text
stringlengths 1
24.2k
| label
int64 0
5
|
---|---|
Badi Mchomola DIRISHA
la usajili nchini England lilifungwa Agosti 8, mwaka huu huku uhamisho
uliotikisa ni ule wa beki Harry Maguire akitokea Leicester City na kujiunga na
Manchester United. Mchezaji
huyo raia wa nchini Uingereza alikamilisha uhamisho wake kwa kitita cha pauni
milioni 80 kwa mkataba wa miaka mitano. Mkaba
huyo utamfanya mchezaji huyo awe anachukua kiasi cha pauni 190,000 kwa wiki,
ambazo ni zaidi ya milioni 527 za Kitanzania. Maguire
ametajwa kuwa beki wa kwanza duniani kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha
katika historia ya soka. Kuna
sababu mbalimbali zinazowafanya wachezaji kuhama timu moja kwenda nyingine na
wengine kuamua kukaa kwenye timu moja kwa kipindi kirefu. SPOTIKIKI
leo inakuonesha tofauti ya uhamisho wa Maguire na kiungo wa zamani wa Chelsea na
timu ya taifa ya Brazil, Oscar dos Santos ambaye kwa sasa anakipiga katika
klabu ya Shanghai SIPG inayoshiriki Ligi Kuu nchini China. Kwenye
soka kila mchezaji anakuwa na ndoto zake, wapo ambao wanakuwa na ndoto za
kucheza soka kwenye klabu kubwa barani Ulaya, wengine wanaangalia klabu ambayo
atapata fedha nyingi kwa ajili ya kuikomboa familia yake na mambo mengine
mengi. Harry Maguire Kikubwa
kilichomfanya Maguire ajiunge na Manchester United sio fedha, lakini kulikuwa
na mambo mawili nakubwa. Jambo la
kwanza lililomfanya ajiunge na Manchester United ni kutimiza ndoto zake, tangu
alipoanza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Sheffield United mwaka 2011,
ndoto zake kubwa zilikuwa kuja kucheza soka ndani ya Manchester United. Alijua
sio kazi rahisi kufanikisha hilo, lakini aliamini kwenye suala la kujituma
kungeweza kumfanya awindwe na klabu yoyote duniani. Mchezaji
huyo alikuwa kwenye kiwango kizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini
Urusi mwaka jana huku England ikifanikiwa kufika hadi hatua ya nusu fainali na
baadae kuwania nafasi ya tatu lakini ilijikuta ikiishia nafasi ya nne. Baada ya
hapo Manchester United wakaanza kuingia vitani kuwania saini ya beki huyo,
hivyo ikiwa ni sehemu moja wapo ya kutimiza ndoto zake. Suala la
pili lilikuwa kuweka rekodi ya uhamisi wake. Pauni milioni 80 haijawai kutoka
kwa beki yeyote kuwekewa mezani kiasi hicho kikubwa cha fedha, hivyo aliona
bora aingie kwenye historia ya kipekee duniani kuwa beki wa kwanza kusajiliwa
kwa kiasi kikubwa cha fedha. Mbali na
kusajiliwa kwa fedha hizo, lakini mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England,
Manchester City walikuja na ofa ya pauni 278,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya milioni
771 kwa wiki, lakini Maguire alikataa na kutaka kutimiza ndoto za kucheza
Manchester United. Hivyo
kilichompeleka Manchester United sio fedha, ila ni kutimiza ndoto zake, kama ni
fedha angeenda Man City ambapo angekuwa anachukua kiasi kikubwa cha fedha
kuliko anachochukua sasa Man United. Oscar dos Santos Alikuwa
mmoja kati ya wachezaji ambao walikuwa kwenye kiwango kizuri wakati anakipiga
katika klabu ya Chelsea kuanzia mwaka 2012 hadi 2017 alipoondoka na kujiunga na
klabu ya Shanghai SIPG inayoshiriki Ligi Kuu nchini China. Maamuzi
ya mchezaji huyo kujiunga na Shanghai SIPG yaliwashangaza wengi hasa kutokana
na umri wake kuwa na miaka 25 wakati huo. Huo ni
umri ambao wachezaji wengi wanalitangaza jina katika klabu kubwa mbalimbali
kutokana na ubora wao, Oscar alikuwa na ubora husiopingika ndani ya Chelsea
kutokana na kuitawala safu yake ya kiungo. Wachezaji
wengi wanataka kuonekana duniani, soka ambalo linaongozwa kutazamwa kwa kiasi
kikubwa duniani ni Ligi ya England pamoja na Hispania, lakini ofa ambayo
iliwekwa na Shanghai SIPG, Oscar hakufikiria suala la kuonekana tena. Shanghai
SIPG waliweka mezani kiasi cha pauni milioni 60, pamoja na kitita cha pauni
400,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi ambapo ni zaidi ya bilioni 1 za
Kitanzania. Wakati
awali alikuwa anachukua kiasi cha pauni 90,000 kwa wiki zaidi ya milioni 249 za
Kitanzania, hivyo alikuwa na kila sababu ya kuondoka. Hii
ilionesha wazi kuwa, ndoto za mchezaji huyo ni kuingiza fedha kwenye mchezo wa
soka na sio kuangalia anakwenda kucheza soka kwenye klabu gani. Tangu amekimbilia
China, jina lake limeshuka kwenye ramani ya wachezaji wanaotikisa soka duniani
tofauti na wengi walivyotarajia makubwa kutoka kwa mchezaji huyo, hata kwenye
kikosi cha timu ya taifa Brazil haonekani kwa kuwa yupo kwenye ligi ambayo
haina ubora mkubwa. Kwa kuwa
ndoto zake zilikuwa ni kuwa tajiri kwa kuingiza fedha nyingi bila ya kuangalia
anacheza kwenye timu gani au ligi gani, ndoto hizo amefanikiwa, bado anaingiza
fedha kila wiki zaidi ya bilioni 1. | 2 |
NA REHEMA SIMON (TUDARCO) WASANII nyota wa muziki hapa nchini, Ali Kiba, Joh Makini, Dogo Janja, Madee na Lulu Diva, ni miongoni mwa wasanii waliosajiliwa ili kutoa burudani katika tamasha la Tigo Fiesta 2017-Tumekusoma. Wasanii hao pamoja na wengine lukuki, walisajiliwa katika matukio yaliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, lakini lile la Mbagala Zakheem likionekana kutia fora kutokana na kuwahusisha wasanii wakali hapa nchini, wakiongozwa na Ali Kiba. Wengine ni Shilole, Jux, Vannesa Mdee, kundi la Weusi likiongozwa na Joh Makini, Stamina, Roma Mkatoliki, Mr Blue, Maua Sama, Fid Q, Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Said Kalori na wengineo wengi. Kati ya wasanii wote hao, Ali Kiba ndiye anayeonekana kuvuta hisia za wengi zaidi jijini humo, huku wimbo wake wa Seduce Me ambao umetokea kubamba vilivyo, ukitarajiwa kufunika. Lakini mbali ya wimbo huo, pia kuna ule wa Zimbabwe, ulioimbwa na Roma ambapo iwapo mwana hip hop huyo atapanda jukwaani na kuimba, ni wazi vumbi litatimka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, litakakofanyika tamasha hilo la aina yake. Kwa mujibu wa waratibu wa tamasha hilo, msimu huu wataanzia kukinukisha jijini Arusha Jumamosi hii, kabla ya kuhamia kwenye maeneo mengine. Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Tigo, William Mpinga, alisema kwa watakaonunua tiketi za tamasha hilo la Jumamosi kwa Tigopesa, watapata punguzo la asilimia 10. Mpinga aliwashauri wapenzi wa Tigo Fiesta kuchukua fursa hii kupata tiketi zao kwa Sh 9,000 tu, hii ikiwa ni punguzo la asilimia 10 ya bei halisi ya Sh 10,000 kwa watakaonunua kwa fedha taslimu. “Kununua tiketi ni rahisi. Fuata utaratibu wa kawaida wa kutuma pesa na tuma TZS 9,000 kwenda namba ya TigoPesa 0678 888 888. Hapo hapo utapokea ujumbe mfupi wa SMS unaothibitisha manunuzi yako ya tiketi. Hifadhi huo ujumbe mfupi. Baadaye utapokea maelekezo ya jinsi na wapi pa kwenda kuchukua tiketi yako,” alisema Mpinga. Aliongeza: “Tigo inajiandaa kutoa ofa nyingine kibao katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2017, kwa hiyo wateja wetu na wapenzi wote wa Tigo Fiesta 2017 wakae tayari kufurahia ofa hizi bomba kadri ya tutakavyokuwa tunazitangaza.” Mwaka huu msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma utajumuisha mikoa ya Arusha, Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora, Dodoma, Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara, kabla ya kuhitimishwa jijini Dar es Salaam. | 4 |
SHANGHAI, CHINA CHINA yenye soko kubwa zaidi la magari duniani, ina mpango ya kupiga marufuku uundaji na uuzaji wa magari yanayotumia dizeli na petrol. Naibu Waziri wa Viwanda nchini humo, Xin Guobin, alisema jana kuwa umefanyika utafiti lakini bado hawajaamua ni lini amri hiyo itaanza kutekelezwa. “Hatua hizo bila shaka zitaleta mabadiliko makubwa katika sekta yetu ya magari,” alisema Guobin. China ilitengeneza magari milioni 28 mwaka uliopita ikiwa ni takriban theluthi moja ya magari yote yaliyotengenezwa duniani. Uingereza na Ufaransa tayari zimetangaza mipango ya kupiga marufuku magari mapya yanayotumia dizeli na petroli ifikapo mwaka 2040 kama sehemu ya hatua za kuzuia uchafuzi wa hali ya hewa duniani. Kampuni ya China ya kutengeneza magari ya Volvo, ilisema Julai mwaka huu kuwa magari yake yatatumia umeme ifikapo mwaka 2019. Makampuni mengine duniani yakiwamo Renault-Nissan, Ford na General Motors yote yanashughulikia mipango ya kutengeneza magari yanayotumia umeme. | 3 |
WIZARA ya Nishati imelitaka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuhakikisha haiachi wala kukiruka kijiji katika kuviunganishia umeme, kwani awamu ya sasa ndiyo ya mwisho ijulikanayo kama ‘baba lao’.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kwenye kitongoji cha Migude kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati akizindua uwashaji umeme.Pia alizindua kisima cha maji ya kunywa kinachotumia mashine ya kuvuta maji inayotumia umeme kwenye kitongoji hicho.Mgalu amesema awamu hiyo ndiyo ya mwisho ya REA awamu ya tatu mzunguko wa pili wa kusambaza miundombinu ya umeme kwenye vijiji ili ifikapo Juni 31 mwaka 2021 inapaswa kuvifikia vijiji vyote kabla ya kuhamia kwenye vitongoji.“Awamu hii ndiyo ya mwisho ya kuvipelekea umeme vijiji kabla hatujahamia vitongoji hivyo, nawasihi Tanesco na REA kupitia vijiji vilivyobaki ili tukamilishe hili kwa vijiji kama alivyoagiza Rais John Magufuli kuwa ifikapo kipindi hicho vijiji vyote vipate umeme,” alisema.Hadi sasa wamevifikia vijiji 8,115 kati ya vijiji 12,000 kote nchini ambapo bado vijiji 4,000 na hadi kufikia Juni 2020 vijiji 10,336 vitakuwa vimefikiwa na umeme na lengo litatimia Juni 2021.“Pia naomba kuwashauri kuwa kuna haja ya kuwakopesha wateja hasa kwa wale wateja wa mijini ambao gharama zao ni tofauti kwani wao wanalipia kuanzia Sh 320,000 hadi Sh 500,000 tofauti na wale wa vijijini ambao wanaunganishiwa kwa Sh 27,000,” amesema Mgalu.Aidha amesema kuwa kuna haja ya kuwakopesha umeme halafu walipe kidogo kidogo kupitia ankara zao za umeme kwani serikali inatumia gharama kubwa kuweka miundombinu ya umeme.“Suala la gharama ya kuunganisha umeme kwenye manispaa na majiji hauwezi kuunganishwa kwa Sh 27,000 kwani Tanesco inajiendesha kwa mapato yake, hata hivyo serikali imesikia hoja ya kutaka bei hiyo iwe maeneo yote,” amesema.Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa amesema umeme umesambazwa vijiji vingi lakini baadhi havijafikiwa.Kawambwa alivitaja baadhi ya vijiji ni pamoja na Mataya, Magole, Baikani, Goba Kimelemeta, Kitopeni A na B, Mtowanyanza, Ukani A na baadhi ya vijiji vya kata ya Fukayosi.Diwani wa Kata ya Magomeni, Mwanaharusi Jarufu alisema jambo kubwa katika maendeleo ni umeme na barabara pamoja na maji. | 1 |
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ametengua uteuzi wa nafasi ya Ofi sa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Paul Misuzi na wakuu wa idara za ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji.Hatua hiyo imekuja baada ya watendaji hao, kushindwa kutekeleza maagizo waliyopewa ikiwemo kushindwa kukusanya mapato ya serikali. Waziri huyo alichukua hatua hiyo katika kikao cha pamoja na watumishi wa idara ya ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji, kilichofanyika mjini Kigoma.Alisema kuwa watendaji hao, licha ya kushindwa kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa kwao, pia wameshindwa kuthibitisha uwezo wao wa kusimamia majukumu yaliyopo chini yao. Misuzi ni Afisa ardhi Mteule pekee kwa mkoa Kigoma, ambaye kitaaluma na kiutumishi, kwa mujibu wa taratibu za serikali, alikuwa na uwezo wa kusaini nyaraka kwa ajili ya mchakato wa utoaji wa hati za umiliki wa viwanja na majengo akiwa ameletwa mkoa Kigoma kwa mchakato maalum baada ya mkoa huo kutokuwa na Afisa Ardhi Mteule kwa muda mrefu.Pamoja na sifa hiyo na nafasi nyeti ya mtumishi huyo, naibu waziri huyo alisema kuwa Misuzi alishindwa kutekeleza mpango wa utoaji hati kwa waombaji, waliokuwa wakitaka kupatiwa hatimiliki za viwanja na majengo, licha ya kuwepo kwa maombi mengi kutoka kwa wananchi. Wengine waliotenguliwa katika sakata hilo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Brown Nziku na Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Emanuel Maghembe.Viongozi hao wanadaiwa kwa miaka miwili tangu mwaka 2017, Naibu Waziri alipotoa maagizo, wameshindwa kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na kuandika taarifa zenye visingizio lukuki, ambavyo vinathibitisha kuwa uwezo wao wa kiutendaji ni wa chini. Jambo moja kubwa ambalo lilimuudhi naibu waziri huyo ni kitendo cha watendaji hao waandamizi wa idara ya ardhi, kushindwa kusimamia makusanyo ya fedha za serikali kupitia kodi za ardhi wakati suala hilo liko kwenye uwezo wao.Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, walipanga kukusanya Sh bilioni 1.1, lakini kilichokusanywa ni Sh milioni 337. Naibu Waziri alisema kuwa watendaji hao, wameshindwa kutekeleza agizo la kuingiza kwenye mfumo wa malipo ya serikali ya ukusanyaji maduhuli viwanja vyote, ambavyo vimesharasimishwa kutokana na idadi ndogo ya viwanja ambavyo vimeingizwa kwenye mfumo huo, huku watendaji hao wakiwa hawajui takwimu za kiasi cha viwanja, ambavyo kiuhalisia vinapaswa kuingizwe kwenye mfumo huo.Kutokana na hali hiyo, naibu waziri alisema watendaji hao wamevuliwa hadhi na nyadhifa zao na watabaki kuwa watumishi na watendaji wa kawaida wa idara ya ardhi kwenye maeneo yao ; na nafasi zao zitatafutiwa watumishi wengine wa kuziongoza. Awali, Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Brown Nziku akitoa taarifa kwa naibu waziri alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2018, viwanja 15,529 vimeingizwa kwenye mfumo wa ukadiriaji wa kodi ya ardhi huku viwanja 43,000 vikiwa vimefanyiwa michoro na kupangwa. | 1 |
Mohamed Hamad Waziri wa maji na umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa ametimiza ahadi yake
ya kuchimba visima vitatu vya maji mjini Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara. Ahadi hiyo ilitokana na Mbunge wa Jimbo la Kuteto, Emmanuel Papian CCM
kumweleza Waziri Mbarawa kero ya maji inayowakabili wananchi wilayani humo. Papian alisema wananchi wa mji wa Kibaya, ambako ni makao makuu ya
Wilaya ya Kiteto wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji na kusababisha kutofanya
shughuli zingine za maendeleo “Mhe Waziri hawa wananchi wa Kiteto, Serikali tumefanikiwa kutoa huduma
ya maji safi na salama kwa asilimia 40% tu kiasi kilichobaki wanajitafutia
wenyewe ambapo wanakunywa maji ambayo si safi na salama na kupata magonjwa
mbalimbali tunaomba utusaidie kuchimba visima kupunguza adha hii,”
alisema. Prof Mbarawa akikagua mradi wa maji chini ufadhili wa The Islamic
Foundation shule ya sekondari Kiteto, na mradi wa maji Kijiji cha Nchinila na
Kazingumu baada ya kujionea hali ilivyo alitoa ahadi ya kuchimba visima vitatu
vya maji. “Nitahakikisha tunaondoa kero hii kwa kuchimba visima vya maji vitatu
hapa kwani tatizo hili ni kubwa na linaweza kuleta madhara kwa wananchi,”
alisema Mbarawa. Visima vitatu vya maji vimechimbwa mjini Kibaya ambapo kimoja kipo eneo
la mnadani, Kageze iliyopo Kijiji cha Bwagamoyo na Kaloleni mtaa wa Majengo
mapya. | 1 |
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM BENKI ya I&M Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, lakini inang’ara kwa kutoa bidhaa na huduma za kipekee ambazo zinakidhi mahitaji yote ya mteja katika soko. I&M Tanzania ilitambulisha akaunti mpya ya wanawake ya Tunaweza inayotoa suluhisho kwa wanawake wa ngazi zote kuanzia mmoja mmoja, wajasiriamali hadi kikundi au taasisi. Akaunti hiyo inajitofautisha kwa kutoa huduma bila malipo yoyote, haina makato ya kila mwezi na viwango vyake vya riba vinavutia kwenye akiba. Akizungumza leo jijini Dar es Salaa, katika maonyesho hayo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya I&M, Anitha Pallangyo, alisema kuwa bidhaa hiyo mpya imeunganishwa kwenye mtandao wa benki wa kidijitali ili kuwapa wateja huduma bora na endelevu wakati wowote wanapohitaji. Alisema I&M Tanzania ni sehemu ya I&M Holdings Kenya iliyoanzishwa mwaka 1974 kama kampuni ya huduma za kifedha kabla baadaye kubadilishwa kuwa benki ya biashara. “Mwaka huu inasherehekea miaka kumi ya huduma zetu katika soko la Tanzania. Tunafurahi kuendelea kuhudumia wateja wetu na wateja wapya, pia tunashukuru wateja wetu na washikadau wote walioshiriki katikakuiletea benki mafanikio makubwa kwa kipindi chote cha miaka kumi kwenye soko.” “Tunatoa huduma kadhaa za kifedha ikiwa ni pamoja na akaunti ya akiba, current akaunti kwa madhumuni ya biashara, mikopo ya biashara, huduma za kubadili fedha, uhamishaji fedha kitaifa na kimataifa, huduma za kidijitali ambazo hutoa fursa kwa mteja kupata huduma za benki kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *150*32# au kupitia iClick- huduma ya benki kwa njia ya mtandao inayopatikana bila kikomo kwa saa 24,” alisema Anitha Meneja Masoko na Mawasiliano huyo wa benki hiyo, alisema kuwa pia benki yao wanatoa unafuu na urahisi wa kupata mikopo na huduma nyingine kadhaa ambazo ziliwafanya watu waliotembelea banda lake kwenye maonyesho ya Sabasaba lililopo ukumbi wa Karume, upande wa kulia wa lango la kuingilia kuhamasika na kutaka kujua zaidi kuhusu benki hiyo. “I&M inafungua milango kwa Watanzania wote kwenda kujiunga na benki inayojali mahitaji yao, iliyo tayari kuwapa huduma za kipekee za kifedha kupitia wafanyakazi wake wenye uzoefu zaidi katika kutoa huduma bora kwa wateja. “Mbali na kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba, benki hiyo inatoa huduma zake bora kupitia mtandao wa matawi yake yaliyoko maeneo ya Maktaba, Indira Gandhi, Nyerere, Kariakoo, Oysterbay pamoja na mikoani ikiwa ni pamoja na Moshi, Arusha na Mwanza,” alisema Timu ya wafanyakazi wa mauzo na idara ya masoko wa benki hiyo kutoka matawi yake ya Dar es Salaam inayoongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya I&M, Anitha Pallangyo na Ofisa Masoko na Mawasiliano, Debora Mwakyoma wapo kwenye maonyesho hayo ili kuwapa wageni na wale ambao wanataka kuwekeza katika benki inayoaminika na salama ikiwa na huduma za ATM zinazopatikana kwa saa 24. | 0 |
Rais wa China Xi Jinping ameitaka New Zealand kutobagua makampuni ya China
wakati alipokutana na Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, ambaye nchi
yake ilikataa ombi la kampuni la China la masuala ya mawasiliano Huawei kujenga
mtandao wa simu za mkononi wa 5G. Ardern, akiwa katika ziara ya siku moja nchini China, alisema kabla ya
mkutano na Xi kwamba ana matumaini ya kuwa na majadiliano na Serikali ya China
juu ya uamuzi wa shirika la New Zealand la intelijensia kukataa ombi hilo. Mahusiano na China yameingia katika hali ya wasi wasi chini ya serikali ya
Ardern ambayo imeonesha wazi wasi wasi wake juu ya kuongezeka kwa ushawishi wa
China katika eneo la kusini mwa bahari ya Pasifiki. Wakikutana mjini Beijing Xi alimwambia Ardern kwamba China imekuwa wakati
wote ikiiangalia New Zealand kama rafiki na mshirika mwaminifu. | 3 |
RIBEIRA, PORTO MLINDA mlango wa klabu ya Porto, Iker Casillas, amesema amekuwa na furaha kubwa ya kuifunga Chelsea na si kumfunga kocha wake wa zamani Jose Mourinho. Awali wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Real Madrid, lakini Casillas anaamini kuwa kiwango
chake kilishuka kutokana na tabia ya kocha huyo kumuweka benchi katika michezo mbalimbali. Hata hivyo, Casilas mwanzoni mwa Septemba alisema Mourinho amemfanya thamani yake ishuke katika soka hivyo hana uhusiano mzuri na kocha huyo, lakini katika mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ulikuwa wa kwanza kuwakutanisha wawili hao. Katika mchezo huo wa juzi Chelsea ilijikuta ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 na kumfanya mlinda mlango huyo kuwa na furaha kubwa kutokana na ushindi huo. “Sina furaha kwa sababu nimemfunga kocha wangu wa zamani Jose Mourinho, lakini nina furaha kubwa kwa sababu
nimeisaidia timu yangu kuipa ushindi. “Sina tatizo na Mourinho na hata kabla ya mchezo niliweza kusalimiana na kocha huyo kwa kushikana mikono, siwezi kukumbuka ya zamani ambayo alinifanyia nikiwa Madrid, kwa sasa ni kuangalia yajayo,” alisema
Casillas. Mchezo huo ilipigwa katika Uwanja wa Estadio do Dragao na kuwafanya Porto wafanikiwe kushika nafasi ya pili katika kundi G. | 2 |
Tima Sikilo, Dar es Salaam Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema
kufanya usajili kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao itategemea kama
ataendelea kuwepo kwenye kikosi hicho. Aussems alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu
2018/19, kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre
Lechantre hivyo mkataba huo unatarajia kumalizika mara baada ya msimu huu kuisha. Akizungumza na Mtanzania Digital, leo Aprili 5,
Aussems amesema iwapo kama angekuwa na uhakika wa kuwepo msimu ujao wa 2019/20
angejua afanye usajili wa aina gani. “Mkataba wangu upo mwishoni hivyo siwezi kutaja mchezaji ninayetaka kumsajili wakati sijui kama msimu unaofuata nitaendelea kuwa mwongozaji wa gurudumu la kikosi cha Simba ,” amesema Aussems. Aidha, kocha huyo ameweka wazi kuwa tetesi
zilizopo kuhusu Meddie Kagere na Jonas Mkude kutakiwa na timu nyingine ni
habari ambazo anazisikia lakini hafahamu chochote. | 2 |
Nairobi, Kenya WAOMBOLEZAJI
katika mazishi ya Rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi wamehimizwa kuwahi
mapema kwenye mazishi ili wapate maziwa na viburudisho vingine. Serikali ya
Kenya imesema itatoa viburudisho kwa watu 30,000 wa kwanza kufika katika
mazishi hayo yatakayofanyika leo. Mratibu wa
jimbo la Rift Valley, George Natembeya
amesema kuwa kutakuwa na viti, soda, maziwa na mikate pamoja na maji kwa watu
30,000 wa kwanza kufika kwenye mazishi na pia watakalishwa kwenye hema. Natembeya
amesema waombolezaji waliosalia watakaribishwa tu ndani ya eneo la makazi,
lakini hawatapata mahala pa kukaa. Amesema pia
kwamba vitafunio vitatolewa kwa wale wa kwanza watakaohudhuria mazishi. “Atakayefika
kwanza ndiye atakayepewa wa kwanza “, alisema Matembeya huku akiwataka
waombolezaji kufika mapema. Aidha usafiri
utatolewa kuanzia mji wa Nakuru hadi katika makazi ya Moi ya Kabarak yapata
kilomita 20 (sawa na maili 12.4) kutoka Nakuru mjini. Baadhi ya Wakenya
kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa vigezo vya kauli hiyo ya Serikali ya
kutolewa kwa viburudisho vya bure kwa waombolezaji. Kupitia
ukurasa wa Twitter Modal realism@MozDefinitely amesema serikali inaogopa sana
kuwa idadi ya watu watakaojitokeza kwenye mazishi itakua ya chini, kwa hiyo
imelazimika kuwahonga wakenya wasio na ajira kuhudhuria mazishi?. @kamau_wanjohi
anasema njaa na kiu ni kichocheo cha kutosha cha kuwavutia watu kuhudhuria
mazishi. Naye Kimathi
@CounselKimathi ameandika Wakenya wanapaswa kuangaliwa kama wanajua
wanachokitaka. Tunachokihitaji
sio mkate na soda ndogo…tunaweza kujinunulia hizi wakati wowote kwenye maduka.
