content
stringlengths 1k
24.2k
| category
stringclasses 6
values |
---|---|
WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji cha Kilama Kata ya Iyogwe wilayani Gairo, mkoa wa Morogoro wamepata neema kwani hadi Juni 30, mwaka huu.Jumla ya gramu 255. 23 za dhahabu zilinunuliwa katika soko la madini la Morogoro mjini na kupatikana jumla ya Sh milioni 25.3 na Serikali ikiwa imekusanya tozo zinazofi kia kiasi cha Sh milioni 1.8.Kaimu Ofisa Madini Mkazi wa mkoa wa Morogoro , Emmanuel Shija alisema hayo kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika mgodi mpya wa dhahabu wa Kilama uliogunduliwa na wachimbaji wadogo wa eneo la kitongoji cha Mlimani kipindi cha mwishoni mwa mwezi Mei mwaka 2019.Shija alisema tangu uchimbaji umeanza chini ya utaratibu na usimamizi uliowekwa katika eneo hilo, hadi kufikia Juni 30, 2019 gramu 228.3 za dhahabu zilinunuliwa na madalali wa eneo la Kilama , ambapo wanunuzi wa dhahabu watano wamesajiliwa na mgodi huo na kupewa leseni kwa mujibu wa sheria.“Jumla ya gramu 255.23 za dhahabu kutoka mgodi wa Kilama zimenunuliwa katika soko la Madini lililopo Morogoro mjini na dhahabu hizo zimenunuliwa kwa jumla ya Sh 25, 341, 725 . 27 na Serikali imekusanya tozo zake zinazofikia jumla ya Sh 1,849,945 .94,” alisema Shija alipozungumza na gazeti hili. Hata hivyo, alisema leseni nne za utafiti na uchimbaji mdogo wa madini (PML) zimeombwa na Ushirika ulioundwa chini ya utaratibu unaosimamiwa na halmashauri za wilaya ya Gairo.Pamoja na hayo, alitoa rai kwa uongozi wa ushirika ambao umekabidhiwa kuongoza mgodi huo wafanye kazi ya usimamizi kwa weledi na uaminifu ili kuhakikisha wachimbaji wadogo wanafanya kazi wananufaika na mgodi huo lakini pia na serikali inapata stahiki zake zilizo kwa mujibu wa Sheria.Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe aliufungua tena mgodi huo Julai 7, mwaka huu baada ya kufungwa Juni 8, mwaka huu kutokana na wachimbaji watano kufariki dunia kwa kufukiwa na miamba ya mawe na kujeruhiwa pia.Hata hivyo, kufunguliwa kwa mgodi huo kumekuja baada ya wachimbaji wadogo kutimiza masharti yaliyotolewa na Dk Kebwe juu ya kuweka mazingira mzuri ya uchimbaji, kuunda vikundi vya ushirika vya wachimbaji na kusajiliwa na halmashauri ambapo jumla ya vikundi 97 vilikuwa vimesajiliwa. | uchumi |
LIGI Kuu ya wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo minne katika viwanja vinne tofauti.Vinara wa ligi hiyo Alliance Girls yenye pointi 13 wataikaribisha Baobab ya Dodoma yenye pointi moja katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza. Panama Queens yenye pointi tatu itacheza na bingwa mtetezi JKT Queens ambayo ina pointi tisa katika nafasi ya nne, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Samora, Iringa.Katika Uwanja wa Gwambina, Mwanza, TSC Queens yenye pointi sita itacheza na vibonde Tanzanite Queens ambayo haina pointi ikiwa imefungwa mabao 23. Akizungumza jana Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo alisema michezo mitatu imesogezwa mbele kwa sababu mbalimbali.Mchezo wa Simba Queens na Sisterz ya Kigoma ambao ulikuwa uchezwa leo umesogezwa mbele hadi keshokutwa kutokana na Sisterz kuchelewa kufika Dar es Salaam kwa sababu walisafiri kwa treni toka Kigoma, hadi jana ilisemekana walikuwa Kilosa, Morogoro, na ilishindikana kuendelea na safari kutokana na kuwepo ajali ya treni ya mizigo.Pia mchezo wa Mlandizi Queens dhidi ya Marsh na Ruvuma Queens dhidi ya Yanga Princess zitachezwa Jumanne ijayo badala ya leo, michezo hii imesogezwa mbele kutokana na timu hizi kuwa na wachezaji katika kikosi cha timu ya Taifa ya U-20 kilichopo Algeria. | michezo |
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa PSSSF, umeanza kufanya uhakiki wa wastaafu na wategemezi wa mfuko huo kuanzia sasa hadi mwezi Machi, mwaka huu Tanzania Bara na Visiwani.Ili kuweza kufanikisha kazi hiyo, uongozi wa mfuko huo umetaja vigezo vitakavyotumika ili kutambua uhalali wa wastaafu hao, ambapo wahusika wametakiwa kufika katika ofisi za mfuko huo wakiwa na picha moja ya pasipoti, kitambulisho cha Taifa au cha mpiga kura na nakala ya kadi ya benki. Kwa mujibu wa taarifa ya PSSSF iliyotolewa kwa umma jana, wahusika wanaotakiwa kufuata masharti hayo ya uhakiki ni waliokuwa wanachama wa mifuko ya LAPF, GEPF, PSPF na PPF ambapo awali ilikuwa ni mifuko inayojitegemea.Kutokana na kuunganishwa kwa mifuko hiyo, sasa imezaliwa mifuko miwili ambayo ni wa PSSSF unaohusika na watumishi wa umma na Mfuko wa NSSF unaoshughulikia watumishi walio wa sekta binafsi. Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Rais John Magufuli, kuagiza mifuko hiyo kuanza kulipa mafao kwa kutumia mifumo iliyokuwa inatumiwa na mifuko kabla ya kuunganishwa.Alitoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Desemba 28, Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika maagizo hayo, Rais Magufuli pia aliagiza wafanyakazi waliokuwa kwenye ajira za muda zisizokuwa za kitaaluma, kulipwa mafao yao yote, pindi tu mradi husika unapomalizika au wakisitishiwa mkataba wao. Hatua hiyo ya Rais Magufuli iliibua shangwe kutoka kwa wafanyakazi na wastaafu na kufuatiwa na maandamano, yaliyofanyika katika miji ya Dar es Salaam na Dodoma ili kuunga mkono agizo hilo. | kitaifa |
Kahawa hiyo iliuzwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013 hadi Aprili 30 mwaka huu. Meneja Mkuu wa Tanica, Leonidas Nshansha alisema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.Alisema malengo ya kampuni hiyo tangu Mei Mosi mwaka jana yalikuwa ni kuzalisha tani 255 za kahawa ya unga na tani 270 za kahawa ya kukaanga.Alisema hadi sasa kiwanda kimezalisha tani 251 za kahawa ya unga na kahawa ya kukaanga uzalishaji wake unaendelea kwa asilimia 100. Nshansha alisema kuwa kipindi cha mwaka wa fedha unaokaribia kuisha, malengo yanaweza kukamilika kwa kiasi kikubwa, tofauti na mwaka 2012.Mwaka huu mafanikio yataongezeka, japo haijajulikana ni faida kiasi gani watapata ukaguzi utakapofanyika baada ya kufunga mahesabu ya mwaka.Pia alisema kutokana na kuwepo changamoto hasa katika soko la dunia, hususan uwepo wa bei isiyokidhi gharama za uzalishaji, kampuni hiyo imejiimarisha katika soko la ndani, kwa kutoa kipaumbele kwa watumiaji wakubwa wa kahawa hiyo katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Dodoma, Kigoma, Katavi na Rukwa.Pia, kampuni imeendelea kujiimarisha katika soko la Afrika Mashariki, hasa Kenya, ambayo ndiyo nchi inayoongoza kwa kutumia kahawa. | uchumi |
NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imetenga Sh bilioni 88 kulipa wakandarasi mbalimbali nchini wanaotekeleza miradi ya maji.Aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Kabati (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kuhakikisha inawalipa wakandarasi wanaoidai ambao wengi wao hawajalipwa madai yao.Aweso alisema serikali imetenga fedha hizo kwa lengo la kulipa makandarasi wote nchini akiwemo mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji katika mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo ambaye tayari amelipwa zaidi ya Sh bilioni moja.Akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Vedasto Ngombale (CUF) aliyetaka kujua serikali imefanya tathmini ili kujua ni asilimia ngapi ya miradi 10 ya visima 10 katika kila wilaya iliyofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) imefanikiwa au haijafanikiwa.Naibu waziri huyo alisema katika mwaka 2016, wizara iyo ilifanya tathmini ya kina nchi nzima ili kujua idadi ya visima vyote vilivyochimbwa kwa awamu ya kwanza ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji katika halmashauri zote Tanzania Bara. “Idadi ya visima vilivyochimbwa vilikuwa 1,485 kati ya hivyo, visima 990 sawa na asilimia 67 vilipata maji na visima 494 sasa na asilimia 33 vilikosa maji,” alisema.Alisema maeneo ambayo visima vyake vilikosa maji, serikali ilitumia vyanzo vingine mbadala kama vile chemchemi, mito, maziwa au kujenga mabwawa ili kuhakikisha maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mpango wa vijiji 10 yanapata huduma bora ya majisafi na salama.Alisema kwa sasa serikali imeanzisha Mfuko wa Maji wa Taifa ambao unalipa miradi yote iliyochelewa kukamilika na miradi mipya inayoendelea kujengwa katika halmashauri zetu, lengo ikiwa ni kumpatia huduma bora ya maji kwa kila mwananchi. | kitaifa |
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita katika kipindi Oktoba hadi Desemba, mwaka jana, imeokoa zaidi ya Sh milioni 16 za taasisi mbalimbali ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)ambazo zingehujumiwa.Taasisi hiyo imepokea malalamiko ya rushwa 48 kutoka kwa wananchi ambapo malalamiko 10 kati yake yamefunguliwa majalada ya uchunguzi na mengine uchunguzi umekamilika na nane yamepelekwa makao makuu kwa ajili ya hatua zingine.Aidha, Takukuru Mkoa wa Geita imeanza uchunguzi kwa kasi kupitia timu maalumu iliyoundwa inawaoshirikisha watalaamu kutoka sekta tofauti wakiwemo maafisa wa Takukuru kuhusu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo zilizotokana na fedha za huduma za kijamii CSR kutoa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) ambapo baadhi ya watumishi wa mgodi wameanza kuhojiwa.Mkuu waTakukuru Mkoa wa Geita Thobias Ndaro alisema hayo juzi wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu kutoka Oktoba hadi Desemba, mwaka jana, ofisini kwake alipokuwa akizungumza na wanahabari.Ndaro amesema, Sh milioni15 kati ya Sh milioni 16. 6 zilizookolewa zilitokana na kukamatwa kwa mfanyabiashara wa kuuza simu na vifaa vya simu katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro aliyekamatwa kwa kukwepa kulipa kodi wakidaiwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa TRA.Mfanyabiashara huyo alikamatwa wakati wa ujio wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baada ya uchuguzi wa kina ilibainika kuwa kweli na kutozwa kodi ya Sh milioni 15 na uchunguzi dhidi yake ulikuwa bado unaendelea kwa kuangalia rekodi zake za nyuma.Kiasi kingine cha fedha kilichookolewa kilitoka Idara ya Elimu Sh 200,000 na Idara ya polisi kutoka wilaya ya Bukombe Sh milioni 1.1 na Sh 313,000 ziliokolewa kutoka wilayani Chato katika Idara za Elimu, Madini na Ardhi.Mbali na kuokoa fedha hizo Takukuru mkoa wa Geita imeanza kutekeleza kwa kasi uchunguzi wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ya kijamii kutoka mgodi wa Geita kupitia CSR ambapo tayari watu kadhaa wakiwemo watumishi wa GGM wamehojiwa. | kitaifa |
['Chelsea wanavutiwa kumsajili winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha mwezi huu lakini hawako tayari kufikia dau la pauni milioni 80 lililotajwa na klabu hiyo. (Express)', 'Manchester City wanawania kumsajili winga wa Wolves Mhispania Adama Traore, 23. (Calcio Mercato, via Manchester Evening News)', 'Wakala wa kiungo wa Barcelona na Chile Arturo Vidal, 32, atafanya mazungumza na Manchester United kuhusiana na uwezekano wa mchezaji huo kuhamia United mwezi huu. (Corriere Della Sera, via Mirror)', 'Aston Villa wako kwenye mawasiliano na Crystal Palace kuhusu kumrejesha mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 29. (Telegraph, via Birmingham Mail)', 'Villa wamepewa fursa ya kumsajili kipa mkongwe Pepe Reina, 37, kutoka AC Milan. (Mail)', 'Inter Milan inaripotiwa kumfuatilia nahodha wa Manchester United Ashley Young, 34. (Manchester Evening News)', 'Mario Gotze, ambaye alifunga goli la ushindi la Ujerumani katika fainali la kombe la dunia 2014 anajiandaa kuondoka katika klabu ya Borussia Dortmund kwa uhamisho huru pale mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Bild, via Mirror)', 'Newcastle wanavutiwa kumsajili winga wa zamani wa Liverpool, Ryan Babel kutoka Galatasaray. Klabu hiyo ya Uturuki imepanga kumuachia Mholanzi huyo mwezi huu huku klabu ya Ajax ipia ikimpigia hesabu. (Express)', 'Kocha Ole Gunnar Solskjaer amesema wachezaji wengi wa Man United wanacheza kwa ajili ya kesho yao. Kiungo wa England Jesse Lingard, 27 amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake pamoja na kiungo Mserbia Nemanja Matic. Beki wa Mholanzi Timothy Fosu-Mensah, 22 na beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 25 watamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)', 'Everton inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Juventus mfaransa Adrien Rabiot, 24 mpaka mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)', 'Mshambuliaji wa Ujerumani Leroy Sane, 23, anakaribia kurejea kwenye mazoezi ya Manchester City baada ya kuwa nje kwa miezi mitano akiunguza majeraha. (Manchester Evening News)', 'Napoli wanavutiwa na mshambuliaji wa Brighton mfaransa Neal Maupay 23. (Telegraph) '] | michezo |
Hayo yalisemwa Mke wa Mbunge wa Mkuranga, Naima Malima wakati wa kuwapokea wageni kutoka India, ambao ni Chama cha Wanawake Waliojiajiri (SEWA) waliotembelea kikundi cha Kiwalani Women Group.Naima alisema imefika wakati sasa kwa vikundi hivyo, kutafuta masoko mbalimbali yakiwemo ya Kimataifa.“Ni vema mtumie fursa za ujio wa wageni kama hawa, kutangaza bidhaa zenu ili muweze kupata fusra za kuuza nje kwani ubora wa bidhaa zenu ndiyo utawapatia masoko ya nje,” alisema.Alitaka vikundi hivyo kushirikiana, kwani hata wageni wao miaka ya nyuma walikuwa kama wao, lakini kutokana na ushirikiano wameweza kufikia hatua kubwa.Mwenyekiti wa kikundi hicho, Rehema Ngelekele alisema lengo la kuundwa kikundi hicho ni kujiinua kiuchumi kwa kufanya shughuli za ujasiriamali.Ngelekele alisema kuwa kikundi chao kilianzishwa mwaka 2000 ambapo wamepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba, kununua viwanja na mashamba na kusomesha watoto na kusaidia wajane na yatima.Kiongozi wa wageni hao, Shree Kumar alisema lengo la kuja Tanzania ni kuangalia jinsi vikundi vya wanawake vinavyoshiriki katika kujikwamua kiuchumi.Kumar alisema baada ya kutembelea kikundi hicho, wameridhishwa na jitihada zinazofanywa na wanawake wa Tanzania na kuwataka waendelee kujishughulisha.Akizungumzia juu ya ujio wa wageni hao, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mahoteli, Hifadhi na Majumbani (CHODAWU), Said Wamba alisema wamekuja kwa lengo la kukutana na vikundi vya wajasiriamali wanawake. | uchumi |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kutopeleka magari ya Serikali kwenye karakana binafsi kwani Wakala unajitosheleza kwa kuwa na wataalamu na vifaa vya kutosha.Kamwelwe, amesisitiza kwa Wakala huo kuhakikisha unatengeneza magari kwa bei nafuu na muda na mfupi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja wao.Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine alikagua vitendea kazi vya kisasa vilivyofungwa katika karakana ya MT. Depot iliyopo jijini hapo."Ninyi ni taasisi ya Serikali fanyeni vitu viwe nafuu na mtengeneze kwa viwango ili watu wafurahie huduma zenu", amesisitiza Waziri Kamwelwe.Aidha, ametoa wito kwa Wakala huo kutoa ushauri wa magari ya Serikali kwa umahiri na weledi na kutokubali kutengeneza magari ya Serikali endapo gari hilo litaonekana gharama yake ni sawa na kununua gari nyingine. Waziri Kamwelwe ameupongeza Wakala huo kwa kupunguza gharama za kutengeneza taa za barabarani ambazo zinatumia mfumo wa dakika."Wakala umetumia kiasi cha shilingi milioni 150 katika kitengeneza taa hizo badala ya milioni 250 na tayari zimeanza kufungwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro" amesema Waziri Kamwelwe.katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2019/20 Waziri Kamwelwe amefafanua kuwa Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua boti za uokoaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi katika visiwa vya Ukerewe (Ilugwa, Nafuba na Gana).Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TEMESA kwa Waziri huyo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Japhet Masele, amemueleza kuwa Wakala umejipanga kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20 kuanzisha karakana katika ngazi za Wilaya ikiwemo Wilaya ya Kahama, Simanjiro, Same, na Chato lengo likiwa ni kupeleka huduma karibu na wateja hasa kwa walio mbali na karakana za mikoa.Ameendelea kueleza kuwa hadi sasa Wakala umeshafanya uwekezaji wa shilingi bilioni 66 kwa ajili ya kununua vivuko 18 na hivyo kufanya kufikia jumla ya vivuko 31 na boti ndogo tano hapa nchini.Kuhusu kukamilisha ujenzi wa vivuko nchini Masele amesema kuwa tayari wakala umekamilisha ujenzi wa kivuko kipya cha MV Mwanza kinachotoa huduma eneo la kigongo-Busisi, ujenzi wa miundombinu katika kivuko cha Lindi Kitunda na inaendelea kukamilisha ujenzi wa Kivuko cha Kayenze- Bezi kitakachotoa huduma kati ya Kayenze na kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza.Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ulianzishwa chini ya sheria ya Wakala Na.30 ya mwaka 1997 ikiwa na majukumu ya kufanya matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali, matengenezo ya usimikaji wa mifumo ya umeme, uendeshaji wa vivuko vya Serikali, utoaji huduma za ukodishaji wa mitambo ya Serikali, kufanya usanifu na usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa mitambo, umeme na elektroniki. | kitaifa |
VIJANA wawili wa Kitanzania, Zakaria Sheha Ally na Shamsi Mwalimu Said wamechukua nafasi ya kwanza na ya tatu kwenye fainali za 27 za tuzo ya kimataifa ya kuhifadhi Kurani tukufu.Zakaria Sheha Ally (16) kutoka Tanzania Bara na Shamsi Mwalimu Said (19) kutoka Zanzibar wameibuka na kitita cha Dola za Marekani 5,000 na dola 3,000 kila mmoja baada ya kuwashinda wenzao wanane waliofanikiwa kuingia fainali hizo.Walioingia fainali hizo walitokea katika nchi za Afrika Kusini, Sudan, Malaysia, Uturuki, Yemen, Kenya, Burundi na Uingereza. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Gaffari Mohammed (14) kutoka Uingereza ambaye ameibuka na kitita cha dola za Marekani 4,000.Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Kurani Tanzania, mwaka huu yalishirikisha vijana 10 kutoka nchi 10 duniani. Tuzo hizo zilitolewa jana wakati wa kilele cha mashindano ya 27 ya Kimataifa ya Kuhifadhi na Kusoma Kurani tukufu na utoaji tuzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.Akizungumza na mamia ya waumini wa Kiislamu waliofurika kushuhudia kilele cha Tuzo ya Kimataifa ya Kurani iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Kurani nchini, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kuhifadhisha Kurani kunapaswa kuwa msingi imara katika kujenga jamii bora.Aliwataka wazazi wa Kiislamu wahakikishe wanawasimamia vyema watoto wao na kuwahifadhisha Kurani badala ya kutoa msukumo pekee kwenye elimu ya kimazingira.“Sote ni mashahidi kwamba vijana wetu wanao uwezo wa kuhifadhi Kurani na wakati huohuo wakasoma na kuhitimu fani mbalimbali katika elimu ya mazingira,” alieleza. Alisema mafanikio ya duniani na ahera hayapatikani kwingine isipokuwa ni kupitia Kurani.“Hivyo basi, tuwafunze Kurani vijana wetu ili waweze kukabiliana na changamoto nyingi zinazoibuka kwenye ulimwengu wa sasa hususan suala zima la mmomonyoko mkubwa wa maadili.”Alisema njia mojawapo ya kuwasaidia vijana kukabiliana na hali ya sasa ya dunia ya utandawazi ni kuwasomesha na kuwahifadhisha Kurani.“Vijana waliosoma na kuihifadhi Kurani ni vigumu kwenda kinyume na maadili kwani Kurani ndiyo njia pekee ya kuwachunga na kuwafanya waonyeke dhidi ya vitendo vinavyokwenda kinyume na uadilifu.”Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliipongeza Jumuiya ya Kuhifadhi Kurani nchini kwa kuendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mwongozo na msingi wa maisha yao kupitia Kurani kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanawaongezea vijana hao uelewa sahihi wa dini yao na elimu ya kutosha ya mazingira. | kitaifa |
KIKOSI cha Klabu ya Yanga SC, kimeondoka jana kwa ndege kwenda mkoani Shinyanga kuwakabili Mwadui FC kesho, kwenye Uwanja wa CCM, Kambarage katika muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Timu hiyo imeondoka siku moja baada ya kuwasili kutoka mkoani Lindi, ambako ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.Katika mchezo huo vigogo hao walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 katika Uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa. Yanga ina wachezaji wake wote inaowategemea, wakiwemo wale wa timu ya Taifa Stars waliokuwa nchini Lesotho kucheza mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019, ambako walifungwa 1-0. Timu hiyo inaenda kuwakabili wapinzani wao hao katika mchezo wao wa 11 tangu msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara uanze ambapo hadi sasa timu hiyo haijafungwa hata mchezo mmoja.Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera amesharejea nchini kutoka kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alikoenda kwa majukumu ya kuinoa timu ya taifa hilo kwenye michezo ya kufuzu Afcon mwakani. Hata hivyo kocha huyo bado yupo Dar es Salaam kwa mapumziko na ataungana na kikosi hicho leo tayari kwa mpambano huo wa kesho.Yanga inaenda kucheza mchezo wake wa kwanza ugenini tangu msimu uanze, ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ndanda FC mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Wakati huo Mwadui atacheza mchezo huo akiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika uwanja wake wa nyumbani.Ligi hiyo itaendelea leo kwa michezo mbalimbali kuchezwa katika viwanja tofauti baada ya kusimama kwa muda kupisha michezo iliyopo kwenye kalenda ya FIFA na michezo ya kufuzu michuano ya Afcon mwakani Cameroon. Wakati huo huo, Simba Sports inatarajiwa kuikaribisha Lipuli FC Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Kwa upande wake kocha wa kikosi cha Lipuli, Selemani Matola alisema kikosi cha timu hiyo kimejiandaa vyema kuwakabili mabingwa hao watetezi na kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu. “Katika kipindi hiki kifupi cha mapumziko nilikuwa nafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita, ingawa katika mchezo wetu dhidi ya wapinzani wetu nitawakosa wachezaji Paul Ngalema, Malimi Busungu na wamesema hawatarejea kwenye kikosi kwa sababu wana madai na klabu,” alisema. | michezo |
['Kuna uwezekano Manchester United ikashuka daraja msimu huu, kwa mujibu wa kocha wa zamani wa England, Sam Allardyce. (Talksport)', 'Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafutwa kazi endapo timu yake itafungwa na Norwich mwishoni mwa mwezi, ripoti zinaeleza. (Sun)', 'Hata hivyo, vyanzo vingine vinaarifu kuwa uongozi Man United upo tayari kumvumilia na kumpa muda zaidi Solskjaer wa kufanya mageuzi klabuni, licha ya kiwango kibovu cha matokeo ya mwanzo wa msimu kwa miaka 30. (Telegraph)', 'United wanapanga kuwasajili kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 20, na beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, bila kujali mustakabali wa Solskjaer. (Goal) ', 'Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino napanga kuwauza wachezaji kadhaa wa klabu hiyo baada ya kuanza msimu kwa kiwango kibovu. Wachezaji watakaowekwa sokoni mwezi Januari ni; Eric Dier, 25, Christian Eriksen, 27, Serge Aurier, 26, Victor Wanyama, 28, pamoja na Danny Rose, 29. (Times - subscription required)', 'Kocha David Moyes yupo tayari kurudi kuifunza klabu yake ya zamani ya Everton, katika kipindi ambaco kocha wa sasa Marco Silva akiwa katika shinikizo kubwa baada ya timu hiyo kuwa chini ya mstari wa kushuka daraja. (Mirror)', 'Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni ili 22 wamsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, ambaye yupo kwa mkopo Palace toka Januari mwaka huu. (Express)', "Kiungo wa Arsenal Dani Ceballos, 23, amesema alaifanya uamuzi sahihi kujiunga na 'the Gunners' kwa mkopo akitokea Real Madrid baada ya kuitwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania. (Goal)", 'Klabu ya Barcelona itampatia kipa wake Mjerumani Marc-Andre ter Stegen, 27, mkataba wa muda mrefu hivi karibuni. (Marca)', 'Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Kevin Phillips anataka kuchukua nafasi ya ukocha wa timu hiyo baada kufutwa kazi kwa kocha Jack Ross. (Star)', 'Borussia Dortmund wameungana na Arsenal, Juventus na Paris St-Germain katika kufuatilia maendeleo ya winga kinda wa Celtic ya Uskochi, Karamoko Dembele, mwenye miaka 16. (Bild - in German)', 'Mshambuliaji raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, amesema hakuwa na mpango wa kuondoka Juventus msimu huu licha ya kuhusishwa na uhamisho kuelekea vilabu vya Manchester United na Tottenham. (Tuttosport - in Italian)', "Lyon inatarajiwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc baada ya kumtimua kazi Sylvinho. (L'Equipe - in French)", 'Beki wa kati wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, amekasirishwa vikali na kura ya maoni iliyoendeshwa na gazeti la Uhispania la Marca ambapo ametajwa kuwa beki namba mbili mbovu zaidi duniani baada ya Phil Jones wa Man United. ', 'Ushiriki wa klabu za Ligi ya Primia ya England katika michuano ya Champions League utapunguzwa kutoka timu nne zinazofuzu moja kwa moja mpaka timu tatu, chini ya mapendekezo mapya ya kanuni za mashindano. (Mail)'] | michezo |
Rais John Magufuli amewataka wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Teknolojia Mbeya (MUST), Mzumbe na Saint Augustine (SAUT) kutekeleza majukumu yao kwa haki na kutumia muda ipasavyo.Akizungumza wananchi na Jumuiya ya wanataaluma wa vyuo hicho, Rais amesema wanafunzi wanapoteza muda wao mwingi kwa mambo ambayo hayawasaidii katika masomo.Rais Magufuli ameeleza hayo katika Chuo cha must baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa maabara ya chuo hicho, jijini Mbeya, leo, Ijumaa.Amewaonya madhara ya kuendekeza ngono vyuoni kwani mbali na kufeli masomo, wanakuwa hatarini kupata magonjwa ya zina na Ukimwi. “Nawahusia wanangu, mshinde shetani.Najua majaribu ni makubwa…inabidi niwaambie najua hamjazoea hilo,” alisisitiza Rais Magufuli. Hata hivyo, amewataka wahadhiri kutenda haki kwa kutowakosesha wanafunzi maksi wanazostahili ili wafeli.“Walimu mtende haki kwa wanafunzi…msije kuwanyima maksi ili mbembelezwe….mtabembelezwa na wangapi,” Rais alihoji huku wanafunzi wakionekana kufurahia.Rais amehitimisha ziara yake ya siku tisa mkoani Mbeya baada ya kuzungumza na wananchi na kuzindua miradi ya maendeleo huku akiwawataka viongozi kutenga siku maalum ya kutatua kero zinazowagusa wananchi moja kwa moja. | kitaifa |
Mkurugenzi Mkuu wa ATCl, Ladislaus Matindi amesema wamejipanga vizuri ili kujitanua kibiashara na kurudi katika mfumo wa kimataifa wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Ndege (IATA).Amesema ATCL iliondolewa katika mfumo wa kimataifa wa utoaji wa huduma na ununuzi wa tiketi kwa kukabiliwa na madeni makubwa.Kwa mujibu wa Matindi, madeni ambayo yaliitia hasara kubwa ATCL yalitokana na udanganyifu wa mikataba ya huduma, manunuzi na ukodishwaji wa ndege.Amesema kitendo cha kutia saini na kampuni hiyo maana yake sasa ATCL itarudi tena katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kwa kutumia mgongo wa kampuni hiyo inayoheshimika duniani.Matindi amesema, taratibu zote zimefuatwa katika makubaliano na watoaji wa huduma za ndege za kimataifa Hahn Air, ikiwemo kupata baraka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuridhia.Awali Makamu wa Rais wa kampuni hiyo, Steve Krackstedt amesema, wameingia mkataba na ATCL baada ya kuridhishwa na juhudi zake kujiimarisha ili kurudi mfumo wa kibiashara.Amesema kazi kubwa imefanywa na ATCL kuimarisha huduma zake ikiwemo kununua ndege mpya kwa ajili ya safari zake nchini na nje ya nchi ikionesha utayari kufanya biashara. | uchumi |
SERIKALI kwa sasa iko katika hatua ya kuchambua na kupitia upya muundo wa kifedha na kiuchumi, utakaotumika kwenye mikataba ya uchimbaji na utafutaji wa gesi ili kuweza kuinufaisha nchi.Aidha, serikali imebainisha kuwa imejiandaa na haina wasiwasi kwenye malipo ya Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rufiji.Akijibu hoja wakati wa kuhitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Aderaldus Kilangi alisema hatua hiyo imetokana na kubaini upungufu uliokuwepo ndani ya mikataba hiyo baada ya serikali kupitia upya.“Hatua ya kuchambua muundo ni katika kutekeleza mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuchunguza namna taifa inavyoweza kunufaika kwenye sekta ndogo ya gesi na uvuvi,” alisema.Dk Kilangi alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (CCM), kuhusu sababu ya serikali kutotoa leseni mpya za uchimbaji na utafutaji gesi.“Moja ya mapendekezo ya kamati uliyoiunda (Spika Ndugai) kuchunguza sekta ndogo ya gesi na uvuvi, ni kurejea mikataba ya utafutaji na uchimbaji na kazi hiyo ikapewa ofisi ya AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali). Tulianza kazi kuipitia mikataba yote, tukaunda timu kutoka wizara na sekta mbalimbali za serikali,” alisema.Dk Kilangi alisema kuwa ofisi yake ililazimu kuijengea uwezo timu hiyo baada ya kupitia mikataba yote 11 ya utafiti na uchimbaji gesi.“Tuligundua kuna kitu muhimu kukiangalia ambacho ni “Economic and Financially Modeling (muundo wa kiuchumi na kifedha). Siri nzima ipo hapo kama tunapata au kupoteza, hivyo tukaja na awamu nyingine ili ifanye kazi kwa mwezi mmoja.“Tulichokifanya ilikuwa kuangalia muundo gani wa kifedha na kiuchumi uliotumika ikagundulika lazima kama nchi kuangalia inapendekeza mfumo upi ambapo kazi hiyo itafanyika kuanzia Juni 6 hadi 25 mwaka huu,” alisema. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema serikali imejiandaa na haina wasiwasi kwenye malipo ya mradi wa kuzalisha umeme wa mradi wa Rufiji.“Tumeshalipa Sh bilioni 723. Si kama tumefanya makosa hapana. Serikali ilikuwa inafahamu kuwa bajeti iliyopitishwa ni Sh bilioni 700 kamili. Tumefanya hivyo kwa sababu ya umuhimu wa mradi huu.“Kuhusu na hizo Sh bilioni 28 zinazodaiwa kutolewa bila ridhaa ya bunge, mamlaka ya kufanya uamuzi wa kuhamisha mafungu ni ya Waziri wa Fedha na Mipango. Unapokuwa na jukumu la msingi ambalo halipaswi kusubiri yapo mamlaka kwa waziri ambaye alihamisha fedha kutoka fungu 21 hazina kwenda fungu 58,” alisema.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mussa Sima alisema Mradi wa Kuzalisha Umeme kwenye Mto Rufiji, una umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa nchi.Alisema madai kuwa utekelezaji mradi huo, utavunja mkataba wa mbuga ya Selous kuwa urithi wa dunia si kweli, bali mkataba ulikuwa tayari. | uchumi |
