text
stringlengths
10
3.8k
<s>[INST] Idadi inayoathirika kwenye kundi [/INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika hutofautiana kutegemea eneo, idadi ya kupe, maambukizi ya awali ya bakteria hao na mbinu zinazotumika kuangamiza kupe. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ya wanyama wanaofariki baada ya kuambukizwa iko juu. Idadi ya vifo hufika 80% kwa mifugo (kundi la wanyama) wadhaifu kiafya. </s>
<s>[INST] Sehemu ya chini ya Mashavu/Taya kuvimba [/INST] Kukosa utulivu, kushindwa kusimama imara, ulimi kutoka nje, kuinua miguu sana wakati wa kutembea, kufinyilia kichwa mitini au ukutani, kuzungukazunguka,, kiwewe na hisia kali kupita kiasi hadi anapozirai. </s>
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Wanyama wote walio na damu moto wakiwemo kondoo, mbuzi, punda na ngamia wako katika hatari ya kuambukizwa kichaa cha mbwa. Pia huathiri wanadamu na mbwa. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Maambukizi hutokana na kuumwa na mnyama aliyeathirika, hasa mbwa au wanyamapori wa jamii ya mbwa. Binadamu anaweza kuambukizwa kwa kuumwa au kukwaruzwa na mnyama aliyeathirika kama vile mbwa au kutokana na mate ya mnyama aliye na ugonjwa huu. </s>
<s>[INST] Kutoka mate kwa wingi [/INST] Kushindwa kutoa sauti anapojaribu kuroroma au wakati mwingine kukoroma mfululizo hadi kupooza/kulemaa </s>
<s>[INST] Magonjwa yanayosababisha mimba kutoka [/INST] Magonjwa yanayohusiana na uharibikaji wa mimba k.m. Homa ya Rift Valley na Ugonjwa wa Kutupa Mimba, yanaangaziwa katika sehemu hii. </s>
<s>[INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unapatikana sana katika Kaunti ya Garissa, maeneo ya Pwani, Kati ya Kenya, na kaskazini mwa Bonde la Ufa (Naivasha, Baringo, Uasin Gishu na Trans Nzioa). </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mbu hupata virusi hivi kutoka kwa mnyama mgonjwa wanapomnyonya damu. Kisha virusi hivi hupitishwa kwa mnyama mwingine, asiye na ugonjwa huo wakati anaponyonywa damu na mbu hao. Watu hupata ugonjwa huu kwa kugusa damu na majimaji mengine ya mnyama aliyeathirika wanapomchinja, au wanapomsaidia kuzaa au kugusa vitoto/vijusi na uchafu wa vijusi hivyo. Watu wanaweza pia kuugua kwa kula nyama na viungo vya wanyama wagonjwa ambavyo havijapikwa vizuri, au wakiumwa na mbu. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Kwa wanyama wachanga, ugonjwa huu unaweza kuua kati ya asilimia 10-50 ya wanyama hao. Wanyama waliokomaa wanaweza kuambukizwa lakini ni wachache (karibu 10%) hufa. </s>
<s>[INST] Uzuiaji wa ugonjwa huu kwa binadamu [/INST] Ikiwa kuna mkurupuko, mizoga ya wanyama wafu, uchafu wanaoutoa, na vitoto vilivyokufa tumboni, vinafaa kuzikwa kwa njia salama </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kula nyasi, maji na lishe nyingine iliyochanganyika na vijusi na uchafu mwingine wa ng’ombe aliyeambukizwa. Maambukizi haya pia yanaweza kutokea dume anapomtungisha jike mimba. Utungishaji wa mimba kwa mbinu ya kisayansi inayotumia mbegu za kiume/manii yaliyo na ugonjwa huu pia unaweza kusambaza bakteria wanaosababisha ugonjwa huu. Mchoro 15: Mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa wa kutupa mimba. Vijusi vilivyoharibika na tando za vijusi hivyo kutoka kwa wanyama walioambukizwa husambaza viini vya ugonjwa huo kwenye malisho. Wanyama walio katika hatari ya kuambukizwa/wadhaifu kiafya humeza bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanapokula malishoni na kusababisha maambukizi mapya. </s>
<s>[INST] Kupanuka na kufura kwa korodani (kende) moja au zote (miongoni mwa madume) [/INST] Kukosa kutoka kwa baadhi ya viungo vya kuwalinda watoto wanapokuwa tumboni mwa mama (kwa mfano kondo au mfuko wa mimba) </s>
<s>[INST] Uwezekano wa binadamu kuambukizwa [/INST] Binadamu anaweza kuupata ugonjwa huu kutoka kwa wanyama walioambukizwa kwa kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa na kushika vijusi au viungo vya vijusi viliyoathirika. Ili kuzuia binadamu kuambukizwa, chemsha maziwa, pika nyama vizuri na kuepuka kugusana na viungo/tishu zilizoathirika. Wakati wa kusaidia wanyama kuzaa, unafaa uvae mavazi ya kinga. </s>
<s>[INST] Unyonyaji wa maziwa mengi [/INST] Ndama, vifungua mimba (waliozaliwa na ng’ombe jike aliye mchanga kiumri), wako katika hatari kuu ya kuambukizwa kuliko waliozaliwa na ng’ombe aliyewahi kuzaa hapo awali </s>
