id
stringlengths
1
6
url
stringlengths
31
202
title
stringlengths
1
120
text
stringlengths
8
182k
2398
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kisiwa%20cha%20Mafia
Kisiwa cha Mafia
Mafia ni funguvisiwa la Tanzania, pamoja na jina la kisiwa kikubwa ndani yake, linalotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki km 130 kusini kwa Dar es Salaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni km 16. Kisiwa kikuu kina urefu wa km 49 na upana wa km 16; eneo lake ni takriban km² 400. Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole uliokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole kilichopo karibu na kisiwa kikuu kwa umbali wa mita 900. Wilaya Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani ikiwa na wakazi 40,801 (2002). Mji mkubwa na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni. Ina tarafa mbili ambazo ni: Tarafa ya kusini Tarafa ya kaskazini Kata za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo: Baleni Jibondo Kanga Kilindoni Kirongwe Kiegeani Mibulani Ndagoni Ina jumla ya vijiji 23. Uchumi Wakazi walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja na nazi, chokaa na samaki. Kuna utalii unaosifiwa sana lakini idadi ya wageni bado ni ndogo. Hasa Waitalia wamependa kutembelea Mafia pia kwa sababu ya jina la kisiwa ambalo kwa Kiitalia linamaanisha shirika la kigaidi lenye historia ndefu katika Italia ya kusini hadi siku ya leo. Historia Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya utamaduni wa Waswahili kama vile miji ya Chole na Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya Sultani wa Omani (baadaye wa Zanzibar). Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia kutoka kwa Sultani wa Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mwaka 1915, wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, Waingereza waliteka kisiwa wakishambulia kutoka hapa manowari ya Kijerumani ya SMS Königsberg mdomoni mwa mto Rufiji kutoka Mafia. Mnamo 1922, baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika, si tena Zanzibar. Tazama pia Orodha ya visiwa vya Tanzania Hifadhi ya Kisiwa cha Mafia Tanbihi Viungo vya nje http://mafia-island-tanzania.gold.ac.uk/index_swahili.php Archaeology and History of Mafia Island , tovuti ya Mafia Island Tanzania ya Pat Caplan Pat Caplan’s publications on Tanzania, hasa Mafia, in chronological order, as of 120411 Asili ya Kua , kuhusu historia ya mji wa Kua kisiwani Chole, ilivyokusanywa na Pat Caplan mnamo mwaka 1966 Last Century in Mafia Island, blogu ya Mafiaisland.com Mafia kwa Geonames.org Visiwa vya Afrika Visiwa vya Tanzania Visiwa vya Bahari ya Hindi Mkoa wa Pwani
2399
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Mafia
Wilaya ya Mafia
Mafia ni moja kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani katika Tanzania yenye postikodi namba 61700. Eneo lake ni hasa Kisiwa cha Mafia na visiwa vidogo karibu nacho. Mji mkuu na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ilikuwa na wakazi wapatao 46,438 walioishi humo. Kata za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo: Baleni, Kanga na Kirongwe kwa pamoja ni tarafa ya kaskazini, shehia nyingine ni tarafa za kusini. Wilaya hii inajumuisha funguvisiwa pamoja na kisiwa cha Mafia ndani yake inayotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki 130 km kusini ya Daressalaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni 16 km. Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa 50 km na upana wa 8 km; eneo lake ni takriban 400 km². Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini karibu na kisiwa kikuu. Marejeo M
2400
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20%28ziwa%29
Tanganyika (ziwa)
Ziwa Tanganyika ni moja ya maziwa makubwa ya Afrika ya Kati likienea mpakani mwa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia. Ni ziwa kubwa la pili duniani kwa wingi wa maji matamu baada ya Ziwa Baikal (Siberia) kwa kuzingatia kiasi cha maji ndani yake na kina (hadi mita 1,470). Kwa kulinganisha eneo lake (km² 32,893) ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika. Maji yake hutoka kuelekea mto Kongo ha hatimaye katika Bahari Atlantiki. Jina Hatuna uhakika jinsi gani wenyeji walioishi kando ya ziwa hilo waliliita kwa lugha zao mbalimbali. Kutokana na taarifa za wapelelezi Wazungu waliofika huko kwenye karne ya 19 na kushika yale waliyoelewa kutoka kwa wenyeji, kuna ushuhuda fulani kuhusu majina manne ambayo ni "Tanganika", "Liemba", "Kimana" na "Nsaga". Jina la Tanganika limepokewa na Wazungu wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa Ujiji. Henry Morton Stanley aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba watu wa Ujiji hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina, ila tu kwamba lilimaanisha "ziwa kubwa". Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hilo "Tanganika". Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitokana na aina ya samaki walioitwa vile. Baadaye Stanley alikumbuka neno "nika" katika lugha nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotanda" . Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa makabila mengine: watu wa Marungu walisema "Kimana", wale wa Urungu "Iemba" na Wakawendi "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu, yaani "Iemba", inalingana na taarifa ya David Livingstone aliyekuta jina "Liemba" kuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa na jina hili linaendelea kutumiwa kwa meli ya MV Liemba inayosafirisha watu na bidhaa ziwani tangu mwaka 1914. Jina la ziwa limekuwa pia jina la eneo lililokabidhiwa kwa Uingereza kama Tanganyika baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia tangu 1919. Jiografia Maji ya Ziwa Tanganyika yanajaza ufa kubwa kwenye ganda la dunia ambalo ni sehemu ya bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Ni ziwa lenye kina kikubwa katika Afrika. Vipimo Kina cha wastani ni m 570, ni kubwa zaidi katika sehemu ya kaskazini ambako vilindi vyake hufikia kina cha mita 1470. Kutokana na kina kikubwa kinashika kiwango kikubwa cha maji matamu kati ya maziwa yote ya Afrika (18,900 km³) na asilimia 16 ya maji matamu yote duniani. Halijoto ya maji usoni mwa ziwa ni sentigredi 25 na uchungu wake ni pH 8.4 hivi. Urefu wa ziwa ni kilomita 676 kutoka kaskazini hadi kusini na upana wake ni km 50 kwa wastani. Uso wa maji huwa na eneo la km2 32,900 na urefu wa pwani yake ni km 1,828. Kina kikubwa cha ziwa kimesababisha kuwepo kwa safu za maji zisizochanganya maana maji ya chini hayakorogwi kwa upepo au mikondo na maji ya juu, hivyo maji ya chini hayapokei oksijeni na kuwa na uhai kidogo. Samaki na viumbehai wengi hawawezi kuishi katika maji bila oksijeni. Beseni Ziwa linapokea maji yake kutoka mito ya mazingira inayoishia humo. Beseni lake huwa na eneo la km2 231,000 (sq mi 89,000). Mito miwili mikubwa na mito mingi midogo inaishia ziwani. Mto Lukuga hutoka ziwani na kupeleka maji yake kwenda beseni la Kongo. Mto mkubwa zaidi unaoingia ni Ruzizi unaofika upande wa kaskazini kutoka Ziwa Kivu. Malagarasi, ambao ni mto mrefu wa pili nchini Tanzania, inaingia upande wa mashariki. Kubadilika kwa kiasi cha maji Kutokana na mahali pake katika tropiki kwenye jua kali, Ziwa Tanganyika linapotewa na maji mengi kwa njia ya uvukizaji. Kwa hiyo kiasi cha maji ndani yake inategemeana na kiasi cha maji yanayoingia. Kwa sasa chanzo kikubwa ni maji ya Ziwa Kivu. Imegunduliwa ya kwamba uwiano wa ziwa ulibadilika sana katika historia. Mnamo miaka 200,000 iliyopita uso wa ziwa ulikuwa mita 600 chini ya uwiano wa leo. Wakati wa vipindi vya tabianchi yenye mvua nyingi zaidi uwiano ulipanda juu, na kupungua tena kwenye vipindi vya ukame. Vipindi hivi vya mabadiliko vilidumu mara kwa mara miaka elfu kadhaa. Hali ya sasa imepatikana tangu miaka 12,000. Wakati ule volkeno za Virunga vililipuka na kuziba mto uliowahi kubeba maji ya Ziwa Kivu kuelekea mto Naili na baada ya kufikia uwiano wa leo maji ya Kivu yalianza kutoka upande wa Tanganyika kupitia njia ya Ruzizi. Mabadiliko ya uwiano wa maji kwenye ziwa yalitazamwa pia katika historia ya miaka 200 iliyopita kwa kulinganisha kumbukumbu ya wakazi na taarifa za wapelelezi Wazungu walioandika taarifa juu ya safari zao. Baada ya mwaka 1800 maji yalikuwa chini sana, kabla ya 1900 yalikuwa juu sana, tangu 1900 yalishuka tena. Katika miaka ya 1960 ziwa lilijaa tena likabaki hivi hadi sasa. Mabadiliko haya yanalingana na mabadiliko katika kiasi cha mvua inayopokewa katika beseni ya ziwa. Miji na nchi jirani Miji mikubwa ziwani ni bandari za Kigoma kwa upande wa Tanzania na Kalemie kwa upande wa Kongo. Kila bandari ni pamoja na mwanzo wa njia ya reli. Mji mkubwa kabisa ni Bujumbura, mji mkuu wa Burundi. Eneo lote la ziwa limegawiwa baina ya nchi jirani yaani Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia. Sehemu kubwa iko chini ya Tanzania (46%) na Kongo (40%). Visiwa Kuna visiwa mbalimbali ndani ya ziwa Tanganyika. Vikubwa zaidi ni pamoja na Visiwa vya Kavala, Mamba-Kayenda, Milima na Kibishie katika sehemu ya Kongo Visiwa vya Mutonowe na Kumbula katika sehemu ya Zambia Kisiwa cha Lupita katika sehemu ya Tanzania Biolojia Kuna spishi nyingi za samaki aina ya cichlidae zinazokadiriwa kuwa 250 na angalau spishi 75 za samaki wengine. Spishi nyingi wanaishi karibu na mwambao na hadi kina cha mita 180; chini yake kiwango cha oksijeni kinapungua mno. Lakini kiasi kikubwa cha samaki kinapatikana katikati ya ziwa, ila ni spishi chache tu, hasa spishi mbili za kapenta (inayoitwa pia dagaa) na spishi nne za sangala. Cichlidae karibu spishi zote ni wenyeji wa ziwa yaani wametokea hapa. Pia sangala ni wenyeji wa Tanganyika, kwa hiyo hakuna matatizo kama huko Viktoria Nyanza ambako spishi ya sangala iliingizwa miaka 50 iliyopita na kuvuruga ekolojia ya ziwa. Kutokana na mazingira ya pekee ziwa Tanganyika ni mahali pa kutazama matokeo ya mageuko_ya_spishi. Cichlidae wa ziwa Tanganyika wanapendwa kama samaki wa mapambo wakinunuliwa na kufugwa na wenye tangisamaki kote duniani. Ziwani kuna pia spishi nyingi za pekee za konokono na kaa pamoja na crustacea nyingine. Uvuvi Tasnia muhimu katika eneo la ziwa ni uvuvi. Inakadiriwa ya kwamba baina ya 25–40% za protini katika chakula cha milioni 1 ya watu wanaoishi kule ni kutoka samaki wa ziwani. Mwaka 2015 kulikuwa na watu 100,000 hivi waliofanya kazi kuhusiana na uvuvi. Samaki wa ziwani wanauzwa kote Afrika ya Mashariki. Katika miaka ya 1950 uvuvi wa kibiashara ulianzishwa ziwani ukasabisha kupotea kwa samaki: kufikia mwaka 1995 mavuno ya samaki yalipungua hadi tani 180,000. Kampuni nyingi za uvuvi zilizostawi katika miaka ya 1980 ziliporomoka. Usafiri Usafiri ni mgumu kufikia Ziwa Tanganyika kutoka miji mikuu ya nchi zao. Kuna njia za reli zinazoishia Kigoma (Tanzania) kutoka Dar es Salaam, bado kwenye njia ya reli iliyojengwa zamani za ukoloni wa Kijerumani Kalemie (J.D. Kongo) kutoka Lumbumbashi Mpulungu (Zambia) - hakuna reli bado, ila kuna mipango ya kujenga njia hadi hapa hadi njia kuu ya TAZARA Huduma iliyopo hadi sasa ni ngumu na hali za njia za reli si nzuri. Upande wa Tanzania treni zilichelewa mno, masaa hata siku, lakini hali ilianza kuwa afadhali kuanzia Julai 2016. Muhimu kwa ajili ya watu ziwani ni huduma ya feri. Kuna meli 2 zinazobeba abiria na mizigo ambazo ni MV Liemba baina ya Kigoma na Mpulungu halafu MV Mwongozo baina ya Kigoma na Bujumbura. Marejeo Viungo vya nje Food and Agriculture Organization of the United Nations Index of Lake Tanganyika Cichlids Maziwa ya Afrika Maziwa ya Tanzania Maziwa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Maziwa ya Zambia Maziwa ya Burundi Mkoa wa Kigoma Mkoa wa Katavi Mkoa wa Rukwa
2404
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ethiopia
Ethiopia
Ethiopia (kwa Kiamhara ኢትዮጵያ Ityopp'ya; kwa Kiswahili pia "Uhabeshi") ni nchi ya Afrika ya Mashariki iliyoko kwenye Pembe ya Afrika. Nchi zinazopakana na Ethiopia ni Sudan na Sudan Kusini upande wa magharibi, Eritrea na Jibuti kaskazini, Somalia mashariki na Kenya upande wa kusini. Ni nchi ambayo ina historia ya pekee Afrika na hata duniani kwa ujumla. Ethiopia ni moja ya nchi mbili za Afrika ambazo hazikutawaliwa na wakoloni wakati walipong’ang’ania Afrika. Nchi nyingine ni Liberia. Kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Ethiopia ilivamiwa na Waitalia (1936) lakini ilipata uhuru wake tena baada ya miaka michache. Jina la nchi Asili ya jina "Ethiopia" haijulikani. Kuna maelezo mbalimbali lakini yote yanakosa uhakika. Hilo ni sawa pia kwa jina la pili la kihistoria ambalo ni "Habasha" ilikuwa "Uhabeshi". Ethiopia mara nyingi linaelezwa kuwa neno la Kigiriki cha Kale Αἰθιοπία Aithiopia lililotokana na Αἰθίοψ "Aithiops" ; maana yake "uso" (ὄψ) "kuwaka" (αιθw) hivyo labda "uso uliochomwa" ama sura nyeusi. Lakini jina hili halikumaanisha hasa nchi ya Ethiopia ya leo lakini nchi zote zenye watu wenye rangi nyeusinyeusi. Kwa muda mrefu watu wa Ulaya waliita Afrika yote kwa jina "Ethiopia". Pia si wazi kama neno la Kiafrika lenye maana tofauti limechukuliwa na Wagiriki kwa maana ya neno lao la "aithiops". Nchi yenyewe ilijulikana kwa muda mrefu wa historia yake kwa jina la Habasha. Habasha ilikuwa jina la Kiarabu kwa ajili ya nchi ikaingia kama "Uhabeshi" katika Kiswahili au "Abisinia" katika lugha za Ulaya. Asili ya jina hilo haliko wazi; wengine husema ni katika lugha ya kale ya nchi yenyewe kumaanisha "nchi kwenye nyanda za juu"; tena wengine wanadai kwamba jina limetoka Uarabuni wa kusini lilipokuwa jina la kabila moja lililohamia na watu walioleta lugha za kisemiti Ethiopia. Jiografia Tazama pia: Orodha ya mito ya Ethiopia Ethiopia ina eneo la kilometa mraba 1,127,127 (maili mraba 435,071). Nchi yenyewe ni mojawapo ya nchi za Pembe ya Afrika upande wa mashariki. Nchini Ethiopia kuna milima mirefu; sehemu kubwa ya nchi inaundwa na Nyanda za juu za Ethiopia zilizotenganishwa na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, ambalo limepasua kutoka kusini - magharibi kwenda kaskazini – mashariki na kuzungukwa na mbuga maeneo yaliyo chini. Mabonde na milima hasa nchini Ethiopia yanaathiri hali ya hewa, udongo, mimea, na makazi ya watu. Ukweo wa milima na eneo la kijiografia vinasababisha aina mbili za hali ya hewa: eneo lililopoa liko zaidi ya ukweo wa mita 2,400 (futi 7,900) ambapo vipimo vya joto ni kati ya kuganda na 16°C (32°–61°F); vipimo vya joto kwa ukweo wa mita 1,500 na 2,400 (futi 4,900—7,900) joto ni 16°C hadi 30°C (61°–86°F); joto zaidi liko chini ya mita 1,500 (futi 4,900) ni hali ya hewa ya tropiki na hali ya hewa ya ukame na joto saa za mchana ni 27°C mpaka 50°C (81°–122°F). Mvua ya kawaida ni kuanzia kati ya Juni mpaka kati ya Septemba lakini eneo la milima ya kusini mvua hunyesha zaidi ikianzia na mvua kidogo ya Februari ama Machi. Ethiopia ni nchi ambayo ina ikolojia tambakazi. Ziwa Tana, ambalo liko kaskazini mwa nchi, ndilo chanzo cha Mto Naili ya Buluu (kwa Kiarabu: Bahr al Zraq). Eneo la mto huo lina aina za wanyama za pekee kama Gelada - nyani, Walia ibeka na pia Mbwa mwitu. Historia Historia ya awali Historia ya binadamu katika Ethiopia ilianza mapema kabisa. Mifupa ya kale kabisa ya viumbe jamii ya watu imepatikana katika nchi hii kwa sababu zilihifadhiwa katika mazingira yabisi ya nchi. Wataalamu wengi huamini ya kwamba Ethiopia (pamoja na Kenya na Tanzania) inaweza kuwa mahali ambako watu wa aina ya Homo Sapiens walianza kupatikana duniani. Kuna mabaki mbalimbali ya kiutamaduni yanayochunguzwa na akiolojia, lakini sehemu kubwa ya nchi haijaangaliwa bado kitaalamu. Inaonekana kwamba katika karne za K.K. kulikuwa na uhusiano wa karibu na Uarabuni kwa sababu lugha za Kiethiopia ni karibu na lugha za upande mwingine wa Bahari ya Shamu. Inaaminiwa kwamba watu kutoka Uarabuni Kusini walihamia Ethiopia na kuleta lugha yao huko. Biblia ina taarifa juu ya ziara ya malkia wa Sheba aliyemtembelea mfalme Suleimani wa Yerusalemu. Milki ya Sheba imedaiwa kuwepo ama Ethiopia au Yemen na wengine huamini ya kwamba ilikuwa dola la pande zote mbili za mlangobahari wa Bab el Mandeb unaotenganisha Eritrea ya leo na Uarabuni Kusini. Historia ya kale Milki ya kwanza ya Ethiopia inayoweza kutajwa kutokana na mabaki ya majengo na maandishi ilikuwa milki ya D'mt (pia: Da'amot) katika Ethiopia ya kaskazini pamoja na Eritrea ya leo. Kuna mabaki ya hekalu la Yeha pamoja na makaburi ambako majina ya wafalme kadhaa yamehifadhiwa kwa maandishi kwenye mawe. Lugha ilikuwa karibu sana na lugha za kale za Uarabuni. Ilikuwa na athira juu ya sehemu za kaskazini ya Ethiopia kwa kipindi kikubwa cha milenia ya 1 KK. Ilifuata milki kubwa ya Aksum, iliyoanzishwa wakati wa kuzaliwa Yesu. Ufalme wa Aksum ulikuwa milki ya kwanza kutawala maeneo makubwa ya Ethiopia. Nabii Mwajemi Mani aliuweka Ufalme wa Aksum kwa utukufu sawa na Roma, Uajemi na Uchina kama nchi zilizokuwa na nguvu duniani karne ya 3 BK, wakati yeye alipoishi. Ilikuwa karne ya 4 BK ambapo Frumentius, mtu Msiro-Mgiriki aliyekuwa amepotelea baharini kutokana na kuzama kwa jahazi, alishikwa na Wahabeshi na kupelekwa kortini na baadaye kumuongoa mfalme Ezana kuingia Ukristo. Kwa hiyo Wahabeshi wakampa jina Abba Selama. Kwa muda mfupi dini hiyo mpya ilienea kote. Mara nyingi karne ya 6 Aksum ilitawala eneo la Yemeni ng'ambo ya Bahari ya Shamu. Aksum ilistawi hasa kutokana na biashara kati ya Mediteranea na Bara Hindi iliyopita kwenye mlangobahari wa Bab el Mandeb ikatumia bandari ya Adulis (karibu na Massawa ya leo nchini Eritrea). Uenezi wa Uislamu ulivuruga biashara hiyo na Aksum ilipoteza utawala juu ya pwani. Kuporomoka kwa uwezo wa kibiashara kunaonekana katika kusimamishwa kwa uchapaji pesa ya wafalme wa Aksum katika karne ya 7. Nchi ilishambuliwa pia kutoka milki za barani. Mabaki ya ufalme wa Aksum yaliharibiwa mnamo mwaka 900 wakati na malkia Gudit (au Judith) aliyekuwa ama Myahudi ama kiongozi wa makabila ya Kipagani kutoka nyanda za juu. Milki ya Ethiopia Kiongozi wa kabila la Agaw alimwoa binti wa mfalme wa mwisho wa Aksum akaanzisha nasaba ya Zagwe na kuunda upya ufalme wa Kikristo katika nyanda za juu. Kitovu cha ufalme huu kilipelekwa zaidi mbali na pwani. Nasaba hii ilipinduliwa mnamo 1270 na Yekuno Amlak aliyetumia jina la kifalme Tasfa Iyasus. Alianzisha nasaba iliyojiita "Wa Suleimani" kwa kudai ilikuwa ukoo wa mwana wa mfalme Suleimani na malkia wa Sheba. Tasfa Iyasus alitumia cheo cha Negus Negesti ("Mfalme wa Wafalme"). Enzi ya Mfalme Lebna Dengel, Ethiopia iliweza kuwasiliana na nchi za Ulaya na kudumisha ubalozi na nchi kama Ureno. Lakini, Mfalme Susenyos alipojiunga na Kanisa Katoliki mwaka 1622, chakari na misukosuko ilifuata. Wamisionari Wajesuiti walichukiwa na waamini wa Kanisa la Ethiopia, na katika hiyo karne ya 17 Susenyos mwana wa Mfalme Basil aliwafukuza wanamisheni hao. Baadaye Waoromo wakaanza kuasi amri ya Kanisa la Ethiopia na kutafuta njia za dini yao, eneo hili la Uhebeshi. Mambo hayo yote yalifanya Ethiopia itengwe miaka ya 1700. Wafalme wakawa kama wakurugenzi, ambao waliamriwa na masharifu kama Ras Mikael Sehul wa Tigrinya. Ethiopia ilitoka kutoka utengo kwa kufuatia misheni ya Uingereza kufika Ethiopia na kukamilisha muungano kati ya nchi hizi mbili; lakini, hadi milki ya Tewodros II ndipo Ethiopia ilipoanza tena shauri za Duni. Miaka ya 1880 ilikuwa miaka ya Ulaya kung’ang’ania ukoloni Afrika ambapo Waitalia na Waingereza walitafuta kutawala eneo la Assab, bandari iliyoko karibu na mdomo wa bahari ya Shamu. Bedari ya Kusini, karibu na kiingilio cha bahari ya Shamu, ilinunuliwa na Waitalia kutoka sultani mwenyeji Machi 1870 ambayo mwaka 1882 ilizaa koloni la Eritrea. Haya yalizua magombano kati ya Waethiopia na Waitalia na Vita vya Adowa mwaka 1896, ambapo Waethiopia walishtua dunia kwa kupiga nguvu za wakoloni na kulinda madaraka yao kwa uongozi wa Menelik II. Italia na Ethiopia zilisaini mkataba wa amani tarehe 26 Oktoba 1896. Karne ya 20 hadi leo Karne ya 20 miaka ya kwanzakwanza ilimilikiwa na Mfalme Haile Selassie, aliyechukua nafasi ya kuendeleza Ethiopia mpaka uongozi wake ulipokatizwa kwa Vita ya pili ya Uhabeshi na Italia (1936). Waingereza na wazalendo wa Jeshi la Ethiopia wakakomboa nchi mwaka 1941, na Waingereza kukiri madaraka ya Ethiopia kwa mkataba wa Uingereza na Ethiopia mnamo Desemba 1944. Milki ya Haile Selassie ilikoma mwaka 1974, ambapo Wakomunisti wa "Derg" walimpindua na kuanzisha serikali ya kikomunisti chini ya Mengistu Haile Mariam. Mapinduzi hayo yalifuatwa na msukosuko wa vita na migogoro pamoja na ukame na shida za wakimbizi. Mwaka 1977 Somalia ilivamia eneo la Ogaden (Vita vya Ogaden), lakini Ethiopia iliweza kuwafukuza Wasomali kwa msaada wa vifaa vya kijeshi vya Urusi, na majeshi ya Kuba, Ujerumani Mashariki na Yemeni. Usaidizi mwingi kutoka Nchi za Kikomunisti uliwezesha Ethiopia kudumisha mojawapo ya majeshi kubwa Afrika. Lakini hii haikuzuia ukereketwa wa jimbo la Eritrea na Tigray, ambapo ukame wa mwaka 1985 na mapinduzi ya siasa hasa kwa Kambi za Ujamaa, zilileta uongozi wa Derg 1991 kukoma. Chama cha kukomboa Eritrea (EPLF) na Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi Ethiopia (EPRDF), ziliungana kukomboa Ethiopia, wengi wa wanamgambo wakiwa wanaharakati wa Eritrea. Mwaka 1993 jimbo la Eritrea likawa huru kutoka Ethiopia, kufuatia kura ya maoni iliyofanywa ili kumaliza vita hivyo vilivyodumu miaka 20, mmojawapo kati ya migogoro ya muda mrefu zaidi Afrika. Mwaka 1994 Ethiopia kaiweka Katiba mpya ambayo ilileta uchaguzi wa kidemokrasia. Mwaka 1998 magombano ya mipaka na Eritrea yalileta Vita vya Eritrea na Ethiopia ambayo vilidumu hadi Juni 2000. Vita hivyo vilileta uvivu wa uchumi na nguvu ya muungano unaongoza nchi. Siasa Uchaguzi wa Ethiopia ulipitisha wanabaraza 547 Bungeni. Baraza hilo la bunge lilijumuika Juni 1994 na kupitisha katiba mpya ya Jimbo la Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia mnamo Desemba 1994. Uchaguzi huu ulikuwa wa kwanza kuchagua wanabaraza wa kitaifa kwa sifa bungeni na wanabaraza wa majimbo mnamo Mei na Juni 1995. Vyama vingi vya upinzani viligoma kushiriki uchaguzi. Ushindi ulichukuliwa na Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia (EPRDF). Umoja wa Mataifa ukasema vyama vya upinzani vingeweza kushiriki uchaguzi kama zingetaka. Serikali ya Majimbo ya Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia ilichukua mamlaka mnamo Agosti 1995. Rais wa kwanza Negasso Gidada. EPRDF ikaongoza serikali na Waziri Mkuu Meles Zenawi ambaye aliunga mkono majimbo ya kikabila, na kuwapa madaraka viongozi wa kikabila. Ethiopia sasa ina majimbo 9 ambayo yana serikali ya madaraka ya shirika, na hata majimbo haya yanakubaliwa kutoza ushuru na kutumia akiba ya ushuru. Hata hivyo, uhuru wa habari na kisiasa bado umefinywa. Serikali ya Zenawi ilichaguliwa tena mwaka 2000 kwa uchaguzi wa kwanza wa Kidemokrasia, Rais akiwa Girma Wolde-Giorgis. Kutoka 1991, Ethiopia imetafuta urafiki zaidi na Marekani na Umoja wa Ulaya, ili kuweza kukopa fedha za kusaidia uchumi wake na pia kutoka Benki ya Dunia. Mwaka 2004, serikali ilianza kuhamisha watu kutoka maeneo ya ukame wakisema hii itazuia njaa. . Uchaguzi mwingine wa Ethiopia ulikuwa tarehe 15 Mei 2005, ambao ulivutia wapigakura kiasi cha juu zaidi, asilimia 90% ya wananchi waliojiandikisha. Watazamaji wa Umoja wa Ulaya walidai uchaguzi haujafikia kiwango cha kimataifa, lakini Umoja wa Afrika ulitoa ripoti tarehe 14 Septemba kwamba Waethiopia walionyesha kujitokeza na kuheshimu demokrasia, halafu tarehe 15 Septemba, Carter Center, ikasema matokeo ya uchaguzi yaaminika na kuonyesha ushindani wa kisiasa. Uangalizi na ushuhuda wote ulimalizia kuranki Uchaguzi wa Ethiopia na kesi nyingine waipa, asilimia 64% ya matokeo mazuri, na vizuri zaidi kulingana na kesi nyingine 24%. Katika Uchaguzi wa Ethiopia, 2005 EPRDF ilitokea iking’ang’ania uongozi. Tarehe za kwanza za Juni na tena Novemba, polisi kwa amri ya EPRDF wakafyatua risasi na kuua watu kwa maandamano yaliyokuwa yakipinga matokeo ya kura. Ni kwamba vyama vya upinzani vililalamika kwamba EPRDF iliiba kura na kuwazisha wananchi na kusema baraza 299, wapata hitilafu ya wizi wa kura. Hayo yote yalichunguzwa na Watazamaji wa Uchaguzi wa kimataifa na pia Kamisheni ya Uchaguzi Ethiopia. Matokeo ya uchunguzi huo kama haijatokea mnamo Juni 2005, wanafunzi wa chuo kikuu walianza maandamano wakisaidiwa na wanamgambo wa Muungano wa Vyama vya Upinzani. Lakini serikali kwa kutoa amri ya kukomesha maaandamano, mnamo 8 Juni, watu 26 waliuliwa mjini Addis Ababa kwa msukosuko wa maandamano na wengine wengi kushikwa. Mnamo 5 Septemba 2005, Kamisheni ya Uchaguzi Ethiopia, ilitoa matokeo na kusema kwamba (EPRDF) kashinda uchaguzi na kwa hiyo iongoze serikali. Lakini vyama vya upinzani viliongezea viti bungeni kutoka 12 mpaka 176. Muungano wa umoja na demokrasia ulishinda viti vyote vya Addis Ababa, kwa Bunge la Taifa na Baraza la mtaala. Maandamano yalizuka tena mitaani 1 Novemba, ambapo vyama vya upinzani viliitisha mgomo kwa jumla na pia kwa Bunge mpya, wakatae matokeo ya uchaguzi. Polisi tena walijaribu kuzuia maandamano hayo na watu 42 wakafa kwa misukosuko mjini Addis Ababa. Polisi saba pia wakafa na mwingine pia kafa kutokana na majeruhi ya mlipuko wa bomu. Tope la watu walishikwa na kufungwa jela. Februari 2006 watu elfu sita bado walikuwa jela wakingoja hukumu Machi. Mnamo 14 Novemba, Bunge la Ethiopia lilipitisha mkataba kuimarisha Kamisheni huru na kuchunguza visa vya 8 Juni na tarehe 1 na tarehe 2 Novemba. Februari 2006 Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, alitamka kwamba, EPRDF kashinda kura, lakini angetaka kuona Ethipia ikitatua shida zake yenyewe na iendelee katika njia ya demokrasia. . Majimbo ya Kujitawala Ethiopia imegawiwa katika majimbo 9 ya mamlaka ya kikabila (kililoch; umoja: kilil), na maeneo 68. Afar Amhara Benishangul-Gumuz Gambela Harar Oromia Somali Jimbo la Makabila ya kusini Tigray Zaidi ya hayo kuna maeneo ya miji miwili (astedader akababiwoch; umoja: astedader akababi): Addis Ababa na Dire Dawa. Watu Idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa 113,656,596 (2022) ambao wanaongezeka kwa asilimia 2.88 kwa mwaka. Ethiopia ina makabila zaidi ya 80 yenye utamaduni tofautitofauti. Watu wengi huongea lugha za Kisemiti na lugha za Kikushi. Waoromo (34.49%), Waamhara (26.89%), Wasomali (6.20%) na Watigrinya (6.07%) ni zaidi ya 73% ya wananchi wote. Kumbe kuna makabila mengine yenye watu wachache kiasi kama 10,000. Lugha Ethiopia ina lugha 84 za kienyeji (angalia Orodha ya Lugha za Ethiopia). Mifano fulani ni kama ifuatavyo: Kiingereza ndiyo lugha ya kigeni inayoongelewa zaidi na kufunzwa katika shule ya upili. Kiamhara ilikuwa lugha ya ufundishaji katika shule ya msingi lakini sasa sehemu nyingi nafasi yake imeshikwa na Kioromo na Kitigrinya. Dini Wakristo, ambao ndio wengi (67.3%, kati yao Waorthodoksi wa mashariki 43.8%), wanaishi hasa kwenye milima, na Waislamu (31.3%) na Wapagani (0.6%) wengi wanaishi kwenye mabonde. Ukristo Ufalme wa Aksum ulikuwa milki na nchi ya kwanza kukubali Ukristo, ambapo askofu Frumentius wa Taya, aliyetumwa na Atanasi wa Aleksandria kuiinjilisha nchi, alimuongoa Ezana wa Aksum katika karne ya 4. Kwa hiyo Wahabeshi wakampa jina Abba Selama. Kwa muda mfupi dini hiyo mpya ilienea kote. Labda Frumentius alifika tayari na wamonaki kama wamisionari. Lakini umonaki hasa ulianza mnamo mwaka 500 walipofika wamonaki tisa wenye asili ya Siria waliotokea Misri katika monasteri za Pakomi. Hivyo mpaka leo mtindo huo ndio unaotawala kati ya umati wa wamonaki wa Ethiopia, wakati wakaapweke ni wachache, ingawa hawajawahi kukosekana. Athari za Siria na Misri zinajitokeza katika mambo mengi. Wamonaki wanaishi katika vibanda vya binafsi wakikutana kwa sala tu. Wamonaki wanawake (kawaida ni wajane) wanaishi jirani na monasteri ya kiume wakiitegemea kiroho na kiuchumi. Uislamu Uislamu nchini Ethiopia unapatikana kutoka mwanzo wa dini hiyo; ambapo nabii Muhammad aliwaambia Waislamu waepuke kuuliwa Maka kwa kukimbilia Uhabeshi, ambayo ilitawaliwa na Mfalme Mkristu. Hata utamaduni wa Kiislamu wasema Bilal, mfuasi wa Nabii Muhammad, alikuwa ametokea Ethiopia. Uyahudi Wayahudi, ambao wanaitwa Beta Israeli a Wafalasha, walioishi Ethiopia tangu karne nyingi, wengi wao wamehamia Israeli hasa katika karne ya 20. Dini za jadi Mbali na dini hizo za kimataifa, kuna wafuasi wa dini za jadi za Kiafrika. Utamaduni Mnamo Aprili 2005, Mnara wa Aksum, mojawapo ya dafina za kidini Ethiopia, ulirudishwa na Waitalia ambao waliunyakua mwaka 1937 na kuupeleka Roma. Italia ikakubali kuurudisha mnamo 1947 kulingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ethiopia ndiyo Nyumba ya kiroho ya Mwendo wa Rastafari, ambao wanaamini Ethiopia ni Zion. Warastafari wamuona mfalme Haile Selassie I kama Yesu. Sikukuu Ona pia: Kalenda ya Waethiopia Uchumi Ethiopia imebaki nchi fukara mojawapo: Waethiopia wengi wanapewa chakula cha msaada kutoka ng’ambo. Baada ya mapinduzi ya mwaka 1974, uchumi wa Ethiopia ulikuwa uchumi wa kijamaa: amri ya uchumi iliwekwa na jimbo, na upande mkubwa wa uchumi uliwekwa kwa jamii, kutoka viwanda vyote vya kisasa, kilimo cha biashara, taasisi za kukopesha na mashamba yote na mali yote ya kukomboa. Kutoka kati ya 1991, uchumi ulianza kutolewa katika ujamaa na kuendekeza uchumi wa soko huria, serikali inasisitiza uchumi wa rasilimali ili kuzuia uvivu wa uchumi uliojitokeza wakati wa amri ya ujamaa. Mwaka 1993, Ubinafsishaji wa kampuni kaanza, viwanda, mabenki, ukulima, biashara za ndani na biashara za kimataifa. Kilimo ni karibu asilimia 41% ya mapato ya uchumi (GDP), ambayo ni asilimia 80 ya biashara ya kimataifa, na asilimia 80 ya wananchi wanategemea kilimo. Mambo mengi ya biashara hutegemea ukulima, wauzaji, viwanda vya kufunganya na kuuza nje mavuno ya ukulima. Mavuno yanayouzwa nje mengi yanatolewa na wakulima wa kiasi binafsi. Wanazalisha kahawa, nafaka (hasa maharagwe), mbegu za mafuta, viazi, miwa, na mboga. Biashara ya nje hasa ni ya kuuza mazao, kahawa ikiwa ndiyo inayoleta pesa nyingi za kigeni. Mifugo ya Ethiopia inaaminika kuwa ndiyo wengi zaidi Afrika. Mnamo 1987 ilihesabika kuwa asilimia 15 ya mapato ya uchumi yanatokana na mifugo. Michezo Ethiopia ni nchi mojawapo inayotoa wanariadha wazuri zaidi duniani, hasa kama wa mbio wa masafa ya kati na masafa marefu. Kenya na Morocco ni wapinzani wa Ethiopia kwa Michezo ya mabingwa wa Dunia na Olimpiki kwa masafa ya kati na marefu. Machi 2006, Waethiopia wawili walitamalaki mbio za masafa marefu, kwa jina wakiwa: Haile Gebreselassie (Bingwa wa Dunia na Olimpiki) aliyevunja rekodi ya kilometa 10 na sasa pia kilomita 20, NusuMarathoni, na rekodi ya kilomita 25, na kijana Kenenisa Bekele (bingwa wa dunia, mbio za majira (bara), na pia bingwa wa olimpiki), anayeshikilia Rekodi za Dunia za mita 5,000 na 10,000. Huko nyuma Ethiopia ilitoa mwanariadha maarufu katika historia ya mchezo huu duniani, Abebe Bikila. Tazama pia Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia Uislamu nchini Ethiopia Muziki wa Ethiopia Vyakula vya Ethiopia Orodha ya kampuni za Ethiopia Jeshi la Ethiopia Orodha ya Wafalme wa Ethiopia Hifadhi za Taifa Ethiopia Mawasiliano nchini Ethiopia Usafiri nchini Ethiopia Vyuo vikuu vya Ethiopia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Marejeo Deguefé, Taffara (2006). Minutes of an Ethiopian Century, Shama Books, Addis Ababa, ISBN 99944-0-003-7. Hugues Fontaine, Un Train en Afrique. African Train, Centre Français des Études Éthiopiennes / Shama Books. Édition bilingue français / anglais. Traduction : Yves-Marie Stranger. Postface : Jean-Christophe Belliard. Avec des photographies de Matthieu Germain Lambert et Pierre Javelot. Addis Abeba, 2012, ISBN 978-99944-867-1-7. English and French. Reprint, Trenton, NJ: Red Sea, 1995. ISBN 1-56902-009-4. Mauri, Arnaldo (2010). Monetary developments and decolonization in Ethiopia, Acta Universitatis Danubius Œconomica, VI, n. 1/2010, pp. 5–16. and WP Reprint, New York: Olive Branch, 2003. ISBN 1-902669-53-3. Murphy, Dervla (1968). In Ethiopia with a Mule. London: Century, 1984, cop. 1968. N.B.: An account of the author's travels in Ethiopia. 280 p., ill. with a b&w map. ISBN 0-7126-3044-9 Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2003). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 1: A-C. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag. Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2005). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 2: D-Ha. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag. Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2007). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 3: He-N. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag. Siegbert Uhlig & Alessandro Bausi, et al. (eds.) (2010). Encyclopaedia aethiopica, Vol. 4: O-X. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag. Alessandro Bausi & S. Uhlig, et al. (eds.) (2014). Encyclopaedia aethiopica'', Vol. 5: Y-Z and addenda, corrigenda, overview tables, maps and general index. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag. Viungo vya nje Serikali Balozi wa Ethiopia- Washington DC yakupa taarifa za serikali ya Ethiopia Idara ya mambo ya nje Ethiopia idara ya taarifa Ethiopia baraza la wafalme wa Ethiopia Wafalme wa Ethiopia Bunge ya Ethiopia Tovuti rasmi Habari Addis Tribune gazeti la kila wiki online edition allAfrica - Ethiopia news Ethiopian News Agency (ENA) hii ni idara ya serikali Nazret.com Ethiopian news portal Ethiopian Review Uptodate ethiopian news Helm Magazini sanaa, utamaduni, fasheni na heba kutoka Ethiopia Walta Information Center habari Masomo BBC Habari – Umbo wa: Ethiopia Ethiopian Treasures Dafina za Ethiopia- Historia, Utamaduni, Lugha, Dini - Ethiopia CIA - The World Factbook: Ukweli wa mambo kuhusu Duniani Guardian Unlimited - Special Report: Ethiopia 2000 /mktaba wa Congress ya marikani tareki nyingi ni kutoka Julai 1991 Maelekezo meetethiopia.com Portal that introduces and celebrates the rich history, culture and diversity of Ethiopia through the use of a repository that contains Ethiopia-related websites ranging from Arts, Society and Religion to Entertainment, Shopping and Technology Ethio Search Ethiopian on-line directory and search engine Open Directory Project - Ethiopia directory category Stanford University - Africa South of the Sahara: Ethiopia directory category The Index on Africa - Ethiopia directory category Utalii Ethiopian Tourism Commission government agency Lugha English-Amharic Dictionary based on Amsalu Aklilu and G. P. Mosback's dictionary Online Dictionary of the official language of Ethiopia Amharic Dictionary Mashirika ya msaada The Denan Project – inasaidia kihospitali watu wa Denan Mengineyo 4 Films about Ethiopia Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Pembe ya Afrika
2406
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yoweri%20Kaguta%20Museveni
Yoweri Kaguta Museveni
Yoweri Kaguta Museveni (* 1944 Ntungamo, Wilaya ya Ntungamo, Uganda) ni Rais wa Uganda tangu 29 Januari 1986. Alichukua madaraka baada ya kushinda vita vya msituni chini ya kundi la National Resistance Movement na kushinda katika chaguzi za urais za mwaka 1996, 2001 na 2006. Kwa muda mrefu, kabla ya kuwa rais wa Uganda, Museveni aliongoza vita vya msituni dhidi ya serikali za Idd Amin aliyetawala toka mwaka 1971-79, na serikali ya Milton Obote aliyekuwa madarakani mwaka 1980-85. Kutokana na mafanikio ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na kukubali kwake kufuata sera za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, Museveni alipata sifa kubwa toka kwa viongozi wa mataifa ya Magharibi. Mwishoni mwa miaka ya 1990, Museveni alikuwa akielezewa kuwa ni mfano bora wa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika. Hata hivyo uongozi wake umetiwa dosari na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda. Mambo mengine ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kisiasa unaofanywa na serikali yake dhidi ya wapinzani kama vile Kizza Besigye na kitendo cha kubadili katiba ya nchi hiyo ili aweze kugombea urais mwaka 2006. Alichagua Pico Taro (mwanamuziki wa Kijapani) kama balozi wa utalii wa Uganda mnamo Oktoba 6, 2017. Viungo vya nje Tovuti ya Ikulu ya Uganda Marais wa Uganda Watu wa Uganda
2439
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jeshi
Jeshi
Jeshi ni jumla ya watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya dola au kutekeleza maagizo ya serikali dhidi ya maadui wa nje. Neno linatumika hasa kwa kutaja jeshi la ardhi, jeshi la wanamaji na jeshi la anga. Kazi ya jeshi Kazi ya jeshi ni kulinda nchi dhidi ya maadui wa nje kutetea nchi dhidi ya mashambulizi kutoka nje au pia kushambulia nchi nyingine kama hatua hii imeamriwa na serikali halali. Kusudi hilo dhidi ya hatari ya nje ndiyo tofauti kuu na kazi ya polisi ambayo ni mkono mwingine wa serikali ya taifa wenye silaha. Hata hivyo kuna nchi ambako tofauti kati ya jeshi na polisi si wazi vile, hasa kuna nchi nyingi ambako jeshi limepewa wajibu wa ndani ya taifa au ambako wanajeshi walichukua mamlaka mikononi mwao kwa nguvu ya silaha. Katika nchi mbalimbali kuna vikosi vinavyotekeleza shughuli ndani ya taifa lakini vina silaha sawa na sehemu za jeshi na wakati mwingine vinahesabiwa kama sehemu ya jeshi. Kwa mfano vikosi vinavyolingana na FFU ya Tanzania vinaitwa gendarmerie huko Ufaransa na nchi nyingi za Afrika Magharibi au carabinieri huko Italia na kule vinahesabiwa kama mkono wa jeshi ingawa kazi yao ni ya ndani ya nchi. Hali ya jeshi vitani husimamiwa na sheria ya kimataifa ya vita jinsi ilivyoundwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa. Sheria hiyo inalenga kulinda raia wakati wa vita na pia haki za wanajeshi wakikamatwa na adui. Sheria inadai ya kwamba wanajeshi wote wanahitaji kuwa na sare rasmi inayoonekana na kuwatofautisha na raia kuwa chini ya mamlaka rasmi inayoeleweka na kuwajibika kwa serikali yao kubeba silaha zao wazi kutimiza masharti ya sheria ya kimataifa Wanajeshi wanafuata utaratibu huo wanalindwa na sheria inayokataza pia raia kubeba na kutumia silaha na kushiriki katika mapigano. Katika vita nyingi sheria ilipuuzwa lakini kuna mifano kadhaa katika karne ya 20 ambapo jinai za vitani zilifuatiliwa kwa mfano kwenye Kesi za Nuremberg kuhusu jinai za vitani upande wa Ujerumani na kesi zilizofikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai tangu mwaka 2000. Jeshi la ardhi Jeshi la ardhi lina kituo ama kambi ambayo kambi hii yaweza kulinda makundi ya Jeshi, divisheni ama umma wa jeshi. Kukitokea vita, Jeshi huwa wakipeleka divisheni na makundi ya kijeshi kwa vipimo kulingana na vita na mbinu za kusukuma ama kushinda adui kwa vita. Na pia ratili ya vita ikiwapendukia, Jeshi hupeleka wanajeshi pulikiza ili kusukuma adui kabisa ama kumshinda. Jeshi la taifa Jeshi la Taifa ni chombo kilichoanzishwa kisheria chenye silaha na askari wenye mafunzo ya kivita amabao kazi yao ni kupambana kivita kulinda ardhi ya nchi husika dhidi ya uvamizi kutoka nje. Nchi huwa na jeshi moja la kulinda mipaka yake dhidi ya uchokozi kutoka nje, lakini pia huwa na majeshi 'Usu' kadhaaa kwaajili ya kulinda usalaama wa ndani. kwa mfano; majeshi ya nchi ni kama Jeshi la Uganda (UPDF), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF). Majeshi Usu ni kama Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na TANAPA. Shughuli nyingi za majeshi hutofautiana kulingana na kitengo husika cha jeshi, kwa mfano jeshi la nchi kavu,Jeshi la Anga na Jeshi la Majini, haya ndiyo matawi makuu matatu ya jeshi . Kwa historia, Jeshi la anga lilikuwa pamoja na Jeshi la ardhini, hasa kwa historia ya Uchina ama Jeshi la ukombozi wa umma wa Uchina ilichanganya (jeshi la ardhi, jeshi la majini, jeshi la anga, divisheni za makombora na usayari) kwa tawi moja. Majeshi ya kisasa yaitwa pia huduma, ama askari watawala). Hii inaweza kuhusu pia matawi ya Vita: jeshi la nchi kavu, vifaru, makombora, na mhandisi wa jeshi, na pia Wasafirishaji wa matawi kama: mawasiliano, watambuzi, daktari, wapeleka vifaa, na Jeshi la ndege (tofauti na jeshi la anga). Shurutisho la jeshi Jeshi laweza kuwa kubwa kama chama, chama cha Jeshi (Shurutisho) ambalo lina makundi mengi zaidi ya askari. Jeshi tofauti hujigawa kulingana na utamaduni wao — hasa Marekani (Jeshi la kwanza la Marekani). Kwa Jeshi la Uingereza Jeshi kwa shurutisho ni "Jeshi la kwanza", na Marekani ni "divisheni ya kwanza". Jeshi Kikundi ama Jeshi kinara ni shurutisho kubwa zaidi kulingana na umma, utatuzi na ushirikana. Jeshi la Urusi wakati wa Muungano wa Sovieti lilikuwa limegawanywa kwa kundi za askari ambazo zilikuwa chini ya Jeshi shurutisho vitani. Lakini wakati wa amani kundi hizi zilikuwa chini ya tarafa ya Jeshi. Ona pia Vita Historia ya Jeshi Sayansi ya Jeshi Jeshi la umma Silaha
2440
https://sw.wikipedia.org/wiki/Elimuanga
Elimuanga
