id
stringlengths
1
6
url
stringlengths
31
202
title
stringlengths
1
120
text
stringlengths
8
182k
2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Akiolojia
Akiolojia
Akiolojia (kutoka Kiyunani αρχαίος = zamani na λόγος = neno, usemi) ni somo linalohusu mabaki ya tamaduni za watu wa nyakati zilizopita. Wanaakiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki, kwa mfano kwa kuchimba ardhi na kutafuta mabaki ya majengo, makaburi, silaha, vifaa, vyombo na mifupa ya watu. Akiolojia na historia Tofauti na somo la Historia, akiolojia haichunguzi sana maandishi hasa ili kupata ufafanuzi wa mambo ya kale. Historia inatazama zaidi habari zilizoandikwa lakini akiolojia inatazama vitu vilivyobaki kutoka zamani. Wanaakiolojia wanaweza kutumia maandishi na habari za historia wakiamua jinsi gani waendelee na utafiti wao, kwa mfano wachimbe wapi. Lakini hutumia mitindo ya sayansi mbalimbali kuchunguza vitu vinavyopatikana kwa njia ya akiolojia. Kinyume chake, matokeo ya akiolojia ni chanzo muhimu kwa wachunguzi wa historia. Mara nyingi matokeo ya akiolojia yanaweza kupinga au kuthibitisha habari zilizoandikwa au kufungua macho kwa kuzielewa tofauti. Mfano wa Pompei Mfano bora wa akiolojia ni utafiti wa mji wa Pompei huko Italia. Habari za Pompei zimepatikana katika maandishi mbalimbali ya Kiroma, lakini mji uliharibika kabisa na kufunikwa na majivu ya volkeno Vesuvio mwaka 79 B.K. Kuanzia mwaka 1748 wataalamu walianza kuchimba mahali pa mji mpotevu wakaupata. Hadi leo sehemu kubwa ya mji umefunuliwa tena. Chini ya majivu na udongo wa karne nyingi vitu vingi vimehifadhiwa vizuri ambavyo vingepotea kabisa visingefunikwa, kwa mfano picha za Kiroma zenye rangi nzuri kabisa kwenye kuta za nyumba. Hata mabaki ya chakula yamepatikana yakachunguzwa. Afrika na akiolojia Ujuzi wa akiolojia ni muhimu sana kwa ajili ya historia ya Afrika. Tamaduni nyingi za Afrika ziliendela bila maandishi hadi juzi au hata leo. Habari zetu kuhusu utamaduni wa Zimbabwe Kuu au kuhusu uenezi wa Wabantu hutegemea akiolojia kwa kiasi kikubwa sana. Hivyo akiolojia huongeza ujuzi wetu kwa kufunua ushahidi wa nyakati za kale; wakati huohuo kazi ya akiolojia inahatarisha ushahidi huo kwa sababu kazi yake huondoa hifadhi ya udongo. Katika karne za kwanza za akiolojia mabaki mengi ya tamaduni za kale yameharibika kutokana na kufunuliwa kwao. Kuepukana na tatizo hilo ni jukumu muhimu la akiolojia ya kisasa. Viungo vya nje "The World Wide Web Library of African Archaeology Sayansi Historia
10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Daktari
Daktari
Daktari (au dokta; wingi wake unaundwa kwa kutanguliza ma-) ni neno lenye asili ya Kilatini ("doctor") lililoingia Kiswahili kwa kupitia Kiingereza. Hutumiwa kwa maana mbili: 1) Mtaalamu aliyepata mafunzo maalum kwenye chuo kikuu cha kutibu maradhi ya wagonjwa. Mtu wenye ujuzi wa kutibu anaitwa pia mganga (wa), tabibu (ma). Daktari humtibu mgonjwa kwa kutumia sindano, kumtundikia dripu n.k. baada ya kumpima baadhi ya vitu kama: Kumpima damu Kumpima mapigo ya moyo n.k. Maranyingi daktari hufanya kazi yake katika sehemu maalumu iitwayo Hospitali. 2) Kwa kufuata tabia za lugha nyingine daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uzamivu au "PhD" ambayo ni shahada ya juu kabisa. Picha Cheo Elimu Tiba
16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia
Historia
Historia (kutoka Kigiriki ιστορια, historia; pia "tarehe" kutoka Kiarabu تاریخ tarih kwa maana ya "historia": pia tena "mapisi") ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wakati uliopita. Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu"). Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake. Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani. Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani (vita, uhuru, viongozi na mengineyo) zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi. Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa historia ya awali). Kurasa zinazohusiana Historia ya Afrika Historia ya Amerika Historia ya Asia Historia ya Australia Historia ya Ulaya Historia ya Wokovu Historia ya Kanisa Historia ya teolojia Historia ya utawa Historia ya Kanisa Katoliki Historia ya Uislamu Miaka Vita Tanbihi
17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Afrika
Historia ya Afrika
Historia ya Afrika ni historia ya bara hilo lililo asili ya binadamu wote. Kwa ujumla, historia ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbalimbali, na simulizi au hekaya za mapokeo. Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi na hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithbati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia. Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa. Historia ya Afrika Hapo kale, bara la Afrika lilishuhudia matukio mengi ya harakati za mwanadamu kuliko mabara mengine ya ulimwengu. Wataalamu wa athari wamegundua athari za zamadamu zinazorudi nyuma kufikia hadi miaka milioni minne, na athari za ustaarabu wa Wamisri wa Kale huko Misri na Wafoinike huko Tunis na sehemu nyinginezo za Afrika ya Kaskazini katika karne ya 9 KK. Harakati za madola makubwa ya Warumi na Waarabu ziliweza kuonekana kabla ya karne ya 4 BK, na Waarabu walianza kuingia Afrika huko Habasha (Ethiopia) tangu karne ya 7 BK na kutangaza dini ya Uislamu na kuieneza katika maeneo mbalimbali ya Afrika pamoja na kuanzisha biashara na ustaarabu na kuimarisha mamlaka zao katika Sudan ya wakati huo tangu karne ya 8 baada ya Kikristo. Himaya za Ghana, Mali, na Songhai zilikuwa zikijulikana kwa utajiri mkubwa na biashara stawi iliyokuwa ikifanyika wakati huo ya dhahabu na bidhaa nyinginezo. Mwisho wa karne ya 15 BK, himaya ya Songhai ilikuwa na nguvu kuweza kuitia chini ya utawala wake mamlaka ya Mali. Sehemu nyingine za kusini mwa Afrika zilikuwa wakati huu hazijulikani sana, na historia yake ilikuwa bado haijasajiliwa. Baina ya karne ya 1 KK na karne ya 16 BK watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kibantu watokao sehemu za Nigeria na Cameroon ya leo, ndio waliokuwa wameenea kwenye sehemu mbalimbali kusini mwa bara la Afrika, wakiwa wameanzisha vijiji, mashamba na mamlaka katika sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo, za Luba na Mwememutapa, lakini makundi ya wachungaji wa wanyama walianza kuhamia kusini katika karne za 15 na 16 na kukutana na Wabantu. Ndipo walipoanzisha mamlaka zao za Bunyoro, Buganda, Rwanda na Ankole. Ukoloni Wazungu walianza kugundua bara la Afrika katika karne ya 15, wakati Wareno walipokuja kwenye fukwe za bara la Afrika kutafuta njia nyepesi na ya amani ya kufikia India, na kuweza kupata nafasi ya kushikilia biashara ya dhahabu na pembe na watumwa ambayo ilikuwa ikiendelea wakati huo katika bara la Afrika. Katika mwaka 1488 Bartolomeo Dias alizunguka Rasi ya Tumaini Jema (kwa Kiingereza: Cape of Good Hope), na katika mwaka 1498 Vasco da Gama alifika ufukwe wa Afrika Mashariki na kuendelea mpaka India. Baada ya hapo, Ureno ulianzisha vituo vya biashara Afrika, ukifuatiwa na Waholanzi, Waingereza, Wafaransa na Wazungu wengineo, na biashara ya watumwa iliyosimamiwa na Waarabu na baadhi ya Waafrika wenyewe ikashika kani na kuwa na kasi na nguvu. Wakati huohuo Waturuki walishikilia sehemu za kaskazini ya Afrika na Waomani wakashikilia ufukwe wa Afrika Mashariki. Kati ya miaka 1880 na 1912, Wazungu waligawana bara la Afrika, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa Wazungu isipokuwa Liberia na Ethiopia. Wafaransa wakachukuwa Afrika Magharibi na Kaskazini na kwa hivyo nchi za Afrika Magharibi: Dahomey (sasa Benin), Guinea, Mali, Cote d'Ivoire, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (sasa Burkina Faso) zilikuwa chini ya utawala wake. Hali kadhalika, Algeria, Tunisia na Morocco zilitawaliwa na wao. Aidha, Wafaransa walitawala Togoland, Somaliland, Madagascar, Comoro, na Reunion. Waingereza nao wakatawala Afrika Mashariki na Kusini, na kuwa sehemu ya Sudan na Somalia, Uganda, Kenya, Tanzania (chini ya jina la Tanganyika), Zanzibar, Nyasaland, Rhodesia, Bechuanaland, Basutoland na Swaziland chini ya utawala wao na baada ya kushinda katika vita huko Afrika ya Kusini walitawala Transvaal, Orange Free State, Cape Colony na Natal, na huko Afrika ya Magharibi walitawala Gambia, Sierra Leone, the Gold Coast na Nigeria. Wareno wakachukuwa sehemu ya Guinea, Angola na Msumbiji na sehemu na visiwa fulanifulani huko Afrika ya Magharibi. Wabelgiji wakachukua Kongo na Rwanda-Urundi, na Wahispania wakachukua sehemu ya Guinea, Spanish Sahara (sasa Sahara ya Magharibi), Ifni na sehemu nyingine za Morocco. Wajerumani nao wakachukua Togoland, Cameroon na baadhi ya nchi katika Afrika ya Magharibi na Afrika ya Mashariki, lakini baada ya vita vya kwanza vya dunia wakanyang'anywa. Waitalia wakachukua Libya, Eritrea na sehemu kubwa ya Somalia. Uhuru Nchi ya kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910. Misri, katika mwaka wa 1922 walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tangier katika mwaka wa 1925. Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka wa 1956, na wakarudishiwa Tangier. Katika mwaka huu wa 1956, Sudan na Tunisia vile vile walipata uhuru wao, na Ghana katika mwaka wa 1957, Guinea katika mwaka wa 1958, na vile vile Morocco wakarudishiwa Spanish Morocco. Katika mwaka wa 1960 Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo (Brazzaville), Cote d'Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (Burkina Faso). Vile vile, katika mwaka huohuo wa 1960 Congo (Kinshasa), Nigeria, Somalia, na Togo zikapata uhuru, na katika mwaka wa 1961 Sierra Leone na Tanganyika zikapata uhuru, na Afrika ya Kusini ikawa Jamhuri. Katika mwaka wa 1962 Algeria, Burundi, Rwanda, na Uganda zikawa huru, na 1963 zikafuatia Zanzibar, Gambia na Kenya, na katika mwaka wa 1964 Malawi (Nyasaland), na Zambia (Rhodesia ya Kaskazini) zikapata uhuru. Baada ya miaka miwili, katika mwaka wa 1966 Botswana (Bechuanaland) na Lesotho (Basutoland) zikajinyakulia uhuru. Mauritius na Swaziland katika mwaka wa 1968 na vile vile Guinea ya Ikweta. Hispania ikairudisha Ifni katika mwaka wa 1969 katika mamlaka ya Morocco. Aidha, katika mwaka wa 1974 Guinea ya Kireno (Guinea-Bissau) ikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1975 Angola, Cape Verde, Mozambique, Sao Tome na Principe zikapata uhuru. Hispania vilevile ikaitoa Sahara ya Magharibi kwa Morocco na Mauritania katika mwaka wa 1976, lakini wananchi wakakataa kuwa chini ya nchi mbili hizi, kukazuka vita. Mauritania ukaitoa sehemu yake na kuipa Morocco katika mwaka wa 1979, tatizo ambalo mpaka sasa linaendelea baina ya Morocco na Sahara ya Magharibi, na Umoja wa Mataifa unajaribu kutatua tatizo hili. Waingereza wakawapa uhuru Shelisheli katika mwaka wa 1976, na Ufaransa ukatoa uhuru kwa visiwa vya Ngazija (Comoro). Katika mwaka wa 1977 Jibuti (Nchi ya Afars na Issas) iliyokuwa ikitawaliwa na Wafaransa ikarudi kwa wenyewe. Rhodesia (Zimbabwe) ikapata uhuru halisi mwaka wa 1980, na South West Africa, iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika ya Kusini ikapata uhuru katika mwaka 1990 na kuitwa Namibia. Uingereza umebaki na visiwa vya Saint Helena na Ascension, na Ufaransa unaendelea kutawala Mayotte na Reunion. Hispania vilevile unaendelea kutawala visiwa vya Canarias pamoja na Ceuta na Melilla na visiwa viwili vingine vilivyoko karibu na Morocco. Angalia pia Historia Kuu ya Afrika (mradi wa UNESCO na vitabu) Tanbihi Marejeo http://www.infoplease.com/ce6/world/A0856495.html Korotayev A. & Khaltourina D. Introduction to Social Macrodynamics: Secular Cycles and Millennial Trends in Africa. Moscow: URSS, 2006. ISBN 5-484-00560-4 . ! Afrika
20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hesabu
Hesabu
Hesabu (afadhali: Hisabati kutoka neno la Kiarabu vilevile) ni somo linalohusika na idadi na jinsi tunavyoweza kuhesabu kwa kutumia hasa kanuni zifuatazo: kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawa n.k. Hesabu ni sehemu ya msingi ya nadharia ya namba. Hisabati
24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jiografia
Jiografia
Jiografia ni somo la Dunia na vipengele vyake, wakazi wake, na maajabu yake. Neno la Kiswahili jiografia linafuata matamshi ya Kiingereza ya neno la Kigiriki "γεωγραφία", geo-grafia kutoka gê "dunia" na graphein "kuandika". Lina maana ya "kuandika kuhusu Dunia". Neno hili lilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na mwanasayansi Eratosthenes (276-194 KK). Sehemu za jiografia ni vitu kama mabara, bahari, mito na milima. Wakazi wake ni watu wote na wanyama waishio juu yake. Maajabu yake ni vitu vinavyotokea kama vile maji kujaa na kupwa, upepo, na tetemeko la ardhi. Nchi za Afrika Afrika ya Mashariki Burundi Eritrea Jibuti Kenya Komoro Rwanda Shelisheli Somalia Tanzania Uganda Uhabeshi (Ethiopia) Sudan Kusini Afrika ya Kati Gabon Guinea ya Ikweta Jamhuri ya Afrika ya Kati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jamhuri ya Kongo Kamerun Sao Tome na Principe Afrika ya Kaskazini Algeria Libya Misri Moroko Sahara ya Magharibi Sudan Tunisia Afrika ya Kusini Angola Botswana Eswatini Lesotho Malawi Mauritius Msumbiji (Mozambiki) Namibia Afrika Kusini Zambia Zimbabwe Afrika ya Magharibi Benin Burkina Faso Chadi Cabo Verde Ivory Coast Gambia Ghana Guinea Guinea Bisau Liberia Mali Mauritania Niger Nigeria Senegal Sierra Leone Togo Nchi za Amerika ya Kaskazini Kanada Marekani (Maungano wa Madola ya Amerika) Meksiko (Maungano a Madola ya Mexiko) Nchi za Amerika ya Kati Nchi za barani Belize Guatemala Honduras El Salvador Nikaragua Kosta Rika Panama *(Meksiko mara nyingi huhesabiwa katika Amerika ya Kati kwa sababu za kiutamaduni) Nchi za visiwa vya Karibi Antigua na Barbuda Bahamas Barbados Dominica Jamhuri ya Dominika Grenada Haiti Jamaika Kuba Saint Kitts na Nevis Saint Lucia Saint Vincent na Grenadini Nchi za Amerika ya Kusini Argentina Bolivia Brazil Chile Ekuador Guyana Guyana ya Kifaransa Kolombia Paraguay Peru Surinam Uruguay Venezuela Nchi za Asia Asia ya Kati Afghanistan Kazakhstan Kirgizistan Mongolia Tajikistan Turkmenistan Usbekistan Asia ya Kaskazini Siberia (sehemu ya Urusi) Asia ya Mashariki Uchina (pamoja na Taiwan) Japani Korea Kaskazini Korea Kusini Asia ya Kusini-Mashariki Brunei Indonesia Kamboja Laos Malaysia Myanmar (zamani iliitwa Burma) Philippines Singapur Thailand (zamani iliitwa Siam) Timor Mashariki Vietnam Asia ya Kusini Bangladesh Bhutan Uhindi (au India) Maledivi Nepal Pakistan Sri Lanka (zamani iliitwa Ceylon) Asia ya Magharibi Armenia Azerbaijan Georgia Irak Israel Yordani Libanon Palestina Shamu (au: Syria) Uajemi (au Iran au Persia) Uturuki Bara Arabu Bahrain Kuwait Muungano wa Falme za Kiarabu Oman Qatar Saudia Yemen Nchi za Ulaya Nchi za Oceania mfumo wa Jua Jua Utaridi Zuhura (Ng'andu) Dunia (Ardhi) Mirihi (Meriki - Mars) Mshtarii Zohari Uranus Neptun Tazama pia Nchi Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Tanbihi Viungo vya nje Jiografia Sayansi
30
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiesperanto
Kiesperanto
Kiesperanto ni lugha ya kupangwa inayozungumzwa zaidi duniani kati ya lugha hizi. Ilipangwa na Ludwik Lejzer Zamenhof, myahudi aliyetoka mjini Białystok, nchini Urusi (siku hizi ni sehemu ya nchi ya Poland). Alitoa kitabu cha kwanza cha lugha hii mwaka 1887 baada ya kuitengeneza kwa miaka karibu kumi. Nia yake ilikuwa kutengeneza lugha rahisi ili iwe lugha saidizi ya kimataifa, lugha ya pili kwa kila mtu duniani. Waesperanto wengine bado wanataka hiyo, lakini wengine wanapenda kuitumia tu bila nia ya kuieneza duniani kote. Waesperanto wanakitumia Kiesperanto kwa ajili ya kukutana na wageni na kujifunza kuhusu nchi na tamaduni nyingine. Siku hizi, maelfu ya watu wanaitumia mara kwa mara ili kuwasiliana na watu popote duniani. Chunguzi za kitaalamu zimeonyesha kwamba Kiesperanto kinaweza kujifunzwa rahisi zaidi sana kuliko lugha asilia, na pia kwamba kujifunza Kiesperanto kwanza kunarahisisha kujifunza kwa lugha nyingine. Sifa za kiisimu Kwa kuwa lugha ya kupangwa, Kiesperanto hakiko katika familia yoyote a lugha. Maneno yake yanatoka hasa lugha za Kirumi (kama Kifaransa na Kilatini), lakini pia lugha za Kigermaniki (kama Kiingereza na Kijerumani) na lugha za Kislavoni (kama Kirusi na Kipolandi). Maneno mengi yanaumbwa kwa kuunganisha mzizi wa neno moja na viambishi au kwa kuunganisha mizizi ya maneno mbalimbali. Kwa mfano kuna kiambishi awali "mal-" inayoonyesha kinyume: "bona" ni "-zuri" na "malbona" ni "-baya". Kwa hiyo inawezekana kusema mambo mengi baada ya kujifunza maneno machache tu. Matamshi na maandishi Katika Kiesperanto kuna harufi 28 na kuna sauti 28. Kila harufi inaweza kutamka kwa sauti moja tu, na kila sauti inaandikwa kwa serufi moja tu. Harufi za Kiesperanto ni zifuatazo: a b c ĉ d e f g ĝ h ĥ i j ĵ k l m n o p r s ŝ t u ŭ v z Irabu zote (a, e, i, o, u) zinatamka kama kwa Kiswahili. Kwa upande wa konsonanti, b, d, f, g, h, k, l, m, n, p, r, s, t, v na z zinatamka kama kwa Kiswahili. c inatamka kama ts. ĉ inatamka kama ch. Matamshi ya ĝ yanafanana na matamshi ya j kwa Kiswahili (ni sawasawa na matamshi ya j katika neno la Kiswahili "njia"); j ya Kiesperanto inatamka kama y ya Kiswahili. ĵ inatamka kama j ya Kifaransa (inafanana na sh ya Kiswahili, lakini inatamka na sauti, kama z). ŝ inatamka kama sh. ŭ inatamka kama w; ŭ inatumika baada ya a na e tu, ingawa Zamenhof wenyewe na Waesperanto wengine waiunganisha na irabu yoyote, k.m. "sŭahila" (Kiswahili), "ŭato" (wati), tena jina la herufi yenyewe ni "ŭo"; tofauti kati ya au na aŭ ni kwamba au inatamka kwa silabi mbili na aŭ kwa silabi moja. Serufi Nomino (majina) zote zinahitimu kwa kiambishi tawali -o, kwa mfano "arbo" (mti). Wingi wa nomino unahitimu kwa -oj (arboj = miti). Vivumishi vinahitimu kwa kiambishi tawali -a, kwa mfano "alta" (-refu). Vivumishi kwa kawaida vinawekwa kabla ya nomino inayohusu, lakini pia inaweza kuwa baada yake. Wingi pia unaonyeshwa katika vivumishi kwa harufi "j": altaj arboj = miti mirefu. Vitenzi vina viambishi tamati mbalimbali: -i inatumika kwa vitenzi-jina (kwa mfano "fari" = "kufanya") -as inatumika kwa njeo ya wakati uliopo (kwa mfano "mi faras" = "ninafanya" -is inatumika kwa njeo ya wakati uliopita (kwa mfano "mi faris" = "nilifanya" au "nimefanya") -os inatumika kwa njeo ya wakati ujao (kwa mfano "mi faros" = "nitafanya") -us inatumika kwa hali a masharti (kwa mfano "mi farus" = "ningefanya") -u inatumika kwa hali ya kuamuru (kwa mfano "faru!" = "fanya!"; "li faru" = "afanye") Viungo vya nje makala za OLAC kuhusu Kiesperanto lugha ya Kiesperanto katika Glottolog http://www.ethnologue.com/language/epo Maelezo mengine kuhusu Kiesperanto Jifunze Kiesperanto Tangazo la Praha la jamii ya kiesperanto TANGAZO LA PRAHA LA JAMII YA KIESPERANTO (Word-doc.) esperanto-afriko.org Jifunze lugha ya Kiesperanto, 2007, Kozi ya kimataifa Kurso Saluton! Lernu! Lugha Lugha saidizi ya kimataifa
31
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20ya%20kuundwa
Lugha ya kuundwa
Lugha ya kuundwa (au lugha unde) ni lugha ambayo misamiati na sarufi zake zimetungwa na watu badala ya kukua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Kwa kawaida zinaundwa kwa ajili ya kuwasiliana kati ya watu sawasawa na lugha asilia. Nyingi zinatengenezwa ili kuwa lugha saidizi za kimataifa, lakini nyingine zinaundwa kwa ajili ya usiri au majaribio ya isimu au bila sababu fulani. Lugha ya kuundwa inayozungumzwa zaidi ni Kiesperanto. Mara chache lugha ya kuundwa maana yake ni lugha za kompyuta au za kuandaa programu (angalia lugha asilia). Kwa sababu ya utata huo watu wengi, hasa Waesperanto, hawapendi kutumia neno lugha ya kuundwa, na badala yake wanasema lugha ya kupangwa. Msemo lugha ya kupangwa unatumika kwa lugha zile tu ambazo ziliundwa kwa ajili ya utumiaji wa kawaida baina ya watu, kama Kiesperanto. Mfano mwingine wa lugha ya kuundwa ni lugha ya sheng' inayozungumzwa nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana. Lugha hiyo Haina wazawa asilia mahali popote ila tu ilizuka miongoni mwa vijana Kwa kutaka kusitiri mazungumzo Yao. Hivi ni kuunga mkono wazo la hapo awali kwamba lugha unde Huwa Kwa Sababu za kusitiri mazungumzo au kuunda programu za kompyuta kama vile lugha iitwaya "binary language" ambayo hutumika katika vifaa vya kielektroniki Ili kuundia programu zake. Lugha hiyo ndio hueleweka na mashine za kielektroniki kama tarakilishi au kikokotoo. Marejeo TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Massamba, David 2004 "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Lugha Isimu
32
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha
Lugha
Lugha (kutoka neno la Kiarabu: لغة) ni utaratibu wa kuwasiliana kati ya binadamu (wengine wanadai hata kati ya viumbe wenye akili). Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu. Mwaka wa 2008 ulikuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa. Maana ya neno "lugha" Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kuleta mawasiliano. Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu kwa sababu zilitokea kama bahati tu kwa binadamu. Wanyama hawatumii lugha kama chombo cha mawasiliano, kwa kuwa lugha ni sauti zenye maana na kukubaliwa na jamii. Hakuna lugha bora zaidi duniani, kwa kuwa lugha zote zina ubora, mradi zikidhi matakwa ya jamii husika. Mbali na maana ya kawaida kuna pia lugha ya ishara inayotumiwa na watu bubu. Katika fani ya programu za kompyuta ni kawaida kuongea juu ya "lugha ya kompyuta". Umuhimu wa lugha Lugha ni kitambulisho cha jamii Lugha hutolea elimu Lugha huleta mawasiliano katika jamii Lugha hukuza utamaduni lugha huburudisha Tabia za lugha Lugha huwa na tabia zifuatazo: Lugha huzaliwa: ni kutokana na lugha nyingine moja au zaidi zilizotangulia kuwepo. Lugha hukua: lugha hukua (kuongezeka kwa maneno, kuongezeka kwa idadi ya wazungumzaji, kuwa na mawanda mapana, kusanifiwa) kadiri inavyoendelea kutumiwa na jamii. Lugha hutohoa: lugha ina tabia ya kuchukua au kukopa maneno kutoka lugha nyingine. Lugha hufundishika: mtu yeyote anaweza kujifunza walau kiasi lugha yoyote hata kwa njia ya ufundishaji. Lugha huathiriana: lugha yoyote inaweza kuathiriwa na lugha nyingine. Lugha lazima ijitosheleze: kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii inayotumia lugha yenyewe. Lugha zina ubora: lugha zote ni bora hakuna lugha bora kuliko nyingine zote. Lugha hurithiwa: jamii hurithi lugha kutoka kizazi hadi kizazi. Lugha hufa: inapozidi mno kubadilika mwisho si yenyewe tena, lakini pia inapoachwa isitumike tena kwa kuwa wahusika wanapendelea lugha nyingine. Sifa za lugha Lugha lazima iwe inahusu binadamu Sauti-sauti hufanywa na mwanadamu Lugha hufuata misingi ya fonimu, yaani, a, b, ch, d, f, h, z n.k. Lugha huwa na mpangilio maalumu wenye kubeba maana. Mpangilio huo huanza na fonimu ---> Silabi ---> Neno Lugha hujitambulisha ili kuzalisha maneno mengi. Dhima za lugha Lugha hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashiana habari. Lugha hutumika kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii. Lugha hutumika kutunza, kukuza, na kuendeleza utamaduni wa jamii. Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali (ni nyenzo ya kufundishia). Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa kabila/jamii au taifa fulani. lugha hutumika kutoa burudani. Aina za lugha kwa kigezo cha uwasilishaji Kimsingi lugha ni moja. Uwasilishwaji wake ndio huigawa katika tanzu/aina kuu mbili: Lugha ya mazungumzo Lugha ya maandishi Lugha ya mazungumzo Hii ni lugha ambayo huwasilishwa na watu kwa njia ya mazungumzo ya mdomo - na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mazungumzo. Lugha ya mazungumzo ni kongwe, hai na halisi zaidi ya mzungumzaji na ina maana nyingi, kwani mzungumzaji na msikilizaji huwa ana kwa ana katika mazingira mamoja. Stadi za lugha ya mazungumzo ni kuzungumza na kusikiliza. Lugha ya maandishi Hii ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Hii ni kiwakilishi cha lugha ya mazungumzo katika mfumo wa maandishi. Lugha ya maandishi ni changa kwani imeanza milenia za hivi karibuni baada ya kuvumbuliwa kwa maandishi. Stadi za lugha ya maandishi ni kuandika na kusoma: Kwa kawaida, lugha ni sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Lugha ya aina hii inaitwa lugha asilia. Lakini pia kuna lugha za kuundwa. Nyanja za lugha Lugha ina nyanja kuu mbili, nazo ni: Sarufi - hushughulikia kanuni za lugha Fasihi - hushughulikia sanaa zitokanazo na lugha husika ili kuumba kazi mbalimbali za kifasihi. Kukua na kufa kwa lugha Tangu siku za kwanza za binadamu, lugha zimekuwa zikichipuka, kukua, kutangaa na kufa kama kiumbe yeyote mwingine. Kwa hivyo, lugha zilizopo leo ulimwenguni, huenda baada ya karne nyingi kupita zikatoweka na kuzuka nyinginezo. Leo ulimwenguni mathalan, kuna lugha karibu 6,700, zikiwa 1,000 katika bara la kaskazini na la kusini la Amerika, 2,000 zikiwa kwenye bara la Afrika, 230 katika bara la Ulaya, 2,200 katika bara la Asia, na 1,300 katika bara la Oshania (Australia na nchi jirani nayo). Kurasa zinazohusiana Lugha asilia Lugha ya kuundwa Lugha mama Lugha ya pili Tazama pia Lango la lugha Viungo vya nje
33
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20asilia
Lugha asilia
Lugha asilia ni lugha ambayo ilikua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani ambao watu wake wanaiongea kama lugha mama. Ni kinyume cha lugha ya kuundwa (lughaundwe). Mara nyingine lugha asilia maana yake ni lugha yoyote ambayo inaweza kuzungumzwa na watu, huku lugha za kompyuta na za kuandaa programu zinaitwa lugha za kuundwa. Mara nyingine tena lugha asilia ni lugha ambayo mtu huzaliwa nayo au huikuta baada ya kuzaliwa. Hata hivyo lugha asilia huwa chimbuko la watu fulani katika jamii na hutofautisha jamii moja na nyingine. Mara nyingi ni sehemu ndogo tu ya jamii ndiyo huwa na lugha asilia yaani kila ukoo au kabila huwa na lugha yake ya asili. Lugha
65
https://sw.wikipedia.org/wiki/Madola
Madola
Katika mabara, lile lenye nchi nyingi zaidi ni Afrika likiwa na nchi au madola 54, likifuatiwa na bara la Ulaya likiwa na madola 48, kisha Asia likiwa na madola 44, halafu Amerika ya Kaskazini pamoja na Amerika ya Kati likiwa na madola 23, na baada yake ni Australia na Pasifiki (Oshania) likiwa na madola 14, na mwishowe ni Amerika ya Kusini likiwa na madola 12. Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 195 ulimwenguni. Nchi za Ulimwengu (AS)= Asia (AF)= Afrika (NA)= Amerika ya kaskazini (SA)= Amerika ya kusini (A)= Antaktika (EU)= Ulaya na (AU)= Australia na nchi za Pasifiki. (A) Afghanistan (Kabul) (AS) Afrika Kusini (Pretoria, Cape Town, Bloemfontein) (AF) Albania (Tirana) (EU) Algeria (Algiers) (AF) Andorra (Andorra la Vella) (EU) Angola (Luanda) (AF) Antigua na Barbuda (St. John's) (NA) Argentina (Buenos Aires) (SA) Armenia (Yerevan) (EU) Australia (Canberra) (AU) Austria (Vienna) (EU) Azerbaijan (Baku) (AS) (B) Bahamas (Nassau) (NA) Bahrain (Manama) (AS) Bangladesh (Dhaka) (AS) Barbados (Bridgetown) (NA) Belarus (Minsk) (EU) Belize (Belmopan) (NA) Benin (Porto Novo) (AF) Bhutan (Thimphu) (AS) Bolivia (Sucre) (SA) Bosnia na Herzegovina (Sarajevo) (EU) Botswana (Gaborone) (AF) Brazil (Brasilia) (SA) Brunei (Bander Seri Begawan) (AS) Bulgaria (Sofia) (EU) Burkina Faso (Ouagadougou) (AF) Burma/Myanmar (Yangon) (AS) Burundi (Bujumbura) (AF) (C) Cabo Verde (Praia) (Ureno) Cambodia (Phnom Penh) (AS) Chad (N'Djamena) (AF) Chile (Santiago de Chile) (SA) Colombia (Bogota) (SA) Costa Rica (San Jose) (NA) Cote d'Ivoire/Ivory Coast (Yamoussoukro) (AF) Cuba (Havana) (NA) (D) Denmark (Copenhagen) (EU) Djibouti (Djibouti) (AF) Dominica (Roseau) (NA) Dominican Republic (Santo Domingo) (NA) (E) Eire (Dublin) (EU) Ekuador (Quito) (SA) El Salvador (San Salvador) (NA) Eritrea (Asmara) (AF) Estonia (Tallinn) (EU) Eswatini (Mbabane) (AF) Ethiopia (Addis Ababa) (AF) (F) Falme za Kiarabu (Abu Dhabi) (AS) Fiji (Suva) (Australia na Pasifiki) (G) Gabon (Libreville) (AF) Gambia (Banjul) (AF) Georgia (Tbilisi) (EU) Ghana (Accra) (AF) Grenada (St. George's) (NA) Guatemala (Guatemala City) (NA) Guinea (Conakry) (AF) Guinea-Bisau (Bisau) (AF) Guinea ya Ikweta (Malabo) (AF) Guyana (Georgetown) (SA) (H) Haiti (Port-au-Prince) (NA) Hispania (Madrid) (EU) Honduras (Tegucigalpa) (NA) Hungaria (Budapest) (EU) (I) Iceland (Reykjavik) (EU) Indonesia (Jakarta) (AS) Iraq (Baghdad) (AS) Israel (Jerusalem) (AS) Italia (Roma) (EU) (J) Jamaika (Kingston) (NA) Jamhuri ya Afrika ya Kati (Bangui) (AF) Japani (Tokyo) (AS) (K) Kamerun (Yaounde) (AF) Kanada (Ottawa) (NA) Kazakstan (Astana) (AS) Kenya (Nairobi) (AF) Kirgizia (Bishkek) (AS) Kiribati (Teinainano) (AU - Oceania) Komoro (Moroni) (AF) Kongo (Jamhuri ya) (Brazzaville) (AF) Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) (Kinshasa) (AF) Korea, Kaskazini (Pyonyang) (AS) Korea, Kusini (Seoul) (AS) Kroatia (Zagreb) (EU) Kupro (Nicosia) (AS) and/or (EU) Kuwait (Kuwait City) (AS) (L) Laos (Vientiane) (AS) Latvia (Riga) (EU) Lebanon (Beirut) (AS) Lesoto (Maseru) (AF) Liberia (Monrovia) (AF) Libya (Tripoli) (AF) Liechtenstein (Vaduz) (EU) Lithuania (Vilnius) (EU) Luxemburg (Luxemburg) (EU) (M) Madagascar (Antananarivo) (AF) Malawi (Lilongwe) (AF) Malaysia (Kuala Lumpur) (AS) Maldives (Male) (AS) Mali (Bamako) (AF) Malta (Valletta) (EU) Marekani (Washington D.C.) (NA) Marshall Islands (Majuro) (AU - Oceania) Masedonia Kaskazini (Skopje) (EU) Mauritania (Nouakchott) (AF) Mexiko (Mexico City) (NA) Micronesia (Palikir) (AU - Oceania) Misri (Cairo) (AF) Moldova (Chisinau) (EU) Monaco (Monaco) (EU) Mongolia (Ulan Bator) (AS) Morisi (Port Louis) (AF) Moroko (Rabat) (AF) Montenegro (Podgorica) (EU) Msumbiji (Maputo) (AF) (N) Namibia (Windhoek) (AF) Nauru (Yaren)) (AU - Oceania) Nepal (Kathmandu) (AS) Nicaragua (Managua) (NA) Niger (Niamey) (AF) Nigeria (Abuja) (AF) Norwei (Oslo) (EU) New Zealand (Wellington) (AU) (O) Oman (Muscat) (AS) (P) Pakistan (Islamabad) (AS) Palau (Melekeok) (AU - Oceania) Panama (Panama City) (NA) Papua Nyugini (Port Moresby) (AU) Paraguay (Asuncion) (SA) Peru (Lima) (SA) Poland (Warsaw) (EU) (Q) Qatar (Doha) (AS) (R) Romania (Bucharest) (EU) Rwanda (Kigali) (AF) (S) Sahara ya Magharibi (AF) Saint Kitts na Nevis (Basseterre) (NA) Saint Lucia (Castries) (NA) Saint Vincent na Grenadini (Kingstown) (NA) Samoa (Apia) (AU - Oceania) San Marino (San Marino) (EU) Sao Tome na Principe (Sao Tome) (AF) Saudia (Riyadh) (AS) Senegal (Dakar) (AF) Serbia (Belgrad) (EU) Shelisheli (Victoria (Shelisheli)) (AF) Sierra Leone (Freetown) (AF) Singapuri (Jiji la Singapuri) (AS) Slovakia (Bratislava) (EU) Slovenia (Ljubljana) (EU) Solomon Islands (Honiara) (AU - Oceania) Somalia (Mogadishu) (AF) Sri Lanka (Sri Jayawardenapura) (AS) Sudan (Khartoum) (AF) Sudan Kusini (Juba) (AF) Suriname (Paramaribo) (SA) Syria (Damascus) (AS) (T) Taiwan (Taipei) (AS) Tajikistan (Dushanbe) (AS) Tanzania (Dodoma) (AF) Timor ya Mashariki (Dili) (AS) Togo (Lome) (AF) Tonga (Nuku'alofa) (AU - Oceania) Trinidad na Tobago (Port of Spain) (NA) Tunisia (Tunis) (AF) Turkmenistan (Ashgabat) (AS) Tuvalu (Funafuti) (AU - Oceania) (U) Uajemi (Tehran) (AS) Ubelgiji (Brussels) (EU) Ucheki (Prague) (EU) Uchina (Beijing) (AS) Ufaransa (Paris) (EU) Ufilipino (Manila) (AS) Ufini (Helsinki) (EU) Uganda (Kampala) (AF) Ugiriki (Athens) (EU) Uhindi (New Delhi) (AS) Uholanzi (Amsterdam, Den Haag) (EU) Uingereza (London) (EU) Ujerumani (Berlin) (EU) Ukraine (Kiev) (EU) Ureno (Lisbon) (EU) Uruguay (Montevideo) (SA) Urusi (Moscow) (EU, AS) Uswidi (Stockholm) (EU) Uswisi (Bern) (EU) Uthai (Bangkok) (AS) Uturuki (Ankara) (AS) & (EU) Uzbekistan (Tashkent) (AS) (V) Vanuatu (Port Vila) (AU - Oceania) Vatikani (EU) Venezuela (Caracas) (SA) Vietnam (Hanoi) (AS) (Y) Yemen (Sana'a) (AS) Yordani (Amman) (AS) (Z) Zambia (Lusaka) (AF) Zimbabwe (Harare) (AF) Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Marejeo http://www.infoplease.com http://www.worldatlas.com Yale Africa Guide Interactive - Nations of Africa Nchi Orodha za kijiografia nds:Land#Länner sv:Världsgeografi#Lista över länder
71
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayansi
Sayansi
Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa. Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa. Aina za sayansi Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo: Sayansi Asili k.m. Biolojia Jiografia Zoolojia Sayansi Umbile k.m. Fizikia Hisabati Kemia Sayansi Jamii k.m. Historia Elimu Saikolojia Siasa Sayansi Tumizi k.m. Teknolojia Uhandisi Pia, kuna sayansi zinazohusu mada maalumu mbalimbali: Maarifa Astronomia Tiba Mbinu za kisayansi Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli fulani. Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka nadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia. Hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Zisipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika. Sura ya kisayansi Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika jiwe (maada yabisi) kuna uvungu (dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu. Historia Sura ya kiutamaduni Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmojammoja; lakini kadiri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga. Hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo lilionekana kama ni shauku la mtu mmojammoja kama awali. Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa sehemu ya historia ya sayansi. Majina na sifa hutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea. Sayansi na jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe. Sayansi na siasa za dunia Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu. Ingawaje haibainishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu za mamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi. Sayansi na maendeleo Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla. Hivyo roho ya uchunguzi ndiyo iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi. Tazama pia Mtu wa kwanza alitoka wapi Tanbihi Sayansi
72
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sheria
Sheria
