url
stringlengths
18
212
text
stringlengths
608
373k
index
stringlengths
64
64
word_count
int64
100
24.7k
mean_word_length
float64
4.5
15.8
num_sentence
int64
3
547
character_count
int64
502
349k
line_count
int64
1
1
fraction_of_duplicate_lines
float64
0
0
fraction_of_characters_in_duplicate_lines
float64
0
0
symbol_to_word_ratio
float64
0
1
fraction_of_words_without_alpha
float64
0
10
num_of_stop_words
int64
10
2.51k
https://www.vpo.go.tz/news/unep-kuiunga-mkono-tanzania-katika-nishati-safi-ya-kupikia
Tanzania imeahidiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuungwa mkono katika vipaumbele vya mazingira ikiwemo agenda ya nishati safi ya kupikia. Hayo yamejiri wakati wa mazungumzo kati ya Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bi. Elizabeth Mrema Julai 11, 2024 jijini Nairobi, Kenya. Mazungumzo hayo yamefanyika katika kikao cha pembeni baina ya viongozi hao wakati wa Mkutano wa 11 wa Wawakilishi wa Kudumu wa UNEP uliotarajiwa kumalizika Julai 12, 2024. Bi. Mndeme ameishukuru UNEP kwa kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Halikadhalika, ameliomba shirika hilo kuendelea kuunga mkono Tanzania hususan katika utekelezaji wa vipaumbele vya nchi katika sekta ya mazingira vikiwemo agenda ya nishati safi ya kupikia, biashara ya kaboni na uchumi wa buluu. Bi. Mrema ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa michango yake kwenye agenda zilizowasilishwa na kujadiliwa kwa kipindi chote cha mkutano huo. Kutokana na hatua hiyo Naibu Mkurugenzi huyo amepokea michango hiyo na kuahidi kuichukua kwa ajili ya kuweka kwenye vipaumbele kwenye mpango kazi wa Shirika la UNEP katika kipindi cha mwaka 2024-2025 kwa ajili ya kuifanyia kazi. Mkutano wa 11 wa Wawakilishi wa Kudumu wa UNEP unafanyika kwa lengo la kupitia programu za shirika hilo UNEP kwa kipindi cha mwaka 2022- 2023 na kupitia mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2023 – 2024. Pia, katika mkutano huo wajumbe wanapitia utekezaji wa kazi za shirika hilo hususan kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai na uchafuzi wa mazingira. Sanjari na hayo, pia wajumbe wa mkutano huo uliofunguliwa Julai 08, 2024 wamepata wasaa wa kufanya maandalizi ya mikutano ijayo ya Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA - 7). Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Bernad Kibesse.
befb751b82db3d4566477f44aba079b69240621b1bf95d41798e5ff85b8dbc7c
327
5.409786
18
1,769
1
0
0
0
4.89
38
https://www.vpo.go.tz/news/dkt-kijaji-nemc-muongeze-kasi-utoaji-vyeti-ya-tathmini-ya-athari-kwa-mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amelielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuongeza kasi ya utoaji wa vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) katika miradi inayotekelezwa nchini. Dkt. Kijaji amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kutembelea Ofisi za NEMC kwa ajili ya kuzungumza na Menejimenti pamoja na kufahamu majukumu ya kisheria yanayosimamia Baraza hilo. Amesema katika kipindi hiki, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kujipambanua katika kufungua milango kwa wawekezaji wa miradi ya maendeleo nchini, juhudi ambazo zinahitaji kuungwa mkono kwa vitendo na taasisi zote za umma ikiwemo NEMC. “Natambua mmeendelea kufanya kazi nzuri katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Sura 191…Naomba hili la vyeti vya tathimini ya mazingira tuliangalia kwa jicho la kipekee ili kuwezesha utekelezaji wa miradi” amesema Dkt. Kijaji. Aidha Waziri Kijaji amefafanua kuwa Ofisi yake ina imani na matumaini makubwa na watendaji wa Baraza hilo katika kuakisi maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika usimamizi na uhifadhi endelevu wa mazingira ili kulinda afya na maisha ya Watanzania. Ameeleza kuwa NEMC inapaswa kuwa kiungo katika kutoa ushauri wa kiufundi na kitaalamu wakati wa mchakato wa maombi ya vyeti vya tathimini ya mazingira kwa kuhakikisha waombaji wanapatiwa maelekezo ya namna bora ya kushughulikia kasoro na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo ya miradi. “Tunapobaini kasoro au changamoto wakati wa maombi ya vyeti tutoe msaada wa haraka ili waombaji waweze kuzirekebisha na kutoa taarifa na kuwajulisha mapema na pia tusichukue muda mrefu kwa waombaji wakisubiri huduma hii” amesema Dkt. Kijaji. Akifafanua zaidi Dkt. Kijaji amesema Watanzania wana imani na matumaini makubwa na Baraza hilo katika usimamizi endelevu wa mazingira na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa na jamii salama kwa mustakabali wa vizazi vya sasa na vijavyo. Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali itaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa Baraza hilo ikiwemo kusimamia mchakato wa mabadiliko ya muundo wa Baraza hilo ambao upo katika hatua nzuri. Ameongeza kuwa Baraza hilo lina wataalamu wenye ujuzi, weledi na maarifa ya kitaaluma katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira, hivyo utaalamu huo hauna budi kutumika vyema katika kubuni na kubaini miradi inayoweza kutoa suluhisho ya changamoto za uharibifu wa mazingira nchini. “NEMC ina wasomi wazuri wenye fani mbalimbali ambao wakitumika vyema wataisaidia nchi kuweza kupiga hatua kubwa na pia kuandaa mipango itakayosaidia kupata majibu ya changamoto za uharibifu wa mazingira katika taifa letu” amesema Mhe. Khamis. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NEMC, Prof. Esnati Chaggu ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuendelea kuiwezesha Bodi kutekeleza vyema majukumu yake kupitia Mpango Kazi ulioandaliwa na menejimenti ya baraza hilo. Amesema katika kuharakisha kasi ya utekelezaji wa majukumu, baraza limebuni mfumo ya kieletroniki kupitia TEHAMA ambapo huduma mbalimbali zinazotolewa katika mfumo huo ikiwemo vyeti vya tathimini ya mazingira na hivyo kurahisisha utendaji kazi. Kuhusu usimamizi wa Sheria, Prof. Chaggu amesema baraza limeendelea kusimamia utekelezaji wa sheria ya upigaji marufuku wa matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali na sekta binafsi. “Tunaishukuru Serikali kwa ushirikiano unaoipatia baraza..tunaahidi kuongeza kasi, weledi na maarifa zaidi katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ili tuweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa kuzingatia maono ya Viongozi wetu” amesema Prof. Chaggu. Aidha kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware amesema Baraza litaendelea kupokea na kutekeleza maelezo yanatolewa na Viongozi Wakuu wa Serikali katika kusimamia Sheria ya Mazingira Sura 191. “Baraza limeendelea kufanya kazi kubwa…Tupo tayari kwa kazi na tutauwepo majini na ardhini kwani tuna wataalamu wenye weledi katika kutekeleza majukumu tuliyopewa” amesema Dkt. Sware.
8e4c9c8f2519ea360cb2a56c294f65947f922ab069c0ecda4f7d17a1c11f520c
601
5.843594
29
3,512
1
0
0
0.332779
0.17
79
https://www.vpo.go.tz/news/dkt-mpango-maafisa-biashara-msiwe-kikwazo-kwa-wafanyabiashara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka maafisa biashara kutokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wakati wa utekelezaji wa majukumu yao. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kasulu akiwa ziarani mkoani Kigoma mara baada ya kupokea malalamiko ya matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa kuhamisha wafanyabiashara katika maeneo waliyokuwa wanatumia Wilayani hapo. Amesema suala la kutumia nguvu ikiwemo mabomu ya machozi kwa wananchi ambao hawana silaha ni kinyume na sheria na utaratibu. Aidha ameagiza viongozi wa Halmashauri hususani maafisa biashara kuwaelimisha wananchi kuhusu oparesheni mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika ili kuondoa taharuki wakati wa utekelezaji wake. Makamu wa Rais amekemea vitendo vya utozaji ushuru kwa mazao chini ya tani moja kwani serikali tayari ilipiga marufuku suala hilo. Makamu wa Rais amesema serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Kigoma ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine. Amewasihi wananchi wa Kasulu na watumiaji wote wa barabara zinazojengwa kuzingatia matumizi salama ya barabara kwa kufuata sheria ili kuepusha madhara ya ajali ikiwemo vifo na majeruhi. Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amezungumza na wananchi wa mji wa Makere ambapo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kutumia sheria ndogo vema katika kudhibiti uharibifu wa mazingira. Amewahimiza viongozi wa dini na kimila kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na kudhibiti uchomaji moto kwenye misitu. Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha mita zinapatikana ndani ya miezi miwili ili kuwaunganishia huduma ya maji wananchi wa Makere. Amesema mji huo huduma ya maji ni toshelevu lakini wananchi wengi hawajaunganishwa na huduma hiyo sababu ya ukosefu wa mita. Pia Makamu Rais amekemea tabia ya kuharibifu wa miundombinu ya maji na kuagiza watendaji kuwatafuta na kuwachukulia hatua wahalifu wote walioharibu miundombinu ya maji Wilayani Kibondo. Makamu wa Rais amesema Serikali italipa fidia halali kwa waliochukuliwa mashamba ya nyakirigi katika upanuzi wa kambi ya wakimbizi nyarugusu. Akiwa katika eneo la Nyakitonto, Makamu wa Rais ameagiza askari wa uhifadhi kuacha tabia ya kupiga na kuwanyanyasa raia ikiwemo kuchukua mazao yao pale wanapokutwa na makosa na badala yake wapelekwe katika vyombo vya sheria. Pia amewasihi wananchi wa eneo hilo kufuata sheria na makubaliano yaliyowekwa ikiwemo kutovamia maeneo ya hifadhi. Ametoa rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kurekebisha sheria ndogo ambazo ni kandamizi kwa wananchi ikiwemo kutoza fedha za kadi za kliniki kwa kina mama pamoja na faini kwa wakina mama wanaojifungua watoto nyumbani. Vilevile Makamu wa Rais amewasihi wananchi wa Wilaya ya Kasulu kujitokeza katika kutoa maoni yao katika Dira ya Taifa 2050 ili mawazo yao yaweze kutumika katika kuandaa Taifa la mika 25 ijayo. Halikadhalika amewataka wananchi wa Kigoma kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu kwa amani na utulivu. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi – TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amewataka watumishi wanaotoa huduma za afya katika vituo vya afya na zahanati kuzingatia maadili na miongozo iliyowekwa. Amesema ni marufuku kwa mtumishi wa huduma za afya kumtoza mama mjamzito malipo ya kadi ya kliniki pamoja na faini kwa mama anayejifungua mtoto wake nyumbani bila kudhamiria. Katimba amesema ni wajibu kwa watoa huduma za afya na serikali kwa ujumla kuelimisha wananchi faida na umuhimu wa kujifungua watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya.
