text
stringlengths
3
16.2k
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU WAZIRI wa Utumishi wa Umma, Bw Moses Kuria, amepuuzilia mbali madai ya uwepo wa tofauti za kisiasa baina yake na Naibu Rais Rigathi Gachagua. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni Jumatano, Desemba 27, 2023, Bw Kuria alisema kuwa “wana historia ndefu na Bw Gachagua ambayo haiwezi kuwaruhusu kuwa kwenye vita”. “Hatuna tofauti zozote. Nadhani watu wanafasiri visivyo. Sipigwi vita na mtu yeyoye kisiasa. Mimi na Bw Gachagua tumetoka mbali sana,” akasema B Kuria. Akirejelea uhusiano wake na Naibu Rais, alipohudumu kama Mkuu wa Taarafa (D.O), Bw Kuria alisema kuwa kwa wakati mmoja, alimfanyia kampeni katika Kaunti ya Nyeri, wakati wote walikuwa kwenye Chama cha Jubilee (JP). Wakati huo, Bw Gachagua alikuwa akiwania ubunge katika eneo la Mathira huku Bw Kuria akitetea nafasi yake kama mbunge wa Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu. Baada ya uchaguzi mkuu wa 2017, Bw Kuria alisema kuwa kwa wakati mmoja, alikuwa kiongozi wa Bw Gachagua katika Bunge la Kitaifa. “Wakati yeye (Gachagua) alipochaguliwa, alinikuta nikihudumu muhula wa pili, huku nikiwa mkubwa wake kwa wakati mmoja. Huo ulikuwa wakati nilihudumu kama Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Uchukuzi. Yeye alihudumu kama mmoja wa wanachama wa kamati hiyo,” akasema Bw Kuria. Waziri Kuria anasema walifanya kampeni pamoja na Bw Gachagua huku wakihangaishwa sana na serikali ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta. “Sisi sote tunatetea na kupigania maslahi ya Mlima Kenya. Yeye ni mkubwa wangu serikalini na katika Baraza la Mawaziri, hivyo, hatuwezi kuruhusu tofauti ndogo ndogo kututenganisha,” akasema Bw Kuria.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA MWANDANI wa Rais William Ruto, bloga Dennis Itumbi na wakili Miguna Miguna, wamejiunga na wale wanaolilia haki kufuatia mauaji ya kinyama ya bloga maarufu katika Kaunti ya Meru, Daniel Muthiani almaarufu ‘Sniper’. Bw Itumbi anahoji kujivuta kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuhusiana na uchunguzi wa mauaji hayo na kukamatwa kwa washukiwa. Aidha, analalamikia kile anachodai ni unyamavu wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) kuhusiana na suala hilo. “Hivi kumbe mshukiwa mmoja alikamatwa kuhusiana na kutekwa nyara kwa Sniper lakini ODPP haikutoa mwelekeo kuhusu kushtakiwa kwake. DCI iliambia mahakama wanasubiri ODPP. Mbona ofisi hii inachelewesha suala hili? Mbona DPP amenyamaza kindani na hadharani?” Bw Itumbi akalalamika. Kwa upande, wake Miguna Miguna alilalamikia unyamavu wa Inspekta Jenerali wa Polisi (IG) Japhet Koome kuhusiana na kisa cha mauaji ya Muthiani. Wakili huyo amewataka Wakenya kuuliza ukweli kutoka kwa maafisa wa usalama kuhusu mauaji ya bloga huyo, akitaja mauaji yake kama kielelezo cha mwenendo wa dharau kwa sheria uliokithiri nchini. “Kenya ni nchi iliyosheheni vitendo vya maovu na dharau kwa uzingativu wa sheria. Siku hii ya Krismasi, Wakenya wanataka kusikia kutoka kwa DCI na Japhet Koome kuhusu mauaji ya kikatili ya Sniper!” wakili Miguna akaandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, zamani ukijulikana kama Twitter. Maiti ya Muthiani ilipatikana imetupwa katika mto Mutonga, katika kaunti ya Tharaka Nithi mnamo Desemba 16, 2023, siku chache baada ya kutoweka kwake. Alikuwa ametoweka tangu Desemba 2, 2023 Upasuaji uliofanyiwa maiti yake na mwanapatholojia mkuu wa Serikali Dkt Johansen Oduor katika Hospitali ya Marimanti Level 4, ulionyesha kuwa Sniper aliteswa kabla ya kuuawa kinyama. Mwili wake ulipatikana na majeraha shingoni huku mbavu kadha zikiwa zimevunjika. Aidha, kulikuwa na majeraha kichwani. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA TITUS OMINDE VIONGOZI wa kidini kutoka North Rift wametoa wito kwa Wakenya kuendelea kuwa na mshikamano na umoja licha ya hali ngumu ya kiuchumi huku wakimtaka Rais William Ruto kutumia Mwaka Mpya 2024 kama mwaka wa kuangazia ufufuaji wa uchumi. Wakizungumza wakati wa ibada za Krismasi katika makanisa mbalimbali North Rift, viongozi hao wa kiroho pamoja na waumini waliofika maabadani walisema wangependa kuona Rais Ruto akitafuta hekima kutoka kwa Mungu ampe mawazo ya jinsi ambavyo anaweza kusimamia mchakato wa kisera na kiutawala kukabiliana na changamoto za nyakati ngumu za kiuchumi. Walisema wangependa kuona raia nchini wakiwa na pesa mfukoni mwaka 2024. Askofu Wilson Kurui, mlezi wa wahudumu wa injili Uasin Gishu alisema rais Ruto anahitaji mazingira ya amani ili kufufua uchumi. Askofu Kurui alitoa changamoto kwa Rais Ruto kujiepusha na siasa za kulipiza kisasi badala yake azingatie mahitaji ya raia wa kawaida. “Kama Kanisa tunasali ili Rais wetu aongoze Wakenya katika mazingira ya amani na ushauri wangu kwake ni kuachana na siasa za utengano. Ajikusuru kutumikia nchi kama mtumishi wa Mungu kwa kuzingatia sana ufufuaji wa uchumi,” alisema Askofu Kurui. Alitoa changamoto kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuanza kufanya kazi na Rais Ruto kwa manufaa ya nchi. “Kiongozi wa upinzani, Bw Odinga asahau yaliyopita na akubali kumpa sapoti Rais Ruto kwa ustawi wa nchi yetu,” akaongeza Askofu Kurui. Kwa upande wake Askofu Zablon Malema wa Kanisa la Hallelujah mjini Eldoret, aliwaomba Wakenya wote kuendelea kumtakia mafanikio Rais Ruto ili kuishi maisha ya amani ambayo yataleta maendeleo. Askofu Malema alitoa ushauri kwa kiongozi wa nchi kwamba aongoze bila ukabila, hasa katika uteuzi wa maafisa wa serikali kwa kubuni nafasi za ajira kwa Wakenya kutoka jamii zote. “Rais Ruto lazima awe macho ili kuhakikisha kuwa kuna usawa katika uajiri ili kuhakikisha sekta za ajira zinaonyesha sura ya Kenya na kuepuka ukabila katika ajira,” alisema Askofu Malema. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA LABAAN SHABAAN MUUNGANO wa watu wasiomuamini Mungu nchini umesifia agizo la Papa Francis ambaye Jumatatu wiki jana aliagiza viongozi wa kidini wa Kanisa Katoliki kubariki wapenzi wa jinsia moja. Muungano huo ukiongozwa na Harrison Mumia–Rais– ulisema kwenye taarifa kuwa uamuzi wa uongozi wa Kanisa Katoliki kupisha baraka kwa wapenzi wa jinsia moja ni wa maana sana kubadili mtazamo wa utangamano wa kijamii. “Uamuzi huu utabadilisha mambo kwa waumini wa kikatoliki duniani na kwa jumuiya ya wakristo Kenya,” Ilieleza taarifa ya Shirika la Atheists in Kenya mnamo Desemba 24, 2023. Kisha taarifa hiyo ikaongeza: “Uamuzi huu unatuma ujumbe wazi kwa jamii ya Wakristo Kenya na kuwa haki za wapenzi wa jinsia moja ni haki za binadamu na hakuna dhambi kwao kuwa katika uhusiano wa kimapenzi.” Bw Mumia alisema shutuma kwa watu walio katika mwavuli wa LGBTQ zimeongezeka miaka ya hivi karibuni. “Rais William Ruto alisema hawezi kuruhusu ndoa za watu wa jinsia moja nchini Kenya katika muhula wake wa uongozi,” akaeleza. “Tutaendelea na kampeni za kulinda na kudumisha haki za watu wa LGBTQ Kenya zikijumuisha haki ya kuishi, uhuru na usalama,” akaongeza. Mnamo Desemba 19, 2023, Kiongozi wa Kanisa la Katoliki Papa Francis aliridhia mapadri kubariki wapenzi wa jinsia moja, katika mabadiliko ya sera yanayonuiwa kulifanya Kanisa kuwa shirikishi zaidi ila bado ndoa za jinsia moja ni marufuku. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MWANGI MUIRURI WAMILIKI wa lojing’i za mashinani sasa wanasema wanavuna vitamu huku wateja wakifurika. Ingawa hivyo, wengine wanasema baadhi ya wateja wanafika wawili wawili huku baadhi wakionekana waziwazi kuwa ni wa jinsia moja. Pia wakazi wa Murang’a wameshuhudia upekee fulani ambapo vidosho wa mjini wanafika kwa lojing’i wakiwa na vijana wa kiume wa mashinani, hali inayofanya wengi kuulizana maswali ni jinsi gani watu wanatumia sherehe za Krismasi. Je, matendo yao yanaendana na lengo la sikukuu hii? “Mimi nimeshuhudia makubwa. Wanawake wa mijini wanakuja na vijana wa huku mashinani na wanakodisha chumba kwa muda na kisha wanatoka,” akasema Bw Paul Mwangi kutoka mji wa Maragua. Aidha, alisema kwamba wanaume wa Nairobi nao wanafika wakiwa na wanawake wa mashinani na hawana shida kulipa chumba kwa muda tu. “Huku tumezoea watu kuja kukodisha chumba cha malazi kuanzia saa mbili usiku na wakishalipa, huwa wanajifunga na kutoka asubuhi inayofuata mwendo wa saa tatu asubuhi,” akasema. Tofauti, akaongeza, ni siku za soko na Jumamosi ambapo kuna wateja wa uasherati wa walio katika ndoa. “Sanasana sisi tunahudumia walevi mtaani ama waliokuwa wanafika hospitalini wakachelewa. Lakini sasa tunashuhudia wawili kwa wawili wakiingia na kukodisha chumba na baada ya muda wa saa moja au mbili, wanaondoka licha ya kulipa ada sawa na za kukesha,” akasema mhudumu mmoja mjini Sabasaba. Hata hivyo, wahudumu wengine waliteta kwamba wameshuhudia visa vya kukera vya mashoga na wasagaji kusaka hudumu za lojing’i mashinani msimu huu wa Krismasi. “Imenibidi nimetoa amri kwa wahudumu wa vyumba vyangu kusikodishwe chumba kwa washukiwa wa mahusiano ya aina hiyo. Lakini pia nimeshangaa kwamba unapata mwanamume mmoja anaingia kwa lojing’i akiwa na wanawake wawili na tukionekana kushangaa tunachekwa,” akasema mhudumu katika mtaa wa Karugia ulioko eneobunge la Kandara. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WAANDISHI WETU WAKENYA wameungana na ulimwengu kuadhimisha Sikukuu ya Krisimasi leo Desemba 25, 2023, huku maelfu wakiwa kwenye kambi kutokana na athari za mvua ya El-Nino. Wakazi katika kaunti za Tana River, Meru, Taita Taveta, Kwale, Lamu, Isiolo kati ya maeneo mengine, wanateseka kwenye baridi, kung’atwa na mbu na kukosa maji safi na chakula. Isipokuwa tu kaunti ya Lamu, ambako kambi zilizotengenezwa ni za watu waliotoroka makwao kutokana na mashambulio ya kigaidi, kambi zilizo katika kaunti nyingine nchini ni za watu ambao makazi yao yaliharibiwa na mafuriko. Kwa wengi wao, hii itakuwa ni mara ya kwanza kusherehekea sikukuu hiyo bila kuwepo kwenye makazi yao rasmi.Bi Dorothy Halubva, ambaye ni mama wa watoto wanne, kwa sasa anaishi kwenye chumba cha muda katika kijiji cha Gumba, Kaunti ya Tana River. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, amejua uchungu ambao mtu asiye na makazi huwa anapitia. Pia, amekaa kwa siku kadhaa bila chakula. Awali hajawahi kukosa chochote maishani mwake. Hata hivyo, hali ni tofauti mara hii kwani atasherehekea Sikukuu ya Krisimasi kwa namna tofauti kabisa. “Kufikia sasa, ningekuwa nishaweka taa maalum za kurembesha kuta za nyumba yangu. Hata hivyo, mara hii nitawasha tu mshumaa. Ninatarajia kuimba nyimbo za kusherehekea sikukuu hii usiku,” akasema. Bi Mary Hiribae pia hana furaha kuihusu siku hii, ikiwa hatukatokea mtu yeyote wa kumsaidia kutoka kambini. “Sina hema. Ninahangaika sana kupata chakula na makazi. Siwezi kumpa shinikizo yoyote mume wangu kwani hii ndiyo hali inayotukabili sote,” akasema. Mama huyo mwenye watoto wawili, hataimba nyimbo za kuisherehekea sikukuu kwani haoni lolote la kufurahia. “Watoto wangu wanaonekana wenye furaha wakicheza na wenzao lakini Krismasi hii itakuwa tofauti sana kwao,” akasema. Katika Kaunti ya Lamu, hatima ya zaidi ya familia 200 haijulikani, baada ya kuachwa bila makao kutokana na mashambulio ya kigaidi. Kwa miezi saba iliyopita, familia hizo zimekuwa zikikaa katika kambi iliyo katika shule ya msingi ya Juhudi.Mwenyekiti wao, Bw Joseph Ngige, asema zawadi yao kubwa itakuwa kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya kwenye makazi yao. “Hali ni mbaya hapa. Hivyo, tunaiomba serikali iharakishe utengenezaji wa kambi za polisi na jeshi katika vijiji vyetu,” akasema Bw Ngige. Kwa Bi Beatrice Kilinguli, anayetoka katika eneo la Ukunda, Kaunti ya Kwale, maana ya Sikukuu ya Krismasi ni kujumuika pamoja na familia yake. Mama huyo wa watoto wawili anasema kuwa huwa anawategemea wahisani kwa mahitaji yake ya kimsingi. Anasema anatarajia kuwa kuna mtu atakayejitokeza ili kumsaidia. “Tungependa usaidizi zaidi kutoka kwa serikali, hasa wanawake ambao hawana waume na wanahangaika kuzilisha familia zao. Sh2,000 ambazo huwa tunapata kila mwezi kutoka kwa serikali huwa hazitoshi,” akasema Bi Kilinguli. Ijapokuwa yeye ni Mwislamu, Bw Rashid Chano kutoka Kwale ni mwingi wa matumaini kuhusu msimu huu wa Krismasi. Kwake, hali ilivyo siku hii ni ishara kwamba mwaka huu umekuwa mgumu, ijapokuwa unakaribia kufikia mwisho. Katika Kaunti ya Mombasa, kauli ya Bw Darrel Midega, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, inafanana na zile za Bi Keziah Katile na Bw Maxwell Kiche. “Zawadi ambayo serikali inaweza kutupa msimu huu wa Krismasi ni kupunguza gharama ya maisha. Kama mwanafunzi aliye katika chuo kikuu, gharama kubwa ya maisha imetuathiri sana,” akasema. Wakenya wengi walio katika kambi hizo wanasema kuwa misaada ambayo serikali imekuwa ikitangaza kutoa ili kuwasaidia bado haijawafikia. Ripoti za Kalume Kazungu, Siago Cece na Wachira Mwangi You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KALUME KAZUNGU WAKIMBIZI wa mafuriko Kaunti ya Lamu wamepokea fedha na misaada mingine ya kibinadamu ili kuwasaidia kupambana na hali yao ya maisha wakiwa kambini. Kaunti ya Lamu ina karibu kambi 12 za waathiriwa waliohama vijijini mwao baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko. Kulingana na ripoti ya serikali ya Kaunti ya Lamu kuhusiana na janga la El-Nino, jumla ya familia 2,599 zimeathiriwa na mafuriko ambapo familia 822 zimehama makwao baada ya makazi