<s>[INST] Mifugo hupata minyoo hii kutokana na ulaji wa nyasi zilizo na mayai au mabuu ya minyoo hiyo. [/INST] Mchoro 17: Maambukizi ya minyoo hiyo hutokea ikiwa mifugo/wanyama watakula lishe iliyo na kinyesi kilicho na minyoo au mabuu/viluwiluwi hivyo </s>
<s>[INST] Maradhi ya kuvuja/kutokwa na damu [/INST] Magonjwa yanayosababisha umwagikaji/uvujaji mkubwa wa damu, yakiwemo maambukizi ya damu, kimeta na ugonjwa wa chambavu (donda kubwa kwenye paja hasa la mguu wa nyuma), yanaangaziwa katika sehemu hii. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu huwa kwenye mate yanayotoka mdomoni na puani, na katika kinyesi. Huenea kupitia kwa malisho yaliyoambukizwa na mnyama anayeugua au anayebeba viini hivyo mwilini bila kuonyesha dalili. Kupe na nzi wanaouma/pangevipanga, wameripotiwa kuwa wasambazaji wa bakteria hawa. Mchoro 7.1: Maambukizi ya Damu kutokana na kikohozi, malisho yaliyoambukizwa kwa mate au kinyesi. Wanyama wengi hufa kutokana na ugonjwa huu ikiwa watakosa kutibiwa. </s>
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Mara nyingi huathiri wanyama wachache kwenye kundi, na unapatikana sana katika maeneo yenye mafuriko ya maji. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Asilimia kubwa (hadi 80%) ya wanyama wagonjwa hufa. Vifo hivi vinaweza kutokea ghafla lakini wakati mwingine hutokea siku 2—8 baada ya dalili za mwanzo kuonekana. </s>
<s>[INST] Hali hatari zinazochangia maambukizi [/INST] Ugonjwa huu huzuka katika msimu wa mvua. Hasa kutokana na msongo wa mawazo unaohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa k.m. mvua ya ghafla inayotokea punde baada ya kiangazi. </s>
<s>[INST] Dalili za ugonjwa huu kwa wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Viungo vya ndani kufura na kugeuka vyekundu, majimaji kwenye mapafu, majimaji yasiyo na rangi kupatikana ndani ya ngozi na mapafu yaliyoathirika. </s>
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoambukizwa [/INST] Kimeta ni ugonjwa wa wanyama wenye damu moto (kama vile mamalia) wakiwemo ngamia, kondoo, mbuzi na swara n.k. Wanadamu wanaweza pia kupata ugonjwa huu kwa kugusana na damu, viungo vya ndani, na vitu kutoka kwa wanyama walioambukizwa, kuvuta hewa yenye seli za bakteria,kushika au kugusa bidhaa za wanyama hao na ulaji wa nyama iliyoathirika. Kwa hivyo, unahimizwa kuwa mwangalifu sana unapowahudumia wanyama wagonjwa na mizoga ya wanyama. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kimeta husababishwa na bakteria/kiini kinachoweza kuishi udongoni kwa muda mrefu (hadi miaka 60) na sugu/ konachostahimili joto, ukame, baridi kali na kemikali za kuua viini. Ugonjwa huu unaweza kuzuka katika maeneo ambayo wanyama hukusanyika, kwa mfano, mahali pa kunywa na pa kuramba magadi ya udongoni. Huambukizwa kupitia kwa malisho na vyakula vilivyoambukizwa viini hivyo. Nzi na wadudu wengine wanaweza kusambaza ugonjwa huu kutoka kwa mnyama mmoja hadi mwingine. Mchoro 18: Uambukizaji wa kimeta hutokea wanyama wanapomeza viini vya kimeta vinavyoishi udongoni wakati wanapokuwa malishoni. Ugonjwa huu husababisha kifo cha ghafla; Damu nyeusi hutoka kwa wingi hasa mdomoni na kitakoni mwa wanyama waliokufa. Mizoga hiyo isipozikwa na kufukiwa vizuri, bakteria walio katika viungo vya mizoga hiyo huingia kwenye malisho na udongoni. Hiki huwa chanzo cha maambukizi kwa wanyama wanaolishwa kwenye malisho hayo. </s>
<s>[INST] Utupaji/uzoaji mbovu wa mizoga [/INST] Wanyama wanaweza kupata kimeta kwa kugusana moja kwa moja au vinginevyo na wanyama walioathirika au bidhaa zao. </s>
<s>[INST] Mara nyingi, wanyama wanaoonekana kuwa wenye afya katika kundi huambukizwa [/INST] Mara moja moja, mnyama mgonjwa huonyesha dalili za ugonjwa huo kwa mara ya kwanza licha ya kuwahi kuugua maradhi haya bila kuonyesha dalili hapo awali: kupepesuka, kupumua kwa shida, kutetemeka, kuanguka, kuzirai na kupigapiga miguu (degdege kama mtu wa kifafa), damu kutoka kwenye sehemu za mwili zilizo na uwazi, na kifo. </s>
<s>[INST] Dalili za ugonjwa huu kwa wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Damu nyeusi, isiyoganda na kutoka kwa wingi katika viungo vyote vya mwili vilivyo na uwazi (mdomoni, puani na kitakoni) bila kukoma Mzoga haukakamai yaani haujikazi na kuwa mgumu (yaani rigor mortis) kama inavyotarajiwa kwa mnyama aliyekufa. </s>
