text
stringlengths
0
24.2k
label
class label
6 classes
Na Anna Potinus – Dar es salaam Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba amejibu ombi la msanii mwenzake, Nassib Abdul (Dimond Platinum) la kushiriki kwenye Tamasha la muziki la Wasafi Festival linalotarajiwa kuanza Novemba 24 mwaka huu kwamba hatoweza kushiriki kwa kuwa atakuwa na majukumu ya uzinduzi wa kinywaji chake cha Mofaya atakaoufanya nchi za nje. Awali Diamond Platinum alimualika Ali Kiba kwenye tamasha hilo akitamani Ali Kiba angekuwepo katika tamasha hilo wakaimba pamoja kwani kwa kufanya hivyo ingeonyesha kukuwa kwa wasanii badala ya kutengeneza bifu wakuze muziki wao na watengeneze fedha kwa ajili ya kulisha familia zao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba leo Novemba 7 ameandika kwamba hatoweza kushiriki kwenye tamasha hilo kutokana na yeye kuwa balozi wa kinywaji hicho. Hata hivyo ameeleza kwamba yeye na kampuni ya Rosckstar wapo tayari kutoa ushirikiano kwa kampuni ya Wsafi kwa kuwapa udhamini kwenye tamasha hilo. “Tusingependa kuwaacha hivi hivi, tuko tayari kuwapa ushirikiano wa udhamini katika tamasha lenu kupitia Mofaya Energy drink ili kusukuma mbele gurudumu la sanaa Tanzania na Afrika, uongozi wangu utaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya jambo hili kubwa,” amesema Baada ya kuweka ujumbe huo watu mbalambali wamempongeza msanii huyo kwa kuandika maneno ya busara na kiungwana kujibu ombi la msanii mwenzake huyo.    
4burudani
BENKI ya I&M imetenga Sh milioni 75 kwa ajili ya promosheni inayolenga kuwaongezea wateja kipato kwa kipindi cha miezi mitatu ikiwamo kupata fedha mara mbili ya akiba zao. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo ya Jidabo, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa benki hiyo, Lilian Sware alisema imezinduliwa rasmi mwezi huu na itadumu kwa miezi mitatu. Sware alisema kila mwezi wateja watano wa benki hiyo watajishindia fedha mara mbili ya akiba iliyopo kwenye akaunti zao lakini siyo zaidi ya milioni tano.Akizungumza akaunti zinazoweza kuingia kwenye promosheni hiyo alisema ni ya akiba, biashara, mshahara au akaunti ya mtoto. Alisema wateja wa matawi ya benki hiyo nchi nzima wanaweza kushiriki na kujishindia bahati yao. Alisema promosheni hiyo ni kwa ajili ya kuwapa zawadi wateja wa benki hiyo katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo inafanywa sambamba na huduma nyingine rafiki za kibenki katika matawi yote .Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo ya I&M, Emannuel Kiondo alisema hata kama mteja ana kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya Sh milioni tano, kiwango cha juu cha promosheni hiyo ni Sh milioni tano ambazo zitazidishwa mara mbili na mteja kupewa Sh milioni 10 na si zaidi ya hapo.“Mfano mteja ana akiba ya shilingi laki tatu itazidishwa mara mbili na kupewa shilingi laki sita, na kama mteja ana shilingi milioni mfano 10, sisi kiwango chetu cha juu ni shilingi milioni tano, hivyo tutazidisha shilingi milioni tano na kumpa shilingi milioni 10 na si zaidi,” alifafanua Kiondo. Aidha aliwataka pia wateja wapya kujiunga na benki hiyo kwa kufungua akaunti kati ya hizo tajwa na kuweza kuingia kwenye promosheni hiyo itakayoinua kipato chao.
1kitaifa
Na LILIAN JUSTICE -MOROGORO WANANCHI mkoani Morogoro wametakiwa kula matunda na vyakula vyenye virutubisho vya madini ya foliki, ili kupunguza ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi. Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Tawala, Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi, yaliyofanyika mjini hapa. Alisema kwamba tatizo la kuwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi linaepukika, kama wananchi watakuwa mstari wa mbele kula matunda, yakiwamo machungwa na mapapai. Pia, alisema matatizo hayo yatakwisha kama wananchi watatumia vidonge vyenye vitamin ya foliki, ambavyo husaidia kwa kiwango kikubwa kuzuia tatizo hilo. “Binafsi nashangaa kuona Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye tatizo hilo, licha ya wananchi wake kuzalisha matunda kwa wingi. “Kwahiyo, nawaomba wananchi wale matunda kwa wingi badala ya kuyauza kama inavyofanyika sasa,” alisema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi Wenye Watoto Wenye Ulemavu wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBAHT), Abdulhakim Bayakub, alisema pamoja na kufanya jitihada za kusaidia watoto hao kwa matibabu, bado hazifanikiwi zaidi kutokana na ukubwa wa gharama za matibabu hayo. “Gharama za vipimo ni kubwa, kwani mtoto akiwekewa mpira inagharimu kiasi cha shilingi laki tano. “Chama cha ASBAHT kimekuwa kikishirikiana na hospitali zote ambazo matawi yake yapo, lakini bado tunahitaji msaada wa wadau wenye uwezo wa kufanya hivyo,” alisema. Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Rita Lyamuya, alisema kliniki zote zinapaswa kutoa vidonge vyenye vitamini ya foliki acid, ambavyo vinawasaidia wajawazito kujifungua bila matatizo.
1kitaifa
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo alisema, wafanyabiashara ambao walikuwa tayari wameshaanza kutumia mashine hizo wanatakiwa kuendelea kuzitumia, wakati Serikali ikiendelea kuwatambua ambao hawana mashine.“Wafanyabiashara ambao walishanunua mashine hizo na kuanza kuzitumia wanatakiwa kuzitumia na wale ambao bado hawajapata mashine hizo watapewa za bure na Serikali tunaendelea kuwatambua,” alisema Kayombo.Aidha, alisema kwa wafanyabiashara ambao walinunua mashine hizo kwa fedha zao tayari Serikali ilishawarudishia fedha zao wakati wa marejesho ya kodi zao kama walivyoahidiwa.Baadhi ya wafanyabiashara wamelalamikiwa kuuza bidhaa zao bila kutoa risiti za mashine wakidai kuwa hawatumii mashine wanasubiri watakazopewa na Serikali kama ambavyo iliwaahidi.Kayombo alisema TRA iko katika maandalizi ya manunuzi ya mashine hizo na kuweka utaratibu wa kugawa mashine kwa wafanyabiashara ambao wanastahili kuwa nazo.Mwezi uliopita, TRA ilisema inatarajia kuanza kutoa mashine za bure kwa wafanyabiashara stahiki 200,000.Aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango akizungumzia uamuzi huo wa EFD, alisema utoaji huo wa mashine bure, ni uamuzi wa kubadili utaratibu kwa kuwa utaratibu wa awali wafanyabiashara walinunua mashine hizo na kurudishiwa fedha zao wakati wa kulipa kodi.Kwa mujibu wa Dk Mpango, uchambuzi wa wafanyabiashara wanaostahili kupewa mashine hizo, unaendelea nchi nzima kwa kuangalia ukubwa wa biashara ili wapewe mashine hizo kwa lengo la kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi.
0uchumi
['Bingwa wa Olimpiki mbio za marathon Eliud Kipchoge Ijumaa wiki hii ametangazwa mwanamichezo bora katika hafla ya kufana iliyofanyika katika uwanja wa Mombasa Sports Club.', 'Kipchoge pia alichaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa kitengo cha wanaume naye bingwa wa dunia, Hellen Obiri akatwaa tuzo la wanawake.', 'Baadhi ya wanamichezo ambao Obiri aliwabwaga ni Brigid Kosgei ambaye anashikilia rekodi ya dunia na bingwa wa dunia wa marathon Ruth Chpngetich.', 'Miongoni mwa wanamichezo Kipchoge aliwaangusha ni bingwa wa dunia mbio za mita 1,500, bingwa wa Olimpiki na wa dunia mbio za mita 3000 kuruka vizuizi na maji, Conseslus Kipruto.', '"Nafurahia sana kushinda tuzo hii, inamaanisha watu wametambua niliyofanya Vienna kwa kukimbi chini ya saa mbili katika marathon. Napenda kuwaambia watu kuwa hazikua mbio ya ushindi ila kutuma ujumbe ya kwamba hakuna lisilowezekana dunia," anasema Kipchoge.', 'Timu bora kwa wanaume ilikua ni klabu ya mpira ya Bandari na Malkia Strikers kwa wanawake.', 'Malkia Strikers ilishinda taji la voliboli katika michezo ya mataifa ya Afrika nchini Morocco na hatimaye ikashiriki kombe la dunia nchini Japan.', ' "Ushindi huu wa tuzo la timu bora umetuongezea motisha sana. Tunajiandaa sasa kwa michezo ya Olimpiki. ', 'Huko tunaenda kubeba kombe," anasema nahodha wa Malkia Strikers Mercy Moim ambaye anafanya kazi na idara ya Magereza.', 'Mkufunzi wa Malkia Strikers Paul Bitok alishinda tuzo la kocha bora.']
2michezo
MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema uzalishaji katika kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama cha TanChoice kitakachokuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 1,000 na mbuzi na kondoo 4,500 kwa siku, unaanza rasmi mwanzoni mwa mwaka ujao.Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alisema kiwanda hicho ambacho kimejengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 23 na ambacho kitatoa ajira za moja kwa moja kwa watu zaidi ya 500, kilipata leseni ya ujenzi na uendelezaji katika maeneo maalumu ya uwekezaji kutoka EPZA mwaka jana.Alisema kiwanda hiki ambacho kitakuwa na migawanyo mitano ya machinjio inakifanya kuwa kiwanda kikubwa cha nyama Afrika Mashariki na cha pili kwa ukubwa baada ya kile cha Ethiopia ambacho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 3,000 na mbuzi pamoja na kondoo 6,000 na kuzalisha tani 300 za nyama kwa siku moja.“Pamoja na kuwa na asilimia 11 ya mifugo yote barani Afrika, mchango wa sekta ya mifugo kwa pato la taifa bado umekuwa mdogo ambao ni asilimia 7.4, wakati sekta hiyo inakuwa kwa wastani wa asilimia 2.6 kwa mwaka,” alisema na kuongeza: “Kiwanda hiki cha kuchinja na kuchakata nyama kitapunguza kwa kiasi utoroshaji wa mifugo kwenda nchi jirani ambao wamekuwa wakitumia fursa hii kuongeza uzalishaji kwenye viwanda vyao na mauzo nje ya nchi”.Takwimu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaonesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe zaidi ya milioni 13.5, kondoo milioni 5.5, mbuzi milioni 3.6, nguruwe 400,000 na kuku milioni 23.2.Uwekezaji huu mkubwa wa kiwanda cha kuchinja na kuchakata nyama unategemewa kuingizia nchi fedha nyingi za kigeni kwa kuuza nyama nchi za Ulaya na Uarabuni. Sehemu ambapo mradi huu unatekelezwa ni karibu na inapopita treni ya umeme ya SGR, hivyo kukifaidisha kiwanda na wepesi wa kufikisha mizigo bandarini na pia kuleta ng’ombe kutoka sehemu mbalimbali nchini.Kiwanda cha TanChoice kitaweza kutengeneza biashara kubwa kwa vijana inayohusisha unenepeshaji wa mifugo ambayo itahitajika kama malighafi kwenye kiwanda cha nyama.“Mwekezaji huyu hawezi kufanya kila kitu, hivyo wawekezaji wa ndani wanaweza kuchangamkia fursa hii ya kunenepesha mifugo ambayo itahitajika katika kiwanda hiki,” alisema.Mabaki yatakayotokana na kuchinja na uchakataji wa nyama yatauzwa ndani ya nchi na sehemu nyingine zitauzwa China ambako soko lake ni kubwa. Pia mabaki kama damu ya mifugo itakayochinjwa inatumika katika kutengeneza chakula cha kuku hivyo kuongeza fursa kwa wazalishaji wengine wa vyakula vya mifugo. Kwato na pembe za ng’ombe hutumika kutengeneza vifungo vya nguo na mabegi.
1kitaifa
Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM JUKWAA la Wahariri  Tanzania (TEF)  limetoa tamko la kutaka kuwapo maridhiano ya taifa kuhusu mustakabali wa nchi. Limetaka mazungumzo hayo yashirikishe   makundi mbalimbali wakiwamo viongozi wastaafu, asasi za  raia, vyama vya  taaluma, makundi ya rika  mbalimbali kuweza kufanya mjadala huo kama alivyofanya Rais Dk. John Magufuli, alipokutana na wafanyabishara   Ikulu  Dar es Salaam, hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, alisema hivi sasa Taifa linashuhudia malalamiko mbalimbali kutoka kwa jamii jambo ambalo halileti afya kwa ustawi,  umoja na mshikamano wa Watanzania. Alisema   tamko hilo ni maazimo ya wahariri wanachama wa TEF waliokutana juz. Kwenye mkutano huo,  pamoja na mambo mengine, walijadili na kutafakari kwa kina hali na mwelekeo wa nchi kwa sasa ambako malalamiko yamekuwa mengi kwa makundi ndani ya jamii. Alisema malalamiko hayo ambayo baadhi yamekuwa yakiripotiwa na vyombo vya habari yamekuwa yakigusa sehemu kuu tatu ambazo ni kuminywa kwa uhuru wa kutoa maoni hasa kupitia vyombo vya habari, kuzorota  demokrasia nchini kwa ujumla wake na ukuaji wa uchumi ambao kwa sasa haulingani na hali ya maisha ya Watanzania. Alisema kuminywa kwa uhuru wa kutoa  maoni  kimekuwa  kikwazo kikubwa cha utendaji na ufanisi katika vyombo vya habari. Balile alisema vyombo vya habari  kwa  sasa haviko huru kutoa taarifa mbalimbali kama mwanzo kutokana na hofu iliyojengeka miongoni mwa wananchi ambao wamekuwa wakisita kutoa maoni. “Mazingira ya kazi  kwa wanahabari yamekuwa magumu kutokana na baadhi ya watendaji wa vyombo  vya dola kuwabughudhi na kufanya uovu wa wazi dhidi yao wanapokuwa kazini. “Matukio mbalimbali ya polisi kuwanyanyasa waandishi wa habari yakiwamo ya wanahabari kunyang’anywa simu zao, mfano yaliyotokea Dodoma kwa mwandishi kuporwa simu, kupotea kwa mwandishi Azory Gwanda wa Mwananchi na kwingineko,” alisema Balile. Mengine ni mauaji ya Kibiti, kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwiline, kuuawa  askari wanane, kushambuliwa kwa risasi  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, vitendo ambavyo baadhi yake hadi sasa havijapata majibu wala wala wahusika  kupatikana. Alisema hali hiyo inawafanya waandishi na wananchi kwa ujumla kuwa na hofu hasa kwa wale wa habari za uchunguzi. Balile alisema vyombo vya habari vilevile vimekuwa vikifanya kazi katika mazingira magumu na ya woga kutokana na watendaji wake kuitwa na kuhojiwa mara kwa mara na mamlaka kama vile Idara Habari (MAELEZO) na Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania (TCRA) na hata wakati mwingine kupewa adhabu za kulipa faini au kufungiwa. “Vituo vingine vitano vya televisheni kutozwa faini i na TCRA  na kufungiwa kwa magazeti ni baadhi ya adhabu ambazo zimekuwa zikitolewa kinyume na Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016. “Pia mitandao ya  jamii ambayo ilikuwa njia mbadala ya umma au wananchi kujieleza na kupata habari nayo imeanza kuwekewa vikwazo baada ya kutungwa   kanuni zinazotaka kusajiliwa kwa blogs na mitandao mingine, huku waendeshaji wake wakitakiwa kulipa ada,’’ alisema Balile. Alisema suala la kuzuiwa   mikutano ya vyama vya siasa ambavyo ilikuwa moja ya vyanzo vikubwa vya habari, kinyume na sheria ya nchi  huku vyama vya upinzani vikionekana kuathiriwa zaidi, ikizingatiwa   watendaji wa chama tawala (CCM) wanaonekana wakiendelea na shughuli za  siasa katika sehemu mbalimbali nchini kwa hoja kuwa wanakagua utekelezaji wa ilani ya chama. Kaimu Mwenyekiti huyo wa TEF alisema suala la kuzuia matangazo ya televisheni ya moja kwa moja kutoka  bungeni  kwa maelezo ya ukubwa wa gharama na kutoa fursa kwa wananchi kufanya kazi, huku kinyume chake yakiwapo matangazo mengi ya moja kwa moja katika muda uleule, yanayofanywa na taasisi nyingine za serikali. Alisema  kurushwa kwa matangazo hayo ya moja kwa moja na taasisi nyingine za hakujazuia wananchi kufanyakazi zao! “Pia wanahabari wanashindwa kufanya kazi zao sawasawa kwa mfano   uchaguzi mdogo mbalimbali uliofanyika baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015  uliambatana na matukio ya kuogofya yakiwamo mauaji ya watu na kujeruhiwa, hali ambayo iliwafanya waandishi washindwe  kutekeleza wajibu wao  inavyotakiwa,’’ alisema Alisema vilevile kuna dalili za kuzorota kwa shughuli za  uchumi kutokana na kufungwa kwa baadhi  ya biashara na shughuli nyingine za uzalishaji mali, hali ambayo  imesababisha ongezeko la ukosefu wa ajira. “Baadhi ya vyombo vya habari kwa sasa vina hali ngumu na kushindwa kujiendesha kutokana na kuidai serikali na taasisi nyingine mamilioni ya fedha za matangazo ambazo endapo zingelipwa zingeweza kuvikwamua. “Kufungwa kwa baadhi ya biashara au kushuka kwa mapato kwa baadhi ya kampuni kumeathiri biashara ya matangazo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo chanzo cha mapato kwa vyombo vya habari,’’ alisema Balile.
1kitaifa
Hatua hiyo inalenga pia kuufanya mchezo huo kuchezwa mjini na vijijini kama ilivyo michezo mingine. Kamati hiyo ambayo ni mpya imepania kuhakikisha mchezo huo unaboreka zaidi na kufahamika kama ule wa wanaume.Katibu Mkuu wa kamati hiyo Khatma Mwalim akizungumza na Mwandishi wa habari hizi ambaye alitaka kujua mikakati ya uongozi huo mpya, alisema kuwa jambo la kwanza ni kuondoa makundi ambayo yalishaanza kuchomoza ndani ya klabu zao hususan zile kongwe ambazo ni New Generation na Women Fighter.Alisema kuwa katika kutaka kufikia azma yao hiyo ni kudhibiti mvutano huo na kuanza ukurasa mpya kwa mustakabali wa soka lao la wanawake. Hata hivyo alidai kuwa uongozi wake utapata changamoto kubwa kutokana na idadi ya timu zilizopo kwani ni ndogo ukilinganisha na michezo mingine.Katika kukabiliana na hilo Khatma alisema kamati yake inajipanga kuelekea vijijini kuhamasisha soka hilo la wanawake kwa kutumia mbinu mbalimbali za ushawishi.Alizitaja baadhi ya mbinu ambazo watazitumia ni kufanya mazoezi ya pamoja na wanavijiji, kucheza mechi za kirafiki na kutumia hata mikanda ya video inayoonesha soka hilo.Kwa sasa soka hilo la akinadada linajumuisha timu sita ambazo ni New Generation, Women Fighter, Kidimni Queen, Mwenge Sisters, Bungi Sisters zote za Unguja na Mkoani Queens kutoka Mkoani kisiwani Pemba. Kamati ya soka la Wanawake tayari imepata uongozi wake baada ya kufanya uchaguzi na Mwenyekiti wake ni Sabah Bakar Hassan na Khatma Mwalim
2michezo
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, Mbagala Dar es Salaam JKT ilionesha kandanda safi na kutawala mchezo karibu katika vipindi vyote.Mabao ya washindi yalifungwa na Samwel Kamuntu dakika ya 20 na Emmanuel Pius aliyefunga katika dakika ya 52 na bao la United lilifungwa dakika ya 23.Kwa matokeo hayo, Ruvu sasa imezishusha Yanga na Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 16 sawa na vinara Mtibwa Sugar kabla ya mechi hiyo Ruvu ilikuwa na pointi 13.Msemaji wa JKT Mteule Daraja alisema mwendo wao ni wa ushindi katika kila mechi kwani lengo lao ni kutwaa ubingwa. “Tulikuwa tunataka kufika juu kwenye msimamo na tumefika, lengo letu ni kutwaa ubingwa, tunaamini tunaweza,” alisema.
2michezo
Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA RAIS Mstaafu  wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ametaja sababu za kujiuzulu kwake nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa kulitokana na kulinda heshima ya taifa na ya Rais wa awamu ya kwanza. Amesema anasikitishwa kuona chanzo cha kujiuzulu kwake bado hadi sasa kipo, ambacho ni mauaji ya vikongwe jambo ambalo ni fedheha kubwa kwa taifa. Kauli hiyo aliitoa   Dodoma jana katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika mkoani hapa. Alisema   hakuna haja kwa sasa kiongozi kujiuzulu kwa sababu ya mauaji bali Serikali inapaswa kupambana na wauaji wote ili kutoruhusu hali hiyo kuendelea. Alisema mwaka 1976 akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani,  alilazimika kujiuzulu   baada ya kutokea mauaji katika Mkoa wa Shinyanga lakini miaka tisa baadaye akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa   miaka 10. “Kuongezeka kwa wazee ni jambo jema linaloonyesha taifa linapata maendeleo lakini hili la kuwaua vikongwe ni aibu na fedheha kubwa sana, naomba likomeshwe,” alisema Mwinyi. Alivitaka vyombo vya habari kutambuwa kuwa vina jukumu la kutoa elimu kwa jamii wakiwamo watu wenye tabia hiyo ya kuwaua vikongwe. “Mwaka 1976 nilijizulu, kisa ni mauaji ya watu Shinyanga. Nilijiuzulu  ili kumwokoa Rais na fedheha (Mwalimu  Nyerere)…nikaona aibu inipate mimi. “… leo bado risala inasema na tumesikia mama Waziri kasikia, viongozi wamesikia, hakutakuwa na haja ya kujiuzulu ila wao ndiyo wanatakiwa kujiuzulu. “Tunaendelea kukabiliana na mauaji na imani za ushirikina, ni aibu, ila haya yanaendelea kushughulikiwa  na sasa mkazo utaongezwa  katika utoaji wa elimu kwa jamii,” alisema. Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema Serikali imetoa kipaumbele kwa wazee na haitasita kuwahudumia kila inapobidi. Alisema Serikali kila mwezi inapeleka  fedha katika kambi 17 za wazee na  imekwisha kununua bajaji 10 kwa ajili ya kuwahudumia, yakiwamo majiko matano ya kutumia. “Kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili kwa ubora wa afya za wazee katika nchi 11, hivyo katika hili ni lazima tujipongeze,” alisema. Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Taifa, Stebastian Mbulegi alisema   alimwomba Rais Mstaafu Mwinyi kuwafikishia salamu zao kwa Rais Dk. John Magufuli kuhusina na mambo matano ambayo ni pamoja na kuomba itungwe sheria kuhusiana na  Sera ya Taifa ya Wazee ili kuipa nguvu. Pia  alitaka wazee wapate huduma za afya bure na bila malipo kwa vile  wamekuwa wakisumbuliwa katika hospitali na vituo vya afya. “Pia Serikali ikomeshe mauaji ya vikongwe kutokana na imani za ushirikina, itoe malipo ya pensheni kwa wazee wote ikizingatiwa kwa sasa ni asilimia nne tu  ya wazee wanaopata na asilimia 96 hawapati,” alisema Mbulegi. Pia Mwenyekiti huyo alimwomba Rais huyo Mstaafu, wazee washirikishwe katika ngazi mbalimbali za uamuzi kama vile kupatiwa viti maalumu vya ubunge na udiwani.
1kitaifa
RAIS John Magufuli amesema ameanza ziara yake mkoani Rukwa vibaya na kwa majonzi kutokana na ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya Sh bilioni 20 kutelekezwa na mkandarasi Fally Enterprises asiye na sifa wala uwezo ambaye ameagiza achunguzwe na kushitakiwa.Kutokana na hali hiyo, amemwagiza Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuwachukulia hatua kali watendaji wa wizara yake waliohusika kumpatia kazi nyingi zaidi mkandarasi huyo kinyume cha utaratibu.Aidha, amemwagiza Profesa Mbarawa na kumpatia siku saba kuunda tume maalumu ya wataalamu kuifanyia uchunguzi wa kina miradi yote inayotekelezwa na mkandarasi huyo aikiwamo ile ambayo haijaikamilisha.Mbali ya Wizara ya Maji, pia ameagiza Tamisemi, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa na Wakili wa Serikali kufuatilia tuhuma dhidi ya mkandarasi huyo pamoja na hujuma uliyofanywa katika Mradi wa Maji Laela.Pia amempigia simu na kumwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Siro kumwondoa Ofisa Mnadhimu, Polycarp Urio kwa kushindwa kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwa ziarani Rukwa hivi karibuni.Rais Magufuli ametoa maagizo hayo jana katika Mji Mdogo wa Laela Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kabla ya kuzindua barabara ya Tunduma – Laela – Sumbawanga ya kilometa 223.2 iliyogharimu Sh bilioni 375.Mradi huo wa barabara ulikamilika kujengwa tangu mwaka 2015 kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la Millennium Challenge (MCC) na fedha za ndani za Serikali ya Tanzania kwa kiwango cha lami.“Huyu mkandarasi Fally hamalizi ujenzi wa miradi huku mingine ikiwa chini ya kiwango. Nashangaa amepewa miradi yote... lakini hajafutiwa usajili kwa mujibu wa sheria namba 15 ya 1994,” alieleza Rais Magufuli.“Waziri andaa tume maalumu ichunguze miradi yote ya maji anayoijenga pia ifanyiwe upya thathmini pamoja na kubaini kama utaratibu wa manunuzi umefuatwa kwa mujibu wa sheria. Kama mkandarasi huyo amelipwa waziri baada ya kuwasilisha certificate zote mlipaji awekwe ndani kwa mujibu wa sheria,” alizidi kuagiza Rais Magufuli.Alimwagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo kumfuatilia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Nyangi Msemakweli kama amemlipa mkandarasi huyo.Mkandarasi huyo anatuhumiwa kuhujumu miradi ya maji kwa kuijenga kwa viwango hafifu ukiwemo mradi wa maji wa Laela wa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.7 ukiwa umemalizika miaka mitatu iliyopita lakini maji hayatoki.Miradi hiyo iko katika wilaya za Kalambo, Nkasi na Sumbawanga.“Ninazo taarifa kuwa Waziri Profesa Mbarawa ulipokuwa mkoani Rukwa kikazi uliagiza mkandarasi Fally akamatwe lakini akaachiwa. Nataka nimfahamu nani aliyemwachia huru akikaidi agizo la waziri ambaye ni mteule wangu,” amehoji huku akiwataka viongozi wasitishwe na watu wenye fedha.Awali, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy alimweleza Rais Magufuli kuwa mkandarasi Fally hana sifa wala viwango, na amefisadi miradi ya maji huku akijilimbikizia mali kwa kujenda maghorofa sehemu mbalimbali.“Mheshimiwa Rais mafisadi kama Fally wanastahiki adhabu kali ya kunyongwa... Pia azitapike fedha zote kama wengine wanavyozitapika,” alisema mbunge huyo machachari.Baada ya kuzindua barabara, Rais alifika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Laela na kumpigia IGP Sirro na kumuagiza amfukuze Mnadhimu Urio kwa kushindwa kumpatia RPC majina tisa ya askari polisi ambao Waziri Lugola aliagiza wahamishwe kwa makosa ya kuwabambikizia kesi wananchi na kuwanyima dhamana.Rais Magufuli ambaye alitokea mkoani Songwe alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, jana alianza ziara mkoani Rukwa ambayo inaendelea leo. Akimaliza mkoa huo atakwenda kwa ziara nyingine Mkoa wa Katavi.
1kitaifa
Anna Potinus Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amemtoa hofu Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Shukuru Kawambwa, kuhusu kutekelezwa kwa mradi wa umeme katika Kijiji cha Kondo kilichopo katika Kata ya Zinga kilichokuwa kwenye mradi wa REA awamu ya pili, ambacho hadi Juni mwaka 2016 hakikutekelezewa mradi wake. Dk. Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Juni 26, alipokuwa akijibu swali ya nyongeza la mbunge huyo aliyetaka kupata kauli yake juu ya utekelezaji wa mradi huo. Kawambwa amesema ndani ya kijiji hicho kuna Shule ya Msingi ya Kondo na Sekondari ya Zinga na miundombinu yote haina umeme hadi sasa. Akijibu swali hilo, Dk. Kalemani, vijiji vyote vimeshapata umeme na hivi sasa vimebakia vitongoji tu. “Kati ya Wilaya ambazo vijiji vyake vyote vimeshapata umeme ni pamoja na Bagamoyo. “Kuna vitongoji 169 katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge na kati ya hivyo vitongoji 100 tayari vina umeme bado 69 tu ambavyo bado havijapata umeme ambavyo ni pamoja na kitongoji cha Kondo, kwa hiyo nimpe mheshimiwa Mbunge imani kwamba nimeshawaelekeza wakandarasi wakishirikiana na Tanesco wameshaanza kupeleka umeme kwenye kitongoji cha Kondo na watakamilisha Julai 12 hivyo asiwe na wasiwasi,” amesema. Aidha, Dk. Kalemani ameongeza kuwa Mkandarasi aliyeko katika Jimbo la Bagamoyo na Chalinze anapeleka umeme katika vitongoji vyote ikiwemo kijiji kirefu cha Msingi na Magurumatare cha kilomita 28 ambacho hakijapelekewa umeme.
1kitaifa
Derick Milton, Simiyu Shirika la World Vision Tanzania limezindua mradi wa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo Minyoo na Kichocho katika Wilayani Itilima. Kwa mujibu wa Shirika hilo kupitia utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya nchini, Wilaya hiyo imekuwa na kiwango cha juu ya asilimia 30 cha maambukizi ya minyoo na kichocho, hali inayosababishwa na uhaba wa upatikanaji wa maji safi na mazingira salama Wilayani humo. Mbali na hilo Idara ya Afya katika Wilaya hiyo inasema kuwa wananchi wengi wamekuwa na imani potofu juu ya dawa za Minyoo na kichcho wanazopewa pindi wanapopimwa na kukutwa na magonjwa hayo hali ambayo imesababisha pia kiwango cha maambukizi kuwa juu. Mwakilishi wa Shirika hilo Rise Liwa akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huo amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu na utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 864,993.00 sawa na Sh. Bil 1.9 za kitanzania chini ya ufadhili wa Serikali ya Korea(KOICA). Liwa amesema kuwa shirika hilo linatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia ,Wazee na watoto pamoja na ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Arnold Musiba amesema hali ya magonjwa hayo si nzuri kutokana na jamii kubwa ya wakazi wa Wilaya hiyo kuwa na imani potofu juu ya dawa zitolewazo za minyoo na kichocho. Kupitia mradi huo Wordvison itawafikia wananchi 283,972, kata 22, vijiji 102, vitongoji 587 na Kaya 44,171 ambapo shughuli mbalimbali za utoaji dawa za minyoo na kichocho zitafanyika, uchimbaji na usambazaji maji kwa vijiji 10 na uhamasishaji wa usafi wa mazingira kupitia viongozi wa maeneo husika na matumizi ya vikundi vya sanaa.
1kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka Watanzania wanaoweza kuunganisha nguvu na wawekezaji kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kufanya hivyo kwa kuwekeza kwenye viwanda vikubwa.Aidha, Majaliwa aliyeeleza kuvutiwa na Maonesho ya Wiki ya SADC, amesisitiza Watanzania kutumia maonesho ya viwanda ya SADC kukaribisha wageni kwa ukarimu, kutangaza mambo mazuri ya nchi ikiwamo vivutio vya utalii.Alitoa mwito huo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mabanda ya maonesho na kujionea bidhaambali mbali, zinazooneshwa na washiriki kutoka nchi wanachama wa jumuiya. Waziri Mkuu alisema kupitia maonesho hayo, nchi wanachama wa jumuiya wanayo fursa ya kuanzisha viwanda nchini. SADC inaundwa na nchi 16.“Watanzania mnaoweza kuunganisha nguvu na nchi wanachama huu ndiyo wakati,” alisema Majaliwa na kusisitiza kuwa maonesho hayo ni fursa kubwa ya upatikanaji masoko ya bidhaa mbali mbali miongoni mwa nchi wanachama.Akipongeza maonesho hayo, alisema ameona bidhaa za aina mbali mbali zinazozalishwa nchini zikiwa kwenye kiwango cha ubora wa hali ya juu, jambo aliloshauri Watanzania kujitokeza kwa wingi kujionea.Alisema ni vyema watanzania wakatembelea kuona wengine wanafanyaje na pia kujionea bidhaa ambazo wapo baadhi ambao hawafahamu kama zinazalishwa nchini.Miongoni mwa bidhaa zitokanazo na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo zinazooneshwa ni pamoja na nguo, vyakula, kazi za mikono na bidhaa za ngozi.“Ni fursa kubwa kwetu Tanzania kutumia nafasi hii kutangaza biadhaa zetu za ndani,” alisema.Alisisitiza kuwa ni wakati mzuri wa kuhakikisha nchi inaendelea kuhamasisha wawekezaji wa nje kuja kuwekeza nchini kwani mazingira ni mazuri.Kupitia maonesho hayo, Majaliwa alisema Tanzania inao uwezo mkubwa wa teknolojia ya kuendesha mitambo na upatikanaji wa mazao. Alitoa mfano wa miwa na kusema Tanzania haina shida ya sukari kwani fursa ipo nchini.Akisisitiza ukarimu kwa wageni waliofika kushiriki maonesho hayo, alisema “maandalizi yote yamekamilika kwa kiasi kikubwa. Watanzania tutumie nafasi hii kuwakaribisha kwa ukarimu. Tutangaze vivutio vya utalii.”Alitaja vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, fukwe na eneo la Oldupai Gorge ambalo ndilo chimbuko la binadamu, akisema ni wakati mzuri wa kuhakikisha wageni wanayafahamu na kuelewa yalipo.Alitoa mfano wa mlima Kilimanjaro kuwa wapo watu wengine ambao wamekuwa wakitangaza kuwa ni wao. “Watanzania ni fursa kutangaza mambo yote nchini ikiwamo uwekezaji,” alisisitiza.Alisema inafahamika kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii inafanya kazi ya kutangaza utalii na vivutio vilivyopo lakini kwa kipindi hiki cha mkutano kila Mtanzania kwa nafasi yake anapaswa kuutangaza kwa wageni.Maonesho ya viwanda ya SADC yalifunguliwa juzi na Rais John Magufuli ambaye alihimiza nchi wanachama kujizatiti kuwekeza kwenye viwanda.Wageni kutoka nchi wanachama wanaendelea kuwasili nchini kushiriki maonesho hayo yatakayofungwa kesho na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Baadaye watawasili wakuu wa serikali na nchi za SADC kwa ajili ya mkutano wao wa 39 utakaofanyika Agosti 17 na 18.
0uchumi
Mwandishi Wetu, New York Umoja wa Mataifa (UN), umetengeneza historia kwa vijana duniani kwa namna ya pekee kwa kuzindua mkakati wa vijana kuelekea 2030 ikiwa ni moja ya matukio yaliyosubiriwa kwa hamu kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 73 ulioanza leo hapa New York nchini Marekani. Mkakati huo umezinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio Guteres ambapo amesema ni mkakati uliofikiriwa na Umoja huo wa kufanya kazi na vijana kwa ajili ya vijana na kuwapa kipaumbele katika mambo ya msingi katika kutimiza mpango wa maendeleo endelevu. “Ni wazi kuwa katika dunia ya sasa kuna takribani vijana bilioni 1.8 wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 24 likiwa ni kundi kubwa la vijana kuwahi kutokea katika historia ambapo wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na mambo kama utandawazi, kukua kwa teknolojia na mabadiliko ya tabia ya nchi. “Vijana wengi hawako katika ajira shuleni au hata katika mafunzo huku mmoja kati ya wanne akiathiriwa na vurugu za vita kwa namna moja ama nyingine, mamilioni ya wasichana wanapata watoto katika umri mdogo jambo linaliothiri afya zao na kuendeleza mzunguko wa kubaki katika lindi la umaskini,” amesema. Amesema jambo la kushangaza ni kwamba vijana hao kwa kiasi kikubwa hawashirikishwi katika masuala kimaendeleo sambamba na kunyimwa sauti na viti katika ngazi za maamuzi huku wakiwa ni chanzo cha ubunifu, mawazo chanya na suluhisho katika mambo mengi wakipatiwa nafasi. Mkakati huo wa vijana umelenga mambo makuu matano ya msingi katika utekelezaji wake moja ikiwa ni kufungua milango mipya katika kuwashirikisha vijana yakiwamo kuimarisha mpango wa kuhakikisha wanafikiwa na elimu na huduma bora za afya, kuhakikisha wanawezeshwa kiuchumi kupitia mafunzo na utoaji wa ajira, kuhakikisha haki zao zinapewa kipaumbele kuwashirikisha katika mambo ya kijamii na kisiasa na tano kutoa kipaumbele kwa vijana na utatuzi wa migogoro na haki za binadamu kwa kuwashirikisha katika hatua za kulinda amani. Hata hivyo, Katibu Mkuu ametoa wito kwa nchi wanachama wa UN kuupa kipaumbele utekelezaji wa mkakati huo ili kuwaimarisha vijana.
3kimataifa
SERIKALI imesema ni marufuku kwa watu wenye leseni za uwindaji au wale watakaopewa leseni hizo kutumia silaha za kivita kuwinda wanyama kwenye vitalu vya uwindaji. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alipozungumza na gazeti hili.Novemba 6 mwaka huu, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambalo ni shirika la umma chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ilitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuhusu kufunguliwa kwa uwindaji kwa wenyeji na wageni wakazi nchini.Kutokana na kufunguliwa kwa uwindaji huo ambao uliositishwa kupitia Tangazo la Serikali Namba 538 la mwaka 2015, gazeti hili pamoja na mambo mengine, lilitaka kujua ni aina gani ya silaha ambazo haziruhusiwi kutumiwa.Hasunga alisema silaha zilizoruhusiwa ni nyingi, lakini zilizopigwa marufuku ni silaha zote za kivita kama vile SMG, AK 47 na bastola. Aliwataja baadhi ya wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa na wamiliki wa leseni za uwindaji kwenye vitalu ni pamoja na nyati na aina zote za swala. Ili kurahisisha kazi hiyo ya uwindaji, Serikali imetenga vitalu vya uwindaji.Kwa mujibu wa TAWA, kanda hizo tano ni pamoja na Kanda ya Kaskazini mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro ambayo itahusika na kitalu cha uwindaji cha Kitwai Kusini, wakati Kanda ya Kusini mkoani Lindi katika Wilaya ya Kilwa itahusika na kitalu cha uwindaji cha Kilwa Kaskazini, huku Kanda ya Mashariki mkoani Pwani katika Wilaya ya Kisarawe itahusika na kitalu cha uwindaji cha Kisarawe.Kanda zingine ni Kanda ya Magharibi mkoani Tabora/ Katavi katika Wilaya ya Mlele/Kaliuwa ambayo itahusika na kitalu cha uwindaji cha Ugalla Niensi, wakati Kanda ya Kati mkoani Singida itahusika na kitalu cha Simbanguru/Igwemadete.
1kitaifa
Hadija Omary, Lindi Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imetenga Sh 103.8 kwa ajili ya kusambaza umeme  kwenye mitaa inayofanana na vijiji mkoani Lindi. Hayo yameelezwa na waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani juzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa miundobinu ya gesi asilia majumbani mkoani Lindi uliofanyika katika Kata ya Mnazi Mmoja  Manispaa ya Lindi. Kalemani amekiri kuna maeneo ya mjini ambayo mengi yaliitwa kama mitaa na si vijiji wakati kuna mitaa ambayo haina tofauti na vijiji. “Tumeshatoa maelekezo kuwa mitaa yote inayofanana na vijiji iwe kwenye miji, Manispaa ama majiji yote ipelekewe umeme kwa Sh 27,000,” amesema. Aidha, amesema fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020 huku akimsisitiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Kanda ya kusini, Feisian Makota kuzingatia na kuanza kutekeleza maagizo hayo kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Awali akimkaribisha Waziri wa Nishati kuzungumza na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alimuomba waziri huyo kuangalia namna ya kuwaunganisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo sawa na wale wa vijijini ambako miradi ya REA inatekelezwa. Zambi alisema kuna baadhi ya mitaa ndani ya manispaa hiyo ipo vijijini ambayo kuna haja ya Serikali kuwaangalia wananchi wa maeneo hayo walipie malipo ya umeme sawa na yale yanayofanywa na wananchi wa vijijini ambako miradi ya REA imefika.
1kitaifa
 ASHA KIGUNDULA-DAR ES SALAAM MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Yanga leo inashuka dimbani kuumana na Biashara United ya Mara, katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Dare s Salaam. Yanga itaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuvuna pointi tatu katika mchezo wake uliopita uliochezwa Uwanja wa Samora mjini Iringa, baada ya kuilaza bao 1-0 Tanzania Prisons. Wanajangwani hao wanafahamu kuwa wanahitaji ushindi ili kuzidi kujongea juu ya msimamo wa Ligi Kuu msimu huu. Pia wanataka ushindi ili kujiweka katika hali nzuri kisaikolojia, wakati wakisubiri kuumana na Watani wao wa jadi, Simba, mchezo utaochezwa Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hata hivyo, mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa Yanga kwani wapinzani wao Biashara nao wanahitaji matokeo mazuri ya pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo. Biashara United inayofundishwa na Francis Baraza, inahitaji ushindi kwa udi na uvumba, huku ikitaka kuendelea kuweka rekodi ya kutoa kichapo kwa mabingwa hao. Biashara iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wa msimu uliopita uliochezwa Uwanja wa Karume, Musoma.Wachezaji David Molinga, Papy Tshishimbi, Mrisho Ngassa na Denis Kaseke, wanaweza kuleta shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo yenye makao yake makuu, Mtaa wa Twiga, Dar es Salaam. Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 21, ikicheza mechi 10, ikishinda sita, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja. Biashara United inashika nafasi ya 15 miongoni mwa timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo, ikiwa na pointi 15, ikishinda michezo minne, sare tatu na kuchapwa mara sita. Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema afya za wachezaji wake zipo vizuri kwa ajili ya kucheza mchezo huo. “Mchezo dhidi ya Biashara ni muhimu kwetu kushinda ili kuongeza ari ya kikosi kuelekea mchezo na Simba, kwa ujumla hali ya wachezaji wangu zipo vizuri,”alisema Mkwasa. Kwa upande wa Baraza alisema wanafahamu wapo kwenye nafasi isiyoridhisha hivyo watapambana kuhakikisha wanavuna pointi tatu dhidi ya Yanga, ili kujongea juu ya msimamo wa ligi hiyo.
2michezo
BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limejipanga kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini Rais John Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka amewaeleza waandishi wa habari kuwa, nafasi ya baraza hilo ni kubwa katika kufanikisha ujenzi wa viwanda kama taasisi mtambuka inayochagiza maendeleo na ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi.“Tumekuwa tukishirikiana kwa karibu sana taasisi nyingine za serikali kama Kituo cha Uwekezaji (TIC), Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na nyinginezo katika kufanikisha azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda,” amesema Dk Gwamaka.Alisema baraza halitakuwa kikwazo katika kufanikisha ujenzi wa viwanda zaidi ya kuwa mshauri kwa wawekezaji wa viwanda kuzingatia sheria na taratibu za kimazingira bila ya kuathiri afya za wananchi.“Sisi kama baraza tunapenda kumshauri mwekezaji kiwanda tangu anapoanza ujenzi au uzalishaji nini anapaswa kuzingatia ili uwekezaji wake uwe rafiki wa mazingira,” alisema na kuongeza kuwa NEMC inaunga mkono azma ya ujenzi wa viwanda.Dk Gwamaka alisema milango ipo wazi ofisi zote za NEMC makao makuu na zile kanda kwa mtu yeyote anayejenga kiwanda kwenda kupata ushauri kwani baraza limekamilika na lina waatalamu katika sekta mbalimbali.“Tunaweza kuangalia kumshauri mwekezaji wa kiwanda kuwa eneo gani anaweza kuboresha. NEMC ni kampuni wezeshi kwa mtu au mwekezaji yeyote anayefuata na kuheshimu sheria za mazingira,” alisema.Dk Gwamaka alisema uchumi wa nchi yeyote duniani hauwezi kuwa imara na endelevu bila kuwa na viwanda kwani sekta ya viwanda ndiyo ya muhimili au roho ya uchumi.Bosi huyo wa NEMC hakusita kupongeza hatua na juhudi za makusudi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kwa kusema viwanda vitapanua na kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa kitanzania.“NEMC ni mdau mkubwa katika ujenzi wa viwanda. Tunahamasisha viwanda vinavyoleta tija, rafiki kwa mazingira na kulinda afya za wananchi,” alisema Dk Gwamaka.Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani miaka mitatu iliyopita imeweka hadharani dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 na tayari hatua mbalimbali zimeshachukuliwa kufanikisha azma hiyo.
0uchumi
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM TIMU ya Simba imemtema kipa wake Ivo Mapunda, huku ikielezwa kuwa mkongwe huyo ameondoka katika timu hiyo baada ya kusukiwa zengwe ndani ya miamba hiyo. Ivo alitua Simba Desemba mwaka juzi akitokea Gor Mahia ya Kenya, likiwa ni pendekezo la aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mcroatia Zdravko Logarusic na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu uliomalizika Mei mwaka huu. Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga, ambapo Wekundu hao walishinda bao 1-0, Ivo aling’ara na kumkuna Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hans Poppe, aliyedai watampa mkataba wa mwaka mmoja. Lakini hali imekuwa tofauti baada ya uongozi wa Simba kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Haji Manara, kutangaza kuachana na kipa huyo kwa kile walichodai amedengua kusaini mkataba mpya waliompa. “Tumeachana rasmi ya kipa wetu Ivo Mapunda, tulimpa mkataba mpyalakini alishindwa kusaini ndani ya muda tuliowekeana hivyo hatutakuwa naye tena msimu ujao,” alisema. Hata hivyo, habari za kuaminika zilizolifikia MTANZANIA zimedai kuwa kulikuwa na mgongano mkubwa baina ya viongozi wa Simba juu ya kuongezewa mkataba kwa kipa huyo. Taarifa hizo zimedai kuwa kikao kilichoketi hivi karibuni kupitia mambo mbalimbali ya timu hiyo, kilifikia uamuzi huo wa kutompa mkataba wa mwaka mmoja. “Wajumbe wengi walishindwa kuukubali uwezo wa Ivo Mapunda, baada ya kudai hana mapenzi na timu hiyo na alifungwa baadhi ya mabao mepes sana, ikiwemo mchezo muhimu waliofungwa na Mbeya City mabao 2-0 mkoani Mbeya, mechi ambayo ilikuwa muhimu sana na tulitakiwa kushinda ili kuendelea kuifukuza Azam,” alisema. Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Ivo Mapunda kuzungumzia suala hilo, ambaye alikanusha taarifa za yeye kukataa kusaini mkataba na kudai alikuwa hatakiwi ndani ya Simba. “Taarifa za mimi kutemwa nimezisikia kwenye vyombo vya habari, ila si kweli kuwa mimi nimekataa kusaini mkataba mpya. Kama ndio hivyo kwanini mimi nilienda kwenye kambi ya Lushoto hadi nikaumia ndio nikaondolewa kambini kwa matibabu, ila ukweli mimi nilikuwa sitakiwi Simba,” alisema. Alieleza kwa sasa yupo huru kujiunga na timu yoyote hapa nchini, itakayokuwa na ofa nzuri huku akiwa na mipango mingine ya kucheza soka la kulipwa. Kocha wa Simba, Dylan Kerr, akishirikiana na Kocha wa Makipa, Abdul Salim, wameshaanza kusaka kipa mzoefu wa kuziba nafasi yake ikiwa inamjaribu Muivory Coast, Vincent Angban na Mreno Ricardo Andrade, anayetarajia kutua muda wowote kuanzia sasa.
2michezo
Baada ya hapo jana kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga Mkongomani Papy Tshishimbi kunukuliwa na kituo cha redio cha Efm kuwa aelewi kinachoendelea juu ya mkataba mpya  na klabu yake ya Yanga baada ya yeye kutaja kiasi anachokitaka na klabu hiyo kukaa kimya Leo kiungo huyo ameonekana kwenye mkaa makuu ya klanu hiyo akiwa na kabitu mkuu wa klabu hiyo Dk.David Luhaga wakifanya kikao kizito kinachosekana kuwa ni cha kujadili hatma ya kiungo hiyo Bado haijafahamika kikao hicho ni kwa ajili ya mubakisha papy au la kwkaua hakuna gaarifa yoyote ilyotolewa na klabu au mchezaji mwenyewe mpaka sasa Tshishimbi anatarajia kumalia mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na kuna uwezekano mkubwa wa kutimka klabu hapo mara baada ya wapinzani wa yanga Simba Sc kuonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo   
2michezo
MWAMVITA MTANDA WEKUNDU wa Msimbazi, Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya ili mfululizo. Mafanikio ya Simba yametokana na sababu nyingi, ikiwemo ukubwa au  upana wa kikosi hicho, mbinu pamoja na ufundi wa benchi la ufundi la timu hiyo linaloongoza na kocha mbelgiji, Patrick Aussems na ubora wa  mchezaji mmoja mmoja. Ninapozungumzia ukubwa au upana wa kikosi cha Simba , ninamaanisha ubora wa wachezaji wa timu hiyo. Ni ukweli ulio wazi kwamba, kikosi cha sasa cha Simba kinaundwa na wachezaji wenye viwango vya juu na uzoefu mkubwa. Hata hivyo, uwezo wa wachezaji wa timu hiyo kucheza dakika tisini kwa kasi ile ile pasipo kuchoka ni eneo jingine muhimu katika kufikia matarajio ya kikosi hicho. Nani anayesababisha hali hii? Kabla ya msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania  Bara, kikosi cha Simba kilikuwa kikijulikana kwa sifa ya kutomudu vyema mapambano ya dakika 90. Simba haikuwa na uwezo wa kucheza vipindi vyote viwili kwa kasi ile ile. Iliweza kucheza kipindi cha kwanza kwa kasi lakini kadri  muda ulivyozidi kusonga kasi ilipungua. Hata hivyo udhaifu huo  haukushuhudiwa msimu uliopita wa Ligi Kuu na hata katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba ilishiriki. Wachezaji wa timu hiyo walionekana kuwa na nguvu dakika ya kwanza hadi ya tisini. Hapa  ndipo tunapomkuta mtu anayeitwa Adel Zrane. Raia huyu wa Tunisia ndiye mtaalamu wa mazoezi ya viungo katika kikosi cha Simba. Zrane tangu alipoajiriwa na klabu hiyo, ameweza kuwafanya wachezaji kuwa ngangari kiasi cha kutosha. Undani wake Zrane anasema alizaliwa mwaka  1980 katika mji wa Sousse nchini Tunisia. Anasema katika ukuaji wake alikuwa anapenda sana maisha ya soka. Elimu yake Zrane anamiliki leseni ya juu ya utaalamu wa viungo ‘Phisical fitnes’ambayo inatambulika na Shirikisho la Soka Ulaya ‘UEFA’ pamoja na shahada ya uzamivu ‘PHD’ ya maswala ya lishe na viungo. MCHANGO UBINGWA SIMBA Kocha huyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuisadia Simba kupata ubingwa, kutokana na namna ambayo amewajenga wachezaji na kuwafanya kuwa imara. “Mimi kazi yangu ni kuhakikisha wakati wote wachezaji wanakuwa imara ili kuwafanya waweze kumudu mifumo ya kocha Aussems,”anasema. Zrane  amefanya kazi kubwa kwa kuwafanya  wachezaji kuwa tayari wakati wote na hata Aussems alipofanya mabadiliko haikuathiri kiwango cha uchezaji cha timu yake.   ANAVYOITAZAMA SIMBA Anasema anajisikia faraja kufanya kazi ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi na hasa baada ya kuhakikishiwa na mabosi wake kubaki nayo msimu ujao. Anasema mafanikio ya kazi anayofanya na           kikosi cha Simba yanatokana na uelewano kati yake na wachezaji. “Hakika wachezaji wamekuwa wasikivu kwa  kila kinachowafundisha au kuwaelimisha, hii inaifanya kazi yangu kuwa rahisi,”anasema. Anasema endapo wachezaji wa Simba wataendelea kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kama ilivyo sasa, basi watafika mbali zaidi. Anasema,wapo baadhi ya wachezaji aliwakuta wakiwa wamekata tama ya kuendelea kucheza soka kutokana na kutokubalika kwa makocha waliopita  hatua  iliyowafanya kujaa viburi, lakini akapambana kuwanjenga kisaikolojia hadi wakabadilika. “ Nafurahi sana kuwepo Simba, hasa katika nchi hii ya Tanzania, nafanya kazi yangu katika mazingira  mazuri na watu ambao wapo tayari, naweza kusema wachezaji  wote ni marafiki zangu, nawalea kwa kuwafanya wawe na nidhamu nzuri,”anasema Zrane. Wachezaji wanamzungumziaje? Pascal Wawa Ni beki wa kati wa Simba. Raia huyu wa Ivory Coast, ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Asec Memos ya nchini humo anamsifu Zrane kwa kusema ni mtu anayeijua kazi yake sawa sawa. Wawani miongoni mwa wachezaji wakigeni ambao wakati wanajiunga na timu hiyo hawakukubalika kwa mashabiki, hali hiyo ilitokana na uzito mkubwa walioonekana kuwa nao dimbani.  “Ni zaidi ya kaka kwangu, amekuwa karibu na mimi na kunitia moyo  hasa nilipokata tamaa, pia alinijenga na kuanza kufanya vizuri mpaka leo hii nipo fiti kabisa,”anasema.  HAROUNA NIYONZIMA Niyonzima ni kiungo wa Simba, raia wa Rwanda, ambaye alisajiliwa akitoka Yanga. Tayari amewachezea Wekundu hao kwa  misimu miwili. Kiungo huyo ni minongoni mwa wachezaji  walioponea chupu chupu kufungashiwa virago msimu uliyopita kutokana na kushuka kiwango.  Kuporomoka kwa kiwango kwa nahodha huyo wa zamani wa Rwanda kulisababisha asiaminiwe na hivyo kuwa mchezaji anayeanzia benchi. Niyonzima amesema,  mpaka anafanikiwa kurejea katika ubora wake ni matokeo ya programu za kocha Zrane. Anasema amemfanya kuwa na uwezo wa kucheza  dakika tisini kwa kiwango kile kile. “Huwezi kuniambia kitu kwa huyu kocha, amenisaidia sana, kweli nilitaka niondoke kabisa Simba, lakini walishirikiana na kocha Aussems kunijenga kisaikolojia mpaka leo nipo sawa, nina imani kuwa bado nina misimu kadhaa mbele ya kucheza soka hapa,”anasema Niyonzima.
2michezo
NEW YORK, MAREKANI SIKU moja baada ya rapa Jay Z, kutangazwa kuwa bilionea wa kwanza katika muziki wa hip hop, staa wa muziki wa RnB, Robyn Fenty maarufu kwa jina la Rihanna, ameingia kwenye historia mpya ya kuwa msanii wa kwanza tajiri kwa upande wa wanawake. Wasanii wengi wamekuwa wakijikusanyia pato kubwa mara baada ya kuachia albamu au nyimbo ambazo zitafanya vizuri kwenye chati mbalimbali za muziki duniani, lakini imekuwa tofauti kwa Rihanna. Mara ya mwisho kwa Rihanna kuachia wimbo mmpya ilikuwa Januari 27, mwaka 2016, ambapo wimbo huo ulijulikana kwa jina la Anti, uliachiwa chini ya uongoz wa Roc Nation ambao unamilikiwa na rapa Jay Z. Mbali na kukaa muda mrefu bila ya kuachia wimbo au albamu, Rihanna kwa mujibu wa Jarida la Forbes ameingiza kiasi cha dola milioni 600, ambazo ni zaidi ya trilioni moja za Kitanzania. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akiingiza kiasi hicho cha fedha kutokana na kazi zake za muziki, ikiwa pamoja na ziara mbalimbali siku za hivi karibuni na biashara yake ya bidhaa za urembo. Wasanii ambao Rihanna anashindana nao kwa sasa ni pamoja na Madonna ambaye anakadiriwa kuwa na kiasi cha dola milioni 570, Celine Dion dola milioni 450 na mke wa Jay Z, Beyonce mwenye utajiri wa dola milioni 400. Mwezi mmoja uliopita, Rihanna alifanya mazungumzo na The New York Times, aliweka wazi kuwa, anapambana kwa kufanya kazi zingine ambazo hatamani kuzifanya, lakini ikiwa ni lengo la kuutafuta utajiri. “Fedha zipo njiani, lakini nimekuwa nikifanya kazi mbalimbali ambazo zingine sizipendi kuzifanya lakini kwa ajili ya kuutafuta utajiri,” alisema Rihanna. Wimbo wa Anti, unatajwa kuwa miongoni mwa chachu ya ongezeko la kipato chake, inadaiwa kwamba wimbo huo unaongeza mauzo ya biadhaa zake za urembo. Alianza kujiingiza moja kwa moja kwenye biashara ya urembo mwaka 2017 na ikaanza kupenda na idadi kubwa ya wanawake. Mapema mwaka huu, kampuni ya LVMH Moet Hennessy Louis Vuitton, ambayo inatajwa kuwa moja kati ya kampuni zinazotengeneza bidhaa mbalimbali za urembo, iliingia mkataba wa kufanya kazi na Rihanna ambapo msanii huyo anachukua kiasi cha dola milioni 10 kupitia kampuni hiyo. Lakini mbali na mafanikio hayo, mashabiki wake wametumia mitandao ya kijamii wakimuomba aachie wimbo mpya au albamu ili waweze kupata burudani kwa kuwa muda mwingi sasa anautumia kwa ajili ya biashara ya vifaa vyake vya urembo. Mwishoni mwa mwaka jana, msanii huyo aliweka wazi kuwa, yupo kwenye mpango wa kuachia albamu mpya ambayo itakuwa ikijulikana kwa jina la R9, lakini hajaweka wazi ataiachia lini.
4burudani
SAID Suleiman Omar (15) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika msafara wa Waziri Ofi si ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, George Simbachawene huko Masota Shengejuu Mkoa wa Kaskazini Pemba.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Shekhani Mohamed Shekhani alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilisababisha kifo cha kijana huyo anayeishi Dar es Salaam ambaye alikwenda Pemba kwa matembezi ya likizo ya mwisho wa mwaka.Shekhani alisema Said aligongwa na gari moja yenye namba ya SMZ 665 ambayo ilikuwa katika msafara wa Waziri wakati kijana huyo alivuka barabara baada ya gari la tatu lililokuwa kwenye msafari huo kupita.Msafara huo ulikuwa ukitoka Chakechake kuelekea Wingwi ambapo Said alivuka barabara akidhani msafara huo umemalizika na ndipo alipogongwa na gari hiyo ya nne. Jeshi la Polisi linamshikilia dereva aliyesababisdha ajali hiyo aliyefahamika kwa jina la Omar Mohamed Abdallah kwa mahojiano zaidi.Kutokana na ajali hiyo, Waziri Simbachawene alikatisha ziara yake na kwenda kuwapa pole familia ya mtoto Said hapo kijijini kwao. Baba wa mtoto aliyefariki dunia, Suleiman Omar alisema hiyo yote ni mipango ya Mungu.“Nimesikitishwa na ajali hiyo lakini hiyo ni mipango ya Mungu anachotaka ndiyo huwa,”alisema.Waziri Simbachawene yupo ziarani Pemba kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo masuala ya mazingira na athari zake zinazotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
1kitaifa
NA FESTO POLEA, MKALI wa wimbo wa Chura, Snura Mushi ‘Majanga’ amesema  bado wimbo wake umezuiliwa licha ya kupeleka muswada mpya unaoongoza video mpya ya wimbo huo. Snura aliwaambia waandishi wa habari visiwani hapa wakati akijiandaa na show yake ya jana usiku katika tamasha la Ziff kwamba ameshapeleka marudio ya script ya pili aliyotakiwa afanye na mamlaka husika baada ya kwanza kukataliwa. “Wimbo wangu wa Chura bado umezuiliwa lakini kwa sasa nina wimbo mwingine unaitwa ‘Shindwe’ ukimaanisha kishindo huu utaniongezea mashabiki kutokana na kuwa katika mahadhi ya uswahilini, kisingeli,’’ alisema Aliongeza kwamba mashabiki wa ‘Chura’ waendelee kuvuta subira hadi mamlaka husika zitakaporuhusu video hiyo kurudiwa kwa kufuata maadili yanayotakiwa. Onyesho la jana usiku lilikuwa maalum kwa kuitwa ‘Usiku wa Bi Kidude’ ambapo wasanii na majd walioshiriki katika burudani ni wanawake.
4burudani
Ramadhan Hassan -Dodoma SERIKALI imesema bado kuna tatizo la matumizi makubwa ya bangi nchini ambapo mwaka 2015 hadi  Juni, 2020, kilo 188,489.93 za bangi zimekamatwa. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana, Sera na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika siku ya  maadhimisho ya kupinga vita dawa za kulevya duniani. Jenista alisema bado tatizo la matumizi ya bangi ni kubwa nchini ambapo Serikali inajitahidi kulitatua na kwamba wamefanikiwa kukamata kilo 124,080.33 za mirungi kilo 58.46 za Cocaine na kilo 635.57 za heroin. Alisema katika ukamataji huo, watuhumiwa 73,920 walikamatwaa ambapo pia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imefanikiwa kufanya ukaguzi katika makampuni 167 yanayojihusisha na uingizaji  wa kemikali bashirifu. Alisema katika ukaguzi huo, mamlaka imefanikiwa kukamata kiasi lita za ujazo 480,000 na kilo 22,145 za kemikali bashirifu zilizoingia nchini bila ya kufuata utaratibu. Alisema tatizo la dawa za kulevya katika jamii ni mtambuka linalohitaji ushiriki wa sekta mbalimbali katika kupambana nalo. Alisema DCEA inatekeleza majukumu yake  ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na wizara mbalimbali, vyombo vya ulinzi na usalama, na taasisi zingine za Serikali na zisizo za Serikali pamoja na mashirika ya kitaifa na kimataifa. Alisema  mwaka 2015-2020, mamlaka imetekeleza kazi mbalimbali katika kukabiliana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2017. Pia imetoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya ambapo mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu imeweza kuanzisha vilabu vya kupinga dawa za kulevya mashuleni. “Vile vile, elimu bora kuhusu tatizo la dawa za kulevya imekuwa ikitolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile televisheni, magazeti, warsha za kitaifa na makongamano pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu madhara ya dawa hizo pamoja na udhibiti wa uchepushwaji wa kemikali bashirifu. “Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia wimbi la vijana kuingia kwenye matumizi na biashara ya dawa hizo,” alisema. Alisema pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhoofisha na kuvunja mitandao mikubwa ya wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi. Waziri Jenista alisema kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2019 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Tanzania  ilifanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kwa 90%. Pia, mamlaka imeshinda kesi kubwa za wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya. “Upanuzi wa huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya, mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zingine zisizo za kiserikali imefanikiwa kupanua huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya nchini, ambapo hadi mwaka 2016 kulikuwa na vituo vitatu tu nchini ambavyo vilihudumia waathirika 3,500.
