content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
MKAZI wa Boko, Abubakar Hamisi (46) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mkataba wa mauziano ya kiwanja kati yake na aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai, uliandikwa Sh milioni 60 lakini walipewa Sh milioni 80 ili kupata ahuweni ya kodi.Hamisi ni shahidi wa 20 katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato, inayomkabili Gugai na wenzake. Akiongozwa na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Awamu Mbagwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba shahidi huyo akizungumza jana alidai kuwa Gugai ni jirani yake na amewahi kufanya naye biashara.Alidai walifanya makubaliano baina ya familia na Gugai ya kuuziana kiwanja namba 64 kilichopo kitalu C cha Boko Ununio Dar es Salaam, kwa Sh milioni 80 na malipo yalifanyika kwa fedha taslimu. Alidai baada ya familia kufanya makubaliano na Gugai, Mwanasheria wake alienda kuandaa mkataba na walipofika nyumbani kwake jioni aliwapa na kuusoma kisha akawakabidhi fedha. Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa katika mkataba huo uliandikwa Sh milioni 60 tofauti na makubaliano lakini walikabidhiwa fedha taslimu Sh milioni 80.Aliendelea kudai katika mkataba huo uliofanyika nyumbani kwake akiwa na mwanasheria uliandikwa hivyo ili kuweza kupata ahuweni ya kodi. Baada ya maelezo hayo, shahidi huyo aliiomba mahakama kupokea mkataba wa mauziano ya kiwanja kama kielelezo baada ya kuutambua kwa majina na saini. Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Semi Malimi ulipinga kupokewa kwa mkataba huo wakidai kuwa ni nakala na sio nyaraka halisi ya mkataba.Alidai nyaraka yoyote inayotolewa mahakamani lazima iwe halisi kwa mujibu wa sheria kifungu 67 (1) na kama ni nakala yapo mazingira yanayoruhusu ipokewe. Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 11, mwaka huu atakapotoa uamuzi kama kielelezo hicho kipokewe au la. Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo hilo linamkabili Gugai.
kitaifa
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa duka kubwa la kampuni hiyo mjini Dodoma baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ili liweze kuwa la kisasa linalokidhi mahitaji ya mji mkuu.Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma pamoja na kuwapongeza kwa kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini, amewataka wakazi wa Dodoma kutumia nyenzo hiyo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi .“Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel na tunawaomba waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini. Tuko tayari kushirikiana Airtel katika kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za mawasiliano na hatimaye kuwa maisha bora,” alisema Dk Nchimbi.Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Adriana Lyamba alisema:”Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma mbalimbali. “ alisema.Aidha alisisitiza kwamba kupitia duka hilo wateja watapata huduma za pesa mkononi za Airtel Money ,intaneti na kuweza kununua muda wa maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na huduma nyingine nyingi.Lyamba pia alisema Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza Mbeya na Mtwara.Maduka mengine yaliyopo Morogoro, Bukoba na Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Septemba.
uchumi
WAENDESHA bodaboda nchini wametakiwa kutochukua sheria mkononi inapotokea watu wamesababisha ajali wakiendesha barabarani.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema hayo mjini hapa jana wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM). Salma alitaka kujua serikali inachukua hatua gani kuelimisha waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakichukua hatua za papo kwa hapo na kupiga watu waliosababisha tatizo au ajali.Salma alisema pamoja na bodaboda kuleta faida nyingi zikiwemo ajira, usafiri na maendeleo, kumekuwa na changamoto za kuchukua hatua mikononi mara watu wanaposababisha ajali. Masauni alisema waendesha bodaboda hawatakiwi kuchukua hatua wanaposababisha vifo ili waepuke kuingia katika mkono wa sheria wakipelekwa mahakamani na kufungwa.Masauni pia alijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Bhagwanji Maganlal Meisuria (CCM) aliyeuliza serikali ina mkakati gani kukomesha vitendo vya bodaboda kupora mali za abiria zikiwemo simu na mikoba ajalini.Masauni alisema waendesha pikipiki na bajaji wanaopora mikoba na simu za raia au abiria si wema bali wahalifu kama wahalifu wengine na hivyo Polisi wanatakiwa kuwashughulikia. Mbunge wa Musoma Mjini, Vedasto Manyinyi (CCM) alihoji lini serikali itatekeleza mkakati wa kupunguza tatizo la waendesha bodaboda kusababisha ajali za mara kwa mara na wizi. Masauni alisema vipo vyanzo vikuu vitatu vinavyosababisha ajali za barabarani nchini.Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni makosa ya binadamu ambayo huchangia kwa asilimia 76, ubovu wa magari asilimia 16 na mazingira ya barabara ambayo huchangia asilimia nane.Alisema makosa ya binadamu ni uendeshaji wa kizembe/ hatari, mwendo kasi, ulevi, uzembe wa wapanda pikipiki, wapanda baiskeli na watembea kwa miguu na sababu nyingine. Polisi inatoa elimu kwa waendesha boda namna nzuri ya utumiaji pikipiki ikiwemo kuvaa kofia ngumu, kukagua leseni kupunguza waendeshaji wasio na leseni wanaoweza kusababisha ajali.
kitaifa
Alisema asilimia 81 ya mabomba yameshawasili eneo la mradi kutoka China. Idadi ya mabomba inayohitajika ni 440 hali ambayo alisema inamfariji kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati. Aliongeza kuwa mabomba zaidi ya nusu (kilometa 265 ) yameshaunganishwa kati ya kilometa 542 ambazo ndio umbali wa Mtwara hadi Dar es Salaam.Mtaro ambao umechimbwa hadi sasa ni kilometa 114 kazi ambayo Pinda alisema inaendelea vizuri na inasimamiwa na wataalamu wazuri kutoka Afrika Kusini na nchini. Kuhusu ubora wa mabomba, Pinda alihakikishiwa na mtaalamu mwelekezi anayesimamia mradi huo kuwa yana ubora wa hali ya juu.“Hili la ubora linatuhakikishia tusiwe na wasiwasi, kwani hawa wataalamu wamekwenda hadi China, kukagua utengenezaji wa mabomba haya na kuridhika na ubora wao,” alisema Pinda.Aliongeza kuwa uhai wa mabomba hayo chini ya ardhi ni miaka 30, na yakifanyiwa matengenezo yana uwezo wa kudumu miaka 50 hadi 70. Jambo ambalo linaonesha mradi utadumu kwa miaka mingi.Awali akimpa maelezo Waziri Mkuu, Mhandisi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Baltazar Mroso alisema kati ya kazi zinazofanywa ni kuweka zege kwenye mabomba yatakayotandazwa baharini umbali wa kilometa 25.Alisema asilimia 85 ya kazi ya kutandaza mabomba inafanywa na Watanzania, hivyo mradi umesaidia kuongeza ajira nchini.Pinda alikagua kiwanda cha kusiliba mabomba baharini na ya maeneo ya ardhi oevu kwa saruji, alitembelea maeneo wanayochimba mtaro wa mabomba, alikagua eneo linapoibukia bomba la baharini litokalo Songosongo na sehemu mabomba yanakopindwa.
uchumi
WAKATI serikali ikiendelea na ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Mwanza yenye urefu wa kilometa 1,219 na pia kukarabati ile ya zamani maarufu kama `Reli ya Kati’, Shirika la Reli Tanzania (TRL), limetangaza kugeukia ujenzi wa reli za mijini, ikianza na Dar es Salaam na Dodoma.Lengo la reli hizo, limetajwa kuwa ni kuondoa msongamano katika maeneo ya mijini, lakini pia kuziunga sehemu zenye shughuli kuu za kiuchumi kama viwanda, ili kuweza kusafirisha bidhaa kwa urahisi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alipokuwa anazungumzia mikakati mbalimbali ya kuimarisha usafiri wa reli nchini. Alisema kwa Dar es Salaam, mbali ya kuimarisha safari za sasa za ndani ya Dar es Salaam na maeneo jirani kama Pugu, zitajengwa pia reli mpya kati ya Mbezi na Bagamoyo, nyingine itakwenda Mbagala, lakini itakuwepo pia ya kwenda Uwanja wa Ndege.“Mpango huu wa kuwa na mtandao mpana wa reli za mijini unalenga kukabiliana na foleni, hasa ikizingatiwa katika miji na majiji kunakuwa na watu wengi, hivyo kukwamisha katika shughuli zao na foleni.“Ndiyo maana tunaangalia uwezekano wa kuwa na mtandao wa reli, tukianza na Dar es Salaam na Dodoma. Haya mambo yapo katika mipango kwa muda mrefu, ila kwa sasa tunakwenda kutenda. Ni suala la muda tu,” alisema Kadogosa ambaye ofisi yake inajiandaa kufyatua jingo la ghorofa saba eneo la Ihumwa, jirani na mji mkuu wa kiserikali wa Dodoma.Aliongeza kuwa reli hizo zitasaidia pia usafirishaji wa bidhaa kutoka viwandani, kwani zitakuwepo pia zitakazoungwa na viwanda ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na malighafi. Tayari Dar es Salaam kuna safari za treni za ndani ya jiji, ya Tazara- Pugu-Mwakanga, ya Stesheni ya Dar es Salaam-Pugu na Stesheni ya Dar es Salaam-Ubungo, ambazo zimetajwa kusaidia wakazi wake kutumia muda mfupi wa safari tofauti na mabasi ya abiria.Aidha, kwa kutumia usafiri wa treni, abiria wengi wamekuwa wakisafirishwa kwa wakati mmoja. Mathalani, kwa safari moja, treni kati ya Stesheni-Pugu husafirisha zaidi ya abiria 2,000 kutokana na mabehewa yake kati ya 19 na 23. Behewa moja hubeba abiria kati ya 80 na 120 na safari huchukua kati ya nusu saa na saa moja, wakati kwa safari kama hiyo kwa basi, abiria huweza kutumia hata saa 3-4.
kitaifa
Mshambuliaji Elius Maguli anayekipiga klabu ya Dhofar inayoshiriki Ligi Kuu Oman ndiye aliyefunga bao hilo dakika ya 18 kwa shuti. Taifa Stars sasa itamenyana na Zambia katika mechi ya nusu fainali baada ya Zambia kuitoa Botswana juzi katika robo fainali nyingine.Baada ya kufungwa bao hilo, Afrika Kusini walibadilika na kufanya mashambulizi mengi katika lango la Tanzania, lakini washambuliaji wao walikosa umakini na kushindwa kufunga. Taifa Stars walirudi nyuma na kujihami huku wakitumia mashambulizi ya kushtukiza, hadi mapumziko hakukuwa na mabadiliko.Kipindi cha pili, Afrika Kusini waliingia kwa kasi na kulishambulia zaidi lango la Tanzania, lakini washambuliaji wake walipoteza nafasi nyingi. Kocha Salum Mayanga alifanya mabadiliko, dakika ya 49 kwa kumtoa Thomas Ulimwengu na kumuingiza Simon Msuva aliyeonekana kukaa na mpira na kuwasumbua mabeki wa Afrika Kusini.Afrika Kusini walilisakama lango la Taifa Stars mara kwa mara lakini safu ya ulinzi chini ya nahodha Himid Mao na Erasto Nyoni ilihimili. Kocha wa Stars, Salum Mayanga aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonesha juhudi kubwa uwanjani hata kupata matokeo hayo mazuri.Alisema wataendelea kucheza kwa nidhamu nusu fainali ili kutimiza lengo lao la kufika fainali na kutwaa ubingwa wa COSAFA. Maguli alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kukabidhiwa tuzo maalumu. Aliwashukuru mashabiki wa Tanzania waliojitokeza uwanjani hapo kuwashangilia.
michezo
Lulu aliye nje kwa dhamana atapanda kizimbani mahakamani hapo baada ya kusomewa maelezo ya awali karibu miaka miwili na nusu iliyopita. Msanii huyo anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu.Inadaiwa Lulu alimuua Kanumba bila ya kukusudia Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu huyo Sinza Vatican, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu Dar es Salaam jana, kesi hiyo itasikilizwa siku hizo na Jaji Sam Rumanyika. Kesi hiyo inaanza kusikilizwa baada ya kupangiwa Jaji kufuatia upelelezi kukamilika.Mara ya kwanza Lulu alipandishwa kizimbani Aprili 11, 2012 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam wakati huo, Augustina Mbando ambapo alisomewa mashitaka ya mauaji.Hata hivyo, Februari 18, 2014 akisomewa maelezo ya awali Lulu alikiri mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kusema kulikuwepo ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha mwigizaji huyo.Lulu aliachiwa kwa dhamana Januari 29, 2013 baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa Aprili 7, 2012 Sinza Vatican Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia. Lulu alipelekwa rumande gereza la Segerea hadi mashitaka yalipobadilishwa akapata dhamana.
michezo
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ametengua uteuzi wa nafasi ya Ofi sa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Paul Misuzi na wakuu wa idara za ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji.Hatua hiyo imekuja baada ya watendaji hao, kushindwa kutekeleza maagizo waliyopewa ikiwemo kushindwa kukusanya mapato ya serikali. Waziri huyo alichukua hatua hiyo katika kikao cha pamoja na watumishi wa idara ya ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji, kilichofanyika mjini Kigoma.Alisema kuwa watendaji hao, licha ya kushindwa kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa kwao, pia wameshindwa kuthibitisha uwezo wao wa kusimamia majukumu yaliyopo chini yao. Misuzi ni Afisa ardhi Mteule pekee kwa mkoa Kigoma, ambaye kitaaluma na kiutumishi, kwa mujibu wa taratibu za serikali, alikuwa na uwezo wa kusaini nyaraka kwa ajili ya mchakato wa utoaji wa hati za umiliki wa viwanja na majengo akiwa ameletwa mkoa Kigoma kwa mchakato maalum baada ya mkoa huo kutokuwa na Afisa Ardhi Mteule kwa muda mrefu.Pamoja na sifa hiyo na nafasi nyeti ya mtumishi huyo, naibu waziri huyo alisema kuwa Misuzi alishindwa kutekeleza mpango wa utoaji hati kwa waombaji, waliokuwa wakitaka kupatiwa hatimiliki za viwanja na majengo, licha ya kuwepo kwa maombi mengi kutoka kwa wananchi. Wengine waliotenguliwa katika sakata hilo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Brown Nziku na Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Emanuel Maghembe.Viongozi hao wanadaiwa kwa miaka miwili tangu mwaka 2017, Naibu Waziri alipotoa maagizo, wameshindwa kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na kuandika taarifa zenye visingizio lukuki, ambavyo vinathibitisha kuwa uwezo wao wa kiutendaji ni wa chini. Jambo moja kubwa ambalo lilimuudhi naibu waziri huyo ni kitendo cha watendaji hao waandamizi wa idara ya ardhi, kushindwa kusimamia makusanyo ya fedha za serikali kupitia kodi za ardhi wakati suala hilo liko kwenye uwezo wao.Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, walipanga kukusanya Sh bilioni 1.1, lakini kilichokusanywa ni Sh milioni 337. Naibu Waziri alisema kuwa watendaji hao, wameshindwa kutekeleza agizo la kuingiza kwenye mfumo wa malipo ya serikali ya ukusanyaji maduhuli viwanja vyote, ambavyo vimesharasimishwa kutokana na idadi ndogo ya viwanja ambavyo vimeingizwa kwenye mfumo huo, huku watendaji hao wakiwa hawajui takwimu za kiasi cha viwanja, ambavyo kiuhalisia vinapaswa kuingizwe kwenye mfumo huo.Kutokana na hali hiyo, naibu waziri alisema watendaji hao wamevuliwa hadhi na nyadhifa zao na watabaki kuwa watumishi na watendaji wa kawaida wa idara ya ardhi kwenye maeneo yao ; na nafasi zao zitatafutiwa watumishi wengine wa kuziongoza. Awali, Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Brown Nziku akitoa taarifa kwa naibu waziri alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2018, viwanja 15,529 vimeingizwa kwenye mfumo wa ukadiriaji wa kodi ya ardhi huku viwanja 43,000 vikiwa vimefanyiwa michoro na kupangwa.
kitaifa
IKIWA zimebaki siku tatu, kuanza kwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, Jiji la Dar es Salaam limeweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo katika mitaa mbalimbali.Aidha, uongozi wa mkoa, umeahidi kuwa kazi ya kutokomeza mifuko hiyo, haitakuwa ya nguvu wala usumbufu wowote na tayari vikosi kazi vimeshaundwa.Akizungumza jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa viongozi mbalimbali wa jiji hilo, Katibu Tawala wa Mkoa, Abubakar Kunenge amesema mkakati huo una maeneo manne yakilenga katika kusimamia sheria na kanuni ambazo zitasaidia katika kutokomezwa kwa mifuko hiyo ambayo ina madhara makubwa.Alisema katika kutekeleza mkakati huo, elimu kwa umma ni jambo litakalozingatiwa, usimamizi na uratibu, eneo ambalo mifuko hiyo itawekwa pamoja na usimamizi na pamoja na kufanya kazi na wadau mbalimbali.“Dar es Salaam inaendelea kutoa taarifa ya maelekezo kwa wananchi, pia tunaendelea kutayarisha mabango ambapo mpaka sasa yameshatayarishwa saba pamoja na manispaa mbalimbali,” alisema Kunenge na kuongeza kuwa magari yanaendelea kupita mitaani kuelimisha wananchi.Alisema elimu ni suala endelevu kwa wananchi na kwa kiwango kikubwa wameonesha utayari wa kuacha matumizi ya mifuko hiyo, hivyo agizo hilo ambalo lilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa litafanikiwa kwa kiwango kikubwa.Alisema katika eneo la usimamizi tayari vikosi kazi mbalimbali vimeundwa kwa ajili ya kuwajibika na kuripoti kuhusu suala zima la utekelezwaji wa udhibiti wa mifuko hiyo na wakuu wa wilaya watapita katika maeneo yao kuona yaliyopangwa na utekelezaji wake.“Wananchi wameelezwa mahali pa kuweka mifuko hiyo, kuna vituo mbalimbali vya kukusanya vipatavyo 137 na katika vituo hivyo, mifuko haitakiwi kukaa kwa muda mrefu,” alisema Kunenge na kufafanua kuwa katika vituo hivyo vitakuwa vimefungwa kuepuka upepo lakini pia kutakuwa na walinzi kuepusha wananchi kufika na kuchukua mifuko tena.Alisema katika maeneo mbalimbali watu wameshatenga maeneo kuanzia ngazi ya mtaa kwa ajili ya kukusanya mifuko hiyo na kwamba kazi ya kuondoa mifuko pamoja na kupiga faini haitegemewi kuwa ni chanzo cha ufisadi na taarifa zitatolewa mara kwa mara.Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kazi ya kuzuia matumizi ya mifuko hiyo haitakuwa ya kutumia nguvu wala usumbufu wowote.“Jiji hili ndilo linalozalisha na kutumia mifuko hiyo kwa kiwango kikubwa, tukiweza kupiga hatua kwa asilimia 60 itakuwa ni hatua kubwa imefanyika,” alisema.
kitaifa
WAKATI michuano ya soka ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, (Kombe la Kagame) ikianza leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la vyama vya soka ukanda huo, Cecafa, Nicholaus Musonye amesema viongozi wa vyama wanachama wanahujumu.Akizungumza na waandishi wa habari jana Musonye alisema wamejiandaa vizuri kufanikisha michuano hiyo inayoanza leo na kumalizika Julai 13 lakini hakusita kuweka wazi dukuduku lake kuwa viongozi wa vyama wanachama ndio wanaohujumu mashindano hayo kwa kuweka nguvu kwenye mashindano yenye fedha nyingi na kuacha kusapoti kazi ya kukuza michezo katika ukanda wao hali inayofanya kudorora.“Kuna mashindano yanayoendeshwa kwenye nchi zetu na viongozi wa vyama wanayakumbatia kwa sababu yana pesa nyingi na kusahau jukumu letu kama Cecafa la kuandaa mashindano ambayo ndiyo chimbuko la kuendeleza soka kwenye ukanda wetu, mimi nilikuwa Nairobi lakini sikwenda kuangalia,” alisema Musonye na kukataa kutaja amelenga mashindano gani.Pia Musonye alisema yeye amehudumu kwa muda mrefu kwenye Cecafa kama Katibu Mkuu lakini akitakiwa kuondoka ili waweke mtu mwingine yeye yupo tayari.“Kesho (leo) tutafungua mashindano rasmi na naamini tutafanya michuano bora na yenye wachezaji bora wanaoweza kupambana kwani kila timu hasa zile zinazoshiriki mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika zimeleta timu nzima,” alisema Musonye.Aidha Musonye aliziombea timu zilizojitoa kwenye mashindano hayo kwa madai ya kujiandaa na michezo ya kombe la Shirikisho Afrika kufika mbali na hata kutwaa ubingwa kwani hakupenda kuzitamkia maneno mabaya kwa wakati huu.Yanga na St George ya Ethiopia ndizo zilizojitoa kwenye michuano hiyo zikidai kutaka muda wa kujiandaa zaidi na michuano ya Afrika.Kaimu Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani alisema wamejiandaa ipasavyo kukamilisha michuano hiyo ya Kombe la Kagame.Michuano hiyo inazinduliwa leo ambapo mechi ya ufunguzi itakuwa saa nane mchana kati ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Vipers ya Uganda kabla Azam FC haijacheza na Kator ya Sudan Kusini na saa kumi jioni na saa moja usiku utachezwa mchezo wa Kundi C kati ya Singida United na APR ya Rwanda. Mechi zote zitachezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi.
michezo
SERIKALI imezitaka halmashauri zote zinazojenga hospitali za wilaya mkoani Lindi, zimalize kwa wakati uliopangwa bila kutoa sababu na kusababisha ujenzi wa hospitali hizo kuchelewa zaidi.Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo mwishoni mwa wiki wakati alipokagua Hospitali ya Wilaya ya Lindi inayojengwa katika kata ya Kiwalala. Ujenzi wa hospitali hiyo unagharimu Sh bilioni 1.5 zilizotolewa na serikali kuu.Waziri Jafo alisema katika halmashauri nyingi tayari fedha za ujenzi wa hospitali hizo za wilaya zimeshatolewa, hivyo ni vyema ujenzi wake ukamilike mapema bila sababu zisizo za msingi. Alisema amekuwa akipokea sababu nyingi kutoka kwa wakurugenzi kuhusu kutokamilika kwa wakati kwa ujenzi wa hospitali hizo, jambo ambalo kuanzia sasa hatolikubali tena.“Unasikia mkurugenzi anakuambia njia ilikuwa haipitiki, mara maji shida, hizi ni baadhi ya sababu nyingi tu ambazo hazina athari ya kusababisha mradi usiishe kwa wakati unaotakiwa,”alisisitiza. Alisema ni lazima majengo saba ya hospitali mkoani humo yakamilike haraka hadi kufikia Juni 30, mwaka huu, ili wananchi wapate huduma safi na ya karibu ya afya.“Sitamvumilia mkurugenzi yeyote yule anitolee sababu za ujenzi wa hospitali uchelewe kukamilika, mimi sitamuelewa kabisa,’’ alisema. Pamoja na hayo, Waziri Jafo alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea katika hospitali hiyo ya Lindi ambao umefikia katika hatua ya kuezeka bati. Aliimpongeza Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kwa kazi aliyoifanya ya kufuatilia hospitali hiyo mpaka kujengwa hapo Kiwalala wilayani Lindi.Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya, Dismas Masulubu alisema serikali kuu ilishatoa Sh bilioni 1.5 na mpaka sasa zimeshatumika Sh milioni 950. Alisema ujenzi wa hospitali hiyo ulianza Januari na unatakiwa ukamilike Juni 30, mwaka huu ambapo majengo saba, kati ya 22 ya hospitali hiyo yanayotakiwa kujengwa mwaka huu.Dk Masulubu alisema majengo hayo saba yanahusisha pia jengo la wazazi, mapokezi, maabara, x-ray, kufulia nguo, upasuaji na jengo la watoto wachanga. Diwani wa Kiwalala, Mohamedi Chilumba alisema tangu kuanzishwa wilaya ya Lindi mwaka 1983 haijawahi kuwa na hospitali ya wilaya.
kitaifa
['Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars hii leo imeandikisha sare 1-1 na timu ya taifa ya Burundi Intamba Murugamba katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia nchini Qatar 2022.', 'Licha ya kutawala kipindi cha kwanza cha mchezo Tanzania ilishindwa kuona lango la wenyeji wao huku washambuliaji hodari Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya Genk nchini Ubelgiji na Simon Msuva wakishindwa kuwika katika lango la Burundi.', 'Kipa wa Burundi Jonathan alikataa katakata kufungwa na wachezaji hao wawili kupitia uokoaji wa hali ya juu.', 'Udhaifu wa Burundi ulionekana katika utoaji pasi sawala lililopelekea kipindi cha kwanza kukamilika kwa sare tasa.', 'Burundi hatahivyo ilitawala kipindi cha pili cha mchezo mbele ya mashabiki wao baada ya kocha wake Olivier Niyungeko kufanya baadhi ya mabadiliko miongoni mwa wachezaji wake.', 'Mbwana Samatta alikosa bao la wazi akiwa amesalia na kipa wa Burundi aliyepangua shambulizi lake na kuisaidia pakubwa Intamba Murugamba.', 'Hatahivyo kunako dakika ya 81 ni Burundi ndio ilioanza kuona lango la wageni wao kupitia mchezaji Cedric Hamissi anayechezea soka yake nchini Tanzania ambaye alipokea pasi muruwa kutoka kwa Mohamed Amissiwari aliyeingia katia nafasi ya Bienvenue kanakimana.', 'Hatahivyo Tanzania waliimarisha mashambulizi yao kunako dakika hizo za lala salama na haikuchukua muda mrefu wakati Simon Msuva aliposawazisha dakika tatu baadaye.', 'Mechi ya marudio iutachezwa nchini Tanzania wikendi ijayo tarehe 8 mwezi Septemba.', 'Mshindi wa mechi hiyo atafuzu kwa raundi ya pili ya michuano hiyo.']
michezo
AZAM FC jana ilikata tiketi ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba,Kagera.Katika mchezo huo bao pekee lililoifanya Azam kusonga mbele liliwekwa kimiani na Joseph Mahundi dakika ya 79 baada ya kuwatambuka mabeki wa Kagera na kuachia shuti hafifu lilomshinda mlinda mlango wa Kagera Jeremia Kisubi. Azam sasa inaungana na timu za Lipuli FC na KMC kufika hatua hiyo. Robo fainali ya mwisho inatarajiwa kuchezwa leo kati ya Yanga na Alliance.Na baada ya kupata ushindi huo Azam wanatarajiwa kukutana na KMC, kwenye hatua inayofuata ya nusu fainali. Mchezo wa jana ulianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa wakihofia kuruhusu bao la mapema kwenye lango lao lakini mpaka mapumziko hakukuwa na timu iliyoliona lango la mwenzake.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kila timu ikifanya mabadiliko wakiwa na matarajio ya kubadilisha mchezo ili wapate matokeo mazuri . Azam ililazimika kumaliza mechi pungufu baada ya mlinda mlango wake Razak Abarola kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Kagera Sugar nje kidogo ya eneo la hatari.
michezo
SAKATA la askari polisi wanane wanaodaiwa kujihusisha na kashfa ya utoroshaji dhahabu jijini Mwanza, limetua rasmi kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz.Askari hao ambao Januari 4, mwaka huu, waliwakamata watu waliotaka kutorosha kilo 323.6 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 30 na fedha taslimu Sh milioni 305, walitaka wapewe Sh bilioni 1 kutoka kwa watuhumiwa hao. Baada ya mpango wao huo kukwama kutokana na mamlaka za nchi kuingilia kati na watuhumiwa kutiwa mbaroni na askari wenzao, kinachoendelea kwa sasa ni uchunguzi wa suala hilo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.DCI Boaz, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, alisema ofisi yake itakamilisha upelelezi wa jambo hilo hivi karibuni. Alisema kuwa upelelezi unaoendelea, utawasaidia kujua ni makosa ya aina gani watuhumiwa hao wanane, wanakabiliwa nayo ili mashitaka dhidi yao yaweze kufunguliwa. Alisema kwa kuwa watuhumiwa hao ni askari, watapelekwa kwanza kwenye Mahakama ya Kijeshi kwa ajili ya mashitaka ya kinidhamu na kama kutakuwa na jinai yoyote dhidi yao, ndipo watakapopelekwa kwenye Mahakama za Kiraia.Wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, akiwemo Waziri wa Madini, Doto Biteko, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, katibu tawala mmoja na makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Rais John Magufuli aliwaeleza Watanzania mpango mzima ulivyokuwa. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, askari hao baada ya kuwakamata watuhumiwa, waliwafikisha Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza, lakini hawakushushwa kwenye gari, badala yake walichokifanya ni kuwataka watuhumiwa wawepe Sh bilioni 1.Baada ya majadiliano yao, watuhumiwa katika mkupuo wa kwanza, waliwapatia askari hao Sh milioni 300, mkupuo wa pili wakawapa Sh milioni 400 na kuahidi kumaliza mkupuo wa tatu wa Sh milioni 300 watakapofika wilayani Sengerema. Wakiwa njiani kuelekea Sengerema, ndipo walipokutana na kizuizi cha polisi njiani na watuhumiwa wote wakiwemo askari hao wanane wakatiwa mbaroni. Kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na jeshi hilo, Rais Magufuli alimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kwa kazi nzuri iliyofanyika.Ili kufanikisha kazi hiyo ya kufuatilia utoroshaji wa dhahabu na madini mengine nchini, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamanda Ahmed Msangi, alisema kuwa msingi wao mkubwa wa kufanikisha kazi hiyo ni wananchi. Alisema Jeshi la Polisi litafanya kazi kwa karibu na wananchi, ikiwemo kuwapatia elimu ili wananchi hao waweze kushirikiana na jeshi hilo, kwa kutoa taarifa kuhusu utoroshaji huo.
kitaifa
AGIZO la Rais John Magufuli la kumtaka Msajili wa Hazina kuyabana mashirika ya umma ili kulipa gawio kwa serikali, hatimaye ofisi hiyo imevuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 633.39 hadi kufikia Juni mwaka huu, sawa na asilimia 106.Fedha hizo zinatokana na makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka katika taasisi, mashirika na kampuni ambazo serikali ina hisa.Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka amesema wamevuka lengo ambalo waliliweka la kukusanya Sh bilioni 597.77 mwaka huu.“Kwa mwaka 2019 tulijiwekea lengo la kukusanya Sh bilioni 597.77 lakini hadi Juni 21, mwaka huu, tulikuwa tumeshavuka lengo kwa sababu tumekusanya zaidi ya Sh bilioni 633, sawa na asilimia 106 hadi sasa na bado tunaendelea kukusanya,”alisema Mbuttuka.Akizungumzia idadi ya mashirika na taasisi hizo zinazotoa gawio, Mbuttuka alisema zimeongezeka kutoka 13 mwaka 2015 hadi kufika 28 mwaka 2018 na kwamba uchangiaji wa mapato umeongezeka.Akifafanua mgawanyiko wa taasisi hizo na aina ya uchangiaji unaotolewa, Mbuttuka alisema taasisi hizo zimegawanyika katika sehemu kuu tatu: Sehemu ya kwanza ni gawio linalotoka katika mashirika ambayo serikali inamiliki kwa kiasi kikubwa na kampuni ambazo serikali ina hisa chache na kwamba gawio hilo hulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Hazina ya Madaraka.Sehemu ya pili ni michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi kutoka katika taasisi za serikali, ambao unalipwa kwa mujibu wa Kifungu cha 47 cha Sheria ya Fedha Namba 15 ya mwaka 2015 iliyorekebisha Sura ya Msajili wa Hazina Sura ya 370.Sehemu ya tatu ni makusanyo mengineyo ambayo yanajumuisha marejesho ya ziada, marejesho ya mikopo na riba kutokana na serikali kukopesha mashirika (on-lending) na makusanyo ya Mtambo wa Kuhakiki Mawasiliano ya Simu (TTMS).Alisema makusanyo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kuimarika kwa utendaji wa mashirika pamoja na jitihada za Ofisi ya Msajili wa Hazina katika kufuatilia mapato husika.Pamoja na kuimarika kwa makusanyo na utendaji wa mashirika, Mbuttuka alisema kumekuwa na baadhi ya mashirika hayafanyi vizuri na kwamba, jitihada zimefanyika ikiwa ni pamoja na kuimarisha utendaji wa bodi za wakurugenzi na menejimenti.Aidha amezielekeza taasisi hizo, zijikite katika majukumu ya msingi ya uanzishwaji wake kwa kuwa amebaini baadhi ya mashirikia hayo yamekuwa yakitoka nje ya kazi za msingi ambazo zimesababisha athari zisizo za lazima.Pia hatua kadhaa zimechukuliwa, ikiwemo kuongeza mitaji kwa mashirika stahiki baada ya uchambuzi na kujiridhisha na uhitaji huo na mfano halisi ni Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Benki ya Rasilimali nchini (TIB).Alisema hatua nyingine zilizochukuliwa ni kupunguza, kuunganisha na kuhamisha majukumu yanayofanana baina ya taasisi na mashirika ya umma ili kuongeza tija na kupunguza mzigo kwa mashirika hayo.“Tutaendelea kuboresha na kuyapitia mashirika yote yanayotuhusu ili tuone jinsi ya kuyaboresha na yale yasiyoweza tutatafuta njia nyingine ambazo tumeanza kufanya kama ni kuyaunganisha, lengo ni kupata matokeo bora zaidi, lakini kubwa ni kuhakikisha utawala bora unazingatiwa na watumishi wote,” alisisitiza Mbuttuka.Mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa anamuagiza Msajili wa Hazina, kuzibana kampuni za umma zisizolipa gawio serikalini.Mara ya mwisho ilikuwa hivi karibuni wakati akipokea gawio la Sh bilioni 2.1 kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
uchumi
SERIKALI imetoa tahadhari kwa shule 108 za msingi, sekondari na za ufundi kwa kushindwa kukidhi matakwa ya wizara hiyo.Ripoti mpya ya Wizara ya Elimu inasema shule hizo zimebainika kutokidhi viwango vya usafi, matumizi mabaya ya ruzuku, kushindwa kutoa elimu na matumizi mabaya ya vifaa vya teknolojia ya mawasiliano.Hatua hiyo ni mikakati ya wizara kuhakikisha shule zinafuata vigezo vya kutoa elimu bora. Agosti mwaka huu, wizara ilisitisha huduma za shule 57 nchini lakini baadaye zilifunguliwa baada ya kukidhi matakwa ya wizara.Waziri wa Elimu, Eugene Mutimura, alisema serikali haitawavumilia viongozi wa shule zilizoshindwa kufikia viwango. “Kuna shule ambazo hazitafunguliwa Januari ikiwa watashindwa kukamilisha yale waliyoshauriwa wakati wa ukaguzi,” alisema.Aliongeza kuwa shule 31 zilikaguliwa kutokana na matumizi mabaya ya rasilimali za serikali, huku nyingine 17 zikitakiwa kupewa ushauri katika utoaji elimu. Takribani shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi na taasisi za elimu ya juu 900 zilikaguliwa, hivyo hawatawaeleza nini wafanye bali kutimiza wajibu wao katika nyanja zote.