Elimuanga (pia: astronomia, kutoka maneno ya Kigiriki ἄστρον astron "nyota" na νόμος nomos "sheria") ni elimu juu ya magimba ya ulimwengu kama vile nyota, sayari, miezi, vimondo, nyotamkia, galaksi kuhusu nyendo zao, nafasi, umbali, ukubwa na sheria zinazotawala tabia zake. Elimuanga ni tofauti na unajimu ambayo si sayansi bali jaribio la kuona uhusiano kati ya nyota na tabia za wanadamu na pia kutabiri mambo yajayo. Hata hivyo vyanzo vya fani zote mbili zilikuwa karibu sana katika historia ya binadamu hadi kutokea kwa elimuanga ya kisayansi. Chanzo na historia ya elimuanga Elimu ya nyota nyakati za kale Tangu zamani watu waliangalia nyota wakajifunza kuzitofautisha. Mabaharia na wasafiri wakati wa usiku waliweza kutumia nyota kama vielekezi safarini. Walitazama pia mabadiliko ya kurudia kati ya nyota zinazoonekana angani wakati wa usiku. Wakaona mabadiliko haya ya jinsi nyota zinavyoonekana yaweza kuwa uhusiano na nyakati za mvua, baridi na joto, mavuno na ustawi wa mimea katika mwendo wa mwaka. Kutazama nyota vile kulikuwa msaada wa kupanga vipindi vya mwaka na kuunda kalenda. Watazamaji wa nyota walianza kutambua pia tofauti kati ya nyota mbalimbali, kwa mfano nyota zenye mahali palepale kila wakati na nyota chache za pekee zilizobadilisha mahali angani kwa utaratibu wa kurudia na hizi ziliitwa sayari, tena nyota nyingine zilizoonekana kwa muda tu zikibadilisha mahali pake angani zikaitwa vimondo. Kwa karne nyingi wataalamu katika sehemu mbalimbali za dunia walihisi ya kwamba nyota hizo zilikuwa miungu iliyoonekana kwa mbali sana. Katika vitabu vya dini vya kale kuna majadiliano juu ya tabia zao; wakati mitholojia ya mataifa mengi iliona nyota kuwa miungu, Biblia ilifundisha ni taa zilizowekwa angani na Mungu pekee aliye mwumbaji wa ulimwengu. Wataalamu wa kale katika nchi kama Uhindi au Ugiriki ya Kale walianza kutambua mwendo wa sayari na kuunda nadharia yuu ya uhusiano wa dunia, jua na sayari nyingine. Ndiyo chanzo cha imani ya kwamba nyota zinaweza kuwa na tabia fulani na athari juu ya maisha duniani na hasa kama mtu alizaliwa wakati nyota fulani ilionekana, basi tabia zilizoaminiwa kuwa za nyota ziliweza pia kuathiri maisha ya mtu huyo. Hapa kuna asili ya "kupiga falaki" na unajimu wa kisasa. Wakati uleule wataalamu hao walitazama nyota jinsi zilivyo, kuziorodhesha na kupiga hesabu za kalenda. Orodha ya kale iliyoendelea kutumiwa kwa zaidi ya miaka 1,000 ilikuwa ya Klaudio Ptolemaio kutoka Misri. Kupanuka kwa elimu tangu kupatikana kwa darubini na kamera Kwa macho matupu mtu mwenye afya ya macho anaweza kuona takriban nyota 6000 - 7000. Leo hii kuna zaidi za nyota 945,592,683 zilizoorodheshwa katika orodha za kimataifa. Katika karne ya 17 darubini za kwanza zilibuniwa Ulaya. Hivyo utazamaji wa nyota uliboreshwa na magimba ya angani mengi yalianza kuonekana. Galileo Galilei aliweza kuona miezi ya Mshtarii mwaka 1609 iliyokuwa haijajulikana hadi siku ile. Katika karne ya 19 kifaa cha kamera kilileta tena upanuzi wa elimu; upigaji picha uliwezesha uchunguzi wa picha za nyota wakati wowote. Kamera iliwezesha pia kuona nyota zisizoonekana kwa macho tu. Kuingiza mwanga kwenye kamera kwa masaa kunakusanya nuru hafifu na hivyo kuonyesha lakhi za nyota zisizoonekana kwa macho. Sehemu kubwa ya kazi ya wataalamu wa anga ilihama kutoka kwenye darubini kwenda deski ya mtafiti, siku hizi mbele ya kompyuta yenye data. Mitambo mipya Maendeleo ya tekinolojia yalileta mitambo mipya inayowezesha kupima mawimbi yasiyoonekana kwa macho kama vile Mawimbi ya infraredi Mwawimbi ya urujuanimno Mawimbi ya redio Magimba ya anga yanatoa kila aina ya mnururisho kwenye spektra. Vipimo hivi vilipanusha tena elimu tuliyo nayo kuhusu muundo wa ulimwengu. Mnururisho wa mandharinyuma (ing. cosmic background radiation) ulitambuliwa uliothibitisha nadharia kuhusu umri wa ulimwengu tangu mlipuko mkuu. Kuangalia nyota kwenye anga-nje Tangu mwanzo wa usafiri wa anga-nje wataalamu wa anga walipata nafasi ya kuangalia na kupima nyota nje ya athira ya angahewa ya Dunia (inayopunguza kiasi cha nuru inayoonekana) na nje ya ugasumaku wake. Tangu miaka ya 1970 satelaiti mbalimbali zilirishwa zinazobeba darubini za anga-nje. Utafiti wa nyota umepanuka hadi kupima miale ya eksirei na ya gamma inayozuiliwa na ugasumaku na angahewa. Maendeleo yamekuwa makubwa isipokuwa gharama zimekuwa pia kubwa za kuunda vifaa, kuvipeleka kwenye anga-nje halafu kuvitunza , hadi gharama za kupeleka watu huko juu kwa matengenezo. Kati ya darubini za anga-nje zilizokuwa mdhhuri sana ni Darubini ya Hubble. Pamoja na uwezo wa kompyuta wa kushughulikia idadi kubwa za data darubini za anga-nje zmeleta vipimo na data za nyota mamilioni. (itaendelea) Marejeo Viungo vya nje Namna Ya Kuelewa Nyota Za Mbinguni Tovuti ya Unawe Tanzania kwa ajili ya watoto na vijana wanaopenda habari za astronomia Astronomy in Tanzania - tovuti ya Dr. Noorali T. Jiwaji, Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam Astronomy site specifically designed for kids and their parents. Astronomy Picture of the Day Astronomy Around the World Astronomy with sections for beginners and younger people Video kuhusu elimuanga kwa kiswahili
2442
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayari
Sayari
Sayari (kwa Kiingereza planet) ni kiolwa kikubwa cha angani kinachozunguka jua (au nyota nyingine) na kung'aa kutokana na nuru ya jua iliyoakisiwa, tofauti na nyota na jua zinazong'aa peke yake. Kwa macho inaonekana kama nyota, lakini baada ya kuitazama kwa muda wa mwaka inaonekana inabadilisha mahali pake angani, tofauti na nyota kwa jumla. Tofauti kubwa kati ya sayari na nyota ni kwamba, nyota ukiitazama inametameta ila sayari haiwezi. Jina Jina la Kiswahili "sayari" lina asili yake katika neno la Kiarabu كوكب سيار kaukab sayar "nyota inayosogea" . Neno hilo la Kiarabu linalingana au ni tafsiri ya neno la Kigiriki πλανήτης planetes (lenye maana ya "yenye kusogea") ambalo ni asili ya jina "planet" kwa Kiingereza na lugha nyingine za Ulaya. Tangu zamani watazamaji wa anga katika tamaduni mbalimbali walitambua ya kwamba nyota kwa kawaida hukaa mahali pamoja lakini nyota chache zinabadilisha polepole mahali pake kati ya nyota nyingine zikifuata njia zinazorudia kila mwaka. Nyota hizo ziliitwa "nyota zinazosogea". Ufafanuzi wa sayari Zamani kulikuwa na sayari 5 tu zilizoonekana angani kwa macho matupu kama nyota zinazobadilisha mahali. Tangu kupatikana kwa mitambo kama darubini miaka 400 iliyopita idadi ya violwa angani vyenye miendo ya pekee imeongezeka sana lakini imeonekana pia kuna tofauti kubwa sana kati ya violwa hivi. Hivyo wataalamu wa Umoja wa kimataifa wa astronomia (IAU) walikubaliana mwaka 2006 kuhusu ufafanuzi wa sayari. Kiolwa cha angani kinahesabiwa kuwa sayari kama kinatimiza masharti matatu: (a) kama linazunguka jua kwenye obiti yake (b) kama masi na graviti yake zinatosha kufikia umbo linalofanana na tufe (c) kama ni kiolwa tawala cha obiti yake na hivyo limeondoa violwa vingine kwenye obiti kwa graviti yake. Ufafanuzi huo uliamuliwa kwa kura hata kama wanaastronomia wengine hawakukubali. Azimio hili liliondoa hadhi ya sayari kwa Pluto iliyowahi kutazamwa kuwa sayari katika miaka iliyopita. Wakati mwingine kuna violwa vingine ambavyo vinavyoitwa pia "sayari" ingawa havitoshelezi masharti yote matatu. Violwa vya angani katika mfumo wa jua letu yenye umbo la kufanana na tufe yasiyolingana na sharti c) huitwa "sayari kibete" - kwa mfano Pluto. Violwa vinavyozunguka nyota nyingine nje ya mfumo wa jua letu, kama yana masi ya kutosha, huitwa "sayari za nje" (ing. exoplanet). Hadi Mei 2016 kuna 2125 zilizotambuliwa . Violwa vyenye masi ya sayari ambazo si sehemu ya mfumo wa jua lolote lakini zinapita angani zinazoweza kuitwa sayari bila nyota (ing. wandering planets, starless planets, siku hizi zaitwa pia "planemo"). Majina ya sayari Kwa Kiswahili kuna tofauti kuhusu majina ya sayari kati ya vikundi viwili: sayari zinazoonekana kwa macho matupu ambazo ni Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohali. Hizi zilijulikana tangu kale na mabaharia hasa walizitumia kwa kukadiria njia wakiwa baharini mbali na bara. Majina haya yamepokelewa na Waswahili wa Kale kutoka kwa lugha ya Kiarabu pamoja na majina mengi ya nyota. Ila sayari ya pili yaani Zuhura ambayo ni sayari inayong'aa kuliko zote pia ina jina la Kibantu ambayo ni Ng'andu ("mwenye kung'aa). Kwa lugha za Ulaya kama Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani majina ya sayari za jua letu yanatokana na majina ya miungu ya Roma ya Kale au Ugiriki ya Kale. sayari zisizoonekana kwa macho kama Uranus na Neptun pamoja na sayari kibete (Pluto) zilitambuliwa tu bada ya kupatikana kwa mitambo ya darubini. Hatua hii ya kiteknolojia ilitokea Ulaya na hivyo wataalamu wa Ulaya waliendelea katika desturi ya kutumia majina yenye asili katika lugha za kale Kigiriki na Kilatini. Elimu ya sayari hizi za nje zilizokuwa geni kwa mataifa yote mengine ya dunia ilisambaa pamoja na majina ya Kiulaya na hivyo lugha nyingi zinatumia majina haya. Sayari za jua letu Jua letu lina sayari nane ambazo ni Utaridi (Mercury), Zuhura (pia: Ng'andu; Venus), Dunia yetu (Earth), Mirihi (Mars), Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturn), Uranusi na Neptuni. Toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006 Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari hivyo kufanya idadi ya sayari zinazojulikana kuwa tisa. Hata hivyo chama chenye mamlaka juu ya masuala ya sayari na nyota, Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kimetangaza rasmi kuwa Pluto si sayari na kuiita sayari kibete. Vitabu vingi vya shule vimebadilishwa kulingana na uamuzi huo, japo bado kuna vitabu ambavyo bado vinaonyesha Pluto kuwa sayari kweli. Sayari tano za Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohari huonekana kwa macho kama nyota angani. Lakini tangu zamani zilitambuliwa kuwa tofauti kwa sababu hazikai mahali palepale kama nyota ya kawaida bali huhamahama angani. Kutokana na tabia hii zimetazamwa mara nyingi kuwa na nguvu za pekee au hata kuwa miungu. Unajimu umetumia mwendo wa sayari zinazoonekana kwa macho kama msingi muhimu wa makadirio yao. Sayari nyingine katika mfumo wa jua zimetambuliwa tangu kutokea kwa astronomia ya kisayansi kwa darubini. Hizi ni Uranus na Neptun. Katika lugha ya Kiswahili sayari zinazoonekana kwa macho huwa na majina ya asili ya Kiarabu isipokuwa Zuhura ina jina la Kibantu la Ng'andu pamoja na jina la asili ya Kiarabu. Majina mengine ni ya asili ya Kilatini. Jumla ya jua, sayari zote 8 pamoja na miezi yao, sayari kibete, vimondo, nyotamkia na asteroidi inaitwa mfumo wa jua. Aina za sayari Sayari za jua letu hutofautiana kwa ukubwa na muundo. Mshtarii (Jupiter) ni sayari kubwa na masi yake ni mara 318 masi ya dunia yetu. Sayari ndogo ni Utaridi na masi yake ni takriban nusu ya dunia. Kutokana na umbali tunatofautisha "sayari za ndani" kuanzia Utaridi (Mercury) hadi ukanda wa asteroidi, halafu "sayari za nje" kuanzia Mshtarii (Jupiter) hadi Uranus. Muundo wa sayari ni tofauti; kuna vikundi kulingana na mata inayojenga sayari: Sayari za mwamba: sayari hizi zina muundo unaofanana na dunia yetu; asilimia kubwa ya masi ni mwamba. Hizi ni sayari za ndani za mfumo wa jua letu. Zote ni ndogo kuliko sayari za nje. Sayari jitu za gesi: sayari hizi kama Mshtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn) ni kubwa na zimefanywa na hidrojeni na heli. Masi ya Mshtarii ni mara 318 ile ya dunia, Zohali mara 95. Ilhali sayari hizi ni baridi kutokana na umbali mkubwa na jua, hidrojeni inapatikana kwa kiasi kikubwa katika hali mango na kwenye sehemu za ndani hidrojeni ina tabia kama metali kutokana na shinikizo kubwa. Sayari jitu za barafu: hizi ni Uranus na Neptun. Ni kubwa kuliko dunia, lakini si kama sayari jitu za gesi; Uranus huwa na masi 14 za dunia, Neptun na masi 17 za dunia. Ganda la nje ni mchanganyiko wa hidrojeni na methani, na sehemu za ndani ni barafu ya maji na methani. Sayari nje ya mfumo wa jua letu Wataalamu wa astronomia wamegundua sayari-nje (ing. exoplanets) yaani sayari zilizoko nje ya mfumo wa Jua letu zinazozunguka nyota mbalimbali. Kutokana na umbali mkubwa na matatizo ya utazamaji kwa muda mrefu hakukuwa na uhakika kama nyota kuwa na sayari ni jambo la kawaida angani au kama sayari ni chache tu. Tangu 1995 kuwepo kwa sayari-nje kuliweza kukadiriwa kutokana na mabadiliko ya mwendo wa nyota kadhaa yaliyoweza kuelezwa tu kutokana na masi ya karibu inayobadilisha mwendo wa kawaida. Baada ya kuboreshwa kwa vifaa vipimo vya mabadiliko ya mng'aro vimeonyesha mipito ya sayari, maana wakati wa kupita kwa sayari kati ya nyota fulani na mtazamaji duniani sayari inafunika sehemu ya nyota yake, hivyo mng'aro wake unapungua. Kiasi cha mabadiliko ya mng'aro kinaruhusu kukadiria umbali wa sayari na nyota yake na ukubwa wake. Sayari-nje nyingi zimetambuliwa kwa kutumia mbinu huu. Kutokana na maendeleo ya darubini imewezekana tangu mwaka 2004 kutambua sayari-nje kadhaa moja kwa moja lakini idadi yao hadi sasa ni ndogo wa sababu ugunduzi ni vigumu. Hadi Aprili 2019 kuwepo kwa sayari-nje 4,048 kumethibitishwa na kati ya hizi mifumo ya sayari 659 imetambuliwa ambako kuna zaidi ya sayari moja. Nyingi kati ya hizo zilikuwa na ukubwa kufanana na Mshtarii au kubwa zaidi. Lakini sayari ndogo zaidi zimetambuliwa pia. Marejeo Viungo vya nje Tovuti ya International Astronomical Union http://www.bbc.com/news/science-environment-33462184
2443
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyota
Nyota
Nyota kwa mang'amuzi na lugha ya kawaida ni nuru ndogo zinazoonekana angani wakati wa usiku. Nyota ni magimba makubwa Hali halisi nyota ni vitu sawa na Jua letu ambalo ni nyota mojawapo. Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisayansi imegunduliwa ya kwamba ni magimba makubwa sana katika anga-nje yanayong'aa kwa sababu yanatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za mnururisho kutokana na myeyungano wa kinyukilia ndani yake. Lakini ziko mbali sana na kwa hiyo tunaziona kama nukta ndogo za nuru. Kwa jumla nyota zinaonekana kwenye anga kwa mpangilio usiobadilika, na kila nyota huwa na mahali pake pasipobadilika kati ya nyota nyingine, hata kama nyota kwa jumla zinazunguka angani juu yetu kila siku. Leo tunajua ya kwamba nyota zote huwa na mwendo kwenye anga lakini mabadiliko haya hutokea polepole hayaonekani katika muda wa maisha ya binadamu. Lakini tunajua kutokana na habari za kihistoria ya kwamba mabadiliko yapo. Tofauti kati ya nyota zinazoonekana kwa macho Nyota nyingi ni magimba kama jua letu maana masi kubwa ya gesi na utegili wenye hali ya joto kali, ya sentigredi elfu kadhaa. Zinaonekana ndogo kwa sababu ya umbali wao. Galaksi: Nyota tatu zinaonekana kwa macho matupu si gimba moja tu bali kundi la nyota milioni au hata bilioni kadhaa; kutokana na umbali mkubwa zinaonekana kama nukta moja ya nuru. Hizi ni galaksi ya Andromeda na mawingu mawili ya Magellan. Makundi makubwa ya nyota yanaitwa fungunyota kama idadi ya nyota iko chini ya milioni au galaksi kama ni kundi kubwa zaidi linalojitegemea. Kwa darubini galaksi nyingi zimetambuliwa. Sayari: Kati ya nyota zinazoonekana kwa macho kuna chache zinazobadilisha polepole mahali angani kati ya nyota nyingine. Zikihama zinafuata mwendo maalumu unaorudia kila mwaka. Nyota hizi zinaitwa sayari. Tangu kupatikana kwa darubini tunajua ya kwamba sayari ni gimba mango kubwa kama dunia yetu lenye umbo la tufe linalozunguka jua kwenye anga ya ulimwengu. Kwa macho haiwezekani kutofautisha mara moja sayari na nyota nyingine. Kwa hiyo katika lugha ya kila siku sayari huitwa mara nyingi "nyota" ikionekana kwa macho. Lakini tangu milenia nyingi wataalamu waliotazama anga walijua kuna tofauti. Tangu miaka kadhaa inajulikana kuna sayari nyingi hata nje ya mfumo wa jua letu lakini hizi hazionekani kwa macho wala kwa darubini za kawaida. Zinaitwa sayari za nje (kwa Kiingereza exoplanets) Nyotamkia (comets): Mara kwa mara zinatokea nyota mpya ambazo hazikuonekana siku kadhaa zilizopita. Hazikai mahali palepale angani lakini zina mwendo wa kila siku kati ya nyota nyingine hadi kupotea tena. Zikionekana kubwa huonyesha nuru ya pembeni kama mkia, kwa hiyo huitwa nyotamkia au kometi. Hali halisi ni magimba mango yasiyo makubwa sana yanayozunguka jua letu.Sehemu ya mata yao ni barafu inayoyeyuka zikikaribia Jua na hii ni asili ya "mkia" Jua letu ni nyota iliyo karibu na dunia yetu tunapoishi ambayo ni sayari yake. Inaonekana kubwa kushinda nyota zote kwa sababu ni karibu. Wingi wa nuru yake unaficha nyota nyingine wakati wa mchana. Imegunduliwa ya kuwa ni tufe kubwa sana yenye joto kali na kwa hiyo mada yake ni katika hali ya utegili yaani kama gesi ya joto sana. Kipenyo chake ni zaidi ya kilomita milioni 1.3 na umbali wake nasi ni takribani kilomita milioni 150. Kwa jumla karibu nyota zote tunazoona ni jua kama letu yaani magimba kubwa sana ya utegili wa joto. Jua letu ni kitovu cha mfumo wa jua pamoja na sayari, miezi yao, kometi na vumbi nyingi ambazo zinaizunguka. Elimu ya nyota Habari za nyota zinakusanywa na kufanyiwa utafiti na sayansi ya astronomia. Wanaastronomia wanatumia vifaa kama darubini kutazama nyota na kupima nuru yake. Kwa kutumia mbinu za sayansi ya fizikia inawezekana kutambua tabia nyingi za nyota ingawa ziko mbali sana. Tofauti na elimu ya unajimu ambao unatumia mbinu nyingi za kale, lakini haufuati utaratibu wa kisayansi, bali unajaribu kutabiri mambo yajayo kutokana na nyendo za nyota. Idadi ya nyota Nyota zinazoonekana kwa macho wakati wa usiku ni kama 6,000 lakini idadi yake hali halisi ni kubwa mara nyingi zaidi. Hakuna aliyeweza kuhesabu nyota zote; kuna makadirio ya kuwa idadi inaweza kufika 70,000,000,000,000,000,000,000. Galaksi na fungunyota Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kundi la namna hiyo huitwa galaksi. Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wa jua letu, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Tunaona sehemu za nyota zake angani zikionekana kama kanda ya kung'aa linalojulikana kwa jina "njia nyeupe". Kando ya galaksi kuna makundi madogo zaidi yenye nyota mia hadi lakhi kadhaa yanayoitwa fungunyota. Umbali kati ya nyota Kutokana na umbali mkubwa kati ya nyota na nyota umbali huo hautajwi kwa mita au kilomita jinsi ilivyo duniani. Wanaastronomia hutumia hapa vizio vya Mwakanuru na Parsek. Nyota jirani kabisa na jua letu inaitwa Alpha Centauri: umbali wake ni mwakanuru 4.2, maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi ifike kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyokuwa miaka minne iliyopita. Galaksi ya jirani inayoitwa Andromeda ina umbali wa mwakanuru milioni 2.5. Maana yake mwanga wake unahitaji miaka milioni mbili na nusu mpaka kuonekana kwetu au kwa lugha nyingine tunaona galaksi ya Andromeda jinsi ilivyokuwa miaka hiyo milioni mbili na nusu iliyopita. Umbali wa parsek 1 ni sawa na mwakanuru 3.26 au karibu kilomita trilioni 31 au mita 3.0857×1016. Maisha ya nyota Fizikia na astronomia zimegundua ya kwamba nyota hazidumu milele bali zina mwanzo na pia mwisho. Kutokana na tabia hii wataalamu mara nyingi huongea juu ya "maisha", "kuzaliwa" na "kufa" kwa nyota ingawa si viumbehai. Nyota zinaanza katika nebula au katika mawingu makubwa ya gesi kwenye anga ya ulimwengu. Kama wingu, ambalo sehemu kubwa yake ni hidrojeni, ni kubwa sana inaanza kujikaza kutokana na graviti yake. Katika muda wa miaka milioni 10-15 mkusanyiko huu unazidi kuvuta mata kwake na kuongeza graviti yake tena na kujikaza. Katika kitovu cha masi hii shinikizo na halijoto zinapanda. Kadiri gesi inavyojikaza, nguvu ya graviti ndani yake inaongezeka, na atomi zake zinaanza kugusana. Halijoto inazidi hadi kufikia kiwango ambako myeyungano wa kinyuklia (nuclear fusion) unaanza ambako hidrojeni inabadilika kuwa heliamu. Kipindi cha mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kinaendelea kwa miaka bilioni kadhaa hadi sehemu kubwa ya hidrojeni itakapokwisha. Hapo sehemu za nje za nyota hupoa na kupanuka; hali hii huitwa jitu jekundu (red giant) kwa sababu ya ukubwa na rangi yake. Majitu mekundu kadhaa huonekana kwa macho angani yaking'aa kwa nuru nyekundu. Kama masi ya nyota bado ni kubwa mmeyungano nyuklia unaendelea kuzaa elementi nzito zaidi kwa sababu sehemu ya heliamu inaendelea kujibadilisha kuwa elementi za juu zaidi. Inaaminiwa ya kwamba elementi zote ulimwenguni zilianzishwa ndani ya nyota. Mwishoni, kama masi haitoshi tena kuendeleza mmeyungano, mnururisho unapungua na masi inaweza kujikaza. Kutegemeana na ukubwa wa masi nyota inaweza kuingia upya katika mchakato wa myeyungano nyuklia kwa ghafla na kupasuka. Mabaki ya mlipuko huu yanakaa angani tu na mara nyingi huingia tena katika mwendo wa kuzaa nyota mpya; sehemu ndogo za masi hii huwa sayari. Kama masi imejikaza sana shimo jeusi (kwa Kiingereza: black hole) hutokea. Katika hali hii nguvu ya graviti ni kubwa mno: inashika hata nuru yenyewe ambayo haiwezi kutoka nje tena.
2444
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daniel%20Arap%20Moi
Daniel Arap Moi
Daniel Toroitich arap Moi (2 Septemba 1924 - 4 Februari 2020) alikuwa Rais wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002. Maisha na mwanzo wa siasa Moi alizaliwa Sacho, wilaya ya Baringo, Mkoa wa Bonde la Ufa, na alilelewa na mama yake Kimoi Chebii, kufuatia kuaga dunia mapema kwa baba yake. Baada ya kumaliza masomo ya chuo cha upili cha Tambach, aliweza kujiunga na chuo cha ualimu mjini Kapsabet. Alifanya kazi kama mwalimu kutoka mwaka 1946 hadi 1955. Mwaka wa 1955 Moi aliingia siasa akachaguliwa kwa kiti cha wanabaraza wa mkoa wa bonde la ufa. Mwaka wa 1960, Moi na Ronald Ngala waliunda chama cha KADU ambayo kwa Kiswahili ni Muungano wa Demokrasia ya Waafrika wa Kenya kilichoshindana na KANU iliyoongozwa na Jomo Kenyatta. Lengo la KADU, lilikuwa kuhifadhi maslahi ya makabila madogo kama Wakalenjin dhidi ya makabila makubwa kama Waluo na Wakikuyu, makabila ambayo yalikuwa zaidi upande wa chama cha KANU, Kenyatta mwenyewe akiwa Mkikuyu. KADU ilipendelea katiba ya majimbo ambapo mamlaka nyingi zingebaki kwenye ngazi za chini, na KANU ilipendelea mfumo wa serikali ya umoja ambapo mamlaka zingeunganishwa mikononi mwa serikali ya kitaifa. KANU ilipata kura nyingi katika uchaguzi kabla ya uhuru, hivyo serikali ya kikoloni ya Waingereza iliachana na katiba ya majimbo. Mwaka wa 1957, Moi alichaguliwa kwa baraza la Bonde la Ufa tena, na mwaka wa 1961 kwa baraza la bunge kwa kiti cha Baringo ya Kaskazini. Baadaye akawa Waziri wa Elimu mwaka wa 1960–1961, bado kabla ya uhuru wa Kenya. Makamu wa rais Baada ya Kenya kupata uhuru mnamo 12 Desemba 1963, Kenyatta alimsihi Moi ya kwamba KADU na KANU ziungane pamoja kumaliza ukoloni. Kwa hiyo Kenya ikawa nchi ya chama kimoja, ikiimarishwa na muungano wa wengi Wakĩkũyũ-Waluo. Moi, aliweza kupanda cheo na kuwa waziri wa mambo ya ndani mwaka 1964, hasa kwa umuhimu wake kuleta faraja za watu wa bonde la ufa na jumla KADU kwa serikali ya umoja wa Taifa. Baadaye aliweza kupanda cheo zaidi akawa Makamu wa Rais mnamo 1967. Kama kiongozi kutoka kabila dogo, alituliza makabila haya makubwa nchini Kenya. Lakini, Moi alipingwa na wanasiasa wa makabila makubwakubwa, hasa Wakikuyu na Waluo. Walijaribu kubadilisha katiba na kufuta kanuni iliyomfanya makamu wa rais kuchukua nafasi yake wakati rais anaaga dunia. Hata kwa uzee na afya yake Kenyatta kudhoofika, alipinga mipango hii; katiba ilibaki jinsi ilivyokuwa. Urais wa Moi Mzee Jomo Kenyatta alipoaga dunia tarehe 22 Agosti 1978, Moi alichukua kiapo na kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa na sifa nchini, kona zote. Alisafiri sehemu na maeneo yote Kenya, na basi wananchi wakampa faraja na hongera. Alipochukua kiapo kuwa Rais wa Kenya, alinena kwamba atafuata "nyayo" za Mzee Kenyatta, kwa maana ataendelea na sera za Kenyatta na umoja wa Harambee. Ijapokua wapinzani wake wa kisiasa, hasa kutoka makabila makubwa, walimwona Moi kama rais wa mpito tu, asiyeweza kukaa muda mrefu kwa sababu ametoka katika kabila dogo. Mnamo 1 Agosti 1982, kundi la askari wa jeshi la anga la Kenya, wakiongozwa na Hezekiah Ochuka, lilijaribu kumpindua Moi, lakini walikuta upinzani wa mikono mingine ya jeshi na polisi waliosimama upande wa rais na kushinda uasi (Ona uasi wa wanahewa wa Kenya 1982). Moi alichukua fursa hiyo kuwafukuza wapinzani wa kisiasa na kuimarisha nguvu yake. Alipunguza ushawishi wa wafuasi wa Kenyatta kwenye baraza la mawaziri kupitia uchunguzi wa muda mrefu. Uchunguzi huo ulionyesha kwamba wanasiasa kadhaa walikuwa wakishiriki katika uasi. Moi aliwasamehe lakini alifaulu kuwaonyesha kama wasaliti mbele ya jamii ya Kenya. Viongozi wa uasi huo, pamoja na Ochuka walihukumiwa kufa, na hii ilikuwa mara ya mwisho hukumu za mauti zilitekelezwa Kenya . Moi alipandisha ngazi wafuasi wake waaminifu, akabadilisha katiba kuifanya KANU iwe chama cha kisiasa pekee kinachoruhusiwa kisheria nchini. Wasomi wengi hawakukubali mabadiliko hayo walimoona mwelekeo wa kidikteta. Vyuo vikuu vilikuwa chanzo cha harakati ambazo zilitaka kuanzisha mageuzi ya kidemokrasia. Walakini, polisi jasusi iliingilia vikundi hivyo na wanaharakati wengi wa demokrasia walikwenda uhamishoni. Serikali ilipiga marufuku kufundishwa kwa Umarx katika vyuo vikuu vya Kenya. Harakati za siri zilizaliwa, kama vile Mwakenya na Pambana. Moi, alijulikana ng'ambo kama kiongozi anayeunga mkono Ulaya ya magharibi, kwa vita baridi kati ya Ukomunisti na Ukapitalisti. Kenya ilikuwa kwa Muandamano wa kutojiunga. Lakini serikali za Ulaya ya magharibi ziliona Kenya kama nchi inayopinga Ukomunisti na hivyo kambi ya nguvu kwao kushinda ukomunisti. Kwa hiyo Kenya ilipokea misaada kutoka nchi za kibepari zaidi ili kuzuia ujamaa uliotambakaa, Ethiopia, Somalia, Tanzania na pia Vita za Uganda. Kwa hiyo siasa za uhuru na haki za kibinadamu, hazikuwazisha Ulaya ya magharibi hata kidogo. Lakini, vita baridi vilipokwisha kwa kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, mambo hayo mapya yakatokea, mwandamano wa watu na wanasiasa kuitisha demokrasia ya vyama nyingi, wakiongozwa na Matiba na Oginga Odinga. Moi alianza kuonekana kama mdhalimu kwa sababu alianza kuwafunga jela wanamgambo wa kidemokrasia, na pia jela nyingine za kisiri ambazo watu waliteswa kwa kunanuliwa na swali. Ulaya ya Magharibi ikaacha kuipa Kenya usaidizi wa kigeni na kwa kazo pande zote ndani ya Kenya na ng'ambo, Moi kakubali kuruhusu Demokrasia ya vyama nyingi, ambapo Moi mwenyewe kaunga uchaguzi na kukampaini kwa nguvu zaidi kwa kupinga upinzani Kasarani mnamo Desemba 1991. Moi alishinda uchaguzi wa miaka 1992 na 1997, ambapo ulizidi kwa vita vya ukabila mkoa wa bonde la ufa. Moi aliweza kuwagawa watu wa upinzani kwa kukema ukabila, na vyama vya upinzani kupasuka kwa kambi za faraja za kabila. Pia inasemekana wizi wa kura, hasa mkoa wa bonde la ufa na Ukambani. Ufisadi serikalini Mwaka wa 1999 Intidhamu zisizohusika na serikali kama Amnesty na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa zilichapishwa kuonyesha haki za kibinadamu kwa wapizani wa siasa hazikutetewa Kenya Moi akiwa Rais. Jina la Moi lilitajwa kwa Ufisadi wa 'migodi' na uzuiaji wa ufisadi huo, ambapo serikali kwa sahihi za watu wachache ilisemekana imetoa pesa ya kununua na kuuza migodi ng'ambo kwa jina la kampuni bandia Goldenbarg ambapo Kamlesh Pattni, mfanyabiashara wa Kenya, alisemekana kuwa fisadi halisi kwa oparesheni za Goldenbarg na wanasiasa waliohusika. Ilisemekana kwamba Moi aliiona Goldenberg kama njia ya kupata pesa za kigeni nchini Kenya ambapo uchumi, utalii na usaidizi wa kigeni ulipokoma mwaka wa 1992. Hivyo goldenberg ilinunua na kuuza migodi iliyochomolewa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Aibu hii ya Goldenbarg ni gharama ya asilimia 10 ya utolezi wa uchumi mwaka mmoja. Pesa zilizolipwa Goldenbarg, zilikuwa zitolee kenya pesa za kigeni lakini kwa sababu ni mambo fisadi, basi waliopewa pesa hizo wakurudisha na basi serikali ya Mwai Kibaki ilijaribu kuchunguza kesi yenyewe zaidi. Kung'atuka Rais Moi, kazuiwa na katiba kwa Uchaguzi wa mwaka 2002. Wengi kwa faraja za Moi walisema katiba itekelezwe ili achaguliwe mara ya tatu, lakini Moi mwenyewe kawapinga na kutawa, na kumchagua Uhuru Kenyatta, mwana wa Rais wa kwanza, kama mwenyekiti kwa chama cha KANU. Raila Amollo Odinga kwa bidii, alikampainia Mwai Kibaki, ambaye alishinda urais kwa muungano wa NARC na Kukiriwa 29 Desemba 2002. Moi aliishi kwa utawa mjini Kapsabet, ambapo huduma zake za amani na usaidizi azifanyia kwa Chuo cha Moi Afrika. Wakenya wengi wamtambua Moi kwa hoja na vigelegele mahali popote aliposimama. Moi aliunga nchi ya umoja, ambayo inaunganisha makabila yote, juzi siku ya uchaguzi wa maono wa katiba mpya, Moi kaipinga katiba ambayo itagawa watu. Katiba mpya ilipokataliwa na watu, Kibaki kwa hadhara, yasemekana na magazeti kwamba kapanga mkutano na Moi kujadili njia ya kusonga mbele. Tazama pia Siasa ya Kenya Tanbihi Waliozaliwa 1924 Waliofariki 2020 Marais wa Kenya
2447
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kasi%20ya%20nuru
Kasi ya nuru
Kasi ya nuru (pia: kasi ya mwanga, kwa Kiingereza speed of light) ni kasi yake iliyopimwa hata imekubaliwa kuwa nuru inakwenda karibu kilomita laki tatu kwa sekunde moja katika ombwe. Kama nuru inapitia katika hewa kasi yake inapungua. Katika nadharia ya uhusianifu ya Albert Einstein kasi ya nuru inadhaniwa kuwa ileile wakati wowote, pia katika hali yoyote. Yaani kasi inabaki ileile hata kama nuru inatoka katika chombo chenye kasi yenyewe au kama mtazamaji ana mwendo wake mwenyewe. Katika nadharia hiyo hakuna mwendo wenye kasi kushinda nuru. Kasi ya nuru imekuwa kipimo cha msingi katika sayansi za fizikia na unajimu. Kasi hiyo haihusu nuru pekee inayoonekana na macho ya binadamu lakini pia kwa aina mbalimbali ya mnururisho kama mawimbi ya redio n.k. Tangu safari ya kwanza ya watu kufika juu ya mwezi chini ya Mradi wa Apollo wa NASA tabia ya nuru kuwa na kasi ilionekana kwa watazamaji wote. Kila safari kituo cha NASA katika mji wa Houston iliwaita wanaanga kwa redio: jibu lilichukua sekunde kadhaa hadi kufika kutokana na umbali wa kilomita lakhi tatu kati ya dunia na mwezi, hivyo mazungumzo yaliendelea kwa vituo vya kusubiri hadi sauti ilipofika na kurudi. Kama siku moja wanaanga watasafiri mbali zaidi, hadi Mirihi au Zohali ,muda huu utaongezeka kutokana na umbali na kasi ya nuru inayobaki ileile. Tanbihi Vipimo Fizikia
2449
https://sw.wikipedia.org/wiki/Galaksi
Galaksi
Galaksi (ing. galaxy) ni kundi la nyota nyingi zinazoshikamana pamoja katika anga ya ulimwengu kutokana na graviti yao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo. Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wetu wa jua, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya bilioni 300 (3·1011). Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kwa rangi yake kama njia nyeupe au "njia ya maziwa". Umbo lake linafanana na kisahani kikiwa na kipenyo cha miakanuru 100,000 na kikiwa na unene wa miakanuru 3,000. Kwenye kitovu cha galaksi graviti ni kubwa sana kiasa cha kwamba galaksi nyingi huaminiwa kuwa na shimo jeusi kituvoni. Galaksi zilizo karibu angani zinaitwa Mawingu ya Magellan ambayo ni galaksi mbili ndogo zilizopo kwenye umbali wa miakanuru 170,000 na 200,000. Galaksi kubwa ya jirani ni Andromeda na ina umbali wa miakanuru milioni 2.5. Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi zinazoweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana ni mabilioni. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani. Galaksi zinazojulikana zimepewa namba katika orodha ya kimataifa na wanasayansi wa astronomia. Galaksi kati yao hujumuika pia zikiathiriana kwa njia ya graviti yao na kuzunguka kitovu cha graviti cha pamoja. Galaksi hadi 50 zinazoshikamana katika kipenyo cha miakanuru milioni 10 huitwa kundi la galaksi (ing. galaxy group). Kuna pia galaksi mamia hadi maelfu kadhaa zinazoshikamana na hii huitwa fundo la galaksi (ing. galaxy cluster) linaweza kuwa na kipenyo cha miakanuru milioni 10 - 20. Marejeo galaksi
2450
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moshi%20William
Moshi William
TX Moshi William (jina halisi: Shaban Ally Mhoja Kishiwa) alikuwa mmoja wa wanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini Tanzania aliyeweza kurekodi albamu 13. Alizaliwa Tanga mwaka 1958 na kufariki dunia 29 Machi 2006 na kuacha mke mmoja na watoto wanne. Kwa miaka mitatu mfululizo (2003, 2004, 2005) Moshi William alitunukiwa tuzo ya kitaifa ya utunzi bora. Moshi William alijiunga na bendi kongwe nchini Tanzania Juwata Jazz Band mwaka 1982 akitokea Bendi ya Polisi Jazz. Mwanamuziki huyo alijipatia umarufu mkubwa kwa kutunga nyimbo zilizokuWa na mafunzo katika jamii: mfano wa nyimbo kama Ashibae, Mwaka wa Watoto, Msafiri Kakiri, Asha Mwanaseifu, Kaza Moyo, Ajuza, Ndoa Ndoano, Mwanamkiwa, AjaLi, Nyongo Mkaa na Ini, Isihaka Kibene, Harusi ya Kibene, Piga Ua Talaka Utatoa na nyimbo nyingine nyingi. Ukipita mitaa ya Keko Machungwa jijini Dar es Salaam sehemu alikokuwa anaishi mwanamuziki huyu lazima utasikia moja ya nyimbo zake zikipigwa katika klabu mbalimbali au kwenye majumba ya wenyeji. Pia katika miji mbalimbali ya Afrika Mashariki na kati mwanamuziki huyu alifananishwa sana na mwanamuziki Madilu System wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na staili yake ya uimbaji katika Bendi ya Msondo Ngoma na mtoto wake Hassan Moshi William. Kifo cha mwanamuziki Moshi William kiliacha pengo kubwa sana katika Bendi ya Msondo Ngoma. Waliozaliwa 1958 Waliofariki 2006 Wanamuziki wa Tanzania
2452
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nyotamkia
Nyotamkia
Nyotamkia (kometi, pia nyota msafiri, shihabu, Kiing. comet) ni gimba dogo la angani linalozunguka Jua kwa njia ya duaradufu yenye sehemu kubwa mbali na Jua na sehemu ndogo karibu na Jua. Pale inapokaribia Jua inaotesha "mkia" unaoipa jina lake la "nyota yenye mkia". Mkia huu ni hasa mvuke unaong'aa kutokana na nuru inayoakisiwa. Mwili wa nyotamkia ni mchanganyiko wa mawe, vumbi na barafu. Nyotamkia hutokea katika sehemu za mbali za mfumo wa Jua, ng'ambo ya obiti ya Uranus, katika Wingu la Oort. Ukubwa hauzidi kipenyo cha kilomita kadhaa zikiwa na maumbo tofauti tofauti. Muda mwingi nyotamkia iko mbali na Jua pengine haionekani kwa darubini. Ikifuata njia ya mzunguko na kukaribia Jua kiasi cha kutosha inaanza kuonekana kama nyota ikiakisi nuru ya Jua. Ikikaribia Jua zaidi sehemu ya barafu yake inaanza kuyeyuka kuwa mvuke na mvuke huu ni kama angahewa ya muda. Sehemu nyingine ya mvuke huachana na nyotamkia yenyewe na kuonekana kama "mkia". Mkia huu unaelekea kila wakati upande usio wa Jua kwa sababu upepo wa Jua unasukuma mvuke upande ule. Kati ya nyotamkia ni chache tu zinazokaribia kiasi cha kutosha hadi zinaonekana kuwa na mkia kwa macho tu kwa muda wa wiki hadi miezi kadhaa. Zamani ziliaminiwa kuwa ishara kutoka mbinguni au kutoka kwa Mungu zikisababisha wasiwasi na hofu. Historia Kataka tamaduni nyingi za dunia Nyotamkia zilitazamiwa kama tukio nje ya utaratibu wa kawaida na hivyo kama ishara ya balaa fulani inayokaribia. Tangu karne ya 16 Nyotamkia zimetambuliwa kuwa magimba yanayorudi baada ya muda fulani. Mara ya kwanza nyotamkia ya Halley ilitambuliwa na Mwingereza Edmond Halley mwaka 1705 ya kuwa inarudi. Halley alitambua ya kwamba nyotamkia aliyoiona mwaka 1705 ilikuwa ileile iliyowahi kuonekana mwaka 1682. Alitabiri ya kwamba nyotamkia hii itaonekana tena mwaka 1759 ikawa hivyo. Nyotamkia hii iliyopewa jina la "Halley" imeendelea kurudi kila baada ya miaka 76. Wanahistoria waliweza kuthibitisha ya kwamba taarifa mbalimbali katika historia kuhusu nyotamkia tangu mwaka 240 BK ziliihusu "Halley". Ilipoonekana mwaka 1985/1986 nuru yake ilikuwa imepungua kulingana na ziara za awali kutokana na kupungua kwa maada yake iliyopotea katika "mkia". Leo kuna nyotamkia takriban 170 zilizothibitishwa ya kuwa zimerudi. Kuna pia nyotamkia chache zilizoonekana kwa darubini jinsi zilivyopasuka na kuisha wakati wa kupita karibu na Jua. Kutokana na habari hizo zote wataalamu hufikiri ya kwamba kuna nyotamkia nyingi katika mfumo wa Jua letu lakini idadi inaendelea kupungua polepole zikikwisha kutokana na kupungua kwa maada au kukaribia mno Jua au hata kugongana na magimba mengine. Haiwezekani kujua idadi kwa sababu muda wa kuzunguka Jua ambao ni sawa na muda wa kuonekana tena unaweza kuwa miaka mamia, hivyo nyingine hazikuonekana bado tangu mwanzo wa astronomia ya kisayansi. Maendeleo ya utafiti Tarehe 11 Novemba 2014 kifaa cha kutua(lander) ya chomboanga Rosetta ilitua juu ya nyotamkia Churyumov–Gerasimenko baada ya safari ya miaka 10 (zaidi ya kilometa bilioni 6). Ndiyo mara ya kwanza ya chombo kilichotengenezwa na binadamu kutua juu ya nyotamkia yoyote. Hatua hiyo itawezesha kuelewa zaidi hulka na historia ya ulimwengu. Tazama pia Nyotamkia zilizotembelewa na vyombo vya angani Tanbihi
2455
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dedan%20Kimathi
Dedan Kimathi
Kwa maana nyingine, tazama: Dedan Kimathi (kata). Dedan Kimathi (Thenge, tarafa ya Tetu, kaunti ya Nyeri, 31 Oktoba 1920 - 18 Februari 1957) alikuwa Mkenya aliyeongoza harakati za kundi la Mau Mau za kutwaa ardhi iliyokuwa iko mikononi mwa wakoloni toka Uingereza. Kimathi alihukumiwa na kunyongwa kutokana na harakati zake za kuikomboa nchi ya Kenya. Serikali ya wakoloni Waingereza ilimchukua Kimathi kama gaidi, lakini wananchi wengi wa kabila la Gikuyu walimchukua kama mpigania uhuru. Maisha ya mwanzo Alipofika miaka kumi na mitano, Kimathi alijiunga na shule ya msingi, Karuna-ini, ambapo aliweza kujifunza kiingereza halisi. Hii baadaye ilimsaidia kuandika kwa kiingereza kabla ya mnyanyuko na wakati wa mnyanyuko wa Mau mau. Akiwa shuleni alijiunga kwa chama cha ushauri. Alikua muumini wa dini na alibeba Bibilia kila wakati. Alifanyia kazi idara ya misitu kuokota begu za miti, ili aweze kujilipia gharama ya shule. Baadaye akajiunga na shule ya upili ya Tumutumu CSM, lakini akaacha shule kwa sababu ya kutolipa gharama ya shule. Kimathi alifanya kazi kadhaa lakini hakupata msimamo. Mojawapo ya kazi hizo alijiunga na jeshi na kutumwa kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka wa 1941. Lakini, mwaka wa 1944, alifukuzwa jeshi kwa sababu ya makosa kadhaa. Mnamo 1946, alijiandikisha kwa chama cha Muungano wa Waafrika Wakenya. Mnamo 1949, alianza kufunza shule alikosomea, lakini wakamfukuza kazi kwa sababu ya kulaumiwa amefanya ubakaji. La kuaminika ni kwamba alipigwa kalamu kwa makosa ya uchochezi. Maisha Kimathi aliweza kuvutia watu kwa kuonyesha bidii kwa kazi aina zote, alizoweza kufanya. Kimathi alianza siasa za upinduzi mwaka wa 1950. Alianza kuwa mfuasi wa Mau Mau, na baadaye kupanda cheo na kuweza kuwapa wajiunga wapya kiapo cha Mau Mau na kwa hivyo akawa gaidi kulingana na Waingereza. Alijiunga tena na Kikundi ya Arubaini, wakombozi wa Chama cha Kati cha Wakikuyu mwaka wa 1951. Alichaguliwa kama karani kwa chama cha KAU eneo la Ol' Kalou na eneo la Thomson Falls mwaka wa 1952. Alishikwa kwa mmda mwaka huo, lakini akatoroka kwa usaidizi wa polisi wa kijiji. Hii ilileta mwanzo wa Vita vya ukereketwa halisi. Kimathi aliunda baraza la ulinzi wa Kenya, ambayo ilitoa amri kwa wapiganaji wote msituni mwaka wa 1953. Mwaka wa 1956, alishikwa pamoja na bibi yake mmoja, Wambui. (hadithi nyingi za Kimathi zaeleza vile alivyopigwa risasi.) Alihukumiwa kifo na mahakama, na Jaji wa sheria Chifu Kenneth O'Connor, akiwa bado kitandani katika hospitali kuu ya Nyeri. Asubuhi na mapema mnamo 18 Februari 1957 alinyogwa na serikali ya wakoloni Waingereza. Urithi Kimathi alizikwa kwenye kaburi la umma mahali pasipojulikana katika gereza la Kamiti. Serikali ya Uingereza mpaka sasa inapinga maiti ya Kimathi ifukuliwe ili azikwe tena kirasmi, kwasababu wanasema alikuwa gaidi. Lakini Wakenya wengi wamchukulia kuwa Shujaa wa Taifa. Jina la Kimathi linakumbukwa nchini Kenya hasa kutokana na mitaa ya miji, majengo mengi na pia barabara ambazo zimeitwa kwa jina lake. Mchezo wa Kuigiza wa "Mzalendo Kimathi" ama kwa kiingereza The Trial of Dedan Kimathi umeandikwa na Ngugi wa Thiong'o (ndugu wa shujaa wa Mau Mau) akishirikiana na Micere Mugo na mchezo huo unaeleza kisa cha Kimathi. Viungo vya nje A conversation with insurgents who had fought alongside Dedan Kimathi Daily Nation gives his background Kimathi's life Dedan Kimathi's background (article in the middle of the page) Some observations Another interesting article A brief discussion of the uprising A paper that may open up new leads for those who want to research further Waliozaliwa 1920 Waliofariki 1957 Wanaharakati wa Kenya
2456