<s>[INST] Kinga [/INST] Wafahamishe maafisa wa tiba/afya ya mifugo kuhusu visa vyovyote vinavyoshukiwa kuwa kimeta na vifo vyovyote vya ghafla Wanyama wanaoshukiwa kufa kutokana na kimeta hawafai kuchunwa ngozi au viungo vyake kufunguliwa wazi, kwani hewa huwasaidia bakteria kuunda utando au ukingo unaowalinda Maboma ya wanyama hayafai kutumiwa hadi wanyama wote walio kwenye hatari wachanjwe, na mizoga yote kuzikwa na kufukiwa kwenye shimo refu au kuchomwa Hakikisha kwamba mizoga yoyote ya wanyama waliokufa kwa kimeta na vitu vilivyoambukizwa vinazikwa (vinafukiwa) kwenye shimo refu la angalau futi 6. </s>
<s>[INST] Kukabiliana na kimeta miongoni mwa wanadamu [/INST] Kuna aina tatu kuu za kimeta zinazoambukiza wanadamu kulingana na njia ya kuingia kwa bakteria wake mwilini. Kwa kawaida, kimeta huingia mwilini kupitia kwa ngozi (kimeta ya ngozi), ya mapafu (kimeta ya kupumua), au mfumo wa utumbo (kimeta ya utumbo). Aina hizi zote za kimeta hatimaye zinaweza kusambaa katika mwili wote na kusababisha kifo ikiwa hazitatibiwa kwa dawa za kuua vijasumu (antibiotics). </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Uambukizaji hutokea pale mnyama anapomeza nyasi zilizo na bakteria wanaosababisha ugonjwa huu; viini hivi huishi kwenye udongo na njia ya chakula ya mnyama. Miongoni mwa kondoo, ugonjwa huu hasa hutokea baada ya mnyama huyo kupata jeraha. Mchoro 19: Chambavu hutokea pale mnyama anapomeza bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanaoishi kwenye udongo. </s>
<s>[INST] Kulemaa kwa miguu/kushindwa kutembea [/INST] Uvimbe mwekundu na mchungu katika nyama ya sehemu iliyoathirika, kisha baadaye kupoa na uchungu kuondoka </s>
<s>[INST] Damu kuganda haraka [/INST] Sehemu iliyovimba hugeuka kuwa nyeusi, viungo vya ndani hubadilika rangi na kutoa harufu mbaya na viputo vya hewa (air bubbles). </s>
<s>[INST] Magonjwa yanayotambulika kwa mkojo mwekundu [/INST] Sehemu hii inaangazia dalili za ugonjwa wa Mkojo Mwekundu (Babesia, yaani homa ya kupe), ugonjwa unaotambuliwa kwa mnyama kukojoa mkojo mwekundu. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kupe wa bluu/samawati wa kike waliokomaa (wanaojulikana kisayansi kama Rhepicephalus Boophilus) hupata viini kutoka kwa mnyama aliyeathirika. Kisha huvisambaza kwa vizazi vyao kupitia kwa mayai. Kisha mabuu (au kupe wachanga) huvisambaza wanapowafyonza/wanapowanyonya wanyama wengine damu. </s>
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Utokeaji wa ugonjwa huu kwenye kundi hutofautiana, kulingana na sababu kadhaa. Katika maeneo ambayo ugonjwa huu hutokea kwa kawaida, dalili chache sana za ugonjwa huu huonekana. Mikurupuko ya ugonjwa huu inaweza kutokea ikiwa ndama ambao hawajawahi kuathiriwa na kupe wakiwa wachanga zaidi, watapelekwa kwenye eneo lililoathiriwa na/au ikiwa kupe walioambukizwa watavileta viini hivyo katika eneo lisilo na kupe. </s>
<s>[INST] Magonjwa mengine ya kieneo [/INST] Magonjwa ya kieneo hupatikana sana katika maeneo ya ufugaji wa ng'ombe kwa wingi. Sehemu hii itaangazia ugonjwa wa malale (Nagana), ndigana baridi na kititi/ugonjwa wa kiwele </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ng’ombe wanaweza kuupata ugonjwa huu kwa kuumwa na mbung'o au wadudu wengine wanaouma kama vile nzi wa kumma yaani pange kipanga (kisayansi wanaitwa Tabanids na Stomoxys mtawalia). Mchoro 23: Uambukizaji wa malale kupitia kwa mbung'o waliomuuma mnyama aliyeambukizwa hadi kwa yule aliye katika hatari ya kuambukizwa. </s>
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika [/INST] Tafiti zinaonyesha kwamba hadi thuluthi moja (1/3) ya wanyama kwenye kundi hupata ugonjwa huu, lakini hili hutofautiana kulingana na idadi ya mbung'o na nzi hao wengine wa kuuma. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Karibu wanyama wote walio na ugonjwa huu hufa ikiwa hawatatibiwa. Maradhi haya hukaa sana kabla ya kusababisha kifo. Katika hali za kawaida, hadi 3% hufa kutokana na ugonjwa huu. </s>
<s>[INST] Hupatikana sana katika maeneo ya wanyama wengi wa porini. [/INST] Wanyama wengi huugua punde msimu wa mvua unapoisha kutokana na kuongezeka kwa mbung'o na nzi wa kuuma. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kupe husambaza viini/vimelea hivyo kutoka kwa wanyama walio na ugonjwa huo mwilini hadi kwa wanyama wazima wanapowafyonza damu. Ugonjwa huu unaweza pia kusambazwa kupitia kwa nzi wanaouma. </s>