Tunataka kuona maendeleo” aliandika kupitia Twitter; Ken Mapesa
alishauri tofauti, ambapo alisema wangetoa maziwa badala ya soda wakati wa
mazishi ili wakumbuke maziwa aliyoyatoa Moi wakati wa utawala wake kwa watoto
wa shule yaliyojulikana kama Maziwa ya Nyayo: Rais mstaafu
Moi aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Jumanne wiki iliyopita na Wakenya
mbalimbali wamekua wakipata fursa ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa
mwili wa kiongozi huyo aliyeliongoza taifa lao kwa muda wa miaka 27. Mwili wa
Hayati Moi utazikwa katika makazi yake ya Kabarak eneo la Nakuru siku ya
Jumanne. | 3 |
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ leo inashuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Cosafa dhidi ya wenyeji Afrika Kusini mchezo utakapoigwa Uwanja wa Gelvandale saa 10:00 jioni.Tanzanite iliingia hatua hiyo baada ya kushinda michezo yake miwili dhidi ya Botswana mabao 2-0 na dhidi ya eSwatini mabao 8-0 na kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Zambia kwa mabao 2-1.Kocha wa timu hiyo Bakari Shime amesema kwa kuwa wanatambua ugumu wa mchezo huo, wamejipanga vyema kuhakikisha wanafanya vizuri ili kutinga hatua ya fainali.Alisema anatambua mchezo huo ni wa mtoano hivyo mikakati aliyoweka ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kutambua kuwa timu itakayofungwa itakuwa imeaga mashindano hayo yanayofanyika Afrika Kusini.“Tunatambua utakuwa mchezo mgumu, lakini kwa upande wetu tumejipanga vizuri kushinda mchezo huo na kucheza fainali kwa upande wetu tumejipanga vizuri,” amesema Bakari Shime.Mchezo wa kwanza wa hatua hiyo utakuwa kati ya Zimbabwe na Zambia utakaochezwa saa nane mchana katika uwanja mmoja na mchezo wa Tanzanite na Afrika Kusini.Tanzanite ni timu pekee mpaka sasa inaongoza kwa kuwa na mabao mengi katika michuano hiyo mabao 11 ikifuatiwa na Zambia yenye mabao 10 timu zote kutoka Kundi B. | 2 |
MWANDISHI WETU-PWANI Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, imeanza mkakati wa kuwaandaa vijana zaidi ya 52 kwa kuwapatia mafunzo ya utalii na kutambua fursa zilizopo katika sekta hiyo ikiwa ni mkakati wa kuinua utalii wilayani humo pamoja na kujiandaa kupokea wageni ambao watakuwa wanapita hapo kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ambapo amesema kuwa vijana ndani ya wilaya hiyo kwa sasa wameamka na wapo tayari kuchangamkia fursa mbalimbali za utalii hasa kwa kuzingatia wamebarikiwa kuwa na kila aina ya vivutio vya utalii. Amesema kuwa hakuna sababu ya vijana kuendelea kubaki nyuma wakati fursa zipo hivyo wahakikishe kwamba kila wanachokiona Wilayani humo ni fursa niwajibu wao Sasa kuchangamkia fursa hizo. “Wilaya Kisarawe inafursa kubwa ya utalii kwani inavivutio vingi na ukizingatia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, imepandisha hadhi msitu wa Pugu pamoja na Kazimzumbwi na pia kuna mapango mengi ya utalii hivyo zote hizo ni fursa,” amesema Jokate Alisema kuwa Kisarawe imekuwa ni chachu ya kuongeza mapato ya halmashauri hiyo ambapo miaka kadhaa ilikuwa inakusanya Sh bilioni moja na kwa sasa yamepanda zaidi na kufikia kukusanya Sh bilioni 2.7 kwa mwaka. Mkuu huyo wa wilaya amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuweza kuona umuhimu wa kujenga barabara ya Kisarawe kwenda Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kwa kiwango cha lami jambo ambalo sasa litachochea maendeleo kutokana na shughuli za utalii. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dk. Shogo Sedoyeka amesema kuwa Kisarawe ni eneo zuri na limejaliwa kuwa shughuli nyingi ikiwamo kuwa lango la utalii kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. | 1 |
Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM TIMU ya Simba leo inajitupa katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, kucheza na Mwadui FC huku kiungo wa kimataifa wa Congo, Mussa Ndusha, akianza kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Tayari Simba imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya Ndusha ambaye anatarajiwa kuanza kwenye mechi hiyo ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu kuanza kwa ligi hiyo. Tangu kuanza kwa ligi msimu huu, beki huyo ameonekana kushindwa kufanya kazi iliyomleta Simba kutokana na kukosa ITC. Ndusha alitua Simba na kupewa mkataba wa miaka miwili, alionekana uwanjani na Simba katika mechi mbili za kirafiki za kimataifa wakati waliposhinda mabao 4-0 dhidi ya AFC Leopard na katika sare ya bao 1-1 dhidi ya URA, zote zilichezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba wanaongoza ligi hivi sasa kwa pointi 29 ikiwa imecheza mechi 12, itaingia katika mechi hiyo wakitoka kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto Africans. Mechi nyingine za ligi hiyo zitakazochezwa leo, Mbeya City wataikaribisha Majimaji katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, Ndanda watakuwa ugenini kucheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani huku African Lyon ikiwa wenyeji kwa Tanzania Prisons katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. | 2 |
CHAMA cha Msalaba Mwekundu Tanzania kimesema baadhi ya watu na taasisi wanatumia vibaya nembo yake kwa manufaa binafsi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Julius Kejo ametaja baadhi ya taasisi na makundi yanayoruhusiwa kutumia nembo hizo ni wanachama, wafanyakazi, maofisa wa kujitolea, taasisi zenye mikataba na Msalaba Mwekundu kutoa huduma kwa mujibu wa taratibu za taasisi hiyo na vikosi vya tiba jeshini.Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni endelevu ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya nembo ya chama hicho, Kejo aliviomba vyombo vya habari visaidie kuelimisha jamii dhidi ya matumizi yaliyo sahihi.Alisema matumizi hayo yasiyo sahihi yanafanywa na baadhi ya hospitali binafsi, maduka ya dawa, waganga wa jadi, wahalifu wa kivita na baadhi ya watu binafsi. “Mfano, katika baadhi ya hospitali za binafsi na maduka ya dawa wamekuwa wakitumia kimakosa nembo ya Red Cross (Msalaba Mwekundu) kama ishara ya kuwapo huduma zao, na hata baadhi ya waganga wa kienyeji nao utakuta wanaweka alama ya Red Cross, ni makosa,” alisema Kejo.Alisema kwa kutokujua, baadhi ya watu na taasisi wanaweza kuwa wanaitumia nembo hiyo bila kujua kuwa hawana mamlaka ya kuitumia. Kwa mujibu wa Kejo, nembo hiyo inayo kazi na matumizi maalumu hivyo, haipaswi kutumiwa kiholela kwa kuwa katika maeneo mbalimbali duiniani, baadhi ya wahalifu wa kivita wamekuwa wakiitumia kinyume na makusudio ya kuwapo kwake.Katika ufafanuzi wa maswali, Kejo alisema ni makosa kuamini kuwa alama hiyo inahusiana na ishara za imani au dini. “Hii nembo haina uhusiano na imani yoyote ya kidini kwa kuwa hata muundo wake si sawa na ule wa baadhi ya imani.Hii blocks (vyumba) zake tano zote zinalingana, lakini hizo za kiimani, sehemu nyingine ni ndefu kuliko nyingine,” alisema. Akasema: “Kwa nchi kama Tanzania yenye amani, hatuwezi kujua kirahisi ubaya na hatari ya matumizi mabaya ya nembo hii, lakini huwezi kujua nani anaitumia vibaya kufanikisha mambo yake mwenyewe.”Chama cha Msalaba Mwekundu kilianzishwa mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge Namba 71 na mwaka 1963, chama hicho kikatambuliwa rasmi na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC). Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu anaweza kuadhibiwa kwa kutu | 1 |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewaomba wananchi wa Jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam, kumchagua mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, Asia Msangi, kwani hatawasaliti wananchi wa jimbo hilo, bali atawatumikia kwa uaminifu mkubwa.Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Majohe jimboni humo, wakati akimnadi mgombea huyo wa ubunge.“Mchagueni Asia. Mgombea wetu ana historia nzuri, ni Mcha Mungu na ni kiongozi katika makanisa, lakini pia ni mtu ambaye amejitoa kuwasaidia watu kupitia kazi mbalimbali hasa kina mama,” alisema Dk Mashinji.Pia Mashinji alisema hakuna nchi inayoendeshwa kwa Ilani ya chama fulani, bali kwa Mpango wa Maendeleo. Alieleza kuwa vyama vya siasa havina mpango unaoongoza nchi.“Hata sisi Chadema hatuwezi kuendesha nchi kwa mipango au Ilani yetu, vyama visitudanganye. Baada ya chama kushinda uchaguzi na kuingia madarakani unaandaliwa mpango wa serikali wa miaka mitano unapelekwa bungeni na kupitishwa, huu ndio mpango unaotekelezwa na serikali na si Ilani ya chama fulani,” alisema Dk Mashinji.Alisema mwanasiasa ambaye anakihama chama kwa madai kuwa anakwenda kuunga mkono utendaji wa serikali, madai hayo sio ya msingi kwani mpango wa serikali unatekelezwa na vyama vyote.Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Mdogo katika jimbo hilo, Frederick Sumaye alihamasisha amani, utulivu na umoja katika uchaguzi huo, utakaofanyika Jumapili wiki hii. Mgombea wa chama hicho, Sia, aliwaomba wananchi wa kata hiyo ya Majohe, kumchagua yeye kwani amejitoa kushirikiana nao. | 1 |
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekanusha habari inayosambaa katika mitandao ya kijamii, ikidai kuwa TRA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetangaza nafasi za kazi 500 za uelimishaji uchangiaji kodi na ukusanyaji wa kodi ya majengo vijijini.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi ya TRA, wananchi wameombwa kuipuuza habari hiyo.“TRA inakanusha taarifa hiyo na inauomba umma kuipuuza kwa sababu haina ukweli wowote,” ilifafanua taarifa hiyo ya TRA jana.Taarifa hiyo imesema hata mawasiliano ya kwenye habari hiyo si rasmi ya TRA hivyo wananchi wawe makini ili kuepuka kutapeliwa.Kumekuwepo na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari, “Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na Benki Kuu (BOT)” kutangaza ajira 500.Hatua hiyo ndiyo iliyoifanya TRA kukanusha na kutahadharisha wananchi kuhusu taarifa hiyo. TRA imewaomba wananchi kupiga simu bure Kituo cha Huduma kwa Wateja kupitia namba 0800 750 075 au 0800 780 078 au kutuma barua pepe: huduma@tra.go.tz, au kutembelea tovuti www. tra.go.tz.Pia, wanaweza kutuma ujumbe kwa njia ya WhatsApp kwenda namba 0744-233-333 ili kupata ufafanuzi wa masuala yao. | 1 |
WAZIRI wa Nishati Dk Medard Kalemani ameagiza kuunganishwa kwa huduma ya umeme kwa vijiji viwili vya Busomeke na Mizanza vilivyopo katika Kata ya Mwisi wilayani Igunga, Tabora kufuatia ziara aliyoifanya katikati ya wiki hii. Waziri Kalemani maagizo hayo katika ziara yake wilayani Igunga huku akisisitiza kuwa matarajio yake ni kuona suala hilo linatekelezeka mapema ili hadi inapofika Oktoba Mwaka huu. Katika mkutano wake na wananchi wa Kata ya Mwisi Waziri Kalemani aliekeleza umeme huo kupelekwa katika vitongoji vyote vilivyopo katika kata hiyo na Vijiji Vyote na kumtaka mkandarasi aliyepo katika eneo hilo kuhakikisha analitekeleza suala hilo kwa muda alioutoa.“Lengo la ziara hii ni kuhakikisha lengo la Serikali la vijiji vyote kuunganishwa na Nishati ya Umeme linafikiwa ifikapo mwaka 2012 ili kuwaondolea adha Wananchi la ukosefu wa huduma ya umeme ambayo ni muhimu kwa maendeleo yao na Nchi kwa ujumla” alisema Dk Kalemani | 1 |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amechukizwa na kusuasua kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Hamai kilichopo Wilaya ya Chemba.Jafo alionesha kuchukizwa kwake wakati wa ziara ya kukagua miradi ya afya inayoendelea kujengwa katika halmashauri hiyo, hasa baada ya kuwa fedha za ujenzi wa kituo hicho kufikishwa kituoni hapo zaidi ya miezi 10 iliyopita. “Kituo cha Hamai kimepokea fedha tangu Januari 2018, lakini mpaka sasa ujenzi haujakamilika wakati vituo vingine vyenye mazingira magumu zaidi vimekwishakamilisha ujenzi tena kwa ubora wa hali ya juu,” alisema Jafo.Alisema fedha zilizoletwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ni Sh milioni 400 ambazo zinadaiwa kutumika zote, huku wakihitaji Sh milioni 29 ili kukamilisha ujenzi huo. “Nashindwa kuelewa ni kitu gani cha gharama kilichowekwa katika kituo hiki ambacho kimesababisha fedha hizo kwisha kabla ya ujenzi kukamilika. Inakuwaje halmashauri zingine wametumia kiasi hicho cha fedha kukamilisha miundombinu yao, lakini kwa Chemba fedha hizo zisitoshe kukamilisha kituo, kuna tatizo gani hapa?” alihoji Jafo. Jafo aliongeza: “Hakuna fedha itakayoongezwa katika kituo hiki cha Hamai, nataka majengo yote yaliyojengwa hapa yakamilike haraka iwezekanavyo na kwa ubora unaotakiwa bila kuwa na sababu zingine zozote.Mkurugenzi nendeni mkatafute fedha popote pale mkamilishe kituo hiki.” Aidha, akizungumza na wananchi, Jafo alitumia fursa hiyo kuwaeleza kinagaubaga kuwa Halmashauri ya Chemba ni miongoni mwa halmashauri zilizopata fedha nyingi za ujenzi wa vituo vitatu vya afya na hospitali ya wilaya. “Sitavumilia kuona fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na hospitali zikitumika vibaya. Nitasimamia sheria na atakayekwenda kinyume na maelekezo atachukuliwa hatua kali,” alisema.Aidha, alitoa wiki mbili kwa uongozi wa halmashauri hiyo, kukamilisha ujenzi wa kituo hicho na kuahidi kurejea tena Hamai ifikapo Januari 15, mwaka huu kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia alisema kusuasua kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Hamai, kunatokana na ujanja ujanja wa baadhi ya watumishi kutaka kufanya vitu wenyewe bila kushirikisha kamati za ujenzi. “Mara nyingi tulipowashauri hawakutaka kusikiliza ushauri huo na ndio baadhi ya sababu zilizochangia kutokamilika kwa ujenzi huo wa kituo kwa wakati,” alisema Nkamia.Awali, akitoa maelezo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba, Dk Semistatus Mashimba alisema uhaba wa watumishi hususani katika idara ya ujenzi na manunuzi, ndio uliochangia ucheleweshaji katika ujenzi huo. “Katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo hiki tumekumbana na changamoto kadhaa, ikiwamo ya uhaba wa watumishi hususan katika idara ya ujenzi na manunuzi ambazo ndio muhimu katika kusimamia shughuli zote za ujenzi wa vituo vya afya,” alisema. Vituo vitatu vya afya katika Wilaya ya Chemba, vimepokea Sh milioni 400 kwa kila kituo, za ujenzi wa miundombinu ya afya ya vituo vya Hamai, Mrijo na Kwamkoro. Pia, serikali ilitoa Sh bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya. | 1 |
AFRIKA ikiwemo Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), inahitaji Dola za Marekani trilioni sita katika kujenga na kuimarisha miundombinu ya uwekezaji ikiwemo barabara, bandari, reli, nishati, teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehema) ifikapo mwaka 2030.Hayo yamebainishwa na wadau na washiriki wa Wiki ya Maonesho ya Nne ya Viwanda ya SADC, yanayoendelea jijini Dar es Salaam.Akiwa miongoni mwa watoa mada, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko alisema Afrika na SADC zinahitaji fedha hizo Dola za Marekani trilioni sita katika kutekeleza miradi ya miundombinu mbali mbali ya uwekezaji ili kukuza uchumi na maendeleo ya kitaifa na kikanda.Kakoko alisema tofauti na Asia na Ulaya na mabara mengine, suala la uwekezaji katika miundombinu halijapewa umuhimu wa kutosha barani Afrika.Hivyo, alisema kuna haja kwa serikali za bara hilo na SADC kuona namna gani zinaweza kuongeza uwekezaji katika miundombinu ili kuongeza uzalishaji, mapato, ajira, kuimarisha ajira zilizopo pamoja na kuboresha maisha ya watu.Katika hilo, alitoa mfano kuwa asilimia 80 ya biashara ya kimataifa, inafanyika kwa njia ya maji, hivyo ni muhimu kuimarisha miundombinu ya bandari kwa kuwa ndiyo milango inayotumika kuingiza bidhaa au kusafirisha bidhaa nje ya nchi.“Maendeleo ya ukanda wa SADC yanategemea sana miundombinu imara kama bandari au reli kwa sababu ukosefu wa miundombinu au uwepo wa miundombinu duni inadumaza ufanisi wa kibiashara wa kikanda, kwa mfano Bandari ya Dar es Salaam inahudumia nchi sita kwa upande wa magharibi ambazo pia zinafanya biashara na nchi zingine kama Japan, China na India, kwa upande wa mashariki inazihudumia nchi za Mashariki ya Kati na Mashariki ya Mbali, hayo yote yanawezekana kwa sababu Tanzania iko kati kati kijiografia na inaweza kufanya biashara ya kibandari na nchi zingine,” amesema Kakoko.Alisema asilimia 40 mpaka 50 ya bajeti ya Tanzania, inaelekezwa kwenye ujenzi na uimarishaji wa miundombinu mbali mbali ikiwemo ya usafiri na usafirishaji, nishati na mawasiliano, jambo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya watu.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Profesa Damian Gabagambi alisema moja ya changamoto zinazozikabili nchi za Afrika na SADC ni upatikanaji wa fedha za kuwekeza katika ujenzi na uimarishaji wa miradi ya miundombinu.Alisema pamoja na hilo, pia kuna ugumu katika SADC wa kuvutia mtaji kutoka sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa miradi ya miundombinu, kwa kuwa hawana uhakika wa usalama wa fedha zao.Kwa mujibu wa Profesa Gabagambi, katika kipindi cha miaka 50 sasa, Afrika imeshindwa kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu kutokana na hatari mbali mbali zinazoweza kujitokeza na kuwatia hasara. | 0 |
SERIKALI imesema hadi Desemba 31, mwaka huu, Watanzania wote wenye sifa za kupata vitambulisho vya Taifa watakamilisha usajili wa kuchukua alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki, kazi inayoendelea kufanywa sasa.Sambamba na hilo, serikali imesema itanunua mashine mpya za uzalishaji wa vitambulisho vya taifa zenye uwezo mkubwa zaidi kwa lengo la kuharakisha upatikanaji vitambulisho hivyo.Hayo yalibainishwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Buyuni, Christopher Chiza (CCM). Mbunge huyo alihoji serikali ina mpango gani wa kuharakisha zoezi la kutoa vitambulisho vya taifa wavitumie kwa shughuli za maendeleo.Akijibu swali hilo, Masauni alisema serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inaendelea kukamilisha usajili kwa watu wote wenye sifa ikitarajiwa kukamilisha kazi ya uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki Desemba 31, mwaka huu.Alisema hadi sasa vitambulisho milioni tano vya taifa vimeshatolewa na kwamba vingine milioni 13 vipo hatua za mwisho kutolewa na kwamba hadi ifikapo Desemba mwaka huu, lengo lao ni kutoa jumla ya vitambulisho milioni 24.4. “Wananchi waendelee kuwa watulivu na wale waliokamilisha uchukuaji alama za vidole, saini na picha na hawajapata vitambulisho, huenda ndio hivyo milioni 13 vilivyo hatua za mwisho kutolewa,”alisema Naibu Waziri Masauni.Aidha alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila kukwama ikiwemo wale wanaojisajili kibiashara Brela, NIDA imefungua dawati maalum la usajili katika ofisi hizo. Alisema usajili huo unafanywa kwa kuzingatia sifa bila kuathiri masharti ya kisheria na kanuni.Akijibu swali kuhusu utaratibu gani umewekwa na serikali wa kuwapa vitambulisho wananchi wanaokaa mipakani bila kuathiri malengo ya utoaji vitambulisho hivyo, Waziri Masauni alisema utaratibu wa kuwapa vitambulisho hautofautiani na ule wa kawaida uliopo. | 1 |
Ngoma alitarajia kuwasili Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga, lakini pia mshambuliaji huyo alishafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Simba na inasemekana ujio wake ulikuwa ni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo msimu ujao.Kwa mujibu wa Mtandao wa KickOff.com, Ngoma raia wa Zimbabwe, amekamilisha zoezi lake la usajili kwenye klabu hiyo, baada ya kuwa huru kufuatia kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na mabingwa wa soka Tanzania Yanga.Taarifa hiyo imesema Ngoma alisaini mkataba huo wa miaka mitatu baada ya kufuzu vipimo vya afya na anatarajiwa kujiunga na miamba hao wa ligi ya ABSA,ambao kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo. Akiwa Polokwane City, Ngoma anatarajiwa kukutana na Mzimbabwe mwenzake, George Chigova aliyewahi kucheza naye FC Platinum chini ya kocha Norman Mapeza. | 2 |
Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam BAADA ya ujio wa magwiji wa zamani wa timu ya Real Madrid kufanyika kwa mafanikio makubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ameeleza kuwa anafanya uwezekano wa kuileta timu halisi ya Real Madrid yenye nyota, Cristiano Ronaldo au Barcelona yenye staa, Lionel Messi. Magwiji hao walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya magwiji wa zamani wa Tanzania ‘TSN Tanzania Eleven’, iliyoisha kwa Real Madrid kushinda kwa mabao 3-1, huku nyota wa mechi akiwa mshambuliaji, Ruben de la Red aliyefunga mabao matatu ‘hat trick’. Rais Kikwete alieleza nia yake hiyo juzi usiku kwenye hafla ya kula chakula cha usiku na magwiji wa timu hizo, huku akisema tayari wameanza mazungumzo na Real Madrid, kufanikisha ujio wa timu hiyo halisi. “Nimefarijika na ujio huu mkubwa nchini, ila kwa sasa nia yetu ni kuileta timu halisi yenyewe, tunafanya nao mazungumzo na timu hiyo hivi sasa ili kufanikisha hilo na hata magwiji hawa watatuunga mkono kwa hilo kutusaidia,” alisema akiwaambia wachezaji wa kikosi cha ‘TSN Tanzania Eleven’. “Magwiji hawa waliotua nchini wametuambia ni rahisi Madrid kuja hapa, katika kipindi cha kujiandaa na msimu mpya wa ligi ‘pre season’ na sio nyakati kama hizi ambazo ipo kwenye mashindano,” alisema. Kikwete alizidi kuongeza kuwa endapo nia ya kuileta Madrid itashindikana, basi watahamia pia kwa wapinzani wao Barcelona, kwa kuwatumia moja ya wadhamini wao Kampuni ya bia ya Castle Lager yenye maskani yake nchini Afrika Kusini, kwa kuwashawishi kuwaleta nchini. “Unajua nia ya mdhamini ni kupata soko la matangazo, hivyo tutakapowatumia Castle ni rahisi sana kupeleka ushawishi wao na kuileta Barcelona nchini, kwani ni njia mojawapo ya kujitangaza,” alisema. Katika hatua nyingine, wachezaji wa zamani wa Tanzania wakiongozwa na makocha wao, Boniface Mkwasa, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Fred Minziro walimshauri Kikwete kutumia fursa hiyo ya ujio huo, kuwapeleka wachezaji wetu vijana kwa ajili ya kupata mafunzo ya soka na kutanua wigo wa kucheza soka la kulipwa huko. Ujio wa magwiji hao nchini umeratibiwa na Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), kwa kushirikiana na Rais Kikwete pamoja na kampuni nyingine kama vile Tropical Electronics, Vodacom Tanzania, Fast Jet, Hoteli ya Ladger Plaza, Binslum Tyres na ATN Petroleum. | 2 |
PAMOJA na serikali kudhibiti matumizi na uingizwaji wa dawa za kulevya nchini kwa asilimia 90, lakini baadhi ya watu wamebuni mbinu mpya za matumizi ya dawa hizo, imeelezwa.Miongoni mwa mbinu mpya ni kwa watumiaji kutumia dawa rasmi za hospitalini zikiwemo za usingizi na wakati mwingine kuzichanganya na kemikali na kutumika kama dawa za kulevya. Aidha, baadhi ya watu wamekuwa wakisafirisha dawa za kulevya zikiwemo bangi na mirungi, kwa kuzichanganya na mazao ya biashara na chakula.Mbinu hizo mpya ziliwekwa bayana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam jana, wakati akifungua mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na biashara ya dawa za kulevya, uliohudhuriwa na washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi 55. Alisema, mkutano huo ujulikanao kama (28th HONLEAAfrika), umelenga kuweka mipango ambayo nchi za Afrika zinaweza kuitekeleza katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya sambamba na kudhibiti mianya ya matumizi ya dawa hizo.“Tanzania tumeshaanza mikakati hiyo na kwa kiasi kikubwa tumedhibiti matumizi ya dawa za kulevya, lakini tumebaini kuwa bado kuna matumizi ya aina za dawa za hospitalini ambazo zinapelekea watu kupata kilevi zinatumiwa vibaya,” alisema. Alisema, “Mikakati hii tunaendelea nayo kwa kuwa pia kuna matumizi ya kemikali ambazo zinatumika vibaya kuchanganywa na dawa... lengo letu ni kumaliza kabisa matumizi ya dawa za kulevya na kupitia mkutano huu tutaweka mikakati na kubadilishana mawazo kwa nchi zetu ili kufikia hatua ambazo zitasaidia kudhibiti dawa za kulevya,” alisema.Kutokana na hayo, Majaliwa alizitaka nchi hizo za Afrika, kutengeneza sheria ya pamoja ya kudhibiti matumizi na usafirishaji kwa kuwa kila nchi ina utamaduni wake na mazingira yake. Alitoa mapendekezo kwa wajumbe wa mkutano huo, ikiwemo kuangalia namna bora ya kuweka msingi mzuri wa usimamaizi wa udhibiti uzalishaji na kuweka mpango mkakati wa pamoja wa kudhibiti dawa za kulevya, kwani hatua zisipochukuliwa, hatua hali itaendelea kuwa mbaya.Pia aliomba kwamba ziangaliwe na kupendekezwa njia nzuri za kushirikisha taasisi zinazotumia kemikali zinazotengenezwa viwandani, ambazo kwa wasio waaminifu wanazitumia kutengeneza madawa ya kulevya ili waweze kuwadhibiti. Alisema wamekuwa wakichukua hatua mara moja kwa wale walioathirika na madawa hayo, ambapo pia taasisi za kimataifa zimekuwa zikisaidia kujenga maeneo na vituo vya kuwahudumia walioathirika. Alitaka nchi hizo za Afrika kuunganisha nguvu ili kuzuia mianya ya kusafirisha dawa za kulevya, sambamba na kuangalia njia za kuwadhibiti baadhi ya watu haswa vijana ambao wamekuwa wakifanya biashara ya usafirishaji wa dawa hizo.Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi, ambazo zimeimarisha sheria ya kupambana na udhibiti wa dawa za kulevya, hivyo nchi zote za Afrika zikaona ni vyema kufanyia mkutano huo Tanzania “Katika mkutano huu pia watazungumzia namna nzuri na mikakati ya kudhibti uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya na usafirishji wa njia zote za dawa za kulevya kwa bahari, nchi kavu, usafirishaji wa binadamu na matumizi ya fedha haramu,” alisema.Mapema, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Vitendo vya Uhalifu(UNODC) Ukanda wa Afrika Mashariki, Dk Amado Philip de Andres alisema imebainika kwamba wafanyabiashara wakubwa hasa wa heroin ndiyo wafadhili wa ugaidi haswa katika bara la Afrika. | 1 |
Na AGATHA CHARLES WAKUU wa mikoa 13, makatibu wakuu wanne, ma-naibu katibu wakuu 6, makatibu tawala wanne na viongozi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Magereza wako katika mafunzo ya siku tano katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Kunduchi, Dar es Salaam. Wakuu hao na mikoa yao kwenye mabano ni John Mongella (Mwanza), Mrisho Gambo (Arusha) na Anthony Mtaka (Simiyu). Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya nne chuoni hapo jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Issa Haji Gavu alisema washiriki 45 wanapatiwa mafunzo ya muda mfupi chuoni hapo. “Malengo ya chuo ni kutayarisha viongozi kwa ajili ya ulinzi na usalama. Viongozi kufahamu masuala ya ulinzi na usalama ni vyema ili kukabiliana na matishio yoyote yanapofika,” alisema Waziri Gavu. Alisema katika mafunzo hayo, washiriki watajifunza masuala ya ulinzi na usalama kwa upana wake. Waziri Gavu, alisema hakuna tishio la usalama bali ni kuandaa viongozi kukabiliana na hali yoyote ya maafa au janga. Naye mkuu wa chuo hicho, Dk. Matern Lumbanga alisema kozi hiyo itawafundisha washiriki misingi ya uadilifu, masuala ya uongozi wa umma na utendaji wa kila siku wa viongozi. Mmoja wa washiriki hao, Mtaka alisema kozi hiyo ni nzuri hasa kwa vijana. “Ni kozi ya msingi kwa viongozi, si kozi ya kukosa kwa wenye dhamana hasa vijana na ni muhimu katika kuelekea uchumi wa nchi yetu na viwanda,” alisema Mtaka. Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi, alisema ana matarajio makubwa katika kuelewa masuala ya usalama na kujua viashiria vyake katika mkoa na hata nchi. Alisema kwa sasa mkoa wake uko shwari katika suala zima la usalama. Washiriki hao wanatarajia kuihitimu mwishoni mwa wiki hii. | 1 |
VITA dhidi ya ujangili imeanza kuzaa matunda ikiwemo kuongezeka kwa wanyama na kupungua kwa vitendo vya ujangili ambapo kiwango cha mauaji ya tembo kimepungua kutoka tembo 194 mwaka 2016 hadi kufi kia tembo 23 hadi kufi kia Juni 2018.Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolph Mkenda wakati akifungua mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa wa Polisi, Waendesha Mashtaka wa Serikali, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka za Hifadhi za Taifa, katika kukabiliana na ujangili.Profesa Mkenda alisema katika kipindi hicho meno 211 na vipande 413 vya meno ya tembo, silaha 355 na risasi zaidi ya 20,000 vilikamatwa. Alisema kulingana na kauli za wadau wa utalii katika Pori la Akiba la Selous idadi ya wanyama imeongezeka. “Selous idadi ya wanyama imeongezeka, kwenye Mbuga ya Ruaha wawekezaji wanasema wamekiri kuongezeka kwa idadi ya wanyama na kutaka jitihada zaidi kuongezeka ili kukabiliana na vitendo vya ujangili,” alisema. Aliwataka kuhakikisha wanapambana na ujangili na uharifu katika Sekta ya Misitu na wanyama.Alisema jitihada za kikosi kazi haziwezi kuzaa matunda bila kuungwa mkono na Jeshi la Polisi. Naye Mkurungezi wa Pams Foundion Elisifa Ngowi alisema wamekuwa wakifadhili mapambano ya ujangili kwa mafanikio makubwa sana na hatua hiyo ya kuunganisha nguvu kwa vyombo vyote itasaidia kufikia mauaji ziro ifikapo mwaka 2024, pia inasaidia kupunguza mlolongo mrefu wa mapambano dhidi ya mauaji ya wanyama.Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji Ujangili na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi Taifa cha Kuzuia na Kupambana na Ujangili, Robert Mande alisema mkutano huo umehudhuriwa na washiriki 136. | 1 |
PARIS, UFARANSA NYOTA wa mchezo wa tenisi namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic, amefanikiwa kutwaa taji la tano la michuano ya wazi ya BNP Paribas, iliyofanyika nchini Ufaransa. Bingwa huyo ametwaa taji hilo baada ya kumshinda mpinzani wake, Milos Raonic, kwa seti 6-2 6-0. “Imezidi kuwa siku ya furaha kubwa kwa upande wangu kwa kutwaa taji hili, ninaamini huu ni mwanzo mzuri kwa ajili ya michuano mingine,” alisema Djokovic. Kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka, amefanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kumshinda mpinzani wake, Serena Williams, ambaye ni nyota namba moja kwa ubora kwa wanawake. Victoria alifanikiwa kuibuka kidedea kwa kumshinda seti 6-4 6-4. Hata hivyo, Victoria amedai kwamba japokuwa wameshinda, lakini alikuwa na ushindani mkubwa na mpinzani wake. | 2 |
Na DERICK MILTON WANANCHI wa Kijiji na Kata ya Ngulyati Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wamedai kuwapo mchezo mchafu kutoka kwa wahudumu wa Kituo cha Afya Ngulyati kuandika taarifa za wagonjwa hewa. Madai ya hayo ya wananchi yalitolewa juzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka kwenye mkutano wa hadhara ulifanyika mjini Ngulyati. Wananchi hao walisema wahudumu hao wamekuwa wakifanya hivyo ili kutumia dawa kwa matumizi yao binafsi huku wazee wakinyimwa huduma za matibabu bure kama inayotakiwa. Mmoja wa wananchi hao, Ramadhani Kuyege, alisema imekuwapo tabia ya wahudumu wa afya katika kituo hicho kuandika taarifa za wagonjwa hewa. Alisema watumishi hao pia wamekuwa wakitumia dawa hizo kinyume na malengo yaliyokusudiwa, hali ambayo imesababisha kituo hicho kukosa dawa kwa muda mrefu. “Huu mchezo ni mkubwa kwenye hiki kituo, wanaiba dawa wanapeleka kwenye maduka yao na nyingine wanawauzia wenye maduka ya dawa na sisi wananchi tunakosa tunabaki kuhangaika kila siku,” alisema Kuyege. Minza Maduhu alidai kuwa kila mara kituo hicho cha afya kimekuwa kikosa dawa na wamekuwa wakiambulia dawa moja tu ya Panadol. “Sisi wazee kila siku tunafukuzwa, tunaambiwa lazima tutoe fedha hakuna huduma za bure wakati kila siku viongozi wanatueleza wazee wanapata huduma bure. “Kituo hiki hakina dawa kila siku wagonjwa wananunua dawa kwenye maduka ya dawa muhimu,” alisema Minza. Kutokana na malalamiko hayo, RC alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kumpelekea taarifa ya matumizi ya Sh milioni 10 ambazo zinatolewa na Wizara ya Afya kwenye kituo hicho. “Kituo hiki kipata pesa kila mwaka Sh milioni 10 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya… niagize kufikia Jumatatu mkurugenzi afike ofisini kwangu kuniletea taarifa ya matumizi ya fedha hizo,” alisema Mtaka. | 1 |
Kwa maana hiyo timu hiyo sasa inarudi Mbande na itakuwa ikifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kwa vile wenyewe (Azam) watakuwa Zanzibar.Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alisema mwanzoni mwa wiki iliyopita kwamba Twiga itaweka kambi Zanzibar ili kubadili mazingira.Hakuna kiongozi yeyote aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo la kukosekana kwa kambi, lakini habari za uhakika kutoka ndani ya TFF zinasema kuwa chanzo cha kambi hiyo kukwama ni kukosekana kwa uwanja wa kufanyia mazoezi.Aidha kocha wa timu hiyo Rogasian Kaijage alisema kukosa mechi za kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya All African Game kunawanyong’onyesha.Twiga Stars ina wiki tatu za kujiandaa dhidi ya michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Congo Brazzaville ambapo Kocha huyo alihitaji mechi za kimataifa kwa ajili ya kujipima kabla ya kuelekea huko.Akizungumza jana baada ya mazoezi yao ya Karume, Kaijage alisema walitamani kucheza mechi za kujipima ili kujua nafasi zao lakini ni gharama na timu haiwezi kumudu.“Hatuna jinsi, tutaendelea na mazoezi yetu na kucheza na timu za wanaume. Tulitaka mechi za kimataifa lakini hakuna pesa za kuwaleta,” alisema.Pia, alizungumzia ukata katika timu hiyo imesababisha timu kushindwa kupata baadhi ya vitu muhimu katika maandalizi yao.Kaijage ameomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo katika maandalizi yake ili kwenda kufanya vizuri katika michuano hiyo ya kimataifa.Kwa mujibu wa Kaijage, leo watahamishia kambi yao Mbande na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, kutokana na kuwa na mazingira tulivu kwa maandalizi yao.Alisema licha ya hali ngumu wanayokutana nayo, lengo lao ni kuhakikisha wanakwenda kushiriki na kushinda. | 2 |
ANDREW MSECHU – DAR ES SALAAM MWANAHARAKATI wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Fatma Karume
amewataka vijana kuwa jasiri katika kudai haki zao, kwa kuwa ndio wanaotakiwa
kuamua hatma ya taifa la kesho. Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana wa
ACT Wazalendo jana Dar es Salaam, ambapo Fatma alisema kuwa vijana wanatakiwa
watambue kuwa hakuna kitu cha kukiogopa isipokuwa woga wenyewe kwa sababu woga
ni kama jela uliyoitengeneza mwenyewe na kujiweka mwenyewe. “Woga humfanya mtu ajisitishe na kujikwamisha mwenyewe, hivyo vijana
wasikubali kutiwa woga ili washindwe kutimiza malengo yao,” alisema Fatma. Alisema katika hilo, vijana wanatakiwa kutokuwa waoga katika kudai na
kutetea demokrasia kwa kuwa haijawahi kuombwa kwa mtu, bali ni haki ya msingi
inayohitaji kupiganiwa. “Na niwaambie, kama mnangoja kugawiwa demokrasia mtanyang’anywa kila
siku. Msifikiri kwamba kwenye nchi yetu ambayo kuna chama kimeamua kuhodhi
dola, mambo haya yatakuwa mepesi mepesi,” alisema Fatma ambaye pia ni
mwanasheria na wakili wa kujitegemea. Alisema mapambano ya kisiasa katika mazingira kama yaliyopo nchini
huwa yanaonyesha matokeo baada ya muda, hivyo wanasiasa lazima wawe na pumzi. “Ninaposema muwe na pumzi, mfano mmoja ni kwa Nelson Mandela ambaye
ilimchukua miaka 27 jela hadi walipoamua kuvunja mfumo wa ubaguzi wa rangi na
kutengeneza katiba mpya. “Katika mapambano haya msitegemee kirahisi kuona matokeo ya moja kwa
moja leo wala kesho, maana CCM imeshasema imeshahodhi dola, hivyo si jambo la
lelemama. “Aliyekuwa na pumzi ndiye atakayeshinda katika mapambano haya. Kazi
hii ni muhimu kwa ngome ya vijana kwa sababu vijana ndio waishio leo na tumaini
letu kwa siku zijazo,” alisema Fatma. Alisisitiza kuwa vijana ndiyo leo ya taifa kwa sababu ni muhimu kwa
walioko kwenye madaraka waambiwe kuwa vijana ndio mtakaoongoza nchi kwa siku
zijazo. Fatma alisema ni vyema vijana watambue kuwa maisha yao bado yapo kwa
hiyo wanatakiwa kujitambua na kujenga taifa la leo na kuamua wanataka
kukumbukwa kama mambo waliyoyafanya kwenye maisha yao kwa siku zijazo. Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu
aliwataka washiriki wote kupokea matokeo na kuunga mkono kwa kutoa ushirikiano
kwa atakayekuwa ameshinda kwenye uchaguzi wa ngome ya vijana. Alisema kwa watakaopata fursa waambiwe jukumu wanalokwenda kulibeba
siyo lele mama hasa wakati huu aliodai kuwa demokrasia ya nchi hii imedorora,
na vijana wengi wamekuwa waoga. “Demokrasia tunayoihubiri kwingine, ambayo tumekuwa tukipiga kelele
pale Serikali ya Magufuli inapoivunja, leo kifanyike humu ndani,” alisema Dorothy.