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi%20simulizi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama kwenye fasihi andishi) kama njia kuu ya kufikisha ujumbe. Ni sehemu ya msingi ya utamaduni na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla. Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo Kwa mdomo na kihifadhiwa katika maandishi kwa mfano: utenzi, ngano au nyimbo za jadi. Hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi. Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Lakini mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake hayaendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi. Sifa za fasihi simulizi Fasihi simulizi ina sifa za kipekee ambazo huipambanua na fasihi andishi. Sifa hizo ndizo huipa uhai fasihi hii. Miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na: Utendaji wa fasihi simulizi hushirikisha utendaji wa fanani na hadhira moja kwa moja (ana-kwa-ana) Fanani kuwepo kwa fanani ambaye husimulia, huimba, hupiga makofi na kubadilisha miondoko na mitindo ya usimuliaji. Hadhira kuwepo kwa hadhira ambayo hushiriki kwa kuuliza maswali, kupiga makofi, kushangilia, kuimba, kuiga na kadhalika - kutegemea jinsi ambavyo fanani atawashirikisha. Fasihi simulizi huingiliana na mabadiliko ya kiwakati na kimazingira; baadhi ya tanzu au vipera vya fasihi simulizi vinaweza kuwa vimepitwa na wakati lakini bado vinaweza kubadilishwa na vikaafikiana na wakati mahususi. Fasihi simulizi ni mali ya jamii nzima, humilikiwa na kila mtu katika jamii. Sifa hii ndiyo huipa uwezo wa kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Fasihi simulizi huzaliwa, hukua na hata hufa. Kuzaliwa: fasihi simulizi huzaliwa kutokana na mambo yanayotokea katika jamii. Kukua: fasihi simulizi hukua kadri inavyojadili matatizo yanayojitokeza. Kufa: fasihi simulizi hufa kwa namna mbili. Hii ni kutokana na maendeleo ya mazingira ambayo hufuata mfumo wa jamii husika. Kwa mfano kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasihi inaweza kuhifadhiwa kwenye maandishi na kwenye kanda mbalimbali za kurekodi. Fasihi simulizi ina mandhari maalumu ya kutendea; ni sehemu ambayo imetengwa rasmi kwa ajili ya aina/kipera fulani cha fasihi simulizi. Mandhari hayo yanaweza kuwa porini, misituni, mtoni, pangoni, nyumbani na kadhalika. Fasihi simulizi ina sifa ya "kuwa na utegemezi".Utegemezi wa fasihi simulizi hutegemea zaidi sanaa za maonesho hasa sanaa za ghibu yaani muziki,kwa sababu,fasihi simulizi huchota uhai wake kutokana na vitendo na tabia za fanani,mahadhi na toni za kimuziki na vipengele vingine vya sanaa za maonesho. Tanzu na vipera vya fasihi simulizi Hadithi Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Ni masimulizi ambayo yanatumia lugha ya mjazo au nathari na mtiririko wake huwa mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi hutofautiana kutoka kitanzu/kipera kimoja hadi kingine. Kwa jumla zipo hadithi ambazo ni za kubuni na zingine za kihistoria. Baadhi ya vipera vya utanzu huu ni: Ngano Hizi ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika kuelezea au kuonya kuhusu maisha. Vijipera vya kipera hiki ni: Soga Ni hadithi ndogo ndogo zinazohusisha utani na ucheshi kwa kiasi fulani. Hizi ni hadithi ambazo hutambwa katika mtiririko wa matukio ambao huzua kicheko. Soga hudhamiria kuchekesha na pia kukejeli. Visakale Masimulizi ya kimapokeo juu ya wahenga au mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya chuku na historia. Kwa mfano hadithi za Liyongo. Mapisi Maelezo ya historia bila kutia mambo ya kubuni. Tarihi Hizi ni hadithi ambazo husimulia au zimejengwa kwenye matukio ya kihistoria. Inawezekana matukio yanayosimuliwa yakawa ya kweli, yaani yalipata kutokea kihistoria. Hadithi hizi hutokea zaidi katika maandishi. Visasili Ni utanzu unaofungamana na imani za dini na mizungu ya jamii. Hizi ni hadithi za kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe, na maana na shabaha ya maisha yao. Mara nyingi hadithi hizi huaminiwa kuwa ni kweli tupu, na hutumika kuelezea au kuhalalisha baadhi ya mila na madhehebu ya jamii inayohusika. Ushairi Huu ni utanzu wa fasihi simulizi unaowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya uimbaji au ughani badala ya usemaji wa kawaida. Katika utanzu huu kuna vipera viwili ambavyo ni nyimbo na maghani. Nyimbo Nyimbo ni kila kinachoimbwa. Kipera hiki kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa. Maghani Maghani ni istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa kwa kalima au maneno badala ya kuimbwa. Kipera hiki kina vijipera vitatu ambavyo ni maghani ya kawaida, sifo na maghani masimulizi. Maghani ya kawaida Hilo ni kundi ambalo tunaweza kuingiza fani mbalimbali za ushahiri simulizi kama vile ushairi wa mapenzi, siasa, maombolezo, kazi, dini ilimradi unaghanwa katika namna ya uwasilishwaji wake. Sifo Hizi ni tungo za kusifu ambazo husifu watu, wanyama na mimea. Baadhi ya sifo huwa zinakashifu au kukejeli. Sifo huwa na tanzu muhimu kama vile vivugo (majigambo), pembezi na tondozi. Semi Semi ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa zitumiazo picha na tamathali kuelezea maudhui yanayobeba maana au mafunzo muhimu kwa jamii. Kundi hili lina vipera au tanzu sita ambazo ni: Methali Vitendawili Nahau Misemo Mafumbo Mizungu Lakabu Methali Methali ni semi fupi fupi zenye mpangilio maalumu wa maneno ambazo huelezea kwa muhtasari mafunzo, mafumbo na mawazo mazito yaliyotokana na uzoefu wa kijamii. Mara nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamathali hasa sitiari na mafumbo. Methali nyingi huundwa na vipande viwili vya maneno vyenye fikra yurani. Kipande cha kwanza huashiria tendo au sharti na kipande cha pili huashiria matokeo ya tendo au sharti hilo. Au sehemu ya kwanza huanzisha wazo fulani, na sehemu ya pili hulikanusha au kulikamilisha wazo hilo. Kwa mfano; mwenda pole hajikwai, aliye juu mngoje chini. Mifano ya methali Mcheka kilema,hali hakija mfika. Kupotea njia, ndiko kujua njia. Mchelea mwana kulia, utalia wewe. Maana ya methali hutegemea muktadha au wakati maalumu katika jamii. Kazi za methali Methali zina kazi nyingi katika jamii yoyote ile kama vile: Kuionya jamii inayohusika au inayopewa methali hiyo. Kuishauri jamii inayopewa au kutamkiwa methali hiyo. Kuihiza jamii inayohusika. Kukejeli mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya jamii husika. Vitendawili Ni semi zilizofumbwa ambazo hutolewa kwa hadhira ili izifumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo, na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki, mbali na kuwachemsha bongo zao. Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali vilivyomo katika maumbile. Misimu Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya kutosha katika jamii huweza hatimaye kuingia katika kundi la methali za jamii hiyo. Mafumbo Ni semi za maonyo au mawaidha ambazo maana zake za ndani zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha na hadhira maalum, hivyo ni tofauti na methali au vitendawili ambavyo ni semi za kimapokeo. Lakabu Haya ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo. Majina haya huwa ni maneno au mafungu ya maneno yenye maana iliyofumbwa. Mara nyingi majina haya huwa ni sitiari. Baadhi ya majina haya humsifia mhusika, lakini mengine humkosoa au hata kumdhalilisha; Mifano: simba wa yuda- Hali Selassie, Baba wa taifa – Mwl Nyerere. Sanaa za maonyesho. Ni maonesho au maigizo ambayo hutumia watendaji na mazingira maalumu kwa kuiga tabia na matendo ya watu au viumbe wengine ili kuburudisha na kutoa ujumbe fulani kwa hadhira. Viungo vya nje blogu ya Eric Ndumbaro kuhusu Fasiki simulizi ya Kiafrika Fasihi
2458
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bujumbura
Bujumbura
Bujumbura, ni mji mkuu wa Burundi unaokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 300,000. Mji upo kaskazini mashariki mwa Ziwa Tanganyika, na ni mji mkubwa zaidi Burundi, kitovu cha mawasiliano na uchumi nchini humo. Bujumbura ni mji pekee Burundi ambao una bandari ya kupakia mali na bidhaa mbalimbali za kuuza nje, kama vile kahawa, pamba, ngozi na madini ya stani. Historia Bujumbura ilipanuka toka ilipokuwa kijiji kidogo kilichokuwa kambi ya Jeshi ya Wajerumani. Eneo hili lilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mwaka wa 1889. Lakini, baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Bujumbura ilichukuliwa na Ubeljiji ambapo Shirikisho la Mataifa ilisimamia Ruanda-Urundi. Jina la mji likabadilishwa kutoka Usumbura hadi Bujumbura. Burundi ilipopata uhuru, mwaka wa 1962. Bujumbura ni mji ambao umeshuhudia vita vya ukabila kati ya Wahutu na Watutsi kwa kung'ang'ania uongozi wa Burundi. Vivutio Katika mji huo kuna majengo ni yale ya kikoloni na pia kuna soko, uwanja wa taifa, msikiti mkubwa na Kanisa kuu. Pia kuna Jumba la Makumbusho ambalo linaitwa jumba la makumbusho ya maisha na jumba la makumbusho ya jiologia. Mambo mengine ya kuchangamsha ni kama Hifadhi ya Rusizi, na Kiamba hapo Mugere, ambapo panasemekana kwamba David Livingstone na Henry Stanley walikutana. (Lakini watu wengi wasema walikutana Ujiji), Kigoma, nchini Tanzania ambapo panasemekana ni mwanzo wa mto unaosemekana kuwa ndio mwanzo wa Mto Nile). Viungo vya nje Tovuti rasmi Miji Mikuu Afrika Ziwa Tanganyika Miji ya Burundi
2459
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maumau
Maumau
Maumau lilikuwa kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakipinga utawala wa kikoloni wa Waingereza toka mwaka 1952 hadi 1960. Kundi lilianzishwa mwaka wa 1946, na viongozi wa hao mashujaa walikuwa Jomo Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga, Paul Ngei, Ronald Ngala, Harry Thuku na wengineo. Walifanya kazi nzuri sana, kwanza juu ya kuonyesha vile watu wanavyoweza kufika mbali wakiwa kitu kimoja. Kama haingekuwa kwa maungano hawangeweza kufanya chochote. Ingawa vuguvugu la Maumau halikuwa na mafanikio makubwa kijeshi, upinzani wao ulichangia sana katika kuharakisha upatikanaji wa uhuru wa Kenya mwaka 1963. Chanzo cha jina la kundi hili, Maumau, hakieleweki vyema. Kuna hali ya kutokukubaliana juu ya chanzo na maana ya jina lenyewe. Baadhi wanadai kuwa ni jina la vilima fulani huko Kenya, wengine wanaamini kuwa jina hilo lilitoka kwa walowezi wa Kiingereza lililokuwa na nia ya kudhalilisha kundi hilo. Wako pia wanaosema kuwa jina hilo ni kifupi cha: Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru. Sehemu kubwa ya kundi la Maumau iliundwa na watu wa kabila la Gikuyu huku kukiwa na baadhi ya wanachama toka Embu na Meru. Wagikuyu wenyewe hawakuwa wakiliita kundi hili Maumau bali "Muingi" (vuguvugu), "Muigwithania" (anayeunganisha), "Muma wa Uiguano" (kiapo cha umoja) au KCA (Kenya Central Association, chama kilichotangulia kupigania haki za Wakikuyu. Historia ya Kenya Ukoloni
2460
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bonde%20la%20Ufa
Bonde la Ufa
Bonde la Ufa kwenye fani ya jiolojia ni bonde ambalo limetokana na mwendo wa mabamba ya gandunia mahali yanapoachana. Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki ni mojawapo kati ya mabonde maarufu zaidi duniani. Mabonde ya ufa hutokana na mvutano wa tektoniki. Mwendo huu huleta utengano wa mabamba hayo. Bonde la ufa latokea kama mabamba ya gandunia huachana na kuacha nafasi. Mabonde ya ufa ni mahali ambako volkeno pamoja na matetemeko ya ardhi hujitokeza. Mabonde ya ufa makubwa kabisa yapo chini ya maji kwenye misingi ya bahari. Gandunia
2462
https://sw.wikipedia.org/wiki/Vita%20Kuu%20ya%20Dunia
Vita Kuu ya Dunia
Vita Kuu ya Dunia ni jina linalotumika kwa ajili ya vita inayohusu nchi nyingi katika sehemu mbalimbali za dunia badala ya eneo la nchi kadhaa pekee. Kwa kawaida vita mbili za karne ya 20 huitwa "Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia" (1914-1918) na "Vita Kuu ya Pili ya Dunia" (1939-1945). Jina hilo limepatikana tangu mwanzo wa karne ya 20 katika miaka kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ilipoonekana ya kwamba vita ikianzishwa itahusu sehemu kubwa ya dunia kutokana na mapatano kati ya mataifa makubwa ya Ulaya yaliyotawala nchi nyingi duniani chini ya mfumo wa ukoloni. Wanahistoria wengine hudai ya kwamba hali halisi vita kuu ya kwanza ilizohusu dunia yote ilikuwa vita ya miaka saba (1756-1763) kati ya Uingereza na madola ya Kijerumani ya Uprusi na Hannover dhidi ya Ufaransa, Urusi, Austria, Uswidi, Saksonia na Hispania. Mapigano yalitokea Ulaya, Amerika ya Kaskazini, Visiwa vya Karibi, India, Asia ya Mashariki, Afrika na baharini kote duniani. Viungo vya nje Historia ya Vita Kuu ya Kwanza (Kiingereza) Vita
2470
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kemia
Kemia
Kemia (labda jina limetokana na neno la Kiarabu al-kemia) ni sayansi ya mata kwa kiwango cha atomi. Kemia yahusu tabia ya elementi na viungo vya atomi, ni somo la kujua mabadiliko ya mata na uhusiano wa mata na mata ndogo tofauti, na pia huhusika wa nishati. Kimsingi kemia ni somo la atomi na mkusanyo wa atomi kwa molekyuli, bilauri ama madini ambavyo vinajenga mata za kawaida. Kulingana na kemia ya kisasa ni ujenzi wa mata kwa kiwango cha atomi. Utangulizi Kemia wakati mwingine yasemekana kuwa somo la sayansi la kati, kwa sababu inaunganisha sayansi nyingine, kama vile fizikia, biolojia na jiologia. Kemia ina matawi mengi yaliyo maalumu kwa masomo na watalaamu wa matawi hayo, mahususi wa kemia, kwa mfano waruhusu utengenezaji wa vitu vipya, uoteshaji au uendelezaji wa madawa ili kutibu magonjwa, na kutambua umekanika wa harakati za maisha. Moja ya majawabu kwa kemia ni ati radhi imehusika. Kwa kemia radhi yaweza kuhusika na radhi nyingine, ama, ihusike radhi na harakati za nishati. Uhusiano ambao unajulikana zaidi ni uhusiano wa kiini ama viini na viini vingine kwa jawabu ya kemikali ambapo kiini kimoja au viini za penduliwa kwa ainanyingine. Hii yahusu mnururishi wa samaku (kama kwa nuru ya kemia) Ambapo jawabu ya kemikali ya tokea kwa sababu ya papo ya nuru. Jawabu za kemikali ni masomo mengine ya tawi ya kemia mbapo ya stadi radhi kwa mifano mingine. Kemikali ya Kispektroskopi kwa mfano wa stadi uhusiano wa nuru na radhi, bila jawabu lolote kutokea. Wanasayansi ambao wanadumisha sayansi hii wanaitwa wanakemia. Kulingana nao radhi zote zina viungo vya atomi ama radhi ndogo zaidi zinazounda atomi. Atomi zaweza kuungana na kutoa radhi kubwa kama ioni, molekyuli ama bilauri. Mjengo wa Dunia ambao tumeuzoea na mitambo ya radhi tumezoea zahakikishwa na jawabu ya viini vya kemikali na uhusiano wa jawabu hizi. Chuma cha pua ni chuma ngumu kwa sababu atomi zake zimeshikana pamoja kwa mshono wa bilauri. Mbao huchomeka kwa sababu ya jawabu pesi ya oksijeni kwa jawabu za kemikali kwa kiwango fulani cha joto. Maji ni kiowevu kwa joto inayodumisha maisha kwa sababu, molekyuli za maji zasonga zaidi kuliko mango ya barafu, lakini kidogo kwa mvuke. Binadamu au mnyama yeyote aweza kuona kwa sababu ya uhusiano wa nuru na molekyuli za unyama nyuma ya macho. Kwa hili eneo kubwa la masomo, ni vigumu sana kuhekima kila stadi kwa kemia na kuhtasari stadi yote kwa jumla. Hata kwa wataalamu zaidi wa kemia, wengi ujuzi wao umetia maanani kwa stadi kadhaa walizotia maanani zaidi kwa masomo yao. Kemia ina matawi mengi sana, yanayoitwa tawi za kemia, ambazo wanakemia watia makini. Kemia ambao hufunzwa kwa shule ya upili na miaka ya kwanza ya chuo kikuu, yenyewe huitwa kemia ya msingi ambayo huwapa wanafunzi masomo ya kemia kwa msingi ili kuimarisha masomo pana ya kemia, kulingana na tawi lolote la kemia mwanafunzi atakayofuata. Kwa kemia ya msingi, stadi yenyewe haimalizii kwa utaalamu lakini wataalam wengi hutumia masomo haya ya msingi wa kemia kueleza kazi yao kwa sababu jibu lenyewe ni ngumu zaidi kueleza kwa ujuzi ama jibu lenyewe ni laghai. Sayansi ya Kemia ni maendeleo ya kisasa kulingana na historia, lakini mizizi yake ni kutokana na alkemia ambayo ilikuwa desturi kwa milenia katika dunia nzima. Jina la kemia ni kutoka alkemia; lakini, etimologia ya alkemia haijavumbuka zaidi (ona alkemia). Historia ya Kemia Jina al-kemia yatoka katika Kiarabu al-kīmiyaˀ au al-khīmiyaˀ (الكيمياء or الخيمياء), kilichotanguliza al- kwa neno la Kigiriki χημεία, khemeia, ambalo linamaanisha "kuunganisha pamoja", "kumwaga pamoja", "kuchomelea", "aloi ya chuma", na kadhalika. Msingi wa kemia waweza kutokana na kuchoma. Moto ulikuwa nguvu ambayo iligeuza vitu kutoka ain amoja hadi nyingine, na hiyo ndiyo iliyoleta shauku ya binadamu. Ni moto ulioleta ufumbuzi wa chuma na glass. Baada ya migodi kugunduliwa na kuwa madini ya mali, watu wengi walitamani kugundua njia ya kupindua madini mengine kuwa migodi. Hii ilileta sayansi ya kujaribu ambayo iliitwa Alkemia. Wanaalkemia waligundua taratibu aina nyingi za kemikali ambazo zilileta maendeleo ya Kemia ya kisasa. Kemia kama vile twaijua leo iligunduliwa na Antoine Lavoisier ambaye alile sheria ya kuhifadhi uzito mwaka wa 1783. Ugunduzi wa radhi za Kemikali ina historia ndefu ya uedelezaji wa jedwali iliopagwa kwa ufumbuzi wa Dmitri Mendeleev. Tuzo ya Nobel ya Kemia ilioanzwa mwaka wa 1901, ina historia jema kuhusu uvumbuzi wa kemia miaka 100 iliopita. Utabiri wa Kemikali Utabiri wa kemikali ni utabiri unaoweza kuelezwa na kemia na unahusu viungo na nishati. Utabiri wa kemikali unahusika na mapenduzi ya tabia ya viini panapotokea majawabu ya kemikali. Moto ni mojawapo ya utabiri uliowahi kushangaza zaidi. Wanakemia wao hujaribu kutabiri mambo yote kuhusu Tabiri za kemikali zinazojulikana, na kugundua tabiri ambazo hazijajulikana na kuziweka kwa kundi ya jedwali kulingana na tabia ya viini vya kemikali. Mfano, Viini ambavyo zaitikia jawabu ya oksijeni, ilikutoa majibu kwa aina ya viini vingine, husemekana kwamba zime oksijeniwa; hata hivyo kundi ya kemikali za kali ama alkali za weza jawabu na kutuliza athari, utabiri ambao wajulikana kama utulizaji wa athari za kemikali. Viini vinaweza kua pia dhoofu ama ziendelee kujiunda kutoka viini vingine kwa njia ya jawabu aina nyingi. Jawabu za kemikali zinahusika na mapenduzi au uhifadhi wa bidii, utabiri huu wasomwa kwa stadi ya kemia inayoitwa, Kemikali ya SiyaraJoto/ kemia ya athari-joto. Na pia, viini vingine hutoa nuru bila kuashwa moto, utabiri huu waitwa fosfati nuru. Matawi ya Kemia Kemia imegawiwa katika matawi makuu kadhaa. Kuna pia matawi mengine ya kitaalamu ambayo yanahusika na kemia. Kemia ya Uchambuzi ni Uchambuzi wa vifaa, ili kuelewa Viini vya kemikali na ujenzi. Kemia ya Uchambuzi ya husu majaribio mbinu ilkanun za kemia. Hzi mbinu za weza kutumika kwa Kemia aina yeyote, lakini si kwa Kemia fasihi ya nadhari. Biokemia ni stadi ya Kemikali, jawabu za kemikali na uhusiano unaofanyika kwa vitu vilivyo hai vijumba. Biokemia na kemia ya mahuluku zi karibu na Kemia ya madawa. Kemia Si Mahuluku ni stadi ya tabia na jawabu za viungo vya kemikali mbazo siyo mahuluku. Tafauti ya kemia mahuluku na si mahuluku haijategwa zaidi makusudi, bado kuna mlinganisho hapa napale hasa kwa tawi ya Kemia ya mahuluku madini. Kemia ya mahuluku ni stadi ya muundo, tabia, viungo, umekaniki, na jawabu ya Viungo vya mahuluki. hasa, ni stadi ya viini vinavyo radhi ya kaboni. Kemia ya fizikia ni stadi ya asili ya kemikali, taratibu na mifumo ya kemikali. Bidii na siyara ya mifumo hii ya kemikali inavutia wana kemia ya fizikia. Eneo nyingine za stadi muhimu ni kama Kemikali ya siyarajoto, Kemikali ya mwendo wa bidii, kemia ya umeme, Umekaniki wa statistiki, na spektroskopi. Kemia ya fizikia inahusika sana na Fizikia ya molekyuli. Kemia ya fizikia inahusu matumizi ya hesabu za(kalikilasi) kwa kuonyesha milingano. Kemia ya nadhari ni ustadi wa kemia kwa kutumia fikira (hasa kwa kutumia Hesabu ama fizikia), ina fafanua tabia ya shenga au zikiwa chenga. Hasa kwa matumizi ya umakanika kwanta na kwa kemia yaitwa kemia kwanta. Kutoka mwisho wa vita vya pili vya Dunia, uendelezaji wa compyuta umeruhusu mfumo wa uendelezaji wa Kemia ya uanga na compyuta, ambayo ni usanifu wa kutengeneza na kutumia miradi ya kompyuta ili kutatua hesabu za kemicali. Kemia ya nadhari ya husika zaidi na fizikia ya molekyuli. Kemia ya Nuklia ni stadi ya vile viini vilivyo kwa atomi vinavyo jiunganisha pamoja na kujenga nuklia. Mageuzo ya radhi ni mambo ya kisasa na ni masomo makubwa ya kemia ya kinuklia, na jedwali la vinuklia ni matokeo muhimu na kifaa cha elimu hii. Elimu nyingine za Kemia ni kama Kemia ya Sayari, Kemia ya Anga, Uhandisi wa Kemikali, Kemia ya maarifa, Kemia ya umeme, Kemia ya mazingira, jeo-kemia, Kemia ya kijani kibichi, Historia ya Kemia, Sayansi ya Vifaa, Kemia ya Dawa, Biolojia ya molekyuli, Molekyuli za Jenetika, Technologia ya nukta, Kemia ya mahulukulu madini, Petrokemia, Famakolojia, Photochemistry, Kemia ya bidii za nuru na kemikali, Kemia ya polima, Kemia ya molekyuli jitu, Kemia ya Wajihi, na Kemia ya athari-joto. Kanuni za ujuzi Mifumo ya Kemia Mifumo ya kemia, ni taratibu zinazo husika kwa eneo hii kupea majina ya viungo vya kemikali. Kuna mifumo fumbuzi zaidi ya kupa majina kemikali zilizogudulika. Viungo mahuluku zapewa majina kulingana na mifumo ya mahuluku. viungo si mahuluku za pewa majina kulingana na mifumo ya si mahuluku. Atomi Atomi ni muungano wa radhi ambazo zimepata sitima ya kuunga kwa kiini (kwa nuklia ya atomi) ambayo ina protoni na niutroni, napia elektroni kadhaa ili kupima nguvu viini vilivyo na stima ya kuunga. Kiini Kiini ni atomi ambazo zina kiwango cha nambari za protoni na nuklia sawa. Hii nambari yaitwa namba ya atomi ya kiini. Kwa mfano, atomi zote zina 6 protoni kwa nuklia ni atomi za kiini cha kemikali caboni, na atomika zote zina 92 protoni kwa nuklia ni atomi za kiini cha urani. Maonyesho mazuri ya nambari za viini za kemikali ni jedwali, ambayo huweka viini vya kemikali ambazo zina tabia sawa ya kemikali pamoja. Orodha ya viini kwa jina, kwa ishara na kwa nambari ya atomi, na pia kwa kuongezea kuna orodha ya aisotope. Viungo Kiungo ni kifaa kilicho na hakiba tosha ya viini vya kemikaliambazo za zaleta viungo, an mpango wa kujiunganisha ambao unaleta tabia fulani ya kemikali. Mfano, maji ni kiungo ambacho kina viini vya hidrojeni na oksijeni kwa uwiano wa mbili kwa moja, na oksijeni kati ya hidrojeni, na kwa pembe ya 104.5° kati. Viungo vi na tengenezwa na kubomolewa kwa Jawabu ya kemikali Molekyuli Molekyuli ni kiungo asili kidogo zaidi kwa Viungo au kiini, ambacho hakiwezi kugauika mara nyingi, na kia tabia za kemikali. Molekyuli hasa yaweza kuwa na atomi mbili ama zaidi, zinazo kujiunga kikaza pamoja. Ioni Ioni ni kifaa kilicho na stima, ama atomi ama molekyuli ambayo imepoteza au kuongeza elektroni. Iliyoongeza yaitwa kationi (kama natiri kationi Na+) na iliyopoteza elektroni yaitwa anioni (kama klorini Cl-) ambazo zaweza kutulizana kama chumvi kwa kemikali (ni natiri ya kloroni NaCl). Mfano wa ioni za poliatomi ambazo hazigawani wakati wa Jawabu za kali-alkali ni kama haidroksaidi (OH-), ama fosfeti (PO43-). Kifaa Kifaa cha kemikali yaweza kuwa ni Kiini, Kiungo ama mchanganyiko wa Kiungo, Viini ama Viungo na viini. Radhi nyingi twaziona kilasiku kwa maisha yetu na mchanganyiko mwingine nikama anga, aloi, na radhi za biolojia na zaidi ya vitu vingine nyingi. Tazama pia Orodha ya elementi Mfumo radidia Tuzo ya Nobel ya Kemia Tanbihi Marejeo Marejeo mengine Kwa umati Atkins, P.W. Galileo's Finger (Oxford University Press) ISBN 0-19-860941-8 Atkins, P.W. Atkins' Molecules (Cambridge University Press) ISBN 0-521-82397-8 Kean, Sam. The Disappearing Spoon - and other true tales from the Periodic Table (Black Swan) London, 2010 ISBN 978-0-552-77750-6 Levi, Primo The Periodic Table (Penguin Books) [1975] translated from the Italian by Raymond Rosenthal (1984) ISBN 978-0-14-139944-7 Stwertka, A. A Guide to the Elements (Oxford University Press) ISBN 0-19-515027-9 Kwa wasomi wa wastani Atkins, P.W., Overton, T., Rourke, J., Weller, M. and Armstrong, F. Shriver and Atkins inorganic chemistry (4th edition) 2006 (Oxford University Press) ISBN 0-19-926463-5 Chang, Raymond. Chemistry 6th ed. Boston: James M. Smith, 1998. ISBN 0-07-115221-0. Voet and Voet Biochemistry (Wiley) ISBN 0-471-58651-X Kwa wasomi wa juu Atkins, P.W. Physical Chemistry (Oxford University Press) ISBN 0-19-879285-9 Atkins, P.W. et al. Molecular Quantum Mechanics (Oxford University Press) McWeeny, R. Coulson's Valence (Oxford Science Publications) ISBN 0-19-855144-4 Pauling, L. The Nature of the chemical bond (Cornell University Press) ISBN 0-8014-0333-2 Pauling, L., and Wilson, E. B. Introduction to Quantum Mechanics with Applications to Chemistry (Dover Publications) ISBN 0-486-64871-0 Smart and Moore Solid State Chemistry: An Introduction (Chapman and Hall) ISBN 0-412-40040-5 Stephenson, G. Mathematical Methods for Science Students (Longman) ISBN 0-582-44416-0 Viungo vya nje Jedwali la Elementi kwa Kiswahili kutoka Kamusi Hai : ndogo na kubwa MIT mafunzo wazi | kemia Wikidchem, hakiba ya kemia mbayo nibure Chemical Glossary Chemistry Information Database Chemistry Forum IUPAC Nomenclature Home Page, see especially the "Gold Book" containing definitions of standard chemical terms Experiments videos and photos of the techniques and results More experiments - lots of information about the elements too. Material safety data sheets for a variety of chemicals Material Safety Data Sheets Sayansi
2471
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hugh%20Masekela
Hugh Masekela
Hugh Masekela (amezaliwa 4 Aprili 1939) ni mpulizaji mashuhuri wa tarumbeta wa Muziki ya Jazz. Alizaliwa mji wa Wilbank, Afrika Kusini. Hugh Masekela anafahamika ulimwenguni kote kwa aina ya kupiga Jazz la mtindo wa Afri Jazz na hasa upulizaji wake wa tarumbeta; uongozi wa bendi ya muziki; tena kama mtunzi na mwandishi mahiri wa mashairi ya muziki. Masekela alijifunza kupuliza tarumbeta akiwa shuleni na mwalimu wake ni Padri Trevor Huddleston. Padri Trevor alikuwa ni mkuu wa shule yao Huddleston. Masekela alifanya ziara New York, Marekani ambako alikutana na msanii maarufu wa kimarekani Louis Armstrong na aliporudi Afrika Kusini alibeba tarumbeta alizopewa na Armstrong ambazo zilimzindua Masekela na kuanza kufahamika. Akiwa na umri wa miaka ishirini Masekela alikuwa akitumbuiza muziki ya aina tofauti, hasa ya Jazz; Bebop; Funk na Afrobeat wakati huo alikuwa na kundi la Jazz Epistles; kundi hilo lilikuwa na wasanii maarufu kama mpiga kinanda mahiri Abdillah Ibrahim. Mwaka 1960 Masekela alikwenda London, Uingereza ambako alijiunga na shule ya muziki ya Guildhall School of Music na baadaye alikwenda New York, Marekani ambako alisoma katika mji wa Manhattan. Mwaka 1962 alitoa albamu yake ya kwanza iitwayo Trumpet Africa. Miaka miwili baadaye alitoa nyingine iitwayo The Americanisation of Ooga Booga ambayo ilitamba mpaka kushika chati, hasa baada ya kupigwa na kituo kimoja cha radio cha mjini California. Mpaka kufikia Agosti 2000 alikuwa ameuza nakala milioni 50 na kumfanya apate tuzo ya Platinum. Hugh ameshirikiana na wasanii kama Miriam Makeba wa Afrika Kusini na Paul Simon wa Marekani kwenye albamu ya Graceland. Tarumbeta lake limesikika zaidi kwenye wimbo wa Gumboots na Diamonds on the soles of her shoes. Albamu Trumpet Africaine (Mercury 1963) Grrr (Mercury 1965) The Americanization of Ooga Booga (MGM 1966) Hugh Masekela's Next Album (MGM 1966) The Emancipation of Hugh Masekela (UNI 1966) The Lasting Impression of Hugh Masekela (MGM 1968) Hugh Masekela's Latest (UNI 1967) Hugh Masekela is Alive and Well at the Whiskey (UNI 1967) The Promise of a Future (Uni 1968) Masekela (Uni 1968) Reconstruction (Chisa 1970) Hugh Masekela & Union of South Africa (Chisa 1971) Home Is Where the Music Is (Chisa 1972) I Am Not Afraid (Chisa 1974) The Boy's Doin' It (Casablanca 1975) Colonial Man (Casablanca 1976) Melody Maker (Casablanca 1976) You Told Your Mama Not to Worry (Casablanca 1977) Live in Lesotho (Down South 1980) Home (Moonshine 1982) Techno Bush (Jive Afrika 1984) Waiting for the Rain (Jive/Arista 1985) BBC Radio I Live in Concert (Strange Fruit 1985) Tomorrow (Warner 1986) Sarafina! (Shanachie 1987) Uptownship (Novus 1989) In Concert - Vukani (BMG 1990) Beating' Around the Bush (Novus 1992) Homecoming Concert (Shanachie 1991) Hope (Triloka 1993) Notes of Life (Columbia 1995) Black to the Future (Sony Jazz 1997) The Best of Hugh Masekela on Novus (RCA 1999) Sixty (Sony Jazz 2000) Grazing in the Grass: The Best of Hugh Masekela (Sony 2000) Time (Sony Jazz 2001) Almost Like Being in Jazz (Straight Ahead 2004) Revival (Heads Up 2004) The Chisa Years: 1965-1975 (BBE 2006) Live at the Market Theatre (Four Quarters End 2006) The Best of Hugh Masekela (Jive 2007) Na Jazz Epistles Jazz Epistle: Verse 1 (Continental 1959) Na Herp Albert Herb Alpert/Hugh Masekela (Horizon 1978) Main Event Live (A&M 1978) Na wengine John Mehegan, Jazz in Africa (Continental 1959) King Kong: The Original Stage Cast (1959) The Long Road to Freedom: An Anthology of Black Music (Buddah) Miriam Makeba, The Many Voices of Miriam Makeba (Kapp 1962) Harry Belafonte, The Many Moods of Belafonte (RCA) Miriam Makeba, The World of Miriam Makeba (RCA 1963) Miriam Makeba, The Voice of Africa (RCA 1964) Miriam Makeba, Makeba Sings! (RCA 1965) Harry Belafonte na Miriam Makeba, An Evening with Belafonte/Makeba (RCA 1965) The Byrds, Younger Than Yesterday (Columbia 1966) The Monterey International Pop Festival Stu Gardner, To Soul with Love (Revue 1967) Johannesburg Street Band, Dancin' Through the Streets (UNI 1968) Letta Mbulu, Letta (Chisa 1970) Hedzoleh Soundz, Introducing Hedzoleh Soundz (Chisa 1973) When We Were Kings (DAS/Mercury 1974) Johnny Nash, Tears of My Pillow (CBS 1975) Randy Crawford, Everyhing Must Change (Warner Bros 1976) Lamont Dozier Dozier, Peddlin' Music on the Side (Warner Bros 1977) Miriam Makeba, Country Girl (Disques Esperance 1978) Ralph MacDonald, The Path (Marlin 1978) Eric Gale, Blue Horizon (Elektra Musician 1982) African Sounds for Mandela (Tsafrika 1983) Sakhile, New Life (Jive Afrika 1984) Barney Rachabane, Blow Barney Blow (Jive Afrika 1985) Jewel of the Nile (1985) Blancmange, Believe You Me (Sire 1985) Aswad, To the Top (Mango 1986) Manu Dibango, Afrijazzy (Enemy 1986) Artists Against Apartheid, Freedom Beat (Video Arts 1986) Kiki Dee, Angel Eyes (Columbia 1986) Paul Simon, The Graceland Concert (Warner 1987) Miriam Makeba, Sangoma (Warner Bros 1987) Hamiet Bluiett, Nali Kola (Soul Note 1987) Marc V., Too True (Elektra 1988) Ziggy Marley and the Melody Makers, Conscious Party (Virgin 1988) Mbongeni Ngema, Time to Unite (Mango 1988) Sarafina! The Music of Liberation (RCA 1988) Sipho Mabuse, Chant of the Marching (Virgin 1989) Dave Grusin, Migration (GRP 1989) Paul Simon, The Rhythm of the Saints (Warner Bros 1989) Jonathan Butler, Deliverance (Jive 1990) Miriam Makeba, Eyes on Tomorrow (Polydor 1991) 29th Street Saxophone Quartet, Underground (Antilles 1991) Ivan Lins, Awa Iyô (Reprise 1991) René McLean, In African Eyes (Triloka 1992) Cindy Lauper, Hat Full of Stars (Epic 1993) Sekunjalo - Now Is the Time - The Official ANC Album (Mango 1993) Tandie Klaasen, Together As One (HKM 1995) Mandela: Son of Africa, Father of a Nation (Mango 1995) Simply Red, Life (Eastwest 1995) Place of Hope (Warner Bros 1995) MarcAlex, Enjoy (Gallo 1995) Rebecca Malope, Live at the State Theater (CCP 1995) Hedzoleh Soundz, Wala (Alive) (Edzo 1996) Brenda Fassie, Brenda Fassie Live (VBREN1 1996) Stewart Sukuma, Afrikiti (Tropical Music 1998) Wendy Mseleku, Powerhouse (Columbia 1999) Smooth Africa (Heads Up 1999) Jazz Crusaders, Power of Our Music: The Endangered Red Species (Indigo Blue 1999) Themba Mkhize, Tales from the South (Sony Jazz 1999) Family Factor, Deliverance (Epic 1999) Sibongile Khumalo, Immortal Secrets (Columbia 2000) Orlando Cachaito Lopez, Cachaito (World Circuit/Nonesuch 2001) South Africa Freedom Day: Concert on the Square (Image Entertainment 2001) Umoja: The Spirit of Togetherness (Sting 2001) Brothers of Peace, Zabalaza: Project B (Kalawa-Jazmee 2001) Jimmy Dludlu, Afrocentric (Universal 2001) Prisca Molotsi, Where Are You Going? (Jigsaw 2001) Joy Denalane, Mamani (Four Music 2002) Tsepo Tshola, A New Dawn (Columbia 2002) Ten Minutes Older: The Trumpet (Colosseum 2002) Amdanla! A Revolution in Four-Part Harmony (ATO) Jeff Maluleke, Mambo: The Collection (CCP 2003) Busi Mhlongo, Freedom (Columbia Chissa 2003) Mafikizolo, Kwela (Kalawa-Jazmee 2003) Solidarity Forever: A Tribute to South African Workers by South African Artists (Gallo 2003) Andy Narell and Calypsociation, The Passage (Heads Up 2003) Enzo Avitabile na Botari, Save the World (Wrasse 2004) The Trio, My Pride, My Joy (Kisanji 2004) Poncho Sanchez, Do It! (Concord Picante 2004) Spikiri, Spikiri Featuring Hugh Masekela (Vega 2005) Tsepo Tshola, Winding Rivers and Waterfalls (Chissa/Heita 2005) Ladysmith Black Mambazo, Long Walk to Freedom (Heads Up 2005) Ngwako, Ramelodi (Chissa 2005) Corlea, Shades of the Rainbow (Chissa 2005) In for a Mez, Rocking the Cradle (Chissa 2005) The Bala Family, Genesis (Bala Brothers/Chissa 2006) Sam Bridges & the Levite Camp, Some Bridges (Concord 2006) Nathi, Soze (Chissa 2006) Keiko Matsui, Moyo (Shout Factory) Waliozaliwa 1939 Wanamuziki wa Afrika Kusini
2473
https://sw.wikipedia.org/wiki/Thomas%20Jefferson
Thomas Jefferson
Thomas Jefferson (2 Aprili 1743 – 4 Julai 1826) alikuwa Rais wa tatu wa Marekani kuanzia mwaka wa 1801 hadi 1809. Pia alikuwa mwandishi wa katiba ya Marekani aliyetumia nadharia ya John Locke na kupanga hoja za kupinga Marekani kuendelea kuwa chini ya mfumo wa utawala wa kifalme chini ya Uingereza. Viungo vya Nje White House biography Thomas Jefferson Papers: An Electronic Archive Thomas Jefferson collection The Papers of Thomas Jefferson Jefferson, Thomas, Summary View of the Rights of British America (1774), katika World Digital Library The Thomas Jefferson Hour The Papers of Thomas Jefferson Collection of Thomas Jefferson Manuscripts and Letters http://tjrs.monticello.org/letter/44 Waliozaliwa 1743 Waliofariki 1826 Marais wa Marekani Virginia (jimbo)
2474
https://sw.wikipedia.org/wiki/John%20Locke
John Locke
John Locke (29 Agosti 1632 – 28 Oktoba 1704) alikuwa mwanafalsafa Mwingereza aliyetoa nadharia ya "Mkataba Jamii": mkataba huu unahusisha watawala na watawaliwa ambapo watawaliwa huwapa watawala madaraka ya kuongoza kwa kufuata matakwa ya watawaliwa. Nadharia hii ilisaidia kwa kiwango kikubwa kujengwa kwa taifa la Marekani kutoka katika utawala wa Kifalme uliokuwa chini ya Uingereza. Waliozaliwa 1632 Waliofariki 1704 Wanafalsafa wa Uingereza
2479
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pasaka
Pasaka
Pasaka ni sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh). Pasaka ya Kiyahudi ni ukumbusho wa ukombozi wa Wanaisraeli kutoka Misri wakati wa Musa mnamo miaka ya 1200 KK. Pasaka ya Kikristo ni ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa kwake, mnamo Aprili 30. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo. Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kufa na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo limeendelea kutumika kwa ajili ya sherehe ya Kikristo. Tarehe ya Pasaka Pasaka ni sikukuu inayobadilika tarehe yake katika kalenda ya kawaida kila mwaka. Pasaka ya Kiyahudi inafuata kalenda ya Kiyahudi: ni tarehe 15 Nisan ambayo ni siku baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya sikusare ya machipuko (mnamo 21 Machi). Kwa kawaida Pasaka ya Kikristo, tangu karne ya 1 au karne ya 2 inaunganisha siku ya Jumapili (ni Jumapili kila mwaka kwa sababu ndiyo siku ya ufufuko katika mapokeo ya Kikristo) pamoja na kumbukumbu ya pasaka ya Kiyahudi. Tangu mtaguso wa kwanza wa Nikea Wakristo walipatana kusheherekea Pasaka kwenye Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu unaotokea baada ya sikusare ya tarehe 21 Machi. Kwa hiyo Pasaka inaweza kutokea kati ya 22 Machi hadi 25 Aprili. Tangu masahihisho ya kalenda ya Juliasi na kuanzishwa kwa kalenda ya Gregori mara nyingi kuna tofauti kati ya Pasaka ya Ukristo wa magharibi (sehemu kubwa ya Kanisa Katoliki na makanisa ya Uprotestanti) na Pasaka ya Ukristo wa mashariki kwa sababu Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda ya Juliasi kwa ajili ya kukadiria sikukuu zao. Majina ya Pasaka ya Kiyahudi na Pasaka ya Kikristo katika lugha mbalimbali Katika lugha nyingi, asili hii bado inaonekana, ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa maumbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya Kikristo. Viungo vya nje Liturujia 50 Catholic Prayers for Easter Liturgical Resources for Easter Holy Pascha: the Resurrection of Our Lord (Orthodox icon and synaxarion) Desturi Liturgical Meaning of Holy Week (Greek Orthodox Archdiocese of Australia) Easter in the Armenian Orthodox Church Roman Catholic view of Easter (from the Catholic Encyclopedia) Easter traditions from around the world Easter in Belarus: in pictures on the official website of the Republic of Belarus Hesabu A Perpetual Easter and Passover Calculator Julian and Gregorian Easter for any year plus other info Almanac – The Christian Year Julian or Gregorian Easter and associated festivals for any year Easter Dating Method for calculator Dates for Easter 1583 – 9999 Orthodox Paschal Calculator Julian Easter and associated festivals in Gregorian calendar 1583–4099 About the Greek Easter and Greek Easter calculator Orthodox Paschal calculator with technical discussion and full source code in javascript Sikukuu Kalenda Liturujia
2481
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pasaka%20ya%20Kikristo
Pasaka ya Kikristo
Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Pasaka, pia Pasaka ya Kiyahudi na Kipindi cha Pasaka Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ambayo Wakristo karibu wote hufanya kila mwaka ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake. Umuhimu wake Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika madhehebu mengi ya Ukristo, kwa sababu ufufuko huo ndio msingi wa imani ya Kikristo. Mtume Paulo aliandika kwamba Kristo asingefufuka, imani hiyo ingekuwa haina maana, kwa kuwa asingeondolea dhambi za watu. Pamoja na kifo cha Yesu, ndio kiini cha kanuni ya imani ya Wakristo wa kwanza kama alivyoipokea Paulo mwenyewe alipoongoka miaka sita baada ya matukio hayo. Katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho aliandika: 15:1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, 2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. 3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 5 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. 9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini. 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. 19Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. 20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. 28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote. Jina la Pasaka Jina la "Pasaka" limetokana na sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi linaloitwa "פסח" (tamka: pasakh) kwa lugha ya Kiebrania. Kinyume cha Kiingereza, ambacho kina maneno mawili, Passover na Easter, katika Kiswahili na lugha nyingine nyingi majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi hazitofautiani. Asili yake ni kwamba kusulibiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mnamo Aprili ya mwaka 30 BK. Wakristo wa kwanza, ambao wote walikuwa Wayahudi, walisheherekea sikukuu ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu ya ufufuko wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti, ingawa bila kwenda mbali sana. Badiliko kubwa zaidi lilikuwa lile la Wakristo kuadhimisha daima Pasaka siku ya Jumapili kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko, wakati Wayahudi wanadhimisha Pasaka kwa kuangalia tarehe, bila kujali ni siku ipi ya juma. Tarehe ya Pasaka </small> Tarehe ya Pasaka inafuata kuonekana kwa mwezi angani, kwa hiyo sikukuu hiyo haina tarehe imara katika kalenda ya kawaida. Inapatikana katika Machi au Aprili. Pasaka haifuati mwezi pekee lakini tarehe yake imefungwa pia kwa sikusare (au ekwinoksi), kwa hiyo haiendelei kuzunguka mwaka wote kama tarehe za Kalenda ya Kiislamu. Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325 uliamua ya kwamba Pasaka itasheherekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya 21 Machi (tarehe ya sikusare machipuo ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku, hivyo mwanzo wa majira ya kuchipua kaskazini mwa dunia). Kwa kuwa mwezi mpevu baada ya 21 Machi inaweza kutokea kati ya 22 Machi na 19 Aprili, tarehe ya Pasaka, ambayo ni Jumapili inayofuata, hutokea kati ya 22 Machi na 25 Aprili. Katika Ukristo kuna kalenda mbili zinazotumika, hivyo pia tarehe mbili za Pasaka. Kanisa la magharibi, yaani Wakatoliki wengi na Waprotestanti, hufuata Kalenda ya Gregori (ambayo imekuwa kalenda ya kawaida ya kimataifa), lakini Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda iliyotangulia, yaani Kalenda ya Juliasi. Ndiyo maana mara nyingi Pasaka inaendelea kuadhimishwa katika Jumapili tofauti kati ya pande hizo mbili. Hata hivyo kuna majadiliano yenye lengo la kufikia makubaliano ili kuadhimisha Pasaka pamoja. Kwa sasa tofauti ya kalenda inaleta Kanisa la Mashariki kusheherekea Pasaka wakati mwingine hata katika mwezi wa Mei wa kalenda ya Gregori, ingawa kwao bado ni Aprili kufuatana na kalenda ya Juliasi. Tanbihi Viungo vya nje Liturujia 50 Catholic Prayers for Easter Liturgical Resources for Easter Holy Pascha: The Resurrection of Our Lord (Orthodox icon and synaxarion) Mapokeo Liturgical Meaning of Holy Week (Greek Orthodox Archdiocese of Australia) Easter in the Armenian Orthodox Church Roman Catholic View of Easter (from the Catholic Encyclopedia) Easter in Belarus: In Pictures on the official website of the Republic of Belarus Polish Easter Traditions Hesabu A Perpetual Easter and Passover Calculator Julian and Gregorian Easter for any year plus other info Almanac—The Christian Year Julian or Gregorian Easter and associated festivals for any year Easter Dating Method for calculator Dates for Easter 1583–9999 Orthodox Paschal Calculator Julian Easter and associated festivals in Gregorian calendar 1583–4099 About the Greek Easter and Greek Easter Calculator Orthodox Paschal calculator with technical discussion and full source code in javascript Ukristo Kalenda Sikukuu za Ukristo
