content
stringlengths
1
17.8k
category
stringclasses
5 values
label
int64
0
4
IDARA ya Uhamiaji imeanzisha utaratibu mpya wa kulipa malipo ya hati za kusafi ria kupitia simu za mkononi. Uzinduzi wa huduma hiyo ulifanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam.Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni alisema huduma hiyo iitwayo ‘Malipo ya Pasipoti kwa M-pesa’ inalenga kuwawezesha wananchi kufanya malipo kwa haraka na urahisi. “Napenda kuwataarifu wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwamba, sasa wanaweza kulipia hati zao uhamiaji kwa kupitia MPesa.”“Lengo letu ni kuhamasisha Watanzania wapate hati mpya za kielektroniki lakini pia kuwasogezea huduma za malipo viganjani kwao, ndio maana tumeona umuhimu wa kushirikiana na Uhamiaji kufanikisha hili,” alisema.Naye Kamishna wa Hati za Kusafiria wa Uhamiaji, Mary Palmer, alisema huduma hiyo ina lengo la kuwawezesha wananchi kufanya malipo kirahisi na kuiwezesha idara hiyo kufanya kazi kwa urahisi zaidi.
Kitaifa
0
SERIKALI imetakiwa kuleta mabadiliko ya sheria yatakayoiwezesha Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuwa mamlaka ili isimamie sekta hiyo ipasavyo. Wabunge waliitaka serikali kuleta mabadiliko hayo wakati wakichangakia jana katika mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) alisema iwapo TFS itapandishwa hadhi itaweza kusimamia ipasavyo ukuaji na uendelezaji wa sekta ya misitu nchini. “Ikiwa mamlaka, TFS itakuwa na madaraka yake na pia kupanga maendeleo ya sekta kama zilivyofanya Tanapa, Ngorongoro na mamlaka zingine, wakati umefika wa kufanya mabadiliko,” alisema Sakaya.Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Immaculate Semesi (Chadema), ameitaka TFS kuhangalia jinsi ya kulinda na kutunza misitu hasa ile iliyopo kwenye ukanda wa bahari ili kujilinda na majanga na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. “Tumekata miti katika ukanda wa Bahari ambayo ni kinga kwetu wakati wa majanga, tushukuru kimbuga Kenneth hakijatufikia, kama ilivyotabiriwa la sivyo madhara yangekuwa makubwa sana,” alisema Dk Semesi.Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwale (Chadema) akichangia hotuba hiyo alisema umefika wakati sasa wa serikali kuibadilisha TFS kuwa mamlaka kama ilivyo Tanapa ili ifanye kazi zake kwa ufanisi zaidi.Katika hatua nyingine, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania imepewa jukumu la kuanzisha majaribio ya upandaji miti, ukuaji, uhifadhi, matumizi ya miti ya asili na kigeni, kuratibu tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi ya teknolojia bora, mpya ya miti, hifadhi ya udongo, wanyama na mimea.Hayo yalielezwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla wakati akitoa hotuba yake wakati wa kuwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Alisema taasisi hiyo imeanzisha majaribio 30 ya utafiti wa upandaji sahihi wa miti kwenye eneo la hekta 95 katika Kanda ya Ziwa, Kati, Mashariki, Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini.Kwa mujibu wa Waziri Kigwangalla, matokeo ya majaribio hayo yataongeza wigo wa spishi za miti ya asili zitakazokuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.Alisema taasisi imekusanya na kusambaza taarifa kuhusu janga la moto wa misitu kwa kutumia takwimu za satelaiti na kuwa taarifa hiyo inaonesha kuwa janga la moto ni kubwa na limeathiri eneo la misitiu lenye kilometa za mraba 100,903 ambao ni sawa na asilimia 11 ya eneo lote la Tanzania Bara.Aliyataja maeneo yaliyoathirika kuwa ni mikoa ya Lindi, Katavi, Mbeya, Tabora na Ruvuma na kuongeza kuwa wizara kwa kushirikliana na wadau inaendelea kuelimisha umma kuhusu kuchukua tahadhari na kuzuia moto wa misitu.Katika kupunguza madhara ya moto kwenye mashamba ya miti na misitu ya hifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umefanya kampeni za uhamasishaji wa matumizi sahihi ya moto katika vijiji 318 vilivyoko karibu na amshamba ya miti na misitu ya asili.
Kitaifa
0
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa a alisema maonesho hayo ya mifuko yanafanyika kwa mara ya kwanza na yameandaliwa na baraza hilo ambapo wananchi wataweza kupata fursa ya kufahamu huduma zinazotolewa na mifuko hiyo.“Wananchi wanahitajika kushiriki maaonesho haya yenye lengo la kutoa elimu kwao juu ya huduma za mifuko,” na katika maonesho haya wajasiriamali wa sekta mbalimbali walionufaika kupitia mifuko hii watashiriki ili kuonesha matokeo ya uwezeshaji wa,” alisema Issa.Alisema mifuko itakayoshiriki katika maonyesho hayo ni Mfuko wa Kuendeleza Wajasiriamali Wananchi, Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi, Mfuko wa Pembejeo za kilimo, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mfuko wa Dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, na Mfuko wa Dhamana za Mikopo kwa Mauzo ya Nje ya Nchi.“Mifuko mingine ni Mfuko ya Kuwasaidia Makandarasi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Mfuko wa Misitu Tanzania, SELF Microfinance Fund na Asasi ya Kusaidia Uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo nchini ( PASS),” alisema.Alifafanua kwamba kaulimbiu ya maonesho haya ni “Wezesha wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda.”
Biashara
1
Makubaliano haya ni awamu ya kwanza ya uendelezaji wa hekta 110 za eneo hilo huru la bandari, ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali.Hekta hizo 10 zitaendelezwa kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa na kisha kugawiwa kwa kampuni za kimataifa, zinazofanya kazi za kutoa huduma mbalimbali kwa kampuni zinazofanya kazi ya utafiti wa mafuta na gesi katika Mkoa wa Mtwara.Kitakapomalizika, kituo hiki cha huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti wa gesi na mafuta mkoani Mtwara kitakuwa cha kipekee, si kwa Tanzania pekee bali katika ukanda mzima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.Utiaji saini makubaliano hayo ya kihistoria mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dk Adelhelm Meru na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande.Utiaji saini ulishuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Dk Mwakyembe alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa kampuni za kimataifa, zinazotoa huduma kwa kampuni za utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta kuwekeza Mtwara na pia kutoa huduma zake katika Afrika.Waziri Mwakyembe alisema kampuni saba ziko tayari kuwekeza katika eneo hilo. Alitaka mamlaka husika kuhakikisha zinafanya haraka na kwa usahihi matayarisho yote yanayotakiwa ili kampuni hizo ziweze kuanza kufanya kazi mara moja.“Mamlaka husika hazina budi kumaliza haraka na kwa usahihi matayarisho yanayotakiwa ili uwekezaji huu uanze mara moja,” alisema.Alisema kabla ya hapo kampuni hizo zilikuwa zikitoa huduma zake kutokea Mombasa, Kenya na Afrika ya Kusini. Waziri Teu alisema hatua hiyo ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania.“Mtwara na Tanzania sasa vinafunguka zaidi,” alisema, na kuongeza kuwa baada ya kuanza kazi, kampuni hizo zitazalisha ajira kwa Watanzania na kuongeza wigo wa kodi kwa Serikali.Kwa upande wake, Dk Meru alisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa kampuni hizo zitatoa huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta katika nchi za Kusini na Mashariki ya Afrika Alisema ujio wa kampuni hizo pia utasaidia katika kuendeleza sekta nyingine kama hoteli na kilimo katika Mkoa wa Mtwara.Baadhi ya kampuni zilizoonesha nia ya kuwekeza katika eneo hilo la hekta 10 ni Schlumberger, Weatherford and Halliburton International Inc kutoka Marekani.Nyingine ni Lena, FFF (T), Alpha Group and Queensway kutoka Dubai na Uingereza; Altus Tanzania Ltd kutoka Singapore; Tans Ocean Industries & Services Ltd ya Dubai na Intershore Tanzania Ltd ya Afrika Kusini.
Biashara
1
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika amebainisha hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea bandari hiyo ili kushuhudia tishari hizo.Alisema ununuzi wake umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 10 na yanatarajiwa kuongeza tija na ufanisi utakaoiwezesha TPA kuwahudumia wateja wake kwa kasi kubwa zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.“Kwa kuwa tishari moja lina uwezo wa kubeba tani 3,500 au makasha 198 ya futi 20 kwa mara moja, hatua hiyo ni dhahiri itatupunguzia gharama za uendeshaji ambazo ni mizunguko ya kwenda nangani, mteja atapunguziwa muda wa kusubiri kwa kuwaongezea tija maradufu”, alisema.Hata hivyo alisema pamoja na ununuzi wa tishari hizo, TPA kwa kushirikiana na serikali inaendelea na mpango wake wa ujenzi wa bandari mpya Mwambani ambayo itawezesha meli kutia nanga moja kwa moja.Bandari ya Tanga ndiyo ya pili kwa ukubwa nchini ukiacha ile ya Dar es Salaam, ina gati lenye urefu wa mita 381 na kina kifupi cha maji ambacho hulazimisha mzigo kuhudumiwa mara mbili nangani na gatini ambapo shughuli za kupakia na kushusha hufanyika kwa kutumia tishari pamoja na meli za kuvuta vyombo.
Biashara
1
Alitoa kauli hiyo juzi usiku wakati akizungumza na mabalozi na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam na miaka 50 ya kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Vietnam, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.“Huu ni wakati muafaka kwa nchi zetu kuangalia ni aina zipi za uwekezaji zinafaa kuchukuliwa kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake. Nitumie fursa hii kuwakaribisha wawekezaji kutoka makampuni ya Ki-Vietnam waje kuwekeza kwenye usindikaji wa korosho, utengenezaji wa saruji na viwanda vya nguo,” alisema Waziri Pinda.Aliyataja maeneo mengine ambayo wenye kampuni wanaweza kuwekeza kuwa ni nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ujenzi wa nyumba za kuishi.Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vietnam (VIETTEL) kwa uamuzi wake wa kutenga Dola za Marekani bilioni moja ambazo zitatumika kuendesha shughuli zake nchini.“Huu ni mtaji mkubwa sana, siyo tu hapa Afrika Mashariki na Kati bali hata barani Asia. Uwekezaji huu utazalisha ajira za moja kwa moja 1,700 na ajira nyingine 20,000 ambazo si za moja kwa moja,” aliongeza.Kwa upande wake, Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Vo Thanh Nam alisema tangu ipate uhuru wake hadi, nchi hiyo imekwishaanzisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi 185 na wakati huo huo imekwishaweka uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi 220.
Biashara
1
Serikali imetoa onyo wazazi na walezi kutowatelekeza watoto wenye mahitaji maalum wafikishwapo shuleni.Wito huo umetolewa leo Ijumaa, bungeni, Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Conchester Rwamlaza aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali juu ya huduma katika shule za watoto wenye mahitaji maalum.Akifafanua kuhusu suala hilo, Waitara amesema kuwa serikali na jamii kwa ujumla wana wajibu wa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kuwapatia watoto mahitaji muhimu.“Kwa kweli jambo hili ni jukumu la jamii na sio serikali pekee yake….tukishikamana serikali na jamii jambo hili litakuwa jepesi sana”Akifafanua baadhi ya changamoto zinazokwamisha katika utoaji wa mgao wa fedha za utoaji huduma katika shule hizo Waziri Waitara amesema kuwa baadhi ya watoto hawawekwi katika mfumo rasmi huku baadhi ya Halmshauri zikishindwa kufikisha taarifa sahihi za mahitaji muhimu ya shule hizo.“Nitoe wito kwa wabunge, madiwani na viongozi wa vijiji na mitaa tupatiane takwimu sahihi tukipata taarifa sahihi tutapeleka pesa kulingana na uhitaji wa eneo hilo” amesema Waitara
Kitaifa
0
Yanga inahitaji sare ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kushinda bao 1-0 katika mechi ya awali iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam wiki iliyopita.Nsajigwa aliliambia gazeti hili jana wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wanajivunia maandalizi waliyoyafanya na kwamba ushindi ndio kipaumbele chao.“Nikweli tunacheza ugenini na mechi tunatarajia itakuwa ngumu lakini ushindi ni jambo la muhimu kwasababu tumekuja tukiwa tunawajua vizuri wapinzani wetu hivyo hawawezi kutusumbua kama ilivyokuwa mechi ya kwanza tuliyocheza nyumbani,”alisema Nsajigwa.Kocha huyo alisema pamoja na kwamba wanaongoza kwa bao moja lakini hawatocheza kwa kujilinda badala yake watashambulia kama ilivyokuwa mechi ya kwanza ili kuwazuia wapinzani wao wasilisogelee lango lao na ikiwezekana wapate bao la mapema ili kuwachanganya zaidi.Alisema kila mchezaji kwenye kikosi chao anatambua umuhimu wa ushindi katika mchezo wa leo hivyo anaamini hawatokuwa na mzaha zaidi ya kutekeleza walichokikusudia ambacho ni ushindi.Nsajigwa alisema pamoja na wapinzani wao kuonekana wazuri lakini kwa ari na mikakati waliyokwenda nayo Shelisheli anauhakika wa kuvuna ushindi na kuendelea na safari ya kufika hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika.
