text
stringlengths
0
24.2k
label
class label
6 classes
*Aipongeza kutokuwa tawi la Simba na Yanga *Aeleza imepunguza ukame wa vikombe NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewatakama bingwa wapya wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,Azam kutoishia kushinda Kombe la Kagame pekee badala yake isonge mbele na kushinda mataji makubwa ya ubingwa Afrika. Kikwete alitoa changamoto hiyo jana Ikulu wakati alipokutana na mabingwa hao wapya wa Kagame kwa ajili ya kumkabidhi kombe hilo ambapo aliwapongeza. Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Kikwete aliwataka kuhakikisha kuwa wanaulinda ubingwa huo kwa kuhakikisha wanashinda kombe hilo la Kagame mara tatu mfululizo, ili iweze kulifanya kombe hilo mali ya klabu hiyo na Tanzania. “Nimefurahi sana kusikia mmeshinda kombe hili, mmetutoa mchanga wa macho kwa maana Watanzania wanapenda mchezo wa soka, lakini mchezo wenyewe hauwapendi. “Changamoto yangu kwenu ni kwamba, sasa twende zaidi ya Afrika Mashariki hapa tumefanya vizuri, tumecheza mechi zote bila kufungwa hata bao moja. Hii safi Sasa twende mbele kwenye ubingwa wa Afrika na tucheze michuano ya ubingwa huo siyo kwa nia ya kufikia fainali bali kushinda Kombe la Ubingwa wa Afrika. Na tunaweza. “Tuna ukame wa vikombe katika nchi yetu, kila tunaposhindwa kazi yetu imekuwa ni kutunga hadithi na maelezo ya kusingizia kwanini tumeshindwa, kazi yetu ni kutafuta watu wa kuwalaumu, mara atakuwa huyo mara yule tunatafuta mchawi tu, ifike wakati Watanzania waondokane na tabia ya kutunga hadithi na maelezo marefu na visingizio vya kushindwa kwa timu zetu katika michuano ya kimataifa,” alisema. Rais huyo mpenda michezo, alieleza kuwa anafurahi kuona Azam imeendelea kuwa kama ilivyoanza, kwasababu moja ya mambo makubwa yanayoua timu zetu nchini ni timu kujifanya kivuli cha timu zetu kubwa Simba na Yanga, kwani ukishakuwa kivuli cha timu kubwa basi huwezi hata kuifung ahiyo timu ambayo unajifanya kivuli chake. Hata hivyo, Kikwete alitoa rai kwa timu hiyo kuendelea na moyo wa kujituma na kufanya vizuri kwenye soka. Azam FC ilitwaa ubingwa wa Kagame kwa kuitandika Gor Mahia ya Kenya bao 2-0 katika mchezo wa fainali wa michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja waTaifa jijini Dar es Salaam.
2michezo
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa adhabu kwa wachezaji wawili wa klabu za Simba Jonas Mkude na Yanga Bernard Morrison kutokana na makosa mbalimbali waliyotenda kwenye michezo iliyopita kwenye ligi kuu bara. Wachezaji wote wawili wamepewa adhabu ya kutocheza michezo miwili na kupigwa faini ya shilingi Laki Tano kila mmoja. Kilichopelekea Mkude kupata adhabu hiyo ni kitendo alichokifanya kwenye mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Biashara United kwa kumpiga kiwiko  mchezaji wa Biashara United kwenye mchezo ulipigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Kwa Upande wa Morrison yeye amepata adhabu hiyo baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prison kwenye mchezo wa Ligi kuu bara.
2michezo
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kuondoka leo kwenda Misri ikiwa na wachezaji 32, huku ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon 2019.Kabla ya kuanza kwa fainali hizo Juni 21, mwaka huu nchini humo, timu hiyo itaweka kambi ya wiki mbili na kucheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu dhidi ya Misri na Zimbabwe au Nigeria. Akizungumza jana wakati anakabidhiwa bendera na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta alisema wanaenda kupambana ili kuleta sifa kwa Tanzania.“Kwa niaba ya wachezaji tunashukuru kwa kuwa nasi hapa na kututakia heri, nafikiri haya ni mashindano makubwa kila mmoja anafahamu, tunaenda kupambana kuleta kitu kitakachoipa sifa serikali hii ya Rais John Magufuli, na tunawaomba muendelee kuwa nasi bega kwa bega kipindi chote cha mashindano,”alisema.Kocha Mkuu Emmanuel Amunike alisema wanaenda Misri wakiwa na malengo ya kufanya vizuri na kwamba anaamini kujituma kwa wachezaji wake kunaweza kubadilisha historia nyingine, kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea.“Tangu tumeanza safari hii Agosti mwaka jana hadi hapa tulipofika kumetokana na juhudi za wachezaji, leo tunaenda Misri tukiwa na ahadi na malengo ya kufanya vizuri, lolote linawezekana kama ambavyo baada ya miaka 39 imetokea,” alisema. Alisema watu wa Tanzania wanastahili kuona mafanikio zaidi kwa sababu kuna wachezaji wengi wenye vipaji. Kocha huyo alimshukuru Waziri Shonza kwa kuwatembelea akisema kuwa wamefurahi ujio wake kwa kuwa umewapa hamasa kama timu.Awali, Shonza aliwatakia heri wachezaji hao na kusema kuwa ana matumaini watafanya vizuri na kurudi na ushindi. Alisema macho ya Watanzania yapo kwao hivyo, waende wakapambane, waoneshe nidhamu na kushikamana ili kuandika historia nyingine nzuri. “Twende Misri tukashinde na serikali ya awamu ya tano iko pamoja nanyi, tunaomba msituangushe bali mkawe wazalendo mkapigane kufa au kupona kupata matokeo mazuri,”alisema.
2michezo
LOS ANGELES, Marekani RAPA Snoop Dogg huwa hajiulizi mara mbili anapotaka kufanya alichoamua. Iko hivi, juzi alianika majina ya mastaa wanaotumia dawa za kulevya aina ya bangi, orodha ambayo pia inawahusisha walioaga dunia. Alichokifanya mkali huyo wa muziki wa Hip Hop ni kutaja miezi yote 12, kila mmoja ukiwa na jina la staa mvutaji bangi. Mfano, kwa shabiki wake aliyezaliwa Januari, Snopp alisema amekuja duniani siku moja na Bob Marley aliyekuwa mvutaji bangi. Kwa mujibu wa orodha ya Februari, aliyezaliwa Februari, alikuja na mvutaji bangi mwingine aitwaye Rihanna.
4burudani
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo anatarajiwa kuwa Shahidi wa kwanza katika kesi namba 351 ya mwaka jana inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mke wake Neema Lema. Mbele ya Hakimu Nestory Barro wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, katika kesi hiyo ya uchochezi Lema na mkewe wanadaiwa kutoa kauli za kukashifu dhidi ya Gambo ambapo leo watuhumiwa hao wamesomewa hoja za awali za shitaka linalowabili. Lema alikuwa akitetewa na Wakili John Mallya na Sheck Mfinanga,huku Serikali ikiwakilishwa na Wakili Alice Mtenga. Alice alidai Lema na mkewe walituma ujumbe mfupi wa sms, “Karibu tutakudhibiti kama uarabuni wanavyodhibiti mashoga”, ujumbe unaodaiwa wa kumuudhi na kumuumiza Gambo. Baada ya kusomewa hoja hizo watuhumiwa hao walikana kutenda kosa hilo ambapo pia Wakili Mallya alitoa notisi ya pingamizi la mdomo la kuipinga hati ya mashitaka iliyowashitaki watuhumiwa hao kutokana na kuwa na mapungufu ya kisheria na kuwa baadaye wataiomba Mahakama iitupilie mbali hati hiyo. Hakimu Barro aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 3 mwaka huu,hoja za pingamizi hilo zitakapowasilishwa kwa njia ya mdomo.
1kitaifa
Mara kwa mara busu na kupigana pambaja ni jambo ambalo huchukuliwa kuwa la kawaida kati ya wapendanao, lakini je umewahi kufiria kuhusu faida zake za kiafya. Nam, si siri tena, kubusiana kuna faida chungu nzima, kando na kuwa ishara ya mapenzi. Hizi ni baadhi ya faidi za kubusiana: 1. Huamsha homoni za furaha Kubusu kunaamsha akili ili kutoa kemikali kadhaa ambazo huutekenya mwili na kuuacha ukiwa umechangamka kwa furaha. Kemikali hizi ni pamoja na Oxytocinm Dopamine na Serotonin, kemikali hizi ni muhimu katika kuichangamsha mwili na akili kwa jumla. 2.Kuimarisha uhusiano Kemikali ya Oxytocin inafanya kazi muhimu ya kuimarisha uhusiano kati ya wapenzi. kemikali hii hutolewa na akili wakati wa kubusiana. 3.Huondoa msongo wa moyo Imebainika kuwa busu ni njia muhimu katika kupunguza msongo wa moyo. Kando na kubusu, ni vyema kumkumbatia na kumwambia mpenzi maneno matamu wakati wa kumbusu ili kuondoa kabisa msongo wa moyo. 4.Kupunguza shinikizo la damu Kubusu kunaimarisha mpigo wa moyo na hivyo kusaidia katika kuongeza kasi ya damu mwilini. Kasi ya damu mwilini inapoimarika nalo shinikizo la damu linapunguka. 5.Kupunguza uchungu wa hedhi Imebainika kuwa mwanadada ambaye hubusu mara kwa mara hawi na uchungu wakati wa hedhi ama kwa wengine hupunguka kabisa. Hii ni kwa sababu damu hupata urahisi wa kuteremka katika mishipa. 6.Huimarisha kinga ya mwili Utafiti uliofanyika 2004 ulibaini kuwa wapenzi ambao hubusiana mara kwa mara huwa na homoni moja katika mate yao. Hii husadia katika kuimarisha kinga ya mwili maana mwili unakuwa tayari kwa kemikali zisizo zake. Kilicho muhimu ni kuwa kubusu kuna faida kubwa pasi kuzingatia anayebusiwa wala wa kubusu. Kubusu kunaleta msisimko wa aina yake ambao husaidia katika kuuchangamsha mwili.
4burudani
“Tutatumia nafasi hiyo kumuombea Rais ili aweze kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa na Watanzania kuongoza Taifa letu ili aweze kufanikiwa,” alisema Askofu Malassy.Pia Askofu Malassy ameongeza kuwa watatumia mkesha huo kumshukuru Mungu kwa kuijalia Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, kumuombea Rais afya njema na utendaji mzuri anaoendelea kuufanya kwa maendeleo ya Taifa kwa kuwa mara zote amesisitiza kufanyiwa maombi na Watanzania.Aidha Askofu Mallassy amewataka wananchi wote kutumia siku hiyo kumuomba na kumshukuru Mungu kwa amani iliyopo nchini kwa vile ndio msingi mkubwa wa shughuli za kila siku zinazosaidia kupata kipato na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.Naye Mchungaji Olivia Mallonga alisema kwamba wao kama wadau wanaendeleza desturi ya kuliombea Taifa amani ili lisije kutumbukia kwenye machafuko kama nchi nyingine.“Watanzania wana dini ndio maana wanatumia imani zao kufanya maombi ili Mungu awalinde na maovu au machafuko yanayoweza kutokea kutokana na sababu yoyote,” alisema Mchungaji Olivia.
2michezo
Vijana hao wa Shime leo wanashuka dimbani kucheza na wenyeji India baada ya Jumapili kutoka sare ya 1-1 na Marekani.Shime alitamba kikosi chake kuwafunga India, wenyeji wa michuano hiyo inayofanyika ili kuipa baraka India kabla ya fainali za Kombe la Dunia kwa vijana mwaka kesho.Katika mchezo wa Jumapili, Marekani ndio waliotangulia kufunga bao dakika ya tano lililowekwa kimiani na Jean Julien wakati bao la kusawazisha la Serengeti lilifungwa na Mohammed Abdallah katika dakika ya 16.Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo maalumu, Serengeti Boys watacheza na Korea Kusini Alhamisi ya Mei 19 kabla ya kumalizia kwa kukipiga na Malaysia siku mbili baadaye. Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25.
2michezo
BARCELONA, HISPANIA NGULI wa soka wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, Ronaldinho Gaucho, ameweka wazi kwamba, atakuwa na furaha sana endapo staa wa taifa hilo Neymar, atarudi katika klabu yake hiyo ya zamani. Neymar alikuwa katika klabu ya Barcelona kwa kipindi cha miaka minne kabla ya mwaka jana kujiunga na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 198, alidaiwa kuondoka Barcelona kutokana na kushindwa kutamba mbele ya Lionel Messi. Hata hivyo Neymar amekuwa na mchango mkubwa ndani ya PSG tangu alipojiunga japokuwa alikuwa majeruhi, lakini kumekuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo anataka kurudi kucheza soka la nchini Hispania hasa klabu ya Real Madrid. Kutokana na taarifa hizo, Ronaldinho amedai kwamba, atakuwa na furaha sana endapo atamuona nyota huyo akirudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona kuliko Real Madrid. “Kitu muhimu kwa Neymar ni furaha. Napenda kumuona rafiki yangu akiwa na furaha, lakini kwa upande wangu nitakuwa na furaha zaidi endapo nitamuona mchezaji huyo akirudi Barcelona. Hata hivyo sina uhakika kama jambo hilo linaweza kutokea,” alisema Ronaldinho.
2michezo
Na JUDITH NYANGE SERIKALI imeombwa kutoa elimu ya namna ya kujiokoa kwa abiria wanaotumia usafiri wa majini   kuepusha vifo vya watu wengi kama ilivyokuwa katika ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea Mei 21, mwaka 1996. Mmoja wa watu walionusurika katika ajali hiyo,   Charles Limbu, alikuwa akizungumza  wakati wa kumbukumbu ya miaka 21 tangu kutokea kwa ajali hiyo, zilizofanyika juzi katika makaburi ya Igoma wilayani Nyamagana jijini Mwanza. Alisema ni wakati sasa serikali kuhakisha elimu   na vifaa vya kujiokoa vinakuwepo katika vyombo vyote vya usafiri wa majini. “Abiria wengi hawafahamu namna ya kutumia maboya na vifaa vingine vya kujiokoa vilivyopo katika vyombo vya usafiri wa majini. “Ni vema serikali ikahimiza na kuhakikisha wasafiri wanapatiwa elimu ya kutumia vifaa hivyo vya kujiokoa  kupunguza madhara  inapotokea ajali. “Katika ajali ya MV Bukoba wengi tuliopona ni kwa sababu tuliweza kuzingatia elimu tuliyopatiwa wakati tunaanza safari. “Nilipoona meli imeanza kupoteza uelekeo nilikimbia  kuchukua boya ambalo lilinisaidia  kujiokoa, laiti kama abiria wote wangekuwa wanafahamu  namna ya kutumia vifaa hiyo kusingetokea vifo vya watu wengi,” alisema Limbu. Limbu aliitaka serikali kuhakikisha vifaa hivyo vinakuwapo sehemu za wazi ambako abiria wote wanaweza kuvifikia na  kwa idadi sawa kulingana na uwezo wa chombo husika.     Kiliphece Herman ambaye pia alinusurika katika ajali hiyo, alisema chanzo cha ajali hiyo ni  umasikini wa kutumia kifaa chakavu kusafirishia abiria, ujinga wa jamii na viongozi wanaowajibika kusimamia usafiri   na uzembe kwa wanaopewa jukumu la kuendesha na kusimamia vyombo hivyo. “Bila mambo hayo kutatuliwa ajali za mara kwa mara zitaendelea kutikoea, nawashauri viongozi wa  serikali  kuichukua jukumu la kupunguza umaskini na kuhakikisha vinakuwapo vifaa bora vya usafiri. “Kuondoa ujinga kwa walio na jukumu  na mamlaka zinazohusika kusimamia vyombo vya usafiri hasa wa majini na kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kufanya uzembe kwa kukiuka na kuvunja sheria zilizopo,” alisema Herman. Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSC), Eric Hamissi, aliwataka wananchi kuacha kuwa na hofu. Aliwashauri  wasione baada ya ajali hamna usalama wa usafiri wa majini kwa sababu  baada ya tukio hilo zilichukuliwa  hatua kubwa za kuhakikisha halijirudii na usalama wa abiria  katika meli zao unazingatiwa kwa kiwango cha juu. Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema serikali ipo mbioni kununua meli mpya kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri ndani ya Ziwa Victoria pamoja na kuzifanyia marekebisho na ukaguzi wa mara kwa mara  kuhakikisha usalama wa abiria wakati wote. “Kila  mtanzania kwa imani yake aendelea kuwaombea marehemu wote waliotangulia mbele ya haki na  wote wenye jukumu na dhamana ya suala la usafirishaji. “Kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake katika eneo lake ili kukomesha kabisa matukio ya ajali,”  alisema Mongella. Tukio hilo kubwa la historia la kuzama kwa meli  ya MV Bukoba  lilitokea alfajiri ya Mei 21, mwaka 1996 zikiwa zimebaki kilometa 56   kufika Bandari ya Mwanza. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 800  ambako watano kati yao  walitambulika na familia zao na 130 waliweza kuokolewa.
1kitaifa
MKUTANO wa 13 wa Baraza la tisa la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza Jumatano ambapo jumla ya miswada miwili itasomwa kwa mara ya kwanza huku maswali na majibu 146 yakiulizwa na kujibiwa na mawaziri husika wa wizara.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Raya Issa Mselem alisema marekebisho ya sheria mbalimbali za mwaka 2018 na mambo mengine yanayohusiana na hayo yatajadiliwa.Aidha Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Wakala wa Serikali wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo pamoja na mambo mengine utasomwa. “Kwa mujibu wa ratiba yetu ya kikao cha wiki mbili cha Baraza la Wawakilishi tutakuwa na miswada miwili pamoja na maswali na majibu 146,” alisema.Aidha alisema ripoti za kamati za kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa mwaka 2018-2019 zitawasilishwa na wenyeviti wa kamati hizo. Aidha katika kikao hicho mwelekeo wa Mpango wa Taifa wa Uchumi utawasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Mohamed.Katika kikao hicho kamati teule ya kuchunguza majengo ya shule 19 za sekondari zilizojengwa Unguja na Pemba itawasilisha ripoti yake mbele ya wajumbe. Wajumbe katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichopita waliibana serikali na kulitaka Baraza kuchunguza mradi wa ujenzi wa shule 19 zilizojengwa chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ambapo baadhi ya majengo inadaiwa yamejengwa chini ya kiwango.
1kitaifa
Hatimaye Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu leo ameonekana hadharani katika baadhi ya picha zilizotumwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Katika picha hizo, Lissu anaonekana amenawiri na akiwa na afya njema na tabasamu huku akipunga mkono kama ishara ya kusalimia akiwa na watu mbalimbali na nyingine akiwa peke yake amekaa katika kiti cha magurudumu (wheelchair) na nyingine akiwa amelala kitandani. Jana akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa picha na video zinazomuonyesha Lissu alivyo sasa baada ya kupigwa risasi na matibabu anayoendelea nayo nchini Kenya. Lissu ambaye alipigwa risasi Septemba 7, mwaka huu mkoani Dodoma na watu wasiojulikana, amekuwa jijini kwa zaidi ya siku 40 akitibiwa majeraha ya risasi alizopigwa ambapo amefanyiwa upasuaji mara 17 na anatarajiwa kupelekwa nje kwa matibabu zaidi mwishoni mwa mwezi huu.
1kitaifa
Editha Karlo – Kibondo SHIRIKA la Madaktari wasiyokuwa na Mipaka la Umoja wa Mataifa (MSF), linalotoa huduma katika makambi ya wakimbizi ya Nduta na Mtendeli mkoani Kigoma,  limejipanga kupambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa corona ili kuhakikisha havisambai. Mratibu wa shirika hilo ofisi ya Kigoma, Maclle Homme aliyasema hayo jana, wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi wilayani Kibondo. Alisema wanayo timu ya dharula iliyopewa mafunzo maalumu, iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa ebora,sasa iko tayari kwa ajili ya kudhibiti corona ‘’Wote tunafahamu hali halisi inayoikabili dunia, virusi vya corona,tunaendeleza nguvu huko na tuko tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kusaidia kuzuia maambukizi kuanzia kwa wakimbizi na jamii inayozunguka maeneo haya,”alisema baadhi ya wadau wengine Shirika la Chakula Duniani (WFP), lililowakilishwa na Said Johari,na Oxfam Josephat Joseph ambao nao wanahudumia wakimbizi, walisema wanafanya kazi kuhakikisha wakimbizi wanafuata maelekezo yote ya wataalamu wa afya, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kutosalimiana kwa kushikana mikono na mikusanyiko yasiyokuwa yalazima  ambayo yanaweza kusababisha maambukizi “Tunagawa chakula cha zaidi ya siku 30 kwa wakimbizi ili kupunguza makusanyiko ya mara kwa mara kwa wakimbizi maana awali walikuwa wanapewa kwa siku saba, tumewagawa katika makundi wanaopokea jioni  na wengine asubuhi ili kupunguza muda wa kuwa pamoja na muda mrefu na tunataraji kutoa chakula cha zaidi ya muda huo ili wakimbizi wakae pamoja kwa muda mrefu ili yasije yakatokea maambukizi,’’ alisema Saidi Ofisa Afya Wilaya ya Kibondo, Steven Janks alisema kamati ya dharula ya wilaya imejipanga kuhakikisha ndoa zote zitakazofanyika kipindi hizi lazima zitolewe taarifa kwa kuombewa kibali kabla ya kufungwa ili wataalamu watoe ushauri na haitafungwa ndoa itakayokusanya idadi kubwa ya watu  na sherehe zote zifanyike nje ya kumbi na kwa kuzingatia umbali kati ya mtu na mwenzake mita mija na nusu hadi mbili Alisema sasa wanawapima joto abiria wote wanaoshuka  kwenye mabasi kituo cha Kibondo ili kuhakikisha maambukizi yanazuiliwa kuingia. Mkuu wa Wilaya hiyo, Luisi Bura alisema ni vizuri kuwapo uzingatiaji na utekelezaji wa kila kinacho amriwa akisisitiza watu wanaohitaji kufunga ndoa na  sherehe zingine kuhakikisha wanaomba kibali toka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kibondo ili wataalamu wa afya wahusishwe na kushauri ili kutotoa mianya ya kuwepo maambukizi
1kitaifa
RAMADHAN HASSAN-DODOMA VIONGOZI  wa umma 11,330, sawa na asilimia 83 hadi kufikia Desemba 20M mwaka huu  hawajarejesha tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma kwa Kamishna wa Maadili. Hayo yalielezwa hapa jana na  Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Harold Nsekela wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa tathmini ya   hali ya urejeshaji wa tamko la rasilimali na madeni ya viongozi wa umma. Alisema hadi Desemba 20, mwaka huu, tathmini inaonesha  hali ya urejeshaji mpaka sasa si nzuri. Alisema   kati ya viongozi wa umma 13,699, wanaotakiwa kuwasilisha tamko, 2,369 sawa na asilimia 17 ndio waliowasilisha matamko yao.  “Kwa maoni yangu, kama hali itabaki hivi mpaka Desemba 31, haitaleta taswira nzuri  hasa ukizingatia kwamba nchi yetu  inafuata misingi ya utawala bora,unaohimiza ,uwazi na uwajibikaji sambamba na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu,”alisema. Alisema viongozi wa umma kushindwa kuwasilisha tamko, ni kosa chini ya kifungo cha 15 (a),aliwatahadharisha viongozi ambao watashindwa kutekeleza matakwa hayo kuwa Sekretariet ya Maadili haitasita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kupelekwa kwenye Baraza la maadili. Alipoulizwa ni viongozi wangapi wamewapelekwa kwenye Baraza la Maadili mpaka sasa “Ukikiuka maadili sisi hatuendi kwenye mahakama za kawaida, tuna utaratibu wetu unaishia katika Baraza la Maadili,kuna  hatua kama mbili hivi kabla ya kufikia kwenye baraza. “Kuna mwingiliano, ila makosa ya kimaadili ukikiuka, tuna utaratibu wetu chini ya sheria yetu tunaweza tukakupeleka kwenye baraza la maadili na faini ni milioni moja mpaka 5. Alisema uvunjaji wa maadili ndiyo chanzo cha makosa makubwa ambayo yanatokea.  “Hatupendelei unaweza ukaonywa tukazungumza yakaishia hapo hapo kwa sababu unapelekwa huko ili iweje,kama kurejesha fomu lazima tukupeleke baraza la maadili kama hutatoa taarifa za kuridhisha,”alisema Kamishna huyo. Aliwahimiza viongozi ambao bado hawajawasilisha matamko yao kutumia vizuri muda uliobaki kutekeleza matakwa hayo ya kisheria na hakutakuwa na muda wa nyongeza  wa kuwasilisha nje ya muda huo. “Napenda ieleweke wazi,sheria ya maadili ya viongozi wa umma haiwataki tu viongozi wa umma kuwasilisha matamko yao ya rasilimali na madeni, bali kutoa taarifa za kweli ndani ya matamko yao,”alisema. Alipoulizwa kuhusu mafisadi waliopelekwa mahakamani pamoja na wala rushwa sheria ya maadili inasema,Nsekela alisema sheria hawairuhusu  kuwashughulikia watu wa namna hiyo. “Sasa ukikutwa kwa kosa la ufisadi humu kwetu halimo kwenye sheria hii, kwahiyo sisi hatuwezi kukushughulikia kwani suala la  ulaji wa rushwa halipo huku kwetu “Ni kweli inawezekana kunatokea kukiukwa maadili mfano kupokea zawadi kwa sisi viongozi sio kosa ila ni ukiukwaji wa maadili ukipokea zawadi zaidi ya shilingi  200,000 unatakiwa umweleze mkuu wako wa kazi kwamba nimepokea zawadi ya shilingi 200,000.
1kitaifa
Upendo Mosha, Moshi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Zefrin Lubuva asilipwe mshahara wa Februari hadi atakapojirekebisha. Hatua hiyo imekuja baada ya Mghwira kukasirishwa na kitendo cha mkurugenzi huyo kushindwa kujibu maswali aliyomuuliza kwanini halmashauri hiyo imeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu. Sakata hilo limetokea leo Ijumaa Februari 14, katika kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya mkoa cha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika leo. “Mkurugenzi wa Mwanga kila wakati umekuwa ukishindwa kujibu maswali vile inavyopaswa sijajua ni nani anakulipa mshahara, ila mamlaka inayohusika kukulipa isikulipe mshara wa mwezi huu,” amesema.
1kitaifa
WASHINGTON, MAREKANI MTOTO wa kike wa rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan amesemavhakuna la kujitetea  kutokana na kauli aliyoitoa baba yake mwaka 1971 katika mazungumzo ya simu akiuelezea ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kama “tumbili”. Mkanda mpya wa sauti ndio uliofichua kuwa  Reagan akisema hayo wakati huo akiwa Gavana wa California. Binti yake,  Patti Davis amelaani vikali katika waraka wake uliochapishwa katika gazeti. “Hakuna la kujitetea ,hakuna ufafanuzi wa maelezo, hakuna ufafanuzi mzuri juu ya kile ambacho baba yangu alikisema ,” aliandika. Davis aliandika katika waraka kwa ajili ya gazeti la Washington Post kwamba alikuwa anajiandaa kumtetea baba yake kabla ya kusikia kanda ya sauti, lakini alishituka baada ya kusikia kile alichokisema rais huyo wa zamani. “Siwezi kuwaambia kuhusu mwanaume aliyekuwa akiongea kwa simu…si mwanaume niliyemfahamu mimi,” aliandika Sauti iliyorekodiwa hivi karibuni ilionekana kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Atlantic. Reagan alitoa kauli katika mazungumzo na rais wa Marekani aliyekuwa madarakani wakati huo  Rais Richard Nixon. Ronald Reagan aliuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kama ”tumbili” Alikuwa akiuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa(UN), ambao walikuwa upande wa wapinzani wa Marekani katika kura dhidi ya kuitambua Uchina na kuiondoa Taiwan katika Umoja wa Mataifa. Reagan – ambaye alikuwa anaiunga mkono Taiwan – alimpigia simu rais siku iliyofuata akimwambia : “Aaangalie hao … tumbili kutoka hizo nchi Afrika – ambao bado hawafurahii kuvaa viatu,”. Nixon anasikika kwenye mkanda huo akiangua kicheko kwa sauti kubwa baada ya kauli hiyo. Ronald Reagan alikuwa rais wa Marekani kuanzia mwaka 1981 hadi 1989 Yeye mwenyewe pamoja na kuwaita Watanzania tumbili aliwahi kuandika jinsi alivyopambana dhidi ya ubaguzi alipocheza soka ya chuoni na baadae alipoingia madarakani alipopewa uanachama wa klabu ya taifa ya ritzy mjini Los Angeles ambayo aliikataa kwasababu haikuwaruhusu Wayahudi au Wamarekani wenye asili ya Afrika. Binti yake aliandika kuwa maneno aliyoyasikia “Yatabaki nami daima, ” na  akaongeza kuwa kama baba yake angekuwa bado hai “angeomba msamaha ” kama angesikia sauti yake iliyorekodiwa kwa sababu  haiwezi kueleweka kwa maneno mengine isipokuwa ubaya. Aliongeza kuwa anatumaini watu watamsamehe rais huyo wa zamani wa marekani “kwa maneno ambayo hayangepaswa kutamkwa katika mazungumzo yoyote yale. Wakosoaji wanamshutumu Reagan kuwa mbaguzi wa rangi katika kipindi chake chote cha maisha ya kazi. Alipokuwa akigombea kiti cha ugavana wa California mwaka 1966, mchezaji huyo wa zamani wa filamu alisema “kama mtu binafsi anataka kuwabagua waniga (Negroes) au wengine katika kuuza au kukodisha nyumba, ni haki yake kufanya hivyo “. Hata hivyo Reagan alikanusha shutuma za ubaguzi wa rangi dhidi yake.
3kimataifa
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepokea shehena ya dawa, vifaa na vifaa tiba kutoka serikali ya India, zikiwemo dawa za kuzuia kifafa kwa wajawazito, chanjo ya homa ya ini na za matibabu ya saratani.Dawa hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni mbili zenye lengo la kuongeza nguvu katika kuimarisha sekta ya afya zitasambazwa nchini kote haraka.Alisema atahakikisha dawa hizo ambazo asilimia kubwa ni dawa muhimu, ikiwemo ya kuzuia kifafa kwa wajawazito, chanjo ya homa ya ini na dawa kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wa saratani, zinasambazwa haraka katika vituo vilivyokusudiwa kwa mfumo wa maoteo. Ummy alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa miongoni mwa dawa ambazo zimetolewa na serikali ya India ni Amoxline kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya bakteria kwa watoto ambazo ni dozi 19,800.“Dawa nyingine ni dozi 3,000 za kuzuia wanawake kuvuja damu nyingi muda mfupi baada ya kujifungua na dozi 3,000 za kutibu kifafa cha mimba ambazo tutahakikisha shehena hii ya dawa muhimu zinasambazwa haraka ili kupanua wigo wa upatikanaji wa dawa nchini,” alisema. Alisema dawa hizo ni msaada, hivyo zitatolewa bure katika hospitali za karibu ili ziweze kutumiwa mapewa kwa sababu ni nyingi na baadhi zina miaka miwili kumaliza matumizi yake.Alisema ameelekeza kwa upande wa dawa za chanjo ya homa ya ini, zitumike kukinga watoa huduma za afya na madaktari ambao wapo katika hatari kubwa ya maambukizi. “Watoa huduma wetu ndio wenye changamoto kubwa ya kuugua homa ya ini kwa kuwa wanakutana na kutoa huduma kwa wagonjwa wakiwa hawana kinga hivyo naelekeza dawa hizo zitumike kwao na tutahakikisha wanapata chanjo ya pili hadi kumaliza dozi,” alisema.