2485
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pasaka%20ya%20Kiyahudi
Pasaka ya Kiyahudi
Pasaka ya Kiyahudi (pia Passah au Pessah; Kiing. Passover) ni kati ya sikukuu muhimu zaidi za dini ya Uyahudi. Sikukuu hiyo inakumbuka Wanaisraeli walivyotoka katika utumwa walimokuwemo huko Misri. Pasaka ya Kiyahudi imekuwa na athira kubwa juu ya sherehe ya Pasaka ya Kikristo kuhusu tarehe, liturujia na desturi mbalimbali. Jina la Pasaka Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh) lenye maana ya "kupita juu, kukaa juu ya (kama mlinzi)" katika kitabu cha Biblia cha Kutoka 12:23. Humo imeandikwa ya kwamba Mungu "atapita" juu ya milango ya nyumba za Wanaisraeli huko Misri katika usiku kabla ya kutoka kwao, na kuzuia maovu ambayo Wamisri waliathiriwa nayo. Tarehe ya Pasaka ya Kiyahudi Pasaka ina tarehe kamili katika kalenda ya Kiyahudi: inaanza 15 Nisan na kusheherekewa kwa siku saba hadi 22 Nisan. Siku ya kwanza na ya mwisho ni sikukuu hasa. Katika nchi ya Israel siku hizi mbili ni siku za kupumzika kazi. Wayahudi wengine, hasa nje ya Israel, husheherekea siku 8. Kwa sababu kalenda ya Kiyahudi ni kalenda ya mwezi tarehe zake hubadilika katika hesabu ya kalenda ya Gregori yaani kalenda ya kawaida ya kimataifa. Kwa jumla Pasaka ya Kiyahudi inasheherekewa wakati wa miezi Machi au Aprili kwa sababu Nisan ni mwezi wa kwanza wa majira ya kuchipua. Asili ya Pasaka Katika Biblia, kitabu cha Kutoka, sura ya 12, kuna taarifa juu ya kutoka kwa Wayahudi katika Misri wakati wa Musa mnamo mwaka 1200 KK. Taarifa ni kwamba Musa alitumwa na Mungu kuwaondoa Wanaisraeli katika hali ya utumwa huko Misri na kuwaongoza kwenda nchi ya ahadi. Lakini mfalme wa Misri mwenye cheo cha Farao alikataa, hivyo Mungu alituma mapigo dhidi ya Misri ili Farao alazimishwe kukubali. Pigo la mwisho tena kali mno lilikuwa kifo cha kila aliyezaliwa kama mtoto wa kiume wa kwanza katika Misri. Hapo Wanaisraeli waliambiwa kuchinja mwanakondoo na kupaka damu yake milangoni kwao ili malaika akipita kuua watoto wa kwanza asiguse watoto wa Wanaisraeli. Baada ya pigo hilo Farao alikubali Wanaisraeli watoke. Tendo hilo la kuwaweka mababu yao huru linakumbukwa na Wayahudi kote duniani katika siku zinazoanza 15 Nisan. Sherehe ya Pasaka Sherehe ya Pasaka inaanza masaa ya jioni kabla ya siku yenyewe, kwa sababu katika kalenda ya Kiyahudi mwanzo wa siku si usiku kati wala macheo bali wakati wa machweo jioni inayotangulia. Maandalizi ya sikukuu ni pamoja na kufanya usafi mkubwa kabisa katika nyumba. Hakuna kitu kilichochachuka kinachobaki katika nyumba kufuatana na Kutoka 12:20, yaani kitu chochote chenye nafaka au unga wake ulioguswa na maji, hata punje yake kama vile mkate, keki au spagetti. Tendo hili ni la kukumbuka jinsi Wanaisraeli walipaswa kukimbia Misri haraka bila muda wa kutengeneza mikate ya kawaida yaliyochachuka. Kwa hiyo wanawake wao walioka mikate yasiyochachuka ambayo yamekuwa chakula cha Pasaka hadi leo. Mikate hii huitwa "matze". Familia na marafiki hukutana kwa chakula cha pekee wakizunguka meza ya Seder (seder = "utaratibu") yenye vyakula vya pekee. Kati ya vyakula hivyo, mboga chungu inakumbusha uchungu wa utumwa, matunda ya kupondwa yenye rangi ya kahawia-nyekundu yanakumbusha udongo wa matofali ambayo Wanaisraeli walipaswa kutengeneza, maji ya chumvi yanakumbusha machozi huko Misri, mayai ni ishara ya matumaini, na vingine. Vyote huliwa katika utaratibu (=seder) maalumu pamoja na masomo na sala kutoka vitabu vya Haggada vinavyoshikwa na wote mezani. Pasaka Pasaka
2486
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda%20ya%20Juliasi
Kalenda ya Juliasi
Kalenda ya Juliasi ni kalenda iliyoanzishwa katika Dola la Roma kwa amri ya Julius Caesar mnamo mwaka 46 KK Ilichukua nafasi ya kalenda ya Kirumi iliyotangulia. Kalenda ya Juliasi ilibadilishwa na kalenda ya Gregori kuanzia karne ya 16 BK lakini ilikuwa kalenda rasmi katika nchi mbalimbali kama Urusi hadi karne ya 20. Mpaka leo ni kalenda ya liturgia katika Kanisa la Kiorthodoksi. Matengenezo ya mwaka 46 KK Juliasi Kaisari alikuwa mtawala wa Kirumi aliyeamua kubadilisha kalenda ya kale iliyokuwa ya aina ya kalenda ya mwezi. Majira yalikosa tarehe kamili katika kalenda hiyo, hali iliyosababisha matatizo ya kiutawala, hasa kwa sababu tarehe ya malipo ya kodi ilitakiwa kuwa baada ya mavuno, wakati wakulima walipokuwa na uwezo wa kulipa. Hivyo Caesar alimwajiri mtaalamu Mmisri Sosigenes atunge kalenda mpya inayofuata mzunguko wa jua. Kalenda hiyo iliitwa kwa heshima yake Kalenda ya Juliasi. Ilikuwa na miezi 12 yenye siku 30 au 31 isipokuwa mmoja mfupi wenye siku 28 ambao ni mwezi wa Februari ili kukamilisha siku 365 za mzunguko wa kandokando ya jua. Vipindi hivyo viliendela kuitwa "mwezi/miezi" ingawa havikufuata tena mwendo wa mwezi wenyewe. Kwa sababu muda wa mwaka wa jua ulijulikana kuwa na siku 365 1/4, kila mwaka wa nne siku ya nyongeza iliingizwa kama siku ya 29 ya mwezi wa Februari. Mwaka 46 KK wenyewe ulirefushwa kwa ajili ya sahihisho lile ukawa na siku 445 ambao Warumi waliukumbuka kama "mwaka uliochanganyikiwa". Majina na hesabu ya miezi Sosigenes alitumia majina ya miezi ya kalenda ya kale yanayoendela kutumika hadi leo. Isipokuwa mwaka 44 KK baada ya kifo cha Caesar mwezi wa "Quintilis" ulipewa jina la marehemu ukaitwa "Julius" ndiyo Julai kwa Kiswahili. Mtawala mkubwa aliyefuata baada ya Julius Caesar alikuwa Augusto (anayehesabiwa kuwa Kaisari wa kwanza wa Kirumi) na mwezi wa Sextilis ulipewa jina kwa heshima yake: ni mwezi wa Agosti kwa Kiswahili. Hata watawala wengine walijaribu kupachika majina yao kwenye mwezi fulani lakini ni majina ya Kaisari Juliusi na Augusto pekee yaliyodumu. Miezi ya Septemba hadi Desemba inatunza kumbukumbu ya kwamba ilikuwa miezi ya saba hadi kumi katika kalenda ya kale ya kirumi. Jina la mwezi - Nambari ya Kilatini Septemba - septem (7) Oktoba - octo (8) Novemba - novem (9) Desemba - decem (10) Lakini hapakuwa na mapatano kuhusu mwanzo wa mwaka ni mwezi gani. Maeneo mbalimbali yalitumia mwanzo tofauti. Ni tangu karne ya 13 BK tu kwamba 1 Januari ilianza kukubaliwa polepole kuwa mwanzo wa mwaka katika nchi za Ulaya. Kasoro za Kalenda ya Juliasi Kalenda ya Juliasi ilikuwa na kasoro ambayo haikujulikana mwanzoni. Muda kamili wa mwaka wa jua si siku 365 1/4. Hivyo mwaka wa kalenda ya Juliasi ulipita muda kamili ya mwaka wa jua kwa dakika 11 na sekunde 14. Hadi karne ya 14 BK tofauti hiyo ilikuwa imefikia tayari jumla ya siku 7. Hayo yalionekana hasa wakati wa Pasaka ambayo haikufuata tena utaratibu uliowekwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea. Kwa sababu hiyo Mtaguso wa Trento wa Kanisa Katoliki uliamua kusahihisha kalenda. Ni Papa Gregori XIII aliyeita wataalamu waliofanya makadirio mapya. Tangu mwaka 1582 kalenda ya Gregori ilipoanzishwa ikawa leo kalenda ya kimataifa. Kalenda
2487
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda%20ya%20mwezi
Kalenda ya mwezi
Kalenda ya Mwezi ni kalenda inayohesabu miezi kufuatana na mwendo wa Mwezi kwenye anga. Mwezi una muda wa siku 29,5 kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya. Faida yake ni ya kwamba mwezi unaonekana na watu wote. Hali hii inasaidia kuelewana haraka kati ya watu juu ya tarehe fulani katika mazingira ambako hakuna mitambo wala maandishi. Mwaka wa miezi hii 12 una siku 354. Kwa sababu hiyo kalenda za kale katika mataifa na tamaduni mbalimbali mara nyingi zilikuwa hasa kalenda za kufuata mwezi. Kalenda ya mwezi ina mwaka wa siku 354 ambao ni fupi kuliko mwaka wa jua mwenye siku 365 1/4. Kutokana na hiyo kalenda haiwezi kutabiri majira yanayoenda sambamba na mwendo wa jua. Hii ilileta ugumu katika makadirio ya mambo yote yanayohusu mpangilio ya kilimo kinachofuata majira ya joto na baridi au ukame na mvua. Hali hizi zote zinategemea hali ya jua na kukadiriwa katika mwaka wa jua. Ugumu huu uligusa pia mambo ya utawala na serikali kwa sababu uwezo wa wakulima kulipa kodi inategemea mavuno. Kalenda ambayo haisaidii kupanga wakati wa mavuno hivyo kupatikana kwa mapato ya serikali ina faida kidogo tu. Kutokana na sababu hizo kalenda za mwezi zilirekebihswa mara nyingi kwa njia ya kuingiza siku za nyongeza ili muda wa mwaka ilingane na mwaka wa jua. Kalenda ya Kiyahudi ni mfano hadi leo jinsi mwaka wa mwezi unasahihishwa kwa kuingiza miezi ya nyongeza. Katika utaratibu wa kipindi cha miaka 19 kuna miaka 12 ya kawaida na miaka saba yenye mwezi wa nyongeza inayobadilishana ili kulinganisha kalenda ya mwezi na mwendo wa jua hivyo mwezi wa mavuno inabaki katika majira yake. Kalenda ya mwezi tupu ambayo ni muhimu hadi leo ni kalenda ya kiislamu. Tarehe zake zinabadilika kila mwaka katika kalenda ya Gregori ambayo ni Kalenda ya kimataifa inayofuata jua. Kwa mfano Ramadhani iko mwaka 2006 BK wakati wa Novemba; kila mwaka inasogea mbele itafika miezi ya Agosti, Mei, Januari na kadhalika hadi kurudi tena Novemba katika mwendo wa miaka wapitao 33. Kalenda
2488
https://sw.wikipedia.org/wiki/Madagaska
Madagaska
Jamhuri ya Madagaska (au Madagasikari) inaenea katika kisiwa cha Madagaska (pia: Bukini) kilichopo katika Bahari Hindi mashariki kwa pwani ya Afrika. Jina Jina Madagaska lina maana ya "Kisiwa kikubwa" na linatokana na lugha ya wenyeji, Wamalagasi ambao waongea Kimalagasi. Jiografia Kisiwa chenyewe ni cha nne kwa ukubwa duniani. Upekee wa kisiwa unatokana na kwamba kilimeguka kutoka India miaka milioni 88 hivi iliyopita, halafu kilibaki bila watu hadi karne ya 5 hivi BK. Ekolojia Kisiwa hicho ni pia mazingira makubwa ya aina ya violezo ambayo ni asilimia 5 ya violezo vyote vya mimea na wanyama vya dunia nzima. Asilimia 90 ya viumbehai asili ni maalumu wa Madagaska, kama vile wanyama aina ya kima awali wanaoitwa lemuri, ndege ambao waambukiza ugonjwa na mti wa mbuyu. Historia Madagaska ni kati ya maeneo ya mwisho kufikiwa na kukaliwa na binadamu. Wa kwanza kufika walitokea visiwa vya Indonesia (kama mwaka 350-550 BK). Baadaye tu walihamia watu kutoka bara la Afrika (mwaka 1000 hivi) na wengineo (Waarabu, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k.). Kuanzia mwaka 1787 hadi mwaka 1897 kisiwa kilizidi kuunganishwa kisiasa chini ya Ufalme wa Merina. Watawala walikuwa watu kutoka familia ya Andrianampoinimerina, mwanzilishi wa taifa hilo, ambaye alikuwa ametokea katika kabila la Wamerina Kabila hilo lilikuwa kubwa na muhimu kuliko yote 18 ya kisiwa hicho. Makazi yake yalikuwa katika uwanda wa juu wa kati lakini lilienea sehemu kubwa ya Bukini. Wamerina walikuwa na makao makuu ya utawala wao Antananarivo; baada ya kugawiwa kwa ufalme wao mnamo 1710 kitovu cha malaka kati ya Wamerina ikahamia kwenye mlima wa Ambohimanga lakini tangu kuunganishwa kwa Wamerina mnamo 1794 mji mkuu ukulikuwa tena Atananarivo. Kutoka hapo waliweza kueneza mamlaka yao katika sehemu nyingine za kisiwa hicho. Makabila yote ya wenyeji yalizungumza lugha moja na yalikuwa na mila na desturi zinazofanana, hivyo yaliweza kujenga umoja wa kiutamaduni uliowafanya wawe jamii moja kimsingi. Watawala hao wa kifalme waliweza kutekeleza mambo mbalimbali kuendeleza Bukini katika vipindi vyao kabla ya kuja kwa wageni kutoka Uingereza na Ufaransa ambao kwa kiasi fulani ulidhoofisha mamlaka ya kifalme. Kisiwa hicho hatimaye kiligeuzwa kuwa koloni la Ufaransa. Hii ni kwa kuwa, ingawa sera ya kuisasisha ya Bukini kwa namna fulani iliimarisha uwezo wa nchi hiyo wa kutetea uhuru wake, lakini kwa ujumla sera hiyo ilidhoofisha ufalme huo kwa kuongeza utegemezi wake kwa mataifa ya kigeni. Watu Mwaka 2018 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa milioni 26.3. Wenyeji wengi wana mchanganyiko wa damu: DNA inaonyesha kuwa wakazi wa kwanza kutoka Indonesia wameichangia asilimia 50 hivi na Waafrika vilevile. Wanaoishi sehemu za ndani ni wa Kiindonesia zaidi, wakati wale wa pwani ni wa Kiafrika zaidi. Lugha Lugha ya taifa ni Kimalagasi. Lugha rasmi za Madagaska ni Kimalagasi na Kifaransa (angalia pia orodha ya lugha za Madagaska). Dini Mwaka 1993 nchini Madagaska kulikuwa na dini za jadi (52% hivi), Ukristo (41%, Waprotestanti wakiwazidi kidogo Wakatoliki), Uislamu (7% hivi) n.k. Tangu hapo wafuasi wengi wa dini za jadi wameongokea Ukristo, hasa wa Kiprotestanti. Utamaduni Pamoja na kutokea mazingira tofauti sana, Wamalagasi wamechanganyikana sana na kuwa na utamaduni na lugha aina moja, ya Kiindonesia zaidi. Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo Viungo vya nje Country Profile from BBC News Madagascar from UCB Libraries GovPubs Key Development Forecasts for Madagascar from International Futures Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Visiwa vya Afrika Visiwa vya Bahari ya Hindi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
2490
https://sw.wikipedia.org/wiki/Itifaki
Itifaki
Itifaki (kutoka neno la Kiarabu; pia "protokali", kutoka Kiingereza "protocol") ni orodha au mpangilio wa visa unaotumika katika kuendesha sherehe, mkutano, mjadala na kadhalika kutokana na utaratibu uliowekwa. Mathalani katika shughuli za mikutano ni kiongozi gani anatakiwa kuingia kwanza, kisha nani afuatie na nani awe wa mwisho kuingia katika sehemu ya mkutano. Mwenyeji wa mkutano anatakiwa kukaa upande gani na mgeni mwalikwa anatakiwa kukaa upande gani. Kama ni shughuli ya kitaifa ni wimbo wa taifa gani unatakiwa uanze, ule wa Rais mwenyeji au wa Rais mgeni? Baada ya mkutano nani anatakiwa kutoka kwanza na nani awe wa mwisho. Mambo kama haya au utaratibu kama huu ndio huitwa itifaki. Ila mwanafunzi afahamu kwamba itifaki ikitumika katika isimujamii inaleta dhana tofauti na maelezo haya. Pia ni maelewano au maridhiano maalumu kati ya mataifa. Tena ni programu ya kompyuta. Kompyuta Utamaduni Elimu jamii
2492
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Caesar
Julius Caesar
Gaius Julius Caesar (tamka gayus yulius kaesar - 100 - 44 KK) alikuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Roma ya Kale. Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo. Baadhi ya mafanikio hayo ni: Kama kiongozi wa kijeshi aliteka Gallia (leo: Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa ni karibu sana na Kilatini, lugha ya Roma ya Kale. Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa mungu. Jina lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani). Aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa leo (Kalenda ya Juliasi). Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai. Katika historia ya Roma alifunga kipindi cha Jamhuri - kilichofuata ni Dola la Roma aliloliwekea misingi. Kupanda ngazi Alizaliwa katika familia ya makabaila wenye nafasi katika Senatus ilivyoitwa bunge la Roma. Aliingia katika siasa, akachaguliwa kwa vyeo mbalimbali kwa vipindi vya kawaida wa miezi kadhaa hadi mwaka moja. Cheo chake muhimu cha kwanza kilikuwa mkuu wa koloni la Kiroma la Hispania. Alifaulu kushinda ghasia ya Wahispania wenyeji waliojaribu kuwafukuza Waroma kutoka nchini mwao. Caesar aliporudi Roma alitajirika na kujipatia sifa kama kiongozi wa kijeshi pia mwanasiasa aliyeokoa koloni muhimu la Hispania. Baadaye Caesar alijiunga na wanasiasa wawili wengine: Gnaeus Pompeius Magnus aliyekuwa mkuu wa wanajeshi na Marcus Licinius Crassus aliyekuwa tajiri kushinda Waroma wote. Wote watatu waliunda umoja ulioitwa "triumviratus", yaani umoja wa wanaume watatu, wakashika mamlaka katika dola. Caesar alichaguliwa kwa cheo kikuu yaani Konsul kwa mwaka 59 KK. Baada ya mwisho wa kipindi chake alijipatia cheo cha Prokonsul au gavana wa eneo la Gallia ya Kiroma (Italia ya Kaskazini na eneo dogo la Ufaransa ya Kusini). Vita ya Gallia Alitumia nafasi hii kuanzisha vita dhidi ya makabila ya Gallia huru yaani eneo lote la Ufaransa, Uswisi na Ubelgiji ya leo. Katika miaka minane ya 58 - 51 KK alitwaa Gallia yote. Aliingia pia ndani ya Germania (Ujerumani) na kuvuka bahari aliposhambulia upande wa kusini wa Britannia. Aliandika kitabu cha "De bello gallico" (yaani Vita ya Gallia) akieleza mapigano yake. Kitabu hicho kina habari muhimu za kihistoria juu ya utamaduni wa makabila ya Gallia, Germania na Britannia aliyopigana nayo. Vita vya wenyewe kwa wenyewe Baada ya kufanikiwa Gallia na kujenga jeshi kubwa tena hodari, wanasiasa wengine huko Roma walianza kumwogopa wakajaribu kumzuia asirudi Italia. Mwenzake Crassus alikuwa amekufa tayari vitani mashariki mwa dola; mwenzake Pompeius aliomwogopa Caesar akajaribu kushawishi viongozi wengine kumsimamisha. Lakini mwaka 49 KK Caesar aliongoza wanajeshi lake warudi Italia. Pompeius na wapinzani wake walitoka Roma wakaenda Ugiriki iliyokuwa jimbo la Kiroma. Mwaka 48 KK Caesar akachaguliwa tena kuwa Konsul. Akamfuata Pompeius kwa jeshi lake akamshinda katika mapigano. Pompeius alikimbia kwenda Misri lakini mfalme Ptolemaio XIII alimwogopa Caesar akamwua Pompeius akampatia Caesar kichwa chake alipofika Misri. Caesar alikutana na dada yake Ptolemaio Kleopatra akampenda na kuzaliana naye mwana wake pekee. Akamsaidia Kleopatra kuwa malkia na mtawala wa Misri. Kuchaguliwa dikteta hadi kifo Caesar alirudi Roma kutoka Misri akiwa mshindi dhidi ya wapinzani wote. Bunge la Senatus lilimpa cheo na madaraka ya dikteta kwa miaka 10. Baada ya ushindi mwingine dhidi ya wapinzani huko Hispania bunge lilibadilisha azimio hilo kumpa cheo cha dikteta wa maisha. Caesar alipokea azimio hili. Sasa sehemu ya wabunge waliogopa ya kwamba nia yake ilikuwa kuwa mfalme wa Roma - jambo lililokuwa marufuku katika jamhuri ya Roma. Kikundi cha wabunge -wote makabaila wa familia za kale- kiliunga mikono wakamwua Caesar bungeni tarehe 15 Machi 44 KK kwa kumdunga kisu mara 23. Caesar anasemekana alimtambua mpwa wake Brutus akamwuliza kwa maneno yake ya mwisho: "Hata wewe mwanangu?" Caesar hakuwa na watoto ila huyu mwana wa Kleopatra asiyekuwa Mroma. Kabla ya kifo chake alikuwa amempanga mtoto mpwa wake Oktaviano. Huyu Oktaviano -aliyejulikana baadaye kama Augusto na mtawala wa kwanza wa Dola la Roma- alilipiza kisasi chake katika kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe na kuua wapinzani wote wa Caesar. Miaka miwili baada ya kifo chake bunge lilimtangaza Caesar kuwa mungu. Marejeo Kaisari Watu wa Roma ya Kale Waandishi wa Kilatini
2494
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurow
Kurow
Ukitafuta mji wa Poland, uone Kurów. Kurow ni mji mdogo kwenye bonde la Waitaki kwenye kisiwa cha kusini cha New Zealand katika wilaya ya Otago. Mazingira ya Kurow ina miradi mbalimbali ya kutengeneza umeme kwa nguvu ya maji. Kuna kilimo cha matunda hasa mizabibu. Kuna mvutano kuhusu asili ya jina la mji kama imetokana na neno la Wamaori wazalendo au kutoka kwa mji wa Kurów. Miji ya New Zealand
2495
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gallia
Gallia
Gallia ni jina la kihistoria kwa ajili ya Ufaransa pamoja na maeneo ya jirani. Eneo la Gallia Gallia ilikuwa jina la kilatini kwa ajili maeneo yaliyokaliwa na "Wagallia". Hili ilikuwa namna jinsi Waroma wa Kale walivyowaita majirani wao Wakelti. Kijiografia eneo hili lilijumlisha Ufaransa, Uswisi, Ubelgiji na Italia ya Kaskazini ya leo. Wakelti au Wagallia walikalia pia Uingereza ya Kusini (=Britania) na Hispania (=Iberia) lakini maeneo haya hayakuhesabiwa kuwa sehemu ya "Gallia" na Waroma. Wakelti walikuwa pia kati ya wakazi wa kale wa Ujerumani kabla ya uvamizi huko wa Wagermanik wenyewe. Habari za Gallia Karibu habari zote za kimaandishi kuhusu Gallia na Wagalli zimetokana na Waroma wa kale. Sehemu kubwa ya habari zinapatikana katika kitabu cha Caesar "Vita ya Gallia". Kuna pia mabaki ya kiarkolojia hasa makaburi pamoja na vitu vya maisha ya kila siku vilivyoweka makaburini kwa imani ya kwamba vitawasaidia marehemu katika ahera. Arkiolojia ya makaburi inaonyesha ya kwamba Wakelti (Wagallia) walikuwa sehemu ya biashara ya kimataifa pia walikuwa na mafundi wenye uwezo wa kutengeneza vitambaa na nguo, pia na wahunzi na wafinyanzi. Wagallia na Waroma Mnamo mwaka 390 KK kabila fulani la Wagallia chini ya kiongozi Brennus lilivamia Italia na mji wa Roma lakini walishindwa kuteka boma la mji. Kwa muda mrefu Waroma walihofia majirani ya kaskazini. Kuanzia mwaka 200 KK Waroma walikuwa waliendelea kisiasa, kiuchumi na kijeshi wakafaulu kuteka "Gallia Cisalpina" (Gallia upande wa kusini wa milima ya Alpi) ambayo leo hii ni Italia ya Kaskazini. Ikawa jimbo la Kiroma. Kuanzia mwaka 125 KK Waroma walianza kuvamia sehemu za pwani la Gallia pamoja na bonde la mto wa Rhone. Ikawa jimbo la Gallia Narbonensis. Mji mkuu ulikuwa mji wa Narbo (leo: Narbonne). Sehemu nyingine ya Gallia imebaki nchi huru ya makabila yaliyojitawala. Mwaka 58 KK mwanasiasa na jenerali Mroma Caesar akawa gavana wa Gallia Cisalpina pia Narbonensis. Alichukua nafasi ya vita kati ya makabila ya Wagallia katika eneo la Uswisi kuingilia ndani ya mambo ya Gallia huru. Katika vita ya miaka nane alishinda wapinzani wote. Mwaka 51 KK Gallia yote ikawa chini ya utawala wa Kiroma. Jimbo la Kiroma Katika karne zilizofuata Gallia imekuwa sehemu halisi ya Dola la Roma. Inaonekana Wagallia wenyewe walikubali utawala wa Kiroma hasa baada ya kupewa uraia wa Kiroma. Lugha ya Kilatini ilitumika kwa ajili ya habari za kiutawala ikapokelewa polepole na wenyeji. Kilatini hiki kilikuwa msingi wa lugha ya Kifaransa kilichotokea baadaye. Roma ya Kale Historia ya Ufaransa Nchi za kihistoria za Ulaya
2497
https://sw.wikipedia.org/wiki/Misri
Misri
{| border="1" cellpadding="2" cellspacing="0" align="right" width="330px" style="margin-left:15px; border-collapse:collapse; border-color:#f2f2f4" |+Jamhuri ya Kiarabu ya Misri (Kiswahili)Gumhūriyyat Misr al-ʿarabiyya (Kiarabu)</font> | align="center" colspan="2" | |---- | Lugha rasmi || Kiarabu |---- | Mji Mkuu || Cairo |---- | Mji Mkubwa || Cairo |---- | Serikali || Jamhuri |---- | Rais || Abdel Fattah el-Sisi |---- | Eneo || km² 1,010,408 |---- | Idadi ya wakazi || 100,075,480 (2020) |---- | Wakazi kwa km² || 99 |---- | Uchumi nominal || Bilioni $302.256 |---- | Uchumi kwa kipimo cha umma || $3,047 |---- | Pesa || Lira au Pauni ya Misri = 100 Piaster |---- | Kaulimbiu || "Haki - Amani - Kazi" |---- | Wimbo wa Taifa || 'Biladi, Biladi, Biladi (nchi yangu, nchi yangu, nchi yangu)</center> |---- | colspan="2" align="center"| |---- | Saa za Eneo || UTC +2 |---- | Mtandao || .eg |---- | Kodi ya Simu || +20 |} Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia. Ni nchi yenye wakazi milioni 100 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani (zaidi ya milioni 9). Ni kati ya nchi za dunia zenye historia ndefu inayojulikana. Jina la nchi Jina la Misri kwa Kiswahili linalingana na jina rasmi la مصر Miṣr katika lugha ya Kiarabu. Ni jina la Kale jinsi inavyoonekana katika Biblia ya Kiebrania ambako inaitwa Mitzrayim (מִצְרַיִם, wingi wa Misri kumaanisha Misri ya Juu na Misri ya Chini). Maana ya jina hili ni "nchi". Katika enzi ya Misri ya Kale nchi iliitwa na wenyeji Km.t (Kemet) inayomaaniosha "nchi nyeusi" kwa kutaja ardhi "nyeusi" (=yenye rutuba) ya bonde la Naili, tofauti na ardhi nyekundu ya jangwa. Majina ya Kizungu ya "Egypt" (ing.), "Egypte" (far.), "Ägypten" (jer.) yanatokana na jina la Kigiriki Αίγυπτος (aigyptos). Hakuna hakika juu ya maana asilia ya neno. Wengine huamini neno limetokana na jina la hekalu muhimu mjini Memphis. Neno hili ni pia asili ya jina "Wakopti" na hii ni jinsi wenyeji wa Misri walivyojiita wakati wa utawala wa Dola la Roma Jiografia Misri imepakana na Bahari ya Mediteranea, Israel, Eneo la mamlaka ya Palestina, ghuba ya Suez, ghuba ya Aqaba, Bahari ya Shamu, Sudan na Libya. Umbo la nchi hufanana na trapeza. Tabianchi ni yabisi sana na maeneo makubwa ni jangwa, pamoja na oasisi na maeneo ya savana ya miiba. Karibu wananchi wote huishi ndani ya kanda nyembamba ya bonde la mto Naili. Bonde hili linavuka nchi kuanzia mpakani na Sudani katika kusini kuelekea kaskazini hadi mdomo wa mto kwenye Bahari ya Mediteranea. Ardhi pande zote mbili za mto inamwagiliwa na kulimwa. Kwatika umbali mdogo kutoka mto jangwa inaanza. Takriban kilomita 250 kabla ya mdomo Naili inagawanyika katika mikono mbalimbali na kuunda delta ya mto. Kanda hili bichi si zaidi ya asilimia 5 za eneo lote la nchi, ila 98% za wananchi wote huishi humo. Kwa hiyo Naili huitwa "Baba wa Misri", kwa maana bila mto huo pasingekuwepo taifa hili. Mji mkuu wa Kairo uko mwanzoni mwa eneo la delta. Nchi yote huwa na kanda asilia zifuatazo: Oasisi ya mto Naili: mto umechimba bonde kama mfereji katika mwamba asilia ya nchi. Ndani ya bonde hili jembamba lenye upana hadi kilomita 25 kuna kanda la ardhi yenye rutuba kuanzia Ziwa Nasser hadi Kairo. Delta ya Naili: upande wa kaskazini wa Kairo Naili inajigawa katika mikono miwili mikuu na kati ya mikono hiyo miwili kuna eneo la delta yenye km² 23,000 kwa umbo la pembetatu. Inajaa ardhi ya rutuba kutokana na matope ya Naili iliyopelekwa huko na mafuriko katika muda wa miaka elfu kadhaa. Eneo hili linalimwa kote na kumwagiliwa likiwa na mikono midogo ya kando ya Naili. Jangwa la Magharibi: ni eneo kubwa upande wa magharibi wa Naili lisilo na milima mikubwa. Kaskazini mwake kuna tambarare ya Lybia iliyo takriban mita 240 juu ya uwiano wa bahari. Kusini mwake linainama eneo la mbonyeo wa Qatara hadi mita 133 chini ya UB, halafu jangwa linapanda tena juu kuelekea kusini magharibi. Ndani ya eneo hili kubwa kuna beseni kadhaa pamoja na oasisi za Siwa, Bahariyya, Farafra, Dakhla na Charga. Kilomita 100 upande wa kusini-magharibi wa Kairo kuna oasisi kubwa ya Fayyum pamoja na ziwa la Warun lenye eneo la km² 230. Jangwa la Mashariki: ni eneo upande wa mashariki wa mto Naili. Huko kuna milima inayopanda juu ya mita 2,000 pamoja na wadi yaani bonde kali. Jangwa linatelemka hadi mfereji wa Bahari ya Shamu ambao ni sehemu ya Bonde la Ufa linaloanza Palestina na kuendelea hadi Ziwa Nyasa. Rasi ya Sinai: ni eneo la jangwa na milima inayofikia hadi mita 2637 (Jabal Katharina). Historia Nchi hiyo ni kati ya vitovu vya ustaarabu wa binadamu, na kwa sababu hiyo inavutia watalii wengi. Historia ya awali Katika kipindi cha historia ya awali tangu takriban miaka 6000 KK wakazi wa Misri walikuwa na kilimo cha nafaka. Walikuwa na teknolojia ya Zama za Mawe. Wakati ule Jangwa la Sahara lilipanuka na kuwalazimisha watu kukaa karibu zaidi kwenye mto Nile na kwenye oasisi kama Faiyum. Katika mazingira ya jangwa bonde la Nile liliwavuta watu kutokana na rutuba kubwa ya ardhi iliyoongezwa kila mwaka upya kwa njia ya mafuriko yaliyotandaza matope kutoka nyanda za juu kwenye ardhi. Utafiti wa akiolojia umegundua ya kwamba wakazi hao wa bonde walianzisha tamaduni mbalimbali zilizokuwa tofauti kati yao lakini zilizowasiliana kibiashara. Mifano ya kwanza ya mwandiko wa hiroglifi imepatikana kwenye vyungu vilivyofinyangwa mnamo 3200 KK. Misri ya Kale Katika karne zilizofuata, mnamo 3000 KK yalitokea muungano wa sehemu mbalimbali wa Misri chini ya wafalme wenye nguvu wanaotajwa kwa cheo cha farao. Katika historia iliyotungwa na waandishi Wagiriki wa Kale ni kwa kawaida Farao Menes anayetajwa kuwa mtawala wa kwanza aliyeunganisha Misri ya Kaskazini na Misri ya Kusini kuwa milki moja. Lakini leo hii inajulikana kuna wafalme waliomtangulia waliokuwa tayari na milki kubwa. Hata hivyo Menes alianzisha utawala wa nasaba mbalimbali zilizofuatana, pamoja na vipindi vya kati ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe na mafarakano katika nasaba ziliweza kugawa nchi tena kwa muda. Mafarao wa Misri ya Kale walifaulu mara kadhaa kupanua mamlaka yao hadi ndani ya Sudani ya leo, na pia kwa vipindi juu ya sehemu za Palestina na Syria ya leo. Mara kadhaa wavamizi kutoka nje walifaulu kushika utawala juu ya Misri kama vile Wahyksos kutoka Palestina / Kanaan, Wakushi kutoka Nubia au watu kutoka Lybia. Wavamizi hao walitumia pia cheo cha Farao wakijaribu kuendeleza tabia nyingi za milki za awali. Hatimaye wote walipinduliwa tena na viongozi wazalendo walioanzisha nasaba mpya. Mwaka 525 KK mfalme wa Uajemi aliteka Misri. Kwa kipindi kifupi Wamisri waliweza kuwaondoa tena na kuendelea chini ya watawala wazalendo. Misri ya Ptolemi (Wagiriki) na chini ya Roma Uvamizi wa Aleksander Mkuu mwaka 332 KK ulianzisha kipindi cha Misri ya Kigiriki. Mji mpya wa Aleksandria ulikuwa mji mkuu mpya. Jemadari wa Wagiriki walitumia pia cheo cha Farao na kutawala kama nasaba ya Ptolemi, lakini tabaka ya watawala ilikuwa na utamaduni tofauti sana na wananchi wakulima wa kawaida. Wakati wafalme Wagiriki waliendelea kutawala milki mpya ilienea kutoka magharibi ya Mediteranea iliyokuwa Dola la Roma. Malkia wa mwisho wa Misri alikuwa Kleopatra. Baada ya kifo chake Misri ilikuwa jimbo la Dola la Roma. Utawala wa Kiroma uliendelea kwa karne 6. Katika muda huu Ukristo ulianza kuenea katika Misri. Nchi ilikuwa haraka kitovu muhimu cha imani mpya na Ukristo wa Kikopti uliendeleza liturgia na mapokeo ya pekee na kupeleka mfumo huu wa Ukristo hadi Sudani na Ethiopia. Lakini hali ilikuwa ngumu baada ya magavana wa Roma na baadaye wa Bizanti kujaribu kuwalazimisha Wakopti kufuata liturgia na mafundisho ya Kanisa rasmi yaani Kanisa la Kiorthodoksi. Uvamizi wa Kiarabu na Misri ya Kiislamu Kwenye mwaka 639 jeshi la Waarabu Waislamu lilivamia Misri na kuteka nchi yote katika muda wa miaka 3. Wenyeji wengi waliokuwa Wakristo Wakopti hawakuwapinga kwa sababu walipendelea Waislamu kuliko Wakristo Waorthodoksi waliowahi kuwakandamiza vikali katika miaka iliyotangulia. Kwa karne kadhaa idadi kubwa bado walikuwa Wakristo lakini kuanzia karne ya 12 idadi ya Waislamu ilikuwa kubwa zaidi kwa sababu Wakristo walipaswa kulipa kodi zaidi na vipindi kadhaa vya mateso vilitokea na yote ilisababisha kuhamia kwa wananchi kwenda dini mpya. Watawala wapya hawakutumia Aleksandria kuwa mji mkuu bali walianzisha mji mpya wa Fustat karibu na Babylon ya Misri, pale ambako mto Nile unajigawa na kuanzisha delta yake. Hadi mwaka 969 Misri ilitawaliwa na watawala Waislamu Wasunni waliokuwa kwa jina magavana na wawakilishi wa makhalifa huko Dameski au Baghdad, lakini zaidi watawala wa kujitegemea hali halisi. Mwaka 969 Wafatimi kutoka sehemu za Tunisia ya leo walivamia na kuteka nchi wakianzisha ukhalifa wao. Wafatimi walikuwa Waismaili, wakati ule mwelekeo wa kimapinduzi ya Shia. Walianzisha makao makuu yao nje ya Fustat na Babylon wakaiita "Al-Qahira", yaani mwenye ushindi, na hii ilikuwa chanzo cha Kairo ya leo. Wakati wa vita za misalaba Wafatimi walishindwa na askari wa Wasunni waliendelea kuunda nasaba ya masultani wa Mamluki wa Misri. Jimbo la Milki ya Osmani Mnamo mwaka 1517 Waosmani walivamia na kuteka Misri. Hadi karne ya 19 Misri ikaendelea kama jimbo la Milki ya Osmani, kisheria hata hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Hali halisi nchi ilikuwa na kipindi kifupi kama milki ya kujitegemea wakati wa karne ya 19, hadi kusimamiwa na Uingereza hasa kwa shabaha ya kutawala mfereji wa Suez na kushuka kwa ngazi ya nchi lindwa. Mwaka 1914 ilitangazwa kuwa nchi lindwa chini ya Uingereza; tangazo la uhuru la mwaka 1922 bado liliacha athira kubwa kwa Uingereza. Uhuru Tangu mwaka 1952 Misri imepata uhuru kamili, na tangu hapo ilitawala pia mfereji wa Suez. Watu Wakazi wengi (91%) ni Wamisri asili. Wengine ni Waazaba, Waturuki, Wagiriki, Wabeduini, Waberberi, Wanubi n.k. Wahamiaji kutoka Sudan na nchi nyingine ni milioni 5 hivi, wakati Wamisri wanaoishi ugenini ni milioni 2.7. Lugha rasmi ni Kiarabu Sanifu cha Kisasa, wakati wananchi wanatumia kwa kawaida aina mbalimbali za Kiarabu, hasa Kiarabu cha Kimisri (68%) Upande wa dini, sheria zinazitambua 3 tu: Uislamu, ambao ndio dini rasmi, Ukristo na Uyahudi. Uwiano wa wafuasi wa dini hizo haujulikani vizuri, lakini Waislamu (hasa Wasunni) ni kama 90%, Wakristo (hasa Wakopti wanaoendelea kufuata Ukristo uliokuwa unatawala kabla ya Waarabu kuteka nchi katika karne ya 7) ni walau 10%, wakati Wayahudi wamehama karibu wote. Tazama pia Mikoa ya Misri Orodha ya miji ya Misri Historia ya Misri Misri ya Kale Orodha ya Marais wa Misri Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Serikali Egypt's Government Services Portal (Arabic, English) Egypt Information Portal (Arabic, English) Egypt Information and Decision Support Center (Arabic, English) Egypt State Information Services (Arabic, English, French) Chief of State and Cabinet Members Egyptian Tourist Authority Taarifa za jumla Country Profile from the BBC News Egypt profile from Africa.com Egypt Maps – Perry-Castañeda Library Map Collection, University of Texas at Austin Biashara World Bank Summary Trade Statistics Egypt Mengineyo History of Egypt, Chaldea, Syria, Babylonia, and Assyria in the Light of Recent Discovery by Leonard William King, at Project Gutenberg. Egyptian History (urdu) By Nile and Tigris'' - a narrative of journeys in Egypt and Mesopotamia on behalf of the British museum between 1886 and 1913, by Sir E. A. Wallis Budge, 1920 (DjVu and layered PDF formats) Napoleon on the Nile: Soldiers, Artists, and the Rediscovery of Egypt . Nchi za Kiarabu Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Maeneo ya Biblia Mashariki ya Kati
2498
https://sw.wikipedia.org/wiki/Libya
Libya
Libya ni nchi ya Afrika ya Kaskazini kwenye Bahari ya Mediteraneo, inayopakana na Misri, Sudan, Niger, Chad, Algeria na Tunisia. Eneo kubwa la nchi (90%) ni sehemu ya jangwa la Sahara. Chini yake kuna akiba kubwa ya petroli, ambayo ndiyo utajiri wa nchi. Miji mikuu ni Tripoli, Benghazi na Misratah. Historia Wakazi asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki. Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea. Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi. Katika karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao. Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20. Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941 ilipotekwa na Waingereza ambao, baada ya Vita vikuu vya pili kwisha, waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji, Idris I, aliyekuwa amepinga ukoloni tangu mwaka 1920 (Vita vya Libya dhidi ya Italia). Kisha kumpindua mfalme huyo, Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011 kwa mkono wa N.A.T.O. Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mwaka 2020 kulikuwa na makubaliano ya kusimamisha vita na kuunda serikali ya pamoja ili kuandaa uchaguzi mkuu. Watu Wakazi wa Libya ni hasa mchanganyiko wa Waberberi, Waarabu na Waturuki (74%), mbali na Waberberi (25%) ambao ndio wakazi asilia, lakini wengi wao wameanza kutumia lugha ya Kiarabu pia. Kuna pia wahamiaji kutoka nchi za jirani, za kandokando ya Bahari ya Kati na kutoka Bara Hindi. Wakazi wameongezeka tangu mwaka 1970 kutoka milioni 2.5 hadi kuwa karibu milioni 7 mwaka 2022. Nusu ya wakazi wote ni vijana chini ya umri wa miaka 16. Sehemu kubwa kabisa (80%) huishi sehemu za pwani. Lugha kuu ni Kiarabu pamoja na lugha kadhaa za Kiberberi. Ndizo: Kinafusi (wasemaji 101.000) Kighadames (wasemaji 42.000) Kitamascheq (Tuareg; wasemaji 17.000) Upande wa dini, unatawala Uislamu (97%). Wakristo ni zaidi ya 100,000, wakiwemo hasa Wakopti (60,000) na Wakatoliki (40,000). Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Libya profile from the BBC News. Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi za Kiarabu Nchi za Waberber Maeneo ya Biblia
2499
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tripoli
Tripoli
Tripoli ni neno la asili ya Kigiriki (Τρίπολις - Trípolis au Τρίπολη - Trípoli) linalomaanisha "miji mitatu" au "mji mwenye sehemu tatu". Asili yake ni maungano ya miji mitatu ya jirani kuwa mji au dola moja. Katika lugha ya Kiarabu neno limekuwa "Trablus" au "Tarablus" (طرابلس). Neno linataja miji mbalimbali ya kisasa au ya kihistoria ndiyo hasa mji mkuu wa Libya, Tripoli (Libya) au Trablus/Libya mji wa pili wa Lebanon Tripoli (Lebanon) au Trablus/Lebanon mji wa Ugiriki, Tripoli (Ugiriki) mji wa Marekani, jimbo la Iowa, Tripoli (Iowa) mji wa Marekani, jimbo la Pennsylvania, Tripoli (Pennsylvania) jina la kihistoria la mji wa Tirebolu, Uturuki jina la kihistoria kwa dola ndogo katika Syria/Lebanon wakati wa vita za msalaba meli ya kijeshi ya Marekani USS Tripoli Makala zinazotofautisha maana
2501
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahore
Mahore
Mahore (Kifaransa: Grande-Terre) ni kisiwa kikubwa cha eneo la ng’ambo la Ufaransa la Mayotte. Kisiwa cha pili ni Pamanzi (Kifaransa: Petite-Terre). Mahore ina urefu wa 39 km na upana wa 22 km. Milima yake ni Mont Benara (660 m), Mont Choungui (594 m), Mont Mtsapere (572 m) et Mont Combani (477). Mji mkubwa ni Mamoudzou. Kitovu cha kiuchumi ni Kawéni. Kijiografia kisiwa ni sehemu ya funguviwa ya Komoro. Mayotte Visiwa vya Bahari ya Hindi Visiwa vya Afrika
2509
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maulid
Maulid
Maulid (pia: maulidi, kwa kirefu: Maulid an-Nabii) ni sikukuu ya dini ya Uislamu ya kuadhimisha kuzaliwa kwake Mtume Muhammad takriban mwaka 570 BK. Neno lenyewe ni la asili ya Kiarabu kutokana na مولد النبي , maulid an-nabi, au ميلاد النبي , milaad an-nabi). Sikukuu inafuata kalenda ya Kiislamu. Waislamu wa dhehebu la Sunni husheherekea tarehe 12 Rabi'-ul-Awwal kwa mujibu ya kalenda ya Kiislamu ya Alhijria na Waislamu wa dhehebu la Shia husheherekea tarehe 17 Rabi'-ul-Awwal. Wataalamu wa historia wengine wanasema ya kwamba sherehe ya Maulid imeanzishwa mnamo karne ya 12 BK. Kuna Waislamu kadhaa wanaokataa sherehe hiyo kwa sababu hakuna sunna wala hadith ya Muhammad mwenyewe kuhusu kusheherekea maulid yake. Lakini kwa ujumla ni sikukuu inayopendwa sana na Waislamu wengi duniani. Misri maulid ni kati ya sikukuu za Kiislamu zinazokumbukwa sana na Waislamu. Katika Afrika ya Mashariki sherehe ya maulid huko Lamu imejulikana hasa ikivuta wageni kutoka pande zote za Afrika ya Mashariki hadi Uarabuni. Kati ya desturi ni mikutano, kusikia mashairi juu ya maisha ya mtume a mengine. Tarehe za Maulid katika kalenda ya Gregori Maulid kama vile sikukuu zote za Kiislamu inafuata kalenda ya Kiislamu ambayo ni kalenda ya mwezi. Kwa sababu hiyo tarehe yake hubadilikabadilika katika kalenda ya Gregori iliyoenea kimataifa. Kalenda ya kiislamu hubadilika kulingana na kuandama kwa mwezi. Zifuatazo ni tarehe za maulid kwa ajili ya miaka 2006 - 2021. Tarehe ya kwanza ni ile ya Wasunni (12 Rabi'-ul-Awwal) na tarehe ya pili katika mabano ni ile ya Washia (17. Rabi'-ul-Awwal). Tarehe hizo zinaweza kuwa tofauti na tarehe halisi kwa sababu kuna tofauti kati ya nchi na vikundi vya Waislamu jinsi gani kukubali kuhusu mwanzo wa miezi. 2006: 12 Aprili, (17 Aprili) 2007: 31 Machi, (5 Aprili) 2008: 20 Machi, (25 Machi) 2009: 9 Machi, (14 Machi) 2010: 26 Februari, (3 Machi) 2011: 15 Februari, (20 Februari) 2012: 4 Februari, (9 Februari) 2013: 24 Januari, (29 Januari) 2014: 13 Januari, (18 Januari) 2015: 2 Januari, (7 Januari) 2016: 22 Desemba, (27 Desemba) 2017: 11 Desemba, (16 Desemba) 2018: 30 Novemba, (5 Desemba) 2019: 19 Novemba, (24 Novemba) 2020: 8 Novemba, (13 Novemba) 2021: 28 Oktoba, (2 Novemba) Viungo vya nje Islamic Holy Days Mawlid Video Russian Mawlid Turkish Mawlid Sikukuu za Uislamu
2511
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mayotte
Mayotte
Mayotte ni eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: Départment de Mayotte). Linaundwa na visiwa vya Mahore na Pamanzi pamoja na vingine vidogo. Eneo hili kijiografia ni hasa muungo wa funguvisiwa la Komoro lakini si kisiasa. Mayotte iko katika kaskazini ya Mfereji wa Msumbiji kwenye Bahari Hindi, kati ya Madagaska upande wa mashariki-kusini na Msumbiji bara upande wa magharibi. Iko kilometa 295 magharibi kwa Madagaska na km 67 kusini mashariki mwa Anjouan. Ardhi ya Mayotte ina eneo la takriban km² 374. Ni mwamba wa matumbawe. Mji mkuu ni Mamoudzou tangu mwaka 1977. Mji mkuu wa zamani ni Dzaoudzi kwenye kisiwa cha Pamanzi. Historia Mayotte inaonekana kuwa imekaliwa na watu kutoka karne ya 7, wakitokea Madagaska, wengine wenye asili ya Asia na wengine wenye asili ya Afrika. Kati ya karne ya 8 na karne ya 11 wakazi walisilimu, na kuna msikiti mkongwe (katika Tsingoni) wa karne ya 14, pamoja na mirhab ya matumbawe (1532). Visiwa vyote vya Komoro vinafuata utamaduni wa Kiswahili vikiwa pamoja na Mayotte. Mwaka wa 1841, wakati idadi ya watu ilipungua kwa wakazi chini ya 3000, sultani wa mwisho Andriansoly (kutoka Madagaska) aliuza kisiwa kwa Ufaransa kwa kubadilishana ya ulinzi wa nchi hiyo, hivyo Mayotte ikawa koloni la Kifaransa. Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komoro walidai uhuru na kuunda Umoja wa Comoro, Mayotte iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni. Lugha na dini Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayotte, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska. Upande wa dini, asilimia 97 ni Waislamu na 3% ni Wakristo. Utalii Kisiwa cha Mayotte kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500). Usafiri Reli: kilomita 0 Barabara: Jumla: kilomita 93 (mi 58) za lami kilomita 72 (45 mi) za vumbi: kilomita 21 (13 mi) Vilindi vya kung’oa tanga: hakuna Bandari: Dzaoudzi Uwanja wa ndege: 1 (2002) Viwanja vya lami: 1 Tazama pia Jiografia ya Mayotte Watu wa Mayotte Siasa ya Mayotte Uchumi wa Mayotte Mawasiliano ya Mayotte Maeneo ya ng’ambo ya Ufaransa Wizara za serikali ya Ufaransa Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje CIA World Factbook - Mayotte cha maelezo, Mayotte - Mayotte wa lugha za Mayotte (na Kifaransa) Shimaore (na Kifaransa) Komori Visiwa vya Afrika Visiwa vya Bahari ya Hindi Eneo la ng'ambo la Ufaransa
