haraka na ipi ya muda mrefu.Kuhusu kipindi mikusanyiko hiyo ilipochukuliwa, alisema ilichukuliwa wakati wa utawala wa ukoloni na kwa sasa Tanzania inachonufaika nacho ni Tanzania kutangazwa kwa watalii mbalimbali, wanaoingia katika Makumbusho ilipohifadhiwa mikusanyiko hiyo na mahali ilipopatikana.Mjusi huyo aina ya Dinosaur ni mjusi mkubwa kuliko hata tembo anayeaminika kuwa ndiye mnyama mwenye umbo kubwa wa nchi kavu na mwenye uzito mkubwa, aliyehifadhiwa katika Makumbusho ya Viumbehai ya Berlin, Ujerumani. Mjusi huyo alivumbuliwa katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi miaka 100 iliyopita.Mjusi huyo ambaye ana uzito wa tani 50 ni kivutio adimu katika makumbusho ya Berlin, masalia ya mjusi huyo katika eneo la Tendaguru, yalikusanywa na kupelekwa Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho ya Berlin yaliyojen
kitaifa
.Rais John Magufuli amesema bado kuna ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watumishi wa idara ya mahakama nchini, hali ambayo haimfurahishi.Akihutubia jijini Dar es salaam katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini, Rais Magufuli amesema kuwa ukosefu huo wa maadili miongoni mwa watumishi wa idara ya mahakama umekua ukisababisha wananchi kukosa haki, kuwepo kwa idadi kubwa ya mahabusu zaidi ya wafungwa na kucheleweshwa kusikilizwa kwa kesi mbalimbali.“Hii inadhihirisha kwamba tatizo la uchelewashaji kesi bado lipo, na hili Mheshimiwa Jaji Mkuu amelisema, jambo hili linawahusu zaidi wapelelezaji, mwakilishi wa IGP yupo na vyombo vingine vya TAKUKURU vipo hapa viharakishe suala la upepelezaji, linawanyima haki Wananchi,” amesema Rais Magufuli.Amewataka watumishi wote wa idara ya mahakama nchini kuzingatia maadili ya taaluma zao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kushirikiana na vyombo vingine kuhakikisha idadi ya wafungwa magerezani pamoja na mahabusu inapungua.“Wafungwa ni 13,000 na kitu mpaka leo, lakini mahabusu ni 17,632. Bado katika eneo hili haijafanyika kazi vizuri, na hili siyo suala la mahakama kwani ninyi majaji na mahakimu mnasubiri kuletewa,” amesema Rais Magufuli. Kauli mbiu ya siku ya sheria nchini kwa mwaka huu ni Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.
kitaifa
KATIKA toleo lililopita, kulikuwa na makala yaliyoelezea namna sekta ya kilimo inavyochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kupitia makala hayo, pamoja na masuala mengine yalieleza namna utekelezaji wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2011 ulivyosaidia kuwezesha utambuzi wa mifugo nchini kwa kuondoa mifugo yote ya nje, kupunguza wizi na kupunguza migogoro.Endelea. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina anaamini katika kuboresha kosaafu za mifugo nchini, umeandaliwa mkakati wa kuziboresha. Umeandaliwa na kuzinduliwa kwa madhumuni ya kuzalisha ndama bora wa maziwa na nyama milioni moja kwa mwaka. Programu hiyo itahusisha matumizi ya teknolojia za uhimilishaji (MOET) na madume bora.Katika uhimilishaji mbegu, zitazalishwa katika Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa (NAIC) na kusambazwa kupitia vituo vya kanda vya uhimilishaji kwa bei elekezi ya Sh 5,000 kwa dozi.Aidha, uzalishaji wa viinitete utafanyika katika maabara ya kituo cha Taliri Mpwapwa iliyojengwa kwa gharama ya Sh milioni 400. Mafunzo kuhusu teknolojia ya uhimilishaji yalitolewa kwa wahimilishaji 204 kutoka maeneo mbalimbali nchini.Ukarabati wa kituo cha uhimilishaji cha taifa (NAIC) Usa River-Arusha, umefanyika kwa kununua vifaa vya maabara, trekta, reki na mtungi wa lita 2,000 kwa ajili ya kusafirishia kimiminika baridi cha nitrojeni na mitungi mitano ya lita 50 kwa Sh bilioni 1.3. Maofisa ugani wa mifugo waliwezeshwa vitendea kazi vya pikipiki 200 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za uhimilishaji.Mafunzo ya teknolojia ya uhimilishaji yalitolewa kwa wahimilishaji 204 kutoka maeneo mbalimbali nchini. Aidha, mafunzo ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa ikiwa ni pamoja na uhimilishaji yalitolewa kwa wafugaji 25,659 kwa njia ya mitandao ya kijamii.Kwa upande mwingine, waziri Mpina anasema katika kueneza ufugaji wa mifugo bora kupitia mikopo ya mifugo kwa wafugaji watakaojiunga katika vikundi kupitia miradi ya kopa ng’ombe/mbuzi lipa ng’ombe/mbuzi au kopa ng’ombe/mbuzi lipa maziwa. Madume bora ya mbegu za ng’ombe wa maziwa 20 yalitolewa kwa wafugaji katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini na mitamba 419 ilisambazwa katika vikundi vya wafugaji nchini.Vilevile Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imenunua na kusambaza mitamba 350 kwa wafugaji wa mkoa wa Tanga. Madume bora ya mbegu 11 kwa ajili ya NAIC yenye thamani ya Sh milioni 250 yamenunuliwa kutoka Afrika Kusini (5) na New Zealand (6) yenye uwezo wa kuzalisha mbegu bora takribani dozi 1, 320,000 kwa mwaka.Pia amesema uzalishaji wa mitamba kwenye mashamba inakozalishwa na kuweka mazingira wezeshi kwa Sekta Binafsi kuendelea kuzalisha mitamba ili kuhamasisha ufugaji wa kisasa.Jumla ya mitamba 35,698 ilizalishwa na kusambazwa kutoka katika mashamba ya serikali, kampuni ya Narco na sekta binafsi. Ili kuongeza uzalishaji wa mitamba ya ng’ombe wa maziwa, jumla ya ng’ombe aina ya borani 408 walinunuliwa na Narco na ng’ombe 70 aina ya fresian walinunuliwa na Taliri kwa madhumuni ya kuongeza kundi la ng’ombe wazazi.Anaongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, serikali ilitenga hekta 519,918.38 kuwa maeneo ya ufugaji kwenye vijiji 748 katika wilaya 80 za mikoa 22 na kufanya jumla ya eneo lililotengwa hadi sasa kufikia hekta milioni 2.535. Jumla ya hati za kumiliki ardhi kimila 48 zimetolewa kwa wafugaji katika wilaya za Ngorongoro, Longido, Simanjiro, Hanang na Monduli.Hati nne miliki za kimila za pamoja zinazohusisha vijiji vya Orkitkit, Lerug, Engonguangare na Ngapapa (Kiteto) zimeandaliwa na eneo la malisho lenye ukubwa wa hekta 30,000 limemilikishwa kwa wafugaji. Aidha, vijiji sita katika wilaya ya Kiteto vimeandaa mpango wa matumizi ya pamoja na kutenga hekta 125,000 kwa ajili ya ufugaji. Vilevile, Serikali kupitia Narco, imetenga maeneo yake hekta 125,610 yatumiwe na wafugaji wakati maalumu.Serikali pia, imefuta mikataba ya uwekezaji katika vitalu 34 vyenye ukubwa wa hekta 97,869.34 ambazo zitagawiwa kwa wafugaji. Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mahamoud Mgimwa anapongeza wizara kwa kuboresha miundombinu ya ujenzi wa mabwawa matatu ya Masusu (Ngorongoro), Olyapasei (Kiteto) na Kwamaligwa (Kilindi) umekamilika.Aidha, ujenzi wa malambo 1,378 na visima virefu 101 katika maeneo mbalimbali nchini umekamilika. Wizara inakamilisha ujenzi wa visima vitatu virefu katika wilaya za Manyoni, Iringa na Ngorongoro. Aidha, ujenzi wa lambo katika kijiji cha wafugaji cha Chamakweza unaendelea. Vilevile ukarabati wa malambo ya Wami-Dakawa (Mvomero) na Nyakanga (Butiama) unaendelea.Ujenzi na ukarabati wa minada ya Upili na Mpakani ya Longido, Kirumi, Nyamatala, Buhigwe, Murusagamba, Kasesya, Mutukula, Kizota, Pugu, Korogwe na Weruweru umefanyika. Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel anasema wizara imenzisha mashamba darasa ya malisho katika kila halmashauri ya wilaya ili wafugaji wa asili wajifunze jinsi ya kuboresha na kuhifadhi malisho hususani wakati wa kiangazi na ukame.Anasema mashamba darasa ya uzalishaji malisho bora yameanzishwa katika halmashauri 16 sawa na wastani wa hekta 112 ambazo ziko katika halmashauri za Morogoro Vijijini, Mvomero; Kilosa; Misungwi; Babati; Njombe; Mufindi; Rungwe; Mbeya Vijijini; Mbozi na Chamwino. Utekelezaji unaendelea katika Halmashauri za Itilima; Maswa; Meatu; Misenyi na Karagwe.Marobota 4,581,873 yenye wastani wa uzito wa kilogramu 12 kila moja yalizalishwa kutoka kwenye mashamba ya serikali, taasisi na sekta binafsi. Aidha, mbegu bora za malisho aina ya nyasi tani 11.2 na pingili/mapandikizi ya Napier /Guatemala /Brachiaria tani 45 na aina ya mikunde tani 3.5 zimezalishwa na kusambazwa.Pia anasema katika kuimarisha huduma za ugani na mafunzo kwa kuongeza udahili wa maofisa ugani, udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 2,137 mwaka 2015/2016 hadi 2,700 mwaka 2017/2018.Wizara imeanzisha mkakati wa kuwawezesha vijana wahitimu kutoka katika vyuo vya mifugo ngazi ya cheti, stashahada na shahada kwa kuwaweka katika maeneo ya taasisi kwa kipindi maalumu kwa lengo la kuwajengea uzoefu na ujuzi na kuwaunganisha na taasisi za kifedha. Mwandishi wa makala haya ni Kaimu Katibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi anapatikana kwenye namba 0784 441180
kitaifa
BUNGE limeishauri serikali kuhakikisha fedha zote zinazoingia nchini kutekeleza miradi ya Ukimwi, zikaguliwe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), licha ya fedha hizo kutoingia kwenye mfumo mkuu wa serikali.Akisoma taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi katika kipindi cha Januari 2018 hadi Januari 2019, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Oscar Mukasa alisema ili kumpa mamlaka CAG kukagua, ni vyema sheria inayomnyima mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho. “Sheria inayomnyima mamlaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali irekebishwe ili kumpa CAG mamlaka ya kufanya ukaguzi katika taasisi hizo zisizo za kiserikali ili kuona kilichotekelezwa ikilinganishwa na mawasiliano yaliyowasilishwa kwa wafadhili.Kwa kufanya hivyo kutaongeza utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazoelekezwa katika mapambano dhidi ya Ukimwi,” alisema Mukasa. Alisema fedha za mapambano ya Ukimwi ni fedha za umma, ambazo upatikanaji wake unahusisha serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa nje na ndani ya nchi.Mukasa alisema pia kamati imependekeza Sheria ya Ukimwi, kufanyiwa mapitio ili kuzingatia hali halisi hasa kutokana na kuwapo kwa ukinzani baina ya Sheria ya Ukimwi katika suala la umri wa mtu kupima kwa hiari awe na miaka 18 au kwa ridhaa ya mzazi kwa walio chini ya miaka 18, wakati Sheria ya Ndoa inayoruhusu mtoto chini ya miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya mzazi.Alisema kamati pia imeishauri serikali kuharakisha mchakato wa tozo maalumu, kwa ajili ya Mfuko wa Ukimwi wa Taifa (ATF) na kubuni uwekezaji wa kushirikiana na sekta binafsi ili kuwekeza katika miradi ambayo sehemu ya faida itakuwa chanzo cha mapato kwa ajili ya mfuko. Pia, kamati imeshauri serikali kuwa na utaratibu utakaoandoa migogoro ya takwimu, kwani imekuwa inaathiri shughuli za watumiaji wa takwimu.Kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Ukimwi kuhusu umri wa mtu kupima VVU na Upimaji wa mtu binafsi, Mukasa alisema takwimu zinaonesha kuwepo kwa asilimia 40 ya maambukizi mapya ya VVU kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi-24 na kwamba asilimia 80 ya maambukizi mapya ni miongoni mwa jinsia ya kike. “Tanzania haijafanya vizuri katika malengo ya 90 ya kwanza ya mapambano ya Ukimwi, ipo haja ya serikali kufanya tafakari juu ya machakato wa upimaji wa mtu binafsi.” alisema.Akichangia, Mbunge wa Viti Maalumu, Jackline Ngonyani alishauri kuanza na wabunge ambao watabainika kutofanya tohara, kufanyiwa mara moja ili kupambana na maambukizi ya Ukimwi, kwa sababu watu wasiotahiriwa huchangia maambukizi ya Ukimwi na kansa ya kizazi.Hata hivyo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku “Msukuma” (CCM) alitoa taarifa kuwa kusema: “Hoja ya mbunge Jackline ya kupima wasiotahiriwa ni nzuri sana, lakini pia takwimu zinaonesha kuwa hata wanawake waliokeketwa pia wanachangia maambukizi ya Ukimwi, hivyo tuwekewa mashine ili wakati tunapima wanaume wasiotahiriwa basi tupime na wanawake waliokeketwa.”
