content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema wizara hiyo inatarajia kuja na mkakati maalumu wa kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kwa kunadi maeneo ya vivutio vya utalii badala ya kuinadi nchi kwa ujumla na vivutio vyake.Pia amesema maeneo hayo yatakuwa yakinadiwa kwa mfumo wa vifurushi hali itakayosababisha mtalii akija nchini atatembelea maeneo ya hifadhi, misitu ya mazingira asilia pamoja na maeneo ya utalii wa kiutamaduni.Kanyasu alisema lengo la kuja na mkakati huo ni kusaidia maeneo hayo kujulikana pamoja na kumwezesha mtalii kuvifahamu vivutio vinavyopatikana katika eneo hilo kwa undani badala ya kuitangaza nchi kwa kujumuisha vivutio vya utalii vilivyopo kwa ujumla wake.Alisema mkakati huo utasaidia kuongeza idadi ya watalii katika maeneo yenye vivutio ya utalii, lakini kwa sasa yamekuwa yakipata idadi ndogo ya watalii kwa vile yamekuwa hayafahamiki ipasavyo.Alisema mkakati huo utalenga zaidi katika maeneo yenye utalii wa kiutamaduni na maeneo ya misitu asilia, ni utalii mpya ambao kwa Tanzania haufahamiki unaojikita kuangaliia viumbe ambao wapo hatarini kutoweka.
uchumi
WATAALAMU wa afya wameshauri wazazi kuacha kuwapa watoto wao vyakula vyenye sukari ili kupunguza ongezeko la ugonjwa wa kisukari kwa watoto wadogo.Vyakula ambavyo wazazi wanatakiwa kuepuka kuwapa watoto ni pamoja na chipsi, baga, soseji na vile vyenye mafuta mengi, sukari nyingi, ikiwemo vinywaji kama soda, juisi za viwandani na bidhaa nyingine za aina hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa masuala ya afya kwa nchi za Afrika (AMREF), Daktari Githinji Gitahi kutoka Kenya kupitia ukurasa wake wa twitter alisema “natamani niandike hata mara 1,000 wazazi waache kuwanunulia watoto wao soda na vyakula vyenye mafuta tafadhali nawaomba sana.” Githinji alisema ugonjwa wa sukari umekua janga kwani kwa sasa ndio unaongoza kuua zaidi watoto na hata watu wazima.Kauli hiyo imeungwa mkono na Dk Andrew Suleh ambaye alisema kisukari aina ya pili ndio imekithiri kwenye nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kutokana na mfumo wa maisha watu kutokana na msongo wa mawazo, kutofanya mazoezi, kula vyakula visivyofaa sukari kupita kiasi, pamoja na pombe.Kwa upande wa aliyekuwa daktari mkuu kitengo cha magonjwa ya sukari Hospitali ya Mwananyamala ambaye kwa sasa amestaafu, Nurdin Mavura akizungumzia ugonjwa huo alisema sukari ni ugonjwa wa kurithi, kama wazazi baba au mama, wajomba, mashangazi, kama wanao ni rahisi pia kurithi. Alisema kisukari cha watoto ni aina ya kwanza ambayo ni ya kinasaba na moja kwa moja huanza na sindano ya insulin.Alisema aina ya kwanza ya kisukari mtoto mpaka agundulike ni kuanzia umri wa miaka minne na huathiri zaidi watoto na vijana na kwamba aina hii ya kisukari ikiwa seli maalumu zinazotengeneza homoni ya insulin zinapokosekana katika tezi kongosho. Pia kongosho inapoharibika kutokana na sababu yeyote ile husababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu na kwamba matibabu aina hii ya kisukari ni hatari kwa kuwa watoto hawawezi kujidhibiti katika vyakula hivyo sindano pekee ndio inayotumika katika matibabu.Dk Mavura alisema katika aina hii ya pili ya kisukari, insulini huzalishwa kwa kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi na utendaji kazi wake na kwamba mara nyingi mtu hupatikana na aina hii kisukari ukubwani. Naye daktari wa masuala ya afya na chakula, Sweetbeth Njuu akizungumza na HabariLeo kuhusiana na suala hilo alisema watoto walio kwenye hatari zaidi ya ugonjwa wa sukari ni wale wanaozaliwa na uzito mkubwa na wale wanaozaliwa na uzito mdogo.Alisema kwa kawaida mtoto anapaswa kuzaliwa akiwa na kilo mbili na nusu hadi tatu na nusu, zikizidi hapo mtoto anakuwa kwenye hatari ya kuzaliwa na ugonjwa wa sukari na pia zikipungua chini ya kilo mbili na nusu pia mtoto anakuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo. Dk Njuu alisema janga la kisukari cha utotoni linatokana na ulaji mbovu, na wazazi ndio wanachochea, kwa kuwa watoto hawana tamaa wala hawana uchaguzi wa chakula, anamtegemea mzazi. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2017 ya shirikisho la kimataifa la ugonjwa wa kisukari karibu watu milioni 15.5 waliyo na umri kati ya miaka 20-79 wanaishi na ugonjwa huo Barani Afrika.Ugonjwa wa kisukari hutokea pale kongosho inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya insulini au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho. Hali hiyo husababisha ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu (hyperglycemia). Msimamizi wa Huduma za Kisukari kwa Watoto kutoka Chama cha Kisukari nchini (TDA), Herieth Mganga alikarirwa akisema ugonjwa wa kisukari kwa watoto upo lakini baadhi ya wazazi bado hawajakubali na kuongeza kuwa hadi sasa kuna watoto 2,488 ambao wanatibiwa kisukari katika kliniki 34 zilizopo nchini.
kitaifa
['Unai Emery amedokeza kuwa alikaribia kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na raia wa Brazil Fabinho, 26, alipojiunga na Arsenal kama kocha mkuu mwaka jana. (Evening Standard)', 'Manchester City imeongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 23, na pia ilituma wataalamu wake kufuatilia mechi ya Jumatano ya Champions League dhidi ya Red Bull Salzburg. (Guardian)', 'Tottenham inamfuatilia mshambuliaji wa Gremio raia wa Brazil Everton Soares, huku mtaalamu mkuu soka Steve Hitchen akimtazama mchezaji huyo wa miaka 23 katika michuano ya Copa Libertadores. (Sky Sports)', 'Manchester United ina mpango wa kuwasajili wachezaji wawili wa safu ya mashambulizi baada ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kuomba kuimarisha kikosi chake zaidi. (Star)', 'Arsenal itawasilisha ombi la kutaka kupunguziwa bei ya kumnunua beki wa kati na nyuma wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 20, kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi cha Unai Emery. (Sun)', 'Monaco wana nafasi ya kumnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 31, anayewachezea kwa mkopo huku tetesi zikisema kwa ada hiyo ni robo ya £29m iliyolipwa mwaka 2016. (Sky Sports)', 'Real Madrid imemtambua kipa wa Athletic Bilbao Mhispania Unai Simon, 22, kama mchezaji ambaye huenda akachukua nafasi ya kipa wao wa sasa Mbelgiji Thibaut Courtois, 27. (El Desmarque, via AS)', 'Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemtaja Harry Kane wa Tottenham kama mshambuliaji mahiri lakini amekiri kuwa haoni kama klabu yake itafanikiwa kumhamisha nyota hiyo wa miaka 26 kutoka London kaskazini. (Evening Standard)', 'Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema angelipendelea kumsajili Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye mkataba wake katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwezi Januari. (ESPN)', 'Brendan Rodgers amemwambia kiungo wa kati James Maddison kuwa Leicester ni mahali anapoweza "kujikuza" licha ya Manchester United kuonesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 22. (Leicester Mercury)', 'Juventus inafanya mazungumzo na Mario Mandzukic kuhusu uhamisho wake kutoka klabu hiyo mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Croatia wa miaka 33 amekuwa akilengwa na Manchester United. (Mirror)', 'Vilabu vya Derby, Huddersfield na Swansea vinamfuatilia mchezaji wa safu ya kati wa Fleetwood Kyle Dempsey, 24. (Football Insider)', 'Mchezaji wa zamani wa Liverpool wa safu ya kati Dietmar Hamann anasema kuwa amepata fununu kwamba Reds "wanahamu sana" ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. (Sky Germany - via Mirror)', 'Real Madrid imemwambia kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz, 20, kwamba inataka kumuuza kama sehemu ya kuondokeana nae kabisa. (Mail)', 'Barcelona imepinga madai kuwa imeilipa Atletico Madrid euro milioni 15 kumaliza mzozo kati yake na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Sport)', 'Mchezaji wa safu ya kati ya Real, Isco, 27, amekubali kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka klabu hiyo mwezi January mwakani. (Mail)', 'Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Paris St-Germain na Juventus, Zlatan Ibrahimovic,38, anataka kurejea katika ligi kuu ya Italia, Serie A. ', 'Meneja wa chuo cha mafunzo ya soka ya Manchester United Nicky Butt anasema klabu hiyo inawachezaji wengi ambao wanaweza kufuata nyayo za mshambuliaji Marcus Rashford na kuleta mabadiliko katika kikosi cha kwanza. (Goal)']
michezo
MADHARA ya mama mjamzito asiyekuwa na kinga au kupata chanjo ya ugonjwa wa rubella, husababisha kuzaa watoto wenye matatizo ya matundu kwenye moyo, fi go na hata kuwa na shida ya viungo.Dalili za ugonjwa wa rubella hazina tofauti na za ugonjwa wa surua, ambapo mtoto huanza kwa kupimwa kwanza surua kisha kupatiwa chanjo. Meneja wa Taifa wa Mpango wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dafrosa Lyimo alisema hayo jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya wiki ya chanjo. Wiki ya chanjo hufanyika kila mwaka katika wiki ya mwisho ya mwezi wa Aprili.Alisema chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella hutolewa moja na chanjo hiyo ilianza kutolewa rasmi nchini kuanzia mwaka 2014. Alisema surua na rubella husababishwa na virusi na huenezwa kwa njia ya hewa na dalili zinafanana, ambapo kati ya siku 8 hadi 21 za maambukizo mtoto atakuwa na dalili za joto kupanda, vipele vidogovidogo kuanzia usoni hadi miguuni na macho kuwa mekundu.Kuhusu chanjo, alisema mpango wa taifa wa chanjo ulianzishwa mwaka 1975 kwa lengo la kuwakinga watoto, wasichana na jamii kwa ujumla dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. “Mpaka sasa jumla ya magonjwa 13 yanayozuilika kwa chanjo yapo katika mpango wa taifa wa chanjo,” alisema Dk Dafrosa na kuongeza kuwa kauli mbiu ya wiki ya chanjo ni ‘Chanjo ni kinga, kwa pamoja tuwakinge’.Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na kupooza, surua, rubella, pepopunda, dondakoo, kifaduro, kifuakikuu, kuharisha, kichomi, saratani ya mlango wa kizazi, homa ya ini na mafua makali. Kuhusu huduma za chanjo, alisema imethibitika kitaalamu kuwa chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya kuambukizwa.Alieleza kuwa pia hupunguza gharama kubwa ambazo familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Alisema malengo ya mpango wa taifa wa chanjo kuanzia mwaka 2016 hadi 2020, ni kumfikia kila mtoto kwa chanjo kwa usawa, kuongeza wigo wa utoaji huduma za chanjo kwa watu wote.
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa amekuwa mchezaji wa tatu msimu huu kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja, hat-trick, baada ya kufanya hivyo katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance mchezo uliopigwa jana Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.Chirwa alifunga mabao hayo dakika ya tano, 24 na 68 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji Shaban Chilunda, ambaye alifunga mabao mengine mawili katika dakika ya 32 na 52 kufuatiwa kazi nzuri ya Chirwa na beki Nicolas Wadada.Wengine ambao tayari wameshafunga hat-trick msimu huu ni Ditram Nchimbi wa Polisi Tanzania dhidi ya Yanga na Daluwesh Saliboko wa Lipuli walipocheza dhidi ya Singida United. Baada ya ushindi huo, Azam imesogea mpaka nafasi ya nne ikiwa na pointi 19 sawa na Namungo, ambao wote walishinda mechi zao za mwisho.Katika mchezo huo wa jana, Azam ilitawala kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kutengeneza nafasi nyingi, ambazo hazikuzaa matunda kutokana na kukosa umakini kwa washambuliaji wa timu hiyo.Licha ya kutawala mchezo huo, Azam iliendelea kuwa na uchu wa mabao, baada ya kufanya mabadiliko ya kutoka Obrey Chirwa na kuingia Shaban Hamis na kutoka Mudathir Yahya na kuingia Donald Ngoma.Mabadiliko hayo yaliendelea kuifanya timu hiyo kuendelea kumiliki mpira na kukosa umakini wa eneo la mwisho baada ya kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na viungo wa timu hiyo akiwemo Salum Abubakar. Matokeo mengine ya michezo ya jana ni Mbao ilishinda 2-0 dhidi ya KMC, Mtibwa ikaifunga Kagera mabao 3-1, Biashara ikaifunga Lipuli 1-0, Mbeya City ikiwa Sokoine ikalala 2-1 dhidi ya Mwadui na JKT Tanzania ilishinda 2-1.Wakati huohuo, Yanga wanaondola leo inaifuata Alliance ya Mwanza ambayo itacheza nayo keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
michezo
['Leicester imeanza mazungumzo na kocha Brendan Rodgers kuhusu mkataba mpya ili kuiwekea ukuta nia ya Arsenal kumnasa kocha huyo. (Telegraph)', 'Kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino hatakuwa kocha wa Bayern Munich.(Bild)', 'Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri amesema hatarejea kuwa meneja mpaka kipindi cha majira ya joto lakini anafanya mafunzo ya kiingereza kutokana na kuhusishwa na timu za ligi kuu ya England. (ESPN)', 'Manchester United bado wana matumaini ya kumsajili kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27, mwezi Januari baada ya mchezaji huyo kuwakataa.(Mirror)', 'Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland, 19, anaweza kuuzwa kwa kitita cha pauni milioni 17 mwezi Januari kwa mujibu wa mkataba wake.(Manchester Evening News via Bild)', 'Chelsea wana mpango wa kumsajili mshambualiaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 27, kipindi kijacho cha majira ya joto.(Independent)', 'Unaweza pia kusoma', 'Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 33, hataiacha klabu hiyo mwezi Januari huku vilabu vinavyomtaka vikiamua kusubiri mpaka mchezaji huyo atakapopatikana kwa uhamisho wa bure. (Sun)', 'Borussia Dortmund wana mpango wa kumbakisha mshambuliaji Jadon Sancho, 19 mpaka mwishoni mwa msimu.(Telegraph)', 'Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amehojiwa kwa ajili ya nafasi ya ukocha katika klabu ya Watford. (Times)', "Kocha wa zamani wa West Ham, Newcastle na West Brom Alan Pardew amesema anapenda kuifundisha Everton lakini amesema kocha wa zamani wa Everton David Moyes 'anafaa kwa nafasi hiyo'.(Mail)", 'Wakala wa mshambuliaji wa Barcelona KOusamne Dembele,22, amekutana na uongozi wa Chelsea na Manchester City. (El Desmarque - in Spanish)', 'West Ham watajaribu kumuuza mlinda mlango Roberto mwezi Januari na kutengana na mkurugenzi wa michezo aliyemuingiza kwenye klabu hiyo.(Guardian)', 'Mshambuliaji wa miaka 17 Ansu Fati ametia saini mkataba mpya wenye kipengele ambacho kitamfanya anunuliwe kwa Pauni milioni 337.5. (FC Barcelona)']
michezo
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesitisha uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege na kumteua Fred Luvanda kushika nafasi hiyo kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo, kutenguliwa kwa Nyabundege kumezingatia Kifungu Namba 33(2) na 33(2) (f) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006. Taarifa hiyo pia ilisema uteuzi wa Luvanda umezingatia Kifungu Namba 33(2)(b) cha Sheria za Mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006 na kuongeza kuwa hatua ya mabadiliko hayo, imetokana na mwenendo usioridhisha wa benki hiyo chini ya uongozi wa Nyabundege.Luvanda anachukua nafasi hiyo, akitokea Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha ya benki hiyo, ambaye kwa sasa amepewa jukumu la kusimamia shughuli zote za kiutendaji za benki ya TIB Corporate.“Hatua hizi zilizochukuliwa zina lengo la kuboresha usimamizi na utendaji wa mabenki yanayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki Kuu inauhakikishia umma kuwa Benki ya TIB Corporate itaendelea kutoa huduma na madai yote yaliyoiva yatalipwa kama kawaida” ilisema taarifa hiyo. Ilisema Benki Kuu itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki ili kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa stahimilivu.
kitaifa
BIASHARA ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika kwa ujumla, inatajwa kukua kwa kiwango cha chini ikiliganishwa na kanda nyingine ulimwenguni.Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda na Biashara katika Sekretarieti ya SADC, Calicious Tutalife amesema ikilinganishwa na kanda nyingine duniani, biashara iko chini katika SADC na Afrika.Akieleza shughuli za kurugenzi ya maendeleo ya viwanda na biashara kwa waandishi wa habari jana Dar es Salaam, alisema thamani ya biashara ya ndani imeendelea kubaki chini kwa asilimia 22 ya biashara yote ya SADC.Alisema kasoro hiyo ni miongoni mwa zilizobainika kupitia maadhimisho ya wiki ya viwanda yaliyohitimishwa hivi karibuni jambo ambalo ameshauri ifanyike mikakati kuondokana nazo.Akisisitiza jumuiya kuweka kipaumbele cha biashara ndani ya ukanda, alisema pia inapaswa kutatua matatizo ya miundombinu, kupunguza vikwazo, kuboresha ubunifu na utafiti.Amesema baraza jipya la biashara lililozinduliwa, linapaswa kushirikiana na nchi wanachama kuboresha na kuwezesha mazingira ya ushindani kwa kuhusisha ukanda, nchi na sera za ndani kiasi cha kuwezesha kuleta matokeo chanya katika maendeleo ya kiuchumi.Amesema pia uwekezaji katika utafiti, maendeleo na ubunifu umeendelea kubaki chini huku nchi nyingi zikiwekeza chini ya asilimia moja ya pato la ndani (GDP).“Upo umuhimu wa kuboresha mfumo wa elimu ikiwamo teknolojia mpya, kuwekeza kwenye miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano, vituo vya umahiri, ubunifu na vituo vya viwanda ili kuongeza fursa za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda,” amesema.Alishauri kuwa pia upo umuhimu wa kusaidia fedha za kuanzisha nyenzo za kuunga mkono ubunifu na maendeleo ya teknolojia.
uchumi
WAKATI mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yakiendelea kunoga, wapinzani wao Guinea ya Ikweta wanatarajiwa kutua nchini leo alfajiri tayari kwa pambano la kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcom 2021 nchini Cameroon.Kambi ya Taifa Stars ilikamilika juzi baada ya kutua kwa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi, Mbwana Samatta kutoka Ubelgiji na Simon Msuva anayecheza soka Morocco, huku ushindani ukingezeka kwa wachezaji kugombea namba.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema wachezaji wote wanaonesha kiwango kizuri mazoezini kila mmoja akisaka nafasi ya kuwamo katika mchezo huo wa kesho kwenye Uwanja wa Taifa. Mchezo huo wa kwanza wa Afcon 2021 dhidi ya timu hiyo ya Guinea ya Ikweta, utaanza saa 1:00 usiku na viingilio ni Sh 5,000 VIP na 3,000.“Vijana wako katika ari ya juu, kila mmoja anaonesha kiwango ili aweze kupata namba katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo, tunaamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema.Mchezaji huyo wa zamani wa Stars alisema jambo la muhimu ni mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kuwatia nguvu wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuanza kwa ushindi mchezo huo wa kwanza kabla ya kucheza na Libya katika mchezo wa pili. Kwa upande wake, Kocha Msaidizi Juma Mgunda, alisema maandalizi yanakwenda vizuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.Alisema wachezaji waliopo kwa kipindi hiki watasaidia kutimiza lengo la kwanza la kutafuta ushindi katika mchezo huo wa kwanza wa kufuzu kabla ya kuelekea Tunisia kuwakabili Libya. Taifa Stars inasaka kwa mara ya pili mfululizo kufuzu kucheza fainali za Afcon baada ya mwaka huu kushiriki zile za Misri, lakini ilitolewa katika hatua ya makundi baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza miaka 39 iliyopita.
michezo
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amemkabidhi Katibu Mkuu wa Hazina, Doto James madini ya dhahabu, madini ya vito na fedha za kigeni kwa pamoja zenye thamani zaidi ya Sh bilioni tisa zilizotaifi shwa kutokana na kesi za uhujumu uchumi. Mbali na kiwango hicho cha fedha, kiasi kingine cha madini ya Tanzanite gramu 888 zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni saba ambazo ziko Arusha bado hazijakabidhiwa. Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dar es Salaam jana, Biswalo alisema madini yaliyotaifishwa ni pamoja na kilo 25.546 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 913,954.72 na Tani 76 za madini ya vito zenye thamani ya Dola za Marekani 2,638,349.95.Biswalo pia alikabidhi carrats 2,849 zenye thamani ya Dola za Marekani 3,803.32 pamoja na fedha za kigeni za mataifa 15 zenye thamani ya Sh 1,023,608,515.12. Katika makabidhiano hayo ambayo yalishuhudiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango na Waziri wa Madini, Doto Biteko, DPP aliwataja Wakaguzi wa Madini, Omary Pima na Donald Njonjo na baadhi ya askari kuwa ndiyo waliohusika katika kukamata madini hayo, lakini pia alimtaja Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori kwa kusimamia kesi hizo ambapo robo tatu ya madini yaliyotaifishwa yalitokana na umahiri wake wa kazi.Madini na fedha hizo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye makasha makubwa manne ambayo Katibu Mkuu wa Hazina alizikabidhi kwa Benki Kuu ya Tanzania ili zihifadhiwe mpaka hapo matumizi yake yatakapoainishwa. Mara baada ya kukabidhiwa madini na fedha hizo, Doto alisema dhahabu hizo ambazo amezikabidhi BoT kwa ajili ya kuhifadhiwa ni nyongeza katika akiba ya fedha za kigeni na kuwa mbali na dhahabu, madini ya Tanzanite nayo yamekuwa yakitoroshwa nje ya nchi hususani nchi jirani, hivyo serikali imejidhatiti katika kuziba mianya hiyo ya utoroshaji wa madini. Akisisitiza utunzaji wa madini hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango alisema: “Inaumiza sana, haiwezekani katika umaskini huu wa Watanzania halafu kuna watu wengine wanapora mali za maskini, nawapongeza Ofisi ya DPP kwa kushinda vishawishi mbalimbali baada ya kukamata mali hizi, sitarajii mali hizi tunazozihifadhi hapa BoT nije kusikia eti zimegeuka vioo vilivyosagwasagwa, nitajiuzulu mara moja”. Kauli hiyo ya Dk Mpango kuwa hatarajii kusikia madini hayo yamegeuka kuwa vioo vilivyosagwa ilikuja baada ya Waziri Biteko kusema kuwa kwenye miaka 1990, dhahabu iliyokuwa imehifadhiwa BoT ilionekana kugeuka na kuwa dhahabu feki.Dk Mpango aliiomba Wizara ya Katiba na Sheria kuwapatia cheti cha kumbukumbu maofisa wake waliosimamia vizuri ukamataji na utaifishwaji wa mali hizo, lakini pia alimwomba Katibu Mkuu wa Hazina naye kuwafanyia kitu cha kumbukumbu kutokana na kazi hiyo nzuri walioifanya. Alitoa wito kwa mahakama na vyombo vya dola kutokuwa na huruma na watu wanaohujumu rasilimali za nchi, bali wawashughulikie ipasavyo. Naye Waziri wa Madini, Doto Biteko aliwaonya watu wanaodhani kuwa wanaweza kuiweka serikali mfukoni kwa kuendeleza vitendo vya utoroshaji wa madini.Biteko alisema kwenye mkutano wa Rais John Magufuli na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika jijini Dar es Salaam, wachimbaji hao walilalamika kuhusu uwepo wa kodi kwenye sekta hiyo, ukosefu wa masoko ya madini pamoja na urasimu mambo ambayo serikali iliyafanyia kazi lakini cha kushangaza bado wapo baadhi ya watu wanaendeleza vitendo viovu vya utoroshaji wa madini. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Augustine Mahiga alisema Mahakama na Ofisi ya DPP wamefanya kazi nzuri ambayo imewezesha madini na fedha hizo kurudi serikalini na kuongeza kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na madini mengi ya aina mbalimbali, hivyo serikali itaendelea kuisimamia sekta hiyo kwa faida ya taifa. Baada ya kukabidhiwa madini na fedha hizo, Naibu Gavana wa BoT, Dk Yamungu Kayandabila alisema kuwa mali waliyokabidhiwa wataihifadhi vizuri na hawataingusha serikali kwa kushindwa kufanya hivyo
kitaifa
SAKATA la malumbano makali yaliyodumu kwa zaidi ya wiki mbili baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kudai Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amelidhalilisha Bunge kwa kuliita dhaifu, limechukua sura mpya baada ya CAG kukubali kuitikia mwito huo wa Spika.Katika hatua nyingine, Spika Ndugai amepuuza madai kuwa amevunja Kamati mbili za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zinazofanya kazi kwa ushirikiano na CAG.Amefafanua kuwa kilichotokea ni wajumbe wa kamati hizo, kutawanywa kwenye kamati zingine wakati huu ambao hawana kazi ya kufanya. Januari 7 mwaka huu, Spika Ndugai alivieleza vyombo vya habari jijini Dodoma kuwa CAG na Mbunge wa Kawe jijini Dar e s Salaam, Halima Mdee ambaye aliunga mkono kauli ya CAG kuwa Bunge ni dhaifu, wanapaswa kufika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21 na 22 ili wahojiwe.Kauli hiyo ya Spika ilizua mjadala mkali katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwa madai kuwa Spika hana mamlaka kisheria, kumwita na kumhoji CAG kwa kuwa CAG analindwa kikatiba kutoitwa na kutohojiwa na mamlaka au mtu yeyote.Baada ya sakata hilo kudumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa, hatimaye CAG Prof Assad alijitokeza jijiini Dar es Salaam jana mbele ya vyombo vya habari na kusema kuwa amepokea mwito huo wa Spika Jumanne ya Januari 15, na kuthibitisha kuwa atakwenda mbele ya Kamati hiyo ya Bunge Januari 21 ili kuhojiwa.CAG alisema kuwa majibu yake aliyoyatoa kwenye mahojiano nje ya nchi kuwa Bunge ni dhaifu, hayakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge. Alisema maneno “udhaifu” na “mapungufu” ni lugha ya kawaida kwa wakaguzi, katika kutoa maoni ya utendaji wa mifumo ya taasisi mbalimbali, japo yanaweza kuchukua tafsiri tofauti kwa watu wengine.“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni chombo ambacho hakiwezi kufikia ufanisi unaohitajika katika utendaji wake, kama ripoti zake hazitafanyiwa kazi ya kuridhisha na kwa wakati na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Bunge ni taasisi ambazo lazima zielewane na kufanya kazi kwa karibu sana; ninaamini kuwa mpaka sasa nina mahusiano mazuri na yenye tija, si tu kati yangu na Spika, bali na Bunge zima,”alieleza CAG CAG Assad.Alisema uhusiano huo ni muhimu kati ya pande hizo mbili katika kutekeleza majukumu yao ya kikatiba, hivyo hauna budi kuenziwa na kudumishwa. Profesa Assad alisema kuwa ofisi yake, haina namna ya kuathiri tafsiri ya viongozi, wanasiasa na wachangiaji wa kawaida, bali kitu cha muhimu ni uungwana kutawala katika mawasiliano yao.Spika Ndugai akanusha kuvunja kamati Mapema jana asubuhi, Spika Ndugai akiwa na Kamati ya uongozi ya Chama cha Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, alivieleza vyombo vya habari kuwa katika mfumo wa Jumuiya ya Madola, CAG ni ofisa wa Bunge. Ndugai alisema kwa mantiki hiyo, CAG ambaye ni Ofisa wa Bunge hawezi kumgomea Spika.Alisema CAG anatoka katika Mhimili (Bunge) ambao kazi yake kikatiba ni kuisimamia Serikali, hivyo badala ya wabunge kufanya kazi ya kufuatilia hesabu za Serikali, wanamwajiri CAG kufanya kazi hiyo na baadaye kuwapelekea majibu aliyoyapata.Alisema kwa kuwa Bunge lina wajibu wa kuisimamia serikali, ripoti ya CAG inalisadia Bunge kuishauri na kuielekeza serikali, hivyo sakata hilo kati yake na CAG litakwisha kwa kuwa si jambo kubwa.Kutokana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) kulivalia njuga sakata hilo la Spika na CAG, Spika Ndugai alisema kuwa anapata taabu sana na Zitto kwa kuwa chama chake, kina mbunge mmoja tu, ambaye ni Zitto mwenyewe, hivyo akimfukuza atasababisha chama hicho kukosa uwakilishi bungeni.Spika alisema kuwa Zitto anahangaika na jambo hilo, kwa lengo tu la kupotosha na kujipatia umaarufu. Lakini, alisema uvumilivu utakapomwishia, atachukua hatua dhidi yake.Madai kuwa Spika amezifanyia mabadiliko Kamati za LAAC na PAC, Ndugai alipuuza vikali madai hayo. Alisema baada ya Kamati za Bunge kumaliza shughuli zake ndani ya wiki mbili, wajumbe hao wa LAAC na PAC wataendelea na majukumu yao kama kawaida Bunge litakapoanza.Aidha, Kamati ya Uongozi ya Chama cha Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, ilikutana jana kwa siku moja jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Spika wa Kenya, Justin Muturi, kupitisha bajeti ya jumuiya ya hiyo ya mwaka 2020 Kanda ya Afrika.
kitaifa
MCHEZO wa fainali Kombe la Shirikisho la Azam (FA) ulizozikutanisha timu ya Mtibwa Sugar na Singida United, uliingiza mapato ya uwanjani ya Sh milioni 20 mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa.Mashabiki wa soka walifurika kushuhudia mtanange huo kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa Arusha, ambao Mtibwa Sugar waliibuka na ushindi dhidi ya Singida United ya Singida. Taarifa iliyotolewa na Chama cha Soka mkoa Arusha (ARFA), kupitia kwa mwenyekiti wake Peter Temu ilieleza kuwa mchezo huo uliwakutanisha jumla ya watazamaji 11,400 waliokata tiketi na kuingia uwanjani wakati uwanja huo unabeba watazamaji 12,000.Kutokana na mapato hayo, serikali ilifaidika kupitia kodi ya VAT kwa mgao wa Sh 3,050,847.46, wakati gharama ya tiketi ilikuwa Sh 2,622,000.00, huku wamiliki wa uwanja, ambao ni Chama cha Mapinduzi (CCM, waliondoka na Sh 2,149,072.88, Timu ya Mtibwa Sugar FC ilipata 3,581,788.14 sawa na wenzao wa Singida United. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lenyewe liliondoka na Sh 2,865,430,Baraza la Michezo Tanzania (BMT) 143,271.53, wakati gharama za mchezo ilikuwa sh 1,289,443.73 na Chama cha Soka mkoa wa Arusha (ARFA) kilipata 716,357.63 kufanya jumla ya jumla ya Sh 20,000,000 kwa idadi ya watazamaji 11,400. Ikumbukwe kuwa viingilio katika mchezo huo vilikuwa bwerere, ambapo jukwaa kuuu (VIP A) ilikuwa ni Sh 10,000, jukwaa B1 na B2 Sh 2,000 na jukwaa C, ambalo ni mzunguko, watazamaji walilipa Sh 1,000 kwa kichwa.Mchezo huo wa fainali ulimalizika kwa timu ya Mtibwa kuibuka mabingwa baada ya kuichakaza Singida United kwa mabao 3-2 na kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.
