text
stringlengths
0
24.2k
label
class label
6 classes
Na BENJAMIN MASESE MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, amewatahadhirisha wananchi kutodhubutu kupewa pipi na mtu yeyote ndani ya gari binafsi au basi la abiria. Amesema  baadhi ya pipi hizo hupakwa dawa za kulevya na kusababisha kupoteza fahamu. Amesema tayari madhara ya ulaji wa pipi yalimkuta mtumishi mmoja wa Serikali ambaye alipewa pipi ndani ya basi na kujikuta akizinduka akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekeo Toure, akipatiwa matibabu. Tahadhari hiyo aliitoa alipozungumza na wananchi wa Kata za Igoma na Kishili kuhusu  mambo mbalimbali ya ulinzi na usalama ndani ya wilaya ya Nyamagana. Tesha ambaye hakutaka kutaja jina lake la mtumishi huyo aliyekula pipi lakini alidokeza cheo chake kuwa ni mkurugenzi. Alisema  alipewa pipi na abiria mwenzake aliyekuwa jirani na muda mfupi alisinzia na kupoteza fahamu. “Naombeni wananchi tuwe na tahadhari sana juu ya ulaji wa vitu  ndani ya vyombo  vya usafiri, hili nalisema wazi kwani limekuwa likijitokeza. “Hivi karibuni kuna mtumishi mmoja alikuwa anasafiri  ambako alipopewa pipi na abiria mwenzake kumbe ilikuwa imepakwa dawa za kulevya. “Mtumishi huyo ambaye tena ni mkurugenzi alijikuta akizindukia Sekeo Toure, hajui alifikishwa vipi katika hospitali hiyo. “Epukeni ulaji wa pipi pia kwa sababu umekuwapo   utapeli kwa njia ya simu nao umeendelea kutikisha nchi na watu kuibiwa mamilioni ya fedha,”alisema. Tesha alizungumzia  suala la wana wanafunzi  waliofaulu  mtihani  wa darasa la saba akiwaonya wazazi  watakaoshindwa kuwapeleka kuanza kidato cha kwanza watafikishwa mahakamani. Alisema ifikapo Januari 31, 2017 ataanza ziara ya kutembelea shule zote ndani ya Nyamagana  kubaini wanafunzi walioshindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza na kuwachukulia hatua wazazi wao. Wananchi wa Igoma na Kishili walimweleza DC  kwamba   kumekuwapo na kero ya kukatika daraja la Fumagila linalounganisha wilaya za Misungwi na Nyamagana na kusababisha wananchi kushindwa kwenda shule hasa   mvua inaponyesha. Akitoa majibu, alisema tayari Serikali imetenga Sh milioni 300 kwa ajili ya kujenga daraja la Fumagila na kuwataka wazazi kuwasindikiza wanafunzi na kuwavusha upande wa pili  mvua inaponyesha.
1kitaifa
ASHA BANI-DAR ES SALAAM WAUAJI wilayani  Rufiji Mkoa wa Pwani ‘wamembipu’ Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon  Sirro, kwa kuua mtu mwingine usiku wa kuamkia jana katika Kitongoji cha Kazamoyo Kijiji cha Ikwiriri Kaskazini wilayani humo. Wauaji hao   walivamia  kijijini hapo   na kumpiga risasi shingoni,  Erick Mwarabu (38) ambaye ni  fundi rangi. Kwa mujibu wa mtoa taarifa,  Mwarabu akiwa nyumbani kwake   saa 8.00 usiku juzi, wauaji hao walifika na kumpiga     risasi   shingoni ambayo ilitokea kichwani upande wa kulia   kati  ya jicho na sikio na akafariki dunia papo hapo.   Mkuu wa  Wilaya ya Rufiji,  Juma Njwayo, aliithibitishia MTANZANIA  kwa  simu kwamba tukio hilo la mauaji lilitokea usiku wa kuamkia jana. Alisema   tayari mwili wa marehemu umekwisha kufanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake  kwa mazishi. Kifo cha Mwarabu kinafanya   idadi ya watu waliouawa   hadi sasa katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani kufikia 30. Kutokana na vitendo hivyo vya mauaji, hivi karibuni IGP Sirro, alitangaza mkakati wake ikiwamo jinsi ya kukomesha mauaji katika maeneo hayo.   IGP Sirro aliapa kupambana na wauaji hao huku akiahidi donge nono la   Sh milioni 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kuwezesha kukamatwa wauaji hao. Alisema polisi  wanaendelea na operesheni mbalimbali  kuhakikisha  vitendo hivyo haviendelei na kwamba lazima watafanikiwa kubaini mzizi wa mauaji hayo. Mei 21  mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alitembelea eneo hilo na kuteta na askari wa operesheni maalumu ya kuwasaka wauaji wilayani Kibiti.  Alisema  mauaji hayo sasa yametosha akisisitiza  Serikali haitakuwa tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea kama ilivyo  Somalia. Ziara hiyo ya ghafla ya Waziri Nchemba ilitokana na   mauaji ya mara kwa mara ya raia  ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana. Akizungumza baada ya kuwatembelea   polisi  katika kambi maalumu ya operesheni ya kusaka wahalifu katika Kata ya Bungu, alisema  Serikali  imejipanga kukomesha hali hiyo kwa sababu kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama. “Tunaendelea kufuatilia kazi   mnayoendelea kufanya,   tuendelee kusonga mbele. Nikiziangalia takwimu na mwenendo, nazidi kupata maswali na naendelea kuona kuwa kuna kamchezo kanachezwa.  “Mauaji haya waliyoyafanya inatosha. Lazima tuwatie nguvuni, hatuwezi kuruhusu jambo hili likaendelea na kamchezo haka kakaendelea. “Anayefanya mauaji haya, anayeshirikiana na anayeshangilia hiki kinachofanyika wote tunawaweka katika kundi moja. Kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama,”alisema. Nchemba  aliwataka polisi hao kukaa kimkamkati kuwakamata wauaji hao. Alisema ni muhimu polisi waondokane na dhana kwamba wametokomea kusikojulika bali wawakamate.
1kitaifa
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa ikipokea wagonjwa wengi wa moyo kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati na 217,016 wameshahudumiwa. Kaimu Mkurugenzi wa Upasuaji wa JKCI, Dk Angela Swai, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.Alisema wagonjwa hao wamepatiwa huduma hiyo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Wapo wagonjwa kutoka Zimbabwe, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi, Ethiopia na hata katika visiwa vya Comoro ambao wamekuwa wakipatiwa huduma hapa ikiwamo za shida za mishipa ya moyo iliyoziba.”“Gharama sio kubwa sana hata kwa wagonjwa wanaotoka nje ya nchi, hatujazitofautisha sana na wagonjwa wa ndani, gharama hizo ni sawa na zile anazotoa mgonjwa anayetibiwa katika hospitali za binafsi,” alisema.Alisema ni muhimu wananchi wakatambua huduma za moyo zinazotolewa katika taasisi hiyo na kuchukua hatua pindi wanapobaini kuwa na shida za aina hiyo. Dk Angela alisema tangu kuanzishwa kwa JKCI Septemba 2015, imekuwa ikihudumia wagonjwa kutoka mikoa yote nchini ambao wamekuwa wakipewa rufaa kutoka hospitali za mikoa kwa ajili ya kupata huduma ya kiwango cha juu cha tiba ya moyo.“Wagonjwa katika taasisi hii hupata huduma za matibabu za kibingwa za magonjwa yote ya moyo zikiwamo za upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua, urekebishaji wa mfumo wa umeme wa moyo, tiba ya mishipa ya damu na utayarishaji wa wagonjwa wanaokwenda kupandikizwa figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” alisema.Kuhusu viwango vya vifo katika taasisi hiyo kila upasuaji unaofanyika, alisema JKCI hufanya uchunguzi kwa mwezi kwa wagonjwa waliofariki, jambo ambalo huwasaidia kujitathmini zaidi kiutendaji. Lengo la tathmini hii ni kujipima katika ufanisi wa utoaji wa huduma za upasuaji wa moyo na kuweza kujipanga zaidi kwa huduma zilizo bora kwa kipindi kingine.Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Moyo katika taasisi hiyo, Dk Tulizo Sanga, alitoa mfanokuwa, kwa kipindi cha miaka mitatu imeweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje ya nchi 217,016, huku waliolazwa wakiwa ni 11,587 na waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua ni 1,098.Alisema hali hiyo inatokana na kuwapo kwa huduma madhubuti zinazotolewa na wataalam wazalendo wanaofanya kazi ya kuwahudumia wananchi wenye matatizo na wasio na matatizo ya moyo kwa kutoa mada mbalimbali zinazowasaidia kujikinga na maradhi hayo.
1kitaifa
Vijana, licha ya kufungwa na Pazi vikapu 82-76 bado inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 ikifuatiwa na JKT yenye pointi 13, ambayo iliifunga Jogoo kwa vikapu 68-55 lakini pia ikafungwa na Ukonga vikapu 54-47.Oilers inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo sita na kushinda yote, ABC ambayo iliifunga Mabibo vikapu 60-50 inashika nafasi ya tano baada ya kucheza michezo saba, ikishinda mitano na kupoteza miwili.Ukonga Kings inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo saba, ikishinda mitano na kufungwa miwili, Jogoo inashika nafasi ya nane licha ya kufungwa na Kigamboni vikapu 71-63 ikiwa imecheza michezo saba, kushinda minne na kupoteza mitatu na kujikusanyia pointi 11.DonBosco Youngstars inashika nafasi ya tisa ikiwa imecheza michezo sita na kushinda minne na kufungwa miwili na ina pointi 10, Mabibo Bullets inashika nafasi ya kumi baada ya kucheza michezo saba, ikashinda mitatu na kufungwa minne na kukusanya pointi 10.Kurasini Heat inashika nafasi ya 11 ikiwa imecheza michezo nane, ikashinda miwili na kufungwa michezo sita na kukusanya pointi 10, Magnet ipo nafasi ya 12 ikiwa imecheza michezo saba, ikashinda mitatu na kufungwa minne na kujikusanyia pointi 10 Kigamboni inashika nafasi ya 12 ikiwa imeshuka dimbani mara nane na kushinda mchezo mmoja na kukusanya pointi nane, UDSM Insiders ambayo iliifunga Tanzania Prisons vikapu 66-56 ikiwa ni ushindi wa kwanza baada ya kucheza michezo saba ina pointi nane na Magone inaburuza mkia ikiwa na pointi nane baada ya kucheza michezo nane na kufungwa yote.Kwa upande wa timu za wanawake, Ukonga Queens inaongoza msimamo ikiwa na pointi nane, DonBosco Lionesses inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi saba sawa na JKT Stars, Jeshi stars ina pointi tano sawa na Oilers Princesses na Vijana Queens inaburuza mkiwa ikiwa na pointi nne.
2michezo
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeelezea masikitiko yake kutokana na kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ikisema ameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mihayo Juma N’hunga wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika duniani kote jana. N’hunga alisema Dk Mengi atakumbukwa kwa mambo mengi mema akiwa miongoni mwa wawekezaji wa mwanzo kuitumia fursa ya kuanzishwa vyombo vya habari nchini.Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa imesaidia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo ajira kwa waandishi wa habari wanaomaliza elimu kwa viwango mbalimbali. “Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar natoa salamu za masikitiko kufuatia kifo cha mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi ambaye ametumia muda wake mwingi katika kuwekeza kwenye sekta ya habari na ajira,” alisema Naibu Waziri N’hunga.Aliwataka waandishi wa habari na wawekezaji wengine kuiga mfano wa Mengi aliyetumia utajiri wake kwa ajili ya uwekezaji na kutoa ajira kwa watu wengine. “Watu wengine ikiwemo matajiri waige mfano wa Mengi katika kutumia utajiri wake kwa ajili ya kuwanufaisha wengine,” alisema. Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Hassan Mitawi alisema baraza litamkumbuka Mengi kwa ushirikiano wake mkubwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vimetoa mchango wa hali ya juu katika uhuru wa vyombo vya habari.Alisema wakati waandishi wa habari wakiadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wanatakiwa kukumbuka mchango wa Dk Mengi aliyesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari nchini. “Mengi tutamkumbuka kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari nchini sambamba na uhuru wa taaluma hiyo ikiwemo kutoa ajira kubwa kwa waandishi wa habari,” alisema. Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) Zanzibar, Dk Mzuri Issa alisema taaluma ya uandishi wa habari imepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Dk Mengi.
1kitaifa
Na CHRISTOPHER MSEKENA STAA wa filamu za Kibongo Irene Uwoya, ameendelea kugonga vichwa vya habari za burudani baada ya mume wake, Hamad Ndikumana aliyefunga naye ndoa ya Kikristo kufariki dunia mapema wiki hii akiwa nyumbani kwake, Kigali nchini Rwanda. Kwa wiki tatu mfululizo Uwoya amekuwa hakuauki kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa tukio aliloliita ni ndoa ya Kiislamu aliyofunga na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz  Chende ‘Dogo Janja’, ndoa ambayo Janjaro alithibitisha siyo filamu, licha ya Uwoya kudai ni filamu. Mfululizo wa tukio la ndoa mpya na msiba wa mume wake, Ndikumana yamepokewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki wake. Wapo waliompa pole huku wengine wakimtusi. Wanaomtusi wanahusisha tukio lake la ‘ndoa tata’ na Janjaro kuwa huenda limemuumiza Ndikumana kiasi cha kupata mshtuko wa moyo na kupoteza maisha. Hata hivyo, kwa jumla wengi wameonyesha kuguswa na msiba huo na kuonyesha hisia zao. Katika kundi hilo ambalo lina watu wengi zaidi, wamekwenda mbali zaidi na kuumizwa kwa msiba huo kiasi cha kufananisha na pigo alilopata mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady baada ya kufiwa na aliyekuwa mumewe Ivan Don. NDOA Uwoya aliolewa na kocha huyo msaidizi wa Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda mwaka 2009 na katika maisha yao ya ndoa walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume   aitwaye Krish, ambaye amekuwa akiishi naye jijini Dar es Salaam. Upande wa Zari, naye alifunga ndoa ya kimila na mfanyabiashara wa Uganda, Ivan Ssemwanga ‘Ivan  Don’  miaka mingi iliyopita na katika maisha yao ya ndoa walifanikiwa kupata watoto watatu wa kiume. CHANGAMOTO NDANI YA NDOA Mwezi uliopita, Uwoya na mzazi mwezake marehemu Ndikumana, walianza kutupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii ambapo Ndikumana alitoa malalamiko kwa mrembo huyo kuwa katika maisha yao hakuwa mkweli ikiwa ni pamoja na kumnyima haki ya kumsalimia mtoto wao, Krish anayeishi Bongo na yeye akiwa anaishi Rwanda. Malalamiko hayo, Uwoya aliyakanusha na zaidi aliendelea kufanya mitikasi yake ikiwa ni pamoja na kula bata nchini China hata aliporejea nchini, Octoba 27, mwaka huu akadai kufunga ndoa na Dogo Janja, jambo ambalo lilionekana kutomuumiza Ndikumana. Alichofanya Ndikumana ni kujibu mashambulizi kwa kumtangaza mpenzi wake mpya wa Kinyarwanda, aliyemtaja kwa jina la Asmah na kuendelea na maisha yake ya furaha huku akionyesha kutokuwa na presha na ndoa ya Uwoya na Dogo Janja kwani mrithi wake  aliweza kurudisha tabasamu lake lililopotea. Hiyo ilikuwa Oktoba 31, mwaka huu. Upande wa Zari, raia huyo wa Uganda aliachana na mume wake Ivan Don mwaka 2014 baada ya kunasa kwa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambapo mpaka sasa wamepata watoto wawili, Tiffah na Nillan. Zari alikuwa karibu mno na watoto wake aliozaa na Ivan Don licha ya vijana hao wa kiume kuishi na baba yao Uganda na Afrika Kusini lakini hakuwahi kuonyesha nia ya kumrudia mumewe zaidi ya kuboresha panzi lake jipya na Diamond Platnumz. Ivan Don kwa muda wote huo akiwa mbali na mke wake alionyesha kuwapenda watoto wake, kusimamia miradi yake iliyopo Afrika Kusini na Uganda pamoja na kula bata na kundi lake la Rich Gang bila kuwa karibu na mrembo mwingine. VIFO VYA WAUME ZAO Kifo cha Ndikumana kimetokea ghafla usiku wa kuamkia Jumatano ya wiki hii, akiwa nyumbani kwake. Inadaiwa alipata tatizo la maumivu ya kifua kabla ya mauti kumkuta. Siku nzima kabla ya kifo chake alikuwa mzima,  hata jioni yake alikuwa mazoezini akiwanoa wachezaji na yeye mwenyewe akishiriki mazoezi. Afisa Habari wa klabu hiyo aitwaye Gwakaya alisema Ndikumana alipata maumivu makali ya kifua na akaomba soda ya baridi, alipomaliza kunywa kidogo akatapika kisha akakata kauli hivyo anadhaniwa amekufa kwa ugonjwa wa moyo. Ndikumana ni baba wa watoto wawili wa kiume Baasit na Krish. Alizikwa Jumatano kwenye mjini Nyamirambo, Rwanda. Kifo cha Ivan Don, kilikuja baada ya tajiri huyo kuugua na Zari kushiriki katika kumuuguza kwenye Hospitali ya Stive Biko Academy, Afrika Kusini mpaka alipofariki kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo, Mei 25, mwaka huu na kuzikwa Nakarilo, Uganda. UWOYA AVISHWA VIATU VYA ZARI Kama unavyoona hapo juu, matukio yaliyotokea kwenye maisha ya Zari yanawiana kidogo na yale yaliyomtokea Irene Uwoya kwa kuwa wote waume zao wamepoteza maisha baada ya ndoa zao kuvunjika. Mungu ailaze roho ya marehemu Hamad Ndikumana mahali pema peponi – Amina.
4burudani
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora inahitaji mwekezaji ajenge kiwanda cha tumbaku.Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adam Malunkwi amesema ofisini kwake mjini Urambo kuwa, tumbaku ni zao mama na linalimwa katika kila eneo wilayani humo.Amewaeleza waandishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, Halmashauri hiyo imetenga eneo la kujenga kiwanda hicho na linafikika kwa kuwa miundombinu ipo, na pia kuna umeme na maji.“Kwa hiyo tukipata mwekezaji anayeweza kusaidia kujenga kiwanda cha tumbaku utakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwenye wilaya yetu ya Urambo na maandalizi ya awali kama nilivyosema tulishayaweka vizuri. Kwa hiyo hilo ndiyo ningeomba liwe la kwanza katika vipaumbele vyetu kwa upande wa viwanda” amesema Malunkwi.Amesema, Urambo pia inahitaji mwekezaji wa pembejeo za kilimo kwa kuwa hilo limekuwa tatizo kubwa katika eneo hilo.“Upatikanaji wa pembejeo za kilimo kama tunaweza tukapata mwekezaji mzuri akadhamini jambo hili kwa uhakika katika mkoa wetu wa Tabora hasa wilaya yetu ya Urambo inaweza kutusaidia. Na pembejeo zinazosumbua ni hizo za zao la tumbaku na zao la mahindi”amesema.Makunkwi amesema, Urambo pia inahitaji mwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa maeneo yapo na kuna fursa za kutosha.“Kama tunaweza tukapata wawekezaji katika masuala ya umwagiliaji tuna imani kabisa masuala ya kilimo hasa mpunga tunaweza tukalima mara mbili kwa mwaka, watu wanaweza wakalima bustani za vitunguu, nyanya na mazao mengine ambayo yanaweza yakasaidia vipato kwa wananchi wetu wa wilaya ya Urambo” amesema.Kwa mujibu wa Malunkwi, Urambo pia imetenga eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo.
0uchumi
Anna Potinus – Dar es Saaam Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), wametangaza kushirikiana na kampuni ya Wasafi Ltd katika kupeleka ujumbe kwa jamii kuhusiana na suala la afya kupitia tamasha la Wasafi festival ambapo wasanii watapata fursa ya kutoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 10, katika ofisi za Tacaids zilizopo Posta jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi na mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’, amesema lengo kuu la ushirikiano huo ni kuangalia ni namna gani wasanii wanaweza kutumia vipaji vyao kuelimisha jamii. “Tuliona tuandae tamasha la Wasafi festival ambalo litatukutanisha na kutumia sanaa yetu katika njia zilizo sahihi hivyo tukaona sasa imefikia muda kutumia ushawishi tulionao na katika kulifanikisha hilo tukasema tukishirikiana na Tacaids pengine tutafikisha ujumbe mzuri zaidi,” amesema. “Hauwezi kutimiza ndoto zako kama hauna afya bora hivyo tukiwa kama wasanii ambao Mungu ametupa Baraka za ushawishi tunaweza tukafikisha ujumbe kwa wenzetu wakatuelewa hivyo tumeshirikiana na Tacaids katika kuwaelimisha vijana namna ya kutumianafasi tulizonazo katika njia chanya zitakazoleta maendeleo katika nchi yetu,” amesema. Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tacaids, Jumanne Issango, amesema vijana ndio kipaumbele katika katika mapambano dhidi ya ukimwi na kwamba ndio kundi lenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi “Utafiti uliofanyika 2016/17 unaonyesha kwamba maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kundi la vijana kati ya miaka 15-24 wanachangia asilimi 40 ya maambukizi mapya kati ya maambukizi ya idadi ya watu 72,000 kitaifa kwa mwaka hivyo baada ya kuzindua utafiti huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwa Tume kutumia wasanii kufikisha ujumbe na elimu ya VVU na Ukimwi na kuhamasisha suala la upimaji kwa vijana,” amesema Issango. “Majukwaa ya wasanii ni mengi lakini mwaka huu tumebahatika kushirikiana na Wasafi tumeambiwa takribani wasanii 20 wana ushawishi hivyo tumeona ni fursa nzuri katika kuwafikishia ujumbe vijana juu ya maambuziki ya virusi vya ukimwi, eneo muhimu ambalo tutaliwekea msisitizo ni pamoja na matumizi ya Condom, upimaji na sasa hivi vijana wako katika mtandao kwahiyo tutahakikisha tunatumia akaunti za wasanii hawa kupitishia jumbe,” amesema Issango. Aidha Issango amesema kupitia tamasha hilo wanatarajia kuwafikia vijana milioni 15 na kutakuwa na utoaji wa elimu, ugawaji wa condom na vipeperushi vitakavyokuwa na maelezo juu ya maambukizi hayo ambapo ametoa wito kwa wasanii wengine kufuata mfano wa wasafi wa kutoa elimu juu ya maambikizi ya ukimwi.
5afya
CHAMA cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) kimeibana serikali ya Afrika Kusini, kikiitaka iwalinde raia wa mataifa ya Afrika wanaoshambuliwa, kuuawa na kuharibiwa mali katika mashambulizi ya kibaguzi.Msimamo huo wa CPA ulitangazwa bungeni jana na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alipozungumzia maazimio ya Mkutano wa Mabunge wanachama wa CPA uliomalizika Zanzibar hivi karibuni. Ndugai alisema wanachama na washiriki wa mkutano huo aliosema umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya washiriki kuliko miaka mingine, wamesaini azimio maalumu kuhusiana na msimamo wao huo.“Tumesaini andiko la pamoja lenye tamko ya kulaani na kupinga mauaji yanayofanyika Afrika Kusini yanayojulikana kama Xenophobia (Ubaguzi kwa wageni). Tumepinga vikali ukatili huu unaofanywa kwa Waafrika wenzetu. Tumewataka viongozi wa serikali ya Afrika Kusini kuchukua hatua za haraka za kuwalinda raia wa kigeni kutoka mataifa ya Afrika,” alisema Ndugai. Alieleza kuwa jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa raia hao wa Afrika Kusini hawaui wazungu, wala wahindi au wageni wengine weupe bali walengwa ni waafrika.“yaani waafrika sasa tunauana wenyewe kwa wenyewe,” Alisema ukatili na unyama unaoendelea kufanywa na raia hao wa Afrika Kusini hauwezi kuachwa ukaendelea kuota mizizi na ndio sababu wabunge wa CPA wameamua kufikisha andiko lao kwa viongozi wa Afrika Kusini.
1kitaifa
KUTOKANA na kuongezeka kwa abiria katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kuanzia Jumatatu wiki ijayo, litaongeza safari za Dar es Salaam-Moshi kutoka nne kwa wiki (mbili kwenda na mbili kurudi) hadi sita.Hatua hiyo inatokana na mahitaji makubwa yaliopo tangu treni ya abiria irejee kufanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi Ijumaa Desemba 6, mwaka huu baada ya miaka 25 ya kusitishwa, ambapo kwa safari moja zaidi ya abiria 500 walisafiri.Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema jana kuwa mahitaji yameongezeka tangu kuanza kwa safari hizo, hasa kutokana na sherehe za mwisho wa mwaka, hivyo wanaangalia namna ya kuongeza safari ili kukidhi mahitaji.“Mpangilio wetu tangu turejeshe safari za abiria ni kwenda Moshi mara mbili na Dar es Salaam mara mbili, inayofanya safari nne kwa wiki. Sasa tunataka iwe mara sita, ‘discussion’ (majadiliano) inaendelea hivi sasa,” alisema Kadogosa.Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRC, Focus Sahani alipoulizwa, alifafanua kuwa wanasubiri idhini ya mkurugenzi mkuu waongeze safari hizo Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kwa kuwa mahitaji yameongezeka na kufanya lazima ya ruti tatu kwenda na tatu kurudi kutoka mbili kwenda na mbili kurudi za awali.“Mahitaji yapo mpaka Kigoma na Mpanda katika sherehe hizi za mwisho wa mwaka. Lakini kwa hii ya kaskazini, tumepanga kuongeza ruti tatu badala mbili na mabehewa mawili kutoka tisa na tunasubiri idhini ya DG (mkurugenzi) malengo yetu ni kuanza next week (wiki ijayo) Jumatatu,” alisema Sahani.Sahani alifafanua kuwa ruti moja ya kulala inabeba abiria 72, na daraja la pili kukaa ni mabehewa mawili yanayobeba abiria 120 huku daraja la tatu likiwa na mabehewa matatu yanayobeba abiria 240 na kufanya idadi ya abiria 432.Alisema kuna behewa moja ambalo ni hoteli na baa. Hata hivyo, alisema abiria hupanda na kushuka njiani na abiria wa Moshi hawapendi kusongamana, hivyo abiria wengi hupenda kukaa na wachache wanaopanda njiani kwa safari fupi kama Pugu, Korogwe, Kidomole baadhi husimama na kufanya idadi kufikia kati ya 550 hadi 600 kwa ruti moja.Kuhusu mapato, Sahani alisema wanashirikiana na maofisa wa TRC wa Moshi na Dar es Salaam kuweka sawa hesabu. Aliahidi ataeleza mapato hayo tangu kuanza kwa safari leo.Alisema nauli ya kukaa ni Sh 16,500 ikilinganishwa na mabasi Sh 32,000 na daraja la kulala ni Sh 39,000 na daraja la tatu ni Sh 10,700. Usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, ulisitishwa mwaka 1994 na treni ya mizigo ya Dar es Salaam- Arusha ilisitishwa 2007 na kurejea Julai mwaka huu huku ya abiria ikirejeshwa Desemba 6, mwaka huu.
1kitaifa
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Haji Manara amewaponda wote waliokuwa mstari wa mbele kumshawishi Ramadhani Singano kuikacha timuhiyo na kuhamia Azam kufuatia mchezaji huyo kuwa kwenye orodha ya majina ya wachezaji wa Azam waliochwa msimu huu. Manara amesema Singano alishauriwa vibaya na kutoa onyo kwamba iwe funzo kwa vijana wadogo wanaonyanyukia kisoka ili kutengeneza mustakabli mzuri wa maisha yao ya baadaye. “Mguu wake wa kushoto ulikuwa kama kijiko,ni dribbler mzuri na ana akili nyingi but alishauriwa hovyo na wanaojiona wajuaji,matokeo yake leo Azam wanakwenda kumuacha (sio kosa lao).” “Iwe funzo kwa vijana wadogo wanaonyanyukia kisoka,hawa wajuaji sidhani hata kama wanajishughulisha nae tena!! Nikuombe dogo utulie naiamini miguu yako, soon utarejea ktk uwezo wako na cc klabuni tulishakusamehe kwa yale maneno uliolishwa utubeze na wajuvi feki,” ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram. “Bado ni mchezaji mwenye akili nyingi, uwezo wake hasa wa kutumia mguu wa kushoto na maamuzi ya haraka, hivyo ni muda sahihi kutulia kabla ya kurejea kwenye ubora licha ya kuachwa na Azam FC,” amesema. Messi aliachana na Simba msimu wa mwaka 2014-15 na kujiunga na Azam FC ambapo usajili wake ulizua sintofahamu kutokana na mvutano uliokuwa baina ya mchezaji huyo na Simba, ikidaiwa kuwa bado alikuwa na mkataba na klabu hiyo. Maoni ya mashabiki na wadau mbalimbali  
2michezo
NEW YORK, MAREKANI MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amesema mtoto wake, Royalty, amembadilisha kitabia na mfumo wake wa maisha kwa sasa. Awali msanii huyo alikuwa akitumia muda mwingi kufanya mambo yasiyo na maana kwa jamii na familia yake, lakini tangu alipoanza kumlea mtoto huyo amekuwa na mabadiliko makubwa katika maisha yake. “Royalty amekuwa na mchango mkubwa wa kubadilisha maisha yangu, kutokana na hali hiyo ninatakiwa kumfanyia kila kitu ambacho anapaswa kufanyiwa. “Maisha yangu ya sasa yamekuwa ya kiutu uzima ila haya yote yanatokana na kuitwa baba,” alieleza Chris. Msanii huyo kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Zero’, wiki iliyopita aliachia albamu yake mpya ‘Mix tap’ yenye wimbo alioshirikiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Rihanna.