UONGOZI wa timu ya soka ya Yanga umesema hauna mpango wa kubadilisha kikosi chake katika mchezo wao na Azam FC ambao utachezwa leo usiku kuanzia saa 2:15 wa Kombe la Mapinduzi Timu hizo zinakutana leo katika dimba la Amaan, Azam inashuka ikiwa na pointi moja baada ya mchezo wake wa kwanza kutoka sare na Jamhuri na Yanga wana pointi tatu kufuatia kushinda katika mchezo wake wa juzi na timu ya KVZ na kuongoza Kundi A, ambalo linaundwa na timu hizo.Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub Cannavaro alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo dhidi ya KVZ na kushinda bao 1-0. Alisema kuwa kikosi ambacho wamekuja nacho kwenye mashindano hayo ndio hicho hicho watakachokichezesha kwa michezo yote ya michuano hiyo. Hata hivyo alisema kuwa hicho wanakiamini sana na ana uhakika wa lufanya vizuri katika mashindano hayo ya Mapinduzi na hata katika mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC.“Tunakiamini kikosi chetu hichi na ndicho tutakachokitumia kwa mechi zote hatuna mpango wa kuongeza wachezaji wengine kwa kuwa tunacheza na Azam”, alisema. Aidha alisema kuwa timu ya Azam wanaifahamu kutokana na kwamba wameshakutana mara nyingi katika ligi na kuwaahidi mashaki wao kutokuwa na wasiwasi wowte na wakiamini kikosi chao.“Mpira ni dakika 90, kuwa na wachezaji wazuri haimaanishi ndio washindi na ndani ya dakika hizo lolote linaweza kutokea lakini tunajiandaa kwa ajili ya ushindani na kushinda”, alisema Canavaro. Hii ni mara ya pili kwa timu hiyo kuleta kikosi B katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo mwaka mmoja iliwaleta na kuondolewa mapema kwenye michuano hiyo. | michezo |
KAMPENI ya kuwastiri Watoto wa kike kupata nguo za ndani (chupi na sidiria), imezinduliwa jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia watoto 1,000 wa mkoani Lindi na Arusha hususani wilayani Karatu.Kampeni hiyo ya siku 40 inaendeshwa na mradi wa Girls in Action Initiative iliopo chini ya Kampuni ya Christom Solution.Akizungumza na wandishi wa habari leo Ijumaa, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Miriam Lukindo alisema walifanya utafiti katika mkoa wa Lindi na Karatu kubaini changamoto zinazowakabili Watoto wa kike ukiachilia ile ya taulo maalum ‘Pads’.Lukindo alisema kuwa utafiti huo walifanya kwenye baadhi ya shule za msingi mbali na kugawa taulo lakini walibaini kuna changamoto kubwa ya Watoto kukosa nguo za ndani.‘Karatu kuna shule tulizotembelea, kati ya watoto 400, watoto wawili tu ndio wamevaa nguo za ndani, wengine wote hawana nguo za ndani, ni changamoto kubwa.“Changamoto zaidi inawakabili pale ambapo wanaingia kwenye siku sawa, kuna mmoja alituambia yeye anatumia gunzi la mahindi kujistiri kipindi cha hedhi.“Anachofanya anachukua pads, anaiweka juu ya gunzi kisha anajiweka huko chini na kuibana na miguu yake, kwa hiyo kipindi cha hedhi mabinti wengi hawaendi shule na hii inawafanya washuke kimasomo.Naye mhamasishaji katika kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘Sadaka Ghandi ‘Ant Sadaka’ alisema baadhi ya watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 15 hawapendi miili yao kutokana na changamoto zinazowakabili kiasi cha kuwafanya washindwe kujiamini.“Tuwakoe watoto kupata vishawishi vya kupewa pewa pesa ili wakidhi mahitaji yao, changamoto kwa watoto wengi vijiji ni nguo za ndani na taulo za kike, tuungane kwa pamaja katika kampeni hii kwa kuchangia shilingi 1,000 tu kwenye namba 0677 069428,” alisema Sadaka. | kitaifa |
NYUMBA 336 katika vijiji vya Kipeta na Kilyamatundu Kata ya Kipenta katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, zimebomoka na zingine kuezuliwa paa na kuta baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha kwa takribani dakika 45.Aidha, mkazi wa kijiji cha Kipeta, Elizabeth Manamba (85) amepoteza maisha baada ya kuta za nyumba alimokuwa amelala kumwangukia na kumuumiza vibaya kifuani huku watu 50 wakiwa wamejeruhiwa na kutibiwa katika Kituo cha Afya Kilyamatundu.Miongoni mwa waliojeruhiwa ni Ofisa Tarafa wa Kipeta, Jacob Nkungwe na mkewe, huku kuta za nyumba waliokuwa wakiishi zimeanguka na paa kuezuliwa. Mvua hiyo ilileta madhara makubwa katika Shule ya Sekondari Kipeta kwa kubomoa vyumba vitano vya madarasa, ofisi ya walimu, mabweni mawili nyumba moja ya mwalimu na vyoo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo. Alisema mvua hiyo ilianza saa tano usiku juzi na kudumu kwa saa 45. Akizungumzia tukio hilo, Mganga wa Kituo cha Afya Kilyamatundu, Neema Nyondo alisema usiku huo wa tukio, majeruhi wapatao 36 walipokewa kituoni hapo kwa matibabu huku baadhi yao wakiwa wamevunjika mikono, mbavu na miguu.Akimzungumzia marehemu Elizabeth Manamba, Nyondo alisema usiku huo alifikishwa katika kituo hicho akiwa amepoteza fahamu, baada ya kujeruhiwa vibaya kifuani kwa kuangukiwa na kuta za nyumba yake.Ndugu wa karibu wa marehemu, walidai kuwa wauguzi wa Kituo cha Afya Kilyamatundu waliwashauri wamkimbize mgonjwa wao Hospitali ya Kamsamba iliyopo wilaya ya Momba mkoa wa Songwe kwa matibabu zaidi, lakini wao waliamua kurejea naye nyumbani, ambapo alifariki dunia usiku huo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Kalolo Ntila alisema hasara iliyosababishwa na mvua hiyo, haijafahamika na kwamba timu ya wataalamu itatumwa kufanya tathmini.Ofisa Mtendaji, January Ninde aliwataka wananchi wawahifadhi waathirika katika nyumba zao na kuwapatia msaada wa hali na mali, ikiwemo chakula na malazi. Baadhi ya waathirika walilieleza gazeti hili kuwa usiku huo wa tukio, walijaribu kujibanza uvunguni mwa vitanda ili kujiokoa, kutokana na mvua hiyo kuwa kubwa na upepo mkali. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfany Haule na kamati ya ulinzi na usalama, jana walitembelea kata ya Kipeta ili kujionea wenyewe athari iliyosababishwa na mvua hiyo na kuwapa pole waathirika. | kitaifa |
Hayo yalisemwa Mjini hapa jana na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Vicoba cha watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu.Alisema wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa kwani mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa katika mikoa mingi hapa nchini.Alisema mafanikio hayo yanatokana na ushirikishwaji katika kuanzisha na kusimamia vikundi jambo ambalo limewavutia wananchi wengi.Mama Pinda alisema anatumaini kuwa vicoba wataendelea kuimarisha mfumo wa kuanzisha vikundi vipya, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uongozi, kibenki na mbinu mbalimbali za kibiashara, kimaisha na nidhamu ya kutumia fedha.Alisema licha ya Vicoba kukabiliwa na changamoto mbalimbali ni muhimu kwa uongozi kuhakikisha kunakuwa na tahadhari za mapema ili vikundi viwe salama.Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kuibuka kwa wadau wasiofuata kanuni za Vicoba, namna ya kutunza kumbukumbu, gharama za uendeshaji ofisi, miundo tofauti ya taasisi zinazojihusisha na jamii na ukosefu wa fedha za kutathimini mpango.Akisoma risala ya kikundi cha Vicoba, Lucy Rutahinirwa alisema kikundi hicho kilianzishwa Septemba 13, mwaka jana na sasa kina wanachama 60 ambapo kati yao wanawake ni 46 na wanaume ni 14.Alisema wanachama wa kikundi hicho wameweza kununua hisa zenye thamani ya Sh milioni 13.6 ambao ndiyo mtaji katika kutimiza lengo la kujiimarisha kiuchumi jumla ya wanachama 48 wamekopeshwa mkopo unaofikia Sh milioni 22.5 na marejesho ya mkopo yanaendelea vizuri.Alisema lengo la kikundi hicho ni kuona wanachama wanaongeza hisa ili kuwa na mtaji mkubwa zaidi wa kuendesha kikundi.“Bado tunaendelea kushawishi watumishi wenzetu nchi nzima ambao sio wanachama kujiunga na Vicoba kama njia ya kuongeza kipato na kuwajengea wafanyakazi uwezo mkubwa wa kujiimarisha zaidi kiuchumi kwa kupewa mikopo yenye masharti nafuu,” alisema.Katika uzinduzi huo, jumla ya Sh milioni 18 zikiwa ni ahadi na fedha taslimu zilipatikana ambapo mke wa Waziri Mkuu aliahidi kutoa Sh milioni tano na Rais wa Vicoba Tanzania Devota Likokola aliahidi kutoa Sh milioni mbili. | uchumi |
BAADA ya kupoteza pointi nne kwenye michezo miwili iliyopita vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameapa kufi a uwanjani kusaka pointi tatu muhimu kwenye mechi dhidi ya African Lyon itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.Mchezo huo wa 30 kwa Yanga ambayo inaongoza ligi hiyo kwa pointi 68 baada ya kucheza mechi 29, inahitaji ili kujiongezea pointi baada ya hivi karibuni kutoka sare ya 1-1 na Ndanda FC mjini Mtwara.Timu hiyo pia bado ina machungu ya kufungwa 1-0 na wana Kamwene, Lipuli ya Iringa katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora hivi karibuni, hivyo inahitaji ushindi ili kurejesha matumaini katika mbio za ubingwa.Yanga katika mechi mbili dhidi ya Lipuli na Ndanda, imepoteza jumla ya pointi nne, hivyo ni jukumu lake sasa kuhakikisha inashinda katika mchezo huo wa leo.Hadi sasa bado vinara hao wana presha kubwa kutokana na mwenendo huo wa kusuasua kupata matokeo huku Azam FC ambao wanashika nafasi ya pili kwa pointi 62 wakiwa wamecheza michezo sawa na Yanga wamekuwa na muendelezo mzuri wa kupata matokeo chanya.Mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba wanaoshika nafasi ya tatu kwa pointi 57 wakicheza mechi 22, wenyewe ndio wanaonekana kuwa tishio zaidi kwa Yanga baada ya kushinda kila mechi zote hivi karibuni na kuwa na viporo vingi.Kuelekea kwenye mchezo huo kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema hawana jambo jingine zaidi ya kufikiria kupambana na kushinda na kuondoka na pointi zote tatu.“Tumefanya makosa kwenye michezo iliyopita hatuna kingine zaidi ya kupambana muda wote kutafuta pointi tatu zitakazotuongezea ari ya kuendelea kupambana kwa michezo iliyo mbele yetu na kuendelea kubaki kileleni,” alisema Zahera.Hadi sasa Lyon wanashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 22 baada ya kucheza michezo 32 kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu, hawapewi nafasi kubwa ya kushinda kwani mwenendo wao sio mzuri.Huo ni mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kwa Yanga, tangu mabingwa hao wa zamani nchini wachague Uwanja wa CCM Kirumba kuwa uwanja wao wa nyumbani ili kupisha ule wa Taifa kuchezewa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, ambayo Tanzania ndio mwenyeji. | michezo |
Waziri huyo anaongoza ujumbe wa maofisa mbalimbali wa Serikali katika kukagua barabara kuu hususani mizani kutoka jijini Dar es Salaam-Tunduma hadi Mji wa Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).Barabara hiyo inatumiwa na magari ya mizigo ya wafanyabiashara wa DRC kutoka Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kwa kukagua maeneo ya mizani, serikali inataka kuondoa kero zinazosadikiwa kukumba wafanyabiashara katika usafirishaji.“Tanzania imebarikiwa kuzungukwa na nchi sita zisizo na bahari na tuna ukanda wa bahari wenye urefu zaidi ya kilometa 1500…lazima tutumie bahati hii kujiletea maendeleo,” aliwaambia waandishi wa habari baada ya kutembelea kituo cha kupimia magari cha Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani.Ziara ya ujumbe huo, ilianzia katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande alitoa taarifa fupi kwa Waziri huyo kuhusu shughuli bandarini hapo. Pia, ujumbe ulitembelea Kitengo cha kupakia na kupakua kontena (TICS) bandarini hapo.Maeneo mengine yaliyotembelewa ni pamoja na bandari za nchi kavu (ICDs) maeneo ya Kurasini na kushuhudia msongamano mkubwa wa malori ya mizigo katika njia hiyo. “Tunataka kubadilika, lazima tubadilike,” alisema Waziri Mwakyembe.Ujumbe huo unaosafiri kwa barabara kupata taarifa za moja kwa moja kutoka kwa wahusika, unajumuisha pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba pamoja na mjumbe wa kamati hiyo, Zarina Madabida.Akizungumza baada ya kukagua kituo cha mizani cha Mikese, Serukamba alisema wanataka kuangalia na kufahamu kila tatizo kwa kina hatimaye ufumbuzi wa kudumu upatikane.“Tuko katika ushindani mkubwa, lazima kama nchi tubadilike kwa haraka,” alisema Serukamba.Alitoa mfano wa kasoro zilizopo katika vituo vya kupima mizigo na kusema muda unaotumika kushughulikia gari moja ni mrefu na hivyo kupunguza ufanisi.Mwakyembe alisema kasoro hizo na nyingine, zitapatiwa ufumbuzi hivi karibuni kutokana na mikakati iliyopo. Ziara hiyo ya kikazi ya zaidi ya kilometa 2,000, itahitimishwa kwa kufunguliwa kwa ofisi ya TPA Alhamisi wiki hii katika Mji wa Lubumbashi, ambayo ni moja ya mikakati ya kuongeza ufanisi wa bandari katika kuhudumia nchi jirani.Ujumbe huo unajumuisha pia maofisa waandamizi kutoka TPA na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra). Takwimu za hivi karibuni zinaonesha shehena yote ya mizigo ya nchi sita zitumiazo Bandari ya Dar es Salaam, yaani Zambia, D R Congo, Burundi, Rwanda, Malawi na Uganda, imeongezeka kutoka tani milioni 3.55 mwaka 2011/12 hadi kufikia tani milioni 4.05 mwaka 2102/13, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2. | uchumi |
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa kiwango chochote kwenye simu zao kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia.Kila siku wateja watakaoongeza salio wataingizwa kwenye droo ya “Airtel MKWANJIKA” ambapo washindi wanne wataibuliwa na kutakiwa kuingia katika sanduku la pesa la Airtel (Airtel Mkwanjuka Boksi) na kujikusanyia pesa hadi kiasi cha shilingi milioni moja ndani ya dakika moja.Akizindua promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Airtel, Anethy Muga alisema; ” tumezindua promosheni hii mwisho wa mwaka ili kuwezesha wateja wetu kujishindia zawadi zitakazobadili maisha yao katika msimu huu wa sikukuu.‘‘ Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja Uhusiano, Jackson Mmbando alisema wateja wanaotumia mtandao wa Airtel wanaongezeka kila siku, hivyo kuwataka kushiriki kwa wingi, akisisitiza promosheni hiyo ni kwa wateja wote wa Airtel, hakuna gharama ya ziada.“Washindi wote watakaopatikana wakati wote wa promosheni watapigiwa simu kwa namba 0683 442 244 na watapatiwa kiasi cha pesa alichoweza kujikusanya na kushinda kutoka kwenye kisanduku cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money, ” aliongeza Mmbando. Droo ya kwanza ya promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itafanyika Desemba 23 na nyingine nyingi zaidi kufanyika Januari 2016 na kuendelea. | uchumi |
Nchemba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki bungeni mjini hapa wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2015/16.Akijibu hoja hizo, ambazo nyingi zilitolewa na wabunge wa vyama vya upinzani wakisema serikali haijafanya chochote katika miradi ya maendeleo bali kilichoongezeka ni deni ya taifa, Nchemba alisema hata kama TRA na Halmashauri zote nchini zingekusanya mapato kwa asilimia 100, zingefikia asilimia 62 ya bajeti.“Kwanza watu wanaotazama bunge hili huko nje wakiwasikia hawa wanaosema serikali haijafanya chochote watawashangaa, wengi wanalalamika deni la taifa limeongezeka, ila miradi ya maendeleo iliyofanywa hawaioni…”,alisema Nchemba.Alifafanua, ikiwa TRA pekee ingekusanya mapato kwa asilimia 100 fedha hizo zingekuwa ni asilimia 57 ya bajeti na kwamba kama rais angeamua asikope taifa lingekuwa wapi hivi leo, hakuna nchi iliyotulazimisha kukopa,ila hiyo asilimia inayobaki ya bajeti ni lazima ipatikane kwa wahisani,” alisema Nchemba.Na kuwashangaa wabunge wa upinzani ambao wamekuwa wakibeza miradi mbalimbali na kusema kama wanapenda miradi iliyofanywa ni lazima wapende na deni lililopo.“Hivi unalipendaji jengo la bunge tunalokaa humu ndani ambalo tumelijenga kwa mkopo halafu usiupende mkopo wenyewe, utakipendaje Chuo Kikuu cha UDOM, kilichojengwa kwa mkopo alafu usipende deni lake”, hivyo hivyo kwa miradi ya barabara, umapita kwenye barabara nzuri halafu hampendi madeni yake,” alihoji Nchemba.Na kusema miradi ipatayo 360 iliyotekelezwa nchini imekamilika na mingine iko kwenye hatua za mwisho kutokana na fedha za mikopo kutoka kwa wahisani wa maendeleo, na kwamba hata reli ambayo inagharimu Sh trilioni 15 ni fedha za mkopo.“Ni vyema tukatimiza wajibu wetu, na ni heri aliyechoka kwa kufanya kazi kuliko yule mvivu aliyechoka kwa kutotambua kazi zilizofanywa,” alisisitiza Nchemba.Na kusema deni la nchi lililofikia takribani Trilioni 30, Nchemba alisema bado linalipika kwani kuna viashiria vyote vinavyoonesha ulipikaji wake na kwamba nchi haiwezi kuendelea bila kuwa na mikopo.“Tumekopa nchi mbalimbali, India, China, Japan na nchi nyingine na fedha zimetumika kwenye miradi ya maendeleo na leo mmeona mafanikio yake , kuna mtandao wa barabara za lami ambao umerahisisha usafiri kwa wananchi na kuokoa muda. | uchumi |
Akiwa kwenye mabaki ya iliyokuwa nyumba yao miaka takribani tisa iliyopita, bado ni mahala anapoishi na kupata usingizi wake. Lakini Salah Jaar mwenye umri wa miaka 32 sasa, hayuko peke yake.Pembeni mwake kuna nusu dazani ya paka ambao huchangia kumpa faraja kwamba bado kuna uhai wa watu na viumbe wengine katika mji huo.“Inanifariji wakati paka wanapokuwa karibu yangu,” anasema. “Inanifanya nione mabomu, uharibifu wa nyumba, mateso na athari zake kuonekana siyo za kutisha sana,” anasema.Mji huo wa Kafr Nabl, ambao amezaliwa na kukulia, Salah anasema ulikuwa na wakazi zaidi ya 40,000, lakini kwa sasa kuna wakazi chini ya 100 waliobaki. Wakati idadi ya watu ikiwa kidogo hivyo, paka wanakadiriwa kuwa mamia kadhaa kama si maelfu.“Watu wengi wameikimbia Kafr Nabl au kuuawa kiasi kwamba idadi ya watu sasa ni ndogo sana. Paka wanahitaji watu wa kuwajali na kuwapa chakula, maji na matunzo mengine kwa hiyo wengi wamehamia kwenye nyumba ambazo bado zina watu wachache. Kila nyumba sasa ina paka takriban 15, wakati mwingine hata zaidi,” anasema Salah.Salah bado anafanya kazi kama mwandishi wa habari wa kituo cha redio cha Fresh FM. Ingawa studio zao za awali zimepungua ukubwa baada ya kulipuliwa kwa bomu katika mapambano ya angani, lakini kwa bahati nzuri shughuli za kituo zilikuwa zimehamishwa siku chache kabla ya bomu hilo na hivyo kusalimika. Kituo hicho cha redio, ambacho kimekuwa kikitangaza maonyo kuhusu uvamizi, kuhubiri umuhimu wa amani na programu za habari, ucheshi na simu, nacho kimekuwa makazi ya paka pia waliohamia hapo.Mwanzilishi wa redio hiyo, Raed Fares, kabla kuuliwa na waasi Novemba mwaka 2018, alitenga kiasi maalumu cha fedha kwa ajili ya kuwanunulia paka maziwa na jibini, hatua inayoendelezwa na warithi wake hadi sasa. “Paka wengi walizaliwa katika jengo hilo la redio. Mmoja wao, ambaye alikuwa mweupe na madoa ya hudhurungi, aliendeleza uhusiano maalumu na Raed.Angeenda kila mahali pamoja naye na hata kulala karibu yake,” Salah anasema. “Wakati mwingine tunapotembea mitaani utaona karibu paka 20 mpaka 30 wakitufuata. Wengine wao huja nyumbani na sisi.”Anasema chochote wanachokula binadamu paka hao waliojikuta na hali ngumu kwa kuwa hawawezi kukimbia mji huo kama wanavyofanya wanafdamu wengi, pia hulazimika kula; iwe mikate, mbogamboga na kadhalika.Anasema ingawa hata paka hufa na kujeruhiwa na mabomu, lakini wanaosalimika wengi hao kupatiwa makazi na hata matibabu ingawa matibau hata kwa binadamu ni taabu pia katika mji huo. Na vikosi vya Rais Bashar al-Assad vikiwa karibu kuuchukua mji wa Kafr Nabl, Salah anakiri kuwa na wasiwasi, sio wa yeye mwenyewe na marafiki zake, bali pia paka wa mji huo ambao wanazidi kubaki ‘yatima’. | michezo |
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesitisha likizo zote za watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari.Mndeme ametoa agizo hilo wakati wa kikao na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vyumba vipya 142 vikamilike kujengwa.Viongozi aliozuia likizo zao ni Katibu Tawala Mkoa, wakuu wote wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, Ofisa Elimu Mkoa na wale wa wilaya zote, pia wahandisi wa ujenzi wa halmashauri.“Nataka katika halmashauri zote zenye upungufu wa madarasa hakuna kiongozi kwenda likizo ya mwisho wa mwaka hadi madarasa mapya yakamilike kujengwa, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 waingie darasani ” amesema.Awali, akitoa taarifa fupi ya hali ya miundombinu ya madarasa, Katibu Tawala Mkoa, Profesa Riziki Shemdoe alisema jumla ya wanafunzi wapya 1,556 watahitaji madarasa mapya ya kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari.Aidha, Mndeme amezuia safari za mafunzo za madiwani wote katika halmashauri nane za Ruvuma hadi watoto wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hapo mwakani watakapoingia darasani. | kitaifa |
['Real Madrid itataka kumsaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen mwezi Januari.(Marca)', 'Real Madrid pia wanaisaka saini ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, 19 raia wa Norway Erling Haaland, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United. (AS)', 'Beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 26, amefichua kwamba alitaka kuondoka mjini London mwisho wa msimu uliopita na amekiri kwamba hajui hatma yake iko vipi katika klabu hiyo. (Football.London)', 'Aston Villa imehusishwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25. (Birmingham Mail)', 'Kazi ya Unai Emery kama mkufunzi Arsenal huenda ipo hatarani iwapo kikosi chake kitashindwa kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu . (Times - subscription required)', 'Mchezaji wa zamani wa Uingereza na nahodha David Beckham anamlenga mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kama mteja wake wa kwanza katika kazi yake mpya kama ajenti . (Mail)', 'Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Man United Mark Robins amesema kwamba ilikuwa rahisi kwake kukataa kuwa mkufunzi wa Sunderland na kuamua kutia saini kandarasi mpya na klabu ya Coventry. (talksport)', 'Ajenti mmoja raia wa Urusi anadai kwamba aliiomba klabu ya Zenit St - Petersburg kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexander Lacazette ambaye alikuwa anagharimu £61m . (mirror) ', 'Kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba ,26, anakaribia kupona jeraha tayari kucheza mechi dhidi ya Liverpool mnamo tarehe 20 mwezi Oktoba licha ya ripoti ya kuvunjika kidole. (sun) ', 'Man United inaweza kutarajia ufadhili wa shati utaokagharimu £450m huku wakisaka kandarasi mpya.(ESPN)', 'Kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Matty Longstaff , aliyefunga bao la ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Man United mwezi huu , kwa sasa analipwa £850 kwa wiki na klabu hiyo. (sun) ', 'Kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Jaoa Moutinho 33 anatarajiwa kukubali kuweka kandarasi mpya katika uwanja wa Molineux. (Birmingham Mail)', 'Wolves ina mpango wa kuimarika katikati ya safu ya ulinzi pamoja na safu ya katikati wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari (The Athletic, via Inside Futbol)', 'Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amemwambia Aliyekuwa mshambuliaji wa Sunderland Kevin Phillips kwamba heri anemsajili yeye badala ya Francis Jeffers. (Mirror)', 'Kiungo wa zamani wa Man United Marouane Fellaini, 31 raia wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya China ya Shandong Luneng, anasema kwamba Jose Mourinho hakupewa muda wa kutosha katika uwanja wa Old Trafford. (Mail)'] | michezo |
KUMEKUWA na ongezeko la mashauri ya migogoro ya ndoa katika kipindi cha miezi tisa kuanzia Julai, mwaka 2018 hadi Machi, mwaka huu, ambapo jumla ya mashauri 16,832 yameripotiwa ikilinganishwa na mashauri 13,282 katika kipindi cha mwaka 2017/18 ambayo ni sawa na asilimia 34.5.Mkurugenzi wa Idara ya Watoto, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Mwajuma Magwiza, alisema hayo juzi wakati wa hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya familia duniani yaliyofanyika kimkoa. Alisema katika familia nyingi nchini changamoto kubwa ambayo imekuwa ikizikabili ni kukithiri kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake.Alisema kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kuongezeka katika familia nyingi nchini huku watendaji wa matukio hayo wakiwa ni wanafamilia au watu wa karibu na watendewa wa ukatili huo. “Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi kwa mwaka 2017 zinaonesha jumla ya matukio ya ukatili 13,457 yameripotiwa ukiwemo ukatili wa kingono 3,583 na mimba za utotono 1,323,” alisema.Pia alisema taarifa hiyo inaonesha mikoa ya kipolisi yenye takwimu kubwa za ukatili ni Kinondoni (2,426), Dodoma (1,283), Tanga (1,064), Temeke (984) na Arusha (972). “Migogoro hiyo si tu inaathiri ukuaji wa familia, pia inachangia kurudu- sha nyuma maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla,” alisema. Aidha, alisema vitendo hivyo ambavyo kwa kiasi kikubwa vinatokana na mmomonyoko wa maadili kwa familia na kutokuwajibika kikamilifu kwa wazazi kunakosabaisha migogoro ya ndoa.Alitaja changamoto nyingine kuwa pamoja na kukosekana kwa usawa kunakoongeza migogoro katika familia zinapombana na kuondokana na umaskini. “Vijana walio katika balehe wanaoishi katika kaya maskini mara nyingine wanajiingiza katika hatari nje ya familia zao ili wapate vitu au yale wasiyoweza kuyapata nyumbani kwao,” alisema. Pi alisema kuhamahama kwa wazazi kunakosukumwa na mahitaji ya kiuchumi na sababu nyingine ambapo matokeo yake ni familia kuwa mbali na ndugu na matandao wa jadi wa kijamii pia huchangia familia kutokuwa na ubora wa kutimiza wajibu kikamilifu. | kitaifa |
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua shindano la uchoraji nchi nzima linalojulikana kama ‘Jiachie na Kili Canvas Competition 2020’ linalotarajiwa kufanyika Januari 22, Golden Tulip, Dar es Salaaam.Akizungumza jana Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema shindano hilo litashirikisha wachoraji kutoka nchi nzima na mshiriki atatakiwa kuja na kazi aliyochora kwenye kitambaa kigumu cha kuchorea kisichozidi sentimita 60 kwa sentimita 50.“Mchoraji anapaswa kutumia vitambulishi vya bia ya Kilimanjaro kumuongoza katika uchoraji. Vitambulishi hivyo ni Mlima Kilimanjaro, Twiga, nyota tano na michoro ya kiafrika iliyo kwenye lebo,” alisema Kikuli Pia alisema kazi zitapitiwa na kuchunjwa na majaji kupata washindi watano ambao watapewa nafasi ya kuchora papo hapo na mshindi atapata nafasi ya kuchora mchoro maalum ambao utatumika kuelekea kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon pamoja na pesa taslimu Sh milioni mbili.“Mashindano yanafanyika kwa ajili ya kutoa fursa kwa wachoraji ili waonyeshe kazi zao kwa jamii, kuibua vipaji vipya pamoja na kuongeza muamko wa tasnia ya uchoraji nchini,” alisema Kikuli.Aidha alisema shindano litafanyika ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mbio za Kilimanjaro Marathon 2020 ambazo hufanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro. Naye jaji mkuu wa shindano hilo, Nathan Mpangala, aliwaomba wachoraji kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo ambayo itawatangaza, kumkutanisha na watu mbalimbali, kuwajengea kujiamini na kuwapatia kipato.Mbali mshindi wa kwanza kupata Sh milioni mbili pia washindi wa pili hadi wa tano ataondoka na kifuta jasho cha Sh laki mbili kila mmoja. Pia kazi itakayoshinda itapelekwa kwenye mbio za Kili Marathon ambazo zitafanyika Machi 1, Viwanja vya Ushirika. | michezo |
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amechaguliwa bila kupingwa kuwa Rais wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) katika uchaguzi mkuu uliofanyika mjini Kampala, Uganda jana. Uchaguzi huo ulifanyika baada ya viongozi waliokuwepo kumaliza muda wao tangu mwezi uliopita.Karia ataongoza baraza hilo kwa miaka minne, akichukua mikoba iliyoachwa na rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Sudani (SFA) Mutasim Gafaar aliyemaliza muda wake. Katika uchaguzi huo, makamu wa kwanza wa rais amechaguliwa Francis Amin kutoka Sudan Kusini na makamu wa rais wa pili ni Esayas Jiro wa Ethiopia.Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Karia alisema mambo atakayofanyia kazi ni pamoja na suala la udhamini.“Tutajipanga ili kupata wadhamini lakini hawawezi kuja hivi hivi bila sisi wenyewe kuwa wawazi na kuwajibika kuwa waadilifu na kuhakikisha kwamba angalau kile kidogo tunachokipata tunafanya mambo yanayoonekana,”alisema.Alisema uhakika wa wadhamini kuja upo kwani tayari wapo baadhi wamekuwa wakiunga mkono kama Shirikisho la soka la kimataifa (Fifa) na lile la Afrika (Caf) na la Ulaya Uefa. Rais huyo alisema mashirikisho hayo yamekuwa yakiwasaidia hasa kwenye soka la vijana ila michuano ya Chalenji wamekuwa wakibeba jukumu wenyewe.Alisema iwapo watatengeneza mipango mikakati mizuri wataleta misaada itakayosaidia kuendesha mashindano ya Cecafa. Kuhusu kutanua soka la ufukweni, alisema watahakikisha na nchi nyingine za ukanda huo zinashiriki kikamilifu huku akizitaja Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini na Eritrea.Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alitangaza jana kuwa huo ni muula wake wa mwisho wa kuiongoza Cecafa kwa nafasi hiyo. | michezo |