2512
https://sw.wikipedia.org/wiki/Funguvisiwa
Funguvisiwa
Funguvisiwa ni kundi la visiwa vinavyokaa sehemu pamoja baharini. Mara nyingi kundi la namna hiyo lina asili moja, kama vile kuwa mabaki ya kisiwa kikubwa zaidi kilichogawika kutokana na mmomonyoko wa ardhi yake au kuwa na asili ya volkeno. Atolli inaweza kuonekana pia kama kundi la visiwa lakini huhesabiwa zaidi kama kisiwa kimoja hata kama sehemu kadhaa ziko chini ya maji. Katika Bahari ya Pasifiki na Bahari Hindi kuna mafunguvisiwa ya atolli. Funguvisiwa kubwa kabisa duniani ni lile la Indonesia pamoja na Ufilipino linaloitwa pia Funguvisiwa la Malay. Bahari ya Pasifiki ina mafunguvisiwa mengi, pia sehemu ya Karibi ya Bahari ya Atlantiki karibu na Amerika ya Kati. Mafunguvisiwa muhimu ya Afrika ni Zanzibar, Shelisheli na Komoro katika Bahari Hindi, halafu Visiwa vya Kanari na Visiwa vya Madeira katika Atlantiki. Mafunguvisiwa madogo karibu na pwani ya Afrika ya Mashariki ni kama vile ya Lamu, Kilwa na Kirimba. Visiwa Jiografia Bahari
2513
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lamu%20%28maana%29
Lamu (maana)
Lamu ni neno la kutaja mahali pafuatapo katika Kenya: Lamu (mji) - ni kati ya miji ya kale sana ya Waswahili kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki; uko kwenye orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" Lamu (kisiwa) ni kisiwa chenye mji wa Lamu Lamu (funguvisiwa) ni funguvisiwa lenye visiwa vya Lamu, Pate, Manda, Kimayu na vingine Lamu (wilaya) ilikuwa wilaya ya kiutawala wa Jamhuri ya Kenya iliyounganisha funguvisiwa pamoja na sehemu za bara jirani nayo Kaunti ya Lamu ndiyo sehemu ya utawala tangu mwaka 2010 Makala zinazotofautisha maana
2516
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya
Wilaya
Wilaya ni mgawanyo wa kiutawala au eneo lililotengwa kwa ajili ya utawala. Mikoa ya Tanzania na Kenya imegawiwa kwa wilaya. Asili ya neno ni Kiarabu "ولاية" (wilaayatun - Kituruki: vilayet). Katika Dola la Osmani "vilayet" ilikuwa ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala ikimaanisha jimbo au mkoa. Mkuu wake au gavana alikuwa na cheo cha "Wali". Neno hili la "wilaya" limepatikana katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Uislamu au lugha ya Kiarabu kama vile Uturuki, Algeria, Tunisia, Oman, Mauritania, Sudan, Malaysia, Indonesia, Afghanistan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan. Katika Kiarabu cha Kisasa "wilaayatun" inamaanisha pia dola ndani ya shirikisho - kwa mfano madola kama vile Texas ndani ya Marekani. Katika matumizi ya Kiswahili huko Kenya na Tanzania "wilaya" imekuwa mgawanyo wa ngazi ya pili yaani ni kitengo chini ya ngazi ya kwanza ya mikoa. Vitengo vya wilaya ni tarafa. Na vitengo vya tarafa ni kata zinazoitwa shehia katika Zanzibar na chini yake vijiji au mitaa. Algeria ni nchi nyingine ambako wilaya inamaanisha ngazi ya pili ya kiutawala. Ugawaji wa nchi
2517
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmomonyoko
Mmomonyoko
Mmomonyoko (kwa Kiingereza erosion) ni hali ya kuvunjika au kumegekamegeka kwa udongo au mwamba kutokana na athira ya upepo, maji, barafu, joto au mwendo wa ardhi. Kazi za binadamu zimekuwa pia sababu muhimu ya mmomonyoko. Katika mazingira yanayokaliwa na binadamu, na hasa kwa kilimo, mmomonyoko unaleta hatari. Mmomonyoko wa asili Mmomonyoko ni kati ya nguvu muhimu zinazofinyanga uso wa dunia. Uso wa mabonde na milima ya dunia ni matokeo ya mmomonyoko. Mmomonyoko wa maji Maji ni kati ya nguvu kuu za mmomonyoko. Mwendo wa maji unasukuma sehemu ndogo za ardhi na kuzipeleka mbali kabisa. Hata vipande vya mwamba vinaweza kukatwa hasa kwa mawe madogo yanayorushwa na maji dhidi ya miamba mikubwa. Mwendo wa maji ya mito unaweza kuchimba mabonde makubwa. Ukali wake unategemea na kiasi cha maji, kasi yake na aina ya ardhi, kama ina mtelemko mkubwa au kama maji yamepita kwenye ardhi au juu ya miamba. Kama mtelemko ni mkubwa na ardhi ni laini ni rahisi kwa maji kukata bonde refu na kubwa. Hata mtelemko wa mvua unaleta mmomonyoko. Matone yenyewe hugongagonga sehemu ndogo za ardhi na kuzibeba kidogo jinsi inavyoonekana vizuri baada ya mvua kwenye eneo penye mchanga. Maji ya mvua yakitelemka milimani yanaweza kubeba udongo mwingi. Udongo wote pamoja na mawe madogo unaobebwa na maji hutuamishwa mahali fulani kama mashapo. Kwa njia hiyo maji yanaweza kutenganisha aina mbalimbali za mashapo. Kwa kawaida sehemu nzito hutelemka kwanza na kukaa kama mwendo wa maji unaanza kupungua wakati mto umetoka kwenye mtelemko na kuingia eneo la tambarare. Kwa njia hii aina za mashapo kama vile changarawe, mchanga, matamahuluku na udongo kabisa zinapatikana. Mmomonyoko wa pwani Mmomonyoko kwenye mwambao wa bahari au ziwa ni aina ya pekee ya mmomonyoko wa maji. Unatokea hasa kutokana na nguvu ya mawimbi na mikondo. Mikondo ya baharini hubeba muda wote mashapo kwa kuyachukua hapa na kuyatuamisha pale. Kama kiasi kilichochukuliwa kinazidi kiasi kilichotuamishwa mmomonyoko unatokea. Pale panapotuamishwa zaidi kuliko kuchukuliwa fungu linatokea. Watu wakijenga karibu mno na bahari -kwa mfano mahoteli ya kitalii- wataona mara nyingi ya kwamba nyumba zinachukuliwa na bahari baada ya miaka kadhaa kwa sababu ya mmomonyoko wa pwani wa kawaida. Mmomonyoko wa upepo Upepo unaweza kupuliza chembe ndogo za udongo kama udongo huu ni laini na kavu. Aina hii ya mmomonyoko hutokea hasa pasipo na mimea inayofunika udongo wa juu. Jangwani kiasi kikubwa cha udongo au mchanga huhamishwa na dhoruba. Upepo ukibeba machanga unaweza kusababisha hata mmomonyoko kwa miamba. Mchanga unarushwa na upepo kwa kasi kubwa dhidi ya mwamba na kuisagasaga. Mmomonyoko wa barafu Barafu ikipatikana kama barafuto (ganda nene la barafu inayoanza kutiririka polepole na kujisukuma mbele)ina uwezo wa kuvunja mawe na miamba mikubwa kabisa na kuzisukuma mbali. Barafuto isipoishia baharini inatoa mito inayoendeleza kazi ya mmomonyoko wa maji. Njia nyingine ya barafu kufinyanga uso wa dunia hutokea pale ambako maji yanaingia kwa mashimo au safu ndogo katika mwamba. Hali ya hewa ikishuka chini ya 0° C majai haya yanaganda na kupanuka hivyo kuvunja mwamba. Mmomonyoko uliosababishwa na wanadamu Mabadiliko kutokana na kazi za kibinadamu yalisababisha mara nyingi mmomonyoko wa ghafla unaoshtusha na kuleta hasara. Mfano ni kukata miti hasa kwenye mitelemko ya milima au kulima milimani. Kazi hizi zinapunguza au kuondoa kabisa funiko la mimea na kuacha udongo bila hifadhi. Maji ya mvua na upepo hazina vizuizi tena. Matokeo yake ni mafuriko ya ghafla kwa sababu wakati wa mvua maji huteremka haraka na mara moja yakichimba mifereji, kuharibu nyumba, kuua watu na kuondoa ardhi yenye rutuba kwenye mashamba. Njia nyingine ni mmomonyoko kutokana na kuzidi kwa mifugo. Kazi ya kukanyaga kwa miguu mingi hasa kwenye njia zilezile zinazotumika kuzunguka kati ya boma, maji na sokoni kumeleta uharibifu mwingi. Kwato za mifugo kama ng'ombe, mbuzi, punda na wanyama wengine wafugwao huathiri udongo mara wanapokanyaga mara kwa mara na hivyo hufanya udongo huo kuwa rahisi kusombwa na wakala wa mmomonyoko, kama vile maji, barafu na upepo. Jiolojia Ekolojia
2522
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liwali
Liwali
Kwa "wali" kama chakula tazama wali (chakula) Liwali au wali ni cheo cha msimamizi wa eneo fulani. Cheo cha Kiarabu Asili ni neno la Kiarabu "الوالي" al-wali linalomaanisha mtawala wa mahali au eneo asiyejitegemea bali aliyeteuliwa na serikali kushughulikia mambo ya utawala katika eneo fulani. Mara nyingi katika nchi za utamaduni wa Uislamu Wali alisimamia "wilaya". Kazi yake ililingana na "gavana". Cheo cha Uswahilini Katika eneo la Waswahili neno al-wali lilikuwa "liwali" na lilimtaja mkuu wa mahali au wa mji. Masultani wa Zanzibar waliteua maliwali kwa ajili ya miji ya pwani waliokuwa wawakilishi wa sultani mahali walipo. Mwaka 1886 kulikuwa na maliwali wafuatao wa Zanzibar kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki: Tungi, Mikindani, Lindi, Kilwa Kivinje, Kikunye, Kisiju Cheo cha kikoloni Katika mfumo wa utawala wa Kiingereza katika Afrika ya Mashariki liwali ilikuwa cheo cha afisa wa ngazi ya juu zaidi kilichopatikana kwa wazawa katika utawala wa miji. Cheo hiki kiliendelezwa kwenye pwani ya Kenya baada ya Uingereza kuchukua mamlaka juu ya pwani kutoka Sultani wa Zanzibar; liwali alipaswa kuwa Mwislamu. Alisimamia mahakama ya liwali iliyokuwa ngazi ya juu za mahakama za Kiislamu zilizoamua kesi za mali, ndoa na urithi baina ya Waislamu waliokuwa Waafrika wazalendo au kutoka nchi nyingine, Waarabu au Wahindi. Katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Wajerumani waliendelea mwanzoni na maliwali waliorithi kutoka kwa Sultani lakini baadaye nafasi yao ilichukuliwa na afisa Mjerumani. Baada ya eneo kutekwa na Uingereza na kuitwa Tanganyika cheo cha liwali kilirudishwa mwaka 1921 kama cheo cha "native administration" ya miji. Kwa mfano mjini Dar es Salaam liwali alikuwa daima Mwislamu kutoka ukoo wa Kiarabu hadi uhuru. Aliwajibika na usimamizi wa mahakama yake alikoshika pia nafasi ya jaji akasimamia pia ukusanyaji wa kodi. Alikuwa na haki ya kuamulia adhabu ya kiboko "hadi viboko sita". Tanbihi Marejeo James Norman Dalrymple Anderson, Islamic Law in Africa, reprint Routledge, 2008, ISBN 0415426006, 9780415426008 James R. Brennan & alii, Dar es Salaam. Histories from an Emerging African Metropolis, African Books Collective, 2007, ISBN 9987449700, 9789987449705 James R. Brennan, Taifa: Making Nation and Race in Urban Tanzania, Ohio University Press, 2012, ISBN 0821444174, 9780821444177 Cheo
2523
https://sw.wikipedia.org/wiki/Azimio%20la%20Dodoma
Azimio la Dodoma
Azimio la Dodoma ni makubaliano ya wanablogu wa Kiswahili wa Tanzania waliokutana jijini Dodoma kuhusu njia za kuendeleza blogu za wanablogu wa Tanzania kwa kuwa na maadili yanayoendana na utu, heshima, na kanuni za uandishi wa habari. Mkutano huo ulifanyika 7 Aprili 2006. Viuongo vya nje Azimio la Dodoma Blogu za Kiswahili Blogu za Watanzania Blogu za Wakenya Mradi wa Global Voices Masomo kwa wanablogu wapya Blogu Dodoma
2529
https://sw.wikipedia.org/wiki/Urithi%20wa%20Dunia
Urithi wa Dunia
Urithi wa Dunia ni maeneo yenye thamani kubwa ya kiutamaduni au kimazingira duniani yanayoangaliwa na shirika la UNESCO. Hadi Septemba 2023 sehemu 1,172 katika nchi 166 zimekubaliwa. Nchi zinazoongoza kwa wingi wa mahali ni Italia (59) na China (57) zikifuatwa na Ujerumani (52), Ufaransa (51) na Hispania (50). Afrika ina mahali 147 (8.56%) katika nchi 46, zikiongoza Afrika Kusini (10), Ethiopia na Moroko (9), Tunisia (8), Algeria, Misri, Senegal na Tanzania (7). Orodha rasmi ya UNESCO ina mahali 913 pa urithi wa dunia wa kiutamaduni na mahali 220 pa urithi wa dunia wa kimazingira, mbali ya 39 pa mseto. Mwanzo wa jitihada za kuhifadhi urithi wa dunia ulikuwa ujenzi wa bwawa la Assuan lililoelekea kuzamisha majengo mbalimbali ya utamaduni wa Misri na Nubia wa kale chini ya maji. Wakati ule UNESCO ilifaulu kukusanya pesa ili hekalu la Abu Simbel liweze kuhamishwa mlimani kabla ya kujaa kwa bwawa. Tangu 1972 kuna mkataba wa kimataifa wa Stockholm kuhusu hifadhi ya urithi wa dunia kiutamaduni na kimazingira. Kila mahali panapopendekezwa ili pakubaliwe panahitaji angalau sifa moja kati ya sita zifuatazo: kuwa na thamani ya pekee ya kisanii kuwa na athira muhimu katika eneo fulani au kipindi cha historia kuwa kitu cha pekee kisichopatikana tena au kuwa na umri mkubwa kuwa mfano bora wa kipindi fulani cha historia ya ujenzi kuwa muhimu katika uhusiano na fikra muhimu au watu muhimu wa historia Kamati ya Urithi wa Dunia hukutana kila mwaka na kuangalia maombi ya kupokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Kamati inapokea taarifa kuhusu hifadhi na hali ya urithi uliopo tayari orodhani. Kila baada ya miaka miwili orodha inatolewa upya. Viungo vya nje Tovuti rasmi kwa Kiingereza UNESCO World Heritage portal – Official website (in English and French) The World Heritage List – Official searchable list of all Inscribed Properties KML file of the World Heritage List – Official KML version of the list for Google Earth and NASA Worldwind UNESCO Information System on the State of Conservation of World Heritage properties – Searchable online tool with over 3.400 reports on World Heritage sites Official overview of the World Heritage Forest Program Convention Concerning the Protection of the World Cultural and Natural Heritage – Official 1972 Convention Text in 7 languages The 1972 Convention at Law-Ref.org – Fully indexed and crosslinked with other documents Protected Planet — View all natural world heritage sites in the World Database on Protected Areas World Heritage Site – Smithsonian Ocean Portal Time magazine. The Oscars of the Environment – UNESCO World Heritage Site UNESCO chair in ICT to develop and promote sustainable tourism in World Heritage Sites Umoja wa Mataifa UNESCO !
2532
https://sw.wikipedia.org/wiki/Somalia
Somalia
Somalia (kwa Kisomali: Soomaaliya), ambayo inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika Pembe ya Afrika. Kijiografia, imezungukwa upande wa kaskazini-mashariki na Ethiopia na Jibuti, na upande wa magharibi ya kati na Kenya; Ghuba ya Aden nayo iko mashariki. Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Mogadishu (wakazi 2,120,000). Jiografia Historia Ukoloni wa Italia Kuanzia mwaka 1888 Italia ilijipatia mikataba ya ulinzi na masultani mbalimbali waliotawala maeneo madogo kwenye Pembe ya Afrika. Walitangulia 1889 na sultani ya bandari ya Hobyo na mtawala wa usultani wa Majerteen. Mwaka 1892 Usultani wa Zanzibar ulikodisha bandari ya Banadir kati ya Mogadishu hadi Brava kwa Italia. Mwaka 1905 Italia ilinunua eneo hili kutoka Zanzibar na kulitangaza kuwa koloni na Mogadishu kuwa mji mkuu. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waitalia walikabidhiwa na Uingereza eneo la Kismayu. Walilitawala kwa jina la "Oltre Giuba" (ng'ambo ya mto Juba) na kuliunganisha na Somalia ya Kiitalia tarehe 30 Juni 1926. Wakati uleule waliamua kumaliza hali ya sultani za Majarteen na Hobyo kuwa nchi lindwa na kuzifanya sehemu kamili za koloni. Mipango hiyo ilisababisha vita kali ya miaka miwili kwa sababu masultani waliona mikataba yao ya ulinzi ilivunjwa wakapinga jeshi la Italia. Mwaka 1936 Somalia ikaunganishwa na Ethiopia kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kiitalia. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia makoloni ya Italia yalivamiwa na Uingereza uliotawala Somalia tangu 1941. Mwaka 1949 Somalia ilirudishwa mikononi mwa Italia ilisimamie kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Ukoloni wa Uingereza Uingereza uliingia katika eneo hili baada ya Misri kuondoka mwaka 1885 kwa kushindwa na jeshi la Mahdi huko Sudan. Uingereza uliingia kwa sababu iliona umuhimu wa kutawala pande zote mbili za Bab el Mandeb ikihofia uenezaji wa nchi nyingine za Ulaya, hasa Ufaransa iliyokuwa na koloni la kwanza ya Ubuk (Obok) katika Jibuti ya leo tangu 1862. Pamoja na hayo Waingereza walitegemea kununua nyama kwa ajili ya mji wa Aden na meli zilizopita hapo kati ya Uhindi na Ulaya. Somaliland ilitawaliwa awali kama mkoa wa Uhindi wa Kiingereza ikawa baadaye chini ya wizara ya makoloni huko London. Hata kama Uingereza haukuwa na nia ya kuingilia mno maisha ya wenyeji ulikutana na upinzani mkali kuanzia mwaka 1899 kutoka kwa kiongozi wa dini Diiriye Guure, aliyeitwa na Waingereza "Mullah majununi". Waingereza walijibu kwa ukatili katika vita vya miaka 20 iliyoua takriban theluthi moja ya wakazi wote wa eneo. Mwishowe Uingereza iliweza kumaliza upinzani kwa teknolojia mpya ya eropleni za kijeshi zilizotumia mabomu na bunduki za mtombo kutoka angani kwa mara ya kwanza katika Afrika. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia eneo likatwaliwa na Italia katika Agosti 1940 lakini lilichukuliwa tena na Uingereza katika Machi 1941. Uhuru Mwaka 1960 utawala wa kikoloni ulikwisha na Somalia ikapata uhuru wake, ikiunganisha makoloni mawiliː la Waitalia (kusini) na la Waingereza (kaskazini). Baada ya mwaka 1991 nchi ya Somalia ilibaki haina serikali wala umoja wa taifa, bali iligawiwa na wakereketwa na wanamgambo wa ukoo na eneo, hasa Somaliland, Puntland na Galmudug upande wa kaskazini. Katika miaka 2008-2013 ilihesabika kama nchi filisika. Kwa sasa ni nchi dhaifu lakini inaanza kujengwa upya kama shirikisho na kujiandaa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Watu Tazama pia: Orodha ya lugha za Somalia Wakazi asili wa Somalia ni Wasomali (85%) wa makabila yafuatayo: Isaaq Hawiye Dir Darod Digil & Mifle Wengine (15%) ni: Wabantu Waarabu n.k. Kisomali ndiyo lugha ya kawaida ya wakazi wengi na lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Kati ya lugha nyingine zinazotumika nchini, mojawapo ni Kiswahili (lahaja za Chimbalanzi na Kibajuni). Upande wa dini, 99.8% ni Waislamu, hasa Wasuni. Wakristo hawafikii 0.1%. Utawala Maeneo (umoja: gobolka, wingi: gobollada) ya Somalia, ambayo imegawiwa tena katika wilaya, ni 18: Mawasiliano Mawasiliano ya Jamhuri ya Somalia ilikaribia kuangamia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa sasa kampuni za binafsi za mawasiliano ya mitambo, zimetwaa karibu miji yote Somalia, na hata kutoa huduma njema kuliko nchi zilizo jirani. Somalia ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina mawasiliano ya bei rahisi zaidi, pengine kwa kuwa Somalia haikuwa na serikali iliyotoza ushuru; (Telecoms thriving in lawless Somalia) Kampuni zinazohudumia watu wa Somalia ni kama: SOMTEL Galkom Global Internet Company Hormuud Telcom Nationlink Netco STG Dahabshiil Tazama pia Utamaduni wa Somalia Uislamu nchini Somalia Waandishi wa Somalia Muziki wa Somalia Uchumi wa Somalia Vita vya Mogadishu Mawasiliano nchini Somalia Orodha ya kampuni za Somalia Jeshi la Somalia Usafiri nchini Somalia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo Mauri, Arnaldo, Somalia, in G, Dell'Amore (ed.), "Banking Systems of Africa", Cariplo-Finafrica, Milan, 1971, pp. 209–217. Shay, Shaul. Somalia in Transition Since 2006. Piscataway, NJ: Transaction Publishers, 2014. Viungo vya nje Federal Government of Somalia Somalia profile from the BBC News Habari, mitandao inayojadili kuhusu Somalia. AllAfrica.com - Somalia Habari International Freedom of Expression eXchange: Somalia Somalia - A Country Study Habari za kawaida BBC habari barabara - Somalia: Kutoka kwenye mbomoko? interneti- CIA World Factbook - Somalia Somali Planet Networks'' US State Department - Somalia includes Background Notes, Country Study and major reports Better off Stateless: Somalia Before and After Government Collapse Watambuzi Anarchy and Invention: Vipi Kampuni za Somalia zaweza kufanya biashara bila serikali? Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi za Kiarabu
2550
https://sw.wikipedia.org/wiki/Barafuto
Barafuto
Barafuto huitwa pia "mto wa barafu". Ni kanda kubwa la barafu iliyoanza kutambaa kutokana na uzito wake ikifuata graviti kwenye mtelemko. Kwa sababu hiyo barafuto zinapatikana hasa mlimani. Asili ya barafu ya barafuto Barafuto zimetokana na theluji inayokaa miaka mingi bila kuyeyuka katika mazingira baridi. Theluji mpya inakaa juu ya theluji ya miaka iliyotangulia. Uzito wa theluji ya baadaye inakandamiza ile ya chini. Kutokana na shindikizo hili theluji ya chini hubadilika kuwa barafu kabisa. Barafuto ni kati ya nguvu kubwa za mmomonyoko duniani. Afrika ina barafuto ndogo kadhaa juu ya mlima Kilimanjaro na mlima Kenya lakini zinaelekea kupotea kutokana na uhaba wa mvua itakayobadilika kuwa theluji mpya. Zamani za enzi ya barafu kiwango cha barafu kwenye ncha ya kaskazini kilikuwa kikubwa kiasi cha kusababisha barafuto kutokea zilizosukuma barafu hadi Ulaya ya Kati. Jiografia
2551
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utaridi
Utaridi
Utaridi (alama: ; kwa Kiingereza Mercury) ni sayari iliyo karibu zaidi na jua letu katika mfumo wa Jua. Jina la sayari Jina lake limetokana na Kiarabu عطارد (soma ʿuṭaarid) inayomaanisha "mwendo wa haraka" kwa sababu kasi ya Utaridi inapita mwendo wa sayari nyingine kutokana na njia yake fupi ya kuzunguka Jua katika siku 88 pekee. Majina ya Wagiriki wa Kale "Hermes" na Waroma wa Kale "Mercurius" yalikuwa majina ya mungu wao aliyekuwa na kazi ya kuwasilisha habari za miungu wengine aliyeaminiwa kuwa na kasi kubwa kwa kazi hii: chaguo hili lilitokana na tabia ileile ya sayari. Jina hili la Kiroma Mercurius limeingia katika lugha nyingi za Ulaya. Umbo la Kiarabu limekuwa jina la watu katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Kiislamu, pia jina la sayari ya kwanza kwa mfano katika Kituruki na Kimalaysia. Katika vitabu kadhaa vya Kiswahili sayari inaitwa Zebaki lakini hii inaonekana ni kosa lililotokana na jina la Kiingereza "Mercury" kwa sayari hii. Mercury ni pia jina la metali inayoitwa zebaki kwa Kiswahili kutokana na Kiarabu زئبق (soma ziʾbaq). Mara chache neno "utaridi" limetumiwa kutaja sayari kibete ya "Pluto" lakini hii ni kwa kukosea pia. Tabia za Utaridi Utaridi ni sayari ndogo. Kipenyo chake kwa ikweta ni 4879.4 km. Kwa sababu iko karibu sana na jua ina mbio za haraka. Mwaka wa Utaridi ambayo ni muda wa kuzunguka jua ni siku 88 za dunia pekee. Inazunguka kwenye mhimili wake katika muda wa siku 58.6 za dunia. Kutokana na kuwa karibu na jua kuna joto kali upande unaotazama jua lakini upande wa usiku ni baridi kabisa kutokana na uhaba wa hewa inayoweza kutunza halijoto. Halijoto ya wastani ni +178.8 °C, (usiku -183.15 °C na mchana +426.85 °C). Mwaka 2012 barafu ya maji ilitambuliwa kwenye data kutoka chombo cha angani MESSENGER iliyochunguza sayari hii. Barafu inapatikana karibu na ncha ya kaskazini isiyofikiwa na miale ya jua. Uhaba wa hewa umesababisha uso wa sayari kujaa mashimo ya kasoko. Kasoko hizi zimesababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Angahewa kama duniani ingeangamiza meteoridi ndogo na kusababisha kupasuka kwa kubwa lakini Utaridi zote zinafika usoni bila kizuizi. Alama za meteoridi ni mmomonyoko wa pekee unaoonekana hakuna dalili ya mmomonyoko kutokana na hewa au maji ya awali. Kutokana na kuwa karibu sana na jua Utaridi inaonekana kama nyota kwa macho katika masaa ya pambazuko na machweo pekee. Tanbihi Sayari
2552
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mshtarii
Mshtarii
Mshtarii (alama: ; pia Mshiteri, Mushtarii au Mshatira, kutokana na Kiarabu المشتري al-mushtari; na hata Jupita kutokana na Kiingereza Jupiter) ni sayari ya tano toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake. Mshtarii ni sayari kubwa kabisa ya jua letu. Masi yake inazidi mara mbili na nusu masi ya sayari zingine zote pamoja. Angahewa Mshtarii haina uso unaoonekana. Sehemu kubwa ya masi ya sayari ni elementi nyepesi kama hidrojeni na heli ambazo ni gesi katika mazingira ya duniani. Hii ndiyo sababu ya kwamba sayari kubwa za Mshtarii pamoja na Zohali huitwa "sayari jitu za gesi". Kadiri gesi hizo zinavyopatikana chini zaidi (yaani kuelekea ndani) uzito wa matabaka ya juu unaongeza shinikizo katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili (majimaji) inayobadilika kuwa mango (imara) ndani zaidi. Zamani iliaminika ya kwamba sayari yote ni ya gesi iliyoganda lakini siku hizi wataalamu wa astronomia huamini kwamba kuna kiini cha mwamba au metali. Doa jekundu linaloonekana usoni mwa angahewa ni dhoruba ya tufani kubwa sana iliyotazamwa tangu darubini za kwanza zilipopatikana. Duniani tufani zinapotea kwa kawaida baada ya wiki kadhaa lakini doa jekundu limeendelea bila kusimama kwa miaka 300. Miezi Mshtarii ina miezi 79 iliyotambuliwa hadi mwaka 2018. Miezi minne mikubwa ilitambuliwa mwaka 1610 na Galileo Galilei aliyekuwa kati ya wanaastronomia wa kwanza kutumia darubini. Ndiyo Io, Europa, Ganimedi na Kallisto. Ukubwa wa Ganimedi unakaribia kipenyo cha Utaridi ukipita kile cha Pluto. Miezi 63 huwa na kipenyo chini ya kilomita 10. Mwezi mdogo kabisa wa Mshtarii unajulikana kwa namba tu na una kipenyo cha km 1. Tanbihi Sayari Mshtarii
2553
https://sw.wikipedia.org/wiki/Laki
Laki
Laki (pia Lakhi) ni neno lenye asili ya Kihindi linalotumika kutaja namba 100,000, ambayo inafuata 99,999 na kufuatwa na 100,001. Inaweza kuandikwa pia 105. Kwa mfano, Mji una wakazi laki tano, yaani mia tano elfu. Namba 650,000 inaweza kusomwa "laki sita na nusu". Neno limeingia katika Kiswahili kutokana na historia ndefu ya mawasiliano ya kibiashara kati ya Bara Hindi na pwani ya Afrika ya Mashariki. Pengine inasikika kwamba wingi wake ni neno lukuki, lakini matumizi ya kawaida ni tofauti. Viungo vya nje Namba
2555
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi
Mwezi
Mwezi (alama: ) ni gimba la angani linalozunguka sayari, sayari kibete au asteroidi fulani. Kuna miezi mingi katika anga-nje. Vipindi vya kuonekana kwa mwezi wa Dunia vilisababisha matumizi ya "mwezi" kama majira ya wakati. Mabadiliko ya kuonekana kwake yalisababisha katika Kiswahili neno "mwezi" litumike kama kipindi cha wakati. Awamu zake nne pengine ndizo chanzo cha majuma ya siku sabasaba. Miezi ya sayari na sayari kibete Sayari inaweza kukosa mwezi au kuwa na miezi mingi. Mshtarii na Zohali ina miezi zaidi ya 80, mingine mikubwa kama sayari ndogo, mingine midogo yenye kipenyo cha km 1 tu. Dunia yetu ina mwezi mmoja tu. Utaridi haina mwezi. Mwezi hauna nuru ya kwake yenyewe bali unang'aa kutokana na nuru ya jua inayoakisiwa usoni mwake kama kwenye kioo. Sayari na sayari kibete zenye miezi katika mfumo wa jua: Dunia: mwezi 1 Mirihi: miezi 2 Mshtarii: miezi 80 Zohali: miezi 83 Uranus: miezi 27 Neptun: miezi 14 Orkus: mwezi 1 Pluto: miezi 5 Haumea: miezi 2 Kwaoar: mwezi 1 Makemake: mwezi 1 Gongong': mwezi 1 Eris: mwezi 1 Sayari na sayari kibete zisizo na miezi katika mfumo wa jua: Utaridi Zuhura (Ng'andu) Ceres Sedna Mwezi wa Dunia yetu Mwezi wa dunia yetu ni kati ya miezi mikubwa kwenye mfumo wa Jua. Hakuna jina tofauti kuliko "Mwezi" isipokuwa watu wametumia pia jina la Kilatini "Luna" wakitaja Mwezi wetu ili kuutofautisha na miezi ya sayari nyingine. Katika Wikipedia hi tunajitahidi kuandika "Mwezi" kwa gimba linalozunguka Dunia na "mwezi" kama habari inahusu sayari nyingine. Mwezi wetu huwa na umbo la tufe lakini si tufe kamili. Kipenyo cha wastani ni kilomita 3,476 ambacho ni takribani robo ya kipenyo cha Dunia. Mwezi unazunguka dunia yetu kwenye obiti chenye umbo la duaradufu. Umbali wake na Dunia ni baina ya kilomita 363,300 hadi 405,500 kutoka Dunia. Huwa tunaangalia uso wake upande mmoja, tena uleule tu. Sababu yake ni ya kwamba mzunguko wa Mwezi kwenye mhimili wake ni sawa na kipindi cha obiti ya kuzunguka Dunia mara moja. Kipindi cha obiti yake ni siku 27 , masaa 7, dakika 43 na sekunde 11.5. Upande wa nyuma wa Mwezi uko gizani wakati sisi tunaona mwezi mpevu. Wakati wa mwezi mwandamo kwetu upande wa nyuma unapokea nuru ya Jua. . Nuru ya Mwezi hautoki kwake bali ni nuru ya jua inayoakisiwa na uso wake. Uso wa Mwezi unajaa mashimo ya kasoko yaliyosababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Mwezi hauna angahewa inayozuia mapigo ya meteoridi ndogo au kupunguzu nguvu yao jinsi ilivyo duniani. Mwezi kama kipimo cha wakati Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo linapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamo. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupita mara moja ni siku 29 na robo. Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamo hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamo tena ni kati ya siku 28 hadi 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi kinaonekana kwa watu wote.Hivyo muda wa kurudi kwa Mwezi ulikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu pamoja na kipindi cha siku. Inawezekana kipimo cha siku saba katika juma kilianza kwa kuzingatia robo 4 za mwezi wenye siku 28. Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ambayo ni kalenda ya Kiislamu. Inapanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi. Safari kwenda mwezini Mwezi wetu ni gimba la angani la kwanza ambako wanadamu wamefika. Tarehe 21 Julai 1969 mwanaanga Mmarekani Neil Armstrong alikuwa mtu wa kwanza wa kukanyaga uso wa mwezi. Wanaanga wengine 11 kutoka Marekani waliendelea kufika mwezini hadi mwaka 1972.Baadaye safari za kwenda mwezini hazikufanywa tena kutokana na gharama kubwa. Mwezi mali ya watu? Hata kama Warusi na Wamarekani walifikisha bendera zao mwezini, hawadai kuwa na mali huko. Katika mkataba kuhusu anga-nje nchi 192 za Dunia zimekubaliana kuwa Mwezi utaangaliwa sawa na maeneo ya kimataifa ya bahari. Walikubaliana kuwa ni marufuku kupeleka silaha kali kama za nyuklia angani. Mataifa mengi ya Dunia yametia sahihi mkataba huo, isipokuwa nchi chache hususan za Afrika ikiwemo Tanzania. Lakini kuna watu binafsi wanaodai kuwa na mali kwenye Mwezi. Tangu mwaka 1980 yupo Mwamerika mmoja aliyefaulu kuandikisha Mwezi kwa jina lake kwenye ofisi ya msajili wa viwanda mjini San Francisco akiendelea kuuza hati za kumiliki maeneo mwezini. Kuna pia familia moja pale Ujerumani iliyorithi hati ambako mfalme wa Prussia kwenye mwaka 1756 alitoa zawadi ya Mwezi kwa mzee wao. Taasisi ya Sheria ya Anga-Nje (International Institute of Space Law) ilitoa tamko kuwa madai haya hayana msingi wa kisheria . Vyanzo
2556
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28maana%29
Mwezi (maana)
Mwezi ni neno la kutaja mwezi (gimba la angani) - msindikizaji wa sayari mwezi (wakati) - mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka mwezi - namna ya kutaja siku za hedhi za wakinamama Makala zinazotofautisha maana
2557
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwezi%20%28wakati%29
Mwezi (wakati)
Mwezi ni mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka. Muda wa mwezi unategemea aina ya kalenda inayotumika. Mwezi kama kipimo cha wakati Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo lapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamo. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupita mara 1 ni siku 29 1/4. Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamo hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamo tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu. Inawezekana kwamba juma la siku saba lilianza kwa kuzingatia robo 4 za mwezi wa siku 28. Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ndiyo kalenda ya Kiislamu inayopanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi. Kalenda ya mwezi Katika kalenda ya mwezi ni sawa na kipindi kutoka awamu ya mwezi mpya angani hadi mwezi mpya unaofuata ni 29.53 siku. Mwezi mpya unaanza sawa na kuonekana kwa mwezi mpya jinsi ilivyo katika kalenda ya Kiislamu. Kalenda ya jua Kwa kalenda ya jua muda wa mwezi unakaribia tu muda kati ya awamu za mwezi. Katika kalenda ya Gregori miezi ina kati ya siku 28 hadi 31. Lakini vipindi hivi havina uhusiano tena na hali halisi ya awamu za mwezi wa angani mwenyewe. "Mwezi" ni lugha tu haimaanishi gimba la angani tena. Majina ya miezi Kwa Kiswahili nchini Tanzania miezi inatofautishwa kwa namba; mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu ... hadi mwezi wa kumi na mbili. Pamoja na njia hiyo, kuna majina ya Kilatini iliyofika kwenye Kiswahili kupitia lugha za wakoloni, yaani Kijerumani na Kiingereza. Ndiyo yanayotumika zaidi nchini Kenya. Majina ya miezi yenye asili ya Kilatini (majina ya Kilatini katika mabano) Januari (Ianuarius), siku 31 Februari (Februarius), siku 28* Machi (Martius), siku 31 Aprili (Aprilis), siku 30 Mei (Maius), siku 31 Juni (Iunius), siku 30 Julai (Iulius), siku 31, Agosti (Augustus), siku 31 Septemba (September), siku 30 Oktoba (October), siku 31 Novemba (November), siku 30 Desemba (December), siku 31 Februari huongezeka siku moja kufikia 29 katika miaka mirefu kufuatana na utaratibu wa kalenda ya Gregori. Majina ya Kiarabu ya miezi (Kalenda ya Kiislamu) Muharram محرّم Safar صفر Rabi`-ul-Awwal (Rabi' I) ربيع الأول Rabi`-ul-Akhir (Rabi' II) ربيع الآخر أو ربيع الثاني Jumaada-ul-Awwal (Jumaada I) جمادى الأول Jumaada-ul-Akhir (Jumaada II) (Jumaada II) جمادى الآخر أو جمادى الثاني Rajab رجب Shaaaban شعبان Ramadan رمضان Shawwal شوّال Dhul Qaadah ذو القعدة Dhul Hijjah ذو الحجة Miezi hii haina wakati maalumu katika kalenda ya jua yenye miezi Januari - Desemba, bali inabadilika kila mwaka. Kalenda Wakati Vipimo vya wakati
2559
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda
Kalenda
Kalenda ni utaratibu wa kupanga wakati. Hupatikana kama orodha ya vipindi vya wakati kama vile siku, juma, mwezi na mwaka. Kalenda mbalimbali zimejua pia vipindi vya miaka kadhaa. Kalenda inayotumika zaidi leo kimataifa ni kalenda ya Gregori iliyo muhimu kwa uchumi na biashara. Kuna pia nchi zinazotumia hasa kalenda zao za kitaifa au kalenda mbalimbali sambamba. Hasa maisha ya kidini hupangwa kufuatana na kalenda maalumu. Kihistoria palikuwako na kalenda nyingi. Migawanyo asilia ya wakati Mchana na usiku Kwa watu wengi duniani mabadiliko ya mchana na usiku ni utaratibu wa kwanza unaogawa wakati. Mchana na usiku pamoja inahesabiwa kama siku moja. Lakini kuna njia tofauti jinsi gani kuanza hesabu hiyo: asubuhi (mwanzo wa mchana) au jioni (mwanzo wa usiku) zilikuwa njia za kawaida za kuhesabu siku mpya. Tangu kupatikana kwa saa zinazoonyesha masaa hata gizani ni saa sita usiku (katikati ya usiku) inayoangaliwa kuwa mwanzo wa siku mpya. Awamu za mwezi Awamu za mwezi huonekana vizuri kwa kila mtu. Kwa sababu hii awamu hizi zilikuwa mbinu unaoeleweka rahisi kupanga siku kwa vipindi. Kipindi kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya ni kipimo kinachopatikana katika kila nchi ni siku 29 1/2. Majira kama msingi wa hesabu ya mwaka Majira au badiliko la vipindi vinavyorudi vya joto na baridi au vya ukame na mvua vilikuwa utaratibu mwingine ulioonekana kwa watu. Ila tu hesabu hii ilitegemea na mazingira na hali ya hewa katika eneo fulani. Hasa katika nchi ambako majira yanatofautiana vikali na kufuata utaratibu wa kurudia hata mimea na wanyama hufuata mwendo wa majira. Katika mazingira kama hii imewezekana kutofautisha matokeo katika maisha kufuatana na idadi ya vipindi vya baridi au vya joto au vya mvua vilivyopita tangu tokeo fulani. Mabadiliko ya mimea hutegemea mwendo wa jua na idadi ya mwanga pamoja na joto linalopatikana katika sehemu mbalimbali za dunia. Katika nchi karibu na ikweta tofauti hizi mara nyingi si kali sana na majira hazionekani vizuri isipokuwa majira ya mvua na ukame. Katika nchi hizi kalenda za kale mara nyingi zilitegemea nyota hasa Zuhura (Ng'andu) na mahali angani inapoonekana asubuhi au jioni kwa wakati fulani. Kilimo na mwanzo wa Kalenda Inaaminika ya kwamba tangu kuanza kilimo watu wameanza pia kushika kumbukumbu ya wakati. Katika nchi nyingi kupanda na kuvuna kunategemea mwendo wa majira yanayorudia. Kazi ya pamoja inahitaji mpangilio na lugha ya pamoja. Hapa ni mwanzo wa kalenda. Aina za kalenda Kutokana na migawanyo asilia ya wakati zilitokea njia mbalimbali jinsi ya kupanga wakati katika kalenda. Kutokana na hapo kuna hasa kalenda ya mwezi, kalenda ya jua na kalenda ya lunisolar (=kalenda jua-mwezi) inayounganisha mwaka kufuatana na mwendo wa jua na vipindi halisi vya mwezi. Kalenda za mwezi Kalenda hizi hufuata awamu za mwezi. Kutoka mwezi mwandamu (=mwezi mpya) hadi mwezi mwandamu unaofuata ni muda wa siku 29 na nusu. 12 za vipindi hivi ni takriban sawa na mwaka 1 yaani kipindi hadi kurudia kwa majira kama joto au baridi. Lakini kuna tofauti kati ya mwaka wa jua unaotawala kurudi kwa majira baada ya siku 365 ¼ na muda wa miezi halisi 12 mwenye siku 354 pekee. Hii ni hasara ya kalenda ya mwezi ya kwamba baada ya miaka kadhaa hailingani tena na majira kwa hiyo ni vigumu kupanga kilimo kufuatana na kalenda hii. Lakini katika maeneo ya dunia ambako majira si muhimu vile kalenda za mwezi zinaendelea kutumiwa. Mfano maarufu wa kalenda ya mwezi ni kalenda ya Kiislamu; hapo kipindi cha „mwezi kinalingana kabisa na awamu za mwezi angani na baada ya miezi 12 ya aina hii mwaka mpya mwenye muda wa siku 354.3 unaanza tena. Ilhali mwaka huu una upungufu ya siku 11-12 kulingana na mwaka wa jua sikuu zake „zinatembea“ kutoka majira hadi majira; katika mazingira ya jangwa ya Uarabuni ulikotokea kilimo na majira hayakuwa muhimu vile. Kalenda ya Jua Nchi nyingi za dunia zinategemea kilimo. Kilimo hufuata majira ya hali ya hewa. Majira haya hutawaliwa na jua yaani na kiasi cha mwanga na nishati zinazofika dunianikutoka kwa jua na hii inabadilika kutokana na umbali wa jua unaobadilika katika mwendo wa dunia kuzunguka jua letu. Mwendo huu wa dunia kuzunguka jua unachukua siku 365 ¼ kwa hiyo watu katika tamaduni mbalimbali baada ya kugundua muda huu walitunga kalenda zilizoshika mwendo huo. Kalenda hizi zinaweza kugawiwa kwa namna mbalimbali lakini mara nyingi zinatumia vipindi 12. Vpindi hivi vinaweza kuitwa „mwezi“ lakini havina uhusiano tena na awamu halisi za mwezi. Kalenda ya jua maarufu ni kalenda ya Gregori iliyokwa kalenda ya kimatifa hasa. Kalenda jua-mwezi (lunisolar) Kalenda jua-mwezi zinalenga kuunganisha mwaka wa jua na mwendo wa majira kwa pande mmoja na awamu halisi za mwezi kwa upande mwingine. Kwa hiyo kalenda hizi zinatumia vipindi vya mwaka vya mwezi yaani miezi halisi 12. Kila baada ya miaka 2 – 3 kuna mwaka mrefu mwenye miezi 13. Kwa njia hii upungufu wa mwaka wa mwezi kulingana na mwaka wa jua unasawazishwa. Mifano mashuhuri wa hesabu hii ni kalenda ya Kiyahudi na Kalenda ya Kichina. Hesabu ya mwaka Kalenda zote hutumia hesabu inayoanza kwenye tarehe fulani ya chanzo. Kalenda ya kimataifa (=Kalenda ya Gregori) huanza hesabu yake katika mwaka ulioaminiwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo na hesabu hii huitwa baada ya Kristo. Hesabu hii imefikia baada ya mwaka 2010. Kalenda ya Kiislamu huanza hesabu yake katika mwaka wa hijra yaani kuondoka kwa Muhamad kutoka Maka kwenda Madina. Hesabu hii imefika zaidi ya miaka 1430. Kalenda ya Kiyahudi inaanza hesabu katika mwaka ulioaminiwa kuwa uumbaji wa dunia na leo imefikia hesabu ya zaidi ya miaka 5770. Kalenda za Kisasa Hata leo hii kuna kalenda mbalimbali zinazotumiwa duniani. Kalenda inayotumiwa zaidi kimataifa ni kalenda ya Gregori inayohesabu miaka tangu Kristo kuzaliwa. Kalenda hii imepokea muundo wake kutoka kalenda ya Roma ya Kale hasa miezi na idadi ya siku zao. Kalenda nyingine inayotumiwa katika nchi kadhaa ni kalenda ya Kiislamu inayohesabu miaka tangu hijra ya Muhamad; kalenda hii hutumiwa na Waislamu wote kwa kukadiria sikukuu zao hata wakitumia menginevyo kalenda ya Gregori. Kalenda nyingine ni kalenda kama ile ya Kichina, ya Kihindi na kadhalika zinazotumiwa kwa makadirio ya sikukuu katika dini au utamaduni wao lakini kwa maisha ya kawaida watu wengi wanatumia kalenda ya Gregori. Nchi kadhaa huwa pia na namna ya pekee za kalenda kwa mfano Ethiopia hufuata kalenda yake inayohesabu tangu kuzaliwa kwake Kristo lakini kwa tofauti ya hesabu ya miaka 7 na miezi 3; ina miezi 13. Kalenda ya Uajemi huhesabu miaka tangu hijra lakini tofauti na Waislamu wengi hutumia mwaka wa jua si mwaka wa mwezi kwa hiyo kuna tofauti ya takriban miaka 40 hivi. Wiki Hesabu ya wiki haifuati kalenda ni kipindi cha siku 7 kinachorudia mfululizo bila kujali mwisho au mwanzo wa mwaka. Asili yake iko katika Mashariki ya Kati hasa Babeli ikasambazwa kupitia imani ya Uyahudi na Ukristo. Inaanza kwa siku ya Jumapili inayotazamiwa kidini kama siku ya kwanza ya uumbaji wa dunia na kwa wakristo pia siku ya ufufuo wa Yesu unaotazamiwa kama uumbaji wa pili. Kwa kusudi la kupanga maisha na hasa kazi wiki za mwaka zinahesabiwa kuanzia 1 - 52; hapo wiki ya kwanza na wiki ya mwisho kwa kawaida si kamili kwa sababu siku kadhaa zimo katika mwaka uliotangulia au kufuata. Tangu kuenea desturi ya wikendi yaani mapumziko ambako wengi hawafanyi kazi siku za Jumapili na Jumamosi kalenda nyingi huonyesha siku ya kwanza ya wiki ambayo ni Jumatatu kama chanzo cha wiki ya kazi. Mpangilio wa wiki kama hesabu ya siku ya kupumzika na siku za kazi umeenea kote duniani hasa kwa ofisi za serikali ingawa katika nchi nyingi watu maskini hawana nafasi za kupumzika mara kwa mara. Tazama pia Kalenda ya Gregori Kalenda ya Juliasi Kalenda ya Kiislamu Kalenda ya Kiyahudi Kalenda ya Jua Kalenda ya Mwezi Mwaka wa Jua !