1kitaifa
Aliyekuwa beki wa kati wa KMC, Ally Ahmed Ally amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC. Ally ametambulishwa leo makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam baada ya kusaini mkataba huo akitokea KMC ya Kinondoni aliyoichezea kwa msimu mmoja akitokea Mwadui FC ya Shinyanga. Ally anakuwa mchezaji mpya wa tisa kusajiliwa Yanga SC na wa pili tu mzawa baada ya kiungo wa ulinzi, Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar. Wengine saba wote ni wa kigeni, Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana), Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia. Yanga SC imedhamiria kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, baada ya misimu miwili ya kuzidiwa kete na mahasimu wao, Simba SC. Baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu mfululizo 2015, 2016 na 2017, Yanga SC wakapokonywa taji hilo na Simba SC 2018 ambao wamefanikiwa kulitetea 2018.
2michezo
SAM  BAHARI – SHINYANGA. WADAU wa elimu Mkoa wa Shinyanga wamekemea  tabia ya wanafunzi wa kike wanaosoma shule za msingi na sekondari  kuwatongoza wavulana kwa lugha ya kuvutia na  yenye  kushawishi  kushiriki vitendo vya mapenzi. Licha ya kuibuka tabia hiyo, wadau wameiomba Serikali kupitia upya sheria inayosimamia  wanafunzi  wa kike wanaopewa mimba na kukatisha masomo yao. Akizungumza wakati wa kikao cha kutangaza matokeo ya darasa la saba juzi,  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba alisema imebainika wanafunzi wa kike kipindi hiki wameanza  kuwatongoza  wavulana na kufanya ngono  isiyo salama na mwisho wa siku hupata ujauzito. Alisema wasichana  kuamua kubadilika tabia na kuanza kuwatongoza  wavulani, ni kutokana na ulegevu wa sheria inayotumika kwa watu wanaowapa mimba hukamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani tofauti na mtoto wa kike ambaye hubaki huru. “Sheria hii inayohusu wanafunzi wetu wa kike kupewa mimba, inatafasiri   mwanaume aliyempa mimba mwanafunzi akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili,  lakini mtoto wa kike anayetiwa mimba hubaki huru,”  alisema. Akitangaza  ufaulu wa matokeo ya mitihani wa darasa la saba, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albart  Msovela alisema kwa mara ya kwanza mkoa huo umeshika nafasi ya 17 kitaifa. Alisema mkoa uliandikisha watoto 40,292 kuanza darasa la kwanza mwaka 2013 na waliosajiliwa kufanya mtihani wa mwisho kuingia kidato cha kwanza mwaka 2020, ni 30,393 na waliofaulu ni 23,634 sawa na asilimia 77. 76.
1kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema dhamira ya serikali ya kudhibiti mifuko ya plastiki nchini ipo pale pale na kinachofanyika kwa sasa ni maandalizi na serikali haitoi vibali vipya vya utengenezaji wa mifuko hiyo katika kipindi hiki cha mpito.Alisema wale wenye mpango wa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya mifuko ya plastiki huko mbele wasije wakalalamika wamepata hasara itakapozuiwa kwa kuwa jambo hilo limeshaelezwa wazi.January aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowashirikisha wadau wa mazingira pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Joyce Msuya.“Kwa sasa tupo kwenye kipindi cha mpito cha tafakari...Hatua ambazo tunachukua ni kutafuta takwimu na kutengeneza mpango kukabiliana na changamoto za uzuiaji wa mifuko ya plastiki,” alisema January.Alisema kuzuia mifuko ya plastiki kunahitaji uratibu wa kitaasisi kwani hauwahusishi wao tu bali pia Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato (TRA), viwanja vya ndege, Serikali za Mitaa, Baraza la Taifa la Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na wadau wengine.“Tumezungumza na UNEP namna ambayo tunaweza kushirikiana nao kuhusu jambo ikiwemo ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi wa aina ya uchumi mpya unaoweza kuibuka wa mifuko mbadala,” alifafanua.Naibu Mkurugenzi wa UNEP, Msuya alisema changamoto tatu zinazoikabili sekta ya mazingira duniani ni mabadiliko ya tabianchi, ukataji wa miti hovyo pamoja na utupaji wa taka ngumu.Mshiriki wa mkutano huo, Maria Sarungi alipendekeza mikutano ya wadau wa mazingira kujadili changamoto ifanyike angalau mara nne kwa mwaka badala ya kusubiri maadhimisho siku ya mazingira.
1kitaifa
SHIRIKA la Habari la China, Xinhua na Kampuni ya Magazeti ya Serikali Daily News, Habari Leo (TSN), zimeaidi kudumisha ushirikano ikiwa ni pamoja na kuendeleza programu ya lugha ya Kiswahili kwa Wachina.Hayo yalisemwa jana na Mhariri wa HabariLeo, Nicodemas Ikonko wakati akimkaribisha Mhariri Mkuu wa Shirika la Habari la Xinhua ambaye pia ni mjumbe wa China Communist Part, Ping He walipotembelea kampuni ya TSN ikiwa ni mkakati wa kudumisha ushirikiano uliopo kati ya China na Tanzania.Ikonko alisema kwa kuwa China imetilia maanani kuendeleza uhusiano wa kirafiki na nchi za Kiafrika hususani Tanzania tangu kuasisiwa kwake, TSN ipo tayari kutoa mafunzo ya kiswahili kwa Xinhua kupitia gazeti la HabariLeo na mtandao wa Tsn Online kwa ajili ya kuzidisha mwingiliano na uelewano pamoja watu China na Tanzania.Alisema kwa kufanya hivyo anamini kutaweza kusaidia ufundishaji wa Kiswahili kupitia gazeti katika kukuza na kueneza Kiswahili nchini China. Mhariri wa Dailynews Pudensiana Temba alisema ushirikiano wa Tanzani na China ni wa muda mrefu ulioasisiwa na baba wa mataifa yote mawili ambao ni hayati Julius Nyerere na Mao Zedong.Alisema uhusiano huo umekua mzuri kwa fursa mbalimbali za maendeleo kwa pande zote mbili ambapo katika sekta ya habari TSN imekuwa ikishirikiana vyema na Xinhua pamoja na chombo kingine cha habari cha People’s Daily ambapo zaidi ya waandishi 20 walishakwenda kupata mafunzo ya muda mfupi na mrefu nchini China ikiwa ni pamoja na kubadilisha uzoefu.Aidha Temba aliushukuru pia ubalozi wa China nchini Tanzania ambao umekuwa ukitoa udhamini wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Tanzania. Kwa upande wa Mhariri Mkuu wa Xinhua Ping He alisema ni mara ya kwanza kutembelea TSN na kuahidi kudumisha uhusiano uliopo kwa kuwa vyombo vyote viwili vinamilikiwa na serikali na pia ni vyombo vikubwa kwenye nchi zote mbili.Alisema kwa sasa Xinhua inapatikana katika nchi 23 duniani Tanzania ikiwemo na kuhaidi kuipa ushirikiano TSN ili iweze kupiga hatua katika sekta ya habari. Kwa upande wa Kaimu Mhariri wa TSN Baraka Katemba alisema ujio huo wa Ping He na jopo lake utasaidia kukuza taaluma ya habari kwa pande zote mbili kwa kuwa lengo la ujio wao ni kukuza mahusiano kati ya China na Tanzania katika masuala ya vyombo vya habari . Wakati huo huo, ujumbe wa wafanyabishara 25, kutoka Kampuni 15 za Jimbo la Zhejiang China, utafanya ziara ya siku tatu nchini kusaka fursa za biashara.Ujumbe huo utakuwa na ziara kati ya Julai 20 hadi 23, mwaka huu na utafanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini. Taarifa kutoka kitengo cha Mawasiliano cha Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilisema kuwa ujumbe huo utaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Jimbo hilo, GE Huijun.Taarifa hiyo ilisema lengo la ziara hiyo ni kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini na inalenga kukuza mahusiano ya kiuchumi baina ya Jimbo la Zhejiang na Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile teknolojia, mawasiliano, ujenzi na uchukuzi, afya na madini.Tayari China na Tanzania zina mahusiano ya muda mrefu zaidi ya miaka 45 ambapo bidhaa mbalimbali zinaingizwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na vyakula, magari, nguo, bidhaa za viwandani, vipuri vya magari na mitambo, vifaa vya umeme na vile vya chuma wakati Tanzania inauza kwenda China vyakula vya baharini, ngozi mbichi, magogo, shaba, Mihogo na vifaa vya mbao.
1kitaifa
WAKATI Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Ettiene Ndayiragije akitarajiwa kutangaza kikosi chake leo baadhi ya wadau wamehimiza apewe muda ili timu ifanye vizuri.Juzi, Kamati ya Utendaji ya dharura ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ilikutana na kumtangaza Kocha huyo akichukua nafasi ya Emmanuel Amunike. Kazi ya kwanza ya Ndayiragije ni kushiriki mechi ya kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan, zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. TFF ilivunja mkataba na Amunike hivi karibuni baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Misri.Ndayiragije aliyejiunga na Azam FC msimu huu atasaidiana na makocha Seleman Matola wa Polisi Tanzania na Juma Mgunda wa Coastal Union. Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti baadhi ya wadau hao walisema makocha wote ni wazuri na wanahitaji muda kwani kufundisha klabu ni tofauti na timu ya taifa. “Ndayiragije ni kocha mzuri na ameonyesha uwezo hasa wa kuibua vijana wengi katika klabu tofauti. Anahitaji kupewa muda ili kuleta manufaa,” alisema mchambuzi wa soka nchini na mchezaji wa zamani Ally Mayay.Alisema kama taifa kunahitajika mipango ya muda mrefu na mfupi, hivyo, iwapo amechaguliwa awe wa muda mfupi huenda ikawa shida kwani wengi wanataka matokeo. Kwa upande wake kocha Kenny Mwaisabula ‘Mzazi’ alisema makocha hao wanahitaji kuungwa mkono ingawa tatizo kwa soka la Tanzania sio kwa kocha bali ni mfumo unaotakiwa kutengenezwa kwa muda mrefu.“Sio makocha wabaya wote ni wazuri cha msingi tuwaunge mkono ingawa wana mtihani mzito na kwamba kama watashinda itakuwa ni jambo la kheri lakini ikishindikana kuna haja ya serikali kushirikiana na TFF kuandaa vijana kwa ajili ya wakati ujao,”alisema.
2michezo
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeleta mtikisiko kwa vyama vya upinzani, hasa Chadema na ACT- Wazalendo ambavyo viongozi wake wametangaza kujiunga na chama hicho tawala. Vigogo hao kutoka upinzani, walitangaza uamuzi huo katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dk. John Magufuli. Waliotangaza kujiondoa Chadema ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Patrobas Katambi na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha. Kutoka ACT-Wazalendo ni aliyekuwa mshauri wa chama hicho ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, aliyekuwa Katibu Mkuu Samson Mwigamba, Mshauri wa Sheria, Albert Msando na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Edna Sunga. Akizungumza katika kikao hicho, Katambi alisema upinzani wa sasa umekuwa haujadili matatizo na kuyatafutia suluhu, bali unajadili mambo binafsi. “Leo hii nasaliti ubinafsi na umimi kwa kuamua kujiunga na CCM. Tunachosema jukwaani si kile tunachokiishi, upinzani umegubikwa na ubinafsi, umimi na makundi ya hapa na pale. “Kijana ndani ya upinzani ni karai linalojenga ghorofa. Karai huonekana takataka baada ya ghorofa kukamilika,” alisema Katambi. Naye Profesa Mkumbo alisema ameamua kujiunga CCM ili awe sehemu ya kuleta mapinduzi ya kiutawala, kisera, kiitikadi na ya wananchi. “CCM kina nguvu kubwa kwa sababu ni chama cha wanachama, watu wanakiogopa chama na si chama kuwaogopa watu. “Hata nasi tulijaribu kujenga misingi hii huko tulipokuwa upinzani, lakini tumeshindwa,” alisema Profesa Mkumbo. Kwa upande wake, Msando, alisema kuwa anajivunia kuwa mwana CCM. “CCM ni chama kinachoonyesha kuwajali watu, mimi kama kijana ninajivunia kuwa mwanachama wa CCM. “CCM kiliahidi kupambana na umasikini, kutengeneza ajira, kurudisha nidhamu na uwajibikaji. Tuna kila sababu ya kupongeza kwa haya mambo mazuri. “Nina imani sasa mnajenga chama na chini ya uongozi wa Rais Magufuli CCM mpya inapatikana. Sioni aibu kuwa CCM, kipindi cha nyuma mtu alikuwa anaogopa kusema yeye ni mwana CCM, lakini kwa sasa mtu anajivunia kwa sababu yaliyoahidiwa kwenye ilani yanatekelezwa kwa vitendo. “Chama kiliahidi kupambana na ufisadi na rushwa, lakini sasa hivi tunaona ni watu wa aina gani wanachuchumaa mahakamani, zamani ilikuwa unaweza ukapiga simu mtu akapewa dhamana hata saa 6 usiku, lakini siku hizi haiwezekani… nidhamu na uwajibikaji unarudi,” alisema Msando. Naye Masha alisema ameamua kurudi CCM kwa sababu ni nyumbani kwani alizaliwa ndani ya chama hicho. “Nilipohama nilimficha baba, alinipigia na kuniuliza nimefanya nini na mimi nilimuuliza wewe uko chama gani… akasema yeye alifukuzwa na mimi nimehama, hivi ni vitu viwili tofauti. “Nimekuja hapa kuwaombeni mnipokee mwana mpotevu nimerudi, niko imara na nitakuwa mwaminifu kwa chama na Serikali, ukinihitaji nitumie,” alisema Masha. Kwa upande wake, Sunga, alisema ameamua kujiunga na CCM kwa sababu ameona inapambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo. “CCM kina dhamira ya dhati ya kuirudisha Tanzania katika misingi yake, inapambana na dhuluma, wizi na unyonyaji,” alisema Sunga. Mwigamba alisema ameamua kujiuga na CCM ili kuijenga iendelee kudumu na kuwa imara na Serikali yake ifanye vizuri zaidi. “Tumechagua kutokuwa vuguvugu, tumeamua kuwa moto na wako watu ambao watadhani sisi ni wasaliti, lakini kadiri watakavyopiga kelele tutazidi kuwa wa moto zaidi,” alisema Mwigamba.  KAULI YA JPM Baada ya kupokewa kwa wanachama hao, Rais Magufuli alisema ni mfano mzuri wa Watanzania wanaojitambua, lakini akawatahadharisha wasije wakabadilika tena. “Wako watu wengi wanataka kuingia CCM, leo niliombwa karibu na watu 10 na wengine wamesafiri, lakini kuna wanachama wengine karibu 200 walikuwa viongozi katika mikoa mbalimbali wameamua kurudi CCM. “Nimeamua wakati mwingine mwafaka tutawakaribisha ili waje wajitambulishe rasmi. Mtembee kifua mbele ninyi ni wana CCM, niwaombe msibadilike tena, msije mkaingia huku kwa majaribio, msimame imara kukitetea chama… hata pakitokea nafasi ya kugombea ya chama ninyi mkagombee tu,” alisema.  SOPHIA SIMBA ARUDI KUNDINI Baada ya tukio hilo, Rais Magufuli, alitangaza kusamehewa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Sophia Simba. Machi 11, mwaka huu, wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dodoma, Sophia alifukuzwa uanachama kwa madai ya kukisaliti chama katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Hatua hiyo ilisababisha apoteze ubunge wa Viti Maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama. Katika kikao hicho, Rais Magufuli, alisoma barua ya Sophia ya kuomba radhi mbele ya wajumbe ambao waliridhia kwa kauli moja kumsamehe kigogo huyo. Rais Magufuli alisema kati ya wanachama wote waliofukuzwa, Sophia ndiye pekee aliyeandika barua mbili za kuomba radhi. “Katika wote tuliowafukuza na kuwapa adhabu, huyu (Sophia) ndiye aliandika barua ya kuomba radhi. Amekuwa akiandika barua za kuomba radhi na tumekuwa tukikaa kimya tunamwangalia wala hatumjibu chochote… lakini inaonekana mwenendo wake amekuwa kweli akiomba radhi. “Wengine wawili waliandika barua kukubaliana na maamuzi yaliyotolewa, lakini wengine walikaa kimya, sasa niliguswa na huyu ambaye aliomba radhi mara nyingi,” alisema. Rais Magufuli alisoma barua hiyo kisha akawauliza wajumbe kama wanaridhia Sophia asamehewe. “Sasa nimeona niwaulize wajumbe, mnasemaje tumrudishie uanachama, tumsamehe (wajumbe walinyoosha mikono na kusema asamehewe)… wanaosema sio waseme (hakuna mjumbe aliyesema). “Katibu Mkuu utamjulisha na mimi nitaandika hapa kwamba NEC imekusamehe,” alisema Rais Magufuli.  BARUA YA SOPHIA KWA JPM Sehemu ya barua ya kuomba msamaha iliyoandikwa na Sophia Machi 14, mwaka huu ilisomeka hivi: Mheshimiwa Mwenyekiti kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, niruhusu nichukue fursa hii kukuomba radhi wewe binafsi, wajumbe wa Kamati Kuu, wajumbe wa NEC na CCM kwa ujumla. Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naikubali adhabu niliyopewa na ambayo ilitolewa na vikao halali vya chama changu, nimeipokea kwa mikono mikunjufu kwani nimekukosea wewe Mwenyekiti wangu na nimekikosea chama changu. Naandika barua hii kuonyesha majuto yangu kwako na kwa chama changu, naandika barua hii kuomba mnisamehe kwa sababu maisha yangu yote kuanzia kwa wazazi wangu nimekuwa ndani ya TANU na CCM na kila kilichofanikiwa hapa duniani nimekipata kwa sababu ya CCM nikipendacho na kukithamini sana na bado naahidi na namuomba Mwenyezi Mungu anijalie niendelee kuwa mpenzi na mkereketwa wa CCM mpaka mwisho wa maisha yangu. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba radhi tena kwani mzigo huu ni mzito sana na sijui jinsi ya kuubeba, kwani hii ni adhabu yangu ya kwanza kupewa na chama changu, na ndiyo adhabu kubwa na ya mwisho, naomba mnihurumie na Mwenyezi Mungu anihurumie. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na yote hayo, napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa azma yako ya kuleta nidhamu ndani ya CCM, naamini sana katika chama kuzaliwa upya na katika mabadiliko makubwa ya uchumi wa viwanda, nidhamu na Serikali kwa ujumla. Naomba nimalize kwa kuomba radhi tena, nisamehe sana na naiomba huruma yako na ya chama changu. JPM ATAJA VIONGOZI WATAKAOBAKI CCM Akizungumza katika kikao hicho, Rais Magufuli, alisema viongozi watakaobaki katika chama hicho ni wale tu wenye imani thabiti na mapenzi mema na si CCM masilahi. Rais Magufuli alisema viongozi wa namna hiyo ndiyo watakaoweza kusimamia Serikali ipasavyo katika ngazi zote. “Tunahitaji viongozi wachapakazi, waaminifu, waadilifu, wenye kuchukizwa na rushwa, wanaochukia ubadhirifu wa mali za umma na za chama, wapole, wanyenyekevu, lakini wakali kwenye mambo ya ovyo. “Tunahitaji viongozi wanaoishi imani na ahadi za chama, wasiohongeka, lakini wanaokubalika kwa wanachama na wananchi, si kwa fedha zao bali kwa mienendo yao mema na maono waliyonayo. “Ukiwa kiongozi wa namna hii chama chetu kitakuwa imara na madhubuti zaidi na kitasimamia haki za wanachama na wananchi wote, hasa wanyonge. “Viongozi wa namna hii ndio watakaoweza kusimamia Serikali ipasavyo katika ngazi zote na hawa ndio aina ya viongozi ambao chama chetu kinaendelea kuwapata katika uchaguzi wa mwaka huu,” alisema. Alisema pia mageuzi yanayoendelea kufanywa na chama hicho yamekuwa mwiba mkali kwa wachache ambao walizoea maisha ya kidesturi yasiyoheshimu misingi ya chama. UCHAMBUZI WA MAJINA Rais Magufuli alisema wanachama 3,004 walijitokeza kugombea nafasi za uongozi wa mikoa na jumuiya za chama kitaifa wakati nafasi zinazohitajika ni 261. Alisema majina hayo yalichambuliwa kwa wiki mbili na kwamba kila jina lilichambuliwa pamoja na taarifa nyingine.  KIKAO KUFANYIKA IKULU Kuhusu kikao hicho kufanyika Ikulu, Rais Magufuli alisema: “Hapa Ikulu ni kwenu kwahiyo siwezi kuletwa hapa mimi na wana – CCM halafu niwazuie kuja ambako ni kwenu. Tembeeni kifua mbele mmepaandaa ninyi.” Awali Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 115 kati ya 119 kutoka mikoa 32 nchini.  BAVICHA WATOA NENO Akizungumzia na waandishi wa habari jana kuhusu kuondoka kwa wanachama wao na kujiunga na CCM, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick ole Sosopi, alisema kuwa huu si muda mwafaka wa kuwajadili na badala yake watawatumia ujumbe baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa madiwani. Alisema kwa sasa wana kazi kubwa ya kujipanga kuhakikisha wanapata madiwani wengi katika chaguzi zijazo. “Si muda mwafaka kwetu kuwajadili wanaokihama chama, ila tunaamini ni mradi wa chama tawala kuwaaminisha wananchi kama wamebadilika na wanakubalika na ndiyo maana wanawachukua viongozi wetu… “Historia ya siasa inaonyesha wazi wapo waliohama chama na mambo yakaendelea, hivyo tuna imani tutafaya vizuri zaidi ya sasa kwani tupo imara,” alisema Sosopi.
1kitaifa
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema wizara yake inaangalia namna bora ya kuimarisha soko la chumvi inayozalishwa nchini, yenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndani na ziada, kwa kuzuia ile inayoingizwa kutoka nchi za nje.Nyongo amesema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya kutembelea mgodi wa kuzalisha chumvi wa kampuni ya Stanley and Sons ulioanzishwa mwaka 1948/49 uliopo katika Kijiji cha Kitame wilayani humo.Akizungumzia uzalishaji chumvi, Nyongo ametoa mfano wa mgodi pekee wa Stanley kuwa huzalisha chumvi kati ya tani 4,000 hadi 6,000 kwa mwaka kulingana na hali ya hewa, licha ya kuwepo migodi mingi ya uzalishaji chumvi katika baadhi ya mikoa nchini ambapo mara nyingi wazalishaji wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa soko la chumvi wanayozalisha.Alitaja baadhi ya mikoa yenye migodi ya kuchimba na kuzalisha chumvi kuwa ni Pwani yenye zaidi ya mgodi mmoja, Kigoma eneo la Uvinza, Lindi na Mtwara.Amesema, chumvi ni bidhaa mtambuka inayotumika kama chakula, dawa na ni madini, hivyo aliwataka wachimbaji na wazalishaji wa chumvi kusindika chumvi hiyo katika ujazo tofauti na kwa bei nafuu ili kila mmoja aweze kununua kwa matumizi ya nyumbani, viwandani na kwa ajili ya mifugo.Mmoja wa wakurugenzi katika mgodi wa chumvi wa Kampuni ya Stanley and Sons, Richard Stanley ameiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara itakayorahisisha usafirishaji ya chumvi hiyo.
0uchumi
Akizungumza na gazeti hili, Meneja Mawasiliano wa GGM, Tenga B. Tenga alisema wamesikitishwa na hukumu iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kupitia Kamati ya Nidhamu ya shirikisho chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa.“Mgodi wa Geita Gold uliidhamini timu hii kama sehemu ya kuendeleza michezo na kwa vijana wanaouzunguka mgodi. Menejimenti ya Mgodi wa Geita Gold imesikitishwa na maamuzi ya Kamati ya Nidhamu,” alisema.Aliongeza kuwa, kutokana na maamuzi hayo ya TFF, uongozi wa GGM utajadili na kutoa maamuzi rasmi kuhusu udhamini huo na kama wataendelea kuidhamini klabu hiyo aliyosisitiza si mali ya mgodi, bali imesajiliwa kivyake na inajitegemea kuanzia uongozi hadi taratibu zake, isipokuwa udhamini tu.Kamati ya Nidhamu ilimkuta na hatia kocha msaidizi wa klabu ya Geita Gold, Choke Abeid na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu na kipa wa timu hiyo Dennis Richard amefungiwa miaka 10 pamoja na kulipa faini ya Sh milioni 10 huku timu hiyo ikishushwa hadi daraja la pili kwa madai ya kupanga matokeo.Geita ilidaiwa kupanga matokeo baada ya kuifunga JKT Kanembwa mabao 8-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma huku Polisi Tabora nao wakidaiwa kupanga matokeo katika mchezo wao dhidi ya JKT Oljoro, ambapo walishinda 7-0.
2michezo
NEW YORK, MAREKANI BAADA ya kukutwa na hatia ya kumshambulia shabiki wake nchini Sweden, rapa Rakim Mayers maarufu kwa jina la ASAP Rocky, ametangaza kusitisha ziara zake za muziki kwa kipindi hiki cha Julai kwa ajili ya kumaliza kesi yake. Wiki moja iliopita msanii huyo alikuwa nchini Sweden kwa ajili ya tamasha la muziki, lakini siku moja kabla ya tamasha hilo msanii huyo alikamatwa na polisi baada ya kumsukuma shabiki yake hadi kuanguka kwa madai hakutaka kupiga naye picha. Chanzo cha karibu na msanii huyo kimeweka wazi kuwa, Julai hii hatoweza kufanya chochote katika kazi zake za muziki hadi akimalizana na kesi yake ambayo inamkabili. Hata hivyo, hadi sasa msanii huyo anashikiliwa na polisi nchini Sweden kutokana na tukio hilo. Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wameaza kupaza sauti zao kutaka mamlaka yatoe maamuzi ili msanii huyo aweze kuwa huru na kazi zake.
4burudani
Na PENDO FUNDISHA, MBEYA MFANYABIASHARA maarufu jijini Mbeya, Steven Samweli maarufu kwa jina la Maranatha, ametiwa nguvuni akituhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Kutiwa nguvuni kwa mfanyabiashara huyo ni mwendelezo wa nia ya Serikali ya kupambana na biashara ya dawa hizo nchini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi juzi kwamba, Maranatha alikamatwa juzi usiku akiwa katika moja ya maduka yake ya dawa baridi. “Baada ya polisi kupata taarifa za mfanyabiashara huyo kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, tuliweka mtego na hatimaye kufanikiwa kumtia nguvuni. “Kwa sasa tunamshikilia kwa mahojiano na baada ya uchunguzi kukamilika, atafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Kidavashari. Pamoja na hayo, kamanda huyo wa polisi alisema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kunafikisha idadi ya watu wanane waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya mkoani Mbeya. “Miongoni mwa hawa tunaowashikilia, baadhi yao walikutwa na vielelezo, hivyo watafikishwa mahakamani wakati wowote wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. “Kwa hiyo, nawaomba wananchi mkoani hapa, waachane kabisa na biashara ya dawa hizo kwa sababu wakikutwa nazo, watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola,” alisema Kamanda Kidavashari.
1kitaifa
Mkoa wa Pwani umeahirisha maonesho ya viwanda yaliyopangwa kuanza Oktoba Mosi mwaka huu ili kutoa fursa kwa wadau wengi zaidi kushiriki.Mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo amewaeleza waandishi wa habari mjini Kibaha kuwa, maonesho hayo yataanza Oktoba 17 na kumalizika Oktoba 23 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM SabaSaba.Awali mkoa huo ulipanga kuwa na maonesho ya viwanda kwa wiki moja sanjari na Kongamano la Fursa na Biashara na Uwekezaji Oktoba tatu.“Tarehe kumi na tisa siku ya Jumamosi kama leo ndipo kutakuwa na kongamano la uwekezaji. Tumesukuma mbele kama wiki mbili baada ya tarehe 14 mwezi wa 10 ambapo Mwenge unazimwa Lindi na sisi kama mkoa tutashiriki kikamilifu kule tuwape nafasi wenzetu wa Lindi wafanikishe tukio hili kubwa”amesema.Ndikilo amesema tathmini iliyofanywa ya idadi ya washiriki wa maonesho hayo na kongamano hilo imeonesha kuwa idadi ya washiriki bado ni ndogo kulinganisha na matarajio.“Kwenye maonyesho ya viwanda tulitarajia kupata washiriki 400 lakini mpaka tarehe ya jana 27 waliokuwa wamethibitisha ni wenye viwanda 173” amesema.Ndikilo amesema wameshawafikia washiriki zaidi ya 400 kwenye mkoa wa Pwani na mikoa ya kanda ya mashariki ukiwemo wa Dar es Salaam, Tanga na Morogoro.Kiongozi huyo amesema, miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni wenye viwanda 53, wajasiriamali 100 na wenye viwanda vidogo 20, na kwamba, idadi ya waliothibitisha kushiriki ni chini ya 50% kulinganisha na matarajio.“Na waliokuwa wamethitisha kwenye kongamano la wawekezaji tulitarajia namba hiyo hiyo 400 lakini walikuwa kwenye mia moja hamsini, mia moja na sabini kati ya idadi ya 400 ambao tuliwatarajia”amesema.Kwa mujibu wa mhandisi Ndikilo, wakati wa kongamano Mkoa wa Pwani utazindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo hivyo wanatarajia watu wengi watafika kushuhudia tukio hilo kubwa.
0uchumi
Akizungumza na gazeti hili baada ya pambano hilo Majiha alisema maandalizi mazuri aliyofanya kwa muda mrefu yamemsaidia kumkabili mpinzani wake huyo na kujiwekea rekodi yake ya kipekee.“Nashukuru Mungu kwa kushinda kwa sababu nilijipanga vizuri kwa maandalizi ya muda mrefu nilimsoma mpinzani wangu na hatimaye kutimiza kile ambacho nilitaka kukifanya,”alisema.Aidha katika mapambano ya utangulizi yaliyopigwa siku hiyo Kalama Nyilawila alitoka sare dhidi ya chipukizi toka Tanga, Jakobo Maganga katika pambano la raundi nane.Licha ya uzoefu wake Nyilawila bado hakuweza kuonesha ukongwe baada ya Maganga kumng’ang’ania hadi mwisho.Naye bondia Juma Fundi alimshinda kwa pointi Shadrack Juma huku Deo Samwel akitoka sare dhidi ya Mwinyi Mzengela na Harid Manje akimpiga kwa KO Rashid Ally raundi ya nne.
