id
stringlengths
1
6
url
stringlengths
31
202
title
stringlengths
1
120
text
stringlengths
8
182k
1876
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20ya%20maoni
Kura ya maoni
Kura ya maoni zinatumika katika demokrasia ili kuchagua viongozi wa nchi au kuamua kama sheria fulani itumike. Kawaida kura ya maoni hupigwa na wale wote wenye umri halali wa kupiga kura ili kukubali au kukataa pendekezo, sera, sheria, mabadiliko ya katiba, katiba mpya, kukataa au kumuunga mkono kiongozi fulani. Kura ya maoni huchukuliwa kuwa ni aina mojawapo ya demokrasia ya moja kwa moja. Siasa
1877
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kura%20juu%20ya%20katiba%20mpya%20ya%20Kenya%20%282005%29
Kura juu ya katiba mpya ya Kenya (2005)
Kura ya maoni juu ya katiba mpya ya Kenya ilipigwa tarehe 21 Novemba 2005. Asilimia 58 ya Wakenya waliopiga kura waliikataa. Rais wa Kenya na baadhi ya mawaziri walipiga kampeni kutaka Wakenya waiunge mkono katiba hiyo. Kundi lililokuwa likiiunga mkono katiba mpya lilikuwa likiwakilishwa na alama ya ndizi na kundi lililokuwa likiipinga lilitumia alama ya machungwa. Ingawa watu wanane walikufa katika fujo zilizohusiana na kura hiyo, kwa ujumla zoezi hili lilifanyika kwa amani. Suala ambalo lilikuwa likijadiliwa sana ni kiasi cha madaraka ambacho rais anapaswa kupewa. Katiba mpya ilikuwa impe madakaraka makubwa sana rais wa Kenya wakati ambapo wanaoipinga katiba hiyo walitaka kuwe na Waziri Mkuu ambaye atagawana madaraka na Rais. Suala la umiliki wa ardhi nalo lilipewa kipaumbele kwenye mjadala wa kufaa au kutofaa kwa katiba hiyo. Katiba mpya ilikuwa ikiweka vikwazo kwa watu wasio Wakenya kumiliki ardhi, ilikuwa iruhusu wanawake kumiliki ardhi (kwa kurithi), na ilitaka iundwe tume ya ardhi ambayo ingekuwa na wajibu wa kugawa ardhi na kuondoa uwezekano wa viongozi wa serikali kupeana ardhi. Tume hii pia ingekuwa ndio msikilizaji mkuu wa kesi za ardhi na ingekuwa na jukumu la kurudisha ardhi kwa makundi na watu binafsi ambao waliipoteza miaka iliyopita. Siasa ya Kenya Historia ya Kenya
1878
https://sw.wikipedia.org/wiki/Demokrasia%20ya%20moja%20kwa%20moja
Demokrasia ya moja kwa moja
Demokrasia ya moja kwa moja ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, kijamii, kisheria, na kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kama vile bunge. Uwezo huu wa wananchi kutoa maamuzi unaweza kuwapa wananchi hata uwezo wa kimahakama ingawa mara nyingi wananchi hupewa uwezo wa kutunga au kupitisha sheria tu. Muundo wa demokrasia ya asili uwezo huu wa kutunga au kupitisha sheria na kupitisha maamuzi ulikuwa uko mikononi mwa wananchi wenyewe na sio wawakilishi wao. Kutegemeana na mfumo wenyewe wa demokrasia ya moja kwa moja, wananchi huwa wana uwezo wa kutunga sheria, kupitisha sera, kuwaweka madarakani na pia kuwaondoa madarakani viongozi. Demokrasia ya moja kwa moja ni tofauti na demokrasia inayofuatwa katika nchi nyingi duniani hivi sasa ambapo wananchi huchagua wawakilishi wao katika uchaguzi. Siasa
1879
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bunge
Bunge
Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka katika dola. Mihimili mingine ni mahakama na serikali. Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani. Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wa utawala wa Mfalme Henri III katika karne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili, Bunge la Makabwela na Bunge la Mabwanyeye. Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni. Shughuli za bunge husimamiwa na mbunge aliyechaguliwa kama mwenyekiti, rais au spika wa bunge. Kuna aina mbili za bunge: Bunge la "chumba kimoja" ambako wawakilishi wote wa wananchi hukaa na kufanya maazimio pamoja Bunge la "vyumba viwili" ambako kitengo kikubwa zaidi kina kazi ya kutunga sheria na wabunge wake huchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika majimbo ya uchaguzi yanayotakiwa kuwa takriban na idadi ya wapiga kura sawa. Kitengo kingine mara nyingi huitwa "senati" au "chumba cha juu" kwa kawaida ni kidogo zaidi, wabunge wake huchaguliwa ama na wawakilishi wa mikoa au majimbo au wanateuliwa pia kufuatana na kanuni za katiba (k.m. kwa shabaha ya kuwakilisha makundi maalumu katika jamii) na madaraka yake kwa kawaida ni madogo lakini inathibitisha au kukataa sheria zilizoamuliwa na bunge la kwanza; lakini hapa kuna tofauti nyingi kati ya nchi na nchi. Mabunge ya Afrika Orodha ya Wabunge wa Tanzania Ona pia Bunge la Tanzania Marejeo Viungo vya nje Bunge la Tanzania Bunge la Afrika Kusini Bunge la Umoja wa Afrika Bunge la Ghana Bunge la Uingereza Bunge la Ulaya Siasa Sheria
1890
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mahakama
Mahakama
Mahakama ni mfumo wa wataalamu na kamati maalumu ambao unatafsiri na kutumia sheria katika jina la wananchi, la jamhuri au la mfalme. Mahakama pia inatoa mfumo wa kutatua migogoro. Chini ya mfumo wa mgawanyo wa madaraka mahakama kwa ujumla haitungi wala haiundi sheria (ambayo ni kazi ya bunge) wala kutekeleza sheria (ambayo ni wajibu wa serikali), bali inatafsiri sheria na kutumia na kutekeleza katika ukweli wa kila kesi. Mahakama ina kazi ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote. Kwa kawaida kuna mahakama za ngazi mbalimbali; mahakama za juu zinapokea rufaa dhidi ya kesi za ngazi za chini hadi mahakama ya rufaa ya mwisho inayoitwa mahakama kuu au mahakama ya katiba. Tawi hili la mahakama lina uwezo wa kubatilisha sheria zisizolingana na katiba ya nchi. Neno "mahakama" pia hutumika kumaanisha kwa pamoja maafisa ndani yake kama vile majaji, mahakimu na makarani wengine. Mahakama na sheria Kimsingi mahakama ina kazi ya kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya matumizi yao. Hali halisi sheria haziwezi kutaja kila kitu kinachoweza kutokea hivyo ni mahakama zinazoamua kwa njia ya kulinganisha kesi, sheria na maazimio ya mahakama yaliyotangulia. Kwa hiyo mahakama zinashiriki kiasi katika kazi ya kutunga haki hasa pale ambako sheria za bunge zinaacha pengo. Kidesturi muundo wa haki na sheria katika Uingereza na Marekani unaziachia mahakama nafasi kubwa zaidi kuendeleza taratibu za kisheria. Tazama pia Mgawanyo wa madaraka Serikali Bunge Masomo zaidi Cardozo, Benjamin N. (mwaka wa (1998). The Nature wa mchakato wa kimahakam. New Haven: Yale University Press. Feinberg, Kenneth, Jack Kress, Gary McDowell, na Warren E. Burger (1986). The High Cost and Effect of Litigation, matoleo 3. Frank, Jerome (1985). Law and the Modern Mind. Birmingham, AL: Legal Classics Library. Lawi, Edward H. (1949) An Introduction to Legal Reasoning. Chicago: University of Chicago Press. Marshall, Thurgood (2001). Thurgood Marshall: His Speeches, Writings, Arg, maoni na Reminiscences. Chicago: Lawrence Hill Books. McCloskey, Robert G., na Sanford Levinson (2005). The American Supreme Court, toleo la 4. Chicago: University of Chicago Press. Miller, Arthur S. (1985). Politics,Democracyand the Supreme Court:Essays on the Future of Constitutional Theory. Westport, CT: Greenwood Press. Tribe, Laurence (1985). God Save This Honorable Court: How the Choice of Supreme Court Justices Shapes our History. New York: Random House. Zelermyer, William (1977). The Legal System in Operation. St Paul, MN: West Publishing. Maandiko ya Chini Sheria
1891
https://sw.wikipedia.org/wiki/Katiba
Katiba
Katiba ni sheria au kanuni zinazoaInisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao. Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi. Kuna aina kuu mbili za Katiba ambazo ni: (a) Katiba isiyo ya maandishi (ya kimapokeo) (b) Katiba ya maandishi. Katiba ya India ndiyo katiba ndefu kuliko katiba yoyote duniani. Tazama pia Katiba ya Kenya Viungo vya nje [http://www.odele.ru/law/ Constitution Siasa Sheria
1899
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukimwi
Ukimwi
Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi UKIMWI; kifupisho cha Kiingereza AIDS) ni ugonjwa unaotokana na virusi ambavyo kwa Kiswahili vinaitwa kifupi VVU ("Virusi vya UKIMWI"; kwa Kiingereza: HIV, yaani "Human Immunodeficiency Virus") na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maambukizi nyemelezi yanayosababisha maradhi. Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya binadamu kwa kuwa husababisha vifo (yaani kupotea kwa uhai wa watu hao). Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kufikia mwaka 2014 ugonjwa huu umeua watu milioni 39, hasa kati ya wanaoishi barani Afrika upande wa kusini kwa Sahara. Kwa mwaka 2015 pekee wamefariki watu milioni 1.2 na kati yao watoto wengi. UKIMWI umekuwa na madhara makubwa katika jamii, kama ugonjwa wa mwili na kama chanzo cha ubaguzi. Kuna sintofahamu kuhusu UKIMWI kama vile kwamba eti, unaweza kusambazwa kwa kugusana tu bila ngono. Ugonjwa huu pia unasababisha madhara ya kiuchumi ambayo ni makubwa, hasa kwa nchi maskini. Hadi hivi sasa, UKIMWI hauna chanjo wala tiba, lakini ugonjwa huu unaweza kuepukika kwa kuachana na ngono, ambayo ndiyo husababisha sana ugonjwa huu. Pia, watu wanaweza kujikinga kutokana na ugonjwa huu kwa kuepuka kuchangia vifaa au vitu vyenye ncha kali. Kimsingi zaidi ni kwamba ugonjwa huo umetokana na kuenezwa hasa na maadili mabovu. Dhidi yake watu wanahitaji kuelewa tangu utotoni na ujanani maana ya jinsia na maisha kwa jumla, kwamba vinadai upendo, nidhamu na uwajibikaji, si kufuata tamaa tofautitofauti daima. Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya UKIMWI duniani. Maana ya jina UKIMWI ni kifupisho cha "Upungufu wa Kinga Mwilini" Upungufu maana yake UKIMWI unaharibu uwezo wa mwili kupambana na magonjwa. Si UKIMWI moja kwa moja unaoweza kuua lakini mashambulio ya magonjwa ambayo kwa kawaida yasingekuwa tatizo kubwa. Kinga inahusu mfumo wa kingamwili ambao ni uwezo wa mwili kujitetea dhidi ya ugonjwa. Mwili usio na kinga unapatwa na matatizo mbalimbali kwa sababu mfumo wa kinga umeharibika, na hauwezi kupigana na ugonjwa wowote. Jina la Kiingereza ni AIDS = Acquired Immuno Deficiency Syndrome. acquired - maana mtu hawezi kuwa na hali hii kiasili, ameipata immuno - hii inataja ya kwamba tatizo linahusu "immune system" yaani mfumo wa kingamwili deficiency - inamaanisha ya kwamba kuna kasoro syndrome - ni mkusanyiko wa matatizo ya kiafya; ilhali kingamwili haufanyi kazi tena, mgonjwa anaathiriwa na magonjwa mbalimbali na kuonyesha dalili za magonjwa hayo yote. Mfumo wa kingamwili na VVU Kila mtu huwa na mfumo wa kingamwili ndani yake. Seli za ulinzi zinazunguka mwilini na kutafuta vidubini vya nje vinavyoweza kuleta mvurugo na zinaviharibu. Kati ya seli hizi za ulinzi ni seli nyeupe za damu (lukosaiti) ambazo ni muhimu sana. Ukimwi unasababishwa na VVU. Kama virusi vyote, VVU vinaingia katika mwili kwa kusudi la kuzaa. Virusi haviwezi kuzaa peke yake: vinahitaji seli vinapoweza kuingia ndani yake na kutumia mfumo wa seli kwa kunakili DNA yake. Kwa kawaida virusi vinashambuliwa na mfumo wa kingamwili na kuharibika. Lakini VVU vina tabia mbili za pekee ambazo zinavifanya vvya hatari hasa: vinafaulu mara nyingi kuepukana na seli za ulinzi mwilini vinaingia hasahasa katika seli nyeupe za damu za aina "seli za T". VVU vikianza kuongezeka katika seli nyeupe ya damu vinadhoofisha na hatimaye kuharibu seli hii. Maana yake VVU vinashambulia moja kwa moja seli ambazo ni sehemu ya kingamwili na zinazohusika kukinga mwili. Kuenea kwa VVU mwilini kunapunguza idadi ya seli za ulinzi na hivyo kupunguza kiwango cha kingamwili. Baada ya kupungua kwa kingamwili vidubini vingine vinaendelea kufika mwilini lakini sasa vinaenea zaidi kwa sababu seli za ulinzi zimekuwa chache. Kila ambukizo linaendelea kwa muda mrefu zaidi na hivyo mwili kwa jumla unateswa kwa muda mrefu zaidi. Kadiri Ukimwi unavyoendelea vipindi vya magonjwa vinakuwa virefu zaidi na nguvu za mwili zinapunguapungua. Katika ngazi za mwisho idadi ya maambukizo inazidi uwezo wa mwili wa kupambana nayo na hapo mtu unakaribia kifo. Dalili or symptoms. UKIMWI ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili wa binadamu unaosababishwa na virusi vya ukosefu wa kinga mwilini.Mwanzoni, baada ya kuambukizwa, mtu anaweza kukumbwa na kipindi kifupi cha maradhi ya aina ya mafua. Kwa kawaida, hali hii hufuatwa na kipindi kirefu kisicho na dalili. Ugonjwa huu huendelea kutatiza kingamwili jinsi unavyozidi, hivyo kumfanya mtu kuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi, ikiwa ni pamoja na maambukizi nyemelezi, na kansa ambayo kwa kawaida hayawaathiri watu walio na kingamwili njema. Kuna awamu tatu kuu za maambukizi ya VVU: maambukizi makali, awamu fiche na UKIMWI. Maambukizi makali Kipindi cha kwanza kufuatia maambukizi ya VVU huitwa VVU vikali, VVU vya kimsingi au dalili kali za kudhibiti virusi. Watu wengi hupata maradhi ya mfano wa mafua au maambukizi ya mfano wa mononukleosi wiki 2 - 4 baada ya kuambukizwa ilhali wengine hawana dalili zozote kuu.Dalili hutokea katika asilimia 40-90 ya visa vyote na mara nyingi hujumuisha homa, tezi kubwa na chungu za limfu, inflamesheni ya koo, upele, maumivu ya kichwa, na/au vidonda vya kinywa na sehemu za uzazi.Upele huu, unaotokea katika asilimia 20 - 50 ya visa, hutokea katika kiwiliwili, na kwa kawaida huwa wa makiulopapula. Baadhi ya watu pia hupata maambukizi nyemelezi katika awamu hii.Dalili za tumboni na utumboni kama vile kichefuchefu, kutapika au kuharisha zinaweza kutokea, sawa na dalili za kinuroni za niuropathia ya pembeni au sindromu ya Guillain-Barre. Muda ya dalili hutofautiana, ingawa kwa kawaida huwa wiki 1 - 2. Kufuatia sifa zake za kutokuwa dalili maalum, hizi mara nyingi haziwezi kutambulika kama dalili za maambukizi ya VVU. Hata visa vinavyotambuliwa na daktari wa familia au katika hospitali mara nyingi hutambulika vibaya kama baadhi ya visababishi vingi vya magonjwa ambukizi yaliyo na dalili zinazoingiliana. Kwa hivyo, inapendekezwa kuchunguza VVU katika watu wanaoonyesha homa isiyoelezeka ambao wanaweza kuwa na vipengele hatari vya kuambukizwa. Awamu fiche Dalili za kwanza hufuatwa na awamu fiche (VVU visivyo na dalili au VVU vya muda mrefu).Bila ya matibabu, awamu hii ya pili ya historia asilia ya maambukizi ya VVU inaweza kudumu kutoka miaka 3 hadi zaidi ya miaka 20; (wastani wa miaka 8).Ingawa kwa kawaida mwanzoni kuna dalili chache, au hata zisiwemo, karibu mwishoni mwa awamu hii, watu wengi hupatwa na homa, kukonda, matatizo ya tumbo na utumbo, na maumivu ya misuli. Kati ya asilimia 50 na 70 ya wagonjwa pia hupata limfadenopathia ya mwili wote inayorejea, ambayo hudhihirika kwa uvimbe usio na kisababishi na usio chungu wa zaidi ya kikundi kimoja cha tezi za limfu (ila katika sehemu za uzazi) kwa zaidi ya miezi 3 hadi 6. Ingawa watu wengi walioambukizwa VVU-1 wana kiwango cha virusi kinachoweza kutambulika, na ambacho bila matibabu kitaendelea na kuwa UKIMWI, idadi ndogo (5%) huwa na kiwango kikubwa cha seli za CD4+(seli saidizi za T) bila matibabu ya kudhibiti virusi kwa zaidi ya miaka 5. Watu hao huainishwa kama wadhibiti wa VVU au watu wasioendeleza kwa muda mrefu, ilhali wale ambao pia hudumisha kiwango cha chini au kisichotambulika cha virusi bila matibabu hujulikana kama "wadhibiti hodari" au "wagandamizaji hodari" . Ukosefu wa Kinga Mwilini Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI) hufasiliwa kwa msingi wa kiwango cha seli za CD4 + cha chini ya seli 200 kwa kila µL au kutokea kwa magonjwa maalumu yanayohusiana na maambukizi ya VVU. Bila matibabu maalum, takriban nusu ya watu walioambukizwa VVU hupata UKIMWI katika muda wa miaka 10.Hali zinazotokea mara nyingi zaidi kudhihirisha uwepo wa UKIMWI ni numonia ya numosistisi (40%), kakeksi kwa muundo wa dalili dhoofishi za VVU (20%) na kandidiasi ya umio.Dalili nyingine ni pamoja na maambukizi ya njia ya pumzi. Maambukizi nyemelezi yanaweza kusababishwa na bakteria, virusi, kuvu na vimelea ambavyo kwa kawaida hudhibitiwa na mfumo wa kingamwili.Maambukizi yanayotokea hutegemea, kwa upande mmoja, aina ya viumbehai vinavyopatikana kwa wingi katika mazingira ya mtu.Maambukizi hayo yanaweza kudhuru karibu kila mfumo wa viungo. Watu walio na UKIMWI wako katika hatari kuu zaidi ya kupata saratani nyingi zinazosababishwa na virusi, kama vile: Sakoma ya Kaposi, limfoma ya Burkitt, limfoma ya mfumo mkuu wa neva na saratani ya seviksi.Sakoma ya Kaposi ndiyo saratani inayotokea mara nyingi, yaani katika asilimia 10 hadi 20 ya watu wenye VVU.Saratani inayoifuata ni limfoma, ambayo imesababisha vifo vya karibu 16% ya watu wanaoishi na UKIMWI, na ndiyo dalili ya kwanza ya UKIMWI katika asilimia 3 - 4 ya watu.Saratani hizi mbili huhusishwa na virusi vya hepesi ya binadamu aina ya 8.Saratani ya seviksi hutokea mara nyingi zaidi katika watu walio na UKIMWI kwa sababu ya jinsi inavyohusiana na virusi vya papiloma ya binadamu. Isitoshe, watu hao mara nyingi huwa na dalili za kimfumo, kama vile homa ya muda mrefu, jasho (hasa usiku), tezi za limfu zilizofura, ubaridi, udhaifu na kupoteza uzito.Kuharisha ni dalili nyingine inayotokea katika takriban 90% ya watu wenye UKIMWI. Lini na wapi VVU vilianza UKIMWI huchukuliwa kama janga — yaani mlipuko wa ugonjwa katika eneo kubwa, na ambao ungali unaenea. UKIMWI ulitambuliwa mara ya kwanza na Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa huko Marekani mwaka 1981, ilhali kisababishi chake - VVU - kilitambuliwa mwanzoni mwa muongo huo nchini huko. Matukio ya kwanza yalikuwa katika kikundi kidogo cha waraibu wa dawa za kudungia na wanaume shoga wasiokuwa na visababishi bayana vya udhaifu wa kingamwili na walioonyesha dalili za numonia ya Pneumocystis carinii, maambukizi nyemelezi yanayotokea kwa nadra na maarufu katika watu wenye kingamwili dhaifu sana. Punde baadaye, idadi isiyotarajiwa ya mashoga wakapata Sakoma ya Kaposi (SK), saratani ya ngozi iliyokuwa nadra sana hapo awali.Visa vingine vingi vya NPC na SK vilitokea huku vikitahadharisha Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani, hivyo kikosi cha kiutendaji kikaundwa ili kuudhibiti mzuko huu. Katika siku za kwanza, kituo hicho hakikuwa na jina rasmi la ugonjwa huu, mara nyingi wakitumia majina ya magonjwa mengine yaliyohusishwa nao, kwa mfano, limfadenopathi, jina ambalo baadaye wavumbuzi wa VVU waliviita virusi hivi. Wavumbuzi pia walitumia “Sakoma ya Kaposi na Maambukizi nyemelezi”, jina lililokuwa la kikosi cha kiutendaji kilichoanzishwa mwaka wa 1981. Wakati mmoja, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kiliunda msemo "ugonjwa wa 4H", kwani sindromu hii ilionekana kuwaathiri watu wa Haiti, mashoga (homosexuals), wenye hemofilia na watumiaji wa heroini. Katika vyombo vikuu vya habari liliundwa neno "GRID" (lililosimamia "gay-related immune deficiency", yaani "ukosefu wa kinga uliohusishwa na mashoga". Hata hivyo, baada ya kutambua kuwa VVU havikuwaathiri jamii ya mashoga pekee, ilibainika kuwa neno GRID lilikuwa likipotosha, hivyo neno UKIMWI likaanzishwa kwenye mkutano mnamo Julai 1982. Kufikia Septemba 1982, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kilianza kuuita UKIMWI. Mnamo 1983, vikundi viwili tofauti vya watafiti vilivyoongozwa na Robert Gallo na Luc Montagnier bila kutegemeana vilitangaza kuwa retrovirusi mpya ilikuwa ikiwaambukiza wagonjwa wa UKIMWI, hivyo wakachapisha matokeo yao katika jarida la Science. Gallo alidai kuwa virusi vilivyokuwa vimetambuliwa kwa mara ya kwanza na kikundi chake kilikuwa sawa katika umbo na virusi vya binadamu vya limfotrophia-T. Kikundi cha Gallo kiliviita virusi hivi HTLV-III. Wakati huohuo, kikundi cha Montagnier kilitambua virusi kutoka kwa mgonjwa aliyekuwa na uvimbe wa tezi za limfu kwenye shingo na udhaifu wa mwili ambazo ni dalili mbili bainifu za UKIMWI. Huku wakikanusha ripoti ya kikundi cha Gallo, Montagnier na wenzake walionyesha kuwa viini vya protini vya virusi hivyo vilikuwa tofauti na HTLV-I kiukingamwili. Kikundi cha Montagnier kiliviita virusi walivyovitambua virusi vinavyohusishwa na limfadenopathi. Virusi hivi vilibainika kuwa sawa mwaka wa 1986 na kubadilishwa na kuitwa VVU. Leo wanasayansi wengi wanaamini VVU-1 na VVU-2 vimetokana na jamii ya sokwe huko Afrika Magharibi na ya Kati mwishoni mwa karne ya 19 au mwanzoni mwa karne ya 20, wakati virusi vya SIV kutoka kwa nyani au sokwe vilikwenda kwa binadamu. VVU-1 vinaaminika kutoka kusini mwa Cameroon kupitia kugeuka kwa VSVU(cpz), (virusi vya sokwe vinavyosababisha ukosefu wa kinga mwilini) vinavyoambukiza sokwe wa mwituni (VVU-1 hutokana na mzuko wa magonjwa ya VSVUcpz katika nususpishi ya sokwe iitwayo Pan troglodytes troglodytes). Virusi vinavyohusiana kwa karibu na VVU-2 ni VSVU(smm) ambavyo ni virusi vya mangabi mwenye masizi (Cercocebus atys atys), tumbili wa kale anayeishi Afrika Magharibi (kutoka kusini mwa Senegali hadi magharibi mwa Côte d'Ivoire). Tumbili wa kisasa kama vile tumbili bundi wana ukinzani wa maambukizi ya VVU-1 kwa sababu ya uunganishaji wa jeni mbili zinazokinzana na virusi. VVU-2 inadhaniwa kuruka kizuizi cha spishi katika angalau matukio matatu tofauti, hivyo kupelekea vikundi vitatu vya virusi hivi ambavyo ni M, N na O. Kuna ushahidi kuwa wanadamu wanaoshughulikia nyama za mwituni kwa kuwinda au kuziuza, kwa kawaida hupata VSVU.Hata hivyo, virusi hivyo ni dhaifu na hukandamizwa na mfumo wa kingamwili baada ya wiki kadhaa za kuambukizwa. Inadhaniwa kuwa maambukizi kadhaa ya virusi hivyo kutoka kwa mtu hadi mwingine katika mfululizo wa haraka huhitajika ili vipate wakati unaotosha kubadilika na kuwa VVU. Zaidi ya hayo, kwa sababu ya kiwango chake kidogo cha kuambukiza kutoka kwa mtu hadi mwingine, virusi hivyo vinaweza tu kuenea katika wingi wa watu iwapo kuna njia moja au mbili za hatari ya kuambukizana ya kiwango cha juu. Njia hizi zinadhaniwa kutokuwepo barani Afrika kabla ya karne ya 20. Njia maalumu za hatari kubwa ya maambukizi zinazoruhusu virusi hivi kubadilika ili kuweza kuishi katika wanadamu na kuenea katika jamii yote hutegemea wakati uliopendekezwa wa kuvuka kutoka kwa mnyama hadi mwanadamu. Tafiti za kijeni za virusi hivi zinadokeza kuwa chanzo cha hivi karibuni zaidi cha VVU-1 ya kikundi M kilitokea mnamo 1910. Wanaotaja kipindi hicho maalumu huhusisha mzuko wa janga la VVU na kuibuka kwa ukoloni na ukuaji wa miji mikubwa ya kikoloni ya Afrika, huku ukisababisha mabadiliko ya jamii pamoja na kiwango kikubwa cha uasherati, uenezi wa ukahaba na matukio mengi ya vidonda vya viungo vya uzazi (kama vile kaswende) katika miji iliyochipuka. Ingawa viwango vya uambukizaji wakati wa ngono ya kupitia uke viko chini katika hali ya kawaida, kuna ongezeko kubwa iwapo mmoja wa wapenzi hao ana ugonjwa wa zinaa unaosababisha vidonda vya viungo vya uzazi. Miji ya kikoloni ya miaka ya kwanza ya 1900 ilijulikana kwa maambukizi ya viwango vya juu kutokana na ukahaba na vidonda vya viungo vya uzazi, hivi kwamba, kufikia mwaka 1928, 45% ya wanawake wakazi wa mashariki mwa Kinshasa walidhaniwa kuwa makahaba. Kufikia mwaka 1933, takriban 15% ya wakazi wote wa mji huo walikuwa wameambukizwa aina mojawapo ya kaswende. Maoni mengine yanadokeza kuwa hatua zisizo salama za uuguzi barani Afrika katika miaka ya baada ya Vita vya pili vya dunia, kama vile kutumia tena na tena sindano zisizosafishwa kuchanja umati, antibayotiki na kampeni dhidi ya malaria ndizo njia za kwanza zilizoruhusu virusi hivyo kujibadilisha vikiwa ndani ya wanadamu kisha kuenea. Visa vilivyonakiliwa vyema vya VVU katika mwanadamu ni vya mwaka 1959 katika eneo la nchi ya Kongo. Kuna uwezekano kuwa virusi hivyo vilikuwemo huko Marekani mwaka 1966,lakini maambukizi mengi yanayotokea nje ya Kusini kwa Sahara yanaweza kufuatiliwa hadi kwa mtu mmoja aliyeambukizwa na VVU katika nchi ya Haiti na kisha kuyapeleka maambukizi hayo nchini Marekani takriban mwaka 1969. Janga hili kisha lilienea kwa haraka katika vikundi vilivyo katika hatari kubwa ya kuambukizwa (mwanzoni ilikuwa ni wanaume waliofanya ngono na wanaume). Kufikia mwaka 1978, maambukizi ya VVU-1 katika mashoga wenyeji wa New York na San Francisco yalikadiriwa kuwa 5%, kuonyesha kuwa maelfu ya watu nchini Marekani tayari walikuwa wameambukizwa. Uambukizaji VVU husambaa hasa kupitia njia tatu kuu: ngono (ikiwa ni pamoja na ulawiti na hata ngono ya mdomoni), kuingiliana na viowevu vya mwili vilivyoambukizwa (hasa kuongezewa damu au kudungwa sindano) na kutoka kwa mama hadi mtoto wakati wa ujauzito, kuzaa au kunyonyeshaBaadhi ya viowevu vya mwili, kama vile mate na machozi, havisambazi VVU. Kupitia ngono Kufanya ngono zembe kumepelekea visa vingi zaidi vya maambukizi ya VVU kote ulimwenguni, huku mwingiliano baina ya watu wa jinsia tofauti ukichangia visa zaidi ya mwingiliano wa mashoga kote ulimwenguni (kwa sababu mashoga ni wachache zaidi). Hata hivyo, mtindo wa usambazaji hutofautiana pakubwa baina ya mataifa mbalimbali. Nchini Marekani, visa vingi zaidi vya usambazaji wa kingono vilitokea katika wanaume wanaofanya ngono na wanaume (kwa sababu huko ushoga umeenea zaidi)huku idadi hii ikichangia 64% ya visa vyote vipya. Kuhusu ngono zembe baina ya watu wa jinsia tofauti, makadirio ya hatari ya kusambazwa kwa VVU kwa kila kitendo cha ngono yanaonekana kuwa zaidi kwa mara 10 katika mataifa yasiyostawi kuliko mataifa yaliyostawi.Katika mataifa yasiyostawi, hatari ya usambazaji wa mwanamke hadi mwanamume imekadiriwa kuwa 0.38% kwa kila kitendo, huku usambazaji wa mwanamume hadi mwanamke ukiwa 0.30%; makadirio mbadala katika mataifa yaliyostawi ni 0.04% kwa kila kitendo katika usambazaji wa mwanamke hadi mwanamume, na 0.08% kwa kila kitendo katika maambukizi ya mwanamume hadi mwanamke. Hatari ya kuambukizwa kutokana na ngono ya kinyeo (ulawiti) iko juu sana, ikikadiriwa kuwa 1.41.7% kwa kila kitendo (katika ngono ya watu wa jinsia moja na tofauti pia). Ingawa hatari ya kuambukizwa kupitia ngono ya mdomoni iko chini, bado ipo. Hatari ya kila kitendo imekadiriwa kuwa 00.04% kwa ngono pokezi ya mdomoni. kwa kuwa visa vichache vimeripotiwa. Katika miktadha inayohusisha ukahaba kote ulimwenguni, hatari ya maambukizi ya mwanamke hadi mwanamume imekadiriwa kuwa 2.4% kwa kila kitendo, huku maambukizi ya mwanamume kwa mwanamke yakiwa 0.08% kwa kila kitendo. Hatari ya kuambukizwa huongezeka katika wingi wa magonjwa ya zinaa na vidonda vya uzazi.Vidonda vya sehemu za uzazi vimekisiwa kuongeza hatari hadi mara tano. Maambukizi mengine ya zinaa, kama vile kisonono, klamidia, trikomoniasi, vaginosi ya kibakteria, huhusishwa na aghalabu ongezeko dogo la hatari ya kuambukizwa. Wingi wa virusi kwa mtu aliyeambukizwa ni suala kuu la hatari katika usambazaji wa kingono na pia wa kutoka kwa mama hadi mtoto. Katika miezi 2.5 ya kwanza baada ya kuambukizwa VVU, uwezo wa mtu kuambukiza ni mara 12 zaidi kwa sababu ya wingi wa virusi. Iwapo mtu yuko katika awamu za mwisho za VVU, viwango vya kuambukizana ni takriban mara 8 zaidi. Ngono shari inaweza kuwa suala linalochangia ongezeko la hatari ya kuambukizwa. Ubakaji pia unaaminika kuongezeka hatari ya kusambaza VVU kwa sababu ni nadra kondomu kutumika, huwa na uwezekano wa kujeruhiwa ukeni au kinyeo, na pia kuna uwezekano wa magonjwa ya zinaa yanayoambatana na VVU. Viowevu vya mwili Njia ya pili maarufu zaidi ya usambazaji wa VVU ni kupitia kwa damu na mazao yake. Usambazaji wa kupitia damu unaweza kuwa kupitia sindano inayotumiwa na watu wengi wanapoongezwa viowevu mwilini, majeraha ya sindano, kuongezwa damu chafu au mazao ya damu, au kudungwa kwa vifaa visivyotakaswa. Hatari inayotokana na kutumia sindano baina ya watu wengi wakati wa kudungwa dawa ni kati ya 0.63-2.4% kwa kila kitendo, wastani wake ukiwa 0.8% Hatari ya kuambukizwa VVU kwa sindano iliyotumiwa na mtu aliyeambukizwa VVU hukadiriwa kuwa 0.3% (takriban mara 1 kwa 133) kwa kila kitendo, ilhali hatari inayofuatia tando za ute kuingiliana na damu iliyoambukizwa ni 0.09% (takriban 1 kwa 1000) kwa kila kitendo. Nchini Marekani, watu wanaodungwa dawa ndani ya misuli walichangia 12% ya visa vyote vipya vya VVU mwaka wa 2009, huku 80% ya watu katika sehemu fulani wanaodungwa dawa wakiwa wameambukizwa VVU. Kuongezewa damu iliyoambukizwa huchangia maambukizi kwa takriban 93% ya visa vyote.Katika mataifa yaliyostawi, hatari ya kuambukizwa VVU kutokana na kuongezewa damu iko chini sana (chini ya 1 kwa 500,000) ambapo viwango vya juu vya kuchagua mtu atakayetoa damu na pia upimaji VVU hufanywa. Kule Uingereza, hatari iliyoripotiwa ni 1 kwa milioni 5. Hata hivyo, katika mataifa yenye mapato ya chini, nusu tu ya damu inayoongezwa huwa imepimwa vyema (kufikia mwaka wa 2008). Inakadiriwa kuwa hadi 15% ya maambukizi ya VVU katika maeneo hayo hutokana na kuongeza damu au mazao ya damu yaliyoambukizwa, hii ikiwa ni asilimia 5 - 10 ya maambukizi ya ulimwengu mzima. Sindano za tiba zisizo salama huchangia pakubwa katika kueneza UKIMWI katika eneo la Kusini kwa Sahara. Mnamo 2007, kati ya 12% na 17% ya maambukizi katika eneo hilo yalichangiwa na matumizi ya sindano hizo. Shirika la Afya Duniani linakadiria hatari ya kuambukizwa kupitia sindano hizo barani Afrika kuwa 1.2%. Hatari kuu huhusishwa na taratibu vamizi, kusaidiwa kuzaa na utunzaji wa meno katika sehemu hii ya dunia. Watu wanaochanja au kuchanjwa chale, chale za mwili na kutia kovu hudhaniwa kuwa katika hatari ya kuambukizwa, ingawa hakuna visa vilivyothibitishwa ambavyo vimenakiliwa. Haiwezekani mbu au wadudu wengine kusambaza VVU. Mtu anaweza pia kupata VVU kwa kuchanga sindano na wenzake. Hii ina maana ya kutumia sindano ambayo haijawahi kusafishwa baada ya mtu mwingine kuitumia. Baadhi ya watu ambao, kinyume cha sheria, huchukua madawa ya kulevya kama heroin na cocaine huchukua dawa hizo kwa sindano. Baadhi yao wanachanga sindano moja. Kama mmojawao ana virusi ya UKIMWI na anashirikisha sindano yake, anaweza kuambukiza HIV kwa watu wengine. Mama hadi mtoto VVU vinaweza kusambazwa kutoka kwa mama hadi mtoto wakati wa ujauzito, kuzaa au kunyonyesha. Njia hii ni ya tatu kwa umaarufu wa kusambaza VVU kote duniani. Bila matibabu, hatari ya kusambazwa wakati wa au baada ya kuzaliwa ni takriban 20%, na 35% kwa watoto wanaonyonya.Kufikia mwaka wa 2008, usambazaji wima ulichangia takriban 90% ya visa vya VVU katika watoto. Hatari ya kusambazwa kutoka kwa mama hadi mtoto inaweza kupunguzwa hadi 1% kwa kutumia matibabu mwafaka. Matibabu ya kukinga hujumuisha mama kutumia dawa za kudhibiti virusi wakati wa ujauzito na kuzaa, kuchagua kuzaa kwa kupasuliwa, kutonyonyesha na kumpa mtoto dawa za kudhibiti VVU.Hata hivyo, idadi kubwa ya mbinu hizi hazipatikani katika mataifa yanayostawi. Iwapo damu itachafua chakula wakati wa mtoto kutafuna, itaongeza hatari ya kuambukiza. VVU na UKIMWI Virusi vyenyewe VVU ndivyo kisababishi cha mkusanyiko wa magonjwa yanayojulikana kijumla kama VVU/UKIMWI. VVU ni retrovirusi ambavyo hasa huambukiza vipengele vya mfumo wa kingamwili ya binadamu kama vile seli za CD4+T, makrofaji na seli za dendraiti. Virusi hivi huharibu seli za CD4+ T moja kwa moja au vinginevyo. VVU ni mshirika wa jenasi ya Lentivirus, sehemu ya familia ya Retroviridae. Virusi vyote vya lenti huwa na sifa sawa za kimofolojia na biolojia. Spishi nyingi za mamalia huambukizwa na virusi vya lenti, ambavyo haswa huwa ndivyo visababishi vya maradhi ya muda mrefu yaliyo na kipindi cha kupevuka kirefu.Virusi vya lenti husambazwa kama virusi vya RNA chanya za uzi mmoja hisia zilizo ndani ya kigamba. Inapoingia ndani ya seli iliyolengwa, jenomu ya RNA ya virusi hugeuzwa (hubadilishwa kinakala) na kuwa DNA ya nyuzi mbili ambayo husafirishwa pamoja na jenomu ya virusi katika chembe ya virusi vile. DNA ya virusi inayoundika huingia katika kiini cha seli ambapo huchangamana na seli ya DNA kwa kutumia integresi iliyofasiliwa kama virusi, na pia vipengele husika vya kiini kikuu. Vinapochangamana na DNA ya seli, virusi hivi vinaweza kuingia katika awamu fiche, hivyo kuwezesha virusi hivi pamoja na seli inayovipokea kuepuka kutambuliwa na mfumo wa kingamwili. Aina mbili za VVU zimetambulika: VVU-1 na VVU-2. VVU-1 ni virusi vilivyotambulika kwanza (na ambavyo mwanzoni vilijulikana pia kama LAV au HTLV-III). Virusi hivi vina sumu kali, vyenye kuambukiza, na ndivyo visababishi vikuu vya visa vingi vya maambukizi ya VVU kote ulimwenguni. Kiwango cha chini zaidi cha uambukizaji wa VVU-2 ikilinganishwa na VVU-1 huonyesha kuwa watu wachache zaidi walio katika hatari ya VVU-2 wataambukizwa kila wanapokumbana na virusi hivi. VVU-2 hupatikana zaidi Afrika Magharibi kwa sababu ya uwezo wake wa chini wa kuambukiza. Baada ya virusi kuingia mwilini, kuna kipindi cha kugawanyika kwa virusi, hali inayopelekea wingi wa virusi katika damu ya pembeni. Katika kipindi cha kwanza cha maambukizi, kiwango cha VVU kinaweza kufika milioni kadhaa za chembe za virusi kwa kila mililita ya damu. Mwitikio huu huandamana na kiwango kikubwa cha kushuka kwa idadi ya seli za CD4+ T zinazozunguka. Viremia kali mara nyingi huhusishwa na kuwezeshwa kwa CD8+ seli za T, ambazo huangamiza seli zilizoambukizwa VVU na kisha kuhusishwa na kuzalishwa kwa zindiko, au kuzalishwa kwa zindiko mpya. Mwitikio wa seli za CD8+ T huchukuliwa kuwa muhimu katika kudhibiti viwango vya virusi, ambavyo hupanda na kushuka, huku viwango vya seli za CD4+ T vikirejea. Mwitikio bora wa seli za CD8+ T umehusishwa na kupungua kwa mwendo wa ugonjwa na pia prognosi bora zaidi, ingawa mwitikio huu hauondoi virusi. Pathofisiolojia ya UKIMWI ni tata. Mwishowe, VVU husababisha UKIMWI kwa kuharibu CD4+seli za T. Hali hii hudhoofisha mfumo wa kingamwili hivyo kuwezesha mambukizi vamizi. Seli za T ni muhimu kwa mwitikio wa kingamwili, hivyo bila ya seli hizi, mwili hauwezi kukabiliana na maambukizi wala kuharibu seli za saratani. Utendakazi wa kuharibiwa kwa seli za CD4+ T hutofautiana katika awamu kali na za muda mrefu. Katika awamu kali, lisisi ya seli inayosababishwa na VVU, na pia kuangamizwa kwa seli za T angamizi huchangia katika kuharibiwa kwa seli za CD4+ T, ingawa apoptosi pia inaweza kuchangia hali hii. Katika awamu ya muda mrefu, matokeo ya uwezeshaji wa kijumla wa kingamwili ukiandamana na udhaifu wa pole pole wa uwezo wa mfumo wa kingamwili kuzalisha seli mpya za T hukisiwa kuchangia kupungua kwa pole pole kwa idadi ya seli za CD4+ T. Ingawa dalili za udhaifu wa kingamwili kama ulivyo katika UKIMWI hazitokei kwa miaka mingi baada ya kuambukizwa, kiwango kikubwa cha kuharibika kwa seli za CD4+ T hutokea katika wiki za kwanza baada ya kuambukizwa, hasa katika ute wa utumbo, ambao huwa na kiwango kikubwa cha limfosaiti zote za mwili. Sababu ya kiwango hiki kikubwa cha kuharibiwa kwa seli za CD4+ T ni kuwa kiwango kikubwa cha seli za ute za CD4+ T huzalisha protini ya CCR5 inayotumika na VVU kama kipokezi kishiriki ili kuweza kufikia seli hizo, ilhali kipande kidogo tu cha seli za CD4+ T katika mkondo wa damu hufanya hivyo. VVU hutafuta na kuharibu CCR5 inayotolesha seli za CD4+ T katika awamu kali ya maambukizi. Mwitikio mkubwa wa kingamwili hatimaye huyadhibiti maambukizi hayo kisha kuanzisha awamu fiche ya kiutambuzi. Seli za CD4+ T katika tishu za ute husalia zikiwa zimeathiriwa sana. Ugawanyikaji endelevu wa VVU husababisha hali ya uwezeshaji wa kijumla wa kingamwili, ambao hudumu katika awamu yote ya muda mrefu. Uwezeshaji wa kingamwili, ambao hutambulika kwa ongezeko la uwezeshaji wa hali ya seli za kingamwili na kutoleshwa kwa saitokini inayosababisha inflemesheni, husababishwa na utendakazi wa zao la jeni na mwitikio wa kingamwili dhidi ya ugawanyikaji wa VVU unaoendelea. Uwezeshaji wa kingamwili pia huhusishwa na kuharibika kwa mfumo wa uchunguzi wa kingamwili wa kizuizi cha ute wa tumbo na utumbo, hali inayosababishwa na kuangamizwa kwa seli za CD4+ T za ute katika awamu kali ya ugonjwa huu. Hivyo si kila mtu aliye na VVU ana UKIMWI. Wakati watu wanapata VVU, wanaweza kuwa na afya kwa miaka mpaka akakutwa na aina maalumu ya magonjwa na vipimo vya damu vikionyesha kuwa ina idadi ndogo sana ya seli nyeupe za damu ambazo ndizo zinazopambana na maambukizi. Kuna maradhi ambayo kwa kawaida ni ishara kwamba mtu ana UKIMWI kwa kuwa watu wenye afya njema hawapati magonjwa haya, kwa sababu mfumo wa kinga mwilini una nguvu ya kutosha ya kupigana na magonjwa hayo. Hivyo kupata ugonjwa wa aina hiyo ni ishara kwamba mfumo wa kinga umeharibika. Baadhi ya magonjwa hayo ni: Sarkoma ya Kaposi - aina ya kansa ambayo kwa kawaida huathiri ngozi (mara nyingi husababisha vidonda vyekundu au zambarau, au majeraha juu ya ngozi). Wakati mwingine huathiri tu ngozi, bali pia mifumo mingine katika mwili. Retinitis - virusi zinashambulia nyuma ya jicho. Pneumocystis carinii (kifupi PCP) - aina ya pneumonia, magonjwa ya kuambukiza ya mapafu. PCP ni maambukizi ya kawaida kwa wagonjwa wa UKIMWI. Toxoplasmosis - ugonjwa unaosababishwa na vimelea, ambao unaweza kusababisha matatizo katika mifumo ya ubongo na mingine katika mwili. Kansa ya kizazi - ambayo huwa inaenea. Utambuzi VVU hutambuliwa kupitia uchunguzi wa kimaabara kisha kuainishwa kiawamu kwa msingi wa uwepo wa dalili au ishara fulani. Watu walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa hupendekezwa kupimwa VVU, ikiwa ni pamoja na mtu yeyote aliye na ugonjwa wa zinaa Katika maeneo mengi ya ulimwengu, 1/3 ya watu wenye VVU hutambua kuwa wameambukizwa katika awamu za mwishoni mwa ugonjwa huu wakati UKIMWI au ukosefu mkuu wa kingamwili umekuwa wazi. Uchunguzi wa VVU Watu wengi walioambukizwa VVU huzalisha zindiko maalum (yaani kuzalisha zindiko mpya) katika wiki 3 hadi 12 tangu maambukizi ya kwanza. Utambuzi wa VVU vya kimsingi hufanywa kabla ya kuzalishwa kwa zindiko mpya kwa kupima RNA ya VVU au antijeni ya p24. Matokeo chanya yanayopatikana kwa kupima MAP au zindiko huthibitishwa kwa zindiko au MAP tofauti. Vipimo vya zindiko kwa watoto wa umri wa chini ya miezi 18  kwa kawaida huwa kasoro kwa sababu ya uwepo endelevu wa zindiko za mama. Kwa hivyo, maambukizi yanaweza kutambulika tu kwa vipimo vya MAP vya VVU, RNA au DNA, au kupitia kupima uwepo wa antijeni ya p24.Sehemu kubwa ya ulimwengu haina uwezo wa kupata vipimo bora vya MAP huku watu wa sehemu nyingi wakisubiri hadi dalili za watoto wao kuendelea au watoto hao kukua hadi kuwa na uwezo wa kupimwa kikamilifu. Kufikia mwaka wa 2007-2009 katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, kati ya asilimia 30-70 ya watu walikuwa wakifahamu hali yao ya VVU. Mnamo mwaka wa 2009, kati ya asilimia 4-42 ya watu hawa walipimwa. Takwimu hizi zinaonyesha ongezeko kubwa kutoka miaka ya awali. Uainishaji wa maambukizi ya VVU Mifumo miwili mikuu ya uainishaji hutumika kuainisha VVU na magonjwa husika kwa ajili ya uchunguzi: mfumo wa uainishaji wa magonjwa wa Shirika la Afya Duniani, na mfumo wa VKM wa uainishaji wa maambukizi ya VVU. The VKM hutumika zaidi katika mataifa yaliyostawi. Kwa vile mfumo wa uainishaji wa SAD hauhitaji vipimo vya mahabara, mfumo huu ni mwafaka kwa mataifa yanayostawi ambayo kwa kawaida yana upungufu wa vifaa, ambapo unaweza pia kutumika kuongoza udhibiti wa kimatibabu. Ingawa mifumo hii miwili ni tofauti, yote huwezesha ulinganishaji kwa ajili ya malengo ya kitakwimu. Shirika la Afya Duniani lilipendekeza ufasili wa UKIMWI mara ya kwanza mwaka wa 1986. Tangu hapo, ufasili wa Shirika hili umedurusiwa na kurefushwa mara kadhaa, toleo la hivi karibuni likiwa la mwaka wa 2007. Mfumo wa SAD hutumia vikundi vifuatavyo: Maambukizi ya kimsingi ya VVU: Yanaweza kuwa bila dalili au yakihusishwa na sindromu kali ya retrovirusi. Awamu ya I: Maambikizi ya VVU huwa bila dalili yakiwa na kiwango cha seli za CD4+ T (ambacho pia huitwa kiwango cha CD4) cha zaidi ya 500/uL. Maambukizi haya yanaweza kujumuisha kuvimba kwa tezi za mwili wote. Awamu ya II: Dalili ndogo zinaweza kuhusisha kiwango cha chini cha kudhihirika kwa za tando za ute na maambukizi yanayorejea ya sehemu ya juu ya njia ya pumzi. Kiwango cha seli za CD4 cha chini ya 500/uL.. Awamu ya III: Dalili kuu zinazoweza kujumuisha hali ya kuharishaya muda mrefu isiyo na kisababishi maalum kwa zaidi ya mwezi mmoja, maambukizi makali ya bakteria ikiwa ni pamoja na tiibii ya mapafu na pia kiwango cha seli za CD4 cha chini ya 350/uL. Awamu ya IV ya UKIMWI: dalili kali zinazojumuisha toksoplasmosi ya ubongo, ukungu wa umio, trakea, bronkasi au mapafu na sakoma ya Kaposi. Kiwango cha seli za CD4 cha chini ya 500/uL.. Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani pia kilianzisha mfumo wa uainishaji wa VVU, kilichoudurusu mwaka wa 2008. Katika mfumo huu, maambukizi ya VVU yameainishwa kulingana na kiwango cha CD4 na dalili za kiutambuzi, nayo hueleza maambukizi kwa awamu tatu: Awamu ya 1: Kiwango cha CD4 cha seli ≥ 500 /uL na hakuna hali zinazoashiria UKIMWI Awamu ya 2: Kiwango cha seli za CD4 200 hadi 500 /uL na hakuna hali zinazoashiria UKIMWI Awamu ya 3: Kiwango cha seli za CD4≤ 200 cells/uL au hali zinazoashiria UKIMWI. Tashwishi: iwapo habari iliyopo haitoshi kufanya uainishaji uliopo juu Kwa sababu za kiuchunguzi, utambuzi wa UKIMWI hubakia iwapo baada ya matibabu kiwango cha seli za CD4+ T kitapanda zaidi ya 200 kwa kila µL ya damu au iwapo maradhi mengine yanayoashiria UKIMWI yataponywa. Matibabu Hakuna tiba au chanjo; hata hivyo, matibabu ya kudhibiti virusi yanaweza kupunguza mwendo wa ugonjwa huu na huenda yakapelekea urefu wa maisha kuwa karibu na kawaida. Ingawa matibabu ya kupunguza makali hupunguza hatari ya kifo na matatizo yanayotokana na ugonjwa huu, matibabu haya ni ya bei ghali, hivyo yanaweza kuhusishwa na madhara mbadala. Kuna dawa za kusaidia watu wenye UKIMWI. Hizi zinaitwa dawa za kurefusha maisha. Dawa za kurefusha maisha haziwezi kutibu UKIMWI. Hii ina maana kwamba haziwezi kufanya virusi vyote kuondoka mwili wa mtu. Lakini zinaweza kuwasaidia watu kupambana na virusi vya UKIMWI kwa mifumo yao ya kinga kufanya kazi vizuri zaidi. Hivyo dawa za kurefusha maisha si tiba kabili kwa virusi ya UKIMWI. Watu wenye VVU/UKIMWI ambao huchukua dawa za kurefusha maisha wanaweza kuishi muda mrefu, bila kupata maradhi yanayothibitisha UKIMWI. Lakini baada ya muda mrefu, virusi za HIV zisizouawa na dawa hizo hujifunza jinsi ya kupambana nazo na hivyo zinakuwa sugu kwa dawa hizo. Wakati mwingine VVU ni sugu kwa dawa moja, lakini dawa nyingine inaweza kutumika. Ili kupunguza uwezekano wa upinzani kutokea, watu wenye UKIMWI huchukua dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Wanaweza kuchukua madawa 2-4 kwa mara moja. Hii wakati mwingine inaitwa cocktail ya UKIMWI. Lakini baada ya muda mrefu, VVU kujifunza kuwa sugu kwa dawa nyingi. Hapo hakuna zaidi ya kuwatibu. Hivyo wanasayansi kuendelea kujaribu kupata dawa mpya ya kupambana na VVU. Dawa tano muhimu za wenye VVU ni: D4T (stavudine) 3TC (Lamivudine) NVP (nevirapine) AZT (zidovudine) EFZ (efavirenz) Bila dawa hizo, kwa kawaida mtu mwenye VVU anaweza akaishi miaka 9-11. Njia za kujikinga na UKIMWI Kuna njia nyingi za watu kupambana na janga hilo. Kuzuia maambukizi ya VVU, hasa kupitia kondomu na miradi ya kubadilishabadilisha sindano, ni mikakati mikuu inayotumika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu. Lakini wengine wanahoji kwamba bila kubadili tabia, teknolojia peke yake haitaweza kushinda ugonjwa huo. Chanjo Njia bora ya kuzuia VVU ni wazo la kuwa na chanjo. Wanasayansi wengi wanatafuta chanjo ya VVU ili kuokoa uhai wa mamilioni ya watu, lakini kufikia mwaka 2012, hakuna chanjo mwafaka dhidi ya VVU/UKIMWI.Jaribio moja la chanjo ya RV 144 iliyotolewa mwaka 2009 lilipelekea kupunguza hatari ya kuambukiza kwa takriban 30%, hivyo kuchochea matarajio ya jamii ya utafiti ya kutengeneza chanjo mwafaka zaidi. Majaribio zaidi ya chanjo ya RV 144 yanaendelea. Kondomu Vitendo vya kijinsia ni njia kuu ya kupata VVU. Kama watu wanatumia kondomu wanapofanya mapenzi, kuna nafasi ndogo zaidi ya kuambukizana VVU, lakini ukweli kamili ni kwamba hakuna ngono salama kwa hakika. Matumizi ya kondomu ya kila mara hupunguza hatari ya kuambukizana UKIMWI kwa takriban 80% katika muda mrefu wa usoni. Iwapo mwenzi mmoja ameambukizwa, kutumia kondomu kila mara hupelekea viwango vya chini ya 1% kwa mwaka vya huyo mwingine kuambukizwa. Kuna ushahidi mdogo unaoonyesha kuwa kondomu za wanawake una kiwango sawa cha kinga. Dawa za ukeni Kutumia mafuta ya ukeni yanaliyo na tenofovir muda mfupi kabla ya ngono hukisiwa kupunguza viwango vya maambukizi kwa takriban 40% miongoni mwa wanawake wa Kiafrika. Kinyume na hili, matumizi ya spemisidi nonoxynol-9 yanaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa kwa sababu ya uwezo wake wa kuleta mwasho wa uke na rektamu. Tohara Tohara katika eneo la Kusini kwa Sahara "hupunguza uambukizaji wa VVU katika wanaume wanaohusiana na wanawake kimapenzi kwa kati ya 38% na 66% kwa muda wa miezi 24". Kwa msingi wa tafiti hizi, mashirika ya SAD na UNAIDS yalipendekeza tohara kama mbinu ya kuzuia uambukizaji VVU kutoka kwa mwanamke hadi mwanamume mwaka 2007. Haijabainika wazi iwapo njia hii huzuia uambukizaji kutoka kwa mwanamume hadi mwanamke na iwapo mbinu hii ina manufaa katika mataifa yaliyostawi na haijabainika miongoni mwa mashoga. Baadhi ya wataalamu wanahofia kuwa dhana ya kiwango cha chini cha hatari miongoni mwa wanaume waliotahiriwa inaweza kupelekea mienendo hatari zaidi, hivyo wanapinga faida ya mbinu hii katika kukinga. Wanawake waliofanyiwa ukeketaji wana hatari zaidi ya kuambukizwa. Mawaidha na elimu Njia muhimu ya kuzuia VVU/UKIMWI ni elimu kwa kuwa hiyo inawezesha kuelewa maana ya jinsia na kukwepa sababu za maambukizi yake. Ni kwamba watu wanaweza kupata VVU kutokana na ngono na kutokana na damu. Watoto wanaweza pia kupata VVU kutoka kwa mama zao (wakati wa kukua ndani ya akina mama wajawazito na wakati wa kunyonya maziwa ya mama.) Kuna baadhi ya watu ambao hawataki watu wajue kuhusu kondomu na sindano safi, au hawataki wawe na kondomu au sindano safi. Hao wanaamini kuwa watu wakijua kuhusu kondomu na kuwa na kondomu watafanya ngono zaidi na hivyo kuzidisha maambukizi badala ya kuyapunguza kwa sababu kinga hiyo si madhubuti. Vilevile wanaamini kuwa watu wakiwa na sindano safi watatumia dawa za kulevya zaidi. Wengi wa wanaodhani hivyo ni pia kwa sababu ya dini zao kukataza uzinifu na ulevi kama tabia zinazoharibu binadamu binafsi na jamii kwa jumla. Hao huhimiza upendo na uaminifu katika ndoa, usafi wa moyo na utunzaji wa afya. Miradi inayohimiza kujinyima ngono haijatambulika inaathiri vipi hatari ya kupata VVU. Ushahidi wa manufaa ya elimu ya rika pia hautoshi. Elimu ya ngono inayotolewa shuleni inaweza kupunguza mitindo hatari, lakini inaweza pia kuchochea wanafunzi wakajaribu wenyewe ngono. Vijana wengi wanajihusisha katika vitendo hatari licha ya kufahamu kuhusu VVU/UKIMWI, huku wakipuuza hatari ya kuambukizwa. Dawa kabla ya hatari Asilimia 96 ya watu walikingwa dhidi ya maambukizi iwapo wenzi wao walioambukizwa walipata mapema dawa za kudhibiti VVU Proflaksisi ya kabla ya hatari pamoja na kipimo cha kila siku cha dawa ya tenofovir (ikiwa na au bila emtricitabine) ni mwafaka kwa vikundi fulani, ikijumuisha: mashoga, wachumba wa wenye VVU na vijana wa Afrika wanaovutiwa na watu wa jinsia tofauti. Hadhari za jumla katika mandhari ya utunzaji wa afya zinaaminika kufaulu kupunguza hatari ya VVU. Matumizi ya dawa zinazodungwa mishipani ni kipengele muhimu cha hatari, hivyo mikakati ya kupunguza madhara kama vile miradi ya kubadilisha sindano na matibabu ya kubadilisha opioidi yanaonekana kufaulu kupunguza hatari. Dawa baada ya hatari Vipimo vya dawa za kudhibiti VVU zinazotolewa kati ya saa 48 hadi 72 baada ya hatari kwa damu yenye VVU au viowevu vya uzazi hujulikana kama proflaksisi ya baada ya hatari. Matumizi ya dawa moja ya zidovudine hupunguza mara tano hatari ya kupata VVU kutokana na jeraha la sindano. Matibabu hupendekezwa baada ya ubakaji iwapo mshukiwa anatambulika kuwa na VVU lakini yanakumbwa na utata iwapo hali yake haijulikani. Taratibu za matibabu ya sasa hutumia lopinavir/ritonavir na lamivudine/zidovudine au emtricitabine/tenofovir na yanaweza kupunguza hatari zaidi. Kwa kawaida, muda wa matibabu huwa wiki nne na mara nyingi huhusishwa na athari kali (zidovudine ikiwa na takriban 70% ya visa, ikijumuisha 24% kichefuchefu, 22% uchovu, 13% mafadhaiko na 9% maumivu ya kichwa. Kuzuia maambukizi ya mama kwa mtoto Hatua za kuzuia kusambaza VVU kutoka kwa mama hadi mtoto zinaweza kupunguza kiwango cha maambukizi kwa asilimia 92-99. Kimsingi, hatua hizi hujumuisha kutumia mwungano wa dawa za kudhibiti VVU katika ujauzito na baada ya kuzaa, na pia kunywesha kwa chupa badala ya kunyonyesha.Ikiwa itakubaliwa kulisha, inafaidi, inawezekana kumudu gharama yake, na ni salama, kina mama hawapaswi kuwanyonyesha watoto wao. Hata hivyo, iwapo haiwezekani, kina mama hushauriwa kunyonyesha tu katika miezi ya kwanza. Ikiwa kunyonyesha pekee kutatekelezwa, kumpa mtoto proflaksisi ya kudhibiti VVU kwa muda mrefu zaidi hupunguza hatari ya kuambukizwa. Dawa za kudhibiti virusi Kwa sasa hakuna tiba au chanjo ya VVU mwafaka. Matibabu hujumuisha dawa tendi za kudhibiti VVU za kiwango cha juu zinazopunguza mwendo wa ugonjwa huu. Kufikia mwaka 2010, zaidi ya watu milioni 6.6  wa nchi za mapato ya chini na ya kati walikuwa wakitumia dawa hizo. Matibabu pia huhusisha hatua za kuzuia na kutibu maambukizi nyemelezi. Chaguo za kisasa za KNKN ni michanganyiko ya angalau dawa tatu za angalau aina au "vikundi" viwili vya ajenti za dawa za kudhibiti VVU. Mwanzoni, matibabu kwa kawaida huhusisha kizuizi kisicho cha nukliosidi kinachozuia kugeuzwa kwa nakala (KKNKN) pamoja na vidonge viwili vya kifanani cha nukliosidi kinachozuia kugeuzwa kwa nakala (KNKN). KNKN kwa kawaida hujumuisha: zidovudine (AZT) au tenofovir (TDF) na lamivudine (3TC) au emtricitabine (FTC). Mwungano wa ajenti zinazojumuisha kizuizi cha protisi (KP) hutumika utaratibu huu ukipoteza utendakazi. Wakati wa kuanzisha matumizi ya dawa za kudhibiti VVU ni mada ambayo ingali inajadiliwa. Shirika la Afya Duniani, miongozo ya Ulaya na pia Marekani hupendekeza dawa za kudhibiti VVU kwa vijana waliobalehe, watu wazima na kina mama wajawazito walio na kiwango cha CD4 cha chini ya 350/uL au walio na dalili, bila kuzingatia kiwango chao cha CD4.Hali hii huwezeshwa na ukweli kwamba kuanzisha matibabu wakati huu hupunguza hatari ya kifo. Isitoshe, Marekani imependekeza matibabu hayo kwa watu wote wenye VVU bila kuzingatia kiwango cha CD4 au dalili, ingawa inatoa pendekezo hili ikiwahofia watu wenye kiwango cha juu cha CD4. Shirika la Afya Duniani pia linapendekeza matibabu kwa watu wenye maambukizi nyongeza ya kifua kikuu na hepatitisi B tendi ya muda mrefu. Matibabu yanapoanzishwa, inapendekezwa yaendelezwe bila "kupumzika". Watu wengi hutambuliwa punde tu baada ya wakati ambao matibabu yalipaswa kuanzishwa. Katika matibabu, matokeo yanayotarajiwa ni kiwango cha HIV-RNA ya plasma ya muda mrefu cha chini ya nakala 50/mL.Viwango vya kuthibitisha ikiwa matibabu ni mwafaka hupendekezwa kwanza baada ya wiki nne na punde viwango hivi vinaposhuka chini ya nakala 50/mL. Vipimo vya kila baada ya miezi 3-6 kwa kawaida huwa mwafaka. Udhibiti usio mwafaka huchukuliwa kuwa zaidi ya nakala 400/mL. Kulingana na kigezo hiki, matibabu huwa mwafaka kwa zaidi ya 95% ya watu katika mwaka wa kwanza. Manufaa ya matibabu hujumuisha upungufu wa hatari ya kuendelezwa kwa VVU na kupunguka kwa hatari ya kifo.Katika mataifa yaliyostawi matibabu pia huboresha afya ya mwili na ya akili. Matibabu hupelekea kupunguza kwa 70% hatari ya kupata kifua kikuu. Manufaa ya nyongeza hujumuisha upungufu wa hatari ya kusambazwa kwa ugonjwa huu hadi kwa wenzi kingono, na upungufu wa kusambazwa kwa maambukizi kutoka kwa mama hadi mtoto. Ubora wa matibabu hutegemea pakubwa maafikiano. Sababu za kutoafikiana hujumuisha: ufikiaji duni wa huduma za kimatibabu,huduma duni za kijamii, ugonjwa wa akili na uraibu wa madawa. Isitoshe, utata wa utaratibu wa matibabu (kufuatia idadi ya tembe na idadi ya marudio ya kumeza tembe) na athari kali zinaweza kusababisha kutoafikiana kwa kimakusudi.Hata hivyo, viwango vya uafikiano ni sawa katika nchi zinazostawi na zilizostawi Matukio makuu huhusishwa na ajenti inayotumika. Baadhi ya visa vinavyotokea mara nyingi hujumuisha: sindromu ya lipodistofi, dislipidemia na kisukari tamu hasa pamoja na vizuizi vya protisi. Dalili zingine zinazotokea mara nyingi hujumuisha: kuhara, na ongezeko la hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa. Hata hivyo, athari kali huwa katika matibabu mapya yaliyopendekezwa. Gharama huenda ikawa tatizo kwani baadhi ya dawa huwa ghali. Hata hivyo, hadi mwaka wa 2010, 47% ya watu waliohitaji dawa hizo walikuwa wakizitumia katika nchi zinazostawi na za mapato ya wastani Dawa fulani zinaweza kuhusishwa na ulemavu wa kuzaliwa hivyo hazifai kutumiwa na wanawake wanaopanga kupata watoto. Matibabu yanayopendekezewa watoto hutofautiana kidogo na ya watu wazima. Katika nchi zinazoendelea, kufikia mwaka wa 2010, 23% ya watoto waliohitaji dawa hizi walikuwa wakizitumia. Shirika la Afya Duniani na Marekani inapendekeza matibabu kwa watoto wote wa umri wa chini ya miezi 12.Marekani hupendekeza matibabu kwa watoto wa umri wa mwaka 1-5 walio na kiwango cha VVU-RNA cha zaidi ya nakala 100,000 /mL na kwa walio zaidi ya miaka mitano watibiwe iwapo kiwango cha CD4 ni chini ya 500/ul. Kuzuia maambukizi nyemelezi Mikakati ya kuzuia maambukizi nyemelezi hufaa watu wengi wenye VVU/UKIMWI. Matibabu ya dawa za kudhibiti virusi huboresha na kupunguza hatari ya kupata maambukizi nyemelezi kwa wakati huo na baadaye.Chanjo dhidi ya hepatitisi A na B hupendekezwa kwa watu walio katika hatari ya VVU kabla ya maambukizi, ingawa yanaweza kutolewa baada ya kuambukizwa. Kinga ya Trimethoprim/sulfamethoxazole kati ya wiki 4-6 na kukoma kunyonyesha watoto waliozaliwa na mama mwenye VVU hupendekezwa katika sehemu zenye upungufu wa raslimali. Pia inapendekezwa kuzuia PCP kiwango cha CD4 kikiwa chini ya 200 /uL na kwa wenye PCP au waliokuwa nayo awali. Watu wenye ugandamizaji wa kingamwili pia hushauriwa kupata kinga ya toksoplasmosisi na Meninjitisi ya kriptokokasi. Mikakati mwafaka ya kinga imepunguza kiwango cha maambukizi kwa 50% katika miaka 1992-1997. Matibabu mbadala Takriban 60% ya watu wenye VVU nchini Marekani hutumia mbinu mbalimbali za matibabu mbadala. Ubora wa matibabu hayo hata hivyo haujathibitishwa. Kwa kuzingatia ushauri wa kilishe na UKIMWI, kuna ushahidi unaoonyesha manufaa ya nyongeza za virutubishi vidogo. Ushahidi wa manufaa ya nyongeza za seleniamu unaonyesha kuwa manufaa yake si mengi sana. Kuna ushahidi mdogo kuwa nyongeza ya vitamini A kwa watoto hupunguza vifo na kuboresha ukuaji. Nyongeza ya vitamini nyingi kwa kina mama wajawazito wenye lishe duni na wanaonyonyesha imeboresha afya ya kina mama na watoto barani Afrika Kutumia virutubishi vidogo ndani ya lishe katika viwango vya KMS kwa watu wazima wenye VVU kumependekezwa na Shirika la Afya Duniani. SAD linasema kuwa takwimu kadhaa zimeonyesha nyongeza ya vitamini A, zinki na ayoni inaweza kuwaathiri pakubwa watu wazima walio na VVU. Hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha manufaa ya miti shamba. Matarajio ya kuishi Katika sehemu nyingi ulimwenguni UKIMWI umekuwa ugonjwa wa muda mrefu, si ugonjwa mkali tu. Prognosi ni tofauti katika watu mbalimbali, na kiwango cha CD4 pamoja na wingi wa virusi huwa muhimu katika kutabiri matokeo. Wastani wa muda wa kuishi baada ya kuambukizwa unakadiriwa kuwa kati ya miaka 9-1  bila matibabu, ikitegemea aina ya VVU. Baada ya utambuzi wa UKIMWI, iwapo matibabu hayapo, uwezo wa kuishi huwa kati ya miezi 6-19. KKNKN na uzuiaji mwafaka wa Maambukizi nyemelezi hupunguza kima cha vifo kwa 80% na kuongeza matarajio ya urefu wa maisha hadi miaka 20-50 kwa mtu mzima wa kimo aliyetambuliwa na maambukizi karibuni. Hii ni kati ya 2/3 na karibu na kiwango cha umma. Matibabu huwa hayafaulu yanapoanzishwa yakiwa yamechelewa katika prognosi, kwa mfano, matibabu yakianzishwa kufuatia utambuzi katika kiwango cha UKIMWI, matarajio ya urefu wa maisha huwa miaka~10–40. Wasipotibiwa, nusu ya watoto wachanga wanaozaliwa na VVU hufa kabla ya miaka miwili. Sababu kuu ya vifo vinavyotokana na VVU/UKIMWI ni Maambukizi nyemelezi na saratani ambayo mara nyingi hutokana na matatizo endelevu ya mfumo wa kingamwili. Hatari ya saratani huonekana kuongezeka ikiwa kiwango cha CD4 kitashuka chini ya 500/uL. Kiwango cha kuendelea kwa ugonjwa wa kiutambuzi hutofautiana pakubwa katika watu mbalimbali na kimedhihirika kuathiriwa na vipengele kadhaa, kama vile uhatarisho na utendaji wa kingamwili; uwezo wa kufikia huduma ya afya na uwepo wa maambukizi pacha; pamoja na aina ya (au za) virusi husika. Maambukizi pacha ya kifua kikuu ni mojawapo ya visababishi vikuu vya vifo vya watu wenye VVU/UKIMWI, huku yakipatikana katika 1/3 ya watu walioambukizwa VVU na husababisha 25% ya vifo vinavyohusiana na VVU. VVU pia ni kipengele kikuu zaidi cha hatari ya kifua kikuu. Hepatitisi C ni maambukizi mengine pacha yanayotokea mara nyingi, ambapo kila ugonjwa huongeza uendeleaji wa ugonjwa mwingine Saratani zinazotokea mara nyingi zaidi ambazo huhusishwa na VVU ni sakoma ya Kaposi na limfoma isiyo ya Hodgkin. Hata wakitibiwa kwa dawa za kudhibiti VVU, watu walio na VVU huenda wakakumbwa na matatizo ya kiniuroni ya ufahamu, osteoporosi, nuropathia, saratani, nefropathi, na ugonjwa wa moyo na mishipa baada ya muda mrefu. Haijulikani ikiwa hali hizi hutokana na kuambukizwa kwa VVU kwenyewe au ni athari kali za matibabu yake. Watu wangapi wana UKIMWI? VVU/UKIMWI ni janga la kimataifa. Kufikia mwaka 2018 walau watu wapatao 37,900,000 walikuwa wakiishi na VVU na kila mwaka watu milioni 2 wengine wanambukizwa. Zaidi ya nusu ni wanawake na milioni 2.6 ni watoto chini ya miaka 15. Hata hivyo watu wengi wenye VVU hawajui kuwa navyo. Kwa sababu hiyo, idadi halisi ya watu wanaoishi na VVU haijulikani. Hali hii ilisababisha karibu vifo milioni 1.8 mwaka 2010 ikilinganishwa na milioni 3.1 katika mwaka 2001. Kwa jumla watu 32,000,000 wameshakufa kwa ugonjwa huo. Wengi kati ya watu wenye VVU huishi Afrika kusini kwa Sahara (20,600,000). Wengi kati ya watoto ambao hufariki dunia kutokana na UKIMWI pia wanaishi barani Afrika. Katika mwaka wa 2010, kadirio la 68% (milioni 22.9 ) la visa vyote vya VVU na 66% ya vifo (milioni 1.2 ) vilitokea katika eneo hili. Hii inamaanisha kuwa karibu 5% ya watu wazima wana virusi hivi na vinaaminika kuwa kisababishi cha 10% ya vifo vyote vya watoto. Wanawake wa eneo hili huchangia karibu 60% ya visa vyote tofauti na maeneo mengine. Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya watu wenye VVU ulimwenguni kote, ikiwa ni watu milioni 5.9 . Kiwango cha matarajio ya urefu wa maisha kimepungua katika nchi zilizoathirika zaidi kutokana na VVU; kwa mfano, mwaka wa 2006, ilikadiriwa kuwa kiwango hiki kilipungua kutoka miaka 65 hadi 35 nchini Botswana. Asia Kusini na Kusini Mashariki ni eneo la pili lililoathirika zaidi; mwaka wa 2010, eneo hili lilikuwa na kadirio la visa milioni 4  au 12% ya watu wote wanaoishi na VVU, hivyo kupelekea vifo vya takriban watu 250,000. Takriban milioni 2.4  ya visa hivi viko India Ukithiri wa VVU uko chini katika maeneo ya Uropa Magharibi na Kati ikifikia 0.2% na Mashariki mwa Asia ikiwa na 0.1%. Mwaka wa 2008 nchini Marekani, takriban watu milioni 1.2 walikuwa wakiishi na VVU, hivyo kupelekea takriban vifo 17,500. Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kilikadiria kuwa, mwaka wa 2008, 20% ya Wamarekani waliokuwa na VVU hawakujua hali yao. Nchini Uingereza, kufikia 2009 kulikuwa na takriban visa 86,500 vilivyopelekea vifo 516. Nchini Kanada, kufikia 2008 kulikuwa na visa 65,000 vilivyopelekea vifo 53. Jamii na utamaduni Unyanyapaa Unyanyapaa dhidi ya watu walio na UKIMWI zipo kote ulimwenguni kwa namna mbalimbali, zikiwemo kutengwa, kukataliwa na jamii, ubaguzi na kuepuka watu walioambukizwa VVU, kulazimishwa kupimwa VVU bila idhini au ulinzi wa usiri, vurugu dhidi ya watu walioambukizwa au waliodhaniwa kuambukizwa VVU; na karantini ya watu waliombukizwa VVU. Vurugu zinazohusiana na unyanyapaa au hofu ya vurugu huzuia watu wengi kupima VVU, kurudia matokeo ya vipimo na kutotafuta matibabu. Hali hizi hugeuza ugonjwa wa muda mrefu unaoweza kudhibitiwa kuwa hukumu ya kifo na kuendeleza ueneaji wa VVU. Unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na UKIMWI, umegawanywa zaidi katika vikundi vitatu kama ifuatavyo: Unyanyapaa Mkuu wa UKIMWI -mawazo ya woga na wasiwasi unaoweza kuhusishwa na ugonjwa wowote aunaoua au kuambukiza. Unyanyapaa wa kiishara wa UKIMWI -kutumia VVU/UKIMWI kuonyesha mitazamo fulani dhidi ya vikundi vya jamii au mitindo ya maisha inayohusishwa na ugonjwa huu. Unyanyapaa wa kihisani wa UKIMWI- Unyanyapaa dhidi ya watu wanaohusishwa na suala la VVU/UKIMWI au watu walio na VVU. Mara nyingi, unyanyapaa wa UKIMWI huonyeshwa pamoja na unyanyapaa wa aina moja au nyingine, hasa unyanyapaa unaohusiana na ushoga, uasherati, ukahaba na kutumia dawa za kulevya. Katika nchi nyingi zilizostawi, kuna uhusiano kati ya UKIMWI na ushoga.Hata hivyo, njia kuu ya kuenea kwa UKIMWI ulimwenguni kote inabakia kuwa maambukizi kati ya wanaume na wanawake, kwa kuwa ndio ngono ya kawaida. Athari za kiuchumi VVU/UKIMWI huathiri uchumi wa watu na nchi. Pato la ndani la uzalishaji la nchi zilizoathiriwa zaidi limepungua kufuatia ukosefu wa rasilimali ya kibinadamu.Bila lishe bora, huduma za afya na dawa, watu wengi hufariki kutokana na matatizo yanayohusiana na UKIMWI. Kando ya kutoweza kufanya kazi, watu hao pia huhitaji kiwango kikubwa cha huduma za afya. UKIMWI hupunguza idadi ya watu wanaoweza kulipa ushuru Kwa kuwaathiri hasa vijana, hivyo kupunguza raslimali zilizopo za matumizi ya umma kama vile huduma za elimu na afya ambazo hazihusiki na UKIMWI. Hali hii husababisha upungufu wa pesa za nchi na wa ukuaji wa uchumi. Hali hii kisha hupelekea upungufu wa ukuaji wa msingi wa ushuru, athari ambayo huongezeka iwapo kuna matumizi zaidi katika matibabu, mafunzo (ili kuchukua nafasi ya wafanyakazi wanaougua), kuwalipa wafanyakazi wagonjwa na kuwatunza mayatima wa UKIMWI. Hali hii hutokea hasa iwapo ongezeko kubwa la vifo vya watu wazima litapelekea kubadilika kwa wajibu wa kuwatunza mayatima hawa kutoka kwa familia hadi kwa serikali. Katika kiwango cha familia, UKIMWI husababisha upungufu wa mapato na pia ongezeko la matumizi katika huduma za afya. Utafiti katika nchi ya Côte d'Ivoire ulionyesha kuwa familia zilizo na mgonjwa aliye na VVU/UKIMWI zilitumia pesa mara mbili zaidi ya familia nyingine. Matumizi hayo ya ziada pia hupelekea kiwango kidogo zaidi cha mapato ya kutumia katika elimu au uwekezaji wa kibinafsi au wa kifamilia. Mayatima Watu wengi ambao wanakufa kutokana na UKIMWI, hasa katika Afrika, huacha watoto ambao bado ni hai, na ambao wanaweza wanahitaji msaada na huduma. Inakadiriwa kuwa kufikia mwaka wa 2007, diadi ya watoto yatima kutokana na UKIMWI  milioni 12. Wengi wao hutunzwa na nyanya na babu wazee. Dini na UKIMWI Mada kuhusu dini na UKIMWI imekuwa ikikumbwa na utata mwingi katika miaka thelathini iliyopita, hasa kwa sababu baadhi ya viongozi wa dini wametangaza hadharani kwamba wanapinga utumiaji kondomu. Mashirika mengine ya dini yamedai kuwa maombi yanatosha kutibu VVU/UKIMWI. Mwaka 2011, BBC iliripoti kuwa baadhi ya makanisa huko London yalikuwa yakidai kuwa maombi yanatibu UKIMWI. Kituo cha Utafiti wa Afya ya Kiuzazi na VVU cha Hackney kiliripoti kuwa watu wengi waliachma kutumia matibabu, wakati mwingine kwa kushauriwa na wachungaji wao. Jambo hili lilipelekea vifo vya watu wengi. Synagogue Church Of All Nations ilitangaza maji ya upako ili kuwezesha uponyaji kutoka kwa Mungu, ingawa ilikana kuwa iliwashauri watu kukoma kutumia matibabu. Katika vyombo vya habari Kimojawapo kati ya visa maarufu zaidi vya UKIMWI kilikuwa cha Mmarekani Rock Hudson, muigizaji shoga aliyekuwa ameoa kisha kutalaki hapo awali. Hudson alifariki tarehe 2 Oktoba 1985 baada ya kutangaza ana VVU tarehe 25 Julai mwaka huohuo. Yeye alikuwa ametambuliwa kuwa na ugonjwa huo mwaka 1984. Mgonjwa mashuhuri kutoka Uingereza mwaka huo alikuwa Nicholas Eden mwanasiasa shoga na mwana wa Waziri Mkuu, marehemu Anthony Eden. Tarehe 24 Novemba 1991, virusi hivi vilipelekea kifo cha mwanamuziki wa aina ya muziki wa rock, Mwingereza Freddie Mercury. Mercury, aliyeongoza bendi iliyojulikana kama Queen alifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI baada ya kujulikana kuwa na ugonjwa huo siku iliyopita tu. Hata hivyo, Mercury alikuwa ametambuliwa kuwa na ugonjwa huo mwaka 1987. Kimojawapo kati ya visa maarufu zaidi vilivyotokana na ngono kati ya watu wa jinsia tofauti ni kile cha Arthur Ashe, mchezaji tenisi Mmarekani. Ashe alitambuliwa kuwa na VVU tarehe 31 Agosti 1988; baada ya kuambukizwa alipokuwa akiongezewa damu akifanyiwa upasuaji wa moyo awali miaka ya 1980. Vipimo zaidi katika saa 24 baada ya utambuzi wa kwanza vilionyesha kuwa Ashe alikuwa na UKIMWI, lakini hakuwambia watu kuhusu utambuzi huu hadi Aprili 1992. Ashe alifariki kutokana na UKIMWI akiwa na umri wa miaka 49 tarehe 6 Februari 1993. Picha ya Therese Frare ikionyesha mwanaharakati wa ushoga David Kirby akifariki kutokana na UKIMWI huku akizungukwa na familia yake, ilipigwa Aprili mwaka wa 1990. LIFE magazine ilisema kuwa picha hiyo ilikuja kufahamika kama picha maarufu zaidi kuwahi kuhusishwa na janga la UKIMWI/VVU.'' Picha hiyo iliyochapishwa na gazeti hilo ilishinda tuzo la World Press Photo, kisha kupata umaarufu ulimwenguni kote baada ya kutumiwa na United Colors of Benetton katika kampeni ya utangazaji ya mwaka 1992. Ukanushaji, njama na hila Kikundi kidogo cha watu kingali kinakana uhusiano wa VVU na UKIMWI, uwepo wa VVU au ubora wa vipimo vya VVU na njia za matibabu. Madai hayo, yanayojulikana kama ukanaji UKIMWI, yamechunguzwa na kukataliwa na jamii ya kisayansi.Hata hivyo, madai hayo yana athari kuu kisiasa, hasa nchini Afrika Kusini. Hatua ya serikali ya nchi hiyo kukubali kirasmi ukanaji wa UKIMWI ilipelekea mwitikio usiofaa wa janga hili, na imelaumiwa kupelekea visa vingi vya maambukizi ya VVU na mamia ya maelfu ya vifo ambavyo vingeepukwa. Urusi ulianzisha Operesheni INFEKTION, uhamasisho wa ulimwengu mzima kueneza habari kuwa VVU/UKIMWI ulitengenezwa na Marekani. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu wanaamini na wanaendelea kuamini madai hayo. Kuna aina nyingi za dhana potovu kuhusu VVU na UKIMWI. Dhana tatu kuu ni kwamba UKIMWI unaweza kusambazwa kwa kumgusa mtu, kuwa ngono na bikira itatibu UKIMWI na kuwa VVU vinaweza tu kuambukiza mashoga na watumiaji wa madawa. Dhana nyingine potovu ni kuwa tendo lolote la ngono ya kinyeo kati ya mashoga wasioambukizwa linaweza kupelekea maambukizi. Utafiti unavyoendelea Utafiti wa kuboresha matibabu ya kisasa unajumuisha kupunguza madhara ya ziada ya dawa zilizopo, kurahisisha kanuni za kutumia dawa na kuboresha ubora na kuamua utaratibu bora wa kanuni ili kudhibiti ukinzani wa dawa. Hata hivyo, chanjo pekee ndiyo inayodhaniwa kuweza kusitisha janga hili. Hii ni kwa sababu chanjo ni ya bei nafuu, hivyo mataifa yanayostawi yanaweza kuimudu, na haitahitaji matibabu ya kila siku. Hata hivyo, baada ya miaka 20 ya utafiti, imekuwa vigumu kupata chanjo dhidi ya VVU-1, hivyo tiba bado haijapatikana. Upandikizaji seli kuu Mwaka wa 2007, Timothy Ray Brown, mwanaume wa umri wa miaka 40 aliyekuwa na VVU, pia anayejulikana kama "the Berlin Patient" alipewa huduma ya pandikizo la seli kuu kama mojawapo ya matibabu ya lukemia sugu ya mieloidi (LSM).Pandikizo la pili lilifanyika mwaka uliofuata baada ya kuugua tena. Mfadhili alichanguliwa sio tu kwa kuwa ana upatanifu wa kijeni lakini pia kwa kuwa alikuwa na utangamano wa kubadilika kwa CCR5-Δ32 ambayo huwezesha ukinzani dhidi ya maambukizi ya VVU. Baada ya miezi 20 bila matibabu ya dawa za kudhibiti VVU, iliripotiwa kuwa viwango vya VVU kwenye damu ya Brown uboho na matumbo vilikuwa chini ya kiwango cha kutambulika.Virusi hivi vilibakia katika kiwango hicho kwa miaka mitatu baada ya upandikizo wa kwanza.Ingawa watafiti na baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa matokeo haya ni tiba, wengine wao wanadokeza kuwa virusi hivi vinaweza kuwa vimejificha ndani ya tishukama vile ubongo (unaotumika kama hifadhi). Matibabu ya seli kuu yamebakia chini ya kuchunguzwa kwa sababu ya asili yake ya kinadharia, ugonjwa wenywe na hatari ya kufa inayohusishwa na upandikizaji wa seli kuu na ugumu wa kupata wafadhili mwafaka. Matibabu ya kuboresha kingamwili Matibabu saidizi za kudhibiti uigaji wa virusi, matibabu ya kingamwili zinazoweza kusaidia kuboresha mfumo wa kingamwili zilizochunguzwa awali, na juhudi zinazoendelea ni pamoja na IL-2 na IL-7. Kutofaulu kwa chanjo kadhaa kukinga dhidi ya maambukizi ya VVU na kuendelea kwa UKIMWI kumepelekea mwelekeo mpya wa kuzingatia taratibu za kibayolojia zinazosababisha ufiche wa VVU. Kipindi kifupi cha matibabu ya kuunganisha dawa za kudhibiti VVU na dawa zinazolenga hifadhi fiche siku moja kinaweza kutokomeza maambukizi ya VVU.Watafiti wamegundua abusaimu inayoweza kuharibu eneo la kufungia protini ya gp120 CD4. Protini hii hupatikana katika aina zote za VVU kwa sababu ndiyo ncha ambapo limfosaiti za B hujishikisha kisha kuafikiana kwa mfumo wa kingamwili. Tanbihi Marejeo Viungo vya nje AIDSinfo – HIV/AIDS Treatment Information, U.S. Department of Health and Human Services Shirika la Afya Duniani Mashirika 3 na 5 Initiative Médecins Sans Frontières: Kampeni ya upatikanaji wa madawa muhimu WHO Mpango wa VVU / UKIMWI Elimu UKIMWI Mfumo wa Taarifa za Global Kutoka Taasisi ya Taifa ya Marekani ya Afya New England Journal of Medicine Ibara "Ruhusu dhidi ya Wagonjwa? Kurefusha maisha Tiba katika India" AIDSPortal maarifa mtandao Tovuti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi, UNAIDS HIV InSite sida.fr • un centre pour les malades du SIDA • infos • tèmoignages • actualités Dalili Ukimwi
1901
https://sw.wikipedia.org/wiki/Desemba
Desemba
Desemba ni mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya Gregori na ni kati ya miezi saba katika kalenda hiyo yenye siku 31. Tarehe 21 ya mwezi huo wa Desemba (katika miaka mingine inawezekana kuwa tarehe 20 au 22) ni siku ya solistasi ya Kusini (kutoka Kiingereza solstice), yaani wakati Jua linapokuwa kusini kabisa mwa Ikweta. Neno Desemba limetokana na neno la Kilatini "decem" linalomaanisha "kumi." Desemba ulikuwa ni mwezi wa kumi katika kalenda ya Kirumi. Miezi Kalenda
1904
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mmea
Mmea
Mimea (kwa Kiingereza: "plants", kutoka Kilatini "Plantae") ni moja kati ya makundi ya viumbe hai duniani likijumuisha miti, maua, mitishamba na kadhalika. Kuna zaidi ya aina 300,000 ya mimea. Sayansi inayochunguza mimea huitwa botania ambayo ni kitengo cha biolojia. Kwenye uainishaji wa kisayansi mimea hujumlishwa katika himaya ya plantae kwenye milki ya Eukaryota (viumbehai vyenye kiini cha seli na utando wa seli). Kwa hiyo mimea huwa na utando wa seli wenye selulosi. Mmea unapata sehemu kubwa ya nishati kutoka nuru ya jua kwa njia ya usanisinuru, yaani hujilisha kwa msaada wa nuru. Ndani ya majani ya mimea kuna klorofili, dutu ya rangi ya kijani, inayofanya kazi ya kupokea nuru na kupitisha nishati yake kwa sehemu nyingine ya mmea ambamo inatumiwa kujenga molekuli zinazotunza nishati kwa njia ya kikemia na kutumiwa katika metaboli ya mwili. Mimea kadhaa imepoteza uwezo wa kutengeneza klorofili ya kutosha, hivyo inajipatia nishati kama vimelea kutoka kwa mimea au viumbehai wengine. Mimea mingi inazaa kwa njia ya jinsia, yaani kwa kuunganisha seli za kiume na kike; mara nyingi viungo vya kiume na vya kike vinapatikana ndani ya mmea mmoja. Kuna pia mimea inayozaa kwa njia isiyo ya kijinsia, kwa mfano kwa kuotesha mzizi wa hewani ambao unaingia ardhini na kuendelea kama mmea wa pekee. Mimea ni msingi muhimu kwa viumbehai wengine duniani kwa sababu sehemu kubwa ya oksijeni katika angahewa ya dunia inatengenezwa na mimea.. Mimea inatoa chakula kwa binadamu kama vile nafaka, matunda na mboga za majani, pia lishe kwa wanyama wa kufugwa. Picha Tanbihi Mimea Biolojia
1907
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usanifu%20majengo
Usanifu majengo
Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo. Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu majengo". Wanahitaji elimu ya ujenzi, hesabu, sanaa, teknolojia, elimu jamii na historia. Msanifu wa kwanza anayejulikana kwa jina ni Imhotep wa Misri ya Kale. Mbinu za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana, hali ya hewa, hali ya jamii, utaratibu wa siasa yake, hali ya uchumi na mengine mengine. Nchi na tamaduni mbalimbali ziliunda aina tofauti za usanifu majengo. ujenzi sanaa
1908
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mipango%20miji
Mipango miji
Mipango miji ni sayansi na sera kuhusu maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kimazingira katika miji na vitongoji vyake. Mgiriki Hippodamus anasemekana kuwa ndiye baba wa mipango miji kutokana na ubunifu wake wa mji wa Miletus ingawa kumekuwa na miji iliyopangwa kabla yake. Taaluma ya mipango miji imechipuka toka kwenye taaluma za usanifu majengo na uhandisi. Miji Ujenzi Sayansi ya Jamii
1910
https://sw.wikipedia.org/wiki/IRC
IRC
Internet Relay Chat (IRC) ni aina ya mawasiliano ya papo kwa hapo kupitia mtandao wa Intaneti. Teknolojia hii imeundwa hususan kwa ajili ya mawasiliano ya watu wengi kwa wakati mmoja, lakini pia mawasiliano ya mtu mmoja kwa mmoja yanawezekana. Teknolojia hii ilitengenezwa na Jarkko Oikarinen Agosti 1998 ili kuchukua nafasi ya teknolojia nyingine kama hii iliyokuwa ikiitwa MUT huko Ufini. IRC ilipata umaarufu pale ilipotumika kuripoti jaribio la kuipindua serikali ya Urusi mwaka 1991. Teknolojia hii ilitumiwa pia kuripoti uvamizi wa Kuwait na nchi ya Iraki. Viungo vya nje - Tovuti ya IRC Intaneti
1911
https://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu%20za%20mkononi
Blogu za mkononi
Blogu za mkononi ni aina ya blogu zinazotumia zana zinazoshikika mkononi kama vile simu za mkononi. Kwahiyo, habari, maoni, au visa vinatolewa katika mtandao wa kompyuta kwa kutumia zana hizi. Teknolojia hii ilianza huko Japan ambapo simu za mkono zenye kamera zilianza kupatikana kwa urahisi. Inasemekana utumaji wa habari kwenye mtandao wa kompyuta toka katika zana za mkononi ulifanywa na Steven Mann hapo mwaka 1955 alipotumia kompyuta inayovalika. Mwaka 2000 ndipo utumaji wa habari katika mtandao wa kompyuta toka katika simu ya mkono ulifanywa na Tom Paamand nchini Udeni. Adam Greenfield ndiye aliyeanzisha matumizi ya neno "blogu za mkononi." Aliandaa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Blogu za Mkononi jijini Tokyo, Japani mwaka 2003. Teknolojia Blogu Uandishi wa Raia
1912
https://sw.wikipedia.org/wiki/Paul%20Simon
Paul Simon
Paul Simon ni mwanamuziki wa country, anaimba na kupiga gitaa. Amewahi kushirikiana na wanamuziki wengi; moja ya makundi hayo ni Ladysmith Black Mambazo. Nyimbo alizowahi kuimba ni "Homeless", "Mother and child reunion" na "Diamond in the sole of her shoes". Paul Simon alizaliwa tarehe 13 Oktoba 1941 katika mji wa Newark Height, New Jersey. Huko alifahamika kama muimbaji na mtunzi mwenye asili ya kiyahudi. Aliwahi kufunga ndoa mara tatu, ana watoto wanne. Mmojawapo ni mpigaji gitaa kama baba yake. Waliozaliwa 1941 Wanamuziki wa Marekani New York City
1928
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shaaban%20Robert
Shaaban Robert
Shaaban Robert (1 Januari 1909 - 22 Juni 1962) alikuwa mshairi na mwandishi wa riwaya. Mchango wake katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa kwani kazi zake zinaheshimika katika fasihi ya Kiswahili na pia zinatumika shuleni. Maisha Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 katika kijiji cha Vibambani, jirani na Machui, kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga. Wazazi wake wote wawili walikuwa wa ukoo wa Mganga wa kabila la Wayao, lakini hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili. Kabla ya baba yake kuitwa Roberto , mwanzo alifahamika kwa jina la Ufukwe na jina hili lilitokana na Mzee Robert kuzaliwa karibu na ufukwe . Jina la Roberto lilitokana na tajiri mmoja aliyekuwa amemuajiri baba yake (babu yake Shaabani Robert). Baada tu ya Shaaban Robert kuingia katika shule za Wazungu alibadili jina kutoka Roberto na kuwa Robert. Alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-Salaam kati ya miaka 1922 na 1926, akawa mtu wa pili katika wanafunzi kumi na mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka chuoni, yaani School Leaving Certificate. Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani miaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Waswahili tena mahali patulivu kulisaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili. Tangu mwaka 1944 hata 1946 alihamia ofisi nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga (tokea mwaka 1952 hata 1960). Alipandishwa cheo kuwa Grade III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa Grade II Local Service. Kwa ujumla Shaaban Robert aliandika vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na Nduguze, Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini, Utubora Mkulima. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Kichina, Kiingereza na Kirusi. Mbali na maandiko yake alikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na Tanganyika Languages Board. Alikuwa pia mwanachama wa Tanga Township Authority. Alifariki dunia huko Tanga tarehe 22 Juni 1962 akazikwa Machui. Aliacha wake watatu na watoto watano, ingawa aliwazaa kumi. Mke wa kwanza alikuwa Mdigo. Pia aliacha dada yake (wa baba mmoja) Mwana Saumu, na mama yake. Alitunza kwa zawadi ya waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa nishani ya M.B.E. Vitabu vyake Mwafrika Aimba (1969), Nelson. Nairobi Almasi za Afrika (1971), Nelson, Nairobi Koja la Lugha (1969), Oxford, Nairobi Insha na Mashairi (1967), Nelson, Nairobi Ashiki Kitabu Hiki (1968), Nelson, Nairobi Pambo la Lugha (1968), Oxford, Nairobi Kielezo cha Fasili (1962), Nelson, Nairobi Masomo Yenye Adili (1959), Art & Literature, Nairobi Mapenzi Bora (1969), Nelson, Nairobi Tenzi za Marudi Mema na Omar Khayyam (1973), TPH, Dar-es-Salaam Utenzi wa Vita vya Uhuru (1961), Oxford, Nairobi Almasi za Afrika Na Tafsiri Ya Kiingereza (1960), Art & Literature, Nairobi Mashairi ya Shaaban Robert (1971), Nelson, Nairobi Sanaa ya Ushairi (1971), Nelson, Nairobi Nathari Kufikirika (1968), Oxford, Nairobi Wasifu wa Siti Binti Saad (1967), Art & Literature, Nairobi Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini (1949), Nelson, Nairobi Kusadikika (1951), Nelson, Nairobi Adili na Nduguze (1977), TPH, Dar-es-Salaam Utu Bora Mkulima (1968), Nelson, Nairobi Siku ya Watenzi Wote (1968), Nelson, Nairobi Kielelezo cha Insha (1954), Witwatersand, Nairobi Barua za Shaaban Robert 1931- 1958, (2002), TUKI, Dar-es-Salaam Mithali na Mifano ya Kiswahili (2007), TUKI, Dar-es-Salaam. Tanbihi Viungo vya nje (en) Shaaban Robert Waliozaliwa 1909 Waliofariki 1962 Waandishi wa Tanzania Washairi wa Tanzania Fasihi ya Kiswahili
1930
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbeya
Mbeya
Mbeya ni jina la: Mji wa Mbeya Mkoa wa Mbeya katika Tanzania Kusini-Magharibi Wilaya za Mbeya mjini na vijijini Jimbo Kuu la Mbeya la Kanisa Katoliki Tanzania Makala zinazotofautisha maana
1950
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Mbeya
Mkoa wa Mbeya
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, ukipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa, mbali na mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka ule wa Mbeya upande wa magharibi mwaka 2016. Una Postikodi namba 53000. Kabla ya kugawiwa kulikuwa na wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya, Momba na Mbarali. Tangu 2016 mkoa umekuwa na wilaya za Busekelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe. Kadiri ya sensa ya mwaka 2022 idadi ya wakazi ni 2,343,754 Jiografia Kijiolojia mkoa wa Mbeya ni eneo la kukutana kwa mikono miwili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki inayoendelea hapa katika ziwa Nyasa. Mkoa wa Mbeya inapakana pia na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe imejaa maziwa ya kasoko. Mito mikubwa ni Songwe na Kiwira. Chanzo cha mto Ruvuma kiko pia Mbeya katika tambarare ya Usangu. Wilaya ya Rungwe ni eneo lenye mvua nyingi katika Tanzania, ila maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.. Mkoa kwa ujumla ni mmojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi. Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu na waishio huko zaidi ni Wanyiha. Vivutio vya kitalii Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za ziwa Nyasa, Mlima ya Mbeya, Mlima ya Rungwe, Uwanda wa juu wa Uporoto, Uwanda wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii. Mkoa wa Mbeya una idadi ya vivutio vya kitalii ambavyo ni pamoja na: . Ziwa Ngosi . Ziwa Kisiba . Hifadhi ya Taifa Kitulo . Pori la Akiba Mpanga Kipengere . Maporomoko ya maji (Kapologwe, Malamba, Kimani, Isabula) . Vilele vya Mlima Mbeya, Mlima Loleza, Mlima Rungwe . Safu za Milima ya Kipengere (Livingstone) Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Busokelo : mbunge ni Atupele Mwakibete (CCM) Ileje : mbunge ni Janeth Mwamben (CCM) Kyela : mbunge ni Ally Jumbe Mlaghila (CCM) Lupa : mbunge ni Masache Njelu Kasaka (CCM) Mbarali : mbunge ni Haroon Mullah Pirmohamed (CCM) Mbeya Mjini : mbunge ni Tulia Ackson Mwansasu (CCM) Mbeya Vijijini : mbunge ni Oran M. Njeza (CCM) Mbozi : mbunge ni George Mwenisongole (CCM) Momba : mbunge ni Condester Michael Sichalwe (CCM) Rungwe : mbunge ni Sauli Henry Amon (CCM) Songwe : mbunge ni Philipo Mulugo (CCM) Tunduma : mbunge ni Mwakajoka Frank (Chadema) Vwawa : mbunge ni Hasunga Ngailanga (CCM) Waandishi toka mkoa wa Mbeya Godfrey Mwakikagile Christopher Richard Mwashinga Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Mbeya Orodha ya mito ya mkoa wa Mbeya Viungo vya nje Tovuti rasmi ya Mkuu wa Mkoa Tovuti ya habari mbeyayetu Mbeya Region Socioeconomic Profile katika TZOnline Marejeo M