2560
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sudan
Sudan
Sudan (jina rasmi: Jamhuri ya Sudan) ni nchi ya tatu kwa ukubwa katika bara la Afrika na ya kumi na sita duniani Imepakana na Misri kaskazini, Bahari ya Shamu kaskazini-mashariki, Eritrea na Ethiopia mashariki, Sudan Kusini kusini-mashariki, Afrika ya Kati na Chadi magharibi, na Libya kaskazini-magharibi. Kijiografia nchi hii huhesabiwa kama sehemu ya Afrika ya Kaskazini. Mji mkuu ni Khartoum. Majimbo ya Sudan Kusini yalikuwa sehemu ya nchi hiyo lakini yalipiga kura ya kujitenga yakapata kuwa nchi huru kuanzia tarehe 9 Julai 2011. Jiografia Ona pia: Orodha ya mito ya Sudan, Orodha ya miji Sudan Sudan iko upande wa Afrika ya kaskazini, ina pwani kwenye bahari ya Shamu kati ya Misri na Eritrea. Imetamalikiwa zaidi na mto Nile na mikono yake. Ina eneo la kilomita mraba 1,886,068 (sq mi 728,215). Ardhi yenyewe ni kiwara, lakini kuna milima upande wa mashariki na magharibi. Hali ya anga ni ya mwangaza kusini, na mikuranga kaskazini. Mvua yapatikana miezi ya Aprili na Oktoba. Uharibifu wa mazingira hasa ni kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo na utapakazi wa jangwa. Majimbo Nchi imegawiwa katika wilaya 18, zilizogawiwa tena katika kata 133. Historia Historia ya awali Nchi ilikuwa na makazi ya kudumu kuanzia milenia ya 8 KK. Katika milenia ya 5 KK watu walizidi kuhama Sahara ikigeuka jangwa wakasogea katika eneo la Sudan ya sasa (bonde la mto Nile). Mchanganyiko wa watu hao uliunda ufalme wa Kush kwenye 1700 KK. Makao makuu yalikuwa Kerma. Katika karne ya 8 KK watu wa ufalme huo waliteka Misri na kuitawala kwa karne moja hadi waliposhindwa na Waashuru. Baadaye makao makuu yalikuwa Meroe, ambapo ufalme uliendelea hadi karne ya 4 BK ukiwa maarufu kwa uhunzi kwa jina la Ethiopia. Ufalme kusambaratika Ufalme huo uliposambaratika, zilitokea falme mbalimbali katika eneo lake, mmojawapo ukiwa ule wa Nubia. Huko Ukristo ulienea katika madhehebu tofauti: yale ya Kikopti kutoka Misri na yale ya Kibizanti kutoka Roma ya mashariki. Baadaye Uislamu pia ulijitokeza katika falme hizo ukazidi kuenea hadi kuanzisha usultani wa Sennar. Mwaka 1821 mtawala wa Misri chini ya himaya ya Waturuki aliteka Sudan kaskazini. Katika miaka ya 1870 juhudi za Wazungu za kukomesha biashara ya utumwa zilisababisha kutokea kwa Mahdi. Dola la Mahdi Dola la Mahdi (kwa Kiarabu المهدية, "mahdiyya") lilianzishwa na Muhammad Ahmad Al-Mahdi mwaka 1881 alipojitangaza kuwa mahdi kufuatana na imani ya Kiislamu akaongoza uasi dhidi ya Misri iliyotawala Sudan ikisimamiwa yenyewe na Uingereza. Muhammad Ahmad Al-Mahdi alifaulu kukusanya wafuasi wengi na kushinda Wamisri. Tarehe 26 Januari 1885 jeshi lake lilitwaa mji mkuu Khartum na kumwua gavana Gordon Pasha. Al-Mahdi alianzisha mji mkuu mpya ng'ambo ya mto Nile kwa kuunda Omdurman. Wamisri na Waingereza wakatoka nje ya Sudan. Baada ya ushindi wake Al-Mahdi alikufa na homa ya matumbo. Ugomvi ulitokea kati ya makamu wake hadi 1891 wakati Abdallahi ibn Muhammad mwenye sifa ya kuwa aliongoza jeshi la mahdi wakati wa mashambulio dhidi ya Khartum alikubaliwa wa viongozi wa mahdiyya akajiita "khalifa". Khalifa Abdullahi aliimarisha utawala wake wa kuwaua wapinzani bila neema, kati yao wanafunzi na ndugu za mahdi mwenyewe. Akajenga jumba mjini Omdurman linalosimama hadi leo. Khalifa Abdullahi alijaribu kutumia teknolojia mbalimbali. Akanunua meli za mvuke za mtoni alizoziona Waingereza walizitumia pia akajenga kiwanda cha kutengenezea bunduki. Akaanzisha nyaya za mawasilaino kwa simu. Lakini kwa ujumla vita na utawala wa mahdiyya zilikuwa ziliharubu uchumi iliyoendelea kuzorota. Khalifa alifaulu kupanua utawala wake juu ya maeneo karibu yote ya Sudan ya leo lakini alishindwa kufikia jimbo la Ikweta ambako Emin Pasha aliendelea kutetea mabaki ya Sudani ya Kimisri. Itikadi ya kupanua utawala wa mahdiyya kwa njia ya jihad ilimsababisha khalifa kushambulia nchi jirani ya Ethiopia iliyotawaliwa na kaisari wa Kikristo. Mwaka 1887 akaongoza jeshi la askari 60,000 hadi Gondar. Waethiopia wakajibu kwa kushambulia Sudan mwaka 1889. Kifo cha Kaisari Yohane IV katika mapigano ya Metemma tarehe 9 Machi 1889 ililazimisha Waethiopia kurudi kwao. Lakini jeshi la mahdiyya lilipoteza wanajeshi wengi pia likadhoofika. Wakati huohuo jemadari wa khalifa Abd ar-Raħmān an-Nujumī alishambulia Misri lakini alishindwa kwenye mapigano ya Tushkah. Hii ilikuwa mara ya kwanza ya jeshi la mahdiyya kushindwa. Majaribio ya vita za jihadi dhidi ya Wabelgiji katika jimbo la Ikweta na dhidi ya Waitalia katika Eritrea yalishindikana pia. Mwaka 1895 mkuu wa jeshi la pamoja la Misri na Uingereza, jenerali Horatio Kitchener aliamua kulipiza kisasi kwa vita ya 1885 akaongoza jeshi kubwa dhidi ya Sudan. Kwa kutumia meli za mvuke kwenye mto Nile na kujenga reli akasongea mbele hadi Omdurman. Tarehe 2 Septemba 1898 jeshi la mahdiyya lilishindwa kabisa katika mapigano ya masaa matano. Safari hiyo Waingereza waliandaliwa vizuri zaidi, pia silaha mpya kama bunduki ya mtombo ziliwapa ushindi. Upande wa khalifa walikufa askari 11,000, upande wa Waingereza na Wamisri watu 400 pekee. Khalifa mwenyewe alitoroka akajenga jeshi upya na kutawala kusini mwa Sudan, lakini akauawa mwaka 1899 katika mapigano ya Umm Diwaykarat. Hivyo Waingereza walitawala Sudan pamoja na Misri hadi 1956, na Kitchener akawa gavana mkuu wa kwanza. Baada ya Uhuru Baada ya uhuru wa nchi (1956), makabila ya kusini, ambayo hayakukubali kusilimishwa, yalipigania vita ndefu hadi kupata uhuru wao. Darfur ni eneo lenye majimbo matatu ambayo imeathiriwa na vita vya kisiasa, vita vya Darfur. Kutokana na vita nyingi serikali hazikuwa imara na kulikuwa na mabadiliko ya mara kwa mara baada ya uhuru. Mapinduzi ya kijeshi ya kwanza yalitokea mwaka 1958, kisha jenerali Ibrahim Abboud alitawala hadi 1964 wakati alipopaswa kujiuzulu kutokana na upanuzi wa vita katika Sudan Kusini na upinzani wa wananchi kwenye mji mkuu. Utawala wa Nimeiry Kilichofuata kilikuwa kipindi cha serikali 3 za kiraia hadi 1969. Tarehe 25 Mei 1969 jeshi, chini ya kanali Gaafar Nimeiry, lilipindua tena serikali. Nimeiry alikuwa waziri mkuu, wakati bunge na vyama vyote vilipigwa marufuku. Nimeiry alitawala hadi 1985, na tangu 1971 alikuwa rais. Mwaka 1972 alifaulu kumaliza awamu ya kwanza ya vita ya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Sudan Kusini kwa mapatano ya Addis Ababa. Sudan Kusini ilipewa mamlaka ya kujitawala katika mambo ya ndani chini ya serikali ya kieneo. Mwanzoni Nimeiry alijaribu kuiga siasa ya Gamal Abdel Nasser nchini Misri na kutekeleza sera kadhaa za ujamaa. Utawala wake uliona upinzani kutoka kwa Wakomunisti na pia kutoka Waislamu wenye itikadi kali. Baada ya kupinduliwa kwa siku kadhaa na Wakomunisti alivunja ushirikiano na Urusi na kuanza kupokea wanasiasa wenye mwelekeo wa Uislamu mkali katika serikali yake. Tangu miaka ya 1980 alisogea zaidi upande wa Uislamu wa kisiasa. Mwaka 1983 alitangaza sharia kuwa msingi wa sheria zote na kubadilisha sheria za jinai ipasavyo. Hatua hii ilisababisha upinzani katika sehemu za nchi zisizokaliwa na Waislamu. Alivunja pia serikali ya kieneo kwa Sudan Kusini na hivyo vita ya wenyewe kwa wenywewe ilianza upya. Nimeiry alitangaza hali ya dharura iliyompa tena mamlaka za kidikteta. Mwaka 1985 aliruhusu kunyongwa kwa mwanafalsafa Mwislamu Mahmoud Mohammed Taha kwa kosa la "uasi dhidi ya Uislamu". Miezi minne baadaye Nimeiry alipinduliwa kwenye mwaka huohuo. Utawala wa Bashir Sudan ilirudi kwa miaka michache chini ya serikali ya kiraia. Mapinduzi yaliyofuata mwaka 1989 yalileta utawala wa jenerali Omar al-Bashir. Vita ya wenyewe kwa wenye iliendelea hadi mwaka 2005 ikamalizika kwa Mapatano ya Naivasha baina ya Sudan na SPLA. Sudan Kusini ilipewa miaka hadi 2011 kujitawala halafu kuwa na kura ya wananchi wa kusini kuhusu uhuru uliotangazwa mwaka uleule. Tangu mwaka 2003 Bashir alisimamia pia vita ya jeshi lake na wanamgambo dhidi ya wakazi wasio Waarabu wa Darfur waliopinga utawala wake. Tarehe 11 Aprili 2019 Bashir alipinduliwa na jeshi lake baada ya wiki kadhaa za maandamano ya wananchi wa Khartum na miji mingine dhidi yake. Kupinduliwa kwake pamoja na kipindi cha serikali ya mpito ya kijeshi vilitangazwa na waziri wa ulinzi, jenerali Awad Mohammed Ibn Auf. Ilhali waandamanaji waliendelea kupinga serikali ya kijeshi, Ibn Auf alijiuzulu tarehe 12 Aprili na siku iliyofuata, tarehe 13 Aprili, jenerali Abdel Fattah Burhan alitangaza wanajeshi wanatafuta ushirikiano wa karibu na wapinzani wa utawala wa awali<ref>[https://www.bbc.com/swahili/habari-47919489 Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapa kuung'oa utawala], BBC News Swahili 13-04-2019</ref>. Watu na makabila Kadiri ya sensa za mwaka 2008, wakazi walihesabiwa kuwa zaidi ya milioni 21.6. Kadirio ni kwamba wakazi ni karibu milioni 48 mwaka 2022. Umma wa miji kama Khartoum (pamoja na Omdurman, na Khartoum ya kaskazini) waongezeka zaidi: umma wa miji hiyo yakadiriwa milioni 6-7 na wengine wahamiaji milioni 2 ambao wamekimbia vita vya kusini, magharibi, mashariki na pia wengine kwa sababu ya ukame. Sudan ina aina mbili za utamaduni — Waafrika walio na Uarabu na Waafrika wasio Waarabu — na maelfu ya makabila na migao ya kabila, lugha tofautitofauti kwa makundi au kabila – migawanyiko hii uleta siasa za utengo na ubaguzi. Majimbo ya Kaskazini hasa ndio makubwa nchini Sudan, na pia miji mikubwa iko katika majimbo haya. Zaidi ya milioni 22 wanaoishi katika majimbo haya ni Waislamu-Waarabu na wanaongea Kiarabu, lakini wengi pia huongea lugha 70 za kikabila hasa Kinubi, Kibeja, Kifur, Kinuban, Kiingessana, kwa kikundi hiki kuna wale wavutia zaidi kama: Wa-Kababish kutoka Kordofan kaskazini, watu hawa wanaofuga ngamia; Ga’alin (الجعلين), Rubatab (الرباطاب), Manasir (المناصير) and Shaiqiyah (الشايقيّة); makabila ambao makao yao ni karibu na mito ni kama Baggara wa Kurdufan na Darfur; Wakiham Beja eneo ya bahari ya Shamu na Wanubi wa Nile kaskazini, ambao wengine wamehamishwa karibu na mto Atbara. Eneo la Shokrya kwa Wabutana, Wabataheen wamepakana na Waga’alin na Washorya, upande wa kusini-magharibi eneo ya Butana. Pia kuna Warufaa, Wahalaween na makabila mengine mingi eneo la Gazeera na kwa ufuo wa Bluu Nile na eneo ya Dindir. Hata Wanubi kusini mwa eneo la Kurdufan na Wafur upande wa magharibi. Makabila makuu Waja'alein Washigia Warubatab Washokrya Waababda Waazande Wabaggara Wabeja Waberta Wabornu Wadaju Wadinka Wafulani Wafur Wagumuz Wahausa Waingessana Wakoalib Wamahas Wamanasir Wamasalit Wamidob Wamoro Wanuba Wanuer Wanyimang Warashaida Watagale Watama Wazaghawa Lugha Nchini Sudan kuna lugha zaidi ya 70. Kati yake, muhimu zaidi ni Kiarabu, ambacho ndicho lugha rasmi pamoja na Kiingereza. (Angalia Orodha ya lugha za Sudan.) Dini Dini kubwa zaidi nchini ni Uislamu (97%). Wakristo ni hasa Waorthodoksi wa Mashariki (Wakopti, Waethiopia na Waeritrea, lakini pia Waarmenia), halafu Waorthodoksi, Wakatoliki na Waprotestanti. Elimu Vyuo Vikuu vya Sudan ni kama vile: Akademia ya Sayansi ya Utabibu Chuo Kikuu cha Wanawake cha Ahfad Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Bayan Chuo cha Watu wa Compyuta Chuo Kikuu cha Omdurman Ahlia Chuo Kikuu cha Gezira Chuo kikuu cha Khartoum Senta ya Utafiti, Mycetoma Chuo Kikuu cha Sudan cha Sayannsi na Teknolojia Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Orodha ya miji ya Sudan Uislamu nchini Sudan Elimu nchini Sudan Utamaduni wa Sudan Muziki wa Sudan Orodha ya waandishi wa Sudan Mgogoro wa Darfur Makabila ya Sudan Haki za kibinadamu nchini Sudan Janjaweed Kush Jeshi la Sudan Nubia Josefina Bakhita Marejeo Tanbihi Vitabu Brown, Richard P.C. (1992) Public Debt and Private Wealth: debt, capital flight and the IMF in Sudan. Macmillan Publishers London ISBN 0-333-57543-1. Churchill, Winston (1899; 2000). The River War — An Historical Account of the Reconquest of the Soudan. Carroll & Graf Publishers (New York City). ISBN 978-0-7867-0751-5. Clammer, Paul (2005). Sudan — The Bradt Travel Guide. Bradt Travel Guides (Chalfont St. Peter); Globe Pequot Press. (Guilford, Connecticut). ISBN 978-1-84162-114-2. Evans-Pritchard, Blake; Polese, Violetta (2008). Sudan — The City Trail Guide. City Trail Publishing. ISBN 978-0-9559274-0-9. El Mahdi, Mandour. (1965). A Short History of the Sudan. Oxford University Press. ISBN 0-19-913158-9. Fadlalla, Mohamed H. (2005). The Problem of Dar Fur, iUniverse (New York City). ISBN 978-0-595-36502-9. Fadlalla, Mohamed H. (2004). Short History Of Sudan. iUniverse (New York City). ISBN 978-0-595-31425-6. Fadlalla, Mohamed H. (2007). UN Intervention in Dar Fur, iUniverse (New York City). ISBN 978-0-595-42979-0. Jok, Jok Madut (2007). Sudan — Race, Religion and Violence. Oneworld Publications (Oxford). ISBN 978-1-85168-366-6. Mwakikagile, Godfrey (2001). Slavery in Mauritania and Sudan — The State Against Blacks, in The Modern African State — Quest for Transformation. Nova Science Publishers (Huntington, New York). ISBN 978-1-56072-936-5. O'Fahey, Rex Seán; Spauling, Jay Lloyd (1974). Kingdoms of the Sudan. Methuen Publishing (London). ISBN 978-0-416-77450-4. Covers Sennar and Darfur. Peterson, Scott (2001). Me Against My Brother — At War in Somalia, Sudan and Rwanda — A Journalist Reports from the Battlefields of Africa. Routledge (London; New York City). ISBN 978-0-203-90290-5. Prunier, Gérard (2005). Darfur — The Ambiguous Genocide. Cornell University Press (Ithaca, New York). ISBN 978-0-8014-4450-0. Welsby, Derek A. (2002). The Medieval Kingdoms of Nubia — Pagans, Christians and Muslims Along the Middle Nile. British Museum Press (London). ISBN 978-0-7141-1947-2. Zilfū, ʻIṣmat Ḥasan (translation: Clark, Peter) (1980). Karari — The Sudanese Account of the Battle of Omdurman. Frederick Warne & Co (London). ISBN 978-0-7232-2677-2. Makala "Quo Vadis bilad as-Sudan? The Contemporary Framework for a National Interim Constitution". Law in Africa'' (Cologne; 2005). Vol. 8, pp.  63–82. Viungo vya nje (kutoka kitabu cha wadadisi wa Marekani) Serikali Tovuti rasmi Majlis Watani makala rasmi ya bunge . Maarifa ya kawaida Congressional Research Service (CRS) Reports regarding Sudan –(Kutoka taarifa za baraza ya Marekani) (Idara ya mambo ya kigeni ya Marekani- Sudan yahusu maandiko zingatizi juu ya usomi na habari kuu za nchi. Habari AllAfrica.com - Sudan Viungo via Habari. Forced Migration Review Sudan issue taratibu za kutua amani Guardian Unlimited - Special Report: Sudan Sudan News Agency (SUNA) and SunaSMS government sites Yahoo! News Full Coverage - Sudan news headline links Sudan Tribune France-based (in English) Picha Sura mpya Za Sudan Picha nyingine Utalii Mengineyo Sudan.net portal Sudaneseonline.com portal Sudani.com Portal Slavery in Sudan Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi za Kiarabu Afrika ya Kaskazini Nchi za Kiarabu Bahari ya Shamu Maeneo ya Biblia
2561
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zimbabwe
Zimbabwe
Jamhuri ya Zimbabwe (iliyojulikana wakati wa ukoloni kama Rhodesia ya Kusini) ni nchi isiyo na bahari iliyoko upande wa kusini wa Bara la Afrika, kati ya mto Zambezi na mto Limpopo. Imepakana na Afrika ya Kusini upande wa kusini, Botswana upande wa magharibi, Zambia upande wa kaskazini-mashariki, na Msumbiji upande wa mashariki. Jina Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale. Eneo Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200. Mikoa ya Zimbabwe ni: Bulawayo (mji), Harare (mji), Manicaland, Mashonaland ya Kati, Mashonaland Mashariki, Mashonaland Magharibi, Masvingo, Matabeleland Kaskazini, Matabeleland Kusini na Midlands. Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni: Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa Harare, mji mkuu Chitungwiza Mutare Historia Historia ya awali Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani. Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa. Ukoloni Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890. Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia. Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu. Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980. Baada ya uhuru Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi. Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe. Watu Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k. Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi. Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) . Mawasiliano Mawasiliano ya simu na mitambo yake yanaendeshwa na Tel-One0, kampuni ya serikali. Kuna kampuni 3 za simu za mikononi: Econet Wireless, Net*One na Telecel. Tazama pia Wilaya za Zimbabwe Kata za Zimbabwe Orodha ya miji ya Zimbabwe Mawasiliano Zimbabwe Utamaduni wa Zimbabwe Orodha ya lugha za Zimbabwe Muziki wa Zimbabwe Waandishi wa Zimbabwe Mambo ya kigeni Zimbabwe Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Viungo vya nje Serikali Tovuti rasmi ya Bunge la Zimbabwe Tovuti rasmi ya serikalimirror site Habari Ardhi na siasa -BBC usanifu wa utekelezaji wa arthi. Zimbabwe destruction: (hadithi ya mtu mmoja) New Zimbabwe UK-Based independent daily newspaper AllAfrica.com - Zimbabwe news headline links IFEX - Zimbabwe press freedom violations The Sunday Mirror weekly newspaper Zimbabwe Independent weekly newspaper The Zimbabwean UK-based independent weekly newspaper (gazeti ya wiingereza) The Herald State-owned daily newspaper Zimbabwe Situation A comprehensive collection of news stories concerning Zimbabwe from different sources Haikona! Zimbabwe News Blog Taarifa ya habari Zimbabwe Wanamgambo Sokwanele Zvakwana Maelekezo (Chuo kikuu cha kolombia - Zimbabwe maelekezo ya WWW-VL Open Directory Project - Zimbabwe maelekezo Stanford University - Afrika kusini mwa Sahara: Zimbabwe maelekezo Yahoo! - Zimbabwe maelekezo Utalii Travel Overview of Zimbabwe Facts about Zimbabwe Nyingine Amnesty International (Zimbabwe) Dariro (makala ya kutafuta vifungu vya Zimbabwe) itsbho.com Leading Zimbabwean entertainment website RSF report on Zimbabwe from 2003 Writers of Zimbabwe – (makala ya muadishi kwa waandishi wa Zimbabwe) Zimbabwe Human Rights NGO Forum-(haki za kibinadamu) ZIMBABWE (viungo via taarifa) "Dead Capital" in Zimbabwe 5 year archive of Zimbabwe news updated daily Zimbabwe Crisis Habari za kuazua zilizo chapishwa wakati wa kura mnamo 2000. ZimFest Miziki ya Zimbabwe kila mwaka, Marekani kaskazini. Zimbabweb lango la taarifa Zimbabwe zwnews Lango la habari Zimbabwe Economic Development Bulletin (Maelezo ya maedeleo ya uchumi) kupoteza haki ya mali Zimbabwe na udhoofu wa uchumi. Cato Journal Kifungu cha kuanguka kwa nchi ya Zimbabwe Center for Global Development (senta ya maedeleo ya dunia) garama na mwanzo wa misukosuko Zimbabwe. Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Nchi zinazoongea Kiingereza
2563
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilindi
Kilindi
Kilindi inaweza kutaja mahali mbalimbali pamoja na Wilaya ya Kilindi katika Mkoa wa Tanga nchini Tanzania Kilindi (Kilindi), kata ya Wilaya ya Kilindi Kilindi (Chakechake), kata ya Wilaya ya Chake Chake katika Mkoa wa Pemba Kusini, Tanzania Kilindi (Unguja Kaskazini), kata ya Wilaya ya Unguja Kaskazini 'A' katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Tanzania Kilindi (Matiri), kiji katika kata ya Matiri, Wilaya ya Mbinga kwenye Mkoa wa Ruvuma, Tanzania
2565
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilaya%20ya%20Handeni
Wilaya ya Handeni
Handeni ilikuwa wilaya ya Mkoa wa Tanga katika Tanzania hadi kugawiwa katika Wilaya ya Handeni Mjini na Wilaya ya Handeni Vijijini mnamo mwaka 2012. Imepakana na wilaya ya Kilindi upande wa magharibi, wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Kilimanjaro upande wa kaskazini, wilaya ya Pangani upande wa mashariki na Mkoa wa Pwani kwa kusini. Mwaka 2002 ilikuwa na wakazi 249,572. Tarafa Wilaya ya Handeni ilikuwa na tarafa 7 kata 19 na vijiji 112. Tarafa zilizopo ni Chanika, Sindeni, Mkumburu, Magamba, Kwamsisi, Mzundu na Mazingara. Kata zilizopo nia kama zifuatazo: Chanika Kabuku Kang'ata Kiva Komkonga Kwaluguru Kwamatuku Kwamkonje Kwamsisi Kwasunga Kwedizinga Mazingara Mgambo Misima Mkata Ndolwa Segera Sindeni Vibaoni Viungo vya nje Handeni District Homepage for the 2002 Tanzania National Census H
2569
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rungwe%20%28wilaya%29
Rungwe (wilaya)
Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 8 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania yenye Postikodi namba 53500. Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya Mjini kwa magharibi. Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu. Jina la wilaya limetokana na kituo cha misioni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban km 20 kutoka Tukuyu. Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa lililoitwa kihistoria pia "Konde". Mwaka 2002 wilaya ilikuwa na wakazi 307,270. Mnamo mwaka 2013 kata 11 zilitengwa na Rungwe na kuunda Wilaya ya Busekelo. Barabara kuu kutoka Daressalaam - Iringa - Mbeya kwenda Malawi inapita eneo la wilaya. Rungwe inapokea mvua nyingi na iko kati ya maeneo yenye rutuba sana katika Tanzania. Kati ya mazao ya sokoni kuna mashamba makubwa ya chai. Tanbihi Marejeo Rungwe District Homepage for the 2002 Tanzania National Census Tanzanian Government Directory Database Wilaya za Mkoa wa Mbeya Mkoa wa Mbeya
2579
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kur%C3%B3w
Kurów
Ukitafuta mji wa New Zealand uone Kurow. Kurów ni kijiji katika Poland ya Kusini-Mashariki kwenye mto wa Kurowka. Iko katikati ya miji ya Pulawy na Lublin katika wilaya ya Lublin. Ina wakazi 2811 (2005). Katika karne ya 15 BK kijiji kilipewa cheo cha mji chini ya sheria ya mji ya Magdeburg. Katika karne ya 16 BK ikawa kati ya miji ya Poland iliyopokea Uprotestanti. Wakati wa migawanyiko ya Poland ikawa mwanzoni chini ya Austria, baadaye chini ya Urusi. Tangu 1918 imekuwa tena sehemu ya dola la Poland iliyoanzishwa upya. Wojciech Jaruzelski aliyekuwa kwanza waziri mkuu, halafu rais wa Poland kati ya 1981 hadi 1990 alizaliwa Kurow. Poland
2580
https://sw.wikipedia.org/wiki/Angola
Angola
Angola ni nchi kubwa iliyopo upande wa kusini magharibi wa bara la Afrika ikipakana na Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia. Upande wa magharibi kuna pwani ndefu ya Bahari Atlantiki. Mkoa wa Kabinda umetenganika na sehemu nyingine za nchi na unapakana na Jamhuri ya Kongo pia. Angola ni nchi tajiri kwa mafuta na madini: almasi ndiyo muhimu zaidi. Lakini nchi ni maskini kutokana na vita vya miaka 29; kwanza vita vya kupigania uhuru dhidi ya Ureno iliyofuatwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 2002. Nchi yenyewe hasa ni ya kidemokrasia na inajulikana kama Jamhuri ya Angola (kwa Kireno: República de Angola, kwa matamshi ya IPA: //; kwa lugha za wenyeji: Repubilika ya Ngola). Asili na historia ya jina 'Angola' Jina Angola linatokana na neno la lugha ya Kibantu "N’gola", ambalo lilikuwa jina la kiongozi wa ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili. Jiografia Maeneo ya Angola Angola imegawiwa katika mikoa 18 (províncias), wilaya 162 (municípios) na kata 559. Mikoa ni: Historia Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani. Katika karne za kwanza BK kutoka kaskazini walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Kuanzia karne ya 14, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, kwa mfano Dola la Kongo, Dola la Lunda na Dola la Kasanje. Dola la Kongo Dola la Kongo lilikuwa ufalme ulioenea ndani ya nchi za leo za Angola, Kongo (Kinshasa) na Kongo (Brazzaville). Ulianzishwa katika karne ya 14 ikadumu hadi karne ya 17. Mtawala wake alikuwa na cheo cha "Mwene Kongo" au "Manikongo" wa kabila la Bakongo. Ufalme huo umejulikana zaidi kihistoria kwa sababu ya mawasiliano yake ya kimataifa. Katika karne ya 15 meli za Wareno zilifika mwambaoni mwake. Wakati wa kukutana na Wareno Ufalme wa Kongo labda ulikuwa na eneo la km² 300,000 ukaunganisha robo ya magharibi ya Kongo (Kinshasa) pamoja na sehemu za Angola na Kongo (Brazzaville). Manikongo mbalimbali walijenga uhusiano na Ureno na Kongo ilikuwa taifa la kushikamana na Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kile taarifa mbalimbali ziliandikwa zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo. Manikongo alikaa katika mji wa M'banza-Kongo. Baada ya wafalme kuwa Wakristo Wakatoliki na kujengwa kwa kanisa kuu, jina la "São Salvador do Congo" (kwa Kireno: "Mwokozi Mtakatifu wa Kongo") lilikuwa kawaida kwa mji mkuu wa milki. Ufalme ukawa na majimbo, wilaya na vijiji. Majimbo yalikuwa saba ya Mpemba, Nsundi, Mpangu, Mbata, Mbamba na Soyo. Kwa mikataba ya baadaye falme za Kakongo, Loango na Ngoy likatokea shirikisho ya sehemu nne. Dola la Lunda Dola la Lunda lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1600 hadi 1850 hivi kandoni kwa mto Kasai, mpakani kwa nchi za kisasa za Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Dola la Kasanje Dola la Kasanje lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1620 hadi 1910 hivi kandoni kwa mto Kwango, upande wa kaskazini wa nchi ya kisasa ya Angola. Lilianzishwa na viongozi kutoka Dola la Lunda. Mwaka 1910 lilivamiwa na Wareno na kuingizwa katika koloni lao la Angola. Dola la Ndongo Dola lingine la kusini lilikuwa lile la Ndongo, lililopambana na Wareno miaka 30 chini ya malkia Njinga katika karne ya 17. Vita vya uhuru Mwaka 1966 Jonas Savimbi alianzisha tapo la UNITA (kwa Kireno: União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno. UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana. UNITA ilianza kama kikundi cha kikomunisti kufuatana na itikadi ya Mao Zedong. Uadui kati ya Wakomunisti wa Uchina na Urusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya MPLA (kwa Kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho) iliyosaidiwa na Urusi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe Baada ya uhuru mwaka 1975 MPLA ilitawala mji mkuu na kuunda serikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga. Savimbi alipata kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali duniani ili kuiondoa madarakani serikali ya MPLA. Savimbi alikuwa akipata misaada ya fedha na silaha toka serikali za Marekani, China, Afrika Kusini, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikijulikana kama Zaire), Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba, na Nicaragua. Tarehe 22 Machi 2002, Jonas Savimbi aliuawa vitani. Muda mfupi baadaye UNITA na MPLA zilikubaliana kusimamisha mapigano. UNITA ilichukua nafasi ya chama cha upinzani. Hata hivyo taratibu za kidemokrasia zilichelewa hadi chaguzi za miaka 2008 na 2012 na toleo la katiba mpya la mwaka 2010. Watu Sensa ya mwaka 2014 ilihesabu watu 24,383,301 na kufikia mwaka 2016 walikuwa 25,789,024. Wakazi wengi ni Waafrika, hasa wa makabila ya Waovimbundu (37%), Waambundu (23%) na Wakongo (13%). Machotara ni 2%, Wachina 1,6% na Wazungu 1%. Ingawa lugha za Kibantu zinaongoza, na 6 kati yake zina hadhi ya lugha ya taifa, lugha rasmi ni Kireno. Upande wa dini, inakadiriwa kuwa zaidi ya nusu ni Wakatoliki na robo ni Waprotestanti wa madhehebu mia tofauti. Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Orodha ya lugha za Angola Wanawake wa Angola Tanbihi Viungo vya nje Serikali Republic of Angola lango rasmi la serikali National Assembly of Angola makala rasmi(kwa kireno) Ubalozi wa angola Washington DC Habari allAfrica - Angola - viungo via habari Angola Press -idara ya Taarifa na habari ya Angola (kwa kireno, kifaransa na kingereza) Angonoticias (kwa kireno) -lango la habari lenye sifa Angola Mangole (kwa kireno) - ya habari nchini Angola na pia maelekezo ya makala kwa kompyuta. Jornal de Angola (kwa kireno) - Gazeti lenye sifa Angola Maoni BBC - Country profile: Angola CIA World Factbook - Angola US State Department - Angola includes Background Notes, Country Study and major reports Radio na Muziki Site Official de Kizomba Radio Canal Angola ONLINE Maelekezo Columbia University Libraries - Angola directory category of the WWW-VL Open Directory Project - Angola Angola kwenye Open Directory Project Stanford University - Africa South of the Sahara: Angola Tovuti mbalimbali kuhusu Angola Utalii Mambo mengine Angola Conflict Briefing Umoja wa Afrika Angola Nchi za Afrika Nchi zinazotumia Kireno Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
2581
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi%20ya%20Kenya
Shilingi ya Kenya
Shilingi ya Kenya (KES au Ksh) ni fedha za Kenya. Shilingi moja imegawanywa kwenye senti mia moja. Shilingi ya Kenya ilianzishwa mwaka 1966 baada ya kuvunjwa kwa bodi ya fedha ya Afrika ya Mashariki iliyosimamia fedha ya pamoja ya Kenya, Tanzania na Uganda iliyoitwa East African Shilling iliyotumiwa katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Kuna sarafu za shilingi 1, 5, 10, 20 na 40. Sarafu za senti zipo za zamani za senti 1, 5, 10, 20 na 50 lakini hazinunui kitu tena. Noti zilitolewa za shilingi 5, 10, 20, 50, 100, 200, 500 na 1000 ingawaje noti za shilingi 5, 10 na 20 ni nadra sana kuonekana. Shilingi 1 = Senti 100 Majina ya zamani: Thumuni 1 = Senti 50 Peni 1 = Senti 10 Ndururu 1 = Senti 5 Sarafu Benknoti Pesa Kenya
2582
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ikweta
Ikweta
Ikweta ni mstari unaogawa dunia katika sehemu mbili (kaskazini na kusini) kwenye umbali sawa kati ya ncha ya kaskazini na ya kusini. Baina ya nchi za Afrika ni Somalia, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Gaboni na Sao Tome na Principe ambazo ziko kwenye mstari wa ikweta. Katika Amerika ikweta inapita Ekwado (jina limetokana na neno la ikweta kwa Kihispania), Kolombia na Brazili. Katika Asia ikweta inapita funguvisiwa ya Indonesia. Jiografia
2587
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamerun
Kamerun
Jamhuri ya Kamerun (pia: Cameroon) ni jamhuri ya muungano katika Afrika ya Magharibi. Imepakana na Nigeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Guinea ya Ikweta na Ghuba ya Guinea. Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kifaransa (kinachoongoza kwa zaidi ya asilimia 80) na Kiingereza. Jiografia Mito Milima Maeneo kiutawala Kamerun imegawiwa katika mikoa (regions) 10 na wilaya (départements) 58. Mikoa ni: Mkoa wa Adamawa, Mkoa wa Kati, Mkoa wa Mashariki, Mkoa wa Kaskazini ya Mbali, Mkoa wa Pwani, Mkoa wa Kaskazini, Mkoa wa Kaskazini-Magharibi, Mkoa wa Magharibi, Mkoa wa Kusini, na Mkoa wa Kusini-Magharibi Ona pia: Orodha ya miji ya Kamerun Historia Historia ya awali Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki. Wakati wa ukoloni Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa. Tangu uhuru hadi leo Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru. Wananchi wa Kamerun ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kamerun. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kamerun. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun. Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao. Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kamerun (kwa Kifaransa République du Cameroun''). Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kamerun, lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha. Siasa Uchumi Watu Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini. Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi. Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote. Utamaduni Elimu Tazama pia Ukristo nchini Kamerun Kanisa Katoliki nchini Kamerun Uislamu nchini Kamerun Mawasiliano nchini Kamerun Mambo ya kigeni ya Kamerun Orodha ya miji ya Kamerun Jeshi la Kamerun Usafirishaji nchini Kamerun Chama cha Wanaskauti Kamerun Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Viungo vya nje Serikali Urais wa Nchi ya Kamerun Tovuti rasmi ya serikali Bunge ya Kamerun Tovuti rasmi Habari allAfrica - Cameroon viungo via habari CRTV - Cameroon Radio Television ya serikali The Post – Gazeti lenye sifa linalochapwa huko Buea Le Messager Gazeti la binafsi Radio Siantou Elimu Chama cha Wakamerun cha wanainjinia na wanasayansi za compyuta Uchambuzi BBC News - Country Profile: Cameroon (Kitabu cha wadadisi wam marekani) - Cameroon Makabila na koo Baka Pygmies of Cameroon Utamaduni na miziki ya watu wa Kamerun Anthropological researches in Cameroon Fieldwork among Cameroonian populations Bamileke, watu wa Kamerun Bakweri, watu wa Kamerun ya Kiingereza. Miongozo CMCLICK Online! Cameroon Portal - Cameroon Cameroon Internet Community. Cameroon Business Directory. Cameroon Information. Cameroon Culture. Open Directory Project - Cameroon directory category Stanford University - Africa South of the Sahara: Cameroon Maelezo kuhusu Afrika, kusini kwa Sahara. University of Pennsylvania - African Studies Center: Cameroon directory category Yahoo! - Cameroon uelekezo, kamerun Utalii Cameroon tourism Picha kuhusu utalii kamerun Cameroon In Colour Picha za Kamerun Umoja wa Afrika Nchi za Afrika Jumuiya ya Madola Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa
2591
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sarafu
Sarafu
Sarafu (kar. صرافة badilisha) ni kipande cha metali iliyotolewa na serikali ya nchi kama namna ya pesa. Mara nyingi sarafu ina umbo la duara kama kisahani. Kuna pia sarafu za pembe tatu, pembe nne au pembe zaidi. Zamani sarafu ilikuwa umbo la kawaida ya pesa. Sarafu za kwanza zinazojulikana dunia zimepatikana kutoka Lydia katika Anatolia ya Magharibi iliyokuwa wakati ule sehemu ya utamaduni wa Wagiriki wa Kale. Sarafu zilitengenezwa hasa kwa kutumia metali ya thamani kama dhahabu na fedha, pia ya shaba na wakati mwingine ya chuma. Thamani ya sarafu ililingana na kiasi fulani cha metali hizi. Siku hizi sehemu kubwa ya fedha inatolewa kama noti yaani kama karatasi. Karibu popote duniani sarafu hutumika kwa ajili ya pesa ndogo tu. Isipokuwa sarafu za dhahabu zinatolewa kwa idadi ndogo hasa kwa ajili ya watu wanaopenda kukusanya aina mbalimbali za sarafu zenye thamani ingawa hazitumiki kama pesa ya kulipia. Sarafu za kihistoria Pesa
2592
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiolwa%20cha%20angani
Kiolwa cha angani
Kiolwa cha angani (pia: gimba la angani, kwa Kiingereza: astronomical object au celestial body) ni jina la jumla kwa ajili ya vitu vinayopatikana katika anga ya ulimwengu. Kwa Kiingereza istilahi "object" (kiolwa) na "body" (gimba) mara nyingi hutumiwa kama visawe. Lakini ilhali kila gimba la anga-nje ni pia kiolwa cha anga-nje, kinyume chake si kweli. Gimba la anga-nje ni kitu kimoja cha pekee, kama vile sayari, mwezi, asteroidi. Kiolwa cha anga-nje ni wazo pana zaidi, likitaja pia mambo kama galaksi au nebula yenye sehemu nyingi ndani yake. Kati ya violwa vya anga-nje huhesabiwa: Jua Sayari Sayari kibete Miezi Vimondo (pia meteori au meteroidi) Asteroidi Nyotamkia Nyota Galaksi Nebula Mawingu katika anga Hivyo vyote ni violwa asilia. Vitu vilivyoko kwenye anga-nje vilivyotengenezwa na binadamu ni vyombo vya anga-nje. Hapa kuna swali kama mabaki kutokana na vyombo vya anga-nje vilivyovunjika au takataka ya angani yanayotokana na safari za anga-nje yanastahili kuitwa kwa neno hili. Elimu ya violwa vya anga-nje ni astronomia.