2michezo
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma inamshikilia Mtendaji wa kata ya Mlowa Bwawani, Luis Pearson (37) na mgambo katika ofi si hiyo, Josphat Msambili (37) kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa ya Sh 400,000.Watuhumiwa hao ni wakazi wa kijiji cha Mlowa Bwawani Wilayani Chamwino, Dodoma na wanadaiwa kufanya kosa hilo kinyume cha kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya 2007. Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo alisema watuhumiwa hao wawili walimweka mahabusu Samweli Chilulumo, mkazi wa kijiji cha Wiliko kata ya Mlowa Bwawani kutokana na ugomvi wa kifamilia.“Wakati Chilulumo yupo mahabusu ndio watuhumiwa walimtaka awape rushwa ya Sh 600,000 ili wamwachie huru lakini aliomba apunguziwe hadi Sh 400,000,” alisema.Chilulumo aliomba atolewe mahabusu ili akatafute fedha hizo, watuhumiwa hao walikataa na kuamua kwenda kutafuta mteja wa mbuzi 10 alizokuwa nazo nyumbani kwake. Kibwengo alisema uchunguzi wa Takukuru ulibaini mtuhumiwa Msambili alienda kutafuta mnunuzi wa mbuzi hao na kumpeleka kwa Chililumo na mnunuzi huyo alienda nyumbani kwa mahabusu kuwakagua mbuzi na akarudi tena kwa mahabusu ndipo wakakubaliana bei.“Takukuru imethibisha mnunuzi huyo alitoa fedha ambazo watuhumiwa walizipokea ndio wakamtoa mahabusu na kumwachia huru,” alisema.Alisema Takukuru imekamilisha uchunguzi wao na watuhumiwa wanapandishwa kizimbani. Kibwengo alitoa mwito kwa watendaji wa kata, mitaa na vijiji Dodoma kufanya kazi kulingana na maadili ya kazi na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani havina nafasi katika mkoa huo.Aliwapongeza wananchi wanaotoa taarifa za vitendo vya rushwa na kuwasihi waendelee kuwa sehemu ya mapambano hayo kwa kutoa taarifa wanapona uonevu kama huu ukitendeka. Alisema kutokana na Chilulumo kutoa taarifa kwa diwani, viongozi wa wilaya hadi mkoa na baadaye Takukuru, atakuwa shahidi katika kesi hiyo ya kushawishi na kupokea rushwa.
1kitaifa
NEW YORK, MAREKANI STAA wa filamu nchini Marekani mwenye asili ya nchini Kenya, Lupita Nyong’o, amewataka warembo barani Afrika kujivunia urembo wa rangi zao ili kulitangaza bara lao. Mshindi huyo wa tuzo za Oscar, amedai kwa upande wake anajivunia rangi pamoja na mwonekano wa nywele zake za Kiafrika katika kazi zake za mitindo na burudani. “Nimekuwa nikipata kazi mbalimbali kutokana na rangi yangu na nywele za Kiafrika, nafanya vizuri katika tasnia ya filamu Hollywood kama walivyo watu wengine. “Hivyo huu ni wakati wa wasichana wengine wenye rangi na nywele kama zangu kujivunia vile walivyo, hakuna sababu ya kujibadilisha kwa ajili ya kutaka kufanana na watu fulani, kila mmoja ajivunie kile alichopewa na Mungu,” alisema Lupita.
4burudani
KINSHASA, DRC UPINZANI umepanga kutumia nguvu ya umma baada ya Taume ya Uchaguzi nchini hapa kusema uchaguzi wa rais atakayechukua nafasi ya Rais Joseph Kabila hauna uwezekano wa kufanyika mwaka huu. Hilo huenda likazua upya machafuko yaliyoshuhudiwa mwaka jana kwa vile bi ukiukaji wa makubaliano yaliyoyasitisha mwaka jana, ambayo yalimruhusu Kabila kuendelea kubaki madarakani hadi mwishoni mwa mwaka huu. Kugoma kwa Kabila kuondoka madarakani mwishoni mwa muhula wake wa pili Desemba mwaka jana kuliibua machafuko yaliyoua makumi ya watu. Upinzani haukuchukua muda kuibuka kulaani tangazo hilo la Rais wa Tume, Corneille Nangaa, ikisema huko ni ‘kutangaza vita.’ “Rasilimali tulizo nazo, zinatupa sababu zaidi za kuamini kuwa Desemba, haitawezekana kufanyika uchaguzi kama ilivyopangwa,” Nangaa alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa, TV5Monde. Chini ya makubaliano yaliyofikiwa Desemba 31 mwaka jana kati ya wawakilishi wa Kabila na viongozi wa upinzani, Kabila, aliye madarakani tangu 2001, pia alizuiwa kujaribu kubadili katiba ili awanie urais kwa muhula wa tatu. Hata hivyo, Kabila alisema uchaguzi utafanyika tu pale tume ya uchaguzi itakapomaliza kuorodhesha mamilioni ya wapiga kura. Katika kuitikia kauli za Nangaa, kiongozi wa upinzani Felix Tshisekedi aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa rais wa tume ametangaza vita kwa watu wa Kongo na ameonya watachukua hatua kali kushirikisha nguvu ya umma mitaani.
3kimataifa
Mwandishi Wetu, Dodoma Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa nchini, John Shibuda, amewataka Watanzania wajitokeze kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Jumapili Novemba 24, mwaka huu. Pamoja na hali hiyo amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuchagua kiongozi anayemtaka kwani hatua hiyo itasaidia kujenga misingi ya utawala bora katika upatikaji wa viongozi hao. Shibuda amesema hayo leo Ijumaa Novemba 22, leo kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari ambapo amewataka Watanzania kujitokeza na kwenda kupiga kura kuchagua viongozi hao pamoja na wajumbe wao. “Natoa wito kwa umma wote mjitokeze na kwenda kupiga kura. Wito unazingatia kwamba kamati ya uongozi ya baraza la vyama vya siasa tayari imechukua hatua ya kusimamia kutendeka kwa hatua za kutakatisha hitilafu zote, zinazoathiri sifa za uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019. “Kwa hiyo sasa, nashauri kila mtu mwenye sifa za kupiga kura na alikuwa amekwazika na kero za watendaji waitwao waborongaji wa kanuni za uchaguzi huu. Sasa nawashauri watu wote  muwe na ufikiri mwema wa kuunda uamuzi mpya wa kushiriki katika uchaguzi huu wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa. Kwa hiyo jitokezeni mkapige kura siku ya Novemba 24,” amesema Shibuda. Pamoja na mambo mengine, amewataka wananchi, wanasiasa na wakereketwa wa demokrasia na siasa za ushindani wa vyama vingi kutambua kwamba kususia upigaji kura si ubani wa sadaka ya kafara la kuondoa matendo batili ya kuundika kwa mazalia ya hila za athari za kiini macho kwa haki na usawa za mfumo wa vyama vingi. “Ukombozi dhidi ya tabia za matendo ya watekelezaji maovu ya hulka potofu, dawa yake ni vikao vya kukosoana tupate masahihisho ya kujenga. Stahiki katika utungwaji wa kanuni mpya za uchaguzi. “Kwa hiyo sasa, nawashauri wananchi, viongozi wa siasa na wakereketwa wa siasa kataeni kuwa mateka wa hasira za kuwapa ushindi waborongaji na waparaganishi wa kukwaza dhamiri zenu za kushiriki katika upigaji kura,” amesema. Shibuda ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa vyama vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti, amesema Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa  ndiyo sauti kuu, hivyo vikao hivi vitawaarifu kuhusu matokeo ya kikao cha majadiliano na wasimamizi wa uchaguzi huu wa serikali za mitaa.
1kitaifa
NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans Van Der Pluijm, amesema ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni kitu kidogo sana kwake, kwani bado nafsi yake inatamani kitu kikubwa zaidi kwa klabu hiyo. Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-1dhidi ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi uliofanyika Jumatatu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kufikisha jumla ya pointi 53, zilizopelekea klabu hiyo kutangazwa kuwa mabingwa wapya msimu huu. Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema tayari amejipatia sifa hapa nyumbani kwa kuipa ubingwa Yanga, akieleza sasa ni wakati wa kuonyesha maajabu kimataifa. Pluijm alisema kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, tayari mikakati yake yote ambayo alijiwekea kabla ya mchezo huo wa marudiano imekamilika. “Ubingwa wa ligi ni kitu kidogo kwangu, hapa kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuelekeza nguvu zote kimataifa,” alisema Pluijm. Mholanzi huyo alisema wakati anakabidhiwa kikosi cha Yanga, alijiwekea dhamira ya kuwapa ubingwa na hilo limeweza kutimia. “Nilipokuwa naingia mkataba nilisema lazima timu ninayoifundisha ichukue kombe la ligi, bado nataka kuishuhudia ikifanya kitu kikubwa zaidi,” alisema Pluijm. Timu hiyo inatarajiwa kuvaana na Etoile du Sahel katika mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita. Tayari timu hiyo imetua Tunisia kwa ajili ya mchezo huo.
2michezo
Timu 14 kati ya 16 zinazoshiriki Ligi Kuu msimu huu wa 2015-16 zitacheza kwenye viwanja tofauti huku kila moja ikiwa na shauku ya kutaka kushinda. Mabingwa watetezi, Yanga ndio wanaoshikilia usukani kwa pointi 12 wakilingana na Azam FC na Mtibwa Sugar, lakini wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa huku Simba ikishika nafasi ya nne.Yanga wanakutana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Je, watafanikiwa kuvunja mwiko wa kutowafunga Mtibwa uwanjani hapo? Mara ya mwisho walipokutana uwanjani hapo msimu uliopita Yanga walifungwa mabao 2-0. Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm alisema ana matumaini ya kushinda kwani malengo waliyojiwekea ni kushinda kila mchezo. “Tuna imani ya kufanya vizuri katika mchezo wetu na Mtibwa.Tunataka kuvunja huo mwiko kwani kikosi changu kiko vizuri kwa mapambano,” alisema kocha huyo raia wa Uholanzi. Yanga inahitaji kushinda mchezo huo kama inataka kuendelea kuongoza ligi, na ikiwa itafungwa na Azam FC wakashinda, basi Yanga watashuka hadi nafasi ya tatu au ya nne na kuwaruhusu Mtibwa na Azam kuwa juu yao.Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema timu yao imejipanga kufanya vizuri katika mchezo huo. “Tunaichukulia Yanga ni timu ya kawaida haiwezi kututisha. Waje watakiona cha moto,” alisema Kifaru na kuongeza kuwa safari hii ni zamu yao kushinda kwa kila mchezo ulioko mbele yao ili kuchukua ubingwa wa ligi.Kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi wenyeji watashuka dimbani kuvaana na Coastal Union ya Tanga. Azam FC wamedhamiria kuendeleza rekodi yao ya kutokupoteza mchezo wowote. Tayari wameshinda michezo yote ya ugenini na nyumbani iliyokwisha kucheza hadi sasa.Mara ya mwisho Azam FC kukutana na Coastal Union Machi mwaka huu, Azam waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Leo zinakutana Azam Complex hivyo bado Azam ina nafasi ya kufanya vizuri zaidi na kuwafunga Coastal kwa mara nyingine ambao wameanza vibaya ligi wakishikilia nafasi ya 15 kwenye msimamo wakiwa na pointi mbili.Licha ya ubora wa Azam FC, hawatakiwi kuidharau timu hiyo ya Tanga kwa vile inawafahamu na lolote linaweza likatokea kwa sababu nao wanataka matokeo mazuri. Kwa upande mwingine, Simba wanaikaribisha Stand United ya Tanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakitoka kujeruhiwa vibaya kwa kufungwa mabao 2-0 na watani wao wa jadi, Yanga.Simba inayoshika nafasi ya nne kwa pointi tisa na Stand United inayoshika nafasi ya tano kwa pointi sita, zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja huo msimu uliopita. Itapania kushinda leo ili kuwathibitishia mashabiki wao kuwa iliteleza tu kwa Yanga.Mchezo mwingine itakuwa ni Majimaji ya Songea dhidi ya Ndanda FC katika mchezo utakaochezwa mkoani Songea, Ruvuma ikiwa ni mara yao ya kwanza. Majimaji ikishika nafasi ya sita ikiwa na pointi sita wakati Ndanda FC inashika nafasi ya 10 kwa pointi nne. Zote zinahitaji ushindi.Kwa upande wa Kagera Sugar yenye pointi nne inacheza na JKT Ruvu wanaoshikilia mkia. Kagera Sugar wana nafasi ya kufanya vizuri kwa vile wako nyumbani. Africans Sports itacheza na Mgambo kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Tanzania Prisons wataikaribisha Mwadui FC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
2michezo
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, amesema amekuwa akitumia akili zaidi anapokuwa katika eneo hatari  la wapinzani, hatua inayomfanya kufunga mabao ambayo yamekuwa yanaisaidia timu yake. Kagere juzi alifunga bao pekee la Simba katika ushindi wa 1-0 dhidi ya mtani wake Yanga, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bao hilo lilimfanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Gor Mahia kufikisha mabao tisa msimu huu akiwa na kikosi hicho cha Msimbazi, akilingana na mpachika mabao wa Alliance, Dickson Ambundo. Kwa ushindi wa juzi, Simba ilifikisha pointi 39 na kusogea hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitoka nafasi ya nne baada ya kushuka dimbani mara 16, ikishinda michezo 12, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja. Akizungumza baada ya pambano lao na Yanga kumalizika, Kagere alisema baada ya kufanikiwa kuvuna pointi tatu, kwa sasa wanaangalia mbele kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo yao ijayo. “Unapokuwa eneo la hatari la mpinzani wako, unatakiwa kuongeza umakini ili uweze kupata kile unachokihitaji, unatakiwa kutumia akili zaidi kuliko nguvu, umri  si kitu sana, mara nyingi napenda kujipa changamoto mwenyewe, licha ya mechi kuwa na ushindani mkubwa nashukuru tumepata pointi tatu muhimu,” alisema Kagere aliyewahi kukipiga  Piliso Rwanda. Alisema kwa sasa anautazama mchezo wao unaofuata dhidi ya African Lyon, unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha. Wakati huo huo, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amemzungumzia mshambuliaji huyo kwa kusema ni mchezaji tishio anapokuwa eneo la hatari la wapinzani. “Simba ilicheza kwa kiwango bora kuliko sisi, wachezaji wangu walishindwa kutambua tunahitaji nini, ukiangalia hata bao tulilofungwa mabeki walikosa umakini na kushindwa kutambua pale alikuwepo mshambuliaji wa aina gani,” alisema Zahera. Kagere ameonekana kuwa mwiba  mchungu kwa mabeki wa timu  mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara na katika michuano ya kimataifa, ambapo Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Kabla ya  kuipa ushindi juzi dhidi ya Yanga, Kagere pia aliiongoza Simba kuitungua Al Ahly ya Misri bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pia alionyesha  umahiri wa kupachika mabao wakati Simba  ilipoumana na Mbabane Swallows ya nchini Swaziland, akifunga bao moja Wekundu waliposhinda 4-1 Uwanja wa Taifa kabla ya kufunga idadi hiyo hiyo iliposhinda  4-0 ugenini. Alithibitisha ubora wake wakati Simba ilipoitungua Nkana Red Devils ya nchini Zambia mabao 3-1, ambao alifunga bao la pili kwa kichwa kabla ya kuifungia mabao mawili Simba ilipopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya J.S Saoura ya Algeria.
2michezo
ZAIDI ya asilimia 47 ya watu walio katika uhusiano, wanaombwa na wapenzi wao wabadilike kitabia. Japo siyo kila tabia kitaalamu unapaswa kuibadili hata kama mwenzako anakwambia japo asimilia kubwa ya tabia za wahusika zinapaswa kubadilika. Ila swali la msingi, huwa unamuelewa mwenzako anapolalamika kwamba anataka ubadilike? Unajua anataka nini katika mabadiliko yako? Ifahamike, mara nyingi mwenzako anapotaka ubadilike, kuna kitu ama vitu vinamkera katika tabia yako. Hivyo kilio chake cha kutaka ubadilike ni kuhitaji uachane na vitu hivyo ili afurahie zaidi kuw ana wewe katika uhusiano. Kilio cha mwenzako juu ya mabadiliko ya tabia yako mara nyingi huwa ni kwa faida yako na yake. Mfano, labda anahisi unamsaliti kutokana na tabia yako fulani. kilio chake cha kutaka ubadilike tafsiri yake ni kwamba anataka kuwa na amani na furaha na wewe. Kama ukiachana kubadilika, hawezi kuwa na furaha na amani. Unajua tafsiri ya yeye kutokuwa na furaha akiwa na wewe? Mwenzako akiacha kuwa na amani na wewe kwa sababu ya kutokuwa na imani juu ya tabia yako juu yake, huenda pia asione sababu na maana ya yeye kuendelea kuwa muaminifu na mwenye kukuheshimu. Athari ya jambo hili ni yeye kuwa mtu wa hovyo kwa sababu ana amini na wewe pia ni mtu wa hovyo kwake. Kumbuka binadamu huwa anaziamini na kuheshimu zaidi hisia zake kuliko maneno anayoambiwa. Hivyo ni vema kuwa na tabia ama mwenendo unaochochea hisia chanya kwa mwenzako kuliko hasi.  Ni kosa kubwa kuacha kufikiria kwanini mwenzako anataka ubadilike. Ni kweli, siyo kila jambo mwenzako analokwambia halitaki basi unapaswa kuliacha. Hawezi kukwambia acha kupokea simu ya bosi wako ama ya wateja wako unapokuwa nyumbani kisha na wewe ukakubali kwa kigezo cha kutaka kumfurahisha. Ila pia ni vema kumueleweshwa mwenzako juu ya umuhimu wa kupokea simu hizo na siyo kuonyesha dharau juu yake.  Unapoonesha dharau kwa mwenzako, unahamasisha hisia za mwenzako ziamini kwamba yeye sio wa muhimu na hana thamani kwako. Kitu hiko sio tu kitamfanya aumie ila pia kitamfanya  ajione yuko sehemu isiyo sahihi katika maisha yake. Kilio cha mwenzako juu ya mabadiliko ya tabia yako inabidi ukipe nafasi muhimu katika akili yako. Mpaka mwenzako anakutaka ubadilike ujue tabia yako fulani inamfanya asiwe na amani na furaha. Sasa mtu ataendelea vipi kujivuia wewe katika maisha yake na humfanyi kuwa na amani na furaha?  Mahusiano yanapaswa kuwa sehemu ya kufurahishana, kupeana hamasa ya maisha na kubadilishana raha. Kama humfanyi mwenzako kupata vitu hivyo kwa sababu ya tabia yako, abadani hawezi kujiona yuko katika mahusiano kamili.  Na kama mtu asipojiona yuko katika mahusiano kamili unajua nini kitafuata? Binadamu toka enzi za kale ni mtu mwenye kuhangaika kutafuta sehemu ya kumpa, furaha amani na pumziko. Kama kwao pia anaona sio sehemu ya kumfanya ajidai, sio ajabu sana kuhama na kuondoka kusaka sehemu bora zaidi.  Mahusiano mengi yanapovunjika ni kwa sababu wahusika hawapeani yale wanayotarajia kwa kila mmoja. Kama mwenzako analitarajia kupata raha na utulivu kwa kuwa na wewe na anaona hapati, unafikiri atakuwa na sababu gani ya kuendelea kuwa na wewe? Kuwa chanzo cha raha kwa mwenzako ikiwa unahitaji aendelee kuwa sehemu ya maisha yako. Hakuna mtu anayeingia katika mahusinoa ili apate karaha na maudhi. Iangalie vema tabia yako kama inampa mwenzako sababu ya kujivunia kuwa na wewe. Instagram: g.masenga Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia ( Psychoanalyst)   ramadhanimasenga@yahoo.com
5afya
MMOJA wa wasichana watatu wa Uingereza waliotoroka kwao miaka minne iliyopita na kwenda kuolewa na wanamgambo wa dola la Kiislamu nchini Syria (ISIS), Shamima Begum (19) amejifungua katika kambi ya wakimbizi nchini Syria.Shamima ambaye wiki iliyopita akiwa mjamzito alisema anataka kurudi nyumbani akihofia usalama wa mtoto aliyetarajiwa kuzaliwa wakati wowote, amekaririwa katika mahojiano na BBC akiomba msamaha kuwa karibu na kundi hilo la kigaidi lililosababisha maafa katika maeneo mbalimbali.Februari 2015, Shamima na wenzake; Amira Abase akiwa na umri wa miaka 15 na Kadiza Sultana aliyekuwa na miaka 16 walisafiri kutoka London kwenda Istanbul, Uturuki Februari 17 kisha kuvuka mpaka na kwenda Syria ambako waliolewa na wapiganaji wa kikundi hicho.Taarifa ya familia iliyochapishwa na BBC kwenye mtandao inasomeka:“Sisi wanafamilia ya Shamima Begum tumejulishwa kwamba Shamima amejifungua mtoto wa kiume na yeye na mtoto wake wana afya nzuri. Kwa kuwa hatuna mawasiliano ya moja kwa moja na Shamima, tunatarajia kuyatafuta ili tuthibitishe hili”.Awali, mwanasheria wa familia ya binti huyu, Mohammed Tasnime Akunjee, aliiambia Radio 4 katika kipindi chake cha The World This Weekend kuwa wana furaha kwa kuwa Shamima amejifungua, ana afya njema hivyo wanataka arudi nyumbani.Alisema familia ilisikitishwa na taarifa juu ya vifo vya watoto wake wawili .Alisema watoto hao; wa kike mwenye mwaka mmoja na wa kiume mwenye miezi mitatu walifariki dunia kutokana na matatizo yanayohusishwa na utapiamlo na ukosefu wa dawa katika eneo hilo la vita.Akizungumza na Sky News, Shamima alisema jamii haina budi kumhurumia kwa mambo yote aliyopitia.Alipoulizwa kama alifanya makosa kusafiri hadi Syria, alisema, “kwa namna moja, ndiyo, lakini sijuti kwa sababu imenibadilisha mimi kama binadamu. Ilinifanya kuwa imara na jasiri. Niliolewa na nisingeweza kupata mtu kama huyu nchini Uingereza,” alisema.Aliendelea kusema: “Nilipata watoto, nilikuwa na wakati mzuri hapa. Ni kwa sababu tu mambo yamekuwa magumu na siwezi kuvumilia tena.” Gazeti la The Times ndilo lilimuibua Shamima kwa mara ya kwanza kupitia mahojiano yaliyofanyika Februari 13 mwaka huu na kukaririwa akisema ni mjamzito na kwamba watoto wake wawili walifariki.Mwandishi wa gazeti hili, Anthony Loyd alisema alimgundua katika kambi ya wakimbizi baada ya kusikia lafudhi yake.Shamima alipoulizwa na Sky News kama alikuwa anafahamu vitendo vya mauaji vilivyokuwa vikiendelea kufanywa na kundi la ISIS, alisema alifahamu mambo hayo yote na hakuwa na tatizo juu ya hayo.“Kwa sababu nilishakuwa mcha dini kabla ya kuondoka nchini, nilisikia kuwa katika uislamu hayo yanaruhusiwa,” alisema.Pamoja na Shamima kuomba msamaha kwa mauaji yaliyofanywa yakihusishwa na ISIS ikiwamo tukio la Manchester, lakini alisema anaona ni aina fulani ya kulipiza kisasi kwa kuwa pia kundi hilo la kigaidi lilikuwa linalengwa.Alijitetea kwamba kipindi chote alichokaa nchini humo alikuwa mama wa nyumbani na hajawahi kutoa usaidizi kwa kundi hilo.Binti huyo alisema wiki mbili zilizopita, alitoroka kutoka Baghuz; yaliyokuwa makao makuu ya IS, Mashariki mwa Syria. Mumewe, ambaye ni Mholanzi, inasadikiwa kwamba alijisalimisha kwa makundi ya wapiganaji ya serikali.Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na mjadala kuhusu endapo Shamima aruhusiwe au asiruhusiwe kurejea nchini Uingereza.Miongoni mwa waliohojiwa ni pamoja na wakazi wa eneo la Bethnal Green ambako alikuwa akisoma, ambao baadhi walitaka aruhusiwe kurudi nchini huku wengine wakihoji kama serikali itakubali.Baba yake Shamima alishutumu maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano akisema wapo vijana wanaokuwa waathirika wa dunia ya kidijitali hivyo mambo mengi yanaweza kutokea.
3kimataifa
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM KILA mwanadamu ameumbwa na milango ya fahamu, milango ya fahamu ambayo inaonekana kwa nje ya mwili wake ipo mitano. Ambayo ni pua, macho, sikio, ngozi na ulimi (mdomo). Hii hufanya kazi ya kupeleka taarifa kwenye ubongo kwa njia mbalimbali. Ngozi hupeleka taarifa kwa njia ya kugusa, sikio – kusikia, pua – kunusa, ulimi – kuonja na macho – kuona. Ulimi wa binadamu una vionjo vinne ambavyo ni utamu, uchungu, ugwadu na ukali. Vionjo vyote hivyo hupeleka taarifa katika ubongo na hivyo wenyewe kutoa tafisiri juu ya kitu alichoonja mwanadamu iwapo ni kitamu, kikali, kigwadu au kichungu. Hata hivyo pamoja na milango hiyo ya fahamu ambayo wengi wetu tunaifahamu na tunaiona kwa macho, ipo pia milango mingine ya fahamu ambayo yenyewe huwezi kuiona kwa macho ya kawaida wala kuigusa. Mtaalamu wa Tiba ya Utengamao na Mazoezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Rosemary Kauzeni, anasema wataalamu wa afya pekee wakiwamo wa tiba ya mazoezi ndiyo wanaoweza kuielezea milango ya fahamu isiyoonekana. “Kuna ambao upo kwa ajili ya kufanya mwili uweze kupata uwiano, kitaalamu wanaita ‘vestibular sense’ wenyewe upo katikati ya masikio na kichwa cha mwanadamu. “Mlango huu kazi yake kubwa ni kuhakikisha mwili unapata uwezo wa kukaa, kusimama, kutembea au kufanya jambo lolote pasipo kuanguka (kudondoka). Dk. Kauzeni anasema mlango mwingine wa fahamu upo ndani kabisa ya ufahamu yaani kwenye ubongo. “Huu hutafsiri na kutoa taarifa juu ya eneo alilopo mtu, kuna hali ya namna gani, labda ni joto au baridi na mambo mengine kama hayo,” anasema. Anasema humsaidia mtu kupata hisia mbalimbali na kwamba ili mwili na ubongo ufanye kazi kwa ufanisi ni lazima milango yote ya fahamu isiyoonekana na inayoonekana ifanye kazi sawa sawa. Anasema sehemu za mwili wa mwanadamu zimeungwa kwa viungio na katika viungio hivyo kuna vishipa vidogo vidogo vinavyoitwa kwa jina la kitaalamu ‘ligaments’. “Vishipa hivi vinaunganisha misuli ya mwili na kuifunika na nyama, milango yote hii lazima ipeleke taarifa kwenye ubongo na inashirikiana kwa ukaribu,” anasema. Anasema ubongo hupokea taarifa na kuzitafsiri kisha kugawa kazi kwa viungo vya mwili, kwamba kiungo kipi kifanye kazi gani na kwa wakati gani. “Hivyo, utendaji bora wa milango ya fahamu huchangia utendaji bora wa ubongo na mwili kwa ujumla,” anasema.   Hupata athari Daktari huyo anasema milango ya fahamu nayo huweza kupata athari mbalimbali kama ilivyo kwa viungo vingine vya mwili. “Inapotokea imepata athari hufanya ubongo nao kushindwa kutafsiri vema taarifa ambazo hupokea na au kutoa tafsiri zisizo halisi,” anasema. Anasema hali hiyo huweza kutokea iwapo ubongo unaweza kupokea taarifa nyingi zaidi au kidogo kuliko vile unavyopaswa kupokea. “Inapotokea hali hiyo, yaani ubongo unapokea taarifa nyingi zaidi au kidogo tunasema ubongo umepata ajali. “Hali hiyo inapotokea binadamu hujisikia vibaya. Si mara zote milango yote inaweza kuathirika, unaweza kuathirika mlango mmoja, miwili au mitatu na mingine ikaendelea kustahimili na isipate madhara kabisa.   Ubongo na idara zake Anasema ubongo una idara zake ambazo hueleza namna gani mtu atende. “Kuna idara zinatafsiri uoni, hisia za ngozi, vionjo. Milango ya fahamu inaposhindwa kufanya kazi sawa sawa husababisha utendaji kazi wa idara hizo nazo kutetereka,” anasema. Dk. Kauzeni anasema wataalamu wameligawa tatizo hilo katika maeneo manne. “Eneo la kwanza ni pale utendaji kazi wa mtu unapoweza kuvurugika kwa urahisi, kwa mfano sauti kidogo ikipenya masikioni mwake huwa kero kubwa na hata kudhani dunia yote imejaa sauti,” anabainisha. Anasema milango ya fahamu inapofanya kazi yake vizuri ni rahisi mtu kuchuja sauti anayohitaji ipenye katika masikio yake. “Yaani akikaa mahala hata kama kuna sauti nyingi kiasi gani, anao uwezo wa kuruhusu sauti moja pekee ipenye masikioni mwake na akaendelea kufanya kazi zake kama kawaida. “Ndiyo maana anakuwa na uwezo wa kukaa; kwa mfano, darasani na kukawa na kelele nyingi zinapigwa na wanafunzi lakini akaendelea kujisomea na hata kufanya vema katika mitihani yake,” anasema. Anasema mtu mwenye tatizo katika mlango wa fahamu wa ngozi wakati mwingine anaweza kulalamika anaumia hata anapoguswa na kitu fulani. “Unakuta mtu analalamika hata akikatwa kucha, akinyoa nywele, ndevu au hata wakati mwingine anaweza kukwepa kuvaa baadhi ya nguo zake akidai zinamuumiza,” anabainisha. Anaongeza: “Unakuta anachangua aina ya nguo za kuvaa kwa sababu zingine akivaa zinamuumiza kwani kiwango chake cha hisia huwa kipo juu mno kuliko kawaida. “Wapo wengine huwa hawataki kutumia hata mashuka mazito (blanketi), au kuvaa sweta kwa sababu anaona zinamuumiza.” Anasema tatizo jingine ni kukosa usingizi. Kwamba anakaa muda mwingi bila kupata usingizi na hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu hupata maumivu ya kichwa, yote hii ni kwa sababu milango yake ya fahamu inakuwa haifanyi kazi yake sawa sawa kwa pamoja,” anasema. Dk. Kauzeni anasema wakati mwingine hushindwa kuhimili vionjo na anapoonja kitu chochote huona kero kubwa na wengine wakiona mwanga uwe mkali au mdogo kwao huwa ni kero.   Watoto Anasema watoto wenye tatizo hilo mara nyingi hupenda kukimbia kimbia, kuruka ruka bila kujali kwamba wanaweza kuumia kulingana na mazingira waliyopo. “Hupendelea kusukuma vitu ovyo kutoka sehemu moja hadi nyingine na wanaweza kushika kitu kigumu muda mrefu wakitembea nacho huku na huko,” anasema. Anasema wakati mwingine wanapochukua kitu kutoka sehemu moja hadi nyingine hudondosha kila mara. “Wakati mwingine wanapowekwa juu ya vitu kwa mfano, kwenye bembea huwa wanaogopa na hata wakitembea hupepesuka. “Huonekana walegevu, huchoka haraka, hawana utulivu na wakikaa huwa hawakalii makalio (wanakaa kama vile wanataka kulala),” anasema na kuongeza: “Watoto wenye tatizo hili ukiwabeba huwa ni wazito mno kama vile jiwe na uzito huo huwa upo zaidi katika eneo la kifua na mgongo. “Ukiangalia unyao wao utaona hauna uvungu wenyewe huwa upo ‘flat’ hivyo ni muhimu wazazi kuwachunguza watoto wao,” anasema. Anasema changamoto nyingine ambayo watoto wenye tatizo hilo hukabiliana nayo ni kupangilia shughuli zao. “Hupata wakati mgumu kufanya kazi bila kusaidia mpangilio wa kazi husika, kama hawapewi mpangilio wa kazi husika huwa ni rahisi ‘kuvurugika’ kwa haraka na shughuli hiyo haitaweza kufanyika,” anasema. Dk. Kauzeni anaongeza: “Kama tayari ni mwanafunzi utaona ushikaji wake wa kalamu si wa kawaida, yaani unakuta ameishika yote. “Hata mpangilio wake wa mwili jinsi anavyokaa au kuandika huwa si wa kawaida, unakuta kama vile amelala kidogo,” anabainisha.   Watu wazima Anasema kwa upande wa watu wazima mara nyingi huwa na hasira na wakati mwingine hupendelea kukaa kimya. “Huwa hawapendi kuzungumza na utendaji wao wa kazi huwa hafifu pindi wanapobadilishiwa kazi hata kama awali alipangilia vizuri, awamu hiyo hataweza kuifanya tena. “Hata mpangilio wao wa mwili huharibika na unapoharibika hujikuta wakipata maumivu ya viungo, mgongo, shingo, misuli kubana na kwenye viungio. “Wengine misuli yao hulegea kupita kiasi na kujikuta mgongo nao ukilegea kwa sababu zile nyama za mgongo huwa hazishikilii tena uti wa mgongo ili uwe sawa,” anasema.   Visababishi Anasema hadi sasa dunia haijatambua kwanini milango ya fahamu hupata ajali lakini viashiria vikubwa wametaja mazingira mtu anayokulia. “Kuanzia tumboni mwa mama kama hakukuwa na uchangamfu wa kutosha mtoto kuweza kuzunguka na kucheza ukuaji wa mlango huwa mdogo. “Baada ya mtoto kuzaliwa pia kunaweza kutokea shida kama mtoto hawezi kuwekwa kwenye mazingira yatakayomfanya milango yake ichangamke, ni namna gani ataweza kupata taarifa inavyotakiwa,” anasema na kuongeza: “Wakati mwingine mazingira nayo yanaweza kuchangia mtu kupata tatizo hili, kwa mfano, ukiwa katika eneo ambalo lina kelele nyingi.   Uhusiano na magonjwa mengine “Usafi nao ni jambo la msingi kulizingatia, kwa sababu kama mtu ana tatizo hili la milango ya fahamu, akakakutana na harufu kali labda ya choo ubongo wake unaweza kutafsiri tofauti. “Anaweza kuanguka na kupoteza fahamu na mtu anapodondoka ikiwa atajipigiza kichwa chini misuli inaweza kupasuka na hivyo kumsababishia kupata tatizo la kiharusi,” anabainisha.   Mazoezi ni tiba Anasema tatizo hilo linatibika kwa njia ya mazoezi na dawa maalumu ambazo wataalamu huwapatia wagonjwa. “Mazoezi ni muhimu kwa afya, unapofanya mazoezi kwa mfano ya kutembea mwili huwa unawasiliana na ubongo  moja kwa moja. “Ubongo ulivyoumbwa ni kama vile kifaa cha CPU kwenye kompyuta, wenyewe unaushughulisha mwili wa binadamu,” anasema. Anasema katika kliniki yao kwenye Idara ya Tiba ya Mazoezi na Utengamao Muhimbili kwa siku huwa wanapokea na kutibu watoto 20 na watu wazima 10 wenye tatizo hilo. “Matibabu huchukua hadi siku 14 na mtu hupona kabisa lakini hutegemea wakati mwingine kwa watoto huchukua hadi siku 30,” anasema.
5afya
WATUMIAJI wa magari wanaofi ka kupata huduma katika vituo vya mafuta wametakiwa kuhakikisha kuna stika maalumu ya Wakala wa Vipimo (WMA) katika pampu za mafuta kabla ya kupatiwa mahitaji yao. Akizungumza jana wakati wa kukagua pampu za mafuta katika Kituo cha Total kilichopo Mlimani City, Kaimu Meneja wa WMA Mkoa wa Kinondoni, Charles Mavunde, alisema stika hizo zinasaidia kujua kituo cha mafuta kimehakikiwa na mamlaka husika. Alisema kila mwaka huwa wanafanya uhakiki na ukaguzi wa vipimo mbalimbali ambavyo vinatumika katika biashara na kwamba kituo hicho ni kati ya vituo 85 vilivyopo katika Mkoa wa Kinondoni ambavyo vinafanya vizuri katika kuwahudumia wananchi.“Kila pampu ya mafuta ambayo imehakikiwa na mkaguzi wa vipimo hubandikwa stika inayoonesha mwezi na mwaka wa ukaguzi na alama inayomzuia mmiliki wa pampu ya mafuta kuichezea, na hata ikitokea ameichezea hairudishiki,” alisema Mavunde. Alifafanua kuwa mfanyabiashara atakayebainika kuchezea pampu ya mafuta anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kutozwa faini kati ya Sh 300,000 hadi Sh milioni 50 ama kifungo cha miaka saba jela. Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Total Mlimani City, Ally Mohamed, alisema wamekuwa wakizingatia matumizi sahihi ya vipimo ili kumlinda mlaji. “Kila baada ya miezi mitatu wakala wa vipimo huwa wanapita kukagua pampu za mafuta na mpaka sasa hatujawahi kupata matatizo yoyote ya vipimo,” alisema Mohamed. Meneja Uhusiano wa Wakala wa Vipimo, Irene John, aliwashauri wananchi pindi watakapoona wamepunjwa katika bidhaa mbalimbali watoe taarifa katika ofisi za wakala huo zilizopo nchi nzima au kupiga simu ya bure namba 08001197
1kitaifa
Baada ya juzi wanariadha watatu kutwaa medali kwenye michezo hiyo inayofanyika Los Angeles, jana wanariadha watano waliibuka na medali.Akizungumza kwa njia ya mtandao jana, Mkuu wa msafara, Frank Macha alisema Tanzania imeendelea kujinyakulia medali baada ya juzi kupata medali tatu.“Wachezaji wetu wamefanikiwa kupata medali nyingine tano baada ya zile tatu ambazo zilinyakuliwa awali."Waliopata medali ni Blandina Patrick (dhahabu) na Deonatus Manyama (fedha) wote kwenye mbio za mita 800. Wengine ni Faraja Meza aliyepata medali ya dhahabu, Riziki Chilumba medali ya fedha na Aisha Kaoneka medali ya shaba kwenye mbio za mita 100.Wachezaji wengine ambao walishajinyakulia medali ni Godfrey Jabuya, Blandina Patrick na Deonatus Manyama kwenye mbio za mita 400 hivyo hadi sasa Tanzania imefikisha jumla ya medali nane, dhahabu tatu, fedha tatu na shaba mbili.Timu hiyo ina wachezaji wanane, wanawake wanne na wanaume wanne, itashiriki tena katika mchezo wa riadha katika mita 100, 200, 400, 800, 5000, nusu marathon na mita 4x100 kupokezana vijiti
2michezo
WAWAKILISHI pekee wa Afrika Mashariki katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Simba SC wamewatanguliza mashushushu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuwachunguza wapinzani wao AS Vita Club watakayokutana nao Jumamosi katika mchezo wa Kundi D.Simba inaongoza katika kundi lake, inatarajia kuondoka kesho Alhamisi kwenda Kongo tayari kucheza dhidi ya AS Vita iliyopo katika nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi hilo.Katika mchezo wa kwanza dhidi ya klabu ya Algeria ya JS Saoura, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi jioni huku AS Vita ikifungwa 2-0 katika mchezo uliofuata dhidi ya Al Alhly ya Misri huko Alexandria.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana kuhusu mikakati yao kuelekea kwenye mchezo ujao Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Crescentius Magori alisema mipango ya maandalizi inaenda vizuri ingawa hawataki kuweka wazi mipango yao kutokana na Wakongo wengi kuishi nchini.Alisema wanaofia mipango na mikakati yao kufichuliwa, lakini alisisitiza kuwa tayari Simba imetuma watu wake `wapelezi’ kuifuatilia AS Vita na kuiandalia Simba sehemu ya kufikia na mambo mengine.“Hadi sasa tumetuma watu kuanza kufanya maandalizi ya awali kuelekea kwenye mchezo wetu na wapinzani wetu ili kuhakikisha mipango yetu ya kuvuna ushindi inaenda sawa, tunajua timu za Kongo zinajua fitina kwenye soka na ndio maana hatuwki mipango yetu yote hadharani, “amesema Magori.Amesema idadi ya kikosi kinachoondoka kuelekea kwenye mchezo huo kitawekwa wazi na kocha wa kikosi hicho Patrick Aussems muda wowote baada ya kufanya mazoezi ya jana ya kujiweka fiti kwa mchezo .Hadi sasa gharama za kusafiri mashabiki kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye mchezo huo imeshawekwa wazi tiketi ya ndege kwenda na kurudi kwa Kenya Airways kwa Alhamisi ni dola za Marekani 760 sawa na Sh. 1,748,563 kwa siku ya Ijumaa ni dola 850 sawa na Sh. 1,955,757 wakatoi malazi ni dola 70 sawa na Sh. 161,074 wakati viza ni dola 50, sawa Sh 115,052.
2michezo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wajiondoe katika kufanya biashara na halmashauri hiyo kwa kuwa wanakiuka maadili ya utumishi wa umma.Ametoa agizo hilo wakati anazungumza na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora na Hospitali ya Rufaa ya Kitete katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.“Madiwani mjiondoe kuwa wasimamizi wa kampuni zinazozofanyakazi na halmashauri yenu na wakuu wa idara nanyi muwe makini mfanye kazi na kampuni huru ili muweze kuchukua hatua pale linapotokea tatizo,” amesema.“Nyie madiwani ndio mnaopaswa kuisimamia halmashauri, sasa kama watu mliopewa dhamana mkiingia katika kufanya shughuli nyingine mnawakwaza wakuu wa idara na kuharibu mambo. Fanyeni kazi yenu ya kuisimamia halmashauri kwa mujibu wa dhamana mliyopewa.” amesema Waziri Mkuu.Ametoa mfano wa mradi wa ununuzi malori mawili na makontena 20 ya kukusanyia taka mitaani ya Manispaa hiyo na kampuni inayomilikiwa na diwani ilipewa zabuni ya kununua vifaa hivyo, ambapo ilikabidhi lori moja likiwa bovu na kukataliwa.“Yeye akaenda kulipaka rangi na kuwaletea, walilikataa tena,” alieleza.Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Msalika Makungu aifanyie uchunguzi ofisi ya Mweka Hazina wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora baada ya kuwepo kwa utafunaji wa fedha za umma kwa visingizio mbalimbali.Amesema zaidi ya Sh milioni 12.4 zimelipwa na Mweka Hazina wa halmashauri ya manispaa hiyo, Abbas Mwanzori kwa ajili ya malipo ya wahasibu waliofanya kazi muda wa ziada na watumishi, huku kukiwa hakuna fomu zilizojazwa na watumishi hao.“Hatuwezi kwenda mbele tukiwa na watu wa namna hii. Halmashauri haiwezi kuendelea mtu anatumia vibaya ofisi kwa manufaa yake binafsi. Na kati ya fedha hizo sh. milioni 8.4 mlizitoa kwa kutumia ‘password’ ya Halima (Mhasibu) bila ya kumjulisha na alipogundua akahoji mkamuhamishia sokoni, Naagiza arudishwe mara moja,” alisema.
1kitaifa
Kwa muda sasa, China imepata mafanikio makubwa katika uhifadhi wa mazingira. Taifa hilo lenye watu wengi zaidi duniani, linaongoza katika harakati za kuongeza maeneo yenye mimea,kutokana na mpango wake kabambe wa upandaji miti na kufanikisha kilimo bora.Takwimu zilizopo zinaonyesha  eneo la misitu nchini humo kumeongezeka kutoka asilimia 12.5  miaka ya 1950 hadi asilimia 21.7 mwaka 2017. Pamoja na mafanikio hayo, mamlaka ya misitu ya China imeapa kuongeza eneo hilo hadi asilimia 26 ifikapo mwaka 2035.Miradi kama ile ya kupambana na jangwa kubwa la Kubuqi, mkoa wa Mongolia ya Ndani, inabaki kuwa mfano katika jitihada za kuhifadhi mazingira nchini China.Hii ni hatua kubwa, kwani kulingana na wataalamu, majangwa husababisha changamoto kubwa katika maendeleo ya uchumi kutokana na kukosekana kwa misitu, hali ya mazingira isiyotabirika,  uwezo wa chini wa uzalishaji, pamoja na miundombinu mibovu.Lakini licha ya hali hiyo, China ilikubali changamoto ya kukabiliana na jangwa hilo, ambalo baadaye limekuwa mfano wa maendeleo katika misitu.Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limepongeza juhudi za China katika kugeuza mojawapo ya majangwa makubwa zaidi kuwa sehemu ya misitu. Zaidi ya  kilomita 6,000 za mraba katika jangwa la Kubuqi tayari limerejeshwa katika hali nzuri.Kubuqi ni jangwa la saba kwa ukubwa nchini China. Jangwa hilo lipo kilomita 800 kutoka Beijing na lilikuwa chanzo cha dhoruba ya mchanga iliyokuwa ikiupiga mji mkuu wa China, Beijing,  kwa muda mrefu. Jangwa la Kubuqi lipo katika mkoa wa Mongolia ya Ndani na lina ukubwa wa kilomita za mraba 20,000 .    Kihistoria jangwa la Kubuqi halikuwa limefunikwa kwa mchanga kutoka mwanzo. Kwa mujibu wa kumbukumbu za kihistoria, sehemu hii ya nchi ilikuwa makazi ya watawala katika karne ya nyuma na ilikuwa na ardhi yenye rutuba nyingi.  Katika siku hizo, inasemekana Kubuqi ilikuwa imejaa rangi ya kijani, mji mahiri na wa kusisimua.Hata hivyo karne ya malisho iliyofuata ilisababisha kuharibiwa kwa mimea yote ardhini. Miaka 200 iliyopita, shughuli hizi za malisho ziligeuza sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba, kuwa jangwa na kumaliza vyote vilivyofanya eneo hilo kuwa la kuvutia. Sehemu yote ya ardhi karibu na Kubuqi ilibaki kuwa kame. Wenyeji walibatiza sehemu hiyo kama "bahari ya mauti" kutokana na hali ngumu sana ya maisha wakati huo.Lakini miaka 30 iliyopita, juhudi za kupigana na jangwa na kulirejesha eneo hilo katika hali yake ya awali zilianza. Kwa uratibu za serikali za mitaa na makampuni, pamoja ushiriki wa wakulima na wafugaji, kwa kuzingatia sayansi na teknolojia, eneo hilo lilianza kurutubishwa Hivyo haikuwa jambo la kushangaza wakati ripoti ya UNEP ilipoonyesha kupungua kwa dhoruba ya mchanga iliyokuwa ikipiga Beijing, kutoka 50 mwaka 1988 hadi moja tu mwaka 2016.Aidha, jitihada za kuboresha ardhi ya misitu kwa mujibu wa ripoti hiyo pia zilisaidia zaidi ya watu 102,000 katika eneo hilo kujikwamua kutoka kwenye umasikini.Hiyo iliwezekana baada ya Shirika la China la Elion Resources Group, likishirikiana na wenyeji na serikali ya Beijing, kuwa na lengo moja la kuzuia kuenea kwa jangwa na kurejesha mazingira.Kwa miongo mitatu, kampuni hiyo pamoja na wanasayansi na wenyeji waliungana katika moja ya miradi kabambe zaidi ya kupambana na jangwa katika karne ya 20.Wakiwa wamejihami na teknolojia shirikishi, mashine na kemikali, waliobebeshwa jukumu hili walifanya kazi bila kuchoka katika juhudi za kugeuza jangwa kuwa ardhi ambayo sasa ina uwezo wa kukuza matunda na miti.Katika mradi huo wa urejesho, wenyeji walipewa motisha kwa kupanda mmea aina ya susi au licorice ambayo haihitaji maji mengi na pia inaweza kuuzwa kwa matumizi ya dawa ya jadi ya Kichina. Mpango huu ulikuwa na mafanikio kwani  mmea huo uliendana na hali ya mazingira ya Kubuqi.Mwaka 2013, kutokana na dhana ya maendeleo ya sekta ya mchanga ya " nuru zaidi, maji kidogo, teknolojia ya juu, na faida nyingi", kampuni ya Elion iliinua mpango huu hadi kiwango kingine baada ya kuwekeza mamilioni ya dola na kutumia teknolojia mpya ya “germplasm” na teknolojia ya upandaji kutokana na uzoefu wake wa zaidi ya miaka 27 ya kurejesha ikolojia kuboresha hali ya Kubuqi.Kwa sasa, eneo hilo lina hekta 3,500 ambayo hasa inatumika katika kukuza nyasi na miti yenye thamani ya juu ya dawa za jadi za Kichina. Hii iliashiria uzinduzi wa uzalishaji na upandaji wa susi na spishi nyingine kwa njia kubwa.Ili kupima rutuba kwa udongo wa jangwa baada ya mafanikio ya susi, kampuni hiyo ilifanya majaribio ya maendeleo ya kilimo cha kisasa ikilenga  kulima matunda na mbogamboga katika eneo hilo la kiikolojia. Mchakato wa uhifadhi uliifanya kampuni hiyo kuanzisha vyumba vya vioo vya kisasa katika eneo la kiikolojia ambavyo vitatumiwa hasa kukuza miche ya susi. Mradi mwingine wa kulea miche ya matunda na mboga pia ulianzishwa.Tangu wakati huo, theluthi moja ya jangwa imerejeshwa na sehemu ya ardhi yenye mchanga inaendelea kupungua. Elion ni kampuni maarufu katika juhudi za kurejesha ardhi iliyoharibika. Shughuli yake kubwa ni marejesho ya mazingira, na kuzalisha nishati safi. Kampuni hiyo ilitunukiwa tuzo ya taifa ya kuboresha mazingira kutoka kwa  serikali ya China na pia ilitambuliwa kama bingwa wa nchi kavu na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na kuenea kwa jangwa (UNCCD). Takwimu kutoka serikali za mitaa zinaonyesha kwamba juhudi za kuongeza misitu katika jangwa la Kubuqi zimebadilisha maisha ya wakulima na wafugaji zaidi ya 100,000. 
1kitaifa
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ameitaka Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha inasambaza dawa kwa wakati, ili kuepusha tatizo la dawa kuisha muda wake wa matumizi zikiwa kwenye maghala yao.Dk Ndugulile ameyasema hayo baada ya kufanya ziara katika ghala la MSD Kanda ya Kaskazini na kushuhudia dawa nyingi zimeisha muda wake wa matumizi na nyingine muda wake unakaribia kuisha.Alisema ametembelea baadhi ya hospitali mkoani hapa na kuona wagonjwa wanaambiwa wakanunue baadhi ya dawa muhimu, wakati zipo kwenye ghala na nyingine muda wake wa kutumika umeisha.Dk Ndugulile amesema, jambo hilo halivumiliki na kuwataka wasisubiri mpaka dawa za bure au zilizonunuliwa na serikali ziishe muda wake wa matumizi, wahakikishe wanaweka utaratibu wa kuzisambaza kwa wakati ili zisiharibike zikiwa kwenye maghala yao.Amesema, dawa zinazokaribia kuharibika wazipeleke kwa wateja ambao wanaweza kuzitumia kwa muda mfupi, ikishindikana wazigawe bure na zilizoisha muda watafute kibali cha kuziteketeza.“Ni bora dawa zitumike bure kuokoa maisha ya Watanzania kuliko zikabaki na kuharibika kwenye maghala, hii dhambi sitawasamehe na Serikali haitavumilia jambo hili,” amesema.Aidha amesema vipimo vingi havifanyiki katika hospitali kwa sababu hakuna vitendanishi, hivyo wawasiliane na wateja hasa katika hospitali za wilaya ili kuhakikisha vipimo vyote vinapatikana.Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Kaskazini, Billy Singano, amesema bohari hiyo inahudumia vituo vya afya 488, hospitali mbili maalum na hospitali tatu za rufaa katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.Amesema ongezeko la dawa limefikia asilimia 80 na wanahakikisha dawa zinapofika zinafungwa na kupelekwa kwa wateja kulingana na uhitaji wao.Pia wamerahisisha utendaji wa kazi kwa kufunga mfumo ambao watoa huduma wote wanaona idadi ya dawa zilizopo katika ghala lao.
1kitaifa
KIWANDA cha viatu cha Bora kimeanza kuliuzia viatu Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ikiwa ni sehemu ya matunda ya kilio kilichowasilishwa na uongozi kwa Rais John Magufuli alipokutana na wafanyabiashara Dar es Salaam. Hatua hiyo imekuja ikiwa imepita miezi miwili tangu Rais Magufuli alipofanya mkutano huo ambao Ofisa Usalama wa Kiwanda cha Bora, Sylivery Buyaga alimwambia kuwa licha ya kutengeneza buti nzuri za jeshi kwa miaka mitatu sasa, taasisi hiyo hainunui viatu kwao.Akizungumza juzi kwenye Maonesho ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Buyaga alisema JKT wameanza kununua viatu kutoka kwao. “Jozi 10,000 zimeshachukuliwa na jeshi,” alisema Buyaga ingawa alilalamikia soko la ndani ya nchi kutokuwa zuri kutokana na uingizaji wa viatu kutoka nje vinavyouzwa kwa wananchi kwa bei ya chini, vikioneshwa kuwa ni ngozi halisi wakati siyo. Alisema licha ya viatu vyao kuwa na ubora unaochangiwa na matumizi ya teknolojia ya hali ya juu kutoka Ujerumani, wateja wa ndani hukimbilia vyenye bei ndogo wakiamini vina viwango sawa jambo ambalo siyo. Alisema ili kulinda bidhaa za ndani, mamlaka zenye dhamana ya kuruhusu uingizaji bidhaa zinapaswa kuzuia zisizo na ubora ambazo jamii huaminishwa kuwa ni ngozi halisi, lakini zikiuzwa kwa bei ya chini. Ofisa usalama wa kiwanda hicho cha Bora chenye wafanyakazi 400, alisema licha ya kufanya upanuzi wa mtambo, lakini wanafanya kazi kwa asilimia 25 kutokana na ufinyu wa soko. Buyaga alisema kungekuwapo sera inayohimiza matumizi ya bidhaa za ndani miongoni mwa taasisi za serikali, ingesaidia viwanda vya ndani kuongeza uzalishaji. “Kungekuwa na sera ya sare za shule, kwenye migodi kutumia bidhaa za ndani ikiwamo mabuti ya usalama na taasisi nyingine, tungeongeza uzalishaji,” alisema. Akishukuru hatua ya jeshi kusikia kilio chao, Buyaga alisema hiyo ni hatua nzuri ambayo licha ya kusaidia kuongeza mapato na ajira, pia inawapa nguvu ya kujitanua kusaka masoko katika majeshi ya nchi nyingine. “Awali, tulipokwenda nchi nyingine kuomba kuuzia majeshi viatu, walitaka kuona kama tunauza pia kwa jeshi ndani ya nchi yetu,” alisema. Buyaga alisema wakati wakiendelea na mkakati wa kuhimiza umma kuthamini bidhaa za nchini, pia wanaendelea kutafuta masoko ya nje zaidi. Kwa sasa wanauza viatu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Uganda na Rwanda. Akielezea soko katika nchi jirani ikiwamo DRC ambayo ni nchi mwanachama SADC, alisema aina ya viatu wanavyopeleka ni buti za usalama wakati Uganda wanauza zaidi viatu vya shule. Alisema kupitia maonesho ya viwanda ya SADC yaliyohitimishwa rasmi jana, amekutana na kuzungumza na kampuni moja ya Zimbabwe ambayo imeonesha utayari wa kuwa msambazaji wa viatu wanavyozalisha. Wakati huo huo, kiwanda hicho kimefunga maduka yake, badala yake, kazi ya uuzaji viatu itafanywa na mawakala. Buyaga alisema walikuwa na maduka Dar es Salaam, Kahama, Mwanza, Mbeya, Arusha lakini sasa yamebaki mawili yaliyoko Mnazi Mmoja na Msimbazi, Dar es Salaam.
1kitaifa
MBUNGE wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ataweka mashine 40 za kuchuja maji katika vituo vya kutolea huduma za afya maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.Akizungumza wakati akifungua mradi wa maji Shule ya Sekondari Mpunguzi, jijini Dodoma, Mavunde amesema anakusudia kuagiza mashine hizo 40 kuweka maeneo ya kutolea huduma za afya ili wananchi wapate maji safi ya kunywa.Mavunde ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira amesema, mashine hizo moja inagharimu Sh 900,000.Amesema zitawekwa maeneo hayo ya kutolea huduma za afya vituo vya afya na zahanati, ili wananchi wanaofika vituoni wanywe maji hayo.Alisema lengo ni kuhakikisha maji yanayotoka kwenye mabomba au matangi yanachujwa na kuwa safi na salama kwa watu wote kuyatumia.Akikabidhi mashine hiyo katika sekondari ya Mpunguzi, Mavunde alisema, wanafunzi wa shule ya sekondari hiyo watatumia vikombe vyao kupata maji kutoka kwenye mashine hiyo ili kuhakikisha afya zao zinakuwa salama.Akizungumzia mradi huo wa kuchuja maji, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari, Menrad Mtewele, alimpongeza mbunge kwa kutekeleza ahadi ya kufikisha maji shuleni hapo na kuwapa mashine ya kuchuja maji.Mtewele alisema, mbunge Mavunde alitoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya mwaka jana, na katika kipindi kifupi ametekeleza ahadi kwa kufikisha maji na kuweka tangi na mabomba shuleni hapo.Akizungumzia uwezo wa mashine hizo, Joan Khone alisema zinaweza kuchuja maji kwa zaidi ya asilimia 99 na asilimia moja inayobaki moja inachujwa kwa chujio lingine la mashine hiyo.Alisema kuchuja maji kutaepusha wananchi kupata magonjwa yakiwemo yanayotokana na uchafu, kipindupindu na homa za matumbo.“Mashine hizo zina chujio ndogo ambazo hazipitishi wadudu wa aina yoyote isipokuwa maji tu na zinaweza kuhakikisha maji ya kunywa yanakuwa safi na salama,” alisema.Alisema mashine hizo zinasaidia kuweka maji safi na salama, tofauti na kutumia vyombo vya kuchemsha kama sufuria au kingine ambacho kinaweza kuongeza uchafu kama ukungu.Alisema mashine yenye uwezo wa kuchuja maji ya ziwani, mtoni na mabwawa kwa asilimia 99, ina uwezo wa kuchuja maji yenye chumvi kwa asilimia 60, hivyo ni mashine bora.
1kitaifa
Nyemo Malecela -Kagera MUUGUZI aliyetumbuliwa wakati wa kuondoa watumishi hewa mkoani Kagera, Dezber Solomon (49) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa darasa la sita, Alinda Reverian (14) baada ya kumfanyia jaribio la kumtoa mimba. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bukoba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Februri 8, mwaka huu saa sita mchana katika eneo la Kilimani nyumbani kwa Vedastina Chreophas. Kamanda Malimi alidai kuwa Alinda aliyefanyiwa jaribio la kutoa mimba kwa njia isiyokuwa halali na salama, alikuwa anasoma darasa la sita Shule ya Msingi Kilimani iliyoko Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera. “Siku ya tukio marehemu alikwenda nyumbani kwa Solomon ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kibwenge kilichopo Halmashauri ya Bukoba, ambaye aliwahi kufanya kazi katika Zahanati ya Buzi iliyoko katika halmashauri hiyo. “Lakini alifukuzwa kazi na Serikali katika zoezi la kuondoa watumishi hewa waliojipatia kazi kwa kutumia vyeti vya kughushi, ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa hana cheti cha kidato cha nne, lakini akaendelea kuhudumia wagonjwa mtaani bila kibali na kwa kificho,” alidai Kamanda Malimi.  Alisema marehemu alikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa ambako inadaiwa alipatiwa matibabu ya maumivu ya tumbo kitendo ambacho ndugu na jamaa wanashuku ndicho kilichosababisha kifo chake. Kamanda Malimi alisema mtuhumiwa amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi wakati mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kagera. “Uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni kutobolewa kwa mfuko wa uzazi na kuingiziwa madawa sumu katika jaribio la kutoa mimba,” alidai Kamanda Malimi. Katika tukio lingine, Februari 9, mwaka huu saa tano usiku katika Mtaa wa Rwazi, Kata ya Kahororo, Manispaa ya Bukoba, Buberwa Mberwa (14) mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Kahororo alikutwa akiwa amejinyonga kwa kujitundika kwenye nondo ya dirisha kwa kutumia mkanda wa begi ambao alikuwa akiutumia kufunga suruali. Alisema marehemu alikuwa anaishi na mama yake pekee baada ya baba yake kuwatelekeza na kusababisha hali yao ya maisha kuwa ngumu. Inadaiwa kuwa marehemu aliwahi kuwa na tatizo la afya ya akili. “Inaelezwa kwamba kabla ya tukio hilo, saa 12 jioni marehemu aliporejea nyumbani, aliwakuta watoto wa baba yake mdogo ambao ni Kakuru Laurent (8), mwanafunzi wa darasa la pili Kahororo na Kato Laurent (8), mwanafunzi wa shule hiyo wakichezea mkanda huo akawataka wampe mkanda wake wakamkatalia. “Walipomuona kachukia waliamua kumpa mkanda wake na kuondoka kwenda kwao kutoka alipokutwa amejinyonga,” alisema Kamanda Malimi.
5afya
THE HAGUE, UHOLANZI KIKAO cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague, Uholanzi kilisitishwa ghafla jana baada ya mmoja wa washtakiwa, Slobodan Praljak, kudaiwa kunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu. Praljak (72), alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa kijeshi wa Bosnia wenye asili ya Croatia, ambao walikuwa wanasikiliza uamuzi wa mwisho wa rufaa uliokuwa ukitolewa na Mahakama Maalumu ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uhalifu uliofanyika Yugoslavia (ICTY) nchini hapa. Vyombo vya habari vya Croatia, vinasema mshtakiwa huyo alifariki dunia, lakini mahakama hiyo ya UN ilisema haiwezi kuthibitisha mara moja taarifa hizo. Alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 mwaka 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar. Baada ya kusikiliza hukumu kuwa majaji wamepitisha kifungo hicho, alimwambia jaji, ‘nakunywa sumu, mimi si mhalifu wa kivita’ huku washtakiwa wenzake wakimwangalia bila kuamini kinachotokea. Uhalifu huo wa kivita unatokana na vita ya mwaka 1992-95 baina ya Wacroatia wa Bosnia na Waislamu. Praljak alisimama na akainua mkono wake hadi kwenye kinywa chake, kisha akainamisha kichwa chake nyuma na kuonekana kunywa kitu kutoka katika kichupa kidogo. Jaji Mwandamizi Carmel Agius, mara moja alisitisha shughuli na gari la kuwabeba wagonjwa likaitwa. “Sawa,” alisema Jaji Agius na kuendelea: “Tunaahirisha, pazia tafadhali, usiondoe kichupa ambacho amekitumia alipokunywa kitu.” Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kutoka The Hague, Anna Holligan, alisema kuwa kabla ya pazia kurejeshwa, ukumbi wa mahakama ulionekana kujawa na mkanganyiko. Gari la kuwabeba wagonjwa lilifika baadaye nje ya ukumbi, huku helikopta ikiruka juu angani na wafanyakazi kadhaa wa uokoaji kuingia ukumbini na vifaa vyao. Zaidi ya saa moja baada ya tukio hilo, mlinzi mmoja aliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa Praljak alikuwa bado anatibiwa, lakini baadaye taarifa za vyombo vya habari zilisema amefariki dunia. Praljak, anadaiwa kutochukua hatua zozote akiwa kamanda wa wahudumu wakuu wa Jeshi la Walinzi wa Wacroatia wa Bosnia (HVO) wakati walipokuwa wakiwakamata Waislamu majira ya joto mwaka 1993. Aidha hakuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa kuwa mauaji yalikuwa yamepangwa, na mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa na kuharibiwa kwa daraja la kale la mji wa Mostar na misikiti. Mahakama hiyo, ambayo iliundwa 1993, itamaliza kazi  yake mwisho wa mwaka huu.