532e4ff10b7dc9d85327bd1393dff5abb613a615e47781332d455667659d8917
545
5.702752
24
3,108
1
0
0
0
0.55
79
https://www.vpo.go.tz/news/makamu-wa-rais-aisisitiza-utoaji-wa-elimu-kuepuka-maradhi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesisitiza umuhimu wa wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuwasaidia wananchi kwa kutoa elimu kuepukana na maradhi mbalimbali. Makamu wa Rais ametoa wito huo mara baada ya kutembelea Zahanati ya Kijiji cha Kasumo akiwa wilayani Buhigwe mkoani Kigoma. Amesema maradhi yanayotajwa kuwasumbua wananchi wa Kijiji hicho ikiwemo magonjwa ya mfumo wa hewa pamoja na magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasio salama yanaweza kudhibitiwa kwa kutoa elimu kupitia mikutano mbalimbali ya Kijiji. Amewahimiza wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuwatembelea wanakijiji katika maeneo yao na kuwaelimisha namna ya kuwalinda watoto dhidi ya michezo katika maji machafu pamoja na unywaji maji yasiochemshwa. Amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuweka utaratibu wa kuchemsha maji kabla ya kunywa na kuondokana na imani waliyonayo kwamba maji ya kuchemsha sio matamu. Makamu wa Rais amewapongeza wanakijiji hao kwa kwa kujitoa katika kukamilisha zahanati hiyo ambayo imekua msaada kwa wananchi wa Kijiji hicho na vijiji Jirani. Amewasihi wananchi wa Kijiji hicho kuendelea kujitolea na kushirikiana katika shughuli za maendeleo ili kuboresha Maisha yao kwa vizazi vya sasa na baadae. Aidha ametoa wito kwa wanakijiji hao kuanzisha nguvu mpya ya ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika zahanati hiyo. Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amekagua shuguli za maendeleo katika Wilaya ya Buhigwe ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari Kahimba pamoja na ujenzi wa barabara kiwango cha lami ya Muyama – Kasumo – Kabanga. Amewataka wakandarasi kuhakikisha wanaongeza kasi katika ujenzi wa barabara hiyo wakati huu wa kiangazi ili ikamilike kwa wakati na kufungua shughuli za kiuchumi na kijamii katika Wilaya hiyo na maeneo Jirani. Makamu wa Rais amesema serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itakamilisha miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Kigoma ili kuvutia zaidi uwekezaji na kurahisisha shughuli za ufanyaji biashara.
65a73f94926fc4ffefe5328d1759caed8a9e24754669aa43f8a9ef64e9b409ce
307
5.570033
14
1,710
1
0
0
0
0.65
49
https://www.vpo.go.tz/news/makamu-wa-rais-ataka-ulinzi-maeneo-ujenzi-wa-miradi-kuepusha-migogoro-ya-ardhi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kulinda maeneo yaliyotengwa kwaajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuepusha kuvamiwa na hivyo kuepelekea migogoro baadae. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akikagua eneo la ujenzi wa Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi na Ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili (MUHAS) Kanda ya Magharibi yaliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati akiwa ziarani mkoani Kigoma. Amesema Miradi hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya mkoa wa Kigoma na kanda nzima ya magharibi kwa ujumla hivyo yanapaswa kutengenezewa mpaka wa barabara ili kuepusha uvamizi. Makamu wa Rais ameagiza Wakala ya Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha inaanza ujenzi wa barabara kuelekea katika eneo hilo la mradi ili kurahisisha upelekaji wa vifaa vya ujenzi wakati wa utekelezaji wa mradi. Aidha ametoa wito wa kuzingatia ratiba katika kuanza kutekelezwa kwa miradi hiyo ambayo imetengewa shilingi bilioni 4 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 katika kuanza ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD. Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa kuongeza hekari 50 zinazohitajika kama nyongeza katika mradi huo. Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amekagua kupokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege Kigoma unaoendelea kutekelezwa mkoani humo. Akizungumza na wananchi wanaofanya kazi katika mradi huo, Makamu wa Rais amesema serikali itahakikisha miradi hiyo inawanufaisha wananchi na kuwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na uaminifu kwa manufaa ya mkoa na Taifa kwa ujumla. Kazi ya ukarabati na upanuzi wa Uwanja huo inahusisha Ujenzi wa Jengo la Abiria, maegesho yan ndege, njia za kurukia ndege, mnara wa kuongoza ndege, taa za kuongoza ndege pamoja na barabara za kuingia na kutoka katika uwanja huo. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Desemba 2025.