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kupitia Bandari ya Mtwara itakuwa na uwezo wa kuhudumia tani zaidi ya milioni moja za mizigo kwa mwaka kutoka tani 400,000 za sasa, mara ujenzi wa gati namba mbili utakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu.Bandari hiyo ambayo imeelezwa kuwa lango kuu la biashara au uchumi kwa ukanda wa kusini mara baada ya kukamilika kwa gati hiyo, imejipanga kuwahudumia sio tu wateja wa ndani ya nchi bali na wa nchi jirani za Malawi, Zambia na Msumbiji.Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu bandarini hapo jana, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Juma Kijavara alisema kukamilika kwa ujenzi wa gati namba mbili kutaifanya bandari hiyo pia kuwa na uwezo wa kuhudumia tani zaidi ya milioni mbili kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Alisema bandari hiyo tangu ijengwe enzi za ukoloni mwaka 1953, ilivunja rekodi kwa kusafirisha tani 377,590 za mizigo katika Mwaka wa Fedha wa 2016/2017, huku mwaka 2018/19 ilisafirisha tani 363,286 na mwaka 2014/15 ilisafirisha tani 296,577.Tofauti na gati zingine zilizopo nchini na nchi jirani, gati namba mbili linalojengwa katika Bandari ya Mtwara lina kina cha asili cha mita 13 maji yanapokupwa, jambo linaloifanya bandari hiyo kuwa bora katika ukanda wa kusini ikilinganishwa na kina cha mita 9.5 cha bandari za nchi jirani.Akieleza kuhusu ujenzi huo, Mhandisi wa bandari hiyo, Norbert Kalembwe, alisema unatekelezwa na wakandarasi kutoka China ambao ni Kampuni za China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) na China Railway Major Bridge Engineering Group Co. Ltd (CRMBEG) kwa gharama ya Sh bilioni 137.4 ambazo ni fedha za serikali, lakini pia wakandarasi hao wanafanya kazi chini ya mhandisi msimamizi ambayo ni Kampuni ya Inros Lackner ya Ujerumani.Kwa mujibu wa Kijavara, shehena kubwa ya mizigo inayohudumiwa na bandari hiyo ni zao la korosho ambalo ndiyo zao kuu la biashara kwa mikoa ya kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Shehana zingine ni saruji inayozalishwa na kiwanda cha Dangote.“Gati hili linalojengwa lina urefu wa mita 300 na ujenzi umefikia asilimia 52, likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia meli zenye ukubwa wa tani 65,000 ikilinganishwa na gati la awali lenye uwezo wa kuhudumia meli zenye uwezo wa tani 45,000, lakini pia litakuwa na eneo la kuhifadhia mizigo lenye ukubwa wa mita za mraba 79,000 na uwezo wa kuhudumia tani zaidi ya milioni moja kwa mwaka,” alieleza.Pamoja na kuhudumia shehena za mafuta yanayokuja kwa ajili ya mikoa ya Lindi na Mtwara, Meneja huyo alisema bandari yake pia imejipanga kusafirisha tani 500,000 za makaa ya mawe kwa mwaka, tani zaidi ya 50,000 za jasi na tani zaidi ya 300,000 za saruji kwa mwaka inayozalishwa na kiwanda cha Dangote.Ofisa Utekelezaji wa bandari hiyo, Ibrahim Ruzuguma, alisema Bandari ya Mtwara inapokea wastani wa meli tatu za mizigo kwa wiki, hivyo kwa mwezi inapokea meli 12 ikiwemo meli moja ya mafuta kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambayo inakuja bandarini hapo kila mwezi.Kwa kuwa bandari ni sehemu ya uchumi wa nchi, Ofisa Ulinzi wa Bandari ya Mtwara, Khalid Kitentya, alisema wamewekeza akili, taaluma na fedha na katika kufanya hivyo, kitengo cha ulinzi bandarini hapo siyo tu kwamba kina jukumu la kuzuia uhalifu ukiwemo wizi wa mali za wateja na vitu vingine, bali pia kuhakikisha uchumi wa nchi uko salama. | uchumi |
SERIKALI imeamua kuendesha mnada wa wazi mtandaoni katika msimu wa mauzo ya zao la korosho kwa mwaka huu ili kuwe na uwazi, usawa na kupata bei nzuri. Aidha, katika msimu wa mauzo uliopita ambao serikali ilichukua jukumu la kununua korosho zote zilizovunwa, mpaka sasa serikali imebaki ikidaiwa na wakulima Sh bilioni 50 pekee ambazo hazijalipwa kati ya Sh bilioni 723 zilizotakiwa kulipwa kwa wakulima. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema kuwa serikali katika msimu wa mwaka 2019/2020 ambao unaanza mwezi huu, korosho zote zitauzwa kupitia minada ya wazi.“Tayari Bodi ya Korosho imeanza kusajili wanunuzi wenye kampuni nchini kwa kutumia mfumo huo ili kununua korosho, lengo la utaratibu huu mpya ni kupanua wigo wa soko ambapo utaongeza ushindani na kupata bei nzuri zaidi kulingana na mwenendo wa soko la dunia,” alisema Hasunga. Waziri Hasunga alisema kupitia utaratibu huo wakulima watalipwa mapema zaidi ambapo alisema kutakua na mkutano wa wadau wa sekta ya korosho Septemba 30, mwaka huu utakaofanyika jijini Dar es Salaam utajadili pia mambo mbalimbali na kuelezea utaratibu huo Aidha, alisema awamu ya kwanza ya mauzo ya korosho hiyo itakuwa kwa wenye viwanda vya kubangua korosho nchini chini ya utaratibu maalumu utakaowekwa na bodi na baada ya hapo wataanza kuuza kwa utaratibu wa minada itakayofanyika nchi nzima kwa kila ghala.Aliongeza kuwa mpaka sasa serikali haijaingia mkataba na mnunuzi yoyote isipokuwa wanunuzi wote watanunua kwa kupitia utaratibu wa manunuzi kupitia jukwaa la Solo la Bidhaa Tanzania (TMX) ambapo hakutakuwa na utaratibu wa awali wa watu kutumbukiza vikaratasi kwenye kisanduku kisha kufunguliwa kesho yake kupata mshindi. Alisema kupitia mnada huo, wanunuzi wa nje ya nchi wataweza kushiriki na hawatalazimika kufungua akaunti hapa nchini bali watadhaminiwa na benki za malipo zinazotambuliwa na TMX. “Wanunuzi wote wa korosho watasajiliwa na Bodi ya Korosho kupitia Mfumo wa Wizara ya Kilimo wa Kusimamia Biashara za Kilimo (ATMIS) na wanunuzi watatakiwa kulipa kinga ya dhamana kutegemea na kiasi cha korosho anachotaka kwenye akaunti suluhishi inayomilikiwa na soko la bidhaa.Alisema wanunuzi hao wataruhusiwa kununua korosho ghafi kwa mafungu kati ya tani 50 hadi 500 kulingana na mahitaji ambapo korosho zitapangwa kulingana na ubora na daraja. Aidha, alisema mnunuzi atalazimika kununua kiasi cha korosho kilichopo katika fungu katika kikao kimoja ili kuwezesha utoaji wa korosho katika ghala kwa kutumia utaratibu wa korosho za kwanza kuingia ndizo za kwanza kutoka. Aidha, Waziri huyo alisema pia wanunuzi kwenye leseni watapewa namba maalumu (code) watakazotumia kuingia kwenye mfumo wa mnada na mnunuzi akishinda atalazimika kulipa ndani ya siku tatu na malipo yote ni kupitia benki na minada hii itafanyika siku mbili kwa wiki katika maghala yote yaani Jumanne na Alhamisi.Aliongeza kuwa lengo la serikali ni kuona wakulima wanalipwa fedha zao moja kwa moja kwenye akaunti zao binafsi katika benki zilizopo maeneo yao na kwamba Bodi ya Korosho inaendelea kuwasajili wakulima wote wa korosho waliopo nchini. | uchumi |
Gawio hilo lilitolewa Jumamosi jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyoandaliwa na NSSF.Akikabidhi hundi ya fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Dk Ramadhani Dau, Kaimu Mkurugenzi wa Katani Ltd, Juma Shamte alisema katika kipindi cha Mwaka 2006/2013 , NSSF imeshatoa kiasi cha Sh bilioni 14.8 kwa uwekezaji wa katani, ambao unakua kwa kiwango kwa kasi na kuchangia pato la taifa.Kwa mujibu wa Shamte, uwekezaji huo wa NSSF katika Kampuni ya Katani, umeiwezesha Kampuni kupata faida kubwa, kiasi cha Sh bilioni 13 mwaka jana, na hivyo kuanza kutoa gawio kwa wanahisa wake.Akizungumza wakati wa kupokea fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema: “NSSF imekuwa na muendelezo wa kuchangia katika uwekezaji wa ndani unaomgusa mwananchi moja kwa moja”.NSSF, kwa mujibu wa Dau, itaendelea kuwekeza kwenye miradi itakayowanufaisha Watanzania walio wengi zaidi, na kutoa kwa wadau wengine wa maendeleo kuwekeza kwenye miradi kama hiyo ili kuchochea kasi ya maendeleo ya Watanzania na Taifa kwa ujumla. | uchumi |
FAINALI za kumsaka mshindi wa Bongo Star Search 2019, zilizofanyika juzi katika ukumbi wa Next Door Arena, Dar es Salaam, Meshack Fukuta kutoka Mbeya aliibuka mshindi.Mshindi wa pili alikuwa Leonard Sunday na ushindi wa tatu ulikwenda kwa Frank Charles, wa nne, Patricia Zephania na wa tano, Patrick Alsina. Kabla ya Jaji Mkuu, Rita Paulsen, hajatangaza jina la mshindi, mashabiki ukumbini walikuwa wakipiga kelele za kushangilia jina la Meshack hali iliyomfanya mwandaaji huyo kutulia kwanza na baadae kuendelea kuchana bahasha na kusoma jina la mshindi.Mshindi huyo alipewa tuzo na hundi ya Sh milioni 50, ambapo kati ya fedha hizo, Sh milioni 20 zitatumika kwa ajili ya mkataba wa kurekodi na kusimamiwa kazi zake zote za muziki kwa mwaka mzima.Mshindi wa pili, Leonard Sunday na mshindi wa tatu Frank Charles, walijipatia televisheni kila mmoja. Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, alimpongeza Rita Poulsen kwa kuandaa shindano hilo na kuwataka washiriki kutumia fursa waliyoipata kujiendeleza zaidi ili waweze kufika mbali.Aliwatolea mfano, Harmonize na Peter Msechu, kuwa ni miongoni wa walioibuliwa na BSS ambao pamoja na kwamba hawakushinda lakini wakaendelea na kuwa wasanii maarufu. BSS ni shindano la kusaka vipaji vya kuimba ambalo limefanyika kwa msimu wa 10 sasa. | michezo |
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege ameagiza vitengo vya ukaguzi wa ndani katika ofi si za mikoa na halmashauri kuhakikisha inabainisha na kudhibiti mianya ya ubadhirifu kwenye mifumo ya kukusanyia mapato na usimamizi wa fedha.Pia amesema wizara yake imeomba kibali cha ajira kwa wakaguzi wa ndani wapatao 100 ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada hiyo katika sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.Kandege ameyasema hayo jijini hapa kwenye kikao kazi cha wakaguzi wa ndani na kuongeza kuwa ni wajibu wa vitengo hivyo kuhakikisha suala la ubadhirifu na upotevu wa fedha katika meneo yao unadhibitiwa.Aidha, Kandege alisema ofisi yake inatambua changamoto ya uhaba wa kada ya wakaguzi wa ndani katika ofisi za mikoa na kwenye halmashauri na ndio maana imepeleka maombi ya kupewa kibari cha ajira.“Wakaguzi wa ndani ni watu muhimu hususani katika suala zima la usimamizi wa fedha katika sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa, wakaguzi wa ndani ndio jicho la kwanza la serikali. Kandege aliongeza:“Bila kada hii ya watumishi serikali haiwezi kuona vitu ambavyo vinatokea na kutendekea kinyume kwenye matumizi ya fedha. Serikali inawaamini na kutambua mchango wao katika usimamizi wa fedha na uwajibikaji hivyo ni vyema rasilimali watu ikawa ya kutosha ili kazi hii iweze kufanyika kwaufanisi.”Kuhusu changamoto ya ufinyu wa bajeti kwa vitengo vya ukaguzi, Kandege alisema Serikali imeongeza bajeti za vitengo vya ukaguzi kutoka Sh bilioni 5.6 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia Sh bilioni 6.4 kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.3.Kandege pia aliziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha inazipatia majibu hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili hoja hizo zifungwe.Aidha, Kandege alitumia fursa hiyo kumpongeza aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga kwa kazi aliyoifanya katika kada ya ukaguzi kabla ya kustaafu utumishi wa umma na kumtaka kuendelea kutoa mchango kwenye shughuli za kiuchumi za kujenga Taifa.Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Nyamhanga amesema kutokana na umuhimu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani fedha zilizotengwa kwa ajili ya kitengo hicho zitalindwa na kuhakikisha zinatumika kwa ajili ya kazi za kitengo pekee. | kitaifa |
MSHIKEMSHIKE wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea tena leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwa kuwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba SC dhidi ya Mwadui FC.Simba itamalizia hasira zake kwa Mwadui baada ya kufungwa 5-0 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika uliofanyika Alexandria, Misri wiki iliyopita.Kabla ya mechi za jana, Simba ilikuwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 33 Mwadui ikiwa nafasi ya 16 na pointi zao 24.Simba itahitaji kupata ushindi leo kwa udi na uvumba ili kujipoza na kipigo walichokipata Jumamosi iliyopita cha mabao 5-0 kutoka Al Aly na pia kujiwekea mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wao.Mwadui wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya, kwani mara ya mwisho timu hizi zilipokutana Septemba 23 mwaka jana, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-1, mabao ya Simba yakifungwa na John Bocco aliyepiga mawili na jingine Meddie Kagere.Nahodha wa Simba, Bocco amesema, mashabiki wa timu yao watulie na wasiwe na wasiwasi kwani matokeo mabaya waliyoyapata katika mechi iliyopita ya klabu bingwa hayatawaathiri katika mechi zao za ligi.“Tumetoka katika michezo ya kimataifa, tumeshamaliza na mechi iliyopita tupo tayari na mchezo wa ligi ili tufanye vizuri,” alisema Bocco.Kwa upande wa Mwadui katibu wa timu hiyo, Ramadhani Kilao alisema kuwa wao wamejiandaa kwa lolote kuweza kuwakabili Simba na wamepanga kuondoka na pointi katika mchezo huo.“Kikosi chetu kipo hapa Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo tunachokiangalia ni kupata pointi tatu ili kujitengenezea mazingira ya kujiweka sehemu salama ya msimamo wa ligi,” amesema Kilao. | michezo |
Wafanyabiashara hao zaidi ya 500 wakiwa wamekusanyika katika eneo la Masuka mjini hapa, kutaka kufanya maandamano kwenda kuonana na mkuu wa mkoa ofisini kwake kumuelezea kero hizo ili zipatiwe ufumbuzi, ambapo maduka mengi yalionekana kufungwa.Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na waandishi wa habari, kabla ya kuanza maandamano kwenda ofisi za Mkuu wa Mkoa, Mrisho Emiliani, Joseph Molel, Salvatory Shayo, Salum Magona walilalamikia mashine hizo za risiti kuuzwa Sh 800,000 na wakilazimishwa kununua maeneo ambayo TRA imepanga, fedha ambazo ni nyingi kulinganisha na mitaji ya maduka yao kama wajasiriamali.Walidai kuwa kinachowaumiza zaidi ni kukatwa asilimia 18 kama kodi kwa bidhaa wanazouza, huku soko huria likiwa na bei ya kupanda na kushuka kulingana na msimu, na wakati mwingine bidhaa husika haina faida kama ambavyo serikali inafikiria.Meneja wa TRA mkoa wa Morogoro, Kilomba Kanse, alifika eneo hilo la Masika kujaribu kuzungumza na wafanyabiashara hao bila mafanikio, ambapo aliwaeleza kuwa alipokea taarifa juzi saa 10 jioni kuwa Serikali imeongeza muda wa matumizi ya risiti hadi Desemba 31 mwaka huu badala ya Novemba 15 mwaka huu, na kwamba kama kungekuwa na maelekezo zaidi ya Serikali ni baada ya tarehe hiyo.Ingawa mwandishi wa habari hizi alishuhudia tangazo la kuhimiza matumizi ya risiti katika gari ya TRA siku hiyo hiyo ya mgomo wa wafanyabiashara majira ya saa 4:00 asubuhi, bado Kanse alidai matangazo yaliyokuwa yakitolewa yalisitishwa kutokana na tamko hilo la Serikali.Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao wa kati, Ali Mamba, alikataa kuwasilisha kero zao kwa TRA, kwa madai imeshindwa kuwasikiliza kwa muda mrefu, ndio maana wanataka kumuona Mkuu wa mkoa ambapo jitihada zao zilizaa matunda kwa Mkuu wa Mkoa kuwaruhusu wafanyabiashara wanane kuwawakilisha wenzao kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, ingawa wafanyabiashara wengine waliendelea na maandamano hadi katika ofisi hizo huku wakizuiwa na Polisi. | uchumi |
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda kushirikiana na serikali ili kuhakikisha soko la bidhaa mbalimbali wanazozizalisha linakuwa kubwa kwenye nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Jumuiya ya Afrika Mshariki (EAC).Bashungwa amesema hayo alipokutana na wafanyabishara na wamiliki wa viwanda wa Tanzania ikiwa ni wiki chache kabla ya wiki ya viwanda ya SADC inayotarajiwa kuanza Agosti 5 hadi 9, mwaka huu jijini Dar es Salaam.Alisema serikali imejipanga kushirikiana na wamiliki wa viwanda hivyo pale ambapo itahitajika kufanya hivyo ili kujenga uchumi wa viwanda ambao upo katika mpango kabambe chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.Bashungwa alisema wazalishaji wanatekeleza asilimia 30 ya kuwepo kwa kiwanda hivyo serikali inapaswa kusaidia asilimia 70 iliyobakia inatimia.Alisema masoko, mazingira sahihi na mikakati mingine inapaswa kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau. Aliwataka wamiliki wa viwanda kutumia wiki hiyo ya viwanda ya SADC kama fursa pekee kuthibitishia umma wa nchi wanachama uwezo wa Tanzania katika uzalishaji.“Ili sekta ya viwanda iwe na tija nchini ni lazima wadau wote washiriki kwenye mikakati kwa kutumia uhusiano wa kikanda wa SADC na EAC,” alisema.Alisema mkakati wake ni kuona viwanda vinavyozalisha kwa sasa vinatatua changamoto zake ili viweze kukua na itasaidia kuhamasisha viwanda vipya. Waziri Bashungwa alisema kasi hiyo ya kuimarisha viwanda inatakiwa kuendana na utekelezaji wa mkakati wa ufanyaji biashara huru (Blue Print).“Iwapo soko la kanda hizo litatumika vizuri ni wazi matarajio ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania ya uchumi wa viwanda yatatimia,” alisema. Waziri Bashungwa alisema wapo kwenye mapitio ya sheria na sera ya uendelezaji viwanda vidogo. | uchumi |
WATU wa kada mbali mbali wameunga mkono hatua ya Rais John Magufuli ya kuwaalika watu wa kada mbalimbali kukaa nao pamoja ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa pamoja.Walisema ili nchi iweze kusonga mbele, inahitajika michango ya pamoja kutoka sekta mbalimbali ya nchi, kitu ambacho Rais Magufuli amekuwa akifanya.Wakasema ni kutoakana na kukaa na watu wa kada mbalimbali, imemuwezesha kufanya mabadiliko katika nafasi mbali mbali huku wakihimiza watumishi na watendaji kumuelewa kwamba anachohitaji ni uwajibikaji na si kingine.Wakizungumzia mkutano wa juzi kati ya Rais Magufuli na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini, walisema umedhihirisha dhamira nzuri na diplomasia katika kutafuta suluhu ya matatizo yanayoathiri ufanisi wa sekta binafsi.Akizungumza na gazeti hili jana, Mshauri binafsi wa masuala ya uchumi, Profesa Kitojo Wetengere alisema uwajibikaji ni suala muhimu kwa kila Mtanzania na kwa sekta zote hivyo wateule wa rais wanapaswa kufahamu hilo.“Kuna pengo kubwa kati ya kile ambacho Magufuli anataka na kinachotendeka na ndiyo maana mheshimwa anaendelea kubadilisha viongozi,” alisema Profesa Wetengere akiunga mkono mabadiliko aliyofanya rais jana katika Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA).Rais Magufuli amemteua Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kuchukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.Aidha, amemteua Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa TRA akichukua nafasi ya Charles Kichere ambaye uteuzi wake pia umetenguliwa jana.Profesa Wetengere alisisitiza, “inakuwaje rais aitishe mkutano wakati wizara na TRA ipo…. Watu wapimwe kulingana na utendaji na uwajibikaji na si karatasi (vyeti).Wapimwe kwa ubunifu wao na mabadiliko.” Alisema mambo yaliyoibuliwa ni mengi na yaliwezekana kutatuliwa. “Jambo la kujiuliza ni kwa nini yameendelea kuwapo kwa muda wote bila kutatuliwa?..Kulikuwa na hujuma nyingi … ndiyo maana rais ameona mabadiliko yawepo.Kiukweli lazima mabadliko makubwa yaendelee kufanyika serikalini.” Akizungumzia mkutano huo wa juzi Ikulu Dar es Salaam, Profesa Wetengere ambaye ni mshauri wa uchumi akibobea zaidi katika eneo la diplomasia, alisema ulikuwa wa kidiplomasia ambao umedhihirisha kwamba mambo yaliyokuwa yakisemwa kuhusu sekta ya biashara na viwanda yalikuwa sahihi.Akishauri kuhusu mfumo wa kodi, alisema upo umuhimu wa kujifunza kutoka nchi nyingine wanavyofanya kuhakikisha kunakuwa na mfumo wa kitaalamu na unaotenda haki.Vile vile alisema sheria za kodi zinapaswa kubadilika kulingana na mazingira zisaidie badala ya kugeuka kikwazo. “Unapoweka kodi kubwa lazima rushwa itaingia,” alisema.Mshauri huyo wa uchumi alisisitiza umuhimu wa kupanua wigo wa kodi. Alisema wasomi na wataalamu wanapaswa kukaa na kuibua maeneo hayo badala ya wataalamu kuendelea kujielekeza kwa watu wachache na kuwabebesha mzigo wa kodi na kuleta manung’uniko.Mdau mwingine upande wa viwanda, Akida Mnyenyelwa alisema mkutano huo ulikuja wakati muafaka na umewasuuza nyoyo.Mnyenyelwa ambaye anatoka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), alisema waziri aliyeteuliwa, Bashungwa waliwahi kufanya naye kazi kwa karibu ni mtu anayefahamu sekta ya biashara na changamoto zake.Hata hivyo, alisisitiza kuwa maoni hayo ni yake kwa kuwa msemaji wa CTI ni mwenyekiti. “Binafsi, naona uteuzi umekuja mahali ambako ni muafaka anafahamu sekta ya biashara na changamoto zote,” alisema Mnyenyelwa na kuunga mkono hatua za rais kufanya mabadiliko akisisitiza kuwa ndiye anayefahamu upungufu uliopo katika eneo lolote.Alisisitiza, “Rais anajua mapungufu yako wapi ndiyo maana anataka kurekebisha kasi ya utendaji. Kiundani hatuwezi kujua mambo yanayoendela; kama kuna kasoro, hata akiteua mara kwa mara ni sawa.” Alisema wafanyabiashara na wenye viwanda wanachotaka ni kuona urasimu na uonevu unakwisha.“Kunapokuwa na ukandamizaji, biashara haziendi hiyo haikai vizuri. Kwa hiyo kama rais anaona mapungufu sisi kama wadau tunalipokea,” alisema Mnyenyelwa.Wakizungumzia mabadiliko aliyofanya Rais Magufuli katika TRA na Wizara ya Viwanda na Biashara, baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali waliozungumza na gazeti hili walishauri viongozi wa juu kuratibu utendaji wa walio chini yao kwa kuwa ndiyo wanaowaangusha.“Mimi sasa hivi ni mjasiriamali lakini nilikuwa na maduka ikabidi niyafunge kwa kushindwa kuyamudu kutokana na kodi kubwa… vijana ndiyo wenye kusumbua hawafuati maelekezo ya wakubwa. Na sisi wajasiriamali tunatamani tuwe na mkutano na rais,” alisema Shenaz Issa mkazi wa Morogoro.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema katika Serikali ya Awamu ya Tano viongozi hawapaswi kubweteka kwa kuwa watakapokwenda kinyume cha matarajio ya rais lazima hatawavumilia.Kwa upande wake, Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Lenny Kasoga alisema uamuzi wa rais unatuma ujumbe kwa walio madarakani kufanya kazi kwa ufanisi.Alisema tangu Rais Magufuli aingie madarakani aliahidi kuwa hatasita kuwatumbua wasio fanya kazi kwa tija. Saa 24 baada ya rais kufanya mkutano na wafanyabiashara Ikulu Dar es Salaam, jana alifanya mabadiliko TRA na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kutengua uteuzi wa vigogo wake na kuteua wengine wa kushika nyadhifa husika.Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Bashungwa ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhede amekuwa Kamishna Mkuu wa TRA kuchukua nafasi ya Kichere aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe | kitaifa |
MKOA wa Ruvuma umetakiwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwavutia wawekezaji kuchangamkia fursa za uwekezaji na kuufanya mkoa huo kuwa moja ya maeneo yenye viwanda vingi nchini.Akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Joseph Simbakalia, amesema kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na miundombinu muhimu kama barabara, umeme na maji ni hitaji muhimu ambalo kila mwekezaji hupenda kujua kabla ya kufanya uamuzi wa kuwekeza.Mkoa wa Ruvuma kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, ulikuwa kati ya mikoa 11 iliyokuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa. Simbakalia alisema miongoni mwa majukumu ya msingi la mamlaka hiyo ni kuainisha maeneo ya uwekezaji na kuwavutia wawekezaji.“Jukumu hili halipaswi kutekelezwa na EPZA peke yake bali tunahimiza serikali za mikoa na wilaya kushirikiana kwa karibu katika kutenga maeneo na kuboresha mazingira ya biashara ili kusudio la ujenzi wa uchumi wa viwanda liende kwa kasi zaidi,” alisema.Mwongozo huu uliozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, unalenga kuanisha fursa za uzalishaji na kupanua utoaji habari za uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.Kwa sasa mkoa wa Ruvuma una viwanda vidogo na vya kati 19 vikiwa katika manispaa ya Songea na mji mdogo wa Mbinga na viwanda vipya vya kuchakata mahindi kimoja kikiwa kinaendelea kujengwa ni sehemu ya viwanda hivyo.Takwimu zinaonyesha asilimia 75.8 ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma ni wakulima hasa mazao ya kahawa, karanga, mahindi, viazi, tumbaku, mihogo, korosho, matunda, mtama, nazi na ufuta. | uchumi |
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na mshambuliaji wa klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amefurahishwa na mbinu za Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije na kueleza zinawasaidia kuwa na ari ya kupambana uwanjani na kuahidi kufanya makubwa chini yake.Samatta aliyasema hayo alipokuwa kambini na Taifa Stars katika michezo miwili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia, ambapo walifanikiwa kufuzu hatua ya makundi baada ya kuifunga Burundi kwa panalti 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa baada ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali uliochezwa Burundi.“Ndoto kubwa ninayoiota kwa sasa ni siku moja kuja kucheza michuano ya Kombe la Dunia, japo matumaini ya kufikia hatua hiyo kuna ugumu hivyo tunatakiwa kupambana,” alisema Samatta. Kuhusu michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu, Samatta alisema kwake ni jambo kubwa kupata nafasi ya kucheza katika Uwanja wa Anfield unaomilikiwa na klabu ya Liverpool kwa kuwa ni klabu kubwa, lakini alipendelea zaidi kama wangepangwa kundi moja na Barcelona au Real Madrid za Hispania.“Unaposhiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya huwezi kukosa kukutana na vigogo kama hao, mabingwa wa nchi mbalimbali.Lakini ningependa zaidi kukutama ama na Barcelona au Real Madrid, ila hata hivyo Anfield pia ni moja ya sehemu bora sana, si mbaya kucheza na timu kama Liverpool na Napoli,” alisema. Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, ambapo katika kundi la Genk kuna timu za Liverpool, Napoli na Salzburg. Pia atacheza kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Uingereza pindi atakapovaana na Liverpool katika dimba la Anfield. | michezo |
KAULI ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaasha Tumbo kuwa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo haina mtendaji wa sekta ya ardhi anayeweza kuvaa viatu vya ukuu wa idara iwapo anayeshikilia nafasi hiyo, Salehe Kang’e ataondolewa, imemwokoa mkuu huyo wa idara kutumbuliwa.Kauli hiyo ilikuja baada ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula kueleza kuwa Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri hiyo hafai kuwa mkuu wa idara ya ardhi kutokana na kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Bakari Mhando alimwomba Anjelina kutomwondoa katika nafasi hiyo Kang’e, akidai upungufu aliouonesha atahakikisha unarekebishwa kwa mwezi mmoja.Akiwa katika ziara ya kustukiza katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga juzi, Dk Angelina Mabula alionesha kuchukizwa na mkuu huyo wa idara ya ardhi kushindwa kusimamia ukusanyaji kodi ya ardhi ikiwemo kutoa hati za madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi wilayani humo.Kang’e amebakiza mwaka mmoja kustaafu kazi. Halmashauri hiyo imeingiza viwanja 3,000 katika mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki na mashamba 1,009, lakini imetoa hati moja ya madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi.Angelina alisema alichotegemea baada ya kuingizwa viwanja na mashamba kwenye mfumo huo wa ulipaji kodi kielektroniki, mkuu wa idara ya ardhi angehakikisha wadaiwa wote sugu wanafuatiliwa ili walipe kodi, lakini kinyume chake kazi hiyo haijafanyika na ni mdaiwa mmoja tu aliyepelekewa hati ya madai.Alisema msisitizo wa Serikali ni kukusanya mapato yakiwemo ya kodi ya ardhi ili kusaidia shughuli za maendeleo ambazo haziwezi kupatikana iwapo serikali haitakuwa na makusanyo mazuri ya kodi.“Haya yanayofanyika ununuzi wa ndege na ujenzi wa SGR (Reli ya Kisasa) bila ya kukusanya kodi hayawezi kufanyika na Rais John Magufuli anasisitiza ukusanyaji kodi, watu hawako makini,” alisema.Alimpa mwezi mmoja kuhakikisha wadaiwa wa kodi ya ardhi wanapelekewa hati za madai na watakaokaidi wafikishwe katika mabaraza ya ardhi na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kaskazini ifuatilie utekelezaji wa agizo hilo. | kitaifa |