| 1 |
SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogo(machinga), wafanyabiashara hao wamesema wamepokea uamuzi huo kwa shangwe kubwa na tayari baadhi ya maeneo wameanza kugawiwa.Aidha, wamesema maelekezo ya Rais kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) kutazama upya viwango vya kodi, yatasaidia wafanyabiashara wengi kutokwepa kodi na pia kutotumia njia za panya kuingiza biashara zao.Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga hapa nchini, Steven Lusinde akizungumza na gazeti hili jana, alisema kuwa wanapongeza uamuzi huo wa Rais, kwani walisubiri jambo hilo kwa miaka mingi.“Nashukuru sana kwa uamuzi wa Rais kutupatia vitambulisho na mimi nilikuwepo na nimepewa kitambulisho namba moja, tunapongeza sana uamuzi huu kwani jambo hili tulilisubiri tangu nchi yetu ipate Uhuru na sisi tutambuliwe.Tunaahidi tutamsaidia kwa nguvu zetu zote Rais,” alisema Lusinde. Rais Magufuli juzi alitoa vitambulisho maalumu 670,000 kwa ajili ya wamachinga na mamalishe, ambavyo vitagawiwa nchi nzima kwa lengo la kuwasaidia kufanya biashara zao kwa uhakika na kutambuliwa na TRA.Pia, Rais aliagiza TRA kutazama upya viwango vya kodi, viwe rafiki ili watu wengi waweze kulipa, ambapo alisema anakerwa na makusanyo hafifu ya mapato ya serikali. Katibu wa Wamachinga wa Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, Bruno Mathew alisema wafanyabiashara wa Kariakoo, wamefurahishwa na uamuzi wa Rais kuwapatia vitambulisho.Alisema kuwa kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, tayari wana mfumo wa kuwatambua. “Kwa upande wetu Ilala tayari tulikuwa kwenye mfumo, tayari tulishajisajili kwa hiyo wamachinga wanasubiri tu kupewa vitambulisho vyao kwani wanaamini sasa watafanya biashara katika mazingira ya utulivu,” alisema Bruno.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema tayari wameanza kutekeleza agizo la Rais, ambapo jana walianza kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara na utaratibu huo utaendelea mpaka vitambulisho 25,000, walivyopewa na Rais vitakapoisha na wataomba vingine.“Uamuzi wa Rais kutoa vitambulisho ni jambo jema na sisi leo (jana) tumeanza kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wetu na uzuri ni kwamba tulikuwa tumeshatengeneza kanzi data yetu kuwatambua wamachinga, ambapo tuna wafanyabiashara hawa wadogo 6,236,” alisema Mjema.Alisema wiki ijayo wataanza kutoa vitambulisho hivyo kwa mama lishe pamoja na wafanyabiashara ndogo wengine barabarani. Kiongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Mchungaji Silver Kiondo alipongeza maagizo ya Rais Magufuli kutaka TRA kutazama upya viwango vya kodi, ambapo alisema itasaidia wafanyabiashara wengi kutokwepa kodi.“Tunampongeza Rais Magufuli kutoa maelekezo kwa TRA kuangalia viwango vya kodi viwe rafiki kwa walipa kodi, wafanyabiashara wengi watalipa kodi na serikali itapata mapato, lakini kwa sasa ni watu wachache wanabeba mzigo wa kulipa kodi huku wengi hawalipi,” alisema.Alisema kuwapo na uwazi bandarini na pia kodi zinazolipika, kutasaidia wafanyabiashara kutotumia njia za panya kuingiza mizigi yao. Hata hivyo, alitoa angalizo katika utoaji wa vitambulisho kwa wamachinga uangaliwe kwa umakini, isije kuwa wafanyabiashara wengine wanaficha biashara zao ili waonekane ni wafanyabiashara wadogo wenye mtaji chini ya Sh milioni nne wakapewa vitambulisho. | 1 |
Mashindano hayo ya 15 ya dunia ya mbio za nyika yalifanyika Uganda na kushirikisha wanariadha zaidi ya 500 kutoka nchi 47.Katika mashindano hayo, Tanzania ilipeleka timu kamili ya wachezaji 28 walioshiriki katika mbio za vijana wenye umri chini ya miaka 20 kwa wanaume na wanawake, timu mchanganyiko ya kupokezana vijiti na timu ya wakubwa ya wanaume na wanawake.Kabla ya kuondoka kwenda Uganda, uongozi wa Riadha Tanzania pamoja na makocha wa timu hiyo walitamba kuwa timu hiyo imeweka rekodi kwa kupeleka timu kamili na itarudi na medali.Hata hivyo, katika mbio za kupokezana vijiti za mchanganyiko, Tanzania iliambulia nafasi ya nane baada ya kutumia dakika 24:13.Katika mbio za wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20 kwa wanaume, mwanariadha wa kwanza wa Tanzania alikuwa ni Francis Damian aliyemaliza mbio hizo katika nafasi ya 26 kwa kutumia dakika 25:15 huku Mganda, Muethiopia na Mkenya ndio walimaliza wa kwanza hadi wa tatu.Watanzania wengine katika mbio hizo ni Ramadhani Hamisi, Elisha Wema, Joshua Sulle, Anthony Wema na Yohana Sule waliomaliza katika nafasi ya 34. 36, 41, 45 na 49.Kwa wanawake; Asha Samwe alishika nafasi ya 43, Noela Khaday alikuwa wa 55, Amina Mgoo alikuwa wa 68, Elizabeth Ilanda alikuwa wa 82 na Shamima Salum alikuwa wa 88.Kwa upande wa wanawake wakubwa, Failuna Abdi aliongoza kwa Watanzania baada ya kumaliza wa 16 kwa kutumia dakika 33:48, huku Magdalena Shauri akimaliza wa 28 kwa dakika 35:13 na Angelina Tsere alimaliza wa 38 kwa 35:49.Wengine ni Maylelina Mbua alimaliza wa 50 kwa dakika 36:31 wakati Sara Ramadhan alimaliza katika nafasi ya 51 kwa muda wa 36:32 na Siata Kalinga alimaliza wa 83 kwa dakika 40:13.Washindi wa mbio hizo walikuwa Wakenya, Irene Cheptan, Alice Nawowuna na Lilian Rengeruk waliotumia dakika 31:57, 32:01 na 32:11.Habari zingine kutoka timu ya Tanzania zinadai kuwa baadhi ya makocha wamedai kuwa timu hiyo haijafanya vizuri kwa sababu ya uchovu baada ya kutumia usafiri wa barabara kwenda Uganda.Hata hivyo, timu ya Kenya iliyofanya vizuri katika mashindano hayo nayo ilisafiri kwa basi kutoka Nairobi hadi Kampala.Hayo ni mashindano makubwa kwa Tanzania kushiriki tangu uongozi mpya wa RT ulipoingia madarakani mapema mwaka huu, na Katibu Mkuu wake Wilhelm Gidabuday kuahidi kurudi na medali katika mashindano hayo.Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha, IAAF, washindi sita wa kwanza wa kila mbio ukiondoa zile za vijana, mbali na medali wanapata na zawadi za fedha. | 2 |
RAIS John Magufuli amesema mgogoro wa ardhi wa vijiji 33 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kati ya wananchi na wawekezaji, utapatiwa ufumbuzi hivi karibuni, kwa kuwa ripoti ya Tume ya mawaziri wanane aliyoiunda, imeshakabidhiwa serikalini.Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilikuja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kumweleza kuwa kazi aliyowatuma wameshaimaliza na tayari ripoti wameikabidhi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye pia na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Kwa mujibu wa Lukuvi, wakazi wa vijiji hivyo 33 walipaswa kuondolewa kupitia Tangazo la Serikali Namba 28 kutokana na vijiji hivyo kuwa ndani ya hifadhi.Hata hivyo, uamuzi huo ulisitishwa na Rais Magufuli na kuamua kuunda Tume ya Mawaziri wanane ili kufuatilia suala hilo ili uamuzi wa haki, utolewe kwa upande wa wananchi na upande wa serikali.Lukuvi alimweleza jana Rais Magufuli kwenye mkutano wake wa hadhara na wananchi wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuwa kazi ya kupitia upya maeneo, taarifa mbalimbali na sheria kuhusu mgogoro huo wameshaikamilisha. Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, Tume hiyo imeshakabidhi ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawiziri ili iweze kujadili katika Baraza la Mawaziri chini ya uenyekiti wa Rais Magufuli na kisha kutolewa uamuzi wa ama kuwaondoa wananchi katika vijiji hivyo 33 au la.“Kazi tumeimaliza, tumepata taarifa ya mkoa, tumezungumza na viongozi na wananchi hawa, Baraza la Mawiziri litaketi chini yako na kukushauri na ikikupendeza uamuzi wa vijiji hivi 33 na vijiji vingine vilivyokuwa na matatizo kama hapa Mbarali uweze kutolewa, kwa hiyo Wanambarali suala ya GN 28 limekwisha, msubiri matokeo yakayotolewa na vikao halali,”alieleza Lukuvi.Kuhusu mgogoro wa mashamba ya Kapunga na Highland, Lukuvi alisema nao umeshafanyiwa kazi. Alisema mashamba hayo yalibinafsishwa na serikali kwa mujibu wa sheria na wanunuzi walipatikana. Alisema shamba la Kapunga lilinunuliwa na Kampuni ya Tanzania Export Trading Company ya Patel, wakati shamba la Highland lilinunuliwa na Mbunge wa Mbarali wa sasa, Haroon Mulla Pirmohamed.Baada ya hayo yote, Lukuvi alisema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, iliamua kufunga ekari 4,675 zilizokuwa zimeingizwa kwa mwenye shamba wakati zilitakiwa kuwa za wananchi na kuongeza kuwa kazi ya kuzirudisha ilikamilika mwaka 2016 wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa Abbas Kandoro.“Baada ya mgogoro kati ya vijiji 11 na mmiliki wa shamba la Highland, tulifanya uhakiki ili kujiridhisha kama kweli shamba hili liliingia kwenye mipaka ya wananchi, baada ya uhakiki, ekari 1,352 zilikatwa kutoka shamba hili na kurudishiwa wananchi na mwaka 2018 Highland alipewa hati nyingine ambayo ina pungufu ya eneo la awali kwa ekari 1,352, na shamba namba 77 na 78 pia limerudishwa ambazo ni eakari 1,375,”alieleza Lukuvi.Bonde la Mto Ruaha Kuhusu uharibifu wa Bonde la Mto Ruaha, ambalo pia hujulikana kama Bonde la Usangu ni moja ya mabonde manne makubwa hapa nchini likiwemo Bonde la Mto Kilombero na Rufiji chini, alisema Bonde hilo lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 85,554 sawa na asilimia 47 ya Bonde la Rufiji. Alisema vijiji 33 katika eneo hilo, viliathirika kutokana na Tangazo Namba 28 la Serikali ambapo kabla ya tangazo hilo, eneo hilo lilikuwa na ukubwa wa hekta 10,000, lakini baada ya tangazo likaongezwa na kuwa hekta 20,000.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, katika hilo, kuna mambo ambayo serikali ilikosea na kuna mambo ambayo wananchi nao pia walikosea. Alisema kwa upande wa serikali wakati inatoa tangazo hilo la kufuta vijiji 33 vilivyokuwa na wakazi takribani 40,000, haikuelezwa wananchi hao wataenda wapi. Lakini, pia alihoji ni kweli kwamba serikali ilikuwa inalihitaji eneo lote hilo. Kwa kuwa Mto Ruaha Mkuu unaundwa na mito tisa, matumizi ya maji yaliyofanywa na wananchi wa eneo hilo kwa kilimo cha umwagiliaji, ulitishia uhai wa mto huo ambao ni muhimu kwa uzalishaji wa umeme kwa mabwawa ya Mtera na Kidatu na maporomoko ya Mto Rufiji ya Stiegler’s Gorge.Mbali na shughuli hizo za kilimo, wananchi pia walikuwa wakikata miti hovyo, kuingiza mifugo holela na shughuli holela za uchimbaji madini, ambavyo vyote viliathiri ustawi wa mto huo. Alisema kwenye miaka ya 1960, maji ya mto huo yalikuwa yakimiminika wakati wote. Lakini, kwa sasa maji hukatika hata kwa miezi sita na kusababisha vifo vya wanyama wakiwemo viboko na samaki.Kijiji cha Machimbo Kuhusu wananchi wa Kijiji cha Machimbo kutaka kulipwa fidia, Rais Magufuli alisema wananchi hao walishalipwa fidia ya Sh milioni 800 na waliobaki wanatakiwa kulipwa Sh milioni 31 tu. Alisema wananchi hao baada ya kuchukua fidia hiyo, hawakuhama na waliendelea na shughuli zao, hivyo hawatalipwa na wanatakiwa kuondoka.Alisema kama watabaki, watatakiwa kurudisha fedha hizo. “Kuna mradi mmoja uligharimu zaidi ya shilingi bilioni 20, baadaye mradi huo ukagawiwa kwa wananchi na kila mmoja alipata hekta 1 ili walime, lakini wananchi wale wakaanza kuuza maeneo yao kwa wafanyabiashara na waliowauzia wanajulikana, baada ya kuwauzia yakaenda kwenye mikono ya wajanja na wajanja hao wakaanza kuwakodishia wananchi kwa shilingi milioni 1,” alisema Rais Magufuli.Kuhusu ekari 4,675 na ekari 1,300 alizoagiza zirudi kwa wananchi, Rais Magufuli alitaka kujiridhisha kuhusu hilo na kuwaagiza Waziri wa Ardhi, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, wampatie orodha ya watu waliopewa ekari hizo kwa sababu zinaweza kuwa ekari hewa. Rais Magufuli pia alisema Mwekezaji wa Shamba namba 77 na 78, alipewa kihalali na aliamua kukodisha mashamba hayo kwa wananchi kwa gharama ya Sh 2,295 kwa ekari, lakini madalali waliyauza maeneo hayo kwa kuyakodisha kwa Sh 600,000 hadi Sh 700,000, hivyo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ahakikishe madalali hao wanatafutwa. | 1 |
NEW YORK, MAREKANI RAIS wa Marekani, Barack Obama, amekutana na baadhi ya wasanii wa nchini humo kwa ajili ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya. Wasanii waliopewa mwaliko huo ni pamoja na Nicki Minaj, Pusha T, Rick Ross, Busta Rhymes, Common, J. Cole, Alicia Keys na wengine wengi, walipokutana na rais huyo walijadili namna watakavyopambana na matumizi ya dawa za kulevya. Obama aliwataka wasanii hao watumie uwezo wao kuandika kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa kuzuia utumiaji na uuzaji wa dawa hizo. Kupitia akaunti ya Instagram, Minaj alidai kwamba ana furaha kubwa kukutana na Rais huyo na kujadili suala hilo. “Rais anaamini kuwa wasanii tunaweza kufikisha ujumbe kwa watu wengi wanaotuzunguka, kwa upande wangu nina furaha kwa kupata mwaliko Ikulu,” aliandika Minaj. | 4 |
NAIROBI, KENYA MWANAMITINDO mwenye vituko vingi nchini Kenya, Huddah Monroe, amesema haogopi kufanya lolote kwa ajili ya maisha yake kwa kuwa anaamini hawezi kumfurahisha kila mtu. Alisema anapata kiasi kikubwa cha fedha kinachomwezesha kufanya chochote anachotaka kwa ajili ya maisha yake na si kila wanalotaka watu wengine. “Ninaingiza kiasi kikubwa cha fedha, naishi nitakavyo na nafanya nitakacho na siwezi kamwe kufanya anachotaka shabiki, ila ushauri kwa shabiki fata mazuri yangu na mabaya yangu niachie mwenyewe. “Siwezi kumfurahisha kila mtu bali najifurahisha mwenyewe kwa ninachoona kizuri kwangu kwa kuwa sifanyi vya watu, bali ni vyangu na haya ndiyo aina ya maisha ninayoyataka,” aliandika Huddah. | 4 |
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema Serikali haitoruhusu kusafirisha korosho ghafi kwenda nje ya nchi na badala yake itaingia makubaliano na wabanguaji ili shughuli ya ubanguaji ifanyike kwani itasaidia kujenga heshima ya ajira na viwanda kwa watanzania.Kakunda ametoa msimamo huo mkoani Mtwara wakati wa kikao kazi na wadau wa zao la korosho katika mikoa inayolima korosho hapa nchini.Waziri Kakunda ameisema wapo watu ambao walikuwa wakitumia viwanda kwa kununua korosho hapa nchini ambapo hivi sasa serikali imeamua kununua bidhaa hiyo.Amesema lengo la mkutano huo na wadau hao ni kuona wale wamiliki wa viwanda vikubwa, vidogo na vya kati sasa vinabangua korosho kwa mchakato wote.Waziri Kakunda amesema ni wajibu wa wabanguaji hivi sasa kushirikiana na serikali kuona namna wanavyoweza kuanza kuanzia jana adi inapofika Desemba 10 mwaka huu wafanye uzinduzi rasmi wa kazi ya ubanguaji wa korosho.“Maana ya viwanda vya Tanzania ni kutoa ajira kwa watanzania maana nyingine ya viwanda ni nini...ni kuiongezea thamani korosho na thamani yake ni hapa hapa nchini Tanzania,” alisema Kakunda.Waziri Kakunda alisema katika msimu huu 2018/2019 matarajio ni kukusanya zaidi ya tani 200,000 hivyo ni wajibu wa kila mbanguaji kuhakikisha anakuwa mkweli katika hilo.Wadau wa korosho kwenye kikao hicho akiwemo meneja kutoka kampuni ya Yalin Cashewnut Compan Limited, Sulemani Millanzi amesema, kiwanda chao kina uwezo wa kubangua tani 10,000 kwa mwaka na kuajiri zaidi ya watu 30,000.Mbanguaji mdogo wa korosho, Afisa Mwalimu amepongeza jitihada hizo za serikali na kwamba matumaini yao makubwa ni kupata nafasi katika shughuli hiyo ya kubangua korosho hapa nchini na itawezesha kukuza uchumi wao. | 0 |
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa Sh milioni 10 kutoka Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), kwa watu waliothirika na tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Akikabidhi msaada huo, Askofu Mkuu wa EAGT, Dk. Brown Mwakipesile, alisema kanisa limeona lina wajibu wa kuisadia Serikali kuwapunguzia machungu watu waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko hilo lililotokea Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17. “Tumeona ni vema kanisa la EAGT lishiriki kuisadia Serikali kuwafariji wananchi waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo. Tumeona ni wajibu wetu kwa sababu waliopatwa na maafa ni watu wetu wote. Tunawaombea wote waliopatwa na shida waweze kupata nafuu mapema zaidi,” alisema. Akipokea msaada huo, Waziri Mkuu alisema Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa kwa walengwa. “Nawashukuru viongozi wa dini zote kwa jinsi mnavyoisaidia Serikali na mlivyoguswa na kuamua kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa, “Tunatambua juhudi zinazofanywa na taasisi za dini zote kuunga mkono juhudi za Serikali, tunafarijika mno na tunawashukuru kwa moyo huo,” alisema. Aidha, alimuomba askofu huyo na viongozi wengine wa dini, kuwaombea viongozi waliopo madarakani ili awape hekima na busara na awawezeshe kuwaongoza vema Watanzania. Tetemeko hilo la ardhi liliharibu miundombinu ya barabara, shule, zahanati na kujeruhi watu 440, nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zikipata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali. | 1 |
Na Safina Sarwatt, Hai WATUMISHI wa watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kuvunjwa kwa moja ya ofisi zao na kuibwa kompyuta sita. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, wizi huo ulitokea Juni 27 mwaka huu saa tano asubuhi huku akidai kuwa tukio hilo limegubikwa na utata mkubwa ndani yake. “Taarifa iliyoripotiwa katika ofisi yangu ni jumla ya kompyuta mpakato tatu aina Dell ambazo thamani yake ni Sh milion 12, tukio hilo limegubikwa na utata mkubwa ndani yake hivyo tunaendelea kuwahoji watumishi hao,”alisema Kamanda. Alisema kuwa ofisi hiyo iliyovunjwa ni ya kuhifadhi kumbukumbu za vizazi na vifo na kwamba mpaka sasa ripoti iliyotolewa polisi ni kuibiwa kwa kompyuta mpakato tatu tu. Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Yohana Sintoo alikiri kuibwa kwa vifaa hivo. “Kweli ofisi ya NIDA ilivunjwa juzi usiku wa kuamkia jana, wezi hao waliingia na kuchukua kompyuta sita tu ambazo zilikuwa zinatumika kuhifadhia kumbukumbu nakuacha,”alisema Sintoo. | 1 |
Mwandishi Wetu -Singida BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 katika wilaya kadhaa nchini. Misaada iliyotolewa na benki hiyo inayoongoza kwa kutengeneza faida kati ya benki zote zinazofanya biashara humu nchini ndani ya miezi mitano mwaka huu, inahusisha vifaa vya ujenzi, madawati na vifaa vingine vinavyowezesha ukamilishaji wa miradi ya afya,elimu na usalama wa raia. Benki ya NMB imeshatoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa mikoa ya Kanda ya Kati. Akifafanua kuhusu misaada hiyo wakati akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani ingida, Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Nsolo Mlozi, alibainisha kuwa misaada hiyo ya zaidi ya Sh milioni 200 iliyotolewa imelenga sekta ya elimu, afya na majanga kwa mikoa mitatu ya Kanda ya kati. Akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, MkoaniSingida, katika shule ya Sekondari ya New Kiomboi, Mlozi alisema fedha hizo zilizotolewa na NMB zimetumika kununua madawati, viti vya shule za sekondari,vitanda na vifaa tiba kwenye sekta ya afya. Aidha, alisema lengo la misaada hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali. Pia alisema misaada hiyo imekabidhiwa kwa baadhi ya shule, zahanati, hospitali katika mikoa ya Singida, Dodoma na Manyara. Pia NMB walikabidhi madawati 250 na vitanda 80 vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 29.5 kwa baadhi ya shule za Wilaya ya Iramba mkoani humo. Katika hatua nyingine, Benki hiyo imevipatia kituo cha Polisi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro pamoja na shule ya msingi Msowelo mabati 160 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa ajili ya kuezekea maboma. NMB iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni mpango wa kuzipunguza baadhi ya changamoto kwa taasisi za serikali hapa nchini, Meneja wa NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus, alisema na kubainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia kuinua miradi ya maendeleo. Baraka alisema kuwa kati ya mabati hayo, kituo cha polisi wilaya kimepa tamabati 80 huku shule ya msingi Msowelo nayo ikipata mabati 80. | 0 |
Mwamuzi wa mechi hiyo Erick Onoka wa Arusha na Kamisaa Omar Juma walifikia uamuzi wa kuahirisha mechi hiyo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya jana na kuharibu uwanja.Taarifa hizo zilisema kuwa uwanja ulijaa maji na kwamba mechi isingewezekana kuchezwa na kwa vile leo uwanja huo utatumika katika mechi nyingine ya Ligi Kuu kati ya Stand United na Mtibwa Sugar, hivyo mechi hiyo itachezwa kesho.Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kutokana na timu hizo kuwania kumaliza kwenye nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi. Timu hizo zipo kwenye nafasi ya tatu na ya nne kwenye msimamo wa ligi, Simba ikiwa na pointi 29 na Kagera pointi 24.Simba inataka kushinda mechi hiyo si tu kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza ligi kwenye nafasi za juu, lakini pia ikitaka kulipa kisasi kwa Kagera Sugar kwani katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wekundu hao wa Msimbazi walilala kwa bao 1-0.Timu hizo zinakutana zote zikiwa zimetoka kupata matokeo mazuri katika mechi zilizopita ambapo Simba iliifunga Ruvu Shooting mabao 3-0 na Kagera Sugar ikiifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1. | 2 |
Na SHOMARI BINDA MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amewaonya watu ambao wamekuwa wakikwepa kujiandikisha vitambulisho vya taifa kuwa baada ya hatua hiyo kukamilika ataagiza polisi kuwasaka waliopuuzia. Alisema watu hao watatakiwa waeleze sababu za kutojisajili na kupata vitambulisho. RC alikuwa akizungumza juzi baada ya kumalizika siku 90 za usajili na uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa Mkoa wa Mara. Alisema hatua hiyo imekamilika kwa kusajili wananchi 718,647 kati ya 763,142 waliostahili kusajiliwa hivyo kufanya idadi ya wananchi waliodahiliwa kufikia asilimia 94. Alisema katika hatua hiyo pia wamesajili wageni wakazi 224 ambao wamekuwa wakiishi halali mkoani humo. Rc aliwaonya ambao hawakujiandikisha kutumia siku za marekebisho kujisajili na kujiandikisha. “Wale waliojiandikisha baada ya hatua hiyo kumalizika watapata vitambulisho vyao na wasiokuwa navyo tutawahesabu kuwa siyo wenzetu. “Zipo wilaya ambazo zimefanya vizuri katika hatua hii ni Musoma na Bunda ambazo zimesajili kwa asilimia 112 zinastahili kupongezwa,” alisema. Hata hivyo alisema licha ya kukamilika hatua hiyo itaendelea katika ofisi za wilaya hivyo kuwaomba wale ambao hawakupata fursa hiyo wafike kukamilisha kuanzia Mei hadi Juni 2018. | 1 |