2593
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nebula
Nebula
Nebula ni neno linalotumika kwa ajili ya kutaja eneo angavu na jeupejeupe linaloonekana angani ama kwa macho au kwa darubini. Zamani hata galaksi ziliweza kuitwa "nebula". Galaksi ya Andromeda iliyokuwa galaksi ya kwanza kutambuliwa angani ilikuwa inaitwa "Andromeda Nebula". Siku hizi neno linataja wingu kubwa linalong'aa. Maada yake inaweza kuwa gesi ya moto, vumbi na utegili. Gesi ya moto na utegili zinang'aa pekee yake; vumbi linaweza kuakisi nuru ya nyota za karibu. Mara nyingi nebula ni mahali pa kuzaliwa au kutokea kwa nyota mpya. Wakati mwingine wingu ni mabaki tu ya nyota aina ya nova, yaani nyota iliyokufa katika mlipuko mkubwa. Nebula
2594
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili
Utegili
Utegili (plasma) ni neno la kumaanisha Utegili (damu) ni yale majimaji yanayobaki kwenye damu baada ya kuondolewa kwa seli za damu kwenye damu ya vetebrata Utegili (seli) ni majimaji ndani ya seli za mwili Utegili (fisikia) ni hali ya mada kama gesi ya joto sana inaachana na elektroni Makala zinazotofautisha maana
2595
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utegili%20%28fizikia%29
Utegili (fizikia)
Utegili (pia: plasma) katika lugha ya fizikia, ni hali ya nne ya maada. Hali hiyo ni kama gesi ila ni ya kiioni. Nyinginezo ni hali mango (imara), kiowevu (majimaji) na gesi (kama hewa). Mfano wa maada mango ni jiwe la mwamba, maada kiowevu ni maji, na maada gesi ni hewa. Hivyo plasma ama utegili ni hali ya nne ambayo si ya asili katika maisha yetu ya kila siku. Huonekana katika mifumo ya kimaada iliyo katika joto kali. Plasma ni hali halisi ya jua. Lenyewe linafanyika na maada lakini si tena katika hali ya kawaida tunayoijua hapa duniani. Nayo ni kama gesi inayolipuka masaa yote na kufanya mnururiko wa nishati inayotufikia kama joto, mwanga na pia mawimbi ya plasma itufikiayo na kujidhihirisha kama aurora katika ncha ya kaskazini ya Dunia. Ikiwa gesi ni ya joto kali sana elektroni zake zinaanza kuachana na atomu zao. Tabia ya hali hii ni tofauti na hali ya gesi yenyewe. Elektroni zisizoshikwa na atomu pamoja na atomu hizo katika hali ya ioni zote zinajibu kwa uga wa sumakuumeme. Asilimia kubwa ya maada ulimwenguni iko katika hali ya utegili kwa sababu imo ndani ya nyota za angani. Kwa ajili ya matumizi ya mitambo hali ya utegili yaani ya kuionika husababishwa pia kwa leza au kwa uga wa sumakuumeme. Fizikia
2596
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghuba
Ghuba
Ghuba ni hori kubwa ya bahari inayopakana na nchi kavu pande mbili au tatu. Mara nyingi ghuba hutokana na misogeo ya ganda la dunia inayosababisha maji kujaa nafasi iliyojitokeza. Baadhi ya ghuba zinazojulikana ni kama vile Ghuba ya Guinea, Ghuba ya Uajemi, Ghuba ya Mexiko au Bahari ya Shamu. Bahari
2597
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yuri%20Gagarin
Yuri Gagarin
Yuri Alexeyevich Gagarin (kwa Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин; 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi - 27 Machi 1968) alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye Anga-nje. Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga ya Urusi mwaka 1955. Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga-nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani. Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108. Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow. Kuhusiana na kifo Cha Gagarin, maombolezo ya kitaifa yalitangazwa katika Umoja wa Kisovyeti (kwa mara ya kwanza katika historia ya USSR kwa kumbukumbu ya mtu ambaye hakuwa mkuu wa nchi). Kwa heshima ya cosmonaut ya Kwanza Ya Dunia, idadi ya makazi yalipewa jina, barabara na njia zilipewa jina. Makaburi mengi ya Gagarin yamejengwa katika miji tofauti ya ulimwengu. Stempu na sarafu Waliozaliwa 1934 Waliofariki 1968 Watu wa Urusi Wanaanga
2600
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Afrika%20ya%20Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati (kwa Kisango Ködörösêse tî Bêafrîka) ni nchi ya bara bila pwani katika Afrika ya Kati. Imepakana na Chadi upande wa kaskazini, Sudan na Sudan Kusini upande wa mashariki, Jamhuri ya Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa kusini na Kamerun upande wa magharibi. Jiografia Nchi hii, hasa inashikilia mbuga ya Sudani-Guinea, lakini pia jangwa la Sahara upande wa kaskazini na msitu wa ikweta kusini. Theluthi mbili za eneo la nchi zimetapakaa kwa mabia ya mto Ubangi unaotiririka kusini kwa Mto Kongo, na theluthi ya eneo katapakaa kwa mabia ya mto Shari, unaotiririka kusini kwa Ziwa Chadi. Historia Historia ya Kale Ukoloni wa Ufaransa Kwa sababu ya utapakazi wa eneo kwa mabia ya mto Ubangi na mto Shari, Wafaransa wakati wa ukoloni waliita nchi hii Ubangi-Shari (Oubangui-Chari kwa Kifaransa). Ilipokuwa koloni la Ufaransa, Ubangi-Shari ziliwekewa mamlaka ya madaraka kama eneo la Jamii ya Wafaransa mwaka wa 1958, lakini baadaye ilipata uhuru tarehe 13 Agosti 1960. Uhuru Kwa miongo mitatu kutoka uhuru, ‘Jamhuri ya Afrika ya Kati’ ilitawaliwa na serikali za mabavu zilizonyakua mamlaka bila kufuata taratibu za demokrasia. Kwa namna ya pekee Jean-Bédel Bokassa alitawala kuanzia tarehe 31 Desemba 1965 hadi Septemba 1979, akijifanya kaisari tarehe 4 Desemba 1976. Mwaka wa 1993, kura za kidemokrasia za kwanza zilifanywa na kumchagua Ange-Félix Patassé kuwa Rais. Lakini Rais Patassé alipinduliwa na Jenerali François Bozizé mwaka wa 2003. Baadaye huyo alishinda uchaguzi mnamo Mei 2005 na kuiongoza nchi mpaka Machi 2013 alipolazimika kukimbia. Kati ya Novemba 2012 na tarehe 23 Julai 2014 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba kwa ukatili na vinaendelea hadi mwaka 2020. Eneo Jamhuri ya Afrika ya Kati imegawiwa katika maeneo 14, yanayoitwa préfectures, na pia maeneo 2 ya uchumi (préfectures economique) na mji mmoja (commune). Maeneo hayo yamegawiwa zaidi katika wilaya 71 zinazoitwa sous-préfectures. mikoa ni: Bamingui-Bangoran, Basse-Kotto, Haute-Kotto, Haut-Mbomou, Kémo, Lobaye, Mambéré-Kadéï, Mbomou, Nana-Mambéré, Ombella-M'Poko, Ouaka, Ouham, Ouham-Pendé, na Vakaga; maeneo ya uchumi ni Nana-Grébizi na Sangha-Mbaéré; na mji ni Bangui. Watu Nchi ina watu 4,666,368 waliogawanyika katika makabila 80, kila moja likiwa na lugha ya pekee. Ile inayowaunganisha katika mawasiliano ni Kisango, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kifaransa. Kadiri ya sensa ya mwaka 2003, kati ya wakazi, 80.3% ni Wakristo (51.4% Waprotestanti na 28.9% Wakatoliki). Waislamu ni 10% na wengi wa waliobaki wanafuata dini za jadi. Tazama pia Orodha ya lugha za Jamhuri ya Afrika ya Kati Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Habari allAfrica - Jamhuri ya Afrika ya Kati kiungo cha taarifa ya habari Uchambuzi BBC News - Country Profile: Central African Republic CIA World Factbook - Central African Republic Maelekezo Open Directory Project - Central African Republic directory category chuokikuu cha Stanford – Afrika kusini mwa sahara: Central African Republic directory category The Index on Africa - Jamhuri ya Afrika ya Kati directory category chuo kikuu cha Pennsylvania – Masomo ya afrikar: Jamhuri ya Afrika ya Kati maelekezo Yahoo! - Jamhuri ya Afrika ya Kati maelekezo Makabila na koo African Pygmies Utamaduni na muziki wa watu wa Jamhuri ya Afrika, picha na ulezaji wa ukoo. Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa
2601
https://sw.wikipedia.org/wiki/Algeria
Algeria
Algeria (pia: Aljeria; kwa Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir; kwa Kiberber: Dzayer, ⴷⵣⴰⵢⴻⵔ; kwa jina rasmi "Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria") ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia. Algeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara. Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa lugha ya Kiarabu. Jiografia Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa, Sahara iko upande wa kusini. Asilimia 20 za eneo la Algeria upande wa kaskazini ni makao kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya ni pwani ya Mediteranea na milima ya Atlas. Atlas inapanda hadi kimo cha mita 2,308 juu ya UB. Sahara inaanza kusini kwa Atlas na kanda yenye nyasi chache, halafu inafuata eneo la matuta ya mchanga pasipo mimea yote. Kusini kwake tena ni nyanda za juu ambazo ni hasa maeneo ya miamba mitupu. Kusini kabisa kuna milima kama Tassili n'Ajjer na Ahaggar inayopanda hadi mita 2,918 na kuwa kama visiwa vya uoto katika jangwa. Mito ya kudumu iko kaskazini tu, sehemu za pwani. Mabonde ya mito ya ndani ni makavu, isipokuwa baada ya mvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa. Hali ya hewa Kanda la kaskazini lina hali ya hewa inayoathiriwa na Bahari ya Mediteranea. Huko halijoto kwenye mwezi Agosti ni 25 °C na 12 °C wakati wa Januari. Kwenye sehemu za juu kuna baridi na hata barafu kwenye majira ya Januari lakini joto ni kali zaidi wakati wa Julai/Agosti. Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C katika siku moja. Wakati wa joto halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka chini ya °C kwenye saa za usiku. Mvua ni haba mno: kuna miaka mfululizo bila tone hata moja. Katika milima ya Ahaggar kuna usimbishaji kidogo kutokana na ukungu, kwa hiyo miti kadhaa na mimea mingine iko. Historia Historia ya kale Historia inayojulikana ilianza na Waberber ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi asilia. Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwa Karthago uliopanua utawala wake hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini). Kumbe Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania. Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma, hivyo wakapata uhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Algeria moja kwa moja. Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa huko. Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wa Algeria na Dola la Roma lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu katikati ya karne ya 7. Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja. Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7 uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma. Uvamizi wa Waarabu Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada ya uhamisho wa serikali ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski, Waumawiya walikaza jitihada huko Afrika ya kaskazini. Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Algeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Algeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu. Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu. Ukoloni wa Wafaransa Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya miaka 1830 na 1962. Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angalia Orodha ya Marais wa Algeria. Kwa sasa Algeria inajenga upya umoja wa kitaifa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka 2002. Nchi imebaki na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wa kabila la Waberber ambao kihistoria ndio wakazi asilia. Lakini kwa lugha, utamaduni na historia Algeria ya leo ni sehemu ya dunia ya Kiarabu. Wilaya za Aljeria Kuna vitengo vya utawala 48 vinavyoitwa wilaya, zinazolingana zaidi na mikoa katika nchi zingine. Miji Algiers Annaba Mascara-Oran Temurssen Watu Wakazi wengi wana mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na ya Kiberber na wachache ya Kituruki na ya Kiberber; karibu wote (98%) wanafuata dini ya Uislamu. Wakristo ni 1%, wakiwemo Waprotestanti na Wakatoliki, lakini wengine wanashindwa kujitokeza kutokana na hofu ya dhuluma. Lugha rasmi ni Kiarabu (72%) na Kiberber (27-30%), lakini wengi sana wanaongea pia Kifaransa. Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Kujisomea Ageron, Charles-Robert (1991). Modern Algeria – A History from 1830 to the Present. Translated from French and edited by Michael Brett. London: Hurst. ISBN 978-0-86543-266-6. Aghrout, Ahmed; Bougherira, Redha M. (2004). Algeria in Transition – Reforms and Development Prospects. Routledge. ISBN 978-0-415-34848-5. Bennoune, Mahfoud (1988). The Making of Contemporary Algeria – Colonial Upheavals and Post-Independence Development, 1830–1987. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-30150-3. Fanon, Frantz (1966; 2005 paperback). The Wretched of the Earth. Grove Press. ASIN B0007FW4AW, ISBN 978-0-8021-4132-3. Horne, Alistair (1977). A Savage War of Peace: Algeria 1954–1962. Viking Adult. ISBN 978-0-670-61964-1, ISBN 978-1-59017-218-6 (2006 reprint) Laouisset, Djamel (2009). A Retrospective Study of the Algerian Iron and Steel Industry. New York City: Nova Publishers. ISBN 978-1-61761-190-2. Roberts, Hugh (2003). The Battlefield – Algeria, 1988–2002. Studies in a Broken Polity. London: Verso Books. ISBN 978-1-85984-684-1. Ruedy, John (1992). Modern Algeria – The Origins and Development of a Nation. Bloomington: Indiana University Press. ISBN 978-0-253-34998-9. Stora, Benjamin (2001). Algeria, 1830–2000 – A Short History. Ithaca, New York: Cornell University Press. ISBN 978-0-8014-3715-1. Sidaoui, Riadh (2009). "Islamic Politics and the Military – Algeria 1962–2008". Religion and Politics – Islam and Muslim Civilisation. Farnham: Ashgate Publishing. ISBN 0-7546-7418-5. Viungo vya nje Serikali El Mouradia official presidential site (in French and Arabic) National People's Assembly official parliamentary site Chief of State and Cabinet Members Maelezo zaidi Algeria from UCB Libraries GovPubs Photos From Algeria Ministère de l'Aménagement du Territoire, de l'Environnement et du Tourisme Map of Algeria Nchi za Afrika Nchi za Kiarabu Nchi za Waberber Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa
2602
https://sw.wikipedia.org/wiki/Melilla
Melilla
Melilla (tamka: me-li-ya; kwa Kiarabu: مليلية, Meliliya; jina rasmi: Ciudad Autónoma de Melilla = Mji wa kujitawala wa Melilla) ni mji wa Hispania kwenye pwani ya Mediteranea unaozungukwa na eneo la Moroko upande wa bara. Umbali na Hispania bara ni takriban km 170 kuvuka bahari. Mji ulio karibu upande wa Moroko ni Nador kwenye umbali wa km 15. Pamoja na mji wa Ceuta kisiasa ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya, kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Watu Melilla ina wakazi 65,500 (mwaka 2005) katika eneo la km² 20. Zamani wakazi walio wengi walikuwa Wakatoliki wenye asili ya Hispania pamoja na Wayahudi na Waislamu Waarabu au Waberber wenye asili ya Moroko. Miaka ya nyuma idadi ya Waislamu imeongezeka ambao wengi wao wanapendelea kujiita Waberber kuliko Waarabu; Wayahudi wamepungua sana. Inasemekana ya kwamba wakazi karibu wote wanajiangalia kuwa Wahispania bila kujali kama ni Wakatoliki au Waislamu. Uchumi unategemea uvuvi pamoja na biashara ya mpakani. Pesa rasmi ni Euro. Historia Historia yake ilianza zaidi ya miaka 2000 iliyopita ikaundwa kwa jina la Rusadir. Ikawa sehemu ya Dola la Roma katika jimbo la Mauretania Tingitana. Eneo lake lilipiganiwa kuanzia mwaka 429 BK kati ya wavamizi Wavandali na Bizanti. Karibu kabla ya mwaka 700 BK Waarabu Waislamu walivamia eneo la pwani ya Moroko wakielekea Hispania. Mji ulipata jina la Meliliya ukabaki chini ya utawala wa Kiislamu hadi mwaka 1497 ulipotekwa na Wahispania. Wahispania walifaulu kubaki na mji katika vita mbalimbali za karne zilizofuata. Mwaka 1936 vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania vilianza Melilla kwa uasi wa wanajeshi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Hispania. Miji ya Hispania
2606
https://sw.wikipedia.org/wiki/Guinea%20ya%20Ikweta
Guinea ya Ikweta
Jamhuri ya Guinea ya Ikweta (kwa Kiswahili pia: Ginekweta) ni nchi mojawapo ndogo ya Afrika iliyopo upande wa magharibi wa Afrika ya Kati. Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon upande wa kusini na mashariki, na Ghuba ya Guinea upande wa magharibi, ambapo visiwa vya São Tomé na Príncipe vinapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya Ikweta. Jina Jina la nchi linatokana na kuwa karibu na Ghuba ya Guinea na Ikweta. Jiografia Nchi ina sehemu mbili kuu. Eneo kubwa liko kwenye bara la Afrika katika kanda ya Rio Muni. Ndipo walipo wakazi wengi zaidi. Sehemu iliyoendelea zaidi, pamoja na mji mkuu, iko kwenye kisiwa cha Bioko. Pamoja na visiwa vingine, hasa Annobon, hiyo kanda ya Visiwa ni sehemu ya pili ya nchi. Historia Ilikuwa koloni la Hispania kwa jina la Guinea ya Kihispania likiwa na maeneo mawili ambayo yalijulikana kama Río Muni (bara na visiwa vidogo kadhaa), na kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Poo) ambako uko mji mkuu, Malabo (ambayo iliitwa awali Santa Isabela). Siasa Uchumi Mikoa Guinea ya Ikweta imegawiwa katika mikoa 8 iliyopo katika kanda mbili: Mkoa wa Annobón (mji mkuu wa mkoa: San Antonio de Palé) Mkoa wa Bioko Norte (Malabo) Mkoa wa Bioko Sur (Luba) Mkoa wa Centro Sur (Evinayong) Mkoa wa Kié-Ntem (Ebebiyín) mkoa wa Litoral (Bata) Mkoa wa Wele-Nzas (Mongomo) Mkoa wa Djibloho (Ciudad de la Paz) Watu Wananchi wengi (80%) ni wa kabila la Wafang, ambao ni wa Kibantu. Lugha Ni nchi pekee ya Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya taifa, hasa ukiacha Ceuta na Melilla (maeneo ya Hispania yaliyozungukwa na Moroko) na Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu (nchi isiyotambulika kimataifa). Pamoja nacho, Kifaransa na Kireno pia ni lugha rasmi. Dini Wananchi wengi wanafuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (88%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (5%). Wanaofuata dini asilia za Kiafrika na Baha'i ni 5%. Waislamu ni 2%. Utamaduni Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Marejeo Max Liniger-Goumaz, Udogo siyo urembo : Hadithi ya Guinea ya ikweta (French 1986, translated 1989) ISBN 0-389-20861-2 Ibrahim K. Sundiata, Equatorial Guinea: Colonialism, State Terror, and the Search for Stability (1990, Boulder: Westview Press) ISBN 0-8133-0429-6 Viungo vya nje Tovuti rasmi (Kihispania), makala maalum ya serikali ya Guinea ya Ikweta makala ya Elimu Guinea ya ikweta makala ya wanasiasa wa upinzani Habari allAfrica - Equatorial Guinea taarifa ya habari Uchambuzi na Maelekezo BBC News Country Profile - Guinea ya ikweta CIA World Factbook - Equatorial Guinea Open Directory Project - Equatorial Guinea maelekezo Stanford University – Afrika kusini mwa Sahara: Guinea ya ikweta Maelekezo Guinea ya ikweta, Afrika - Ikweta-Guinea Chuo kikuu cha Pennsylvania - African Studies Center: Ikweta-Guinea Maelekezo Yahoo! - Guinea ya ikweta maelekezo Koo na Makabila African Pygmies (Utamaduni na mziki wa watu wa Guinea ya ikwete / picha na ukoo.) Utalii Uchumi Sahuri za benki, Guinea ya ikweta, from the Fair Finance Watch (Uhifadhi wa biashara, guinea ya ikweta) nchini Hispania Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi zinazotumia Kihispania Nchi zinazotumia Kireno Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa
2607
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tana
Tana
Tana kwa kisambaa maana yake ni nzuri au jema. Lakini pia ni neno linaloweza kumaanisha: Tana (ziwa) katika Ethiopia Mto wa Tana (Kenya) katika Kenya Wilaya ya Mto wa Tana, Kenya Mto wa Tana (Norway) Tana (Norway) ni mji Tana (barafuto), Alaska Tana, kifupi cha Antananarivo, mji mkuu wa Madagaska Makala zinazotofautisha maana
2608
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tana%20%28ziwa%29
Tana (ziwa)
Ziwa la Tana ni ziwa kubwa la Ethiopia ambalo ni asili ya Nile ya Buluu. Beseni lake liko takriban km 370 kaskazini-magharibi kwa Addis Ababa katika nyanda za juu za Ethiopia. Umbo la ziwa limebadilika katika karne iliyopita kutokana na mashapo. Kamusi ya mwaka 1888 ilitaja kina cha mita 100, lakini leo ni mita 14 pekee. Eneo la ziwa hubadilika na majira ya mvua au ukame yaani kuwa na maji mengi au kidogo. Mito mingi inaingia ziwani ikiwa mikubwa, kati yake ni mito ya Reb na Gumara. Mto Abbai (jina la Kiethiopia la Nile ya buluu) unatoka katika ziwa. Eneo la Ziwa la Tana ni kitovu cha kihistoria cha Ethiopia ya Kikristo. Katika visiwa vidogo ziwani kuna makanisa na monasteri 20 zilizojengwa tangu karne ya 14 BK. Picha Viungo vya nje Maziwa ya Ethiopia
2615
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jangwa
Jangwa
Jangwa ni eneo kavu lenye mvua au usimbishaji kidogo tu. Kutokana na ukavu kuna mimea michache tu, pia wanyama wachache. Wanyama walioko hufanya shughuli zao hasa wakati wa usiku. Kipimo cha usimbishaji kinachotambulika kimataifa ni kiwango cha chini ya mm 250 kwa mwaka. Uoto wa mimea hufunika chini ya asilimia 5 za eneo lake. Wakati mwingine huitwa jangwa hata maeneo ambayo ni makavu kutokana na baridi kali. Aina za maeneo makavu: jangwa na mibuga Maeneo makavu yanaweza kutofautishwa kuwa yabisi sana (en: extremely arid) pasipo usimbishaji kwa muda wa miezi 12 mfululizo (maana yake hakuna mvua kila mwaka), yabisi (en: arid) pasipo usimbishaji zaidi ya mm 250 kwa mwaka, nusu yabisi (en:semiarid) penye usimbishaji kati ya mm 250 and 500 kwa mwaka. Maeneo yabisi sana na maeneo yabisi ni jangwa. Maeneo nusu yabisi yenye nyasi huitwa mbuga. Takriban theluthi moja ya uso wa nchi kavu duniani ni yabisi sana, yabisi au nusu yabisi. Athari ya uvukizaji Kiasi cha usimbishaji peke yake hakitoshi kila mahali kutofautisha maeneo makavu. Mm 200 za mvua katika eneo la joto zitasababisha eneo kuonekana kama jangwa kabisa kwa sababu kiasi kikubwa cha maji yale kidogo yanayoneshewa hupotea kutokana na uvukizaji. Kuna mifano ya kwamba eneo penye kiasi kilekile cha 200 mm halionekani kuwa jangwa tayari kwa sababu kutokana na halijoto na mawingu (hata yasiponyesha mvua) kiasi kidogo cha maji yanavukiza. Kama uvukizaji unapita kiasi cha mvua hata eneo penye mvua zaidi ya 250 mm inaonekana kama jangwa. Aina za jangwa Mara nyingi majangwa hutofautishwa kutokana na uso wake: Jangwa la mchanga — uso lake huonyesha hasa mchanga. Mchanga umetokea kutokana na mmomonyoko wa changarawe na kokoto kama mawe haya ni hasa ya shondo. Punje ndogo za mchanga husukumwa na upepo na kutokea kama matuta makubwa ya mchanga. Jangwa la mchanga ni mahali pagumu mno kwa maisha ya kila aina. Mfano bora ni jangwa la Rub al-Khali katika Uarabuni Saudi. Sahara ina pia sehemu za jangwa la mchanga. Jangwa la changarawe — uso lake huonyesha hasa changarawe. Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au miamba - punje ndogo zaidi zimeshapulizwa mbali na upepo. Hii ni sababu ya majangwa mengi kuwa na maeneo ya mchanga na changarawe yanayobadilishana. Changarawe hupatikana pia pale ambako zamani barafuto zilisaga mawe na kuzisukuma mbele ya barafu zao pale zilizobaki. Ni ajabu kutafakari ya kwamba sehemu fulani ilikuwa ya barafuto tukisimama leo mahali penye joto kali lakini mabadiliko ya hali ya hewa yalileta baridi au joto kila sehemu ya dunia yetu katika mamilioni ya miaka iliyopita. Jangwa la mawe — uso lake huonyesha miamba na mawe makubwa. Maana yake hapo udongo wote mwenye rutba na mchanga vimeshapulizwa mbali na mwamba umebaki. Athira za joto na baridi zinaweza kupasua mwamba. Mmomonyoko wa upepo hutokea. Jangwa la chumvi — mara nyingi penye beseni yabisi za mashapo bila njia ambako maji ya mvua (au mto) yanaweza kutoka. Maji yote huvukiza na kuacha chumvi yake katika udongo. Kiasi cha chumvi kinaendelea kuongezeka polepole katika udongo wa beseni hizi. Maji Jangwa ni eneo kavu lakini maji hutokea. Maji ya chini Mara nyingi kuna maji chini ya ardhi. Pale ambako maji haya si chini mno mimea inaweza kuyafikia kwa mizizi yao. Mahali kadhaa chemchemi hutokea. Sehemu kama hizi zinaonekana kama oasisi penye miti, wakati mwingine hata na bwawa. Mahali pengine wakazi wa jangwa wamechimba kisima kirefu pasipo na mimea kinachosaidia maji ya watu na wanyama hasa wa misafara. Maji ya mvua Mvua ikionyesha unaweza kutokea kwa wingi. Maji yake hukusanyika katika mabonde na kutokea kama mto wa muda. Kuna mifano mingi ya wasafiri jangwani waliokufa kwa sababu walipiga kambi katika bonde penye kivuli lakini walizama kwa sababu mto mkali ulijitokeza kwa ghafla kutokana na mvua ulionyesha katika umbali mkubwa. Sehemu nyingine mvua husababisha kutokea kwa mbwawa hata maziwa kwa muda. Mito inayopita jangwa Mito kadhaa kama Nile ina maji ya kutosha ili ivuke neo la jangwa. Inawezesha maisha ya mimea, wanyama na watu katika mabonde yao. Mito mingine inakwisha jangwani kwa sababu maji yote hupotea na kuvukiza. Mfano wake ni delta ya mto wa Okavango unaokwisha katika jangwa la Kalahari huko Botswana. Delta hii ni eneo la mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa. Mto wa Ewaso Nyiro katika Kenya ya kaskazini kwa kawaida hukwisha katika nchi yabisi za Usamburu. Lakini kila baada ya miaka makumi kadhaa baada ya mvua kubwa sana inaendelea kuvuka jangwa la Somalia ya kusini na kufikia Bahari Hindi jinsi ilvyotokea wakati wa El-Nino 1998. Majangwa makubwa duniani Marejeo Sura ya nchi
2616
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usimbishaji
Usimbishaji
Usimbishaji (kwa Kiingereza: precipitation) ni maji yanayonyesha kutoka hewa hadi ardhini. Maji hayo ni pamoja na mvua, theluji, mvua ya mawe na umande. Usimbishaji unaanza pale ambapo hewa yenye joto na mvuke hupanda juu. Juu zaidi halijoto yake inapungua na mvuke ndani ya hewa unaanza kuwa matone ya maji. Kila wingu hufanywa na matone mengi madogo yanayoendelea kuelea hewani pamoja. Upepo unakoroga matone yale madogo mpaka yanagongana na kuunganika na hivyo kukua. Kama matone ni makubwa ya kutosha yanaanza kuanguka chini kama mvua, theluji au mvua mawe. Hali inategemea halijoto katika mawingu na hewani pale matone yanapotelemka. Kiasi cha usimbishaji ni muhimu kwa ajili ya tabia za hali ya hewa katika nchi au eneo fulani. Kufanya mvua kwa mitambo Watu wameanza kufanya mvua kwa kukamua mawingu. Hapo punje ndogo za iodidi ya fedha zinatupwa mawinguni kwa njia ya ndege au makombora. Punje hizo zinakuwa viini vya kutonesha mvuke na kusababisha matone kukua hadi mvua kunyesha. Teknolojia hiyo inatumika katika maeneo makavu. Inatumika pia katika maeneo ya kilimo ili kuzuia mvua mawe isiharibu mavuno. Marejeo Metorolojia
2618
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uvukizaji
Uvukizaji
Uvukizaji (pia: mvukizo; ing. evaporation) katika fizikia ni mwendo wa kiowevu (majimaji) kugeuka gesi. Kuna dutu kama maji zinazoanza kuvukiza kabla ya kufikia kiwango cha kuchemka. Viowevu vyote huvukiza vikifikia kiwango maalumu cha kuchemka. Kama molekuli katika kiowevu zinapashwa moto mwendo wake unaongezeka. Zinagonganagongana na kuachana mbali zaidi hadi kuwa gesi. Katika metorolojia uvukizaji ni hasa mwendo wa maji kuwa mvuke au gesi. Mwendo huu ni nguvu muhimu sana katika dura ya maji duniani. Maji ya baharini au unyevu nchini vinapashwa moto hasa na mionzi ya jua hadi kuwa mvuke unaopanda juu kuunda mawingu. Fizikia Metorolojia
2620
https://sw.wikipedia.org/wiki/Moroko
Moroko
Moroko (pia Maroko, kwa Kiarabu المغرب), au kirefu Ufalme wa Moroko (المملكة المغربية al-mamlaka al-maghribiya yaani "ufalme wa magharibi") ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari za Atlantiki na Mediteranea; upande wa bara imepakana na Algeria na Mauretania. Maeneo ya Kihispania ya Ceuta na Melilla yamezungukwa na Moroko kwenye pwani ya Mediteranea. Mpaka wa kusini haueleweki vizuri kwa sababu Moroko inadai ya kwamba Sahara ya Magharibi ni sehemu ya eneo lake, hali isiyokubaliwa na jumuiya ya kimataifa tangu Moroko ilipovamia Sahara ya Kusini mwaka 1975. Jina Jina la "Moroko" limetokana na mji mkuu wa kale Marakesh. Jiografia Eneo la Moroko ni km² 446,550. Sehemu kubwa ni jangwa la Sahara. Watu walio wengi huishi kwenye sehemu za rutuba karibu na pwani. Kuna milima inayofunika maeneo makubwa. Milima ya Rif inaongozana na pwani ya Mediteranea yenye mwelekeo kutoka kaskazini-magharibi kwenda kaskazini-mashariki. Milima ya Atlas iko katikati ya nchi kutoka kusini-magharibi kwenda kaskazini-mashariki. Miji mikubwa Mji mkuu ni Rabat wenye wakazi milioni 1.2. Mji mkubwa ni Casablanca (kwa Kiarabu: الدار البيضاء dar al-baiDa = nyumba nyeupe). Miji yote miwili mikubwa ni miji ya bandari. Miji mitano mikubwa ni kama ifuatavyo (namba za sensa ya mwaka 2004): 1. Casablanca: wakazi 2.933.684 2. Rabat: wakazi 1.622.860 3. Fes: wakazi 946.815 4. Marakesh: wakazi 823.154 5. Agadir: wakazi 678.596 Historia Makala: Historia ya Moroko Moroko ya Kale Habari za kimaandishi za kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani lilibaki nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale (usiuchanganye na nchi ya kisasa Mauretania) uliounganisha sehemu kubwa ya Moroko ya kaskazini. Wamauretania wa kale walishirikiana na Dola la Roma hadi kuwa jimbo la dola hili kwa jina la "Mauretania Tingitana". Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Roma kuanzia mwaka 400 BK kukawa na uvamizi wa Wavandali. Uvamizi wa Kiarabu Karne ya 7 BK ilileta uvamizi wa Waarabu walioteka nchi na kusababisha polepole Waberber (waliokuwa Wayahudi, Wakristo au wafuasi wa dini za jadi) kuwa Waislamu. Mwanzoni Moroko ilikuwa sehemu ya milki ya khalifa ya Waomawiyya waliotawala Dameski (Siria). Baada ya kupinduliwa kwa Waomawiyya na Waabasiya wa Baghdad (Iraq) mkimbizi Mwarabu Idris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea. Hii ilikuwa mwanzo wa Moroko kuwa milki ya Kiislamu inayojitawala. Watawala wa kienyeji Vipindi vya historia husebabiwa kufuatana na familia zilizofuatana za wafalme Waarabu au Waberber. Moroko ilitawaliwa na familia za (miaka BK) Waidrisi (788-974) Wamaghrawa (987-1070) Wamurabitun (Almoravi)(1073-1147) Wamuwahidun (Almohad) (1125-1269) Wamarini (1258-1420) Wawattasi (1420-1547) Wasaadi (1509-1659) Waalawi (1631 hadi leo) Murabitun na Muwahidun Wafalme wa Wamurabitun (Almoravi) (1073-1147) na wa Wamuwahidun (Almohad) (1147-1269) walieneza utawala wao hadi Afrika ya Magharibi (Mauretania, Senegal na Mali ya leo) na sehemu kubwa ya Andalusia (Hispania ya Kiislamu), tena hadi mipaka ya Misri. Wamuwahidun waliendelea kupanuka kuelekea Misri lakini baadaye walidhoofika wakapaswa kuwaachia Wahispania Wakristo sehemu za Andalusia. Athira ya milki ya Moroko ilipungua baadaye hadi Hispania yote ikarudishwa kwa watawala Wakristo mwaka 1492; pia utawala kusini kwa Sahara haukuendelea. Wareno wa Wahispania waliendelea kuteka miji kwenye pwani za Moroko. Utawala wa Hispania juu ya Ceuta na Melilla leo ni mabaki ya nyakati zile. Sehemu za nchi zilianza kujitawala bila kukubali tena mamlaka wa juu, kwa mfano makabila ya Waberber milimani au miji ya Rabat na Sale iliyounda dola dogo la Jamhuri ya Bou Regreg katika karne ya 17 na kujishughulisha na uharamia. Waalawi (1666 hadi leo) Katika karne ya 17 familia ya Waalawi walishika mamlaka wakaendelea nayo hadi leo. Waliweza kutunza uhuru wa nchi hadi mwanzo wa karne ya 20. Lakini mwanzo wa karne ya 20 Ufaransa na Hispania walimlazimisha mfalme Mulay Abdelaziz kukubali mkataba uliofanya Moroko kuwa kama koloni chini ya nchi hizo mbili. Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilidhoofisha Ufaransa pamoja na kuingia kwa wanajeshi Waamerika na Waingereza na ahadi zao za kuleta uhuru tokeo lililohamasisha wazalendo wa Maroko kupigania upya uhuru wa nchi. Baada ya vita Wafaransa walijaribu kukandamiza mwendo huo wakamwondoa Sultani Mohammed V nchini 1953. Ghasia zikaongezeka, Sultani akarudi na nchi ikapewa uhuru mwaka 1956. Utawala wa mwanae Hassan II kuanzia mwaka 1961 uliitwa "miaka ya risasi" kwa sababu mfalme alikataa kukubali utaratibu wa kidemokrasia. Chaguzi zilikuwa za uwongo, wapinzani wakatupwa jela au kuuawa. Hassan II alishinda majaribio mbalimbali ya kumpindua. Siasa ya kushikamana na Marekani ilimsaidia mfalme kimataifa lakini baada ya mwisho wa "vita baridi" alilazimishwa na Wamarekani kulegeza utawala wake. Mtoto wake Muhamad VI akawa mfalme kijana mwaka 1999 akaanza mageuzi ya kisiasa ya wazi zaidi. Watu Mnamo 60 % (Januari 2005) za wakazi milioni 32.7 huishi mijini. Kiasili wakazi wengi ni Waberber na Waarabu, pamoja na watu wa asili ya Andalusia (Hispania) na wa Afrika kusini kwa Sahara. Waberber ndio wenyeji asilia. Kaskazini mwa nchi ambako kitovu chake ni Fes kuna zaidi tabia ya Kiarabu, wakatu kusini ambako kitovu chake ni Marakesh kuna tabia ya Kiberber zaidi. Lugha Lugha rasmi ya nchi ni Kiarabu na Kiberberi. Waberber wengi, hasa kaskazini, wameacha lugha yao na kutumia Kiarabu lakini walileta maneno yao katika lahaja ya Kiarabu cha Kimaroko. Hata Kifaransa kinatumika sana. Dini Uislamu ndio dini rasmi na ndio unaofuatwa na wakazi wengi sana (98.9%), hasa Wasunni. Wengine ni Wakristo (0.9%) na Wayahudi (0.2%). Wakristo karibu wote ni wa asili ya Ulaya. Wayahudi waliwahi kuwa wengi kidogo, lakini idadi yao imepungua katika miaka ya nyuma kutokana na uhamaji hata kama hali yao katika taifa ni nzuri kulingana na nchi nyingine za Kiarabu. Uchumi Nguzo za uchumi wa nchi ni kilimo na magodi ya kuchimba madini, pamoja na uvuvi na utalii. Zaidi ya asilimia 40 za wananchi hulima. Kwa jumla asilimia 18 za eneo la Moroko zinatumiwa kwa kilimo, hasa katika magharibi na kaskazini-magharibi. Nchi hii ina akiba kubwa ya fosfati inayochimbwa na kuuzwa nje kwa matumzi ya mbolea. Akiba ya fosfati ni kubwa duniani. Moroko ina nafasi ya tatu katika uzalishaji baada ya China na Marekani. Umuhimu wa utalii kwa uchumi umezidi kukua; mwaka 2018 idadi ya watalii ilifikia milioni 12.3 Vivutio vya kitalii ni pamoja na mahali pa urithi wa dunia kama vile Medina ya Fez Medina ya Marrakesh Ksar au mji-ngome wa Ait Benhaddou Mji wa kihistoria ya Meknes Eneo la akiolojia la Volubilis Medina ya Tetouan Medina ya Essaouira Mji wa Kireno wa Mazagan Rabat Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Official website of the government of Morocco Official bulletins of the government of Morocco Parliament of Morocco Census results of 1994 and 2004 Forum press Morocco Morocco profile from the BBC News Maroc Paradise, Beauty of Morocco Tribes of Morocco Key Development Forecasts for Morocco from International Futures EU Neighbourhood Info Centre: Morocco World Bank Summary Trade Statistics Morocco Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi za Kiarabu Nchi za Waberber Afrika ya Kaskazini
2621
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Moroko
Historia ya Moroko
Historia ya Moroko inahusu eneo ambalo leo ni nchi ya Afrika kaskazini-magharibi. Moroko ya Kale Habari za kimaandishi za kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani lilibaki nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale (usiuchanganye na nchi ya kisasa Mauretania) uliounganisha sehemu kubwa ya Moroko ya kaskazini. Wamauretania wa kale walishirikiana na Dola la Roma hadi kuwa jimbo la dola hili kwa jina la "Mauretania Tingitana". Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Roma kuanzia mwaka 400 BK kukawa na uvamizi wa Wavandali. Uvamizi wa Kiarabu Karne ya 7 BK ilileta uvamizi wa Waarabu walioteka nchi na kusababisha polepole Waberber (waliokuwa Wayahudi, Wakristo au wafuasi wa dini za jadi) kuwa Waislamu. Mwanzoni Moroko ilikuwa sehemu ya milki ya khalifa ya Waomawiyya waliotawala Dameski (Siria). Baada ya kupinduliwa kwa Waomawiyya na Waabasiya wa Baghdad (Iraq) mkimbizi Mwarabu Idris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea. Hii ilikuwa mwanzo wa Moroko kuwa milki ya Kiislamu inayojitawala. Watawala wa kienyeji Vipindi vya historia husebabiwa kufuatana na familia zilizofuatana za wafalme Waarabu au Waberber. Moroko ilitawaliwa na familia za (miaka BK) Waidrisi (788-974) Wamaghrawa (987-1070) Wamurabitun (Almoravi)(1073-1147) Wamuwahidun (Almohad) (1125-1269) Wamarini (1258-1420) Wawattasi (1420-1547) Wasaadi (1509-1659) Waalawi (1631 hadi leo) Murabitun na Muwahidun Wafalme wa Wamurabitun (Almoravi) (1073-1147) na wa Wamuwahidun (Almohad) (1147-1269) walieneza utawala wao hadi Afrika ya Magharibi (Mauretania, Senegal na Mali ya leo) na sehemu kubwa ya Andalusia (Hispania ya Kiislamu), tena hadi mipaka ya Misri. Wamuwahidun waliendelea kupanuka kuelekea Misri lakini baadaye walidhoofika wakapaswa kuwaachia Wahispania Wakristo sehemu za Andalusia. Athira ya milki ya Moroko ilipungua baadaye hadi Hispania yote ikarudishwa kwa watawala Wakristo mwaka 1492; pia utawala kusini kwa Sahara haukuendelea. Wareno wa Wahispania waliendelea kuteka miji kwenye pwani za Moroko. Utawala wa Hispania juu ya Ceuta na Melilla leo ni mabaki ya nyakati zile. Sehemu za nchi zilianza kujitawala bila kukubali tena mamlaka wa juu, kwa mfano makabila ya Waberber milimani au miji ya Rabat na Sale iliyounda dola dogo la Jamhuri ya Bou Regreg katika karne ya 17 na kujishughulisha na uharamia. Waalawi (1666 hadi leo) Katika karne ya 17 familia ya Waalawi walishika mamlaka wakaendelea nayo hadi leo. Waliweza kutunza uhuru wa nchi hadi mwanzo wa karne ya 20. Lakini mwanzo wa karne ya 20 Ufaransa na Hispania walimlazimisha mfalme Mulay Abdelaziz kukubali mkataba uliofanya Moroko kuwa kama koloni chini ya nchi hizo mbili. Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilidhoofisha Ufaransa pamoja na kuingia kwa wanajeshi Waamerika na Waingereza na ahadi zao za kuleta uhuru tokeo lililohamasisha wazalendo wa Maroko kupigania upya uhuru wa nchi. Baada ya vita Wafaransa walijaribu kukandamiza mwendo huo wakamwondoa Sultani Mohammed V nchini 1953. Ghasia zikaongezeka, Sultani akarudi na nchi ikapewa uhuru mwaka 1956. Utawala wa mwanae Hassan II kuanzia mwaka 1961 uliitwa "miaka ya risasi" kwa sababu mfalme alikataa kukubali utaratibu wa kidemokrasia. Chaguzi zilikuwa za uwongo, wapinzani wakatupwa jela au kuuawa. Hassan II alishinda majaribio mbalimbali ya kumpindua. Siasa ya kushikamana na Marekani ilimsaidia mfalme kimataifa lakini baada ya mwisho wa "vita baridi" alilazimishwa na Wamarekani kulegeza utawala wake. Mtoto wake Muhamad VI akawa mfalme kijana mwaka 1999 akaanza mageuzi ya kisiasa ya wazi zaidi. Historia ya Moroko
2624
https://sw.wikipedia.org/wiki/Changarawe
Changarawe
Changarawe ni mawe madogo. Kama ukubwa wa kila kijiwe ni chini ya 2 mm ndipo mchanga. Kama ni kubwa zaidi kuliko 60-75 mm (kawaida hutofautiana kati ya nchi na nchi) si changarawe tena ni jiwe. Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au mwamba. Idadi kubwa ya changarawe hutokana na mmomonyoko katika mito. Njia nyingine ni mmomonyoko wa barafuto. Changarawe inapatikana pia kama miamba au mawe makubwa yanaanguka mlimani na kupasuka. Changarawe ni jambo muhimu katika ujenzi. Kama kokoto inatumika chini ya barabara au kuchanganywa na simiti kwa ajili ya misingi ya majengo. Jiolojia
2626
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tuta%20la%20mchanga
Tuta la mchanga
Tuta la mchanga ni kilima cha mchanga kilichojengwa na upepo kwa kupuliza na kusukuma punje za mchanga. Kama halishikwi na mimea inaweza kuhamahama. Matuta ya mchanga hutokea penye mchanga usiofunikwa na udongo au mimea ya kutosha. Mifano ni: Kando la bahari: mahali pengi ufukoni ni kawaida kuwa na mstari mmoja au miwili ya matuta ya mchanga kando la maji. Jangwani: penye jangwa la mchanga maeneo makubwa yanaweza kutokea kama matuta ya mchanga. Matuta ya mchanga ni hatari kwa ajili ya binadamu kwa sababu yanaweza kufunika mashamba, nyumba hata kijiji kizima. Kama upepo ni mkali yanaweza kuhama mita makumi kila nafasi ya dhoruba. Kuna majaribio mengi ya kusimamisha matuta yasihame. Njia mojawapo ni kupanda manyasi katika maeneo penye mvua wa kutosha. Hii ni kazi inayohitaji uangilifu. Lazima kurudia kupanda pale ambako majani yamekufa. Lazima kuzuia wanyama na watu wasikanyage kati ya manyasi haya. Mradi wa kuhifadhi mazingira ya Umoja wa Mataifa unasaidia miradi ya aina hii kote duniani. Jiografia Sura ya nchi
2627
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sahara
Sahara