kitaifa
WATANI wa jadi Simba na Yanga, kila mmoja anatafuta namna ya ‘kuchomoka’ kwenye mechi yao ya Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii kwa kila mmoja akipanga mbinu zake.Miamba hiyo inatarajiwa kumenyana Jumapili ya wiki hii kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems aliyeamua kupiga kambi yake jijini Dar es Salaam, ameamua kukiongezea kikosi chake dozi ya mazoezi na sasa badala ya kufanya mara mbili kwa siku, itakuwa mara tatu kuanzia jana, leo na kesho ili kuivuruga Yanga katika mchezo huo.Akizungumza kwenye mazoezi ya timu yake yanayofanyika uwanja wa Boko Veterani, Aussems alisema mchezo huo ni muhimu kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo lakini kwake anauchukulia kawaida na kujiandaa kama ilivyo kwa mechi nyingine.“Kila mmoja yuko imara, tunafanya mazoezi katika hali ya hewa nzuri, tunajiandaa vyema dhidi ya Yanga na ni mchezo ambao ni muhimu kwetu kushinda haina tofauti na mingine, tunachohitaji kwetu ni pointi tatu,” alisema. Alisema wanajiandaa kufanya vizuri na anaamini baada ya dakika 90 mshindi atajulikana.Kocha huyo aliongeza kuwa ameridhishwa na kambi yao ya mazoezi iliyoko Kunduchi kwani kuna hali ya hewa nzuri inayovutia na mazingira ni tulivu kwao. “Kuna utofauti gani wa kwenda kwingine kubadilisha mazingira na kukaa hapa kwenye mazingira tulivu na hali ya hewa nzuri, tunaendelea vizuri na tunafurahia maandalizi yetu,” alisema.Kwa upande wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema hana hofu na Simba kwani ameifahamu kupitia mikanda ya video. Yanga imeweka kambi yake Morogoro na inatarajiwa kurejea kesho kwa ajili ya mechi hiyo. “Nimekuwa nikiisoma Simba kupitia mikanda ya video niliyoomba nipatiwe kila baada ya mechi yao, kwa hiyo sina hofu naamini maandalizi tunayoyafanya yatatusaidia kuibuka na ushindi,” alisema.Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza zikiwa na makocha wapya kila mmoja akiingia uwanjani akiwa na historia yake tofauti katika mechi zilizopita. Aussems ameiongoza Simba kushinda michezo mitatu kati ya mitano, akipata sare moja na kupoteza mmoja dhidi ya Mbao huku Zahera anaiongoza Yanga ikitoka kushinda mechi zote nne ilizocheza. Mara ya mwisho timu hizo zilikutana Aprili mwaka huu ambapo Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na beki Erasto Nyoni.
michezo
WALIOKUWA wafanyakazi wa muda kwenye sekta mbalimbali zikiwamo za madini, ujenzi wa barabara, madaraja na nyinginezo wameanza kuwasilisha uthibitisho wao kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya malipo ya mafao yao.Wafanyakazi hao ni miongoni mwa walioandamana hivi karibuni hadi ofisi za NSSF Ilala kabla ya kuelekea Makao Makuu yaliyopo katikati ya Jiji kudai malipo ya Fao la Ukosefu wa Ajira kwa wafanyakazi wasiokuwa na taaluma.Maandamano hayo yalikuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kuagiza kupitia kikao chake na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kuwa kila Mfuko uendelee na mfumo wa kikokotoleo waliokuwa wanautumia kuwalipa wastaafu kabla ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo na kutokea kwa mifuko miwili wa NSSF unaohudumia sekta binafsi na PSSSF unaoshughulikia sekta ya umma.Katika maagizo hayo Rais Magufuli pia aliagiza wafanyakazi waliokuwa kwenye ajira za muda zisizokuwa za kitaaluma kulipwa mafao yao yote pindi tu mradi husika unapomalizika au wakisitishiwa mkataba wao. Kutokana na agizo hilo, uongozi wa NSSF hivi karibuni uliwataka wanufaika na fao hilo kuanza kuwasilisha maombi yao kwenye ofisi zake ili hatua stahiki zichukuliwe ambapo jana gazeti hili lilishuhudia wafanyakazi hao kuanza kuwasilisha nyaraka zao. Juma Nasor aliyekuwa akifanya kazi kwenye ujenzi wa barabara alibainisha kuwa wamevutiwa na uamuzi huo wa NSSF wenye kutekeleza agizo hilo la Rais Magufuli.Hivi karibuni Meneja Kiongozi wa Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi alibainisha kuwa malipo yatalipwa mara tu baada ya mfanyakazi husika kuhakikiwa. Alisema uhakiki huo utachukua siku 30 tangu mfanyakazi kuwasilisha ombi lake na kuwa kwa maombi yatakayotiliwa shaka yatafanyiwa uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja. Alisema NSSF imejipanga vyema kutekeleza uhakiki huo kwa wakati na muda mwafaka ili kila mwenye haki apewe haki yake kwa wakati huku akiwataka wenye kustahili kulipwa fao hilo kutosita kuwasilisha maombi kwenye ofisi za NSSF zilizopo kila Mkoa.“Tumejipanga kuwalipa kwa wakati hawa wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ajira ya muda na ambao labla ajira imesitishwa au mradi kuisha, hawa watapewa mafao yao yote,” alisema. Alifafanua zaidi kuwa kila mhusika akishapewa fedha zake zote alizokuwa amechangia NSSF ataongewezewa na asilimia nyingine ya fedha kama nyongeza. Alisema kwa wafanyakazi ambao wanafanya kazi za kitaaluma na walikuwa wakichangia zaidi ya miezi 18 wakisitishiwa ajira zao watalipwa asilimia 33.3 ya mshahara waliokuwa wakilipwa kwa miezi sita kabla ya kupata ajira nyingine. Alibainisha kuwa kwa wale waliokuwa wakichangia chini ya miezi 18 watalipwa asilimia asilimia 50.
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala na Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dodoma na kamati ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, kuhakikisha ujenzi unaanza wiki ijayo na kukamilika ndani ya miezi sita ijayo.Aidha, ametaka hospitali hiyo ijengwe na moja ya majeshi na kutaka utumike mchoro wa hospitali inayojengwa Tunduma. Jafo alitoa maagizo hayo baada ya kutembelea eneo ambalo hospitali hiyo inapaswa kujengwa huku kukiwa hakuna kitu chochote kinachoendelea, jambo ambalo lilimfanya kutoridhika na maelezo aliyopewa.Imepita takribani miezi sita tangu Rais John Magufuli aagize fedha kiasi cha Sh milioni 995 ambazo zilikuwa imetengwa kugharamia maadhimisho ya Siku ya Uhuru mwaka jana zitumike kujenga Hospitali ya Uhuru katika Jiji la Dodoma.Pia hivi karibuni ameagiza kiasi cha Sh bilioni 2.3 kati ya Sh bilioni 5 ambazo zimetolewa kama gawio na Kampuni ya Bharti Airtel International zitumike katika ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inajengwa wilayani Chamwino huku wananchi wakitoa ekari 109 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo. Akitoa maelezo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe alisema ujenzi wa hospitali hiyo umechelewa kutokana na kuchelewa kwa michoro na kutotolewa fedha.Dk Kiologwe alisema: “Tumepata taarifa kuwa sasa kuna hatua ya kazi, awali ilipitishwa kuwa utumike mchoro wa hospitali za wilaya zinazoendelea kujengwa, baada ya maelezo yako (Jafo) ya kutaka hospitali hii kuwa ya kipekee na kuwa ya ghorofa na maelezo ya Tamisemi ni kwamba pengine itumike michoro ya hospitali inayojengwa Tunduma na sisi kama mkoa, tunasubiri tuweze kupata michoro hiyo kwa ajili ya kuendelea na ujenzi”.Mkuu wa Mkoa, Dk Binilith Mahenge alisema: “Na kama alivyoeleza mtaalamu sisi mkoa pamoja na Tamisemi tuliunda kamati na majukumu waligawana kwa hiyo kukawa na kazi tatu, ya kwanza ilikuwa kupata eneo na ambalo limepatikana, suala la pili ilikuwa kufuatilia fedha na kazi ya tatu ilikuwa kufuatilia michoro, sasa haya majukumu mawili yamechukua muda mrefu sana. “Changamoto ya pili ni hizo fedha ufuatiliaji wake, tulianza kufuatilia ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Katibu Tawala lakini baadaye kwa pamoja na Tamisemi wakaamua kufuatilia kupitia Hazina.”Baada ya maelezo hayo, Jafo alisema: “Nimekuja hapa kuangalia kazi inaendeleaje, sarakasi nyingine hata sizielewi, sijui mmenielewa? Yaani haya maneno mengine siyaelewi nimekuja kuangalia kazi inaendeleaje, na kwa bahati mbaya haya maneno ninayoyapata hapa kutoka kwa viongozi mbalimbali sijaridhika nayo kabisa. “Nchi hii tukifanya kazi kwa utaratibu huu hatuwezi kwenda wala kuwasaidia wananchi, kila mtu akitengeneza urasimu hatuwezi kwenda hata kidogo.“Kwa hiyo Mkuu wa Mkoa kifupi niseme mimi sijaridhika kabisa, asilimia mia moja sijaridhika kabisa na hii sijui fedha hazijafika, sijui vipi vipi naona yote ni kwamba tumeshindwa kuwa na watu walio makini kuona jambo hili linatekelezwa, mimi nilitarajia kukuta jengo kwa hiyo kifupi sijaridhika. “Naomba nitoe maelekezo yafuatayo kwa sababu sijaridhika na nataka kazi hapa ifanyike bila ya blaa blaa tena kwa ubora, jambo la kwanza nataka hospitali hii ijengwe na moja ya majeshi yetu.“Ajenda ya mchoro nimezunguka maeneo mbalimbali nimekuta mchoro mmoja unaweza kukafanana. Kuna mchoro ambao tunaujenga Tunduma na umebuniwa na TBA (Wakala wa Majengo) naagiza kuwa ndio utumike na TBA ndio wasimamie hii kazi kama washauri maana mchoro wao ndio wameubuni na kama kuna marekebisho ya kuongeza kwenye baadhi ya maeneo zitangezwa.“RC mimi nataka kuanzia wiki ijayo kazi ianze hapa, hivyo wataalamu wa Mkoa na Tamisemi wote wiki ijayo kazi ianze, vinginevyo hizi bla bla hatuwezi kufika maana nimesikia sijui kuna kikao, aitwe nani na nani yaani ubabaishaji tu, miezi sita mizima mnaitana tu, vikao haviishi. “Wataalamu wiki ijayo kazi ianze, anayesema kazi haianzi anyooshe kidole... (kimya) kwa hiyo wote tumekubaliana wiki ijayo kazi inaanza, nikija hapa Alhamisi ijayo nikute maeneo yote yameshasafishwa na kazi imeanza.”
kitaifa
KWA kauli moja Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne, waliotenda makosa mbalimbali wakiwa wenyeviti wa chama hicho ngazi ya mikoa na wilaya.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally, waliosamehewa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na aliyekuwa Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa. Wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mara, Christopher Sanya na aliyekuwa Mwenyekiti Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.Pamoja na hayo, Dk Bashiru alisema NEC kwa kauli moja imeamua kumuweka katika uangalizi, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, ambaye ameomba kurejeshewa uanachama wa CCM baada ya kufukuzwa kwa makosa ya kimaadili. Alisema pia halmashauri hiyo, imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa.Nafasi hizo ziliachwa wazi baada ya waliokuwa katika nafasi hizo kupangiwa majukumu mengine ya kiserikali au kufariki dunia. Uchaguzi mdogo Temeke Aidha, pia imepitisha jina na mgombea wa CCM wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Temeke Dar es Salaam, Abdallah Mtolea ambaye pia ndiye aliyekuwa anashikilia jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), kabla ya kujivua uanachama na kujiunga na CCM.Akitaja majina ya wagombea hao, alisema katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa walioteliwa kuwania nafasi hiyo ni Dk Damas Kashegu, Asha Feruzi, Galila Wabanhu na Makene Boniphas. Katika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa walioteuliwa kuwania nafasi hiyo ni Dk Abel Mwendawile, Amani Mwamwindi na Sabas Mushi. Na nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Simiyu ni Mashaka Makongoro, Mayunga Ngokolo na Heri Zebedayo.Dk Bashiru alisema katika nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mwanza, walioteuliwa na halmashauri hiyo ni Bahebe Ezekiel, Nyiriza Nyiriza, Masso Jane na Misogalya Kassile. Katika nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mwanza walioteuliwa kuwania nafasi hiyo ni Salum Chima, Yusuph Gwayaka, Bertha Nakomolwa na Philemon Kiemi.Katika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, walioteuliwa ni Amina Kobo, Lemmy Ludovick na Hamidi Shebuge. Kwa mujibu wa Dk Bashiru, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pia imeiagiza Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kurudia mchakato wa kupendekeza majina ya mgombea wa nafasi ya Mjumbe wa NEC. Uamuzi pingamizi mbalimbali Wakati huo huo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kauli moja imetupilia mbali pingamizi zilizowekwa dhidi ya viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali na kuagiza viongozi hao waendelee na nyadhifa zao.Alisema pingamizi hizo ziliwekwa dhidi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Lindi, Aisha Ally, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Salim Mohamed na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara, George Rubagora.Alisema pamoja na kutupilia mbali pingamizi hizo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewaagiza walezi wa mikoa yote, ambayo viongozi wake waliwekewa pingamizi, wakutane na wanachama na kukiunganisha chama. Dk Bashiru alisema katika kikao hicho, kimemuagiza Zubeir Majaliwa (aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Uvinza) ambaye Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Uvinza ilimsimamisha uanachama, kuwasilisha rufaa yake kuanzia ngazi husika wakati adhabu yake ikiendelea.Aidha, Halmashauri Kuu ya CCM imetoa adhabu ya karipio kwa mwanachama wa CCM, Hasnain Murji kutokana na kukabiliwa na makosa ya kimaadili. Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilifanyika jana jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Rais John Magufuli.Kwa mujibu wa katibu mkuu huyo, pamoja na kikao hicho kutoa maamuzi hayo, kilipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na taarifa ya chama juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya mwaka 2015. Alisema pia kikao hicho kilipokea taarifa kuhusu masuala ya maadili, kilipokea na kuridhia marekebisho ya kanuni mpya za fedha na mali za chama na jumuiya zake na kimepokea na kuridhia uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM.