4burudani
Derick Milton – Simiyu Meneja wa Wakala wa Mejengo ya Serikali (TBA), mkoani Simiyu Mhandisi Loishorwa Naunga amesema kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi majengo mawili ya upasuaji mkubwa mionzi na maabara katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo miezi miwili kabla ya muda wa mkataba wake ambao ni Oktoba mwaka huu. Akizungumza na Mtanzania leo Mei 23, Naunga mesema kuwa majengo hayo yanayojengwa kwa gharama za sh.Bilioni 3.5 ambapo mpaka sasa wamepokea kiasi cha sh. Bilioni 1.6 “Tunategemea kama serikali itatuletea kiasi cha pesa kilichobaki tuna uhakika kuwa mwezi Agosti tutakamilisha ujenzi mzima kabla ya muda wa mkataba, ” amesema. Mganga mafawidhi wa hospitali hiyo Dk. Matoke Muyenjwa amesema kuwa kasi ya mkandarasi ni kubwa na wanategemea kukabidhiwa majengo mapema kabla ya muda wa mkataba. Dk. Muyemjwa amesema kuwa katika jengo la maabara mkandarsi amekamilisha ujenzi huku jengo la mionzi na upasuaji likiwa kwenye hatua za ukamilishwaji wake.
1kitaifa
Mholanzi huyo amepoteza kazi saa chache baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na Uganda, The Cranes juzi katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN).Katika mechi hiyo ya kwanza ya kuwania kufuzu kwa fainali hizo za mwakani nchini Rwanda, Stars ilipoteza kwa kipigo hicho kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar mbele ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo ilikuwa na kikao chake cha kawaida saa chache kabla ya mechi hiyo iliyochezwa usiku.Saa chache baada ya mechi, TFF ilitoa taarifa ikieleza kuhusu kikao hicho na kwamba imeamua kusitisha ajira ya Mholanzi huyo aliyepewa mkataba wa miaka miwili kuanzia Aprili mwaka jana.“Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo (jana) pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.“Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo; ajira ya Kocha Mkuu Mart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia tarehe 21 Juni, 2015,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa benchi lote la Ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia jana na punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa litatangazwa.Kabla ya mechi hiyo, baada ya kelele za wadau kuzidi, TFF ilimpa masharti kocha huyo kwa kueleza kuwa mechi dhidi ya Uganda ambayo marudio yatakuwa wiki mbili zijazo jijini Kampala, ilikuwa kipimo chake cha mwisho na akishindwa kuipeleka timu Rwanda 2016, atafukuzwa kazi.Hiyo ilitokana na Stars kupoteza mechi zote tatu za makundi za michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini ambako ilialikwa mwezi uliopita, na kipigo dhidi ya Misri katika kufuzu kwa Afcon 2017, kilifuatia matokeo hayo mabaya.Mechi ya juzi ilikuwa ya tano mfululizo kwa Nooij kupoteza na kufanya acheze mechi 18 tangu aajiriwe na kati ya hizo, ameshinda mechi tatu tu, akitoka sare saba na kupoteza mechi nane.Mholanzi huyo aliyezaliwa Julai 3, 1953 mjini Beverwijk, akiitwa Martinus Ignatius au maarufu kwa jina la Mart Nooij, aliwahi kuwa Mkufunzi wa Chama cha Soka cha Uholanzi, na amewahi kufanya kazi Marekani na Kazakhstan.Alikuwa kocha wa timu ya vijana ya Burkina Faso ya miaka 20 katika Kombe la Dunia mwaka 2003 kabla ya mwaka 2004 kuwa kocha msaidizi wa muda wa FC Volendam ya Uholanzi. Mwaka 2007, aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Msumbiji, na akiwa na timu hiyo ilifuzu kwa fainali za Afcon mwaka 2010 baada ya kuzikosa kwa miaka 12.Baada ya kushindwa kufuzu kwa fainali za Afcon za 2012, Nooij alijiuzulu kazi hiyo Septemba 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani Gert Engels.Aprili 19, 2012, aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Santos, lakini akafukuzwa Desemba 18, mwaka huu.Novemba 2013, Nooij aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Saint George ya Ethiopia na miezi mitano baadaye, alikubali kuifundisha Tanzania kuanzia Aprili 25, 2014 akichukua nafasi ya Kim Poulsen wa Denmark.Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa anatajwa kuwa mrithi wa muda wa Nooij atakayeiongoza Stars katika mechi ya marudiano nchini Uganda, kabla ya kuteuliwa kwa kocha wa kudumu.
2michezo
WANANCHI wenye makazi na wanaofanya shughuli zao kwenye hifadhi za wanyama wilayani Songwe, wametakiwa kuhama kutoka maeneo hayo kwa kuwa si salama na yanahatarisha maisha yao kutokana na uwapo wa wanyama wakali. Kwa mujibu wa ofisa maliasili kata ya Kapalala, wilayani Songwe, Benard Nenje, kumekuwapo na matukio mengi ya wakazi wa maeneo yaliyo jirani na hifadhi kushambuliwa na wanyama sambamba na kuharibiwa mali zao ikiwamo mazao shambani.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Nenje alisema kwa mwaka jana pekee, wananchi 24 walipata madhara ya kuvamiwa na wanyama, ambapo kati yao 22 wanatokea kata ya Gua na wawili kata ya Ngwala ambao serikali ililazimika kuwalipa fidia kutokana na mazao yao kuliwa na tembo. Alisema kwa mwaka huu wananchi 30 wanatakiwa kulipwa fidia kutokana na tembo kula mazao yao na wengine kujeruhiwa na simba na fisi.Ofisa huyo alisema asilimia kubwa ya wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi wanakuwa hawaelewi madhara yake hivyo kujikuta wakijenga makazi na kujishughulisha na kilimo bila kuujulisha uongozi wa kijiji pamoja na kata ili kupata utaratibu. “Watu hao wamekuwa wakijeruhiwa na wanyama wakali wakiwamo simba pamoja na mazao yao kuliwa na tembo jambo linaloigharimu serikali kuwalipa fidia kutokana na kosa walilofanya wenyewe,” alisema.
1kitaifa
VIONGOZI wa dini kwa pamoja na wadau mbalimbali katika ngazi tofauti tofauti jijini Dar es Salaam wamepewa elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola.Maeneo waliyojifunza ni namna ya kujikinga, kutoa taarifa na hata kutoa msaada kwa watakaokuwa wameathirika. Aidha chini ya utaratibu huo, wahudumu wa afya ngazi ya jamii, watapita nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya afya kwa ngazi ya jamii kuhusu athari za ugonjwa huo, ambao hadi sasa haujaingia nchini.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tafiti za Afya, mkoa wa Dar es Salaam na Msimamizi wa Uelimishaji wa Ugonjwa wa Ebola, Dk Ndeniria Swai alisema elimu hiyo kwa viongozi ni muhimu kwa sasa, muda ambao ugonjwa huo haujaingia nchini ili kuwa na utayari.Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na elimu hiyo kuratibiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu (Redcross) nchini.Akizungumza, Dk Ndeniria alisema mafunzo hayo yanalenga kufanya kazi kwa pamoja na kada mbalimbali ili kufikisha elimu kuhusu athari za ugonjwa wa ebola, namna ya kukabiliana nao pindi utakapotokea, ilikuepusha maambukizi kwa walio wengi.Shehe Seif Sadiki Muyenga kutoka Kigamboni, alisema elimu hiyo kwao ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na wao kama viongozi wa dini na wajumbe wa kamati ya amani ni lazima kulipokea hilo kwa mikono miwili na kulifanyia kazi .Muyenga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Amani, mkoa wa Dar es Salaam, alisema mwili ukiumwa na akili ama nafsi lazima kukosa amani, hivyo baada ya kuelekezwa wataenda kuufanyia kazi kwa waumini na wengine wataendelea kupeleka taarifa hizo.
1kitaifa
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kupangwa kwa maeneo yote itakapopita Reli ya Kisasa (SGR), ili shughuli zitakazofanyika katika wilaya na vijiji inakopita reli hiyo kwenda sambamba na shughuli za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.Aidha, Lukuvi alisema wakati wa kupanga maeneo hayo, hakuna mwananchi yeyote atakayenyang’anywa eneo lake, bali maeneo hayo yatapangwa kimji na kuainishwa matumizi yake, kama vile ujenzi wa viwanda, mahoteli na maduka makubwa, hivyo kuwataka wananchiwanaotaka kufanya uendelezaji mdogo kusubiri mpango huo.Lukuvi alisema hayo jana katika vijiji vya Kwala na Soga vilivyopo Kibaha Mkoa wa Pwani, alipozungumza na wananchi wa maeneo hayo kuwaelezea mpango wa wizara yake kupanga na kupima maeneo yote inakopita SGR ili kuendana na fursa za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.“Wilaya na vijiji vyote reli ya SGR itapita ardhi yao itapangwa na wale wananchi walio kando ya reli itakapopita wasubiri wasiwe na wasiwasi ardhi ya maeneo yao itengenezewe mpango na muongozo kuhusiana na maeneo hayo utatolewa,” alisema Lukuvi.Alisema, lengo la serikali kupanga maeneo hayo ni kutaka mpango mzima wa uendelezaji ukanda wa kiuchumi katika maeneo hayo, ufahamike kitaifa na kimataifa ili kuvutia wawekezaji, watakaotaka kuja kuwekeza na kubainisha kuwa fedha kwa ajili ya mpango huo zishatengwa.Aliwatahadharisha wananchi wa vijiji hivyo kutokubali kuanza kuuza maeneo yao, kwa kuwa baada ya kupangwa kwa maeneo hayo thamani ya ardhi itapanda na tayari baadhi ya watu wajanja kutoka nje ya vijiji, hivyo washaanza kutafuta maeneo kwa ajili ya fursa hiyo.Alisema, si vyema kila wilaya ikawa na mpango wake wa uendelezaji maeneo itakapopita reli hiyo, bali serikali inachotaka ni kuwa na mpango wa kitaifa utakaotoa mwongozo kwa wilaya zote, kusisitiza kuwa ardhi katika maeneo hayo itasimamiwa na wilaya husika.“Tukiacha maeneo ya kandokando ya reli bila kupanga na kupima kutafanyika vitu vya ajabu, reli hii ina faida kubwa, hivyo lazima kupanga maeneo inakopita ili kwenda sambamba na shughuli za kiuchumi za maeneo hayo,” alisema Lukuvi.Kwa mujibu wa Lukuvi, kuna timu imeundwa kwa ajili ya Mpango wa Uendelezaji Ukanda wa Kiuchumi katika eneo inakopita reli ya SGR na timu hiyo inashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kama vile za nishati, uchukuzi, reli na mawasiliano, lengo likiwa kuwa na mpango utakaokidhi mahitaji ya uendelezaji ukanda kiuchumi katika eneo linakopita reli hiyo.Mapema akiwa katika eneo inapojengwa Bandari Kavu kijiji cha Kwala Kibaha Vijijini, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshana alimueleza Waziri Lukuvi kuwa wilaya yake ilipanga kuitumia fursa ya reli hiyo na Bandari Kavu katika eneo la Kwala kwa ujenzi wa hoteli, maduka makubwa (malls), nyumba za kupangisha (apartments) ili wale wote watakaoitumia bandari hiyo kutoka maeneo tofauti waweze kupata malazi.Akiwa katika Kijiji cha Soga, Lukuvi aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa, eneo lao lishapandishwa hadhi na kuwa mji, hivyo ujenzi holela hautaruhusiwa na hati miliki za ardhi zitakazotolewa eneo hilo ni miaka 99.Aliwataka wakazi wake kuitumia fursa ya reli ya SGR kujiendeleza kiuchumi. Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa alimueleza Lukuvi kuwa kazi ya kuandaa mpango katika maeneo hayo, iende sambamba na uboreshaji miundo mbinu katika vijiji hivyo, ili kuwawezesha watu watakaoenda katika maeneo hayo, kutokumbana na changamoto kama vile barabara, maji na umeme.
0uchumi
Na WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM KIUNGO wa zamani wa Simba, James Kotei, bado hajaisahau raha ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, baada ya kusema leo ataketi mahali tulivu kuufatilia ‘live’. Timu hizo zitaumana, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kuanzia saa 11 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kotei aliicheza Simba kwa mafanikio makubwa, akiisaidia kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, kabla ya kutimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kisha FC Slavia-Mozyr ya Belarus. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kotei alisema mchezo huo ni mkubwa hivyo ataungana na Wanasimba kuisapoti timu yake hiyo ya zamani. “Najua kama kesho ni mchezo wa ‘derby’ ya Kariakoo, nitaangalia mechi hii hapa hapa nilipo, nakumbuka shamrashamra zake, Simba Nguvu Moja. “Kitu kikubwa ninachokumbuka katika mchezo huu ni jinsi mashabiki wanavyoufanya mchezo huo kuwa na mvuto wa aina yake na ndicho kinanifanya niangalie,”alisema Kotei.
2michezo
Madini itaikaribisha Simba kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Machi 18 mwaka huu kucheza nayo mechi ya robo fainali.Akizungumza na gazeti hili kocha huyo wa timu hiyo ya ligi daraja la kwanza alisema timu yake inaendelea na mazoezi kama kawaida kwa ajili ya mchezo huo.“Tutashinda kwani vijana wangu wapo katika kupambana na ninawashukuru mashabiki wa soka walivyojitokeza kutuunga mkono katika mechi dhidi ya JKT Ruvu tunawaomba wajitokeze tena kwani huo ndio uzalendo,” alisema Juma.Aidha, mashabiki wa soka mjini hapa wameeleza kufurahia ujio wa Simba kwenye mechi hiyo wakisema muda mrefu hawajaona timu kubwa mkoani mwao.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini hapa mashabiki hao walisema kuwa ujio wa Simba utavuta hisia za masabiki mbalimbali kutoka ndani na nje ya jiji.Mmoja wa mashabiki hao, Athuman Hassan alisema wakazi wa Arusha na vitongoji vyake hawajaiona timu kubwa kama Simba kwa takriban miaka saba sasa hivyo hiyo ni fursa adhimu kwao. “Imekuwa faraja kwetu kushuhudia tena Simba ikicheza kwenye uwanja huu, tunatarajia tutaona burudani safi siku hiyo,” alisema Hassan.Naye Elibarick Siyangi alisema mchezo huo utafanya mzunguko wa fedha kuongezeka Arusha kwani watu wengi watakwenda kuushuhudia.“Hii sasa ni changamoto kwa klabu zetu hasa vinazoshiriki ligi daraja pili na ligi daraja la kwanza ziache mazoea na zipambane zicheze Ligi Kuu,” alisema.
2michezo
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa mwezi ujao na hivyo anatarajiwa kujiunga na timu hiyo kipindi hiki ambacho ligi imekwisha hadi msimu mpya ujao. Kocha wa muda wa Zimbabwe, Norman Mapeza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo huo wa Kundi G dhidi ya Liberia.Kumusoko anakuwa mchezaji pekee wa Zimbabwe aliyeitwa katika kikosi hicho cha taifa akiwaacha raia wenzake watano wanaocheza ligi ya Tanzania. Kikosi hicho ni makipa; Edmore Sibanda (CAPS United, Zimbabwe), Ariel Sibanda (Highlanders, Zimbabwe), Petros Mhari (FC Platinum) Mabeki: Denis Dauda (CAPS United, Zimbabwe), Partson Jaure, Qadr Amin (both Ngezi Platinum, Zimbabwe), Onesimo Bhasera (SuperSport United), Teenage Hadebe (Chicken Inn, Zimbabwe), Jameson Mukombwe (Black Rhinos, Zimbabwe), Erick Chipeta (Ajax Cape Town), Sydney Linyama (Black Rhinos).Viungo: Thabani Kamusoko (Yanga SC, Tanzania), Devon Chafa, Ronald Chitiyo (both CAPS United, Zimbabwe), Simon Shoko (FC Platinum, Zimbabwe), Kuda Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns), Marvelous Nakamba (Vittese Arnhem, Holland), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum, Zimbabwe), Ovidy Karuru (AmaZulu). Washambuliaji: Tendai Ndoro (Orlando Pirates), Evans Rusike (Maritzburg United), Knowledge Musona (KV Oostende) na Prince Dube (Highlanders, Zimbabwe).
2michezo
Anna Potinus Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amewataka viongozi nchini kuachana na tabia ya kujikweza mbele za watu na badala yake kuishi kama binadamu wa kawaida kwani kwa kufanya hivyo hakuwapunguzii cheo walicho nacho. Amesema watanzania hatutakiwi kubaguana kwa dini wala kabila na kwamba Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ukubwa aliokuwa nao kama rahisi alikuwa mtu wa kawaida mbele ya watu wengine kwa namna alivyokuwa anahusiana na watu hali iliyopelekea mtu akikaa naye hapati hofu ya kwamba amekaa na rais. Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza katika kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jijini Dar es Salaam. “Ni jambo la muhimu viongozi kutambua kuwa kujishusha hakukufanyi usiwe kiongozi wasababu una wakati wa kutimiza majukumu yako lakini unapokuwa na binadamu wenzako wako kama wewe,”. “Orodha ni ndefu ya mambo ya mwalimu kwa sisi ambao tumebahatika kuwa karibu naye ametuachia urithi wa mambo mengi muhimu katika nyanja zote za maisha ya Watanzaniani sasa ni wajibu wetu kuutambua urithi huo na kuutunza, baadhi ya mambo hayo yameshakuwa tunu za taifa na ndizo zinazolea taifa hili,”.  “Watanzania wenzagu, wanachama wenzangu wa CCM na vyama vingine vya siasa, wa rangi zote, makabila yote na madhehebu yote ya dini tushikamane katika kusimamia tunu hii, amani na umoja hauna kabila wala chama na mtu yeyote anayepuuza mambo haya haitakii mema nchi yetu wala yeye mwenyewe,” amesema Dk. Kikwete.
1kitaifa
PARIS, UFARANSA MSHAMBULIAJI wa timu ya PSG, Neymar Jr, amefunguka na kusema kwa sasa ana furaha na amani kuwa ndani ya kikosi hicho, hivyo yupo tayari kuipigania timu hiyo. Mshambuliaji huyo raia wa nchini Brazil, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Septemba 2, alikuwa na lengo la kutaka kuondoka huku akihusishwa kuwindwa na klabu yaka ya zamani Barcelona pamoja na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, lakini dili hilo lilishindikana. Kutokana na hali hiyo mashabiki wa PSG walikuwa wanamzomea mchezaji huyo mara baada ya kurudi kikosini msimu huu, lakini aliweza kuwanyamazisha mashabiki hao kwa kuifungia timu hiyo mabao manne kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu nchini Ufaransa. Akizungumza na waandishi wa habari huko Rio nchini Brazil wakati wa maandalizi wa mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Senegal, Neymar alisema lengo lake kubwa kwa sasa ni kuisaidia PSG. “Kila mmoja ameona kilichotokea wakati wa soko la uhamisho majira haya ya kiangazi, ukweli ni kwamba nilikuwa na lengo la kutaka kuondoka PSG. “Lakini baada ya kushindwa kuondoka bado nina furaha ya kuwa PSG, sisemi haya kwa kuwa nipo na timu ya taifa, ila naongea hivyo nimeona msimu huu umeanza vizuri kwangu, hivyo nipo tayari kuipigania kwa meno na kucha zangu. Nina asilimia 100 ya kuwa na mafanikio makubwa msimu huu. “Kiangazi kilikuwa kirefu kwangu, lakini nilijiandaa kwa lolote, hivyo ninamshukuru Mungu msimu umeanza vizuri kwangu, ninaamini hali hii itaendelea hivi,” alisema Neymar. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alikuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu katika msimu wa 2018-19 kutokana na kusumbuliwa na mguu. Hivyo anaamini kwa sasa angekuwa bora zaidi endapo hasingepata majeraha hayo.
2michezo
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM WADAU mbalimbali wa mchezo wa soka nchini wameitaka Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutafakari upya vigezo wanavyotumia kumpata kocha sahihi wa kuifundisha timu ya soka ya Taifa. Hatua hiyo inatokana na matokeo mabaya ya timu ya Kilimanjaro Stars waliyopata katika michuano ya Kombe la Cecafa, yanayoendelea nchini Kenya. Kilimanjaro wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji, Kenya na kumaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi A, wakiwa na pointi moja katika mechi nne walizocheza, wakifungwa mechi tatu na kwenda suluhu mchezo mmoja, huku wakifunga mabao mawili pekee katika michezo yote. Wakizungumza kwa wakati tofauti na MTANZANIA jana, wadau hao walisema Kamati ya Ufundi iweke wazi vigezo vilivyotumika kumteua kocha wa timu, kutokana na ukakasi uliopo, kwa kile kilichotokea kwenye michuano ya Cecafa Kenya. Kocha wa zamani wa timu ya Mbeya City na Yanga, Juma Mwambusi, alisema wasiwasi wake upo kwa wahusika waliomteua kocha huyo ili kuifundisha timu ya taifa. “Mimi ni Mtanzania kama wengine, naumia nikiona hali hii kama ilivyo kwa wengine, TFF ndio wenye jukumu la kumteua kocha, ila sijui kama walitumia vigezo sahihi kumpata Ninje. “Timu ya taifa si ya kufanyia majaribio, hata kama alikuwa mchezaji wa zamani na alisomea ukocha je, anafahamu mazingira ya hapa nchini? Aliwahi kufundisha timu yoyote na alitambua utayari wa wachezaji aliokabidhiwa?” alihoji Mwambusi. Mchezaji wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay, alisema waliomteua Ninje kuwa kocha wa timu ya taifa walisahau mahitaji ya Watanzania. “Hatukwenda Kenya kujifunza, badala yake tulitaka kushinda taji kwa kuwa  michuano ya Cecafa tunaimudu, tulifanya hivyo katika michuano ya mwaka 2010 na tulikuwa na uwezo wa kufanya tena mwaka huu, ndiyo maana kuna wachezaji wazoefu,” alisema Mayay. Kocha wa timu ya Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio‘, aliishauri Kamati ya Ufundi ya TFF kutojali zaidi vyeti, badala yake wajikite kwenye ubora wa kocha. “Kocha bora Tanzania kwa sasa ni Meck Maxime, lakini TFF hawakuliona hilo, wao wakavutiwa na kocha anayejua kuzungumza lugha ya Kiingereza. “Kwa hili TFF na kamati husika wanatakiwa wajitafakari upya na nitakwenda kumweleza Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi, bila kumwonea haya kwamba uteuzi wake haukuwa sahihi,” alisema Julio. Kocha wa Kagera Sugar, Meck Maxime, alisema licha ya TFF kuwa na viongozi wanaofahamu mpira, wanatakiwa kujifunza kutokana na makosa, kabla ya kuwapa makocha majukumu ya kitaifa. “Wahusika wanatakiwa kujifunza na kubadilika, makocha wanaofahamu mazingara ya hapa nyumbani wapo wengi, hao ndio waliotakiwa kutumiwa na si vinginevyo,” alisema Maxime.   Kocha Ammy Ninje  ana leseni ya ukocha daraja A la Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) na tayari ameshawaomba radhi Watanzania,  akiahidi kutengeneza kikosi bora   kitakachoshiriki michuano ijayo. Akizungumza baada ya kuondolewa katika michuano hiyo, Ninje alisema mpango wake ulikuwa kurudi na kombe hilo nchini, ila kutokana na matokeo hayo anarejea kujipanga upya michuano ijayo. “Tatizo lipo kwa wachezaji namna tulivyowalea, hawakuwa na kasi, ukiacha mchezo dhidi ya Zanzibar, iliyobaki yote tulicheza vizuri, ingawa hatukupata matokeo mazuri. “Tunaomba Watanzania watusamehe kwa kuwaangusha, kwani halikuwa lengo letu, tunawaomba waendelee kuisapoti timu yao na tunawaahidi kuboresha tulipokosea,” alisema Ninje.
2michezo
Yanga itakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) nusu fainali dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kutokana na mchezo huo muhimu, uongozi wa klabu hiyo uliamua kupeleka kikosi cha vijana kilichocheza dhidi ya Jeshi Kombaini na kutoka sare ya bao 1-1.Kitendo hicho cha kupeleka kikosi cha vijana kilimkasirisha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyetaka uongozi wa Yanga kwenda kutoa ufafanuzi, kwa nini haikupeleka kikosi cha kwanza kama walivyoahidi.Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema juzi kuwa uamuzi wa kutopeleka kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo, ulikuwa ni kwa maslahi mapana ya Yanga katika kufanya vizuri michuano ijayo ikiwemo dhidi ya Mbao FC na ligi.Lakini pia, alisema kulikuwa na dosari kadhaa katika kufikia makubaliano ya ushiriki wa mechi hiyo hasa upande wa Yanga, upana wa kikosi, ukaribu wa mechi ya FA na kuwataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu hasa kipindi hicho cha mpito.“Niwaombe radhi wote waliosikitishwa na uamuzi huo japo una manufaa kwa klabu. Pia, naomba tushikamane tuwe kitu kimoja, kuelekea kutwaa makombe tunayoshiriki kwa sasa na kuendelea kuichangia Yanga,”alisema.Aidha, kikosi kilichowafuata Mbao ni Deogratius Munishi, Beno Kakolanya, Ally Barthez, Haji Mwinyi, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Vicent Endrew, Said Juma, Kelvin Yondani, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko. Wengine ni Obrey Chirwa, Amis Tambwe, Geofrey Mwashiuya, Hassan Kessy, Emmanuel Martin, Juma
2michezo
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imewataka aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba, Hans Pope na mkurugenzi wa kampuni ya Ranky Infrastructure & Engineering, Franklin Lauwo, wajisalimishe wenyewe katika ofisi zao kutokana na tuhuma za makosa mbalimbali ya rushwa yanayowakabili. Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Naibu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungu, amesema juhudi mbalimbali za kuwatafuta watu hao zimegonga mwamba hivyo wanatakiwa watii amri na kujisalimisha wao wenyewe. Naibu mkurugenzi huyo amesema Pope anatuhumiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuhusiana na malipo ya kodi. Kati ya Machi 10,2016 na Septemba 30, 2016, mshitakiwa huyo akishirikana na washitakiwa wenzake, Evans Aveva na Geofrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za TRA, kwamba klabu ya Simba imenunua nyasi bandia kutoka Ninah Guangzhou Trading Limited kwa thamani ya dola za kimarekani 40,577. “Ukweli ni kuwa nyasi hizo zilinunuliwa dola za kimarekani 109,499 lengo ikiwa ni kukwepa kulipa kodi ya mapato sahihi kwa TRA,” Ameeleza. Amesema kwa upande wa Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi na aliupata kwa njia ya rushwa kwa sababu hakuwa na sifa na sio mkandarasi ambae amesajiliwa na bodi ya makandarasi nchini. “Kati ya Machi na Septemba 2016, mshitakiwa alifanya kazi ya ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa klabu ya Simba uliopo Bunju, Kinondoni kwa thamani ya zaidi ya bilioni mbili wakati hajasajiliwa na bodi ya makandarasi, kisheria kufanya kazi hiyo,” amefafanua. Aidha Brigedia Mbungu ameongeza kwamba mtu yeyote atakayesaidia kutoa taarifa za ukweli zitakazosaidia kupatikana kwa washitakiwa hao atapewa zawadi nono.
2michezo
MKUTANO wa mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa unaanza leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, mkutano huo unawashirikisha mawaziri wa nchi 16 za SADC ukilenga kujadiliana namna bora ya kutekeleza sera, mikakati na programu zinazohusu sekta hizo.Programu moja wapo ni mpango wa kuongeza kasi ya mtandao wa intaneti kupunguza gharama za huduma za mtandao kwa kuunganisha watoa huduma za Tehama kwenda kwenye vituo vya kitaifa na kikanda (SADC Regional Internet Exchange points).Alisema maunganiko hayo yatawezesha mawasiliano ya intaneti yanayofanyika ndani ya nchi kubaki kwenye nchi husika wanachama wa SADC bila kwenda kwenye nchi nyingine na kupunguza umbali na gharama ya kusafirisha mawasiliano ya nchi husika.“Kwa upande wa Tanzania tayari tuna vituo sita vya maunganisho ya watoa huduma za intaneti yaani ‘Internet Exchange Point’,” alisema waziri huyo.Kwa mujibu wa waziri, maeneo yatakayojadiliwa katika mkutano huo unaotanguliwa na vikao vya wataalamu wa sekta hizo wa SADC ni pamoja na miundombinu ya mawasiliano, usalama wa mtandao, sera, utafiti katika sekta ya mawasiliano, masuala ya posta, habari na matumizi ya pamoja ya huduma za mawasiliano.Mengine ni sekta ya uchukuzi; hali ya hewa, usafiri wa anga, reli, barabara, bandari, ujenzi na kuhuisha sera, sheria na kanuni zioane kikanda; miundombinu ya mawasiliano na maunganisho yake na kutumia teknolojia ya kisasa kufanikisha utoaji wa huduma na usafirishaji wa bidhaa kwa kutumia biashara mtandao na ushirikiano wa kikanda.Kamwelwe alisema mkutano huo utaanza leo hadi Septemba 20 mwaka huu na pamoja na vikao vya wataalam pia Septemba 19 kutakuwa na Kongamano maalumu la Ubunifu na Teknolojia Zinazochipukia la mawaziri wa SADC wa sekta hizo pamoja na wadau wengine.“Vile vile nchi wanachama wa SADC waliandaa mwongozo wa sheria za mfano wa usalama wa mtandao.Madhumini ya kuwa na mwongozo huo ni kuhakikisha kuwa kila nchi inatunga na kusimamia utekelezaji wa sheria za usalama mtandaoni kwa kuwa masuala ya usalama wa mitandao hayatambui mipaka,” alisema Kamwelwe.