5afya
Msanii wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amemkataa Mwana FA ambaye jana alitangazwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona na sasa yupo karantini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya. Dimpoz alionyesha kumkataa Mwana FA kupitia video aliyopost katika ukurasa wake wa instagramu ambapo mtu alimpiga simu kuumuuliza iwapo amekutana na msanii huyo hivi karibuni lakini alimkwepa akisema hana ukaribu naye siku hizi. Katika video hiyo ambayo pengine ni ya kuigiza Ommy alisema Mwana FA marafiki zake ni waimbaji wa Hip Hop, tajiri wa GSM na Alberto Msando. Hata hivyo kuonyesha kuwa yalikuwa ni masilahala maelezo ya video hiyo ya Ommy ilikuwa ikiwashauri watu kutowakimbia waathirika na badala yake kupima. “Dawa sio kuwakataa marafiki zetu kisa Wamekutwa na Maambukizi,Dawa ni kwenda kupima kama ukijiona una Dalili Zilizotajwa za Corona” Dawa sio kuwakataa marafiki zetu kisa Wamekutwa na Maambukizi,Dawa ni kwenda kupima kama ukijiona una Dalili Zilizotajwa za Corona #StaySafe #StayHome #WashHands A post shared by Ommy Dimpoz (@ommydimpoz) on Mar 20, 2020 at 5:24am PDT  
4burudani
NEW YORK, MAREKANI BAADA ya mkali wa muziki Shad Moss ‘Bow Wow’ kuachana na mpenzi wake wa zamani, Erica Mena, sasa msanii huyo ameweka wazi kwamba anatoka na mkali wa muziki wa RnB, Keyshia Cole. Kupitia akaunti yake ya Twitter, juzi Bow Wow aliweka picha akiwa na mrembo huyo na kusema kwamba ‘Kichwa kimepata sehemu ya kutulia’ Hata hivyo, rafiki wa karibu na Bow Wow alisema kwamba wawili hao kwa sasa wapo katika uhusiano, lakini mambo yao yanafanyika chini kwa chini. Bow Wow kwenye akaunti yake ya Instagram aliandika kwamba uhusiano wake wa sasa ni bora zaidi ya mwaka jana, hivyo anaamini atadumu kwa muda mrefu na mpenzi mpya, japokuwa hakumtaja ni nani. Msanii huyo alikuwa chini ya kundi la Young Money Cash Money, lakini mwaka jana aliamua kujitoa na kufanya kazi pamoja na Snoop Doggy, ambaye ndiye aligundua kipaji cha masanii huyo.
4burudani
PARIS, UFARANSA BINGWA namba mbili kwa ubora wa nchini wa tenisi duniani kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal, juzi alionesha ubora wake na kutwaa ubingwa wa French Open baada ya kumchapa mpinzani wake Dominic Thiem kwa seti 6-3, 5-7, 6-1, 6-1. Pambano hilo ambalo lilitumia saa tatu na dakika moja, lilimfanya Nadal kuonesha ubora wake kwa wachezaji wa mchezo huo kwenye udongo. Kuna viwanja mbalimbali vya viwanja ambavyo vinatumika kwa ajili ya mchezo huo, miongoni mwa viwanja hivyo ni pamoja na sehemu yenye udongo, hivyo Nadal ameripotiwa kuwa bingwa wa viwanja hivyo. Huu ni ubingwa wake wa 12 wa michuano hiyo ya wazi ya nchini Ufaransa, lakini bado hajamfikia mpinzani wake Roger Federer ambaye anashika nafasi ya tatu kwa ubora, lakini anaongoza kuwa na mataji mengi ya Grand Slam ambapo anayo 20, huku Nadal akiwa na 18. Hata hivyo, Nadal amempongeza mpinzani wake Thiem kwa ushindani aliouonesha kwenye mchezo huo wa fainali huku akiamini anaweza kuja kufanya makubwa kwenye michuano mingine siku za hivi karibuni. “Ameonesha ushindani ambao sikuutarajia, amestahili kufika fainali, nampongeza kwa kile alichokifanya, ninaamini atakuja kuwa bora zaidi ya hapo kwa siku za hivi karibuni kama vile kwenye michuano ya Austrian. “Msimu huu ushindani ulikuwa mkubwa sana, lakini kila mmoja alipambana kuhakikisha anafanya vizuri, ninaamini nimeweza kutwaa ubingwa huu kutokana na maandalizi yangu kuwa bora zaidi. “Ninawashukuru wote ambao walikuwa na mimi katika kipindi hiki chote tangu mwanzo hadi siku ya mwisho ninatwaa ubingwa, nianze kwa familia yangu, mke wangu pamoja na mashabiki kwa kuonesha sapoti ya nguvu kwangu, ninaamini bila ya wao sidhani kama ningekuwa na nguvu ya kufanya hivi, asanteni sana,” alisema bingwa huyo.
2michezo
Tanzanite ina kibarua kigumu cha kupenya hatua inayofuata kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa vijana wa umri huo zitakazofanyika mwakani Papua New Guinea.Ugumu huo unatokana na timu hiyo kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Zambia nyumbani na hivyo italazimika kushinda kuanzia mabao 5-0 katika mechi ya marudiano inayotarajiwa kufanyika keshokutwa Lusaka, Zambia.Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwenda Zambia jana, nahodha wa timu hiyo Stumai Abdallah alisema mechi iliyo mbele yao ni ngumu hivyo wanaomba dua za Watanzania kufanikisha ushindi.“Kwa kweli tunakwenda kupambana, tunajua mechi ilivyo ngumu, tunaona wenzetu tunaowaacha nyumbani mtuombee jamani tusonge mbele,” alisema.Naye kocha mkuu wa timu hiyo, Rogasian Kaijage alitaka mashabiki wa soka nchini kutokatishwa tamaa na matokeo ya kwanza ya timu hiyo.“Tumefungwa idadi kubwa ya mabao, lakini hiyo isiwe sababu ya kukata tamaa, tunaweza kubadili matokeo,” alisema.Aidha, mkuu wa msafara wa timu hiyo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Blassy Kiondo alisema timu iko vizuri na matumaini ya kupata ushindi yapo.“Vijana wa ari kwa kweli, timu yetu ipo vizuri, mwalimu amerekebisha makosa yaliyojitokeza mwanzo tunaamini mechi ya marudiano itakuwa kali sana na tutapata matokeo ya kuridhisha,” alisema. “Unajua mpira ni mchezo wa makosa, hakuna sababu ya kukata tamaa, kama wao (Zambia) walitufunga hapa nyumbani basi hata sisi tunaweza kuwafunga kwao, kwa nini tushindwe,” alisema.
2michezo
SWAGGAZ RIPOTA AGIZO la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu kuchunguzwa kwa nyota wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, kama anatumia bangi au laa ili aweze kukamatwa, limenifikirisha vitu vingi na kufanya nianze kutazama kwa ukaribu mwenendo wa hivi karibuni wa memba huyo wa WCB. Licha ya mazuri mengi ambayo amekuwa akiyafanya kama vile kusaidia walemavu, kutoa mitaji kwa wanawake na vijana wajasiliamali, kufanya shoo kubwa zinazoacha gumzo pamoja na kuzidi kupaa kimuziki, Harmonize amekuwa tofauti kitabia na yule wa kipindi kile anaatoka. Ukitazama ukurasa wake wa picha ambao mpaka sasa una wafuasi zaidi ya milioni 2.9, utagundua mambo kadhaa ambayo hapo awali hakuwanayo. Mengi ni mabaya yanayofunika mazuri, jambo linalowaumiza wanaopenda mafanikio yake. TABIA YA KUVUTA SIGARA Katika agizo la mlezi wa WCB, Paul Makonda alilolitoa juzi katika kikao chake na wasanii, alisema tabia ya ajabu ni miongoni mwa sababu zinazokwamisha wasanii wengi kupata dili kwa kuwa kampuni nyingi zinataka mtu safi asiye na uchafu mbele ya jamii. Ndiyo maana akiwa kama baba wa WCB, alimwomba gavana wa Accra, Ghana amchunguze kijana wake Harmonize kama anachovuta hadharani ni sigara au bangi ili kama ni dawa za kulevya basi akitua Bongo, aweze kuwekwa rumande na kufunguliwa kesi kama ile ambayo ilimkuta mrembo Wema Sepetu. Hiyo yote imetokana na tabia mpya ya staa huyo, kuvuta sigara hadharani jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya vijana wadogo wanaomtazama kama kioo pia hata kwa afya yake akiwa kama msanii wa muziki anayeiwakilisha vyema Tanzania huko ulimwenguni. MGUU NDANI MGUU NJE WCB? Harmonize kwa sasa ni msanii mkubwa. Ukitazama msafara wake wenye walinzi mbavu nene wapatao wanne utagundua jamaa siyo wa mchezo na tayari ameanza kujijengea ‘empire’ au utawala wake akiwa bado ni memba wa WCB. Licha ya mambo kadhaa yanaonyesha, Harmonize bado ni msanii wa WCB, kuna tetesi zilizotokana na mwenendo wa msanii huyo na  viongozi wa WCB kuwa kwa sasa Konde Boy, mguu mmoja ndani na mwingine upo nje ya lebo hiyo kubwa Afrika. DIAMOND ASHANGILIA AGIZO LA MAKONDA Wakati Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akitoa kauli ya Harmonize kushughulikiwa kutokana na tabia yake ya kuvuta hadharani kitu kinachotoa moshi unaofanana na bangi, Diamond Platnumz alionekana akipiga makofi. Hiyo ni ishara kuwa anapongeza na amefurahishwa na agizo hilo ambalo kama ni kweli linakwenda kumtia matatani Harmonize ambaye ni msanii wake. SAPOTI IMEKUWA NDOGO Tetesi zimeendelea kudai kuwa huwenda Harmonize hayupo sawa na Diamond Platnumz au viongozi wake kutokana na sapoti ndogo ambayo amekuwa akipewa hivi karibuni tofauti na ilivyokuwa huko nyuma. Mfano wimbo Paranawe wa Harmonize aliofanya na Rayvanny, Diamond Platnumz, hakuwahi kuuposti katika ukurasa wake wa Instagram kama ilivyokawaida yao kusapotiana. Hata mameneja wao kama Sallam Sk, Babu Tale na Mkubwa Fella hawakuupa sapoti mtandaoni wimbo huo kama ambavyo wanawapa kina Rayvanny, Mbosso, Lavalava na wasanii wengine. Hali kadharika hivi karibuni Harmonize, anaachia albamu yake fupi (EP) inayoitwa Afro Bongo. Hii ni albamu kubwa inayotarajia kusumbua chati mbalimbali za muziki Afrika akiwa ameshirikiana na staa wa Nigeria, Burna Boy. Jambo la kusangaza, Harmonize amekuwa akiipa promo yeye mwenyewe bila sapoti ile kubwa ambayo tumezoea kuioa WCB wakipeana. HARMONIZE ANAKWAMA WAPI? Hakuna anayeweza kubisha kuwa Harmonize ni msanii bora zaidi kwa sasa, tazama nyimbo zake zinavyoweka rekodi kubwa, fuatilia shoo zake anazofanya, utagundua ni msanii ambaye atadumu kwa muda mrefu kwenye muziki. Harmonize, anakwama pale ambapo anaanza kulewa sifa kipindi hiki ambacho Afrika imempokea vizuri na tayari ameanza kuuwakilisha vyema ukanda huu wa Afrika Mashariki kama mwenyewe anavyojiita ‘East African Young Star’. Anaweza asione mapungufu hayo lakini ni vizuri akasikia kelele za mashabiki wanaompenda, wakimuonya kuwa siyo vizuri kwa afya yake kutumia moshi, siyo jambo jema  kujikweza ila vizuri kujilinda, kuwekekeza kwenye kazi na kusaidia jamii ili aendelee kudumu miaka na miaka.
4burudani
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza Kamati ya Maadili kufuatilia ukweli kuhusu tuhuma za upangaji wa matokeo zilizotolewa na kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili.Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema baada ya TFF kusikia tuhuma hizo zilizotolewa na Kabwili kupitia vyombo vya habari, sekretarieti imeiandikia barua Kamati yake ya Maadili kufanyia kazi suala hilo.“TFF itavijulisha vyombo vingine vya usalama ili visaidie uchunguzi na kuchukua hatua stahiki,” alisema Ndimbo.Kabwili ambaye ni kipa wa tatu Yanga, amenukuliwa na kituo kimoja cha redio nchini akiishutumu Simba kutaka kumpa hongo kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kupanga matokeo.Alidai Simba ilimshawishi afanye kosa kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania litakalomfanya aoneshwe kadi ya njano na kufikisha idadi ya kadi zitakazomsababisha akose mechi iliyofuata dhidi ya watani wa jadi katika soka ya Tanzania.Hata hivyo, Kabwili aliyesimama langoni kwenye mechi dhidi ya Simba Februari 16, mwaka jana, Yanga ikifungwa 1-0, bao pekee la mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 72 alisema hakukubali kushiriki mpango huo.Wakati mchezaji huyo akisubiri kwenda kwenye Kamati ya Maadili ya TFF, Klabu ya Simba imepinga na kukemea vikali kauli ya Kabwili.Katika mtandao wao wa Instagram jana, Simba walisema wanapinga vikali kauli hiyo aliyoitoa juzi katika kituo cha Redio cha East Afrika, na kusisitiza kwamba inaamini kauli za aina hii kutoka kwa wachezaji ni za kuchukiza na sio za heshima ambazo zinaashiria upangaji wa matokeo ya mechi kama ilivyotuhumiwa na mchezaji huyo.Ilisema: “Kauli hizi zina madhara makubwa kwenye uadilifu wa klabu ya Simba na uongozi wake, heshima kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania inawekwa mashakani kama kauli za namna hii hazitachukuliwa hatua stahiki”. Taarifa hiyo ilisema Simba inafurahishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na TFF dhidi ya kauli kama hizi kwa vyombo husika.“Simba inaamini jambo hili lipo mbele ya mikono ya vyombo husika na litachukuliwa hatua stahiki haraka,” sehemu ya taarifa hiyo ilisisitiza.Wakati huo huo, TFF imempongeza mshambuliaji Thomas Ulimwengu baada ya kusajiliwa na Klabu TP Mazembe kwa mkataba wa miaka miwili. Sehemu ya taarifa hiyo ya TFF inasema: “Hongera Thomas Ulimwengu kwa kujiunga na TP Mazembe, tunakutakia kila la kheri ”.Ulimwengu amerejea Mazembe ambako aliondoka mwaka 2016 na kwenda klabu ya FC Athletic Eskilstuna kisha FK Sloboda Tuzla kati ya mwaka 2017-18 zote za barani Ulaya.Mwaka 2018 alirejea barani Afrika na kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Sudan na mwaka 2019 alijiunga na klabu ya JS Saoura ya Algeria na alicheza michuano ya klabu bingwa Afrika na kikosi hicho. Ulimwengu amerejea kuimarisha safu ya ushambuliaji ya TP Mazembe na jana alitua Lubumbashi kuanza kazi rasmi.
2michezo
TIMU za soka Azam na Simba zinatarajiwa kushuka dimbani leo kucheza fainali ya michuano ya kusheherekea miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Timu hizo zitashuka katika dimba la Gombani ambako ndiko kunakofanyika fainali hiyo, ambapo Azam ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga KMKM mabao 3-0 na Simba iliishinda Malindi kwa penalti 3-1 baada ya mchezo wao kumaliza dakika 90 wakiwa suluhu.Mchezo huo wa fainali utapigwa majira ya saa 9:00 za alaasiri na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye ndiye atakuwa mgeni rasmi na kukabidhi zawadi kwa washindi.Azam hii itakuwa ni mara ya tatu mfululizo kufikia hatua hiyo ya fainali, na iwapo itanyakuwa tena kombe hilo, itaondoka kabisa na kombe hilo.Wakizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya Simba, Nico Kiondo alisema kuwa wanatarajia kupambana na kurekebisha makosa yao waliyoyafanya katika mchezo wa nusu fainali ili kuweza kushinda mchezo huo.Alisema kuwa katika fainali hiyo mpaka sasa hajawa na uhakika wa kuongeza kikosi isipokuwa inategemea na uwamuzi wa wakuu wao lakini ikiwezekana wataongeza ili kukiongezea nguvu kikosi hicho.Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema wao wamejipanga kucheza na timu yoyote watakayokutana nayo fainali.Alisema kuwa wao mashindano ya Kombe la Mapinduzi wameyapa uzito mkubwa na ndio maana hata ujaji wao wanakuja na kikosi kamili ili kuweza kutoa ushindani.“Tunmejipanga kutetea ubingwa wetu na tukishinda itakuwa ni historia mpya kwani tutakuwa kombe ni mali yetu rasmi, tunamuomba mungu atujaalie hilo”, alisema Iddi.Michuano ya kombe la Mapinduzi ilikuwa ikishirikisha timu tisa, sita kutoka Zanzibar na tatu Tanzania Bara, ambazo ziligawiwa katika makundi mawili.Bingwa wa michuano hiyo mwaka huu, atapata Kombe, Medali za Dhahabu na Sh Milioni 15 wakati mshindi wa pili ataondoka na kitita cha Sh Milioni 10.
2michezo
VINARA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Yanga wamesema watapambana na wekundu wa Msimbazi Simba katika harakati za kuwania taji la Ligi Kuu msimu huu.Akizungumza na waandishi wa habari juzi usiku kwenye kambi yao Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema walipoanza msimu hawakuwa na malengo yoyote wakijua wanaweza kuwa katika nafasi ya tano au sita, lakini baada ya kuona mwenendo wao ni mzuri sasa anatangaza rasmi lazima wapiganie taji. “Hatuwezi kujificha hasa ikizingatia kwamba tulifanya vizuri mzunguko wa kwanza na wa pili pia, tumeanza vyema, natangaza rasmi kwamba tutapambana na Simba kuwania taji la Ligi Kuu,” alisema.Zahera alisema mwenendo wao ulikuwa mzuri isipokuwa walianza kupoteza baadhi ya mechi kwa madai ya waamuzi kushindwa kuchezesha kwa haki. Alisema wanachokiangalia katika michezo iliyobaki ni kuhakikisha wanafanya vizuri mpaka mwisho na kuchukua taji hilo sambamba na kubeba Kombe la Shirikisho la Azam (FA). Yanga kwa sasa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 67 katika michezo 27 kiasi cha kujiamini na kuona kuwa ina nafasi ya kupigania taji hilo linaloshikiliwa na Simba. Wanafuatiwa na Azam yenye pointi 56 na Simba pointi 51 lakini ikiwa na michezo saba kibindoni.Kilio Bodi ya ligi Kocha huyo alilalamikia ratiba ya Ligi Kuu kuwabana katika mechi zijazo ikionesha kutakiwa kucheza kila baada ya siku tatu katika mikoa iliyoko mbali na kwamba licha ya kupeleka barua kuomba kuliangalia hilo, Bodi hiyo imewakatilia na kuweka msimamo kuwa ni lazima wacheze. “Mchezaji akicheza mechi anatakiwa apumzike saa 72 kwa sababu mwili unakuwa umechoka ili mwili uweze kurejea katika hali ya kawaida, lakini sasa unakuta safari ya kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine mpaka ufike haupumziki wala kupata muda wa kufanya mazoezi,” alisema na kutolea mfano wanatakiwa wacheze Mwanza kisha waanze safari ya Mtwara. Alisema kwa ratiba hiyo ngumu hata kubeba kombe lenyewe itakuwa ni kazi kubwa.Wachezaji wafundwa Katika mkutano huo wa waandishi ulihudhuriwa na wachezaji, viongozi na wadau wa klabu wakiwafunda wachezaji kujitambua na kujipanga kimaisha. Kwa upande wa kocha aliwataka wachezaji kujua kuwa kuna maisha baada ya mpira hivyo, wanapaswa kujipanga wakati wowote kama baba wa familia. Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay aliwataka wachezaji kujiandaa na maisha kwa kuhakikisha wanawekeza kibiashara au hata kimasomo ili mwisho wa siku wakiachana na soka wawe na kitu kingine cha kufanya.
2michezo
POLISI jijini Mwanza inawashikilia watu 46 kwa tuhuma za kujihusisha na makosa mbalimbali. Makosa hayo ni unyang’anyi, kupatikana na dola bandia za Marekani (utapeli), wizi wa vipuri vya magari, usafirishaji, uuzaji, matumizi ya dawa ya kulevya na uhalifu wa kuvunja nyumba usiku na kuiba.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema watu hao walikamatwa kwenye operesheni inayoendelea, iliyoanza Juni 4 mwaka huu. Kamanda huyo alisema wahalifu sugu wa matukio ya unyang’anyi walikamatwa Juni 7 mwaka huu ndani ya ziwa Victoria katika maeneo ya Kunene, Bwiro, Kweru na Irugwa wilayani Ukerewe.Wengine walikamatwa katika Manispaa ya Ilemela katika visiwa vya Bezi na Makoba na eneo la Sengerema katika visiwa vya Kasarazi, Zilagura, Iyozi na Maisome. Watuhumiwa 21 wakiwa na injini 21 za mitumbwi, walikamatwa na kutambuliwa na wamiliki. “Pia tumefanikiwa kukamata nyavu haramu 195 na pikipiki mbili moja aina ya San LG na nyingine Nissan ambazo namba zikiwa zimefutwa,” alisema.Kamanda Muliro alisema kwenye operesheni iliyofanywa na polisi kuhusu matukio ya utapeli, kupatikana na dola bandia za Marekani na fedha bandia za Tanzania, kuanzia Juni 28 hadi Juni 30, mwaka huu watu sita walikamatwa.Alisema watu hao walikamatwa katika wilaya za Nyamagana na Sengerema, ambapo watuhumiwa watano wa dola bandia walikamatwa wilayani Nyamagana wakiwa na dola bandia noti 599 za Sh 100 zenye namba moja inayofanana na mtuhumiwa mmoja, alikamatwa wilayani Sengerema akiwa na noti bandia 32 za Sh 10,000. Kwa upande wa wizi na vifaa vya magari, katika kipindi hicho hicho, wezi tisa wa vifaa vya magari (vipuri) walikamatwa kwenye makazi ya watu wakiwa na taa za magari, vitasa, redio ya gari na vioo vya magari (side mirrors).Kwa upande wa wavunjaji wa nyumba na kuiba usiku, Kamanda Muliro alisema watuhumiwa watano walikamatwa pamoja na runinga saba zilizokuwa zimeibwa pamoja na mitungi ya gesi na kompyuta mpakato. Vifaa hivyo vimepatikana na baadhi ya vitu vimetambuliwa na wamiliki.Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa, wakiwemo watuhumiwa wa dola bandia na shilingi bandia za Tanzania kuwa ni Joseph Okwalo (23) na Fredy Joseph (19), mfanyakazi wa mabasi ya Friends ambao kwa pamoja ni wakazi wa Bugando Mission.Wengine ni Anatory Shilinde maarufu kama White(26) mkazi wa Ndofe-Igoma- Mwanza, Kukundakwe Karukwanzi(38) meneja wa mabasi ya Friends, Aida Mkumbo(40) karani wa mabasi ya Friends na Osca Haji (22) mkazi wa Nyamkumbo mkoani Geita
1kitaifa
Mahitaji   Jinsi ya kuandaa Katakata vipande vidogo vidogo vya embe Weka chumvi katika sufuria, kaanga hadi iwe rangi ya kahawia (usiweke maji). Acha ipoe, pasha mafuta moto halafu acha yapoe kidogo, baada ya hapo weka paprika, pilipili, binzari na viungo vyote, changanya vizuri. Weka chumvi na maembe changanya vizuri. Funika mchanganyiko, acha ikae usiku kucha ili embe ilainike. Siku ya pili tayari kwa kutumia, unatakiwa kuiweka juani ili embe ilainike vizuri zaidi. Lakini ni hiari, si lazima.
5afya
WIZARA ya Kilimo imeunda timu ya watu watano kuhakiki ulipwaji wa fedha kwa wakulima wa korosho kwa msimu wa 2018/2019 baada ya kunusa ufi sadi katika malipo hayo.Aidha imemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kuchunguza na kuhakiki matumizi wa fedha za uliokuwa Mfuko wa Wakfu kutokana na kuwepo kwa matumizi yasiyofaa ya fedha Sh bilioni 53.2 .Taarifa hizo mbili zinatakiwa kuwa zimekamilika ifikapo Januari 15 mwakani kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki kwa watakaobainika.Hayo yamebainishwa jana jijini hapa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa malipo ya korosho zilizonunuliwa na Serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa mwaka 2018/2019.Alisema mpaka mwisho wa msimu, takribani tani 222,561.2 za korosha ghafi zilikuwa zimekusanywa zikiwa na makadirio ya thamani ya Sh bilioni 723.8.Alisema kati ya korosho hizo zilizokuwa daraja la kwanza zilikuwa tani 204,476.1 zenye thamani ya Sh 674,771,522,700 na zile za daraja la pili zilikuwa tani 18,084.9 zenye thamani ya Sh Sh 47,744,294,400.“Hivyo kumeifanya Serikali iwe imelipa wakulima kwa korosho kwa tani 217,786 zenye thamani ya Sh bilioni 707.8.“Azama ya serikali ilikuwa ni lazima kulipa malipo ya wakulima wote, lakini hadi leo tunapozungumza hapa, malipo ya wakulima bado hajaisha, na hii inatokana na mambo ambayo yamejitokeza kwenye malipo.”Hasunga alisema pamoja na kuwa kamati ya ulinzi na usalama na ile ya kilimo kufanya uhakiki, wamebaini kuwapo udanganyifu mkubwa katika malipo ya wakulima.“ Sasa kutokana na udanganyifu huo unatupa shaka kama viongozi wa wizara kwamba huenda hata baadhi ya ya wakulima waliolipwa sio sahihi.”Hasunga alitolea mfano Chama cha Msingi cha Sangasanga AMUCOS ambacho kimefanya udanganyifu kwa kuongeza kilo zaidi ya 7,000 huku wakilipwa malipo hewa ya zaidi ya Sh milioni 222.2Aidha alisema kuna baadhi ya watu waliolipwa sio wakulima, na ambao hawakuleta korosho kwenye chama cha msingi lakini majina yao yapo kwenye malipo ya mwisho na fedha ambazo zimelipwa kwa watu ambao sio wakulima ni Sh 222, 328, 867 na hii ni kwenye chama kimoja tu cha Sangasanga.Alisema pia katika baadhi ya vyama uhakiki uliweza kuokoa zaidi ya Sh bilioni 1.6 ambazo zingelipwa kwa wakulima hewa.“ Kuna vyama vingine pia tumepata changamoto kama hizo, kule Tandahimba kama isingekuwa uadilifu wa wale waliosimamia uhakiki kulikuwa na Sh bilioni 1. 6 zilikuwa zinapotea na maeneo mengine imeonekana upo udanganyifu.”Hasunga alisema timu hiyo ya watu watano iliyoundwa inatakiwa kuhakikisha inaangalia kama korosho zilizopokelewa ndizo zilipo na ndio kiasi kilichouzwa na kama kuna upungufu ni kiasi gani.Hasunga alisema Timu hiyo pia inatakiwa kuhakiki kama kuna wakulima ambao mpaka sasa bado hawajalipwa.Aidha, Hasunga alisema wizara yake pia imemuagiza CAG kufanya uchunguzi na uhakiki wa matumizi ya fedha Sh bilioni 53.2 za uliokuwa Mfuko wa Wakfu ambazo zililenga kujenga viwanda vitatu, maghala na kuendeleza zao la korosho.“Mwishoni wa mwaka 2016, serikali iliamua kufuta Mfuko a Wakfu na wakati huo kwenye akaunti ya mfuko huo kulikuwa na kiasi cha Sh bilioni 53.2 kwa ajili ya kujenga viwanda vya kubangulia korosho Mkinga mkoani Tanga, Tunduru-Ruvuma na Mkuranga-Pwani.“ Kilichojitokeza Bodi ya Korosho badala ya kutekeleza maagizo ya serikali wakabadilisha matumizi ya fedha, viwanda havikujengwa, maghala hayakujengwa na wakatumia fedha tofauti na maagizo ya serikaliHasunga aliongeza: “ Kilichotushtua mwaka huu wakati minada inaendelea wale walioagiza magunia kwa misimu iliyopita kwamba wanaidai serikali kiasi cha Sh bilioni 12 kwa ajili ya magunia ya msimu wa mwaka 2017/2018.Alisema wakati huo, utaratibu uliokuwepo mnunuzi wa korosho ndiye aliyetakiwa kulipia magunia hayo.“Swali linakuja kuwa fedha za magunia, ni kwanini hazijalipwa na leo Serikali inadaiwa?” alisema.Alisema katika matumizi yaliyoanishwa na Bodi ya Korosho pia ilikuwa ni kuvipa Vyama Vikuu vya ushirika kulipia madeni yao ya nyuma ya benki ambako chama cha TANEKU Ltd kilipewa Sh bilioni 1.87 na chama cha CORECU kilipewa Sh bilioni 2.12.