kimataifa
TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya nchi hizo, lengo likiwa kufungua milango zaidi ya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).Mbali ya Tanzania na Uganda, nchi nyingine wanachama wa EAC, jumuiya yenye wakazi zaidi ya milioni 170 ni Kenya, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo hivi karibuni jijini Kampala, Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia masuala ya EAC, Dk Philemon Mateke alisema jukwaa linatarajiwa kuwa `daraja’ muhimu katika sekta ya biashara baina ya Tanzania na Uganda.“Hatuna sababu za kutofanya biashara kwa uwazi na kisasa zaidi kwani nchi zote hizo zimetengeneza mazingira mazuri ya biashara. Nchi zote zina amani, miundombinu mizuri na kadhalika.Ni wakati wa kuchangamka kibiashara,” alisema Dk Mateke. Kutokana na kuzinduliwa kwa jukwaa hilo, alisema kwa siku mbili kuanzia Septemba 4 mwaka huu, wadau muhimu watakutana Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yatakayoboresha ustawi wa biashara. Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Richard Kabonero alisema mkutano huo utafanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), ukiwa na kaulimbiu ‘Ukuzaji Biashara na Uwekezaji kwa Ukuaji na Maendeleo Endelevu’.Miongoni mwa washiriki watakuwa viongozi wa taasisi za kibiashara, watunga sera, wadau wa biashara na wengine, ili pamoja na mambo mengine kuchambua fursa zilizopo baina ya nchi hizo mbili na jinsi zinavyoweza kuleta neema kwa watu wa mataifa hayo.Alisema wakati wa mkutano, watazungumza pia na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania, Dk John Magufuli juu ya masuala mbalimbali na changamoto za kibiashara baina ya nchi zao. Naye Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Aziz Mlima, alisema mikakati ya kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo mbalimbali inafanyiwa kazi ili kutengeneza mazingira bora ya biashara.
kitaifa
WAHADHIRI wa vyuo vya elimu ya juu wameunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kwamba baadhi ya shahada zinazotolewa na vyuo vikuu sasa hazina hadhi bali wanafunzi wanamaliza vyuo ili kupata vyeti.Aidha wameshauri kufanyika kwa maboresho ya elimu na kuwe na msukumo wa kuwajali walimu kimaslahi lakini pia kuwaendeleza kitaaluma.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wasomi hao wamesema tatizo la shahada za ‘kudesa’ katika vyuo vikuu nchini ni kubwa na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha nchi inapata wasomi wazuri wanaomaliza vyuo na vyeti vinavyolingana na elimu waliyoipata.Juzi Rais Magufuli akizindua Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha shahada wanazotoa zina viwango vya juu na si shahada za ‘kudesa’ na kuwataka wahadhiri kuwa wakali.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Frank Tillya alisema walimu wanaowafundisha wanafunzi hao nao pia wanachangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa elimu ya vyuo vikuu."Walimu nao wanachangia kwa kiasi kikubwa, wengi hawana maadili kwa sababu kama una maadili huwezi kukubali kuona mwanafunzi anatoka hajui kitu, wanafunzi wengi wanatoka hawana kabisa quality (kiwango) ya shahada kwa sababu hawakufundishwa kufikiri," alisema.Alisema wanafunzi wengi wanafanya tu mitihani ili kufaulu, lakini elimu yao haiakisi hadhi ya shahada hata wanapomaliza vyuo, jambo ambalo linaleta changamoto katika kupata kazi kwani wanakuwa hawana uwezo wa kushindana."Hata ukiangalia 'interview' za kazi utabaini tatizo kubwa kwani vyeti wanavyokuja navyo vinakuwa na ufaulu mkubwa lakini wanapohojiwa unabaini kichwani hawana ujuzi unaofanana na ufaulu wao,” alisema.Dk Frank alisema ingawa Rais Magufuli hakueleza kwa kirefu ukubwa wa tatizo hilo, lakini ni suala linalohitaji mjadala wa kitaifa ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema shahada ya sasa haimfanyi mhitimu kupata uwezo wa kuchanganua mambo wala kufikiri kwa mapana."Hili ni tatizo la kitaifa sijui tumejikita zaidi katika elimu nyingine, kijana amehitimu chuo lakini ukimwambia akuandikie barua au mpe habari ya kurasa tatu mwambie aifupishe hawezi," alisema Dk Bana.Hata hivyo, Dk Bana alisema moja ya sababu ya kushinda kuimarika kwa kiwango cha elimu ni mfumo wa elimu ya juu ambao alisema hauvidhibiti vyuo kuzalisha elimu bora kwa kiwango cha kutosha.Aidha alisema baadhi ya walimu wanatekeleza wajibu tu lakini hawana moyo wa kuwasaidia wanafunzi kupata maarifa na wengine hawana sifa kabisa za ualimu ambapo alishauri kufanyike maboresho ya elimu ya juu.Alisema elimu ya vyuo vikuu inashuka hasa vyuo vinavyoanzishwa sasa na kwamba mwanafunzi anavyojibu mtihani wake na alama anazopewa na mwalimu wake havilingani na kwamba wanafunzi wanataka matokeo mazuri bila kuyasumbukia.Na aliyewahi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwete amesema uongozi wa vyuo uwe tayari kushughulikia tatizo hilo ili kuongeza ubora wa elimu nchini.Alisema tatizo hilo lipo katika vyuo vingi kwani wanafunzi wengi hawana bidii ya kujisomea ili kupata maarifa badala yake wanataka kuhitimu ili wapate vyeti safi vya kwenda kutafutia ajira.
kitaifa
BAADA ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, Yanga wametamba kuifunga Pyramids katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga watashuka dimba CCM Kirumba Jumapili kuikaribisha Pyramids ya Misri katika mchezo wa ply-off wa kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.Timu hizo zinatarajia kurudiana Novemba 3 Misri. Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila (pichani) alisema kwa sasa akili na nguvu zao zote wanazielekeza katika mchezo huo wa Jumapili na wana matumaini makubwa ya kushinda, Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka wa timu yao wajitokeze kwa wingi katika kuipa timu yao sapoti iweze kufanya vizuri zaidi na kurahisisha njia yao ya kufuzu.Akielezea kuhusu mchezo wao dhidi ya Mbao FC,Mwandila alisema mchezo huo ulikuwa ni mgumu sana, lakini timu yake ilicheza vyema kwa kupambana zaidi na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.Aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kuibuka na ushindi licha ya ugumu wa mchezo huo. Alisema wapinzani wao wa Mbao FC walipambana pia huku akiwa na matumaini ya timu yake kupambana Jumapili na kupata matokeo mazuri. Alisema ushindi wa Mbao FC ni kiashiria kuwa timu yake itaifunga timu ya Pyramid FC kutoka nchini Misri.Kwa upande wake nahodha wa timu ya Yanga Pappy Tshishimbi alisema wamejipanga kuhakikisha na wanapata ushindi katika mchezo wa Jumapili na ule wa marudiano nchini Misri ili kutinga makundi.
michezo
KUPITIA Mfumo wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) Serikali imepata zaidi ya Sh bilioni 93.6 fedha ambazo kama sio mfumo huo zingekuwa kwenye mifuko ya watu.Takwimu hizo zilitolewa Dar ea Salaam jana na Rais John Magufuli wakati akikabidhiwa rasmi mfumo huo ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuthibiti mawasiliano pamoja na mapato ya huduma ya Mawasiliano ya simu hapa nchini. Rais Magufuli alisema:“Bila kuwa na mfumo huu huwezi kuhakiki mapato yatokanayo ya Mawasiliano ya simu, TRA hawakuweza kukusanya kodi iliyostahili, mtambo huu unahakiki mapato.”Mfumo huo ulikabidhiwa na Kampuni ya TMS na GBG kwa TCRA ambapo Rais Magufuli alisema sasa kila kitu kiko wazi katika sekta hiyo kwani hakuna fedha itakayopotea.Alisema kupitia mfumo huo kampuni za kutoa huduma ya mawasiliano pia zimenufaika kwa kupata Sh Bilioni 173.93 na mkandarasi Sh bilioni 53.52 na Sh bilioni 13.3 wamepata TCRA kupitia simu za kimataifa.Rais Magufuli aliipongeza TCRA kwa kazi wanayoifanya sasa kwani alipoingia madarakani hakupendezwa na utendaji kazi wao palikua na mchezo mbaya. “Palikua na mchezo mbaya sana, Tanzania tumeibiwa mno, tumechapwa ukweli, tumeliwa kweli, tumedhulumiwa vya kutosha,” alisema.Alisema 2015 alipoingia madarakani aliamua kuutafuta mkataba wa wakandarasi hao ambapo mkataba halisi ulifichwa na kuwa kipengele kilichohusu kukusanya fedha kwenye kampuni za mawasiliano kilifichwa hivyo ilibidi atumie vyombo vya ulinzi akaupata mkataba huo.“Nilichofanya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Simba nikatengua uteuzi wake nikamtoa kwanza tukapeleka mabadiliko kwenye Bunge na Spika na watu wake wakakiweka kipengele kilichokua kimefutwa kwa ujanja ujanja uliofanywa na baadhi ya viongozi waliokuepo serikali ni,” alisema Rais Magufuli.Alisema baadaye mkandarasi aliamriwa kurudi kukamilisha kipengele kilichofichwa kwenye mkataba na baada ya kutimiza sasa wamekabidhi kazi. Rais Magufuli alisema aliongeza mkataba wa miaka mitano zaidi kwa mkurugenzi Mkuu wa TCRA ili aendelee kufanyia kazi mfumo huo.Alisema takwimu za kidunia zimeonesha kuwa sekta ya Mawasiliano ni nyeti na muhimu na inakua kwa kazi duniani, zaidi ya watu bilioni tano wanatumia simu duniani kote na wanaotumia data ni milioni 3.9 na kwa Tanzania, wanaotumia simu ni zaidi ya watu milioni 42.“Biashara nyingi ya rejareja zinaendeshwa kwenye mitandao na kwa mwaka 2017 biashara hiyo iliyofanyika kwenye mitandao zilikua na thamani ya dola za Marekani trilioni 2.3 kupiku biashara za kwenye maduka makubwa na maduka ya kawaida,” alisema rais.Aidha alisema sekta ya mawasiliano imewezesha kupatikana kwa huduma ambazo awali hazikuwepo mathalani afya, elimu, usafiri wa teksi, kibenki ambapo zaidi ya watu milioni 20 wamejiunga na huduma za kibenki mitandao na pia ndio uliosaidia serikali kufingia simu hafifu milioni moja na kufahamu vifaa vyote vinavyotumia mtandao.Alisema sekta hiyo imetoa ajira zaidi ya milioni 28 za moja kwa moja na kufanya sekta hiyo kuitwa kisima kipya cha mafuta au mgodi wa madini. Hata hivyo, alisema sekta hiyo inachangamoto zake ambazo ni pamoja na uhalifu wa mtandao na kuathirika mila na desturi.“Kukabiliana na changamoto hizi serikali imekua ikianzisha mamlaka na mfumo mbali mbali kudhibiti na sisi tumeanzisha mamlaka kutunga sera, sheria na kuweka miundombinu pamoja na mfumo huu wa TTMS kufatilia takwimu za Mawasiliano,” alisema.Rais Magufuli pia alitoa mwito kuujengea uwezo mfumo huo na kuusimamia isitokee yaliyotokea katika mfumo wa kukusanya kodi wa TRA, EFD. “Wote tunajua yaliyotokea katika mfumo wa EFD, mtambo haukua Tanzania lakini sasa tumebadili uko hapa nchini nchini ya Wizara ya Fedha,” alisema.Rais aliagiza pia taasisi zote za serikali ambazo zinahusika na ukusanyaji mapato ya serikali kutengeneza mfumo wa kukusanya mapato na pia kuunganishwa na mfumo wa taifa. “Kati ya taasisi 667 ni taasisi 339 tu zimeunganishwa, Waziri wa fedha nataka uwaandikie barua nakala apewe Waziri Mkuu na mimi nipewe nakala yangu ili niweze kufuatilia,” alisema.Rais Magufuli pia aliwashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kumuombea na kuongeza kuwa vita ya uchumi inahitaji maombi na kuwa matatizo yaliyopo sasa serikali hii isipoyatatua hayatatatuliwa tena. Akizungumzia mfumo huo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema kukamilika kwa mfumo kumewezesha kuonesha taarifa mbalimbali zinazopita katika Mawasiliano hapa nchini.Aidha, alisema Mfumo unaiwezesha TCRA kupata takwimu za Mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje, kuhakiki mapato ya watoa huduma, kupata takwimu zinazohusiana na huduma za mawasiliano ya sauti, data na ujumbe mfupi, kubaini Mawasiliano ya ulaghai, kutambua takwimu za fedha za mitandaoni na kusimamia ufanisi na ubora zaidi viwango vya mawasiliano kwenda kwa watoa huduma, kuwasililisha mapato ya Mawasiliano ya kimataifa.“Toka mwaka 2013 mfumo ulipoanza kufanya kazi mpaka Septemba 2018 serikali imepata chanzo kipya cha Mawasiliano yanayotokana na Mawasiliano ya kimataifa zinazoingia na kuishia hapa nchini na kiasi cha Sh bilioni 93 ziliwasilishwa serikalini,” alisema.Aidha alisema pato la kodi limeongezeka na kwamba simu za kimataifa zilikua zinaingia kiulaghai. Mfumo umewezesha kubaini watu wenye mfumo mingine ya ulaghai kuingiza simu za nje kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, sasa simu zinazoingia kwa njia za ulaghai ni asilimia kumi wakati awali zilikua zaidi ya asilimia 60.Malaba alisema sasa TRA na BOT zinapata taarifa ya kiasi cha fedha na kuwa awali zilikua Sh trilioni nane kwa mwezi na kwa mwaka jana kufikia Sh trilioni 11. Mkurugenzi huyo aliahidi wataendelea kuboresha mfumo huo kutanua wigo ili kuendelea kutoa huduma na kuongeza mapato kwa serikali ambapo aliahidi mamlaka hiyo kuutunza mfumo wa TTMS.Alisema chimbuko la kuanzishwa mfumo huo ni Bungeni baada ya malalamiko ya gharama za simu zinazoingia nchini kushuka kila kukicha hali ambayo ilipunguza mapato kwa watoa huduma na pia kodi kwa serikali na mchango katika uchumi.“Ilionekana hitaji la mfumo huu, TCRA ilisimamia manunuzi ya mfumo huu na Machi 22, 2013 kwa lengo la kutekeleza mradi ikiwa ni kujenga kuendesha na kuhamisha umiliki Octoba mosi 2013 mkataba wa miaka mitano Septemba 2018 mkataba huo umemaliza muda wake,” alisema.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema gharama ya kuunganisha mitandao imepungua kutoka Sh 30.58 iliyokuwepo mwaka 2015 hadi kufikoa Sh 10 kwa dakika kwa mwaka huu na itaendelea kupungua ifike Sh mbili mwaka 2022.Alisema ilani ya Chama cha Mapinduzi ilielekeza kulinda wananchi dhidi ya wizi wa mtandao ambapo wanaendelea kusajili kwa kutumia alama za vidole kuendelea kuzuia wizi huo.
kitaifa
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Bangata, wilayani Arumeru, Michael Silamoi kwa tuhuma za kumshambulia hadi kumsababishia kifo mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho.Mbali na Mwenyekiti huyo, wengine wanaoshikiliwa ni askari mgambo wawili wa kijiji hicho waliofahamika kwa majina ya Balozi Andrea na Wariael Obedi pamoja na mkazi mwingine aliyefahamika kama Onesmo Siyoi.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), Hassani Omary akizungumza na gazeti hili jana alithibitisha Mwenyekiti huyo na wenzake watatu kuendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa tangu kukamatwa kwao Januari 8, mwaka huu.“Ni kweli Mwenyekiti wa kijiji cha Bangata na wenzake watatu tunaendelea kuwashikilia kwa tuhuma za kumpiga hadi kusababisha kifo cha Stalei Samwel (29) kilichotokea Januari 3, na jalada la kesi hiyo tumeshalipeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria,” alisema.Mkuu huyo wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha aliongeza kuwa watuhumiwa hao hawawezi kuachiwa kwa dhamana kutokana na kuwa wanatuhumiwa kwa mauaji na kinachosubiriwa ni taratibu zikamilike ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo, baba mzazi wa marehemu huyo, Samwel Lukumay (77), alisema kuwa kijana wake alikamatwa na mwenyekiti huyo akiwa na watuhumiwa hao wanaoshikiliwa na Polisi pamoja na mwenyekiti wa usalama wa kijiji hicho, Nuruel John ambaye alitoroka baadaye.Alisema kuwa kijana wake alifungiwa katika ofisi ya kijiji na kuanza kushambuliwa na watuhumiwa hao na kwamba chanzo cha tukio hilo ni mwanawe kudaiwa kumjeruhi mmoja wa wanakijiji.Alisema viongozi hao walimjeruhi mwanawe sehemu mbalimbali za mwili wake na kufikia kumnyoa nywele zake kwa kutumia panga, hali iliyosababisha hadi ngozi ya kichwa kutoka.Mzee huyo aliongeza kuwa baada ya viongozi hao kuona hali ya kijana wake ni mbaya walimpeleka katika Kituo cha Polisi Baraa wakidai kuwa alikuwa ni mwizi na kwamba alishambuliwa na wananchi wenye hasira kali jambo ambalo polisi walilitilia shaka na kutoa PF3 ili akapatiwe matibabu kutokana na hali yake aliyokuwa ambapo alifariki
kitaifa
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars Juma Mgunda amesema wanakwenda Sudan kupindua matokeo na kukata tiketi ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani zitakazofanyika Cameroon mwakani. Taifa Stars ikiwa kwenye nyumbani ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Sudan na kujiweka kwenye wakati mgumu wa kufuzu kwa mara ya pili kwenye fainali hizo ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni mwaka 2009. Mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Mbrazili Marcio Maximo Taifa Stars ilifuzu kwa mara ya kwanza fainali hizo kwa kuifunga Sudan ambapo kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kabla ya kwenda kupata ushindi mwingine wa mabao 3-1, Kartoum. “ Nawaomba watanzania wawe na subira na watusamehe kwa matokeo tuliyopata, bado tuna nafasi kubwa kwenye mchezo wa marudiano kwa kusahihisha makosa tuliyofanya na kwenda kupindua matokeo ” alisema Mgunda.Mgunda, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na Coastal Union alisema kiuhalisia matokeo waliyopata sio mazuri hasa ukichukulia walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani.“Tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa bahati mbaya hatukuweza kuzitumia. Usipotumia nafasi unazopata wenzako wakipata wanakuadhibu.“Nawaomba mashabiki wawasamehe wachezaji kwani na wao ni binadamu ila nina imani tunaenda kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano,”alisema Mgunda ambae pia ni kocha wa Coastal Union ya Tanga. Taifa Stars itarudiana tena na Sudan mwezi ujao mchezo utakaopigwa Uganda kufuatia nchi ya Sudan kuwa kwenye machafuko ya kisiasa. Kabla ya kukutana na Sudan, Taifa Stars iliitoa timu ya taifa ya Kenya kwa mikwaju ya penalti, baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika michezo yote miwili.
michezo
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amewataka wahitimu wa shahada za ualimu, kujiandaa kisaikolojia kufundisha shule za msingi, badala ya sekondari kama walivyotarajia.Alisema hayo juzi kwenye mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Elimu Mkwawa (MUCE), Iringa baada ya kuwatunuku wahitimu shahada.Alisema, serikali hivi sasa inawapeleka walimu waliohitimu shahada za ualimu, kufundisha shule za msingi, jambo ambalo halikupokelewa vyema na walimu, wakidai kushushwa hadhi, kwa kuwa waliamini stahili yao ni sekondari. Tunaungana na wadau wa elimu, kumpongeza Dk Kikwete kwa kuwaasa walimu kujiandaa kufundisha shule za msingi, kwani mwelekeo wa serikali sasa ni mapinduzi ya viwanda na mapinduzi ya elimu.Ni matarajio yetu walimu waliohitimu juzi na waliohitimu zamani, sasa wameelewa vyema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha elimu ya msingi na kujenga msingi bora wa elimu ya juu. Ni vizuri wakauelewa na pia kuupokea vyema mpango huo wa serikali, unaolenga kuboresha elimu ya msingi na pia kuwahakikishia ajira kubwa wahitimu wa ualimu kutokana na shule za msingi, kuhitaji walimu zaidi wenye shahada.Kwa wasioelewa maana ya mpango huo ni vyema wakarejea kauli ya Rais mstaafu Kikwete kuhusu mabadiliko, ambayo mfumo wa elimu nchini umepitia tangu ukoloni hadi leo. Kimsingi, mpango huo umelenga kuboresha utoaji wa elimu ya msingi ili kwenda na wakati, teknolojia na utandawazi kuziba pia ombwe la walimu wa darasa la saba (UPE), kidato cha nne (Daraja C) na wa diploma walioostaafu au kufa.Kwa kuwa elimu yetu inapita katika vipindi na mfumo tofauti, ni vizuri wahitimu wa ualimu wakaelewa mantiki ya serikali kuamua walimu wenye shahada, wakafundishe shule za msingi ili kuboresha taaluma ili tushindane na nchi za nje. Wazazi, walimu, wadau wa elimu na wanafunzi ni mashahidi wa malalamiko kuhusu ubora wa elimu inayotolewa, kufuatia baadhi ya wahitimu kutokidhi matarajio ya viwango vya waajiri. Malalamiko hayo yakiwemo ya wahitimu shule za msingi kutojua vyema Kiingereza, yanaelekea kupata jibu sahihi, kwa hatua hizi za serikali kwa kuboresha sifa za walimu watakaofundisha.Ni muhimu basi kama Taifa, kila mmoja kwa nafasi yake, ashiriki mageuzi haya ya elimu kwa kushirikiana na serikali kuboresha mfumo mzima wa utoaji elimu ili ukidhi mahitaji ya soko. Serikali inatekeleza sera ya viwanda, ambayo inahitaji wasomi wenye weledi wa kuendesha viwanda na kufanya biashara. Hivyo, ni muhimu kwa vyuo vye elimu kubadili mitaala, kukidhi utoaji elimu bora, utakaokidhi matarajio hayo.
kitaifa
MABINGWA watetezi wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Azam FC watawakosa nyota watano katika michuano hiyo kutokana na sababu mbalimbali.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii na Azam imepangwa kundi A pamoja na timu za JKU ya Zanzibar, Kator FC ya Sudan Kusini na Vipers kutoka Uganda.Ratiba inaonesha kuwa mabingwa hao watetezi ambao walilinyakua taji hilo mwaka 2015 mara ya mwisho kufanyika michuano hiyo, wataanza kucheza na Kator kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja wa Azam FC, Philip Alando, amesema, kikosi chao kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo licha ya kuwakosa wachezaji wake watano wa kikosi hicho.Aliwataja wachezaji hao kuwa ni beki wao Yakub Mohammed, Daniel Amoah, Iddy Kipagwile, Salim Hoza na kiungo waliyemsajili hivi karibuni kutoka Singida United, Tafadzwa Kutinyu.Amesema, Kipagwile pamoja na Hoza wamepata likizo fupi baada ya wote wawili kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, huku Amoah akiwa bado anasumbuliwa na majeraha na waliobakia wapo kwenye mapumziko ya kawaida na wanatarajiwa kurudi mwanzoni mwa mwezi ujao.“Timu inaendelea na mazoezi yake ya kuelekea michuano hiyo ambayo kwetu ni muhimu kama unavyojua sisi ndio mabingwa watetezi, baada ya kucheza mechi ya kirafiki na Green Warriors na kutoka sare ya kufungana bao 1-1, leo (jana) tutataendelea na mazoezi ya pamoja.
michezo
TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania imeiadhibu Zimbabwe kwa mabao 6-2 katika mchezo wa fainali za mashindano ya kwanza ya COPA Coca-Cola kwa vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Mataifa ya Afrika na kutwaa ubingwa.Tanzania ilionesha kiwango cha juu na kuibuka mshindi katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye viwanja vya MPESA Foundation Academy mjini Thika, Kenya jana. Taarifa kutoka Kenya zinasema kwamba mshindi wa kiatu cha dhahabu, Paul Nyerere alifunga mabao 3 ‘hat trick’ katika kipindi cha kwanza wakati wa fainali hiyo. Nyerere ameibuka mfungaji bora baada ya kufikisha mabao 7 kwenye michuano hiyo.Mabao mengine yaliwekwa kimiani na Ndile Haruni, Rai Mohambi, Boniface Raphael na kuiwezesha Tanzania kutwaa taji la mabingwa wa Kombe la COPA Coca- Cola Afrika 2019.Akizungumza mara baada ya mashindo hayo kuisha, Kocha wa Tanzania, Alex Mtweve alisema, timu yake ilistahili taji hilo.“Tuliutawala mchezo tangu mwanzo na vijana wangu walionyesha ujuzi, kwa kweli tulikuja kwenye mashindano haya na lengo la kutwaa ubingwa, nashukuru vijana hawajaniangusha.”Mtweve aliongeza kuwa siri ya ushindi wake imekuwa ni kucheza mchezo wa kushtukiza na kushambulia kwa nguvu. Mlinzi wa timu ya Tanzania, Chuma Ramadhan alifanya kazi kubwa pia ya kuiwezesha timu yake kutawala mchezo baada ya kuokoa hatari kadhaa golini kwake na kuzuia penalti moja wakati wa mchezo huo wa fainali.Akizungumza baada ya mechi hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chama ambaye alishuhudia fainali hiyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana hao na kuwatakia kila la heri.
michezo
Miji hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Mbeya na pia safari ya kimataifa kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini.“Kwa mwaka mmoja sasa Fastjet imeona Watanzania wakisafiri kwa ajili ya mikutano ya kibiashara na kutembelea ndugu na jamaa hivyo kuepusha uchovu na muda mwingi wa kusafiri kwa saa nyingi kwa kutumia barabara,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Fastjet, Ed Winter.Kwa mujibu wa Winter, kampuni ilianza kwa safari mbili kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kilimanjaro.Baada ya mahitaji ya safari za ndege kuongezeka, iliitikia mwito kuongeza safari mbili za nchini na moja ya kimataifa kwenda Johannesburg ndani ya mwaka mmoja. Winter alisema wana mpango wa kuongeza safari nyingine ya kimataifa kwenda Zambia ambayo ipo katika hatua nzuri.“Usafiri wa ndege wa bei nafuu ni muhimu sana kwa ajili kukuza uchumi wa Afrika,” alisema Winter. Kampuni hiyo ambayo nauli zake zinatajwa kuwa nafuu, zinaanzia Sh 32,000 na kwa safari za kimataifa, inaanzia Sh 160,000 lakini bila ada na kodi za Serikali.Wakati huo huo katika kusherehekea mwaka mmoja wa huduma zake, kampuni imetoa ofa maalumu leo ambako tiketi za safari kati ya Januari 6 na Machi 29 mwakani zitauzwa kwa bei ya chini ya Sh 32,000.
uchumi
KAMPUNI ya teknolojia ya malipo ya kimataifa, Visa imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini Tanzania. Huduma hiyo itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Visa kwenye simu ili wafanye malipo ya biashara kwa salama na kuweka na kutoa fedha kwa mawakala wa Visa.Mteja yeyote wa HaloPesa ikiwa ni pamoja na wale ambao hawana akaunti ya benki, watafaidika na huduma hii. Lengo la huduma hii ni kuunganisha Watanzania zaidi kwenye mfumo wa malipo ya kimataifa, kuleta huduma ya malipo ya Visa ya usalama na urahisi kwa watumiaji na wafanyabiashara. “Tunafurahia ushirikiano huu na mojawapo wa kampuni maarufu ya simu ya Halotel. Ushirikiano wetu na Halotel utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya malipo ya QR kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji na wafanyabiashara zaidi ya 40,000. “Pia itasaidia kuongeza ushirikishaji wa kifedha kwa watumiaji ambao sasa wataweza kufaidika na kushiriki katika mfumo wa ecoVisa,” alisema Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Kevin Langley. Halotel ni kampuni ya simu inayokua kwa haraka zaidi nchini Tanzania ambayo ilianzishwa mwaka 2015. Ndani ya miaka mitatu, imepata wateja zaidi ya milioni nne na ambao zaidi ya milioni moja wanatumia huduma ya Halopesa. Pia kampuni inao wakala 40,000 kote nchini. “Tunajivunia kushirikiana na Visa katika mpango huu.Kwa ushirikiano huu, tutaweza kuwa na uwezo wa kuwaletea wateja wetu huduma za kimataifa za malipo za Visa na kuwawezesha wateja wetu kulipia na kulipwa kwa urahisi zaidi,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son. Kupitia ushirikiano, HaloPesa itawapa watumiaji fursa ya kufanya malipo kutumia codi ya QR ya Visa nchini Tanzania na kote duniani.
uchumi
MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Ally Mchungahela ametangaza rasmi uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga kwamba utafanyika Mei 5 mwaka huu.Uchaguzi huo umetangazwa kufanyika siku hiyo kutokana na agizo la Serikali kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT), kuitaka TFF isimamie klabu hiyo ifanye uchaguzi wake ndani ya siku 30.Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo Karume Ilala jana, Mchungahela alisema wametoa taarifa ya kufanyika uchaguzi huo kwa lengo la kuwajulisha wapenzi na wanachama wa Yanga maendeleo ya mchakato wa uchaguzi yalipofikia na kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali zitaanza kutolewa leo makao makuu ya Yanga.Alisema kwa wale waliochukua fomu awali kwa ajili ya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi hawatachukua tena na badala yake watasubiri kupigiwa kura siku ya uchaguzi huo mkuu kwa vile walishafanyiwa usaili na kufanya kampeni. “Hakuna asiyefahamu uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika hapo awali lakini baadae ulishindwa kufanyika kwa sababu za kisheria na sasa uchaguzi utafanyika kwa tarehe tuliyopanga na si vinginevyo kwa ushirikiano wa wanayanga wenyewe chini ya uangalizi wa Shirikisho la soka nchini kwa sababu ni chombo kinachosimamia mpira,” alisema Mchungahela.Mchungahela alisema wao wana mamlaka ya mwisho kutangaza tarehe ya uchaguzi. Tarehe hiyo ni tofauti na ile iliyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Baraza la wadhamini la Yanga chini ya George Mkuchika kwamba Aprili 28 ndio uchaguzi ungefanyika.Mchungahela alisema tarehe hiyo iliyopangwa na baraza la wadhamini kutakuwa na fainali za Afcon kwa vijana zinazotarajiwa kuanza Aprili 14 nchini hivyo wengi watakuwa wakifuatilia fainali. Wajumbe Yanga waliohudhuria kwenye mkutano huo ni Omary Kaaya, Zayumba Hamis, Karume Benjani, Mwamedi Mtengulwa ambaye ni mbunge kutoka Rufiji na wakili Sam Mapande. Mchungahela alisema hadi sasa wameshapata daftari la leja linaloonesha orodha ya wanachama hai wa timu hiyo na kwamba hiyo ni ishara njema kwa wanachama.