michezo
2
["Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka 2019 si mwingine bali ni Lionel Messi, ambaye amejichukulia kinyang'anyiro cha kuwa mchezaji bora zaidi kwa mara ya sita.", 'Mchezaji huyo wa Argentina mwenye miaka 32 amenyakua tuzo hiyo baada ya kuikosa toka mwaka 2015 na hii ni kutokana na kuweza kufunga mara 54 katika klabu ya nchini kwake kwa mwaka 2018-19 .', 'Virgil van Dijk alikuwa mshindi wa pili - yeye ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Liverpool katika saba bora, akiwemo Sadio Mane.', 'Mchezaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, aliwahi kutunukiwa tuzo hiyo mara tano na amekuwa watatu katika kura.', 'Toka mwaka 2008 tuzo hiyo maarufu zaidi ya wasakata kandanda duniani imetawaliwa na washambuliaji hatari katika kizazi cha sasa Messi na Ronaldo. ', 'Mpaka kufikia mwaka 2017, kila mmoja wao akishinda mara tano. ', 'Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa la Croatia Luka Modric aliingilia ufalme wa Messi na Ronaldo baada ya kunyakua tuzo hiyo mwaka jana. ', 'Na sasa Messi amerejea kileleni kwa kumpiku Ronaldo na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kunyakua tuzo hiyo mara sita. ', 'Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa mwaka huu kwa Messi, Ronaldo na Van Dijk kuwania tuzo moja kwa pamoja.', 'Mara ya kwanza walikutana katika tuzo za Mchezaji Bora wa Ulaya (Uefa) mwezi Agosti ambapo Van Dijk aliibuka na ushindi. ', 'Mara ya pili wakaminyana katika tuzo za Mchezaji Bora wa Fifa ambapo Messi aliibuka mshindi.', "Tano Bora ya Ballon d'Or", '1. Leonel Messi (Barcelona na Argentina)', '2. Virgil van Dijk (Liverpool na Uholanzi)', '3. Cristiano Ronaldo (Juventus na Ureno)', '4. Sadio Mane (Liverpool na Senegali)', '5. Mohammed Salah (Liverpool na Misri)', "Ballon d'Or ni nini?", "Tuzo ya Ballon d'Or imekuwa ikitolewa nchini Ufaransa kila mwaka toka 1956, na mshindi wake wa kwanza alikuwa mchezaji kutoka Uingereza Stanley Matthews.", 'Awali tuzo hiyo ilikuwa ni kwa wachezaji wa Ulaya tu kabla ya kufanyika mabadiliko mwaka 1995 na kujumuisha wachezaji wa mataifa yote duniani, mradi wanasakata kandanda katika vilabu vya Ulaya. ', 'Orodha ya majina ya wachezaji 30 bora huandaliwa na baadae kupigiwa kura na wanahabari wa michezo kutoka sehemu tofauti duniani, ambapo kila nchi hupiga kura moja. ', 'Kutoka mwaka 2010 mpaka 2015 tuzo hiyo iliunganishwa na ile ya Fifa lakini zilitengana mwaka 2016 ambapo Fifa ilianza kundaa tuzo zao wenyewe. ']
michezo
2
AGIZO la Rais John Magufuli la kutaka kila kijiji kupata umeme, limeungwa mkono na Mtanzania anayeishi nchini Poland, Julius Zellah, ambaye amejitolea kuzalisha nishati ya umeme katika eneo la Ilungu, Mbeya Vijijini.Kampuni ya Mtanzania huyo, ya Texpol Development Company (TDC) Limited, kwa kushirikiana na Light for Africa ya Poland ambayo ni taasisi ya Diaspora wa Tanzania nchini humo, zimechukua hatua ya kusaidia wananchi waishio katika vijiji vya eneo hilo kuwa na umeme, unaotokana na maporomoko ya maji kwenye mito mikubwa na milima.Akizungumza kutoka Poland, Zellah ambaye ni mlezi wa mradi huo, anasema wamepania kumsaidia Rais Magufuli na Waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani. Anampongeza Rais Magufuli, kwa hatua anazochukua za kuhakikisha wananchi wanyonge na wenye kipato cha chini, wanapata umeme ili uwasaidie kurahisisha huduma za jamii, ikiwemo zahanati na shule na kwa ajili ya uzalishaji mali, kama viwanda vidogo. Zellah anamuomba Dk Kalemani kutembelea Ilungu, kukagua mradi ulipoishia na kumalizia vijiji vilivyobaki ili wananchi wapate nishati hiyo waliyoisubiri tangu uhuru. Anasema ni faraja kubwa kwa Serikali kuona wananchi hao wanatoka kwenye giza na kupata mwanga.Zellah amewajengea bure chanzo cha umeme wananchi wa vijiji 10 vya Kata ya Ilungu katika Wilaya ya Mbeya Vijijini, bila kutumia fedha za serikali. Anasema huo ni mchango wake kwa serikali ambayo imepania kujenga viwanda. Vijiji vilivyopata umeme ni Ifupa, Shango, Itiwa, Mwela, Mashese, Ngole, Nzumba, Isyonje, Nyalwela A na Nyalwela B.Katika mradi huo, ameweza kupeleka umeme na maji katika Shule ya Sekondari ya Serikali ya Ilungu, shule sita za msingi na zahanati tano. Umeme huo umepelekwa pia kwenye nyumba zote za wafanyakazi wa taasisi za serikali katika kata hiyo. Kata ya Ilungu haifikiki kwa urahisi kwa sababu iko milimani, karibu meta 2,800 kutoka usawa wa bahari.Usafiri huwa ni mgumu maradufu wakati wa kipindi cha mvua. Kata hiyo ya Ilungu iko umbali wa kilometa 52 kutoka Mbeya mjini. Ipo katika barabara inayounganisha miji ya Mbeya na Njombe na inapakana na Kata za Kitulo, Makete, Igurusi, Igoma na Irambo. Kazi ya kujenga miundombinu hiyo ya umeme,ilianza mwaka 2013 baada ya wakazi wa Kijiji cha Ifupa kumsomea risala ndefu Zellah ya kukosa umeme, ulioahidiwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) zaidi ya miaka 10.Mtanzania huyo aliwasihi wananchi wa kata yote ya Ilungu wasiilaumu serikali kutokana na kuwa na majuku mengi, bali wampe baraka zao aweze kuwajengea miundombinu ya kuzalisha umeme; na washirikiane naye katika kazi hiyo ngumu na yenye gharama kubwa. Hadi mwaka 2018, mradi huo ulikuwa umekamailika kwa asilimia karibu 90 na wananchi zaidi ya 16,000 wamenufaika na umeme huo.Gharama za ujenzi wa kazi hiyo hadi sasa ni takribani Sh bilioni 6.8 na utakapokamilika, itakuwa Sh bilioni 7.4. Zellah na kampuni yake ya Texpol, alikubaliana na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) kuwa mradi wa Ilungu utakapopatikana fedha ya serikali itaenda kuokoa maeneo mengine ya mkoani Mbeya. Baadaye ilipopatikana pesa ya serikali, Rea walitumia fursa hiyo kusambaza umeme katika Wilaya ya Chunya, kitu ambacho ni faida kubwa kwa Serikali ya Tanzania.Baada ya kumaliza usambazaji umeme, Zellah alianza jitahada za kujenga umeme wa maji kwa kutumia maporomoko ya Mto Ishinga, nje kidogo ya Kijiji cha Mwela. Ili kufanikisha kazi hiyo, kampuni hiyo ya Texpol ikishirikiana na taasisi ya Light for Africa Foundation kutoka Poland, inayounga mkono mradi huo, walianza kutafuta vyanzo vya fedha kutoka taasisi za fedha Poland.Walilenga kukamilisha umeme kwenye maeneo mengine ya vijiji vya Kata ya Ilungu na uliobaki kuunganisha kwenye mkongo wa taifa. Vijiji vilivyobaki kuunganishwa ni Nyalwela C, Nkumburu na Mabande, vyenye watu zaidi ya 6,000. Taasisi ya Light for Africa Foundation ikiongozwa na Alicja Bajowska (Mama Waka Waka) kutoka Poland, wamesaidia miradi kadhaa ya jamii katika Wilaya ya Mbeya Vijijini, ikiwemo kupeleka majiko ya kisasa, viti na meza 200.Vingine ni vitanda 123 vya chuma kwa mabweni ya wasichana wa Shule ya Sekondari ya Serikali ya Ilungu, ambako kwa muda mrefu wanafunzi walikuwa wanalala sakafuni na kusababisha waugue kila mara. Pia, taasisi hiyo imepeleka vifaa vya afya 500 (mama kit) vya kisasa vya kusaidia akina mama wakati wa kujifungua. Mwaka juzi Balozi wa Poland nchini Tanzania, Dk Ewelina Lubieniecka alimkabidhi vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Vijijini. Miundombinu ya usambazaji wa umeme ni sehemu ya kuendeleza mradi wa umeme wa maji wa karibu megawati 6.5 katika Kata ya Ilungu, uliobuniwa na kampuni ya Texpol Development Company (TDC) Limited, ikisaidiwa na Light for Africa.Lengo la kuendeleza mradi wa nguvu ya maji ni kuwezesha wananchi wa Kata Ilungu, kupata umeme wa gharama nafuu ili waanzishe viwanda vidogo kama vile useremala, kusaga nafaka, kuchomelea milango na madirisha, kutunza vyakula na kuendesha kwa ufanisi shule na vituo vya afya. Umeme wa maji utasaidia pia kurudisha gharama kubwa, zilizotumika kujenga miundomninu ya umeme kwa kata nzima.Ikumbukwe kuwa, tangu mwaka 2003, wananchi wa Kijiji cha Ifupa Kata ya Ilungu, wamekuwa wakiomba umeme kutoka Tanesco na kuahidiwa kupata nishati hiyo huku wakitakiwa kufanya kutandaza nyaya (wiring) katika nyumba zao. Baadhi walitandaza nyaya hizo, lakini hadi 2013 TDC ilipokubali mchakato wa kujenga mradi wa umeme, wakawzi walikuwa hawajapata umeme kutoka Tanesco.Wakati utafiti wa uwezekano wa mradi wa umeme wa maji unaendelea, TDC iliona kuwa ni busara kujenga miundombinu ya usambazaji karibu na eneo la mradi ili umeme huo usaidie pia wananchi. hadi makala haya yanakwenda mitamboni, Texpol bado haijamaliza mradi wake kutokana na pesa yote kutumika kwenye miundombinu ya umeme huo. Kampuni ya Texpol ilihamasishwa na wananchi wa kata nzima na ikatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme. Pesa hiyo ilitoka ndani na nje ya nchi, hasa Poland anakoishi Mtanzania huyo, Zellah, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Diaspora Tanzania nchini Poland.Ujenzi wa miundombinu hiyo ulianza kwa kilovoti 33 kutoka mkongo wa Tanesco unaotoka Mbeya kwenda Makete na kupeleka umeme huo hadi Kijiji cha Ifupa na baadaye, kata nzima ya Ilungu. Umeme huo ulijengwa chini ya usimamizi wa Tanesco. Texpol walilipa ada zote zinazohitajika kwa Tanesco kwa kusimamia kazi hiyo ngumu.Kampuni ya Texpol ilipata nyaraka zote muhimu za kisheria kwa kazi hiyo, ikiwemo leseni ya uuzaji umeme kutoka Tanesco. Vibali vingine vya kisheria ni kutoka Wizara ya Nishati, REA, MFA, NEMC, TANESCO, TIC na Mamlaka ya Bonde la Maji Rufiji.Zellah na Mama Waka Waka wanawataka Watanzania duniani kote, wasisubiri serikali ifanye kazi hiyo peke yake, bali waige mfano huu na kuisaidia kuzalisha umeme mbadala na kuusambaza kwa wananchi katika maeneo ambayo serikali bado haijafanya hivyo. Hatua hiyo itawezesha vijiji vyote vya Tanzania, kupata umeme kwa muda mfupi na kwa gharama ndogo.
Kitaifa
0
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), imebuni taa za kuongoza magari zinazosimamiwa na mtu, badala ya kujiendesha kwa lengo la kuokoa maisha ya askari wa usalama barabarani wanaogongwa na madereva wazembe.Pia kuondoa msongamano wa magari kwenye barabara iliyozidiwa. Hayo yalibainishwa na Mwalimu wa Madereva wa Magari Makubwa na Mabasi kutoka VETA-Kionda, William Munuo wakati akizungumzia ubunifu huo kwenye banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) yanayoendelea.Alisema walifanya utafiti wa taa zilizopo nchini kwenye makutano mbalimbali ya barabara na kugundua wakati wa msongamano, askari hulazimika kuingilia kati taa na kuanza kuongoza magari kwa kuyaita, jambo ambalo wakati mwingine ni hatari kwa maisha yao. “Tuliona tubuni taa zitakazomsaidia askari kuongoza magari akiwa pembeni ya barabara mahali salama, lakini pia zitakazotumika kuondoa msongamano kwenye barabara yenye foleni kwa wakati huo,” alisema.Akiuelezea mfumo huo, alisema taa walizobuni zinafungwa kwenye makutano ya barabara husika, kisha swichi ya kuziongoza inafungwa pembeni mwa barabara kwenye kichumba na askari hatakiwi kusimama barabarani bali ndani ya kichumba hicho ili aonapo foleni imezidi barabara fulani ndiyo anabonyeza taa ya kijani kuyaita.Alisema taa hizo ni rahisi kutumia badala ya taa za sasa ambazo zinaongoza magari kwa kufuata muda uliopangwa, hivyo hata foleni ikiwa barabara moja taa hizo haziwezi kutoa kipaumbele magari kupita.Aidha alisema taa hizo bunifu zinawasaidia polisi wa usalama barabarani kutochomwa jua au kunyeshewa mvua na pia kuwaepusha na moshi wa magari kwa kukaa ndani ya chumba chenye swichi ya taa na kuongoza magari ambacho kina utulivu na kivuli.Alisema hata dereva akiwa mzembe au akifeli hawezi kumgonga askari, kwa sababu hayupo barabarani na hiyo inamfanya askari huyo afanye kazi kwenye mazingira bora na kwa utulivu.Munuo alisema hivi sasa wamepeleka ubunifu huo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kuwaonesha jinsi unavyofanya kazi na wao kuona na kusema watakutaka na wadau kuzungumzia ubunifu huo.
Kitaifa
0
MKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka amesema baraza limeshachukua tahadhari zote za kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa wa Stiegler’s Gorge.“Tumejipanga kuhakikisha vyanzo vyote maji katika mto Rufiji katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Dodoma, Njombe, Mbeya na Ruvuma vinatuzwa na kuwa endelevu,” Dk Gwamaka aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam waliotaka kujua hatua ambazo baraza limechukua kulinda mazingira kwenye eneo la Mto Rufiji.Alisema mradi wa kuzalisha umeme wa Stigler’s Gorge ni muhimu sana katika kujenga uchumi imara wa viwanda na hivyo hatua za makusudi zimechukuliwa kulinda vyazo vyote vinavyotiririsha maji kwenye mto Rufiji.Alisema NEMC kama zilivyo taasisi mtambuka ipo mstari wa mbele kuchagiza maendeleo ya uchumi na viwanda nchini kwa kuhakikisha shughuli zote za kimaendeleo haziathiri mazingira yaliyopo.“NEMC ipo makini kwa miradi yote ambayo inafanyika maeneo yaliyopo na vyanzo vya maji. Tunahakikisha vinalindwa na kuwa endelevu kwa faida ya vizazi vilivyopo na vile vijavyo,” amesema.Alisema baraza litaendelea kusimamia sheria na taratibu zote zinazosimamia mazingira hapa nchi ili kuyalinda kwani kufanya hivyo kutaiweka Tanzania katika nafasi nzuri kuelekea ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.“NEMC inapongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ambavyo kimsingi vitaongeza ajira kwa Watanzania,” alisema.Dk Gwamaka aliziomba taasisi, mamlaka mbalimbali na Watanzania kwa ujumla kushirikiana na NEMC kuhakikisha kuwa mazingira katika maeneo husika yanatunzwa na kulindwa kwa faida ya vizazi vijavyo.Mwaka jana, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) iliwaagiza wakurugenzi wote wa miji, manispaa na majiji kuainisha vyanzo vyote vya maji katika maeneo husika ili viwekewe utaratibu wa kulindwa.Kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la umeme la Stigler’s Gorge mbali ya kumaliza tatizo la umeme nchini, utachochea kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda na kuleta mageuzi makubwa ya uchumi na kijamii ambapo megawati 2,100 za umeme zinatarajiwa kuzalishwa.Ulitiaji saini wa mkataba wa kuanza ujenzi wa mradi huo mkubwa wa umeme ulishuhudiwa na Rais Magufuli, Waziri Mkuu wa Misri na viogozi mbalimbali wa dini Ikulu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka jana.