1kitaifa
Kavumbagu amekuwa na msimu mbaya chini ya kocha Stewart Hall, kiasi cha kumfanya kujutia maamuzi yake ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo aliyojiunga nayo misimu miwili iliyopita akitokea Yanga.Akizungumza na gazeti hili, Kavumbagu raia wa Burundi, alisema benchi limemchosha na hayupo tayari kushawishika kuongeza mkataba kutokana na kuhofia kuua kiwango chake kwa kukaa benchi.“Nashukuru wachezaji wenzangu na uongozi mzima wa Azam kwa kipindi chote cha misimu miwili niliyochezea timu yao, kwa sasa mkataba wangu umekwisha na nimeona inatosha ni vyema nikasake changamoto sehemu nyingine nitakapopata nafasi ya kucheza na kuimarisha kiwango changu,” alisema Kavumbagu.Mshambuliaji huyo aliyeifungia Azam mabao msimu huu kwenye mechi za ligi, alisema hajajua ni timu gani ataichezea msimu ujao, lakini angependa kujiunga na timu kubwa za Yanga na Simba kama zitamuhitaji .Alisema amekuwa akivutiwa na timu hizo mbili nchini kutokana na namna zilivyo na ushindani mkubwa na mashabiki wengi ambao wanazipenda na alikuwa na wakati mzuri wakati akiichezea timu ya Yanga.
2michezo
WAZIRI wa Uwekezaji, Angellah Kairuki ameliambia Bunge kuwa mwaka ujao wa fedha nchi itakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuvutia wawekezaji. Kairuki alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kassim Ahmed (CUF).Katika swali la nyongeza mbunge huyo alisema nchi ina tatizo kubwa kwenye uboreshaji wa mazingira ya biashara kutokana na mfumo wa kodi uliopo na kuhoji ni lini serikali itaandaa mfumo rafiki wa kodi ulio wazi. Aidha, alisema kwa sasa Tanzania iko kwenye nafasi ya 144 ya uwezeshaji kibiashara lakini Rwanda ni nchi ndogo lakini iko kwneye nafasi nzuri ya 29 huku Kenya ikiwa nafasi ya 40 na kuhoji serikali haioni inapoteza wawekezaji kutokana na mfumo wa kodi usio rafiki.Akijibu swali hilo, Kairuki alimhakikishia mbunge huyo kuwa mwaka ujao wa fedha nchi itakuwa inafanya vizuri zaidi na hivyo wabunge na wawekezaji wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.“Lakini ukiangalia kwa sasa Juni hadi Julai mambo mengi yamefanywa na serikali na juzi tu nilikuwa na mkutano na Benki ya Dunia jijini Washington nchini Marekani na Dar es Salaam kuhakikisha tunawasilisha vilelezo vya kuonesha ni kwa namna gani kama nchi tumefanya maboresho mbalimbali na tumepiga hatua katika kuboresha viashiria 11 ambavyo vinatumika kupima wepesi wa kufanya baishara,” alisema Kairuki.Alisema katika mkutano huo aliongezewa muda wa kuwasilisha vilelezo vingine vya namna gani serikali imeboresha mazingira na mifumo ya biashara kwa wawekezaji na wafanyabiashara. “Maboresho tuliyofanya ni pamoja na kuanzisha biashara, taratibu za baishara mipakani hivyo niwatoe hofu watanzania na wabunge kila mmoja atimize nafasi yake ili kuona ni namna gani tunaboresha huduma hiyo na naamini ifikapo 2020/21 ripoti yetu na nafasi ya Tanzania tutafanya vizuri zaidi,” alisema.Awali akijibu swali hilo, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha alimhakikishia mbunge huyo kuwa serikali imekuwa ikiweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi na ndio maana kwenye kila bunge wamekuwa wakipata matukio mbalimbali ya kodi ili kuendelea kuboresha mazingira yawe ya ushindani.“Nimhakikishie kuwa pamoja na changamoto zilizopo serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kodi na kumhakikishia kuwa mazingira ya biashara yataendelea kuboreshwa hivyo kuvutia wawekezaji,” alisema Ole Nasha. Katika swali la msingi, mbunge huyo alisema mazingira ya kufanya biashara nchini ni magumu kwa wafanyabiashara wa ndani na wa nje.Je, ni lini serikali itaondoa urasimu ili wananchi waweze kunufaika. Ole Nasha alisema serikali imekuwa ikibuni na kutekeleza mikakati na mipango mbalimbali kwa kuhakikisha uwepo wa mazingira bora ya ufanyaji biashara nchini. Alisema kwa mwaka 2017 serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ilifanya uchambuzi wa kina wa mazingira ya biashara nchini kwa sekta zote na kubaini changamoto mbalimbali zikiwemo mwingiliano wa sheria.Alibainisha kuwa kufuatia changamoto hizo serikali iliandaa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa mazingira ya biashara nchini ambao umeridhiwa na baraza la mawaziri kwa ajili ya utekelezaji. “Mpango huo utasaidia kuondoa muingiliano wa sheria na kupunguza urasimu kwa wafanyabiashara wakati wa kupata huduma katika taasisi mbalimbali za serikali. Mpango wa utekelezaji wa Blue Print umekamilika,”alisema.
1kitaifa
UWEZO wa madaktari wazalendo kufanya upasuji wa masikio yenye matatizo ya kusikia nchini umefi kia asilimia 90 huku uwezo wa kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia watoto waliopandikizwa vifaa kwa watoto waliozaliwa wakiwa hawasikii ukiongezeka na kufi kia asilimia 100.Daktari Bingwa wa Upasuaji Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila), Godlove Mfuko alisema hayo jana hospitalini hapo na kuongeza mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, hospitali hiyo ilifanyia upasuaji watoto watatu huku wengine wawili wakiwashiwa vifaa vyao waweze kusikia sauti.Alisema jitihada za kuboresha sekta ya afya nchini, zimesaidia wataalam wazalendo kutoa huduma zao kwa ufanisi zaidi, vifaa na vifaatiba vikiimarishwa na kuongezwa. Dk Mfuko alisema tangu waanzishe huduma ya kuwekea watoto vifaa vya usikivu Juni 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), watoto 34 wamewekewa vifaa hivyo maalum vya kusaidia kusikia.Alisema kufanyika kwa huduma hizo nchini ni mwendelezo wa wataalam hao wazalendo kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kuhakikisha wananchi wanafikiwa kwa urahisi na huduma za afya kule kule waliko.Alisema gharama za upasuaji mgonjwa au mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha masikioni kumsaidia kusikia ni Sh milioni 36 wakati akipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayo hugharimu Sh milioni 80 hadi Sh milioni 100 mgonjwa mmoja. Alisema watoto wawili wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia MNH - Mloganzila na wamewashiwa vifaa hivyo waweze kusikia sauti mara ya kwanza tangu wazaliwe.Aidha, mtoto Uebert Kigala amerekebishiwa sauti kifaa alichopandikiziwa ili kumsaidia kusikia ikiwa ni mwendelezo wa wataalam kufuatilia maendeleo yake ili kuhakikisha kifaa kinafanya kazi kwa ufanisi.“Hawa watoto hawajawahi kusikia sauti tangu wazaliwe hivyo leo wataanza kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka baada ya kuunganisha vifaa hivi na kuviwasha’’ alisema Dk Mfuko. Dk Mfuko alitoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kupima afya zao kwa sababu asilimia 20 ya watu wenye tatizo la usikivu nchini ndio wanaoenda hospitali huku asilimia 80 wakidaiwa kubaki majumbani.
1kitaifa
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa ya wizi wa kompyuta katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Kanda ya Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema wamepokea taarifa hiyo Jumanne asubuhi (Oktoba 15, mwaka huu).Kamanda Mambosasa alisema mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika wa wizi huo ambao hata hivyo hakuwa tayari kutaja ni kompyuta ngapi zimeibwa. Alipopigiwa simu, DPP Biswalo Mganga kuhusu wizi huo, alisema yupo kwenye kikao na hajui atazungumza muda gani kwa sababu ana mambo mengi.Kutokana na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), haijajulikana kama kompyuta hizo zimewahi kuhifadhiwa kesi zinazoendelea katika mahakama mbalimbali. Tukio hilo la wizi limetokea ikiwa ofisi hiyo iko katika mchakato wa kujadiliana na kuingia makubaliano na washitakiwa mbalimbali wa kesi za uhujumu uchumi.Miongoni mwa kesi ambazo ziko katika hatua ya makubaliano ni kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili vigogo wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IndependentPower Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sethi na James Rugemalira wanaodaiwa kusababisha hasara na utakatishaji zaidi ya Sh bilioni 309.Washitakiwa wengine ambao wako kwenye makubaliano ni Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera anatuhumiwa kukwepa kodi na kutakatisha jumla ya Sh milioni 173 na mwingine ni Yusuf Ally maarufu ‘Mpemba wa Magufuli’ anayekabiliwa na mashitaka ya kusafirisha nyara za serikali zenye thamani zaidi ya Sh milioni 200.Miongoni mwa washitakiwa ambao tayari wameshahukumiwa kwa kutumia utaratibu huo wa makubaliano ni wafanyabiashara wawili ambao ni Magdalena Uhwello na Halima Nsubuga ambao wameingiza serikalini Sh bilioni moja baada ya kukiri kufanya biashara ya upatu.Wengine ni mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuiibia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mohamed Yusufali (39) Sh milioni saba kila dakika na wenzake kuingiza serikalini Sh 24,303,777,424.70 pamoja na kutaifisha nyumba nne zinazomilikiwa na Yusufali. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Arifal Paliwalla (44) na Sameer Khan (40) ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya I& M. Washitakiwa hao mpaka sasa wamelipa Sh 1,201,000,000.Pia yupo Mkurugenzi Mkuu wa Benki M (Tanzania), Sanjeev Kumar (63) ametakiwa kulipa fidia ya zaidi ya Sh bilioni sita ndani ya miezi 24 ambapo mpaka sasa tayari ameshalipa Sh milioni 690. Wengine ni vigogo sita wa Kampuni ya Six Telecom akiwamo Wakili maarufu, Dk Ringo Tenga ambao wametakiwa kulipa fidia ya Dola za Marekani 3,748,751.19 sawa na Sh bilioni nane na tayari wamelipa Dola za Marekani 150,000 pamoja na kutaifisha nyumba ya washitakiwa iliyopo Mikocheni.Mbali na Tenga, wengine ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha, Kampuni ya Six Telecoms na Frank Mwalongo.
1kitaifa
*Mahakama Kuu Dar yatengua hukumu yake ya miezi sita baada ya kubaini hati ya mashtaka dhidi ya warufani, ilikuwa na upungufu  Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam MBUNGE wa  Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema) aliyehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero kwenda jela miezi sita bila faini, ameachiwa huru na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa yake huku akiwa amekaa gerezani siku 79, ambazo ni takribani miezi mitatu. Lijualikali (30) ambaye hukumu iliyompeleka jela ilitikisa nyanja za siasa na sekta ya sheria, aliachiwa huru jana baada ya mahakama kubaini hati ya mashtaka iliyomtia hatiani awali ilikuwa na upungufu mkubwa. Mahakama hiyo ilimuachia huru jana baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na mrufani aliyewakilishwa na Wakili Tundu Lissu, Fred Kiwelo na Enock Edwin. Mwingine aliyeachiwa pamoja na  Lijualikali baada ya hukumu yake kutenguliwa ni Stephano Mgata (35) aliyepewa adhabu ya kifungo cha nje cha  miezi sita. Lijualikali na mwenzake huyo, awali walitiwa hatiani kwa kosa la kufanya vurugu na kusababisha taharuki wakati wa mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Ifakara. Uamuzi wa kuwaachia huru warufani hao ulitolewa na Jaji Ama-Isario Munisi, baada ya kukubaliana na hoja za warufani kwamba hati ya mashtaka dhidi yao ilikuwa na upungufu mkubwa usioweza kurekebishika katika hatua ya rufaa. “Ushahidi uliotolewa na Jamhuri katika Mahakama ya Wilaya ya Kilombero haujitoshelezi kuweza kuwatia hatiani washtakiwa hao. “Upungufu katika hati ya mashtaka ni mkubwa hivyo mahakama inatengua adhabu za vifungo walizopewa washtakiwa na inaamuru waachiwe huru,”alisema Jaji Munisi. Awali Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kilombero, Timothy Lyon, aliwatia hatiani Lijualikali na mwenzake na kuwapa adhabu walizokuwa wakizitumikia. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Januari 11 mwaka huu, Hakimu Lyon, alisema Mahakama inawatia hatiani washtakiwa kwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili. Lijualikali alikuwa na kesi tatu huko nyuma ambazo alitiwa hatiani na kuhukumiwa, mahakama ilimuona ni mkosaji mzoefu hivyo kumuhukumu kwenda jela miezi sita. Kesi ambazo mbunge huyo alitiwa hatiani na kuhukumiwa ni kesi namba 338 ya mwaka 2014, kesi namba 220 ya mwaka 2014 na kesi namba 340 ya mwaka 2014. Mshitakiwa wa pili Mahakama hiyo ilimwona mshtakiwa wa pili  Mgata kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza hivyo kumuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na ndani ya kipindi hicho hakutakiwa kutenda kosa lolote la jinai. Adhabu hiyo ilipingwa, kupitia mawakili wao walikata rufaa ambayo ilisajiliwa na kupewa namba 60 ya mwaka 2017, wakipinga adhabu hiyo wakiwa na sababu tano ikiwemo hati ya mashtaka ina upungufu mkubwa ambao hauwezi kurekebishika. Walidai hati hiyo ya mashtaka ilikuwa haiendani na maelezo ya kosa, hivyo washtakiwa walitiwa hatiani kwa kitu ambacho hakipo. Jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa mahakamani na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ambaye alipinga hoja hizo za rufani akidai hati ya mashtaka ilikuwa inakubalika kwa mujibu wa sheria na makosa yaliyoko yanarekebishika. Alidai ushahidi uliotolewa Mahakama ya Kilombero ulijitosheleza kuwatia hatiani washtakiwa. LISSU Siku moja baada ya Lijualikali kuhukumiwa Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, alisema hukumu hiyo inatokana na vita vya kisiasa kati ya Chadema na Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Lijualikali na Lema (Godbless-Arusha Mjini) kwa sasa yuko nje kwa dhamana baada ya kukaa mahabusu miezi mitatu kutokana na kunyimwa dhamana akituhumiwa kutoa lugha ya uchochezi, wote hawa ni wafungwa wa kisiasa. “Adhabu ya kifungo bila faini imetolewa kwa sababu za kisiasa. Kwanza walimshitaki mara mbili, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu ili wamfunge na asiweze kuendelea na kampeni. Haikuwezekana kumfunga na alishinda ubunge. “Baadaye walimfungulia kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu ambako nako tuliwashinda vibaya. Wamekata rufaa Mahakama ya Rufani ya Tanzania nako tutawashinda na wanajua hivyo,” alisema Lissu. Alisema waliamua kumfunga mbunge huyo bila faini wakiamini kuwa uamuzi huo utamfanya akose sifa za kuwa mbunge. Huku akinukuu Ibara ya 67 (2) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Lissu alisema adhabu hiyo haina athari yoyote, kwa maelezo kuwa mtu anakosa sifa za kuwa mbunge iwapo atafungwa gerezani zaidi ya miezi sita. “Si kifungo tu cha miezi sita, pia lazima awe amekutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu. “Adhabu ya kifungo aliyopewa Lijualikali haijazidi miezi sita. Pia kosa la kumpiga askari polisi, hata kama lingekuwa la kweli si kosa la utovu wa uaminifu,” alisema.
1kitaifa
DERICK MILTON NA SAMWEL MWANGA, ITILIMA SERIKALI imeanza ujenzi wa hospitali mpya ya kisasa katika eneo la kijiji cha Nguno katika  Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu kwa lengo la kuwaondolea kero wananchi ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya. Akizungumza kwenye ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo uliofanywa wilayani humo baada ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru, Mganga Mfawidhi, Anorld Musiba amesema zoezi hilo litasaidia kupunguza changamoto wanazopitia wananchi hao. “Mwaka jana vimetokea vifo vya watu watano, mwaka huu mpaka sasa vimetokea vifo vya watu wawili na vyote ni akina mama wajawazito, serikali imeamua kujenga hospitali wilayani hapa ambapo ujenzi wake unaendelea na utakamilika Juni 30, mwaka huu. “Ujenzi huu utahusisha majengo saba na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5, hadi sasa gharama zilizotumika ni shilingi bilioni 2.1 sawa na asilimia 81 ya utekelezaji, tunategemea ujenzi huu utasaidia kumaliza vifo vya kina mama wajawazito na tunatarajia hospitali hii itahudumia wananchi zaidi ya 300,000. Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge, Mkongea Ali amesema ameridhishwa na ujenzi huo na  ametaka kuongezwa kwa kasi ya ujenzi huo kabla ya mwaka wa fedha 2018/19 kuisha.  Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo walishukuru serikali kwa kuwaletea hospitali ambapo wameomba kuharakishwa kwa ujenzi wake ili kuanza kupata huduma mapema. “Tulikuwa tunateseka sana kwenda Bariadi, ukiangalia huku ni vijijini na miundombinu ya barabara ni mibovu tumekuwa tukitumia muda mrefu kupata matibabu,” amesema Janeth Saguda.
1kitaifa
Tayari Yanga ilitua Mbeya kwa ndege kwa ajili ya pambano hilo la kuthibitisha ubingwa baada ya juzi Yanga kutoshuka dimbani licha ya kupewa ubingwa baada ya Simba kulambwa 1-0 na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa.Baada ya kipigo hicho cha Simba na ushindi wa Azam FC wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Simba ilishushwa katika nafasi ya pili na kuangukia ya tatu.Tayari Yanga imeshacheza michezo 27 na kufikisha pointi 68 ikiwa na michezo mitatu mkononi ambazo kama Simba itacheza michezo mitatu iliyobaki bado haitamfikia kwa kuwa itafikisha pointi 67 na Azam FC ikimaliza michezo miwili iliyobakiza itafikisha pointi 66.Pia, inakutana na Mbeya City ambayo hata ikishinda haina nafasi tena ya kuchukua ubingwa wala ikipoteza haitaweza kushuka daraja, kwani ina pointi 33 na inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi. Iwapo itashinda mchezo wa leo na miwili iliyobaki itaendelea kujitengenezea rekodi yake ya kipekee kwa kufikisha pointi 71 na zaidi.Hata ikipoteza michezo yote iliyobaki haina hasara yoyote kwa kuwa wameshatetea ubingwa wao. Kikosi cha Kocha Mkuu Hans Pluijm baada ya mchezo huo wa Mbeya, Mei 14 kitasafiri hadi Mtwara ambako watacheza na Ndanda ambako pia watakabidhiwa mwali wao.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, Yanga ilitangaza ubingwa juzi jioni baada ya Simba kupoteza mchezo wake dhidi ya Mwadui, muda ambao haukutosha kwa maandalizi ya kutawazwa sherehe za kukabidhiwa kombe. Alisema kuwa Yanga itakabidhiwa ubingwa huo katika mchezo dhidi ya Ndanda FC mwishoni mwa wiki hii.
2michezo
Na JUSTIN DAMIAN, SHIRIKA la Maendeleo la Ufaransa (AFD), lipo katika majadiliano yatakayoiwezesha Serikali kupata mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 65 (zaidi ya Sh bilioni 150) kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini, Emmanuel Baudran, aliliambia MTANZANIA katika kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa linaloendelea jijini Dar es Salaam, kuwa mkopo huo unalenga kuboresha uwanja huo – terminal 2, ili uweze kuendana na ongezeko la abiria. Baudran alisema majadiliano hayo yapo katika hatua nzuri na kuongeza kuwa mkataba wa mkopo huo unaweza kusainiwa mwezi ujao. “Tunaamini kuwa usafiri wa anga ni kichocheo muhimu cha maendeleo na Tanzania imekuwa ikipokea watalii wengi. Biashara kati ya mkoa mmoja na mwingine zinakua pia na kwa kuwa nia yetu ni kusaidia sekta zenye mchango kwa maendeleo, tunaona eneo hili ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,” alisema Baudran. Alisema shirika hilo lipo katika majadiliano na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo wa masharti nafuu kukarabati viwanja vingine vya ndege vilivyopo katika mikoa mbalimbali. “Tanzania ina  viwanja vya ndege zaidi ya 15, ikiwa ni pamoja na vikubwa na vidogo. Baadhi ya viwanja hivi havipo katika hali nzuri na AFD ipo tayari kusaidia ukarabati wake,” alisema. Alisema katika mpango wa ukarabati wa viwanja 11 vya ndege ambao Serikali inao, shirika hilo lipo tayari kufadhili baadhi ya viwanja ambavyo Serikali itatoa kipaumbele na kutaka fedha kwa ukarabati na upanuzi.
1kitaifa
MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amedai kwamba ameshitushwa na uwezo wa nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, aliouonesha juzi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, juzi alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo dhidi ya Arsenal, ambapo alipachika mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-2. Kutokana na kiwango hicho, Wenger amedai kwamba hakutarajia kuona uwezo mkubwa ambao aliuonesha mchezaji huyo. “Kwa upande wetu, tulishindwa kuwa na mipango mizuri ya kutafuta mabao kutokana na nafasi ambazo tulizipata, lakini katika mchezo huo nilikuja kushangazwa na uwezo wa nyota mpya wa Man United, Rashford. “Nadhani haikuwa kwangu tu, ilikuwa kwa kila mmoja kushangazwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye alifanikiwa kufunga mabao mawili, alikuwa na akili ya kwenda na mchezo na kujua wapi sehemu sahihi ya kukaa. “Ninaamini atakuja kuwa na uwezo wa hali ya juu endapo ataendelea na aina ya mchezo ambao anacheza na kama hatalewa sifa,” alisema Wenger. Nyota huyo alianza kuonesha uwezo wake wa kupachika mabao katika mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya Midtjylland, ambapo katika mchezo huo alifanikiwa kupachika mabao mawili.
2michezo
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda pamoja na timu nzima ya Wizara ya Kilimo, wamefanya ziara kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kufuatilia sakata la ununuzi wa korosho.Viongozi hao walioapishwa juzi Ikulu Dar es Salaam na Rais John Magufuli, walilazimika kusafiri juzi usiku hadi kwenye mikoa hiyo ili kuhakikisha agizo lilitolewa na Rais kuhusu serikali kununua korosho zote linatekelezwa.Wakizungumza kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1) jana mchana, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa alisema ziara yao hiyo imewapa fursa ya kujiridhisha kiwango cha korosho kilichopo, zipo kwenye hali gani pamoja na kuona kama kuna ziada pia.Bashungwa alisema uamuzi wa serikali wa kununua korosho hizo umeungwa mkono na kufurahiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa mikoa hiyo ya kusini.“Serikali ya Rais Magufuli inataka kufungamanisha sekta ya kilimo na sekta ya viwanda kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.Kiwanda hiki cha kubangua korosho cha BUCCO kilikuwa kimefungwa, lakini baada ya kauli ya Rais, kimefunguliwa,” alieleza Naibu Waziri Bashungwa. Kwa upande wake, Waziri Kakunda aliwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi na kuvitaka viwanda vinavyochakata mazao ya wananchi kuzingatia hilo.Alisema uamuzi wa Rais Magufuli kukikabidhi kiwanda cha BUCCO kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni kwa sababu wanajeshi ni wazalendo, waadilifu na waaminifu. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alisema mpaka jana jumla ya tani 4,453 za korosho zilikuwa zimeshapokewa kwenye maghala.Zambi alisema kazi ambayo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepewa na serikali ni kulinda maghala ya korosho, kusafirisha korosho hizo kutoka kituo kimoja hadi kingine, na kuendesha kiwanda hicho.“JWTZ hawanunui korosho, kazi ya kununua korosho inafanywa na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kupitia vyama vikuu vya ushirika, na vyama hivyo vya ushirika ndivyo vinavyowalipa wakulima,” alieleza Zambi.Wataalamu wa uchumi na biashara, walisema kushindwa kwa wanunuzi binafsi kununua korosho kwa bei elekezi ya serikali, ni kutokana na kubadilika kwa bei katika soko la kimataifa.Mtaalamu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Razack Lokina alisema serikali siyo tu ina uwezo wa kununua kwa bei iliyoipanga, lakini pia ina uwezo wa kuzihifadhi korosho hizo na kuziuza wakati wowote ambapo bei ya soko iko vizuri. Profesa Lokina alisema uamuzi wa serikali ni sahihi kwa kuwa unamlinda mkulima asipate hasara.Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Mchungaji Silver Kiondo, alisema mkulima anapaswa kulindwa na uamuzi huo wa serikali wa kuzinunua korosho hizo ni sahihi.Mchungaji Kiondo alisema kwa kuwa haieleweki sababu iliyowafanya wanunuzi hao kushindwa kununua korosho hizo, ni vyema ukafanyika utafiti ili kujua sababu iliyowafanya washindwe kuzinunua kwa bei elekezi ya serikali.
1kitaifa
NA GEORGE KAYALA MWIMBAJI chipukizi katika muziki wa Injili nchini, Mary Msigwa, amelalamikia wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo kutowathamini, vyombo vya habari na wadau wa muziki huo pindi wanapotaka msaada kwa ajili ya kukuza muziki wao. Msigwa alilalama kwamba nyimbo za wasanii chipukizi hazipewi nafasi ya kuchezwa kwenye redio na runinga mbalimbali bila sababu za msingi. Mary alisema changamoto nyingine zinazowakabili waimbaji wachanga ni kukosa fedha kwa ajili ya kurekodia, kushindwa kujitangaza kiasi kwamba wanashindwa kutambulika kwa jamii. “Wasanii chipukizi hatuthaminiwi na hii imesababisha baadhi ya wenzetu kushindwa kuendelea na huduma hii kwani hata kama ukifanikiwa kurekodi kwa kujibana shida inakuwa kwa watangazaji wa redio na televisheni ambao huwa hawazipi nafasi nyimbo zetu na hii inasababisha tushindwe kufahamika kwenye jamii,” alisema mwimbaji huyo.
4burudani
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM), amesema anakusudia kuwasilisha muswada binafsi bungeni utakaoweka sharti la kurejewa mjadala wa Katiba Mpya. Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema muswada huo atauwasilisha katika kikao cha tisa cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Novemba 7  mwaka huu mjini Dodoma. Alisema Katiba ya nchi ni mkataba wa wananchi ambao utadumu kwa miaka mingi hivyo hautakiwi kufanywa kama dharura au kuogopwa bali unahitaji umakini. “Mchakato ulianza ukatumia fedha nyingi na kuhusisha watu wengi lakini haukukamilika, na hapa katikati ulighubikwa na sintofahamu nyingi. “Na kwa namna yoyote ile ili tuweze kuwa na Katiba bora itakayohusisha wadau wote kwa maana ya wananchi, viongozi wa vyama vya siasa na upande wa serikali itakuwa ni muhimu mchakato uanze kwa kuzingatia rasimu ya katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba,” alisema Nyalandu. Alisema anatarajia kuwa wabunge wa chama chake na wabunge wa upinzani watamuunga mkono   hoja hiyo iweze kurudi upya na wadau wote wapate fursa ya kujadili ipatikane Katiba Mpya. “Wabunge tuna nafasi yetu ya kujadili na kupeleka maoni ya binafsi na yale ya pamoja. “Katiba imempa nafasi mbunge mmoja mmoja bila kujali ametoka chama gani, hivyo mimi naona ni hoja ambayo ni lazima ipate nafasi kama hoja nyingine na kufanyiwa kazi. MATOKEO YA TWAWEZA Wakati huohuo, Taasisi ya Twaweza jana ilitangaza matokeo ya utafiti ambayo yanaonyesha Watanzania wawili kati ya watatu wanahitaji Katiba Mpya. Utafiti huo uliopewa jina la ‘Zege Imelala’ ulilenga kupata maoni ya wananchi kuhusu kukwama kwa mchakato wa kuunda Katiba Mpya. Akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alisema ulifanyika kati ya Juni hadi Julai mwaka huu na kuhusisha watu 1,745 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara. “Asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu kwa Tanzania kupata katiba mpya na nusu ya wananchi wanasema mchakato wa katiba uanze upya na tume mpya,” alisema Eyakuze. Kulingana na utafiti huo, asilimia 49 ya wananchi wanafahamu juu ya mchakato wa kukusanya maoni uliofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba na asilimia 21 wanafahamu kuwa vipengele vya rasimu ya Warioba viliondolewa na Bunge Maalumu la Katiba kupitia Katiba Inayopendekezwa. “Wananchi hawakubaliani na mabadiliko mengi yaliyofanywa na BMK chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba Mpya, Andrew Chenge,” alisema. POLEPOLE Akizungumza baada ya kutangazwa   matokeo hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, alikiri kuwa inahitajika Katiba Mpya lakini kwa sasa wameamua kushughulikia kwanza   shida za wananchi. “CCM inaamini katika utafiti kama nyenzo ya kutuarifu juu ya yale tunayoyatenda. Hata mimi na serikali ya CCM inataka Katiba, lakini kwa sasa tumeamua kushughulika na shida za watu suala la katiba litakuja baadaye. “Tuna miaka mitano kupanga ni kuchagua, mageuzi ya katiba yatafanyika pale ambapo tumefanikiwa kufanya mageuzi ya taasisi za siasa, jamii  na serikali…itaandikwa pale ambako nidhamu ya viongozi na watumishi itakuwa imenyooka,” alisema Polepole. Alisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa BMK lakini walikwama kwa sababu kulikuwa na masilahi binafsi ya viongozi wa vyama vyote ambao walishindwa kuwa na uelewa wa pamoja juu ya nini Watanzania wanataka na  muafaka na maridhiano pia havikuwapo. ACT WAZALENDO Katibu wa Itkiadi na Uenezi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, alisema katiba mpya bado ni kipaumbele cha Watanzania na kuinyoosha nchi bila katiba ni kazi bure. ASASI ZA KIRAIA Mwakilishi wa Asasi za Raia, Deogratias Bwire, alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kumshauri Rais Dk. John Magufuli aupe kipaumbele mchakato wa Katiba Mpya. “Serikali inafanya mambo mengi mazuri kama vile ya kulinda rasilimali za nchi je, haya yote yanalindwa kwenye nyaraka gani. “Tunapotaka kunyanyua maisha ya mtu mnyonge halafu mwisho wa siku hakuna sehemu anapoweza kwenda kuidai haki yake tunakuwa tunamdanganya,” alisema Bwire. CHADEMA Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Profesa Mwesiga Baregu, aliishauri Serikali isikilize maoni ya wananchi.  