1kitaifa
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema amepokea ujumbe mfupi kutoka kwa watu 5,763 na majina 100 ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja baada ya kutoa rai kwa wananchi kuwataja.Makonda akiwa katika msiba wa mwandishi wa habari nchini, Isack Gamba, Dar es Salaam, aliwataka wananchi kuwataja wasichana wanaojiuza katika mitandao ya kijamii na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja baada ya uwepo wa watu wanaotuma picha hizo katika mitandao ya kijamii.Akizungumza na gazeti hili jana, Makonda alisema mpaka asubuhi ya jana tayari amepokea jumbe hizo pamoja na majina ya watu mbalimbali wanaojihusisha na tabia hizo ambazo ni kinyume cha sheria za nchi.“Nimetoa taarifa hii jana (juzi) nikiwataka wananchi wanitumie ujumbe na kupiga simu. Simu ni nyingi mpaka nyingine nimeshindwa kupokea, lakini ujumbe ndio huo nimepokea mpaka sasa na majina yanayotajwa yanajirudia naamini mpaka jioni nitakuwa nimepata taarifa nyingi zaidi,” amesema Makonda.Alisema kwa sasa kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili ambao unafanyika kwenye mitandao ya kijamii ambako watu wameamua kuweka mambo ya faragha kwenye mitandao hiyo.“Wanapotangazia umma wanaleta madhara makubwa kwa watoto ambao wengi kwa sasa wanashika simu na kuona mambo ambayo ni kinyume na maadili ya kitanzania,” alieleza Makonda.Alisema kuanzia Jumatatu ijayo atakuwa na timu maalumu pamoja na madaktari ambao watawashughulikia watu hao na wale watakaobainika kujihusisha na mambo hayo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Aliongeza kuwa hawatoishia kwa watu hao pekee, bali hata wale wanaofanya nao uchafu huo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.“Hakuna asiyejua sheria ipo wazi na wale wanajihusisha na mambo haya sheria inasema wanastahili kifungo cha miaka 30 au maisha, kwa hiyo ni lazima na wale wanaojihusisha kushiriki kitendo hiki wachukuliwe hatua,” alisema.Aidha, alisema mbali na watu wanaojihusisha na mapenzi na jinsia moja na wasichana wanaojiuza kupitia mitandao ya kijamii, pia kuna baadhi ya watu wanahamasisha vitendo vya ngono kwenye mtandao wa ‘WhatsApp’ watashughulikiwa kwa kuwa tayari wanashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kwa hatua zaidi.Alisema wanataka mambo ya mapenzi ya jinsia moja, udhalilishaji na kila aina ya vitendo vya uvunjifu wa maadili ya utu wa Mtanzania, maadili ya dini na imani zote yadhibitiwe katika mkoa ili kuepusha madhara kwa vizazi vijavyo.Aliongeza kuwa endapo wakiwaacha watu hao baadaye taifa litazalisha mashoga na wasichana wanaojiuza katika mitandao ya kijamii na kuondoa sifa ya nchi. Alisema tayari watu waliorusha picha zao chafu kwenye mitandao, akiwemo Amber Rutty pamoja na mpenzi wako mikononi mwa polisi tangu alipoagiza wafike.“Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam yeyote anayemfahamu shoga au anayefanya mambo kinyume maadili na sheria nipatie jina nataka wiki hii mpaka Jumapili napokea majina na kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kuna timu itaanza kuwashughulikia,” alisema mkuu wa mkoa.Katika hatua nyingine, baada ya wasanii wa filamu kusambaza picha zao za ngono kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo, TCRA imewaonya wasanii wa filamu na muziki na watumiaji wa mitandao dhidi ya tabia hiyo chafu.Katika tangazo lao kwenye gazeti hili jana, TCRA ilisema ni kosa kisheria kutengeneza na kusambaza picha, sauti na maandishi ya ngono au yenye muelekeo wa kingono katika mitandao ya kijamii.Kwa kuwa jambo hilo ni kosa la kijinai kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na Kanuni za Maudhui za mwaka 2018, Mamlaka hiyo imeutaka umma wa Watanzania kuzingatia matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano na mitandao ya kijamii nchini. Ikumbukwe kwamba, hivi karibuni, muigizaji wa filamu, Wema Sepetu aliingia kwenye matatizo na mamlaka za serikali na tasnia ya filamu baada ya picha yake yenye maudhui ya kingono kusambaa kwenye mitando ya kijamii.Mbali na Wema, msanii mwingine maarufu ‘Amber Rutty’, naye amekuwa gumzo baada ya picha yake ya video inayomuonesha akifanya vitendo vya ngono kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Baada ya Wema kukiri kosa, Bodi ya Filamu Tanzania ilimfungia muigizaji huyo kujishughulisha na masuala yote yanayohusu filamu na uigizaji kwa muda usiojulikana hadi hapo bodi itakapojiridhisha kuwa amejirekebisha.Taarifa ya TCRA imetoa onyo kwa watu au wasanii wote wenye tabia ya kusambaza jumbe picha, sauti, katuni au maandishi ya ngono, ponografia na yasiyo ya kimaadili katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, Twitter na makundi ya WhatsApp.TCRA ilisema hatua kali za kisheria zimeshachukuliwa dhidi ya wahusika na zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na utengenezaji, usambazaji wa picha, sauti, vibonzo au maandishi ya ngono yenye mwelekeo wa kingono yasiyo ya maadili.
1kitaifa
WATANZANIA wametumia Swala ya Idd el – Haji kuombea nchi kuepukana na majanga kama lile la watu 75 kupoteza maisha baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro, Jumamosi iliyopita.Akizungumza katika Swala ya Idd el Haji Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya Msikiti wa Kibadeni Chanika jijini Dar es Salaam jana; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo aliyekuwa mgeni rasmi, aliwawataka watanzania kuungana pamoja kuendelea kuliombea taifa kuepuka na majanga mbalimbali.Waziri huyo alisema Watanzania wanapaswa kuliombea Taifa ili liondokane na majanga kama lile la Morogoro ambapo pia aliwataka watanzania kuwaombea watu waliopoteza maisha na waliojeruhiwa kutokana na tukio hilo.“Janga hili la juzi linatukumbusha janga lililotokea katika Kijiji cha Isongore Mkoani Mbeya miaka ya nyuma, lilitokea na watu wengi walipoteza maisha, janga kama hili si Tanzania pekee, sehemu nyingine kama Ghana, Nigeria, Congo limeshawahi kutokea hivyo tujitahidi kuombea majanga kama haya yasitokee,” alisema Waziri Jafo.Kwa upande wake Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeir amekemea shutuma kuwa baadhi ya kauli ndani Bakwata zinaipotosha serikali na kusema hawatavumilia kusemwa vibaya.Mufti Zubery alisema, baraza hilo hutoa elimu hivyo watu wasiwachonganishe na serikali kwa kutafsiri vibaya kauli zake. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Taifa Bakwata, Hamisi Mataka alisema ni muhimu baraza hilo kufanya mazungumzo ili kuondoa tofauti inayoendelea ya Waislamu wa nchi moja kuswali Sikukuu ya Idd siku tofauti na kwamba hali hiyo inaondoa umoja.Kutoka Dodoma; Shehe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amesema kazi ya Mola haina makosa alipangalo Mola huwa hakuna wa kulaumiwa kutokana na vifo vya ajali ya moto vilivyotokea mkoani Morogoro ambapo amewaomba Watanzania kuwaombea waliofariki dunia pamoja na majeruhi wa tukio hilo.Akizungumza jana katika Swala ya Iddi iliyofanyika katika Msikiti wa Gaddaf jijini hapa, Shehe Rajabu pia alipongeza viongozi wa ngazi za juu katika serikali kwa kuwasaidia majeruhi wa tukio hilo pamoja na kuwahifadhi wale ambao wamefariki dunia mjini Morogoro.Kutoka Mwanza; Bakwata Mkoa wa Mwanza imetoa salaamu za pole kwa Rais Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Stephen Kebwe na wakazi wa mkoa wa Morogoro kwa ujumla kufuatia tukio la ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro Agosti 10 mwaka huu na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70.Shehe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke akihutubia waumini wa dini ya kiislamu kwenye sherehe za Sikukuu ya Idd el Haji ambayo ilifanyika katika uwanja wa Nyamagana alisema tangu kutokea kwa ajali hiyo, serikali yote imehamia mkoani Morogoro akiwemo Waziri Mkuu, Mawaziri na viongozi wengine wa serikali ambao wameonesha ushirikiano wa pamoja katika kukabiliana najanga hilo.Kutoka Zanzibar; Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ameitaka jamii kuacha kusuluhishana matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia. Akilihutubia Baraza la Idd katika uwanja wa Dole Kizimbani Wilaya ya Magharibi Unguja, Dk Shein alisema hakuna mtu aliye juu na sheria na anayefanya vitendo vya udhalilishaji afikishwe mbele ya vyombo vya dola.Aidha amewataka viongozi wa dini ya kiislamu pamoja na mashehe kwa ujumla kutoa elimu na mawaidha kuhusu njia ya kukabiliana na vitendo hivyo ambavyo haviendani pamoja na tabia ya binadamu. Imeandikwa na Regina Mpogolo, Dar, Magnus Mahenge, Dodoma, Nashon Kennedy, Mwanza na Khatib Suleiman, Z’bar
1kitaifa
JOSEPH HIZA NA MITANDAO CLAUDIA Wanjiru ni mwanamtindo mwenye makovu usoni, ambayo aliyapata baada ya kunusurika mkasa wa moto akiwa mwanafunzi wadarasa la saba. Kabla ya mkasa huo, Claudia, ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya alikuwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo. Lakini licha ya makovu usoni, amehakikisha ndoto hiyo anaitimiza. Akizungumza namna alivyopatwa na makovu hayo,anasema “tulipokuwa kwenye hoteli tukiwekewa chakula, jiko la gesi lililipuka na mafuta yakanimwagikia usoni. Nilianza kukimbia nikitafuta maji”. Alichukuliwa kisha akapelekwa hospitalini. Alikuwa ameungua kwa asilimia 14 usoni. Alikaa hospitalini kwa muda wa miezi mitatu. Hali hii ilifanya maisha yake kubadilika, hata kukosa marafiki. “Baada ya kuungua, watoto ambao walikuwa wadogo kwangu kiumri, walikuwa wananiogopa, na wale wa rika langu, walikuwa wananicheka na kunitania. Nikiwa shuleni, nilikuwa napata barua za matusi na mwalimu alipokuwa akitupatia zoezi la kufanya kwa makundi, hakuna mtu aliyekuwa akikubali kuwa naye kundi moja,” anasema. Hali hii ilipelekea Claudia kukumbwa na msongo wa mawazo kutokana na namna watu walivyomtendea na kumsema. “Watu walisema nilijaribu kubadilisha rangiya ngozi yangu lakini dawa zikagoma; Wengine walidai eti nina Ukimwi. Nilikuwa najipendekeza kwa watu ili nipate marafiki, lakini mtu aliyekuwa anakubali kuwarafiki yangu alikuwa na lengo fiche.” “Kutokana na kukosa marafiki, nilijaribu kujitoa uhai kwa kuweka jiko katika chumba changu na kufunga mlango na madirisha, lakini sikufa, nikajua Mungu ameniokoa.” “Nilijua kwamba Mungu amenipatia nafasi nyingine na kuwa ananipenda si lazima nipendwe na mtu kwa kuwa yeye ndiye aliyenipatia maisha haya, ni yeye ndiye aliniweka duniani.” Aliponusurika baada ya kujaribu kujitoa uhai, akaamua kujikubali na kujitahidi kufikia ndoto yake ya kuwa mwanamitindo. “Nikaanza uanamitindo, ili niwasaidie wasichana wengine ambao pengine wanazuiwa kushiriki kwa sababu ni wanene ama niwafupi. Lengo, wasome historia yangu ili wajue kuna matumaini.” Amejaribu kwenda katika mashindano ya uanamitindo lakini kila wakati mawakala humbagua. “Kuna wakati nilienda kujisajili katika mashindano ya uanamitindo lakini wakala akanizuia mlangoni na kuniambia niwanamitindo pekee walioruhusiwa kuingia,” anasema. Lakini alijua kukataliwa kwake ni kwasababu ya makovu yake. Licha ya kukataliwa na mawakala, Claudia ambaye pia anajitambulisha kama ‘Vanilla Afrika’ kama  jina lake la kisanii, hakukata tama. Kwa msaada wa wanafunzi wenzake, hupigwa picha katika mazingira tofauti na kuziweka katika mtandao wa Instagram. Makovu pia yamemkosesha mchumba. “Mvulana ambaye nilikuwa namchumbia, kila wakati tukikosana, ananikumbusha juu ya alamazangu usoni. Huniambia anavumilia kuwa na mimi kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunipenda na alama hizo.” Hata hivyo, msichana huyu anaulezea urembo kulingana na anavyotambua. “Urembo ni tabia, ni kumsaidia mtu, kumheshimu mtu, urembo ni utu… Hii ndiyo maana ya urembo, kwasababu mtu anaweza kuwa na sura ya kupendeza, lakini hana tabia za kupendeza. “Kama mimi mwenyewe niko na hizi alama, najiambia kwamba mimi ni mrembo, kwasababu si alama zinanipatia jina, alama ni ngozi tu, kila mtu anayo.”
3kimataifa
Maonesho hayo yatakayofanyika nchini kwa mara ya kwanza yameandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade).Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo, Boniventure Mwalongo, wadau mbalimbali wa tiba asili na tiba mbadala wanatarajia kushiriki katika Maonesho hayo.Mwalongo alisema washiriki hao ni pamoja na watabibu wa tiba asili, watengenezaji wa dawa asili, wakunga wa tiba asili, kampuni za dawa asili na vipodozi vya dawa asili, wasambazaji wa tiba asili na tiba mbadala, watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na tiba mbadala.Aidha, Mwalongo alisema wanaendelea na taratibu za kufanya maongezi na wadhamini mbalimbali ambapo watatoa taarifa rasmi baada ya kufikia tamati ya maongezi, ikiwa ni pamoja na kutoa ratiba nzima ya maonesho hayo.Wadau wasiopungua 280 wameonesha nia ya kushiriki.
0uchumi
SERIKALI itaboresha kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kumwezesha kijana kupata fursa ya mkopo kuendeleza miradi mbalimbali itakayomkwamua kiuchumi.Hayo yameelezwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Sh milioni 92 iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Alisema serikali imeweka mikakati ya kuwawezesha vijana kiuchumi waweze kuanzisha au kuendeleza uzalishaji mali.Alisema serikali ilianzisha kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la kutoa mikopo yenye riba nafuu. Kwa kulitambua hilo, alisema serikali imeamua kuangalia utaratibu mzuri utakaokuwa unatoa fursa ya kuwezesha vijana kupata mikopo hiyo, ikiwemo suala la kumwezesha kijana mmoja mmoja kuwa na nafasi ya kupata mikopo hiyo.“Mfano kijana akiwa ana mradi wake na akawa na vigezo vya kukopesheka ni vyema akapatiwa mkopo ajiendeleze kiuchumi kwa kuwa atakuwa na uwezo kuzalisha ajira kwa wengine,”alisema.Alisema awali lengo la kutoa mkopo huo kwa vijana ilikuwa ni kuwawezesha kuendeleza miradi ya uzalishaji mali wanayoifanya pamoja na kuinua kipato chao wajikwamue kiuchumi.“Nipongeze vikundi vya vijana 12 wa wilaya ya Chato, Geita na Bukombe vilivyopewa mkopo. Hatua mliyofikia itachangia uanzishaji viwanda vidogo ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kuongeza ukuaji wa uchumi,”alieleza Mavunde.Mbunge wa Chato ambaye ni Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amesema vikundi 783 vimesajiliwa Geita na baadhi ya vikundi ni vya vijana wa Wilaya Chato waliopata mkopo na kuanzisha shughuli za kiuchumi za ufugaji, kilimo, uchimbaji wa madini, uvuvi na biashara.Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu alieleza programu ya kukuza ujuzi inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ni vyema ikiwawezesha vijana kupata stadi za kazi katika utoaji huduma za hoteli kukuza utalii.
1kitaifa
WAKATI tama- sha la Utamaduni la Afrika Mashariki (JAMAFEST) likitarajiwa kufungwa Leo, mambo yalikuwa ni moto usiku wa juzi baada mastaa wa vichekesho na muziki kupanda jukwaani kwa burudani, huku wakishukuru kwa kuwa miongoni mwa walioweka historia mpya. Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ aliyetumia sanaa yake ya uchekeshaji kuwa- furahisha watu alisema anashukuru kwa kupata nafasi ya kupanda jukwaa la JAMAFEST kwani ameonekana katika nchi sita kwa wakati mmoja. “Nashukuru kwa kupata nafasi hii kwani nimekuwa mmoja wa walioweka historia, ni heshima kwa sababu hili ni jukwaa kubwa na tumeonekana Rwanda, Kenya, Uganda, Burundi na hapa nyumbani inaonesha sasa hata sanaa yetu in- azidi kukua na kutambulika, “alisema. Tamasha halikubagua watu hadi wasanii wa muziki wa Injili walipata fursa kutumbuiza na miongoni mwao ni Joel Lwaga aliyesema anashukuru kupata nafasi ya kutumbuiza katika jamii kwani amefarijika. “Kupata nafasi kumenitia moyo na nguvu kubwa kwa kuwa hili ni tamasha kubwa la kijamii na jumbe zangu nyingi kupitia nyimbo ninazoimba zimekuwa zikiwagusa vijana kwa sababu maisha wanayopitia hata mimi nimetoka huko, “alisema. Mbali na hao, nani analikumbuka kundi la muziki la Segera ? Nao waliibukia kwenye tamasha na kuamsha shamrashamra kutokana na aina ya uimbaji wao unaovutia kucheza bila kujali ni mtoto, kijana, mzee au mama. Kiongozi wa kundi hilo, Siza Mazongela alisema wamerudi tena na kitendo cha kupata nafasi katika jukwaa hilo la kimataifa kumewafanya kuwa na furaha na kupandisha mzuka wao wa kazi.“Nimejisikia raha sana kupata nafasi hii ya kuchangamsha, hatukupotea ila tulikuwa tunaendelea na matamasha sehemu mbalimbali na baada ya hapa kuna lingine linakuja Novemba la muziki wa taarabu, “alisema. Wasanii wengine walioburudisha ni Ben Paul, Maua Sama, Bendi ya muziki ya Rwanda, Kundi la vicheke- sho kutoka Kenya na vikundi mbalimbali vya ngoma vya nchi za Afrika Mashariki.
2michezo
KATIBU Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Balozi John Kijazi amezindua vikundi kazi vya baraza hilo kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kuibua changamoto na kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania.Akizungumza baada ya uzinduzi wa vikundi kazi hivyo jijini Dar es Salaam juzi, Balozi Kijazi alisema madhumuni ya kuunda vikundi kazi hivyo vilivyowajumuisha wataalamu katika sekta mbalimbali, vitawezesha majadiliano juu ya changamoto zijadiliwe kwa kina zaidi kabla ya kupelekwa katika ngazi ya Baraza.“Jumla ya vikundi kazi vinne nimevizindua leo (juzi) ikiwa ni pamoja na Kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara, Viwanda, Misitu na Kilimo vitavyokwenda kuibua changamoto na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera na miongozo iliyopo,” alisema Balozi Kijazi.Alisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma, unahitajika ili kuweza kubaini changamoto na kuzijadili na kuja na mapendekezo yatakayoleta tija katika mustakabali wa kujenga uchumi wa Taifa.“Serikali itapokea mapendekezo yote yatakayowakilishwa na timu za wataalamu kutoka katika vikundi kazi hizi na tutayafanyia kazi mapendekezo yote, zaidi kwa mengine yanayoweza kuchukuliwa na maamuzi kwa ngazi yenu endeleeni lengo ni kupanga majadiliano katika ngazi ya taifa,” alisema Balozi Kijazi.Alisisitiza kuwa mijadala ya vikundi kazi hivyo vifanyiwe kazi kwa uhuru na usawa kwa kutohofia cheo cha mtu au mali, bali wote wawe kitu kimoja ili majadiliano yaweze kuleta tija na mapendekezo yatakayofanya mazingira ya biashara kuboresheka zaidi.“Vikundi kazi hizi vikapitiwe Sera, Miongozo na Sheria zilizopo ili waje na mapendekezo yatakayoboresha mazingiria ya biashara kuwa rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini,” alisema.Alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya tozo, mamlaka za udhibiti na kero mbalimbali katika uanzishaji wa biashara nchini, hivyo ni muhimu vikundi kazi hivyo vikatoa mapendekezo katika maeneo hayo ili yafanyiwe kazi. “Uongozi wa awamu ya tano umefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara, hivyo ni matumaini yangu tutakwenda kumaliza kabisa changamoto zilizopo na kupelekea nchi yetu kupiga hatua kiuchumi,” alisema Balozi Kijazi.Pia, Balozi Kijazi alisema kikosi kazi cha kilimo kisimamie utekelezaji wa nguzo kumi za kilimo kwanza na pia kufanya mapitio ya Mpango wa Awamu ya Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP- II) na kuleta mapendekezo ya utekelezaji wake. “Lengo letu ni kutizama azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, vikundi kazi hivi ndiyo vitatupa mwanga wa kufikia malengo kwa kuja na mapendekezo yenye tija na utekelezaji ufanywe maendeleo yapate kuonekana,” alisema Balozi Kijazi.
1kitaifa
SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutoka kuwa baraza na kuwa mamlaka kamili ili litekeleze majukumu yake kwa ufanisi zaidi.Nia hiyo ya serikali imeelezwa juzi na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima, kwa wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea Makao Makuu ya NEMC jijini Dar es Salaam.“Kuna kila sababu ya kuifanya NEMC mamlaka kutokana na umuhimu wa mazingira,” amesema Simba na kuongeza serikali imekwishatambua suala la kulinda mazingira ya Tanzania ni muhimu mno na kwa hiyo NEMC kama chombo chenye dhamana ya kuhifadhi na kusimamia mazingira kinahitaji kuongezewa nguvu na mamlaka.Mwenyekiti wa kamati, Suleiman Saddiq Murrad alisema pendekezo hilo ndiyo kwanza wanalisikia kutoka upande wa serikali.“Kamati kama mshauri wa Bunge tumelipokea, tutalijadili katika vikao vya kamati na kupeleka mapendekezo bungeni, alisema Murrad.Murrad kwa niaba ya kamati, amesifu kazi zinazofanywa na baraza na kuahidi kamati itaendelea kuunga mkono NEMC ili kusudi majukumu ya baraza yatekelezwe kikamilifu. Kuhusu changamoto wanazokumbana nazo hasa upungufu wa watendaji, mwenyekiti alisema kamati itazitolea mapendekezo kwa serikali na suala la upungufu wa wafanyakazi italipa uzito unaostahiki ili baraza lipate watendaji wa kutosha kwa sababu mazingira yanagusa maeneo ya uhai na ustawi wa Taifa.Kamati ilielezwa kwamba kwa sababu ya upungufu wa wafanyakazi zaidi ya miradi 10,000 iliyosajiliwa haikufuatiliwa au kukaguliwa.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesisitiza baraza lazima lisimamie Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 katika kutekeleza majukumu yake.“Sheria ya Mazingira inampa nguvu mtendaji katika kutimiza majukumu yake hivyo ni lazima kusimamia sheria zilizopo ili kuhakikisha mazingira yanabaki salama,” alisema January.Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka aliahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na kamati na serikali na hasa kusimamia sheria ya mazingira na nyingine ili kuyalinda mazingira ya Tanzania.Kamati ilikagua mradi wa ujenzi wa ofisi mpya za NEMC na kutembelea maabara ya vyura wa Kihansi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako kamati ilielezwa historia ya vyura hao na utunzwaji wake.
1kitaifa
NEW YORK, MAREKANI UMOJA wa Falme za Kiarabu (UAE) utayaunga mkono mapendekezo ya Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu mazungumzo mapya ya kutafuta amani Yemen. Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE, Anwar Gargash, amesema walifanya mazungumzo ya tija na mjumbe maalumu wa UN kuhusu Yemen, Martin Griffiths, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Kauli hiyo ya UAE inakuja wiki mbili baada ya mkutano wa kutafuta amani Yemen uliofanyika mjini Geneva, Uswisi kushindikana baada ya waasi wa Houthi kutohudhuria. Waasi hao waliushutumu muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia kuwazuia kusafiri kwenda kwenye mazungumzo hayo.
3kimataifa
OFISA Mtendaji wa Kata ya Mpwayungu wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Selemani Kibakaya amesema wamefanikiwa kuzuia ndoa za utotoni nne na kulazimisha wazazi wao kurudisha mahari walizochukua.Alikuwa akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Mradi wa Sauti Yangu unaotekelezwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Women Wake Up (Wowap), unafadhiliwa na Shirika la Child Fund Korea kupitia Jukwaa la Haki za watoto.“Wiki iliyopita nimefanikiwa kurudisha mahari za watu wanne waliotaka kuoa watoto chini ya miaka 18,kuna sababu nyingi zinafanya watoto waolewa mapema ikiwa ni pamoja na kufuata mkumbo na yote haya ni sababu ya umaskini.”Alisema kila mwanajamii, viongozi wa dini wana jamii ya kueleza kuhusu haki za watoto, wawakilishi wa watoto ikiwezekane waingine kwenye baadhi ya vikao vya serikali ili watoe changamoto zao.“Mara nyingi watoto wanasemewa lakini ifike wakati tuwasikilize ili kuweza kubaini changamoto zinazowakabili.”alisema Alisema wamekuwa wakipambana na matukio na kesi za wanaowapa mimba wanafunzi lakini tatizo kubwa ni ushirikiano kutoka kwa wananchi. Alisema walikuwa wakikamata wanaowapa mimba wanafunzi lakini cha kushangaza fomu ya matibabu (PF 3) zilikuwa zikipotelea polisi na hivyo ushahidi muhimu kukosekana.“Tukaamua kupambana na hilo, binti akipelekwa hospitali tunaomba nakala tatu za PF 3 ambazo zinakwenda shuleni, polisi na kwa mtendaji na hiyo ikawa ajenda yetu ya kudumu.”Alisema kesi za kuwapa mimba wanafunzi zinatakiwa kuwa na ushahidi wa kutosha ili wahusika wachukuliwe hatua. Kibakaya alisema sasa wameweza kupunguza tatizo la mimba kwenye kata hiyo.“Tangu mwaka huu uanze kuna wasichana wawili tu waliopata ujauzito kutoka kwenye mimba saba zilizokuwepo mwaka uliopita” alisema Alisema kuna umuhimu wa wanafunzi kupimwa mimba mara kwa mara.Kwa upande wake, mwalimu kutoka shule ya Sekondari ya Dodoma, Esther Simchimba alisema kupitia mradi wa sauti yangu watoto hawana sababu za kuingia kwenye mahusiano katika umri mdogo kwani madhara yake ni kufukuzwa shule.Mchungaji Baraka Kisimula wa kanisa la Anglikana Chang’ombe Dodoma alisema amekuwa mdau wa malezi ya vijana 240 wanaotoka katika mazingira magumu na kinamama 36 waliotelekezwa na waume zao.Alisema malezi ya watoto yanahitaji upendo kwani kila mtoto anataka kupendwa. Mratibu wa Wowap Nasra Suleiman alisema mradi huo unatekelezwa ambazo ni Manchali na Mpwayungu wilaya ya chamwino na na kata ya Chang’ombe.Pia klabu za wanafunzi zimeundwa katika shule ya Dodoma sekondari na Lukundu sekondari. Alisema wanafundisha watoto kushirikiana na vyombo vya ulinzi wa mtoto vilivyopo katika maeneo yao ili kuboresha mifumo ya ulinzi wa mtoto na kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto.
1kitaifa
NA AGATHA CHARLES, DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli ameteua mabalozi 21, kati yao wapya 15, wakiwamo wanasiasa wenye majina makubwa. Mabalozi hao walioteuliwa ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika balozi za Tanzania zilizoko nchi mbalimbali duniani, miongoni mwao ni wanasiasa maarufu, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. Pindi Chana na Rajab Luhwavi ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Luhwavi anayeshikilia wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu Bara, CCM na Dk. Chana ambaye ni Kaimu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) pia ni wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho. Taarifa ya uteuzi huo ilitolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na kusambazwa kwenye vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa. Hata hivyo, taarifa hiyo haikuchanganua nchi ambazo mabalozi hao watapelekwa zaidi ya kutaja orodha ya nchi zilizo wazi na nyingine sita ambazo Tanzania imefungua balozi zake mpya. Mbali na akina Nchimbi, wengine walioteuliwa ni Balozi Mbelwa Kairuki, ambaye ni mume wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, Balozi Samuel Shelukindo, Balozi Silima Haji na Balozi Abdallah Kilima. Wengine ni Balozi Joseph Sokoine ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Sokoine, Balozi Baraka Luvanda na Balozi Dk. James Msekela aliyewahi kuwa mbunge wa Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Dodoma. Katika orodha hiyo, wamo pia Sylvester Ambokile, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Mella, Grace Mgovano, Mohamed Bakari na Job Masima. Kundi hilo linawajumuisha pia aliyepata kuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya nne, Omar Yusuf Mzee, Matilda Masuka, Fatma Rajab, Sylvester Mabumba ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Dole na mwenyekiti katika Bunge la 10, Profesa Elizabeth Kiondo na George Madafa (ambaye uteuzi wake ulishatangazwa). Licha ya taarifa hiyo ya Ikulu kusema kuwa vituo vya kazi vya mabalozi hao 21 vitatangazwa baadaye, lakini iliviorodhesha vile vinavyohitaji wawakilishi hao kuwa ni Beijing-China, Paris-Ufaransa, Brussels-Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya, Muscat-Oman, Roma-Italia, New Delhi-India na Pretoria-Afrika Kusini. Vituo vingine ni Nairobi-Kenya, Brasilia-Brazil, Maputo-Msumbiji, Kinshasa-Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kampala-Uganda, Abuja-Nigeria, Moroni-Comoro na Geneva-Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, mabalozi sita watakwenda katika balozi mpya zitakazofunguliwa hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki. “Wale waliobaki katika vituo ambavyo si kati ya 15 vilivyotajwa, wataendelea na nafasi zao za uwakilishi katika vituo walivyopo,” ilieleza taarifa hiyo ikimnukuu Balozi Kijazi.   HESABU KALI Uteuzi wa wanasiasa kama Dk. Nchimbi, Dk. Chana na Luhwavi ambaye ni mmoja wa waliofanya kazi kwa ukaribu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipata kuwa mmoja wa wasaidizi wake, umetoa taswira ya kufanyika kwa mabadiliko makubwa ndani ya CCM, hususani Kamati Kuu na Sekretarieti katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika mwakani. Si hilo tu, uteuzi wa Dk. Nchimbi, ambaye amekuwa mjumbe wa miaka mingi wa CC, wakati fulani akipata kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Naibu Waziri na baadae Waziri katika wizara mbalimbali, nao umetoa taswira kwamba sasa Rais Magufuli anajenga CCM moja. Kitendo cha Rais Magufuli kutomteua Dk. Nchimbi katika Serikali yake kilizua maswali mengi. Julai, mwaka jana Dk. Nchimbi akiwa na wajumbe wenzake wa Kamati Kuu ya CCM, Sophia Simba na Adam Kimbisa, walijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kudai kujitenga na uamuzi wa chombo hicho kwa kuwa kilikiuka Katiba ya CCM wakati wa mchakato wa kupata jina la mgombea urais. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemhamisha Balozi Modest Mero kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva, kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) yaliyopo New York-Marekani, ambako atakuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania. Taarifa hiyo ilieleza kuwa Balozi Mero anachukua nafasi ya Balozi Tuvako Manongi ambaye atastaafu Desemba 6. Pia Rais Magufuli amemteua Grace Martin kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa. Uteuzi huo wa Grace aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ulianza jana. Wengine walioteuliwa ni Balozi Peter Kallaghe ambaye sasa anakuwa Ofisa Mwandamizi Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC). Kabla ya uteuzi huo, Balozi Kallaghe alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
1kitaifa
             Na MWANDISHI WETU, Lagos, Nigeria MARAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya na Nana Akufo-Addo wa Ghana wamewataka vijana Bara la Afrika kuwa wabunifu na kumchangamkia fursa za kiuchumi ili kuiweza kusaidia nchini zao. Kauli hizo wametoa hivi karibuni jijini Lagos nchini Nigeria kwenye jukwaa la nne la kila mwaka lililoandaliwa na Taasisi ya Tony maarufu Tony Elumelu Foundation (TEF), Entrepeneurship Forum. Rais Uhuru Kenyatta, aliwahimiza vijana kutoka bara la Afrika kutumia ubunifu wao ili kuleta mabadiliko. “Viongozi vijana wabunifu kutoka Afrika wanapigana na mabadiliko yenye nia njema kwa kutumia teknolojia. Kuwa bora iwezekanavyo kwa familia, jamii, taifa yako lakini muhimu wewe mwenyewe,” amesema Rais Uhuru alisisitiza ushauri wake kwa vijana kufanya kazi ili kuwa bora kwa taaluma ambayo wamechagua. Tukio hilo ni fursa pekee ya kukusanya vipaji vya biashara kwa vijana, kujenga mitandao yenye nguvu na kupeleka ujumbe kwa watunga sera kwamba sekta binafsi iliyo mahiri na inawajibika inauwezo wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi. Baada ya kupata mafunzo ya miezi tisa, ushauri na ufadhili, jumla ya vijana 4,470 walifaidika na programu hiyo iliyoshuhudia zaidi ya vijana laki tatu wakituma maombi. Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, alisisitiza kuendelea kujitolea kuhakikisha maendeleo ya uchumi Afrika kwa kusaidia mafunzo ya kizazi kipya cha wajasiriamali ambao mafanikio yao yanaweza yakabadili bara hili ikwemo kutengeneza ajira. “Ujasiriamali ni muhimu kufungua maendeleo ya uchumi katika bara letu. Naamini kwa dhati mafanikio yanaweza yakaleta demokrasia na kama tunaweza kubadili tamaa na kuwa fursa, hiki kizazi cha ajabu kinaweza kufanikiwa kwa kila jambo,” alisema Tony Elumelu Naye Rais wa Ghana, Nana Akudo-Addo, aliwasisitizia wawakilishi wa sekta ya umma kuhimiza, kusaidia na kuiga kazi inayofanywa na Taasisi ya Tony Elumelu. “Hakuna kinachobadilika au kujiendeleza kivyake. Watu lazima waamke, waonge, wajadili na kubadilisha mada,” alisema Rais Nana Akufo-Addo. Tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, imeweza kuwasaidia wajasiriamali Waafrika kutoka pembe zote za Bara la Afrika na washindi katika mashindano mbalimbali katika jukwaa la mwaka huu walipata ufadhili wa dola za Marekani 5000 (takribani Shilingi milioni 11.4 kila mmoja).