michezo
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata ole Sanare, amewaonya wafanyabiashara wasio waaminifu katika mkoa huo kuacha kuingiza bidhaa kwa njia ya magendo ikiwamo vipodozi vilivyozuiwa kwa matumizi ya binadamu na kuonya watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo hilo wakati wa utoaji vyeti na zawadi kwa askari waliofanya kazi vizuri zaidi kwa mwaka 2018/2019 mkoani Morogoro. Alitoa onyo hilo baada ya Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Willbord Mutafungwa, kumueleza askari wake hawatumiki katika operesheni zinazoendeshwa na mamlaka zinazosimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali wanapokwenda kudai kodi kwa wafanyabiashara.“Wafanyabiashara msijifiche kwa kusingizia mnadaiwa kodi kwa njia ya mtutu kwani baadhi yenu mnajihusisha na biashara za magendo ya kuficha sukari,” alisema ole Sanare. Alisema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya wafanyabiashara katika mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wafanyabiashara na wawekezaji mbele ya mawaziri hazikuwa za kweli walipodai kuwa wanadaiwa kodi kwa njia ya mtutu wa bunduki.“Nimefuatilia jambo hili kwa kina, nimepata taarifa kuwa wafanyabiashara wanaolalamika ni wale waliokuwa wameficha sukari ya magendo iliyokamatwa na polisi,” alisema.Katika hafla hiyo iliyoambatana na maonesho ya namna ya kukabiliana na uhalifu yaliyooneshwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mkuu huyo wa mkoa pia alioneshwa sehemu ya sukari ya magendo iliyokamatwa.Alitua halfa hiyo kumtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro asisite kuchukua hatua kwa askari ambaye atabainika kuvujisha siri za watoa taarifa za wahalifu kwani vitendo hivyo vinahatarisha amani na usalama wao.Naye Kamanda Mutafungwa alisema katika kipindi cha mwaka 2018/2019, jumla ya askari 37 wametambuliwa na kustahili kupata pongezi maalumu kwa kazi nzuri waliyofanya mkoani humo.
michezo
Mahadhi aliyesajiliwa Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga ameandika ujumbe mrefu kwenye mtandao wake wa Instagram. “Assalam alykum ndugu zangu katika imani haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapenzi wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba sana radhi.“Haja ya moyo wangu ni kutaka kufikia malengo yangu niliyojiweka lakini kwa mwaka 2017 ilikuwa ngumu sana kutokana na changamoto nilizokutana nao,” aliandika Mahadhi. Pia Mahadhi alisema ombi lake mashabiki, viongozi na benchi la ufundi anawaomba radhi kama aliwakosea, kwani bado anahitaji nafasi anaamini hawezi kurudia kosa.Aidha, alisema anaamini kilio chake kimewafikia anahitaji kuanza mwaka mpya akiwa kijana mwema na mpya na anawapenda wote. Mahadhi amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga na Mei 2017 zilisambaa tetesi kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Union huenda angetolewa kwa mkopo kwenda Singida United lakini yeye alisema ni bora aondoke jumla kuliko kutolewa kwa mkopo.
michezo
Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Marekani, Dave Sarachan alitangaza orodha ya wachezaji kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki Machi 27 itakayofanyika Cary, kaskazini mwa Carolina, ambayo itashirikisha wachezaji 17 kati ya 22 wenye umri wa miaka 24 au chini ya hapo.Weah, 18, anajiunga kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo ya timu ya taifa ya Marekani baada ya kukichezea mara mbili kikosi cha kwanza cha PSG wakati ikishinda 2-0 huko Troyes na ule wa 5-0 dhidi ya Metz.Wamarekani wameamua kumuinua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na siku 84 kwa ajili ya kukutana na nchi hizo, ambazo zimeshindwa kufuzu kwa Kombela Dunia Juni nchini Urusi."Mchezo huu kwa mara nyingine tena unawakilishwa na baadhi ya sura mpya,” alisema Sarachan. "Sehemu kubwa ya kundi hili ni wachezaji vijana ambao tunafikiri watakuwa na muda mrefu na timu hiyo ya taifa pamoja na wachezaji wengine wazoefu.”Weah ni mmoja kati ya wachezaji watano walioitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Marekani, pia kinamjumuisha mabeki Antonee Robinson wa Bolton Wanderers, Erik Palmer-Brown wa Ubelgiji. Wengine ni Bortrijk wa Ubelgiji na Shaq Moore anayeichezea klabu ya Hispania ya Levante pamoja na mshambuliaji Andrija Novakovich wa timu ya Uholanzi ya Telstar."Huu ndio muda sasa kuwapatia hawa vijana uzoefu wa mechi za kimataifa,”alisema Sarachan.“Watapimwa dhidi ya timu yenye uzoefu ya Paraguay." Palmer-Brown hivi karibuni lisajiliwa na vinara wa Ligi Kuu ya England ya Manchester City na yuko kwa mkopo katika klabu ya Ubelgiji, ambako alianza kuichezea wiki mbili zilizopita.Mzaliwa wa Uingereza Robinson ameichezea mara 29 timu ya Daraja la Kwanza ya Bolton.
michezo
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro De Oliveira na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika utafi ti wa mafuta na gesi na ununuzi wa mafuta.Mazungumzo kuhusu ushirikiano huo, yalifanyika juzi mjini hapa na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa petroli na gesi, Marwa Petro, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Mataragio na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Angola nchini.Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Angola, kwa kuwa tayari ina uzoefu kwenye masuala ya utafiti wa mafuta na gesi na tayari imeshagundua mafuta.Aliongeza kuwa Tanzania ina maeneo kadhaa yenye viashiria vya mafuta, mfano Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika, hivyo serikali inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa nchi inapata mafuta kama ilivyo kwa Angola, ambayo ipo pia katika Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta Duniani (OPEC).Alitoa muongozo wa nini kinachotakiwa kufanywa, baada ya mazungumzo ya viongozi hao wawili ili lengo hilo la ushirikiano liweze kufanyiwa kazi na wataalamu wa nchi hizo mbili, likiwemo suala la Angola kuiuzia mafuta Tanzania.Balozi Oliveira alisema wakuu wa nchi za Angola na Tanzania, wanafahamu kuhusu suala hilo, hivyo ni muhimu kwa watendaji wa pande zote mbili kulifanyia kazi suala hilo na kutoa taarifa kwa viongozi hao wakuu, badala ya kusubiri viongozi hao kuulizia utekelezaji wa suala hilo.Wakati huohuo, Waziri wa Nishati, Dk Kalemani alikutana na watendaji wa kampuni ya ORMAT ya Marekani ambao wameeleza nia ya kampuni hiyo kushirikiana na Taasisi ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika masuala ya utafiti na uzalishaji umeme kwa kutumia jotoardhi.Meneja Mwandamizi wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Raphael Swerdlow alimueleza Kalemani kuwa kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1965, inazalisha umeme kutokana na jotoardhi kwenye maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Kenya, ambapo wanazalisha megawati 139.Waziri Kalemani aliwaeleza watendaji wa kampuni hiyo kuwa serikali inahitaji kampuni makini na yenye nia ya dhati ya kushirikiana na TGDC, kuweza kuzalisha umeme kutokana na chanzo hicho, ambacho hakijaanza kuzalisha umeme nchini, licha ya kuwa na maeneo mengi nchini yenye viashiria vya jotoardhi.
uchumi
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amewataka Watanzania kuwekeza kwenye lishe kwani kuna uzalishaji mkubwa wa chakula na hakuna sababu za kuwepo kwa udumavu na hata utapiamlo.Hasunga alisema hayo mjini hapa jana wakati akifungua warsha ya wadau wa kilimo hifadhi.Alisema Tanzania ni wazalishaji wa mazao ambayo yamekuwa yakiuzwa ndani na nje na kwamba nchi haitakiwi kuwa na wananchi wenye udumavu wa mwili au akili.“Hatutakiwi kuwa na udumavu wa mwili, akili na utapiamlo. Kuna magonjwa mengi kwa sababu watu hawali vizuri. Ni lazima kuwekeza kwenye lishe badala ya kusubiri ugonjwa ili utibiwe kwa kuwa magonjwa mengi yanatokana na dawa tunazotumia,” alisema.Alisema jitihada kubwa zimefanyika katika kuongeza uzalishaji kwenye kilimo.“Lazima tuunganishe mnyororo wa kuongeza thamani ya mazao tunayozalisha, ifike mahali udongo wetu tuupime. Tunataka kujua kila mkoa ardhi yake ikoje na virutubisho vipi vinakosekana hata kama ni mbolea iendane na udongo wa aina fulani,” alisema.Pia alisema juhudi zimefanyika za kuendeleza kilimo kwa kushirikiana na serikali kwa maendeleo ya wakulima na taifa kwa ujumla.Alisema katika mwelekeo wa kufikia uchumi wa viwanda kwa kukuza uzalishaji wenye tija, jitihada hizo zinaendana na Sera ya Kilimo ya Mwaka 2013 na programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili.Sera na programu hizo zinahimiza usimamizi endelevu wa matumizi bora ya maji na ardhi, kuongeza tija na faida katika uzalishaji, biashara na kuongeza thamani ya mazao na kuiwezesha sekta katika uratibu, ufuatiliaji na tathimini.Aidha, alisema wakati mwingine jitihada za kuongeza uzalishaji zinakuwa na mafanikio madogo kutokana na kutotumia teknolojia sahihi zinazoendana na mahitaji ya wakati.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mahamoud Mgimwa amesema asilimia 65 ya Watanzania wameajiriwa katika kilimo na mchango wa sekta hiyo, ni mkubwa hivyo, ni vyema wakulima wabadilike na kuingia kwenye kilimo hifadhi.“Ili nchi iweze kuendelea lazima kuwekeza kwenye eneo hilo miaka ya nyuma serikali ilitenga asilimia moja ya bajeti yake kwenye eneo la utafiti lakini fedha nyingi zaidi zinatakiwa kuwekeza kwenye utafiti ili kilimo kiwe na tija, asilimia 75 ya mbegu hazitokani na utafiti. Pamoja na dhana ya kwenda kilimo hifadhi lazima serikali iongeze fedha kwenye utafiti,” alisema.Meneja wa Kilimo Hifadhi Tanzania, Hamis Dulla alisema wamekuwa wakihamasisha kilimo hifadhi ili kuwa na kilimo chenye tija.
kitaifa
KOCHA wa Simba, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amelalamikia bao la Yanga akidai kuwa lilifungwa wakati mchezaji wake akipatiwa matibabu nje ya uwanja.Alisema kuwa wakati mchezaji huyo akiomba kuingia uwanjani, mwamuzi hakumuona na goli likafungwa. Hatahivyo hakutoa lawama kwa mwamuzi Jonesia kwani alisema dakika zote alikuwa sahihi.“Siwezi kumlaumu mwamuzi lakini tulifungwa bao wakati mchezaji wetu akiwa nje ya uwanja bila mwamuzi kufanya uamuzi wowote, “alisema Vandenbroeck. Naye kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema mchezo huo ulikuwa mgumu, hasa pale walipokuwa nyuma kwa mabao mawili, “lakini mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani wa hali ya juu. Alisema kuwa walipania kushinda mchezo huo, lakini walitarajia matokeo hayo.“Mtokeo tuliyatarajia wachezaji walikuwa vizuri, licha ya kwamba tulitaka matokeo yaushindi katika mchezo huo, “alisema Mkwasa.Alisema baadhi ya wachezaji ambao hawakupewa nafasi katika mchezo huo atawatumia katika mechi zijazo ili kuhakikisha anatengeneza timu bora zaidi na yenye ushindani katika mbio za kuwania ubingwa.
michezo
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema ujenzi wa viwanda umewezesha uchumi wa wilaya hiyo kukua kwa kasi kubwa na kukuza mapato ya halmashauri maradufu.Amesema ofisini kwake mjini Mkuranga kuwa, kwa kuzingatia hali ilivyokuwa kabla ya kuingia Serikali ya Awamu ya Tano na sasa, kuna mabadiliko makubwa, na kwamba, viwanda vimekuwa neema kwao.Amewaeleza wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano mapato ya halmashauri yalikuwa chini sana lakini sasa yameongezeka kwa kiasi kikubwa.“Pia mapato ya Serikali kuu naongelea hapo TRA yameongezeka. Kwa mfano kule nyuma lengo la wilaya lilikuwa chini ya bilioni mbili sasa hivi tunacheza kwenye bilioni sita makusanyo hayo kwa mwaka” amesema.Sanga amesema kuna viwanda zaidi ya 71 Mkuranga na vingine sita vipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi.Amesema kiwanda cha aina yoyote kinaweza kujengwa wilayani humo kwa kuwa mahitaji ya msingi yapo na wametenga zaidi ya ekari 10,000 kwenye Kijiji Cha Msufini kata ya Mbezi kwa ajili ya uwekezaji.
uchumi
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar as Salaam, Daniel Chongolo amezindua kampeni kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulipa kodi ya majengo na kodi ya mabango.Chongolo amesema kampeni hiyo itaenda sambamba na kampeni ya nyumba kwa nyumba ikilenga kuhakikisha wamiliki wote wanalipa kodi kwa wakati kukusanya Sh bilioni saba.Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Chongolo amesema lengo ni kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ya majengo na mabango.Amesema hatua hiyo inatokana na wananchi wengi kujitokeza siku ya mwisho kulipia kodi hizo na kusababisha msongamano, jambo ambalo halipendezi kwani linaua ufanisi wake.Chongolo amesema kufanikisha kampeni hiyo viongozi wa wilaya, wakiwamo watendaji mitaa na kata watashirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuhamasisha wananchi wajue umuhimu kulipa kodi ya majengo na mabango.“Kutakuwa na utaratibu maalumu wa kila mwenye jengo kupewa stakabadhi yake na kisha atakwenda kulipa na watendaji watakuwa wakiwaelekeza wananchi kulipa kodi yao.“Serikali kwa kuwajali wananchi wake imeamua kodi ya jengo kuwa moja ambayo ni Sh10,000 tu. Mwenye nyumba moja atalipa kiasi hicho na mbili atalipia kila moja Sh 10,000,” amesema,Amesema baada ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya majengo, yeye akishirikiana na viongozi wa kata, mitaa na maofisa wa TRA watapita nyumba hadi nyumba kukagua wasiolipa.Meneja wa TRA wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, Masota Masatu alisema wamejipanga kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na watafanya hamasa maeneo yote.
uchumi
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema, baada ya Jukwaa la Fursa za Biashara Novemba 21 hadi 23 Tabora haitakuwa kama ilivyo sasa na ameziagiza halmashauri zote ziwe na miradi miwili mikubwa ya viwanda na kilimo.Mwanri amesema, mkoa umeziagiza halmashauri nane za mkoa huo ziwasilishe mipango yao na kwamba, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri watakaoshindwa kutekeleza maagizo hayo wataondolewa katika nafasi zao.Ameyasema hayo mjini Tabora katika ukumbi wa Chuo Cha Chuo Kikuu Cha Askofu Mkuu Mihayo (AMUCTA) wakati wa mkutano wa wadau wa Jukwaa la Fursa za Biashara Tabora.Watu kadhaa wamehudhuria mkutano huo wakiwemo viongozi wa dini, wajasiriamali, viongozi na wanafunzi katika chuo hicho na waandishi wa habari.“Kwa kifupi hakuna halmashauri ambayo haitakuwa na jambo la kufanya, zote nimezitaja, na zote nimezielekeza na hivi ninavyozungumza wanaandaa maandiko...“Tumezungumza na Benki ya Kilimo Tanzania. Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kupitia miradi niliyoisema zitatakiwa zikusanye kiasi kipatacho asilimia thelathini za mradi unaouzika. Na asilimia sabini itatolewa na benki hii ya kilimo ambayo Mheshimiwa Rais wetu ametuanzishia” amesema Mwanri.Amesema kila halmashauri inapaswa kuonesha kitu watakachobaki nacho baada ya jukwaa na viongozi katika halmashauri wasidhani jambo hilo la kama mdundiko kwamba litapita tu.“Hatukakubali, hatutakubali, hatutakubali ngonjera, hatutakubali. Wenzetu waliopo katika Serikali kwa maana ya Halmashauri wasipotuonesha kitu ambacho wataondoka nacho baada ya jukwaa linalokuja tutawaambia hawatoshi na tutawaondoa katika nafasi zao. Tutawaambia hawatoshi tutawaondoa katika nafasi zao…“Kwa hiyo kama kuna kiongozi yoyote katika halmashauri anayefikiri jambo hili ni kama mdundiko na kwamba litapita tu halitapita na jambo hili lazima liweke alama”amesema Mwanri.
uchumi
WANANCHI katika vijiji vya Kitongosima na Shinembo katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, wamepongeza na kushukuru Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) kwa kuwapa mafunzo wanayosema yamewazindua kimaisha.Walitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti katika vijiji vyao, ambavyo ni vya mfano wa urasimishaji ardhi na mashamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu, walipozungumza na gazeti hili mintarafu manufaa wanayoyaona katika mafunzo ya urasimishaji ardhi na biashara yanayoratibiwa na kuendeshwa na Mkurabita wilayani Magu.Baadhi ya wanavijiji hao waliopimiwa mashamba na kupewa hati za hatimiliki za kimila, walisema mafunzo kuhusu namna ya kutumia hati hizo, yamewapa mwanga wa namna ya kuanzisha na kuendesha kilimo biashara kitakachowapa tija na kuondokana na kilimo cha mazoea cha kujikimu.Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitongosima, Nzunda Francis alisema baada ya mafunzo hayo kijijini kwao sasa wananchi wengi waliokuwa wanasita kuchukua hati zao, wanamimika kukamilisha mchakato wa kuzichukua. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Victoria Saccos cha kijijini Kitongosima, Nyangeta Liso alisema: “Mafunzo haya ya Mkurabita yametusaidia sana maana tangu tuanzishe Saccos yetu tulikuwa tunakopeshana tu, lakini sasa tumeanza kufikiria kufanya biashara nyingine hasa kujenga ukumbi wa kukodisha ili ukuze mapato yetu.”Wanakijiji Beatus Masalu (78) na Beatus Nzunda (60) walisema tangu wapimiwe mashamba yao na kupata hati, hawajatumia hati zoe kwa namna yoyote mbali na kuzitunza nyumbani kwa kuwa hawakuwa na mafunzo yoyote. “Sasa nimefumbuka macho nimeanza kushughulika ili nizitumie kutafutia mkopo benki ili nifanye kilimo cha kisasa kwa ajili ya biashara.Nataka kulima dengu na mahindi kitaalamu na kwa wingi,” alisema Nzunda. Mjumbe na Mwakilishi wa Kikundi cha TASAF Dindiliani B cha kijijini Shinembo, George Alex alisema: “Mafunzo yametusaidia maana tumegundua asilimia 90 ya vikundi vyetu, vinafanya kazi kwa mfumo wa aina moja usio endelevu maana kila mwisho wa mwaka tunagawana pesa na kuvunja vikundi kisha tunaanza upya.Kumbe kweli ndiyo maana hatuendelei.” Katibu wa Kikundi cha Masaugula Ikulicha Shinembo, Daud Paul alisema mafunzo yamewaongeza mbinu za kupanua fursa za soko na kutafuta mtaji. Kijijini Kitongosima, Petro Nyama (35) alisema alikuwa miongoni mwa waliosita kupimiwa na kurasimisha mashamba yao wakidhani yatataifishwa, lakini baada ya kuelimishwa wametambua urasimishaji ni tija kwao na kwa umma mzima. “Tumefumbuliwa macho kwamba hizi hati ni mtaji mkubwa na kila mtu sasa anaona Mkurabita ni kitu cha faida; ni kitu kizuri; ni mkombozi wa sisi wanyonge vijijini,” alisema Nyama.
kitaifa
WATU wanne wamefariki na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya basi la abiria la Kampuni ya Fikosh, walilokuwa wakisafiria, kupata ajali baada ya kuacha njia na kupinduka.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alisema ajali hiyo ni ya juzi katika eneo la Mnarani wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, uliosababisha dereva wa gari hilo, Abdallah Ramadhani kushindwa kumudu gari katika mteremko wa eneo gari hilo lilipopindukia. Aliitaja gari hiyo ni aina ya scania lenye namba za usajili T AUV 400, iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Kigoma. Kwamba wakati ajali hiyo inatokea gari hiyo ilikuwa ikitokea Mwanza kupitia mkoa Tabora.Kamanda Otieno alisema baada ya ajali hiyo, majeruhi walichukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa Kigoma ya Maweni akiwemo dereva wa gari hilo, Abdallah Ramadhani. Walifikishwa Maweni baada ya kupatiwa huduma ya kwanza kwenye Kituo cha Afya Uvinza. Akizungumza kuhusu ajali hiyo jana mchana, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Kigoma ya Maweni, Dk Osmund Dyegula alisema wagonjwa 22 ndiyo walikuwa wamebaki hospitalini, akiwemo mmoja ambaye hali yake ni mbaya. Mganga huyo alisema majina ya abiria waliofariki kwenye ajali hiyo, bado hawajatambua na kwamba maiti za abiria hao zimehifadhiwa chumba cha maiti cha hospitali hiyio ya mkoa.
kitaifa
RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka ameahidi kutoa Sh 500,000/- kwa kila mwanariadha atakayefikia viwango vya kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020.Mtaka aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akiwaaga wanariadha wanane wa Tanzania watakaoshiriki mbio za kimataifa za Nagai Marathon zitakazofanyika Oktoba 21, ambazo zinatambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF).Amesema, yuko tayari kutoa kiasi cha Sh milioni 4 endapo wanariadha hao wote wanane watafuzu kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki 2020, ambapo viwango hivyo pia vitawawezesha kushiriki mashindano mbalimbali kuanzia mwakani.Amesema ni vizuri endapo wanariadha hao watafuzu mapema kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki kwani watakuwa na muda mwingi wa kufanya maandalizi ya kushiriki michezo hiyo.Pia alisema watakuwa pia wamefuzu kwa mashindano yote makubwa ya mwakani, hivyo aliwataka kwenda Nagai kupambana iwezekanavyo ili kufuzu kwa michezo hiyo mikubwa na kupata fedha hizi.Alisema moja ya jukumu la RT mwakani kuwa na idadi kubwa ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na imeahidi kuandaa wanariadha wazuri , walioandaliwa vizuri, ambao pia watafanya vizuri kwa ajili ya mashindano.Aliwaambia kuwa watumie vizuri mchezo huo kwani utawawezesha kupata fedha nyingi, ajira na hata vyeo kwa wale walioajiriwa tayari.Alisema kwa wale walio majeshini endapo watakuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali, watapanda vyeo haraka na kuwapita hata wale walioingia jeshini kwa ajili ya visomo vyao.Alisema matarajio ya RT ni kuona vijana hao nane wanaokwenda Nagai, wanafuzu kwa ajili ya michezo hiyo ya Olimpiki na kuahidi kuwaweka kambini mapema kwa ajili ya maandalizi ya mashindano mbalimbali.Balozi wa Hiyari wa Shirika la Misaada ya Kimaendeleo la Japan (Jica), Juma Ikangaa aliwataka wanariadha hao kutotoa visingizio endapo watafanya vibaya katika mbio hizo na zingine.Mkuu wa msafara wa timu hiyo iliyoondoka nchini jana kwenda Nagai, Mohamed Kiganja alisema kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika mbio hizo na kuwataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi wowote.Wanariadha hao wakiwa Nagai, Japan watashiriki katika mbio za kilometa 21 na 42, yaani nusu marathon pamoja na zile za full marathon.Wanariadha waliomo katika timu hiyo ni pamoja na Sylivia Masatu, Amina Mohamed, Marco Joseph, Fabian Sulle, Angelina John, Rozalia Fabian, Nilbaldo Peter na Neema Gadiye.Mbali na Kiganja, viongozi wengine katika msafara huo ni pamoja na katibu msaidizi wa RT, Ombeni Zavalla, Lucy Henry wa Jica, Kassim Saleh, Benson Chacha wa BMT na Ikangaa.
michezo
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake watano, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka 100, ikiwemo ya utakatishaji fedha.Mbali na Maimu, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7/2019 ni Meneja Biashara wa NIDA, Aveln Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.Washitakiwa hao walifutiwa mashitaka 27 juzi katika mahakama hiyo, baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kutoa kibali cha kufutwa kwa mashitaka hayo na baadaye washitakiwa hao walikamatwa tena na jana walipandishwa kizimbani kusomewa mashitaka hayo 100.Wakili wa Serikali Wankyo Saimon akisaidiana na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 24 ya utakatishaji fedha, mashitaka 23 ya kughushi, mashitaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, kula njama kwa nia ya kulaghai mawili kujipatia fedha njia ya udanganyifu mawili.Pia, wanadaiwa kuwa na mashitaka matano ya kuisababishia hasara NIDA, mashitaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka, ambalo linamkabili Maimu na Sabina.
kitaifa
MFUKO wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umetenga Sh bilioni 127.3 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kilimo nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwakani. Rais wa IFAD, Gilbert Fossoun Houngbo aliyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam jana alipofanya mazungumzo na Rais John Magufuli.Pamoja na kutenga fedha hizo, Houngbo ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Togo alimpongeza Rais Magufuli na serikali anayoiongoza kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kukuza uchumi, ikiwemo utekelezaji mzuri wa miradi inayofadhiliwa na IFAD, kutilia mkazo umuhimu wa uwekezaji usiokuwa tegemezi, unaolinda utu, unaozalisha kipato kwa wananchi na unaojenga misingi endelevu ya kujitegemea.Alibainisha kuwa baada ya kutenga fedha hizo, IFAD inasubiri upande wa Tanzania kuainisha maeneo mahususi ya miradi ya kilimo ambako fedha zitaelekezwa. Aidha, alieleza kuwa ana matumaini miradi hiyo itafanikiwa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na namna serikali ilivyo na dhamira ya maendeleo. Kwa upande wake, Dk Magufuli aliishukuru IFAD kwa ushirikiano wake mzuri na Tanzania na kumhakikishia Houngbo kuwa ushirikiano na uhusiano huo ulioanza mwaka 1978 utadumishwa kwa maslahi ya Watanzania.Alisema fedha zilizotengwa katika mpango huo wa miaka mitatu zitaelekezwa katika maeneo yenye maslahi mapana ya sekta ya kilimo, ikiwemo kuwezesha matumizi ya zana bora za kilimo katika uzalishaji, kuzalisha mbegu bora za mazao, kutatua changamoto ya masoko ya mazao na kuboresha ufugaji. Pia aliipongeza IFAD kwa kutoa fedha pasipo kuweka masharti ya maeneo zinakopaswa kuelekezwa.Rais Magufuli aliagiza Wizara ya Kilimo kuharakisha mchakato wa kuainisha maeneo yatakayopokea fedha hizo ili utekelezaji wa mpango huo uanze. Wakati huo huo, Rais Magufuli alifanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden, Peter Eriksson.Baada ya mazungumzo hayo, Waziri Eriksson alimpongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya rushwa na ameeleza dhamira ya Sweden kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania.
kitaifa
TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), imepangwa Kundi B katika mashindano ya Afrika Mashariki ya Cecafa 2019 yatakayofanyia Uganda, imeelezwa.Ngorongoro Heroes katika Kundi B imepangwa na Kenya na Zanzibar katika mashindano hayo yatakayofanyika Uganda kuanzia Septemba 21.Wakati katika Kundi A kutakuwa na wenyeji Uganda, Sudan, Eritrea na Djibouti huku Kundi C likiwa na timu za mataifa ya Burundi, Sudan Kusini na Somalia.Kwa mujibu wa ratiba hiyo, timu tatu za juu kutoka katika Kundi A na B zitasonga mbele katika robo fainali na kuungana na timu mbili za kwanza kutoka Kundi C.Kikosi cha awali cha Tanzania chini ya Kocha Mkuu, Zuberi Katwila chenye wachezaji 35 kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ya Uganda.Kikosi cha awali cha Ngorongoro Heroes: Ramadhan Kabwili – Yanga, Ally Salim – Simba, Abdul Seleman-U18, Oscar Masai – Azam, Lusajo Mwaikenda – Azam, Dickson Job – Mtibwa, Gustapha Simon – Yanga, Onesmo Mayaya – Mtibwa, Kelvin Kijiri – KMC na James Kahimba – Coastal Union.Wengine ni Ally Msengi – KMC, Ally Ng’anzi – Madison (Marekani), Kelvin Nashon –JKT, Lenny Kissu – Biashara, Yahya Mbegu – Simba, Frank Kahole – Mtibwa, Andrew Simchiba – Coastal, Mohamed Abdllah – Mtibwa, Razack Ramadhan –Mtibwa, Wilbore Maseke – Azam na Gadafi Said – Azam.Wengine ni Novatus Dismas – Biashara, Abubakar Juma – Mtibwa, Israel Mwenda – Alliance, Samwel Jackson – Azam, Omar Banda – Azam, Kassim Shaban – Sahare, Kibwana Shomari – Mtibwa, Tariq Seif – Biashara, Agiri Ngoda – Azam, Tepsi Evance – Azam, Nickson Kibabage – Al Jadida, Morocco Zanda Said – Azam, Kelvin John -U17 na Herbert Lukindo-Mbao.
michezo
SERIKALI ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (JICA) inakusudia kuipatia Tanzania mkopo nafuu na ruzuku wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 345 za Marekani, sawa na takriban Sh bilioni 794, kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya maendeleo.Miradi hiyo ni ukarabati wa barabara ya Arusha hadi Holili, ukarabati wa Bandari ya Kigoma na Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Visiwani Zanzibar. Ahadi hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la JICA anayesimamia Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Hiroshi Kato, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, mjini Washington D.C nchini Marekani. Aliitaja miradi hiyo iliyoko mezani kwao inayosubiri kupatiwa fedha wakati wowote kuanzia sasa kuwa ni pamoja na mradi wa ukarabati wa barabara ya Arusha-Holili utakaopatiwa mkopo wa dola milioni 221.Aliutaja mradi wa pili kuwa ni wa majisafi na usafi wa mazingira Zanzibar utakaopatiwa fedha kupitia mkopo wa dola milioni 99 na mradi wa upanuzi wa Bandari ya Kigoma ambao Japan itatoa ruzuku ya dola za Marekani milioni 25. Kato alisema kuwa Japan inajivunia ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Tanzania na kwamba iko tayari kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuitaka serikali kuwasilisha miradi yake ya kimkakati ambayo Japan itafadhili kupitia mikopo yenye riba nafuu pamoja na ruzuku.
kitaifa
UTAFITI umeonesha kuwa maambukizi mapya ya Ukimwi yameongezeka kwa kiwango kikubwa kwenye kundi la vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 24 ambapo asilimia 40 kati ya asilimia 80 yako kwa wasichana wa umri wa miaka 15 hadi 19.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa alisema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana (AGYW) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Alisema utafiti wa viashiria vya Ukimwi kwa mwaka 2016/17 umeonesha kuwa Tanzania ina jumla ya vijana milioni 12 wa umri wa miaka 10 hadi 19 ikiwa ni asilimia 24 na milioni tano wa umri wa miaka 20 hadi 24 ikiwa ni asilimia 31 ya idadi ya Watanzania wapatao milioni 44.Alisema Ukimwi umeendelea kuwa tishio la uchumi na maendeleo ya nchi na madhara yake yanaendelea kuwa ni changamoto katika kufikia malengo ya Mpango wa Taifa wa Miaka mitano. “Janga hili ni matokeo ya mchanganyiko wa sababu nyingi za kibaolojia, kijamii, kimila na kiuchumi. Madhara ya Ukimwi yameathiri mtu binafsi, familia, jamii na nchi kwa ujumla”.“…Hivyo, udhibiti wake unahitaji nguvu za pamoja. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa mwanzo wa kumalizika kwa ugonjwa wa Ukimwi upo mikononi mwetu sisi sote,” alisema. Aliongeza kuwa miradi hiyo ya majaribio inayowalenga wasichana balehe na wanawake vijana imekuwa ikitekelezwa katika mikoa tisa ya Shinyanga, Dar es Salaam, Kagera, Dodoma, Morogoro, Singida, Mbeya, Iringa na halmashauri 24.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango alisema malengo yao ifikapo mwaka 2020 ni kufikia wananchi wote kwa kujua hali zao ili wale walioathirika wawe kwenye dawa. Alisema kwa kuwa kundi la vijana maambukizi ya Ukimwi ni mabaya wamekuwa wakiwawezesha ili wajitambue kuhusu afya zao na kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha kundi hilo linapata taarifa sahihi na kupata fursa za kiuchumi.