Kitaifa
0
TIMU ya soka ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti boys jana iliifunga Malawi mabao 2-1 katika mchezo wa mashindano ya Vijana kwa nchi za kusini mwa Afrika (COSAFA) uliochezwa Gaborone, Botswana.Habari kutoka Gaborone zinasema, Serengeti boys ambayo ilianza vibaya kwa kufungwa na Angola mabao 2-0 wiki iliyopita, jana ilipata bao dakika ya saba likifungwa na Kelvin Pius ’Mbappe” na kudumu hadi mapumziko ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo. Kipindi cha pili Malawi walicharuka na dakika ya 59 walisawazisha bao lililofungwa na Mwungulu lakini Serengeti boys waliongeza bao la ushindi dakika ya 78 likifungwa na Suleiman Juma.Baada ya mchezo huu Serengeti boys imebakisha mchezo mmoja katika Kundi B ambao itacheza na Afrika Kusini kesho ambapo ikishinda itacheza nusu fainali.Afrika Kusini jana waliifunga eSwatini mabao 2-0. Akizungumza baada ya mechi hiyo kocha wa Serengeti Boys Oscar Mirambo alisema wamefurahi kupata ushindi na kuahidi ushindi tena dhidi ya Afrika Kusini. “Nafurahi wachezaji wamefanya kile nilichowaagiza tukapata ushindi, nawaomba watanzania waendelee kuwa na imani na timu yao kuwa itafanya vizuri,” alisema Mirambo.Serengeti inashiriki mashindano hayo kama timu mwalikwa na inatumia mashindano hayo kupata uzoefu wa kujiandaa na fainali za Afrika za Vijana ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini mwakani
michezo
2
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Jennifer Omollo amesema, Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Pwani ni fursa kwa halmashauri hiyo kwa kuwa viwanda kwenye eneo hilo vinahitaji soko la bidhaa.Amesema ofisini kwake mjini Kibaha kuwa, pia wajasiriamali wadogo wanahangaika kupata soko la bidhaa zao hivyo wakikutana na wenzao wenye viwanda vikubwa wanaweza kuuza wanachozalisha.Ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.Maonesho hayo ya pili ya viwanda mkoani Pwani yatafanyika kuanzia Oktoba Mosi hadi saba kwenye viwanja vyaa CCM Sabasaba Picha ya Ndege, na Kongamano litafanyika Oktoba tatu.“Kwa hiyo kongamano hilo kwa mji wa Kibaha ni fursa kubwa kwa sababu wananchi pia wataona ni jinsi gani Serikali inawekeza katika eneo la viwanda lakini pia wataona maendeleo ambayo Halmashauri ya Kibaha na Mkoa wa Pwani imepiga katika masuala mazima ya viwanda” amesema Omollo.Amesema, Halmashauri hiyo ina miradi kadhaa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na kujenga soko kubwa katikati ya mji lenye uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 4,000.“Tunawaalika, ni vizuri watu wakaja wakapata maeneo katika lile soko ili weweze wakafanya biashara…lakini pia Halmashauri inajenga machinjio ya kisasa kwa mpango wa miradi mkakati” amesema na kuongeza kuwa fedha za miradi hiyo zimetoka Serikali kuu.
Biashara
1
RAIS John Magufuli amesema kuwa kitendo cha timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 kufungwa mechi zote kimemfehedhesha kwa kiasi kikubwa nani aibu kwa taifa.Kwa matokeo hayo mabaya, Rais amesema kuwa anatamani angekuwa Waziri wa Michezo apange timu ya ushindi. Tanzania ilikuwa mwenyeji wa michuano ya Afcon kwa vijana wa chini ya miaka 17 iliyomalizika wiki iliyopita lakini timu mwenyeji, Tanzania, haikufanikiwa haikuambulia ushindi hata mmoja kati ya mechi tatu iliyocheza.Rais ametoa yake ya moyoni leo, Jumanne, wilayani Kyela, mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi Nyanda za Juu Kusini. “Haiwezeki taifa la watu wa milioni 55 tunafungwa na taifa la watu 10. Hii ni aibu kwetu….tunaaibika sote,” Rais Magufuli alisema.Rais alimsifia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kwa uchapaji kazi wake lakini kitendo cha timu ya vijana kufanya vibaya kimebaki kuwa aibu kwake pia.
michezo
2
HALMASHAURI za Wilaya na Manispaa ya Lindi mkoani hapa, zimetakiwa kujenga nyumba za walimu ili kutimiza ahadi iliyotolewa miaka mitatu iliyopita na serikali ya mkoa.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliyasema hayo wakati alipozungumza viongozi wa serikali ya wilaya, Manispaa ya Lindi katika Shule ya Sekondari ya Mingoyo mjini hapa.Alisema makubaliano yalikuwa kati ya mamlaka hizo na serikali ya mkoa kwa kila mwaka kujenga nyumba 10 za walimu za gharama nafuu.Zambi alisema utekelezaji wake uko chini mno, ukilinganisha muda uliotolewa, ambapo bado mwalimu anasumbuliwa kwa kukosa nyumba ya kukaa shuleni hapo. Alisema manispaa zilijengwa nyumba tatu tu za walimu katika Shule ya Msingi ya Mtuleni.“Mfano hapa shule hii ya sekondari ya Mingoyo mwalimu anatoka Mnazi Mmoja anakuja kufundisha hapa, hamuoni kuwa atachelewa kufika shuleni kutokana umbali uliopo,” alihoji mkuu huyo wa mkoa.Aidha, alisema ujenzi wa nyumba walimu, uende sambamba na hosteli za wanafunzi kutokana baadhi yao wanatoka katika mitaa ya Nayani, ambako njia sio rafiki kwani kuna msitu.Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mingoyo, Mwichande Kalyoma alisema shuleni hapo kuna walimu 20, ambao baadhi yao wanaishi katika nyumba za kupanga Mnazi Mmoja na Mahumbika. Alisema kuna changamoto kutokana kutokuwapo nyumba za walimu kwani wanahitaji nyumba zingine 17.“Changamoto nyingine ni ukosefu wa matundu ya vyoo, jengo la utawala kwa sasa tunatumia darasa moja kuwa ofisi kutokana kutokuwepo jengo la utawala na chumba cha kuhifadhia kompyuta,” alisema.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, JoumarySatura alimueleza mkuu huyo wa mkoa kuwa mipango iko mbioni, kukamilisha yote hayo kwa wakati huu.Alisema kinachosubiriwa ni bajeti ya mwaka ujao ndiyo itatekeleza baada ya kupatikana mapato ya ndani ya manispaa hiyo.Aliongeza tatizo la nyumba lipo na litatuliwa katika shule za Kitumbwikwera na Mingoyo, ambako kuna umbali kutoka mashuleni mwao hadi katika makazi yao.
Kitaifa
0
TANZANIA Bara imeshika nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inayoshirikisha timu za wasichana chini ya umri wa miaka 17.Michuano hiyo iliyoshirikisha timu sita ilifanyika kwenye viwanja vya FUFA Technical Centre, Njeru, Jinja na kumalizika jana. Bara, ilimaliza ya pili katika michuano hiyo iliyochezwa kwa mtindo wa ligi licha ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Djibouti katika mechi yake ya mwisho jana.Ushindi huo umeifanya Bara kufikisha pointi 11 na kushika nafasi ya pili nyuma ya vinara Uganda waliotwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 13. Mabao ya Tanzania Bara jana yalifungwa na Aisha Masaka alifunga mabao saba katika dakika ya nane, tisa, 16, 27, 28, 30 na 33, Thabea Munga dakika ya tatu, Shamim Salum dakika ya 40 na Lucia Sabasi dakika ya 51.Uganda imekuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo, ikiifunga Kenya mabao 2-0 katika mechi ya mwisho jana. Kenya iliambulia nafasi ya tatu ikiwa na pointi saba na Burundi iliyoifunga Eritrea mabao 4-0 ilimaliza ya nne.Mabao ya Uganda jana yalifungwa na Fauzia Najjemba dakika ya 31 na Juliet Nalukenge dakika ya 44 wakati Burundi mabao yake yalifungwa na Nzohabonayo dakika ya 63, Ineza Bora dakika ya 71 Ciza Nandine dakika ya 76 na Kalenzo Lydia dakika ya 79.Akizungumza jana, Kocha wa Tanzania Bara, Bakari Shime alisema walijipanga kurudi na ubingwa lakini uchezeshaji mbovu wa waamuzi umewakosesha ubingwa. “Nashukuru leo (jana) tumeshinda lakini lengo letu halikuwa kushika nafasi ya pili, tulijiandaa kutwaa ubingwa lakini waamuzi walichezesha kwa maagizo ya timu fulani ishinde kwa lazima,” alisema Shime.
michezo
2
Jumla ya wafungwa na mahabusu 300 kutoka kwenye magereza ya Butimba, Bariadi, Mugumu, Tarime, Bunda na Kahama wameachiwa huru.Hii ni kufuatia kutekelezwa kwa agizo lililotolewa na Rais John Magufuli hivi karibuni kwa Wizara ya Sheria na Katiba na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupita kwenye magereza nchini na kupitia upya kesi za wafungwa na mahabusu ili walifungwa kimakosa waachiwe huru.Haya yamesemwa leo, Alhamis na Rais Magufuli katika ziara yake wilayani Kongwa alipokuwa akizungumza na wananchi.“Siwezi kutawala nchi na machozi, yataniumiza, na niwaombe polisi wasiwabambikizie kesi wananchi wanyonge, sio suala zuri,” aliongeza. Rais Magufuli ameeleza kuwa zoezi hilo la kupitia kesi hizo, litaendelea nchi zima, lengo ikiwa ni kuhakikisha haki inatengendeka ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
Kitaifa
0
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Katavi, Amos Makala kuunda mara moja timu ya kuchunguza tuhuma za unyanyasaji wa ngono zinazofanywa na viongozi wa juu wa wanaume wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele dhidi ya watumishi wa umma wa kike.Alitoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele ambapo alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili na kutembelea, kuagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri zote tano zilizopo mkoani humo.“Wizara yangu imepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma wa kike wa halmashauri hiyo ya wilaya wakiwatuhumu viongozi wa juu wa halmashauri hiyo wakitumia nyadhifa zao kuwanyanyasa kingono... hivyo namuagiza mkuu wa mkoa wa Katavi aunde mara moja timu itakayochunguza malalamiko hayo na tuhuma hizo ili hatua za kinidhamu na kijinai ziweze kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa,” aliagiza.Alisisitiza kuwa baada ya timu hiyo kukamilisha uchunguzi wake taarifa iwasilishwe na kufanyiwa kazi na Mkuu wa Mkoa na kuwa baada ya utaratibu huo kukamilika mapendekezo ya timu hiyo yawasilishwe wizarani kwake kwa maamuzi .Alisema kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwalinda watumishi wa umma wa jinsia zote wanaofanya kazi kwa uhuru na amani na sio kwa kunyanyaswa na watumishi wenzao.“Nawaasa watumishi wote wa umma nchini endeleeni kufanya kazi zenu kwa uhuru na amani, nawaonya viongozi wa umma wa kiume wanaoendekeza tabia mbaya ya kuwanyanyasa watumishi wa kike kwa kutumia madaraka yao hawatabakia salama, hatua kali dhidi yao zitachukuliwa iwapo watabainika ili iwe fundisho kwa wengine,”alionya.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Makala alimuhakikishia Waziri Jafo kuwa atatekeleza agizo hilo haraka iwezekanavyo kwa kushirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi .“Mara tu timu ya uchunguzi nitakayounda ikiwasilisha taarifa yake ofisini kwangu nitaifanyia kazi mara moja na kuiwakilisha wizarani kwa kuwa kama mkoa sipendi kabisa kusikia watumishi wa umma wa kike wananyanyaswa kingono na wakuu wao wa kazi ambao wanatumia madaraka yao vibaya,” alisisitiza.Baadhi ya watumishi wa umma wa kike katika halmashauri hiyo waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini kwa kuwa sio wasemaji wamedai kuwa wako tayari kuwataja viongozi hao timu hiyo ya uchunguzi itakapoundwa kwa kuwa wanafahamika.