3kimataifa
Mabingwa hao watetezi wanapewa nafasi ya kushinda mechi hiyo kutokana na ubora wao lakini pia kutokana na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mechi ya kwanza iliyochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Ushindi ni muhimu kwa Yanga leo, kwani ikitereza itatoa mwanya kwa mpinzani wake Simba inayokimbizana nayo kwenye kutwaa taji hilo.Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 59 huku Simba ikiongoza kwa kuwa na pointi 62. Kabla ya mechi ya leo, Yanga imebakiza mechi nne kumaliza ligi na Simba imebakiwa na mechi mbili na hivyo Yanga kuwa kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa ikishinda mechi zake zote hata kama Simba pia itashinda.Akizungumzia mechi hiyo Kocha, Juma Mwambusi, alisema hautarajiwi kuwa mchezo rahisi kutokana na mazingira yalivyo licha ya kupata ushindi mnono katika mechi ya kwanza. “Mchezo wetu wa raundi ya kwanza tulishinda kule, Kagera ni timu nzuri ambayo inaweza kuufanya mchezo kuwa mgumu, kikubwa kwetu ni kujipanga vizuri kwa vita,” alisema.Hali ya ushindani pia ipo kwenye timu za chini zinazopigania kubaki Ligi Kuu, ambapo zinatafutwa timu mbili zitakazoungana na JKT Ruvu kushuka. Ndanda Fc ipo nafasi ya 11, ikifuatiwa na African Lyon, Mbao FC, zote zikiwa na pointi 30, na zimebakiza mechi tatu kila moja ambapo zikishinda zote zitafikisha pointi 39 na hivyo kuziachia msala Majimaji na Toto zenye pointi 29 kila moja.Timu hizo zinatakiwa kujitahidi kushinda mechi zake huku zikiomba timu za juu ziharibu kwa sababu Majimaji ikishinda mechi zote itafikisha pointi 35 na Toto ikishinda zote ita- bakiza pointi 38 na h i v y o kuwa kwenye wakati mgumu wa kusalia kwe - nye ligi.
2michezo
Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Barrick Gold ya nchini Canada, imesema wiki ijayo timu ya wataalamu wake watakuja nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzao na Serikali kuhusu uendeshaji wa migodi yake. Tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kuwa iwapo Barrick inayoimiliki Kampuni ya Acacia itachelewa kuja kufanya mazungumzo ataifunga migodi yao. Wakati kampuni hiyo ikijiandaa kuja nchini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tayari imepeleka madaia ya Dola za Marekani bilioni 190 ambazo ni sawa na Sh trilioni 424), kwa Kampuni ya Acacia, ikiwa ni malimbikizo ya kodi kutoka mwaka 2000. Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Financial Post juzi ilisema. “Kampuni ya Barrick Gold kupitia ripoti yake ya robo mwaka imesema itaanza majadiliano na Serikali ya Tanzania wiki ijayo kuhusu marufuku ya kusafirisha nje madini na masuala mengine yaliyoikumba kampuni inayoimiliki ya Acacia. “Taarifa hiyo ya mazungumzo inakuja baada ya Jumatatu wiki hii Tanzania kuwasilisha bili ya dola bilioni 190 kwa Accacia yenye makao makuu Uingereza. “Serikali ya Tanzania inaituhumu Acacia, ambayo inamilikiwa na Barrick kwa asilimia 63.9 kudanganya mapato yake ili kukwepa kodi na hivyo kuitaka ilipe malimbikizo pamoja na faini. Acacia imekana tuhuma hizo. “Tanzania pia iliweka marufuku ya kusafirisha mchanga wa dhahabu (makinikia) na fedha Machi mwaka huu, hatua ambayo inaweza kuathiri asilimia sita ya uzalishaji wa wakia milioni 5.3 hadi milioni 5.6 ya dhahabu kwa mwaka katika migodi ya Acacia. “Barrick ilisema inasubiri hadi Acacia itakaporekebisha mwongozo wake wa uzalishaji kabla ya kubadili mwelekeo mzima wa uzalishaji wake kwa mwaka,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo ilisema, Barrick yenye makao yake makuu Toronto, Canada iliripoti kuongezeka kwa mapato kufikia Dola bilioni 1.08 robo iliyoishia Juni 30, kutoka dola milioni 138 kwa mwaka mwaka jana. “Hilo lilichochewa na mafanikio makubwa ya mauzo ya hisa katika mgodi wa Veladero na mradi wa Cerro Casale. Mtiririko wa fedha kwa kipindi hicho ulikuwa dola milioni 43 ukiwa umeshuka kutoka dola milioni 274 kwa kipindi kama hicho mwaka jana kutokana na kiwango cha juu cha kodi, ongezeko la mtaji na ongezeko lililopangwa kwa ajili ya matumizi ya ukuaji wa badaye,” ilisema. Juni 14 mwaka huu, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Profesa John Thornton na Ikulu ikatoa taarifa kwa umma kwamba, katika mazungumzo hayo, kampuni hiyo imesema  ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini. Julai 21, 2017 akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Rais Magufuli alisema. “Nitasimamia haki siku zote katika maisha yangu, na niliwaambia nimeanzisha vita hii ya kiuchumi, vita ya kiuchumi ni mbaya sana, wakubwa wale huwa hawafurahi, kuna viongozi wengi tu mliona yaliyowapata ni kwasababu nchi zao zilikuwa na mali. “Lakini wale wakubwa wakataka kuchezea hizo mali, kwa manufaa yao na siyo kwa manufaa ya wananchi wa pale, walitumia mbinu nyingi za kila aina, lakini Mungu wangu ni mwema na Watanzania ni wema watasimama kwa ajili ya taifa hili. “Ninayoongea nayajua ni matrilioni ya fedha ambayo yameibiwa, na kwasasa hivi tumewaita waje wafanye mazungumzo, wamekubali lakini wakichelewachelewa  nitafunga migodi yote. “Ni mara 10 migodi hii tukaigawana Watanzania wachimbe wawe wanauza tuwe tunapata kodi, kuliko kuchimbwa na watu wanaojiita wawekezaji halafu hawalipo kodi. “Walikuwa wanazungumza mle wanachimba dhahabu, madini machache tu, matatu. tumegundua mle kuna madini mengi. “Tanzania hii ni nchi tajiri, lakini imekuwa ikiibiwa mno, tumechezewa sana, mimi nipo serikalini na mimi ndiye najua siri za serikali, tumechezewa sana kwa kuibiwa sana mali zetu, kwenye dhahabu huku tumeibiwa mno, ukiyajua yale yaliyokuwa yanafanyike mle unaweza ukalia. “Unaweza ukatamani usiishi, mtu anachimba anapokea anapeleka na anashirikiana na baadhi ya watu tuliowaamini kwenda kulisimamia hili. “Anasema hapa tunasafirisha mchanga na Watanzania wote tunaamini tunasafirisha mchanga, mbona hawajaja Kibondo kuchukua mchanga wa hapa mbona na penyewe tunao? “Lakini tunaamini, wanaupeleka kwenye makontena wanapeleka Ulaya na wakisha enda kuusafisha kule ule mchanga unaobaki wala hawaurudishi, ulikuwa ni utapeli wa ajabu, na ni aibu kubwa kuona utapeli huu unafanywa na watu ambao ni wakubwa. Julai 26 akiwa mkoani Singida, Rais Magufuli tena alisema “Haiingii akilini watu wanakuja wanachukua mali zetu na kuondoka nazo, ifike mahali tuamke, tumeibiwa vya kutosha, nendeni mkachimbe madini, hizo fedha tutagawana sisi, hata kama hatufanyi kazi hizo fedha tutagawana. “Wapo wachina wanakuja kuchimba barabara hapa nchini, tunashindwaje kuwatumia hawa wakachimbe madini yetu kisha wakatuachia dhahabu yetu halafu wao wakaondoka? “Mimi ndiye Rais, hakuna anayejua siri za serikali kama mimi na nawaambia mmepata mtu ambaye anazungumza ukweli, ningeweza kunyamaza kwa vingine ninavyoviona, lakini nataka kujenga Tanzania mpya. “Yale makontena yote ningeweza kuwaambia tugawane mzee, hata kingereza ninajua, ningeweza kuwaambia give me ten percent (asilimia 10). “Ningejenga mahoteli na kuwa na kampuni nyingi kwani wapo Watanzania wamejenga huko nje lakini nyumba za wazazi wao zimechakaa, mimi nimezaliwa hapa, ninaishi hapa na nitakufa hapa,” alisema Rais Magufuli.
1kitaifa
BEATRICE KAIZA Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Mkoa wa Ilala, inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha kijamii (CCK), Renatus Muabhi kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Serikali kutoka katika taasisi hiyo na kuomba rushwa ya kiasi cha Sh 50,000,000. Akizungumza na Mtanzania Digital Mkurugenzi wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema uchunguzi wa takukuru umebaini kuwa dhumuni lake lilikuwa  ni kuomba rushwa hiyo ili kumsaidia Mkurugenzi wa kampuni ya Bharya Engeneering & Contracting Company Limited (BECCO), Manraj Bharya katika tuhuma zake zilizokuwa zikimkabili. “Mtuhumiwa alikamatwa Desemba 12 mwaka huu katika ofisi za kampuni ya BECCO akiwa amepokea fedha za mtego wa rushwa kiasi cha Sh. 1,000,000,’’ amesema Myava. Pia Myava ametoa rai kwa wananchi kujihadhari na matapeli wa aina hiyo na kujiepusha nao, na endapo wakibaini wahalifu wowote watoe taarifa Takukuru ili uchunguzi ufanyike ili waweze kubainika na kuchuliwa hatua stahiki. Uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
1kitaifa
WASHINGTON, MAREKANI   BUNGE la Marekani linatarajia kupiga kura makubaliano yanayounga mkono bajeti itakayobakisha sehemu kubwa ya programu za misaada kwa Afrika na kutoa dola bilioni moja kukabiliana na tishio la njaa. Makubaliano hayo yalitangazwa jumatatu wiki hii baada ya wabunge kukataa mpango wa kupunguza misaada unaokusudiwa kufanywa na Rais Donald Trump anayetokea Chama cha Republican. Matokeo hayo yanatokana na kutokuwa tayari kwa wabunge waandamizi wa Republicans kukata fedha za programu hizo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo Marekani (USAid). Sehemu kubwa ya wabunge wanaomuunga mkono Trump, waliopendekeza kukatwa kwa misaada walijikuta wakikosa nguvu baada ya uamuzi wa viongozi wa Republican kuingia makubaliano na wabunge wa Chama cha Democrat walio wachache kuukataa mpango wa Rais. Kutokana na uamuzi huo, Rais Trump amepata pigo katika juhudi zake za kuweka ‘Marekani Kwanza’ kwa gharama ya nchi masikini. Hata hivyo, Rais Trump amesema hana jinsi atakubaliana na mpango wa matumizi ya serikali kuu unaowasilishwa na Bunge.
3kimataifa
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wajasiriamali nchini kutumia fursa ya kupima na kupewa nembo ya ubora bure kuboresha bidhaa zao.Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha TBS, Rhoida Andusamile amesema shirika hilo limetoa fursa hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu ikiwa ni pamoja na kuinua uzalishaji wa bidhaa bora na sekta ya viwanda vidogo.Amesema kwa bidhaa za wajasiriamali kuwa na nembo ya ubora kutoka TBS itawasaidia kuingia kwa urahisi katika soko la ndani na nje na pia kuhimili ushindani wa soko.Andusamile alisema anachotakiwa kufanya mjasiriamali ni kutuma maombi TBS akiambatanisha na barua ya utambulisho kutoka Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA) kwa wanaozalisha bidhaa za vyakula."Tukishapokea maombi, tunakuja kuchukua sampuli na kuipima bila gharama yoyote, na kama imekidhi viwango, nembo ya ubora inatolewa kwenye bidhaa husika," amesema.Alisema nembo ya ubora itatumika kwa miaka mitatu bila malipo na baadaye mjasiriamali ataanza kuchangia mwaka wa nne asilimia 25 ya gharama ya leseni, na baadaye asilimia 10 na hatimaye asilimia 100."Tunafanya hivi mchango wake uweze kuwasaidia wajasiriamali wengine wanaochipukia na wakiamini kuwa kwa kipindi hicho mjasiriamali huyo atakuwa amekuwa katika uzalishaji,""Hivyo ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ambayo yatatumiwa na wajasirimali katika eneo husika yaliyo safi na salama." alisema.Akizungumza ushiriki wao katika maonesho ya wajasiriamali wanawake, Andusamile alisema wanatumia fursa hiyo kutoa elimu namna ya kupata nembo ya ubora na faida za kuwa na nembo hiyo.“Pia tunatumia fursa hii kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kununua bidhaa zenye uthibitisho wa ubora kutoka TBS. TBS ndiyo mdhamini wa walaji wa bidhaa, kama bidhaa itamletea shida ni rahisi kupata fidia kulingana na madhara, lakini kama haitakuwa na uthibitisho na nembo ya ubora kutoka shirika letu hawezi kusaidiwa.”Alisema faida za uwekaji nembo ya ubora pia humpa uwezo wa kushindana sokoni, humuondolea usumbufu wa kupima bidhaa kwa kuzingatia matakwa ya mnunuzi na humthibitishia mlaji kuwa bidhaa husika inafaa kwa matumizi, umuhakikishia usalama kiafya na ulinda mazingira."Tunataka kumpatia mjasiriamali elimu bora juu ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na umuhimu wa kuweka nembo ya ubora ili kufikia uchumi wa kati kwani wao ndio msingi wa kupata viwanda vya kati
0uchumi
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imesema imesema askari wa Tanzania wanakwenda kwenye nchi mbalimbali kulinda amani na si kushiriki kwenye mapigano.Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hussein Mwinyi amesema bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa kuwa Tanzania ina wajibu wa kulinda amani kwenye nchi hizo kwa kuwa ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya za kikanda za EAC, SADC na jumuiya ya nchi za maziwa makuu.Ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Bumbwini, Muhammed Amour Muhammed. Mbunge huyo alitaka kufahamu mtazamo wa Serikali kuhusu askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaokwenda kwenye maeneo yenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na wanapoteza maisha.Waziri Mwinyi amesema, Tanzania itaendelea kushiriki kulinda amani katika nchi mbalimbali ili kutimiza wajibu kimataifa na itachukua tahadhari kuepuka maafa yaliyowahi kutokea."Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limechukua hatua ya kutoa mafunzo ya kutosha kwa vikosi vyetu vinavyopewa jukumu hili pamoja na kuwaongezea vifaa vua kisasa ili waweze kujilinda dhidi ya mashambulio ya vikundi vya waasi," amesema.
1kitaifa
Derick Milton, Simiyu Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Simiyu ‘Miss Simiyu’ linalo tarajiwa kufanyika Julai 6, mwaka huu litashirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mkoani humo. Shindano hilo ambalo litafanyikia katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi, Mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson. Akiongea na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Simiyu Talent Company, Zena Mchujuko ambao ndiyo waandaaji wa shindano hIlo amesema kuwa Miss Simiyu mwaka huu itakuwa kubwa. Mchujuko amesema kuwa kwa kushirikiana na Grace Entertainment wameamua kuifanya Miss Simiyu kuwa ya kipekee zaidi lengo likiwa mrembo atakayepatikana afike ngazi ya kitaifa hadi dunia. “ Tutakuwa na mwanamuziki kizazi kipya Diamond Platinumz, ambaye atatoa burudani wakati wa shindano na mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson,” amesema. Mchujuko amesema kuwa tiketi zimeanza kupatikana katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bariadi, ambapo kiingilio cha chini ni 10,000, 50,000 na VIP 100,000.
4burudani
    Na JOSEPH SHALUWA WAKATI soko la filamu za Kibongo likiendelea kudorora, kumeibuka kituko kwenye tasnia hiyo. Kichekesho hicho ni kinachoitwa bifu la Duma (Daudi Michael) na Gabo (Salim Ahmed). Kwa hakika ni kituko. Kwamba, watu waache kufikiria namna ya kutoka kwenye matope, tuanze kuwajadili wao. Katika mitandao ya kijamii, upepo umebadilika na wanajaribu kukuza hiki kinachoitwa bifu. Nilianza kufuatilia huu mchezo tangu mwishoni mwa Septemba, mwaka jana. Sikutia neno. Wiki hii tena wameibuka kwa sura ileile. Nimeona kuna haja ya kuandika kuhusiana na jambo hili. Hapa nitaelezea kwa kadiri nilivyoelewa bifu hili katika sura tofauti. GABO ZIGAMBA… Namfahamu Gabo muda mrefu kisanii. Nimeanza kumfahamu zaidi alipoanza kucheza sinema za Jerusalem Film Company ya mwigizaji Jacob Stephen ‘JB’. Tangu nimeona kazi yake ya kwanza, nimekuwa nikifuatilia kazi zake kwa karibu. Niseme ukweli, ni msanii ambaye niliona uwezo wake tangu mapema kabisa. Nilipomuona kwenye Fikra Zangu, baadaye Majanga nikampa maksi zangu 90 katika uwezo wake wa kuigiza. Anafanya kazi nzuri, mapungufu ya hapa na pale yapo kama msanii hasa kutokana na mazingira ya kazi hapa  Bongo. Lakini kwa ujumla wake, unapotaja wasanii 10 wa kiume wenye uwezo, jina la Gabo kamwe huwezi kuliweka kando. Namfahamu kama msanii anayejitambua, asiyependa makundi, mwenye ndoto za kufika mbali, anayeishi kwenye malengo na asiyekata tamaa. Huyo ndiye Gabo ninayemfahamu. DUMA NAYE… Nilipomuona Duma kwa mara kwanza kwenye Tamthilia ya Siri ya Mtungi, nilisema yes! Bongo Muvi imelamba dume. Tangu hapo nikaanza kumfuatilia. Kwa ujumla niliona uwezo mkubwa wa msanii huyu. Hata nilipomfuatilia kwenye Tamthilia nyingine za Nyota na Huba nilijiridhisha pasipo shaka kuwa kijana kazi anaiweza. Kimsingi Duma amekuja na moto na kiukweli hajawahi kupoa tangu alipoanza kukubalika kwenye game. Ni msanii wa aina yake, mwenye uwezo wa kufikisha mbali sanaa na sanaa ikabadilisha maisha yake. SURA ZA BIFU LENYEWE Natazama bifu lao katika sura mbili – la ukweli au la kupanga. Huenda wamekubaliana kufanya bifu ili wakubalike zaidi kwa mashabiki. Kama ndivyo, hii itakuwa kiki ya kipuuzi kuwahi kutokea. Na mnufaika hapo atakuwa Gabo. Kama ni kweli, siyo kiki basi Duma anajiharibia mwenyewe! Nimemuona akiongea zaidi na social media, akitumia nguvu nyingi kumponda Gabo. Anamsema kwa mengi. Mara hajui kuvaa, hana dili za nje ya nchi kama yeye. Anamwita Gabo ni virus na yeye ni anti virus! Anajisifu kwa safari za Kenya, Uganda na nchi nyingine za nje. Anasema Gabo hatumii vizuri uaminifu anaoaminiwa na Watanzania kwa kutoa kazi nzuri kila wakati. Eti ana tuzo nyingi, lakini hajafanya kitu kikubwa. Iwe kiki au bifu la kweli, hapa Duma amechemka na anaharibu jina lake alilolisotea. JB, Richie (Single Mtambalike) na Bishanga (Alen Raymond) kwa pamoja waliamua kukaa pembeni ya soko kwa muda mrefu, tena wakaanza kujishughulisha na kazi nyingine kabisa nje ya sanaa, lakini walipoamua kurudi waliingia kwa miguu miwili! Richie ameendelea kuwa msanii mzuri mpaka sasa, kadhalika JB na Bishanga ambaye huonekana kwa nadra  kwenye filamu, lakini thamani yao haijawahi kushuka. Filamu nyingi siyo ubora katika kuigiza. Kuandika script hakumthibitishi mtu kama msanii bora. Wapo waandishi wengi wa miswada ya filamu siyo waigizaji. Kuandika ni taaluma. Kuigiza hasa ni kipaji. Duma anachanganya madawa hapa iwe kwa kujua au  kutojua. DUMA HAJAWAJUA MASHABIKI Duma ajue kuwa thamani yake kwa mashabiki ni kubwa. Na kama walikubaliana na Gabo kuwa watengeneze kiki, atambue kuwa ameingizwa choo cha kike! Ni kiki itakayomgharimu badala ya kumpandisha. Kwa tambo zake, kwamba anaigiza tamthilia za kimataifa, anaigiza na wasanii wa kimataifa, anajua kuvaa nk, mashabiki watatafsiri kama maringo, mwisho wake watamuonea huruma Gabo, kisha watamchukia (Duma). Huo ndiyo ukweli. Kama basi haijapangwa, atambue kuwa jamii inamuona hivyo na muda mfupi ataona malipo ya anachokifanya. Kama ni dili avunje, maana ni hatari kwa sanaa yake. Katika mtazamo wa kawaida; kwa Gabo ambaye amefanya kazi nyingi nzuri kama Bado Natafuta, Safari, Safari ya Gwalu na nyinginezo, tena akiwa na tuzo kibao mkononi ikiwemo ya kimataifa ya Sinema Zetu (SZIFF), kuingia kwenye vita ya maneno naye, tena ukiwa mzungumzaji zaidi wewe, lazima watu wataona una wivu. Kwa namna yoyote ile, Duma ajiondoe kwenye hili tatizo ambalo kama halijampata, basi linamnyemelea. TUJIKUMBUSHE YA RAY NA KANUMBA Marehemu Steven Kanumba alikuwa na bifu la kisanii na swahiba wake, Vincent Kigosi ‘Ray’. Lile lilikuwa bifu la kibiashara kwelikweli. Walitengeneza bifu la maana na likawa na manufaa kwao wote. Walikuwa na tambo kwenye kazi, lakini kwa maneno ya staha. Hakuna mahali popote tulipata kuwasikia wakigombana au kurushiana maneno yasiyo na staha. Walitambiana magari, walishindana kuagiza vitendea kazi nje na kazi bora. Lakini mwisho wa siku, walikuwa wakikutana na kufanya kazi pamoja zilizozidi kuwapaisha kisanii (tukumbuke Oprah na Off-Side). Hivyo basi, kama Gabo na Duma wameamua kutengeneza bifu la kibiashara, wabadili sura. Ama kama ni kweli wapo kwenye bifu, Duma aelewe kuwa litamtafuna yeye na kuzidi kumpandisha Gabo. Natamani ninachokiona kiwe ndoto. Kwa sababu ni halisi, basi ni hamu yangu kiishe mara moja. Turudi kwenye mstari wa kujadili mkwamo wa sinema zetu, siyo bifu za kuzidi kuua sanaa.
4burudani
BARCELONA, HISPANIA MSHAMBULIAJI wa timu ya Barcelona, Antoine Griezmann, ameweka wazi kuwa, kucheza soka ndani ya kikosi hicho sio kazi rahisi, lakini anaamini atapambana kuhakikisha anapigania nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Staa huyo amejiunga na Barcelona wakati wa uhamisho wa kiangazi mwaka huu akitokea Atletico Madrid, lakini tangu kujiunga kwake bado hajaonesha kiwango ambacho wengi walitarajia kikuona. Hali hiyo inatokana na mabadiliko ya namba akiwa Atletico Madrid na Barcelona ni tofauti, hata hivyo kuna ushindani mkubwa wa namba. Katika michezo 11 aliyocheza msimu huu mchezaji huyo amefanikiwa kupachika manne ya Ligi Kuu nchini Hispania huku akitoa pasi tatu za mwisho, hivyo mashabiki wamedai mchezaji huyo bado yupo chini ya kiwango. Mashabiki waliamini ujio wa mchezaji huyo utakuwa na mchango mkubwa wa mafanikio ya timu huku akiweza kuziba nafasi ya aliyekuwa nyota wa timu hiyo Neymar Jr ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya PSG. Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde, aliweka wazi kuwa kiwango cha Griezmann kitakuja kubadilika endapo atakubali kufuata misingi ya timu hiyo, lakini mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Eric Abidal amedai mchezaji huyo bado yupo chini ya kiwango. “Barcelona sio sehemu rahisi kucheza mpira, hii ni timu mpya kwangu, nimetoka kwenye timu nyingine ambayo niliizoea, nimekutana na mbinu mpya, nafasi nyingine ya kucheza, lakini haijalishi, huu ndio muda sahihi wa kupambana kwa ajili ya kupigania timu na kupigania namba yangu kikosini. “Ninajivunia maamuzi yangu ya kuwa hapa kwa sasa, ninaamini kila kitu kitakuwa sawa, lengo langu kwa sasa ni kuhakikisha ninakuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi, kucheza dakika nyingi, kufunga mabao mengi, kutoa pasi na kuifanya timu inafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa,” alisema mchezaji huyo.
2michezo
Hayo yalisemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, juzi wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo mjini Morogoro.Waziri Kigoda alisema Serikali inatambua umuhimu wa shirika hilo hapa nchini hususan katika kuchangia uchumi wa nchi, kusimamia afya, usalama na ustawi wa watu, kusaidia kuwalinda walaji, kuchangia biashara za ndani na nje ya nchi na kusimamia ushirikiano wa Kimataifa katika nyanja za viwango.Kwa mujibu wa Waziri huyo, changamoto kubwa zinazolikabili shirika hilo ambazo ni pamoja na uhaba wa watumishi, vifaa vya maabara, fedha za maendeleo na matumizi ya kawaida, uelewa mdogo wa umma na Jumuiya ya Wafanyabiashara juu ya dhana nzima ya viwango na ubora.“Changamoto hizi Serikali inazifanyia kazi na kwa mwaka ujao wa fedha kwa maana 2014/2015 ,Serikali inatarajia kuongeza wafanyakazi 200 ambao wengi wao watasaidia katika kuweka na kusimamia viwango,” alisema.Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBS, Profesa Cuthbert Mhilu, alisema kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 , TBS ilipewa vibali vya kuajiri wafanyakazi 45 na mwaka huu wa fedha wa 2014/2015 inatarajia kupewa vibali vya kuajiri wafanyakazi wapatao 200 , zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia viwango vya ubora.
0uchumi
Mwandishi wetu WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa ebola ambao umeendelea kuwepo katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda. Majaliwa alisema hayo jana wakati akiahirisha Mkutano wa 15 wa Bunge la Bajeti jijini Dodoma. Alisema kutokana na mwingiliano wa nchi hizo, Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kukabiliana tishio la ugonjwa huo. “Ugonjwa huu wa ebola umeendelea kuwepo Congo, umelipuka tena Uganda sote tunatambua upo mwingiliano wa nchi hizi, katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti. “Lakini pia nitoe wito kwa Watanzania kuchukua hatua kutokana na hatari iliyopo katika ugonjwa huu,”alisema. Akizungumzia kuhusu ugonjwa dengue, Majaliwa alisema Janauri hadi Juni zaidi ya watu 4,282 waliathiriwa na ugonjwa huo na wanne walipoteza maisha. Alitaja mikoa ambayo inaongoza kwa idadi ya wagonjwa wa dengue ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Singida, Pwani na Kilimanjaro. Aidha, Majaliwa aliwataka wabunge kushiriki kwa wingi katika mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), utakaofanyika nchini Agosti. Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba, aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha na kupiga kura. Kuhusu Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blueprint),  Majaliwa alisema kuanzia Julai Mosi Serikali itaanza kuutekeleza kwa lengo la kurahisisha mazingira ya kufanya biashara. Alisema wakati kazi hiyo inaendelea Serikali itafanya ufutialiaji kuhusu utekelezaji wa mpango huo na kutathmini kama lengo limefikiwa. “Utekelezaji wa mpango huo unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kurahisisha mazingira ya kufanya biashara nchini, unaojidhihirisha kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo imefuta tozo kwamishi 54 zilizobainishwa kwenye mpango huo.” Waziri Mkuu ametaja tozo zilizoondolewa au kupunguzwa ni pamoja na zinazosimamiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi hususan kwenye Sekta ya Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Maji Kadhalika, Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unaleta tija, ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara ishirikiane na Ofisi ya Waziri Mkuu kusambaza blueprint pamoja na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa wizara zote kwa ajili ya kusimamia utekelezaji katika maeneo yao. Amesema kupitia mpango wa bajeti ya 2019/2020, Serikali itaendelea kuweka mazingira rahisi ya ufanyaji biashara kwa kutoa unafuu katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli nyingine jumuishi. Wakati huohuo,Waziri Mkuu amesema katika kukabiliana na kilimo tegemezi cha mvua hususani kwenye zama hizi za mabadiliko ya tabia nchi, Serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuwatoa wananchi katika kilimo hicho. Amesema hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni pamoja na kuunda upya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo inalenga kuiwezesha tume hiyo kusimamia ipasavyo shughuli za umwagiliaji. Pia Serikali imehamishia tume hiyo Wizara ya Kilimo ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuendeleza kilimo nchini. ”Ili tuweze kufikia lengo la kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 475,056 za sasa hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025, tayari nimeielekeza Wizara ya Kilimo isimamia kwa karibu na kutekeleza majukumu yake kwa weledi.” Waziri Mkuu amesema Wizara ya Kilimo inatakiwa ihakikishe inasimamia vema miradi 22 ya umwagiliaji inayoendelea sasa pamoja na miradi mipya minane itakayojengwa nchini katika pindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.
1kitaifa
NA THERESIA GASPER MSANII wa RnB kutoka mji kasoro bahari, Morogoro, Abednego Damian ‘Belle 9’, ameweka wazi kwamba umaarufu wa mkali wa kunogesha video za wasanii nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’, umetokana na wimbo wake wa ‘Masogange’. Akizungumza juzi alipotembelea Ofisi za New Habari Limited (2006) zinazochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba na Rai, Belle 9 alisema huwa anaamini kipaji cha mtu ndio maana wengi aliowashirikisha katika nyimbo zake wamepata umaarufu mkubwa. “Nimefanya kazi na wasanii wasiotambulika akiwemo Masogange na wamepata umaarufu mkubwa pia nimefanya kazi na maprodyuza wengi wasiojulikana lakini baada ya kazi hizo wamejulikana, hivyo huwa sidharau uwezo wa mtu ninachoangalia ni ubora wa kazi zake na si jina lake hata kama ni chipukizi,” alisema. Kati ya video alizofanya na waongozaji wasio na majina makubwa na zimefanya vizuri ni ‘Burger’ na ‘Movie Self’ inayotarajiwa kuachiwa kesho ambayo ameshirikiana na wasanii Izzo Bizness, Jux, Mr Blue, G. Nako na Nandy. “Audio ilishatoka ilifanywa na mtayarishaji Tuddy Thomas huku video ikiwa chini ya prodyuza chipukizi QG kutoka Morogoro, naamini kazi yake mtaifurahia,” alimaliza Belle 9.