kitaifa
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema madaktari wote waliosoma kwa fedha za serikali watapangiwa vituo vya kazi.Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Nanyamba, Abdalah Chikota (CCM). Katika swali lake lake, Chikota alitaka kujua mpango wa muda mfupi wa serikali wa kupeleka madaktari bingwa katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula (Mtwara).Alisema kwa sasa wapo madaktari ambao wanasoma katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) na kuwa mara watakapomaliza masomo yao watapangwa na serikali kule ambako kuna mahitaji ya madaktari hao.Dk Ndugulile alisema katika wakati huu wa mpito wakiwa wanasubiri kupeleka madaktari hao Serikali pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF wamekuwa wakiweka kambi mabalimbali wakiwa na madaktari bingwa ili kutoa huduma za kibingwa. Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mtwara Mjini, Hawa Ghasia (CCM), Dk Ndugulile alisema wizara imefanya tathimini ya mahitaji ya madaktari bingwa na fani zao katika Hospitali zote za mikoa, Kanda maalumu na Hospitali ya Taifa Muhimbili.Alisema tathmini hiyo itawezesha utekelezaji wa uamuzi wa kuwapanga upya madaktari bingwa kwa uwiano kulingana na mahitaji ya kila hospitali hizo. “Lengo ni kuwa kila hospitali hizi zinakuwa na madaktari bingwa wa fani nane. Fani hizo ni pamoja na daktari bingwa magonjwa ya uzazi na wanawake , watoto, magonjwa ya ndani, upasuaji, upasuaji wa mifupa, daktari wa huduma za dharura na magonjwa ya ajali,” alisema.Alisema pia madaktari wengine bingwa wanaohitajika katika Hospitali hizo ni pamoja na daktari bingwa wa huduma za usingizi na daktari bingwa wa huduma ya Radiolojia. Kwa mujibu wa Ndugulile katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/18 wizara iliwapeleka madaktari bingwa wa fani za upasuaji wa kawaida na upasuaji wa mifupa 125 katika Chuo Kikuu cha MUHAS. Alisema madaktari hao wanatarajia kumaliza masomo yao katika mwaka wa fedha wa 2020/21.
kitaifa
SERIKALI itaibadilisha menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kupata watendaji wanaotekeleza majukumu yake inavyostahili kwa kuwa kwa sasa wanakosa kuwa na mipango thabiti.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Magomeni Kota. Eneo hilo ni lililokuwa na nyumba ndogo ndogo za wananchi zilizobomolewa zijengwe mpya baada ya kuwa katika hali mbaya na kaya zaidi ya 600 zikisubiri kukamilika kwa mradi huo.Hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 40. Nyumba hizo zilibomolewa mwaka 2016 baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara eneo hilo na kuitaka TBA kukamilisha ujenzi huo ndani ya mwaka mmoja kuanzia 2017 ambapo hadi sasa haujakamilika kutokana na changamoto mbali mbali. Kuhusu TBA, Kamwelwe alisema amekagua kwa mara ya kwanza mradi huo kuona unavyoendelea na hajaridhishwa mbali ya hivi karibuni, serikali ilitoa fedha Sh bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi huo.“Maendeleo ya mradi huu, hayajaridhisha nimebaini eneo hili limelala, halionekaniki kama kuna mtu anafanya kazi,” alisema Kamwelwe na kuongeza anashangazwa kuona hali hiyo akielezwa sababu ni ukata Alisema kwa sasa ataitengeneza TBA ili izalishe kwa kiwango kinachotakiwa na kwamba hatawanyang’anya ajira lakini wanachelewa kupanga huku waking’ang’ania vitu ambavyo sio vya kwao.“Nilitamani nikute ujenzi ukiendelea, mnashindwa kuingia mkataba hata wa watu kuleta kokoto kweli, hilo nalo waziri awasaidie, mnakosa plan, miradi isimamiwe na wenye weledi iweze kwenda,” alisema. Alisema kuna watendaji TBA wamevamia fani za watu na waliojivalisha vyeo atavifuta. “Namsubiri tu Katibu Mkuu akija tutabadilisha menejimenti hii ili mambo yaende, watu wanajenga jiko halina hata dirisha, tunalaumiwa mno bungeni wakati mwingine tunashindwa hata kujibu,” alisema Kamwelwe.Aliwaahidi wananchi kuwa na yeye kuanzia sasa atalala hapo ili kusimamia kazi iende kwa kasi zaidi na kuhakikisha mwishoni mwa mwaka huu wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo wanaingia kuishi hapo. Alitoa maagizo kwa Katibu Mkuu (Ujenzi), kubadilisha wafanyakazi wa TBA na kutafuta wasimamizi wakuu wa mradi ambao ni wa ujenzi ili kufanya kazi katika mradi huo.Alimtaka ahakikishe miradi yote nchini ya majengo inayosimamiwa na TBA, majina ya wasimamizi wakuu wa miradi yanapelekwa kwa waziri ili kuona taaluma zao kwa kuwa fedha za serikali sio za kufanyia mafunzo katika ujenzi. Alisema katika mradi huo, msimamizi mkuu sio mwenye taaluma ya ujenzi ndio kazi hiyo haiwezi kufanyika ipasavyo. Alisema kila mradi wa majengo nchini unahitaji kuwa na msimamizi wake wa ujenzi na isiwe kama mkoa wa Songwe ambako mhusika ni mmoja akisimamia miradi kwenye halmashauri zote.“Miradi hii anatakiwa msimamizi wa ujenzi kuwa eneo la kazi muda wote, alale hapo na kuamkia hapo na mapendekezo yangu ni kuweka mwenye taaluma ya ujenzi wa majengo kazi isogee mbele,” alisema. Awali akisoma taarifa ya mradi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushauri TBA, Kileo Yusuf alisema eneo hilo lina kaya 644 na muda wa ujenzi ulikuwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 2017 na mradi ulitakiwa kukamilika mwaka jana, lakini kutokana na changamoto sasa utakamilishwa mwishoni mwa mwaka huu.Alisema awali TBA ilipokea Sh bilioni 20 na majengo yote yamejengwa kwa ghorofa na kutokana na eneo hilo kuwa ni lenye mchanga, imekuwa changamoto kubwa kwa ujenzi huo kuanzia ngazi ya msingi.
kitaifa
SIMBA leo inashuka dimbani kucheza nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi utakaochezwa Uwanja wa Amaan Unguja, Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku.Azam FC ambayo ni bingwa mtetezi inacheza na Simba ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga katika fainali zilizopita kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Gombani Pemba, hivyo mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Akizungumza kocha msaidizi wa Simba, Suleman Matola alisema mfumo wa mtoano umezidi kuifanya mechi kuwa ngumu, lakini wamejipanga kuondoka na ushindi dhidi ya Azam .Nahodha wa Simba, John Bocco alisema mchezo huo utakuwa wa ushindani kwa sababu Azam FC watakuwa wanatafuta ushindi ili wafuzu fainali kutetea Kombe lakini na wao wanahitaji kufuzu fainali na ili warudi na taji hilo Dar es Salaam kuwapa raha mashabiki wao.“Azam FC ina wachezaji wazuri kama ilivyo Simba hivyo mchezo huu tumeuchukulia kwa uzito mkubwa na tutaingia uwanjani kwa lengo la kutafuta ushindi ili tufuzu fainali na kombe lije Dar es Salaam,” alisema Bocco.Naye kocha wa makipa wa Azam FC, Iddi Abubakar alisema wamekuja katika mashindano kushindana sio kushiriki, hivyo wataonesha ushindani kudhihirisha kuwa ndio mabingwa watetezi .Naye nohodha wa Azam FC, Aggrey Morris alisema wamejiandaa kuikabili Simba na wanaamini watashinda mchezo huo na kutinga fainali.“Tunajua tunakwenda kucheza na timu bora ila hata sisi ni bora ndio maana tumefika kwenye hatua hii, hivyo tumejipanga kushinda ili tufuzu fainali,” alisema Moris.Simba iliifunga Zimamoto kwa mabao 3-1 na Azam FC iliifunga Mlandege kwa bao 1-0 hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani ukizingatia kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Simba inaongoza ikiwa na pointi 35 na Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 26.Kwa msimu huu kwenye ligi hiyo, Simba iliifunga Azam FC kwa bao 1-0 na baada ya kipigo hicho ikaamua kuachana na kocha Etienne Ndayiragije na kumchukua Aristica Cioaba ambaye yupo na kikosi hicho hadi sasa.Mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa wa Mapinduzi ni mwaka 2011 baada ya kuifunga Yanga kwa mabao 2-0 na mwaka jana ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa na Azam FC kwa mabao 2-1.Mashindano haya ya 13 yalishirikisha timu nne za Zanzibar ambapo zote zimeaga mashindano na timu nne za Tanzania Bara na yanachezwa kwa mtindo wa mtoano ambapo bingwa anatarajiwa kuondoka Sh Milioni 15 pamoja na Kombe. Timu ambazo zimeaga mashindano kutoka Kundi A ni Mlandege na Jamhuri na Kundi B timu za Zimamoto na Chipukizi.Mashindano hayo maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 56 ya Mapinduzi yalianza mwaka 2007 na hufanyika kila mwaka ambapo Azam ndio bingwa mtetezi, ambapo aliifunga Simba mabao 2-1 mwaka jana katika Uwanja wa Gombani Pemba. Fainali za mashindano hayo zitafanyika Januari 13 katika Uwanja wa Amaan majira ya saa 2:15 usiku.
michezo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela, Novat Kaberwa, baada ya kukiri kumuua bila kukusudia mke wake, Clara Munisi.Katika kesi hiyo, Kaberwa alikuwa akikabiliwa na shtaka la kumpiga mke wake baada ya kurudi nyumbani saa 3:00 usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda na baadaye kurudi akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoacha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo, alitoa hukumu hiyo jana baada ya mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kumuua mke wake bila kukusudia.Mazengo alisema amezingatia hoja zote zilizotolewa na mawakili wa utetezi kuwa mshitakiwa ameipunguzia gharama Mahakama kwa kukiri kosa na pia amezingatia mazingira ya tukio lilivyotokea.Kabla ya adhabu hiyo kutolewa, Wakili wa Utetezi, Venance Victor, akishilikiana na Hashimu Mziray na Neema Kalabuha, aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wao kwa sababu ni kosa lake la kwanza na pia ana watoto wawili ambao hawana mtu wa kuwaangalia.Victor alidai mteja wao alikaa mahabusu tangu Julai 15, 2016 na kipindi hicho cha zaidi ya miaka mitatu amejifunza na amebadilika na hakuna kosa lolote alilolitenda akiwa gerezani na pia anajutia alichokitenda.Pia, wakili huyo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake kutokana na kuwa ni mhandisi ambaye amesomeshwa na serikali mchepuo wa sayansi na serikali ina muhitaji ili aweze kukamilisha miradi ambayo aliyopewa.“Kumbukumbu zinaonesha mshitakiwa pamoja na kampuni yake ya Best World Engineering alikuwa ikimepewa mradi wa kurekebisha barabara ya Mikumi - Kilosa, hadi sasa serikali imeshindwa kutekeleza kwa wakati kwa sababu mshitakiwa yupo ndani,” alisema Victor.Wakili huyo, pia alidai katika tukio hilo hakuna silaha yoyote iliyotumika kuonesha alifanya kitendo hicho kwa kudhamiria na kwamba marehemu hakufia eneo la tukio bali alifia hospitali.
kitaifa
TIMU ya Azam FC imelazimishwa suluhu ya bila kufungana na Mbao FC, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na kuendelea kujiweka katika mazingira magumu kwenye mbio za kuwania ubingwa.Matokeo hayo yamewafanya Azam kufikisha pointi 63 baada ya kucheza michezo 30 katika muendelezo wa ligi hiyo inayoongozwa na Yanga yenye pointi 68 wakicheza michezo.Hiyo ni mechi ya kwanza kwa kocha Abdul Mingange na msaidizi wake, Iddi Cheche kupata pointi moja tangu wakabidhiwe jukumu la kukinoa kikosi hicho baada ya kutimuliwa kwa benchi zima la ufundi la Hans Van Der Pluijm.Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikiwa makini wakihofia kuruhusu bao la mapema, ambapo hali hiyo iliendelea hadi mapumziko na kuzifanya timu hizo kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa suluhu.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mabadiliko ambayo hayakuzaa matunda kwa pande zote.Azam walipata pigo baada ya nahodha wao kupata kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Mbao.Hadi mwisho wa mchezo, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kila mmoja kuondoka na pointi moja.
michezo
Pia alikutana na wawakilishi wa kampuni ya Price Waterhouse Coopers (PwC) wakiongozwa na David Tarimo kutoka Tanzania, John Gibbs (Kanda ya Afrika) na Anne Eriksson (Kanda ya Afrika Mashariki) na kuzungumza nao masuala ya nishati na gesi asilia, miundombinu na upatikanaji wa rasilimali fedha.Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alikutana na mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni ya Invest Africa, Robert Hersov na wenzake wanne na kumweleza Waziri Mkuu nia yao kuwekeza Tanzania kwenye maeneo ya usindikaji mazao, ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao na ufadhili wa miradi inayokubalika kiuchumi na ambayo ni rahisi kupatiwa mikopo.Naye Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Globeleq, Mikael Karlsson ambapo alimweleza Waziri Mkuu haja ya kampuni hiyo kuzalisha umeme wa upepo kama njia mbadala ya kuongeza nishati hiyo badala ya kutegemea gesi.Akijibu hoja zao kwa nyakati tofauti, Waziri Mkuu aliwaeleza wajumbe wa timu hizo kwamba Tanzania ni mahali pazuri kwa uwekezaji lakini pia ni lazima pande zote mbili ziwe makini ili kuhakikisha katika kila mradi inapatikana mizania sawia ya maendeleo.Akizungumza na Karlsson, Waziri Mkuu alisema fursa ya kuzalisha umeme wa upepo iko katika mikoa ya Singida, eneo la Makambako (Njombe), Katavi na Rukwa.“Sasa hivi mbali ya upepo, mnaweza pia kuangalia uzalishaji wa nishati inayotokana na jotoardhi katika eneo lililopo kwenye Bonde la Ufa. Kati ya megawati 40,000 zinazotarajia kuzalishwa ndani ya eneo hili, megawati 5,000 ziko kwenye Bonde la Ufa la Tanzania,” alifafanua.Kampuni ya Globelec pia inamiliki mitambo ya SONGAS ambayo inazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.Waziri Mkuu aliwasili jijini London kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaohusu uwekezaji barani Afrika akimwakisha Rais Jakaya Kikwete na ameshiriki mjadala huo pamoja na Rais John Mahama wa Ghana, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
uchumi
MBUNGE wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kutotumia vyombo vya ulinzi na usalama ‘kumfinyafinya’ sana.Lema alitoa rai hiyo juzi wakati alipopewa nafasi na Gambo kusalimia wananchi wa Jiji la Arusha katika ufunguzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) iliyopo Njiro jijini Arusha.Amesema amejionea serikali ilivyofanya uwekezaji wa kutosha katika maabara hiyo ya kisasa mkoani Arusha na kuishukuru kwa ujenzi wa maabara hiyo ya pekee barani Afrika.“Nashukuru serikali kwa kujenga maabara hii, lakini naviomba vyombo vya ulinzi na usalama visinifinye sana, najua RC Gambo ameshasema mara nyingi mimi ni rafiki yake sikatai, lakini tufanye maendeleo kwa sababu bado nina likizo ndefu ya kutohudhuria bungeni hadi mwakani,”amesema Lema.Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Catherine Magige alimtoa hofu Lema kuwa asiwe na wasiwasi kwani kero za wananchi anaziwasilisha vyema bungeni ingawa yeye hayupo bungeni kwa sasa.Pia aliishukuru serikali kwa kujenga maabara hiyo ya kisasa mkoani Arusha, huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha, Joseph Massawe alisisitiza kuwa serikali itandelea kuboresha mambo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha usalama wa wananchi unaimarishwa na upatikanaji wa maendeleo.Gambo alishukuru kufunguliwa kwa maabara hiyo jijini Arusha na kusema kuwa hivi sasa wapinzani wanajua serikali inataka nini ndio maana wanashiriki katika mambo ya kimaendeleo na kumshukuru Lema kwa kujua umuhimu wa kutunza amani na utulivu mkoani humo.
kitaifa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura na kumtaka kulipa fi dia ya Sh 100,998,121 kwa awamu tano.Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashitaka kumfutia Wambura mashitaka ya uhujumu uchumi na kumsomea mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo alikiri kutenda kosa hilo.Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina alisema mshitakiwa atatakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu tano kuanzia jana ( Sh 20,000,000), Desemba 31, mwaka huu (Sh 20,249,531), Machi 31,2020, Juni 30 na Septemba 30, 2020 ambapo fedha atakazotakiwa kulipa ni Sh 20,249,531 kama ilivyopangwa kwa miezi.Pia alisema mshitakiwa atatakiwa asifanye kosa la jinai kwa miezi 12 na kwamba rufaa ipo wazi kwa asiyeridhika. Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai hawana rekodi ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe fundisho kwake na wengine.Wambura kwa upande wake alidai ni kosa lake la kwanza hivyo mahakama impe adhabu itakayomsaidia kushiriki kufanya shughuli nyingine za kijamii. Awali, akisoma makubaliano hayo, Simon alidai kuwa wameingia makubaliano na mshitakiwa huyo baada ya kukiri kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Alidai wameamua kuondoa mashitaka ya kughushi, kutoa nyaraka za uongo na utakatishaji fedha ambayo ni mashitaka ya uhujumu uchumi.Alidai Wambura na upande wa serikali wamekubaliana kulipa fedha yote kwa awamu tano. Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Mhina alimuapisha mshitakiwa na kumuuliza kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.Akisoma mashitaka mapya, Wakili Simon alidai Julai 6,2004 na Oktoba 30,2015 maeneo ya Ilala kwa udanganyifu Wambura alijipatia Sh 100,998,121 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa lengo la kuonesha malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 kutoka Kampuni ya Jekc System Limited.Katika maelezo ya awali, Simon alidai Wambura kipindi hicho akiwa katibu Mkuu wa TFF, Novemba 28,2002 waliingia makubaliano ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 lengo kufadhili michuano ya Chalenji kipindi hicho mwenyeji alikuwa Tanzania.Alidai Wambura alisaini makubaliano hayo kwa niaba ya TFF na kwamba walitakiwa kurudisha fedha zote pamoja na riba ya asilimia tano baada ya mashindano kukamilika. Alidai Januari 13,2014 Kampuni ya Jekc System Limited iliandika barua kwa mshitakiwa na kwa njia ya udanganyifu Wambura aliilaghai TFF kwa kujaribu kuonesha alichaguliwa na kupewa mamlaka ya kisheria kukusanya fedha hizo kwa niaba ya TFF.Wambura alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akiwa na mashitaka 17 ikiwemo ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutoka nyaraka za uongo na utakatishaji fedha. Katika hatua nyingine, MKAZI wa Buguruni, Thomas Mgoli (37) ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba kukiri mashitaka ya uhujumu uchumi ikiwemo ya kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa anayetaka kumsaidia aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi.Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina alidai kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa. Alidai taratibu za makubaliano kati ya mshitakiwa na upande wa mashitaka bado hazijakamilika na kwamba zitakapokamilika wataomba mahakama iruhusu mshitakiwa kuletwa mahakamani.Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Desemba mosi, 2017 na Agosti mwaka huu katika eneo la Mahabusu ya Keko, huko Temeke, mshitakiwa alijifanya kama mtumishi wa umma aliyeajiriwa kitengo cha Usalama wa Taifa (TISS) Katika mashitaka ya pili imedaiwa kuwa, kati ya Agusti 17 na 29,2019 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dare es Salaam, mshtakiwa kwa kudanganya alijipatia ambapo alijipatia Sh 280,500 kutoka kwa Lucy Ngongoseko kupitia namba mbili za simu tofauti za mtandao wa Airtel akijifanya kuwa yeye ni Ofisa Usalama kutoka TISS anayetaka kusaidia kesi namba 213/2017 ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Jamal Malinzi katika mahakama ya Kisutu.Pia inadaiwa siku na mahali hapo, mshitakiwa alitumia fedha kiasi cha Sh 280,500 wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Wakati huohuo, Hatima ya vigogo sita wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ikiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wake, Dickson Maimu kujulikana leo kama wote watakiri mashitaka ya uhujumu uchumi au la.Mbali na Maimu washitakiwa wengine ni Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, na Xavery Kayombo. Vigogo hao wanakabiliwa na mashitaka 100 kati ya hayo, 24 yakiwa ni ya utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.1, 23 ya kughushi nyaraka; 43 ni kuwasilisha nyaraka za uongo ili kumdanganya mwajiri wao na kuisababishia mamlaka hiyo hasara.Jana, Wakili wa serikali Mwandamizi Ladislous Komany alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally kuwa wanatarajia kubadilisha hati ya mashitaka katika kesi hiyo na kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini ( DPP) ametoa hati ya kuipa ruhusa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo. Alidai kati ya washtakiwa sita ni washitakiwa wawili tu ndio waliofika mahakamani hapo ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Ndege na Kayombo.Alidai kesi hiyo haiwezi kuendelea kwa kuwa kwa sababu hatua zote hizo zinatakiwa kwenda sambasamba na uwepo wa washitakiwa wote mahakamani kwa ajili ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao mapya. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi leo na mahakama ilitoa hati ya kutolewa washitakiwa hao gerezani.Mashitaka mengine yanayowakabili washitakiwa hao ni ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu (mawili), mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na mashitaka mawili ya kula njama. Wanadaiwa kati ya Julai 19, mwaka 2011 na Agosti 31, mwaka 2015, washitakiwa wakiwa maeneo tofauti tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kufanya udanganyifu wa sh. bilioni 1.175 dhidi ya NIDA.Maimu na Raymond wanadaiwa Novembe 7, mwaka 2011 wakiwa Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha Kampuni ya Gotham International Ltd kupata faida ya Sh 899,935,494.
michezo
SEKTA za fedha zikiwamo benki na huduma nyingine za kifedha, wadau wa usafirishaji na wamiliki wa hoteli wametakiwa kuchangamkia fursa zitokanazo na mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Agosti, mwaka huu. Mkutano huo utaanza Agost 5 hadi 18, mwaka huu na utaambatana na matukio mbalimbali kati ya matukio hayo ni ufunguzi wa Jengo la Mwalimu Nyerere huku pia Rais mstaafu, Jakaya Kikwete naye ataongoza mjadala wa uchumi utakaofanyika Chuo Kikuu Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano Afrika Mashariki, Dk Faraj Mnyepe alibainisha kuwa mkutano huo utaleta nchini wageni zaidi ya 1000 ambapo kutakuwa na uhitaji wa huduma ya magari zaidi ya 500 kwa siku, uhitaji wa huduma za kifedha, afya, burudani na huduma nyingine muhimu.Alisema uhitaji huo wote ni fursa kubwa kwa watanzania ambapo aliwataka kuzitumia vema na kwa uadilifu ili kujiongezea kipato na kuliletea sifa taifa. Dk Mnyepe aliongeza kuwa Wizara yake imejipanga kushirikiana na watoa huduma hao kwa kuwapatia nafasi maalum za ushiriki huku akiwataka watanzania wengine kujitokeza kwenye kongamano la uchumi katika wiki ya viwanda itakayoanza Agost 5 hadi 9, mwaka huu. Alisema katika kipindi hicho cha mwezi Agosti kutakuwa na fursa nyingi ambazo watanzania watapaswa kuzitumia huku akitolea mfano wa kongamano hilo la kiuchumi kuwa watanzania wengi wanapaswa kuhudhuria ili kujua fursa za kibiashara na mataifa ya nje. Akizungumzia kuhu- siana na huduma za hoteli alibainisha kuwa kutakuwa na wageni wengine ambao watataka kutumia hoteli zilizopo nje ya kidogo ya jiji na kuwataka wamiliki wa hoteli hizo kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wageni hao. “Wapo wageni ambao moja kwa moja serikali itawahudumia usafiri na huduma za hoteli lakini kama wanakuja na ujumbe ambao ni mkubwa zaidi usioku- wapo kwenye mpango wetu wa kuwahudumia hawa wanaweza kuhitaji kukodi usafiri au hata kwenda kupata huduma za hoteli kwa gharama zao wenyewe... hivyo hapo ndio wadau binafsi wa usafiri wanapoingia na hata wamiliki wa hoteli hata zile za nje kidogo ya jiji, ninawatakia maandalizi mema ya mkutano huu na pia sekta ya habari nina imani imejipanga kusaidiana na serikali katika kuutangaza mkutano huu,” alisema.Alisema kuwa pia SADC itaadhimisha miaka 27 tangu kuanzishwa kwake ambapo jengo la Mwalimu Nyerere lililopo katikati ya jiji litafunguliwa ikiwa ni heshima ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambaye ni kati ya waasisi wa SADC.Kabla ya mkutano huo kutakuwa na mikutano kad- haa ambapo kuanzia Agost 5 hadi 9 kutakuwa na ma- onesho ya wiki ya viwanda ikifuatiwa na mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu utakaoanza Agost 9 hadi 12 na kuanzia Agost 13 hadi 15 kutakuwa na mkutano wa Mawaziri kabla ya kufanyika wa wakuu wa nchi Agost 17 na 18. Utahudhuriwa na wakuu wa nchi 16 na wageni zaidi ya 1,000 ambapo ndani yake wapo watu ambao walishawahi kuishi hapa nchini ambapo kwa mujibu wa Dk Mnyepe wageni hao wame- onesha nia ya kutembelea sehemu mbalimbali za kitalii nchini na maeneo waliyowa- hi kuishi wakati wakiwa hapa nchini.
kitaifa
WAKAZI wa Dar es Salaam wapatao milioni 4.3 wanatarajiwa kumeza kingatiba dhidi ya magonjwa ya matende na mabusha pamoja na minyoo ya tumbo kuanzia Jumamosi ya wiki hii hadi Desemba 20.Aidha, imeelezwa kuwa mbu wa aina zote wakiwemo wale wanaoambukiza ugonjwa wa malaria wana uwezo wa kuambukiza ugonjwa wa matende na mabusha. Kadhalika, alisema jiji hilo lina wanaume 3,000 wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa mabusha, ambapo msisitizo unatolewa kwa wananchi kushiriki katika kumezeshwa dawa za kingatibapango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Upendo Mwingira alisema kampeni hiyo ni kingatiba na sio chanjo kwa kuwa wahusika watameza dawa hizo ambazo zitawasaidia kutatua tatizo hilo.Aliongeza kuwa dawa za minyoo ya tumbo zitaanza kutolewa kuanzia kwa w. Mratibu wa Menye umri wa miaka mitano na kuendelea. Akifafanua zaidi alisema kampeni hiyo hutoa dawa mara moja kwa mwaka huku akiyataja magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele kuwa ni pamoja na usubi, vikope, matende, mabusha na minyoo ya tumbo. Kuhusu mbu kuambukiza matende na mabusha alisema ugonjwa huo husababishwa na minyoo midogo ambayo vimelea vyake huenezwa na mbu wa aina zote, ikiwemo mbu aina ya anopheles anayeambukiza malaria.Kwa upande wake Ofisa Mpango wa Taifa wa magonjwa hayo, kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Oscar Kaitaba alisema waathirika wakuu wa magonjwa hayo ni wananchi wa mazingira duni kutokana na mazingira kutokuwa katika hali safi na salama kwa afya.