kitaifa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mbeya Mjini kimepata wanachama wapya 280, wakiwamo 30 waliohamia wakitokea vyama vingine vya siasa.Wanachama hao ambao walikuwa na nyadhifa mbalimbali ni pamoja na aliyekuwa mgombea Ubunge 2015 kupitia Chausta, Martha Komba. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole aliongoza mapokezi ya wanachama hao kwenye mkutano uliolenga kuzungumza na viongozi wa mashina, matawi na kata wilaya ya Mbeya Mjini ziara ya kuimarisha chama.Katibu wa CCM Mbeya Mjini, Gervas Ndaki alisema kati ya wanachama wapya 280, kati yao 250 hawakuwahi kuwa na chama chochote huku wanachama 30 wakitokea vyama vingine. Ndaki alisema miongoni mwa wanachama waliotoka vyama vingine asilimia kubwa walikuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao baadhi yao walikuwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.Wengine waliopokewa ni aliyekuwa kiongozi wa walinzi wa Chadema (Redbrigedi) wa Mkoa, Paul Ambele Mwakajila ambaye pia alikuwa mlinzi wa viongozi wa Chadema Taifa. Katibu huyo alisema pamoja na hao, pia alipokelwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa Wazazi Mkoa wa Mbeya kutoka Chama cha ACT- Wazalendo, Mbuza Mbuza. Akizungumza baada ya kuwapokea na kuwakabidhi kadi mpya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mwakasole alisema waliopokelewa kutoka vyama vya upinzani wanatakiwa waoneshe utofauti na vyama walikotoka.Aidha aliwapongeza wanachama hao wapya kwa kuhama vyama vyao na kufuata maendeleo. Aliwataka waunge mkono juhudi zinazofanywa na serikali chini ya Rais John Magufuli. Mwakasole alitoa mwito kwa wanachama wa CCM ambao wamekuwa wakijitokeza katika nafasi mbalimbali kugombea katika chaguzi kukubaliana na matokeo ya kushindwa na kuepuka kulipiza visasi kwa kutochaguliwa.Alisema kulipiza kisasi kwa kushindwa kwenye chaguzi huchangia kuleta mgawanyiko na migogoro ndani ya chama hivyo kusababisha chama kizima kushindwa katika uchaguzi. Alisema Watanzania wana sifa ya pekee duniani ya umoja hivyo kila mwananchi anapaswa kujivunia na kuulinda kwa nguvu zote kwani umoja uliopo ukipotea kuupata si kazi rahisi.
kitaifa
ILE siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi hapa nchini hatimaye leo imefi ka, ambapo kutakuwa na pambano la ngumi la kukata na shoka litakalowakutanisha bondia wa ngumi za kulipwa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay wa Ufi lipino.Pambano hilo la uzani wa Super Walter lisilo la ubingwa ni la raundi 10 litafanyijka katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Hili ni pambano la kwanza la kimataifa kwa Mwakinyo kucheza katika ardhi ya Tanzania, pambano lake la mwisho lilikuwa Machi mwaka huu nchini Kenya, ambapo alimshinda kwa ‘Technical Knock Out’ (TKO) mpinzani wake, Sergio Gonzalez kutoka Argentina.Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo alisema kuwa alikuwa akilisubiri pambano hilo kwa muda mrefu na amejiandaa vizuri na ameahidi kumuangusha kwenye raundi za mwanzoni.Alisema licha ya kukutana na bondia mwenye uwezo mkubwa kutokana na ukweli kwamba anatokea kwenye gym ya bondia mkubwa duniani, Manny Pacquiao lakini haoni cha kumtisha na kumnyima ushindi mbele yake.“Tumejiridhisha kuwa Tinampaya ni bondia aliyekidhi vigezo vya kupambana na mimi na atanipa upinzani mkubwa, nimejiandaa vizuri kuhakikisha nashinda katika ardhi ya nyumbani ili kudhihirishia umma kuwa nipo vizuri na pia hiyo itakuwa ni chachu ya kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi hapa nchini,” alisema Mwakinyo.
michezo
RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/16, ilifichua udhaifu katika mradi wa bomba la usafirishaji gesi asilia kati ya Mtwara na Dar es Salaam, ilipobainisha kiwango kidogo cha matumizi ya gesi hiyo nchini.Katika ripoti yake hiyo, CAG alieleza kuwa bomba hilo lililojengwa na Kampuni ya Maendeleo ya Petroli na Teknolojia China (CPTDC)kwa gharama ya Dola za Marekani bilioni 1.283 (Dola bilioni 1.225 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya China), ujenzi wake ulifanyika kabla ya kutafuta wateja wa gesi hiyo. CAG alibainisha kuwa hali hiyo inasababisha ukakasi katika marejesho ya mkopo yaliyotegemea kupatikana kwenye mauzo ya gesi asilia baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa bomba na kuanza kutumika kibiashara.Wakati makadirio ya mauzo halisi ya gesi asilia ni futi za ujazo milioni 138.8 kwa siku, CAG alibaini Shirika la Umeme (Tanesco) ndiyo mteja pekee wa gesi hiyo na anatumia wastani wa futi za ujazo milioni 46.61 kwa siku, hivyo matumizi ya bomba hilo ni ya asilimia sita tu ilhali malengo yalikuwa kusafirisha gesi kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, viwandani, kupikia majumbani na matumizi ya magari.Kampuni ya Pan African Energy kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanakiona kikwazo hicho katika matumizi ya gesi asilia na kuanzisha mradi wa kujaza gesi kwenye magari katika kituo chao cha Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Pan African Energy Tanzania, Andy Hanna, anasema wamekuwa wakitoa huduma za kujaza gesi magari kwenye kituo hicho cha gesi wakiwa wabia wa TPDC kwa kuhakikisha huduma za gesi na wameendelea kuhakikisha huduma zinawavutia wengi ili kubadili mfumo.“Tunatoa huduma kwa zaidi ya magari 100 kwa siku na huduma zetu ni za saa 24. Na hii imezidi kuwa njia mojawapo ya kuwavutia watu wengi kupitia wale tunaowahudumia, lakini tatizo lipo kwani kituo ni kimoja tu na hakipo kwenye eneo rafiki kibiashara.“Mifumo hii iliyopo kwenye kituo hiki tuliifunga miaka tisa iliyopita, na hadi sasa idadi ya magari yanayopata huduma ni zaidi ya 300. Kwa sasa, ni watanzania wachache wanafurahia kutumia gharama ndogo kwenye uendeshaji wa magari."Kama wangefahamu wengi zaidi manufaa ya kutumia gesi badala ya mafuta kwenye magari na vituo vikaongezeka, basi wanufaika wangekuwa wengi, lakini pia utunzaji wa mazingira ungeongezeka kwani asilimia 72 ya kinachotoka kwenye mafuta ya petroli na dizeli huchafua mazingira,” anaeleza.Katika kituo hicho cha kujaza gesi kwenye magari, HabariLeo inakutana na dereva teksi, anayejitambulisha kwa jina moja la Ezekiel, anayesema ana miezi saba tangu aanze kutumia gesi kwenye gari lake aina ya Toyota IST analolitumia kwa biashara hiyo.Ezekiel anasema: “Mimi ni dereva wa gari hili la biashara, kwa kweli sasa nafurahia kutumia gesi badala ya mafuta kwenye gari, matumizi ya fedha ni kidogo. Nikiweka kilo 10 za gesi kwenye gari langu, naliendesha kwa kilometa 170 bila ya kupata adhaa yoyote, tena kwa gharama nafuu kwani kilo moja kwa sasa tunauziwa shilingi 1,550.“Zamani nilikuwa nikitumia zaidi ya lita 30 kwa kilometa 170, tena hiyo ni pale unapokuta hakuna msongamano wa magari, na kama unavyojua kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, petroli imekuwa ikiuza kati ya shilingi 2,150 na 2,350,” anasema.Dereva teksi mwingine, James Osward, naye anasifu matumizi ya gesi kwenye magari, akieleza kuwa gharama za nishati kwa ajili ya magari yake sasa zimepungua baadala ya kuanza kutumia gesi.“Nina magari mawili ya biashara, yote ni Toyota IST. Hadi sasa, nina miezi sita tangu nilipobadilishia mfumo wa hili moja na ndilo ninalolitumia ninapokuwa kwenye shughuli zangu za kubeba abiria."Kwa kweli sasa ninafurahia kupata unafuu mkubwa linapokuja suala la matumizi nya fedha kwa ajili ya nishati kwenye gari. Nilipokuwa ninatumia petroli, nilikuwa nikitumia fedha nyingi ukilinganisha na sasa. "Lakini jambo hili wengi wamekuwa hawalielewi mpaka pale mtu atakapopata fursa la kutumia gari linalotumia gesi. Mtazamo wangu ni kuwa miaka ijayo watu wengi watahamia huku maana unapofunga mfumo huu, matumizi yanapungua marudufu,” anasifu.Ramadhani Yasin, dereva wa basi dogo la abiria, maarufu daladala, linalofanya safari zake kutoka Gongo la Mboto na Stesheni, anasema amekuwa na maisha mazuri tangu mwajiri wake alipoamua kuunganisha mfumo wa gesi kwenye gari hilo aina ya Toyota Coaster.“Aisee, siku hizi ninaona fedha imenikubali, kuunganishwa kwa mfumo wa gesi kwenye gari kunanipa faida, na bosi wangu naye anapata."Zamani nilikuwa nikimpelekea hesabu shilingi 80,000 kwa siku, lakini kwa sasa napeleka 'laki moja' (Sh. 100,000) wakati huohuo mimi nabaki na shilingi 50,000 tofauti na zamani ambapo nilikuwa nikipata shilingi 20,000 kwa siku.“Kwenye matumizi, kwa siku ninaweka gesi kilogramu 25 asubuhi na 25 jioni, lakini zamani nilikuwa nikinunua dizeli ya mpaka shilingi 160, 000 kwa siku, faida ilikuwa kidogo,” anaeleza dereva huyo ambaye anasisitiza itakuwa ngumu kukubali kuajiriwa na mmiliki wa gari lisilokuwa na mfumo huo wa gesi.TRILIONI 30 ZAOKOLEWAKwa mujibu wa TPDC, kwa kipindi cha miaka 15, tangu Tanzania ilipoanza kuzalisha na kusambaza gesi, imeokoa kiasi cha Sh. trilioni 30, ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje kwa ajili ya kuzalisha umeme na uendeshaji wa viwanda.Mkurugenzi wa TPDC, Dk James Mataragio anasema kiasi hicho cha fedha kingetumika kwenye ununuzi wa mafuta kwa ajili ya umeme wa mafuta, lakini kutokana na uwapo wa gesi asilia, takribani asilimia 54 ya umeme unaozalishwa nchini unatumia gesi asilia, huku nishati hiyo pia ikitumika viwandani na pia kwenye magari.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha na Utafiti wa Sera (Repoa), Dk. Donald Mmari, anasema utumiaji wa gesi unaweza kuwa chanzo cha mapato makubwa ya taifa.“Nchi nyingine tunaweza kuona kama vile China, Malaysia na India, magari yote ya kijamii yakiwamo mabasi yanatumia gesi asilia na kufanya gharama ya uchukuzi kushuka chini. Ni wakati sasa kuitumia sekta hii,” Dk. Mmari anashauri.VITUO KUONGEZWAKamishna Msaidizi wa Gesi wa Wizara ya Nishati, Sebastian Shana, anasema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya gesi asilia kwenye magari huku huduma hiyo ikiwa inatolewa kwenye kituo kimoja, serikali inakusudia kutengeneza vituo vingine viwili vikubwa kwa ajili ya kusambaza gesi kwenye vituo vingine vidogo vilivyoko jijini. Shana anasema takribani magari 300 nchini yanatumia gesi kama mbadala wa mafuta, huku mengi zaidi yakiendelea kubadilishwa mifumo ili yatumie nishati ya gesi.Agosti 21 mwaka huu, Mkurugenzi wa TPDC, Dk. Mataragio, katika wasilisho lake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema kutokana na ongezeko la magari yanayotumia gesi, kituo cha majaribio kilichoko Ubungo, kinashindwa kuhimili matakwa ya matumizi, hivyo shirika limejipanga kujenga kituo kikubwa eneo la Sam Nujoma jijini humo.