1951
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ladysmith%20Black%20Mambazo
Ladysmith Black Mambazo
Ladysmith Black Mambazo ni kundi la muziki ambalo linaimba bila kutumia ala za muziki. Kundi hili lipo Afrika ya Kusini. Neno "Mambazo" linamaanisha "shoka" kwa Kizulu. Na "Ladysmith" ni kitongoji katika jimbo la Natal alichotoka Joseph Shabalala kiongozi na mwanzilishi wa kundi hili. Ladysmith Black Mambazo lina albamu zaidi ya 40. Kundi hili lilipata umaarufu mkubwa liliposhirikiana na mwanamuziki wa Marekani Paul Simon kutoa albamu ya Graceland ambayo iliwashirikisha pia wanamuziki maarufu duniani kama Miriam Makeba na Hugh Masekela. Wanamuziki wa Afrika Kusini
1952
https://sw.wikipedia.org/wiki/Arusha
Arusha
Arusha ni neno la kutaja watu na mahali katika Tanzania kaskazini-mashariki: Kabila la Waarusha Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arusha Mji wa Arusha ni makao makuu ya mkoa na wilaya, pia makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Tanzania Makala zinazotofautisha maana
1953
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Arusha
Mkoa wa Arusha
Mkoa wa Arusha ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 23000, na ni wa pili kwa utajiri nchini. Wakazi ni 2,356,255. Eneo Eneo lake ni km za mraba 34,526 zikiwemo km² 707 za maji ya ndani.. Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani, kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara. Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini, Ngorongoro na Karatu. Makao makuu yapo Arusha mjini. Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (m 2,878) ni volkeno hai bado, na mlima Meru ni volkeno iliyolala tangu mwaka 1910. Mvua hunyesha kati ya milimita 1,800 kwa mwaka mlimani Arusha hadi mm 508 kwa mwaka katika maeneo makavu. Uchumi Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Tarangire ziko karibu. Barabara ya lami Dar es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi. Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti. Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea. Kati ya wakazi asili wa mkoa ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamasai. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Arumeru Magharibi : mbunge ni Gibson Ole Mesiyeki (Chadema) Arumeru Mashariki : mbunge ni Joshua Nassari (Chadema) Arusha Mjini :mbunge ni Godbless Lema (Chadema) Karatu : mbunge ni Wille Qulwi Qambalo (Chadema) Longido : mbunge ni Onesmo Ole Nangole (Chadema) Monduli : mbunge ni Kalanga Julius Laizer (Chadema) Ngorongoro : mbunge ni William Tate ole Nasha (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Arusha Orodha ya mito ya mkoa wa Arusha Tanbihi Viungo vya nje Tovuti ya Mkoa wa Arusha Arusha
1954
https://sw.wikipedia.org/wiki/Deutsche%20Welle
Deutsche Welle
Redio Deutsche Welle (DW), au Sauti ya Ujerumani ni kituo cha Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa ajili ya matangazo ya nje. Kituo kimeanzishwa mw. 1953 kilitoa matangazo ya Kijerumani kwa ajili ya Wajerumani kote duniani kwa njia ya SW. Leo (2005) kituo hutangaza kwa redio za SM na FM kwa lugha 30 halafu kwa TV kwa lugha 4. Makao makuu ndipo Köln; ofisi za DW-TV ziko Bonn na Berlin. Kwa www.dw-world.de ratiba na matangazo hupatikana pia katika mtandao. Ukurasa wa matangazo ya Kiswahili upo Sauti ya Ujerumani . Ujerumani Redio ya kimataifa
1956
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilomita%20ya%20mraba
Kilomita ya mraba
Kilomita ya mraba (km²) ni kipimo cha eneo; eneo lenye upana na urefu wa kilomita moja Msingi wake ni mita ya mraba (m²). Kilomita ya mraba hutumika kwa upimaji wa maeneo makubwa duniani kama mji, mkoa, nchi au dunia yote. Kilometa 1 ya mraba (km²) ni sawa na: eneo la mraba yenye urefu wa kilomita moja kila upande Mita ya mraba 1,000,000 Hektari 100 Ekari 247.105 381 Maili ya mraba 0.386 102 Au: Mita ya mraba 1 = kilometa ya mraba (km²) 0.000 001 Hektari 1= kilometa ya mraba (km²) 0.01 Maili ya mraba 1 = kilometa ya mraba 2.589 988 Ekari 1 = kilometa ya mraba 0.004 047 Vipimo vya eneo Hisabati de:Quadratmeter#Quadratkilometer
1958
https://sw.wikipedia.org/wiki/Usawa%20bahari%20wastani
Usawa bahari wastani
Usawa wa wastani wa maji ya bahari hutumika kama kipimo cha kulinganisha kimo cha mahali duniani toka usawa wa bahari. Hali halisi usawa wa bahari hubadilika kati ya mahali na mahali na muda hadi muda. Kwa hiyo kuna kadirio la wastani wa vipimo hivyo inayotumika kuwa usawa bahari wastani. Kawaida hutumika katika sentensi kama: "Nairobi iko mita 1644 juu ya usawa wa bahari." Au: "Ndege inasafiri mita 11.000 juu ya usawa wa bahari" Kifupi chake: UB Jiografia Bahari Vipimo
1959
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alfu%20Lela%20U%20Lela
Alfu Lela U Lela
Kitabu cha Alfu Lela U Lela au Usiku Elfu na Moja (كتاب ألف ليلة وليلة kwa Kiarabu au هزار و یک شب kwa Kiajemi) ni mkusanyiko wa fasihi katika muundo wa visa kutoka Mashariki ya Kati. Maandishi na historia yake Visa hivi vinatokana na kitabu cha zamani cha Kiajemi kiitwacho Hazâr Afsâna (Visa vya Ngano Elfu Moja). Inaaminika kuwa mtu aliyekusanya visa hivi na kutafsiri kwa Kiarabu ni mtambaji hadithi maarufu Abu abd-Allah Muhammed el-Gahshigar katika karne ya 14. Tafsiri ya kwanza ya Kiarabu ya kisasa ilichapwa Cairo, Misri mwaka 1835. Inasadikika kuwa visa hivi vilianza kukusanywa wakati Baghdad ilipokuwa kitovu cha biashara na siasa Mashariki ya Kati. Wafanyabiashara toka Uajemi (Persia), China, India, Afrika, na Ulaya walikuwa wakitembelea Baghdad kwa ajili ya biashara. Masimulizi makuu ya Alfu Lela: Mfalme na Shahrazad Mwanzo wa visa hivi ni kuudhiwa kwa mfalme Shahryar wa "kisiwa kilichoko kati ya India na China," na kitendo cha mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa. Shahryar aliamua kumuua mke wake. Kwa kuamini kuwa wanawake wote wako kama mke wake aliyemuua (yaani sio waaminifu) anamwamuru mtumishi wake awe anampatia mke kila usiku. Baada ya kulala na mke wake mpya usiku, kunapokucha anaamuru mke huyo auawe. Hali hii inaendelea hadi pale binti wa huyo mtumishi wake anapounda mbinu maalum na kuamua kujitolea kuwa mke wa mfalme. Binti huyo jina lake ni Shahrazad (Scheherazade au Shahrastini katika vitabu vya Kiingereza). Kila usiku baada ya ndoa yao, binti huyo anatumia masaa na masaa kumsimulia mfalme visa vitamu na vya kusisimua ambapo utamu wake unakuwa umekolea inapofika alfajiri (ule wakati wa kuuawa kwa mke wa mfalme). Kwa nia ya kujua mwisho wa kisa, mfalme alikuwa akiahirisha mauaji ya Shahrazad. Aliendelea kuahirisha kuuawa kwa mke wake hadi akapata naye watoto watatu! Ulipofika wakati huo aliamini kuwa mke wake huyo ni mwaminifu hivyo akabadili uamuzi wa kuua wake zake. Mchanganyiko wa hadithi Visa vyenyewe ni mchanganyiko wa mapenzi, misiba, ucheshi, mashairi, na visa vya dini ya Kiislamu. Visa hivi vinajumuisha pia wanamazingaombwe na majini.Visa maarufu ni pamoja na Taa ya Alladin, Baharia Sindbad, Ali Baba na Wezi Arobaini. Kati ya majina mengi inayotajwa kuna pia majina ya Khalifa Harun ar-Rashid na mshairi Abu Nuwas. Inaaminika kuwa visa vya Alladin na Ali Baba viliingizwa katika mkusanyiko huo karne ya 18 na Antoine Galland ambaye alisikia visa hivyo toka kwa mtambaji hadithi wa Kimaroni tokea nchini Syria. Viungo vya Nje - Tafsiri mbalimbali za Alfu Lela U Lela pamoja na tafsiri ya Sir Francis Burton na John Payne Project Bartleby edition Tafsiri ya Lane na Poole - Tafsiri ya Jonathan Scott Viungo vya Filamu na Luninga Kipindi cha luninga Sinema ya Sinbad: Legend of the Seven Seas Fasihi
1960
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karne
Karne
Karne ni muda wa miaka mia moja. Karne 10 ni milenia moja. Inawezekana kugawa karne kwa miongo 10. Neno hili limetokana na Kiarabu "ﻗﺮﻥ" linamaanisha kipindi cha miaka mia moja. Kwa kawaida karne si miaka 100 yoyote inayofuatana lakini kipindi kati ya miaka kama vile 1901-2000 au 1801-1900. Karne inakwisha katika mwaka wenye "00" mwishoni yaani 1700, 1800, 1900, 2000. Sababu yake ni kwamba hakuna mwaka "0" ya kuanzisha hesabu, hivyo karne ya kwanza ya hesabu ilianza kwa mwaka 1. Hali hii huleta kila karne majadiliano kwa sababu watu wengi husikia karne mpya inaanza wakati tarakimu ya mbele waliyozoea muda mrefu inabadilika. Hivyo watu wengi walisheherekea karne mpya mwanzoni wa mwaka 2000 iliyokuwa mwaka wa mwisho wa karne ya 20, si mwaka wa kwanza wa karne ya 21. Ingawa maoni ya wataalamu hayakueleweka au hayakupokelewa, watu wengine walisema haidhuru. Vipimo vya wakati
1961
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubuntu
Ubuntu
Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko ubinafsi. Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na Kixhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwa Kiswahili "utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana ya neno Ubuntu. Falsafa ya Ubuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi. Msingi wa falsafa hii ni, "mtu si mtu bila watu," kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu." Kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu" Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya Ubuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na ya kidini kwa kuwa imejengwa juu ya upendo wa watu wengine (kama unavyojipenda wewe) na hata mazingira. Viungo vya Nje ubuntu: Falsafa ya Kiafrika Ubuntu na Sheria Afrika Kusini Bill Clinton Akisisitiza Kuhusu Ubuntu video Makala Kuhusu Ubuntu na Dini Tafsiri ya Ubuntu Toka Kwa Askofu Desmond Tutu Video: Mandela Akitafsiri Ubuntu Video ya Mandela Akizungumzia Ubuntu Utamaduni wa Afrika Falsafa ya Kiafrika
1962
https://sw.wikipedia.org/wiki/Malik%20Zulu%20Shabazz
Malik Zulu Shabazz
Malik Zulu Shabazz (amezaliwa mwaka wa 1968 kwa jina la Paris Lewis) ni mwanasheria nchini Marekani na kiongozi wa kundi la New Black Panther Party for Self Defence. Wanasiasa wa Marekani
1963
https://sw.wikipedia.org/wiki/New%20Black%20Panther%20Party%20for%20Self%20Defence
New Black Panther Party for Self Defence
New Black Panther Party for Self-Defense ni kundi la wanaharakati weusi wenye siasa kali na mwamko wa kimapinduzi nchini Marekani. Kundi hili lilianzishwa mwaka 1989 na mtangazaji wa redio, Aaron Michaels, huko Dallas, Texas. Mwanzoni kundi hili lilichukua jina la "Black Panther Party" ambalo lilikuwa ni jina la kundi jingine lililokuwa na itikadi za kimapinduzi nchini Marekani. Wanachama wa kundi la mwanzo la Black Panther walipinga matumizi ya jina hilo yanayofanya na kundi jipya la Aaron Michaels. Michaels na wenzake walidai kuwa Black Panther haikuwa mali ya mtu binafsi bali jamii nzima ya watu weusi, hivyo hakuna ubaya jina hilo likatumika. Hata hivyo waliamua kuongeza neno "New" katika jina hilo. Kundi hili linakua huku likifungua matawi sehemu mbalimbali nchini Marekani. Wafuasi wengi waliojitenga na kundi jingine la Nation of Islam walijiunga na kundi hili wakimfuata aliyekuwa kiongozi wa New Black Panther Party, marehemu Khalid Abdul Muhammad. Khalid Abdul Muhammad alikuwa ni mhubiri wa Nation of Islam kabla hajajiunga na New Black Panther Party. Falsafa za kundi hili ni mchanganyiko wa mahubiri ya Malcolm X, Marcus Garvey, itikadi za uzalendo wa Kiafrika, na uanaharakati wa kimapinduzi. New Black Panther
1968
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bendera%20ya%20Tanzania
Bendera ya Tanzania
Bendera ya Tanzania ni ya mstatili unaokatwa pembe kwa pembe na kanda nyeusi yenye milia za njano kandokando. Pembetatu ya juu ina rangi ya majani, pembetatu ya chini ni ya buluu. Matumizi ya bendera inahifadhiwa chini ya sheria ya "The National Flag and Coat of Arms Act, 15-1971". Historia ya bendera Bendera hii imepatikana tangu 30 Juni 1964 kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Bendera ya Tanganyika ilikuwa na rangi ya kijani ikiwa na kanda nyeusi katikati yenye milia za njano kando. Buluu imepatikana kutokana na bendera ya Zanzibar ya mwaka 1964 ikimaanisha bahari. Hata hivyo toka mwaka 2005, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianza kutumia rasmi bendera ya Zanzibar. Hii ni mara ya kwanza toka kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar kwa funguvisiwa la Zanzibar kuwa na bendera yake lenyewe. Maana ya rangi Rangi zinasemekana kuwa na maana zifuatazo: Kijani kwa ajili ya mashamba, kilimo na misitu. Kijani ni pia rangi ya bendera ya chama cha TANU kilichokuwa chama tawala tangu uhuru. Buluu kwa ajili ya bahari na visiwa. Nyeusi ni rangi ya Waafrika. Njano inakumbusha juu ya utajiri wa madini. Njano ya namna hiyo inaelezwa mara nyingine kuwa ni dhahabu , lakini maelezo rasmi mengine kwa Kiingereza yanataja rangi kuwa "Yellow Pantone 116c" Bendera za kihistoria tangu zamani za ukoloni Marejeo Tanzania Tanzania
1970
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jakaya%20Kikwete
Jakaya Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015. Asili Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwere. Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake. Masomo Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga. Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978. Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi. Kupanda ngazi katika siasa 1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha. Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa. Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote. Miaka kumi ya urais Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo. Kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa Jakaya Kikwete kama Rais wa 4 wa Tanzania kulifanyika Jumatano, tarehe 21 Desemba 2005. Ilikuwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa miaka mitano wa Jakaya Kikwete kama Rais na Ali Mohamed Shein kama Makamu wa Rais. Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania. Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi. Heshima na Tuzo Nishani Shahada za Heshima Marejeo Tanbihi Viungo vya nje Jakaya Kikwete Fans Website Government of Tanzania Ippmedia Interview with Col Kikwete BBC Profile Jakaya Kikwete Swearing-In Ceremony Waliozaliwa 1950 Marais wa Tanzania Watu walio hai
1985
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jens%20Fink-Jensen
Jens Fink-Jensen
Jens Fink-Jensen (alizaliwa Copenhagen, Denmark, 19 Desemba 1956) ni mwandishi katika lugha ya Kidenishi katika nyanja mbalimbali kama vile semi za kawaida na mashairi. Vile vile yeye ni mpigapicha na mwandishi wa vitabu hasa vya muziki na nyimbo. Alianza maisha yake kama mwandishi wa vitabu vya hadithi 4 Juni 1975 wakati alipoandika hadithi fupi ijulikanayo kama Juni 1995. Kitabu hicho kilichapishwa kwenye gazeti la kila siku kwa lugha ya Kidenish lijulikanalo kama "Nipashe Habari'". Hatimaye kwenye mwezi wa Mei katika mwaka wa Elfu Moja na Mia Tisa na Sabini na Sita, akawa mwandishi wa mashairi kwanza kwa kuandika tunzi nne za mashairi zilizo chapishwa kwenye jarida nambari sabini na sita mkwaju moja, na ambalo hujulikana kama “Mbegu ya Ngano” (Hvedekorn). Tunzi zake za mwanzo kwenye nyanja ya mashairi zilichapishwa kwa mara ya kwanza kunako Mwaka wa Elfu Moja Mia Nane na Dhemaanini na Moja na zikajulikana kwa kupewa kicwa cha maneno Dunia Kwenye Jicho. Alianza kukusanya mashairi yalio kua yameandikwa na washairi wengine na kuyaweka katika hali ya vitabu kwenye mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Dhemanini na Sita. Vitabu vyenyewe vilichapishwa vikiwa katika hali ya mkusanyiko wa hadidhi fupi-fupi na vikatambulika kwa jina la Wanyama mwitu. Hatimae kunako mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Tisini na Nne, akaanza kuandika vitabu kwa watoto, baadhi yavyo kikiwa ni kile kiitwacho Jonas na Konokono. Alihitimu masomo yake kwenye shule ya upili kidato cha sita na kupita vizuri katika masomo ya lugha mbali-mbale akiwa katika shule ya bweni ya Herlufsholm kunako mwaka wa Elfu Moja mia Tisa na Sabini na Sita. Baadae alifanya mafunzo ya kijeshi na kuhitimu kwa kutunukiwa cheo cha Kamanda kwenye kikosi kiitwacho Walinzi Hai wa Kifalme (Royal Life Guards). Hatimae kwenye mwaka wa Elfu-moja na Mia Tisa na Dhemaanini na Sita, akajiunga na chuo kitoacho masomo kwenye fani ya ujenzi kilichoko mjini Conpenhagen amboko alitunukiwa shahada ya Mastas katika uchoraji na ujenzi. Katika mwaka wa Elfu moja Mia Tisa na Tisini na Saba, akiwa bado angali kwenye chuo hicho-hicho, aliyaendeleza masomo yake kwa kushiriki kwenye masomo ya ukusanyaji na utoaji wa habari katika misingi inayo husisha matumizu ya mbinu mbali-mbali. Na akiwa kama mojawapo wa waandishi wakongwe walio vuma katika miaka ya Dhemaanini na ambao walipenda kua na uhusiano wa karibu sana na bwana Poul Borum, (mhariri wa Hvedekorn), yeye pamoja na wenzake wengine kama vile Michael Strunge, walichangia katika kubuni onyesho la kusisimua ambalo lilijulikana kama “Kizazi Kipya” na ambalo liliandaliwa katika ukumbi wa Huset ulioko mjini Copenhagen. Hii ilikua ni kwenye mwaka wa Elfu Moja mia Tisa na Dhemaanini. Vile-vile, alijishirikisha kwenye maonyesho ya tunzi mbali-mbali na alishikilia nafasi maalum ya kusoma mashairi yenye kuelezea hali ya furaha na huzuni, huku akionyesha picha zinazo onyeshwa kwenye kuta kwa kutumia miale ya mwangaza. Mengine alio jihusisha nayo yalikua ni Kuleta hali ya uuwiyano katika tunzi mbali-mbali zilizo tungwa na shule mbali-mbali za upili, na kwenye sherehe zingine mbali-mbali zilizo wahi kufanyika wakati huo; Hii ikiwa ni baadhi ya matukio mengine alio jihusisha nayo. Wengine walio shiriki nae ni mwana mziki Fredrik Mellqvist ambae ana uhodari wa kucheza chombo kiitwacho Keyboard. Wengine alio shiriki nao ni pamoja na yule mchezaji wa chombo kiitwacho Saksafoni aitwae Jens Severin. Mwana sanaa huyu Jens Fink-Jensen amewahi vile-vile kuandaa maonyesho ya picha, kwamfano yale yaliyo julikana kama “Meli za Kusini” pamoja na Uso wa Beijing. Mengine yalikua ni pamoja na maonyesho yalio julikana kama Picha za Neno ambazo ziliandamana na picha ambazo huonyeshwa kwa kutumia miyale ya mwangaza na ambazo hushirikisha sauti. Mfano ukiwa ni ile ijulikanayo kama Jicho limulikalo Ulimwengu likiwa ni onyesho lililokua linasimulia kuhusu malighafi inayo tumika ndani ya vitabu. Orodha ya vitabu vingine alivyowahi kuchapisha 1981 Mashairi ya Verden i et øje (Dunia kwenye jicho) 1982 Mashairi ya Sorgrejser (Safari za kufadhaisha) 1983 Mashairi ya Dans under galgen (Kucheza densi kwenye miti ya kunyongea watu) 1986 Hadidhi Fupi za Bæsterne (Wanyama mwitu) 1988 Mashairi ya Nær afstanden (Karibu ya mwendo) (yalio chapishwa kwa lugha ya Kiarabu 1999) 1994 Vitabu kwa Watoto Jonas og konkylien (Jonas na konokono) (ambamo picha za tafsiri zimechorwa na msanii Mads Stage) 1995 Mashairi ya Forvandlingshavet (Bahari ya mageuzi). 1998 Kitabu Kwa Watoto Jonas og himmelteltet (Jonas na hema ipepeayo kwenye mawingu) (ambamo picha za tafsiri zimechorwa na msanii Mads Stage) 2002 Mashairi ya Alt er en åbning (Kila kitu ni ufunguo mpya) 2005 Chaguo Maalum la Mashairi Mia Moja ya kimapenzi ya Syd for mit hjerte (Kusini ya moyo wangu) Viungo vya nje Jens Fink-Jensen Online Waliozaliwa 1956 Waandishi wa Denmark
1989
https://sw.wikipedia.org/wiki/Krismasi
Krismasi
Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki. Jina Kwa Kiswahili kuna majina mawili ya kawaida kwa ajili ya sikukuu hii: Krismasi kutokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo. Noeli kutokana na neno la Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambalo limepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "Noël". Hilo ni ufupisho wa neno la Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa". Historia ya sherehe ya Krismasi Hakuna uhakika kamili ni lini Krismasi ilianza kusheherekewa. Ni sikukuu ya kale katika Ukristo lakini haikuwepo tangu mwanzoni. Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa. Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi. Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200 BK. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari. Lakini kadirio la tarehe 25 Desemba lina asili katika Misri pia. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) wataalamu nchini Misri waliona tarehe 14 Nisan ya kalenda ya Kiyahudi ambayo ni sawa na 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa. Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Krismasi na sikukuu ya Sol Invictus Mjini Roma wakati wa karne ya 4 tarehe ya Krismasi katika Desemba ilitokea pamoja na sikukuu ya Kipagani iliyoitwa "Siku ya Sol Invictus". Hii ilikuwa sherehe ya Jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika"). Hii ilikuwa ibada iliyoingia Roma kutoka Uajemi ambako mungu Mithra aliabudiwa kama mungu wa nuru. Waumini wa dini ya Jua waliona wakati wa Desemba kama kipindi cha pekee kutokana na solistasi ya mwezi huo; katika nusutufe ya kaskazini ya Dunia urefu wa mchana unapungua na usiku unakuwa mrefu tangu sikusare ya 21/22 Septemba hadi tarehe 21/22 Desemba; kuanzia siku za 21/22 Desemba mchana huwa mrefu na nuru inaongezeka. Mwendo huo ulitazamwa kama ushindi wa nuru = Jua juu ya giza. Pale Roma Kaisari Eliogabalus (aliyezaliwa Syria, alitawala Roma 218 hadi 222) alianzisha sherehe ya sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" huko Roma. Baadaye Kaisari Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273. Wakati wa Kaisari Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba. . Hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba. Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kufanya ichukue nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika"). Kwa namna yoyote hata katika Ukristo Jua linatazamwa kama ishara ya Kristo; katika sehemu mbalimbali za Biblia Kristo alifananishwa tayari na Jua na maneno haya yaliandikwa muda mrefu kabla ya kutokea kwa siku ya Sol Invictus. Mifano ni Injili ya Luka 1,78 Ufunuo 21, 23 , Malaki 4,2 (, hivyo katika mashindano na dini ya kuabudu Jua Wakristo walitumia lugha ya Biblia kwa kudokeza Kristo ndiye Jua la kweli. Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo. Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki na sehemu ya Waprotestanti na Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda. Habari za Krismasi katika Biblia Habari za Krismasi kama sherehe hazipatikani katika Biblia kwa sababu zilizotajwa hapa juu na kwa sababu mwanzoni mwa Kanisa mkazo ulikuwa juu ya kifo na ufufuko wa Yesu, tunavyoona hasa katika barua za Mtume Paulo. Baadaye tu, Wakristo walichunguza zaidi asili ya huyo aliyesadikiwa nao kuwa alikufa na kufufuka. Hasa vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo na Luka. Katika Injili ya Mathayo Mathayo anasimulia habari hizo katika mlango wa kwanza kuanzia aya 18 na katika mlango wa pili. Bikira Maria, Mama wa Yesu, alipata mimba wakati alipokuwa mchumba wa Yosefu. Yosefu alitaka kumwacha lakini aliambiwa na malaika aanze kuishi naye na kumkubali mtoto kama wake kwa kumpa jina "Yesu". Mamajusi kutoka mashariki waliwatembelea kijijini Bethlehemu na kuwaletea zawadi kwa sababu waliona nyota ya pekee iliyokuwa kwao alama ya kuzaliwa kwa mfalme mpya katika Uyahudi ikawaongoza hadi mjini Yerusalemu. Lakini walipompitia mfalme Herode Mkuu, huyo alikasirika akimwogopa mfalme mpya. Hata hivyo aliwaelekeza Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika. Yosefu alipata tena ujumbe kutoka kwa malaika akaondoka na mtoto na Maria kukimbilia Misri kabla ya askari wa Herode hawajaweza kumuua Yesu. Baada ya kifo cha Herode walirudi kutoka Misri lakini hawakuenda tena Bethlehemu bali walihamia Nazareti katika mkoa wa Galilaya. Katika Injili ya Luka Katika taarifa ya Luka (mlango wa 1 na 2) Maria alipokea huko Nazareti ujumbe wa malaika mkuu Gabrieli kwamba atapata mimba halafu mtoto wa pekee. Yosefu na Maria walikwenda Bethlehemu kwa sababu ya sensa iliyowataka kwenda katika mji asili wa ukoo wa Yosefu, mjukuu wa mfalme Daudi. Hapo Yesu alizaliwa katika hori la kulishia wanyama; wachungaji mabondeni walitangaziwa na malaika habari hiyo wakaja kumwona mtoto. Baada ya kuzaliwa wazazi walimpeleka Yesu Yerusalemu katika hekalu kufuatana na sheria ya Agano la Kale (Kitabu cha Kutoka 13,2; 13,15) halafu wakarudi kwao Nazareti. Habari za Krismasi katika Korani Korani pia ina habari za kuzaliwa kwake Yesu (nabii Isa). Sura ya tatu (Al Imran, 42-47) ina habari za tangazo la malaika kwa Bikira Mariamu zinazofanana na Luka 1. Sura ya 19 (Mariamu, 16-34) inarudia tangazo la malaika kwa Mariamu na inasimulia kuzaliwa kwake Yesu chini ya mti wa mtende, halafu majadiliano kati ya Mariamu na ndugu zake. Mtoto mchanga Yesu akaanza kusema wakati wa kuzaliwa akimtetea mama yake dhidi ya ndugu zake. Krismasi katika liturujia Kama kawaida, imani na liturujia ya Kikristo zinaitikia haja za binadamu. Mojawapo ni kukutana na watu wa kupendeza kwa wema wao. Kipindi cha Noeli kinatimiza haja hiyo, kwa kuwa kinaadhimisha kuzaliwa kwa mtu mpya kabisa ambaye anatuvutia kwa wema wake na ambaye tukimuona tumemuona Mungu, tena tukimpokea tunazaliwa upya kama wana wa Mungu. “Leo amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”. Tunapoadhimisha Noeli tangazo hilo la malaika kwa wachungaji linatufikia sisi. Si kujidanganya, kana kwamba Yesu angezaliwa leo, wala hatukumbuki tu tukio la zamani, bali fumbo la kuzaliwa Bwana linatufikia leo katika liturujia na kutuletea neema zake. Hivyo tunaweza tukazaliwa upya kwa kushiriki kuzaliwa kwa kichwa chetu. Liturujia inashangilia hivi, “Lo! Mabadilishano ya ajabu! Mwana wa Mungu anakuwa mtu kusudi mtu awe mwana wa Mungu!”. Tena si binadamu tu, bali viumbe vyote vinapata heshima mpya kwa Neno wa milele kujifanya kiumbe. Desturi za Krismasi Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo. Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio (Italia ya Kati) na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa. Mapambo ya Krismasi: ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemu inawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka. Mti wa Krismasi - ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kama mwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi. Zawadi za Krismasi - Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2. Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira. Baba Krismasi Tanbihi Marejeo The Battle for Christmas, by Stephen Nissenbaum (1996; New York: Vintage Books, 1997). ISBN 0-679-74038-4 The Origins of Christmas, by Joseph F. Kelly (August 2004: Liturgical Press) ISBN 978-0-8146-2984-0 Christmas Customs and Traditions, by Clement A. Miles (1976: Dover Publications) ISBN 978-0-486-23354-3 The World Encyclopedia of Christmas, by Gerry Bowler (October 2004: McClelland & Stewart) ISBN 978-0-7710-1535-9 Santa Claus: A Biography, by Gerry Bowler (November 2007: McClelland & Stewart) ISBN 978-0-7710-1668-4 There Really Is a Santa Claus: The History of St. Nicholas & Christmas Holiday Traditions, by William J. Federer (December 2002: Amerisearch) ISBN 978-0-9653557-4-2 St. Nicholas: A Closer Look at Christmas, by Jim Rosenthal (July 2006: Nelson Reference) ISBN 1-4185-0407-6 Just say Noel: A History of Christmas from the Nativity to the Nineties, by David Comfort (November 1995: Fireside) ISBN 978-0-684-80057-8 4000 Years of Christmas: A Gift from the Ages, by Earl W. Count (November 1997: Ulysses Press) ISBN 978-1-56975-087-2 Viungo vya nje Christmas: Its Origin and Associations, by William Francis Dawson, 1902, from Project Gutenberg Liturujia Sikukuu za Ukristo Yesu Kristo Krismasi Rozari
1991
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mto%20Kagera
Mto Kagera
Mto Kagera (kwa Kinyarwanda: Akagera) ni kati ya mito inayounda mto Nile, pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza. Unaanzia Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela km 400 hadi kuingia ziwa Viktoria. Mto Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale unapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho ya njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza km kama 40 kaskazini kwa Bukoba. Jina la mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania. Tazama pia Orodha ya mito ya Tanzania Orodha ya mito ya Uganda Orodha ya mito ya mkoa wa Kagera Tanbihi Viungo vya nje Geonames.org Mto Kagera Mito ya Burundi Mito ya Rwanda Mito ya Uganda Mito ya Tanzania Ziwa Viktoria Nile Mkoa wa Kagera Mediteranea
1992
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Kagera
Mkoa wa Kagera
Mkoa wa Kagera kati ya mikoa 31 ya Tanzania ndio mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa wenye postikodi namba 35000. Jina lake linatokana na mto Kagera. Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mingine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na Geita. Eneo lake ni km² 28,953 za nchi kavu na km² 11,885 za maji ya ndani, hasa ya Viktoria Nyanza, jumla km² 40,838. Mkoa wa Kagera uko mnamo mita 1000 juu ya uwiano wa bahari. Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba. Kiutawala eneo la mkoa limegawiwa kwa wilaya saba: Bukoba, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa pamoja na eneo la manisipaa ya Bukoba. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012. Sensa ya mwaka 2022 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,989,299 inayoendelea kuongezeka kasi. Mkoa huu una makabila makubwa manne ambayo ni: Wanyambo, Wahangaza, Wahaya na Wasubi. Wanyambo huishi kwa wingi katika wilaya za Kyerwa na Karagwe, Wahangaza huishi kwa wingi katika wilaya ya Ngara, Wahaya huishi kwa wingi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Misenyi na Wasubi huishi kwa wingi katika wilaya ya Biharamuro. Makabila ya Wanyambo na Wahaya hupenda kula ndizi kwa wingi na asilimia kubwa wanafuata mila na desturi za mababu: Zamani Wanyambo na Wahaya walikuwa hawawezi kuoana na hiyo bado sasa ipo kwa kiasi kidogo. Pia mkoa huu una wakimbizi wengi, kwa asilimia kubwa wanatokea nchi za Rwanda na Burundi wakipitia wilaya ya Ngara. Jiografia Hali ya hewa ni nzuri kwa kuishi, kilimo, uvuvi. Mkoa huo ni maarufu kwa ulimaji wa kahawa, ndizi, miwa na chai. Pia una mbuga za wanyama na umezungukwa na mto Kagera. Historia ya mkoa Mkoa huu unapatikana ukanda wa ziwa Viktoria. Katika mkoa huu kuna mambo mengi ambayo yalitetemesha nchi ya Tanzania. Mambo hayo ni pamoja na vita ya Uganda na Tanzania, vita ambavyo vilihusishwa na mkoa huu; ilikuwa mwaka 1978. Ndipo Idd Amin Dada aliyekuwa Rais wa Uganda alipoliamru jeshi lake kuvamia mkoa wa Kagera. Walianza kuvamia wilaya ya Missenyi. Hapo Julius K. Nyerere aliyekuwa rais wa Tanzania aliamuru jeshi lake kufukuza wavamizi hadi kuvamia nchi ya Uganda. Agizo hilo lilikuwa zuri lakini vijana wa mkoa wa Kagera walipata shida kwa sababu walilazimishwa kufuzwa Uanamgambo mara moja na kupelekwa vitani. Walipoanza tu vita hivyo raia wa Uganda walishirikiana na jeshi la Tanzania kufichua maficho ya jeshi la Uganda. Jeshi la Tanzania liliwapiga na kuwapora mali zao, vifaa vya kivita na kuwateka wanajeshi wao. Mwanzoni mwa mwaka wa 1979 Idd Amin Dada alikimbia na Tanzania kushinda vita hivyo. Mara baada ya vita hivyo Watanzania walichukua mali za Uganda, hasa mifugo, na walipofika nchini Tanzania walifurahia na kusherekea ushindi huo. Mwaka 1996 meli ya MV Bukoba ilizama ikisafirisha abiria kutoka mkoa wa Kagera kwenda Mwanza; watu wengi walikufa na lilikuwa pigo kwa serikali, kwa ndugu na majonzi makubwa kwa Watanzania kwa ujumla. meli hiyo ilikuwa ina mkoani mwanza katika ziwa la victoria Katika mkoa huohuo mwaka 2016 lilitokea tetemeko la ardhi lililoleta maafa makubwa: watu walikufa, wengine walipoteza mali zao, hususani majumba yao. Uongozi wa mkoa wa Kagera uliomba kila Mtanzania kuchangia angalau shilingi 100 na kuwasaidia. Elimu Katika mkoa huu elimu bado haijaenea kwa watu wote walioko vijijini. Elimu inakua kwa kasi ndogo na watu wengi wa mkoa huu hawajasoma: wengi wanafanya kazi ya kulima. Hali hiyo hufanya taifa kurudi nyuma kimaendeleo maana taifa kama taifa huongozwa na wasomi ili kukua kiuchumi. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Biharamulo : mbunge ni Oscar Rwegasira Mukasa (CCM) Bukoba Mjini : mbunge ni Steven L. Byabato (CCM) Bukoba Vijijini : mbunge ni Rweikiza Jasson (CCM) Karagwe : mbunge ni Innocent Luugha Bashungwa (CCM) Kyerwa : mbunge ni Innocent Sebba Bilakwate. (CCM) Muleba Kaskazini : mbunge ni Charles Mwijage ((CCM) Muleba Kusini : mbunge ni (CCM) Ngara : mbunge ni Alex Gashaza (CCM) Nkenge : mbunge ni Diodorius Kamala (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Kagera Orodha ya mito ya mkoa wa Kagera Tanbihi Viungo vya nje Tovuti ya Mkoa wa Kagera Kagera – Bukoba – the official webguide – Tourist Office Bukoba / Kagera United Republic of Tanzania: Kagera Region Utamaduni wa Kagera -en K
1993
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kagera
Kagera
Kagera ina maana mbalimbali: Kagera ni mto katika Tanzania Mkoa wa Kagera ni mkoa katika Tanzania. Kagera (Ukerewe) ni kata ya wilaya ya Ukerewe kwenye mkoa wa Mwanza (Tanzania) {maana}} Makala zinazotofautisha maana
1996
https://sw.wikipedia.org/wiki/Yesu
Yesu
Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK). Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi. Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu). Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6). Misingi ya ujuzi wetu juu yake Yesu hakuacha maandiko yoyote. Habari zake zinapatikana hasa katika Biblia, kwa namna ya pekee katika Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya. Nje ya Ukristo kuna habari fupi kuhusu Yesu katika maandiko ya waandishi wa Roma, Wagiriki na Wayahudi. Habari hizo zinaangaliwa sana kwa sababu zimetungwa na watu wasiomwamini Yesu kidini. Kwa ujumla zinathibitisha ya kwamba Yesu alikuwepo, na kwamba wakati hao walipoandika alikuwa na wafuasi huko Roma na ya kwamba awali Waroma hawakuelewa tofauti kati ya wafuasi wake na Wayahudi. Kati ya waandishi hao muhimu ni hasa: 1. Mtaalamu Myahudi Flavius Josephus: huyo aliandika mnamo 90 BK kitabu cha "Antiquitates Judaicae“ (Habari za historia ya Wayahudi) akitaja kifo cha "Yakobo ndugu wa Yesu“ (sura ya 20, 200). 2. Mwandishi Mroma Tacitus: huyo aliandika mnamo mwaka 117 ya kwamba Kaisari Nero alishtaki kikundi cha “Chrestiani” ya kuwa wamechoma moto mji wa Roma. Aliongeza: “Mtu ambaye ni asili ya jina hilo ni Chrestus aliyeuawa wakati wa Tiberio kwa amri ya Pontio Pilato” (Annales XV,44). 3. Mwandishi Mroma Svetonius: huyo alimtaja “Chrestos” katika kitabu chake juu ya maisha ya Kaisari Klaudio (25,4) ya kwamba huyu amesababisha fujo kati ya Wayahudi wa Roma hivyo Kaisari aliwafukuza wote mjini. 4. Mwanasiasa Mroma Gaius Plinius Caecilius Secundus: huyo aliacha barua kadhaa zinazotaja Wakristo mnamo mwaka 100 BK. Alimwuliza Kaisari Traianus jinsi ya kushughulikia Wakristo waliokataa kutoa sadaka mbele ya sanamu za Kaisari. Mazingira yake Nchi ambayo Yesu alizaliwa akafundisha ni nchi ileile ambayo Mungu aliwaahidia Waisraeli tangu zamani za Abrahamu, ni nchi ileile waliyoiteka chini ya Yoshua, ni nchi ileile waliyoirudia kutoka utumwani Babeli. Lakini wakati wote wa Agano Jipya, yaani tangu Yesu alipozaliwa hadi mwisho wa maisha ya mitume wake, nchi hiyo haikuwa huru, bali chini ya himaya ya Warumi, ingawa pengine hao waliwakabidhi vibaraka, yaani watawala wenyeji waliowekwa na wakoloni. Vibaraka hao ni Herode Mkuu (37 KK-4 KK) na wazawa wake, ambao tena hawakuwa Waisraeli halisi bali Waedomu ingawa kabila lao lililazimishwa kuingia dini ya Uyahudi karne iliyotangulia. Ukoo huo unajulikana kwa ukatili, uchu wa madaraka na uzinifu wake. Vilevile maliwali wa Kirumi waliowekwa pengine kutawala nchi au sehemu fulani walionyesha mara nyingi ukatili na dharau kwa Waisraeli na dini yao, hata kusababisha chuki na mapigano kati ya jeshi na wananchi. Mfano mmojawapo ni Ponsyo Pilato aliyesimamia Uyahudi kuanzia mwaka 26 hadi 36 BK. Mbali na hayo, utawala wa Dola la Roma, ulioenea Ulaya Magharibi na Kusini, Afrika Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati kupakana na Iraq ya leo, kwa jumla ulihakikisha hali ya amani kwa muda wote wa Agano Jipya na karne za kwanza za Kanisa. Hali hiyo, pamoja na umoja wa dola hilo lote, na urahisi wa mawasiliano kwa njia ya barabara zilizotengenezwa na Warumi, na uenezi wa lugha ya kimataifa (Kiyunani, yaani Kigiriki cha zamani), ilichangia kasi ya uenezaji wa habari njema (Injili). Lugha hiyo ndiyo iliyotumiwa na waandishi wote wa Agano Jipya ili vitabu vyao viwafaidishe watu wengi zaidi, ingawa baadhi yao hawakuijua vizuri. Lugha mama ya Yesu na ya Mitume ilikuwa Kiaramu ambacho ni jamii ya Kiyahudi na ambacho polepole kilishika nafasi yake kati ya Wayahudi kuanzia karne ya 6 KK. Hao wote walitokea mkoa wa Galilaya, uliokuwa na mchanganyiko wa watu (Waisraeli na mataifa), kiasi kwamba huko Wayahudi wenyewe walifuata kwa urahisi desturi za Kiyunani hata wakadharauliwa na wenzao wa Kusini (Yerusalemu na mkoa wa Yudea). Kati ya mikoa hiyo miwili ulienea mkoa wa Samaria ambao wakazi wake walijenga uadui mkubwa na Wayahudi baada ya uhamisho wa Babeli, walipokataliwa kuchangia ujenzi wa hekalu la pili la Yerusalemu. Maisha yake Dionisi Mdogo, mmonaki aliyeanzisha (mwaka 533 hivi) mtindo wa kuhesabu miaka tangu kuzaliwa Yesu kurudi nyuma (K.K.) au kwenda mbele (B.K.), alikosea hesabu zake. Leo tunakisia Yesu alizaliwa mwaka 6 hivi K.K. kwa sababu alizaliwa Bethlehemu chini ya Herode Mkuu aliyefariki tayari mwaka 4 K.K. Huyo alipojaribu kumuua mtoto Yesu, familia takatifu ilikimbilia Misri mpaka baada ya kufa kwa Herode. Hapo ikarudi Galilaya hata Yesu akajulikana kwa jina la kijiji cha Nazareti kilichodharauliwa na Wagalilaya pia. Ndipo alipokulia na kuishi akifanya kazi ya ufundi. Hivyo Yesu alitumia sehemu kubwa ya maisha yake kijijini akiwatii wazee wake Maria na Yosefu na kufanya kazi za mikono. “Alishuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii” (Lk 2:51). Kwa namna hiyo ametuachia kielelezo cha utakatifu katika maisha ya familia na ya kazi ambayo ndiyo njia ya kawaida ya kukomaa kiutu na kumtumikia Mungu. “Mnyenyekeane katika kicho cha Kristo” (Ef 5:21). Mwaka 26 hivi BK ndugu yake Yohane Mbatizaji aliacha maisha ya jangwani alikokulia na kuanza kuhubiri toba kandokando ya mto Yordani. Kwa kuwa Waisraeli walikosa manabii kwa muda mrefu, na walitamani sana ukombozi, walimuendea kwa wingi hata wakamtia hofu Herode Antipa. Ingawa huyo akamfunga mapema akamuua, kazi ya Yohane ilikuwa imetimia kwa sababu aliweza kuwaandaa Waisraeli wengi (hasa watu wadogo na wakosefu) wampokee Yesu aliyebatizwa naye. Katika nafasi hiyo Yohane alimtambulisha kama Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu. Ndipo Yesu naye alipoanza kuhubiri, lakini pia kutenda miujiza ya kila aina, akapata haraka wafuasi wengi. Kati yao akachagua Mitume wake 12 kama msingi mpya wa taifa la Mungu badala ya Israeli ya kale. Alifanya kazi hizo kuanzia Galilaya, akitangaza ujio wa ufalme wa Mungu, kwa maana ya kwamba ufalme uliotazamiwa na Wayahudi umewajia kwa njia yake. Ingawa hakupitia shule yoyote ya Biblia, Yesu alionekana anafundisha vizuri kuliko walimu wa sheria wa kawaida, kama mtu mwenye mamlaka juu ya Torati. Mafundisho yake yalilingana na yale ya Mafarisayo kuliko na yale ya Masadukayo, lakini alishindana pia na hao wa kwanza. Kijicho na upinzani vikazidi hasa Yerusalemu, walipoanza kufanya njama za kumuua. Ingawa Yesu alijua hayo, alijikaza kwenda katika huo mji mtakatifu autangazie habari njema na kufia huko. Baada ya kupokewa kwa shangwe kabla ya sherehe ya Pasaka ya mwaka 30 (au 33) akakamatwa na baraza la Israeli kwa tuhuma ya kufuru ya kujilinganisha na Mungu, halafu akakabidhiwa kwa liwali wa Kirumi aliyekuwa na mamlaka ya kutoa adhabu ya kifo. Baada ya kikao ambapo Wayahudi walitafuta kisingizio cha kisiasa, Ponsyo Pilato akalazimika kuagiza Yesu asulubiwe, na kisha kufa kwake kaburi lilindwe na askari. Hata hivyo siku ya tatu kaburi likaonekana tupu, na Yesu akaanza kuwatokea wanafunzi wake wa kike na wa kiume kwa muda wa siku arubaini, halafu akapaa mbinguni mbele ya macho yao. Habari hizo zikatangazwa kwa sauti tu kwa miaka kadhaa, halafu zikaanza kuandikwa. Kanisa linaheshimu kwa namna ya pekee, kama ushuhuda mkuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu na kama moyo wa Maandiko matakatifu yote, Injili nne zilizoandikwa na Marko, Mathayo, Mwinjili Luka na Yohane kati ya mwaka 65 na 100 hivi. Ni muhimu kujua maisha ya Yesu kwa sababu matendo na maneno yake, pamoja na kimya na sala yake, na hasa kifo na ufufuko wake, yote yanatufunulia Baba na matakwa yake kwetu. “Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote” (Lk 24:19). Baada ya kujua maisha ya Yesu tunapaswa kujilinganisha naye hadi aundwe na kuishi ndani mwetu akitushirikisha uhai, kifo na ufufuko wake. “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu, na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu… Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu!” (Gal 2:20; 4:19). Sala zake (Math 11:25-26) Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako (Yoh 11:41-42) Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. (Yoh 17:1-26) Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. Mimi nimewapa neno lako, na ulimwengu umewachukia, kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli. Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, hao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo, ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao. (Mk 14:36) Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe. (Mk 15:34) Eloi, Eloi, lama sabakthani? (maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?) (Lk 23:46) Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu. Imani juu yake Waumini wake wanaunda Kanisa la Kikristo ambalo linapatikana leo katika madhehebu mengi. Karibu wote wanamwamini kuwa Mungu aliyechukua umbile la mwanadamu au, kwa lugha nyingine, kuwa Mwana wa Mungu. Kwa imani hiyo, Yesu ni Mungu na mtu kwa pamoja, ndiyo sababu ni mshenga pekee kati ya Mungu na watu. “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1Tim 2:5). “Katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol 2:9). Hivyo ni Mungu kweli na mtu kweli. Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake. “Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, ‘Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu’” (Mk 15:39). Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele. “Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake” (Yoh 14:10). Hapa duniani Yesu alizaliwa na Bikira Maria kama malaika alivyomuambia: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo, hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Lk 1:35). Hata hivyo Wakristo wachache wanaamini kuwa yeye ni mtume wa pekee wa Mungu ila si Mungu. Katika dini ya Uislamu, Yesu anajulikana kama Nabii Isa. Waislamu wanaamini kuwa yeye alikuwa nabii wa Mungu ila hakuwa mwana wa Mungu wala Mungu. Maadhimisho yake Maisha yake yamekuwa msingi wa sikukuu mbalimbali zinazosheherekewa katika nchi nyingi duniani, kama vile Noeli au Krismasi (kuzaliwa kwake), Epifania (kuonekana kwake na kubatizwa kwake), Majilio (kuandaliwa kwa ujio wake wa kwanza na kutarajia ujio wa pili), Kwaresima (mafungo na mateso yake), Ijumaa Kuu (kifo chake); muhimu kuliko zote ni Pasaka (kufufuka kwake). Tazama pia - Makala "Yesu Kristo": mafundisho ya Kikristo kuhusu Yesu - Makala "Isa": mafundisho ya Uislamu kuhusu Yesu - Makala juu ya cheo "Kristo" Tanbihi Marejeo Viungo vya nje Complete Sayings of Jesus Christ in parallel Latin and English. Yesu Waliozaliwa 6 KK Waliofariki 30 Yesu Kristo Ukristo Watu wa Biblia Watu wa Israel Manabii wa Agano Jipya Wafiadini Kristolojia Utatu Mtakatifu Bikira Maria