Natumai wengi tulikua tunajiuliza ya nini kilichotokea katika video ya wimbo wa Nisamehe wa Kala Jeremiah aliomshirikisha msanii Aslay . Utalia Wimbo Mpya wa Kala Jeremiah, Je Aslay Kakimbia Video? Katika video hiyo msanii huyo hakutokea na leo Kala Jeremiah anafunguka juu ya kile kilicho tokea wakati wa kushuti video hiyo. Akizungumza na mtandao wa SNS, Kala Jeremiah anasema walifuata utaratibu kama ilivyo kawaida na waliongea na management ya Aslay na kuwaambia siku ya kushoot a video na management ya Aslay ikasema hamna neno ila siku ya kushuti Aslay hakutokea location. Aslay ndiye aliyeimba kiitikio katika wimbo huo wa ‘nisamehe’ amekua recentry kuwa na kasumba hiyo ya kutokutokea kwenye mambo mbalimbali yanayomhusu kama unakumbuka katika tamasha la ZIFF mwaka jana alizuiwa kuperform Zanzibar mpaka alipoomba radhi na mamlaka mjini humo kwa madai kuwa hakutokeaga kwenye moja ya show aliyotakiwa aperform. Kala Jeremiah anasema Tulifuata utaratibu wa kawaida kwanza tuliongea na management tukaomba ushiriki wa msanii ,akasema haina shida kila kitu kitakuwa sawa , basi nikasubiri hiyo siku kukawa na dharula hawakutokea Kala Jeremiah anadai kuwa wakapanga siku ya pili na bado pia msanii huyo hakutokea na wakaamua kuendelea na production bila yeye, Pia akaendelea kufunguka juu ya kumtumia msanii huyo hela ya mafuta na bado akamchomesha mahindi. Sikuombwa chochote ..lakini niliprovide hadi mafuta nikamtumia manager wake ..kwamba wakati mwingine sisi wassanii mimi mwenyewe huwa nakwama! Licha ya watu wengi kumlaumu Aslay, Kala Jeremiah amedai kuwa anamshukuru sana msanii huyo kwa kumpigia bonge la chorus. | 4 |
ADAM MKWEPU Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM HOMA ya pambano la watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga, inazidi kupanda huku kila timu ikijinadi kwa upande wake kuelekea katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Timu hizo tayari zimeanza maandalizi ya kuelekea kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kubeba hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, ambapo Simba wako visiwani Zanzibar wakati Yanga imejichimbia Morogoro. Kocha wa Yanga, George Lwandamina, atakiongoza kikosi chake akiwa na kumbukumbu ya kushindwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka huu walipokabiliana na Simba na kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3. Kocha huyo ameshindwa kutamba katika michezo yote aliyokutana na kocha wa Simba, Joseph Omog, ukiwemo wa ligi kuu msimu uliopita Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1. Omog aliiongoza tena Simba kuifunga Yanga kwa penalti 4-2 kwenye Kombe la Mapinduzi mwaka huu, kabla ya kuibuka tena na ushindi wa penalti 4-3 kwenye Ngao ya Jamii. Timu hizo zote zimekusanya pointi 15 baada ya kucheza michezo saba ya ligi hiyo, huku Simba ikiongoza msimamo kutokana na kufunga mabao mengi, ambapo imezifumania nyavu mara 19, huku Yanga wakiwa na mabao 10. Akizungumza na MTANZANIA jana, Omog alisema Yanga ni timu nzuri lakini kikosi chake ni bora zaidi ya mabingwa hao watetezi ambao wanalifukuzia taji la nne mfululizo la ligi hiyo. “Nimeifunga Yanga mara mbili na kutoka sare mara moja katika mechi sita nilizocheza nao nikiwa kocha wa Simba, kwa hiyo najivunia rekodi hiyo ambayo naamini itanibeba na kupata matokeo mazuri katika mechi ya Jumamosi na hata mechi nyingine za ligi na michuano mengine,” alisema Omog. Kocha huyo alisema kambi yao ya Zanzibar itakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwaweka sawa wachezaji wake na kuwakumbusha mambo muhimu yatakaowasaidia kupata ushindi na kujilinda ili wasipoteze mchezo. Omog alisema anawajua Yanga lakini si timu tishio kwake kutokana na ubora wa safu ya ushambuliaji na ulinzi imara aliyoandaa dhidi ya mshambuliaji, Ibrahim Ajibu,anayeonekana kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na aina ya mabao aliyofunga katika mechi zilizopita. Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu Yanga, Dismas Ten, alisema hawana hofu wala presha kuelekea kwenye mechi hiyo kwa sababu wanashiriki ligi ili kusaka ubingwa. “Simba wakienda kuweka kambi Zanzibar hayo ni mapendekezo yao, si lazima tuwafuate huko ingawa mara nyingi imekuwa hivyo, sisi tunapambana kupata matokeo mazuri yatakayotuwezesha kutetea taji letu. “Hatushiriki ligi sababu ya Simba, kwani nao ni moja ya timu 16 zinazoshiriki ligi kuu, ndio maana kila kikosi kinapambana kwa hali na mali kufanya vizuri,” alisema Ten. Ten alieleza wanachokitegemea wao ni kupata matokeo ya kuridhisha, kupitia kwa wachezaji wao ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha kikosi chao kinatoka uwanjani na ushindi. | 2 |
Mwandishi wetu, Tanga MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itawasaidia wafanyabiashara wanaokwepa kodi kuacha vitendo hivyo vya kuikosesha Serikali mapato. Shigela ameyasema hayo ofisini kwake alipotembelewa na maafisa wa TRAwanaofanya kampeni hiyo mkoani humo ambayo imelenga kuwaelimishawafanyabiashara kuhusu masuala ya kodi ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati. Amesema kuwa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikwepa kulipa kodi pengine kwa kujua au kutokua, jambo ambalo linahitaji elimu ya uelewa ili kila mwananchi afahamu wajibu wake kwenye ulipaji wa kodi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Akiizungumzia kampeni hiyo, Shigela ameipongeza TRA kwa kuendesha zoezi hilo katika mikoa mbalimbali na kusema litaongeza ukusanyaji wa mapato baada ya wafanyabiashara kuelimishwa na kufahamu kuwa maendeleo ya nchi yanasababishwa na ulipaji wa kodi kwa ajili ya kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, barabara, umeme na maji. Shigela amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari bila kusubiri kubugudhiwa na serikali, huku akieleza kuwa serikali itaendelea kupambana na wakwepa kodi wanaoingiza bidhaa za magendo nchini kwa kupitia bandari bubu zilizopo kandokando ya Bahari ya Hindi. “Nchi yoyote haiwezi kupiga hatua ya maendeleo bila wananchi wake kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa sababu kodi ndio kila kitu huwezi kujenga barabara kama wafanyabiashara hawataki kulipa kodi, huwezi kuimarisha huduma za afya kama hakuna kodi na pia huwezi kuimarisha mifumo ya elimu bila kodi,” alisema Shigela. Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Tanga, Specioza Owure amesema kuwa, maafisa hao wa TRA wanaofanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi, watafika maeneo mbalimbali yenye wafanyabiashara katika mkoa wa Tanga na watawaelimisha kuhusu umuhimu wa kodi na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati. “Maafisa hawa wanatumia jitihada zote kuwaelimisha wafanyabiashara, tunafanya hivi ili kila mmoja afahamu wajibu wake wa kulipa kodi sambamba na kusogeza huduma za TRA karibu na wateja,” alisema Owure.Kampeni ya elimu kwa mlipakodi mkoani Tanga inatarajia kumalizika Juni 30, 2020 ambapo lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, kusikiliza maoni na changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati. | 0 |
NEW YORK, MAREKANI MUME wa zamani wa Mariah Carey, Nick Cannon, ameweka
wazi chanzo cha ugomvi wake na rapa Eminem ni mke wake. Cannon aliongea maneno hayo wakati wa mahojiano na
kipindi cha Daytime Talk Show, alisema hakuwa na lengo la kutaka kuingia kwenye
mgogoro na Eminem lakini aliyekuwa mke wake Mariah ndiyo chanzo. “Mariah na Eminem walikuwa na bifu lao wenyewe, hivyo
sikuweza kuwa mnyonge hasa pale rapa huyo alipomzungumzia mke wangu kwenye
wimbo wake wa Bagpipes from Baghdad, nikaona na mimi nionyeshe uwanaume wangu. “Eminem hakuwa na shida na mimi, lakini nilinunua
kesi, mwisho wa siku sisi ni wanaume, nikaona nikae chini kujaribu kuyamaliza
ila haikuwa kazi rahisi,” alisema Cannon. Bifu hilo lilianza mwaka 2009, kabla ya Cannon na
Mariah kuachana 2014 huku tayari wakiwa na watoto wawili mapacha. | 4 |
HALMASHAURI nchini zimeagizwa kuendelea kukagua mashamba yote yaliyotaifi shwa wakati wa Azimio la Arusha ili yaandaliwe mipango ya matumizi ya ardhi na kupimwa.Aidha, viongozi wa vijiji na kata wametakiwa kuacha tabia ya kuwagawia ardhi kwa mtindo wa kuwakodisha wananchi, kwani kufanya hivyo ni kinyumecha utaratibu na sheria za nchi.Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu.Katika swali lake, Komu alihoji ni lini serikali itatekeleza ahadi yake ya mara kwa mara ya kuyapima upya mashamba yaliyotaifishwa wakati wa Azimio la Arusha ambayo hivi sasa yamebadilishwa matumizi na kujengwa shule, zahanati, hospitali, makazi. Akijibu swali hilo, Mabula alikiri kuwa kuna mashamba kadhaa nchjini yaliyotaifishwa wakati wa Azimio la Arusha.“Baadhi ya mashamba hayo yaligawiwa kwa mashirika na taasisi za umma kwa ajili ya kuendeleza hususan kwa kilimo cha kahawa na mkonge,”alisema. Hata hivyo, alisema baadhi ya mashamba hayo yamebadilishiwa matumizi na yamekuwa yakitumiwa na wananchi kwa matumizi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ikiwemo makazi, shule, zahanati, hospitali.“Wizara yangu kwa kushirikiana na halmashauri nchini imeendelea kukagua, kuyaandalia mipango ya matumizi ya ardhi na kupima upya baadhi ya mashamba hayo,”alisema.Aidha, Mabula alisema baadhi ya mashamba ambayo Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri imeyaandalia mpango wa matumizi ya ardhi ni pamoja na kihuhwi Estate, Sagulas Estate, Lewa Estate, Bombwera Estate, Geiglitz Azimio Kipapula pamoja na Kibaranga yote ya mkoa Tanga.“Mashamba mengine ni New Msowero Farm, Mvumi Farms/Estate Kilosa na Luipa Estate yaliyopo mkoani Morogoro,Kimsingi jukumu la kuandaa mipango ya matumizi ya mashamba hayo ni la Halmashauri husika yalipo mashamba hayo,”alisema.Alitoa rai kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kupanga na kupima mashamba husika ili yaweze kutumika kwa tija kulingana na mahitaji halisi ya sasa.Aidha, Mabula alitaka viongozi wa vijiji na kata kuacha tabia ya kuwagawia ardhi kwa mtindo wa kuwakodisha wananchi, kwa kufanya hivyo ni kinyumecha utaratibu na sheria za nchi.Pia alitoa rai kwa wananchi kutumia ardhi yao kwa tija kwani ardhi haiongezeki wakati idadi ya watu, mifugo na shughuli za uzalishaji zinazohitaji ardhi zinazoongezeka.Mabula alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Sonia Magogo(CCM) aliyeuliza, Je, Serikali ina mpango gani kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya handeni ambao wanakosa ardhi ya kuendesha shughuli zao za kilimo kwa sababu ya kumilikiwa na wachache? | 1 |
Derick Milton, Simiyu Kampeni inayolenga kuhamasisha jamii kuwa na vyoo bora inayojulikana kama ‘Nyumba ni Choo’ imezinduliwa rasmi mkoani hapa huku ikidaiwa kaya 6,459 sawa na asilimia tatu, hazina vyoo.Kampeni hiyo itaendeshwa kwa siku 20 ikiongozwa na msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto. Kabla ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka, Katibu Tawala wa Mkoa Jumanne Sagini amesema mbali na hilo kaya 215,316 sawa na asilimia 97 ndizo zenye vyoo ambapo kati ya hizo zenye vyoo bora ni 97,536 sawa na asilimia 46.7 ya kaya zote. “Katika kuhakikisha suala hilo linatiliwa mkazo mkoa umejipanga kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya ikiwa pamoja na kutiliwa kwa mkazo wa sera za usafi wa mazingira,” amesema. Naye Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Anyitike Mwakitalima amesema kupitia kampeni hiyo wamelenga kuongeza uwepo wa vyoo bora kwa kipindi cha muda mfupi. “Mbali na hilo kampeni hiyo itahakikisha inaboresha hali ya afya katika nchi sambamba na kukabiliana na uchafu kwa njia zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ujenzi wa vyoo bora kwenye ngazi ya kaya na taasisi,” amesema. Awali, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema tatizo la kutokuwa na vyoo bora linasababishwa na baadhi ya tamaduni ambapo katika baadhi ya jamii baba mkwe hatumii choo kimoja na mkwe wake. | 1 |
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezitaka taasisi za utafiti na ugunduzi nchini, kuwekeza zaidi katika utafiti ili kutoa mchango mkubwa katika kutimiza malengo ya serikali ya kufikia nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025.Taasisi zilizoagizwa ni Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA), vyuo vya elimu ya kati, vyuo vya ufundi, vyuo vya elimu ya juu, wanafunzi mbalimbali wa sekondari pamoja na taasisi mbalimbali za utafiti na ugunduzi nchini.Profesa Ndalichako alisema hayo wakati akizindua Mwongozo na Mashindano ya Ubunifu yenye lengo la kutambua na kuendeleza wabunifu na ugunduzi nchini. Alisema mwongozo huo unatakiwa kutumika na wabunifu, wagunduzi na watafiti kama msahafu kutambua na kuendeleza ubunifu na ugunduzi.Profesa Ndalichako alisema katika kuhakikisha utafiti na ugunduzi na ubunifu unaendelea nchini, serikali itaendelea kuandaa mazingira wezeshi kuhakikisha wabunifu na wagunduzi hao wanaendelezwa ili kufikia malengo yao.“Serikali itaendelea kusaidiawabunifu na wagunduzi nchini kutokana na kutambua wazi wataendeleza sayansi na teknolojia nchini lakini hasa wataongeza zaidi ajira na tija ,” alisema.Alisema katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini, sayansi ya ubunifu na ugunduzi ni muhimu kwani ina mchango mkubwa katika kuhakikisha sayansi na teknolojia zinaleta mapinduzi makubwa ya viwanda nchini.Profesa Ndalichako alisema kaulimbiu ya mwongozo huo ni ubunifu katika kukuza ujuzi wa wabunifu kwa maendeleo ya viwanda nchini inayoonesha wazi ubunifu na ugunduzi ni nyenzo muhimu kufikia azma ya kuwa na uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda nchini.Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba alisema kama nchi inataka kusonga mbele, lazima kuwekeza fedha za kutosha katika utafiti na ugunduzi la sivyo haitafika.Alisema uzinduzi wa mwongozo ni jambo la kihistoria, hivyo alisifu wizara hiyo kuanzisha ubunifu huo utakaowasaidia kuwapa dira na mwelekeo, wabunifu na wagunduzi kwa utafiti wakitumia maelekezo yaliyo ndani yake.Serukamba alisema nchi itasonga mbele kwa kutumia sayansi na teknolojia hivyo kwa kuwa na mwongozo huo kama dir, kutasaidia watafiti na wabunifu kuleta maendeleo katika nchi.Akizungumzia uzinduzi wa mwongozo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe alisema wizara hiyo ipo tayari kuandaa mazingira wezeshi kwa wabunifu na wagunduzi kuendeleza taaluma. | 1 |
MWANAFUNZI wa kidato cha nne, Jasmini Ngoye (18) wa Shule ya Sekondari Lupanga mkoani Morogoro, anadaiwa kujilipua kwa risasi kooni iliyofumua utosi wa kichwa chake.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana. Alisema tukio hilo ni la Februari 19, saa 12 asubuhi katika maeneo ya Kola B Manispaa ya Morogoro. Kwamba mwili wa mwanafunzi huyo, ulionekana ukiwa na jeraha la risasi kichwani.Kamanda Mutafungwa alisema taarifa za kuonekana kwa mwili huo, zilifikishwa kituo cha polisi na askari walifika eneo la tukio, ambapo uchunguzi ulionesha kuwa jeraha hilo la risasi, liliingia kwenye koo na kutokea kwenye utosi wa kichwa chake.Alisema pembeni mwa mwili wake, ilipatikana silaha (bastola) aina ya bereta yenye namba H.11135 ikiwa na magazini moja na ganda la risasi moja lililotumika. Kwa mujibu wa kamanda huyo, walipowahoji watu mbalimbali kuhusu tukio hilo, alijitokeza Profesa Hamis Mahigi (69) mkazi wa Kihonda, aliyesema anamtambua marehemu kuwa ni shemeji yake na alikuwa akiishi naye Kihonda na alitoweka tangu Februari 18, mwaka huu saa 10 jioni.Alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo, umeonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo wa muda mrefu aliokuwa nao mtu huyo kabla ya kifo chake. Alisema kuwa walifanikiwa kupata kitabu chake cha kumbukumbu (diary), ambayo aliandika ujumbe mbalimbali. Moja ya ujumbe ulisomeka “Ni mtoto asiyejua wazazi wake na asiyejua kazaliwa wapi.Mtoto huyu anatamani kukiona kifo chake wakati wowote na muda wowote, mtu yeyote atakayeisoma diary hii ndiye atakayeandika siku, tarehe ya kifo changu.” Alisema kuwa aliikabidhi diary hiyo kwa rafiki yake siku hiyo ya tarehe 18, aitwaye Imelda Milanzi, ambaye pia ni mwananfunzi wa Shule ya Sekondari Lupanga kidato cha nne.Kamanda Mutafungwa alisema kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea. Kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa uchunguzi zaidi. Alisema kuwa Prof Maiga ambaye ndiye mmiliki wa bastola, amekamatwa na anahojiwa kuhusu tukio hilo. | 1 |
HATIMAYE Kivuko cha Mv Nyerere kilichozama siku nane zilizopita katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza, kimeinuliwa rasmi huku ikipatikana maiti moja ya mtoto mdogo na kufanya idadi ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufi kia watu 228.Pamoja na hayo, serikali jana ilitarajia kupeleka kivuko cha Mv Ukara kisiwani hapo kwa ajili ya kusaidia usafiri katika visiwa ambavyo baada ya Mv Nyerere kuzama, vilikosa usafiri, huku ikiendelea na mchakato wa kupata kivuko kikubwa zaidi kumaliza tatizo la usafiri katika eneo hilo.Akizungumza kisiwani hapo jana, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema baada ya kivuko hicho kuinuliwa na kusimama kabisa, ilipatikana maiti ya mtoto mdogo.Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Jenerali Venance Mabeyo, alielezea namna walivyoanza kuinua kivuko hicho ambapo hadi jana asubuhi walifanikiwa kukiinua kikaa ubavu na baadaye kikasimama kabisa. “Kivuko hiki kilikuwa kimelala kifudifudi, tulikilaza ubavu na baadaye kikasimama kabisa, kazi iliyopo ni kukitoa majini na kukivuta nchi kavu kwa ajili ya matengenezo,” alieleza Jenerali Mabeyo.Kivuko hicho kilipinduka na kuzama mchana wa Alhamisi ya Septemba 20, mwaka huu wakati kikikaribia kutia nanga katika gati la Ukara ikitokea Bugolora na kusababisha vifo vya watu 228, huku 41 wakiokolewa. Katika hatua nyingine, Rais John Magufuli amewataka watendaji wenye dhamana ya kuongoza taasisi, wizara na mamlaka walizopo kujitafakari na kujifunza kupitia ajali ya kuzama kwa Kivuko cha Mv Nyerere.Aliitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuzindua Daraja la Juu la Mfugale eneo la Tazara na kusema Taifa bado liko kwenye simamzi kubwa ya kuzama kwa kivuko hicho na kuwataka watendaji wote wakiwemo Watanzania kujifunza kupitia tukio hilo.Awali, aliwashukuru marafiki wa nchi mbalimbali kwa salamu zao za pole kwani zimewafariji Watanzania na pia shukrani hizo amezitoa kwa watanzania wote kwa mshikamano walioonesha tangu kutokea kwa ajali hiyo na kusema japokuwa nchi bado inaomboleza, lakini ni vyema pia kazi zikafanywa. | 1 |
Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM MSANII wa muziki wa kundi la Weusi, John Makini, amesema mipango yake ni kuhakikisha anafanya kazi bora zaidi zitakazoweza kumtangaza kimataifa. Makini ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Kata Leta’ aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria Davido, alisema ili msanii aweze kufanikiwa lazima ajitangaze kwa kufanya kazi zenye ubora. Alisema tasnia nzima ya muziki kwa sasa imeonyesha ushindani wa hali ya juu, si kwa wasanii Watanzania tu hata wale wa nje ya nchi. “Mipango yangu ni kufanya kazi bora zaidi na zaidi, hivyo mara baada ya kuachia ‘Kata Leta’ kazi nyingine kali itafuata. “Nimegundua ili uweze kujitangaza lazima uvuke mipaka ya Tanzania, kutafuta wasanii wakubwa wa kimataifa ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuwashirikisha kwenye kazi zako,” alisema Makini. Msanii huyo hadi sasa amefanikiwa kuwashirikisha wasanii watatu wa kimataifa katika kazi zake tofauti ambao ni Chidinma na Aka. | 4 |
WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar imesema njia pekee ya wakulima kupiga hatua kubwa ya uzalishaji wa mpunga ni kutumia kilimo cha umwagiliaji.Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Rashid Ali Juma alisema kilimo cha umwagiliaji ndio mkombozi wa wakulima ambao kwa sasa wanaweza kulima muda wowote mwaka mzima. Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sasa inatekeleza mradi mkubwa wa umwagiliaji maji mashambani ambao ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Exim ya Korea ya Kusini.‘’Serikali tayari inatekeleza mradi mkubwa wa umwagiliaji maji mashambani ambao unatekelezwa na wenzetu Benki ya Exim kutoka Korea ya Kusini ikiwa ni mkopo,’’ alisema. Juma alisema mradi huo wa umwagiliaji ulianza Desemba, 2018 ambapo kazi kubwa ni ujenzi wa mitaro ya kupitishia maji inayoenda mashambani pamoja na kujenga pia njia zake.Aidha, alizitaja kazi nyingine zitakazofanyika ni kuchimba visima vya uzalishaji wa maji 49 vitakavyotumika kusambaza maji mashambani na ujenzi wa mabwawa manne ya maji. ‘’Hizo ndiyo kazi zitakazofanyika katika utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji maji mashambani wenye lengo la kukuza uzalishaji wa mpunga kwa wakulima wetu, ‘’ alisema.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Ahmada Kassim Haji alisema kama wakulima wa mpunga watajikita zaidi katika uzalishaji wa mpunga kwa umwagiliaji maji, yapo matumaini makubwa ya kujitosheleza kwa chakula. Alisema kilimo cha mpunga cha kutegemea mvua hakina uhakika kupata mavuno mazuri. ‘’Serikali imejikita katika kuimarisha kilimo cha umwagiliaji maji mashambani ambacho matarajio ni kukomboa wanawake, ‘’alisema. | 1 |
Ofisa Mikopo wa Sido mkoani Singida, Reuben Mwanja alisema mjini hapa juzi kuwa walengwa 1,089 walionufaika na mikopo hiyo na kati yao, 675 ni wanawake na 414 ni wanaume.Mwanja alisema mikopo ya Sh milioni 354.8 ilitolewa kupitia wateja 774 wa vikundi; wanawake wakiwa 509 na wanaume 265 wakati Sh milioni 150.7 zilitolewa kwa mteja mmoja mmoja.Kwa mujibu wa Mwanja vikundi vingi vya vijijini vilivyopewa mikopo hiyo, ni vilivyopo kwenye utaratibu wa Vicoba, ambavyo ni Mhintiri, Igombwe na Ikungi vyote vya Wilaya ya Ikungi “Marejesho ya mikopo hii ni asilimia 98 hali inayoridhisha mno,” alisema Mwanja. | 0 |
NA JESSCA NANGAWE SIMBA imeendelea kujitengenezea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, baada ya jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli, katika pambano lililochezwa Uwanja wa Samora, Iringa. Mshambuliaji John Bocco ndiye aliyeipa Simba pointi tatu katika mchezo wa jana, baada ya kufunga bao pekee la Wekundu hao dakika ya 23. Bocco alifunga bao hilo ambalo ni la tatu kwa upande wake msimu huu, baada ya kupokea pasi murua ya Fransis Kahata. Kwa ushindi wa jana Simba imefikkisha pointi 56, baada ya kushuka dimbani mara 22, ikishinda michezo 18, sare mbili na kupoteza mara mbili. Baada ya kichapo cha jana, Lipuli imeshuka kwa nafasi moja ikitoka ile ya tisa hadi ya 10, baada ya kucheza michezo 22, ikishinda nane, sare tano na kupoteza tisa hivyo kujikusanyia pointi 29. Mchezo huo ulianza kwa kasi na kila timu kuonekana kudhamiria kupata mabao ya haraka. Hatua hiyo ilisababisha kuwapo kwa kosa kosa tangu mwanzoni mwa mchezo, zilizotokea kila upande. Dakika ya saba, mshambuliaji na nahodha wa Lipuli jana, Daruwesh Saliboko alishindwa kupachika bao kutokana na kutojpanga vema. Dakika ya tisa, kipa wa Simba, Aishi Manula alipangua mchomo wa Kennedy Masumbuko. Dakika ya 12, kipa wa Lipuli, Deogratias Munishi ‘Dida’ aliokoa mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere. Dakika ya 31, beki wa Lipuli Paul Ngalema alionywa kwa kadi ya njano kutokana na kupinga uamuzi wa mwamuzi. Kipindi kila upande ulijaribu kuzichanga karata zake, Lipuli ikitaka kusawazisha kabla ya kuongeza na Simba ikitaka kufunga mabao zaidi.