Hayo yalibainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nasanda Massama, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX), iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Dar es Salaam, hivi karibuni.Alisema kwa upande wa kampuni za ndani masoko hayo ya mitaji mchango wake umeongezeka kutoka asilimia sita, mwaka 2005 hadi asilimia 24, mwaka huu.“Hali hii inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la kampuni zilizoorodheshwa katika masoko ya mitaji. Kwa sasa kuna kampuni 25 kutoka kampuni sita zilizoorodheshwa wakati wa kuanzishwa kwa masoko haya,” alisisitiza Massanda.Kwa upande wake, Rais Kikwete alipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini kwa ajili ya kuboresha masoko ya mitaji, hisa na bidhaa, hali ambayo alisisitiza itasaidia kukuza uchumi wa Tanzania na kutimiza lengo la kuwa moja ya nchi zenye uchumi wa kati.Hata hivyo, alisema pamoja na kwamba Serikali inajitahidi kukuza uchumi huo wa nchi kupitia kilimo, kutokana na Tanzania kuwa na idadi kubwa ya wakulima, bado kuna haja ya kushirikisha hadi sekta binafsi kwa ajili ya kutafuta jawabu la uhaba wa maghala ya kuhifadhia chakula.“Nafurahi kuona namaliza muda wangu kama kiongozi wa Tanzania, lakini jitihada nilizofanya zikianza kuonekana. Sasa mageuzi ya kilimo ndio yanaanza kupitia soko la bidhaa TMX, kilimo chetu kitaimarika, lakini bila kupata jawabu la maghala ya kuhifadhia mazao, ukuaji wa kilimo utakua mgumu,” alisisitiza Rais Kikwete.Aidha alisema sera ya kilimo kwanza inafanya vizuri, ingawa bado suala la stakabadhi ghalani limekuwa likipigwa vita, kwani wakulima wengi wamekuwa wakizalisha mazao mengi kiasi cha mengine kukosa maghala ya kuhifadhia.“Uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni tani 150,000 tu, lakini mazao yamekuwa mengi sana na wakulima wanafikiri kuwa NFRA ndio mnunuzi pekee wa mazao yao. Natumaini kupitia soko la bidhaa TMX, soko la mazao haya litaimarika. | uchumi |
KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeipongeza Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc) kwa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa malengo ya ubinafsishaji na kuendeleza azma ya serikali ya viwanda.Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyoratibiwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na pia kuhudhuriwa na Naibu Waziri waViwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya na watendaji wengine kutoka wizara hiyo.Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Sadiq`Murad' ameipongeza TCC Plc kwa mafanikio hadi sasa na kuongezea kuwa kamati yake iliridhishwa na walichokiona na kuutaka uongozi na wafanyakazi kuendeleza kazi hiyo nzuri.“TCC Plc ni mfano mzuri wa kweli unaopaswa kuigwa kwa wengine kwani utatambua imekuwa imara katika ulipaji wa kodi serekalini.. Kamati yangu imezichukua changamoto zao na tutaishauri serikali inavyostahili ili kuhakikisha wawekezaji kama TCC Plc wanafanya shughuli zao bila wasiwasi,” amesema.Mwenyekiti huyo pia aliipongeza TCC Plc kwa kukuza vipaji vya ndani kwani hadi sasa kuna wakurugenzi watano wa kitanzania katika Menejimenti ya Juu inayoundwa na wakurugenzi wanane.Hivi karibuni kampuni hiyo imeshuhudia uteuzi wa Sam Mandara kama Mkurugenzi wa uzalishaji ambaye ni mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kampuni hiyo ibinafsishwe.Manyanya alisema TCC Plc imekuwa mfano wa kweli katika mafanikio ya ubinafsishaji kwani mashirika mengine yaliyobinafsishwa wakati mmoja na TCC Plc yalishindwa kujiendesha na yamekufa wakati kampuni hiyo imeendelea kukua na kujiendesha kwa faida miaka yote.Aliipongeza kampuni hiyo kwa kuwekeza katika nishati ya umeme wa gesi kwani hatua hiyo haijahakikisha tu gesi inayozalishwa nchini inatumika, bali pia imehakikisha wakazi wa maeneo ya Chang’ombe, Temeke hawapati adha za mgawo wa umeme, kwani kampuni hiyo haitumii umeme mwingi kutoka kwenye gridi ya taifa.Meneja Mkuu na Mtendaji Mkuu wa TCC Plc, Allan Jackson ameishukuru kamati hiyo kwa kuwa bega kwa bega nao hadi sasa ambapo imeiwezesha TCC Plc kufikia malengo yake tangu kuanzishwa kwake.Aliongeza kusema kwa mwaka jana pekee TCC Plc ililipa serikalini kodi ya ongezeko la thamani (VAT), mapato na ushuru wa bidhaa kiasi cha Sh bilioni 227, jambo ambalo wabunge wanatakiwa kujivunia.Aliwakumbusha wabunge kuwa TCC Plc ni mali ya watanzania na kuwa yeye na wafanyakazi ni wasimamizi tu kwa niaba ya wanahisa wa kampuni hiyo. | uchumi |
BONDIA machachari nchini, Hassan Mwakinyo ameiomba Serikali isapoti mchezo wa ngumi ili utumike katika kulitangaza taifa nje ya mipaka yake.Mwakinyo ambaye ni balozi wa Kampuni ya Sportpesa ameyasema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwelekeo wa ngumi za kulipwa nchini.Nyota huyo amesema kuwa mabondia wengi wamekuwa na nia ya kulitangaza taifa nje ya mipaka yake kwa kuhakikisha wanashinda mapambano lakini sapoti ya serikali imekuwa ni ndogo ukilinganisha na ile inayoenda kwenye michezo mingine. “Kazi yetu ni kubwa na ngumu, Serikali imekuwa ikitupa sapoti lakini bado haitoshi isipokuwa tunaomba izidi kutusaidia kwani bado safari ni ndefu…“…tunaona jinsi wanavyoipa sapoti timu ya taifa ya mpira wa miguu, sasa na sisi tunahitaji sapoti ya namna hiyo ili tuzidi kuipeperusha vyema bendera yetu,” amesema Mwakinyo.Ameongeza kuwa anaamini kuwa serikali ni sikivu na itaunga mkono timu hiyo.Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni Oktoba 26 na inaelezwa kuwa huenda atavaana na bondia kutoka Argentina, Ufilipino, Italia, Marekani au Urusi. | michezo |
Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu kinachotarajiwa kuanza kazi Oktoba mwaka huu.Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Doto Biteko baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kitakachochenjua na kusafisha dhahabu kwa asilimia 99.9.Amesema mbali na kusaidia wafanyabiashara nchini katika kuchenjua na kusafisha dhahabu zao, pia uwepo wa kiwanda hicho utawezesha nchi kuwa na akiba ya madini hayo yatakayonunuliwa na Benki ya Kuu (BoT).Januari mwaka huu, Rais John Magufuli aliagiza BoT kuwa na akiba ya dhahabu na kuhimiza haja ya serikali kudhibiti usafirishaji wa madini kutokana hapa nchini ambayo ni nchi ya nne kwa kuzalisha dhahabu.“Tunatakiwa kuanza kununua dhahabu, BoT inatakiwa kuwekeza kwenye hili. Tunatakiwa kuwa na akiba yetu si tu kwenye dola bali hata kwenye dhahabu, kwa sababu dhahabu ni fedha,” amesema Rais Magufuli.Biteko amesema kuanzia Oktoba mwaka huu, BoT itaanza kununua dhahabu iliyosafishwa ambayo itaweka kwenye “akiba ya Taifa ya dhahabu’ na hatimaye kusaidia nchi kuuza dhahabu na kushindana kwenye soko la kimataifa.Amesema hatua ya kuanzisha kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu nchini ni takwa la kisheria kutokana na mabadiliko ya hivi karibuni ya Sheria ya Madini, na kuongeza kuwa mpaka sasa tayari serikali imetoa leseni mbili za kuanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu mkoani Dodoma na Mwanza.Amesema walijitokeza jumla ya waombaji 24 na waliopewa vibali wa uendeshaji wa shughuli za kurefine na ku-smelte ni sita.“Kati ya viwanda hivyo sita vitakavyojengwa nchini viwanda viwili ni vya kurefined madini ya dhahabu, copper na silver ambavyo vipo katika mikoa ya Dodoma na Geita,” amesema na kuongeza kuwa viwanda vinne vya Smelter ambavyo vimejengwa Kyerwa mkoani Kagera, Mpwapwa (Dodoma) na Kahama (Shinyanga).Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Ferenc Milnar alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uliogharimu dola za Marekani milioni 2, umekamilika kwa asilimia 75 na kwamba hivi sasa wanasubiri vifaa kutoka nchini Italia.Alisema baada ya kufika vifaa hivyo nchini mwezi ujao, watatumia siku saba kuvifunga. Molnar pia alimuhakikishia waziri kuwa watahakikisha kiwanda hicho ndani ya muda uliopangwa.Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha hicho, Prince Mugisha alisema wataanza kwa usafishaji wa mfano ambao utakuwa kilo 30 hadi 50 kwa siku. Alisema mwakani watakuwa wakisafirisha kilo 1,000 kwa siku.Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema utekelezaji wa sehemu wa Sheria ya Madini inayotaka theluthi moja ya mrahaba utolewe kama dhahabu utaanza kutekelezwa mara baada ya kiwanda cha uchenjuaji wa dhahabu cha kwanza kukamilika kati ya Oktoba.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge aliwahakikisha wawekezaji wanaotaka kuwekeza mkoani humo kuwa watapata msaada unaotakiwa na kufika ofisini kwake kama wanakumbana na urasimu wa aina yoyote. | uchumi |
MABONDIA Francis Cheka na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ kila mmoja amejigamba kuonesha ubabe wake katika pambano litakalofanyika keshokutwa katika ukumbi wa Sabasaba PTA, Dar es Salaam. Dullah Mbabe mwenye umri wa miaka 24, amecheza michezo 28 mpaka sasa, kashinda mapambano 22 ambapo 21 kati ya hayo ameshinda kwa KO, akipoteza mapambano matano na kutoa sare pambano moja.Akizungumza kuelekea pambano hilo, Dullah Mbabe alisema siri ya kushinda kwa KO katika mapambano yake ni kutokana na nguvu nyingi alizonazo. “Mimi nina nguvu kama mdudu, yaani ukigombana na mimi ni sawa umegombana na kifaru, sijamuona wa kunipiga bado hapa nchini, labda mwaka 2025 nitakapokuwa mzee ndiyo nitapigwa,” alisema Dullah Mbabe. Kwa upande wa mkongwe Cheka mwenye umri wa miaka 36, amecheza michezo 44, na kushinda mapambano 32, kupoteza mapambano 10 na kutoa sare mapambano mawili, alisema kumpiga Dulla Mbabe ni suala la kawaida kwake wala haongei sana. “Ninaamini kumpiga Dullah Mbabe ni suala la kawaida kwasababu nimeshakwepa mishale mingi mpaka sasa, kila mtu atakayekuja pale ulingoni ataona, wala siongei sana.” “Ni kweli huwezi kuwa bingwa milele, hilo linafahamika kuwa watu huwa wanapokezana kwa muda lakini kwa sasa hivi mimi ndiyo namba moja, nimeshinda ubingwa wa dunia mara tano, bingwa wa Afrika mara nne na bingwa wa mabara mara mbili na sasa hivi ninachofanya ni kuhamasisha vijana wanaokua,” aliongeza Cheka. Viingilio vya pambano hilo ni Sh 7,000 kwa mzunguko na Sh 15,000 kwa VIP. | michezo |
BUNGE limeridhia kubadilisha hadhi mapori ya akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika-Orugundu katika ukanda wa Kaskazini- Magharibi kuwa Hifadhi za Taifa ambako kutasaidia kuimarisha ulinzi, kujenga mazingira bora na kukuza Pato la Taifa.Pia serikali ipo katika kampeni ya kuchora upya ramani na vivutio mbalimbali vya utalii nchini kwa lengo la kuongeza, kubadili na kupanua vivutio vya utalii nchini.Akiwahoji wabunge jana kabla ya kupitia azimio hilo bungeni, Spika wa Bunge, Job Ndugai alishangaa wabunge wote walivyokubaliana kuridhia azimio la kupandisha hadhi mapori hayo kuwa hifadhi za taifa.Akihitimisha hoja za wabunge, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla alisema kwa Bunge kuridhia kupandisha hadhi mapori hayo, Taifa litapata manufaa yakiwemo ya kuimarisha uhifadhi wa maliasili hasa wanyamapori, mimea na mazalia na makuzio ya samaki na viumbe wengine kwenye maji.Pia utaongeza Pato la Taifa kwa msingi ubadilishaji hadhi utasaidia hifadhi hizo kuwa vivutio vya utalii.Alisema uhifadhi na usimamizi endelevu wa mapori haya ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimazingira kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Usimamizi huo utawezesha kuondoa uharibifu wa mazingira, uvamizi wa mifugo, ujangili na uingizwaji wa silaha haramu za kivita.Akisoma maoni ya kamati, Makamu wa Mwenyekiti, Timotheo Mnzava alisema uamuzi wa kupandisha hadhi mapori hayo kuwa hifadhi za taifa utaimarisha ulinzi.Alisema kamati inalishawishi Bunge kupitisha azimio hiyo kwani hatua hiyo itajenga mazingira bora kwa ajili ya kuendeleza utalii na kukuza pato la taifa.Lakini inashauri ili kuepusha uwezekano wa hifadhi mpya kuwa na migogoro, kamati inashauri serikali kuhakiki mipaka husika kwa kushirikisha wananchi ili kuepuka kuwepo kwa migogoro ya mipaka.Akitoa maoni yake, Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM) alisema ni vema kupandisha hadhi mapori hayo na serikali inatakiwa kukumbuka na mikoa ya Kusini kwani Watanzania wote ni wamoja.Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate (CCM), alisema kupandishwa hadhi kwa mapori kutapunguza tatizo la uhalifu kwani wenyeji wa Kagera walitakiwa kupita mapori hayo wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) alisema kupandisha hadhi kutatoa faida ya kuongeza Pato la Taifa, kuongeza ajira na kuongeza watalii kupitia uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko (CCM) alisema wakati wanapandisha hadhi mapori hayo wanatakiwa pia kukumba mapori ya Kigosi na Mayowosi kwani yapo katika ekolojia moja.Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) alipongeza uamuzi wa kupandisha hadhi mapori hayo lakini akataka wasitelekeze mkakati wa kuboresha korido ya Kusini ambayo mradi wa uendelezaji ukanda huo ulishaanza.Sasa kuna hifadhi 14, Serengeti, Ziwa Manyara, Arusha, Ruaha, Mikumi, Gombe, Tarangire, Kilimanjaro, Katavi, Rubondo, Milima Mihale, Udzungwa, Saadani, Kitulo, Mkomazi na Kisiwa cha Saanane.Usimamizi wa maeneo ya wanyamapori unahusisha hifadhi za Taifa 16 zinazosimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), mapori ya akiba 28 na mapori tengefu 42 yanayosimamiwa na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (Tawa). | kitaifa |
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wataendelea kusota gerezani hadi Januari 3, mwakani kesi yao ya uchochezi inayowakabili na wenzao saba, itakapotajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Sababu ya washitakiwa hao kusota rumande ni kutokana na kufutwa kwa dhamana yao na kuwa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam tangu Novemba 23, mwaka huu. Hatua hiyo ilikuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusitisha usikilizwaji wa rufaa ya kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana washitakiwa hao hadi hapo rufaa ya upande wa serikali itakaposikilizwa Mahakama ya Rufani.Wakili wa Serikali, Wankyo Simon akisaidiana na mwenzake Salum Msemo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa. Wakili Simon alidai hawana taarifa ya kinachoendelea mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.Hata hivyo, Wakili Faraja Mangula alidai Wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, mwakani. Akijibu hoja hiyo, Wakili Simon alidai wanaiachia mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa. Hakimu Mashauri alisema Januari 4, mwakani atakuwa na kazi nyingine hivyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 3, mwaka huo.Baada ya kuelezwa hayo, Mbowe na Matiko waliwatakia wafuasi wao heri ya sikukuu wakiamini kuwa hawawezi kutoka gerezani kwa kipindi hiki kutokana na kutojua kinachoendelea mahakamani. Mahakama Kuu baada ya kukubali rufaa yao ya kufutiwa dhamana iweze kusikilizwa upande wa serikali ulipinga maamuzi ya mahakama hiyo kwa kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga usikilizwaji wa rufaa hiyo kwa sababu mahakama haina mamlaka.Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani. Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam. | kitaifa |
Simba juzi iliingia mkataba wa miaka miwili na Okwi, ambaye ataanza kuichezea tena timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, utakapoanza Agosti mwaka huu.Akizungumza na gazeti hili, Kaburu alisema baada ya kuinasa saini ya Okwi, sasa usajili wao umekamilika kwa asilimia 90 na wamebakiza asilimia 10, ili kufunga zoezi hilo na kumkabidhi kocha Joseph Omog, timu yake kwa ajili ya kuwapa mafanikio waliyokusudia kuanzia msimu ujao.Kiongozi huyo alisema kuwa na kikosi ghali kama hicho kinakupa uhakika wa kufikia malengo ambayo mmejipangia na wao kama uongozi hawaoni sababu ya Simba kushindwa kufanya vibaya katika michuano yote kwani wana nyota wote wenye kikosi chao.Alisema sababu ya kusajili timu kama hiyo ni kutaka kumaliza manung’uniko ya mashabiki wao ambayo yamekuwa hawafurahishwi na mwenendo wa timu yao, hasa katika usajili na safari hii wameamua kulimaliza jambo hilo kwa kufanya kufuru ya kuwabeba nyota wote wanaotamba nchini.Alisema baada ya kufanikisha hilo ana imani watakuwa wamekata kiu ya mashabiki wao na kazi iliyobaki ni moja ambayo ni kuisapoti timu hiyo ili iweze kufanya vyema na kufikia malengo ambayo wanayakusudia.Nyota wenye majina makubwa ambao wametua Msimbazi ni John Bocco, Aishi Manula na Shomari Kapombe wote kutoka Azam mwingine ni Haruna Niyonzima, kutoka kwa mahasimu wao Yanga, pia wapo wachezaji Emmanuel Mseja na Ally Shomary. | michezo |
WADAU wa kilimo cha alizeti mkoani Dodoma, wameiomba serikali kuandaa mafunzo maalumu kwa maofi sa ugani, hatua itakayowaongezea uwezo wataalamu hao katika kutoa elimu stahiki kwa wakulima wa zao hilo.Ombi hilo lilitolewa na wadau hao wakati wa kikao cha wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT), ambao walifanya ziara hivi karibuni mkoani Dodoma kwa lengo la kujifunza na kuona changamoto zinazowakabili wakulima wa zao hilo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao katika Wilaya za Bahi na Kongwa walisema, changamoto kubwa ambayo wakulima hao wanakabiliana nazo ni kukosekana kwa wataalamu wa kilimo waliobobea katika kilimo cha zao hilo.Walisema pamoja na changamoto hiyo, pia kuna idadi ndogo ya maofisa ugani ukilinganisha na mahitaji halisi ya idadi ya wakulima waliopo katika maeneo mengi mkoani humo.Mmoja wa wadau hao, Yohana Mwanjara ambaye anajihusisha na usambazaji wa mbegu na pembejeo kwa ajili ya alizeti alisema, licha ya jitihada kubwa ambayo serikali imekuwa ikifanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, bado tatizo la ukosefu wa wataalamu wenye weledi wa zao hilo ni kikwazo kikubwa. Alisema wengi wa wataalamu waliopo hawaendani na mabadiliko na teknolojia za kilimo zilizopo na hivyo kuwa kikwazo katika kumsaidia mkulima.“Unamkuta mkulima anahangaika kupata maarifa ya nini cha kufanya lakini hawezi pata msaada matokeo yake unakuta mkulima huyu anaishia kulima tu kwa mazoea,” alisema Mwanjala.Akiielezea changamoto hiyo, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija alikili kuwepo kwa tatizo hilo na kuongeza kuwa mbali na changamoto ya elimu duni ya zao la alizeti kwa maofisa ugani, aliitaja changamoto nyingine kuwa ni uwepo wa idadi ndogo ya maofisa ugani kama kikwazo kingine katika kumfikia mkulima mmoja mmoja.“Idadi yetu ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wakulima waliopo, hali hii imetulazimu wakati mwingine kuwatumia maofisa mifugo kusaidia kwenye maeneo ambapo hatuwezi kufika na hii kiukweli ni changamoto kubwa maana hata ambapo tunaweza fika wakati mwingine unakuta baadhi yetu uelewa wa zao hili kuwa ni mdogo na hata kuzidiwa maarifa na wakulima,” alisema Shija.Hadi sasa takribani maofisa kilimo 38 pekee ndio wanaotajwa kupata mafunzo maalumu kuhusu zao hilo ndani ya mkoa huo, idadi inayotajwa kuwa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wakulima takribani 33,400 waliopatiwa mafunzo rasmi ya zao hilo.Katika kuhakikisha mkoa wa Dodoma unaondokana na changamoto hiyo, na kulifanya zao hilo kama mojawapo ya mazao ya kibiashara yanayotegemewa na mkoa huo, uongozi wa Serikali mkoani humo umeanza mkakati wa kuwapatia mafunzo maalumu maofisa ugani ili kuwaongezea umahili katika kutoa elimu na huduma kwa wakulima.Hatua hiyo inatajwa kuwa itachochea katika kuongeza hamasa kwa wakulima wengi kujihusisha na kilimo cha zao hilo na hivyo kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza viwanda vitakavyokuwa vikichakata mazao yatokanayo na zao hilo. | kitaifa |
KIPA Juma Kaseja amesema juhudi zake ndizo zilizomfanya aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars. Kaseja alikuwa kipa namba moja ‘Tanzania one’ kwa muda mrefu kabla ya kuachwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Stars miaka sita iliyopita.Mwishoni mwa wiki iliyopita, kocha wa muda wa Taifa Stars, Etiene Ndayiragije alimjumuisha Kaseja kwenye kikosi chake kitakachocheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa kwa wachezaji wa ndani , Chan, dhidi ya Kenya mwishoni mwa mwezi huu.Akizungumza na gazeti hili, Kaseja ambaye kwa sasa ni kipa wa KMC alisema, amekuwa akifanya juhudi kubwa golini, ndio maana kocha Ndayiragije na benchi lake wameona anafaa kurudi tena Stars.“Nimefurahi kuitwa kwenye timu ya taifa baada ya miaka sita, naamini bado ninao uwezo wa kulipigania taifa langu langoni,” alisema. “Nikiangalia wachezaji walioitwa, naamini safari hii timu itafanya vizuri,” alisema.Kaseja aliyewahi kudaka Simba na Yanga kwa nyakati tofauti aliachwa kwenye timu ya taifa baada ya kuingia kwenye mgogoro na aliyekuwa kocha wa Stars Marcio Maximo aliyedai kipa huyo hakuwa mzalendo.Ilidaiwa Kaseja alifurahia timu ilipofungwa na Senegal kipa wa mechi hiyo akiwa Ivo Mapunda, ndipo Maximo alipochukia na kusema hatomwita kwenye timu yake tena. Inadaiwa pia Kaseja na Mapunda mpaka leo hawana maelewano mazuri. Akizungumzia kuhusu kujifua, Kaseja alisema hana muda wa kupumzika kwa sababu mpira ndio maisha yake.Kaseja na wachezaji wenzake wa KMC walipewa mapumziko ya siku tatu na kocha Jackson Mayanja, lakini Kaseja ameendelea na mazoezi kwa siku zote. Akizungumza jana katika mazoezi ya peke yake Kaseja alisema mpira ndio maisha yake na ili acheze vizuri anahitaji mazoezi hivyo hakuona umuhimu wa kupumzika“Mpira ndio maisha yangu na ili nifanye vizuri nahitaji mazoezi hivyo naendelea na mazoezi ili kujiweka sawa kwani natamani Taifa Stars ifanye vizuri tufike mbali,” alisema Kaseja. | michezo |
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi amesema hawezi kufungua shauri lolote mahakamani la kuomba ufafanuzi wa kikatiba kuhusu mgogoro uliopo kati ya Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad uliodumu kwa takribani miezi minne sasa.Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili hivi karibuni, walisema kuwa miongoni mwa watu ambao wanaweza kusaidia kupata ufumbuzi wa mgogoro huo kati ya Bunge na CAG ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Chama cha Mawakili. Miongoni mwa watu waliotoa ushauri huo ni Wakili wa Kujitegemea, Onesmo Mpinzile aliyesema kuwa kama busara ikishindikana katika kuumaliza mgogoro huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye Mlinzi Mkuu wa Katiba, anaweza kufungua shauri la kikatiba ili kuomba ufafanuzi wa kikatiba kuhusu mamlaka hizi mbili na kuiomba mahakama kutoa uamuzi.Baada ya kuulizwa jana kama yuko tayari kuufanyia kazi ushauri huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kilangi alisema hawezi kufanya hivyo kwa kuwa katika mgogoro huo hakuna jambo lenye mashaka litakalomfanya ahitaji tafsiri ya kisheria au jambo analolalamikia ili Mahakama itoe uamuzi. Kwa mujibu wa Profesa Kilangi, watu wanakwenda mahakamani kama kuna jambo ambalo tafsiri yake haieleweki vizuri ili Mahakama isaidie kutoa tafsiri au kuiomba mahakama ifanye kitu fulani juu ya jambo husika, na siyo kuomba namna nzuri ya kutatua mgogoro.Alisema kama kuna jambo linampa mtu mashaka au jambo analolalamikia ikiwemo jinai kama vile kupigwa, kuibiwa au madai kama vile kudhulumiwa, kuporwa kiwanja, hivyo mhusika anaweza kwenda kufungua shauri mahakamani kwa ajili ama ya kupata tafsiri ya kisheria au Mahakama itoa uamuzi wa jambo husika. “Katika mambo haya mawili, sijaona jambo la kunifanya niende mahakamani, kwa sababu ninapokwenda mahakamani kufungua shauri, naenda kulalamika au kudai kuhusu nini,” kama tafsiri, Katiba ipo na sheria zipo, naenda kuomba tafsiri ya kitu gani,” alieleza Profesa Kilangi.Alipoulizwa nini nafasi yake kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kupata suluhu ya mgogoro kati ya Bunge na CAG, Profesa Kilangi alisema yeye ana wajibu wa kuushauri mhimili wa utendaji na Bunge lina mwanasheria wake ambaye ana wajibu wa kulishauri Bunge, Spika au Katibu wa Bunge. Profesa Kilangi alisema pale anapotakiwa kutoa ushauri, huutoa ushauri huo kimya kimya kule alikoombwa kama ni kwa Rais, Waziri Mkuu, Waziri au mamlaka nyingine yoyote iliyoomba ushauri kwa kuwa mmiliki wa ushauri ni yule aliyeomba si aliyetoa ushauri.Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Rugemeleza Nshala, alisema kwa sasa TLS haijachukua uamuzi wowote kuhusu sakati hilo kati ya Bunge na CAG ikiwemo kufungua shauri mahakamani. Dk Nshala alisema TLS haiwezi kufungua shauri mahakamani mpaka Baraza la Utawala likae na kuamua kama kuna haja ya kufanya hivyo.Alisema hata kama kutakuwa na haja ya kuingilia kati mgogoro huo kwa ajili ya kupata ufumbuzi, si lazima wafungue shauri mahakamani, bali wanaweza kwenda kuonana na kila upande na kuwashauri ili hatimaye suala hilo liishe. Alisema ni vyema inapotokea tofauti kama hizo kwa viongozi wakazimaliza kimya kimya badala ya kuziweka hadharani. Mgogoro huo umeifanya jamii kugawanyika kimtazamo, kwa kuwa wapo wanaounga mkono uamuzi wa Bunge na wengine wanaunga mkono msimamo wa CAG. | kitaifa |
['Barcelona ingelimsaini mshambuliaji wa Tottenham Lucas Moura, 27, msimu huu lakini ilishindwa kufikia bei yake ya £45m. (Mundo Deportivo)', 'Juventus itawauza mshambuliaji Mario Mandzukic, 33, na kiungo wa kati Emre Can, 25, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari. (Goal)', 'Atletico Madrid bado inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, na wako tayari kuweka dau kubwa mwezi Januari. (AS - Spanish)', 'Juventus pia inawfuatilia wachezaji watatu wa Manchester United miongoni mwao kipa David de Gea, 28, Eric Bailly, 25, na Nemanja Matic, 31, kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufunguliwa msimu ujao. (Daily Mirror via Gazzetta Dello Sport)', 'Beki wa Liverpool Dejan Lovren, 30, amesema anatathmini uwezekano wa kuhamia AC Milan na Roma msimu huu wa joto. (Sportske Novosti via Liverpool Echo)', 'Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, alilia machozi alipoambiwa kuwa hawezi kujiunga tena na klabu yake ya zamani Barcelona. (El Chiringuito radio via Esporte - Portuguese)', 'Mshambulizi wa Barcelona Luis Suarez, 32, amesema Neymar alikua amefanya kila awezalo kuondoka Paris St-Germain. (Fox Sports Radio via Barca Blaugranes)', 'Callum Hudson-Odoi, 18, amabye ni mshambuliaji wa Chelsea yuko tayari kujitolea kwa mustakabali wake wa muda mrefu na klabu hiyo. (Football.london)', 'Winga wa zamani wa Liverpool Ryan Kent, 22, anasema wachezaji wawili wa zamani wa klabu hiyo Steven Gerrard na Michael Beale, ambaye sasa ni msimamizi wa Rangers, walikua kiungo muhimu katika mchakato wa wake kuhamia klabu ya Glasgow. (Express)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati anayelengwa na Manchester United Bruno Fernandes, 24, anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya na klabu ya Sporting Lisbon. (Record via Manchester Evening News)', 'Nottingham Forest walimtaka kiungo wa zamani wa Tottenham Marcus Edwards, 20, msimu huu. (The Athletic)', 'Aston Villa imewasilisha dau la £9m la kumnunua mshambulizi wa Celta Vigo Pione Sisto, 24, msimu wa joto. (Faro de Vigo - Spain)', 'Ndugu yake kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa miaka 26 atatumia muda wake mwingi Old Trafford kujiimarisha bada ya jaribio lake la kuhama klabu hiyo msimu huu kugonga mwamba. (El Chiringuito via Metro)', 'Mshambuliziwa Borussia Dortmund Marco Reus, 30,anasema yuko tayari kufanya kila awezalo katika uwezo wake kuhakikisha kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 20, anaungana nae katika klabu hiyo. (Sport1 via Lancashire Live)', 'Vilabu vya Real Sociedad na Athletic Bilbao nchini Uhispani vinajiandaa kumnyakua beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 30, ikiwa mchezaji huyo atapatikana. (Express)', 'Manchester United ina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, mwezi Januari mwakani kwa bei iliopunguzwa kandarasi yake ikiingia mwaka wa mwisho katika klabu hiyo .(Sun)', 'United itamenyana na Inter Milan kupata saini ya Eriksen. (Express)', 'Jaribio la Bayern Munich kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, msimu wa juto limetibuka baada ya kushindwa kufikia masharti ya mshahara wa mchezaji huyo. (Manchester Evening News)', 'Mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling, ambaye awali alijiunga na Roma kwa mkopo huenda akasalia katika klabu hiyo ya Italia zidi ya msimu huu. (Manchester Evening News)', 'Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa akidai kuwa amekataa ofa ya vilabu kadhaa vilivyotaka kumsajili. (mail)', 'Liverpool na Chelsea wanapania kumsajili mshambuliaji wa Wigan Athletic wa miaka 17- Muingereza Joe Gelhardt, ambaye ameshirikishwa mara tatu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Mirror)', 'Winga wa Chelsear Willian, 31, ananyatiwa na kocha wake wa zamani Maurizio Sarri ambaye sasa ni mkufunzi wa Juventus, wakati kandarasi ya nyota huyo Stamford Bridge ikiingia mwaka wa mwisho. (Express)'] | michezo |