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Kulingana na idadi ya kupe walioathirika katika eneo, na aina ya ng’ombe walioathirika. Ng’ombe wa aina za kiasili kama vile Zebu na Boran hawaathiriwi sana kwa sababu ya ustahimilivu wao wa maambukizi ya kupe. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Ng'ombe wa umri wa kati ya mwaka mmoja na miwili huonyesha ghafla dalili za ugonjwa huu, ambazo hujitokeza kama homa/joto mwilini, kukataa chakula, kupumua kwa juujuu na kwa haraka, kusita kutembea na tando za kamasi kubadilika rangi, lakini kifo si rahisi. Ng'ombe wa maziwa walioathirika pia hupunguza kiwango chao cha maziwa. Ng'ombe wanaozidi miaka miwili huonyesha dalili za ugonjwa huu ghafla kisha kufa kwa ghafla. Mara nyingi wanyama hawa hupatikana wamekufa. Idadi ya vifo inaweza kuanzia asilimia 30 — 50 kwa wanyama wanaozidi miaka miwili ambao wameonyesha dalili za ugonjwa huu. Wanyama walioambukizwa huendelea kuwa na ugonjwa huu mwilini maishani mwao na ndio huambukiza wengine kwenye kundi. </s>
<s>[INST] Hali hatari zinazochangia maambukizi [/INST] Kuleta ng’ombe mgeni aliyeathirika kwenye kundi na uwepo wa wadudu wanaoambukiza (kupe na nzi wa kuuma) </s>
<s>[INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Mara nyingi wanyama huwa hawaonyeshi dalili yoyote ya ugonjwa huu. Hata hivyo, kwa nadra dalili huwa: </s>
<s>[INST] Dhibiti kupe [/INST] Tafuta usaidizi wa Afisa wa Afya ya Mifugo na kutibu ugonjwa huo haraka iwezekanavyo punde dalili zinavyojitokeza </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu husambazwa kutoka kwa mnyama mmoja hadi mwingine kupitia kwa mikono iliyoambukizwa na kutodumisha usafi kwenye maboma ya mifugo. Mchoro 25: Maambukizi ya bakteria wanaosababisha kititi. Hii hutokea mtu asipozingatia usafi wakati wa kukama.Husambaa hasa unapomkama ng’ombe aliyeambukizwa, kabla ya kuwakama wanyama ambao hawajaambukizwa. Bakteria wanaosababisha kititi huhamishwa kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa hadi kwa yule aliye hatarini kwa kutozingatia usafi. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Kifo kinaweza kusababishwa na kititi kipevu (hatari) kinachotokana na bakteria wenye sumu ndani ya damu </s>
<s>[INST] Ng’ombe wanaotoa maziwa mengi wako kwenye hatari zaidi [/INST] Matumizi ya mbinu zisizo za kawaida za kukama kama vile kutumia mkojo na mate kulainisha matiti unapokama. </s>
<s>[INST] Kiwele (robo moja au zaidi) kufura, kuwa kigumu, na moto, kikishikwa kinaweza kugeuka chekundu [/INST] Rangi yake kubadilika, kiwango cha maziwa kupungua na maziwa yasiyokuwa ya kawaida (kuwa na damu au kugeuka rangi ya manjano) </s>
<s>[INST] Mradi wa Kuzidisha Ubora wa Chakula cha Siku zijazo (AVCD) nchini Kenya - Kitengo cha Mifugo [/INST] Mwongozo wa nyanjani wa magonjwa ya mifugo kwa kutegemea dalili zao katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya </s>
<s>[INST] Awamu ya 2: Magonjwa ya wanyama wadogo wa kucheua [/INST] Dibaji
Magonjwa ya mifugo hupunguza kiwango cha ufugaji na biashara za mifugo, hasa katika maeneo ya ufugaji ambako huduma za tiba ya mifugo ni adimu. Mifumo mipana ya ufugaji inayotumiwa maeneo haya- kama vile ufugaji wa kuhamahama, uhamaji wa kila msimu na mifumo-mseto ya ufugaji na ukuzaji wa mazao kwa pamoja- inazua changamoto zaidi kutokana na ulishaji wa pamoja wa mifugo, uhamaji wa kila mara na mwingiliano kati ya mifugo na wanyamapori. Tafiti za hivi majuzi katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya (miongoni mwa jamii za Waborana, Warendille, Waturkana, Wasomali na nyingine za wafugaji) zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuambukiza kama vile Homa ya Mapafu inayosambaa haraka, ugonjwa wa mapafu ya mifugo, Sotoka ya Wanyama wa Kucheua (PPR), kimeta, ugonjwa wa vinundu vya ngozi na ugonjwa wa miguu na midomo hutokea kila mara. Tafiti hizo, kadhalika, zinaonyesha kuwa jamii hizi hutumia kiwango kikubwa cha dawa za tiba ya mifugo kudhibiti magonjwa haya lakini tiba nyingi hutumika bila ushauri wa kitaalamu. Kwa hivyo, kuna uwezekano kwamba nyingi ya tiba hizi hazifai. Hata muhimu zaidi ni kuwa, kipindi cha baada ya matumizi ya dawa hizo ni kifupi kuliko inavyotakiwa, hali inayozua hofu kuwa bidhaa za mifugo kama hao zina kiwango kikubwa cha mabaki ya dawa. Idara ya Huduma za Afya ya Mifugo (DVS), kwa ushirikiano na mashirika ya kimaendeleo ya humu nchini na kimataifa, imetekeleza mikakati mseto ya kuhamasisha na kuzuia magonjwa katika eneo la kaskazini mwa Kenya. Hata hivyo, hatua hizi zinapaswa kutekelezwa na wadau wote