“Kituo hicho kinachotarajiwa kukamilika Oktoba 2020, kitatumika kujazia gesi katika magari pamoja na kupeleka gesi maeneo ambayo miundombinu ya mabomba ya gesi bado haijafika,” aliahidi.MWENDOKASI KUNEEMEKADk Mataragio pia alisema TPDC inalenga kuupatia gesi asilia mradi wa mabasi ya mwendokasi (DART), akieleza kuwa kwa kuanzia, kituo cha kujazia gesi kwenye magari kitajengwa eneo la DART, depoti ya Ubungo Oktoba mwakani.Alisema shirika lilikubaliana na DART kuwezesha kuweka vituo maalum vya gesi katika depoti ya Gongo la Mboto na Mbagala ili kupunguza gharama za uendeshaji wa mabasi hayo, lakini pia kupunguza nauli kwa wananchi.Mratibu wa Mradi wa Matumizi ya Gesi Asilia kwenye Magari (CNG Vehicle Project) kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Dk Esebi Nyari anasema wanaendelea kuunganisha magari kwenye mfumo wa matumizi ya gesi asilia badala ya petroli na kwamba hadi sasa, magari zaidi ya 100 yameunganishwa kwenye karakana yao.Dk. Nyari anasema mfumo huo wa kuunganisha gesi asilia unasaidia kupunguza gharama kwa wamiliki wa magari na kwamba kiasi kidogo cha gesi asilia kinatumika kwa umbali mrefu.“Mfumo huu una faida nyingi, kilogramu moja ni shilingi 1,550 huku petroli lita moja ikiwa ni wastani wa shilingi 2,200, ukiweka gesi asilia kilogramu moja unaweza kwenda zaidi ya kilometa 20 huku petroli lita moja inakwenda kilometa zisizozidi 12. "Mtungi wa gesi asilia wa kilogramu 15 (shilingi 23,250) unaweza kutumika kutembea zaidi ya kilometa 200 tofauti na petroli,” anafafanua.Kuhusu gharama za kubadili mfumo, mtaalamu huyo anasema kuwa mwenye gari lenye 'cylinder' nne, wanatoza Sh milioni 1.8 na kwa zaidi ya hapo bei inapanda kidogo."Cylinder 'nne ni shilingi milioni 1.8, ukiwa na gari lenye 'cylinder' zaidi ya hapo bei inapanda lakini hii ikitokea kutatokea kampuni au taasisi mbalimbali za ufundi zitafanya kazi ya kuunganisha magari, basi bei ya uunganishaji itashuka..."...Serikali pia ikiangalia namna fulani ya kutoa msamaha wa kodi kwa baadhi ya vifaa vya kuunganishia vinavyotoka nje ya nchi, huenda watu wanaotumia gesi wanaongezeka kutoka 300 waliopo sasa kwani bei ya kuunganisha itakuwa chini," anasema Dk Nyari.Kwenye kuunganisha mfumo, DIT ndiyo pekee inafanya kazi hiyo kwa sasa nchini kwa inashirikiana na kampuni ya wazawa ya Energo Tanzania Limited ambayo inashughulikia teknolojia na DIT hao wanahusika zaidi kwenye ufundi wa mfumo huo.Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, anasema ni wakati sasa nchi kuongeza kasi kwenye uvunaji wa gesi asilia. Anasema ili uchumi wa nchi upige hatua, ni vyema rasilimali zake zikatumika kwa usahihi.Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, anasema: “Wenye maamuzi (serikali) waangalie jinsi gani watafanyia kazi utafiti uliofanywa na wadau mbalimbali wakiwamo Repoa kuhusu gesi. "Kuna juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John Magufuli pamoja na wasaidizi wake, lakini tunahitaji kuongeza kasi kwenye uvunaji wa gesi ili iweze kunufaisha taifa. Dunia haitusubiri, tuvune tulichonacho kwa ajili ya vizazi. Kama vitatumika vizuri, tutafika mbali.
uchumi
WADAU wa Muswada wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafi ri wa Ardhini (LATRA), wameshauri Jeshi la Polisi lisihusike na kukagua magari badala yake jukumu hilo liachiwe mikononi mwa mamlaka hiyo mpya ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa leseni za usafi ri na usafi rishaji.Akizungumza na gazeti hili jijini hapa jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Hawa Chakoma alisema taasisi za usafiri na usafirishaji takribani 10 walifika mbele ya kamati hiyo kutoa maoni yao kuhusu kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018.Chakoma alisema wadau walishauri LATRA ndio wabaki na jukumu la kukagua magari kwani ndio wenye mamlaka ya kutoa leseni kwa magari hayo kinyume cha muswada unataka Polisi kuendelea kufanya kazi hiyo. Alisema wadau wanaona mwingiliano wa kazi kati ya Sumatra na Polisi wa kukagua magari unaongeza urasimu, hivyo walishauri Polisi waichie mamlaka hiyo suala la kukagua na kutoa leseni za magari.Alitaja wadau waliofika mbele ya kamati kuwa ni viongozi wa Chama cha Usafirishaji wa Mizigo Tanzania (TATOA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (DABOA), Road Safety Ambassador (RSA) na wadau wengine.Kuhusu faini, alisema wadau walishauri muswada wa sheria unaonesha kwamba kutakuwapo na faini, lakini unasema adhabu na tozo zitaingizwa kwenye kanuni, wadau walishauri ni vema vyote vikaingizwa kwenye sheria ili zipate nguvu ya kujadiliwa kwenye bunge badala ya kumwachia waziri anayetunga kanuni.Kuhusu faini ya Sh milioni tatu au kifungo kisichopungua miaka miwili au vyote viwili kwa mtu aliyefanya kosa au kampuni iliyofanya kosa kutozwa Sh milioni tano, wadau walishauri muswada huo huo uoneshe pia kiwango cha faini hiyo ni kwa makosa gani, aina gani na ukubwa gani wa gari linatozwa faini hiyo.Wadau pia walishauri pamoja na kuwepo kiwango hicho cha faini, muswada huo unatakiwa kuonesha kiwango cha juu na kiwango cha chini cha faini kwa aina mbalimbali ya magari na ukubwa wake.Kwa kutenganisha kiwango cha juu cha faini na kidogo cha faini, Chakoma alisema wadau walishauri pia zingeonesha aina ya gari kama ni bajaji, bodaboda, daladala, basi au chombo kingine cha usafiri wa ardhini, kitendo cha kuweka faini za jumla, kinaweza kuua biashara ya magari madogo.Alisema muswada ulisema muda wa kupeleka malalamiko wa mtu aliyefanya kosa ni siku 14, wadau wakashauri ni vema ungeonesha pia ni muda gani mtu au kampuni husika malalamiko yake yatafanyiwa kazi.Alisema kuhusu malalamiko hayo, muswada unasema yatashughulikiwa na kamati ndogo ya marejeo itakayokuwa imechaguliwa na bodi ya mamlaka hiyo, wadau walishauri muswada ungepunguza madaraka na mamlaka ya kamati hiyo ya kufanya kazi kama Tume ya Ushindani.
kitaifa
Promosheni ya Airtel Mkwanjika imekuwa ni promosheni ya kipekee inayowapatia wateja wanne wa Airtel kila siku kuchaguliwa kupitia droo inayoendeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nafasi ya kuingia kwenye kisanduku kinachopeperusha pesa na kupewa dakika moja ya kujikusanyia pesa kisha kuondoka na mkwanja wao wa pesa taslimu.Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Huduma za Ziada wa Airtel, Nassor Abubakar alisema ;“mpaka sasa tunao washindi 128 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini kati yao washindi 96, wameshajishindia kiasi cha pesa walichoweza kujikusanyia ndani ya sanduku la pesa, hivyo tunajisikia furaha kuwawezesha Watanzania na wateja wetu kwa ujumla kuboresha maisha yao kwa kuwapatia kiasi cha pesa kama zawadi ya ushindi wao kupitia promosheni hii ya Airtel Mkwanjika ”.Nassor aliwataja washindi hao kuwa ni Jafari Twaha kutoka Arusha, Lisa Vedastor, Hajattussimena Byron Martin kutoka Bukoba, Philimon Shayo, Gidion Vedasto, Mariam Juma na Michael Enas kutoka Dar es Salaam, Barton Andrea kutoka Dodoma na Bury Umary kutoka Manyara.Pia aliongeza, Said Suleiman na Said Azizi kutoka Mtwara, Sospeter Paulo na Angolina Gillioni kutoka Morogoro, Maganga Masesa, Neema Michael kutokaTabora, Arafa Idd kutoka Pwani, Emilson Emilton, Rehema Pamela na Anabela Samson kutoka Mwanza, Christian Paul kutoka Shinyanga na Sandari Mustapher kutoka Songea.Kwa upande wake Nassor aliongeza kwa kusema ,kila mteja wa Airtel ana nafasi ya kujishindia, ni rahisi mteja anachotakiwa kufanya ni kununua vocha yake, kukwangua na kuingiza kwenye simu yake au kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money au kununua vifurushi vya Airtel Yatosha na namba yake itaingizwa moja kwa moja kwenye droo ya promosheni ya Airtel Mkwanjika.“Natoa wito kwa Watanzania na wateja wetu nchi nzima kuendelea kutumia huduma zetu na kuongeza salio ili kupata nafasi ya kuibuka kuwa washindi kupitia promosheni hii ya Airtel Mkwanjika,” alisisitiza.
uchumi
WANAFUNZI wawili wa kitanzania wanatarajia kupeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya kimataifa ya uimbaji kwa lugha ya Kichina yatakayofanyika Machi mwaka huu, jijini Beijing, China.Wanafunzi hao wanaiwakilisha nchi baada ya kuibuka vinara wa mashindano yaliyofanyika hapa ambayo yaliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na yalishirikisha wanafunzi 12 kutoka shule na vyuo vikuu mbalimbali vya hapa nchini. Walioibuka vinara katika mashindano hayo ni Tausi Nzimano anayesoma Kichina mwaka wa kwanza kutoka UDOM aliyepata asilimia 97.13 na Mercy Geoffery wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Mathew ya jijini Dar es Salaam kwa kupata asilimia 97.5.Akizungumzia ushindi huo, Geoffrey alisema haikuwa kazi rahisi licha ya kuwa alijiamini kuibuka kinara wa mashindano. “Awali wakati tunaanza mashindano haya ngazi ya shule, ilifika wakati nilikata tamaa, lakini wazazi walinitia moyo nikaongeza juhudi na sasa nimeibuka kinara kwenda China kupeperusha bendera yetu,” alisema. Nzimano yeye alisema haikuwa kazi rahisi kufikia hatu hiyo kwani changamoto kubwa ilikuwa kwenye matamshi ya lugha hiyo.Aliomba serikali kutoa elimu kwa jamii ili itambue umuhimu wa mashindano ikiwemo ya uimbaji kwa lugha ya Kichina ambayo yana fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kusoma nje ya nchi. Washindi hao wanawaomba Watanzania kuwaombea katika shindano hilo ili waweze kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje. Naye Mhadhiri Msaidizi katika Idara ya lugha za kigeni (Kichina) Udom, Sasha Abubakari alisema, haikuwa kazi rahisi kuwapata washiriki wa shindano hilo kwani maeneo mengine wazazi walikuwa wanakataza watoto wa kike kusafiri.“Kuna shule changamoto hiyo ilijitokeza, mwalimu anayefundisha Kichina ni mwanaume na wanafunzi wanaotakiwa kuwakilisha shule ni wa kike, wazazi wanakataa watoto wao kusafiri na mwalimu huyo, lakini tulivyowaelewesha walielewa,” alisema. Akizungumzia umuhimu wa mashindano hayo, Abubakari alisema wengi wanaoshiriki katika ngazi ya kimataifa wanapata nafasi ya kusomeshwa Kichina nchini China, akisema hata yeye alikuwa ni miongoni mwa waliosoma nchini humo.Kaimu Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Peter Msofe aliwataka Watanzania kujifunza lugha mbalimbali na kichina kupata fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na nchi hiyo. Aliwataka wanafunzi hao kujifunza kichina hata kama hawatapata nafasi ya kushiriki mashindani hayo kimataifa ya lugha nje. Mkurugenzi wa Chuo cha Confucius Udom, Dk Yang Lun alisema China ilianzisha chuo kinachofundisha kichina kukuza lugha hiyo, utamaduni na kudumisha uhusino wake.