Kitaifa
0
MKUTANO mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar, ZFA, leo umepitisha katiba mpya ya chama hicho bila kupingwa. Katiba hiyo itaanza kutumika rasmi katika shughuli zote za soka la Zanzibar.Mkutano mkuu huo ulifanyika kisiwani Unguja katika Ukumbi wa uwanja wa Amaan huku ukihudhuriwa na wajumbe 9 kati ya 10 wa mikoa mitano ya Zanzibar. Wajumbe hao waliopitisha katiba hiyo ni Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote ya Unguja na Pemba.Katika upitishwaji wa katiba hiyo wajumbe tisa waliokuwepo ukumbini hapo walikubali kupitisha katiba hiyo huku mjumbe mmoja kutoka mkoa wa mjini Magharibi hakuhudhuria kutokana na matatizo ya kiafya na aliwasilisha kwa njia ya maandishi ikifanya katiba hiyo kupita bila kupingwa.Katiba hiyo sasa inaiondoa jina la Chama cha Soka, ZFA na kuwa Shirikisho la Soka Zanzibar, ZFF ili kufikia malengo ya kukuza soka la Zanzibar katika ngazi zote kuanzia chini.Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mkutano huo jana, katibu wa ZFA Mohamed Ali alisema mchakato unaofuata hivi sasa ni kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho kupitia katiba hiyo mpya.Alisema kamati ya uchaguzi itakapotangazwa na wao watakuwa na jukumu la kushughulikia taratibu hizo za uchaguzi wa Rais, Makamu na wajumbe wa kamati ya utendaji.Aidha, akizungumzia katiba hiyo mpya alisema imeweka mambo mengi yatakayochangia kukuza soka la Zanzibar pamoja na kwenda na wakati kama mashirikisho mengine ya soka.Alisema miongoni mwa mambo muhimu ni kupiga hatua ya kuitwa shirikisho jambo ambalo linahitaji jitihada kubwa ili kufikia lengo la jina hilo ikiwemo kuwa na soka bora na litakalotoa wachezaji wazuri watakaowakilisha ndani nan je ya Zanzibar.“Katiba hii ina mambo mengi ambayo yatapeleka soka letu mbele kuanzia chini kabisa, kikubwa viongozi watakaochaguliwa waifuate na wahakikishe kile ambacho kilichopendekezwa katika katiba kinafanyiwa kazi,”alisema.
michezo
2
['Manchester City wamekerwa na mchakato wa Arsenal kumfuatilia kocha wao msaidizi Mikel Arteta na wameionya Arsenal kuwa itawapasa watoe donge nono ili wamnyakue kocha huyo. (Mirror)', 'Arteta anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa Arsenal Josh Kroenke Jumatatu usiku kwa ajili ya kufanya usaili wa tatu na wa mwisho huku akikaribia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Unai Emery aliyetimuliwa mwezi uliopita. (Mail)', 'Kocha wa zamani wa Chelsea, AC Milan, Real Madrid na Napoli Carlo Ancelotti amefikia makubaliano ya jumla kuwa kocha wa klabu ya Everton. (Sky Sports)', 'Chelsea wamewajumuisha washambuliaji Mjerumani Timo Werner wa klabu ya RB Leipzig, 23, na Mfaransa wa klabu ya Lyon Moussa Dembele, 23, katika orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili mwezi Januari. (Mail)', 'Mmiliki wa Napoli Aurelio De Laurentiis ametupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, akisema kuwa klabu yake inabidi ianze kujinga upya kutokea chini. (Goal.com)', 'Klabu ya Leicester inatajwa kuwa na utashi wa kiwango cha juu kumsajili beki wa klabu ya Juventus na Uturuki mwenye thamani ya pauni milioni 25 Merih Demiral,21, kwenye dirisha dogo la usajili mwezi ujao. (Leicester Mercury)', 'Mlinzi raia wa England Ashley Young, 34, anatarajia kuihama klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu na yupo tayari kuanza mazungumzo na vilabu mbalimbali kuanzia mwezi ujao. (ESPN)', 'Wachezaji waandamizi wa Tottenham wamemshauri kocha wao Jose Mourinho kumsajili mshambuliaji wa Wolves Adama Traore, 23, baada ya mchezaji huyo raia wa Uhispania kuonesha kiwango kizuri dhidi yao Jumapili iliyopita (Football Insider)', 'Winga wa Ujerumani Leroy Sane, 23, ameeleza kuwa hatimaye amereje kwenye uwanja wa mpira wakatiakikaribia kurejea kwenye kikosi cha Manchester City. Sane hajacheza toka mwezi Agosti alipopata majeraha makubwa. (Manchester Evening News)', 'Kocha Unai Emery amekataa ofa ya kuifundisha Everton akiamini bado ni mapema kufundisha klabu nyengine ya Ligi ya Primia baada ya kufurushwa na Arsenal mwezi uliopita. (Marca)', 'Vilabu vya Leicester City, Newcastle, Southampton na Leeds United vinagombea saini ya mshambuliaji raia wa England Jarrod Bowen, 22, anayechezea klabu ya Hull City. (Mirror, via Leicester Mercury)', 'Liverpool wameonesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Coventry City raia wa England Sam McCallum, 19. (90min.com)']
michezo
2
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Luzangi, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa sasa ufanisi wa bandari hiyo, umezidi kuwa wa kisasa na haraka.“Maboresho yanayofanywa na Mamlaka yanazaa matunda hivyo nchi jirani zizidi kutumia bandari yetu, ili wapate thamani halisi ya fedha yao,” alisema.Akifafanua, Janeth alisema Bandari ya Dar es Salaam katika mwaka 2012/13, ilihudumia shehena ya tani milioni 12.5 ikilinganishwa na tani milioni 10.9 zilizohudumiwa mwaka 2011/12, sawa na ongezeko la asilimia 15.Katika shehena yote iliyohudumiwa mwaka 2012/13, shehena ya nchi zitumiazo bandari ilikuwa tani milioni 4, ambayo ni asilimia 32 ya shehena yote.Kwa mujibu wa Janeth, jitihada zinaendelea kufanywa na Mamlaka, wadau wa bandari na Serikali katika kuimarisha njia kuu za usafirishaji za reli na barabara na kupunguza vikwazo vya biashara.“Hii itasaidia kuimarisha huduma ya ndani na nchi jirani,” alisema na kuongeza kuwa jitihada za masoko zinafanywa na Mamlaka na wadau wengine kuvutia wateja ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji kazi wa bandari.Akitoa takwimu zaidi, Janeth alisema shehena yote ya mizigo ya nchi 6 zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam, yaani Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Malawi na Uganda, zimeongezeka kutoka tani milioni 3.55 mwaka 2011/12 hadi kufikia tani milioni 4.05 mwaka 2102/13, sawa na ongezeko la asilimia 14.2.“Ongezeko hilo ni kutokana na kuendelea kukua kwa uchumi wa nchi hizo na vile vile mazingira mazuri ya biashara humu nchini Tanzania na uboreshaji wa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam,” alisema.Akizungumzia ushindani, alisema Bandari ya Dar es Salaam iko katika nafasi nzuri zaidi ya ushindani, ikilinganishwa na bandari nyingine katika eneo la Afrika Mashariki na Kati, kutokana na eneo zuri kijiografia na kuwa nchi inayofanya kila kinachotakiwa ili kufanya vizuri.Pia, kumekuwepo na punguzo kubwa la mlundikano wa mizigo na kufanikiwa kukomesha vitendo vya upotevu wa mizigo na wizi kwa kiasi kikubwa. Kwa upande wa mapato, mwaka 2012/13 wastani wa Sh bilioni 371.7 zilikusanywa, sawa na ongezeko la asilimia 14.3 ikilinganishwa na Sh bilioni 325.3 mwaka 2011/12.
Biashara
1
Katika mchezo wa kwanza, Yanga wakiwa nyumbani walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0, hivyo katika mchezo huo wawakilishi hao wa Tanzania Bara, wanahitaji sare au ushindi wa namna yoyote ili kusonga mbele hatua inayofuata.Akizungumza na gazeti hili kabla ya timu kuondoka, msemaji wa Yanga Dismas Ten, alisema wamekwenda Shelisheli wakiwa na uhakika na ushindi kutokana na maandalizi mazuri ambayo wameyafanya tangu mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Majimaji.“Timu imefanya mazoezi ya kutosha na kocha ameridhishwa nayo, lakini pia wachezaji wote wapo fiti kiafya na kiakili kwa ajili ya pambano hilo hivyo tunakwenda kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi ambao utatuvusha raundi ya kwanza ya michuano hiyo ya Afrika,” alisema Ten.Msemaji huyo alisema katika mchezo huo watamkosa mshambuliaji wao Obrey Chirwa, kutokana na kukabiliwa na maumivu ya misuli ya paja aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Majimaji siku chache zilizopita.Ten alisema wanakwenda wakijua ubora wa wapinzani wao St Louis, na kocha wao George Lwandamina anatambua mbinu mbadala ambazo zitawasaidia kuhakikisha wanaibuka na ushindi wakiwa ugenini.Nyota 20 ambao wameondoka na kikosi cha Yanga jana asubuhi kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya wakipitia Nairobi, Kenya na baadaye Shelisheli, ni Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Juma Abduli, Hassan Ramadhani, Said Makapu, Geofrey Mwashiuya, Rafael Daud, Kelvin Yondani na Pius Buswita.Wengine ni Emmanuel Martin, Said Mussa, Ibrahim Ajibu, Youth Rostand, Patto Ngonyani, Nadir Haroub, Andrew Vicent, Papy Tshishimbi, Amiss Tambwe na Buruan Akilimali.
michezo
2
WAKATI mzunguko wa pili wa ligi ya mpira wa wavu ikitarajia kufi ka tamati Agosti 4, timu nne za wanawake na nyingine nne za wanaume zimeingia kucheza hatua ya mtoano.Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi na Uratibu ya Chama cha Mpira wa Wavu mkoa wa Dar es Salaam (Dareva), Rogson Joseph alisema raundi ya pili inatarajiwa kumalizika Agosti 4. “Keshokutwa (kesho) zitachezwa mechi tano katika Uwanja wa Shule ya msingi ya wasichana ya Uhuru, Ilala na Agosti 4 zitachezwa mechi sita na mshindi wa kwanza hadi wa nne atacheza hatua ya mtoano,” alisema Rogson.Rogson alisema timu za wanaume ni bingwa mtetezi Tanzania Prisons, Faru, JKT na Chui na kwa upande wa wanawake ni bingwa mtetezi Tanzania Prisons, Makongo, Jeshi Stars na JKT. Timu za keshokutwa CDS itacheza na Makongo, Mjimwema itacheza a Victory Sports, Faru itacheza na Makongo, CDS na Mjimwema na kwa upande wa wanawake Mjimwema itacheza na Dar Stars.Agosti 4 JKT itacheza na Tanzania Prisons, CDS dhidi ya Victory Sports, Mjimwema itacheza na IP Sports, Tanzania Prisons itacheza na Chui na kwa upande wa wanawake, Tanzania Prisons itacheza itacheza michezo miwili dhidi ya Makongo na Mjimwema.
michezo
2
ARSENE Wenger amekiri kujisikia vibaya kutokana na mweneno mbaya wa Arsenal. Mfaransa huyo alitumia miaka 22 akiwa na the Gunners, alipoanza kibarua chake tangu mwaka 1996.Wakati akiondoka klabuni hapo mwaka 2018, Arsenal ilikuwa na mataji matatu ya Ligi Kuu ikiwemo walilolitwaa kwa kuweka rekodi ya kutopoteza mechi msimu wa mwaka 2003/04, chini yake ilitwaa makombe saba ya FA na kucheza fainali za Ligi ya Mabingwa.Masikitiko ya Wenger si kwa Arsenal pekee bali kwa soka ya England, iliyojaa mabadiliko kadhaa ya kushangaza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70 amekiri kwa namna Gunners ilivyokuwa ikicheza, ni tofauti na ilivyo sasa.Wenger alisema: “Siku hizi, kuna klabu pengine zinawazuia kuendeleza utamaduni waliokuwa nao katika kucheza.”“Nilipofika Arsenal, tulikuwa watu 80. Nilipoondoka walikuwa 750 na kunapokuwa na watu 750 kwenye kampuni moja kila mmoja anafikiria namna ya kujihudumia badala ya kusonga mbele.”“Majuto yangu kwa Arsenal ni kuondoka kwenye kiwango cha utu na kukiwa na kiasi kikubwa cha uongozi, miaka 10 unaona mchezaji mzuri, unamleta, unampa suti za michezo na anakuwa sehemu ya timu.”“Hayo yameshapita, sasa kama unamtaka mtaalamu mpya wa utimamu wa mwili, utapata maombi 300. Hivyo ndivyo ilivyo Arsenal, taratibu nilihisi klabu inaanza kuporomoka.”
michezo
2
Timu ya Taifa ya Nigeria imetwaa nafasi ya tatu katika michuano ya #Afcon2019 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya dhidi ya Tunisia usiku wa kuamkia leo.Katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Al- Salam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 kwa wakati mmoja, jijini Cairo, goli la mapema lililowekwa kimiani na Odion Ighalo katika dakika ya tatu lilitosha kabisa kuipa Eagles nafasi hiyo ya tatu.Hii ni mara ya nane kwa Nigeria kushika nafasi ya tatu katika mashindano hayo makubwa zaidi Barani Afrika. Kikosi cha tai hao wa Nigeria kiliongozwa na nahodha wao, John Obi, Mikaeli anaye kipiga katika klabu ya Trabzonspor nchini Uturuki, Odion Ighalo, Ahmed Musa, Alex Iwobi na Samueli Chukwueze.
michezo
2
Washindi hao kutoka mkoa wa Dar es Saalam ni pamoja na Luteni Kanali Mstaafu wa JWTZ, Habib Shabani Mazome, mwalimu wa shule ya sekondari ya Jitegemee, Emma Mkede Mosha na mama wa nyumbani Fatema Hussein Mawji.Akizungumza wakati wa hafla Mkurugenzi Rasilimaliwatu, Patrick Foya alisema Airtel itaendelea na kampeni yake ya kuwafurahisha wateja wake kila siku ili kubadili maisha yao.“Kila siku mtu wa Airtel anapata bahati ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kwa kununua na kujiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha vinavyokidhi mahitaji yake. Mpaka sasa tunao washindi 31 waliokwisha jishindia na promosheni bado inaendelea, bado tunayo magari mengi ya kutoa kwa wateja wetu. Natoa mwito kwa wateja na Watanzania kuendelea kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha na kupata nafasi ya kujishindia,” alisema.Akizungumza baada ya kukabidhiwa gari lake, Fatema Hussein Mawji alisema hakuamini wakati, alipoambiwa kwamba yeye ni mshindi. Alisema akiwa kama mama wa nyumbani gari litanisaidia katika shughuli zangu za sokoni, kuhudumia familia na katika shughuli za kijamii kwa ujumla.