1997
https://sw.wikipedia.org/wiki/Azania
Azania
Azania (kwa Kigiriki: Ἀζανία) ni jina la kihistoria la sehemu mbalimbali za pwani ya Afrika ya Mashariki. Asili yake ni zamani za Waroma na Wagiriki wa kale kwa eneo lililokuwa la watu wa Lugha za Kikushi. Mapokeo ya Waroma na Wagiriki wa Kale Mara ya kwanza jina hili limepatikana katika mwandishi Mroma Plinio Mzee (Gaius Plinius Secundus) aliyeishi wakati wa karne ya 1 B.K. Kufuatana na maelezo yake, Azania ni sehemu zile zilizoanza katika eneo la Adulis (leo: Eritrea) na kuelekea kusini. Kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mabaharia "Periplus ya Bahari ya Eritrea" (karne ya 2 BK) kinatoa maelezo zaidi zinazoonyesha ya kwamba jina la Azania labda lilimaanisha pwani ya Afrika ya Mashariki kutoka Eritrea hadi Tanzania ya leo. Mwandishi Cosmas Indicopleustes wa karne ya 6 B.K. aliandika Azania ni nchi chini ya utawala wa ufalme wa Aksum, basi hapo isingeenea sana kusini kwa pembe la Afrika. Zanj ya Waarabu Katika karne zilizofuata umbo la "Azania" halikutumika tena. Inawezekana ya kwamba sababu yake ilikuwa Waarabu Waislamu walichukua nafasi ya Wagiriki na Waroma wakitawala biashara ya nje ya pwani ya Afrika ya Mashariki. Kuna uwezekano ya kuwa Waarabu walitumia umbo tofauti la neno kuwa "Zanj" kwa ajili ya eneo lilelile. Zanj imekuwa asili ya neno Zanzibar. Matumizi ya neno Azania katika karne ya 20 Kuingia katika jina la "Tanzania" Katika karne ya 20 jina la Azania limefufuka tena. Nchi huru za Tanganyika na Zanzibar ziliungana tarehe 26 Aprili 1964 kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jina jipya lilitafutwa. Hapo jina lile la kihistoria "Azania" lilikumbukwa tena; kwa kuunganisha maneno ya Tanganyika, Zanzibar na Azania jina la nchi "Tanzania" limepatikana. Kutaja Afrika Kusini Kwa namna tofauti jina la Azania lilitumika pia Afrika Kusini. Wakati wa siasa ya ubaguzi wa rangi sehemu ya wapinzani wa siasa hii hawakutaka kutumia jina rasmi la "South Africa / Zuid Afrika" tena. Walitafuta jina katika historia iliyotangulia kufika kwa Makaburu wakichukua jina la Azania. Ni hasa vyama vya PAC na Azanian People´s Organization waliotaka kubadilisha jina la Afrika Kusini kuwa Azania. Lakini chama kikubwa cha ANC haikukubali, hivyo mipango ilishindikana. Tanbihi Madola Afrika ya Mashariki
2000
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jumuiya%20ya%20Madola
Jumuiya ya Madola
Jumuiya ya Madola (jina la Kiingereza ni Commonwealth of Nations) inaunganisha nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake. Umoja huu umeanzishwa mw. 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Dola la Kibritania au Dola la Kiingereza ambayo ilikuwa dola kubwa kabisa katika historia ya dunia lakini maeneo yake yalianza kuachana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokana na kudhoofishwa kwa Uingereza vitani na miendo ya kupigania uhuru katika nchi mbalimbali hasa Uhindi. Leo zipatao asilimia 30 ya watu wote duniani (watu 1,800,000) huishi katika nchi wanachama za Jumuiya ya Madola. Nchi za jumuiya hii wenye wakazi wengi ni hasa Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Nigeria. Kuna pia nchi ndogo sana kama Tuvalu yenye wakazi 11,000 pekee. Nchi kadhaa zilisimamishwa uanachama au kuondoka kwa hiari zao. Mfano Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa hiyo hazipo tena lakini mpya ya Tanzania imekuwa nchi mwanachama. Vilevile Newfoundland iliondoka katika jumuiya baada ya kujiunga na Kanada kama jimbo. Pakistan ilisimamishwa uanachama mara kadhaa kwa sababu serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi walioanzisha serikali ya kijeshi. Imerudishwa tena. Zimbabwe ilisimamishwa uanachama baada ya uchaguzi bandia 2002 ikaamua kujiondoa kabisa mwaka 2003. Jamhuri ya Ueire iliamua mwaka 1949 kuacha viungo vyote na Uingereza ikajitangaza kuwa jamhuri isiyokubali athira ya nje kama hali ya malkia wa Uingereza kuwa mkuuw a dola hivyo ikaondoka katika jumuiya. Afrika Kusini ilijiondoa 1961 kwa sababu ya upinzani wa jumuiya dhidi ya sheria za apartheid. Baada mwisho wa ubaguzi wa rangi nchi ilirudi katika jumuiya. Fiji imesimamishwa mara kadhaa baada ya uasi wa kijeshi uliopindua serikali. Nchi wanachama za Jumuiya ya Madola Nchi wanachama za zamani Viungo vya nje Tovuti ya Bunge la Jumuiya ya Madola Jumuiya ya Madola Mashirika ya kimataifa
2002
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mzunguko%20wa%20Bahari%20Nyekundu
Mzunguko wa Bahari Nyekundu
Mzunguko wa Bahari Nyekundu (kwa Kiingereza: Periplous of the Erythrean Sea) ni kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mabaharia kilichoandikwa mnamo mwaka 70 BK. "Periplous" ni neno la Kigiriki linalomaanisha tendo la kuzunguka bara kupitia bahari kwa merikebu; "Bahari ya Eritrea" ni jina la kale kwa ajili ya Bahari ya Shamu (hadi Bahari Hindi). Jina hilo lilitungwa na watu wa nchi za mashariki ya Bahari ya Kati na Misri waliotumia lugha ya Kigiriki miaka 2000 iliyopita. Kitabu hicho kimeandikwa na mwenyeji wa Aleksandria / Misri uliokuwa mji mkubwa wakati ule na kitovu cha biashara ya kimataifa kati ya Dola la Roma, Afrika ya Mashariki na Bara Hindi. Kitabu kinaeleza juu ya bandari kuanzia Misri hadi Afrika ya Mashariki kwa upande mmoja na hadi Bara Hindi kwa upande mwingine. Kinataja majina ya bandari, bidhaa zilizopelekwa huko na bidhaa zilizopatikana kila mahali. Pia kuna habari za kando juu ya watu, watawala na mila zao. Maelezo ni mengi kuhusu pwani ya Eritrea na Somalia hadi Pembe ya Afrika; kuelekea kusini majina ya bandari ni machache; mwisho wa eneo lililojulikana ni mji wa Rhapta katika nchi za Azania, lakini hadi leo wataalamu hawajaelewana Rhapta na Azania zilikuwa wapi. Bahari ya Hindi Historia ya Afrika Afrika ya Mashariki
2003
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Eritrea
Bahari ya Eritrea
Bahari ya Eritrea (kwa Kigiriki ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa) ni jina la kale la Bahari ya Shamu na Bahari Hindi. Neno "erythra" katika lugha ya Kigiriki inamaanisha rangi nyekundu ("thalassa" = bahari). Hivyo bahari ile iliitwa "Bahari Nyekundu" (linganisha Kiingereza "Red Sea"). Inasemekana ya kwamba jina hilo limetokana na aina ya mwani unaoonyesha rangi hiyo wakati mwingine. Inaonekana ya kwamba waandishi wa kale hawakutofautisha kati ya Bahari ya Shamu na Bahari Hindi. Merikebu za zamani zile zilisafiri muda wote karibu na pwani kwa sababu dira haikulikana bado nje ya Uchina. Hivyo haikuwa rahisi kuvuka bahari moja kwa moja na kupata picha kamili ya umbo la bahari. Nahodha wa merikebu hizo walitumia maandiko kama Periplus ya Bahari ya Eritrea wakipanga safari zao. Bahari ya Hindi Bahari ya Shamu
2004
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Shamu
Bahari ya Shamu
Bahari ya Shamu (kwa Kiingereza Red Sea; kwa Kiarabu البحر الأحمر Baḥr al-Aḥmar, al-Baḥru l-’Aḥmar; kwa Kiebrania ים סוף Yam Suf; kwa Kitigrinya ቀይሕ ባሕሪ QeyH baHri) ni ghuba kubwa ya Bahari ya Hindi. Jina la kihistoria katika lugha ya Kigiriki lilikuwa Bahari ya Eritrea (ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa). Kaskazini kuna rasi ya Sinai pamoja ghuba ndogo za Aqaba na Suez; pia kwa sasa imeunganika na Mediteranea kwa njia ya Mfereji wa Suez. Kusini Bahari ya Shamu imeunganika na Bahari Hindi kwa njia ya mlango wa bahari wa Bab el Mandeb. Ghuba yote ina urefu wa takriban kilomita 2000; upana wake ni kati ya km 300 na 20 tu kwenye Bab el Mandeb. Eneo lake ni km² 450,000. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 2500 chini ya uwiano wa bahari. Vilindi hivyo ni sehemu ya Bonde la Ufa. Halijoto ya maji ni kati ya 21-25 °C. Nchi za kando Nchi zinazopakana na Bahari ya Shamu ni: Upande wa Kaskazini: Misri Israeli Yordani Upande wa Magharibi: Misri Sudan Upande wa Mashariki: Saudia Yemen Upande wa Kusini: Eritrea Jibuti Somalia Bahari ya Hindi Bahari ya pembeni
2006
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jamhuri%20ya%20Watu%20wa%20Zanzibar
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingawa inajitawala katika mambo ya ndani. Hadi mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 nchi hiyo ilijulikana kama Usultani wa Zanzibar. Jina Etimolojia ya Neno Zanzibar Jiografia Eneo lake ni sawa na funguvisiwa la Zanzibar lililopo mbele ya mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Tanganyika (Tanzania bara). Linajumuisha visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo, lakini si kile cha Mafia kilichopo kusini zaidi. Kiutawala Zanzibar imegawanyika katika mikoa mitano, 3 kisiwani Unguja na 2 kisiwani Pemba. Pemba Pemba Kaskazini Pemba Kusini Unguja Unguja Mjini Magharibi Unguja Kaskazini Unguja Kusini Historia Historia inaonyesha kwamba kwa kiasi cha miaka 20,000 kumekuwepo makazi ya binadamu katika visiwa vya Zanzibar. Visiwa hivyo ni sehemu ya kumbukumbu ya kihistoria ya ulimwengu wakati Waajemi wafanyabiashara walivigundua na kuvifanya makao makuu kwa safari kati ya Mashariki ya Kati, India na Afrika. Katika kipindi cha karne ya 3 na ya 4, Wabantu walianza biashara na Waarabu waliofika Afrika ya Mashariki. Katika karne ya 7, Waarabu walifika Zanzibar kibiashara pamoja na kusambaza dini ya Uislamu; Waarabu ndio walioipa jina ZANZIBAR kutokana na maneno ya Kiajemi ZINJI BAR yaani sehemu ya Watu Weusi. Lugha ya Kiswahili ilianza kutumika kiasi cha karne ya 13 ikitokana na mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za Kiafrika. Katika karne ya 16 Wareno walifika Zanzibar lakini utawala wao ulifuatiwa na kutokuwepo utulivu, lakini biashara ya utumwa iliwaweka watu pamoja. Waarabu kutoka Oman walichukua utawala Zanzibar katika karne ya 17 na Zanzibar ilikuwa makao makuu ya utawala wa Waomani. Miaka 1820-1870 Zanzibar ilifaidi matunda mazuri ya kiuchumi na maendeleo yaliyosababishwa na utawala wa masultani na hivyo kupelekea kuenea kwa dini ya Kiislamu Zanzibar pamoja na kuwa na mwakilishi nchini Marekani. Katika karne ya 19 Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa Oman, mwaka 1830 Zanzibar ilikuwa inaongoza kwa kilimo cha karafuu, na hiyo kupelekea haja ya watumwa kuongezeka kutumika katika kilimo. Hatimaye watumwa walikuwa 90% za wakazi wote. Mwaka 1885 kamisheni kutoka Uingereza na Ujerumani iliamua kuigawa Zanzibar kutoka katika utawala wa Kisultani na ndio ulikuwa mwisho wa utawala wa kujitegemea kwa Zanzibar. Mnamo mwaka 1886 sultani alikubali maridhiano hayo. Mwaka 1890 Zanzibar ilikuwa chini ya uangalizi wa Waingereza rasmi, lakini uchaguzi wa mwanzo ulifanyika mwaka 1957, na miaka iliyofuata kukawepo fujo na machafuko kutoka kwa Waafrika wanaodai uhuru dhidi ya utawala wa Kiarabu. Mwezi Desemba mwaka 1963 Waingereza waliipa uhuru Zanzibar chini ya jumuiya ya madola, na tarehe 12 Januari 1964 Zanzibar ilifanya mapinduzi kujikomboa kutoka katika utawala wa sultani. Muda mchache baadaye iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA. Siasa Kwa jumla mikoa mitano ya Tanzania imo ndani ya Zanzibar ikiwa mitatu iko Unguja na miwili Pemba. Zanzibar inatawaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Zanzibar ina bunge lake linaloitwa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar lenye wabunge 50 wanaochaguliwa kwa muda wa miaka mitano. Mji mkuu na makao makuu ya serikali ni Jiji la Zanzibar ambalo liko kisiwa cha Unguja. Mji mkuu wa kisiwa cha Pemba ni Chake Chake. Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilianzishwa baada ya mapinduzi ya 1964 yaliyomaliza Usultani wa Zanzibar. Rais wa kwanza alikuwa Abeid Amani Karume hadi mwaka 1972. Alifuatwa na Aboud Jumbe (1972-1984). Rais wa tatu aliyemfuata alikuwa Ali Hassan Mwinyi (1984-1995) aliyeendelea kuwa rais wa Tanzania tangu 1985. Rais Amani Abeid Karume ambaye ni mwana wa rais wa kwanza na alikuwa mgombea wa CCM alichaguliwa mara ya pili na wananchi wote tarehe 30 Oktoba 2005 katika kura iliyopingwa na chama cha upinzani CUF. Rais aliyefuata ni Ali Mohamed Shein (2010-2020), halafu Hussein Ali Mwinyi. Watu Watu wa Zanzibar ni wa asili mbalimbali, hasa watu wa asili ya Afrika Bantu, yakiwemo makabila ya Wahamidu na Watumbatu; halafu Waasia, awali kutoka India na nchi za Kiarabu. Idadi ya wakazi wa Zanzibar ilikuwa 1,303,569 mwaka 2012, tarehe ya sensa ya mwisho, iliyoonyesha ongezeko la 3.1% kwa mwaka. Karibu theluthi mbili ya watu wanaishi katika kisiwa cha Zanzibar (Unguja). Mkoa wa mjini magharibi ndio wenye idadi kubwa ya wakazi, kiasi cha watu 205,870. Pemba ina jumla ya makazi sawa. Mji mkubwa ni Chake Chake, ukiwa na idadi ya 19,283, mengine ni Wete na Mkoani. Dini Dini ya Uislamu ina kiasi cha 97% za wananchi wote. Waliobaki ni hasa Wakristo. Wa kwanza walikuja wakati wa utawala wa Kireno, halafu wakati wa masultani kuwepo Zanzibar na wa ukoloni wa Uingereza. Kulikuwa na Wahindu pia lakini wengi wao walikimbia nchi au kuuawa wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964. Kuna misikiti 51, ambayo waadhini wake hugongana wakati wa maombi, pamoja na mahekalu ya Uhindu sita na makanisa kadhaa, yakiwemo Kanisa Kuu Katoliki na Kanisa Kuu la Anglikana katika mji wa Zanzibar Stonetown. Hasa hilo la mwisho ni maarufu kwa sababu lilijengwa mahali pa soko la watumwa lililofungwa, altari ikiwa imejengwa juu ya nafasi ya mti wa kuwafunga watumwa walioadhibiwa kwa viboko, na batizio kuwa mahali walipotupwa watoto watumwa ambao hawakuuzwa pamoja na mama zao. Hata hivyo makanisa kadhaa yalichomwa moto katika miaka 2005-2015. Afya Upande wa huduma ya afya, vifo vya watoto wachanga bado ni 83 kati ya wazaliwa 1000, na inakadiriwa kuwa utapiamlo huathiri mmoja katika watu watatu wa visiwa. Matarajio ya maisha wakati wa kuzaliwa ni miaka 48, wakati maambukizi ya VVU / UKIMWI ni madogo sana kwa Zanzibar kuliko Tanzania kwa ujumla (0.6% ya idadi ya watu dhidi ya wastani wa kitaifa wa 8%). Uchumi Uchumi wa Zanzibar unategemea kilimo na utalii. Mazao yanayouzwa nje ni hasa karafuu, basibasi, mdalasini na pilipili. Uchumi wa Zanzibar ni uchumi duni kabisa ambao mwananchi wa kawaida anaishi kwa kiasi cha chini ya dola moja kwa siku au hana uhakika wa kupata chochote. Wastani wa mapato ya kila mwaka ya US $ 250 na ukweli kwamba karibu nusu ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Lakini kuna tofauti kubwa katika kiwango cha maisha kati ya wakazi wa Pemba na Unguja, tena kati ya wakazi wa mijini na vijijini. Hilo linatokana na viongozi kutoonesha mori katika kutatua matatizo au kuweka mbinu za kuleta maendeleo, badala yake ni kujadili siasa kwa muda mwingi. Zanzibar ni nchi yenye matumaini katika uchumi lakini, kutokana na migogoro ya kisiasa, imekuwa katika hali duni kabisa, na mabalozi wa Marekani na nchi nyingine walisisitiza mara nyingi umuhimu wa kuwepo ushirikiano katika siasa ili kuiwezesha Zanzibar kuinuka katika hali ya uchumi. Viungo vya nje www.tanzabradford.webs.com/umoja wa watanzania Bradford www.tzgr.ewebsite.com/Umoja wa Watanzania Greece Tovuti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Takwimu Picha za Zanzibar Ramani ya Zanzibar na Tanganyika 1886 Makala ya BBC kuhusu bendera mpya Historia na utamaduni wa Zanzibar Zanzibar links Zanzibar Network kwa Utalii wa Ushirika - NGO Umoja Tanzania Zanzibar
2007
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tsunami
Tsunami
Tsunami ni wimbi kubwa sana katika bahari linalosababishwa na tetemeko la ardhi, mlipuko wa volkano au matokeo mengine yanayoleta mshtuko wa ghafla chini ya maji. Mshtuko huo unasababisha kutokea kwa wimbi kali linaloanza kupaa juu likifika katika maji kame na kwenye ufuko wa bahari. Neno tsunami linatokana na lugha ya Kijapani likimaanisha "wimbi la bandarini". Tsunami huweza kutokea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Wakati mwingine inaweza kutokea bila kuleta madhara yoyote. Tsunami ya Krismasi 2004 Tsunami ya Krismasi 2004 ilikuwa mojawapo kati ya maafa makubwa yaliyotokea katika historia ya dunia yetu iliyoua malakhi ya watu huko Asia Kusini na kuleta madhara hadi pwani ya Afrika ya Mashariki. Tarehe 26 Desemba 2004 lilitokea tetemeko la ardhi chini ya Bahari Hindi karibu na pembe ya kaskazini ya Sumatra kwenye mstari ambako bamba la Uhindi linajisukuma chini ya bamba dogo la Burma. Siku ile km 1,200 za pembizo la bamba la Uhindi zilisogea mbele katika muda wa dakika chache kwa urefu wa takriban mita 15 chini ya bamba la Burma. Bamba la juu lilisukumwa na kupaa juu hadi mita 30. Mshtuko huo ulianzisha wimbi kubwa chini ya bahari lililotoka juu kwa umbo la tsunami iliyoua takriban watu 275,000. Katika maji marefu ya bahari wimbi halikuwa na hasara likaonekana kuwa na cm 30 pekee. Lakini ilifika mwambaoni kwenye maji kama likaanza kupaa juu kufikia hadi m 30. Kutoka kitovu cha tetemeko la ardhi mawimbi ya tsunami yalienea kotekote. Yalipiga vikali sana pwani za Indonesia, Sri Lanka, Thailand na India. Mawimbi yalifikia hadi pwani ya Afrika na kusababisha vifo Somalia, Kenya, Tanzania na Afrika Kusini. Athari za tsunami kwa afya Baada ya kuokoa watu, jambo la msingi kwa afya ya umma ni kusafisha maji ya kunywa, chakula, makazi, na utunzaji wa majeraha. Maji ya mafuriko yanaweza kuleta hatari za kiafya kama vile maji na vyakula vilivyochafuliwa. Upotezaji wa makazi huwaacha watu katika hali ya kutangamana na wadudu, joto na hatari zingine za kimazingira. Vingi vya vifo vinavyohusiana na tsunami husababishwa na kuzama, lakini majeraha ya kisaikolojia ni tatizo la msingi pia. Majeraha kama vile kuvunjika mikono au miguu na majeraha ya kichwa husababishwa na athari za kimwili za watu wanaosukumwa na maji kwenye vifusi kama vile nyumba, miti na vitu vingine visivyosonga. Maji yanapopungua, uvutaji na uondoaji wa vifusi kwenye maeneo yaliyo na watu wengi unaweza kusababisha majeraha zaidi na kudhoofisha majengo na huduma. Utunzaji wa kimatibabu ni muhimu sana katika maeneo ambapo kuna huduma finyu ya afya. Madhara ya baadaye Mikasa ya kiasili haisababishi ongezeko la magonjwa ya kuambukiza katika mkurupuko. Hata hivyo, maji na vyakula vilivyochafuliwa na aidha ukosefu wa makazi na huduma ya afya vinaweza kuwa na madhara ya baadaye ya kukithiri kwa maradhi yaliyo kwenye sehemu iliyoathiriwa. Miili inayooza husababisha hatari ndogo sana ya mkurupuko mkuu wa ugonjwa. Watu walio hatarini zaidi ni wale wanaoshughulikia miili au kuiandaa kwa mazishi. Athari za mkasa hudumu kwa muda mrefu. Mahitaji makuu ya kifedha huwa miezi ya mkasa, yakiwemo: ukaguzi na ufuatiliaji wa magonjwa ya kuambukiza na yanayosambazwa na maji au nzi; ugeuzaji wa vifaa vya matibabu kutoka sehemu zisizoathiriwa ili kukidhi mahitaji ya sehemu zilizoathiriwa; udumishaji wa huduma za afya za kimsingi, mifumo ya maji, makazi, na ajira; na kusaidia jamii kurejea katika hali ya kawaida kisaikolojia na kijamii baada ya mkasa. Usalama wa chakula baada ya tsunami Ili kuzuia magonjwa yanayotokana na chakula, nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kula au kutayarisha chakula na baada ya kutumia choo au bafu. Iwapo huna maji safi, tumia visafisha mikono visivyo na maji hadi maji safi yatakapopatikana. Usile chakula chochote ambacho hakijahifadhiwa kwenye vyombo visivyoingiza maji (vyombo vya mikebe au vya plastiki vilivyofungwa) na kile ambacho huenda kimetangamana na maji yasiyotibiwa, kama vile maji ya bahari, mafuriko, mto au dimbwi. Tupa chakula chochote kilicho katika mikebe isiyofungwa au inayoingiza maji ambacho kimetangamana na maji yasiyotibiwa. Vyakula vya mikebe ambavyo havijaharibika vinaweza kuokolewa. Ondoa vitambulisho kwenye mikebe, safisha sehemu ya nje ya mikebe hiyo kwa maji ya sabuni, na uue viini kikamilifu kwenye mikebe hiyo kwa mchanganyiko wa kikombe 1 (aunsi 8; takribani lita 0.25) cha klorini (asilimia 5.25) katika galoni 5 (takribani lita 19) za maji safi yaliyotibiwa. Tumia kalamu kuandika yaliyomo na tarehe ya kuharibika kwenye mikebe hiyo. Iwapo mikebe ya chakula iliyofunguliwa ina vifuniko vyenye hesi, meno, vilivyokunjwa (vifuniko vya chupa za soda), vilivyopinda, au vya kubingirika, au ikiwa imetengenezwa nyumbani, itupe ikiwa imetangamana na maji ambayo hayajatibiwa. Haiwezi kutiwa kiua viini. Ikiwa hunyonyeshi, katika kulisha watoto wachanga tumia chakula cha mtoto kilichotengenezwa na kuhifadhiwa mikebeni kisichohitaji kuongezwa maji. Ikiwa barafu kavu itapatikana, inaweza kutumiwa kudumisha ubaridi wa chakula — pauni 25 (takribani kilogramu 11.5) za barafu kavu zitadumisha friza ya futi 10 (lita 283) chini ya kiwango cha kuganda kwa siku 3 hadi 4. Kuwa makini unaposhughulikia barafu kavu, kwa sababu hugandisha kila inachogusa. Vaa glavu kavu na nzito ili kuepuka majeraha. Barafu kavu inapoyeyuka hubadilika kutoka hali ngumu na kuwa gesi. Pitisha hewa safi (ondoa hewa) kwenye magari au vyumba unaposafirisha, kuhifadhi au kutumia barafu kavu. Bila kupita kwa hewa safi, gesi inayotoka kwenye barafu inayoyeyuka inaweza kuongezeka polepole na kusababisha madhara, yakiwemo kupoteza fahamu na kifo. Tatizo la maji baada ya tsunami Tsunami inaweza kutengeneza mbingiriko wa maji ya bahari ambayo inaweza kutapakaa sehemu kubwa ya kijiografia. Maji ya bahari yakiendelea kusongea ufuoni, maji ya kunywa ya visima yanaweza kuzamishwa na kuweza kuchafuliwa na vidubini (bakteria, virusi, parasiti) na kemikali ambazo zinaweza kuathiri afya ya binadamu. Chumvi ya baharini inayohusishwa na maji ya chumvi inayofurika maji ya kunywa ya pwani si tishio la haraka kwa afya. Kwa sababu ya ladha mbaya ya maji ya chumvi, watu wengi hawawezi kumeza (kunywa) maji mengi: hiyo itasababisha shida za afya mara moja. Hata hivyo, ugonjwa unaosababisha vidubini husambaa kupitia mafuriko kwa kawaida huwa haitoi ladha nzito. Ikiwa maji yaliyona ugonjwa-yanayosababisha vidubini yatanyiwa, hata kwa kiwango kidogo, inaweza kusababisha shida za afya kwa maisha kama vile uharishaji ulio sugu, kipindupindu, na maambukizi hatari. Matumizi ya maji chafu kusafisha vidonda yanaweza kuleta maambukizi hatari. Zaidi ya hayo, uchafu wa kemikali unaopatikana katika mafuriko ya maji unaweza kuchafua visima kwa urahisi. Uchafu wa kemikali unaweza kujumuisha bidhaa za fueli kutoka kwa tangi za fueli zilizoanguka, au dawa za kuua wadudu ambazo zimehifadhiwa katika meneo ya mafuriko. Ukinywa maji yaliyo na aina hii ya uchafu wa kemikali inaweza kuwa hatari kwa afya na maisha. Baada ya visima kusafishwa vizuri na kuanza kujaza maji kutoka kwa mpenyo wa mwamba, kiwango kikubwa cha chumvi (kuwa na chumvi nyingi) unapaswa kupungua. Visiwa vifupi vinaweza kuathiriwa zaidi kuliko visima vyenye kina ndefu kwa sababu ya kuwepo kwa maji ya chumvi katika eneo la juu ya udongo. Ingawa kuanza upya kwa visima vinaweza kuwa pole pole kuliko ile ya visima vyenye kina ndefu, kuwepo kwa chumvi kwa visima vinapaswa kuwa kidogo kwa muda. Baada ya tsunami, watu katika sehemu zilizoathirika wanapaswa kusikiza matangazo ya umma kuhusu usalama wa kupeana maji. Visima vya kibinafsi vilivyofurika vinapaswa kuchunguzwa na kusafishwa baada ya maji ya mafuriko kupungua. Ikiwa harufu mbaya, ladha na rangi isiyo kuwa ya kawaida, au matokeo ya awali ya uchunguzi wa maji yatafanya watu washuku kuwa visima vya eneo hilo vimechafuliwa na fueli, dawa ya kuua wadudu, au hata kemikali zingine, uchunguzi wa kemikali ya maji ya kunywa unahitaji sana. Maswali kuhusu uchunguzi yanapaswa kutolewa kwa viongozi wa eneo hilo. Maji mazuri ya kunywa, kupikia, na usafi wa kibinafsi inajumuisha maji yaliyowekwa kwa chupa, chemshwa, au kutibiwa. Baada ya tsunami, asili ya maji yanaweza kuchafuliwa na maji ya chumvi. Ukitumia maji ya chumvi (mchanganyiko wa maji ya chumvi na maji isiyotiwa chumvi) kwa kunywa na kupika kwa muda mrefu yanaweza kusababisha shida za afya kutoka kwa viwango vya juu ya chumvi yanayoweza kunyiwa. Viongozi wa eneo lako wanaweza kupanga mapendekezo maalum kwa uchemshaji na uwekaji wa kemikali maji katika eneo lako. Ukipata maji kutoka kwa tangi la maji au kisima, tafadhali rejelea ujumbe wa kusafisha matangi ya maji au visima. Usipopata maji kutoka kwa tangi la maji au kisima, fuata sheria hizi kuhusiana na maji ya kunywa, kupikia, na usafi wa kibanfsi. Mashauri muhimu Usitumie maji yaliyochafuliwa kuosha vyomba, kusugua meno, kuosha na kutayarisha chakula, kuosha mikono, kutengeneza barafu au kutayarisha fomyula ya mtoto. Ikiwezekana, tumia fomyula ya mtoto isiyohitaji kuongezwa maji. Unaweza kutumia kisafisha mikono chenye alkoholi ili kuosha mikono. Ikiwa utatumia maji ya chupa, hakikisha kuwa yametolewa katika chanzo salama. Ikiwa hujui iwapo maji hayo yalitolewa kwenye chanzo salama, unapaswa kuyachemsha au kuyatibu kabla ya kutumia. Tumia maji ya chupa, yaliyochemshwa au yaliyotibiwa tu hadi maji ya chanzo chako yatakavyochunguzwa na kupatikana kuwa salama. Kuchemsha maji, kunapowezekana, ndiyo njia bora zaidi ya kuua bakteria na parasiti. Kuchemsha maji kwa dakika 1 kutaua vimelea vingi. Hata hivyo, kuchemsha maji ya chumvi kwa zaidi ya dakika 5 kunaweza kuongeza kukolea kwa chumvi za bahari na vichafuzi vingine. Iwapo hautaweza kuchemsha maji, unaweza kuyatibu kutumia tembe za klorini, aidini au dawa ya klorini ya nyumbani isiyo na harufu (asilimia 5.25 ya sodium hypochlorite): Ukitumia tembe za klorini au aidini, fuata maagizo yanayokuja na tembe hizo. Ukitumia dawa ya klorini ya nyumbani, ongeza 1/8 ya kijiko cha chai (takriban mililita 0.75) ya klorini kwa kila galoni ya maji ikiwa maji haya ni safi. Kwa maji yasiyo safi, ongeza 1/4 ya kijiko cha chai (takriban mililita 1.50) ya klorini kwa kila galoni. Changanya mmumunyo huu kikamilifu kisha uuache kwa dakika 30 kabla ya kutumia. Fahamu: Kutibu maji kwa tembe za klorini, aidini au dawa ya majimaji hakutaua parasiti. Tumia mmumunyo wa dawa ya klorini kukamua vyombo vya maji kabla ya kuvitumia tena. Tahadhari unapotumia tangi za kuhifadhi maji na aina zingine za vyombo. Kwa mfano, tangi za maji za zimamoto na makopo au chupa zilizotumika awali huenda zimechafuliwa na mikrobu au kemikali. Usitegemee matumizi ya vyombo ambavyo havijajaribiwa vya kusafisha maji. Kuua viini vya maradhi kwenye Matangi ya Maji na Mifumo Mingine ya Kunasa Maji ya Mvua Baada ya Mafuriko Katika maeneo mengi ulimwenguni, watu hupata maji ya kunywa kwenye mifumo ya kunasa (kukusanya) maji ya mvua na kuyahifadhi. Hata inapotengenezwa na kutumika inavyofaa, mifumo hii huchafuliwa kwa urahisi na viinitete vinavyoweza kusababisha magonjwa. Baadhi ya mifumo ya kusambaza maji hutumia sehemu kama vile paa ili kukusanya maji na kuyaelekeza kwenye tangi la maji (tangi la kuhifadhi). Ikiwa hupati maji yako kutoka kwa tangi au kisima, rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na Usafi wa Kibinafsi kwa habari kuhusu kuua viini kwenye maji yako. Maji ya matangi ya maji na mifumo sawa yanapotangamana na maji ya mafuriko, watu wanapaswa kuchukulia kuwa maji yao ya kunywa yamechafuliwa. Ikiwa unasikitika kuhusu kuchafuliwa kwa chanzo cha maji yako ya kunywa, tafadhali rejelea Maji ya Kunywa, Kupika, na Usafi wa Kibinafsi kuhusu uchafuzi wa maji chumvi, uchafuzi wa kemikali na athari za kiafya. Moja ya mbinu zifuatazo inaweza kutumika kuua viini kwenye matangi ya maji na mifumo mingine ya kunasa maji ya mvua katika hali za mikasa kwa kuzingatia iwapo chanzo cha maji ya kunywa kinapatikana tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unasafishwa (Mbinu ya 1) au iwapo tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unahitaji kutumika kwa haraka zaidi kama chanzo cha maji ya kunywa (Mbinu ya 2). Iwapo bidhaa za fueli au vichafuzi vingine vya kemikali vimetangamana na tangi la maji au mfumo wa kunasa maji ya mvua, au iwapo kuna harufu ya fueli au kemikali zingine katika mazingira karibu na mfumo huo, tumia tu Mbinu ya 1 kwa uuaji viini. Mbinu ya 1—Tumia mbinu hii ikiwa maji safi ya kunywa yanapatikana kutoka kwenye chanzo kingine tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unaposafihshwa. Mbinu hii ni bora, lakini huchukua muda mrefu zaidi, kwani tangi la maji/mfumo ni lazima utolewe maji yote na kujazwa tena mara mbili. Safisha kikamilifu sehemu ya kunasa maji (kwa mfano, paa) na uondoe vifusi vyote. Ondoa maji kwenye tangi la maji kikamilifu. Ondoa vifusi vyote kwenye tangi. Bila kuingia kwenye tangi, sugua sehemu ya ndani vizuri iwezekanavyo kwa brashi dhabiti au ufagio na mmumunyo wa kikombe 1 (aunsi 8; takriban lita 0.25) wa asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu (sodium hypochlorite) katika galoni 10 (takriban lita 38) za maji. Jaza tena tangi hilo kwa maji ya mvua au kutoka kwenye chanzo kingine. Iwapo hufahamu kiasi cha tangi, tumia fomyula ifuatayo kutambua kiasi cha maji linachoweza kuhifadhi: Kwa tangi la umbo la mstatili, zidisha kina cha tangi (katika futi) kwa urefu (katika futi) na kwa upana (katika futi), kisha uzidishe matokeo kwa 7.5 ili kupata idadi ya galoni zitakazojaza tangi hilo. Kwa tangi la mviringo, zidisha urefu (katika futi) kwa matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe, zidisha matokeo kwa 3.14, na kisha uzidishe matokeo hayo kwa 7.5 ili kupata galoni. Ikiwa hakuna mbinu kati ya hizi inayoweza kutumika, unaweza kukadiria kiasi kwa galoni kwa kufanya "kisio la kidhahania," kisha uzidishe kiasi cha dawa itakayotumika mara mbili katika mmumunyo wa kuua viini. Kipimo kwa mita: Katika vipimo vya mita, zidisha urefu (mita) X upana (mita) X kina (mita) X 1,000 = kiasi katika lita. Kwa matangi ya mviringo, zidisha kina X matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe (mita) X 3,140 = kiasi katika lita. Ongeza vikombe 4 (aunsi 32; takribani lita 1) vya asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu kwa kila galoni 100 (takribani lita 380) za maji katika tangi. Hii inapaswa kukupa ukolezi wa klorini wa takribani sehemu 100 kwa kila milioni. Fungua maji kwenye paipu zote zinazotumika kwa maji ya kunywa nyumbani kwako hadi utakapotambua harufu kali ya klorini. Wacha mmumunyo huo utulie kwa saa 24. Ondoa maji yote kwenye tangi. Jaza tangi kwa maji ya mvua au ulijaze kwa maji yanayoweza kunyweka. Foka paipu zote za nyumbani kwako hadi harufu ya klorini itakapoisha kabisa kabla ya kuanza kutumia mfumo huu tena. Mbinu ya 2— Tumia mbinu hii ikiwa maji safi ya kunywa yanapatikana kutoka kwa asili nyingine wakati tangi/mfumo unaambukuliwa. Mbinu hii si bora kama ilivyo Mbinu ya 1, lakini huchukua muda mfupi kwani tangi/mfumo unahitaji kutolewa maji na kujazwa tena mara moja tu. Safisha kikamilifu sehemu ya kunasa maji (paa) na utoe vifusi vyote. Iwapo haufahamu kiasi cha tangi, tumia fomyula ifuatayo kutambua kiasi cha maji kinachoweza kuwekwa ndani ya tangi: Kwa tangi la mstatili, zidisha kina cha tangi (katika futi) kwa urefu (katika futi) na kwa upana (katika futi), kisha uzidishe matokeo na 7.5 ili kupata idadi ya galoni. Kwa tangi la mviringo, zidisha urefu (futi) kwa matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo kwa chenyewe, zidisha matokeo kwa 3.14, kisha uzidishe matokeo hayo kwa 7.5 ili kupata idadi ya galoni zinazoweza kulijaza. Ikiwa hakuna mbinu kati ya hizi inayoweza kutumika, unaweza kukadiria kiasi kwa galoni kwa kufanya "kisio la kidhahania," kisha uzidishe kiasi cha dawa itakayotumika mara mbili katika mmumunyo wa kuua viini. Kipimo kwa mita: Katika vipimo vya mita, zidisha urefu (mita) X upana (mita) X kina (mita) X 1,000 = kiasi katika lita. Kwa matangi ya mviringo, zidisha kina X matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe (mita) X 3,140 = kiasi katika lita. Ongeza vikombe 4 (aunsi 32; takribani lita 1) vya asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu kwa kila galoni 100 (takribani lita 380) za maji katika tangi. Hii inapaswa kukupa ukolezi wa klorini wa takribani sehemu 100 kwa kila milioni. Fungua maji kwenye paipu zote zinazotumika kwa maji ya kunywa nyumbani kwako hadi utakapotambua harufu kali ya klorini. Wacha mmumunyo huo utulie kwa saa 24. Ondoa maji yote kwenye tangi. Ondoa vifusi vyote kwenye tangi. Bila kuingia kwenye tangi, sugua vizuri sehemu ya ndani ya tangi kwa brashi dhabiti au ufagio na mmumunyo wa kikombe 1 (aunsi 8; takriban lita 0.25) wenye asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu (sodium hypochlorite) katika galoni 10 (takribani lita 380) za maji. Ondoa mmumunyo wote wa kiua viini kwenye tangi. Jaza tena tangi kwa maji. Foka paipu zote za nyumbani kwako hadi harufu ya klorini itakapoisha kabisa kabla ya kuanza kutumia mfumo huu tena. Kuua viini kwenye visima Baada ya tsunami, huenda visima katika maeneo yaliyoathiriwa vikawa vimechafuliwa. Tafadhali rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na ya Usafi wa Kibinafsi kuhusu uchafuzi wa maji chumvi, uchafuzi wa kemikali na athari za afya. Iwapo unashuku kuwa kisima chako kimechafuliwa, wasiliana na mamlaka za eneo lako kwa ushauri mahususi zaidi. Iwapo haupati maji yako kutoka kwa tangi au kisima, rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na ya Usafi wa Kibinafsi kwa habari kuhusu kuua viini kwenye maji yako. Yafuatayo ni baadhi ya maagizo ya jumla ya kuua viini kwenye visima. Kuua viini kwenye Visima Vilivyotobolewa au Vilivyochimbwa Vuta maji yote kutoka kwa kisima. (Fahamu: Katika sehemu zisizo na nguvu za umeme, jenereta ya kubeba inaweza kuhitajika kuendesha pampu.) Tumia mifereji ya nje kuondoa maji kwenye kisima iwapo inapatikana. Tumia Jedwali 1 kukokotoa kiasi cha dawa ya klorini (kimiminiko au chembe) cha kutumia. Ili kubainisha kiasi kamili cha kutumia, zidisha kiasi cha kiua viini kinachohitajika (kulingana na kipenyo cha kisima) na kina cha maji kwenye kisima hicho. Kwa mfano, kisima chenye kipenyo cha futi 5 huhitaji vikombe 4½ vya dawa ya klorini kwa kila futi ya maji. Iwapo maji katika kisima hicho ni futi 30 kwenda chini, zidisha vikombe 4½ na futi 30 ili kubainisha idadi kamili ya vikombe vya dawa ya klorini vinavyohitajika (4½ X 30 = vikombe 135). Mfumo wa mita: Katika mfumo wa mita, kisima chenye kipenyo cha takribani mita 1.5 huhitaji takribani lita 1.1 za dawa ya klorini kwa kila mita ya maji. Iwapo kisima ni takribani mita 9.1 kwenda chini, zidisha lita 1.1 na mita 9.1 ili kubainisha idadi kamili ya lita za dawa klorini itakayohitajika (1.1 X 9.1 = lita 10). Futi moja ya urefu wa maji = mita 0.305. Weka idadi hii kamili ya kiasi cha kiua viini katika galoni 10 za maji (lita 38). Rashia mchanganyiko huu kwenye ukuta au bitana ya kisima. Hakikisha kuwa kiua viini hicho kinagusa sehemu zote za kisima hicho. Funga kabisa sehemu ya juu ya kisima hicho. Fungua mifereji yote na uvute maji hadi utakapotambua harufu nzito ya dawa ya klorini kwenye kila mfereji. Kisha simamisha pampu na uwache mmumunyo huo kwenye kisima kwa saa 24 au, kwa kiwango cha chini, usiku kucha. Siku itakayofuata, endesha pampu kwa kufungua mifereji yote, kuendelea hadi harufu ya klorini itakavyoisha. Weka sawa mtiririko wa maji kwenye mifereji au vyombo vinavyopeleka maji kwenye mifumo ya maji chafu iweze kutiririka polepole ili kuepuka kujaza mno mfumo wa utupaji. Kuua viini kwenye visima vilivyotoboka Foka kisima hadi maji yawe safi. (Fahamu: Katika maeneo yasiyo na stima, genereta inayoweza kusogezwa kutoka mahali pamoja hadi pengine itahitajika ili kutumia pampu.) Tumia mifereji ya nje kutoa maji kutoka kwa kisima ikiwa inapatikana. Tambua kiasi cha maji katika kisima kwa kuzidisha galoni kwa kila futi ya kina cha kisima kwa futi (Jedwali 2). Kwa mfano, kisima kilicho na kipenyo cha inchi 6 ina galoni 1.5 ya maji kwa kila futi. Ikiwa kina cha kisima hiki ni futi 120, zidisha 1.5 kwa 120 (1.5 X 120 = galoni 180). Kipimo cha mita: Katika kipimo cha mita, tambua kiasi cha maji kwenye kisima kwa kuzidisha lita kwa kila mita kwa kina cha kisima kwa mita. Kwa mfano, kisima chenye kipenyo cha sentimita 15.2 kina lita 18.6 za maji kwa kila mita. Ikiwa kina cha kisima hiki ni mita 36.5, zidisha lita 18.6 kwa mita 36.5 ili kutambua idadi jumla ya lita za maji katika kisima (18.6 X 36.5 = lita 679). Kwa kila galoni 100 (lita 380) za maji kwenye kisima, tumia kiasi cha klorini (aina ya maji au chembechembe) kama ilivyoashiriwa katika Jedwali 3. Changanya kiasi chote cha klorini ya maji au chembechembe na takriban galoni 10 (lita 38) za maji. Weka mmumunyo katika eneo la juu la kisima kabla ya kufunika. Unganisha mpira wa maji kutoka kwa mfereji ambapo maji hutokea kwa tangi kwa kifuniko cha kisima. Endesha pampu. Nyunyiza maji ndani ya kisima na uoshe pande za kifuniko kwa angalau dakika 15. Fungua mfereji yote katika mfumo na uache maji yapite hadi utakaponusa klorini. Kisha funga mifereji yote na uzibe sehemu ya juu ya kisima. Acha kisima kwa saa 24, au kwa muda mchache zaidi, usiku kucha. Baada ya kuacha maji ndani ya kisima, endesha pampu kwa kufungulia mifereji yote na kuendelea hadi harufu ya klorini inapoisha. Sawazisha mwendo wa mifereji ya maji au chombo kinachotoa maji hadi kwa mifumo ya maji machafu hadi kufukia mwendo wa polepole ili kuepuka kuweka shinikizo katika mfumo wa maji machafu. Usafi baada ya Tsunami Ni muhimu kukumbuka kutekeleza usafi wa kimsingi katika kipindi cha dharura. Osha mikono kila mara yako kwa sabuni na maji yaliyochemshwa au yaliyotiwa kiua viini. Maji yaliyochemshwa ndiyo bora zaidi. Mifano ya nyakati za kuosha mikono yako ni: kabla ya kutayarisha au kula chakula; baada ya kutumia choo; baada ya kushiriki katika shughuli za kushafisha baada ya mafuriko; na baada ya kushika vitu vilivyochafuliwa na maji ya mafuriko au maji taka. Maji safi yasipopatikana, unaweza kutumia bidhaa zenye spiriti zilizotengenezwa kwa ajili ya kuosha mikono. Maji ya mafuriko yanaweza kuwa na kinyesi kutoka kwa mifumo ya maji taka yanayoenea kwenye ardhi na mapato ya ziada ya kilimo na viwanda. Ingawa mgusano wa ngozi na maji ya mafuriko kwa wenyewe hauleti hatari kubwa ya afya, kuna hatari ya magonjwa kutokana na kula au kunywa chochote kilichochafuliwa na maji ya mafuriko. Ikiwa una vidonda wazi ambavyo vitatangamana na maji ya mafuriko, hakikisha umevisafisha vyema iwezekanavyo kwa kuviosha kwa sabuni ili kudhibiti maambukizi. Kidonda kikianza kuwa chekundu, kuvimba au kuwa na mtiririko, tafuta usaidizi wa kimatibabu mara moja. Isitoshe, wazazi wanahitaji kuwasaidia watoto kuepuka maradhi yanayoenezwa na maji. Usiwaruhusu watoto kucheza katika maeneo yenye maji ya mafuriko, osha mikono ya watoto mara nyingi (kila mara kabla ya kula) na usiwaruhusu kuchezea vinyago vilivyochafuliwa na maji ya mafuriko ambavyo havijatiwa kiua viini. Unaweza kutumia mmumunyo wa kikombe kimoja cha klorini katika galoni 5 za maji kwa kuua viini kwenye vinyago. Vinyago vingine kama vile wanyama waliojazwa nguo na vinyago vya watoto haviwezi kutiwa kiua viini; vinapaswa kutupwa. Tazama pia Madhara ya ongezeko la joto Duniani Bahari Maafa asilia Afya