kitaifa
WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, kikiendelea kujifua vilivyo nchini Misri baada ya kupata mechi mbili za majaribio dhidi ya wenyeji Misri na Zimbabwe kabla ya kuingia rasmi kwenye fainali hizo ambazo wanatarajia kushiriki kwa mara ya pili tangu walipofanya hivyo miaka 39 iliyopita.Taifa Stars iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1980 iliishia katika hatua ya makundi, hivyo mwaka huu ina kibarua cha kuhakikisha inavunja rekodi yake kwa kufuzu kwa hatua ya pili, ambayo ni 16 bora.Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana, huku Taifa Stars ikitarajia kuanza kutupa karata zake kesho kwa mchezo dhidi ya vigogo vya Afrika, Senegal. Misri imekuwa mwenyeji wa mashindano hayo baada ya kupokwa kwa Cameroon kutokana na kushindwa kukamilisha maandalizi kwa wakati. Cameroon pia ndio mabingwa watetezi wa taji hilo.MIAKA 39 SASABaada ya kushiriki kwa mara ya mwisho fainali za Afcon mwaka 1980, imechukua takribani miaka 39 kwa Tanzania kurejea katika fainali za mashindano hayo, ambayo sasa hufanyika kila baada ya miaka miwili.Taifa Stars ilibuku nafasi ya kwenda Misri kwa staili ya aina yake baada ya kuwafunga majirani zao Uganda, The Cranes kwa mabao 3-0 siku ya mwisho ya mechi za makundi, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Katika fainali hizo za mwaka 1980 nchini Nigeria, Tanzania haikushinda mchezo hata mmoja katika hatua hiyo ya makundi, na ilimaliza katika nafasi ya mwisho ikiambulia pointi moja baada ya kutoka sare mechi moja na kufungwa mbili.Tanzania ilikuwa moja ya timu za mwisho kufuzu kwa fainali hizi za Afcon 2019 katika mchezo ulipigwa Machi 24 mwaka huu. Sasa Taifa Stars inaangalia kuvunja rekodi yake ya mwaka 1980 ya kucheza hatua ya makundi na ikivuka tu na kucheza hatua ya 16 bora, ndoto ya kocha Amunike itakuwa imetimia.Kikosi cha Stars kiliondoka nchini kikiwa na msafara wa wachezaji 32, ambapo kupitia mechi hizo za kirafiki wachezaji hao walichujwa na kubaki 23, idadi ambayo itahudumiwa na Shirikisho la Soka Afrika, Caf. KUPAMBANA STARS Wachezaji hao ni wazi wana kila sababu ya kupambana kwa jasho na damu kuhakikisha wanaipeperusha bendera vyema na kuwatoa kimasomaso Watanzania zaidi ya milini 50.Watanzania wana imani kubwa na kikosi hicho, lakini naweza kusema hicho nikipimo tosha kwa kocha wa kikosi hicho, Emmanuel Amunike kuwaonesha na kuwaaminisha watu waliokuwa na mtizamo hasi juu huku wakihoji uwezo na kazi hiyo.Kikosi hicho kimekita kambi nchini Misri baada ya kuridhishwa na miundombinu ya matayarisho ya wachezaji yatakayochangia wachezaji kupata morali na ari ya kufanya vizuri katika michezo ya kundi lao kisha kutinga hatua inayofuata.Taifa Stars wamepangwa Kundi C pamoja na majirani zao Kenya na timu vigogo Senegal na Algeria ambazo zimefanya uwekezaji mkubwa kwenye soka la vijana na wamepata uzoefu wa kushiriki mara nyingi michuano hiyo.Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa ufupi ni shindano kubwa lililoanzishwa mwaka 1957 lakini tangu mwaka 1968, fainali hizo zilikuwa zinafanyika kila baada ya miaka miwili makala haya yanakuletea uchambuzi mdogo kwa mataifa yaliyotwaa taji hilo mara nyingi na wachezaji waliofunga mabao mengi.MISRIMisri ndiyo taifa pekee lenye rekodi na historia kubwa ya kutwaa taji la michuano hiyo mara saba na kuyazidi mataifa mengine yaliyopata kushiriki kwa nyakati tofauti. Mafarao hao kwa mara ya kwanza walitwaa mwaka 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.GHANA NA CAMEROONMataifa hayo yanafuatia kwa kushika nafasi ya pili kwa kutwaa taji hilo mara nyingi baada ya Ghana walitwaa miaka ya 1969, 1965, 1978, huku Cameroon wakianza mwaka 1984, 1988, 2000 na 2002 na 1982.WABABE NIGERIAKitabu cha kumbukumbu kinaonesha Nigeria wanashika nafasi ya tatu, wamelitwaa taji hilo mara tatu, ikiwa ni mwaka 1980, 1994 na 2013.DR CONGO, IVORY COASTWanashika nafasi ya nne huku kila mmoja wao akiwa amechukua mara mbili, ambapo Congo wamechukua miaka ya 1968 na 1974 wakati Ivory Coast 1992 na 2015.WALIOFUNGA MABAO MENGIWachezaji 10 waliopata kutikisa kwenye michuano hiyo kwa kufunga mabao mengi na wanazidi kubaki kwenye kumbukumbu ya kitabu cha michuano hiyo mikubwa barani Afrika, Caf.Samuel Eto’o mshambuliaji na raia timu ya taifa ya Cameroon anashikilia uongozi kwa kufunga mabao 18, Laurent Pokou raia wa Ivory Coast ametumbukia nyavuni mara 14 akifuatiwa na Rashid Yekini raia wa Nigeria amefunga mabao 13. Wengine ni Hassan Shazly (Misri) 12, Hossam Hassan (Misri) 11, Ndaye Mulamba (Dr Congo) 10, Didier Drogba (Ivory Coast) 10, Joel Tieh (Ivory Coast) 10, Kalusha Bwalya (Zambia) 10.
michezo
WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema kati ya mwaka 2017 na 2018 Tanzania imeendelea kuwa na urari chanya katika mauzo ya bidhaa zake katika nchi za Afrika. Hayo yamo katika bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyosomwa bungeni jana na Waziri Joseph Kakunda wa wizara hiyo. Waziri Kakunda alisema Tanzania imeuza zaidi kuliko kununua kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa asilimia 10.63; Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC- kwa asilimia 29.84 na Umoja wa Afrika – AU- kwa asilimia 5.63. Akifafanua alisema mauzo kwa EAC yalikuwa ni Dola za Marekani milioni 447.5 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 349.6 zilizopatikana mwaka 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 21.88. Ongezeko hilo limetokana na mauzo ya bidhaa za chai, mahindi, ngano, alizeti, mchele, bidhaa za karatasi,mabati, vigae, vyandarua, kemikali, saruji na mafuta ya kupaka.Tanzania iliagiza kutoka EAC bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 302 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 220.4 kwa mwaka 2017 ikiwa ni ongezeko la asilimia 27.24.Akizungumzia SADC alisema mauzo ya Tanzania yalikuwa Dola za Marekani milioni 999.34 mwaka 2018 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 877.8 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 12.16.Aidha, Tanzania iliagiza bidhaa za Dola za Marekani milioni 604.32 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 600.64 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 0.61. Kwa upande wa Umoja wa Afrika, mauzo ya bidhaa za Tanzania yalikuwa Dola za Marekani milioni 1,485.05 mwaka 2018 ikilinganishwa na Dola milioni 1,419.84 kwa mwaka 2017 sawa naongezeko la asilimia 4.39. Ongezeko hilo limetokana na mauzo ya bidhaa za madini, pamba, chai, kahawa, mahindi, ngano, alizeti, mchele, bidhaa za karatasi, mabati, vigae, vyandarua, kemikali, saruji na mafuta ya kupaka. Tanzania katika kipindi hicho iliagiza bidhaa za Dola za Marekani milioni 989.01 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 895.88 kwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.42.Katika soko la China Tanzania iliongeza mauzo yake kufikia Dola za Marekani milioni 1.98 kutoka dola milioni 142.3 kwa mwaka 2017 hadi kufikia dola milioni 144.28; wakati China iliuza Tanzania bidhaa za Dola za Marekani milioni 356.Kwa utendaji huo katika soko kuna urari hasi wa biashara wa asilimia 21.79 katika kipindi husika. Katika soko la India mauzo ya Tanzania kwa mwaka 2018 yalikuwa Dola za Marekani milioni 734.27 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 977.6 kwa mwaka 2017. Tanzania imeagiza kutoka India bidhaa za Dola za Marekani milioni 1,218.07 ikilinganishwa na dola milioni 1,077.60 zilizoagizwa mwaka 2017. Akizungumzia soko la Japan, Waziri Kakunda alisema Tanzania iliuza bidhaa za Dola za Marekani milioni 66.72 ikilinganishwa na dola milioni 75.7 zilizouzwa mwaka 2017 ikiwa ni sawa na upungufu wa asilimia 13.47 ya mauzo. Mwaka 2018 Tanzania iliagiza bidhaa za dola za Marekani milioni 398.13 kutoka Japan ikilinganishwa na bidhaa za dola za Marekani milioni 365.2 za mwaka 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 8.27. Mataifa ya India, Japan na China ndio wafanyabiasha wakubwa na Tanzania.Pamoja na taifa kuendelea kuongeza kasi ya biashara ya nje, kumekuwepo na changamoto ambazo Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imetaka serikali kuzifanyia kazi. Jumuiya hiyo imesema kwamba mazingira ya biashara bado sio bora kutokana na utoaji huduma hafifu bandarini, mawasiliano hafifu baina ya mamlaka za Tanzania na wafanyabiashara wa DRC, kuwepo na udanganyifu wa badhi ya wafanyabiahara, mawakala na watumishi wa serikali wasiokuwa waaminifu.
