BUFFET / xlsum /swahili /xlsum_1_21_dev.tsv
akariasai's picture
Upload 147 files
2fbc8cc
raw
history blame
1.56 kB
text: Mama yake Isla-Rose anasema ''hakutarajia'' kumpeleka mwanae kwa daktari wa meno akiwa na umri mdogo Mama wa Isla-Rose Heasman, Jasmin kutoka Plymouth Devon nchini Uingereza, alisema ''hakutegemea'' kuwa angempeleka binti yake kwa daktari wa meno katika umri mchanga. ''Ilibidi atolewe jino, ilikuwa inaogopesha.Alikuwa jasiri kuliko mimi, hakulia kabisa,''Alieleza Kituo hicho cha tiba ya meno kimesema kuwa Isla-Rose ni ''mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi'' kuwahi kutokea, na alipatiwa beji kama zawadi Watoto wengi huota meno wanapofikia umri wa miezi sita wengine wakiwa na miezi na wengine mpaka baada ya mwaka mmoja. Isla-Rose alipatiwa dawa ya kumkinga na maumivu kabla ya kutolewa jino, alipatiwa zawadi kwa kuwa alikuwa jasiri ''Ilinibidi nitoke nje ya chumba nikiwa nalia kwa sababu sikuweza kuvumilia kutazama mwanangu akiwa katika maumivu. Daktari wa meno alimpatia Isla-Rose zawadi ya karatasi yenye maandishi kama zawadi ya kuwa shujaaa Kwa mujibu wa shirikisho la wataalamu wa afya ya meno nchini humo,BDA, takriban mtu mmoja kati ya 2000 huzaliwa wakiwa na jino. Huwa yanalegea kwa sababu mizizi ya meno inakuwa bado haijaimarika. Profesa Damien Walmsley, anasema: ''hali hiyo inaweza kusababisha matatizo ya kunyonyesha,ulimi wa mtoto kupata vidonda, na hatari ya jino kuchomoka na kuingia kwenye mapafu ya mtoto.Hata hivyo changamoto hizi ni nadra kutokea Jino lilitolewa na kuwekwa kwenye mkebe kwa ajili ya familia kwenda nalo nyumbani Mtoto mchanga wa kike aliyezaliwa akiwa ameota jino moja ameng'olewa jino hilo akiwa na siku 12.