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sophia Kaduma, wakati akifungua warsha ya wadau wa kilimo, kujadili mpango mkakati wa Tadb, Dar es Salaam jana.Kwa mujibu wa Wassira, benki hiyo itaweza kutoa mikopo ya bei nafuu endapo itashirikiana na Wizara ya Fedha, pamoja na wizara za kisekta, ikiwemo ya Kilimo, kutafuta fedha za gharama nafuu.“Kwa sababu nia yetu ni kuhakikisha uchumi unakua kupitia kilimo, tumedhamiria kushirikiana na TADB kutafuta fedha za gharama nafuu, zitakazowawezesha wakulima kugeukia kilimo bora cha kisasa, wapate maendeleo na kuchangia kukuza uchumi,” Wassira anasema na kuongeza kuwa, mapinduzi ya kilimo yanawezekana kwa kuwa Serikali iko tayari kutoa mchango wake.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Adolf Mkenda alisema, TADB ni chachu ya kuleta mageuzi kiuchumi, hivyo wizara yake haina budi kuhakikisha inafanikiwa kumwezesha mkulima mtaji, ajikite kwenye kilimo chenye tija.“Mtu mmoja akiwezeshwa kwa mkopo nafuu anaweza kuzalisha mazao ya kilimo mengi ya kutosha kuuzwa na kulisha idadi kubwa ya watu. Watu wanne wakiwezeshwa kulima kilimo chenye tija pia wataweza kulisha wengi na kuuza ziada itakayo kuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla. Hivyo ndivyo kilimo cha tija kinavyoleta mabadiliko, tutahakikisha benki hii inafanikiwa,” alisema Mkenda.Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Thomas Samkyi alisema lengo la Serikali kuanzisha benki hiyo si kuishindanisha na ningine bali kuwasaidia wakulima kimitaji, wapate maendeleo na kuchangia kukuza uchumi.“Tunachokifanya sasa ni kuangalia maeneo ya vipaumbele ili, ndani ya muda mfupi tuweze kuanza kuwakopesha wakulima wa ngazi zote, wageukie kilimo chenye tija,”Samkyi alisema. | uchumi |
WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko ameitaka kampuni inayochimba madini ya urani katika mto Mkuju wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, Uranium One kutosita kuwasiliana naye pindi wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa mradi wao.Aliyasema hayo katika kikao chake na watendaji wa kampuni hiyo kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma.Aidha, Biteko alisema maombi yote ya leseni kubwa za uchimbaji wa madini zinawasilishwa katika Baraza la Mawaziri ili kuridhiwa baada ya wawekezaji kuonesha nia na kuwasilisha maombi ya leseni hizo.Biteko amekiri kuwa ana uelewa wa kile kinachoendelea katika uwekezaji huo kutokana na ushirikishwaji alioupata kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Angella Kairuki kupitia vikao mbalimbali alivyoshiriki.Akizungumzia lengo la ujio wao katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uranium One, Frederick Kibodya amesema ni kuelezea maendeleo waliyofikia katika uwekezaji huo pamoja na kumpongeza Biteko kwa kuteuliwa kuongoza wizara hiyo.Kibodya amesema, “Uteuzi huo umelenga katika kukuza sekta ya madini ikiwa ni pamoja na mradi wa uchimbaji wa madini ya urani”.Akizungumzia uwekezaji uliofanyika mpaka sasa katika mradi huo, amesema ni dola za Marekani milioni 200 (zaidi ya Sh bilioni 500) kutoka mradi ulipoanza mwaka 2009.Akizungumzia manufaa ya mradi huo, Kibodya amesema ni pamoja na kusaidia katika kukuza teknolojia nchini. Alisema madini hayo yakichimbwa yanatumika katika kuzalisha umeme ambayo ni teknolojia mpya nchini.Mradi utasaidia katika kuongeza ajira nchini. Aliendelea kufafanua kuwa kwa kipindi cha ujenzi wa mradi wanatarajia kuajiri Watanzania 1,600 kwa kipindi cha miezi 18.Alibainisha kuwa kutakuwepo na uzalishaji wa ajira zisizo rasmi kiasi cha watu 4,500 wakati wa ujenzi na 2,300 pindi uzalishaji utakapoanza.Amesema mradi utasaidia katika kuhamisha utaalamu kutoka kwa wawekezaji kwenda kwa wazawa na mradi umelenga katika kutoa elimu ya ajira na utaalamu kwa wazawa.Pia Kibodya amesema mradi unatarajia kuliingizia Taifa pato la dola za Marekani milioni 220 kama kodi kwa mwaka, kiasi ambacho kitakuwa kikibadilika kadri uzalishaji unavyoongezeka.Mradi wa uchimbaji madini ya urani katika mto Mkuju unafanywa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na mbia wa Kampuni ya Mantra anayejulikana kama Rosatom. | uchumi |
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya HabariLeo, Daily News na SpotiLeo, imetoa washindi watano katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018, zinazotolewa kila mwaka na Baraza la Habari nchini (MCT).Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya 10, zimekuwa zikishirikisha waandishi wa habari wa kada mbalimbali kutoka katika vyombo tofauti vya habari, yakiwamo magazeti, runinga na redio.Katika tuzo hizo, Alfred Lasteck wa HabariLeo alishinda Tuzo ya Kodi na Ukusanyaji Mapato kwa habari yake ya jinsi baadhi ya wafanyabiashara wanavyoidanganya serikali katika eneo maarufu la kibiashara la Kariakoo, Dar es Salaam kwenye suala la kodi.Adam Lutta wa Habari- Leo naye alitwaa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Habari za Usalama Barabarani, wakati Tuzo ya Mpigapicha Bora wa Magazeti ilikwenda kwa Rahel Palangyo kwa picha inayowaonesha polisi wakimbeba msobesobe shabiki wa mpira wa miguu.Mwandishi Mkongwe wa Daily News, Meddy Mulisa alishinda Tuzo ya Utalii na Uhifadhi kwa habari yake ya Tathmini ya Hifadhi ya Taifa ya Bugiri kuvutia watalii zaidi. Wakati huohuo, tuzo ya Mwandishi Bora wa Habari za Michezo na Burudani, ilikwenda kwa Sauli Gilliard anayeandikia gazeti la Daily News.Waandishi wengine walioteuliwa kuwania tuzo hizo kutoka kampuni ya magazeti ya serikali, ambao walifanikiwa kukabidhiwa vyeti, kama ishara ya kutambuliwa kwa mchango wao katika tasnia ya habari ni Abdallah Msuya (Daily News) na Frank Leonard (HabariLeo).Mshindi wa tuzo za habari za kodi, Lasteck alishukuru kwa ushindi huo akisema, “Haikuwa kazi rahisi kushindana na waandishi wengine bora waliopo nchini. Ni bahati lakini pia juhudi zilikuwa mbele.“Pia uongozi thabiti wa TSN ukiongozwa na wahariri mahiri wa Habari- Leo, ulichangia kwa kiasi kikubwa kunifanya nishinde tuzo hii. “Ni heshima kwangu na kwa kampuni yetu ya Serikali.”Kwa upande wake, Rahel Palangyo ambaye aliibuka miongoni mwa wanawake waliojinyakulia tuzo katika hafla hiyo alisema, “Nashakuru kupata tuzo hii ambayo ina maana kubwa sana, hasa ukizingatia changamoto mbalimbali wanazopitia wanawake katika jitihada za kupata mafanikio kwenye nyanja mbalimbali.”Akiwapongeza washindi hao, Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah alisema kuwa siri ya mafanikio ya TSN kwenye tuzo hiyo, inatokana na kampuni kuwekeza nguvu kwenye maendeleo ya kitaaluma ya waandishi, lakini kujikita kuandika habari zinazoigusa jamii.Tuma alisema, “Mafanikio haya ni makubwa na ya kipekee kwetu. Tumekuwa na waandishi ambao wamekuwa na hamasa kubwa ya kufanya uandishi kwa kugusa maisha ya wanajamii, lakini pia wenye weledi na uwezo mkubwa wa kufuatilia mambo kwa undani.“Wengi wao tunawawezesha kwa kuwapa mafunzo mbalimbali, lakini pia tunashauriana nao jinsi wanavyoweza kuandika habari bora na zenye kiwango bora.“Hata baada ya ujio wa mitandao ya kijamii ambayo imekuja kuongeza uharaka wa kutoa habari, sisi tumeangalia kama fursa ya kuanza kufuatilia habari kwa undani ili tuweze kuzichapisha kwenye gazeti.”Tuma aliahidi wasomaji na watanzania kuwa magazeti hayo yataendelea kutoa habari zenye kugusa jamii.Meneja Masoko na Mauzo, Januarius Maganga aliwaambia washindi hao kuwa ushindi walioupata ni heshima kubwa na wataendelea kuthamini jitihada hizo kwa maendeleo ya kampuni kwa ujumla. Mhariri wa gazeti la Daily News, Pudenciana Temba alisema:“Hongereni sana, tunajivunia ushindi wenu kama ishara ya kielelezo cha ubora wa kazi mnazofanya, haikuwa rahisi lakini nyie mmeweza.”Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Tuzo hizo, Kajubi Mukajanga aliwashukuru waandishi waliojitokeza kuwasilisha kazi zao, ambapo jumla ya kazi 644 zilipokewa ambazo ni ongezeko la asilimia 18 ukilinganisha na mwaka uliopita. Jopo la kuteua washindi wa tuzo hizo, lililoongozwa na Mhariri mkongwe, Kiondo Mshana.Vyombo vya habari vya kielektroniki viliongoza kwa kuingiza kazi 359 sawa na asilimia 55.7, vikifuatiwa na magazeti ambapo kazi 285 sawa na asilimia 44.3 ziliwasilishwa.Akimkaribisha mgeni rasmi, Profesa Chris Maina Peter kwenye hafla hiyo, Mukajanga alisema jumla ya waandishi wa habari 449 nchini kote walishiriki, ambapo kati yao wanaume ni 314 sawa na asilimia 70 na wanawake ni 135 sawa na asilimia 30.Hafla hiyo ya utoaji tuzo ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ambaye alishuhudia wateule 81 wakipanda jukwaani kuwania tuzo hizo ambapo kati yao 48 ni wanaume sawa na asilimia 59 na wanawake 33 sawa na asilimia 41, ambapo mshindi wa jumla alikuwa ni Salome Kitomary wa gazeti la Nipashe. | kitaifa |
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Mendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine ametoa mwito kwa vyama vya ushirika katika zao la korosho, kuwekeza kwenye viwanda vya kubangua korosho ili kuongeza thamani na kupata bei nzuri sokoni.Ametoa mwito huo alipofanya ziara ya Operesheni ya Korosho wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, kujionea hali ya zao la korosho lilivyo na kufanya ukaguzi wa awali kwa ajili ya malipo ya zao hilo, pia kutazama uwezo wa viwanda vya kubangua korosho kama inajitosheleza.“TADB ipo tayari kutoa mkopo kwa vikundi ushirika kuanzisha viwanda vya kubangua korosho nchini ili kuongeza thamani zao hilo ili liwe na soko zuri duniani, lengo kubwa ni kumhakikishia mkulima soko la korosho yake,” alisema Justine.Aliongeza kuwa jambo kubwa ni utayari wa wana ushirika katika kuandaa mpango wa biashara, utakaoongeza thamani ya zao hilo kwa kujenga maghala, viwanda vya kubangua korosho ili faida iliyokuwa ikipotea kwa kuuza korosho ghafi iweze kubaki kwa mkulima.“Uwezo wa kuanzisha viwanda hivi upo kwa Shirika la Kuhudumia Maendeleo Viwanda Vidogo (SIDO) lina teknolojia na wataalamu wanaoweza kusimamia ujenzi wa kiwanda cha kubangua na kuweka kwenye vifungasho,” alieleza Justine.Alisema kinachotakiwa ni vyama vya ushirika kuunda kampuni ambayo wao watakuwa wanahisa na TADB itatoa mkopo wa kuweza ujenzi wa viwanda hivi, lengo likiwa kumuondolea mkulima changamoto ya kukosa soko ya korosho ghafi.“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli inalenga kumsaidia zaidi mtu wa hali ya chini akiwemo mkulima na kama benki imejipanga kutekeleza azma hiyo serikali ya kuwaondolea changamoto wakulima katika maeneo mbalimbali hapa nchini.Alisema nchi ina uwezo wa kuzalisha korosho kuanzia tani 200,000 na kuendelea hivyo, kama juhudi za kuziongezea thamani zitafanya soko kuimarika na kuongeza hamasa kwa wakulima kulima zaidi korosho nchi. Justine alisema vyama vya ushirika na wawekezaji nchini waiangalie hiyo fursa ya kuanzisha kiwanda cha kubangua korosho, kitakachosaidia kuongea thamani zao hilo ambalo lina soko zuri duniani.“TADB itaendelea kutoa ushirikiano kwa wakulima kwa kutoa mikopo ya pembejeo na dhana za kilimo ili kuweza kukuza uzalishaji wa korosho hapa nchini,” alisema. Alisema kuwa benki yake ipo katika kuchagiza maendeleo ya sekta ya kilimo hapa nchini.Alisema utekelezaji wa Mpango wa Awamu ya Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP- II), unategemea ushiriki wa wadau wote kutoka sekta za binafsi na umma, hivyo TADB ni miongoni mwa wadau katika kufanikisha utekelezaji wake. Mapema Juni mwaka huu, Rais Magufuli alizindua ASPD-11 lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji zaidi utakaofanikisha ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025. | kitaifa |
HUKU takwimu zikionesha kuongezeka kwa ukatili wa watoto hapa nchini, Mbunge Salma Kikwete ameshauri kuwepo kwa kampeni kwa lengo la kuepusha vitendo hivyo vinavyoathiri kundi hilo kimwili, kiakili na kihisia. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, 2016, watoto 10,000 walifanyiwa ukatili huku mwaka 2017 watoto zaidi ya 13,000 ambapo mikoa inayoongoza kwa vitendo hivyo ikiwa ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Tabora na Singida. Ripoti hiyo ya utafiti inaonesha wasichana watatu kati ya 10 na mvulana mmoja kati ya saba walisema walifanyiwa ukatili wa kijinsia kabla ya kufikisha miaka 18.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Malenzi Chanya, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Thrive For Community Elevation Foundation (TCE), Marynsia Mangu, zaidi ya asilimia sita ya wasichana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 24 walipata mimba ambapo kila tukio moja la ujauzito, ukatili ilifanyika.“Kushikwa bila ridhaa au kutomasa na jaribio la kufanya ngono ndio udhalilishaji uliofanywa mara nyingi ukifuatiwa na jaribio la kufanya ngono, asilimia asilimia 6.9 ya wasichana na asilimia 2.9 ya wavulana walilazimishwa au walishurutishwa kufanya ngono kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.Naye mwenyekiti wa TCE, Rahim Ndambo alisema mkakati wa taasisi hiyo ni kuzunguka kata hadi kata katika kila mkoa ikiwa ni pamoja na kampeni mbali mbali kwenye vyombo vya habari ili watoto wapate haki zao za msingi na wazazi waache kuwachpa, ikiwa ni pamoja na kuwafanyia vitendo vingine vya ukatili ikiwemo kuwaingilia kingono. | kitaifa |
MAOFISA Madini nchini wametakiwa kutobagua migodi midogo kwa kuelekeza nguvu kwenye migodi mikubwa tu huku wakisisitizwa kutatua migogoro kwenye maeneo yao ya kazi na kuelezwa kuwa, watakaobainika wakibagua migodi hiyo na kutotatua migogoro wataondolewa kwenye nafasi zao.Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini aina ya Sapphire wakati wa ziara yake katika kijiji cha Masuguru, wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara hiyo ikilenga kukagua shughuli za uchimbaji madini wilayani humo pamoja na kusikiliza kero za wachimbaji katika migodi hiyo na alipokea kero za kutaka kutengewa maeneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji, bei elekezi za madini ikiwemo kuunganishwa na huduma ya umeme kwenye migodi yao.Akizungumza kijijini hapo, alimtaka Ofisa Madini Mkoa wa Ruvuma hukakikisha anaishughulikia kero hiyo na kuitatua mara moja na kuongeza kuwa, Rais anataka wachimbaji nchini wachimbe madini, hivyo maofisa madini kote nchini wahakikishe wanashughulikia kero katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kusuluhisha migogoro.Alisema kuwa kama mgogoro ni mkubwa wapo viongozi wa vyama vya wachimbaji wahakikishe kuwa wanafikisha migororo hiyo sehemu husika ili iweze kutatuliwa.Akijibu ombi la ruzuku, aliwataka wachimbaji wadogo kujiunga katika vikundi vidogo vidogo ili iwe rahisi kwa wachimbaji hao kufikiwa ikiwemo kupatiwa huduma za leseni, elimu, vifaa, kuwamilikisha, kuwapatia mikopo na kuwafuatilia jambo ambalo litapelekea wafanye kazi kwa urahisi na kwa kulipa kodi za serikali na wao kubaki na kipato kitakachowezesha maisha bora.Akizungumzia suala la madalali aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni ya kufanya shughuli hizo ikiwemo vifaa vya kupimia madini na kuwataka kulipa kodi na kuwatahadharisha wachimbaji wanaoshirikiana na madalali wasiokuwa na leseni kuacha kwani kwa kufanya hivyo wote wanahesabika kuubia taifa.Kwa upande wake, Ofisa Madini Mkoa wa Ruvuma, Abraham Nkya alisema kuwa mkoa huo tayari umetenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kwamba watashirikiana na wachimbaji hao ili suala hilo liweze kuwasilishwa Tume ya Madini kwa ajili ya hatua zaidi. | kitaifa |
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Johnson Mfinanga wakati aliitaja baadhi ya mikakati iliyoundwa juu ya msingi wa serikali ya awamu ya nne katika kuboresha zaidi huduma za kampuni hiyo.“Ni katika kipindi hiki cha awamu ya nne chini ya Rais Kikwete ndio tuliweza kuanzisha safari zetu za kwenda visiwa vya Comoro na tumekuwa tukizidi kuongeza safari zetu zaidi kuelekea huko kwa kuwa tumebaini uamuzi huu umekuwa na tija kwa wananchi wa mataifa haya mawili,’’ alibainisha Mfinanga.ATCL kwa sasa imeongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa hivyo kutoka mara tano hadi kufikia mara nane kwa wiki. Kwa sasa ATCL ndio kampeni pekee ya ndege hapa nchini inayotoa huduma zake kutoka Dar es Salaam kuelekea visiwa vya Comoro.Mfinanga alibainisha mpango wa kampuni hiyo wa kutambulisha safari zake za moja kwa moja baina ya visiwa vya Comoro na Zanzibar kabla ya mwisho wa mwaka huu kutokana na uhitaji mkubwa wa soko linachochewa na fursa za kibiashara baina ya visiwa hivyo.Aliongeza kuwa pamoja na mipango hiyo ATCL pia inaendelea kuboresha huduma zake kuelekea mkoani Mtwara na imekuwa ikijivunia kuwa kiungo muhimu katika usafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoa huo ambao kwa sasa unajipanga kuchangamkia fursa ya uchumi wa gesi iliyovumbuliwa hivi karibuni.Akizungumzia mipango ya ATCL katika kujipanua zaidi, Mfinanga alisema kwa sasa kampuni hiyo inaandaa mpango mkubwa wa miaka mitano ambao unatarajiwa kukamilika na kuwekwa wazi hivi karibuni. | uchumi |
MESUT Ozil ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Arsenal na hakuna wa kumlinganisha naye kwa wachezaji wanaocheza nafasi yake kwenye kikosi cha washika bunduki hao.Bado anaonekana kutoendana sana na mfumo wa kocha Unai Emery, lakini hakuna namna zaidi ya kocha huyo wa zamani kujitahidi kupata kile ambacho Ozil anaweza kumpa na ambacho wengine hawana uwezo huo. Inaelezwa Emery, kocha wa zamani wa Sevilla na Paris Saint-Germain anataka kumuona kiungo huyo kutoka Ujerumani akihusika zaidi katika kukaba na kuisaidia timu kupata matokeo, mfumo ambao unaelekea kumshinda Ozil.Alimuweka kando kwenye mchezo wa kombe la Carabao dhidi ya wapinzani wao wakubwa Tottenham Hotspurs ambapo Arsenal ilifungwa mabao 2-0 kwa kile alichokuja kueleza baadae kuwa ilikuwa ni kwa sababu za kimbinu, aliona Ozil asingetosha mahitaji ya mchezo huo. Kitendo hicho kilizusha hasira kwa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii ambao wanaona kocha huyo kutoka Hispania hamtendei haki Ozil na kwamba timu bila yake inakosa ubunifu kwenye eneo la ushambuliaji.Henrik Mikhitaryan, Alex Iwobi na nyota wengine wote wanaocheza nafasi moja na Ozil hawana ubunifu wa kuitengenezea Arsenal nafasi za mabao, lakini pia hawana utulivu wa kukaa na mpira na kuituliza timu wakati wanashambulia kama ambavyo Ozil anafanya. Alirejea kwenye kikosi cha kwanza kwenye ushindi wa Arsenal wa mabao 3-1 ambapo alihusika kwenye mabao mawili yaliyofungwa na Pierre Emerick Aubameyang na lile lililofungwa na kiungo wa kimataifa wa Nigeria Alex Iwobi.Katika mchezo huo, Mesut Ozil alivaa kitambaa cha unahodha cha timu hiyo ambapo mbali na kuhusika na mabao haya mawili lakini pia alipiga mpira mkubwa na kusababisha kupata sifa nyingi kutoka kwa vyombo vya habari vya England na wachambuzi. Unai Emery anamhitaji Ozil, anapaswa kuelewa namna ya kumbadilisha Ozil ili nyota huyo awe na mchango ule anaotaka kwenye kikosi chake. Ni mchezaji wa kipekee na hakuna wachezaji wengi wa aina yake katika dunia ya leo.Philip Lahm ambae aliwahi kucheza na Ozil kwenye timu ya taifa ya Ujerumani aliwahi kusema kuwa Ozil ni kiungo mwenye akili kuliko viungo wote katika bara la Ulaya, lakini kocha Jose Mourinho alisema hakuna nakala ya Ozil hata ile mbaya. Sifa hizo na nyingine nyingi zinathibitisha ubora wa kipekee aliyonao kiungo huyo mwenye asili ya Uturuki ambapo Unai Emery anatakiwa kujua namna gani ya kumtumia na kupata ubora wake.Mesut Ozil anaweza asiwe mzuri sana kwenye kukaba lakini ana ubora mkubwa ambao hata wachezaji wenye ubora wa kukaba hawana uwezo wa kufanya kile Ozil anaweza kukifanya kwa Arsenal. Ozil kama walivyo viungo wengi wachezeshaji duniani wanatakiwa kuzungukwa na viungo wenye uwezo mkubwa wa kukaba ndivyo unaweza kupata ubora wake.Kwenye kikosi cha Arsenal, Ozil anaonesha kiwango bora na kukupa kile ambacho wachezaji wengine kwenye kikosi cha timu hiyo wanashindwa kukupa kama akipangwa sambamba na kiungo Lucas Torreira wa Uruguay. Mechi nyingi Ozil alizopangwa kucheza na Lucas Torreira kwenye kiungo huku kwenye kiungo cha juu akicheza Granit Xhaka, Arsenal imekuwa ikicheza soka la hali ya juu na Ozil amekuwa akitoa mchango muhimu mfano kwenye ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Leicester.Kumbe pamoja na mapungufu yake kwenye ukabaji Ozil akichezeshwa na viungo sahihi wenye uwezo mkubwa wa kukaba, anakupa mara mbili zaidi ya kile anachokupa. Hakuna sababu ya kocha Unai Emery kuhangaika na sifa moja tu ambayo Mesut Ozil anakosa na kuacha sifa nyingi ambazo kiungo huyo mchezeshaji anazo; kama anakuwa bora zaidi ukimpanga na Lucas Torreira basi anatakiwa kufanya hivyo sio kumuweka benchi. | michezo |
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Emma Oriyo alisema programu hiyo ya mafunzo ni ya miaka minne mfululizo na awamu ya kwanza inaanza mwezi huu na kukamilika Machi 3 mwaka ujao.Emma alisema programu imelenga kuwanufaisha wauzaji wadogo wa bidhaa zao nchi nzima ambapo awamu ya kwanza watawafundisha wauzaji 1226 kwa kuwapatia mafunzo maalumu kwa ajili ya kuboresha na kuendeleza biashara zao.“Mafunzo haya yatakuwa yakiendeshwa kikanda kwa muda wa siku nne. Yataanzia Kanda ya Pwani na Kusini na kumalizia Kanda ya Ziwa,” Alisema Emma na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wauzaji wadogo kukuza biashara zao na kuimarisha kipato na maisha yao kwa ujumla.Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Meneja Mauzo wa TBL, Patrick Swai alisema kampuni yao imeamua kuwapa elimu wauzaji wadogo kwani wengi wao hawana uwezo wa kugharamia mafunzo hayo ambayo hulipiwa gharama kubwa. Alisema katika kutoa mafunzo hayo, TBL inashirikiana na wataalamu wa ushauri wa biashara. | uchumi |
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema gharama za matibabu nchini hazijabadilika badala yake, zimezidi kupungua ili wananchi wamudu na kupata hduuma bora za afya.Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Idara Kuu ya Afya, kumekuwapo na taarifa za upotoshaji umma juu ya mapendekezo mapya ya gharama za matibabu kwa hospitali za umma. Taarifa hiyo imeeleza serikali imejizatiti kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwenye vituo vya afya nchini huku ikiongeza bajeti ya dawa, vifaa na vifaa tiba.“Wizara inapenda kutaarifu umma kuwa gharama za matibabu hazijabadilika, badala yake, zimekuwa zikipungua ili kwamba wananchi hata wenye kipato cha chini waweze kuzimudu,” ilieleza taarifa hiyo. Kuhusu upotoshwaji wa gharama za matibabu, taarifa hiyo ilisema wizara imebaini kuwepo kwa taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kupotosha umma. Ilieleza kuwa taarifa hiyo potofu iliyosambaa kupitia akaunti ya mtandao wa Facebook ya Hamenya Salehe, Mwana Ukawa ikidai kuwa serikali imetoa mapendekezo mapya ya gharama za matibabu.Aidha, kupitia mtandao huo, taarifa hiyo potofu imeonesha kuwa gharama za kujifungua kwenye hospitali ya umma zitakuwa ni Sh 300,000 na Sh 25,000 kwa ajili ya kadi ya kliniki. Taarifa hiyo ilieleza wizara inakemea taarifa hizo za upotoshaji zinazochafua taswira ya serikali katika jamii, na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayebainika kusambaza taarifa potofu kwa umma. Imeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuchukua hatua kwa wapotoshaji wa aina hiyo.Kupitia ukurasa huo wa facebook iliandikwa mapendekezo mapya ni ada ya kujifungua hospitali kuwa Sh 300,000 na kadi ya kliniki Sh 25,000 na kuwa mbali na mapendekezo hayo, mengine yaliyopangwa ni kuwa wagojwa wa Ukimwi na Kifua Kikuu (TB) watakuwa wanajigharamia dawa kwa fedha zao. Ukurasa huo ulidai mapendekezo mengine ni kununua vidonge vya uzazi wa mpango kutokana na wahisani kusitisha udhamini katika huduma hizo kutokana na serikali kudaiwa kukiuka haki za binadamu. | kitaifa |
['Klabu ya Arsenal imefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania na Barcelona, Luis Enrique kuhusu mpango kuchukua nafasi ya Unai Emery. (El Confidencial, kupitia Metro)', 'Klabu ya Tottenham wapo tayari kutoa ofa ya pauni 50m kwa Memphis Depay mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, ambaye alihamia Klabu ya Ufaransa Lyon kutoka Manchester United mnamo Januari 2017.(Sunday Mirror)', 'Manchester United inajipanga kumsajili tena mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 27, katika msimu ujao wa kiangazi. (The Sun on Sunday)', 'Chelsea inataka kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 24, kama adhabu ya kufungiwa itafutwa mwezi Januari. (Sunday Mirror)', 'Pia timu ya Chelsea wanataka $ 5m kutoka kwa klabu yoyote inayotaka kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud, 33, mnamo Januari.(Sunday Express) ', "Paris St-Germain kwa mara ya kwanza wamefanya majadilano ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappé lakini hakuna ofa yoyote iliyotolewa. (L'Equipe, via Marca)", 'Meneja wa Liverpool Jürgen Klopp hayupo tayari kumuachia Dejan Lovren, mwenye umri wa miaka 30, aondoke klabuni hapo kwenye dirisha dogo la uhamisho Januari.(Football Insider)', 'Juventus wanaweza kuwatoa wachezaji wake wanne kwenda Manchester United akiwemo mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic, 33, kiungo wa Ujerumani Emre Can, 25, beki wa Italia, Dani Rugani, 25, na kiungo wa Ufaransa, Blaise Matuidi, 32, kubadilishana na kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Tuttosport, kupitia Sunday Express)', 'Manchester City ipo tayari kumpatia Mholanzi Giovanni van Bronckhorst fursa ya kufanyiwa majaribio kama mrithi wa Pep Guardiola kwa kumteua kuwa kocha kwa klabu mwenza New York. (Sunday Mirror)', 'Everton inapokea maombi ya kumuuza kipa wa Uholanzi Maarten Stekelenburg Januari, huku mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu. (Football Insider)', 'Wolves watakamilisha usajili wa mlinzi mwenye umri wa miaka 17 wa PSV Eindhoven, Nigel Lonwijk kwa kitita cha £200,000 ifikapo Januari. (ED, via Birmingham Mail) ', 'Uefa inatazamia kuandaa fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya 2024 nchini Marekani, huku New York ukiwa ndio mji unaopigiwa upatu katika hatua itakayochangia mechi hiyo kuchezwa kwa mara ya kwanza nje ya Ulaya. (Morning Consult)'] | michezo |
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu Serikali itaanza kutekeleza utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blue print) kwa lengo la kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.Alisema hayo jana wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, jijini Dodoma na kuongeza kuwa wakati kazi hiyo inaendelea Serikali itafanya ufuatialiaji kuhusu utekelezaji wa mpango huo na kutathmini kama lengo limefikiwa.“Utekelezaji wa mpango huo unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kurahisisha mazingira ya kufanya biashara nchini, unaojidhihirisha kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo imefuta tozo kwamishi 54 zilizobainishwa kwenye mpango huo,” alisema. Waziri Mkuu ametaja tozo zilizoondolewa au kupunguzwa ni pamoja na zinazosimamiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi hususan kwenye Sekta ya Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Maji.Kadhalika, Waziri Mkuu alisema katika kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unaleta tija na kuelekeza Wizara ya Viwanda na Biashara ishirikiane na Ofisi ya Waziri Mkuu kusambaza blue print pamoja na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa wizara zote kwa ajili ya kusimamia utekelezaji katika maeneo yao. Alisema kupitia mpango wa bajeti ya 2019/2020, serikali itaendelea kuweka mazingira rahisi ya ufanyaji biashara kwa kutoa unafuu katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli nyingine jumuishi.Wakati huohuo,Waziri Mkuu alisema katika kukabiliana na kilimo tegemezi cha mvua hususani kwenye zama hizi za mabadiliko ya tabia nchi, serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuwatoa wananchi katika kilimo hicho. Alisema hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni pamoja na kuunda upya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo inalenga kuiwezesha tume hiyo kusimamia ipasavyo shughuli za umwagiliaji na pia Serikali imehamishia tume hiyo Wizara ya Kilimo ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuendeleza kilimo nchini.“Ili tuweze kufikia lengo la kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 475,056 za sasa hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025, tayari nimeielekeza Wizara ya Kilimo isimamia kwa karibu na kutekeleza majukumu yake kwa weledi,” alisema. Waziri Mkuu alisema Wizara ya Kilimo inatakiwa ihakikishe inasimamia vema miradi 22 ya umwagiliaji inayoendelea sasa pamoja na miradi mipya minane itakayojengwa nchini katika pindi cha mwaka wa fedha 2019/2020. | kitaifa |