michezo
['Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard)', 'Barcelona na Paris St-Germain zimekubali malipo ya uhamisho wa mchezaji wa miaka 27 wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, lakini majadiliano yanaendelea kuhusu makubaliano ya mkataba huo. PSG inataka mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 22, kuwa sehemu ya mpangilio huo. (Mirror)', 'Hatahivyo, Ajenti wa Dembele anasema mchezaji huyo hatoondoka Nou Camp, hatua ambayo huenda ikachangia kupromoka kwa pendekezo la uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona. (Daily Mail)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25, amekubali makubaliano ya kujiunga upya na Monaco kwa mkopo - huku kukipangiwa malipo ya £31.8m ka mkataba wa kudumu.(RMC Sport, kupitia Sun)', 'Mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal, mwenye umri wa miaka 33, c huenda akarudi katika klabu alikotoka Uhispania kaba ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu, huku Real Sociedad ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Osasuna na Malaga. (Evening Standard)', 'Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England Sam Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, ametambuliwa na timu bingwa ya Italia AC Milan na Juventus kama mchezaji anayelengwa baada ya kuridhisha maajenti katika mshindano ya ubingwa wa Ulaya wa timu za wachezaji walio chini ya umri wamiaka 17 mapema msimu huu wa joto. (Sun)', 'Manchester United italipa kitita cha £300,000 cha malipo ya Alexis Sanchez ya £400,000 kwa wiki wakatimchezaji huyo wa kiiungo cha mbele wa Chile akiwa uhamishoni kwa mkopo huko Inter Milan. (Metro)', "Mchezaji wa kiungo cha mbele wa RB Leipzig na anayelengwa na Liverpool, Timo Werner, mwenye umri wa miaka 23, bado hajakata tamaa ya uhamisho kwenda ng'ambo katika siku za usoni licha ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Ujerumani kusaini mktaba mpya katika klabu hiyo kwenye ligi ya Bundesliga. (Mirror)", 'Kipa wa Bournemouth Asmir Begovic, mwenye umri wa miaka 32, huenda akaondoka baada ya kuipoteza nafasi yake kwa mchezaji wamiaka 21 wa England Aaron Ramsdale. (Sun)', 'Mshambuliaji wa Reading Sam Baldock, mwenye umri wa miaka 30, anavutia vilabu kadhaa katika ligi ya Ujerumani Bundesliga 2, huku mlinzi mwenye miaka 19 wa timu ya taifa ya England Tom Holmes akitarajiwa kujiunga na KSV Roeselare huko Ubelgiji kwa mkopo. (Get Reading)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City Giannelli Imbula, mwenye miaka 26, anakaribia kuhamia kwa mkopo kwenda klabu katika ligi ya Serie A. (Sport Italia)', 'Tottenham hawana uhakika na nia ya Christian Eriksen kutokana na kuvunjika kwa mahusiano kati ya mwenyekiti wao Daniel Levy na wakala wa kiungo huyo mwenye miaka 27 raia wa Denmark. (Guardian)', 'Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini Eriksen anatakiwa kuanza kwenye mechi za Spurs licha ya kutokujulikana kwa hatma yake ya mbeleni. (Talksport)', 'Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 26 aliondoka Manchester United kwa sababu alichoshwa na klabu hiyo , kwa mujibu wa kocha wa Belgium Roberto Martinez. (Mirror).', 'Kaka yake Paul Pogba, Mathias mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Deportivo Manchego, amesema mdogo wake anayechezea Manchester United itapendeza zaidi kama atahamia Real Madrid. (AS)', 'Mshambuliaji wa Everton Cenk Tosun anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ana mpango wa kuhamia Eintracht Frankfurt. (Turkish Football)', 'Liverpool imesema kuwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wake Bobby Duncan na imekataa kutumia mbinu za Fiorentina. (Liverpool Echo)', 'Mchezaji wa Brighton, Jurgen Locadia, 25 anaweza kusajiliwa kwa mkopo na Bundesliga side Hoffenheim. (Argus)', 'Olympiakos wako katika mazungumzo na klabu ya Leicester katika mpango mpya wa kumsajili mshambuliaji wa Foxes ambaye ni raia wa Algeria Rachid Ghezzal, 27. (Sky Sports)', 'Manchester City wapo katika mipango ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Hearts Aaron Hickey kwa dau la paundi milioni 1.5 ili kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ifikapo mwezi Januari. (Sun)', 'Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion, Rekeem Harper mwenye umri wa miaka 19 amepewa nafasi kubwa katika mipango ya kocha mkuu wa klabu hiyo Slaven Bilic katika msimu huu. (Express and Star)']
michezo
SIMBA sasa bado pointi tano tu kumfikia mpinzani wake mkubwa Yanga anayeongoza Ligi Kuu Soka ya Tanzania Bara baada ya jana kuifunga Biashara ya Mara kwa mabao 2-0.Ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa mkoani Mara unaifanya Simba kufikisha pointi 69, pointi tano nyuma ya Yanga yenye pointi 74.Huo ni muendelezo wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania Bara kucheza mechi zake za viporo vilivyotokana na ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba sasa imecheza mechi 27.Aidha, matokeo hayo yanazidi kuichimbia kaburi la kushuka daraja kwa Biashara ambapo inashika nafasi ya pili toka mwisho ikiwa na pointi 34 katika michezo 32.Mabao yote mawili ya Simba yalipatikana kipindi cha kwanza yakiwekwa kimiani na nahodha wa timu hiyo John Bocco na kumfanya kufikisha mabao 14 kwenye ligi hiyo mpaka sasa.Ilimchukua dakika 33 kwa nahodha huyo kuiandikia Simba bao la kuongoza akiunganisha kwa shuti kali la mguu wa kushoto pasi nzuri iliyopigwa na kiungo Mzamiru Yassin.Dakika tano kabla ya mapumziko Bocco tena aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi wa beki Asante Kwasi aliyecheza badala ya Mohamedi Hussein’Tshabalala’ Biashara ikicheza mbele ya mashabiki wake ilishindwa kutengeneza nafasi kipindi cha kwanza na kutoa nafasi kubwa ya Simba kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo.Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa John Bocco na kumuingiza Emmanuel dakika ya 58 na dakika ya 66 beki Paul Bukaba alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga kwa shuti lake kuokolewa na kipa Nourdin Abalora na kuondoshwa na mabeki wa Biashara.Simba ilipata pigo dakika ya 71 kwa kiungo wake Mnyarwanda Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Biashara.Haikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji Meddie Kagere baada ya kupoteza nafasi ya wazi dakika ya 73 kwa shuti lake kutoka pembeni kidogo ya lango la biashara na dakika ya 74 alitolewa na kuingia Hassan Dilunga.
michezo
Huduma hiyo ambayo inatolewa kwa kushirikiana na Kampuni ya AFB, imelenga kubadilisha maisha ya wafanyabiashara wadogo ambao wanahitaji mikopo kuimarisha mitaji yao.Huduma hiyo itakayojulikana kama “Airtel Money Timiza” ni sehemu ya juhudi za Airtel ya kuungana na Serikali katika kuwezesha wananchi na wateja wa Airtel wote kujipatia mikopo ya haraka na ya muda mfupi kwa marejesho nafuu ya siku 7 hadi 28.Akizungumza wakati wa uzinduzi, Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipongeza huduma hiyo na kusema ni motisha kwa wafanyabiashara wadogo.Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso alisema: “Leo uzinduzi wa huduma yetu ya Airtel Money Timiza unadhihirisha dhamira ya dhati ya Airtel ya kutoa huduma iliyo bora na nafuu ili kugusa maisha ya kila siku ya wateja wetu hapa Tanzania .”Alisema ni matumaini yake kwamba huduma hiyo itaongeza kasi ya ukuzaji wa uchumi miongoni mwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikundi vya wanawake, wajasiriamali na watu binafsi.Kwa upande wake, Mwanzilishi wa AFB, Andrew Watkins-Ball alisema huduma hiyo ya mikopo ya Airtel Money Timiza ni ya kipekee tofauti na benki ambayo mara nyingi mteja hulazimika kuwa na historia ya uwekaji na utoaji katika benki hiyo.Alisema mikopo hiyo ya Airtel kwa kushirikiana na AFB, inatolewa kutokana na jinsi ambavyo mteja anatumia simu.
uchumi
WATU 26 wakiwemo Watanzania watatu wamekufa katika shambulio la bomu lililofanyika katika hoteli mjini Kismayo, Somalia.Mwandishi wa habari maarufu mwenye uraia wa Canada na Somalia, Hodan Nalayeh na mumewe, Farid, ni miongoni mwa waliokufa katika shambulio hilo linalosadikiwa kufanywa na kundi la wapiganaji wa al shaabab katika hoteli ya Easey.Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), raia wengine waliokufa katika tukio hilo ni Wakenya watatu, Wamarekani wawili na Muingereza.Watu wengine 50 wamejeruhiwa katika shambulio hilo ambalo inadaiwa pia washambuliaji wanne waliuawa.Kuhusu vifo vya Watanzania, HabariLeo halikufanikiwa kupata msemaji upande wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuthibitisha taarifa hizo zilizoripotiwa na shirika la BBC.Mashuhuda wa tukio hilo walisema maofisa wa ngazi za juu wa kisiasa akiwemo mgombea urais katika uchaguzi ujao katika jimbo la Jubaland, ameuawa katika shambulio hilo la juzi usiku.Aidha, ofisa usalama, Abdi Dhuhul aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) kwamba waziri mmoja wa utawala wa eneo hilo pamoja na wakili ni miongoni mwa waliofariki katika shambulio.Wanasiasa wa eneo hilo pamoja na viongozi wengine walikuwa ndani ya hoteli hiyo wakijadili kuhusu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katika ukanda huo.Vikosi vya usalama katika mji huo ulio mwambao wa Kusini mwa Somalia, vilikabiliana na kundi hilo usiku kucha.Kwa saa kadhaa, vikosi vya usalama vilikabiliana na wapiganaji waliokuwa na silaha nzito hadi asubuhi.Walioshuhudia walisema walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari kulipuka. Miili ya watu iliondolewa kutoka kwenye hoteli hiyo wakati vikosi vya usalama vikiendelea na msako.
kitaifa
SERIKALI haina mpango wa kuvibadili vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa VETA. Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Willam Ole Nasha wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa (CCM). Mchengerwa alisema katika swali: “Serikali imerejesha vyuo vilivyokuwa vya maendeleo kuwa chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya kusema hayo, alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kukibadili chuo cha Maendeleo Ikwiriri FDC kuwa VETA ili kubadili fikra za wananchi wa Rufiji, Kibiti na hatimaye kuleta mwamko wa elimu. Akijibu swali hilo, Waziri Ole Nasha alisema elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi hutolewa katika shule na vyuo katika kiwango na madaraja mbalimbali kulingana na malengo yake. Alisema ngazi ya shule za sekondari, elimu ya ufundi hutolewa kumuandaa mwanafunzi kujiunga na vyuo vya ufundi stadi na ufundi wa kati.“Vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi huandaa mafunzi mchundo na vyuo vya ufundi wa kati huandaa mafundi sanifu. Aidha, vyuo huandaa wahandisi katika fani mbalimbali zinazohusiana na ufundi.” Waziri Ole Nasha alisema vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilianzishwa kwa lengo la kumsaidia mwananchi kukabiliana na changamoto za kimaendeleo katika mazingira yake kwa kumpatia maarifa na stadi anuai Alisema kwa sasa serikali haina mpango wa kuvibadili vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa VETA na badala yake imejikita katika kuviboresha vyuo hivyo kwa kuvikarabati na kuviongezea vifaaa vya kujifunzia na kujifundishia ili viweze kutoa mafunzo bora zaidi. Waziri Ole Nasha alisema awamu ya kwanza ukarabati wa vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 20 ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji, na awamu ya pili inatarajiwa kuanza mapema Juni mwaka huu. “ Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ikwiriri kilikuwa katika awamu ya kwanza na ukarabati umekamilika,” alisema. Aidha, Ole Nasha alisema katika mwaka wa fedha 2019/2020 Rufiji ni miongoni mwa wilaya zilizotengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya cha VETA.
kitaifa
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ameshauri wakuu wa mikoa nchini kuhamasisha matumizi ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi.Pia ameiomba Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) kuwezesha suala la anuani ya makazi kufanikiwa. Hayo yamo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi. Kikao hicho kililenga kujenga uelewa wa pamoja na kuhamasisha utekelezaji wa matumizi ya mfumo huo.Alisema wakuu wa mikoa kama watafanya jitihada za kuhamasisha matumizi ya mfumo huo, kutakuwepo na mafanikio na hivyo kurahisisha mawasiliano na utambuzi. Pia alishauri Tamisemi na Wizara ya ujenzi kuweka jitihada katika kuhamasisha, kujenga uelewa na uwezo katika utekelezaji wa matumizi ya mfumo, ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ambatanishi ya Tehama ili uwe na tija katika utoaji huduma hususani katika biashara mtandao.Pia alizitaka Wakala wa Barabara vijijini (Tarura), Wakala wa Barabara (Tanroads), Wakala wa Majengo (TBA), Shirika la Nyumba (NHC) na taasisi nyingine zote zenye majukumu ya kuweka miundombinu kuhakikisha mipango yao inakuwa na anwani ya makazi na postikodi kulingana na viwango vilivyopo. Aidha alizitaka taasisi mbalimbali zilizoko Dodoma kuanza mara moja kutumia anwani za makazi na postikodi katika kutoa huduma.Aidha, alizitaka Halmashauri zote kuweka mazingira ya kupatikana kwa urahisi na gharama nafuu nguzo zenye majina ya barabara, njia na vibao vyenye namba za nyumba ili endapo taasisi au wananchi watahitaji kwa ajili ya maeneo wapate bila usumbufu. Pia aliwataka watoa huduma, wafanyabiashara na wenye nyumba za biashara kuhakikisha maeneo yao ya huduma au biashara yanatumia anwani za makazi na postikodi katika huduma zao.“Tunatambua kuwa Dodoma ni mji wa kiserikali hivyo tunapaswa kuifanya kuwa na hadhi ya kiserikali, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mifumo imara ya utoaji wa huduma. hatuna budi kuwa mfano kitaifa katika kutekeleza na kuutumia kwakuwa utaongeza tija na ufanisi,”alisema.Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Jim Yonazi alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili mfumo huo kuwa ni ufinyu wa bajeti unaochangiwa na halmashauri kutotenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Pia mwamko mdogo wa taasisi na wananchi kushiriki katika kuchangia utekelezaji, barabara na mitaa mingi kutokuwa na majina yaliyorasimiwa na uharibifu wa muundombinu wa mfumo uliopo.
kitaifa
Maswi alitoa agizo hilo mjini Mbeya jana, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Madini mkoani Mbeya, ambako alipatiwa taarifa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kuhusu kampuni kubwa tatu zinazogoma kulipa maduhuli stahiki kwa Serikali, kwa madai ya kuwa na hati ya msamaha wa kodi katika baadhi ya maeneo.“Hili jambo mbona ni rahisi kwa kuwa sekta yetu hii ya madini inaendeshwa kwa kuzingatia sheria, na sheria inatamka wazi kuwa ni lazima kila mwekezaji wa madini alipe maduhuli kulingana na kiasi alichouza.“Kamishna wa Madini fuatilia hili na kama kweli kuna hizo hati…kwani zinatoka wapi? Si zimetoka serikalini basi zifutwe, hawa walipe malipo stahiki,” alisisitiza Maswi.Awali akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wa TMAA katika Mkoa wa Mbeya, Ofisa Mfawidhi wa wakala huo mkoani hapa, Jumanne Abdallah, alisema ofisi yake imekuwa ikikabiliwa na wakati mgumu katika ukusanyaji wa maduhuli kutoka kampuni hizo za madini na kushindwa kukusanya malipo stahiki.Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kulipa Sh milioni nne kwa mwezi kodi ya maduhuli, lakini kutokana na madai ya kuwa na hati hizo, zimekuwa zikilipa kila mwezi Sh milioni 3.
uchumi
WATU watano wa familia moja wamekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi ambayo pia iliwajeruhi watu watatu wa Kijiji cha Isongwa, Kata ya Mkole, Wilaya ya Sikonge, Tabora.Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi Emanuel Nley ilisema mvua kubwa iliyonyesha juzi usiku ikiambatana na radi ilisababisha vifo.Kamanda Nley alisema tukio hilo lilitokea saa nne usiku Aprili 22, mwaka huu watu hao wakiwa wamelala katika chumba kimoja kwao.Aliwataja waliokufa kwa radi hiyo kuwa ni Mhindi Petro (38) aliyeunguzwa kifuani na mguu wa kulia na Vailet Juma (16) aliyeungua usoni, ziwa la kushoto na mkono wa kulia.Wengine ni Grace Juma (13) aliyeunguzwa usoni, Kulwa Lukanya (12) mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Igalula aliyeungua tumboni na mkono wa kulia na Nyanzobe Juma (7) aliyeunguzwa usoni na mguu wa kulia.Majeruhi waliotibiwa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge na kuruhusiwa ni Dotto Lukanya (12), mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Igalula ambaye aliunguzwa ubavu wa kushoto.Kamanda Nley aliwataja majeruhi wengine wa tukio hilo ni Pendo Machiya (11), mwanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Igalula aliyeunguzwa mguu wa kulia na Masanja Juma (11) aliyejeruhiwa mkono wake wa kushoto.Kamanda huyo alisema radi hiyo iliingilia dirishani chumba ambacho walikuwa wamelala wanafamilia hao wanane na kutokea ukutani upande wa pili na kusababisha ukuta kupasuka kutokana na kujengwa kwa miti na udongo.Alitoa pole kwa familia hiyo kutokana na tukio hilo na aliwataka watu waliobaki katika familia hiyo kuwa watulivu hasa katika kipindi hiki cha majozi ya kupotewa na ndugu na jamaa zao.Tukio hilo la vifo vinavyotokana na radi ni la pili kutokea kwa mwaka huu, kwani tukio kama hilo liliwahi kutokea miezi mitano iliyopita katika Wilaya ya Uyui baada ya radi kuua watu watatu wa familia
kitaifa
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto anampa taabu sana na ameomba ushauri amfanye nini.Ndugai amesema jijini Dar es Salaam kuwa, Zitto anampa taabu kwa sababu chama cha ACT Wazalendo kina Mbunge mmoja tu kwenye Bunge la Tanzania hivyo akimfukuza chama hicho kitakosa uwakilishi bungeni.“Niseme ukweli huyu amekuwa akinipa taabu sana, nisema tu ukweli wa moyoni kwa sababu ni Mbunge wa kipindi karibu cha tano anapaswa kuwa anafahamu mambo mengi”amesema.“Sasa huyu yaani ni mmoja tu kwenye chama chake, ukifukuza hakuna tena uwakilishi na mtaniuliza maswali waandishi maana yake ninyi hamchoki, sasa huyu umemfukuza mzee sasa, kwa hiyo wakati mwingine nahitaji hata ushauri wenu, hivi mtu kama huyu unamfanyaje…“he he he, hee chama ambacho kina Mbunge mmoja tu, sasaa heeh, maana sio minority tena, yaani ni, si jui nini, katika wabunge 393 karibu na mia nne yaani mmoja tu, ndiyo maana mnamuona anahangaika mahakamani peke yake tu”amesema Spika Ndugai.Amesema Zitto anahangaika na mambo yake peke yake kutafuta umaarufu, bado hajafikiria kumuita, watamvumilia ila ipo siku watachukua hatua.“Yupo huku Dar es Salaam wenzake wapo Dodoma, anadanganyadanganya watu huku, kuzunguka zunguka kwenye makorido, kaenda na kesi ya ajabu ajabu ile, sijui ya vyama vya siasa imeenda wapi. Na ule muswada upo kule niwaambieni unaendelea kama kawaida, sasa hivi kwenye ngazi ya kamati, likianza Bunge muswada unaingia”amesema Ndugai.
kitaifa
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amewataka wawekezaji, wafanyabiashara, taasisi za fedha na wajasiriamali kuwa na uthubutu na kuchangamkia fursa, zinazoibuliwa Lindi ili kuujenga mkoa huo, ambao ni kati ya mikoa yenye utajiri uliojifi cha.Pia, amewataka Watanzania na wawekezaji, kuchangamkia fursa zinazoibuliwa katika mikoa mbalimbali nchini na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ili kuijenga Tanzania ya viwanda.Makamu wa Rais amesema hayo mjini Lindi jana katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji, lililoandaliwa na TSN kwa kushirikiana na Mkoa wa Lindi.Hotuba ya Makamu wa Rais ilisomwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.Amesema kampuni hiyo ya magazeti kwa muda mrefu, imekuwa ikitembelea mikoa na kuweka kambi kupitia timu yake ya waandishi wa habari, ambayo huingia hadi vijijini na kuibua fursa zilizopo katika mkoa huo na kuzitangaza kupitia vyombo vyake vya habari.TSN ni wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo, SpotiLeo, Daily News na HabariLeo Digitali.“Jukwaa hili ni njia ya busara iliyochaguliwa na TSN kushawishi majitu ya miraba minne hapa Tanzania ambayo bado yameatamia fursa kubwa. Huyaamsha na kuyaonesha kuwa yameatamia utajiri mkubwa na kuuonesha utajiri huo kupitia vyombo vyake vya habari kwa lengo la kuvutia wawekezaji,” ameeleza.Alisema pamoja na kuamshwa kwa mikoa hiyo, lakini pia majukwaa hayo huvutia taasisi mbalimbali za serikali ambazo hutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara, wawekezaji na hata wajasiriamali katika maeneo mbalimbali nchini.“Kule Arusha kwenye moja ya majukwaa haya, wafanyabiashara wengi waliogopa kujitokeza kuzungumza kwa kuhofia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini baada ya mwakilishi wa mamlaka hiyo kuzungumza, hali ilibadilika na wengi walifurahi kupata elimu ambayo awali walikuwa hawana na walikuwa wakihofia bure tu,” alisema.Alisema wazo la kuendesha majukwaa hayo ni ubunifu tu wa TSN ili kuleta ari mpya ya kuibua fursa za kiuchumi kwenye mikoa na kuhamasisha umma, kampuni, taasisi za kibiashara kuchangamkia fursa zinazoibuliwa.Akizungumzia Jukwaa la Lindi, alisema Lindi si tu ni jitu la miraba minne lililolala, bali pia limeatamia utajiri mkubwa na hakuna anayethubutu kuliamsha kwa hofu ya kudhurika au likanuna na kusifanyike kitu chochote.“Lakini TSN imekuja na njia ya staha imeishawishi Lindi na kuelezea faida za kuibuliwa kwa fursa zake, na sasa inaamka polepole,” alisisitiza.Alisema mpaka sasa mkoa huo utajiri wake umeshaibuliwa na kutangazwa na kilichobaki ni wawekezaji, taasisi za fedha, wafanyabiashara na wajasiriamali, kugeuza macho yao Lindi ambako ni sawa na mgodi ‘uliotema’.“Nimethibitisha kuwa Lindi ni hazina ya Taifa kwa kuwa na fursa nyingi, kuna kilimo cha korosho, ufuta, madini grafaiti, gypsum, utalii wenye fukwe zenye viwango vya kimataifa, utalii wa mambo ya kale, utalii wa urithi wa harakati za ukombozi wa Afrika, wanyama na uwindaji, misitu na mazao yake,” alisema.Alisema uwekezaji wowote ili ufanikiwe, lazima uwe na uthubutu na alitoa mfano namna alivyofanikisha ujenzi wa uwanja wa taifa kupitia mfadhili mpya na kumuondoa mfadhili wa awali, ambaye alikuwa hachangii chochote.Pamoja na hayo, aliwataka wawekezaji na wenye viwanda, kuhakikisha wanatumia malighafi zinazozalishwa nchini, jambo litakalowapatia faida, lakini pia kuinua wazalishaji wa ndani.“Lindi mmeshaonesha njia, lakini kama leo hii mmeweza kushinda mikoa sugu kama Dar es Salaam ambako wengi wanakimbilia huko, lakini mkawa wa kwanza katika kuanzisha viwanda vidogo, ni wazi kuwa mtapiga hatua kubwa,” amesema.Dk Mwakyembe alisema Makamu wa Rais alipenda sana kuhudhuria jukwaa hilo, lakini imeshindikana kutokana na kuibuka kwa shughuli nyingine za kitaifa zilizohitaji uwepo wake.“Ametutakia mjadala mzuri na ametaka apewe mrejesho wa mwitikio wa wana-Lindi katika jukwaa hili,” alisema.Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah alielezea lengo kuu la TSN kuanzisha majukwaa hayo kuwa ni kuhakikisha inaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuifikia serikali ya viwanda kwa kuibua fursa zilizopo kwenye mikoa hiyo na kuzitangaza.“Tuliamua kwenda mikoani baada ya kuona kuna fursa nyingi ambayo hata wananchi wa mikoa husika wenyewe hawazifahamu. Mpaka sasa tumeshafanya majukwaa haya kwenye mikoa nane na huu wa Lindi ni wa tisa,” alisisitiza Tuma.Mikoa iliyokwishafanya majukwaa hayo ya kuibua fursa za biashara kupitia TSN ni Simiyu, Geita, Shinyanga, Mwanza, Zanzibar, Arusha, Tanga na Tabora. Alisema mkoani Lindi, kampuni hiyo ilituma waandishi wake wiki tatu zilizopita, ambao waliziibua fursa za Lindi na wiki hizo mfululizo wamekuwa wakizitangaza.“Leo (jana) hii gazeti letu la HabariLeo lina kurasa 48, kati hizo kurasa 35 zina habari za Mkoa wa Lindi pekee,” alisema.Mwenyekiti wa Bodi ya TSN, Hab Mkwizu aliwataka washiriki wote wa jukwaa hilo, kuhakikisha wanaondoka na funzo ambalo watalitumia kuwasaidia katika biashara zao ili majukwaa hayo yawe na tija.Aliwashukuru wadhamini wa jukwaa hilo na uongozi mzima wa mkoa wa Lindi kwa kufanikisha jukwaa hilo kufanyika, ambalo pia linamalizika rasmi leo.
uchumi
MAZIKO ya aliyekuwa mmiliki wa timu ya Pallson ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha, Thomas Mollel maarufu Askofu yanatarajiwa kufanyika Jumatatu, nyumbani kwake Mbuguni.`Askofu’ ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini ya tanzanite na mmiliki wa migodi hiyo iliyoko wilayani Simanjiro mkoani Manyara, alifariki juzi mkoani Dodoma baada ya kuanguka ghafla bafuni saa 4 usiku sehemu alikofikia. Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya kichama ya Meru, Shabani Mdoe alisema kuwa kwa sasa chama kinaangalia namna ya kusafirisha mwili huo kwa njia ya ndege hadi katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).Mdoe alisema ratiba ya ndege inaonesha kuwa mwili utawasili Arusha Jumapili Mei 26. Alisema kwa sasa wanakaa na familia kuangalia kama watakubaliana na ratiba hiyo na kama itashindikana, basi kuna uwezekano wa kusafirisha mwili kwa njia ya barabara ili mwili uweze kuja mapema Arusha kuwahi maziko siku ya Jumatatu kama ilivyopangwa.Katibu alisema Askofu ambaye aliwahi kuwa diwani na kabla ya mahuti kumkuta alikuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Meru alikwenda Dodoma na wafuasi wengine kumsindikiza Mbunge mteule Dk John Pallangyo aliyepita bila kupingwa kwenda kuapishwa bungeni.Alisema `Askofu’ mbali ya kuwa mwanasiasa ni mpenzi mkubwa wa soka na alianzisha timu ya Pallson iliyotamba hadi Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini sasa timu hiyo haiko tena katika ulimwengu wa soka.Naye Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), Zakharia Mjema alisema chama kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha `Askofu’ kwani alikuwa mdau mkubwa wa soka mkoani Arusha na msaada mkubwa kwa chama cha soka. Alisema kuwa mmiliki huyo wa Pallson atakumbukwa kwa mambo mengi katika tasnia ya soka mkoani Arusha na nchi kwa ujumla kuwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi siku ya mazishi ya mpenzi huyo wa soka Arusha ikiwa ni njia ya kumuenzi.Naye mchezaji wa zamani wa Pallson, Fidelis Nzowa maarufu kwa jina la Chief amepokea taarifa ya kifo cha `Askofu’ kwa masikitiko, kwani alikuwa sio mmiliki tu wa timu bali alikuwa mzazi kwa wachezaji wote waliowahi kuichezea timu hiyo. Naye Denis Shemtoe timu Meneja wa zamani wa timu ya AFC ya Jijini Arusha alisema anamfahamu vizuri Askofu na kamwe pengo lake halitazibika katika soka la Mkoa wa Arusha.
michezo
UJENZI wa reli ya kisasa unaoendelea katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam- Morogoro na Dodoma, umetajwa kuviachia neema kubwa viwanda vya ndani kutokana na malighafi yenye thamani ya mabilioni kununuliwa nchini.Kwa sasa viwanda vya saruji na nondo, ndivyo vinavyoonekana kunufaika zaidi kutokana na mahitaji makubwa ya malighafi hizo, zinazotumika zaidi katika ujenzi wa reli ya kihistoria barani Afrika, ulioanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya utawala wa Rais Dk John Magufuli.Meneja Mradi wa reli hiyo kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kipande cha Dar es Salaam na Morogoro, kitakachokuwa na jumla ya kilometa 300, Machibya Masanja, alisema juzi kuwa pamoja na mradi kulenga kunufaisha nchi, anafurahi kuona kwamba karibu asilimia 90 ya malighafi zinatoka nchini, hivyo kuongeza mzunguko wa fedha katika viwanda vya ndani.“Ni bahati ya aina yake kwa mradi mkubwa kama huu kutegemea malighafi chache sana kutoka nje. Hapa kwetu labda ni vyuma vyenyewe vya reli tu ndivyo huagizwa kutoka Japan, lakini vingine kwa asilimia 90 pesa inabaki hapa hapa,” alisema.Alitoa mfano kuwa kwa upande upande wa saruji, mahitaji kati ya Dar es Salaam na Morogoro ni mataruma ya reli 500,100, hivyo saruji inayotumika kwa mataruma pekee ni zaidi ya tani 200,000, kwani kila taruma moja lenye uzito wa kilo 380 kwa asilimia 40 hutengenezwa kwa saruji.Saruji hiyo ni mbali na ile inayotumika katika madaraja makubwa na madogo katika sehemu korofi, zenye miinuko au mabonde. Aidha, kwa upande wa Dar es Salaam, kipande cha kilometa 16 kati ya Steshenei Kuu na Gongo la Mboto, litakalokuwa na njia za reli za juu katika baadhi ya maeneo, linatarajiwa kubeba mirunda ya zege 510, achilia mbali nguzo zinazosimika ili kubeba mirunda hiyo.Mrunda mmoja wa zege unatengenezwa kutokana na tani 12 za saruji, sawa na mifuko 240, huku ukisukwa kwa vipande vya nondo vya ukubwa tofauti. “Sasa ukiangalia hapo unaweza kuona jinsi viwanda vyetu vinavyonufaika kutokana na ujenzi huu.Hapo tumezungumzia vitu vichache tu, lakini ukiachililia mbali faida za mradi kiuchumi baada ya kukamilika kwake, tayari mradi umechangia katika kukuza uchumi wa viwanda, kutoa ajira na mengineyo mengi.“Kama tusingekuwa na malighafi hizi, ni dhahiri fedha zingekwenda nje ya nchi, na hata ajira zingekwenda huko.” Masanja, akiwa katika eneo la kiwanda cha mataruma eneo la Soga mkoani Pwani, alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha mataruma 1,080 kwa siku, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ajira kwa Watanzania wa kada mbalimbali.Mradi ya Dar es Salaam – Morogoro umeajiri asilimia 96 ya Watanzania. “Ndiyo hali halisi, tunatengeneza vitu vyetu kwa ubora wa kimataifa na tunapata malighafi kama saruji, kokoto, mchanga, maji na nondo hapa hapa nyumbani, hivyo tunatekeleza mradi huku tukikuza tukikuza pato na nchi,” alisema Machibya huku akishangiliwa na kundi la vijana wa Kitanzania wanaonufaika na ajira katika mradi huo.Kwa sasa, ujenzi umeshika kasi na kukamilika kwa asilimia 36, lakini meneja huyo akisema hawaoni tena kikwazo cha kutokamilika kwa mradi mwishoni mwa mwaka kesho. “Hakuna kikwazo, kila kitu kipo. Tunatarajia Novemba 2, mwaka 2019 tutakabidhiwa rasmi mradi kwa kipande cha Dar es Salaam- Morogoro ili tuweze kuanza kuuendesha wakati vipande vingine vya Morogoro- Makutupora na kuendelea hadi Mwanza ujenzi wake ukiendelea.Mradi huo hadi kukamilika unatarajiwa kuwa wa kilometa 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu Sh trilioni 7.1.Mradi umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kitakachogharimu Sh trilioni 2.7. “Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa kilometa 422 ambacho kitagharimu shilingi trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora kilometa 376.5, Tabora hadi Isaka kilometa 162.5 na Isaka hadi Mwanza kilometa 311.25,” alisema Kadogosa.Katika maeneo mbalimbali kati zinazoendelea kwa sasa ni kuweka matuta, madaraja, kupasua miamba kwa sehemu zenye milima, kuweka mataruma, kusimika nguzo za umeme, kujenga madaraja ya mjini ambayo treni itapita juu na sasa utandikaji wa reli.Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo Aprili mwaka huu, Rais Magufuli, alisema anatamani kuiona Tanzania ikiwa kama Ulaya kwa upande wa miundombinu, akisisitiza kuwa miundombinu imara ya usafiri ni kichocheo muhimu cha ukuaji uchumi katika nchi na kwamba bila miundombinu hiyo ni ndoto kupata maendeleo.“Kukosekana kwa miundombinu imara na ya uhakika, imesababisha gharama za usafiri kuwa juu kulinganisha na maeneo mengine duniani,” alisema Rais Magufuli na kutoa mfano kuwa, wastani wa bei ya kusafirisha kontena moja la futi 20 kwenye nchi za Afrika Mashariki umbali usiozidi kilomita 1,500 ni Dola za Marekani 5,000 na kwamba bei hiyo ni sawa na gharama ya kusafirisha kontena lenye ukubwa kama huo kutoka China hadi Tanzania umbali wa kilomita 9,000.“Tafiti zinaonesha pia kukosekana kwa miundombinu imara ya usafiri kunashusha pato la nchi za Afrika kwa asilimia kati ya moja na mbili na kuongeza gharama za usafirishaji kwa asilimia 40. Hali hii inasababisha nchi zetu zishindwe kushindana na nchi zingine katika masuala ya biashara, uwekezaji na maendeleo ya viwanda,” alisema.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ya 2015 kuhusu usafiri wa reli, inaonesha usafiri wa reli ni muhimu, kwani ni mhimili mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na usipoboreshwa, Afrika haitaweza kutumia rasilimali na utajiri ilionao. Alisisitiza kuwa, ili nchi yoyote iweze kujitegemea, ina wajibu wa kumiliki vitu muhimu kama reli, bandari, nishati, barabara, mawasiliano na vingine.Aliongeza kuwa, ujenzi wa reli ya kisasa utaongeza tija na ufanisi katika usafiri wa reli nchini kwani utarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria. Mathalani, safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza inayotumia saa 36 kwa usafiri wa reli ya kawaida, sasa itapungua mara nne na kufikia saa 7 hadi 9 tu. Dar es Salaam na Morogoro safari yake itakuwa chini ya saa 1:30 wakati kwenda Dodoma hazitazidi saa 3.Kwa upande wa biashara, alisema itaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda, Uganda, Zambia na kadhalika ambazo hazina bahari, hivyo kutegemea kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam. Treni za mizigo zinatarajiwa kubeba tani milioni 17 kwa mwaka. Hii si tu itapunguza uharibifu wa barabara kutokana na malori ya mizigo, lakini itaongeza pia kasi ya biashara nchini na nchi za jirani pia.Reli ya kisasa ya Tanzania itakuwa na kasi ya kilometa 160 kwa saa, hivyo kuifanya kuwa ya aina yake kwa reli za masafa marefu barani Afrika. Ni ya mizigo na abiria na ina urefu wa kilomita zaidi ya 722 pamoja na njia za kupishania kutoka Dar es Salaam –Morogoro mpaka Dodoma ukitoa njia za kupishania ni zaidi ya kilomita 500 kutoka Dar es Salaam – Dodoma huku ikiwa ni ya mizigo na abiria”.Katika nchi tisa zenye miradi ya SGR barani Afrika, Afrika Kusini, Morocco na Tunisia wamejenga reli ambazo ni fupi zenye urefu wa kilomita 80 mpaka 100 zina kasi kubwa ambayo ni kilomita 200 kwa saa zikiwa treni maalumu kwa abiria tu.