2008
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanganyika%20African%20National%20Union
Tanganyika African National Union
Tanganyika African National Union (TANU) kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hiki na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar ulipounda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. TANU ilianzishwa 7 Julai 1954 kutokana na Tanganyika African Association (TAA). TAA ilikuwa na mwelekeo wa kitamaduni zaidi ya siasa. Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere. TANU ilishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961. Katiba ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini ikifuata mfano wa nchi za kijamaa zenye muundo wa siasa ya chama kimoja. Mtiririko wa upatikanaji uhuru Mtiririko wa kupigania uhuru wa Tanganyika na mchango wa Mwalimu katika kupigania uhuru: 1929: TAA yaundwa ikiwa na wajumbe wafuatao: Kleist Sykes Mzee bin Sudi Ibrahim Hamis Zibe Kidasi Ali Said Mpima Suleiman Majisu Raikes Kusi Rawson Watts Cecil Matola 1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kujenga mawasiliano na chama cha Kenya African Union (KAU). 1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la TAA; likiwa na wajumbe wafuatao: Abdulwahid Sykes (Katibu) Sheikh Hassan bin Amir Hamza Kibwana Mwapachu Said Chaurembo Dk. Kyaruzi. John Rupia Stephen Mhando 1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika Arusha. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, Dossa Aziz na Stephen Mhando. 1952: Abdulwahid alichaguliwa kuwa Rais wa TAA. 1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika. Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid. Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano. 1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU. Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Mohammed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate na Mwinjuma Mwinyikambi. Wengine walikuwa Rajab Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidar Mwinyimvua na Idd Faiz Mafongo. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia na Mashado Ramadhani Plantan. Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa. 1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, , Abubakar Ilanga na Saadan Abdu Kandoro. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia. Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine. Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi Titi Mohamed kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25. Tazama pia Kura Tatu TANU TANU
2009
https://sw.wikipedia.org/wiki/Benjamin%20Mkapa
Benjamin Mkapa
Benjamini William Mkapa (12 Novemba 1938 - 24 Julai 2020) alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM. Wasifu Mkapa alizaliwa Lupaso karibu na Masasi katika kusini-mashariki ya Tanganyika. Kuanzia 1945 hadi 1951 alsoma shule za msingi pale Lupaso na Ndanda. 1952/53 alisoma shule ya seminari ya Kigonsera akaendelea kwenye shule ya sekondari ya watawa Wabenedikto pale Ndanda hadi kumaliza O-level. 1958/59 alimaliza A-levels pale St Farncis, Dar es Salaam (leo hii Pugu Secondary). Alipokelewa kwenye Chuo Kikuu cha Makerere alipohitimu 1962. Hatua za maisha ya kazi Aprili 1962: Afisa tawala Dodoma Aprili 1962: Mkuu wa Wilaya Agosti 1962: alijiunga na Utumishi wa wizara ya mambo ya nje Mei 1966: Mhariri mkuu, gazeti la Uhuru Aprili 1972: Mhariri mkuu, Daily News Julai 1974: Afisa habari katika Ofisi ya Rais, Dar es Salaam Julai 1976: Mwanzilishi na mhariri mkuu wa Shirika la habari la Tanzania (SHIHATA) Oktoba 1976: Balozi wa Tanzania pale Nigeria Februari 1977: Waziri wa Mambo ya Wje Novemba 1980: Waziri wa Habari na Utamaduni Aprili 1982: Balozi wa Tanzania pale Kanada Februari 1983: Balozi wa Tanzania pale Marekani Aprili 1984: Waziri wa Mambo ya Nje 1990: Waziri wa Habari na Utangazaji Mei 1992: Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Novemba 1995: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais wa Tanzania Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kuuungwa mkono kwa nguvu na rais wa zamani Julius Nyerere . Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi. Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha kampuni zilizomilikiwa na serikali akaweka sera za soko huria. Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali. Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi vilevile matumizi mabaya ya fedha za umma. Utawala wake ulikuwa na matumizi sana na maposho bila kikomo. Alitumia £ 15 milioni kununua ndege ya binafsi ya kirais, vilevile karibu £ 30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalamu waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi. Ilikuwa juu ya ununuzi huo wa mwisho ndipo katibu wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania. Baada ya kutoka ofisini kwa kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa alikumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo. Kwa kujibinafsishia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu. Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007. Heshima na Tuzo Nishani Mnamo Desemba 7, 2019, alitunukiwa Nishani ya Heshima ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kuanzisha vyuo vikuu binafsi, hivyo kukifanya Chuo Kikuu cha Iringa kuwa chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini Tanzania wakati wa utawala wake. Shahada za Heshima Marejeo Viungo vya nje 2001 mahojiano na Public Broadcasting Station "Serikali ya Uingereza yagawanyika juu ya mfumo wa radar wa Tanzania" "Blair ashtumiwa juu ya mpango wa rada wa Tanzania" "Mpango wa rada wa Tanzania "upotezaji wa fedha" "Umiliki wa mradi wa nguvu ya makaa ya mawe ya Kiwira : Uhusiano wa Mkapa-Yona" "Rais mstaafu Benjamin Mkapa Kutunukiwa Nishani ya Heshima kwa Kuanzisha Vyuo Vikuu Binafsi Nchini Wakati wa Utawala Wake.1661870/ Benjamin Mkapa bio katika Tume ya Afrika Waliozaliwa 1938 Waliofariki 2020 Marais wa Tanzania Waliohudhuria Chuo Kikuu cha Makerere Chama Cha Mapinduzi
2010
https://sw.wikipedia.org/wiki/Reli%20ya%20Kenya-Uganda
Reli ya Kenya-Uganda
''Makala hii yaeleza habari za njia ya reli ya kihistoria kati ya Mombasa na Uganda. Kwa habari za Shirika ya Reli ya Uganda ya kisasa tazama Uganda Railways Corporation. Reli ya Kenya-Uganda ni jina kwa reli kati ya Mombasa na Kampala iliyojengwa na Waingereza kuanzia mwaka 1896. Mwanzoni ilijulikana kwa jina la "Reliya Uganda" tu. Reli hii ilisababisha Uingereza kutafuta utawala juu ya eneo ambako njia ya reli ilipita. Eneo hili lilikuwa baadaye koloni na nchi ya Kenya. Hali halisi njia ya reli hii ilijengwa katika Kenya pekee hadi ziwa Viktoria Nyanza ambako usafiri uliendelea kwa njia ya meli hadi Uganda. Tangu 1931 kulikuwa na nyongeza ya njia ya reli hadi Uganda yenyewe. Utanguliza wa kujenga reli Biashara ya Uganda Reli ilijengwa kwa sababu Kampuni ya Kifalme ya Uingereza kwa Afrika ya Mashariki IBEA (Imperial British East Africa Company) ilitaka kuboresha usafiri wa kwenda Uganda baada ya Uganda ilitangazwa nchi lindwa na Uingereza na kampuni ilitaka kuchukua nafasi hii ya kuanzisha mashamba ya kibiashara huko yasiyokuwa na faida bila usafiri wa kupeleka mazao kwenye masoko ya dunia. Mwenye kampuni ya IBEA William MacKinnon alianzisha biashara kati ya Mombasa na Uganda lakini safari hizi kwa magari ya maksai zilikuwa ngumu na ghali sana. MacKinnon alianza kushawishi Serikali ya Uingereza na kudai reli ijengwe. Awali serikali ya Uingereza ilisitasita kwa sababu faida ya kiuchumi haikuonekana pia Uingereza wakati ule haikupenda kuongeza idadi ya koloni zake ikipendelea kuwaachia watu binafsi na makampuni yao shughuli za kufungua masoko mapya katika nchi kama Uganda. Maeneo ambayo ni Kenya ya leo yalifikiriwa wakati ule kukosa thamani ya kiuchumi kabisa. Mashindano na Wajerumani Mipango hii ya kujenga biashara ya kampuni ilikuwa hatarini kutokana na uenezaji wa Ujerumani katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1890 mwakilishi wa kampuni kikoloni ya kijerumani Karl Peters alifaulu kusaini mapatano na Kabaka; wakati uleule Wajerumani walionekana kupanusha eneo la Witu kwenye pwani la Kenya na Somalia. Hapo serikali za nchi zote mbili ziliamua kumaliza mashindano kati ya makampuni haya kwa kuelewana juu ya mipaka ya maeneo katika Afrika kwa mapatano kati ya Uingereza na Ujerumani ya 1890. Azimio la kujenga reli na mwanzo wa Kenya Mkataba huu ulifanya shughuli za Afrika ya Mashariki kuwa rasmi chini ya serikali ya Uingereza. Kutokana na azimio hili Uingereza iliamua 1894 kuitangaza Uganda kuwa chini ya ulinzi wake na pia kujenga reli kama njia ya kuhakikisha utawala wake na kuweka msingi wa uzalishaji mali huko Uganda kwa ajili ya soko la dunia. Baada ya azimio la kujenga reli Uingereza iliona haja ya kulinda njia ya reli yenyewe hivyo ikatangaza eneo lote kati ya Mombasa na Uganda kuwa chini ya ulinzi wake kuanzia tar. 01.07.1895. Kwa njia hii mipango ya kujenga reli ilikuwa mwanzo wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza iliyokuwa Kenya baadaye. Ujenzi wa reli Mwezi wa Mei 1896 ujenzi ulianzishwa Mombasa chini ya uongozi wa mhandisi George Whitehouse. Alikuwa na bajeti ya BP 3,250,000. Kazi ilionekana ngumu sana kwa sababu ya maeneo magumu kama vile jangwa, kinamasi, milima, Bonde la Ufa na mtelemko wake, kwa ujumla zaidi ya 1000 km. Wafanyakazi kutoka Bara Hindi Waingereza waliamua kuchukua wafanyakazi kutoka Bara Hindi kwa sababu katika majaribio ya kwanza Waingereza hawakuelewana na wenyeji wa pwani ambao waliajiria awali. Kwa ujumla zaidi ya Wahindi 13,000 walichukuliwa kufanya kazi ya reli. Kwa jumla walitoka hasa katika mikoa ya Gujarat na Panjab, na lugha hizi zinatumika hadileo katika Afrika ya Mashariki. Wengi walikuwa wafanyakazi wa mkono,lakini wengine pia mafundi na makarani. Wengi walikufa kwa sababu ya ugumu wa kazi, magonjwa, ajali na wanyama witu kama vile simba walioitwa wala-watu wa Tsavo walioua wafanyakazi 135. Mwanzo wa Nairobi Mwaka 1899 reli ilifika eneo la Nairobi ya leo. Whitehouse aliamua kujenga hapa kambi kubwa kwa sababu mahali palikuwa na maji, tena takriban katikati ya Mombasa na Kampala, halafu kabla ya njia kupanda juu kwa milima inayoongozana na Bonde la Ufa. Kambi hii ilidumu ikawa mji wa Nairobi. Tar. 20.12.1901 reli imefika Port Florence (leo: Kisumu)ufukoni wa ziwa la Viktoria Nyanza. Kutoka hapa bidhaa zilipelekwa kwa meli hadi Port Bell / Kampala. Njia ya reli yenyewe ilifika Kampala mw. 1931 kutoka Nakuru. Mafanikio na matatizo Ni sawa kabisa kusema ya kwamba reli hii ilikuwa mwanzo na mbegu wa Kenya. Biashara ya Uganda haikuleta kabisa faida ya kiuchumi za kurudisha gharama za ujenzi lakini reli ilifungua sehemu kubwa za Kenya kwa ajili ya biashara ikawezesha kilimo ya kibiashara. Hivyo reli ilikuwa msingi kwa ajili ya mipango ya baadaye ya "White Highlands" ya kuunda koloni ya walowezi kama Afrika ya Kusini. Wahindi wengi walibaki wakawa mwanzo wa jumuiya ya Wakenya na Wauganda wenye asili ya kiasia. Gharama zilikuwa kubwa. Bajeti ya kifedha haikutosha kabisa iliongezeka mara mbili. Gharama za maisha zilikuwa nzito zaidi. Wafanyakazi wahindi walikuwa wa kwanza kulipa bei hiyo. Magonjwa yaliyokuja nao yalisababisha vifo vingi kati ya wenyeji hasa Wakikuyu; makabila kama Wanandi waliopinga ujenzi wa reli yalikandamizwa vikali na Waingereza. Viungo vya Nje History of the Uganda Railway Kenya Uganda Afrika ya Mashariki Usafiri wa Uganda Historia ya Kenya Historia ya Uganda
2011
https://sw.wikipedia.org/wiki/Port%20Bell
Port Bell
Port Bell ni mji mdogo karibu na Kampala/ Uganda ufukoni wa ziwa la Viktoria Nyanza. Jina la mji limetokana na Sir Hesketh Bell aliyekuwa kamishna (gavana) Mwingereza huko Uganda kuanzia mwaka. 1905-1909. Port Bell ni bandari kwa ajili ya Kampala. Feri zinatoka kwenda Jinja, Kisumu na Mwanza. Kuna viwanda kadhaa kama vile Kiwanda cha Bia cha Uganda Breweries; bia ya Bell Lager inatengenezwa hapa. Kuna pia kiwanda cha pombe kali aina ya Waragi na kiwanda cha chai. Miji ya Uganda Kampala Wilaya ya Kampala
2012
https://sw.wikipedia.org/wiki/Chad
Chad
Chad (pia: Chadi) ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger. Mji mkuu ni Ndjamena. Jiografia Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote . Kaskazini kuna milima ya Tibesti. Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20. Historia Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni hiyo. Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu. Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba. Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu. Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021. Watu Wakazi walikuwa 15,500,000 mwaka 2018. Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake: Kaskazini wako hasa watu walioathiriwa sana na utamaduni wa Uislamu (55% za wakazi wote, wengi wakiwa Wasuni). Mifano ni Waarabu (12.3%), Wafulbe, Wahaussa, Wazaghawa na wengineo. Wengi wao walikuwa wafugaji na sehemu ya makabila inaendelea hadi leo maisha ya kuhamahama. Kusini wako hasa watu wanaofuata Ukristo (41%, Wakatoliki wakiwa wengi kidogo kuliko Waprotestanti) au dini asilia za Kiafrika (1%) kama Wasara (27.7%). Wengi wao hulima. Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile. Lugha rasmi ni Kiarabu na Kifaransa. Tazama pia Orodha ya miji ya Chad Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Marejeo Alphonse, Dokalyo (2003); "Cinéma: un avenir plein d'espoir }}", 214. "Background Note: Chad". September 2006. United States Department of State. Bambé, Naygotimti (April 2007); "[http://www.cefod.org/spip.php?article915 Issa Serge Coelo, cinéaste tchadien: On a encore du travail à faire] [http://www.cefod.org/spip.php?article915 Issa Serge Coelo, cinéaste tchadien: On a encore du travail à faire] ", Tchad et Culture 256. Botha, D.J.J. (December 1992); "S.H. Frankel: Reminiscences of an Economist", The South African Journal of Economics 60 (4): 246–255. Boyd-Buggs, Debra & Joyce Hope Scott (1999); Camel Tracks: Critical Perspectives on Sahelian Literatures. Lawrenceville: Africa World Press. ISBN 0-86543-757-2 "Chad". Country Reports on Human Rights Practices 2006, 6 March 2007. Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor, U.S. Department of State. "Chad". Country Reports on Human Rights Practices 2004, 28 February 2005. Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor, U.S. Department of State. "Chad". International Religious Freedom Report 2006. 15 September 2006. Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor, U.S. Department of State. "Amnesty International Report 2006 ". Amnesty International Publications. "Chad" (PDF). African Economic Outlook 2007. OECD. May 2007. ISBN 978-92-64-02510-3 "Chad ". The World Factbook. United States Central Intelligence Agency. 15 May 2007. "Chad " (PDF). Women of the World: Laws and Policies Affecting Their Reproductive Lives – Francophone Africa. Center for Reproductive Rights. 2000 . Freedom of the Press: 2007 Edition. Freedom House, Inc. "Chad". Human Rights Instruments. United Nations Commission on Human Rights. 12 December 1997. "Chad". Encyclopædia Britannica. (2000). Chicago: Encyclopædia Britannica, Inc. "Chad, Lake". Encyclopædia Britannica. (2000). "Chad – Community Based Integrated Ecosystem Management Project" (PDF). 24 September 2002. World Bank. (PDF). Cultural Profiles Project. Citizenship and Immigration Canada. ISBN 0-7727-9102-3 "Chad Urban Development Project" (PDF). 21 October 2004. World Bank. "Chad: Humanitarian Profile – 2006/2007" (PDF). 8 January 2007. Office for the Coordination of Humanitarian Affairs. "Chad Livelihood Profiles" (PDF). March 2005. United States Agency for International Development. "Chad Poverty Assessment: Constraints to Rural Development" (PDF). World Bank. 21 October 1997. "Chad (2006) ". Country Report: 2006 Edition. Freedom House, Inc. . Country Analysis Briefs. January 2007. Energy Information Administration. "Chad leader's victory confirmed", BBC News, 14 May 2006. "Chad may face genocide, UN warns", BBC News, 16 February 2007. Chapelle, Jean (1981); . Paris: L'Harmattan. ISBN 2-85802-169-4 Chowdhury, Anwarul Karim & Sandagdorj Erdenbileg (2006); . New York: United Nations. ISBN 92-1-104540-1 Collelo, Thomas (1990); Chad: A Country Study, 2d ed. Washington: U.S. GPO. ISBN 0-16-024770-5 Dadnaji, Dimrangar (1999); East, Roger & Richard J. Thomas (2003); Profiles of People in Power: The World's Government Leaders. Routledge. ISBN 1-85743-126-X Dinar, Ariel (1995); Restoring and Protecting the World's Lakes and Reservoirs. World Bank Publications. ISBN 0-8213-3321-6 Gondjé, Laoro (2003); "[http://www.cefod.org/spip.php?article231 La musique recherche son identité] ", Tchad et Culture 214. "Chad: the Habré Legacy" . Amnesty International. 16 October 2001. Lange, Dierk (1988). "The Chad region as a crossroad" (PDF), in UNESCO General History of Africa – Africa from the Seventh to the Eleventh Century, vol. 3: 436–460. University of California Press. ISBN 978-0-520-03914-8 (PDF). . N. 3. September 2004. Macedo, Stephen (2006); Universal Jurisdiction: National Courts and the Prosecution of Serious Crimes Under International Law. University of Pennsylvania Press. ISBN 0-8122-1950-3 Malo, Nestor H. (2003); "[http://www.cefod.org/spip.php?article236 Littérature tchadienne : Jeune mais riche] ", Tchad et Culture 214. Manley, Andrew; "Chad's vulnerable president", BBC News, 15 March 2006. "Mirren crowned 'queen' at Venice", BBC News, 9 September 2006. Ndang, Tabo Symphorien (2005); " " (PDF). 4th PEP Research Network General Meeting. Poverty and Economic Policy. Pollack, Kenneth M. (2002); Arabs at War: Military Effectiveness, 1948–1991. Lincoln: University of Nebraska Press. ISBN 0-8032-3733-2 "Rank Order – Area ". The World Factbook. United States Central Intelligence Agency. 10 May 2007. "Republic of Chad – Public Administration Country Profile " (PDF). United Nations, Department of Economic and Social Affairs. November 2004. . Government of Chad. Spera, Vincent (8 February 2004); "Symposium on the evaluation of fishery resources in the development and management of inland fisheries". CIFA Technical Paper No. 2. FAO. 29 November – 1 December 1972. "". . UNESCO, Education for All. "http://www.crisisgroup.org/~/media/Files/africa/central-africa/chad/French%20translations/Chad%20Back%20towards%20War%20French.pdf " (PDF). International Crisis Group. 1 June 2006. Wolfe, Adam; , PINR, 6 December 2006. World Bank (14 July 2006). World Bank, Govt. of Chad Sign Memorandum of Understanding on Poverty Reduction. Press release. World Population Prospects: The 2006 Revision Population Database. 2006. United Nations Population Division. "Worst corruption offenders named", BBC News, 18 November 2005. Young, Neil (August 2002); An interview with Mahamet-Saleh Haroun, writer and director of Abouna ("Our Father"). Viungo vya nje Vya serikali Serikali ya Chad Official presidency site Chief of State and Cabinet Members Vingine Chad country study from Library of Congress Chad profile from the BBC News Key Development Forecasts for Chad from International Futures Chad Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa Nchi zinazotumia Kiarabu
2016
https://sw.wikipedia.org/wiki/Athi
Athi
Athi ni jina la mto katika kaunti ya Kitui, Kenya, Afrika Mashariki. Sehemu za mto hujulikana pia kwa majina ya Galana na Sabaki, kwa hiyo mto wote huitwa pia Athi-Galana-Sabaki. Ina urefu wa kilomita 390, na beseni lenye eneo la Km² 70,000. Mto wa Athi umeupatia jina lake mji wa Athi River karibu na Nairobi pia kwa kampuni ya Athi River Mining. Athi inaanza karibu na Nairobi ikielekea Bahari Hindi. Inapita Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki pia tambarare ya juu ya Yatta ilipotafuta njia yake kuvukia eneo kubwa la mawe ya kivolkeno. Baada ya maporomoko ya maji ya Lugard inapokea mto Tsavo ikibadilika jina lake. Mto unaitwa kuanzia hapa kwa jina la Galana. Kabla ya kufika katika Bara Hindi karibu na Malindi upande wa kaskazini jina linabadilika tena kuwa Sabaki. Tazama pia Mito ya Kenya Orodha ya mito ya kaunti ya Kitui Tanbihi Viungo vya nje Geonames.org Mito ya Kenya Mto Galana Bahari ya Hindi Kaunti ya Kitui
2017
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ludwig%20Krapf
Ludwig Krapf
Johann Ludwig Krapf (11 Januari 1810 – 26 Novemba 1881) alikuwa mmisionari wa kwanza wa Uprotestanti nchini Kenya katika karne ya 19 akatunga kamusi ya kwanza ya lugha ya Kiswahili. Masomo Ujerumani na Uswisi Krapf alizaliwa tarehe 11 Januari 1810 katika kijiji cha Derendingen karibu na Tübingen, eneo la Württemberg, Ujerumani wa Kusini-Magharibi katika familia ya wakulima wadogo Walutheri. Alisoma shule ya msingi kijijini kwake halafu shule ya sekondari Tübingen. Akiwa mwanafunzi alipenda sana masomo yote yaliyohusu jiografia na lugha. Pamoja na Kilatini na Kigiriki alisoma pia Kifaransa na Kiitalia. Alipokuwa na umri wa miaka 16 alitembelea mara ya kwanza nyumba ya Misioni ya Basel, Uswisi. 1827 – 1829 alijiunga na kozi ya kuandaa wamisionari huko Basel lakini hakupendezwa na maisha ya pamoja; akishikwa na wasiwasi kuhusu wito wake akarudi nyumbani na kuingia masomo ya teolojia katika Chuo Kikuu cha Tübingen. Krapf alimaliza masomo yake mwaka 1834. Vituo vya huduma kama mchungaji msaidizi na mwalimu vilifuata. Wakati ule alikutana na mmisionari aliyempa moyo kurudi Basel. Ethiopia 1837-1842 Mwaka 1836 alikutana na mwakilishi wa Church Missionary Society (CMS) aliyemkaribisha kufanya kazi na CMS. Misioni ya Basel ilimpa ruhsa akapokea wito wa kwenda Ethiopia. Krapf alianza mara moja kujiandaa akisoma Ge’ez (lugha ya Kale ya Ethiopia) na Kiamhari (lugha ya kisasa ya Wakristo katika nyanda za juu Ethiopia). 1837-1842 Krapf alifanya kazi ya umisionari huko Ethiopia. Mpango wa misioni ya CMS ilikuwa kuwaamsha Wakristo Waorthodoksi kwa matumaini ya kwamba watakuwa wenyewe wamisionari bora kwa wenzao Wapagani au Waislamu. Lakini Krapf hakuelewa vema Ukristo wa kiorthodoksi wa Waamhari. Alishindwa kuelewa maana ya liturgia, mila na desturi nyingi. Hakuelewa hasa kwa nini Wakristo Waorthodoksi walisoma Biblia katika lugha ya kale ya Ge’ez hata wasipoelewa lugha hiyo badala ya kutumia tafsiri ya Kiamahari aliyokuwa amefanya. Hivyo Krapf alijisikia amevutwa zaidi na Wagalla – hili ni jina la zamani za watu wanaojulikana leo kama Waoromo au Borana. Wagalla kwa jumla walikuwa wakifuata dini zao za kiasili, athira za kiislamu zikianza kuonekana. Krapf alijifunza lugha yao alianza kutafsiri sehemu za Agano Jipya katika Kigalla (Kioromo). Mwaka 1842 Krapf alipaswa kuondoka Ethiopia pamoja na wamisionari wengine wa Kiprotestanti, akiwa na ndoto ya kurudi na kufanya kazi kati ya Wagalla. Alikaa muda kidogo Kairo (Misri) akafunga ndoa, bibiarusi alikuwa amemfuata kutoka Ujerumani. Wakati ule kwake nyumbani Tübingen Chuo Kikuu kilikuwa kimefuata taarifa zake na 1842 kikampa cheo cha udaktari (PhD) kwa ajili ya utafiti wake katika lugha na historia ya Ethiopia. Afrika ya Mashariki 1844-1853 Ethiopia ilikuwa imefunga milango yake, hivyo Krapf aliwaza njia nyingine. Alikuwa amesikia ya kuwa Wagalla waliwahi kufika hadi pwani za Afrika ya Mashariki. Hivyo akasafiri hadi Zanzibar kwa lengo la kuwafikia Wagalla kupitia eneo la Kenya ya leo. Sultani Seyyed Said alimpa ruhusa ya kuanzisha kituo cha misheni huko Mombasa. Mwaka 1844 Krapf alifika Mombasa akianza mara moja kujifunza Kiswahili pamoja na lugha ya wazalendo wa eneo la Mijikenda. Huko mke na mtoto waliugua malaria wakafa. Krapf alihamia Rabai iliyoko katika vilima juu ya Mombasa penye joto kidogo akaanzisha kituo cha Rabai Mpya. Mwaka 1846 mmisionari mwingine (Johannes Rebmann) alikuja kufanya kazi pamoja naye. Huko Rabai Mpya Krapf alitunga kamusi na sarufi ya kwanza ya Kiswahili. Krapf na Rebmann walikuwa Wazungu wa kwanza walioona milima yenye theluji Afrika. Rebmann aliona Kilimanjaro, Krapf aliona Mlima wa Kenya. Taarifa zao zilipofika Ulaya zilichekwa na wataalamu waliodai milima yenye theluji haiwezekani Afrika. Krapf aliendelea kuwa na matatizo ya afya akarudi Ujerumani mwaka 1853. Urithi wake Hadi kifo chake aliendelea kuboresha vitabu vyake kuhusu utamaduni na lugha za mataifa mbalimbali ya Afrika. Kwa jumla aliandika kamusi au kutafsiri sehemu za Biblia katika lugha zifuatazo: Ge’ez, Kiamhari, Kioromo, Kiswahili, Ki-mijikenda, Kikamba, Kimasai. Ludwig Krapf alitoa mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kwani aliweza kutafsiri Injili ya Luka na ya Mathayo ,pia aliweza kuandika sarufi ya Kiswahili inayohusu jamii ya Wasambaa. Nyumba yake huko New Rabai imekuwa makumbusho chini ya Museums of Kenya. Jengo la Ubalozi wa Kijerumani huko Nairobi limepewa jina lake. Krapf alikuwa Mlutheri, lakini Kanisa Anglikana linamkumbuka kama mwanzilishi wa madhehebu yake nchini Kenya. Marejeo Krapf, Ludwig: A dictionary of the Suahili language, London 1882 Raupp, Werner: Gelebter Glaube. Metzingen/Württemberg 1993, 278 - 287: "Johann Ludwig Krapf - Bahnbrecher der ostafrikanischen Mission". Gütl, Clemens. 2001. Johann Ludwig Krapf - "Do' Missionar vo' Deradenga" zwischen pietistischem Ideal und afrikanischer Realität. Hamburg, 2001 (Beiträge zur Missionswissenschaft und interkulturellen Theologie, Bd. 17); ISBN 3-8258-5525-2. Gütl, Clemens: "Memoir on the East African Slave Trade" ya Johann Ludwig Krapf aliyoiandika mwaka wa 1853 bila kuichapisha rasmi. Imetolewa na Gütl pamoja na maelezo katika jarida. Vienna, 2002 (Beiträge zur Afrikanistik, 73). Eber, Jochen: Johann Ludwig Krapf: ein schwäbischer Pionier in Ostafrika. Riehen/Lahr 2006. Raupp, Werner: Johann Ludwig Krapf. Missionar, Forschungsreisender und Sprachforscher. 1810–1881. In: Gerhard Taddey, Rainer Brüning (Hrsg.): Lebensbilder aus Baden-Württemberg, Band 22. Stuttgart 2007, (182) - 226. Raupp, Werner: Johann Ludwig Krapf, "dr Missionar vo Deradinga". In: Hin und weg. Tübingen in aller Welt. Hrsg. von Karlheinz Wiegmann. Tübingen 2007 (Tübinger Kataloge, 77), (90) - 99. Raupp, Werner: Morgenroth des Reiches Gottes. In: Tübinger Blätter'' 96 (2010), 70 - 73. Watu wa Ujerumani Wamisionari Kiswahili
2018
https://sw.wikipedia.org/wiki/Komori
Komori
Komori (kwa Kiswahili pia: Visiwa vya Ngazija; kwa Kikomori: قمر, Komori, kwa Kifaransa: Comores) ni nchi huru kwenye funguvisiwa katika Bahari Hindi upande wa Mashariki wa Afrika. Iko katika Kanali ya Msumbiji kaskazini kwa Madagaska na mashariki kwa Msumbiji. Jina limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo Juzur al-Qamar (جزر القمر) linamaanisha "visiwa vya mwezi". Katika Afrika iko kati ya nchi tatu ndogo kabisa. Pesa: 1 Frank ya Komori (FC) = 100 centimes. 1€ = 491,9677 FC Sikukuu ya Taifa: 4 Julai Jiografia Komori ina visiwa vitatu vikubwa: Grande Comore (Ngazidja), Anjouan (Nzwani) na Moheli (Mwali). Kisiwa cha Mayotte ni sehemu ya funguvisiwa kijiografia lakini kisiasa ni sehemu ya Ufaransa kwa sababu wakati wa kupata uhuru watu wa Mayotte walitamka kwa kura nyingi (73%) ya kwamba wanataka kukaa na Ufaransa. Lakini Komori inadai ni sehemu ya eneo lake. Komori ni sehemu ya bara la Afrika. Ina pia visiwa mbalimbali vidogo. Hali ya hewa ni ya kitropiki. Kuna mvua miezi yote. Kitovu cha kisiwa kikubwa zaidi (Grande Comore) ni mlima wa volkano hai Karthala wenye mita 2,461 juu ya UB. Safari iliyopita Karthala ililipuka mwaka 1977 ikaharibu kijiji kimoja. Miji Miji mikubwa ni (wakazi mwaka 2005): Moroni 42.872, Mutsamudu 23.594, Fomboni 14.966, Domoni 14.509 na Tsémbehou 11.552. Historia Visiwa vya Komori vimekaliwa na watu mbalimbali kutoka Afrika na Asia Kusini katika historia ndefu. Wanaakiolojia walitambua mabaki ya makazi ya watu kutoka karne ya 6 kwenye kisiwa cha Nzwani lakini haijulikani kama watu walitangulia kufika mapema bila kuacha mabaki ya kutambulika. Waswahili wa kwanza walifika kama sehemu ya uenezi wa Wabantu tangu karne ya 9 BK. Kipindi cha kwanza huitwa kipindi cha Dembeni (karne ya 9 - 10) ambako Waswahili walianzisha kijiji kimoja katika kila kisiwa. Wakati wa karne ya 11 hadi ya 15 biashara iliongezeka na Madagaska pia na wafanyabiashara kutoka Uarabuni. Vijiji vidogo vikaongezeka na vijiji vya awali vikakua vikawa miji. Kumbukumbu ya wenyeji hutaja mara nyingi majina ya Waarabu kutoka Yemen na Saba' kama mababu wa koo asilia lakini hakuna uhakika kama kumbukumbu hizo zinalingana na historia halisi. Athira ya Kiarabu na ya Kiislamu ikaongezeka kutokana na biashara ya watumwa, dhahabu na pembe za ndovu kati ya Afrika ya Mashariki na nchi za Kiislamu. Waarabu na Waajemi walijenga vituo kwa ajili ya biashara yao pamoja na misikiti na kueneza dini ya Uislamu kwenye visiwa. Hata kama Komori si karibu sana na pwani, hata hivyo kutokana na mwendo wa upepo ni kituo muhimu cha jahazi kwenye safari kati ya Kilwa na Msumbiji iliyokuwa bandari kuu ya dhahabu ya Zimbabwe. Siasa Kufuatana na katiba ya uhuru ya mwaka 1975 Komori ilitangazwa kuwa jamhuri ya Kiislamu. Serikali zilipinduliwa mara kwa mara na wanajeshi au na mamluki. Katiba mpya ya mwaka 2001 imeondoa tabia ya kidini ya dola na iliunda utaratibu wa urais kuzunguka kati ya visiwa vitatu vikubwa. Katika muundo huo rais wa jamhuri atateuliwa kila baada ya miaka minne kutoka kisiwa tofauti. Katika uchaguzi ya mwaka 2002 rais Azali Assoumani alichaguliwa kutoka kisiwa cha Ngazidja (Komori Kuu). Katika uchaguzi wa 2006 rais amechaguliwa kati ya wagombea kutoka kisiwa cha Anjouan. Wananchi wa Anjouan walipiga kura ya kwanza. Wagombea watatu wenye kura nyingi wameteuliwa na kusimamishwa mbele ya wapiga kura wa visiwa vyote watakaomchagua rais wa jamhuri. Rais wa mwaka 2010 alitoka katika kisiwa cha Moheli, baadaye tena rais kutoka Ngazidja, n.k. Katika uchaguzi wa 2010 ndiye Ikililou Dhoinine aliyepata kura nyingi. Watu Watu wa Komori ni mchanganyiko wa Waarabu, Wamadagaska, Waafrika wa bara ambao mababu walikuwa watumwa, Wahindi na Wazungu kadhaa. Kutokana na uhaba wa ajira Wakomori wengi wamehamia nje, hasa Madagaska. Wakazi wengi ni Waislamu (98%, hasa Wasunni), wakifuatwa na Wakristo (2%). Karibu nusu ya wananchi wote hawajui kusoma. Ina lugha rasmi tatu ambazo ni Kifaransa, Shikomor (inayofanana na Kiswahili) na Kiarabu. Nje ya Kifaransa, Kiarabu na Kimalagasy Sanifu, kuna lugha tatu za asili ambazo huzungumzwa na Wakomori, yaani Kimwali, Kindzwani na Kingazidja ambazo ziko karibu na Kiswahili. Uchumi Komori ni kati ya nchi maskini zaidi duniani. Kilimo, uvuvi, uwindaji na misitu ni misingi ya uchumi wote. Barabara na mawasiliano ya meli au ndege ni haba, idadi ya watu inakua haraka, elimu ni duni; haya yote yanasababisha kudumu kwa uchumi wa kijungujiko na uhaba wa ajira. 80% ya wafanyakazi wote wanashughulika kilimo. Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Tovuti rasmi Anjouan.net Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Visiwa vya Afrika Visiwa vya Bahari ya Hindi Nchi za visiwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
2021
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jomo%20Kenyatta
Jomo Kenyatta
Jomo Kenyatta (1893-1978) alikuwa rais wa kwanza wa Kenya. Jina lake halisi lilikuwa Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagĩkũyũ wanauita kenyaata. Maisha Alisoma katika shule ya kanisa la wamisionari wa Kiskoti. Baada ya kuhitimu aliajiriwa kama karani na msoma mita wa manispaa ya Nairobi, alioa mke wake wa kwanza ambaye ni Grace Wahu. Kabila lake lilikuwa ni Mgĩkũyũ. Azma yake ya kutaka kuikomboa ardhi ya Wagĩkũyũ ilimfanya aweze kuwaunganisha, naye akawa katibu wao mwaka 1928. Mwaka 1930 alizuru Marekani na Uingereza ambako aliishi miaka kumi na mitano na hata kuoa mwalimu wa Kiingereza ambaye aliitwa Edna Kenyatta. Alirudi Kenya mwaka 1946 na alichaguliwa kuwa rais wa chama cha siasa cha Kenya African Union (KANU). Alihamasisha kukomeshwa ubaguzi wa rangi; kuwa na mwamko kisiasa pamoja na mambo mengine yanayompa Mwafrika heshima na utu. Aliandika kitabu kiitwacho Facing Mount Kenya kilichohusu ukombozi na historia ya Wagĩkũyũ. Alikuwa pia mwanzilishi na mhariri wa gazeti la kwanza kwa lugha ya Gĩkũyũ ambalo liliitwa Mũigũithania. Kutokana na kuhusishwa na harakati za vita vya msituni vya kundi la Mau Mau alihukumiwa miaka saba jela mwaka 1952. Huwezi kuzungumza historia ya Kenyatta bila ya kuitaja Maumau. Baadaye alioa mke wa tatu aliyeitwa Mama Ngina Kenyatta ambaye alikuja kuwa mke wa rais wa kwanza na ambaye ndiye mama yake Uhuru Kenyatta, rais wa sasa. Licha ya Waingereza kuwa na matumaini ya kuwapa wapinzani Waafrika mamlaka "ya wastani" zaidi, ilikuwa Kenya African National Union (KANU) ya Jomo Kenyatta, mfungwa wa zamani, ambayo iliunda serikali muda mfupi kabla ya Kenya kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963. Tarehe 1 Juni 1963 Kenya ilipata madaraka na Jomo Kenyatta alitawazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya. Mwaka mmoja baadaye, Kenyatta akawa rais wa kwanza wa Kenya juu ya uanzishwaji wa jamhuri. Chama kidogo cha Kenya African Democratic Union (KADU), kilichowakilisha muungano wa makabila madogo ambayo yaliogopa utawala wa makabila makubwa, kilijitoa na kujivunja mwaka wa 1964 na wanachama wake wakajiunga na KANU. Chama kidogo cha upinzani, Kenya People's Union (KPU), kilianzishwa mwaka 1966, kiongozi wake akiwa Jaramogi Oginga Odinga aliyewahi kuwa makamu wa rais Kenyatta. KPU ilipigwa marufuku, na kiongozi kuwekwa kizuizini baada ya chachari za kisiasa zilizohusishwa na ziara za Kenyatta katika Mkoa wa Nyanza. Hakuna vyama vingine vya upinzani vilivyoanzishwa baada ya 1969, kupelekea Kenya kuwa mfumo wa chama kimoja chini ya KANU. Kenyatta alifariki mjini Mombasa tarehe 18 Agosti 1978 na kuzikwa jijini Nairobi kwenye jengo la bunge. Marejeo ! Waliozaliwa 1893 Marais wa Kenya Waliofariki 1978
2022
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwanza%20%28sarafu%29
Kwanza (sarafu)
Kwanza (kifupi: KZ) ni pesa inayotumika kwa malipo halali katika nchi ya Angola. Wakati wa uhuru Angola ilirithi pesa ya escudo kutoka Ureno. Mwaka 1977 Kwanza yenye Lwei 100 imeingizwa nchini kama pesa ya kwanza ya kitaifa. Kutokana na kushuka kwa thamani ya fedha mara kwa mara pesa ya Kwanza imebadilishwa mara nne tangu 1977: 1977 Kwanza 1977 Kwanza Novo (Kwanza Mpya) 1995 Kwanza Reajustado (Kwanza iliyosahihishwa) 1999 Kwanza (Kwanza Reajustado milioni moja zilibadilishwa kuwa Kwanza mpya 1) Sarafu za centavos 10 na 50 hazipatikani kwani hazinunui kitu tena. Pesa Angola
2023
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwanzaa
Kwanzaa
Kwanzaa ni sikukuu inayosherehekewa kati ya Wamarekani Weusi nchini Marekani kwa muda wa siku saba toka tarehe 26 mwezi wa disemba hadi tarehe 1 mwezi wa Januari. Sikukuu hii ilianzishwa Kalifornia na Maulana Ron Karenga tarehe 26 Diesemba mwaka 1966. Karenga alitunga neno jipya "Kwanzaa" kutokana na neno la Kiswahili "Kwanza" inayochukuliwa kumaanisha "matunda ya kwanza". Herufi "a" iliongezwa katika neno hilo ili kulifanya neno hilo kuwa na herufi saba, sawa na idadi ya siku za kusherehekea sikukuu hii. Baadhi ya waamerika weusi huchukulia sikukuu hii kuwa na umuhimu sana kwao kama vile ilivyo Hanuka kwa Wayahudi au Krisimasi kwa Wakristo. Karenga aliagiza kutumia maneno kadhaa ya Kiswahili katika sikukuu hizi kwa kuonyesha uhusiano na utamaduni wa Afrika. Sherehe hii imejengwa juu ya maadili ya kitamaduni ya Kiafrika na huchukuliwa kuwa ni kama aina za sherehe za makabila mbalimbali Afrika wakati wa mavuno. Maadili haya ya Kiafrika yamegawanywa katika dhana iitwayo Nguzo Saba. Kwa siku saba, kila siku huwa na nguzo yake ya kukumbuka na kuenzi. Nguzo hizo ambazo zinafahamika kwa Kiswahili ni: Umoja, Kujichagulia, Ujima, Ujamaa, Nia, Kuumba, na Imani. Nguzo saba hizi hutumiwa kama moja ya njia ya kuimarisha umoja wa kifamilia miongoni mwa jamii za Wamarekani Weusi na pia njia ya kuwakumbusha historia na utamaduni wao. Sikukuu hii inatumia alama kadhaa ambazo nazo zinatambulika kwa lugha ya Kiswahili. Alama hizo ni: Mazao Mkeka Kinara Muhindi Mishumaa Saba Kikombe cha Umoja Zawadi Kati ya shughuli zinazofanywa wakati wa sikukuu hii ni kuwasha mishumaa saba (mshumaa mmoja kila siku) na kutoa tambiko la kuenzi mababu na mabibi waliotangulia. Mishumaa hii huwa ina rangi za kijani, nyekundu na nyeusi. Mshumaa mweusi huwekwa katikati na ndio huwa wa kwanza kuwashwa. Huwashwa siku ya kwanza. Rangi nyeusi huwakilisha watu weusi, rangi nyekundu hukumbusha mapambano na masahibu yaliyowakumba walitangulia, na rangi ya kijani humaanisha utajiri wa bara la Afrika na pia matumaini mema ya watu weusi. Tanbihi Viungo vya nje Tovuti Rasmi ya Kwanzaa Sikukuu Utamaduni wa Marekani
2024
https://sw.wikipedia.org/wiki/Visa%20vya%20Esopo
Visa vya Esopo
Visa vya Esopo vinatokana na masimulizi ya Esopo, ambaye inaaminika kuwa alikuwa ni mtumwa wa Kiafrika aliyeishi kati ya mwaka 620 na 560 Kabla ya Kristo katika Ugiriki wa Zamani. Visa vyake hutumiwa kutoa mafunzo na kuburudisha. Visa hivi hutumiwa kwa wingi katika vitabu vya watoto na vikaragosi. Historia ya Esopo haijulikani vyema. Inaaminiwa kuwa alikuwa ni mtumwa aliyeachiliwa huru na baadaye alikuja kuuliwa na Wadeliphi. Baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa hakuna mtu aliyewahi kuishi katika historia aliyeitwa Esopo. Viungo vya Nje Visa vya Esopo kupitia Mradi wa Gutenberg Fasihi
2026
https://sw.wikipedia.org/wiki/Guinea
Guinea
Guinea (pia: Gine, Gini) ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Guinea-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Guinea-Bissau na Guinea ya Ikweta. Imepakana na Guinea-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Côte d'Ivoire, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari Atlantiki upande wa magharibi. Eneo lake ni chanzo ya mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia. Jina Jina la "Guinea" liliwahi kutaja sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberberi. Watu Makabila yaliyopo nchini ni 24. Kubwa zaidi ni lile la Wafulani (40%). Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wakazi wanatumia zaidi lugha asilia kadiri ya makabila, hasa Kipular, Kimaninka, Kisusu, Kikisi, Kikpelle na Kiloma, Upande wa dini, 85% ni Waislamu (hasa Wasuni), 8% ni Wakristo (hasa Wakatoliki) na 7% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. Tazama pia Orodha ya lugha za Guinea Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Serikali Serikali ya Guinea Permanent UN Mission of the Republic of Guinea'' Habari CIA World Factbook - Guinea BBC News Country Profile - Guinea Muziki Cora Connection West African music resources Orodha Open Directory Project - Guinea directory category Stanford University - Africa South of the Sahara: Guinea directory category The Index on Africa - Guinea directory category University of Pennsylvania - African Studies Center: Guinea directory category Yahoo! - Guinea directory category Nchi za Afrika Umoja wa Afrika
2027
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abu%20Nuwas
Abu Nuwas