BAADA ya kusimama kwa siku kadhaa kupisha mechi za kimataifa, Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea tena mwishoni mwa wiki hii huku kila timu ikiwa na moto wa kutaka kushinda. Ligi ilisimama kuipisha timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza na Uganda mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Mataifa Afrika, Afcon 2019, mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Kampala na kumalizika kwa suluhu.Timu zote 20 zipo kwenye maandalizi kabambe kuhakikisha zinafanya vizuri kwenye mechi hizo ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi. Washindi wa pili msimu uliopita, Azam wataendelea na kampeni zao Ijumaa wakiwa ugenini kucheza na Mwadui FC ya Shinyanga saa nane mchana huku kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, African Lyon ikiwaalika Wagosi wa Kaya, Coastal Union kutoka Tanga.Azam inaingia uwanjani na nguvu mpya baada ya kurejea kwa mshambuliaji wake mpya Donald Ngoma iliyomsajili msimu huu kutokea Yanga. Ngoma hajaonekana uwanjani muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, lakini sasa anaendelea vizuri na ameshaanza mazoezi takriban wiki mbili zilizopita. Jumamosi, mabingwa watetezi Simba watakuwa ugenini uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara kumenyana na Ndanda iliyoahidi kupindua meza na kufuta uteja wa kufungwa na Simba mara nyingi. Siku hiyohiyo, Prisons itaialika Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.Mechi nyingine siku hiyo ni kati ya Mbao watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikaribisha JKT Tanzania huku KMC ikiwaalika Singida United kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Lipuli FC itakuwa nyumbani uwanja wa Samora Iringa kuwakabili Mtibwa Sugar na mechi ya mwisho siku hiyo itakuwa Mara ambako wenyeji Biashara watakwaana na Kagera Sugar.Jumapili ya Septemba 16 kutakuwa na mechi mbili, mabingwa wa zamani Yanga wakiwa nyumbani Uwanja wa Taifa kuwaalika Stand United ya Shinyanga na kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya wenyeji Mbeya City watacheza mechi yao ya kwanza nyumbani msimu huu dhidi ya Alliance ya Mwanza. Mpaka sasa Mbao FC, ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja huku Azam FC wakiwa nafasi ya pili na pointi zao sita sawa na mabingwa watetezi Simba waliopo nafasi ya tatu.Yanga wapo nafasi ya 10, baada ya kucheza mechi moja na kuchukua pointi zote tatu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ufunguzi. Na timu za Mwadui FC na Mbeya City zinaburuza mkia zikiwa hazina pointi, City wakipoteza michezo yote mitatu wakati Mwadui michezo miwili. Kiujumla timu tatu zinazoshika nafasi za juu zimeonekana kufanya vizuri kwenye mechi za awali hasa Azam FC ambao mpaka sasa katika mechi mbili wamefunga mabao matano huku wakiwa hawajaruhusu nyavu zao kutikishwa.Wanafuatiwa na Simba ambao wamefunga mabao matatu yote yakifungwa na mshambuliaji wake nyota Meddie Kagere na wao hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa wakati vinara Mbao FC wao wameruhusu bao moja na kufunga mabao matatu kwenye mechi zao tatu walizocheza. Simba, Yanga na Lyon zilitumia mapumziko kujiweka sawa kwa kucheza mechi za kirafiki ambapo Simba ilicheza dhidi ya AFC Leopard ya Kenya na kushinda mabao 4-2 huku Yanga ikijipima na Lyon na kushinda bao 1-0. | michezo |
MWIGIZAJI maarufu nchini Wema Sepetu ameachiwa huru kuendelea na shughuli zake za filamu baada ya Bodi ya Filamu kujiridhisha kuwa ametekeleza adhabu waliyompa kwa asilimia 75.Wema alifungiwa tangu Oktoba mwaka jana kujihusisha na filamu kwa muda usiojulikana, baada ya kusambaa kwa picha yake kwenye mitandao ya kijamii iliyokuwa na maudhui ya ngono.Akizungumzia kumfungulia msanii huyo jana, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisoo amesema:“Kuna masharti kadhaa tuliyompa ya adhabu ametekeleza na tumeridhishwa tukiamini sasa hivi matukio yake hayatajirudia.“Masharti tuliyompa ni pamoja na kumtaka atuandikie changamoto anazopata kwenye kazi yake ambapo alieleza kukosa fedha za kutoa filamu yake iliyopita na rushwa ya ngono. Pia, alieleza mafanikio ni kupata tuzo za sinema zetu kupitia filamu ya Heaven Sent, pamoja na kueleza shughuli za kijamii anazofanya,” amesema.Pia, amesema Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006, ameahidi kubadilika na kwamba itaendelea kumfuatilia mwenendo wake kwani bado asilimia 20 ambazo anatakiwa kuzitekeleza.Fisoo alisema lengo la serikali sio kumkomoa mtu bali ni kumsaidia na kumtaka msanii huyo kutobweteka na kuahidi iwapo msanii huyo atarudia matukio yake atachukuliwa hatua kali zaidi.Kwa upande wake, Wema alisema “nadhani mnajua jinsi ninavyoipenda kazi yangu, naihusudu, naithamini kwa hiyo mtegemee vitu vingi sana vipya kutoka kwangu vizuri, nawaahidi watanzania kuwa sitowaangusha”.Amesema: “Watanzania waendelee kuniunga mkono, watu wanaamini bado ninaweza, naomba niwahakikishie wasitegemee mambo mabaya tena,”.Wema alitambulishwa katika sanaa ya uigizaji mwaka 2007 na marehemu Steven Kanumba na kuanza kuonekana katika filamu ya Point of No Return.Ameigiza pia katika filamu nyingine nyingi kama Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny, Basilisa zilizompatia umaarufu na mafanikio makubwa. | michezo |
MKURUGENZI wa Mashitaka (DDP), Biswago Mganga amesema serikali imetaifisha rasmi mali za Wakili maarufu jijini Arusha, Median Mwale zenye thamani ya Sh bilioni 1.2 kutokana na makosa ya kutakatisha fedha haramu.Mganga amesema, mali hizo zilizotokana na zao la utakatishaji fedha haramu baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kumtia hatiani na kuamuru mali hizo zitaifishwe na serikali.Akizungumzia na waandishi wa habari jana mjini Arusha wakati wa makabidhiano kati ya ofisi ya DPP na Hazina, Mganga alitaja mali hizo kuwa ni magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.Mali zingine zilizotaifishwa ni nyumba mbili ikiwemo iliyopo Plot Namba 261 Block C Njiro na nyumba nyingine iliyopo Plot Namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kutaifisha mali hizo na kwamba Aprili 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasmi na kuwa mali ya serikali.“Kwa mujibu wa sheria mali zinapotaifishwa kuwa mali ya serikali zinakuwa chini ya Katibu Mkuu Hazina” alisema.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Hazina, Benezeth Rutta alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa Wizara ya Fedha na zinapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa.“Mali hizi baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada” alisema Rutta.Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Selemani Nyakulinga amesema mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dola za Marekani milioni 17.2.Alisema fedha hizo zilikuwa zinaibwa kutoka mfuko wa Global Fund kwa ajili ya kusaidia kutibu Ukimwi nchini Tanzania zikitoka Hazina ya nchi ya Marekani.Amesema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni raia wa Kenya, wakishirikiana na Watanzania akiwemo Wakili Mwale .AMesema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua mali mbalimbali, zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama kuridhia na kutaifisha mali hizo kuwa za serikali. | kitaifa |
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma leo inazindua kitengo kitakachotibu magonjwa yanayohusiana na mfumo wa njia ya mkojo na pia kitashughulikia upasuaji wa tezi dume.Katika taarifa iliyotolewa na Kitendo cha Mawasiliano na Uhusiano katika Hospitali ya Benjamini Mkapa inaonesha kwamba kitengo hicho kitakuwa na vifaa vyote vinavyotakiwa katika kutoa huduma hiyo.Mkuu wa kitengo hicho, Dk Remigius Rugakingira, amesema mwishoni mwa wiki, “Kitengo hicho kitakuwa na vifaa vya hali juu vya kubaini magonjwa yanayohusiana na mfumo wa njia ya mkojo.”Dk Rugakingira alisema katika kitengo hicho utafanyika upasuaji ambao utafanywa kwa kutumia njia ya upasuaji wa matundu madogo.“Nawaomba wakazi wa Dodoma na mikoa jirani wenye matatizo katika mfumo wa njia ya mkojo kuja katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kutumia huduma hii. Hospitali hii imeweka vifaa vya kisasa kufanya uchunguzi wa kitabibu katika mfumo wa njia ya mkojo,” amesema.Dk Rugakingira amesema kitengo hicho kitatoa matibabu kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa njia ya mkojo kwa wanawake na wanaume, ambavyo viungo vya mfumo wa njia ya mkojo ni pamoja na figo, tezi, kibofu cha mkojo na viungo vya uzazi wa wanaume.Amesema wataalamu wa tiba wa BMH watashirikiana na wenzao wa Taasisi ya tiba ya Open Medical (OMI) kutoka Viena, Austria katika kuanza kutoa matibabu ya mfumo wa njia ya mkojo.Dk Rugakingira alisema wataalamu wa tiba kutoka OMI ambayo iko chini ya mfuko wa ushirikiano baina ya Marekani na Austria, pia watatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wenzao wa Hospitali ya Benjamin Mkapa.“Lengo la mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo ni kutuwezesha kuendesha kitengo hicho kipya kwa ufanisi. Ushirikiano wetu na wataalamu hao kutoka OMI utatupa jukwaa ambapo tunaweza kubadilishana uzoefu kutoka katika matibabu ya mfumo wa njia ya mkojo,” alisema. | kitaifa |
KAMISHNA Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Anna Makakala amepewa salamu za heshima kutoka kwa mataifa mbalimbali kwa kuindoa Tanzania kuwa uchochoro wa vitendo vya rushwa na kupitisha dawa za kulevya kwenda Ulaya.Nchi zilizotoa pongeza na kumpa heshima kwa kutambua mchango wa Kamishna Makakala ni China, Marekani, India, Ujerumani, Uingereza na Saudi Arabia. Salamu hizo za heshima zilitolewa Dra es Salaam juzi kwenye kongamano la viongozi wa dini lililoandaliwa na Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini nchini na kushirikisha wajumbe 437 kutoka mikoa yote ya bara na visiwani.Aidha wajumbe kutoka mataifa hayo akiwemo Profesa Yi gen kutoka China, Dk Brooks Lasmax wa Ujerumani , Shehe Dk Syudih Muhmed wa Saudia Arabia, Askofu Owen kennedy kutoka Marekani, Mchumi George Frank kutoka Uingereza na Dk Surani Snjaly wa India walisema kwa nyakati tofauti kuwa mabadiliko chanya katika masuala ya uhamiaji sio tu yamesaidia kwa asilimia kubwa kupungua kwa biashara ya dawa za kulevya nchini Marekani na Ulaya lakini imeiletea heshima Tanzania kwa kutokuwa tena barabara ya kupitisha dawa za kulevya.Walidai kuwa siku za zamani wakiwa wageni waliokuwa wakipita mara kwa mara na kuingia Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA), maofisa uhamiaji walikuwa wanapokea mgeni kwa kumuuliza atampa dola ngapi kabla hata hajafanya ukaguzi na walikuwa wakipewa Dola za Marekani 100 mgeni hakaguliwi kabisa lakini sio sasa.Dk Surajy walimwagia sifa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa kuigeuza idara hiyo kuwa chombo cha heshima kwa nchi mbalimbali na kuongeza kuwa hivi sasa raia wa India wanatamani kuja Tanzania kujifunza njia rahisi ya kuondoa rushwa. | kitaifa |
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa siku 68 kwa halmashauri nne kurejesha fedha za Mradi wa Elimu (Equip) zilizotumika kinyume cha utaratibu.Pia ameagiza ndani ya siku saba Mweka Hazina wa Manispaa ya Iringa, Saad Ishabairo kuchunguzwa na ikibidi ashushwe cheo mara moja.Jafo aliyasema hayo hayo jana jijini hapa na kufafanua kuwa halmashauri hizo ni kati ya halmashauri nane zilizotumia kiasi cha Sh milioni 912.7 kinyume cha utaratibu.Alizitaja halmashauri hizo zinazotakiwa kurejesha fedha kuwa ni Kigoma Ujiji, Butiama, Liwale na Bahi. Halmashauri nane zilibainika kutumia fedha za elimu kiasi cha Sh milioni 912.7 kinyume cha malengo ya fedha hizo na kutakiwa kiwa kurejesha, hata hivyo hamashauri nne zilitolitii agizo hilo.“Tumekuwa tunatekeleza miradi mbalimbali katika halmashauri zetu, katika sekta ya elimu tuna Mradi wa Equip 2 ambao utekelezaji wake umebainika kuwa na changamoto ya matumizi mabaya ya fedha za miradi ambazo zilitolea ili kuhakikisha tunasukuma mbele suala zima la elimu,” alisema Jafo.“Takribani Sh 912,720,559.40 zilitumika vibaya na halmashauri nane, ambazo ni Kigoma Manispaa, Busega, Butiama, Liwale, Lindi Manispaa, Mpwapwa, Chemba na Bahi. “Tamisemi iliamua kutoa maelekezo mahususi baada ya kuwaita wakurugenzi na maofisa wao kufanya kikao Morogoro na iliagizwa fedha zilipaswa kurudishwa ifikapo Desemba 31, mwaka jana.Jafo aliongeza: “Katika suala hilo halmashauri kadhaa ziliweza kurudisha, lakini bado nne hazijakamilisha, jambo hili kwetu sisi kama Tamisemi limetuhuzunisha sana kama tunatoa maelekezo lengo ni kutekelezwa.“Baada ya kuwasikiliza wakurugenzi wa halmashauri hizo ambao nimewaita na kukutana nao nimesikitishwa sana na Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Butiama hali zao ni mbaya. Kutokana na hali hiyo kwa halmashauri zote nne ziwe zimerejesha fedha ifikapo Machi 28, mwaka huu, lengo la kutekeleza miradi kama ilivyokusudiwa.”Aliagiza wakurugenzi wote kuhakikisha matumizi ya fedha yanaendana na utaratibu uliwekwa katika fedha hizo.“Sitarajii fedha yoyote ya maendeleo iliyotengwa kwa ajili ya mradi wowote ikatumika kinyume na utaratibu,” alisema na kuongeza kuwa pia ametoa wiki moja kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kumchunguza Mweka Hazina wa Manispaa ya Iringa, Ishebairo kutokana na kutotimiza wajibu wake akiwa Halmashauri ya Bahi,“Katika matumizi mabaya ya fedha kuna watu walishindwa kutimiza wajibu wao. Kwa mfano, Butiama unaona wazi kwamba katika fedha hizi Ofisa Mipango hakutimiza wajibu wake, aliyekuwa Mweka Hazina na mkurugenzi, pia hivyo basi namuelekeza mamlaka ya nidhamu ya ofisa mipango na aiyekuwa mweka hazina hatua za kuwashusha kuwaondoa katika nafasi zao na mkurugenzi taratibu zingine za kiofisi zinaendelea,” alieleza.“Kwa Bahi, aliyekuwa Mkurugenzi (Rachel Chuwa ambaye alisimamishwa) uchunguzi unafanyika na aliyekuwa Mweka Hazina Saad Ishabairo kwa halmashauri hiyo alishindwa kutimiza vizuri wajibu wao. Pamoja na kuwa amehamishiwa katika Manispaa ya Iringa, kwa sababu hii inaweza kuwa kasumba anaharibu hapa anaenda kwingine namuelekeza katibu mkuu afanye uchunguzi wa kina kubaini kilichojiri.“Hata kama mtu amestaafu atafutwe ahojiwe nini kilitokea mpaka fedha hizo zimeweza kupotea provide mtu huyo yupo, ni lazima kila mtu atabeba msalaba wake kwa sasa kwa sababu hatutaweza kuvumilia mambo yoyote ambayo yanaleta hujuma katika kuwahudumia wananchi.“Lakini naomba niwatahadharishe wakurugenzi wote katika mamlaka ya serikali za mitaa maelekezo yangu ya leo yanagusa katika maeneo mbalimbali kumekuwa na vitendo vya hovyo watu wanachukua fedha wanatumia kinyume na maelekezo na wala hawataki kufuata miongozo halali iliyowekwa ya matumizi ya serikali,” amesema.Katika hatua nyingine, Jafo ametoa maelekezo kwa Naibu wake, Mwita Waitara kuhakikisha anapitia na kukagua miradi yote ya elimu na kuangalia kama fedha zilizotengwa katika sekta hiyo zimetumika kama ilivyokusudia na kumtaka kuwa mkali anaposimamia miradi hiyo. | kitaifa |
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo mjini Morogoro jana, Herman Kessy kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa benki hiyo.Aidha, aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, benki hiyo pia itaanzisha uwakala wa benki ambayo itashirikiana na mawakala wa sehemu mbalimbali na ili kuhakikisha inafikisha huduma za kibenki kwa wananchi wote kwa urahisi, uhakika na unafuu.“Kupitia huduma hii, wateja wataweza kupata pesa zao kupitia mawakala au kupakua programu maalumu kwenye simu zao za kiganjani zitakazowezesha kulipa huduma za maji, umeme pia kutuma pesa kutoka kwenye akaunti zao kwenda kwenye huduma maalumu ya benki kwa njia ya simu,” alifafanua.Akizungumzia hali ya taasisi za kifedha nchini, Kessy alisema MCB iko imara licha ya changamoto zilizojitokeza hivi karibuni kutokana na agizo la serikali kuelekeza taasisi zake zote za umma kuhamisha na kupeleka fedha zote Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na hivyo wateja wakubwa wa serikali kufunga akaunti zao na kuhamishia fedha zao BoT.“Lakini sio hilo tu, hata uhakiki wa watumishi wa umma uliobaini watumishi hewa 19,000 umetuathiri kwa sababu wakati wa uhakiki uliofanyika kwa zaidi ya siku 90 urejeshaji wa makato ulisitishwa, hivyo basi benki ikiwemo yetu hatukupata marejesho ya mikopo kutoka kwa wafanyakazi walioathiriwa na uhakiki huo na pia kukosa mapato yatokanayo na r | uchumi |
FOMU za kushiriki mbio za Ngorongoro Race 2019, ambazo zinatarajia kufanyika Aprili 20 zitaanza kutolewa Ijumaa mjini Karatu, imeelezwa.Mratibu wa mbio hizo, Meta Petro alisema juzi tayari baadhi ya wanariadha nyota wamethibitisha kushiriki mbio hizo za kilometa 21, akiwemo Alphonce Simbu ambaye hivi karibuni alifikia viwango vya kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020. Simbu pia amefuzu kwa mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika Doha, Qatar Septemba mwaka huu.Petro alisema kuwa mbali na wanariadha wa hapa nchini, pia wanariadha kibao kutoka Kenya wameonesha nia ya kushindana katika mbio hizo, ambazo mshindi wa kwanza anatarajia kuondoka na kitita cha Sh milioni 1. Alisema kuwa wameamua kuweka kituo kimoja cha usajili wa wanariadha ili kuhakikisha kila mwanariadha anayenunua fomu anapewa risiti na pesa stahiki inaingia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia mashine ya kielectoniki ya EFD.“Tutaanza usajili Ijumaa na kila mwanariadha atakayenunua fomu atapewa risiti ya TRA ili serikali ipate fedha zake stahiki kwa ajili ya maendeleo ya taifa, “alisema Petro, ambaye ni kocha wa timu ya taifa iliyoshiriki mbio za dunia za nyika Denmark Machi 30 mwaka huu. Alisema fomu ya wanaotaka kushiriki mbio za kilometa 21 zitatolewa kwa Sh 20,000 wakati zile za kilometa tano kila moja itauzwa kwa Sh 10,000 na kilometa 2.5, ambazo zitashirikisha watoto zitapatikana kwa Sh 5,000 kila moja.Alisema kuwa mbio hizo ambazo zitaanzia katika lango kuu la kuingilia na kutokea katika Hifadhi ya Ngorongoro, zinadhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro (NCAA) na zitamalizikia katika viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu, Arusha. Patro akitaja zawadi zingine alisema mshindi wa pili wa mbio za nusu marathon ataondoka na Sh 500,000 wakati mshindi watatu atapewa Sh 200,000, huku mshindi wa nne atapewa 100,000.Kwa upande wa kilometa 5, mshindi wa kwanza atapewa Sh 300,000 huku wa pili 200,000 wakati watatu atapewa Sh 100,000 huku zawadi zikiendelea kutolewa kuanzia mshindi wa nne hadi wa 10. Wakati huohuo, NCAA kupitia kwa Kaimu Meneja Mawasiliano wao Joyce Mgaya, washiriki 100 wa kwanza kumaliza mbio za kilometa 21 watapata ofa ya kutembelea hifadhi hiyo. | michezo |
WATU sita wanaosadikiwa kuwa majambazi, wakiwemo raia wa Burundi, wameuawa katika majibizano ya risasi na kikosi kazi maalumu cha kupambana na ujambazi katika maeneo ya Ubungo UFI, Dar es Salaam.Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na silaha tatu aina ya AK 47, risasi 217, magazini nane, mabomu manane ya kutupa kwa mkono pamoja na kitambulisho chenye namba OP 0216239 jina la Theophili Manirakiza, mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana na taarifa za kiitelijensia zilidai kwamba watuhumiwa hao wana mafunzo makubwa waliyoyapata nchini Burundi na wamefanya matukio mengi ya uhalifu hapa nchini.Alisema watuhumiwa hao waliuawa baada ya mtego uliowekwa na askari kutokana na taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa ambao ni Willy Irakozes maarufu Commando raia wa Burundi, Jean Mugisha raia wa Burundi na Mtanzania Omary Nassoro.Alisema watuhumiwa hao walipanga kwamba Novemba 29, mwaka huu saa 10:30 alfajiri wangempora mfanyabiashara aliyekuwa akisafiri kuelekea Morogoro akisadikiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha."Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa matukio ya uhalifu yaliyotokea Mabibo External Novemba 3, mwaka huu ambapo mfanyabiashara wa Tigopesa/M-Pesa aliporwa Sh milioni 50 na tukio jingine la eneo la Tegeta Novemba 15, mwaka huu ambapo mfanyabiashara raia wa China aliporwa Sh milioni 10," alisema.Aidha alisema Irakozes amekuwa akitafutwa kwa kufanya matukio mbalimbali ya unyang'anyi wa kutumia silaha hasa katika tukio la kuvamia Benki ya NMB Temeke ambapo anadaiwa kuwaua askari wawili na raia.Pia Machi 15, 2011 mtuhumiwa huyo akiwa anashikiliwa kituo cha Polisi Kagongwa Kahama kwa makosa mbalimbali yeye na wenzake walitoroka baada ya kuwaua askari polisi wawili na kutoroka na silaha mbili aina ya AK47.Aidha matukio mengine waliyoshiriki watuhumiwa hao ni pamoja na kuteka mgodi wa Tulawaka Geita mwaka 2011 na pia kuvamia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, Zanzibar.Mwaka 2012 watuhumiwa hao wanadaiwa kuvamia kituo cha mafuta Kagera na kufanya mauaji ambapo pia walivamia maduka yaliyopo karibu na Kituo cha Polisi Chato kwa kukishambulia kituo hicho ili kurahisisha uporaji.Alisema watuhumiwa hao walipora Sh milioni tatu na mwaka 2010 walivamia mgodi wa Nyamongo na kufanya mauaji ya askari mmoja na kujeruhi wengine."Tumetangaza kwamba Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu hatutakuwa tayari kuona watu wanatafuta fedha haramu kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Tumejipanga vizuri na tutachukua hatua pale tunapoona ni vyema kufanya hivyo," amesema.Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa salama na kuwaonya ambao wamekuwa wakiwapokea raia wa kigeni na kuwasaidia kufanya uhalifu na kusema Tanzania inataka wageni lakini wenye kufuata sheria na taratibu za nchi. | kitaifa |
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera, katika hotuba yake kwenye sherehe ya TCCIA kutimiza miaka 25 iliyofanyika hivi karibuni mjini hapa.Mbali na kutoa pongezi hizo alitumia fursa hiyo kuipongeza kwa kuwezesha kumaliza tatizo la mashine za kielectroniki (EFDs), ambao ni mfumo mpya wa kutoa risiti.Hata hivyo alisema ingawa bado changamoto zinaendelea kutolewa juu ya matumizi ya mashine hizo, suala hilo linaweza kujadiliwa kwa mapana zaidi na mamlaka zinazohusika.Mbali na hayo, aliipongeza TCCIA Mkoa wa Morogoro kutokana na juhudi na busara iliyozionesha kwa kutoa ushirikiano mzuri wakati wa mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Mkundo, wilayani Mvomero.Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Morogoro, Bachoo Sadik Bachoo, alisema pamoja na kutimiza miaka hiyo, mambo mengi mazuri ya kitaifa na Mkoa yamefanyika ndani ya miaka hiyo 25.Alisema kwa Mkoa wa Morogoro, TCCIA imefanikisha kutatua migogoro ya wafanyakazi wakiwemo wa soko kuu, kuondolewa kwa malipo ya mabango kwenye nyumba zinazomilikiwa na Shirika la Nyumba (NHC) kwa nchi nzima.Alisema TCCIA Mkoa pia imefanikisha kuondoa misuguano kati ya TRA na jamii ya wafanyabiashara na badala yake kumekuwa na uhusiano mwema unaoleta mafanikio katika ukusanyaji wa kodi.Hata hivyo alisema TCCIA Mkoa imefanikisha kufungua matawi katika wilaya nne kati ya sita za mkoa, ambapo lengo ni kuwa na matawi kwenye wilaya zote.Akizungumzia malengo ya baadaye, Mwenyekiti huyo wa TCCIA Mkoa wa Morogoro, alisema wanatarajia kuanzisha harambee ili kukusanya fedha ambazo zitawezesha kununua eneo kwa ajili ya kujenga jengo la kisasa la TCCIA. | uchumi |
KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema, kilichowafanya wapoteze mchezo wao mbele ya Lipuli FC ni wapinzani wao hao kuwazidi uwezo hivyo mbinu zao zote walizozitumia hazikufanya kazi.Yanga walifungwa mabao 2-0 na Lipuli katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, FA, uliopigwa katika Uwanja wa Samora, Iringa juzi. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo, kocha huyo raia wa DR Congo, alisema kuwa hakutarajia kama atakutana na upinzani mkali kama ule licha ya kuwajua Lipuli ni moja kati ya timu ngumu nchini.Alisema kuwa mbinu alizoingia nazo aliamini kabisa zitawapa ushindi lakini kadiri muda ulivyozidi kusogea akaona wanapata wakati mgumu na kumlazimu kuzibadili. Alifafanua kuwa alifanya mabadiliko ya mfumo kwa kuwatoa Ibrahim Ajib, Haji Mwinyi na Mohammed Issa ‘Banka’ na kuwaingiza Amis Tambwe, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Juma Abdul lakini bado mambo yakawa magumu.“Niliona Lipuli ni wagumu kufungika ndio maana nilimuingiza Tambwe, Juma na Ninja nikamtoa Ajib, Mwinyi na Banka ili kufanya tupandishe mashambulizi na kushambulia kwa kasi, tutumie mipira ya krosi kupata mabao lakini ikashindikana,” alisema Zahera. Kwa upande wa Kocha wa Lipuli, Seleman Matola alisema kuwa kilichowasaidia kupata ushindi katika mchezo huo ni kuzisoma mapema mbinu za Yanga.Alisema kuwa walifanikiwa kuwadhibiti kila upande na kuutawala mchezo na kama wachezaji wake wangeongeza umakini wangeweza kupata mabao zaidi ya mawili lakini akawashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya kuipeleka timu fainali kwa mara ya kwanza. “Hii ni zawadi ya mashabiki wa Lipuli pamoja na watu wa Iringa kwa ujumla, tulitengeneza nafasi nyingi za kupata mabao lakini tukafanikiwa kufunga mawili, kwakuwa tumeenda fainali hayo tuliyoyapata yanatosha. | michezo |
WAPINZANI wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe wanatarajiwa kuwasili leo mchana tayari kwa mchezo wa hatua ya robo fainali unaotarajiwa kupigwa mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Kuelekea kwenye mchezo huo, Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara alisema kikosi cha timu yao kipo kwenye maandalizi mazuri na kwamba hawawahofii wapinzani wao hao zaidi ya kuwaheshimu. Alisema siku zote mashabiki wao ni sehemu muhimu kwenye ushindi wao kwa namna wanavyojitokeza uwanjani na kuujaza uwanja na kuwaomba wajitokeze kwa wingi dhidi ya TP Mazembe Jumamosi hii.“Wapinzan wetu wanawasili kesho( leo), tunathamini mchango wa mashabiki wetu na kuelekea kwenye mchezo huu tumeweka viingilio vya bei ya chini kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi kama kwenye michezo iliyopita,kama mashabiki wasingekuwa wanajitokeza uwanjani tusingefikia hatua hii tuliyofika,“ alisema Manara wakati wa kutangaza viingilio vya mchezo huo.Akitaja viingilio kwa ajili ya mchezo huo, Manara alisema viti vya mzunguko bei yake ni Sh 4000, VIP, Sh 20,000, VIP B Sh 10, 000, wakati viti vya platnumz ni Sh 100,000 na kusisitiza lengo ni kuhakikisha kila mwanachama na shabiki wa timu hiyo wanaichangia timu kwa kulipa kiingilio uwanjani. | michezo |
KOCHA Emmanuel Amunike ameita kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, The Cranes na hakumjumuisha hata mchezaji mmoja wa Mtibwa Sugar.Mchezo huo wa kundi L utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 24 ni muhimu kwa Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika ambapo mara ya mwisho kufuzu kwa fainali hizo ni miaka 38 iliyopita.Kwa mara ya kwanza, Mtibwa Sugar imeshindwa kutoa mchezaji hata mmoja kwenye kikosi cha Taifa Stars lakini kocha wa timu hiyo, Zubery Katwila alisema hayo ni maamuzi yake na yeye hawezi kumuingilia.“Siwezi kumchambua kocha mwenzangu kwanini hajamuita hata mchezaji mmoja kwenye kikosi changu, hilo nawaachia wachambuzi.“Kama kocha, ni wazi Amunike ana vigezo vyake juu ya wachezaji wa aina gani awaite kwenye kikosi chake na ambao anaamini watampa matokeo mazuri na kama mtanzania niko nyuma yake kuona timu yetu ya taifa inapata matokeo mazuri,” amesema Katwila ambaye amewahi kuichezea Taifa Stars.Tangu nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Nigeria atangaze kikosi chake kitakachoivaa timu ya taifa ya Uganda Machi 24, kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki na wachambuzi juu ya uteuzi wake.Wengi wamekuwa wakitaja majina ya wachezaji kama vile Salim Ayee, Ibrahim Ajibu, Mohamedi Hussein’Tshabalala’, Paul Godfrey na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kuwa walistahili kuitwa kwenye kikosi hicho. | michezo |