kitaifa
Besson anayeiwakilisha Kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa, alitembelea wizara kufahamu fursa za uwekezaji zilizo katika sekta ya nishati na madini.“Kampuni unayoiwakilisha ni kubwa, yenye teknolojia ya kisasa na inafanya uwekezaji mkubwa duniani hivyo kama mna nia ya kuwekeza katika uendelezaji wa vitalu vya gesi mnaweza kuingia katika ushindani wa kumiliki vitalu hivyo kwani muda bado unaruhusu,” alisema Profesa Muhongo.Waziri Muhongo alisema Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), linamiliki vitalu viwili vya gesi karibu na mpaka wa Msumbiji, lakini linahitaji mbia mwenye nia ya dhati atakayeshirikiana naye katika hatua zote za uendelezaji wa vitalu.Kuhusu usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa Muhongo alimweleza Besson kuwa TPDC pia itahitaji kupata uzoefu na pengine mbia aliyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na TPDC katika usimamizi. Profesa Muhongo alisema Serikali itasambaza gesi katika makazi ya watu kupunguza uharibifu wa mazingira.Alitoa mfano kuwa jiji la Dar es Salaam pekee linatumia si chini ya magunia 50 ya mkaa kwa siku hivyo gesi itapunguza uharibifu wa mazingira.Alisema huo ni mpango endelevu kwani tayari kuna bomba la kilometa 6.3 kutoka Ubungo hadi Mikocheni linalotoa gesi majumbani na bei yake haizidi shilingi 12,500 kwa mwezi.Alisema kuwa TPDC itahitaji mbia katika utekelezaji wa mpango huo wa usambazaji gesi majumbani na katika sehemu ambazo bomba la gesi haliwezi kupita kutahitajika mitungi ya gesi ili wananchi wote wafaidi gesi hiyo.
uchumi
RAIS John Magufuli amedokeza kisa kilichosababisha kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), James Mataragio ambaye ameamuru arudishwe katika nafasi yake.Akizungumza jana katika hafla ya makabidhiano ya dhahabu za Tanzania zilizokamatwa Kenya, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Magufuli alisema Mataragio alisimamishwa kazi baada ya kukataa kupokea rushwa ili agawe vitalu viwili vya gesi baharini.Kwa mujibu wa Rais Magufuli; Mataragio akiwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, alikataa kupokea rushwa ili kuruhusu kuuzwa kwa vitalu hivyo vya gesi baharini na badala yake alisimamia msimamo wa kuzuia kitalu kimoja cha Mnazi Bay kubakia serikalini ili kiingize fedha kwa serikali.Alisema msimamo wake ulilenga katika kuwezesha uchimbaji wa gesi katika kitalu hicho kuanza na kuwawezesha wafanyabishara wanunue gesi ambayo Tanzania imepewa na Mungu kutoka serikalini.Kauli ya Rais Magufuli imekuja siku chache baada ya kuagiza Mkurugenzi huyo wa TPDC kurejeshwa katika nafasi yake ili aendelee na kazi.Mataragio alisimamishwa kazi Agosti 20 mwaka 2016 na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo chini ya Profesa Sufian Bukurura.Hata hivyo Bodi hiyo ilimaliza muda wake Juni, mwaka huu. Kusimamishwa kazi kwake kulitokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015 iliyoeleza kuwa, TPDC ilikiuka taratibu za manunuzi ya umma kwa kuipa upendeleo kampuni ya Marekani kutafiti mafuta na gesi katika maeneo ya Kaskazini na Magharibi mwa Ziwa Tanganyika, Songosongo, Mandawa na Eyasi. Machi, 16, 2018 Mataragio na wenzake wanne walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya Sh bilioni saba.Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kaimu Meneja wa Uvumbuzi, George Seni, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala, Wellington Hudson, Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu, Kelvin Komba na Edwin Riwa ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango.Hata hivyo, juzi Rais Magufuli aliagiza Wizara ya Nishati kumrejesha mara moja Mataragio katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mkuu ili kuendelea na majukumu yake.Mataragio alishika nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete Desemba 15, 2014, kabla ya hapo aliishi na kufanya kazi Marekani akiwa mtaalamu wa miamba mwandamizi wa Kampuni ya Bell Geospace ya Houston. Jana Mkurugenzi huyo Mkuu wa TPDC alizungumza na gazeti hili na kusema;“Nimeripoti kazini leo (jana), presha ya kazi ni kubwa sana, kazi ni nyingi kutoka kwa huyo aliyekuwa anakaimu, tumefanya makabidhiano ya ofisini, nikitulia nitakua kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza zaidi, ” alisema.
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesisitiza kuwa zuio la mifuko ya plastiki, litakuwa la kisheria na hivyo hakutakuwa na msalie mtume.Akizungumza Dar es Salaam jana, January alisisitiza kuwa marufuku ya mifuko hiyo, lengo lake ni kulinda afya za wananchi na mazingira. “Madhara yanayotokana na matumizi ya mifuko hiyo ni makubwa sana na hivyo si rahisi kwa mtu kuona katika hali ya kawaida,” alisema. Aliongeza kuwa wizara yao, itahakikisha zuio hilo linafanikiwa bila vikwazo na kwamba wananchi wataendelea kuelimishwa.“Katika kukabiliana na zuio hili, changamoto ni nyingi ikiwemo kutokuwa na ufahamu mpana wa wananchi juu ya athari zake, lakini tumejipanga kuhakikisha linafanikiwa na hatua muhimu zaidi ni kutoa elimu kwa wananchi,” alisisitiza. Aliongeza, “Katazo la kitu kama hiki halikosi vikwazo, kelele na hata vitisho kutoka kwa watumiaji na wazalishaji. Hivyo tumejipanga kukabiliana na yote hayo.”Alisisitiza kuwa elimu ya kutosha, itatolewa kuhusu madhara ya mifuko ya plastiki na njia mbadala zitaanza kutumika wakati wa kipindi cha zuio. “Tumejipanga kiasi cha kutosha juu ya namna ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza na jambo muhimu sana ni ushirikiano kwa kuwa mazingira ni suala muhimu kwa kizazi cha leo na kesho; hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuyalinda,” alisema January.
kitaifa
WADAU wa usalama barabarani wakiwemo wabunge wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya usalama barabarani ya mwaka Sheria ya mwaka 1973 na kubadilisha vipengele ambavyo vimekuwa vikwazo katika kupunguza madhara ya ajali.Akizungumza jijini hapa jana katika mkutano ulioshirikisha wadau, wakiwamo waandishi wa habari katika kilele cha siku ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani ambapo kwa Tanzania wanaadhimisha kwa mara ya tatu, Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Twafiq ambaye naye ni mwathirika wa ajali.Aliwataka baadhi ya askari kutenda haki na kuacha uonevu kwa kuchukua rushwa na kupoteza haki za waathirika wa ajali za barabarani. Alizungumzia suala la upakizaji wa mishikaki kwa abiria unaofanywa na dereva wa bodaboda na huku askari wakifumbia macho jambo hilo licha ya kupita mbele yao.“Sheria ya uvaaji kofia ngumu, faini iongezwe ili kuweka mkazo kwa abiria na madereva wanaofanya uzembe katika eneo hilo, matumizi ya simu kwa madereva wakati wakiendesha vyombo vya moto na kutofunga mkanda kwa abiria ambapo ni visababishi vikubwa vya ajali za barabarani.Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM) alisema madereva wa serikali ndio wamekuwa chanzo kukibwa cha ajali za barabarani kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kwenda mwendo kasi na kutosimama kwenye alama za pundamili.Bura alisema licha ya serikali kupiga marufuku matumizi ya pombe aina ya Viroba lakini bado Viroba vinatumika ambapo madereva wanatumia pombe aina ya gongo ya kienyeji ambapo wanaweka katika chupa za maji, ili mtu akiona ajue anakunywa maji kumbe sio.Mbunge wa Bahi, Omary Badweli (CCM) alikiri kuwapo kwa upungufu kwenye sheria hiyo na kusisitiza uwepo wa baadhi ya askari wa barabarani ambao wamekuwa wakipindisha ukweli pindi ajali inapotokea hivyo kumnyima haki mwathirika wa ajali. Beatrice Matemba aliyekatwa miguu yote kutokana na ajali, alisema ajali zimekuwa zikiwaletea masikini na mateso kwa waliopata ulemavu kutokana na ajali na kutengwa kwa jamii.Naye mwathirika wa ajali, Alex Mhando alisema bado kuna changamoto na usumbufu kwa waathirika kulipwa fidia na watu wa bima mara baada ya kupata ajali na kutoka kuwepo Sheria inayowabana na kuwalazimisha moja kwa moja wahusika kulipa fidia wahanga wa ajali.Naye mwakilishi na Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ulemavu (Shihivyawata), Felician Mkude alishauri mamlaka zinazohusika na barabara kuzingatia alama za barabarani na haki za watembea kwa miguu badala ya kuwathamini watumiaji wa vyombo vya moto pekee.Pia alitoa rai kwa wanaharakati kufanya uchambuzi na kuainisha maeneo ambayo wanapata madhara waathirika wa ajali hizo za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na mwendokasi. Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), John Seka alisema lengo la wadau hao kukutana ni kujenga ushawishi utakaochagiza mabadiliko ya kina ya sheria ya usalama barabarani ili kuondoa mapungufu yaliyopo katika sheria hiyo.Akisoma tamko la mtandao wa wadau katika kilele, Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Gladness Munuo aliiomba serikali kufanya mabadiliko katika sheria ya usalama barabarani katika vipengele vitano vyenye mapungufu zaidi.Aliyataja maeneo hayo kuwa ni mwendokasi kuwa kilomita 30 kwa saa katika maeneo ya makazi, shule, makanisa, matumizi ya mkanda kwa abiria wa nyuma, matumizi sahihi ya kofia ngumu kwa abiria na dereva, matumizi ya kilevi na vizuizi vya watoto.Mtandao ulioshiriki kuandaa maadhimisho ya siku hiyo kuwa ni Tamwa, TLS, Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Mfuko wa vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Shihivyawata na shirika lisilo la kiserikali la Sikika.
kitaifa
TIMU sita za netiboli zitacheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya kufanya vizuri katika mashindano yaliyomalizika juzi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bandari mjini Mtwara.Mashindano hayo ya Daraja la Pili yalishirikisha jumla ya timu nane, huku mbili zikishuka daraja wakati zingine nne zikipigwa faini ya Sh 500,000 baada ya kushindwa kutokea wakati zilithibitisha kushiriki mashindano hayo.Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Judith Ilunda alisema jana kuwa timu za Tamisemi, Jiji Dodoma na JKT Makutopora zote za Dodoma, Magereza Lindi, Smart Queens na Eagle Queens zote za Dar, ndizo zilizopanda daraja.Alisema kuwa timu hizo zilipanda daraja baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Daraja la Pili Taifa na kuungana na zingine za Daraja la Kwanza kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano ya netiboil.Ilunda alizitaja timu ambazo zimekumbana na lungu la kulipa faini ya Sh 500,000 kila moja baada ya kushindwa kushiriki mashindano hayo ni pamoja na Magereza Mahabusu, Kigamboni Queens na Kinondoni Queens.Baadhi ya timu zilizopo Daraja la Kwanza ni pamoja na mabingwa watetezi, Uhamiaji, JKT Mbweni, Jeshi Stars, Polisi Moro, JKT Mgulani, Magereza Moro, Sedico, Arusha Queens, Bandari Dar, Coca-Cola Kwanza, Zimamoto na Polisi Arusha.Akizungumzia timu zilizoshuka daraja kutoka Daraja la Pili kwenda `mchangani’, ni pamoja na Lindi Queens na Ruvuma Kombaini, ambazo zitakwenda kuanzia wilani na mikoani katika msimu ujao.Aidha, Ilunda alisema kuwa timu za Uhamiaji, Magereza, Polisi Morogoro, Polisi Arusha na Jeshi zitawakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya Ligi ya Muungano yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 2.
michezo
JUMLA ya makontena 34 yenye seti za meza na viti 22,000 vimewasili bandarini Zanzibar na vinatarajiwa kuanza kusambazwa katika shule za Unguja na Pemba.Mwenyekiti wa kamati ya madawati kitaifa, Waziri Haroun Ali Suleiman amesema madawati hayo yamewasili kutoka China ambapo yametengenezwa na Kampuni ya Guangzhou Everprety Furniture Limited.Amesema kamati hiyo ilipewa jukumu la kuchangisha wadau mbalimbali madawati kwa ajili ya matumizi ya shule za Unguja na Pemba ambazo zinakabiliwa na tatizo hilo.Amesema jumla ya Sh bilioni 3.8 zimetumika kwa ajili ya kutengeneza samani hizo ambapo kabla kumefanya wanafunzi wengi kusoma sakafuni.''Tumepokea shehena ya makontena yenye seti za samani ikiwemo madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao wanakabiliwa na tatizo hilo kiasi cha kusoma na kukaa chini,''amesema.Amesema kiasi hicho cha madawati kwa kiasi kikubwa kitapunguza tatizo hilo ambalo limeongezeka kutokana na serikali kutangaza elimu ya maandalizi kuwa ya lazima.Alifahamisha kwamba hiyo ni awamu ya kwanza ya madawati, ambapo awamu ya pili inatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao.Mapema Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema wizara itahakikisha madawati hayo yanatunzwa huku walimu wakuu wote wakitakiwa kuwa wasimamizi wakuu.Alisema juhudi zaidi zinahitajika katika kutafuta madawati ambapo upo upungufu wa madawati 17,950.''Licha ya kupata kiwango kikubwa cha madawati bado tunakabiliwa na uhaba wa madawati yapatayo 17,950 kwa shule za Unguja na Pemba,'' amesema.Mwaka 2017 Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliunda kamati ya watu 11 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi tatizo la uhaba wa madawati kwa shule za Unguja na Pemba.
kitaifa
KUTOKANA na ufanisi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) katika uagizaji wa mbolea kwa pamoja, sasa Bodi ya Sukari imeomba ushirika na wakala huo katika uagizaji sukari.Aidha, PBPA imepanga kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuweka utaratibu wa flowmeter katika mabomba yatokayo bandarini kwenda kwenye kampuni zenye maghala ya kuhifadhia mafuta ili kujua kiasi kilichoshushwa.Haya yamebainishwa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PBPA, Erasto Simon wakati wa kutoa mada kuhusu shughuli za uagizaji mafuta kwa pamoja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.Amesema baada ya mafanikio ya mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja (BPS), na pia kufanikisha kikamilifu uagizaji wa mbolea kwa pamoja, sasa Bodi ya Sukari imeomba ushirika huo katika uagizaji sukari.“Kutokana na ufanisi wa mfumo huu, PBPA imeshiriki kikamilifu katika uanzishwaji wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja na sasa Bodi ya Sukari imeomba ushirika wa PBPA katika kuanzisha mfumo wa BPS katika uagizaji wa sukari,” amesema.Alisema mpaka sasa mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja, umekuwa na mafanikio kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwa na uhakika wa usalama wa upatikanaji wa mafuta kwa muda wote na kuwezesha kupanga bei elekezi.Simon alisema mfumo umesaidia kuwa na takwimu za uhakika na kuwezesha serikali kupanga ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia takwimu sahihi.“Hii imerahisisha sana katika kupanga mapato na matumizi ya serikali na pia udhibiti.“Mfumo umesaidia suala la usalama wa upatikanaji wa mafuta kwa muda wote, kuongezeka kwa sehemu za kupokelea mafuta Tanga na Mtwara na kudhibiti ubora wa mafuta yanayoingia nchini,” alisema.Simon alisema pia imesaidia kuwa na chanzo kimoja cha uagizaji wa mafuta, hivyo kuziwezesha kampuni mpya kuweza kununua mafuta bila kupata changamoto zozote na kujua sehemu, ambapo masoko yanapatikana.“Mfumo umesaidia kuweka mazingira sawia kibiashara kwani gharama uagizaji wa mafuta nchini ziko sawa kwa kampuni zote na kupata bei nzuri kutokana na wingi wa mafuta yanayoagizwa.“Pia kuondoa mianya ya rushwa katika uagizaji wa mafuta kwani ufunguzi wa zabuni hufanyika kwa uwazi na washiriki wote kuridhika na matokeo ya zabuni,” alisema.Akizungumzia changamoto, Simon alitaja changamoto iliyopo ni wapokeaji wa mafuta, kushindwa kukamilisha taratibu za ulipaji wa mafuta kwa wakati, kama inavyoelekezwa kwenye mikataba.Simon alisema changamoto nyingine ni mleta mafuta kuchelewa kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa kwa mpokeaji wa mafuta ili kukamilisha taratibu za malipo kwa wakati.Alitaja changamoto nyingine ni kusitishwa kwa meli kushusha mafuta kutokana na mafuta ambayo hayajalipiwa kukosa hifadhi na hivyo meli kusubiri mpaka hifadhi kupatikana.Akizungumzia mikakati inayofanyiwa kazi, Simon alisema TBPA imepanga kufanya tathmini ya namna bora ya kuanza uingizaji wa pamoja wa LPG kwa kuzingatia maoni kutoka kwa wadau.Simon alisema PBPA kushirikiana na EWURA kuweka utaratibu wa kufunga ‘flowmeter’ katika mabomba yote, yatokayo bandarini kwenda katika kampuni zenye maghala ya kuhifadhia mafuta ili kuwana uhakika wa kiasi cha mafuta kilichoenda kwenye maghala husika.“ Mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja umekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na ongezeko la mafuta anayoingizwa kwa ajili ya matumizi ya ndani na yanapita kwenda nchi jirani” alisema.
uchumi
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa badhi ya wakazi wa mjini Sumbawanga wanalazimika kutumia pumba za mpunga kupikia chakula baada ya mkaa kupanda kwa kasi.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa gazeti hili jana mjini hapa, baadhi ya wakazi hao wamekiri kushindwa kununua mkaa huo kwa bei ya kati ya Sh 40,000 na 45,000 kwa gunia. Wiki mbili zilizopita gunia moja la mkaa kwa bei ya rejareja lilikuwa likiuzwa Sh 30,000.“Hali ya maisha imekuwa ngumu na chungu kwangu heri ya mwaka jana, sababu ni kwamba kutokana na kipato changu kuwa cha chini siwezi kumudu kununua gunia la mkaa kwa bei ya Sh 40,000. Kilichotokea ni kwamba sasa natumia pumba za mpunga kupikia chakula,”amesema Mariam Joseph ambaye ni mama wa watoto wanne.Alisema changamoto anazozipata wakati akipika kwa kutumia pumba hizo za mpunga ni pamoja na kuwa na moshi mwingi ambao akiuvuta anakohoa sana.Naye mkazi wa kitongoji cha Kizwite, Manispaa ya Sumbawanga, Lucy Ngomeni alisema “Nalazimika kutumia pumba hizo kupikia chakula lakini kiafya naathirika sana, hii wiki ya pili natumia pumba hizo kupikia chakula baadaye tunalazimika kushinda pia kulala na njaa kwa sababu msimu huu wa mvua pumba zinakuwa zimelowa”.Kupanda kwa bei hiyo kunaelezwa kumechochewa na ushuru unaotozwa na Idara ya Maliasili na halmashauri za wilaya kupitia ofisi za vijiji, kuongezeka.
uchumi
SERIKALI itaendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wa umma watakaofanya ubadhirifu katika miradi ambayo serikali imeweka fedha nyingi kwa maendeleo.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha ameyasema hayo alipozungumza na watendaji wa serikali ya mkoa wa Morogoro baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya elimu kutoka Ofisa Elimu mkoa, Mwalimu Joyce Baravuga.Amesema sekta ya elimu imepewa kipaumbele kikubwa na serikali ya awamu ya tano kwa kutengewa fedha nyingi.Ukiacha miundombinu, wizara yake pekee inapokea Sh trilioni 1.4 katika bajeti ya mwaka na kwenye fedha za maendeleo upatikanaji wake ni asilimia 100.“Tanzania inasifiwa Afrika kuwa kati ya nchi ya kwanza kuongeza bajeti ya elimu hadi asilimia 21.2 ya bajeti ya taifa,” amesema Waziri Nasha.Naibu Waziri huyo alisema kipaumbele kikubwa cha serikali ya awamu ya tano ni sekta ya elimu hivyo ni wajibu wa viongozi wenye dhamana kusimamia na kufuatilia miradi yake ya maendeleo ngazi ya mikoa na wilaya kwa kutoka ofisini na kwenda kufuatilia utekelezaji wake pasipo kusubiri viongozi wa ngazi za juu.Alisema kuanzia mwaka 2016, serikali inatekeleza mpango wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na imekuwa ikitumia kila mwezi, Sh bilioni 20.8.Ameipongeza Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA) Kanda ya Mashariki na Chuo cha Veta Kihonda kwa kutumia vyema fedha za ujenzi wa karakana mbili ya fani ya useremala na ya umeme wa magari chuoni zilizogharimu Sh bilioni 1.8 zilizotolewa na serikali.Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Ofisa Elimu wa mkoa wa Morogoro, Baravuga alisema wana uhaba wa walimu 4,248 wa shule za msingi na 796 wa sekondari, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, madawati, ofisi za walimu na maabara.
kitaifa
NAHODHA wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta leo anatarajia kuichezea kwa mara ya kwanza Aston Villa tangu akuposajiliwa kutoka Genk ya Ubelgi.Aston Villa inashuka dimbani kumenyana na Leicester City katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Carabao utakaofanyika kwenye Uwanja wa Villa Park, huku Samatta akitegewa katika safu ya ushambuliaji.Samatta alisajili wa Aston Villa hivi karibuni huku akitegemewa sana na timu hiyo ambayo ilikuwa haifanyi vizuri katika Ligi Kuu ya England.Tayari kocha wa timu hiyo, Dean Smith amethibitisha kutaka kumpanga Samatta huku akiwa na matumaini makubwa na mshambuliaji huyo baada ya safu ya ushambuliaji ya Aston Villa kuwa na matatizo baada ya kukumbwa na majeruhi na wengine kuondoka katika timu hiyo.Hata hivyo, nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, anatarajia kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa beki kisiki Mturuki Caglar Soyuncu.Aidha, mchezo huo ambao unatarajiwa kutazamwa na mamilioni ya Watanzani wengi baada ya Samatta kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika klabu ya Ligi Kuu ya England.Licha ya Villa kupewa nafasi ya kuibuka na ushindi kwa faida ya uwanja wa nyumbani, bado mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote kutokana na matokeo ya mechi ya awali, ambayo walitoka sare ya 1-1, na ubora wa Leicester kwa sasa.Kocha Smith aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Samatta amekuwa na mwenendo mzuri mazoezi tangu ajiunge na klabu hiyo, hivyo kuna nafasi kubwa ya kumchezesha katika mchezo huo wa leo.
michezo
Wataalamu hao wakiongozwa na Paolo Mauro, walisema katika taarifa yao jana kwa vyombo vya habari, kuwa hata ukuaji wa uchumi nchini bado ni imara.“Kutokana na mwendelezo mzuri wa sera ya fedha na wa bei za vyakula katika kanda, mfumuko wa bei unatarajiwa kushuka zaidi katikati ya mwaka huu hadi kufikia lengo la muda wa kati la asilimia 5,” ilisema taarifa hiyo.Iliongeza kuwa nakisi ya urari wa mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi iliongezeka zaidi mwaka jana, kutokana na kupungua kwa bei za mauzo ya dhahabu na mazao asilia katika soko la dunia.Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/13, iliongeza taarifa, kulijitokeza matumizi makubwa ya Serikali kuliko ilivyotarajiwa na kusababisha kiwango halisi cha ukopaji wake, kutoka taasisi za ndani kuzidi lengo lililokubaliwa chini ya mpango wa Serikali na IMF kwa asilimia 1.2 ya Pato la Taifa.“Katika mwaka huu wa fedha (2013/14), makusanyo ya mapato yanaendelea kuwa chini ya makadirio yaliyoingizwa katika bajeti iliyopitishwa na Bunge.“Ili kufikia nakisi ya bajeti ya karibu na asilimia 5 ya Pato la Taifa, Serikali imechukua hadhari katika kupeleka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti,” ilisema taarifa.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wa mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka, inatarajiwa mgawo wa matumizi kupunguzwa ili yaendane na makusanyo ya mapato. Wakati huo huo, malimbikizo ya madeni yameongezeka kwa kiasi kikubwa, hasa kwa miradi ya barabara.Ilishauriwa kuwa ili kutunza heshima ya mchakato wa bajeti na sera ya fedha, hatua zaidi za kisera zinahitajika ili kuepuka malimbikizo mapya na kulipa yaliyopo baada ya ukaguzi."Kuendeleza utulivu wa uchumi ni muhimu kwa ajili ya uchumi kuendelea kukua kwa haraka katika kipindi cha muda wa kati … changamoto kubwa ni kuendelea kuiwezesha bajeti kukidhi uwekezaji katika miundombinu na matumizi kwa ajili ya vipaumbele vya jamii, na wakati huo huo kuendelea kupunguza nakisi ya bajeti ili kulifanya deni la Taifa kuendelea kuwa himilivu,” ilisema IMF.Mageuzi yanayoandaliwa katika sera za kodi za Serikali ikiwa ni pamoja na mapitio ya sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) yana uwezo wa kuongeza ufanisi na kukusanya mapato zaidi na kuleta usawa katika kugawana mzigo wa kodi, ilisema.Hata hivyo, uzoefu katika mwaka huu wa fedha wa makusanyo ya mapato yasiyotosheleza matumizi, vinapaswa vitumike kuona umuhimu wa kuwa na makadirio halisi ya mapato katika mzunguko ujao wa bajeti."Makubaliano yalifikiwa katika ngazi ya wataalamu juu ya hatua za kisera ambazo zitachangia kuhitimisha mapitio ya mwisho chini ya mpango mpya wa Ushauri wa Sera za Uchumi (SCF). Uhakiki wa mwisho unategemea idhini ya Baraza la Mawaziri na Bodi Tendaji ya IMF.“Makubaliano ya jumla yalifikiwa kwenye muhtasari wa mpango ambao hatimaye unaweza kuwa mpya wa PSI wakati ikisubiri kukamilika kwa majadiliano ya kina,” ilisema.Taarifa ilieleza kuwa mkutano ujao wa Bodi Tendaji ya IMF kuhusu Tanzania umepangwa kufanyika mwishoni mwa Aprili.“Timu ya wataalamu wa IMF inatoa shukrani kwa majadiliano ya uwazi na yenye tija kwenye masuala ya kisera na kwa ukarimu wa dhati wa Serikali,” ilihitimisha taarifa hiyo.Ujumbe huo wa IMF ulikutana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu na maofisa waandamizi wa Serikali.
uchumi
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe alitoa mwito huo kwenye mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert Paschal alipomtembelea ofisini kwake.Gembe alisema benki hiyo ina wajibu wa kutoa elimu ya kina kuhusu kilimo cha kisasa kwa kutilia mkazo miundombinu muhimu ya kilimo kama vile skimu za umwagiliaji.“TADB mna wajibu wa kuhamasisha kilimo cha kisasa na cha kibiashara kwa wakulima wadogo waweze kubadilisha fikra zao kutoka kilimo cha mazoea na kufikiria kilimo cha kisasa chenye tija kitakachoongeza kipato cha wakulima hao,” alisema Gembe.Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilombero alisema benki inapaswa kutekeleza kwa vitendo juhudi za serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini kupitia kilimo ambacho kinaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi.Alisema ili kufikia malengo yake, benki inapaswa kuwa na wataalamu wa utafiti na maendeleo waweze kuratibu taarifa za utafiti na maendeleo ya kilimo, hali ya hewa, udongo unaofaa kwa kilimo, pamoja na hatua nyingine za kuhuisha maendeleo kwenye kilimo.Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Paschal alisema wamejipanga kutoa mikopo ya kilimo katika makundi matatu. Nayo ni mikopo ya muda mfupi, wa kati na wa muda mrefu.Paschal alisema kwa kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo manane ya minyororo ya uongezaji wa thamani. Alisema benki inahitaji kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine izielekeze kwenye kuendeleza kilimo.Mkurugenzi huyo wa mikopo alimuomba ushirikiano Gembe kuhakikisha mikopo hiyo inarudishwa kwa wakati.