3kimataifa
Na Nathaniel Limu-Ikungi  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, ameagiza Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Paulo Makaka, asimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabali ikiwamo ya upotevu wa vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais Dk John Magufuli. Makaka anatuhumiwa kupoteza vitambulisho 580 vyenye thamani ya Sh milioni 14 pamoja na upotevu wa kitabu cha leseni chenye namba 801 hadi 900. Dk. Mwanjelwa alitoa agizo hilo juzi wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri huyo.  “Huyu ofisa biashara sio mwaminifu hata kidogo. Naagiza asimamishwe kazi kuanzia leo (10/01/2020) asikanyange ofisini. Mtumishi huyu amechafuka na hasafishiki.  “Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa) telekelezi majukumu yenu chunguzeni  tuhuma zinazomkabili afisa biashara huyu,” alisema Dk. Mwanjelwa Aidha aliwataka wakurungezi wa halmashauri nchini, kuchukua hatua stahiki haraka, dhidi ya watumishi ambao wanakwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. “Mkurugenzi au mkuu wa idara asiyekemea uovu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, atakuwa ni sehemu ya uovu husika. Mkurugenzi au mkuu wa idara, unapashwa uwajue watumishi wako ambao wanafanya mambo kinyume na sheria, kanuni na taratibu. Ukiwatambua washughulikie haraka,” alisema Dk. Mwanjelwa. Katika hatua nyingine, aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya nchini, kutenga muda kufanya mikutano ya mara kwa mara kupokea kero zinazowakabili watumishi walio chini yao. Vile vile kupokea ushauri, mapendekezo yatakayotolewa na watumishi hao. Alisema kuwa mikutano hiyo itasaidia kuimarisha mahusiano mazuri ya karibu, yatakayosababisha kufanya kazi kama timu moja.  Aliwataka wasiwe miungu-watu, wasikilize changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia majawabu. Kwa upande wa watumishi wa umma, Dk. Mwanjelwa, amewataka wathamini na kupenda kazi walizopewa. Wachukulie kazi kama fursa, katika ustawi wa maisha yao. “Niwapongezeni kwa kupata fursa hii ya kuwa watumishi wa umma. Kupitia kazi zenu, mnaaminika mbele ya jamii. Mtumishi wa umma anakopesheka haraka kuliko mtu mwingine. Ninyi ni vioo kwa jamii”,alisema na kuongeza;  “Lakini baadhi ya watumishi mavazi yao tu yanawaondoa kwenye utumishi wa umma. Watu wanaanza kuulizana hivi huyo ni mtumishi wa umma kweli. Hakikisha unakuwa mtanashati wakati wote na vitendo vyako visiwe vya ajabu ajabu,” alisisitiza. Wakati huo huo, Dk. Mwanjelwa aliipongeza Halmashauri ya Ikungi kwa kusimamia vema utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
1kitaifa
KAMPALA, UGANDA RAIA wa Uganda wanaotumia mitandao ya jamii kama vile Facebook na WhatsApp, huenda wakalazimika kulipa ili waruhusiwe na Serikali kuitumia. Hii ni baada ya Bunge kuidhinisha muswada huo tata juzi Jumatano. Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa leo, wanaotumia mitandao ya jamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda (shilingi 100 za Tanzania) kila siku. Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, ambazo zitakuwa zikitozwa asilimia moja ya thamani yake. Mwezi uliopita, Rais Yoweri Museveni, alikaririwa na vyombo vya habari akisema mitandao ya jamii inatumiwa zaidi kwa taarifa za udaku. Lakini wanaharakati wa haki za binadamu hawakubaliani na madai yake. “Ni sehemu tu ya majaribio ya kubana uhuru wa kujieleza,” Mwana Blogu Rosebell Kagumile aliliambia Shirika la Habari la Reuters. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wabunge watatu walikosoa sheria hizo mpya na kuzitaja kama ‘utozaji wa kodi maradufu’. Wabunge hao; Robert Kyaggulanyi, maarufu kama Bobi Wine (Kyaddondo Mashariki) na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon, walisema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia muda wa salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki. Mbunge mwingine, Patrick Nsamba wa chama tawala, alisema ushuru huo utawaumiza zaidi masikini. Ni rahisi kwa mbunge kusema asilimia moja ni kiasi kidogo cha kosi, lakini kwa watu wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku itawaumiza zaidi.
3kimataifa
SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Nchini (Tanesco) mkoa wa Pwani, linatarajia kuongeza vituo vidogo vya uzalishaji umeme ili wawekezaji wa viwanda wapate umeme wa kutosha.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonyesho ya Viwanda jana, Ofisa Mwandamizi wa Tanesco mkoa wa Pwani, Alex Mosha alisema kwa sasa mkoa unapata umeme wa megawati 80 hadi 85 ambazo zinatosheleza mahitaji lakini kutokana na kasi ya uanzishwaji wa viwanda umeme huo hautatosheleza. Alisema kuwa kuna vituo kadhaa vitakavyojengwa ili kupeleka umeme kwenye viwanda vya mkoa huo na kwamba kwa sasa wanatumia vituo vyaa Ubungo, Mlandizi na Chalinze.“Vituo vipya ni Luguruni ambacho kitakuwa na transfoma mbili za MVA 60 kila moja, Zegereni ambako ndiko kwenye eneo la viwanda ambao kwa sasa wanatumia kituo cha Mlandizi. Alisema kituo cha Mlandizi ambacho kimeelemewa na kwamba watabadilisha transfoma mbili za MVA 10 na zitawekwa za MVA 20,” alisema Mosha.Alisema Mkuranga wanatumia kituo cha Mbagala ambacho kimeunganishwa na ilala na Kunduchi na kwamba ikitokea tatizo Mkuranga hutumia kituo cha Bunju. Kwa mujibu wa Mosha umeme wa Bunju unakwenda Bagamoyo na Zinga hadi Chalinze kwa ajili ya wilaya hiyo ya Bagamoyo.
1kitaifa
KAMISHINA wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Gabriel Malata ametoa siku saba kuanzia jana kwa Kampuni ya Kichina, inayofanya kazi ya ujenzi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam (CHEC), kuhakikisha inawapa mikataba ya ajira wafanyakazi wote wa kampuni hiyo ambao hawana mikataba.Mikataba hiyo imeelezwa kuwa itawasaidia wafanyakazi hao kulipiwa kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kwa kufanya hivyo, Serikali nayo itapata mapato kupitia Kodi ya Mapato ya Mshahara (PAYE).Malata ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wake na vyombo vya habari, baada ya kusuluhisha mgogoro huo, uliozuka tangu mwaka jana kati ya kampuni hiyo na wafanyakazi wake.Kwa mujibu wa Malata, wafanyakazi wa CHEC walikuwa na malalamiko kadhaa dhidi ya mwajiri wao, hali iliyosababisha kuwepo kwa mgomo wa chini chini, ambao aliumaliza juzi baada ya kuwa na majadiliano ya siku mbili na pande hizo husika.Miongoni mwa malalamiko ya wafanyakazi hao dhidi ya mwajiri wao ni kupewa mikataba kandamizi ya kazi, ambayo ilikuwa haioneshi muda wa uhai wa mkataba pamoja na wafanyakazi kuachishwa kazi kinyemela kwa madai kuwa mkataba maalumu umekwisha.Malata alitaja malalamiko mengine ya wafanyakazi hao kuwa mkataba huo, ulikuwa unampa nguvu mwajiri kufanya mabadiliko ya majukumu ya mfanyakazi pasipo kuzingatia maslahi na nafasi husika, lakini pia kupitia mkataba huo, malipo ya mshahara kwa sasa yanawatambulisha wafanyakazi hao kama vibarua, hivyo kuwaondolea haki ya kupata mikopo katika taasisi za kifedha.“Kwa mujibu wa taarifa ya mwajiri ambayo bado tunaendelea kuifanyia kazi, kampuni ina jumla ya wafanyakazi 370, kati yao 88 hawana mikataba ya kazi kwa kuwa ni waajiriwa wa chini ya mwezi mmoja, hata hivyo mwajiri hakuweza kuthibitisha idadi kamili ya wafanyakazi alionao, hivyo nimeagiza hawa wote 88 wapewe mikataba ya ajira ndani ya wiki moja kuanzia leo (jana),” alieleza Kamishina.Malata pia alitoa mwezi mmoja kwa mwajiri kuanzia jana, kuhakikisha maazimio mengine yote waliyokubaliana, yanatekelezwa na ofisi yake ipewe taarifa, la sivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.Miongoni mwa maazimio hayo ambayo yalitokana na kiini cha mgogoro kati ya wafanyakazi na mwajiri ni mwajiri kuhakikisha anakomesha vitendo vya unyanyasaji, ikiwemo matumizi ya lugha chafu kwa wafanyakazi yanayofanywa na wafanyakazi wa kigeni, ubaguzi kwa baadhi ya huduma, matibabu kwa wafanyakazi ikiwemo kuwapima afya wanapoingia, wanapokuwa kazini na wanapoondoka.Mengine wafanyakazi kuruhusiwa kukopa katika taasisi za fedha baada ya kurekebisha mikataba yao, mwajiri kushiriki kikamilifu mfanyakazi anapokufa akiwa kazini ikiwemo kutoa rambirambi, kununua jeneza na kusafirisha mwili, chama cha wafanyakazi na wafanyakazi kutafuta suluhisho la matatizo na mwajiri kwa mazungumzo, badala ya kuhamasisha migomo mahali pa kazi.Mkurugenzi wa bandari hiyo, Freddy Liundi alisema mgogoro uliokuwepo kati ya wafanyakazi na mwajiri, haukuathiri shughuli za ujenzi wa upanuzi wa bandari kwani ulidumu kwa saa nane kabla ya kupatiwa ufumbuzi.Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi (TASIWU), Likulile Ally alimshukuru Kamishina Malata kwa kuutatua mgogoro huo kwa muda mfupi na kuahidi kushirikiana na mwajiri katika kutimiza kazi zao.
1kitaifa
Yanga ambayo ilianza vyema michuano hiyo haijafungwa mchezo hata mmoja baada ya kushinda michezo mitatu na mabao tisa, huku ikiwadhibiti wapinzani kwa kutoruhusu bao hata moja katika nyavu zake.Aidha, KCC ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo, pia wamekuwa wakifanya vizuri baada ya kushinda michezo miwili na kupata sare moja katika mchezo wao wa kwanza.Akizungumza na kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na Azam Tv, Kitambi alisema sababu kubwa ya kuzipa nafasi timu hizo katika hatua ya fainali ni kutokana na upinzani waliouonesha tangu kuanza kwa michuano hiyo.“Kwangu mimi nazipa nafasi timu hizi kwa sababu ndizo ambazo zimekuwa zikinivutia soka lake, ingawa kuna changamoto ndogo zilizoonekana, lakini nikilinganisha na timu nyingine naona hizo zina afadhali,” alisema.Alisema Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amekuwa akifanikiwa kutokana na mfumo ambao hutumia.Alisema Yanga wanaweza kufanikiwa katika mchezo wa robo fainali utakaopigwa leo dhidi ya JKU kama timu hizo zitaendelea kucheza kwa mifumo tofauti kama ilivyoonekana katika michezo iliyopita.Kitambi alisema timu ya Azam Fc ilijitahidi lakini bado inasua sua ndio maana hakuipa nafasi huku akisema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog hajakipanga kikosi vizuri kiasi cha kuonesha wazi kuwa hajapata 11 bora ya kikosi cha kwanza.
2michezo
NA ZAINAB IDDY, WAWAKILISHI Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga wameendelea kupoteza mwelekeo katika harakati za kutinga nusu fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Ndoto ya Yanga kutinga hatua hiyo ilianza kuyumba baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 wakiwa ugenini nchini Algeria walipocheza na Mo Bejaia, kabla ya kuja kufungwa nyumbani idadi kama hiyo hivyo na TP Mazembe ambao ni mabingwa wa mwaka jana katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Kilio cha Wanajangwani na Watanzania kwa ujumla ni kuona Yanga inawatoa kimasomaso kwa kuingia fainali kama ilivyokuwa kwa watani zao, Simba mwaka 1993. Lakini juzi Yanga walijikuta wakilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Medeama ya Ghana. Kwa matokeo ya michezo mitatu iliyocheza Yanga, imeambulia pointi moja, ikiwa inaburuza mkia katika kundi lake A, iliyopo sambamba na Medeama walio nafasi ya tatu, Bejaia walioshika namba mbili na Mazembe walioongoza kundi kabla ya mchezo wao wa jana na Bejaia. Ni wazi matokeo hayo yanaifanya Yanga kupoteza matumaini ya kutinga nusu fainali licha ya kocha wake mkuu, Hans van de Pluijm, kusema kuwa wana nafasi ya kuingia nusu fainali jambo ambalo linaonekana ni sawa na ndoto za mchana kulingana na pointi walizonazo wapinzani wake pamoja na mechi zilizobaki kwa Wanajangwani hao. Iwapo kama tutatumia usemi wa Kiswahili unaosema yaliyopita  yamepita tugange yajayo, basi ni wazi Yanga inawalazimu kuchukulia mashindano hayo kama sehemu ya kujifunza kwa ajili ya mashindano ya mwakani ambayo tayari wameshakata tiketi ya kushiriki. Kwa hivi sasa ni wazi hatua iliyofikia Yanga ni somo kwao hivyo wanapaswa kulitumia kujiandaa na mwakani, lakini pia wakitakiwa kutambua kuwa kuna vitu lazima wavifanyie kazi, ili kutimiza nia yao iliyoelekea kuwashinda mwaka huu, miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na:- Ushindi wa nyumbani Kosa kubwa ambalo mwaka huu Yanga wamelifanya katika michezo yake kimataifa ya klabu ingwa kisha kombe la shirikisho baada ya kuangukia pua, ni kuruhusu kupoteza mechi za nyumbani. Licha ya rekodi kuonyesha Wanajangwani mara nyingi wamekuwa na matokeo mazuri ugenini, lakini mara nyingi ushindi wa nyumbani unaibeba timu. Ni wakati wa kocha Hans van de Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, kutafuta plani B ambayo itawawezesha kuwa na matokeo mazuri nyumbani. Usajili wa kiungo mshambuliaji Tatazo la kiungo mshambuliaji linaendelea kuiandama Yanga, kwani hivi sasa wanamtumia Thaban Kamusoko ambaye hana uwezo mzuri wa kupandisha na kushusha mpira uwanjani. Awali, alikuwa akiimudu nafasi hiyo Salumu Telela, lakini baada ya Yanga kuamua kuachana naye kumekuwa na tatizo kubwa kwenye kiungo mshambuliaji. Ni wakati wa benchi la ufundi kuangalia namna wanavyoweza kulimaliza tatizo la kiungo mshambuliaji ambaye atakuwa na sifa stahiki, ili kuisaidia katika mechi za kimataifa mwakani. Semina elekezi ya CAF Ni kawaida kabla ya kuanza mashindano yoyote lazima kutolewe semina elekezi itakayotoa mwongozo wa jinsi gani timu zitashiriki michuano hiyo. Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), kama ilivyokuwa katika mashindano lilitoa waraka kwa timu zilizokuwa zinacheza kuwania kuingia hatua ya makundi (Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho) kupeleka majina ya maofisa watakaohudhuria semina ya namna ya kuratibu mechi hizo kuelekea fainali lakini pia walitakiwa kupeleka vivuli (photocopies) vya hati zao za kusafiria. Maofisa waliohitajika ni meneja wa timu, daktari wa timu na ofisa habari wa timu, TFF iliwafikishia ujumbe Yanga kabla ya kucheza na Esperanca ya Angola kwa kuwataka kutuma nyaraka hizo kati ya Aprili 26 na Aprili 28, 2016. Cha ajabu Yanga wanaojiita wa kimataifa, walishindwa kutekeleza maagizo hayo licha ya taarifa hizi na hata ukumbusho (reminders) zilipelekwa kwa barua pepe, simu na hata kuonana ana kwa ana kwa Katibu Mkuu wa Yanga, ofisa habari na viongozi wengine wa klabu. Madhara ya kutoshiriki semina hiyo yaliweza kuonekana katika mchezo wa kwanza wa Yanga dhidi ya Mo Bejaia pale walipozuiliwa kutumia baadhi ya vitu vyao ikiwemo maji na jezi zenye nembo ya wadhamini Kilimanjaro. Siku moja kabla ya washiriki kuanza kuwasili Cairo, Misri, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga alituma nyaraka kama zilivyotakiwa na wakatumiwa tiketi tatu (3) na CAF. Pamoja na tiketi kuletwa Yanga bado watu hao hawakusafiri wakidai klabu haijatoa ruhusa. Umri wa wachezaji Tatizo kubwa lililopo sasa ndani ya timu ya Yanga ni kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa jambo ambalo linasababisha kutoendana na kasi iwapo watakutana na wachezaji wanaokimbia na mpira. Wachezaji kama Kamusoko, Kelvin Yondani, Nadir Harub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite na wengineo, licha ya kucheza kandanda safi lakini mara nyingi hawawezi kuendana na kasi ya kimchezo wanapokutana na wanandinga damu zao zinazochemka. Ifike wakati Yanga isiangalie kiwango cha mchezaji pekee  bali izingatie umri wa mwanandinga, kwani kusajili mchezaji mkubwa kiumri kunasababisha kuitumikia timu kwa muda mfupi kuliko thamani ya fedha alizosajiliwa.
2michezo
Miongoni mwa vifaa hivyo ni mashine ya kukaushia nywele, vifaa vya kuoshea nywele, viti na masinki. Vitendea kazi hivyo mbalimbali vitamuwezesha kupanua wigo wa huduma zinazopatikana katika saluni yake.Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel , Hawa Bayumi alisema sambamba na kuongeza idadi ya huduma zitakazopatikana katika saluni ya Prisca, vifaa hivyo vitamuwezesha kuhudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja.Alisema hali hiyo itamuwezesha Prisca kuajiri vijana wenziwe ili kuendeleza biashara na kukuza kipato chake.Bayumi alisema mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali vijana ili kuwaongezea kasi ya maendeleo ya kibiashara ni sehemu ya kurudisha mapato ya kampuni hiyo kwa jamii kwa namna inayoleta tija kwa taifa.“Sisi tumeona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa,” alisema meneja huyo.Awali akipokea msaada huo Prisca ameshukuru kwa vifaa hivyo na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa.“Naahidi kuongeza juhudi na kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara yangu lakini pia nitatoa fursa kwa vijana wenzangu,” alisema Prisca. Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali.
0uchumi
Yanga juzi ilikuwa ugenini Uwanja wa Kambarage Shinyanga kupambana na Mwadui FC, na kulazimishwa sare ya 2-2, matokeo ambayo yameiweka rehani nafasi yake ya kuongoza ligi hiyo.Akizungumza na gazeti hili Pluijm, alisema safu yake ya ulinzi iliwanyima pointi tatu kwenye mchezo huo kitu ambacho kinaweza kuwagharimu kutokana na ushindani mkali uliopo kati yao na wapinzani wao Azam FC.“Hatukucheza kwenye kiwango chetu cha kawaida, lakini tulistahili ushindi kutokana na namna ambavyo wachezaji wangu walivyocheza kwa kujitolea na kupata mabao yale mawili.“Hata hivyo safu yetu ya ulinzi ilituangusha kwa kuruhusu bao la kusawazisha la dakika za mwisho,” alisema Pluijm. Mholanzi huyo alisema matokeo hayo siyo mabaya, lakini wanalazimika kupambana kwenye mchezo wao unaokuja dhidi ya Kagera Sugar ili kurudisha wimbi lao la ushindi na kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya ubingwa msimu huu.Alisema katika mchezo huo wapinzani wao Mwadui, walionekana kucheza kwa kutumia nguvu nyingi na kuwakamia, kitu ambacho kiliwasumbua wachezaji wake kushindwa kuonesha kiwango chao cha kawaida ambacho wamekuwa wakikionesha kwenye michezo iliyopita.“Mchezo ulikuwa mgumu kwa sababu tulicheza na timu ambayo ilipania kutuvurugia mipango yetu kwa kucheza vurugu, lakini nimefurahi kupata sare hiyo kwa sababu vijana wangu walilazimika kubadilika na kuendana na hali ya mchezo ilivyokuwa,” alisema Pluijm.Katika mchezo huo mabao ya Yanga yote mawili yalifungwa na Mzimbabwe Donald Ngoma, huku yale ya Mwadui yakifungwa na Poul Nonga na Bakari Kigodeko na kuifanya timu hiyo ya Jangwani kufikisha pointi 20 katika mechi nane ilizocheza msimu huu.
2michezo
Ramadhan Hassan, Dodoma Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Makubaliano Kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya Rom Solution Company Ltd ya nchini Romania wanatarajia kuhojiwa leo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma. Wajumbe hao sita wameitwa katika mahojiano hayo wakiwa na laptop walizopewa na Kampuni ya Rom Solution. Kwa mujibu wa Takukuru wanaohojiwa leo ni Kamishna wa Zimamoto, Mbaraka Semwanza, Naibu Kamishna wa Zimamoto, Fikiri Salala, Naibu Kamishna wa Zamamoto, Lusekela Chaula, Naibu Kamishna wa Zimamoto, Ully Mburuko, Ofisa Ugavi Mkuu wa Zimamoto, Boniface Kipomela na Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Felis Mshana.
1kitaifa
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM NJOMBE Mji imesisitiza bado haijapotea njia na kilichotokea kwenye mechi zao mbili zilizopita ni upepo tu lakini hali itakuwa tulivu. Njombe Mji imevurunda mechi zake zote mbili za Ligi Kuu msimu huu, ikianza kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Prisons kabla ya kubanduliwa bao 1-0 na Yanga wikiendi iliyopita. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Njombe Mji, Erasto Mpeka, alisema licha ya kupoteza michezo yote waliyocheza mpaka sasa, hali hiyo haijawakatisha tamaa badala yake wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. “Malengo yetu ni yale yale toka mwanzo ya kumaliza nafasi tatu za juu, kama tukishindwa kabisa basi tusikosekane kwenye 10 bora,” alisema Mpete. Hata hivyo, alisema bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa hasa ya kifedha lakini wanapambana kusaka wadhamini ili kuzitatua. “Kuna changamoto kadhaa hasa katika gharama, lakini tunajitahidi kwenda nazo sawa, tunategemea sapoti kubwa sana ya wapenzi wa soka hapa Njombe,” alieleza mwenyekiti huyo. Njombe Mji itashuka dimbani Jumapili kuumana na Mbeya City katika pambano la ligi hiyo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
2michezo
MOSCOW,  Urusi URUSI na Misri zimesema zitaendelea kushirikiana katika nynja mbalimbali ili uhusiano baina ya mataifa haya mawili uweze kufika ngazi nyingine. Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa hapa,  Sergey Lavrov kupitia ujumbe aliouandika katika jarida la  Time-Tested Friendship na kuchapishwa katika tovuti ya gazeti la  Al-Ahram  la  Misri. Lavrov alisema uhusiano  wa siasa kati ya nchi hii na Misri unazidi kukua na biashara baina ya mataifa haya mawili inazidi kuchanua tangu ilipofikia wastani wa dola  bilioni 6.5  kwa mwaka. “Ushirikiano katika nyanja za jeshi unawezesha vikosi vya Misri na utekelezaji wa sheria kupinga vitisho vya ugaidi kwa ufanisi zaidi,” alisema waziri huyo. “Aina mpya za ushirikiano katika nyanja hii zinajaribiwa kwa ufanisi. “Oktoba 2016 katika mkutano uliofanyika katika ardhi ya  Misri na   Septemba 2017 katika  mkutano uliofanyika  Urusi kwa pamoja tulikubaliana  kupambana  dhidi ya ugaidi  na katika mkutano wa utetezi wa urafiki uliofanyika mwaka  2016  na mwaka  2017  ambao ulivihusisha vikosi vya anga vya mataifa haya mawili,”aliongeza waziri huyo. Alisema Urusi na Misri zimekuwa zikishirikiana kwa karibu katika kutatua migogoro mbalimbali duniani  kujenga umoja miongoni mwa jamii.
3kimataifa
Mwanamzuiki Naseeb Adbul (Diamond) amesema alikuwa akimsikitia msanii mwenzie Vanessa Mdee pindi aliposaini mkataba wa kujiunga na kampuni ya Universal Music kwa ajili ya kusimamia kazi zake za muziki. Diamond amesema yeye ana uzoefu juu ya mikataba ya makampuni ya kimataifa ya lakini alikaa kimya kwakaua alijua kama angeongea kuhusu ugumu wa kufanya kazi na makampuni hayo angeonekana mbaya mbele za watu. “Nisiwe mnafiki, Nimefanya kazi na Universal takribani miaka miwili na nusu nimemalizana nao mwaka huu. Nisiwe mnafiki ninapoona msanii yeyote akisaini mara ya kwanza namsikitikia. Dada yangu vanessa mdee alivyosigniwa niliwaambia uongozi kwamba duuh natamani ajue anachoenda kukutana nacho. Lakini mimi sio mtu wa kuongea mitandaoni nakaaga tu kimya” amesema Diamond. Ikumbukwe mapema mwezi Juni Vanessa Mdee alitangaza kuacha muziki kutokana na tasnia hiyo kujaa na mambo ambayo hayapo hayafurahishi na kutishia uhai wake.   @diamondplatnumz akiongelea suala la vanessamdee kuilaumu Lebo ya Universal, kuwa ni moja ya sababu iliyompelekea Kuacha Muziki. Leo kwenye press conference ya @wcb_wasafi ! #HiiNiYetuSote #IAMZUCHU18JULY A post shared by Maulid Kitenge (@kitengemaulid) on Jul 13, 2020 at 12:49pm PDT
4burudani
WATU wanne wamekufa papo hapo katika ajali iliyohusisha magari mawili yaliyogongana na kulipuka katika eneo la Nyangoye katika Kata ya Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Revocatus Malimi amesema ajali hiyo ilitokea juzi saa tatu usiku ikihusisha gari lenye namba za usajili T869CHT aina ya Toyota Hiace iliyokuwa inatoka maeneo ya Hamugembe pamoja na gari la mizigo aina ya Mitsubishi Canter lenye namba za usajili T223 ATK, lililokuwa linatokea Rwamishenye kwenda Mjini Kati.Kamanda Malimi alisema magari hayo yaligongana na kuanguka pembeni mwa barabara na kuanza kuungua, na kusababisha vifo vya watu wanne ambao ni Niece Gerevace (30), dereva wa Hiace mkazi wa Rwamishenye, Prudence Themistocles (30), mkazi wa Rwamishenye, dereva wa bodaboda aliyesababisha ajali ya magari hayo.Wengine ni Peter Ifunya (31) aliyekuwa kondakta wa Hiace mkazi wa Rwamishenye na Dickson Bakuza ambaye alikuwa dereva wa Mitsubishi Canter aliyekuwa amebeba matikiti maji katika gari lake.“Tulichokibaini ni kwamba ajali imetokana na uzembe wa madereva ambapo dereva wa Hiace alijaribu kumpita dereva wa pikipiki na baadaye akajikuta amegongana na Canter na magari yao kupinduka pembeni ya barabara na kuanza kuwaka moto,” amesema Kamanda Malimi.Alitoa mwito kwa madereva kuwa makini na eneo hilo na kufanya kazi yao kwa umakini kwani eneo hilo lina mlima na bado lina kona hivyo wanapaswa kuzingatia sheria za barabarani wanapokuwa wanaendesha.Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, na kuna majeruhi wawili ambao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo. Hao ni Amry Mohamed (35) na Joseph Athanazi (30).Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa, Felix Otieno amethibisha kupokea miili ya watu wanne na majeruhi watatu, na kwamba majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu na afya zao zinaendelea vizuri.
1kitaifa
Mama wa nyota wa Bongo Fleva Diamond platnumz na mumewe maarufu kwa jina la Uncle Shamte wameendelea kujivinjari kila kona kwa kuonesha mapenzi yao. Tangu mwanaume huyo ahusishwe na tuhuma za kuchepuka, wawili hao ni kama wanazidi kuwa wapya kutokana na mapenzi kedekede wanayoendelea kuoneshana hadharani kupitia mitandao ya kijamii. Lakini jambo la kushtua licha ya mapenzi motomoto anayoonesha kwa mumewe huyo, familia ya Shamte wala haina muda na mama huyo. Hii imekuja baada ya Mama Dangote kupewa za uso na dada wa mumewe na kumwambia asijipendeze kwani familia hiyo haimuhitaji. Mama Dangote na mumewe ShamteMama Diamond ameambiwa maneno hayo baada ya kuposti picha ikimuonesha Shamte na wadada wawili na kuweka maelezo yanayosema hiyo ni familia ya Shamte. Haya ndiyo maelezo ya aliyoandika Mama Dangote kwenye picha hiyo; Shamte’s family ….Ahmada Shamte Shamte's family….👨‍👧‍👧💞💞💞 @estercaree Ahmada shamte A post shared by Sandrah…! (@mama_dangote) on Aug 24, 2019 at 12:08am PDT Baada ya posti hiyo, dada wa Shamte ambaye anajulikana kwa jina la Raya amwambia Mama Dangote aache kutumia jina la familia hiyo kwani wao hawatambui mahusiano ya wawili hao. Maoni ya watu mbalimbali wisdom_and_joy Karma is truly a bitch 😩. What bibi did to Hamisa is coming back to bite her. 🙌🏾 tupilike_mwakajange Yaan Mungu. Wetu nae kaona. Arahisishe. Kipengere cha malipo duniani. Yani analipa fasta fasta . wtu tunaenjoy….. Mwmbien mama enu na bado maana warugulu. Sio wanafki😅😅 sala.gloria Thanks lord god is good karma is a bitch maman dangote you got wat you deserve 👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽 This is not the first time Rally Jone’s sister is proving that her family does not like Sandra. After Rally’s baby mama gave birth, she went to see the baby something that caused an uproar on social media.