kitaifa
['Klabu ya ligi ya Uchina Beijing Guoan wamepania kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale. Klabu hiyo, ina mpango wa kumfanya winga huyo mwenye miaka 30 kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uchina. (telegraph)', 'Manchester United, ambao awali walikuwa wakimnyemelea Bale wamejitoa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo. (Manchester Evening News).', 'Man United hatimaye imekubali masharti ya kumsajili beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atawasili katika uwanja wa Old Trafford kwa dau la £80m . (Bleacher Report)', 'Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Kolscielny amekubali kujiunga na klabu ya Rennes. (RMC Sport).', 'Arsenal inatarajiwa kuishinda Tottenham katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos. Mchezaji huyo wa Uhispania atajiunga kwa mkopo.(Mirror)', 'Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza James Milner ,33, amesema hajui hatma yake katika klabu hiyo licha ya kwamba anataka kusalia. (Liverpool Echo)', 'Bayern Munich wanapigiwa upatu kumsaini winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha ,26, baada ya kushindwa kumsaini Leroy Sane na Gareth Bale. (90min)', 'Ombi la Crystal Palace la £20m kumsaini beki wa Uingereza Reece James limekataliwa na Chelsea. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alihudumu msimu uliopita akiichezea Wigan.(Star)', 'Arsenal, Chelsea, Manchester United na West Ham wote wana hamu ya kumsajili mchezaji wa Dynamo Kiev na Ukraine Mykola Shaparenko. (Caught Offside)', 'Real Madrid wamekataa ofa sita za kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, ambaye anahusishwa na uhamsho wa kuelekea Liverpool. (Cadena SAR)', ' Winga wa Nigeria na Arsenal Alex Iwobi ameonya kuihama Arsenal iwapo mchezaji anayedaiwa kuwa na thamani ya $80m Wilfried Zaha atajiunga na Arsenal na kuchukua nafasi yake', 'Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anafikiria kumsajili Andy Caroll kurudi katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 na raia wa Uingereza yuko huru baada ya kuachiwa na klabu ya West Ham mnamo mwezi Juni. (Sun on Sunday)', 'Mshambuliaji wa Tottenham na Uholanzi Vincent Janssen 25 anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kuelekea katika timu ya Mexico Monterrey mapema wiki ijayo.(Football London) ', 'Mlinda lango wa Uhispania David De Gea 28 amekubali kuandikisha kandarasi mpya ya miaka sita ambayo itamfanya kuwa mlinda lango anayelipwa mshahara mkubwa duniani.(Sunday Telegraph', 'Manchesater City inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa ArgentinaThiago Almada, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Velez Sarsfield nyumbani kwao. Mabingwa hao wa Premia wameripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa takriban £16m . (Sun on Sunday) ', 'Manchester United imeimarisha mazungumzo na Lille kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast Nicolas Pepe kwa dau la £70m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amevutia hamu kutoka Liverpool , Arsenal na Everton.(Sunday Times)', 'Arsenal ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Itali Moise Kean, 19, na tayari wamewasiliana na ajenti wake (Mail on Sunday)', 'Watford wameanza mazungumzo na klabu ya Ufaransa Rennes kuhusu uwezekano wa kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 21 kutoka Senegal Ismaila Sarr. (Sky Sports)', 'Newcastle ina hamu ya kumsajili winga wa Burnley anayedaiwa kuwa na thamani ya £30m Dwight McNeil, lakini mkufunzi mpya Steve Bruce amejiandaa kutoa ofa ya £15m. (Sun on Sunday)', 'Aston Villa inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kasimpasa na Misri Egypt Trezeguet, 24, katika makubaliano ya thamani ya £8.75m. (Sunday Telegraph)', 'Crystal Palace imefanya mazungumzo na Liverpool kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mchezaji mwenye umri wa miaka 28 Nathaniel Clyne. The Eagles wanataka raia huyo wa Uingereza ambaye aliichezea Bournemouth kwa mkopo msimu uliopita kuchukua nafais yake Aaron Wan-Bissaka, ambaye alijiunga na Manchester United mwezi June. (Mail on Sunday) ', 'Beki wa Saint-Etienne na Ufaransa William Saliba, 18, atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya Jumanne katika klabu ya Arsenal kabla ya uhamisho wake wa £28m (Sunday Mirror)', 'Tottenham italazimika kulipa £67m iwapo watamsajili kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Giovani lo Celso, 23, msimu huu . (Evening Standard)', 'Sheffield United na Aston Villa zote zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford Neal Maupay. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ufaransa ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na timu hiyo. (Sun on Sunday)', 'Everton wako tayari kuipa changamoto Arsenal kumuwania mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, ambaye anauzwa na klabu yake ya Crystal Palace kwa kitita cha pauni milioni 80. (Evening Standard)', 'Manchester United, Everton na Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Juventus kuhusu kumsajili Blaise Matuidi. (Le Parisien)', 'Manchester United wanaongeza jitihadi kumpata kiungo wa Lazio, mzaliwa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Mirror)', 'Inter Milan wanamtaka mchezaji wa Man United Lukaku.', 'Livepool inamtaka beki wa kushoto wa Augsburg Philipp Max, 25, (Sport)', 'Tottenham na West Ham wanamtolea macho Diego Llorente, 25 wa Real Sociedad. (El Mundo Deportivo)', 'Wolverhampton Wanderers wanataka kumsajili mshambuliaji wa Italia na AC Milan Patrick Cutrone mwenye thamani ya takriban pauni milioni 20. (Express & Star)', 'Tottenham imempa mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji Fernando Llorente. (Mail) ', "'Arsenal kuwasajili wachezaji maarufu na ghali zaidi'", 'De Ligt safarini kukamilisha usajili na Juventus ', 'Crystal Palace imetangaza dau la pauni la milioni 8 kumpata kiungo wa Everton James McCarthy. (Sky Sports)', 'Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amemaliza matumaini ya Everton kwa kumsajili Kurt Zouma ambaye aliutumia msimu uliopita akiwa Goodison Park kwa mkopo. (Mirror) ', 'Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko, 33, huenda akaondoka Roma baada ya miaka mitatu, huku Inter Milan ikiwa na mpango wa kupata saini ya mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 15.(Sportitalia)', 'Mchezaji wa Chelsea, 18, Ethan Ampadu amefanya vipimo vya kiafya kabla ya kuhamia RB Leipzig ya Ujerumani. . (Sky Sports)', 'Klabu ya Brugge ya Ubelgiji ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Afrika Kusini Percy Tau, aliyecheza michuano ya kombe la mataifa Afrika. (Argus)', 'Derby County inataka kumsajili mlinda mlango wa Watford Daniel Bachmann, 25, kwa mkopo. (Derby Telegraph)']
michezo
TIMU za Simba na Mbao FC za Tanzania jana zilitakata baada ya kushinda mechi zao na kutinga nusu fainali za mashindano ya Kombe la SportPesa kwenye Uwanja wa Taifa katika muda tofauti.Mbao ndio ilikuwa ya kwanza kutinga nusu fainali na sasa itacheza dhidi ya Kariobang Ijumaa saa 10 jioni katika hatua hiyo baada ya kuwatoa mabingwa watetezi Gor Mahia ya Kenya kwa penalti 4-3, huku Simba ikashinda 2-1 dhidi ya AFC Leopard na sasa itacheza dhidi ya Bandari katika hatua hiyo kuanzia saa 8:00 mchana. Simba ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 13 lililofungwa na Mganda Emmanuel Okwi baada ya kupata krosi kutoka kwa Zana Coulibaly na kumchambua beki mmoja wa AFC Leoparxdna kuujaza mpiira wavuni.Cletus Chama aliifungia Simba bao la pili dakika tatu tangu kuanza kwa kipindi cha pili kwa bao baada ya kupata pasi kutoka kwa Okwi aliyeng’ara jana baada ya mara kwa mara kuichachafya ngome ya wapinzani. Simba ilikosa mabao kadhaa katika dakika ya 19, 39, 57 Okwi na Hassan Dilunga walivyoshindwa kuipatia timu yao mabao licha ya kupata nafasi nzuri ya kufunga kama wangekuwa watulivu.AFC Leopard walipata bao la kwanza katika dakika ya 61 lililowekwa kimiani na Oburu Vecent akiunganisha wavuni krosi ya Okaka Aziz, ambaye aliingia muda mfupi kabla ya kupatikana kwa bao hilo kuchukua nafasi ya Marita Brian. Wakati huohuo, katika mchezo uliotangulia jana, timu nyingine ya Tanzania, Mbao FC ya Mwanza iliwavua ubingwa Gor Mahia ya Kenya baada ya kuifunga kwa penalti 4-3 katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Waliopata penalti zao kwa Mbao FC ni Said Khamisi, Aboubakar Ngalema, Hamim Abdukarim na David Mwasa huku Ibrahim Mwasa alikosa wakati waliofunga kwa Gor Mahia ni Francis Kahata, Jack Tuyisenge na Ndaki Robert huku Harun Shakavavah na Shafiq Batambuze walikosa.Timu hizo ilibidi kwenda katika hatua ya matuta baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya kufungana bao 1-1, ambapo Gor Mahia walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Dnis Oliech katika dakika ya 32 baada ya mchezaji mmoja wa Mbao kuunawa mpira katika eneo la hatari na kuwa penalti.Mbao walisawazisha katia dakika ya 76 lililofungwa na aboubakar Ngalema baada ya kutokea piganikupige katika lango la Gor Mahia. Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Zana Coulibaly, Rashid Juma, Emmanuel Okwi/ Mzamiru Yassin, Cletus Chama, Rashid Juma, Lamine Moro, Pascal Wawa/Juuko Murshid, Jonas Mkude/James kotei, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hunlede Kisimbo/Meddie Kagere.
michezo
UKOMA ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea aina ya bakteria wa jamii ya “Mycobacterium”. Maambukizo ya wadudu hao hufanyika kwa njia ya hewa kwa mgonjwa kwenda kwa mtu mwingine.Ukoma ni jamii moja na ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao pia huenezwa kwa njia ya hewa. Vimelea vya ukoma hushambulia mishipa ya neva na ngozi, wakati vile vya kifua kikuu huzaliana katika mapafu na kuenea katika viungo vingine. Ukubwa wa madhara ya ukoma na kifua kikuu hutegemea kiwango cha kinga za mwili alizo nazo mwathirika.Ukoma, katika miaka ya nyuma ulikuwa ni ugonjwa uliotikisa na kuwa tishio kubwa kwa jamii. Kwa sasa, ugonjwa huo umepungua kwa kiwango kikubwa nchini kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoka na kutoa elimu kwa jamii ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo pamoja na tiba.Kupungua kwa ugonjwa wa ukoma nchini kumewafanya Watanzania wengi wadhani kwamba ugonjwa huu haupo tena, lakini kama yalivyo magonjwa mengine, ukoma haujapotea kabisa. Mratibu wa Taifa wa Ugonjwa wa Ukoma kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Deus Kamara, anasema: “Zipo halmashauri za wilaya 20 kutoka mikoa nane nchini hazijafikia kiwango cha kutokomeza ugonjwa wa ukoma.” Dk Kamara anataja vigezo vya kutokomeza ugonjwa wa ukoma vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ni uwepo wa mgonjwa mmoja eneo la utawala kati ya watu 10,000, na kwamba halmashauri hizo zipo juu ya kiwango hicho.Dk Kamara anasema hayo katika taarifa yake kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, kabla ya kufungua semina ya uhamasishaji wa uongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero kuhusu ukoma. Semina hiyo imekuja siku chache kabla ya kufanyika kwa maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani yanayofanyika kitaifa Jumapili ijayo (Januari 27), katika Kitongoji cha Chazi, kijiji cha Kigugu, Wilayani Mvomero, Morogoro.Hatua hiyo inakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Ujerumani linalojishughulisha na ukoma pamoja na kifua kiuu (German Leprosy and Tuberculosis Relief-GLRA). Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya ukoma mwaka huu 2019 ni “Tutokomeze ubaguzi, Unyanyapaa na Chuki dhidi ya Waathirika wa Ukoma.”Mratibu huyo wa Taifa wa ugonjwa wa ukoma ametaja maeneo ambayo bado yana changamoto ya ugonjwa wa ukoma kuwa ni halmashauri 20 zilizo katika mikoa minane ya Lindi, Mtwara, Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Tanga, Geita na Morogoro. “Maadhimisho haya yanalenga kuikumbusha jamii na kuielimisha juu ya ugonjwa wa ukoma tangu kuanzishwa kwa Siku ya Ukoma Duniani mwaka 1954,” anasema Dk Kamara. Anasema katika Mkoa wa Morogoro, wagonjwa wa Ukoma kuanzia mwaka 2014 walikuwa ni 269 na miaka mingine na idadi yao katika mabano ilikuwa kama ifuatavyo: Mwaka 2015 (257), 2016 (320), 2017 (270) na mwaka 2018 wagonjwa 181.Dk Kamara anasema ugonjwa huu umeendelea kuwepo nchini ingawa si kwa kiwango kikibwa na kwamba wizara inaendelea na mpango wake wa kitaifa wa kutokomeza kifua kikuu na ukoma. Anasema mikoa inapaswa kutengeneza mkakati wa kuwasaka, kuwafikia, kuwaibua na kuwaweka katika matibabu stahili wale wote wenye ukoma au dalili zake.Anasema hatua hiyo ni pamoja na kuzifikia kaya zote zenye wagonjwa wa ukoma kwa kufanyiwa uchunguzi ili wale ambao hawajaugua wapatiwe tiba kinga ili kutokomeza ukoma katika halmashauri zote ifikapo mwaka 2020. Naye Mwakilishii Mkazi wa Shirika la GLRA, Buchard Rwamtoga, anaema shirika hilo mwaka huu linatimiza miaka 60 ya kuwepo hapa nchini katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania kutokomeza ugonjwa wa ukoma. Anasema GLRA ni Shirika lisilo la kiserikali la Kimataifa (NGO) lenye Makao yake Makuu katika jiji la Wurbzurg, Ujerumani na kwamba lilianzishwa mwaka 1957 nchini Ethiopia.Anasema shirika hulo lilianza kazi ya huduma kwa wagonjwa wa Ukoma nchini Tanzania mwaka 1959. Mradi wao wa Kwanza anasema ilikuwa ni kusaidia kituo cha wagonjwa wa Ukoma cha Peramiho – Songea, mkoani Ruvuma kinachoendeshwa na watawa wa Mtakatifu Benedict. Katika kutimiza miaka 60 ya uwepo wake nchini, Rwamtoga anasema GLRA limefanikisha kujengea makazi bora kwa familia 120 miongoni mwa familia 739 za watu waliougua ukoma hapa nchini.“Dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba kupitia michango ya wadau mbalimbali, shirika linaweza kusaidia mashirika na taasisi nyingine hasa katika mpango wa taifa wa kudhitibi ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma katika kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya,” anasema Rwamtoga. Anataja mafanikio waliyoyapata kwa miaka 60 kuwa ni pamoja na kutoa viatu maalumu kwa walioathirika na ukoma jozi 94,500 kwa watu 47,250, miguu bandia, magongo na baiskeli kwa watu 2,655.Halikadhalika anasema shirika katika kipindi hicho limenunua magari 270 kwa ajili ya Tanzania bara na Zanzibar. Rwamtoga anataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kusaidia masuala ya elimu kwa wanafunzi 3,765 pamoja na kuwezesha vikundi vya kusaidiana vipatavyo 50, vyenye wanachama 677 kwa familia za watu wenaoishi na ugonjwa wa ukoma.Naye Mshauri wa Watu wenye Ulemavu na uwezeshwaji wa shirika hilo, Grace Mwasuka, anasema miongoni wa kazi za GLRA ni kuwajengea uwezo wadau wao kwa kutoa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa miradi kwa waratibu wa miradi, wajumbe wa kamati za miradi na maofisa ustawi wa jamii katika wilaya husika. “Tunatoa mafunzo ya ujasiriamali, mikopo midogo na tathimini na ufuatiliaji kwa vikundi vya kusaidiana. Pia GLRA imetoa mafunzo na vifaa vya kuendeshea ofisi kwa Chama cha Ukoma Tanzania na Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu,” anasema Mwasuka. Anasema wamekuwa wakitoa mitaji midogo kwa vikundi vidogo vya kusaidiana na mikopo ya vifaa kwa vijana waliomaliza mafunzo ya ufundi.Anasema wametoa pia vifaa vya kutendea kazi zikiwemo pikipiki, baiskeli na simu za mkononi kwa waratibu wa miradi, na kushiriki katika kutengeneza miongozo, sheria na mipango ya serikali. Anasema shughuli nyingine ambazo wamekuwa wakizifanya ni pamoja na kutengeneza na kuchapisha vijarida, vipeperushi na mabango yanayotoa elimu juu ya ukoma, ulemavu kwa ujumla na haki za watu wenye ulemu.Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari anawataka wananchi wa mkoa huo na halmashauri zake kutowaficha wagonjwa wenye ukoma majumbani ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa ifikapo mwaka 2020. “Serikali inawajali sana wananchi wake hivyo wananchi hampaswi kuwaficha wagonjwa majumbani kwani dawa na vipimo zinatolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini,” anasema Tandari Anasema mkoa utaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza ugonjwa wa ukoma kwani wajibu wao ni kuwasaidia watu wenye maradhi hayo kupona ili warudi kwenye kazi zao za kila siku.
kitaifa
WAZIRI mpya wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (40) amesema amepokea kwa mikono miwili uteuzi huo na kuwa amejipanga kuitumikia nafasi hiyo kwa umakini na kuleta maendeleo makubwa yanayotakiwa.Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo kabla ya uteuzi wa jana asubuhi uliofanywa na Rais John Magufuli, alisema anaifahamu wizara hiyo, kwa kuwa amewahi kufanya nayo kazi kwa ukaribu hivyo anazijua kero na changamoto, na atashirikiana na wafanyakazi kuiletea mabadiliko wizara husika.Aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara. Mbunge huyo wa Karagwe mkoani Kagera, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Novemba 10, mwaka jana kutokana na mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri. Kwa mujibu wa wasifu wake katika tovuti ya Bunge, Bashungwa aliyezaliwa Mei 5, 1979, ana Shahada ya Umahiri katika Masuala ya Kimataifa akijikita katika Sera za Kiuchumi na Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, na Shahada ya Kwanza ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John’s.Anakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa tatu katika utawala wa Rais Magufuli akitanguliwa na Charles Mwijage ambaye pia alikuwa akishughulikia Uwekezaji, na Kakunda ambaye pia aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Novemba 10, mwaka jana akitokea kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi.Akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wake, Kakunda ambaye ni Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora, alisema anakubali matokeo kwa kuwa alikuwa akijua fika kuwa rais angemwondoa kwenye wizara hiyo kutokana na mazingira yaliyojitokeza juzi kwenye kikao cha Rais na wafanyabiashara hao kutoka wilaya zote nchini.Kakunda alisema mabadiliko ni sehemu ya kuongeza tija na anamini aliyekabidhiwa kijiti ataendeleza yale mazuri kwa kuwa alifanya kazi ya maendeleo ya wizara hiyo kwa kushirikiana na wafanyakazi na waliifanya kama timu ya wafanyakazi wote kwa pamoja.Rais Magufuli alifanya mabadiliko hayo ya mawaziri pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) jana ikiwa ni siku moja baada ya kikao chake kizito na wafanyabiashara hao. Katika baadhi ya malalamiko ya wafanyabiashara hao walionesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara huku wengine nao wakielekeza malalamiko yao moja kwa moja kwa TRA.Moja kati ya kero zilizolalamikiwa hiyo juzi ni ufungaji hovyo wa viwanda uliofanywa na watendaji wa wizara hiyo, baada ya wafanyabiashara hao kudai watendaji wa wizara wamekuwa wakijisifu kwa kuwafungia viwanda vyao.Lakini pia wafanyabiashara hao walilalamikia utitiri wa vibali kwa ajili ya ufunguaji wa viwanda kuwa umekuwa kero kwa maendeleo ya viwanda. Kwa upande wa TRA, wafanyabiashara hao walisema baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wanachangia ukwepaji wa kodi kutokana na kuwawekea mazingira magumu yanayoshawishi watoe rushwa.Kutokana na malalamiko hayo na mengine, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Charles Kichere wa Kamishna Mkuu wa TRA na kumteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edwin Mhede kushika wadhifa huo katika mamlaka hiyo iliyoanzishwa mwaka 1996.Mhede ni mchumi aliyewahi kufanya kazi katika taasisi mbali mbali za serikali, na anakabidhiwa jukumu la kuongoza TRA akiwa ni Kamishna Mkuu wa tano katika utawala wa Rais Magufuli hadi sasa akitanguliwa na Risherd Bade, Eliakim Maswi, Alphayo Kidata.
kitaifa
Kwa mujibu wa Kamusi Kuu ya Kiswahili “mtu ni kiumbe mwenye utashi mkubwa kuliko viumbe wengine wote walioko duniani” na “binadamu ni kiumbe mwenye maumbile na sifa tofauti na wanyama wengine na hasa ya kuweza kutambua mema na mabaya”.Kimsingi, ufafanuzi hizi mbili zimetumia maelezo tofauti, lakini hazioneshi tofauti kubwa katika maana. Mtu yeyote angeulizwa kwa haraka, angeweza kujibu kuwa mtu ni binadamu na binadamu ni mtu.Hata hivyo, wahenga wapya wametumia ubunifu mkubwa katika matumizi ya maneno haya mawili ili kuonesha tofauti yake ambayo mwandishi nimeitafsiri hivi: Viumbe wote waliotolewa tafsiri za hapo awali, katika Kamusi Kuu ya Kiswahili wanaitwa watu. Lakini katika kundi hilo la watu, wapo ambao wana sifa za ziada zinazowatofautisha na wengine. Sifa hizo ni pamoja na kuwajali wengine, kuwatendea mema wengine na mengine mengi mazuri. Hao wanaitwa binadamu. Hivyo, binadamu ni wachache katika kundi kubwa la watu.Mwisho wa mawindo mbwa hana thamani: Ujumbe huu pia niliusoma katika lori la kubeba mafuta. Maana niliyoipata ni kuwa, mtu anapokuwa na shida anaweza kutumia kila mbinu kufanikisha shida yake. Aidha, mtu mwingine anaweza kusaidia katika utatuzi wa shida hiyo. Wakati wa harakati za utatuzi mtatuaji au anayesaidia kutatua anaweza kuwa na thamani kubwa, lakini shida ile inapotatuliwa mtatuzi huwa hana thamani tena.Hivyo, wasaidizi au watatuzi wa tatizo wamefananishwa na mbwa ambaye wakati wa kwenda kuwinda atabembelezwa na kupewa hata vyakula vizuri ili apate nguvu za kufanikisha lengo la mwindaji. Kwa kumwezesha kufanya hivyo, mbwa atawinda kwa bidii na wakati mwingine hata kujiingiza hatarini ili aweze kumwezesha bwana wake kupata kitoweo.Baada ya mawindo, mbwa akimsogelea bwana wake mara nyingi huambulia kufukuzwa, kupigwa na kupewa nyama zisizo na thamani ambazo bwana wake hawezi kuzila. Vilevile, usemi huu unaweza kufananishwa na wamiliki wa kampuni za uzalishaji ambao huwahamasisha wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii ili kampuni izalishe na kupata faida.Lakini kampuni inapopata faida na kukua, wafanyakazi waliochangia mafanikio hayo hawakumbukwi kwa lolote. Ukiona manyoya ujue kaliwa: Usemi huu unanikumbusha wafugaji wa kuku wa kienyeji wanaowaachia (kuku) wazunguke na kujitafutia chakula wenyewe. Kila asubuhi hutoka nje na kuzurura kila mahali ili kujitafutia chochote na kila jioni hurejea makwao.Mfugaji kwa kawaida huwatambua kuku wake kwa rangi za manyoya na inapotokea mmoja haonekani, huwa ni kazi yake kuzunguka kwa majirani kuulizia kama kuku huyo alikosea na kwenda nyumba ya jirani, badala ya kurudi nyumbani kwake. Jambo ambalo siyo la kawaida kwa kuku ni kupotea nyumbani. Hivyo, ikitokea akakuta manyoya ya rangi ya kuku wake, basi mfugaji hukata tamaa na kuamini kuwa kuku wake ama ameliwa na wanyama au ndege wanaokula kuku, au ameliwa na watu katika nyumba ya jirani.Katika hali ya kawaida, kuku anakuwa na manyoya yake wakati wote hivyo hawezi kuacha manyoya yake na yeye kuendelea na safari. Mfugaji akiona manyoya ajue kuku wake kaliwa. Hali hii inaweza kubeba dhana ya ndege wote wanaofugwa ikiwa ni pamoja na kuku, njiwa, bata, kanga na ndege wengine. Ujumbe huu unafananisha na maisha ya kawaida ambayo mtu unaweza kupambana sana katika kutafuta maisha, lakini usijue mwisho wako na kisha juhudi zako kuishia ukingoni utakapoona dalili za kukatisha tamaa.Kazi mbaya ukiwa nayo: Ujumbe huu niliusoma katika daladala ukiwa na msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii. Kaulimbiu ya uongozi wa awamu ya tano nchini Tanzania ni Hapa Kazi Tu. Wimbo unaotawala kwa sasa ni kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato. Mhenga mpya hapa alitafakari kauli za watu wenye kazi ambao hawazithamini wala kuzijali kazi zao na kuona kama ni jambo la kawaida kwa wao kuwa na kazi hizo. Aidha, alitafakari pia wale ambao hawana kazi na wanamwomba Mungu kila siku awajalie wapate kazi.Watu hawa wawili wana mawazo tofauti. Aliye na kazi anaona ni jambo la kawaida na huenda akawa anachelewa kazini, anafanya kazi kwa mazoea na hata kufikia mahali kuiona kazi aliyonayo huenda siyo ya hadhi yake na kutamani kupata kazi nyingine. Asiye na kazi anaahidi akipata kazi ataitumikia kwa uwezo wake wote ili asije akapoteza bahati ya kuwa nayo.Hata hivyo, pamoja na ahadi zake huenda atakapoipata kazi mawazo yake yatabadilika na kuwa kama ya yule aliye nayo. Ikitokea kazi hiyohiyo inayoonekana haifai ikapotea ama kwa kufukuzwa au kwa kumaliza mkataba ndipo thamani yake huongezeka. Msemo huu unafanana na methali nyingine kama mdharau mwiba mguu huota tende na ukiona cha nini mwenzio anasema nitakipata lini.Ujumbe mwingine niliousoma katika gari kubwa la mizigo ni Punguza maneno muda si rafiki. Huu pia unasisitiza mtu kuacha maneno na kuchapa kazi kama kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu inavyosema.Mchana nzi usiku mbu: Kutokana na msemo huu, nilipata dhana ya mateso na mahangaiko au shida anazozipata mtu kila siku, ambapo mchana kutwa anahangaika na nzi na usiku anapotarajia kulala ili apumzike anakutana na mbu. Watu wote tunafahamu kero ya nzi wanapokuwapo katika maeneo tunayokaa au kupumzika. Lakini pia tunafahamu fika usumbufu wa mbu tunapotaka kulala. Wadudu wote wawili zaidi ya usumbufu wao, pia wanaambukiza magonjwa ambayo ni hatari. Nzi wanaambukiza kipindupindu na homa ya matumbo na mbu wanaambukiza malaria na hivi sasa kuna matangazo kila kona yanayotutahadharisha na ugonjwa wa kidingapopo au dengi unaoenezwa na mbu.Wahenga wapya kwa kutafakari mihangaiko anayoipata binadamu mchana na usiku akipambana na maisha wafananisha na hekaheka za nzi na mbu. Tatizo siyo bosi, ila hesabu: Ujumbe huu niliusoma katika daladala. Wengi tunaweza kubashiri kile ambacho mwendesha daladala alikuwa akikifikiria wakati anaandika ujumbe huu. Ni kawaida kwa biashara ya daladala kupanga kiasi cha fedha ambacho ni lazima kikusanywe kila siku. Dereva hukabidhiwa gari na kupewa maagizo ya kuwasilisha kwa bosi kiasi hicho.Hivyo, huenda siku moja dereva alitafakari hekaheka zinazompata ili kukamilisha kiasi hicho ambacho kwa siku hiyo aliona ni vigumu. Akatafakari tatizo liko wapi kwa bosi, kwake, abiria au hesabu? Kwake tatizo aliona ni hesabu. Hesabu ni neno la Kiswahili ambalo katika mazingira ya biashara ya daladala ni kiasi cha fedha ambacho dereva anatakiwa kuwasilisha kwa mmiliki wa gari kila siku.Ujumbe mwingine ambao niliufananisha na huu uliandikwa tatizo siyo mchungaji, bali kondoo. Ujumbe wa mwisho kwa leo ni huu, kila kilema na mwendo wake. Wahenga wapya hawakuwa na lengo la kuwadhalilisha wala kuwabeza walemavu. Dhana yao ilikuwa kwamba kila tatizo linalompata mtu linatatuliwa kwa namna tofauti. Vilevile, tatizo moja linaweza kuwapata watu tofauti na kila mmoja akawa na njia tofauti ya kulitatua. Tafsiri zote nilizozitoa kwa semi za wahenga wapya ni kwa kadiri ya mawazo, uelewa na maoni yangu.Aidha, wahenga wapya wana mchango mkubwa katika ukuzaji na uimarishaji wa lugha ya Kiswahili. Wahenga hao wapya wamekuwa na matumizi mapana na yenye ubunifu mkubwa wa lugha na hivyo. Ninaendelea kutafiti iwapo maneno na semi ambazo siku hizi tunaziita za wahenga zilianzaje? Huenda zilianza kama wahenga wapya walivyoanza katika siku za hivi karibuni.Iwapo zilianza hivyo, basi huenda dhana za wahenga hawa wapya zikapata mashiko na kutumika kama methali, nahau au misemo kwa vizazi vijavyo. Ikitokea hivyo basi wahenga wapya wataungana na wahenga wa zamani na wote kwa pamoja wataitwa WAHENGA. Tujivunie Kiswahili Mwandishi wa makala haya ni Mchunguzi Lugha katika Idara ya Istilahi na Kamusi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita).
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imetoa kipaumbele kwenye matumizi ya tehama kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi.Amewataka wananchi kutumia vizuri teknolojia hiyo ya habari na mawasiliano kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta mbalimbali kukuza uchumi na kuwapunguzia wananchi umaskini na pia kuongeza ajira. Alisema hayo jana katika sherehe za utoaji tuzo za mashindano ya Tehama ya Huawei yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.Aliwaonya watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii nchini. “ Watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii waache. Ni vema wakatumia mitandao hiyo kwa kuhamasishana mambo mema zikiwemo shughuli mbalimbali za maendeleo. Watakaokiuka sheria ipo,” alisema. Alisema serikali inaamini matumizi ya Tehama yataongeza ufanisi katika kuhudumia wananchi.Mfano katika sekta ya elimu, mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wengi kutoka katika shule tofauti kwa wakati mmoja. “Matumizi ya Tehama kwa kiasi kikubwa yatapunguza gharama za uendeshaji kwani yatafanikisha mawasiliano binafsi, warsha na maelekezo mbalimbali kuwafikia walengwa bila kusafiri nje ya vituo vya kazi,” alisema.Alitoa mfano Juni 2017, Rais Magufuli alizindua mfumo wa ukusanyaji mapato ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa kielektroniki na kudhihirisha sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni mhimili muhimu wa maendeleo kwenye viwanda, utalii, ujenzi, elimu, afya, kilimo, uvuvi na ufugaji.“Kwa kuzingatia hayo, Juni mwaka huu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Serikali ilizindua mifumo tisa ya Tehama inayolenga kuimarisha utendaji wa serikali hususan kuwahudumia wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, ukusanyaji mapato na utoaji wa taarifa,” alisema. Waziri Mkuu, Majaliwa alisema serikali itaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza mifumo ya tehama ili kutekeleza kwa vitendo azma ya kuwapa wananchi vijijini maendeleo na huduma bora kwa wakati.Alisema Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ina uwezo wa kuona na kubaini makusanyo yanayokusanywa katika halmashauri mbalimbali nchini na kiasi kinachoingizwa benki kwa kupitia Tehama. Waziri Mkuu alisema serikali imeendelea kuunganisha mkongo wa taifa wa mawasiliano kwenye taasisi zake ili kufanikisha azma ya kutumia serikali mtandao, hatua inayoenda sambamba na kuunganisha shule za msingi, sekondari, ofisi za wakuu wa wilaya, polisi, hospitali za wilaya, vyuo vikuu na Posta.
kitaifa
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza jana mjini hapa katika ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya SHIMUTTA.Amesema wafanyakazi wakishiriki mashindano hayo wataweza kuwasaidia katika matumizi yao kwa kupunguza gharama za matibabu pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwani watakuwa wamefanya mazoezi.Makamu wa Rais ambaye ni mlezi wa shirikisho hilo aliwaasa waajiri kuacha kuwazuia wafanyakazi kwenda kushiriki michezo hiyo dakika za mwisho.“Kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa wafanyakazi kushiriki shughuli za michezo kama mlezi wa SHIMMUTA sifurahishwi hata kidogo na tabia hiyo,” alisema.Makamu huyo wa Rais alisema suala la kutofanya mazoezi na michezo katika maeneo ya kazi ni jambo ambalo halikubaliki.“Ikumbukwe kuwa serikali ilianzisha michezo hii kwa lengo la kuimarisha afya na kujenga mahusiano mema baina ya wafanyakazi ili hatimaye waweze kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao,” alisema.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nicholas Mkapa alisema serikali itaendelea kusimamia michezo ikiwemo ya SHIMMUTA.“Tunakuahidi kusimamia kwa vitendo yale yote uliyoyaagiza ikiwemo kusimamia kwa karibu michezo ikiwemo hii ya SHIMMUTA,” alisema.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SHIMMUTA, Khamis Mkanachi alimshukuru makamu wa Rais kwa kuwatafutia udhamini wa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu katika mkoa utakaopangwa baadae. mwisho
michezo
JUMLA ya Sh milioni 44.9 zimepatikana katika kipindi cha siku nne kuanzia Mei 6 hadi 9, mwaka huu, kutokana na ushuru na kodi mbalimbali zitokanazo na madini tangu serikali ilipoanzisha uratibu wa kufungua vituo vya kuuza na kununua madini mkoani Ruvuma.Takwimu hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme wakati akifungua soko la kuuza dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru. Alisema kati ya fedha hizo, Sh milioni 9.9 zimetokana na mrabaha na Sh milioni 2.5 ni ushuru. Alieleza kuwa tangu serikali ilipoweka sheria ya kuanzishwa kwa soko la madini kumekuwa na mafanikio makubwa, ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya serikali na udhibiti wa madini ambayo kabla ya sheria hiyo kulikuwa na vitendo vingi vya utoroshaji madini na ukwepaji kodi.Alisema katika kipindi hicho gramu 2,824.2 zilipatikana, kati ya hizo gramu 2,540 za vito na dhahabu iliyopatikana ni gramu 364.2. Aidha, Mndeme aliagiza kufanyiwa ukaguzi wa mizani na vifaa vingine vya kupima madini hasa baada ya kubaini kuwa baadhi ya vipimo vinavyotumika haviko sahihi, jambo linaloweza kusababisha udanganyifu na hivyo kuikosesha serikali taarifa za mapato halisi.Alisema, lengo ni kufahamu thamani ya madini kwani kwa muda mrefu kumekuwa na udanganyifu mkubwa unaofanywa na wafanyabiashara wa madini. Alisema, ufunguzi wa soko la madini katika wilaya ya Tunduru na Songea mkoani humo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli linalolenga kupata uhakika wa takwimu za madini, soko na uhakika wa bei na kuondoa unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo unaofanywa na wanunuzi.Aliwataka wananchi na wachimbaji wadogo wa madini mkoani humo kuwa walinzi wazuri wa rasilimali za madini na kusisitiza kuwa yeyote atakayekamatwa anatorosha madini atachukuliwa hatua, ikiwemo kufikishwa mahakamani sambamba na kufutiwa leseni.Aidha, Mkuu wa Mkoa aliziomba taasisi za fedha zikiwemo benki kufungua huduma za fedha katika eneo la kuuzia madini ili kuwaondolea usumbufu wanunuzi na wauzaji madini kufuata fedha mbali. Aliwataka pia wachimbaji wadogo kuhakikisha wanafungua akaunti badala ya kutembea na fedha nyingi mifukoni, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao. Awali, Ofisa Madini wilaya ya Tun- duru, Juma Kapela alisema, wilaya ya Tunduru imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali ya thamani kama dhahabu, madini ya vito na shaba.Kapela alisema, ofisi ya ofisa madini mkazi inasimamia jumla ya leseni hai 342 za uchimbaji mdogo na imeshapokea maombi mapya 56 ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini yaliyo katika hatua za kupitiwa kama yanakidhi vigezo ili yaweze kutolewa leseni. Alisema hadi sasa jumla ya leseni 239 zimepewa hati za makosa na leseni 1,342 zimefutwa kwa kutotimiza masharti ya umiliki wa leseni hizo kwa mujibu wa sheria.Alisema kufunguliwa kwa soko la madini katika wilaya ya Tunduru kutafungua milango kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini walioko katika wilaya ya Tunduru na maeneo jirani kupata sehemu ya kuuzia na kununua madini. Kwa upande wao, wachimbaji wadogo wa madini, walimpongeza Rais John Magufuli kwa kukubali kukutana na wadau wa sekta ya madini ili kusikiliza kero za sekta ya madini.Hata hivyo, waliiomba serikali itengeneze mazingira mazuri ya soko la ununuzi wa madini ya vito kwa sababu wanunuzi hao wapo katika kampuni tofauti hivyo kukaa chumba kimoja zaidi ya mnunuzi mmoja inaondoa usiri wa kampuni kwa kampuni na mchimbaji anayehitaji kuiuzia. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo wa Madini, Mohamed Mlangwa alisema, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba madini ya vito hayana bei maalumu kama ilivyo kwa dhahabu.