uchumi
RAIS John Magufuli amewaagiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kutotoa rushwa na kuripoti wanapoomba rushwa. Akizungumza na wafanyabiasha Ikulu jana, Rais Magufuli aliwapongeza wafanyabiashara hao kufika katika mkutano huo kwa gharama zao na pia kutoa michango yao kwa lengo la kuboresha huduma za serikali lakini pia mazingira ya biashara.Alisema lengo la mkutano huo ilikuwa ni kueleza changamoto mbalimbali zinazosababisha kodi isikusanywe ipasavyo ambapo alikumbusha kuwa kazi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) ni kukusanya kodi. Aliwashukuru wafanyabiashara hao kwa kusema ukweli na wameeleza kodi inayokusanywa labda asilimia tatu ndio inakwenda serikali na asilimia kubwa inapotea kutokana na rushwa.Alisema kodi isipokusanywa kama nchi itaingia katika matatizo makubwa na kuongeza kuwa maendelo yote yanayofanyika ni kutokana na kodi za wananchi. “Vituo vya afya, hospitali vyote vinajengwa kwa kodi za wananchi. Kuna hospitali 67 zinajengwa ni kodi zetu, ukarabati wa shule kongwe 88 ni kodi …mradi wa kufua umeme Rufiji unagharibu Sh Trilioni 6.5, treni za spidi hivi vyote vinajengwa kwa fedha zenu..mfano mradi wa umeme tutaumia leo lakini baadaye umeme utakuja kushuka kwa faida yenu,” alisema na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara na ununuzi wa ndege vyote ni kutokana na kodi za Watanzania.Alisema Watanzania wote kwa pamoja wakishirikiana Tanzania itainuka. Kwa mujibu wa Rais Magufuli aliyataka majadiliano hayo na wafanyabiashara ili wale wanaosumbua wafanyabiashara wajulikane na kuwekwa wazi. “Kamishna wa TRA na makamishna wote tunahitaji kodi lakini sio kodi kwa manyanyaso. Sipendi kuona mfanyakazi wa TRA akimnyanyasa mfanyabiashara na nyie wafanyabiashara acheni kunyanyasa wafanyakazi wa TRA, maana kuna wafanyabiashara wengine mna maneno ya mabaya na ya jeuri,” alisema na kuongeza hata kwenye maandiko watoza ushuru wanachukiwa.Alikiri kuwa wapo wafanyakazi wa TRA waaminifu na wanafanyakazi vizuri na ndio wamekuwa chanzo cha kodi kuongezeka na kuwataka wafanyabiashara kukataa rushwa na kitendo cha kukubali kutoa rushwa ndio chanzo cha kunyanyasika. “Halafu naomba niwaambie akija mfanyakazi wa TRA na kukutisha kuwa ametumwa na uongozi wa juu, sijui wamepewa maagizo kutoka juu, waambie wawaoneshe hao wako wa juu, maana mara nyingine usikute wametumwa na mapepo maana nao wanakaa huko huko juu,” alisema.Kudai kodi bila mitutu ya bunduki Alionya pia tabia ya maofisa kodi kwenda kudai kodi na mitutu ya bunduki na kuongeza kuwa biashara ni mahusiano nasio kutishana. Rais Magufuli pia aliwakanya wafanyabiashara tabia ya kuoneana wivu na kupigana vita, kwani vitendo hivyo vitawarudisha nyuma na sio kusongambele. Alisema pia anatambua dhambi zao ndogo ndogo kwani wako wanaodaiwa wameshindwa kurudisha mikopo na kuwataka wanaporudi wakatengeneze.Rais aliwataka wafanyabiashara kuwataja wanaowazungusha na kuwasumbua wanapokwamishwa kusafirisha bidhaa zao kwenda nje. “Ukweli ni kwamba tusipokusanya kodi kama nchi tutakuwa na tabu sana, tunazungumza vituo vya afya 355 fedha za kujenga vituo hivyo ni kodi za watanzania, ukarabati wa shule kongwe zaidi ya 88 fedha zile ni kodi, kujenga miradi mkubwa wa reli wa trilioni 7.5 ni kodi,” alisema.Alisema gharama za umeme ni changamoto kwa kuwa nchi nyingine gharama yake ni ndogo tofauti hapa nchini ambapo huuzwa kwa senti 11 hadi 12 kwa uniti moja. Aliwataka pia wafanyabiashara kutokutoa rushwa kwa maofisa wa TRA kwa maelekezo kwamba ni maagizo ya juu.“Msikubali kwamba ni maelekezo ya juu pengine ni maelekezo ya pepo,” alisema.Hata hivyo alitoa angalizo kwa wafanyabiashara kuangalia hizo mamlaka ambazo zinakwenda kukusanya kodi na kudai ni maelekezo kutoka juu kuwa wengine wanaweza kuwa ni majambazi. Aliwataka TRA kuwasikiliza wafanyabiashara katika makadirio na ulipaji wa kodi. “Ukiwa huna mwambie bwana sina nitalipa polepole, na nyie TRA wasikilizeni, biashara ni mahusiano sio uadui, wasikilizeni,” alisema Rais Magufuli.Aidha, alisema taifa linalojitambua linawathamini wafanyabiashara wake, na kwamba kuna fursa mbalimbali ndani ya nchi pamoja na ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo wafanyabiashara wanaweza kuzitumia. Aliwataka pia wafanyabiashara hao kukaa katika vikao vya kanda kuzungumza na kupeleka mapendekezo yao ya kikodi pamoja na changamoto nyingine katika wizara husika. Rais Magufuli alisema kila mmoja akitimiza wajibu wake taifa litafanikiwa na kwamba kuna watu wananyanyasika lakini hawazungumzi.“Ombi langu mkazungumze yale ya kweli yanayowagusa Watanzania, hayo ndio ambayo napenda kuyasikia mimi,” alisema. Aliagiza pia benki ziwasaidie wafanyabiashara kuendelea kwani hakuna nchi itakayofanikiwa bila wafanyabiashara. Ataka waache kuoneana wivu Rais Magufuli alisema kuwa wafanyabiashara waache kuoneana wivu “Unakuta mfanyabiashara huyu hampendi huyu, huyu anampiga vita huyu, haijengi… eneo la kufanya biashara ni kubwa, ninawaomba sana tutakapoondoka sisi tuwe na watu zaidi ya milioni 100 mabilionea,” alisema Rais Magufuli.Alisema hakuna vyama katika wafanyabiashara, chama chao ni fedha hivyo wafanye biashara yao kwa uwazi na uhuru. Rais Magufuli aliwataka kujipanga katika biashara zao huku akitolea mfano walikuja wafanyabiashara kutoka Uturuki, walipokutana na wafanyabiashara wa hapa nchini kuna ambao hawakua hata na kadi za mawasiliano. Aliwataka pia wafanyabiashara kuwa wazalendo kuitangaza Tanzania vizuri wanapoenda nje ya nchi sio kuipaka matope na kuichafua.Majaliwa: Wanaoisemea ukweli TRA wasionewe Kwa upande wake Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza mtu yoyote asiadhibiwe kwa kusema ukweli juu ya changamoto za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo wamezieleza katika kikao hicho. Waziri Mkuu alisoma ujumbe alioandikiwa na mfanyabiashara katika mkutano huo uliosema kuwa watu wengi wanaogopa kuisema TRA kwa sababu mkutano huo uko mubashara, watashughulikiwa kwasababu mamlaka hiyo ni miungu watu wanawaathibu wafanyabiashara.Alisema mafanikio yanayoletwa na serikali yanatoka katika kodi zinazotokana na kodi za wananchi na kwamba serikali inatambua jitihada za wafanyabiashara na ina nia njema kwao. Alisema serikali imefanya ziara katika sekta zote kusikia changamoto zao za kibiashara na pia kukutana na TRA na sekta nyingine za kibiashara na kubaini kuwa kuna tozo nyingi zinazofanana. Alisema pia kuwa wamebaini kuwa TFDA na TBS zinafanya kazi zinazofanana hivyo serikali inaangalia namna ya kuunganisha na kuwa chombo kimoja, wanasubiri ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG).“Tulichokifanya tumeziambia sekta hizo wakae pamoja na kuunganisha zile zinazofanana tuziainishe ili kuacha tozo moja kwa taasisi moja ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara, pia mamlaka hizi TFDA na TBS wote wanamashine zinazofanana kwanini tusiwe na chombo kimoja,” alisema. Alimuagiza Kamishna Mkuu wa TRA, kufatilia mianya ya rushwa, kodi kubwa, kufunga maduka ya watu bila kutoa elimu na timu nyingi za ukaguzi kaguzi ambazo haina uhakika kwamba ni za mamlaka hiyo.“Wafanyabiashara wanaambiwa hii ni timu kutoka juu, nilikutana na wafanyabiashara Kariakoo walizungumza mengi, uonevu … kuna mzigo wa mwananchi umekaa miaka mitatu amerudishiwa mwaka huu baada ya kufatilia,” alisema Waziri Mkuu ambapo Rais Magufuli ameagiza waliohusika kukamatwa na kupelekwa mahakamani na mfanyabiashara kulipwa fidia.Waziri Mkuu alisema atahakikisha serikali inajenga mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara, kuimarisha biashara za mipakani na kushirikiana na wafanyabiashara kuhakikisha wanapata faida kubwa na kulipa kodi.Alisema pia kuwa serikali meweka mkakati wa kulinda bidhaa za ndani na kwamba imeongeza kodi kwa mabomba yanayotoka nje ya nchi na kuwataka wakandarasi kutumia mabomba ya ndani katika miradi ya serikali. Aidha, alisema serikali imeboresha mazingira ya kilimo na kuongeza mazao ya kibiashara ambayo ni mkonge na michikichi, imepangua tume ya umwagiliaji na kupanga timu mpya lengo ni kuhakikisha kilimo kinapata nafasi kubwa. “Wawekezaji wote sekyta ya kilimo njooni wizarani leteni mapendelezo yenu, uzeni mazao nje lakini tuwe na takwimu ni kiasi gani yanauzwa nje,” alisema Waziri Mkuu.Alisema amepokea changamoto ya serikali kutojibu barua zote kwani wajibu wa serikali ni kujibu barua hizo bila kujali umuhimu wake. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema serikali imeamua kupiga marufuku matumizi ya baadhi ya mifuko ya plastiki na kuwataka wafanyabiashara wapiti sheria na kanuni zilizopo. “Naomba mkasimamie ili wote huko muwe walinzi tunaomba sana na nyie muwe mabalozi huko,” alisema. Alisema wafanyabiashara ndio ambao wataifikisha Tanzania katika uchumi wa kati, hivyo ni vizuri kueleza changamoto zao zikafanyiwa kazi na mazingira ya biashara kuboreshwa.Samia onya Taasisi za Udhibiti Samia alisema Taasisi za Udhibiti zimegeuka kuwa vyanzo vya mapato kwa sababu badala ya kuwa wasimamizi na hiyo ni kwa sababu katika miongozo yao kuna sehemu wamelekezwa adhabu, amewataka kufanya kazi yao ya udhibiti na si vinginevyo. Aidha, alisema anakubaliana na wafanyabiashara kwamba ofisi ya Mazingira na ya NEMC zilikua hazifanyi kazi vizuri lakini sasa yamefanyika mabadiliko. Samia alishauri pia mapendelezo yatakayoletwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi yapelekwe kwa kanda na si kwa mikoa jambo ambalo litakua rahisi kufanyiwa kazi.TPSF na kilimo cha tija Mkurugenzi wa Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye alisema kuwe na kampeni madhubuti kupiga vita urasimu kati ya sekta binafsi na ya umma. Pia alimuomba Rais kusimamia serikali kulipa madeni ya serikali ambayo inadai wafanyabiashara ambao wamefanya miradi mbalimbali ya serikali kwasababu madeni hayo yamekuwa ni makubwa.“Kuna watu wameua mitaji yao yote, juhudi zifanyike madeni yote ya nyuma yalipwe, muweke malengo kwamba mpaka kufikia mwezi Desemba madeni ya nyuma yawe yamelipwa na hii inawezekana, na kuweka maazimio kwamba mikataba itakayoingiwa sasa wawe na pesa kama ni mkopo uwe na riba,” alisema Simbeye. Simbeye alimuomba Rais Magufuli kubadili kilimo kiwe cha tija, alisema bila mapinduzi ya kilimo kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda itakua ni ndoto. Alishauri mabaraza ya biashara katika ngazi ya Mkoa na Wilaya yafanyike, isiwe kwa mapenzi ya Mkuu wa Mkoa au wa Mkuu wa Wilaya na kwamba wametayarisha mfumo madhubuti ya mabaraza hayo.Alisema kwa upande wa sekta binafsi wameamua kujirekebisha na kujisimamia wafanye kazi zao kwa uzalendo mkubwa. Lukuvi amshushua Kiluwa Kwa upande wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alimshushua mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa, Mohammed Kiluwa kwa kumtaka wawekezaji anaodai wametoka nchini Chini kuwapeleka Mamlaka ya Uwekezaji (TIC) badala ya kulalamika lamika. Katika hili, Rais Magufuli alichomela msumari kwa kudai ni yeye aliyefuta hati ya ardhi ya heka 1,000 alizochukua akidai kuwa anajenga viwanda kumbe ameiuza kwa wawekezaji.Rais Magufuli alisema alimshangaa mfanyabiashara huyo amepata wapi nguvu hiyo kwani sera inasema ardhi itapewa kwa Mtanzania tu na ambaye si raia atapewa kupitia TIC. “Haiwezekani ukachukua ardhi kwa bei rahisi halafu wewe ukaiuza kwa bei kubwa, nilienda kufungua kiwanda lakini nikajua sio kiwanda chake kwa sababu wanaotoa maelezo ni Wachina lakini nikakaa kimya tu, akaniomba nataka kuongezewa nikamwambia eneo lina heka ngapi, akasema heka 50, nikamwambia utakapojaza watakupa eneo lingine,” alisema.Alisema kama mfanyabiashara huyo ana wawekezaji kwanini wasiende moja kwa moja serikalini. Waziri Lukuvi awali akielezea tukio hilo alisema Kiluwa aliomba kumiliki ardhi kibaha na bei ya ardhi kwa wakati huo ilikuwa ni Sh milioni 5.8 kwa heka, lakini ofisi ya Mkoa wa Kibaha ilimuuzia kinyume cha bei yaani kwa Sh milioni moja tu. “Lakini ukiangalia kuna kampuni ya Mrusi ya Kamaka ina shea 6,500 na nyingine ya Kiluwa ina shea 1,500 na ndani yake kuna Wachina, Kamaka alikuja ofisini kwangu anadai Sh bilioni 4 alizompa Kirua atalipwa na nani,” alisema.Alisema Kamishana wa ardhi alibaini kuwa watu hao hawana viwanda, walimtaka Kiluwa awapeleke wawekezaji anaodai wana viwanda kwa Mkurugenzi wa TIC. “Hakuna muwekezaji atakuja anyimwe ardhi na Bwana Kiluwa nakwambia leo ni mara ya mwisho viwanja vimefutwa, hao watu wapeleke TIC, huyu Kamaka ni Mrusi yuko hapa miaka 25 ana nia gani ampe pesa huyu Kiluea amnunulie” alisema Lukuvi. Alisema wafanya biashara wengi wana tatizo la kulipa kodi ya ardhi kwa wakati na pia kuendeleza ardhi zao.Lukuvi alitoa mwito pia kwa wafanyabiashara hao kuwekeza kwani bado serikali ina ardhi ya kutosha kwaajili ya uwekezaji. Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Kiluwa, awali alimwelezea Rais kuwa aliomba eneo na alikuwa katika ujenzi wa kiwanda cha saruji lakini amesimamishwa ujenzi akiambiwa kwamba eneo limefutwa na Rais, alimuomba amrudishie eneo hilo na ndani ya miezi mine atajenga viwanda 10.Aidha, alisema awali Rais apokwenda kufungua kiwanda cha Kiluwa Steel aliomba eneo la kujenga viwanda vingine. “Nilikuwa na heka 50 ukasema jaza hizo taratibu nyingine mfuate RC na nilifanya hivyo baada ya hapo niliomba eneo lingine heka 1,000 niliomba nikaenda halmashauri nikalipia bilioni 1 na kulipia kodi na taratibu zote,” alisema.Mwanasheria na mikataba ya blue Print Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilagi alisema serikali inashughulikia mkataba wa blue Print na sheria zote zenye vikwazo kwenye biashara kwa uratibu wa ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha alisema kuwa wamepewa kupitia sheria ya uwekezaji na nyingine zinazoathiri biashara na uwekezaji kuondoa vikwazo na kwamba mpaka mwezi Septemba mwaka huu kutakua na mabadiliko makubwa.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Diwani Athuman alisema penye rusha hakuna haki, utulivu, usalama na maendeleo hivyo vita hiyo inatakiwa kusimamiwa na watu wote. “Kila mmoja popote alipo, ili tuweze kufanikiwa na kuwepo na dhati ya pamoja ni lazima wote tushiriki kwa dhati,” alisema. Aidha, alisema moja ya kazi zinazofanywa na Takukuru ni kufanya tafiti, katika tafiti hizo imeonesha wafanyabiashara wanashirikiana na baadhi watumishi wa umma kukwepa kodi.Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Florens Luoga alisema kazi ya BoT ni kuhakikisha huduma za benki zinamfikia kila mwananchi, hata wa vijijini na kwamba kazi yao ni kusikiliza mipango yao ya kutanuka mpaka vijijini. Aidha, akizungumzia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, Profesa Luoga alisema kuwa serikali haijachukua fedha za wafanyabiashara na kwamba kuanzia wiki ijayo uchunguzi umeanza kufanyika wanaostahili watachukuliwa hatua.“Hakuna pesa zilizonyang’anywa na wiki iliyopita tumeanza kufanya uchunguziwanaostahili wachukuliwe hatua, sio sahihi wanavyosema kwamba wamenyang’anywa,” alisema Profesa Luoga. Alisema kwa sasa BoT inaimarisha mfumo wa uingizaji na usafirishaji nje ya nchi kwani wafanyaji wa biashara hizo awali walikua wanabeba fedha kwenye mabegi hawatumii benki.Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala alisema sekta ya utalii inaendelea vizuri, changamoto ya tozo, tozo hizo ziko katika taasisi nyingine na tumeanzisha mfumo wakielektoniki taasisi zote zitalipwa kwenye dirisha moja. Sheria ya uwekezaji Sheria ya uwekezaji ni ya muda mrefu ina miaka 22 sasa inahitaji kupitiwa na kwamba kongamano la elimu Tabora litaandaliwa kama walivyoomba na pia yataandaliwa makongamano ya sekta nyingine. Sera ya sekta binafsi inaandaliwa. Blue print ndani ya mwaka mmoja itakuwa katika hatua nzuri na itasaidia wafanyabiashara.Mawaziri waonesha njia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchikaalitoa mwito kwa wafanyabiashara kutokubali kutoa rushwa, wanapoombwa rushwa na watumishi wa umma watoe taarifa. Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Joseph Kakunda alisema wizara yake inajitahidi kulinda viwanda vya ndani na kwamba wajiandae kuongeza uzalishaji pamoja na kuboresha bidhaa wanazozalisha. Waziri wa Kilimo, Josephat Hasunga alisema kuwa nchi ina utoshelevu wa chakula kwa zaidi ya asilimia 100 na kwamba changamoto zilizopo ambazo ni mbegu, viwatilifu na mbolea sekta binafsi inaweza kuchukua fursa hiyo na kuwekeza.Aidha, alisema kuwa changamoto kwa maofisa ugani ambapo atazungumza na Tamisemi ili waweze kutumika vizuri katika kuboresha kilimo. Waziri wa Fedha na Mipango, Philiph Mpango alisema kuwa ni wakati sasa wa kufanya maboresh katika mfumo wa kodi na tozo kwani umekuwa ni wa muda mrefu. Rais atoa maagizo Katika mkutano huo Rais Magufuli alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutumia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, madini, uvuvi, mifugo, biashara na pia fursa zilizopo katika Jumuiya ambazo Tanzania ni mwanachama ambazo ni Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Aidha aliwataka kwenda kukaa katika kanda zao na kuainisha maeneo yote ambayo wangependa Serikali iyaboreshe na kuwasilisha kwa Waziri Mkuu na pia ameitaka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kujitathmini upya ili utendaji wake uakisi na kuwagusa wafanyabiashara wote nchini badala ya kuonekana ni taasisi inayofanya kazi na watu wachache waliopo Dar es Salaam.Kufuatia changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na wafanyabiashara katika mkutano huo, Rais Magufuli alichukua hatua za papo hapo zikiwemo kuagiza Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro (RCO), SSP Asifiwe Ulime kusimamishwa kazi na kuchunguzwa kufuatia unyanyasaji uliofanywa na Polisi dhidi ya watumishi wa Kiwanda cha Tumbaku (TLTC), kuchunguzwa na kuvuliwa madaraka kwa Meneja wa TRA Mkoa wa kikodi wa Ilala Jijini Dar es Salaam , Abdul Mapembe kufuatia kufungwa kampuni ya kazi za sanaa ya Steps Entertainment bila sababu za msingi na kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa maoafisa watatu wa TRA ambao walizuia mzigo wa mfanyabiashara mmoja kwa miaka mitatu huku wakishinikiza kupewa rushwa. Baada ya kumaliza mkutano huo, Rais Magufuli alimkabidhi Waziri Mkuu Majaliwa orodha ya kampuni 17,447 ambazo zinajihusisha na udanganyifu wa kodi.
kitaifa
KIKOSI cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo asubuhi kinatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20 kwenda Iringa kukabiliana na Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, bila ya baadhi ya wachezaji wake nyota.Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora keshokutwa. Katika msafara huo watakosekana nyota wake watano wanaoumwa ambao wamekuwa tegemeo na mhimili kwenye kikosi hicho kutokana na mchango wanaoutoa wakiwa uwanjani.Akizungumza na gazeti hili Mratibu wa Kikosi hicho, Hafidhi Saleh alisema mipango yote ya maandalizi iko sawa kuwakabili wapinzani wao na wanakwenda kwa basi kuwakabili Lipuli.“ Katika msafara wetu tutawakosa wachezaji wetu, Ibrahim Ajib, Juma Abdul, Ramadhan Kabwili, Andrew Dante, Abdallah Sahibua ambao wanaumwa kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa daktari wetu, hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi chetu,” alisema.Saleh amesema, pamoja na kuwakosa wachezaji hao, lakini kikosi chao kamwe hakiwezi kutetereka kwani wana uhakika wa kuendeleza makali yao huko Iringa.Yanga ambao hadi sasa wapo kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa hazina ya pointi 67 wanaenda kucheza mchezo huo wa 28 wakiwa na matarajio ya kupata ushindi ili kuhakikisha wanatimiza shabaha yao ya kutwaa taji hilo msimu huu.Wanaenda kucheza na Lipuli wanaoshika nafasi ya tano kwenye msimamo huo kwa pointi 39, ambao kwenye michezo uliopita kwenye uwanja huo walitoka suluhu na Mbao FC.Mbali na wachezaji, Yanga pia inakwenda Iringa bila kocha wao, Mwinyi Zahera ambaye amekwenda katika majukumu ya timu ya taifa ya Congo, ambaye yeye ni kocha msaidizi, huku Lipuli nao wakitarajia kumkosa kocha wao, Selemani Matola aliyefungiwa.
michezo
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Rais ameridhia hifadhi tatu mpya kuingizwa katika orodha ya Hifadhi za Taifa.Alibainisha hayo jana wakati akihitimisha na kujibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika hotuba yake ya makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.“Hapa nina hati kutoka kwa Rais, ameridhia hifadhi mpya tatu kuingia katika orodha ya hifadhi za taifa,” alisema na kuzitaja hifadhi hizo mpya kuwa ni Hifadhi ya Burigi Chato, Hifadhi ya Rumanyika Karagwe na Ibanda Kyerwa. Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla amesema biashara ya kuuza wanyama hai nje imefungwa na haitafanyika tena hata awe mnyama mdogo wa aina gani.“Biashara hii ya kuuza wanyamapori hai nje ya nchini haitafanyika tena, imefungwa, kama bado mimi ni waziri katika wizara hii nimeifunga na sitaifungua na haitafanyika kamwe, hata awe chawa…haijalishi mnyama ana ukubwa gani,” alisema. Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Muheza Adadi Rajabu.Akichangia mada Msigwa aliomba biashara ya kuuza wanyamapori hai irejeshwe kwa kile alichodai waliokuwa wakifanyabiashara hiyo wameingia katika umasikini na wengine kupoteza maisha kutokana na kukosa biashara wakati Adadi akichangia hoja alitaka biashara ya kuuza vipepeo nje ya nchi iruhusiwe.“Hakuna mnyama hai akayetoka na kuuzwa nje ya nchi iwe kwa njia halali au la…naona Msigwa ananiangalia uniangalie tu vizuri, biashara hii imefungwa, hata Adadi pia alichangia lakini uamuzi ndio huo hakuna kipepeo au mnayama hai atatoka nje… kuna vipepeo wanapatikana msitu wa Amani, ni wa kipekee hakuna sehemu wengine tunaendelea kuboresha ili watalii wazaidi wafike kuangalia lakini pia kwenye maporomoko yaliyopo karibu na pale,” alisema.Waziri Kigwangalla alisema kama kuna mtu anafuga wanyamapori wake basi afungue ‘Zoo’ watu waende wakaangalie kwenye hifadhi hizo binafsi, lakini hakuna biashara ya kununua wanyama hapa nchini na kuuzwa nje ya chini hata awe mdogo kiasi gani. Awali wakichangia hoja ya wizara hiyo wabunge walisema utalii ni biashara kubwa, hivyo serikali inatakiwa kutafuta namna ya kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo badala ya kupoteza muda katika kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu.Pia wameitaka serikali kujipanga na kuangalia namna ya kupunguza tozo nyingi ambazo walieleza zimekuwa kikwazo katika sekta hiyo muhimu nchini ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha mapato ya kigeni kwa asilimia 25.Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ni nyeti na inahitaji uwekezaji mkubwa, lakini imekuwa ikicheleweshwa na migogoro ya muda mrefu kati ya mamlaka ya hifadhi na wananchi. “Tumekuwa badala ya kufanya biashara ya utalii ni kutatua migogoro tu, tuseme sasa inatosha tufanye biashara kwa kupata suluhisho la kudumu... tuichukulie biashara ya utalii kwa upeo wa kibiashara zaidi kama wenzetu katika nchi nyingine wanavyofanya na tutajiingizia mapato zaidi ya tunayopata sasa,” alisema Msigwa na kuongeza kuwa serikali iangalie haraka mipaka na kumaliza kabisa suala la migogoro ya ardhi.Msigwa pia alizungumzia kukinzana kwa sheria mbali mbali na kusababisha utekelezaji wake kuwa mgumu na kukwamisha mazingira ya kuvutia biashara ya utalii. “Wizara hii inategemewa kuleata mapato, acheni urithi, tunaona kuna sehemu ya kazi inafanyika na mawaziri waliopo sasa... mkiendelea kazi hii nzuri, tutaondokana na hali ya kufukuzana fukuzana katika wizara hii nyeti,” alisema mbunge huyo.Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema), alisema sekta ya utalii imekuwa ikichangia asilimia 17.5 ya Pato la Taifa, lakini imekuwa haichukuliwi kwa umakini na kutaka serikali kujipanga kwa kutegemea fedha zake za ndani badala ya wadau wa nje ili kuiingua sekta hiyo.Owenya pia alizungumzia kodi ambazo alizielezea kuwa ni nyingi na kutoa mfano kwenye hoteli wamekuwa wakitozwa kodi na Osha Sh milioni 1.5, Cosota kodi sh milioni 1.5, Nemc Sh milioni 1.5 na taasisi zingine na kuhoji tozo hizo zote fedha zake zinapelekwa wapi na zinafanyia kazi gani ya kumfaidisha mfanyabiashara wa hoteli. Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema anaona kodi ya wizara hiyo ni ndogo na kupendekeza serikali iache maduhuli ya wizara hiyo angalau kwa miaka mitano ili watumie kuendelea kuboreshea wizara ili iweze kufikia mafanikio makubwa zaidi na kuliingizia taifa kipato. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), alichangia alisema tozo zimekuwa nyingi kwa wadau wa utalii na kuwa sekta hiyo haiwezi kuendelea kwa kujaza matozo kwenye biashara ndio maana hazikui. Aliitaka wizara hiyo kuwa na mbinu za kuutangaza utalii wa Tanzania na kutoa mfano wa Malaysia imekuwa ikipata watalii milioni 25 kwa mwaka na kuwa wamekuwa wakitumia vitu vya kawaida tu kutangaza utalii wao. Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba iidhinishiwe na Bunge Sh 120, 202,638, 734 kwa matumizi ya wizara, na kati ya fedha hizo, Sh 71,312, 649,000 ni matumizi ya kawaida na Sh 48,889,988, 734 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
kitaifa
KOCHA wa mabingwa wa soka wa Tanzania Bara Simba, Patrick Aussems bado ubingwa uko wazi kati yao na wapinzani wao wakubwa Yanga. Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 18 wakiwa nyuma ya Azam wanayoshika nafasi ya pili kwa pointi sita.Yanga inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza mechi 25 na kuwa mbele ya wapinzani wao Simba kwa tofauti ya pointi 12. Kihesabu hadi sasa Simba wamebakiwa na michezo 20 na kama watafanikiwa kushinda yote watafikisha pointi 105, watakuwa wamewapiga bao watani wao,Yanga ambao hata kama wakishinda mechi zilizobaki watafikisha pointi 100.“Niseme tu timu zote zilizopo juu kwenye msimamo wa ligi hasa Yanga ina nafasi ya kuchukua ubingwa, hii inafanya kila mechi tunayocheza kwa sasa kuwa ngumu.“Tutahakikisha tunashinda kila mechi yetu kuweza kutetea ubingwa wetu na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani,” alisema Aussems. Simba itakuwa wageni wa Lipuli kwenye muendelezo wa mechi zake za Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Samora kesho. Mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
michezo
WASOMI wamesema kauli ya ‘maagizo kutoka juu’ iliyokuwa ikitumiwa na baadhi ya watumishi wa umma, ililenga kuwashughulikia wananchi kama wahalifu.Kauli hiyo ambayo imekuwa ikutumiwa na baadhi ya watumishi wa umma, imezua gumzo nchini baada ya Rais John Magufuli kupitia ujumbe wake wa Mwaka Mpya kwa taifa, kuwataka watumishi wa umma kuchapa kazi, wajiamini na kuachana na kauli ya ‘maagizo kutoka juu’ katika kila kitu wanachofanya. Rais Magufuli alisema huo ni ugonjwa, ambao umeanza kuwapata watumishi wa umma wa kutojiamini, hata kama wanayoyafanya ni kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa wakati mwingine hakuna maagizo yoyote kutoka juu kama wanavyodai.Kutokana na hilo, baadhi ya wasomi waliozungumza na gazeti hili, walisema kinachofanywa na baadhi ya watumishi hao kupitia kauli hiyo ni sawa na kuwahudumia wananchi kama wahalifu, wanapokwenda kupata huduma badala ya kuwahudumia kwa heshima. Aliyewahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Mwanza ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima, alisema watumishi wa umma wanapaswa kujua kuwa Rais Magufuli, anataka utendaji bora kwa kuzingatia sera na kanuni na siyo kuwatesa wananchi, kwa kisingizio kuwa ni maagizo kutoka juu.“Kwa mfano baadhi ya watu kwenye sekta binafsi wanateseka kwa kufungiwa biashara zao ambazo zinatengeneza ajira, kuongeza mzunguko wa fedha na kuboresha maisha ya watu, kwa madai ni maagizo kutoka juu, wajibu wa kwanza wa mtumishi wa umma ni kulea na kutoa elimu kabla ya kuchukua hatua,” alieleza Dk Kitima. Kwa mujibu wa Dk Kitima, baadhi ya taasisi za umma ikiwemo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Waziri William Lukuvi, imekuwa mfano bora wa kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia sheria na kanuni.Alisema wizara hiyo imejitahidi kwa kiasi kikubwa, kutoa ufumbuzi wa migogoro ya ardhi nchini kutokana na watendaji wake wakiongozwa na Lukuvi kufika maeneo yenye migogoro, kukaa na wananchi na kusikiliza kero zao, na hatimaye kuja na suluhu ambazo zimekuwa msaada kwa wananchi. Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Alexander Makulilo, alisema kuwa utumishi wa umma unaongozwa na sheria, kanuni, sera, maadili na miongozo mbalimbali katika kutimiza wajibu wa kila siku.
kitaifa
['Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi ametia saini kandarasi ya muda mrefu na Liverpool. ', 'Raia huyo wa Ubelgiji, mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Liverpool kutoka Lille 2014 kwa mkataba wa miaka mitano kabla ya kuhudumu misimu miwili kwa mkopo. ', 'Lakini alirudi na matokeo mazuri akifunga mara mbili dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya kabla ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Tottenham katika fainali ya kombe hilo. ', "''Hisia zangu ni kwamba nilitaka kusalia katika klabu hii . Kuna kitu maalum kinachoendelea hapa''.", 'Manchester City wanakaribia kumsaini mchezaji wa Uhispania Rodri kutoka klabu ya from Atletico Madrid kwa dau litalakovunja rekodi ya klabu hiyo la £62.8m baada ya kulipa ada ya kumuachilia kulingana na timu hiyo ya Uhispania.', 'Atletico imesema kuwa wakili wa mchezaji huyo na wawakilishi wa City walilipa ada hiyo ya kuwachiliwa kwa mchezaji huyo siku ya Jumatano. ', 'Rodri mwenye umri wa miaka 23 tayari amevunja mktaba wake na Atletico ambao ulitarajiwa kukamilika ,mwezi Juni 2023. ', 'Itaipiku rekodi ya awali ya City ya £60m wakati walipomsaini Riyad Mahrez mwaka 2018.', 'Rodri alijiunga na Atletico mnamo mwezi Mei 2018 baada ya kuhudumu miaka mitatu katika klabu ya Villarreal na aliichezea kwa,mbau hiyo mara 34.', 'Tottenham imesajili kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele kutoka klabu ya Lyon kwa dau lililovunja rekodi la £53.8m .', 'Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ametia saini kandarasi ya hadi 2025 na dau hilo huenda likaongezeka hadi Yuro 70m akiongezewa marupurupu. ', 'Rekodi ya uhamisho ya awali katika timu hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Davinson Sanchez aliyesajiliwa kutoka Ajax kwa dau la £42m. ', 'Ndombele alijiunga na Lyon 2017 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya tatu katika ligi ya Ufaransa msimu uliopita.', 'Pia alicheza mara mbili dhidi ya Manchester City katika mechi za raundi ya muondoani za kombe la mabingwa Ulaya.', 'Manchester United imemsaini mchezaji wa Uingereza na beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka kwa dau la £50m .', 'Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye aliichezea Palace mara ya kwanza mwaka uliopita amekubali kutia saini kandarasi ya miaka mitano ambayo itamfanya kupokea £80,000 kwa wiki.', 'United tayari imelipa £45m mapema , na kumfanya Wan-Bissaka kuwa mchezaji wa tano aliyesainiwa kwa dau kubwa , baada ya Paul Pogba, Romelu Lukaku, Angel di Maria na Fred. ', 'Man United ilithibitisha usajili wake siku ya Jumamosi', 'Mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer alisema kuwa Wan-Bissaka alikuwa beki bora anayechipuka katika ligi ya Premia.', 'Arsenal imekamilisha uhamisho wa kwanza msimu huu baada ya kumsaini kinda wa Brazil Gabriel Martinelli.', 'Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ametia saini kandarasi ya muda mrefu , Arsenal imethibitisha. ', 'Martinelli amejiunga na Arsenal kutoka klabu ya Ituano ambapo alikuwa amefunga magoli 10 katika mechi 34 baada ya kuanza kuichezea klabu hiyo ya Brazil 2017.', "''Nataka mchezo wangu kufanana na ule wa Ronaldo'', alisema Martinelli.", 'Ni mchezaji ambaye anafanya kazi kwa bidii akiweka juhudi za kuafikia malengo yake. Kila mara anapigania kushinda mataji.', 'Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ametia saini makubaliano ya mshahara wa £200,000 kwa wiki ili kusalia katika klabu hiyo hadi mwezi June 2023, akiwa na fursa ya kuongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja. ', 'Mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na United akiwa na umri wa miaka saba kabla ya kuanza kukichezea kikosi kikuu cha timu hiyo 2016 akiwa na umri wa miaka 18.', 'Chelsea imemsaini kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic kutoka Real Madrid kwa dau la £40m, licha ya kuhudumia marufuku ya miaka miwili.', 'Kovacic alihudumu misimu miwili iliopita kwa mkopo akiichezea The Blues , akiwasaidia kushinda kombe la Yuropa na anajiunga kwa mkataba wa miaka mitano. ', 'Chelsea tayari iliukuwa imemsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 wakati alipokuwa kwa mkopo hivyobasi hakuhitaji usajili upya. ', 'Marufuku hiyo ya uhamisho iliotolewa na Fifa itahudumu hadi 2020 Januari.', 'Manchester United wamemuongezea kipa wa Uhispania David de Gea mashahara katika harakati za kumrai kusalia katika timu hiyo.', 'Mkataba wa De Gea unakamilika baada ya miezi 12 na juhudi za kumfanya mchezaji huyo kutia saini kandarasi mpya zimegonga mwamba.', 'Inajulikana kwamba ofa iliotolewa na Man United itamfanya kuwa kipa anayelipwa zaidi dunini.', ' Karibia ajiunge na Real Madrid 2015.']