Hata hivyo, safu za ulinzi za kila upande zilifanya kazi nzuri kuepusha madhara langoni mwao na kufanya dakika 90 za patashika hiyo kumalizika kwa Simba kutakata kwa bao 1-0. Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Cloutas Chama, Meddie Kagere, John Bocco na Francis Kahata. Kikosi cha Lipuli: Deogratius Munishi, Duchu, Paul Ngalema, Mwassa, Mwangosi,Lufunga, Mwinyi,Tangalu, Joshua, Daruesh Saliboko, na Kennedy Masumbuko. Michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana, Azam ilijikuta ikiendelea kuwa mteja wa Coastal Union, baada ya kucharazwa mabao 2-1, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ikumbukwe kuwa, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza kati ya timu hizo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Coastal ambayo ilikuwa mwenyeji ilishinda bao 1-0. Mabao ya Coastal yalifungwa na Ayoub Lyanga na Mudathir Khamis. Kwa mtokeo hayo, Coastal imepanda hadi nafasi ya nne, ikitoka ile ya sita ya awali, baada ya kufikisha pointi 37. Bao la Azam lilipachikwa na dakika ya 90 na mshambuliaji, Obrey Chirwa. Hata hivyo, Azam inayofundishwa na kocha Mromania Aristica Cioaba, imesalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa imejikusanyia pointi 44. Kagera Sugar iliiadhibu Mbao mabao 2-0, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Mabao ya Kagera Sugar yaliwekwa kimiani na Yusuph Muhilu na Godfrey Mwashiuya. Mhilu amefikisha mabao 10 msimu huu na kumkaribia Kagere anayekamata uongozi akiwa na mabao 12. Polisi Tanzania iling’ara baada ya kuitandika KMC mabao 3-2, huku Singida ikilazwa bao 1-0 na Ndanda na kuzidi kujiweka kwenye mazingira hatarishi zaidi ya kushuka daraja. Nao Maafande wa Ruvu Shooting wakatakata bao 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Mwadui na Namungo zikagawana pointi moja moja baada ya sare yao ya bao 1-1 Uwanja wa Kambarage. Mtibwa iliendelea kudorora baada ya kutandikwa bao 1-0 na ya JKT Tanzania huku Biashara ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Alliance, Uwanja wa Karume, Mara. | 2 |
Na SARAH MOSES, DODOMA
KILO 99 za dawa za kulevya zimekamatwa mkoani hapa.
Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme, alipokuwa akizungumza na wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji mjini hapa.
Alisema kuwa, Wilaya ya Dodoma ndiyo inayotumiwa na wafanyabiashara hao, kupokea dawa hizo kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.
“Kuna kesi 168 zinazowakabili watu 240 kwa utumiaji na uuzaji wa dawa za kulevya. Hivyo basi, nyie viongozi watajeni watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo hata kama ni wanasiasa au watu wenye uwezo kifedha,” alisema Mndeme.
Aliyataja maeneo yanayoongoza kwa kuuza dawa hizo za kulevya kuwa ni Miyuji, Hazina, Airport, Mlezi na Chinangali West.
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini, Daniel Shillah, aliwataka wananchi kuwa makini na watu waliowapangisha kwenye nyumba zao kwani wengi wao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.
“Wenyeviti ninyi mnawajua vizuri wananchi wenu, hivyo basi kuweni makini nao na kama kuna mtu unajua anatumia au anauza, njoo utoe taarifa na sisi Jeshi la Polisi tutamshughulikia.
“Adhabu ya mtu ambaye nyumba yake itakutwa na dawa za kulevya, atatozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kuruhusu nyumba yake iwe na dawa hizo na mtumiaji atatozwa faini ya shilingi milioni tatu.
“Kwa kifupi ni kwamba, Wilaya yetu ya Dodoma Mjini inaongoza kwa kuwa na bangi pamoja na mirungi na maeneo yaliyoathiriwa na dawa hizo ni pamoja na Makutupora, Msalato, Veyula, Kizota, Majengo, Mailimbili, Chadulu, Zuzu, Bahiroad na Mbabala. | 1 |
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imeagizwa kurudisha mchakamchaka shuleni kama zamani. Agizo hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya kufanya mazoezi kitaifa ambayo imelenga kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza. “Zamani wakati sisi tunasoma, tulikuwa tunakimbia mchakamchaka na uliwekwa makusudi kwani tulipata fursa ya kufanya mazoezi. “Leo hii shuleni hakuna mchakamchaka, Waziri wa Elimu aurudishe kama awali, wanaweza kusema kwamba umbali wanaotembea watoto tayari ni mazoezi, hapana, mchakamchaka una nafasi yake na ni wa muhimu, wapange jinsi itakavyokuwa,” alisema. Pia aliziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinarudisha viwanja vya michezo vilivyouzwa ili wananchi wavitumie kwa kufanya mazoezi. “Kila halmashauri ihakikishe viwanja vya michezo vilivyouzwa vinarudi kwa wananchi, wakishindwa watafute vingine na Jeshi la Polisi lisimamie bodaboda na bajaji zisipite kule katika njia za watembea kwa miguu, maana watu wanafanya mazoezi ya kukimbia,” alisema. Akizungumzia kampeni hiyo, Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema imezinduliwa kutokana na kuongezeka kwa watu wanaougua magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza. “Tunaendekeza usasa, usharobaro, hatutaki mazoezi, lakini tunajiumiza, nawaagiza wakuu wa mikoa na wilaya watenge kila Jumamosi ya pili ya mwezi watu wafanye mazoezi. Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza yanachangia asilimia 27 ya vifo vyote duniani. “Utafiti wa mwaka 2012 hapa nchini uliohusisha wilaya 53, ulionyesha viashiria hatarishi vya magonjwa haya. Asilimia 26 walionekana kuwa ni wanene kupita kiasi, asilimia 26 walikutwa na lehemu nyingi mwilini, asilimia 33 wana mafuta mengi, asilimia 9.1 wana ugonjwa wa kisukari, huku asilimia 25.9 wakiwa na shinikizo kubwa la damu,” alisema Ummy. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema anatamani kila mwananchi katika mkoa wake atakayebainika kuugua kwa uzembe magonjwa yasiyoambukizwa, atozwe gharama ya matibabu mara mbili. “Wengi wanaougua kwa kutokufanya mazoezi, gharama inakuwa kubwa kwa Serikali, leo (jana) imeitishwa kampeni, lakini wengine wamelala, natamani kupendekeza atakayeugua kizembe, atozwe mara mbili, kama ni Sh 300,000 basi atozwe 600,000 ili tubadilike,” alisema Makonda. | 1 |
Wakati Mbio za kuziba nafasi za uongozi katika klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), Malangwe Mchungahela ametoa onyo kwa wanachama wa klabu hiyo ambao wanaowatishia wagombea kwenye matawi yao.Akizungumza leo Jumanne, Malangwe amesema kuwa matawi ni mali ya klabu ya Yanga na siyo mali ya mwanachama, hivyo yeyote atakayefanya fujo wakati wa kampeni, Jeshi la Polisi litamshughulikia ipasavyo.“Kama hutaki kusikiliza sera za mgombea ni bora ukaondoka na siyo kufanya fujo kuzuia kampeni za mgombea, Jeshi la Polisi lipo makini na litahakikisha wote watakaojaribu kuzuia au kufanya fujo wanadhibitiwa kabla ya kutimiza azma yao,” alisema Mchungahela.Naye ofisa usalama wa TFF, Caf na Fifa, Inspekta Abdallah Hashim ametangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 13 katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam. | 2 |
WAKULIMA wilayani Sikonge, Tabora wanaotaka kulima zao la pamba wametakiwa kuvumilia hadi serikali ijiridhishe tishio la mdudu funza mwekundu halipo maeneo jirani yaliyopigwa marufuku kulima zao hilo.Ushauri huo umetolewa juzi Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati wa kikao cha robo ya kwanza Baraza la Madiwani. Alisema Wizara ya Kilimo iliweka karantini kwa wilaya zinazopakana na mikoa ya Rukwa na Mbeya kutolima pamba kutokana na kuwepo funza wekundu wanaoshambulia zao hilo.Mkuu wa Mkoa alisema hawezi kuruhusu watu walime hadi hapo wataalamu wa wizara waje wajiridhishe na watoe tamko kuhusiana kutokuwepo kwa tishio la mdudu huyo.Katika agizo lake, Mkuu wa Mkoa aliwataka madiwani wasiende kuwahamasisha wananchi kulima zao la pamba kabla hawajapata msimamo wa serikali ili wasije kupata hasara.Mwanri alisema kitendo cha kuruhusu kulimwa kwa zao hilo kabla ya matokeo ya wataalamu hayajatoka kunaweza kutia hasara kubwa ndani na nje ya Mkoa wa Tabora, ambapo funza huyo mwekundu anasambaa maeneo ambayo hayupo.Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila aliishauri serikali iwaruhusu walime pamba kama zao mbadala la tumbaku ambayo inapigwa vita kimataifa.Aliomba serikali iwaruhusu kulima pamba kwa kuwa maeneo ya jirani zao ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku wameanza kulima na wana vyama vya msingi vya zao hilo. Nzalalila alisema wakazi wengi wamehamasika kulima pamba wanachosubiri kibali kushiriki kilimo hicho kwa ajili ya kuondoa umaskini.Katika hatua nyingine madiwani na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wametakiwa kutumia mvua zinazonyesha kuhimiza wananchi kujielekeza kulima kwa kanuni za kilimo bora. | 1 |
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam KESI iliyofunguliwa na wanachama wa Simba kuomba zuio la Uchaguzi Mkuu, imetawaliwa na utata mtupu baada ya mwanachama mmoja kuibuka na kuomba kuingia katika kesi kwa madai kwamba kuna mchezo mchafu ndani yake. Mwanachama huyo, Shaaban Omari, anataka kuieleza mahakama mchezo mchafu uliopo katika kesi hiyo na kwamba ni vigumu kupata zuio bila kuwepo kwa kesi ya msingi mahakamani. Utata huo ulionekana jana wakati maombi hayo ya zuio yalipotakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji, Augustine Mwarija. Maombi ya zuio yalikwama baada ya mahakama kubaini kwamba, Rais wa Simba, Ismail Aden Rage hakuwepo mahakamani japo Wakili wa wadai, Revocatus Kuuli kudai kwamba alipokea hati ya kuitwa. “Mheshimiwa Jaji tunaomba tuendelee kusikilizwa, tuko tayari,” alidai Kuuli. “Rais wa Simba alipelekewa hati ya kuitwa mahakamani na kama alipelekewa uthibitisho uko wapi? Alihoji Jaji Mwarija. Wakili Kuuli aliomba shauri liahirishwe ili waweze kuleta uthibitisho au Rage afike mahakamani. Jaji Mwarija aliamuru maombi hayo yasikilizwe leo na Rage afike mahakamani. Wakati wanachama hao wakiomba zuio ndipo mwanachama huyo, Shaabani Omari akiwakilishwa na Wakili Jerome Msemwa na kuwasilisha maombi ya kuingia katika kesi kwa kujitegemea ili kuieleza mahakama mchezo mchafu unaoendelea ndani ya maombi ya zuio. Akizungumza na MTANZANIA kuhusu maombi hayo yaliyowasilishwa, Wakili Msemwa alidai kwamba tayari kuna maombi ya mteja wake mahakamani na aliamua kufanya hivyo baada ya kuona kuna mchezo mchafu. “Tumewasilisha maombi namba 302/2004, mteja wangu anataka kuieleza mahakama kinachoendelea, wanachama wa Simba wamewasilisha maombi bila ya kuwepo kwa kesi ya msingi, zuio litatolewaje bila kuwepo kwa kesi ya msingi, kinachotangulia mahakamani ni kesi ya msingi. “Wagombea hawakuhusishwa katika kesi, wadai wamewasilisha maombi ya zuio bila kuambatanisha Katiba ya Simba, sisi tumeambatanisha Katiba ya Simba katika maombi ya kujiunga, tunataka Jaji aone kilichomo ndani yake. “Katika Katiba ya Simba, Ibara ya 55 inasema kwamba hairuhusiwi kutafuta msaada katika mahakama za kawaida za sheria. Uamuzi wa mwisho uliochukuliwa na vyombo vya Simba Sports Club, maamuzi ya aina hiyo hayana budi kuwasilishwa katika Mamlaka ya Baraza la Usuluhishi. Ukiukwaji wa kanuni hii utasababisha kufukuzwa kutoka Simba Sports Club,” alidai Msemwa akinukuu ibara hiyo. Msemwa alidai katiba hiyo inatamka kwamba rufaa inatakiwa kwenda TFF kisha inakwenda FIFA, lakini kufikisha suala hilo mahakamani ni kwenda kinyume na Katiba ya Simba. Maombi ya Shaabani ni dhidi ya Josephat Waryoba, Said Monero, Hassan Hassan, Rais wa Simba na Bodi ya Wadhamini. | 2 |
WATU watatu akiwemo mwanamke, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kujifanya maofisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).Wanaokabiliwa na mashitaka hayo ni Levina Mwaikeke (42) mfanyabiashara na mkazi wa Mwakibete jijini Mbeya, Peter Herman (32) na Daniel Simwinga (31) wakulima na wakazi wa Ilomba jijini Mbeya. Sambamba na kujifanya maofisa wa Tanapa, makosa mengine ni kula njama ya kutenda kosa na kutoa taarifa za uongo kwa mwajiriwa wa serikali.Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, Nemes Chami, ilidaiwa na waendesha mashitaka, Peter Mirisho na Sadam Kitembi kuwa washitakiwa walifanya makosa hayo Januari 17, mwaka huu katika Kijiji cha Mkwajuni wilayani Songwe. Waendesha mashitaka walidai washitakiwa katika kosa la kwanza la kula njama, walilifanya kinyume cha Kifungu Namba 384 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Iliyorekebishwa mwaka 2002.Walidai kosa la pili washitakiwa walijifanya maofisa wa Tanapa kutoka mkoani Iringa, kinyume cha Kifungu Namba 369 (i) cha sheria hiyo na kosa la tatu kumdanganya mwajiriwa wa serikali, askari polisi kinyume cha Kifungu Namba 122 (a). Walidai siku ya tukio, watu hao wakiwa kijijini Mkwajuni, walijitambulisha kwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi aliyetambulika kwa jina moja la Kahabi katika kituo cha polisi kuwa ni maofisa wa Tanapa wakitokea Iringa. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 27, mwaka huu itakapotajwa tena na washitakiwa wako nje kwa dhamana. | 1 |
Na LEONARD MANG’OHA-ALIYEKUWA KIBAHA WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Tanzania, Charles Mwijage, amesema ukuaji wa uchumi unapaswa kwenda sambamba na kasi ya kukuwa kwa maendeleo nchini. Ametoa kauli hiyo jana wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni na vipodozi cha Kampuni ya Keds Tanzania Limited ya nchini China, kinachotarajiwa kuanza ujenzi hivi karibuni. Waziri Mwijage alisema hatua iliyofikiwa na kampuni hiyo kuelekea ujenzi wa kiwanda hicho ni miongoni mwa kazi nzuri ya kujivunia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuhakikisha Tanzania inafikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda. “Kiwanda hiki kikikamilika kitakuwa kinazalisha tani 50,000 kwa mwaka huku mauzo ya kampuni yakiwa ni dola za Marekani milioni 33 kwa mwaka, hii inatoa matumaini kufikia lengo sekta ya viwanda kutoa walau asilimia 40 ya ajira zote. “Kinachonifurahisha na kuona kuwa wataanza uzalishaji mapema ni kuwa shughuli ya kutayarisha eneo la ujenzi wa kiwanda hiki umechukua siku 28 tu na wameniambia kuwa ndani ya miezi saba wataanza uzalishaji,” alisema Waziri Mwijage. Alisema Serikali itahakikisha inaendelea na juhudi zake za kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini ili kuhakikisha wanawekeza mikoa yote nchini na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya nyingine kwenda wilayani Kibaha kujifunza namna ambavyo wilaya hiyo imefanikiwa kuwavutia wamekezaji kuwekeza. “Niwaeleze tu uongozi wa Kampuni ya Keds, hakuna sababu ya kwenda nchi nyingine, zalisheni hapa mkauze katika nchi hizo ambako mtaona kuna soko la bidhaa zenu,” alisema. Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda hicho kinachotarajiwa kuwekeza kiasi cha dola za Marekani milioni 12, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Cliord Tandari, alisema kuwa utakuwa na faida kuwa kwa wananchi. “Kwanza kitazalisha ajira za moja kwa moja 2,000 na ajira zisizo za moja kwa moja 2,000 lakini pia utasaidia kupunguza matumizi ya fedha zetu za kigeni kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi na pengine niwatake kuendelea kuwa mabalozi wazuri na kuendelea kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini,” alisema Tandari. Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Keds Tanzania Limited, Jack Feng, alisema kampuni hiyo itaendelea na shughuli za uwekezaji katika maeneo mengine hasa katika uwekezaji wa viwanda. “Tutaendelea pia kuwashawishi wenzetu kuja kuwekeza Tanzania kwa kuzingatia kuwa Tanzania ina amani na kuna miundombinu mizuri ya kutuwezesha kwenda mahali popote, hata ukiangalia hapa tunapojenga tuko karibu na barabara kuu ya Morogoro,” alisema Feng. | 1 |
Mwanachama huyo wa Yanga ambaye kwa mujibu wa Dk Tiboroha, si hai kwa kuwa hajalipa kadi yake tangu mwaka 2012, amesema leo ataweka hadharani vielelezo kuhusu uanachama wake, huku akidai Katibu Mkuu huyo hana ufahamu mzuri kuhusu Katiba ya klabu hiyo.Akizungumza jana, Kaswahili ambaye juzi alilalamikiwa na klabu ya Yanga kwa kile ilichodai kuwa amekosea kutangaza tarehe ya uchaguzi ya klabu hiyo, alidai anamwona katibu huyo ni sawa na mtu ambaye haijui vyema Katiba ya Yanga na kuwa anatakiwa kujifunza mengi kwanza kabla ya kulaumu.Alidai akiwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi anayo haki ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kila wakati halali ukifika.Alisema anashangaa kuona kuwa licha ya juhudi zake za kuandika barua kutaka uchaguzi huo ufanyike, lakini hajaona harakati zozote zikifanyika za kutaka hayo kufanyika.Akizungumzia kuhusu uamuzi wa Yanga wa kumpeleka mahakamani kwa kosa la kuchukua michango ya wanachama kwa ajili ya kupewa fomu za uchaguzi, alidai masuala ya soka hayatakiwi kupelekwa mahakamani, bali kujadiliwa katika ngazi za klabu.Alisema kuwa kama anaweza kuwatangazia wanachama kujitokeza kuchukua fomu ni kwa nini asiwaambie watoe michango kabisa wakati hayo ni mambo ambayo yanaendana na shughuli za uchaguzi.Katika taarifa yake ya awali, Dk Tiboroha alisema kuwa anampeleka mahakamani Kaswahili kwa kosa la kukusanya michango ya wanachama huku akiwa sio mwanachama hai, kitu ambacho Kaswahili amekanusha na kudai kuwa leo anawasilisha kwa wanahabari vielelezo vya uanachama wake.“Mimi ninamshangaa huyo mtu ambaye ameingia majuzi tu madarakani na kujidai kuwa ndio anaijua Yanga vilivyo huku akishindwa kufahamu hata masuala madogo madogo katika Katiba ya klabu anayoiongoza,” alidai Kaswahili. | 2 |
DIWANI wa kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Mkoa Dodoma, Keneth Yindi, kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamewakabidhi vitambulisho vya bima ya afya wazee 600 venye thamani ya Sh milioni 2.1.Akizungumza kwenye makabidhiano hayo yaliyofanyika kata ya Buigiri diwani huyo amesema, vitambulisho hivyo vitawawezesha wazee hao kupata huduma ya afya iliyoboreshwa na uhakika.Aidha amesema, wazee hao wataondokana na kero ya kukaa muda mrefu bila kupata huduma za afya kutokana na ukosefu wa fedha za kuweza kulipia huduma.Akizungumza kwenye makabidhiano hayo ambayo pia yaliambatana na siku ya kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kuwa wazee wao waliokabidhiwa vitambulisho ni kutoka vijiji vitatu vikiwemo Mwingamile, Chinangali na Buigiri."Wengi wao hawa wazee mara nyingi wanapopatwa na matatizo ya magonjwa hufika kwangu na kuomba fedha ili waweze kwenda hospitalini kutibiwa, lakini kikubwa na cha kusikitisha zaidi wengine wamelazimika kuuza hata maeneo yao ya mashamba ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kupata matibabu," alisema.Kwa upande wao wadau wa maendeleo, Dk Ombeni Msuya na Dk Jacob Seni ambao ni wahadhiri wa Chuo Kikuu cha UDOM wakizungumza kwenye makabidhiano hayo walisema kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanawafikia wana jamii katika kusaidia huduma za kiafya zilizoboreshwa.Dk Msuya alisema kuwa juhudi hizo za uboreshaji wa huduma za afya, wao kama wadau wa maendeleo ni mojawapo kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuondoa kikwazo kikubwa kwa wazee ambao walikuwa wakikosa huduma hiyo ya msingi ya afya."Sisi kama wadau wa maendeleo tutahakikisha tutaendelea kushawishi wengine kuchangia katika juhudi hizo ili kuleta maendeleo.Kaimu Mkurugenzi, Huduma za afya ustawi wa jamii lishe ofisi ya Rais, Tamisemi, Dk James Kengie aliwataka madaktari pamoja na watoa huduma ya afya kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha kuwahudumia kwa wale wanaofika kupata huduma. | 1 |
MICHUANO ya Ligi Kuu Bara imesimama kupisha mechi za timu za taifa lakini imesimama ikiwa na msisimko mkubwa kulingana na matokeo na matukio yaliyojiri katika mechi zilizopigwa siku tatu za mwisho.Kwanza ligi hiyo imesimama ikiwa na matokeo ya kibabe na yasiyotarajiwa kulingana na mwendo wa timu husika tangu kuanza kwa ligi. Ukianza kwa Mbao, ilivyoshindwa kurudia ubabe iliouonesha mbele ya Simba na kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mbao ambayo ilianza kwa moto mkali ikiongoza ligi kisha kuichapa Simba bao 1-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kuzidi kuimarika, kipigo cha juzi kimezidi kuishusha katika msimamo wa ligi na kujikuta katika nafasi ya saba huku Yanga ikizidi kupaa ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi zake 16 baada ya mechi sita.Achana na kipigo hicho, lakini jina la Ibrahim Ajibu siku hiyo ndiyo lilikuwa gumzo zaidi kuliko ushindi wenyewe kutokana na pasi ya mwisho ya bao la kwanza aliyoipiga kabla ya baadaye kufunga bao la pili kwa mtindo wa ‘tik-tak’ lililomuibua mpaka Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kusifia ufundi wa kijana huyo.Upande wa wapinzani wa Yanga, Simba nao walikuwa moto baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon na kuzidi kujitengenezea njia ya kutetea ubingwa wao msimu huu. Mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya baada ya kukaa muda mrefu bila ya kucheka na nyavu.Hayo ni mabao ya kwanza kwa kila mmoja tangu kuanza kwa msimu huu, bahati mbaya wamefunga wakati ligi inasimama, hivyo nao wamesimama na moto wao ulioanza kuwaka katika mechi yao hiyo ya mwisho.Si unamkumbuka Donald Ngoma? Naye pia juzi kafunga bao lake la kwanza msimu huu akiwa na Azam katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Coastal Union. Ngoma amefunga bao hilo ikiwa ni mechi yake ya pili kuichezea Azam tangu atoke majeruhi ikiwa na maana ameshaanza kuzoea mazingira na anazidi kuwa bora, hivyo wapinzani wanapaswa kukaa sawa kutokana na kufahamika moto wa mshambuliaji huyo anapokuwa fiti.Kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya kulikokuwa na ‘derby’ ya Prisons dhidi ya Mbeya City nako kama ulivyosikia, Prisons ilitoka imeinamisha kichwa chini baada ya Eric Kyaruzi kuiandikia City bao la ushindi dakika ya 87 na kuzima tambo za Wajela-jela hao siku hiyo kwa matokeo ya 2-1.Singida United nayo iliendeleza mchakachaka wake wa ushindi wa tatu mfululizo baada ya kuibutua Ndanda kwa mabao 3-1. Singida iliyoanza kwa kuyumba mwanzoni mwa msimu, sasa inaonekana kuimarika ambapo kabla ya Ndanda ilishinda dhidi ya City kwa mabao 3-0 kisha kuifunga Lipuli 1-0 na sasa imepanda mpaka nafasi ya nne na pointi zake 16.JKT Tanzania timu pekee iliyopanda daraja msimu huu ambayo haijafungwa mpaka sasa nayo ilishikwa shati na vibonde Alliance kwa matokeo ya sare ya 1-1. Alliance waliinyima pointi tatu JKT kwa bao lao la dakika 90 lililowekwa na Juhudi Philimon.Mbali na matokeo hayo lakini kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo bado hakujatulia. Hata Azam inayoongoza kwa pointi zake 18 bado haina uhakika na uongozi huo kutokana na Mtibwa Sugar aliyekaa nafasi ya pili na pointi 17.Lakini presha kubwa kwa Azam ni Yanga ambayo ina pointi 16, wamepishana pointi mbili tu huku Yanga ikiwa imecheza mechi sita pekee, Azam ikiwa imeshacheza michezo minane mpaka sasa.Azam sasa inaomba Yanga iliyo kwenye moto wake iteleze ili yenyewe izidi kujiimarisha kileleni. Aidha, kileleni kunaonekana bado kuna utata kwa sababu hata bingwa mtetezi, Simba ina pointi 14 baada ya michezo saba, ikipishana pointi mbili na Singida na Yanga zilizo juu yake lakini ikipishana pointi tatu na Mtibwa na pointi nne na Azam.Kama Simba itashinda mechi yake inayofuata itakuwa sawa na Mtibwa na kuzipiku Yanga na Singida kisha kumpumulia Azam kwa tofauti ya pointi moja. Ni wazi ligi bado mbichi na imesimama wakati ambao kila timu iko moto, inataka kwenda kileleni kujihakikishia usukani mapema lakini takwimu za mechi na idadi ya pointi imebaki kuwa kizungumkuti na kuzidisha utamu na msisimko wa ligi. | 1 |
MWANDISHI WETU -PWANI MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeagizwa kuongeza muda wa kufanya kazi ya uandikishaji na uchakataji wa taarifa kwa ajili ya vitambulisho vya Uraia kutoka saa nane hadi 16. Agizo hilo ni kuhakikisha wananchi wanapata vitambulisho au namba kwa ajili ya kukamilisha zoezi la usajili wa laini za simu zinazotarajiwa kufungwa baada Januari 20 mwaka huu. Pia wameagizwa kuhakikisha wanaongeza wafanyakazi (watendaji wa dharura) katika vituo vya kuandikishia ambavyo vipo katika kila wilaya nchini. Maagizo hayo yalitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni jana alipotembelea ofisi za NIDA Kibaha mkoani Pwani ili kujionea zoezi hilo linavyoendelea. Masauni mbali na kuwaagiza NIDA kufanya kazi kwa saa 16 pia amefuta likizo na mapumziko ya mwisho wa juma kwa wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika kitengo cha uchakataji wa taarifa za vitambulisho vya uraia ili kuwezesha wananchi wote kupata vitambulisho kwa wakati. Masauni alisema wameamua kuongeza muda wa ziada wa kufanya kazi kwa wafanyakazi hao baada ya kutembelea kitengo hicho na kubaini kuwa kuna changamoto ya wafanyakazi wachache na wanafanya kazi kwa saa chache huku wananchi wakiendelea kuhangaika kupata vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini zao. “Lakini vitu ambavyo nimeviona vya msingi na tumekubaliana vifanyiwe kazi haraka, ni kitengo kinachohusika na uchakataji ama uchunguzi wa taarifa mbalimbali ambao kasi yao ni ndogo sana. “Na kasi hii ndogo inatokana na kwanza uchache wa wafanyakazi na pia uchache wa muda wa kufanya kazi, kwa maelekezo yangu na ambavyo tumekubaliana kwanza wataongeza muda wa kufanya kazi kutoka saa nane hadi 16 kwa siku zote 18 na hakutakuwa na ‘holiday’ likizo wala hakutakuwa na weekend (mapumziko ya siku za mwisho wa wiki)”alisema Masauni. Alisema pia ameagiza NIDA kuongeza wafanyakazi wa dharura ili kuongeza nguvu. “Vile vile tumekubaliana kwamba tutawatumia wafanyakazi wa dharura kwa ajili ya kuongeza nguvu katika makao makuu ya NIDA kwa lengo la kuweza kuchakata zile taarifa za kiuchunguzi”aliongeza Naibu Waziri huyo wa Mambo ya Ndani. Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Arnold Kihaule alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa ofisi zake kila wilaya zinafanya kila liwezekanalo kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa wakati na kuahidi kuwa watafanya kazi saa 24 siku zote za juma. “Sisi NIDA kwa upande wetu tunamhakikishia Waziri kuwa tunafanya kazi saa 24, tunafanya kazi jumamosi na jumapili na kwa ushahidi tumefungua kituo Mnazi mmoja tangu Disemba 22 mwaka jana hivyo hatukuwa na Krisimas, Boxing day wala Mwaka Mpya,”alisema Dk Kihaule. Aidha alisisitiza wananchi ambao tayari wamepata namba kuhakikisha wanakwenda kusajili laini zao kwa alama za vidole kabla muda haujaisha. “Kuna watu tayari wana namba za NIDA bado hawajaenda kusajili laini za simu, kwa hiyo nawaomba wale wote wenye namba waende kusajili laini zao,”alisema Mkurugenzi huyo wa NIDA. Mei mwaka jana Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ilitangaza kuanza kwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole na kuweka kitambulisho cha Taifa kama kigezo muhimu. Mwisho wa usajili huo ulikuwa ni Disemba 31 mwaka jana, kabla ya hivi karibuni Dk. John Magufuli hajaongeza siku 20 kuanzia Januari Mosi hadi 20 mwaka huu. Umuhimu wa kitambulisho cha Uraia umekuwa ni mkubwa kutokana na kuhitajika katika michakato mbalimbali. Maeneo mengine ambayo bila kitambulisho cha taifa huwezi kupata huduma ni pamoja na upatikanaji wa Pasipoti (Hati ya Kusafiria). Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nayo imeweka kigezo kimojawapo ambacho mwanafunzi anahitajika kuwasilisha ili aweze kupata mkopo ni Kitambulisho cha Taifa. Sehemu nyingine zinazohitaji vitambulisho ni wakati wa usajili wa kampuni kwa Wakala wa usalili wa Kampuni (BRELA), Kupata leseni ya udereva, umiliki wa ardhi na hata ajira katika baadhi ya makampuni ya sekta binafsi Pia Sekretarieti ya ajira iliwahi kutoa tangazo la ajira na kuweka kigezo kimojawapo kwa waombaji wa ajira ni kuwa na kitambulisho cha Taifa. Tangazo hilo lilieleza kwamba kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika mfumo wa ajira nchini waombaji walitaarifiwa kuwa kuanzia mwishoni mwa Septemba mwaka 2019 kuwa na vitambulisho vya Taifa. Katika kuonyesha umuhimu wa kitambulisho hicho pia mwaka jana Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma alielekeza mahakama zote nchini kutoa dhamana kwa mshitakiwa mwenye Kitambulisho cha Taifa au wenye vitambulisho hivyo kuwadhamini watu ambao kesi zao zinadhaminika. Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Jaji Mkuu kutoa mapendekezo hayo kwani Julai 19 mwaka jana wakati wa mahafali ya 60 ya mawakili wapya katika shule ya Sheria Jaji Mkuu alitoa mapendekezo hay ya kutumia kitambulisho cha Taifa. Wakati sasa akizielekeza Mahakama kuanza kutumia vitambulisho hivyo, wakati huo alipendekeza kitambulisho hicho kitumike kwenye dhamana pasipo kutaka mshitakiwa kuonyesha mali. Pendekezo hilo alilitoa ikiwa ni katika kushauri namna ya kutatua changamoto ya msongamano wa mahabusu magerezani kwa kulegeza mashariti ya dhamana. | 1 |