1kitaifa
NA JOSEPH SHALUWA NI mrefu, mwenye ngozi yenye rangi ya dhahabu. Ana macho meupe, pua fupi, midomo minene iliyofunika meno yaliyopangika vyema kinywani na kutengeneza mwanya mdogo wa kichokozi katikati. Sauti yake nyembamba ni kivutio kingine, shingo ndefu kama ya twiga ni kati ya sifa zinazomuacha kwenye orodha ya warembo wa Tanzania wenye mvuto kwa mwaka wa kumi sasa. Usisahau kwamba mwaka 2013 alishinda Tuzo ya Msichana Mwenye Mvuto Zaidi (Sexiest Girl Award) ya gazeti moja la wiki nchini akiwamwaga washiriki wenzake waliongia fainali, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Nelly Kamwelu, Jacqueline Wolper na Jokate Mwegelo. Wema Isaac Sepetu ni kati ya warembo wachache nchini kutokea Miss Tanzania wenye kismati cha aina yake. Wamepita warembo wengi sana tangu yalipoanzishwa mashindano hayo mwaka 1994, lakini wengi wameshapotea kwenye ramani. Achana na walioshinda nyuma yake, tangu aliposhinda Wema mwaka 2006, warembo wengine takribani wanane waliomfuata, wengi wamesahaulika kabisa. Nitakukumbusha mwishoni. Ni rahisi kusema mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa bahati kwa washiriki na hasa wale walioshinda nafasi za juu. Kati ya warembo watano waliongia Tano Bora, wanne mpaka sasa wanaendelea kutesa kwenye sanaa mbalimbali. Nyuma ya Wema kuna Jokate Mwegelo ambaye ni modo, mwigizaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lisa Jensen – mwanamitindo na mwigizaji na Irene Uwoya aliyechukua namba 5 akitesa kwenye filamu za Kibongo. Pamoja na kwamba warembo wote wanne kutokea Miss Tanzania 2006 wapo kwenye game, Wema anaonekana kukubalika zaidi na mashabiki. Hiyo ni nyota ya ajabu kwa mlimbwende huyu. Kwa lugha nyepesi, naweza nikasema Wema ni brand – bidhaa. Ni taasisi kubwa ambayo inaweza kutengeneza fedha nyingi. Wema ni utajiri. Kupitia kipaji chake, anaweza kupata fedha nyingi mbali na umaarufu ambao pengine unamsaidia mambo mengi. Nimesukumwa kuandika makala haya ili kumuibua usingizini na kama alikuwa analitambua hili, basi ajue kuwa wapo wanaliona hilo kwa jicho pana, hivyo ingekuwa bora na faida kwake kama akianza haraka mapema ili kutengeneza umilionea.   MVUTO WA WEMA Kama unabisha kuwa Wema siyo brand, hakubaliki na hana kismati, fanya uchunguzi mwepesi ambao utakupa majibu ya haraka. Andika chochote kuhusu Wema mtandaoni ukimsema vibaya, uone kazi ya mashabiki! Wema hana sababu ya kujibu chochote. Hata ukimchafua kwa staili gani, wapo mashabiki zake huko, watasimama kwa ajili yake. Wema anapendwa, anakubalika. Kingine kinachomsaidia kukubalika na kupendwa ni namna anavyoguswa na mambo mbalimbali ya kijamii. Amewasaidia wengi wakiwemo mastaa. Kajala Masanja ni miongoni mwao. Wakati akiwa kwenye sakata la kwenda jela au alipe faini, ni Wema ndiye aliyotoa Shilingi milioni 13 kumsaidia kurejea uraiani na kupishana na mateso ya nyuma ya nondo. Wema hachafuki!   NINI KIMEMPATA WEMA? Wakati anaanza alijitahidi kuonyesha nia ya kusaka mafanikio, lakini kwa sasa spidi yake imepungua. Wema alikuwa na kasi ya kucheza sinema. Alikuwa miongoni mwa wasanii wa kike wanaolipwa ghali zaidi. Katika kundi hilo walikuwemo Aunt Ezekiel, Rose Ndauka, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na Shamsa Ford. Mwaka 2013, Wema alifungua kampuni yake ya utayarishaji filamu, Endeless Fame Films. Lilikuwa wazo zuri la kibiashara. Lakini wazo hilo hakulitendea haki, kwani mwaka mmoja baadaye alifunga ofisi hiyo. Nini kimetokea? Wema anapaswa kujitazama upya na kuangalia namna ya kusimama tena. Mtaji bado anao – ni jina lake tu.   MANAGEMENT ZAIDI Wema anaweza kutengeneza fedha zaidi kama akiwa na uongozi imara zaidi. Haina maana kwamba, Martin Kadinda siyo meneja mzuri, la hasha! Kadinda ni kijana mjanja, mchakarikaji na mbunifu. Ndiye aliyeharakisha na kushughulikia wazo la bidhaa ya lipstick yenye jina la Kiss by Wema Sepetu. Duka linalouza bidhaa hizo lipo Mwenge jijini Dar es Salaam. Hongera sana Kadinda. Lakini tukiangalia mafanikio ya mastaa wengi, si ya kutegemea meneja mmoja. Unaweza kuwa na mmoja anayesimamia jumla, lakini wengine wawili au watatu wakawa wa kubuni idea zaidi za biashara na kutoa ushauri. Sipati picha, ikiwa watu kama Ruge Mutahaba, Said Fella au Babu Tale wangekuwa kwenye crew ya management ya Wema ingekuwaje! Naamini tungekuwa tunamwongelea Wema mwingine. Si dhambi kuwa na meneja zaidi ya mmoja. Mwangalie Diamond anavyotusua kimafanikio, ni kwa sababu amezungukwa na mameneja wanaoshindana kuumiza vichwa kubuni mawazo ya biashara ya kumpaisha zaidi na zaidi. Hata Wema pia anaweza kutumia mbinu hiyo ili kutumia jina lake kujiweka pazuri kimafanikio. Kama kuna mtu amepata kumwambia kuwa eti jina lake limeanza kuchuja, anamdaganya sana. Muda bado unao Wema. Ni wewe tu.
4burudani
Na MWANDISHI WETU SELIMUNDU (sickle cell) ni ugonjwa wa kurithi ambao hutokea baada ya mwili wa binadamu kuwa na upungufu katika umbile la seli, ambapo hubadilika na kuwa nusu duara au umbile la mundu (zana ya mkulima) badala ya mduara. Hali hii ya umbile la seli kufanana na mundu, ndio iliyosababisha iitwe iitwe selimundu au kwa jina la kitaalamu sickle cell. Ni ugonjwa unaorithishana vizazi kwa vizazi, lakini endapo mzazi mmoja tu akiwa na vinasaba vya ugonjwa huu basi huwa ni vigumu kusababisha mtoto kuvipata, bali endapo wazazi wote wawili ikitokea wana vinasaba hivyo. Kwa Afrika, Nigeria ni nchi ya kwanza kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na selimundu huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu, ambapo kila mwaka watoto takribani 11,000 huzaliwa na matatizo hayo. Kutokana na kuongezeka kwa tatizo hilo, wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) wameamua kufanya utafiti na kutafuta njia ya kuutibu ikiwa ni pamoja na kupandikiza uboho (born marrow) na vinasaba kwenye mifupa. Kwa kawaida, chembe nyekundu ya damu ni mviringo, husafiri kupitia mishipa midogo kabisa ya damu kwa urahisi na kwa wagonjwa wenye selimundu, chembe zao za damu huvunjika na kupoteza umbo hilo la mviringo na kuchukua umbo la ndizi au mundu. Chembe hizo nyekundu za damu zenye umbo la mundu hukwama katika mishipa midogo ya damu mwilini na mtiririko wa damu kwenda sehemu fulani ya mwili unapopungua huku hewa safi ya oksijeni ikizuiwa na kusababisha maumivu makali ya ghafla. Kutokana na hali hiyo, husababisha maumivu makali katika mifupa na vifundo, maumivu yasiyotabirika ambayo yanaweza kutokea mara chache au mara nyingi kama kila mwezi kwa mgonjwa mwenye matatizo hayo. Dalili Dalili ya kwanza huanza kuonekana kwa mtoto pindi anapotimiza umri wa miezi sita tangu kuzaliwa kwake. Huanza kuugua mara kwa mara, kuvimba miguu, kuishiwa damu pamoja na ubongo wake kushindwa kukua ipasavyo. Hali hiyo inapotokea, mzazi anashauriwa kumpeleka hospitalini ili aweze kufanyiwa vipimo na kuanza matibabu mapema ili kupunguza ukubwa wa tatizo. Daktari Akizungumzia ugonjwa huo, Daktari wa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mloganzila, Moses Karashani, anasema sasa hivi kuna ongezeko la rufaa kwa watoto wanaougua selimundu. Anasema watoto hao ni wale wenye umri kuanzia miezi sita hadi miaka 14 ambapo kati yao nusu ni wale walio chini ya miaka minane. Anasema mara baada ya kuonekana kwa dalili zilizopo hapo juu, mtoto anapaswa kufikishwa hospitali mapema ili aweze kupata huduma za matibabu kwa haraka. “Mtoto ambaye wazazi wake wote wawili (baba na mama) wana vinasaba vya selimundu, kuna uwezekano wa asilimia 25 kupata ugonjwa huo na mtoto ambaye mzazi mmoja hana vinasaba hivyo hawezi kurithi,” anasema Dk. Karashani. Anaongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, walimua kuanzisha kliniki ya watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huo siku ya Jumanne na Alhamisi hospitalini hapo ili waweze kupata huduma bora za matibabu. Anasema watoto waliopewa rufaa kutoka hospitali mbalimbali nchini zikiwamo za Mkoa wa Dar es Salaam, wanafikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu. Anasema pia wamekuwa wakipokea watoto wenye ugonjwa huo kutoka majumbani, jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa. Anasema katika siku hiyo, zaidi ya watoto 20 wanafika hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu kuanzia umri wa miezi sita hadi miaka 14, ambapo kati yao, nusu yake ni wale wenye umri chini ya miaka minane, jambo ambalo linadhihirisha ukubwa wa tatizo. Anasema licha ya jitihada mbalimbali zinazotolewa na serikali katika kuhakikisha watoto wanapata huduma bora za matibabu, hadi sasa idadi ya watoto wanaougua ugonjwa wa selimundu ni kubwa. “Idadi ya wagonjwa wa selimundu inaongezeka siku hadi siku, juhudi za ziada zinahitajika ili kuhakikisha wanapatiwa matibabu bora,” anasema. Anasema watoto wanaougua ugonjwa huo, baadhi yao wanapitia changamoto nyingi ikiwamo kukimbiwa na mzazi mmoja au unyanyapaa. Anasema wazazi wengine huamua kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji wakiamini kuwa wamerogwa, jambo ambalo si kweli. Anasema hali hiyo imesababisha idadi kubwa ya watoto wanaofikishwa hospitalini kulelewa na mzazi mmoja. “Kwa sababu ugonjwa huu unahusisha udumavu wa ukuaji wa ubongo na maradhi ya mara kwa mara, baadhi ya wazazi wanaamua kuwakimbia wake zao na wengine kuwapeleka kwa waganga. Hii imechangia wengi wao kuletwa hospitali wakiwa kwenye hatua mbaya,” anasema. Anasema katika za Marekani na India, mtoto mara baada ya kuzaliwa anafanyiwa vipimo maalumu ‘screening’ ili kubaini matatizo aliyonayo, hii huwasaidia kuanza matibabu mapema pindi anapobainika kuwa na matatizo. Dk. Karashani anasema Chuo cha Afya ya Tiba Muhimbili (Muhas) walifanya utafiti kuhusiana na vipimo hivyo maalumu ‘screening’ katika hospitali za Temeke na Mwananyamala na kufanikiwa. “Kwa mfano, baadhi ya hospitali binafsi nchini, wanaweka ‘full package’ ya mjamzito na gharama za malipo yake ikiwamo ya kumfanyia ‘screening’ mtoto mara baada ya kuzaliwa, hali ambayo inasaidia kujua matatizo yanayomsumbua,” anasema. Anasema vipimo hivyo ni muhimu kwa sababu vinasaidia kujua maradhi ambayo mtoto anaweza kuzaliwa nayo. Dk. Karashani anasema ili waweze kupiga hatua zaidi ya kuwatibu watoto, Serikali inapaswa kuboresha sera zake na kuanzisha mpango maalumu wa kuwafanyia vipimo maalumu watoto hao mara baada ya kuzaliwa. Anasema kuboreshwa kwa sera hizo kutasaidia kuwalazimisha wajawazito kulipia gharama za matibabu zikiwamo za kuwafanyia screening watoto wakiwa wachanga. Anasema hiyo itasaidia kutambua matatizo ya mtoto kuanzia tumboni hadi anapozaliwa, jambo ambalo pia linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo. Anasema lakini pia serikali inapaswa kuanzisha utaratibu wa utoaji wa elimu kwa wagonjwa wa selimundu kuanzia ngazi ya mtaa ili kuhakikisha elimu ya ugonjwa huo inawafikia watu wengi zaidi. Hii itapunguza unyanyapaa na kuondoa imani potofu na kudhani kuwa wamerogwa. Mmoja wa wazazi aliyezungumza na gazeti hili, Amina Omary, ambaye mtoto wake wa umri wa miaka mitano anasumbuliwa na maradhi haya, anasema awali alikua hajui kama ana ugonjwa huo hivyo alimpeleka kwa mganga wa kienyeji ili kupatiwa matibabu. “Nilipojifungua mwanangu alikuwa anaumwa mara kwa mara pamoja na kukaukiwa damu, nilidhani amerogwa, nikaanza kuhangaika kwa waganga tofauti ili kutafuta tiba, lakini hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya mtoto kuendelea kuugua,” anasema Amina. Anaongeza kuwa, wakati anaendelea kuhangaika kutafuta tiba ya mtoto wake, mzazi mwenzie aliamua kumkimbia hivyo akawa katika mazingira magumu huku akihangaika mwenyewe ukizingatia kuwa hana kipato cha kutosha. Anasema mwishowe aliamua kurudi hospitali na kuanza vipimo, ndipo mtoto wake alipogundulika kusumbuliwa na selimundu, akatakiwa kuanza matibabu haraka kwa sababu alikuwa amechelewa. “Mimi na familia yangu tulidhani mwanangu amerogwa hivyo nikaamua kwenda kwa waganga, tuliposhindwa tukarudi hospitali na kuanza vipimo ndipo alipogundulika kwamba anaumwa selimundu,” anasema. Anasema katika kipindi chote hicho, baadhi ya ndugu, jamaa na familia walikuwa wanamnyanyapaa mtoto wake kwasababu ya maradhi yanayomsumbua. Anaiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kuanzia ngazi ya vijiji ili kila mmoja aweze kuujua ugonjwa huo na dalili zake, hii itasaidia kuwafikisha watoto mapema hospitalini. Naye Mariam Hussein ambaye mwanawe hana ugonjwa huo, anasema elimu kuhusu selimundu haijatolewa vya kutosha, ndio maana wananchi hukimbilia kwa waganga wakidhani wamerogwa. “Mimi mwenyewe sina elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huo, ndio maana tunapoona mtoto anaugua mara kwa mara tunaamini karogwa,” anasema. Anaongeza: “Ikiwa watapatiwa elimu ya kutosha, itasaidia wazazi wengi kuwahi hospitali na wanaume kushindwa kuwakimbia wake zao.”
5afya
Vijana hao wa Hans van Pluijm na Charles Boniface Mkwasa, wanashuka dimbani wakitoka kuifunga Coastal Union mabao 8-0 katikati ya wiki hii na kujiwekea historia ya kufunga ya kuwa timu iliyoshinda mechi moja kwa mabao mengi katika msimu huu wa 2014/15 unaoelekea ukingoni.Yenyewe Mbeya City yenye makazi yake jijini Mbeya, katika mchezo wake dhidi ya Azam FC katikati ya wiki, ililazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na leo ita kuwa Uwanja wa Taifa, kusaka pointi tatu za kuiweka pazuri zaidi kuliko ilivyo sasa.Aidha, Yanga na Mbeya City zinakutana kwa mara ya pili, baada ya mzunguko wa kwanza kukutana kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 3-1.Mbeya City ni timu ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa inaongoza kwa sare 10 baada ya ndugu zao, Tanzania Prisons kuongoza kwa sare 11 kabla ya michezo ya jana.Wakati Yanga ikiongoza kwa pointi 43, Mbeya City wana pointi 25 wakiwa katika nafasi ya nane, lakini timu hiyo ya Mbeya ikiwa mbele kwa kucheza michezo 21 huku Yanga wakicheza 20.Timu zote mbili zimelenga kushinda mchezo wa leo ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri. Mbeya City ambao walianza vibaya msimu huu, kwa sasa wako vizuri na waliwabana mabingwa watetezi Azam FC kwenye uwanja wao wa nyumbani kwani wamekuwa wakionesha hamu ya kutaka ushindi.Itaingia Uwanja wa Taifa ikipania kushinda, lakini itakuwa na kazi ngumu dhidi ya Yanga iliyo katika kiwango bora kwa sasa huku wachezaji wake wa safu ya ushambuliaji Simon Msuva, Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa, Haruna Niyonzima wakiwa katika viwango vyao vya ubora.Katika kiungo, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’ wako vizuri, sawa na safu yao ya ulinzi chini ya nahodha Nadir Haroub na kipa wao, Ally Mustapha ‘Barthez,’ hivyo Mbeya City ambayo msimu uliopita iliingia ligi kwa kishindo na kumaliza nafasi ya tatu, itabidi ifanye kazi ya ziada kutokana na pointi Taifa leo.Mchezo wa leo utakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ambao wanatarajia kucheza mechi ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho mwishoni mwa wiki ijayo dhidi ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia kwenye Uwanja wa Taifa.Mechi nyingine itakayochezwa leo ni Stand United wakiwakaribisha maafande wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Katika mchezo wa kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.Polisi Morogoro ambao walianza vizuri Ligi Kuu, kwa sasa hawako katika hali nzuri, hadi kusababisha aliyekuwa kocha wake, Mohamed Rishard ‘Adolf’ kutimuliwa.Ni timu ambayo iko katika hatari ya kushuka daraja kwani inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 21 wakati Stand United inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 24, nayo ikiwa haina uhakika wa kubaki Ligi Kuu.
2michezo
  Na Tiganya Vincent SERIKALI mkoani Tabora imeliagiza jeshi la polisi   kuendesha   ukaguzi wa magari yote yanayotoa huduma za usafirishaji wa abiria   kuhakikisha   mabovu yanazuiwa kutoa huduma hiyo. Kauli hiyo ilitolewa   wilayani Sikonge baada ya  ajali mbili za basi la Kampuni ya Adventure iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na la Kampuni ya HBS.  Ajali hizo zilitokea hivi karibuni. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alisema hatua hiyo itasaidiz kuzuia ajali zinazototokea kutokana na ubovu wa vyombo hivyo. Alisema   baada ya kuangalia gari la HBS  namba T960 AHH, bodi yake  ilionekana imechakaa ingawa lilikuwa linaendelea kutoa huduma ya usafiri. Alimwagiza Kamanda wa Polisi Usalama wa Barabarani Mkoa wa Tabora (RTO)  kuanza mara moja ukaguzi wa magari yote ya abiria kila siku. Mwanri alisema haiwezekani magari mabovu yaendelee kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na kuendelea kuhatarisha  maisha ya watu. Alisisitiza kuwa gari lisiruhusiwe kusafiri likiwa bovu hadi   litakapofanyiwa maboresho ya kuondoa ubovu huo. Ilielezwa kuwa  ajali ya basi la HBS ilisababishwa na uzembe wa dereva   ambaye alijaribu kulipita gari jingine katika upande usioruhusiwa na kujikuta akiingia katika daraja  na basi kupinduka. Tukio hilo lilisababisha abiria  zaidi ya 20 kujeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge. Mmoja wa majeruhi wa gari hilo,   Sada Shabani alikiri dereva wa gari lao hakuwa makini   alipokuwa anapishana na gari jingine na kujikuta akiingia katika daraja, Alisema   ajali hiyo ingeweza kuepukika kama dereva huyo angesubiri lori la mafuta lipite na yeye   aendelee na safari yake. Wakati huohuo, Mwanri  aliagiza jeshi la polisi kuwatafuta madereva wa mabasi yote mawili waliosababisha ajali na kukimbia ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
1kitaifa
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata na kumfi kisha mahakamani, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (Chadema) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh milioni mbili kati ya Sh milioni 10 alizoomba.Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla mtuhumiwa huyo hajafikishwa mahakamani jana, Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali alisema Kimbe alikamatwa na maofisa wa Takukuru juzi katika Hoteli ya Gentle Hills mjini Iringa.Kimbe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Isakalilo mjini Iringa, anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa mzabuni wa manispaa hiyo, Nancy Hassan Nyalusi anayefanya kazi ya kukusanya ushuru katika stendi ya mabasi ya mjini Iringa.Kilimali alisema Meya huyo alipokea fedha hizo za mtego wa rushwa kwenye gari yake aina ya Nadia yenye rangi ya maroon ikiwa na namba za usajili T456 CKD iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegeshea magari ndani ya hoteli hiyo ya Gentle Hills.Katika hatua nyingine, Kimbe aliyekuwa akishikiliwa na Takukuru tangu akamatwe juzi jioni, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa jana majira ya saa saba mchana.Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, Liad Chamshana, mwanasheria wa Takukuru, Lestituta Kessy alisema Kimbe (42) anatuhumiwa kwa mashtaka mawili ya rushwa kinyume na Kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.Alitaja shitaka la kwanza kuwa ni kushawishi kiasi cha Sh milioni 10 kutoka kwa Nancy Nyalusi kama zawadi ya kumpatia mkataba wa kukusanya ushuru katika maeneo ya stendi kuu ya mabasi mjini Iringa kitu ambacho kina mahusiano na kazi za mwajiri wake ambaye ni Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.Katika shitaka la pili, Kimbe anatuhumiwa kama Meya wa Manispaa ya Iringa kujipatia Sh 1,990,000 kutoka kwa Nancy Nyalusi kama zawadi baada ya kumpatia mkataba wa kukusanya ushuru katika stendi ya mabasi.
1kitaifa
Mkuu wa Upelelezi wa wilaya, Charles Chalula, alipoulizwa juu ya tukio hilo jana alikiri taarifa kufika ofisini kwake, na tayari jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo mhudumu wa hoteli hiyo. Pia alisema atawasiliana na mkurugenzi wa hoteli hiyo, aliyemtaja kwa jina moja la Haule ili aweze kurudisha fedha za wachezaji, ambazo walilipa kukaa hapo hadi Mei 2 mwaka huu michezo itakapokamilika.“Ni kweli wachezaji wamekuwa na hofu na usalama wao na mali zao, nitamtafuta mmiliki wake akiwezekana arudishe fedha zao leo hii hii (jana) ili waweze kuhamia hoteli nyingine, ila nitahakikisha suala la upelelezi tunalifanya haraka ili hivi vitu vilivyoibwa vipatikane haraka,” alisema Chalula.Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo gazeti hili, wizi huo ulitokea majira ya saa 10:00 jioni wakati wengi wa wachezaji hao wakiwa Uwanja wa Jamhuri kuishangilia timu ya soka soka iliyokuwa inapambana na CDA ya hapa. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.Mbali ya soka, wachezaji wengine wa Uchukuzi ni wa michezo ya kuvuta kamba, bao, drafti na karata. Mmoja wa wachezaji hao, Ally Suleiman katika chumba chake ameibiwa kompyuta mpakato yenye thamani ya Sh milioni 1.2, fedha taslimu Sh 120,000 na mashine inayohifadhia nyaraka mbalimbali yenye thamani ya Sh 180,000.Suleiman aliyefungua kesi ya wizi iliyopewa jalada namba IR/3844/2016 pia aliibiwa vitu mbalimbali ikiwemo kadi ya Bima ya Afya na leseni ya udereva.Mchezaji mwingine, Tracius Dionis alisema wezi hao waliingia chumbani kwake na kutawanya vitu kwenye begi lake, lakini hawakuiba chochote zaidi ya kuchukua seti ya televisheni, mali ya nyumba hiyo ya kulala wageni.Aliongeza kuwa, walifungua chumba cha mchezaji mwingine, Aminiel Ombeni ambaye amesafiri kwenda Moshi kuzika baada ya kupata msiba wa mama yake, na bado haijajulikana vilivyoibwa kwani begi lake lilikutwa katika chumba cha mteja aliyefika juzi mchana.Naye Katibu Mkuu wa timu ya Uchukuzi, Alex Temba alisema wamesikitishwa na tukio hilo kwani haijawahi kutokea katika mikoa yote waliyowahi kushiriki michezo ya Mei Mosi.Temba aliomba jeshi la polisi kuonyesha ushirikiano kama lilivyoahidi siku ya kwanza timu ziliporipoti mkoani hapa kuwa watatoa ulinzi mkubwa, basi watekeleze ahadi yao kutokana na wachezaji wote ni wageni mkoani hapa.“Suala hili limetusikitisha sana huyu ni mfanyakazi mwenzetu pamoja na kwamba tupo katika suala la michezo lakini aliendelea na kazi za ofisi na jana tu alikuwa akituma taarifa mbalimbali, basi tunawaomba polisi watusaidie hivi vitu vipatikane, na hata waongeze ulinzi kwani ni tukio la aibu kuwaibia wageni,” alisema Temba.
2michezo
OSCAR ASSENGA, TANGA Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema kuwa ifikapo Januari mwakani viwanja vyote nchini vitatumia mfumo wa kieletroniki katika ukataji tiketi za kuingia uwanjani. Karia amesema hayo leo Desemba 1 alipofungua mkutano wa baraza kuu la TPLB lililofanyika mjini Tanga. Amesema wataanza mazungumzo na Chama cha Mapinduzi pamoja na Halmashauri mbalimbali zinazomiliki viwanja ambavyo hutumiwa na baadhi ya timu za zinzaoshiriki Ligi kuu bara. “Labda niwaambie kwamba viwanja vyote hapa nchini ifikapo Januari vitatakiwa kuwa na mashine kwa ajili ya ukataji wa tiketi na zoezi hilo litaanza mazungumzo na halmashauri pamoja na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),” amesema Rais Karia. Karia amesema zoezi hilo litafanyika kama linavyofanyika katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Uhuru, Chamazi na Taifa vya jijini Dar es Salaam.