michezo
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) ni moja ya sekta zilizonufaika na Mkutano wa 39 wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana jijini Dar es Salaam.Aidha, shirika hilo limeazimia kumaliza changamoto za ucheleweshaji wa safari, uahirishaji wa safari na utoaji wa taarifa kwa abiria pindi kunapokuwa na hitilafu ili kuondoa adha hiyo kwa abiria na kuwapo sokoni kimataifa.Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la Wafanyakazi la ATCL jijini Dar es Salaam.Kuhusu mkutano wa SADC, mkurugenzi huyo wa ATCL alisema shirika hilo limenufaika kwa kuwa kati ya marais 15 waliofika nchini kuhudhuria mkutano huo, Rais wa Comoro alitumia ndege ya shirika hilo kwa safari ya kuja na kurudi nchini kwake.Alisema wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo pia wametumia usafiri wa shirika hilo kuja nchini na kurudi katika nchi zao.Kuhusu changamoto zinazolikabili shirika hilo, Matindi alisema linaingia katika soko la kimataifa ikiwa tayari limepata ufumbuzi changamoto mbalimbali ikiwamo ya ucheleweshaji wa ndege kwa abiria.“Kwa mfano suala la ucheleweshaji wa ndege hakuna anayetaka ila sababu zinazotokana na uzembe zikomeshwe na zile nyingine kuwe na mpango wa kudhibiti hali hiyo mapema.”“Ucheleweshaji mara nyingine unatokana na kuharibika kwa ndege na kwa kuwa ni chache zinafanyika jitihada za kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa,” alisema.Kwa upande mwingine, Matindi alisema kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita wamekuwa wakipata soko la mizigo kwani wamesafirisha tani 59 za mizigo kutoka India kuja Tanzania.“Mizigo hiyo ikifika Tanzania ipo inayobaki hapa hapa na mingine inapelekwa nchi nyingine,” alisema.Alisema wanaendelea na mazungumzo na nchi za Botswana na Namibia ili wanapopeleka abiria Afrika Kusini wawe wanachukuliwa kutoka hapo na kupelekwa katika nchi hizo.Akifunga baraza hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ATCL, Emmanuel Koroso, alisema bodi hiyo mpya ina mtazamo mpya tofauti na ya zamani ambayo ilikuwa na mikataba isiyoeleweka pamoja na watu kuweka maslahi binafsi hali iliyozorotesha shirika hilo.
uchumi
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (pichani) amezitaka kampuni zinazotakiwa kulipa fi dia katika maeneo ya uchimbaji kufanya hivyo kwa wakati ili kuondoa migongano na wananchi.Nyongo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua lini serikali itawalipa fidia wananchi ambao wamefanyiwa tathimini lakini hawajalipwa fidia yao kwa miaka mingi? Nyongoi alisema Sheria ya Ardhi Namba 4, 1999 inataka waliothaminiwa ardhi kupisha maeneo kulipwa fidia ndani ya miezi sita.Alisema, baada ya hapo mwekezaji anatakiwa kulipa kwa riba na ikizidi miaka inatakiwa kufanyika uthamini upya kwenda na wakati. “Hivyo nizitake kampuni ambazo zinatakiwa kulipa fidia kupisha maeneo ya uchimbaji kufuata sheria kwa kuwalipa wananchi kwa wakati unaoelekezwa na sheria,” alisema.Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) alisema wizara kupitia Ofisi ya Madini Mkoa wa Geita itasimamia na kukagua eneo la mtaa wa Mgusu.Katika swali la msingi, Peneza alisema: “Wananchi wa Mtaa wa Mgusu wanaoishi ndani ya mipaka ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita Gold wanaathirika na uchafuzi wa mazingira wa taka zinazomwagwa karibu na wananchi.” Peneza alitaka kujua ni lini serikali itatoa agizo kwa Mgodi wa Geita kulipa wananchi fidia ili watoke katika eneo lililomilikishwa mgodi. Nyongo alisema wananchi wa mtaa wa Mgusu wanajishughulika na uchimbaji mdogo madini.“Hata hivyo, tathimini ya mazingira iliyofanywa na mgodi wa GGM haioneshi uwepo madhara yanayohitaji kuhamishwa kwa wananchi wa kitongoji hicho,” alisema Waziri Nyongo. Alisema Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Kifungu cha 96(1) na 97(1) (a) na (b) vinaeleza fidia inapaswa kulipwa kwa mujibu wa Sheria. Alisema mwekezaji anatakiwa kuanza kuchimba madini baada ya kushauriana na mamlaka za serikali za mtaa husika na kujiridhidhsha juu ya madhara yanayoweza kusabishwa na uchimbaji huo.Aidha, Nyongo alisema Mtaa wa Mgusu uko Kilometa 4,5 kutoka eneo la uchimbaji la Nyamulilima Star na Commet la GGM ambapo uchimbaji unaendeshwa njia ya chini kwa chini. “Kwa umbali huo ni vigumu kwa taka ngumu kufika katika mtaa huo, hata hivyo, ukingo wa miamba isiyo na madini umewekwa kuzuia miamba hiyo kutoka nje ya eneo la uchimbaji.”
kitaifa
KATIKA mchezo wa jana, kati ya Simba na Yanga kulishuhudia matukio matano kabla ya mchezo huo kuanza, Yanga kugoma kuingia kushuka katika basi lao.-Yanga walifika Uwanja wa Taifa saa 9:25 alasiri, lakini wachezaji wao walikaa ndani ya gari kwa takriani dakika 20, huku baadhi ya makomandoo wakiwafukuza waandishi wa habari waliokuwa karibi na gari hilo. Ilikuwa tofauti kwa Simba, ambao wenyewe baada ya kufika uwanjani hapo walishuka katika gari lao na kuingia moja kwa moja katika chumba chao cha kubadilishia nguo.SIMBA WAIFUNIKA YANGAKishangiliaji au kuchangamka, Simba waliifunika Yanga kabisa kabla ya kuanza mchezo huo. Dakika 15 kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, mashabiki wa Simba walionekana kuwa wenye wenye furaha kubwa baada ya hamshahamsha yao kubwa iliyowafunika kabisa wenzao wa Yanga, ambao walionekana kama vile hawataki kabisa kelele baada ya kutulia vitini kimya, wakisubiri mtanange kuanza. Pamoja na hilo, kwa mtazamo tu ilionekana mashabiki wa Simba walijitokeza kwa wingi uwajani kushuhudia pambano hilo la watani wa jadi.VURUGU KWENYE MAGETIMashabiki wa pande zote mbili walionekana kuwa na usongo mkubwa wa kuingia ndani ya uwanja kushuhudia mpambano huo, walikutana na changamoto kubwa kutokana na idadi kubwa ya mashabiki waliotaka kuingia uwanjani kwa wakati mmoja, huku wasimamizi wa milangoni wakioneoneana kutojiandaa kupokea watu wengi kwa wakati mmoja.Baadhi ya mashabiki waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kuwa, walikata tiketi lakini walizuiwa kuingia uwanjani baada ya mashabiki wa timu zote mbili kujaa uwanjani mapema na wengine kushindwa kupata sehemu ya kukaa, Wengine walikosa uvumilivu na kuamua kuondoka hata kabla mchezo haujaanza huku baadhi yao akilalamika wakidai mpangilio haukuwa mzuri na waliobaki wakijazana milangoni, walikutana na adha ya kufukuzwa na kutakiwa kukaa mbali kabisa.
michezo
MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema wakuu wa idara jijini humo, wamekosea kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo kwa kuwafuata wafanyabiashara hao ndani ya masoko, badala ya nje ya masoko.Madeni ameyasema hayo jana katika baraza la madiwani la Jiji la Arusha ambapo baadhi ya madiwani wa jiji hilo walidai agizo alilolitoa Rais John Magufuli kuhusu machinga kutokubughudhiwa baada ya kuwa na vitambulisho vya machinga, limekiukwa.Mmoja wa madiwani hao, Isaya Doita amesema baadhi ya vitambulisho hivyo vimegaiwa kwa wafanyabishara wa ndani ya vizimba ambao mitaji yao ni Sh milioni tano.Pia kugawiwa kwa baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi huku wakishindwa kufundisha wanafunzi madarasani. Alisema baadhi ya madiwani wamenunua vitambulisho hivyo kwa hoja ya kumuunga mkono Rais Magufuli.“Lakini jambo la kushangaza madiwani hao wanaungaje mkono hoja hiyo ilihali hawafanyi biashara, wamechukua vitambulisho vya nini? Huu utaratibu umekiukwa na hivi sasa hali ya masoko yetu ya NMC, Kilombero na Soko Kuu katika ukusanyaji wa mapato imeshuka,” alisema na kuongeza:“Sasa hapa mnamfurahisha nani maana mapato ya Jjiji yanashuka halafu leo hii Rrais akisema anahitaji ‘database’ ya machinga Jiji la Arusha waliopata vitambulisho ni wangapi mtasemaje?Kwa upande wake, diwani Abdulrasul Tojo, alimtaka Ofisa Biashara Jiji la Arusha, Godfrey Edward aeleze Arusha ina jumla ya wafanyabiashara wadogo wangapi na idadi ya vitambulisho vilivyogaiwa ili ifahamike kwa nini jiji hilo mpaka sasa linakosa vyanzo vya mapato kwenye masoko.Mbunge wa Arusha, Godbless Lema alihoji kwa nini agizo la Rais Magufuli limekiukwa kwa vitambulisho kugawiwa kwa watu wasiostahili.Alisisitiza kuwa utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho hivyo ukasitishwa badala yake fedha za masoko zipelekwe serikalini kwani awali masoko yalikuwa yakikusanya Sh milioni 10 kwa siku au milioni tano lakini kwa sasa yanakusanya Sh 10,000 hadi 40,000 kwa siku.Kutokana na hoja hiyo ya dharura , Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Madeni alihoji wakuu wa Idara za Jiji la Arusha kwa nini wameenda kugawa vitambulisho ndani ya masoko kwa wafanyabishara wasiostahili, badala yake wangetakiwa kugawa nje ya masoko.“Hii hujuma mnamfanyia rais, mapato ndio usalama wa nchi na usalama wa nchi ni mapato, nawauliza kwa nini mmegawa vitambulisho kwa wasiostahili na angalieni mmeleta madhara kama haya, mapato yameshuka sababu ya kugawa vitambulisho kwa
kitaifa
['Nyota wa soka Cristiano Ronaldo hatakabiliwa na shtaka lolote baada ya kutuhumiwa na madai ya unyanyasaji wa kingono, waendesha mashtaka wa Marekani wamesema.', 'Kathryn Mayorga, 34, alidai kuwa mchezaji huyo wa klabu ya Juventus alimbaka katika hoteli moja mjini Las Vegas mwaka 2009.', 'Iliripotiwa kuwa Bi Mayorga alikubaliana na nyota huyo kusuluhisha kesi hiyo kimya kimya nje ya mahakama mwaka 2010.', 'Lakini aliamua kufungua tena kesi hiyo mwaka 2018, baada ya Ronaldo kupinga madai hayo.', 'Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, waendesha mashitaka wa Las Vegas walisema madai hayo hayakuweza kutibitishwa.', '"Hakuna shitaka litakalotolewa," taarifa hiyo ilisema.', 'Gazeti la kila wiki la Ujerumani Der Spiegel, lilichapisha taarifa kuhusu madai hayo mwaka jana. ', 'Gazeti hilo liliandika kuwa Bi. Mayorga alitoa ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya tukio hilo.', 'Mwaka mmoja baadae, ripoti ilitolewa ikimhusu Ronaldo kukubali kutoa kitita cha dola milioni 375,000 ili kesi hiyo imalizike kimya kimya bila kutoa taarifa kwa umma kwa kulinda heshima yake.', 'Uamuzi wa wanasheria wa Bi Mayorga kuvunja kimya chao kuhusu unyanyasaji huo wa kingono ulitokana na kampeini ya #MeToo movement.']
michezo
JESHI la Polisi mkoani Katavi linawasaka askari wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa tuhuma za kuwapiga risasi na kuwajeruhi vibaya watu watano, wanne kati yao wakiwa ndugu wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Ikongwe kilichopo katika wilaya ya Mpanda .Watu hao wamelazwa Hospitali Teule ya mkoa wa Katavi iliyopo katika Mji wa Mpanda. Wakazi hao wanadaiwa kuvamia Hifadhi ya Misitu Msaginya ulioko katika Halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda, ambao unahifadhiwa na kumilikiwa na TFS na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo. Majeruhi hao wametambuliwa kuwa ni Filbert Patrick (40) ambaye amejeruhiwa mguuni na wadogo zake watatu Joseph Patrick (27) ambaye amejeruhiwa kifuani, Geofrey Patrick (39) ambaye amejeruhiwa mkono wa kushoto na Januari Patrick (22) aliyejeruhiwa begani. Mwingine ni Nkuba Sai aliyejeruhiwa mkono wake wa kushoto.Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba alifika eneo hilo la tukio na kuokota ganda tupu la risasi ya SMG . “Tayari nimeshaagiza kukamatwa mara moja kwa askari wote wa TFS waliohusika katika tukio hilo ili wahojiwe na sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa wale watakaobainika kutenda uhalifu huo.”Kwa upande wake, Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo alisema amesikitishwa na na kitendo kilichofanywa na askari wa TFS huku akisisitiza kuwa hawakuwa na sababu yoyote ya kutumia nguvu kubwa kiasi hicho. Akisimulia mkasa huo kwa kirefu, Diwani wa Sitalike, Adamu Chelehani alieleza kuwa siku hiyo ya tukio baada ya kupata taarifa kuwa mahindi yanafyekwa na askari wa TFS ambao walikuwa na silaha nzito ...wakazi wa kijiji hicho wapatao 10 walifika eneo hilo na kuwasihi askari hao waache kuyafyeka mahindi kwamba wanayategemea kulisha familia zao.“Hata hivyo, askari hao wa TFS walikaidi na kuendelea kufyeka mahindi ambayo yalikuwa yamekomaa yakitarajiwa kuvunwa mwezi ujao, jambo hilo lilisababisha waanze kuwazomea askari hao ..... Baada ya kuwa wamemaliza kufyeka mahindi kwenye mashamba ya wanakijiji hao, askari hao wa TFS wakiwa na silaha nzito walipanda kwenye gari lao aina ya Land Cruiser huku wanakijiji hao wakiendelea kuwazomea kwa nguvu zao zote,” alieleza. Alidai wakati gari hilo linaondoka askari hao walianza kuwashambulia wananchi hao kwa kuwapiga risasi za moto.
kitaifa
.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa vyama vya siasa nchini havijazuliliwa kufanya shughuli zake za kisiasa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.Akijibu maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa utaratibu uliopo sasa unaoonekana kama kuvinyima nafasi vyama vya siasa kufanya shughuli zake unalenga kuwawezesha Wanasiasa kufanya shughuli za kisiasa katika maeneo yao pasipo kubughudhiwa na Wanasiasa kutoka nje.Waziri Mkuu Majaliwa alikua akijibu swali la Papo kwa Papo kutoka kwa Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe ambaye alitaka kufahamu ni lini Serikali itaviruhusu vyama vya siasa kufanya shughuli zake kama ilivyokua miaka ya nyuma.Kuhusu  suala la kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi, Waziri Mkuu Majaliwa amesistiza kuwa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi iliyopo sasa ni huru kwa kuwa imekua ikitekeleza majukumu yake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote awe Kiongozi ama Mwanasiasa.Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa si kweli kwamba nchi inaongozwa kibabe kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, bali inaongozwa kwa kufuata misingi ya Kidemokrasia.
kitaifa
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekemea tabia ya baadhi ya halmashauri kuuza viwanja kwa bei jambo ambalo amesema itakuwa vigumu masikini kumilika ardhi iliyopangwa.Lukuvi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wataalamu wa ardhi nchini wapatao 800 ambao wamekutana jijini hapa kwa kwa siku tatu. Alisema tabia ya halmashauri kuuza viwanja kwa bei kubwa kwa lengo la kupata mapato ya ndani mengi, ni kero kwa wananchi na kusisitiza hali hiyo itafanya wanaoendelea kumiliki ardhi kuwa ni matajiri na masikini kushindwa kumudu Lukuvi alihimiza uwepo wa bei elekezi ya upimaji wa viwanja na mashamba.“Hivi sasa baadhi ya halmashauri zina uza viwanja kwa bei kubwa sana isiyolingana kabisa na gharama walizoingia kwa tamaa ya kupata mapato mengi ya ndani. Kuna wimbi sasa kila halmashauri inajivuna tumepata fedha nyingi, wamelanga kwenye ardhi, hii hapana, hakuna ulanguzi wa ardhi hapa…ninyi halmashauri mna ardhi, lakini hatukuwaambia muwe nyarubanja mlangue bei mnayoitaka, sasa tutaingilia kati, tunataka watalaamu wa ardhi msimamie na kuelekeza bei,” alisema.Waziri Lukuvi aliongeza kuwa wanafanya tathimini na gharama zote kwa Sh 100, halafu wanataka wapate Sh bilioni moja, matokeo yake wanaongeza kero kwa wananchi na wasiokuwa na fedha wataendelea kuwa na makazi holela tu.“Wataona bora kuendelea kujenga mahali ambapo hapajapangwaa maana ni rahisi zaidi kuliko viwanja vyako vilivyopangwa. Kwa hiyo suala hili la uuzaji wa viwanja na upangaji ni zuri lakini lazima liwekewe utaratibu ili viwanja vyenyewe viuzwe kwa bei inayohimilika, isiwe kila mtu tu anaamua, umasikini wote na posho zote za madiwani na wilaya zitokane na uuzaji wa viwanja haiwezekani. Yaani umasikini wote wa wilaya na madeni yenu myabambike kwenye ardhi, hapo mnafanya ardhi ionekane ni ya watu matajiri, masikini hawatamudu kununua viwanja vilivyopangwa,” alisema.Waziri Lukuvi alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa ofisi za kanda za mikoa ambazo zinaanzishwa kushirikiana na halmashauri katika kukokotoa gharama za upimaji wa ardhi.“Kwa hiyo wale watendaji wa ofisi yangu ya mkoani, watashirikiana na halmashauri kukokotoa gharama na kushauriana juu ya bei ya kuuzia kwa mradi na upimaji wa mashamba lazima uwe na bei elekezi. Wananchi wanataka kupima mashamba yao lakini wanaibiwa, maana anaweza kuja mpimaji mmoja anasema kupima eka moja ni Sh 300, nataka kila mkoa uweke vigezo vya gharama ya upimaji wa mashamba na gharama za upimaji wa viwanja, mkikaa sekretarieti ya mkoa mnaweza kuweka vigezo ili wananchi waweze kumiliki ardhi iliyopangwa na salama na kupewa nyaraka kwa gharama nafuu,” alisema.
kitaifa
RAIS John Magufuli ametoboa siri ya kumkabidhi Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, kamusi na vitabu vya kusoma na kujifunza lugha ya Kiswahili viliyoandikwa na walimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza lugha hiyo kwa kasi.Marais hao wawili walikutana juzi na kufanya mazungumzo katika Ikulu ya nchi ya Afrika Kusini katika Jiji la Pretoria.Rais Magufuli baada ya mazungumzo hayo na Rais Ramaphosa alisema anatarajia uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini utaimarishwa zaidi katika masuala ya uchumi na kukuza lugha ya Kiswahili.“Ndio maana tumemkabidhi Kamusi ya Kiswahili iliyoandikwa na walimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hatua ambayo itasaidia kukitangaza Kiswahili hapa Afrika Kusini.“Lakini pia tutaleta walimu wa Kiswahili ili wafanye kazi ya kufundisha lugha ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali ya hapa Afrika Kusini,” alisema Rais Magufuli.Rais Magufuli alimpongeza Rais Ramaphosa kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na alimhakikishia kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria na nchi hiyo ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Nelson Mandela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha African National Congress (ANC).Alibainisha kuwa anatarajia uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini utaimarishwa zaidi katika masuala ya uchumi na kukuza lugha ya Kiswahili.Kwa upande wake, Rais Ramaphosa alimshukuru Rais Magufuli kwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake na alimhakikishia kuwa Afrika Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika ukombozi wa Taifa hilo na kwamba katika kipindi chake cha uongozi wake atauendeleza na kuuza zaidi uhusiano huo.Alisema kufuatia uamuzi wa Afrika Kusini kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo katika shule za msingi na sekondari.Aidha, aliahidi kufanya ziara rasmi ya Kitaifa nchini Tanzania kabla ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliopangwa kufanyika mwezi Agosti, mwaka huu nchini Tanzania na pia atahudhuria mkutano huo.Rais Magufuli jana aliondoka Afrika Kusini na kutua Namibia ambako anafanya ziara rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Namibia,
kitaifa
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agness Kijazi ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kipindi cha miaka minne 2019-2022.Dk Kijazi ambaye ni mwakilishi wa kudumu Tanzania katika Shirika hilo anakuwa mwanamke wa kwanza na mjumbe wa kwanza kutoka nchi zinazoendelea kushika nafasi hiyo.Inaelezwa kuwa atakuwa na majukumu ya kumsaidia Rais kuongoza shirika hilo katika kutekeleza majukumu yenye tija kwa wanachama wake ikiwemo Tanzania. Akizungumzia ushindi wake mbele ya wapiga kura wa mkutano wa 18 wa WMO na wajumbe waalikwa, Dk Kijazi alitoa shukrani zake kwa wote waliomuamini na kumuunga mkono hadi kufika kupata nafasi hiyo na kuahidi kuitumia nafasi hiyo kwa weledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya shirika hilo.“Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote waliokuwa pamoja na mimi kwa kuniunga mkono na kunichagua kwa kura zote, naahidi kuitumikia nafasi hii kwa weledi mkubwa na kuhakikisha WMO inafikia malengo yake,” alisema Dk Kijazi.Akizungumzia ushindi huo, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Dk Atashasta Nditiye alisema ni heshima kubwa sana kwa nchi, Wizara inampongeza sana Dk Kijazi na kuamini kuwa ataiwakilisha nchi vizuriAidha alimshukuru Rais wa Tanzania kwa ushirikiano aliouonesha kwa kukubali Tanzania kuwakilishwa na Dk Kijazi kwani jitihada zake katika kuboresha sekta ya hali ya hewa kumeendelea kuiletea sifa nchi kwa ujumla Kaimu Balozi, Ubalozi wa Kuduma Umoja wa Mataifa, Geneva Robert Kahendaguza alisema kuwa ushindi wa Dk Kijazi ni kielelezo cha umadhubuti wa kidiplomasia wa Tanzania na sifa zake binafsi ikiwemo uzoefu wa muda mrefu na elimu ya ngazi ya juu katika nyanja ya sayansi ya hali ya hewa.Uchaguzi wa viongozi wa WMO hufanyika kila baada ya miaka minne kwa kuchagua viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Mkuu, Rais, Makamu wa Rais wa kwanza, wa pili na wa tatu, ambapo kwa mwaka huu umefanyika katika mkutano wa 18 wa shirika hilo baada ya muda wa viongozi hao kuisha.Katika uchaguzi huo, alichaguliwa Profesa Petteri Taalas kutoka Finland (Katibu Mkuu), Profesa Dk Gerhard Adrian kutoka Ujerumani (Rais), Profesa Celeste Saulo kutoka Argentina (Makamu wa kwanza wa Rais), Dk Albert Martis kutoka Curacao (Makamu wa Pili wa Rais) na Makamu wa Tatu wa Rrais, Dk Agness Kijazi kutoka Tanzania.
kitaifa
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imekiri kuwepo kwa changamoto nyingi baada ya serikali kuanzisha mfumo wa elimu bila malipo kwa shule za msingi.Akijibu swali la mbunge wa Handeni, Omar Kigoda (CCM), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwita Waitara amesema serikali imejipanga kutatua changamoto hizo.Amesema moja ya njia za kutatua changamoto hizo itahamisha walimu zaidi ya 11,000 wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi.Waitara amesema kwa sasa wamepata kibali cha kuajiri walimu kwa awamu na pia waalimu 6,000 wanatarajia kuajiriwa hivi karibuni ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu.Akizungumzia kuhusu umaliziaji wa maboma ya vyumba vya madarasa 15 katika Halmashauri wa Mji wa Handeni yaliyoanza kwa nguvu za wananchi, Waitara alisema maboma sita yapo katika hatua ya lenta.Amesema hadi Januari mwaka huu, halmashauri hiyo imeshapokea jumla ya Sh milioni 46.6 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma yaliyoanza kwa nguvu za wananchi ili yaanze kutumika.Waitara amesema serikali kwa kushirikiana na wadau kupitia Programu ya Lipa kwa Matokeo (EP4R) na Programu ya kuimarisha Ubora wa Elimu Tanzania itaendelea kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kwaajili ya ukamilishaji wa maboma.Amesema halmashauri ya zinahimizwa kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma yaliyopo kabla ya kuanzisha miradi mipya.Katika swali lake Kigoda alitaka kujua ni lini Halmashauri ya Handeni na zinginezo zitakamilisha majengo ya madarasa yaliyotokana na nguvu za wananchi.
kitaifa
WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar imesema njia pekee ya wakulima kupiga hatua kubwa ya uzalishaji wa mpunga ni kutumia kilimo cha umwagiliaji.Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Rashid Ali Juma alisema kilimo cha umwagiliaji ndio mkombozi wa wakulima ambao kwa sasa wanaweza kulima muda wowote mwaka mzima. Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sasa inatekeleza mradi mkubwa wa umwagiliaji maji mashambani ambao ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Exim ya Korea ya Kusini.‘’Serikali tayari inatekeleza mradi mkubwa wa umwagiliaji maji mashambani ambao unatekelezwa na wenzetu Benki ya Exim kutoka Korea ya Kusini ikiwa ni mkopo,’’ alisema. Juma alisema mradi huo wa umwagiliaji ulianza Desemba, 2018 ambapo kazi kubwa ni ujenzi wa mitaro ya kupitishia maji inayoenda mashambani pamoja na kujenga pia njia zake.Aidha, alizitaja kazi nyingine zitakazofanyika ni kuchimba visima vya uzalishaji wa maji 49 vitakavyotumika kusambaza maji mashambani na ujenzi wa mabwawa manne ya maji. ‘’Hizo ndiyo kazi zitakazofanyika katika utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji maji mashambani wenye lengo la kukuza uzalishaji wa mpunga kwa wakulima wetu, ‘’ alisema.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Ahmada Kassim Haji alisema kama wakulima wa mpunga watajikita zaidi katika uzalishaji wa mpunga kwa umwagiliaji maji, yapo matumaini makubwa ya kujitosheleza kwa chakula. Alisema kilimo cha mpunga cha kutegemea mvua hakina uhakika kupata mavuno mazuri. ‘’Serikali imejikita katika kuimarisha kilimo cha umwagiliaji maji mashambani ambacho matarajio ni kukomboa wanawake, ‘’alisema.
kitaifa
CHAMA cha Wakulima wa Zabibu na Masoko Mpunguzi (UWAZAMAM) jijini hapa, kimeipongeza serikali kwa kupunguza tozo ya ushuru wa mchuzi wa zabibu kutoka Sh 3,315 hadi 450, kikisema hatua hiyo itainua uchumi wa mkoa na wakulima wa zao hilo.Hata hivyo, Uwazamam kimewaomba wanunuzi wa mchuzi huo, kuongeza bei kutoka Sh 1,540 za awali hadi Sh 2,000 kwa lita, hasa baada ya serikali kupunguza tozo hilo ili wakulima wanufaike na punguzo hilo.Katibu wa chama hicho, Emmanuel Temba amesema jijijni Dodoma kuwa, wanachama wa chama chao wanasindika na kuuza mchuzi wa zabibu, lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya tozo kubwa, hali iliyosababisha wanunuaji kushindwa kununua mchuzi huo. Temba alimpongeza Rais John Magufuli na Bunge, kwa kuliona hilo na kuamua kupunguza tozo hiyo.Amesema anaamini wasindikaji wadogo, watapata soko kwa kuwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya soko kutokana na wanunuzi kusuasua kwa madai tozo ni kubwa.Hata hivyo, Temba alisema tayari wanunuaji wakubwa wameonesha nia na wanachangamkia fursa ya kununua mchuzi huo kutokana na punguzo la tozo lililotangazwa na Bunge hivi karibuni.“Kwa kuwa viwanda vikubwa vinavyochukua mchuzi huu vitakuwa vimepunguziwa kodi, basi tunaomba waangalie uwezekano wa kuongeza bei kwenye ununuzi kutoka Sh 1,540 hadi 2,000,” amesema Temba.Temba alisema waliamua kubuni kusindika mchuzi huo kutokana na hasara waliyopata wakulima ya kuharibika zabibu kwa kukosa wanunuzi.Amesema katika kipindi cha masika, walinunua zabibu tani 19 zenye thamani ya Sh milioni 11.4 na kupata mchuzi lita 15,000 ambao uliuzwa kwa Sh milioni 18, huku msimu wa mwaka 2016 wakati wa kiangazi walinunua tani 62.6 zenye thamani ya Sh milioni 75.1 na walipata lita 48,000 ambazo waliuza kwa thamani ya Sh milioni 86.4.Amebainisha kuwa msimu wa kiangazi mwaka 2017 walinunua tani 108 kwa Sh milioni 129.6 na kupata mchuzi wa lita 84,000 ambao uliuzwa kwa Sh milioni 151.2.Aidha, alisema wataendelea kuongeza uzalishaji wa mchuzi huo kutokana na kupata soko la uhakika kwa kuuza mchuzi huo kwa wadau wa mazao ya kuzalisha zabibu wa ndani na nje.
uchumi
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaweka kitimoto wakuu wa idara mbalimbali zilizopo katika halmashauri za wilaya na jiji hilo kwa kuwataka kujiandaa na uhamisho kwenda mikoani endapo idara zao zitabainika kukwamisha miradi mbalimbali.Akizungumza katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Makonda alisema tayari ofisi yake imeanza kulifanyia kazi suala hilo ikishirikiana na Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa hatua hiyo. Kwa mujibu wa Makonda baadhi ya watendaji hao hususani waliokaa katika ajira zao ndani ya Jiji hilo kwa zaidi ya miaka 10 bila uhamisho wowote, wamekuwa kikwazo katika mikakati mbalimbali iliyo katika Mpango wa Maendeleo kutokana na mazoea waliyoyajenga na wadau mbalimbali wakiwemo wakandarasi.“Baadhi yenu hapa wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi miradi hiyo, wamekuwa wakiwakwamisha wakurugenzi, mameya, wakuu wa wilaya na hata mimi mkuu wa mkoa. Kifupi watambue kuwa mwisho wao ndani ya Jiji hili ni mwezi ujao,” alisema Makonda.Aidha Makonda alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Ilala, Jumanne Shauri kumsimamisha mmoja wa wakandarasi ambaye siku za hivi karibuni alilalamikiwa na mmoja wa madiwani wa halmashauri hiyo kwa kufanya kazi aliyopewa chini ya kiwango. “Nakutaka mkurugenzi kumsimamisha kazi mkandarasi huyo mara moja na kama wapo wengine wasimamishe hatuwezi kuona fedha zikipotea kwa kazi sizizo na ubora,” alisema Makonda.Alisema wao kama viongozi vigezo vyao vya utendaji kazi vinapimwa kutokana na kazi wanazozifanya na kwamba hawapo tayari kuona wanapoteza kazi hizo kutokana na makosa yanayofanywa na watu wengine tena kwa kuzembea. Katika hatua nyingine, Makonda amedai kubaini matukio ya ubadhirifu wa fedha katika miradi ya ujenzi wa barabara inayotekelezwa kupitia Mpango wa Uendelezaji wa Miji (DMDP), suala alilolitaka baraza hilo kulifanyia kazi ili kujiridhisha nayo.
kitaifa
WATU wawili wameuawa katika matukio tofauti wilayani Muleba mkoani Kagera kwa imani za kishirikina na kujichukulia sheria mkononi akiwemo mtoto aliyenyofolewa sehemu zake za siri. Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba mtu mmoja anashikiliwa na polisi, mkoani humo.Alisema Aprili 17 mwaka huu, katika kijiji cha Ihunga, kata ya Kishanda, wilayani Muleba, wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kumshambulia Colletha Frances (65) kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia kifo na kuamua kumchoma moto nyumba yake pamoja na kufyeka mashamba ya migomba na kuyachoma.Kamanda Malimi alisema chanzo cha mauaji hayo ni kumtuhumu Colletha kuwa ni mchawi na kumhusisha na kifo cha Ismail Hamisi (7) aliyetoweka tangu Aprili 5 mwaka huu na mwili wake kugundulika ukiwa umezikwa kwenye shamba la mama huyo umbali wa mita 60 kutoka ilipo nyumba yake, Aprili 17 mwaka huu.Aliongeza kuwa baada ya mwili kuonekana eneo hilo wananchi walikusanyika na kuhamasishana kuvamia nyumba ya Colletha, wakamtaka atoke nje na alipotoka alikuta umati mkubwa wa watu walioanza kumshambulia na silaha za jadi hadi kumuua.Kamanda Malimi alisema chanzo cha ukatili huo ni kumtuhumu na kifo cha Ismail kuanzia mazingira ya kupotea kwake hadi kifo na aliongeza kuwa mwili wa Ismail uligundulika kuwa umenyofolewa sehemu zake za siri. Alisema kuhusu tukio la mauaji ya mtoto huyo hakuna anayeshikiliwa isipokuwa katika tukio la kujichukulia sheria mkononi uchunguzi umeanza na mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano zaidi, akituhumiwa kuwa mhamasishaji mkuu. Hata hivyo hakumtaja jina kwa sababu za kiuchunguzi.