Biashara
1
SERIKALI ya Tanzania imesema inatambua umuhimu wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (Af- CHPR) katika kuhamasisha misingi ya haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia na ndio maana imekuwa ikipeleka wanasheria wake kujibu madai mbalimbali ambayo yamekuwa yakifikishwa mahakamani hapo.Aidha Serikali imesema licha ya gharama kubwa ya kushughulikia kesi mbalimbali zinazofunguliwa na walalamikaji katika Mahakama hiyo haitaweza kudharau wito wa mahakama hiyo kwa kuwa inatambua umuhimu wake.Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa serikali anayeshughulikia Haki za Binadamu, Alecia Mbuya alisema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye ripoti za sheria pamoja na hukumu mbalimbali zilizotolewa na mahakama hiyo tangu mwaka 2006 hadi 2016.“Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizochangia kutunga sheria na maamuzi ya mahakama hii pamoja na ripoti ya kitabu hiki tunachokizindua, kwa wale mnaofatilia maendeleo ya utendaji kazi wa mahakama zaidi ya nusu ya kesi zilizofunguliwa hapa na ambazo bado zinasubiri zinatoka nchini kwetu zikiwa zimefunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi,” alisema Mbuya.Alisema pia kutokana na umuhimu wa mahakama hiyo,Tanzania ndio nchi ambayo kesi zake nyingi zilizopelekwa na watu pamoja na mashirika binafsi zimetolewa maamuzi ambayo serikali imeyaheshimu kwa kutekeleza maagizo ya Mahakama hiyo. “Hivi sasa katika mahakama hii kuna kesi zaidi ya 60 ambazo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na sasa Wakili Mkuu wa serikali imekua ikifika katika mahakama hii kutekeleza wajibu wake, ukiangalia kwa karibu gharama za kushughulikia kesi hizi ni kubwa sana jambo ambalo hatukua nalo hapo awali, lakini hatutaweza kuacha,” alisema Mbuya.Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Ben Kioko alisema uzinduzi wa ripoti ya kisheria utasaidia nchi wanachama kusoma hukumu ambazo zimetolewa tangu uhai wa mahakama hiyo ambayo ilianza kufanya kazi nchini Ethiopia kabla ya kuamishiwa jijini Arusha mwaka 2006.
Kitaifa
0
CHAMA cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) tawi la Namanga, kimemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aingilie kati mgogoro kati yake na Wakala wa Vipimo (WMA) unaowalazimisha kulipia tozo mpya kwa kila bidhaa, badala ya kutumia utaratibu wa awali wa kulipia tozo kwa mzigo wote.Aidha, TAFFA imesema haipo tayari kufanya kazi na wakala huo hadi hapo utakapowaonesha sheria hiyo mpya inayowalazimisha kuitekeleza bila kuwepo kwa makubaliano yoyote, kitendo wanachodai kuwa kinawaumiza. Walitoa msimamo huo jana kwenye kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wao, Ismail Lukas, kilichofanyika Namanga, wilayani Longido.Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, walikuwa wakitumia sheria ya zamani ya mwaka 2016 ambayo walikuwa wakilipia asilimia 0.2 ya thamani ya mzigo ambapo kiwango cha chini cha malipo kilikuwa Sh 100,000 kwa mzigo. Alisema wanachopinga ni WMA kuamua kuwatoza malipo ya Sh 100,000 kwa kila aina ya bidhaa badala ya mzigo mzima kama sheria inavyoelekeza.“Tunamuomba Waziri Mkuu aje Namanga kuzungumza na sisi juu ya huu mgogoro kwani tukiendelea na utaratibu huu tutakosa wafanyabiashara. Hakuna mtu aliye tayari kupata hasara kwa sababu jinsi tunavyopandishiwa gharama za tozo ndivyo hivyo hivyo bei za bidhaa zitakavyopanda,”alisema Mwenyekiti huyo.Meneja wa tawi wa kampuni ya EDPAC, Wilson Mkanza alisema kwa sasa hawapo tayari tena kufanya shughuli yoyote bila kupata muongozo wa sheria mpya inayowalazimu wao kutumia utaratibu mpya wa kulipa tozo ya Sh 100,000 kwa kila bidhaa badala ya mzigo kama utaratibu wa awali.Alisema walipokea barua Mei 15, mwaka huu ya ufafanuzi wa kanuni ya ada za ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi kutoka kwa Kaimu Meneja wa WMA mkoa, Dismas Maturine.Alieleza kuwa barua hiyo iliwataka kulipia bidhaa moja moja badala ya kutozwa kwa mzigo mzima, kama ilivyokuwa awali bila kushirikishwa chochote kabla ya kupewa barua hiyo. Janeth Mero kutoka kampuni ya Beam Tanzania Limited, alisema uwepo wa utaratibu huo wa kulipa kwa kwa bidhaa moja moja unatengeneza mazingira ya rushwa, hivyo kuwataka kuendelea na utaratibu uliokuwepo wa awali ili walipe bila migogoro yoyote.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi kutoka WMA makao makuu, Stella Kahwa, alisema ameyapokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyia kazi. Alisema utaratibu utakaoendelea kutumika ni ule uliokuwa ukitumika awali.
Kitaifa
0
WATENDAJI wa mifuko ya hifadhi ya jamii wametakiwa kuhakikisha wanatii na kutekeleza kwa ufanisi maagizo ya Rais John Magufuli aliyotoa kuhusu wastaafu.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa agizo hilo wakati alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mjini hapa.Waziri Jenista alitaja maagizo hayo kuwa ni pamoja na kuendelea kutumia vikokotoo vya zamani vya mafao kwa kila mfuko na kuhakiki kikamilifu wastaafu wote ili kujiridhisha kuwa hakuna wastaafu hewa.Akiwa katika siku yake ya kwanza kutembelea mikoa yote nchini kuona iwapo maagizo hayo ya Rais Magufuli yanatekelezwa ipasavyo, Mhagama pia ameagiza watendaji wa mifuko hiyo kuhakikisha wanaachana na miradi isiyo na tija na kuzingatia kubana matumizi yasiyo ya lazima.Alisema kuwa jukumu kuu la Wizara hiyo ni kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali ili kufikia matarajio na malengo ya Rais Magufuli huku akitoa ujumbe kwa watumishi wote wasiotaka kuendana na kasi hiyo kuondoka kwa hiyari."Tunahitaji watumishi waadilifu na walio na weledi, hivyo watumishi wanaoenda kinyume na matakwa yetu ni vizuri wakajiondoa wenyewe mapema badala ya kusubiri kuondolewa kwa aibu," alionya .Aliupongeza uongozi wa PSSSF kwa kuendesha uhakiki kwa kiwango cha hali ya juu jambo ambalo pia liliungwa mkono na wateja mbali mbali aliowakuta ofisini hapo ambao hawakuficha furaha yao kwa kitendo cha Rais Magufuli kurejesha kikokotoo cha zamani.Hata hivyo, waziri hakuridhishwa na utendaji kazi wa NSSF katika kushughulikia wateja wao, hasa kwenye suala la fao la kujitoa, ambapo mmoja wa wateja alilalamika mbele yake uwa inamchukua muda mrefu kupata malipo yake.Awali, Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa alimwambia waziri kuwa mteja wao huchukua siku 14 kupata hundi yake baada ya kutimiza masharti yote yaliyowekwa na mfuko huo.Kwa mujibu wa taarifa aliyopewa waziri, PSSSF mkoa wa Singida una wateja 122,000 wakati NSSF ina zaidi ya wateja 18,000 .
Kitaifa
0
['Tottenham imemtambua meneja wa England Gareth Southgate kama anayepigiwa upatu kuichukua nafasi ya Mauricio Pochettino. (Star Sunday)', 'Wachezaji wa Spurs wameanza kuamini kuwa meneja Pochettino hivi karibuni ataondoka katika klabu hiyo, huku Manchester United ikiwa ndio klabu anayovutiwa nayo. (Sun on Sunday)', 'Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho anajitayarsha kurudi Real Madrid, huku rais Florentino Perez akimpanga raia huyo wa Ureno kuichukua nafasi ya Zinedine Zidane. (Sunday Times)', 'Liverpool inataka kumsajili mchezaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 David Neres kutoka Ajax. (Calciomercato)', 'Liverpool inahofia huenda meneja Jurgen Klopp akavutiwa na wadhifa wa kuwa kocha wa Ujerumani baada ya kumalizika kwa kipindi cha uhudumu cha Low. (Sunday Mirror)', 'West Ham ipo tayari kuweka thamani ya £100m kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya England Declan Rice ili kuilemaza Manchester United katika jitihada zake za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa miaka. (Sunday Express)', 'Barcelona ipo tayari kufufua azimio lake la kumfukuzia winga wa Chelsea Willian mwenye umri wa miaka 31. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Brazil unakamilika mwishoni mwa msimu. (Mundo Deportivo)', 'Meneja Pep Guardiola anasema Manchester City haitonunua wachezaji wowote mwezi Januari kwasababu klabu hiyo haina pesa. (Sky Sports)', 'Manchester City inataka kumsajili beki wa kati wa Leicester City mwenye umri wa miaka 23-Caglar Soyuncu. (Fotospor kupitia Metro) ', 'Manchester City imempatia ocha wa Uholanzi Giovanni van ¬Bronckhorst jukumu la ndani ya klabu wakati ikijitayarisha kwa siku ambayo Guardiola hatakuweko. (Sunday Mirror)', 'Wakal wa mlinzi wa Manchester United Victor Lindelof, mwenye umri wa miaka 25, anasema mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Sweden alifukuziwa na Barcelona wakati wa majira ya joto. (Sport Bladet kupitia Manchester Evening News)', 'Uamuzi wa beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt kuhamia Juventus msimu huu wa joto ulitokana na hatua ya Barcelona kumfukuzia Lindelof. (Sunday Express)', 'Manchester United itaitisha £20m kwa kipa wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 wa England Dean Henderson, mwenye umri wa miaka 22, anayeichezea Sheffield United kwa mkopo, mwishoni mwa msimu. (Sun on Sunday)', 'Meneja wa Chelsea Frank Lampard ianaongoza jitihada za kutaka kumsajili mshambuliaji anayepigiwa upatu mwenye umri wa miaka 17 wa Wigan Joe Gelhardt. (Sunday Express)', 'Kocha wa Kipa wa Uhispania David de Gea, Emilio Alvarez ameondoka Manchester United baada ya kushuka kwa kiwango cha mchezaji huyo wa mwenye miaka 28 msimu uliopita, hatua iliozusha maswali kuhusu mbinu anazotumia. (Mail on Sunday)', 'Barcelona haina raha na mchezaji wa kiungo cha kati Arthur, mweny umri wa miaka 23, baada ya kujivinjari usiku kucha na mshambuliaji wa Paris St-Germain na raia mwenzake wa Brazil, Neymar. (Marca)', 'Meneja wa Juventus Maurizio Sarri ana hamu ya kumrudisha upya mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Emre Can, mwenye umri wa miaka 25, katika timu yake baada ya Mjerumani huyo kushindwa kuhamia PSG wakati wa majira ya joto. (Le10sport)', 'Ajax inatarajia kufikia makubaliano ya mkataba ulioimarika na mchezaji wanayemlenga wa Real Madrid, Donny van de Beek katika jitihada ya kufukuza klabu kuvutiwa na mchezaji huyo wa miaka 22 raia wa Uholanzi. (Voetbal International)']
michezo
2
BAADHI ya wachezaji wa Simba wametuma ujumbe wakionesha mipango yao ya kuingamiza AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa Agosti 8, mwaka huu.Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha tamasha la Simba Day linalofanyika Agosti 8 ya kila mwaka.Simba hutumia tamasha hilo kutambulisha wachezaji wake, benchi la ufundi na jezi itakazotumia kwa msimu mzima.Kwenye jumbe mbalimbali walizotuma baadhi ya wachezaji hao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wanawataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwani wamejipanga vizuri kwa mechi yoyote mbele yao kuhakikisha wanafanya vizuri.“Tuko poa tumejiandaa vizuri dhidi ya msimu mpya na tamasha la Simba, tuko tayari kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri siku hiyo na naomba mashabiki wajitokeze kwasababu tutaingia uwanjani kibingwa zaidi,” mshambuliaji Emmanuel Okwi.“Tupo na kocha wetu anatuelekeza nini cha kufanya tunaamini mambo yatakwenda vizuri siku hiyo,” alisema.Beki Mohamed Hussein alisema wapinzani watapata tabu sana kwani jinsi walivyojiandaa wana nafasi ya kufanya vizuri.“Yeyote tutakayekutana naye atapata tabu siku hiyo kikubwa ni mashabiki wetu wajitokeze na kuona namna tulivyojipanga kwa msimu mpya,” alisema.Kwa upande wake, James Kotei alisema “matendo yataonekana uwanjani kwani maandalizi waliyofanya ni mazuri kufanya kazi siku ya tamasha”. Naye mshambuliaji mpya wa Simba, Adam Salamba alisema:“Tunajiandaa vizuri huku Uturuki, napenda kuwaambia mashabiki wetu wa Simba tunajiandaa vizuri huku nchini Uturuki, tunampa mwalimu wetu ushirikiano wa kutosha, niwatake mashabiki wetu terehe 8 mwezi wa nane wahudhurie kwa wingi… Simba kibingwa zaidi.”Simba ipo Uturuki ikiendelea na mazoezi ya kujifua ambapo leo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki kujipima kisha itaendelea na mazoezi hadi Agosti 5, itakaporejea tayari kukipiga na AFC Leopards ya Kenya.
michezo
2
Serikali imekusanya mapato ya jumla ya bilioni 93.6/- tangu uanze kutumika mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) mwaka 2014.Haya yamesemwa na Rais John Magufuli kwenye hafla ya makabidhiano ya mfumo huo kutoka kwa mkandarasi wake kwenda kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo, mapema leo, Ijumaa, jijini Dar es Salaam.Rais Magufuli alieleza kuwa fedha hizo zimekusanywa baada ya kupungua kwa kiwango cha udanganyifu kwenye simu za kimataifa, kutoka 65% hadi 10% kutokana na mfuo huo wa TTMS.“Kati ya bilioni 93.6/ iliyokusanywa na serikali kupitia TTMS, bilioni 82.2/- zimewekwa Hazina, huku bilioni 11.4/- zikipelekwa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) na kampuni za kutoa huduma pia zikipata bilioni 173/-,” alisema.Rais Magufuli ameongeza kwamba mfumo huu utakuwa na manufaa makubwa katika kusimamia ubora na takwimu sahihi za mawasiliano, kubaini mawasiliano ya simu za kimataifa zinazofanyika kwa njia za udanganyifu, pamoja na kufuatilia miamala ya kifedha inayofanyika kimtandao.Tofauti na hayo, manufaa mengine ni pamoja na mfumo huo kutambua namba za utambulishi za simu za kiganjani yaani IMEI, kuhakikisha vifaa vyote vilivyounganishwa na mitandao ya watoa huduma, vinakidhi viwango vya kimataifa, pamoja na kuhakiki mapato yanayotokana na mawasiliano ya simu.