2michezo
TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa sasa ipo nchini Misri ambapo imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21. Kikosi kilikuwa na jumla ya wachezaji 39 awali ambapo mchujo wa kwanza ulichuja wachezaji saba na mchuju wa pili ulichuja wachezaji 9 na kufanya wachujwe jumla ya wachezaji 16 na kufanya wabaki wachezaji 23. Mchujo Wachezaji saba walioachwa kwenye kikosi kabla ya kukwea pipa ulikuwa namna hii 1. Ibrahim Ajibu- Yanga 2.Jonas Mkude- Simba 3.Ally Ally -KMC 4.Shomari Kapombe- Simba 5.Ayoub Lyanga- Coastal Union 6.Kenedy Wilson- Singida United 7.Kassim Khamis- Kagera Sugar Wachezaji tisa walioachwa kutoka kwenye kikosi kilichokwea pipa mpaka kambini nchini Misri ni:- 1. Claryo Boniphace – U20. 2. Selemani Salula – Malindi FC. 3. David Mwantika – Azam FC. 4. Abdi Banda – Baroka FC 5. Fred Tangalu – Lipuli FC. 6. Miraji Athuman – Lipuli FC. 7. Shiza Kichuya – ENPPI. 8. Shaban Chilunda – Tenerife. 9. Kelvin John – U17. Hawa hapa ndio watakaoshiriki Afcon  
2michezo
Na CLARA MATIMO- MWANZA WATOTO 45 wamekatiwa bima ya afya na Shirika la Foundation Dart linalosaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mwanza. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi watoto hao bima hizo katika kituo cha afya Buzuruga jana, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dorocella Reuben, alisema hiyo ni zawadi muhimu kwa walengwa kwa kuwa sasa watakuwa na uhakika wa matibabu endapo wataugua. Alisema tangu shirika hilo lianzishwe mwaka 2012, limekuwa likitoa misaada mbalimbali kwa watoto wa kike ambao wanaishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kielimu kwa kuwanunulia vifaa vya shule, kuwalipia ada na mafunzo ya ufundi, lakini wanapougua huingia gharama kubwa kwa ajili ya kuwapatia matibabu. “Tulikaa na viongozi wenzangu tukatafakari tukaona ni bora tuwakatie bima watoto wetu hawa ili wawe na uhakika wa matibabu, tumeanza na hawa wachache lakini tutaendelea kuwakatia wengine kadiri Mungu atakavyotuwezesha, naomba Watanzania wenzangu wenye uwezo wawatafute watoto ambao familia zao hazijiwezi wawakatie bima. “Tumeamua kuwakabidhi leo hizi bima zao ikiwa tunaelekea katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na mwaka mpaya kama sehemu ya zawadi za shirika kwao, maana hakuna zawadi kubwa kama ya uhai, unapokuwa na bima una uhakika wa kuokoa maisha,” alisema. Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buzuruga, Dk. Masoud Masele, alipongeza shirika hilo kwa kuwakatia watoto hao bima hizo za afya zenye thamani ya Sh 180,000. Alisema hivi sasa watakuwa na uhakika wa kupata matibabu katika hospitali zilizo ndani ya Manispaa ya Ilemela.
1kitaifa
Mwandishi Wetu-Dodoma SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kuwa limefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh bilioni 23.5 ambazo zilikuwa zikitumika kila mwaka kuendeshea mitambo ya umeme. Pia katika kipindi cha miaka minne shirika hilo limeweza kupata megawati 400 za ziada ambazo awali hazikuwepo. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dodoma kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano,  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, alisema kuwa fedha hizo zilikuwa zinatumika katika uendeshaji wa mitambo ya kusukuma umeme katika vituo mbalimbali hapa nchini. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni Mtwara, Tunduru, Namtumbo, Songea, Madaba, Ruvuma na Liwale ambavyo vyote hivyo  awali vilikuwa vikitumia mafuta kupeleka umeme maeneo mbalimbali hapa nchini. “Tunashukuru sasa hivi tumefanikiwa kuokoa kiasi hicho cha fedha tokea mwaka 2018, na tunaamini tutazidi kupiga hatua kwa hii miradi tunayoifanya,” alisema Dk. Mwinuka. Alisema shirika hilo limeongeza ukusanyaji wa mapato hadi kufikia Sh trilioni 1.53. kutoka Sh trilioni 1.2 mwaka 2012/13. Dk. Mwinuka alisema mafanikio mengine waliyoyapata ni  kwenye ufuaji wa umeme, ununuzi, usafirishaji pamoja na eneo la uwekezaji. Alisema kuacha kufua umeme kwa kutumia mafuta, kumetokana na uwekezaji ambao wameufanya ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta hiyo. Mbali na hilo, alisema ili kutatua changamoto za umeme Dar es Salaam wamefanikiwa kuboresha kituo cha Ubungo cha kupooza umeme kutokana na kuzidiwa. “Hivi karibuni tumeboresha kituo cha Ubungo, kutokana na mahitaji ya jijini kuwa makubwa na kusababisha kituo kuzidiwa na megawati 240, hii imesaidia kutatua tatizo la umeme,” alisema Dk. Mwinuka. Alisema wamefanikiwa kufunga transfoma mpya ambayo ina wezo wa kufanya kazi katika maeneo mbalimbali tofauti na ilivyokuwa awali. Dk. Mwinuka alisema kuwa mwaka 2015 mita zilizofungwa ni 1,648,386 ambapo hadi kufikia mwaka jana mita zilizofungwa ni 2,700,682 sawa na ongezeko la mita 1,052,292 sawa na asilimia 63.84. Alisema Mtwara kulikuwa na tatizo la umeme na wameweza kuongeza mitambo miwili ya gesi asilia yenye KV 4. Dk. Mwinuka alisema katika kipindi cha miaka minne wameweza kupata megawati 400 za ziada ambazo awali hazikuwepo. “Kwa ujumla kwa kipindi cha miaka minne tumeweza kupata megawati 400 za ziada ambazo hatukuwa nazo kabla ya 2015,” alisema Dk. Mwinuka. Alitaja mafanikio mengine ni kushuka kwa gharama za umeme kuanzia mwaka 2016 katika maeneo ya malipo ya huduma pamoja na gharama za maombi. “Ilikuwa ukitaka kuomba umeme ilikuwa lazima ulipie, hata gharama ya uniti moja iliteremshwa kutoka 2.4 hadi 1.5 kwa uniti na ilitegemea na mteja wa aina gani na hilo ni moja ya fanikio katika huduma yetu ya umeme,” alisema Dk. Mwinuka.
1kitaifa
Derick Milton, Simiyu Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe amesema wamepata taarifa kuwa baadhi ya wasambazaji  waliopewa dhabuni ya kusambaza viuatilifu vya kuua wadudu kwenye zao la pamba wanaihujumu serikali. Bashe amesema kuwa wamegundua wasambazaji hao wamekuwa wakiuzia serikali dawa hizo kupitia bodi ya pamba kwa bei kubwa kuliko wanavyowauzia watu wenye maduka ya kuuza viuatilifu hivyo. Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akipokea chupa 13,000 za viuatilifu vya pamba kutoka bodi ya pamba kwa ajili ya kuwapatia wakulima wa Mkoa wa Simiyu. Bashe amesema kuwa wamegundua kuwepo kwa hujuma hizo, kwani viuatilifu hivyo vinavyouzwa kwenye maduka hayo bei yake imekuwa rahisi, kuliko vinavyouzwa na bodi ya pamba nchini. Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri huyo ameiagiza bodi ya pamba, kufanya operesheni kali kwenye maduka yote yanayouza dawa hizo kuangalia kama bei ya viuatilifu inayotumika inalingana na ile ambayo wanatumia bodi. “Hatuwezi kuwa na wasambazaji wa aina hii, waliomba wenyewe tukawapa masharti, lazima wayatekeleze, hatuwezi kuendelea kumkandamiza mkulima, bodi ya pamba ifanye opereisheni kila duka kuangalia bei za uko,” amesema Bashe.
1kitaifa
Aidha uzinduzi huo umeenda sanjari na kutoa huduma stahiki na bidhaa halisi za kampuni hiyo zinazouzwa na kupata waranti ya miaka miwili endapo bidhaa hizo zitaharibika.Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo nchini, Mike Seo wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa bidhaa hizo pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa duka hilo.Alisema lengo la kufungua duka hilo ni kukidhi mahitaji ya wateja wa kampuni hiyo kwani Arusha ni mji wa kiuchumi, kitamaduni pia ni kitovu cha utalii na diplomasia Afrika Mashariki.Naye Mikidad Mubaraka ambaye ni moja kati ya wadau wa kampuni hiyo, alisema lengo la kuzindua kituo hicho jijini hapa ni kusogeza huduma karibu na wateja na kuboresha mahusiano ili wateja kununua bidhaa halisi badala ya kukimbilia bidhaa feki.Aliongeza kuwa teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu zaidi ya 236,000 kwenye inchi 79 na inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia kuingia kwenye teknolojia mpya ya matumizi ya simu za kisasa na luninga.
0uchumi
IMEELEZWA kwamba, kitendo cha baadhi ya madaktari kukataa kutoa ushahidi mahakamani na polisi kushindwa kufanya uchunguzi unaojitosheleza ni miongozni mwa vikwazo kwa kesi za udhalilishaji wa kijinsia kushindwa kusikilizwa kwa wakati.Hayo yalisemwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, Makame Mshamba, baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa mikoa ya Kaskazini Unguja na Mkoani Pemba juzi.Alisema baadhi ya madaktari wamekuwa wakisumbua kutoa ushirikiano, huku wakikataa kufika mahakamani wakati wanapotakiwa kutoa ushahidi kwa mtu aliyefikwa na tukio la udhalilishaji wa kijinsia ikiwamo kubakwa au kulawitiwa. Alisema ni kosa kwa mtu anapoitwa mahakamani kutoa ushahidi kukataa wito huo na inachukuliwa ni sawa na kukwamisha Mahakama kutekeleza majukumu yake.“Madaktari wanatusumbua sana katika uendeshaji wa kesi zetu kwa sababu wamefanya kazi ya uchunguzi wa kitabibu kwa muathirika sasa wanapoitwa waje wathibitishe mahakamani hawataki, hii si sawa,” alisema.Alisema zipo baadhi ya kesi zimekwama kwa sababu ya kushindwa kupatikana kwa ushahidi kutoka kwa madaktari waliofanya kazi ya kupima mtu aliyedhalilishwa. Alipoulizwa kwa nini madaktari hao wanakataa kufika mahakamani kutoa ushahidi wa mtu waliyemfanyia uchunguzi, alisema wanadai kwamba hiyo si kazi yao.Naye ofisa kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Rashida Ahmed, alisema baadhi ya kesi zinazowasilishwa kutoka Jeshi la Polisi uchunguzi wake kwa kiasi kikubwa huwa haujakamilika huku ukiacha maswali mengi ya msingi yanayotakiwa kufanyiwa kazi.“Tunaletewa baadhi ya kesi za udhalilishaji wa kijinsia kutoka polisi lakini uchunguzi wake kwa kiasi kikubwa huwa haujakamilika na ndiyo maana tunazifuatilia zaidi kwa kutaka kujua mambo ya ziada,” alisema.Kwa mujibu wa taarifa fupi ya uchunguzi wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia iliyofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) Zanzibar, matukio hayo yamekuwa yakiongezeka ukiwamo ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kiume na wanawake visiwani hapa.
1kitaifa
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Tava, Agustino Agapa alisema wachezaji wa wavu ufukweni hawana gharama kutokana na kuwa timu inaundwa na wachezaji wawili pekee.“Ni wakati muafaka kwa makocha wetu katika mikoa mbalimbali kutafuta vipaji ambavyo vitashiriki katika mchezo huu ambao ni mzuri kwa watalii kwa kuwa huchezwa ufukweni zaidi,” alisema.Alisema pia kuwa hata ikihitajika kusafirishwa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ni rahisi kuwamudu kwa gharama na kufanya vyema. Mwenyekiti huyo alisema katika kuhakikisha mpango wa kuibua vipaji unafanikiwa walifanya mafunzo hivi karibuni kwa makocha 27 wa Dar es Salaam na mikoani na kuwaelimisha kuhusu mchezo huo.Alisema makocha hao walielimishwa namna ya kufundisha mchezo huo, hivyo anaamini wataenda kutengeneza timu zitakazoleta ushindani katika ligi ya kitaifa.Agapa alisema mchezo huo bado ni mchanga lakini iwapo utatumiwa vyema ni sehemu ya kuvutia utalii hasa katika hoteli zinazojengwa katika fukwe mbalimbali.
2michezo
SERIKALI imesema walimu hawapaswi kudai malimbikizo ya nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa miaka ambayo nyongeza hiyo haikutolewa.Hayo yalibainishwa bungeni jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Bakar (Chadema) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.Katika swali lake, Bakar alisema: “walimu wote nchini wameingia katika mkataba na mwajiri wake ambao pamoja na mambo mengine unaonesha uwepo wa nyongeza ya mshahara kila ifikapo Julai. Tangu iingie madarakani serikali ya awamu hii walimu hawajapewa hiyo.”Alitaka kujua kama serikali itawalipa walimu kama malimbikizo au imeshapoteza. Akijibu swali hilo, Waitara alisema serikali imekuwa ikitekeleza miongozo mbalimbali iliyowekwa kuhusu maslahi ya walimu ikiwa ni pamoja na kutoa nyongeza za mwaka za mishahara kulingana na utendaji mzuri wa kazi na kwa kuzingatia tathimini ya utendaji kazi ya kila mwaka.“Kwa mujibu wa Kanuni E. 9 (1) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009 Toleo la Tatu, nyongeza ya mwaka ya mishahara haipaswi kuombwa au kudaiwa na walimu, bali serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza hiyo kutokana na sera za kibajeti kwa mwaka husika,”alisema. Alisema watumishi wa umma wakiwemo walimu wanastahili kupewa nyongeza ya mwaka ya mshahara iwapo bajeti ya mishahara inaruhusu.Waitara alisema kutokana na ufinyu wa bajeti, nyongeza hiyo haikutolewa kwa watumishi katika mwaka wa fedha 2003/4, 2004/5, 2008/9, 2011/12, 2012/13 na 2016/17. “Hata hivyo, kwa kutambua utendaji mzuri wa kazi, Serikali ya Awamu ya Tano ilitoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wote ikiwemo walimu katika mwaka 2017/18,”alieleza na kuongeza: “Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kuwa serikali itatoa nyongeza ya mishahara ya mwaka kwa watumishi kadri ya uwezo wa kulipa utakavyoruhusu. Hivyo walimu hawapaswi kudai malimbikizo ya nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa miaka ambayo nyongeza hivyo haikutolewa.”
1kitaifa
['Kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumrithi Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa Manchester United. (Manchester Evening News)', 'Tottenham wapo tayari kupokea ofa za usajili za chini ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)', 'Spurs haina mpango wa kumsajili kiungo Mserbia anayechezea Manchester United Nemanja Matic, 31. (Manchester Evening News)', 'Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin amesema teknolojia ya usaidizi ya mwamuzi ama VAR ni "uozo" japo "haiwezekani kurudi nyuma". (Mirror)', 'Arsenal wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Valencia Marcelino wakati klabu hiyo ikiendelea kusaka kocha mpya wa kudumu. (Goal - in Spanish)', 'Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ameacha kumfuatilia kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25, kutokana na kuwa na dau la pauni milioni 85 katika mkataba wake. (Mail)', 'Kocha wa Manchester United Solskjaer amesema anataka klabu hiyo kufanya maamuzi ya haraka katika dirisha la usajili, akiashiria kuwa mwenyekiti mtendaji Ed Woodward hakufanya maamuzi ya haraka mwishoni mwa msimu wa uliopita. (Evening Standard)', "Manchester City wameingia katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez. Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye miaka 22. (Sky Sports Italia, via Calciomercato - in Italian)", 'Mshambuliaji raia wa Ufaransa Olivier Giroud atafanya mazungumzo magumu na klabu yake ya Chelsea. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33 anataka kuondoka klabuni hapo mwezi Januari. (Evening Standard)', 'Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amefanya maamuzi ya kutofanya usajili wowote mwezi Januari licha ya klabu hiyo kupwaya kwenye safu ya ulinzi. (Independent)', 'Klabu yeyote ya Ligi ya Primia ambayo itataka kumsajili kocha wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez italazimika kulipa fidia ya zaidi ya pauni milioni 20 kwa klabu yake ya sasa, Dalian Yifang ya Uchina. (Mail)', 'Tetesi bora za Jumanne ', 'Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, anatarajiwa kugoma kurejea katika ligi ya Primia na badala yake kusaini mkataba na klabu yake nyengine ya zamani ya AC Milan. (Telegraph)', 'Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Arsenal inamtaka nahodha wa zamani wa klabu hiyo Mikel Arteta kuchukua mikoba ya kocha aliyetimuliwa Unai Emery. Kwa sasa Arteta ni kocha msaidizi wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City. (Mirror)', 'Arsenal ipo tayari, ikibidi, kupitia rekodi na kufanyia usaili mpaka wakufunzi 12 ambao watawania nafasi iliyoachwa wazi na Emery aliyetimuliwa juma lililopita. (Mirror)', 'Everton wanatarajiwa kutomfukuza kocha wao Marco Silva kabla ya mchezo na mahasimu wao wa jadi Liverpool hapo kesho Jumatano. (Express)', 'Kocha Manuel Pellegrini amejiongezea muda wa kuifunza klabu ya West Ham baada ya kuifunga Chelsea. Kibarua cha kocha huyo mzoefu pia kipo mashakani kutokana na timu yake kutokuwa na matokeo mazuri. (Mail)', 'Kocha aliyetimuliwa na klabu ya Tottenham hivi karibuni Mauricio Pochettino amefungua milango ya kurejea katika ligi ya Primia akitamba kuwa yupo tayari kuzamia tena kwenye bahari ya ukufunzi. (Fox Sports, via Mirror)', 'Mlinzi wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, anaamini Pochettino amekuwa mhanga wa mafanikio yake mwenyewe klabuni hapo na kuwa wachezaji wote wanahisi kusababisha kufutwa kazi kwa kocha huyo raia wa Argentina. (Evening Standard)']
2michezo
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya watendaji ikiwa ni pamoja na kubadili Msemaji wa Jeshi hilo.Katika mabadiliko hayo IGP Sirro amemteua aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar.IGP Sirro amemteua kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.Taarifa ya Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii kwenye jeshi hilo, Mussa Mussa imeeleza kuwa, IGP Sirro amemhamisha aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai Zanzibar Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Maulid Mabakila kumpeleka makao makuu ya Polisi, Dar es Salaam.DCP Msangi amesema, mabadiliko hayo ni ya kawaida kuboresha utendaji wa Jeshi la Polisi.SACP Misime amewaomba waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kuendeleza ushirikiano wa Polisi na waandishi wa habari katika kuielimisha jamii iache vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
1kitaifa
Dirisha la usajili Ulaya limefungwa jana usiku, ambapo AS Roma wameanikiwa kumsajili kiungo mchezeshaji wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan kwa mkopo wa mda mrefu. Miamba hao wa Serie wamefanikiwa kunasa huduma ya nyota huyo kufuatia kutokuwa na nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza hapo emirates tangu aondoke Manchester United. Raia huyo wa Armenia huenda sasa anaungana na Nacho Monreal na Mohammed Elneny ambao wamejiunga na Real Sociedad na Beşiktaş mtawalia. Lakini Mkhitaryan alibadilishwa katika dabi ya jana na pia alichezeshw akwenye mechi dhidi ya Newcastle huku pia mshahara wake wa yuro laki mbili kwa wiki ukiwa kikwazo. Iwapo Mkhitaryan atakamilisha uhamisho huo wa mkopo atajiunga pamoja na Chris Smalling aliyewai kucheza naye katika klabu ya Manchester United. Maoni ya mashabiki
2michezo
Koku David, Dar es Salaam Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kodi wa Temeke, imewataka wamiliki wa majengo kulipa kodi hiyo sanjari na madeni ya nyuma. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatano Februari 5, katika semina iliyoshirikisha wamiliki wa majengo wa Kata ya Makangarawe, Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke, Paul Walalaze amesema majengo yote yanatakiwa kulipiwa kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba kila mmiliki mwenye deni la nyuma anaruhusiwa kulipa taratibu. Amesema TRA imepewa agizo la kufanya kazi na taasisi za serikali ili kuhakikisha lengo la kukusanya kodi kwa kila anayestahili linafikiwa. “TRA inamjali mlipa kodi na ndiyo maana imeboresha huduma, lakini pia inapokea maoni na kero za walipa kodi ili kuangalia namna nzuri ya kuweza kuzitatua,” amesema Walalaze. Kwa upande wake Ofisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mkoa wa Temeke, Catherine Mwakilagala amesema msamaha wa kodi ya majengo huombwa kila mwaka na mhusika wa msamaha mwenye umri wa kuanzia miaka 60 na zaidi. Amesema iwapo muombaji wa msamaha huo nyumba yake itakuwa na madeni ya nyuma sheria inamtaka kuyalipa kama kawaida. “Pia muombaji huyo wa msamaha wa kodi ya majengo anatakiwa kuwa anaishi kwenye nyumba hiyo ambayo yeye ndiye mmiliki halali na si nyumba ya mtoto wake. “Aidha kuna baadhi ya wazee wanamiliki nyumba mjini na vijijini ambazo zote wanaziombea msamaha, kwa mujibu wa sheria hawaruhusiwi kuombea msamaha nyumba mbili na badala yake atasamehewa nyumba moja tu,” amesema Catherine. Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makangarawe, Baraka Mwasaka amesema wakazi wengi wa eneo hilo hawakuwa na uelewa kuhusu kodi ya majengo hivyo semina hizo zitasaidia kuwaelimisha. Chiku Sadiki, mkazi wa Kata ya Makangarawe Mtaa wa Abiola amesema elimu hizo zitawasaidia kujua maana ya kodi ya majengo na umuhimu wake.
1kitaifa
Beki kisiki wa Singida United, Keneddy Wilson Juma ”mwili jumba’ leo ametangazwa kujiunga na kikosi cha Simba kwa kandarasi ya miaka miwili. Juma anakuwa mchezaji wa pili mpya kwa Simba kupewa mkataba mpya baada ya mlinda mlango Beno Kakolanya kusaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba. Taarifa rasmi kutoka ukurasa wa Instagram wa Simba imesema: “Ingizo jipya kwenye kikosi cha Mabingwa, beki wa kati Kennedy Wilson Juma amesaini mkataba wa miaka miwili. Uwepo wa Kennedy kwenye kikosi kwa kushirikiana na mabeki wengine tulionao ni hakika safu yetu ya ulinzi itakuwa imara zaidi,” Kennedy anasifika kwa matumizi ya nguvu awapo uwanjani.     Ingizo jipya kwenye kikosi cha Mabingwa, beki wa kati Kennedy Wilson Juma amesaini mkataba wa miaka miwili. Uwepo wa Kennedy kwenye kikosi kwa kushirikiana na mabeki wengine tulionao ni hakika safu yetu ya ulinzi itakuwa imara zaidi. #NguvuMoja A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania) on Jun 18, 2019 at 3:00am PDT
2michezo
LONDON, ENGLAND RATIBA ya mzunguko wa tano wa michuano ya Kombe la FA imewekwa wazi, ambapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, wanatarajia kukutana na Manchester City kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Huu ni mchezo ambao unatarajiwa kugusa hisia za mashabiki wa soka kutokana na uwezo wa klabu hizo na kuwa na mashabiki wengi duniani. Kocha wa Chelsea, Guus Hiddink, amesema kuwa huo utakuwa ni mchezo ambao utawakusanya mashabiki wengi kama ilivyo katika michezo ya fainali. “Naweza kusema kuwa huu utakuwa ni mchezo wa fainali kwetu, timu zote zina wachezaji wenye uwezo mkubwa, hivyo natarajia kuona mashabiki wengi katika mchezo huo,” alisema Hiddink. Wakati huo klabu ya Ligi Daraja la Kwanza, Shrewsbury Town, ambayo imeonesha ushindani wa hali ya juu, itakuwa kwenye Uwanja wa New Meadow dhidi ya wapinzani wao, Manchester United. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya Kombe la FA, Arsenal, watakumbana na Hull City, ambao walikutana katika fainali mwaka 2014. Hii itakuwa ni mara ya tatu mfululizo klabu hizi kukutana katika michuano hii, huku mwaka jana, Arsenal ikiishambulia klabu hiyo kwa mabao 2-0. Michezo mingine ambayo itapigwa ni pamoja na Reading dhidi ya West Brom au Peterborough, Watford dhidi ya Leeds, Blackburn dhidi ya Liverpool au West Ham, wakati huo Tottenham ikipambana na Crystal Palace, huku Bournemouth ikicheza na Everton. Michuano hiyo inatarajia kuendelea kutimua vumbi Februari 19, mwaka huu, kwenye viwanja mbalimbali.  
2michezo
Amina Omari, Handeni Zao la Muhogo linalolimwa wilayani Handeni mkoani Tanga, soko lake litachuana na nchi za nje zinazolima kwa wingi zao hilo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa wa wilaya hiyo, Godwin Gondwe wakati Mwenge wa Uhuru ulipokagua shamba la mfano la zao hilo lililopo katika kata ya Mkata. Amesema ubora wa zao hilo unaozalishwa wilayani humo hauna tofauti na unaozalishwa katika nchi za Cambodia, Thailand na Vietnam.  “Kutokana na ubora wa mihogo yetu ndiyo maana kwa mwaka huu tayari makampuni matatu ya nchini China tayari yameshakuja na kuonyesha nia ya kununua muhogo mkavu kutoka kwa wakulima wilayani kwetu,” amesema Gondwe. Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally alisema ili kufikia Tanzania ya viwanda ni lazima tuongeze kasi ya uzalishaji wa malighafi zitakazotumika katika viwanda hivyo. “Ni vema kuja na mikakati madhubuti ya kuhakikisha zao hilo linachakatwa lote bila ya kutupa kitu ili wakulima wetu waweze kunufaika kiuchumi na serikali kupata mapato yake,” amesisitiza.
1kitaifa
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema jana kuwa hivi karibuni wataanza kuzipitia CV hizo ili kujua kocha gani atakayewafaa.“Tumeandaa utaratibu maalumu kuwashirikisha wataalamu ili kuweza kupata kocha bora atakayetupa mafanikio na kuturudisha kwenye ushindani wa Ligi Kuu,“ alisema Hans Poppe.Alisema wanahitaji kocha atakayekuwa na viwango vya kimataifa zaidi, mwenye kulijua vizuri soka la Afrika, pamoja na mazingira wanayoishi wachezaji wake, hivyo anaamini katika CV zilizopo ofisini kwao wanaweza kupata mwenye sifa wanazozihitaji.Alisema wamechoshwa kuona timu yao ikikosa ubingwa katika misimu mitatu iliyopita na wanachotaka kuanzia msimu huu kuwa na benchi imara la ufundi ambalo litaweza kusimamia vizuri uwajibikaji wa timu na wachezaji ili ufikia malengo wanayoyahitaji.Alisema wamemchukua Jackson Mayanja, kuwa Kocha Msaidizi kwa kuwa wanajua uwezo wake wa ufundishaji aliokuwa nao na wanachotaka kumletea mtu wa juu yake ambaye watasaidiana kutumia uwezo waliokuwa nao kuifanya Simba kuwa timu inayotisha.
2michezo
Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli, amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kwamba Jenerali Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye amestaafu kazi Januari 31, mwaka huu. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali James Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali. Luteni Jenerali James Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance  Mabeyo, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. “Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye,” ilieleza taarifa hiyo. Januari 30, mwaka jana Rais Dk. John Magufuli , alimuongezea muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye amekamilisha muda wake Januari 31, mwaka huu kwa mujibu wa katiba na sheria. Akizungumza na waandishi wa habari mwaka jana katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam, Jenerali Mstaafu Mwamunyange alisema alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote walistaafu mwaka jana.  “Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016, lakini Rais na Amri Jeshi Mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo Januari 30, 2016 hadi Januari 31, 2017,” alisema Jenerali Mwamunyange Akitaja sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumuongezea muda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo . Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange alisema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi. Pamoja na hilo pia Rais Dk. Magufuli alifanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo wa nyadhifa mbalimbali.  Walioteuliwa mwaka jana na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk. Magufuli  ni Meja Jenerali James Mwakibolwa  kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu, ambaye alichukua nafasi ya Meja Jenerali Salum Kijuu aliyestaaafu kazi mwaka jana baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria. Kabla ya uteuzi huo, Meja Mwakibolwa alikuwa ni Mkuu wa Tawi la Utendaji wa Kivita na Mafunzo Makao Makuu ya Jeshi. Jeneral Mwamunyange alimtaja pia Kamanda mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi kuwa  Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasilia na Utalii, nafasi ambayo anahudumu nayo. Meja Jenerali Sirakwi alikuwa Mratibu Msaidizi Mkuu Baraza la Usalama wa Taifa- BUT. Mwingine  aliyeteuliwa  na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali George William Ingram kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga akichukua nafasi ya  Meja Jenerali Joseph  Pwani aliyestaafu Januari 31, mwaka huo kwa mujibu wa sheria. Brigeda Jenerali Ingram alikuwa Ofisa Mnadhimu katika Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Anga. Safari ya Mabeyo Septemba 12, mwaka 2014 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, alimpandisha cheo Venance Mabeyo kutoka Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali. Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ndiyo ilikuwa ni mwanzo wa kuelekea kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ambayo ilitimia jana kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa ndani ya nchi. Kikwete ambaye pia alikuwa Amiri Jeshi Mkuu kwa wakati huo alimteua Mabeyo kwa mujibu wa Kanuni za Majeshi ya Ulinzi, Aya ya 7.01 Kifungu cha (3). Mbali naye pia aliwapandisha  cheo kuwa Meja Jenerali  maofisa wengine sita, ambao ni  Brigedia Jenerali Gaudence Milanzi, Jenerali Mwakibolwa, Ndetaulwa Zakayo,  Simon Mumwi, Issa Nassor, Rogastian Laswai. Wote hao walivishwa vyeo hivyo na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange kwa niaba ya Rais.