kitaifa
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala inawashikilia watu watatu akiwamo mmiliki wa Kampuni ya Motrax, Chandulal Ladwa kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Sh200,000.Mtuhumiwa huyo alitoa rushwa kwa wakili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Goodluck Mwangomango ili ampe upendeleo kwenye kikao cha kujadili marejeo ya mikataba ya miradi ya chama hicho.Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa Mei 29, mwaka huu, saa 4 asubuhi, maeneo ya Sea View Upanga kwenye mgahawa wa Central Park, Ladwa ambaye ni mpangaji wa maeneo ya biashara ya CCM alitoa kiasi hicho ili apewe upendeleo kwenye kikao cha kufanya marejeo ya mikataba.Alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani jana chini ya Kifungu cha 15 (1), (b) cha Sheria ya Takukuru Na.11/2007 ili kujibu tuhuma hizo. Alisema CCM wanaendelea kufanya uhakiki wa mali zote za chama ikiwa ni agizo la Rais John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa. Alisema kiwanja ambacho mtuhumiwa amepanga ni mali ya CCM hivyo mtuhumiwa aliomba kukutana na wakili huyo wa CCM ili apate kipaumbele cha kupatiwa tena eneo alilopanga maeneo ya Oysterbay.Wakati huo huo, maofisa wawili wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa), Selaman Ally na Issa Khalifan wanashikiliwa na Takukuru kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 150,000.Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala Myava alisema tukio hilo lilitokea Aprili 24, mwaka huu, saa saba mchana, maeneo ya Tabata Kisukuru baada ya kuomba rushwa kutoka kwa mtoa taarifa ili wamrekebishie ankara ya maji na kumrejeshea huduma hiyo. Myava alisisitiza wananchi kutoa taarifa na ushirikiano kwa Takukuru ili kutokomeza vitendo vya rushwa nchini. Pia alitoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa kutoa taarifa za watu wanaofanya ubadhirifu wa mali za vyama hivyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
kitaifa
KUFUATIA kuwepo kwa taarifa zilizoenea za kusimamishwa kwa baadhi ya benki katika biashara ya kubadilisha fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imebainisha kuwa ilichokifanya ni kuzisimamisha ushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni na si kubadili fedha reja reja.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na benki hiyo kupitia Idara ya uhusiano wa Umma na Itifaki, ilisema kuwa benki za Barclays , Exim, UBA, BancABC na Azania zimesimamishwa kushiriki katika Soko la jumla la fedha za kigeni kati ya benki za kibiashara (IFEM), kwa kuvunja kanuni na taratibu kama inavyowataka kufanya.Hatua inatajwa kuchukuliwa baada ya benki hizo, kushindwa kutoa taarifa kwa Benki Kuu ya Tanzania juu ya miamala yote ya kifedha inayofanyika. Taarifa hiyo ilifafanua kuwa soko la fedha za kigeni kati ya mabenki (IFEM), lina kanuni na taratibu zake, ambazo zinaeleza kinagaubaga namna washiriki wote wanavyotakiwa kufanya biashara hiyo na kwamba washiriki wote katika soko hilo, wanatakiwa kutoa taarifa BOT kuhusu miamala waliyofanya kwa siku.Hata hivyo, inaeleza kuwa washiriki wa IFEM ambao watavunja kanuni na taratibu za soko hilo, hufungiwa kushiriki katika kuuza na kununua kwenye soko hilo kwa kipindi maalum. “Hivyo kwa benki hizo tano, kufungiwa kwake kunahusu tu ushiriki katika soko la fedha za kigeni kati ya mabenki na sio biashra rejareja ya fedha,” ilisema taarifa hiyo na kusema kuwa benki hizo zinaruhusiwa kuuza fedha za kigeni kwa wateja wake au kununua kutoka kwao.Soko la jumla la fedha za kigeni kati ya benki za kibiashara (IFEM), linawezesha benki za biashara na taasisi za fedha kuuza na kununua (kubadilishana) dola za kimarekani na shilingi kati yao. Taarifa hiyo ilieleza kuwa soko hilo, husaidia kuamua kiwango rasmi cha kubadilisha dola dhidi ya shilingi kwa siku husika. Benki Kuu ya Tanzania pia inashiriki kuuza na kununua fedha za kigeni pale inapolazimu, wakati mwingine huingilia soko ili kuhakikisha hakuna mabadiliko makubwa.
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amechukizwa na kukemea utendaji kazi wa watendaji wa wilaya ya Kongwa wa kufanya kazi kwa maigizo.Pia, ameagiza Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Nelson Milanzi kujieleza kwa maandishi kwa kushindwa kuwajibika katika utekelezaji wa miradi ya elimu na kutaka maelezo hayo kufika kwa Katibu Mkuu Tamisemi ifikapo Ijumaa.Jafo ambaye juzi alitembelea miradi kadhaa katika wilaya ya Kongwa na kukuta shughuli za ujenzi katika shule mbili za sekondari ukiwa kwenye hatua ya msingi ikiwa ni miezi sita tangu kutolewa kwa fedha.Akiwa katika shule ya Sekondari ya Kongwa, Jafo alimuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Kongwa kumpigia simu Ofisa Elimu Milanzi ambaye yuko Mtwara kwenye mashindano ya Umiseta kurejea kwenye kituo chake cha kazi, kujieleza kimaandishi na kurejesha fedha za safari alizopewa kwa siku ambazo alitakiwa kuwepo kwenye mashindano.“Mpigieni simu arudi, na akifika aandike barua ya kujieleza kwa katibu mkuu kwanini ameshindwa kutimiza wajibu, nimetoa nafasi hii kwa sababu napenda kutenda haki, pengine kuna jambo nyuma ya ukuta,” alisema. “Nataka tumsikilize na yeye pengine kwenye ofisi yenu mnakwamishana mwenyewe apime, akishajieleza Katibu Mkuu atapima maelezo yake na kuamua ama kumbakisha au akapangiwe kazi zingine maana anaweza kurudi kufundisha, kuwa afisa elimu kata,” alisisitiza.Hatua ya Jafo ilitokana na maelezo yaliyotolewa kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Wilaya, Deo Ndejembi na Mkurugenzi, Dk Omary Nkulo waliodai kuchelewa kujengwa kwa majengo katika shule ya Sekondari Kongwa na Sejeli kutokana na kuwapo kwa mvutano wa ama watumie mfumo wa Force Account au watumie mkandarasi.Maelezo kama hayo pia yalitolewa wakati Jafo akikagua mradi wa shule ya Sekondari ya Sejeli ambako ujenzi wake pia uko katika ngazi ya msingi. Akiwa kwenye shule ya Sejeli, Jafo alisema: “ Hapa nikuambie ni uzembe hakuna sababu yoyote, hata hii kazi kwa kiasi kikubwa imeanza kufanyika leo (juzi) na kwa sababu Jafo amekuja anaweza kutembelea shule.Kama tunaenda kanisani na misikitini nani anaweza kusimama na kusema naongopa anyoshe mkono hapa, hata machinjio ya kuku pia yametelekezwa.” Alisema fedha kwa ajili ya shule hizo zilitolewa na kupokewa tangu Januari, mwaka huu, lakini hakuna kitu kilichofanyika wakati maeneo mengine waliyopelekewa fedha kama hizo wamemaliza mabweni na wamajiandaa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano.“Hapa kazi sijaridhika na mnamuangusha Spika (Job Ndugai) ambaye ametafuta fedha kwa ajili ya wananchi wake, kwa kweli sijaona sababu ya msingi, nendeni Bahi ina watumishi kama ninyi, lakini wanajenga mabweni, madarasa, hospitali ya wilaya na mambo yanaenda vizuri ila hapa sijaridhika,” alisema.
kitaifa
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeanza operesheni maalum kubaini wamiliki hewa wa viwanja zaidi ya 9,000, vilivyoandikishwa kumilikiwa na watumishi wa wizara hiyo kwa njia isiyokuwa halali.Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ilibainisha kuwepo kwa idadi kubwa ya viwanja, vinavyomilikiwa na wafanyakazi hao kwa majina bandia au anuani za uongo. Alisema watumishi hao wamejimilikisha isivyo halali ili waje kuviuza kwa wananchi kwa njia za udanganyifu na kuwa wapo watumishi, ambao wamepima viwanja vya wananchi mara mbili mbili na kuwasababishia kero wananchi hao. Aliongeza kuwa idadi kubwa ya viwanja hivyo havijalipiwa kodi na pia havijaendelezwa kwa kuwa vimeachwa kwa muda mrefu bila ya shughuli za kibinadamu kufanyika hali inayowaathiri wakazi wengine wa maeneo hayo.Alisema,“wizara imejipanga kunasa viwanja vyote ambavyo umiliki wake una mashaka na vitachukuliwa na kurejeshwa serikalini hivyo basi wananchi mnaombwa kutoa ushirikiano stahiki ili operesheni hii iwe na tija.” Akizungumzia kuhusu athari zaidi za kutoendelezwa kwa viwanja hivyo, alisema kuwa ni sawa na kuwadhurumu haki wananchi wengine kumiliki ardhi na kuongeza kuwa kwa kutokuendelezwa huko, kunasababisha uwepo wa nyoka, uchafu au hata uharifu kwa wananchi waishio maeneo husika au jirani.Aliwataka wananchi waishio jirani na maeneo yasiyoendelezwa kwa zaidi ya miaka 10 bila ya kuwaona wamiliki wake kutoa taarifa ili yaanze kuchunguzwa. Kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, viwanja hivyo na idadi yake ni Mbweni Mpiji viwanja 3,544, Mbweni JKT viwanja 1,424, Mivumoni viwanja 1,508 na Bunju viwanja 4,868. Kwa upande wa Temeke ni maeneo ya Tuangoma yenye viwanja 3,384 na Kizota ikiwa na viwanja 2,362.Kwa upande wa Wilaya ya Kigamboni, maeneo yenye viwanja vya aina hiyo ni Mtoni Kijichi, viwanja 1,776, Mwongozo viwanja 2,754 na Vijibweni viwanja 38. Maeneo mengine ni Kibada viwanja 6,223 na Gezaulole viwanja 1,128, wakati Wilaya ya Ilala eneo la Buyuni Chanika viwanja 7,570 na Mwanagati viwanja 2,164. Waziri Lukuvi aliwataka watu wenye taarifa za watu wanaomiliki viwanja visivyoendelezwa kwa muda mrefu kwenye maeneo hayo, kumpigia simu yake ya mkononi namba 0755 333334 huku akiwahakikishia usalama wao kuwa hawatajulikana kuwa ndio wametoa taarifa hizo.
kitaifa
KATIBU Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Balozi John Kijazi amezindua vikundi kazi vya baraza hilo kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kuibua changamoto na kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania.Akizungumza baada ya uzinduzi wa vikundi kazi hivyo jijini Dar es Salaam juzi, Balozi Kijazi alisema madhumuni ya kuunda vikundi kazi hivyo vilivyowajumuisha wataalamu katika sekta mbalimbali, vitawezesha majadiliano juu ya changamoto zijadiliwe kwa kina zaidi kabla ya kupelekwa katika ngazi ya Baraza.“Jumla ya vikundi kazi vinne nimevizindua leo (juzi) ikiwa ni pamoja na Kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara, Viwanda, Misitu na Kilimo vitavyokwenda kuibua changamoto na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera na miongozo iliyopo,” alisema Balozi Kijazi.Alisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma, unahitajika ili kuweza kubaini changamoto na kuzijadili na kuja na mapendekezo yatakayoleta tija katika mustakabali wa kujenga uchumi wa Taifa.“Serikali itapokea mapendekezo yote yatakayowakilishwa na timu za wataalamu kutoka katika vikundi kazi hizi na tutayafanyia kazi mapendekezo yote, zaidi kwa mengine yanayoweza kuchukuliwa na maamuzi kwa ngazi yenu endeleeni lengo ni kupanga majadiliano katika ngazi ya taifa,” alisema Balozi Kijazi.Alisisitiza kuwa mijadala ya vikundi kazi hivyo vifanyiwe kazi kwa uhuru na usawa kwa kutohofia cheo cha mtu au mali, bali wote wawe kitu kimoja ili majadiliano yaweze kuleta tija na mapendekezo yatakayofanya mazingira ya biashara kuboresheka zaidi.“Vikundi kazi hizi vikapitiwe Sera, Miongozo na Sheria zilizopo ili waje na mapendekezo yatakayoboresha mazingiria ya biashara kuwa rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini,” alisema.Alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya tozo, mamlaka za udhibiti na kero mbalimbali katika uanzishaji wa biashara nchini, hivyo ni muhimu vikundi kazi hivyo vikatoa mapendekezo katika maeneo hayo ili yafanyiwe kazi. “Uongozi wa awamu ya tano umefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara, hivyo ni matumaini yangu tutakwenda kumaliza kabisa changamoto zilizopo na kupelekea nchi yetu kupiga hatua kiuchumi,” alisema Balozi Kijazi.Pia, Balozi Kijazi alisema kikosi kazi cha kilimo kisimamie utekelezaji wa nguzo kumi za kilimo kwanza na pia kufanya mapitio ya Mpango wa Awamu ya Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP- II) na kuleta mapendekezo ya utekelezaji wake. “Lengo letu ni kutizama azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, vikundi kazi hivi ndiyo vitatupa mwanga wa kufikia malengo kwa kuja na mapendekezo yenye tija na utekelezaji ufanywe maendeleo yapate kuonekana,” alisema Balozi Kijazi.
kitaifa
SIMBA itacheza nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mchezo wa mashindano ya Mapinduzi yanayochezwa visiwani Zanzibar kesho kutwa.Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Amaan, Unguja baada ya jana kuifunga Zimamoto kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Gombani, Pemba. Azam FC ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, anakutana na Simba ambayo katika fainali zilizopita waliifunga kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Gombani Pemba, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Simba ambayo ipo Kundi B iliifunga Zimamoto jana kwa mabao 3-1 inakutana na Azam FC ambayo ipo Kundi A ambayo iliitoa Mlandege kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Amaan kwa bao la Obrey Chirwa dakika ya 57.Simba ilianza kupata bao la kwanza dakika ya nne likifungwa na John Bocco na dakika tano baadaye iliongeza bao la pili lililofungwa Sharaf Shiboub katika dakika ya tisa akiunganisha kona iliyopigwa na Ibrahim Ajibu, lakini dakika ya 28 Zimamoto walipata bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Ahmada na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa 2-1.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na katika dakika ya 53 Ibrahim Ajib aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Zimamoto, bao lililodumu hadi dakika 90 kipyenga cha mwisho kilipopulizwa.Kwa mara ya kwanza Simba ilimchezesha Louis Mequissone raia wa Msumbiji iliyemsajili juzi katika dirisha dogo ambaye aliingia dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga.Baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba, John Bocco, alisema wanakwenda kuangalia makosa yao na kuyafanyika kazi na mchezo wao dhidi ya Azam FC utakuwa wa ushindani na wao watahitaji kushinda mchezo huo ili kuwapa raha mashabiki.“Azam FC ina wachezaji wazuri kama ilivyo Simba hivyo mchezo huo tumeuchukulia kwa uzito mkubwa na tunakwenda kujiandaa ili tuweze kushinda,” alisema Bocco.Mtibwa Sugar ambayo ipo Kundi B inatarajiwa kucheza nusu fainali kesho na mshindi wa mchezo wa Yanga dhidi ya Jamhuri ambao ulichezwa jana usiku. Mtibwa Sugar iliifunga Chipukizi kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba, ambapo kipa Said Mohammed ‘Ndunda’ aliokoa penalti mbili.Chipukizi ilitangulia kufunga bao dakika ya tano lililofungwa na Suleiman Nassor na Haroun Chanongo kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 63. Shujaa wa Mtibwa alikuwa Nduda ambaye aliokoa penalti za Jumaa Kassim na Abdallah Mohamed, huku penalti za Mtibwa Sugar zikifungwa na Omar Sultan, Abdulhalim Humud, Riffat Khamis na Dickson Job na zile za Chipukizi zilifungwa na Salim Abui na Abdallah Khalisan.Mashindano hayo ya 13 yanashirikisha timu nne za Zanzibar na timu nne za Tanzania Bara na mecho zitachezwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo bingwa anatarajiwa kuondoka na Sh milioni 15 pamoja na kombe. Fainali za mashindano hayo zitafanyika Januari 13 katika Uwanja wa Amaan majira ya saa 2:15 usiku.
michezo
SERIKALI imejizatiti kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa ukienda sanjari na ujenzi wa viwanda vya sukari, kupunguza nakisi iliyopo.Akizungumza na Habarileo hivi karibuni, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha viwanda vilivyopo vinaongeza uzalishaji wa sukari na kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa.Mwaka jana, Rais John Magufuli alipokutana na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, aliwataka kuwekeza zaidi katika viwanda vya sukari, kukabili nakisi inayosababisha nchi kuagiza sukari kutoka nje.Rais Magufuli alisema mahitaji ya sukari ni tani 590,000 kwa mwaka huku tani 455,000 zikiwa ni sukari ya kula na 135,000 ya viwandani. Upo upungufu wa tani 125,000 wa sukari ya kula na tani 135,000 ya viwandani.Alitaja Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwamba ina mkakati mkubwa wa miaka mitatu wa kuongeza uzalishaji wa miwa mara mbili.“Sasa wanazalisha zaidi ya tani 130,000 na wamesema wana uwezo wa kuzalisha hadi tani 250. Wanataka kupanua mashamba na wazalishaji wa nje wa miwa waongeze uzalishaji,” alisema.Viwanda vya Kagera na Mtibwa pia vinatajwa kuwa na mpango wa kupanua uzalishaji wa miwa. Kwa upande wa TPC Moshi, Hasunga alisema wanashindwa kufanya upanuzi kwa sababu ya eneo kuwa dogo.Waziri Hasunga alitaja miradi mipya ambayo serikali inaiwekea mkazo ni Mkulazi 1 na Mkulazi 2 mkoani Morogoro.Mmoja una uwezo wa kuzalisha tani 50,000 za sukari na mwingine tani 200,000 hadi 250,000.Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia kampuni yake ya Mkulazi Holding na Jeshi la Magereza, ndiyo imeanzisha kiwanda katika Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.“Kwa sasa hivi wameshapanda miwa maeneo mengi na walioko nje wamepata miwa mingi, kinachosubiriwa sasa ni viwanda vitakavyosindika hiyo miwa,” alisemaAlitaja kampuni nyingine ya miwa ya Morogoro, ambayo pia imewekeza katika kilimo cha miwa kwa wingi ianze uzalishaji . Ingawa alisema siyo mzalishaji mkubwa, lakini alisema itachangia uzalishaji wa sukari.
uchumi
WAGONJWA 400 wa mabusha na matende wamefanyiwa upasuaji wa ugonjwa huo katika Wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo, hatua iliyotokana na elimu mbalimbali inayoendelea kutolewa kwa wananchi.Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Dk Grace Maghembe wakati wa semina iliyoendana na uzinduzi rasmi wa kampeni ya utoaji dawa za kingatiba za magonjwa ya mabusha na matende inayotarajiwa kuanza leo katika wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.Katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Dk Maghembe alisema wagonjwa hao wamepatikana tangu kuanza kwa kampeni hiyo miaka mitano iliyopita ambapo mbali na wagonjwa hao, asilimia 80 ya wananchi wamepatiwa dawa za kingatiba. “Tunawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika unywaji wa dawa za kuzuia mabusha na matende ili kusaidia kulinda afya zao, ikumbukwe kuwa tiba ni bora kuliko kinga hivyo ni vyema wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki kampeni hiyo” alisema Dk Maghembe.Pia alisema kampeni ya unywaji wa dawa kinga hizo utahusisha watu wa jinsi zote kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea na kuwasisitiza wanawake kujitokeza kwa wingi kunywa dawa hizo kwa kuwa magonjwa hayo huwapata watu wa jinsia zote.Alisema ili kufanikisha suala hilo, vituo 923 vya huduma ya kudumu na 671 vya huduma za kuhama pamoja na mikoba 252 kwa kata na mitaa yote ya Jiji la Dar es Salaam vitatoa huduma hiyo, lengo ni kufikia asilimia 90 ya wananchi kwa mwaka huu pekee. Kwa upande wake, Makonda aliwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi kunywa dawa hizo ili kufanikisha kutokomeza magonjwa hayo katika Mkoa wa Dar es Salaam.Alisema kufanyika kwa kampeni hiyo kumelenga kutokomeza kabisa ugonjwa huo na malengo kwa mwaka huu ni kufikia asilimia mia huku akiahidi kuanzisha kampeni dhidi ya ugonjwa tezi dume kwa wananchi wa Jiji hilo. Alisema kuanzishwa kwa uchunguzi na tiba ya ugonjwa huo katika hatua ya kaya hadi kaya, kumelenga kutokomeza ugonjwa huo ambao siku za hivi karibuni umeonekana kuwakumba wananchi wengi nchini, wakiwemo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
kitaifa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa kesho Jumatatu atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya kitaifa ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (Umisseta) yatakayofanyika mjini Mtwara.Michezo hiyo itakayoshirikisha takribani washiriki 3,304 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na miwili Zanzibar, itafanyika hadi Juni 21 na kufungwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako.Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Idara ya Elimu (Tamisemi), Leonard Thadeo alisema jana kwa njia ya simu kuwa kila kitu kimekamilika na tayari yeye na timu yake wako Mtwara kwa ajili ya michezo hiyo.Alithibitisha kuwa Majaliwa ndiye atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michezo hiyo mwaka huu, ambayo itashirikisha michezo ya soka, netiboli, riadha, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mikono kwaya pamoja na ngoma.Aidha, Thadeo alisema kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ndiye atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Umoja wa Michezo ya Shule za Msingi (Umitashumta) utakaofanyika Juni 25 wakati wachezaji wataanza kuwasili siku mbili kabla.Alisema kuwa michezo ya Umitashumta yenyewe itashirikisha mikoa 26 ya Tanzania Bara tu na inatarajia kufungwa Julai 3 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo.Thadeo aliongeza kuwa lengo lao kubwa la kwanza ni kuwawezesha wanafunzi kucheza michezo, ambayo ni sehemu ya elimu na wale wanaohusika na kuendeleza vipaji wanatakiwa kuwaendeleza watoto hao.Alisema mfano shule za michezo na mashirikishi au vyama vya michezo kama Chaneta (Netiboli), TFF (Soka), TBF (Kikapu) Taha (Mpira wa Mikono), Tava (Wavu) na RT (Riadha), ndizo zenye majukumu ya kuwaendeleza vipaji vya watoto hao
michezo
LEO, Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kwa michezo mitatu katika viwanja tofauti ukiwemo ule utakaowakutanisha mabingwa mara 27 wa ligi hiyo, Yanga SC ambao watawaalika Mbao FC katika Uwanja wa Taifa.Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa Mei 22 mwaka jana katika uwanja huo huo ambapo Yanga walitoka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa dakika ya 22 na Thaban Kamusoko kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni.Yanga ina matokeo mazuri tangu kuanza msimu huu ambapo katika michezo yake mitano imeshinda minne na sare moja huku Mbao wakiwa wamecheza michezo minane wameshinda minne, sare mbili na kufungwa miwili.Kabla ya mechi za jana, Mbao walikuwa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 14, Yanga walikuwa nafasi ya nne na pointi zao 13.Mbao wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya matokeo mbaya kwenye mechi zao mbili mfululizo za ugenini, walitoka sare ya 1-1 na Coastal Union, Mkwakwani na kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting wakati Yanga ambao mechi zao zote wamecheza kwenye uwanja huo wakiwa na rekodi nzuri ya ushindi mara nne na sare moja.Yanga ndio wanaonekana kuwa wakali zaidi katika kufumania nyavu za wapinzani wao ambapo wamefunga mabao tisa na kufungwa manne tofauti na Mbao ambao wamefunga sita na kufungwa idadi sawa na Yanga.Mechi zingine zitakazochezwa leo ni kati ya Biashara United itakayokuwa nyumnbani kwenye Uwanja wa Karume, Mara kuwakaribisha wachimba madini wa Mwadui FC ambao wanaburuza mkia, nao Maafande wa JKT Tanzania watakabiliana na Alliance ambao wanashika nafasi yapili kutoka mkiani mwa msimamo.
michezo
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeingia katika ushirikiano na kampuni ya Samsung Mobile pamoja na kampuni ya usambazaji ya Yellow box kuzindua ingizo jipya la simu za kisasa aina ya Samsung A series.Airtel na Samsung imeingia ubia huo huku ikizindua OFA maalumu kupitia Samsung A10 na A2 core inayolenga kuwafaidisha wateja wake katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, alisema Airtel imeingia kwenye ushirikiano mpya na Samsung Mobile pamoja na Yellow Box kwa kuzindua simu za kisasa kwa lengo la kuongeza watumiaji zaidi wa huduma za intaneti kutokana na uhitaji wa wateja wetu”.“Kwenye ulimwengu wa kidijiti kwa jinsi ambavyo teknolojia inakua, Airtel tunaona ni vyema pia wateja wetu ambao ni muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara zetu kuendana na ukuaji huo. Katika msimu huu wa Saba Saba tunawaletea smartphone mpya kabisa za Samsung A series zenye ofa kabambe kupitia A10 na A2 core,” alisema Mmbando.Mmbando alisema hiyo ni fursa ya kipekee kwa wateja wa Airtel kujipatia simu mpya aina ya Samsung A series ikiwemo hii ya A10 na A2 core na kujipatia ofa ya bando ya 36GB kwa muda wa miezi 12 bure. Simu za Samsung A series na A10 na A2 core zitapatikana pia kwenye maduka yote ya Airtel Money Branch, maduka ya Airtel nchi nzima na katika maonesho ya Sabasaba.Naye Meneja Biashara wa Samsung Mobile, Suleiman Mohammed alisema ushirikiano baina ya Samsung na Airtel ni muhimu sana, kwani utakuza watumiaji wa simu za kisasa nchini.
kitaifa
MABONDIA Watanzania wametakiwa kujiaandaa vyema kabla ya kwenda kushiriki kwenye mashindano makubwa.Rai hiyo imetolewa baada ya mabondia wa Tanzania, Swedi Mohamed na Suleiman Said kupigwa kwa Knockout (KO) katika mapambano ya utangulizi kabla ya pambano la marudiano kati ya Andy Ruiz na Anthony Joshua lililofanyika nchini Saudi Arabia juzi.Akizungumzia mapambano hayo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBRC), Yahya Poli alisema mabondia ni vema kujiandaa kabla ya kukubali pambano kuepuka fedheha ya kupata kipigo.“Kupigwa katika ndondi ni kitu cha kawaida lakini tunaangalia umepigwa pigwaje, hivyo nawashauri mabondia kujiandaa vema kabla ya kukubali pambano kwani kufanya hivyo kunawajengea heshima,” alisema Poli.Swedi Mohamed alichapwa na Ivan ‘Hopey’ Price wa Uingereza katika raundi ya tatu kwenye pambalo la uzito wa Super Bantam na Suleiman Said alipigwa hadi akakaa raundi ya kwanza na Mmarekani Diego Pacheco katika uzito wa kati Katika usiku huo wa masumbwi Anthony Joshua alifanikiwa kurejesha mataji yake ya WBA, WBO, IBO na IBF baada ya kumshinda kwa pointi za majaji, 118-110 mara mbili na 119-109, Andy Ruiz.Joshua alipokonywa mataji yake ya WBA, WBO na IBF baada ya kupigwa na Ruiz kwa Knockout (KO) raundi ya saba katika pambano lililofanyika Juni mwaka huu ukumbi Madison Square, New York, Marekani.Ikumbukwe juzi bondia mwingine, Mtanzania, Bruno Tarimo ‘Vifua Viwili’ alifanikiwa kutwaa taji la IBF International uzito wa Super Feather baada ya kumshinda kwa pointi mwenyeji, Nathaniel May ukumbi wa ICC Exhibition Centre mjini Sydney, Australia.Bondia huyo mzaliwa wa Rombo, mkoani Kilimanjaro alimzidi mpinzani wake kwenye pambano hilo la raundi 10 na haikuwa ajabu kutangazwa mshindi jana.Hilo lilikuwa pambano la 28 kwa Tarimo tangu ajiunge na ngumi za kulipwa Desemba 25, mwaka 2013 akiwa ameshinda mara 25, mara tano kwa KO, amepigwa mara mbili zote kwa KO na droo moja.
michezo
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa chuo hicho, Profesa Mathew Luhanga, katika hotuba yake iliyosomwa na Profesa Eliuter Mageni katika mahafali ya 48 ya chuo hicho mwishoni mwa wiki.Alisema kwamba ufugaji wa nyuki ni eneo linalokua kwa kasi hapa nchini hivyo chuo hicho kinajipanga kutoa mchango wake kwa jamii katika eneo hilo.“Tayari elimu ya awali juu ya bidhaa za nyuki imeanza kutolewa kwa baadhi ya wanafunzi ndani ya chuo,” alisema Profesa Luhanga na kuongeza mitaala imezingatia utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali ambayo dhamira yake ni kufanya utafiti, kutoa huduma za ushauri na mbinu za kutafuta masoko na mitaji kwa wajasiriamali.Katika mahafali hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliyewakilishwa na Naibu wake, Gregory Teu, jumla ya wahitimu 2,272 katika ngazi za astashahada, stashahada na shahada ya uzamili walitunukiwa.Aidha, kulikuwa na wahitimu waliomaliza mafunzo ya lugha ya Kifaransa daraja la kwanza na wanane wa daraja la pili.Katika mahafali hayo, ambayo Desemba 14 yataendelea kwenye Kampasi ya Mwanza, Mkuu wa Chuo, Profesa Emmanuel Mjema aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoa ushirikiano katika kukiendeleza chuo kimuundombinu.