katika sekta hiyo ili zifanikiwe. Wamiliki wa mifugo, kwa mfano, wanao mchango mkubwa katika ufuatiliaji wa matukio ya magonjwa kwa kutoa ripoti kuhusu mikurupuko ya magonjwa hayo. Usahihi wa taarifa zinazotolewa unaweza kuimarishwa kupitia ufundishaji wa wafugaji kuhusu dalili na ishara za magonjwa wanayokumbana nayo mara kwa mara. Mwongozo huu utatumiwa kuwapa mafunzo wafugaji wa kieneo, watoaji wa taarifa za magonjwa katika kiwango cha kijamii, matabibu/wahudumu wa kibinafsi wa afya ya wanyama, wauzaji wa dawa, wafanyabiashara na wadau wengine wahusika kuhusu magonjwa na mbinu za kuyadhibiti magonjwa ya kieneo ili kuimarisha uwezo wao wa kusaidia kufaulisha juhudi za utekelezaji wa mikakati ya ufuatiliaji na ukabilianaji na magonjwa hayo. Muundo wa Mwongozo huu umechochewa na Mwongozo wa Nyanjani wa Magonjwa ya Wanyama unaotegemea Dalili (yaani A Field Manual of Animal Diseases by Syndromes) - uliochapishwa mwaka wa 2013 na Mradi wa Viwango, Mbinu na Taratibu za Afya ya Wanyama (yaani Standards Methods and Procedures in Animal Health -SMP-AH) kama sehemu ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, Ukanda wa Afrika Mashariki; Ofisi ya Umoja wa Afrika ya Inter-African kuhusu Rasilimali za Wanyama; Idara ya Marekani ya Kilimo - Kitengo cha Kilimo cha Kigeni; na Chuo Kikuu cha Georgia, Athens nchini Georgia. Hata hivyo, mwongozo huu ni sehemu ya jozi/awamu tatu za miongozo inayoangazia magonjwa ya kieneo ambayo huathiri hasa ng’ombe, kondoo, mbuzi na ngamia katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya. Hii ni tofauti na mwongozo wa SMP-AH uliokarabatiwa mahsusi kwa ajili ya magonjwa yanayoathiri biashara za mifugo. </s>
<s>[INST] Utaratibu wa mwongozo huu [/INST] Mwongozo huu umewasilishwa katika awamu tatu; Awamu hii ya 2 inaangazia magonjwa ya wanyama wadogo wa kucheua. Magonjwa hayo yameanishwa katika makundi tisa kulingana na dalili zayo kuu; yaani, kuathiriwa kwa mfumo wa kupumua, maambukizi/uvamizi wa ngozi, madonda ya miguu na midomo, ukosefu wa utulivu, kuharibika kwa mimba/ujauzito, kuhara/mharo, magonjwa ya kutokwa na damu ghafla, mkojo mwekundu na magonjwa mengine ya kieneo. Mada zilizoangaziwa chini ya kila ugonjwa huo ni; majina ya wenyeji, wanyama wanaoathiriwa, uambukizaji, idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi, idadi ya vifo, usambaaji/msambao, hali hatari zinazochangia maambukizi, dalili za ugonjwa, wanyama waliokufa/mizoga, na kinga. Mwongozo huu ni nakala inayoweza kuimarishwa baada ya muda kwa kutegemea michango kutoka kwa wadau mbalimbali watakaohusishwa. </s>
<s>[INST] Shukrani [/INST] Watu wengi walichangia katika utayarishaji wa mwongozo huu. Wanajumuisha maafisa wa afya ya wanyama kutoka kaunti za Turkana, Marsabit, Isiolo, Garissa na Wajir walioshiriki katika warsha za mafunzo; Michael Baariu, Dabasso Barako, Changayo Orkhobeshe, Ehele Haile, Stephen Mutahi, Boku Bodha, Adano Umuro, Dennis Mwongela, Joseph Muriira, John Koskei, Siyat Onle Takal, Abubakar Siraj, Job Ronoh, Jane Akale, Daud Abukar na Anthony Ngugi. Joseph Mathooko kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo pia alishiriki. Pia tunatambua michango ya Waratibu wa Nyanjani wa AVCD (Adan A. Kutu (Isiolo), Abdisemed Osman (Wajiri), Simon Chuchu (Marsabit) na Viola Chemis (Turkana) katika kaunti lengwa walioboresha mwongozo huu kwa kutegemea maoni yaliyotolewa na maafisa wa nyanjani katika kaunti, Watoaji Taarifa kuhusu Magonjwa katika Jamii (CDRs) na wafugaji katika ngazi ya kijiji. </s>
<s>[INST] Marejeleo yaliyopendekezwa: [/INST] Bett, B., Kihu, S., Wamwere-Njoroge, G. Hambe H. and Kiara, H. 2019. Field manual for livestock diseases based on syndromes in pastoral areas in northern Kenya. Small ruminant diseases (Volume 2). Accelerated Value Chain Development (AVCD) Livestock Component. Nairobi, Kenya: ILRI. </s>
<s>[INST]
Magonjwa yanayoathiri Mfumo wa kupumua [/INST] Magonjwa yanayoangaziwa katika sehemu hii hubainika kwa kuangalia jinsi mnyama anavyopumua kama dalili kuu ya ugonjwa. Homa ya mapafu (CCPP) miongoni mwa mbuzi ndio ugonjwa maarufu zaidi unaoangaziwa katika sehemu hii . </s>