1kitaifa
Alisema hayo juzi Dar es Salaam wakati wa semina ya ubunifu katika sayansi na Teknolojia, iliyohusisha wafanyabiashara kutoka taasisi za umma na binafsi.Alisema kwa njia hiyo bidhaa, huduma, ubunifu, biashara pamoja na ufumbuzi wa mambo mbalimbali utaweza kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuchangia katika maendeleo ya nchi."Nina furaha kuona Finland tunajihusisha kwa kiasi kikubwa katika kuunga mkono maendeleo ya mfumo wa ubunifu Tanzania kupitia ushirikiano wa kimaendeleo uliopo baina yetu," alisema.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Patrick Makungu alisema lengo la semina hiyo ni kuangalia mchango unaoweza kupatikana katika uhusiano wa kimataifa .
0uchumi
Ruvu Shooting ambayo imepanda daraja na itacheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, imesema ipo kwenye mchakato wa usajili, lakini hawatasajili wachezaji kutoka Simba wala Yanga.Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa Klabu hiyo, Masau Bwire, alisema hawawezi kusajili wachezaji kutoka timu hizo kongwe, kwani licha ya kutocheza kwa kujituma pia nidhamu zao ni mbovu.“Hatuna mpango wa kusajili makapi ya Simba na Yanga, kwani wachezaji hao huwa mara nyingi hawana moyo wa kupambana na pia nidhamu zao ni mbovu,” alisema Bwire.Alisema kocha wao, Tom Olaba amependekeza kikosi chao kusajili wachezaji saba wenye vipaji, ambapo uongozi unalifanyia kazi jambo hilo ili kutimiza matakwa ya kuwa na timu imara msimu ujao.Ruvu Shooting ambayo ilishuka msimu uliopita imepanda daraja pamoja na timu za African Lyon ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza.
2michezo
JENNIFER ULLEMBO NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM WAKATI klabu ya Yanga ikiendelea kusajili nyota wake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo Mholanzi, Hans Van der Pluijm, amewashtukia viongozi wa timu hiyo akieleza anahisi baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hadi sasa hakuwapendekeza katika ripoti yake. Klabu hiyo hadi sasa imefanikiwa kupata saini za wachezaji watatu ambao ni Deus Kaseke aliyetoka Mbeya City, Haji Mwinyi wa Zanzibar na Benedicto Tinoco kutoka Kagera Sugar. Akizungumza na MTANZANIA jana kutoka Ghana, Pluijm alisema mbali na wachezaji hao, pia amepata habari za chini chini kuwa viongozi wanaosimamia masuala ya usajili wamepanga kuongeza wachezaji wengine ambao hawapo kwenye listi yake. “Habari zote za usajili zinavyoendelea nazipata na nafuatilia kwa umakini, tayari nimeanza kugundua mambo yanaenda tofauti na nilivyopanga,” alisema Pluijm. Mholanzi huyo ambaye anatarajiwa kurejea nchini Juni saba mwaka huu, alisema hatasita kufanya mabadiliko pindi atakapowasili na kugundua wachezaji waliosajiliwa hawana kiwango. “Tukiharibu kwenye usajili ndiyo basi, hakuna tena muda wakuanza kurekebisha hasa ukizingatia tunakabiliwa na mashindano ya kimataifa na lazima msimu ujao tutetee taji letu la Ligi Kuu. Ukikosea kufanya usajili mara baada ya msimu kumalizika ujue utabeba mizigo hadi msimu mwingine kwani hata usajili wa dirisha dogo ni wamaboresho,” alieleza Pluijm. Alisema yeye ni mwalimu hivyo anajua mapungufu ya timu hiyo, kama viongozi watafanya kinyume timu itakapoboronga asilaumiwe kwa lolote. Pluijm ameeleza atakaporudi nchini atavianika vifaa vipya alivyopendekeza kutua Jangwani, ambapo anatarajiwa kurejea nchini wiki ijayo tayari kuanza mazoezi ya kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame). Pluijm tayari amehakikisha kiungo mchezeshaji raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima na beki Mrundi Mbuyu Twite wanaendelea kuitumikia klabu hiyo. “Kwa sasa nipo mapumzikoni, ni vigumu kuzungumzia mambo ya wachezaji wapya wanaosajiliwa Yanga kwa ajili ya msimu ujao, lakini mambo yatakuwa mazuri zaidi tukakapoanza mazoezi Juni 8, mwaka huu,” alisema. Mbali na Niyonzima na Twite, klabu hiyo pia imemsainisha mkataba wa miaka miwili kipa, Deogratius Munishi ‘Dida’ ambaye alikuwa akiwaniwa na watani wao wa jadi Simba. Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pia wanawania saini ya winga Haroun Chanongo, kuziba pengo la Mrisho Ngassa aliyejiunga na klabu ya Free State ya Afrika Kusini na kusaini mkataba wa miaka minne. Pluijm alisema ana mipango ya kuandaa kikosi imara kitakachoonyesha ushindani katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ili kiweze kufika mbali zaidi ya hatua waliyofikia kwenye Kombe la Shirikisho. Hakuna mchezaji mpya wa kulipwa aliyesaini Yanga, licha ya uongozi wa klabu hiyo kukiri kuwa na majina saba mezani wakiwemo walioomba wenyewe na walioitwa kwa majaribio.
2michezo
WATANZANIA wanapaswa kumshukuru Mungu kwa nchi kuendelea kupata viongozi, wanaodumisha uhuru na umoja kwa vitendo, mambo ambayo yanalifanya taifa kuheshimiwa na kuwa na maendeleo.Kauli hiyo ilitolewa na mmoja wa wanawake mashujaa wa uhuru wa Tanzania Bara, Mwasaburi Ally (98) ambaye alikuwa bega kwa bega na Mwalimu Julius Nyerere kupigania uhuru wa nchi.Mwasaburi ni miongoni mwa wanawake mashujaa wa uhuru wachache walio hai, ikiwa ni miaka 58 tangu Tanzania Bara ilipopata Uhuru. Ni mzee kwa umri, lakini mchangamfu, mwenye nguvu, Mungu amemjalia afya njema na anasikia vizuri bila matatizo, licha ya uoni hafifu alionao kwa sasa kutokana na umri wake mkubwa.Hivi karibuni, Habari- Leo ilimtembelea nyumbani kwake eneo la Ilala Mtaa wa Tabora na Kilwa jijini Dar es Salaam na kumjulia hali, kisha kuzungumza naye kuhusu harakati za uhuru wa Tanzania Bara.Akizungumzia harakati za uhuru, Mwasaburi ambaye anaonekana mwenye nguvu tofauti na umri wake huo, anafahamu mambo mengi ya harakati za kuikomboa Tanganyika wakati huo, na kuanzishwa kwa chama tawala cha wakati huo cha Tanzania African National Union (TANU).Kwa wasiomfahamu, Mwasaburi ni mke wa pili wa marehemu Aziz Ally aliyekuwa mmoja wa watu maarufu na wenyeji wa jiji la Dar es Salaam enzi hizo, ambaye alijaliwa kuwa na watoto wakiwemo kina Dossa Aziz na Abdu Sykes.Hao walikuwa marafiki wa Mwalimu Julius Nyerere, waliompokea jijini humo na kuishi naye eneo la Magomeni Kota, ambako walikuwa wakipanga jinsi ya kuikomboa Tanganyika.Akizungumzia hali ilivyokuwa kabla ya uhuru, baada ya uhuru na sasa, Mwasaburi alisema, “Wakati wa mkoloni ilikuwa ni amri za kikoloni tu na tulitawaliwa vibaya na kutekeleza ya wazungu, ndio maana Nyerere aliona sio sawa, akaanzisha harakati za uhuru na mimi nikamsaidia tukajikomboa, leo bado nchi iko salama, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kuendelea kupata marais wanaodumisha uhuru’’.Alisema wakati wa harakati za uhuru, wanawake wengi hawakuwa wamesoma, na familia zilijikita zaidi kuwafundisha dini watoto wao hususan wa kike. Kwamba hiyo ilikuwa changamoto kwa wanawake wengi, kutoshiriki kwenye harakati za ukombozi, kwa kuwa jamii iliwaona ni watu wa kukaa nyumbani.“Mimi niliolewa nikiwa mdogo mwenye umri wa miaka 15, tulijaliwa watoto wanne na mume wangu alifariki nikiwa na miaka 25, wakati huo Nyerere alikuwa akifika Mtaa wa Gerezani kwa kina Dossa na Abdu ambapo alikuwa akiwaeleza nia yake ya kutaka kuikomboa nchi kutoka kwa wakoloni,”alisema Mwasaburi na kuongeza… ”Nyerere alipokuja kwa kina Dossa, rafiki zake, aliniona akawa ananipenda kwa vile nilikuwa mtundu, akauliza nimesoma nikamwambia nilisoma tu Kurani, ndipo akanisomesha pale Anautoglou lugha ya Kiswahili na Kiingereza,”alisema Mwasaburi.Alisema Nyerere ndiye aliyekuwa akimlipia ada na kukagua maendeleo yake na alipomaliza, alishiriki rasmi kwenye mikutano aliyokuwa akifanya Nyerere.
1kitaifa
KAMPUNI ya magazeti ya serikali (TSN) imeendelea kutesa baada ya waandishi wake wawili kushinda kwa mara nyingine tuzo za uandishi wa habari zinazohusu masuala ya watoto zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).Waandishi hao ni Anne Rhobi wa Daily News aliyekuwa mshindi wa jumla katika kundi la waandishi wa habari waliojikita katika uandishi wa habari za watoto na Sifa Lubasi wa HabariLeo kutoka mkoani Dodoma Washindi kutoka vyombo vingine vya habari ni Anold Jovin kutoka Redio Kwazera mkoani Kagera na Mwanza ni Kiembe wa ABM FM Radio ya Dodoma.Wengine ni Lilian Lugakingira (Nipashe na EATV ) Kagera, Suleyman Abeid (Majira) mkoani Shinyanga, Tumaini Msowoya na Rehema Matowo (Mwananchi).Akizungumza wakati akikabidhi tuzo hizo, Mkuu wa mawasiliano, utetezi na uhusiano wa Unicef, Manisha Mishra alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Jukwaa la Wahariri katika kuwawezesha waandishi wa habari kuihabarisha jamii kuhusiana na ukatili wanaotendewa watoto katika maeneo mbalimbali nchini.“Tunatambua kwamba waandishi wa habari ni watu pekee wa kupaza sauti na kufichua yanayotendeka kuhusu watoto kwa hivyo Unicef tutaendelea kushirikiana na jukwaa la wahariri kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa ufanisi,” alisema Mishra.Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Nevile Meena alisema mwakani watahakikisha wanaongeza idadi ya maeneo ya kushindanisha ili kupanua wigo wa ushiriki kwa waandishi wengi zaidi.Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo, Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alivitaka vyombo vya habari nchini kutambua wajibu wao wa kuendelea kuzipa kipaumbele habari zinazohusu masuala ya watoto na kufichua vitendo vyote vya ukatili wanavyotendewa ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kukabiliana na vitendo hivyo.Balile alisema iwapo vyombo vya habari nchini vitajenga utamaduni wa kutoa kipaumbele kwa habari za watoto ni wazi serikali na wadau wengine wa watoto wataweza kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha mtoto wa Tanzania analindwa na kupata haki zake za msingi.
1kitaifa
Na Joseph Lino, Tanzania ina utajiri wa mifugo ambayo haijaweza kustawi vizuri katika kuinua hali ya maisha ya wananchi wengi wanaofuga kutokana na uhafidhina. Kwa sababu hiyo, malighafi nyingi zinazotokana na mifugo hupotea na kutopewa kipaumbele, hali inayosababisha wafugaji kutofaidika na sekta hiyo. Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuwa na mifugo wengi ambao ni moja ya sekta yenye tija ya kuleta maendeleo nchini. Ngozi ni moja ya mazao yanayotokana na mifugo, lakini sekta ya ngozi bado ipo nyuma kimaendeleo kama walivyo wenye mifugo hiyo. Kwa mujibu wa Jukwaa Huru la Wadau wa Kilimo (ANSAF), kuna viwanda tisa vya kusindika ngozi zenye uwezo wa kuchakata ngozi mita za mraba milioni 40 kwa mwaka, hata hivyo viwanda hivyo vina uwezo mdogo wa kusindika malighafi inayopatikana nchini. ANSAF inasema  ngozi za ng’ombe 4,643,000 pamoja na ngozi  za mbuzi na kondoo  22,820,000 husindikwa kila mwaka, lakini husindikwa  kwa kiwango cha chini. Sekta ya ngozi bado haijaendelezwa kwa kiasi kikubwa ambacho kwa sasa sekta hiyo imetengeneza ajira chache ikilinganisha na mifugo iliyopo nchini. Kwa  mfano, wastani uzalishaji wa ng’ombe 1,000 na mbuzi 1,500 ambao huchinjwa kila siku katika machinjio ya Dodoma Mjini. ANSAF inaelezea kuwa kiasi cha Sh milioni 15 kuhitajika kujenga kiwanda cha kusindika bidhaa za ngozi. “Ngozi ya ng’ombe hununuliwa kwa Sh 8,000 na ya mbuzi Sh 2,000 na ikisindikwa huuzwa Sh 40,000 na matokeo yake kutengeneza viatu jozi nne,” inaeleza ANSAF. Kwa mantiki hiyo, mtu anaweza kutengeneza jozi  30 au 35 ambazo zinaweza kuuzwa Sh milioni 1.75 kila mwezi. Nafasi ya Tanzania  kuwa na idadi nyingi ya mifugo Kusini mwa Jangwa la Sahara, hivyo ina uwezo wa kuuza viatu na bidhaa zote zinazotokana na ngozi masoko ya nje. ANSAF inapendekeza kwamba Serikali iingie mikataba na makampuni ya nje ambayo yanaweza kutengeneza ajira na kuchangia kwenye Pato la Taifa. Kwa takwimu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaonesha katika mwaka 2015/16, vipande ghafi 187,000 vya ngozi za ng’ombe vyenye thamani ya Sh bilioni 2.4 na vipande ghafi 124,000 vya ngozi za mbuzi/kondoo vyenye thamani ya Sh milioni 121.5 viliuzwa nje ya nchi. Aidha, ngozi zilizochakatwa ni vipande 1,575,139 vya ng’ombe vyenye thamani ya Sh bilioni 45 na vipande vya ngozi za mbuzi/kondoo 1,124,000 vyenye thamani ya Sh bilioni 7.5. Kwa upande mwingine, mifugo iliyouzwa ndani kupitia minadani ni ng’ombe 1,470,805, mbuzi 1,161,840 na kondoo 253,243 wenye thamani ya Sh bilioni 976.474. Katika mwaka 2015/16, idadi ya mifugo nchini inafikia ng’ombe milioni 25.8, mbuzi milioni 17.1 na kondoo milioni 9.2. Hata hivyo, uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 597,757 (ng’ombe 319,112; mbuzi na kondoo 124,745, nguruwe 54,360 na kuku 99,540) mwaka 2014/2015 hadi tani 648,810 (ng’ombe 323,775; mbuzi na kondoo tani 129,292). Takwimu hizo zinaonesha kuwa juhudi  zinafanywa na wadau pamoja na Serikali kuongeza mazao yatokanayo na mifugo, haswa   ng’ombe lakini  inaonesha bado iko chini sana  kwani wafugaji wengi hawajaenda shule na wana utamaduni wa  kujali sana uwingi kuliko ubora wa mifugo hiyo. Watu wa makamo wanakumbuka wakati  wa awamu ya kwanza ya utawala wa nchi chini  ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati  ng’ombe kulikuwa na kampuni mahiri saba zinamshughulikia. Kurudia mwenendo huo si kosa ila tutafanikiwa vilivyo.
1kitaifa
Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM   BAADHI ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wa Jiji la Dar es Salaam, wamechangamkia fursa ya kuuza vifaa vya shule katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo ikiwa ni siku chache kabla ya kufunguliwa shule. MTANZANIA jana lilishuhudia mitaa mingi ya Kariakoo na Manzese ikiwa na machinga wakiuza bidhaa za shule zikiwamo masanduku ya chuma, mabegi ya shule, sare za shule, vitabu, daftari na kalamu. Katika uchunguzi huo, machinga hao wamekuwa wakiuza vifaa hivyo kwa bei sawa na ile ya dukani jambo ambalo linawarahisishia kupata wateja kwa urahisi. Mmoja wa machinga hao, Hemedi Juma, alisema kuwa vifaa hivyo wanavipata katika maduka ya jumla ambapo wao huongeza faida kidogo. “Bei tunayouza sisi ni sawa na wenye maduka ya jumla lakini watu kwa kuwa wamezoea kununua madukani ndio maana unaona msongamano ni mkubwa,” alisema Juma. Katika duka maarufu la kuuza vifaa vya shule lililoko Kariakoo la Tahfif katika makutano ya mitaa ya Tandamti na Swahili, watu mbalimbali walikuwa wamepanga foleni ya kuingia dukani humo. Maduka ya vitambaa vya sare za shule pia yalionekana yakiwa na watu wengi wakinunua bidhaa huku mafundi nao wakiendelea na kazi ya ushonaji. Mmoja wa mafundi anayefanya shughuli zake katika eneo la Manzese Uzuri, Joachim Mkude, alisema kwa sasa nguo nyingi anazoshona ni sare za shule. “Kwa sasa mafundi tumezidiwa na sare za shule kwa kuwa shule ziko karibu kufunguliwa na nguo zinahitajika haraka,” alisema.
1kitaifa
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, limemchagua Asia Chikwale kuwa Naibu Meya mpya wa manispaa hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja. Meya wa Halmashauri ya manispaa hiyo, Abdul Mshaweji ameongoza kazi ya uchaguzi wa Naibu Meya katika mkutano wa Baraza la Madiwani hao uliofanyika kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Songea. Kikao hicho pia kimewashirikisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Tina Sekambo na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema pamoja na watumishi wa idara na vitengo wa manispaa hiyo. Mshaweji alieleza umuhimu wa uchaguzi katika kulijenga Taifa kwa kuwa kiongozi anayechaguliwa atashirikiana vyema na viongozi wa serikali na wananchi kuleta maendeleo ya Manispaa ya Songea na Taifa kwa ujumla. Kwa upande wake, Naibu Meya aliyemaliza muda wake, Judith Mbogoro alitoa shukrani kwa madiwani wote na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Songea kwa ushirikiano aliupata katika kipindi chote alichokuwa Naibu Meya na ameahidi kuwa atakuwa pamoja na kiongozi aliyechaguliwa ili kuhakikisha manispaa hiyo inasonga mbele. “Najitambua na kujijua nitatoa ushirikiano daima,” alisema Mbogoro. Naye Naibu Meya mpya, Asiah Chikwale alisema nafasi aliyoipata ataitumia vizuri kwa kushirikiana na viongozi wengine kuleta maendeleo ya Manispaa ya Songea, Mkoa na Taifa kwa ujumla wake. Manispaa ya Songea ina kata 21 na mitaa 95 ikiwa na jumla ya madiwani 28. Wakati huo huo, Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imekagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Ruvuma katika Manispaa ya Songea na kuridhishwa na hatua za ujenzi unaotarajiwa kukamilika wakati wowote. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Oddo Mwisho alisema serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo wa vituo vya afya ili kusogea huduma kwa wananchi. Aliagiza watendaji wa manispaa kuhakikisha wanaanza huduma mara moja katika kituo kwani wananchi wanachosubiri ni kuanza kupata huduma jirani hali itakayopunguza msongamano Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Akitoa taarifa ya mradi huo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Dk Mamerita Basike alisema walipokea fedha kutoka serikalini Sh milioni 400 kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Ruvuma Juni 24, 2018. Dk Basike alisema mradi huo umekamilika kwa kazi zote ambazo ziliainishwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI na kwamba kinachosubiriwa hivi sasa ni ununuzi wa vifaa tiba na dawa ili huduma zianze kutolewa.Aliyataja majengo manne yaliyokamilika katika kituo hicho kuwa ni la wagonjwa wa nje, la mama na mtoto, la upasuaji, la maabara, ujenzi wa shimo la choo na shimo la kondo la nyuma na ujenzi wa kichomea taka.“Halmashauri imeomba vifaa na madawati kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kituo cha afya kianze kutumika kituo hiki kitahudumia wananchi wa kata za Ruvuma, Mateka, Majengo, Subira, Mfaranyaki na Lizaboni,” alisema.
1kitaifa
Kinshasa, Congo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inajiandaa kumwapisha Felix Tshisekedi, kuwa rais mpya wa taifa hilo. Sherehe za kuapishwa zinatarajiwa kufanyika Alhamisi, wiki hii na zitashuhudiwa Tshisekedi, akiapishwa kuwa rais akichukua mikoba ya Joseph Kabila, aliyeitawala Congo, tangu mwaka 2001. Awali sherehe hizo zilikuwa zifanyike leo Jumanne, lakini Msemaji wa Muungano wa Upinzani (CACH) ambao ulimuunga mkono Tshisekedi, alisema uwezekano wa kuapishwa ni Alhamisi. Mahakama ya katiba ilitupilia mbali madai ya mgombea aliyeshika nafasi ya pili Martin Fayulu, na kumthibitisha Tshisekedi, kuwa rais mteule wa Congo. Tanzania, Burundi na Kenya ni miongoni mwa Mataifa kadhaa ya Afrika yaliyompongeza Tshisekedi,  ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC.
3kimataifa
Mwandishi Wetu TAASISI ya Dk Reginald Mengi Kwa Watu Wenye Ulemavu (DRMF) imetangaza utaratibu wa kumuenzi Dk Mengi kwa mwezi mzima, kupitia shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika mwezi wa Mei 2020. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Shimimana Ntuyabaliwe, alisema mwezi wa Mei ni muhimu kwao kwa sababu umebeba matukio matatu muhimu ambayo ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu muasisi wa DRMF alipofariki Mei 2, 2019, pia siku yake ya kuzaliwa ni  Mei 29 na Mei 18 2018 taasisi hiyo ndipo iliposajiliwa rasmi. “Kwa hiyo, katika mwezi huo tutaendesha kampeni ya kuwahamasisha Watanzania popote pale walipo, taasisi, mashirika, na vikundi vya kijamii kuutumia mwezi wa Mei kila mwaka kufanya matendo mbalimbali ya kujitolea kwa kumbukumbu ya Dk. Reginald Mengi. Kampeni hii itajulikana kwa jina la Ubuntu. “Ubuntu ni neno la kabila la wazulu kutoka Afrika ya Kusini likimaanisha ‘Utu’ au ‘Moyo wa kujitolea kwa binadamu wenzako’ hivyo taasisi yetu inaamini kuwa neno hili moja Ubuntu linatosha kumtambulisha marehemu Dk. Mengi kikamilifu,” alisema Ntuyabaliwe. Aliseam katika uhai wake Dk. Mengi alijitolea na kufanya mambo mengi katika jamii ya watanzania n mkono wake ulikuwa mrefu na mpana na alijitoa akiwa na tabasamu la bashasha bila kuchoka, kwa kugusa na kuleta tofauti katika maisha ya Watanzania wengi aliowafikia. “T
1kitaifa
VITENDO vya ukeketaji na ukatili wa jinsia vimeendelea mkoani hapa kutokana na kinachodaiwa kuwa wazazi kuamua kumaliza matatizo hayo kwa njia ya majadiliano na upande wa wahalifu. Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa Dawati la Jinsia, Mkaguzi wa Polisi, Iddah John, wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Ilongero wilayani Singida. Alisema wanafunzi wa kile wanapopata mimba, wazazi wa binti husika humalizana kwa mazungumzo na wazazi wa mwanaume aliyesababisha hali hiyo. “Wazazi wa mwanafunzi huyo wa kike huficha kwa makusudi tukio hilo lisijulikane kabisa, wao watafanya mazungumzo na upande uliomfanyia binti ukatili wa kijinsia. “Kwa ujumla katika mazungumzo hayo hufanyika makubaliano ya upande ulioathirika kupata ‘kitu kidogo’, kisha kitakachofuata ni kunywa supu ya mbuzi,” alisema. Akifafanua zaidi, Iddah alisema ni ukweli usiopingika kwamba wazazi hao, watakuwa wamemfanyia ukatili wa kijinsia binti yao kwa vile atakuwa amekatishwa masomo yake. Mratibu huyo alisema maadhimisho hayo yanalenga kuhimiza jamii mkoani hapa kutoa ushirikiano kusaidia kutokomeza vitendo hivyo pamoja na ukeketaji. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Veronica Mure, alisema ukatili wa kijinsia unafanywa na kila mtu kwa kujua au kutokujua. “Kwa hali hiyo, vitendo hivi ambavyo vipo kinyume na haki za binadamu, ni jukumu letu sisi sote kuvitokomeza, tujitambue na tuamue kwa dhati kushiriki kuvitokomeza vitendo hivyo kupitia Serikali, asasi na mashirika ya kiraia,” alisema. Aidha mkurugenzi huyo, alisema jamii ina upungufu katika mapambano hayo, ikiwamo kushindwa au kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola katika kuvitokomeza. “Kitendo cha ukatili wa kijinsia au ukeketaji kikitolewa taarifa polisi au mahakamani, kwanza mhanga wa tukio atafichwa na mbaya zaidi hakuna mtu au watu watakaokuwa tayari kushirikiana na polisi au kutoa ushahidi mahakamani,” alisema.
1kitaifa
WAFANYABIASHARA maarufu watano mkoani Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na vifungashio vya bidhaa mbalimbali ambavyo si halisi na bidhaa ambazo zimefi ka ukomo wa muda wa matumizi.Kukamatwa kwa wafanyabiashara hao kunafuatia operesheni iliyofanywa na kikosi maalumu kilichoshirikisha vyombo vya Ulinzi na Usalama, Bodi ya Sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakala wa vipimo na wataalamu kutoka kiwanda cha sukari Kilombero.Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nlei alisema kuwa oporesheni hiyo ilifanyika Juni 10 na 11, mwaka huu ikilenga ukaguzi na ukamataji wa vifungashio mbalimbali vya bidhaa ambavyo si halisi hasa mifuko ya sukari, mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine. Hata hivyo, Kamanda Nlei hakuwa tayari kuwataja wafanyabiashara hao kwa madai kwamba bado wanaendelea na mahojiano nao wala thamani halisi ya mali iliyokamatwa.Alisema katika ukaguzi huo walifanikiwa kukamata mifuko tupu ya 1430 ya sukari ya kiwanda cha Mtibwa, mifiko tupu 110 ya sukari kutoka nje ya nchi, mifuko 36 mipya ya kampuni ya sukari ya Kilombero ambayo ni ya kughushi, mashine tano za kushonea mifuko ya kuhifadhia sukari na mizani mbili ambayo haijahakikiwa na wakala wa vipimo.Alivitaja vitu vingine vilivyokamatwa kuwa ni maboksi 550 ya kufungashia mafuta ya korie, ndoo 30 za kufungashia mafuta ya kula lita 20 na nyingine 10 za lita kumi zote zikiwa zimepunguzwa ujazo, sukari ya Kilombero mifuko miwili ambayo imefungwa mara ya pili ( Repack ). Kamanda Nlei alisema kuwa watuhumiwa watano wamekatwa baada ya kukutwa na vifungashio hivyo na wanaendelea kuhojiwa ambapo upelezi ukikamilika jalada litafikishwa kwa mwendesha mashitaka wa serikali ili wafikishwe mahakamani.Alitoa wito kwa wananchi na wakazi wote wa mkoa wa Tabora kuwa makini wakati wananunua bidhaa kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaendelea kuuza bidhaa zilizokwisha muda wake na wakibaini watoe taarifa. Katika hatua nyingine, jeshi la polisi limekamata dawa za binadamu ambazo ni mali ya bohari ya madawa (MSD) zilizoibwa ambazo zilikutwa zikiuzwa. Kamanda Nlei alisema kuwa watu wanne wanashikili kuhusiana na dawa hizo aina ya artemether Lumefantrine (ALU) maarufu kama mseto.Alisema kuwa watuhumiwa wawili kati yao, ni watumishi wa ghala la kuhifadhia dawa la Msd Mkoa wa Tabora na wawili ni raia, japo hakuwa tayari kutaja majina yao kwani upelelzi haujakamilika. Watuhumiwa hao wanne walikamatwa Juni 9, mwaka huu mjini Tabora wakiwa na mifuko miwili mikubwa ya sandarusi ikiwa imejaa dawa hizo ambazo thamani yake bado haijafahamika.
1kitaifa
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amekiri kuwa sasa timu yake inaweza kuonyesha uwezo mkubwa kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na hata kutwaa ubingwa kulingana na mikakati waliyojiwekea. Akizungumza na MTANZANIA akiwa nchini Zambia, Hall alisema kupitia mashindano hayo Azam inazidi kuimarika na kumpa uhakika wa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa ambayo wataanza kushiriki mwezi Machi. “Mashindano haya yametusaidia sana kwani nidhamu kwa wachezaji imeongezeka na kuzidi kunipa moyo wa kufanya vizuri kimataifa na katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ili kukamilisha mpango wa kunyakua mataji yote makubwa,” alisema. Alisema hawana mpango wa kutafuta mechi za kirafiki kwa maandalizi zaidi kwani mashindano wanayoshiriki yametimiza vigezo vya mahitaji yao na kupunguza gharama ambazo zingetumika kusaka mechi za kimataifa nje ya nchi. Hall alisema kwa kutumia mashindano hayo ameweza kurekebisha makosa madogo madogo na kufanyia kazi mapungufu ambayo yamekuwa yakiwasumbua wachezaji wake mara kwa mara. Mabingwa hao wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, wanatarajia kushuka tena dimbani Jumatano hii kuvaana na Zanaco FC ya Zambia.