uchumi
CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimevishauri vyuo vikuu nchini kuona umuhimu wa kufundisha masuala ya mazingira, madini na mafuta katika mitaala yao, ili kuijengea jamii uelewa mpana katika maeneo hayo.Rais wa TLS, Dk Rugemeleza Nshala alisema hayo Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo, itasaidia kudhibiti mianya ya wizi kwa rasilimali hizo, huku jamii ikipata manufaa katika nyanja mbalimbali.Akizungumza kuhusu mafunzo ya rasilimali zinazokwisha, kwa mawakili wa serikali, binafsi, wadau wa mazingira na madini kutoka serikalini yaliyofadhiliwa na nchi ya Canada, Dk Nshala alisema uelewa kuhusu masuala ya madini ni mdogo kwa sababu vyuo vingi hapo awali vilikuwa havifundishi masuala hayo na kuhamasisha kwa sasa kubadilika na kufundisha. Alisema kwa sasa nchi ina miradi mingi ya uchimbaji mafuta na madini, hivyo ni vyema kuwajengea uwezo wa kielimu wananchi wake ili kuhakikisha nchi inanufaika na rasilimali zake.“Ni vyema kufanya jitihada za kuwajengea uwezo wa kielimu kuhusu masuala ya madini, mafuta na mazingira wananchi wetu ili waweze kufahamu haki zao na sheria zilizopo,” alisema Nshala na kuwataka wanafunzi pia kuona umuhimu wa kujikita katika maeneo hayo kwa manufaa ya baadae. Alisema ipo haja sasa kwa vyuo vingi hapa nchini kuanza kutoa elimu hiyo ili pengo la uelewa mdogo wa masuala ya mazingira na madini likazibwa.Nshala alisema Watanzania wanaoishi maeneo ya madini wakifahamu sheria, kupigania haki zao, majukumu ya serikali za vijiji yakatekelezwa itasaidia rasilimali zilizopo kutumika kwa manufaa ya jamii.Kwa upande wake, Mshiriki ambaye ni Mwanasheria kutoka Baraza la Mazingira (NEMC), Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Naomi Joshua, alisema mabadiliko ya sheria ya mazingira ya mwaka 2017 yamechagiza uwezo wa shughuli za kimazingira hasa katika sekta ya madini. Alisema NEMC imekuwa ikijitahidi kufuatilia miradi mbalimbali na kuangalia athari za kimazingira na namna ya utekelezaji kabla ya kuanzisha kwa mradi.“Wanaokwenda kinyume tumekuwa tukiwachukulia hatua na tutahakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika bila kuathiri mazingira,” alisema Naomi. Alisema mafunzo hayo ana imani yatawasaidia wanasheria wengi kufahamu mambo mbalimbali kuhusu mazingira, madini na mafuta kabla na baada ya kusaini mikataba ya uchimbaji madini. Mwanasheria wa Serikali, Godfrey Nyamsenda alisema, ni vyema kulinda na kuangalia masuala ya mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
kitaifa
MBUNIFU wa teknolojia ya umwagiliaji wa shamba kwa kutumia simu janja, Ramadhani Bakari kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, amebuni mfumo wa umwagiliaji unaomwezesha mkulima kumwagilia kwa kutumia simu ya mkononi akiwa ndani au nje ya nchi.Bakari ambaye ni Mhitimu wa Stashahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), chuoni hapo alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo na kuongeza kuwa ametumia simu janja yenye ‘application’ ambayo inawasiliana na mfumo maalum.Alisema mfumo huo unaunganishwa na pampu ya maji, mabomba na kifaa cha kieletroniki ambacho ndicho kinachosaidia mfumo kufanya kazi kupitia simu ya mkononi.“Unakwenda kwenye simu na ku download application inayoitwa Blwnk, ukiifungua utakutana na kitufe kinaitwa washa ukibonyeza tu hapo unakuwa unafanya mawasiliano na mfumo wako popote ulipo kwa kuwa unajiwasha na shamba linaanza kupata maji,” alisema.Alisema lengo la kubuni teknolojia hiyo ni kupunguza changamoto ya umwagiliaji kwa wakulima kwani wamekuwa wakiajiri watu au kutumia nguvu kazi kubwa mashambani. Pia kuzuia upotevu wa maji unaweza kufanywa na wafanyakazi wazembe.Alisema utafiti huo upo katika hatua ya kujifunzia, Ulianza mwaka jana, na kwamba ukiendelezwa teknolojia hiyo inaweza kufanya kazi hadi kumwagilia eka 10. Naye Mkuu wa Idara ya Masomo ya Elimu ya Juu chuoni hapo, Dk. Philip Daninga alisema chuo kinafundisha Tehama ili wanafunzi waweze kujiajiri pale wanapomaliza masomo yao pasipo kutegemea kuajiriwa kwani ajira zimekuwa ni changamoto.Dk. Daninga alisema ulimwengu wa sasa unategemea Tehama hivyo chuo kinahakikisha kozi zinazofundishwa zinamsaidia mwanafunzi akimaliza aweze kuzifanyia kazi kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuwa mbunifu anayeweza kuangalia mazingira yanayomzunguka na kubuni kitu.Dk. Daninga alisema kijana anapokuwa mbunifu inakuwa rahisi hata kupata ajira hivyo kama chuo wamekuwa wakihusisha mitaala kwa namna ambayo mwanafunzi anapomaliza masomo yake anakuwa na uwezo wa kujiajiri.
kitaifa
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewakumbusha wananchi kudai risiti sahihi kila wanapofanya manunuzi ya bidhaa, la sivyo haitasita kuwatoza faini na hata kuwashitaki mahakamani.Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee alisisitiza hilo alipozungumza na HabariLeo jijini hapa juzi kuhusu wajibu wa mnunuzi wa bidhaa katika kuwezesha upatikanaji wa kodi za serikali.“Kutodai risiti sahihi wakati wa manunuzi ya bidhaa ni kushiriki kukwepa kodi, ndio maana sasa tumeanza kutoza faini ya Sh 30,000 hadi Sh milioni 1.5 kwa mtu anayebainika kukwepa wajibu huo wa kisheria,”alisema.Kwa upande mwingine, mfanyabiashara anayebainika kufanya mauzo bila kutoa risiti sahihi hutozwa faini ya Sh milioni tatu hadi milioni 4.5 na kushitakiwa mahakamani anaporudia kukwepa kodi kwa mbinu hiyo.Hatua hizo za TRA ni sehemu ya kusimamia utekelezaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) wakati wa mauzo na manunuzi ya bidhaa mbalimbali.Dundee ametaja faida kuu za kutoa na kudai risiti kila yanapofanyika manunuzi ya bidhaa kuwa ni kutunza kumbukumbu za msingi za kuthibitisha bidhaa au mali na uzalendo wa kushiriki katika kuwezesha upatikanaji wa kodi halali za serikali.Faida nyingine ni kuongeza uwajibikaji ambapo kwa mfano, kumbukumbu husaidia TRA kufanya makadirio sahihi ya kodi na mlipakodi kupata haki stahiki ya kikodi ikiwemo ya unafuu unaotokana na sheria za kodi.Aidha, mfanyabiashara huweza kufanya manunuzi sahihi ya kuendeleza biashara kutokana na kumbukumbu alizonazo ikiwa ni pamoja na kuboresha biashara, kuomba mkopo wa fedha na kuweka mipango endelevu.Kutoa risiti pia kunamsaidia mfanyabiashara kuimarisha na kujiongezea fursa za kibiashara ikiwemo kupata zabuni mbalimbali kutoka kwa wateja wakubwa ambao ni serikali na taasisi zake, kampuni, mashirika yasiyo ya serikali (NGOs) na wafanyabiashara wakubwa.Makisio ya mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 ni Sh trilioni 32.9 zikiwamo trilioni 18 zinazotarajiwa kukusanywa na TRA kutokana na kodi mbalimbali.
uchumi
OFISI ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira mkoani Lindi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 200 kwa vikundi vya uzalishaji mali vya vijana tujiajiri 53 kwa nyakati tofauti.Vijana hao wanatoka vikundi vya uzalishaji vilivyoko katika halmashauri sita za wilaya za Kilwa, Liwale, Nachingwea, Lindi, Ruangwa na Manispaa ya Lindi mkoani humo. Ofisa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira kutoka makao makuu mkoani Dar es Salaam, Atupokile Mhalila alisema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na vikundi mbalimbali vya uzalishaji.Mhalila alisema mikopo hiyo imegawanyika katika sehemu kuu mbili, kwanza kuanzisha miradi na pili kuendeleza vijana wanaounda makundi hayo. Mhalila alisema lengo kuu ni kuwanyanyua vijana kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili iwawezeshe kujiajiri wenyewe na kupata kipato kwa kuanzisha viwanda vidogo. Alisema kila kikundi kinakuwa na vijana kumi na hupewa mkopo baada ya kuomba mradi wanaotaka kuufanya na kuutekeleza.Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Lindi, Iddi Maketa alisema kuwa wizara ya nchi, ofisi ya waziri mkuu inayoshughulikia sera, kazi, bunge, ajira na vijana ilitoa mikopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kiasi cha Sh milioni 90 kwa vipindi tofauti, navyo ni 2014/15, 2016/17 na 2018. Alisema vikundi vya hapa mjini vinajishughulisha kuongezea thamani mbao kwa kutengeneza samani za viti, vitanda na aluminium kwa madirisha, ya vioo na uchomoleaji wa milango ya vyuma pamoja na madirisha yake.Abdul Said kutoka kikundi cha Mshikamano cha kata ya Wailes mjini hapa aliishukuru serikali kwa kuwapa mkopo wa Sh 3,000,000 na uliwawezesha wanachama watano. Alisema walitumia fedha hizo kununua mashine za kuchomea na vifaa vinginevyo vya mradi wao wa kikundi hicho na kutoa ushauri kwa serikali badala ya kutoa fedha za mkopo wakopeshe vifaa vya kufanyia kazi siyo kutoa mkopo wa fedha.
kitaifa
USHINDI wa Azam FC wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa juzi, ni salamu kwa Yanga kuwa wako tayari kupambana kuelekea katika mchezo utakaowakutanisha kesho.Azam FC ilishinda mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuatia Uwanja wao wa Azam Complex, kuwa katika matengenezo ambao mabao yalifungwa na Shaban Chilunda na Joseph Mahundi.Wakati wanalambalamba hao wa Chamazi wakifurahia ushindi huo, Yanga walikula kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar hivyo huenda mchezo wa kesho ukawa mgumu kwao.Akizungumzia ushindi katika mchezo huo , Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema walifanikiwa kujua mapungufu ya Lipuli ndio maana walipata matokeo mazuri.“Nashukuru Mungu wachezaji walipewa maagizo nini cha kufanya, mchezo ulikuwa mgumu mwanzo mwisho ila tulipata pointi tatu kwa sababu tulitumia mapungufu yao kuwaadhibu,” alisema.Naye Kocha wa Lipuli, Julio Ellieza alisema kilichowagharimu wakafungwa ni kwa sababu walifanya makosa na walipambana kwa uwezo wao ila bahati haikuwa yao.“Tumefanya makosa wametuadhibu, tulipambana kadiri ya uwezo wetu lakini imeshindikana, naamini makosa yaliyojitokeza tutaenda kuyafanyia kazi ili tufanye vizuri katika michezo inayokuja,” alisema.
michezo
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada katika hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G pamoja na huduma za kibenki kwa njia ya simu kutoka kampuni ya Zantel.Alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na sekta za mawasiliano na fedha, lakini bado ipo changamoto kubwa ya kuyafikia maeneo mengi yanayohitaji kuboreshewa huduma hasa upatikanaji wa huduma hizo vijijini.“Nafurahi kuona kuwa Zantel na Benki ya watu wa Zanzibar imeanza vizuri katika hili katika kuhakikisha mnakuwa mstari wa mbele kuisaidia Serikali kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi wake,” alisema Ahmada.Alisema serikali itaendelea kuhakikisha huduma za kifedha kwa pamoja na mawasiliano zinawafikia Wazanzibari wote kwa urahisi kabisa.Alisema katika kuhakikisha hilo linafanyika Serikali ya Zanzibar imeendelea kufanya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu hasa barabara, njia za mawasiliano na utengenezaji wa sera zilizo stahiki pamoja na kupigana na umasikini na ukosefu wa elimu kwa wananchi wa Zanzibar.Kuhusu huduma ya kibenki, alisema mteja wa Zantel atajipatia huduma mbalimbali za kibenki kwa njia ya simu kama vile kuweka na kutoa fedha, kulipia ankara za huduma mbalimbali kama vile maji, umeme au kununua vocha za simu, na hata kupata mikopo ya benki ambapo huduma hizo zote zinazingatia kanuni na misingi ya Kiislamu.Alitoa mwito kwa wananchi wa Pemba kuchangamkia fursa hizo adimu kutoka Zantel ambao wanashirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar ili kuendelea kujipatia maendeleo.Aitoa rai kwa uongozi wa Zantel na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kuhakikisha kuwa wananchi wa Pemba wanapata huduma hizo kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na kampuni hiyo katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wao.
uchumi
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haikusudii kuiondoa Kampuni ya Fastjet kufanya kazi zake nchini, badala yake inatakiwa kufuata masharti ya sheria za uendeshaji wa shughuli za usafiri wa anga ili kuepusha madhara, ikiwamo ajali.Kuhusu Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet, Lawrence Masha kujichagua kuwa Meneja Uwajibikaji, imeelezwa kuwa, kwa mujibu wa sheria, Meneja Uwajibikaji anapaswa kuwa na utaalamu wa masuala ya ndege na matengenezo.Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, Dar es Salaam jana kutokana na kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mamlaka hiyo inalenga kuwaondoa Fastjet na kuipendelea ATCL.Taarifa hizo zilisambazwa kwenye mtandao wa Jamii Forums, pamoja na mazungumzo ya Mwenyekiti huyo Mtendaji wa Kampuni ya Fastjet, Masha kupitia kipindi cha Amka na BBC cha Shirika la Utangazaji la Uingereza. Johari alisema TCAA haiipendelei Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kuionya Fastjet kuwa isipokuwa makini katika kipindi hiki cha notisi ya siku 28, itakufa endapo hawatafanyia kazi upungufu wao. Aidha, imekiri kupokea barua pepe kutoka kwenye Kampuni ya Fastjet kuomba kuleta ndege mbili zenye usajili wa Afrika Kusini, andiko kuhusu uwezo wao kifedha kufanya biashara hiyo na barua ya kumtaja Meneja Uwajibikaji.Johari alisema wanataka kila shirika la ndege kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na kwamba hawana lengo la kuua mashirika hayo, kwa sababu wanataka ushindani wa kibiashara. Alieleza kuwa kazi ya kurusha ndege angani ikiwa na abiria ni hatarishi, hivyo ili kuhakikisha usalama wa abiria kuruka na kufika salama, inahitaji fedha pamoja na meneja uwajibikaji ambaye ana uelewa wa uendeshaji wa ndege, matengenezo na uzoefu wa menejimenti.Alisema Desemba 2008 iliifungia ATCL mpaka Januari 6, 2009 ndio ilikamilisha taratibu za kisheria na kuruhusiwa kuendelea na biashara hiyo, hivyo kitendo wanachokifanya ni kwa sababu sheria imewapa mamlaka hayo. Mkurugenzi huyo alisema Desemba 17, mwaka huu walitoa taarifa kwamba Fastjet imepoteza sifa kwa mujibu wa sheria pamoja na mabadiliko baada ya Waingereza kujitoa kuwekeza fedha katika kampuni hiyo.Alifafanua kuwa baada ya kuuzwa kwa hisa na wazawa kuchukua kampuni hiyo, kwa mujibu wa sheria inawataka ndani ya siku 14 kueleza kilichojiri ikiwemo uwezo wa kifedha kwa sasa, kumtaja Meneja Uwajibikaji baada ya aliyekuwepo kujitoa. “Fastjet mpaka sasa bado inadaiwa na mamlaka hii Dola za Marekani 156,000, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inawadai shilingi bilioni 2.1, Kampuni ya Swissport inadai shilingi bilioni 2.1, Kampuni ya EYACO ya Mwanza inadai shilingi bilioni 1.1 na Kampuni ya Maendeleo ya Uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KADCO) inadai shilingi milioni 286.Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (1) (cha sheria ya mamlaka ya anga) kinaelekeza kwamba madeni yote yanayodaiwa kwa shirika yalipwe ndipo usajili ufutwe,” alisisitiza. Johari alieleza baada ya kutoa notisi hiyo, Fastjet iliwalipa TCAA Sh milioni 760 na Dola za Marekani 54,000 huku watoa huduma wengine wakiwa wanawadai, na kwamba ni matakwa ya sheria kulipa madeni hayo hivyo walizuia ndege zao ambazo zilitakiwa kurudishwa kwa mtu aliyezikodisha ili kufidia madeni.Kwa mujibu wake, hawakuizuia Fastjet kuingiza ndege nchini kwa sababu wanachotaka ni ushindani kwenye mashirika ya ndege na kwamba hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kuleta ndege mbili aina ya Boeing 737- 500. Alisema katika maelezo yao wameeleza kuwa wataleta ndege hizo na mojawapo ni ile waliyoizuia kufanya kazi zake, pia waliandika maelezo ya fedha za kuendesha biashara kwa mujibu wa kifungu cha 25 (1) cha udhibiti uchumi cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Anga, na kupeleka barua ya kumchagua Masha kuwa Meneja Uwajibikaji.Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu Masha kujichagua kuwa Meneja Uwajibikaji, Johari alisema kwa mujibu wa sheria, Meneja Uwajibikaji anapaswa kuwa na utaalamu wa masuala ya ndege na matengenezo na kwamba watapitia maelezo yake kuona kama anastahili au la. Pia alisema watapitia andiko kuhusu masuala ya fedha na kama hawatakidhi vigezo vyote vya kisheria hawatawasaidia kwa sababu wanaweza kusababisha ajali.Alisisitiza kuwa kabla ya mzawa kuchukua kampuni hiyo alishauriwa ni vitu gani anatakiwa kufanya na serikali inamsaidia mwekezaji kwa kumtaka afuate sheria na taratibu zilizowekwa. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alisema TCAA inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, na sio lengo la kuondoa kampuni binafsi kufanya kazi hizo. Simbeye alisema mwaka 2015 sekta binafsi walivyokutana na Rais John Magufuli moja ya maelekezo aliyoyatoa ni sekta binafsi kuwekeza kwa wingi kwa kufuata sheria na kulipa kodi. Aliongeza kuwa ni lazima wawekezaji wazawa kufuata sheria kwa sababu hakuna nchi inayofanya uwekezaji bila kufuata sheria. Jana, vyombo vya habari hasa magazeti yalimkariri Masha mwenye asilimia 68 ya hisa za Fastjet Tanzania, akiiomba TCAA imruhusu kuingiza ndege kisha kulipa madeni baada ya kufanya biashara. Alisema madeni hayo aliyakuta baada ya kununua hisa za kampuni hiyo ya usafiri wa anga.
kitaifa
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema udanganyifu ni tatizo kubwa linalokabili mfuko huo na kwamba hadi sasa wameweza kuokoa Sh bilioni 4 ambazo zingeliwa na wajanja kwa udanganyifu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga kwenye kikao cha mfuko huo na wahariri, kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam juzi. Mbinu zinazotumika katika udanganyifu huo ni baadhi ya watoa huduma kuongeza gharama za matibabu kwa wenye kadi za NHIF, au kutumia kadi za NHIF kujipatia fedha katika maduka ya dawa au kuchelewesha kuwapatia huduma wenye kadi za NHIF ili baadaye kufanya udanganyifu. Ili kupambana na udanganyifu huo, Konga alisema kwanza wameanzisha kitengo cha kupambana na udanganyifu (fraud) na kina wataalamu mbalimbali, wakiwamo madaktari. Pili, wameamua kushirikisha taasisi za uchunguzi kupambana na udanganyifu huo, kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Polisi na vyombo vya usalama.Tatu, aliviomba vyombo vya habari kusaidia kuweka wazi tatizo hilo kwa jamii ili wananchi na watoa huduma waepukane nalo. Kuhusu idadi ya wanachama walio nao, Konga alisema NHIF imejipanga kuongeza wanachama kutoka asilimia 32 ya sasa hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2020 na baadaye kuwezesha Watanzania wote kunufaika na bima ya afya.Aidha, alisema mfuko huo umetoa mikopo mingi ya vifaa tiba, dawa, vitendanishi na ukarabati wa majengo. Alizungumzia pia suala la utafiti, ambapo alisema NHIF inaendelea kufanya utafiti ili kuongeza vifurushi, huduma na vituo vinavyohitajika. Pia, alisema wanafanya utafiti wa programu mpya ya Tehama, itakayowezesha wateja kujua aina ya dawa, matibabu na gharama zake. Alisema NHIF imeingia mkataba na vituo 7,000 nchini vya kutolea huduma na vingi ni vya serikali. Aidha, wahariri hao walisimama kwa dakika moja, kukumbuka kifo cha aliyewahi kuwa Meneja Mawasiliano wa mfuko huo, Rehani Athumani kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa miaka mingi kwa mfuko huo.
kitaifa
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 2:00 usiku.Ni mchezo mgumu na muhimu kwa timu zote kushinda kwani atakayepata matokeo mazuri ndiye atakayesonga mbele hatua ya nusu fainali. Azam Complex inapewa nafasi ya kusonga mbele kutokana na sababu zifuatazo.Mara nyingi inapocheza kwenye uwanja wa nyumbani hupata matokeo mazuri lakini pia, timu hiyo bado ipo kwenye kiwango bora kwani ipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi.Kadhalika, Mtibwa Sugar ina nafasi kutokana na kwamba ni timu isiyotabirika kwani mwanzoni mwa msimu huu raundi ya kwanza walionekana wako vizuri kiasi cha kuzitisha timu kubwa ingawa baadaye walikuja kuanguka na kushuka.Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.Hivyo, yeyote ana nafasi kutokana na namna atakavyojiandaa.Katika mechi sita tofauti kwa kujumuisha ligi na FA kwa timu zote, kati ya hizo kwa upande wa Azam imeshinda nne na kupata sare mbili huku Mtibwa kwa idadi hiyo ya mechi, ikishinda mchezo mmoja pekee, ikifungwa nne na kupata sare moja.Kwa kutizama matokeo hayo inaonesha ni jinsi gani Azam wako vizuri kuliko Mtibwa ingawa hata hivyo, dakika 90 ndizo zinazoweza kutoa mshindi. Mchezo mwingine utakaochezwa leo ni Tanzania Prisons wakiikaribisha JKT Tanzania kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.Prisons wana nafasi ya kusonga mbele kwa maana kama wataweza kutumia uwanja wa nyumbani vizuri lakini pia, ni miongoni mwa timu zilizoonesha kiwango bora msimu huu ikiwa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.Hata JKT ina nafasi ya kufanya vizuri kwani ina kocha mzoefu wa ligi, Bakari Shime ambaye aliiongoza timu hiyo kupanda Ligi Kuu msimu huu ikiwa ni miongoni mwa timu zilizotikisa Daraja la Kwanza msimu huu.
michezo
MCHUNGAJI wa Kanisa la Gospel Revival Center (GRC), lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ amewataka Watanzania kumpa muda Rais John Magufuli katika kazi yake ya kuliunganisha taifa na kuleta maendeleo na kwamba watahoji utendaji wake mara baada ya kutoka madarakani.Amesema kuwa demokrasia ipo nchini na kwamba endapo serikali itaruhusu kufanyika kwa maandamano ya mara kwa mara hakutakuwa na nchi ya amani kama ilivyo sasa.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mchungaji Lusekelo amesema kutokana na miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi ambazo wananchi wake watakuwa na maisha mazuri.Alisema Rais Magufuli amesaidia kuipeleka nchi mahali salama katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio ya ujambazi nchini.Alisema kuwa baada ya kuingia madarakani, hakuna udini, ukanda wala ukabila na badala yake watoto wa masikini wanasomeshwa kupitia kodi za matajiri ambazo wanalipa kutokana na biashara mbalimbali.‘’Sio kwamba najipendekeza kwa kutaka Ukuu wa Wilaya au Mkoa lakini nataka kuwaambia kuwa siwezi kuona aibu kusema mema anayoyafanya kiongozi wowote kwani hata katika maandiko matakatifu yanatuelekeza kuwa ni mwiko kumsema vibaya mkuu wa nchi yako,’’ alisema Lusekelo.Aliongeza kuwa ni lazima apewe nafasi afanye kazi kwa mujibu wa sheria, katiba, mila na desturi za Kitanzania na kwamba watamhoji utendaji wake baada ya kukamilisha uongozi wake kama wanavyofanya kwa viongozi waliopita.Alifafanua, Rais amehakikisha kunakuwapo muungano imara wa Tanganyika na Zanzibar ambao haupaswi kufanyiwa biashara wala kugusa misingi yake, na badala yake kama kuna maboresho wanapaswa kuzungumza kwa hekima.Pia alisema yapo mabadiliko makubwa yanaendelea kufanyika nchini ikiwemo masuala ya usafiri wa anga kwa kusaidia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuwa na ndege nane na kutumia fedha za ndani kununua zao la korosho.‘’Tungepata Magufuli kama 30 hivi nchi ingenyooka lakini tunapaswa kusema asante kwa kiongozi huyu kwa sababu ndiye ambaye Mungu ametuletea. Mnaweza msione matokeo ya uongozi huu kwa saa lakini baadaye mtasema asante Yesu,’’ alisisitiza mchungaji huyo.Akijibu maswali ya waandishi kuhusu demokrasia nchini, Lusekelo alisema kuwa kwa mara ya kwanza alishuhudia Watanzania milioni sita wakiwapigia kura wapinzani na kwamba wapo wabunge na madiwani wengi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na vyama vingine.Alieleza uwepo wa wawakilishi hao wa vyama vingi inamaanisha kuwa demokrasia ipo na hivyo ni lazima kuwepo wakati wa kusema na kunyamaza na wakati wa kusema na kutekeleza mambo mbalimbali.
kitaifa
Waziri Mwakyembe ametoa ojnyo hilo mjini Kigoma wakati anafunga mafunzo ya ngazi ya chini (Grass Root) ya ualimu wa mpira wa miguu kwa walimu kutoka shule za msingi na sekondari, ikiwa ni programu ya kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini.Alisema amekuwa akipitia video zilizofungwa katika uwanja huo na kuona baadhi ya watu wakionekana kunyunyuzia dawa kwa maana ya kuroga ili kupata ushindi na kusema kuwa vitendo hivyo lazima vikomeshwe na adhabu kali zitatolewa.Waziri huyo wa michezo alisema kuwa sambamba na viongozi wa klabu na wapenzi wao pia serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya soka watakaojihusisha na vitendo hivyo ikiwemo kusafiri na waganga nje ya nchi kwa nia ya kupata ushindi.Aidha Waziri huyo alisema kuwa serikali inasikitishwa na kilio cha gharama kubwa ya kuingiza vifaa nchini kinachotolewa na uongozi wa TFF na kwamba ameamua kulisimamia jambo hilo kwa kulifikisha kwa Waziri wa Fedha ili kuona namna ya kusaidia kuondoa kodi katika uingizaji wa vifaa vya michezo nchini.Alisema, vifaa ni muhimu katika mazoezi na maandalizi ya michezo na kwamba kilio cha muda mrefu katika hilo lazima kipatiwe ufumbuzi sasa kwa kulifikisha jambo hilo kwa Waziri wa Fedha na kumshauri namna ya kulishughulikia.
michezo
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amekuwa mbogo kwa watendaji wanaochelewesha ugawaji na usambazaji vitambulisho vya wajasiriamali katika maeneo yao mkoani humo. Dk Mahenge alisema hayo baada ya kutembelea halmashauri mbalimbali, kukagua namna vitambulisho hivyo vilivyotolewa kwa wajasiriamali na Rais John Magufuli Desemba 10, mwaka jana vinavyosambazwa kwa wajasiriamali wadogo. Hali ya usambazaji au ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali katika halmashauri hizo mkoani humo, haujashika kasi kubwa, hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ili kufikia lengo la kukamilisha vitambulisho hivyo. Mkuu wa Mkoa alifanya ziara katika halmashauri za Chamwino, Kongwa, Kondoa na ziara bado inaendelea katika maeneo mengine ili kuhakikisha usambazaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo unakamilika mapema. Akiwa katika ziara wilayani Kondoa, Dk Mahenge aliwataka watendaji kuharakisha usambazaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi na viongozi wanatakiwa kuhamasisha wananchi kuvichukua. Alitawaka watendaji kuongeza kasi kugawa vitambulisho lakini kusimamia na kuhakikisha kwamba wajasiriamali wasio na vitambulisho hivyo hawaruhusiwi kufanya biashara au shughuli zozote. akiwa wilaya ya Chamwino, Dk Mahenge alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athuman Masasi kuharahakisha usambazaji wa vitambulisho hivyo vya wajasiriamali, badala ya kufanya kazi bila kuwa na vitambulisho. Mkuuu wa Mkoa wa Dodoma alikabidhiwa na Rais Magufuli vitambulisho vya wajasiriamali 25,000, ambavyo alivigawa katika halmashauri zake kwa uwiano wa wingi wa idadi ya watu katika wilaya hiyo. Katika mgawanyo huo, Jiji lilipata vitambulisho 5,000, Chamwino 4,000, Kongwa 3,750, Mpwapwa 3,500, Bahi na Chemba zote zilipata vitambulisho 2,750 kila moja, Kondoa Mji 2,500 na Kondoa Vijijini 750. Vitambulisho vilivyogawiwa Dodoma ni sehemu ya vitambulisho vya wajasiriamali 670,000 nchini alivyovigawa Rais Magufuli kwa wakuu wa mikoa Desemba 10, mwaka jana. Vitambulisho hivyo jijini Dodoma vinatolewa katika jengo la bima, Chamwino katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Bahi katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Kondoa katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Kongwa katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Mpwapwa katika engo la ofisi ya mkuu wa wilaya na Chemba katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya.
kitaifa
SIMBA, leo inatarajiwa kukabidhiwa taji lake la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya mechi dhidi ya Biashara United itakayofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mechi hiyo ni ya 37 kwa Simba ambayo imeshatangaza ubingwa tangu wiki iliyopita ilipoifunga Singida United mabao 2-0 na kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume Musoma, Simba ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Biashara hivyo ni kazi kwao kuendeleza ubabe dhidi ya timu hiyo ngeni kwenye Ligi Kuu au Biashara kupindua matokeo ili kujiweka salama zaidi kubaki msimu ujao.Ugumu wa mechi ya leo unatokana na Simba kutana kukabidhiwa kombe lake kwa heshima kwani msimu uliopita ilikabidhiwa kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja huohuo wa Taifa, hivyo haitakubali kurudia kosa, huku Biashara ikitaka ushindi kujiweka vizuri zaidi kubaki msimu ujao.Biashara wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa wanashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 43 na kumbukumbu ya kutoka kuibuka na ushindi kwenye mchezo ulipita kwa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting.Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kubeba ubingwa haimaanishi kwamba kazi imeisha hivyo wanahitaji ushindi katika michezo yote iliyosalia ili watwae ubingwa na pointi nyingi. Katika hatua nyingine kocha huyo amezungumzia mechi dhidi ya Sevilla waliyofungwa mabao 5-4 juzi akisema alilazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa lengo lakuwapa wachezaji fursa kutengeneza historia ya kucheza na timu kubwa.Alisema kila mchezaji alikuwa anahitaji kucheza na timu hiyo kubwa inayocheza ligi kubwa hivyo aliona ni busara kila mmoja acheze kwa kuwa ushindi haukuwa kipaumbele chao zaidi ya kuwapa wachezaji fursa wapate changamoto ya kujifunza. Kocha huyo amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mashabiki waliojitokeza kuisapoti timu hiyo kulitupia lawama benchi la ufundi kwa kufanya mabadiliko yaliyopelekea kikosi hicho kupoteza mchezo.