Staa anayewakilisha lebo ya muziki ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny awakutanisha kwenye remix wakali kutoka Tanzania, Congo, Miami na Aruba kwenye Hit-track yake ya Tetema. Rayvanny kwenye ukurasa wake wa Instagram, ameweka wazi ujio wa remix hiyo kupitia cover ya ngoma hiyo aliyoipandisha na kueleza kuwa, ngoma hiyo itaatoka rasmi wiki ijayo. can’t wait for the world to hear this one. From #EastAfrica #Congo #Miami and #Aruba! #TetemaRemix ft My Brothers @pitbull @mohombimusic and @jeon_arvani @diamondplatnumz OUT NEXT WEEK ! Exec. produced by @s2kizzy @africancleopatra @mohombiMusic #WCBWasafi #PowerHouse #HausOfAfro #SwahiliNation #FromAfricaToTheWorld A post shared by VANNYBOY (@rayvanny) on Jul 31, 2019 at 1:30pm PDT Tetema Remix imesheheni wasanii kama Pitbull, DiamondPlatnumz Jeon, na Mohombi. Hadi sasa Tetema ‘original’ aliyomshirikisha DiamondPlatnumz imefikisha watazamaji milioni 24 kwenye mtandao wa Youtube. diamondplatnumz
DROOOOOP ITTTTTT!!!!!! juma_jux
Never regular harmonize_tz
🔥🔥 vanessamdee
💫💫💫💫💫 tuerny_cuty
Naitwa tuerny naishi marekani naitaji mwanaume wa kunioa awe tayari kuishi New york america. rafiki_wa_diamondplatnumz
😂😂😂😂Rayvanny Sema Kweli Basi Kumamam*k* s2kizzy
🔥🔥🔥🔥🔥 world 🚀🚀 shit fabrizio_allay
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 kameboy_j
💥💥💥💥 diamondplatenumz
Lazima tuvunjevunjeee🔥🔥🔥 3classic_baby
VannyBoy hii km movie sijui tuite movie gani maana🔥🔥🔥 shekie22
Waaat | 4 |
MZUNGUKO wa kwanza wa ligi daraja la kwanza ngazi ya taifa unaendelea leo kwa timu za AFC na Dodoma kushuka kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku kila mmoja akitoa tambo zake kuelekea mchezo huo.Arusha FC inashuka dimbani ikiwa tayari imecheza michezo minne ikitoka sare michezo miwili na kupoteza michezo miwili,iko nafasi ya Pili kutoka mwisho kwa pointi 2. Dodoma FC imeshuka dimbani Mara nne imeshinda michezo miwili na imetoka suluhu mchezo mmoja na kupoteza mmoja iko nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B.Akizungumzia mchezo huo kocha mkuu wa timu ya AFC David Nyambele alisema amejiandaa kuchukua pointi 3 na makosa yote yaliyojitokeza katika michezo miwili iliyopita hayatajirudia na kwamba anawaheshimu wapinzani wao ila wamejiandaa na hawezi kukubali kupoteza tena mchezo nyumbani."Dodoma wasitarajie mteremko hawatatoka na ushindi sisi tuko imara nyumbani tutapambana kupata alama tatu na tunashukuru pia mashabiki wetu wanatuunga mkono na ninawasihi waje kwa wingi uwanjani.''Kwa upande wao Dodoma FC kupitia kwa katibu mkuu wao Johnson Fortnatus alisema AFC ni timu kibonde na haiwezi kuifunga Dodoma FC. "Uwezo wa timu yetu ni Mkubwa na tupo na maandalizi mazuri na siku zote unapopoteza mchezo mmoja,ule unaofuata unaenda kucheza kwa tahadhari hivyo tumerekebisha kile tulichokosea ," alisema Fourtnatus Wakati AFC ikiikaribisha Dodoma ,Arusha United itaikaribisha Transit camp kesho kwenye uwanja huohuo. | 1 |
BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuhamia Dodoma na imeahidi kuidhinisha Dola za Marekani milioni 455 (sawa na zaidi ya Sh trilioni 1.5) kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato sambamba na ujenzi wa barabara za mzunguko jijini humo.Rais wa AfDB, Dk Akinwumi Adesina aliyasema hayo makao makuu ya benki hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast kwenye mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.Dk Adesina alisema benki hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), lakini pia kwa Tanzania.Alisema benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha Dola za Marekani milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma ; na kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, kinatarajiwa kuidhinishwa na mapema mwezi ujao.Dk Adesina aliongeza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ina imani na mageuzi ya kiuchumi yanayotekelezwa chini ya uongozi wa Rais Magufuli ikiwamo utoaji wa huduma za kijamii kama elimu bila malipo, afya na maji na mapambano dhidi ya rushwa na kuleta uwajibikaji katika taaisisi za umma, na iko tayari kuunga jitihada hizo za serikali kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu.Aidha, alielezea nia yake ya kutaka kushuhudia Bara la Afrika likipiga hatua kubwa za maendeleo sasa na kwa haraka na sio kusubiri baadaye. Kwamba katika kipindi chake cha uongozi AfDB, atahakikisha azma hiyo inatekelezeka.Profesa Kabudi aliishukuru AfDB kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, inayotekelezwa na Rais Magufuli ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimaye bara zima la Afrika.Alimtaka Dk Adesina kuimarisha ofisi za kanda za AfDB ili zitoe huduma zote za kibenki karibu na wanufaika wake sambamba na kuunga mkono miradi ya kimkakati, inayounganisha nchi na nchi Afrika ili kuboresha na kurahisisha huduma ya usafiri na hivyo kuwezesha biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na kujiletea maendeleo.Profesa Kabudi yuko Abidjan kushiriki mkutano wa siku mbili wa dharura wa mawaziri wa fedha, uliondaliwa na AfDB. | 1 |
Kwa miaka mingi, Uganda imekuwa ikisubiri medali kwa mchezaji mmoja mmoja katika mashindano hayo ya dunia ya nusu marathon, ambapo sasa itabidi kuendelea kusubiri medali hiyo hadi mwaka 2020 Gdynia, Poland.Kwa mara nyingine, taifa hilo la Afrika Mashariki limeshindwa kupata nafasi ya kupanda stejini kutokana na kuendeleza ukame wa medali katika mashindano haya ya riadha, ambapo kwa mara ya mwisho ilipata medali mwaka 2004 wakati wanariadha watatu, Wilson Busienei, Martin Toroitich na Joseph Nsubuga waliposhinda medali ya shaba kwa timu mjini New Delhi, India.Jumamosi, Uganda ilitwaa kiasi hicho cha fedha baada ya kushika nafasi ya tano kwa upande wa timu katika mbio za wanaume za kilometa 21, mbio ambazo mshindi ni Mkenya, Geoffrey Kamworor aliyeshinda mbio hizo kwa mara ya tatu mfululizo.Kamworor, ambaye alichomoka kwa kasi zikiwa zimebaki kilometa nne kabla ya kumalizika kwa mbio hizo, alishinda kwa kutumia saa 1:02 na kuongeza taji la mwaka 2014 na 2016 huko Copenhagen na Cardiff.Hatahivyo, bado Fred Musobo ndiye mwanariadha bora wa Uganda baada ya kumaliza katika nafasi ya 20 baada ya kuposti muda wake bora binafsi wa saa 1:01:38. Hilo lilimfanya kocha wa Uganda, Gordon Ahimbisibwe kutamka awali kuwa Kenya walikuwa wakiihofia Uganda kabla ya kufanyika kwa mbio hizo.Chakuvutia zaidi, Jackson Kiprop ndiye mwanariadha wa mwisho wa Uganda kumaliza ndani ya 10 bora wakati alipomaliza katika nafasi ya saba katika mashindano yaliyofanyika Karvana, Bulgaria miaka sita iliyopita.Ethiopia iliiongoza Kenya na Bahrain katika orodha ya medali katika timu kwa upande wa wanaume na wanawake, ambapo Jemal Yimer, Getanneh Molla na Betesfa Getahun walikosa nafasi ya kupanda stejini lakini walimaliza katika nafasi ya nne, tano na sita.Kwa upande wa wanawake, Muethiopia Netsanet Kebede kidogo avunje rekodi ya dunia kwa sekunde 14 alipomaliza kwa kutumia saa 1:06:11, wakishinda zawadi ya dola za Marekani 50,000. | 2 |
NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zimedhamiria kuweka mifumo ya kuzuia athari kubwa za majanga na kujenga satelaiti ya pamoja ili kuhifadhi na kudhibiti taarifa za intaneti, zisitoke katika ukanda huo na kwa nchi husika.Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua Mkutano wa Mawaziri wa nchi 16 za SADC, unaotanguliwa na vikao vya makatibu wakuu na maofisa watendaji wa jumuiya hiyo.Mkutano huo wa siku tano, unafanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.Unajadili sera, miradi, mipango na mikakati ya sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Usafirishaji (Uchukuzi), Hali ya Hewa na Mawasiliano.“Wote tunakumbuka nchi za wenzetu Zambia, Zimbawe, Malawi, zilipata mafuriko kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mwaka jana. Mabadiliko ya hali ya hewa yana taarifa lakini pia huwa na dalili kuna kitu kinakuja”, alisema.“Kwa kukua kwa teknolojia sasa hivi mnaweza mkapata dalili na mkapeana taarifa ili majanga haya ya kiasili yanapotokea yasilete madhara makubwa kwa wananchi ili waweze kujiandaa, Tanzania ilikuwa ya kwanza kupeleka chakula, dawa. Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli alifanya kazi kubwa sana, “ alisema Kamwelwe.“Sasa vikao vyetu hivi, vitapitia hayo matatizo, na kukua kwa teknolojia kutaweza kutupa taarifa mapema tuweze kupunguza madhara. Huu ni mkutano muhimu sana, ajenda mahususi za kutuwezesha kujitegemea kwa kiwango kikubwa wenyewe badala ya kutegemea wenzetu, zitajadiliwa,” alisema Kamwelwe.Kuhusu satelaiti alisema, “Tunategemea wataalamu hawa watakaa, tunao mainjinia wa kutosha katika nchi zote 16 , tuna vyuo vikuu, vijana wataalam tunataka kuwaunganisha hawa pamoja na kujenga satelaiti.“Hatuna satelaiti Afrika ambayo ni ya SADC. Tunataka kufikiria tuwe na ‘baloon’ tuwe na satelaiti ya pamoja ya nchi 16 ili taarifa tuwe tunapeana sisi wenyewe, siyo kwamba tutaacha kushirikiana na dunia, hapana, lakini tutakuwa tunashirikiana na kuwa na mchango wa nchi za SADC kwamba kuna teknolojia tulizozibuni kama ambavyo mnaona TMA (Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania) wamebuni fomula mbili ambazo zinatumika duniani na zimekubalika.Maeneo mengine wataojadili ni usafirishaji wa anga, reli na barabara na kuimarisha miundombinu kwa ajili ya usafirishaji pamoja na kuwezesha upatikanaji wa fedha kujenga miradi inayounganisha nchi hizo kikanda.Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa SADC, Dk Stergomena Tax, Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretarieti ya jumuiya hiyo, Mapolao Mokoena, alisema jumuiya hiyo iliongeza vifaa kwa nchi zilizoathirika kwa majanga, Zimbabwe, Msumbiji na Comoro.Alisema mikutano ya watendaji na wataalamu wa SADC inayoendelea kabla ya mkutano wa mawaziri wa sekta hizo, inachambua namna ya kuifanya jumuiya hiyo kusonga mbele kiuchumi kwa kuwa na mifumo ya Tehama, hali ya hewa, usafirishaji na ujenzi wa miundombinu bora na itapeleka mapendekezo makini kwa mawaziri.Alishukuru kwa makaribisho na uendeshaji mzuri wa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika Dar es Salaam Agosti 17 na 18 mwaka huu na kuitaka nchi ya Msumbiji inayopokea kijiti cha uongozi mwakani, kufanya vizuri kama Tanzania.Awali, Kamwelwe aliwakaribisha wageni kutoka nchi hizo 16 na kuwashauri wahakikishe hawaondoki Tanzania bila kutembelea Kisiwa cha Zanzibar ambacho ni maarufu kwa kilimo cha karafuu, Mlima mrefu Afrika, Kilimanjaro na Mbuga ya Wanyama ya Serengeti kujionea uzuri wa Tanzania. | 1 |
MIAMI, MAREKANI NYOTA wa Tenisi nchini Uingereza, Andy Murray, ameondolewa katika michuano ya wazi ya Miami dhidi ya mpinzani wake, Grigor Dimitrov. Murray, ambaye anashika nafasi ya pili kwa ubora wa mchezo huo duniani, ametolewa katika mzunguko wa tatu kwa seti 6-7, 6-4, 6-3, sawa na alama (1-7). Katika mchezo huo Murray, mwenye umri wa miaka 28, alianza kwa kasi ya juu na kumtisha mpinzani wake kwa kuwa hadi mapumziko nyota huyo alikuwa akiongoza kwa seti moja. Lakini Dimitrov ambaye ana umri wa miaka 26, alirejea uwanjani huku akionekana kuwa na mipango mipya ya ushindi na kufanikiwa kumtupa nje mpinzani wake. “Mchezo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na lazima mmoja ashinde na mwingine aweze kuyaaga mashindano, nimekosa bahati ya kusonga mbele kutokana na mpinzani wangu kufanikiwa kutumia nafasi. “Lakini ninaamini nitajifunza kutokana na makosa ambayo nimeyafanya katika michuano hii, pia nampongeza mpinzani wangu kwa kunipa changamoto kubwa na kufanikiwa kusonga mbele na namtakia kila la heri,” alisema Murray. | 2 |
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula (pichani) amewaonya viongozi wanaotoa siri za vikao, kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili na kuagiza wanaobainika wachukuliwe hatua.Mangula alitoa onyo hili jana mkoani Simiyu wakati wa mkutano wa Halmashauri ya CCM ya wilaya na mkoa na watendaji wa serikali wa halmashauri sita za wilaya za mkoa wa Simiyu.Alisema viongozi wanaotoa siri za vikao hawafai kuongoza chama na wanapobainika ni vema wakachukuliwa hatua za kinidhamu.“Kumekuwa na tabia chafu kwa baadhi ya viongozi ndani ya chama chetu ambao wanatoa siri za ndani za vikao...na kama hamjui kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za chama na kama kuna viongozi watakaobainika kufanya hivyo wachukuliwe hatua za nidhamu,” alisema.Aliagiza viongozi wa chama na serikali wazingatie taratibu na kanuni za utendaji wa majukumu yao na kuacha majungu ndani ya ofisi zao ili kuondoa migongano na migogoro.Alionya pia tabia ya baadhi ya viongozi wa chama kutumia madaraka yao kubughudhi watendaji wa serikali na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kwa ujenzi shule bora na zahanati.Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amemhakikishia Mangula ushirikiano na chama ili kutimiza maono ya Rais John Magufuli na kuwaomba watendaji kuzidisha kasi ya kusikiliza malalamiko ya wananchi. Mwenyekiti wa Wilaya ya Maswa, Paul Jidai alisema viongozi wengi wamekosa mafunzo ya uongozi ndio maana huwa wanakosa uadilifu. Jidai alisema ni vema chama kikawapeleka viongozi katika mafunzo ya uongozi ili waendane na uhalisia wa nafasi wanazopata. | 1 |
RAYMOND MINJA – IRINGA Naibu katibu Mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania
bara(UWT), Jeska Mbogo, amewataka
wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa kuelekeza akili zao na nguvu zao kwenye
masomo badala ya kuzipeleka kwenye mambo ya
anasa. Mbogo ameyasema hayo leo Juni 18, wakati akizunguza na
wanafunzi wa vyuo vikuu vinne ambao ni wanachama wa UWT ambapo amewakabidhi
rasmi kadi za jumuiya hiyo na kuwataka wajikubali jinsi walivyo na kuachana na
tabia ya kujibadilisha maumbile kwa kutumia dawa za kachina. “Ndugu zangu kitu cha kwanza kwenye Maisha yako kama
mwanafunzi ni kujitambua jua umefuata nini chuoni acheni kujirahisisha mnatumika
sana ,wengine mnajibebisha kwa walimu wenu ili muweze kuongezewa alama kwenye
mitihani yenu achene kujirahisisha vivyo
nye ni dhahabu subirini muda wenu ufike,”
amesema. Aidha amewataka wazazi kutenga muda wa kuwa karibu na watoto
wao na kuzungumza nao kwani wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda
wao mwingi kutafuta fedha na kuwasahau watoto wao jambo ambalo linazidisha mmomonyoko
wa maadili kwa watoto wengi. Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa
Rose Tweve amewataka vijana hao kujiamini katika Maisha yao na kutokuwa watu
wakulaumu na kulalamika bali wawe ni watu wa kufanya kazi kwa vitendo
kulisaidia Taifa lao. | 1 |
Ofisa Madini Mkazi katika wilaya ya Chunya, Ronald Mremi alimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage kuwa katika kipindi hicho, ofisi hiyo pia imefanikiwa kukusanya kiasi ch Sh milioni 187.6 ikiwa ni makusanyo yanayotokana na ada mbalimbali.Mwijage alikutana na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo, akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme ya awamu ya pili inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) katika Kanda ya Kusini.Kuhusu utengaji wa maeneo kwa wachimbaji wadogo katika wilaya hiyo, Mremi alisema Wizara ya Nishati na Madini imetoa maeneo mawili, mojawapo ni eneo la Itumbi B lenye ukubwa wa kilometa za mraba 12.78 ambapo lilifanyiwa michoro ya kukata viwanja na kupata viwanja zaidi ya 300. | 0 |
SHULE ya Msingi Pugu Kajiungeni, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam imekabidhiwa jengo la vyoo kwa ajili ya wanafunzi kikiwamo chumba maalumu cha wasichana wenye mahitaji staha. Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT) ilikabidhi jengo hilo lenye vyumba 12 lililogharimu Sh milioni 65. Licha ya chumba cha wasichana wenye mahitaji maalumu, jengo hilo pia lina vyumba viwili kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi vyoo hivyo jana kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Pugu Kajiungeni, Rophina Kawishe, katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, walimu, wanafunzi na wawakilishi kutoka Shirika la Water Aid. Balozi Maajar alisema, “tumefurahia kukamilisha mradi huu wa kwanza.Kwa kipindi kirefu huko nyuma HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati 10,000 na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini”. Alisema kampeni ilifanikiwa kuhamasisha umma kuona wajibu wa kuboresha mazingira ya shule si wa serikali pekee bali wa kila mtu na kila taasisi.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alipongeza HMT kwa kuamua kukabili changamoto za kuboresha mazingira ya elimu kwa kutoa misaada ya madawati, huduma za maktaba na kujenga miundombinu ya vyoo. Taasisi ya WaterAid imesaidia shule hiyo, kwa kuipa vifaa vya kuvuna maji ya mvua, hali iliyoongeza ubora wa vyoo vilivyojengwa na taasisi kwani mazingira ya vyoo yatakuwa safi na ya afya zaidi. | 1 |
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Finland, Timo Soini amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli za kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji.Alitoa pongezi hizo alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga ambaye yupo nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia Februari 25 hadi 26, mwaka huu. Kwenye mazungumzo yao, mawaziri hao walisisitiza umuhimu wa Tanzania na Finland kuboresha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za biashara, uwekezaji, mafunzo ya ufundi, ajira kupitia sekta ya misitu, ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa kwa kuzingatia usawa na kuwajengea uwezo wanawake na watoto.Aidha, Soini alitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na mchango mkubwa katika usuluhishi wa migogoro inayozikabili baadhi ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Walikubaliana kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama, ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu na matishio ya ugaidi.Kabla ya mazungumzo hayo, Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Sampo Suihko, Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha OMNIA Espoo, ambaye alieleza utayari wa taasisi yake wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kubadilishana uzoefu wa kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi yanayoendana na soko la ajira. Dk Mahiga pia alifanya mazungumzo na Matti Ahtisaari, Rais mstaafu wa Finland na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro.Ahtisaari aliipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya katika utatuzi wa migogoro katika nchi za Maziwa Makuu na kusihi kuendeleza jitihada hizo kwa ustawi wa dunia nzima. Vilevile, Dk Mahiga alifanya mazungumzo na Jukka Kallio, Makamu wa Rais wa Helsinki. Katika mazungumzo hayo, uongozi wa Bandari ya Vuosaari umeahidi kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kuboresha mifumo ya kidijiti itakayoongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.Katika kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini, Mahiga alifanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara (Business Finland) na makampuni makubwa ya kibiashara nchini humo. Wafanyabiasha hao walipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na waliahidi kuwekeza na kushawishi makampuni mengine, kuona umuhimu wa kuwekeza nchini Tanzania. | 1 |
KULWA MZEE – DAR ES SALAAM Katibu wa itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amewasili katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufata utaratibu, wa kulipa faini
ya Sh milioni 30 ili kumnusuru DK Vicent Mashinji aliyetiwa hatiani jana. Polepole amefikia hatua hiyo baada ya Mahakama hiyo mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwatia hatiani viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti
Freeman Mbowe na wenzake wanane. Mahakama hiyo iliwahukumu kwenda jela kwa kila kosa miezi mitano au
kulipa faini jumla Sh milioni 350. Adhabu hiyo ilitolewa kwa makosa 12 na kosa moja la kula njama
washtakiwa wote waliachiwa kwani halikuthibitika. Akizungumza katika viwanja vya mahakama akiwa ameambatana na wanachama
wengine wa chama hicho pamoja na mke wa mfungwa huyo , Polepole amesema amefika
kufuata utaratibu ili wamtoe Mashinji. “Tayari tumeshapewa control namba, tunaenda kulipa kisha tutarudi
Mahakama ya Kisutu ili tupewe utaratibu wa kwenda kumtoa gerezani,” amesema
Polepole. | 1 |
Mwandishi Wetu ,Dodoma CHANZO cha kuwapo mauzo ya kangomba kwenye zao la korosho kimetajwa kuwa ni kutokana na gharama kubwa za kuandaa mashamba, kupalilia pamoja na bei kubwa za viuatilifu. Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Christine Ishengoma amesema bungeni leo, Mei 17 kuwa kuna gharama kubwa ambazo wakulima wa kawaida hawawezi kuzimudu hivyo kuingia mikataba ya kupata fedha zitakazosaidia kuhudumia mashamba yao “Hali hii inatokana na wakulima kukosa usaidizi wa Serikali wakati wa kuandaa msimu mpya wa mazao.”amesema Dk Ishengoma | 1 |
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM KAMATI ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, jana imevunjwa rasmi baada ya kumaliza kazi yao iliyokuwa inawakabili ya kuhamasisha mechi dhidi ya Algeria. Kamati hiyo iliyoundwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ilikuwa na kazi ya kuhakikisha Taifa Stars inafanya vema kwenye michuano ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia 2018 nchini Urusi. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Farough Baghouzah, alisema kuwa kamati hiyo imevunjwa rasmi kwa kuwa wamemaliza utekelezaji wao. “Tunawashukuru Watanzania wote kwa kuweza kusapoti timu yao pamoja na hatua zote tulizopitia, licha ya kutolewa kwa jumla ya mabao 9-2 dhidi ya wapinzani Algeria,” alisema. Naye Mlezi wa kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, alisema kamati hiyo ilifanya kazi ipasavyo, licha ya kukumbwa na ukata. Wakati huo huo, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Michael Wambura, alisema kazi kubwa ya kamati hiyo ilikuwa ni kurudisha hamasa kwa mashabiki na morali kwa wachezaji wa timu hiyo. “Tulianza bila fedha, ndio sababu ya kupitisha harambee ambayo baadaye tulipata Sh milioni 124 kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na mashabiki wa timu hii ambapo fedha hizo ndizo zilitusaidia kufanikisha malengo mbalimbali tuliyojiwekea,” alisema Wambura. Alisema lengo lao lilikuwa ni kupata Sh milioni 300, ambazo hata hivyo zilikosekana na kupata milioni 124, fedha hizo zilitumika kwa posho za wachezaji, kulipia hoteli, gharama za tiketi za Afrika Kusini walipoweka kambi na Algeria kwenye mechi ya marudiano. Akifafanua Sh milioni 500 zilizodaiwa kuahidiwa na kamati hiyo kama timu ingefanya vema kwenye michuano hiyo, Wambura alisema fedha hizo hazikuwa kwenye kamati kama ilivyoripotiwa, bali ni ahadi tu iliyotolewa na mashabiki. “Kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam kamati iliahadi kutoa milioni 50 kama pongezi kwa wachezaji ambapo baada ya kupata sare ilibidi wapewe milioni 25, lakini hizo milioni 500 hazikuahidiwa na kamati bali ni mashabiki tu, walisema watatoa iwapo timu hiyo itafanya vema kwenye mchezo wa marudiano,” alisema. Akifafanua zaidi, Wambura alisema shabiki mmoja aliahidi atatoa Sh milioni 300, mwingine milioni 100 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Farough milioni 100, ambazo zote zingefika idadi ya Sh milioni 500, lakini fedha hizo hazikutolewa kutokana na matokeo waliyopata kikosi hicho. Kamati hiyo ya Saidia Stars ilimaliza vema kwa kuwashukuru wadau mbalimbali, akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alitoa Sh milioni 20 kwenye kamati hiyo pamoja na ushauri. | 2 |