2michezo
  VATICAN CITY, VATICAN PAPA Francis amekosoa kiwango kidogo cha uzazi barani Ulaya na kutaka vijana wadogo wasaidiwe wajiandae kwa njia nzuri za wakati ujao katika jamii. “Ulaya ambayo inajibaini yenyewe kama jamii, ni chanzo cha maendeleo yake na dunia nzima,” Papa aliuambia mkutano wa ‘(Re) Thinking Europe’, mradi unaofadhiliwa na Baraza la Maaskofu wa Katoliki Ulaya (COMECE). “Ulaya, inaugua kwa kipindi kibaya cha ‘utasa’. Si tu kwa sababu Ulaya ina watoto wachache na wengi kunyimwa haki za kuzaliwa, bali pia kwa sababu kuna kushindwa kutengeneza utamaduni mzuri wanaohitaji vijana kukabiliana na wakati ujao.” Hii si mara ya kwanza Papa huyo raia wa Argentina kuonyesha kukerwa na kiwango kidogo cha uzazi barani humo kwani mwaka 2014, wakati akilihutubia Bunge la Ulaya aliueleza Umoja wa Ulaya kama ‘bibi mchovu’, ambaye hana uwezo tena wa kuzaa. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya, Frans Timmermans na Mtendaji Mkuu wa Bunge la Ulaya, Antonio Tajani. Walimsikia Papa Francis akisisitiza Ulaya si chombo cha takwimu au taasisi, bali kilichoundwa na watu, ambao hawapaswi kupukutishwa. Aidha alisisitiza kuwa viongozi wa Ulaya wana wajibu wa kuhamasisha Ulaya iliyo na jamii jumuishi, badala ya ile ya uwiano mbaya baina ya walio nacho na wasio nacho.
3kimataifa
['Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Cameroon Joel Tagueu hatoshiriki katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu kutokana na matatizo ya moyo.', 'Picha aliyopigwa wakati wa mazoezi ya timu hiyo ya Indomitable Lions huko Qatar ziligundua tatizo katika mshipa wa moyo wa mshambuliaji huyo.', 'Taarifa katika mtandao wa shirikisho la soka nchini humo inasema hakuna "hakikisho la kuondosha hatari kwa mchezaji huyo kufariki ghafla uwanjani".', 'Kocha mkuu Clarence Seedorf anatarajiwa kuita mchezaji za ziada kuichukuwa nafasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.', 'Kwa mujibu wa daktari wa kikosi hicho Prof William Ngatchou, Tagueu, aliyeichezea timu ya Ureno Maritimo, msimu uliopita amekuwa akifanyiwa ukaguzi sawa na huo na alipigwa picha kwa takriban miaka minane lakini matokeo yalishindwa kudhihirisha matatizo yoyote.', 'Kikosi cha Cameroon kinashuka dimbani leo dhidi ya Guinea Bissau leo katika mashindano hayoya kombe la mataifa ya Afrika mwendo wa saa mbili usiku saa ya Afrika mashariki.']
2michezo
Na ESTHER MBUSSI-DODOMA SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameitaka serikali kutoa tamko kuhusu wanafunzi waliokosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Elimu ya Juu (HELSB), kwa sababu ya kukosa fedha za kulipia ada ya usajili chuoni. Ndugai aliyasema hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCM) kuomba mwongozo wa Spika kuhusu wanafunzi hao akisema wanapofika vyuoni wanalipishwa ada ya usajili ili kupata mkopo huo. “Inashangaza wanafunzi waliodahiliwa wamekosa nafasi ilihali wana sifa lakini pia wengi waliopata nafasi hawajapata mkopo na wakati Rais alisema walio na sifa za kupata mkopo wasisumbuliwe lakini wanasumbuliwa ada ya usajili. “Ingawa idadi ya wanafunzi wanaopata mkopo imeongezeka lakini wanafunzi wanaopata mkopo ni wachache halafu bado wanapata taabu kuupata, naomba mwongozo wako kuhusu suala hili,” amesema Mlata. Akijibu, Spika Ndugai alisema jambo hilo ni muhimu likatolewa ufafanuzi kwa sababu si wanafunzi wa mwaka wa kwanza pekee wanaopata madhila hayo. “Naiomba serikali itoe tamko kesho (leo), haiwezekani mtoto afike chuoni alipie fedha ili apate haki yake ya mkopo. “Ndiyo maana wamezagaa tu mitaani maskini. Hawa ni watoto wa maskini, naomba kesho saa nne serikali itoe tamko au maelezo ya nini kinaendelea kuhusu watoto hawa,” alisema.
1kitaifa
Na Mwandishi wetu -Dar es Salaam WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amefanya mazungumzo na baadhi ya mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini na kuwahakikishia Tanzania ipo salama na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki. Mabalozi waliofanya naye mazungumzo ni Kaimu Balozi wa Marekani, Dk. Imni Patterson, Manfredo Fanti (Umoja wa Ulaya – EU), Sandro De-Oliveira (Angola) na Mubarak Alsehaijan (Kuwait). Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dar es Salaam jana, Simbachawene alisema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini.  “Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali la hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakuwa wa huru na haki,” alisema Simbachawene.  Pia aliwahakikishia ushirikiano zaidi kati ya wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi. “Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” alisema Simbachawene.  Aliwashukuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumwona wanakaribishwa ofisini kwake. “Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote. Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Simbachawene.
1kitaifa
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM MIAKA ya nyuma ilikuwa ni nadra kusikia mtu amefariki dunia ghafla hasa akiwa usingizini, wazee wetu waliishi maisha marefu kuliko ilivyo miaka ya sasa. Waliishi maisha ya kiasili ambayo yaliwasaidia kujiepusha kupata maradhi mengi. Leo hii maisha yamebadilika mno… wengi wanapenda kuishi kisasa bila kujua tunajiumiza wenyewe miili yetu. Siku hizi si ajabu tena kusikia mtu amefariki ghafla usingizini, kifo cha namna hiyo huwa kinauma mno na kuliza wengi. Mtindo mbovu wa maisha tulionao miaka ya sasa unatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza. Watu wengi hupenda kula vyakula visivyokuwa vya asili, hawafanyi mazoezi wala kupima afya mara kwa mara kujua mwenendo wake. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Pedro Pallangyo anasema kutozingatia ulaji bora, kutokufanya mazoezi na kupima afya ni hatari kwa afya zetu. Wengi hufa usingizini Anasema vifo vingi vinavyotokea watu wakiwa usingizini, sababu yake kuu huwa ni kuziba kwa mishipa ya damu. “Tatizo la kuziba mishipa ya damu tulizoea zamani lilikuwa linazikabili zaidi nchi zilizoendelea pekee, lakini sasa ni tatizo kubwa hadi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania,” anasema. Anasema tatizo hilo lilikuwa nchi zilizoendelea kwa sababu ndipo ambapo kulikuwa na sababu hatarishi zinazosababisha mishipa kuziba kuliko nchi zinazoendelea ambako hazikuwapo. “Sababu hatarishi zinazotajwa hapa ndizo hizo, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, kutokufanya mazoezi, unywaji wa pombe kupita kiasi na kuvuta sigara. “Nyingine ni uzito mkubwa kupindukia kulinganisha na urefu wa mtu husika, magonjwa ya shinikizo la damu na sukari,” anasema. Dk. Pallangyo anaosema vitu vyote hivi vinapokuwa kwa mtu ndivyo hujiongezea hatari ya kupata tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu. “Yaani unakuta mtu ni mvutaji wa sigara wakati huo huo ana kisukari na shinikizo lake la damu lipo juu, mtu huyu uwezekano wa kupata tatizo la kuziba kwa mishipa yake ya damu lazima utaongezeka,” anasema. Anasema visababishi vyote hivyo huashiria kuongezeka kwa kiwango cha mafuta kwenye damu. Anasema athari za kuwapo kwa kiwango cha mafuta kikiwa kingi kwenye damu kwa muda mrefu huwa hakijitokezi mapema kwa watu wengi. “Miaka ya nyuma, wengi walianza kuona athari za mafuta kwenye damu mara walipofikisha umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea. Lakini leo hii athari zinajitokeza zaidi kwa watu walio katika umri wa ujana, yaani chini ya miaka hiyo,” anasema. Dk. Pallangyo anasema kadri mafuta yanavyotanda mwilini hupunguza uwazi wa damu kupita au huziba kabisa na hivyo damu kushindwa kupita. “Kwa kawaida mshipa wa damu hautakiwi kuwa na mafuta yeyote lakini uwazi unapokuwa umezibwa kwa kiwango cha asilimia 50 na kuendelea, huyu mtu lazima apate shida kwa sababu damu inakuwa inapita chini ya asilimia 50 inavyotakiwa,” anasema. Anaongeza; “damu inapokuwa inapita chini ya kiwango cha asilimia 50 au kuendelea, ni lazima tumfanyie uchunguzi mgonjwa na kumfanyia upasuaji ili kuzibua mishipa iliyoziba. Ushuhuda wa mgonjwa Faustine Mwandike ni miongoni mwa wagonjwa waliofanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa na tatizo hilo ambapo tayari amefanyiwa upasuaji wa kuzibuliwa mshipa wake wa damu uliokuwa umeziba. Anasema kabla hajachukua hatua ya kwenda hospitalini, alianza kuhisi maumivu makali katika upande wa kushoto wa mwili wake (kwenye moyo). “Maumivu hayo yalikuwa yakijirudia mara kwa mara, baadae nilianza kuona mkono wangu wa kushoto unapoteza nguvu na maumivu yalikuwa yakishuka wakati mwingine hadi kwenye miguu,” anasimulia. Anasema ilifika mahali akawa anashindwa kumudu kuendesha vema gari lake kwani maumivu hayo yalikuwa makali mno. “Nikachukua hatua ya kwenda hospitalini, nikaanza kufanyiwa vipimo mfululizo tangu Januari 11, mwaka huu, madaktari waliona kuna umuhimu wa kuchunguza moyo wangu hasa mishipa ya damu. “Waligundua tatizo lilikuwa ni kuziba baadhi ya mishipa ya damu, mmoja ulikuwa umeziba kwa kiwango cha asilimia 66 na mwingine ambao ni wa kuingiza na kutoa damu kwenye moyo uliziba kwa asilimia 80,” anasema. Anasema baada ya uchunguzi huo alirejea jijini Arusha kwenye makazi yake na kwenda moja kwa moja JKCI, Januari 23 kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. “Kulikuwa na kambi ya upasuaji, Januari 25, nilifanyiwa upasuaji na mishipa hiyo ikazibuliwa, namshukuru Mungu sasa ni mzima,” anasema. Sababu “Ni mfumo mbovu wa maisha niliokuwa nikiishi na nadhani kama nisingewahi kufika hospitalini basi hali yangu ingekuwa mbaya zaidi kwani mishipa mingi ingeziba, sasa nafuata ushauri wa madaktari kuzingatia mtindo bora wa maisha,” anasema. Dalili za tatizo Dk. Pallangyo anataja dalili ya kwanza ni mtu kulalamika kuhisi  maumivu ya kifua upande wa moyo mara kwa mara hata akifanya shughuli nyepesi. “Kawaida mtu akifanya shughuli yoyote mahitaji ya damu yanakuwa makubwa, sasa yanapoongezeka damu haiwezi kupita kwa sababu ule uwazi wake umeshapunguzwa kutokana na hayo mafuta,” anasema. Anasema baadae mtu hupata mshtuko wa moyo hatimaye kufariki ghafla. “Dalili hizi huwa ni muendelezo, huanza kupata maumivu ya kifua, mshituko hatimaye kufariki ghafla, hali hii hutokea pale ambapo mshipa unakuwa umeziba kwa asilimia 100, damu hushindwa kabisa kwenda kwenye moyo na katika sehemu zingine za mwili. Mshipa unapoziba damu na hewa ya oxygen huwa zinashindwa kupita,” anasema. Wengi wanaugua Daktari huyo anasema kila siku watu watatu hadi saba hufika katika taasisi hiyo na kufanyiwa uchunguzi na wanaokutwa na tatizo hufanyiwa upasuaji wa kuzibuliwa. “Idadi hii kwa wiki ni sawa na watu 35 na kwa mwezi ni sawa na watu wapatao 140. Kwa mwaka jana pekee tuliwafanyia uchunguzi watu wapatao 400 katika mtambo wetu wa ‘cath lab’ kati yao asilimia 45 waligundulika kuwa na tatizo,” anasema na kuongeza kuwa mishipa ilikuwa imeziba kwa kiwango ambacho walihitaji kuzibuliwa au kuwekewa mrija (stand) kuizibua. Anasema hata hivyo si wote ambao hufanyiwa upasuaji bali wale ambao mishipa yao imeziba kwa kiwango cha asilimia 50 na kuendelea. “Wale ambao huwa imeziba chini ya kiwango hicho huwa tunawapa dawa za kutumia,” anasema. Ushauri Anasema kwa kuwa tabia hatarishi zinazosababisha tatizo hili zinaepukika watu wabadili mtindo wa maisha. “Matibabu yake ni gharama kubwa, wanaomudu ni wale wenye bima, kipimo na upasuaji hufikia hadi Sh milioni nne, wengi wasiokuwa na bima hushindwa kumudu hivyo ni vema wakakate sasa,” anashauri.
1kitaifa
WAZIRI wa Afya, Hamad Rashid Mohamed amewakumbusha watendaji wa wizara hiyo kuwa huduma za matibabu ikiwemo ya afya kwa wanawake na watoto zinatolewa bure.Alisema serikali haitamvumilia mtendaji ambaye atawatoza fedha wananchi kwa ajili ya kupata huduma za afya ikiwemo dawa ambazo zipo. Hamad alisema hayo wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Kituo cha Afya cha Fuoni ambapo hivi karibuni wananchi wakiwemo wajawazito walitoa malalamiko ya kutozwa fedha kwa ajili ya baadhi ya vipimo. Alisema huduma za upimaji kwa wajawazito na watoto zinatolewa bure, ambapo katika bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2018-2019 serikali imeongeza bajeti ya huduma za afya.Alisema kwamba lengo la kuongeza bajeti ni kuwawezesha wananchi ikiwemo wajawazito na watoto kupata huduma hizo bure. ‘’Nasisitiza tena ni marufuku kwa watendaji wa Wizara ya Afya kuwatoza fedha wananchi ikiwemo wajawazito wanaokuja hapa kwa ajili ya kupima afya zao, Rais Shein(Ali Mohamed) amekataza kabisa suala la kutoza fedha wananchi na ndiyo maana bajeti ya afya imeongezwa,’’alisema. Aidha amewataka watendaji katika bohari kuu kuwasilisha orodha ya mahitaji yao mapema ili waweze kuingizwa katika orodha ya kupata dawa zinazohitajika.‘’Tuna dawa za kutosha, tatizo lipo kwa watendaji wanachelewesha kuwasilisha mahitaji ya dawa katika vituo vya afya,’’alisema. Daktari wa Wilaya ya Mjini Magharibi Unguja, Rahma Maisara alisema watahakikisha hakuna tatizo la upungufu wa dawa zinazohitajika kwa wananchi ikiwemo mahitaji ya wajawazito na vipimo vyake. Aidha aliwakumbusha watendaji wa Kituo cha Afya cha Fuoni na vituo vingine kwamba huduma za afya zinatolewa bure na hakuna sababu ya mwananchi kutozwa fedha kwa ajili ya kupata matibabu. ‘’Katika Kituo cha Afya cha Fuoni tutahakikisha hakuna mgonjwa atakayetozwa fedha kwa ajili ya kupata huduma za afya ikiwemo vipimo kwa wajawazito,’’alisema.
1kitaifa
TEHRAN, IRAN SERIKALI ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imekanusha taarifa zilizosambaa kuwa imeomba mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump. Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran, Bahram Qassemi, aliyenukuliwa na shirika la habari la nchi hiyo, IRNA amesema hakuna ukweli wowote katika taarifa za kwamba Iran iliomba kukutana na Trump wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambao umeanza wiki hii. Qassemi amesema taarifa zilizomnukuu Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, kwamba Iran inataka kukutana na Trump zimejaa uongo na zinapaswa kupuuzwa. Aidha, Qassemi amesema Rais wa Iran, Hassan Rouhani, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo, lakini hakuna mpango wowote wa kuzungumza na Trump. Mvutano umeongezeka kati ya Iran na Marekani, baada ya Trump kujiondoa katika mkataba wa kihistoria wa nyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani mwezi Mei mwaka huu na kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran. >>>>>>>>>>>>>   Chama cha siasa kali chapata umaarufu BONN, UJERUMANI UCHUNGUZI mpya wa kura za maoni unaonyesha kuwa Serikali ya muungano wa Ujerumani, inapoteza uungwaji mkono wa wapiga kura, huku chama cha siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia cha AfD kikizidi kupata umaarufu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Deutschlandtrend na shirika la utangazaji la umma, ARD, umeonyesha jana kuwa chama cha AfD kimekipiku chama cha Social Democratic (SPD) ambacho ni mshirika katika Serikali ya muungano na kuwa chama cha pili chenye nguvu nyuma ya vyama ndugu vya kihafidhina vya Kansela Angela Merkel, ambavyo ni Christian Democratic Union (CDU) na Christian Social Union (CSU). AfD kilionyesha kuimarika kwa nyongeza ya asilimia mbili tangu uchunguzi wa mwisho wa Septemba 9 na kujikusanyia asilimia 18 ikiwa ni moja zaidi ya mshirika wake mdogo wa Serikali ya muungano SPD, ambacho kilipoteza pointi moja. Kundi la Merkel la CDU na CSU ambalo limeongoza Serikali tofauti za Ujerumani tangu 2005, pia limepoteza pointi na kufikia asilimia 28, yakiwa matokeo mabaya kabisa tokea utafiti huo ulipoanzishwa mwaka wa 1997.
3kimataifa
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Kampeni ya Wazazi Nipendeni iliyofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, mwanamuziki nyota nchini, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ alisema wakati wa jamii kubadilika umewadia.Mheshimiwa Temba na Said Juma maarufu Chege Chigunda ni wasanii wanaounda Kundi la TMK Family lililokuwapo kwenye uzinduzi huo uliopambwa na burudani iza kuvutia.“Tubadilike, jamii ibadilike na kufanya uamuzi sahihi hasa linapokuja suala la uzazi salama na mapambano dhidi ya maradhi mbalimbali kama vile malaria. “Mimi nimefurahi sana kushirikishwa katika tamasha hili lenye malengo mazuri na muhimu katika kusaidia jamii yetu. Ninaamini kuwa kupitia kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni’, Watanzania mijini na vijijini wataelewa umuhimu wa uzazi salama,” alisema Mheshimiwa Temba.Aliwaomba wananchi kuipokea kampeni hiyo na kutoa ushirikiano kwa wadau wote hasa watakapoanza ziara kutembelea mikoa mbalimbalii nchini. Kwa upande wake, Chege alisema suala la kupanga uzazi salama ni kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) katika maisha ya sasa si la kusubiri tena, bali ni la kuanza mara moja.“Hakuna sababu ya kusubiri tamasha au kampeni kama hii. Ninawahimiza Watanzania wenzangu na kuwaambia kuwa kila mtu ajipe jukumu la kutembelea vituo vya afya vilivyopo karibu na anakoishi. “Afya yako ni muhimu kwa maendeleo ya taifa na ubora wa kizazi kijacho,” alisema Chege, mmoja wa wasanii wanaokubalika miongoni mwa vijana nchini.Mdau wa muziki wa muda mrefu nchini, Said Fela, alisema kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni’ inatoa fursa kwa wananchi kufahamu vyema masuala ya uzazi wa mpango na kupima afya zao.Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja Mradi huo, Waziri Nyoni, alisema Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID) inasimamia kampeni hiyo kwa lengo la kuwahamasisha Watanzania kushiriki katika kupanga uzazi.“Sasa tumezindua kampeni hii kwa mara ya pili na kwa kushirikiana na wasanii, tutahakikisha elimu ya uzazi salama inawafikia wananchi wengi iwezekanavyo jijini hapa na mikoa yote,” alisema Nyoni. Kampeni hiyo ilizinduliwa Ijumaa iliyopita kwa tamasha kubwa la muziki lililoambatana na ushauri wa kiafya na upimaji maradhi mbalimbali.
2michezo
ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Shao ameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuweka utaratibu mzuri unaofahamika, utakaowawezesha makundi ya watu mbalimbali, kupata huduma za mchanga bila ya usumbufu.Askofu Shao alisema hayo nje ya kanisa baada ya ibada ya Krismasi katika Kanisa la Minara Miwili lililopo eneo la Mji Mkongwe Zanzibar. Alisema matumizi ya rasilimali ya mchanga ni makubwa kwa jamii ya watu wa kawaida na upatikanaji wake umekuwa na utaratibu mrefu wenye usumbufu kwa wananchi.Aidha, alisema matumizi ya kazi za ujenzi yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kufuatia kuimarika kwa familia, kwa hivyo utaratibu mzuri unahitajika kuwekwa ili watu wafaidike na nishati hiyo.“Tunaiomba serikali iweke utaratibu mzuri ambao utawawezesha watu wa kawaida kupata huduma za mchanga kwa shughuli za ujenzi wa nyumba na mambo mengine,” alisema.Aidha, aliitaka jamii nayo kuchukua juhudi za kulinda mazingira na vyanzo vya maji ili kuepuka uharibifu unaoweza kuleta maafa makubwa. Alisema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko ya tabianchi, ambapo vyanzo vya maji hukabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo vingine kupungua uzalishaji maji. Zanzibar inakabiliwa na tishio kubwa la uhaba wa rasilimali ya mchanga, kiasi ya kuweka kiwango maalumu cha watu na kampuni binafsi kupata huduma hiyo.SMZ ipo katika hatua za mwisho za kuweka wakala, ambaye atahusika na usambazaji wa mchanga kwa matumizi ya watu wa kawaida. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Dk Makame Ali Ussi alisema utaratibu wa kuweka wakala, atakayehusika na masuala ya manunuzi ya mchanga ni muhimu, kwa sababu utaondosha urasimu kwa watu wa kawaida kupata huduma hiyo, ikiwemo kuandika barua kwenda kwa sheha.
1kitaifa
Na LEONARD MANG’OHA SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la Tanzania Social Support Foundation (TSSF) linalojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, limetolea ufafanuzi taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa shirika hilo ni la kitapeli na halijasajiliwa. Akitoa ufafanuzi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Donati Salla, alisema taarifa hizo zinalenga kuichafua TSSF na huenda zinatolewa na washindani wao ambao wamekuwa wakitoza riba kubwa kwa wanufaika wa mikopo hiyo kutoka kwenye taasisi zao. Alisema TSSF imesajiliwa kwa mujibu wa sheria na imekuwapo nchini tangu mwaka 2011, na limekuwa likijihusisha na shughuli mbalimbali ikiwamo za bima ya afya na maendeleo ya elimu. Ujumbe unaosambaa kuwa tunataka kuwatapeli wanafunzi wa elimu ya juu  si wa kweli, kwa sababu haujatolewa na Serikali wala shirika lenyewe na isitoshe sisi si kampuni kama walivyoeleza, sisi ni shirika na tumesajiliwa kisheria. “Kabla ya kufikia uamuzi wa kutoa mikopo hiyo tulifanya utafiti na kubaini kuwa kuna idadi kubwa ya watu wenye uhitaji wa mikopo, lakini wanakosa fursa hiyo. “Tulifanya semina kwa Serikali za wanafunzi na tulitoa taarifa katika taasisi za elimu zinazodahili kwa ngazi ya shahada,” alisema Salla. Alisema katika mchakato wao walitumia njia zinazokubalika kisheria kutoa taarifa kwa umma, ambapo walitoa matangazo katika magazeti mbalimbali likiwamo MTANZANIA. Alisema kabla ya kutoa matangazo hayo taarifa zao zilichapishwa katika magazeti mbalimbali nchini, zikieleza kuwa wanafunzi 50,000 walikosa mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, wataweza kunufaika na mikopo kutoka katika shirika hilo. “Tunaelewa kuna watu ambao tayari walikuwa wameomba mikopo na hawajapata, huenda taarifa hii inaweza kuwa imewasababishia ‘shock’, tunaomba waendelee kuwa watulivu na waendelee kuomba. Kazi yetu si kukaa na kusema Serikali imeshindwa au kulaani, bali ni kuisaidia pale inapokuwa haina uwezo wa kutoa mikopo hiyo, maendeleo tunaweza kuyapata kwa kuungana pamoja, tukiendelea hivi hatutafika mbali,” alisema. Alishangazwa kuona watu wanaamini taarifa zilizotolewa na vyanzo visivyo rasmi, huku zile zilizotolewa katika mfumo rasmi zikipotoshwa na kupuuzwa. Alionya kuwa atakayebainika kulichafua shirika hilo atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia mitandao vibaya. Alisema hadi sasa jumla ya wanafunzi 256 walijitokeza kuomba mikopo katika taasisi hiyo na 198 kati ya hao wamepata mipopo hiyo. Wakati huo huo, Salla alisema Novemba 30 mwaka huu, watakutana na makamu wakuu wa taasisi za elimu ya juu nchini kujadili namna ya kutekeleza mpango huo wa udhamini kwa wanafunzi waliokosa mikopo kutoka HESLB.
1kitaifa
Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerry alisema hivi karibuni kuwa ili kupima kikosi chake anahitaji mechi tano za kirafiki za kimataifa. Akizungumza na gazeti hili juzi kwenye mazoezi ya Simba, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Collin Frisch alisema klabu hiyo ipo tayari kumpatia kocha huyo kila kitu anachohitaji.“Sisi kazi yetu ni kuhakikisha tunampatia kocha kila anachohitaji. Kama amesema anahitaji mechi tano tutamtafutia ilimradi tuone kuwa anakisaidia kikosi chetu kutimiza yale tuliyokusudia,” alisema Frisch.Alisema timu atakazochagua ni zile ambazo zitashiriki michuano ya Kagame kwani itafanyika nchini na kushirikisha timu nyingi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.Kwa mujibu wa ratiba ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kuna makundi matatu.Kundi A, litakuwa na timu za Yanga kutoka Tanzania Bara, Gor Mahia kutoka Kenya, Telecom kutoka Djibouti, KMKM ya Zanzibar na Khartoum National kutoka Sudan. Kwa mujibu wa Cecafa, katika kundi hili timu tatu zitatinga kwenye hatua ya robo fainali.Kundi B, litakuwa na timu za APR kutoka Rwanda, Al- Ahly Shendi kutoka Sudan, Lydia Ludic ya Burundi pamoja na Hegan FC ya Somalia. Kwenye kundi hili, timu mbili zitafuzu kwenda hatua ya robo fainali.Kundi C, litakuwa na timu za Azam FC ya Tanzania, Malakia kutoka Sudan Kusini, Adama City kutoka Ethiopia pamoja na KCCA kutoka Uganda.
2michezo
MWENYEKITI wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodogar Tenga amemtaka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallence Karia kuacha  kuliongoza shirikisho hilo kirafiki.Tenga amesema hayo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.Amesema hakuna mtu asiyekuwa na rafiki, lakini urafiki una mipaka na ukiweka urafiki mbele katika majukumu ya kazi ya kila siku ya shirikisho hilo, basi unaweza kukwama mbele na kuanza kulaumiwa.Mwenyekiti huyo alimtaka Rais wa TFF kuacha urafiki katika kuliongoza shirikisho hilo na badala yake alimtaka kuongoza kwa kufuata misingi ya Katiba ya TFF.‘’Kila mtu ana rafiki hapa tulipo na kamwe usiruhusu urafiki uingilie kazi yako ya kuliongoza shirikisho hilo lenye katiba na kanuni katika kuongoza,’’ alisema Tenga, ambaye aliwahi kuwa Rais wa TFF.Tenga alimsifu Gambo kwa kushirikiana na TFF katika kuongoza soka la nchi hii na kusema kuwa hajawahi kuona kiongozi wa mkoa mwenye moyo kama mkuu huyo wa mkoa.
2michezo
NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, amesema ana mpango wa kuihamishia studio ya Mwanalizombe kwenye jimbo lake ili aweze kutekeleza ahadi ya kuinua sanaa. Akizungumza na MTANZANIA, Profesa Jay alisema kuwa moja ya ahadi alizowaahidi wakazi wa Mikumi kwenye kampeni zake ni kuibua vipaji vipya ndiyo maana ameamua kuihamishia studio hiyo huko ili aweze kutekeleza ahadi hiyo. “Mikumi kuna vipaji vingi vya muziki lakini hakuna aliyeweza kuviibua kwa miaka mingi, ila mimi nikiwa kama Mbunge wao nitatekeleza ahadi hii kwa kuihamishia studio yangu Mikumi ili wasanii chipukizi waweze kufanya kazi zao,” alisema Profesa Jay. Mwanalizombe ni studio inayomilikiwa na msanii huyo ipo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es salaam na imeshatoa nyimbo kali kama Makamanda wimbo wa Sugu, Tatu Chafu na Kipi Sijasikia chini ya mtayarishaji Villy.