Sheria (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza law ) ni mfumo wa kanuni, ambazo kwa kawaida hutekelezwa kupitia seti ya taasisi maalumu. Inaunda siasa, uchumi na jamii kwa njia mbalimbali na huratibu mahusiano baina ya watu. Sheria ya mkataba huongoza kila kitu, kuanzia kununua tiketi ya basi hadi biashara katika masoko. Sheria ya mali inafafanua haki na wajibu unaohusiana na uhamisho wa jina la mali ya binafsi na mali ya kweli. Sheria ya hifadhi inatumika kwa mali yanayotumika kwa uwekezaji na usalama wa kifedha, huku sheria ya kukiuka wajibu inaruhusu madai ya fidia ikiwa haki au mali za mtu zinafanyiwa madhara. Ikiwa madhara ni kinyume cha sheria, sheria ya jinai inatoa mbinu zinazoweza kutumiwa na taifa ili kumshtaki mhusika. Sheria ya kikatiba inatoa utaratibu wa utungaji wa sheria, ulinzi wa haki za kibinadamu na uchaguzi wa wawakilishi wa kisiasa. Sheria ya utawala inatumika kuangalia upya maamuzi ya vyombo vya serikali, huku sheria ya kimataifa inatawala shughuli baina ya nchi huru zinazohusu mambo kama vile biashara, vikwazo vya kimazingira na hatua za kijeshi. Akiandika mnamo 350 K.K., mwanafalsafa wa Ugiriki ya Kale Aristotle alisema, "Utawala wa sheria ni bora kuliko utawala wa mtu yeyote binafsi." Mifumo ya sheria inaelezea haki na majukumu kwa njia mbalimbali. Tofauti ya jumla inaweza kufanywa kati ya maeneo yanayotawaliwa na mfumo wa sheria ya kiraia, ambayo huandika sheria zao, na yale yanayofuata sheria za kawaida, ambapo sheria haijaundwa kwa utaratibu maalumu. Katika baadhi ya nchi, sheria ya dini bado hutumika kama sheria maalum. Sheria ni chanzo kikuu cha uchunguzi wa kitaalam, wa historia ya sheria, falsafa ya sheria, uchambuzi wa kiuchumi wa sheria au somo la kijamii kuhusu sheria. Sheria pia huibua masuala muhimu na magumu kuhusu usawa, uadilifu na haki. "Katika usawa wake wa ajabu", alisema mwandishi Anatole France mnamo mwaka 1894, "sheria inakataza matajiri na mafukura kulala chini ya madaraja, kuombaomba barabarani na kuiba mikate." Katika demokrasia ya kawaida, taasisi za msingi za kutafsiri na kuunda sheria ni matawi matatu makuu ya utawala, ambayo ni mahakama isiyo na upendeleo, bunge na serikali yenye kuwajibika. Ili kutekeleza na kutumia nguvu za kufanya sheria ifuatwe na kutoa huduma kwa umma, urasimu wa serikali, jeshi na polisi ni muhimu. Vyombo hivyo vyote vya dola viliundwa na kutawaliwa na sheria, taaluma ya kisheria iliyo huru na jamii yenye bidii zinajulisha na kusaidia maendeleo. Masomo ya sheria Mifumo yote ya kisheria inahusu na masuala ya msingi, lakini kila taifa inaainisha na kubainisha masomo yake ya kisheria kwa njia mbalimbali. Tofauti ya kawaida ni kuwa "sheria ya umma" (maneno yanayohusika kwa karibu na taifa, na kuhusisha sheria ya kikatiba, kitawala na ya jinai), na "sheria ya kibinafsi" (inayohusisha mkataba, sheria ya kukiuka wajibu na mali). Katikamifumo ya sheria ya kirai , mkataba na kukiuka wajibu zinapatikana chini ya sheria ya majukumu huku sheria ya hifadhi inapatikana chini ya serkali za halali au mikataba ya kimataifa. Sheria ya Kimataifa, kikatiba, kitawala, jinai, mkataba, kukiuka wajibu na mali na hifadhi zinatambulika kama "masomo msingi ya jadi", ingawa kuna masomo zaidi ambayo yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa zaidi wa kiutendaji. Sheria ya Kimataifa Sheria ya kimataifa inaweza kuashiria mambo matatu: sheria ya umma ya kimataifa, sheria ya kibinafsi ya kimataifa au mgongano wa sheria na sheria ya mashirika makubwa ya kimataifa. Sheria ya Umma ya Kimataifa inajihusisha na uhusiano kati ya mataifa uhuru. Vyanzo vya maendeleo ya sheria ya umma ya kimataifa ni desturi, mwenendo na mikataba kati ya nchi huru Mikataba ya Geneva. Sheria ya umma ya kimataifa inaweza kutengezwa na mashirika ya kimataifa, kama vile Umoja wa Mataifa (ambao ilianzishwa baada ya kushindwa kwa Shirikisho la Kimataifa kuzuia Vita vya Vikuu vya Pili vya Dunia), Shirika la Kimataifa la Ajira, Shirika la Kimataifa la Biashara, au Shirika la Fedha la Kimataifa. Sheria ya kimatifa ya umma ina hadhi maalum kama sheria kwa sababu hakuna kikozi cha kimataifa cha polisi, na mahakama (kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Haki kama tawi la kimsingi la Umoja wa Mataifa la mahakama) halina uwezo wa kuadhibu kutokutii. Hata hivyo, miili michache, kama vile WTO, ina mifumo yenye ufanisi ya utatuzi wa kudumu na utatuzi wa mogogoro inayoambatana na vikwazo vya kibiashara. Mgongano wa sheria (au "sheria ya kibinafsi ya kimataifa" katika nchi za sheria ya kiraia) unahusisha maeneo ya kimamlaka ya kisheria ya mgogoro wa kisheria baina ya watu wa kibinafsi unafaa kusikizwa na sheria za maeneo gani ya kimamlaka ya kisheria ndiyo inayofaa kutumika. Leo, biashra zinazidi kuwa na uwezo wa kusongeza minyororo ya ugavi ya mtaji na ajira kuvuka mipaka, na pia kufanya biashara na kampuni za nchi za ng'ambo, hivyo kulifanya swali kuhusu nchi ipi ndiyo inayomamlaka ya kisheria kuwa muhimu zaidi. Idadi kubwa zaidi ya biashara zinachagua usuluhishi wa kibiashara chini ya Mkataba wa New York wa mnamo mwaka1958. Sheria ya Umoja wa Ulaya ndiyo ya kwanza, kufikia sasa, ambayo ni mfano wa sheria kuu ya kimataifa. Kutokana na mwenendo wa kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi Duniani, mikataba mingi ya kikanda — hasa ya Umoja wa Nchi za Amerika Kusini — zimeanza kuufuata mfano kama huu. Katika Umoja wa Ulaya, nchi huru zimekusanya mamlaka yao katika mfumo wa mahakama na taasisi za kisiasa. Taasisi hizi zinapewa uwezo wa kutekeleza kanuni za kisheria dhidi ya au kwa nchi wanachama na raia katika namna ambayo haiwezekani kupitia sheria ya umma ya kimataifa. Kama Mahakama ya Ulaya ya Haki yalivyosema katika miaka ya 1960, sheria ya Umoja wa Umoja wa Ulaya hujumiusha "muundo mpya wa sheria ya kimataifa" kwa ajili ya faida inayotegemeana ya kijamii na kiuchumi wa nchi zote wanachama. Sheria ya kikatiba na ya kiutawala Sheria ya kikatiba na kiutawala zinasimamia mambo ya nchi. Sheria ya kikatiba inahusisha uhusiano baina ya serikali, bunge na mahakama na haki za kibinadamu au uhuru wa kiraia wa watu binafsi dhidi ya nchi. Maeneo mengi ya kisheria, kama vile Marekani na Ufaransa, zina katiba moja iliyoandikwa kwa makini, iliyo na Muswada wa Haki. Katiba chache kama vile Uingereza, hazina hati kama hiyo."Katiba" kwa ufupi ni zile sheria ambazo zinajumuisha mwili wa kisiasa, kutoka kanuni, sheria za uamuzi na mkataba. Kesi kwa jina Entick dhidi ya Carrington ilionyesha wazi kanuni ya kikatiba inayotokana na sheria ya kawaifa. Nyumba ya Bwana Entick ilifanyiwa upekekuzi na Afisa mmoja wa polisi aliyeitwa Carrington. Wakati Bwana Entick alipolalamika mbele ya mahakama, Afisa Carrington alidokeza kwamba kibali kutoka waziri wa Serikali, Ali wa Halifax, kilikuwa na mamlaka halali. Hata hivyo, hakukuwa na sheria iliyoandikwa au mamlaka ya kimahakama ambayo yalitoa uwezo huo.Hakimu mkuu, Bwana Camden, alisema, Mwisho mkubwa, ambao ulifanya watu kuingia katika jamii, ilikuwa kupata mali. Haki hiyo imetunzwa na ni takatifu na haiwezi kuondolewa wakati wowote, ambapo haijaondolewa au kufupishwa na sheria fulani ya umma kwa manufaa ya wote...Hakuna sababau inayoweza kupatikana au kutolewa, kimya cha vitabu ni mamlaka dhidi ya mshtakiwa, na aliyeathiriwa lazima atendewe haki. Kanuni ya kimsingi ya kikatiba, ilitokana na John Locke, inadokeza ya kwamba mtu binafsi anaweza kufanya isipokuwa kile ambacho kimekataliwa kisheria. Sheria ya utawala ndiyo mbinu msingi ya kufanya mashirika ya umma yawajibike. Watu wanaweza kutumia mapitio ya kimahakama kwa matendo au uamuzi uliofanywa na za halmashauri za mitaa, huduma za umma au wizara za serikali, kuhakikisha kuwa zinazingatia sheria. Mahakama ya kwanza ya maalum ya kiutawala yalikuwa mahakama ya Conseil d'État yaliyoundwa mnamo mwaka wa 1799, wakati Napoleon Bonaparte alipochukua mamlaka nchini Ufaransa. Sheria ya jinai Sheria ya jinai, inayojulikana pia kama sheria ya kuadhibu, inahusisha makosa na adhabu. Kwa hivyo inapima ufafanuzi wa adhabu ya makosa yaliyopatikana kuwa na madhara yanaonekana kuwa na uwezo wa kusababisha uharibifu lakini, kwa undani, haifanyi uamuzi wa kimaadili kumhusu mkosaji wala kuwekea jamii vikwazo ambavyo vinakataza watu kimwili wasifanye makoa mwanzoni. Investigating, apprehending, charging, and trying suspected offenders is regulated by the law of criminal procedure. Kesi ya kidhana ya uhalifu inatokana na ushahidi, kuzidi shaka ya kuridhisha, kuwa mtu ana hatia ya mambo mawili. Kwanza, mshtakiwa lazima awe amefanya kitendo ambacho kinatazamwa na jamii kuwa hatia, au actus reus (kitendo cha hatia). Pili, lazima mshtakiwa awe na dhamira ya kufanya uharibifu ya kufanya kitendoo fulani cha jinai, au mens rea (akili ya hatia). Hata hivyo, kwa kile kinachojulikana kama hatia za "dhima kali", actus reus haitoshi. Mifumo ya jinai ya utamaduni wa sheria ya raia zinatofautisha kati ya nia katika dhana pana (dolus directus na dolus eventualis), na uzembe. Uzembe hauna jukumu la jinai isipokuwa ambapo hatia fulani una adhabu yake maalum. Mifano ya uhalifu ni mauaji, kushambulia, udanganyifu na wizi. Katika mifano maalum utetezi unaweza kutumika kwa vitendo maalum, kama zile kuuwa ili utetezi wa kibinafasi, au katika nyakati maalum kujitetea kuwa wazimu. Mfano mwingine ni katika kesi ya karne ya 19 ya Jamhuri dhidi ya Dudley na Stephens, iliyopima utetezi wa "kimahitaji". Meli ya Mignonette, iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Southampton kuelekea mji wa Sydney, ilizama. Wafanyikazi watatu wa meli hiyo na Richard Parker, kijana aliyekuwa na umri wa miaka 17, walibaki katika meli iliyoundwa na vijiti. Walikuwa na njaa na kijana yule alikuwa karibu kufa. Kwa sababu ya kuwa na njaa iliyokithiri, wafanyikazi hao walimuuwa kijana yule na kumla. Wafanyikazi hao waliokolewa, lakini wakafikishwa mahakamani huku wakiwa na hatia ya mauaji. Walijitetea kwa kusema kwamba ilihitajika kwa lazima kwa wao kumuuwa kijana yule ili kuyaokoa maisha yao. Bwana Coleridge, akieleza kukataa kukubwa, aliamua, "kuhifadhi maisha ya kibinafsi ni, kwa kuzungumza kijumla, wajibu, lakini inaweza kuwa jukumu kuu kuyatoa maisha hayo kama kafara." Wanaume hao walihukumiwa nyonga, lakini maoni ya umma uliunga mkono haki ya wafanyikazi wale wa meli kuyaokoa maisha yao. Mwishowe, Ufalme ulipunguza hukumu zao hadi miezi sita gerezani. Makosa ya jinai yanatambulika si tu kama makosa dhidi ya waathirika binafsi, lakini jamii pia. Taifa, kawaida likisaidiwa na polisi, huongoza mashitaka, basi hiyo ndiyo sababu mbona katika nchi zenye sheria ya kawaida kesi hutajwa kama "Watu dhidi ya..." au "Jamhuri (kwa "Rex" au Regina) dhidi ya..." Pia, jopo la waamuzi ambao hutokana na raia wa kawaida hutumika kuamua hatia ya washitakiwa kutokna na pointi zinazoweza kubainika ukweli: jopo la waamuzi haliwezi kubadilisha kanuni za kisheria. Baadhi ya nchi zilizostawi bado hutumia adhabu ya kifo kwa matendo ya jinai lakini adhabu ya kawaida ya uhalifu itakuwa ni kufungwa gereza, faini usimamizi wa taifa (kama vile probesheni), au huduma ya kijamii. Sheria ya kisasa ya jinai imeathiriwa vilivyo na sayansi ya jamii, hasa kuhusu kuhukumu, utafiti wa kisheria, kuunda sheria, na kuwasaidia wahalifu kurekesha mwenedo wao. Katika ngazi ya kimataifa, nchi 108 wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ambayo ilianzishwa kuwahukumu watu kwa hatia dhidi ya ubinadamu. Sheria ya mkataba Sheria ya mkataba inahusu ahadi zinazowezwa kutendwa, na inaweza kuandikwa kwa ufupi katika maneno ya Kilatinipacta sunt servanda (ahadi lazima zitimizwe). Katika maeneo ya kimamlaka ya sheria ya kawaida, vipengele vitatu muhimu kuhusu utengenezaji wa mkataba vinahitajika: kutoa na kukubali, kutilia maanani na nia ya kutengeneza uhusiano wa kisheria.Katika kesi ya Carlill shisi ya Kampuni ya Carbolic Smoke Ball kampuni ya matibabu ilitangaza kuwa dawa yake mpya ya ajabu, smokeball, ingewatibu watu kutokana na mafua, na ikiwa haingefaulu kuwatibu, wanunuzi wangepata £ 100. Watu wengi waliwasilisha kesi mahakamani ili wapate £100 zao wakati dawa hiyo iliposhindwa kuwatibu. Ikiogopa kufilisika, Kampuni ya Carbolic ilijitetea kwa kusema kuwa tangazo lile lilikuwa mzaha tu, na kwa hivyo halikuwa toleo lenye nguvu za kisheria. Lilikuwa karibisho, mchezo tu. Lakini mahakama ya rufaa yaliamua kuwa kwa mtu mwenye kufikiria kwa kawaida kampuni ya Carbolic ilikuwa imefanya toleo. Watu walikuwa wametoa kusudi la kununua bidhaa ile kwa kupitia "shida bayana" ya kutumia bidhaa yenye hitilafu. "Soma tangazo vile utakavyo, na ulibadilishe tangazo hilo vile utakavyo", alisema Hakimu Lindley, "haa kuna ahadi maalum ilitajwa katika lugha isyokuwa na utata wowote". "Kutilia maanani" knaonyesha ukweli kwamba vyama vyote katika mkataba vimebadilisha kitu fulani chenye maana. Baadhi ya mifumo ya sheria ya kawaida, ikiwemo Australi, zinasonga mbali kutoka dhana ya kutilia maanani kama mojawapo ya mahitaji ya mkataba. Dhana ya "estoppel" au culpa in contrahendo, inaweza kutumika kuunda wajibu wakati mazungumzo kabla ya kuingia mkataba Katika maeneo ya kisheria ya kiraia, kutilia maanani si lazima kwa mkataba kuwa na nguvu ya kisheria. Nchini Ufaransa, mkataba wa kawaida unasemekana kutokea ambapo "kukutana kwa akili" au kwa "kuwa na nia zinazowiana". Ujerumani ina mtazamio maalum kuhusu mikataba, ambayo inayusisha sheria ya mali. Kanuni ya dhana ya kiakili (Abstraktionsprinzip wanayoitumia, inamaanisha kuwa wajibu wa kibinafsi wa mkataba unaundwa kando na jina la mwenye mali yanayokabidhiwa. Wakati ambapo mikataba inavunjwa kwa sababu fulani (kwa mfano mnunuzi wa gari amelewa kiasi kwamba hana uwezo wa kisheria wa kufanya mkataba) Wajibu wa kimkataba wa kulipa unaweza kuvunjwa tofauti na jina la mwenye gari. Sheria ya kutajirika kusio kwa haki, badala ya sheria tya mkataba, basi inatumika kurudisha jina kwa mmiliki halali. Sheria ya ukiukaji wa wajibu Sheria ya ukiukaji wa wajibu, ambayo wakati mwingine huitwa kosa la jinai, ni makosa ya raia. Kuwa na kosa la ukiukaji wa wajibu, mtu lazima awe amekiuka wajibu aliukwa anafaa kumtendea mty mwingine, au kukiuka haki fulani ya awali ya kisheria. mfano unaweza kuwa kumgonga mtu kimakosa na mpira wa mchezo wa kriketi. Chini ya sheria ya uzembe, ambayo ndiyo aina ya ukiukaji wa wajibu maarufu zaidi, mtu aliyepatwa na madhara anaweza kuomba fidia kwa ya majeraha yake kutoka kwa mtu mwenye uwajibikaji. Kanuni za uzembe zinaonyeshwa na kesi ya Donoghue dhidi ya Stevenson. Rafiki mmoja wa Bi. Donoghue aliagiza chupa isiyopenyeka nuru la pombe ya tangawizi (iliyokusudiwa kutumika na Bi. Donoghue) katika mkahawa katika eneo la Paisley. Baada ya kunya kunya nusu ya bia ile , Bi, Donoghue alimimina iliyosalia katika bilauri. Mabaki yaliyooza ya konokono yalielea juu ya pombe. Alidai kuwa alipigwa na bumbuwazi, na kupata ugonjwa wa kuchomeka ndani ya matumbo, na ilimbidi kumpeleka mtengenezaji pombe kwa kuruhusu kinywaji kuchafuka ovyo. Nyumba ya Mabwana iliamua kwamba mtengezaji pombe aliwajibika kwa ugonjwa wa Bi. Donoghue. Bwana Atkin alikuwa na mtazamo maalum wa kimaadili, na akasema, Dhima ya upuuzaji ... bila shaka ina msingi wake katika mawazo ya kijumla ya umma kuhusu makosa ya kimaadili amabyo mkosaji lazima alipe ... Kanuni ya kuwa unafaa kumpenda adui yako, kisheria inakuwa, haufai kumjeruhi jirani yako; na swali la wakili, nani ndiye jirani yangu? linapokea jibu lenye vikwazo. Lazima uwe na uwangalifu wa kuepuka na vitendo au visa ambapo hautendi lolote inapofaa, ambavyo unaweza kutazamia kuwa vikamjeruhi jirani yako. Huu ulikuwa msingi wa kanuni nne za upuuzaji; (1) Bwana Stevenson alimdai Bi. Donoghue wajibu wa kujali wa kuuza vinywaji salama (2) yeye alivunja wajibu wake wa kujali (3) madhara hayangefanyika isipokuwa kwa kuvunja kwake kwa wajibu wa kujali na (4) tendo lake lilikuwa sababau ya karibu, au haikuwa tokeo la mbali, la madhara yaliyompata mtu fulani. Mfano mwingine wa ukikaji wa wajibu unaweza kuwa wa jirani ambaye anapiga kelele nyingi sana na na mashine katika nyumbani kwake. Chini ya dai la kero kelele hiyo inaweza kukomeshwa. Ukiukaji wa wajibu pia inaweza kuhusisha vitendo vya kimakusudi, kama vile ushambulizi, vita au kuvuka na kuingia katka maeneo yaliyopigwa marufuku. Sheria ya ukiukaji wa wajibu inayofahamika vyema ni ile ya kumharibia mtu jina, ambayo inafanyika, kwa mfano, wakati gazeti linapochapisha madai yasiyokuwa na msingi ambayo yanaharibu sifa ya mwanasiasa fulani. Ukiukaji wa wajibu ambao ni mbaya zaidi ni zile wa kiuchumi, ambao huwa msingi wa sheria ya ajira katika baadhi ya nchi kwa kufanya vyama vya kibiashara kuwa na dhima kwa sababu ya migomo, Wakati ambapo amri ya kisheria haipatiani kinga. Sheria ya mali Sheria ya mali inatawala vitu vya thamani ambavyo watu huvitambua kama 'vyao'. Mali ya kweli wakati mwingine huitwa 'mali isiyohamishika' inahusu umiliki wa ardhi na vitu vilivyojikita katika ardhi hiyo. Mali ya kibinafsi, inaashiria mambo mengineyo; vyombo vinavyowezwa kusongeshwa, kama vile tarakilishi, magari, mapambo na mikate au turathi haki, kama vile akiba na hisa. Haki ya in rem ni haki ya kipande maalum cha mali, ikitofautishwa na haki in personam ambayo inaruhusu fidia kwa hasara, lakini si kwa kurudishiwa kitu fulani. Sheria ya ardhi inajumuisha msingi wa aina nyingi za sheria za mali, na ndiyo ngumu zaidi. Inahusisha mogeji, mikataba ya kukodisha, leseni, maagano, ruhusa na mifumo ya kisheria kwa usajili wa ardhi. Kanuni kuhusu matumizi ya ardhi ya kibinafsi chini ya haki miliki, sheria ya kampuni, hifadhi na sheria ya biashara. Mfano wa kesi msingi ya ya sheria nyingii za mali ni Armory v Delamirie. Kijana wa kufagia chimni alipata pambo lenye mawe ya thamani. Alichukua pambo lile kwa muundaji wa vifaa vya dhahabu ili thamani yake ikadiriwe. Mwanafunzi wa muundaji wa vifaa vya dhahabu aliangalia pambo lile, akaiba mawe yale ya thamani, ma kumuambia kijana yule kuwa thamani yake ilkuwa nusu peni tatu na kuwa angeinunua. Kijana yule alimwambia kuwa angepenga arudishiwe pambo lile, kwa hivyo mwanafunzi wa muundaji vifaa alimrudishia pambo, lakini bila mawe yale ya thamani. Kijana yule alimpeleka mtengenezaji wa vifaa vya dhahabu kotini kwa jaribio la mwanafunzi wake kumdanganya. Bwana Hakimu Mkuu Pratt aliamua kuwa ingawa kijana hangesemekana kuwa mumiliki wa pambo lile, angefaa kutazamwa kama mpataji aliyefaa ("mpataji muwekaji") hadi mumiliki wa kiasili anapopatikana. Kwa kweli mwanafunzi na kijana yule wote walikuwa na haki ya umiliki wa pambo lile (dhana ya kiufundi, inayomaanisha kuwa kitu fulani kingeweza kumilikiwa na mtu fulani), lakini nia ya kijana yule ya kumiliki ilitazamiwa kuwa bora zaidi, kwa sababu ingeweza kudhihirishwa kuwa ya kwanza katika wakati. Umiliki unaweza kuwa sehemu tisa kwa kumi ya sheria, lakini si yote. Kesi hii hutumika kudhihirisha mtazamo wa mali katika maeneo ya kisheria ya kawaida, kuwa mtu anayeweza kuonyesha dai bora zaidi la kipande cha mali, dhidi ya chama kingine, ndiye mumiliki. Kwa kulinganisha, mbinu ya kiklasiki ya sheria ya raia kuhusu mali, iliendelezwa na Friedrich Carl von Savigny, ni kuwa ni haki nzuri dhidi ya Ulimwengu. Wajibu, kama mkataba na ukiukaji wa wajibu hutazamwa kama haki nzuri dhidi ya watu binafsi. Dhana ya mali inaibua maswala mengi zaidi ya kifalsafa na kisiasa. Locke alidokeza kwamba "maisha, uhuru na nyumba" zetu ni mali yetu kwa sababu tunamiliki mali yetu na tunachangayana ajira yetu na mazingira yetu. Usawa na amana Usawa na amana ni mwili wa sheria ulioibuka nchini Uingereza kando na "shera ya kawaida". Sheria ya kawaida ilisimamiwa na mahakimu. Bwana Chansela kwa upnade mwingine, kama muwekaji dhamiri wa mfalme, angeweza kupuuza sheria iliyotengenezwa na hakimu ikiwa alifikiria kuwa ilikuwa sawa kufanya hivyo. Hili lilimaanisha kuwa usawa ulianza kufanya kazi zaidi kupitia kanuni bali si sheria ambazo hazikubadilika. Kwa mfano, ambapo mifumo ya sheria ya kawaida au sheria ya raia haiwaruhusu watu kugawa umiliki wa kutoka kwa udhibiti wa kipande kimoja cha mali, usawa unaruhusu hili kupitia mpango unaoitwa 'amana'. Kudhibitiwa kwa mali na 'wenye amana' ambapo kwa upande mwingine umiliki 'wenye manufaa' (au 'yenye usawa') wa mali ya amana inashikiliwa na watu wanojulikana kama 'wadhamini'. Wadhamini wana wajibu kwa walengwa wao wa kuyachuna vyema mali waliyokabidhiwa. Katika kesi ya awali ya Keech dhidi ya Sandford mtoto alirithi haki ya kokodisha katika soko katika eneo la Ramford, mjini London. Bw, Sandford alikabidhiwa mali hayo hadi wakati ambapo mtoto angekomaa. Lakini kabla ya hapo, kipindi cha kukodisha kilikwisha. Kabaila alikuwa (inaonekana) amemwambia Bw. Sandford kuwa hakutaka mtoto yule awe na kukodisha kupya. Lakini bado kabaila alikuwa amefurahi (inaonekana) kumpa Bw. Sandford fursa ya kukodisha. Bw Sandford aliichukua. Wakati ambapo mtoto (sasa Bw. Keech) alikuwa mkubwa, alimpeleka Bw. Sandford mahakamani kwa faida aliyokuwa akipata kwa kupata kukodisha kwa soko. Bw. Sandford alifaa kuaminika, lakini alijiweka katika nafasi ya mgongano wa maslahi. Bwana Kansela, Bwana Mfalme, alikubali na kumuamuru Bw. Sandford kutoa faida ile na kumlipa Bw. Keech. Aliandika, Bila shaka, Bwana Mfalme LC alikuwa na wasiwasi kwamba wadhamini huenda wakatumia fursa ya kutumia mali ya amana wenyewe badala ya kuyachunga. Wadadisi wa kibiashara wanaotumia hifadhi walikuwa wamesababisha kuaguka kwa soko la hisa katika siku hizo. Wajibu mkali kwa wadhamini ulijumuishwa katika sheria ya serikali na kutumika kwa wakurugenzi wa makampuni na maafisa watendaji wakuu. Mfano mwingine wa jukumu la mdhamini unaweza kuwa kuwekeza mali vizuri au kuiuza. Hii hasa ndiyo kesi kwa fedha za pensheni , aina muhimu kwa zote ya amana, ambapo wawekezaji ndio wadhamini wa akiba za watu hadi wastaafu. Lakini amana pia zinaweza kuundwa kwa madhumuni ya hisani, mifano maarufu ikiwa Makavazi ya Uingereza au Shirika la Rockefeller. Utaalamu zaidi Sheria huenea mbali kuliko masomo ya msingi hadi karibu kila eneo la maisha. Ngazi tatu zimetajwa hapa ili kurahisiha majadiliano, ingawa masomo mbalimbali hufanana na kutegemeana. Sheria na jamii Sheria ya ajira ni somo la uhusiano wa mara tatu wa kiwandani kati ya mfanyikazi, muajiri na chama cha wafanyikazi. Hili linahusisha kupunguza kufanya biashara kwa pamoja, na haki ya kugoma. Sheria ya kuajiriwa kwa binafsi inaashiria haki za maeneo ya kazi, kama zile usalama wa kazi, afya na usalama au mshahara wa chini zaidi. Haki za kibinadamu, haki za kiraia na sheria ya haki za kibinadamu ni maeneo muhimu katika kumhakikishia kila mtu uhuru na haki za kimsingi, Haya yanapatikana katika maadiko kama vile Azimio la Ulimwenguni la Haki za Kibinadamu, Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu (iliyoanzisha Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu) na Mswada wa Marekani wa Haki za Kibinadamu. Mkataba wa Lisbon unafanya Mkataba wa Haki za Msingi za Umoja wa Ulaya uwe na nguvu za kisheria katika nchi zote wanachama isipokuwa Polandi na Uingereza. Utaratibu wa Kiraia na utaratibu wa jinai unahusisha kanuni ambazo mahakama lazima yafuate kadiri trial na rufaa zinapoendelea. Yote yanahusu haki ya raia kupata kuhukumiwa kwa haki au kesi yake kusikizwa kwa haki. Ushahidi. Sheria ya ushahidi inahusu vifaa vinavyofaa kutumika mahakamani ili kesi ijengwe. Sheria ya Uhamiaji na sheria ya utaifa zinahusu haki za wageni kuishi na kufanya kazi katika taifa ambalo si lao na kupata na kupoteza uraia. Yote yanahusu haki ya hifadhi na shida ya watu wasiokuwa na nchi Usalama wa Kijamii. Sheria ya usalama wa kijamii inahusu haki za watu kuwa na bima ya kijamii, kama vile pesa zinazopewa watafuta kazi au faida za makazi. Sheria ya familia inahusu kesi za ndoa na talaka proceedings, haki za watoto na haki za kuwa na mali na pesa ikiwa wenye kufanya ndoa watatengana. Sheria na biashara Sheria ya kikampuni ilitokana na sheria ya amana, ikitegemea kanuni ya kutenganisha umiliki na udhibiti. Sheria ya kisasa ya kampuni ilianza na Sheria ya Kampuni za Pamoja za Akiba ya mwaka 1856, iliyopitishwa nchini Uingereza, ambayo iliwapa wawekezaji mbinu rahisi ya usajili ili kupata dhima ya kupimika chini ya dhana ya mtu tofauti wa kampuni. Sheria ya kibiashara inahusu mkataba tata wa mkataba na mali. Sheria ya shirika, sheria ya bima, bili za kubadilishana, ufilisi na Sheria ya kuufungwa kwa biashara na sheria ya uuzaji zote ni muhimu, na zinarudi nyuma hadi dhana ya Lex Mercatoria ya zama za kati. Sheria ya Kuuza Bidhaa ya Uingereza na Kodi Sawa ya Biashara ya Marekani ni mifano ya kanuni za kibiashara ya sheria ya kawaida Sheria ya maji na Sjeria ya Maji zinaweka muundo msingi wa biashara huru na biashara Duniani kote Baharini, ambapo yamo nje ya eneo la udhibiti wa nchi fulani. Makampuni ya meli yanafanya kazi kwa kutumia kanuni za kawaida za sheria ya biashara, ambazo zimefanywa kuwa jumla kwa soko la kimataifa. Sheria ya maji inajumuisha masuala muhimu kama vile kama vile kuokoa vifaa kutoka baharini, lieni za maji, na majeraha kwa abiria. Miliki Sheria inalenga aims at safeguarding creators and other producers of intellectual goods and services. These are legal rights (copyrights, trademarks, patents, and related rights) which result from intellectual activity in the industrial, literary and artistic fields. Fidia inashughulika na kupata mapato ya mtu mwingine, bali si fidia kwa hasara ya kibinafsi Kutajirika isipofaa ndiyo nguzo ya tatu ya sheria ya raia (pamoja na mkataba na ukiukaji wa wajibu). Wakati ambapo mtu fulani ametajirishwa isipofaa (au kuna "kutokuwepo kwa msingi" wa biashara) kwa gharama ya mawingine, tukio hili linazalisha haki ya fidia ili kugeuza faida hiyo. Sheria na vikwazo Sheria ya kodi inahusu kanuni kuhusu kodi ya thamani iliyoongezwa, kodi ya kampuni, kodi ya mapato. Sheria za kibenki na kanuni za kifedha zinaweka viwango vya chini zaidi kuhusu idadi ya mtaji ambao benki zinaweza kuwa nao, na sheria kuhusu utendaji bora wa uwekezaji. Hili ni kwa minajili ya kuhakikisha ulinzi dhidi ya taabu za kiuchumi, kama vileKunguka kwa soko la Wall Street mnamo mwaka wa 1929. Vikwazo vinashughulika na utoaji wa huduma za umma na usimamizi wa vifaa vya umma.Sheria ya maji ni mfano mmoja. Hasa tangu ubinafshaji uwe maarufu na uchukue usimamizi wa huduma kutoka kwa sheria ya umma, makampuni ya kibinafsi ambayo hapo yalikuwa yakifanya kazi iliyodhitiwa na serikali hapo awali yamefungwa na vyeo mbalimbali vya wajibu wa kijamii. Nishati, gesi, mawasiliano na maji zinadhibitiwa na viwanda katika nchi nyingi za OECD. Sheria ya mashindano, nchini Marekani inajulikana kama sheria dhidi ya amana, ni eneo linalozidi kubadilika ambalo lilianza katika kutokana na amri za Kirumi dhidi ya kuweka bei na mafundisho ya Uingereza ya biashara ya makini. Sheria ya kisasa ya mashindano inatokana na sheria za Marekani dhidi ya biashara za magendo na dhidi ya ukiritimba (Sheria ya Sherman na Sheria ya Clyaton) ya mwisho wa karne ya 20. Inatumika kudhibiti biashara zinazojaribu kutumia ushawishi wao wa kiuchumi kubadilisha biashra za sokoni bila kujali maslahi ya mnunuzi. Sheria ya mnunuzi inaweza kujumuisha chochote kuanzia kanuni kuhusu vifungu vya mikataba ambavyo si sawa hadi maelekezo kuhusu bima ya mizigo ya ndege. Sheria ya mazingira inazidi kuwa muhimu, hasa katika mwanga wa Itifaki ya Kyoto na hatari inayoweza kutokana na mabadiliko ya hali ya anga. Ulinzi wa kimazingira pia intumika kuwaadhibu wanaoharibu mazingira katika mifumo ya kisheria ya kiinchi Mifumo ya sheria Kwa ujumla, mifumo ya kisheria inaweza kugawanywa kati ya mifumo ya kisheria ya kiraia na mifumo ya kisheria ya kawaida. Maneno "sheria ya kiraia" yanayoashiria mfumo wa kisheria hayapaswi kuchanganyishwa na "sheria ya kiraia" kama kundi la masomo ya kisheria ambayo ni tofauti na sheria ya umma au ya jinai. Aina ya tatu ya mfumo wa kisheria—inayokubalika bado na baadhi ya nchi ambazo zina utengano wa kanisa na taifa—ni sheria sheria ya kidini, ambayo ina msingi wake katika maandiko ya kidini. Aina ya mfumo amabo nchi inatumia kutawala mara nyingi kudhamiriwa na historia yake, uhusiano wake na nchi zingine au kushikilia kwake kwa viwango vya kimataifa. Vyanzo ambavyo maneneo fulani ya kisheria hutumia kama kama zenye uwezo wa kuwa nguvu za kisheria ndizo sifa fafanuzi za mfumo wowote wa kisheria. Hata hivyo, uainishaji ni jambo la umbo kuliko maana, kwani sheria sawa mara nyingi hutawala. Sheria ya kiraia Sheria ya kiraia ni mfumo wa kisheria unaotumika katika nchi nyingi Duniani. Katika sheria ya kiraia vyanzo vinavyotambulika kama kuwa na mamlaka, ni, haswa, uundaji wa sheria—haswa sheria zilizoandikwa katika katiba au amri zinazopitishwa na serikali—na tamaduni. Sheria za kuandikwa zinapatikana hata katika miaka mingi ya awali , huku mfano mmoja ukiwa Codex Hammurabi ya Kibabeli. Mifumo ya sheria za kiraia ya kisasa inatokana na mazoezi ya kisheria ya Dola la Kirumi ambalo maadiko yake yalipatikana katika Ulaya ya Zama za Kati. Sheria ya Kirumu katika siku za Jamhuri ya Kiruma na Dola la Kirumi lilitegemea sana utaratibu, na ilikosa daraja la kitaaluma. Badala uake mtu wa kawaida aliyeitwa, iudex, alichagukiwa kufanya uamuzi. Kesi za awali hazikuripotiwa, kwa hivyo sheria yoyote yenye msingi katika kesi iliyoibuka ilifichwa na hata kutotambulika. Kila kesi ilikuwa ilimuliwe upya kutokana na sheria za nchi, ambayo ni sawa na kupungua kwa umuhimu (kinadharia) wa uamuzi wa mahakimu kwa kesi za siku za usoni kwa mufumo ya kisheria siku za leo. Katika kipindi cha karne ya 6 NK katika Dola la Mashariki la Roma, Kaisari Justinian I aliandika na kuzikusanya pamoja sheria ambazo zilikuwa zinapatikana hapo awali katika Roma, ambapo kile kilichobakia kilikuwa sehemu moja juu ya ishirini ya kiwango cha maandiko ya kisheria kutoka awali. Hili ikawa inafahamika kama Corpus Juris Civilis. Kwa mujibu wa mwanahistoria mmoja wa kisheria, "Justinian alitazama kwa uangalifu hadi miaka ya dhahabu ya nyuma ya sheria ya Kirumi na alilenga kuirejesha hadi upeo wake wa karne tatu za awali." Wakati uo huo, Ulaya ya Magharibi ilitumbukia polepole katika Zama za Giza, na haikuwa hadi karne ya 11ambapo wasomi katika Chuo Kikuu cha Bologna walipoyagundua upya maandiko yaliyokuwa yamepotea na kuyatumia kuzitafsiri sheria zao. Maandiko ya sheria za kiraia yenye msingi unaofanana kwa karibu na sheria ya Kirumu, sambamba na ushawishi mchache kutoka sheria za kidini kama vile sheria ya Kikanoni na sheria ya Kiislamu, iliendelea kuenea kote baranii Ulaya hadi Kutaalmika; kisha, katika karne ya 19, Ufaransa, na Sheria iliyoandikwa ya Kiraia, na Ujerumani, Bürgerliches Gesetzbuch, zilifanya sheria zao zilizokuwa zimeandikwa kuwa za kisasa. Sheria hizi mbili zilizoandikwa zilisukuma vilivyo si tu mifumo ya kisheria ya nchi katika Bara Ulaya (kama vile Ugiriki), lakini pia tamaduni za kisheria za Ujapani na Kikorea. Leo, cnhi ambazo zina mifumo ya kisheria ya kiraia ni kama vile Urusi na Uchina na maeneo mengi ya Marekani ya Kati na Marekani ya Kilatini. Marekani inafuata sheria ya kawaida inayofafanuliwa hapa chini. Sheria ya kawaida na usawa Sheria ya kawaida na usawa ni mifumo ya kisheria ambapo uamuzi wa mahakama yanakubalika wazi kuwa vyanzo vya sheria."Mafundisho ya utangulizi", au stare decisis (Kilatini kwa "kusimama kwa uamuzi") unamaanisha kuwa sumauzi unaofanywa na mahakama yenye mamlaka kubwa yanafunga mahakama yenye mamlaka ya chini. Mifumo ya kisheria ya kawaida hutumia amri mara chache sana, zinazopitishwa na bunge, lakini huenda zikafanya jaribio ambalo si la kitaratibu kuandika sheria zao kuliko katika "mfumo wa sheria wa kiraia". Sheria ya kawaida ina asili yake nchini Uingereza na imerithiwa na karibu nchi zote ambazo hapo awali zilihusika na Dola la Uingereza (isipokuwa Malta, Scotland, na jimbo la Marekani la Louisiana, na jimbo la Kanada la Quebec). Katika Uingereza wakati wa zama za kati, ushindi wa Norman ulisababisha kuungana kwa desturi mbalimbali za kikabila na hivyo basi kuunda sheria ya "kawaida" ya nchi yote. Labda ikisukumwa na mazoea ya kisheria ya Kiislamu wakati wa Krusedi, sheria ya kawaida iliendelea ambapo Mfalme wa Kiingereza alikuwa amefanywa kuwa dhaifu na gharama kubwa ya vita vywa kudhibiti sehemu kubwa za Ufaransa. Mfalme Yohana alikuwa amelazimishwa na mabaroni wake kutia saini hati iliyoweka vikwazo kwa mamlaka yake ya kupisha sheria. "Mkataba huu mkuu" au Magna Carta wa mwaka 1215 pia ulihitaji jopo la mahakimu wa Mfalme kufanya mikutano yao ya kimahakama na uamuzi wao katika "mahali maalum" badala ya kutoa haki ya kibepari katika maeneo yaliyokuwa magumu kutabiri kote. Kundi la mahakimu walsomi na waliokolea walipata jukumu muhimu katika kuunda sheria chini ya mfumo huu, na ikilinganishwa na wenzao Barani Ulaya mahakama ya Uingereza ilikuwa na urasimu mwingi zaidi. Kwa mfano, mnamo mwaka wa 1297, wakati ambapo mahakama kuu ya Ufaransa yalikuwa na mahakimu hamsini na wawili, Mahakama ya Uingereza ya Maombi ya Kawaida yalikuwa na watano. Mahakama haya yenye nguvu na yaliyoshikamana yalisababisha mfumo wa kikiritimba. Kufuatana na hilo, kadiri wakati ulivyopita, idadi iliyoongezeka ya raia waliomba Mfalme kupuuza sheria ya kawaida, na kwa niaba ya Mfalme Bwana Chansela alitoa uamuzi kufanya kile ambacho ni sawa kwa kila kesi. Kuanzia wakati wa Thomas More, wakili wa kwanza kuteuliwa kama Bwana Chansela, mwili wa kimfumo wa usawa uliongezeka kando ya sheria ya kawaida yenye ukiritimba, na ilianzisha Mahakama yake ya Chancery. Mwanzoni, usawa ulikosolewa kuwa ulikosa kukosa utaratibu, na kuwa ulibadilika kulingana na urefu wa mguu wa Chansela. Lakini baada ya muda iliunda kanuni, hasa chini ya Bwana Eldon. Katika karne ya 19 mifumo hiyo miwili iliunganishwa pamoja. Katika kuendeleza sheria ya kawaida na usawa, waandishi wa kitaaluma wamekuwa na jukumu muhimu. William Blackstone, kuanzia kipindi cha 1760, alikuwa mwanachuoni wa kwanza kuelezea na kufunza usawa. Lakini kwa kuelezea tu, wasomi walitafuta melezo na miunso msingi walibadilisha polepole jinisi sheria ilivyofanya kazi. Sheria ya kidini Sheria ya kidini inatokana na maagizo ya dini. Baadhi ya mifano ni Halakha ya Kiyahudi na Sharia ya Uislamu — ambazo zote mbili zinamaanisha "njia ya kufuata" — huku sheria za Kanisa za Ukristo nazo hutumika katika madhehebu machache, kama vile Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiorthodoksi na la Anglikana. Mara nyingi dini inadai kutobadilika kwa sheria, kwa sababu neno la Mungu haliwezi kufanyiwa marekebisho wala kupingwa na mahakimu au serikali. Hata hivyo mfumo fasaha wa sheria kwa jumla unahitaji upanuzi upande wa binadamu. Kwa mfano, Torati au Vitabu Vitano vya Musa katika Agano la Kale. Vitabu hivyo vina kanuni na sheria za msingi za Uyahudi, ambayo baadhi ya jamii ya Kiisraeli huchagua kutumia. Halakha ni kanuni ya sheria za Kiyahudi inayofanya muhtasari wa baadhi ya ufafanuzi wa kitabu cha Talmud. Hata hivyo, Sheria za Israeli zinaruhusu mlalamikaji kuchagua mbinu za kidini ikiwa tu anataka. Mfano mwingine ni Korani ambayo ina sheria, na inakuwa kama chanzo cha sheria zaidi kupitia ufafanuzi, Qiyas (kulinganisha), Ijma (kufikia muafaka) na yaliyokwishatokea. Hili hasa hupatikana katika mkusanyo wa sheria na falsafa ya kisheria inayojulikana kama Sharia na Fiqh. Hadi karne ya 18, Sharia ilitekelezwa kote katika Ulimwengu wa Kiislamu katika mfumo ambao haukuwa umeandikwa kwa ufasaha, huku sheria ya Mecelle ya Dola la Ottoman katika karne ya 19 ilikuwa ya kwanza kuandika vipengele vya Sharia. Tangu miaka ya kati ya 1940, majaribio yamefanywa, katika nchi nyingi, kufanya sheria hizo zifanane zaidi na hali na dhana za kisasa. Katika nyakati za sasa, mifumo ya kisheria katika mataifa mengi ya Kiislamu hutegemea sheria za kiraia na sheria ya kawaida na pia sheria na tamaduni za Kiislamu. Katiba za baadhi ya nchi za Kiislamu, kama vile Misri na Afghanistan, zinatambua Uislamu kama sheria ya taifa, hivyo kuyafanya mabunge katika nchi hizo yasiwe na budi kufuata Sharia. Saudia inatambua Korani kama katiba, na inatawaliwa kwa msingi wa sheria ya Kiislamu. Iran pia imeshuhudia kurudi kwa sheria ya Kiislamu katika mfumo wake wa kisheria baada ya mwaka 1979. Katika miongo michache iliyopita, mojawapo ya tofauti kuu ya harakati ya mwamko wa Kiislamu imekuwa wito wa kuirejesha Sharia, wito ambao umeibua kiasi kikubwa cha maandishi na kuathiri siasa duniani. Nadharia ya sheria Historia ya Sheria Historia ya sheria inashikamana kwa karibu na maendeleo ya ustaarabu. Sheria ya Misri ya Kale, iliyorudi nyuma mbali hadi mnamo 3000 KK, ilikuwa na mkusanyiko wa sheria ambao huenda ulikuwa umegawanjwa katika vitabu kumi na viwili. Ilizingatia dhana ya Ma'at, iliyokuwa na sifa ya mapokeo, hotuba za kushawishi, usawa wa kijamii na uaminifu. Kufikia karne ya 22 KK, mtawala wa zamani wa Kisumeri, Ur-Nammu alikuwa ameandaa mkusanyiko wa sheria, ambao ulihusisha kauli za kimjadala ("ikiwa ... basi ..."). Kufikia mwaka wa 1760 KK, Mfalme Hammurabi aliboresha zaidi Sheria ya Babeli, kwa kuikusanya na kujandika katika jiwe kubwa. Hammurabi aliweka nakala kadhaa za jiwe lile kote katika milki ya Babeli kama stelae, ili watu wote waitazame; hii ilikuja kufahamika kama Mkusanyiko wa Sheria za Hammurabi. Nakala iliyobaki ambayo haijaharibika sana wa stelae hizi iligunduliwa katika karne ya 19 na Waingereza wasomi wa mambo ya milki ya Assyria, na tangu wakati huo imenakiliwa upya na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali, zikiwemo Kiingereza, Kijerumani na Kifaransa. Agano la Kale lilianza mnamo 1280 KK, na linachukua umbo la amri za kimaadili kama mapendekezo ya jamii nzuri. Mji-dola wa Ugiriki ya Kale, Atheni ya Kale kuanzia karne ya 8 KK ilikuwa jamii ya kwanza kuwa na msingi wake katika kuhusisha raia kwa upana; isipokuwa wanawake na daraja la watumwa. Hata hivyo, Atheni haikuwa na sayansi ya kisheria, na hapakuwa na neno la "sheria" isipokuwa kama dhana ya kiakili tu. Bado sheria ya Ugiriki wa Kale ilikuwa na uvumbuzi mkubwa wa kikatiba katika kuendeleza demokrasia. Sheria ya Kirumi ilisukumwa sana na falsafa ya Kigiriki, lakini maelezo yake ya kina yaliendelezwa na wanasheria wa kitaaluma, na yalikuwa magumu sana. Katika kipindi cha karne zilizopita kati ya kupanda na kushuka kwa Dola la Roma, sheria imebadilishwa ili kukabiliana na hali za kijamii zilizokuwa zikibadilika, na ilikusanywa na kuandkiwa vilivyo wakati wa utawala wa kaisari Justinian I. Ingawa ilipungua kwa umuhimu mwanzoni mwa Karne za Kati, Sheria ya Kirumi iligunduliwa upya wakati wa karne ya 11 ambapo wasomi walianza kutafiti mkusanyiko wa sheria za Kirumi na kuyatumia mawazo yao. Katika Uingereza ya Zama za Kati, mahakimu wa Mfalme waliunda mwili wa utangulizi, ambao baadaye ulijulikana kama sheria ya kawaida. Sheria ya biashara ya Ulaya mzima iliundwa ili kuwapa wafanyabiashara uwezo wa kufanya biashara kwa kutumia viwango sawa vya mazoezi; badala ya kutumia sheria za kimtaa zenye pande nyingi. Hiyo Lex Mercatoria, mtangulizi wa sheria ya kisasa ya biashara, ilihimiza uhuru wa mkataba na kuwekwa mbali kwa mali. Kadiri utaifa ulipozidi katika karne za 18 na 19, ndipo Lex Mercatoria ilipozidi kujumuishwa katika sheria za kimanispaa za nchi mbalimbali chini ya mkusanyiko mpya wa sheria za kiraia. Mkusanyiko wa Sheria za Napoleoni na sheria za Kijerumani ulikuwa na ushawishi mkubwa zaidi. Ikitofautishwa na sheria ya kawaida ya Uingereza, ambayo ina idadi kubwa ya sheria za kesi, mikusanyiko ya sheria katika vitabu