Na JANETH MUSHI-MONDULI WAKULIMA wadogo wa shayiri kutoka vijiji vinne vilivyopo Kata za Monduli Juu na Emairete wilayani hapa, wameiomba Serikali kuwatafutia masoko ya zao hilo kama ilivyofanya kwa zao la korosho mkoani Mtwara. Walitoa ombi hilo jana katika Kijiji cha Emairete wakati wa mkutano wa wakulima uliohudhuriwa na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. Mmoja wa wakulima hao, Loretu Meyan, alisema kwa zaidi ya miaka 20 Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya Kampuni ya Kimataifa ya ABInBev, ilikuwa ikiwakopesha mbegu na dawa kisha hununua shayiri hiyo, ila kuanzia mwaka huu hawajaingia nao mkataba tena. Meyan alisema katika kata hizo mbili wamekuwa wakitegemea kilimo cha shayiri kujiongezea kipato na kusomesha watoto, hivyo kuanzia sasa hawajui kilimo cha kuendelea nacho kwani msimu wa kupanda mazao mengine umeshapita. “Serikali ituangalie kwa jicho la huruma kwani zaidi ya hekari 3,000 hazijapandwa, tulikuwa tunasubiri mbegu za mkopo mwaka huu ili tupande shayiri, tulikuwa tunasomesha watoto kupitia zao hili ambalo limekuwa na faida kwetu kwa kiasi kikubwa. “Tunaiomba Serikali itutafutie masoko ili tukipanda zao hili tujue pa kuuzia au ifanye kununua shayiri kutoka kwetu kama ambavyo ilifanya kule Mtwara kununua korosho,” alisema Meyan. Naye Mboyo Kayai alisema nia ya Serikali ya kuelekea uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025 itatekelezeka zaidi iwapo itaangalia wakulima wadogo. “Falsafa ya Serikali ya ‘hapa kazi tu’ na ‘kuelekea uchumi wa kati wa viwanda’ itatekelezeka vipi kama tunarudisha majembe nyuma? Kilimo hiki kina msaada mkubwa kwetu kwani sasa hivi husikii Masai kaiba ng’ombe, tumejikita katika kilimo,” alisema Kayai. Naye Katibu wa Chama cha wakulima Monduli Juu, Moloimet Sane, alisema Serikali iangalie namna ya kuwasaidia wakulima na kwamba Januari 13 ndipo walipopewa taarifa za kutokuendelea na mkataba wa awali. Kwa upande wake, ofisa ushirika kutoka halmashauri hiyo, Ester Tarimo, aliwaeleza wakulima hao kuwa watafuatilia na kupeleka suala hilo ngazi za juu kutafutiwa ufumbuzi. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli, Salim Omary, alisema licha ya wananchi hao kukosa mbegu hizo, halmashauri hiyo pia itapoteza mapato waliyokuwa wakitegemea. “Tutafuatilia suala hili kwani hata zao la mtama mnaloambiwa mlime linahitaji utaalamu siyo la kubahatisha, tukiwa kama Serikali tutafuatilia na kupeleka suala hili ngazi husika,” alisema Omary. | 1 |
KIKOSI cha Simba kimewasili salama mjini Istanbul, Uturuki jana baada ya kuondoka alfajiri ya juzi tayari kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 22.Baada ya kuwasili, Simba walipumzika kidogo kabla ya kwenda kufanya mazoezi yao ya kwanza jana jioni, ambayo pia ni mazoezi ya kwanza timu hiyo ikiwa chini ya kocha Mbelgiji Patrick Aussems.Simba iliondoka na wachezaji wote iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao chini ya kocha wake mpya, Aussems atakayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma aliyekuwa msaidizi pia wa makocha wawili waliopita, Mcameroon Joseph Omog na Mfaransa, Pierre Lechantre.Ikiwa nchini Uturuki, timu hiyo itapata mazoezi katika mazingira na viwanja bora, pamoja na mechi za kirafiki za kujipima nguvu kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 8, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara watauanza msimu kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Azam Sports Federation Cup (ASFC), Mtibwa Sugar Agosti 18, katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa na Bodi ya Ligi, wekundu hao wa Msimbazi wataanza kwa kucheza dhidi ya Tanzania Prisons Agosti 22 kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa 1:00 usiku.Timu hiyo itakutana na mahasimu wao, Yanga Septemba 30, mwaka huu katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa taifa kuanzia saa 10:00 jioni. | 2 |
MKAZI wa Kijiji cha Kagera wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, Celestin Masatu (39) amejichoma kisu tumboni, kujikata kolomeo na kufa baada ya kumfanyia ukatili mkewe Jenifa Julias (30) wa kumchanachana mwilini na kisu, huku akiacha ujumbe akiomba msamaha kwa Rais John Magufuli kwa kitendo alichokifanya.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 7.15 usiku, katika nyumba ya kulala wageni ya Emma iliyoko eneo la kata ya Nakatungulu mjini Nansio.Alisema baada ya kumchoma visu mkewe na baadaye kujichoma kisu na kujikata kolomeo, majeruhi hao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya mjini Nansio usiku huo huo ili kupatiwa matibabu lakini Masatu alipoteza maisha asubuhi siku iliyofuata wakati mkewe akihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.Kamanda huyo alisema kabla ya kujidhuru kwa kujichoma na kisu tumboni, kisha kukatakata utumbo wake na baadaye kolomeo, Masatu alimchoma visu tumboni na shingoni mkewe na kusababisha utumbo na mfuko wa kizazi uliokuwa na mtoto mchanga wa miezi miwili kutoka nje.Alisema wawili hao, awali waliwahi kuishi pamoja kama mme na mke na walijaliwa kupata watoto wawili kabla ya mwanamke kuamua kuondoka na vifaa vya nyumbani na kwenda kuishi peke yake katika kijiji cha Bukongo.Alisema hata hivyo katika siku za hivi karibuni walirejesha mahusiano yao ya ndoa na hadi siku hiyo ya tukio walikubaliana wakutane lakini kumbe mwanaume alikuwa na mpango wa kumdhuru mwenzake kwa sababu ya wivu wa mapenzi.Baada ya Polisi kufanya upekuzi kwenye chumba walichofikia, mbali ya kupata kisu kilichotumika kuwadhuru na vitu vyao vingine kama nguo na viatu, pia lilipatikana daftari lenye maandishi yanayosadikika kuandikwa na Masatu akiomba msahama kwa Rais Magufuli kwa kosa alilolifanya na mgawanyo wa mali zake.“Sehemu ya barua hiyo imeandikwa hivi, nanuku: ‘Naomba radhi kwa serikali inayoongozwa na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kitendo nilitakachofanya kwa hiari yangu.’ Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Emma, Musiba Mayunga alisema alishitushwa na kelele za mwanamke akiomba msaada usiku wa manane na alipowataka wafungue mlango, mwanaume alikataa ndipo aliomba msaada wa uongozi wa kitongoji na Polisi.Alisema kelele hizo ziliwaamusha wageni wengine waliofikia kwenye nyumba yake na ndio waliofanikiwa kuvunja mlango wa chumba na kuwatoa wanandoa hao wakiwa na majeraha.Mwenyekiti wa kitongoji cha Sokoni, Kata ya Nakatungulu, Celestin Mangwesa alisema baada ya kujulishwa na kufika eneo la tukio, alishuhudia mwanamke akitoka nje ya chumba utumbo ukiwa nje. Alisema mwanaume aligoma kutoka hadi Polisi walipowasili na kuamua kuingia ndani ndipo akatolewa akiwa amepoteza fahamu kutokana na majeraha makubwa aliyokuwanayo. | 1 |
Na CHRISTIAN BWAYA
KUJIFUNZA tabia mpya kunaweza kuwa kazi ngumu kama ilivyo kujaribu kuacha tabia usiyoipenda. Sababu ni kwamba mwili, kama ulivyo ufahamu wa mtu, unapenda kufanya kilichozoeleka. Nakumbuka nilipoazimia kuanza kufanya mazoezi kila siku alfajiri nilipata shida kuzoea. Ilinichukua muda mrefu kidogo mazoezi kuwa sehemu ya maisha yangu ya kila siku. Kila nilipojaribu kuamka alfajiri, nilikabiliana na mpambano mkali na mwili usiotaka kuamka. Japo nilikuwa na nia ya dhati ya kufanya mazoezi, bado kiuhalisia haikuwa rahisi. Nilijikuta nikijipa sababu za kutosha kuahirisha kwenda kwenye mazoezi kwa matumaini kuwa ningeendelea kesho yake. Wakati mwingine hiyo kesho ilifika baada ya wiki moja au zaidi. Baada ya muda mrefu wa kupambana na upinzani wa ndani kwa ndani, niliamua kuweka malengo mahususi yatakayonisukuma kujenga tabia mpya ya mazoezi. Kwa hiyo, pamoja na ugumu wake, niliazimia mazoezi yatakuwa sehemu ya ratiba yangu ya kila siku. Kwamba ikipita siku sijafanya mazoezi, basi hiyo itamaanisha ninaelekea kushindwa. Watu wengi hushindwa kujenga tabia mpya wanazozihitaji kwa sababu hawazifanyi tabia hizo kuwa sehemu ya mambo wanayoyafanya kila siku. Wanafikiri kutamani tu kujenga mazoea mapya kunakuja bila jitihada zozote. Matokeo yake, wanaendelea kuwa na tabia zile zile miaka nenda – rudi. Ikiwa unataka kuanza kusoma vitabu, kwa mfano, hakikisha usomaji unakuwa sehemu ya ratiba yako ya kila siku. Siku isipite hujasoma. Kwa kawaida, mwanzoni akili na mwili vitakupa upinzani mkali kwa sababu havijazoea tabia hiyo mpya. Siri hapa ni kuendelea kufanya kile kile unachotaka kukifanya bila kujali unajisikiaje. Lakini pia, kuna tatizo la kuanza tabia mpya kwa ‘fujo.’ Nakumbuka siku ya kwanza tu nilikimbia kwa kasi kubwa utafikiri nilikuwa kwenye mashindano ya mita 400. Kitu ambacho sikukifahamu ni kwamba kwa kufanya hivyo niliuchosha mwili kwa kuulazimisha kufanya kitu ambacho hakijazoeleka. Siku ya pili ilikuwa vigumu kuamka. Mwili wote ulikuwa unauma. Nilikuja kujifunza baadae kwamba sikuwa na sababu ya kukimbia kwa kasi kubwa. Nilihitaji kukimbia kwa mwendo mdogo usiochosha na kwa umbali mdogo. Kwa kufanya hivyo, niliuwezesha mwili kuzoea tabia mpya. Unapambana kuanzisha tabia ipi mpya? Huenda unajaribu kujenga desturi ya maombi kila unapoamka; kufanya sala kabla hujala chakula; kukamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa; kujibu ujumbe unaotumiwa kwa wakati. Mahali pa kuanzia ni kujipa muda wa kuanza kidogo kidogo. Usitake kufanya kwa ukamilifu ndani ya muda mfupi. Jiruhusu kupata mafanikio hatua kwa hatua. Wakati mwingine tunajikuta ‘tunaishangaza’ akili kwa sababu tunataka badiliko liwe kubwa ndani ya muda mfupi. Tunapoona tabia mpya haionekani kuleta matunda kwa wakati tunataka tamaa. Tunataka ‘matokeo makubwa sasa.’ Tunasahau waswahili walisema, ‘Haraka haraka haina baraka.’ Mambo mazuri hayahitaji haraka. Kujifunza kuzizoesha fahamu zetu kuzoea tabia mpya hatua kwa hatua ni jambo la msingi. Hapa ndipo tunapohitaji kujifunza jambo la tatu. Unapoanzisha tabia mpya lazima kujiwekea mfumo mzuri wa motisha. Tabia mpya isipokupa motisha itakuwa vigumu kwako kuendelea nayo. Kuna namna mbili za kujipa motisha. Mosi, kuyaona matokeo ya kile unachojaribu kujifunza. Jiulize kwa nini unajaribu kujenga tabia mpya? Kilichonihamasisha kufanya mazoezi ni matokeo. Nilijiona nikidhibiti uzito wa mwili. Hiyo ilikuwa hamasa tosha. Lakini pili, weka utaratibu wa kujikumbusha kile unachojaribu kujifunza. Fahamu zetu zina tabia ya kupuuza jambo tusilolipa uzito. Namna nzuri ya kujikumbusha ni kujisemea maneno yanayosisitiza mpango ulionao. Andika maneno yatakayokukusha mazoea mapya mahali pa kuonekana. Bandika vikatarasi kwenye kioo cha kabati lako; mlango wa jokofu lako; kwenye dashboard ya gari yako. Kokote unakoweza kuona maneno hayo, bandika. Kwa namna hii utajikumbusha kwa urahisi. Pia, unaweza kuwachagua watu makini unaowaamini ukawaambia unachojaribu kukijenga. Mimi nilimwambia mke wangu. Ingawa na yeye alilazimika kuungana nami kufanya mazoezi, kumwambia kunisaidia kuwajibika zaidi kuliko kama ningekuwa najifanyia mazoezi kwa siri. Mshirikishe rafiki yako au mtu unayemini atakayekuwa hakimu pale utakapojisahau. Baada ya muda, utashangaa unaifanya tabia mpya bila kufikiri. Inakuwa sehemu ya maisha yako.
Christian Bwaya ni mnasihi na mhadhiri wa Saikolojia Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0754870815 au barua pepe bwaya@mwecau.ac.tz kwa msaada zaidi. | 5 |
WIZARA ya Madini imeutaka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kulipa fidia inayofikia Sh bilioni 12 kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo ulioko mkoani Mara.Waziri wa Madini, Doto Biteko na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila wamekutana na uongozi wa Mgodi wa North Mara juzi mjini hapa na kuutaka ulipe fidia ya ardhi kwa wananchi hao.Akizungumza katika kikao hicho, Biteko aliwaeleza wajumbe hao walipaswa kuchukua hatua kadhaa kuonesha wanatii maagizo ya serikali, lakini kutokana na wao kuhisi serikali haina cha kufanya, wakaamua kutulia kwa miezi minne ambapo wamefika ofisini kueleza masuala ambayo hayajafanyiwa kazi.“Hatuwezi kuwa tunakaa, tunafikia maamuzi ninyi mnayapinga, ni nani yupo juu ya serikali,” alihoji. “Mnajua suala la ardhi ni kubwa, mnajua ni maelekezo ya Rais, sasa Rais ameagiza halafu hakitokei kitu.Mimi sielewi. Afadhali watu wangeanza kulipwa unaweza sema sasa hatua za malipo zinafanyika.” Aliwaeleza wajumbe hao uongozi wa mgodi huo hawamfuati mtu mahususi katika kutatua suala hilo na kubainisha mgogoro huo hautatatuliwa na wizara isipokuwa ni watu wenye mamlaka na masuala ya ardhi.Akizungumzia chanzo cha mgogoro kuchukua muda mrefu, alieleza tatizo la kuongezeka gharama za malipo limetokana na mgodi kuchelewesha malipo ya tathimini ya awali ambayo ilikuwa Sh bilioni 1.6, hivyo kusababisha kufanyika ya pili iliyofikia kiasi kikubwa cha Sh bilioni 12 ukilinganisha na awali.Alisema baada ya tathmini kufanywa kwa ajili ya malipo ya fidia, malipo yanapaswa kufanyika si zaidi ya miezi sita baada tu ya tathmini kufanyika; aidha, mgodi ulipaswa kutoa tangazo ili kusimamisha uendelezaji wa maeneo kwani maeneo yakiendelezwa na tathmini kutolipwa kwa wakati kiasi kilichothaminishwa awali kinakuwa si dhahiri tena maana uwekezaji katika eneo husika unaongezeka.Akifafanua hilo baada ya kuzungumza na Mthaminishaji Mkuu wa Serikali kwa simu, Biteko alisema ameelezwa tathmini inayofuatwa ni ile iliyofanyika awamu ya pili na kukazia hawawezi kufuata ya awali kutokana na kwamba muda wa kuwalipa fidia hizo ulipaswa kutozidi miezi sita tangu tathmini kufanyika.Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Profesa Msanjila alisema haiwezekani aje mtu asiyekuwa na uamuzi, waziri atoe uamuzi halafu mtu aliyeko Uingereza (mwekezaji) ayapinge, akisema huo ni udhalilishaji.“Maamuzi ya mwisho yakishafanywa na serikali hakuna serikali nyingine au kampuni iyapinge! Maamuzi yanayotolewa Tanzania hayawezi kwenda kujadiliwa London sio sheria hiyo, ndio maana kampuni lazima iwe imesajiliwa Brela, hakuna mambo ya kusema mshauri yupo London au Afrika Kusini,” alisema.Aliwataka makubaliano waliyoafikiana vikao vya nyuma kuwa kama kiongozi wa North Mara anafahamu hana mamlaka kufanya uamuzi, basi asihudhurie vikao vinavyolenga kupitisha uamuzi, yazingatiwe.Awali Jane Lekashingo ambaye ni mmoja wa viongozi kutoka Mgodi wa North Mara alisema kiongozi mkuu wa masuala ya kisheria katika mgodi huo yupo Uingereza na kama kuna suala lolote la kisheria ni sharti ashirikishwe ili kufanya uamuzi wa pamoja.Baada ya mahojiano makali na yaliyochukua muda mrefu, viongozi wa Mgodi wa North Mara walielewa na kukiri baadhi ya wananchi waliofanyiwa tathmini ya malipo yako sahihi na kuahidi kufanya malipo.Waliahidi baada ya kufika katika vituo vyao vya kazi watakwenda kuendelea na taratibu za malipo ili kuonesha uungwana na kuonesha utii kwa serikali kwa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa nchi.Pamoja na kukiri wamejifunza kutokana na kikao hicho, viongozi hao walisema wataendelea kujifunza kwani wameona kuchelewa kwao kulipa fidia hizo, kumesababisha kampuni kutumia kiasi kikubwa cha fedha kulipa wananchi kutokana na shughuli za kimaendeleo walizoendelea kufanya katika maeneo yao. | 1 |
Azam FC imefuata nyayo za Yanga kucheza hatua inayofuata baada ya juzi kutoka sare ya kufungana 1-1 na APR ya Rwanda na kupata ushindi wa jumla ya mabao 3-2 kufuatia ushindi wa 2-1 Kigali, Rwanda.Azam ilifanya shambulio la nguvu katika dakika ya 17 na Ramadhani Singano nusura afunge lakini alipaisha mpira huo. Dakika ya 22 Kipre Tchetche aliifungia Azam FC bao la kuongoza baada ya kupata pasi kutoka kwa Ramadhani Singano.Jordan Ilam nusura afunge katika dakika ya 28 kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake lilipaa juu ya lango. John Bocco (Adebayor) aliifungia Azam FC bao la pili baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Tchetche. Bidvest waliandika bao la kwanza katika dakika ya 43 lililofungwa na Shongwe Jabulani.Mchezaji huyo aliingia katika dakika ya 42 kuchukua nafasi ya Mosiathaga Kolekantse. Azam FC ilipata bao la tatu katika dakika ya 54 lililofungwa na Kipre Tchetche baada ya kutumia makosa yaliyofanywa na mabeki wa Wits.Waafrika Kusini waliandika bao la pili katika dakika ya 58 kupitia kwa Mosiatihaga Koletantse baada ya kupata pasi kutoka kwa Jordan Liam. Farid Mussa alikosa bao la wazi katika dakika ya 79 akiwa ndani ya mita 18 lakini alipiga shuti pembeni.Tchetche aliifungia Azam bao la nne ambalo ni la tatu kwake katika dakika ya 87 baada ya kumpiga chenga kipa wa Bidvest na kuujaza mpira wavuni. Dakika moja kabla ya mchezo kumalizika Bidvest walipata bao la tatu lililofungwa na Botes Nenrico baada ya kuunganisha krosi ya Mosiatihaga Koikantse kwa kichwa.Mpira ulimalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 na hivyo kuifanya kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-3. Ushindi huo unaifanya Azam FC sasa kukutana na Esperance ya Tunisia katika raundi ya pili itakayofanyika mwezi ujao.Kikosi cha Azam FC: Aishi Manula, John Bocco, Shomari Kapombe, Ramadhani Singano, Aggrey Moris, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Michael Bolou, himid Mao, Salum Aboubakar na Kipre Tchetche. | 2 |
TIMU ya soka ya JKU imewapeleka kwa mkopo wachezaji wake saba katika klabu mbalimbali vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar ba Ligi Daraja la Kwanza Kanda.Hayo yameelezwa na Katibu wa timu hiyo, Saadu Ujudi alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na hali ya timu yao ilivyo kwa sasa katika zoezi zima la dirisha la usajili na uhamisho.Alisema kuwa wachezaji hao ambao wamewatoa wamewapeleka baada ya kuonekana viwango vyao vya soka vimeshuka katika msimu uliopita wa ligi.Alisema kuwa wachezaji hao hawana kiwango cha kuridhisha, ambacho timu yake JKU inakitaka kulingana na kasi ya Ligi Kuu ya Zanzibar ilivyokuwa na ushidani kwa hivi sasa.“Tumewatoa kwa mkopo Ili wakasake kiwango kizuri maana kiwango walichoonesha msimu uliopita hakiendani na kasi ya timu yetu, hivyo matumaini yangu huko watafanya vizuri na kupandisha kiwango chao, “alisema.Alieleza kuwa kati ya wachezaji hao, wachezaji watano wamewapeleka kwa mkopo katika timu ya Polisi na wawili wamewapeleka katika timu ya Kilimani City inayoshirikisha Ligi Daraja la Kwanza Kanda.Aliwataja wachezaji waliowapeleka Polisi ni Ali Suleiman golikipa namba tatu, kwa upande wa walinzi ni Khamis Abdallah (Teri) na Edward Peter Mayunga, kiungo ni Ali Vui Hassan na Mbarouk Chande ambaye anacheza winga.Aidha, alisema wachezaji wawili waliopelekwa katika timu ya Kilimani City kwa mkopo, ambao wote ni viungo wa kati ni Is-haka Othman (Bopa) na Hassan Bamzu.Katibu huyo aliongeza kuwa timu hiyo tayari imeanza mazozei kwa ajili ya maanfalizi ya Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu. | 2 |
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo, Profesa Elisante ole Gabriel amezitaka taasisi za fedha nchini kuchangamkia soko la usindikaji wa maziwa linalohitaji uwekezaji wa kimkakati kutokana na kiasi kidogo cha maziwa kusindikwa. Gabriel ametoa rai hiyo katika kongamano la 10 la Wiki ya Maziwa kitaifa nchini. Alisema kiwango cha maziwa kwa mwaka ni lita bilioni 2.7 wakati kiwango cha maziwa kinachosindikwa ni lita milioni 56 hatua inayomnyima mapato mazuri mfugaji nchini. “Nitoe mwito kwa taasisi za fedha kuchukua fursa hii muhimu kwa kuwekeza kwa nguvu kwenye mnyororo wa thamani ili kuyapa thamani maziwa yetu. Ipo fursa kubwa ambayo itawasaidia wafugaji na taasisi zenu kupata faidi,” alisema Gabriel. Kongamano hilo la wadau kutoka mikoa mbalimbali nje ya nchi linajadili namna ya kuongeza uzalishaji bora wa maziwa nchini. Pia linajadili kukabiliana na changamoto za upatikanaji mbegu bora za uhamilishaji, malisho ya mifugo, masoko ya maziwa na uhaba wa viwanda vya usindikaji wa maziwa nchini. Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa nchini, Lucas Malunde alisema viwanda zaidi vinahitajika kuongeza kiwango cha maziwa yaliyosindikwa kumpa faida mfugaji na mtumiaji wa maziwa. Alisema kiwango cha matumizi ya maziwa kwa mtu mmoja hapa nchini kipo chini kiasi cha lita 49 kwa mwaka wakati lengo ni kumwezesha mtu kutumia lita 200 za maziwa kwa mwaka. Ofisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu alisema wametenga Sh bilioni 500 kwa tasnia ya maziwa kwa ujumla. Alisema wapo wajasiriamali walionufaika kwa kuchukua mkopo wa Sh bilioni 30 kutokana na kuongezeka mahitaji ya maziwa nchini. Alisema mikopo yao imelenga kupata mbegu bora za ng’ombe, vituo bora vya kukusanyia maziwa, vifaa vya kisasa vya usindikaji maziwa, malisho na huduma za chanjo na matibabu. | 1 |
MABINGWA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba watamenyana na Yanga Julai 5, mwaka huu katika mechi ya Kundi C ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kuwania Kombe la Cecafa Kagame.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13, mwaka huu kwenye viwanja vya Taifa na Azam Complex Chamazi na kushirikisha klabu 12 kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda, Ethiopia, Burundi Somalia na Sudan.Akizungumzia michuano hiyo jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye aliishukuru Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji akisema ana imani watu watafurahia kutokana na kuwahi kuwa msisimko miaka ya nyuma. “Namshukuru Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kukubali mashindano haya, mdhamini Azam Media na mtendaji wake, Tido Mhando na Rais Paul Kagame ambaye ni mlezi wetu kwa mipango ya kuimarisha mashindano haya,”alisema.Alitaja makundi matatu ya michuano hiyo na Kundi A linaongozwa na mabingwa watetezi wa Cecafa Azam FC, timu ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC ya Sudan Kusini.Kundi B lina timu za Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djiboit. Kundi C kuna Yanga na Simba za Tanzania, St. George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia. Alisema ratiba hiyo itaanza Juni 29, mwaka huu lakini vigogo Simba na Yanga vitakutana Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza kuwa ni zaidi ya Sh milioni 60, mshindi wa pili zaidi ya Sh milioni 40 na mshindi wa tatu ni zaidi ya Sh milioni 20. Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Mhando alisema lengo la kudhamini michuano hiyo ni kuona yanakuwa kwa kiwango cha juu na chachu ya maendeleo ya soka nchini.Alisema wataitumia michuano hiyo kukizindua kituo chao cha Redio, Uhai FM huku akiwahakikishia mashabiki kuwa licha mashindano hayo kufanyika sambamba na Kombe la Dunia, hawataharibu ratiba kwani yatafana. Rais wa TFF, Walace Karia alisema wamekubali kuwa wenyeji ili kurudisha hadhi na kuziwezesha klabu zinazoshiriki michuano ya kimataifa ikiwemo Yanga, Gormahia, Rayon na KCCA kujiimarisha zaidi. | 2 |
Na UPENDO MOSHA-MOSHI SHAHIDI wa tisa katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite, Erasto Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi 22, amesema hakuona umuhimu wa kuchukua nguo za marehemu kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo. Aliieleza mahakama kwamba hakuona umuhimu wa kuchora ramani katika eneo la pili la tukio ambalo ilikutwa pikipiki namba T 316 CLP, aina ya Toyo ambayo ilitumika katika mauaji. Shahidi huyo wa tisa ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi, Samuel Maimu, aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa ushahidi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, alipokuwa akihojiwa na Wakili wa Utetezi, Emanueli Safari ambaye anamwakilisha mtuhumiwa wa tatu, Musa Mangu. “Sikuwapo wakati marehemu anavuliwa nguo na pia sikuona umuhimu wa kukusanya nguo hizo kama kielelezo katika kesi hii. “Pia, sijui baada ya kuvuliwa nani alikabidhiwa kwa sababu mimi siyo mpelelezi wa kesi mpaka ninayetakiwa kujua nguo ni sehemu ya ushahidi. Mahojiano hayo yalikuwa kama ifutavyo. Wakili: Shahidi hebu isaidie mahakama, ulisema wakati unaandaa ramani uliandaa ramani ya tukio lenyewe, ni wapi ulionyesha vielelezo? Shahidi: Nilisema nilitoa katika mwili wa marehemu na sikuweka alama yoyote. Wakili: Ulisema uliweka alama za kudumu katika eneo la tukio na kama mpelelezi ni lazima utajua masuala ya kijiografia, je unafahamu? Shahidi: Ndiyo nafahamu Wakili: Ulitumia vipimo gani katika ramani yako? Shahidi: Futi ili kuonyesha mita Wakili: Je ulianzia wapi? Shahidi: Katikati ya lami Wakili: Nani alikushikia futi wakati wa kupima? Shahidi: Siwezi kukumbuka maana si sehemu ya ushahidi kwa sababu siyo kielelezo. Wakili: Una elimu gani? Shahidi: Elimu ya kidato cha sita. Wakili: Tuambie katika kesi hii nani mpelelezi mkuu? Shahidi: Kesi zote zipo kwa RCO na tunafanya kazi chini yake. Wakili: Je, unaweza kukumbuka zilikuwa ni risasi ngapi ulizozikuta? Shahidi: Ndiyo ni risasi 30 nilizitoa katika magazine. Wakili: Kuna aina ngapi za risasi? Shahidi: Nyingi Wakili: Risasi hizo zilikuwa ni aina gani? Shahidi: Ni za kawaida na zilikuwa hazina ncha kali. Wakili: Je, wakati unafanya kazi hiyo, RCO alikuwa wapi? Shahidi: Siwezi kujua. Wakili: Ulisema katika eneo la tukio, kulikuwa na watu wengi ni wangapi? Shahidi: Hapana siwezi kujua. Wakili: Shahidi, katika ushahidi wako ulisema ulipigiwa simu na raia akikuarifu kuna pikipiki ilitelekezwa na washitakiwa na mlienda na timu yenu, mlikuwa wangapi? Shahidi: Tulikuwa askari sita na ilikuwa ni timu kutoka katika ofisi ya RCO, Mkoa wa Kilimanjaro. Wakili: Ulisema ulipima na futi, je, kutoka katika eneo alilokuwa marehemu hadi hapo ilipotelekezwa pikipiki, ilikuwa ni umbali gani? Shahidi: Ilikuwa ni zaidi ya kilometa moja Wakili: Je, eneo la pili ulichora ramani kama ulivyofanya katika eneo la kwanza? Wakili: Hapana. Wakili: Kwa nini? Shahidi: Sikuchora kwa sababu ya uhalisia wenyewe wa eneo lenyewe. Ningefanya hivyo ningeweza kuidanganya mahakama kwa sababu eneo hilo lilikuwa limekaa kwa muda mrefu na tayari raia walikuwa wameshafika na kuharibu eneo. Wakili: Je, hukuweza kumshirikisha mtu katika shughuli hiyo? Shahidi: Hapana kwa sababu Jeshi la Polisi halisemi uongo na tulikuwa chini ya kiapo Wakili: Je, baada ya hapo ulienda wapi? Shahidi: Nilikwenda katika Kituo cha Polisi Bomang’ombe na nililala mpaka asubuhi katika gari. Wakili: Ulisema katika gari ulikuwa na dereva ambaye pia ni polisi, je, una uhakika gani kama hakusogeza vielelezo? Shahidi: Hakusogeza nina uhakika. Wakili: Ile briefcase ya marehemu ilienda wapi? Shahidi: Siwezi kujua. Wakili: Je, utakubalina na mimi kwamba briefcase ya marehemu mliondoka nayo kwa sababu ilikuwa na fedha? Shahidi: Sijazungumza habari za briefcase maana sijui suala hilo. Wakili: Je, marehemu alivuliwa nguo wapi? Shahidi: Sikuwapo na sijui. Wakili: Je, utakubaliana na mimi, kwamba risasi huwa inatoboa nguo, si ndiyo? Shahidi: Ndiyo ni kweli. Wakili: Je, hukuona umuhimu wa kuwa na hizo nguo? Shahidi: Mimi siyo mpelelezi wa kesi. Wakili: Je, wakati unakusanya vielelezo katika eneo la tukio, hukuona umuhimu wa kukusanya nguo za marehemu? Shahidi: Sikuona umuhimu na pia sikuwapo wakati wakimvua hizo nguo. Wakili: Je, ulipata ushahidi wa mtu aliyemvua nguo marehemu? Shahidi: Hapana, kwa sababu sikuwapo Wakili: Hivyo utakubaliana na mimi katika ukusanyaji wa vielelezo kuna baadhi ya vielelezo vilipotea? Shahidi: Hapa sikubaliani na wewe. Wakili: Je, ulikagua mifuko ya marehemu? Shahidi: Ndiyo. Wakili: Je, hukukuta fedha au leseni ya udereva? Shahidi: Hapana sikukuta kitu. Wakili: Je, marehemu anawezaje akaendesha gari pasipo kuwa na leseni ya udereva? Shahidi: Hapana, siwezi kujua. Mbali na Wakili Safari kumuhoji shahidi huyo pia wakili Hudson Ndusyepo anayemtetea mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Sharif Muhamed, alimhoji shahidi huyo na mahojiano yao yalikuwa hivi: Wakili: Kama ulivyosema shughuli zako za upelelezi, moja ya jukumu lako jingine ni kukagua makosa ya jinani, je, ulishakagua mangapi? Shahidi: Matukio ni mengi, siwezi kukumbuka. Wakili: Katika hayo matukio mengi uliyokagua na kuchorea ramani yalikuwa ni mangapi? Shahidi: Bado ni mengi. Wakili: Je, ni zaidi ya 10? Shahidi: Ndiyo, yanaweza kufika na zaidi Wakili: Je, unaweza kusema ramani inakuwa ni kielelezo au nini? Shahidi: Uchoraji wa ramani unasaidia kuonyesha uhalisia wa tukio. Wakili: Ina maana yoyote? Shahidi: Ndiyo, ina maana kwa sababu inaelezea vielelezo vilivyookotwa kwa ajili ya kukamilisha ushahidi. Wakili: Je, pale panapotokea utata wa ramani unaweza kusaidia mahakama kwenda hadi eneo la tukio kuonyesha vitu vilivyopo kwenye ramani? Shahidi: Ndiyo, vingine unaweza kuonyesha na vingine usionyeshe. Wakili: Ni vitu gani unaweza kuonyesha kwa mujibu wa ramani? Shahidi: Ni vitu ambavyo haviharibiki. Wakili: Ramani huwa ni siri au ni faida ya mahakama? Shahidi: Siyo siri. Wakili: Naomba nikurejeshe katika kielelezo cha P3 kilichotolewa na upande wa Jamhuri, je, umekiona? Shahidi: Ndiyo. Wakili: Unafanya kazi kwa PGO 229, ni kweli au si kweli? Shahidi: Ni kweli ila sina uhakika na kifungu namba hicho kwa sababu PGO ni kubwa. Wakili: Je, Agosti mwaka 2013, kati yako na OC- CID wa Hai ambaye ni shahidi namba moja wa upande wa Jamhuri, wewe na yeye nani alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio? Shahidi: Yeye ndiye alikuwa wa kwanza Wakili: Yeye OC-CID anasema bastola aliikuta kwenye briefcase nyeusi na wewe unasema ilikuwa katika mwili wa marehemu, sasa hapo ni yupi mkweli? Shahidi: Mahakama itaamua, lakini pia siwezi kumsemea shahidi maana sikuwapo. Bilionea Msuya ambaye alikuwa mfanyabishara wa Madini ya Tanzanite, Arusha, aliuawa Agosti 7, mwaka 2013 kwa kupigwa risasi 22, saa sita mchana, kandokando ya barabara kuu ya Arusha kuelekea Moshi, jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Kesi hiyo namba 12 ya mwaka 2014, inasikilizwa na Jaji Salma Maghimbi na inawakabili washitakiwa saba, ambao ni Sharifu Mohamed, Shaibu Said, Musa Mangu, Jalila Said, Sadik Jabiri, Karim Kihundwa na Ally Musa. Kesi hiyo, itaendelea leo. | 1 |