yao kuharibiwa na mafuriko hayo. Miongoni mwa kambi za wahanga wa mafuriko Lamu ni Moa, Kitumbini, Lumshi A na B, Mikinduni B miongoni mwa nyinginezo. Wiki jana, jumla ya familia 200 za wakimbizi wa mafuriko zilifikiwa na kupokezwa misaada ya fedha, malazi, vyandarua, chakula, sabuni, dawa zikiwemo zile za kutibu maji, sodo za kusaidia wanawake na wasichana kujisitiri kipindi cha hedhi miongoni mwa misaada mingine. Shirika la World Vision Kenya kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Lamu, walifikisha misaada hiyo kwa wakimbizi hao wa mafuriko, hasa wale walioko kwenye kambi mbili kuu za Moa na Kitumbini. Kila familia ilipokezwa jumla ya Sh10,300 kwenye mpango huo, maarufu cash transfer. Akizungumza wakati wa shughuli ya kuwakabidhi misaada wakimbizi hao, Afisa Mkuu wa World Vision Kenya anayesimamia kaunti za Lamu, Tana River na Garissa, Bw Michael Mulei, alisema shirika hilo litaendelea kujitahidi na kushirikiana na serikali za ugatuzi katika kuhakikisha kila mwaathiriwa wa mafuriko nchini anasaidiwa. Bw Mulei alitaja kuwa World Vision Kenya tayari imetafuta na kupata  fedha za kima cha Sh45 milioni  zitakazotumika kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko kote nchini. Alisema kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Lamu, World Vision pia itaendeleza upokezaji wa mafunzo na elimu ya kusaidia waathiriwa kukabiliana Na changamoto zinazochangiwa na mafuriko,ikiwemo maradhi na afya kwa ujumla. “Tumetembelea wakimbizi wa mafuriko hapa Moa na Kitumbini kuwakabidhi fedha, vyakula, dawa, vyandarua na misaada mingine. Twafanya haya ili kusaidia hizi familia kukabiliana na athari za mafuriko. World Vision tutazidi kushirikiana na kaunti mbalimbali kote nchini kuona kwamba wote walioathiriwa na janga la mafuriko litokanalo na El-Nino wanafikiwa na kusaidiwa,” akasema Bw Mulei. Waziri wa Afya Kaunti ya Lamu Dkt Mbarak Bahjaj, alisema kaunti itaendelea kushirikiana na wahisani katika kuwafikia waathiriwa wa mafuriko na kuwasaidia. Alitaja changamoto ya maradhi ya kipindupindu inayochangiwa na mafuriko ambayo imeacha watu watatu wakifariki ilhali zaidi ya 100 wakitibiwa kwenye hospitali mbalimbali za Lamu. Dkt Bahjaj hata hivyo alisema serikali imefanya kila jitihada na kudhibiti hali hiyo ya kipindupindu. “Serikali ya kaunti ya Lamu, chini ya uongozi wa Gavana Issa Timamy, itaendelea kushirikiana na wahisani katika kuwafikia na kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko. Tuko imara,” akasema Dkt Bahjaj. Bi Fatima Hussein,mmoja Wa wakimbizi,alishukuru kaunti Na wahisani Kwa kuwafikishia misaada hiyo. “Twashukuru. Mafuriko yalituganya kupoteza kila kitu. Hatuna chochote tulichookoa. Twafurahia kwamba World Vision Kenya na kaunti inatujali,” akasema Bi Hussein. Mohamed Shongolo, mkimbizi mwingine, aliomba wahisani na mashirika zaidi ya kibinadamu kujitokeza na kuwasaidia. Alisema kambi zao kila mara zimekuwa zikipokea watu wapya,hivyo kuongeza idadi ya wanaoishi kwenye kambi hizo. Bi Halima Kulisa alisema mbali na pesa, vyakula, vyandarua na malazi, ipo haja ya kaunti na wahisani pia kufikiria kuwajengea nyumba zao zilizobomolewa na mafuriko. “Wakati umewadia kaunti itenge ardhi maeneo ya nyanda za juu ambayo itatumika kutuhamisha sisi ambao tunaishi sehemu ambazo zina changamoto ya mafuriko. Wakifanya hivyo watazuia