JUKWAA la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora linamalizika leo baada ya kufanyika kwa siku tatu mfululizo. Limekuwa ni jukwaa la kwanza kati ya saba yaliyokwishafanyika, kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na mawaziri wengine watatu kwa mpigo.Ni jukwaa ambalo pia lilitia fora kwa kuhudhuriwa na wabunge wengi kulinganisha na mengine yaliyotangulia. Mawaziri waliohudhuria Jukwaa la Tabora ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara.Jukwaa la Tabora, kama mengine yaliyotangulia, huandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na mikoa husika. Mpaka sasa mikoa iliyokwisha fanya majukwaa hayo ukiondoa Tabora ni Simiyu, Mwanza, Geita, Arusha, Tanga na Zanzibar.Kwa mujibu wa Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah, TSN iliamua kuandaa majukwaa hayo ili kutoa mchango wake katika kuibua fursa mbalimbali za mkoa husika. Anasema kampuni hiyo katika kuandaa majukwaa hayo hutuma timu yake ya waandishi wa habari kwenda kwenye mkoa husika na kutafuta habari zinazoibua fursa za kiuchumi, biashara na uwekezaji na kuzitangaza kupitia vyombo vyake vya habari.Anasema moja ya vitu TSN ilivyogundua kupitia majukwaa hayo ni utayari mkubwa wa wananchi katika kujitafutia maendeleo yao. TSN ni wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo, Spotileo na pia hutangaza habari zake kupitia mtandao ya kijamii na chaneli ya Youtube ya Daily News Digital.Kutokana na jitihada hizo za TSN za kuibua fursa za kiuchumi katika mikoa mbalimbali, Waziri Mkuu, Majaliwa, wakati akifungua jukwaa la biashara Tabora juzi alisema serikali inafarijika kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na TSN. Anasema kampuni hiyo imeendelea kutekeleza wajibu wake kwa ufasaha kwa kuhabarisha na kuelimisha jamii kupitia majukwaa ya fursa za biashara na uwekezaji ya mikoa.Anasema TSN imekuwa ikiandaa majukwaa hayo kwa miaka miwili sasa na kwamba katika mikoa yote walikopita, TSN imeibua fursa za biashara na uwekezaji na kuzitangaza kwa kuziandika kwenye vyombo vyake vya habari na pia kuzitangaza kupitia majukwaa hayo wanayoyaandaa. “Majukwaa haya yamesaidia sana kupata wawekezaji mbalimbali.Lakini pia yamekuwa na faida nyingi mfano kusaidia upatikanaji wa mitaji, teknolojia, ajira na kuongeza mapato ya serikali,” anasisitiza Waziri Majaliwa. Alisema hata Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, walikuwa wanajua uwepo wa Jukwaa la Biashara Tabora na hivyo kumtuma alete salamu nyingi kwa wananchi wa mkoa wa Tabora na waandaaji wa jukwaa hilo.Ni kwa msingi huo, Waziri Mkuu anaihimiza kampuni hiyo ya magazeti ya serikali kuendelea kuandaa majukwaa hayo ya biashara na fursa za uwekezaji katika mikoa mingine. “Ni matumaini yangu kuwa kila baada ya jukwaa kama hili (la Tabora lililokutanisha watu zaidi ya 500), kutafanyika tathmini za kina na kupima matokeo yaliyotarajiwa.“Ni matumaini yangu pia kwamba siku nyingine mtaandaa haya majukwaa hadi mikoa ya kule…” anasema Waziri Mkuu akiacha fumbo ambalo wafumbuaji wanasema alimaanisha mikoa ya Kusini ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidaiwa kuwa nyuma kimaendeleo licha ya kuwa na raslimali lukuki. Waziri Mkuu pia anatoa wito kwa TSN kwamba baada ya kukamilisha majukwaa ya mikoa iangalie uwezekano wa kuandaa majukwaa hayo katika ngazi za wilaya na ngazi ya kisekta.“Kwa mfano katika ngazi ya kisekta mnaweza kuangalia zao moja la kilimo, au mkaangalia madini, ufugaji au ujasiriamali ili msaidie kuziibua na kuzitangaza fursa zilizopo kwenye sekta husika kama mnavyofanya sasa,” anafafanua.Waziri Mkuu pia anaziagiza idara zote za serikali katika ngazi za mikoa na wilaya kushirikiana katika kubuni njia zitakazosaidia kuibua fursa zilizopo ili zipate uwekezaji haraka. Anasema suala la uchumi wa viwanda ndio azma ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ambayo imeazimia kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025.“Mikoa yote lazima ijikite katika kufikia azma hii, lengo ni kujenga fursa za ajira. Uchumi utakapokua utaiwezesha serikali kutengeneza mipango ya maendeleo ya wananchi,” anasema. Anafafanua kuwa jitihada hizo zitasaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaohitimu masomo na kozi mbalimbali na hivyo kutumia rasilimali na fursa zilizopo kuzalisha mali.Anasema uchumi wa viwanda unaojengwa nchini, unategemea zaidi rasilimali zinazozalishwa na wakulima wadogo, wa kati na wakubwa. Anaagiza kwamba fursa zote za biashara na uwekezaji zilizobainishwa kupitia Jukwaa la Tabora ziandaliwe na kuandikwa vizuri ili wenye mitaji kutoka ndani na nje ya nchi wazione na kuja kuwekeza.Katika mkoa huo wa Tabora fursa lukuki zilibainishwa mbele ya Waziri Mkuu huku ikielezwa kwamba mpaka sasa ardhi inayotumika kwa makazi, kilimo na uwekezaji mkoani Tabora ni asilimia 50 tu ya ardhi yote inayofaa kwa mambo hayo.Ikaelezwa kwamba Tabora kwa sasa ina miundombinu bora zikiwemo barabara za lami zinazounganisha mkoa wa Tabora na mikoa mingine, reli ya kati lakini pia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR). Fursa nyingine inayotajwa ni itokanayo na misitu na mazao yake kama vile uzalishaji wa mbao, asali na nta.Pia zinatajwa fursa za utengenezaji wa samani kwa kiwango cha kimataifa, kilimo cha tumbaku, mpunga, zao mkakati la korosho, alizeti, karanga pamoja na pamba. Majaliwa anaigeukia mikoa mingine akisema: “Nitoe wito kwa viongozi wote wa mikoa yote nchini, wahakikishe wanashirikiana na makundi yote, kuzibaini fursa, kuziorodhesha na kuzitangaza kwenye vyombo vya habari na majukwaa ya biashara na uwekezaji bila kukawia.”Anasema fursa za uwekezaji nchini ni nyingi na serikali ya awamu ya tano imetengeneza mazingira mazuri na wezeshi ya uwekezaji na ufanyaji biashara ikiwemo kuanzisha benki mbalimbali kwa ajili ya kutoa mikopo. “Sote tunatambua juhudi za serikali katika kusaidia maendeleo ya kilimo nchini. Serikali kwa makusudi imeunda Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia wakulima.Naomba tuitumie benki hii vizuri kwani ipo tayari kutoa mitaji kwa wanaotaka kuwekeza katika kilimo na ufugaji,” anabainisha. Pamoja na benki hiyo, Waziri Majaliwa anaipongeza benki ya NMB kwa kutenga kiasi cha Sh bilioni 500 kwa ajili ya kilimo.“Na jambo zuri ni kwamba Tabora imenufaika na Sh bilioni 30 kupitia fedha hizo,” anasema Kwa upande wake, Waziri wa habari, Dk Mwakyembe, anaeleza namna majukwaa hayo ya fursa za uwekezaji na biashara yanavyoendelea kuleta manufaa nchini na kwamba kadri yanavyoendelea kufanyika ndiyo yanavyoboreka zaidi.Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda. anaipongeza kampuni ya TSN kwa kuandaa jukwaa hilo, ambalo limezitangaza na kuziibua fursa za uwekezaji na biashara za Tabora. “Nakiri mbele yako, hakuna washauri wazuri kama watalaamu katika tasnia ya habari kwani kazi yao inagusa kwa weledi kila sekta,” anasema.Anawataka wananchi wa Tabora kufanyia kazi fursa zilizoibuliwa wakati wa jukwaa hilo ili kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mwita Waitara, anapongeza hatua ya kuandaliwa kwa jukwaa hilo akisema ni kutekeleza maagizo ya viongozi wakuu wa nchi wa kuhakikisha kila mkoa unakuwa na viwanda angalau 100.Akimwakilisha Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, Waitara anasema tathamini iliyofanywa huko nyuma ilionesha kwamba viwanda vilivyoanzishwa vilikuwa viwanda 2,280 sawa na asilimia 46 lakini katika tathmini itakayofanyika baadaye mwakani, matarajio ni kuwa na viwanda asilimia 90. Tangu aingie madarakani mwishoni mwa mwaka 2015, Rais John Magufuli alitangaza kwamba serikali yake imedhamiria kujielekeza katika kujenga uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025. | kitaifa |
KOCHA wa Azam FC Ettiene Ndayiragije amesema mchezo wa leo wa fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Kombe la Kagame ni wa kisasi.Akizungumzia mchezo huo jana kupitia sauti iliyotumwa na Msemaji wa klabu hiyo Jaffar Maganga, Ndayiragije alisema kwa kuwa mchezo wa kwanza wa makundi walipoteza 1-0 dhidi ya KCCA, hawatakubali tena iwe hivyo.“KCCA ni timu nzuri tulikutana nao hatua ya makundi tulikuwa bado hatujaunganika vizuri, tunawafahamu nina imani mechi itakuwa bora zaidi na sisi tunahitaji kulipiza kisasi,”alisema.Ndayiragije alikiri kuwa mchezo hautakuwa rahisi kwa kila mmoja kutokana na umuhimu wake, wakitaka kuweka historia ya kulichukua mara tatu mfululizo na KCCA wanataka kuweka historia ya kulitwaa baada ya kulikosa kwa miaka mingi. Mabingwa hao watetezi walifanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kuitoa AS Maniema ya DR Congo kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya kucheza dakika 120 bila kufungana.Aidha, wapinzani wao KCCA walitinga hatua hiyo baada ya kuwaondosha Green Eagles ya Zambia kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia kupata sare ya mabao 2-2 ndani ya muda wa nyongeza.Azam FC ambayo ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), inahitaji kutetea taji hilo ililotwaa msimu uliopita baada ya kuifunga Simba mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Iwapo watafanikiwa kulitwaa tena itakuwa ni mara ya tatu.Mara ya kwanza walilitwaa mwaka 2015 kwa kuichapa Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.KCCA wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kulikosa taji hilo mwaka 1979 walipocheza fainali dhidi ya Abaluya FC kwa sasa inajulikana kama AFC Leopards ya Kenya baada ya kupoteza kwa bao 1-0.Ushindi dhidi ya Azam FC leo utawafanya kuweka historia nyingine mpya kwao kuchukua taji hilo kwa mara ya pili baada ya kulichukua kwa mara ya kwanza mwaka 1978. | michezo |
KIKOSI cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba jana kilifi ka salama mjini Rustenburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.Msafara wa wachezaji 22 na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo uliondoka jana asubuhi na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania. Simba ipo kwenye maandalizi ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu pamoja na michuano ya kimataifa.Ligi Kuu Bara imepangwa kuanza Agosti 23 ambapo Simba itaanza JKT Tanzania, kabla ya mechi hiyo itacheza mechi ya ngao ya hisani dhidi ya mabingwa wa FA, Azam Agosti 17. Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili Rustenburg, meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema wamefika salama na kilichobaki ni kuelekeza nguvu kwenye maandalizi ya michuano inayowakabili na wanaamini watakaporudi watakuwa moto wa kuotea mbali.Alisema waliondoka na wachezaji 22, wachezaji wengine wanne wataungana nao kuanzia leo. “Awali ya yote tunamshukuru Mungu leo (jana) tumeondoka na msafara wa wachezaji 22 kwenda Afrika Kusini kwa ndege ya Air Tanzania na wengine watafuata kuanzia kesho (leo) au keshokutwa (kesho) kutokana na walichelewa kuja nchini kwa matatizo ya viza, hivyo watashughulikiwa taratibu waje kuungana na kikosi Afrika Kusini,” alisema Rweyemamu.Alisema kwenye benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu wa mabingwa hao Patrick Aussems kuna watu sita ambao wapo na kikosi hicho kuhakikisha maandalizi hayo yanakuwa na tija kuelekea kwenye michezo ya ligi na ya kimataifa. Simba itarejea nchini siku moja kabla ya Agosti 8 kwa ajili ya tamasha la Simba Day linalofanyika Agosti 8 ya kila mwaka, ikiwa ni mahsusi kutambulisha wachezaji na jezi zao za msimu kwa wanachama wao. | kitaifa |
['Mwaka 1969, mataifa ya El Salvador na Honduras yalipigana kwa siku nne na kuacha maelfu wakipoteza maisha na maelfu wengine wakipoteza makazi- umwagaji huo wa damu baado unakumbukwa kama Vita vya Mpira wa Miguu. ', 'Matokeo yalikuwa 2-2 baada ya dakika 90 katika uga wa Azteca jijini Mexico City. Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu baina ya Honduras na El Salvador ndani ya wiki chache; wote wakisaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 1970. Michuano ambayo mataifa hayo mawili walikuwa hawajawahi kushiriki. ', 'Honduras walipata ushindi mwembamba kwenye mechi ya kwanza wa 1-0 katika mji mkuu wao wa Tegucigalpa, kishaEl Salvador wakaandikisha ushindi wa 3-0 nyumbani San Salvador.', ' Ripoti za vurugu zilitawala mech izote. ', 'Katika mechi ya tatu, dakika 11 ya nyongeza huku matokeo yakiwa 2-2 mchezaji wa El Salvador Mauricio "Pipo" Rodríguez alichomoka kwa kasi katika eneo la penati na kunganisha krosi iliyomshinda kipa wa Honduras Jaime Varela.', '"Nilipofunga lile goli, Nilifikiri muda usingetosha kwao kupata tena matokeo ya suluhu dhidi yetu," anakumbuka Rodríguez, miaka 50 baada ya mchezo huo. "Nilikuwa nahakika kuwa kwa goli lile tutashinda." ', 'El Salvador kweli waliibuka na ushindi wa 3-2. Wachezaji wakakumbatiana, wakapeana mikono na kutoka uwanjani. ', 'Baada ya wiki tatu, mataifa hayo yakaingia vitani. ', 'El Salvador - ambayo ni ndogo mara tano kwa eneo la kijiografia kwa Honduras - ilikuwa na idadi ya watu milioni 3 mwaka 1969.', 'Sehemu kubwa ya ardhi ilikuwa ikimilikiwa na mabwanyenye wachache, huku wakulima maskini wakiachiwa maeneo machache.', 'Honduras yenyewe licha ya kuwa kubwa kieneo ilikuwa na idadi ya watu miioni 2.3.', 'Matokeo yake yalikuwa ni, katika kipindi chote cha karne ya 20, raia wa Salvador walikuwa wakihamia Honduras ili kuendeleza ardhi kwa kilimo binafsi na kufanya kazi katika makampuni ya matunda kutoka Marekani.', 'Kwa mwaka 1969, inakadiriwa watu 300,000 walihama l Salvador na kuingia Honduras.', 'Mambwanyenye wa El Salvador walikuwa wakiunga kono hama hama hiyo, kutokana na kuwa iliipunguza presha ya watu kutaka kuchukua ardhi yao na kugawana. ', 'Lakini kwa wakulima masikini wa Honsuras hawakulipenda kabisa suala hilo sababu wao pia walikuwa wakitaka mabwanyenye wao. ', 'Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Honduran ikaja na mpango wa cha kufanya. Sheria ya ardhi ilipitishwa ili kuondosha suitafahamu hiyo.', 'Lakini sheria yenyewe haikuyadhibiti mashamba ya Wamarekani bali aardhi iliyotwaliwa na wageni kutoka El Sarvador. ', 'Rais wa Honduras Oswaldo López Arellano akaanza kuwatimua maelfu ya wahamiaji kutoka El Salvador. ', 'Kama hilo halitoshi, kulikuwa na mgogoro juu ya mpaka wa ardhini n majini. ', '"Kwa kiasi kikubwa vita ilikuwa ni ya kugombea ardhi, watu wengi katika eneo dogo la ardhi, huku mabwanyenye wakikuza mambo kupitia vyombo vya habari," anasimulia Dan Hagedorn, mwandishi wa kitabu cha Vita ya Saa 100, kinachoelezea mgogoro huo. ', 'Rais wa El SalvadorFidel Sánchez Hernández na serikali yake walikuwa wakihangaika juu ya namna ya kupokea maelfu ya raia wake waliokuwa wakirejea nyumbani, huku mabwanyenye wa nchi hiyo wakitoa msukumo wa jeshi kujibu mapigo.', 'Taarifa za uchochezi juu ya kuuawa watuna hata tuhuma za ubakaji zikaripotiwa magazetini. ', 'Yote hayo yalipelekea kuongezeka kwa hasira nchi hizo zilipokutana uwanjani. ', '"Ilikuwa ni zaidi ya mambo ya kisiasa," anaeleza Ricardo Otero, mtangazaji wa michezo raia wa Mexico. "Kukatokea hizo mechi tatu za kufuzu kuelekea kombe la dunia la mwaka 1970. Haikusaidia kutatua mgogoro. Mpira wa miguu huku Amerika Kusini ni mchezo unaopendwa sana - kwa mabaya na mazuri. " ', '"Tuliona ni jambo la lazima na uzalendo kwetu kushinda kwa ajili ya nchi yetu El Salvador," Rodríguez anaeleza. " Nafikiri wote tulikuwa na woga wa kupoteza mchezo, kutokana na yale yaliyokuwa yakendelea basi tungekuwa tunaoandamwa na aibu maisha yetu yote."', '"Ambacho tulikuwa hatujui ni umuhimu wa ushindi na goli lile la dakika za lala salama - kuwa lingetumika kama lama ya vita." ', "'Nini kinachoendelea?'", 'Juni 27, 1969 wakati wachezaji wakijiandaa na mpambano uwanjani, El Salvador ikavunja mahusiano ya kidiplomasia na Honduras.', 'Waziri wa mambo ya ndani Francisco José Guerrero akasema takribani Wasalvador 12,000 waliondoka Honduras baada ya mechi ya pili huku gazeti la Uingereza la Guardian likiripoti kuwa waziri huyo "alilaumu juu ya mauaji yatokanayo na mechi ya kimataifa ya mpira." ', 'Siku moja baada a mchezo, Shirika la habari la Marekani la UPI liliandika taarifa yenye kichwa cha habari El Salvador yashinda "Vita ya Soka 3-2". ', 'Taarifa hiyo ilidai kuwa polisi 1,700 wa Mexico walitumika kuzuia ghasia huku mashabiki wa Salvador wakiwaita mashabsikili wakiimba "wauaji, wauaji" wakiwalenga Hoduras. ', '"Watu wa ughaibuni ndio walioanza kusema goli langu limechochea vita," anasema Rodríguez. "Vita ingetokea hata kama goli lisingefungwa." ', 'Baada ya mechi, ghasia za mpakani ziliongezeka.', ' Julai 14, El Salvador ilitoa amri kwa vikosi vyake kuivamia Honduras, na ndege za kivita zikaingia mawinguni kushambulia nchi jirani. ', 'Mwandishi wa habari raia wa Poland Ryszard Kapuscinski alikuwepo eneo hilo pale vita ilipoanza. ', 'Ameandika kwenye kitabu chake cha mwaka 1978, chenye jina la Vita vya Mpira (The Soccer War) kuwa kulikuwa na michoro ya ukutani zilizosomeka "Hakuna anayeweza kuipiga Honduras" na "Tutalipiza kisasi 3-0".', 'Pale ambapo nchi za Amerika zilikuwa zimefanikiwa kusuluhisha mgogoro huo Julai 18, tayari watu 3,000 walikuwa washapoteza maisha. Wengi zaidi walikuwa wamepoteza makazi. ', 'Baada ya shinikizo kali la kimataifa El Salvador iliondoa vikosi vyake Honduras mwezi Agosti.', 'Lakini maumivu hayakuishia hapo. Biashara ikasimama kwa miongo kadhaa baina ya mataifa hayo mawili kufuatiwa kufungwa kwa mpaka. ', 'Dkt Mo Hume, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Glasgow, anasema matatizo ya ndani kwa El Salvador ambayo yalisababisha Vita ya Soka - idadi ndogo ya mabwanyenye wamiliki ardhi tofauti na idadi kubwa ya aikna pangu pakavu tia mchuzi- yataendelea kuiandama nchi hiyo ya miongo kadhaa ijayo. ', 'Bado kuna uhusiano wa mashaka baina ya mataiafa hayo mawili.', 'Lakini kwa bwana aliyefunga goli lilozaa vita anasema goli hilo kwake linaendelea kuwa la kujivunia na si vinginevyo. ', '"Kwangu, goli lile ni chachu ya kujivunia utaifa kupitia michezo," anasema Rodriguez ambaye sasa ana miaka 73. '] | michezo |
Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet nchini, Nico Bezuidenhout amesema mwishoni mwa wiki kuwa, makubaliano hayo yatakuza biashara ya Fastjet kwa kutanua wigo wa kuuza tiketi duniani.Amesema wateja wataweza kufanya maandalizi ya safari, kununua tiketi na kuona mfumo wa safari za Fastjet kirahisi na kutumia huduma zao."Kwa kuwa hata IATA imesema Fastjet itakuza biashara yake kwa asilimia 8 kwa mwaka huu, makubaliano haya na Travelport yataiunganisha Fastjet na mawakala wa safari za anga zaidi ya 68,000 hivyo kwetu ni fursa kubwa ya kukuza biashara," alisema Bezuidenhout alipozungumza na waandishi wa habari.Makamu wa Rais wa Travelport kwa Bara la Ulaya, nchi za Kiarabu na Afrika, Philip Saunders, alisema teknolojia ambayo kampuni yake inatumia itaiongezea mauzo Fastjet kwa kuwa itafahamika kwa mawakala zaidi duniani.Saunders alisema wanatarajia kufanya kazi bega kwa bega na Fastjet katika kufanikisha malengo yake na wakati huo huo kuifanya Travelport kuendelea kuwa kiongozi kwenye sekta ya ukataji tiketi za usafiri wa anga Afrika. | uchumi |
MAOFISA Tarafa nchini wametakiwa kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ya kazi vinginevyo, atakayeshindwa kufanya hivyo atadhihirisha kuwa hamudu kazi hiyo. Rais John Magufuli amewataka viongozi hao kutambua mipaka ya kazi yao huku akiasa Maofisa Tarafa kugeuzwa wasaidizi wa Makatibu Tawala wa Wilaya (DAS) badala ya kushirikiana ili majukumu ya serikali katika maeneo yao yatekelezwe kwa ufanisi mkubwa. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli alitoa rai hiyo juzi alipokutana na Makatibu Tawala wa wilaya zote na maofisa tarafa wa tarafa zote nchini, Ikulu jijini, Dar es Salaam.Kutokana na mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo na Katibu Mkuu wa Utumishi, Dk Laurian Ndumbaro kwa wakati tofauti walimpongeza Rais Magufuli kwa kuandika historia ya kuwa Rais wa kwanza kukutana na maofisa tarafa wa nchi nzima. Rais Magufuli alisema hatarajii kuona ofisa tarafa akijihusisha na ukiukaji wa maadili na utovu wa nidhamu; hafuatilii utekelezaji wa miradi mikubwa iliyopo ama inayopita katika eneo lake kwa kuwa kufanya hivyo kutakuwa kunadhihirisha kuwa haimudu kazi hiyo. Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais aliwataka maofisa tarafa kufanya kazi kwa kujiamini, kuzingatia sheria na taratibu na kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo inayotekelezwa.Alisema DAS wanapaswa kutambua nafasi walizonazo maofisa tarafa na wote kufanya kazi kwa ushirikiano badala ya kuwageuza wasaidizi wao. Aliwataka maofisa tarafa kujenga utaratibu wa kutembelea, kusikiliza na kutatua kero na migogoro inayokabili wananchi na kuchukua hatua pale mambo hayaendi sawa hasa utekelezaji mbaya wa miradi kama ujenzi wa majengo ya serikali, barabara na miradi ya maji. Aliwataka viongozi hao kutambua mipaka ya kazi yao, kusimamia vizuri ukusanyaji mapato, kusimamia utoajivitambulisho vya wajasiriamali wadogo, kuhamasisha watu kufanya kazi za uzalishaji mali, kusimamia ulinzi na usalama, kukomesha wizi na ufisadi wa mali za umma. Wametakiwa pia kutangaza mafanikio ya serikali kuwapa matumaini wananchi. Kabla ya kuzungumza na viongozi hao, Rais Magufuli alisikiliza maoni na changamoto mbalimbali kutoka kwa viongozi hao. Rais Magufuli aliwaahidi kuwa serikali itatoa Sh bilioni moja ili kuwanunulia pikipiki Maofisa Tarafa 399 ambao hawajapata mgawo. Vile vile alimwagiza Waziri na Katibu Mkuu wa Utumishi na Utawala Bora kuondoa sharti la kutopandishwa cheo kwa Ofisa Tarafa ambaye hajapatiwa mafunzo mafupi ya utumishi. “Maofisa tarafa wenye pikipiki ni 171 na wasio na pikipiki ni 399, kwa hiyo nimeamua kutoa maelekezo zinunuliwe pikipiki kwa wote ambao hawana pikipiki, lakini nawasihi mtumie vyombo hivyo kwa uangalifu, isije ikawa ndio chanzo cha kuwapa ulemavu,” alisema Rais Magufuli. Rais Magufuli aliwapongeza wanaofanya kazi vizuri na kwa ushirikiano na watumishi wenzao wa umma waliopo katika maeneo yao.Kutokana na utendaji kazi mzuri wa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Engarenaibor Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Thomas Ngobei, Rais aliagiza apandishwe cheo na kuwa ofisa tarafa.Wakizungumza katika mkutano huo kwa nyakati tofauti, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu waliwataka maofisa tarafa kujenga uhusiano mzuri na watumishi wengine wa umma, kutoa taarifa za mambo yanayotokea katika maeneo yao na kufanya kazi kwa kutanguliza uzalendo na mshikamano wa taifa. | kitaifa |
KUTOKANA na kusambaa kwa taarifa kwa njia ya video fupi kwenye mitandao ya kijamii, ikieleza uwepo wa viashiria vya vitendo vya ugaidi nchini, serikali imewatoa hofu wananchi na kuwataka kuipuuza taarifa hiyo.Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi imebainisha kuwa video hiyo ni ya mwaka 2016, iliyorushwa na Kituo cha Televisheni cha China (CCTV-Africa).Amesema msingi wa taarifa hiyo ya mwaka 2016 ni ripoti yenye kurasa 53, iliayoandaliwa na wataalamu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi cha Mashariki mwa Afrika (IGAD), ambayo haikujikita kwenye utafiti wa kina na wa moja kwa moja kuhusu Tanzania na ugaidi, isipokuwa hisia za watu na makundi mbalimbali kuhusu ugaidi kwenye nchi za Kenya, Ethiopia na Somalia.Amesema ofisi yake imewasiliana na kituo cha CCTV- Afrika, ambapo kimekiri kuwa taarifa hiyo haikuwa na ushahidi wa maana ;na kwamba si wao walioisambaza tena video hiyo.Hivyo, amesema kwa kusambazwa tena kwa video hiyo, kunaashiria dhahiri kuwapo kwa watu wenye nia mbaya, wanaoisambaza tena kwa malengo hasi na nchi ya Tanzania.”Kwa siku kadhaa kumekuwa na taarifa inayosambaa kwa njia ya video, hivyo basi tunawaomba wananchi waipuuze, kwa kuwa si kweli kuwa nchi yetu si salama.“amesema.Amesema vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania, vipo tayari muda wote kukabiliana na kila aina ya vitisho, vinavyoweza au vinavyolenga kuharibu mazingira ya usalama wa nchi. | kitaifa |
Rais John Magufuli amesema, Tanzania na Afrika Kusini zinaongoza kwa kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, mwaka jana biashara baina ya nchi hizo ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.18 kutoka Dola za Marekani bilioni 1.11 mwaka 2017.Ameyasema hayo baada ya kuzungumza faragha na pia kufanya mazungumzo rasmi na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Ikulu, Dar es Salaam.Magufuli amesema, mwaka jana 70% ya mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenye nchi za SADC yalifanywa Afrika Kusini na kiasi hicho ni sawa na asilimia 16.7 ya mauzo yote ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi.Amesema, Afrika Kusini imepiga hatua kubwa kwa maendeleo ya viwanda, inashika nafasi ya pili kwa ukubwa wa uchumi Afrika na ni nchi pekee kwenye bara hilo iliyo kwenye kundi la nchi tajiri 20 duniani (G20).Amesema, tangu mwaka 1990 Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili mitaji 228 kutoka Afrika Kusini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 803.15.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, miradi hiyo imetoa ajira kwa 21,000.“Hii imefanya nchi ya Afrika Kusini kushika nafasi ya 13 kwa kuwekeza nchini na kuwa nafasi ya nne katika nchi zote zilizowekeza nchini ambazo zipo ndani ya Bara la Afrika."amesema. | uchumi |
WATU 18 akiwemo mkuu wa shule ya Shule ya Sekondari Tumaini Lutheran Seminary iliyopo wilayani Malinyi, Mkoa wa Morogoro, baadhi ya walimu, wasimamizi wa mitihani na baadhi ya wanafunzi wamefi kishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ulanga wakikabiliwa na makosa yanayohusu udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Willbroad Mutafungwa alibainisha hayo jana wakati akizungumzia hatua ambazo zimechukuliwa na polisi kutokana na sakata la wizi wa mitihani ya kidato cha nne 2018.Sambamba na washitakiwa hao raia kufikishwa mahakamani, Kamanda Mutafungwa amesema pia wamemtia mbaroni askari mwenye namba G 7281 Konstebo Khamisi na kumfikisha mahakama ya kijeshi kufuatia tuhuma za kujihusisha kwake, kushiriki kwa kupanga njama na kufanya udanganyifu wa mitihani wa kidato cha nne wa shule hiyo.Alibainisha kuwa askari huyo kulingana na kanuni za jeshi atafikishwa kwanza katika mahakama ya kijeshi ili taratibu nyingine ziweze kuchukuliwa na baada ya hapo atafikishwa mahakama ya kiraia kwa mujibu wa sheria za nchi.Kwa sasa wilaya ya Malinyi bado haina mahakama ya wilaya ambapo mashauri yake yanayohusiana na ngazi ya mahakama ya wilaya yanashughulikiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ulanga.Hivi karibuni Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde akizungumza Dodoma na waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne 2018 alisema baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walifutiwa matokeo kutokana na kubainika kufanya udanganyifu kwa kuingia na notes ( nondo), kwenye chumba cha mtihani.Dk Msonde amesema katika hali ya kusikitisha, uongozi wa sekondari hiyo yenye namba za usajili S0983, ulionekana kupanga mbinu za ushindi kwa kuandaaa miundombinu ya kufanya udanganyifu, jambo lililolifanya Baraza la Mitihani Tanzania kufuta matokeo ya wanafunzi 57.Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, walimu wote waliohusika na hujuma hiyo walikamatwa, kuhojiwa na kukiri kuhusika kwa kufanya udanganyifu katika mitihani ya masomo ya Hisabati, Jiografia, Historia na Kemia ambayo yalikuwa yameshafanyika.Dk Msonde, alizitaka Mamlaka husika ziwachukulie hatua stahiki walimu na askari polisi walioshiriki udanganyifu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi na Sheria za nchi.Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Januari 24, mwaka huu lilitangaza matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2018, pamoja na ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 1. 29 kutoka asilimia 77. 09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018. | kitaifa |
WANANCHI wa Kenya wanatumia fedha nyingi katika kugharamia sherehe za harusi nchini humo. Kwa mwaka jana pekee, inakadiriwa zimetumika zaidi ya Shilingi za Kenya bilioni 15, sawa na Shilingi za Tanzania bilioni 300.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jijini humu na Kampuni ya Samantha Bridal, inayojihusisha na shughuli za harusi na mitindo ya maisha.Imeonesha kuwa kutokana na matumizi makubwa ya fedha katika harusi, Kenya imeweza kutengeneza mapato yapatayo shilingi bilioni 30 kwa mwaka katika miaka michache iliyopita.Kwa wastani, Wakenya wanafunga harusi 28,000 kwa kila mwaka, ambapo kila harusi moja inagharimu kati ya shilingi za Kenya 500,000 (Sh milioni 10 za Tanzania) kwa maharusi wa kawaida na shilingi za Kenya milioni 43 kwa maharusi matajiri, gharama zote hizo zikijumuisha na kipindi kifupi cha fungate.“Wakenya wanachelewa kuoa au kuolewa wakiwa na lengo la kuimarisha maisha ya utafutaji ili baadae wakitaka kuoa au kuolewa wawe na uwezo wa kugharamia shughuli za harusi kwa gharama wanazotaka wao,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.Gwiji wa mipango ya harusi na Mmiliki wa kampuni ya Aura Events, Fatemi Bhaiji akizungumza na Business Daily alisema ripoti hiyo imeonesha hali halisi ya maisha ya wananchi wa Kenya. | kitaifa |
MWALIMU wa Shule ya Msingi Forest katika Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro, Pendo Manyama (29) na wanawe wawili wamekufa baada ya mtungi wa gesi iliyokuwa imevuja, kujaa ndani ya chumba na kulipuka.Moto huo ulilipuka mama huyo alipoingia ndani na jiko la mkaa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Wilbroad Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea Desemba 26, mwaka jana saa 8:30 mchana maeneo ya Mtaa wa Kola B katika Manispaa ya Morogoro nyumbani kwa Baltazar Kineneko (37). Kwa mujibu wa Kamanda inaonekana mtungi wa gesi ulifunguliwa na kusababisha gesi kujaa ndani.Alisema mke wa Baltazar, Pendo Manyama ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Forest, bila kujua aliingia na jiko la mkaa na kusababisha moto kulipuka na kuwaunguza mama na watoto wawili, Angela na Adrian Baltazar (2) na kusababisha vifo vyao watatu hao. Kutokana na tukio hilo, Kamanda Mutafungwa alitoa mwito kwa wananchi kuwa waangalifu wakati wote wanapokuwa wakitumia vyombo hivyo vya nyumbani ili kujiepusha na madhara yoyote yale.Katika tukio jingine, mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye pia jina lake halikutajwa, ameuawa kwa kupigwa risasi sehemu ya kichwani na mlinzi wa Kampuni ya New Bantu ambaye ni mlinzi wa Hoteli ya Green Leaf iliyopo maeneo ya Mtaa wa Mji, Kata ya Tungi katika Manispaa ya Morogoro.Kamanda Mutafungwa alisema mauaji hayo yametokea saa 9.15 usiku wa kuamkia Desemba 31, 2018 wakati mtu huyo akiwa na wenzake wawili wakiruka ukuta wa uzio wa jengo hilo kisha kuvunja na kuingia ndani ya stoo kupitia dirishani kujaribu kuiba jenereta aina ya Boss iliyohifadhiwa stoo. Kutokana na kitendo hicho, ndipo mlinzi huyo ambaye jina lake halikutajwa alifyatua risasi iliyompata kichwani huku wenzake wawili wakikimbia.Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na mlinzi anaendelea kuhojiwa. Wakati huo huo, basi lenye namba za usajili T 190 DGK aina ya Yutong mali ya Kampuni ya OTTA likiendeshwa na Jackson Kanza likitokea Dar es Salaam kwenda Bukoba limemgonga mwanamke mtembea kwa miguu asiyefahamika kwa jina anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50-55 na kusababisha kifo chake papo hapo. Kamanda Mutafungwa alisema ajali hiyo imetokea Desemba 30, 2018 saa 5.30 asubuhi Sokoine Shuleni katika Barabara Kuu ya Morogoro – Dodoma. | kitaifa |