michezo
['Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar.', 'Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban.', 'Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa ziada Rami Bedoui kujifunga kupitia kichwa dakika za lala salama alipogusa mpira kwa mara ya kwanza.', 'Wakati huohuo Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Mali 1-0 ili kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon.', 'Mshambuliaji huyo wa Crystal Palace ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal aliufukuza mpira wa adhabu uliopigwa na Sylvain Gbohouo na kuupata kabla ya kipa Djigui Diarra. ', 'Mali ilikuwa imepoteza nafasi chungu nzima kupitia Moussa Marega na Moussa Djenopo, wote wakikosa nafasi nzuri baada ya pasi safi. ', 'Ivory Coast sasa itacheza dhidi ya Algeria katika mechi ya robo fainali siku ya Alhamisi. ', 'Ndovu hao wameibuka washindi wa komnbe hilo mara mbili mwaka 1992 na 2015 lakini walisonga mbele katika raundi ya muondoani wakiwa katika nafasi ya pili baada ya kushindwa 1-0 na Morocco. ', 'Tunisia ilikuwa inaongoza kupitia goli la mshambuliaji wa IsmailiaTaha Yassine Khenissi aliyepata krosi nzuri kutoka kwa Wajdi Kechrida.', 'Mshambuliaji wa Leeds Ekuban ndiye mchezaji wa pekee aliyekosa mkwaju wake katika penalti hizo huku Ferjan Sassi akifunga goli la ushindi. ', 'Tunisia sasa itakabiliana na Madagascar iliopo katika nafasi ya 108 duniani siku ya Alhamisi licha ya kutoshinda mechi hata moja katika dakika 90. ', 'Mwewe hao walitoka sare mechi zao zote tatu kabla ya mikwaju hiyo ya penalti dhidi ya Ghana. ', 'The Black Stars walitawala kipindi cha mwanzo cha mchezo huku shambulio la kichwa la Nuhu Kassim likigonga mwamba wa goli. ', 'Walipata bao la kwanza lakini likakataliwa . Thomas Partey alimpigia pasi Jordan Ayew ambaye naye alitoa pasi murua kwa nduguye Andre na kufunga kupitia kisigino. ', 'Refa aliamuru kwamba Partey alikuwa ameunawa huku refa wa kutumia Video VAR akitarajiwa katika mechi za robo fainali, lakini kiungo huyo wa Atletico alikuwa ameuzuia mpira huo kwa kifua. ', 'Tunisia ilitawala mechi wakati Wahbi Khazri ambaye alikuwa na jeraha alipoingia kunako dakika ya 68. ', 'Muda mfupi baadaye kona yake iligonga mwamba wa goli kupitia kichwa cha Khenissi. ', 'Hatahivyo bahati ya Tunisia ilisimama wakati Khazri alimpigia pasi ya kisigino Kechrida ambaye krosi yake ilifagiliwa hadi wavuni na Khenissi. ', 'Shambulio la kiungo wa Ghana Mubarak Wakaso lilipanguliwa kabla ya kuchangia katika bao la kusawazisha. ', 'Beki Bedoui aliingia katika nafasi ya Khenissi katika dakika ya mwisho ili kuongeza ulinzi-lakini alifunga mkwaju wa adhabu wa Wakaso hadi wavuni mwa goli la Tunisia. ', 'Pande zote mbili zilikuwa na fursa dakika za lala salama -lakini zilishindwa kuzitumia hivyobasi mechi ikaishia kuamuliwa kupitia mikwaju ya penalti.']
michezo
KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emanuel Amunike ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachocheza na Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) mchezo utakaochezwa Septemba 8 kwenye Uwanja wa Namboole Kampala, Uganda.Akizungumza jana, Amunike alisema timu hiyo itaingia kambini Agosti 27 na kwa kushirikiana na wasaidizi wake kocha Emeka Amadi na Hemed Morocco watajitahidi kufanya kile ambacho Watanzania wanatarajia. “Najua Watanzania wana imani na sisi na mimi ni sehemu ya Tanzania kwa sababu ninakula chakula cha hapa na ninakunywa maji ya hapa, hivyo tutajitahidi kuhakikisha timu inafanya vizuri ila siwezi kusema tutafanya maajabu,” alisema Amunike.Kikosi kilichoitwa ni makipa Aishi Manula (Simba), Mohammed Adbulrahman (JKU) na Benno Kakolanya (Yanga). Walinzi ni Shomari Kapombe (Simba), Hassan Kessy (Nkana FC Zambia), Gadiel Michael (Yanga), Kelvin Yondan (Yanga), Abdi Banda (Baroko FC Afrika Kusini), Aggrey Morris (Azam FC) na Andrew Vicent (Yanga).Viungo wakabaji ni Himid Mao (Petrojet Misri), Mudathir Yahya (Azam FC), Jonas Mkude (Simba) na Erasto Nyoni (Simba) Viungo washambuliaji ni Simon Msuva (Al Jadida Morocco), Shiza Ramadhani (Simba) Rashid Mandawa (DBF Botswana), Hassan Dilunga (Simba), Feisal Salum (Yanga) na Farid Mussa (Tenerife Hispania) Washambuliaji ni Mbwana Samatta (Genk KRC Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (Al Hilal Sudan), Shaban Idd (Tenerife- Hispania), Yahya Zayd (Azam FC) na John Bocco (Simba) Kwa sasa Uganda Cranes inaongoza Kundi L ikiwa na pointi tatu baada ya kuifunga Cape Verde bao 1-0 na Tanzania na Lesotho zina pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani. Amunike amesema kwamba katika kukinoa kikosi hicho, atasaidiwa na Mnigeria mwenzake, Emeka Amadi pamoja na Mzalendo, Hemed Suleiman ‘Morocco’.
michezo
Aidha kampuni hiyo iliyopo chini ya Kampuni ya Toyota Tanzania Limited imeamua kupunguza bei ya pikipiki zake aina ya Yamaha kwa lengo la kuwavutia vijana wengi na kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda ambayo imesaidia vijana wengi kujiajiri na kuepuka kujitumbukiza kwenye matukio ya uhalifu.Meneja wa kampuni hiyo tawi la Arusha, Meetal Shah alisema kampuni yake imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kuchangia ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda.“Tunachokifanya ni kuwaunganisha wateja wa pikipiki wasio na fedha taslimu na benki ambazo zimekubali kuwakopesha kwa riba nafuu na sisi kama Kampuni ya City Motors tutawapatia pikipiki na benki ndiyo itakayotulipa sisi, ’’alisema Shah.Kwa upande wa waendesha pikipiki, John Jumanne (39) mkazi wa Sombetini aliyepatiwa pikipiki aina ya Yamaha kupitia mpango huo, ameishukuru kampuni hiyo ya City Motors kwa kueleza kuwa kabla ya hapo alikuwa akiendesha pikipiki ya mtu kwa makubaliano ya kumlipa Sh 7,000 kwa siku na hivyo kujikuta akibakiwa na fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kutunza familia yake.
uchumi
MSIMU mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa rasmi Tanzania katika hafla iliyofanyika klabu ya burudani ya Lifepark Mwenge mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkurungezi Mkuu wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios amekiri kufurahishwa na vipaji na uwezo wa wasanii Watanzania watakaoshiriki kwenye msimu huu mpya. Tanzania itawakilishwa na wasanii tano watakaotumbuiza katika msimu wa sita wa Coke Studio.Mkurugenzi wa mauzo na masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa, aliwatambulisha wasanii watakaowakilisha kwenye msimu huo ni Faustina Charles’ Nandy’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Juma Jux na Mimi Mars.Amesema wasanii hao wataungana na wasanii wengine 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kutimiza idadi ya wasanii 25.“Nchi nyingine msanii huchukuliwa mmoja lakini kwa Tanzania imekuwa tofauti kidogo, hii yote inaonesha ni namna gani muziki Watanzania yaani bongo fleva umekuwa ukikubalika na wasanii wake kupendwa,” amesema.Kwa upande wao wasanii akiwemo Rayvanny alishukuru kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika msimu huu huku akieleza hii ni mara yake ya pili.Nandy amesema “kushiriki Coke Studio kunakusaidia kukutana na wasanii kutoka Afrika wenye vipaji lukuki... nafasi hii kwa msanii yeyote ni kitu cha kujivunia sana na pia inasaidia kutengeneza kazi tofauti na kufanya jina au brand ya msanii kuimarika na nguvu katika soko la muziki Afrika na dunia nzima.”Jux amesema Coke Studio ni kitu kikubwa, na hakuwahi kutarajia kukutana na msanii mkubwa kama Skales kutoka Nigeria ambaye ameurudia wimbo wa Ninogeshe na kumuelezea kuwa ni msanii ambaye ana ushirikiano mzuri.
michezo
JIJI la Dodoma limetenga maeneo matatu kwa ajili ya kuwaweka wafanyabiashara wadogo wanaopanga biashara zao barabarani. Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yunu akizungumza na gazeti hili alisema maeneo hayo yaliyotengwa ni pamoja na pembeni ya soko la sabasaba ambalo ndio stendi kubwa ya mabasi yanayozunguka maeneo mbalimbali ya jiji.“Maeneo mengine ambayo jiji limetenga ni pamoja na soko la Bonanza karibu na Chang’ombe na eneo la karibu na Soko la Dk Rehema Nchimbi,”alisema. Alisema mkakati huo wa soko unawalenga wafanyabiashara ndogo 150 waliojiandikisha awali, hata kama idadi yao inazidi kuongezeka kutokana na watu wengi kuhamia jijini humo.Yunu alisema mkakati huo ambao umewekwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi unalenga kuhamisha wafanyabiashara ndogo wanaopanga bidhaa zao barabarani.Kunambi alitoa agizo hilo kwa ofisa biashara huyo kuhakikisha ndani ya muda mfupi wafanyabiashara ndogo waliozagaa pembeni ya barabara wanaondolewa. Lengo la kuwaondoa ni kuhakikisha jiji linakuwa safi, linakuwa katika mpango mzuri wa namna ya kufanya biashara yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao wadogo.“Pia wanalenga kuhakikisha kwamba mazingira ya jiji, ikiwemo mitaa na barabara zinatunzwa vizuri kwa ajili ya matumizi ya watu mbalimbali wala si kwa ajili ya biashara,”alisema.Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara ndogo jijini hapa kufanya biashara pembeni ya barabara, hivyo kuzuia magari na wapita njia, jambo ambalo linaleta kero kwa wapitaji.Kutokana na serikali kuhamia Dodoma, jiji hilo limekuwa katika mkakati mahususi wa kupanga jiji lake na kuacha maeneo ya barabara na yasiyotakiwa kufanya shughuli zozote. Jiji la Dodoma lilishafanya mpango mwingine mara baada ya kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo ya Jamatini ambao walikwenda Makole na eneo la Sabasaba.
kitaifa
MARAIS Dk John Magufuli na Profesa Arthur Peter Mutharika wa Malawi wamekubaliana kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi zao.Akiwa nchini humo, Rais Magufuli jana alifungua msimu wa soko la tumbaku na kusema nchi za Afrika zina haja ya kufanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo, kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji vitakavyoongeza thamani mazao na kuokoa uharibifu wa asilimia 40, ya mazao yanayovunwa na kukosa mahali pa kuhifadhia. Kauli hiyo ya Rais Magufuli aliitoa jana mjini Lilongwe nchini humo, ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake aliyoifanya kutokana na mwaliko wa Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika.Akizungumza kabla ya kufungua rasmi msimu huo, Rais Magufuli alisema uchumi wa Bara la Afrika kwa asilimia kubwa unategemea sekta ya kilimo na kwamba nusu ya watu wake wameajiriwa kwenye sekta hiyo huku pia nchi hizo zikitegemea kilimo kwa usalama wa chakula, lakini bado kinatekelezwa kwa njia duni. Alisema nchini Malawi asilimia 80 ya wananchi wake wanategemea kilimo kupata ajira huku asilimia 60 ya fedha za kigeni zinatoka kwenye mazao na asilimia 37 ya Pato la Taifa hilo hutegemea kilimo hivyo kuna haja ya kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hiyo kwa kufungua zaidi viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani mazao.Rais Magufuli pia alitoa mfano kwa Tanzania akisema kilimo kinategemewa kwa asilimia 100 kwenye usalama wa chakula, lakini pia asilimia 70 ya wananchi wanategemea ajira huku malighafi za viwandani ikitegemewa kwa asilimia 60. Aidha, kilimo kina mchango kwenye fedha za kigeni ambako asilimia 25 za fedha hizo hutokana na mazao ya kilimo, huku pia pato la nchi likitegemea kilimo kwa asilimia 30 na kusema hiyo inathibitisha kuwa kilimo barani Afrika ni sekta muhimu ya kukuza uchumi inayohitaji kufanyiwa mapinduzi makubwa.Akizungumzia zao la tumbaku, Rais Magufuli alisema zao hilo sio tu muhimu nchini Malawi, bali pia Tanzania kwani ni miongoni mwa mazao yanayoingiza fedha nyingi za kigeni na kutolea mfano kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo, kuanzia 2014 zaidi za Sh bilioni 1.33 zimetokana na zao hilo. Kwa upande wa Malawi, alisema kwa msimu uliopita nchi hiyo imepokea dola za Marekani milioni 300 kwa mauzo ya tumbaku na fedha hizo zingeweza kuongezeka maradufu iwapo wangekuwa na viwanda vya kusindika zao hilo.“Msimu uliopita nimeambiwa ulipata dola milioni 300 kwa mauzo ya tumbaku, sasa kama tungekuwa na viwanda vya usindikaji ina maana tungepata fedha nyingi zaidi, kuliko kuuza malighafi, tunahitaji mageuzi kwenye kilimo na nyie nasikia mmeanza, ni vizuri hongereni,” alisema Rais Magufuli. Kuhusu changamoto za kilimo, Rais Magufuli alisema bado Afrika inakabiliwa na matumizi madogo ya pembejeo, mbinu za zamani za kilimo na matumizi madogo ya mbolea na zana za kisasa hivyo tija haiongezeki.Alisema mbali na changamoto hiyo, pia kuna ukosefu wa maghafa ya kutosha ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa, takwimu zikionesha asilimia 40 ya mazao yaliyovunwa huharibika kwa kukosa maghala ya kuhifadhia. Aidha, Rais Magufuli alitaja changamoto nyingine kwenye kilimo kuwa ni ukosefu wa masoko ya mazao kwa sababu kilimo cha Afrika kwa asilimia kubwa kinategemea masoko ya kimataifa ambayo bei zake hazitabiriki na wakati mwingine hazina faida kwa mkulima.
kitaifa
KAZI ya kutandaza mabomba ya gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa Mkoa wa Lindi inatarajia kuanza mwisho wa mwezi huu.Hayo yamebainishwa bungeni na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM), aliyetaka kujua ni lini wananchi wa Lindi watafikishiwa huduma ya gesi nyumbani.“Katika swali la msingi, inaonesha utekelezaji mradi ya usambazaji wa gesi nyumbani kwa mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara, lakini sijasikia kuhusu Mkoa wa Lindi, je ni lini wananchi wa Lindi watafikiwa na huduma hiyo?” amehoji Salma.Amesema kwa upande wa Mkoa wa Lindi kazi ya kutandaza mabomba ya kusambaza gesi nyumbani itaanza mwisho wa Mei.Hivi karibuni, Dk Kalemani ameagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhakikisha inaongeza kasi ya kusambaza gesi ya kupikia ili angalau robo ya nyumba za Jiji la Dar es Salaam ziwe zimefikiwa na huduma hiyo ndani ya miaka mitatu ijayo.Awali, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kwa sasa TPDC inaendelea na utekelezaji wa mradi kwa kuagiza na kujenga miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na katika taasisi mbalimbali kwa mikoa ya Mtwara, pwani na Dar es Salaam. Mgalu alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge Newala Vijijini, Rashidi Akbar (CCM) aliyeuliza:“Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa gesi kutoka Mtwara na Songosongo inatumika kwa asilimia sita tu, je, kwanini kiwanda cha saruji cha Dangote na Mtwara Cement mkoani Mtwara havijapatiwa umeme wa gesi asilia hadi leo.Pia aliuliza, je, kwa nini wananchi wa Mtwara wasiunganishiwe gesi asilia kwenye nyumba zao?Akijibu maswali hayo, Mgalu alisema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza gesi asilia mkoani Mtwara imeshaanza ambapo kwa sasa kazi ya ununuzi wa mambomba, mita za kupima gesi pamoja na vifaa vya kupunguza mgandamizo wa gesi inaendelea.“Inategemea zaidi kata 120 za awali zitaunganishiwa mabomba ya gesi mkoani Mtwara kwa matumizi ya nyumbani ifikapo Juni mwaka 2019,” alisema Mgalu.Kuhusu viwanda vya Dangote na kiwanda cha saruji cha Mtwara kuunganishiwa umeme, Mgalu alisema kwa sasa kiwanda cha saruji cha Dangote kimeunganishiwa na miundombinu ya gesi asilia ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa kuwezesha matumizi ya gesi asilia kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda cha Dangote ilikamilika na kuanza kufanya kazi Agosti, 2018.“Hadi kufika Aprili mwaka 2019, Kiwanda cha Dangote kiemanza kutumia wastani wa futi za ujazo milioni 5 kwa siku kwa kuzalisha umeme,” amesema.Amesema awamu ya pili ya mradi ilikamilika Desemba 2018 na sasa Kiwanda cha Dangote kinatumia gesi ya wastani wa futi za ujazo milioni 15 hadi 20 kwa siku kwa ajili ya uzalishaji wa saruji. “Jumla ya gharama za mradi ni Shilingi bilioni 8.2,” amesema Mgalu.
kitaifa
HOMA ya ugonjwa wa dengue imeendelea kutikisa mikoa ya Dar es Salaam na Tanga ambapo mpaka sasa watu zaidi ya 2,900 wamethibitika kuugua ugonjwa huo, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jana, wagonjwa wawili walipoteza maisha kwa dengue iliyoendelea kuitesa Dar es Salaam na Tanga.Ili kuepukana na madhara, serikali imesema wananchi wanaweza kujikinga na ugonjwa huo kwa njia mbalimbali ikiwemo kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi, kuondoa vitu vinavyoweza kuweka mazalia ya mbu, vifuu vya nazi, makopo na magurudumu ya magari.Njia nyingine za kujikinga na dengue ni kufyeka vichaka karibu na makazi, kufunika mashimo ya maji taka, kutumia dawa za kufukuza mbu, kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu na kuweka nyavu madirishani na milangoni.Hata hivyo, serikali imesema idadi ya wanaougua ugonjwa huo imeendelea kupungua ikilinganishwa na wiki mbili zilizopita ambapo kwa wastani wagonjwa walioripotiwa kwa wiki walikuwa 525 ikilinganishwa na wagonjwa 420 kwa wiki kwa sasa na juhudi za kuudhibiti zaidi zinaendelea.“Wananchi zipuuzeni taarifa za kwenye mitandao ya kijamii zikiwemo video zinazosadikiwa kuwa ni za miaka ya nyuma zenye taarifa za upotoshaji ambazo zilitolewa ufafanuzi,” ilisema wizara.Pamoja na kwamba ugonjwa huo umeendelea kutishia maisha ya watu, wizara imesema homa ya dengue siyo ugonjwa mpya kwa kuwa hujitokeza nyakati za mvua sehemu mbalimbali duniani. Ilisema mwaka 2016 watu milioni 390 waliugua ugonjwa huo ikilinganishwa na watu milioni 216 waliougua malaria katika mwaka huo 2016.Wiki moja na nusu iliyopita, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi, alisema idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi vya homa hiyo au kuwahi kuugua ilikuwa 1,901 kipindi kuanzia Januari hadi Mei 15 mwaka huu.Alisema serikali inaendelea kuimarisha upatikanaji wa vipimo vya homa hiyo katika vituo vyake vya kutolea huduma katika maeneo yaliyoathirika.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yudas Ndungile, alisema taratibu za kupata mashine ya kupulizia dawa kutokea angani ili kuua mbu hao makazi ya watu jijini zinaendelea.Serikali imeendelea kusisitiza kuwa ugonjwa huo unaombukizwa na mbu aina ya Aedes hauna tiba wala chanjo ya moja kwa moja mpaka sasa na tiba pekee kwa sasa ni panado pamoja na kunywa maji mengi. Mbu wa madoadoa meupe ya kung’aa hupendelea kuuma asubuhi, mchana na jioni.
kitaifa
Wadau wengine ni Wakala wa usafirishaji mizigo bandarini (TAFFA), Wakala wa vipimo (WMA), Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya Kuhudumia Kontena Bandarini (TICS) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA).Wengine ni Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Shirika la Viwango nchini (TBS), Wakala wa Barabara (Tanroads), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kitengo cha afya cha bandari na Chama cha wamiliki wa Malori nchini (Tatoa).Mwinjaka, alisema, "Kila mmoja atawajibika, ikitokea mwenzetu mmoja hawajibiki ipasavyo atajibu kwanini hafanyi kazi yake ipasavyo."Mwanjaka alisema eneo maalumu limeshapatikana kwa ajili ya benki ambapo kwa sasa CRDB na NMB tayari zimepewa eneo lakini pia benki za kimataifa.Alisema pia nchi nyingine ambazo zinachukulia mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, zinatafutiwa eneo kwa ajili ya kufanyia kazi zingine za msingi wakiwa bandarini hapo."Kusaini makubaliano haya haina maana itakuwa mwisho wa kutekeleza majukumu mengine yaliyopo, kila mmoja atawajibika pale yatakapojitokeza na kwa pamoja yatashughulikiwa," alisema Mwanjaka.Kwa upande wake, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga alisema, makubaliano hayo yabane pande zote mbili Serikali na wateja ikiwa mmoja kati yao atabainika kuchelewesha mzigo apigwe faini."Yeyote atakayethibitika kuchelewesha, apigwe faini, siyo ikandamize upande mmoja hapo tutaweza kwenda sawa," alisema. Alisema kwa sasa kupanda kwa bidhaa mbalimbali kunasababishwa na gharama zilizopo bandarini."Mtu anapandisha bei pale Kariakoo kwa ajili afidie pesa yake, mzigo unafikia lakini uzembe unatokea upande mmoja anayetozwa ni huyu mteja," alisema.
uchumi
SERIKALI imesema vyuo vya elimu ya juu nchini, havifanyi vizuri katika eneo la machapisho kwa kutokuwa nayo ya kutosha, jambo ambalo husababisha kushuka katika upangaji wa nafasi za vyuo vikuu kitaifa na kimataifa.Imeeleza katika eneo la taaluma, vyuo hivyo viko vizuri, lakini mara nyingi havishiki nafasi nzuri, huku wakitakiwa kuongeza machapisho. Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimesema wanataaluma wake wasiokuwa na machapisho kwa takriban miaka saba, wanaangalia uwezekano wa kupelekwa kufundisha shule za sekondari nchini.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifunga Wiki ya Tano ya Utafiti, iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani (UDSM). Kuhusu machapisho, Profesa Ndalichako alisema vyuo vya elimu ya juu vya ndani ya nchi, vinatakiwa kubadilika kwamba pamoja na kufanya tafiti, lakini waongeze machapisho yakipelekwa kitaifa na kimataifa.Alisema kila mwaka, kuna taasisi zinazopanga nafasi ya vyuo vikuu kitaifa na kimataifa katika ubora wake. Lakini, vyuo vya ndani vimekuwa haviko katika nafasi nzuri, hali hiyo ikisababishwa kuwa na machapisho na majarida yanayotambulika kitaifa na kimataifa. Aidha, alivitaka vyuo vya elimu ya juu nchini, kuiga kile kilichofanywa na UDSM kwa kutenga fedha kufanya tafiti na wao kuanza kutenga fedha za utafiti kwa kuwa wanalipwa fedha nyingi zikiwemo ada na mishahara.“Kupanga ni kuchagua, chagueni kufanya tafiti, utafiti unalipa iwapo mtawekeza kwa kiwango kinachostahili,” alisema Profesa Ndalichako na kupongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wiki hiyo ya utafiti.Alisema wiki hiyo inatoa fursa kwa wadau, kupata jukwaa na aina za tafiti zilizofanyika kwa kuwa ni eneo ambalo limekuwa likiwashirikisha watunga sera na umma kwa ujumla. Alisema serikali imeendelea kutoa ruzuku kwa ajili ya ubunifu na ugunduzi, na wizara inaandaa mwongozo wa kutambua na kuthamini utafiti, kwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa likiongeza mchango wa maendeleo nchini.
kitaifa
UCHAGUZI mdogo wa kujaza nafasi za uongozi Yanga umekuwa kizungumkuti baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwake.Awali, uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Januari 13, mwaka huu, ukasogezwe mbele wagombea wakiwa katika hatua ya kujinadi kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi mahakamani ya kupinga kufanyika. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Malangwe Mchungahela alifanya mazungumzo na waliofungua kesi na kukubaliana kuzifuta huku akisema wakati wowote atatangaza tena tarehe ya kuendelea pale walipoishia lakini mambo yanaonekana kukwama baada ya kushindwa mpaka sasa ikiwa inakaribia wiki ya pili.Akizungumza Dar es Salaam, Mchungahela alisema wanachosubiri ni wanachama hao kumalizia ufutaji wa kesi hizo na anaamini mambo yatakuwa mazuri. “Hatujakwama, tunaendelea kuzungumza nao ili kumaliza utaratibu wa kesi na wakati wowote tutatangaza pale tulipoishia wagombea wataendelea kujinadi na kufanya uchaguzi,”alisema. Alisema uchaguzi huo utafanyika kwa ushirikiano na Kamati ya uchaguzi ya Yanga kama walivyokubaliana. Nafasi zinazotakiwa kujazwa wazi ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne.
michezo
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imewaagiza maofisa elimu mikoa na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kushughulikia nyongeza ya mishahara ya walimu waliopandishwa madaraja nchini ili waanze kulipwa stahiki zao kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.Agizo hilo lilitolewa jana jijini hapa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Tixon Nzunda wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kikazi baada ya kuitembelea Shule za Msingi Bukumbi na Kigongo zilizopo wilayani Misungwi.Aliagiza walimu hao waongezewe mishahara yao kuanzia mwezi ujao. Shule za Msingi Kigongo na Bukumbi ni kati ya zinazotekeleza Mradi wa Fursa kwa watoto tangu mwaka 2014 hadi 2018 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Children in Crossfire(CIC) linalohusika na malezi na makuzi ya awali ya watoto kwa kushirikiana na Shirika la Uchumi wa Nyumbani (TAHEA). Nzunda alitoa agizo hilo kutokana na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya walimu wa shule hizo waliopandishwa madaraja waliodai kutoongezewa mishahara yao zaidi ya miezi mitano sasa.“Wakurugenzi hakikisheni kila mwezi mnaingia kwenye mfumo kuangalia kwa sababu viongozi wanaweza kutengeneza mazingira ya rushwa ndipo stahiki zao zishughulikiwe,” alisema.Alisema katika kushughulikia stahiki za walimu au watumishi wengine wa umma, serikali kamwe haitawavumilia baadhi ya watendaji walioko serikalini ambao wamekuwa vinara katika kuwakandamiza watumishi wenzao wasifanikiwe na wasipate stahiki zao na kusisitiza uongozi wa aina hiyo haufai. “Tunataka viongozi wanaowezesha wanaowaongoza kufanikiwa.Hivyo nawaagiza nyie ambao mnawaongoza hawa walimu kushughulikia nyongeza yao ya mishahara,” alisema na kuagiza wamjulishe yeye kama tatizo ni kuthibitisha madai ya walimu ili awasiliane na Katibu Mkuu wake kwa ufumbuzi.
kitaifa
WIZARA ya Miundombinu imeelekeza watoa huduma ya usafiri wa pikipiki maarufu bodaboda kutumia mfumo wa kisasa wa abiria kutolipa fedha taslimu Julai 1, mwaka huu.Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya kuhakikisha matumizi ya fedha taslimu katika huduma zote yanakoma ifikapo mwaka 2024.Uamuzi wa kuanza na pikipiki umefikiwa baada ya baraza la mawaziri kuidhinisha mkakati wa taifa wa usafiri wa pikipiki kibiashara.Waziri wa usafirishaji, de Dieu Uwihanganye, amesema mkakati huo utaondoa ulipaji nauli kwa abiria na wamiliki wa vyombo vya usafiri.Alisema mkakati huo utasaidia upatikanaji wa huduma za usafiri na kuimarisha usimamizi wake, hivyo kufikia Julai lazima wenye pikipiki kujisajili katika mifumo ya YegoMoto au Pascal Technology Ltd, ambazo ni kampuni zinazowezesha ulipaji kwa kuwekewa meta.Serikali pia iko katika mchakato wa kupanga gharama mpya za nauli kwa kilometa kwa usafiri wa taxi-moto, gharama watakayokubaliana baada ya majadiliano na wadau.“Meta zitasaidia mambo mengi, kwani itasaidia polisi kufuatilia watakaokiuka sheria za usalama barabarani na kuwatoza faini halali,” alisema.Nchini hapa kuna leseni za biashara za pikipiki 25,000 na inakadiriwa 20,000 hawajasajiliwa, lakini wanatoa huduma na mpaka sasa pikipiki 7,000 zinatumia malipo bila fedha taslimu.Mkakati huo ni kuwezesha malengo ya nchi kufikia uchumi wa kutotumia fedha taslimu mwaka 2024.Alisema mkakati huo utasaidia pikipiki kuhakikisha usalama wa barabarani,usalama wao, kwani ajali nyingi husababishwa na pikipiki, hivyo mfumo huo utasaidia kufuatilia pikipiki zitakazoibiwa kwa kutumia GPS. Takwimu zinaonesha ajali 145 zimetokea Januari mpaka Machi mwaka huu na asilimia 50 zimesababishwa na pikipiki na vifo vya watu 108, asilimia 38 vimesababishwa na pikipiki.Rais wa Shirikisho la Vyama vya Waendesha Pikipiki Rwanda (FERWACOTAMO), Daniel Ngarambe alisema watafanya kazi na wenye pikipiki, wasimamizi na wawekezaji, kwani kuna changamoto ya mtandao hivyo, ni vema kufanyiwa kazi mapema huduma ikamilike
uchumi
KUTOKANA na kuwepo kwa matendo ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto Shirika lisilo la Kiserikali la Compassion International Tanzania limeiomba serikali ione uwezekano wa kuweka somo la ulinzi wa mtoto kwenye mitaala ya elimu.Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania, Agness Hotay wakati akitoa salamu kwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya shirika hilo tangu lianze kuhudumia watoto wahitaji nchini.Alisema kuwa shirika hilo lilianzishwa kwa malengo ya kuwasaidia watoto wenye uhitaji wanaotoka katika familia ambazo hazina uwezo kwa lengo la kuwafanya watoto hao waweze kuishi maisha yenye furaha.Akitoa salamu, mkurugenzi huyo alisema kuwa shirika lina wajibu wa kuhakikisha kuwa kila mtoto bila kujali jinsi, dini au kabila ana uthibitisho kuwa anapendwa, analindwa na kujulikana.Alisema uwakili wa shirika ni pamoja na kumtetea mtoto na kusimamia stahiki za mtoto husika ili kuhakikisha kuwa anafikia ndoto anazotarajia.Alisema kuwa tangu kuanza kwa shirika hilo nchini Tanzania na kutimiza miaka 20 sasa limefikia vijana 135,750 ambapo hadi sasa vijana 99,671 bado wapo kwenye huduma na 36,133 wameshamaliza na kutoka kwenye mpango wa kuhudumiwa na Compassion Tanzania.“Kupitia makanisa ambayo ni washirika wenza na Compassion International Tanzania yameweza kutoa ajira zaidi ya 1,300 hivyo kushiriki katika kuondoa uhaba wa ajira kwa kutengeneza ajira na kuongoza pato la Taifa.“Shirika limeweza kuwezesha makanisa kutengeneza miundombinu, kuhamasisha ujenzi wa madarasa, uchimbaji wa visima, ujenzi wa vyoo vya kisasa na jiko, uanzishwaji wa karakana za mafunzo mbalimbali, uanzishwaji wa VICOBA na ujalismali,” alisema Hotay.Kwa upande wake, Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu, Stella Ikupa, alisema maadhimisho hayo yawatake vijana kutumia fursa zilizopo kujipatia maendeleo.Mbali na hilo, aliwasihi viongozi wa dini kutoa elimu kwa watoto wenye ulemavu ili jamii iweze kuwapa haki sawa na watu wengine.“Naomba niwasisitize viongozi wa dini kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ili wasiwachukulie watoto wenye ulemavu sehemu ya mkosi hata ifike hatua hata kwenye mahusiano mtu mwenye ulemavu asikose kuoa au kuolewa kwa kigezo cha kuwa na ulemavu,” alisema Ikupa.Ikupa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, alisema kitendo cha shirika hilo kujitolea kuwahudumia watoto wenye uhitaji ni sehemu ya kulifanya taifa kuwa na watu ambao wamelelewa katika maadili mazuri na wenye kufanya kazi kwa uadilifu.