8b4afbabb798555976f67203a8549c909ac0456f2fcab4677f5badfbc5f5bd5c
291
5.42268
12
1,578
1
0
0
0
1.37
41
https://www.vpo.go.tz/news/dkt-mpango-upatikanaji-wa-vitambulisho-vya-taifa-utakuwa-wa-uhakika
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema tayari maelekezo yametolewa kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha inaharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa ili kuondoa adha wanayopitia wananchi wa Kigoma na maeneo mbalimbali nchini. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa eneo la Mnanila akiwa ziarani mkoani Kigoma. Amesema kukosekana kwa vitambulisho hivyo kunawanyima fursa mbalimbali wananchi hao ikiwemo kukosa ajira katika miradi inayotekelezwa mkoani humo. Makamu wa Rais ameusisitiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kushughulikia changamoto ya kukataliwa kupata ajira za kawaida katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa sababu ya ukosefu wa vitambulisho vya Taifa. Amesema suala hilo linapaswa kushughulikiwa kwa wananchi kupata ajira hizo kwa kutumia vitambulisho mbadala kama vile leseni na vitambulisho vya kupigia kura. Ameongeza kwamba wananchi wataweza kulinda vema miradi hiyo kama watashiriki katika ujenzi wake. Amewahakikisha wananchi wa eneo hilo kwamba serikali italipa fidia kwa madai halali ya wote waliochukuliwa maeneo yao kwaajili ya ujenzi wa forodha. Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amezungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi kilichopo Wilaya ya Kigoma ambapo amewasihi kulinda na kutunza amani iliyopo nchini. Amewasihi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha wanachagua viongozi bora watakaowatumikia vema. Pia amewahimiza kufanya kazi kwa bidii pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira. Vilevile Makamu wa Rais amezungumza na wananchi wa Wilaya ya Buhigwe ambapo amewahakikishia kwamba Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya mkoa wa Kigoma ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kiuchumi kirahisi ikiwemo biashara. Amesema adha iliyowakabili wananchi kwa muda mrefu ya ukosefu wa miundombinu bora inakaribia kumalizwa kabisa na serikali ya Awamu ya Sita. Aidha amewaeleza wananchi hao dhamira ya serikali katika kuufungua mkoa wa Kigoma kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya kupooza umeme Nguruka pamoja na Kidahwe ambavyo vitawezesha mkoa wote wa Kigoma kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa. Makamu wa Rais amesema serikali inaendelea kutekeleza kikamilifu miradi ya ujenzi wa barabara kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine ya Tanzania ambapo kwa upande wa barabara ya Tabora – Kigoma ni kilometa 51.1 pekee zimesalia kukamilika na zinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi 2024. Pia amesema kwa upande wa barabara ya Kagera – Kigoma ni kilometa 16 pekee zimesalia kuunganisha mikoa hiyo. Halikadhalika Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa uwanja wa ndege wa kisasa unaojengwa mkoani Kigoma kutafungua fursa ya utalii na biashara mkoani humo. Pia amesema Mkoa huo unatarajiwa kuondokana na changamoto ya kufuata huduma za afya katika maeneo mengine ya nchi kwa kuwa serikali inatarajia kujenga Hospitali ya Kanda ya Magharibi katika eneo la Ujiji mkoani humo. Makamu wa Rais ameongeza kwamba Mkoa wa Kigoma unatarajia uwepo wa Chuo Kikuu cha masuala ya afya kutokana na mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili (MUHAS) katika eneo la Ujiji mkoani humo. Makamu wa Rais amewahimiza wananchi wa Buhigwe kuzingatia katika kuhakikisha watoto wanapata elimu kwa kuwa serikali imerahisisha suala hilo kwa kutoa elimu bila ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita. Pia amewasihi kuwafuatilia watoto mashuleni wanayojifunza ili kukabiliana na wimbi la elimu isiyofaa kwa maadili ya kitanzania. Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amewaahidi wananchi wa Kigoma kuwakabidhi barabara ya Kasulu – Buhigwe hadi Manyovu (KM 68.25) na barabara ya Kasulu Kibondo (KM 16) ifikapo mwezi Machi 2025 ili kurahisisha shughuli za kibiashara na uwekezaji mkoa wa Kigoma.