Kitaifa
0
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda ameipongeza kampuni inayojihusisha na utoaji wa huduma za msimbomilia (barcodes) GS 1 Tanzania kwa kuwezesha bidhaa nchini kutambulika kimataifa na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kwa taasisi zote zinasimamia ubora na viwango wa bidhaa nchini.Katika hatua nyingine, Kakunda amepongeza makubaliano yaliyoingiwa baina ya kampuni hiyo na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo ambayo yatawezesha kupeleka elimu ya msimbomilia kwa wananchi.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya kampuni hiyo pamoja na utiaji saini wa makubalino na TSN, Waziri Kakunda alisema kuanzishwa kwa Kampuni ya GS 1 Tanzania kumesaidia kuleta mafanikio makubwa kwa Taifa hususani katika jumuiya ya wafanyabiashara.Alisema awali kabla ya ujio wa kampuni hiyo, wafanyabiashara walilazimika kwenda hadi nje ya nchi hususani katika mataifa ya Kenya, Afrika Kusini na Ubelgiji ili kupata huduma hiyo, suala alilosema kuwa lilikuwa likiwasababishia usumbufu kwa kiwango kikubwa.Alisema pamoja na changamoto iliyokuwa ikiwakuta wao na bidhaa wanazozizalisha kukosa kutambulika katika mifumo ya kimataifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), pia ilichangia kutokukua kwa makampuni madogo na ya kati hatua iliyosababisha bidhaa zinazozalishwa na kampuni hizo kushindwa kuingia katika maduka makubwa ya kisasa sanjari na serikali kukosa mapato.“Ni jambo la kujivunia kwa sasa kuona Tanzania ni miongoni mwa nchi Barani Afrika iliyoingia katika utaratibu huu wa Barcodes na kuungana na nchi zingine za Algeria, Misri, Ivory Coast, Kenya, Libya, Mauritius, Morocco, Nigeria na Afrika Kusini, hatua hii ni muhimu kwa maendeleo katika Sekta ya Biashara na Taifa kwa ujumla,” alisema Kakunda.Pia aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali nchini kote kuhakikisha wanaongeza thamani kwa kusajili bidhaa zao na huduma hiyo ili kujitanua kimataifa sambamba na kujiongezea kipato.Kuhusu ushirikiano na wa GS 1 na TSN, Waziri Kakunda alisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa itasaidia kuwasambazia elimu wananchi nchini kote juu ya umuhimu wa kuwa na alama za msimbomilia katika bidhaa zao tofauti na ilivyo sasa ambapo wananchi wengi bado hawana uelewa juu ya suala hilo.
Biashara
1
Jumatano Yanga itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo ambao kocha huyo ameahidi kuchukua pointi zote tatu kutokana na maandalizi wanayoyafanya hivi sasa.Akizungumza na gazeti hili Lwandamina, alisema michuano ya Mapinduzi imemsaidia kuongeza ushindani wa kujituma uwanjani kwa wachezaji wake hicho ndicho kitu ambacho alikuwa anakitaka akiamini kila atakayepata nafasi atakuwa akicheza kwa bidii kuhakikisha anaendelea kucheza kikosi cha kwanza.“Yanga hii haitegemei ukubwa wa jina, mchezaji ambaye ataonesha kujituma mazoezini ndiye atakayecheza mechi hata kule kwenye Kombe la Mapinduzi makocha waliopo ndiyo wametumia mfumo huo na mafanikio yameonekana,” alisema Lwandamina.Mzambia huyo alisema wanakwenda kuivaa Mwadui akijivunia maandalizi waliyofanya na ushindi kwao ni kitu cha muhimu kutokana na nafasi waliyopo hivi sasa, ambayo haiwaruhusu kuendelea kupoteza hata pointi moja.Yanga imeshuka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, kutokana na ushindi wa timu ya Mtibwa Sugar ambayo sasa imepanda hadi nafasi ya nne ilipocheza na Lipuli ya Iringa na kushinda bao 1-0.
michezo
2
KIWANDA cha kukamua mafuta ya kula kinachojengwa jijini Dodoma, kinatarajia kuanza uzalishaji Juni mwaka huu.Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alipozungumzia mikakati ya serikali ya kuhakikisha mafuta ya kula yanapatikana nchini. Hasunga alisema hatua hiyo ni katika kuondokana na uagizwaji wa mafuta ya kula nje ya nchi, ambao umekuwa ukiigharimu serikali na pia kuzalisha masoko ya mazao nchini. “Kutokana na mahitaji makubwa ya mafuta ya kula, na nchi kutumia fedha nyingi kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi, serikali imeweka mikakati ya kutosha ikiwa ni pamoja na kujenga kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti jijini Dodoma,” alisema waziri huyo.Alisema kwa sasa serikali imekuwa ikitumia zaidi ya Sh bilioni 400 kwa mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi. Hasunga alisema ili kufikia azma hiyo, serikali imeamua kuweka mkazo kwenye uzalishaji wa mazao ambayo yatumika kuzalisha mafuta nchini yakiwemo uzalishaji wa tija wa mbegu za alizeti, michikichi na karanga. “Kwa hiyo tumeamua kuweka mkazo kwenye uzalishaji wa baadhi ya madhao ambayo yatatumika katika kutengeneza mafuta ya kula hapa nchini na baadhi yake ni mbegu alizeti, michikichi na karanga na mengineyo.“Katika kuhakikisha hilo linatekelezeka, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko tumeiwezesha ili wajenge kiwanda cha kuchakata mafuta hapa Dodoma. Mitambo imeshafika tunakusudia kuwa ifikapo mwezi Juni kiwe kimesimama na kimanza uzalishaji,” alisema Hasunga.Alisema pia kutokana na mahindi kutumika kuzalisha unga na kutoa mafuta, serikali inakusudia kujenga kinu kingine Dodoma, ambacho mbali na kuchakana unga wa kutosha, pia kitatengeneza vyakula vya mifugo. “Tuna imani kwa jitihada hizi sasa tutakuwa tumetengeneza na kupata masoko vizuri na uhakika kwa mazao yanayozalishwa na wakulima wetu,” alieleza. Alisema kukamilika kwa kiwanda hicho, kutatoa fursa zaidi ya ajira kwa Watanzania kwani kitaajiri zaidi ya Watanzania 250.
Kitaifa
0
KOCH A wa timu ya taifa ya Rwanda, Vincent Mashanmi ana matumaini Amavubi bado inaweza kufuzu kwa fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019 licha ya kuanza vibaya kampeni zake katika hatua ya makundi.Kimsimamo, Amavubi wako mkiani mwa Kundi H, ikiwa haina pointi yoyote, baada ya kucheza mechi mbili. Kwa upande mwingine, G uinea, ambayo Amavubi itakabiliana nayo baadae mwezi huu, inaoongoza katika msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi zote mbili za mwanzo. Timu za taifa za Ivory Coast pamoja na ile ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) iko katika nafasi ya pili na tatu, kila moja ikiwa na pointi tatu.Kufuatia kutangaza kikosi cha awali cha wachezaji 27 wiki iliyopita kwa ajili ya kupambana dhidi ya vinara G uinea, Mashami amewataka wachezaji wake kuchukulia kwa umakini mkubwa na kuhakikisha wanashinda mechi mbili dhidi ya timu hiyo ya Afrika Magharibi. Alisema kuwa ushindi dhidi ya G uinea itaiwezesha timu yake kurejesha matumaini ya kufuzu kwa fainali hizo za Afcon 2019 nchini Cameroon.“Tumeita karibu wachezaji wote waliounda kikosi kilichocheza dhidi ya Ivory Coast, na ninaamini kuwa wachezaji tuliowaita watakamilisha lengo letu la kupata ushindi katika mechi zote zilizobaki za hatua ya makundi, tukianzia na mbili dhidi ya G uinea,”alisema Mashami. Timu hiyo ya taifa ya G uinea itaikaribisha Amavubi katika mchezo wa kwanza utakaofanyika O ktoba 12 jijini Conakry, kabla hawajarudiana katika mchezo itakaofanyika jijini hapa kwenye Uwanja wa Kigali O ktoba 16.Kocha huyo wazamani wa APR ameita wachezaji watatu wapya katika kikosi hicho akiwemo kipa wa Rayon Sports, Abouba Bashunga na kiungo Djabel Manishimwe pamoja na mshambuliaji Jacqu es Tuyisenge anayeichezea G or Mahia ya Kenya. Mshambuliaji huyo alikosa mchezo dhidi ya Ivory Coast kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu wakati akiiwakilisha klabu yake katika Kombe la Shirikisho.“Bado tuna nafasi ya kufuzu kwa fainali za Afcon, lakini nafasi hizo zitakuwepo endapo tu tutashinda mechi zetu mbili zijazo dhidi ya G uinea, na ndio maana nimewaomba wachezaji kupambana ili kuondoka na pointi zote,,,, “alibainisha kocha huyo. Kocha huyo wazamani wa APR na Bugesera F C alielezea zaidi kuwa Bashunga na Manishimwe walifanya kazi kubwa na kufanikiwa kupata nafasi katika timu ya taifa ya Rwanda. Kikosi cha Rwanda ikitarajia kuanza kambi jana Jumatatu na kitaondoka nchini O ktoba 8 kwenda G uinea.
michezo
2
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inaanza kazi maalumu ya kuwapanga wafanyabiashara ndogo katika maeneo ambayo yamewekwa rasmi kwa biashara yakiwemo masoko ya Jiji.Pia wafanyabiashara hao wametakiwa kutofanya biashara zao sehemu zisizo rasmi na badala yake wafuate sheria na kanuni kwa kufanya shughuli zao katika maeneo yaliyoruhusiswa.Akizungumza na waandishi wa habari, mwishoni mwa wiki Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna alisema halmashauri ya Jiji ina maeneo rasmi yaliyopangwa kwa ajili ya biashara na si barabarani.“Kwa jitihada kubwa zinazofanywa na halmashauri, hivi sasa yapo maeneo mengi rafiki kwa shughuli za kufanya biashara ikiwepo kwenye masoko kama vile Bonanza, Soko Kuu la Majengo, Sabasaba, Chang’ombe na soko maalumu la jioni la Nyerere Square,” amesema.Yuna alisema ni vema masoko hayo yakatumika kwa wafanyabiashara hao badala ya kuzagaa mitaani na barabarani ambako wanaweza kusababisha ajali na watembea kwa miguu kukosa uhuru.Pia alisema ufanyaji biashara wa hovyo huchangia jiji kuwa chafu. Aidha, Yuna aliwataka wafanyabiashara hao kuzingatia maelekezo sahihi ya halmashauri ya Jiji ili biashara zao ziwe na tija kiuchumi kwao binafsi na Jiji pia.
Kitaifa
0
['Mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi cha Manchester United Paul Pogba amegoma kuongea na waandishi baada ya timu yake kuifunga Perth Glory ta Australia 2-0.', 'Mchezo huo ni wa kwanza kwa United katika kampeniyake ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.', 'Magoli ya ipindi cha pili kutoka kwa Marcus Rashford na James Garner yalitosha kwa Man United kutoka na vicheko kwenye uwanja wa Optus nchini Australia. ', 'Pogba alitoa pasi iliyozaa goli la Rashford.', 'Huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Pogba akiwa na United toka alipotangaza nia yake ya kutaka kuondoka kwenye kikosi hicho. ', 'Nia hiyo ya Pogba imesharejelewa mara mbili na wakala wake Mino Raiola katika siku za hivi karibuni. ', 'Kiungo huyo aligoma kuongea na maripota baada ya mchezo akisema "hakuna haja" ya kufanya hivyo. ', 'Vilabu vya Real Madrid na Juventus vinaripotiwa kutaka kumsajili kiungo huyo Mfaransa mwenye miaka 26 japo hakuna kati yao ambaye amepeleka maombi rasmi ya kutaka kumnunua.', 'United inaaminika itataka kulipwa pauni milioni 150 ili kumuachia Pogba aende zake. ', 'Pogba hakupewa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo huo na kuvaliwa na Juan Mata, japo kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer alisema kabla kuwa mchezaji huyo anaweza kupewa majukumu ya unahodha msimu huu. ', '"Sidhani kama jambo hilo linahitaji kutolewa maelezo, tutalijadili baadae," alisema Solskjaer alipoulizwa kuhusu hatima ya unahodha kwa Pogba. ', 'Kuhusu uhamisho, Solskjaer amesema kuwa klabu hiyo haijapokea ofa yoyote ya wanaomtaka Pogba ama mshambuliaji wa Ubelgiji Romelo Lukaku, "tusubiri kuona msimu utakavyoanaza," alisisitiza Solkjaer. ', "Pogba alisema mwezi Juni kuwa ''sasa inaweza kuwa muda mzuri wa kuhamia sehemu nyingine''.", 'Ni dhahiri kuwa si Solskjaer wala uongozi wa Man United unaotaka mchezaji huyo nyota kuondoka Old Trafford katika dirisha hili la usajili la majira ya joto. ', 'Wiki iliyopita, wakala wa mchezaji huyo Raiola aliliambia gazeti la The times kuwa mchezaji wake anataka kuondoka, na klabu hiyo inajua fika nia ya mteja wake. ', '"Mchezaji (Pogba) hakufanya kosa lolote," Raiola aliuambia mtandao wa Talksport.', '"Amekuwa na heshima na weledi. Klabu imekuwa ikijua hisia zake kwa muda mrefu.', '"Ni aibu kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kukosoa bila ya kuwa na taarifa sahihi, na ninasikitishwa kuwa klabu haichukui hatua yoyote kwa wanaofanya hivyo."', 'Hata hivyo, kocha Solskjaer anaamini kuna ajenda dhidi ya mchezaji huyo. ', "''Ni ajenda dhidi ya Paul, ni mchezaji mzuri, mzuri sana, hakujawahi kuwa na shida, ana moyo wa dhahabu,'' alisema kocha huyo.", "''Paul hakuwahi kujiweka nje ya timu, mara zote amekuwa akitoa mchango wake mzuri na siwezi kuripoti chochote , isipokuwa maneni ya mawakala ya wakati wote.", "''Siwezi kukaa hapa kumzungumzia Paul na kila wanachokisema mawakala, tuna miaka michache iliyobaki kwenye mkataba wake na ni mchezaji mzuri.''"]
michezo
2
KAIMU Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema umefika wakati wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuweka mapenzi kwa timu na sio mchezaji mmoja mmoja.Kauli ya kiongozi huyo imekuja kutokana na utamaduni uliojengeka kwa wanachama kumpenda mchezaji mmoja hivyo, asipokuwepo kwenye timu wanaanzisha minong’ono.Akizungumzia suala hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu Haruna Niyonzima kutokuwepo kwenye kikosi kilichotambulishwa, alisema wachezaji wote wana umuhimu, kama mmoja hayupo bado ataendelea kubaki mchezaji wa klabu.“Wote ni wachezaji wa klabu, hatupaswi kumtizama mtu mmoja kama hayupo timu itaendelea kucheza, tuipende klabu na sio kuangalia labda fulani hayupo ndio basi,” alisema.Kwenye tamasha la Simba Day juzi, walitambulisha kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu huku jina la Niyonzima likiwa halijatajwa.Mchezaji huyo wa Rwanda hajatokea tangu timu hiyo ilipoanza mazoezi ya kujifua Uturuki na haijulikani alipo licha ya viongozi wa klabu hiyo kumtaka mapema kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya ligi.Kikosi kilichotangazwa juzi ni Ally Salum, Abdul Suleimani, Rashid Juma, Paul Bukaba, Mohamed Hussein, Said Ndemla, Shomari Kapombe, Muzamiru Yassin, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Nicholas Gyan.Wengine ni Mohamed Ibrahim, James Kotei, Yusuph Mlipili, Asante Kwasi, Aishi Manula, Deogratius Munishi, Marcel Kaheza, Adam Salamba, Shiza Kichuya, Hassan Dilunga, Paschal Wawa, Mohamed Rashid, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Cletus Chama na John Bocco.
michezo
2
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Ibrahim Kombo, alisema mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Dodoma.Alisema zawadi za kushindaniwa katika shindano hilo ni televisheni moja ya nchi 32, simu aina ya tab galaxy, kamera 3, home theatre, microwave tatu na simu moja aina ya galaxy grand.“Leo hii (jana) tayari tumepata washindi 10 wa mwezi Mei, ambao walishinda zawadi hizo kupitia droo iliyochezeshwa ya E-warranty (dhamana), lengo likiwa ni kuwasisitizia Watanzania kutambua na kuthamini bidhaa zenye viwango na si bidhaa feki,” alisisitiza.Alisema kampuni hiyo imeanzisha mfumo wa kutoa dhamana ya miezi 24 kwa bidhaa za simu na bidhaa zake nyingine ili kumsaidia mteja ili kuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa aliyonunua.