UBALOZI wa Thailand nchini umeanza mikakati ya kutenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na kujenga viwanda kwa ajili ya kuchakata zao hilo.Huu ni uzalishaji wa kisasa ambao utashuhudia Uganda ikizalisha mpunga maradufu kutokana na uwepo wa ardhi yenye kufaa kwa kilimo hicho. Akizungumza katika siku ya kitaifa ya Thailand wiki iliyopita, Balozi huyo, Cherdkiat Atthakor ambaye anawakilisha katika eneo lote la Afrika Mashariki, alisema ofisi yake imewasiliana na wawekezaji wa Thailand kwa ajili ya kuja kuwekeza katika Kanda ya Afrika Mashariki.“Mbali na kiwanda cha mpunga, pia tutatengeneza kiwanda cha dawa ili kuwa rahisi kwa wakulima kupata dawa na kuvutia watalii wengi kwa maslahi ya Thailand na Uganda,” alisema balozi. “Mwaka jana tuliwaalika wafanyabiashara wakubwa kutoka nchini Thailand ili kujipatia soko kubwa la bidhaa zao lililopo hapa Uganda, wamefurahishwa na kufanya biashara barani Afrika,” aliongeza balozi huyo.Aliongeza kuwa watalii takribani milioni 25 wanaitembelea Thailand kila mwaka, hivyo kuna mipango ya kufanya utalii wa Uganda kuwa mashuhuri duniani kwa sababu Uganda imebarikiwa kuwa na vivutio vizuri. Balozi mdogo wa Thailand, Barbra Mulwana alisema Uganda inaendelea kufaidi matunda ya uhusiano mzuri kati yake na Thailand. Alisema upande wa elimu, kuna nafasi za wanafunzi 35 za ufadhili wa masomo nchini humo. | kitaifa |
YANGA inatarajiwa kuwa ugenini Nairobi kesho kumenyana na Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Tayari wawakilishi hao wa Tanzania wameshawasili Nairobi kwa ajili ya mechi hiyo, wakitamba kufanya vizuri licha ya kuacha nyota wake kadhaa wanaodaiwa kugoma kutokana na kutolipwa fedha zao.Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aliliambia gazeti hili kuwa anatarajia kupata matokeo mazuri katika mechi hiyo, licha ya changamoto zinazowakabili. Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr amekiri kuwa michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni Dar es Salaam, ilikuwa kipimo kizuri kwa timu yake kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga.Yanga haikushiriki michuano hiyo baada ya kujitoa kutokana na madai ya kutokuwa na wachezaji kwani wengi walikuwa hawajalipwa. Gor Mahia ilipata ushindi mwepesi baada ya kuifunga timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar kwa mabao 2-0 na kumaliza katika nafasi ya tatu ya michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam.Mchezaji Mburundi wa Gor Mahia ndiye aliyefunga bao la kuongoza ndani ya dakika saba tangu kuanza kwa kipindi cha pili kabla Samuel Onyango hajafunga bao la ushindi. “Tulipata nafasi tisa za kufunga mabao, lakini tulifanikiwa kufunga mawili tu. Siwezi sema kuwa hatujaifanyia kazi, tunachotakiwa ni kuimarika zaidi,” alisema kocha Kerr.“Nawapongeza wachezaji wangu, wameonesha uwezo mzuri, ambao utatusaidia kuelekea katika mchezo ujao dhidi ya Yanga,” aliongeza. Katika michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu, Azam FC ilifanikiwa kutetea taji lake baada ya kuwafunga mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kwa mabao 2-1. Azam waliwatoa Gor Mahia katika nusu fainali ya mashindano hayo.Mechi ya mwisho Yanga kucheza kwenye kundi lake ilikuwa dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ambapo zilitoka suluhu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Wawakilishi hao wa Bara wanacheza na Gor kesho wakiwa na pointi moja pekee iliyoipata kwenye mechi na Rayon. Mechi ya kwanza ilicheza dhidi ya MC Alger ya Algeria na kufungwa mabao 4-0. Ni muhimu kwa Yanga kuifunga Gor ili ijiweke kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye kundi D linaloongozwa na Alger yenye pointi nne, ikifuatiwa na Gor yenye pointi mbili sawa na Rayon Sports huku Yanga ikishika mkia kwa pointi moja. | michezo |
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameliagiza Baraza la Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kuimarisha kitengo cha biashara na kufanya uchunguzi wa hujuma mbalimbali dhidi ya kampuni hiyo.Akifungua kikao cha tatu cha Baraza la Wafanyakazi la ATCL, Nditiye alisema hivi karibuni baadhi ya njia katika baadhi ya maeneo, zimekuwa hazijai kutokana na abiria kuambiwa kuwa ndege zimejaa, wakati kiuhalisia sio kweli, hivyo aliwataka wafanye uchunguzi na kulitafutia ufumbuzi suala hilo.Aidha, alisema baadhi ya mawakala wanaonwa na kampuni nyingine ili wauze kwanza tiketi zao na baada ya ndege za kampuni nyingine kujaa, ndio wanauza za ATCL, hivyo alimuagiza mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo kulifanyia kazi na kwamba anataka usafiri wa ATCL uwe namba moja kisha wengine wafuate.“Kuna maneno pia kuwa baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakifanya hujuma kwa kusema tiketi zimejaa, hiyo ni hujuma. Kwa nini uhujumu kampuni wakati ndio inakulipa mshahara?” alihoji. Aliagiza wafanyie uchunguzi madai hayo na ikibainika kuwepo kwa wafanyakazi kufanya hujuma, wachukuliwe hatua. “Tunahitaji tija ya wazi hatuhitaji hujuma, kama kuna vurugu vinafanyika ni lazima zifuatiliwe, ni lazima ndege zetu zijae kwanza ndipo zingine zifuate,” alisema.Aidha, alisema ndege za kampuni hiyo ni mpya na huduma zote ndani ni nzuri na zina nauli ndogo pia, tofauti na kampuni nyingine za ndege ambazo zinatoza gharama kubwa na hakuna huduma yoyote ndani. Hivyo, aliwataka kuimarisha kitengo cha biashara kwani wanahitaji kampuni hiyo ilete tija kwa wananchi. “Kwenye biashara kuna mambo mengi, unaposikia maneno lazima uyachukue na uyafanyie kazi ili kuleta tija,” alisema Naibu Waziri.Aidha, aliwataka kutambua kuwa watumishi wa umma, wana wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, ambao ngiyo wateja wao, hivyo aliwataka pia kuhakikisha kuwa wanaweka malengo halisi ya kazi ili kuwezesha kufikia kiwango cha juu kabisa katika utendeji wao wa kazi.Aliwataka kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu ikiwamo kuonesha heshima na kujali wajibu wao na kutumia maarifa, ujuzi na utaalamu wao ili kupata ufanisi wa upeo wa juu katika utendaji wao wa kazi.“Hampaswi kutumia madaraka kwa manufaa yenu binafsi, kuwapendelea marafiki na jamaa zenu au kuwakandamiza wengine,” alieleza. Hivyo, aliwataka kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha na mali ya umma, waliyokabidhiwa na kwamba ni wajibu wao kuzuia uharibifu, upotevu au ubadhirifu usitokee kutokana na uzembe au manufaa ya mtu binafsi au kundi fulani ikiwa ni pamoja na kujihusisha na vitendo vyovyote.Aliwataka kutambua kuwa msingi wa mafanikio ya usafirishaji wa anga ni utoaji huduma bora na uwajibikaji, wanapaswa kuwahudumia wateja wao na watumishi wenzao kwa heshima.Aliwataka kuhakikisha wanawahudumia kwa umakini zaidi wananchi wanye mahitaji ya kipekee wakiwemo wazee, wanawake, watoto, wagonjwa, walemavu na kundi lolote la watu ambao wapo katika hali ngumu. Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema wao ni wafanyabiashara lazima wasikilize wateja na wadau wao, hivyo malalamiko hayo walishaanza kuyachukulia hatua mbali mbali. | kitaifa |
MTOTO anayesumbuliwa na kitovu chenye ukubwa usio wa kawaida, ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa baada ya wataalamu kumchunguza na kuelekeza utunzaji wake ikisubiriwa umri sahihi wa kuweza kumfanyia upasuaji.Habib Kassim mwenye umri wa miezi minane kutoka Nzega mkoani Tabora alikuwa amelazwa katika wadi ya upasuaji ya watoto kabla ya kuruhusiwa juzi baada ya madaktari kumuona.Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Erasto Sima ambaye kwa kushirikiana na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ndio waliosaidia kumfikisha hospitalini hapo, alisema matibabu yamefanyika na imeonekana sasa upasuaji hauwezi kufanyika hadi atakapofikisha umri wa miaka minne na kuendelea. Kwa mujibu wa Sima, jopo la madaktari lilisema wakimfanyia upasuaji sasa, tumbo lake bado ni dogo hivyo haiwezekani kurudisha utumbo wote uliojikusanya ndani ya kitovu. Walieleza kwamba kadri anavyokua, utumbo utakuwa unarudi na inawezekana ikifika umri huo unaostahili, upasuaji usihitajike. Alisema madaktari walisema mtoto huyo ataishi kama mtoto mwingine isipokuwa cha muhimu ni kuwa na utunzaji aweze kukaa vizuri. Wataalamu hao walisema baada ya miaka mitatu atapaswa kurudi Muhimbili kwa ajili ya kuangaliwa. Alisema ipo dawa aliyoandikiwa atakayokuwa akipaka kwenye eneo la kitovu ambayo ataipata katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Walezi wa mtoto wamepewa barua itakayowawezesha kupata dawa hiyo katika hospitali hiyo. Akieleza hatua za kumsaidia mtoto huyo, alisema aliona makala katika gazeti hili (HabariLeo) iliyomwelezea mtoto na namna familia ilivyokosa nauli ya kumpeleka hospitali ya rufaa Bugando, jijini Mwanza. “Nilipoona habari hizi ndipo nikamtafuta katibu wa wilaya ya Nzega nikaagiza wamtafute mtoto,” alisema na kuongeza kwamba awali, walitaka wampeleke Bugando lakini Mbunge Bashe alisema yuko tayari kugharimia kila kitu. Mtendaji huyo wa jumuiya ya wazazi ametaka jamii ijenge utamaduni wa kusaidiana hususani katika masuala ya ugonjwa.Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Nzega, Regina Ndulu aliyeongozana mtoto, bibi na mama mdogo wa Habibu kuja jijini Dar es Salaam, alisema amefurahishwa na matibabu pamoja na ushauri uliotolewa na madaktari kwa kuwa umesaidia familia kuwa na amani.“Wamesema mtoto aendelee kuwekewa dawa aliyokuwa akiwekewa baadaye ngozi itaendelea kukomaa na akifikisha miaka mitatu, arudishwe Muhimbili wamwangalie,” alisema Ndulu.Akizungumza jana, bibi wa Habib, Hadija Gogati alishukuru gazeti hili sambamba na wasamaria waliofanikisha kufika Muhimbili kwa matibabu. “Bila ninyi na hawa (jumuiya ya wazazi) tusingeweza kufika hapa,” alisema. Aliendelea, “sasa hivi nina amani kwa sababu madaktari wamenieleza namna ya kumhudumia mtoto. Wamesema haiwezekani kumfanyia upasuaji sasa hivi. Walinieleza vizuri na nimeelewa kuwa baadaye hili tatizo litapungua kidogo kidogo.”Makala iliyofanya wasamaria hawa wajitokeze ilichapishwa hivi karibuni ikieleza familia ilivyoshindwa kuzingatia miadi ya Februari mwaka huu kumpeleka hospitali ya rufaa Bugando kutokana na kukosa nauli na fedha za kujikimu wawapo jijini Mwanza. | kitaifa |
RAIS wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf), Ahmad Ahmad amekamatwa jana asubuhi jijini Paris, Ufaransa akituhumiwa kwa rushwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali.Gazeti la kila wiki la Afrika la Jeune Afrique lilidai kuwa rais huyo wa Caf alikuwa akiishi jijini Paris katika hoteli moja wakati akihudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Shirikisho la Kimataifa la Soka, Fifa.Wakati taarifa hizo zikiwa bado hazitawekwa wazi, inadaiwa kuwa Ahmad mwenye umri wa miaka 59 alikamatwa kutokana na tuhuma zinazohusu rushwa kutoka katika kampuni moja.Rais wa Caf Ahmad alikamatwa jana asubuhi majira ya saa 2:30 katika hoteli ya Berri Hotel jijini Paris, Ufaransa kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari. Kukamatwa huko kunahusishwa na suala la mkataba wa Puma, ambao unaipendelea kampuni nyingine.Kwa mujibu wa ripoti Ahmad alisaini mkataba unaonufaisha kampuni ya Technical Steel, ambao bosi wao mmoja alisema alilipa kiasi cha Euro 739 000 kwa Rais huyo wa Caf ili kufanikisha mpango huo. Inaelezwa kuwa kesi hiyo inayomhusu Ahmad itasikilizwa na ofisi kuu dhidi ya rushwa. | michezo |
[' Siku ya Jumanne mashabiki wa mojawapo wa timu kongwe Tanzania watakusanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kusherehekea "Simba Day".', 'Ni katika kuidhinisha wiki ya Simba au kwa umaarufu "Simba Week" na inahusisha mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia pamoja na mechi za timu za wanawake walio chini ya miaka 20.', 'Shughuli zilizopangwa kwa siku saba zimenuiwa kuongeza ukaribu na ushirikiano baina ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo pamoja na Simba kuisaidia jamii kupitia miradi tofuati.', 'Ni sehemu ya azimio la Bilionea Mohammed Dewji, mmiliki mwenza wa klabu hiyo anayeitaka klabu hiyo ikuwe ndani na nje ya uwanja ili kuhakikisha ufanisi zaidi.', '"Niliwahi kukutana na mojawapo ya viongozi wa Zamalek (mnamo 2003) na niligundua wakati huo kuwa bajeti ya Zamalek ni mara 50 zaidi ya bajeti ya Simba," anaielezea BBC Sport."', '"Naweza kuilinganisha na dereva anayeendesha Toyota na mwingine anayeendesha Ferrari - mtu hufanya awezalo." ', 'Azimio la Dewji', 'Aliporudi Tanzania baada ya mashindano hayo ya ubingwa barani Afrika, Dewji alifahamu kuwa mambo yanahitaji kubadilika katika namna ambavyo klabu hiyo inaendeshwa iwapo inataka kushindana.', 'Kwa wakati huo, pendekezo lake la kubadilishi mfumo wa umiliki wa klabu hiyo, haukupokewa vizuri na alijitoa Simba mnamo 2004.', 'Miaka 11 baadaye, katika televisheni nchini humo alijadili atakachokifanya kuongeza mara tatu bajeti ya klabu hiyo, kuwekeza katika miundo mbinu na namna ambavyo wangeliliziba pengo katika kufikia klabu kubwa barani Afrika.', '"Ilikuwa kama mzaha tu lakini Simba ilikuwa haifanyi vizuri na mzaha ukashika kasi," alifafanua.', "Miaka miwili baadaye 'mzaha' huo ulimfanya shabiki sugu wa Simba arudi na kumiliki 49% ya hisa katika klabu hiyo.", 'Umiliki na mageuzi hayo yalioidhinishwa na wafuasi wa klabu ya Simba ulikuwa kama kivuko kuingia katika ufanisi wa klabu hiyo msimu uliopita.', 'Mnamo 2018 walifanikiwa kuidhinisha usajili wa wachezaji mahiri katika safari ya Uturuki na ilionuiwa kuimarisha ushindani wa klabu hiyo nchini na kimataifa.', ' Zaidi ya hapo walifanikiwa kuwekeza katika miundo mbinu msingi, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa kisasa na wa kufanya mazoezi.', 'Simba ilifikia malengo yake msimu uliopita - kwa kushinda katika ligi na kufika kiwango cha makundi katika ligi ya mabingwa, walifanikiwa zaidi kwa kufuzu katika robo fainali ya mashindano ya klabu barani.', 'Licha ya kufanikiwa kuiongeza bajeti ya mwaka zaidi ya mara mbili kwa klabu hiyo, Dewji anafahamu kuwa ipo kiwango cha chini ikilinganishwa na klabu nyingine barani zilizofanikiwa, lakini anaamini itazifikia kifedha katika miaka mitano ijayo.', '"Miaka miwili iliyopita tumeongeza bajeti yetu mara mbili kutoka takriban $1m kwa mwaka hadi $2.5m," Dewji amefafanua.', '"Tutashirikiana na makampuni kama Mohammed Enterprises na Total. Tunafahamu kuwa kila Mtanzania ni lazima anunuwe mafuta, mchele na sukari.', '"Iwapo mashabiki watanunua bidhaa kutoka Mohammed Enterprises watapata punguzo la bei, na kwa upande wao, washirika watawapa thamani ya kutosha ya mauzo hayo."', 'Kuwaleta mashabiki', 'Njia nyingine ambayo klabu hiyo inatumai kushindana ni kwa kuimarisha ushirikiano na mashabiki wake.', '"Tunawavutia. Tumekusanya taarifa kuwahusu. Tumelenga thamani inayostahili katika suala la kiingilio," Dewji ameendelea kusema.', '"Tumezusha shauku kubwa. Tumeidhinisha ukaribu na magazeti na vituo vya redio. Nadhani ndio mwanzo mkoko unaalika maua."', 'Simba imejaribu kuifanya soka iwe na bei nafuu na inayowavutia kila mtu aliye na fikra kama vile tiketi za gharama ya chini zinazo wavutia walio na kipato cha chini.', 'Wakati huo huo kuna tiketi za gharama ya juu - platinum level - kwa wanaojiweza na inayojumuisha fulana ya Simba, usafiri wa basi kwenda na kutoka uwanjani, na viti vya watu muhimu.', 'Shauku ya mashabiki wao 60,000 katika mechi za nyumbani zimewavutia watazamaji wengi wa soka Afrika.', '"Nilikuwa ninazunguma na rais wa shirikisho la soka Caf Ahmad na amesema hajawahi kuona mashabiki wa Afrika wakijaza uwanja katika mechi za nje kama ilivyokuwa kwa Simba. Mpango wetu wa kuwa na uwazi una manufaa."', 'Uwazi huo umehimiza ushirikiano wa karibu baina ya mashabiki na Dewji amesisitiza umuhimu wa hilo kwa wanachama wa bodi yake.', '"Simba ni klabu kubwa. Ni nembo kubwa," aliongeza.', '" Ni jukumu letu kama viongozi wa klabu hii na kama mmiliki wa klabu hii kwamba A) tuwe na maadili katika tunachokifanya B) Tunahitaji kuwa na uwazi mkubwa katika tunachokifanya na C) tunahitaji kuwasiliana na mashabiki wetu kupitia vyombo vya habari kufafanuwa azimio letu ni lipi."', 'Ufanisi wa Simba umeathiri pia timu ya taifa ya Tanzania wakati Taifa Stars ilipofuzu kwa mara ya kwanza katika miaka 39 kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika.', 'Dewji aliongoza kamati iliyohakikisha mechi muhimu ya kufuzu kwa Tanzania dhidi ya Ugnada ilipata uungwaji mkono mkubwa wa mashabiki.', '"Kuwaona mashabiki wengi kulitupatia nguvu ya kwenda na kupambana na kufuzu," alisema mchezaji wa kiungo cha kati wa timu hiyo ya taifa Himid Mao, anayeichezeka klabu ya Misri Petrojet.', '"Tulipokuwa njiani tukielekea uwanjani, tukawaona mashabiki wengi ilitufanya tuhisi kama tuna deni la kuwalipa."', 'Mpango ulifanikiwa huku mashabiki wakiwashangilia, timu hiyo ilipata ushindi wa 3-0 ikiwemo mkwaju wa penalti wake Erasto Nyoni wa klabu ya Simba dhidi ya majirani zake na kufanikiwa kufuzu katika mashindano hayo nchini Misri.', 'Nyoni wa Simba ni moja kati ya wanne waliocheza katika kikosi cha Tanzania katika kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri akiwemo pia Kipa John Bocco, Aishi Manula, na mchezaji wa ziada Mohamed Hussein.', 'Na kulikuwa na wachezaji wawili pia wa Simba katika kikosi cha Uganda nchini Misri, nao ni Murushid Juuko na Emmanuel Okwi, ambaye ameondoka kujiunga na Al Ittihad ya Misri.', 'Matumaini ya Simba sasa ni kushinda katika ligi ya mabingwa na kwa mkono wa biashara wa Dewji anayeushikilia usukani, gari hilo ambalo halikuweza kushindana katika siku za nyuma, linaonekana kusogea katika muelekeo mzuri na linashika kasi.'] | michezo |
['Kevin de Bruyne amekuwa kiungo muhimu wa Manchester City msimu huu, akitengeza nafasi chungu nzima zaidi ya mchezaji mwengine yeyote mbali na kuongoza jedwali miongoni mwa wachezaji waliotoa pasi nyingi zilizosababisha magoli. ', 'Ni ndoto ya mshambuliaji yeyote yule, kucheza mbele ya De Bruyne kutokana na pasi zake murua anazotoa. ', 'Anaweza kukupatia kile unachohitaji mbali na kwamba pia anaweza kufunga. ', 'Goli lake dhidi ya Newcastle wiki iliyopita lilikuwa bora zaidi - lakini sishangai anapofanya vitu kama hivyo ambazo ni ishara za mchezaji mzuri-anaweza kufanya kila mara.', 'Sio lazima uwe bora ndio ufanye vizuri katika timu - kama alivyo kiungo wa kati wa Man United Scott Mc Tominay ambapo ameimarika na kuwa miongoni mwa viungo wa kati wazuri zaidi kuwahi kuichezea Man United. ', 'Hawezi kufananishwa na wachezaji wengine katika kutengeneza nafasi za magoli lakini kwa sababu tofauti , atakuwa muhimu katika timu yake katika debi ya Jumamosi.', "'McTominay ndiye mtu anayetegemewa United'", 'McTominay atakuwa mmojawapo wa majina ya kwanza katika kikosi cha United katika uwanja wa Etihad na mara nyengine alionyesha kwa nini siku ya Jumatano alishinda dhidi ya Tottenham. ', 'Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uskochi alirudi baada ya mechi mbili za ligi ambapo alikuwa amejeruhiwa na kuleta nguvu nyingi katika safu ambayo ilikuwa hafifu. ', 'Mkufunzi wa United alipongeza uongozi wake na uwezo wake na kusema ni mchezaji ambaye hawezi kuachwa nje baadaye na sasa naona kwa nini. ', 'McTominay amekuwa tegemeo kubwa sana kwake , katika eneo ambalo timu hiyo imekuwa hafifu na United itahitaji nidhamu na mipango katikati iwapo wanataka kuinyamazisha City. ', 'City imekuwa na matatizo katika idara hiyo, huku Rodri akitumia muda mwingi kupata uzoefu katika jukumu lake la kuchukua nafasi ya Fernandinho kama kiungo wa kati. ', 'Lakini Rodri alikuwa muhimu dhidi ya Burnley siku ya Jumanne usiku , hatua ambayo ni ishara nzuri kwa City kabla ya mechi ya wikendi. ', 'Aliweza kuwazuia wachezaji wa timu hiyo mara kwa mara kila walipojaribu kupenya katika lango la City. ', 'Walimuhitaji kwasasabu imekuwa rahisi kupita safu ya ulinzi katika mechi zilizopita. ', 'Ni vyema kwa Guardiola ambaye anasema kwamba walishambuliwa mara mbili pekee na Newcastle siku ya Jumamosi lakini magoli yote yaliingia.', 'Ilikuwa wiki njema kwa klabu zote mbili za Manchester na zote mbili zitaingia siku ya Jumamosi zikiwa na sababu za kuamini kwamba zitafanikiwa.', "City walicheza kana kwamba wana sababu ya kudhihirisha dhidi ya Burnley siku ya Jumanne usiku na jinsi 'walivyofurahia ilionyesha umuhimu wa mechi hiyo. ", 'Kwa nini ushindi huo ulikuwa muhimu? , ukweli ni kwamba kila mtu anazungumzia kuhusu Liverpool na Leicester katika ushindani wa taji la ligi. ', "Ilifikia wakati ambapo klabu ya Guardiola ilikuwa imesahaulika katika kinyang'anyiro hicho na walikuwa nyuma na pointi 11. ", 'Walikua hawajacheza vizuri katika kipindi cha wiki chache zilizopita na nikaona kwamba watakuwa na wakati mgumu wakicheza dhidi ya Burnley. ', 'Vilevile ushindi wa Jumatano dhidi ya Tottenham ulikuwa mkubwa kwa klabu kama United . ', 'Kiwango cha mchezo wao kilikuwa kizuri na walionyesha mchezo mzuri kuanzia mwanzo. ', 'Napenda jinsi walivyocheza dhidi ya Spurs kutoka mwanzo wa mchezo, na jinsi walivyopanda baada ya Tottenham kusawazisha na baadaye kuwazuia vizuri mwisho. ', 'Hakuwakuweza kufanya vitu kama hivyo mara kwa mara katika majuma ya hivi karibuni. United wanaelekea katika uwanja wa Etihad wakitafuta kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya timu kubwa. ', 'Mchezo wao mzuri dhidi ya timu bora za ligi ya Uingereza ni ishara tosha kwamba watafanikiwa.', 'Kikosi cha Solskjaer bado hakijapoteza dhidi ya timu ambayo ilimaliza katika nafasi sita bora za ligi ya Uingereza na ni miongoni mwa timu mbili pekee ambazo zimefanikiwa kuilaza Leicester City 2019- 20. ', 'Ushindi wao dhidi ya Spurs ndio uliodaiwa kuwa mzuri zaidi dhidi ya timu ambayo inafunzwa na mkufunzi wao wa zamani Jose Mourinho ambaye angewatia motisha wachezaji kwa mara ya kwanza akirudi katika uwanja wa Old Trafford tangu afutwe na Man United.', 'Ndio wanahitahi uzoefu kuthibitisha kwamba wanaweza kuzifunga timu ambazo hazina upinzani mkubwa. ', 'Huku City ikitarajiwa kutawala mchezo siku ya Jumamosi , tisho la United katika uvamizi inamaanisha kwamba hawatajali. ', 'United inapenda kucheza dhidi ya timu zinazpenda kuvamia na kushambulia lango lake kwa kuwa wana kasi ya kuwatia jeraha wanapovamia na nina hakika watapa nafasi Etihad. ', 'Marcus Rashford alionyesha kiwango kizuri cha mchezo dhidi ya Spurs na alifanya kila kitu alichohitajika kufanya. ', 'Alionekana amenolewa na atajaribu kufunga magoli zaidi wikendi hii.'] | michezo |
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka maofisa ardhi na mipango miji mkoani humo kutoa elimu kwa umma juu ya hifadhi na matumizi bora ya ardhi, kama njia moja ya kuepusha migogoro.Aliyasema hayo Fuoni Kipungani baada ya kuirudisha serikalini eneo la ekari tatu lililokuwa likitumiwa na Said Mbaraka na Maulidi Ramadhan Saleh baada ya kukiuka masharti ya umilikaji wa ardhi hiyo.Aliwataka watendaji wa taasisi hizo kushirikiana na uongozi wa shehia kulihifadhi na kupanga matumizi ya eneo hilo.Alisisitiza kuwa uongozi wa Mkoa wa mjini magharibi Unguja utaendelea na uchunguzi. Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi, ardhi yote ya Zanzibar ni mali ya serikali, mtu aliyekabidhiwa ni sawa na aliyepewa dhamana.''Wananchi wote wanatakiwa kufahamu kwamba ardhi yote ni mali ya serikali na ipo chini ya mikono ya rais ambaye humpa dhamana kiongozi husika,''amesema.Ofisa wa Idara ya Ardhi, Saleh Kombo alisema serikali imegawa ekari tatu kwa ajili ya shughuli za kilimo na matumizi yoyote kinyume na hayo hayakubaliki ambapo ekari italazimika kurudishwa serikalini.''Ekari tatu zilizotolewa na hayati Abeid Amani Karume matumizi yake ni kwa ajili ya shughuli za kilimo tu na si vinginevyo...mtu atakayebainika akifanya kinyume yake atanyan’ganywa umiliki wake,''amesema.Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa B, Ali Said Natepe amesema wanaendelea elimu kuhusu umuhimu wa kutunza ekari tatu ambapo hivi sasa baadhi ya wamiliki wake wameziuza na kukatwa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kudumu.''Tunajua ekari tatu nyingi zimevamiwa na kujengwa nyumba kwa ajili ya makazi ya kudumu, kitendo ambacho hakikubaliki,''amesema. | kitaifa |
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na TPA ya kati ya Julai 2013 na Machi 2014 kuhusu utekelezaji wa mkakati huo, imeonesha pamekuwa na maendeleo makubwa na kuongezeka kwa ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam, ikilinganishwa na kabla ya Julai mwaka jana.Pamoja na mambo mengine, mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa unalenga kubadilisha bandari za Tanzania na hasa ile ya Dar es Salaam kuwa kitovu kikuu cha uchumi Tanzania na kutoa ushindani katika ukanda wa Afrika.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, pamekuwa na ongezeko la mizigo katika bandari hiyo kwa muda huo unaofikia tani milioni 10.95, ikiwa ni mafanikio kwa asilimia 84.2 kabla ya kufikia lengo la tani milioni 13 kwa mwaka 2013/2014.Muda wa meli kukaa bandarini kwa mwezi Machi mwaka huu, ilikuwa siku 6.1 kwa meli, mafanikio ya asilimia 82.0 kabla ya kufikia lengo la siku 5 kwa meli.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, muda wa kukaa kwa mizigo bandarini kutoka nje kwa Machi mwaka huu, ilikuwa siku 10.0 kwa kontena, ikilinganishwa na lengo la siku 7 kwa kontena.“Hali hii imesababishwa na miundombinu mibovu ya reli na kutegemea usafirishaji kwa njia ya barabara kwa kiwango kikubwa,” imeeleza ripoti hiyo. Uwezo wa kutoa magari bandarini, umeongezeka kwa asilimia 100.7 kwa mwezi Machi mwaka huu, na magari 604 yakitolewa kwa awamu.Ripoti hiyo ilisema kuwa kwa Machi 2014, lengo la kutumia siku tatu kwa lori moja la mizigo kuwa limeondoka bandarini, limefikiwa kwa asilimia 81.1, kwani sasa lori moja linatumia siku 3.3.Kwa sasa kwa mujibu wa ripoti hiyo, juhudi za kufanya bandari hiyo kufanya kazi kwa saa 24 kwa siku saba za wiki, ziko katika hatua za mwisho.Ripoti ya makubaliano ya wadau wote wa Serikali na sekta binafsi, iliyofikiwa Februari mwaka huu, itajadiliwa hivi karibuni tayari kwa utekelezaji.Ikizungumzia mfumo wa Kituo Kimoja cha Huduma za Bandari, unaolenga kurahisisha kazi za nyaraka bandarini hapo, ripoti hiyo inasema tayari mfumo huo umeshaanza kutumika tangu Aprili 25, mwaka huu. | uchumi |
IDADI ya watu waliopoteza maisha kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa, imeongezeka na kufi kia watano huku idadi ya watu ambao hawana makazi ikifi kia 2,205.Pia mvua hiyo pia imeharibu nyumba 441, shule mbili na makanisa mawili. Aidha wakazi 165 kutoka Kijiji cha Mshete wilayani Nkasi kujikuta hawana makazi baada ya nyumba zao 33 kubomolewa na mvua za masika juzi huku mwananchi mwenye umri wa miaka 80, akipoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake.Awali wiki mbili zilizopita, watu wengine wanne walipoteza maisha akiwemo Elizabeth Manamba (85) mkazi wa Kijiji cha Kipeta na mwingine ni mtoto mwenye umri wa miaka minane kutoka Kijiji cha Tunko wilayani Sumbawanga aliyepigwa na radi. Wengine ni watoto wawili waliokuwa wakiishi katika Kijiji cha Matala, Laiton Kalindo (10) aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Matala wilayani Nkasi na Mathias Anselimu (8).Mbali ya hayo, watu wapatao 57 wamejeruhiwa huku paa za Shule ya Sekondari Kipeta zimeizuliwa zote. Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo alielezwa kushtushwa kwake na maafa hayo ambayo amekiri kuwa ni changamoto kubwa huku akisisitiza kuwa yanaweza kuwa makubwa zaidi kwa kuwa hizi ni mvua za awali za masika.“Hofu yangu ni kwamba maafa yanaweza kuwa makubwa ya kutisha kadri mvua za masika zinavyoendelea kunyesha hizi ni za awali tu na zimesababisha maafa makubwa kiasi hiki ni changamoto kubwa kimkoa pekee yetu hatuwezi tunahitaji misaada ya mali na hali kutoka ndani na nje ya mkoa,” alisisitiza. Alisema harambee kubwa inatarajiwa kufanyika ili kuwasaidia waathirika ambao wamepoteza kila kitu huku Shule ya Sekondari Kipeta ambayo imeachwa taabani na mvua hiyo ukarabati wake unahitaji zaidi ya Sh milioni 470.“Wanafunzi wapatao 500 wanaosoma katika Shule ya Sekondari Kipeta iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga hawataweza kuanza masomo shule zitakapofunguliwa Januari mwakani kutokana na miundombinu yake ikiwemo vyumba vya madarasa kuharibiwa na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali,” alieleza. Shule hiyo ina wanafunzi wanaosoma Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Sita ikiwa ni shule ya bweni na mchanganyiko. | kitaifa |
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Bara ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Zuberi Katwila amesema anaamini kikosi chake leo kitashinda dhidi ya Sudan. Timu hiyo leo inakutana na Sudan mjini Gulu, Uganda katika mechi ya nusu fainali za michuano ya kombe la Chalenji kwa vijana wa umri huo.Tanzania Bara ilifuzu nusu fainali baada ya kuwafunga wenyeji Uganda Hippos kwa mabao 4-2 katika mchezo wa robo fainali na Sudan iliifunga Sudan Kusini kwa bao 1-0. “Tumefanya maandalizi kwa ajili ya kuikabili Sudan na tunaamini mchezo wa kesho (leo) tutashinda, kikubwa watanzania watuombee kwani kila nchi imejiandaa na kuna wachezaji wenye vipaji,” alisema Katwila. Pia Katwila alisema anajivunia kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji kuanzia safu ya ushambuliaji hadi walinzi.Naye kocha wa Sudan, Mohamed Mousa alisema anaamini anakutana na timu bora lakini wamejiandaa kushinda. Tanzania Bara haijapoteza mchezo wowote tangu hatua ya makundi kwani ilishinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja na kuwa kinara wa kundi B ikiwa na pointi saba.Katika mchezo mwingine Kenya ambayo iliitoa Burundi kwa mabao 2-1 itaivaa Eritrea iliyofika hatia hiyo kwa kuifunga Zanzibar mabao 5-0.Fainali za michuano hiyo inayosimamiwa na Baraza la vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) inatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii. | michezo |