7235ddf6bb0f3077a74197de1fbd5ee9b74f6ee0108d66a79fb0bf3cc1554fdb
563
5.740675
23
3,232
1
0
0
0
1.6
73
https://www.vpo.go.tz/news/serikali-yaiomba-unep-kuiunga-mkono-tanzania-katika-nishati-safi-ya-kupikia
Serikali ya Tanzania imeliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuendelea kuungana na Tanzania kwenye Agenda ya Nishati Safi ya Kupikia ambayo itasaidia kukabiliana na uharibifu wa mazingira. Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amesema hayo wakati ashiriki Mkutano wa 11 wa Wawakilishi wa Kudumu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) unaofanyika Julai 08 hadi 12, 2024 jijini Nairobi, Kenya. Amesema agenda hiyo ni muhimu kuungwa mkono kwani ina manufaa makubwa kwa utunzaji wa mazingira kwani itachagiza kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo huchangia ukatajai wa miti. Pamoja na hayo pia, Mndeme ametoa wito kwa shirika hilo kuunga mkono katika Biashara ya Kaboni na Uchumi wa Buluu, masuala ambayo yanaleta tija katika kuinua pato la wananchi na taifa kwa ujumla. Akizungumzia mkutano huo, alisema Tanzania kama nchi mwanachama itapata fursa ya kuelewa shughuli za UNEP kwa mwaka uliopita na kueleza vipaumbele vya nchi ili viweze kujumuishwa kwenye mipango ya UNEP kwa mwaka mwingine wa utekelezaji wa mpango – (2024 – 2025). Halikadhalika, Bi. Mndeme ametoa shukrani kwa UNEP kuendelea kuisaidia Tanzania hususan kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai na uchafuzi wa mazingira. Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Berdard Kibesse ameishukuru UNEP kwa jitihada za kupambana na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Hivyo, Balozi Mhe. Dkt. Kibesse aliahidi Tanzania kuendelea kuwa wa mstari wa mbele katika kupambana na uharifu wa mazingira unaoikabili dunia na kuleta athari kubwa. Aidha, mkutano huo unafanyika kwa lengo la kupitia programu za UNEP kwa kipindi cha mwaka 2022- 2023 na kupitia mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2023 – 2024. Pia, katika mkutano huo wajumbe wanapitia utekezaji wa kazi za shirika hilo hususan kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai na uchafuzi wa mazingira pamoja na kufanya maandalizi ya mikutano ijayo ya Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA - 7).
d85265ce9621dcd2f01b103b37675af0730d2e9188a065a554f9f64bc2a5cc37
317
5.400631
16
1,712
1
0
0
0
4.73
39
https://www.vpo.go.tz/news/sima-serikali-inaandaa-mkakati-kulinda-uchimbaji-endelevu
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema Serikali inaandaa mkakati wa muda mrefu unaotokana na mapendekeo ya Kamati Maalum ya wadau iliyoundwa na Ofisi hiyo kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuwa na uchimbaji endelevu wa mchanga na usiokiuka Sheria za nchi. Aliongeza kuwa zitafanyika tafiti na kuendeleza teknolojia za ujenzi zinazoweza kutumia mchanga kidogo na kuelimisha wananchi kuhusu athari za uchimbaji holela wa mchanga na kuzuia uchimbaji holela. Aidha, Sima alisema kuwa mamlaka mbalimbali zikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mamlaka za Mabonde na Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Madini Mkoa wa Dar es Salaam, zimekuwa zikifanya ukaguzi wa mara kwa mara na hatua stahiki kwa mujibu wa sheria huchukuliwa, “Kuhusu uchafuzi wa mazingira uliokithiri, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 Kifungu 139(1) imetoa mamlaka kwa Serikali za Mitaa kuzuia au kupunguza taka ngumu, taka vimiminika, gesi taka na taka zenye madhara. Serikali itaendelea kuelimisha wananchi na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisisitiza Sima.
bfdb827eaf725e86b7ca2221b346753f625882d043e3c3889d0d8da91b4e4235
178
5.544944
5
987
1
0
0
0
1.12
23
https://www.vpo.go.tz/news/ofisi-ya-makamu-wa-rais-yatoa-mafunzo-ya-kurejeleza-gesi
Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali. Tafiti zimethibitisha kuwa kumong’onyoka kwa tabaka la ozoni kumetokana na kurundikana angani kwa kemikali/gesi zinazotumika kwenye mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupoozea joto. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Faraja Ngerageza jijini Dar es Salaama wakati akifungua warsha ya mafunzo ya kurejeleza gesi zilizotumika na madhara yatokanayo na matumizi ya gesi feki iliyotolewa kwa Wakufunzi wa Chuo cha VETA. Alisema kuwa Serikali imeaandaa Programu mbali mbali kwa ajili ya utekelezaji wa Itifaki ya Montreal. Mkakati wa kitaifa chini ya mipango ya nchi ni pamoja na kuimarisha uwezo wa Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa Itifaki ya Montreal, kukusanya takwimu za uingizaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka la ozone. Pia uhamasishaji juu ya umuhimu wa kulinda tabaka la ozoni, kujenga uelewa kwa Wakufunzi juu ya urejelezaji wa gesi iliyokwisha tumika katika mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupozea joto, Kuhamasisha matumizi ya kemikali rafiki kwa tabaka la ozoni na Kuweka utaratibu wa udhibiti wa uingizaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni. Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kuandaa warsha za mafuzo ya aina hiyo kwa Wakufunzi wa vyuo vya VETA Nchini wanaohusika na masuala ya mafriji, viyoyozi na mitambo ya kupoozea joto. Washiriki wa warsha hiyo wametoka katika vyuo vya VETA vifuatavyo Dar es Salaam, Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Pwani na Kigoma.