kitaifa
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema wanajipanga kuja na mikakati mitatu kuhakikisha wanasuka kikosi cha KMC kukifanya kiwe na ushindani kuelekea kwenye michuano ya kimataifa msimu huu.KMC wamepata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na Azam FC wakiungana na Simba na Yanga kwa Ligi ya Mabingwa baada ya Tanzania kupata nafasi ya kuingiza timu nne baada ya kushika nafasi ya 12 bora kwa ngazi ya Klabu Barani Afrika.Akizungumza jana baada ya kupokea taarifa hizo njema kwao, Sitta alisema wamefuhi kupata fursa hiyo kwa msimu wa kwanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa. Alisema wakati anaingia kwenye umeya aliikuta timu hiyo ikiwa na miaka miwili ikipambana kwenye Ligi Daraja la Kwanza na kuweka mipango ya kupanda ligi Kuu, ambapo alisema kwao ni mafanikio makubwa. “Tuna maeneo matatu ya kuyaweka sawa, kwanza kuboresha benchi la ufundi, kuimarisha kikosi kwa kuongeza wachezaji wa kimataifa na kujenga uwanja wetu pale Mwenge, lakini kubwa zaidi kujenga brandi ya timu ili watanzania wapende kuichezea KMC,” alisema Sitta ambaye ni mwenyekiti wa timu hiyo. Alisema kwa sasa uwanja wa bora ambao ni maalumu kwa mazoezi umekamilika na wanaendelea kufanya mazungumzo na kocha wa kikosi hicho, Etienne Ndayiragije ambaye mkataba wake uliisha mwishoni mwa mwezi uliopita. Ndayiragije inadaiwa tayari ameanza kufanya mazungumo na Azam FC tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo nayo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
michezo
WAKATI Serikali ya Kenya imelaani matamshi ya kibaguzi dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua maarufu kwa jina la Jaguar, mbunge huyo amekamatwa.Taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa mbunge huyo alikamatwa na vyombo vya dola kwa amri ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wa nchi hiyo kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya wageni.Alikamatwa jana nje ya ukumbi wa Bunge na kupelekwa katika kituo cha polisi, ambacho hakijajulikana. Jumatatu wiki hii, mbunge huyo aliipa serikali ya nchi hiyo muda wa saa 24 kuhakikisha inawaondoa na kuwarudisha kwao wafanyabiashara wote wa kigeni waliopo kwenye jimbo lake, wakiwemo Watanzania.Njagua alisema kama Serikali ya Kenya itashindwa kufanya hivyo, atashirikiana na wananchi wa jimbo hilo kuvamia maduka ya wafanyabiashara hao na kuwatoa kwa nguvu, ikiwemo kipigo na kuwapeleka uwanja wa ndege ili serikali iwarudishe kwao. Moja ya sababu zilizomfanya mbunge huyo kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni ni kwamba wananchi wa jimbo lake hawana uwezo wa kushindana kibiashara na wafanyabiashara hao kutoka Tanzania, Uganda, China na mataifa mengine.Tamko la Serikali ya Kenya Jana Serikali ya Kenya kupitia kwa Msemaji wake, Kanali mstaafu Cyrus Oguna, ilisema inalaani matamshi ya mbunge huyo na kuwataka wafanyabiashara wa kigeni kuwa watulivu na kuendelea kufanya biashara zao, kwa kuwa serikali inawahakikishia usalama wao na wa biashara zao. Oguna kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema kauli za kibaguzi hazina nafasi katika mazingira huru ya utandawazi, lakini pia ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Kenya.“Mara nyingi Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akisisitiza kuhusu dhana ya uwazi na ukaribishaji kwa Waafrika wenzetu na jumuiya ya kimataifa kuitembelea nchi yetu, kushirikiana na Wakenya na kuwekeza kwa uhuru nchini mwetu.“Kwa bahati mbaya mtu mmoja anatumia vibaya uhuru wa kujieleza kwa kuwahamasisha wananchi kuvunja utamaduni wetu wa ukarimu kwa wageni, serikali haikubaliani na kauli hizi za kibaguzi za Njagua,”alieleza Oguna. Kutokana na kadhia hiyo, serikali ya Kenya imesema kauli ya Njagua si msimamo wa serikali na kuwahakikishia raia wote wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo usalama wao binafsi na biashara zao. Lakini, pia serikali hiyo ilisema ina matumaini kuwa nchi zote jirani na jumuiya ya kimataifa, zitaendelea kushirikiana na Wakenya mahali popote walipo duniani.Jaguar ni nani? Nje ya siasa, Jaguar ambaye jina lake halisi ni Charles Njagua Kanyi ni bilionea aliyeokolewa kimaisha kupitia kipaji chake cha muziki. Ingawa aliishi katika umasikini `kupindukia’ ikiwa ni pamoja na kuosha magari ili ajipatie pesa ya kumudu mlo wa siku, Jaguar alianza kubadilisha maisha yake baada ya kujikita katika muziki, akifyatua kazi moja baada ya nyingine na kujipatia mashabiki lukuki ndani na nje ya Afrika Mashariki. Miongoni mwa kazi zake za muziki ni pamoja na nyimbo za “Utaweza Kweli”, “Kigeugeu”, “Kipepeo” na “Kioo”.Hakuishia kupata mashabiki na umaarufu tu, bali alivuna pia pesa alizozitumia vyema, kwa kuwekeza katika katika biashara mbalimbali, ikiwemo nyumba za kisasa anazoishi na kupangisha. Kiwango chake cha utajiri kinachomfanya kuwa mmoja wa wasanii waliofanikiwa mno kimaisha, kinapimwa pia na maisha yake mengine, kwani anamiliki ndege binafsi na ana kampuni mbalimbali za usafirishaji, ikiwemo utitiri wa magari ya kifahari yanayokadiriwa kumgharimu zaidi ya Sh bilioni moja.Baadhi ya magari hayo ni Range Rover Sport, Bentley, Mercedes Benz E240 na Lexus GL 450, BMW 5 Series, Toyota Mark X na kadhalika. Umaarufu wake na kukubalika kwake kwa watu wa rika mbalimbali, ndiko kulikomfanya ajitose kwenye siasa.Kwa mara ya kwanza aliingiza kete yake ya kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, akiwania ubunge katika Jimbo la Starehe na kuibuka mshindi. Wakati anawania ubunge, Jaguar ambaye ni mmoja wa wabunge vijana nchini Kenya, alisema ameguswa na njia za nyota wa muziki wa kizazi kipya wa Tanzania, Joseph Haule `Profesa Jay’ aliyeng’ara kimuziki na baadaye kufanikiwa kuingia bungeni mwaka 2015.Hivyo, naye aliahidi kuingia katika siasa, ndoto ambayo ameitimiza, ingawa uchonganishi wake dhidi ya raia wa kigeni, umeitia doa nyota yake. Madai ya mkenya kutekwa Dar Katika hatua nyingine; Jeshi la Polisi limethibitisha kuwepo na taarifa zilizoripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay za kutoweka kwa mfanyabiashara wa Kenya, Raphael Ongangi katika mazingira ya kutatanisha huku watu watatu wasiojulikana wakidaiwa kutoweka naye.Akizungumzia tukio hilo la Juni 24, mwaka huu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mussa Taibu alisema mke wa mfanyabiashara huyo, Veronica Kundya aliripoti kituoni hapo taarifa za kukamatwa kwa mumewe na watu wasiojulikana.“Ni kweli tuna taarifa zimeripotiwa za kukamatwa kwa Ongangi na watu wasiojulikana, sisi hatuwezi kusema ametekwa au la kwa sababu tuna vyombo vingi vyenye mamlaka ya kumkamata mtu na kumhoji juu ya jambo fulani, sasa hatujajua kama ametekwa au la, ila tunaendelea na upelelezi kubaini amekamatwa na nani na wapi yuko,”alisema Kamishna Taibu.Awali, taarifa za tukio hilo zilitumwa kwenye baadhi ya mitandao na nyingine kutumwa kwa vyombo vya habari, zikisema mfanyabiashara huyo raia wa Kenya alitekwa akiwa njiani kurejea nyumbani akiwa na mkewe na watoto. Taarifa hiyo ilisema tukio hilo ni la juzi saa tatu na nusu usiku kwenye makutano ya barabara za Karume na Msasani, eneo la Oysterbay, jirani na Ubalozi wa Uganda.Akizungumzia tukio hilo kwenye taarifa hiyo, mke wa mfanyabiashara huyo ambaye ni Mtanzania, alisema wakiwa kwenye gari yao aina ya Land Rover Discovery Sport , watu watatu walikuja ghafla na kuwalazimisha wafungue milango na kuingia, kisha kumlazimisha Veronica kuendesha gari kuelekea eneo la Safari Beach, jirani na soko la samaki la Msasani.Taarifa hiyo ilisema kamera za CCTV zilizokuwa eneo la tukio, zilionesha magari matatu na pikipiki mbili na wanaume wengine, wakilifuata gari la mfanyabiashara huyo na kumtoa ndani ya gari lake na kumpandisha kwenye gari nyingine na kumuacha mkewe na gari.Hata hivyo zipo taarifa zinasema baada ya mkewe kuachwa, alipewa maagizo ya kusubiri maelekezo na baada ya saa moja kupita, mumewe alimpigia simu huku akipewa masharti na watu waliomshikilia kumtaka mkewe aende nyumbani na asitoe taarifa popote.Baada ya maelekezo hayo, Veronica aliondoka na kwenda moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Oysterbay, kutoa taarifa na kisha akaenda kutoa pia taarifa Ubalozi wa Kenya juu ya tukio hilo. Inasemekana, Ongangi anaendesha kampuni ya usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam na nchi jirani zikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia na Rwanda.
kitaifa
Taarifa kutoka Yanga zinasema kocha huyo aliondoka jana Dar es Salaam kwenda Morogoro, ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Simba.Zahera alikuwa kwenye benchi la ufundi la timu ya taifa ya Congo, The Leopard na amewahi kufundisha soka nchini Ufaransa.Ujio wa Zahera unathibitisha kuwa Yanga imeachana rasmi na Mzambia George Lwandamina aliyerejea kwao wiki mbili zilizopita kukamilisha mipango ya kujiunga tena na klabu yake ya zamani, Zesco United baada ya kuitumikia Yanga tangu Novemba mwaka 2016.Zahera anakuja Yanga akitokea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako alikuwa msaidizi wa Florent Ibenge tangu Septemba 30, mwaka jana pia amewahi kuzifundisha DC Motema Pembe ya DRC tangu Machi 1, mwaka 2015 hadi Machi 10, 2016.Pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa AFC Tubize ya Ubelgiji kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, mwaka 2014, ambayo alijiunga nayo baada ya kuachana na timu ya taifa ya DRC kati ya Agosti 14 na 28, mwaka 2017 chini ya kocha Ibenge.Zahera alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962 kabla ya kuanza soka mwaka 1975 akiichezea klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka 1980.Baadaye akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu, akijiunga na Chuo cha Teknolojia (ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka ya kulipwa.Zahera alicheza kwa misimu miwili Antwerp FC ya Ubelgiji kabla ya kumaliza mkataba wake na kwenda Ufaransa alikochezea timu za Daraja la Pili, Amiens, Beauvais na Abbeville hadi akastaafu soka. Baada ya hapo akaanza kupata mafunzo ya ukocha ambako alitunukiwa advance na leseni C, B na A za Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).Amewahi kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Ubelgiji kuifundisha Tubize na baadaye kurejea DRC na sasa yuko nchini kwa ajili ya kuifundisha Yanga.Kwa sasa Yanga ipo kambini Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Yanga inazidiwa na Simba kwa pointi 11, lakini ina viporo viwili na ili kutetea ubingwa inalazimika kushinda mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu na Simba ipoteze mechi mbili, jambo ambalo ni ngumu kutokana na uwezo wake kwani haijafungwa.Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alipoulizwa kuhusu ujio wa kocha huyo alitaka atafutwe msemaji wa klabu hiyo, Dismas Teni, ambaye alipopigiwa mara kadhaa, simu yake haipokelewa.
michezo
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza.Mabao ya Simba yalifungwa na Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi.Ushindi huo unawafanya wekundu hao kufikisha pointi 63 ikiikaribia Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 66 katika michezo 32.Simba ikishinda mchezo unaofuata dhidi ya KMC itafikisha pointi 66 sawa na Azam lakini itaishusha kwenye msimamo kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao.Niyonzima aliiandikia Simba bao la uongozi dakika ya 20 baada ya kupokea pasi ya Mzamiru Yassin lililodumu kwa kipindi kizima cha kwanza.Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hassan Dilunga, Adam Salamba na John Bocco na kuingia Clatous Chama, Okwi na Meddie Kagere.Mabadiliko hayo yalisaidia kuongeza kasi ya wekundu hao baada ya Okwi kuifungia timu yake bao la pili dakika ya 75 akiwachambua mabeki wa Alliance na kupiga shuti lililomshinda kipa wa timu hiyo.Alliance walijaribu kuingia ndani ya eneo la Simba mara kadhaa na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.Kadhalika kwa wekundu hao, walipoteza nafasi kwa vipindi tofauti kutokana na kubanwa na mabeki wa timu pinzani.Kitendo cha Alliance kupoteza kinazidi kuwaweka hatarini katika nafasi ya 16 ikikaribia mstari wa kushuka daraja baada ya kucheza michezo 33 na kujinyakulia jumla ya pointi 37.
michezo
WATU wanne wamekufa baada ya magari mawili waliokuwa wakisafi ria kugongana katika eneo la Ubena, Zomozi lililopo upande wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Francis Semwene alithibitisha kupokelewa kwa miili ya watu watatu ikiwemo ya mwanamke mmoja majira ya saa tano asubuhi jana.Dk Semwene alisema miili ya watu watatu ilisafirishwa kutoka eneo la tukio hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kuhifadhiwa chumba cha maiti na mwingine mmoja ambaye ni Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ulichukuliwa eneo la tukio na kwenda kuhifadhiwa Kituo cha Afya Ngerengere kilichopo Wilaya ya Morogoro.Kwa mujibu wa Kaimu Mganga mkuu huyo ,watu waliokufa, wawili ni wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi wa Reli ya Mwendeokasi (SGR) , mmoja ni Askari wa Jeshi ambaye alikuwa na gari lake binafsi pamoja na mwanamke mmoja alikuwa amepewa msaada ‘lifti’ na haikujulikana alikuwa kwenye gari lipi miongoni mwa zilizogongana.Dk Semwene alitaja majina ya watu waliokufa na miili yao kupokelewa Hospitali ya Rufaa ya mkoa kwa ajili ya kuhifadhiwa kuwa ni Modriki Mwaisyupa (41), Innocent Dastan (37) na mwanamke Zainabu Shija (32). Hata hivyo Dk Semwene alisema kabla ya kuchukuliwa kwa miili hiyo, wanaifanyia uchunguzi ili kubaini chanzo cha vifo vyao.Kufuatia ajali hiyo, gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Wilboad Mutafungwa ili kuthibitisha lakini alisema ajali hiyo ilitokea Ubena Zomozi na ni upande wa mkoa wa Pwani na hawezi kulizungumzia kwa kuwa ni mamlaka ya mkoa mwingine.Hata hivyo pamoja na jitihada za kumpata Kamanda mwenzake wa mkoa wa Pwani na kuulizwa kuhusiana na ajali hiyo alieleza kuwa, hakuwa na taarifa ya tukio hilo na kama lingetokea upande wake angelijulishwa na vijana wake na hivyo kushindikana kupatikana kwa namba za magari hayo wala kujua chanzo cha ajali hiyo.
kitaifa
Rais Kikwete alisema kuwa kiwango hicho kinaufanya uwekezaji wa China katika Tanzania kushika nafasi ya tano kwa thamani ya fedha, na kuwa uwekezaji huo utaiwezesha Tanzania kupata ajira 77,335 baada ya kukamilika kwa miradi yote kukamilika ambayo ujenzi wake unaendelea.Aidha, Rais Kikwete alisema uzuri wa uwekezaji huo kutoka China ni kwamba miradi mingi, 354 kati ya miradi hiyo yote 522 ya wafanyabiashara kutoka China ni kwenye sekta ya uzalishaji.Rais alisema hayo juzi wakati alipofungua Mkutano wa Tatu wa Uwekezaji wa Tanzania na China, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Nyumba ya Kulala Wageni ya Serikali ya Diaoyutai mjini Beijing, China ambako Rais anafanya ziara ya Kiserikali.Akizungumza na wafanyabiashara, Rais Kikwete alisema uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China umekua kiasi cha kwamba kati ya Julai na Septemba mwaka huu, 2014, thamani ya miradi imefikia dola za Marekani milioni 533.9 kulinganisha na miradi yenye thamani ya dola za Marekani 124.14 kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka jana.Rais Kikwete alisema ongezeko hilo lilifuatia kufanyika kwa Mkutano wa Pili wa Uwekezaji Kati ya Tanzania na China uliofanyika Dar es Salaam Juni 23 hadi 25, mwaka huu, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa China katika Tanzania, Li Yuanchao ambaye alifuatana na wafanyabiashara 100.Rais Kikwete alisema pia kuwa biashara kati ya Tanzania na China imeongezeka, lakini kwa kutilia maanani ukubwa wa uchumi wa China ambao ni wa pili duniani kwa ukubwa, bado biashara hiyo inaweza kukua zaidi.