Sahara ni jangwa kubwa kaskazini mwa Afrika. Ni jangwa kubwa kabisa barani, ni la kwanza duniani kati ya majangwa joto na jangwa la tatu kwa ukubwa ulimwenguni baada Bara la Antaktiki na Aktiki. Ina eneo la kilometa za mraba 9,200,000, sawa na eneo la Marekani au karibu sawa na eneo lote ya Ulaya. Jina lake ni neno la Kiarabu (صحراء, sahra') linalomaananisha "jangwa". Sahara inafunika sehemu kubwa ya Afrika Kaskazini isipokuwa kanda lenye rutuba kwenye ufuko wa Bahari Mediteranea, milima ya Atlas kwenye Maghreb na bonde la mto Naili huko Misri na Sudan. Inaenea kuanzia Bahari ya Shamu upande wa mashariki hadi Atlantiki upande wa magharibi, na kutoka Mediteranea upande wa kaskazini hadi kanda la Sahel upande wa kusini. Wataalamu wa jiografia husema Sahara haikuwa hivyo wakati wote. Kutokana na utafiti wa dalili katika udongo na mawe yake eneo la Sahara katika milenia zilizopita lilikuwa na vipindi vya ukame vikifuatana na vipindi vya mvua. Jiografia Sahara iko kaskazini mwa Afrika. Ina nchi za Moroko, Algeria, Tunisia na Libya upande wa kaskazini. Upande wa kusini kuna nchi za kanda la Sahel kama Chad, Mali, Mauritania na Niger. Sahara ya Magharibi ina sehemu ufukoni mwa Atlantiki, na upande wa mashariki ni Sudani na Misri ambako oasisi ya mto Nile inakata eneo lake. Upande wa magharibi Sahara inaanza kwenye pwani ya Atlantiki ikielekea hadi pwani ya Bahari ya Shamu kwa umbali wa km 5000. Kwa jumla maeneo ya Sahara ni takriban asilimia 30 za bara lote la Afrika. Uso wa Sahara ni takriban asilimia 80 mawemawe na miamba. Takriban asilimia 20 umefunikwa na mchanga unaosukumwa na upepo kuwa na umbo la matuta ya mchanga ambao yanaweza kuwa na kimo cha mita 180 au zaidi. Kama kila jangwa uso wake unafanyizwa na upepo na maji kutokana na mvua inayonyesha mara chache. Kuna milima ambayo mara nyingi ina asili ya kivolkeno kama vile Aïr, Ahaggar, Tibesti, Adrar des Iforas na milima ya Bahari ya Shamu. Mlima mrefu ni volkeno ya Emi Koussi iliyo sehemu ya safu ya Tibesti kaskazini mwa Chadi. Mito ya Sahara haiendelei mwaka wote ikiwa na maji kwa majira tu au hata kila baada ya miaka kadhaa kama mvua imenyesha. Mfano pekee wa kinyume ni mto Naili unaovuka jangwa lote kutoka vyanzo vyake katika Afrika ya Kati hadi kuishia katika Bahari Mediteranea. Tabianchi ni ya joto na yabisi. Halijoto ni kati ya +58 °C wakati wa mchana ikishuka usiku hadi +13 °C (mlimani hadi -10 °C). Wastani wa mvua katika Sahara ni mm 45.5 kwa mwaka lakini kuna miaka bila mvua yoyote. Katikati yake Sahara ni yabisi sana, uoto ni haba mno. Katika sehemu za kaskazini na kusini kuna maeneo yenye kiwango cha nyasi na vichaka vidogo kadhaa. Kama unyevu unaweza kudumu kwa muda katika mabonde, vichaka vinakuwa vikubwa zaidi na huko na huko kuna pia miti. Sehemu za milima ya juu ambako joto si kama vile kuna kiwango kidogo cha usimbishaji na hapo mabaki ya misitu ya zamani yapo. Sehemu za katikati ambazo ni yabisi sana mara nyingi hazipokei mvua kwa miaka mfululizo. Upande wa kaskazini katika Misri na sehemu za Libya jangwa la Sahara linafika moja kwa moja hadi ufuko wa Mediteranea. Lakini katika nchi za Maghreb jangwa linaishia mguuni pa milima ya Atlas ambayo ina tabianchi ya Kimediteranea yenye majira ya joto na ya baridi pamoja na mvua. Halihewa hiyo inaruhusu uoto wa miti na misitu pamoja na kilimo. Mpaka wa kaskazini wa Sahara unalingana na mpaka wa kaskazini wa kilimo cha mitende na pia mpaka wa kusini wa uoto wa manyasi ya esparto ambayo ni nyasi ya Maghreb na rasi ya Iberia. Mpaka wa kaskazini unalingana pia na mwisho wa maeneo yanayopokea angalau milimita 100 za mvua kwa mwaka. Upande wa kusini Sahara inapakana na Sahel ambayo ni kanda la savana kavu yenye majira ya mvua na kanda hili laenea upana wote wa Afrika kutoka magharibi hadi mashariki. Mpaka wa kusini wa Sahara unalingana na mstari wa mwisho wa maeneo yanayopokea angalau milimita 150 za mvua kwa mwaka. Miji muhimu katika Sahara ni pamoja na: Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania; Tamanrasset, Ouargla, Béchar, Hassi Messaoud, Ghardaïa na El Oued nchini Algeria; Timbuktu, Mali; Agadez, Niger; Ghat, Libya; Faya, Chad. Jiolojia Sahara haikuwa jangwa wakati wote. Michoro ya watu wa zamani katika milima ya Tibesti na Air inaonesha wawindaji na wanyama kama viboko na mamba wanaohitaji maji mengi. Wataalamu wamegundua kutokana na utafiti wa mawe na udongo ya kwamba eneo la Sahara lilikuwa na vipindi vikavu na vipindi vya mvua nyingi. Mnamo miaka 7000 iliyopita Sahara ilikuwa eneo nusu yabisi lenye maji katika mito mirefu. Inawezekana kuilinganisha na Kenya Kaskazini ya leo. Watu waliwinda na kufuga wanyama. Mnamo miaka 5000 iliyopita Sahara ilikauka hadi kufikia hali yabisi kama leo. Lakini maji ya mvua ya nyakati zile bado yapo chini ya ardhi. Misri na Libya ina miradi mikubwa ya kutumia maji yale kwa pampu na kuanza kilimo jangwani kabisa. Flora na fauna Flora ya Sahara ina mimea tofauti sana kulingana na mazingira mbalimbali ndani yake. Kuna kanda tatu za flora ambazo ni kaskazini, kati na kusini. Zinatofautiana kwa kiwango cha mvua inayonyesha. Wataalamu hutofautisha pia kanda mbili za mpito - mpito wa Mediteranea-Sahara na mpito wa Sahel. Kuna spishi 2800 za mimea ya juu, na robo ya spishi hizi inapatikana katika Sahara pekee. Nusu ya spishi ni za kawaida katika jangwa kuanzia huko hadi Uarabuni. Sahara ya Kati, ambayo ni kanda yabisi zaidi, ina spishi 500 za mimea pekee. Hii ni idadi ndogo kulingana na ukubwa wa eneo. Mimea kama miti, mitende, vichaka na manyasi imerekebisha kwa ajili ya mazingira haya kwa kuwa ndogo zaidi, kuhifadhi maji katika shina, na kukuza mizizi ya mlalo kwa kusudi la kukusanya maji na unyevu na pia kuwa na majani yenye ngozi nene (au umbo la sindano) ili kutopoteza maji mengi kwa njia ya uvukizaji. Mimea ina uwezo wa kukauka kabisa halafu kurudi baada ya miaka wakati mvua inanyesha. Fauna ya Sahara pia ina spishi zilizorekebisha maumbile au maisha kulingana na mazingira. Kuna spishi za bweha na spishi za paa na swala. Paa anayeitwa addax anaweza kuishi mwaka mzima bila kunywa. Duma ya Sahara imepungua sana kutokana na uwindaji lakini bado yuko Algeria, Togo, Niger, Mali, Benin na Burkina Faso. Lakini idadi ni chini ya duma 250 kwa jumla. Paka huyu anaepukana na jua kuanzia Aprili hadi Oktoba akipumzika wakati wa mchana mahali pa kivuli. Tanbihi Marejeo Chris Scott. Sahara Overland. Trailblazer Guides, 2005. Michael Brett and Elizabeth Frentess. The Berbers. Blackwell Publishers, 1996. Charles-Andre Julien. History of North Africa: From the Arab Conquest to 1830. Praeger, 1970. Abdallah Laroui. The History of the Maghrib: An Interpretive Essay. Princeton, 1977. Hugh Kennedy. Muslim Spain and Portugal: A Political History of al-Andalus. Longman, 1996. Richard W. Bulliet. The Camel and the Wheel. Harvard University Press, 1975. Republished with a new preface Columbia University Press, 1990. Eamonn Gearon. The Sahara: A Cultural History. Signal Books, UK, 2011. Oxford University Press, USA, 2011. János Besenyő. Western Sahara (2009), free online PDF book, Publikon Publishers, Pécs, ISBN 978-963-88332-0-4, 2009 Lizzie Wade. Drones and satellites spot lost civilizations in unlikely places, Science (American Association for the Advancement of Science), DOI: 10.1126/science.aaa7864, 2015 Viungo vya nje About Sahara subsurface hydrology and planned usage of the aquifers Sahara Jangwa Jiografia ya Afrika Jiografia ya Misri Jiografia ya Libya Jiografia ya Mali Jiografia ya Niger Jiografia ya Chad Jiografia ya Sudan Jiografia ya Mauritania Sahara ya Magharibi Jiografia ya Moroko Jiografia ya Algeria Jiografia ya Tunisia
2628
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kituo%20cha%20Nishi%20Isahaya
Kituo cha Nishi Isahaya
Nishi-Isahaya (kwa Kijapani: 西諫早駅,にしいさはやえき) ni kituo cha treni katika mji wa Nagasaki, nchini Ujapani. Kilifunguliwa mwaka wa 1985. Japani
2633
https://sw.wikipedia.org/wiki/Gabon
Gabon
Jamhuri ya Gabon (kifupi: Gabon) ni nchi huru ya Afrika magharibi ya kati. Imepakana na Guinea ya Ikweta, Kamerun, Jamhuri ya Kongo na Ghuba ya Guinea. Nchi hii ina umma mdogo, madini na mali kwa wingi, na wafanyabiashara kutoka nchi za kigeni wameweza kufanya Gabon iwe nchi yenye maendeleo makubwa. Jiografia Maeneo ya utawala Gabon imegawiwa katika mikoa 9 nayo ina jumla ya wilaya (départements) 37. Mikoa ni: Estuaire, Haut-Ogooué, Moyen-Ogooué, Ngounié, Nyanga, Ogooué-Ivindo, Ogooué-Lolo, Ogooué-Maritime, na Woleu-Ntem. Historia Jamhuri ya Gabon, tangu kupata uhuru kutoka Ufaransa tarehe 17 Agosti 1960, imeongozwa na Rais watatu, Léon M'ba, El Hadj Omar Bongo ambaye amekuwa kiongozi kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake (2009: ndiye aliyekuwa kiongozi barani Afrika aliyeshikilia uongozi kwa muda mrefu zaidi), halafu mwanae Ali aliyepinduliwa na wanajeshi tarehe 30 Agosti 2023. Siasa Mwaka wa 1990 Gabon ilianza demokrasia ya vyama vingi na katiba ya kidemokrasia ili ruhusu ukweli wa uchaguzi na uwajibikaji wa idara za serikali, lakini hali iliendelea kuwa karibu ileile. Uchumi Gabon ni nchi yenye neema sana kuliko nchi jirani. Uchumi wake, hasa chumo cha umma, ni mara nne ya nchi za Afrika kusini kwa Sahara. Hii hasa ni kwa sababu ya uzalishaji wa mafuta ambao umeleta utajiri na mali, lakini usambazaji wa mali hii ya mafuta bado umedhoofika. Gabon ilikuwa mwanachama wa Muungano wa Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) kutoka mwaka wa 1975 mbaka 1995. Mwaka 1990, udhaifu wa pesa CFA frank uliacha Gabon katika shida ya kulipa deni za kimataifa; Ufaransa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wameipa Gabon mkopo na usaidizi kwa uelewano kwamba Gabon itageuza uchumi wake barabara. Watu Yasemekana mambo ya mazingira yalifanya umma wa Gabon kutopanda kwa sensa kati ya miaka 1900 na 1940. Ni nchi ambayo ina umma mdogo zaidi katika Afrika bara, na upungufu wa wafanyakazi ni mojawapo ya mambo yanayofanya hasa uchumi kutovuma zaidi. Umma hasa kwa ujumla ni kama watu milioni 2.4. Gabon hasa ina makabila zaidi ya 40 ambayo yana utamaduni na lugha tofauti lakini karibu wote (95%) ni wa jamii ya Bantu. Wafang ndio kabila kubwa zaidi nchini Gabon, wengine ni Wamyene, Wabandjabi, Waeshira, Wabapounou na Waokande. Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi ya taifa ambayo hutumika kwa mawasiliano (wakazi wanaoimudu ni 80%). Wafaransa 10,000 wanaishi Gabon, na Ufaransa unaathiri mambo ya kigeni, utamaduni na biashara nchini Gabon. Upande wa dini, imekadiriwa kwamba 75.6% za wakazi ni Wakristo (hasa Wakatoliki), 12.2% ni Waislamu (hasa wageni), na 5.7% wanafuata dini asilia za Kiafrika (Bwiti). Utamaduni Makabila ya Gabon Muziki wa Gabon Orodha ya lugha za Gabon Tazama pia Mawasiliano nchini Gabon Mambo ya kigeni ya Gabon Orodha ya kampuni za Gabon Jeshi la Gabon Historia ya Gabon Uchukuzi nchini Gabon Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo David E. Gardinier and Douglas A. Yates, Historia elekezo ya Gabon, tolezi ya 3. (The Scarecrow Press, Inc., 2006) David E. Gardinier, Kamusi ya Historia ya Gabon, tolezi ya 2. (The Scarecrow Press, Inc., 1994) – kazi inayohusu maelezo biografia ya vifaa 1,453 James F. Barnes, Gabon: Beyond the Colonial Legacy (Boulder: Westview, 1992) Viungo vya nje Serikali Le Gabon : makala rasmi ya Jamhuri ya Gabon Assemblée nationale du Gabon makala rasmi. Gabonese Embassy in London arithio za serikali Le Sénat de la République Gabonaise makala rasmi (kwa kifaransa) Habari AllAfrica.com - Gabon viungo via taarifa ya habari Uchambuzi BBC News Country Profile - Gabon Kitabu cha wa dadisi wa Amerika - Gabon Koo na makabila Baka watu wafupi wa Kamerun na Gabon Utamaduni na wakazi wa kwanza Gabon Maelekezo Open Directory Project - Gabon maelekezo Chuo kikuu cha Stanford – Afrika kusini mwa sahara: Gabon maelekezo Chuo kikuu cha Pennsylvania – Ustadi wa-Afrika: Gabon maelekezo Yahoo! - Gabon directory category Utalii Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa jumuiya ya Madola
2634
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utendi
Utendi
Utendi (pia: utenzi; kutoka kitenzi "kutenda") ni aina ya ushairi na tanzu mojawapo ya fasihi simulizi. Kwa kawaida, utendi husimulia maisha na matendo ya mhusika shujaa au wa visasili. Maarufu katika fasihi ya Ulaya, kuna tendi kama wimbo wa Troya, wimbo wa Odisei na wimbo wa kabila la Nibelungi; India kuna wimbo wa Mahabharata; Afrika kuna utendi wa Sundiata na wimbo wa Oduduwa. Hizo zote mara nyingi hudondolewa kama mifano ya utendi. Siku hizi hata riwaya au filamu, hasa kama ni ndefu sana pamoja na wahusika wengi au nyakati nyingi, huitwa utendi. Kwa Wakristo wanaotumia Kiswahili tahajia "utenzi" inataja hasa nyimbo za kiroho. Tenzi maarufu za Kiswahili Utenzi wa Tambuka (kazi ya Bwana Mwengu, karne ya 18) Utenzi wa Shufaka (mtunzi na wakati hawajulikani) Utenzi wa Mwana Kupona (kazi ya Mwana Kupona, karne ya 19) Utenzi wa Inkishafi (kazi ya Sayyid Abdallah Bin Ally) Utendi wa Fumo Liyongo (kazi ya Muhamad Kijumwa) Utenzi wa Hayati Sokoine (kazi ya Charles Mloka, karne ya 20) Tenzi za Enjili (kazi ya Julius Nyerere) Utenzi wa Hati na Adili (Kazi ya Shaaban Robert) Mwanangu Nakuusia (kazi ya Audax Kahendaguza Vedasto) Tanbihi Marejeo Chum, Haji & H.E. Lambert (1962). Utenzi wa vita vya Uhud (The epic of the battle of Uhud), collected and compiled by Haji Chum, edited with a translation and notes by H. E. Lambert. (Johari za Kiswahili, vol. 3). Nairobi. Gérard, S. (1976) "Structure and values in three Swahili epics", Research in African Literatures, 7, 1, 7-22. Knappert, Jan (1967). Traditional Swahili poetry: an investigation into the concepts of East African Islam as reflected in the Utenzi literature. Leiden: Brill. Knappert, Jan (1977). Het Epos van Heraklios. Uit het Swahili vertaald in het oorspronkelijke metrum. Amsterdam: Meulenhoff. (Dutch translation in the original meter). Knappert, Jan. (1999). A Survey of Swahili Islamic Epic Sagas. Lewiston [etc.]: Edwin Mellen Press. Wamitila, K. W. (1999). "A Rhetorical Study of Kiswahili Classical Poetry: An Investigation into the Nature and Role of Repetition", Research in African Literatures, 30, 1, Spring 1999, 58-73. Fasihi Fasihi ya Kiswahili
2635
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ali%20Hassan%20Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi
Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa 8 Mei 1925) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996. Kabla ya hapo alikuwa Rais wa tatu wa Zanzibar baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi kwenye Januari 1984. Urais wa Zanzibar ulimfanya kuwa makamu wa rais wa Tanzania; hivyo aliteuliwa kugombea urais wa kitaifa wakati Julius Nyerere alipoamua kutogombea tena kwenye mwaka 1985. Mwinyi alichaguliwa akaacha cheo chake cha Zanzibar akawa rais wa Tanzania. Visiwani alifuatwa na Idris Abdul Wakil. Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais. Maisha Mwinyi alizaliwa Kivure kwenye Mkoa wa Pwani wa Tanzania bara lakini wazazi wake walihamia Unguja alipokuwa mdogo. Kuanzia mwaka 1933 alipokea elimu ya msingi na sekondari kwenye shule za Mangapwani na Dole Secondary School alikohitimu mwaka 1942. Baada ya masomo ya ualimu aliendelea kwenye Chuo Kikuu cha Durham nchini Uingereza . . Alianza kufundisha shuleni akaendelea kuwa mkuu wa chuo cha ualimu Unguja hadi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya elimu ya Zanzibar baada ya mapinduzi kwenye mwaka 1963. Mnamo 1970 alipewa uwaziri wa nchi katika ofisi ya rais akaendelea na vyeo mbalimbali katika serikali ya Zanzibar, pamoja na waziri wa afya, wa mambo ya ndani na wa utalii. Alihudumia pia miaka mitano kama balozi wa Tanzania nchini Misri. Kwenye Januari 1984 aliteuliwa kuwa rais wa Zanzibar baada ya mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi alilazimishwa kujiuzulu. Katika nafasi kama rais wa Zanzibar alikuwa pia makamu wa rais wa maungano; katika uchaguzi wa 1985 aliteuliwa na CCM kuwa mgombea kwa nafasi ya raisi wa taifa akachaguliwa bila mpinzani katika mfumo wa chama kimoja. Wakati wa urais wa kitaifa wa Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huria zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, Mwinyi alianzisha Tume ya Nyalali iliyopendekeza kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini. Wakati wa awamu yake kwenye mwaka 1995 ulitokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya kisiasa nchini Tanzania. Sera za soko huria za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mwinyi mwenyewe, baada ya kustaafu, hakujiingiza katika mambo ya siasa tena. Anaendelea kuishi huko Dar es Salaam. Heshima na Tuzo Nishani Shahada za Heshima Tazama Pia Orodha ya Marais wa Tanzania Chama Cha Mapinduzi Marejeo Waliozaliwa 1925 Watu walio hai Marais wa Tanzania Watu wa Zanzibar
2637
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kondoa
Kondoa
Kondoa ni jina la Mji wa Kondoa Wilaya ya Kondoa Tanzania Makala zinazotofautisha maana
2638
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hamed%20bin%20Mohammed%20el%20Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamad bin Muhammad bin Juma bin Rajab el Murjebi (amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip; 1837 – 14 Juni 1905) alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika Afrika ya Mashariki na ya Kati wakati wa karne ya 19. Alikutana na wapelelezi mashuhuri kama David Livingstone, Henry Morton Stanley na Hermann von Wissmann. Kwa miaka kadhaa alikuwa gavana wa Kongo ya Mashariki kwa niaba ya mfalme wa Ubelgiji. Alitunga tawasifu kuhusu maisha yake. Mfanyabiashara Baba yake alikuwa mfanyabiashara Mwarabu Muhammed bin Juma, mama yake Bint Habib bin Bushir, alikuwa Mwarabu wa tabaka la watawala toka Muscat. Hamed aliingia katika shughuli za biashara tangu umri wa miaka 12 akafaulu katika biashara ya misafara kati ya Zanzibar na Kongo. Akiwa na umri mdogo, Hamad aliongoza kundi la wanaume 100 kwenda Afrika ya Kati kutafuta watumwa na pembe za ndovu. Baada ya kuvamia maeneo mengi alirudi Zanzibar kuimarisha vyanzo vyake na kukusanya watu wa kumsaidia ili arudi bara. Hapa alipokea jina la Tippu Tip. Kwa mujibu wake mwenyewe, jina hilo lilitokana na mlio wa bunduki yake wa 'tiptip. Alipanga misafara ya mahamali waelfu akipeleka bidhaa kutoka Bagamoyo kupitia Tabora hadi Ujiji kwa Ziwa Tanganyika na ndani ya Kongo. Bidhaa alizobeba alizitumia kujipatia pembe za ndovu na watumwa; watumwa walisaidia kubeba pembe za ndovu njia ya kurudi hadi pwani. Hamed alitajirika sana. Athira yake ilipanuka katika Kongo ya Mashariki hadi alitawala eneo kubwa sana. Kukutana na wapelelezi Wazungu Hamed akapata jina huko Ulaya kwa sababu alikutana na wasafiri na wapelelezi Wazungu kama David Livingstone, Veney Cameron, Henry Morton Stanley, Eduard Schnitzer (Emin Pascha), Hermann von Wissmann na Wilhelm Junker ambao mara nyingi walipata misaada muhimu kutoka kwake. Kati ya mwaka 1884 na 1887 alikuwa mtu mwenye mamlaka katika sehemu kubwa za Mashariki ya Kongo. Gavana wa Mfalme wa Ubelgiji Wabelgiji walipoanza kujenga ukoloni wao Kongo walimkuta kama mtawala wa Kongo ya Mashariki wakapatana naye na kumpa cheo cha gavana ya Mkoa wa Chutes Stanley ("maporomoko ya Stanley", leo Kisangani) mwaka 1887 alichoshika kwa miaka michache. Mwanzoni mwa 1887, Stanley aliwasili Zanzibar na kumtaka Hamad awe gavana wa Wilaya ya Stanley Falls kwenye Dola Huru la Kongo, iliyokuwa koloni binafsi la mfalme wa Ubelgiji. Mfalme Leopold II wa Ubelgiji na Sultani Barghash bin Said wa Zanzibar walikubaliana na tarehe 24 Februari 1887, Hamad alikubali. Wakati huohuo alikubali kuongoza safari za Stanley ili kwenda kumuokoa Mjerumani Emin Pasha (E. Schnitzer), gavana wa Kiosmani wa Equatoria (eneo la Misri ya Kiosmani, Sudan Kusini ya leo). Kurudi Zanzibar Mabadiliko ya ukoloni yaliharibu biashara yake akarudi Zanzibar 1890/1891 alipobaki bila misafara mipya hadi kifo chake mwaka 1905. Hamed amejipatia nafasi katika historia ya Afrika ya Mashariki kwa kuandika yeye mwenyewe tawasifu au kumbukumbu ya maisha yake. Katika lugha ya Kiswahili ndio mfano wa kwanza wa tawasifu. Pia ni mfano wa pekee wa kumbukumbu ya kimaandishi ya matokeo ya siku zile zisizoandikwa na Mzungu lakini na mwenyeji. Aliandika kwa lugha ya Kiswahili akitumia mwandiko wa Kiarabu. Mfasiri katika Ukonsuli wa Ujerumani kwenye kisiwa, Heinrich Brode alinakili muswada wake kwa herufi za Kilatini na kuongeza tafsiri ya Kijerumani iliyochapishwa huko Berlin katika sehemu mbili mwaka 1902 na 1903 , . Brode alitumia kazi hiyo kutunga kitabu chake juu ya Hamed kilichochapishwa mwaka 1905 na kutafsiriwa kwa Kiingereza mwaka 1907. Vita ya Waarabu katika Kongo na kuporomoka wa urithi wa Tippu Tip Baada ya kuondoka kwake Hemed katika Kongo, vita ya Waarabu katika Kongo ilianza. Waarabu na Waswahili wa Kongo Mashariki walipigana na serikali ya kikoloni ya Dola Huru la Kongo ilhali pande zote mbili zilitumia askari Waafrika wengi walioongozwa na viongozi wa nje, ama Waarabu /Waswahili au Wazungu. Tippu Tip alipoondoka Kongo, uwezo wa Dola Huru la kikoloni la Mfalme Leopold bado ulikuwa hafifu sana katika sehemu za mashariki. Mamlaka ilikuwa mkononi mwa Waarabu au Waswahili waliofanya biashara ya pembe za ndovu na watumwa kwenda Zanzibar. Kati yao walikuwa Sefu bin Hamed, mwana wa Tippu Tip, na mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la Rumaliza katika maeneo upande wa magharibi ya Ziwa Tanganyika. Mwaka 1892 Sefu bin Hamed alishambulia Wabelgiji waliofanya biashara ya pembe za ndovu iliyokuwa hatari kwa biashara ya Waswahili. Serikali ya koloni ya Dola Huru la Kongo ilituma kikosi chini ya kamanda Francis Dhanis kwenda sehemu za mashariki. Dhanis alifaulu mapema kushawishi kiongozi Mwafrika Ngongo Lutete aliyewahi kushirikiana na Sefu ahamie upande wake. Jeshi lake lilikuwa na silaha bora na nidhamu bora kati ya askari wake, likafaulu kumshinda Sefu mara kadhaa hadi ifo chake kwenye Oktoba 1893. Kutoka hapa Dhanis aliendelea kumshambulia Rumaliza na hatimaye kumlazimisha akimbie katika eneo la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kwa njia hii Wabelgiji walifaulu kuvunja nguvu ya Waarabu na Waswahili katika Kongo Mashariki. Kisiasa hakuna kitu kilichobaki na juhudi za Hemed bin Mohammed el Murjebi kujenga milki yake katika Kongo, ila tu kiutamaduni Hemed na wenzake walifaulu kueneza lugha ya Kiswahili katika sehemu zile. Kifo Hamad alifariki kutokana na ugonjwa wa malaria tarehe 13 Juni 1905 katika nyumba yake kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar. Jina lake linajulikana kama mfano wa mabaya ya biashara ya watumwa iliyoharibu maeneo makubwa huko Kongo kabla ya mwanzo wa ukoloni. Yeye mwenyewe aliona watumwa ni sehemu tu ya biashara yake akitajirika hasa na biashara ya pembe za ndovu. Marejeo Vyanzo Bennett, Norman Robert. Arab vs. European: Diplomacy and war in Nineteenth-Century East Central Africa. New York: Africana Publishing Company, 1986. Brode, Heinrich. Tippoo Tib: The Story of His Career in Zanzibar & Central Africa. Translated by H. Havelock with preface by Sir Charles Elliot. London: Arnold, 1907 (Online version). Edgerton, Robert B. (2002). The Troubled Heart of Africa: A History of the Congo. New York: St. Martin's Press. ISBN 0-312-30486-2. Maisha ya Hamed bin Mohammed el Murjebi yaani Tippu Tip kwa maneno yake mwenyewe, kimefasiriwa na W.H. Whitely (toleo la Kiswahili - Kiingereza), East Africa Literature Bureau 1974 Sheriff, Abdul. Slaves, Spices & Ivory in Zanzibar: Integration of an East African Commercial Empire into the World Economy, 1770-1873. London, Nairobi, Tanzania, Athens,OH: James Currey, Heinemann Kenya, Tanzania Publishing House, Ohio University Press, 1987. Waliozaliwa 1837 Waliofariki 1905 Watu wa historia ya Tanzania Waandishi wa Tanzania Wafanyabiashara wa Tanzania Utumwa
2640
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20za%20Kibantu
Lugha za Kibantu
Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo. Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Eswatini na Afrika ya Kusini. Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310. Neno Bantu, maana yake ni watu katika lugha nyingi za kundi hilo. Shina lake ni -ntu, na kiambishi awali cha ba- kinaonyesha uwingi wa viumbehai. Kwa sababu hiyo, mtaalamu Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek (aliyeishi tangu mwaka 1827 hadi 1875) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo. Kuna mamia ya lugha za Kibantu; wataalamu wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu Malcolm Guthrie aliziainisha kulingana na maeneo ya kijiografia. Kila eneo limepata herufi yake — A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S — na ndani ya kila eneo kuna tarakimu tena. Pia, Guthrie alichunguza lugha ya nasaba ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu. Tabia za Kibantu na historia ya lugha Lugha za Kibantu zina tabia mbalimbali za pamoja. Kati ya tabia hizo kuna viambishi awali na ngeli za nomino. Kutokana na sifa hizo wataalamu wamekadiria kwamba asili ya lugha za Kibantu ilikuwa katika maeneo ya Kamerun ya Kusini; kutoka huko wasemaji asilia wa Kibantu katika milenia ya pili KK walihamia Kongo hadi Zambia. Waliendelea kuhamahama na kupanuka hadi kufika maeneo yote walipo sasa. Sehemu kubwa ya maeneo ya wasemaji wa lugha za Kibantu zilikaliwa awali na wasemaji wa lugha za Khoisan. Wataalamu wamekisia kwamba Wabantu walifaulu kuenea kutokana na maarifa yao ya kilimo na hasa matumizi ya chuma katika zana za kilimo na pia silaha. Lugha za Kibantu zenye wasemaji wengi Kati ya lugha za Kibantu zinazotumika zaidi kuna Kiswahili na Kilingala. Lugha zenye wasemaji wengi kama lugha ya kwanza ni Kizulu na Kishona. (Idadi ya wasemaji ni makadirio tu; bado ina tofauti kati ya makala na makala) Kiswahili na lahaja zake (wasemaji milioni 150): Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Komori, Mayotte, Msumbiji, Somalia. Kinyarwanda-Kirundi : (wasemaji milioni 15): Rwanda, Burundi Lingala (wasemaji milioni 10): Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon Chichewa (wasemaji milioni 9) : Malawi Kizulu (wasemaji milioni 9) : Afrika Kusini Kisukuma (wasemaji milioni 9) : Tanzania. Kishona (wasemaji milioni 7) : Msumbiji, Zambia, Zimbabwe Gikuyu (wasemaji milioni 7) : Kenya Kikongo (wasemaji milioni 6) : Angola, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Chiluba (wasemaji milioni 6) : Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola Tanbihi Makundi ya lugha Lugha za Afrika Lugha za Kibantu
2644
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abuja
Abuja
Abuja ni mji mkuu wa Nigeria. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 178,462 . Mwaka wa 1976, serikali ya Nigeria iliamua kuanzisha mji mkuu mpya badala ya Lagos. Wakachagua katikati ya nchi, na mipango ya ujenzi ikaundwa chini ya makampuni matatu ya Marekani: PRC Corporation; Wallace, McHarg, Roberts na Todd; na Archisystems. Mipango hiyo ikabadilishwa baadaye na Kenzo Tange, msanifu majengo maarufu wa Japani. Abuja ikatangazwa rasmi kuwa mji mkuu wa Nigeria tarehe 12 Desemba 1991. Iko mahali pa 9, 10, Kaskazini na 7, 10, Mashariki. Balozi za nchi nyingi zikahamishwa Abuja kutoka Lagos. Historia Sifa muhimu ya Abuja ni Mlima wa Aso ambao ni mwamba ulio na urefu wa mita 400. Upande wa kusini wa mlima huo, kuna Ikulu ya Rais, Bunge la Nigeria, Mahakama Kuu na sehemu nyingi za mji. Majengo maarufu mengine ni Msikiti wa Taifa (Nigerian National Mosque) na Kanisa Kuu la Madhehebu (National Ecumenical Centre Cathedral). Kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa (Nnamdi Azikiwe International Airport), karibu na Mlima wa Zuma. Sehemu nyingine za mji hazijajengwa ilivyopangwa, na majengo mengi yanaendelea kujengwa. Mji wa Abuja unagombea kuwa mahali pa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa mwaka wa 2014 (2014 Commonwealth Games). Marejeo ya nje Official site of Nigeria's Federal Capital Territory (FCT) and City of Abuja Makala ya WorldPress inayohusu mabadiliko kwenye Abuja Abuja Bid Announcement Picha za Abuja Miji ya Nigeria Miji Mikuu Afrika
2645
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakarta
Jakarta
Jakarta (zamani iliitwa Batavia) ni mji mkuu wa Indonesia. Iko kwenye kisiwa cha Java, na mahali pake ni 6, 11, Kusini, na 106, 50, Mashariki. Ukubwa wa eneo lake ni 661.52 km². Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa 8,792,000 (mwaka wa 2004). Miji ya Indonesia Miji Mikuu Asia
2647
https://sw.wikipedia.org/wiki/Windhoek
Windhoek
Windhoek ni mji mkuu wa Namibia, na uko mahali pa 22.56 S 17.09 E. Idadi ya wakazi wake ni takriban 230,000. Mji huu ni kituo muhimu kwa biashara ya ngozi za kondoo. Zamani ulikuwa makao makuu ya mtemi wa kabila la Nama aliyewashinda kabila la Waherero wakati wa karne ya 19. Mwaka wa 1885, nchi ilivamiwa na wakoloni kutoka Ujerumani, na mji wa Windhoek ukawa makao makuu ya serikali ya ukoloni mwaka wa 1892. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi ilivamiwa na majeshi ya Makaburu kutoka Afrika ya Kusini ambao wametawala nchi ya Namibia hadi mwaka wa 1990. Namibia ilipopata uhuru, mji wa Windhoek ukawa mji mkuu wa Jamhuri ya Namibia. Miji ya Namibia Miji Mikuu Afrika Namibia
2648
https://sw.wikipedia.org/wiki/Koigi%20Wamwere
Koigi Wamwere
Koigi Wamwere ni mwanasiasa, mwanaharakati, na mwandishi kutoka nchi ya Kenya. Koigi alizaliwa mwaka wa 1949 huko Bahati, wilaya ya Nakuru. Koigi anajulikana kwa kujaribu kupindua serikali za Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi. Koigi aliwekwa kizuizini na watawala hawa, na baadaye alikimbilia uhamishoni nchini Norway miaka ya 80. Baada ya kurudi Kenya miaka ya 90, Koigi alikamatwa na kushtakiwa kwa madai ya kuhusika na uhaini na uporaji kwa kutumia silaha. Kutokana na kampeni kubwa ya kimataifa dhidi ya kesi hiyo ambayo ilichukuliwa kuwa na nia ya kumnyamazisha, serikali ya Kenya ilimwachia huru. Koigi ni mwandishi wa vitabu na makala kadhaa. Vitabu vyake ni "A Woman Reborn", "Justice on Trial", na "I Refuse to Die". Hivi sasa Koigi ni mbunge wa jimbo la Subukia na waziri msaidizi wa Habari katika serikali ya Mwai Kibaki. Koigi, ambaye huko nyuma alikuwa na nywele msokoto (dreadlocks), alinyoa nywele zake baada ya kuangushwa kwa serikali ya chama cha KANU kutimiza ahadi yake kuwa atanyoa nywele baada ya ushindi dhidi ya chama hicho kupatikana. W
2650
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lusaka
Lusaka
Lusaka ni mji mkuu wa Zambia. Jiji la Lusaka liko Kusini ya Kati ya Zambia, na mahali pake ni 15°25' Kusini, 28°17' Mashariki . Iko futi 4200 (au mita 1400) juu ya UB. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 1,391,000 (mwaka wa 2000). Mji wa Lusaka ulianzishwa mwaka wa 1905 na wakoloni Wazungu kwenye mahali pa kijiji ambacho mwenyekiti wake aliitwa Lusaaka. Kwa vile Lusaka iko katikati ya nchi, mwaka wa 1935 wakoloni Waingereza walihamishia mji mkuu wao wa Rhodesia ya Kaskazini huko kutoka mji wa Livingstone. Baada ya kupata uhuru, Lusaka ikaendelea kama mji mkuu wa Zambia hadi hivi sasa. Lusaka hufikika kupitia kiwanja cha ndege cha kimataifa (Lusaka International Airport), au kupitia garimoshi kwenye njia ya reli inayoelekea kutoka mji wa Livingstone kwenda mji wa Kitwe. Tazama pia Orodha ya miji ya Zambia Marejeo ya nje Zambia Tourism page on Lusaka Ramani ya Lusaka Miji Mikuu Afrika Miji ya Zambia
2655
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kunguru
Kunguru
Kunguru ni ndege wakubwa kiasi wa familia Corvidae. Spishi nyingine huitwa vinubi. Wanatokea mabara yote isipokuwa Antakitiki. Spishi nyingi ni nyeusi au nyeusi pamoja na rangi ya nyeupe, kijivu au kahawa; nyingine zina rangi mbalimbali kama buluu, pinki n.k. Hula nusra kila kitu: wanyama na ndege wadogo, wadudu, mizoga, matunda, nafaka n.k. Hulijenga tago lao kwa vijiti juu ya mti au jabali. Spishi nyingine huyajenga matago kwa makundi. Jike huyataga mayai 3-10. Kunguru na binadamu Baadhi ya kunguru huonwa kuwa ni waharibifu na inajulikana kwamba kunguru mkubwa kaskazi (Corvus corax), kunguru mkubwa wa Australia (Corvus coronoides) na kunguru mlamizoga (Corvus corone) wanaweza kuua wanakondoo dhaifu. Lakini mara nyingi hula mizoga iliyouawa karibuni kwa namna nyingine, ugonjwa k.m. Wengine wanaweza kuiga sauti ya binadamu, lakini hawawezi kuongea kama kasuku. Kunguru waliofundishwa kuongea, huonwa kama sehemu muhimu ya Asia ya Mashariki, kwa sababu kunguru huonwa kama alama ya bahati. Baadhi ya watu wanafuga kunguru kama wanyama wa nyumbani. Japo binadamu hawawezi kuwatambua kunguru, kunguru wanaweza kuwatambua watu na kuelewa kwamba hawa ni watu wabaya au la. Kwa tamaduni nyingi za kienyeji za kaskazi ya mbali sana kunguru, spishi kubwa hasa, wamekuchwa kama viumbe vya kirobo au miungu. Katika Afrika Waxhosa wa Afrika Kusini waliwachukulia kunguru kuwa ni ndege wa Mungu. Hadithi ya kixhosa kuhusu shujaa aitwaye Gxam inasimulia kwamba kunguru walirudishia shujaa aliyefanywa upofu uwezo wake wa kuona. Hadithi nyingine ya Wasara wa Chadi na Sudani inasimulia kwamba Mungu mkuu, Wantu Su, alimpa mpwa wake wa kiume Wantu ngoma iliyokuwa ndani yake na mifano ya kila kitu kilichokuwamo mbinguni. Wantu alitarajiwa kuwapatia binadamu vitu hivi, lakini alikuwa akishuka kamba iliyounga mbingu na dunia, kunguru alipiga ngoma. Ngoma akaanguka duniani, akavunjika na akatawanya wanyama, samaki na mimea duniani kote. Uwindaji Huko Marekani kunguru huwindwa kwa kibali cha serikali. Isipokuwa kwanzia Agosti mpaka Machi, msimu wa uwindaji kunguru sababu huwa wengi na hapo watu huruhusiwa kuwinda kunguru. Huko Uingereza ni marufuku mpaka pale mtu atakapopewa kibali. Tabia Kunguru anamaamuzi ya haraka sana, na anamacho yenye uwezo mkubwa wa kuona, pia kunguru anaonekana kuwa na ujasiri mkubwa hamwogopi binadam wa kike (mwanamke) Milio Kunguru hutoa milio mbalimbali. Suala kwamba kuna mawasiliano ya kunguru ni aina ya lugha ni mjadala mkubwa mpaka leo. Kunguru pia wamejifunza kuitika milio ya wanyama wengine na tabia hii hubadilika kwa misimu kadhaa. Milio ya kunguru ni tata na migumu kuelewa, na milio yao hutofautiana kwa spishi tofauti na hasa ugumu wa kujifunza milio huja pale ambapo inafahamika kuwa kunguru wanauwezo wa kusikia sauti ndogo sana ambazo binadamu hawezi kuzisikia. Akili Kama kundi, kunguru wameonekana kuwa na akili sana na majaribio mbalimbali yamethibitisha hili. Kunguru wamepata alama za juu sana kwenye tafiti za awali. Kunguru wa huko Israeli wamejifunza kutumia vipande vya mkate kama chombo cha kuvulia samaki. Spishi moja, New Caledonian Crow, wamefanyiwa tafiti sana kutokana na uwezo wao wa kutengeneza zana za matumizi ya kila siku. . Ujuzi mwingine ni ule wa kuangusha mbegu ngumu kwenye barabara inayopitisha magari makubwa ili yapasue, na kisha kusubiri taa za barabarani kuruhusu watu wapitie watawanye mbegu hizo. Na tafiti hivi karibuni zinaonesha kuwa kunguru wana uwezo wa nyuso za watu. Virusi Kunguru wa Amerika wanaathirika sana na virusi vya Naili Magharibi ugonjwa ulioanza hivi punde tu huko Amerika kunguru hufa ndani ya wiki moja tu tangu waupate ugonjwa huu na wachache sana hufanikiwa kupona. Kunguru wa huko huathirika sana na, kiasi cha kwamba kifo chao sasa kinaonesha athari ya virusi hao kwenye maeneo yao. Uainishaji Tangu miaka mingi wataalamu hawakubali kuhusu undugu wa familia Corvidae na jamaa yake. Mwishowe ilionekana kwamba kunguru wametokana na wahenga wa kiaustralasia na walitawanyika duniani kote. Majamaa yao ya karibu sana ni ndege wa peponi (birds of paradise), mbwigu na Australian mudnesters. Kumbukumbu ya visukuku vya kunguru (mifupa yao) inaonyesha kwamba walikuwa wengi sana Ulaya lakini husiano baina ya kunguru wa kabla ya historia hazieleweki vizuri. Kunguru wa makubwa ya jackdaw, kunguru rangi-mbili na kunguru domo-nene wanaonekana kuwa walikuwepo tangu zamani sana. Kunguru waliwindwa na binadamu hadi enzi ya chuma, kitu ambacho kinaonyesha mabadiliko ya spishi za kisasa. Kunguru wa Marekani hawana historia sahihi inayoaminika. Chakushangaza spishi nyingi zimekwisha hivi sasa baada ya uvamizi wa binadamu, katika visiwa kama Nyuzilandi, Hawaii na Grinlandi hasa. Spishi za Afrika Corvus albicollis, Kunguru Kisogo-cheupe (White-necked Raven) Corvus albus, Kunguru Rangi-mbili (Pied Crow) Corvus capensis, Kunguru Mwangapwani (Cape Rook au Cape Crow) Corvus corax (Northern au Common Raven) Corvus c. tingitanus, Kunguru Mkubwa ( North African Raven) Corvus crassirostris, Kunguru Domo-nene (Thick-billed Raven) Corvus edithae, Kunguru Somali (Somali Crow au Dwarf Raven) Corvus rhipidurus, Kunguru Mkia-mpana (Fan-tailed Raven) Corvus ruficollis, Kunguru Shingo-kahawia (Brown-necked Raven) Corvus splendens, Kunguru Bara-Hindi (Indian House Crow) Garrulus glandarius, Kunguru Rangirangi (Eurasian Jay) Pica pica, Kinubi Rangi-mbili (Eurasian Magpie) Pica p. mauritanica, Kinubi Rangi-mbili wa Afrika ( North African Magpie) Ptilostomus afer, Kinubi (Piapiac) Pyrrhocorax graculus, Kunguru-milima Domo-njano (Alpine Chough) Pyrrhocorax pyrrhocorax, Kunguru-milima Domo-jekundu (Red-billed Chough) Zavattariornis stresemanni, Kunguru Mweupe (Stresemann's Bush Crow) Spishi za mabara mengine Aphelocoma californica (California Scrub Jay) Aphelocoma coerulescens (Florida Scrub Jay) Aphelocoma insularis (Island Scrub Jay) Aphelocoma ultramarina (Transvolcanic Jay) Aphelocoma unicolor (Unicolored Jay) Aphelocoma wollweberi (Mexican Jay) Aphelocoma woodhouseii (Woodhouse's Scrub Jay) Calocitta colliei (Black-throated Magpie-jay) Calocitta formosa (White-throated Magpie-jay) Cissa chinensis (Common Green Magpie) Cissa hypoleuca (Indochinese Green au Yellow-breasted Magpie) Cissa jefferyi (Bornean Green Magpie) Cissa thalassina (Javan Green Magpie) Coloeus dauuricus (Daurian Jackdaw) Coloeus monedula (Western Jackdaw) Corvus bennetti (Little Crow) Corvus brachyrhynchos (American Crow) Corvus caurinus (Northwestern Crow) Corvus corax (Common Raven) Corvus cornix (Hooded Crow) Corvus corone (Carrion Crow) Corvus coronoides (Australian Raven) Corvus cryptoleucus (Chihuahuan Raven) Corvus culminatus (Indian Jungle Crow) Corvus enca (Slender-billed Crow) Corvus florensis ( Flores Crow) Corvus frugilegus (Rook) Corvus fuscicapillus (Brown-headed Crow) Corvus hawaiiensis (Hawaiian Crow au 'Alala) – zamani Corvus tropicus Corvus imparatus (Tamaulipas Crow) Corvus insularis (Bismarck Crow) Corvus jamaicensis (Jamaican Crow) Corvus kubaryi ( Mariana Crow) Corvus leucognaphalus (White-necked Crow) Corvus levaillantii (Eastern Jungle Crow) Corvus macrorhynchos (Large-billed Crow) Corvus meeki (Bougainville Crow) Corvus mellori (Little Raven) Corvus minutus (Cuban Palm Crow) Corvus moneduloides (New Caledonian Crow) Corvus nasicus (Cuban Crow) Corvus orru (Torresian Crow) Corvus ossifragus (Fish Crow) Corvus palmarum (Hispaniolan Palm Crow) Corvus sinaloae (Sinaloan Crow) Corvus tasmanicus (Forest Raven) Corvus t. boreus (Relict Raven) Corvus torquatus (Collared Crow) Corvus tristis (Grey Crow) Corvus typicus (Piping Crow) Corvus unicolor (Banggai Crow) Corvus validus (Long-billed Crow) Corvus violaceus (Violet Crow) Corvus woodfordi (White-billed Crow) Crypsirina cucullata (Hooded Treepie) Crypsirina temia (Racket-tailed Treepie) Cyanocitta cristata (Blue Jay) Cyanocitta stelleri (Steller's Jay) Cyanocorax affinis (Black-chested Jay) Cyanocorax beecheii (Purplish-backed Jay) Cyanocorax caeruleus (Azure Jay) Cyanocorax cayanus (Cayenne Jay) Cyanocorax chrysops (Plush-crested Jay) Cyanocorax cristatellus (Curl-crested Jay) Cyanocorax cyanomelas (Purplish Jay) Cyanocorax cyanopogon (White-naped Jay) Cyanocorax dickeyi (Tufted Jay) Cyanocorax heilprini (Azure-naped Jay) Cyanocorax luxuosus (Green Jay) Cyanocorax melanocyaneus (Bushy-crested Jay) Cyanocorax mystacalis (White-tailed Jay) Cyanocorax sanblasianus (San Blas Jay) Cyanocorax violaceus (Violaceous Jay) Cyanocorax yncas (Inca Jay) Cyanocorax yucatanicus (Yucatan Jay) Cyanolyca argentigula (Silvery-throated Jay) Cyanolyca armillata (Black-collared Jay) Cyanolyca cucullata (Azure-hooded Jay) Cyanolyca mirabilis (White-throated Jay) Cyanolyca nana (Dwarf Jay) Cyanolyca pulchra (Beautiful Jay) Cyanolyca pumilo (Black-throated Jay) Cyanolyca turcosa (Turquoise Jay) Cyanolyca viridicyana (White-collared Jay) Cyanopica cooki (Iberian Magpie) Cyanopica cyana (Azure-winged Magpie) Dendrocitta bayleyi (Andaman Treepie) Dendrocitta cinerascens (Bornean Treepie) Dendrocitta formosae (Grey Treepie) Dendrocitta frontalis (Black-faced au Collared Treepie) Dendrocitta leucogastra (White-bellied Treepie) Dendrocitta occipitalis (Sumatran Treepie) Dendrocitta vagabunda (Rufous Treepie) Garrulus lanceolatus (Black-headed au Lanceolated Jay) Garrulus lidthi (Lidth's Jay) Gymnorhinus cyanocephalus (Pinyon Jay) Nucifraga caryocatactes (Spotted Nutcracker) Nucifraga columbiana (Clark's Nutcracker) Nucifraga multipunctata (Large-spotted Nutcracker) Perisoreus canadensis (Gray au Canada Jay au Whiskeyjack) Perisoreus infaustus (Siberian Jay) Perisoreus internigrans (Sichuan Jay) Pica hudsonia (Black-billed Magpie) Pica nuttalli (Yellow-billed Magpie) Pica pica (Eurasian Magpie) Pica p. sericea (Korean Magpie) Platylophus galericulatus (Crested Jay) – labda ni jamaa ya Prionopidae au ya Laniidae Platysmurus leucopterus (Black Magpie) Podoces biddulphi (Biddulph's Ground Jay) Podoces hendersoni (Henderson's Ground Jay) Podoces panderi (Pander's Ground Jay) Podoces pleskei (Pleske's au Persian Ground Jay) Psilorhinus morio (Brown Jay) Temnurus temnurus (Ratchet-tailed Treepie) Urocissa caerulea (Taiwan Blue Magpie) Urocissa erythrorhyncha (Red-billed Blue Magpie) Urocissa flavirostris (Yellow-billed Magpie) Urocissa ornata (Sri Lanka Blue Magpie) Urocissa whiteheadi (White-winged Magpie) Spishi za kabla ya historia Corvus antecorax (Mwisho wa Pliocene – mwisho wa Pleistocene ya Ulaya) Corvus antipodum (New Zealand Raven) Corvus antipodum antipodum (North Island Raven) imekwisha sasa Corvus antipodum pycrafti (South Island Raven) imekwisha sasa Corvus betfianus Corvus fossilis Corvus galushai (Mwisho wa Miocene ya Big Sandy, Wickieup, MMA) Corvus hungaricus Corvus impluviatus ( High-billed Crow) imekwisha sasa Corvus larteti (Mwisho wa Miocene ya Ufaransa) Corvus moravicus Corvus moriorum (Chatham Islands Raven) imekwisha sasa Corvus neomexicanus (Mwisho wa Pleistocene ya Dry Cave, MMA) Corvus praecorax Corvus pliocaenus (Mwisho wa Pliocene – mwanza wa Pleistocene ya Ulaya ya Magharibi-kusini) Corvus pumilis (Puerto Rican Crow) – labda nususpishi ya C.nasicus/palmarum Corvus simionescui Corvus viriosus (Robust Crow) imekwisha sasa Pica mourerae (Mwisho wa Pliocene – mwanzo wa Pleistocene ya Mallorca) Picha Kunguru na jamaa Wanyama wa Biblia