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoathirika [/INST] Ugonjwa huu hasa huambukiza mbuzi. Hata hivyo, unaweza kuathiri kondoo wanaochanganywa na mbuzi wagonjwa. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama mgonjwa anaweza kuusambaza ugonjwa huu kupitia matone ya pumzi (droplets) yake anayopumua nje kisha mbuzi mzima kiafya kuyavuta ndani ya mwili wake anapopumua. Wanyama wazima kiafya wanaogusana au kusogeana karibu na mnyama aliyeambukizwa huwa katika hatari kuu ya kuupata ugonjwa huu. Mchoro 1.1.1 Unaonyesha jinsi ugonjwa huu wa mapafu (CCPP) unavyosambazwa. Mnyama aliyeathiriwa husambaza kiini kinachousababisha kupitia matone (droplets) yanayomtoka anapokohoa. Wanyama walio hatarini ambao wako karibu naye huvuta ndani kiini hicho kilichoingia hewani (kwenye matone), na kuongeza hatari ya kusababisha maambukizi. </s>
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Karibu wanyama wote kwenye kundi ambao hawajawahi kuambukizwa viini hivi wanaweza kuupata ugonjwa huu. Hata hivyo, ni takribani nusu yao huonyesha dalili za ugonjwa huo. </s>
<s>[INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unapatikana katika maeneo yote ya wafugaji na huenea polepole katika maeneo yote ambayo wanyama hao huhamishiwa. </s>
<s>[INST] Kufadhaika/kiwewe [/INST] Kuwepo wa wanyama wadhaifu kiafya (ama kwa sababu hawajawahi kuambukizwa viini hivyo au hawajachanjwa). </s>
<s>[INST] Kiwango cha juu cha joto/homa [/INST] Kiwango cha vifo hutofautiana (kiko juu katika maeneo ambayo hayajawahi kuushuhudia, na katika wanyama wachanga kiumri) </s>
<s>[INST] Magonjwa yenye maambukizi na uvamizi wa ngozi kwa jumla [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa ambayo dalili yake kuu ni maambukizi ya ngozi. Haya yanajumuisha upele unaowasha ambao huathiri jamii zote za mifugo, pamoja na tetekuwanga ya kondoo na mbuzi </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama mzima kiafya hupata ugonjwa huu kwa kugusana moja kwa moja na mnyama aliyeathiriwa, au kujisugulia katika sehemu ambazo wanyama wenye ugonjwa huu walijisugulia. Pia wanaweza kuupata wanapolala katika sehemu ambazo wanyama walioambukizwa walilala. Husababishwa na vimelea (aina fulani ya viroboto) vinavyojipenyeza ndani ya ngozi. Vimelea hivyo vinaweza kuishi katika mazingira kama hayo kwa muda wa hadi wiki mbili. Mchoro 2.1.1 Unaonyesha jinsi upele unaowasha unavyosambazwa kutoka kwa wanyama walioathiriwa hadi kwa wanyama wazima kiafya. Mchoro huu, aidha, unaonyesha wanyama walioathiriwa wakijisugulia kwenye miti (kama mfano). Katika harakati hii ya kujisugua, wanaacha hapo chembechembe za ngozi zilizo na vimelea vya upele ambao unaweza kuwaambukiza wanyama wazima kiafya wanaojisugulia kwenye miti iyo hiyo. </s>
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi [/INST] Kwa kutegemea mfumo wa ufugaji na mbinu za kuudhibiti zinazotumika, thuluthi (mmoja kwa watatu) ya wanyama kwenye kundi huathiriwa. </s>
<s>[INST] Katika aina fulani ya upele unaowasha, uvimbe hutokeza kwenye ngozi [/INST] Sehemu zilizoambukizwa huanza kuwasha na kusababisha mnyama kuanza kujiuma na kujisugulia kwenye kuta, miti n.k </s>
<s>[INST] Tumia dawa inayofaa kulingana na ushauri wa afisa wa tiba ya mifugo [/INST] Picha 2.12 (b) Mbuzi anayeugua upele unaowasha akionekana kupoteza manyoya, kuwa na mabaka magumu ngozini na kujisugua sehemu iliyoathiriwa kutokana na mwasho </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mate na majimaji mengine kutoka kwenye ngozi hubeba virusi. Madonda au mabaka ya ngozi pia yanaweza kusababisha maambukizi mapya hata baada ya muda mrefu. Madonda hayo yanaweza kudumisha virusi hivyo katika kivuli kwa hadi miezi sita. Wanyama wazima kiafya wanaweza kugusana na wale walioathiriwa na hivyo kuambukizwa. Kondoo wanaweza kuwaambukiza kondoo wengine pekee tetekuwanga ya kondoo huku mbuzi nao wakiwaambukiza mbuzi wenzao pekee. Maambukizi yanaweza kusambazwa kupitia hewani wakati wa kulisha kundi la wanyama. Nzi wanaouma pia wanaweza kusambaza virusi vya tetekuwanga. Mchoro 2.1.3 Waonyesha jinsi tetekuwanga ya kondoo na mbuzi inavyosambaa kupitia migusano au hewa kutoka kwa wanyama walioambukizwa hadi kwa wale wazima kiafya wakati wanapolishwa pamoja. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Katika maeneo yanayoshuhudia ugonjwa huu, wanyama wachache, karibu asilimia 5-10 hufa. Wana wa mbuzi na kondoo huwa katika hatari kuu ya kufa. Hata hivyo, katika maeneo ambayo hayajawahi kushuhudia ugonjwa huu, wanyama wengi, hadi asilimia 100, hufa. </s>