hali ya kila mara kunaposhuhidiwa mvua kubwa sisi ndio tunaopoteza nyumba na mali. Tumechoka,” akasema Bi Kulisa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WANDERI KAMAU WAZIRI wa Ulinzi Aden Duale, ameunga mkono juhudi zinazoendeshwa na idara tofauti nchini kukabili matumizi ya Shisha, akisema kuwa wale wote watakaopatikana wakitumia ‘mihadarati’ hiyo wanafaa kukabiliwa kisheria. Mnamo Ijumaa usiku, Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Matumizi ya Mihadarati nchini (Nacada) iliendesha operesheni kali dhidi ya vituo vya burudani ambako kileo hicho kimekuwa kikitumika. Operesheni hiyo ilifanyika katika eneo la Kilimani, jijini Nairobi, ambako watu kadhaa walikamatwa, huku misokoto kadhaa ya bidhaa hiyo pia ikinaswa. Kutokana na operesheni hiyo, Bw Duale alisema kuwa uvutaji wa Shisha ulipigwa marufuku nchini mnamo 2017, hivyo yeyote anayepatikana akiitumia ama akiiuza anafaa kukabiliwa kisheria. “Waraibu wa Shisha lazima wakabiliwe kisheria, kwani ilipigwa marufuku nchini tangu 2017. Maafisa wa usalama lazima wavamie vituo vyote vya matumizi au uuzaji wa vileo hivyo,” akasema Bw Duale. Mnamo Ijumaa usiku, maafisa wa Nacada waliwakamata watu 25 katika mkahawa na kilabu cha Yejoka Gardens kilichoko Kilimani, Nairobi, baada ya kuwapata wakitumia Shisha na kutafuna miraa. Operesheni hiyo iliongozwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa mamlaka hiyo, Bw Anthony Omerikwa. Bw Omerikwa alisema kuwa lazima sheria zote ziizowekwa kukabili matumizi ya vileo hivyo zizingatiwe. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili.
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na...
Malkia wetu leo ni  Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu...
Sayfer Godez ni mkaazi wa Nakuru .Anapenda kushiriki kwenye majukwaa ya mapambo na urembo.Uraibu wake ni kusafiri na kujumuika na... Sylvia Wangeci 23 ni mzaliwa wa Molo, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha MKU tawi la Nakuru.Uraibu wake ni kusafiri na... Mical Abulatsia Imbukwa, 28, ni mwanahabari katika shirika moja jijini Nairobi. Uraibu wake ni kutazama filamu za Afro sinema na kujumuika... Faith Karungari mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafasheni na mwanamitindo maarufu kutoka Nakuru.Uraibu wake ni kuogelea na kusikiliza muziki... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ya Juu jana ilianza kusikiza rufaa ya mpango wa kubadilisha katiba (BBI) huku Mwanasheria Mkuu Bw Paul... Na BENSON MATHEKA
RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alisema kuwa ndoto yake ya kubadilisha katiba ya Kenya iliyopitishwa 2010 kupitia... Na CHARLES WASONGA
KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa... Na JOSEPH WANGUI
Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa... Na Gitonga Marete
KIONGOZI wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesisitiza kuwa Bunge linapaswa kurejelea Mpango... Na Leonard Onyango
NAIBU wa Rais William Ruto amewataka wabunge kujadili masuala nyeti yanayoathiri Wakenya badala ya kujaribu kufufua... Na CHARLES WASONGA
JUHUDI za wabunge wanaoegemea mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kutumia bunge kupitisha... Na WALTER MENYA
JUHUDI za kuokoa mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI) zimefikishwa rasmi katika Mahakama... Na FRANCIS MUREITHI