Biashara
1
["Mshindi mara mbili wa michuano ya Olimpiki Caster Semenya amesema ''hajawahi kuhisi kuungwa mkono'' na wanawake wengine kwenye michezo.", 'Mshindi mara tatu wa mbio za mita 800 hatatetea taji lake mjini Doha mwezi Septemba baada ya kugonga mwamba mahakamani kuhusu kutumia dawa za kupunguza homoni za testosterone kwa wakimbiaji wa kike.', "''Wananilenga kwasababu hawaniwezi,'' alisema mwanadada huyo mwenye miaka 28.", "''Tangu nilipokuwa mwanamichezo, sikuwahi kwa kweli kujihisi kuungwa mkono, sikuwahi kuhisi kutambuliwa na wanawake.''", "Akizungumza katika mkutano wa wanawake mjini Johannesburg, Semenya aliongeza: ''Ninafikiri", 'Semenya amepinga sheria mpya za mashirikisho ya mchezo wa riadha kuwa yeye na wengine kama yeye wenye kiwango kikubwa cha homoni kutumia dawa za kupunguza ili kuweza kushindana kuanzia mbio za mita 400 mpaka maili moja, au kubadili mbio watakazoshiriki.', 'Semenya kukosa mashindano ya ubingwa duniani ', 'Castor Semenya: Kwanini kesi yake ni muhimu', 'Semenya ashinda dhahabu mbio za 800m London', 'Semenya alikata rufaa mara mbili dhidi ya sheria zashirikisho la mchezo wa riadha IAAF zinazomzuia kukimbia bila kutumia dawa.', "Kuhusu kile kinachoelezwa kutokuungwa mkono na wakimbiaji wenzie wa kike, Semenya ameongeza: ''Mimi ninafanya vizuri sana.Ukifanya vizuri duniani watu husumbuka na kutokana na unachokifanya''.", "''Labda mimi ni tatizo kwasababu nina mafanikio makubwa kupitiliza hivyo , hivyo watu wanakuwa kama wanataka kukushughulikia.'' ", "''Yeyote atakayenizuia kukimbia anapaswa kuniondoa kwenye mstari wa kukimbia. Sina cha zaidi cha kusema kuhusu suala hili. Ninachoweza kusema ni kwamba nipo kwenye kiwango cha juu.''"]
michezo
2
KOCHA wa muda wa timu ya Alliance FC, Daddy Gilbert amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana.Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Martin Kigii katika dakika ya 90 baada ya kuunganisha vyema pasi ya Godlove Mdumule.Ushindi huo umeipandisha Alliance FC mpaka nafasi ya 17 ikiwa na alama 10 baada ya michezo 13. Daddy Alisema timu yake ilicheza vyema na ilifanikiwa kutawala mchezo huo katika vipindi vyote.Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha wanashinda michezo yote ya ligi iliyopo mbele yao.Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Mwanza wajitokezee kwa wingi katika kusapoti timu hiyo, ambayo inashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza.Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliochezwa mkoani Mara juzi katika Uwanja wa CCM Karume, wenyeji Biashara United walilazimisha sare ya bila kufungana na Mbao FC.Kocha wa msaidizi wa Biashara United, Omary Madenge alisema timu yake ilicheza vizuri lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizotengeneza.Kocha Mkuu wa Mbao FC, Amri Saidi `Stam’ alisema atajipanga upya ili timu yake ipate ushindi dhidi ya timu ya Ndanda FC katika mchezo wao ujao.
michezo
2
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samata amesema watapambana na Algeria na Senegal kwa lengo la kujiinua kisoka.Samata ameyasema hayo siku chache baada ya droo ya fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ kupangwa na Tanzania kuwekwa kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya. Fainali hizo zitafanyika Misri kuanzia Juni 21 mpaka Julai 19 mwaka huu.Akizungumzia droo hiyo, Samata alisema Senegal na Algeria ni timu ngumu katika kundi lao lakini watapambana ili washinde waweze kuinua soka la nchi.“Algeria na Senegal wamepiga hatua katika soka miaka mingi, hivyo ni lazima tuwaheshimu lakini ni lazima tupambane kuonesha tunakwenda walipo na tuna uchu wa kufika huko,” alisema Samata.Pia Samata amesema wanaiheshimu Kenya kwa sababu ni majirani ila hawajaipita Tanzania.“Tunawaheshimu Kenya ni majirani zetu wako vizuri katika maendeleo ya soka, lakini hawajafika mbali sana kuipita Tanzania,” amesema.Aidha amesema Kundi C ni gumu, kwani linawakutanisha na timu kubwa za Afrika zilizowapita katika viwango kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kukawa na maandalizi madhubuti ili kushindana na kujaribu kupenya katika hatua ya mtoano na Tanzania inatakiwa kujiwekea malengo ya kushiriki kila fainali za AFCON kuanzia sasa.Taifa Stars ilifuzu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi nane, nyuma ya Uganda walioongoza kwa pointi 13 na kuiacha Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.
michezo
2
Wamesema hatua hiyo ya serikali imeonesha namna serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilivyo sikivu kwa wananchi inaowaongoza na ndiyo sababu ikawasikia na kukijali kilio chao.Viongozi wa waendesha boda boda hao, walitoa pongezi hizo katika kikao chao na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) Aman Kajuna aliyekutana nao ili kujua mapendekezo yao juu ya kero zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.Viongozi hao waliotokea katika wilaya mbalimbali za mkoani hapa, ikiwemo Mbeya Mjini na Mbeya Vijijini, Chunya na Rungwe waliwapongeza pia wanahabari nchini wakisema walikuwa kiunganishi kizuri kati yao na serikali wakati wakitoa kilio cha kubadili namba za usajiri. “Katika mafanikio ya jambo hili hatuwezi kuwaacha wenzetu wanahabari. Walikuwa kiunganishi baina yetu na viongozi wa serikali. Tunaamini wao wamewezesha kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa maafikiano mazuri juu ya jambo hili,” alisema mmoja wa viongozi hao, Paul Christophe kutoka Mbeya.Kwa upande wake Noah Mwakajebele kutoka Tukuyu wilayani Rungwe, alishauri maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kuutumia muda ulioongezwa kupita katika kanda za bodaboda na kutoa elimu juu ya ubadilishwaji wa namba za usajili za pikipiki sambamba na kushauriana juu ya kero zinazoleta mkanganyiko juu ya shughuli hiyo.
Biashara
1
UTAFITI uliofanywa kwa nchi nne za Afrika umetegua kitendawili cha miaka 30 baada ya kubaini kwamba uzazi wa mpango hauchangii ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa wanawake.Matokeo hayo yamepatikana baada ya kufanyika utafiti ulioshirikisha wanawake 7,829 wenye miaka 16 hadi 35 kutoka Kenya, eSwatini, Afrika Kusini na Zambia waliofanyiwa utafiti kwenye maeneo 12.Asilimia 3.81 ya wan- awake waliofanyiwa utafiti walipata maambukizi ya VVU ambao ni 397 kati ya 7829 sawa na wanawake wanne kati ya 100 hivyo hakuna jibu la mwisho kuwa njia hizo zinachangia.Matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa Alhamisi katika mkutano wa Ukimwi Afrika Kusini yalibainisha kuwa wanawake waliofanyiwa utafiti walitumia njia za uzazi wa mpango wa sindano, kitanzi na vipandikizi.Akitangaza utafiti huo wakati wa semina maalumu ya kuchambua utafiti huo nchini, mhamasishaji jamii wa virusi vya Ukimwi na afya ya uzazi, Dk Lilian Mwakyosi ulioandaliwa na Shirika la Habari la Internews Tanzania alisema maambukizi kwa wanawake hususan wasichana yamekuwa yakiongezeka kila siku.Inaelezwa kuwa kati ya watu milioni 37 wanaoishi na virusi vya Ukimwi duniani zaidi ya nusu ni wanawake huku kukiwa na takribani maambukizi mapya 600,000 kila mwaka kwa wanawake vijana.Alisema wanawake milioni 700 wanatumia njia za uzazi wa mpango duniani kati yao milioni 58 kutoka Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Miaka 30 maambukizi ya VVU kwa wanawake yameongezeka.Alisema utafiti wa Desemba 2015 hadi Oktoba 2018, eSwatini kituo kimoja wanawake 502, Kenya kituo kimoja wanawake 901, Afrika Kusini vituo tisa wanawake 5768 na Zambia kituo kimoja wanawake 658.Alisema wanawake 2,609 walitumia njia ya kupanga uzazi ya sindano, 2,607 kitanzi, 2,613 vipandikizi na kufuatiliwa kila mwezi kufika vituoni na kupatiwa vifaa vya kujikinga na ukimwi na matibabu bure.