vidogo ni rahisi kuuza nje ili mahakimu waweze kuitumia. Hata hivyo, hivi leo kuna ishara kuwa sheria ya kiraia na sheria ya kawaida zinazidi kukaribiana. Sheria ya Umoja wa Ulaya imekusanywa katika mikataba, lakini huendelezwa kupitia utangulizi unaofanywa na Mahakama ya Ulaya ya Haki. Sheria ya Kiislamu na falsafa ya sheria zilianza katika kipindi cha Zama za Kati. Mbinu ya kisheria ya utangulizi na kufikiria kupitia mlinganisho (Qiyas) iliyotumika katika sheria ya mapema ya Kiislamu ilifanana na na ile ya baadaye ya mfumo wa Sheria ya Kawaida ya Uingereza. Hii ilitumika hasa katika shule ya Maliki ya sheria ya Kiislamu iliyopatikana sana katika eneo la Afrika Kasakazini, Uhispania wa Kiislamu na baadaye Sicily ya Kiemereti. Kati ya karne za 8 na 11, sheria ya Maliki iliendeleza taasisi nyingi zilizokuwa sambamba na taasisi za baadaye za sheria ya kawaida. Sheria ya kale ya Uhindi na Uchina zinawakilisha mapokeo tofauti ya sheria, na kihistoria yamekuwa na shule huru za kinadharia na mazoezi. Arthashastra, ambayo pengine iliandikwa mnamo 100 BK (ingawa ina maandiko ya awali kidogo), na Manusmriti (100–300) yalikuwa mikataba ya uanzilishaji nchini Uhindi, na ilikuwa na maandiko yanayofikiriwa kuwa wongofu wenye mamlaka wa kisheria. Falsafa kuu ya Manu ilikuwa kuvumiliana na Mfumo wa Vyama Vingi, na ilitajwa kote katika eneo la Asia ya Kusini Mashariki. Mapokeo haya ya Kihindu, pamoja na sheria ya Kiislamu, yalibadilishwa na na sheria ya kawaida wakati ambapo Uhindi ilifanywa kuwa sehemu ya Dola la Uingereza. Malaysia, Brunei, Singapore na Hong Kong pia ilianza kutumia sheria ya kawaida, Mapokeo ya sheria ya Asia ya Kusini yanaangazia mkusanyiko maalum wa ushawishi wa kidunia na kidIni. Ujapani ilikuwa nchi ya kwanza kuufanya mfumo wake wa sheria uwe wa kisasa sambamba na ule wa nchi za magharibi, kwa kuagiza sehemu za mkusanyiko wa sheria za Ufaransa, lakini hasa mkusanyiko wa sheria za Kijerumani. Hili lilionyesha kwa kiwango fulani hadhi ya Ujerumani kama nguvu yenye uwezo mkubwa zaidi katika kipindi cha mwisho cha karne ya 19. Pia, sheria ya mapokeo ya Uchina ilifungua njia kwa kubadilishwa na nchi za magharibi kuelekea miaka ya mwisho ya nasaba ya Ch'ing kupitia njia ya mkusanyiko wa sheria tatu za kibinaFsi zilizokuwa na msingi katika muundo wa Ujapani wa sheria ya Ujerumani. Leo sheria ya Taiwan inabaki na mshikamano wa karibu zaidi na mkusanyiko wa sheria kutoka kipindi hicho, kwa sababu ya mgawanyiko kati ya wanataifa wa Chiang Kai-shek, ambao walitoroka kutoka sehemu hiyo, na wakomunisti wa Mao Zedong waliopata ushindi wa kudhibiti bara mnamo mwaka wa 1949. Muundombinu wa sasa wa Jamhuri ya Watu wa Uchina ilishawishika pakubwa na Sheria ya Kisoshalisti ya Umoja wa Kisovyeti, inayopea sheria ya utawala umuhimu mwingi kuliko haki za sheria ya kibinafsi. Kwa sababu ya kuongezeka kwa kasi kwa viwanda, leo Uchina inapitia machakato wa wa marekebisho, angalau katika nyanja ya haki za kiuchumi, ikiwa si haki za kijamii na kisiasa. Sheria mpya ya mkataba ya mwaka wa 1999 ilikuwa ishara ya kusonga mbali na kuwa na utawala mwingi. Isitoshe, baada ya mazungumzo yaliyodumu miaka kumi na mitano, mnamo mwaka 2001 Uchina ilijiunga na Shirika la Biashara Duniani. Falsafa ya sheria Falsafa ya sheria kwa kawaida inaitwa jurisprudensi. Jurisprudensi unaozidi kuongezka wenyewe ni falsafa ya kisiasa, na unauliza "sheria inafaa kuwa nini?", huku jurisprudensia ya uchambuzi inauliza "sheria ni nini?". Jibu la kiutumikaji la John Austin linajibu kuwa sheria ni "amri, zinazoandamana na matishio ya vkwazo, kutoka kwa mtawala, ambaye watu wote wamezoea kumtii". Mawakili wa sheria ya kimaumbile kwa upande mwingine, kama vile Jean-Jacques Rousseau, wanadokeza kwamba sheria inaangazia sheria isiyobadilika ya tabia ya kimaumbile. Dhana ya "sheria ya kimaumbile" iliibuka katika falsafa ya Kigiriki ya zamani kwa wakati mmoja na kwa pamoja na dhana ya haki, na iliingia mkondo wa utamaduni wa Magharibi kupitia maandiko ya Thomas Aquinas na maoni ya mwanafalsafa wa Kiislamu na mwanasheria Averroes. Hugo Grotius, mwanzilishi wa mfumo uliotegemea dhana za kiakili pekee ya sheria ya kimaumbile, alidokeza kuwa sheria inatokana na msukumo wa kijamii—jinsi Aristotle alivyokuwa amesema—na kufikiria. Immanuel Kant aliamini kuwa amri ya kimaadili inahitaji sheria "zichaguliwe kana kwamba zinafaa kushikilia kama sheria za ilimwenguni kote za kimaumbile". Jeremy Bentham na mwanafunzi wake Austin, wakimfuata David Hume, waliamini kuwa hili liliongeza utata wa "kilicho" na kile ambacho "kinafaa kuwepo". Bentham na Austin walisisitiza kuwe na sheria ya uchanya; na kuwa sheria ya kweli ni tofauti kabisa na "maadili". Kant pia alikosolewa na Friedrich Nietzsche, ambaye alikataa kanuni ya usawa, huku akiamini kuwa sheria hutokana na nia kwa nguvu, na haiwezi fanywa kuwa ya "kimaadili" au "utovu wa nidhamu". Mnamo mwaka wa 1934, mwanafalsafa wa Kiaustria, Hans Kelsen, alizidi na mapokeo ya uchanya katika kitabu chake Nadharia Safi ya Sheria. Kelsen aliamini kuwa ingawa sheria ni tofauti na maadili, inapewa "ukawaida"; kumaanisha kuwa tunfaa kuitii. Ingawa sheria ni taarfa chanya za "ni" (k.m. faini ya kuendesha kwa kurudi nyuma katika barabara kuu ni €500); hii sheria inatuelezea kile "tunachofaa" kutenda. Kwa hivyo kila mfumo wa sheria unaweza kudadisiwa kuwa na kanuni ya msingi (Grundnorm) ianyotupea amri ya kutii. Mpinzani mkuu wa Kelsen, Carl Schmitt, alikataa uchanya na dhana ya utawala wa sheria kwa sababu hakukubali umuhimu wa kanuni za kidhana za Uchanya badala ya mitazamo na uamuzi bayana wa kisiasa. Kwa hiyo, Schmitt alipendekeza falsafa ya sheria ya maalum (hali ya dharura), ambayo ilikanusha kuwa kanuni za kisheria zingezunguka uzoefu wote wa kisiasa. Baadaye katika karne ya 20, H. L. A. Hart alimshambulia Austin kwa kurahisisha kwake kwa suala hilo na Kelsen kwa kutunga kwake kwa mambo ya kihadithi katika kitabu cha Dhana ya Sheria. Hart alidokeza kuwa sheria ni mfumo wa kanuni, zilizogawanywa kuwa (kanuni za maadili) ambazo ndizo za kimsingi na sheria za upili (zinazowalenga maafisa kusimamia kanuni msingi). Kanuni za upili zimegawanywa zaidi kuwa sheria za uamuzi (kutatua migogoro ya kisheria), kanuni za mabadiliko (zinazoruhusu sheria kuwa tofauti) na sheria ya utambuzi(inayoruhusu sheria kutambulika kama halali). Wawili kati ya wanafunzi wa Hart waliendeleza mjadala: Ktaika kitabu chake Dola la Sheria, Ronald Dworkin alimshabulia Hart na wachanya kwa kukataa kwao la kufanya sheria iwe suala la kimaadili. Dworkin anadokeza kuwa sheria ni dhana ya "kitafsiri", inayowataka mahakimu kupata suluhisho bora zaidi kwa mgogoro wa kisheria, kwa mujibu wa mila zao. Joseph Raz, kwa upande mwingine, anawataka alitetea mtazamo wa kichanya na kukosoa mtazamo wa Hart wa "nadharia laini ya kijamii" katika kitabu chake Mamlaka ya Sheria. Raz anadokeza kuwa sheria ni mamlaka, yanayotambulika kupitia vyanzo vya kijamii na bila kurejelea hoja za kimaadili. Katika maoni yake, uainishaji wowote wa kanuni zozote zaidi ya majukumu yao kama vifaa vya kimamlaka katika upatanisha ni bora yaachiwe elimu ya jamii, badala ya falsafa ya sheria. Uchambuzi wa kiuchumi wa sheria Katika karne ya 18 Adam Smith aliwasilisha msingi wa kifalsafa wa kuelezea uhusiano kati ya sheria na uchumi. Taaluma hiyo ilitokana na mchango wa ukosoaji dhidi ya vyama vya wafanyikazi na sheria dhidi ya amana nchini Marekani. Watetezi wa taaluma hii waliokuwa na ushawishi mkubwa zaidi, kama vile Richard Posner na Oliver Williamson na kinachojulikana kama Shule ya Chicago ya wanauchumi na mawakili ikiwemo Milton Friedman na Gary Becker, kwa jumla ni watetezi wa uouguzaji wa udhibiti na ubinafsishaji, na ni maadui wa udhibiti wa serikali au kile wanachokiona kuwa vikwazo dhidi ya unedeshaji wa masoko huru. Mchambuzi maarufu zaidi wa kiuchumi wa sheria ni mshindi wa Tuzo la Nobel la mnamo 1991 Ronald Coase, ambaye makala yake makuu ya kwanza, Hali ya Kampuni (1937), kulidokeza sababu za kuwepo kwa makampuni mbalimbali (makampuni, ubia, n.k.) ndiyo kuwepo kwa gharama za biashara. Binadamu ambao hufikiria kawaida hufanya biashara kupitia mikataba ya bilaterala katika masoko wazi hadi wakati ambapo gharama ya biashara kunamaanisha kuwa kutumia makampuni ya kihalmasahhuri ili kuzalisha bidha ni ya ufanisi mwingi zaidi.Makala yake makuu ya pili, Shida ya Gharama ya Kijamii (1960), yalidokeza kuwa tunaishi katika Dunia bila gharama za kibiashara, watu ambao huongea kuhusu gharama pamoja wanatengeneza mgao sawa wa rasilimali, buila kujali jinsi mahakama yanavyoweza kuamua katika migogoro kuhusu mali. Coase alitumia mfano wa kesi ya kero iliyoitwa Sturges dhidi ya Bridgman, ambapo mtengenezaji peremende ambaye alipiga kelele nyingi na daktari mtulivu walikuwa majirani na walienda mahakamani ili wajue nani kati yao ndiye angefa kuhama. Coase alisema kuwa bila kujali ikiwa hakimu aliamua kuwa mtengenezaji peremende angefaa kuwacha kutumia mashine zake, au ikiwa ingembidi daktari kuvumilia kelele ile, wote wawili wangefikia mapatano ya pamoja kuhusu nani ndiye angefaa kuhama ambayo yanafikia matokeo sawa na mgawanyo wa rasilimali. Ni kuwepo tu kwa bei za biashara kunaoweza kuzuia hili. Kwa hivyo sheria infaa kutazamia kile ambacho huenda kikafanyika, na kuongozwa na ufumbuzi wenye ufanisi. Wenye kuunda mipango serikalini wanaamini wazo kwamba sheria na vikwazo si muhimu au zenye ufanisi katika kuwasaidia watu. Coase na wengine kama yeye walitaka mabadiliko ya mbinu, ili kuweka mzigo wa ushahidi katika serikali iliyokuwa ikiingilia soko, kwa kuchambua gharama za hatua. Elimujamii ya sheria Somo la kijamii la sheria ni taaluma pana ya masomo inayotazama mwingiliano kati ya sheria na jamii na inahusiana kwa karibu na falsafa ya sheria, uchambuzi wa kiuchumi wa sheria na masomo maalum zaidi kama somo la jinai. Taasisi za ujenzi wa jamii na mifumo ya kisheria ni maeneo muhimu ya uchunguzi wa taaluma hii. Mwanzoni, wananadharia wa kisheria walishuku taaluma hii. Kelesen alimshambuliwa mmoja wa waanzilishi wake, Eugen Ehrlich, ambaye alitaka kuweka wazi tofauti kati ya sheria ya uchanya, ambayo mawakili wanajifunza na kutumia, na aina zingine za 'sheria' au kanuni za kijamii zinazodhibiti maisha ya kila siku, na kwa jumla kuzuiwa migogoro isiwafikie mawakili mahakamani. Katika kipindi cha mwaka 1900 Max Weber alifafanua mbinu yake ya "kisayansi" ya sheria, huku akitambua "umbo la kimantiki ya sheria" kama aina ya utawala, ambao si chanzo cha watu lakini kwa dhana za kiakili. Umantiki wa kisheria yalikuwa maneno yake aliyoyatumia kuelezea mwili wa sheria zinazoeleweka na zinazoweza kuhesabika na zilikuwa hatua ya kwanza ya maendeleo ya kisasa ya kisiasa na taifa la ukiritimba la kisasa na kuibuka sambamba na ubepari. Msomi mwingine wa somo la jamii, Émile Durkheim, aliandika katika Mgawanyo wa Ujira na Jamii kuwa kadiri jamii inavyozidi kuwa kubwa, ndivyo mwili wa sheria ya kiraia unaohusika hasa na fidia unapozidi kukuwa kwa gharama ya sheria za jinai na vikwazo vya kisheria. Ili kupitisha sheria, idadi kubwa ya Wabunge lazima wapige kura ili muswada (sheria inayopendekezwa) upitishwe katika kila nyumba. Kawaida kutakuwa na kusoma kwingi na marekebesho mengi yaliyopendekezwa na makundi tofaiti ya kisiasa. Ikiwa nchi ina katiba inayofuatiliwa vyema, idadi maalum ya mabadiliko katika katiba yanahitajika, hivyo kufanya iwe gumu kubadilisha sheria. Serikali kwa kawaida huongoza mchakato huo, ambao unaweza kujumuisha Wabunge (k.m. nchini Uingereza na Ujerumani). Lakini katika mfumo wa kiraisi, serikali inachagua baraza la mawaziri kutawala kutoka kwa washirika wake kisiasa ikiwa wamechaguliwa au la (k.m. nchini Marekani au Brazili), na jukumu la bunge linapunguza liwe kukubali au kukataa. Serikali Mtendaji katika mfumo wa kisheria hutumika kama kituo cha serikali cha mamlaka ya kisiasa. Katika mfumo wa kibunge, kama vile nchini Uingereza, Italia, Ujerumani na Ujapani, mtendaji hujulikana kama serikali, na huwa na wanachama wa bunge. Mtendaji huchaguliwa na Waziri Mkuu au Chansela, ambaye ofisi yake ina nguvu za chini ya imani ya bunge. Kwa sababu uchaguzi wenye watu wengi huteua vyama vya kisiasa kutawala, kiongozi a chama anaweza kubadilika katika kipindi kabla ya uchaguzi mwingine. Mkuu wa Taifa ni kando na mtendaji, na kimfano hupitisha sheria na huwa kama mwakilishi wa nchi. Baadhi ya mifano ni Rais wa Ujerumani (anayeapishwa na Bunge); Malkia wa Uingereza (wadhifa wa kurithi), na Rais wa Austria (anachaguliwa kwa kura ya wengi). Mfano mwingine muhimu ni mfumo wa kirais, unaopatikana nchini Ufaransa, Marekani na Urusi. Katika mifumo ya kirais, mtrndaji huwa kama mkuu wa taifa na mkuu wa serikali, na ana nguvu za kuchagua baraza la mawaziri pekee yake. Chini ya mfumo wa kirais, tawi la mtendaji ni kando na bunge ambapo haiwajibiki mbele ya bunge. Ingawa jukumu la mtendaji ni tofauti toka nchi moja hado nyingine, kawaida itapendekeza wingi wa sheria, na kupendekeza ajenda ya serikali. Katika mifumo ya kirais, mtendaji mara nyingi ana nguvu za kukataa sheria. Mara nyingi mtendaji katika mifumo yote ana wajibu wa sera za mahusiano ya nje, jeshi na polisi na urasimu. Mawaziri au maafisa wengine wanasimamia ofisi za nchi, kama vile wizara ya nje au wizara ya ndani. Uchaguzi wa mtendaji tofauti kwa hivyo ina uwezo wa kupindua mtazamo wa nchi nzima wa serikali. Jeshi na polisi Ingawa mashirika ya kijeshi yamekuwepo kwa muda mrefu kama serikali yenyewe, dhana la kikosi cha polisi kilicho tayari ni dhana ya kisasa. Mfumo wa Uingereza ya Zama za Kati ya mahakama ya jinai ya kusafiri, au assize, ilitumia kesi za maonyesho na unyongaji hadharani kufanya jamii ziwe na hofu na hivyo kudumisha udhibiti. Polisi wa kwanza wa kisasa pengine walikuwa wale wa Paris wa karne ya 17, katika mahakama ya Louis XIV, ingawa Polisi wa Mkoa wa Paris ndio wanadai kuwa wao ndio waliokuwa wa kwanza kuvaa sare. Weber yu maarufu kwa kudokeza kwamba taifa ni lile ambalo linadhibiti kihalali utumizi wa kipekee wa vurugu. Majeshi na askari wanalinda usalama kufuatana na amri ya serikali au mahakama. Maneno taifa lililopangarayika yanaashiria taifa ambalo haliwezi kutekeleza au kulazimisha sera; askari wao na majeshi hawana uwezo wa kulinda usalama na amani na jamii inaelekea vurugu pekee, wakati serikali inapokosekana. Urasimu Asili ya neno "Urasimu" kwa Kiingereza (bureaucracy) ni neno la Kifaransa la "ofisi" (bureau) na neno la Kigiriki cha Zamani cha "nguvu" (kratos). Kama tu wanajeshi na polisi, watumishi wa mfumo wa kisheria wa serikali na miili inayounda urasimu wake hufuata maagizo ya Mtendaji. Mojawapo ya marejeo kwa dhana yalifanywa Baron de Grimm, mwandishi wa Kijerumani aliyeishi nchini Ufaransa. Mnamo mwaka wa 1765 aliandika, Roho halisi ya sheria nchini Ufaransa ni urasimu amabo marehemu Monsieur de Gournay alikuwa akilalamika sana kuhusu; hapa ofisi, makarani, makatibu, wasimamizi na wanaonuia kufanya kazi fulani hawaapishwi kufaidi maslahi ya umma, kwa hakika maslahi ya ummayanaonekana kuanzishwa ili ofisi hizo ziwepo. Wasiwasi kuhusu "utawala wa kiofisi" bado ni kawaida, na utendaji wa watumishi wa umma kawaida hutofautishwa na wa kampuni za kibinafsi zinazoendeshwa na lengo la faida. Kwa kweli kampuni za kibinafsi, hasa zile kubwa, pia zina urasimu. Mtazamo mbaya wa "urasimu" kando, huduma za umma kama vile elimu, afya na shughuli za polisi au uchukuzi wa umma ni kazi muhimu nchi hivyo basi kufanya urasimu wa umma chanzo cha nguvu za serikali. Akiandika mapema katika karne ya 20, Max Weber aliamini kuwa sifa muhimu ya nchi iliyoendelea ilikuwa imekuwa msaada wake wa kirasimu. Weber aliandika kuwa sifa za kawaida za urasimu wa kisasa ni kuwa maafisa wanafafanua lengo lake, wigo wa kazi umefungwa na kanuni, usimamizi unajumuisha wataalamu wa wataalamu wa kitaaluma, amabo ambao husimamia kuanzia juu kuenda chini, wakiwasiliana kupitia kuandika na kufunga uwezo wa wafanyikazi wa umma kufanya watakavyo kwa kutumia kanuni. Taaluma ya sheria Hitimisho la utawala wa sheria ni kuwepo kwa taaluma ya kisheria yenye uhuru wa kutosha wa kuweza kuomba mamlaka ya mahakama huru; haki ya usaidizi kusaidiwa na wakili mahakamani uanatokana na hitimisho hili—nchini Uingereza kazi ya wakili inatofautishwa na ile ya mshauri wa kisheria. Kama mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu yanavyosema, sheria inafaa kupatikana na kila mtu na waty wanfaa kutabiri jinsi sheria itakavyowaathiri. Ili kudumisha utaaluma, zoezi la sheria kawaida linachungwa na serikali au mwili huru kama vile chama cha mawikili, baraza la mawakili au jamii ya sheria. Mawakili wa kisasa wanapata utambulisho maalum wa kisheria kupitia taratibu maalum za kisheria (k.m. mafanikio katika mitihani), yanahitajika na sheria ili kuwa na cheti maalum (elimi ya kisheria inayompa mwanafunzi Shahada ya Sheria, Shahada ya Sgeria ya Kiraia, au Shahada ya Juris Doctor), na zinawekwa ofisini kwa kutumia fomu za kisheria za kuapishwa (kukubaliwa katika baraza la mawakili). Nchi nyingi za Kiisalmu zina sheria sawa kuhusu elimu ya kisheria na taaluma ya kisheria, lakini zingine bado zinaruhusu mawakili wenye mafunzo katika sheria ya Kiislamu ya jadi katika taaaluma ua sheria katika mahakama ya hadhi ya kibinasfi. Nchini Uchina na katika nchi zingine za ulimwengu unaoendelea hakuna watu wa kutosha wenye mafunzo ya kisheria kufanya kazi katika mifumo ya mahakama iliyopo katika nchi hizo, na, kufuatana na hilo, viwango rasmi si vikali sana. Baada ya kupata kukubalika, wakili mara nyingi atafanya kazi katika kampuni ya sheria, katika vyumba kama wakili wa kipekee, katika wadhifa wa kiserikali au katika shirika la kibinafsi kama mshauri wa ndani. Isitoshe wakili anaweza kuwa utafiti wa kisheria|mtafiti wa kisheria anayepeana uatafiti wa kisheria unapoitishwa kupitia maktaba, huduma ya kibiashara au kazi isiyokuwa na muajiri mmoja. Watu wengi wenye mafunzo katika sheria walitumia utafiti wao katika taaluma nyingine tofauti kabisa. Adhimu kwa zoezi la sheria katika mapokeo ya sheria ya kawaida ni utafiti wa kisheria kujua hali ya wakati wa sasa wa sheria. Hili linahushisha kuchunguza ripoti za kesi, majarida ya kisheria na sheria. Zoezi la sheria pia inahusu kuandika hati kama vile kuiitia kwa mahakama, [[brifu [sheria)|brifu]], mikataba, au amana. Majadiliano na ujuzu wa kusuluhisha migogoro (ikijumuisha mbinu za ADR) pia ni muhimi kwa zoezi la sheria, ikitegemea na aina ya taaluma. Mashirika ya kijamii Dhana ya Kiripablikani wakati kulipokuwa na madaraja mbalimbali ya kijamii ya "mashirika ya kijamii" ilianzia wakati wa Hobbes na Locke. Locke aliona mashirika ya kijamii kama watu wenye "sheria sawa na mahakama kurejelea , yenye mamlaka ya kuamua utata baina yao." Mwanafalsafa wa Kijerumani Georg Wilhelm Friedrich Hegel alitofautisha "taifa" na "mashirika ya kijamii" (burgerliche Gesellschaft) katika kitabu chake Vipengele vya Falsafa ya Sawa. Hegel aliamini kuwa mashirika ya kijamii na taifa zilikuwa kinyume kabisa, katika mpangilio wa nadharia yake ya historia. Taifa la kisasa lenye pande hizi mbili–mashirika ya kijamii lilizaliwa tena katika nadharia za Alexis de Tocqueville na Karl Marx. Siku hizi katika nadharia ya wakati wa baada ya kisasa za mashirika la kijamii lazima iwe chanzo cha sheria, kwa kuwa msingi ambapo watu wanaunda maoni na kushwishi yale wanayoamini sheria inafaa kuwa. Kama wakili wa Kiaustralia na mwandishi Geoffrey Robertson QC alivyoandika kuhusu sheria ya kimataifa, ... mojawapo ya vyanzo vyake vya kisasa inapatikana katika majibu ya kawaida ya wanaume na wanawake, na mashirika yasiyo ya kiserikali, amabyo wengi huunga, kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu amabyo wengi huona kwenye runinga wakiwa sebuleni nyumbani mwao. Uhuru wa kujieleza, uhuru wa kujumuika na sheria zingine nyingi za kibinafsi zinawaruhusu watu kukusanyika, kujadili, kukosoa na kufanya serikali zao kuwajibika, ambapo msingi wa demokrasia ya majadiliano inaibuka. Watu wanapozidi kujihusisha mamlaka ya kisheria na na kuwa na uwezo wa kubadilisha jinsi mamlaka ya kisiasa yanapotumika maishani mwao; ndivyo sheria inapozidi kuwa halali kwa watu. Taasisi ambazo ni za kawaida sana za mashirika ya kijamii ni masoko ya kibiashra, kampuni zenye malengo ya kupata faida, familia, vyama vya kibiashara, hospitali, vyuo vikuu, shule, mashirika ya msaada, vilabu vya kujadili, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, vitongoji, makanisa, na vyama vya kidini. Tazama pia Haki za kibinadamu Uchumi Historia Sayansi ya Kisiasa Falsafa Tanbihi https://www.path-2-happiness.com/sw Marejeo Printed sources . See original text in Perseus program. {{cite journal |last=Coase |first=Ronald H. |authorlink=Ronald H. Coase |year=1960 |month=Oktoba |title=The Problem of Social Cost (this online version excludes some parts) |journal=Journal of Law and Economics |volume=3 |pages=1–44 |url=http://www.sfu.ca/~allen/CoaseJLE1960.pdf The Problem of Social Cost |accessdate=2007-02-10 |doi=10.1086/466560 |archive-date=2005-03-31 |archive-url=https://web.archive.org/web/20050331232727/http://www.sfu.ca/~allen/CoaseJLE1960.pdf |dead-url=yes }} Hamilton, Michael S., and George W. Spiro (2008). The Dynamics of Law, 4th ed. Armonk, NY: M.E. Sharpe, Inc. ISBN 978-0-7656-2086-6. Locke, John (1689). Second Treatise'' Online sources Viungo vya nje Legal news and information network for attorneys and other legal professionals Encyclopaedic project of academic initiative in Jurispedia Legal articles, news, and interactive maps WorldLII - World Legal Information Institute CommonLII - Commonwealth Legal Information Institute AsianLII - Asian Legal Information Institute (AsianLII) AustLII - Australasian Legal Information Institute BaiLII - British and Irish Legal Information Institute CanLII - Canadian Legal Information Institute NZLII - New Zealand Legal Information Institute PacLII - Pacific Islands Legal Information Institute Elimu jamii Historia Falsafa
73
https://sw.wikipedia.org/wiki/Siasa
Siasa
Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji, taifa, au hata dunia nzima (siasa ya kimataifa). Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka. Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi. Hapa chini, mifumo mbalimbali ya kisiasa huelezwa kifupi: Utawala wa Kifalme ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka ya dola na ya serikali Mfalme. Katika mfumo huu madaraka hurithiwa na mtu wa familia ya kifalme. Utawala wa Kiimla ni mfumo wa uongozi unaotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa kiongozi. Katika utawala huu watu binafsi hawana haki na uhuru katika maamuzi. Utawala finyu ni mfumo unaowapa wachache kati ya wengi nguvu za maamuzi katika dola na serikali. Nafasi ya wachache hawa hutokana na haiba na uwezo wao kiuchumi, kijamii, kijeshi au kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni nadra sana siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa makabaila. Utawala wa Umma ni utawala unaotokana na jamii kuamua misingi ya kujiongoza, hivyo unatoa fursa ya madaraka kwa umma moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama demokrasia na umegawanyika katika sehemu zifuatazo: Demokrasia Chama ni aina ya demokrasia ya kura. Inashirikisha watu wote kuwa wanachama. Demokrasia Baguzi ni aina ya demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi. Demokrasia Duni ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu kuunda serikali mfano: chama - serikali. Demokrasia Endelevu ni aina ya demokrasia inayotoa fursa ya usawa na kupinga matabaka katika jamii. Demokrasia Shirikishi katika aina hii ya demokrasia wachache hupewa dhamana na wengi katika uwakilishi wa jamii katika maamuzi. Wachache huchaguliwa na wengi kwa njia ya demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba ya nchi hiyo. Mfano: Wabunge huwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi. Siasa
78
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ushairi
Ushairi
Ushairi ni utungo wa kisanaa ulio na madhumuni ya kutumbuiza au kuelimisha. Tena, ushairi ni tawi mojawapo la fasihi andishi. Kinyume chake ni nathari. Inawezekana kutunga mashairi yenyewe au kutumia lugha ya kishairi katika aina nyingine za sanaa, kwa mfano tamthiliya au nyimbo. Ushairi una historia ndefu. Kwa mfano, mwanafalsafa Aristotle katika kitabu chake Ushairi ("Poetics" kwa Kiingereza) anachunguza matumizi yake katika hotuba, tamthiliya, nyimbo na futuhi. Ushairi una vipera vitano ambavyo ni: 1. nyimbo 2. ngonjera 3. mashairi mepesi 4. maghani 5. tendi 6. rara 7. rara nafsi Maana na tafsiri ya ushairi kulingana na washairi wakubwa Katika kujenga hoja mbalimbali za ushairi ni nini. Wakongwe na magwiji wa ushairi wa awali walieleza maana mbalimbali za ushairi kulingana na utunzi. Wakongwe hao waliamini kuwa mtunzi ana uhuru wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira. Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi. Marejeo Fasihi
654
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20saidizi%20ya%20kimataifa
Lugha saidizi ya kimataifa
Lugha saidizi ya kimataifa ni lugha ya kuundwa iliyoundwa kwa ajili ya mawasiliano kati ya watu toka mataifa mbalimbali. Lugha saidizi ya kimataifa inayozungumzwa zaidi ni Kiesperanto. Nyingine ni kama Kivolapuki, Kiido, Kiinterlingua na Kislovianski. Lugha saidizi ya kimataifa nl:Kunsttaal#Internationale hulptalen
660
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hisabati
Hisabati
Hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu. Kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo. Hisabati linaundwa na masomo mbalimbali, kama hesabu, jiometria na aljebra. Neno hisabati katika lugha ya Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu حسابات (halisi: hesabu (wingi)). Somo hili huweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu kisayansi. Hivyo hutumiwa na masomo mengine kama Fizikia, Jiografia, Kemia katika mafunzo yake. {|style="border:1px solid #ddd; text-align:center; margin:auto" cellspacing="15" ||| || || |- |Mantiki ya kihisabati || Nadharia ya seti || Nadharia ya kategoria || Nadharia ya kuhesabu |} Historia ya Hisabati Mwanahisabati Mjerumani Carl Friedrich Gauss aliita hisabati malkia wa sayansi ambayo inasaidia katika uvumbuzi wa kisayansi. Somo la hisabati lilikita mizizi kwa sababu ya uchu wa wanasayansi kupenda kutatua shida kama vile za biashara, ugavi wa ardhi na masomo ya sayari na katika kukisia uzani. Tanbihi Marejeo Courant, Richard and H. Robbins, What Is Mathematics? : An Elementary Approach to Ideas and Methods, Oxford University Press, USA; 2 edition (July 18, 1996). ISBN 0-19-510519-2. du Sautoy, Marcus, A Brief History of Mathematics, BBC Radio 4 (2010). Eves, Howard, An Introduction to the History of Mathematics, Sixth Edition, Saunders, 1990, ISBN 0-03-029558-0. Kline, Morris, Mathematical Thought from Ancient to Modern Times, Oxford University Press, USA; Paperback edition (March 1, 1990). ISBN 0-19-506135-7. Oxford English Dictionary, second edition, ed. John Simpson and Edmund Weiner, Clarendon Press, 1989, ISBN 0-19-861186-2. The Oxford Dictionary of English Etymology, 1983 reprint. ISBN 0-19-861112-9. Pappas, Theoni, The Joy Of Mathematics, Wide World Publishing; Revised edition (June 1989). ISBN 0-933174-65-9. . Peterson, Ivars, Mathematical Tourist, New and Updated Snapshots of Modern Mathematics, Owl Books, 2001, ISBN 0-8050-7159-8. Marejeo mengine Benson, Donald C., The Moment of Proof: Mathematical Epiphanies, Oxford University Press, USA; New Ed edition (December 14, 2000). ISBN 0-19-513919-4. Boyer, Carl B., A History of Mathematics, Wiley; 2nd edition, revised by Uta C. Merzbach, (March 6, 1991). ISBN 0-471-54397-7.—A concise history of mathematics from the Concept of Number to contemporary Mathematics. Davis, Philip J. and Hersh, Reuben, The Mathematical Experience. Mariner Books; Reprint edition (January 14, 1999). ISBN 0-395-92968-7. Gullberg, Jan, Mathematics – From the Birth of Numbers. W. W. Norton & Company; 1st edition (October 1997). ISBN 0-393-04002-X. Hazewinkel, Michiel (ed.), Encyclopaedia of Mathematics. Kluwer Academic Publishers 2000. – A translated and expanded version of a Soviet mathematics encyclopedia, in ten (expensive) volumes, the most complete and authoritative work available. Also in paperback and on CD-ROM, and online. Jourdain, Philip E. B., The Nature of Mathematics, in The World of Mathematics, James R. Newman, editor, Dover Publications, 2003, ISBN 0-486-43268-8. Maier, Annaliese, At the Threshold of Exact Science: Selected Writings of Annaliese Maier on Late Medieval Natural Philosophy, edited by Steven Sargent, Philadelphia: University of Pennsylvania Press, 1982. Viungo vya nje Chama cha Hisabati Tanzania , Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Free Mathematics books Free Mathematics books collection. Encyclopaedia of Mathematics online encyclopaedia from Springer, Graduate-level reference work with over 8,000 entries, illuminating nearly 50,000 notions in mathematics. HyperMath site at Georgia State University FreeScience Library The mathematics section of FreeScience library Rusin, Dave: The Mathematical Atlas . A guided tour through the various branches of modern mathematics. (Can also be found at NIU.edu .) Polyanin, Andrei: EqWorld: The World of Mathematical Equations. An online resource focusing on algebraic, ordinary differential, partial differential (mathematical physics), integral, and other mathematical equations. Cain, George: Online Mathematics Textbooks available free online. Tricki , Wiki-style site that is intended to develop into a large store of useful mathematical problem-solving techniques. Mathematical Structures, list information about classes of mathematical structures. Mathematician Biographies. The MacTutor History of Mathematics archive Extensive history and quotes from all famous mathematicians. Metamath. A site and a language, that formalize mathematics from its foundations. Nrich, a prize-winning site for students from age five from Cambridge University Open Problem Garden, a wiki of open problems in mathematics Planet Math. An online mathematics encyclopedia under construction, focusing on modern mathematics. Uses the Attribution-ShareAlike license, allowing article exchange with Wikipedia. Uses TeX markup. Some mathematics applets, at MIT Weisstein, Eric et al.: MathWorld: World of Mathematics. An online encyclopedia of mathematics. Patrick Jones' Video Tutorials on Mathematics Citizendium: Theory (mathematics). du Sautoy, Marcus, A Brief History of Mathematics, BBC Radio 4 (2010). MathOverflow A Q&A site for research-level mathematics Math – Khan Academy Teachoo Maths National Museum of Mathematics, located in New York City ! Sayansi
692
https://sw.wikipedia.org/wiki/Sheng
Sheng
Sheng ni lugha ya mitaani nchini Kenya inayochanganya Kiswahili na Kiingereza pamoja na lugha mbalimbali za kienyeji kama vile Kikikuyu, Kijaluo n.k. Sanasana hutumiwa na vijana katika mji wa Nairobi. Hata hivyo lugha hii inasambaa katika sehemu mbalimbali za Kenya na watu wa matabaka mbalimbali wanaitumia. Sheng inatumiwa kwenye mabasi, redio, muziki, na hata wakati mwingine kwenye bunge la Kenya. Sheng ilianza kutumika mwanzoni mwa miaka ya 1970 katika kitongoji cha Eastlands katika jiji la Nairobi. Wanamuziki, hasa wa mtindo wa "rap" wamefanya lugha hii kujulikana na kuanza kukubalika. Wanamuziki kama vile Kalamashaka jua kali na Nonini wamekuwa wakiitumia sana kwenye nyimbo zao. Ingawa misamiati mingi, muundo, na kanuni za Sheng zinatoka kwenye lugha ya Kiswahili, Sheng inatumia maneno ya Kiingereza na pia lugha za makabila nchini Kenya. Ingawa kuna watu wengi wanaoipenda na kuitetea Sheng, wako wengine, wakiwemo walimu wa lugha shuleni na vyuoni, wanaoipinga kwa maelezo kuwa inaharibu lugha ya Kiswahili na pia inahatarisha uwezo wa watoto na vijana kumudu Kiingereza na Kiswahili sanifu. Baadhi ya maneno ya Sheng manzi, slay queen mshi, dame, chikidee, chile, chick, mradi, mresh, msupa = msichana fiti!, fiti sana! = mzuri, okay Kanairo = Nairobi sasa = habari yako (ya sasa, ya saa hizi) chali, mhi, kijanaa, aguy, jamaa = mvulana kitu zii sana = kitu kibaya kucheki = kuangalia kuenda tao = kuenda mjini kukatia = kumwambia unayempenda maneno matamu ("flirting") kujiskia, kufeel fly/poa, kuji-do (do = fanya) = kuwa na maringo kupata ball = kupata mimba kugonga wall, kugonga mawe = kujaribu kumwongelesha msichana lakini hataki kujihusisha nawe kulapa mtu = kujidai kuwa humwoni mtu tia ritho = kuangalia (literally: put to the eye); katika Kikuyu, jina 'ritho' lamaanisha 'jicho'. kushona = kupata mimba. Mfano: Dame ameshona kuchill = hali ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa kusota = hali ya kuwa bila pesa ama hela (being broke) kuhanya = kufanya mapenzi holelaholela keroro, kamunyueso = mvinyo, pombe kugotea = kusalimia kuwa gauge = hali ya kuwa mlevi mahaga = sehemu ya nyuma ya msichana, matako ndae = gari kutia ndani, kuishi = kula kupewa = kunywa pombe Karao, Daewoo, = polisi (Daewoo kutoka jina la gari linalotumiwa na polisi nchini Kenya) mchoro = mpangilio wa kufanya kitu (plan) mgondi = jambazi (thug) juala, CD = kondomu kutia zii = kuachana na kitu ambacho unafanya kula vako = kuamini uwongo. Mfano: Alikula vako eti dame yangu ni mlami (He/she believed that I have a white girlfriend) veve = miraa kindugulu = bangi quarantei = karantini kujiaisolet= hali ya kuwa peke yako/kujitenga kuwa single = bila mke chapa na tarimbo/kemba/nyandua = kujamiana kimapenzi radha/ngori = shida risto = hadithi nichapie risto vajoo = bikra kamunyueso/wain =pombe bazenga = mtaalamu mi ni bazenga wa kucheza bukla motino/dogi = mbwa fwaka, fegi = sigara mushogi = gari la aina ya matatu kristi = mnunuaji njege, sange, mabeast = polisi yeng' = mwanamke chums, dooh, weng' = pesa sooh = shilingi mia moja finje = hamsini ashu = kumi mbao =ishirini kutypa = kumbuka bazu = mheshimiwa kuchum, kukis = kubusu Sa Good = Mungu mosmos = polepole chapchap = harakaharaka Njege = polisi Tanbihi Marejeo Abdulaziz, Mohamed H. and Ken Osinde. 1997. Sheng and Engsh: development of mixed codes among the urban youth in Kenya. International Journal of the Sociology of Language 125 (Sociolinguistic Issues in Sub-Saharan Africa), pp. 45–63. Bosire, Mokaya. 2006. Hybrid languages: The case of Sheng. Selected Proceedings of the 36th Annual Conference on African Linguistics, ed. Olaoba F. Arasanyin and Michael A. Pemberton, 185-193. Somerville, MA: Cascadilla Proceedings Project. Fee, D., & Moga, J. 1997. Sheng dictionary.Third edition. Nairobi: Ginseng Publishers. Githinji, Peter. 2005. Sheng and variation: The construction and negotiation of layered identities. PhD dissertation, Michigan State University. Githinji, Peter. 2006. Bazes and Their Shibboleths: Lexical Variation and Sheng Speakers’ Identity in Nairobi. Nordic Journal of African Studies 15(4): 443–472. Githiora, Chege. 2002. Sheng: peer language, Swahili dialect or emerging Creole? Journal of African Cultural Studies Volume 15, Number 2, pp. 159–181. Kang’ethe, Iraki. 2004. Cognitive Efficiency: The Sheng phenomenon in Kenya. Pragmatics 14(1): 55–68. Kießling, Roland & Maarten Mous. 2004. Urban Youth Languages in Africa. Anthropological Linguistics 46(3): 303-341 Mazrui, Alamin. 1995. Slang and Codeswitching: The case of Sheng in Kenya. Afrikanistische Arbeitspapiere 42: 168–179. Ogechi, Nathan Oyori. 2002. Trilingual Codeswitching in Kenya – Evidence from Ekegusii, Kiswahili, English and Sheng. Doctoral dissertation, Universität Hamburg. Ogechi, Nathan. 2005. On Lexicalization in Sheng. Nordic Journal of African Studies 14(3): 334–355. Samper, David. 2002. Talking Sheng: The role of a Hybrid Language in the Construction of Identity and Youth Culture in Nairobi Kenya. PhD Dissertation, University of Pennsylvania. Spyropoulos, Mary. 1987. Sheng: some preliminary investigations into a recently emerged Nairobi street language. Journal of the Anthropological Society 18 (1): 125-136. Viungo vya nje Dikshonari ya sheng Tupitie ucheki ma words za sheng za tene na zile nira Tasnifu kuhusu Sheng Talking Sheng: The role of a hybrid language in the construction of identity and youth culture in Nairobi, Kenya. Kamusi ya Sheng/Kiingereza, Kiingereza/Sheng Blogu ya Sheng Bloki ya Osporne Lugha Lugha za Kenya
693
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiswahili
Kiswahili
Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (35%), lakini sasa ya Kiingereza pia (10%), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki. Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya. Historia ya lugha Lugha ilianza takribani miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu. Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani, waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu, walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasiliano yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba karibu theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu. Kando ya Kiarabu toka zamani pia kuna athira ya lugha mbalimbali kama Kiajemi, Kihindi na Kireno. Kuanzia karne ya 20 hadi sasa maneno mengi yamepokewa kutoka Kiingereza, na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kifaransa, lakini pia kutoka lugha nyingine, hasa Kiarabu. Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawahili au لغة سواحيلية lugha sawahiliya). Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi iliandikwa mwaka 1848 na Dokta Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa. Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi kutokana na lugha mbalimbali za Kibantu zilizochangia katika eneo husika. Tangu karne ya 19 lugha ilianza kuenea barani kwa njia ya biashara. Wakati wa ukoloni wa Uingereza lugha ilisanifishwa na Kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye msingi wa lahaja ya Unguja. Wasemaji Hakuna hakika kuhusu idadi ya wasemaji wa lugha hiyo; idadi zinazotajwa zinatofautiana, lakini ni kati ya milioni 100 na 200 , kwa sababu wasemaji wanaoitumia kama lugha ya kwanza hawapungui milioni 20, na wasemaji wanaoitumia kama lugha ya pili ni zaidi ya milioni 90. Tena idadi ya wasemaji wa lugha ya kwanza inakua haraka, kwa sababu lugha inaenea katika maeneo ambapo hapo awali lugha nyingine zilitawala; hasa katika miji ya Tanzania imekuwa lugha kuu, badala ya lugha za kikabila, kutokana na mchanganyiko wa watu hata ndani ya nyumba moja, kama vile wanapooana watu wa makabila tofauti, jambo ambalo limekuwa la kawaida hasa Tanzania, ambayo inaongoza kwa matumizi ya Kiswahili. Kwa watoto wengi kimekuwa lugha mama. Kati ya nchi nyingine ambapo Kiswahili kinatumika kuna Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia, Zambia, Malawi na visiwa vya Bahari Hindi kama Visiwa vya Ngazija (Komoro). Lugha rasmi Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika nchi zifuatazo: Tanzania: ni lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, makanisani, misikitini, redioni, kwenye runinga na idadi kubwa ya magazeti. Serikali inatakiwa kukiendeleza Kiswahili kwa sababu ni lugha ya taifa. Sera ya elimu ya mwaka 2015 imechagua Kiswahili katika miaka 10 ijayo kiwe lugha ya kufundishia katika ngazi zote, ikiwemo ile ya chuo kikuu, ingawa utekelezaji wake umesimama. Kenya: ni lugha ya taifa tena lugha rasmi, sawa na Kiingereza, baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa tarehe 4 Agosti 2010; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo lenye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Hata hivyo, lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au za kikabila. Uganda: kimetangazwa kuwa lugha ya taifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo. Ni lugha ya polisi na jeshi, hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumiwa na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani. Wona UBC, WBS tv. Mwaka 2005 bunge lilipiga kura kukifanya lugha rasmi ya pili kwa kuwa kinazungumzwa zaidi (nje ya Buganda). Rwanda: tarehe 8 Februari 2017 bunge lilifanya Kiswahili lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, Kifaransa na Kiingereza. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa (pamoja na Kilingala, Kiluba na Kikongo), pia lugha ya jeshi. Kiswahili kilifika mashariki ya nchi na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani ya Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba. Lugha ya kwanza, lugha ya pili Kiasili Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza tu ya wakazi wa miji ya Waswahili kwenye pwani, katika sehemu za pwani pia kijijini. Baada ya kuenea kimekuwa lugha ya watu wengi mjini hasa Tanzania lakini pia Kenya. Kimeenea zaidi kama lugha ya mawasiliano na biashara pale ambako watu wa makabila mbalimbali wanakutana. Pamoja na nchi zinazotajwa hapo juu Kiswahili kinatumika Kaskazini mwa Msumbiji, Kusini kabisa ya Somalia, Mashariki mwa Burundi. Maeneo ya mpaka wa Tanzania kuna pia wasemaji kadhaa huko Malawi na Zambia. Tanzania na Kenya zilipokea wakimbizi wengi waliojifunza Kiswahili lakini hakuna uhakika kama bado kinatumiwa nao baada ya kurudi Afrika Kusini, Rwanda, Sudan Kusini, Somalia n.k. Kimataifa Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, na hasa Afrika, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali, na kukusanya kwake watu wa makabila na nchi kadha wa kadha wakaweza kufahamiana kwa lugha moja, hasa ilivyokuwa ni lugha mojawapo katika lugha kubwa za Afrika ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni na wakoloni, kama Kiarabu, Kiurdu, Kiebrania, Kireno na kadhalika. Leo imekuwa inatumiwa katika kusambaza habari katika vituo mbalimbali ulimwenguni kama vile Sauti ya Amerika, BBC, Deutsche Welle, Monte Carlo, RFI, na nchi nyinginezo kama vile Uchina, Urusi, Irani. Aidha, imekuwa ni mojawapo ya lugha muhimu zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini Marekani, Uingereza, Ulaya bara, Urusi, Uchina, na barani Afrika. Mwaka 2018 Afrika Kusini ilikubali Kiswahili iweze kufundisha shuleni kama somo la hiari kuanzia mwaka 2020. Botswana ilifuata mwaka 2020, na Namibia ina mpango kama huo. Pia Ethiopia na Sudan Kusini zimeanza kufundisha Kiswahili. Maendeleo ya Kiswahili Lugha ina maendeleo: inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili. Kuna mzaha unaosimuliwa hasa Tanzania: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kilikua Tanzania Bara, kikafa Kenya na kuzikwa Uganda. Hali halisi Kiswahili kina maendeleo yake katika nchi hizo zote labda zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo matumizi yake ni kwa njia ya lahaja za Kingwana. Lakini itategemea pia juhudi za serikali kama umoja wa lugha utatunzwa kwa sababu kuna athari nyingi kutoka lugha za kila eneo zinazoingia katika ukuzi wa Kiswahili kwa namna zinazotofauitiana. Taasisi zinazokuza Kiswahili Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda. Nchini Tanzania kuna Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) ilhali nchini Kenya kuna Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA). BAKITA na CHAKITA pamoja na wawakilishi kutoka Uganda wanaandaa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki (BAKAMA). Uchunguzi wa Kiswahili huendelea pia katika idara za vyuo vikuu vingi duniani, kwa mfano katika Institute National des Langues et Civilisations Orientales, jijini Paris, Ufaransa. Kamusi za Kiswahili Kati ya shughuli muhimu za taasisi hizo, mojawapo ni kazi ya kukuza misamiati ya Kiswahili yaani kutafuta maneno mapya au kupanua matumizi ya maneno yaliyopo ili kutaja mambo ya maisha ya kisasa yaliyobadilika. Utunzi wa kamusi za Kiswahili hupanua elimu hiyo. Faida za kutumia Kiswahili kwa mataifa ya Afrika Faida za kutumia lugha ya Kiswahili zinatajwa kama ifuatavyo: 1. Husaidia kuleta umoja wa bara zima. 2. Hudumisha utamaduni wa Kiafrika kuliko kufuata kasumba. 3. Hufanya Waafrika waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni. 4. Hurahisisha mawasiliano baina ya watu wa Afrika Mashariki. 5. Husaidia kuwa na mahusiano ya kibiashara na watu mbalimbali. 6. Ni ishara ya kuwa huru na kushikamana. 7. Ni utambulisho wa jamii husika (utaifa). 8. Husaidia kukuza na kuendeleza sanaa. 9. Husaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika taifa husika. 10. Husaidia kupata ajira katika vyuo na shule mbalimbali zinazofundisha lugha ya Kiswahili hata nje ya nchi. 11. Husaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wa lugha hiyo watakaofanya vizuri katika masomo kwa kuyaelewa zaidi. 12. Husaidia kuikuza na kuieneza ndani na nje ya jamii. Mengineyo Siku ya Kiswahili Duniani ilianzishwa na UNESCO mnamo mwaka 2021 ili kuadhimishwa kila tarehe 7 Julai kuanzia mwaka 2022. Tazama pia Historia ya Kiswahili Uenezi wa Kiswahili Lahaja za Kiswahili Kamusi za Kiswahili Tanbihi Marejeo Ashton, E. O. 1944. Swahili Grammar (Including Intonation). London: Longmans. Hinnebusch, T. J. 1979. "Swahili". Katika: T. Shopen (mhariri) Languages and Their Status, uk. 209-293. Cambridge, Massachusetts: Winthrop. Hinnebusch, T. J., and S. M. Mirza. 1979. Kiswahili: Msingi wa Kusema, Kusoma na Kuandika. Lanham, MD: University Press of America. Shihabdin Chiraghdin et Mathias E. Mnyampala. Historia ya Kiswahili. Oxford University Press, 1977. Nurse, D. and Hinnebusch, T. J. 1993. Swahili and Sabaki: A Linguistic History. Berkeley and Los Angeles: University of California Press. Ohly, Rajmund, Warsaw: Wydawnictwa Uniwersytetu warszawskiego, Język suahili, Ⅰ. Zarys gramatyki ⅠⅠ. Wybór tekstów, 1969 ; Ⅴ Teksty suahili w piśmie arabskim wraz z ćwiczeniami i wprowadzeniem metodologicznym, 1972, Literatura suahili, 1972. Ohly, R., Kraska-Szlenk, I., and Podobińska, Z., Język suahili, Warsaw: Wydawnictwo Akademickie Dialog, 1998. Wald, B. 1987. "Swahili and the Bantu Languages". Katika: B. Comrie (mhariri) The World's Major Languages, uk. 991-1014. New York: Oxford University Press. Whiteley, W. 1969. Swahili: The Rise of a National Language. London: Methuen. Zawawi, S. 1971. Kiswahili Kwa Kitendo: An Introductory Course. New York: Harper & Row. Viungo vya nje makala za OLAC kuhusu Kiswahili lugha ya Kiswahili katika Glottolog http://www.ethnologue.com/language/swh "Kiswahili, lugha moja ya Tanzania (Kiingereza) Jifunze Kiswahili (Kiingereza) Kamusi Hai ya Kiswahili/Kiingereza Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Tovuti kwa Kiitaliano yenye maelezo mafupi kuhusu lugha ya Kiswahili, Kozi kwa mtandao na Kamusi ya Kiitaliano - Kiswahili Mwana Simba: Kiswahili? Hakuna matata! (Kiingereza/Kifaransa) Swahili Literatur/Fasihi ya Swahili (Kijerumani/Kiswahili) Woerterbuch/Kamusi Kiswahili/Deutsch Deutsch/Kiswahili (Kijerumani/Kiswahili) Vitabu vya Kiswahili na du Kijerumani / Swahili-Buecher und Übungen Mafunzo ya Kiswahili kwa video Afrika Lugha za Burundi Lugha za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Lugha za Kenya Lugha za Rwanda Lugha za Tanzania Lugha za Uganda Lugha za Kibantu Waswahili Jumuiya ya Afrika Mashariki
882
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwanzo
Mwanzo
<center> Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili <small> Idadi ya makala: Idadi ya kurasa zote: (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.) Idadi ya hariri: Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: Idadi ya wakabidhi: Idadi ya watumiaji hai: (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita) Takwimu ya WIkipedia ya Kiswahili kwa jumla Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya. Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali hapa kwenye takwimu za makala (fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa) na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani. (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku) Michango ya wanawiki: angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia ( andika jina la mtumiaji kwenye sanduku) Jumuia za WikimediaWikipedia kwa lugha nyingine
888
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiarabu
Kiarabu
Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة‎‎, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu. Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu. Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu. Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau. Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi. Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele. Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali. Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini). Asili ya lugha ya Kiarabu Kiarabu, pamoja na lugha ya Kiebrania (ya Uyahudi) na Kiaramu (ya Mashariki ya Kati) na Kiamhari (ya Ethiopia) zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi vile vile ambazo zinatokana na asili hii, kama Kiashuri, Kifinisia, Kibabili na kadhalika. Baadhi ya hizi lugha zimekufa au kuwa na wazungumzaji wachache, na kwa hiyo umuhimu wake umekuwa si mkubwa kama ulivyo umuhimu wa lugha ya Kiarabu. Aina za Kiarabu Kuna aina tatu kubwa za lugha hii ya Kiarabu: Kiarabu Fasihi ambacho kilikuwa kikitumika zama za Ujahili kabla ya kuja Uislamu, na kuendelea kutumika baada ya kuja Uislamu katika Qurani na Sunnah za Mtume Muhammad, Kiarabu Mamboleo ambacho kinatumika katika maandishi na mazungumzo rasmi baina ya Waarabu wote kwa jumla, na Kiarabu Lahaja ambacho kinatumika na watu maalumu katika sehemu fulani za nchi au vijiji, na ni lugha ya mahali tu, kama vile Kiyemeni au Kimasri au Kishami au Kimaghribi, na lugha hizi au lahaja hizi zinakuwa zinatofautiana sana baina yake katika misamiati na matumizi. Kiarabu fasihi Kiarabu ni lugha ya zamani sana (tarehe yake inarudi nyuma zaidi ya miaka 2000), nayo pamoja na lugha nyinginezo za Kisemiti zilikuwa zikitumika katika nchi za Mashariki ya Kati. Kiarabu Fasihi ilianza kuwa na nguvu zaidi baada ya kuteremshwa Qurani kwa lugha hiyo na kuhifadhiwa Hadithi za Mtume Muhammad na kuwa ndio chanzo cha lugha zote nyinginezo za Kiarabu zilizokuweko wakati huo. Fasihi ya Kiarabu isiyo na tabia ya kidini ilikuwa hasa Ushairi. Washairi kama Abu Nuwas, Omar Khayyam, Hafiz, ibn Qayyim al-Jawziyyah wanakumbukwa hadi leo. Masimulizi kama Alfu Lela U Lela hayakuwa fasihi yenyewe, hata kama yamepata umaarufu katika nchi za Ulaya. Maandishi mengine ya Kiarabu yaliyokuwa muhimu sana ni maandiko ya falsafa na sayansi. Waarabu walitafsiri maandiko ya Wagiriki wa Kale wakaendeleza ujuzi wao. Katika karne zilizopita Ulaya ilipokea sehemu kubwa ya elimu yake kutoka kwa Waarabu kwa njia hiyo. Tangu karne ya 19 na katika karne ya 20 fasihi ya Kiarabu imepata uamsho mkuu. Khalil Jibran wa Lebanon yuko kati ya washairi wanaosomwa zaidi kimataifa. Nagib Mahfuz wa Misri ni mwandishi Mwarabu wa kwanza aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 1988. Tanbihi Viungo vya nje makala za OLAC kuhusu Kiarabu lugha ya Kiarabu katika Glottolog http://www.ethnologue.com/language/arb Lugha za Kisemiti Lugha za Algeria Lugha za Iraq Lugha za Libya Lugha za Mauritania Lugha za Misri Lugha za Moroko Lugha za Sudan Lugha za Tunisia Lugha za Syria Lugha za Saudia Lugha za Yemen Lugha za Oman Lugha za Falme za Kiarabu Lugha za Katar Lugha za Bahrain Lugha za Kuwait Lugha za Somalia Lugha za Chad Lugha za Israel Lugha za Palestina Lugha za Komori Lugha za Gambia
889
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu
Uislamu
Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام al-islam) ni dini inayotokana na mafunzo ya Mtume Muhammad. Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,800 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,400. Uislamu ni ile imani kuwa muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija. Imani na kitabu chake Imani katika Uislamu ni kumwamini Mungu mmoja tu peke yake anayeitwa Allah, ambaye hajazaa wala hajazaliwa na hafanani na yeyote yule. Kitabu kitakatifu cha Waislam ni Qur'an ambayo inaaminiwa ilifunuliwa kwa Mtume Muhammad kutoka kwa Mwenyezi Mungu mbinguni kupitia malaika Jibrili; ni kawaida kusema Qurani "iliteremshwa" kwa Muhammad. Kwa imani hiyo, kabla yake walioteremshiwa kitabu ni Musa (Torati), Daudi (Zaburi) na Isa (Injili). Pamoja na Qurani kuna mafundisho ya Sunna na Hadith ambayo ni maneno ya mtume Muhammad na masimulizi juu ya matendo yake ambayo pengine hutazamiwa kama mwongozo katika Uislamu. Allah ndiye Mungu pekee na muumba wa kila kitu. Qurani inasisitiza kwamba hana mshirika, hana baba wala mwana, hakuzaa wala hakuzaliwa, na hana mwanzo wala mwisho. Pamoja na amri mbalimbali kuna mfumo wa sheria za kidini zinazoitwa kwa jumla "sharia"; inajumlisha maagizo kuhusu mambo mengi ya maisha ya kila siku, uchumi na siasa. Historia ya chanzo cha Uislamu Muhammad alizaliwa mnamo mwaka 570 BK kama mtoto wa mfanyabiashara mjini Maka uliopo kwenye Bara Arabu. Kufuatana na mapokeo ya Kiislamu malaika Jibril alimtokea alipokuwa na umri wa miaka 40 yaani mnamo mwaka 610. Kutoka kwa malaika alipokea maneno ya Kurani na ufunuo huu uliendelea hadi mwisho wa maisha yake. Mtume alitangaza yale aliyosikia kwa wafuasi wake na maneno haya yalianza kukusanywa tayari wakati wa maisha ya mtume. Baada ya kifo chake mwaka 632 khalifa wa tatu Uthman ibn Affan alikusanya muswada na kumbukumbu zote na kuziweka pamoja na kuwa kitabu kamili. Ujumbe uliohubiriwa na Muhammad huko Maka ulipata wasikilizaji wachache, lakini viongozi wengi wa Kikuraishi, waliokuwa kabila kubwa Maka, waliwaona kama hatari kwa Maka na mwaka 622 Waislamu walipaswa kutoka Maka wakahamia Yathrib mji wa jirani uliojulikana baadaye kama Madina. Uhamisho huu unaitwa hijra na tangu khalifa wa pili Umar ibn al-Khattab huhesabiwa kuwa ni chanzo cha kalenda ya Kiislamu. Mjini Yathrib mtume aliendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi. Alifanya mapatano na watu wa Yathrib iliyoitwa baadaye "madinat an-nabi"" ikajulikana kwa kifupi kama Madina. Kutoka Madina mtume alianza kushambulia misafara ya watu wa Maka akawashinda mara kadhaa. Wakati huohuo aliwafukuza Wayahudi wa Yathrib. Mwaka 628 viongozi wa Maka walilazimishwa kufanya mapatano na Waislamu na mwaka 630 jeshi la Waislamu liliingia mjini Maka. Mtume alipoaga dunia mwaka 632 sehemu kubwa ya Bara Arabu ilikuwa chini ya Uislamu tayari. Mafunzo ya Uislamu Uislamu unawafunza wafuasi wake mambo mengi yanayohusiana na maisha, ikiwa yale yanayohusu ibada kama Sala, Zakat, Saumu na Hija; ambazo pamoja na kauli ya Shahada ("Nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wake") huitwa nguzo za Uislamu au yale yanayohusu maingiliano baina ya wanadamu, yakiwa maingiliano ya kijamii kama ndoa na talaka na ujirani mwema, au ya kiuchumi kama biashara, au ya kisiasa kama kawaida za kumchagua kiongozi wa dola, au ya uhusiano baina ya mataifa mbali mbali ulimwenguni. Uislamu unatazamwa kuwa mfumo kamili wa maisha ya binadamu, kiimani, kimaisha, kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ibada katika Uislamu Ibada katika Uislamu ni vile vitendo ambavyo Muislamu anamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake, kwani ibada yoyote haitakikani iwe na ushirikina ndani yake, na wakati itakapokuweko aina yoyote ya shirki basi ibada ile inakuwa haina maana wala thawabu wala ujira wowote, ni kazi ya bure. Kwa hiyo, kila Muislamu anatakikana wakati anapofanya ibada yake afanye kwa ajili ya Mola wake aliyemuumba akampa kila aina ya neema na kumtukuza kuliko viumbe vingine vyovyote, kwa kumpa akili, fahamu na elimu.Nguzo zauislamu :(Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]. Nguzo tano za Uislamu Kuna matendo kadhaa ambazo zinaitwa "Nguzo za Uislamu". Kwa kawaida ni tano zinazofundishwa katika madhehebu ya Wasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini. Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi kwa nguzo tano halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano . Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu. Salat: (Kiarabu: صلاة‎) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari. Zakat: (Kiarabu: زكاة‎‎) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri. Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo. Hajj (Kiarabu: الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni. Maingiliano katika Uislamu Uislamu umeweka kawaida mbali mbali katika maisha wakati watu wanataka kuweka uhusiano fulani baina yao ili mambo yaende vizuri na uhusiano uzidi kuwa mwema baina yao. Katika maingiliano yaliyowekewa kawaida na nidhamu katika Uislamu ni mambo yanayohusu: Nikaha au ndoa baina ya Waislamu Biashara na mambo yanayohusu uchumi Uhusiano wa kijamii baina ya watu katika mtaa au kijiji au mji au nchi Uhusiano wa kimataifa baina ya madola mbali mbali, yakiwa ya kiislamu au yasiyokuwa ya kiislamu. Vikundi na madhehebu Kuna mielekeo mikubwa miwili ndani ya Uislamu ambayo ni vikundi vya Wasunni 85-90% na Washia 10-15%. Kundi kubwa ni Wasunni waliopata jina kutokana na Sunna ("kawaida") ya mtume; takriban asilimia 85-90 ya Waislamu wote huhesabiwa humo. Kati yao kuna madhehebu 4 ambao ni Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafii. Tofauti katika mafundisho si kubwa, zinahusu hasa sharia na fikh. Kundi dogo zaidi ni Washia ambao wamegawanyika kati yao katika vikundi vingi. Washia walijitenga na Wasunni baada ya makhalifa wanne wa kwanza kuhusu swali ni nani anayefaa kuongoza Waislamu. Washia ni wale waliosisitiza sharti awe mtu kutoka ukoo wa Muhammad kupitia binti yake Fatima. Vikundi vya Washia vinatofautiana juu ya viongozi hawa. Jumuiya kubwa ya Washia ni Ithnashara walio wengi huko Uajemi, Irak na Lebanoni. Viungo vya nje Qurani Tukufu - Qurani Tukufu http://www.islamhouse.com tovuti ya Uislam - Mawaidha Alhidaaya - Tovuti ya Kiislamu Makasisi Waingia Uislamu Mazungumzo ya Mwislamu na Mkristo
890
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani
Kurani
Kurani (kwa Kiarabu: القرآن, Qur'an) ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinaaminiwa na Waislamu kuwa ni "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hicho kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad. Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake" Kurani imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,445. Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran na Waislamu, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu. Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile si ya Qur'an tukufu wala si ya kweli; ni nakala ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli. Waarabu wa kabla ya Uislamu waliunda hadithi na hadithi juu ya miti, visima na milima, na waliunda ibada zinazohusiana na miamba na milima huko Safa, Marwa, Abu Kubeys, Arafat, Mina na Muzdalifah. Ingawa Qur'ani ilifuta ibada nyingine, haikupingana na maandiko ya Kiarabu yenye mizizi, badala yake, iliendeleza sana ibada hizo. Wakati mwingine inakuwa vigumu kuelewa Qur'ani bila kujua mazoea ya zamani; kihistoria, wanadamu hawakutumia kipimo cha wakati kikubwa kuliko mwezi. Hivyo, mtu ambaye alisema, "Nina umri wa miaka 200." alikuwa akihesabu miezi, sio miaka. Kwa kweli alikuwa na umri wa miaka 16. "Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa kati yao kwa miaka elfu, isipokuwa miaka hamsini." (Ankebut: 14) Kwa kuongezea vyanzo vilivyoandikwa, masomo mengi na mashujaa, ambayo mengine ni tu katika utamaduni wa hadithi za Kiarabu, yamefunikwa kwa kifupi katika lugha ya Kurani, na marejeo madogo yanafanywa. Hadithi za Yusuf na Züleyha, İsa, Musa, İskender / Zülkarneyn ni hadithi ndefu zaidi. Hadithi za uumbaji na mafuriko, ibada ya Ibrahimu na Dhabihu, hadithi za manabii wa Kiebrania, imani ya Kiyahudi na historia, kama vile kutoka kwa Waisraeli kutoka Misri, zinachukua nafasi kubwa katika Kurani. Historia Waislamu wanaamini kwamba Qur'an mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti yake ilipomfikia. Qur'an haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani. Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Qur'an na kuwa kitabu kitakatifu. Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Qur'an tukufu. Elementi, Sura, Mistari, Aya Kuna sehemu 30 katika Qur'an, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari. Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina. Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Ma'ida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Ra'd, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan. Mahusiano baina ya Qur'an na Biblia Katika Qu'ran , inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizo pamoja na Uislamu huitwa Dini za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano hayo. Kuna baadhi ya kurasa za Qu'ran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Qu'ran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abrahamu, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Ayubu, Zekaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu. Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Qu'ran inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu. Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Qu'ran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo. Kurani na ulimwengu wa leo Sheria zinazotegemea matamshi na ufafanuzi wa Kurani ni shida leo kuzilinganisha na haki za binadamu, usawa wa kijinsia na dini ya binafsi na uhuru wa kusema. Tazama pia Historia ya uandishi wa Qurani Tanbihi Marejeo Al-Quran (Qurani) online kwa Kiarabu na tafsiri zaidi ya 100 katika lugha 20 pamoja na Kiswahili Quran.com Swahili Quran Tasfir by Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani Misahafu Uislamu
891
https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad
Hadithi za Mtume Muhammad
Hadithi au Sunnah ni maneno na vitendo ambavyo Mtume Muhammad alikuwa akisema au akifanya katika kipindi chake cha utume. Hadithi hizi ni mmoja kati ya miongozo ya imani kwa Waislamu. Hadithi hizi zinajumuisha pia mambo aliyoyaona au kuyasikia katika muda wa utume wake akalinyamazia kimya au akawa hakulipinga na akalikubali. Asili Muhammad aliishi miaka kama arobaini bila kuwa na imani ya Mungu pekee. Kisha Mwenyezi Mungu akamletea mjumbe kutoka kwake aitwaye malaika Jibrili anayeaminiwa na Waislamu kuwa ndiye aliyempa aya zilizoko katika msahafu wa Waislamu, Kurani. Inaelezwa kuwa Jibrili alimpa Muhammad aya hizo kwa muda wa miaka ishirini na mitatu mpaka alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 63. Hadithi za Mtume Muhammad zimekusanywa katika vitabu vingi sana na wanazuoni mbalimbali wa Hadithi, lakini vitabu vya hadithi ambavyo ni muhimu na vinategemewa na wengi katika Uislamu ni hivi vifuatavyo: Vitabu vya Hadithi 1- Sahih Al-Bukhari 2- Sahih Muslim 3- Sunan An-Nasai 4- Sunan At-Tirmidhi 5- Sunan Ibn Majah 6- Sunan Abu Daud 7- Muwatt'a Ibn Maalik 8- Musnad Ahmad bin Hanbal Mtume Muhammad alikuwa hapendelei Hadithi zake ziandikwe wakati mmoja na Kurani, yasije yakachanganyika maneno yake na yale ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Hadithi zilichelewa kuandikwa mpaka baada ya kufariki kwake dunia kwa muda mkubwa kidogo, na kwa sababu hiyo Hadithi zikatawanyika sehemu mbalimbali kulingana na usahihi wake au udhaifu wake au uwongo wake. Hivyo kuna Hadithi aina nne kulingana na fahamu na kutegemewa kwa msimulizi wa hiyo Hadithi: Hadithi Sahihi, Hadithi Hasan (Nzuri), Hadithi Dhaifu na Hadithi Maudhu'u (Hadithi ya Uwongo). Vile vile, kuna aina nyingine za Hadithi zilizogawanyika kwa mujibu wa mambo mengine kama vile: kwa mujibu wa wapokezi, au mfululizo wa wasimulizi, au idadi ya wasimulizi katika kila sehemu ya mfululizo, au kwa mujibu wa simulizi lenyewe na msimulizi wake. Hadithi kwa mujibu wa fahamu na kutegemewa kwa msimulizi Hadithi Sahihi huwa imesimuliwa kutegemewa ukweli wake na dini yake na mtu ambaye anafahamu nini anasimulia, na kuieleza hadithi kama alivyoipokea kutoka kwa Mtume Muhammad. Hadithi Hasan au Nzuri huwa inajulikana asili yake na wasimulizi ni watu maarufu. Hadithi Dhaifu huwa ile isiyofikia daraja ya Hasan, kwa sababu ya upungufu wa mmoja katika wasimulizi, au mfululizo wa wasimulizi haufikii mpaka kwa Mtume unakatika kwa mojawapo ya Masahaba, au mmoja katika wasimulizi si wa kutegemewa, na kuna kasoro fulani katika mambo haya. Hadithi Maudhu'u (ya Uwongo) ni ile hadithi iliyobuniwa ikatiwa katika Hadithi za Mtume, na huwa kawaida inakwenda kinyume na Qurani au Hadithi nyinginezo Sahihi au Hasan, au kutonasibiana na maneno yake Mtume au kuwa msimulizi wa Hadithi hii ni mwongo, au kuwa msimulizi hakukutana na yule ambaye amesema amepokea kwake katika mfululizo wa wasimulizi waliotajwa, au kuweko kasoro fulani katika maelezo au matukio yaliyotajwa ndani ya Hadithi hio. Hadithi kwa mujibu wa wasimulizi Hadithi Qudsi ni ile hadithi ambayo Mtume Muhammad ameisimulia kutoka kwa Mola wake Hadithi Marfu'u ni hadithi iliyopokewa na mfululizo wa wasimulizi na kufikishwa mpaka kwa Mtume Hadithi Mauquf ni ile hadithi iliyosimuliwa na masahaba lakini wasiseme kuwa wameipokea kutoka kwa Mtume mwenyewe. Hadithi Maqtu'u ni ile hadithi iliyokatika silsila au mfululizo wake . Viungo vya nje http://www.hadiths.eu Uislamu Misahafu
904
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Ukristo (kutoka neno la Kigiriki Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta" ) ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa kwa Waisraeli katika historia ya wokovu ya Agano la Kale na hasa Yesu Kristo katika Agano Jipya ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1. Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inalenga kuenea kwa binadamu wote, na kwa sasa ni kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi 2,400,000,000 (33% kati ya watu 7.274 bilioni), ambao nusu ni waamini wa Kanisa Katoliki na nusu ya pili wamegawanyika kati ya Waorthodoksi (11.9%) na Waprotestanti (38%) wa madhehebu mengi sana. Karibu wote wanakubali Utatu Mtakatifu, yaani kwamba milele yote Mungu ni nafsi tatu zenye umoja kamili: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni kwa jina lao kwamba mataifa yote wanahimizwa kubatizwa kwa maji, ili kuzaliwa upya, kadiri ya agizo la Yesu ili kuingizwa katika fumbo la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe. Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinajulikana kama Biblia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya. Wakati wa Mababu wa Kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na Mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo. Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwaokoa binadamu. Baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuka, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya Baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasiotubu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao. Hivyo, kati ya madhehebu ya Ukristo, karibu yote yanamkiri Yesu kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli: katika umoja na nafsi yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili. Yote yanamkiri kuwa Mwokozi wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa dunia kwa hukumu ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana. Vilevile yote yanamchukua kama kielelezo cha utakatifu ambacho - kwa msaada wa Roho Mtakatifu na wa sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia ile ya ubatizo - kiwaongoze ndani ya Kanisa katika maadili yao maalumu, kuanzia unyenyekevu na upole hadi upendo unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote, hata adui. Asili Chimbuko la Ukristo ni mtu huyo aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko Mashariki ya Kati, katika kijiji cha Bethlehemu kilichopo hadi hivi leo kwenye mipaka ya Palestina; alikuwa akiitwa Yesu wa Nazareti (kijiji alikokulia) au mwana wa Yosefu mchonga samani,mama yake akifahamika kwa jina la Bikira Maria. Kwa kumuita pia Kristo, wafuasi wake walikiri kwamba ndiye aliyetimiza utabiri wa manabii wa kale, kama unavyopatikana katika vitabu vya Biblia ya Kiebrania na Deuterokanoni. Habari za maisha na mafundisho yake zinapatikana kirefu zaidi katika Injili nne zilizokubalika, katika Agano Jipya kwa jumla, lakini pia ziliandaliwa na kutabiriwa na Agano la Kale. Yesu kama Masiya aliyetarajiwa Ukristo ni matokeo ya utume wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye Masiya, yaani mkombozi aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa binadamu. Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia nyoka, yaani shetani, kuhusu mwanamke kwamba "uzao wake utakuponda kichwa" (Mwa 3:15). Baadaye Abrahamu, babu wa taifa la Israeli, kwa imani na utiifu wake kwa Mungu, aliahidiwa kwamba katika uzao wake mataifa yote yatabarikiwa. Musa, mwanaharakati aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 KK (kabla ya kuzaliwa kwa Yesu), ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi kwa niaba ya Mungu ujio wa Masiya au Kristo (Kumb 18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake na atasema nao yote niliyomwamuru." Kuja kwake kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika Agano la Kale. Kwani Musa alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na manabii na makuhani. Yesu alizaliwa miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya Injili vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo mwongozo wa imani hiyo. Maisha na kazi ya Yesu vimeibua mambo mengi katika historia. Ndiyo sababu kalenda iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu ni mchango mmojawapo wa Ukristo katika ustaarabu. Mafundisho ya msingi ya Yesu Yesu alifanya ishara za kustaajabisha, au miujiza. Matokeo ni kwamba, watu wengi wakamwamini. Nikodemu, mshiriki mmojawapo wa baraza la Sanhedrini, ambalo lilikuwa pia mahakama kuu ya Wayahudi, alivutiwa na kutaka kujua zaidi kuhusu siri ya miujiza hiyo na ujumbe kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kuona ishara zile kutoka kwa Mungu. Yesu akamjibu kwamba hakika mtu hawezi kuingia ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na Roho Mtakatifu. Pia akajieleza kuwa mpatanishi wa ulimwengu wa dhambi na Mungu na kwamba kila anayemgeukia kwa imani hatapotea, bali atarithi uzima wa milele: alisema mwenyewe ni mfano wa nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa. (Yoh 2:23-3:21; Hes 21:9). Akiwa kando ya Ziwa la Galilaya, Yesu alikuta umati wa watu umekusanyika. Basi akapanda mashuani na kuenda mbali kidogo na ufuoni, akaanza kuwafundisha kuhusu Ufalme wa mbinguni kupitia mfululizo wa mifano. Mmojawapo ni huu ufuatao: "Ufalme wa mbinguni ni kama punje ya haradali ambayo mtu anaipanda. Ingawa ni mbegu ndogo sana inakua na kuwa mti wa mboga mkubwa kuliko yote. Inakuwa mti ambao ndege wanauendea, wakipata makao katika matawi yake". (Math 13:1-52; Mk 4:1-34; Lk 8:4-18; Zab 78:2; Isa 6:9,10). Kanisa siku za mwanzo Jumuia ya Wakristo inaitwa Kanisa, yaani "mkusanyiko" kama lilivyotajwa na Yesu mwenyewe hasa katika Injili ya Mathayo 16:18: "Wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu, nitalijenga kanisa langu. Wala milango ya kuzimu haitalishinda". Yesu aliita wengine 11 pamoja na Petro kuunda kundi la mitume wake. Idadi yao ilipangwa kwa kusudi la kudokeza kwamba ndiyo mwanzo mpya wa taifa la Mungu, kama vile watoto 12 wa Yakobo Israeli walivyokuwa mwanzo wa taifa lake la kale. Yesu aliwapa hao Thenashara mamlaka ile aliyopewa na Mungu Baba ili kuokoa watu. Yesu na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa Wayahudi. Yaani walizaliwa katika uzazi wa Abrahamu wakiwa watoto wa Agano lililofanywa kati ya Mungu na taifa lake la Israeli zamani za Musa. Wakati wa Yesu Waisraeli hao waliitwa "Wayahudi". Walio wengi waliishi nje ya nchi ya Israeli/Palestina, kutokana na vita vingi vya zamani vilivyosababisha wakimbizi kuhamia nchi zenye usalama zaidi. Jumuiya za Wayahudi zilipatikana katika miji yote mikubwa ya Afrika Kaskazini (hasa Misri na Libia), Ulaya Kusini na Asia Magharibi mpaka Uajemi. Kwa upande mmoja Wayahudi walitoka katika ukoo wa Ibrahimu, hasa waliokaa Israeli/Palestina. Lakini watu wengine wenye asili ya mataifa tofauti waliwahi kujiunga na imani ya Wayahudi na kuchukua hatua ya kuongoka na kutahiriwa. Katika mazingira yao Wayahudi walikuwa watu wa pekee waliomshuhudia Mungu mmoja tu. Walikuwa tofauti na wengine kwani hawakushiriki katika ibada ya miungu ya serikali, tena walitunza utaratibu wa sabato yaani kutotenda kazi siku ya saba. Mitume wa Yesu walizunguka awali hasa katika jumuiya za Wayahudi kila mahali walipokwenda. Mwanzoni Kanisa lilionekana kama dhehebu la Kiyahudi tu. Baada ya kupokea watu kutoka mataifa bila kuwatahiri hali ilibadilika: Kanisa likawa taifa la Mungu kutoka kwa Wayahudi na kwa Mataifa. Ujio wa Roho Mtakatifu Mara baada ya Yesu kwenda zake katika tukio linalotajwa kupaa kwake mbinguni, wafuasi wake wakarudi Yerusalemu, yapata mwendo wa sabato, na walipoingia huko, wakapanda ghorofani walipokuwa wakikaa Mtume Petro na wenzake. Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwapo wote mahali pamoja. Ukaja upepo toka juu kama upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukatokea na ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia. (Mdo 1:12-14, 2:1-4). Hii ilifuatiwa na Petro na wenzake kuanza kuhubiri ufufuko wa Bwana Yesu na hatimaye kugusa watu 3,000 waliokubali kubatizwa siku hiyo. (Mdo 2: 37-40). Ustawi wa jumuia ya kwanza ya wafuasi wa Kristo Watu walipokuwa wakidumu katika fundisho la mitume, sala, kumega mkate na katika ushirika, wengi wakaona ishara zao nyingi basi nao wakauza mali zao, na vitu walivyokuwanavyo, na kugawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Basi, siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakila pamoja na kushiriki kwa moyo mweupe. Hivyo ndivyo jumuia ilivyozaliwa na kufahamika kama Kanisa. (Mdo 2:42-47). Kukutanika na kushiriki mafumbo makuu, kushukuru na kusifu, pamoja na uwepo wa vipaji na karama za Roho Mtakatifu, hufanya Kanisa liwe hai. Uenezi wa awali wa Kanisa Ujumbe wa Yesu ulienea haraka toka Yerusalemu hata Lida, Yafa, Kaisaria, Samaria, Damasko n.k. na kuanzisha jumuia nyingi. Nazo jumuia kwa bidii za waamini wa mwanzo zikafika Foinike, Kipro, Antiokia, ambako waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza, kutokana na waamini wa mataifa mengine kuwazidi wale wenye asili ya Kiyahudi (Mdo 11:1-23). Imani na desturi za mikusanyiko hiyo zenye asili ya Kiyahudi zilitapakaa na hivyo kuanza kusuguana na mapokeo ya jamii mbalimbali zilipopenya. Hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi wa siku zile tayari walikuwa na imani zao walizokuwa wakizitunza. Basi ukaja wakati ambao Wakristo wakaanza kukosoana kuhusu dhamiri zao na huduma. Ndiyo asili ya nyaraka mbalimbali ambazo zinaunda sehemu muhimu wa Agano Jipya. Uongozi wa Kanisa Kila jumuiya inatumia mbinu zake za uongozi. Mkuu wa jumuiya ya wanafunzi tangu mwanzo ni Bwana Yesu. Lakini kama kundi ni kubwa kazi ya uongozi ni tofauti. Haiwezekani kufanya kila kitu pamoja watu wakiwa wengi. Ipo lazima ya kugawana kazi na madaraka. Suala hili limekuwa muhimu sana katika historia ya Ukristo. Njia mbalimbali za uongozi ambazo zilitafutwa na kujaribiwa zinaonyesha tofauti muhimu kati ya madhehebu mbalimbali. Kwa jumla njia hizo zote zinajaribu kuiga mifano ya ushirika wa kwanza inayopatikana katika Biblia. Vyeo na shughuli maalumu zilizopo katika Ukristo leo, vina asili na mwanzo katika ugawaji wa madaraka ulivyokuwa wakati wa mitume. Katika nyaraka za Paulo (ambazo ni maandiko ya kwanza katika Agano Jipya) tunaona hali ya Ukristo mwanzoni kabisa. Paulo anataja mitume, manabii, walimu, wenye vipawa mbalimbali (1Kor 12,28 n.k.), au maaskofu na mashemasi, pia wazee. Kwa jumla hakuna picha kamili ya utaratibu mmoja uliokuwepo kila mahali. Katika ushirika wa kwanza kule Yerusalemu Mitume, yaani marafiki wa Yesu wa karibu waliotumwa naye na kupewa kazi ya kueneza Habari Njema, ndio waliokuwa viongozi. Lakini baada ya muda mfupi kazi zilikuwa nyingi, hivyo wakaongeza "Wasaidizi saba". Hao saba walishughulikia hasa huduma za upendo, yaani kuwagawia wajane na wazee misaada. Baada ya Mtume Petro kuhama Yerusalemu, Yakobo Mdogo ndiye aliyeongoza ushirika huo. Mwishoni mwa karne ya 1 cheo cha "Askofu" kiliimarika sana, lakini pia vikundi vya Wakristo wenye vyeo maalumu vya utumishi vilianza kutokea. Pamoja na Askofu vyeo vya Kasisi na Shemasi vilikuwa kawaida. Mashemasi wa kike walipatikana pia mwanzoni, lakini walipotea baadaye, kutokana na utamaduni uliokazia kipaumbele cha wanaume. Kuanzia mwaka 100 hivi Kanisa likaitwa "katoliki" maana yake Kanisa moja kwa ajili ya nchi zote na watu wote, tofauti na vikundi vilivyojitenga nalo. Kila mji ulikuwa na askofu wake aliyeongoza kanisa. Maaskofu wa eneo au mkoa mmoja walikuwa chini ya Askofu Mkuu. Maaskofu wa Roma (Ulaya hadi Afrika Kaskazini-Magharibi), Aleksandria (Afrika) na Antiokia (Asia), waliheshimiwa kuliko maaskofu wengine wote wakaitwa "Papa" na "Patriarki". Cheo cha Patriarki kilipatikana pia kwa Askofu wa Bizanti (leo nchini Uturuki) baada ya makaisari wa Roma kuhamia kule, na vilevile kwa Askofu wa Yerusalemu. Katika karne za baadaye vikundi mbalimbali vilianza kupinga kuwapo kwa vyeo maalumu vya utumishi. Walisisitiza zaidi "ukuhani wa Wakristo wote" maana yake kila Mkristo hushiriki utumishi ulio mmoja tu katika Kanisa. Madhehebu mengine ya Kiprotestanti, yakikumbuka sana matatizo ya utaratibu wa kiaskofu wakati wa karne za kati, yaliona afadhali kuendelea bila cheo hicho. Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki pamoja na Wamoravian na Waanglikana wamehifadhi ngazi za kale yaani Uaskofu, Ukasisi na Ushemasi. Nchini Tanzania Walutheri pia Wabatisti wa aina ya A.I.C. wanaheshimu cheo cha Uaskofu. Lakini kimataifa sehemu kubwa ya Walutheri, na hasa Wapresbiteriani (Reformed) na Wabatisti hawana Askofu, wakisisitiza zaidi uwezo na haki ya kila Mkristo kushiriki katika shughuli zote za utumishi akichaguliwa. Imani ya Ukristo ni juu ya Yesu. Alikuja kwelikweli hapa duniani. Alichagua kuja katika nchi ile ya Israeli miaka 2000 iliyopita. Akawachagua wanafunzi wake ambao tunawaita "mitume". Hakika alikuwa na maana kufanya hivyo. Mitume ndio waliotekeleza maagizo ya Yesu, "Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyoamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dhahari" (Math 28:19-20). Biblia inatupa habari za aina hii: wale Mitume ni mifano ya Ukristo wetu katika nguvu au karama zao, lakini pia katika udhaifu wao. Petro Petro ni jina lenye maana ya "mwamba". Alikutana na Yesu akiwa mvuvi, akaendelea kuwa rafiki yake wa karibu sana. Yesu alipokamatwa, Petro alitaka kutumia upanga wake ili amtetee. Lakini alipoulizwa baadaye kama yeye ni rafiki wa Yesu aliogopa akasema hamjui. Katika ushirika wa Yerusalemu alikuwa kiongozi muhimu. Alikuwa Mtume wa kwanza kumpokea katika Kanisa watu wasio Wayahudi bila kudai watahiriwe kwanza. Baadaye akawa katika mji mkubwa wa Antiokia. Katika taarifa ya Luka tunamwona tena Yerusalemu alipokutana na Paulo na kushauriana juu ya kupokea Wapagani katika Ukristo. Agano Jipya ina nyaraka mbili zilizoandikwa kwa jina lake. Kumbukumbu ya kale inasema alifika mpaka Roma. Hapo aliuawa pamoja na Paulo katika mateso ya kwanza ya Wakristo chini ya serikali. Petro ni mfano mzuri wa nguvu na udhaifu katika maisha ya Kikristo. Alikuwa na moyo mkuu kumtetea Yesu kwa upanga asikamatwe - lakini mpaka siku ile hakuelewa kwamba njia ya Yesu si njia ya silaha. Alitaka kuwa karibu na Yesu - lakini kwa hofu akamkana. Alimwingiza katika Kanisa jemadari Mpagani - lakini baadaye akawaogopa waliosema kwamba Mpagani asiingie katika ushirika mpaka awe ametahiriwa na kuwa Myahudi kwanza. Mwishoni mwa maisha yake Petro akawa shahidi wa damu kwa Bwana wake kule Roma akafa msalabani kama Yesu. Kanisa la Roma linamkumbuka kama askofu wake wa kwanza. Kila Papa wa Kanisa Katoliki huitwa "mwandamizi wa Petro" kwani anashika cheo cha Askofu wa Roma kinachoaminika kuwa cha kwanza kati ya maaskofu wote duniani. Paulo Paulo hakuwa mfuasi wa Yesu alipokuwa duniani. Alikuwa Myahudi Farisayo mzaliwa wa Tarso (mji wa Kilikia, leo nchini Uturuki). Alikwenda Palestina kwa masomo ya kidini. Tunasikia habari zake alivyohusika na kifodini cha Stefano (Mdo 6). Baadaye akatumwa na Baraza Kuu la Kiyahudi kuwatafuta Wayahudi waliojiunga na Ukristo na kuwakamata kama wakosaji. Aliposafiri hadi Dameski (mji mkuu wa Siria) kwa ajili hiyo, Yesu alimtokea katika ono akaongoka kuwa Mkristo. Hivyo mtesaji wa Wakristo akawa mhubiri mkuu wa Injili. Hakuna mwingine kati ya mitume wote aliyesafiri, kuhubiri na kuanzisha shirika kama Paulo. Katika safari kubwa tatu alizunguka Asia Magharibi na Ulaya Kusini. Akaendelea kufundisha shirika alipoondoka kwa njia ya barua (au nyaraka). Nyaraka zake mbalimbali zimehifadhiwa katika Agano Jipya. Katika nyaraka hizo Paulo anaonekana kuwa mtaalamu wa Sheria ya Kiyahudi ilivyo katika Agano la Kale. Akatetea kupokea Wapagani katika Kanisa akafundisha jinsi gani uhuru katika Kristo unavyopita masharti ya sheria ya kale. Mwishoni akakamatwa kule Yerusalemu akashtakiwa ya kuwa amehatarisha amani. Kama mzaliwa wa Tarso alikuwa na uraia wa Roma akadai haki yake ya kukata rufaa kule, mbele ya Kaisari. Akapelekwa Roma (Mdo 28). Hatuna hakika juu ya kesi yake. Labda alipata nafasi ya kusafiri tena na kuhubiri Injili mpaka Hispania. Lakini kumbukumbu ya kale inatuambia kwamba aliuawa baada ya Petro kwa kukatwa kichwa katika mateso ya kwanza ya Wakristo (64-68 BK). Paulo ni mfano mzuri jinsi gani mtu aliyepinga Injili vikali aliongozwa kuihubiri. Nyaraka zake zinatuonyesha jinsi gani Mkristo anaweza kutumia akili yake pamoja na imani. Katika maandishi yake tunapata mtu aliyebebwa na imani katika matatizo na mateso makubwa. Anatufundisha kutoangalia Ukristo kama sheria au amri tu (Fanya! Acha!) bali kama jibu la upendo la mtu aliyeelewa upendo wa Mungu kwanza. Thoma Mtume anayekumbukwa sana kule India ni Thoma (au: Tomaso) aliyefika mpaka Bara Hindi. Kaburi lake huonyeshwa katika mji wa Madras. Mpaka leo wako "Wakristo wa Thoma" kusini-magharibi mwa Bara Hindi. Kwa muda mrefu walikosa mawasiliano na Wakristo wengine waliokuwa mbali, lakini siku hizi wanashiriki katika umoja wa Kanisa duniani. Muhtasari wa historia ya Kanisa Ukristo ulianza Mashariki ya Kati kama madhehebu ya Uyahudi ukaenea haraka kwa watu wa mataifa mengine mengi ya Asia, Afrika na Ulaya hivi kwamba waamini wenye asili ya Kiyahudi walizidi kuwa asilimia ndogo hasa kufikia mwisho wa karne ya 1. Kwa juhudi za Mitume waliowahi kuchaguliwa na Yesu na za wengineo, hasa Mtume Paulo. Ukristo ulienea hasa ndani ya mipaka ya Dola la Roma na kupokea yaliyo mema kutoka umataduni hasa wa Wagiriki (mashariki) na Walatini (magharibi), bila kukwamishwa na dhuluma za serikali zilizodumu kwa kwikwi miaka karibu 250 (64-313). Hata nje ya dola hilo, Ukristo ulikabiliana na dhuluma, kama vile Mesopotamia na Uajemi, ambapo ulidumisha zaidi sura asili ya Kisemiti. Wakati wa maisha ya Mitume, dhuluma zilizotabiriwa na Yesu zilianza kutoka kwa Wayahudi wasiomuamini na kutoka kwa watu wengine. Wa kwanza kuuawa alikuwa Stefano, na kati ya Mitume Yakobo Mkubwa. Kabla ya kufa, wengi kwa kuuawa, mitume waliweka waandamizi wao, ambao kati yao maaskofu mwanzoni mwa karne ya 2 walikuwa wameshika uongozi wa makanisa wakisaidiwa na mapadri na mashemasi. Wakati huohuo vitabu vingi vya Kikristo vilivyotungwa katika nusu ya pili ya karne ya 1 vilizidi kuenea na kukusanywa hadi vikaunda Agano Jipya. Baada ya hapo vitabu viliendelea kuandikwa kwa kutetea, kutangaza na kufafanua imani sahihi: ndiyo mwanzo wa teolojia kama fani maalumu. Tofauti za ufafanuzi huo, kama zile kati ya shule ya Aleksandria na shule ya Antiokia, ndizo chanzo cha mabishano yaliyochangia mafarakano makubwa yaliyotokea hasa katika karne ya 5, ingawa kuanzia mwaka 325 mitaguso mikuu ilikusanya maaskofu wengi kutoka sehemu mbalimbali ili kumaliza migogoro. Tofauti za lugha na utamaduni, pamoja na utaifa, zilichangia sana mafarakano. Maendeleo mengine muhimu yalipatikana katika maisha ya Kiroho kwa uanzishaji wa umonaki wa Kikristo, kwanza katika majangwa ya Misri, halafu sehemu nyingine zote. Juhudi za watu hao zilichochea waumini wenzao pia kuwa waaminifu katika ulimwengu uliozidi kuwashawishi badala ya kuwatesa. Ni kwamba kufikia mwisho wa karne ya 4 Ukristo ulikuwa dini rasmi ya Dola la Roma ambalo kabla ya hapo kwa miaka karibu 250 (64-313) lilikuwa limeukataza kikatili. Kabla yake Armenia ilikuwa nchi ya kwanza kupokea Ukristo kama dini ya taifa (301). Ushindi huo ulifanya wengi watamani vyeo ndani ya Kanisa, kwa kuwa viliendana sasa na heshima na mali: hivyo ubora ulipungua. Dola la Roma Magharibi lilipozidi kudhoofiwa na uvamizi wa Wagermanik na makabila mengine yasiyostaarabika, askofu wa Roma kama mchungaji mkuu alilazimika kuwajibika ili kuokoa jahazi. Ndivyo walivyofanya hasa Papa Leo I na Papa Gregori I. Kwa juhudi za wamonaki Wabenedikto na wengineo, ustaarabu wa kale uliokolewa katika vitabu vyake na uinjilishaji uliendelea katika Ulaya ya Kati. Kumbe, uenezi wa Uislamu kuanzia karne ya 7 ulidhoofisha na pengine kukomesha kabisa Ukristo katika nchi nyingi, ukirudisha nyuma ustawi wa Kanisa lote. Hata hivyo, mwanzoni mwa karne ya 8, Uislamu ulizuiwa na Wafaranki kuenea zaidi Ulaya bara. Kabila hilo kubwa la Kigermanik liliwahi kujiunga na Kanisa Katoliki likawa msaada mkubwa kwa Mapapa. Isipokuwa kwa kuwaachia watawale Italia ya Kati, walisababisha Papa aanze kuwa kama mfalme wa dunia hii, jambo lililoathiri sana majukumu yake ya kiroho hadi mwaka 1870. Katika Karne za Kati Ulaya yote ilikwisha kuwa ya Kikristo. Kutoka huko ulienea, pamoja na ustaarabu wa magharibi ulioathiriwa sana na Ukristo, katika Amerika yote na sehemu nyingine za dunia. Mafarakano makuu kati ya Wakristo Katika historia ndefu ya Ukristo, yalitokea mafarakano mengi, waamini wa Yesu wakizidi kutofautiana. Makundi makubwa zaidi ni: Kanisa Katoliki, Makanisa ya Waorthodoksi na ya Waorthodoksi wa Mashariki na madhehebu ya Uprotestanti. Hasa tangu mwaka 1910 madhehebu mengi yanashiriki juhudi za ekumeni kwa ajili ya kurudisha umoja wa awali. Wakatoliki Zaidi ya nusu ya Wakristo wote wanashikamana katika imani na sakramenti chini ya maaskofu wenye ushirika kamili na yule wa Roma, ambaye kwa kawaida anaitwa Papa. Kati yao umoja unazingatiwa sana kama sifa ya kwanza ya Kanisa inayotambulisha wanafunzi wa Yesu. Neno "Katoliki" tunaendelea kulitumia zaidi kwa maana ya madhehebu maalumu yenye wafuasi wengi duniani. Kiteolojia linamaanisha "Kanisa lililopo popote, lililo moja tu kila mahali na kila wakati". Kwa maana hiyo kila Mkristo yumo katika Ukatoliki, kwani mbele ya Kristo Kanisa ni moja tu, kila mahali duniani. Waanglikana, Walutheri, Wamoravia na wengineo huamini kabisa kwamba wenyewe ni sehemu ya Kanisa lile moja la Bwana Yesu lililopo mahali popote. Upande mwingine, hata Kanisa “Katoliki" linaloongozwa na Askofu (Papa) wa Roma ni la "Kiinjili" kwani linakubali na kutangaza Injili (= “habari njema”) ya Yesu Kristo. Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki Wakristo wengi walioishi upande wa mashariki wa Dola la Kirumi na ng'ambo ya mipaka yake ya mashariki walitengana na Wakatoliki hasa katika karne V (Waorthodoksi wa Mashariki) na karne XI (Waorthodoksi). Hata hivyo msimamo wao wa imani si tofauti sana, kwa kuwa wanachanga mapokeo ya awali ya Kanisa la Mitume na la Mababu. Waprotestanti Utitiri wa madhehebu ya Waprotestanti ndio wenye tofauti kubwa zaidi kati yao wenyewe na kati yao na Wakristo waliotajwa kwanza. Hiyo ilitokana na msimamo wa msingi wa urekebisho wa Kiprotestanti wa kutaka kila mmoja aweze kutafsiri Biblia alivyoielewa, bila kutegemea mapokeo wala mamlaka rasmi ya Kanisa, ila msaada wa Roho Mtakatifu. Umoja halisi wa Kanisa unaweza kupatikana tu katika ukweli wa Injili ya Yesu Kristo. Ni habari mbaya kwamba katika karne ya 16 kuupigania ukweli huo kulivunja umoja wa Ukristo wa magharibi. Haiwezekani kushangilia mafarakano ya wafuasi wa Yesu. Yale ya karne hiyo yalitokana na kuelewa tofauti kweli za imani ya Kikristo na yalikuwa na ukali kwa sababu pande zote zilisadiki kwamba kushikilia kwa usahihi ufunuo wa Mungu ni suala la wokovu wa milele. Kwa mfano, Martin Luther aliandika,«Sikubali mafundisho yangu yahukumiwe na yeyote, hata kama ni malaika. Asiyekubali mafundisho yangu hawezi kufikia wokovu». Pamoja na hayo, mambo mengi yalichangia farakano, si teolojia tu, bali siasa, uchumi, jamii na utamaduni. Wakati huo mara nyingi hoja za imani na malengo ya kisiasa vilichanganyikana: wanasiasa wengi walitumia hoja hizo ili kufikia malengo ya kiutawala, na vilevile wanateolojia walitumia siasa kutetea mafundisho yao ili kuvuta watu. Ndiyo sababu Luther alichorwa kama shujaa wa taifa la Ujerumani. Mara nyingi pande zote zilipotosha maana ya wapinzani na kuwachora vibaya wakivunja amri ya nane inayokataza uongo dhidi ya jirani. Hata waliojitahidi kusema ukweli tu juu ya wengine kwa kawaida hawakujitahidi vya kutosha kuelewa msimamo wao na kuona kwamba pengine si mbaya zaidi. Kila mmoja alitaka ushindi akachangia ugomvi uliorithishwa kwa vizazi vilivyofuata. Hivyo, kilichosababisha zaidi farakano si masuala ya imani yaliyojadiliwa na Waprotestanti, bali lawama zao dhidi ya hali mbaya ya Kanisa la wakati huo iliyokuwa inakera wengi na kuwaelekeza kuunga mkono urekebisho. Hapo kale neno hilo (kwa Kilatini reformatio) lilihusu badiliko la hali mbaya iliyopo ili kurudia hali nzuri zaidi ya awali. Katika Karne za Kati lilitumika mara nyingi kwa marekebisho ya umonaki. Katika karne ya 15 haja ya urekebisho ilionekana wazi si tu kwa mashirika ya kitawa bali kwa Kanisa lote. Hasa Mtaguso wa Konstanz (1414-1418) ulidai kabisa ufanyike «katika kichwa na katika viungo». Lakini kwa jumla mitaguso yote ya Karne za Kati na mikutano mingi ya Bunge la Dola la Ujerumani ililenga urekebisho wa Kanisa. Kwa kweli Karne za Kati zilikuwa na mchanganyiko wa mambo yaliyopingana: ibada za nje tu na za dhati kabisa; teolojia iliyoelekeza kutenda kwa msingi wa nipe nikupe na hakika ya kwamba binadamu anategemea kabisa neema ya Mungu; kutojali wajibu hata upande wa viongozi wa Kanisa na marekebisho safi ya mashirika ya kitawa. Karne ya 15 ilikuwa kipindi cha umotomoto wa pekee katika Kanisa, ambapo walei wengi zaidi na zaidi walipata elimu nzuri, hivyo walitamani hotuba bora na mafundisho ya kuwasaidia kuishi Kikristo zaidi. Luther aliitikia haja hizo zilizomgusa sana kama mtu wa wakati wake. Luther alitumia kwa nadra neno urekebisho, lakini likaja kuwa jina la kawaida la matukio yale mengi ya miaka 1517 - 1555, yaani kuanzia uenezi wa hoja 95 za Martin Luther hadi amani ya Augsburg. Kati yake chanzo, yaani mabishano ya Kikanisa yaliyosababishwa na teolojia ya Luther, yalichanganyikana mapema na siasa, uchumi na utamaduni, kutokana na hali halisi ya wakati huo, mbali kuliko mwenyewe alivyofikiri. Viongozi mbalimbali wakaiga mfano wa Luther, ila juhudi zao zikatofautiana: ndio mwanzo wa madhehebu mengine yanayoitwa ya "Kiinjili". Jina hilo linataka kusisitiza kwamba yanasimama kwenye msingi wa Injili tu, kinyume cha Kanisa Katoliki lililoona mapokeo yake kuwa na umuhimu pamoja na Biblia. Kumbe wafuasi wa Luther na wengineo waliitwa na Wakatoliki "Waprotestanti", maana yake "wapinzani" (to protest = kupinga): neno hilo lilianza kutumika tangu wafuasi wa Luther walipopinga azimio la bunge lililotaka Wajerumani wote warudi chini ya Papa wa Roma. Tangu mwaka 1907 tapo la Wapentekoste limeenea duniani kote (linakadiriwa kuwa na waumini milioni karibu 300) na kuathiri hata madhehebu yote ya zamani (ambapo mara nyingi waumini wa aina hiyo wanaitwa "Wakarismatiki"). Kanisa leo Kwa miaka 100 ya mwisho asilimia za Wakristo kati ya watu wote zimebaki 33, yaani mmoja kwa watatu, lakini uwiano kati ya mabara umebadilika sana, kwa maana katika Afrika, Asia na nchi nyingine zinazoendelea Wakristo wameongezeka, kumbe Ulaya na Amerika Kaskazini wamepunguaPew Research Center inakadiria kwamba mwaka 2050, watazidi bilioni tatu.. Wakati huo Wakatoliki na Waprotestanti huenda wakalingana kwa idadi. Kuhusu maeneo ambako Wakristo wanapungua, ni kwamba, kutokana na historia ya Kanisa kuwa na mchanganyiko wa mazuri na mabaya, wengine wanahisi kuwa halina maana tena. Pia kuna makundi kama Wakomunisti na Wamasoni ambayo yanakusudia kabisa kufuta Ukristo kwa kutangaza kasoro za waumini na viongozi wao, pamoja na kuhimiza watu kwenda kinyume cha maadili. Hali hii inajionyesha hasa pale ambapo waamini wengi, hasa Ulaya, wameacha kwenda kanisani isipokuwa siku ya Krismasi na Pasaka au kwenye harusi na misiba. Pia kutokana na mgawanyiko wa madhehebu, kumekuwa na mkanganyiko kuhusu kazi ambazo zinalipasa Kanisa la leo. Sala na ibada Mafundisho ya Yesu kuhusu sala hayatii maanani taratibu maalumu. Badala yake yeye alisisitiza msimamo wa ndani wa kumuendea Mungu kwa imani na unyofu kama vitoto wanavyohusiana na baba zao. Ndivyo mwenyewe alivyosali katika Roho Mtakatifu aliyewaahidia wafuasi atawaongoza badala yake. Kwa msingi huo, katika historia ya Kanisa namna nyingi za kusali zimetokea kwa maisha ya Kiroho ya Mkristo binafsi na kwa jumuia nzima pamoja. Kwa kawaida, taratibu za kuendesha ibada zinaitwa liturujia (kutoka maneno ya Kigiriki yenye maana ya “kazi ya hadhara”). Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Waanglikana, Wamethodisti, Walutheri na wengineo wanafuatilia desturi kama walivyozipokea. Mtiririko wa ibada zao huandikwa na hujulikana kama Liturujia. Madhehebu mengine, hasa yale ya Kipentekoste, huwa na ibada ambazo hazijaandikwa kitabuni: kiongozi wa ibada wa siku hiyo huja na madondoo yake na mtiririko wa ibada huenda kama "Roho" atakavyoongoza siku hiyo. Kwa sababu hiyo husema kwamba hawafuati desturi au mapokeo. Ukiangalia zaidi utaona kuwa ibada zao pia huwa na mtindo na mtiririko fulani, kama vile kuimba mapambio ya harakaharaka wakiwa wanapiga makofi, kucheza na kurukaruka. Mapambio hayo hufuatiliwa na mengine ya taratibu wakiinua mikono kuabudu. Inawezekana kusema hao nao wana utaratibu au liturujia yao ingawa haijaandikwa kwenye vitabu. Wakristo wanahesabu ufufuko wa Yesu kuwa msingi mkuu wa imani yao (1Kor 15:14): ndiyo sababu karibu wote wanaabudu hasa Jumapili, ambayo ndiyo siku ya tukio hilo kuu la historia yote. Ila asilimia 1 inashika Sabato, iliyo siku ya wiki ambapo Wayahudi hupumzika na kuabudu. Haki na amani Upande mwingine wanakanisa wanajaribu kuonyesha jitihada zao katika jamii, ikiwa ni pamoja na kuleta amani na maendeleo na kutoa misaada ya kijamii. Kuna uwezekano kwa madhehebu kadhaa kubadilisha mkazo wao kuutoa kwenye imani tu na kuuweka kwenye huduma za jamii au elimu: hii inafanya yaonekane kama moja ya mashirika ya hisani. Katika nchi nyingi Kanisa limekuwa nguvu ya kutetea haki za binadamu. Tumesikia habari za Desmond Tutu kule Afrika Kusini au za Janani Luwum katika Uganda, jinsi walivyojaribu kutetea haki za wananchi dhidi ya utawala mbaya. Ikiwa Wakristo wanajisikia wito wa kusimama na kusema mbele ya wakubwa hukumbuka manabii wa Agano la Kale hadi Yohane Mbatizaji. Wanakumbuka pia Wakristo wengi katika historia walioweza kusimama mbele ya wafalme na kutetea haki za watu. Labda tunamkumbuka Askofu Ambrosi wa Milano (aliyemvuta kijana Agostino kuwa Mkristo) alivyomtenga Kaisari na Kanisa kwa sababu ya uuaji wa wananchi wengi wasio na kosa uliofanywa na wanajeshi wa serikali. Msingi wake ni katika mafundisho juu ya kazi ya uumbaji. Mbele ya Mungu tuko sawa: kuna msingi gani kuona wengine ni sawa zaidi? Lakini si Wakristo wote wanakubali na kufurahia msimamo wa aina hiyo. Wengine huona imani ya Kikristo haihusiki na taratibu za dunia hii au huona ni wajibu wa Mkristo kutii serikali yoyote wakikumbuka maneno ya Mtume Paulo katika Rum 13. Pamoja na hayo katika Ukristo yapo mapokeo ya kutoshindana na wenye mamlaka bali kuwavumilia katika yote. Labda huona hofu ya kuwa dini inaingizwa mno katika siasa. Binadamu wa karne ya 21 wanahitaji jibu litakalosaidia kuwakwamua kutoka matatizo yao. Wenye dini mbalimbali, hususan Wakristo, wanadai kujua ufumbuzi wa matatizo makuu ya binadamu, ingawa wachache tu wameweza kuonyesha dhahiri matatizo yaliyotatuliwa kabisa kwa dini. Wakati mwingine wanadini wenyewe wamekuwa chanzo cha matatizo badala ya kuyatatua. Jibu linaweza kupatikana katika maneno ya Yesu mwenyewe, aliposema kwamba wafuasi wake ni chumvi ya dunia, ambayo ilete ladha katika maisha ya watu, lakini kama chumvi hiyo inapoteza ladha yake, haifai kitu, isipokuwa kutupwa na kukanyagwa kwa dharau. Hivyo changamoto ya Wakristo ni kufuata vema mafundisho ya imani yao ili kukidhi hitaji la nyakati hizi la kuishi kwa amani, furaha na upendo duniani kote . Uhusiano na dini nyingine Ukristo na dini nyingine zinahusiana kwa kiasi tofauti, kadiri ya mazingira asili, historia, mafundisho kuhusu imani na maadili, desturi, ibada n.k. Ukristo na Uyahudi Ni wazi kuwa Ukristo unahusiana zaidi na dini ya Uyahudi, kwa sababu unatokana nayo na kutumia vitabu vyake vitakatifu (Tanakh na pengine Deuterokanoni pia). Haiwezekani kumuelewa Yesu kwa kumweka nje ya mazingira ya Kiyahudi. Dini hizo mbili zilitengana moja kwa moja miaka 50 hivi baada ya Yesu kuaga dunia. Ni kwamba Wayahudi wa shule ya Jabneh (mwaka 80 hivi B.K.) waliamua kuwatenga kama wazushi wananchi wenzao waliomuamini Yesu Kristo, hasa baada ya kuona hawakusaidia vita vya ukombozi dhidi ya wakoloni Warumi vilivyosababisha maangamizi ya Hekalu la pili na mji wa Yerusalemu mwaka 70 B.K. Tangu hapo Wakristo hawakushiriki tena ibada pamoja na Wayahudi, wakazidi kuzingatia sakramenti ya Kumega Mkate katika Siku ya Bwana (Jumapili, siku inaposadikika Yesu alifufuka) badala ya Sabato (Jumamosi, siku ya pumziko ya Wayahudi). Kabla ya hapo Wakristo wa Kiyahudi walikuwa wanashika siku zote mbili. Ukristo na Ubuddha Hakuna uhusiano wa kihistoria kati ya Yesu na Ubuddha. Hata hivyo mambo kadhaa yanafanana. Yesu alifundisha kuhusu nidhamu mbili zinazompelekea mtu kuwa mwadilifu na hatimaye kuurithi utukufu wa kiroho ambao karama yake ni uzima wa milele: hizo ni kumpenda Mungu kwa moyo wako wote na kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote, na jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Buddha alifundisha hali ya kutodhuru viumbe hai wowote, tena kuwa na moyo mkuu wa mapenzi kwa vitu vyote. Hii ni miongozo inayolenga mtu atambue tabu anazodumisha yeye mwenyewe, kwa matendo yake na upeo ulio na mipaka, katika maisha yake ya kila siku. Baada ya hili, mafundisho ya Kristo yanatofautiana katika kuchukulia hali hii. Kwa mujibu wa Kristo, dhambi, matendo yenye kukosea kanuni za kiroho na hata za kimaumbile, hufutwa na toba; wakati katika mafundisho ya Buddha, makosa yote yanatokana na kutokuwa makini. Hivyo, kwa mujibu wa Buddha, njia pekee ya kumkomboa mtu na shida zake ni kufuata mwongozo wa Nguzo Nane ambazo humweka katika hali ya kuweza kuamka kiroho wakati utulivu wa kimwili na wa kiakili unapofikiwa. Haya ndiyo yanayofanya Ubuddha kuwa ni njia inayojali sana nidhamu ya mtu kimatendo, wakati Ukristo hufuata sana moyo wenye kukiri makosa, na kutafuta uadilifu wa kweli wa kiroho. Huu ni uzuri wa pekee kutoka kwenye mafundisho ya Yesu: Tubuni kwa kuwa saa ya ukombozi ni sasa... Jingine lenye tofauti ni kuwa Kristo hufundisha kuhusu Upendo kwamba ni Mungu, kwa kuwa Upendo una maana kuliko elimu yote ya binadamu, nao ndio unaounganisha na kutunza vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Hilo hutambulika kupitia Kristo ambaye hujidhihirisha kwa yule mwenye kumpokea Roho wa Mungu. Upande wa Buddha, hukanusha nafsi na pia Mungu, akisema: Ni Buddha mwenye ufahamu wa milele, tena hana nafsi isipokuwa Utupu; na ni wenye furaha isiyo kifani izidiyo yote yenye kufanyika ulimwenguni, yaani Nirvana; kila mtu ni Buddha aliyesahau asili yake ya ndani kabisa. Ukristo na Uislamu Ukristo na Uislamu vinafanana zaidi kwa sababu Muhammad alifahamu Wayahudi na Wakristo wengi katika nchi yake na katika safari zake. Dini hizo tatu zinajulikana kwa kushika imani katika Mungu Pekee, muumba wa vitu vyote, na kwa kumchukua Abrahamu kama kielelezo cha imani na rafiki wa Mungu. Mafundisho ya msingi ya Uislamu ni unyenyekevu kwa Mola mmoja aitwaye Allah , mwingi wa rehema na mwingi wa fadhila; nguzo ya Uislamu ni kumuabudu. Katika Uislamu, unyenyekevu wa mtu katika kumcha Mola kwa ibada na swala humpa kukirimika na kuhifadhika kwa Mola wake mwenye fadhila, ambaye atamtunuku haki yake. Naye mnyenyekevu kwa Mola ataishi kuona utukufu mwingi wa Mola wenye kutajwa katika Kurani kwa majina 99 ya Allah. Kati ya sifa na utukufu huo ulio na majina mengi, baadhi yake ni Al Rahman (kwa Kiarabu, "Mwenye rehema"), Al Nur ("Mwenye nuru") n.k. Hayo hufanana na neno la Nuru ya Bwana, rehema na ukombozi kuwa utukufu wa Mbingu katika mwongozo wa Kikristo. Pia Uislamu unafundisha udugu miongoni mwa Waislamu yaani mzizi wa neno linalotumika sana katika Kurani: Waly (Wala, Wilayat, Mawla, Awla) katika kueleza jinsi Mwislamu apasavyo kuishi karibu na mwenzake. Nalo husisitiza upendo na kulindana kwa heri na pia kuepushana na shari. Hilo linafanana na upendo ambao katika Ukristo ndio adili kuu kuliko yote: Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo... mimi si kitu kabisa. (1 Wakorintho 13:1-11). Lakini katika Ukristo upendo hauna mipaka wala masharti. Unatakiwa kuenea kwa maadui pia na kusamehe kila mara kufuatana na mfano wa Baba wa Mbinguni. Mwislamu kadiri ya wingi wa unyenyekevu na usafi wa moyo wake huakisi sifa za Mola wake. Uislamu hufundisha kuhusu vita vya ndani ambavyo muumini hupigana na nafsi yake yenye matamanio ya chini, ambayo huzaa chuki, dhuluma, wivu na maovu mengine ili kuishinda kwa utukufu wa Mola na kudumisha dini (mwongozo) yake katika ngazi zote za maisha. Kabla yake Yesu alihimiza wote wafuate mfano wake wa upole na unyenyekevu wa moyo, akitoa kielelezo katika Heri Nane za hotuba ya mlimani. Tofauti ya msingi ni kuwa kwa mujibu wa Kristo, ni kwa neema ya imani katika Neno la Uzima kwamba mtu hukombolewa kutoka matamanio yake ya kibinadamu, mbali ya kwamba anapaswa kujitahidi asije akapotewa na neema hiyo na kurudia utumwa wa dhambi. Ni imani ya Wakristo na ya Waislamu kwamba Yesu atarudi duniani kwa utukufu, ingawa jambo hilo wanalitafsiri kwa namna tofauti. Uhusiano wa Wakristo na Waislamu una umuhimu wa pekee kwa ajili ya amani na maendeleo ya nchi. Katika sehemu mbalimbali Wakristo na Waislamu waliwahi kushirikiana vema katika mambo mengi ya kijamii lakini uhusiano huo umeanza kuwa mgumu. Sababu moja ni mzigo wa historia tunaoubeba mara nyingi bila kujua. Mzigo huo ni urithi wa mahusiano magumu kati ya Waislamu na Wakristo kule Ulaya na Asia. Itakuwa muhimu sana kwa vijana wa leo kukataa mzigo wa historia na kuvumiliana. Kwa mfano, Waislamu wanaweza kutumia neno "jihadi" wakiongea juu ya jitihada za kuimarisha jumuiya yao au kueneza imani yao, lakini Wakristo walio wengi wanasikia neno hilo vibaya kwa sababu "vita vitakatifu" vya Waislamu vilivyoitwa "jihadi" vilileta mateso mengi kwa Wakristo katika nchi mbalimbali. Kumbe neno halimaanishi vita hasa ila liliwahi kutumika hivyo tangu muda mrefu. Vilevile Wakristo wengi hawaoni tatizo kutumia neno "Crusade" kwa ajili ya mikutano ya kiroho. Lakini Waislamu wanaweza kuchukua neno hili vibaya pia kwani kiasili "Crusade" (maana yake "Vita vya Msalaba") linamaanisha hasa kipindi cha miaka 800 hivi iliyopita. Wakati ule Wakristo wa Ulaya Magharibi walijaribu kufuta utawala wa Kiislamu katika nchi za Mashariki ya Kati kwa vita vilivyoendelea kwa kwikwi muda wa miaka 200. Ukristo na Uislamu viko karibu katika mambo mengi lakini hutumia mafundisho yanayogongana katika sehemu nyingine, hivyo mpaka leo hii kwa Waislamu ni vigumu sana kupokea Injili. Wakati wa vita vya msalaba Fransisko wa Asizi aliona hakuna njia ya kuwavuta Waislamu kwa mabavu. Mashindano pekee yanayoruhusiwa kwa Mkristo ni yale ya upendo ya kumfuata Yesu. Kwa jumla mawazo ya Mt. Fransisko yamethibitishwa na historia. Kwa hiyo si vibaya kujiandaa kushirikiana na Waislamu Kikristo kwa kufahamu kidogo imani yao na kutambua sifa nzuri zilizopo katika maisha na mafundisho yao pia. Wakristo kwa jumla wasijivunie sifa zao kuwa bora kuliko za Waislamu. Anayesoma "Historia ya Kanisa" ataona mifano mingi ya jinsi Wakristo walivyosahau mafundisho ya Yesu na kutendeana kwa unyama. Kwa hiyo mtu asijivune kwamba Ukristo ni dini ya upendo au imani yenye maendeleo kama mwenyewe si mfano wa upendo huo na maendeleo hayo. Kwa Wakristo wengi ni fumbo kwa nini Mungu alikubali kutokea kwa dini hiyo mpya. Lakini mwanzoni mwa Uislamu Mfalme Mkristo wa Ethiopia alipokea na kuhifadhi wakimbizi Waislamu kutoka Maka. Mapokeo ya Kiislamu yanasema mfalme huyu aliyekuwa na jina "Negasi" aligeukia Uislamu baadaye. Lakini "Negasi" si jina la mtu fulani, ni cheo cha wafalme wote wa Ethiopia hadi mwaka 1974 (kwa kawaida huandikwa "Negus"). Halafu hakuna kumbukumbu ya kwamba mfalme yeyote wa karne zile aliacha Ukristo wake. Ukristo na dini za jadi Kuhusu wanaofuata bado imani asilia pia ni kwamba wanatunza katika mila na desturi zao urithi wa utamaduni. Hata maadili mengine yanayofundishwa kwao yanalingana na sehemu za Biblia. Hakika si vema Wakristo wakiwacheka na kuwaita kwa majina ya dharau kama "Wapagani". Hata juu ya imani hizo za jadi ni kweli kwamba zilimjua Mungu kwa namna fulani kutokana na uumbaji wake jinsi alivyoandika Mtume Paulo katika Rom 1. Tazama pia Ukristo barani Afrika Ukristo barani Amerika Ukristo barani Asia Ukristo barani Australia Ukristo barani Ulaya Tanbihi Marejeo Albright, William F. From the Stone Age to Christianity. Alexander, T. Desmond. New Dictionary of Biblical Theology. Bahnsen, Greg. A Reformed Confession Regarding Hermeneutics (article 6)] . Ball, Bryan; Johnsson, William (ed.). The Essential Jesus. Pacific Press (2002). ISBN 0-8163-1929-4. Barrett, David; Kurian, Tom and others. (ed.). World Christian Encyclopedia. Oxford University Press (2001). Barry, John F. One Faith, One Lord: A Study of Basic Catholic Belief. William H. Sadlier (2001). ISBN 0-8215-2207-8 Benton, John. Is Christianity True? Darlington, Eng.: Evangelical Press (1988). ISBN 0-85234-260-8 Bettenson, Henry (ed.). Documents of the Christian Church. Oxford University Press (1943). Bokenkotter, Thomas. A Concise History of the Catholic Church . Doubleday (2004). ISBN 0-385-50584-1 Bruce, F.F. The Canon of Scripture. Chambers, Mortimer; Crew, Herlihy, Rabb, Woloch. The Western Experience. Volume II: The Early Modern Period. Alfred A. Knopf (1974). ISBN 0-394-31734-3. Coffey, John. Persecution and Toleration in Protestant England 1558–1689. Pearson Education (2000). Cross, F. L.; Livingstone, E. A. (ed.). The Oxford Dictionary of the Christian Church. Oxford University Press (1997). ISBN 0-19-211655-X. Deppermann, Klaus. Melchior Hoffman: Social Unrest and Apocalyptic Vision in the Age of Reformation. ISBN 0-567-08654-2. Dilasser, Maurice. The Symbols of the Church. Collegeville, MN: Liturgical Press (1999). ISBN 0-8146-2538-X Duffy, Eamon. Saints and Sinners, a History of the Popes. Yale University Press (1997). ISBN 0-300-07332-1 Elwell, Walter A.; Comfort, Philip Wesley. Tyndale Bible Dictionary, Tyndale House Publishers (2001). ISBN 0-8423-7089-7. Esler, Philip F. The Early Christian World. Routledge (2004). Farrar, F.W. [http://www.tentmaker.org/books/mercyandjudgment/mercy_and_judgment_ch1.html Mercy and Judgment. A Few Last Words On Christian Eschatology With Reference to Dr. Pusey's, "What Is Of Faith?". Macmillan, London/New York (1904). Ferguson, Sinclair; Wright, David, eds. New Dictionary of Theology. consulting ed. Packer, James. Leicester: Inter-Varsity Press (1988). ISBN 0-85110-636-6 Foutz, Scott. Martin Luther and Scripture] Martin Luther and Scripture. Fowler, Jeaneane D. World Religions: An Introduction for Students, Sussex Academic Press (1997). ISBN 1-898723-48-6. Fuller, Reginald H. The Foundations of New Testament Christology Scribners (1965). ISBN 0-684-15532-X. Froehle, Bryan; Gautier, Mary, Global Catholicism, Portrait of a World Church, Orbis books; Center for Applied Research in the Apostolate, Georgetown University (2003) ISBN=1-57075-375-X Funk, Robert. The Acts of Jesus: What Did Jesus Really Do?. Polebridge Press (1998). ISBN 0-06-062978-9. Glenny, W. Edward. Typology: A Summary Of The Present Evangelical Discussion. Gonzalez, Justo L. The Story of Christianity: The Early Church to the Dawn of the Reformation, Harper Collins Publishers, New York (1984). Hanegraaff, Hank. Resurrection: The Capstone in the Arch of Christianity. Thomas Nelson (2000). ISBN 0-8499-1643-7. Harnack, Adolf von. [http://www.ccel.org/ccel/harnack/dogma1.ii.iii.iii.html History of Dogma (1894). Hickman, Hoyt L. and others. Handbook of the Christian Year. Abingdon Press (1986). ISBN 0-687-16575-X Hinnells, John R. The Routledge Companion to the Study of Religion (2005). Hitchcock, Susan Tyler. Geography of Religion. National Geographic Society (2004) ISBN 0-7922-7313-3 Kelly, J.N.D. Early Christian Doctrines. Kelly, J.N.D. The Athanasian Creed. Harper & Row, New York (1964). Kirsch, Jonathan. God Against the Gods. Kreeft, Peter. Catholic Christianity. Ignatius Press (2001) ISBN 0-89870-798-6 Letham, Robert. The Holy Trinity in Scripture, History, Theology, and Worship. P & R Publishing (2005). ISBN 0-87552-000-6. Lorenzen, Thorwald. Resurrection, Discipleship, Justice: Affirming the Resurrection Jesus Christ Today. Smyth & Helwys (2003). ISBN 1-57312-399-4. McLaughlin, R. Emmet, Caspar Schwenckfeld, reluctant radical: his life to 1540, New Haven: Yale University Press (1986). ISBN 0-300-03367-2. MacCulloch, Diarmaid, The Reformation: A History. Viking Adult (2004). MacCulloch, Diarmaid, A History of Christianity: The First Three Thousand Years. London, Allen Lane. 2009. ISBN 978-0-7139-9869-6 Marber, Peter. Money Changes Everything: How Global Prosperity Is Reshaping Our Needs, Values and Lifestyles. FT Press (2003). ISBN 0-13-065480-9 Marthaler, Berard. Introducing the Catechism of the Catholic Church, Traditional Themes and Contemporary Issues. Paulist Press (1994). ISBN 0-8091-3495-0 Mathison, Keith. The Shape of Sola Scriptura (2001). McClintock, John, Cyclopaedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature. Harper &Brothers, original from Harvard University (1889) McGrath, Alister E. Christianity: An Introduction. Blackwell Publishing (2006). ISBN 1-4051-0899-1. McGrath, Alister E. Historical Theology. McManners, John. Oxford Illustrated History of Christianity. Oxford University Press (1990). ISBN 0-19-822928-3. Meconi, David Vincent. "Pagan Monotheism in Late Antiquity", in: Journal of Early Christian Studies. Metzger, Bruce M., Michael Coogan (ed.). Oxford Companion to the Bible. Oxford University Press (1993). ISBN 0-19-504645-5. Mullin, Robert Bruce. A short world history of Christianity. Westminster John Knox Press (2008). Norman, Edward. The Roman Catholic Church, An Illustrated History. University of California (2007) ISBN 978-0-520-25251-6 Olson, Roger E., The Mosaic of Christian Belief. InterVarsity Press (2002). ISBN 978-0-8308-2695-7. Orlandis, Jose, A Short History of the Catholic Church. Scepter Publishers (1993) ISBN 1-85182-125-2 Ott, Ludwig. Grundriß der Dogmatik. Herder, Freiburg (1965). Otten, Herman J. Baal or God? Liberalism or Christianity, Fantasy vs. Truth: Beliefs and Practices of the Churches of the World Today.... Second ed. New Haven, Mo.: Lutheran News, 1988. Pelikan, Jaroslav; Hotchkiss, Valerie (ed.) Creeds and Confessions of Faith in the Christian Tradition. Yale University Press (2003). ISBN 0-300-09389-6. Putnam, Robert D. Democracies in Flux: The Evolution of Social Capital in Contemporary Society. Oxford University Press (2002). Riley-Smith, Jonathan. The Oxford History of the Crusades. New York: Oxford University Press, (1999). Robinson, George. Essential Judaism: A Complete Guide to Beliefs, Customs and Rituals. New York: Pocket Books (2000). Schama, Simon . A History of Britain. Hyperion (2000). ISBN 0-7868-6675-6. Servetus, Michael. Restoration of Christianity. Lewiston, New York: Edwin Mellen Press (2007). Simon, Edith. Great Ages of Man: The Reformation. Time-Life Books (1966). ISBN 0-662-27820-8. Smith, J.Z. (1998). Spitz, Lewis. The Protestant Reformation. Concordia Publishing House (2003). ISBN 0-570-03320-9. Sproul, R.C. Knowing Scripture. Spurgeon, Charles. A Defense of Calvinism . Sykes, Stephen; Booty, John; Knight, Jonathan. The Study of Anglicanism. Augsburg Fortress Publishers (1998). ISBN 0-8006-3151-X. Ustorf, Werner. "A missiological postscript", in: McLeod, Hugh; Ustorf, Werner (ed.). The Decline of Christendom in Western Europe, 1750–2000. Cambridge University Press (2003). Walsh, Chad. Campus Gods on Trial. Rev. and enl. ed. New York: Macmillan Co., 1962, t.p. 1964. xiv, [4], 154 p. Woodhead, Linda. An Introduction to Christianity. Marejeo mengine MacCulloch, Diarmaid. Christianity: The First Three Thousand Years (Viking; 2010) 1,161 pages; survey by leading historian Roper, J.C., Bp. (1923), et al.. Faith in God, in series, Layman's Library of Practical Religion, Church of England in Canada, vol. 2. Toronto, Ont.: Musson Book Co. N.B.: The series statement is given in the more extended form which appears on the book's front cover. Viungo vya nje "Christianity". Encyclopædia Britannica Online. A number of introductory articles on Christianity. The origin of Christianity Adena, L. The 'Jesus Cult' and the Roman State in the Third Century , Clio History Journal, 2008. Dini Yesu Kristo