a29dd6840667557a9f73b70c4785d849f3a8d50079c84c4cf1045f4a3bff2a38
255
5.521569
8
1,408
1
0
0
0
0
40
https://www.vpo.go.tz/news/makamu-wa-rais-amuahidi-balozi-wa-sweeden-tanzania-kuimarisha-uhusiano
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Sweeden katika Sekta ya Elimu, Uwekezaji wa Biashara, Utalii na Mazingira. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Januari 17,2020 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg. Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano kati ya Nchi mbili hizi katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Uwekezaji wa kibiashara na Mazingira wakati Tanzania ikiwa mbioni kuelekea katika Uchumi wa Viwanda. Nae Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg amemuahidi Makamu wa Rais kwamba Nchi yake itashirikiana Bega kwa Bega na Tanzania katika kuhakikisha kuwa Nchi mbili hizi zinafikia Malengo.
6e4f75b9edca5e84282caaeb6042d1a2ce7a414dc9bbd5311a435431c4e081c2
135
5.814815
8
785
1
0
0
0
0.74
20
https://www.vpo.go.tz/news/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa-mawaziri-wa-mazingira-maliasili-na-utalii-wa-sadc
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, amesema kuwa, mkutano huo utajadili mwenendo wa hali ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya utalii na misitu katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Aidha amesema kuwa, mkutano huo utajadili utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira na kupitia mikakati na miongozo juu ya masuala hayo katika kutekeleza majukumu ya kila nchi ndani ya jumuiya hiyo ya SADC. Wakati huo huo, Tanzania imekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Mashauriano ya Kisheria la Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organization (AALCO) 58th Annual Session). Mkutano huo umefunguliwa na mikutano ya Wataalamu wa Sekta ya Wanyamapori na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii ulioanza leo Oktoba 21 hadi 24, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Mapema mwezi Agosti mwaka huu, nchi ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendelea ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais John Pombe Magufuli alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la uenyekiti wa jumuiya hiyo.
df3fa293a0ac06564c574cd88b22eb59a30fa0ca370be93cffabe8ef5d5787dc
230
5.269565
7
1,212
1
0
0
0
1.3
19
https://www.vpo.go.tz/news/samia-azma-ya-kuifanya-dodoma-ya-kijani-iko-pale-pale
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema azma ya kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani iko pale pale. Hayo yamesemwa leo mara baada ya kutembelea shamba la miti lililopo katika eneo la Mzakwe katika Kambi ya Jeshi la Makutupora Jijini Dodoma, ikiwa ni ufuatiliaji wa Kampeni aliyozindua mwaka 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora, Wakala wa Misitu Tanzania na Watendaji wa Ofisi yake kwa kuhakikisha miti iliyopandwa mwezi Desemba 2017 inastawi. “Vitabu vya dini vinasema Moja kati ya sadaka endelevu ni kupanda miti, miti hii imekuwa na kustawi kwasababu ya jitihada zenu za kuimwagilia na kuitunza, msikate tamaa, endeleeni na kazi hii njema ambayo matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa mifumo ya hali ya hewa ambayo huimarisha shughuli za kilimo na maendeleo ya viwanda.” Alisisitiza Makamu wa Rais Nae Mkuu wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kuwa miti 2300 ilipandwa tarehe 21/12/2017 na kati ya hiyo miti 2076 imekuwa na kustawi ikiwa ni sawa na asilimia 90.3 ya miti yote iliyopandwa. “Katika miti iliyooteshwa awali baadhi haikuota, hivyo tumefanya jitihada za kuirudishia, tumepanda takriban miti 300 ya ziada” alisema Luteni Kanali Mbanga. Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha tafiti zinakamilika mapema kutoka katika sampuli ya udongo iliyochukuliwa ili kubaini aina ya miti inayostawi katika eneo hilo na Jiji la Dodoma kwa Ujumla. Kampeni ya Kukijanisha Dodoma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 21/12/2017 katika eneo la Mzakwe Jijini Dodoma ambapo miti 2300 ilipandwa siku hiyo.