uchumi
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jakaya Kikwete amewataka wahitimu wa shahada za ualimu kujiandaa kisaikolojia kufundisha shule za msingi badala ya shule za sekondari kama yalivyo matarajio yao.Ameyasema hayo kwenye mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Elimu Mkwawa cha mjini Iringa baada ya kutunuku Shahada za kawaida kwa wahitimu 1,340 na Stashahada ya Uzamili kwa wahitimu sita.“Serikali sasa inapeleka wanafunzi wenye shahada kufundisha shule za msingi, jambo hili halikupokewa vizuri na wale wa mwanzo, waliona kama wanashushwa hadhi kwa sababu stahili yenu ni kufundisha sekondari,” alisema na kuongeza kuwa maamuzi hayo ya Serikali ni sehemu ya mapinduzi makubwa ya elimu yanayoendelea kutokea nchini na kwa mazingira ya sasa hayaeupikiki.“Tulikuwa na walimu wa shule za msingi waliokuwa wahitimu wa darasa la saba na la nane, leo hawapo sasa tuna wa daraja la tatu A ambao ni wa kidato cha nne ambao nao watapotea kwa sababu ya ongezeko la walimu wa Diploma na Shahada,” alisema.Akizungumzia mapinduzi ya elimu katika nchi zilizoendelea, Kikwete alisema walimu wanaofundisha kuanzia chekechea hadi sekondari katika nchi hizo ni wale wenye elimu ya chuo kikuu.Kutokana na mabadiliko hayo amesema uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umeanza kuangalia namna utakavyobadili mitaala yake ili wahitimu wa shahada za ualimu katika vyuo vyake waweze kumudu kufundisha wanafunzi wa ngazi ya msingi hadi sekondari.Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye aliwataka wahitimu hao kutumia elimu yao kuikomboa jamii badala ya kuibomoa.Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema baraza linaendelea kushirikiana na wadau kuimarisha chuo na kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali.Katika hotuba yao iliyosomwa na mhitimu aliyefanya vizuri kuliko wanafunzi wote, Emanuel Kayuni, wahitimu hao waliwaasa wanafunzi wenzao wanaobaki chuoni hapo kujituma katika masomo yao, kudumisha umoja, nidhamu, hekima na mshikamano.
kitaifa
['Timu ya kandanda ya taifa Stars kutoka tanzania imeiondoa timu ya harambee Stars kutoka kenya katika mashindano ya CHAN 2020', 'Timu ya Kenya Harambee Stars ilidondoka katika michuano ya kufuzu kombe la CHAN 2020 baada ya kupoteza kwa Tanzania taifa Stars 4-1 kupitia mikwaju ya penalti katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi baada ya kutoka sare 0-0 katika dakika 90 za mchezo. ', 'Mkufunzi wa Harambee Sebastien Migne alichagua washambulia waliokuwa na kasi akiwemo Samuel Onyango na Duke Abuya lakini hawakuweza kucheka na wavu, na ilipofikia majira ya penalti Taifa Stars ilithibitisha kwamba wao ndio magwiji watakaoelekea Camroon ambapo michuano hiyo itachezwa mwezi Januari.', 'Harambee Stars walikuwa wametoka sare ya 0-0 siku ya Jumapili iliopita mjini Dar es Salaam na kufuatia ushindi huo Taifa Stars sasa itakutana na Sudan katika raundi ya pili na ya mwisho ya kufuzu.', 'Safu ya mashambulizi ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wa mashambulizi lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya safu ya ulinzi iliowekwa na Taifa Stars. ', 'Joash Onyango alionyesha umahiri wake katika safu ya ulinzi ya Kenya na kuzuia hatari iliokuwa ikisababishwa na Jonas Mkudde.', 'Safu ya mashambulizi ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wa mashambulizi lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya safu ya ulinzi iliowekwa na Taifa Stars. ', 'Joash Onyango alionyesha umahiri wake katika safu ya ulinzi ya Kenya na kuzuia hatari iliokuwa ikisababishwa na Jonas Mkudde.', 'Iddi Alli alikosa bao la wazi kufuatia uvamizi wa Taifa Stars katika lango la Kenya baada ya Isuza kupokonywa mpira.', 'Kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare tasa lakini Harambee Stars ilikaribia kufunga katika kipindi cha pili baada ya Miheso wa Kenya kuvamia lango la taifa Stars.', 'Tanzania ilikaribia kufunga kupitia mshambuliaji wake Mkudde lakini ulinzi mzuri wa Miheso ulimzuia mshambuliaji huyo matata.', 'Kunako dakika za mwisho Mkudde alivamia tena lango la Harambee Stars baada ya kumpokonya mpira Oyemba wa Kenya na kusalia na goli lakini mshambuliaji huyo mrefu wa Tanazania akapiga nje.']
michezo
BENKI ya Dunia imeisifu Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli katika kupunguza umasikini na kujenga miundombinu imara ya kukuza uchumi wa Taifa. Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Denis Biseko alitoa pongezi hizo jana, jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi nchini Tanzania bara mwaka 2017/18. Mwakilishi huyo alisema juhudi zinazofanywa na serikali katika kupunguza umasikini na kuwa taasisi inayoshughulikia suala hilo, ni kubwa na hivyo kui- pongeza serikali na Ofisi ya Takwimu nchini. Katika uzinduzi huo, ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi, ilielezwa kuwa uma- sikini wa mahitaji ya msingi miongoni mwa wananchi wa Tanzania Bara umepungua kutoka asilimia 28.2 katika mwaka 2011/12 hadi 26.4 katika mwaka 2017/18. Vile vile, kiwango cha umasikini wa chakula Tanza- nia Bara kimepungua kutoka asilimia 9.7 katika mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 katika mwaka 2017/18.Awali, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema umasi- kini wa mahitaji ya chakula katika jamii umepungua kutoka asilimia 28.2 katika mwaka 2011/12 hadi 26.4 katika mwaka 2017/18 kuto- kana na uwekezaji katika miundombinu mbalimbali na miradi mikubwa ya kitaifa.Dk Kijaji alisema juhudi zinatakiwa zaidi ili kuon- geza kasi ya kupungua kwa umasikini kwa kasi zaidi kunahitaji juhudi na maarifa ya ziada. Akizindua ripoti hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kiwango cha umasikini wa mahitaji ya msingi katika mwaka 1991/92 kilikuwa asilimia 39.0 hadi sasa kimepungua kwa asilimia 13 katika kipindi cha miaka 26.Akimnukuu Waziri mwenye dhamana, Waziri Mkuu alisema matokeo ya utafiti huu ni kupungua kwa umasikini wa chakula kutoka asilimia 22 mwaka 1991/92, asilimia 19 mwaka 2000/01, asilimia 17 mwaka 2007, asilimia 10 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18.Alisema hali ya chakula nayo imeendelea kuimarika kwa zaidi ya asilimia 124 na hivyo, kuwa kiashiria tosha cha utoshelevu wa chakula kwa msimu wa 2019/2020. Waziri Mkuu alisema kwa upande wa huduma ya maji, matokeo yameendelea kuonesha kuwa asilimia 73 ya kaya Tanzania Bara kwa mwaka 2017/2018 zilitumia maji ya kunywa kutoka vyanzo bora vya maji katika kipindi cha kiangazi ikilinganishwa na asilimia 61 mwaka 2011/12. Alisema kaya zinazoishi kwenye nyumba zenye paa la kisasa zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutoka asilimia 68 mwaka 2011/12 hadi kufikia asilimia 84 mwaka 2017/18 wakati kuta za kudumu zimeongezeka kutoka asilimia 46 mwaka 2011-12 hadi kufikia asilimia 79 mwaka 2017/18. Kuhusu hali ya umasi- kini, Waziri Mkuu alisema si wa Tanzania peke yake, Kenya kiwango cha umasi- kini wa mahitaji ya msingi ni asilimia 36.8 katika mwaka 2015, Afrika ya Kusini (55.5), Rwanda (38.2), Zambia (54.4), Ethiopia asilimia (23.5) na Zimbabwe (72.3). Waziri Mkuu aliagiza Ofisi ya Takwimu Taifa kusambaza watendaji katika ngazi ya halmashauri na katika mikoa ili kupata tak- wimu za kutosha kwa ajili ya maendeleo ya nchni. Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa alisema katika utafiti huo uliokusanya viashiria vina- vyohusu upatikanaji wa maji safi na salama, nishati ya umeme, hali ya vyoo katika kanya na viashiria vingine wamebaini kwamba asilimia 93 ya watanzania bara wanatumia vyoo jambo ambalo ni mafanikio makubwa ya serikali ya awamu ya tano.Kwa upande wa matu- mizi ya akaunti, asilimia 12.3 ya kaya zote nchini Tanzania bara angalau mwanakaya mmoja anamiliki akaunti katika benki yoyote ile nchini.Juhudi zinatakiwa kufanya na benki ili kuongeza idadi ya watanzania wanaotumia benki kwani inahitaji kuchangia kupunguza umasikini wa mahitaji ya watu kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.
kitaifa
SERIKALI imewaagiza wadau wa ngumi za kulipwa nchini, kuheshimu Kamisheni Mpya ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) ili kuweza mchezo huo kupata maendeleo makubwa na kuwanufaisha mabondia.Mwito huo ulitolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa mjadala wa mwisho wa Katiba ya Kamisheni hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Dk Mwakyembe alisema kuwa Tanzania ina mabondia wengi wenye vipaji na viwango vya dunia, lakini mpaka sasa wameshindwa kufaidika na vipaji vyao na kubakia maskini. Alisema kuwa kuna mabondia wengi wametwaa ubingwa wa dunia na kupata sifa kibao, hata hivyo wamebaki kuwa na maisha duni na kusikitisha.Alifafanua kuwa hali hiyo imesababishwa na usimamizi mbaya wa mchezo huo umepelekea mabondia hao kukosa malipo stahiki, huku wengine wakipigana nje ya nchi kwa ajili ya kuongeza rekodi za mabondia wengine. Alisema kuwa mabondia pia wamekuwa wakitumika kama makontena ya kubeba dawa za kulevya kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa faida ya kubeba dawa za kulevya Alisema kuwa wanatarajia kuona matunda chanya ya mchezo wa kulipwa nchini ili kuinua vipaji na vile vile kuwawezesha mabondia kupata vipato stahiki.Mwenyekiti wa muda wa kamisheni hiyo, Emmanuel Saleh alisema kuwa wamepitia changamoto nyingi mpaka kufikia hatua ya mwisho ya Katiba yao kujadiliwa. Saleh alisema kuwa pamoja na kukatishwa tamaa huko, lakini waliweza kusimama kidete na kuifikia hatua hiyo ya mwisho. “Kuna wengine walidhani kuwa tutashindwa, hapana, tulipata Baraka zako Mheshimiwwa na kufanikisha zoezi hili, ambapo baada ya majadiliano, tutafikia muafaka,” alisema Saleh.
michezo
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula ametoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhakikisha viwanja 150 vinaingizwa katika mfumo wa malipo ya kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki.Dk Angelina ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika Halmashauri ya Mkinga iliyoko mkoani Tanga kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Machi 2018.Amesema wizara imeamua kuweka mfumo rahisi wa kielektroniki utakaowezesha kutambua na kufuatilia wamiliki wa ardhi, badala ya mfumo wa zamani wa kutumia majalada ambao wakati mwingine huleta ugumu wa kufuatilia.Katika taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkuu wa Idara ya Ardhi ambaye pia ni Ofisa Mipango Miji katika halmashauri hiyo, Obed Katonge amesema halmashauri yake ina jumla ya viwanja 784 na kati ya hivyo, viwanja 634 vimeingizwa katika mfumo na 100 havijaingizwa.“Natoa mwezi mmoja kuanzia leo(juzi) hadi kufikia mwishoni mwa Februari viwanja vyote viwe vimeingizwa katika mfumo kwa asilimia 100, kwani kwa siku mnaingiza viwanja vingapi mpaka mshindwe kuviingiza katika mfumo?,” amesema.Naibu Waziri alisema hali ya mapato katika halmashauri nyingi hairidhishi na utumiaji mfumo wa malipo ya kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki mbali na kuwezesha uwepo wa kumbukumbu sahihi za wamiliki wa viwanja, lakini pia utasaidia kukusanya mapato ya serikali katika sekta ya ardhi.Akigeukia suala la utoaji hati za madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi, Dk Mabula alisema muda wa ulipaji kodi ya ardhi kwa hiyari umeshapita tangu Desemba mwaka jana, hivyo halmashauri hiyo inatakiwa kutoa hati za madai kwa wadaiwa wote na wale watakaokaidi hatua za kuwafikisha katika mabaraza ya ardhi zichukuliwe.Ameiagiza halmashauri hiyo kuhakikisha inaandaa na kutoa hati za madai 200 kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi ndani ya wiki moja lengo likiwa kuiwezesha serikali kukusanya mapato kupitia kodi ya ardhi.Katika taarifa yake, Mkuu wa Idara ya Ardhi amesema halmashauri hiyo inadai Sh 47,331,170 kutoka kwa wadaiwa sugu wa mashamba yanayoanzia hekta 20 na kuendelea na wadaiwa hao wapo 15.