921
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kiingereza ni lugha ya jamii ya Kigermanik cha Magharibi iliyokua nchini Uingereza kwa muda wa miaka 1,400. Leo, zaidi ya wasemaji milioni mia nne duniani wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya kwanza. Watu wengi zaidi wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya pili, kwa sababu ni muhimu sana kwenye nyanja za mawasiliano, sayansi na uchumi wa kimataifa. Historia ya Kiingereza Mwanzo wa lugha Lugha ya Kiingereza ilianzia huko Uingereza kutokana na kuingiliana kwa lugha mbalimbali, hasa lugha za kale za Ujerumani, Denmark na Ufaransa. Sehemu ya kusini ya kisiwa cha Britania ilikuwa ndani ya Dola la Roma hadi mwanzo wa karne ya 5. Wenyeji walitumia lugha ya Kikelti pamoja na Kilatini cha Waroma, hasa mjini. Uvamizi wa Waanglia-Saksoni: kuja kwa Kigermanik Baada ya Waroma makabila kutoka Ujerumani ya kaskazini na Denmark walianza kuvamia kisiwa hicho. Katika mwendo wa karne mbili waliteka sehemu kubwa ya Uingereza ya leo isipokuwa sehemu za magharibi kama vile Cornwall na Wales na sehemu za kaskazini walipoishi Waskoti. Wavamizi walileta lugha zao za Kisaksoni na Kianglia (Ujerumani ya Kaskazini) zilizounganika kuwa lugha ya Kiingereza cha Kale ambacho kilikuwa karibu sana na Kijerumani cha Kale. Inaonekana ya kwamba wenyeji Wakelti walio wengi walianza polepole kutumia lugha ya watawala wapya, wengine waliuawa au walihamia sehemu zisizo chini ya Waanglia-Saksoni. Lugha hii iliathiriwa mara mbili. Kwanza Wadenmark ndio waliojaribu kujenga ufalme wao kisiwani. Waliteka sehemu za Uingereza ya Magharibi. Kiasi cha maneno kutoka lugha yao kimeingia Kiingereza cha kale kama Wales. Uvamizi wa Wanormandy: kuja kwa Kifaransa, lugha mbili kando Mwaka 1066 jeshi la Wanormani kutoka Ufaransa ya Kaskazini walivamia na kuteka Uingereza. Wanormani walikuwa wa asili ya Skandinavia lakini walikuwa wameshaanza kutumia lugha ya Kifaransa cha kale. Wanajeshi hao walikuwa mabwana wapya wa Uingereza wakitumia Kifaransa chao. Kwa karne kadhaa lugha mbili zilitumika kandokando: Kiingereza cha Kianglia-Saksoni cha watu wa kawaida na kile Kifaransa cha Kinormandy cha tabaka la watawala. Kwa jumla watawala walianza kutumia lugha ya raia lakini lugha hii ilibadilika pia kwa kupokea maneno mengi kutoka Kifaransa. Kuna makadirio ya kwamba zaidi ya theluthi moja ya maneno yote ya Kiingereza yana asili ya Kifaransa. Kuingiliana kwa lugha zote mbili: Kiingereza cha Kati Kipindi hiki cha kuingiliana kati ya Kifaransa cha mabwana na lugha ya kawaida kilileta Kiingereza cha Kati. Hadi leo asili ya maneno kutoka Kijerumani na Kifaransa ni wazi kabisa. Mfano mzuri ni maneno tofauti kwa wanyama kadhaa na nyama yao: ng'ombe huitwa "cow" (sawa na Kijerumani wa Kaskazini "Kau") lakini nyama yake ni "beef" (kutokana na neno la Kifaransa kwa ng'ombe "boeuf"); vilevile "sheep" kwa mnyama kondoo na "mutton" kwa nyama yake (Kijerumani ya Kaskazini: "Schaap" - Kifaransa: "mutton"), vilevile swine=mnyama – pork=nyama (nguruwe) na calf=mnyama – veal=nyama (ndama). Wakulima wafugaji walitumia lugha yao kwa mnyama - mabwana wasiogusa mnyama lakini hula nyama yake waliendelea kutumia neno la Kifaransa kwa ajili ya mnyama yuleyule. Maneno yote mawili yaliingia katika Kiingereza cha Kisasa lakini kwa mambo mawili tofauti. Kiingereza cha Kisasa Kiingereza cha Kisasa kimeanza na tafsiri ya Biblia ya William Tyndale; baadaye na washairi muhimu kama William Shakespeare. Teknolojia ya uchapaji vitabu ilisambaza lugha hii nchini kote na kupunguza athira ya lahaja mbalimbali. Wakati ule Kiingereza kilipokea pia maneno mengi kutoka lugha za Kilatini na Kigiriki zilizokuwa lugha za taaluma na sayansi hadi karne ya 18 kote Ulaya. Kiingereza cha Kisasa kimeendelea kurahisisha lugha. Lakini urekebisho wa tahajia umeshindikana hadi leo hata kama kulikuwa na majaribio mbalimbali. Kutokana na historia yake Kiingereza kimebaki na tahajia isiyolingana na matamshi ya maneno. Mwandishi George Bernhard Shaw alionyesha tatizo hilo kwa pendekezo la dhihaka kwamba neno "fish" (samaki) liandikwe "ghoti": gh kama sauti ya "f" katika "cough", o kama sauti ya "i" katika "women", na ti kama sauti ya "sh" katika "nation". Pamoja na hayo, lahaja za Kiingereza zinazidi kutofautiana, zile muhimu zaidi zikiwa zile za Britania na Marekani. Uenezi wa Kiingereza duniani Pamoja na Dola la Uingereza na makoloni yake, lugha ilienea duniani kati ya karne ya 17 na 19. Tangu karne ya 19 idadi kubwa ya wasemaji wa Kiingereza hawaishi tena Uingerezea bali Marekani. Katika karne ileile Kiingereza kilikuwa lugha ya utawala katika maeneo makubwa ya makoloni ya Dola la Uingereza. Baada ya makoloni kuwa nchi huru mara nyingi Kiingereza kimeendelea kuwa lugha rasmi za nchi hizo. Kutokana na matukio hayo yote, na Marekani kujitokeza katikati ya karne ya 20 kama nchi tawala kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia, Kiingereza kimekuwa leo lugha ya kwanza ya mawasiliano duniani hata kama si lugha yenye wasemaji wengi wa lugha ya kwanza. Pia aina nyingi za Krioli na Pijini zimetokana na Kiingereza na kudumu hadi leo. Kiingereza ni lugha rasmi pekee katika nchi za Uingereza, Marekani, Australia, Nyuzilandi, Jamaica, na nchi nyingine. Kiingereza ni lugha rasmi pamoja na lugha nyingine katika nchi nyingi, kwa mfano Kanada (pamoja na Kifaransa), India (pamoja na Kihindi na lugha za majimbo), Ireland (pamoja na Kigaelik), Philippines (pamoja na Kitagalog). Kwa jumla ni lugha rasmi katika nchi karibu 60, mbali ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Kiingereza barani Afrika Nchi nyingi za Afrika zinatumia Kiingereza kama lugha rasmi, lakini ni Waafrika wachache (isipokuwa Waafrika Kusini) wanaoitaja kuwa lugha ya kwanza kwao. Nchi hizo ni Afrika Kusini, Eswatini, Ghana, Kamerun, Kenya, Lesotho, Liberia, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, Zambia na Zimbabwe. Kiingereza kinazumgumzwa pia katika nchi nyingine za Afrika ambapo si lugha rasmi. Lugha nyingi za Afrika zimekopa maneno ya Kiingereza. Maneno hayo yamerekebishwa kulingana na sauti ya lugha nyingine, kwa mfano: Kiingereza: train --> Kiswahili: treni. Marejeo Viungo vya nje makala za OLAC kuhusu Kiingereza lugha ya Kiingereza katika Glottolog (en) Muhtasari kuhusu Kiingereza kwenye Ethnologue Kamusi Hai ya Kiingereza - Kiswahili - Kiingereza (en) More than 20000 English words recorded by a native speaker (en) Re-Romanization of English Kiingereza Lugha za Kigermanik Lugha za Ulaya Lugha za Uingereza Lugha za Marekani Lugha za Kanada Lugha za Australia Lugha za New Zealand Lugha za Eire Lugha za Uhindi Lugha za Afrika Kusini Lugha za Malta Lugha za Jamaika Lugha za Ghana Lugha za Lesotho Lugha za Liberia Lugha za Kamerun Lugha za Ufilipino Lugha za Kenya Lugha za Nigeria Lugha za Sierra Leone Lugha za Uswazi Lugha za Zambia Lugha za Zimbabwe
923
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara kubwa pekee zaidi ya Afrika. Jina Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale. kwa jina hilo Waroma wa Kale walitaja eneo katika Tunisia ya leo, hawakumaanisha bara lote. Inasemekana asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile,lakini kuna pia maelezo mengine tofautitofauti. Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteranea, upande wa magharibi wa Misri. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua). Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara zima. Jina la "Afrika" limekuwa la kawaida kuanzia karne ya 16 BK. Jiografia Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wa kaskazini mashariki na bara la Asia kwenye rasi ya Sinai . Upande wa kaskazini iko Bahari ya Mediteranea, upande wa mashariki kuna Bahari Hindi pamoja na Bahari ya Shamu na upande wa magharibi iko Bahari Atlantiki. Kuna kisiwa kikubwa cha Madagaska na funguvisiwa mbalimbali. Barani kuna nchi huru 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee na madola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa. Kuna umbali wa kilomita 8,000 kutoka Ras ben Sakka nchini Tunisia (37°21' N, sehemu ya kaskazini kabisa) hadi rasi ya Cape Agulhas nchini Afrika Kusini (34°51'15" S, sehemu ya kusini kabisa). Umbali ni km 7,400 kutoka upande wa magharibi (rasi ya Cape Verde, 17°33'22" W) hadi mashariki (Ras Hafun nchini Somalia, 51°27'52" E). Pwani yote ya Afrika ina urefu wa kilomita 26,000. Nchi kubwa ya Afrika ni Algeria na nchi ndogo ni funguvisiwa la Shelisheli katika Bahari Hindi. Nchi ndogo Afrika bara ni Gambia. Kijiolojia Afrika iko kwenye bamba la Afrika. Lile bamba la gandunia la Afrika linaenea mbali zaidi kuliko maeneo tunayotazama kuwa Afrika kijiografia, ni pamoja na maeneo chini ya bahari linapopakana na mabamba ya Ulaya-Asia, Uarabuni, Uhindi na Australia, Antaktika, Amerika ya Kusini na Kaskazini. Upande wa mashariki wa bamba la Afrika kuna ufa unaozidi kupanuka ikielekea kujitenga kutoka Afrika kama bamba la Somalia. Tabianchi Tabianchi ya Afrika ni pana, kuanzia kanda za tropiki hadi kufikia maeneo ya nusu-aktiki (baridi) kwenye ncha za milima mirefu. Nusu ya kaskazini ya bara ni jangwa au angalau yabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo ya savanna na kanda za msitu wa mvua. Afrika ni bara lenye joto kuliko mabara yote na asilimia 60 za uso wake ni maeneo yabisi au jangwa. Nchi za Afrika Wakazi Wataalamu wengi wanakubaliana kutambua Afrika kama asili ya binadamu wote walioko duniani. Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipita bilioni 1. Ni kwamba idadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita, ikipiku zile za Ulaya na Amerika. Ilhali mwaka 1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka 1990 na milioni 1200 mnamo 2014. Hivyo asilimia ya watoto na vijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi ya nusu ya wananchi wako chini ya umri wa miaka 25. Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote; mwaka 2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4. Lugha Zaidi ya lugha elfu za Kiafrika zinazungumzwa barani leo, ingawa nyingi zinazidi kufifia. Kusini mwa Afrika, Afrika Mashariki na ya Kati watu wengi ni wasemaji wa lugha za Kibantu (kwa mfano Kiswahili). Asili yao ilikuwa pande za kusini za kanda ya Sahel na kutoka kule walienea katika sehemu nyingi za Afrika upande wa kusini kwa Sahara. Kuna pia vikundi vya wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara waliofika hadi Afrika ya Mashariki. Wakazi asilia siku hizi wako wachache, wakionekana kama wasemaji wa lugha za Khoisan au za Wabilikimo. Watu wa Afrika Magharibi husema zaidi Lugha za Kiniger-Kongo hasa zisizo za Kibantu, pamoja na wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara. Watu wa Afrika ya Kaskazini kiasili walikuwa hasa wa makundi matatu: Waberber upande wa magharibi Wamisri upande wa mashariki wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara Waarabu waliovamia eneo hilo lote tangu karne ya 7 BK wameleta lugha yao pamoja na dini ya Uislamu. Lugha yao imekuwa lugha ya watu wengi siku hizi. Wasemaji wa Kiberber bado wako wengi kidogo Moroko na Algeria na wachache katika sehemu za Tunisia na Libya. Kutokana na ukoloni, lugha za Kihindi-Kiulaya zinazumgumzwa pia, hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Kiafrikaans ni lugha ya pekee ya Afrika Kusini yenye asili ya Ulaya. Katika kisiwa cha Madagaska kwenye Bahari ya Hindi, inatumika lugha ya Kimalagasy, ambayo ni kati ya lugha za Austronesia. Dini Waafrika wana imani za dini nyingi tofauti, lakini takwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwa serikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vile Nigeria, Ethiopia na Tanzania. Kadiri ya World Book Encyclopedia, Islam ndiyo inayoongoza, ikifuatwa na Ukristo. Kumbe kadiri ya Encyclopedia Britannica, 45% za wakazi ni Wakristo, 40% ni Waislamu na 10% wanafuata dini asilia za Kiafrika. Wachache tu ni Wahindu, Wabuddha, Wabaha'i au hawana dini yoyote. Tazama pia Historia ya Afrika Orodha ya milima ya Afrika Mito mirefu ya Afrika Maziwa ya Afrika Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Tanbihi Marejeo Moore, Clark D., and Ann Dunbar (1968). Africa Yesterday and Today, in series, The George School Readings on Developing Lands. New York: Praeger Publishers. Naipaul, V. S.. The Masque of Africa: Glimpses of African Belief. Picador, 2010. ISBN 978-0-330-47205-0 Besenyő, János. Western Sahara (2009), free online PDF book, Publikon Publishers, Pécs, ISBN 978-963-88332-0-4, 2009 Wade, Lizzie. Drones and satellites spot lost civilizations in unlikely places, Science (American Association for the Advancement of Science), DOI: 10.1126/science.aaa7864, 2015 Petringa, Maria. Brazza, A Life for Africa, 2006. ISBN 978-1-4259-1198-0. Viungo vya nje History of Africa Marco Notari, for Africa African & Middle Eastern Reading Room from the United States Library of Congress Africa South of the Sahara from Stanford University The Index on Africa from The Norwegian Council for Africa Aluka Digital library of scholarly resources from and about Africa Africa Interactive Map from the United States Army Africa Historia African Kingdoms The Story of Africa from BBC World Service Africa Policy Information Center (APIC) Habari allAfrica.com current news, events and statistics Focus on Africa magazine from BBC World Service Bara
1163
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kuki
Kuki
Kuki ni tafsiri ya muda ya neno la Kiingereza cookie, ambalo maana yake asili ni biskuti au keki ndogo, lakini katika utarakilishi linatumika ili kompyuta yenye kurasa za tovuti iweze kuwasaliana na watazamaji. Programu za tovuti hizi zinahifadhi habari kadhaa za mtazamaji au mtumiaji (k.m. jina la mtumiaji, neno la siri, ruhusa, mapendekezo) kwenye kompyuta ya mtazamaji mwenyewe. Hivi mtazamaji anatambuliwa kila wakati anaingia kwenye tovuti hii. Marejeo Viungo vya Nje Orodha ya maneno ya tarakishi ya mradi wa Kilinux kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Intaneti
1165
https://sw.wikipedia.org/wiki/Panzi
Panzi
Panzi ni aina za wadudu wanaokula mimea. Wameainishwa katika nusuoda Caelifera ya oda Orthoptera. Takriban spishi zote huchupa mbali kwa kutumia miguu yao ya nyuma ambayo ina nguvu sana. Nyingi zinaweza kuruka angani. Panzi wana vipapasio vifupi kuliko mwili wao. Panzi wakubwa ambao wanajikusanya kwenye makundi makubwa huitwa nzige. Kuna panzi wakubwa wengine wenye miiba mikubwa kwenye miguu ya nyuma lakini wasiojikusanya katika makundi. Panzi hao hufanana na ndege wadogo wakiruka juu na huitwa parare. Panzi majike wana vali mwichoni kwa fumbatio zinazowawezesha kuchimba ndani ya ardhi na kutaga mayai yao katika vibumba. Vibumba vya mayai huweza kuwa na mayai kumi na tano hadi zaidi ya mia moja. Mayai ya spishi nyingi za panzi huingia kwa diaposi kupitia majira ya baridi au kiangazi. Hali ya hewa ikiwa nzuri mayai yaendelea kupevuka halafu tunutu wanatoka. Tunutu (panzi wachanga bila mabawa) hubambua ngozi yao mara tano hadi mara saba kufuatana na spishi. Kila hatua ya ukuaji ni ndefu kuliko ile iliyotangulia. Wakati wa ubambuaji wa mwisho panzi wenye mabawa anatoka na kuwa mpevu ndani ya siku au wiki chache. Kuna wadudu ambao wanafanana na panzi lakini wana vipapasio virefu kuliko mwili wao. Hawa ni wana wa nusuoda Ensifera. Spishi moja kati yao anaitwa senene na huliwa na watu. Jike ana mrija wa kutaga unaofanana na kitara. Anataga mayai juu ya au ndani ya mimea. Panzi huliwa sehemu nyingi duniani kwa sababu wana virutubishi vya (protini) vingi. Wanajeshi huambiwa wakamate panzi na kuwala wakipungukiwa chakula. Mwainisho Kuna familia nyingi za panzi, lakini takriban spishi zote za Afrika ya Mashariki ni wanafamilia wa Acrididae na Pyrgomorphidae. Mwainisho wa sikuhizi ni kama ufuatao (familia zote hazionyeshwi): Nusuoda Caelifera Oda ya chini Tridactylidea Familia ya juu Tridactyloidea (panzi wachimbaji Familia Cylindrachetidae Familia Ripipterygidae Familia Tridactylidae Oda ya chini Acrididea Familia ya juu Tetrigoidea Familia Tetrigidae Kundi la familia za juu Acridomorpha Familia ya juu Acridoidea Familia Acrididae (panzi wa kawaida, parare na nzige) Familia Dericorythidae Familia Lathiceridae Familia Lentulidae Familia Lithidiidae Familia Ommexechidae Familia Pamphagidae (panzi-chura) Familia Pamphagodidae Familia Pyrgacrididae Familia Romaleidae Familia Tristiridae Familia ya juu Eumastacoidea (panzi-njiti, panzi-kima, panzi-jani) Familia Chorotypidae Familia Episactidae Familia Eumastacidae Familia Euschmidtiidae Familia Mastacideidae Familia Morabidae Familia Thericleidae (panzi vibete) Familia ya juu Pneumoroidea Familia Pneumoridae Familia ya juu Proscopioidea (vijiti warukaji) Familia Proscopiidae Familia ya juu Pyrgomorphoidea (panzi wa rangi nyingi) Familia Pyrgomorphidae (ngeda n.k.) Familia ya juu Tanaoceroidea Familia Tanaoceridae Familia ya juu Trigonopterygoidea Familia Trigonopterygidae Familia Xyronotidae Familia na nusufamilia za Afrika ya Mashariki Acrididae Acridinae Calliptaminae Catantopinae Coptacrinae Cyrtacanthacridinae Euryphyminae Eyprepocnemidinae Gomphocerinae Hemiacridinae Oedipodinae Oxyinae Spathosterninae Teratodinae Tropidopolinae Dericorythidae Dericorythinae Euschmidtiidae Euschmidtiinae Pseudoschmidtiinae Stenoschmidtiinae Lentulidae Lentulinae Pamphagidae Porthetinae Pneumoridae Pyrgomorphidae Orthacridinae Pyrgomorphinae Thericleidae Afromastacinae Chromothericleinae Plagiotriptinae Thericleinae Picha Panzi na jamaa Wanyama wa Biblia
1166
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nzige
Nzige
Nzige ni jamii ya panzi wenye uwezo wa kujikusanya kwenye makundi makubwa na kuruka umbali mrefu kwa pamoja. Wanao huitwa tunutu. Nzige wanapokuwa wametawanyika mmojammoja huishi kama panzi wa kawaida. Wanapozaliana na kuongezeka idadi hujikusanya katika makundi. Makundi ya tunutu husafiri kuelekea upande mmoja na kula majani wanakopitia. Makundi ya nzige waliokomaa huweza kufikia idadi ya zaidi ya bilioni na huruka umbali mrefu na kuharibu mazao wanakotua. Udhibiti wa nzige Nzige hudhibitiwa kwa dawa za kikemikali. Ni vema nzige wadhibitiwe wanapokuwa wadogo au tunutu kabla hawajaingia mashamba na kuharibu mazao. Tunutu wanaweza kudhibitiwa kwa mashine zinazobebwa mikononi au mgongoni, au zilizopachikwa juu ya gari la pickup. Makundi ya nzige waliokomaa ni lazima yadhibitiwe kwa ndege. Hivi karibuni dawa ya kibiolojia imeendelezwa na mradi wa kimataifa LUBILOSA. Dawa hiyo ina spora za kuvu Metarhizium acridum ndani yake. Siku hizi kuna vifundiro vya kibiashara vitatu sokoni: "Green Muscle" na "Green Guard" vya kampuni BASF na "NOVACRID" cha kampuni ÉLÉPHANT VERT. Vifundiro hivi vinaweza kupulizwa katika mafuta ya diseli kwa mashine za kiwango kidogo sana (g 50 katika L 0.5-2 kwa ha). Katika Biblia Nzige wanatajwa mara nyingi katika Biblia kati ya vitisho vikubwa kwa binadamu kutokana na njaa wanayoweza kusababisha. Pia wanatajwa kama chakula maalumu cha Yohane Mbatizaji, mtangulizi wa Yesu. Spishi za Afrika Anacridium aegyptium, Nzige-miti wa Misri (Egyptian Locust) Anacridium melanorhodon Anacridium m. melanorhodon, Nzige-miti wa Saheli (Sahelian Tree Locust) Anacridium m. arabafrum, Nzige-miti Arabu (Arabian Tree Locust) Anacridium wernerellum, Nzige-miti Mabawa-meusi (Sudanian Tree Locust) Dociostaurus maroccanus, Nzige wa Maroko (Moroccan Locust) Locusta migratoria, Nzige Msafiri (Migratory Locust) Locusta m. migratorioides, Nzige Msafiri wa Afrika (African Migratory Locust) Locusta m. capito, Nzige Msafiri wa Madagaska (Malagasy Migratory Locust) Locustana pardalina, Nzige Kahawia (Brown Locust) Nomadacris septemfasciata Nzige Mwekundu (Red Locust) Schistocerca gregaria, Nzige-jangwa (Desert Locust) Spishi za mabara mengine Austracris guttulosa (Spur-throated locust) Calliptamus italicus (Italian locust) Ceracris kiangsu (Yellow-spined bamboo locust) Chortoicetes terminifera (Australian plague locust) Locusta migratoria (Migratory locust) Locusta m. manilensis (Oriental migratory locust) Locusta m. migratoria (Asiatic migratory locust) Patanga succincta (Bombay locust) Rhammatocerus schistocercoides (Mato Grosso locust) Schistocerca cancellata (South American locust) Schistocerca piceifrons (Central American locust) Picha Panzi na jamaa Wanyama wa Biblia
1169
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Muhammad (kwa Kiarabu "Mwenye kusifika sana"; jina kamili kwa kirefu ni محمد بن عبد الله بن عبد ﺍﻟﻤﻄﻠﺐ ﺍﻟﻬﺎﺷﻤﻲ Muhammad bin 'Abd Allāh bin 'Abd al-Muţţalib al-Hāshimī) anaaminika katika dini ya Uislamu kuwa ni mtume wa mwisho wa Mungu (Allah) kwa binadamu. Utoto wake Muhammad alizaliwa yatima kwani baba yake alifariki kabla yeye hajazaliwa. Hakuishi sana na mama yake (Amina), kwa kuwa naye alifariki dunia Muhammad akiwa na umri wa miaka sita. Baadaye akachukuliwa na babu yake Abdul Muttalib na kuishi naye kwa muda wa miaka miwili, kisha babu yake naye akafariki. Kazi ya kumlea Muhammad ilimwangukia ami yake Abu Talib ambaye ndiye aliyeishi naye mpaka ukubwa na kumuoza na kumpa himaya wakati alipoanza kazi ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu. Kadiri ya hadithi za Kiislamu, ilipokua karibu atadhihiri Mtume mapadri wa Kinasara na makuhani wa Kiyahudi waliokuwa wakikaa Bara Arabu walikuwa wakiwatahayarisha majirani wao wa Kiarabu waliokuwa wakiabudu sanamu, wakiwaambia: “Karibu ataletwa Mtume katika nchi yenu hii, abatilishe hii ibada yenu mbovu ya sanamu”. Walipoambiwa hivi wale Waarabu waliwauliza jina la Mtume huyo, wakawajibu kuwa jina lake litakuwa Muhammad. Kwa hivyo kila mwenye kusadiki hayo alimwita mwanawe Muhammad. Lakini hayakusikilizana majina haya ila kwa baadhi ya Waarabu waliokua wakikaa Shamu tu na Najran (Yaman) ambako mapadri wengi walikaa, na vilevile katika Madina ambayo nusu ya wakazi wake walikuwa Wayahudi. Hata lilipoanza kutangaa jina la Mtume, waliokuwa wamekwisha kuitwa kwa jina hilo walikuwa wachache tu Bara Arabu nzima. Inasemekana Mtume aliinukia tangu utotoni kwake juu ya sifa zake nzuri na ukomavu wa akili ya kiutu uzima, hakupata kufanya vitendo vya utoto umri wake, wala kuazimia kuvifanya ila mara mbili tu, ambazo mara mbili zote hizo Mwenyezi Mungu alimhifadhi navyo. Kitendo chenyewe alichokiazimia kukifanya mara mbili zote hizo na Mwenyezi Mungu akamhifadhi nacho ni kutaka kwenda kukesha katika ngoma za arusi mbili za marafiki wake waliooa katika mji wa Makka. Lakini Mungu alimpa usingizi mkubwa katika masiku yote hayo mawili hata hakuweza kufumbua jicho, wala kunyanyua miguu kwenda mahali. Hajapata kuhudhuria hata mara moja katika ibada za kuabudu sanamu wala kula chakula kilichochinjwa kwa ajili yao. Moyo wake ulichukizwa na hayo na mambo mengine yaliyo mabaya. Tangu udogo wake Mtume aliondokea na sifa nzuri ambazo hapana hata mmoja katika hirimu zake aliyekuwa nazo zote. Kila sifa zinazohesabiwa kuwa ni njema na Waislamu ndizo alizokuwa nazo tangu utoto wake. Mkewe Aisha alipoombwa kutaja kidogo sifa za Mtume, alisema hivi: “Sifa zake ni zile sifa nzuri zinazosifiwa na Qurani” na katika Qurani zimetajwa chungu ya sifa zilizo nzuri. Mtume mara nyingi alikuwa akisema: “Sikupata kufanya hata siku moja yale mambo waliyokuwa wakiyafanya makafiri”. Kwa hivyo yeye hakupata kuabudu sanamu, kulewa, kuzini, kucheza kamari wala hakumdhulumu mtu kitu chake na kama haya. Lakini alikuwa msemakweli, mwaminifu, mpole na mwenye haya na sifa nyingi nyinginezo bora kama hizi. Watu wa Makka walikuwa wakimsifu kwa tabia zake, hata wakampa jina la Muhammad Al-Amin (mwaminifu). Alikuwa hatajikani ila kwa jina la Al-Amin. Wakubwa na wadogo walikuwa wakimheshimu na kumpa amana zao kuwawekea, hata baada ya utume. Hali yake kabla ya kupewa utume Makureshi ni watu wa biashara, kila Kureshi alipata kufanya kazi hii. Safari moja baadhi yao walipokuwa wakienda Yaman katika biashara zao, baba yake mdogo wa pili Bwana Zubeyr alimshauri ikiwa atapenda kusafiri. Mtume aliridhia akenda naye mpaka Yaman, wakakaa huko muda wa siku tatu tu kisha wakarejea, wakati huu Mtume alikuwa mtoto wa miaka tisa. Hata alipotimia miaka 12 mwaka 582, alisafiri tena pamoja na baba yake mdogo mwingine, Bwana Abu Talib; safari hii waliazimia kwenda Shamu, lakini walipofika Busra – mji wa kusini kabisa katika nchi ya Shamu – walikutana na padri jina lake Bahyra ambaye alimkataza asisogee na mwanawe zaidi kuliko hapo, akamwambia: “Mtoto huyu namwona ana alama zote za Mtume aliyetabiriwa kuwa atakuja, basi naona ni hatari kubwa akienda Shamu, asije akauawa na Wayahudi huko. Nakusihi sana urejee naye, au umpe mtu mwaminifu arejee naye, nawe uende katika biashara zako”. Abu Talib alimpa mtu arejee naye Makka naye akaendelea na safari yake. Huyu padri Bahyra alikuwa mwanachuoni wa Kinasara, na alimbashiri Mtume lakini hakuwahi kumwamini alipoanza utume, ila mwanafunzi wake Salman Al-Farsy Mwajemi mara alipopata habari ya kupata utume wake alisilimu, na aliusaidia Uislamu katika mambo mengi. Baada ya kutimia miaka 15 Mtume aliingia katika kufanya biashara ndogondogo yeye na mwenziwe Saib bin Yazid, lakini biashara yao walikuwa wakiifanyia katika miji iliyokuwa karibu na Makka tu. Alipata sifa kubwa ya uaminifu na ukweli katika biashara zake hizi. Mshirika wake huyu alisilimu siku ilipotekwa Makka, na Mtume alifurahi sana kwa kusilimu rafiki yake huyu. Kuanza utume Muhammad hakuwa akihudhuria sikukuu za Wapagani tangu kufahamu kwake. Alikuwa akipenda kukaa peke yake. Kufanya haya kulikuwa kukimwonjesha raha kubwa kuliko kutoka mbele za watu akaona yale mambo yao mabaya aliyokuwa akiyachukia. Kila usiku ukicha alikuwa akizidi kuyachukia. Lakini alikuwa hajui la kufanya. Hata alipotimiza miaka 38 hakuweza tena kustahimili kuona zile ibada za sanamu na tabia mbovu walizokuwa nazo wenziwe, ilivyokuwa hana la kufanya katika kuzizuia, alifanya shauri kuuacha mji wa Makka na kwenda porini kukaa. Akapata pango zuri katika Jabal Hira Kaskazini ya Makka, inapata maili 3 toka huko Makka. Akawa akikaa huko kwenye Jabal Hira kwa muda wa wiki nyingi, kisha hurejea Makka kuja kumtazama mkewe, wanawe na jamaa zake wengine, na vile vile kwa ajili ya kuchukua chakula kinapokuwa kimekwisha. Wakati mwingine akikaa siku nyingi sana huko porini hata humpasa mkewe Khadija kwenda kumsikiliza na mara nyingine alikuwa akifuatana naye, pamoja na watoto wao. Alidumu katika hali hii muda wa miaka miwili na kitu. Baadaye alisimulia kuwa katika mwezi wa Ramadhani 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 unusu wa umri wake alimuona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumuona wapi katokea, akamwambia: “Soma”. Mtume akamjibu: “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujizunza”. Akaja, akamkamata, akambana, akamwambia tena: “Soma”. Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tatu akamwambia: “Soma – Iqraa Bismi Rabbik - ” akamsomea sura ya 96 mpaka kati yake, kisha Mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qurani, ingawa haijawekwa mwanzo. Mara yule mtu (malaika) akaondoka machoni pake asimwone kaenda wapi, naye akarejea kwake hofu imemshika. Alipofika nyumbani, Khadija alidhani ana homa, akamfunika nguo gubigubi akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka. Homa ilipomwachia alimweleza Khadija yote yaliyomtokea, naye akamtuliza moyo wake, akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara Bibi huyu akaondoka akaenda kwa jamaa yake Waraqa bin Naufal akampa habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite, na Mtume akaenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia: “Huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe ni Mtume wa Umma huu! Nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako, Inshaalla nitakuwa mkono wako wa kulia!”. Wakarejea kwao hofu yote imemtoka Baada ya kuazimia kuwa hatakwenda tena kule pangoni. Pale pale akaondoka akenda pangoni mwake ili aonane na malaika tena, ingawa alikaa huko muda mrefu. Siku ile ya kupata Utume inawafiki mwezi wa Desemba 610. Huyu Waraqa hakuwa akiabudu dini ya sanamu bali alikuwa Mkristo, alipokuwa akisoma vitabu aliona kutatokea Mtume mwingine, ndiyo maana alipohadithiwa habari ile mara moja akaamini kuwa aliyemjia Mtume ni Jibril. Maisha yake Makka Muhammad aliishi Makka kwa muda wa miaka 53, arubaini (40) katika hiyo akiwa ni mtu wa kawaida kabla ya kupewa utume, na 13 akiwa ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Maisha yake Makka yalikuwa ya taabu tangu utotoni mwake, kwani alizaliwa yatima kisha alipokuwa katika ujana wake alikuwa akifanya kazi ya kuchunga mbuzi na kondoo wa watu wa Makka kwa vijipesa kidogo mpaka alipofika umri wa miaka ishirini na tano akapata kazi ya kumfanyia biashara Khadija, bibi mtukufu wa Kikureshi ambaye baadaye alikuja kuwa mkewe, na kuzaa naye aghlabu ya watoto wake. Miaka 13 ya utume Makka Katika miaka 13 aliyoyaishi hapo Makka baada ya kupewa utume, Muhammad alipata kila aina ya mateso na masumbuko, juu ya nafsi yake na juu ya wafuasi wake, naye alisubiri na kustahimili kila aina ya taabu na shida kwa ajili ya Mola wake, mpaka Mwenyezi Mungu alipompa amri ya kuhama mji huo na kuelekea Madina. Katika muda huu alipokuwa Makka, wengi katika jamaa zake na watu wa makabila mengine wa matabaka mbalimbali za jamii waliingia dini yake. Mwaka 622 Wakureshi, wakiona hasara katika mafungamano yao na Waarabu wengine wenye kuabudu miungu mingi, kwa dukuduku zao zilimfanya Muhammad ahame pamoja na sahibu wake Abubakar Assiddiq na wafuasi wake 70 hivi akaishi Yathrib, mji ambao ulikaliwa na Waarabu na Wayahudi pamoja na ambao baadaya ukaitwa Madinat al-Nabi (yaani Mji wa Nabii, kifupi Madina). Mwaka huo ukawa wa kwanza katika Kalenda ya Kiislamu inayotumika tangu wakati wa halifa 'Omar ibn al-Khattàb hadi leo. Kuhamia Madina na mwanzo wa Umma Mtume Muhammad, baada ya kupewa amri ya kuguria Madina, aliondoka na kuhamia mji huo ambao ulimpokea na kumkubali na kumsaidia na kumtukuza na kumlinda na maadui. Ingawa Wayahudi wa Madina walikataa kumsadiki kuwa nabii kama wale wa Biblia, aliendelea kuhubiri huko na tangu mwaka wa kwanza alitunga Hati ya Agano iliyokubaliwa na Wamadina wote: ndiyo asili ya Umma, jamii ya waumini. Mtume Muhammad aliishi Madina kwa muda wa miaka 10 mingine akitangaza dini ya Mwenyezi Mungu na huko watu wengi na makabila mbali mbali ya Kiarabu yaliingia dini ya Uislamu kwa makundi makundi. Wakati huohuo alianza kushambulia misafara ya Wamakka wapagani na kuwashinda kwanza huko Badr (624), akashindwa huko Uhud (625), hatimaye akapata ushindi mkuu huko Madina katika vita vya handaki (627): hapo alifukuza na hatimaye akaangamiza kama wasaliti Wayahudi wote wa Madina na wanaume wote wa Waqurayza, wakati wanawake wao pamoja na watoto wakauzwa kama watumwa huko Syria. Mwaka 630 Muhammad akiwa na nguvu za kutosha aliweza kurudi Makka na kuiteka, akairudisha Kaaba ambayo ndiyo kibla cha Waislamu wote ulimwenguni katika mambo ya Sala na Hija. Hata hivyo akarudi kuishi Madina na kutoka huko akaeneza kazi yake ya kisiasa na ya kidini katika Hijaz yote. Baada ya ushindi wake huko Hunayn dhidi ya Waawazin na wenzao, aliteka au kusilimisha vijiji mbalimbali vya maana upande wa uchumi au wa vita kwa mfululizo wa mapigano kwenye Wadi al-qura. Kwa jumla alihudhuria vita 27, akiua kwa mkono wake mtu mmoja tu. Akiendelea kuishi Madina, alinadhimu kwa Sharia na hukumu nyingi maisha ya jamii ya Waislamu huko, na kuweka chanzo cha dola ya kiislamu ulimwenguni. Sharia na hukumu hizo zinapatikana katika kitabu kitakatifu cha (Qurani), ambacho leo Waislamu wote ulimwenguni wananadhimu maisha yao kulingana nacho. Wake zake Ingawa Kurani inaruhusu wake 4 tu, Muhammad alisema ana idhini ya kuvuka kiwango hicho. Jumla alioa wake 11, ambao majina yao yamepangwa hapa chini kufuatana na tarehe ya ndoa. 1. Khadija binti Khuwaylid (tangu 595 hadi kifo chake Januari 620) ambaye aliwahi kuolewa na waume wawili na kuwazalia watoto 5. Katika maisha mazuri ya ndoa alimzalia Muhamad mabinti 4 (Ruqayya, Umm Khulthūm, Zaynab na Fatima), mbali na watoto 2 wa kiume (Qàsim na ‘Abd Allah) ambao lakini walikufa wakiwa bado wadogo. 2. Sawda binti Zam’a (tangu Machi 620) aliyewahi kuolewa na mume mmoja. 3. Aysha binti Abu Bakr (tangu Januari 623) aliyeolewa na Mohamed akiwa na umri wa miaka 9. 4. Hafsa binti Umar (tangu Novemba 624), aliyewahi kuolewa na mume mmoja. 5. Zaynab binti Khuzayma (tangu Juni 625 hadi kifo chake Agosti 625). 6. Hindi Umm Salama binti Abi Umayya (tangu Februari 626), aliyewahi kuolewa na mume mmoja na kuachiwa watoto wengi. Alikuwa mtoto wa kambo wa shangazi ya Mohamed. 7. Zaynab binti Jahsh (tangu Juni 626) aliyeachwa na mume wake. Alikuwa binamu wa Mohamed. 8. Juwayriya binti Al Harith (tangu Desemba 626). 9. Ramla Umm Habība binti Abi Sufyan (tangu Agosti 628) alipoachana na mumewe aliyeingia Ukristo. 10. Safiyya binti Huyay (tangu Septemba 628) ambaye alikuwa Myahudi akatekwa nyara katika vita vya Khybar. 11. Maymuna binti Harith (tangu Februari 629) aliyekuwa na umri wa miaka 51. Kati yao, wa kwanza tu alimzalia Muhammad watoto, lakini wana wote walifariki kabla ya baba yao, isipokuwa Fatma aliyekufa miezi sita baada yake. Aliwaoa pia, lakini bila ya kulala nao, Asma’ binti Al Nu‘man (mkoma) na ‘Amra binti Yazid (aliyekataa katakata ndoa hiyo akapewa mara talaka). Mbali na wake rasmi, Kurani inaruhusu kuwa na masuria wasio na idadi (dhāt al-yamīn, "waliomilikiwa na mkono wa kuume", yaani watumwa, hasa waliotekwa vitani). Muhammad alikuwa nao 16: kati yao Marya (Mkristo) alimzalia mtoto wa kiume: Ibrahim, aliyefariki mdogo sana, kwa huzuni kubwa ya baba yake aliyemfuata kaburini muda mfupi baadaye. Marejeo KADHI SHEIKH ABDULLA SALEH FARSY, Maisha ya Nabii Muhammad - Mulla Karimjee Mulla Mohamedbhai & Son, Zanzibar 1942 Viungo vya nje Visivyotolewa na Waislamu Muhammad, article on Enyclopaedia Britannica Online Muhammad: Legacy of a Prophet - PBS Site Muhammad: Legacy of a Prophet - UPF (Producer's Site) Encarta Encyclopedia 1911 Encyclopedia article on Mahomet William Muir: The Life of Mahomet The Hero as Prophet A passionate championship of Prophet Muhammad as a Hegelian agent of reform. by Carlyle, Thomas (1795-1881) On Heroes and the Heroic in History. Lincoln, Nebraska: University of Nebraska Press, 1966. Vilivyoandikwa na Waislamu Ar-Raheeq Al-Makhtum (The Sealed Nectar) PDF version of Ar-Raheeq Al-Makhtum The Life of Muhammad by Muhammad Husayn Haykal About the Prophet Muhammad (University of Southern California) Kujisomea Al-Hibri, Azizah Y. (2003). "An Islamic Perspective on Domestic Violence". 27 Fordham International Law Journal 195. US edn. by Inner Traditions International, Ltd. (New edition 1974) Kamusi elezo Uislamu Watu wa Kurani Mitume katika Uislamu