17f975a4ff869244ee22516c6c8f88a8bb9dbd9d30db8c3eb6f9262f4faa09e0
274
5.354015
8
1,467
1
0
0
0
3.28
34
https://www.vpo.go.tz/news/mhandisi-malongo-mradi-wa-umeme-rufiji-unazingatia-mazingira
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amesema azma ya Serikali ya ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme la Julius Nyerere iko pale pale na ujenzi wake unaendelea kwa kasi huku suala la hifadhi ya mazingira likizingatiwa. Akizungumza na Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nuklia kutoka Ujerumani Mhandisi Malongo amesema Tathmini ya Athari kwa Mazingira imefanyika na kuonyesha kuwa ujenzi huo ni salama kwa mazingira. “Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza mradi huu kwa kutumia fedha zake kutoka vyanzo vya ndani. Mradi huu utachukua eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 1,250 ambalo ni sawa na asilimia tatu (3%) tu ya eneo lote la pori la akiba selous lenye ukubwa wa kilomita za mraba 50,000. Malongo alisisitiza. Mhandisi Malongo amesema kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 kifungu cha 81, mradi huu umefanyiwa tathimini ya athari kwa mazingira ili kubaini matokea hasi na chanya na kuweka mipango ya kudhibiti madhara na kuboresha utekelelezaji wake. Amesema kuwa kiwango cha umeme cha megawati 2,100 kitaongezeka kwenye gridi ya Taifa kwa maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na maendeleo ya viwanda na kupunguza uzalishaji wa gesijoto duniani, pamoja na uwepo wa fursa za kilimo cha umwagiliaji na uvuvi ulioboreshwa katika uwanda wa chini kutokana na usimamizi na udhibiti wa mtiririko wa maji. Katika hatua nyingine Mhandisi Malongo amewafafanulia wabunge hao mafanikio yaliyopatikana katika katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini lililoanza kutekelezwa Juni Mosi na kusema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kampeni hiyo imeonyesha mafanikio kwa kiasi kikubwa kwani imepokelewa kwa mtazamo chanya na wanachi ikiwa ni jitihada za kushirikisha taasisi mbalimbali na wadau kwa ujumla. Akiongea kwa niaba ya wenzake kiongozi wa ujumbe huo Mhe. Sylvia Kotting-Uhl ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa mageuzi makubwa yanayofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano na kuahidi ushirikiano na nchi yake katika kujenga uwezo katika nyanja za kusimamia na kudhibiti taka za kielektroniki, Uzalishaji wa Umeme wa jua na kutoa mwaliko kwa ujumbe wa Tanzania kutembelea Ujerumani kujifunza zaidi
e95cb9a1111733b45b132412fdc355132c122e87409e153acf9fc3144922c371
349
5.421203
11
1,892
1
0
0
0
2.01
62
https://www.vpo.go.tz/news/wachimbaji-wadogo-watakiwa-kufuata-taratibu-za-mazingira
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Kata ya Mugusu Mkoani Geita wametakiwa kufuata taratibu za hifadhi ya mazingira ili kunusuru afya zao na kuchukua tahadhari ya kukabiliana na uwezekano wa milipuko ya magonjwa. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kutembelea eneo la Mgusu, kuona uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004. Akiwa katika eneo la Mugusu Naibu Waziri Sima amesema bado kuna tatizo la usafi wa mazingira katika maeneo wanayoyatumia kuchenjua dhahabu kwa kutumia zebaki, na kuna haja wachimbaji hao kukaa na halmashauri ya Geita Vijijini ili kuhakikisha wanakuwa na vyoo bora. Akitoa kauli ya Serikali kuhusu mpango kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika shughuli za uchenjuaji, Sima amewataka wakazi wa Mgusu kuendelea na shughuli za uzalishaji wa dhahabu bila kuathiri sekta ya mazingira kwa kupunguza matumizi ya zebaki inayoharibu mazingira na afya za binadamu. Nimeona namna vijana wanavyojishughulisha kwa ajili ya kujipatia kipato, hili ni jambo jema kwenye Taifa letu, lakini nimetembea hadi chini kwenye ule mto wa Nyamasenge hakuna vyoo, watu wanatumia pori na mto kwa ajili ya haja ndogo na kubwa. Kwa mazingira yetu ni hatari sana, tunaweza kufanya kazi nzuri lakini ugonjwa utasitisha shughuli zetu. Nawasisitiza kuwa Usafi ni jambo la kwanza katika kufanya kazi, huwezi kuwa na nguvu isiyojali usafi, alisema Sima. Awali, Naibu Waziri Sima alitembelea chanzo cha maji cha maji cha Mto Mabubi na kujionea hali mbaya inayotishia kutoweka kwa chanzo hicho kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kandokando ya eneo hilo. Chanzo cha maji cha mto Mabubi, hakitadumu na maji hayatakuwa salama kwa matumizi ya binadamu endapo kitaendelea kuingia kemikali ya zebaki nanyi wachimbaji kujisaidia katika eneo hilo Sima alisisitiza. Diwani wa Kata ya Mgusu Bw. Pastory Ruhusa amesema kuwa ataitisha mkutano wa wananchi mapema iwezekanavyo ili kuweka mikakati ya haraka kutokomeza hali hiyo ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira na kupunguza matumizi ya zebaki.