4burudani
Gurian Adolf, Sumbawanga MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda, ameshauri miongoni mwa wanaume ambao ni muhimu kuwabana ili kukomesha mimba za utotoni ni walimu na waendesha bodaboda kwani wamekuwa wakihusika kwa kiwango kikubwa kuwapa mimba wanafunzi. Ushauri huo aliutoa jana wakati akichangia rasimu ya mkakati wa kukabiliana na mimba za utotoni katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) iliyowasilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,  Bonifas Kasululu. Alisema hivi karibuni kumekuwa na kesi nyingi za walimu wakikuhusika kuwapa mimba wanafunzi kitendo ambacho kinahitaji jitihada ya kukabiliana nacho. Alisema pia wanao endesha boda boda ni kundi jingine ambalo linahusika kutokana na vitendo vya kuwapa lifti wanafunzi wanapo kwenda na kutoka shule, na kuwanunulia zawadi ikiwemo chipsi kutokokana na njaa wanazokuwa nazo wanafunzi pindi wanapotoka shule. Miingoni mwa mikati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, kumaliza tatizo hilo ni kila kijiji kwa na shule ya msingi na kila kata iwe na shule ya sekondari. Alisema mkoa mzima una vijiji 59 ambavyo havina shule za msingi ambapo katika Wilaya ya Kalambo kuna vijiji 14, Nkasi vijiji 17 halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga vijiji 28 na halmashauri ya Manispaa hakuna kijiji kisichokuwa na shule. Alisema katika mkoa mzima kata 25 hazina shule za sekondari ambapo alisema katika wilaya ya Kalambo zipo kata nane, wilaya ya Sumbawanga vijijini kata 10 Nkasi kata sita na Sumbawanga Manispaa kata moja. Alisema kutokana na rasimu hiyo ambayo imepitishwa na kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa, anamatumaini kuwa katika kipindi cha miaka 10 suala la mimba za utotoni na kwa wanafunzi litabaki historia katika mkoa huo.
5afya
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, amewageukia mawaziri ambao kwa sasa wanajipitisha kutaka urais mwaka 2020. Amesema watu hao hivi sasa wameanza kujipitisha kutaka kumrithi Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya muda na kwa hatua hiyo huenda wakapoteza sifa. Kauli hiyo aliitoa juzi Ikulu Dar es Salaam, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Kwa mujibu wa chanzo chetu, Dk. Magufuli aliwaonya makada hao wanaoanza kujipitisha kutaka urais wa Zanzibar kabla ya muda, huku akitaka Dk. Shein aachwe afanye kazi. “Rais Magufuli alikuwa mkali sana, hasa ilipoletwa ajenda ya hali ya kisiasa Zanzibar, ambayo ilikuwa ikiangazia uchaguzi wa marudio na wana CCM waliosaliti chama. “Alisema hivi sasa wapo mawaziri ndani ya CCM wameanza kujipitisha kutaka kumrithi Dk. Shein kabla ya wakati wake na akawaonya kuwa wamuache afanye kazi muda wake,” kilisema chanzo chetu. Chanzo hicho kilisema kutokana na hali hiyo, Dk. Magufuli alisema kuwa ili mtu awe rais ni lazima apitie taratibu zinazokubalika na chama na si vinginevyo. Mawaziri na vigogo kadhaa wanatajwa na wana CCM kwamba huenda wakajitosa katika kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar mwaka 2020 wakiwamo Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni na Waziri wa Miundombinu wa Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume. Nahodha alikuwa mmoja wa vigogo waliojitosa mwaka 2010 kuwania kuteuliwa kuwa mgombea urais, lakini alikuwa mshindi wa tatu akipata kura 33, nyuma ya Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyepata kura 54 na Dk. Shein aliyeibuka mshindi kwa kura 117.   MATOKEO UCHAGUZI PEMBA Mbali na hilo, pia katika ajenda hiyo ya hali ya kisiasa Zanzibar, iliwasilishwa taarifa ya namna chama hicho tawala kinavyoteswa na matokeo ya uchaguzi wa wabunge na wawakilishi kwa majimbo ya Pemba. Kutokana na hali hiyo, juzi NEC iliagiza kuundwa kamati maalumu ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa 2015. Wakati hayo yakiendelea, leo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein, anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati Maalumu ya NEC. Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar – Idara ya Itikadi na Uenezi, Waride Bakar Jabu, ilisema kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi. Alisema kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili mapendekezo ya wanachama wa CCM, wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani. “Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya NEC, ambacho kimefanyika leo (jana) chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa agenda za kikao hicho,” alisema Waride katika taarifa yake.
1kitaifa
Christopher Msekena ALBAMU ya msanii wa Bongo Fleva, Rajab Kahali a.k.a Harmonize, Afro East, imerejea tena mtandaoni baada ya kutoweka kwa ishu zinazohusiana na haki miliki. Afro East, iliyozinduliwa Machi 14, mwaka huu, ilifanikiwa kufanya vizuri katika mitandao ya kuuza, kusikiliza na kupakua muziki duniani lakini juzi ikatoweka ghafla jambo lililozua taharuki miongoni mwa mashabiki zake. Akizungumzia kupotea kwa albamu hiyo, Harmonize alisema: “Niwaombe samahani mashabiki zangu wote kwa albamu yetu, Afro East kupotea kwenye ‘platform’ zote lakini Mungu ni mwema tayari imerudi kwenye mitandao ya Apple Music, Spotify, Tidal, Audiomack, Boomplay Music na YouTube.”
4burudani
Shirikisho la soka barani ulaya (UEFA) limeweka wazi kuwa michezo iliyobaki ya ligi ya mabingwa barani ulaya inatarajia kuanza kucheza mnamo tarehe 7 na 8 ya mwezi Agosti mwaka huu huku hatua inayofuata ikichezwa wiki mbili baadae. Katika taarifa iliyotolewa leo baada ya kikao cha wakurugenzi wa nchi wanachama mechi zilizokuwa zimesalia kwenye hatua ya 16 bora zitacheza kama awali kwenye mpangilio wa nyumbani na ugenini huku hatua inayofuata ya 8 bora ikichezwa kwenye mji mmoja wa Lisbon nchini Ureno. “Kwa timu zilizobakiza mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora zitacheza kama kawaida nyumbani na ugenini na baada ya hapo mechi zote zitachezwa mjini Lisbon kati ya tarehe 12 hadi 23 ya mwezi Agosti na fainali pia itachezwa huko huko” imenukuliwa taarifa hiyo Ikumbukwe kuwa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ilisimama baada ya mlipuko wa ugonjwa wa corona na kulikuwa na uwezekano wa kutokamilika kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo ulio gharimu maisha ya watu milioni 3 duniani kote   BREAKING: The Champions League will return in a eight-club knockout format will all games taking place in Lisbon.⁣ ⁣ The final will be taking place on the 23rd August. 🏆 A post shared by Squawka Football (@squawkafootball) on Jun 17, 2020 at 6:49am PDT
2michezo
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli amemng’oa Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru na nafasi yake kurithiwa na Dk. Osward Mashindano. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana usiku, ilieleza kuwa Dk. Mashindano anachukua nafasi hiyo na Mafuru atapangiwa kazi nyingine. Mafuru, hivi karibuni aliibuka na kauli tata ambayo ilionekana kupingana na Rais Magufuli kuhusu uamuzi wa baadhi ya taasisi za umma kuweka fedha katika Fixed Deposit Accounts (akaunti maalumu). Kauli hiyo aliitoa Novemba 30, mwaka huu katika mahojiano maalumu na redio moja nchini. Alisema haiwezekani kwa watumishi wa umma kuiba fedha zinazowekwa katika Fixed Deposit Accounts kwa sababu miamala ya benki ni ya uwazi. Alisema hizo ni tuhuma tu na Serikali imemwagiza CAG kuchunguza. “Nimefanya kazi katika taasisi za benki kwa miaka 20, sijawahi kuona watumishi wa umma wakichota hela kwenye fixed deposit account. “Pale kwenye benki kuna miamala ya aina mbili tu, ya kuweka na kutoa. Usipoweka wazi wakati wa kuweka, siku utakapozitoa itaonyesha tu,”  alisema Mafuru. Alisema hakuna kosa kwa taasisi za Serikali kuweka fedha katika akaunti hizo, lakini Serikali sasa imeamua kuzihamishia Benki Kuu (BoT) ili iwe rahisi kuzifuatilia. Kauli hiyo ya Mafuru ilitanguliwa na ile ya Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, ambaye alisema si kosa kisheria kwa taasisi kufungua akaunti maalumu katika benki ya biashara. Novemba 26, mwaka huu, Rais Magufuli alifichua siri ya hatua yake ya kuitumbua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Alisema alilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya bodi hiyo kuidhinisha Sh bilioni 26 kupelekwa kuwekwa katika akaunti maalumu (Fixed Account) katika benki kadhaa za biashara. Bodi hiyo ilitoa idhini ya kupelekwa fedha hizo katika benki hizo wakati kuna agizo la Rais la kupiga marufuku taasisi za umma, mashirika ya umma, idara za Serikali, wakala na wizara kuweka fedha zao katika benki za kibiashara. Fedha hizo zinatakiwa zifunguliwe akaunti BoT. Hatua hiyo ilitokana na uamuzi wake wa kuvunja Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, na saa chache akateua Naibu Kamishna Mkuu mpya. Ikulu bila kueleza sababu, ilisema kwamba Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Bernard Mchomvu na kuivunja bodi nzima. Aidha, pamoja na kuivunja bodi hiyo, alimteua Charles Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, kuziba nafasi iliyokuwa wazi kwa mwaka mmoja baada ya Dk. Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Lusekelo Mwaseba. Akihutubia katika mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Makao Makuu ya chuo hicho, Bungo wilayani Kibaha mkoani Pwani, Dk. Magufuli alisema aliitumbua bodi hiyo kutokana na kukiuka taratibu. Alieleza kuwa kitendo chao cha kuidhinisha fedha hizo kuwekwa katika benki tofauti, ni tofauti na maelekezo kwani huo ndio ulikuwa mchezo unaofanywa na taasisi na mashirika mbalimbali. Rais Magufuli alisema kumekuwa na mchezo wa wakuu wa taasisi mbalimbali kuchukua fedha na kuziwekwa kwenye akaunti maalumu ambako serikali inakwenda kukopa kwa gharama kubwa.  MABADILIKO Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa katibu mkuu mmoja na mkuu wa mkoa mmoja na mabadiliko madogo katika wizara na mikoa. Amemteua Profesa Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano. Rais Magufuli amemteua pia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo akichukua nafasi ya Dk. Frolence Turuka aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Dk. Turuka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa balozi. Rais Magufuli amemteua Dk. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia mawasiliano, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Kamuzora ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. “Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano “Aidha, Rais Magufuli amemteua Dk. Aloyce Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,” ilieleza taarifa hiyo.  SENDEKA AONDOLEWA CCM Mbali na uteuzi huo Rais Magufuli, amemteua Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Sendeka anachukua nafasi ya Dk. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
1kitaifa
Ikiwa imebakia takribani miezi minne kueleka kwenye uchaguzi mkuu mwanamuziki Zuena Mohammed (Shilole) amesema kuwa anafikiria kwenda kugombea Ubunge kwenye jimbo la Igunga mkoani Tabora mambo yakikaa sawa. Akizungumza na kituo cha televisheni cha East Africa Shilole amesema anataka kuwapa wananchi kile ambacho yeye anaona kinakosena kwenye jimbo hilo kupitia tiketi ya chama chake cha CCM. “Nimefikiria na natumaini mambo yataenda, nipo vizuri kwenye mapambano, nataka niwe pale kwenye jimbo langu la Igunga, nataka niwape wananchi kile ambacho nataka, mimi ni mwaka huu, chama changu ni @ccm_tanzania” amesema. Shilole anakuwa mwanamuziki wa tatu kutangaza nia ya kugombe ubunge ikiwa ni baada ya Harmonize pamoja na Mwana FA wote kutangaza kuwa wanaweza kufikilia kugombea ubunge.   "Nimefikiria na natumaini mambo yataenda, nipo vizuri kwenye mapambano, nataka niwe pale kwenye jimbo langu la Igunga, nataka niwape wananchi kile ambacho nataka, mimi ni mwaka huu, chama changu ni @ccm_tanzania" @OfficialShilole kuhusu kugombea Ubungehttps://t.co/SZIqcCYlPV pic.twitter.com/sP9TZns95P — eastafricatv (@eastafricatv) June 18, 2020
4burudani
Coastal Union ilikubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa hivi karibuni na kushuka hadi nafasi ya saba ikibaki na pointi zake 24 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Akizungumza na gazeti hili, Kihwelu alisema jambo la msingi hawataangalia walipofungwa kwani wanaendelea kutazama ni wapi walikosea na kujipanga zaidi kwa mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu.“Tulipoteza mchezo dhidi ya Tanzania Priosons, lakini tunaendelea kujiimarisha kuhakikisha tunatatua matatizo yaliyopo kwa ajili ya kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo,” alisema.Alisema anaamini kikosi chake kitaendelea kubadilika na kuleta matokeo mazuri katika michezo ijayo.Coastal Union ilikuwa ikishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, lakini baada ya Mgambo Shooting na Ruvu kushinda michezo iliyopita, timu hiyo imeshuka hadi nafasi ya saba.Tayari Coastal Union imeshacheza michezo 21, imeshinda mitano, sare tisa na kupoteza saba na kubakiza mitano ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kubaki katika ligi msimu ujao
2michezo
Kwa upande wa kampuni tanzu ya Equity imeweza kupata faida ya Sh bilioni 256 katika kipindi kinachoishia mwezi Septemba 2015 ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na Sh bilioni 224 iliyopatikana mwaka jana.Akizungumza na wanahisa kuhusu taarifa ya hesabu za robo ya tatu ya mwaka, Ofisa Mtendaji wa kampuni tanzu ya Equity Dk James Mwangi aliwaambia mkakati ya uboreshaji hii imewezesha Huduma za kibenki kwenye kanda kukua kwa kasi kubwa.Alisema pia uwekezaji mkubwa katika njia mpya za uwakala na huduma ya simu mtandao, mafanikio yaliyopatikana katika upanuzi katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki imechangia kwa kiasi kikubwa faida iliyopatikana katika robo ya tatu ya mwaka huu.Pia faida kabla ya kodi imeongezeka kwa asilimia 14 hadi kufikia kiasi cha Sh bilioni 362 ikilinganishwa na Sh bilioni 318 iliyopatikana katika kipindi cha mwaka jana.Mafanikio haya makubwa ambayo kampuni tanzu ya Equity imeyapata yametokana na mikakati mahsusi na ubunifu katika kuweka mazingira rahisi ya upatikanaji wa Huduma za kibenki na kuwafanya wateja kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa wakati.
0uchumi
KOCHA mkuu wa timu ya Soka ya taifa ya wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens ,Bakari Shime amesema morali ya kikosi hicho ipo juu tayari kwa kuwakabili Sudan Kusini kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi A katika michuano ya kombe la Chalenji.Michuano hiyo inayofanyika chini ya usimamizi wa Baraza la vyama vya soka Afrika Madhariki na Kati, Cecafa inatarajiwa kuanza Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi ikishirikisha timu nane. Queens ambao ni mabingwa watetezi mara mbili mfululizo watakuwa na kibarua hicho mbele ya Sudan siku ya ufunguzi wa michuano hiyo na tayari kikosi hicho kipo kwenye maandalizi kabambe.Akizungumza jana Dar es Salaam Shime alisema morali ya kikosi ipo juu pamoja na kwamba mazoezi mepesi yanaendelea kutolewa kwa kikosi hicho.“Morali ya kikosi cha Queens ipo juu na kwa sasa kwa vile muda bado benchi la ufundi tunaendelea kuwapa mazoezi mepesi kuweka sawa miili yao tayari kwa mchezo wetu ambao tunahitaji zaidi ushindi kubusti malengo yetu,” alisema Shime .Alisema mazoezi anayoendelea kuwapa vijana hao ni namna ya kutoa pasi imfikie mlengwa kwa wakati pamoja na kuwaelekeza nidhamu kwa muda wote wakiwa uwanjani. Shime alisema pamoja na kwamba mechi hiyo itakuwa na upinzani bado anaamini ubora wa mchezaji mmoja mmoja unaweza kuwapa majibu sahihii hususan kwenye kuamua matokeo uwanjani.Timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo ni Tanzania Bara, Zanzibar,Burundi na Sudan zilizo kundi A na kundi B likiwa na timu za Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibouti.
2michezo
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ameitaka Taasisi ya Utafi ti ya Wanyamapori (TAWIRI) kuwa na mkakati na mpango kazi kwa mnyama aina ya twiga katika hifadhi mbalimbali nchini, kwani kuna viashiria vya wanyama huyo kutoweka katika hifadhi hizo.Alisema hayo jana wakati akifungua kongamano la 12, lililoshirikisha nchi 16 la wanasayansi watafiti wa uhifadhi duniani, wakurugenzi na watendaji wa taasisi za uhifadhi wa ndani na nje na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.Dk Kigangwalla alisema katika mpango kazi huo wa miaka mitano wa utafiti wa wanyama, Tawiri wanapaswa kuweka mkazo wa kujua nini kinasababisha twiga kutoweka katika hifadhi za taifa na kuja na majibu ya msingi juu ya hali hiyo ili serikali itayafanyia kazi haraka iwezekanavyo.Alisema twiga ni nembo ya Taifa, hivyo ni wajibu wa wanasayansi watafiti wa Tawiri, kuhakikisha wanapata majibu ya msingi kuhakikisha mnyama huyo hatoweki, bali anaongeze katika mbuga za Taifa.Akizungumzia utafiti mwingine ambao Tawiri inapaswa kuufanyia kazi ni pamoja na aina ya ndege, wajulikanao kwa jina la ndege wa ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Alisema kuwa ndege hao ni kivutio kikubwa katika kuvutia watalii nchini.Alisema katika ukanda huo, kuna ndege aina ya 700 katika eneo hilo la Magharibi mwa Tanzania, hivyo taasisi hiyo inapaswa kufanyia kazi na kuyapeleka mapendekezo yake serikali ili kiwe kivutio kikubwa kwa watalii nchini.Aidha, aliagiza kuweka nguvu zaidi kati suala jingine la migogoro ya binadamu na wanyama na mito kwa mamba na kiboko ili kuwajengea uzio.Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Dk Saimon Mduma alisema changamoto zote, zilizosemwa na waziri asilimia kubwa zimeshaanza kufanyiwa kazi na mapendekezo yake, yatafikishwa serikalini kwa utekelezaji.
1kitaifa
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Bandari, Temeke Dar es Salaam, Rangers walipata bao lao kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Almasi Nkinda.Mchezo huo uliokuwa wenye upinzani mkali, ambapo Faru Jeuri walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga, lakini Rangers ilikuwa makini kuhakikisha lango lao linakuwa salama muda wote.Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Kutokana na ushindi huo Rangers imetinga Nusu Fainali kwa kuiondosha kwenye mashindano timu ya Faru Jeuri kutoka mitaa ya Vingunguti.Timu nyingine ambazo zimekata tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya mashindano hayo ni Abajalo, Goms United na Burudani. Nusu fainali ya kwanza ilitarajiwa kuzikutanisha timu za Abajalo dhidi ya Burudani kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mwalimu Nyerere jana.
2michezo
Ushindi huo uliirudisha Yanga kileleni baada ya kufikisha pointi 59.Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo, Pluijm alisema kiwango ambacho kilioneshwa na vijana wake kilimshangaza na walistahili kupata ushindi licha ya kubadili mfumo mara mbili kutokana na wapinzani wao Mtibwa Sugar kuwabana vilivyo.“Kiwango hiki sijakiona katika mechi tatu zilizopita, ikiwemo ile na Al Ahly ambayo tulipata sare ya 1-1, naamini hii ilitokana na kila mchezaji wangu kutambua umuhimu wa ushindi klabu inahitaji nini kipindi hiki ambacho msimu unaelekea mwishoni,”alisema Pluijm.Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema kwa kiwango hicho kinamfanya aende Misri kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri bila kujali ubora na rekodi waliyokuwa nayo wapinzani wao.Kwa upande wake kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime alisema timu yake haikuwa na bahati katika mchezo huo baada ya kuonesha kiwango kizuri lakini wakapoteza kwa bao 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi Yanga.Maxime alisema kuwa amekubali matokeo hayo ingawa anawapongeza vijana wake kwa kucheza kwa kiwango cha juu na kupoteza nafasi nyingi, kitu ambacho alidai kilisababishwa na kukosa bahati katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.“Tumekubali matokeo tumepoteza mchezo nawapongeza Yanga, kwa ushindi wao walicheza vizuri na walistahili ushindi na baada ya mchezo tunakwenda kupumzika kwa siku mbili tatu baada ya hapo tutaanza mazoezi kujiandaa na mechi zilizopo mbele yetu,” alisema Maxime.Maxime alisema pamoja na kupoteza mechi mbili mfululizo, ana uhakika msimu huu wataweka rekodi kwa kumaliza ligi katika nafasi tatu za juu baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.
2michezo
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam Serikali imesema ni marufuku mwanafunzi yeyote kujiunga na shule ya bweni bila kupimwa maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB). Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo leo Jumanne Machi 20, wakati akizindua dawa maalumu ya kutibu TB ya watoto. Aidha, Waziri Ummy amemuagiza Mganga Mkuu wa Serikali kuhakikisha anasimamia suala hilo na kuwapa maelekezo waganga wakuu wa wilaya na mikoa. Amesema ugonjwa wa TB ni janga duniani, Shirika la Afya Duniani (WHO), linakadiria kila mwaka zaidi ya watu milioni 10.4 huugua ugonjwa huo na wagonjwa milioni moja kati yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18. “Takwimu za mwaka 2016 zinakadiria kila mwaka watu 160,000 nchini huugua ugonjwa huo hata hivyo walioweza kugundulika ni takribani watu 65,900 pekee ambao waliingizwa katika mpango wa matibabu. “Ni changamoto kubwa, yaani kati ya watu 100 wanaogundulika ni watu 40 tu, 60 wote hatuwagundui, wapo majumbani, maofisini, nyumba za ibada na kwingine, ingawa bahati nzuri ni kwamba kati ya watu 100 wanaogundulika na kutibiwa 90 hupona lakini tutawapate ni changamoto,” amesema. Ummy amesema serikali ilitoa mwongozo kwamba kila mtu lazima ahisiwe kuwa na ugonjwa huu na ikaainisha dalili zake, ambapo walipata matokeo mazuri kwani sasa idadi ya wanaogundulika imeongezeka mara mbili zaidi ya awali. “Hivyo Mganga Mkuu wa Serikali fuatilia kuhakikisha wanafunzi hawajiungi na shule za boarding bila kupimwa maambukizi ya ugonjwa huu iwapo wanayo au la,” amesema.
5afya
Na MOHAMED KASSARA KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo kitashuka dimbani ugenini kutafuta ushindi dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za mataifa Afrika (Afcon) utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Praia. Taifa Stars itaingia katika mchezo huo, ikihitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu fainali hizo ambazo kwa mara ya mwisho ilishiriki mwaka 1980, michuano iliyofanyika nchini Nigeria. Mchezo huo utakuwa wa pili kwa kocha raia wa Nigeria, Emmanuel Amunike, aliyekabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili, akichukua nafasi ya mzawa, Salumu Mayanga. Amunike atakuwa akikiongoza kikosi hicho kwa mara ya pili, baada ya kuiongoza Taifa Stars kuvuna pointi moja ugenini dhidi ya Uganda. Timu hizo zimekutana katika michezo mitatu ya mashindano yote, ambapo Taifa Stars ilishinda mmoja, imepoteza mmoja na kutoka sare mmoja. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Taifa Stars ilikubali kipigo cha bao 1-0, ukiwa ni mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za Kombe la Dunia uliochezwa Juni 7 mwaka 2008. Katika mchezo huo, Taifa Stars itawakosa beki, Andrew Vincent ‘Dante’ na viungo Jonas Mkude na Frank Domayo, kutokana na majeraha, wakati  kiungo Salum Kihimbwa na mshambuliaji, Kelvin Sabato, watakosekana kutokana na sababu za kiufundi. Baada ya kutema nyota hao, kocha huyo amewaongeza makipa wawili, Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons na Benedicto Tinocco wa Mtibwa Sugar. Msafara wa kikosi cha wachezaji 23, wakiwemo wachezaji tisa wanaocheza soka nje ya nchi ulitua juzi nchini humo ukiongozwa na nyota wa zamani wa Taifa Stars, Peter Tino. Tino aliiongoza Taifa Stars kufuzu Afcon ya mwaka 1980. Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa Taifa Stars, Dany Msangi, alisema kikosi kitakachoivaa Cape Verde kipo timamu kimwili na kiakili. “Tunashukuru tumefika salama, tulipata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanja tutakaochezea, baadaye tutakuwa na kikao kidogo cha wachezaji na benchi la ufundi kuangalia mbinu za wapinzani wetu. “Wachezaji wote wapo katika morali ya hali ya juu, kila mmoja anaonyesha utayari wa kuipigania nchi yake, pia tunatambua umuhimu wa mchezo huu, hivyo tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda ugenini kabla ya kwenda kumaliza kazi Dar es Salaam,” alisema Msangi. Mchezo wa marudiano kati ya Taifa Stars na Cape Verde utafanyika Oktoba 16, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika michuano hiyo, Tanzania imepangwa Kundi L pamoja na timu za Uganda, Lesotho na Cape Verde. Taifa Stars katika msimamo wa kundi hilo inashika nafasi ya tatu, nyuma ya vinara, Uganda wenye pointi nne, ikifuatiwa na Lesotho yenye pointi mbili sawa na Tanzania, huku Cape Verde ikiwa mkiani na pointi moja. Stars ilizindua kampeni zake kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Lesotho mchezo uliochezwa Juni 10 mwaka jana  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kulazimisha suluhu na Uganda katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Kampala. Cape Verde ilizindua harakati zake kwa kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Praia, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na Lesotho jijini Praia.
2michezo
NA MWANDISHI WETU-MACHAKOS TIMU ya soka ya Tanzania Bara  ‘Kilimanjaro Stars’ imeondolewa kwa aibu katika michuano inayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ baada ya kukubali kichapo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’. Kilimanjaro Stars imeondolewa katika michuano hiyo ikiwa iinashika mkia katika kundi lake A  baada ya kujikusanyika pointi moja,kupitia michezo minne, ikitoka sare mchezo mmoja na kuruhusu kufungwa michezo mitatu. Katika mchezo wa jana dhidi ya Kenya, Kiliman jaro  Stars ilicheza soka lisilokuwa na ladha na kuiruhusu bao  dakika ya 19 kupitia kwa Vincent Ouma Oburu, baada ya beki wa Kilimanjaro Stars,Kenedy Wilson kuchelewa kupokea mpira wa pasi na matokeo yake kuwahiwa na mfungaji. Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za kwanza zilipomalizika,kipindi cha pili mambo yalibadilika huku timu zote zikishambuliana kwa zamu. Mara kadhaa mashuti ya mshambuliaji wa Kilimanjaro Ibrahim Ajib, yaliokolewa na  kipa wa Kenya, Patrick Matasi. Kadri muda ulivyosonga Kenya walizidisha mashambulizi langoni mwa Kilimanjaro Stars yaliyowaongezea  presha vijana wa kocha, Ammy Ninje ambao walionekana kupokonywa mipira kirahisi na wapinzani wao hao. Katika mchezo huo,Ninje alifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza chipukizi, Yahaya Zayd na Aman Kyata, lakini hawakuweza kutengeneza nafasi yoyote ya kuweza kupata bao la kusawazisha. Kwa matokeo hayo sasa Kenya anaungana na Zanzibar kutinga hatua ya nusu fainali, licha ya Zanzibar kupoteza mchezo wake dhidi ya Libya kwa bao 1-0.   Ushindi huo uliifanya Libya kufikisha pointi sita,lakini haukuisaidia isiondolewe katika michuano hiyo baada ya kuzidiwa pointi moja na Kenya ambayo ilifikisha pointi saba kutokana na ushindi wake dhidi ya Kilimanjaro Stars.  Kutoka kundi B, Uganda na Burundi zimefuzu nusu fainali ya michuano hiyo,hivyo kuungana na Zanzibar Heroes na wenyeji Kenya. Ratiba ya fainali inaonyesha kuwa nusu fainali ya kwanza itachezwa Desemba  14, ambapo Kenya watacheza na Burundi, wakati nusu fainali ya pili itafanyika desemba 15, ambapo Uganda watacheza na Zanzibar.
2michezo
NEW YORK, MAREKANI NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Tyrese Gibson, amelianzisha bifu jipya kwa kumwambia mkali wa filamu ya Fast & Furious, Dwayne Johnson ‘The Rock’ kuwa ni mbinafsi sana. Wawili hao ni marafiki wakubwa kutokana na filamu hiyo, lakini kwa sasa wanaonekana kuwa kwenye mgogoro kutokana na ucheleweshaji wa kuachia kwa filamu yao nyingine. “The Rock ninaamini ana ubinafsi sana, kuna mambo yetu ya pamoja anaamua kuyafanya kimya kimya jambo ambalo si zuri, yupo vizuri kwenye kazi lakini ana mapungufu yake makubwa sana. “Sina ugomvi naye lakini lazima niseme ukweli, Fast and Furious 9 ilitakiwa kutoka hivi karibuni lakini imesitishwa hadi 2020,” alisema Tyrese.
4burudani
Na GURIAN ADOLF-KALAMBO MWANAMKE mjamzito, aliyefahamika kwa jina la Maria Kalunde (42), pamoja na mtoto wake Magreth Lui (9) wamekufa maji baada ya kutumbukia katika Mto Kalambo kutokana na kuteleza katika kivuko cha miguu cha mto huo. Tukio hilo limetokea jana katika Kijiji cha Kasitu Kata ya Sopa wilayani Kalambo mkoani Rukwa wakati watu hao wakivuka katika mto huo. Akizungumzia tukio hilo mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Nobert Mwanawima alisema mwanamke huyo mjamzito pamoja na mtoto wake walikufa maji kutokana na eneo hilo kutokuwa na daraja la kuvukia kitendo kilichosababisha wananchi wa kijiji hicho kutengeneza kivuko cha miguu kinachokatisha mto kwa kutumia miti. Alisema kuwa mwanamke huyo alipokuwa akipita katika kivuko hicho pamoja na mwanaye waliteleza na kuangukia mtoni, na kisha walianza kupiga kelele za kuomba msaada, lakini kwakuwa watu walikuwa mbali hawakufanikiwa kufika kwa wakati kuwasaidia. “Siku mbili baadaye walipata taarifa kuwa miili yao ilipatikana katika kijiji jirani na wakazi wa kijiji hicho baada ya kuona kuwa watu hao hawafahamiki waliamua kufanya maziko, ndipo walipoamua kuchukua  msiba na kuusafirisha hadi kijiji cha  Katete walipokuwa wakiishi mama huyo pamoja na mwanaye,” alisema  Naye Jeremia Shigoma mkazi  wa Kijiji cha Kasitu, alisema kuwa kutokana na changamoto ya kutokuwa na daraja katika  eneo hilo watu wamekuwa  wakifa maji kutokana na kusombwa na maji hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika nyakati za masika kwakuwa mto huo unakuwa umejaa maji. Aliiomba serikali kuwajengea daraja katika eneo hilo ili kuepukana na vifo vinavyotokea mara kwa mara kwani wao wamekuwa hawajisikii vizuri kushuhudia watu wakipoteza maisha kila nyakati za masika. Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Gasper kateka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa,  awali hali ilikuwa mbaya zaidi kwakua hakukua hata hicho kivuko lakini kilipatikana baada yawananchi  kujichangisha  fedha  kiasi  cha Sh 10,000 kila mmoja kwaajili ya kuwalipa mafundi waliokitengeneza. Diwani wa kata hiyo,  Richad Kamagari (CCM), alisema tatizo la vifo kutokana na kutumbukia watu mtoni limekuwa likijitokeza mara nyingi na yeye amekwisha toa taarifa katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kalambo. Kwaupande wake Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo, Mahmood  Shauri , amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  ambapo alisema kuwa serikali itajitahidi kutatua changamoto hiyo inayowakumba wakazi wa kijiji hicho.