1171
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fizikia
Fizikia
Fizikia (kutoka neno la Kigiriki φυσικός, physikos, "ya kimaumbile", ambalo tena linatokana na φύσις, physis, "umbile") ni fani ya sayansi inayohusu maumbile ya ulimwengu, hususan asili ya dunia na viumbe vyote. Ni taaluma yenye kushughulika na maada na uhusiano wake na nishati. Fizikia imetoa mchango mkubwa katika sayansi, teknolojia na falsafa. Utangulizi Tangu zama za nyuma kabisa, wanafalsafa ya asili walijaribu kueleza mafumbo, kama vile mienendo ya sayari na asili ya maada. Mlengo huu ulijulikana hapo mwanzo kama Fizikisi (kutoka Kiingereza Physics, ikiandikwa Physike kuiga dhana ya Aristotle). Kuibuka kwa Fizikia kama tawi la sayansi lenye kujitegemea, toka kwenye shina la falsafa asilia, kulitokana na mapinduzi ya kisayansi ya karne ya 16 na ya 17 na kuendelea mpaka pambazuko la sayansi ya Kisasa mwanzoni mwa karne ya 20. Fani hii imekuwa ikiendelea kutanuka kulingana na kukua kwa tafiti na kupelekea gunduzi mbalimbali kama vile: modeli sahili ya chembe za kimsingi na uelezi uliotanuka wa historia ya ulimwengu, sambamba na mapinduzi ya teknolojia mpya kama silaha za nyuklia na semikonda. Leo hii utafiti unaendelea katika mikondo mipana ya kimata; kuhusisha mpitishoumemkuu katika joto la hali ya juu, ukokotoaji wa kikwantumu, utafutaji wa Higg Boson, na jitahada za kuendeleza nadharia ya mtuazi wa kikwantumu. Ulikitwa katika mitazamo na vitendo, na pia seti zilizojisheheneza kwa nadharia zinazodhihirishwa kwa hisabati nzuri. Ugunduzi katika sayansi umegusa kote ndani ya Sayansi Asilia, na Fizikia inaelezwa kama Sayansi ya Msingi kwa sababu nyanja nyingine kama Kemia na Biolojia huchunguza mifumo ambayo tabia zake husimama kwenye kanuni za Fizikia. Kemia, kwa mfano, ni sayansi ya dutu iliyofanyika na atomu na molekuli kwa wingi mmoja, lakini tabia za kampaundi za kikemia zinatathminiwa kwa tabia za kimaumbile za molekuli zinazochipukia kwayo. Fizikia ya vitendo inahusiana kwa karibu na uhandisi na teknolojia. Mwanafizikia anayejihusisha na msingi wa utafiti hufanya muundopicha na kisha kufanya vitendo kwa kutumia vyombotekichi kama kikazanishio mwendo wa chembe na Biru, na angali mwanafizikia anayejihusisha na tafiti zilizotendewa kazi, huvumbua teknolojia kama vile Upigaji Picha Kiusumaku Mtetemiazi (kwa Kiingereza MRI, Magnetic Resonance Imaging) na transista za sifa mbalimbali. Fizikia ya kinadharia ina uhusiano wa karibu na hisabati, ambayo huipa lugha ya nadharia za kimaumbile. Aghalabu ni kweli kwamba shauri la kwanza la Nadharia ni kupembua mahusiano katika sura ya kiulimwengu inayoshabihiana na yatendekayo. Kazi nyingine ya umuhimu sawa ni kufanyiza kanuni za mahusiano kimahesabu. Matumizi ya hisabati katika nadharia huwakilisha dhana ya kimawazo, katika mchakato wa kuibua hitimisho muhimu kutoka kwenye hali ya udhanifu uliopitia sheria rasmi za ukokotoaji. Hata hivyo, nafasi ya hisabati katika nyanja za Fizikia ya Kinadharia inapelekea kwamba, si tatizo la mwanafizikia ya kinadharia kuchetua kidhibiti hakikivu cha kihesabu na, kwa kweli kabisa, mahitaji yaliyokaza sana kwenye hesabu mara nyingi hupingana na kweli za kimaumbile. Mwanafizikia ya Kinadharia mara nyingi vilevile huegamia katika ufuatiliaji tathmini wa kinamba na uchocheaji picha wa kompyuta na hivyo kuona matokeo yake; na ndiyo maana kompyuta na kuprogramu kompyuta vimekuwa na uwanda mpana wenye sura mbalimbali katika kufanya modeli za kimaumbile. Kwa kweli, nyanja ya Hisabati na Ufuatiliaji tathmini kikompyuta ni uwanja uliochangamka katika utafiti. Fizikia ya kinadharia mara nyingi huhusiana na falsafa na metafizikia ambapo inaangukia upande wa mawazo ya kufikirika kama vile nafasi za vizio wakadhaa na ulimwengu sambamba. Nadharia Ingawaje mwanafizikia husoma aina mbalimbali za mafumbo ya maisha, kuna baadhi ya nadharia zinazotumika kwa wanafizikia wote. Kila moja kati ya hizi nadharia imejaribiwa kwa idadi ya vitendo na kuhakikishwa makadirio sahihi ya asili iliyopo ndani ya mizingo yenye kubadilika umakini. Kwa mfano, nadharia ya utafiti. Historia Astronomia inatajwa kama sayansi ya kale zaidi, ambapo jamii zilizokuwa zimestaarabika zamani, kama Wasumeri, Wamisri wa kale na jamii kuzunguka uwanda wa mto Indus, takriban miaka 3000 KK zilikuwa na uelewa juu ya elimu ya utabiri kuhusu mienendo ya jua, mwezi na nyota. Nyota na mwezi mara nyingi zilichukuliwa kama alama za kidini, zikiaminika kuwakilisha miungu yao. Ingawa maelezo ya matukio hayo mara nyingi hayakuwa ya kisayansi, tena yenye upungufu wa vithibitisho, hayo maono ya enzi hizo yalikuwa msingi wa uendelezaji wa elimu ya astronomia baadaye. Kwa mujibu wa Asger Aaboe, chanzo cha astronomia ya kimagharibi kinaweza kupatikana Mesopotamia, na juhudi zote za watu wa magharibi kuelekea sayansi ya uhalisia zimerithiwa kutoka astronomia ya kale ya Kibabuloni. Wanaastronomia wa Misri waliacha alama katika makaburi na kumbukumbu zingine juu ya makundi nyota na mienendo ya maumbo mengine katika samawati (maumbosamawati/magimba) mengine. Homer, mshairi bora wa Ugiriki wa kale, aliandika katika Iliad na Odyssey juu ya maumbosamawati tofauti; baadaye wanaastronomia wa Kigiriki waliyapa majina makundi nyota mengi yanayoonekana katika kizio cha kaskazini cha dunia, majina ambayo yanatumika hadi leo. Falsafa ya asili Falsafa ya asili ina chanzo chake huko Ugiriki wakati wa kipindi cha kale, (650 KK– 480 KK), ambapo wanafalsafa wa kabla ya Sokrates kama Thales waliyakataa maelezo yasiyo ya kiasili kwa matukio ya kiasilia na kutangaza kwamba kila tukio lilikuwa na sababu za kiasili. Walipendekeza kwamba lazima mawazo yathibitishwe na sababu makini na uoni na nyingi katika nadharia zao zilithibitishwa kwa mafanikio makubwa katika majaribio mbalimbali, kwa mfano, nadharia ya atomi ilijulikana kuwa sahihi takribani miaka 2000 baada ya kupendekezwa kwa mara ya kwanza na Leucippus na mwanafunzi wake Democritus. Fizikia ya zamani Isaac Newton (1643–1727) aliandika sheria za mwendo na mvutano ambazo zilikuwa hatua kubwa katika fizikia ya zamani. Fizikia ilipata kuwa somo peke yake la sayansi wakati Wazungu walipoanza kutumia njia za majaribio na upimaji kugundua kile ambacho leo kinachukuliwa ni sheria za fizikia. Maendeleo makubwa katika kipindi hicho yalijumlisha ubadilishaji wa mfumo wa jua uliofuata mfumo wa jiosentriki kuwa mfumo wa heliosentriki wa Copernicus. Sheria zinazotawala miendo ya sayari katika mfumo wa jua ziliamuliwa na Johannes Kepler kati ya miaka 1609 na 1619. Kazi za mwanzo katika darubini na unajimu wa kiuchunguzi vilifanywa na Galileo Galilei katika karne ya 16 na 17, na ugunduzi wa Isaac Newton na muungano wa sheria zake za mwendo na sheria za jumla za mvutano ambazo zilikuja kubeba jina lake ulifanyika. Newton pia aliendeleza kalikulasi, somo la mahesabu ya mabadiliko, ambalo lilileta njia mpya ya kukokotoa matukio ya kiumbo. Ugunduzi wa sheria mpya za joto mwendojoto (thermodynamics), kemia na sumakuumeme ulitokana na juhudi kubwa za uchunguzi katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda kutokana na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa mahitaji ya nishati. Sheria zenye maudhui ya fizikia ya zamani ziliendelea kuwa na matumizi makubwa katika matukio ya kila siku ambapo maada ilisafiri na miendokasi isiyokaribia ule wa mwanga kwa kuwa yalitoa majibu yenye makadirio ya karibu zaidi, na nadharia kama kwanta ya kimakenika na ile ya rilativiti zilirahisika kuelekea kutoa majibu kama yaliyotolewa na fizikia ya awali. Hata hivyo makosa katika fizikia ya zamani hasa kwa vitu vidogo zaidi na vile vyenye mwendo uliokaribia ule wa mwanga vilipelekea kuendelezwa kwa fizikia ya kisasa katika karne ya 20. Fizikia ya kisasa Kazi za Albert Einstein (1879–1955), katika athari za kifotoelektriki na nadharia ya rilativiti, ndiyo iliyopelekea mapinduzi ya fizikia katika karne ya 20. Max Planck (1858–1947) alianzilisha nadharia ya kwanta ya kimakenika na vifurushi kimakenika. Nadharia hizo zote kwa pamoja zilikuja kwa sababu ya majibu yasiyo sahihi sana yaliyotolewa na mekaniki ya zamani katika baadhi ya matukio. Mekaniki ya zamani ilitabiri mabadiliko ya mwendokasi wa mwanga, jambo ambalo lilishindwa kutatuliwa na mwendokasi usiobadilika uliotabiriwa na milinganyo ya sumakuumeme ya Maxwell; utata huo ulirekebishwa na nadharia ya Einstein ya rilativiti maalum, ambayo iichukua nafasi ya mekaniki ya zamani kwa vitu vinavyokwenda kwa spidi kubwa zaidi na ikaruhusu mwendo wa mwanga usiobadilika. Mnururisho wa vitu vyeusi pia ulikuwa tatizo lingine kwa mekaniki ya zamani, ambalo lilitatuliwa wakati Planck alipopendekeza kwamba mwanga husafiri katika mfumo wa vifurushi vidogovidogo vinavyoitwa fotoni; pamoja na athari za fotoniumeme na nadharia nzima inayotabiri ngazi zilizojitenga za njiamzingo za elektroni, ilipelekea kwenye nadharia ya vifurushikimakenika (kwa Kiingereza Quantum mechanics) kushika nafasi ya mekaniki ya zamani katika mizania ndogo sana. Nadharia ya vifurushikimakenika ilianzishwa kutokana na kazi za awali za akina Werner Heisenberg, Erwin Schrödinger na Paul Dirac. Kutokana na kazi hizo za mwanzo kila mmoja katika tasnia yake muundo wa kiwango kinachotambulika wa fizikia ya hardali/vitu vidogo ilipatikana. Kufuatia ugunduzi wa tabia za hardali zinazokubaliana na Higgs boson katika kituo cha CERN mwaka 2012, hardali zote za msingi ziliweza kutabiriwa na muundo unaotambulikana, na hakuna hardali nyingine zilizoonekana kupatikana, hata hivyo fizikia zaidi ya muundo unaotambulika, na nadharia kama za supersymmetry, ni katika mambo yanayoendelea kufanyiwa utafiti hivi leo. Tazama pia Viungo vya nje https://en.m.wikipedia.org/wiki/Physics https://www.famedwritings.com/homeworkhelp/physics/why-physics-is-important/ Fizikia Sayansi
1174
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwenyezi%20Mungu
Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu katika lugha ya Kiswahili ni jina linalotumika kwa Muumba wa kila kitu, Mwenye kuabudiwa kwa haki, kinyume na neno mungu ambalo linamaanisha chochote au yeyote anayeabudiwa ikiwa kwa haki au si kwa haki. Neno Mwenyezi linaunganisha Mwenye na enzi na kumpatia Mungu sifa ya kuweza yote, bila kuzuiliwa na yeyote wala chochote. Kwa uweza huo, Mwenyezi Mungu ni Muumba wa mbingu na dunia na kila kilichomo ndani yake, naye ni Mlezi wa viumbe vyote na Mpaji riziki kwa kila chenye uhai ulimwenguni. Mwenyezi Mungu, katika dini na mila nyingi duniani, ni yule anayestahiki kuabudiwa kwa haki ikiwa peke yake bila kushirikishwa na chochote, au kwa kushirikishwa na viumbe, kwa nia ya kuwa hawa viumbe vinamkurubisha naye. Hii ni kwa sababu, kila dini au mila ina namna yake ya kumsawiri Mwenyezi Mungu, na njia gani sahihi ya kumuabudu, na kwa kuwa hakuna itifaki baina ya hizi dini, mila na madhehebu kuhusu Mwenyezi Mungu na namna anavyotakikana kuabudiwa, hizi tofauti chungu nzima zimetokea. Sifa za Mwenyezi Mungu Mwenyezi Mungu ana sifa mbali mbali kwa mujibu wa dini na mila na madhehebu tofautitofauti, na watu wanamsifu Mwenyezi Mungu kwa namna ambayo wanamjua wao kulingana na mafunzo ya dini na mila zao. Hii ni kwa sababu, watoto tangu wazaliwapo hufunzwa na wazee wao habari za Mwenyezi Mungu na namna ya kumuabudu, na mafunzo haya hubakia katika mawazo na fikra zao, na kukua nayo mpaka ukubwani mwao. Imani ya Waislamu Uislamu, kwa mfano, unaeleza kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu, hana mshirika, hana mwanzo wala mwisho, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hapana yeyote mwenye kufanana au kushabihiana naye, naye ni Mola wa ulimwengu huu wote, na Muumba wa kila kitu. Kwake Yeye inatoka riziki ya kila kiumbe, na ndiye Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha. Marejeo ya viumbe vyote wakisha kufa na kufufuliwa ni kwake Yeye tu siku ya Kiyama. Yeye pekee ndiye Mwenye kuhukumu viumbe siku ya malipo, na ndiye atakayewapa waja wake ujira na thawabu na kuwatia Peponi kwa mema waliyoyafanya, au kuwatia adabu na kuwapa adhabu na mateso na kuwatia Motoni kwa maovu waliyotenda hapa duniani. Waislamu wanafunzwa tangu utotoni mwao kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu peke yake, hana mshirika, naye ndiye mwenye kufaa kuabudiwa kwa haki bila ya kushirikishwa na chochote katika viumbe vyake, na kuwa Yeye ni wa kutegemewa katika kila kitu na kuombwa msaada na kuombwa msamaha wakati wa makosa na madhambi. Yeye hana kitu kilichofanana naye, hakuzaa wala hakuzaliwa, hana mwanzo wala mwisho. Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu, Mtoa riziki, Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha. Hukumu yote ni yake siku ya Kiyama. Mtukufu na Mkubwa. Bwana na Mola wa walimwengu wote. Yeye tu ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa na Yeye tu ndiye Mwenye kufaa kuombwa na kutakwa msaada. Imani ya Wakristo Ukristo unakubaliana na Uyahudi na Uislamu katika mengi ya sifa hizi za Mwenyezi Mungu za kuumba, kuhuisha na kufisha, kuruzuku, kufufua, kuhukumu na kulipa ya kheri kwa mwenye kufanya kheri na ya shari kwa mwenye kufanya shari, lakini aghlabu ya madhehebu ya Kikristo, ijapokuwa si yote, yanampa Mwenyezi Mungu sifa ya kuwa Utatu Mtakatifu, na kumsifu kuwa huyohuyo ni Mungu Baba na Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, na kuwa wote hawa watatu wanachanga Uungu pekee kwa umoja kamili kabisa kwa dhati. Uislamu, kwa upande wake, unakataa katakata masuala ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na kwa hiyo ni Mmoja tu wala hana mshirika wa aina yoyote. Katika majadiliano juu ya hilo, mara nyingi Wakristo wanahisi Waislamu wanakariri imani yao wenyewe bila kusikiliza maelezo ya upande wa pili, kwamba fumbo la Utatu Mtakatifu halimaanishi kushirikisha sifa za Mwenyezi Mungu na wengine wawili nje yake, bali kwamba ndiyo alivyo kwa ndani. Kama vile sifa zote za Mungu (zilizoorodheshwa na Uislamu katika majina 99) zisivyovuruga umoja wake, ndivyo ilivyo kwa Utatu: kwa Wakristo karibu wote nafsi tatu ni za Mwenyezi Mungu yuleyule na zinadokeza kwamba milele yote Yeye (nafsi ya 1) anajifahamu (nafsi ya 2) na anajipenda (nafsi ya 3). Dini nyinginezo Dini nyinginezo, kadhalika, zina tasauri na fikra nyingine kuhusu Mwenyezi Mungu. Kuna wale wanaoabudu viumbe mbalimbali wakichukulia kuwa wanamwakilisha Mwenyezi Mungu, kama kuabudu sanamu, nyota, jua, ngo'mbe, wanyama mbalimbali, mizimu, miti, moto, viumbe wenziwao, malaika, majini na kadhalika. Dini na mila hizi, pengine huchukulia kuwa vitu hivi vinatusaidia kutufikisha kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa bila ya vitu hivi, ibada zetu haziwezi kufika. Ama wengine huwa na imani kuwa vitu hivi ndio Mola mwenyewe wa kuabudiwa na kuombwa na kutakwa msaada. Tanbihi Marejeo Augustino wa Hippo, City of God and Christian Doctrine C.S. Lewis, The Problem of Pain Charles Hartshorne, Man's Vision of God Plato, Sophist Tertullian, Against Praxeas Thomas Aquinas, Summa Theologica Viungo vya nje Internet Encyclopedia of Philosophy entry Stanford Encyclopedia of Philosophy entry Logical Truth and Omnipotence Omnipotence and Free Will in Judaism Dini Mungu Uyahudi Ukristo Uislamu
1175
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia
Dunia
Dunia (; kutoka neno la Kiarabu دنيا, dunyaa; wakati mwingine pia: ardhi na kwa neno asili la Kibantu: nchi) ni gimba la angani ambapo juu yake tunaishi sisi binadamu na viumbehai wengine wengi, tukipata mahitaji yetu, kuanzia hewa ya kutufaa na maji. Dunia ni mojawapo ya sayari nane zinazozunguka Jua letu katika anga-nje. Kati ya sayari za mfumo wa Jua, Dunia yetu ni sayari ya tatu kutoka kwa Jua. Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au kizio astronomia 1. Dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756. Dunia huwa na mwezi 1. Umri wa dunia hukadiriwa kuwa miaka bilioni 4.5. Ni mahali pekee katika ulimwengu panapojulikana kuna uhai ulioaminiwa kuanza miaka bilioni 3.5 iliyopita. Uhai unapatikana kwa spishi milioni 10-14 za viumbe hai pamoja na wanadamu waliokadiriwa kuwa sasa bilioni 7.2. Umbo la dunia Umbo la dunia linafanana na tufe au mpira unaozunguka kwenye mhimili wake. "Mhimili wa dunia" ni mstari kati ya ncha zake. Lakini si tufe kamili. Ina uvimbe kidogo kwenye sehemu ya ikweta; ilhali umbali kati ya ncha mbili ni kilomita 12,713 lakini umbali kati ya sehemu za kinyume kwenye ikweta ni km 12,756, yaani kipenyo hiki kinazidi takriban kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha. Tofauti hii inasababishwa na mzunguko wa dunia. Kani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi. Kwa hiyo mahali duniani palipo karibu zaidi na anga-nje si Mlima Everest kwenye Himalaya bali mlima Chimborazo nchini Ekuador. Kwenye uso wake dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili. Nusu moja ina eneo kubwa la mabara yaani nchi kavu ambayo ni asilimia 47 ya sehemu hii. Kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji ya bahari na eneo la nchi kavu ni asilimia 11 pekee za maeneo yake. Kwa jumla dunia ni sayari pekee katika mfumo wa jua yenye maji katika hali ya kiowevu usoni mwake. Bahari kuu ya dunia inashika asilimia 96.5 ya maji yote yaliyopo duniani. Maji ya bahari huwa na asilimia 3.5 chumvi ndani yake. Kwa pamoja maeneo ya maji hufunika 70.7% za uso wa dunia. Nchi kavu huwa na 29.3% na sehemu kubwa ya eneo la nchi kavu ni bara 7 za Asia, Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antarktika, Ulaya na Australia. (Ulaya inaweza kuangaliwa pia kama sehemu ya Asia ikiwa kama rasi yake ya magharibi. Azimio la kutazama Australia kama bara na Greenland kama kisiwa tu ni azimio la hiari si la lazima). Maeneo ya bahari kuu ya dunia kwa kawaida hugawiwa kwa bahari kubwa 3 za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Sehemu ya chini baharini iko kwenye Mfereji wa Mariana katika Pasifiki (mita 11,034 chini ya UB). Kwa wastani bahari huwa na kina cha mita 3,800. Muundo wa dunia - taz. makala "Muundo wa dunia" - Tumeona dunia ina umbo la mviringo au tufe. Tufe hilo si kipande kimoja kikubwa cha mwamba thabiti. Dunia ina muundo ndani yake. Muundo huo unafanana kiasi na kitunguu, yaani dunia yetu imefanyika kwa matabaka mbalimbali yanayofuatana kutoka nje kwenda ndani. Kila moja lina tabia yake. Kimsingi wataalamu hutofautisha matabaka matatu ambayo ni: Ganda la dunia Koti la dunia Kiini cha dunia Ganda la dunia ni sehemu imara na uhai wote tunaoujua unapatikana juu yake. Katikati hali ya koti na ya kiini ni ya joto kubwa sana na maada yake hupatikana katika hali ya giligili (si imara, kuyeyushwa). Kila ukiingia ndani dunia inazidi kuwa ya moto mpaka ukifika ndani kabisa daraja ya harara hufikia nyuzi 5000-6000 °C. Matabaka hayo yanafanywa kwa elementi za kikemia ambazo ni feri (chuma) (32,1 %), oksijeni (30,1 %), silisi (15,1 %), magnesi (13,9 %), sulfuri (2,9 %), nikeli (1,8 %), kalsi (1,5 %) na alumini (1,4 %). Mabaki ya 1,2 % ni viwango vidogo vya elementi nyingine. Elementi hizo zinapatikana kwa hali safi au katika kampaundi za elementi. Vipimo vimeonyesha ya kwamba matabaka mawili ya koti na kiini huwa tena na mgawanyiko ndani yake, hivyo matabaka yafuatayo yanaweza kutofautishwa. Sehemu ya juu ya koti inafanana kikemia na ganda na sehemu hizo mbili zinaitwa tabakamwamba. Tabakamwamba ina unene wa kilomita 50 - 100. Tabakamwamba imekatika katika vipande vinavyoitwa mabamba la gandunia. Vipande hivi vinaelea juu ya giligili ya koti la ndani. Ndiyo sababu bara lolote si la milele; kila bamba huwa na mwendo wake na ndiyo sababu katika historia ya dunia mabara yameachana na kuungana mara kadhaa. Kwa mfano imepimwa ya kwamba sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ina mwendo wa kuachana na bara la Afrika na dalili yake ni bonde la ufa. Pale ambako mabamba yanapakana, volkeno nyingi zinapatikana na matetemeko ya ardhi hutokea. Ugasumaku wa dunia Dunia inazungukwa na uga sumaku yaani mistari ya nguvu ya kisumaku. Sababu yake ni kwamba kiini cha dunia kinafanywa na chuma chenye tabia kama sumaku kubwa. Tabia hiyo inasababishwa na mwendo wa mikondo ya chuma cha moto kilichoyeyuka katika kiini cha nje cha dunia. Mistari ya nguvu ya sumaku inatoka nje kwenye ncha ya kusini na kurudi ndani ya dunia kwenye ncha ya kaskazini. Tabia hiyo ni msingi wa kazi ya dira ambamo sindano ya dira huvutwa daima na ncha sumaku ya dunia na kuelekea kaskazini muda wote. Ugasumaku wa dunia ni kinga muhimu kwa uhai wote duniani. Dunia inapigwa muda wote na mnururisho kutoka jua kwa njia ya "upepo wa jua". Mnururisho huo ni nuru pamoja miale ya hatari. Ugasumaku unakengeusha sehemu kubwa ya mnururisho hatari hadi unapita kando ya dunia na kutofika kwenye uso wa dunia. Dunia kama mahali pa uhai Dunia yetu ni sayari pekee inayojulikana mpaka sasa ambapo binadamu na viumbe vingine vinaweza kuishi. Wanasayansi bado wanafanya ufafiti kujua kama kuna kuna viumbe hai kwenye sayari nyingine. Hapa kuna sababu mbili zinazofanya viumbehai kuishi dunianiː dunia yetu ina umbali na jua unaofaa kwa maisha kwa sababu sayari zilizoko karibu zaidi na jua (k.m. Zuhura) zina joto kubwa mno na sayari zilizoko mbali zaidi kama Mrihi ni baridi mno. dunia yetu ina angahewa yenye asilimia 78 ya naitrojini, asilimia 21 ya oksijini na asilimia 1 ya aina nyinginezo za hewa, na kwa sababu hii uhai na maisha yanamakinika katika ardhi, kinyume na sayari nyinginezo. Uso wa dunia Sehemu kubwa kabisa ya dunia inafunikwa na bahari, kwani takriban asilimia 70 ya uso wake unafunikwa na maji ya bahari na kutokana na maji yote yaliyokuwepo ardhini, asilimia 97 ni maji ya bahari, na asilimia 3 ni maji matamu. Theluthi inayobaki ni nchi kavu kwenye mabara mbalimali na visiwa vingi. Sura ya dunia ni kilomita mraba 510,000,000, ikiwa nchi kavu imechukua eneo la kilomita mraba 149,430,000 na maji yamechukua eneo la kilomita mraba 360,570,000. Mabara makubwa ni Asia, Afrika, Amerika Kusini na Amerika Kaskazini, Australia na Ulaya. Asia na Ulaya mara nyingi hutazamiwa wakati mwingine kama bara moja ya Eurasia. Angahewa Hewa iliyoko juu ya ardhi vile vile ina matabaka mbalimbali, na kila tabaka lina kazi yake. Hewa kwa jumla ina masafa ya kiasi cha kilomita 560 au maili 348 kuendea juu, na baada ya hapo unaingia kwenye anga-nje. Hewa hiyo ndiyo inayokinga viumbehai na madhara ya Jua na mnururisho wa angani ambao unaingia anga ya dunia na kuteremka chini. Tazama pia Muundo wa dunia Madhara ya ongezeko la joto Duniani Tanbihi Marejeo Cesare Emilliani: Planet Earth. Cosmology, Geology, and the Evolution of Live and Environment. Cambridge University Press 1992, ISBN 0-521-40949-7 Comins, Neil F. (2001). Discovering the Essential Universe (2nd ed.). W. H. Freeman. Bibcode:2003deu..book.....C. ISBN 0-7167-5804-0. Viungo vya nje Earth – Profile – Solar System Exploration – NASA. Earth – Climate Changes Cause Shape to Change  – NASA. Earth – Geomagnetism Program – USGS. Earth – Astronaut Photography Gateway – NASA. Earth – Observatory – NASA. Earth – Audio (29:28) – Cain/Gay – Astronomy Cast (2007). Earth – Videos – International Space Station: Video (01:02) – Earth (time-lapse). Video (00:27) – Earth and Auroras (time-lapse). Sayari Dunia
1178
https://sw.wikipedia.org/wiki/Asia
Asia
Asia ni bara kubwa kabisa kuliko mabara yote mengine ya dunia. Bara hili lina eneo la kilomita za mraba 44,579,000 (maili za mraba 17,212,000), ambalo ni sawa na asilimia 30% ya ardhi yote. Wakazi wa bara la Asia ni 3,701,000,000 kwa mujibu wa makisio 2003. Bara la Asia lina nchi 44 na visiwa mbali mbali vya madola mbalimbali. Mlima mrefu kabisa ulimwenguni ambao ni mlima wa Everesti wenye urefu wa mita 8,850 (futi 29,035) ulioko Nepal pia uko kwenye bara hili. Kadhalika, nchi zenye wakazi wengi zaidi ulimwenguni China na India pia ziko kwenye bara hili. Ziwa kubwa kabisa ulimwenguni, bahari ya Kazwini (Caspian Sea) lenye eneo la kilomita za mraba 394,299 (maili za mraba 152,239) vile vile liko Asia kati ya ya nchi hizi: Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan, na Uajemi. Bara la Asia linaweza kugawanywa katika sehemu zifuatazo: Orodha ya nchi na maeneo Bara Asia
1182
https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa
Isa
Isa ni umbo la jina Yesu katika Qurani na pia katika lugha mbalimbali zilizoathiriwa na Uislamu. Ukurasa huu unahusu imani ya Uislamu kumhusu Yesu kadiri ya Kurani. Kitabu hicho kilichoandikwa miaka 600 hivi baada ya Kristo kina aya 93 zinazomhusu, lakini hakileti mfululizo wa habari za maisha yake wala za mafundisho yake maalumu. Ingawa Waislamu wanakiri pia vitabu vitakatifu vya Torati, Zaburi na Injili, katika ibada wanatumia Kurani tu na kwa kawaida ndiyo chanzo chao cha habari juu ya watu na matukio ya kabla yake. Kwao nabii Isa ni mtume anayeaminiwa kuwa mmojawapo wa mfululizo wa mitume na manabii watukufu 124,000 wa Mwenyezi Mungu walioletwa ulimwenguni kuwapasha wanadamu ujumbe wa umoja wake, ili wamuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani. Mitume na Manabii hao wameletwa katika zama mbalimbali na kwa watu, kaumu na umma mbalimbali, na mfululizo huu ulianza na Adamu, baba wa wanadamu wote, hadi Mtume Muhammad akiwa ndiye wa mwisho. Isa ni miongoni mwa mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahimilivu wao mkubwa: Manabii Nuhu na Ibrahimu na Musa na Isa na Muhammad. Tena ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili. "Masihi Isa bin Mariamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Neno lake tu alilompelekea Mariamu, na ni Roho iliyotoka kwake" (sura ya 4 aya 171). Wakristo wanamuita kwa kawaida Yesu Kristo. Kuzaliwa kwake Nabii Isa alizaliwa na bibi Maryam kimuujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimtuma malaika Jibril kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa, alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwingine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mama yake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba. Huo ni mfano mmoja katika mifano minne ya uumbaji aliyotuonyesha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu bila ya baba wala mama, na akamuumba Hawa bila ya mama, na akamuumba Isa bila ya baba, na akaumba wanadamu wote waliobakia kutokana na baba na mama. Habari za kuzaliwa kwake Nabii Isa zinapatikana katika Kurani, surat "Maryamu" (19) kuanzia aya 16 - 35. Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipojitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mcha Mungu. (Malaika) Akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako ili nikubashirie tunu ya mwana aliyetakasika. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanamume yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? (Malaika) akasema: Ni kama hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lililokwishaamuliwa. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. Ujumbe wake Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahili kuabudiwa kwa haki. Ujumbe huu ndio ujumbe uleule uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu ili kuwaongoza, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kuzipa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Kadiri ya sura ya 3 aya ya 50 alisema ni "msadikishaji wa yale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na ili niwahalalishieni baadhi ya yale mliyoharimishiwa, na nimewajieni na Ishara kutoka kwa Mola wenu, kwa hiyo mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii". Alitabiri kuwa baada yake atakuja Mmoja ambaye atawafundisha wanadamu ukweli wote na kuwaongoza kwenye haki na kuwaeleza kila wanalolihitaji katika maisha yao. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ule wa Mtume Muhammad ambao ndio wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote. Kitabu cha Nabii Isa Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya uongozi na sharia na hekima kwa wafuasi wao. Katika vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii mbalimbali ni Taurati kwa Nabii Musa, Zaburi kwa Nabii Daudi, Injili kwa Nabii Isa, na Qurani kwa Nabii Muhammad. Kitabu cha Nabii Isa kiliteremshiwa Wayahudi ambao ndio walengwa wake wa kwanza wa Nabii Isa, kama ilivyothibitishwa na Qurani wakati aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi! Miujiza ya Nabii Isa Nabii Isa alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbalimbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuhu na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbalimbali. Baadhi ya miujiza ya Nabii Isa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ni kuumba ndege kutokana na udongo, kuponyesha vipofu wakaweza kuona, na kuwaondoshea ukoma wale wenye ukoma, na kuhuisha mtu aliyekufa, na kuwateremshia wafuasi wake chakula kutoka mbinguni ili iwe ni dalili kwao wote. Imani ya Kikristo kuhusu Isa Muhammad alikuta Wakristo au Manasara wakiwa wamehitilifiana katika imani yao kuhusu Nabii Isa, kwani wote walimkiri kuwa Mwana wa Mungu, lakini kwa wengi hii ilikuwa na maana kuwa yeye ni Mungu aliyejifanya mtu, isipokuwa wachache walitafsiri tofauti. Makundi ya namna hiyo yalitengana baada ya Nabii Isa kuondoka ulimwenguni na kuwaachia wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada ya wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walitoa fikra na mawazo yao kuhusu Isa, hivyo baada ya muda waligawanyika makundi mbalimbali. Kurudi kwa Nabii Isa Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake aliyoiacha baada ya kupaa kwenda kwa Mola wake, na haya yanaelezwa katika vitabu vya dini vya Kiislamu na vya Kikristo, lakini wanahitilifiana kuhusu namna na njia aliyoondokea ulimwenguni. Waislamu wanasema kuwa Isa alichukuliwa na Mola wake na kupandishwa kwake mbinguni baada ya Wayahudi kutaka kumuua, na kwa hivyo hawakuweza kumuua wala kumsulubu. Wakristo kwa upande mwingine, wanaamini kuwa aliwahi kusulubiwa na kuzikwa kisha akafufuka siku ya tatu. Muhimu hapa ni kujua kuwa atarudi tena duniani kukamilisha kazi aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Hivyo ni kweli kwamba imani kwa nabii Isa na kwa Yesu Kristo ni tofauti sana katika Ukristo na Uislamu. Dini Uislamu Manabii katika Uislamu Watu wa Kurani Yesu Kristo
1183
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara
Bara
Bara (au kontinenti) ni pande kubwa la nchi kavu la Dunia linalozungukwa na bahari. Kwa kawaida tunatofautisha mabara 7 ya Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antaktiki, Asia, Australia, na Ulaya. Wazo la bara Neno "bara" lamaanisha pande kubwa la nchi kavu , tofauti na bahari au visiwa vidogo karibu na pwani ya nchi kavu kubwa zaidi. Neno "kontinenti" latokana na Kilatini "terra continens" yaani "nchi (kavu) mfululizo". Kwa hiyo elezo la neno bara / kontinenti katika sayansi ya jiografia ni "masi kubwa na mfululizo za nchi kavu zinazotengwa kwa maeneo makubwa ya maji" Lakini hali halisi sehemu kubwa ya mabara saba yanayokubaliwa kwa kawaida hayatengwi kabisa kati yake kwa maji. Kwa mfano Ulaya na Asia hayatengwi kabisa na tofauti yake ni kihistoria na kiutamaduni, si kijiografia. Pia neno "masi kubwa" halieleweki waziwazi kabisa. Kwa nini Greenland yenye eneo la kilomita za mraba 2,166,086 inaitwa "kisiwa" lakini Australia yenye eneo la 7,617,930 huitwa bara? Mabara yote ya Dunia yetu huwa na pwani kwenye bahari kuu ambayo ni moja tu ikigawiwa kwa sehemu mbalimbali na mabara vigezo vingine. Uenezaji wa bara Kwa lugha ya kawaida “bara” ni eneo mfululizo wa nchi kavu. Kwa maana hii “Tanzania bara” ni eneo lote la Tanzania isipokuwa visiwa ambavyo ni sehemu ya nchi ya Tanzania bila visiwa vya Unguja, Pemba, Mafia na kadhalika. Vivyo hivyo “Ulaya bara” ni eneo la Ulaya bila visiwa kama Britania, Eire, Malta na kadhalika. Kwa macho ya jiolojia “bara” ni pana kuliko nchi kavu tu. Tunaangalia eneo lote la miamba inayounda bara. Siku hizi tunajua kwamba kila bara linalingana na kipande cha ganda la dunia tunachoita bamba la bara (continental plate). Kipande hiki kinaendelea pia chini ya uso wa bahari katika tako la bara (continental shelf) katika maji yasiyo na kina kikubwa pamoja na visiwa vya sehemu hizi. Kwa mtazamo huu visiwa vya Britania na Eire ni sehemu za Ulaya na vivyo hivyo Autralia na Guinea Mpya ni bara moja. Kwa maana ya utamaduni wazo la bara linaweza kujumlisha pia visiwa vya mbali kama vile Iceland huhesabiwa sehemu ya Ulaya au hata mikoa ya Ufaransa katika Bahari Hindi kuhesabiwa kisiasa katika Ulaya. Idadi ya mabara Kwenye ramani zinazotumia lugha ya Kiingereza kawaida huhesabiwa mabara saba duniani, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo. Bara la Afrika Bara la Asia Bara la Amerika ya Kaskazini Bara la Amerika ya Kusini Bara la Antaktika Bara la Ulaya Bara la Australia Mara nyingi visiwa vya Pasifiki hujumlishwa pamoja na Australia kama Australia na Pasifiki (Kiing. Oceania) na kuhesabiwa kama bara. Kutofautisha mabara [[File:Continental models-Australia.gif|thumb|450px|Ramani inayoonyesha njia mbalimbali za kugawa dunia kwa mabara. Kutegemeana na mawazo ya wataalamu mabara huweza kuhesabiwa kwa namna tofauti. Kwa mfano Eurasia kwa kawaida huhesabiwa kuwa mabara 2 Ulaya na Asia (nyekundu). Wengine hujumlisha pia Eurasia pamoja na Afrika kuwa bara 1. Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini wakati mwingine hutazamiwa kuwa bara moja ya Amerika. Kutokana na elezo kuu kuwa bara ni masi ya nchi kavu iliyotengwa na bara nyingine kwa maji kuna mawazo tofauti kuhusu idadi ya mabara. Ulaya na Asia kwa pamoja ni masi moja kubwa ya nchi kavu na kijiografia hakuna tofauti. Sababu za kuzihesabu kuwa mabara mawili ni kiutamaduni na kihistoria tu. Kwa hiyo mara kwa mara kuna pendekezo kuzijumlisha kwa jina "Euroasia" au "Eurasia". Afrika imeunganishwa na Asia kwa shingo ya nchi ya Suez. Amerika Kusini na Amerika Kaskazini zinaunganishwa kwa shingo ya nchi ya Panama na hata hapo mara nyingi hujumlishwa kama "bara pacha" Mfumo wa mabara saba hufundishwa kule China, India, Pakistan, Ufilipino, sehemu za Ulaya na katika nchi nyingi zinazotumia lugha ya Kiingereza pamoja na Australia and England Mfumo wa mabara sita (kwa kuhesabu Eurasia bara moja) hutumiwa zaidi pale Urusi, Ulaya ya Mashariki na Japani Mfumo wa mabara sita (kwa kuhesabu Amerika kuwa bara moja) hutumiwa Ufaransa na nchi zilizokuwa koloni zake na Italia, Urenol, Hispania, Romania, Amerika Kusini Ugiriki, na nchi kadhaa nyingine za Ulaya. Kuna pia mfumo wa kuhesabu mabara matano kwa kuacha Antaktika isiyo wa wakazi kwenye msingi wa mabara sita. Huu unatumiwa katika nembo na katiba ya harakati ya Michezo ya Olimpiki. wataalamu wachache hupendelea mfumo wa mabara manne wakihesabu Afro-Eurasia bara moja wakibaki na Amerika, Afro-Eurasia, Australia na Antaktiki. Mabara katika historia ya dunia Mabara jinsi yalivyo leo hayakuwepo tangu mwanzo wala hayakai vile. Ilhali kila bara linalingana na bamba 1 au mabamba ya gandunia ina pia mwendo pamoja na bamba lake. Wanajiolojia huamini ya kwamba miaka mamilioni iliyopita mabara yote yaliwahi kukaa pamoja kama bara 1 kubwa sana lililoendelea kupasuliwa baadaye. Vipande huelea juu ya koti ya dunia ambayo ni kiowevo na moto. Mwendo wa mabamba umepimiwa kuwa sentimita kadhaa kila mwake. Uhindi zamani haikuwepo sehemu ya Asia, na sasa hivi Afrika inaelekea kupasuliwa kwenye mstari wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Eneo la Mabara ya Dunia Eneo la dunia Eneo la dunia yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu. Jiolojia ya mabara Mabara jinsi yanavyoonekana hukaa juu ya mabamba ya gandunia ambayo ni vipande vikubwa vya mwamba vinavyounda uso wa dunia. Mabara tunavyoyajua yanalingana kila moja na bamba lake na kila bamba ina mwendo wake wa polepole. Hii ni sababu ya kwamba baada ya miaka mingi uso wa dunia utaonekana tofauti kuliko leo. Kijiolojia bara haliishi kwenye pwani pale bahari inapoanza. Bara linaendelea chini ya uso wa bahari kama tako la bara. Mabara na mabamba yao ni kama ifuatayo: Afrika (Bamba la Afrika), Antaktika (Bamba la Antaktika), Australia (Bamba la Australia), Ulaya na sehemu kubwa ya Asia (Bamba la Ulaya-Asia), Amerika Kaskazini pamoja na Siberia (Bamba la Amerika ya Kaskazini) na Amerika Kusini (Bamba la Amerika ya Kusini). Mabamba madogo yamejitenga ingawa nchi juu yao inaonekana kuwa sehemu ya bara lingine. Mfano wake ni Bara Hindi iliyokuwa kama bara ndogo au kisiwa kikubwa zamani lakini tangu miaka milioni 10 imejisukuma chini ya bamba la Asia-Ulaya na kuikunja hadi kutokea kwa milima ya Himalaya. Kwa jumla miamba ya sehemu za mabara ni mipesi kushinda miamba ya chini na hii ni sababu ziko juu ya miamba mingine. Nchi za Mabara haya Bara la Asia lina nchi huru 44. Bara la Afrika lina nchi huru 53. Bara la Amerika ya kaskazini lina nchi huru 35. Bara la Antaktika halina wakazi wa kudumu wala nchi huru hata moja ijapokuwa nchi kama 7 zinadai kumiliki sehemu fulani za bara hili. Bara la Australia au Oshania lina nchi huru 14. Bara la Ulaya (au Uropa) lina nchi huru 46. Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi. Marejeo Viungo vya nje "What are continents?" YouTube video by CGPGrey What is a continent Universe today, 2 Sep , 2010 by Jerry Coffey, imetazamiwa 2.04.2016 7 Continents of the World, imetazamiwa 2.04.2016 Defining What Exactly Is A "Continent" on wordatlas.com, imetazamiwa 2.04.2016 ! Jiografia Dunia