Kitaifa
0
RAIS John Magufuli ameendelea kung’ara katika siasa za kimataifa mwaka huu, baada ya Taasisi ya Transparency International (TI), kuitaja Tanzania kuwa moja ya nchi zilizofanya vizuri katika masuala ya kupiga vita rushwa.Ripoti ya TI ya mwaka huu, iliyopatikana Dar es Salam juzi, imesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika vita dhidi ya rushwa kubwa na ndogo, zinazohujumu uchumi na kuumiza wananchi wa kawaida wapatapo huduma.Rais Magufuli amekuwa kinara wa mapambanodhidi ya rushwa tangu aingie madararakani mwaka 2015, ambapo Tanzania imekuwa katika vita dhidi ya uhujumu uchumi na rushwa ndogo, ambayo imekuwa kero kwa wananchi wanyonge, ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki katika taasisi za utoaji huduma, hatua ambayo imeiipandisha chati.Ripoti mpya ya TI iliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi ya Afrobarometer imedhihirisha mafanikio ya Rais Magufuli, kwa kuiweka Tanzania juu kwa upande wa nchi za Afrika (Global Corruption Barometer- Africa (GCB), ambapo TI, shirika la mapambano dhidi ya rushwa duniani, limesema mjini Berlin, Ujerumani kuwa Tanzania inaongoza kati ya nchi 35 za Afrika eneo la ‘Namna Wananchi Wanavyotambua Juhudi za Serikali Kwenye Mapambano ya Rushwa’.Matokeo Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 50 ya waliohojiwa, walisema ndiyo wananchi wa kawaida, wana nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya mafanikio kwenye mapambano dhidi ya rushwa, badala ya kuachia mzigo wote kwa serikali. Ripoti hiyo ya TI imesema takwimu hizo za asilimia 50, zimetokana na swali waliloulizwa wahojiwa kwamba:“Wananchi wa kawaida wanaweza au wana nafasi ya kuwa sehemu ya kufanikisha vita dhidi ya rushwa?”.Mkurugenzi Mtendaji wa TI, Patricia Moreira akiwasilisha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari juzi, alisema kwenye kipengele hicho, nchi tano bora zikiongozwa na Tanzania ni Sierra Leone, Lesotho, Nigeria na Ghana.Taasisi za serikali Kuhusu taasisi za serikali, TI imeonesha kuwapo mafanikio makubwa ya kupungua kwa hisia za kuwapo rushwa katika Ofisi ya Rais na Waziri Mkuu, kutoka asilimia 15 hadi nne, kwa wabunge kutoka asilimia 21 hadi nane.Pia, rushwa iliyodaiwa kuwepo kwa maofisa wa serikali kuu imeshuka kutoka asilimia 25 hadi 12, serikali za mitaa kutoka asilimia 25 hadi 10, tofauti hiyo ni kwa kulinganisha hali ya mwaka 2015 na mwaka huu 2019.Katika takwimu hizo, TI pia inaonesha hisia za kuwapo rushwa imeshuka kwa Jeshi la Polisi kutoka asilimia 50 za mwaka 2015 hadi 36 mwaka huu, majaji na mahakimu kutoka asilimia 36 hadi 21, viongozi wa dini kutoka asilimia 10 hadi tatu, asasi zisizo za kiserikali (NGOs) kutoka sifuri hadi 11, taasisi za biashara ikiongezeka hisia asilimia 31 hadi 32 na viongozi wa kimila asilimia 13 hadi tatu, ukilinganisha takwimu za mwaka 2015 na mwaka huu.Hali ya rushwa katika utoaji huduma Ripoti hiyo ya TI inaonesha mafanikio zaidi ya vita ya rushwa ambapo rushwa imeshuka kutoka asilimia 25 ya mwaka 2015 hadi asilimia 18 ya mwaka huu, shule za umma imeshuka kutoka asilimia 11 hadi asilimia nne, huduma za afya imeshuka kutoka asilimia 20 hadi 11 na Polisi kutoka asilimia 35 hadi 31 kati ya mwaka 2015 na 2019.Kuhusu kama rushwa imepungua katika miezi 12 iliyopita au la, ripoti imesema asilimia 66 walisema iliongezeka mwaka 2015 lakini ni asilimia 10 tu waliosema imeongezeka mwaka huu, waliosema imepungua ni 13 mwaka 2015 huku asilimia 72 wakiamini imepungua.Waliosema kiwango ni kile kile ni asilimia 15 mwaka 2015 na asilimia tisa mwaka huu, waliosema hawajui ni asilimia 6 mwaka 2015 na asilimia tisa 2019 na hakuna waliokataa kujibu.Mapambano ya rushwa Ikizungumzia swali kama serikali inafanya kazi nzuri kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ripoti hiyo ya TI imeonesha mwaka 2015 waliosema inafanya vizuri walikuwa ni asilimia 37 wakati mwaka huu ni asilimia 71, waliosema serikali haifanyi vizuri mwaka 2015 ni asilimia 58 wakati mwaka huu wamepungua hadi asilimia 23 na waliosema sijui, mwaka 2015 ni asilimia tano na mwaka huu ni asilimia sita na hakuna aliyekataa kujibu maswali. Ripoti inaonesha asilimia 18 ya waliohojiwa, wanakiri mtu alikuwa lazima atoe rushwa kupata huduma ya kijamii.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania ya sasa ikilinganishwa na mwaka 2015, imepiga hatua kubwa udhibiti wa vitendo vya rushwa kwenye maeneo ya kutolea huduma za umma kutoka asilimia 25 hadi kufikia asilimia 18.Mafanikio siku za nyuma Mafanikio hayo yametajwa kuwa yametokea mwaka mmoja tangu ripoti nyingine ya TI iliyotathmini mapambano dhidi ya rushwa (Corruption Perception Index) ilipotolewa, ikionyesha Rwanda na Tanzania kuongoza katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2017.Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa na TI Februari 21, mwaka 2018 , juhudi za Serikali ya Rais Magufuli kupambana na rushwa, zimezaa matunda kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Taarifa hiyo iliyokusanya takwimu za mwaka mzima wa 2017, ilionesha Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani, zilizopanda kwa kiasi kikubwa katika kupambana na rushwa huku nyingi zikishuka au kubaki pale pale.Wakati mwaka 2016 Tanzania ilikuwa ya 116 duniani, katika ripoti ya mwaka jana, Tanzania ilipanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 103 huku ikizizidi kwa mbali nchi kadhaa kubwa duniani katika utafiti huo, uliohusisha nchi 180.Kwa Afrika Mashariki, Tanzania ilikuwa nchi ya pili baada ya Rwanda iliyoongoza kwa kupunguza rushwa, ambapo katika alama za mtazamo wa rushwa, Tanzania imepata 36, zikiwa ni nyingi kufikiwa na nchi miaka 10 iliyopita.Takwimu hizo zilionesha Tanzania kufikia nafasi hiyo ya juu, ni matokeo ya kufanikiwa kwa serikali kuziba mianya mingi ya rushwa taasisi mbalimbali za serikali na kubadilika mtazamo wa wafanyabiashara na wawekezaji nchini.Nchi tano za mwisho Pia TI ilibainisha katika ripoti yake hiyo kuwa nchi tano za mwisho Afrika zilizotajwa kwenye ripoti hiyo ambazo bado raia wake hawaoni kama serikali zao zinaonesha juhudi zozote kupambana na vitendo vya rushwa ni Madagascar, Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Sudan, Guinea, Malawi na Morocco.Ripoti imebaini zaidi ya nusu ya watu kwenye nchi zote 35zilizoguswa na utafiti wakati wa kuandaa ripoti hiyo kati ya Septemba 2016 na Septemba 2018, wanakiri rushwa kushika mizizi katika nchi zao na serikali haifanyi kitu.Matokeo jumla Mkurugenzi huyo alisema matokeo ya jumla ya utafiti huo, yameonesha kuwa zaidi ya mtu mmoja kati ya wanne waliotumia huduma za umma kama afya na elimu Afrika, walitoa rushwa mwaka 2018 sawa na watu milioni 130.Ripoti hiyo ya mwaka jana, kama ilivyo ya mwaka huu, pia ilitanguliwa na Ripoti ya Jarida la The Economist, lililoeleza Tanzania iliongoza EAC kwa utawala bora na demokrasia na ile ya Taasisi ya Kiuchumi Duniani (World Economic Forum), iliyoitaja ni ya pili Afrika na ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuishi.
Kitaifa
0
KAMPENI inayohimiza watafi ti kuandika upya historia ya ukombozi wa nchi na Afrika kwa ujumla imeanza, lengo likiwa ni kuwezesha wanafunzi kusoma historia ambayo haijapotoshwa kwa makusudi.Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2019/20 bungeni jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (pichani) alisema mbali na wizara yake kusimamia hilo, pia itafufua kampeni ya kurejesha fuvu la shujaa Leti Hema wa Wanyaturu na mashujaa wengine lililochukuliwa na Wajerumani wakati wa ukoloni.“Wizara itahimiza kampeni... kuwezesha wanafunzi na vijana wetu kusoma historia yetu ambayo haijapotoshwa kwa makusudi na hivyo kuwajengea moyo wa uzalendo, utaifa, mshikamano, umoja na upendo,” alisema Dk Mwakyembe.Akizungumzia sekta ya maendeleo ya utamaduni, Waziri alisema baada ya kujitawala, nchi za Afrika ziliendelea kutumia vitabu vya historia, vilivyoandikwa na waliozitawala, hali iliyosababisha michango ya baadhi ya mashujaa wa harakati za ukombozi, kwa makusudi kutoakisiwa na kutothaminiwa ipasavyo.Alitoa mfano wa shujaa wa Wanyaturu, Leti aliyesimama kidete kuzuia utawala wa Kijerumani kwa zaidi ya miaka mitatu kwa kutumia makundi ya nyuki, yaliyouma wazungu pekee na kuzuia Wajerumani kukaribia kilima cha Ng’ongo Ipembe (sasa Singida Mjini) na maeneo yaliyokizunguka.“Hata alipouawa na Wajerumani baada ya kusalitiwa, wakoloni hao hawakuridhika, waliamua kukata kichwa chake na kukipeleka Ujerumani kwa uchunguzi wa kina ili kubaini kama alikuwa na uwezo maalumu wa kibaolojia wa kufundisha wadudu wenye ubongo mdogo sana kama nyuki kushambulia wazungu tu,” alisema. Kwa mujibu wa Waziri, walikwenda pia kuchunguza kuhusu muujiza aliowaonesha wa kukaa juu ya ncha kali ya mkuki badala ya kigoda cha kawaida, ali-pokutana nao kwa mazungumzo ambayo yalivunjika.Alisema shujaa huyo pamoja na wengine akiwamo Mtemi Isike wa Tabora aliyepigana na Wajerumani kwa zaidi ya miaka minne na hatimaye kuzidiwa nguvu na kujinyonga, hawajaandikwa wala mchango wao kuthaminiwa katika historia ya nchi, iliyoandikwa na wazungu. Waziri Mwakyembe alipongeza wadau wa programu hiyo, wakiwamo wabunge wanaounga mkono juhudi za kuhifadhi historia ya ukombozi wa Afrika kwa kubuni miradi mbalimbali, ikiwamo ujenzi wa makumbusho katika maeneo yaliyotumiwa na wapigania uhuru kutoka nchi za kusini mwa Afrika.
Kitaifa
0
MATUKIO mapya ya malaria kwa kila watu 1,000 katika jamii, yamepungua kwa asilimia 62 kutoka matukio 295 kwa kila watu 1,000 mwaka 2008 hadi matukio 112 kwa kila watu 1,000 .Hiyo ni kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa mwaka 2008/2017 na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto. Aidha vifo vinavyosababishwa na malaria, vimepungua kwa asilimia 73 kutoka vifo 33 kwa watu 1,000 katika jamii kwa mwaka 2008 hadi vifo 9 kwa watu 1,000 kwa mwaka 2017.Mhamasishaji Theresia Shirima kutoka NMCP, akizungumza na wanahabari kwenye semina maalumu ya kuwajengea uwezo Moro- goro hivi karibuni, alisema, “Maambukizi ya malaria katika jamii yamepungua asilimia 60 kutoka asilimia 18.1 mwaka 2008 hadi asilimia 7.3 mwaka 2017; huku jamii inayoishi katika maeneo yenye maambukizi ya malaria ya chini asilimia 10, imeongezeka kutoka asilimia 39 kwa mwaka 2007/2008 hadi asilimia 68 kwa mwaka 2017,” alisema.Alisema jamii iliyoishi katika maeneo yenye maambukizi makubwa, imepungua kutoka asilimia 61 mwaka 2008 hadi asilimia 32 mwaka 2017. Kwamba mafanikio hayo yameletwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kuhakikisha mikakati ya udhibiti wa malaria inatekelezwa kwa ufanisi. Semina hiyo ni sehemu ya kampeni ya ‘Ziro Malaria Inaanza na Mimi,’ ya nchi za Bara la Afrika, ikiratibiwa na RBM Partnership to End Malaria na Umoja wa Afrika (AU) kutokomeza ugonjwa wa malaria Afrika mwaka 2030.Ugonjwa wa malaria unasababishwa na vimelea vya plasmodium, vinavyoenezwa na mbu jike aina ya anofelesi kutoka mtu mmoja kwenda mwingine mbu mwenye vimelea vya malaria anapomuuma na kuacha vimelea mwilini mwake. “Malaria inaendelea kuathiri jamii licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kufuatia utekelezaji mikakati mbalimbali,” alisema.Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji Jamii Kupambana na Malaria kutoka NMCP, Leah Ndekuka alise- ma ”Maambukizi ya malaria hutegemea hali ya hewa na mazingira yanayosaidia maambukizi mapya, mfano joto kali, mvua za kutosha na unyevunyevu. “Mazingira ya hali ya hewa tofauti hutofautiana kiwango cha maambukizi na kijiografia hata baada ya mikakati inayofanana.”Pia, tofauti za kipato na mazingira katika jamii, zinachangia kuwepo viwango tofauti vya maambukizi ya malaria, mfano maambukizi ya malaria maeneo ya watu wenye kipato cha juu ni ya chini, ukilinganisha na ya kipato cha chini. Katika kupambana na malaria nchini, serikali kupitia taasisi zake imeweka Mpango Mkakati wa Awali wa mwaka 2015/2020, kuhakikisha malaria imetoweka katika jamii.Lakini, mpango huo ulipitiwa upya na kuboreshwa kukidhi mahitaji ya hali ya sasa ya maambukizi yake. Ilielezwa baada ya mpango wa awali kufanyiwa marekebisho, serikali ilikuja na mpango mpya wa mwaka 2018/2020 kupunguza maambukizi ya malaria kufikia chini ya asilimia moja mwaka 2020. Linda Nakara ambaye ni Mwezeshaji kutoka NMC chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alisema serikali imejizatiti kutoa elimu ya afya dhdi ya malaria.
Kitaifa
0
IMEELEZWA kuwa hakuna sheria yoyote inayokataza taarifa za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kujadiliwa Bungeni endapo mbunge ataona kuna jambo la kuibua kutoka kwenye taarifa iliyoibuliwa.Akijibu swali la mbunge wa Mgogoni Dk Suleiman Ally Yusuf (CUF), kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha alisema kwamba tume imekuwa ikitimiza wajibu wake na ripoti zake ziwazi. Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alikuwa anataka kujua kwa nini ripoti za tume hiyo haziwekwi wazi kwa umma na kama serikali haioni kuwa wakati umefika kujenga utamaduni wa ripoti hizo kujadiliwa bungeni.Naibu waziri huyo alisema kwamba ni kweli kuwa ibara ya 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ikisomwa kwa pamona na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina ipa tume mamlaka ya kufanya uchunguzi wa uvunjikwaji wa haki za binadamu na baada ya uchunguzi kubaini ripoti zitapelekwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji wa maoni ya tume.Aidha sheria inataka tume kuwasilisha taarifa yake ya mwaka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Mawaziri kupitia kwa mawaziri wanaoshughulikia masuala ya haki za binadamu Tanzania bara na visiwani.
Kitaifa
0
Akizungumza mara baada ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo jana jioni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, alisema uwekezaji huo unatarajiwa kuleta manufaa kwa shirika hilo kwani uwekezaji wake pia utasaidia kutoa elimu kwa vitendo juu ya ufugaji kwa kada mbalimbali.Alisema miaka ya nyuma shirika hilo lilikuwa likisifika kwa ufugaji wa kuku kabla ya kusitisha shughuli hizo kutokana na uwepo wa sababu mbalimbali na kusababisha shirika hilo kukosa mapato yaliyokuwa yakitokana na uuzaji wa kuku na mayai.Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, Cyprian Mpemba alisema uwekezaji huo wa miaka 66, mbali na kuingizia shirika hilo kiasi cha Sh milioni 100 kila mwaka, pia utawawezesha kuvuna kiasi kingine kama hicho kama ada ya uingiaji katika eneo hilo.Alisema itachukua muda wa miaka nane hadi uwekezaji rasmi ukamilike katika eneo hilo ukihusisha idara mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda vya usindikaji wa nyama na utengenezaji wa soseji, huku kila baada ya miaka miwili wakikamilisha ujenzi wa eneo yakiwemo maeneo ya kufugia kuku hao.Mpemba alisema matarajio baada ya mika miwili ijayo mradi huo utaweza kuzalisha kuku milioni 2.7 huku wakitoa ajira kwa watu 120 na ukikamilika utazalisha kuku milioni 165 pamoja na kutoa ajira kwa watu 700 hatua aliyosema itasaidia kuleta mapinduzi katika ufugaji wa kuku hapa nchini sambamba na kutoa elimu kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.Naye Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Hesham Ewies alisema malengo yao ni kuibadilisha Kibaha kwa muda mfupi kwa kulifanya kuwa eneo linalosifika kutokana na shughuli za ufugaji wa kuku huku zaidi wakilenga kuondoa upungufu wa mahitaji ya bidhaa ya kuku yaliyopo kwa sasa nchini.Alisema watarajio yao baada ya miaka michache ijayo, Tanzania itaweza kusifika kwa usafirishaji wa bidhaa zitokanazo na kuku kwenda nje ya nchi na hivyo kuliongeza Taifa mapato.
Biashara
1