90955132af97c54eeb168932a8c36bc0f7d4e7293f8be3508bc1637ccf168616
331
5.495468
12
1,819
1
0
0
0
0.3
53
https://www.vpo.go.tz/news/balozi-seif-atembelea-eneo-la-ujenzi-wa-ofisi-za-smz-dodoma
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi ametembelea eneo ambalo zitajengwa Ofisi za Serikali hiyo eneo la Mahoma Makulu Jijini Dodoma. Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Balozi Iddi ambaye aliambatana na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe Balozi Amina Salum Ali, alishukuru Serikali kwa kupewa eneo hilo.* * Aliahidi kuwa SMZ itaaaza ujenzi wa Ofisi zake katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kama watapata fungu ujenzi utaanza mapema iwezekanavyo ili waweze kuhamia katika Makamo Makuu ya Nchi. Katika ziara hiyo ujumbe huo kutoka Zanzibar ulipokelewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi, Samuel Mwashambwa hiyo na viongozi mbalimbali Balozi Seif alipata nafasi ya kutembelea pia eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba ambako zimejengwa Ofisi 25 za Serikali zikiwemo za Wizara mbalimbali na tayari watumishi wake wamehamia. Akizungumza kuhusu eneo hilo Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe alisema eneo hilo lina ekari 30. Alisema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli alipotangaza Serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi Julai 25, 2016 ulianzishwa mchakato wa kuhamisha watumishi.
a4857fcee2b3d3023811633e1a82c0d1168ff923b80463b2b915bb949f605bae
211
5.436019
7
1,147
1
0
0
0
2.37
18
https://www.vpo.go.tz/news/sima-awataka-wauzaji-mifuzo-mbadala-kutowakandamiza-wananchi
**Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Sima amewataka wafanyabiashara wa mifuko mbadala kutotumia fursa hiyo kuwakandamiza wananchi kwa kuiuza kwa bei ya kubwa.** **Mhe. Sima ametoa kauli hiyo leo mjini Singida wakati aliposhiriki operesheni ya kukagua utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki ambalo limenza Juni mosi mwaka huu.** **Katika opresheni hiyo iliyoambatana na ugawaji wa mifuko mbadala iliyotolewa na Kanisa la Full Gospel kwa wananchi mjini hapa alisema ni busara kwa wafanyabiashara hao kuweka bei inayowawezesha wananchi kuweza kuinunua.** **“Ndugu wafanyabiashara tusiwakomoe Watanzania wasije kuona sasa mifuko hii ni ghali na kuona ni bora turudi katika mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku,” alisema.** **Naibu Waziri Sima ambaye alikuwa mgeni rasmi katika operesheni hiyo** **akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alisema** **wataalamu kutoka serikalini watatembelea viwandani kuona kama bei rafiki kwa mwananchi inatumika.** **Aidha aliwataka wananchi hususan vikundi vya wanawake kutumia fursa hiyo kusuka vikapu kwa ajili ya kubebea bidhaa na hivyo kujipatia kipato ambapo alisema kwa kufanya hivyo tutajenga utamaduni kama wa zamani na kuachana na mifuko ya plastiki. Operesheni ya kukagua utekelesaji wa katazo la mifuko ya plastiki linaloratibiwa na Ofisi ya Makamu ilibaini wananchi wengi kupata uelewa wa madhara ya** **mifuko ya plastiki.** **Wananchi mbalimbali wameitikia wito wa kuanza kutumia mifuko mbadala katika masoko na maduka ambapo wamesema wanaipongeza Serikali kwa kuliona hilo na kupiga marufuku mifuko hiyo.** **Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu kuhusu madhara ya mifuko ya plastiki na fursa za uwekezaji wa mifuko mbadala kama ambavyo ilitolewa na wakaguzi kutoka Baraza la Taifa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Pia mkoa huo ulifanya maandamano ya kuunga mkono katazao hilo na kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala ambapo yalihudhuriawa viongozi mbalimbali kutoka mkoa huo.**
f87a7fb8d93f2e18a5afe2742428d3a96aacc58c59f9f637b2077fffc84e8611
290
5.941379
14
1,723
1
0
0
0
0
45
https://www.vpo.go.tz/news/tanzania-kufaidika-na-fedha-za-mabadiliko-ya-tabianchi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman jijini Seoul nchini Korea Kusini. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mbalimbali wamejadiliana kuhusu utayari wa nchi kuwa mwanachama wa GGGI na kushirikiana na taasisi hiyo kuijengea uwezo Tanzania katika kuandaa programu, miradi na mikakati ya kufaidika na fedha na uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (climate financing). Aidha, Waziri Dkt. Jafo ameshiriki Mkutano Mkuu wa 12 na Kikao cha 16 cha Baraza la Nchi Wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Green Global Growth wenye kujadili masuala mbalimbali kuhusu hifadhi ya mazingira. Taasisi hiyo ya kimataifa yenye makao makuu yake katika Jiji la Seoul nchini Korea Kusini, ina takriban wanachama 48 na kati yao sita wanatoka katika Bara la Afrika Afrika. Katika hatua nyingine akiwa katika ziara hiyo ya kikazi, Waziri Mhe. Dkt. Jafo amepata nafasi ya kushiriki katika mkutano na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini. Mjadala katika mkutano huo mada iliyoandaliwa ni fursa zilizopo katika nchi hiyo za mazingira ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo zikiwemo Biashara ya Kaboni (Carbon Credit), Uchumi wa Buluu (Blue Economy) na Udhibiti wa Taka (Waste Management). Waziri Jafo yupo ziarani nchini Korea Kusini kwa ziara ya kikazi ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hayo ni matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akiimarisha diplomasia na mataifa mbalimbali duniani.
b8742676d0f934ac05a9de0f60149e823ba0d1bb41f82c58978a5114401e58b1
270
5.5
16
1,485
1
0
0
0
1.11
37