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa manispaa ya Morogoro na mkandarasi wa ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari Mji Mpya mkoani hapa kukamilisha ujenzi huo Agosti 30, mwaka huu ili wanafunzi waanze kusoma.Waziri huyo alitoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo mapya ya shule hiyo baada ya awali kubomolewa kutokana na kupitiwa na njia ya reli ya mpya ya kisasa (SGR). Kwa sasa wanafunzi wa shule hiyo wamehamishiwa kwa muda katika shule ya Sekondari Tushikamane iliyopo karibu wakisubiri kukamilishwa kwa ujenzi wa majengo hayo mapya, ambapo serikali imetoa Sh bilioni 1. 4.Alisema manispaa hiyo ilichelewa kuanza ujenzi huo tofauti na ilivyo kwa wenzao wa Shule ya Sekondari Msoga iliyopo mkoani Pwani ambayo ilipitiwa na njia ya reli ya SGR.“Wenzenu baada ya kulipwa fidia walianza ujenzi mara moja na tayari umekamilika na wanafunzi wapo shule tangu zilipofunguliwa Julai, mwaka huu, tofauti na Manispaa ya Morogoro, jambo hili sio kitu kizuri,” alisema.Jafo aliagiza kuwa ifikapo Agosti 30, mwaka huu karibu mwezi mmoja kuanzia sasa, ujenzi wa majengo hayo uwe umekamilika na wanafunzi wanakuwa madarasani na ameahidi kurejea tena kuona utekelezaji wa agizo lake. Pia alimwagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kuweka mazingira mazuri ya shule hiyo kutokana na kuwa na eneo kubwa tofauti na hapo awali.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, John Mgalula, alisema walipokea Sh bilioni 1.4 za ujenzi mpya wa shule hiyo zikiwa ni fidia baada ya kupitiwa na njia ya reli ya kisasa ya treni ya mwendokasi (SGR).Alisema baada ya taratibu kukamilika ilipatikana kampuni ya vikosi vya ujenzi kutoka Wizara ya Ujenzi (Corporation Sole Works Superintendent ) ya Dodoma na kwa mujibu wa mkataba inatakiwa kufanya kazi kwa muda wa miezi minne na kwamba hadi sasa imeshalipwa asilimia 50 sawa na Sh milioni 715 kama malipo ya awali.Kwa upande wake, msimamizi wa ujenzi wa shule hiyo kutoka vikosi vya ujenzi mkoani Dodoma, Simeon Machibya, alimhakikishia Jafo kuwa licha ya kuchelewa kuanza ujenzi huo wataukamilisha Agosti 30, mwaka huu na kukabidhi majengo kwa halmashauri ya manispaa hiyo. Alisema ujenzi huo unahusisha vyumba vya madarasa 20, maktaba moja, vyumba vya kompyuta vitatu, vyoo matundu 36, nyumba nne za walimu na jengo la utawala.
kitaifa
LEO ni tarehe 28 Desemba, zimebaki siku tatu tu kabla ya kukamilisha mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2020, tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kuumaliza mwaka huu na kuingia mwaka mpya salama.Wakati mwaka 2019 unaelekea ukingoni kuna matukio mengi ya kukumbukwa ambayo yametokea katika anga la michezo na burudani ambayo yamekuwa ya kuhuzunisha na mengine ya kufurahisha. Matukio ni mengi mno lakini katika makala haya tumeorodhesha baadhi ya hayo ambayo yaliwagusa watu wengi.Harmonize kujitoa WCB Agosti mwaka huu mashabiki na wafuatiliaji wa muziki wa Bongo Fleva walipata taarifa ya kushangaza baada ya kusikia ‘memba’ wa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdul ‘Harmonize’ kutangaza kujitoa katika kundi hilo.Awali Harmonize hakutangaza wazi kuwa amejitoa katika kundi hilo ambalo ndilo limemtoa kimuziki lakini kulikuwa na uvumi wa kujitoa kwake kwa kipindi kirefu baada ya kutoonekana mara kadhaa katika matamasha ya Wasafi yaliyoandaliwa na kundi hilo.Aliyeweka wazi sakata hilo ni mmoja wa viongozi wa WCB Salam SK alipohojiwa na Wasafi FM katika kipindi cha Block 89, Agosti 21 ambapo alisema kuwa moyo wa Harmonize haupo tena WCB na tayari ameshauandikia uongozi kutaka kujitoa.Babu Seya afunga ndoa Septemba 7 msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Nguza Viking maarufu Babu Seya alifunga ndoa takatifu na aliyekuwa mchumba wake, ambaye ni katibu tawala wilaya ya Muheza, Esterine Haule.Ndoa hiyo iliwaacha midomo wazi mashabiki wengi wa msanii huyo kutokana na kuwa ilifanywa kimyakimya ambapo wawili hao walifunga ndoa yao katika Kanisa Katoliki la Sinza, Dar es Salaam. Babu Seya mwenye asili ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mwanamuziki anayefanya kazi zake nchini, tangu mwaka 2004 alikuwa katika kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kunajisi watoto.Mwaka 2017, Babu Seya alitoka jela kwa msamaha wa Rais John Magufuli, baada ya kutumikia adhabu yake kwa miaka 13. Ilielezwa kuwa Babu Seya alifiwa na mkewe kabla ya kuhukumiwa na tangu alipotoka jela amekuwa akiishi maisha ya upweke. Kifo cha Ruge Mutahaba Februari 26 anga la burudani liligubikwa na huzuni kubwa baada ya kutokea kwa kifo cha Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.Ruge alikuwa mmoja kati ya wadau wakubwa waliochangia kukuza tasnia ya burudani nchini kutokana na harakati zake ikiwemo kusimamia kituo cha radio ya burudani, Clouds FM, kuandaa matamsha ya muziki pamoja na kusimamia kituo cha kukuza vipaji vya sanaa cha Tanzania House of Talent ‘THT’ ambacho kimewatoa wanamuziki wengi akiwemo Barnaba, Mwasiti, Linah, Amini, Rachel na wengine.Ruge hadi umauti unamkuta alikuwa akipatiwa matibabu Afrika Kusini, alikuwa akiugua kwa zaidi ya miezi minne na alianza kupatiwa matibabu katika hospitali za Dar es Salaam, kisha akapelekwa India na baadae Afrika Kusini. Mwili wa Ruge ambaye alizaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970 ulizikwa Machi 4, nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru, Karabagaine, Bukoba mkoani Kagera.Mwakinyo ampiga Mfilipino Taifa Novemba 30 kama sio jiji la Dar es Salaam basi ni nchi kwa ujumla ilisimama kupisha pambano la ngumi la kimataifa lisilo na ubingwa kati ya bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo na Mfilipino Arnel Tinampey.Pambano hilo la aina yake la raundi 10 lilipigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mwakinyo kuibuka na ushindi kwa pointi huku mashabiki wengi walikuwa na imani kubwa kwamba mtanzania huyo atamtwanga Mfilipino mapema kwa KO kutokana na kuwa na rekodi nzuri ya kushinda mapambano yake ya kimataifa. Kabla ya kuzipiga na Tinampey, Mwakinyo alitoka kushinda pambano lake kwa KO dhidi ya Muargentina, Sergio Gonzalez , kabla ya hilo alimpiga kwa KO Muingereza, Sam Eggington.Majaji watatu waliokuwa wakisimamia pambano hilo walitoa pointi kwa kutofautiana ambapo jaji wa kwanza alitoa pointi 97 kwa Mwakinyo na 93 kwa Tinampey, wapili Mwakinyo 98 Tinampey 92 na watatu alitoa 96 kwa kila mmoja. Kifo cha Godzilla Februari 13 tasnia ya muziki wa Hip Hop nchini ilipata pigo baada ya kutokea kwa kifo cha msanii wa muziki huo Golden Mbunda, maarufu Godzilla.Godzilla aliyetambulika kwa nyimbo zake kadhaa ikiwemo La kuchumpa, Jinsi nilivyo, First Class, Mama I made It, Nataka pamoja na Milele aliyomshirikisha Ali Kiba alizikwa Februari 16 katika makaburi ya Kinondoni na maelfu ya mashabiki wake pamoja na wasanii mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Msanii huyo ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii waliokuwa na uwezo mkubwa ‘kufree style’ kwa muda mrefu, alifariki baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwao Salasala na kukimbizwa katika hospitali ya Lugalo kupatiwa matibabu.
michezo
Akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa wajasiriamali wakubwa na wakati juu ya mpango wa serikali wa kuishirikisha sekta binafsi katika miradi mikubwa kupitia PPP Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolf Mkenda, aliwaeleza washiriki kuwa, kuna sheria inayoongoza ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, hivyo hakuna sababu ya sekta binafsi kusitasita katika kushiriki miradi mikubwa.Alisema, nchi nyingi zilizoendelea, hasa katika sekta ya miundombinu, zimeshirikisha zaidi sekta binafsi kwenye miradi mikubwa na kuzisaidia nchi hizo kukuza uchumi kwa kasi.Kiongozi huyo ameomba fursa hii itumiwe na Watanzania wengi kadri inavyowezekana, lakini amefafanua pia kuwa fursa hizo ziko wazi kwa wajasiriamali Watanzania na wageni, na kuongeza kuwa suala kubwa katika jitihada hii ni utoaji wa huduma bora na yenye ufanisi.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Godfrey Simbeye, amekaribisha msukumo huo wa serikali na kueleza sekta binafsi ina nia ya kutumia fursa hiyo.
uchumi
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na semina kwa wajasiriamali wadogo katika Wilaya ya Lushoto kuhusu utekelezaji wa viwango vya kitaifa kwa bidhaa zinazozalishwa na zinazosindikwa.Pia wajasiriamali hao wamepatiwa elimu ya namna ya kupata alama ya ubora kwenye bidhaa wanazozalisha bure bila gharama yoyote.Semina hiyo ilifanyika wilayani hapa juzi na kuhudhuriwa na wajasiriamali 33 walijitokeza kupata elimu hiyo sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo ubora wa bidhaa ikiwahusisha wanaozalisha bidhaa za maziwa, siagi, mtindi, asali, jamu, juisi, mbogamboga, wasindikaji wa nyanya na vitunguu saumu.Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika aliwataka wajasiriamali hao kutumia fursa hiyo kwa kusikiliza kwa makini watakayofundishwa ili watumie elimu hiyo kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa.Ofisa Udhibiti Ubora Mkuu wa TBS, Cunbert Kapilima alisisitiza kuwa shirika hilo linatambua mchango wa wajasiriamali katika kukuza Pato la Taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi.TBS mpaka sasa imeshatoa semina na mafunzo kwa bidhaa mbalimbali kwa washiriki kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Katavi, Kigoma, Tanga, Tabora, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.
uchumi
Alisema shirika litaendelea kugawa faida inayopatikana kutokana na zao hilo kwa kusaidia maendeleo ya jamii kwa kila hali inaporuhusu na fursa inapopatikana ili kujenga imani ya wananchi kuipenda ZSTC na kulipenda zao la karafuu ambapo ndio zao kuu la uchumi Zanzibar.Bai aliyasema hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo huko Chake Chake katika hafla maalumu ya kuzungumza na wajasiriamali wa Soko la Jumapili ambayo yametolewa na shirika hilo la biashara.Bai alisema Shirika la ZSTC sasa limeelekeza nguvu zake katika kuisaidia jamii katika shughuli za maendeleo vikiwemo vikundi vya ushirika vya wajasiriamali na wakulima wa zao la karafuu kwa lengo la kuinua uchumi wao.Alisema miongoni mwa misaada inayotolewa na shirika hilo inaelekezwa zaidi katika miradi ya ujenzi wa barabara za vijijini ikiwemo ya Ng’ombeni Chake na Kiwani, miradi ya ujenzi wa shule, biashara, umeme kwa vituo vya ununuzi wa karafuu na vikundi vya ujasiriamali.Mapema akizungumza na wajasiriamali wa Soko la Jumapili katika eneo la Chakechake, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla aliwasisitiza wajasiriamali hao kutumia mashamiana hayo na kulitumia soko hilo kuendelea kibiashara.Alisema Shirika la biashara la ZSTC limefanya jambo la msingi kuwasaidia wajasiriamali hao kutokana na mahitaji yaliyojitokeza ambapo wafanyabiashara hao wamekusanya nguvu zao kukuza uchumi wao.Amewahakikishia wajasiriamali hao kuwa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba iko pamoja nao katika kuhakikisha kuwa shughuli wanazoziendeleza sokoni hapo zinaendelezwa kwa maslahi yao na taifa.
uchumi
KATIBU Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stergomena Tax (pichani) amesema Tanzania ni nchi pekee katika jumuiya hiyo, iliyofanikiwa kufi kia kigezo kilichowekwa na jumuiya cha kufi kia ukuaji wa uchumi wa asilimia saba.Dk Tax amesema SADC imejiwekea vigezo vya uchumi mpana wa kufikia asilimia saba na hadi sasa Tanzania ndio pekee iliyofika vigezo hivyo.Stergomena ameipongeza nchi hiyo, kwa hatua hiyo ya mafanikio ;na kutaka nchi nyingine zipambane kufikia vigezo hivyo ili kwa pamoja kufikia malengo waliojiwekea.Ameyasema hayo jana alipohutubia ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC. Mkutano huo unawashirikisha viongozi wa nchi 16 za jumuiya hiyo. Dk Tax alisema ukuaji wa uchumi katika SADC, umeendelea kuimarika ingawa kuna changamoto nyingi.Alisema mwaka 2017 ulikua kwa asilimia tatu na mwaka 2018 asilimia 3.1 huku nchi za Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Madagascar na Tanzania zikifanya vizuri.Alisema Pato la Taifa katika kanda liliimarika kutoka Dola za Marekani 4,004 mwaka 2017 hadi Dola za Marekani 4,171 mwaka 2018.Alisema mafanikio hayo, yamewezeshwa na nchi tano pekee ambazo ni Botswana, DRC, Maurituis, Shelisheli na Tanzania. Dk Tax pia alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi na kueleza jinsi SADC ilivyoshiriki katika majanga ya kimbunga Idai katika nchi za jumuiya hiyo.Alimshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake jana, Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob kwa juhudi kubwa za misaada ya kiutu zilizofanywa na nchi wanachama kwa nchi zilizopata matatizo hayo ya kimbunga Idai na Kenneth.Alisema SADC ilitoa msaada wa Dola za Marekani 500,000 kwa nchi tatu zilizoathirika zaidi na kimbunga Idai na kufungua kampeni ya maafa iliyowezesha kukusanya zadi ya Dola za Marekani 203 kwa tatizo hilo.Alisema eneo la kuwashirikisha vijana katika ubunifu na utatuzi wa ajira zilizoanzishwa na Dk Geingob zinaendelea kutekelezwa na sekretarieti ya SADC kwa kuhakikisha kunakuwa na fursa za ujasiriamali na biashara.Alisema SADC inajivunia kuimarika kwa amani hasa katika nchi sita zilizofanya uchaguzi kipindi kifupi kilichopita katika jumuiya hizo ambazo ni eSwatini, DRC, Malawi, Zimbabwe, Madagascar na Comoro.
uchumi
WAKAZI wawili wa Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, Patrick Chirwa maarufu kwa jina la Boy (42), mkazi wa Lizaboni na Ramadhani Nivya (41), mkazi wa Ruhuwiko wamehukumiwa kwenda jela miaka 15 wote wawili katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya kupatikana na betri mbili zinazotumika kuchaji betri zinazotumika kwenye ndege aina ya Bombardier zote zikiwa na thamani zaidi ya Sh milioni 36, mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Songea, mkoani hapa, Clofasi Waane ambapo kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 26/2017 ilifunguliwa mahakamani hapo Oktoba, 26, 2017 na washtakiwa wote wawili wakiwa wanakabiliwa na makosa matatu na waliposomewa mashtaka yao walikana makosa yote.Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Hamimu Nkoleye uliiambia Mahakama kuwa mnamo Oktoba, 12, 2017 ndani ya uwanja wa ndege uliopo Ruhuwiko washtakiwa wote wawili waliingia kwenye huo uwanja na kuiba betri mbili zinazotumika kuchaji betri zinazotumika kwenye ndege aina ya Bombardier.Ilielezwa kuwa kitaalamu betri hizo zinatumika kwenye Ami ground power unit (Ami – 2400-55) zenye namba 245203 na zina thamani ya Sh 36, 963,168, ikiwa ni mali ya Shirika la Ndege la Tanzania. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa shitaka la pili kwa washitakiwa wote lilikuwa ni la kuvunja na kuiba.Mwanasheria Nkoleye pia aliiambia Mahakama kuwa shitaka la tatu lilikuwa likimkabili mshitakiwa wa kwanza, Chirwa ambapo alidai mnamo wa Oktoba 13, 2017 katika njia ya kuelekea Lupapila alikutwa akiwa na betri hizo mbili za kuchajia ndege ikiwa mali ya ATCL.Hata hivyo washitakiwa wote wawili walikana makosa yote matatu, kabla ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ya kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 15 jela wote wawili.Kabla ya Hakimu Waane kusoma hukumu hiyo aliwataka washtakiwa waiombe Mahakama iwapunguzie adhabu ambapo mshitakiwa wa kwanza Chirwa aliyekuwa akitetewa na Mwanasheria wa kujitegemea, Benard Mapunda aliiambia Mahakama kuwa mteja wake ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi na pia amekaa mahabusu kwa muda mrefu, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na Mahakama hiyo. Mshitakiwa wa pili, Nivya akiiomba Mahakama impunguzie adhabu akidai anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu (BP).
kitaifa
WAKATI michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kupamba moto, huku tukishuhudia mtifuano mkubwa wa mbio za marathon kwa mafahali wawili Simba na Yanga, kila mmoja wao akijinasibu kushinda michezo iliyobaki kuhakikisha anatwaa taji hilo msimu huu.Lakini vita nyingine ni kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam au FA, ambapo timu nne zinatarajiwa kuoneshana kazi zilizotinga hatua ya nusu fainali kwenye michuano hiyo, huku kila timu ikiwa na shauku ya kujihakikishia kukata tiketi kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la shirikisho bara Afrika, Caf.Hadi sasa timu nne zimeingia kwenye hatua hiyo ambapo fainali ya kwanza timu kati ya Azam FC na KMC, ambayo ilitarajia kuchezwa jana wakati ile ya pili itazikutanisha Yanga dhidi ya Lipuli Mei 6.NUSU FAINALI YA KWANZAFainali hiyo ilitarajia kuwa ngumu na ilitarajiwa kupigwa jana jioni katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, ambapo wawili hao walikutana baada ya kufanya vyema kwenye michezo ya hatua ya robo fainali,ambapo KMC walipata fursa hiyo baada ya kuifunga timu ya African Lyon mabao 2-0 kwenye mchezo mgumu na wa kusisimua uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru.Huku Azam waliokuwa wa kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kushinda mchezo wa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar. mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.YANGA NA LIPULI FCMchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumatatu katika Uwanja wa Samora mjini Iringa, ambapo Lipuli inatarajiwa kuwa mwenyeji kumkaribisha bingwa wa kihistoria Yanga, mtanange huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na uwezo wa timu zote mbili ulioneshwa kwenye michezo ya hivi karibuni kwenye michezo ya ligi. Kwa mara ya mwisho walipokutana katika uwanja huo katika mchezo wa Ligi Kuu mwenyeji Lipuli alifanikiwa kuibuka na pointi tatu baada ya kuifunga Yanga bao 1-0 mchezo uliotawaliwa na upinzani mkali mwanzo mwisho.Lakini safari hii mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu zaidi kwa kuwa hadi sasa Yanga bado ana wasiwasi ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi licha ya kuonekana hadi sasa anaongoza ligi hiyo kwa pointi 77 lakini bado mpinzani wake wa karibu Simba anashika nafasi ya pili kwa pointi 69 anaonekana kuja kwa kasi huku akiwa na faida ya michezo mitano mkononi ambazo kama atafanikiwa kushinda basi atafanikiwa kutetea ubingwa huo.Yanga walifanikiwa kutinga kwenye hatua hiyo baada ya kuifunga timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Namungo FC ya Lindi kwa mabao 1-0 mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa Lindi, huku Lipuli walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Singida United kwa mabao 2-0.
kitaifa
SIMBA jana ilikuwa uwanjani Dar es Salaam ikimenyana na African Lyon kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara katika harakati zake za kutetea taji lake. Katika mechi hiyo Simba ilishinda 2-1.Lakini wakati mabingwa hao watetezi wakipigania taji hilo, kuna kila dalili uongozi wa klabu hiyo kuachana na kocha wake msaidizi Mrundi Masoud Djouma aliyehudumu kwenye klabu hiyo kwa takriban mwaka mmoja.Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba jana, zilidai kuwa uongozi umeamua kuachana nae ili kuinusuru klabu yao iliyo kwenye harakati za kutetea taji lake la Ligi Kuu Bara. Djouma amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba tangu kuwasili kwake akitokea Rayon Sports ya Rwanda kutokana na mbinu zake uwanjani.“Mpaka leo mchana (jana) uongozi ulishaamua kuachana nae, ilikuwa inasubiriwa akabidhiwe barua tu,” alisema mtoa habari wetu ndani ya Simba.Mapema jana, Kaimu Rais wa SimbaSC, Salim Abdallah ‘Try Again’ alikiri hadharani kwa mara ya kwanza kwamba kocha wake msaidizi Djouma na bosi wake Mbelgiji Patrick Aussems hawana maelewano.Try Again aliviambia vyombo vya habari kwamba kumekuwa na msuguano kwa mabosi hao wa benchi la ufundi, na kwamba hali hiyo ilikuwepo tangu wakati wa Pierre Lechantre aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.Kumekuwa na maneno mengi kuhusu Djuma na bosi wake kutokuwa kwenye maelewano na kwamba ndio sababu ya Mrundi huyo kuachwa Dar es Salaam timu hiyo ilipokuwa na mechi za mikoani.Kwa nyakati tofauti viongozi wamekuwa wakikanusha suala hilo, lakini jana kaimu rais alikiri na kuahidi kuja na tamko rasmi kama uongozi.“Nikweli kumekuwa na matatizo ya kujirudiarudia mara kwa mara baina ya Djuma na benchi la ufundi,hasa kwa makocha wakuu akiwemo Pierre Lechantre aliyeondoka,”amesema.Amesema wamekuwa wakifanya jitihada kubwa ya kusuluhisha tatizo hilo lakini hawezi kuzungumza mengi kwa vile watakuja na tamko rasmi baadaye. “Tutakuja na uamuzi mwafaka wa suala hili kwa maslahi mapana ya klabu,” alisema.Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba Boniface Lihamwike amesema uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Novemba 3 sasa umesogezwa mbele kwa siku moja, hivyo utafanyika Novembe 4 mwaka huu.Alisema, uamuzi wa kusogeza mbele uchaguzi huo umekuja baada ya kubaini Novemba 3 kutakuwa na mechi ya Ligi Kuu kati ya mabingwa hao watetezi dhidi ya JKT Tanzania hivyo ni vyema kutoa nafasi kwa mashabiki kuishuhudia timu yao.Simba inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kwanza tangu kubadilisha mfumo na kuingia kwenye hisa ambapo mwekezaji wake Mohamed Dewji amenunua hisa 49 huku 51 zikibaki kwa wanachama.
michezo
Jiji la Dodoma litaweza kujitegemea kimapato ifi kapo mwaka 2021.“Jiji la Dodoma ifikapo mwaka 2021 jiji hilo litakuwa likijitegemea kwa mapato ya ndani,” amesema Mkurugenzi wa jiji hilo, Godwin Kunambi.Amesema kwa kuwa Dodoma inatekeleza ahadi ya serikali kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani humo, halmashauri inatekeleza mipango ambayo inataka jiji hilo kuwa na vivutio vingi na kuwa na mpangilio mzuri wa maeneo ili wananchi wapate huduma za kijamii bila shida.Kunambi amesema mwelekeo wa utendaji kazi wa halmashauri ya Jiji la Dodoma unalenga kuendelea kuongeza uwezo wa kukusanya mapato kutokana na vyanzo vya ndani ili ifikapo 2021 liweze kujitegemea.Kunambi alisema katika mwaka wa fedha 2018/19 Halmashauri ya jiji la Dodoma ilipanga bajeti ya kukusanya Sh bilioni 68 ambayo ni mapato ya ndani na hadi sasa ilishavuka lengo hilo.Akielezea hali ya maendeleo ya upatikanaji wa huduma za kijamii katika jiji hilo, Kunambi amesema kwa sasa jiji hilo halina shida ya uhaba wa maji wala uhaba wa umeme na huduma za miundombinu ya barabara.Amesema baada ya muda mfupi miundombinu ya barabara mingi zaidi, njia za reli na kiwanja cha ndege kwa ajili ya usafiri wa anga vitakuwa vimeimarika zaidi na kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi pamoja na wafanyakazi waliopo jiji hapa.Kunambi aliwaambia wananchi kwamba Jiji la Dodoma litakuwa tofauti na majiji mengine nchini, kutokana na ukweli kwamba litakuwa na miundombinu rafiki kwa wakazi wa jiji.Katika kuhakikisha suala la miundombinu linakuwa bora, tayari mpango wa kujenga barabara za mzunguko wa ndani ya jiji na nje ya jiji inaandaliwa ili kuhakikisha wasafiri wanaotoka mikoa ya
uchumi
Ofisa Mwandamizi Mkuu Elimu wa TRA, Hamis Lupenja alisema hayo wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyofanyika jijini hapa mwishoni mwa wiki.“Vituo vya mafuta hawatoi risiti za TRA licha ya baadhi yao kuwa mashine za EFD’s, katika kukabiliana na hilo utaratibu wa kufunga kifaa cha kodi ndani ya pampu ili kuondoa ukwepaji kodi unafanyika,” alisema.Alisema mashine za kielektroniki (EFD’s), sio mali ya TRA, bali ni mali ya mfanyabiashara, lakini taarifa za kodi za TRA zipo ndani hivyo wanapoziweka pembeni na kuacha kuzitumia ni njia mojawapo ya kukwepa kodi, ndio maana Serikali inafanya utaratibu mwingine.Alisema ili kutatua tatizo la upatikanaji wa mashine hizo, TRA imeongeza idadi ya watengenezaji wa mashine kutoka wanne hadi kufikia nane na idadi ya wasambazaji, imeongezeka kutoka sita hadi 10.Kwa mujibu wa Lupenja, walifanya utafiti juu ya matumizi ya mashine hizo, ambapo baadhi ya wafanyabiashara walikiri kuwa mfumo wa mashine za EFD’s upo wazi na ni rahisi kujikadiria, kutunza kumbukumbu na kupunguza wizi.Alitaja aina ya mashine hizo kuwa ni pamoja na Rejesta ya Kodi, ambazo hutumika kwa wafanyabiashara wa rejareja wanaotoa risiti kwa maandishi ya mkono ambayo huhamishika.Nyingine ni Printa za Kodi za Kielektroniki, ambazo hutumia umeme na mashine ya alama ya kodi ambayo hutumiwa na kampuni zinazotoa hati za madai.
uchumi
TANZANIA imepanda kwa nafasi sita katika ubora wa viwango vya Fifa vilivyotolewa jana. Kwa mujibu wa viwango hivyo vilivyo kwenye tovuti rasmi ya Fifa, Tanzania imepaa kutoka nafasi ya 137 iliyokuwa mwezi uliopita mpaka nafasi ya 131.Kupanda kwenye viwango hivyo kumetokana na timu ya taifa, Taifa Stars kufuzu fainali za Kombe la la Mataifa Afrika ‘Afcon’ zinazotarajiwa kufanyika Misri Juni mwaka huu. Stars ilifuzu fainali hizo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uganda, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufuzu baada ya miaka 39.Mambo yameonekana kuzinyookea timu za ukanda wa Afrika Mashariki safari hii kwani Burundi nayo imepanda kwa nafasi mbili kutoka 136 hadi 134 huku Uganda ambayo kwa kawaida ndio huwa inaongoza kwa viwango kwa ukanda wa Afrika Mashariki ikishuka kwa nafasi mbili kutoka ya 76 hadi ya 78. Kushuka kwa Uganda kumetokana na kufungwa mechi ya mwisho ya kufuzu Afcon na Taifa Stars ambapo ilifungwa 3-0, hata hivyo Uganda ilicheza mechi hiyo kukamilisha ratiba kwani tayari ilishafuzu mapema. Kenya, imeshuka pia kwa nafasi mbili.Timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ imeshuka nafasi mbili kutoka 106 hadi 108 huku Rwanda ikishika nafasi ya 138 na Sudan Kusini ni ya 167. Nchi za Afrika ambazo zipo kwenye 50 bora ni Senegal (23) Tunisia (28), Nigeria (42), Morocco (45), Congo DR (46) na Ghana (49). Ubelgiji inaongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na mabingwa wa kombe la dunia Ufaransa, Brazil, England, Croatia, Uruguay, Ureno, Uswisi, Hispania na Denmark.
michezo
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ndiye anayetarajia kukabidhi bendera ya taifa na kuiaga rasmi timu hiyo.Alisema kuwa msafara wa timu hiyo, ambao utaongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Yussuf Singo, utakuwa na jumla ya watu 31 wakiwemo wachezaji wa riadha, ndondi, kuogelea na mpira wa meza pamoja na viongozi.Alisema kuwa Singo ataondoka kesho Jumapili kwenda Gold Coast, Australia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuipokea timu hiyo, ambayo itaondoka nchini Alhamisi Machi 29.Alisema kuwa timu za ndondi pamoja na ile ya mpira wa meza ziko katika kambi ya kudumu katika hosteli ya FBF Mkuza Kibaha, ambapo timu ya riadha inayoendelea na kambi mjini Arusha, kesho inatarajia kutua Kibaha kuungana na wenzao kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuondoka.Timu ya riadha itakuwa na Stepheno Huche, Said Makula na Sarar Ramadhani (marathon), Failuna Abdi (meta 10,000), Ali Khamisi Ghulam (meta 100/200) na Anthony Mwanga (miruko na mitupo) wakati makocha wao ni Zakarie Barie na Lwiza John.Mabondia ni pamoja na Kassim Mbutika (Walter), Ezra Paulo (Bantam), Haruna Swanga (Heavy) na Suleiman Kidunda (Middle) wakati kocha wao atakayeongozana na timu hiyo ni Mkenya Benjamin Oyombi wakati kuogelea wachezaji ni Hilal Hilal na Sonia Franco chini ya kocha Khalid Yahya Rushaka.Timu ya mpira wa meza inaundwa na Amon Tumaini, Masoud Mtalaso, Neema Mwaisyula na Fathiya Pazi wakati kocha wao ni Ramadhani Othmani Suleiman.Viongozi ni Dk Singo, meneja wa timu hiyo Nasra Mohamed, daktari ni Joakime Mshanga. Viongozi wengine kwa nafasi zao ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Rais wa TOC Gulam Rashid, Bayi, Pestro Kivike, ambaye ni msaidizi wa Shonza.Hadi sasa Tanzania ina jumla ya medali 21, zikiwemo za dhahabu sita za dhahabu, ambazo tano za riadha na moja ya ngumi, sita za fedha, nne za riadha na mbili za ngumi na tisa za shaba.Kwa mara ya mwisho, Tanzania ilipata medali katika Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2006 Melbourne, Australia wakati wanariadha, Samson Ramadhan na Fabian Joseph walipotwaa medali za dhahabu na fedha katika marathon na mbio za meta 10,000.