4burudani
Na MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuanza kwa mvua za masika na kutahadharisha mamlaka za miji kuweka sawa miundombinu ya kupitisha maji ili kuondoa uwezekano wa kutokea mafuriko ambayo yanaweza kuathiri jamii. Kutokana na hilo, TMA imezishauri Mamlaka ya Maafa na wadau wengine kuchukuwa hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, mipango na kujiandaa kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea kutokana na mwenendo wa mvua. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, alisema mamlaka hizo na wananchi wanashauriwa kuhakikisha wanajiandaa kwa kuweka sawa mindombinu inayowazunguka ili kujihakikishia usalama wakati wa mvua za masika ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa katika baadhi ya mikoa. “Kutokana na uwezekano wa vipindi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa, tunashauri mifumo na njia za kupitishia maji kufanya kazi sawa na hatua hizo zichukuliwe hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani kwa sababu vipindi vifupi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza,” alisema Dk. Kijazi na kuongeza.  “Kutokana na uhaba wa maji salama unaotarajiwa kwa shughuli za binadamu, ikiwamo usafi, wananchi wanashauriwa kuchukua hatua stahiki kuzuia milipuko ya magonjwa,” alisema Dk. Kijazi. Aidha mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kutoakana na hali ya ukame ulioyakumba maeneo mengi ya nchi, sasa yanaweza kupata mvua, hivyo wanatakiwa kupata ushauri wa maofisa kilimo kujiandaa kwa kilimo. “Maeneo ya kusini na pwani ya kusini ambayo ni mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara, mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi isipokuwa katika maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Lindi ambako mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa,” alisema Dk. Kijazi. Ukanda wa Pwani ya Kaskazini unatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani, vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko hafifu wa mvua katika baadhi ya maeneo hayo,” alisema. Kwa mujibu wa Dk. Kijazi, mikoa ya Kanda ya Ziwa Viktoria inatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani, huku Nyanda za Juu Kusini zikitazamiwa kuwa na mvua za wastani au chini ya hapo.
1kitaifa
NDEGE nyingine mpya aina ya Bombardier D8 Q400 na Boeing B787-8 Dreamliner zinatarajiwa kuletwa mwishoni mwa mwaka huu.Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Khadija Nassir Ali (CCM).Mbunge huyo alihoji kwa kuwa serikali inaendelea na ununuzi wa ndege; haioni ni wakati muafaka kuhakikisha ndege hizo zinakwenda kila mkoa wenye kiwanja na nchi jirani kusaidia kushusha gharama za usafiri.Nditiye alisema matarajio ya serikali ni kuwa ujio wa ndege hizo utawezesha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuwa na ndege za kutosha na kutoa huduma za usafiri wa anga kwa ufanisi na tija.Alisema ATCL itakuwa na mtandao wa safari mikoa mingine na safari kikanda na kimataifa.“Uwapo wa ndege mpya za kutosha utaiwezesha ATCL kuhimili ushindani wa kibiashara katika utoaji huduma za usafiri wa anga katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa,” alisema.Alisema upanuzi mtandao wa huduma za usafiri wa anga katika kila mkoa wenye kiwanja cha ndege na nchi jirani, unatekelezwa kwa mpango mkakati wa ATCL wa miaka mitano unaoishia mwaka wa fedha 2021/2022 pamoja na mpango wa biashara unaoandaliwa kila mwaka.Alisema hadi sasa ATCL inasafirisha abiria katika mikoa tisa na nchi tano. Mikoa hiyo ni Dodoma, Mwanza, Kagera, Kigoma, Mbeya, Kilimanjaro, Zanzibar, Tabora na Mtwara.ATCL inatoa huduma Hahaya (Moroco), Harare (Zimbabwe), Bujumbura (Burundi), Entebbe (Uganda) na Lusaka nchini Zambia. Utoaji wa huduma unazingatia uwapo abiria wa kutosha kuifanya kampuni hiyo ijiendeshe kwa ufanisi.Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo (CCM) alitaka kufahamu kwa nini bei ya tiketi za ndege ATCL isishuke kuwezesha watu wengi kumudu usafiri.Naibu waziri alisema bei hupungua kutokana na soko.Alisema ATCL iko kwenye ushindani na mashirika mengine yakitoa huduma, bei itashuka. Ndege hizo mbili zikiwasili zitafanya nchi kuwa na ndege nane zilizonunuliwa na serikali ya awamu ya tano.Ndege zilizopo sasa ni Airbus A220-300 iliyopokewa Januari mwaka huu. Nyingine ni Bombardier Dash 8 Q400 tatu zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, Boeing 787-8 Dreamliner moja yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja.
0uchumi
Yanga iliifunga Mtibwa kwenye Uwanja wa Amaan, katika mchezo wa mwisho wa Kundi B wa michuano hiyo, huku mabao yake yakifungwa na Issouf Boubacar na Malimi Busungu na lile la Mtibwa lilifungwa na Shiza Kichuya.Maxime alisema mechi yao dhidi ya Yanga ilikuwa safi,ambapo aliridhika na matokeo na hana wa kumlaumu kwani walishindwa kimchezo tu. “Natamani kukutana na Yanga katika fainali kwani najua tutacheza soka la kuvutia na siyo la hovyo, unajua zikikutana timu zinazojua mambo huwa mazuri na ni rahisi kucheza kwa mfumo,”alisema Maxime.Mtibwa Sugar leo inacheza na Simba katika mchezo wa mwanzo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi huku Yanga wakishuka baadae usiku kucheza na URA ya Uganda. Mtibwa ilimaliza nafasi ya pili katika Kundi B ikiwa na pointi nne, huku Yanga ikiwa kileleni na pointi saba wakati Mafunzo ilishika nafasi ya tatu na pointi mbili huku Azam FC ikishika mkia ikiwa na pointi mbili tu. W
2michezo
Bakari Kimwanga na Ramadhan Hassan-DODOMA MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, ameeleza masikitiko yake jinsi baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama hicho (UVCCM), walivyoshindwa kuenzi misingi ya chama hicho baada ya  mwenyekiti wa umoja huo, Sadifa Juma Khamis kutiwa mbaroni na Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Sadifa alikamatwa juzi jioni mjini hapa na maofisa wa Takukuru kwa tuhuma za kugawa fedha kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM akidaiwa kuwashawishi wamchague mmoja wa wagombea aliyekuwa akimuunga mkono. Kamanda wa Takukuru  Mkoa wa Dodoma, Emme Kuhanga, alithibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa UVCCM. Akifungua mkutano huo   mjini hapa jana, Rais Dk. Magufuli alisema  baadhi ya vijana wamepoteza dira tofauti na viongozi wa zamani ambao walikuwa wakiandaliwa vema kuwa viongozi wa baadaye. “UVCCM ya zamani siyo sawa na hii ya sasa. Vijana wa sasa wanakwenda kwenye mikutano wanapigana, wengine wanatoa rushwa. “Ninavyozungumza hapa, mwenyekiti wenu (Sadifa Juma Khamis) yupo lock-up kwa kushikwa na rushwa. Huo ndiyo umoja wa vijana tuliokuwa tunakwenda nao, sitaki kusema sana. “Mimi nina imini sana na vijana, mkiamua jambo mnaweza ila bahati mbaya kuna wachache mlipotezwa na watu fulani fulani hapa kati. “Ningependa ieleweke kwamba ujana pekee haukufanyi uwe hazina kwa chama au taifa. Ni lazima uwe mzalendo, mchapakazi, muadilifu na kadhalika, hizo ndizo baadhi ya sifa za kijana. “Kijana ambaye ni fisadi, mvivu, mla rushwa, tapeli, mtumia dawa za kulevya na kadhalika, ana mchango mdogo kwa taifa. Nimeanza kueleza kwa kutaja sifa hizo za kijana kwa makusudi kabisa,” alisema Rais Magufuli Kutokana na kukamatwa kwa Sadifa  leo ndipo itajulikana hatima yaka kama atafikishwa mahakamani au la. Rais alisema   pamoja na kusaidiwa na vijana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, lakini alishangazwa  na umoja huo kushindwa kumpa orodha ya vijana wanaofaa katika uongozi. “Niwaeleze ukweli, vijana walinisaidia sana wakati wa kampeni lakini nashangaa nimekuwa nikiletewa majina ya wanaopendekezwa kwa nafasi mbalimbali ila sikuletewa hata jina moja kutoka UVCCM. “Vijana wengi wa UVCCM walikosa nafasi mbalimbali za uteuzi. Lazima wajumbe mumtangulize Mungu mbele kwa kutambua wajibu wenu kwenye uchaguzi huu kwa sababu  mtakaowachagua ndiyo watakuwa washauri wangu,” alisema. KIONGOZI BORA Rais Dk. Magufuli aliwashangaa wanaotoa rushwa ili wachaguliwe wakati yeye hakutoa hata senti moja kuwahonga wajumbe  wamchague. “Mimi nasema ukweli hata Mungu ananisikia, sikutoa hata senti moja ili nichaguliwe. “Nitashangaa sana kama mtamchagua mwenyekiti aliyewahonga. Kila mwenye uwezo kwenye umoja wa vijana amewekewa vigingi vya kila aina, nawaomba wajumbe tuanzishe ukurasa mpya UVCCM. “Kuonyesha ni kiasi gani ninavyowaamini vijana, kwenye Serikali yangu nimeteua vijana wengi na hawajaniangusha. Msichague mtu kwa sababu ya dini yake, kabila lake, mnatoka ukanda mmoja au fedha zake  ila chagueni mtu sahihi mwenye sifa za kuwa kiongozi. “Ninahitaji mchague viongozi wazuri watakaofanya kazi kuliko ilivyo sasa ambako umoja wetu una vitega uchumi, lakini fedha hazijulikani zinakokwenda. “Pale wana jengo kubwa la UVCCM, lakini wameishia kugawana vyumba tu. Ila kwa dhati ninampongeza Shaka (Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM), amefanya kazi kubwa,” alisema. VIJANA NA KUJITAMBUA Akizungumzia eneo hilo  aliwataka vijana wajitambue kwa kuwa huu ni wakati wao wa kushika uongozi. “Ninawaomba vijana wa UVCCM mjitambue kwa sababu huu ni wakati wenu wa kushika dola. “Nisingependa kuona sisi tunaondoka halafu anachukua kijana anayepokea rushwa, tutakuwa tumeliuza taifa na kukiuka misingi tuliyoachiwa na waasisi wetu. “Kwa sababu kama kiongozi anapokea rushwa, hata akiteuliwa kuwa waziri, atapokea rushwa tu na anaweza kumuuza hata mshikaji wake kwa rushwa. “Mimi siyo rais wa maisha, muda wangu utaisha kama itakavyokuwa kwa Dk. Shein (Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar),” alisema Rais Dk. Magufuli. Aliwaomba vijana wa CCM wajiamini kwa kujibu hoja wala wasisubiri kuambiwa. “Bahati nzuri mimi huwa nasoma, nimemuona Msando akitumia taaluma yake ya sheria kujibu hoja kuhusu ibara ya 45 jana (juzi) na sikumtuma ila alisukumwa na profession yake ya sheria. “UVCCM ilikuwa ni jumuiya ya watu wenye uwezo ambao baada ya kukatishwa tamaa waliamua kuhama na kwenda kwenye vyama vingine, lakini leo wanarudi walikotoka. “Hata Profesa Kitila (Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji), alijaribu kugombea, lakini akazuiwa na kwenda alikokuwa, lakini sasa amerudi,” alisema. AVUNJA BODI UVCCM Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa CCM alihoji kazi za bodi ya wadhamini ya UVCCM kwa kuwa haiwanufaishi vijana. “Leo ndiyo uchaguzi na bodi nayo iondoke … hii hata kama wapo kina Lukuvi (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) iondoke tu. “Na nyie viongozi mliopita ndani ya umoja kama kina Mavunde, muwe mnakuja kuzungumza na viongozi angalau hata kwa kunywa maji na kushauriana, kumbukeni mlipotoka, hilo ni jambo jema,” alisema. Awali, akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa wajumbe wa mkutano mkuu huo, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema wanachama wameongezeka kutoka 200,000 hadi kufikia milioni 1.7. Kwa mujibu wa Shaka, UVCCM imetoa asilimia ipatayo 75 ya watu kwenda kufanya kazi kwenye jumuiya nyingine ikiwamo serikalini. “Kuanzia mwaka 2012 hadi sasa, UVCCM ngazi ya taifa imefanya ziara kwenye mikoa yote nchini na imeendelea kushiriki na kuwa chachu ya ushindi kwenye uchaguzi mbalimbali wa Serikali. “Jumuiya imeendelea kufanya uhakiki wa mali zake, tumenunua magari mawili mapya na tumeruhusu jumuiya ifanyiwe ukaguzi wa hesabu. “Kwa hiyo, Dk. Magufuli tunakuomba utupatie eneo mkoani Dodoma tuwekeze kisasa ikiwamo kujenga jengo la kudumu litakalozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018. WANACHAMA WAPYA Katika mkutano huo, wanachama wapya waliojiunga na CCM walizungumza. Aliyekuwa wa kwanza ni aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF). Katika maelezo yake, alisema  ameacha kila kitu na kujiunga CCM kutokana na kuridhishwa na utendaji wa Serikali. Naye aliyekuwa Mbunge wa Kasulu Mjini, kupitia NCCR-Mageuzi, Moses Machali, alisema alilazimika kuhamia CCM kwa kuwa kuna timu ya ushindi. Aliwataka UVCCM kutumia mitandao ya  jamii kwa kuwa vyombo vya habari vinaweza kuyafanya mambo mazuri yaonekane ni mabaya na mabaya yaonekane ni mazuri. Naye  aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila,  alisema aliamua kuhamia CCM kwa sababu ajenda ya ufisadi imehama. “Sasa kuna utu na usawa nchini. Tanzania ya sasa imebadilika. Tunashuhudia matajiri wakilazwa mahabusu. “Hii imesababisha  kiwango cha ufisadi kupungua nchini. Dhamira ya Dk. Magufuli haina shaka na uzalendo wake ni wa kuigwa,” alisema Kafulila. Aliyekuwa Mwanasheria wa ACT-Wazalendo, Albert Msando, aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuwachagua viongozi wasafi. Wakati hao wakisema hayo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema, Patrobas Katambi, aliwataka UVCCM kutoruhusu watu wengine kutumia nafasi nyingine za demokrasia kuvuruga amani ya nchi.      
1kitaifa
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM KIPA wa timu ya Simba, Hussein Shariff ‘Casillas’, amesema hayupo tayari kutolewa kwa mkopo kwenda timu nyingine, huku akidai bora aache kabisa kuitumikia timu  hiyo na kuwa mchezaji huru. Cassilas amekuwa majeruhi kwa muda mrefu baada ya kuumia goti walipokuwa kambini nchini Afrika Kusini mwaka jana, hali iliyopelekea kukaa muda mrefu bila kucheza, ambapo inadaiwa uongozi wake unataka kumtoa kwa mkopo. Akizungumza na MTANZANIA jana, Cassilas alisema yupo tayari kuondoka Simba, lakini si kwa kutolewa kwa mkopo na kusisitiza kuwa anajiamini kutokana na uwezo mkubwa wa kudaka aliokuwa nao. “Najiamini na kazi yangu ndiyo maana mpaka sasa timu yangu inanihitaji kutokana na kazi yangu ninayoifanya, isitoshe, nimeshakuwa kipa bora kwa misimu miwili mfululizo, kwa hilo najivunia,” alisema. Alisema atakaporudi kazini ataendelea kufanya vizuri zaidi, hivyo mashabiki wategemee mambo mazuri zaidi atakaporudi dimbani rasmi kutokana na kumkosa kwa muda mrefu alipokuwa majeruhi. Kamati ya Usajili ya Simba chini ya Mwenyekiti, Zacharia Hans Poppe, wameiongezea nguvu safu ya langoni baada ya kuonekana kulegalega msimu uliopita na kupelekea Simba kushika nafasi ya tatu. Mpaka sasa imemsajili kipa mpya kutoka JKU ya Zanzibar, Mohamed Abraham Mohamed, aliyefanya safu hiyo kuwa na makipa watano, wengine wakiwa ni mkongwe, Ivo Mapunda, Manyika Peter Jr,  Casillas pamoja na kipa aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, Denis Richard. Hivyo, kuna hofu kubwa ya Casilas na Richard kuenguliwa kwenye usajili wa timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
2michezo
BEI ya kakao kavu kutoka kwa wakulima wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro imeongezeka kutoka wastani wa kilo moja Sh 2,000 hadi 2,500 msimu uliopita hadi Sh 3,500 hadi 5,000 mwaka huu.Ofisa Kilimo wa Kata ya Mbingu wilayani Kilombero, Ally Mohamed Mula amesema hayo hivi karibuni mjini Morogoro alipozungumza na gazeti hili juu ya mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la kakao katika kata hiyo na maeneo mengine ya wilaya yenye kustawi kwa zao hilo jipya ndani ya Wilaya ya Kilombero.Zao la kakao linalimwa zaidi na wakulima wa vijiji vya Kata ya Mchombe, Mbingu na Mngeta katika Tarafa ya Mngeta, na ni zao jingine la kibiashara licha ya mpunga ambao ambalo pia ni la chakula wilayani humo.Mula amesema wilaya hiyo ina wakulima zaidi ya 2,600 wanaozalisha zao la kokoa na wengi wao ni kutoka katika ukanda wa vijiji hivyo vitatu ambao kwa msimu uliopita uzalishaji kiwilaya ulikuwa ni tani 358 za kokoa kavu.Amesema uzalishaji wa kilimo cha kokoa katika maeneo hayo umekuwa uliongezeka kutokana na wakulima kuona hilo ni zao litakalowaongezea kipato kiuchumi kitakachowasaidia kuleta maendeleo yao na familia zao.
0uchumi
Na MWANDISHI WETU HABARI kubwa iliyotikisa nchini Kenya na duniani kwa ujumla wiki hii ni kukamtwa kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Henry Rotich, na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka 24 ikiwamo matumizi mabaya ya ofisi, kupanga udanganyifu na kushiriki kwa miradi pasipo kuwa na mipango. Rotich anashitakiwa pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kamau Thugge, na maofisa wengine 26 wa serikali. Miongoni mwa mashitaka yanayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha ni sakata la mabilioni ya ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror yaliyopo kaunti ya Elgeyo Marakwet. Kufikishwa mahakamani kwa Rotich na wenzake ilikuwa suala la muda tu kwa sababu Machi 6 mwaka huu, waziri huyo wa zamani alifika mbele ya wapelelezi katika makao makuu ya Ofisi za Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na kuhojiwa kwa siku nzima kuhusu mradi huo wa mabwawa. Rotich alitakiwa kueleza nini anachokifahamu kuhusu utata unaozunguka mradi wa mabwawa ya Arror na Kimwarer. Siku iliyofuta mawaziri wengine, Mwangi Kiunjuri (Kilimo), Peter Munya (Afrika Mashariki) na Adan Mohamed (Viwanda) pia walihojiwa. Kiunjuri, moja wa waziri wengine wanaokalika kuti kavu, wakati wa sakata hilo alikuwa Waziri wa Ugatuzi maarufu serikali za majimbo na alikwapo wakati mikataba ikitolewa kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa hayo kwa Kampuni ya CMC Di Ravenna, yenye makazi yake nchini Italia. Ofisi ya DCI iliwahoji makatibu wakuu wote wa zamani na wa sasa kuanzia siku ambayo wazo la kujenga mabwawa hayo ilibuniwa. Sakata hilo ambalo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Noordin Haji, amelieleza kama kesi ya ufisadi mkubwa nchini Kenya katika siku za hivi karibuni, ilisababisha Kenya kuomba msaada kutoka Italia, Uingereza na Dubai hatimaye kupata ushahidi unaohitajika kuanza mashtaka. Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka unaoongozwa na Taib Ali Taib, akisaidiana na Alexander Muteti, Victor Owiti na Emily Kamau huku kikosi cha upande wa utetezi kinawajumuisha Katwa Kigen, Kioko Kilukumi, Philip Nyachoti, Kipchumba Murkomen, Kevin Anami, Mwai Mugo, Stephen Kimathi, Mahat Samane na Jinaro Kibet. DPP Haji aliagiza kukamatwa kwa maofisa hao wakuu serikalini baada ya kufanya uchunguzi uliodumu kwa miezi tisa kuhusu ujenzi wa mabwawa hayo uliokadiriwa kugharimu Shilingi za Kenya bilioni 65. Rotich ni nani? Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya mseto kufuatia machafuko ya Uchaguzi Mkuu 2007, alimvuta Rotich karibu kufanya naye kazi kutokana na uelewa wake wa masuala ya uchumi. Kabla ya kuletwa karibu na Uhuru, Rotich alihudumu akiwa mwanauchumi katika Shirika la Fedha Duniani (IMF) ofisi zake za Nairobi mwaka 2004 baada ya kufanya kazi kwa muda mchache na Benki Kuu ya Kenya. Katika azma ya kukonga nyoyo za Wakenya wakati anasoma bajeti yake ya kwanza akiwa Waziri wa Fedha, Rotich alimwaga fedha kwa miradi kama vile Galana Kulalu irrigation scheme na Standard Gauge Railway ambayo ingebadilisha sura ya Kenya. Lakini kitendo chake cha kukopa mamilioni ya fedha huku kukiwa hakuna maelezo yanayokidhi kuhusu matumizi ya fedha yenyewe, kuliacha maswali mengi na kutumbukiza taifa katika wimbi la madeni makubwa. Haishangazi wakati DPP akitangaza kukamatwa kwa Rotich na wenzake sababu kubwa iliyokuwa inajitokeza ni kivipi mabilioni ya fedha kutoka kodi ya wananchi na nyingine za kukopa yanakosa maelezo ya kina ya namna zilivyotumika. “Ungetarajia hakuna tatizo kwa miradi ambayo ipo kisheria na imefuata taratibu zote lakini kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika na malipo kinyume ya sheria yote yakifanyika machoni mwa maofisa wa Serikali wakishirikiana na taasisi binafsi ziliibua maswali mengi,” alisema Haji. Rotich ambaye ni mzaliwa wa Elgeyo Marakwet, sehemu ambayo mradi huo wa mabwawa ungejengwa, sasa anajikuta katikati ya siasa na kesi ya ufisadi inayomkabili. Wakazi wa eneo hilo ambao waliondolewa na kuahidiwa kulipwa hadi sasa wanalalamika kwamba ahadi haijatekelezwa. Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa hususan anapotoka Naibu Rais, William Ruto, wametafsiri kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Rotich kumefanyika kisiasa lengo likiwa ni kumdhoofisha Ruto anayetajwa kuwania urais 2022. Seneta wa Elgeyo Marakwet, ambaye pia ni kiongozi wa walio wengi Bunge la Seneti, Kipchumba Murkomen, amepinga kukamatwa kwa Rotich akisema haileti picha halisi ya mapambano dhidi ya ufisadi mbali kuwadanganya Wakenya kuonyesha vita dhidi ya ufisadi imeshika kasi. “Nikiangalia ushahidi uliopo na mambo yanayoendelea nyuma ya pazia, nikiangalia watu waliokamatwa, waliyoachwa, namna walivyokamatwa na sababu zinazotolewa ikiwamo miradi inayohujumiwa, nimefikia hitimisho kwamba tunachokifanya ni kuwadanganya Wakenya,” alisema. Rotich na wenzake kwasasa wapo nje kwa dhamana, japo DPP alipinga mahakama kuwapa washukiwa dhamana. Kutokana na mahakama kuwazuia kurudi kazini, Rais Uhuru amemteua Waziri wa Kazi, Ukuru Yatani, kukaimu nafasi ya Waziri wa Fedha huku akifanya mabadiliko katika nafasi za makatibu wakuu.
3kimataifa
MWENYEKITI wa Bodi ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania na aliyewahi kuwa Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu (71) amefariki dunia jana jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Nundu alifikishwa jana hospitalini hapo akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.Aidha, baada ya uchunguzi, waliompeleka hospitali waliamua wakahifadhi mwili wake katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo pia jijini Dar es Salaam.Juni 12, mwaka huu, Rais John Magufuli alimteua Nundu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Uchukuzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu ya Airtel ikiwa ni makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Bharti Airtel International.Kabla ya hapo, mbunge huyo wa zamani wa Tanga Mjini alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Mohamed Mtonga.TTCL kwa upande wake ilithibitisha kifo hicho na kueleza kushtushwa na kifo cha Nundu aliyechaguliwa kuongoza Jimbo la Tanga Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
1kitaifa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na aliyekuwa makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha. Aveva na Kaburu wame- kuwa ndani tangu mwaka 2017 walipokamatwa. Dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili watakao- saini bondi ya Sh.Milioni 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 7 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha. Hata hivyo washitakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wamerudishwa mahabusu ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope. Kutokana na hatua hiyo washtakiwa hao wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sa- babu mashitaka ya utakatisha- ji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo alisema jukumu la kuthibitisha shitaka kwa washitakiwa ni kwa upande wa mashitaka, pia kwa kosa moja moja na sio kwa kutegemeana. Hakimu Simba alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashitaka ambapo amewakuta na kesi ya kujibu washitakiwa hao katika kosa la 1,2,3,4,7,8 na 9 isipokuwa katika shitaka la 6 na 10 ambayo ni ya utakatishaji fedha. “Mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliyokuwa yanawanyima dhamana washitakiwa hayapo, je upande wa mashitaka wana pingamizi na dhamana ?,” Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Takukuru, Leornad Swai alieleza hawana pingamizi ambapo Hakimu Simba aliwapatia masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh Milioni 30 kila mmoja. Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo kwa ajili ya washitakiwa kuanza kujitetea. Katika kesi hiyo shtaka la kwanza, linawakabili Aveva na Kaburu ambapo wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.Katika shtaka la pili la Aveva na Kaburu wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays. Shtaka la tatu linalowakabili Aveva na Kaburu inadaiwa kwa pamoja walighushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa Dola za 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli. Katika shtaka la nne Aveva katika banki ya CRDB anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000. Shtaka la tano, Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola za Marekani 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi. Shtaka la sita, Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia Dola za Marekani 187,817 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi. Shtaka la saba linawakabili Aveva, Kaburu na Hanspoppe ambao wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Marekani 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli. Katika shtaka la nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo kwa Levison Kasulwa kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577. Shtaka la tisa ni, Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577.
2michezo
UMOJA wa Wanawake CCM Wilaya ya Ruangwa (UWT) umewataka wanawake kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi, ili waweze kutoa mchango wao kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano katika harakati ya kuwaondolea kero wananchi wake. Hayo yalielezwa na Mbunge Viti Maalumu, Hamida Abdala (pichani) kwenye kikao cha baraza cha umoja huo, kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM wilaya ya Ruangwa.Hamida ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho, aliwasisitiza wanawake kuiunga mkono serikali na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa kwa juhudi zake anazozifanya. Aidha, Hamida aliwataka wanawake kujipanga kushika nyadhifa za uongozi ndani na nje chama. “Wanawake msiniangushe, zinapotokea nafasi za uongozi, hakikisheni nanyi mnapigania na kuwa viongozi, hata kwa nafasi ya ubunge kwenye majimbo ya mkoa huu, sio vibaya wabunge wanawake wagombee…inawezekana,” alisema Hamida. Kwenye baraza hilo lililoongozwa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya, Adela Ng’onye, Hamida alikabidhi jezi za mpira wa miguu kwa Katibu wa CCM wa Wilaya, Barnabas Essau kwa niaba ya timu ya mpira wa miguu ya Kijiji cha Namienje Kata ya Chibula. UWT Wilaya ya Ruangwa walimhakikishia mbunge huyo kuwa asiwe na wasiwasi, kwani wana muunga mkono na wanaunga mkono juhudi zake yeye kama mbunge wa mkoa huo pamoja na mbunge wa jimbo na serikali.
1kitaifa
TEXAS-Marekani KARIBU  watu 20 wameuawa, huku wengine 26 wakijeruhiwa wakati wa  ufyatuliaji wa risasi katika duka la jumla mjini El Paso, jimboni Texas Gavana wa jimbo hilo, Greg Abbot alilitaja shambulio hilo kuwa mojawapo ya siku mbaya zaidi katika historia ya jimbo  hilo. Maofisa wa polisi, wanachunguza iwapo shambulio hilo ambalo lilifanyika maili chache kutoka kwa mpaka wa Marekani na Mexico, lilikuwa la uhalifu wa chuki. Mtu mwenye umri wa miaka 21, sasa anazuiliwa na maofisa wa polisi. Polisi wanasema, mshukiwa  alikuwa akiishi katika eneo la Allen , Dalla umbali wa  kilomita 1,046 mashariki mwa El Paso. Ametajwa na vyombo vya habari vya Marekani kuwa, ni Patrick Crusius. Kanda za video za CCTV zilizodaiwa kuwa za mshambuliaji huyo ambazo zilionyeshwa katika vyombo vya habari vya Marekani, zinaonyesha mtu aliyekuwa amevalia fulana  nyeusi na vilinda masikio. Shambulio hilo, linaaminika kuwa la nane katika historia ya sasa nchini hapa. Linatokea chini ya 24, baada ya shambulio jingine la kuwafyatulia risasi watu waliokongamana, mjini Dayton Ohio na chini ya wiki moja, baada ya mshambuliaji kijana kuwaua watu watatu katika tamasha la chakula mjini California. Maofisa wa polisi na wenzao wa ujasusi wa Shirika la Upelelezi (FBI), wanafanya uchunguzi iwapo manifesto ya kitaifa iliochapishwa katika kundi moja la mtandao, iliandikwa na mshambuliaji huyo. Chapisho hilo, linadai shambulio lililenga jamii ya Wahispania. Duka hilo ambalo liko karibu na duka jingine kubwa kwa jina Cielo Vista Mall, lilikuwa limejaa wateja waliokuwa wakinunua bidhaa za wanao wao kurudi shule. Rais wa Marekani, Donald Trump alielezea shambulio hilo kama kitendo cha uoga. ”Najua tunaungana na kila mtu katika taifa hili kushutumu kitendo hiki cha chuki, hakuna sababu ambazo zinaweza kukufanya kuwaua watu wasio na hatia” , alindika katika mtandao wake wa Twitter. Waathirika bado hawajatajwa, lakini Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador alisema raia wake watatu, ni miongoni mwa waliofariki dunia, kulingana na Shirika la Habari la Reuters. “Sisi kama taifa tunaungana kuwaunga mkono waathiriwa na familia zao” , alisema Abbot. Ofisa Mkuu wa Polisi wa El Paso, Greg Allen alisema ripoti za mtu aliyekuwa akiwafyatulia watu risasi kiholela ndani ya duka hilo, ziliripotiwa mwendo wa saa za Marekani 10:39 na maofisa walitumwa katika eneo la mkasa huo chini ya dakika sita. Kianna Long, alisema alikuwa katika duka hiyo na mumewe wakati waliposikia mlio wa risasi. ”Watu walikuwa na wasiwasi na kukimbia , wakisema  kulikuwa na mtu aliyekuwa akiwafyatulia risasi, Long aliamba Reuters. Shahidi mwengine,Gleondon Oakley aliambia CNN alikuwa katika duka la bidhaa za michezo karibu na duka la jumla lililopo karibu wakati mtoto mdogo alipotoroka na kuingia ndani na kutuambia kuna mtu anafyatua risasi kiholela katika Walmart.
3kimataifa
Anna Potinus Rais Dk. John Magufuli ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbabwe ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo vimelemaza uchumi wa taifa hilo. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 17, alipokuwa akihutubia wakuu wa nchi Wanachama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo na Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob ambapo ataingoza kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe vinaathiri ushirikiano wake katika Jumuiya ya jumuiya hii ya SADC hivyo ninomba nchi hiyo ipewe nafasi ya pili kwa sababu ina utawala mpya,” amesema. Zimbabwe iliwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi kutokana na hatua ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, kuchukua kwa lazima ardhi ya wahamiaji wenye asili ya kizungu. Aidha Rais Magufuli ameapa kuhakikisha amani inadumishwa ili kukwamua uchumi wa mataifa wanachama wa SADC. “Tunaahidi kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC kuhakikisha kupitia mkutano huu ndoto na mawazo ya Baba yetu wa Taifa pamoja na viongozi wengine waanzilishi wa Jumuiya hii yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo,” amesema.