1kitaifa
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Mkazi wa Kijiji cha Itenka, Wilaya ya  Mpanda kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na nyama ya kiboko zaidi ya kilo 110 yenye thamani y ash milioni 2.3. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga  Ntengwa ametoa hukumu hiyo leo Ijumaa Desemba 8, baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa  mahakamani hapo na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Flavian Shio. Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga  amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani  hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na  mashahidi watano na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote. “Mahakama pasipo shaka yoyote imemuona mshtakiwa   ana hatia kupitia Kifungu cha Sheria Namba 86 (1) na (2) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya  mwaka  2009,” amesema Hakimu Chiganga. Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa  Omary Maganga alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka jana ambapo alikamatwa akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya  Katavi  akiwa na nyama ya  kiboko  yenye  uzito wa kilo 118 yenye  thamani ya  Sh milioni tatu.
1kitaifa
 JESSCA NANGAWE  STAA wa filamu nchini, Irene Uwoya amesema kwa sasa hatumii mitandano ya kijamii baada ya akaunti yake ya Instagram kupata matatizo.  Uwoya ambaye kwa sasa anaonekana kimya huku wengi wakidai amefulia amesema baada ya ile akaunti yake ya kwanza kupotea kutokana na kusahau pasward alitumia nyingine lakini akanyang’anywa na wahusika wa mtandao huo kwa madai si yakwake.  Mrembo huyo amekiri kuwa pamoja na mitandao ya kijamii kuwa sehemu ya yeye kupata kipato kwa kutangaza bidhaa mbalimbali lakini amewaachia wahusika kushughulikia hilo na sasa haingii kabisa kwenye mitandao.  “Nilipoteza namba ya siri ya akaunti yangu ya kwanza ambayo ilikua na watu zaidi ya milioni 4, nikabahatika kupata nyingine nayo nimenyang’anywa kwa madai si yangu, sina tatizo kwa kuwa maisha yangu yanakwenda kama kawaida ila kikubwa kwa sasa sipo kabisa huko,”alisema Uwoya. Hata hivyo alisema matukio mbalimbali anayohusishwa nayo amekua akiyapata kupitia watu wake wa karibu lakini hayamuumizi kwa kuwa si ya kweli. 
4burudani
KATIKA kuelekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha UDP, John Cheyo ameulezea utawala wa Rais Dk John Magufuli kuwa ni wa mafanikio makubwa zaidi kuwahi kupatikana, hasa katika eneo la ulinzi wa rasilimali na ujenzi.Amesema katika kipindi cha miaka minne tangu Rais Magufuli aingie madarakani, ameipaisha Tanzania katika hatua nyingi, ikiwemo kuwaondoa Watanzania katika dhana ya utegemezi.Aidha, ameelezea viongozi wa awamu zingine, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa ndiye aliyejenga umoja na undugu wa Watanzania ; na Ali Hassan Mwinyi kuwa ndiye aliyefungulia fursa za kiuchumi na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa.Kwamba utawala wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ulitoa uhuru zaidi kwa vyama vya upinzani, kushiriki kwenye mabaraza ya maamuzi na Bunge, ubinafsishaji wa mashirika ya umma; na utawala wa Jakaya Kikwete, ulilenga zaidi kupaisha uchumi na kuibadilisha sura ya Tanzania hasa mijini.Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti huyo wa UDP alisema tangu Tanzania Bara ipate Uhuru mwaka 1961, kila Rais alikuja na mbinu zake za utawala, zilizolenga kuleta mabadiliko chanya.Lakini, marais wote kwa pamoja walitekeleza dhana ya kutunza umoja, amani na utulivu wa watanzania.“Utawala wa Rais Magufuli uko zaidi katika ujenzi wa nchi, wanaomlalamikia kwenye masuala ya siasa wanamuonea, huyu nafikiri analala huku akiwaza kesho nijenge nini, lakini pamoja na hayo amefuta kabisa dhana ya Tanzania ya utegemezi, akiamua kujenga reli au barabara anabana kwenye mapato anajenga,” alifafanua Cheyo.Alisema kutokana na aina yake hiyo ya uongozi, kwa kipindi kifupi cha miaka minne, amefanikiwa kuijenga kwa kasi Tanzania, ameanzisha miradi mikubwa iliyomalizika na inayoendelea kujengwa tofauti na tawala nyingine.“Katika rasilimali kwa hili nampongeza kwani amekuwa akijiuliza rasilimali hizi ni za nani? Watanzania watanufaikaje akaamua kuanzisha mifumo ya kisheria kuhakikisha Tanzania kwanza inafaidika. Pia hakusahau watu wake ameanzisha elimu bure, bima ya afya, umeme kila kijiji na sasa anaijenga Tanzania ya viwanda,” alieleza.Hata hivyo, aliomba kupitia awamu hiyo ya tano, isiutupe mfumo wa vyama vingi, kwani ni kati ya tunu zilizoachwa na Baba wa Taifa, Nyerere, lakini pia ndio umekuwa msukumo mkubwa wa maendeleo yanayoonekana nchini.“Naomba tuhakikishe mfumo huu unachangia kuleta mawazo chanya ya kuijenga Tanzania kiuchumi lakini pia kudumisha amani,” alifafanua Cheyo.Akiielezea Tanzania kuanzia kipindi cha uhuru hadi sasa, mwanasiasa huyo ambaye pia aliwahi kuwania nafasi ya Urais mwaka 2005, alisema Tanzania inatakiwa ijivunie kwani kwa kipindi cha miaka yote 58 ya Uhuru, imekuwa na amani na utulivu, tofauti na mataifa mengine. Tanzania Bara husherehekea Siku ya Uhuru Desemba 9 ya kila mwaka.
1kitaifa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa waziri wa wizara hiyo Profesa Joyce Ndalichako ametangaza viwango vipya vya ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo Mwasu Sware, taarifa hizo siyo sahihi na zipuuzwe.“Waziri hajatangaza na wala hajazungumza na chombo chovhote cha habari kuhusu suala la kuwepo kwa viwango vipya,” alisema.Inaelezwa kuwa taarifa ya namna hii imewahi kusambazwa mitandaoni mwaka jana lakini wizara iliikanusha.Sware ametoa wito kwa Watanzania hususani watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa wahakikishe kuwa taarifa zozote wanazozitoa ziwe zimethibitishwa na mamlaka husika.
1kitaifa
Christian Bwaya PAMOJA na faida zake, maendeleo yanaweza kubadili kwa kiasi kikubwa mfumo wa malezi uliozoeleka. Kwanza kabisa, majukumu ya kijinsia yaliyozoeleka katika jamii yanabadilika. Mama aliyezoeleka kuwa mlezi anapoingia kwenye soko la ajira, anaacha nyumbani swali gumu: Nani atabaki na mtoto yeye akiwa kazini? Swali hili ni gumu kwa sababu hata ule utamaduni wa familia tandao nao umeanza kupotea. Shauri ya maendeleo, uwezekano wa ndugu kama shangazi, mama mdogo, wifi, shemeji, binadamu kukaa pamoja unakuwa mdogo na hivyo ule msaada uliozoeleka unakosekana. Matokeo yake inabidi sasa wazazi ambao kwa kawaida wanahitaji kuendelea na shughuli za uzalishaji watafute malezi mbadala. Mojawapo wa mbadala huo ni binti wa kazi maarufu ‘house girls’. House girl, kwa kawaida, ni watoto au vijana wadogo waliokulia katika mazingira ya kawaida, mara nyingi kijijini tena bila elimu kubwa, wanaoajiriwa na wazazi kwa lengo la kuwasaidia kumtazama mtoto wakati wa kazi. Sambamba na malezi, wasichana hawa hufanya kazi za ndani. Walezi hawa hupatikana kwa utaratibu usio rasmi unaotegemea mfumo wa kufahamiana na ndugu, jamaa na marafiki wanaoweza kuwaunganisha wazazi wenye uhitaji na msichana anayetafuta kazi. Hakuna utaratibu rasmi unaowawezesha waajiri wenye uhitaji kuwa na uhakika na historia yake, ujuzi wake pamoja na tabia zake kwa ujumla. Hata hivyo, hutokea wakati mwingine wakapatikana kupitia kwa watu wanaofahamika. Ingawa utaratibu huu wengine huuchukulia kama namna nyingine ya usafirishaji wa binadamu, lakini umekuwa ukiwasaidia wazazi kuwa na uhakika na wapi hasa watoto hawa wanatoka. Mara nyingi, mabinti hawa huajiriwa bila mikataba inayoeleweka na hulipwa kiasi kidogo cha fedha. Hata hivyo, nje na malipo ya fedha taslimu, wazazi wengi huwapa marupurupu kama chakula, matibabu na huduma nyingine za msingi. Ratiba zao za siku hujaa shughuli nyingi zisizolingana na kipato chao. Wengi wao huwa wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala. Waajiri wao huwa na matumaini makubwa kupindukia. Pamoja na kazi kubwa wanayofanya, yamekuwapo matukio ya wasichana hawa kuonewa na waajiri wao kwa namna mbalimbali. Wapo wanaotendewa kama watumwa wasiostahili heshima kama binadamu wengine. Wengine hunyimwa haki zao za msingi. Katika mazingira haya, wasichana hawa, wakati mwingine hujenga tabia zisizofaa ambazo huzorotesha uhusiano na waajiri wao. Hali ya kutokuelewana kati ya mwajiri na mtoto huyu wa kazi husababisha hasira, uchungu na visasi ambavyo mara nyingi huishia kwa mtoto asiye na hatia. Ikumbukwe kuwa wasichana hawa ambao mara nyingi ni watoto, huwa hawana uzoefu na malezi. Utendaji wa wengi wao hutegemea maelekezo ya kila mara kutoka kwa waajiri wao ambao wakati mwingine ni watu wenye uwezo mdogo kiuchumi lakini wenye matarajio makubwa. Tunaposikia matukio ya akina dada hawa kuwafundisha watoto tabia zisizofaa, kuwaonea watoto na kuwatendea vitendo visivyofaa, tunaumia kwa sababu tunafahamu waathirika wakuu ni watoto wasio na hatia wanaolelewa na wasichana hawa ambao wakati mwingine huyafanya yote wayafanyayo kulipa kisasi kwa waajiri wasiojali haki zao. Katika makala ijayo tutatoa mapendekezo matano ya namna tunavyoweza kupunguza changamoto hizi na hivyo kumsaidia mzazi kuwa na amani anapoendelea na shughuli zake za uzalishaji kazini. Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Twitter: @bwaya, Simu: 0754 870 815
5afya
RAIS John Magufuli amewapongeza na kuwazawadia wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kwa kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za michuano ya soka barani Afrika kwa mwaka 2019 (AFCON-2019).Pia, amempongeza na kumzawadia bondia Hassan Mwakinyo, ambaye juzi alishinda pambano lake dhidi ya bondia Sergio Gonzalez wa Argentina, lililofanyika Jijini Nairobi, Kenya. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa, hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Kamisheni ya Ngumi Tanzania (TPBRC) na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli alielezea kufurahishwa kwake na matokeo ya mchezo wa juzi, ambapo Taifa Stars iliifunga timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa magoli 3-0.Aliahidi kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wanamichezo wote, kwa kuwa mafanikio yao yanaliletea taifa sifa na heshima na pia yanatangaza fursa mbalimbali, ikiwemo utalii, biashara na uwekezaji. Rais Magufuli aliwapongeza wachezaji wa Taifa Stars, viongozi wa TFF, Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars na Watanzania wote, kwa kuungana pamoja kuishangilia timu yao katika mchezo wa juzi bila kujali tofauti zao za kidini, itikadi za kisiasa, makabila na kanda wanazotoka.“Kwa kweli jana (juzi) nilifurahi sana jinsi mlivyokuwa mnacheza na jinsi mlivyofunga magoli, Watanzania wanataka furaha, sio kufungwafungwa kama mlivyofungwa kule Lesotho, ile iliniuma sana hadi nilipanga kuwa sitaita tena timu kuja hapa Ikulu, lakini sasa safi. “Nataka niwahakikishie serikali ipo na nyinyi na ni matarajio yangu kuwa mtajiandaa vizuri ili mkafanye vizuri katika michuano ya AFCON huko Misri, sasa vita imeanza,” alisema Rais Magufuli.Rais Magufuli ametoa changamoto kwa wadau wote wa michezo, kuhakikisha wanasimamia uboreshaji wa miundombinu ya michezo, wanajipanga vizuri kwa michezo mbalimbali ya kuiwakilisha nchi, wanarekebisha dosari zote zilizosababisha kusuasua kwa Tanzania katika michezo ya kimataifa. Aliipongeza TFF kwa kufanikiwa kurejesha mgawo wa fedha za maendeleo kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Aliiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kufuatilia uendeshaji wa Uwanja wa Taifa ili kujiridhisha juu ya mapato na matumizi ya fedha za uwanja huo na kuangalia ubora wake, kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa maeneo yanayoharibika, hayafanyiwi matengenezo inavyopaswa.Rais Magufuli alimpongeza bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi alioupata hapo juzi baada ya kumpiga kwa knockout bondia Sergio Gonzalez wa Argentina katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika Nairobi nchini Kenya, pamoja na mapambano mengine ambayo alishinda. Alimtaka kuendelea kufanya vizuri katika mapambano mengine ili kuipatia sifa Tanzania.“Nafahamu kuwa unazo changamoto nyingi ambazo hukusema hapa, lakini nakupongeza sana, juzi umemtandika yule jamaa mpaka akakaa chini na huwa nakuona unavyofanya mazoezi makali kwa kutumia matairi, wewe ni kijana safi sana,” alisema Rais. Rais Magufuli aliipongeza Kampuni ya Serengeti Breweries Limited, ambayo ni wadhamini wa timu ya Taifa Stars na SportPesa, ambao ni wadhamini wa bondia Hassan Mwakinyo kwa mchango wao mkubwa wa kuendeleza michezo.Katika hafla hiyo, Magufuli alikubali maombi yaliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya kusaidiwa maandalizi ya michuano ya AFCON kwa vijana wa chini ya miaka 17 iliyopangwa kuanza Aprili 14, 2019 hadi Aprili 28, 2019 jijini Dar es Salaam huku Tanzania ikiwakilishwa na timu ya Serengeti Boys, ambapo alisema serikali itatoa Sh bilioni moja kusaidia maandalizi hayo.Halikadhalika, Rais Magufuli alitoa zawadi ya kiwanja kimoja cha kujenga nyumba jijini Dodoma kwa kila mchezaji wa Taifa Stars, bondia Hassan Mwakinyo, mchezaji wa zamani na nahodha wa Taifa Stars, Leodegar Tenga na mchezaji wa zamani na mfungaji wa bao lililoiwezesha Tanzania kucheza robo fainali ya AFCON mwaka 1980, Peter Tino ambaye pia amezawadiwa Sh milioni 5.Kwa upande wao, wachezaji wa Taifa Stars ambao waliongozwa na nahodha msaidizi, Himid Mao na bondia Hassan Mwakinyo walimshukuru Rais Magufuli na serikali kwa ushirikiano mkubwa, walioupata hadi kufikia mafanikio hayo na waliahidi kuendelea kufanya vizuri katika michezo inayofuata. Pamoja na kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars na bondia Hassan Mwakinyo, Rais alikula chakula cha mchana na wachezaji hao.
1kitaifa
BWANA harusi aliyekimbiwa na bibi harusi, Omary Mohamed, amesema baada ya tukio hilo amelazimika kudai fedha zake za mahari ili aweze kuendelea na maisha yake. Akizungumza na MTANZANIA jana, Omary alisema kwa sasa hawezi kusema lolote zaidi ya kusubiri kulipwa fedha zake madai ambayo ameyawasilisha kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Manispaa ya Ubungo. “Kwa sasa hatua ninayosubiri ni kulipwa fedha zangu. Na muda huu nipo nyumbani kwangu Buguruni Mtaa wa Ghana, lakini unanihoji badala hata kunitumia hata hela ya kahawa,” alisema kwa kifupi Omary. Kauli ya bwana harusi huyo inatokana na tukio lililotokea juzi baada ya bibi harusi mtarajiwa aliyefahamika kwa jina la Asha Mohamed mkazi wa Kilungule Wilaya ya Ubungo kumkimbia bwana harusi na mshenga wake wakiwa wamepigwa butwaa. Tukio hilo lilitokea saa 7 mchana jana ambapo bwana harusi mtarajiwa aliachwa …..
5afya
Na RAYMOND MINJA- IRINGA MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, amemkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Iringa,  Jesca Msambatavangu, Jah People na Abeid Kiponza, akisema wakati wa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hawakuonyesha uadui kwa upinzani kama ilivyo sasa. Mchungaji Msigwa aliyasema hayo kwa wanahabari jana alipokuwa akizungumzia mustakabali wa siasa za Iringa na kamatakamata aliyodai kufanywa na Jeshi la Polisi kwa Chadema kwa lengo la kuibeba CCM. Alisema ametoa malalamiko kwa Mkuu wa Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, kuhusu jeshi hilo linavyofanya kazi mkoani humo. “Tumefanya siasa na Jah People, Kiponza na Jesca, ilikuwa ni kawaida tukimaliza siasa tunapeana mikono na mambo mengine yanaendelea pasipo hila yoyote,” alisema. Msigwa alisema hivi karibuni jeshi hilo liliwakamata wafuasi wa chama chake kwa maelekezo ya CCM na kuwafikisha mahakamani baada ya siku nane, wakiwahusisha na tukio la kuvunja nyumba ya Diwani wa Kata ya Mwangata aliyejiuzulu, Anjelus Mbogo na kuchoma nyumba aliyokuwa akiishi Katibu wa UVCCM Iringa Mjini, Alphonce Muyinga bila kufanya uchunguzi. Katika kesi hizo, Mchungaji Msigwa alisema amehusishwa pia katika kesi ya kuchoma nyumba ya katibu huyo katika tukio lililotokea akiwa nje ya Mkoa wa Iringa. “Waliponiita polisi niliwaambia sikatai wahalifu wanaweza kuwepo Chadema, lakini pia wanaweza kuwepo CCM, wasio na vyama na matukio kama hayo yanaweza kuwa ya kupangwa na wahusika kwa malengo ya kisiasa au ya kiuchumi, kwa hiyo kabla ya kamatakamata ni muhimu  wakafanya kazi yao kwa weledi na utulivu,” alisema. Mchungaji Msigwa alikwenda mbali zaidi akisema anazo taarifa kwamba, matukio hayo yanatengenezwa na CCM kwa lengo la kuichafua Chadema baada ya mipango yao ya kuwashawishi na kuwanunua baadhi ya madiwani wa chama hicho kuanza kuonekana hayawaongezei umaarufu. “Iringa siwezi kuondoka kwa mkono wa mtu, nitaondoka kwa mapenzi ya Mungu, mwanadamu hawezi kuniondoa, niliwekwa kwa mpango wa Mungu na nitaondoka kwa mpango wa Mungu,” alisema. Msigwa alisema kasi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa kuikataa CCM ilipamba moto wakati wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2014 ilipopoteza mitaa 65 na ikaendelea kwa nguvu kubwa, katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 ilipopoteza halmashauri na Jimbo la Iringa kwa mara ya pili mfululizo.
1kitaifa
Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amehojiwa na Jeshi la Polisi kutokana na kauli zake kuhusu tukio la kupotea kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. Lissu alijisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam jana saa 3:40 asubuhi huku akiwa na wakilishi wake baada ya kutakiwa kufanya hivyo na jeshi hilo. Akizungumza na MTANZANIA baada ya mahojiano hayo, Wakili wa Lissu, Frederick Kihwelo, alisema mteja wake aliitwa na jeshi hilo kwa mahojiano maalumu. Alisema baada ya wito huo, yeye na mteja wake waliwasili katika kituo hicho, ambako alihojiwa na kuruhusiwa kuondoka saa 10 alasiri. “Ni kweli Lissu aliitwa na Jeshi hilo. Amechukuliwa maelezo kutokana na kauli alizozitoa katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Desemba 14, mwaka huu, alipozungumzia kupotea kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Ben Saanane,” alisema Kihwelo. Alisema Lissu alihojiwa na maofisa wa juu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na baadaye kuitwa Ofisi ya Upelelezi wa Mkoa (RCO) ambako alihojiwa tena. Kihwelo alisema mteja wake alihojiwa kama anakifahamu kikosi kazi alichokizungumzia katika mkutano wake huo. “Lissu amejibu kuwa anakifahamu kikosi kazi hicho kwa kusikia baadhi ya watu wanapotafuta ndugu zao huambiwa kuwa wanashikiliwa na kikosi hicho kinachojumuisha Usalama wa Taifa, Polisi na wanajeshi,” alisema. Kihwelo aliongeza kuwa Lissu alihojiwa pia kwanini kila anapotamka jina la Rais humwita Mtukufu sana. “Katika mahojiano hayo, hoja zao zilijikita katika mambo manne aliyoyasema Lissu katika mkutano wake, ambayo alilitaka Jeshi la Polisi kusema kama linamshikilia Saanane, kama yuko nje ya nchi alipitia njia gani kuondoka nchini, mawasiliano ya mwisho aliyoongea nayo kabla ya kupotea na kwanini maiti saba zilizookotwa Mto Ruvu zilizikwa bila kufanyiwa uchunguzi,” alisema Kihwelo. Saanane alipotea ghafla katika mazingira ya kutatanisha takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo jambo ambalo limezua hofu kama yu hai ama la.
1kitaifa
TIMU ya taifa ya Afrika ya Kati (CAR) mara mbili ilitoka nyuma na kuilazimisha sare ya 2-2 na kuwazuia wenyeji Rwanda kupata ushindi wa kwanza katika mchezo wa Kundi H wa mashindano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, kwenye Uwanja wa Huye juzi Jumapili.Sare hiyo mbali na kuifanya Rwanda hadi sasa kutoshinda mchezo wowote kati ya mitano waliyocheza, imewatupa nje ya mbio hizo za kusaka nafasi ya kwenda Cameroon kucheza fainali hizo.Mchezo huo ulianza kwa timu zote kusaka bao la mapema na ilikuwa ndoto ya Amavubi ambao walifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa nahodha wake Jacques Tuyisenge baada ya kupata msaada kutoka kwa Fitina Ombalenga.Hata hivyo, bao hilo halikuwavunja moyo wachezaji wa Afrika ya Kati, ambao haraka haraka walijipanga na kufanya mashambulizi ya nguvu na katika dakika ya 27 Habibou alipiga shuti lililomshinda kipa wa Amavubi, Yves Kimenyi na kujaa wavuni na kufanya ubao wa mabao kuwa 1-1.Katika dakika ya 45, wenyeji Rwanda kupitia kwa Tuyisenge alifunga baada ya pasi kutoka kwa mshambuliaji wa Simba ya Tanzania, Meddie Kagere ambaye kabla ya hapo shuti lake liliokolewa na kipa wa CAR wakati Rwanda ikijaribu kupata bao.Afrika ya Kati haikukata tamaa na juhudi zao zilizaa matunda katika kipindi cha pili kupitia kwa kiungo wake Geoffrey Kondogbia aliyefunga bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi.Kimsimamo, Rwanda wako mkiani mwa kundi lao wakiwa na pointi moja tu, tatu nyuma ya CAR ambao wanashikilia nafasi ya tatu. Baadaye siku hiyo, katika mchezo mwingine wa kundi hilo, vinara Guinea walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Ivory Coast.
1kitaifa
Na MUHAMMED KHAMIS (UOI)-ZANZIBAR POLISI Mkoa wa Mjini Magharibi wamefanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa wanaodaiwa kumchoma Samira Abbas Amin (26), ambaye kwa sasa yupo hospitali anaendelea na matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali, alisema wamefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, Omar Said Omar (24), ambaye anadaiwa kuhusika na tukio la kumchoma moto mwanamke huyo katika eneo la Paje, Kisiwani hapa. Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na mtego waliowekewa na jeshi hilo ambapo walifanikiwa kumtia nguvu katika eneo la Darajani, mjini Unguja. Kamanda Nassir alisema kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo Jeshi la Polisi limezipata, watu hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na walikuwa wakiishi pamoja Paje, kabla ya kutofautiana. “Tulipokea taarifa mapema kutoka kwa raia wema juu ya kijana huyu na dhamira yake ya kukimbia na ndiyo maana tukaweka mtego kuhakikisha tunamkamata akiwa na dereva wa gari walilokuwa wanatumia aina ya Vits yenye nambari za usajili Z 853 GJ,’’ alisema Kamanda Nassir. Kutokana na tukio hilo, hali ya taharuki ilitawala jana katika eneo la Darajani miongoni mwa wananchi baada ya askari waliovalia sare maalumu kuonekana wakiwa kwenye doria maalumu, huku wakizunguka eneo la Kituo Kidogo cha Polisi Mkunazini. Tukio ambalo la kikatili ambalo limevuta hisia za watu kisiwani hapa, limemfanya Mratibu wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mzuri Issa, kusema licha tukio hilo kuwa baya, lakini jambo la kutia matumaini ni hatua ya Jeshi la Polisi kumtia mbaroni mtuhumiwa ili sheria ichukue mkondo wake. Alisema vitendo hivyo vya kikatili kutoka Visiwani Zanzibar havileti picha nzuri ambapo aliiomba jamii kupaza sauti kwa kupinga kwa vitendo, ikiwamo kutoa taarifa kwa Polisi ili kukomesha tabia hiyo mbaya. “Tunaamini kwa hili haki itatendeka, maana ushahidi upo wazi kwa kila kitu, hivyo hatutarajii kuona kesi hii ikibezwa, badala yake tunaamini itakwenda haraka sana na kutolewa hukumu,’’ alisema Mzuri.