michezo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi katika kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake kama wana kesi ya kujibu au la.Hatua hiyo imekuja baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kusema bado hajamaliza kuandika uamuzi wa kesi hiyo. Septemba 2, mwaka huu, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alieleza mbele ya Hakimu Simba kuwa wanafunga ushahidi wao baada ya kupeleka mashahidi 10 kuthibitisha mashitaka hayo.Mbali na Aveva, washitakiwa wengine ni aliyekuwa Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope. Wanakabiliwa na mashitaka 10 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha. Katika mashtaka ya kughushi yanayowakabili washitakiwa wote, inadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016, wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Marekani 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli. Pia katika mashitaka mengine, inadaiwa Aveva, Kaburu na Hans Pope kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577.
michezo
WABUNGE nchini wamemmwagia sifa Rais John Magufuli kwa kufi kiria Taifa hili litakuaje miaka 50 ijayo na kuwataka Watanzania wasijifi kirie wao binafsi, bali Taifa na hatima yake.Aidha, wabunge hao wamesema uwezo wa kufikiri wa Rais Magufuli ni mkubwa kwa kubuni miradi ya kimkakati, ambayo inaiweka nchi katika ramani nzuri na kuipa uwezo mkubwa baadaye wa kuinuka kiuchumi. Kauli hizo zimetolewa na wabunge mbali mbali waliopata nafasi ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliyowasilishwa bungeni juzi.Wabunge hao pamoja na kumpongeza Rais Magufuli, pia waliipongeza wizara hiyo kwa kazi nzuri inayoifanya na kutaka kuimarishwa zaidi kwa mafanikio yaliyopo kwa manufaa ya Taifa.Wabunge hao akiwemo aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tano na Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM); Mbunge wa Bunda Vijijini, Boniface Getere (CCM) na Mbunge wa Fuoni, Kapteni Abbas Ali Mwinyi (CCM), walisema mipango ya serikali hasa ununuzi wa ndege, ujenzi wa SGR ni kuonesha ni kwa namna gani Rais Magufuli ana akili kubwa zaidi ya kufikiri inayofikia IQ 200.Walisema wakati wabunge wengine wakifikiri chini ya kiwango na kuwa na fikira finyu zao binafsi kwa kuzungumza kwa kuogopa kukosa kurejea bungeni, Rais Magufuli anafikia Taifa hili miaka 50 ijayo litakuwa wapi. Akizungumzia kuhusu kubezwa kwa ATCL, Kitwanga alisema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kufikiri na kupanua mawazo kwa ununuzi wa ndege na ujenzi wa SGR na wananchi wanapaswa kumpongeza. Alisema kupitia ATCL uchumi wa kitaifa na mdogo, utaimarika kupitia uletaji wa watalii nchini.Alisisitiza kuwa kufufuliwa kwa kampuni hiyo kutafanya Taifa hili kufaidi matunda ya utalii nchini. Akizungumza kwa mifano, alisema ATCL ikileta watalii mpaka wapagazi watanufaika na kusema kinachostahili kufanywa kwa sasa kuisaidia kampuni hiyo na si kuibeza kwa kuangalia zaidi biashara ya utalii. Alisema Kenya Airways inafanya safari tano kwenda Dar es Salaam na tatu kwenda Zanzibar na kwa sasa ni wajibu wa ATCL kuangalia hilo kwa kuwa hizo ni fedha.Akizungumzia SGR, alisema kwa kuwa na reli maana yake kutakuwa na uwezo wa kuhudumia nchi jirani na hivyo kuliongeza Taifa kipato, kwani kitakachofuata baada ya reli ni maeneo ya kiuchumi ikiwamo bandari kavu. Naye Kapteni Abbas Mwinyi alisema pamoja na kuimarishwa kwa ATCL ni vyema viwanja vingi vikapewa taa na minara ili matumzii ya ndege ziwe asilimia 100, kwani kwa sasa ni chini yake kama asilimia 60. Alisema wanaotakiwa kubadilishwa ni wafanyakazi, lakini ndege muda wote zinatakiwa kuwa hewani.Akizungumzia faida, alisema ni vyema serikali ikatoa fursa zaidi kwa ATCL kuwa na kampuni ya chakula ndani ya ndege upokeaji wa mizigo na uhifadhi ili kutengeneza faida. Alisema dunia nzima inatambua uuzaji wa tiketi pekee, hauwezi kuipatia faida kampuni. Pia alitaka Uwanja wa Ndege wa Seronera, uweke mnara wa kuongezea ndege na taa ili uruhusu ndege za Bombardier kutua na hivyo kupata watalii wanaotaka kufika moja kwa moja maeneo ya utalii, kama ilivyo Masai Mara nchini Kenya.Aidha, mbunge huyo alitaka serikali kutekeleza ahadi zake kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) cha kutoa fedha za kununulia ndege za mafunzo. Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe (CCM) pamoja na kuunga mkono juhudi za kupaisha ATCL, aliitaka serikali kuboresha hanga la Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Pudensiana Kikwembe (CCM) alishukuru kuwepo kwa miradi ya kimkakati na kusema ni kichocheo cha kufungua uchumi wa nchi. Kwa upande wake, Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu (CCM) aliisifu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kazi nzuri zinazoonekana na kila Mtanzania katika sekta zote. Alisema wizara hiyo imebeba wizara nyingi na imefukia mashimo ya wizara nyingine kutokana na kazi zake wanazofanya.
kitaifa
Lipuli ilikuwa ya kwanza kupata bao la lililofungwa na Adam Salamba dakika ya 32 na Simba wakisawazisha dakika ya 66 likifungwa na Laudit Mavugo.Simba itaendelea kuwa kileleni mwa msimamo ikifikisha pointi 59 katika michezo 25 iliyocheza huku mahasimu wao Yanga wanaotarajiwa kucheza leo wakiendelea kuwa katika nafasi ya pili kwa pointi 47 katika michezo 22 waliyocheza.Hii ni mara ya pili wekundu hao wanalazimishwa sare ya bao 1-1 na timu hiyo baada ya raundi ya kwanza kupata matokeo ya aina hiyo kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kipindi cha kwanza timu zote zilicheza vizuri na kushambuliana kwa zamu ambapo Lipuli walipata bao la uongozi lililodumu hadi kumalizika kwa kipindi hicho.Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Juuko Murshid na kuingia Mavugo aliyeisawazishia Simba bao baada ya kupata mpira wa kona uliopigwa na Shomari Kapombe.Timu zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo kila mmoja alikuwa na nafasi ya kupata magoli zaidi lakini walizipoteza. Baada ya Lipuli kupata bao la uongozi walitengeneza nafasi nyingine dakika ya 35 na 36 kwa Salamba lakini hawakuwa makini.Kwa upande wa Simba dakika ya 29 na 38 Shiza Kichuya alipata nafasi na kushindwa kuzitumia ipasavyo na dakika ya 79 Mavugo alipaisha mpira. Lakini hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yaliendelea kubaki 1-1 kila timu ikicheza kwa kiwango kizuri.Simba: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Juuko Murshid/Mavugo dk.45, Yusufu Mlipili, Shomari Kapombe, Shiza Kichuya, James Kotei, Asante Kwasi, Nicholaus Gyan, Emmanuel Okwi na Jonh Bocco.Lipuli: Mahamed Yusuph,Steve Mganga, Paul Ngalema, Ally Mtoni, George Owino, Fred Tangalo, Daluwesh Saliboko, Mussa Nampaka, Adam Salamba, Malimi Busungu na Seif Karie.
michezo
Hayo yalisemwa na Ntibenda wakati alipowahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kimkoa yaliyofanyika jana Viwanja vya Shehe Amri Abeid jijini Arusha. Aliwasihi wafanyakazi kutumia vyema vyama vya wafanyakazi mahali pa kazi ili walete maendeleo kati ya waajiri pamoja na wafanyakazi wenyewe.Alisema ni vyema wafanyakazi wakatumia vyama vyao vya wafanyakazi mahali pa kazi ili kuzungumza mambo yao mbalimbali na kusuluhisha, badala ya waajiri kuwazuia ili kuleta maendeleo.Alitoa rai kwa waajiri kuacha tabia ya kutowapa mikataba ya ajira wafanyakazi wao, badala yake washirikiane kwa pamoja katika kuleta maendeleo, kwani kampuni ikipata maendeleo wanaostahili pongezi ni wafanyakazi mnaoshirikiana nao kwa pamoja.“Fanyeni kazi na mtumieni vyama vya wafanyakazi katika kaleta maendeleo badala ya kuvitumia vyama vya wafanyakazi katika kuleta maendeleo nanyi waajiri acheni tabia ya kuwazuia wafanyakazi katika kuleta maendeleo badala ya kuwakandamiza,” alisema Ntibenda.Pia alisema serikali ipo mbioni kufufua viwanda pamoja na reli ili kuinua sekta ya viwanda pamoja kuinua uchumi kwa mkoa wa Arusha na kusisitiza vijana kufanya kazi badala ya kukimbilia kucheza ‘pool table’ pamoja na kupiga debe kwa kuwanyang’anya wananchi vitu vyao.Cosmas Chikoti ambaye ni Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi mkoa wa Arusha, aliomba serikali iangalie maslahi bora kwa wafanyakazi ikiwemo mikataba ya ajira pamoja na kusisitiza kuwa na mahusiano mema kati ya waajiri na waajiriwa.Hafla hiyo ilienda sambamba na maandamano ya wafanyakazi pamoja na kutoa zawadi kwa wafanyakazi bora ambapo pia wananchi mbalimbali walihudhuria ikiwemo wakuu wa wilaya za Arusha, wakurugenzi watendaji wa halmashauri na makatibu tawala mkoa na wilaya.
uchumi
JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limefanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu, ikiwemo wizi wa kutumia funguo za bandia kwa kufungua milango ya wananchi wanapokuwa wamelala nyakati za usiku.Hayo yalisemwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga, Ally Mkalipa alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Igunga katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sokoine, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya kuimarisha ulinzi shirikishi.Mkalipa alisema katika msako unaoendelea Wilaya ya Igunga wa kuwasaka baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu wamefanikiwa kukamata kundi la vijana ambalo hakutaja idadi wala majina yao, wakiwa na funguo zaidi ya 1,000 wanazofanyia uhalifu.Alisema katika funguo hizo zipo ambazo zinatumika kufungua milango ya aina ya vitasa ambazo zimetengenezwa kwa kutumia nondo na kuongeza kuwa baada ya kuwakamata walipowahoji walikiri kufanya uhalifu maeneo mengi. Sambamba na hayo, Mkalipa alitoa tahadhari kwa wananchi wanaopanda pikipiki kwa kukodi kuwa makini kwa kuwa wapo baadhi ya waendesha bodaboda si waaminifu ambao wamekuwa wakitumia namba za pikipiki tofauti wanapokodiwa kuwasafirisha abiria.Aliwataka wananchi na wafanyabiashara kuimarisha milango yao na kuajiri walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo, ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara mizuri huku akiwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Igunga kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ili kukomesha vitendo vya uhalifu kwa kuimarisha ulinzi.
kitaifa
IKIWA imesalia siku moja kabla ya Yanga kuumana na wapinzani wao, Township Rollers katika kuwania kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu hiyo imejinasibu kuwa ipo tayari kupambana kuhakikisha inapata matokeo na kusonga mbele kulingana na maandalizi waliyokuwa nayo.Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa tangu wawasili Gaborone, Botswana wamekuwa na mazoezi ya kutengeneza fiziki kabla ya kuhamia kwenye mbinu za kutengeneza mashambulizi na namna ya kulishambulia lango la wapinzani wao hao ili wapindue matokeo ya mechi ya kwanza na kusonga mbele.Mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita iliisha kwa sare ya bao 1-1, hivyo kuipa kibarua Yanga kumaliza mchezo huo wa pili kwa ushindi au sare ya kuanzia mabao 2-2 kwa ajili ya kukata tiketi ya kuendelea na hatua inayofuata.“Tumekuwa na maandalizi mazuri na kusuka mipango namna gani tunakwenda mbele, tunatengenezaje nafasi na wangapi wanatakiwa kuwa wapi kwa wakati husika ili kuona jinsi gani tunaweza kupata mabao ya kutosha katika mechi hiyo,” alisema Zahera.Kwa upande wa mshambuliaji wa Yanga, Juma Balinya alieleza kufahamu jinsi gani mchezo huo ni mgumu kwao kutokana na uzuri wa Rollers lakini kulingana na maandalizi yao wanajua wataibuka na ushindi kulingana na udhaifu wa wapinzani wao.Naye Mrisho Ngasa alisema: “Mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wapo kwao lakini sisi wachezaji binafsi tuko vizuri na tuna uwezo wa kufanya vizuri katika mechi hii.
michezo
Tuzo Mapunda SIMBA imeanza vyema msimu huu baada ya kuifunga Azam mabao 4-2 katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.Mechi hiyo inayoashiria kufungua pazia la Ligi Kuu Bara hushirikisha bingwa wa Ligi Kuu (Simba na bingwa wa Kombe la FA (Azam).Simba sasa inatwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo, msimu wa mwaka 2017/18 iliifunga Yanga, 2018/19 ikaifunga Mtibwa Sugar na jana msimu wa mwaka 2019/20 imeifunga Azam.Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 13 likifungwa na Shaaban Chilunda aliyewazidi kasi mabeki wa Simba na kuujaza mpira wa wavuni.Dakika tatu baadaye, Sharaf Shiboub aliisawazishia Simba bao hilo akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Azam, Razak Abarola.Shiboub alifunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jnr’.Simba ilianza mashambulizi mapema mwa mchezo huo ikiliandama mara kwa mara lango la Azam kabla ya Wanalambalamba kukaa sawa na kurudisha mashambulizi.Moto wa Simba uliendelea mpaka katika kipindi cha pili ambapo kama ilivyo kwenye kipindi cha kwanza walimiliki zaidi sehemu ya kiungo.Dakika ya 57, Clatous Chama aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwatoka mabeki wa Azam na kuukokota mpira kabla ya kuachia shuti lililomzidi kipa Abalora. Dakika nne baadaye nusura Meddie Kagere aiandikie Simba bao lakini shuti lake lilipaa juu.Mechi hiyo ilitawaliwa na ubabe na rafu nyingi, hali iliyomlazimu mwamuzi Elly Sasii kuwaonya kwa mdomo mara kwa mara hasa wachezaji wa Azam.Hata hivyo, beki ya Simba ilikuwa ikikatika mara kwa mara na dakika ya 78 iliruhusu nyavu zake kutikiswa baada ya Azam kupata bao la pili lililofungwa na Frank Domayo akimalizia pasi ya Obrey Chirwa.Francis Kahata alizidisha shangwe kwa Wanasimba baada ya kufunga bao la nne katika dakika ya 86 akiunganisha pasi ya Chama na kuachia mkwaju mkali kwenye lango la Azam.
michezo
Naibu Kamishna wa Forodha, Patrick Kisaka ametaja mali hizo kuwa ni mifuko 40 ya sukari kutoka Brazil, ndoo 20 za mafuta ya kupikia kutoka Mashariki ya Mbali na katoni 70 za vigae, ambavyo maofisa wa TRA kwa kushirikiana na askari wa doria, walivikamata Januari 8 katika bandari hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna huyo aliwataka wananchi hususan wanaoishi maeneo ya mipaka na ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kutojihusisha na biashara ya magendo na badala yake kuwafichua watu wanaofanya biashara hizo ambao wanaikosesha Serikali mapato.“Tunaomba watu wanaojihusisha na biashara hizi waache mara moja kabla hawajaangukia mikononi mwetu kwani tutawachukulia hatua za kisheria zikiambatana na kifungo au faini, na huu ni kwa mujibu wa sheria.”Alisema Kamishna huyo. Aidha, Kamishna huyo aliwataka wananchi watoe taarifa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia namba 0789 933 8930 na 0789 338 931 endapo watabaini kuna vitendo vyovyote vya kimagendo hasa kwenye maeneo ya mipaka, ambako biashara hiyo imekuwa ikifanyika kwa kasi na kuahidi zawadi nono itakayolingana na kiwango cha kodi ya bidhaa hiyo.Kisaka aliwahakikishia wananchi kuwa idara yake kwa kushirikiana na askari wa doria wataendelea kupambana na wafanyabiashara wa magendo katika maeneo ya majini na nchi kavu usiku na mchana ili kuhakikisha Serikali inapata mapato yake, ambayo yamekuwa yakipotea kwa njia hizo za kimagendo.‘Sisi tutaendelea kupambana na magendo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutumia rasilimali zetu za nchi kavu na majini. Wenzetu wana boti sisi tutaweka mafuta na kufanya doria katika mipaka yote ya majini na nchi kavu”, alisisitiza Kamishna huyo.Katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja, TRA kupitia idara hiyo imeshakamata mifuko 1158 ya sukari ya kilo 50 kutoka nje ya nchi, iliyokuwa ikiingizwa kwa magendo nchini kupitia doria zake mbalimbali zilizoko maeneo ya mipakani na kuahidi kuendeleza mapambano hayo.Bandari bubu zinazotajwa kuwa ni kinara wa kupitisha bidhaa kimagendo ni Kunduchi na Ununio jijini Dar es Salaam na Mlingotini ya Bagamoyo.
uchumi
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kigoma kimesema tofauti ya kiitikadi iliyopo baina ya vyama vya siasa mkoani humo na nchini kwa jumla isiwe sababu ya kuleta utengano na kuvuruga ushirikiano walio nao Watanzania tangu nchi ipate uhuru.Mwenyekiti wa Chadema Mkoa, Ally Kisala alitoa kauli hiyo katika Jukwaa la Umoja wa Majadiliano lililofanyika juzi jioni mjini Kigoma, akisema kwamba amani, umoja mshikamano na ushirikiano wa Watanzania ni wa asili hivyo hauna sababu ya kuvurugwa na tofauti ya kiitikadi iliyopo kwenye vyama vya siasa. Kisala alisema wakati huu nchi inajiandaa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kumekuwa na lugha kali kutoka kwa vyama vya siasa ambazo ndani yake hazina afya katika kulinda umoja na mshikamano wa Watanzania.Alisema lengo la vyama vyote vya siasa ni kushika dola, lakini pia kila chama kinanadi sera zake kwa kuonesha zinataka kumtumikia Mtanzania, akihoji sababu za mtifuano na mivurugano ambayo haina sababu yoyote. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chama cha NCCR – Mageuzi, Sam Ruhuza aliwataka wabunge kusimamia taratibu za uendeshaji wa Bunge na kuisimamia serikali katika kutekeleza matkwa ya Katiba na sheria za nchi hususan matumizi mbalimbali yanayofanywa na serikali.Ruhuza alisema serikali itekeleze sheria inayolipa Bunge mamlaka na uhalali wa kupitisha bajeti ya nchi katika manunuzi na matumizi mbalimbali hivyo wabunge hawana budi kuhoji matumizi makubwa yanayofanywa na serikali bila kupitia kwenye Bunge.Mratibu wa kongamano hilo, Frank Luhasha ambaye ni Katibu wa Chadema Wilaya ya Kigoma, alisema vyama vya siasa vyote vina lengo moja katika kutekeleza majukumu yake isipokuwa vinapishana njia, vipaumbele na wakati hivyo ni lazima vikumbuke wanayofanya yote yanalenga Watanzania na wakumbuke Watanzania wote ni wamoja. Luhasha alisema wakati huu ambao nchi ina vyama vingi ni wazi lazima vyama vipiganie maslahi ya nchi badala ya kupigania maslahi ya serikali na kwamba lengo kuu la kongamano hilo ni kuviweka pamoja vyama vyote na kujadili umoja, mshikamano na ushirikiano kama Watanzania.Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji, Lumu Hamisi ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo, alisema pamoja na kongamano hilo kuhusisha siasa na viongozi wa siasa, lakini lengo lake kubwa ni kuwafanya viongozi wa vyama vya siasa kutafakari majukumu yao katika kuleta umoja na mshikamano wanaposimamia utekelezaji wa shughuli za vyama vyao.
kitaifa
Hatua hiyo imeelezewa kuwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuhakikisha inawarahisishia wateja wake upatikanaji wa huduma zake kupitia teknolojia ya mawasiliano.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kuzindua kituo hicho, Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Exim, Frank Matoro alisema matumizi ya kituo hicho yatawezesha wateja kupata taarifa za kina kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.“Ni matarajio yetu kwamba wateja wetu watafurahia zaidi huduma bora kutoka kwa wahudumu wenye vigezo na uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala ya kibenki,” alisema.Matoro alisema kituo hicho kimekwisha anza kutoa huduma.Alisema malengo ya kampeni hiyo ni kuhakikisha wateja wanatambua uwepo wa kituo hicho na kutumia ipasavyo huduma zitolewazo na kituo hicho.“Katika kuhakikisha kwamba kampeni hii inaleta mafanikio, itaambatana na droo ndogo zitakazowezesha utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wateja zikiwemo fulana zenye nembo ya benki, muda wa maongezi pamoja na simu mpya aina ya iPhone 5s,’’ alitaja.
uchumi
['Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, bado ana hamu kubwa ya kutaka kuondoka Manchester United kuelekea Real Madrid msimu huu wa joto. (Marca) ', 'Beki wa kati wa England Harry Maguire, mwenye miaka 26, amekataa pendekezo la thamani ya £278,000 kwa wiki kutoka Manchester City badala ya kujiunga na timu hasimu United. (Star)', 'Meneja wa United, Ole Gunnar Solskjaer amefanya mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham, Christian Eriksen kuhusu uwezekano wa uhamisho kuelekea Old Trafford, hatahivyo mchezaji huyo wa miaka 27alikuwa anataka kusubiria uhamisho kuelekea Uhispania. (Manchester Evening News)', 'Mchezaji wa kiungo cha mbele wa United na timu ya taifa ya Chile, Alexis Sanchez, aliye na umri wa miaka 30, yupo tayari kwa uhamisho kuelekea Italia , wakati Juventus, Napoli, AC Milan na Inter Milan zote zikiwania kumsajili. (Mirror)', 'Sanchez atashinikiza uhamisho kuondoka Old Trafford kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya Septemba 2. (Times)', 'Kwa upande mwingine, United imeshindwa kupata mnunuzi wa Sanchez- anayepokea malipo ya £560,000 kwa wiki. (Mirror)', 'Juventus bado inatumai kumuondoa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Argentina, Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho Ulaya - licha ya kwamba mabingwa hao wa Italia bado hawajapokea maombi thabiti kwa mchezaji huyo. (Independent)', 'Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain, Leonardo anasema mchezaji wa kiungo cha mbele wa Brazil, Neymar "amefanya makosa" lakini amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa miaka 27 yupo Paris "kwa miaka mitatu". (RMC)', 'Kipa wa Stoke City na timu ya taifa ya England Jack Butland, aliye na miaka 26, ataomba uhamisho kujilazimisha kuwa katika mipango ya meneja wa England, Gareth Southgate kwa ajili ya mashindano ya Euro 2020. (Mail)', 'Timu ya Brazil Flamengo ilmejitoa katika uhamisho wa mshambuliaji Mario Balotelli baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kuitisha mkataba wa thamani ya £4m. (Mail)', 'Napoli imekubali kumsaini winga wa Mexico mwenye miaka 23 Hirving Lozano kutoka timu ya Uholanzi PSV Eindhoven. (Voetbal International)', 'Napoli imekataa ombi la thamani ya £82m kutoka kwa Manchester United kwa mchezaji wa miaka 28 raia wa Senegal Kalidou Koulibaly kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho England. (Corriere dello Sport, kupitia Calciomercato)', 'Winga wa Bournemouth Jordon Ibe anasakwa na mabingwa wa Uskotchi, Celtic. Timu ya Napoli Italia, tayari imemuulizia mchezaji huyo wa miaka 23. (Sun)', 'Manchester United imewapiga marufuku wachezaji kusaini kumbukumbu au autograph kwa mashabiki katika kiingilio cha uwanja wa mazoezi kutokana na masuala ya usalama.(Telegraph)', 'Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini anasema alitaka kipa wa Liverpool Adrian, mwenye miaka 32, asalie katika klabu hiyo. (Mail)', 'Neymar alikuwa mazoezini mwenyewe siku ya Jumatano, ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapouzwa.(Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza bado kujiunga na PSG ikiwa hatakuwa sehemu ya ofa ya Neymar. (Goal)', 'Beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof, 25, anajiandaa kusaini mkataba mpya kwa ongezeko la mshahara mbali na pauni 75,000 alizokuwa akipata kwa wiki. (Aftonbladet - in Swedish)', 'Bayern Munich huenda wakafufua nia yao ya kumnasa winga wa Manchester City, Leroy Sane, ingawa mchezaji huyo, 23, ana jeraha la mguu, litakalo mfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba. (Bild - in German)', 'Mshambuliaji wa Marseille na Italia Mario Balotelli,29, anajiandaa kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Brescia baada ya kukataa ofa ya Flamengo ya Brazil. (Guardian)', 'Flamengo bado wana matumaini ya kubadili msimamo wa Balotelli, baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kaka yake Enock kucheza katika moja kati ya timu zao nyingine (Gazzetta dello Sport - in Italian)', 'Winga wa klabu ya Everton Alex Iwobi, 23, amesema aliondoka Arsenal katika siku ya mwisho ya usajili kuthibitisha kuwa yeye si mchezaji anayechipukia tena. (Mirror)', 'Tottenham itazungumza na Christian Eriksen, 27,tena kuhusu mkataba mpya kabla kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, tarehe 2 mwezi Septemba, baada ya Real Madrid na Juventus kuonesha nia ya kumnasa kiungo huyo.(Independent)', 'Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, anaonekana kujiandaa kujiunga na timu ya Trabzonspor ya Uturuki kwa dili la pauni milioni 2.8 kwa kila msimu.(Goal)', "Monaco imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwasajili wachezaji kiungo Blaise Matuidi,32, na beki wa kati Daniele Rugani,25, kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport - in Italian)"]
michezo
BAADA ya kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia FC katika mchezo wa makundi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mashabiki na wanachama wa Yanga wameutaka uongozi kufanya uamuzi mgumu kwa kusafisha upya kikosi.Kipigo hicho cha ugenini kimemtoa hadharani mchezaji wa zamani wa Yanga, Abeid Mziba akieleza kutoridhishwa na kiwango cha wachezaji akidai walikwenda kucheza kutimiza wajibu na siyo kushindana na baadhi hawaendani na ukubwa wa Yanga.“Wachezaji wamekata tamaa na mchezo wa jana (juzi) walicheza kwa kutimiza wajibu tu na siyo kushindana. Yanga ina matatizo na kuna wachezaji hawana msaada na timu, hivyo timu haiwezi kuendelea kuwa nao,” alisema Mziba.Pia alisema wachezaji wengine hawapo sawa kisaikolojia kwani wamejitwika matatizo yaliyopo kwenye klabu na kuacha kuonesha jitihada binafsi na kufanya vibaya ndio kunazidi kuwamaliza.Alisema tangu kuondoka kwa Kocha George Lwandamina, Yanga imekuwa na rekodi mbovu kutokana na matokeo mabaya kwani kikosi hakifanyi vizuri. Naye kocha wa zamani wa Yanga, Kenedy Mwaisabula ‘Mzazi’ na kipa wa zamani wa timu hiyo, Peter Manyika walisema timu haikuwa na maandalizi ya mchezo, kwani ilijitoa kwenye mashindano ya Kagame ambayo yangewaweka vizuri hivyo haikuwa vizuri kisaikolojia na kimwili.“Mpira siyo kuendesha baiskeli useme unaendesha. Yanga haikuwa na ‘match fitness’ na hata mazoezi ilifanya kwa siku nne tu halafu ikaenda kucheza na Gor Mahia ambayo ilitoka kwenye Kagame,” alisema Mwaisabula.“Kitaalamu Yanga haikuandaliwa kimashindano kwani kisaikolojia na kimwili haikuwa sawa na maandalizi yake hayakuwa mazuri,” alisema Manyika.Mwaisabula alisema kukosekana kwa Yondani na Hassan Kessy si sababu ya timu hiyo kufungwa mabao hayo, na kwamba hata wangekuwepo bado ingefungwa.“Sana sana wangepunguza idadi ya mabao tu, lakini kufungwa wangefungwa maana kiukweli Yanga haikujiandaa kwa mechi hiyo, ilichofanya ni kutimiza wajibu tu, ikamilishea ratiba basi,” alisema Mwaisabula.“Uongozi ujitizame upya… kama timu hiyo ndio wanaingia nayo kwenye mashindano mengine, kazi itakuwa kubwa, wajipange na wafanye maamuzi mapema,” alisema.Mjumbe wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, ameutaka uongozi wa Yanga kuwafukuza wachezaji wote kwa sababu wamekosa mchango wa kuisaidia timu na kumbakisha Kelvin Yondani pekee.Akilimali alisema matokeo ya juzi yanazidi kuleta taswira mbaya kwa timu hiyo na namna mwenendo mzima wa klabu ulivyo sasa na uongozi kuitisha uchaguzi ili kupata watawala wapya watakaofanya kazi kwa weledi ili kuisaidia timu kuimarika na kurejesha makali yake.“Inabidi Yanga waitishe uchaguzi haraka ili kupata viongozi wapya kuikwamua klabu kutoka kwenye hali ya ukata wa fedha uliopo hivi sasa iweze kujiimarisha kiuchumi,” alisema Akilimali.Yanga imebakisha michezo mitatu za marudiano ambapo itaifuata Rayon ya Rwanda na michezo miwili dhidi ya Gor Mahia na USM Algiers itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga inakamata mkia ikiwa na pointi moja, ikifuatiwa na Rayon Sports ya Rwanda yenye pointi mbili, Gor Mahia ina pointi tano na USM Alger ikiwa kinara na pointi saba.
michezo
Msaada huo ni kwa ajili ya kuwatambua na kuwasaidia wafanyabiashara, wanaofuata sheria ili wafanye biashara zao kiurahisi.Pia, mamlaka hizo zimetakiwa kupambana na wafanyabiashara wasiofuata sheria kwa kuwaelimisha juu ya kutumia njia sahihi za kufanya biashara ndani na nje ya nchi .Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Forodha Duniani, Erick Kieck alisema wametoa msaada huo kuwasaidia wakuu wa forodha kuwaunganisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.Akitoa mfano wa wauzaji wa dawa za kulevya, Kieck alisema kuwa watu hao hawafuati sheria za biashara kwani sio halali na kwamba wanatakiwa kuondokana na biashara hizo.Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Patrick Mugoya alisema kuwa mradi huo wa pili unaojulikana kwa jina la WCO-EAC, uliwakutanisha Makamishna wa EAC huku akieleza kuwa mradi huo ni kuhamasisha wahisani wengi zaidi kusaidia mradi huo.Mugoya alisema kuwa mradi huo unatoa fursa kwa mawakala wa Forodha kuchangia katika ukuaji wa masuala ya biashara za kimataifa.Mkuu wa Mradi huo, Joseph Wambati alisema kuwa wamelenga kupunguza gharama za kufanya biashara kwa kuwasaidia wananchi kuweza kujipatia bidhaa kwa bei nafuu.Pia, alisema katika mradi uliopita, waliweza kufanikiwa kuwapa fursa wafanyabiashara mbalimbali kufanya biashara ndani na nje ya nchi. ‘’Tunataka kuwaelimisha wafanya biashara juu ya kuwa waaminifu katika biashara zao ili kuweza kushindana na watu wengine,’’ alisema Wambati.
uchumi
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amemvua kitambaa cha unahodha mlinzi Kelvin Yondani na kumkabidhi mshambuliaji Ibrahim Ajibu kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kuchelewa kuripoti kambini.“Nilitoa siku tano za mapumziko baada ya mechi na Mbeya City lakini yeye kama nahodha hakuripoti kambini baada ya siku hizo na hajatoa taarifa yoyote, ndio maana nimeamua Ajibu awe nahodha mpya wa timu,” alisema. ‘’Siwezi kumuacha mtu kama yule anayepaswa kuonesha mfano kwa wengine afanye hayo, hivyo nimeamua nimvue unahodha na kuanzia sasa nahodha ni Ibrahim Ajibu,’’ alisema Zahera Yondani na Ajibu wote waliwahi kuichezea klabu ya Simba ambapo baadae Yondani alijiunga na Yanga akitokea Simba mwaka 2013 huku Ajibu akijiunga na Yanga mwaka 2017.Itakumbukwa Mwinyi Zahera alimkataa kikosini mlindalango wa klabu hiyo, Beno Kakolanya kutokana yeye kususia mazoezi kutokana na madai ya pesa za usajili wake mpaka sasa hajajiunga na timu. Kikosi cha Yanga kilichobaki Dar es Salaam jana kilianza mazoezi kwenye viwanja vya Polisi Kurasini baada ya mapumziko na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza pamoja na wale wa U20 wapo Zanzibar kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup.
michezo