Abu Nuwas (kwa Kiarabu أبو نواس) alikuwa mshairi Mwarabu aliyeishi 760-815. Katika utamaduni wa Kiswahili ni jina la mhusika katika hadithi za “Hekaya za Abunuwasi”. Maisha Mshairi Abu Nuwas alizaliwa Ahwaz (Irak). Mama yake alikuwa Mwajemi na baba alikuwa mwanajeshi Mwarabu ambaye hakupata kumjua. Jina lake halisi lilikuwa Hasan ibn Hani al-Hakami; 'Abu Nuwas' ni jina la kutania kutokana na nywele zake ndefu. Akiwa kijana alipelekwa Basra (Iraq) akisaidia katika duka la moja al-Yashira. Huko Basra alihamia nyumba ya mshairi Walibah ibn al-Hubab aliyemfundisha elimu ya sarufi na pia elimu ya dini. Abu Nuwas aliendelea kujifunza mengi hata alikaa mwaka mmoja kati ya Waarabu Bedu jangwani ili aboreshe ujuzi wake wa lugha ya Kiarabu sanifu. Baghdad Akahamia Baghdad, mji mkuu wa Dola la Kiislamu lililotawala wakati ule maeneo makubwa kuanzia Afrika ya Mashariki hadi Afghanistan na Asia ya Kati. Alipendwa sana na watu wa mjini kwa sababu alianzisha aina mpya ya ushairi akiimba juu ya furaha za divai na mapenzi hasa na wavulana kuliko wasichana au wanawake. Abu Nuwas akawa mshairi maarufu wa Kiarabu wa siku zile hadi ameitwa kutoa mashairi yake mbele ya Khalifa Harun ar-Rashid. Hata kama mashairi yake yalisababisha hasira ya wahubiri wa Kiislamu, Abu Nuwasi alilindwa na familia ya Barmaki waliokuwa mawaziri wa Khalifa. Wakati Abu Nuwas alipotupwa jela mara kadhaa waliweza kumwondoa gerezani tena. Mwaka 798 Khalifa Harun ar-Rashid aliwaondoa Barmaki madarakani na kuwafunga jela; Abu Nuwasi alikimbilia Misri. Baada ya kifo cha Harun mwaka 809 alirudi Baghdad akikuta kuwa Khalifa mpya ni Muhammad ibn Harun al-Amin aliyewahi kuwa mwanafunzi wake. Miaka michache ya utawala wa al-Amin ilikuwa miaka ambako Abu Nuwasi alitunga mashairi mengi. Baada ya al-Amin kupinduliwa na kaka yake al-Ma’amun aliyekuwa Mwislamu mkali, Abu Nuwas alianza kutunga mashairi yaliyolingana na mafundisho ya kidini. Lakini alishindwa kumbembeleza khalifa mpya. Mnamo mwaka 815 alikufa ama kwa sababu aliuawa au wakati alipofungwa gerezani. Nafasi kati ya Washairi Wakuu Abu Nuwas anahesabiwa kati ya washairi wakuu wa lugha ya Kiarabu. Alikuwa na athira kubwa kwa washairi wa baadaye kama Omar Khayyám na Hafiz. Pia jina lake limetajwa mara kadhaa katika hadithi za Alfu Lela U Lela. Hadi leo wengine wanampenda sana lakini wengine wanamchukia kama mshairi bila maadili. Abu Nuwas mshairi na Abunuwasi wa Afrika ya Mashariki Waswahili wamejua zaidi umbo la jina kuwa "Abunuwasi" na wamecheka wakisoma "Riwaya za Abunuwasi". Lakini huyu Abunuwasi wa riwaya hana uhusiano na Abu Nuwas mshairi wa kihistoria zaidi ya kumpatia jina lake. Hadithi zote za "Riwaya" zinasimuliwa katika nchi nyingine kwa majina tofauti. Waturuki humwita "Nasreddin Hodja", Wauzbeki "Hodja" pekee, watu wa Algeria "Ben Sikran", Waarabu wengine "Juba (Guba)", Waitalia wa Kusini "Giufa". Huko Iraq kumbukumbu ya Abu Nuwas mshairi imechanganywa na hadithi za huyu mjinga mcheshi mwenye hekima anayejulikana katika nchi zote za Mediteraneo na Mashariki ya Kati. Hadithi katika "Riwaya za Abunuwasi“ zinatumia mapokeo ya urithi huo. Lakini kuna angalau hadithi moja ya Abu Nuwas mwenyewe inayolingana na Abunuwasi wa “Riwaya” – inasaidia kuelewa jinsi gani jina lake limeunganishwa na urithi wa Guba – Nasreddin: Hadithi ya Abu Nuwas na Harun ar-Rashid “Abu Nuwas alipenda divai mno. Siku moja alipatikana hali amelewa sana wakati Khalifa Harun ar-Rashid alipita barabarani pamoja na askari zake. Khalifa Harun alimpenda Abu Nuwas mshairi hata aliwahi kukaa naye na kunywa naye lakini aliona hawezi kumruhusu kulewa barabarani mbele ya watu wote asionekane mwenyewe Khalifa anayedharau sharia ya Allah. Hivyo ar-Rashid akamwendea Abu Nuwas alijeficha chupa nyuma yake akikishika kwa mkono wa kuume. “Unionyeshe mkono wako!” Khalifa alisema. Abu Nuwas alishika chupa kwa mkono wa kulia nyuma yake akionyesha mkono wa kiume. “Unionyeshe mkono mwingine!” alidai ar-Rashid. Tena mshairi alishika chupa kwa mkono wa kushoto akimwonyesha Khalifa mkono wa kulia. Akasema ar-Rashid: “Sasa unionyeshe mikono yote miwili!” Abu Nuwas akakanyaga hatua moja nyuma hadi ukuta wa nyumba akashika chupa kwa matako yake ukutani akimwonyesha Khalifa mikono yote mawili. Huyu alidai akanyage hatua moja mbele. “Ee amirulmuumina”, akajibu Abu Nuwas, “Wewe unajua ya kwamba chupa kitanguka chini nikitembea kitavunjika !” Khalifa na askari wote walicheka sana. Abu Nuwas alitegemea kupokea viboko 80 lakini Khalifa alitangaza: “Mwenye akili kama huyu hawezi kuwa mlevi wala siwezi kumwadhibu kwa tendo la kushika chupa tu. Basi aende!" Marejeo Ewald Wagner: Abu Nuwas Al-Hasan B. Hani' Al-Hakam, makala katika The Encyclopaedia Of Islam New Edition I, Leiden 1986, uk. 143 Sophia Smith Galer: The Arab poet who worshipped wine, tovuti ya BBC Culture, 14th November 2017, iliangaliwa Januari 2021 Esat Ayyıldız. "Ebû Nuvâs’ın Şarap (Hamriyyât) Şiirleri". Bozok Üniversitesi İlahiyat Fakültesi Dergisi 18 / 18 (2020): 147-173. Tanbihi Waliozaliwa 760 Waliofariki 815 Washairi wa Kiarabu Washairi wa Uajemi Waandishi wa Uajemi
2032
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bi%20Kidude
Bi Kidude
Bi Kidude (jina halisi: Fatuma binti Baraka; amefariki Bububu, Zanzibar, 17 Aprili 2013, akikisiwa kuwa na umri wa miaka 102) alikuwa gwiji wa muziki katika bara la Afrika. Bi Kidude alikuwa msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu. Muziki huo, ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrika, umekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko. Maisha Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar. Bi Kidude anasema hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya. Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90. Bi Kidude anasema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji. Alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling'ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji. Bi Kidude hategemei kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya 'wanja' na 'hina' ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa 'Unyago' na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe. Watu wanasema 'Utu uzima dawa' Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu. Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar. Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza. Amekwisha pata tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX ilienda kwake. Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa jang'ombe, na aliimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani. Wanamuziki wa Tanzania Watu wa Zanzibar
2033
https://sw.wikipedia.org/wiki/Binyavanga%20Wainaina
Binyavanga Wainaina
Binyavanga Wainaina (18 Januari 1971 - 21 Mei 2019) alikuwa mwandishi kutoka nchini Kenya. Maisha Alizaliwa Nakuru, nchini Kenya. Alihudhuria masomo ya msingi na sekondari nchini Kenya kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Transkei, Afrika Kusini. Baada ya kumaliza masomo yake alihamia katika jiji la Cape Town ambapo alifanya kazi kama mwandishi wa kujitegemea wa masuala ya chakula na utalii. Mwezi Julai 2002 Binyavanga alishinda Tuzo ya Caine kwa Uandishi wa Kiafrika. Yeye ndiye mwanzilishi wa jarida la fasihi la Kwani?, ambalo linachukuliwa kuwa ndio gazeti kuu la masuala ya fasihi toka Afrika Mashariki. Aliaandika riwaya yake ya kwanza iitwayo The Fallen World of Appearances. Mwaka 2003 alipata tuzo toka Chama cha Wachapishaji wa Kenya (Kenya Publishers Association) kutokana na juhudi zake za kuendeleza fasihi ya Kenya. Alisomea shahada ya pili ya Uandishi wa Ubunifu katika Chuo Kikuu cha East Anglia. Kazi zake zimetoka katika magazeti na majarida mbalimbali kama vile National Geographic, The East African, The Sunday Times (ya Afrika Kusini), The Guardian (ya Uingereza). Baadhi ya kazi alizoandika ni: Discovering Home (Hadithi fupi, G21Net, 2001) An Affair to Dismember (Hadithi fupi) Beyond the River Yei: Life in the Land Where Sleeping is a Disease (Riwaya ya picha pamoja na Steven Torfinn, Kwani Trust). Kupata UKIMWI Tarehe 1 Disemba 2016, katika siku ya UKIMWI Duniani, Wainaina alitangaza kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba amethibitika kuwa na UKIMWI. Kifo Wainaina amefariki dunia baada ya kupata ugonjwa majira ya saa nne usiku ya tarehe 21 Mei, 2019, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wanandugu. Marejeo Viungo vya nje Hadithi fupi ya Discovering Home Mahojiano ya Binyavanga Makala ya BBC kuhusu Binyavanga Waliozaliwa 1971 Waliofariki 2019 Waandishi wa Kenya
2035
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkutano%20huria
Mkutano huria
Mkutano huria ni mkutano ambao unaendeshwa na wahudhuriaji au wajumbe badala ya mwandaaji au waandaaji wa mkutano. Katika mkutano wa aina hii hakuna watoa mada na wapokea mada, hakuna watoa hotuba na wasikilizaji. Wahudhuriaji wote ndio watoa mada na wapokea mada. Dhana hii imepewa umaarufu na wataalamu wawili wa programu ya tarakilishi, Lenn Pryyor na Dave Winer. Viungo vya nje Tofauti kati ya mkutano huria na mkutano wa kawaida Mikutano de:Tagung#Unkonferenz
2036
https://sw.wikipedia.org/wiki/Podikasiti
Podikasiti
Podikasiti ni neno lililoanza kutumiwa mwaka 2004 pale matumizi ya programu ya RSS ilipoanza kutumiwa kusambaza matangazo kwa ajili ya kusikiliza kupitia tarakilishi au zana nyingine za mkononi kama vile aipodi. Podikasiti ni mafaili ya video au sauti ambayo yako kwenye mtandao wa tarakilishi kwa ajili ya yeyote yule anayetaka kutazama au kusikiliza. Wana podikasiti wanasambaza kazi zao kwenye tovuti au blogu zao kwa taratibu mbalimbali. Wako wanaoweka mafaili ambayo mtu yeyote anaweza kuyapakua bure au kwa kulipia, lakini kitu kinachofanya podikasiti kuwa tofauti na mafaili, kwa mfano, ya muziki ambayo unaweza kuyapakua na kusikiliza ni kwamba podikasiti inatumia teknolojia ambayo matangazo mapya yanaletwa kwako bila kukuhitahi wewe kwenda kwenye tovuti au blogu ya mwana podikasiti. Redio nyingi kama vile BBC, NPR (Marekani), hivi sasa zinatuma matangazo yao kwa wasikilizaji kwa kwa kutumia teknolojia ya podikasiti. kompyuta
2042
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Singida
Mkoa wa Singida
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania: mkoa huu upo kanda ya kati, ukipakana na mikoa ya Manyara upande wa kaskazini , Dodoma mashariki, Iringa, Mbeya kusini, Tabora upande wa magharibi na Shinyanga. msimbo wa posta ni 43000. Kuna wilaya sita za Iramba, Manyoni, Singida Vijijini na Singida Mjini, Ikungi na Mkalama. Wakati wa sensa ya mwaka 2022 jumla ya wakazi ilikuwa 2,008,058 kutoka 1,370,637 wa mwaka 2012. Wakazi wa wilaya za Singida mjini na kijijini ni hasa Wanyaturu. Walio wengi Iramba ndio Wanyiramba na wakiwa Wagogo wengi huko Manyoni. Pia kati ya wenyeji kuna Wanyisanzu na makabila mengine madogo. Makabila hayo wanaishi kwa amani na upendo. Lugha kuu ni Kiswahili, lakini pia kila kabila wanaongea yao. Uchumi Singida ni kati ya maeneo maskini zaidi ya Tanzania. Uchumi wake ni hasa ufugaji: idadi ya ng'ombe hukadiriwa kuwa takribani milioni 1.4. mbali na punda, kondoo, kuku. Masoko hayako karibu na barabara si nzuri. Kilimo si kizuri kwa sababu ya hali ya mvua. Ukame huleta njaa. Singida ni kati ya mikoa inayotegemea misaada ya chakula. Kati ya mazao yapo ya chakula na ya biashara. Mazao yanayolimwa mkoani hapo ni mtama, alzeti, vitunguu, uweli, viazi, mahindi, karanga, maharage n.k. Pamoja na kuwa mkoa wa Singida umekuwa ukikumbwa na njaa kwa sababu ya ukame, na hata pale mvua inaponyesha ni duni sana, una shughuli mbalimbali ambazo zinaingiza kipato kwa watu wa mkoa huo. Ikiwa kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea mpaka sasa imekuwa madini ya dhahabu yakigunduliwa katika sehemu mbalimbali mkoani Singida japo kumekuwa aidha hakufanyiwi uchunguzi wa kina kuhakiki kiwango cha hifadhi ya madini iliyopo katika eneo husika au huwa kiwako kilichopo ni kidogo, hivyo kutokuvutia wawekezaji wakubwa katika maeneo hayo. Kati ya madini ambayo yamewahi kugunduliwa katika mkoa wa Singida ni dhahabu ambayo imewahi kugunduliwa huko Londoni na Iruma wilayani Manyoni. Mkoani Singida kuna mapori mengi ya akiba ambayo yamejaa wanyama wa aina nyingi ambao kama mapori hayo yatafanywa kuwa hifadhi kamili za taifa yangesaidia sana kuvutia utalii na kuufanya mkoa wa Singida uongeze pato lake na kupunguza umaskini miongoni mwa wanajamii kwani utatoa ajira kwa jamii inayozunguka hifadhi hizo. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Singida Mjini : mbunge ni Mussa Sima (CCM) Singida Kaskazini : mbunge ni Lazaro Nyalandu (CCM) Iramba Mashariki : mbunge ni Joseph Allan Kiula (CCM) Iramba Magharibi : mbunge ni Mwigulu Nchemba (CCM) Manyoni Magharibi : mbunge ni Yahya Omari Masare (CCM) Manyoni Mashariki : mbunge ni Daniel Edward Mtuka (CCM) Singida Mashariki : mbunge ni Tundu Lissu (Chadema) Singida Magharibi : mbunge ni Elibariki Emmanuel Kingu (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Singida Orodha ya mito ya mkoa wa Singida Tanbihi S
2044
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigermanik
Kigermanik
Lugha za Kigermanik ni kikundi cha lugha zenye asili ya Ulaya ya Kaskazini. Lugha za Kigermanik zenye wasemaji wengi ni Kiingereza (milioni 380) na Kijerumani (milioni 120). Lugha nyingine za Kigermanik ni lugha za Skandinavia, halafu Kiholanzi na Kiafrikaans wa Afrika Kusini. Historia Mwanzo wa lugha hizi uko gizani. Wataalamu wamejaribu kutambua sifa za lugha asilia kwa kulinganisha lugha mbalimbalimbali zilizo karibukaribu ikiwa habari zao zimejulikana. Kutokana na makisio hayo Kigermanik kilianza Ulaya ya Kaskazini, labda Sweden ya Kusini katika miaka elfu ya kwanza K.K.. Wasemaji wa Kigermanik walianza kuhamahama wakati wa Dola la Roma na ndipo habari za kwanza za kihistoria zimepatikana. Matembezi ya Wagermanik yalifika hadi Urusi wa Kusini na Afrika ya Kaskazini. Lugha za Kigermanik hugawanywa katika aina tatu: a) Kigermanik ya Kaskazini: Kiswidi, Kidenmark, Kinorwei, Kiiceland na Kifaroe b) Kigermanik ya Magharibi: Kiingereza, Kijerumani (Kidachi), Kiholanzi, Kiafrikaans, Kijerumani ya Kaskazini, Kifrisia, Kiyiddish (Kiyahudi cha Ulaya) c) Kigermanik ya Mashariki: lugha hizi kama Kivandali au Kigoti zimekufa zote zinajulikana kama lugha za kihistoria tu Germanik Makabila ya Wagermanik
2048
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uganda
Uganda
Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini. Uganda inamiliki sehemu ya ziwa la Viktoria Nyanza ikipakana huko na Kenya na Tanzania. Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa. Jina Jina Uganda lina asili yake katika ufalme wa Buganda ulioko kusini mwa nchi pamoja na mji mkuu, Kampala. Jiografia Tazama piaː Orodha ya milima ya Uganda; Orodha ya maziwa ya Uganda; Orodha ya visiwa vya Uganda; Wilaya za Uganda Uso wa nchi umepata tabia yake kutokana na maziwa makubwa, mito, milima ya juu na tambarare. Upande wa kusini nchi imepakana na Ziwa Nyanza Viktoria ambalo kwa eneo ndilo ziwa kubwa kuliko yote ya Afrika. Maziwa makubwa mengine upande wa magharibi ni Ziwa Albert na Ziwa Edward. Mto mkubwa ni Nile inayopita nchi yote kati ya Ziwa Viktoria hadi Ziwa Albert na kuendelea hadi mpaka wa Sudani ikiitwa mwanzoni Nile ya Viktoria na baadaye Nile ya Albert. Milima ya Ruwenzori ni kati ya milima mikubwa kabisa ya Afrika baada ya Kilimanjaro na Mlima Kenya. Kusini kuna ardhi yenye rutuba na kilimo kinastawi vizuri. Historia Historia ya kale Eneo la Uganda limeona uhamiaji wa vikundi vingi waliowazidi wenyeji asili (walioishi huko tangu miaka 50,000 kama si 100,000 KK). Kusini liliingiliwa hasa na wakulima Wabantu. Kaskazini iliona kufika kwa Waniloti kwa mfano Waluo na baadaye Karimojong. Tangu karne ya 15 himaya mbalimbali zilianza kujengwa na kati ya hizo ni hasa falme za Buganda, Ankole, Bunyoro Toro zilizoendelea kuwa muhimu hadi kuja kwa ukoloni na kwa kiasi fulani kama urithi wa kiutamaduni hata katika Uganda ya kisasa. Ukoloni Karne ya 19 iliona kufika kwanza kwa Waarabu na baadaye kwa Wazungu. Kila mmoja alileta dini yake yaani Uislamu na Ukristo wa Kikatoliki na wa Kianglikana. Katika mashindano juu ya Afrika ya Kati Waingereza walifaulu katika kushindana na Waarabu, Wafaransa na Wajerumani. Walienea kwa mapatano na Buganda wakisaidiana kukomesha upinzani kutoka falme za jirani. Baadaye Waingereza walikuwa na nguvu ya kutosha kuamua hata mambo ya ndani ya Buganda wakatangaza Uganda wote kuwa nchi lindwa tangu mwaka 1894. Baada ya uhuru Uganda ilipata uhuru wake tarehe 9 Oktoba 1962 kwa katiba ya jamhuri yenye serikali ya kibunge. Rais wa kwanza alikuwa Kabaka Sir Edward Mutesa II na waziri mkuu Milton Obote. Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini. Serikali ya Obote ilipinduliwa na mkuu wa jeshi Idi Amini mwaka 1971. Utawala wake ulikuwa kipindi cha udikteta ulioharibu uchumi wa nchi na misingi ya dola. Takriban watu 300,000 waliuawa chini ya Amin ama wapinzani wa siasa yake ama watu wa makabila yaliyotazamwa kuwa maadui wa serikali. Raia wenye asili ya Asia walifukuzwa katika nchi na mali yao yote kutwaliwa na serikali. Mwaka 1978 vikosi vya jeshi la Uganda viliingia Tanzania na kuvamia maeneo ya mpakani kaskazini kwa mto Kagera. Mwaka 1979 Tanzania ilijibu kwa njia ya vita na jeshi lake pamoja na wapinzani wa Uganda walishinda jeshi la Amin na kumfukuza dikteta nchini. Rais wa baadaye Yoweri Museveni alikuwako kati ya wanamgambo waliosaidiana na Watanzania. Uchaguzi wa mwaka 1980 ulimrudisha madarakani Milton Obote aliyeanzisha upya udikteta na kuua watu ovyo. Wapinzani wake wakiongozwa na Museveni walirudi porini wakashika silaha. Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986. Museveni alichaguliwa rais katika kura bila vyama vya upinzani za 1996 na 2001. Mwaka 2005 ulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi wa kwanza. Museveni alipata kibali cha bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akachaguliwa mara ya tatu. Miji ya Uganda Kampala Jinja Port Bell Mbale Mbarara Watu Wakazi wa Uganda wameongezeka kutoka 9,500,000 (1969) hadi 34,634,650 (2014), hivyo wengi wao ni vijana kuliko nchi zote duniani. Umri wa wastani ni miaka 15 tu. Makabila makubwa ni Waganda (16.9%), Wanyankole (8.5%), Wanyoro (7.7%), Wasoga (7.4%), Walangi (7.1%), Wakiga (6.9%), Wateso (6.4%), Waacholi (5.7%), Wagisu (4.6%), Walugbara (4.2%). Wengineo ni 33.6%. Nchini kuna lugha asilia 40 hivi, ambazo zinagawanyika katika makundi makubwa mawili: lugha za Kibantu upande wa kusini na lugha za Kinilo-Sahara upande wa kaskazini. Pia kuna lugha za Kisudani na lugha za Kikuliak. Hata hivyo lugha rasmi ni Kiingereza na Kiswahili. Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2014, 84.5% za wakazi wanafuata Ukristo, hasa katika madhehebu ya Kikatoliki (39.3%) na ya Kianglikana (32%), halafu Wapentekoste (11.1%) na mengineyo. Waislamu ni 13.7%, wengi wao wakiwa Wasuni. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.1% tu. Tanbihi Tazama pia Orodha ya lugha za Uganda Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo Kamusi elezo Appiah, Anthony and Henry Louis Gates (ed). Encyclopaedia of Africa (2010). Oxford University Press. Middleton, John (ed). New encyclopaedia of Africa (2008). Detroit: Thompson-Gale. Shillington, Kevin (ed). Encyclopedia of African history (2005). CRC Press. Vitabu vingine muhimu BakamaNume, Bakama B. A Contemporary Geography of Uganda. (2011) African Books Collective. overview written for younger readers. Chrétien, Jean-Pierre. The great lakes of Africa: two thousand years of history (2003). New York: Zone Books. Hodd, Michael and Angela Roche. Uganda handbook (2011) Bath: Footprint. Jagielski, Wojciech and Antonia Lloyd-Jones. The night wanderers: Uganda's children and the Lord's Resistance Army. (2012). New York: Seven Stories Press. ISBN 9781609803506 Otiso, Kefa M. Culture And Customs of Uganda. (2006) Greenwood Publishing Group. Viungo vya nje Kwa jumla Uganda from UCB Libraries GovPubs. Country Profile from BBC News. Uganda Corruption Profile from the Business Anti-Corruption Portal Welcome To Uganda - The Uganda Guide and Information Portal Ramani Printable map of Uganda from UN.org Serikali na uchumi Chief of State and Cabinet Members Key Development Forecasts for Uganda from International Futures. Masuala ya kiutu Humanitarian news and analysis from IRIN – Uganda Humanitarian information coverage on ReliefWeb Radio France International – dossier on Uganda and Lord's Resistance Army Biashara World Bank Summary Trade Statistics Uganda Utalii Uganda Tourist Board Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Jumuiya ya Madola Jumuiya ya Afrika Mashariki
2050
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Iringa
Mkoa wa Iringa
Mkoa wa Iringa ni mojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 51000. Upo katikati ya nchi, kidogo upande wa kusini. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Njombe, Mbeya, Singida na Dodoma. Makao makuu yako katika manisipaa ya Iringa. Jiografia Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania na kupakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania upande wa kaskazini. Hadi mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na eneo lenye ukubwa wa jumla ya km² 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km² 43,935. Eneo linalobakia la km² 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama milima na misitu. Tangu mwaka 2012 wilaya tatu za kusini zimetengwa na Iringa na kuwa mkoa mpya (Mkoa wa Njombe) kwa hiyo eneo la Iringa limepungua kilomita za mraba 21,347. Wakazi Mwaka 2022 kulikuwa na wakazi 1.192,728 katika wilaya zifuatazo: Iringa Vijijini (wakazi 254,032), Mufindi (wakazi 265,829), Kilolo (wakazi 218,130), Iringa Mjini (wakazi 151,345), na Mafinga Mjini (wakazi 51,902). Wenyeji wa mkoa ni hasa Wahehe; wengine wanatokea makabila ya jirani kama Wabena, Wakinga, Wapangwa, Wasangu, Wawanji, Wagogo n.k. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Iringa Mjini : mbunge ni Jesca Msambatavangu (CCM) Isimani : mbunge ni William Lukuvi (CCM) Kalenga : mbunge ni Godfrey Mgimwa (CCM) Kilolo : mbunge ni Venance Mwamoto (CCM) Mafinga Mjini : mbunge ni Cosato Chumi (CCM) Mufindi Kaskazini : mbunge ni Mahmoud Mgimwa (CCM) Mufindi Kusini : mbunge ni Mendrad Kigola (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Iringa Orodha ya mito ya mkoa wa Iringa Marejeo Viungo vya nje Tovuti ya Mkoa wa Iringa I
2055
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dar%20es%20Salaam
Mkoa wa Dar es Salaam
Dar es Salaam ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Mkoa wa Pwani pande zote barani na Bahari ya Hindi upande wa mashariki. Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani. Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393. Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 5,383,728. Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Ilala : mbunge ni Mussa Azzan Zungu (CCM) Kawe : mbunge ni Joseph Gwajima (CCM) Kibamba : mbunge ni (CCM) Kigamboni : mbunge ni Faustine Ndugulile (CCM) Kinondoni : mbunge ni Abbas Tarimba (CCM) Mbagala : mbunge ni Issa Ally Mangungu (CCM) Segerea : mbunge ni Bonna Mosse Kaluwa (CCM) Temeke : mbunge ni Abdallah Mtolea (CCM) Ubungo : mbunge ni Kitila Mkumbo (CCM) Ukonga : mbunge ni Jerry Silaa (CCM) Tazama pia Orodha ya mito ya mkoa wa Dar es Salaam Kata za Mkoa wa Dar es Salaam Viungo vya nje Sensa ya 2002 Usalama katika Daressalaam D
2059
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Dodoma
Mkoa wa Dodoma
Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 41000. Uko katikati ya nchi na umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida. Eneo lote la mkoa lina km² 41,310. Sehemu kubwa ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB. Katika sensa ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 3,085,625. Kuna wilaya saba zifuatazo: Wilaya ya Bahi, Wilaya ya Chamwino, Wilaya ya Chemba, Wilaya ya Dodoma Mjini, Wilaya ya Kondoa, Wilaya ya Kongwa, Wilaya ya Mpwapwa. Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa kwa wilaya mpya za Chamwino na Bahi. Mnamo Machi 2012 ilianzishwa wilaya mpya ya Chemba. Mawasiliano Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa ) kwenda kusini ni nzuri kwa kiwango cha lami. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege. Hali ya hewa na kilimo Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile mtama, wimbi, muhogo; kilimo cha mahindi hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni karanga alizeti na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa divai katika Tanzania. Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu za mkoa. Wakazi na utamaduni Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru. Kondoa kuna Warangi na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Bahi : mbunge ni Omar Ahmed Badwel (CCM) Chemba : mbunge ni Juma Nkamia (CCM) Chamwino : mbunge ni Deo Ndejembi (CCM) Dodoma Mjini : mbunge ni Antony Peter Mavunde (CCM) Kibakwe : mbunge ni George Simbachawene (CCM) Kondoa Mjini : mbunge ni Sanda Edwin (CCM) Kondoa Vijijini : mbunge ni Dk. Ashatu Kijaji (CCM) Kongwa : mbunge ni Job Ndugai (CCM) Mpwapwa : mbunge ni George Malima Lubeleje (CCM) Mtera : mbunge ni Livingstone Lusinde (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Dodoma Orodha ya mito ya mkoa wa Dodoma Tanbihi D !
2060
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiyunani
Kiyunani
Kiyunani ni jina la Kiswahili cha zamani kwa "Kigiriki", ambayo ni lugha ya nchi ya Ugiriki ("Uyunani") au kwa tabia za Wagiriki ("Wayunani"). Neno la Kiswahili cha zamani limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo يونان yunan linataja kiasili Wagiriki wa eneo la Ionia au wa kabila la Waioni walioishi kwenye pwani ya mashariki ya Bahari ya Aegeis. Leo hii si la kawaida sana, lakini linapatikana bado, hasa katika matoleo mbalimbali ya Biblia. Kwa kuwa kitabu hicho kina miaka 2000-3000 hivi, ni wazi kwamba kinasimulia mambo ya zamani, hivyo pengine neno Kiyunani linatafsiriwa kuwa Kigiriki cha zamani, na Uyunani kuwa Ugiriki ya Kale. Ni kwamba miaka ya nyuma neno "Kigiriki" limezidi kusambaa zaidi kati ya wanaoongea Kiswahili, kutokana na athira ya Kiingereza kinachotumia maneno "Greece, Greek" kutoka Kilatini "Graeci", ambayo ni kawaida katika lugha nyingi za Kiulaya. Wanaotajwa wenyewe hujiita "Helleni", na lugha yao "Helleniki". Lugha za Kihindi-Kiulaya
2062
https://sw.wikipedia.org/wiki/Roma%20%28maana%29
Roma (maana)
Roma (pia: Rumi) ni jina linalotumika kwa mji wa Roma (mji mkuu wa Italia), ama kwa dola la Roma lililokuwa kwa karne kadhaa kabla na baada ya Kristo dola kubwa kuliko zote duniani, tena kwa Kanisa la Roma ambalo ni kiini cha Kanisa Katoliki lote. Lilikuwa pia jina la mungu wa kike katika dini ya Roma ya Kale. Roma au Rumi? Roma ni umbo asili la jina katika Kilatini na Kiitalia; limekuwa pia la kawaida katika Kiswahili cha kisasa. Kumbe "Rumi" ilikuwa kawaida katika Kiswahili cha zamani kutokana na kawaida ya lugha ya Kiarabu (الرُّومُ ar-Rūm). Matoleo ya Biblia ya "Union Version" iliyochapishwa tangu 1952 hutumia "Rumi", "Warumi". Kumbe tafsiri ya Biblia ya "Kiswahili cha Kisasa" hutumia "Roma", "Waroma". Mji wa Roma, jina la mji mkuu wa nchi ya Italia Dola la Roma, dola kubwa katika eneo lote kandokando ya Mediteraneo (Ulaya ya Kusini na magharibi, Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini) mnamo miaka 2400-1600 iliyopita. Liliendelea katika Dola ya Roma ya Mashariki au Bizanti hadi mwaka 1453 B.K.. Miji mingine inayoitwa kwa jina la "Roma" iko Australia, Ecuador na Marekani; pia ni jina la eneo ndani ya mji wa Mexiko. Jina la mji limetumika pia kwa meli ya kijeshi ya Italia; filamu mbalimbali n.k. Kanisa la Roma ni jina la jimbo ambalo majimbo yote ya Kanisa Katoliki yanalitegemea ili kudumisha umoja wa imani na upendo duniani kote. Kwa sababu hiyo jina hilo linatumika pia kumaanisha Kanisa Katoliki lote. Kwa mfano, mtu akisema, "Mimi nasali Roma", anamaanisha kuwa ni muumini wa Kanisa hilo. Historia 21 Aprili 753 KK ndiyo tarehe ya kimapokeo ambayo mji huo ulisemekana kuundwa na mapacha Romulo na Remo. Ukweli ni kwamba ulianzishwa mapema zaidi (1000 K.K. hivi). Makala zinazotofautisha maana Lazio
2064
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilatini
Kilatini
Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule, vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili. Ilikuwa pia lugha ya kimataifa ya elimu na hata leo istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kilatini. Historia Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi, kama Kiitalia, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania n.k. Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wikipedia. Kilikuwa lugha ya Dola la Roma (angalia pia Roma ya Kale) lugha mama ya lahaja zilizoendelea na kuwa lugha za Kirumi lugha ya elimu na sayansi katika Ulaya kwa karne nyingi lugha rasmi ya serikali katika nchi nyingi za Ulaya kati ya mwisho wa Dola la Roma mwaka 476 BK hadi mnamo 1700 BK lugha pekee ya liturgia katika Kanisa la Kilatini hadi mwaka 1965 Hadi leo Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya. Tena ni lugha ya kidini katika Kanisa Katoliki lugha rasmi katika nchi ya Vatikano. Urithi wa Kilatini katika Kiswahili Kiswahili kimerithi maneno yenye asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia hamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k. Mifano: shule limetokana na Kijerumani "Schule" iliyopokewa kutoka Kilatini "schola". gari limetokana na Kiingereza "car" iliyopokewa kutoka Kilatini "carrus". basi limetokana na Kiingereza "bus" ambayo ni kifupisho cha Kilatini "omnibus" (maana "kwa wote"). meza limetokana na Kireno "mesa" iliyopokewa kutoka Kilatini "mensa". familia limetokana na Kiingereza "family" iliyopokewa kutoka Kilatini "familia". mashine limetokana na Kiingereza "machine" (au kutoka Kijerumani "Maschine") iliyopokewa kutoka Kilatini "machina" Kilatini cha kisasa Kilatini kilikuwa na upanuzi mkubwa kuanzia karne ya 16; misingi ya sayansi ya kisasa ilijadiliwa katika Ulaya kwa Kilatini kilichokuwa lugha ya vyuo vikuu kote Ulaya. Katika karne ya 18 na 19 mataifa mengi yaliimarisha lugha zao na kuzitumia kwa ngazi zote za elimu. Lakini wataalamu wa Ulaya na Marekani waliendelea kutumia majina ya Kilatini kwa kutaja habari za kisayansi na kubuni majina mapya kufuatana na kanuni za Kilatini kwa kutaja vitu na viumbe vilivyotambuliwa na kuelezwa kisayansi. Kazi hii iliendelea hata wakati matumizi ya Kilatini kama lugha ya kujadiliana yalishafikia mwisho wake. Katika karne ya 20 kulikuwa na harakati ya wapenzi wa lugha kuunda misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k. Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka 2019. Tazama pia Wikipedia ya Kilatini Viungo vya nje makala za OLAC kuhusu Kilatini lugha ya Kilatini katika Glottolog http://www.ethnologue.com/language/lat Lugha za Kirumi Lugha za Kihindi-Kiulaya Roma ya Kale Kanisa Katoliki
2066
https://sw.wikipedia.org/wiki/Zambia
Zambia
Jamhuri ya Zambia ni nchi ya Kusini mwa Afrika isiyo na mwambao baharini. Imepakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania upande wa kaskazini, Malawi upande wa mashariki, Msumbiji, Zimbabwe na Botswana upande wa kusini, Namibia na Angola upande wa magharibi. Mji mkuu ni Lusaka (wenye wakazi 1,747,152 mwaka 2010). Jina Jina limetokana na mto Zambezi. Jina la zamani za ukoloni (hadi 1964) lilikuwa "Northern Rhodesia". Jiografia Nchi kwa sehemu kubwa ni nyanda za juu kuanzia mita 1.000 hadi 1.400 juu ya UB. Milima ya Muchinga imepanda hadi mita 2.164, kilele cha juu kabisa kiko kwenye mita 2.301 huko milima ya Mafinga Hills. Historia Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na Watwa. Katika karne za kwanza za milenia ya 1 BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Baada ya wapelelezi Wazungu kufika katika karne ya 18, Zambia ikawa nchi lindwa ya Uingereza kwa jina la Northern Rhodesia mwishoni mwa karne ya 19. Tarehe 24 Oktoba 1964, Zambia ikawa huru na waziri mkuu Kenneth Kaunda akawa rais wa kwanza. Chama chake cha kijamaa United National Independence Party (UNIP) kilitawala kuanzia mwaka 1964 hadi 1991, kikiwa chama pekee halali kuanzia mwaka 1972. Baada ya Kaunda kuanguka, Frederick Chiluba wa Movement for Multi-Party Democracy alitawala tangu mwaka 1991, akafuatwa na Levy Mwanawasa (2002-2008). Aliyefuata tena ni rais Rupiah Banda (2008-2011), halafu Michael Sata wa Patriotic Front party (2008-2014). Baada ya kifo chake, Guy Scott alikaimu hadi uchaguzi wa tarehe 20 Januari 2015, ambapo Edgar Lungu alipata kuwa rais wa sita. Watu Wakazi wa Zambia ni wasemaji wa lugha za Kibantu katika makabila 73. Makubwa ndio Wabemba (19%), Watonga (13.6%), Watumbuka, Wachewa, Walozi, Walunda, Waluvale, Wakaonde, Wankoya na Wanyanja-. Hata hivyo lugha rasmi ni Kiingereza. Idadi kubwa ni wakulima wa kujitegemea, ingawa 44% wanaishi mijini. Upande wa dini, karibu wote ni wafuasi wa Ukristo ambao ndio dini rasmi kwa mujibu wa katiba ya nchi. 75.3% ni Waprotestanti, 22% ni Wakatoliki na wengine wana dini ya aina nyingine au ni wakanamungu. Tazama pia Miji ya Zambia Mikoa ya Zambia Orodha ya lugha za Zambia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Viungo vya nje Serikali ya Zambia Tovuti ya Ikulu Zambia Corruption Profile from the Business Anti-Corruption Portal Zambia profile from the BBC News Key Development Forecasts for Zambia from International Futures World Bank Summary Trade Statistics Zambia Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Jumuiya ya Madola Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
2069
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Tabora
Mkoa wa Tabora
Mkoa wa Tabora ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 45000. Makao makuu yako Tabora Mjini. Tabora ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania ya kati. Eneo la mkoa ni km2 76,151; mnamo km2 34,698 (46%) ni hifadhi ya misitu, km2 17,122 (22%) ni hifadhi ya wanyama. Jumla ya wakazi ilikuwa watu 3,391,679 (2022). Wenyeji wa Tabora ni hasa Wanyamwezi. Walio wengi ni wakulima na wafugaji. Kulikuwa na wilaya 6 (idadi ya wakazi kwa mabano): Tabora Mjini (188,808), Nzega (417,097), Igunga (325,547), Uyui (282,272), Urambo (370,796), Sikonge (133,388). Jina la Urambo humkumbuka Mtemi Mirambo aliyekuwa mtawala muhimu wa Wanyamwezi kabla ya kuingia kwa ukoloni. Mnamo Machi 2012 ilianzishwa pia wilaya ya Kaliua. Barabara Mkoa wa Tabora una barabara za lami. Ipo inayoanzia Tabora mjini hadi Nzega kuelekea Mwanza. Pia lami kutoka Nzega kuelekea Igunga mpaka Singida. Barabara nyingine ya lami ipo inayoanzia Tabora mjini mpaka Urambo yenye urefu wa km 93. Pia lami nyingine inaanzia Tabora mjini mpaka Manyoni yenye urefu wa km 254 ukipitia Itigi. Kuna njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa upande moja na kwenda Mwanza kwa upande mwingine. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Bukene : mbunge ni Suleiman Zedi (CCM) Igalula : mbunge ni Ntimizi Rashidi Mussa (CCM)) Igunga : mbunge ni Dk. Dalaly Peter Kafumu (CCM) Kaliua : mbunge ni Magdalena Sakaya (CUF) Manonga : mbunge ni Seif Hamis Said Gulamali (CCM) Nzega Mjini : mbunge ni Hussein Bashe (CCM) Nzega Vijijini : mbunge ni Hamis Kigwangallah (CCM) Sikonge : mbunge ni George Kakunda (CCM) Tabora Mjini : mbunge ni Emmanuel Mwakasaka (CCM) Ulyankulu : mbunge ni John Peter Kadutu (CCM) Urambo : mbunge ni Margareth Sitta (CCM) Uyui : mbunge ni Maige Athumani Almas (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Tabora Orodha ya mito ya mkoa wa Tabora Tanbihi T
2072
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Morogoro
Mkoa wa Morogoro
Morogoro ni jina la mto, mji, wilaya na mkoa wa Tanzania. Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 67000. Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Dodoma na Arusha. Eneo lake ni km² 72 939, ambapo kuna wakazi 3,197,104 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 (kutola 2,218,492 wa mwaka 2012). Hivyo Morogoro ni kati ya mikoa mikubwa zaidi ya Tanzania. Utawala Mkoa ulikuwa na wilaya sita ambazo ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Kilosa (489,513), Kilombero (322,779), Morogoro Vijijini (263,920), Morogoro Mjini (228,863), Mvomero (260,525), Ulanga (194,209). Mwaka 2012 imeongezwa wilaya mpya ya Gairo na Wilaya ya Malinyi Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini. Robo yao huishi katika miji ya mkoa. Eneo Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani ya Bahari Hindi na Nyanda za Juu za Kusini Tanzania. Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero, pia milima ya juu kama Uluguru yenye mlima wa Kimhandu wenye 2646 m juu ya UB. Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndiyo mto wa kutoa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam. Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za wanyama za Mikumi na Udzungwa na sehemu ya eneo la kuwinda wanyama la Selous. Wakazi Kabila kubwa ni la Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru. Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba, Wabena, Wambungu, Wakutu na Wavidunda. Upande wa dini, karibu nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo. Mawasiliano Barabara Kuu za lami za Dar es Salaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero. Uchumi Ardhi ya Morogoro ina takribani rutuba ya kufaa kwa mazao mengi. Lakini kilimo kinategemea hali ya mvua. Karibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi. Mazao ya sokoni hulimwa milimani. Mkoa wa Morogoro ni eneo lililojaliwa na Mungu kwa uzalishaji wa sukari kwa wingi. Hasa Wilaya ya Kilombero ina mashamba makubwa ya miwa. Hifadhi za mkoa Inabidi zitunzwe hifadhi mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wa Morogoro kwa sababu kutunzwa kwa hifadhi hizo kunaweza kukaleta faida mbalimbali kama vile: pesa za kigeni na pia maendeleo katika lugha mbalimbali. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Gairo : mbunge ni Ahmed Shabiby (CCM) Kilombero : mbunge ni Peter Lijualikali (Chadema) Kilosa : mbunge ni Baraka Bawazir (CCM) Mikumi : mbunge ni Joseph Haule (Chadema) Mlimba : mbunge ni Suzan Kiwanga (Chadema) Morogoro Kusini : mbunge ni Prosper Joseph Mbena (CCM) Morogoro Kusini Mashariki : mbunge ni Omar Tibweta Mgumba (CCM) Morogoro Mjini : mbunge ni Abood Mohamed Abdul Aziz (CCM) Mvomero : mbunge ni Ahmed Sadiq Murad (CCM) Ulanga Magharibi/ Malinyi : mbunge ni Dk. Hadji Mponda (CCM) Ulanga Mashariki : mbunge ni Goodluck Mlinga (CCM) Tazama pia Kata za Mkoa wa Morogoro Orodha ya milima ya mkoa wa Morogoro Orodha ya mito ya mkoa wa Morogoro Viungo vya nje Tovuti ya Mkoa wa Morogoro Mrogoro Regional Profile (2007) Tovuti ya mkoa M
2073
https://sw.wikipedia.org/wiki/Morogoro
Morogoro
Morogoro ni jina la> Mto Morogoro Mji wa Morogoro Mkoa wa Morogoro na Wilaya za Morogoro Mjini na Morogoro Vijijini. Tanzania Makala zinazotofautisha maana
2080
https://sw.wikipedia.org/wiki/Michael%20Jackson
Michael Jackson
Michael Joseph Jackson (29 Agosti 1958 – 25 Juni 2009) alikuwa mwimbaji, dansa na mburudishaji kutoka nchini Marekani. Hufahamika zaidi kwa jina la kiheshima-utani kama Mfalme wa Pop. Hutambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote, na moja kati ya waburudishaji wenye mvuto na athira kubwa katika medani ya muziki. Michango yake katika muziki, dansi na fasheni,<ref name="Jackson: A Fashion Retrospective">film.com: [http://www.film.com/celebrities/michael-jackson/story/michael-jackson-a-fashion-retrospective/28853307Michael Jackson: A Fashion Retrospective,] 29. Novemba 2009</ref> na hasa suala la kuanika hadharani maisha yake binafsi, imemfanya awe kioo cha ulimwengu katika tamaduni maarufu kwa ziaidi ya miongo minne . Akiwa pamoja na ndugu zake, Jackson amefanya uongozi wa uimbaji kwa mara ya kwanza akiwa kama mwanachama mdogo kabisa katika kundi la The Jackson 5 mnamo mwaka wa 1964. Ameanza kazi ya usanii wa kujitegemea kunako mwaka wa 1971. Albamu yake ya mwaka wa 1982 Thriller imebaki kuwa albamu yenye mauzo bora kwa muda wote. Mchango waka katika utengenezaji wa muziki wa video umeinua kutoka katika hali ya kawaida hadi katika hali ya kisanii zaidi: video zake kama vile Billie Jean, Beat It na Thriller inamfanya kuwa msanii Mmarekani Mweusi wa kwanza kupata kupigiwa nyimbo yake sana kwenye MTV. Jackson ameipa umaarufu baadhi ya maunja ya kudansi, kama vile robot na moonwalk. Staili ya muziki wake, staili ya sauti yake na zile koregrafia zilitambulika vizazi kwa vizazi, kirangi na hata katika mipaka ya kitamaduni. Jackson ni mmoja kati ya wasanii wachache waliowekwa mara mbili kwenye Rock and Roll Hall of Fame. Mafanikio mengine yanajumlisha Guinness World Records (ikiwa ni pamoja Mburudishaji Mwenye Mafanikio kwa Muda Wote), Tuzo za Grammy 15 (ikiwa ni pamoja na ile ya Living Legend Award na ile ya Lifetime Achievement Award), 26 American Music Awards (24 akiwa kama msanii pekee ya kujitegemea, ikiwa ni pamoja na moja kwa ajili ya Msanii wa Karne)—zaidi ya msanii mwingine yeyote— single zake 17 zimeshika nafasi ya kwanza huko nchini Marekani (ikiwa ni pamoja na nne akiwa kama mwanachama wa kina Jackson 5), na inakadiriwa kafanya mauzo ya rekodi zaidi ya milioni 750 dunia nzima, inafanya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza rekodi zao vilivyo kwa muda wote na haijawahi kutokea. Maisha binafsi ya Jackson yamezua utata kwa miaka kadhaa. Kujibadilisha kwa mwonekano wake ilianza kutambulika tangu mwishoni mwa miaka ya 1970 na kuendelea, kwa kubadilisha pua yake, na rangi ya ngozi yake, imesababisha makisio kadha wa kadha katika vyombo vya habari. Mnamo mwaka wa 1993 alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia kwa mtoto, ingawa hakuna mashtaka yoyote yaliyotolewa dhidi yake. Mnamo mwaka wa 2005 amejaribu kuachana na mashtaka kama yale ya awali. Ameoa mara mbili, kwanza alioa mnamo 1994 na akaja kuoa tena mnamo 1996. Amepata watoto watatu, mmoja alizaliwa kwa mama mwenye kuchukua mimba kwa ajili ya familia fulani. Jackson amekufa mnamo tar. 25 Juni 2009 kwa kuzidisha kiasi cha dawa wakati anajiandaa na ziara ya tamasha lake la This Is It, ambalo lilitakiwa lianze katikati mwa mwaka wa 2009. Ameripotiwa kwamba alitumia dawa aina ya propofol na lorazepam. Afisa uchunguzi wa vifo wa Wilaya ya Los Angeles ameelezwa kuwa kifo chake ni uuaji wa binadamu, na mashtaka yanakwenda kwa daktari wake binafsi kwa kosa la kuua bila kukusudia. Kifo cha Jackson kimeamsha mihemko ya huzuni ulimwenguni, na huduma ya ukumbusho wake uliofanywa hadharani, ulitangazwa duniani, ulitazamwa na maelfu ya watu moja kwa moja. Wasifu Maisha ya awali Michael Jackson alianza kuonekana jukwaani akiwa na miaka mitano tu pamoja na kaka na dada zake. Alitokea familia ya wanamuziki ya Jackson Five. Kuhusu miaka yake ya awali alisimulia mara kadhaa ya kwamba baba alimlazimisha kufanya mazoezi mno ya kucheza na uimbaji hivyo Michael alikosa utoto. Watazamaji wengi wamehisi ya kwamba matatizo ya kisaikolojia ya msanii yalikuwa na chanzo katika kipindi hiki. Michael aliandika nyimbo nyingine maarufu ambazo ni 'Bad' na 'Black or White'. Huyu pia huitwa mfalme wa pop duniani. Maisha binafsi Maisha binafsi ya Michael Jackson yalikuwa yakifahamika sana. Pia, alishawahi kutiwa shaurini kwa unyanyasaji wa mtoto, lakini hakukutanika na kosa. Alifanya upasuaji maalumu ili abadilishe mwonekano wake. Michael aliyezaliwa kwa maumbile ya Mwamerika mweusi mwishoni alikuwa na ngozi nyeupe usoni na baada ya upasuaji kadhaa pua yake likawa nyembamba si pana tena. Mwenyewe alidai ya kwamba badiliko la rangi lilisababishwa na ugonjwa. Watu waliomtazama hawakupatana kama mabadiliko ya kimaumbile yalikuwa ama tokeo la kuona aibu kuonekana kama Mwafrika au jaribio kuwa na uso linalorahisisha mawasiliano yake na watu wa bara zote. Michael, alimwoa Bi. Lisa Marie Presley, binti wa Elvis Presley. Jackson, pia alikuwa akimiliki eneo kubwa lenye makazi lililoitwa Neverland, ambalo baadaye liliuzwa kwa kampuni na nusu bado inamilikiwa na mwenyewe. kifo Michael Jackson amefariki mnamo tar. 25 Juni 2009 baada ya kuwaisha katika hospitali ya UCLA Medical Center. Ilifikiriwa kwamba alipata mshtuko wa moyo, ikiwa na maana kwamba moyo wake ulisimama na imeonekana ya kwamba sababu yake ilikuwa matumizi mabaya ya madawa mengi mno. At 4:36 pm local time, the Los Angeles coroner confirmed Jackson's death. Wakati wa umauti wake, Jackson alikuwa na umri wa miaka 50. Tetesi za habari za kifo cha Jackson, kimevunja rekodi ya mtandao na kusababisha msongamano mtandaoni kwa kuwapa tabu Google, Twitter, Facebook, na Yahoo msongamano mkubwa wa utafutaji wa habari zake. Diskografia Albamu Got to Be There (1971) Ben (1972) Music & Me (1973) Forever, Michael (1975) Off the Wall (1979) Thriller (1982) Bad (1987) Dangerous (1991) HIStory: Past, Present and Future, Book I (1995) Invincible'' (2001) Tazama pia Afya na mwonekano wa Michael Jackson Marejeo Viungo vya nje michaeljackson.com Jackson, Michael Waliozaliwa 1958 Waliofariki 2009 Washindi wa Tuzo za Grammy