3kimataifa
Asha Bani, Dar es Salaam Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea anatarajia kupeleka hoja binafsi bungeni kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Afrika wa haki za binadamu kuhusu haki za watu wenye Ualbino Afrika. Amesema mkataba huo ulipitishwa katika mkutano wa 30 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika mwaka jana hivyo anaiomba serikali kufanya marekebisho ya sera ya watu wenye ualbino iliyotungwa 2004 ili kuwasaidia kukomesha vitendo vya kikatili dhidi yao. Kubenea amesema hayo leo Jumapili Agosti 11, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa ameamua kuwatetea watu hao kutokana na kulipa deni aliloachiwa na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu za IPP, marehemu Regnald Mengi. “Nimeamua kufanya hivi kutokana na kutaka kulipa deni ambalo nimeachiwa na marehemu Mengi, mimi hili ndiyo deni langu kuenzi alichokuwa anakifanya na si vinginevyo,” amesema Kubenea. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Jimbo la Ubungo, Mussa Geuza amesema anawaomba wabunge wengine kumuunga mkono Kubenea kwani hoja yake ina mashiko na ustawi kwao.
1kitaifa
JUMLA ya hospitali 13 zinazomilikiwa na vikosi vya ulinzi, ikiwamo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), zimeanza kupata mgawo wa dawa kutoka serikali kuu. Hayo yalibainishwa jana hapa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar jana na Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed.Mohamed alisema Wizara ya Afya imechukua uamuzi huo baada ya kuridhishwa na huduma za vituo hivyo vya afya, ikiwemo hospitali za jeshi. Alisema hayo wakati akiwasilisha makadirio, mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Afya.Aliliomba baraza kuidhinisha jumla ya Sh bilioni 88.6. kwa kazi za kawaida na maendeleo. Alisema mgawo wa dawa zinazosambazwa katika vikosi vya ulinzi zitatolewa bure kwa wananchi wanaokwenda kupata huduma za afya. Alizitaja hospitali zilizoanza kupata mgawo wa dawa kuwa ni hospitali ya Ali Khamis Camp ambayo ni kambi ya JWTZ Pemba, Hospitali ya Bububu, Hospitali ya inayomilikiwa na KMKM iliyopo Bububu na hospitali ya JKU ya Saateni.‘’Hospitali za vikosi vya Ulinzi vya Jeshi na Polisi tumeanza kuvipatia mgawo wa dawa kwa ajili ya hospitali zao na hata zile za vikosi vya SMZ nao wanafaidika na mgao huo,’’ alisema. Alizipongeza hospitali za vikosi vya ulinzi kwa kufanya kazi kubwa kusaidia huduma za afya kwa wananchi wanaoishi Unguja na Pemba. Alisema hospitali hizo zimekuwa na uhusiano mkubwa na wananchi zikitoa huduma bora.
1kitaifa
NA ADAM MKWEPU UONGOZI wa Yanga umetamba kuendelea kutumbua majipu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha wanashinda michezo yake mbalimbali ya ligi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,  Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa  wamejiandaa kupata ushindi dhidi ya Stand United katika mchezo wao utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya ‘figisufigisu’ wanazoendelea kufanyiwa na  wapinzani wao. “Tutaendelea kutumbua majipu, licha ya wapinzani wetu kutufanyia figisufigisu, lakini tunawaambia watasubiri sana mwaka huu na hawataweza,” alisema. Alitoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kwenda kwa wingi kuishangilia uwanjani katika mchezo wao na Stand. Akizungumza juu ya usajili wao, Muro alisema wamesajili wachezaji wawili, akiwamo aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City na baadaye Mwadui ya Shinyanga, Paul Nonga na Mniger, Issoufou Boubacar. Yanga kwa sasa ipo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 27 mbele ya klabu ya Azam, walio na pointi 26.
2michezo
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA  WAKAZI wa Kijiji cha Zepisa, Kata ya Hombolo Bwawani Manispaa ya Dodoma, wamemwomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, awasaidie ili waweze kupata huduma za afya kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo hivyo wakati mwingine kujifungulia porini. Wakizungumza na MTANZANIA juzi kijijini hapo, walisema kijiji hicho kipo umbali wa kilomita zaidi ya 50 kutoka Dodoma Mjini na wamekuwa wakitembea zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma za afya katika Zahanati ya Nunge iliyopo Hombolo. Leah Musa alisema ameshajifungulia mara mbili porini sababu zikiwa ni kurushwarushwa na pikipiki wakati akipelekwa katika kituo cha afya ili kujifungua. “Nikiwaangalia watoto wangu huwa naona huku nipo porini kabisa japo wanasema tupo Manispaa tusaidiwe tuweze kupata zahanati hapa tunapata shida sana wakati wa kujifungua wengi tunajifungulia maporini.” Naye Mwajuma Issa (80), alisema amewasaidia kujifungua zaidi ya kina mama 200 katika kijiji hicho kutokana na kukosekana kwa kituo cha afya. “Nimechoka kuzalisha watu kienyeji, sasa umefika wakati wa kupatiwa na sisi zahanati ili tujifungue vizuri, kiufupi sisi tumesahaulika katika kila kitu,” alisema. Kwa upande wake Zuhura Manyasi, alisema mimba yake ilipofika miezi 8 ilibidi ahamie kwa ndugu zake Dodoma Mjini kutokana na kuogopa kumpoteza mwanawe au yeye mwenyewe. MTANZANIA lilimtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Kunambi ambaye alikiri kijiji hicho kutokuwa na zahanati na kuahidi suala hilo kulighulikia ili waweze kupata huduma za afya. “Pale ujenzi ulishaanza wa zahanati na ulifikia katika hatua ya jamvi, sasa ngoja tujue tunafanyaje, maana na mimi ni mgeni lakini wale wana shida na kule ni mpakani mwa Manispaa na Wilaya ya Bahi,” alisema.
1kitaifa
CAIRO, Misri SERIKALI nchini Misri, imewatia hatiani watu zaidi ya 700 wa kundi la Muslim Brotherhood, ambao walishiriki maandamano yaliyosababisha kuondolewa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hii, Rais Mohammed Morsi, mwaka 2013. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, katika hukumu hiyo ya juzi, watu 75 walihukumiwa vifo na huku wengine  47 wakihukumiwa kifungo cha maisha jela wakiwamo viongozi wa Kiislamu. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International, limeiita hukumu hiyo si ya haki na imevunja katiba ya nchi hii. Ghasia hizo ambazo zilizuka mwaka  2013 katika viwanja vya Rabaa al-Adawiya square, vilivyopo mjini hapa, mamia ya watu waliuawa na vikosi vya usalama. Mapema mwaka huu, bunge la hapa liliwapa kinga ya kutoshtakiwa maofisa wa vyombo vya usalama waliohusika katika mauaji hayo na uhalifu ambao waliufanya kati ya Julai 2013 na Januari  2016. BBC ilieleza kwamba, wale ambao walihukumiwa katika kesi walishtakiwa juu ya makosa yanayohusiana na usalama ikiwa ni pamoja na unyanyasaji, mauaji na kuandaa maandamano haramu. Shirika hilo la utangazaji lilieleza kuwa  watu  75 walihukumiwa kifo tangu Julai mwaka huu na juzi adhabu hiyo ikathibitishwa na hivyo kuwa mwisho wa kesi hiyo. Liliwataja miongoni mwa watu mashuhuri na wanasiasa kutoka Chama cha Muslim Brotherhood ambacho kilipigwa marufuku ni pamoja na kiongozi wao mkuu, Mohammed Badie, mpiga picha mashuhuri, Mahmoud Abu Zeid, maarufu kama Shawkan, ambaye amehukumiwa kifingo cha miaka mitano jela. Mpigapicha huyo alikamatwa na kutupwa rumande, baada ya kukutwa akipiga picha za vurugu hizo za maandamano.
3kimataifa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipunguze viwango vya riba zinazotozwa kupitia mikopo mbalimbali wanayoitoa kwani inawaumiza wajasiriamali.Majaliwa aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Februari 22, 2019) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bomang’ombe, wilayani Hai, Kilimanjaro. Hata hivyo, kiongozi huyo aliwataka wananchi hususani, vijana, wanawake na wenye ulemavu kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa katika Halmashauri yao.Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu imemnukuu Majaliwa akisema “halmashauri inatakiwa itenge asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha vijana, wanawake na wenye ulemavu kupata mitaji.”Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wakulima wa kahawa wabadilike na kuondoa miti ya zamani na kupanda mipya ili waongeze tija. Waziri Mkuu alisema wakulima hao wanaweza kuweka utaratibu wa kuondoa miche ya zamani kwa awamu na kupanda mipya, hivyo kupata mavuno mengi.
1kitaifa
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’  Emmanuel Amunike. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Julai 8, imesema makubaliano hayo yamekuja baada ya pande zote mbili kufikia muafaka wa kusitisha mkataba wa kocha huyo raia wa Nigeria. TFF itatangaza kocha wa muda atayekiongoza kikosi cha Taifa Stars katika mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN). “Makocha wa muda watatangazwa baada ya kamati ya dharura ya kamati ya utendaji (Emergency Committee), itakapokutana Julai 11, mwaka huu,” imesema taarifa hiyo. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48, aliiongoza Stars katika michezo 10, alishinda miwili, sare mbili na kufungwa sita huku timu hiyo ikitolewa katika hatua ya makundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), zinazoendelea nchini Misri.
2michezo
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha maisha jela raia wa Msumbiji, Ana Moisie Chissano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kukamatwa na dawa za kulevya.Aidha, imeamuru dawa za kulevya aina ya Cocaine alizokutwa nazo mshitakiwa kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili. Akitoa hukumu hiyo leo, Jaji Lilian Mashaka alisema ametoa adhabu hiyo kulingana na kifungu namba 15 (1) (b) cha Sheria namba 5 ya mwaka 2015 ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.Jaji Mashaka alisema sheria hiyo inaelekeza mtu yoyote anayejihusisha na dawa za kulevya anapopatikana na hatia anapaswa kutumikia kifungo cha maisha jela. Tangu afikishwe mahakamani, raia huyo ameshakaa gerezani kwa miaka mitatu.
1kitaifa
NAIROBI, KENYA WATUMIAJI wa simu nchini Kenya huenda wakatozwa ada zaidi katika ununuzi wa muda wa maongezi na huduma ya mtandao. Hii ni baada ya serikali kutangaza mpango wa kuongeza kodi ya ongezeko la thamani(VAT) kutoka asilimia 10 hadi 15. Nyongeza hiyo, imejumuishwa katika pendekezo la Rais Uhuru Kenyatta kwa Bunge kufuatia tamko lake la wiki iliyopita. Pendekezo la tozo hilo jipya la kodi likiidhinishwa na Bunge litazidi kuwaumiza watumiaji wa simu, ambao tayari wanakabiliwa na gharama ya ongezeko la ada ya huduma za kutuma fedha. Serikali iliongeza ushuru unaotozwa huduma hiyo kwa asilimia 10 Julai mwaka huu ili kuwezesha kupatikana fedha za kugharimia mpango wa bima ya afya kwa wote ifikapo mwaka 2022. Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya, ushuru huo utaathiri watumiaji wa simu zaidi ya milioni 44.1. Serikali imekuwa ikihamasisha Wakenya kuzingatia malipo ya kielektroniki ili kuboresha huduma na kupunguza visa vya udanganyifu. Huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu, M-Pesa ilikuwa kwa asilimia 14.2, ambayo ni sawa na Sh bilioni 62.9 za Kenya kwa mwaka wa fedha ulioishia Machi 2018. Kodi mpya inayowalenga watumiaji wa simu za mkononi imetokana na ukosoaji mkali dhidi ya serikali kupinga mpango wake wa awali wa kuongeza kodi ya bidhaa za mafuta kwa asilimia 16. Hoja hii ilizua malalamiko makubwa ya umma hatua, ambayo ilimfanya Rais Kenyatta kuingilia kati suala hilo kwa kuipunguza hadi asilimia 10. Rais Kenyatta amesema kuwa bado kuna pengo katika bajeti ya serikali na ndio sababu ya kupendekeza hatua hizo za kufunga mkanda na kubana matumizi katika idara zote za serikali Mapendekezo hayo, hata hivyo yanatarajiwa kujadiliwa bungeni jana.
3kimataifa
Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM ILIKUWA Februari 2, mwaka 1974, katika mbio za mita 1,500 upande wa wanaume kwenye fainali za mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Christchurch, New Zealand ambapo Filbert Bayi alitumia dakika 3 na sekunde 32.16. Akiongoza kuanzia mwanzo wa mbio hizo hadi mwisho, Mtanzania pekee aliyeweka rekodi duniani, Filbert Bayi, alimaliza mbio hizo ambazo zinaelezwa kuwa ni miongoni mwa mashindano makubwa duniani. Mwanariadha huyu nyota nchini, aliyezaliwa katika mkoa ulioko maeneo ya Bonde la Ufa (Rift Valley), Arusha maarufu kwa kutoa wanariadha wazuri hapa nchini, anasema hali ya hewa na mfumo wa maisha ya watu wa mkoa huo unachangia kutoa maarifa kwa wakimbiaji wa mbio ndefu. “Wazazi wangu walikuwa wakulima, wafugaji wa ng’ombe, nilipokuwa mtoto, nilikuwa naangalia mbuzi na ng’ombe, nikiwa kwenye vichaka nachunga mifugo, nawinda, nakimbia na mbwa, nakimbia na wanyama, nafikiri hiyo ndiyo iliyonifanya niwe na stamina katika ukimbiaji. “Kila asubuhi nilikuwa nakimbia  kwenda shule  na natakiwa kurudi kwa chakula cha mchana, kisha natakiwa kurudi tena kwa masomo ya jioni, hivyo unaweza  kuhisi nilikuwa nakimbia kilomita nane kwa siku,” anasema  Bayi. Kauli hii ya Bayi inaakisi matokeo ya riadha ya mwanariadha, Alphonce Felix Simbu, kutoka Mkoa wa Singida aliyeshiriki mashindano ya Olimpiki mwaka huu na kuibuka mshindi wa tano. Simbu mwenye umri wa miaka 24, ameweka historia kwa taifa kwa kushika nafasi ya tano, akitumia muda saa 2:11:15 katika mbio ndefu ‘marathon’ akiwaacha wanariadha 155 walioshiriki mbio hizo, lakini hakuweza kupata medali yoyote. Kabla ya kuelekea nchini Rio de Jeneiro, Brazil, kushiriki michezo hiyo, Simbu amekuwa akijituma sana katika mazoezi na mke wake, Rehema Daudi, anasema: “Kila siku huwa anafanya mazoezi asubuhi na kwenye maeneo haya ya jirani na nyumbani na hasa maeneo ya milimani na amekuwa akifanya hivyo kila siku,” alisema Rehema. Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka, anasema kabla ya kuelekea kwenye michezo ya Olimpiki, Simbu aliweka kambi miezi sita katika Chuo cha Wakala wa Misitu (FITI), kilichopo Siha mkoani Kilimanjaro chini ya kocha wake, Fransic John, baada ya kufikia viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Dunia la mchezo huo (IAAF). Mfumo huo wa maisha ambao Bayi anasema unachangia kuwawezesha wanariadha kufanya vizuri hivi sasa unatoweka na hivyo wanariadha wanatakiwa kufanya mazoezi kwa mtindo wa kisasa. Akizungumza na MTANZANIA SPOTIKIKI kuhusu wanamichezo walioshiriki michezo ya Olimpiki iliyomalizika, Bayi anasema tunahitaji uwekezaji wa kutosha iwapo tunataka kufanikiwa katika michezo  kwani  wanamichezo wetu hawakuwa na maandalizi ya kutosha. Licha ya mwanariadha, Simbu kufanya vizuri kwa kushika nafasi ya tano, Mkenya, Eliud Kipchoge, alishinda mbio hizo na kutwaa medali ya dhahabu. Bayi ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki nchini (TOC), anasema tunatakiwa kuwekeza kwa wanamichezo kwa kuweka programu za muda mrefu kwa kuandaa wachezaji. Anasema hatuwezi kufanya vizuri kama wenzetu wa nchi zilizoendelea kama Marekani, Ufaransa, Ujerumani kama hatutapata makocha wenye uwezo na viwango vya kimataifa. Aidha, Bayi anasema wachezaji wanatakiwa kuandaliwa kwa muda mrefu kabla ya kwenda kushiriki katika mashindano ya kimataifa. Licha ya mwanariadha huyu kijana kutoka Singida Kijiji cha Mampandu, kufanya vizuri kwa kushika nafasi ya tano, Bayi amedai tunahitaji uwekezaji mkubwa katika riadha kwa kuandaa vijana wakiwa na umri mdogo na kwa muda mrefu. Kama anavyosema Juma Ikangaa ambaye alitamba katika Olimpiki ya mwaka 1984 huko Marekani ambapo alishika nafasi ya sita akikimbia saa 2:11:10 na ile ya mwaka 1988 huko Soul, Korea akikimbia saa 2:13:06 na kushika nafasi ya sita. Wanariadha wenye historia ya kufanya vizuri katika mashindano makubwa hapa nchini ni kama Bayi, Seleman Nyambui na Ikangaa ambao rekodi zao zimekuwa nadra sana kufikiwa na wanariadha wetu hapa nchini. Kiwango alichofikia mwanariadha huyu kijana ni kukimbia muda wa saa 2:19:00 alipokuwa akipeperusha bendera ya Tanzania katika michezo ya Lake Biwa, iliyofanyika Desemba mwaka jana huko nchini Japan. Hata hivyo, mwanzoni mwa mwaka huu, Simbu alivunja rekodi yake mwenyewe pale aliposhika nafasi ya 3 katika mashindano hayo kwa kutumia saa 2:09:19 hivyo kufuzu moja kwa moja katika michezo ya Rio mwaka huu. Dalili za Simbu kufanya vizuri zilianza kuonekana tangu akiwa hapa nyumbani, baada ya kujitosa katika mbio za Bagamoyo Marathon siku chache kabla hajaelekea Rio, ambapo alishika nafasi ya kwanza. Katika mbio hizo za Bagamoyo kwa upande wa wanaume kilomita 21, Simbu kutoka Arusha aliibuka mshindi akitumia saa 1:03:56, ambapo kwa asilimia kubwa mbio hizo ziliongozwa na wanariadha wengi kutoka Arusha. Katika mbio hizo za Bagamoyo, Simbu alikuwa na Mtanzania Saidi Makula aliyeshika nafasi ya nne, ambaye yeye katika Rio 2016 alishika nafasi ya 43 hiyo ikiwa ni baada ya kufikia viwango kwa kukimbia marathon kwa saa 2:13:25 mjini Casablanca, Morocco Oktoba mwaka jana. Na ndoto yake ilitimia Aprili 3 mwaka huu aliposhiriki  marathon ya Daengu, Korea baada ya kukimbia kwa saa 2:12:01. Simbu anasema haikuwa rahisi kwake kushika nafasi hiyo kama watu wanavyofikiria kwani alikuwa akikimbia huku akiwa na wanariadha mashuhuri na wakongwe katika riadha, hivyo kuziona mbio hizo ngumu sana kwake lakini hakukata tamaa. “Sitakuja kusahau pale nilipofika km 20 nikiwa sambamba na Kipchoge, aisee jamaa huyu anakimbia  mbio za mwendokasi na kama ningejaribu kushindana naye basi ningechemka na kubaki mwishoni, lakini niliona ni bora niende na kasi ile ile niliyokuwa nayo na hatimaye nilifanikiwa kushika nafasi hii,” anasema Mwanariadha huyu anaongeza kuwa amejifunza mambo mengi ambayo amesema kwa kiasi kikubwa yatamsaidia katika Olimpiki ijayo hapo mwaka 2020 huko Tokyo, Japan hivyo kutoa wito kwa Serikali kuhakikisha inaanza sasa kampeni ya kutafuta medali. “Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki lakini nimeweza kupambana kufa kupona naamini kuwa kama Serikali itatuandaa mapema na kambi yetu ikiwa ya kisasa tena ikiwezekana nje ya nchi nina uhakika medali itakuja Tanzania,” alisisitiza mwanariadha huyu na kuongeza: “Vita ya kusaka medali ianze sasa hivi na si kusubiri wakati mashindano yanakaribia, nimegundua kuwa wanamichezo wengi waliokuwa Rio waliandaliwa vizuri sana na nchi zao na ndio maana wamepata medali na kama walizikosa basi walishika nafasi za juu,” anaongeza Simbu. Wanariadha wengine ambao nao walishiriki katika michezo ya mwaka huu ni pamoja na mwanamke pekee, Sara Ramadhani ambaye alishika nafasi ya 126 yeye akidai kuwa viongozi wake walimtelekeza akiwa kwenye mbio hizo na kujikuta akiwa mwisho huku akikosa maji. Saidi Makula ambaye na yeye alipambana na kushika nafasi ya 43, anasema mbio hizo ni ngumu hivyo zinahitaji maandalizi ya kutosha na si kama alivyojiandaa yeye. Wakati Fabiano Joseph aliyeshika nafasi ya 112, anadai kabla ya kwenda nchini humo miezi miwili kabla alipata matatizo ya mguu hivyo aliposhiriki mbio hizo alitonesha mguu wake.
2michezo
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) linajivunia mapinduzi ya reli katika maeneo makuu matatu, yaliyowezesha kuongeza mapato kutoka Sh bilioni 23.8 mwaka 2014/2015 hadi Sh bilioni 45.4 mwaka 2018/2019.Maeneo yaliochagiza ukuaji huo wa mapato ni kukarabatiwa reli na mabehewa, kurejesha safari za treni katika maeneo zilikositishwa zaidi ya miaka 30, kuunganisha kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuwa TRC na kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Masanja Kadogosa, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa mapinduzi makubwa yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli katika sekta ya reli na kuwezesha mapato hayo yaliyotokana na ongezeko la mizigo na abiria wanaotumia usafiri huo.Alifafanua kuwa treni za mizigo, zimechangia Sh bilioni 30.04 mwaka 2018/2019 kutoka Sh bilioni 17.4 mwaka 2014/2015, Sh bilioni 10.7 kwa treni za abiria wa mikoani kutoka Sh bilioni 8.4 mwaka 2015/2016, kwa treni za abiria wa mjini Sh bilioni 1.9 kutoka Sh milioni 317 ikiwa ni sawa na abiria 4,280,043 mwaka 2018/2019 kutoka abiria 845,607 mwaka 2015/2016.Alisema katika kipindi cha miaka minne, TRC kwa safari za Reli ya Kati imesafirisha abiria kutoka 411,172 mwaka 2015/2016 hadi abiria 578,439 mwaka 2018/2019 huku ikisafirisha tani 52,709 za mizigo kupitia treni ya Dar es Salaam mpaka Kampala, Uganda kupitia Ziwa Victoria na tani 4,800 kwa safari ya Dar es Salaam-Tanga-Moshi iliyorejeshwa Julai mwaka huu.Kuhusu SGR, Kadogosa alisema ujenzi upo awamu tano na kwa awamu ya kwanza inayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro imefikia zaidi ya asilimia 70 huku Sh trilioni 1.1 kati ya Sh trilioni 2.7 zimetumika.Awamu ya pili kutoka Morogoro-Makutupora (Singida) imefikia asilimia 20 huku Sh trilioni moja zikiwa zimetumika kati ya Sh trilioni 4.4. Fedha zote ni za ndani. Alisema katika awamu hiyo ya pili (Morogoro-Makutupora), upimaji na usanifu wa njia kupitia ardhini na angani umekamilika kwa asilimia 100, utwaaji wa ardhi umefikia asilimia 90 eneo lote la kazi ambalo ni kilometa 295 kati ya kilometa 336.
1kitaifa
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa chama hicho, Masoud Attai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.“Ni kweli Zanzibar imepeleka maombi CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati) kuandaa michuano hiyo tumekubaliwa na kilichobakia ni kuona kwamba tunaandaa mashindano hayo, “ alisema.Aidha alisema kuwa tayari wameshapeleka barua Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar (BTMZ ), na tayari wameshawajibu barua hiyo na kilichobakia ni mipango ya pamoja kati yao na viongozi wa BTMZ, ili kupanga programu ya kucheza michuano hiyo.Attai alisema kwa mujibu wa programu yao viwanja vitakavyotumika ni vya Gombani Pemba na Amani Zanzibar kama hali itaruhusu.
2michezo
Na Fredy Azzah, Dodoma Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hillary (CCM), Aidha, ameeleza kushangazwa na kitendo cha Serikali kutenga Sh bilioni 15 kati ya Sh bilioni 80 zilizoombwa na Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na kwamba iwapo serikali itafunga mipaka ya nchi ili chakula kisiuzwe nje, watashikana mashati bungeni. Akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma leo Ijumaa aprili 6, Aesh amesema fedha hizo zilizotengwa zinatosha kunua mahindi Wilaya ya Sumbawanga pekee. “Kama mkishindwa kununua haya mahindi msifunge mipaka, mwaka jana mmefunga mkaja kufungua wakati muda umekwenda na kuweka masharti magumu, nawaambia safari hii mkishindwa kununua mkafunga mipaka tutashikana mashati humu ndani. “Siyo kazi ya mkulima kuhakikisha nchi haina njaa ni kazi ya Serikali, nashangaa huku mnasema tu tumbaku na pamba, bila mahindi huyo mkulima hawezi kulima hayo mazo yake,” alisema Aesh. Aeshi pia amezungumzia watumishi wenye elimu ya darasa la saba kufukuzwa kazi akisema mmoja wa Madereva waliofukuzwa kazi alimwendesha mpaka Waziri Mkuu Mstaafu (hakutaja jina la waziri huyo). “Huyu dereva alikuwa amebakisha miaka mitano tu astaafu, sasa hivi mmemfukuza kazi hana cha kufanya, suala hili mliangalie upya,” amesema.
1kitaifa
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ameanza operesheni maalumu ya kuzibana Taasisi ambazo ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Dara es Salaam kwa kutembelea ofisi moja hadi nyingine ili zilipe madeni yao katika muda uliopangwa.Katika ziara hiyo taasisi sita kati ya saba alizotembelea zimeahidi kulipa zaidi ya Sh bilioni 4.5 ifikapo Desemba, mwaka huu.Alitembelea taasisi hizo juzi ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisha wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi wanalipa madeni yao kabla ya hatua za kuwafikisha kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya wale watakaokaidi kulipa ambapo adhabu yake ni kulipa ama kupigwa mnada kwa mali za taasisi husika kufidia deni la kodi ya pango la ardhi.Taasisi alizotembelea Naibu Waziri huyo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalodaiwa SH bilioni tatu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Sh bilioni 1.4, EPZA Sh milioni 200, Shirika la Reli Tanzania (TRC) Sh bilioni 2.5, Shirika la Masoko Kariakoo Sh milioni 249 pamoja na Chuo cha Taifa cha Utalii Sh milioni 26.8.Akiwa katika Shirika la Masoko Kariakoo, Naibu Waziri Mabula alishangazwa na Shirika hilo kudaiwa zaidi ya Sh milioni 200 huku likiomba kulipa deni lake katika kipindi cha miaka miwili jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za ulipaji madeni ya kodi ya pango la ardhi ambazo humtaka mdaiwa kulipa nusu ya deni.Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, Hetson Kipsi katika barua yake, Shirika lake liliahidi kulipa kwa awamu deni hilo katika kipindi cha miaka miwili kwa kutoa milioni saba kila mwezi jambo lililokataliwa na Naibu Waziri aliyeeleza kuwa Shirika hilo linapaswa kulipa nusu ya deni kwanza ndipo liingie makubaliano ya kulipa kiasi kilichobaki kwa awamu. Hata hivyo Shirika la Masoko Kariakoo lilikubali kutoa Sh milioni 100 ifikapo Julai 29, mwaka huu na kukamilisha kiasi kilichobaki Desemba, mwaka huu.Kwa upande wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mkurugenzi Mtendaji wake, Masanja Kadogosa alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi kuwa Shirika lake halipingi kulipa deni inalodaiwa bali inachofanya ni kuhakiki upya deni hilo kwa kuwa kumekuwa na uhamisho wa umiliki wa mali za TRC kwenda TBA tangu mwaka 1999 sambamba na baadhi ya nyumba za Shirika kuuzwa kwa wananchi huku baadhi ya mali za TRC zikiwa hazina hati.Kadogosa alisema kiasi cha Sh bilioni 2.4 wanachodaiwa ni kikubwa na hakilingani na uhalisia wa deni la TRC na kubainisha kuwa uhakiki utakapokamilika ana imani deni hilo litapungua kwa kiasi kikubwa.Mabula alimueleza kuwa, Shirika lake linapaswa kulipa robo ya tatu ya deni hilo wakati uhakiki ukiendelea na iwapo itaonekana deni limepungua basi kiasi cha fedha kilichozidi kitarudishwa, hata hivyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TRC alikubali kulipa kiasi cha Sh milioni 400 kwa awamu hadi kufikia Oktoba, mwaka huu wakati kazi ya uhakiki wa deni hilo unaohusisha wataalamu wa shirika hilo na wizara ukiendelea.
1kitaifa
Na Kulwa Mzee-Dodoma KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema bajeti yao ya mwaka 2017/18 ni ya  historia ina kurasa 200  ikiwa na makadirio ya Sh trilioni 29.9. Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo ya bajeti ya Serikali mwaka 2017/18 iliyowasilishwa wiki na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango. “Bajeti ya kambi ya upinzani, itakuwa na kurasa nyingi kutokana na kuongezeka kwa matatizo, itawasilishwa kesho(leo) na Mbunge wa Mbozi, David Silinde ambaye ni Naibu Waziri Kivuli wa wizara hiyo, sijui kama wataweka mwongozo kuhusu mzigo huu au vipi,”alisema. “Bajeti iliyowasilishwa Juni, 8 mwaka huu ina upungufu mkubwa, imelenga kumnyonya mwananchi masikini. “Katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18, takwimu za vitabu vyake vya mapato na matumizi zinatofautiana, kitabu cha mapato kinaonyesha kwa mwaka itakusanya Sh trilioni 23.9, kitabu cha matumizi kinaonyesha inakusudia kutumia Sh trilioni 26.9, ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 3, wakati huo huo sura ya bajeti inaonyesha bajeti kwa mwaka 2017/18 ni Sh trilioni 31.7. “Kambi rasmi ya upinzani bungeni inaungana na wale waliosema bajeti hii ni ya ajabu maana haijawahi kutokea kukawa na mkanganyiko mkubwa namna hii wa takwimu katika bajeti,”alisema. Alisema makadirio ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani ni Sh trilioni 29.9 ambako vipaumbele vyao ni   sekta ya elimu iliyotengewa asilimia 20, viwanda asilimia 15, nishati asilimia 15, kilimo asilimia 10 na sekta nyingine zitapata asilimia 40 iliyobakia. Alitaja vyanzo vipya vya mapato kuwa ni mapato yanayotokana na uvuvi katika bahari kuu Sh bilioni 492.1, sekta ya madini Sh bilioni 5.59, kodi ya mrabaha na payee Sh bilioni 270, kupunguza misamaha ya kodi kuwa asilimia moja ya pato la taifa Sh bilioni 145.2 sawa na  Euro trilioni 2.2. Alisema mapato kutoka sekta ya utalii, Sh bilioni 592.7 na sekta ya michezo ya kubahatisha Sh bilioni 30 ambako jumla ya vyanzo vya mapato ya nyongeza ni Sh trilioni 3.7. “Vipaumbele hivi vikitekelezwa kwa ukamilifu Tanzania tutapunguza umasikini kwa asilimia 50 kwa kuwa ni vipaumbele vitakavyochochea ajira kwa watu wengi,” alisema. Kuhusu bajeti iliyowasilishwa na Waziri Mpango, Mdee alisema ilipotangazwa kuondolewa  kodi ya ada ya mwaka ya ‘Motor Vehicle’ magari, viongozi wengi walifurahia bungeni. “Sisi viongozi wa siasa tuna madeni mengi viporo kutokana na kuwa na magari mengi yanayodaiwa kwa sababu hatulipi.