kitaifa
NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amemwagiza Ofi sa Madini Mkazi wa Kanda ya Mirerani kuhakikisha anaufungua Mgodi wa Gem and Rock Venture na kuanza kufanya kazi mara moja, lakini kwa kufuata masharti ya leseni, kanuni, mipaka na sheria za uchimbaji na sio vinginevyo.Biteko alitoa agizo hilo juzi katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara baada ya kupokea taarifa za pande zote mbili juu ya mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili baada ya Kampuni ya Gem and Rock Venture iliyopo Kitalu B kutoboa Mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na Kampuni ya TanzaniteOne. Alisema serikali iko kwa ajili ya kusimamia sheria na haki kwa wachimbaji wote, wawe wakubwa au wachimbaji wadogo, kwa lengo la kutaka kila mmiliki wa mgodi kufuata sheria ya leseni ya uchimbaji aliyopewa na wizara.Alimwagiza Ofisa Madini Kanda ya Mirerani, Daudi Ntalima kabla ya kuwaruhusu Gem and Rock kuhakikisha anakagua mgodi huo kwanza ili ajiridhishe ikiwamo kuangalia usalama wake, wamiliki wanafuata sheria ya leseni yao ya uchimbaji, kanuni na mipaka ya mgodi na wakifuata masharti hayo, wanapaswa kuruhusiwa kuanza kazi. Akizungumzia malipo kutoka kwa wachimbaji wadogo ambayo walikuwa wakilipwa TanzaniteOne bila mbia Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kufahamu, aliwataka Stamico kuamka na kufuatilia kila kitu kinachofanywa na mbia mwenza.Aliwataka Stamico kukaa kibiashara zaidi kwa kufuatilia kila kitu ikiwamo kuangalia mikataba inayoingiwa na mbia mwenza na malipo mengine ambayo yanaweza kuwa nje ya sheria ya leseni ya madini. “Nimekuagiza RMO (Ofisa Madini Mkoa) kuhakikisha Gem and Rock Venture wanafunguliwa mgodi, lakini kabla ya kuwafungulia hakikisha unakagua mgodi wao kama umefuata sheria za madini, mipaka na kanuni,” alisema.Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, alisema ofisi yake itahakikisha inaangalia mipaka ya Mgodi wa Kitalu C na mpaka wa Kitalu B kama yote iko kisheria na nani anastahili kuifuata, kwa lengo la kuepuka migogoro isiyokuwa na tija kwa wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo. Alisema serikali haiko ili kumnyanyasa mtu yeyote, bali iko kuhakikisha kila mchimbaji kote nchini anapaswa kufuata sheria ya leseni aliyopewa, mipaka na kanuni na ikikiukwa serikali haitakuacha salama.Mkurugenzi Mwenza wa TanzaniteOne, Faisal Juma alisema kampuni hiyo inafuata sheria za leseni waliyopewa na kamwe hawawezi kufanya kazi nje ya masharti ya leseni. Juma alisema mara nyingi wachimbaji wadogo wamekuwa wakivamia mgodi wa TanzaniteOne, wao hawajawahi kuvamia migodi ya wachimbaji wadogo kama inavyoelezwa kwani kampuni hufanya kazi kwa kufuata mpango wa madini ambao unatoa mwelekeo wa uchimbaji salama wenye kufuata sheria. Alisema wakati wanapewa uwekezaji katika mgodi huo, waliona mipaka na majira ya nukta (Cordnets) katika mikataba hivyo wao wanafanya kazi kwa kufuata mipaka hiyo na sio vinginevyo.Akizungumzia suala la kufanya kazi bila kushirikisha Stamico, alisema suala hilo sio sawa kwani wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kupitia MEU (Kitengo cha Ufuatilia na Tathamini), na hakuna kitu kinafanywa bila wao kujua kwani hukaa kila siku asubuhi katika vikao vya menejimenti kufahamu utendaji kazi ndani na nje ya mgodi. Mgogoro kati ya Gem and Rock Venture na TanzaniteOne uliodumu kwa miaka miwili, ulitokana na Gem and Rock kuingia kinyemela na kufanya kazi katika mgodi wa TanzaniteOne mita zaidi 640 kinyume na leseni yao. Kutokana na hali hiyo, Ofisa Madini Mkazi alichukua hatua ya kuufungia mgodi huo na kuamriwa kurudi nyuma kama kanuni za mitobozano zinavyosema.
kitaifa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho anatarajiwa kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Pwani.Mkuu wa mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo amesema mjini Kibaha kuwa, Waziri Mkuu atazindua mwongozo huo kwenye kongamano la uwekezaji mkoa wa Pwani.Kongamano hilo litafanyika sambamba na maonesho ya pili ya viwanda Mkoa wa Pwani yaliyofunguliwa jana kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara mhandisi Stella Manyanya alifungua maonesho hayo kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.Wenye viwanda 329 wanashiriki kwenye maonesho ya mwaka huu wakiwemo kutoka mikoa ya Tanga na Dar es Salaam.Ndikilo amesema, hivi sasa Mkoa wa Pwani una viwanda 1,199 vikiwemo vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana, na kwamba, viwanda zaidi ya 300 vimejengwa katika Serikali ya Awamu ya Tano.Amesema mkoa huo umebaini kuwa, maonesho ya bidhaa zinazozalishwa viwandani ni njia mojawapo ya kukuza biashara za wawekezaji na kutatua changamoto zinazowakabili.Kwa mujibu wa kiongozi huyo, maonesho ya kwanza ya viwanda ya mkoa huo mwaka jana yameleta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuvipatia viwanda masoko wakiwemo wateja kutoka mikoa mbalimbali.
uchumi
Hyness ambaye ni mkulima na mama wa mtoto mmoja, alisema jana kuwa aliarifiwa juu ya ushindi wake akiwa shambani. Alisema anaamini Mungu amemuona na kwa ushindi huo, atabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.“Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa masoko ya mazao, pembejeo za kisasa. Kwa ushindi huu, naamini nitaboresha shughuli zangu za kilimo, ikiwemo kuanzisha biashara ndogo na kuboresha makazi yetu, nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii,” alisema Hyness.Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alimpongeza mshindi huyo na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom, kuchangamkia promosheni hiyo kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda kiasi cha Sh milioni 300 kila siku, mmoja akiondoka na Sh milioni 100 kila siku, 10 kila mmoja akishinda Sh milioni 10 na 100 kila mmoja Sh milioni moja, achilia mbali wengine 15,000 wanaojishindia muda wa maongezi wa Sh 1,000 kila mmoja.Alisema kuwa tangu promosheni hiyo ya siku 100 iliyoanza wiki iliyopita, tayari wateja watano wamejishindia Sh milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.“Promosheni hii itadumu kwa siku mia moja, hivyo leo ni droo ya nane hivyo bado kuna mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544. Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom, kiasi kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki,” alisema.
uchumi
BARAZA la Mawaziri nchini hapa limetangaza kuongeza mishahara kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kwa asilimia 10 katika shule za serikali na binafsi kuanzia Machi mwaka huu.Hatua hiyo imefikiwa na kikao cha mawaziri kilichoongozwa na rais wa nchi hiyo, Paul Kagame. Walimu nchini humo wamefurahishwa na ongezeko hilo na kuwa yamefanyika baada ya maombi ya muda mrefu ya chama chao, hivyo kuamini kuwa mambo mazuri yanakuja. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Rwanda (SNER), Faustin Harelimana, alisema hatua hiyo imeleta ahueni kwani wamekuwa wakiomba kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa muundo wa malipo kwa walimu, malipo kwa walimu inategemea kiwango cha elimu pamoja na uzoefu. Novemba mwaka jana, seneta waliomba serikali kuboresha malipo kwa walimu ili yaendane na ukuaji wa uchumi. Walimu kwa miaka kadhaa wakitaka kiwango cha mshahara kufikia angalau Faranga 80,000 za nchi hiyo ili kuweza kukidhi mahitaji muhimu, kwani walimu wanaoajiriwa wakiwa na vyeti kwa shule za msingi wanalipwa faranga 44,000 ,wale wenye diploma Faranga 90,000, huku wenye shahada wakipokea Faranga 120,000.
kitaifa
MAMLAKA ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema mchakato wa kubadilisha sheria ya uendeshaji mifuko ya hifadhi ya jamii, uliwashirikisha wadau wote muhimu, kabla ya kupitishwa na kuanza utekelezaji wake.Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma ya Mwaka 2018, ambayo ilisainiwa mwanzoni mwa mwaka huu, imekumbwa na ukosoaji kwa baadhi ya watu wachache, huku baadhi ya wadau wakidai kwamba chini ya sheria hiyo, mstaafu atapata malipo ya mkupuo ya asilimia 25 tu. Akizungumzia tuhuma hizo, ambazo zimekuwa zikitolewa dhidi ya sheria kwa miezi kadhaa sasa, Mkurugenzi wa Huduma ya Sheria wa SSRA, Onorius Njole alisema mabadiliko yalifanyika, baada ya mawasiliano na mashauriano ya kina na wadau wote.“Tulipokea michango mingi...ilibainika kwamba mafao yanayotolewa ni zaidi ya uwezo wa mifuko. Tungetakiwa kupunguza mafao au kuongeza kiwango cha uchangiaji ili kuifanya mifuko ibakie imara,” alisema Njole.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mamlaka ilifanya jumla ya mikutano 47 na wadau wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia mwaka 2013 na kwa kipindi chote hicho, wamekuwa wakionesha udhaifu uliopo kwenye mifuko hiyo na kushauri kwamba sheria ibadilishwe. “Tuliishirikisha serikali, vyama vya waajiri na vyama vya wafanyakazi katika kuandaa maazimio ya marekebisho ya sheria,” alisema.Aliongeza kwamba baadaye kwenye mchakato huo, mapendekezo yalifikishwa kwenye wizara yenye dhamana na ajira na maoni ya wadau yalichukuliwa kwa umuhimu wa kipekee. “Baada ya wizara kuyapitia upya mapendekezo na kuongeza maoni mengi ya wadau, mapendekezo hayo yaliandikwa upya na kwa kawaida lazima andiko kama hilo lijumuishe majina ya wadau walioshiriki,” alisema.Njole alisema ilifikia wakati waajiri wakawa wanatoa maoni, kwamba malipo ya mtumishi yalipwe kwa kukokotoa wastani wa mshahara wake, aliokuwa anapata kwa wakati wote wa ajira. “Wazo hilo lingepunguza kwa kiasi kikubwa sana malipo ya mstaafu ya kila mwezi na badala yake tuliamua kwamba mstaafu apate asilimia 72.5 ya mshahara aliopokea miezi mitatu kabla ya kustaafu,” alisema.
kitaifa
UONG OZ I wa Y anga umemshitaki mchezaji wa Si mba, James Kotei kwa Sh irikisho la So ka Tanzania (TFF) ikitaka achukuliwe hatua kwa utovu wa nidhamu.Kotei alimpiga ngumi beki wa Y anga, G adiel Michael wakati timu zao zilipokutana kwenye mechi ya L igi Kuu B ara mwishoni mwa wiki iliyopita. Marudio ya picha za video yalimwonesha Kotei akimpiga ngumi Michael shingoni katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoka suluhu. Akizungumza jana, Mkuu wa Idara ya H abari na Mawasiliano wa Y anga, Dismas Ten alisema wamejaribu kuonesha tukio na kuandika barua ili haki itendeke.“ S iwezi kujua nini kilimkuta Kotei akafanya vile, naamini kama nimchezaji muungwana siku ile angeomba radhi kama wengine wanavyofanya angeeleweka,” alisema. Ten alisema anaamini mchezaji huyo hana matukio mengi ya kihuni, ingetosha kuwaonesha watu hata kwa kuandika ujumbe wa kuomba radhi kwenye mitandao ya kijamii.Katika hatua nyingine, alisema Juma Mahadhi ataukosa mchezo ujao dhidi ya Mbao kwani bado anaendelea kuuguza jeraha la goti. Alitaja wachezaji waliorejea mazoezini kutoka majeruhi kuwa ni Juma Abdul na B aruan Akilimali. Pamoja na hilo alisema wameanza maandalizi ya mechi zao za mikoani baada ya kuona timu nyingine zinavyopata changamoto.Katika kuhakikisha wanafanya vizuri alisema viongozi wa Y anga mikoani wameweka mikakati dhidi ya mechi hizo kujenga umoja na kujua nini timu inataka. Pia, alizungumzia suala la jezi zao za msimu huu kuwa hawajazizindua hivyo wanatarajia kutangaza tenda na wakipata kampuni watatangaza na kutengeneza nyingine kwa ajili ya mechi zijazo. Alisema kampuni waliyokuwa wakifanya nayo kazi Micron wameshindwana na kuwataka mashabiki kuwa watulivu wakati wowote watatangaza jezi mpya za msimu huu.
michezo