<s>[INST] Magonjwa yenye madonda miguuni na midomoni [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa yanayodhihirika kupitia madonda makuu kwenye mdomo na kwato. Maradhi haya yanajumuisha mwozo wa kwato unaoweza kuwaathiri mifugo wote, ugonjwa wa miguu na midomo (FMD), unaoathiri wanyama wote wenye kwato na vidonda vya kuambukizana (orf) ambavyo vinaweza kuathiri mbuzi. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kuzoesha mnyama kwenye unyevunyevu kwa kipindi kirefu kunaweza kusababisha maambukizi ya bakteria wanaokaa ngozini au katika mazingira kwa muda mrefu. Bakteria hao hujipenyeza ndani ya ngozi na kusababisha ugonjwa huu., Pia bakteria hao wanaweza kujipenyeza katika jeraha la kwato na kusababisha kwato kuoza(copy from Cattle Manual). Picha 3.1.1 Inaonyesha kondoo na mbuzi waliofungiwa katika maboma yenye tope/unyevunyevu yanayowaweka katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa mwozo wa kwato. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Wanyama walioathiriwa kwa kawaida huwa hawafi. Hata hivyo, kiwango cha maziwa katika mbuzi wa kukamwa pamoja na uzito wa nyama ya mbuzi walioathiriwa hupungua kutokana na shida ya kutembea na hivyo kupunguza ulaji wa chakula. </s>
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa katika kundi [/INST] Wanyama wote wenye mwanya katika kwato zao wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu. Kondoo na mbuzi wanaweza kuathiriwa na FMD lakini hili ni nadra unapolinganisha na ng’ombe. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Wanyama wenye afya hupata ugonjwa huu wanapogusana au kukaribiana na majimaji yanayotoka mwilini kama vile mate, kamasi, mkojo, maziwa, kinyesi au mbegu za kiume (manii) za mnyama aliyeambukizwa. Virusi vinavyosababisha ugonjwa huo vinaweza kubebwa na upepo; nao wanyama walio katika hatari ya kuambukizwa wanaweza kuathiriwa wanapovuta ndani hewa iliyoambukizwa na virusi hivyo. Vivyo hivyo, virusi hivi vinaweza kuishi kwenye mazingira haya kwa siku kadhaa, hasa katika msimu wa unyevunyevu. Msimu huu huwa ndio kiini cha maambukizi kwa wanyama wadhaifu kiafya. </s>
<s>[INST] Idadi ya wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Husambaa haraka miongoni mwa wanyama wadhaifu kiafya na kuna uwezekano mkubwa kuwa wanyama wote katika kundi kama hilo wanaweza kuambikizwa. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Miongoni mwa wanyama waliokomaa, ugonjwa huu si hatari kwa kuwa wengi wa wanyama hawa hufanikiwa kupona wanapoambukizwa. Hata hivyo, wanyama wachache wachanga hufa kutokana na matatizo ya moyo. </s>
<s>[INST] Uhamishaji au usafirishaji ama utembezaji wa wanyama [/INST] Kutumia eneo moja kuwanyweshwa maji, malisho ya pamoja au maeneo mamoja ya kuramba udongo wenye magadi Msimu wa kiangazi huzidisha utembeaji wa wanyama kwa kuwa visima vyenye maji ya kuwanywesha huwa vichache. Malisho ya pamoja pia huchangiamaambukizi. </s>
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoambukizwa [/INST] Mbuzi na kondoo wote wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu, lakini huathiri mbuzi zaidi. Ngamia pia wanaweza kuathiriwa hasa wale wachanga. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu huambukiza wanyama wazima kiafya kutoka kwa wanyama wagonjwa kupitia kwa kugusana. Wanyama wazima kiafya huwa kwenye hatari ya kuambukizwa wanapojigusisha kwenye madonda au kugusana na wanyama walioathiriwa. Mara nyingi maambukizi huenea kupitia majeraha kwenye ngozi pale wanyama wanapokula nyasi au matawi yenye ncha kali au magumu. Virusi vya ugonjwa huu vinaweza kudumu kwenye vidonda kwa muda mrefu katika maeneo kame. </s>
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Wengi wa wanyama, hasa wachanga, huathiriwa. Ugonjwa huu huathiri sana mbuzi kuliko kondoo. Maambukizi yanayotukia mara ya pili baada ya mnyama kupona huweza kutokea kwa sababu ugonjwa huu huwa haujengi kinga thabiti mwilini (kinga ya daima). </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Upele wa mdomoni wa kuambukizana kwa kawaida hauui, lakini majeraha yanayozuka kwenye mdomo yanaweza kumzuia mnyama mwathiriwa kukosa kula, hasa miongoni mwa wanyama wachanga. </s>
<s>[INST] Vidonda huzuka kwenye mdomo na pua ya mnyama (Picha 3.4) [/INST] Vidonda hivyo hugeuka kuwa madonda magumu kwenye mdomo (Picha 3.5), ingawa wakati mwingine madonda haya yanaweza kuenea hadi ndani ya mdomo, (sehemu za chini ya miguu, na matiti ya majike yanayonyonyesha). </s>