kitaifa
MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima ametoa siku tatu kwa viongozi wa Wilaya ya Tarime kubaini zilipo fedha za huduma zilizotolewa na Mgodi wa Acacia North Mara kwa miaka mitatu kiasi cha Sh bilioni 9.5.Malima alitoa agizo hilo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Charles Kabeho, maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kuchunguza miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Tarime Vijijini.Inadaiwa kuwa baadhi ya watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wa serikali wamehusika katika kuhujumu fedha hizo hivyo hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.Malima amesema hayo katika kikao cha kumtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kabeho kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa wilaya hiyo na watumishi wa halmashauri za Tarime Mjini na Tarime Vijijini, madiwani wote wa halmashauri hizo wakiongozwa na wenyeviti wao, Moses Yomami (Tarime Vijijini), Khamis Nyanswi (Tarime Mjini).Pia walikuwapo wakurugenzi watendaji wa halmashauri hizo, Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya, Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye ‘Namba Tatu’ na viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.Malima alionesha kuwapo kwa vitendo vya hujuma katika halmashauri hiyo ya Tarime Vijijini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambako halmashauri zote mbili zinaongozwa na Chadema.Alisema katika shughuli za maendeleo hakuna itikadi za vyama, na kwamba Halmashauri ya Tarime Vijijini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamepokea Sh bilioni 9.5, akizitaja kuwa ni Agosti 10, 2015 walipokea Sh bilioni 1.1, Januari 18, 2016 (Sh 1.6), Julai 29, 2017 (Sh bilioni 1.334), Februari 7, 2017 (Sh bilioni 1.770), Julai 27, 2017 (Sh bilioni 1.477), Julai 18, 2018 (Sh bilioni 1.253) na Septemba 8, 2018 (Sh bilioni 1.435).Alisema mwezi uliopita walitaka kupewa tena Sh bilioni 1.5, lakini amezizuia kwanza hadi fedha hizo za awali Sh bilioni 9.5 za huduma zilitolewa na Mgodi wa Acacia North Mara, kwa ajili ya miradi ya mandeleo, kujulikana matumizi yake kwani kuna harufu ya ufisadi katika fedha hizo.Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Kiboye alimpongeza Rais Magufuli kwa kusikia kilio cha watu wa Tarime na kumteua Kabeho kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime na kuahidi chama hicho kitampa ushirikiano kwa maendeleo ya wana-Tarime na kuwaonya wahujumu halmashauri kwamba dawa yao inachemka na mwisho wao umefika.
kitaifa
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ana hakika timu hiyo itarejea na ushindi kutoka Cape Verde.Stars ilisafiri alfajiri ya jana kwenda Praia kucheza na wenyeji wao Cape Verde kesho mechi ya kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika iliyopangwa kufanyika Cameroon mwakani.Stars na Cape Verde zipo kundi moja na Uganda na Lesotho na tayari kila timu imecheza mechi mbili huku Uganda ikiongoza msimamo wa kuwa na pointi nne, ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi mbili.Akizungumza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam saa chache kabla timu hiyo haijaondoka, Mwakyembe alisema ameamua kuacha usingizi wake na kwenda kuwasindikiza kutokana na kuwa ana uhakika wa asilimia zote kuwa watarudi na ushindi hivyo wasimuangushe.Kwa upande wa serikali, kiongozi aliyeambatana na Stars ni Mkurugenzi wa Michezo, Yusuf Singo. Mwakyembe aliwataka wachezaji hao kutambua kuwa serikali pamoja na watanzania kwa ujumla wapo nyuma yao hivyo wasiwaangushe na pia kama alivyofanya kuwasindikiza hivyohivyo anatarajia kufanya pia wakati watakaporudi hivyo wanapaswa kuhakikisha wanapata ushindi ili awapokee kwa furaha.Aliwasisitiza kuhakikisha wanakabiliana na wapinzani wao kwa kujiamini na kujituma licha ya kuwa ugenini wakijua fika kuwa wanapigania taifa lao ambalo limepoteza heshima kwenye michuano hiyo kwa miaka 38 sasa tangu kushiriki fainali ikiwa ni mara ya kwanza na mwisho.“Nyie ndio tumaini la Tanzania kuturejeshea heshima iliyopotea kwa zaidi ya miaka 38 haijapata kutokea ni muda mrefu mno, sasa tumechoka, nina uhakika tuna kikosi kizuri sana, benchi la ufundi zuri sana lenye weledi wa kila aina…“Sisi kazi yetu kubwa kuwatia moyo na kuwaombea kwa Mungu mfike salama na vilevile tarehe 12 muoneshe mchezo wa kujiamini, kujituma kupigania taifa lenu mimi nina uhakika moyo wangu hauna dukuduku kabisa najiandaa kuwapokea mkirudi,” alisema Mwakyembe.
michezo
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema amewajenga wachezaji wake kisaikolojia kukabiliana na mbinu za fi tina zinazotumiwa na timu nyingi za Kiarabu wakiwa kwao kujinufaisha kupata matokeo chanya.Aidha, Zahera alisema wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na malengo mawili makubwa, kwanza kujilinda kuzuia wasifungwe na kuhakikisha wanapata ushindi wa mabao mawili ili kusonga mbele kufutia kupoteza mchezo wao wa mkondo wa kwanza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.Zahera alisema amechukua hatua hiyo kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha na soka la kiafrika, hasa kwa timu nyingi zinazotoka kwenye ukanda wa kaskazini mwa Afrika kwani wamekuwa na utamaduni wa kutumia mbinu chafu za kuwadhoofisha wachezaji kabla ya kuingia kwenye mchezo. Zahera amefichua kauli hiyo ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Pyramids unaotarajiwa kupigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa 30 June, Cairo nchini Misri. Zahera anajua mchezo huo utakuwa mgumu kwao kwa kuwa kikosi cha wapinzani wao kimesheheni wachezaji wakubwa na wanatumia akili katika kucheza hivyo watazidisha umakini kwa kutowaruhusu kupata nafasi ya kupata mwanya wa kuwafunga. Alisema kitu pekee kinachozidi kumpatia matumaini ya kwenda kuchomoza na ushindi ni kwamba kwenye mazoezi yaliyopita waliyofanya wachezaji wake walikuwa wanafundishwa mbinu ya kufunga na kujilinda na walicheza kwa kujiamini na walionesha maelewano mazuri.
michezo
UTALII unachangia asilimia 25 ya pato la ndani Zanzibar na asilimia 80 ya fedha za kigeni, jambo ambalo wataalamu wanasema lisingewezekana bila kuwepo kwa matumizi bora ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk Mzee Suleiman Mndewa amesema hayo na kuongeza kwamba licha ya watalii kupata taarifa za utalii wakiwa kwao, pia wanapata fursa ya kuendelea kuwasiliana na jamaa zao wakiwa Zanzibar.“Kwa kuwa ni kisiwa, Zanzibar inahitaji mifumo mizuri ya mawasiliano ili kuwavutia watalii wengi zaidi. Ni jambo lisilopingika kwamba watalii wanahitaji sana kuwasiliana na ndugu zao kwa kipindi chote wanapokuwa hapa,” amesema.Aliongeza pia kwamba uimara wa mifumo ya mawasiliano ni muhimu pia kwa watalii wanaotoka ndani ya Jamhuri ya Muungano, akitolea mfano wa boti zinazokwenda Zanzibar kila siku zikitokea Dar es Salaam.“Kwa kifupi, kila boti inabeba takribani watu 400, kila abiria anayekuja hapa anahitaji kuwasiliana na ndugu zake aliowaacha nyumbani. Hii ndio maana tunaamini kwamba suala la kuimarisha mifumo ya mawasiliano linahitaji kuwekewa mkazo,” amesema.Aliongeza kwamba tehama licha ya kuwa na mchango mkubwa kwenye utalii pia ina mchango mkubwa sana kwenye sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo kilimo na uvuvi.“Kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwenye kilimo, kwa mfano, unaweza kutengeneza mfumo ambao utakuambia muda muafaka wa kufanya jambo fulani la kuhudumia mazao kama muda wa kumwagila…,” alisema.Akitolea mfano wa uvuvi, Dk Mzee amesema kwamba mfumo huo pia unaweza kumwongoza mvuvi kujua ni sehemu gani kuna samaki wengi na wapi anaweza kupata soko la samaki, hivyo kuifanya kazi yake kuwa ya uhakika na yenye tija.
uchumi
MGOMBEA nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika klabu ya Yanga, Athanas Kazige amesema anataka kutumia fani yake kuiwezesha kiuchumi klabu hiyo. Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Mei 5 na sasa wagombea wanajipigia kampeni ili kuwania nafasi wanazogombea.Akizungumza jana na gazeti hili Dar es Salaam, alisema anaona faraja kuitumikia klabu hiyo kwa kutumia mitandao ya kijamii kuiwezesha kiuchumi. “Mimi nikipata nafasi ya kuwa mjumbe nitashirikiana na viongozi waliopo kutengeneza mfumo wa kuandika na watu wakisoma habari, makala kwa kulipa ili klabu iweze kupata fedha,”alisema Kazige.Aliongeza kuwa yeye ni mwanahabari, hivyo atahakikisha anashirikiana na viongozi watakao chaguliwa kufufua gazeti la Yanga Imara. “Ukweli hivi sasa wanachama nimeona kwamba kuna upungufu huo, hivyo nitashirikiana na Ofisa Habari wa Yanga ili kuongeza mapato ya klabu kupitia gazeti na mitandao ya kijamii,” alisema Kazige ambaye anagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo.Aidha, Kazige alisema kuwa mabadiliko ya mfumo ili klabu hiyo iweze kujitegemea ni muhimu kwa sasa. “Naomba wanachama wenzangu mchague viongozi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika klabu yetu, na mimi naahidi kuwa nitatumia taaluma yangu kuisaidia Yanga kiuchumi kwani habari kwa sasa ni fedha,”alisema Kazige ambaye ni mwandishi wa habari mwandamizi nchini.
michezo
SERIKALI imesema hadi Desemba 31, mwaka huu, Watanzania wote wenye sifa za kupata vitambulisho vya Taifa watakamilisha usajili wa kuchukua alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki, kazi inayoendelea kufanywa sasa.Sambamba na hilo, serikali imesema itanunua mashine mpya za uzalishaji wa vitambulisho vya taifa zenye uwezo mkubwa zaidi kwa lengo la kuharakisha upatikanaji vitambulisho hivyo.Hayo yalibainishwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Buyuni, Christopher Chiza (CCM). Mbunge huyo alihoji serikali ina mpango gani wa kuharakisha zoezi la kutoa vitambulisho vya taifa wavitumie kwa shughuli za maendeleo.Akijibu swali hilo, Masauni alisema serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inaendelea kukamilisha usajili kwa watu wote wenye sifa ikitarajiwa kukamilisha kazi ya uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki Desemba 31, mwaka huu.Alisema hadi sasa vitambulisho milioni tano vya taifa vimeshatolewa na kwamba vingine milioni 13 vipo hatua za mwisho kutolewa na kwamba hadi ifikapo Desemba mwaka huu, lengo lao ni kutoa jumla ya vitambulisho milioni 24.4. “Wananchi waendelee kuwa watulivu na wale waliokamilisha uchukuaji alama za vidole, saini na picha na hawajapata vitambulisho, huenda ndio hivyo milioni 13 vilivyo hatua za mwisho kutolewa,”alisema Naibu Waziri Masauni.Aidha alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila kukwama ikiwemo wale wanaojisajili kibiashara Brela, NIDA imefungua dawati maalum la usajili katika ofisi hizo. Alisema usajili huo unafanywa kwa kuzingatia sifa bila kuathiri masharti ya kisheria na kanuni.Akijibu swali kuhusu utaratibu gani umewekwa na serikali wa kuwapa vitambulisho wananchi wanaokaa mipakani bila kuathiri malengo ya utoaji vitambulisho hivyo, Waziri Masauni alisema utaratibu wa kuwapa vitambulisho hautofautiani na ule wa kawaida uliopo.
kitaifa
YANGA imeendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya baad aya kuifunga 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA, hatua ya 32 bora katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kuifunga Tanzania Prisons msimu huu, ambapo kwa mara ya kwanza waliifunga 1-0 na kuwa timu ya kwanza kuifunga timu hiyo katika ligi msimu huu. Kwa ushindi huo, Yanga sasa imetinga hatua ya 16 bora sawa na watani zao Simba, ambao juzi waliifunga Mwadui ya Shinyanga kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo wa Uhuru. Ushindi huo wa Simba ulikuwa ni sawa na kulipa kisasi kwa Mwadui, ambayo hadi sasa ndio timu pekee iliyoifunga Simba katika Ligi Kuu, Tanzania Bara. Mabao ya Yanga yalifungwa na wachezaji wapya wa timu hiyo, Bernard Morrison na Yikpe Gislain na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi huo wa mabao 2-0. Morrison ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia Yanga bao pale alipofunga kwa penalti, katika dakika ya 11, baada ya beki wa Tanzania Prison, Michael Ismail kunawa mpira wa krosi katika eneo la hatari, uliopigwa na Juma Abdul. Mpaka mapumziko, Yanga ilikuwa mbele kwa goli 1-0, licha ya wapizani wao kuonesha uimara wa hali ya juu katika muda wote wa mchezo. Mshambuliaji mwingine mpya, Yikpe alifunga bao katika dakika ya 63 kwa mpira wa kichwa baada ya kutumia vyema pasi ya Haruna Niyonzima, ambaye aling’ara katika mchezo wa jana. Pamoja na matokeo hayo, kivutio kikubwa katika mchezo huo, alikuwa ni mshambuliaji mpya wa Yanga, Morrison ambaye licha ya kufunga goli, alionesha kiwango cha hali ya juu, huku akiuchezea mpira kwa namna anavyotaka.Haikua siku nzuri kwa mshambuliaji David Molinga, ambaye aliumia kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na mfungaji wa bao la pili, Yikpe. Dakika za mwishoni, Deus Kaseke alitoka na nafasi yake kuchuliwa na Patrick Sibomana, wakati Feisal Salum aliingia kuchukua nafasi ya Morrison. Kwa upande wa wapinzani wao, waliongeza nguvu kwa kumtoa Salum Kimenya na kuingia Samson Bangula ambaye hata hivyo hakuleta matokeo chanya kwa timu yake.
michezo
Akizungumzia mfumo huo alisema mfumo huo utatumika kutoa mizigo bandarini, katika viwanja vya ndege na mipakani na wenye kuhusisha wadau mbalimbali.“Awali Idara ya Forodha ilikuwa ikitumia mfumo wa asycuda kwa ajili ya kutolea mzigo ambapo umekuwa na changamoto nyingi zilizokuwa zikisababisha ucheleweshwaji wa kutoa mizigo bandarini,” alisema Silaa na kuongeza kuwa mfumo huo ni wa Watanzania na katika kuutekekeza umegharimu dola za Kimarekani milioni 11.6.Alisema katika mfumo wa awali ulipaji wa mizigo ilikuwa lazima kwenda benki ambapo ulijumuisha pia mifumo mingine midogomidogo ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu haswa wakati wa kuandaa ripoti.Silaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa mfumo huo, alisema baada ya kuona mfumo wa awali ulikuwa na changamoto mbalimbali ndipo idara hiyo ilianza mchakato wa kutafuta mzabuni atakayefanya upembuzi juu ya mfumo huo wenye kukidhi matakwa ya Watanzania.Alisema faida za mfumo huo ni kurahisisha taratibu na kupunguza gharama na muda wa kutoa mizigo kutoka siku tisa hadi tano, kuwa na taratibu za wazi zenye kuleta manufaa katika utoaji wa mizigo na kuunganisha vitengo vya ndani vya TRA.Kuhusu kama mfumo huo utaweza kubaini mizigo haramu alisema mfumo huo utaweka wazi hatua kwa hatua ya mzigo tangu kuingia hadi kuondoka na kwamba nanikafanya nini hali ambayo itarahisisha kubaini watakaohusika na kitendo chochote chenye kutiliwa shaka.“Katika mfumo huu nyaraka za kughushiwa zitapunguzwa, utazingatia uadilifu kwa wanaoutumia kwani utatoa taarifa kila wakati unapotumiwa, kufahamu mzigo ulikocheleweshwa na ni nani aliyehusika, kuondoa uongo na kuondoa kufahamiana wakati wa kufuatilia nyaraka,’ alisema.Kwa upande wake, Vileth Kazimoto wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TRA, alisema chini ya mfumo huo zipo changamoto wanazotarajiwa kukumbana nazo, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa uelewa mdogo wa taaluma hiyo kwa wafanyakazi wengi wa TRA.
uchumi
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amekitangaza kijiji cha Nzali kuwa kituo cha uhamasishaji Mkoa wa Dodoma.Alisema hayo katika kijiji cha Nzali kata ya Chilonwa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 42 tangu kuzaliwa kwa CCM na kubainisha kuwa maadhimisho hayo yatadumu kwa mwezi mzima.Kauli ya Dk Bashiru imekuja wakati wa maadhimisho hayo ambapo zaidi ya vikundi 30 vya ngoma vilijitokeza kwenye uzinduzi wake vikiimba nyimbo za hamasa pamoja na kuelezea miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.Amesema wakati huu ambapo nchi iko katika vita ya kiuchumi kila kitu kinahitaji hamasa.“Tunahitaji kufufua hamasa za kisiasa kwa nyimbo, na sasa tunatakiwa kuwepo na vikundi vya hamasa, tunataka sanaa inayohamasisha kushiriki vita vya kiuchumi” alisema.Alisema yeye pamoja na msemaji wa chama hicho Humprey Polepole watafika kijijini hapo kujifunza watu wanavyojitolea kuwa na hamasa.“Msiishie kukisifia tu chama kikosoeni kwa adabu” alisema.Katibu Mpya Idara ya Oganaizesheni CCM Pereira Ame Silima, amesema tangu aingie kwenye siasa na kuzunguka maeneo mbalimbali nchini hajawahi kuona hamasa kubwa katika aliyoikuta katika kijiji cha Nzali.“Sijawahi kuona hamasa kubwa kama hii niliyokuta kijiji hiki, lazima nikiri hilo. Hapa kuna hamasa kubwa wasanii wanaimba na kupiga ngoma na kueleza umma kazi zinazofanywa na serikali yao” alisema.
kitaifa
WAKATI nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kila moja ikionesha kuridhika na kuwa tayari kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika kampeni za kujiunga na jumuiya hiyo, wadau wengine wa maendeleo nao hawako nyuma.Wasomi, wachumi na wanadiplomasia ni miongoni mwa wanaoiunga mkono DRC kutaka iwe nchi ya saba mwanachama wa EAC, baada ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini, wakisema taifa hilo kubwa.Tayari Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameshawasilisha ombi kwa Mwenyekiti wa EAC, Rais Paul Kagame wa Rwanda juu ya dhamira ya nchi yake kutaka kujiunga na jumuiya hiyo ambayo kwa sasa ina takribani watu milioni 170.Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma katika Sekretarieti ya EAC, Owora Richard Othieno, ombi hilo litajadiliwa katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama Novemba 30, mwaka huu jijini Arusha na kwamba kama kutakuwa na ulazima wa kujadili mapema, mwenyekiti anaweza kuitisha kikao wakati wowote kutokana na unyeti wake.Mhadhiri azungumza Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Razack Lokina alisema DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki itasaidia kutanua soko la bidhaa za ukanda huo na kukuza uchumi wa nchi kutokana na nchi hiyo kuwa na idadi kubwa ya watu.Alibainisha kuwa kwa ushirikiano huo pia kutawezesha maeneo mengi zaidi ya nchi hiyo kutumia bandari ya Dar es Salaam kuingiza bidhaa katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu kwani baadhi ya mikoa kutumia bandari inarahisisha ufanyaji biashara.Profesa huyo alibainisha kuwa lakini jambo la msingi ni kuhakikisha nchi hiyo inakuwa na amani kwani hakuna eneo lisilo na amani kunaweza kufanyika biashara.Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC), Peter Mathuki, anasema ombi la DRC linakuja katika wakati mwafaka na linapaswa kuungwa mkono.Mathuki ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alisema EAC imara itakuwa na nguvu ya kiuchumi na hivyo kuchuana na pande nyingine za dunia.Alisema ukubwa wa DRC ni mtaji tosha, kwani ndiyo nchi ya pili kwa ukubwa Afrika na ya kwanza kusini mwa Jangwa la Sahara. Inatajwa kuwa ya 11 duniani, ikiwa na mtaji wa watu milioni 81 ambao wakichanganya na milioni 170 kutoka nchi wanachama wa sasa wa EAC, ukanda utakuwa na `soko’ la watu milioni 250.Mbali ya ukubwa na mtaji wa watu, DRC ni nchi tajiri kwelikweli, huku asilimia 80 ya ardhi yake ikifaa kwa kilimo. Ina hazina ya asilimia 10 ya shaba ya dunia nzima.Asilimia 30 ya cobalt ya dunia nzima, dhahabu, almasi, platinum, bauxite, risasi, madini ya fedha, zink, uranium na inazalisha asilimia 80 ya madini ya coltan yanayotumika kutengeneza simu, sumaku, iPods, na injini za ‘Jet’.Inaelezwa kuwa, nchini DRC kuna aina 1,100 za madini. Ina Mto Kongo ambao ni mto wa pili kwa ukubwa duniani, ukiwa na maporomoko yanayoweza kuzalisha umeme unaoweza kusambazwa Afrika na Ulaya kwa pamoja. Ina pia utajiri wa mafuta ambayo bado kuchimbwa, misitu, wanyama, vivutio vya utalii vilivyopo Ituri na milima ya Virunga pamoja na mito na mabonde yenye unyevu na rutuba, maziwa na kadhalika.Mdau mwingine, Patience Mutesi ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya TradeMark East Africa nchini Rwanda naye amesifu, akisema ni fursa nzuri kwa ukuaji wa EAC kibiashara.Alisema kwa sasa, tayari DRC ni soko la karibu nusu ya bidhaa zote zinazozalishwa katika nchi za EAC na kwamba, yenyewe pia itafungua milango ya bidhaa zake kwa nchi nyingine wanachama.Takwimu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Uganda inaonesha kuwa, nchi iliuza DRC bidhaa zenye thamani za Dola za Marekani milioni 398 mwaka 2018 na kwamba inakusudia kuongeza na kufikia bidhaa za Dola bilioni 2 ifikapo mwaka 2020. Wakati Uganda ikiuza kiasi kikubwa ch bidhaa, yenyewe iliagiza bidhaa zenye thamani ya Dola milioni 2.5 tu kutoka DRC.Kwa upande wa Rwanda, iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 456.8 mwaka 2018 na iliagiza bidhaa za dola milioni 11.2 tu kutoka DRC, kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Rwanda. Tanzania ilipeleka DRC bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani milioni 153 mwaka 2017 na iliingiza bidhaa zenye thamani ya dola milioni moja tu kwa ajili ya bidhaa za matumizi ya ndani ya nchi, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania. Kenya, kwa mujibu wa Shirika la Takwimu la Taifa Kenya, nchi ilipeleka DRC bidhaa zenye thamani ya dola milioni 150 mwaka 2018, huku ikiingiza bidhaa za dola milioni 12.Mchambuzi wa sera kutoka Nairobi, Kenya, Jeremiah Owiti amekaririwa akisema kuwa, DRC ni nchi muhimu kwa ustawi wa ukanda wowote unaotaka maendeleo ya kweli kiuchumi, kutokana na nchi hiyo kuwa na mtaji wa watu, ardhi nzuri ya kilimo, utajiri mkubwa wa madini duniani na kadhalika.“Kama mchakato wa kuipa uanachama utaharakishwa, kasi ya ukuaji wa kiuchumi itapata msukumo mpya zaidi hivyo kuzidi kuifungua Afrika Mashariki,” alisema Owiti.Mchumi UN Kaimu Mkurugenzi wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa (ECA) katika Kanda ya Afrika Mashariki, Andrew Molde, ameungana na wadau wengine kuelezea umuhimu wa DRC kiuchumi endapo itapokelewa ndani ya EAC.Kwa mujibu wa Rais Tshisekedi, anataka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu za maendeleo ya kiuchumi na usalama wa eneo hilo la Afrika, akiamini wakijiunga EAC huenda usalama ukaimarika kwa nguvu za pamoja kutoka nchi wanachama, hivyo kuelekeza nguvu katika maendeleo kwa ujumla.Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli ameweka hadharani dhamira yake ya kuiunga mkono DRC baada ya Rais Tshisekedi kutaka kuungwa mkono alipokuwa ziarani Tanzania wiki iliyopita.Tshisekedi amekutana pia na marais wa Kenya (Uhuru Kenyatta), Uganda (Yoweri Museveni), Rwanda (Paul Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa EAC) na Pierre Nkurunziza wa Burundi, ili pamoja na mambo mengine, akiomba maombi ya nchi yake yaungwe mkono.Wakati DRC ikiwasilisha ombi la kujiunga EAC, baadhi ya nchi zimewahi kufanya hivyo, lakini zikakwama miongoni mwao ikiwa Sudan. Nchi ya Somalia pia imekuwa ikipigania kujiunga, lakini haijabahatika.
kitaifa
MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema inaendelea kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa, ili kukuza na kuendeleza wajasiriamali waitumie kukuza uchumi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alipozungumzia uwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza kadi za kielekroniki cha DZ Cards Afrika, kilichopo katika Eneo Maalum la Uwekezaji la Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam.Uwekezaji katika kiwanda hiki pekee kilichopo Afrika katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ni zaidi ya Sh bilioni 11.Baadhi ya viwanda vilivyopo katika maeneo maalumu ya uwekezaji wa EPZ ni pamoja na viwanda vya nguo, vinavyochakata nafaka, vya kutengenezea vifungashio, vifaa vya ujenzi na vya bidhaa za ngozi.Maziku alisema kuongezeka kwa mahitaji ya kadi za kielekroniki na kukuza uchumi usiotumia fedha taslimu, ndio imefanya kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko ili kusambaza bidhaa zake katika bara lote la Afrika.“Ongezeko la mahitaji ya kadi za kielekroniki na kukuza matumizi Uchumi usiotumia pesa taslimu ndio imetoa msukumo mkubwa kwa wawekezaji wa kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko zaidi,” alisema Maziku.Kiwanda cha DZ Cards Afrika kilianza uzalishaji miaka minne iliyopita na tangu wakati huo, kimepata wastani wa mauzo ya dola za Marekani milioni 2.9 (zaidi ya Sh bilioni 6.67).Kiwanda hiki huzalisha kadi zenye viwango vya kimataifa zinazotumika katika kufanya miamala katika sekta mbali mbali za uchumi. Baadhi ya kadi hizo ni Mastercard na Visacard.Maziku alisema kiwanda cha DZ Cards Afrika, kitakuwa na uwezo wa kuajiri zaidi ya watu 400 wakati uzalishaji ukiwa katika kiwango cha juu. Kwa sasa kinaajiri watu takribani 100.
uchumi
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imewaonya wafanyabiashara na wafugaji watakaojaribu kutorosha mazao ya mifugo zikiwemo ngozi kwa njia ya panya na kuikosesha serikali mapato, kuwa watachukuliwa hatua kali kisheria.Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel alitoa onyo hilo hivi karibuni wakati alipotembelea Kiwanda cha Ngozi cha ACE kilichopo Mtaa wa Viwanda Kihonda katika Manispaa ya Morogoro.Profesa Ole Gabriel alisema azma ya serikali ni kuona viwanda vyote vya ndani vinaendelea kuzalisha kwa tija kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini kwa lengo la kuwanufaisha Watanzania katika masuala ya kupata ajira.Pia aliwataka wawekezaji wa viwanda vya ngozi kuangalia mahitaji ya soko ikiwamo kuboresha zaidi utengenezaji wa ngozi ili wenye viwanda vidogo vya kutengeneza viatu, mabegi, mikanda na bidhaa nyingine zitokanazo na mazao ya ngozi kupata soko kubwa likiwemo la nchi za kusini mwa Afrika zenye idadi kubwa ya watu.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Ngozi cha ACE, Onorato Garavagilia, alisema kwa sasa kinasindika ngozi vipande 4,000 kwa siku za wanyama wakubwa na vipande 7,000 vya ngozi za wanyama wadogo.Alisema hadi kufikia Septemba mwaka huu, kiwanda kinatarajia kuingiza mitambo mipya ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza ngozi hadi kwa kiwango cha daraja la mwisho kwa ajili ya watumiaji wa viwanda vidogo vya kutengeneza viatu na bidhaa nyingine za mazao ya ngozi.“Kwa sasa hatuna tatizo la soko, tunalo China na India pia nchi za Ulaya, kinachohitajika ni kwetu ni kupokea malighafi za ngozi zenye ubora kutoka wa wateja wetu ili uzalishaji uwe na ubora zaidi,” alisema.Baadhi ya wadau wa sekta ya ngozi akiwemo Meneja Uzalishaji wa zamani wa Kiwanda cha Morogoro Tanneries, Kenneth Boma, alisema ubora wa ngozi inahitajika zaidi.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Gabriel Bura alisema wameanza kuwapatia mafunzo wachunaji ngozi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Manispaa ya Morogoro na hadi sasa uchunaji wa ngozi wenye matatizo umepungua kwa asilimia 80 hadi sasa.
kitaifa
MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga leo wana kazi ya kuhakikisha wanasaka ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Huo utakuwa mchezo wa tatu wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu wa mwaka 2019/20 Yanga ikicheza kwenye uwanja huo ambapo katika miwili iliyopita imepoteza mmoja na kupata sare moja. Lakini kwa Coastal utakuwa ni mchezo wa nne baada ya kucheza michezo mitatu na kati ya hiyo, ikishinda mmoja, sare moja na kupoteza mmoja. Mara ya mwisho timu hizo zilikutana msimu uliopita Februari 2019 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na zilitoka sare ya bao 1-1. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam Yanga ilishinda bao 1-0.Mchezo wa leo huenda ukawa mgumu na wenye presha hasa kwa wenyeji Yanga wanaohitaji ushindi angalau kuwatuliza mashabiki wao baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania katikati ya wiki hii. Sare hiyo haikuwafurahisha mashabiki wao hasa ikizingatiwa kuwa mchezo wa kwanza walipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting hivyo, iwapo watashindwa kupata matokeo mazuri tena leo hali itakuwa ngumu kwa Kocha Mkuu Mwinyi Zahera. Timu zote mbili zina washambuliaji wazuri wenye madhara langoni, ukimtazama David Molinga aliyefunga mabao mawili katika mchezo uliopita anataka kuendelea kufunga ili kuendelea kudhihirisha ubora wake na kwa upande wa Coastal hatari zaidi ni Ayoub Lyanga.Safu ya ulinzi ya Yanga bado haijakaa vizuri sana kwa sababu katika mechi mbili wamefungwa mabao manne na kushinda matatu huku Coastal ikionekana kuwa vizuri baada ya kucheza michezo mitatu kufungwa mawili na kufunga mabao matatu.
michezo