1kitaifa
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amewataka wabunge wa CCM nchini, kuacha kulala usingizi au kutafuta kiki ya kisiasa kwa mgongo wa Rais John Magufuli.Badala yake, amewataka kuwatumikia wananchi katika majimbo yao na kuiga mfano uliofanywa na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama wa kujikita katika kusaidia ujenzi wa ofisi za matawi ya chama jimboni humo. Polepole alitoa kauli hiyo jana katika mkutano mkuu wa jimbo la Peramiho ambapo pia alikabidhi pikipiki 16 zenye thamani zaidi ya Sh milioni 45 kwa ajili ya makatibu kata wa chama hicho. Pia alikabidhi baiskeli 132 kwa ajili ya makatibu wa matawi, bati 835 kwa ajili ya ofisi za matawi na saruji mifuko 1,230 kwa ajili ya matawi hayo na ambavyo vilitolewa na Jenista alisema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa viongozi wa kata na matawi katika kutekeleza majukumu yao.Polepole alisema kuwa jukumu la viongozi wa kata na matawi ni kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo ambavyo ni mali ya chama na kwamba pasitokee kiongozi au mtendaji kutumia vibaya vifaa hivyo ambavyo vimetolewa na mbunge huyo wa jimbo la Peramiho. Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama alisema katika jimbo hilo kulikuwa na matawi ambayo ofisi zake hazifanani na Chama Cha Mapinduzi ambacho ni kikongwe hapa nchini na duniani hivyo ameamua kwa dhati kusaidiana na wanachama kurekebisha hali hiyo.
1kitaifa
BAADA ya vuguvugu na danadana za kutofanyika kwa uchaguzi ndani ya klabu ya Yanga kwa muda mrefu hatimaye Dk Mshindo Msolla amechaguliwa kwa kishindo kikubwa na kuwa mwenyekiti mpya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Msolla ameshinda kwenye nafasi hiyo kwa kura nyingi na kurithi nafasi hiyo ya uwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Yusuf Manji aliyeachia ngazi, na anatarajiwa kuongoza nafasi hiyo kwa miaka minne ijayo.Katika uchaguzi huo mkuu kwenye nafasi ya Mwenyekiti walikuwa wagombea wawili tu, ambapo Msolla alikuwa anachuana na mpinzani wake Dk Jonas Tiboroha baada ya Mbaraka Igangula kujitoa kwenye mchakato huo, huku zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo la uchaguzi.MATOKEO YA UCHAGUZI Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mchungahela alieleza kwamba kura zilizopigwa zilikuwa 1,341 na kura zilizoharibika ni tano, kura halali ni 1,336, ambapo Tiboroha aliambulia kura 60 huku akimtangaza Msolla kuibuka mshindi kwenye kiti hicho kwa kura 1,276 na kumtangaza kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga.Katika nafasi ya makamu, Mchungahela alimtangaza Fredrick Mwakalebela baada ya kuibuka kwa kishindo cha kura 1,206 kati ya kura 1,341 zilizopigwa huku zikiharibika kura 21 na kuwambwaga wapinzani wake, Titus Osoro aliyepata kura 12 Yono Kavela 17 na Janeth Mbene 31.Na katika nafasi ya wajumbe walichaguliwa ni wanne kati ya 21 waliwania kwenye kiti hicho walionyakua ni Hamad Islam 1,556, Dominic Kata 1,088, Frank Kamugisha 1,072, Araphat Haji 1,024, na kura zilizoharibika ni 16.Mara baada ya kumaliza mchakato wa kuwatangaza Msolla aliwashukuru wanachama kwa kumuamini kwa kumchagua kwa kishindo kushika nafasi hiyo na kuwaahidi atavunja makundi yote yaliyotamalaki kwenye klabu hiyo na kuyaweka pamoja ili timu ipige hatua mbele. “Nashukuru kwa kuniamini kunipa nafasi hii ingawa siwezi kufurahi sana kwakuwa huu ni mzigo mzito mlionipa cha kwanza nitavunja makundi yote na kuweka umoja tusonge kwa pamoja” alisema Msolla alieleza atafanya kazi kwa uwazi ikiwemokulipa nguvu benchi la ufundi nguvu ikiwemo kuwapa uhuru wa kufanya kazi yao bila kuwaingilia kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kwenye usajili.Kwa upande wa Makamu Mwakalebela alieleza watahakikisha wanatoa bajeti ya kutosha kwa benchi la ufundi kufanya usajili wa maana kusajili wachezaji wenye hadhi ya kuchezea Yanga ili kuifanya timu hiyo kukidhi matarajio ya wanachama wengi. “Tutaweka bejeti nzuri ikiwemo kumuachia Kocha kusajili mchezaji yeyote anayemuhitaji na kumuuza mchezaji anayetaka “ alisema Mwakalebela.Viongozi wote waliochaguliwa kwenye nafasi ya Mwenyekiti na Makamu kwenye mchakato wa kampeni walijikita kwenye kufanya magezi ndani ya klabu hiyo ikiwemo kuifanya timu hiyo kuendeshwa kwa mfumo wa kisasa kama walivyofanya watani wao Simba na kuhakikisha inapiga maendela yaliyotukuka katika karne hii ya soka la kiushindani.Niwazi baada ya kuchaguliwa kazi iliyobaki ni kuhakikisha wanatimiza sera zao walizokuwa wanapita kuhubiri kwenye matawi ya klabu hiyo wakiomba nia ya kushika nafasi hizo adhimu kabisa. Kitendo cha wanachama kuwachagua viongozi hao wasomi kinaonesha kwa umoja wao wamechoka na shida walizopita miaka 80 iliyopita na kwamba wanahitaji klabu hiyo yenye historia lukuki hapa ni chini na ukanda wa Afrika Mashariki ipige hatua kwa kuleta mipango na dira ya kimaendelea kwa kutoka ilipo na kwenda mbele.Kwa miaka mingi klabu kongwe nchini za Yanga na Simba zilikuwa zikiongozwa na viongozi ambao hawakusoma hivyo walionekana kukosa mipango na maono ya kuzifanya timu hizo kujenga ufalme kwenye soka la Afrika na kuishia kila wanapoingia madarakani wanakuwa na dhamira moja tu ya kumfunga mpinzani wao.Wanachama wa Yanga wanaonekana wamebadilika kwa kukata mzizi wa fitina na kuteswa na kivuli cha Manji na wanakiu ya kuona wanapiga hatua kuliko hata walipofika watani zao Simba na kushindana na timu kubwa Kama TP Mazembe, Esparance na zinginezo zilizofanikiwa kwenye soka barani Afrika.Malengo hayo yote yanawezekana endapo Msolla (dokta) na Mwakalebeka kama wataiendesha Yanga kisayansi na kuachana kabisa na mawazo ya kuifunga Simba ndio mafanikio wakati kuna mambo ya kufanya zaidi hya hilo.UONGOZI MPYASafu hiyo mpya ya uongozi yenye matumaini inaingia ikiwa ni muda mrefu sasa Yanga imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki, ikiwemo ombwe la uongozi dhaifu kwa kushindwa kusimamia mambo muhimu ambayo yangeifanya timu hiyo kupiga hatua matokeo yake imebaki kama ilivyozaliwa mwaka 1935 hadi sasa inafikisha miaka takribani 80.Yanga ni moja ya timu kongwe nchini, lakini hakuna kikubwa ilichofanya katika soka la Afrika, ambacho unaweza kusema kuwa kitakumbukwa na kizazi cha sasa na cha baadae. Klabu hiyo sasa inatakiwa kufanya mfumo wa kiuendeshaji kama walivyofanya wenzao wa Simba, ambao tayari timu yao inayoendeshwa kwa mfumo mpya. Simba ilianzishwa mwaka 1936.MAJUKUMU MAZITOUongozi mpya uliiongia madarakani chini ya Dk Msolla una kibarua kizoto cha kuhakikisha timu hiyo inaingia katika mfumu mpya, kupata fedha za uendeshaji na zile za usajili ili kuiwezesha timu hiyo kuimarika zaidi kwa kuwa na kikosi imara.Yanga imekuwa na tabia ya kutembeza bakuli kila inapocheza mechi za Ligi Kuu ili kuiwezesha timu hiyo kumudu gharama za uendeshaji pamoja na kuwalipa wachezaji posho pamoja na mishahara yao na inafanya hivyo kwa sababu bado haina wategemizi au vyanzo vya uhakika vya kuiingizia fedha.Mbali na vyote hivyo, pia Dk Msolla pamoja na timu yako yote hakikisheni katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wenu mnaiwezesha Yanga inakuwa na uwanja wake wa mazoezi na hata ule wa mashindano, ambao mtaweza kuchezea mechi za ligi na hata zile za kimataifa.Miaka minne sio michache, hivyo Yanga mkijipanga vizuri mnaweza kuanza kutumia uwanja wenu na sio lazima uwe mkubwa kama ule wa Taifa kwani mnaweza kuwa na uwanja unaochukua watu wachcahe, lakini wenye sehemu nzuri ya kuchezea (pitch).MATARAJIO YA WENGIWanachama na wapenzi wengi wa Yanga wana matumaini makubwa na uongozi wa sasa ndio maana Msolla pamoja na Mwakalebela mmechaguliwa kwa kura nyingi, hivyo msiwaangushe wapiga kura wenu.Wanachama wanachotaka ni kwa timu yao kufanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano ya kimataifa ili kuwatambia wenzao wa Simba kwa kufanya vizuri. Msolla na kundi lako mmeaminiwa na wanachama, hivyo msiwaangushe wanachama hao na badala yake mpambane na kuhakikisha Yanga inatisha kimataifa na kwa kuwa moja ya klabu kubwa zaidi barani humo.
1kitaifa
POLISI mkoani Dodoma inamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 28, William Saimon kwa tuhuma za kumkaba, kumbaka hadi kusababisha kifo ajuza mwenye umri wa miaka 77 (jina limehifadhiwa).Pia linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za wizi wa hati na kuuza kiwanja cha Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, na wengine wanne kwa kosa la kutengeneza na kughushi risiti za malipo za kielektroniki (EFDs).Kamanda Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema watu hao wamekamatwa baada ya operesheni mbalimbali na misako katika miji wa Dodoma na wilaya zake.Akizungumzia kifo cha ajuza, amesema alikuwa mkulima wa Bihawana na alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Rufaa Dodoma wakati anapatiwa huduma ya kwanza baada ya kukabwa na kubakwa.“Majira ya saa 2:30 usiku (juzi) huko Bihawana akiwa njiani, ghafla alikutana na mtuhumiwa na kumvutia vichakani na kumkaba shingoni na kumbaka. Watu wema walimfikisha hospitali muda mfupi baadaye alifariki dunia kutokana na maumivu makali,” amesema Kamanda Muroto.Aliongeza kuwa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.Kuhusu walioghushi kiwanja cha Mzee Malecela, alisema wamewakamata watu wanne kwa makosa ya wizi wa hati za viwanja, kughushi, kubadili ramani za mpango mji, kubadili mpango wa matumizi ya ardhi, kukuza viwanja na kuingilia mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu za ardhi.Watu hao ni Msaidizi wa Malecela, Jackson Ndahani, Diwani wa Kata ya Makole katika Manispaa ya Dodoma, Abel Mika (CCM), Elias Stephano na Shaban Msovela.“Msako wa wahusika wengine unaendelea na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika,” amesema Kamanda Muroto.
1kitaifa
Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu  baadhi ya makosa yaliyohusishwa na kampuni hiyo pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo, ikisema kuhusishwa kwake kunatokana na vipengele viwili. Mashtaka hayo ni kushindwa kutoa taarifa za usajiri wa kampuni ya UNEX Company Ltd kwa ajili ya kusajili laini za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo pamoja na kutotimiza majukumu yake vizuri kwa kuuza laini za simu 1000 kwa Kampuni ya UNEX ambayo haijasajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kutokana na makosa hayo mahakama iliitia hatiani kwa kuisababishia Serikali hasara ta Sh milioni 459 kwa kufanya mawasiliano nje ya nchi. Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai, alizungumzia katika hati ya mashitaka iliyosainiwa na mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali Mei 16,  mwaka huu. Alisema  makosa hayo  mawili,   hasa namba  sita na saba,   hayahusiani kampuni hiyo   kwa vile  washtakiwa wengine ambao ni raia wa Pakistan si wafanyakazi wa kampuni hiyo na   hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo.   “Tulipohusika na kuhusishwa kwao ni kosa letu la kuwauzia laini za simu ambazo hazijasajiliwa na kutowasilisha nyaraka zisizo halali. “Sisi ni kampuni inayofanya kazi kwa usajiri na vibali halali tulivyopewa na mamlaka ya nchi hii na tumekuwa wawazi na kufuata taratibu na sheria.
1kitaifa
SERIKALI imewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya watoe taarifa kama maeneo yao yana upungufu wa chakula na ni kiasi gani kinahitajika.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema leo bungeni mjini Dodoma kuwa, wizara ya Kilimo ikipata taarifa hizo itaratibu vizuri na kuona namna ya kufikisha chakula kwa wananchi kwa kuwauzia ili zipatikane fedha za kununua chakula kingine kiwekwe kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Chemba (CCM) Juma Nkamia aliyetaka kauli ya Serikali kwa kuwa baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dodoma, Manyara na Singida ina tatizo kubwa la chakula na huenda baadhi ya wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama hawatoi taarifa sahihi kwa sababu ya woga.“Upungufu wa chakula upo kwa baadhi ya wilaya na maeneo mengine na huu ulitokana na tatizo la hali ya hewa kwamba yapo maeneo msimu uliopita hayakupata mvua ya kutosha. Jambo hili linapotokea kule kwenye ngazi hiyo tunao viongozi…”amesema Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo hapo kutoka kwa wabunge wa Bunge la Tanzania.“Inapotokea kama hali ya hewa imekuwa mbaya Mkuu wa Wilaya akieleza atakuwa anaeleweka kwa sababu pia baada ya kutoa taarifa hiyo timu ya Wizara ya Kilimo itakwenda kuona hali halisi na kuweza kuzungumza na ile mamlaka kuweza kupelekewa chakula kwa bei nafuu” amesema.Amesema jambo hilo limetolewa ufafanuzi mara nyingi na kwamba, Rais John Magufuli hajazuia kutolewa kwa taarifa za upungufu wa chakula isipokuwa kwenye maeneo yenye hali nzuri ya hewa na kila mmoja ana nafasi ya kulima au kufanya kazi lakini yana upungufu wa chakula.“Viongozi waliopo kwenye maeneoi hayo wanao wajibu wa kusimamia kila mmoja anafanya kazi pamoja na kulima mazao ya chakula na biashara ili waweze kujipatia tija inapofikia kipindi kama hiki kila mmoja anakuwa na akiba yake” amesema.Ametoa mwito kwa wafanyabiashara watumie fursa ya tofauti za hali ya hewa kwenye maeneo kuuza chakula sehemu zenye upungufu.Amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wakutane na wafanyabiashara wawashawishi wapeleke chakula kwenye maeneo yenye upungufu ili kuongeza vipato vyao.
1kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa taasisi za kutoa huduma wezeshi kwa wateja kufanya hivyo kwa wakati na kuacha urasimu ili kutowakatisha tamaa wabunifu wakati huu wa uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda hapa nchini.Waziri Majaliwa alisema hayo kwenye viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege wilayani Kibaha wakati wa kufunga maonesho ya Wiki ya Viwanda na kusema kuwa kuchelewa kutoa huduma kwa wakati ni kuzorotesha kasi ya uanzishwaji wa viwanda.Majaliwa alisema kwa kuwa serikali imeweka mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda, hakuna sababu ya kuchelewesha utoaji wa vibali vya wateja ambao wanataka huduma kwenye taasisi wezeshi.Moja ya taasisi hizo ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambalo linadaiwa kumchelewesha mteja ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Budget Motorways ya wilayani Kibaha ambayo ilikuwa na mpango wa kuanzisha utengenezaji wa mabasi, lakini amesubiri kibali mwaka mzima. Alisema kuwa kama tayari mtu keshasema ana uwezo wa kutengeneza kitu fulani, ni kwanini TBS isivipime vifaa vinavyozalishwa na kampuni hiyo kama vinakidhi vigezo au la, kuliko kutofanyia kazi suala hilo na kutoa majibu.“Mnachopaswa ni kumfuata na kupima vipuri anavyozalisha kuona kama vina uwezo wa kuundwa hayo magari kama havina uwezo waambiwe kuliko kukaa kimya muda mrefu kiasi hicho, kwani mnawakatisha tamaa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda,” alisema Majaliwa.Aidha alisema kuwa mpango wa serikali ya Awamu ya Tano ni kuwa na viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini ili kuachana na uagizaji wavifaa kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kuinua uchumi wa nchi na kupunguza gharama za uagizaji kutoka nje ya nchi. Alimtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa na kupata ufumbuzi haraka.“Waziri Mwijage una wajibu kuhakikisha suala hili linakwisha ili kumwezesha huyo mtu anayetaka kuanzisha kiwanda cha kutengeneza magari aweze kupata vibali vinavyostahili na kama vigezo havipo basi ijulikane kuliko kutotoa majibu yoyote, hii haijakaa sawa, shughulikia suala hilo. Haya ndiyo tunayoyataka, watu wenye mawazo mazuri lazima yafanyiwe kazi,” alisema Majaliwa.Alibainisha kuwa serikali imezielekeza taasisi za fedha kutoa fedha za mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji kwa wajasiriamali ambao watakuwa na vigezo kwa ajili ya kuwekeza kwenye viwanda ambavyo vitaongeza wigo wa mapato na kutoa ajira kwa watu wengi.“Tutahakikisha tunakabiliana na changamoto ambazo zilisababisha viwanda kufa ili hivi vinavyojengwa viweze kudumu kwani vitasaidia ukuaji wa uchumi pia mkoa wa Pwani ambapo ni kinara wa kuwa na viowanda vingi uendelee kuhimiza uanzishwaji wa viwanda,” alisema Majaliwa. Kwa upande wake, Waziri Mwijage alisema kuwa mkoa wa Pwani umefanya mageuzi makubwa ya viwanda kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta hiyo na kuufanya uongoze kwa kuwa na viwanda vingi na maonesho hayo watayafanya yawe ya kimataifa ili kuhamasisha wawekezaji.Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alisema ili kuhamasisha mikoa itekeleze kwa vitendo sera ya uanzishwaji viwanda watafanya mashindano kwa mikoa ili kuangalia ni mkoa gani umetekeleza na ulioshindwa.Jafo alisema mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo imetekeleza kwa vitendo sera ya serikali ya awamu ya tano ya kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda ambavyo vitaifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda. Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema kuwa lengo la kuanzisha maonesho hayo ambayo yatakuwa ni endelevu ni kutambulisha bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo pia kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao.Ndikilo alisema lengo lingine ni kuzitangaza bidhaa zao ambazo zinakosa soko kutokana na kutojitangaza, hivyo watu kutojua bidhaa zao pia ni kuwatafutia masoko kwa wananchi na sehemu mbalimbali za nje ya nchi mkoa huo una viwanda 429 vikubwa vikiwa ni 109 na vidogo 320. Maonesho hayo yalifunguliwa Oktoba 29 na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
1kitaifa
“Hatua hii ya Brela ni nzuri, wanastahili pongezi na wengine waige,” alisema Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.Pongezi za Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini, ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi.Akithibitisha maendeleo hayo, mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Vibindo, alisema hivi karibuni alifanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja tu. Brela imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka huu.Mteja wa Brela anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza, anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya kuzaliwa.Anatakiwa kuingia katika mtandao wa Brela ambao ni www.brela. go.tz kisha ataingiza jina na baada ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.Baada ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia mchakato huo wa kimtandao.
0uchumi
ASHA BANI-DAR ES SALAAM MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali 258 yamefutwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kutokana na kufanya majukumu kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs). Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Emmy Hudson, alisema kufutwa kwa NGO hizo kwenye muunganisho wa wadhamini wa taasisi zenye kufanya shughuli zilizoainishwa kwenye sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali sura namba 56, ni kufuatia mabadiliko madogo ya sheria. Alisema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika katika sura ya 318 kupitia sheria ya marekebisho mbalimbali Na.3 ya mwaka 2019 iliyoanza kutekelezwa Juni 30 mwaka huu. “Kuanzia sasa jukumu la kusajili muunganisho wa wadhamini utafanyika kwa taasisi zile tu ambazo zitakuwa katika utaratibu maalumu, ikiwa ni pamoja na taasisi ambazo usajili wake wa awali umefanyika kwa mujibu wa sheria nyingine, lakini zinahitajika kupata utu wa kisheria. “Taasisi hizo ni pamoja na vyama vya siasa, mashirika na taasisi za kidini na vilabu vya michezo,’’ alisema. Aliongeza kuwa taasisi ambazo usajili wake moja kwa moja hufanyika Rita ni zile zinazofahamika kama mifuko inayotoa huduma bila ya kupata faida na usajili wake unafanyika chini ya sheria ya muunganisho wa wadhamini sura ya 318. Pia alisema taasisi ambazo usajili wake umetokana na maelekezo ya kisheria moja kwa moja au maamuzi ya kimahakama yanayoelekeza kuanzishwa kwa muunganisho wa wadhamini wa taasisi hiyo. Emmy alisema taasisi zinazojihusisha na masuala ya kilimo ambazo hazijasajiliwa katika sheria yoyote ya Tanzania na zinahitaji usajili kwa ajili ya kupata utu wa kisheria.  “Hivyo basi kuanzia siku ya tangazo hili, ofisi ya Mtendaji Mkuu  haitasajili tena muunganisho wa wadhamini wa taasisi yoyote ambayo inafanya  shughuli zilizoelekezwa kwa mujibu wa sheria ya NGO. “Ijulikane kwamba kwa taasisi zile ambazo zilishasajiliwa Rita ambazo baada ya marekebisho ya sheria hizo zitafutwa rasmi katika daftari la muunganisho wa wadhamini katika ofisi ya Rita, wadhamini watapaswa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha wanalipia madeni yote wanayodaiwa katika marejesho ya wadhamini kila mwaka kwa kipindi ambacho hawakulipa madeni yao walipokuwa Rita,’’ alisema. Pia alisema wanatakiwa kurejesha hati halisi ya usajili wa wadhamini ambayo walikabidhiwa wakati wa usajili. Baadhi ya mashirika hayo ni Muungano wa Wafugaji na Wawindaji nchini, Maarifa Media Trust (Mamet), Saint Anne Maria, Comprehensive Community Based  Rehabiliation in Tanzania (CCBRT), Mviwata Trust Fund na Human Right Resources Center of Tanzania.
1kitaifa
NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, amesema ofisi yake ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), inapata misukosuko inapochukua sampuli za vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto au wazazi. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili ofisini kwake Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Manyele, alisema mara nyingine wakati wa upimaji kipimo hicho hutokea vurugu, hivyo kulazimika kuwatoa wahusika nje kwa nguvu ili shughuli zao za kiofisi ziendelee. “Kuna wakati baadhi ya wapenzi au wanandoa ulazimika kufikishwa ofisini chini ya ulinzi wa polisi, huku wengine wakikataa kukubaliana na matokeo, hivyo kusababisha vurugu,” alisema. Profesa Manyele alisema kutokana na hali hiyo, upimaji DNA huchukua karibu asilimia 90 ya kazi za GCLA na hivyo kuwapa wakati mgumu katika utendaji kazi zao. Alisema kwa kawaida ofisi hiyo uchukua sampuli za upimaji wa DNA kwa wazazi na mtoto wakiwa pamoja, lakini inapokuwa vinginevyo inaleta shida. “Hivi vipimo kuna muda mwingine tunapata shida kuvipata kwa sababu hatuwezi kumpima mmoja mmoja, lazima wahusika waje kwa pamoja. “Upimaji unakuwa mgumu na kuibua vituko na misukosuko mzazi mmojawapo anapokuwa hayupo tayari… Unakuta mtu wakati mwingine hataki kupima, hivyo hulazimika kuletwa chini ya ulinzi wa polisi,” alisema. Profesa Manyele alisema ili kuepusha hali hiyo, ofisi hiyo huwa inawashauri wanaosimamia vipimo hivyo kuhakikisha wanawaandaa wahusika kisaikolojia ili wawe katika maelewano mazuri kabla uchukuaji wa sampuli zao haujafanyika. Pia alisema wapo watu wanaoshindwa kwenda kupima jambo ambalo ofisi yake inalazimika kutuma wataalamu na kuwafuata walipo ili kuchukua sampuli zao. Alisema wazazi wengine wanafika katika ofisi hiyo na kuanza kulalamikia matokeo ya vipimo yanapotoka tofauti na matarajio yao. “Unakuta mzazi katika hisia zake ameshajihakikishia kuwa huyo mtoto si wake, au wengine wanadhani ni wa kwake. “Sasa ikitokea majibu yakatoka tofauti, mtu anakasirika, anakuja hapa anagonga mlango wa ofisi huku akilalamikia matokeo ya DNA,” alisema. Alisema mara nyingi watu wanaofanya hivyo wanaenda kinyume cha utaratibu kwa kuwa mtu anayepaswa kulalamikia matokeo ni aliyepeleka sampuli za vipimo hivyo. Profesa Manyele alisema kutokana na unyeti wa vipimo vya DNA, ndiyo maana vinafanyika kwa usimamizi wa vyombo vilivyotajwa katika sheria, ikiwamo mahakama, ustawi wa jamii, hospitali, manispaa au mkuu wa wilaya, wakili wa kujitegemea, polisi na vituo vya utafiti. Pia alisema yapo makosa yanayofanywa na watendaji wa manispaa, wilaya na mikoa kwa kushindwa kutunza vizuri matokeo ya DNA baada ya kuyapokea. “Utakuta mhusika anaenda katika ofisi za wilaya au manispaa anamkuta ofisa anamuulizia kuhusu karatasi ya matokeo, anakuwa hajui alipoiweka, akiitafuta unamwona anaitoa chini ya uvungu, unashangaa anawezaje kuweka vile nyaraka muhimu kama ile,” alisema Profesa Manyele na kuongeza: “Kinachotokea watu wanapokea matokeo yale bila kufuata taratibu za kiofisi. Mtu analetewa matokeo hakuna sehemu ambayo anasaini wala kuandika kama amepokea kitu. Kwa kifupi hakuna usiri wa matokeo katika ofisi hizo.” Alitaja makosa mengine wanayoyafanya watendaji ni kusoma au kutoa taarifa za matokeo ya vipimo hivyo mbele ya mtoto husika jambo ambalo si sawa. “Mtoto hatakiwi kujua haya mambo. Waachwe wazazi wenyewe wasikilize. Ikitokea mzazi amekuja na mtoto kuchukua matokeo, watendaji wanapaswa wahakikishe wanamshauri wakati mtoto hayupo. Hii itasaidia kwa ustawi wa mtoto husika,” alisema. Profesa Manyele aliendelea kusema kuwa watendaji wanapaswa kuhakikisha wanawaelimisha wahusika wachukuliwe vipimo kuondoa dhana potofu ya kufikiri  kuwa kipimo hicho pia kinapima Virusi vya Ukimwi (VVU) jambo linalosababisha watu kuogopa. Mbali na kujua uhalali wa watoto au wazazi, pia alitoa sababu za watu kupima DNA kuwa ni pamoja na kutatua malalamiko ya kesi za urithi na kutambua ndugu halali. Alisema pamoja na kesi za watoto wanaopata mimba za utotoni kuwa nyingi, lakini ofisi hiyo haipokei kwa wingi malalamiko hayo kutokana na wahusika kutojua kama chombo hicho kinaweza kuwasaidia. “Maofisa elimu na walimu inabidi wafahamu kuwa ofisi ya mkemia mkuu ina nafasi kubwa sana ya kutatua migogoro ya mimba za utotoni baada ya mtoto kujifungua. Hivyo inakuwa rahisi kwa mhusika kuchukuliwa hatua,” alisema Profesa Manyele.
1kitaifa
Vinara hao wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 21, wanaikaribisha kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hiyo ya Shinyanga ambayo iko katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 28. Imecheza mechi 22.Mwishoni mwa wiki, Yanga ilikumbana na Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.Huenda hasira zao za kushindwa kupata ushindi watazihamishia katika mchezo huo ili kuwafurahisha mashabiki wake ambao walitegemea timu hiyo ingepata ushindi mkubwa katika mchezo huo wa kimataifa.Katika mchezo wa raundi ya kwanza, Yanga ilishinda Stand United mabao 3-1 mjini Shinyanga. Mchezo wa leo utakuwa ni muhimu kwa Yanga kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi, kwani ina pointi 46 ikitofautiana pointi nne na mabingwa watetezi Azam FC wenye pointi 42.Ikishinda mchezo huo na mingine miwili inayokuja dhidi ya Ruvu Shooting na Polisi Morogoro itatwaa rasmi taji hilo. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, wachezaji wote wako vizuri kwa mchezo huo na wamejipanga kuondoka na pointi tatu.“Wachezaji wote wanaendelea vizuri, Telela (Salum) ambaye alikuwa ni majeruhi pia ameimarika na huenda leo akawepo katika kuiua Stand United, jambo la muhimu ni mashabiki wasichoke waje kutuunga mkono,” alisema Muro.Kwa upande wa Stand United, bado ina wakati mgumu kwani inahitaji ushindi kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri. Msemaji wa Stand United, Isaac Edward alitabiri mchezo huo na ujao dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC kuwa migumu kwao ambao wanatafuta nafasi ya kupambana ili wasirudi Daraja la Kwanza baada ya kupanda msimu huu.Edward alisema kikosi chake kiko vizuri na tayari kwa mchezo huo kuhakikisha kinaonesha juhudi kupata pointi tatu. Ligi hiyo inayoelekea ukingoni, itaendelea kesho kwa michezo miwili ambapo Simba itacheza na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa na Polisi Morogoro wataikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.Simba imetoka kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki hii jijini Mbeya, huku msemaji wao, Haji Manara akijifariji kuwa timu hiyo imedhamiria kuondoka na ushindi katika uwanja wake wa nyumbani.Katika mechi za juzi za ligi hiyo, Mtibwa Sugar iliibana Prisons nyumbani kwake Sokoine jijini Mbeya na kwenda sare ya bao 1-1 wakati Ruvu Shooting iliifunga Mgambo JKT mabao 2-1.
2michezo