1kitaifa
 MWANDISHI WETU WAKATI benki ya dunia ikitahadharisha juu ya uchumi wa bara la Afrika,Kusini mwa jangwa la Sahara kuporomoka kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu miaka 25 iliyopita,kutokana na virusi vya Corona, bara hilo pia limeonywa vifo vya malaria kuongezeka mara mbili zaidi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema idadi ya vifo vinavyosababishwa na Malaria katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara inaweza kuongezeka hadi kufikia 769,000 mwaka huu, iwapo nguvu zote zitaelekezwa katika mapambano ya virusi vya corona (COVID-19). Inaelezwa kuwa Afrika inaweza kujikuta njiapanda zaidi kupambana na magonjwa mengine kutokana na kuelemewa na kasi ya maambukizi ya virusi vya corona ambapo hadi sasa imethibitisha kesi zaidi ya 25,000 za virusi hivyo huku vifo vikipindukia 1200. Kwa sasa serikali kwa kushirikiana na WHO, zimejielekeza zaidi kwenye kupambana na janga la corona. Mkurugenzi Mkaazi kanda ya Afrika Dk. Matshidiso Moeti mapema wiki hii alitoa wito kwa nchi zote za kiafrika kuhakikisha kwamba juhudi za kupambana na Malaria zinaendelea. “Uchambuzi wa hivi karibuni ulibaini kwamba vyandarua vilivyowekwa dawa vimeachwa kusambazwa na udhibiti wa kesi umepungua, vifo vya malaria katika nchi za Afrika kusini mwa Sahara vinaweza kuongezeka mara mbili ukilinganisha na mwaka 2018”, amesema Moeti. “Hii itakuwa idadi kubwa ya vifo kuwahi kushuhudiwa katika ukanda huo tangu mwaka 2000”, ameongeza mkurugenzi huyo. Pia aligusia juu ya takwimu za mripuko wa kirusi cha Ebola barani Afrika, na kuonyesha kwamba watu walikufa kutokana na maradhi mengine, ikiwemo malaria, kuliko hata Ebola yenyewe, kutokana na ukosefu wa upatikanaji matibabu. Mwaka 2018, kulikuwa na visa milioni 213 vya malaria na vifo 360,000 vinavyohusiana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika, ikiwa ni asilimia 90 ya kesi zote duniani. WHO imesema kama lengo la kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona itachangia kupungua kwa upatikanaji wa dawa za kupambana na malaria, vifo vitaongezeka mara mbili. “Nchi katika ukanda mzima zina nafasi ndogo na fursa ya kupunguza uingiliaji katika udhibiti wa malaria, matibabu na kuokoa maisha katika kipindi hiki cha mripuko wa COVID-19”, ilisema taarifa ya WHO. Benin, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Sierra Leone na Chad zote zilianzisha programu za kupambana na malaria kipindi hiki cha mripuko wa corona. WHO inasema nchi hizo zinapaswa kuwa mfano kwa mataifa mengine ya Afrika. UCHUMI NA CORONA Wakati corona ikitishia mapambano ya magonjwa mengine pia inatishia hali ya uchumi. Mripuko wa virusi hivyo unaozidi kusambaa na utabiri wa benki ya dunia ni kwamba unatarajiwa kuzisukuma nchi za   Afrika, Kusini mwa Jangwa la sahara katika mporomoko wa kiuchumi katika mwaka huu wa 2020 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25. Ripoti ya benki ya dunia kuhusu hali ya kiuchumi barani Afrika imesema kwamba uchumi wa bara hilo utashuka asilimia 2.1 na kufikia asilimia 5.1 kutoka kiwango cha ukuaji cha mwaka jana cha asilimia 2.4. Aidha mripuko huu wa virusi vya Corona utazigharimu nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika dola bilioni 37 hadi dola bilioni 79 ambayo ni hasara itakayoonekana mwaka huu kufuatia kuvurugwa kwa shughuli nyingi za kibiashara na kiuchumi miongoni mwa sababu nyinginezo. Makamu mwenyekiti wa benki ya dunia kwa upande wa Afrika, Hafez Ghanem amesema janga la ugonjwa wa Covid-19 linapima uwezo wa mwisho wa jamii na nchi zote ulimwenguni na kuna uwezekano hususani kwa nchi za Afrika kuathirika zaidi. Benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF zinakwenda mbio kutoa fedha za dharura kwa nchi za Afrika na nyinginezo kukabiliana na virusi vya Corona ili kupunguza athari zitakazosababishwa na hatua za kufungwa kwa shughuli za kimaisha zinazochukuliwa nchi mbali mbali ulimwenguni kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo vya Corona. Ikumbukwe kwamba janga la virusi vya Corona limesababisha kufutwa kwa safari za kimataifa katika nchi nyingi za bara hilo la Afrika hali ambayo   imeathiri kwa kiwango kikubwa sana sekta mbali mbali kama vile sekta ya utalii, uwekezaji na biashara. Serikali mbali mbali za bara la Afrika zimetangaza hatua ya kufunga miji au nchi kwa maana ya kwamba hakuna shughuli za kawaida za kimaisha haziruhusiwi tena kufanyika au baadhi ya nchi zimetangaza kuzuia watu kutoka nje, na zile ambazo zimeruhusu raia wake wamekuwa waoga na hata wengine kulazimika kufunga biashara zao. Kwa mujibu wa WHO licha ya virusi hivyo kuchelewa kuingia barani Afrika sasa inaonekana kuanza kusambaa kwa kasi. Kutokana na hali hiyo benki ya dunia inasema ukuaji wa pato la ndani utapungua kwa kiwango kikubwa na hasa katika nchi tatu zenye uchumi mkubwa katika bara la Afrika ambazo ni Nigeria,Angola na Afrika Kusini. Kadhalika nchi zinazouza mafuta pia zitaathirika sana. MAREKANI TOFAUTI NA AFRIKA Wakati Afrika ikisubiri ahueni na misaada, Marekani taifa tajiri imechukua hatua ya kupunguza makali yaliyosababishwa na virusi vya corona. Ikiwa inaongoza kwa maambukizi ya virusi vya corona duniani huku raia wake wakipoteza ajira kwa kiwango kikubwa imeamua kuidhinisha karibu dola nusu bilioni katika mpango mpya wa kuuokoa uchumi. Wakati ulimwengu ukipambana na kutafuta mbinu za kuuokoa uchumi unaoathirika kwa janga la virusi vya corona Baraza la Wawakilishi Marekani limepitisha mswada mpya wa kichocheo cha uchumi wa dola bilioni 483. Hatua hiyo imekuja wakati kiwango cha ukosefu wa ajira kutokana virusi vya corona kikipanda na kampuni zikihitaji msaada zaidi. Muswada huo tayari ulikuwa umeidhinishwa na Baraza la Seneti, na Rais Donald Trump ameashiria kuubariki haraka iwezekanavyo kuwa sheria. Mpango huo unaongeza kwa ule wa dola trilioni 2.2 ulioidhinishwa mwishoni mwa Machi mwaka huu. Karibu watu 50,000 wamefariki dunia Marekani kutokana na virusi vya corona, huku idadi ya walioambukizwa ikifikia zaidi ya 866,646. Spika wa bunge Nancy Pelosi amesema mpango huo ni muhimu kwa kuzilinda familia za Marekani na kuhakikisha kuwa kampuni ndogo ndogo zina rasilimali zinazohitaji. “Dola bilioni 60 zitatengwa kwa ajili ya wanawake na jamii za walio wachache, maveterani, wamarekani asili, wanaoishi vijijini na watu ambao hawakuwa na fedha kwenye benki lakini wana mahitaji makubwa ya mikopo.  “Bilioni 60 nyingine ni mikopo na ruzuku kwa biashara ndogondogo. Na kisha dola bilioni 100 kwa mahospitali na upimaji.” Unaeleza muswada huo Bara la Ulaya, ambalo ndilo lililoathirika zaidi na vifo 110,000, viongozi wa Umoja wa Ulaya waliipa Halmashauri Kuu ya umoja huo jukumu la kutayarisha mpango wa kuufufua uchumi kwa ajili ya mporomoko unaotarajiwa, baada ya mazungumzo yaliyosifiwa kupiga hatua moja mbele, japokuwa wengine wameonya kuwa mazungumzo magumu bado yanakuja. Aidha wameidhinisha mpango wa awali wa kipindi kifupi wa euro bilioni 540 na wakautaka mpango huo kuanza kufanya kazi mwanzoni mwa Juni. Ugonjwa huo unaonekana kuongezeka barani Ulaya na Marekani, mataifa mengine yangali katika hatua za mapema za vita hivyo ambavyo mpaka sasa vimewauwa Zaidi ya watu 190,000 na kuwaambukiza milioni 2.7 kote duniani. CHANJO, KIRUSI NA MIALE YA JUA WHO limeonya kuwa hatua kali zinapaswa kuendelea kutekelezwa hadi pale tiba mwafaka au chanjo vitakapopatikana. Juhudi zinaendelea kote duniani, huku Chuo Kikuu cha Oxford kikizindua majaribio ya chanjo kwa binaadamu. Ujerumani imetangaza kuwa majaribio ya aina hiyo yataanza wiki ijayo. Katika Ikulu ya Marekani, wanasayansi wamesema wamegundua kuwa kirusi hicho kinaharibiwa haraka na miale ya jua, na kutoa matumaini kuwa janga hilo litapungua wakati msimu wa joto ukianza. Baadhi ya nchi za Ulaya zimeanza kuondoa taratibu vizuizi vya kupambana na virusi vya corona, lakini marufuku dhidi ya mikusanyiko mikubwa imeongezwa. Migahawa, mabaa na matukio ya michezo bado vimefungwa. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametangaza kuwa serikali itaanza kuondoa vizuizi vilivyowekwa kuanzia Mei mosi. Ramaphosa   amesema utaratibu huo utafanywa kwa umakini na tahadhari kubwa. Watu milioni 58 nchini Afrika Kusini wamefungiwa majumbani mwao kwa wiki tano, isipokuwa tu kama unataka kununua chakula au dawa. Nchi hiyo imerekodi visa zaidi ya 3,953 vya maambukizi na vifo zaidi ya 75 Vizuizi vilivyowekwa na serikali mbalimbali vitaathiri ulimwengu wa Kiislamu ambao wiki hii unaanza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
5afya
Na Joseph Lino, DAR ES SALAAM NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika, amesema wananchi wengi wanashindwa kutumia huduma za kibenki kutokana na makato ya huduma za fedha. Mwanyika alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati akizindua akaunti maalumu ya Kikundi ya Benki ya  Access Tanzania. Alisema huduma za bure zinasaidia watu ambao hawana vigezo vya kupata mikopo kwenye benki nyingine. “Kama inavyojulikana, vikundi vingi vilivyopo vijijini hupata wakati mgumu hasa kwenye kufikiwa na huduma za fedha kutokana na maeneo waliyopo, hivyo kupelekea kutumia njia za zamani ikiwamo kibubu kama njia ya kuhifadhi fedha. “Nina hakika kupitia akaunti hii ya Kikundi, huduma za kibenki za bure zitawezesha wananchi wa kawaida kwa kupitia Access mobile kupata huduma za fedha. “Huduma ya akaunti ya Kikundi ni mahsusi kwa ajili ya vikundi mbalimbali visivyo rasmi kwa kuweka akiba na kukopa vinavyojiwekea akiba kwa njia mbalimbali ili kukopeshana baadaye na inawezesha kwa kushirikaiana na Shirika la Care na Selcom,” alisema. Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Access, Andrea Ottina, alisema akaunti hii inatoa simu tatu kwa wanachama wa kikundi husika ili kuhakikisha usalama wa fedha zao  na kufanya miamala kwa njia ya simu kwa niaba ya kikundi. “Akaunti hii itaviwezesha vikundi kuendelea na shuguli zao bila kuvuruga ratiba zao za kila siku kwa sababu kila kitu hufanyika kupitia simu zao za mkononi,” alisema Ottina. Mwakilishi kutoka Care International, Christian Pennotti, alisema wanasimamia vikundi 10,000 vyenye wanachama 250,000 vinavyohitaji huduma za kibenki.
1kitaifa
NEW YORK, MAREKANI MSANII wa muziki wa RnB nchini Marekani, Tremaine Neverson ‘Trey Songz’, amegombanisha wasichana katika ‘party’ aliyoandaa kwa ajili ya marafiki zake. Msanii huyo aliandaa sherehe hiyo huku akiwaalika rafiki zake wa karibu, lakini furaha ilibadilika baada ya warembo wawili kugombana kwa ajili ya msanii huyo. Sherehe hiyo ilifanyikia kwenye nyumba yake eneo la kuogelea, hivyo warembo hao inadaiwa kwamba kila mmoja alimtambia mwenzake kwamba anampenda msanii huyo kuliko mwenzake. Kupitia akaunti ya Instagram, Trey Songz aliiweka video ya warembo hao wakigombana na kudai kwamba wote ni rafiki zake.
4burudani
Na Masyaga Matinyi – Arusha TANZANIA ipo katika hatari ya kupoteza soko la madini ya vito baada ya Kenya kufuta ushuru wote pindi yanapoingia nchini humo. Hatua hiyo ya Kenya imefikiwa katika mkutano maalumu kuhusu sekta ya madini (Kenya Mining Forum) uliofanyika jijini Nairobi, Desemba 4 hadi 5, mwaka huu na kuhudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na Waziri wa Madini, Dan Kazungu. Katika mpango mkakati uliotangazwa katika mkutano huo ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 200 kutoka mataifa mbalimbali, Serikali ya Kenya ilisema inafungua mipaka yake ili kuruhusu madini ya vito kuingia bila vikwazo vyovyote. “Kufungua mipaka ya Kenya kuruhusu madini ya vito kutoka ukanda wa Afrika kuingia Kenya kwa uhuru bila vikwazo,” ilisema sehemu ya mpango mkakati. Pia katika mkutano huo, Serikali ya Kenya ilisema inaunda Shirika la Madini la Taifa huku ikikusudia kulifanya kuwa shirika kubwa la madini barani Afrika. Mbali na kulifanya kuwa shirika kubwa Afrika, pia itahakikisha linasajiliwa katika masoko makubwa ya hisa duniani, ambayo ni New York Stock Exchange (NSE) na London Stock Exchange (LSE), lengo likiwa kupata mitaji ya uwekezaji katika sekta ya madini. Wakati Kenya ikipanga mikakati hiyo yenye lengo la kuifanya kitovu cha biashara ya madini ya vito katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania imekuwa ikitoza ushuru kwa madini kama hayo yanayoingizwa nchini wakati wa maonyesho yanayofanyika jijini Arusha. Madini ya vito yanayoingizwa nchini hutozwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini (import duty) kutokana na ukubwa wa mzigo. Alipoulizwa kuhusu hatua ambazo Tanzania inachukua au itachukua kukabiliana na changamoto hiyo, Waziri wa Madini, Angela Kairuki, alisema wizara yake ilipeleka mwakilishi katika mkutano huo Nairobi na ripoti inafanyiwa kazi. “Siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja sasa, tulituma mwakilishi, hivyo tunasubiri ripoti yake, kisha tutakaa na kuangalia nini cha kufanya kwa masilahi ya taifa,” alisema Kairuki. Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alisema ameipokea taarifa hiyo na watakutana na wadau wengine serikalini ili kutafuta mwafaka wa kukabiliana na changamoto hiyo ya kibiashara na uchumi. Kwa habari kamili nunua nakala yako ya MTANZANIA
1kitaifa
Kulwa Mzee – Dar es Salaam MWANAFUNZI wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Lumola Kahumbi (30), amedai askari wa Kituo cha Polisi Oysterbay alichukua hela zake Sh 12,500, mwingine akamwambia ajiongeze naye akatoweka akiwa njiani kuelekea chooni alikokuwa anapelekwa. Shahidi huyo wa utetezi amedai alikuwa chini ya ulinzi kituoni hapo, akaomba kwenda chooni, akiwa huko askari mmoja akamwambia jiongeze huku mwingine akizamisha mkono mfukoni kwake na kutoka na kiasi hicho cha fedha akabakiwa na Sh 200. Shahidi huyo wa 13 wa upande wa utetezi alidai hao jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba Alidai alikamatwa na askari eneo la Kinondoni Studio na kupelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay Februari 16 mwaka 2018, mfukoni alikuwa na Sh 12,700. “Tuliambiwa kama kuna mtu anataka kujisaidia aseme, mimi nikataka kwenda, nilisindikizwa na polisi wawili,  kabla hatujafika chooni chini ya mwembe askari mmoja akaniambia  jiongeze, mwingine akanisachi na kuchukula Sh 12,500 kisha akaniambia niondoke na nisigeuke nyuma.  “Februari 16,2018 nilitoka chuo na kupanda daladala la Kariakoo/ Makumbusho kwenda Kinondoni Studio kumuona shangazi yangu saa moja na nusu usiku, niliposhuka studio nilielekea nyumba ya nne kwa shangazi,”alidai. Alidai akiwa kwenye daladala aliona magari ya polisi na yalipofika usawa wa kituo cha daladala cha studio, waliruka kutoka kwenye gari zao wakati huo katika barabara hiyo ya Kawawa wananchi walikuwa wakiendelea na shughuli zao na kwamba ule msafara wa gari za polisi ulileta taharuki. Shahidi huyo wa utetezi alibainisha kuwa katika kituo cha daladala cha studio wakati wa tukio hilo kulikuwepo na gari za daladala tatu zikipakia abiria na kondakta wa gari moja wapo alikamatwa. Alidai askari walipoanza kukimbiza watu na kuwakamata alikimbia kuelekea Magomeni lakini alipofika eneo la wauza vitanda askari walimkamata. Wengine walikamatwa wauza viwanda na wateja wao na walikimbia baada ya polisi kuonesha kama kuna kitu wanafanya wananchi wakataharuki na kuanza kukimbia. Alidai kwamba walikamatwa watu wengi na gari nyingi za polisi zilijaza watu ambapo walipofika katika Kituo cha Polisi Osterbay wote waliwekwa eneo la nje ya geti chini ya mwembe na wengine waliwekwa ndani ya geti. Alidai geti lilipofunguliwa walipata wasaa wa kuonana kwa muda wa nusu saa na wakiwa hapo askari waliwapiga kwa kutumia mikanda. Shahidi alidai mmoja kati ya askari hao alitoka ndani ya kituo hicho cha polisi akiwa na ngoma akampa mmoja wao aipige na kuwalazimisha waimbe wimbo wenye maneno ‘dola si lelemama’. Kahumbi alidai ndani ya dakika 20 kuna askari aliwaambia wanaotaka kakwenda chooni wajitokeze na yeye alikuwa miongoni kwa waliojitokeza kutaka kwenda chooni. Wakati akielekea chooni walipofika eneo la chini ya mwembe askari ndipo akanyang’anywa hela aliyokuwa nayo akabaki na Sh 200. Alidai kwa kuwa Sh 200 nilikuwa haitoshi nauli, aliondoka kwa miguu kutoka kituo cha polisi Osterbay hadi DIT. Baada ya ushahidi huyo kueleza hayo, Wakili wa Serikali Salim Msemo, alimuuliza awali kuwa ni kweli mwanachama wa chama cha siasa na asiye mwanachama wanatofautishwa kwa kadi na hizo kadi zina namba na akajibu ni sahihi. Alidai  hakuna uthibitisho wowote ambao ameutoa mahakamani kuthibitisha ni mwanachama wa CCM kama anavyodai katika ushahidi wake. Shahidi wa 14 Shabani Othman anaendelea kutoa ushahidi ambapo alidai alikuwa wakala wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni na baada ya kuapa hakupewa kiapo  hadi Februari 17 asubuhi siku ya uchaguzi. Mbowe na wenzake nane wanashtakiwa kwa mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi na kufanya maandamano haramu Februari 16 mwaka huu.
1kitaifa
SERA ya Uchumi wa Kati kupitia ujenzi wa viwanda, umepata msukumo baada ya Kampuni ya IPP kuingia ubia wa kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari kutoka Jamhuri ya Korea maarufu kama Korea Kusini, kinachotarajiwa kuzalisha magari 1,000 kwa mwaka.IPP imeingia ubia huo na Kampuni ya Youngsan wenye uwekezaji wa kiasi cha zaidi Sh bilioni 22, sambamba na kutoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi 500, idadi inayotarajiwa kuongezeka kadri ya muda unavyokwenda. Ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kurasini, utaanza mwanzoni mwaka ujao na uzalishaji rasmi unatarajiwa kuanza kati ya Septemba na Oktoba mwaka huo.Makubaliano ya uanzishwaji wa kiwanda hicho yalifikiwa jijini Dar es Salaam kati ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Song Geum-young ambao kwa pamoja walisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho, kumelenga kuunga mkono juhudi za maendeleo nchini.Akizungumzia hatua hiyo, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho, ilikuwa moja ya ndoto zake kama hatua ya kuitikia mwito wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, inayosisitiza kasi ya ujenzi wa viwanda nchini.“Hakuna kinachoshindikana ukiwa na nia, hata Rais wetu anapambana katika mambo ambayo wengi waliona yanashindikana, amenunua ndege na kufanya mengine mengi..hii ni hatua kubwa katika kukuza maendeleo yetu,” alisema Mengi.Alisema kiwanda hicho kikianza kazi, kitatoa ajira kwa Watanzania, pia kitasaidia kuongeza mzunguko wa biashara katika Afrika Mashariki na Kati na kuiingizia mapato serikali kupitia kodi mbalimbali.Aidha, alisema mipango yake ya baadaye ni kuhakikisha wanajenga kiwanda chenye uwezo wa kutengeneza magari kuanzia mwanzo hadi inapokamilika kutoka katika hatua hiyo ya uunganishaji, jambo alilosema litazidi kuitangaza Tanzania.Magari yanayotarajiwa kuunganishwa kupitia kiwanda hicho ni mabasi, malori na magari madogo, ambapo kwa mujibu wa Balozi wa Jamhuri ya Korea, magari hayo ni ya kisasa. Alisema Jamhuri ya Korea imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa magari na kwamba anaamini kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho nchini, kutasaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda na kuleta tija kimaendeleo.
1kitaifa
Na JOSEPH SHALUWA, STAA wa kitambo kwenye filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema baada ya kukaa singo kwa muda mrefu, sasa yupo tayari kuingia kwenye ndoa wakati wowote. Akizungumza na Swaggaz, Johari amesema anatamani sasa naye aingie kwenye ndoa kwa kuwa umri wake unamruhusu kufanya hivyo. “Mimi ni mwanamke kamili, ni mtu mzima. Nimeshakuwa sasa, kwahiyo kiukweli nina kiu ya mume. Mungu akinipa mume bora, nitaolewa. Sitaki kuzungumzia sana mambo yaliyopita, lakini muhimu kwa sasa ni mume,” anasema Johari. Kuhusu sifa za mwanaume anayependa awe mumewe, Johari alisema: “Napenda mwanaume mwenye upendo wa dhati   kwangu na awe mtafutaji, pia aheshimu kazi yangu. “Historia yangu ya mapenzi imenifundisha mengi, najielewa na kujitambua vizuri. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Johari wa zamani na wa sasa. Kwanza nimekomaa kiakili, nimekutana na vitu vingi na nimejua maisha ni nini. Nipo tayari kufanya maisha na mwanaume serious.” Hata hivyo, Johari anasema kuwa ikitokea mwanaume wa kumuoa akichelewa sana, atafikia uamuzi wa kuzaa, kwani ni kati ya ndoto zake za muda mrefu. “Hakuna mwanamke ambaye hapendi kuitwa mama. Hata mimi natamani, nitajisikia fahari sana siku moja nikiitwa  mama. Ingawa siyo vyema kuzaa nje ya ndoa, lakini ikitokea mwanaume wa kunioa anachelewa nitachukua uamuzi huo mgumu,” anasema Johari. UJIO MPYA Johari ambaye pia ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya RJ ya jijini Dar es Salaam akiwa na mkurugenzi mwenza, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema kwa muda mrefu alikaa kimya kisanii, lakini sasa amerejea upya. “Nimeamua kuanza na nyumbani kwetu Mwanza. Nina movie inaitwa Dosari ambayo nimecheza na wasanii wa Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuwasapoti. Ni filamu ya Kampuni ya Freedom Fighter Film inayomilikiwa na Freedom (Edward Kumaliga),” anasema. Anasema filamu hiyo ambayo itasambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es Salaam, imechezwa na wasanii wa Kanda ya Ziwa wakiwemo Freedom na Andrew Ngonyani ‘Braza K’ anayeshiriki kwenye mchezo wa Futuhi unaorushwa na Star TV. “Baada ya kazi hii, kuna mzigo mwingine utaingia sokoni kupitia kampuni yetu ya RJ. Wadau watulie, wasubiri kazi za nguvu kutoka kwangu. Nimepania kurudisha ushindani  uliokuwepo zamani,” anasema Johari. Lakini hata hivyo, Johari alieleza malalamiko yake kuhusu soko la filamu lilivyoshuka nchini tofauti na zamani ambapo alisema sababu kubwa inayosababisha hali hiyo ni kuwa na wasambazaji wengi wasiokuwa na uwezo na kazi hiyo. “Soko la filamu siyo zuri sana kutokana na usambazaji pamoja na wimbi la watengenezaji wengi waliojitokeza pasipokuwa na uwezo na vigezo. Kingine naweza kusema ni uhaba wa wasambazaji wenye uwezo na kazi hiyo,” anasema Johari.
4burudani
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema Serikali itatumia muda mwingi kadri itakavyoona inafaa ili kujiridhisha na manufaa ambayo taifa litapata kabla ya kusaini mikataba ya sekta ya nishati, hususani ya mafuta na gesi.Ameyasema hayo wakati akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Maurel & Prom kutoka Ufaransa, wanaotafiti na kuchimba gesi eneo la Mnazi Bay.Waziri Kalemani ametoa msimamo huo wa Serikali baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa kampuni hiyo iliyowasilishwa na Makamu Mkurugenzi Mkuu, Elias Kilembe ambayo pamoja na mambo mengine, waliomba serikali iharakishe mchakato wa utiaji saini mikataba ya uwekezaji zaidi katika sekta husika, ambayo walishiwasilisha.Waziri Kalemani alisema, serikali haikusudii kumchelewesha mwekezaji bali kinachofanyika ni kujiridhisha hatua kwa hatua, namna taifa litakavyonufaika."Tutatumia muda wa kutosha kujiridhisha, hata kama ni miaka 40, lakini lazima mikataba iwe na manufaa. Huo ndiyo msimamo wa serikali," alisema na kuongeza:"Sisi tunapenda wawekezaji, tunataka waendelee kuwekeza ili tupate manufaa ya gesi na mafuta, lakini tusiibiwe".Aidha, katika ziara hiyo, Waziri Kalemani aliutaka uongozi wa kampuni hiyo kuchukua hatua stahiki za makusudi na haraka katika kudhibiti changamoto ya maji ya bahari kusogea karibu zaidi na kisima cha gesi cha Mnazi Bay, hivyo kuwepo hofu ya maji hayo kuingia kwenye kisima husika.Vilevile, Waziri alipongeza ukamilishwaji wa mfumo wa kuunganisha visima vyote vya gesi vya Mnazi Bay, hali ambayo alieleza itasaidia katika kuimarisha ukaguzi na udhibiti."Naagiza, kuanzia sasa kila gesi inayotoka katika visima vilivyopo, ipite kwenye mfumo huu mpya ili ituwezeshe kujua ni kiasi gani imetoka na kiasi gani kilipwe," alieleza.Akikagua Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, ulio chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Waziri alipongeza kazi nzuri inayofanywa na shirika hilo na kuwataka waongeze bidii zaidi katika usimamiaji wa rasilimali hizo za mafuta na gesi kwa manufaa ya watanzania.Katika ziara hiyo, Waziri pia alikagua utekelezaji wa miradi ya umeme iliyo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika Mtaa wa Ufukoni na Mbae Mashariki, Manispaa ya Mtwara; ambapo aliwaagiza viongozi wa shirika hilo katika maeneo hayo, kuhakikisha wananchi wote waliolipia umeme wanaunganishiwa huduma hiyo ifikapo Desemba 20 mwaka huu.Aidha, alitoa maagizo kwa mameneja wote wa Tanesco nchi nzima kuwa tarehe ya mwisho kuwaunganishia wananchi waliolipia umeme ni Desemba 31 mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
0uchumi
Kulwa Mzee, Dar es Salaam Upelelezi wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mmiliki wa Blogu ya 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe mfanyabiashara Abdul Nsembo (45), haujakamilika. Kesi hiyo imetajwa leo Jumatatu Mei 27, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, ambapo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai mbele ya  Hakimu Mkazi wa Mfawidhi, Kelvin Mhina kesi lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine. Baada ya kudai hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka na Hajra Mungula walidai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi. Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, mwaka huu, washtakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana. Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.
1kitaifa
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wataangalia wachezaji wengine wazuri ambao watasaidia sio tu katika michuano ya kimataifa, bali ikiwezekana kutetea taji hilo kwa msimu ujao.Muro alisema hawatarajii kufanya usajili wa wachezaji kutoka Simba kwani wamejifunza kutokana na makosa. “Usajili tutafanya kwa wachezaji wengine wa kimataifa hivyo hatutarajii uongozi wetu utasajili wachezaji kwa watani zetu Simba, hata kama ni mzuri kwa kiasi gani au ni malaika, hatutafanya wala hatutarajii,” alisisitiza Muro.Kuhusu ni wachezaji gani wataachwa, alisema ni mapema kusema kwa sasa kwani hilo ni suala la benchi la ufundi. Alisema hajui ni nani ataachwa kwani hayo hujulikana baada ya kumalizika kwa msimu na kisha wakishapewa ripoti ya benchi hilo ndipo watajua wanaohitajika na wasiohitajika.Mkuu huyo wa Habari pia alikanusha taarifa za usajili wa Simon Msuva na Haruna Niyonzima Simba kwamba ni za uzushi na kuwataka wanachama wa klabu hiyo kutosikiliza taarifa hizo.Pamoja na hayo, alizungumzia mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Etoile Sportive du Sahel uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Sousse nchini Tunisia kuwa licha ya kutolewa, wamechukulia kama ni sehemu ya changamoto kujipanga kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa mwakani.“Tumeyakubali matokeo, tumejifunza mambo mengi na tunachukulia mapungufu yetu kwa ajili ya kujipanga,” alisema. Yanga ilitolewa baada ya kufungwa bao 1-0 na hivyo kutupwa nje kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Aprili 18, mwaka huu.Aidha, timu hiyo ya Jangwani tayari imetawazwa bingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 25 baada ya kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 13 zinazoshiriki ligi msimu huu. Leo inacheza na Azam FC
2michezo
SERIKALI ya Marekani imeiweka Tanzania katika orodha ya nchi saba, ambazo raia wake watawekewa masharti magumu kuingia nchini humo, huku sababu kubwa ikiwa ni tabia ya Watanzania kuzamia nchini humo pindi wanapopewa viza za kuingia. Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki kupitia Msemaji wake, Emanuel Buhohela imesema kuwa bado haijapatiwa taarifa hiyo rasmi, isipokuwa imeiona taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii. Alisema kuwa katika diplomasia ya nchi na nchi, kuna njia stahiki ya mawasiliano ambayo hutumika kuwasilisha hoja mbalimbali, hivyo kama wizara haina taarifa rasmi. Alisisitiza kuwa kwa sasa haiwezi kusema lolote. Jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii, mijadala ilikuwa ikionesha ni kama vile Tanzania imeshawekewa masharti magumu ya raia wake kupata viza za kuingia Marekani, wapo waliopotosha, wakidai kuwa sababu ya kuwekewa masharti hayo ni kutokana na Marekani kutoridhishwa namna haki za binadamu zinavyoshughulikiwa hapa nchini.Lakini kwa ufuatiliaji wa gazeti hili wa namna suala hilo, lilivyoandikwa kwenye vyombo vya habari mbalimbali Marekani, yakinukuu serikali ya nchini hiyo, umebaini nchi tatu kati ya hizo saba zilizoorodheshwa ni za Afrika, ambazo zimetajwa kuwa raia wake kwa mwaka 2018 walizidisha muda wa kuishi nchini humo. Nchi hizo tatu ni Eritrea ambayo asilimia 24 ya raia wake, waliopatiwa viza za biashara au matembezi kuingia Marekani kwa mwaka juzi walizidisha muda wa kuishi nchini humo. Nyingine ni Nigeria iliyokuwa na asilimia 15 ya raia wake kuzamia Marekani na ya tatu ni Sudan ikiwa ni asilimia 12 lakini kwa Tanzania hakukuwa na takwimu zinazoonesha. Nchi nyingine zilizo kwenye orodha ya nchi saba ni Belarus, Kyrgyzstan na Myanmar. Baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti taarifa hiyo ni The Wall Street, Reuters, Skifs.com na NewYork Post.Ripoti kutoka Wizara ya Usalama wa Mambo ya Ndani ya Marekani ya mwaka 2018, ambayo gazeti hili lilipitia, inaonesha kuwa Watanzania 5,892 walioingia Marekani, walitakiwa kuondoka kurejea Tanzania.Lakini waliozidisha muda na kuzamia kuendelea kuishi Marekani, walikuwa ni Watanzania 204 ambao ni sawa na asilimia 3.46. Hivyo nchi hizo nyingine tatu za Afrika zilizoorodheshwa, zinaonekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya wazamiaji, ikilinganishwa na Tanzania.Sababu nyingine iliyotajwa ya kuwekwa kwenye orodha nchi hizo (sio Tanzania) ni kushindwa kukagua raia wake wanaokwenda Marekani, hivyo kuongeza wasiwasi wa matukio ya kigaidi. Tanzania haina historia ya kuwa na magaidi wala kujihusisha nao huku ikisifiwa kuwa nchi ya amani, ikilinganishwa na nchi hizo nyingine tatu za Afrika katika orodha hiyo. Kwa nchi hizo zote zilizotajwa ikiwamo Tanzania, raia kutokea nchi hizo watakaokumbana na masharti hayo magumu ya viza ni wale wanaotaka kwenda Marekani kwa shughuli za biashara na kutembea. Hivyo, wanaokwenda kwa shughuli za masomo, tiba na mambo mengine, nje ya hayo mawili, hawatakumbana na masharti magumu. Pia masharti mengine magumu ambayo Tanzania imepangwa kuwekewa ni kuondolewa katika orodha ya nchi zinazonufaika na mpango kupatiwa uraia wa Marekani kwa njia ya bahati nasibu maarufu ‘Green Card’. Tangu alipoingia madarakani Rais Donald Trump aliupinga mpango huo wa kupewa uraia wa Marekani kwa njia ya bahati nasibu, huku akitaka wapewe uraia watu wenye ujuzi. Jumanne ijayo Serikali ya Marekani ndipo itatoa msimamo wa mwisho, kama nchi hizo saba, zipitishwe rasmi kwenye mpango huo wa masharti magumu wa viza hizo mbili. Magazeti ya nchini humo yameeleza kuwa kuna uwezekano wa kuongezwa kwa nchi nyingine mbili, kwenye orodha hiyo ya kuwekewa masharti magumu ya kupata viza kuingia Marekani. Siku saba baada ya kuingia tu madarakani, Rais Trump aliweka wazi msimamo wake kuhusu wageni kuingia nchini humo, ambapo alizuia rasmi nchi kadhaa hasa zenye idadi kubwa ya wananchi wa imani ya dini ya Kiislamu kuingia Marekani, hatua iliyozua mjadala mzito duniani. Agizo lake hilo la kwanza, lilikumbana na pingamizi kutoka Mahakama nchini humo huku lile la pili la Machi 2017 lilikumbana na pingamizi pia, ambapo Mahakama nchini humo ilibainisha kuwa lilikuwa ni agizo lenye dalili za ubaguzi wa dini. Septemba mwaka 2017 Rais Trump alitoa agizo jingine la kuziwekea vikwazo nchi kadhaa kuingia Marekani na lilifikishwa mahakamani, ambapo Juni 2018 Mahakama nchini humo ilibainisha kuwa sheria inampatia Rais Trump madaraka ya kuzuia watu kuingia nchini humo. Raia kutoka nchi za Iran, Libya, Somalia, Syria, Yemen na Korea Kaskazini na wanasiasa wa Venezuela, wamewekewa masharti magumu kuingia Marekani. Hata hivyo, orodha ya nchi hizi saba za sasa ikiwamo Tanzania zitakazowekewa masharti magumu, hazina idadi kubwa ya Waislamu, isipokuwa wazamiaji ndio wengi. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Ben Ellis alipoulizwa na gazeti hili kuhusu sababu ya Tanzania kuwekwa kwenye orodha hiyo, alisema kuwa kwa sasa hawezi kusema lolote hadi watakapopata msimamo wa mwisho juu ya uamuzi huo kutoka nchini kwake.
1kitaifa