4burudani
Na HARRIETH MANDARI -GEITA KAMPUNI ya uchimbazaji dhahabu katika Mgodi wa Bulyanhulu Acacia imesema uamuzi wa Serikali kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi kumewasababishia hasara kubwa, hivyo wameufunga mgodi kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji. Meneja Mkuu wa Uhusiano wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo alisema mgodi wa Bulyanhulu (BGML), umepoteza nusu ya mapato yake yote ya awali. Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi wa mgodi huo juzi, Mwaipopo alisema uzalishaji katika mgodi huo umepungua kutoka wakia 300,000 hadi aunzi 2,000 kwa mwezi kiasi ambacho alidai ni kidogo na hakina faida yoyote kwa kampuni. Mwaipopo alisema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kupungua kwa uzalishaji, hivyo kufanya mgodi huo kushindwa kumudu gharama za uendeshaji. Alisema kutokana na hilo Septemba 15 wamefikia uamuzi wa kupunguza rasmi shughuli za uzalishaji sambamba na wafanyakazi 150 akiwamo aliyekuwa Meneja Mkuu wa mdogi huo, Graham Crew ili kuepuka hasara zaidi. “Tumepata hasara kimapato ambayo ni chini ya nusu ya mapato yetu, tumekuwa tukilazimika kutumia akiba ya fedha iliyokuwepo kwa ajili ya kuendesha mgodi na kulipa wafanyakazi,”alisema. Kwa upande wake, Crew alisema tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji na uzalishaji dhahabu katika mgodi huo wamewekeza zaidi ya Sh trilioni 8 huku matumizi yakiwa ni Sh trilioni 6.6 na kodi mbalimbali zikigharimu Sh trilioni 2.2. Aidha katika kuwaandaa wafanyakazi hao, alisema wamekutana mara ikiwa ni pamoja na kuwaeleza kutokata tamaa ya maisha baada ya kuondoka mgodini hapo na kuwataka kutumie vizuri elimu ya ujasiriamali waliyoipata kujikimu kiuchumi. “Wafanyakazi mpeta elimu ya ujasiriamali, nimewaeleza kasimame imara, muwe tayari kukabiliana na maisha nje ya mgodi kwani maisha siyo mgodini pekee yapo hata nje ya hapa…, inawezekana kabisa kufanya shughuli zingine za kiuchumi na maisha yakaendelea,”alisema Crew. Kuhusu hatima ya mgodi huo, Crew alisema kuwa watabakia wafanyakazi wachache ambao wataendelea na uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia tope la makinikia hivyo kuzalisha miche ya dhahabu. “Mgodi huu bado utaendelela kutoa kodi ya huduma kwa asilimia 67 ambayo ni sawa na Sh milioni 176  ambacho hutolewa kwa Wilaya ya Msalala, asilimia 33 na Wilaya ya Nyanghwale ambayo ni sawa na Sh milioni 87,” alifafanua. Hatua ya kufungwa kwa migodi hiyo inatokana na kile wanachodai kupinga uamuzi wa kamati za uchunguzi zilizoundwa Rais Dk. John Magufuli kuchunguza usafirishaji wa mchanga wa dhahabu na masuala ya kiuchumi na kisheria. Ripiti za kamati hiyo ziliibuka masuala mazito ikiwemo  kutosajiliwa kwa kampuni ya Acacia Mining inayojinasibisha kuwa mmiliki wa kampuni za Bulyanhulu Gold Mines, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals. “Kamati imebaini na kuthibitisha kwa mujibu wa nyaraka na maelezo kutoka ofisi ya msajili wa makampuni (Brela) kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc haikusajiliwa nchini Tanzania na wala haina hati ya utambuzi kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura ya 212,” alisema Profesa Osoro.
1kitaifa
Mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala ametangaza kuwa amepona rasmi virusi vya corona vilivyomsumbua kwa takribani miezi miwili Dybala ambaye wiki kadhaa zilizopita aligundulika na ugonjwa huo kwa mara ya nne ndani ya wiki sita ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa sasa yupo safi “Sura yangu inasema kila kitu napenda kutangaza kuwa sasa nipo huru nimepona virusi vya Corona” ameandika huku akiweka picha akiwa ametabasamu Dybala alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa kwanza kabisa wa Juventus kukutwa na virusi vya corona mapema mwezi wa Machi   Mi imagen lo dice todo, finalmente curado de Covid-19 😆💪🏽♥️. My face says it all, i’m finaly cured from Covid-19 💪🏽♥️😆La mia faccia dice tutto: finalmente guarito dal Covid-19! A post shared by Paulo Dybala (@paulodybala) on May 6, 2020 at 9:10am PDT
2michezo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea Sh milioni 27 kutoka kwa Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili ya kuwalipia bima watoto 500 kwa kipindi cha mwaka mmoja.Watoto watakaolipiwa bima hiyo ni wale waliofanyiwa na watakaofanyiwa operesheni ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhiwa hundi ya fedha hizo Dar es Salaam jana, Makonda alisema ubalozi huo umekuwa bega kwa bega na serikali katika kusaidia changamoto mbalimbali zinazowapata wananchi.“Ubalozi huu ni rafiki wa Watanzania, umesaidia kusomesha watoto 100 wa kike, kusaidia kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuturisha misikiti 800, umeleta madaktari 10 kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto Muhimbili na sasa unawalipia bima watoto hawa 500,” alisema Makonda.Alisema amekuwa na kampeni ya kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo na ndipo kupitia ubalozi huo wa UAE chini ya Balozi wake nchini Tanzania Khalifa Abdulrhaman Almarzooqui walileta madaktari hao 10 kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji watoto wenye matatizo ya moyo.Alieleza kuwa katika kampeni hiyo jumla ya watoto 60 walifanyiwa upasuaji, lakini ikaonekana kuwa kuna haja ya kuendelea kuwasaidia wazazi wa watoto hao katika kufuatilia maendeleo yao ikiwemo kuwawekea bima.“Wengi wa watoto hawa na wazazi wao wanaishi katika mazingira magumu, akishafanyiwa upasuaji mzazi atatakiwa kufuatilia afya ya mtoto ikiwemo kwenda kliniki, sasa gharama za yote haya wataiwezaje? Alihoji. Alisema kwa kushirikiana na ubalozi huo wameamua kuanzisha bima hiyo kwa watoto hao 500 ya mwaka mmoja, itakayohusisha watoto hao waliofanyiwa upasuaji na wengine wanaofanyiwa upasuaji hospitalini bila kujali sehemu wanakotoka.“Mwakani tuna mpango wa kufanyia upasuaji watoto wengine 500 wenye matatizo ya moyo, hawa nao tutawaingiza kwenye mfumo huu wa bima,” alisema.
1kitaifa
TANZANIA inashiriki maonesho ya utalii ya kimataifa nchini Uholanzi kwa lengo la kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.Maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika mji wa Utrecht na kushirikisha taasisi mbalimbali kutoka duniani kote, yanajulikana kama ‘Holday Fair 2019 na yalianza tangu Januari 9 mwaka huu na yatakamilika Januari 13, 2019.Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Taasisi mbalimbali na kampuni binafsi za utalii zipo nchini humo kwa ajili ya kushiriki maonesho hayo.Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wizara, Taasisi za Serikali zinazoshiriki maonesho hayo ni pamoja na Bodi ya Utalii Tanznaia (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).Kwa upande wa kampuni binafsi zinazoshiriki maonesho hayo ni into Africa Eco Travel Ltd, Migada Adventures, Mbalaget Tented Camp Ltd, Kili Fair Promotions Ltd, East Africa Camps na Makasa Tanzania Safaris.Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Irene Kasyanju, alisema kuwa maonesho hayo ni fursa muhimu kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake vya utalii.Kasyanju alisema kwa mara ya kwanza mwaka huu, waandaaji wa maonesho hayo wametoa nafasi kwa Balozi za nje zilizopo nchini humo nazo kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizomo katika nchi zao.Kwa mujibu wa Balozi huyo, maonesho hayo yataenda sanjari na Vakantiebeurs Travel Congress, Vakantiebeurs Consumer Day na Vakantiebeurs Trade Day ambapo washiriki watapata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo utasaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake.
0uchumi
Nairobi,Kenya MAHAKAMA imeamuru watu wawili wanaohusishwa na na mauaji ya kasisi wa Kanisa Katoliki. Michael Maingi Kyengo wasipewe dhamana hadi Novemba 6,mwaka huu. Hakimu Mwandamizi, Hellen Onkwani aliagaza watuhimiwa Kavivya Mwangangi na Solomon Mwangangi wazuiliwe kituo cha polisi kwa muda wa siku nane ili uchunguzi zaidi kuhusu kifo cha kasisi huyo ukamilike. “Badala ya usimulie kisa hicho hapa kortini, nitakuruhusu ufanye hivyo katika kituo cha polisi ukiandamana na watu wa familia yako na wakili ndipo urekodi polepole kilichojiri,” alisema Onkwani. Mmoja wa maofisa wanaochunguza kesi hiyo, Julio Mutembei alijibu na kumweleza hakimu kuwa mshukiwa alitaka kutoboa siri jinsi kasisi alivyouawa. “Naomba hii mahakama irekodi maungamo hayo ya mshukiwa huyu,” alisema Mutembei. Hata hivyo, hakimu alikatiza huo ushahidi. Mtuhumiwa mwingine, Michael Mutunga tayari anashikiliwa kwa muda wa siku 10 baada ya kufikishwa mahakamani. Ijumaa iliyopita Mwangangi alisimulia korti jinsi mwendazake alivyofungwa mikono na miguu kabla kuuawa na maiti yake ikafukiwa kando ya mto katika Kaunti ya Machakos. Alisema Padri Kyengo alikuwa amefungiwa ndani ya buti la gari. Alimtaja Mutunga kama rafiki yake wa karibu ambaye alimwomba waandamane akamsaidie ‘kutoa sadaka.’ Alisema pia ni rafikiye ndiye aliyemwamuru kumfunga miguu na mikono marehemu. “Msiniue tafadhali. Tafadhali usiniue,” Mwangagi alikumbuka jinsi kasisi huyo alimsihi Mutunga aliyekuwa amechukua simu ya Kasisi Kyengo. Alieleza kuwa alimwamuru amtajie nambari ya siri ya kufungua simu na pesa alizokuwa nazo kwenye akaunti. “Marehemu alimpa Mutunga nambari ya siri ya simu na akaunti za benki,” alisema Mwangagi. Mtuhumiwa alisema Mutunga alitoa pesa kwa akaunti ya Kasisi Kyengo kisha akamlaza kifudifudi. Mahakama ilielezwa utunga alichukua panga na kumuua Kasisi. Mutembei aliieleza mahakama kuwa sampuli za marehemu zimepelekwa kuchunguzwa katika maabara ya Serikali. Pia alisema nguo, gari, simu na kadi za benki zilichukuliwa na watuhumiwa.
3kimataifa
Kobe pamoja na mwanawe Gianna waliaga dunia kufuatia ajali mbaya ya ndege waliyokuwa wameiabiri pamoja na jamaa wengine saba Wengine hao walikuwa wazazi pamoja na wachezaji waliokuwa wakisafiri kuhudhuria mechi katika Mamba Sports Academy Dunia inaomboleza kifo cha mchezaji hodari wa mpira wa kikapu Kobe Gryant na mwanawe Gianna waliofariki pamoja na wengine saba Jumapili, Januari 26 kufuatia kisa cha ajali mbaya ya ndege iliyotokea Calabasa mjini California. Kobe Bryant has been killed in a helicopter crash in Calabasas, California, on Sunday morning. The 41-year-old former Los Angeles Lakers basketball star's death was confirmed by TMZ. A post shared by Urban News (@urbannews254) on Jan 26, 2020 at 12:00pm PST Kati ya walioiabiri ndege hiyo ni kocha John Altobeli, 56, mkewe Keri Altobelli na mwanao Alyssa, wote wakiripotiwa kuaga dunia papo hapo. Alyssa, msichana mwenye umri wa miaka 13 alikuwa katika timu moja na Gianna, mwanawe Kobe. Christina Mauser ambaye ni naibu kocha katika shule ya kibinafsi ya mpira wa kikapu pia ni kati ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo. Payton Chester ambaye pia alikuwa mwanatimu wa Mamba alikuwa akisafiri pamoja na mamaye wakati wa kisa hicho. Orange County baseball coach John Altobelli, his daughter Alyssa and wife Keri also died in the helicopter crash along with Kobe and Gianna Bryant. My heart goes out to the Altobelli family 💔 A post shared by Katie Couric (@katiecouric) on Jan 26, 2020 at 5:18pm PST Kando na hao, alikuwapo Ara Zobayan, rubani wa ndege hiyo aliyesifika mno kwa uhusiano wake na familia ya Kobe. Jumla ya abiria hao wote tisa waliripotiwa kufariki katika ajali hiyo, majina yao haya hapa: https://www.instagram.com/p/B70msqmA-Cf/?utm_source=ig_embed Kobe Bryant Gianna Bryant – Mwanawe Kobe John Altobelli- babake Alyssa Keri Altobelli- mamake Alyssa Alyssa Altobelli- mwanatimu wa Mamba Christina Mauser- kocha Kobe Bryant Gianna Bryant – mwanawe Kobea John Altobelli- Bakake Alyssa Keri Ara Zobayan – rubani  
2michezo
Akizungumza na gazeti hili baada ya sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi uliowekwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Balozi wa China, Dk. Lu Youqing, Kasongo alisema ujenzi wa uwanja huo utasaidia kuinua soka.“Soka ni ajira na vijana wakipata sehemu za kufanya mazoezi na kufundishwa namna ya kucheza soka itasaidia kuongeza kipato pia kuwaondoa katika makundi maovu,” alisema Kasongo.Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema ujenzi huo unatarajiwa kuanza kesho na utasimamiwa na kampuni ya BCEG kutoka China ambayo ndio iliojenga Uwanja wa Taifa na Uhuru“Uwanja unajengwa na kampuni ya BCEG ambayo ndio iliyojenga uwanja wa Taifa na Uhuru na niwaombe utakapomalizika tuutunze ili hata vizazi vijavyo vifaidi,” alisema Makonda.Uwanja huo unatajiwa kutumia dola za kimarekani laki nne na nusu na utakuwa na jukwaa la VIP, vyumba vya wachezaji, maliwato pamoja na vyumba vya waamuzi.
2michezo
Na JANETH MUSHI-ARUSHA WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema wa Arusha Mjini na Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki, wameweka hadharani ushahidi wa video unaoonyesha jinsi baadhi ya madiwani wao walivyoshawishiwa kukihama chama hicho na kujiunga na CCM. Wabunge hao walibonyeza kitufe jana mbele ya waandishi wa habari kama walivyoahidi Jumapili iliyopita, kwamba wangeanika ushahidi huo hadharani   kuonyesha mbinu walizoziita chafu, zilizofanywa na viongozi wa Serikali kwa madiwani wao. Katika ushahidi huo, madiwani hao wanaonekana kwa nyakati tofauti, wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, Katibu Tawala, Wilaya ya Meru, Timotheo Mzava na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Christopher Kazeri. Mazungumzo kati ya viongozi hao wa Serikali na madiwani hao, yanahusu kuhama kwa madiwani hao na ahadi walizotakiwa kupewa baada ya kutimiza nia hiyo. Katika video ya kwanza inayoonekana kuchukua dakika zipatazo 30 baada ya kurekodiwa Agosti 28, mwaka huu, Mzava anaonekana akiwa ofisini akizungumza na mmoja wa madiwani wa Chadema kwa kumshawishi ahamie CCM. Katika mazungumzo hayo, diwani huyo anaomba kabla hajajiuzulu, atekelezewe miradi miwili ya soko na barabara iliyopo kwenye kata yake. Diwani huyo anasikika akisema ana nia ya kuhama ila ana mashaka na madiwani wengine waliokwisha kuhamia CCM ambao anasema yeye ni tofauti na madiwani hao. Kwenye video hiyo hiyo, inaonekana siku diwani huyo huyo akizungumza na Mkuu wa Wilaya (Mnyeti), Mkurugenzi Kazeri. Katika video hiyo, diwani huyo anaonyesha wasiwasi wa kuhama akisema anahofia kutolipwa fedha hizo baada ya kuhama. Katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Kazeri anasikika akisema tayari wamekwisha kupiga hesabu ya idadi ya vikao walivyobakiza madiwani hao kabla ya kumalizika kipindi chao cha uongozi mwaka 2020. Pia, Kazeri anasikika akimwambia diwani huyo  kwamba ni vema akaangalia mwelekeo wa maisha yake na akimsisitizia diwani huyo kwamba ameshampa maelekezo mweka hazina wa halamshauri yao namna ya kuwalipa kiinua mgongo chao cha miaka mitano pamoja na posho zote ingawa wamekuwa madarakani kwa   mwaka mmoja na nusu. Mnyeti pia anasikika akimweleza diwani huyo  kwamba akishaandika barua ya kujiuzulu na kuhamia CCM, atatafutiwa ajira zitakapotangazwa na kwamba kabla ya ajira rasmi, diwani huyo atakuwa akifanya kazi za kujitolea akisubiri ajira rasmi. Mnyeti anasikika akisema yeye hafanyi uamuzi  lakini ana ushawishi na kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alishachukua wasifu wa madiwani hao (CV). Vilevile Mnyeti anasikika akisema kwa mamlaka aliyonayo, atashughulikia suala hilo na  alimsisitizia diwani huyo  kwamba Rais Dk. John Magufuli, anatarajia kutembelea mkoani Arusha baada ya wiki tatu kuanzia siku waliyokuwa wakizungumza. Mnyeti anaonekana akimshawishi diwani huyo ahame kwa kuwa Rais Dk. Magufuli atakapokuwa Arusha  watapelekwa wakaonane naye usiku. Kwa mujibu wa video hiyo, Mnyeti akiwa nje ya ofisi yake anaendelea kusema madiwani wengine wawili wameshatafutiwa ajira katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii. Mnyeti anazidi kumtaka diwani huyo aandike barua ya kujiuzulu na hata kama hana ajira, yeye yuko tayari kumlipa mshahara  aweze kutunza familia yake. Video hiyo pia inamuonyesha diwani huyo akilalamikia mgao wa Sh milioni mbili alizoahidiwa kupewa kama kianzio huku Mkurugenzi Kazeri akisikika akisema hakuna diwani aliyepewa zaidi ya kiasi hicho cha fedha. Pia  Kazeri anasikika akimwahidi diwani huyo kwamba atatekeleza miradi katika kata yake ili akigombea udiwani kupitia CCM wakati wa uchaguzi mdogo  aweze kuchaguliwa kwa urahisi kwa kuwa ameshatekeleza ahadi kwa wapiga kura wake. VIDEO NYINGINE Video nyingine  inaonyesha aliyekuwa Diwani wa Makiba, Emanuel Mollel, akizungumza na diwani mwenzake akimshawishi mwenzake ambaye haonekani vizuri kwenye picha, kwamba ahame kwa sababu  hata Diwani wa Maroroni, Bryson Isangya, alipokuwa akioa, Mzava ambaye ni Katibu Tawala, ndiye aliyekuwa mratibu wa harusi yake. Diwani huyo anasikika akisema kwamba Kazeri amewahakikisha kuwa uchaguzi mdogo ukirudiwa  watampigia kura ya kutokuwa na imani Mwenyekiti wa Halmashauri, Willy Njau. Katika video hiyo, mkurugenzi huyo anasikika akisema kwamba  katika uchaguzi wowote utakaoitishwa, hakuna mgombea wa Chadema atakayetangazwa hata kama atakuwa ameshinda. Mbali na video hizo, Lema na Nassari walionyesha sauti iliyorekodiwa ambako mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mnyeti, akizungumza na mmoja wa madiwani aliyejiuzuru jimboni kwa Nassari. Katika sauti hiyo, Mnyeti anasikika akimuuliza kama wakati wa vikao vyao kuna mtu alikuwa anawarekodi, lakini mtu huyo anasikika akisema hakukuwa na mtu aliyekuwa akiwarekodi. NASSARI Akizungumza baada ya kuonyesha ushahidi huo ambao nakala zake alizigawa kwa waandishi wa habari kupitia flash, Nassari alisema kufanya siasa na kuongoza wananchi hakuhitaji nguvu bali kunahitaji akili. “Nilishasema sina shida ya diwani kuhama chama, nina shida na watu wanavyohama chama halafu kwa kumtaja rais, hii ni aibu kwa taifa, dola na Serikali kwa ujumla. “Mmeona aina ya rushwa, rushwa ya fedha, ajira, ulinzi, makazi, kiinua mgongo na posho ya miaka mitano ambayo mtu hajaitumikia, lakini anaahidiwa kupewa. “Rais amejipambanua kwamba ni kiongozi anayesimama na kupinga rushwa kwa vitendo. “Katika hili, sikutaka kuiabishia Serikali ndiyo maana nilitaka kukutana na rais nimpe ushahidi ili achukue hatua, lakini kwa kuwa Polepole ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM amejitokeza na kututaka tuwe wazi, na sisi tumeamua kueleza kila kitu. “Juzi niliwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kupitia ujumbe wa maandishi nikimuomba nikutane naye kumpa ushahidi wetu. “Kwa hiyo, kesho asubuhi (leo), tutakwenda Takukuru Dar es Salaam kupeleka ushahidi kwa sababu  kuna ushahidi mwingine hatujauonyesha kwa sababu ni aibu kwa Serikali. “Kwa kifupi, tunao uchafu mwingi ambao tukiuachia hapa, ni aibu kwa dola na hata kwangu mbunge. Kwa hiyo, tunawaomba wachukue hatua , hii ni tamthilia kama Isidingo, yaani hii ni sehemu ya kwanza,” alisema Nassari. LEMA Naye Lema alisema watendaji wa Serikali  waliohusika katika matukio hayo  hawastahili kuwa kwenye ofisi za umma kutokana na makosa waliyoyafanya. “Gharama za kurudia uchaguzi katika kata moja ni kati ya Sh milioni 250 hadi Sh milioni 300. Kwa hiyo, katika kata zote zitakazorudia uchaguzi, zitatumika zaidi ya Sh bilioni 4.5 ambazo zingeweza kujenga kilomita tisa za barabara. “Sina hakika kama kuna hatua zitachukuliwa dhidi ya watu hao, lakini uhakika nilionao  ni kwamba tumetekeleza wajibu wetu. “Lakini tutakenda Takukuru, nyie tumewapa kidogo, wao tunawapa mziki wote  waangalie na mambo ambayo tumeogopa kuwaonyesha hapa   wajue sisi tuna busara,” alisema Lema. Alisema anaamini Takukuru watachukua hatua dhidi ya watumishi hao kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa watu wengine wanaohusika na rushwa. MNYETI Akizungumzia madai hayo, Mnyeti alisema atazungumzia tuhuma hizo leo saa 2.00 asubuhi mbele ya waandishi wa habari. Mkurugenzi Kazeri alipopigiwa simu, alimtaka mwandishi wetu ampigie baadaye na alipopigiwa tena, simu yake haikupatikana. Viongozi wengine waliotajwa kwenye ushahidi huo wa video akiwamo Gambo, Katibu Tawala Mnzava Mollel, hawakupatikana kupitia simu zao za mkononi.
1kitaifa
Alisema hayo jijini Arusha wakati wa kikao chake na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini ya tanzanite na kufuatilia kwa karibu shughuli za uchimbaji na biashara ya madini hayo ili yanufaishe taifa.Alisema tanzanite hiyo ghafi yenye uzito wa gramu 2,015.59, ilikuwa ikitoroshwa na raia wa India, Jain Anurag aliyekuwa akitaka kwenda mji wa Jaipur kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Qatar wiki iliyopita.Alisema madini yaliyokamatwa yameshataifishwa kama ambavyo sheria na kanuni za madini zinavyoelekeza na kwamba ukamataji dhidi ya watorosha madini hufanywa na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Wakala wake wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji.Aidha, amesema Serikali itafuta leseni za wafanyabiashara wa madini watakaobainika kutorosha rasilimali hiyo nje ya nchi ikiwemo kuwakamata wachimbaji na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi stahiki kwa serikali.Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla ametoa saa 24 kwa raia wa kigeni wote wanaojihusisha na biashara ya madini ya tanzanite na madini mengine kinyume cha sheria, kuondoka nchini mara moja na watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
0uchumi
WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani Donald Trump, amevunja utamaduni wa karibu miaka 20 kwa kutoandaa chakula cha jioni kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo inayoandaliwa katika Ikulu ya White House imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu kipindi cha Rais Bill Clinton. Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson anaripotiwa kukataa ombi la kutaka hafla hiyo kuandaliwa. Mei mwaka huu, Shirika la Habari la Reuters lilisema Tillerson alikataa pendekzeo kutoka kwa idara inayohusika na masuala ya dini ya wizara hiyo kuandaa sherehe hiyo. Awali Trump alilaumiwa kutumia maneno makali dhidi ya waislamu ikiwemo kampeni ya kutaka uchunguzi kufanyiwa misikitini nchini Marekani. Alisema katika taarifa: “Kwa niaba ya watu wa Marekani na Melania ninatuma heri njema kwa Waislamu wakati wanaposherehekea Eid al-Fitr. Chakula cha kwanza cha Eid Ikulu mjini hapa kiliandaliwa na Rais Thomas Jefferson mwaka 1805 kwa ujumbe kutoka Tunisia. Sherehe hizo zilifufuliwa tena na Hillary Clinton mwaka 1996 wakati akiwa mama wa kwanza wa taifa. Hafla hiyo ilianza kufanywa kila mwaka tangu mwaka 1999 na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri wa Kiislamu nchini Marekani.
3kimataifa
Na Abdallah Amiri-Igunga MUUGUZI mmoja wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amedaiwa kumbaka binti wa miaka 16 (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mtaa wa Buyumba, Kata ya Igunga Mjini, ambaye alikuwa akimuuguza mama yake aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk. Ruta Deus, alikiri kuwepo kwa tuhuma hizo.  “Ni kweli tukio hilo lipo na hiyo si mara ya kwanza kwani siku za nyuma muuguzi huyo (jina tunalo) akiwa Kituo cha Afya Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hivyo hii ni mara ya pilli na huo ni ukiukwaji wa taratibu na kanuni za kiutumishi,” alisema Dk. Deus. Alisema suala hilo tayari liko polisi na wao wanaendelea kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo, mama wa msichana huyo, Wande Salum (42) aliyekuwa amelazwa wodi no. 3, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 10, mwaka huu, saa 4 usiku.  Wande alidai kuwa muuguzi huyo alifika katika wodi hiyo kuangalia hali yake na baada ya kumuona alimwambia ambadilishe dawa.  Alidai kuwa muuguzi huyo aliomba aondoke na mwanawe aliyekuwa akimuuguza na walipofika ofisini alimchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka kuanzia saa 4 usiku hadi saa 8. Wande alidai baada ya kuona muda umekuwa mrefu pasipo mwanawe kurudi wodini, aliomba msaada kwa baadhi ya wagonjwa wenzake wenye hali nzuri wamsaidie kumtafuta. Alidai kuwa baadhi ya manesi waliokuwa zamu walipopata taarifa hiyo, waliungana na baadhi ya wagonjwa kumtafuta mwanawe na walimkuta eneo la nyasi wanakofulia nguo kina mama akiwa hajitambui, huku akiwa amemwagiwa maji mwilini.  Wande alidai kuwa baada ya kumwondoa katika nyasi hizo, walikuta akivuja damu sehemu za siri kutokana na kubakwa kwa muda mrefu na muuguzi huyo. Aidha mama huyo alisema kitendo alichofanyiwa mwanawe ni cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho, huku akiomba vyombo vya dola kumsaka muuguzi huyo apatikane na kufikishwa mahakamani.  Baadhi ya kina mama wanaokwenda kutibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Rehema Julias na Sada Mwinamila, walisema hivi sasa wameingiwa na hofu kutokana na kitendo hicho na kuiomba Serikali kutofumbia macho suala hilo.  Alipotafutwa muuguzi huyo kwa njia ya simu, ilikuwa imezimwa. Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema bado hajapokea taarifa yoyote dhidi ya muuguzi huyo.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Barnabas Mwakalukwa, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo dhidi ya muuguzi huyo, alisema bado hajapokea taarifa hiyo.
1kitaifa
Serikali ya Gabon imefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi baada ya wananjeshi kadhaa kuvamia kituo cha redio cha taifa na kutangaza kuwa Rais Ali Bongo amepinduliwa.Rais Bongo yupo nchini Morocco kwa mwezi wa pili sasa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kiharusi.Hata hivyo wanajeshi waliohusika na tukio hilo wanashikiliwa , gazeti la The Guardian la Uingereza limeripoti.Msemaji wa serikali hiyo, Guy-Bertrand Mapangou ameripotiwa akisema kuwa tayari kituo hicho cha utangazaji kimesharejeswa chini ya usimamizi wa serikali hivyo mambo sasa yanakwenda shwari.Mapema leo Jumatatu, mtu aliyejitambulisha kama Lt Kelly Ondo Obiang akiwa na walinzi waliovalia mavazi kama ya walinzi wa Rais wa Taifa hilo walitangaza kupitia kituo hicho cha redio kuwa wametwaa madaraka na kila mwananchi asalimu amri.
3kimataifa