2081
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mnazi
Mnazi
Mnazi ni neno linaloweza kutaja: mti wa mnazi (mti) mwenye matunda ya nazi kinywaji cha mnazi (kinywaji) kinachotengenezwa na utomvu wa nazi changa Makala zinazotofautisha maana
2086
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kinywaji
Kinywaji
Kuna vinywaji vingi: Maji Chai Kahawa Maziwa Soda Togwa Maji ya matunda Pombe Mnazi Mvinyo Mbege Bia Kimpumu Chang'aa
2087
https://sw.wikipedia.org/wiki/Swala
Swala
Kwa swala kama ibada ya Kiislamu, taz. Swalah. Swala ni wanyama walao nyasi katika nusufamilia Antilopinae, Aepycerotinae na Pantholopinae za familia Bovidae. Hupatikana katika maeneo yenye nyasi fupi fupi na vichaka vifupi fupi hasa kwenye maeneo mengi ya hifadhi katika Afrika. Spishi nyingine hukimbia kilometa 80 kwa saa na zina uwezo wa kuruka mita 7 hadi 8 juu akiwa kwenye kasi. Rangi yao ni ya mchanga na nyeupe kidogo kwenye koromeo na sehemu ya chini ya mkia. Maadui yao wakubwa ni simba, chatu na chui. Spishi Nusufamilia Aepycerotinae Aepyceros melampus, Swala Pala (Impala) Nusufamilia Antilopinae Ammodorcas clarkei, Swala Dibatag (Dibatag au Clarke's gazelle) Antidorcas marsupialis, Swala Mrukaji (Springbok) Antilope cervicapra, Swala Mweusi (Blackbuck) Dorcatragus megalotis, Swala Beira (Beira) Eudorcas albonotata, Swala wa Mongalla (Mongalla gazelle) Eudorcas rufifrons, Swala Paji-jekundu (Red-fronted gazelle) Eudorcas rufina, Swala Mwekundu (Red gazelle) – imekwisha sasa Eudorcas thomsonii, Swala Tomi au Swala Lala (Thomson's gazelle) Gazella arabica, Swala Arabu (Arabian gazelle) – imekwisha sasa Gazella bennettii, Swala Mhindi (Chinkara au Indian Gazelle) Gazella cuvieri, Swala wa Cuvier (Cuvier's Gazelle) Gazella dorcas, Swala-jangwa (Dorcas au Ariel Gazelle) Gazella erlangeri, Swala wa Neumann (Neumann's Gazelle) Gazella gazella, Swala-milima (Mountain Gazelle) Gazella leptoceros, Swala Pembe-nyembamba (Rhim Gazelle) Gazella saudiya, Swala wa Saudia (Saudi Gazelle) – imekwisha sasa Gazella spekei, Swala wa Speke (Speke's Gazelle) Gazella subgutturosa, Swala Mwajemi (Goitered Gazelle) Litocranius walleri, Swala Twiga (Gerenuk au Waller's au Giraffe-necked Gazelle) Nanger dama, Swala Dama (Dama Gazelle) Nanger granti, Swala Granti (Grant's Gazelle) Nanger soemmerringii, Swala wa Soemmerring (Soemmerring's Gazelle) Procapra gutturosa, Swala wa Mongolia (Mongolian Gazelle) Procapra picticaudata, Swala Goa (Goa) Procapra przewalskii, Swala wa Przewalski (Przewalski's Gazelle) Saiga tatarica, Swala Saiga (Saiga) Nusufamilia Pantholopinae Pantholops hodgsonii, Swala wa Tibeti (Tibetan Antelope) Picha Swala Wanyama wa Afrika Wanyama wa Biblia
2088
https://sw.wikipedia.org/wiki/John%20F.%20Kennedy
John F. Kennedy
John Fitzgerald Kennedy (29 Mei 1917 – 22 Novemba 1963) alikuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 1961 hadi alipouawa. Maisha Alikuwa mtoto wa pili katika familia ya watoto 9. Baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu wa ukoo wenye asili ya Eire. Vita Kuu ya Pili ilipoanza alijiunga na jeshi la wanamaji. Mwaka 1943 alijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na ndege za kivita za Japani. Mwaka wa 1957 Kennedy alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Wasifu kwa ajili ya wasifu ya wabunge wanane wa Senati ya Marekani; kitabu kiliitwa Profiles in Courage. Mwaka 1947 alianza kujiingiza katika siasa na mwaka 1960 alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Ni rais pekee muumini wa Kanisa Katoliki katika historia ya nchi hiyo. Aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 22 Novemba 1963, akiacha mke na watoto wawili. Atakumbukwa kwa kutetea haki za watu wote bila kujali rangi yao. Kati ya mengine alisema "Wamarekani wasiulize Marekani imewatendea nini, bali wajiulize kwanza wao wenyewe wameitendea nini nchi yao". Viungo vya nje Maktaba ya John F. Kennedy tovuti rasmi Waliozaliwa 1917 Waliofariki 1963 Senati (Marekani) Marais wa Marekani Massachusetts
2097
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwarara
Kwarara
Kwarara ni ndege wa nusufamilia Threskiornithinae katika familia Threskiornithidae ambao wana miguu mirefu. Domo refu lao limepindika na hutumika kwa kutafuta chakula ndani ya matope. Spishi nyingi za kwarara huweka matago yao juu ya miti, kwa kawaida pamoja na yange, koikoi au domomwiko. Jike huyataga mayai 2-4. Spishi za Afrika Bostrychia bocagei, Kwarara wa Sao Tome (São Tomé Ibis) Bostrychia carunculata, Kwarara Ndevu (Wattled Ibis) Bostrychia hagedash, Kwarara Hijani (Hadada Ibis) Bostrychia h. brevirostris, Kwarara Hijani Magharibi (Western Hadada Ibis) Bostrychia h. nilotica, Kwarara Hijani Kaskazi (Northern Hadada Ibis) Bostrychia h. hagedash, Kwarara Hijani Kusi (Southern Hadada Ibis) Bostrychia olivacea, Kwarara Kishungi (Olive Ibis) Bostrychia o. akeleyorum, Kwarara Kishungi Mashariki (Eastern Olive Ibis) Bostrychia o. cupreipennis, Kwarara Kishungi wa Kati (Central Olive Ibis) Bostrychia o. olivacea, Kwarara Kishungi Magharibi (Western Olive Ibis) Bostrychia o. rothschildi, Kwarara Kishungi wa Principe (Príncipe Olive Ibis) Bostrychia rara, Kwarara Kidari-mabaka (Spot-breasted Ibis) Geronticus calvus, Kwarara Upara Kusi (Southern Bald Ibis) Geronticus eremita, Kwarara Upara Kaskazi (Northern Bald Ibis) Lophotibis cristata, Kwarara Mabawa-meupe (Madagascar Ibis) Lophotibis c. cristata, Kwarara Mabawa-meupe Kaskazi (Northern Madagascar Ibis) Lophotibis c. urschi, Kwarara Mabawa-meupe Kusi (Southern Madagascar Ibis) Plegadis falcinellus, Kwarara Mweusi (Glossy Ibis) Threskiornis aethiopicus, Kwarara Shingo-nyeusi (African Sacred Ibis) Threskiornis bernieri, Kwarara wa Madagaska (Malagasy Sacred Ibis) Threskiornis b. abbotti, Kwarara wa Aldabra (Aldabra Sacred Ibis) Threskiornis b. bernieri, Kwarara wa Madagaska (Malagasy Sacred Ibis) †Threskiornis solitarius, Kwarara wa Reunion (Réunion Sacred Ibis) imekwisha sasa Spishi za mabara mengine Cercibis oxycerca (Sharp-tailed Ibis) Eudocimus albus (American White Ibis) Eudocimus ruber (Scarlet Ibis) Mesembrinibis cayennensis (Green Ibis) Nipponia nippon (Crested Ibis) Phimosus infuscatus (Bare-faced au Whispering Ibis) Plegadis chihi (White-faced Ibis) Plegadis ridgwayi (Puna Ibis) Pseudibis davisoni (White-shouldered Ibis) Pseudibis papillosa (Black or Red-naped Ibis) Thaumatibis gigantea (Giant Ibis) Theristicus branickii (Andean Ibis) Theristicus caerulescens (Plumbeous Ibis) Theristicus caudatus (Buff-necked Ibis) Theristicus melanopis (Black-faced Ibis) Threskiornis melanocephalus (Black-headed Ibis) Threskiornis moluccus (Australian White Ibis) Threskiornis spinicollis (Straw-necked Ibis) Picha Wari na jamaa
2099
https://sw.wikipedia.org/wiki/Alexander%20Graham%20Bell
Alexander Graham Bell
Alexander Graham Bell (3 Machi 1847 – 2 Agosti 1922) alikuwa kati ya wagunduzi wa mawasiliano ya simu. Alizaliwa katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti lakini baadaye alihamia nchi za Kanada na Marekani. Baba yake alikuwa mwalimu wa watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea. Alifanikiwa katika jaribio lake la kwanza mwaka 1876. Bell hakuwa mtu wa kwanza wa kutengeneza simu kwa mawasiliano lakini mashine yake ilikuwa ya kwanza iliyoweza kutumiwa kibiashara nje ya majaribio na maabara. Alitumia matokeo ya utafiti wa watangulizi hasa Mwitalia Antonio Meucci. Marejeo Waliozaliwa 1847 Waliofariki 1922 Wanasayansi wa Marekani Watu wa Uskoti
2100
https://sw.wikipedia.org/wiki/Karl%20Friedrich%20Benz
Karl Friedrich Benz
Karl Friedrich Benz alizaliwa tar. 25 Novemba 1844 akiitwa Karl Friedrich Michael Vaillant huko Mühlburg / Karlsruhe Ujerumani wa Kusini Magharibi. Baada ya kumzaa mamake Josephine Vaillant akaolewa na babake Johann Georg Benz. Hivyo akaitwa Karl Friedrich Michael Benz lakini baadaye akajiita Carl Friedrich Benz. Alikuwa mhandisi Mjerumani mwenye sifa ya kuwa alitengeza motokaa ya kwanza au gari la kwanza lililotumia nguvu ya nishati ya petroli. Mwaka 1864 alichukua digri ya uhandisi, mw. 1871 alianzisha kampuni yake ya kwanza. Hapo alitengeneza injini ya petroli ya mapigo mawili mwaka 1878/79 aliyoendeleza kuwa injini ya mapigo manne. Benz hakuwa mhandisi wa kwanza kutengeneza injini za aina hii, Mjerumani mwenzake Nikolaus Agosti Otto aliwahi kuchukua hataza ya injini ya mapigo manne mwa. 1876. Injini za aina hii zilifanya kazi viwandani vikiendesha mashine mbalimbali. 1886 Benz alikuwa mtu wa kwanza aliyeweka injini ya petroli kwa gari. Gari lake la kwanza lilikuwa na magurudumu matatu yenye nguvu-farasi 0.8. Mke wake Bertha Benz alifanya safari kubwa ya kwanza kwa gari hili kwa umbali wa km 89 kutoka Mannheim kwenda Pforzheim (yote Ujerumani wa Kusini Magharibi). Alipoishia petroli alipaswa kuinunua katika duka ya madawa kwani hapakuwapo na kituo cha petroli bado. Benz aliendelea kutengeneza gari lenye magurudumu manne. Kwa jina la "Velo" lilikuwa motokaa ya kwanza iliyotengenezwa kwa wingi duniani. Benz aliona kupanuka kwa biashara yake watoto wake wakiendelea kuendesha makampuni yake. Mwaka 1926 kampuni ya Benz iliunganishwa na kampuni ya Gottlieb Daimler kwa jina la "Daimler-Benz". Karl Benz aliaga dunia tar. 4 Aprili 1929. Viungo vya Nje Automuseum Dr. Carl Benz, Ladenburg (Heidelberg) Bertha Benz Memorial Route Waliozaliwa 1844 Waliofariki 1929 Watu wa Ujerumani
2106
https://sw.wikipedia.org/wiki/Isaac%20Newton
Isaac Newton
Isaac Newton (25 Desemba 1642 – 20 Machi 1727) alikuwa mwanahisabati, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka nchi ya Uingereza. Anakumbukwa duniani kote kutokana na michango yake mbalimbali katika sayansi. Ndiye aliyegundua tawi la kalkulasi (sambamba na Leibniz), sheria za mwendo na ya uvutano (graviti). Mchango mwingine wa Isaac Newton upo katika nadharia ya mwanga, akitumia prisma kuonyesha jinsi rangi zinazounda mwanga (kama zinavyoonekana kwenye upinde wa mvua) zinavyotokea. Alichangia pia astronomia kwa kuboresha darubini ya kuakisia (darubini akisi) iliyoleta matokeo mazuri. Alitambua ya kwamba kanuni za mvutano zinatawala pia mwendo wa sayari. Alitunga ramani ya nyota kufuatana na tafiti za Flamsteed. Elimu na imani Newton alipata shahada yake ya kwanza mwaka 1665 na ile ya uzamili mwaka 1668. Kwa kuwa alizaliwa katika familia ya Kianglikana, alitumia muda mwingi kufanya utafiti wa Biblia na theolojia pia. Alilenga kupatanisha elimu ya sayansi na imani yake. Aliandika "Graviti inaeleza miendo ya sayari lakini haiwezi kueleza ni nani aliyeanzisha miendo yao. Mungu anatawala mambo yote na yaliyopo na yanayoweza kuwepo". Tarehe 10 Desemba 1682 alimuandikia Richard Bentley: «Siamini ulimwengu unaweza kuelezwa na sababu za maumbile tu, bali nalazimika kuuona kama tunda la hekima na ubunifu vya mmoja mwenye akili». Hata hivyo, yeye binafsi hakukubali mafundisho juu ya Utatu wa Mungu. Maandishi yake Newton's works – full texts, at the Newton Project The Newton Manuscripts at the National Library of Israel – the collection of all his religious writings Descartes, Space, and Body and A New Theory of Light and Colour, modernised readable versions by Jonathan Bennett Opticks, or a Treatise of the Reflections, Refractions, Inflexions and Colours of Light, full text on archive.org "Newton Papers" – Cambridge Digital Library (1686) "A letter of Mr. Isaac Newton... containing his new theory about light and colors", Philosophical Transactions of the Royal Society, Vol. XVI, No. 179, pp. 3057–3087. – digital facsimile at the Linda Hall Library (1704) Opticks – digital facsimile at the Linda Hall Library (1719) Optice – digital facsimile at the Linda Hall Library (1729) Lectiones opticae – digital facsimile at the Linda Hall Library (1749) Optices libri tres – digital facsimile at the Linda Hall Library Marejeo This well documented work provides, in particular, valuable information regarding Newton's knowledge of Patristics Marejeo mengine Bardi, Jason Socrates. The Calculus Wars: Newton, Leibniz, and the Greatest Mathematical Clash of All Time (2006) excerpt and text search Berlinski, David. Newton's Gift: How Sir Isaac Newton Unlocked the System of the World. (2000); isbn|0-684-84392-7 Buchwald, Jed Z. and Cohen, I. Bernard (eds.) Isaac Newton's Natural Philosophy, MIT Press (2001) excerpt and text search See this site for excerpt and text search. Cohen, I. Bernard and Smith, George E., ed. The Cambridge Companion to Newton. (2002). 500 pp. focuses on philosophical issues only; excerpt and text search; complete edition online  – Preface by Albert Einstein. Reprinted by Johnson Reprint Corporation, New York (1972) Eamon Duffy, "Far from the Tree" (review of Rob Iliffe, Priest of Nature: the Religious Worlds of Isaac Newton, Oxford, Oxford University Press, 2017, ISBN|9780199995356), The New York Review of Books, vol. LXV, no. 4 (8 March 2018), pp. 28–29. Hawking, Stephen, ed. On the Shoulders of Giants. Places selections from Newton's Principia in the context of selected writings by Copernicus, Kepler, Galileo and Einstein Keynes took a close interest in Newton and owned many of Newton's private papers. Newton, Isaac. Papers and Letters in Natural Philosophy, edited by I. Bernard Cohen. Harvard University Press, 1958, 1978; . Newton, Isaac (1642–1727). The Principia: a new Translation, Guide by I. Bernard Cohen; , University of California (1999) Shapley, Harlow, S. Rapport, and H. Wright. A Treasury of Science; "Newtonia" pp. 147–9; "Discoveries" pp. 150–4. Harper & Bros., New York, (1946). (edited by A.H. White; originally published in 1752) Trabue, J. “Ann and Arthur Storer of Calvert County, Maryland, Friends of Sir Isaac Newton,” The American Genealogist 79 (2004): 13–27. Dini Dobbs, Betty Jo Tetter. The Janus Faces of Genius: The Role of Alchemy in Newton's Thought. (1991), links the alchemy to Arianism Force, James E., and Richard H. Popkin, eds. Newton and Religion: Context, Nature, and Influence. (1999), pp. xvii, 325; 13 papers by scholars using newly opened manuscripts Ramati, Ayval. "The Hidden Truth of Creation: Newton's Method of Fluxions" British Journal for the History of Science 34: 417–38. in JSTOR, argues that his calculus had a theological basis Snobelen, Stephen "'God of Gods, and Lord of Lords': The Theology of Isaac Newton's General Scholium to the Principia", Osiris 2nd series, Vol. 16, (2001), pp. 169–208 in JSTOR Wiles, Maurice. Archetypal Heresy. Arianism through the Centuries. (1996) 214 pages, with chapter 4 on eighteenth century England; pp. 77–93 on Newton, excerpt and text search. Viungo vya nje ScienceWorld biography by Eric Weisstein Dictionary of Scientific Biography "The Newton Project" Science in the Making Isaac Newton's papers in the Royal Society's archives "The Newton Project – Canada" "Newton's Dark Secrets" – NOVA TV programme from The Stanford Encyclopedia of Philosophy: "Isaac Newton", by George Smith "Newton's Philosophiae Naturalis Principia Mathematica", by George Smith "Newton's Philosophy", by Andrew Janiak "Newton's views on space, time, and motion", by Robert Rynasiewicz "Newton's Castle" – educational material "The Chymistry of Isaac Newton", research on his alchemical writings The "General Scholium" to Newton's Principia Kandaswamy, Anand M. "The Newton/Leibniz Conflict in Context" Newton's First ODE  – A study by on how Newton approximated the solutions of a first-order ODE using infinite series "The Mind of Isaac Newton" – images, audio, animations and interactive segments Enlightening Science Videos on Newton's biography, optics, physics, reception, and on his views on science and religion Newton biography (University of St Andrews) The Linda Hall Library has digitized Two copies of John Marsham's (1676) Canon Chronicus Aegyptiacus, one of which was owned by Isaac Newton, who marked salient passages by dog-earing the pages so that the corners acted as arrows. The books can be compared side-by-side to show what interested Newton. Waliozaliwa 1642 Waliofariki 1727 Wanafizikia wa Uingereza Wanateolojia wa Uingereza Wanahisabati wa Uingereza Wanaastronomia wa Uingereza
2108
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtakatifu%20Marko
Mtakatifu Marko
Mtakatifu Marko (kwa Kilatini Mārcus; kwa Kigiriki Μᾶρκος) aliishi katika karne ya 1 BK. Alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyeongokea mapema Ukristo pamoja na Maria mama yake. Kanisa la kwanza lilikuwa linakusanyika nyumbani mwao. Alifanya kazi na mitume Paulo na Barnaba katika kuhubiri Injili huko Kupro na Uturuki wa leo. Baadaye alikuwa na Mtume Petro na Paulo katika mji wa Roma hadi walipouawa na serikali ya Kaisari Nero (dhuluma ya miaka 64-68). Ndipo, kwa kufuata mafundisho ya Petro aliyemwita mwanae, alipoamua kuandika Injili ya kwanza, iliyotumiwa na kufuatwa na Mtume Mathayo na Mwinjili Luka, ingawa katika orodha za Biblia inashika nafasi ya pili. Kadiri ya mapokeo alifariki wakati akifanya kazi ya kuanzisha Kanisa huko Aleksandria nchini Misri. Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Aprili. Tazama pia Watakatifu wa Agano la Kale Orodha ya Watakatifu Wakristo Orodha ya Watakatifu wa Afrika Orodha ya Watakatifu Wafransisko Tanbihi Marejeo Viungo vya nje The Life, Miracles and Martyrdom of St. Mark the Evangelist of Jesus Christ H.B. Swete, 'St. Mark in the New Testament' H.B. Swete, 'St. Mark in Early Tradition' St. Mark the Apostle, Evangelist, and Preacher of the Christian Faith in Africa Apostle Mark the Evangelist of the Seventy Orthodox icon and synaxarion Watu wa Biblia Wafuasi wa Yesu Wainjili Watakatifu wa Israeli
2109
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtakatifu%20Paulo
Mtakatifu Paulo
Mtume Paulo (7-67 hivi) ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa. Alitangaza kifo na ufufuko wake katika nchi karibu zote zilizopo kaskazini kwa Bahari ya Kati. Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma wakati wa dhuluma iliyoanzishwa na Kaisari Nero. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sherehe yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Juni pamoja na ya Mtume Petro, lakini pia uongofu wake una sikukuu maalumu, tarehe 25 Januari. Maisha kabla ya wongofu Mtakatifu Paulo alizaliwa kati ya miaka 7-10 BK katika familia ya Kiyahudi ya kabila la Benyamini (Israeli) na madhehebu ya Mafarisayo iliyoishi katika mji wa Tarsus (kwa sasa mji huo uko sehemu ya kusini mashariki ya nchi ya Uturuki). Jina lake la kwanza (la Kiebrania) lilikuwa Sauli, lakini kadiri ya desturi ya wakati ule alikuwa pia na jina la Kigiriki: Paulos kutoka Kilatini Paulus (= mdogo). Mwenyewe alikuwa na uraia wa Roma kama wananchi wote wa Tarsus. Angali kijana alisomea ualimu wa Sheria (yaani wa Torati) huko Yerusalemu chini ya mwalimu maarufu Gamalieli wa madhehebu ya Mafarisayo. Akishika dini yake kwa msimamo mkali akawa anapinga Ukristo kwa kukamata, kutesa na hata kuua Wakristo, kama vile Stefano Mfiadini. Alifanya hivyo mpaka alipotokewa na Yesu Kristo mfufuka akiwa njiani kwenda Damaski, Syria (kwa umuhimu wake katika Historia ya Wokovu habari hii inasimuliwa mara tatu katika kitabu cha Matendo ya Mitume: 9:1-19; 21:12-18 na 22:5-16). Jibu lake kwa Yesu lilikuwa (Mdo 22:10): "Nifanye nini, Bwana?" Habari za wongofu wake katika Mdo 9 1 Wakati huo Saulo alikuwa akizidisha vitisho vikali vya kuwaua wafuasi wa Bwana. Alikwenda kwa Kuhani Mkuu, 2 akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia ya Bwana, awakamate na kuwaleta Yerusalemu. 3 Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga kutoka angani ulimwangazia pande zote. 4 Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: "Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?" 5 Naye Saulo akauliza, "Ni nani wewe Bwana?" Na ile sauti ikajibu, "Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa. 6 Lakini simama sasa, uingie mjini na huko utaambiwa unachopaswa kufanya." 7 Wale watu waliokuwa wanasafiri pamoja na Saulo walisimama pale, wakiwa hawana la kusema; walisikia ile sauti lakini hawakumwona mtu. 8 Saulo aliinuka, na alipofumbua macho yake hakuweza kuona chochote; hivyo wale watu wakamwongoza kwa kumshika mkono mpaka mjini Damasko. 9 Saulo alikaa siku tatu bila kuona, na wakati huo hakula au kunywa chochote. 10 Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, "Anania!" Anania akaitika, "Niko hapa, Bwana." 11 Naye Bwana akamwambia, "Jitayarishe uende kwenye barabara inayoitwa Barabara ya Moja kwa Moja, na katika nyumba ya Yuda umtake mtu mmoja kutoka Tarso aitwaye Saulo. Sasa anasali; 12 na katika maono ameona mtu aitwaye Anania akiingia ndani na kumwekea mikono ili apate kuona tena." 13 Lakini Anania akajibu, "Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kutoka kwa watu wengi; nimesikia juu ya mabaya aliyowatendea watu wako huko Yerusalemu. 14 Na amekuja hapa akiwa na mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu kuwatia nguvuni wote wanaoomba kwa jina lako." 15 Lakini Bwana akamwambia, "Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli. 16 Mimi mwenyewe nitamwonyesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu." 17 Basi, Anania akaenda, akaingia katika hiyo nyumba. Kisha akaweka mikono yake juu ya Saulo, akasema, "Ndugu Saulo, Bwana ambaye ndiye Yesu mwenyewe aliyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa, amenituma ili upate kuona tena na kujazwa Roho Mtakatifu." 18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka macho ya Saulo, akaweza kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Na baada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia. Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasi huko Damasko. 20 Mara alianza kuhubiri katika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. 21 Watu wote waliomsikia walishangaa, wakasema, "Je, mtu huyu si yuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaomba kwa jina hili kule Yerusalemu? Tena alikuja hapa akiwa na madhumuni ya kuwatia nguvuni watu hao na kuwapeleka kwa makuhani!" 22 Saulo alizidi kupata nguvu, na kwa jinsi alivyothibitisha wazi kwamba Yesu ndiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko walivurugika kabisa. Habari za wongofu wake katika Mdo 22 Miaka 22 baadaye, huko Yerusalemu, Paulo alijitetea hivi: 1 "Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni sasa nikijitetea mbele yenu!" 2 Waliposikia akiongea nao kwa Kiebrania wakazidi kukaa kimya zaidi kuliko hapo awali. Naye Paulo akaendelea kusema, 3 "Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti Sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama ninyi wenyewe mlivyo hivi leo. 4 Niliwatesa hata kuwaua wale watu waliofuata Njia hii. Niliwatia nguvuni wanaume kwa wanawake na kuwafunga gerezani. 5 Kuhani Mkuu na baraza lote la wazee wanaweza kushuhudia jambo hilo. Kutoka kwao nilipokea barua walioandikiwa wale ndugu Wayahudi waliokuwa huko Damasko. Nilikwenda Damasko ili niwatie nguvuni watu hao na kuwaleta wamefungwa mpaka Yerusalemu ili waadhibiwe. 6 "Basi, nilipokuwa njiani karibu kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote. 7 Hapo nilianguka chini, nikasikia sauti ikiniambia: `Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?` 8 Nami nikauliza: `Nani wewe, Bwana?` Naye akaniambia: `Mimi ni Yesu wa Nazareti ambaye wewe unamtesa.` 9 Wale wenzangu waliuona ule mwanga lakini hawakusikia sauti ya yule aliyeongea nami. 10 Basi, mimi nikauliza: `Nifanye nini Bwana?` Naye Bwana akaniambia: `Simama, nenda Damasko na huko utaambiwa yote ambayo umepangiwa kufanya.` 11 Kutokana na ule mwanga mkali sikuweza kuona na hivyo iliwabidi wale wenzangu kuniongoza kwa kunishika mkono mpaka nikafika Damasko. 12 "Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii Sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko. 13 Yeye alikuja kuniona, akasimama karibu nami, akasema: `Ndugu Saulo! Ona tena.` Papo hapo nikaona tena, nikamwangalia. 14 Halafu Anania akasema: `Mungu wa babu zetu amekuchagua upate kujua matakwa yake na kumwona yule mtumishi wake mwadilifu na kumsikia yeye mwenyewe akiongea. 15 Kwa maana utamshuhudia kwa watu wote ukiwaambia yale uliyoyaona na kuyasikia. 16 Sasa basi, ya nini kukawia zaidi? Simama ubatizwe na uondolewe dhambi zako kwa kuliungama jina lake.` 17 "Basi, nilirudi Yerusalemu, na nilipokuwa nikisali Hekaluni, niliona maono. 18 Nilimwona Bwana akiniambia: `Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa binadamu hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.` 19 Nami nikamjibu: `Bwana, wao wanajua wazi kwamba mimi ni yule aliyekuwa anapitapita katika masunagogi na kuwatia nguvuni na kuwapiga wale waliokuwa wanakuamini. 20 Na kwamba wakati shahidi wako Stefano alipouawa, mimi binafsi nilikuwako pale nikakubaliana na kitendo hicho na kuyalinda makoti ya wale waliokuwa wanamuua.` 21 Naye Bwana akaniambia: `Nenda; ninakutuma mbali kwa mataifa mengine."` Baada ya wongofu Baada ya kufanya utume katika mazingira ya Kiarabu, Tarsus na Antiokia alianza safari za kitume, akienda mbali zaidi na zaidi, akilenga kumhubiri Yesu mahali ambapo bado hajafahamika, hata Hispania. Ilikuwa kawaida yake kuanzisha makanisa katika miji mikubwa ili toka huko ujumbe ufike hadi vijijini. Muda wote wa utume wake Paulo alipambana na dhuluma kutoka kwa Wayahudi wenzake na matatizo mengine kutoka Wakristo wenye msimamo tofauti na wa kwake, hasa Wakristo wa Kiyahudi juu ya haja ya kufuata masharti ya Agano la Kale ili kupata wokovu. Hatimaye alikamatwa na wapinzani wake Wayahudi mjini Yerusalemu, lakini askari wakoloni walizuia asiuawe. Baada ya hapo alilazimika kukaa gerezani akisubiri hukumu ya Dola la Roma, kwanza Kaisaria Baharini miaka miwili, halafu akakata rufaa kwa Kaisari akapelekwa Roma, alipofika mwaka 61 akakaa miaka miwili tena kifungo cha nje katika nyumba ya kupanga. Kisha kufunguliwa (labda kwa sababu washtaki wake hawakuwasili) alisafiri tena ingawa hakuna hakika alielekea wapi. Kifodini chake Aliuawa nje ya kuta za Roma kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma za Nero kati ya mwaka 64 na 67 B.K. Juu ya kaburi lake lilijengwa kanisa kubwa ambalo liliteketea kwa moto katika karne ya 18 likajengwa upya na hadi leo linapokea hija za Wakristo wengi, hasa katika "Jubilei ya mtume Paulo" iliyotangazwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kwa mwaka 2008/2009. Maandishi yake Kati ya barua nyingi alizoandika (kwa makanisa ya Thesalonike, Korintho, Galatia, Roma, Filipi, Kolosai, Efeso, kwa viongozi Wakristo kama Timotheo na Tito, tena kwa Filemoni), katika Agano Jipya zinatunzwa 13. Ukubwa na ubora wa mchango wa Paulo unaeleweka tukizingatia kwamba alifanya kazi na kuandika kabla ya vitabu vya Agano Jipya kupatikana. Ndiye aliyeanza kuliandika akipanua mawazo aliyoyapokea katika Kanisa kwa kuzingatia Agano la Kale na mafunuo na mang’amuzi yake mwenyewe. Hapo alifafanua vizuri ajabu maisha ya Kikristo kama neema ya kumshiriki Yesu kwa imani, sakramenti na juhudi za kushinda umimi hadi kugeuka sadaka hai, takatifu na ya kumpendeza Mungu. Wokovu huo, utakaokamilika katika ufufuko wa mwili, unapatikana katika Kanisa, ambalo Paulo alilitambulisha kama bibiarusi wa Kristo na mwili wake. Tazama pia Watakatifu wa Agano la Kale Orodha ya Watakatifu Wakristo Orodha ya Watakatifu wa Afrika Orodha ya Watakatifu Wafransisko Marejeo Aulén, Gustaf. Christus Victor (SPCK 1931) Brown, Raymond E. An Introduction to the New Testament. Anchor Bible Series, 1997. ISBN 0-385-24767-2. Brown, Raymond E. The Church the Apostles left behind(Chapman 1984) Bruce, F.F. 'Is the Paul of Acts the Real Paul?' Bulletin John Rylands Library 58 (1976) 283–305 Bruce, F.F., Paul: Apostle of the Heart Set Free (ISBN 0-8028-4778-1) Conzelmann, Hans, the Acts of the Apostles—a Commentary on the Acts of the Apostles (Augsburg Fortress 1987) Davies, W. D. "The Apostolic Age and the Life of Paul" in Matthew Black, ed. Peake's Commentary on the Bible. London: T. Nelson, 1962. ISBN 0-8407-5019-6 Davies, W. D. Paul and Rabbinic Judaism: Some Rabbinic Elements in Pauline Theology. S.P.C.K., 3rd ed., 1970. ISBN 0-281-02449-9 Dunn, James D.G., 1990, Jesus, Paul and the Law Louisville,KY: Westminster John Knox Press. ISBN 0-664-25095-5 Dunn, James D. G., Jesus, Paul, and the Gospels (Grand Rapids (MI), Wm. B. Eerdmans, 2011). Hanson, Anthony T. Studies in Paul's Technique and Theology. Eerdmans, 1974. ISBN 0-8028-3452-3 Harris, Stephen L. Understanding the Bible. Palo Alto: Mayfield. 1985. ISBN 978-1-55934-655-9 Holzbach, Mathis Christian, Die textpragmat. Bedeutung d. Kündereinsetzungen d. Simon Petrus u.d. Saulus Paulus im lukan. Doppelwerk, in: Jesus als Bote d. Heils. Stuttgart 2008, 166-172. Irenaeus, Against Heresies, i.26.2 Maccoby, Hyam. The Mythmaker: Paul and the Invention of Christianity. New York: Harper & Row, 1986. ISBN 0-06-015582-5. Kim, Yung Suk. A Theological Introduction to Paul's Letters. Eugene, Oregon: Cascade Books, 2011. ISBN 978-1-60899-793-0 MacDonald, Dennis Ronald, 1983. The Legend and the Apostle: The Battle for Paul in Story and Canon Philadelphia: Westminster Press. Murphy-O'Connor, Jerome, Jesus and Paul: Parallel lives (Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 2007) ISBN 0-8146-5173-9 Murphy-O'Connor, Jerome, Paul the Letter-Writer: His World, His Options, His Skills (Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 1995) ISBN 0-8146-5845-8 Murphy-O'Connor, Jerome, Paul: A Critical Life (Oxford: Clarendon Press, 1996) ISBN 0-19-826749-5 Ogg, George. “Chronology of the New Testament.” Matthew Black, ed. ‘’Peake's Commentary on the Bible.’’ Nelson, 1962. ISBN 0-8407-5019-6 Rashdall, Hastings, The Idea of Atonement in Christian Theology (1919) Ruef, John, Paul's First letter to Corinth (Penguin 1971) Sanders, E.P., Paul and Palestinian Judaism (1977) Segal, Alan F. Paul, the Convert, (New Haven/London, Yale University Press, 1990) ISBN 0-300-04527-1. Segal, Alan F., "Paul, the Convert and Apostle" in Rebecca's Children: Judaism and Christianity in the Roman World (Harvard University Press 1986). Horrell, David G. "An Introduction to the Study of Paul." T&T Clark Approaches to Biblical Studies. 2nd edition. London: T&T Clark, 2006 Marejeo mengine Bart D Ehrman. Peter, Paul and Mary Magdalene: The Followers of Jesus in History and Legend; 304 pages, Oxford University Press (Machi 2008) Bart D. Ehrman. The New Testament: A Historical Introduction to the Early Christian Writings; 608 pages, Oxford University Press (Julai 2011); ISBN 978-0-19-975753-4 Hyam MacCoby. The Mythmaker: Paul and the Invention of Christianity; 238 pages, Barnes & Noble Books (1998); ISBN 978-0-7607-0787-6 Hans Joachim Schoeps. Paul: The Theology of the Apostle in the Light of Jewish Religious History (Library of Theological Translations); 34 pages, Lutterworth Press (Julai 2002); ISBN 978-0-227-17013-7 Pinchas Lapide, Peter Stuhlmacher. Paul: Rabbi and Apostle; 77 pages, Augsburg Publishing House; (Desemba 1984) Pinchas Lapide, Leonard Swidler, Jurgen Moltmann. Jewish Monotheism and Christian Trinitarian Doctrine; 94 pages, Wipf & Stock Publishers (Mei 2002) Viungo vya nje Jewish Encyclopedia: Saul of Tarsus (known as Paul, the Apostle of the Heathen) Catholic Encyclopedia: Paul of Tarsus Catholic Perspective on Paul Documentary film on Apostle Paul Encyclopædia Britannica: Paul, 1911 Maps of Paul's three missionary journeys and final captive journey Novena to Saint Paul Apostle Paul's mission and letters From PBS Frontline series on the earliest Christians. Representations of Saint Paul "Saint Paul, the Apostle." Encyclopædia Britannica Online. 2009. The Apostle and the Poet: Paul and Aratus Dr. Riemer Faber The Apostle Paul's Shipwreck: An Historical Examination of Acts 27 and 28 Why Paul Went West: The Differences Between the Jewish Diaspora Biblical Archaeology Review Waliozaliwa 7 Waliofariki 67 Mtume Paulo P P Manabii wa Agano Jipya Mitume katika Ukristo Wamisionari Wafiadini Wakristo
2116
https://sw.wikipedia.org/wiki/Baada%20ya%20Kristo
Baada ya Kristo
Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani. Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK. Historia ya hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo" Hesabu hii ilianzishwa mwaka 527 BK na mmonaki Dionysius Exiguus alipokuwa Roma. Wakati ule mahesabu mbalimbali ya miaka yalikuwa kawaida. Mwaka uleule uliweza kuitwa kutokana na muda wa utawala wa Mfalme au Kaisari (kwa mfano: mwaka wa 5 wa Kaisari Iustiniano) na pia kuanzia tarehe ya kuundwa kwa mji wa Roma (kwa mfano: mwaka 1185 ab Urbe Condita = tangu kuanzishwa kwa mji). Mahesabu mengine yaliyokuwa kawaida wakati ule ni makadirio mbalimbali "tangu kuumbwa kwa dunia" na mengineyo. Dionysio baada ya kufanya utafiti alidhani Yesu alizaliwa mwaka 754 tangu kuanzishwa kwa Roma. Hesabu yake haijui mwaka "0"; tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu huchukuliwa kama mwanzo wa mwaka. Kwa hiyo moja kwa moja inaingia katika mwaka "1" na mwaka kabla yake ni mwaka 1 kabla ya Kristo = KK. Hii ndiyo sababu ya kwamba dunia karibu yote ilikosa kusheherekea mwaka 2000 kuwa mwanzo wa milenia mpya. Mwaka 2000 ulikuwa mwaka wa mwisho wa karne iliyoanza mwaka 1901; karne na milenia mpya zilianza mwaka 2001. Kosa la Hesabu ya Dionysio Hesabu ya Dionysio ilikosea miaka kadhaa. Ni kwa sababu wakati wake Dola la Roma lilikuwa limeshakwisha katika Italia, Kaisari alikaa Bizanti au Roma ya Mashariki. Kumbukumbu za Roma yenyewe hazikutunzwa tangu miaka mingi. Leo hii wataalamu wengi hukubaliana ya kwamba kasoro Ya Dionysio ni takriban miaka 4 - 8; yaani mwaka halisi wa kuzaliwa kwake Yesu ulikuwa kama miaka nne hadi nane kabla ya mwaka ambao tumezoea kuhesabu kama "1", kwa kuwa mwaka 4 K.K. ndipo alipokufa mfalme Herode Mkuu aliyejaribu kumuua akiwa mtoto mchanga. Wengi walijaribu kusahihisha kosa hilo lakini habari kamili kabisa haziwezi kupatikana, tena ni vigumu kubadilisha mahesabu yote, vitabu n.k. Uenezi wa Hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo" Mwanzoni hesabu ya Dionysio ilikuwa pendekezo la mtaalamu fulani tu, watu wakiendelea kutumia mahesabu yao mbalimbali. Miaka 60 baada ya Dionysio, Papa Bonifas IV, akiwa mkuu wa Kanisa Katoliki, alitumia tarehe zote mbili za "baada ya Kristo" na "tangu kuanzishwa kwa mji". Wataalamu walianza kutumia zaidi hesabu hiyo mpya. Mnamo mwaka 725 mtaalamu Beda Mheshimiwa alitunga kitabu "Kuhusu ugawaji wa wakati" (kwa Kilatini De Temporum Ratione) alikotumia mfumo ulioundwa na Dionysio akaendelea kuutumia pia katika kitabu kuhusu "Historia ya Kanisa". Kwa kuwa vitabu vya Beda vilikuja kutumiwa kote katika Ulaya ya Magharibi, vilichangia sana uenezi wa hesabu hiyo mpya. Wakati wa Karolo Mkuu, Mfalme (halafu Kaisari) aliyetawala Ufaransa pamoja na Ujerumani, Italia ya Kaskazini na maeneo ya Uholanzi na Ubelgiji, hesabu tangu Kristo ilikuwa rasmi kwa serikali. Lakini bado zilihitajika karne kadhaa hadi hesabu hii iwe imekuwa kawaida katika Ulaya. Kutokana na uenezaji wa uchumi, biashara na utawala wa Wazungu, hesabu "Baada ya Kristo" ilienea kote duniani. Siku hizi ni hesabu pekee katika nchi nyingi. Katika nchi mbalimbali inatumika sambamba na mahesabu mengine. Nchi mbalimbali za Kiislamu hutumia miaka tangu Hijra ya Muhammad (mwaka 622 BK), lakini mara nyingi pamoja na miaka ya hesabu ya Kikristo kwa ajili ya mambo ya biashara na mawasiliano ya kimataifa. Nchi ya Israeli inatumia kalenda rasmi tangu "kuumbwa kwa dunia", isipokuwa kando ya Kalenda ya BK kwa sababu zilizotajwa hapo juu kwa ajili ya nchi za Kiislamu. Japan inatumia hesabu ya miaka ya Kaisari yake - vilevile kando ya Kalenda ya BK. Namna za kutaja Hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo" Dionysio hakutumia msamiati "baada ya Kristo" - alisema "Anno Domini" ("mwaka wa Bwana") akimaanisha Dominus = Bwana ndiye Yesu. Hivyo kifupi katika lugha ya Kilatini ni "AD" kilichoingia pia katika Kiingereza na lugha nyingine kadhaa. Hata miaka kabla ya Kristo kwa Kiingereza huitwa kwa kifupi cha Kilatini "a. Chr" (ante Christum natum = kabla ya kuzaliwa kwake Kristo). Wengine hutumia "BC" = "before Christ". Tazama pia Anno Domini Historia Kalenda
2117
https://sw.wikipedia.org/wiki/Milenia
Milenia
Milenia (kutoka neno la Kiingereza millennium, ambalo mizizi yake ni katika Kilatini: mille, elfu, na annus, mwaka) ni kipindi cha miaka elfu moja. Hii ni sawa na kusema milenia ina karne kumi. Kwa sasa tuko katika milenia ya pili BK iliyoanza tarehe 1 Januari 2001. Lakini watu wengi walisheherekea tarehe 1 Januari 2000 ingawa mwaka 2000 ilikuwa mwaka wa mwisho wa karne na milenia iliyotangulia. ! Vipimo vya wakati
2118
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kaizari
Kaizari
Kaizari ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani "Kaiser", lakini asili yake ni Kilatini "Caesar". Asili ya Kiroma Asili ya cheo ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina likawa cheo. Cheo cha Kaizari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola la Roma ya Mashariki (Bizanti) hadi mwaka 1453. Ulaya Katika Ulaya yenyewe mfalme wa Wafaranki Karolo Mkuu alipokea cheo cha "Caesar" au Kaizari. Baadaye wafalme Wajerumani waliomfuata Karolo Mkuu katika sehemu ya mashariki ya ufalme wake waliendelea kutumia cheo hiki cha Caesar au Kaizari. Neno la Kaizari liliingia katika lugha ya Kiswahili wakati wa ukoloni wa Kijerumani huko Tanzania, kwa kuwa Austria na Ujerumani zilitawaliwa hadi mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia 1918 na wafalme wenye cheo cha "Kaizari". Vilevile mfalme wa Urusi alikuwa na cheo kilekile kilichoitwa "Tsar" kwa Kirusi, ilhali neno hili limeundwa pia kutoka "Caesar". Lugha za Kiingereza na Kifaransa zilitumia cheo tofauti cha macaesar wa Kiroma, ndicho "Imperator" (= mwenye amri, mwenye mamlaka, jemadari) kilichokuwa "Emperor" kwa Kiingereza au "Empereur" kwa Kifaransa. Nje ya Ulaya Kaizari ni cheo cha mfalme aliye juu ya wafalme wengine. Kutokana na uzoefu huu hata Shah wa Uajemi, Tenno wa Japani, Huangdi wa China na Negus Negesti wa Ethiopia hutajwa kwa cheo cha "Kaizari". Malkia Viktoria wa Uingereza alitumia cheo cha Kaizari ("empress") kama mtawala wa Uhindi tangu mwaka 1877. Wakati wa ukoloni mtawala mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani alikuwa Kaizari Wilhelm II wa Ujerumani; kwenye sarafu ya rupia alionyeshwa pamoja cheo kwa lugha ya Kilatini "imperator". Rais Jean-Bedel Bokassa alijitangaza kuwa Kaizari ("empereur") wa Afrika ya Kati mwaka 1977 akiiga mfano wa Napoleon Bonaparte aliyejiwekea taji la Kaizari ya Ufaransa mwaka 1804. Bokassa alipinduliwa mwaka 1979 na nchi kuwa jamhuri tena. Ufalme