<s>[INST] Mipasuko sehemu zilizoathiriwa [/INST] Ugonjwa huu mara nyingi hudumu kwa majuma manne hadi sita, halafu mnyama huyo huanza kupona polepole mwenyewe </s>
<s>[INST] Nyunyiza dawa ya kuua viini katika maboma au maeneo ambako wanyama hukaa [/INST] Osha mikono kwa sabuni baada ya kugusa/kushika madonda ya orf kwa kuwa virusi vyake vinaweza kuambukiza hata binadamu </s>
<s>[INST] Magonjwa yenye dalili za kuhangaika/kiwewe [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa yanayodhihirika kwa dalili za ukosefu wa utulivu kama vile kujizungusha, kufinyilia kichwa mahali n.k. Magonjwa makuu yanayoangaziwa hapa ni maji kujaa kwenye moyo na kichaa cha mbwa (T9). Magonjwa haya yote huathiri jamii nyingi za wanyama. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Viini vinavyosababisha ugonjwa huu husambazwa na kupe, hasa wenye rangi mbalimbali. Kupe wasiokuwa na viini hivi huvipata kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa wakati wanapomnyonya/kumfyonza damu yake. Viini hivyo hukua vikiwa kwenye kupe huyo na kisha kusambazwa wakati kupe huyo anapomnyonnya damu mnyama mwingine. </s>
<s>[INST] Picha 4.11 Kupe wenye rangi mseto wanaosambaza viini vinavyosababisha maji kujaa kwenye moyo [/INST] Picha 4.1.2 Inaonyesha mzunguko wa maambukizi ya viini vinavyosababisha ugonjwa wa maji kujaa kwenye moyo. Kupe hawa wenye rangi mbalimbali) huvipata viini hivyo kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa wakati anapomnyonya damu na kuvisambaza hadi kwa mnyama mwingine anapomnyonya damu pia. </s>
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika katika kundi [/INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika hutofautiana kulingana na wingi wa kupe, maambukizi ya hapo awali na mbinu zinazotumika kukabiliana na ugonjwa huo. </s>
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ya wanyama wanaokufa baada ya kuambukizwa ugonjwa huu huwa juu katika maeneo ambayo haujawahi kushuhudiwa. </s>
<s>[INST] Kifo cha ghafla [/INST] Kukosa utulivu huongezeka muda unavyosonga, hali inayosababisha ukosefu wa uthabiti wa kutembea, utoaji ulimi nje, uinuaji miguu zaidi ya kawaida wakati wa kutembea, ufinyiliaji kichwa mahali na kujizungusha. Mwishowemnyama mgonjwa huanguka na kuanza kupigapiga miguu (degedege). </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu hutokana na kuumwa na mnyama aliyeathiriwa, hasa mbwa na wanyamapori wa jamii ya mbwa. Mate yanayotoka kwa mnyama huyo aliyeathiriwa huwa na virusi ambavyo huingia mwilini mwa mnyama anayeumwa. Mchoro 4.2.1 Unaonyesha mzunguko wa maambukizi ya kichaa cha mbwa, ambao ni ugonjwa wa virusi unaoweza kuambukiza pia binadamu. Mnyama mwenye kichaa hiki kama vile mbwa au mbuzi humuuma mwenzake, na katika hali hiyo kusambaza virusi hivyo kupitia kwa mate yake. Ugonjwa huu ni hatari kwa wanyama. Iwapo mwanadamu ataumwa, osha jeraha haraka kwa kutumia maji yenye sabuni kisha utembelee kituo cha afya kilicho karibu kwa matibabu ya haraka. </s>
<s>[INST] Kukosa kula au kunywa [/INST] Utembeaji usiokuwa wa kawaida na kupungua kwa hisi; kupungua kwa hisi sanasana huathiri miguu ya nyuma. </s>
<s>[INST] Kabiliana na idadi ya mbwa koko [/INST] Wanyama walioambukizwa wanafaa kuuawa kitaalamu (ambako hakuna uchungu) ili kupunguza maambukizi zaidi </s>
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Mifugo wote wanaweza kuathiriwa, lakini ugonjwa huu ni maarufu sana miongoni mwa kondoo na mbuzi. Ugonjwa huu unasababishwa na minyoo wachanga (viluwiluwilu/mabuu) wa tegu miongoni mwa mbwa na wanyama wengine wala-nyama. </s>
<s>[INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] </s>
<s>[INST] Magonjwa yanayosababisha mimba kutoka [/INST] Mabaki ya tegu yanapatikana katika ubongo au uti wa mgongo. Mabaki hayo huwa na urefu wa angaa sentimita tano. </s>
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Magonjwa yanayohusisha mimba kutoka k.m Homa ya Rift Valley (RVF) na ugonjwa wa maziwa (ugonjwa wa kutupa mimba), yameangaziwa kwa kina katika sehemu hii. </s>
<s>[INST] Picha 5.1.1 Mbu wa Aedes ametambuliwa kama msambazaji mkuu wa viini vya RVF [/INST] Mbu hupata virusi vya ugonjwa huu anapomnyonya damu mnyama aliyeambukizwa. Kisha humwambukiza mnyama mzima kiafya anapomnyonya damu. Mbu wa jamii ya Aedes hutambuliwa kama mbebaji wa viini vya ugonjwa huu huku mbu wale wengine kama vile culex, anopheles, na nzi wa kuuma/pange wakitajwa kama wasambazaji wa raundi ya pili ya maambukizi. </s>