Ndumbaro alikata rufaa kwenye kamati hiyo mwishoni mwa mwaka jana kupinga adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa miaka saba.Adhabu hiyo ilitolewa na Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya Ndumbaro kupinga makato ya asilimia tano kwa klabu za Ligi Kuu kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo.Katika kupinga huko, Ndumbaro alisema anaziwakilisha klabu 13 za ligi kupinga makato hayo, mpaka sasa suala la makato hayo halijatekelezwa baada ya vuguvugu hilo la Ndumbaro.Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa, Revocatus Kuuli kwa vyombo vya habari jana ilisema kamati hiyo ilikutana jana kujadili rufaa hiyo, lakini Ndumbaro hakutokea.“TFF iliwakilishwa na Wakili Emmanuel Muga na Dk Ndumbaro hakufika wala hakuwakilishwa na wakili wake,” ilisema taarifa hiyo.Taarifa ilisema, kufuatia kutofika kwa Dk Ndumbaro, kamati kwa azimio moja iliamuru TFF itoe mwito mpya na mpaka Aprili 14 mwaka huu uwe umemfikia Dk Ndumbaro, ukimfahamisha tarehe ya kikao kijacho cha kusikiliza rufaa yake. | 2 |
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM UONGOZI wa klabu ya Simba, umepanga kuvunja benki kwa kuwaongezea mkataba mnono wachezaji wake mahiri na muhimu, akiwamo Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Ibrahim Ajibu, kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Desemba 17 mwaka huu. Simba imefikia uamuzi huo baada ya kuona wachezaji hao wakinyemelewa na mahasimu wao Yanga, huku mikataba yao ikiwa inaelekea ukingoni Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema hakuna mchezaji muhimu watakayempoteza msimu huu kwani wana mpango kabambe wa kuhakikisha wanawapa mikataba wachezaji wote waliomaliza na walio mbioni kumaliza mikataba yao. “Mengi yatazungumzwa, lakini mpango wetu ni kuhakikisha tunawapa mikataba wachezaji wote tunaowahitaji na ukiona hadi tunaanza mzunguko wa pili mchezaji hajapewa mkataba mpya, ujue huyo hatuna mpango naye. “Kila kitu katika klabu yetu kinakwenda kwa utaratibu maalumu, hivyo haraka sana tutahakikisha suala la mikataba linakuwa hadithi,” alisema Manara. Mbali na Tshabalala na Ajibu, wachezaji wengine wanaotarajia kupewa mkataba ni Abdi Banda na Jonas Mkude, huku Awadhi Juma akiwa na hatihati ya kutemwa na klabu hiyo. | 2 |
Hadija Omary – Lindi NI maajabu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya
mwanafunzi wa darasa la tatu wa Shule ya Msingi Pangatena kupata ujauzito. Mwanafunzi huyo ambaye jina limehifadhiwa, ni
miongozi mwa wanafunzi 40 waliopata ujauzito katika Wilaya ya Kilwa mkoani hapa
mwaka huu. Kati ya wanafunzi hao ambao wamelazimika kukatisha
masomo, wamo wa shule za msingi na sekondari. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo. Christopha
Ngubiagai juzi alipozungumza na wananchi wakati wa sherehe ya kumbukizi ya
miaka 114 ya vita ya Majimaji iliyopiganwa mwaka 1905-1907 wilayani humo. Ngubiagai alisema takwimu hizo ni kuanzia Januari
hadi Julai, mwaka huu. Kutokana na hali hiyo, Ngubiagai aliwaasa wazazi na
walezi kuendeleza mapambano dhidi ya janga hilo kubwa na kuvitaka vyombo vya
dola kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika. Alisema ni ajabu kuona Kilwa inaongoza kuwa na idadi
kubwa ya wanafunzi wanaokatishwa masomo, licha ya Serikali kuweka nguvu kubwa
ya kutokomeza mimba za utotoni. “Tarafa ya Pande ndiyo inayoongoza kuwa na mimba
nyingi kwa wanafunzi. Kila mwezi huwa na mwanafunzi mmoja aliyekatisha masomo. “Serikali inachukua hatua kali kali, lakini kuna
watu hawasikii. Katika hili nawaambia tutapambana nalo kila siku,” alisema. Ngubiagai alisema hadi sasa, wanafunzi saba ndani ya
tarafa hiyo wamepata ujauzito, watatu wa shule ya msingi na wanne sekondari. Alisema miongoni mwa watu wanaotajwa kuongoza
kushiriki mapenzi na kuwajaza mimba wanafunzi, ni walimu na madereva bodaboda. Alitolea mfano Kata ya Namayuni inayoongoza kwa
walimu kushiriki uhusiano wa mapenzi na wanafunzi wao. Alisema ni jambo la aibu kuona kama wazee
walipambana na wakoloni wakaamka, leo wanaona vijana wanapambana kuwatia mimba
watoto. “Kama wazee wetu walipambana kumwondoa mkoloni na
wakamwaga damu, vijana tunao wajibu wa kuwasaidia watoto wa kike wasipate
ujauzito wakiwa na umri mdogo. “Ni jambo la aibu, wazee wetu wakiamka leo wakaona haya mambo sidhani kama watatuelewa. “Wakuu wa wilaya wenzangu wananiuliza Kilwa kuna nini
maana kila kidume kinafukuzia katoto, ndugu zangu mnanitia aibu tafuteni saizi
zenu mkamalizane,” alisema Ngubiagai. Alisema Serikali haitasita kuchukua hatua kali za
kisheria kwa mtu yeyote atakayebainika kumpa mimba mwanafunzi ama kushiriki naye
mapenzi. | 5 |
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Stewart Hall, amekiri timu yake kuzidiwa uwezo na wapinzani wao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Esperance ya Tunisia iliyowatoa kwenye michuano hiyo. Mchezo huo wa marudiano wa raundi ya pili ya michuano hiyo ulifanyika juzi Uwanja wa Olimpique de Rades na wenyeji Esperance kushinda kwa mabao 3-0, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2, kutokana na Azam FC kushinda 2-1 jijini Dar es Salaam siku 10 zilizopita. Akizungumza baada ya mchezo huo, Hall alisema Esperance walicheza vizuri hususani kipindi cha pili na kuweza kuyatumia makosa waliyoyafanya wachezaji wake kupata ushindi huo, uliowavusha hatua inayofuata ya michuano hiyo. “Esperance ilicheza vizuri sana hasa kipindi cha pili, walicheza kwa haraka na soka la kushambulia hivyo kusababisha madhara kwa upande wetu na tukajikuta tukifanya makosa ambayo yalikuwa ni faida kwao, timu yangu ilipambana lakini tulizidiwa,” alisema. Alisema kukosekana kwa wachezaji wake Kipre Tchetche, Pascal Wawa na Shomari Kapombe ambao ni majeruhi pamoja na Jean Mugiraneza ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano, pia kumechangia kikosi chake kupwaya hivyo kushindwa kuwadhibiti Waarabu hao. “Kushindwa kudhibiti mpira ni udhaifu mwingine ambao ulionekana kwenye kikosi changu, hivyo kuzidi kuwapa nafasi wapinzani wetu kutushambulia lakini pia baadhi ya wachezaji walionekana kuchoka mapema,” alisema. Alisema atahakikisha anayafanyia kazi mapungufu hayo ili yasiweze kujirudia kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na kuhatarisha harakati zao za kuchukua ubingwa. Kikosi cha Azam kitarejea nchini kesho na kupitiliza moja kwa moja mkoani Mwanza kwa usafiri wa ndege, kujiandaa na mchezo wao wa FA dhidi ya Mwadui FC utakaocheza keshokutwa Uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo. | 2 |
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile, amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini B jambo linaloathiri ukusanyaji wa damu katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.Alisema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Damu Salama, Kanda ya Kaskazini kilichopo mkoani Kilimanjaro.Dk Ndugulile amesema, takwimu za ukusanyaji wa damu katika kanda hiyo zinaonesha kiwango kikubwa cha damu iliyokusanywa mwaka juzi na mwaka jana kimemwagwa baada ya kupimwa na kubainika kina maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini.Amesema maambukizi ya ugonjwa wa ini yanaongezeka kwa kasi kubwa kuliko ya virusi vya Ukimwi (VVU) na kuwataka watanzania kujenga utaratibu wa kupima afya zao ili watakaokuwa hawajapata maambukizi wapewe chanjo.Dk Ndugulile amesema kwa utaratibu wa kawaida, Serikali inatoa chanjo tano kwa watoto wadogo na moja ya chanjo hizo ni ya ugonjwa wa homa ya ini lakini watu wazima wanatakiwa kulipa gharama ili kupata huduma hiyo.Amesema, maambukizi ya ugonjwa huo yanalingana na ya VVU na makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni watumiaji wa dawa za kulevya na wanaofanyakazi kwenye hospitali hasa maabara.Dk Ndugulile alisema katika kuboresha upatikanaji wa damu, Serikali inatarajia kufunga mashine za kisasa na kujenga vituo 10 nchini kwa ajili ya kuhifadhi damu, lakini upimaji utaendelea kufanyika katika vituo vya kanda.Kaimu Meneja wa Damu Salama kanda ya Kaskazini, Richard Komanga amesema, kumekuwa na ongezeko kubwa la wachagiaji damu wa hiyari kutoka asilimia 82 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 94 kwa mwaka huu.Hata hivyo asilimia 3.5 ya damu iliyokusanywa mwaka juzi ilibainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini B, asilimia 1.3 homa ya ini C, VVU 1.8, kaswende 1.5, mwaka jana homa ya ini B 2.9, homa ya ini C 0.2, Kaswende 0.7 na VVU 0.8.Alisema damu zinazokusanywa katika halmashuari mwaka juzi, asilimia nne ilikuwa na maambuki ya ugonjwa homa ya ini B , C 1.1 , Kaswende 1.5 , VVU mbili, mwaka jana asilimia 4.6 homa ya ini B , C 0.3 , Kaswende 1.6 , VVU 0.8. | 1 |
NEW YORK, MAREKANI KAKA wa Kim Kardashian, Rob Kardashian na mpenzi wake Blac Chyna, wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kike Oktoba, mwaka huu. Awali wawili hao walisema ujauzito wa Blac ni wa mtoto wa kiume, lakini kumbe alikuwa hajafanya vipimo, ila wiki hii wamefanya vipimo hivyo na kugundua kuwa watapata mtoto wa kike. Kupitia akaunti ya Twitter, Blac ameonesha kuwa na furaha kubwa baada ya kupokea taarifa hizo za mtoto wa kike. “Familia yangu inatarajia kukua ifikapo mwezi Oktoba, natarajia kupata mrembo tofauti na awali ambapo habari zilienea kuwa nitapata mtoto wa kiume,” aliandika Blac. Hata hivyo inadaiwa kuwa Rob anaonesha kukosa furaha baada ya kuambiwa kuwa ni mtoto wa kike, inaonesha kuwa Rob alijiandaa zaidi kupata mtoto wa kiume. | 4 |
Na WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM JAMII imeombwa kuwafichua wanaotumia vibaya kazi za wasanii na kujinufaisha nazo huku wasanii hao wakibaki masikini. Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa albamu ya msanii wa nyimbo za injili, Lilian Germin, Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scholastica Kevela, alisema kazi nyingi za wasanii hasa wa muziki wa injili zimekuwa zikiuzwa isivyo halali na kuikosesha mapato Serikali na wasanii husika. Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kisima cha Makimbilio lililoko Kimara Kilungule, Benedict Lyimo, alisema injili inayotangazwa kwa njia ya uimbaji huwafikia na kuwakomboa watu wengi. Hata hivyo, Kevela alichangia Sh 700,000 kwa ajili ya uzinduzi wa albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo saba ambazo ni ‘Ahsante bwana yesu’, ‘Haleluya’, ‘Roho mtakatifu’, ‘Tawala bwana’, ‘Wewe ni bwana uniwezeshaye’ na ‘Wewe ni mwema’. | 4 |
GENEVA, USWISI | SIMANZI imetawala duniani baada ya kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN), Kofi Annan. Annan amefariki dunia usingizini nyumbani kwake mjini Geneva, Uswisi jana akiwa na umri wa miaka 80, kutokana na kuugua kwa muda mfupi. Raia huyo wa Ghana, alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa UN na mshindi wa tuzo ya kimataifa ya Amani ya Nobel aliyoipata mwaka 2001. Taarifa ya kifo chake ilitolewa jana kwa pamoja kati ya familia yake na taasisi yake ya Kofi Annan aliyokuwa akiiongoza. “Kwa masikitiko makubwa, familia ya Annan na taasisi ya Kofi Annan Foundation zinatangaza kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa UN na mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel kilichotokea leo (jana) baada ya kuugua kwa muda mfupi na kufariki akiwa usingizini. “Katika kipindi chote alichokuwa akiugua hadi mauti yalipomkuta, alikuwa pamoja na mkewe Nane na watoto wake Ama, Kojo na Nina. “Familia inaomba faragha wakati huu wa maombolezo na mipango ya mazishi itatangazwa baadaye,” ilisema taarifa hiyo. MWEUSI WA KWANZA KUONGOZA UN Annan alizaliwa Aprili 8, 1938 katika Kitongoji cha Kofandros, Kumasi nchini Ghana. Elimu yake ya awali aliipata katika Shule ya Mfantsipim (1954 hadi 1957). Mwaka 1958 alijiunga na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Kumasi (sasa Chuo Kikuu cha Kwame Nkrumah). Baada ya kuhitimu elimu nchini Ghana, alijiunga na Chuo cha Macalester kilichopo Jimbo la Minnesota nchini Marekani. Alikuwa mwanadiplomasia, mpole na mtulivu. Alijulikana kwa kuongoza kwa uthabiti UN katika siasa za kimataifa, tangu mwaka 1997 hadi 2006 akiwa Mwafrika mweuzi wa kwanza kukalia kiti hicho. Wakati akiingia madarakani mwaka 1997, alipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa Katibu mwenza wa Bara la Afrika, Boutros Boutros-Ghali, ambaye ni raia wa Misri. Boutros alilazimika kuondoka madarakani baada ya jaribio lake la kuwania awamu ya pili kukumbana na kura ya turufu (veto) na taifa la Marekani, hivyo kukosa sifa. KABLA YA KUWA KATIBU MKUU Alijiunga na UN mwaka 1962 kama ofisa wa ngazi za chini wa Shirika la Afya la UN mjini Geneva. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UN, alikuwa Mkurugenzi wa vikosi vya kulinda amani vya UN katika nchi ya zamani ya Yugoslavia. Vikosi hivyo yakishirikiana na Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO), yalilinda Jimbo la Bosnia. Kwa sasa Bosnia na Herzegovina ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki katika Rasi ya Balkani. UMAHIRI NA SIFA ZA UONGOZI Akiwa UN, Annan alianzisha Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDG’s), Mpango wa Kupambana na Mambukizi ya Ukimwi (Global Fund to Fight AIDS), Malaria na Kifua Kikuu. Hakuishia hapo, bali amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza kuanzisha taasisi ya UN inayoshughulikia mapambano dhidi ya ugaidi. Mwaka 2001, dunia ilishuhudia mwanadiplomasia huyo akitangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na uongozi wake ndani ya UN. Pia wakati Kamati ya Tuzo ya Amani ya Nobel ilipomtangaza kuwa mshindi, ilimmwagia sifa kutokana na mipango madhubuti ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi barani Afrika na kupinga ugaidi. “Kofi Annan alikuwa injini ya mambo mengi mazuri tuliyonayo. Ni huzuni kumpoteza mtu muhimu kama yeye ambaye amewafundisha wengi masuala ya uongozi wake. “Kwa namna fulani Annan alikuwa ndiye Umoja wa Mataifa. Alipanda ngazi kutoka moja hadi nyingine hadi kuukwaa ukatibu mkuu, akiwa ameacha alama kubwa,” alisema jana Katibu Mkuu wa sasa wa UN, Antonio Guterres. Annan alikuwa kiongozi wa kimataifa aliyepigania amani na utulivu kwenye mataifa mbalimbali duniani. Katika kipindi cha uongozi wake, alipambana kwa kila fursa aliyopata ili kuhakikisha dunia inakuwa sehemu yenye amani, maendeleo, haki na utawala wa sheria. Baada ya kustaafu UN, aliendelea na kazi yake ya usuluhishi na kutafuta amani kupitia taasisi yake na mwaka 2007 alikuwa mwanzilishi wa Asasi ya The Elders yenye dhumuni la kupigania amani na haki za binadamu duniani iliyomjumuisha pia Nelson Mandela. UPATANISHI KENYA Annan alikuwa mpatanishi mkuu wa mgogoro wa kisiasa nchini Kenya baada ya kuzuka ghasia zilizosababishwa na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007. Katika uchaguzi huo, Mwai Kibaki alitangazwa mshindi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Samuel Kivuitu hatua iliyozusha machafuko ikidaiwa haukuwa ushindi halali, huku wengi wakiamini aliyeshinda alikuwa Raila Odinga wa Chama cha ODM. Nchini Kenya, Annan anakumbukwa kama mwanadiplomasia aliyenusuru maisha yao na mtu muhimu katika ustawi wa taifa hilo hadi leo. Katika ghasia hizo, watu zaidi ya 1,000 walifariki dunia na wengine 600,000 wakakimbia makazi yao baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. BENDERA KUPEPEA NUSU MLINGOTI Rais wa Ghana, Nana Addo Dankwa Akufo-Addo, ametangaza kuwa Serikali ya nchi hiyo itahakikisha inapeperusha bendera za taifa nusu mlingoti ikiwa ni ishara ya kuombeleza kifo cha Annan. Taarifa hiyo imetolewa na Akufo mwenyewe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter. “Kwa niaba ya Serikali, wananchi wote wa Ghana, mke wa rais, Rebbeca, tumepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwenzetu Annan kilichotokea Berne nchini Uswisi. “Kwa niaba ya wananchi wa Ghana, wote tumeumizwa na kifo hicho na tunatoa rambirambi kwa mjane wa Annan, Nane Maria, pamoja na watoto wake Ama, Kojo na Nina kwa kumpoteza mtu muhimu maishani mwao. “Hata hivyo, baada ya kuzungumza na mjane Nane Maria, amenijulisha kuwa Annan amefariki kimya kimya akiwa usingizini. “Kofi ni rafiki na mwanadiplomasia mwenye heshima kubwa duniani na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa wa kwanza kutoka ukanda wa nchi za Jangwa la Sahara kushika wadhifa huo. “Nimetoa maagizo, kwamba kwa heshima yake, bendera ya taifa ya Ghana itapepea nusu mlingoti nchini kote na ofisi zote za ubalozi wetu duniani kwa wiki moja kuanzia Agosti 20, mwaka huu. Apumzike kwa amani,” alisema Rais Akufo. VIONGOZI WAMLILIA ANNAN UINGEREZA: Waziri Mkuu, Theresa May, alisema; “Ni huzuni kubwa kusikia kifo cha Kofi Annan. Kioo cha uongozi na mtu aliyefanya mabadiliko makubwa ndani ya Umoja wa Mataifa, mchango wake ni mkubwa ambao umeonekana sehemu mbalimbali duniani. Daima aliamini dunia inaweza kuwa sehemu salama. Natoa pole na rambirambi kwa watu wote pamoja na familia yake.” NEW ZEALAND: Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, alisema; “Dunia imempoteza muungwana, kiongozi na mtu msumbufu wa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake. Pumzika kwa amani Kofi Annan.” AUSTRALIA: Waziri Mkuu wa zamani wa Australia, Kevin Rudd, alisema; “Dunia imempoteza kiongozi mkubwa leo (jana). Kofi ndiye mwanzilishi wa MDG’s. Alifanya jitihada kubwa kuzuia vita ya Irak. Alizungumzia umoja. Hakika nitamkosa sana rafiki mwema kama yeye.” INDIA: Waziri Mkuu wa India, Narenda Modi, ametoa salamu za rambirambi kutokana na kifo hicho na kusisitiza kuwa Afrika na dunia zimempoteza mtu muhimu. EU: Mwenyekiti mwenza wa Bunge la Ulaya la Mahusiano ya Kimataifa na waziri mkuu wa zamani wa Sweden, Carl Bildt, amesikitishwa pia na kifo hicho akisema; “Mtu mtaratibu, mwenye busara na hekima na rafiki ametuacha leo (jana).” KENYA: Spika wa Bunge la Kenya, J. B. Muturi ametoa salamu za rambirambi kwa wananchi wa Ghana na familia yake kwa kueleza; “Kofi Annan, ni Mwafrika mweusi wa kwanza kuongoza Umoja wa Mataifa. Annan alitimiza wajibu na alipenda amani duniani.” | 3 |
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imekifutia usajili kituo cha mjini Moshi cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi(SMMUCo) na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo kuhamishwa.Aidha kimezuia udahili wa wanafunzi wapya na kuamuru kuhamishwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wanaoendelea na masomo katika jumla ya programu tisa. Pia kimeendelea kusitisha udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika vyuo vikuu viwili na kufanya jumla ya vyuo vikuu vilivyositishiwa udahili kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kufikia 12.Akizungumzia na waandishi wa habari leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU alitaka hatua hizo zisichukuliwe kama siasa. Itakumbukwa kwamba mwaka 2016, TCU ilifanya ukaguzi maalum wa kuhakiki ubora katika vyuo vya elimu ya juu nchini na baadhi ya vyuo viligundulika kuwa na mapungufu kadhaa yanayoathiri utoaji wa elimu bora.Aidha alisema tume iliendelea kuvishauri na kuelekeza vyuo kurekebisha mapungufu hayo kwa nyakati tofauti, sambamba na kufanya kaguzi za kawaida na za kushtukiza katika baadhi ya vyuo vikuu. | 1 |
MBARAKA Kolomela (37) mnunuzi wa vyuma chakavu mkazi wa Msangani wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekufa baada ya kulipukiwa na chuma inayodhaniwa kuwa bomu. Aidha katika tukio hilo, watu wawili wamejeruhiwa ambao ni Fatuma Likupila (61), mkazi wa Msangani na Shomary Athuman umri kati ya miaka (24) na (26) mkulima wa Msangani. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo ni la Septemba 20 mwaka huu majira kati ya saa 4 na saa 5 asubuhi eneo la Msangani. Nyigesa alisema kuwa marehemu ni mnunuzi wa vyuma chakavu na alipofika kwa Rajab Nyangare (50), ambaye naye ni muuzaji wa vyuma chakavu, marehemu alianza kuvichambua na kuvitoa upande mmoja na kuviweka upande mwingine ndani ya jengo ambalo halijaisha (Pagala) mali ya Nyangare.“Wakati marehemu na akiendelea kuchambua vyuma hivyo ulitokea mlipuko mkubwa uliosababisha kifo cha marehemu na majeruhi hao watatu ambao walikuwa jirani”,alisema Nyigesa. Alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ), wameokota vipande vitano vya chuma chakavu, vidhaniwavyo kuwa ni mabomu na vimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi.“Kwa upande wa majeruhi Likupila amepata majeraha kichwani, na masikio na alipelekwa Hospitali ya Rufaa Tumbi na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi na hali yake ambayo ni mbaya”, alisema Nyigesa.Aidha alisema kuwa Athuman amepata majeraha tumboni na kwenye paja na anaendelea na matibabu hospitali ya Tumbi kwa ajili ya matibabu zaidi.“Polisi inasisitiza wananchi kuacha tabia ya kuokota vyuma na kuhifadhi majumbani bila ya kuchukua tahadhari na bado wanaendelea kumtafuta mmiliki wa vyuma chakavu, ambaye ametoweka eneo la tukio, lengo ni kumhoji kupata uhalali wa leseni yake ya ununuzi wa vyuma chakavu na mlipuko”,alisema Nyigesa. | 1 |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigamboni inatarajiwa kuendelea kulipa fidia kwa wananchi wa Gezaulole iliyopo Kata ya Somangila katika Mwaka huu mpya wa bajeti ili kuondokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi wa kata hiyo kuhusiana na malipo hayo.Hayo yamebainishwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Charles Lawiso katika kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kililofanyika leo ambapo pamoja na mambo mengine lilipongezwa kwa ufanisi mzuri katika kuiletea maendeleo manispaa hiyo.Hatua imefuatia swali lililoulizwa na Diwani wa Kata ya Somangila Fransis Masanja aliyetaka kufahamu ni lini wananchi hayo watalipwa fidia zao hatua iliyotokana na maeneo yao kuchukuliwa kwa ajili ya mradi wa upimaji viwanja miaka miwili iliyopita.Akijibu swali hiyo Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kimsingi manispaa hiyo imekuwa ikilipa fidia hizo kwa wananchi hao kila mwaka kwa kadri ambavyo fedha zimekuwa zikipatikana, ambapo kwa mwaka huu malipo hayo yataanza kutolewa wakati wowote ikiwa ni baada ya mwaka mpya wa fedha kuanza.“Taratibu kwa ajili ya ulipaji wa fidia hizo zinaendelea, kilichochelewesha hatua hiyo ni kuanza kwa mpango husika unaohusiana na mwaka huu wa fedha, ila kila kitu kipo sawa matarajio yetu wananachi hao watalipwa fedha zao” alisema Masanja.Katika hatua nyingine Manispaa hiyo imesema changamoto ya kukosekana kwa huduma ya choo katika Shule ya Sekondari Kisota inatarajiwa kutatuliwa hivi karibuni mara baada ya muda uliotolewa kwa mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa choo hicho kuisha.Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kigamboni Paskazia Tibalinda alisema matarajio ya kukamilika rasmi kwa moja ya chemba ya choo hicho yanatarajiwa kujulikana jumatano ijayo, lakini kwa wakati huu tayari manispaa hiyo imetoa ruhusa kwa uongozi wa shule hiyo kuanza kukitumia choo hicho.Alisema uamuzi uliochukuliwa na Manispaa hiyo ni kumtaka Mkandarasi husika kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo hadi Jumatano vinginevyo manispaa itafanya kwa fedha zake kisha kumakata mkandarasi hiyo katika fedha walizokubaliana katika mkataba.Kwa sasa wanafunzi wa Sekondari hiyo wanalazimika kwenda kujisaidia katika choo kilichopo shule ya Sekondari ya Abdu Jumbe, inayopakana na sekondari hiyo ya Kisota.Aidha kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo ya Kigamboni Mabadi Hoja alisema ulipaji wa fidia hizo unapaswa kuhakarakishwa ili kutoa fursa kwa wananchi hao kufanya shughuli zao za kimaendeleo.Alisema malipo ya wananchi hao yamekuwa ya muda mrefu kabla ya kutengenishwa kwa manispaa hiyo kutoka manispaa ya Temeke hivyo ni vyema Ofisi ya Mkurugenzi ikalisimamia suala hilo liweze kumalizika | 1 |