2119
https://sw.wikipedia.org/wiki/Duma
Duma
Duma ni mnyama mbuai aliyemo katika jamii ya paka (Felinae) ambaye hupatikana Afrika na kidogo sehemu za Asia. Chakula chake ni wanyama jamii ya swala . Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgongo wa duma huwa kama alama ya "S", tofauti na mgongo wa chui. Macho ya duma yana weusi mkali ukilinganisha na chui. Manyoya yake yana rangi ya manjano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi. Rangi ya duma inashabihiana na mazingira yake ya mawindo hutegemea zaidi mbio na kuona ukilinganisha na wanyama wengine wawindaji ambao hutegemea kunusa na kuvizia katika mawindo yao. Ndiye mnyama anayeaminika kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko wanyama wengine watembeao kwa miguu: hukimbia kilometa 113 kwa saa. Wanapokua, madume hutembea peke yao katika makundi ya duma watatu au wawili. Wanajamiana na majike wanapokuwa kwenye joto tu na si vinginevyo. Picha Paka na jamaa Wanyama wa Afrika
2120
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hijra
Hijra
Hijra (هجرة) ni neno la Kiarabu linalomaanisha tendo la Mtume Muhammad la kutoka Makka na kuhamia Madina mwaka 622 BK. Mwaka huo umekuwa tarehe ya kuanzisha kalenda ya Kiislamu ambayo miaka yake huhesabu miaka baada ya hijra. Maana asili ya neno lenyewe ni "kuachana" au "kutengana", kutokana na historia ya Muhammad limechukua pia maana ya "kukimbilia" au "kuhamia". Historia ya Hijra Muhammad alianza kuhubiri habari za Qurani na za Uislamu katika mji wa Makka alipozaliwa na kuishi. Lakini hakupata wafuasi wengi. Kinyume chake kabila lake yeye mwenyewe la Waquraishi walimchukia na kumtesa kwani viongozi waliogopa ataharibu biashara kubwa iliyoletwa na Kaaba iliyokuwa kama hekalu ya kidini mjini. Hivyo Muhammad aliondoka Makka pamoja na babake mkubwa Abu Bakr; wafuasi wake kama 70 waliwahi kuondoka Makka siku zilizotangulia. Wote walipokelewa na watu wa Madina mji wa jirani. Hapo Madina Muhammad akawa kiongozi aliyekubaliwa na watu wengi katika miaka iliyofuata aliunganisha Waarabu katika Uislamu mwishowe akarudi Makka ambako Waquraishi walipaswa kumkubali yeye na dini ya Usilamu. Katika kumbukumbu ya Waislamu wa kwanza tendo la hijra lilikuwa jambo muhimu sana. Sura za Qurani zilipokusanywa kila moja imeandikwa kama imepatikana kabla au baada ya hijra. Kila sura inaonyesha chini ya kichwa chake maneno ama (imeteremka Makka) au (imeteremka Madina). Pia hesabu ya miaka ilianzishwa wakati wa khalifa wa pili Umar ikihesabu kuanzia tarehe ile ya kuhamia kwake Muhammad Madina. Uislamu
2121
https://sw.wikipedia.org/wiki/Adolf%20Hitler
Adolf Hitler
Adolf Hitler (Braunau, Austria, 20 Aprili 1889; Berlin, Ujerumani, 30 Aprili 1945) alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake. Alihutubia dharau na chuki ya kimbari dhidi ya watu wote wasio Wagermanik na hasa dhidi ya Wayahudi. Alisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia na mateso ya watu milioni kadhaa. Akitangaza shabaha ya Ujerumani Mkubwa alisababisha kushindwa na kugawiwa kwa taifa lake pamoja na kupotewa na maeneo makubwa, hasa upande wa mashariki. Maisha Utoto na familia Alizaliwa nchini Austria mwaka 1889. Wazazi wake walikuwa mtumishi wa forodha ya Austria Alois Hitler na mama yake Klara aliyekuwa mke wa tatu wa Alois. Adolf alikuwa na ndugu watano lakini kati yao ni dada yake Paula pekee aliyeishi kufikia umri wa mtu mzima, wengine wote walikufa mapema. Alikuwa pia na ndugu wawili kutoka ndoa ya mke wa pili wa baba na hao waliitwa Alois mdogo na Angela waliokaa katika familia ya Alois mzee baada ya kifo cha mama. Kutokana na kuhamishwa kwa baba mara kwa mara Adolf alisoma kwenye shule za msingi tofauti kati ya 1895 hadi 1899. Kuanzia mwaka 1900 alisoma kwenye shule ya sekondari mjini Linz lakini hakufaulu, alipaswa kurudia madarasa mawili. Hakupenda somo la dini, lakini alivutiwa na historia na jiografia. Baba alimpiga mara nyingi katika kipindi kile akikasirika juu ya kutofaulu shuleni. Baada ya kifo cha baba Alois mwaka 1903 mamake alimhamisha kwenda shule nyingine mjini lakini alishindwa hapa pia, akarudi nyumbani kwa mama bila ya kumaliza masomo yake. Alipokaa Linz Adolf alifahamika na mafundisho ya kiongozi wa chama cha "Alldeutsch" na hapa alianza kusikia habari za chuki dhidi ya Wayahudi na dharau dhidi ya mataifa ya Waslavi ya Ulaya. Tangu 1906 Hitler alijisikia kuwa msanii alipeleleza nafasi za kusoma uchoraji. Mwaka 1907 aliomba kupokewa katika chuo cha sanaa mjini Vienna, lakini alishindwa. Akarudi nyumbani baada ya kusikia mamake alikuwa mgonjwa wa kansa. Aliangalia nyumba hadi kifo cha mama kwenye Desemba 1907. Mama alitibiwa na daktari Eduard Bloch aliyekuwa Myahudi; Adolf alimshukuru sana kwa juhudi zake na baadaye alimlinda Bloch dhidi ya mateso yaliyoandaliwa kwa Wayahudi katika miaka ya 1930 baada ya Hitler kuwa mtawala wa Ujerumani na tangu 1938 wa Austria pia. Msanii asiyefaulu Vienna na Munich Tangu Januari 1908 alitumia urithi wa mama pamoja na pensheni ya mjane kwa kuhamia Vienna alipokaa hadi 1913. Alijaribu tena kupata nafasi kwenye chuo cha sanaa cha Vienna akashindwa tena. Mtu aliyeishi pamoja naye katika chumba kimoja alisema wakati ule Hitler alivutiwa zaidi na opera za Richard Wagner kuliko siasa. Tangu mwisho wa 1908 alihama mara kwa mara sehemu alipokaa akitafuta kupanga vyumba kwa bei nafuu zaidi; inaonekana matatizo ya pesa yaliongezeka. Miaka 1910-1911 alipaswa kuishi katika bweni la wanaume wasio na nyumba. Tangu 1910 Hitler alikuwa na mapato madogo kwa njia ya kunakili picha alizouza kupitia watu walioishi pamoja naye katika bweni. Wengine waliouza picha kwa niaba yake walikuwa Wayahudi lakini, tofauti na daktari wa mamake, hakuwapa usaidizi wowote baadaye: waliteswa kama Wayahudi wote baada ya kuvamiwa kwa Austria 1938. Hitler alisoma mengi wakati ule na hasa maandiko yaliyotangaza ubora wa mbari ya Kigermanik na chuki dhidi ya Wayahudi. Mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria, Ujerumani. Alikuwa amepokea hela kidogo kutoka urithi wa babake pia alitaka kujiondoa katika wajibu wa kufanya huduma ya lazima ya kijeshi katika Austria-Hungaria. Aliendelea kunakili picha na kuziuza kwenye maduka ya sanaa. Mnamo Februari 1914 alikamatwa na polisi ya Bavaria na kupelekwa Austria lakini huko iliamuliwa hafai kwa huduma ya kijeshi akarudi Munich. Wakati wa kukaa Munich alisoma maandiko ya Houston Stewart Chamberlain kuhusu ubaguzi wa kimbari. Mwanajeshi 1914 - 1918 Kuhamia kwake Munich kulifuatwa na vita mwaka 1914. Mnamo Agosti 1914, wakati wa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alijitolea kwa jeshi la Bavaria ambapo kutokana na bidii na ukakamavu wake alipanda cheo na kuwa praiveti. Mwisho wa vita mwaka 1918 alikuwa na cheo cha koplo. Hakupewa shughuli za kupigania maadui moja kwa moja bali sehemu kubwa ya vita alihudumia kama tarishi aliyebeba habari na barua kati ya maafisa wa ngazi ya juu na hivyo mbali kiasi na eneo la mapigano. Alijeruhiwa mwaka 1916 alipopigwa na kibanzi cha kombora na tena kwenye Oktoba 1918 alipoathiriwa na gesi ya sumu iliyosababisha kipindi cha upofu. Alikuwa hospitalini bado aliposikia habari za mapinduzi katika Ujerumani na azimio la kusimamisha vita tarehe 11 Novemba 1918. Kuingia siasa Mwezi Novemba 1918 Hitler alirudi Munich alipoendelea kuwa mwanajeshi hadi mwaka 1920. Munich iliona kipindi cha vuguvugu ya mapinduzi. Kwa muda alishiriki katika kamati zilizochaguliwa na wanajeshi na kuwawakilisha mbele ya serikali na maafisa. Munich iliona kipindi kifupi cha mapinduzi makali ambako viongozi wake walijaribu kuiga mfano wa Urusi. Kipindi hiki kilikwisha baada ya mashambulio ya sehemu za jeshi zilizofuata amri za serikali kuu ya Berlin. Sasa maafisa wa jeshi walioshika tena amri walipambana na mielekeo ya kikomunisti na kisoshalisti kati ya askari na wafanyakazi wa viwanda. Hapa Hitler aliteuliwa na wakuu wake kwa propaganda dhidi ya wanamapinduzi wasoshalisti. Alipelekwa kwa mafundisho ya kiitikadi akapewa mazoezi ya kuhutubia watu. Inaonekana ya kwamba ilikuwa katika kipindi hiki Hitler alipopokea mafundisho yaliyoimarisha itikadi ya chuki dhidi ya Wayahudi walioshtakiwa na wafuasi wa ufalme kuwa sababu ya kushindwa vitani pamoja na kuchochea mapinduzi. Hitler alitumwa pia na wakuu wake kama mpelelezi kuhudhuria mikutano ya kisiasa mjini. Hapa ilitokea ya kwamba kwenye Septemba 1919 alihudhuria mkutano wa chama kidogo na kichanga kilichojiita "Chama cha Wafanyakazi Wajerumani" (Deutsche Arbeiterpartei, DAP). Hitler alishiriki katika majadiliano akakaribishwa kujiunga na chama hicho. Aliomba kibali cha mkuu wake jeshini kwa hatua hii akawa mwanachama wa 55 wa chama hiki. Aliteuliwa kuwa katibu mwenezi wa DAP na chama kilianza kupokea zawadi kutoka matajiri waliomwona Hiler kama mhubiri mwenye kipaji kikubwa aliyepinga usoshalisti na ukomunisti. Mwezi Februari DAP ilibadilisha jina lake kuwa "Nationalsozialistische Deutsche Arbeiterpartei" (Chama cha Kizalendo - Kisoshialisti cha Wafanyakazi Wajerumani) kifupi NSDAP. Kwenye Aprili 1920 Hitler alitoka katika jeshi akipata riziki yake kwa njia ya kuhutubia mikutano alipolipwa. Sifa zake kama mhubiri zilijulikana kote Munich na alianza kuwasiliana pia na wanasiasa waliokuwa na mielekeo ya kufanana huko Berlin. Mwaka 1921 hatimaye aliweza kushinda viongozi wa awali katika chama na kuwa kiongozi mkuu wa NSDAP ambao hadi wakati ule bado ilikuwa moja ya vyama vingi vidogo vilivyotangaza siasa ya kizalendo dhidi ya ukomunisti na pia dhidi ya demokrasia. Jaribio la mapinduzi 1923 Hitler alivutiwa sana na mfano wa Benito Mussolini, kiongozi wa kifashisti wa Italia, aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma. Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya jimbo la Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin - lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku. Hitler akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Neville Chamberlain aliyedai kwamba kuna mbari mbalimbali za watu zenye tabia na thamani tofauti sana. Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("Mapambano Yangu") alimojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari. Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria", na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria. Kujenga chama Baada ya kutoka gerezani alirudi katika siasa. Aliahidi za kwamba atafuata sheria, hivyo chama cha NSDAP kiliruhusiwa tena. Hitler alisafiri kote Ujerumani akiunda matawi ya chama. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano. Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia. Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS" ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi na kuwa na wajibu hasa kumlinda Hitler. Chama chake hakikufaulu hadi 1929, wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya katika Mdodoro Mkuu. Mamilioni ya watu waliachishwa kazi na kuona njaa. Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali. Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu. Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% za kura na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge la Reichstag. Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933. Chansela na kiongozi wa Ujerumani Tarehe 30 Januari 1933 Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani. Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walikamatwa na kupelekwa katika makambi ya KZ. Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena. Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyoweka mipaka kwa ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa zaidi, akaanzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu" akipiga marufuku vyama vya upinzani. Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi. Siasa dhidi ya Wayahudi Chuki dhidi ya Wajerumani waliokuwa Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milioni 62. Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili. Kwa njia hiyo Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria" (ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini), "Wayahudi nusu" kama mzazi mmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwa katika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali. Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili. Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwelekeo huo uliongezeka. Hasa wanasayansi na wasanii wengi walihamia nchi huru. Siasa yake katika mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Vita Kuu ya Pili Hitler alifuata mwanzoni siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya katika Dola la Ujerumani. Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa kimataifa. Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba 1939 tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza na Ufaransa walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland. Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote. Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya, na inakadiriwa alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya) pamoja na watu vya mbari mbalimbali kama Wasinti (kati ya 200,000 na 1,500,000). Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee. Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti. Mwisho wa vita na kifo Maafisa wachache wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler. Tarehe 20 Julai 1944 kanali Stauffenberg alilipusha bomu katika ikulu ya Hitler pale Prussia ya Mashariki. Hitler alijeruhiwa lakini hakufa. Tangu Januari 1945 Hitler alihamia tena Berlin kutokana na uvamizi wa jeshi la Kirusi katika Ujerumani Mashariki. Hapa alikaa katika boma imara chini ya ardhi. Hakutoka mjini tena. Tarehe 20 Aprili alishehereka mara ya mwisho sikukuu yake na kupokea wageni wachache. Siku iliyofuata vikosi vya kwanza vya jeshi la Urusi vilianz kuingia katika maeneo ya Jiji la Berlin. Tarehe 25 Aprili 1945 Berlin yote ilizungukwa kama kisiwa na jeshi la Wasovyeti na tangu 28 Aprili waliingia katika kitovu cha Berlin. Hitler bado alikuwa na tumaini kwamba vikosi vya jeshi la Kijerumani kutoka magharibi vitafika Berlin lakini majaribio yote yalishindikana. Habari zilipokelewa Berlin ya kwamba makamu zake Hitler kama Himmler na Goering walijaribu kutafuta mapatano na Marekani au Uingereza. Hitler aliwatangaza ni wasaliti akaamuru kuwakamata lakini amri hizi hazikutekelezwa tena maana hawakuwa karibu naye. Katika hali hii Hitler alielewa ya kwamba hakuna njia ya kushinda na wataalamu hukubaliana ya kwamba hapo aliamua kujiua. Usiku wa 27 Aprili alimwoa mpenzi wake wa miaka mingi Eva Braun. Aliendelea kutunga wosia wake ambamo alimtaja mkuu wa jeshi la maji Karl Doenitz kuchukua madaraka yake kama mkuu wa dola na wa jeshi. Kwenye 29 Aprili jioni alipokea habari ya kwamba Benito Mussolini ameuawa huko Italia. Tarehe 30 Aprili aligawa sumu kwa wote waliokuwa pamoja naye katika boma chini ya ardhi akawaruhusu kuondoka; aliagiza sumu ijaribishwe kwa mbwa wake mpendwa "Blondi". Mnamo saa 15.30 Eva Brau alijiua kwa kumeza sumu na Hitler alipigia risasi kichwani. Wasaidizi wa mwisho walibeba maiti hadi bustani ya ikulu na kuziweka katika shimo kutokana na mlipuko wa bomu; hapa wakazichoma kwa petroli. Warusi waliingia saa chache baada ya vifo hivi. Walikuta maiti tarehe 5 Mei bila kutambua ni Hitler na Eva Braun. Tarehe 10 Mei msaidizi wa daktari wa meno wa Hitler aliweza kutambua maiti kutokana na meno. Mabaki yalizikwa baadaye karibu na makao makuu ya jeshi la Kirusi katika Ujerumani ya Mashariki; yalihamishwa mara kadhaa kila wakati makao makuu yalipohamishwa. Mwishoni mabaki ya maiti yalichomwa na Warusi tarehe 5 Aprili 1970, majivu yalisagwa na yote kutupwa katika mto mdogo karibu na mji wa Magdeburg. Taarifa hizi zilitunzwa kama siri kwa miaka mingi hadi mwisho wa Ukomunisti katika Urusi na hivi kulikuwa na uvumi wa kwamba Hitler hajafa na labda alikimbia hadi Amerika Kusini, jinsi idadi ya wasaidizi wake waliofaulu kutoroka. Marejeo Kujisomea zaidi Viungo vya nje Waliozaliwa 1889 Waliofariki 1945 Adolf Hitler Wanasiasa wa Ujerumani Wanasiasa wa Austria Historia ya Ujerumani Wanasiasa katika Historia ya Ujerumani Vita Vikuu vya Pili
2122
https://sw.wikipedia.org/wiki/Miaka%20baada%20ya%20hijra
Miaka baada ya hijra
Miaka baada ya Hijra ni hesabu ya miaka katika kalenda ya Kiislamu. Hesabu hii ilianzishwa miaka 17 baada ya tukio lenyewe (638 BK) kufuatana na azimio la Khalifa Umar ibn al-Khattab. Waarabu waliwahi kuwa na kalenda iliyotumia mwendo wa mwezi lakini hawakuhesabu miaka. Kila mwaka ulitajwa kutokana na tukio fulani. Mwaka wa kuzaliwa kwake Mtume Muhammad hujulikana "Mwaka wa Tembo" kwa sababu mwaka ule Makka ilishambuliwa na jeshi la Waethiopia lililokuwa na tembo wa kijeshi. Hata baada ya Muhammad desturi hii iliendelea. Mwaka wa Hijra wenyewe uliitwa "Mwaka wa kukubaliwa kwa safari," mwaka uliofuata "Mwaka vita ilipoamriwa," n.k. Wakati wa Khalifa Umar ilionekana haja ya kuwa na hesabu inayoeleweka zaidi, hivyo hesabu ya Hijra ikachaguliwa. Hesabu ya Kiarabu na Hesabu ya Kiajemi Waarabu Waislamu waliendelea kuhesabu miaka ya mwezi ya siku 29 au 30 kufuatana na kuonekana halisi kwa mwezi. Hivyo miaka ya Kiislamu ina jumla ya siku takriban 354. Mwaka huo wa Kiislamu una siku 11 pungufu kuliko siku zile 365 za mwaka wa jua katika kalenda ya Kikristo. Mwaka 2006 BK ni 1427 BH (baada ya Hijra). Uajemi hutumia hesabu ya miaka ya Hijra pamoja na mwaka wa jua. Hivyo mwanzo wa 2006 BK huko Uajemi ni mwaka 1384 BH (baada ya Hijra). Tazama pia Kalenda ya Kiislamu Kalenda
2127
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kalenda%20ya%20Kiislamu
Kalenda ya Kiislamu
Kalenda ya Kiislamu ni mtindo wa kuratibu wakati unaopatikana katika nchi mbalimbali za Kiislamu. Tofauti na kalenda ya kawaida inayofuata jua hii ni kalenda ya mwezi inayofuata kuandama kwa mwezi. Pia Waislamu wanaoishi katika mazingira yasiyo ya Kiislamu hutumia kalenda hii kwa ajili ya kupanga maisha yao ya kidini, hasa sikukuu na saumu. Kalenda hii ilianza kutumika rasmi kutokana na tukio la mtume Muhammad kuhama Makka kwenda Madina, tukio ambalo linajulikana kama Hijra. Mahali pengi Kalenda ya Kiislamu hutumika pamoja na kalenda zinazofuata mwendo wa jua, hasa kalenda ya Gregori ambayo ndiyo iliyoenea zaidi duniani. Miezi na mwaka Kalenda ya Kiislamu imepokea kawaida ya mwaka wa Waarabu wa kale wenye miezi 12. Hesabu ya vipindi hivi 12 hufuata muonekano wa Mwezi angani, ambayo ni tofauti na "miezi" katika kalenda ya kimataifa ambayo hayana uhusiano na kuonekana kwa Mwezi kwenye anga. "Mwezi" humaanisha kipindi kamili kati ya kuonekana kwa mwezi wa hilali mara ya kwanza hadi kurudia kwa kuonekana kwake. Kwa sababu muda huo ni siku 29.5, mwezi huhesabiwa kuwa na siku 29 au 30. Waislamu wanaofuata mfano wa Kisaudi hukubali kwamba mwezi mpya umeanza kama umeonekana kwa macho. Kwa sababu desturi hii imeleta matatizo ya kutokubaliana, pia ni rahisi kukadiria mwendo wa mwezi, nchi mbalimbali za Kiislamu hutumia makadirio ya kitaalamu kupanga tarehe za miezi. Idadi ya siku katika mwaka wa Kiislamu ni 354, kwa hiyo ni mfupi kuliko mwaka wa Jua wenye siku 3651/4. Kwa sababu hiyo sherehe zote za mwaka wa Kiislamu husogea polepole katika majira ya mwaka wa kalenda ya kiraia inayofuata Jua. Hesabu ya miaka Taz. makala "Miaka baada ya hijra" Hesabu ya miaka katika kalenda ya Kiislamu hufuta utaratibu wa "miaka baada ya hijra" yaani tangu kuhamia kwake Mtume Muhammad kutoka Makka kwenda Madina. Hijra ilitokea mwaka 622 BK au katika mwaka 1 wa hesabu yenyewe. Njia inayofuata inasaidia kujua takriban tarehe gani ya Kiislamu inalingana na tarehe ipi katika kalenda ya kawaida: K = (32H : 33) + 622 H = (33*(K - 622)): 32 mfano mwaka K= 2017 - 622 = 1395 * 33 = 46035 : 32 = 1438.6 K (Mwaka "baada ya Kristo" katika kalenda ya Kikristo), H (Mwaka "Baada ya Hijra" katika kalenda ya Kiislamu) Kalenda ya Kiislamu ya "Shamsi" ya Iran Huko Uajemi (Iran) na Afghanistan kuna mfumo tofauti wa kupanga wakati. Huko wanatumia kalenda ya jua wakihesabu muda wa mwaka ni siku 365 jinsi ilivyo katika kalenda ya Gregori. Kila mwaka unaanza mnamo tarehe 20 Machi ambayo ni sikusare ya machipuo yaani usawa wa muda wa usiku na mchana kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia. Ni kalenda ya Kiislamu kwa sababu inaanza kuhesabu miaka tangu hijra. Kalenda hii huitwa "Shamsi" (kutoka neno la Kiarabu / Kifarsi شمس shams = Jua). Kwa mfano, mwaka 1396 shamsi ya Iran inalingana na mwaka 1438 wa kalenda ya kawaida ya Kiislamu. Huko wanaita kalenda ya kidini "kalenda qamari" (yaani ya mwezi) na mara nyingi kuchapisha namba ya "mwaka qamari" kando ya "mwaka shamsi". Katika kupanga sikukuu za kidini hufuata kalenda qamari lakini sikukuu za serikali hufuata kalenda shamsi. Mwaka mpya katika kalenda hii inaanza kikamilifu wakati wa sikusare machipuo yaani tarehe 21 au 20 Machi ambayo ni maarufu kama sikuu ya Nowruz. Miezi Miezi yenye sikukuu muhimu ni hasa mwezi wa saumu wa Ramadhani, mwezi wa Haj wenye tarehe 10 ndiyo Idd el Hajj na mwezi wa Rabi' ul-auwali wenye tarehe 12 Idd-ul-maulidi yaani sikukuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (Maulidi-an-Nabii). Mwezi wa Muharram ni muhimu sana kati ya Washia wanaokumbuka mateso na kifo cha Imam Husain wakati wa mapigano ya Karbala. Majina na mfuatano wa miezi ni hivi: Muharram محرّم Safar صفر Rabi`-ul-Awwal (Rabi' I) ربيع الأول Rabi`-ul-Akhir (Rabi' II) ربيع الآخر أو ربيع الثاني Jumaada-ul-Awwal (Jumaada I) جمادى الأول Jumaada-ul-Akhir (Jumaada II) جمادى الآخر أو جمادى الثاني Rajab رجب Shaaban شعبان Ramadan رمضان Shawwal شوّال Dhul Qaadah ذو القعدة Dhul Hijjah ذو الحجة Siku za Juma au Wiki Kalenda ya Kiislamu hutumia juma au wiki ya siku saba jinsi ilivyo kawaida kwa Wayahudi na Wakristo. Siku muhimu zaidi ni Ijumaa ambako Waislamu hukusanyika kwa ajili ya sala ya pamoja. Kwa Kiarabu majina ya siku za juma hufuata hesabu ya Kiyahudi jinsi inavyoonekana katika Biblia. Jumapili inaitwa "siku ya kwanza", Jumatatu "siku ya pili" hadi "siku ya tano" = Alhamisi. Siku ya sita pekee imepewa jina jipya la Kiislamu kutokana na mkutano wa sala ya pamoja. Siku ya saba tena imebaki na jina lake la Kibiblia "Sabato" au siku ya saba. Hii ni kwa sababu utamaduni wa Kiarabu kabla ya Uislamu uliwahi kupokea athira nyingi kutoka kwa Wayahudi na Wakristo, pia walikuwepo Waarabu ambao upande wa dini walikuwa Wakristo na Wayahudi. Majina ya siku katika lugha ya Kiswahili yanaonyesha ya kwamba lugha ilianza katika mazingira ya Kiislamu kabisa, bila athira za moja kwa moja kutoka Uyahudi au Ukristo. Majina ya siku yamepangwa kufuatana na Ijumaa ambayo ni siku muhimu hasa katika maisha ya Kiislamu. Maana ya Jumamosi, Jumapili n.k. ni "Siku ya kwanza, pili, tatu" baada ya Ijumaa. Alhamisi imebaki na jina la Kiarabu. Jumapili: yaum al-ahad (siku ya kwanza) يوم الأحد Jumatatu: yaum al-ithnayna (siku ya pili) يوم الإثنين Jumanne: yaum ath-thalatha (siku ya tatu) يوم الثلاثاء Jumatano: yaum al-arba`a (siku ya nne) يوم الأَربعاء Alhamisi: yaum al-khamis (siku ya tano) يوم خميس Ijumaa: yaum al-jum`a (siku ya mkutano) يوم الجمعة Jumamosi: yaum as-sabt (siku ya sabato) يوم السبت Tanbihi Uislamu
2128
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa%20wa%20Lindi
Mkoa wa Lindi
Lindi ni jina la mji, wilaya na mkoa ulioko Kusini-Mashariki mwa Tanzania. Mkoa wa Lindi ni kati ya mikoa 31 iliyopo nchini Tanzania yenye postikodi namba 65000. Umepakana na mikoa ya Pwani, Mtwara, Ruvuma na Morogoro. Upande wa mashariki hupakana na Bahari Hindi. Eneo la mkoa Mkoa huu umeanzishwa mwaka 1971 na una eneo la km² 67,000. Karibu robo ya eneo lake au km² 18,000 ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Mkoa una wilaya sita za: Lindi Mjini, Mtama (hadi 2019 Lindi Vijijini), Kilwa, Nachingwea, Liwale na Ruangwa. Mito mikubwa ndiyo Lukuledi, Matandu na Mavuji, yote yaelekea Bahari Hindi. Mwinuko huanza mwambaoni ukipanda hadi mita 500, hakuna milima mirefu. Wakazi Mwaka 2022 idadi ya wakazi ilikuwa 1,194,028. Karibu asilimia 90 kati hao ni wakulima. Makabila makubwa zaidi ni Wamwera, ambao wanapatikana hasa wilaya ya Nachingwea na Lindi vijijini katika kata za Rondo, halafu Wamachinga, Wamalaba ambao wako zaidi Lindi mjini, Wamatumbi na Wangindo huko Kilwa. Wakazi kwa wilaya ni (idadi katika mabano): Kilwa (171,850), Lindi Mjini (41,549), Lindi Vijijini (215,764), Liwale (75,546), Nachingwea (162,081), Ruangwa (124,516), Hali ya hewa Hali ya hewa ya Lindi ni ya joto mwaka wote ikiwa na wastani kati ya sentigredi 24,5 na 27. Mkoa hupokea kati ya mm 980 na 1200 za mvua kwa mwaka, hasa kati ya miezi ya Novemba na Mei. Miundombinu ya mawasiliano Kuna barabara chache katika hali nzuri. Ndizo km 155 za barabara ya lami na km 3567 za barabara ya mavumbi, mara nyingi katika hali mbaya. Wakati wa mvua mara kwa mara njia ya kwenda Daressalaam imefungwa. Kuna matumaini ya kuboreka kwa mawasiliano na jiji la Daresalaam tangu kumalizika kwa daraja la Rufiji. Kwa sasa barabara ya kutoka Mingoyo mpaka Dar es Salaam imekamilika kwa kiwango cha lami, kimebaki kipande cha kilometa 60 tu kuanzia Muhoro, wilaya ya Kilwa, mpaka kukaribia daraja la Mkapa juu ya mto Rufiji ambacho kinamaliziwa kwa kiwango cha lami. Kuna kiwanja cha ndege Lindi, Nachingwea na Kilwa Masoko. Lindi na Kilwa Masoko kuna pia bandari. Huduma za simu zimepata maendeleo kiasi tangu kuanzishwa kwa simu za mkononi. Utalii haujafikia umuhimu sana kutokana na matatizo ya mawasiliano magumu, ingawa Lindi ina sehemu mbalimbali zenye uwezo wa kuwavuta watalii: Kilwa Kisiwani ndio mji wa kihistoria wa pwani ya Afrika ya Mashariki pamoja na magofu ya miji mingine ya Waswahili, Selous ni hifadhi kubwa kabisa katika Afrika, ufuko wa mchanga ni wa kuvutia sana, nafasi za zamia majini ni tele. Gesi iliyopatikana baharini karibu na kisiwa cha Songosongo imeleta matumaini ya maendeleo. Kilimo na biashara Mkoa wa Lindi wakazi wake wengi ni wakulima, hasa maeneo ya vijijini wengi wanalima mazao mchanganyiko, yaani ya biashara na chakula. Mazao ya biashara hasa ni korosho, ambazo zinapatikana kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa, Lindi Vijijini, na Nachingwea, pia kuna zao la ufuta na ndizi kama zao la biashara na chakula pia. Mazao ya chakula kuna mahindi, mpunga, muhogo, nyanya, vitunguu: hizi pia hulimwa sana wakati wa masika kutegemea na mvua za vuli. Biashara wakazi wengi wa mkoa wa Lindi wanafanya biashara, hasa biashara ndogondogo zijulikanazo kama "machinga trade": wanauza mazao wakati wa mavuno na huchukua bidhaa nyingi kutoka Dar es salaam na kupeleka vijijini hasa kwenye kata. Elimu Mkoa wa Lindi huko nyuma kielimu kwani shule za sekondari mpaka sasa si nyingi sana na shule hizo hazina walimu wa kutosha kutokana na miundombinu ya barabara na shule zenye kidato cha tano na cha sita mpaka sasa ni Lindi sekondari - Lindi, Mahiwa na Namupa seminari - Lindi vijijini. Pia kuna chuo cha ualimu Nachingwea katika wilaya ya Nachingwea. Majimbo ya bunge Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo: Kilwa Kusini : mbunge ni Selemani Ally Bungara (CUF) Kilwa Kaskazini : mbunge ni Ngombare Edgar (CUF) Lindi Mjini : mbunge ni Hassan Suleiman Kaunje (CCM) Liwale : mbunge ni Zuberi Kuchauka (CCM) Mtama : mbunge ni Nape Nnauye (CCM) Mchinga : mbunge ni Hassan Bobali (CUF) Nachingwea : mbunge ni Hassan Elias Masala (CCM) Ruangwa : mbunge ni Kassim Majaliwa (CCM) Tazama pia Orodha ya milima ya mkoa wa Lindi Orodha ya mito ya mkoa wa Lindi Tanbihi L Mkoa wa Lindi
2131
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilwa
Kilwa
Kilwa ni jina la wilaya na mahali patatu katika mkoa wa Lindi, Tanzania. Wilaya ya Kilwa iko kati ya Dar-es-salaam na Lindi ufukoni wa Bahari Hindi. Kilwa Masoko ni makao makuu ya wilaya. Kilwa Kivinje ni mji wa kihistoria tangu karne ya 18. Kilwa Kisiwani ni kisiwa karibu na mwambao kinachotazama Kilwa Masoko. Hapo ndipo Kilwa ya kihistoria iliyojulikana kama mji mkubwa wa pwani ya Afrika ya Mashariki tangu nusu ya kwanza ya karne ya 14 BK kutokana na taarifa ya msafiri Ibn Battuta. Pamoja na mabaki ya mji wa Songo Mnara, magofu ya Kilwa Kisiwani yameandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage). Kuna pia kata inayoitwa Kilwa katika Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga, Tanzania. Viungo vya nje Makala zinazotofautisha maana
2135
https://sw.wikipedia.org/wiki/Keremkerem
Keremkerem
Keremkerem ni ndege wa familia ya Meropidae. Wana mwili mwembamba wa rangi maridadi. Mdomo wao ni mrefu na mwembamba na mkia wa aina nyingi za keremkerem una mileli mirefu katikati. Ndege hao wanaishi uwandani kwa kanda ya tropiki na nusu-tropiki ya Afrika, Ulaya na Asia. Hula wadudu, nyuki, manyigu na mabunzi hasa, ambao wanakamatwa hewani. Kabla ya kula, ndege anatoa mshale wa mdudu akimgongea tawi la mti au kitu kigumu kingine. Keremkerem hupenda kuwa pamoja kwa makundi. Huchimba mashimo ndani ya kando za mchanga kwa kutaga mayai yao meupe. Familia ya Meropidae imegawika katika nusufamilia mbili: Nyctyornithinae (keremkerem wenye ndevu) na Meropinae (keremkerem wa kawaida). Spishi za Afrika Merops albicollis, Kerem Koo-jeupe (White-throated Bee-eater) Merops apiaster, Kerem wa Ulaya au Polohoyo (European Bee-eater) Merops boehmi, Kerem wa Böhm (Böhm's Bee-eater) Merops breweri, Kerem Kichwa-cheusi (Black-headed Bee-eater) Merops bulocki, Kerem Koo-jekundu (Red-throated Bee-eater) Merops bullockoides, Kerem Paji-jeupe (White-fronted Bee-eater) Merops gularis, Kerem Mweusi (Black Bee-eater) Merops hirundineus, Keremberere (Swallow-tailed Bee-eater) Merops malimbicus, Kerem Kidari-chekundu (Rosy Bee-eater) Merops mentalis, Kerem Masharubu-buluu (Blue-moustached Bee-eater) Merops muelleri, Kerem Kichwa-buluu (Blue-headed Bee-eater) Merops nubicoides, Kondekonde Kusi (Southern Carmine Bee-eater) Merops nubicus, Kondekonde Kaskazi (Northern Carmine Bee-eater) Merops oreobates, Kerem Kidari-marungi (Cinnamon-chested Bee-eater) Merops orientalis, Kerem Kijani (Green Bee-eater) Merops persicus, Kerem Mashavu-buluu (Blue-cheeked Bee-eater) Merops pusillus, Kerem Mdogo (Little Bee-eater) Merops revoilii, Kerem Somali (Somali Bee-eater) Merops superciliosus, Kerem Kiole (Olive Bee-eater) Merops variegatus, Kerem Mkufu-buluu (Blue-breasted Bee-eater) Spishi za Asia Meropogon forsteni (Purple-bearded Bee-eater) Merops leschenaulti (Chestnut-headed Bee-eater) Merops ornatus (Rainbow Bee-eater) Merops philippinus (Blue-tailed Bee-eater) Merops viridis (Blue-throated Bee-eater) Nyctyornis amictus (Red-bearded Bee-eater) Nyctyornis athertoni (Blue-bearded Bee-eater) Picha Viogajivu na jamaa
2137
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mto%29
Pangani (mto)
Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia hapa Pangani Mto Pangani ni kati ya mito mikubwa ya Tanzania. Unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari ya Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani. Jina Mto unapita katika maeneo ya jumuiya zenye lugha tofautitofauti, hivyo kuna majina mbalimbali. Katika karne ya 19 kabla ya ukoloni mwendo hadi maporomoko karibu na Hale (Mnyuzi) ulijulikana zaidi kama "Ruvu", na sehemu ya mwisho kuanzia maporomoko hadi bahari kwa jina "Pangani" kutokana na mji ulipofikia baharini . Kwenye ramani za zamani za ukoloni majina yote mawili yalitumika kandokando: "Ruvu" na "Pangani". Ramani za zamani za uhuru wa Tanzania mara nyingi huwa na maandishi "Pangani or Ruvu River". . Siku hizi imekuwa kawaida kutumia jina "Pangani" kuanzia bwawa la Nyumba ya Mungu. Beseni la mto Beseni la Pangani ni eneo la km2 43,650. Karibu yote imo Tanzania isipokuwa kuna km2 3,914 huko Kenya katika mazingira ya Taveta. Jumla ya wakazi katika beseni la Pangani ni milioni 3.7. Chanzo cha mto Pangani ni maungano ya matawimto Kikuletwa na Ruvu inayokutana leo katika lambo la Nyumba ya Mungu kusini kwa Moshi. Mto Kikuletwa hupokea maji kutoka Mlima Meru na mitelemko ya Kilimanjaro upande wa kusini. Ruvu hupokea maji kutoka mitelemko ya Kilimanjaro upande wa mashariki pamoja na Ziwa la Jipe. Mto Pangani unaendelea km 432 hadi Pangani mjini unapoingia katika Bahari Hindi. Kwenye sehemu ya kwanza baada ya Nyumba ya Mungu mto unaitwa wakati mwingine bado "Ruvu". Uzalishaji wa umeme kwenye mto Pangani Kuna mahali pawili ambako malambo yametengenezwa kutumia umememaji ya mto Pangani Nyumba ya Mungu pale ambako matawimto ya Ruvu na Kikuletwa yanakutana Maporomoko ya Pangani karibu na Hale (kata ya Mnyuzi, Korogwe) Vituo vya umeme vimeathiriwa vibaya na kupungukiwa kwa maji mtoni. Hifadhi ya mazingira na kupungukiwa kwa maji Mto Pangani unategemea misitu panapokusanywa maji yake. Misitu hii imepungua sana kutokana na uenezaji wa mashamba, kukatwa kwa miti kwa ajili ya makaa na matumizi ya ubao. Vilevile machafuko yamekuwa hatari kwa ajili ya afya ya mto na watu wanaotegemea maji yake. Asili ya machafuko ni hasa kilimo, mvua hupeleka mbolea mtoni na kusababisha kukua kwa wingi wa majani yasiyotakika. Uvuvi umezidi vilevile hadi kuhatarisha samaki. Tazama pia Mito ya Tanzania Orodha ya mito ya mkoa wa Kilimanjaro Orodha ya mito ya mkoa wa Manyara Orodha ya mito ya mkoa wa Tanga Tanbihi Viungo vya nje Pangani Basin - A Situation Analysis (Kiingereza, PDF) Ramani (Kiingereza) Geonames.org Mito ya Tanzania Mkoa wa Tanga Mkoa wa Kilimanjaro Mkoa wa Manyara Mto Pangani Bahari ya Hindi
2138
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rhapta
Rhapta
Rhapta ni jina la soko na mji wa kale katika pwani la Afrika ya Mashariki. Habari zake zilipatikana tangu karne ya kwanza katika mwongozo wa kigiriki kwa ajili ya mabaharia. Jina la Rhapta lilitajwa tena katika vitabu vingine hadi karne ya 6 BK lakini baadaye lilipotea au kubadilishwa. Wataalamu walio wengi hukubaliana ilikuwepo ufukoni wa Tanzania lakini hakuna uhakika kuhusu mahali pake kamili. Kuna kisio la kuwa Rhapta ni jina la kale la Pangani lakini hiyo ni kisio tu kutokana na bandari nzuri ya kiasili inayopatikana pale Pangani. Wengine wanaona Tanga au mdomo wa mto Rufiji ilikuwa mahali pa Rhapta. Kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea kilichoandikwa mnamo mwaka 70 BK kinataja Rhapta kuwa soko kuu la Azania barani pia kituo cha mwisho kati ya miji na vituo vilivyofanya biashara na dunia ya Kiroma. Mnamo mwaka 200 mwandishi Mmisri Claudius Ptolemaius anataja Rhapta kuwa mji mkuu wa Barbaria (Afrika ya Mashariki barani). Rhapta ilikuwa mdomoni wa mto mwenye jina la Rhapta pia ambao uliaminika kuwa na asili yake katika "Milima ya Mwezi". Mdomo wa mto ulikuwa karibu na kisiwa cha Menouthis. Hakuna uhakika kama kisiwa hiki ni Pemba au Mafia. Sarafu za kiroma za karne za kwanza BK zimepatikana mahali mbalimbali za pwani; zinathebitisha kuwepo kwa biashara kati ya dunia ya Kiroma na Azania wakati ule. Kufuatana na Periplus biashara ilikuwa ya pembe ya ndovu na gamba la kobe. Historia ya Afrika
2140
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani%20%28mji%29
Pangani (mji)
Pangani ni mji wa Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania, uliopo ufukoni mwa Bahari Hindi kati ya Dar es Salaam na Tanga ukielekea pande zote mbili za mdomo wa mto Pangani. Leo hii ni mji mdogo mwenye wakazi karibu 8n000 na makao makuu ya Wilaya ya Pangani. Lakini ina historia ndefu, hasa kwa sababu kuna bandari nzuri ya kiasili mdomoni wa mto wa Pangani inayofaa kwa jahazi ndogo. Majengo mbalimbali ya kale ni ishara ya historia ndefu ya mji huu. Pamoja na Boma, lililojengwa na Waarabu wa Unguja na kutumiwa na wakoloni wa Kijerumani na wa Kiingereza, kuna nyumba za Waswahili. Eneo la mji limegawiwa kwa kata mbili ambazo ni Pangani Mashariki (pamoja na mji wa kihistoria) na Pangani Magharibi. Jiografia Mji wa Pangani uliundwa kando la hori ya Bahari Hindi mahali ambako mto Pangani unakwisha. Hori ina upana wa kilomita 5 ikiingia barani kilomita 2.5. Mdomo wa mto Pagani una upana wa mita 300 - 500 kwa kilomita kadhaa ndani ya nchi kavu na hivyo ni bandari salama kwa jahazi ndogo. Mji wa Pangani ulianzishwa upande wa kaskazini wa mdomo huo uko kwenye pwani katikati ya visiwa vya Unguja na Pemba. Bandari ya Pangani inafikiwa na jahazi ndogo jinsi zilivyokuwa kawaida kwenye pwani la bahari Hindi. Ndani ya mdomo wa mto merikebu zilikuwa salama hata wakati wa dhoruba baharini. Uzuri wa bandari hii ulikuwa msingi kwa kustawi kwa mji kama kituo cha safari kwenye pwani na mahali pa biashara kati ya bara na visiswa vya karibu vya Unguja (50 km) na Pemba (75 km). Sehemu hii ya pwani ilifaa kama chanzo cha njia ya misafara kufuata bonde la mto Pangani kuelekea Kilimanjaro (290 km) na ndani zaidi. Mazingira ya Pangani inapokea milimita 100 - 1100 kwa mwaka , inayotosha kwa kilimo kwenye kanda la pwani. Kwenye mpangilio wa tabianchi wa Koeppen hii inatazamiwa kama "Aw", yaani tabianchi ya kitropiki ya savana. Historia Pangani ni moja ya miji ya kale ya Waswahili kwenye pwani la Bahari Hindi. Pangani kuwa Rhapta? Wataalamu kadhaa waliochungulia habari za kale walipendekeza ya kwamba mji wa Rhapta ulikuwa sawa na au karibu na Pangani ya leo. Mji huu wa Rhapta unajulikana kutokana na kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea kilichoandikwa mnamo mwaka 70 B.K. Lakini Pangani ni mahali pamoja kati ya patano palipotajwa kuwa mahali pa Rhapta ya kale, hakuna uhakika. Kipindi cha utawala wa Zanzibar Pangani ilikuwa mji muhimu katika utamaduni wa Waswahili. Katika karne ya 19 BK biashara ya misafara kati ya eneo la maziwa makubwa na Zanzibar ilipita mara nyingi hapa; Bidhaa kutoka zanzibar zilipelekwa Pangani na kugawiwa kwa wapagazi wa misafara. Makundi ya watumwa waliobeba ndovu wakati wa kurudi walihamishwa hapa kwenye boti ziizowapeleka hadi soko la watumwa Zanzibar. Tangu uhamisho wa ikulu wa Waarabu wa Omani kuja Zanzibar Pangani iliona maendeleo ya kiuchumi. Makabaila walijipatia mashamba makubwa wakalima miwa wakitumia kazi ya watumwa. Kupanda na kushuka kwa Pangani katika kipindi cha ukoloni Hata kwa wapelelzi wazungu waliofika Zanzibar kwa meli kubwa Pangani ilikuwa mara nyingi mlango wa kungia Afrika bara. Pangani ilikuwa sehemu ya kanda ya pwani iliyokabidhiwa na Sultan Bargash kwa kampuni ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki ya Karl Peters. Mwaka 1889 Pangani ilikuwa mahali palipoanzia vita vya Bushiri dhidi ya utawala wa Wajerumani. Mwakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki Emil von Zelewski alimtendea liwali wa Sultani kwa ukali uliosababisha ghasia ya watu wa Pangani na kuanzisha Vita ya Abushiri. Baada ya kukomeshwa kwa vita hii umuhimu wa Pangani ulipungua sana kwa sababu meli kubwa kutoka Ulaya hazikuweza kuinghia katika mdomo wa mto Pangani, mizigo na abiria walipaswa kuhamishwa kwa boti ndogo kutoka meli hadi mjini. Hivyo Wajerumani walikazia maendeleo ya Tanga penye bandari ya kina kirefu. Hadi sasa Polepole Pangani imerudi nyuma. Uhaba wa mawasiliano na barabara uliongeza mwendo huu. Hadi leo hakuna barabara ya lami kabisa katika wilaya yake. Miaka ya nyumba mahoteli mbalimbali katika mazingira ya Pangani yameanza kutumia nafasi nzuri kwa utalii mwambaoni. Marejeo Miji ya Tanzania Waswahili Mkoa wa Tanga Wilaya ya Pangani
2141
https://sw.wikipedia.org/wiki/William%20Tyndale
William Tyndale
William Tyndale alikuwa mwanatheolojia Mwingereza, kasisi ya kanisa na mtaalamu aliyetafsiri Biblia mara ya kwanza katika Kiingereza cha kisasa. Alizaliwa huko Gloucestershire mnamo mwaka 1494 - aliuawa Vilvoorde (Brabant - Ubelgiji ya leo) tarehe 6.9.1536. Tafsiri yake ya Biblia ilikuwa toleo la kwanza lililochapishwa kwa kutumia mitambo mapya ya uchapaji vitabu. Mawazo yake yalipingwa kwa nguvu zote na watawala na watu wa dini yalionekana kama upinzani wa kidini hivyo aliamua kukimbilia Ujerumani kwa usalama wake, huko alitafuta mchapishaji aliyetoa nakala ya kwanza ya Agano Jipya kwa lugha ya kingereza nakufuatiwa baadaye na agano la kale. Askofu Kardinali Wolsey alimtangaza kuwa mzushi. Lakini ilikuwa tendo la kupinga ndoa na talaka za mfalme wa Uingereza Henry VIII ilikuwa sababu ya kifo chake. Henry VIII alikasirika juu ya Tyndale akamwomba Kaisari Karl V wa Ujerumani kumkamata. Tyndale alishikwa huko Brussels (mji chini ya Kaisari wakati ule) akasoimamishwa mbele ya mahakama iliyotoa hukumu ya mauti kwa sababu ya uzushi dhidi ya kanisa katoliki. Katika mji wa Vilvoorde penye gereza lake alifungwa mtini akachongwa na mwili wake kuchomwa motoni. Historia ya Ukristo Kiingereza