1191
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania
Tanzania
Tanzania (jina rasmi: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki ndani ya ukanda wa maziwa makuu ya Afrika. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi. Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika, upo kaskazini-mashariki mwa Tanzania. Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ilikuwa 61,741,120 (nchi ya 24 duniani) kutoka 44,928,923 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2012, likiwa ongezeko la 3.2% kwa mwaka. Msongamano ni wa watu 47.5 kwa km² (nchi ya 124 duniani). Mji mkuu ni Dodoma (wenye wakazi 410,956), lakini Dar es Salaam ndilo jiji kubwa zaidi, lenye watu 4,364,541. Miji mingine ni kama vile Mwanza (706,543), Arusha (416,442), Mbeya (385,279), Morogoro (315,866), Tanga (273,332), Kahama (242,208), Tabora (226,999) na Zanzibar (223,033). Jina Jina "Tanzania" liliundwa kama mkusanyiko wa majina ya maeneo mawili yaliyoungana kuunda nchi: Tanganyika na Zanzibar. Jina lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na serikali kutafuta jina fupi zaidi kuliko "Republic of Tanganyika and Zanzibar". Mshindi alikuwa mwenyeji wa Dar es Salaam aliyeitwa Mohamed Iqbal Dar. Alipendekeza kuunganisha herufi tatu za kwanza za TANganyika na ZANzibar akafikia "Tanzan". Hakuridhika bado, akaona nchi nyingi za Afrika zina majina yanayoishia na "ia" akaongeza herufi hizi. Mwenyewe alieleza baadaye chaguo lake kwamba aliamua kutumia "I" ya jina lake Iqbal na "A" ya jina la dhehebu lake analolifuata katika Uislamu la Ahmadiyya. Jina "Tanganyika" linatokana na maneno ya Kiswahili tanga (kwa kiingereza "sail") na nyika (kwa kiingereza "uninhabited plain", "wilderness"), yakiunda msemo "tanga nyikani". Wakati fulani inaelezwa kama marejeleo ya Ziwa Tanganyika. Jina la Zanzibar linatokana na "zenji", jina la watu wa eneo hilo (inadaiwa lina maana ya "nyeusi"), na neno la Kiarabu "barr", ambalo linamaanisha pwani au ufukwe. Historia (Kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani) Kabla ya uhuru nchi zote mbili, Tanganyika na Zanzibar, zilikuwa chini ya utawala wa Uingereza lakini hazikuwa makoloni ya kawaida. Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza). Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa lililoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa. Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti hadi 1964, zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais. Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (1985–1995) iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (1995–2005) aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa. Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa (2005–2015), naye aliendeleza sera za watangulizi wake akitokea chama hichohicho cha CCM. Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa rais wa awamu ya tano, John Magufuli (wa CCM vilevile). Kufuatana na kifo chake tarehe 17 Machi 2021, makamu wake, Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa rais wa awamu ya sita. Jiografia Ikiwa na eneo la kilomita za mraba 947,303 (365,756 sq mi), Tanzania ni nchi ya 13 kwa ukubwa barani Afrika na ya 31 kwa ukubwa duniani. Inapakana na Kenya na Uganda upande wa kaskazini; Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi; na Zambia, Malawi, na Msumbiji upande wa kusini. Tanzania iko kwenye pwani ya mashariki ya Afrika na ina ufuo wa Bahari ya Hindi takriban kilomita 424 (885 mi). Pia inajumuisha visiwa kadhaa vya pwani, vikiwemo Unguja (Zanzibar), Pemba, na Mafia. Tanzania ni nchi yenye sehemu za juu na za chini kabisa barani Afrika: Mlima Kilimanjaro, wenye urefu wa mita 5,895 (futi 19,341) juu ya usawa wa bahari, na kina cha Ziwa Tanganyika, katika mita 1,471 (futi 4,826) chini ya usawa wa bahari kwa mtiririko huo. Tanzania ina milima na misitu minene kaskazini-mashariki, ambako kuna Mlima Kilimanjaro. Nchi iko katika eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, hivyo maziwa yanafunika km2 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi. Upande wa kaskazini na magharibi kuna Ziwa Victoria, ziwa kubwa zaidi barani Afrika, na Ziwa Tanganyika, ziwa lenye kina kirefu zaidi barani humo, linalojulikana kwa aina yake ya kipekee ya samaki. Upande wa kusini magharibi kuna Ziwa Nyasa. Eneo la katikati mwa Tanzania ni uwanda mkubwa, wenye tambarare na ardhi ya kilimo. Ukanda wa mashariki una joto na unyevunyevu, huku Visiwa vya Zanzibar vikiwa karibu. Maporomoko ya maji ya Kalambo katika mkoa wa kusini-magharibi mwa Rukwa ni maporomoko ya pili kwa urefu barani Afrika, na yanapatikana karibu na ufuo wa kusini-mashariki wa Ziwa Tanganyika kwenye mpaka na Zambia. Eneo la Hifadhi ya Menai Bay visiwani Zanzbar ndilo eneo kubwa zaidi la bahari lililohifadhiwa. Hali ya hewa Hali ya hewa inatofautiana sana ndani ya Tanzania. Katika nyanda za juu, halijoto huanzia 10 hadi 20 °C (50 na 68 °F) wakati wa msimu wa baridi na joto kwa mtiririko huo. Tanzania hupata majira ya joto katika miezi ya Desemba, Januari na Februari (25–31 °C au 77.0–87.8 °F) huku kipindi cha baridi zaidi kikitokea kati ya Mei na Agosti (15–20 °C au 59–68 °F). Halijoto ya kila mwaka ni 20 °C (68.0 °F). Hali ya hewa ni baridi katika maeneo ya milima mirefu. Tanzania ina vipindi viwili vikuu vya mvua: Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei ingawa zipo tofauti ndogo kati ya sehemu mbalimbali. Kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa. Mabadiliko ya hali ya hewa nchini Tanzania yanasababisha kuongezeka kwa joto na uwezekano mkubwa wa matukio ya mvua kubwa (kusababisha mafuriko) na vipindi vya ukame. Mabadiliko ya hali ya hewa tayari yanaathiri sekta za kilimo, rasilimali za maji, afya na nishati nchini Tanzania. Kupanda kwa kina cha bahari na mabadiliko ya ubora wa maji kunatarajiwa kuathiri uvuvi na ufugaji wa samaki. Tanzania ilitoa Mpango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NAPAs) mwaka 2007 kama ilivyoagizwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi. Mwaka 2012, Tanzania ilitoa Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kukabiliana na wasiwasi unaoongezeka wa athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi katika mazingira ya kijamii na kiuchumi. Wanyamapori na Hifadhi Tanzania ina takriban 20% ya spishi za wanyama wengi wa Afrika wenye damu moto, wanapatikana kwenye mbuga zake za Taifa, hifadhi na bahari. Hifadhi za Taifa na mbuga za wanyama zimeenea katika eneo la zaidi ya kilomita za mraba 42,000 (sq. mi 16,000) na kuunda karibu 38% ya eneo la nchi. Tanzania ina mbuga 21 za taifa, pamoja na hifadhi mbalimbali za wanyamapori na misitu, ikijumuisha Hifadhi ya Ngorongoro. Magharibi mwa Tanzania, Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni kitovu ya uchunguzi unaoendelea wa Jane Goodall wa tabia ya sokwe, ambao ulianza mwaka wa 1960. Tanzania ina bioanuwai nyingi na ina aina mbalimbali za makazi ya wanyama. Katika uwanda wa Serengeti nchini Tanzania, nyumbu (Connochaetes taurinus mearnsi), "bovids" wengine na pundamilia hushiriki katika uhamaji mkubwa wa kila mwaka. Tanzania ni nyumbani kwa takriban spishi 130 za amfibia na zaidi ya spishi 275 za wanyama watambaao, wengi wao wanapatikana Tanzania tu na wamejumuishwa katika orodha ya International Union for Conservation of Nature. Tanzania ina idadi kubwa ya simba Duniani. Tanzania ilikuwa na alama 7.13/10 kwenye Forest Landscape Integrity Index mwaka 2019, ilishika nafasi ya 54 duniani kati ya nchi 172. Miundo ya muungano Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar kufanyika mwaka 1964 Tanzania imekuwa na miundo ifuatayo: Nchi inatawaliwa na serikali ya muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania. Tanganyika au Tanzania bara haina serikali wala bunge la pekee. Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake vinavyoratibu mambo yasiyo ya muungano. Mambo yafuatayo yamekubalika kuwa shughuli za muungano: Mambo ya nje Jeshi Polisi Mamlaka ya dharura Uraia Uhamiaji Biashara ya nje Utumishi wa umma Kodi ya mapato, forodha Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu Utawala Muundo wa uongozi na utawala katika kipindi cha ukoloni ulizingatia mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mitatu ya dola yaani serikali, bunge na mahakama. Tangu uhuru, mgawanyo wa madaraka na uhusiano miongoni mwa mihimili hiyo uliimarishwa kwa kuzingatia wakati, mahitaji ya demokrasia na misingi ya utawala bora na umeainishwa pia katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 4 (1). Kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi pia kulikuwa hatua ya kuendelea kuimarisha utawala wa ushiriki wa wananchi kadiri mahitaji ya upanuzi wa maono na falsafa duniani. Ugatuzi, yaani mgawanyo wa kiutawala, unafuata Katiba ya nchi I 2.2. Tanzania imegawiwa kwa mikoa 31. Kila mkoa huwa na wilaya ndani yake. Jumla ya wilaya ni 169, ambazo kati yake 34 ni miji. Ndani ya wilaya kuna ngazi za tarafa (division) na kata (ward). Chini ya kata kuna vijiji na wakati mwingine ngazi ya chini tena ambayo ni vitongoji. Watu Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kwa wastani kuna mtu mmoja tu kwa kilomita ya mraba (1/km²), lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba na katika Mkoa wa Dar es Salaam ni 3,133 kwa kilomita ya mraba. Asilimia 70 hivi huishi vijijini, ingawa uhamiaji mijini unakwenda kasi. Makabila Jamii nyingi za watu zimeishi na kushirikiana katika eneo la Tanzania bara kwa milenia nyingi. Kati ya jamii hizo, nyingi zilikuja kutoka maeneo mengine ya Afrika. Nyingi katika jamii zilizohamia sehemu hii ziliingia katika makundi madogomadogo kwa amani, ingawa ziko zilizoingia kwa njia ya uvamizi na vita. Baadhi ya jamii zilizovamiwa zilijihami na kuwazuia wahamiaji wasiendelee kuteka maeneo mengine. Kufikia mwaka 1884, wakati Wajerumani walipoanza harakati za kufanya sehemu hii ya Afrika kuwa koloni lao, kulikuwa na makabila zaidi ya 120 katika eneo la Tanzania bara. Kuna makabila 125 hivi. Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya, Wajaluo na Wamakonde. Jambo la pekee kuhusu jamii zilizoishi na zinazoendelea kuishi Tanzania ni kwamba wakazi asili wanawakilisha makundi yote makuu manne ya lugha barani Afrika. 1. Idadi kubwa sana ya Watanzania ni wa jamii ya Wabantu (k.m. Wazaramo, Wapare na Wapogoro). 2. Nje ya hao, kuna Waniloti, kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya. 3. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome, Wasi na Waburunge. 4. Kuna kundi la Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; wanaitwa Wasandawe . Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika ya Kati. Pia kuna asilimia ndogo ya watu wenye asili ya nje ya bara la Afrika, kwa mfano Wahindi, Waarabu, Waindochina, Wafarsi, Wachina, Wagiriki na Waingereza. Hii ilisababishwa na karne za mchanganyiko wa mahitaji ya biashara yaliyofanywa na mabara ya Ulaya na Asia hapo Afrika. Lugha Nchini Tanzania kuna lugha za kikabila zaidi ya mia moja na ishirini, kwa kuwa kila kabila lina lugha yake. Kiswahili ndiyo lugha ya taifa na inazidi kuwa lugha mama kwa watoto wengi, hasa mijini. Walau asilimia 90 za wakazi wanakitumia walau kama lugha ya pili. Kiswahili ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu: hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini, kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu. Kiswahili kinatumika kama lugha baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo rasmi; kwa hiyo ni lugha rasmi ya dhati. Baada ya uhuru, Kiingereza (iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi na kwa elimu kuanzia sekondari ingawa sera mpya inataka Kiswahili kishike nafasi yake hadi chuo kikuu; kwa hiyo ilichukuliwa kama lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi rasmi wa Kiingereza umepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchukulia Kiswahili kama lugha rasmi ya dhati pekee. Sera mpya ya elimu inakusudia kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika ngazi zote kufikia mwaka 2024. Dini Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi inawezekana ni zaidi azimio la kisiasa. Kwenye funguvisiwa la Zanzibar idadi ya Waislamu huaminiwa kuwa takriban 97%. Usafiri Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Nyingine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani ya Bahari Hindi kuna pia usafiri wa meli. Hadi sasa idadi ya barabara za lami si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es Salaam, Mbeya katika kusini-magharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina barabara nzuri na mawasiliano ni magumu. Mashirika mawili ya reli yanayohudumia Tanzania: ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali. Huduma kwa ndege zinatumia hasa viwanja vya ndege 11 vyenye barabara ya lami kwa ajili ya ndege, hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro/Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni. Pia kuna viwanja vingine vya ndege kama vile uwanja wa ndege wa Mwanza, Bukoba na Kigoma. Usafiri wa majini pia unafanyika hasa katika bahari ya Hindi, ingawa hakuna meli ya serikali hapo na mashirika binafsi hutoa huduma. Usafiri wa majini hufanyika pia katika maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa. Miongoni mwa meli ni MV Bukoba iliyozama tarehe 21 Mei 1996 pamoja na abiria karibu 1,000 na MV Nyerere iliyozama tarehe 20 Septemba 2018 pamoja na abiria zaidi ya 200. Katika ziwa Tanganyika ipo meli ya Mv Liemba ambayo ilianza kutumika tangia kipindi cha ukoloni wa Wajerumani: inatoa huduma kati ya miji ya mwambao wa ziwa Tanganyika na nchi jirani. Mwaka 2017 ulianza ujenzi wa awamu ya kwanza ya njia ya geji sanifu nchini Tanzania inayolenga kuunganisha Dar es Salaam na Morogoro. Njia hii inatarajiwa kuendelea hadi Mwanza na hatimaye hadi Burundi. Urithi wa Dunia Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (mwaka wa kukubaliwa – jina la mahali) 1979 – Hifadhi ya Taifa Ngorongoro. 1981 – Hifadhi ya Serengeti. 1981 – Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara. 1982 – Hifadhi ya Taifa Selous. 1987 – Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro. 2000 – Mji Mkongwe wa Jiji la Zanzibar / Unguja. 2006 – Michoro ya Kondoa. Utamaduni na Sanaa Muziki Kuna aina zaidi ya tano za muziki nchini Tanzania, kama zilivyofafanuliwa na BASATA ni pamoja na ngoma (ngoma za asili), dansi, kwaya (muziki wa injili), taarab, na bongo flava (pop/hip hop). ). Ngoma ni muziki wa dansi wa kitamaduni, ngoma hutofautiana kati ya kabila na kabila. Dansi ni muziki wa bendi unatokana na muziki wa soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (au "rumba ya kikongo"). Taarab ni muziki wa Waafrika wa pwani uliopokea athira kutoka tamaduni nyingi, hasa muziki wa Waarabu na Wahindi. Kimsingi ni uimbaji wa mashairi unaofuata muziki wa bendi. Kwaya ni muziki ambao asili yake ni kanisani. Bongo flava ni muziki wa pop wa Tanzania uliozaliwa na muziki wa kizazi kipya, unajumuisha reggae, RnB, na hip hop, uliochanganywa na vionjo vya asili (flava) lakini tangu wakati huo umekua na kuwa muziki wa kipekee wa maeneo ya Maziwa Makuu. Asili mbalimbali za ushawishi zimesaidia kufanya bongo flava kuwa muziki maarufu zaidi Afrika Mashariki, na muziki mmojawapo kati ya ile maarufu zaidi katika bara la Afrika. Tangu kuundwa kwa Tanzania hadi 1993, kurekodi na usambazaji wote wa muziki ulisimamiwa kikamilifu na BASATA, hasa kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD). Ni aina 4 tu za muziki za Kitanzania zilizoruhusiwa kurekodiwa au kutangazwa, ambazo wakati huo zilikuwa ngoma, taarab, kwaya na dansi. Sheria ya Huduma za Utangazaji ya 1993 iliruhusu mitandao ya kibinafsi ya matangazo na studio za kurekodi. Haya ni mojawapo ya mabadiliko muhimu zaidi katika tasnia ya muziki ya Tanzania tangu kuanzishwa kwa nchi miaka 30 kabla. Miaka michache kabla ya Act ya 1993, muziki wa hip hop ulikuwa umeanza kuimarika katika miji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Mwanza. Ilikuwa ikianza mageuzi kutoka kwenye hip hop ya Kiingereza huko Uzunguni, maeneo tajiri kama Oysterbay na Masaki pamoja na shule za kimataifa, hadi kizazi kipya Uswahilini, vitongoji maskini na kutumia Kiswahili. Mara tu baada ya kufunguliwa kwa mawimbi ya redio, bongo flava ilizaliwa ikienea kwa haraka kote nchini, na katika Maziwa Makuu. Fasihi Utamaduni wa kifasihi wa Tanzania kimsingi ni wa simulizi. Tanzu na vipera maaarufu vya fasihi simulizi ni pamoja na ngano, mashairi, mafumbo, methali na nyimbo.  Sehemu kubwa zaidi ya fasihi simulizi iliyorekodiwa Tanzania ni ya Kiswahili, ingawa lugha za makabila ya Tanzania zina mapokeo yake ya simulizi.  Fasihi simulizi ya nchi imekuwa ikipungua kwa sababu ya mabadiliko ya muundo wa jamii, na kufanya uwasilishaji wa fasihi simulizi kuwa mgumu zaidi, pia teknolojia za kisasa zinachangia kushushwa kwa thamani ya fasihi simulizi. Utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu umeenea nchini Tanzania. Fasihi andishi nyingi za Kitanzania ni za Kiswahili au Kiingereza.  Watu mashuhuri katika fasihi andishi ya Tanzania ni pamoja na Shaaban Robert (anatambulika kama baba wa fasihi ya Kiswahili), Muhammed Saley Farsy, Faraji Katalambulla, Adam Shafi Adam, Muhammed Said Abdalla, Said Ahmed Mohammed Khamis, Mohamed Suleiman Mohamed, Euphrase Kezilahabi, Gabriel Ruhumbika, Ebrahim Hussein, May Materru Balisidya, Fadhy Mtanga, Abdulrazak Gurnah, na Penina O. Mlama. Uchoraji na Uchongaji Mitindo miwili ya sanaa ya Tanzania imepata kutambuliwa kimataifa. .  Uchoraji wa Tingatinga umejulikana tangu miaka ya 1970. Mtindo huo umepewa jina la mwanzilishi wake, mchoraji wa Kitanzania Edward Said Tingatinga. Kwa ujumla michoro ya Tingatinga inayoonyesha watu, wanyama, au maisha ya kila siku.  Baada ya kifo cha Tingatinga mwaka wa 1972, wasanii wengine walikubali na kuendeleza mtindo wake, na aina hiyo sasa ndiyo mtindo muhimu zaidi unaolenga utalii katika maeneo ya Afrika Mashariki.: Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Dar es salaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje. Michezo Mchezo maarufu nchini Tanzania ni mpira wa miguu. Ingawa mpira wa miguu (kandanda) unaongoza kwa ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana, michezo mingine kama vile mpira wa kikapu, mchezo wa ngumi na riadha inazidi kuwa maarufu miongoni mwa watu. Baraza la Michezo la Taifa ndicho chombo kinachosimamia michezo nchini chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni chombo kinachosimamia mpira wa miguu nchini. Vilabu maarufu vya soka la kulipwa jijini Dar es Salaam ni Young Africans F.C. na Simba S.C. Wachezaji wa kandanda ambao wamechezea klabu kubwa za kigeni ni pamoja na Mbwana Samatta, Kelvin John, na Morice Abraham. Tanzania iliandaa Kombe la Mataifa ya Afrika U-17 2019. Soka la wanawake ni mchezo unaokuwa kwa kasi zaidi Tanzania. Utamaduni wa wanawake kucheza mpira wa miguu umeanza kueleweka kwa wengie. Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Taifa Queens ni bingwa wa Michuano ya CECAFA kwa Wanawake kwa mwaka 2016 na mwaka 2018. Michuano hii huandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 17 'Serengeti Girls' ilifuzu kucheza Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake nchini India mwaka 2022. Hasheem Thabeet ni Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA).Mwanariadha wa zamani wa Tanzania wa mbio za kati, Filbert Bayi Sanka mwaka 1974 aliboresha rekodi ya mbio ya mita 1500, na mwaka wa 1975 aliboresha rekodi ya mbio ya maili moja. Bado anashikilia rekodi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ya mita 1500. Filamu Tanzania ina tasnia maarufu ya filamu inayojulikana kwa jina la "Bongo Movie". Studio nyingi za utayarishaji filamu za Kitanzania ziko Dar es Salaam. Kabla ya uhuru wa Tanzania mwaka 1961, baadhi ya sinema za kigeni zilirekodiwa Tanganyika na Zanzibar. Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar huandaa maonyesho ya filamu, warsha, muziki pamoja na sanaa zingine za maigizo. Tazama pia Orodha ya Mawaziri Wakuu wa Tanzania Orodha ya Mawaziri Wakuu wa Zanzibar Orodha ya Magavana Wakuu wa Tanganyika Orodha ya Masultan wa Zanzibar Orodha ya watu maarufu wa Tanzania Orodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneo Orodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la Taifa Orodha ya mikoa ya Tanzania na Maendeleo Utawala wa Kijiji - Tanzania Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Viungo vya nje Tanzania Corruption Profile from the Business Ani-Corruption Portal Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Jumuiya ya Madola Jumuiya ya Afrika Mashariki Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
1201
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi
Uhindi
Uhindi (pia: India) ni nchi kubwa ya bara la Asia, upande wa kusini, ikienea hasa katika rasi kubwa ya Bahari ya Hindi. Kwa eneo ina nafasi ya saba duniani, lakini kwa idadi ya wakazi (1,352,642,280 mwaka 2018) ni nchi ya pili baada ya China. Kati ya nchi za kidemokrasia ndiyo yenye watu wengi zaidi duniani. Tena inakadiriwa kwamba miaka ya hivi karibuni itapiku China. Imepakana na Pakistan, China, Nepal, Bhutan, Bangladesh na Myanmar. Kiutawala Uhindi ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo ya kujitawala 29 pamoja na maeneo ya shirikisho 7. Mji mkuu ni New Delhi, lakini mji mkubwa zaidi ni Mumbai. Historia Historia ya awali Binadamu walifika India kutoka Afrika kabla ya miaka 55,000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kama wawindaji-wakusanyaji waliozagaa barani, umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande wa urithi wa kibiolojia, ambayo inapitwa na Waafrika tu. Makazi ya kudumu yalianza magharibi, katika beseni la mto Indus, miaka 9,000 iliyopita, hata kuzaa ustaarabu maalumu (Indus Valley Civilisation) katika milenia ya 3 KK. Kabla ya ukoloni Kufikia mwaka 1200 KK, Kisanskrit cha Kale, mojawapo kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya, kilikuwa kimeenea India kutoka Kaskazini-Magharibi, kikawa lugha ya Rigveda, mwanzoni mwa dini ya Uhindu. Hivyo lugha za Kidravidi zikakoma kaskazini. Kufikia mwaka 400 KK, matabaka ya kudumu katika jamii yalikuwa yamejitokeza katika Uhindu. Hapo dini za Ubuddha na Ujaini zilitokea, zikipinga taratibu hizo za kibaguzi. Katika bonde la mto Gange yalianza madola ya Maurya na Gupta. Ndani yake hadhi ya wanawake ilirudi nyuma, na mtazamo wa kwamba baadhi ya watu hawatakiwi hata kuguswa ukaimarika. Huko India Kusini, Falme za Kati zilieneza maandishi na tamaduni vya lugha za Kidravidi kwa falme za Asia Kusini Mashariki. Kati karne za kwanza baada ya Kristo, dini za Ukristo, Uislamu, Uyahudi na Uzoroastro pia zilitia mizizi katika pwani za Kusini. Majeshi kutoka Asia ya Kati yalivamia kwa kwikwi mabonde ya India, hata kuunda usultani wa Delhi na kuingiza India Kaskazini katika umma wa Kiislamu. Katika karne ya 15 BK, Dola la Vijayanagara liliunda utamaduni wa kudumu wa Kihindu kusini mwa India. Katika Punjab, Usikh ulianzishwa, ukipinga dini rasmi. Dola la Mughal, mwaka 1526, liliwezesha karne mbili za amani na kuacha urithi wa usanifu majengo bora. Wakati wa ukoloni Uhindi wa Kiingereza ni kipindi cha historia ambapo nchi za Bara Hindi ama zilitawaliwa na Uingereza moja kwa moja ama zilikuwa chini ya usimamizi wa Uingereza kama nchi lindwa. Utawala huo ulienea juu ya Uhindi wa leo pamoja na Pakistan, Bangladesh, Nepal na kwa muda pia juu ya Burma (Myanmar). Utawala wa Kiingereza ulikuwa na vipindi viwili vifuatavyo: Utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki (British East India Company) Tarehe 31 Desemba 1600 malkia Elizabeth I alitoa hati ya ulinzi wa kifalme kwa biashara kati ya Uingereza na "Uhindi wa Mashariki". Kampuni iliyopokea hati hii ilikuwa kundi la wafanyabiashara na matajiri wa London waliovutwa na utajiri wa nchi za mashariki na hasa na faida kubwa mikononi mwa wafanyabiashara Wareno na Waholanzi waliotangulia katika biashara kati ya Ulaya na nchi za Asia ya Kusini. Kampuni ilishindana kibiashara na kivita na wafanyabiashara wa Ureno, wa Uholanzi na wa Ufaransa. Iliweza kununua au kuvamia vituo vya biashara na kujenga maboma yake kuanzia mwaka 1644 huko Bombay, Madras na penginepo. Mwaka 1717 kampuni ilipata kibali cha mtawala wa Moghul cha kusamehewa kodi kwa biashara katika Ubengali. Tangu mwaka 1680 kampuni ilianzisha jeshi lake la maaskari Wahindi na kuwa mshiriki katika siasa ya Uhindi. Kati ya miaka 1756 na 1763 Uingereza pamoja na mataifa mengine ya Ulaya ilishiriki katika Vita vya miaka saba viliyokuwa vita vya kwanza vya kimabara. Waingereza walipigana pamoja na Prussia dhidi ya Austria, Ufaransa, Urusi na Uswidi. Jeshi la kampuni liliendesha vita hivyo dhidi ya maeneo ya Ufaransa katika Uhindi. Wafaransa walishindwa wakabaki na vituo vidogo tu katika miji kama Pondicherry na Mahe lakini kampuni iliongeza maeneo yake katika Uhindi. Baada ya mwaka 1757 Kampuni ya Kiingereza ilikuwa enzi muhimu, iliweza kushindana hata na nguvu ya Moghul. Ilianza kutawala sehemu kubwa za Uhindi wa Kusini pamoja na Ubengali. Kampuni ilitumia mbinu mbili: mikataba na madola ya watawala wa Kihindi waliokubali kupokea mabalozi wa kampuni kwao waliokuwa kama washauri wakuu wa Maharaja au Nawab wa eneo; siasa ya nje na mambo ya jeshi ziliwekwa chini ya kampuni uvamizi na utawala wa moja kwa moja, maeneo yale yalikuwa mali ya kampuni. Mafaniko makubwa ya kampuni yalisababisha mgogoro huko Uingereza na sheria mbalimbali za bunge la Uingereza zililenga kuongeza athira ya serikali ya Uingereza juu ya shughuli za kampuni. Katika karne ya 19 kampuni ikawa mtawala wa sehemu kubwa za Uhindi, ama kwa njia ya mikataba na watawala wa kienyeji au kwa utawala wa moja kwa moja. Kampuni ilianza kubadilisha uso wa India kujenga reli na kuanzisha mawasiliano wa kisiasa kwa huduma ya posta na pia simu za telegrafi. Mwaka 1857 ilitokea uasi wa wanajeshi Wahindi wa jeshi la kampuni uliosababisha na mkasi wa mabadiliko na dharau ya viongozi Waingereza kwa utamaduni wa wenyeji. Utawala wa kampuni ulianza kuporomoka; uliokolewa tu kwa kupeleka Uhindi wanajeshi kutoka Uingereza. Uasi ulikomeshwa kwa mabavu. Lakini kuingilia kati kwa serikali ya Uingereza kulikuwa mwisho wa utawala wa kampuni. Mwaka 1858 serikali ya London ilichukua madaraka yote ya kampuni ikafanya Uhindi kuwa koloni la taji la Uingereza. Utawala wa kiserikali kati ya 1858 hadi 1947 Kuanzia mwaka 1858 Uhindi ulitawaliwa kama koloni la Uingereza. Kaisari wa mwisho wa Moghul Bahadur Shah Zafar II aliondolewa nchini. Malkia Viktoria wa Uingereza alichukua cheo chake akaitwa "Kaisari wa Uhindi" (kwa Kiingereza: "Empress of India"; kwa Kihindi: "Padishah-e-Hind") akamuachia utawala gavana wake aliyepewa cheo cha "makamu wa mfalme" (Vice-Roy). Muundo wa utawala uliendelea: maeneo ya kampuni yalikuwa makoloni ya Uingereza. Maeneo ya watawala Wahindi yalibaki yalivyo lakini kila Maharaja au Nawab alipaswa kula kiapo cha utii kwa malkia kama Kaisari au malkia mkuu wa Uhindi na kumkubali mshauri Mwingereza katika jumba lake kama mwakilishi wa Uingereza. Mwisho wa karne ya 19 harakati za kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru. Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu". Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili. Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga. Baada ya uhuru Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi. Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu. Mgawanyiko wa kiutawala Hii ni orodha ya majimbo ya Uhindi: Watu Lugha ya taifa ni Kihindi, ambacho ni lugha ya Kihindi-Kiulaya, pamoja na Kiingereza ambacho pia ni lugha rasmi. Kuna lugha 21 kubwa na lugha nyingi zisizo na wasemaji wengi sana. Kusini mwa Uhindi watu husema lugha za Kidravidi kama Kikannada, Kitelugu, Kitamil na Kimalayalam. Kaskazini husema hasa Kipunjabi, Kibengali, Kigujarati na Kimarathi. Lugha ndogo chache ambazo si lugha za Kihindi-Kiulaya (74 %) wala za Kidravidi (24 %) ni lugha za Kisino-Tibeti, lugha za Kiaustro-Asiatiki na lugha za Kitai-Kadai. Visiwani mwa Andaman, kulikuwa na lugha za Kiandamani lakini nyingi zao zimeshatoweka kabisa. Wakazi walio wengi (79.8 %) hufuata dini ya Uhindu. Takriban 14.2 % ni Waislamu; hivyo Waislamu wa Uhindi ni jumuiya ya tatu katika umma wa Kiislamu duniani baada ya Waislamu wa Indonesia na Pakistan. Dini nyingine ni Ukristo (2.3 %), Usikh (1,7 %), Ubuddha (0.7 %), Ujain (0.4 %), Uzoroastro na Bahai. Tazama pia Majimbo ya Uhindi Orodha ya lugha za Uhindi Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Viungo vya nje Tovuti rasmi India Travel Uhindi katika Curlie (ex-Open Directory Project) India profile from the BBC News India Encyclopædia Britannica entry Indiaat the UCB Government Information Library (archived from original) Nchi za Asia Jumuiya ya Madola
1203
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki
Afrika ya Mashariki
Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Kihindi. Kadiri ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Mashariki ina nchi 18 zifuatazo: (mji mkuu Bujumbura) (mji mkuu Jibuti (mji)) (mji mkuu Asmara) (mji mkuu Addis Abeba) (mji mkuu Nairobi) Komori (mji mkuu Moroni) Madagaska (mji mkuu Antananarivo) (mji mkuu Lilongwe) Morisi (mji mkuu Port Louis) (mji mkuu Maputo (mji mkuu Kigali) (mji mkuu Lusaka) Shelisheli (mji mkuu Victoria) (mji mkuu Harare) (mji mkuu Mogadishu) Sudan Kusini (mji mkuu Juba) (mji mkuu Dodoma) (mji mkuu Kampala) Mayotte na Réunion, zilizokuwa makoloni na sasa ni mikoa ya Ufaransa, zinahesabiwa pia katika orodha hii. Hata hivyo: Malawi, Zambia na Zimbabwe wakati mwingine zinehesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kusini (zamani zilikuwa pamoja kama Rhodesia ya Kusini, Rhodesia ya Kaskazini na Unyasa katika Shirikisho la Afrika ya Kati) Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na Réunion ni visiwa vidogo vya Bahari Hindi vinavyohesabiwa kuwa sehemu za Afrika ya Mashariki. Historia Afrika ya Mashariki inatajwa na sayansi kuwa mahali ambako watu wa kwanza duniani walikopatikana. Majina ya miji ya Afrika ya Mashariki imetajwa mara ya kwanza katika Periplus ya Bahari ya Eritrea (karne ya 1 B.K.). Tangu uenezaji wa ukoloni wa Kizungu upande wa Mashariki wa bara ulianza kuitwa Afrika ya Mashariki. Somalia, Eritrea na Ethiopia za leo zilitawaliwa na Italia kama "Afrika ya Mashariki ya Kiitalia" (Africa Orientale Italiana) katika miaka ya 1936 hadi 1941, Kenya ilitwaliwa na Uingereza kwa jina la "Afrika ya Mashariki ya Kiingereza" (East Africa Protectorate au pia British East Africa) hadi 1920, Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi zilijulikana kama "Afrika ya Mashariki ya Kijerumani" (Deutsch Ostafrika) hadi 1919 na Msumbiji iliitwa mara nyingi "Afrika ya Mashariki ya Kireno" (África Oriental Portuguesa) hadi uhuru. Lugha Wakazi wengi wa Afrika ya Mashariki ni wasemaji wa lugha za Kibantu; sehemu ya kaskazini wasemaji wa lugha za Kihamiti ni wengi (Waoromo, Wasomalia). Katika Ethiopia kuna wasemaji wengi wa lugha za Kisemiti. Pia kuna wasemaji wa lugha za Kiniloti na lugha za Khoisan. Ushirikiano wa nchi za Afrika ya Mashariki Nchi mashuhuri zaidi katika sehemu hii ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa sababu ya kutumia lugha moja katika mawasiliano baina ya wananchi wa sehemu hii, yaani Kiswahili. Aghalabu nchi za Afrika ya Mashariki zinazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kati yao, kwani katika nchi hizi kuna makabila mengi sana na kila kabila lina lugha yake ambayo kawaida inatumika nyumbani baina ya watu wa kabila moja, lakini wakitaka kuwasiliana na makabila mengine, mara nyingi hutumia lugha ya Kiswahili, na hii ni kwa sababu lugha hii ndiyo iliyoenea zaidi na kufahamika zaidi katika eneo hili la dunia. Nchi za Afrika ya Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Tanzania ni nchi ambazo ni karibu tangu zamani. Zimeshirikiana historia, zote zimekaliwa hasa na makabila yanayotumia lugha za Kibantu (Kenya na Uganda wana pia idadi muhimu ya wakazi wasiotumia lugha za Wabantu). Katika nchi zote tatu lugha ya Kiswahili imekuwa lugha muhimu ingawa kwa daraja mbalimbali. Wakati wa ukoloni zilitawaliwa na Uingereza iliyoacha taasisi na taratibu mbalimbali zilizosaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa uhuru. Tanzania, Kenya na Uganda zina ukubwa wa eneo la maili za mraba; Tanzania 360,000 ikifuatiwa na Kenya 224,960 na Uganda 93,980 upande wa mashariki nchi hizi zimepakana na bahari ya Hindi na upande wa kaskazini mashariki zimepakana na Somalia, upande wa kaskazini zimepakana na Ethiopia na Sudan Kusini upande wa magharibi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jamuhuri ya Rwanda na Burundi, kusini ni Zambia, Malawi na Msumbiji. Nchi hizi zimepitiwa na mstari wa ikweta, umepita Kenya na kusini mwa Uganda. Kenya na Tanzania zina ukanda wa pwani wenye bandari za Mombasa; Tanga; Bagamoyo; Dar es Salaam; Zanzibar; Kilwa na Mtwara. Afrika ya Mashariki
1204
https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu
Simu
Simu (kutoka Kiarabu سیم, sim, inayomaanisha "waya") ni chombo cha mawasilianoanga kinachotumia umeme. Matumizi ya simu ni kwa ajili ya watu wawili walio katika sehemu mbili tofauti kuongea. Awali simu ilihitaji iunganishwe na nyaya, lakini leo hii inaweza kutumia redio. Hiyo inaitwa nyayatupu, siwaya au simu bila waya. Historia Watu wengi wanaamini kuwa simu iligunduliwa mnamo 1876 na Alexander Graham Bell, Mskoti mwenye umri wa miaka 29 aliyeishi nchini Marekani. Lakini Mwitalia Antonio Meucci alianzisha matumizi ya simu toka mwaka wa 1871 hukohuko Marekani. Tangu mwishoni mwa karne ya 20 kuna aina mpya ya simu iliyoenea ambayo ni simu ya mkononi. Ingawa haistahili kweli kuitwa tena "simu" kwa maana asilia kwa sababu hakuna simu, ni aina ya mtambo wa mawasiliano uliosambaa haraka sana. Katika nchi nyingi za Afrika simu hizi zina faida ya pekee kwa sababu zinaruhusu mawasiliano hata pale ambako nyaya za Posta hazifiki. Namba za simu Kila simu inapaswa kuwa na namba ya pekee ikiunganishwa katika mtandao wa simu. Isipokuwa ofisi au kampuni inaweza kuwa na namba moja kwa simu zake zote halafu maungio ya simu ya ndani ambako ama mtu au mtambo unaunganisha simu za ndani na mtandao wa nje. Kwa kawaida mtandao wa simu ndani ya nchi inagawiwa kwa maeneo. Maeneo haya yanaweza kugawiwa tena hadi ngazi ya mtandao wa mahali. Kila eneo linafikiwa kupitia namba ya eneo; ndani ya eneo inatosha kutumia namba ya simu yenyewe. Mfano: simu ya namba 556677 iko mjini Dar es Salaam. Namba ya eneo la Dar es Salaam ni 022. Kufikia simu hii ndani ya eneo la Dar es Salaam inatosha kupiga 556677. Mtu anayetaka kuipigia kutoka Dodoma au Arusha anatangulia namba ya eneo na kupiga 022-556677. Simu za mkononi huunganishwa katika mtandao mkubwa wa kitaifa kufuatana na kampuni inayotoa huduma kama vile Airtel, TIGO au TTC yenye mtandao wake wa pekee. Kwa teknolojia bila waya hakuna haja ya ugawaji wa kieneo. Lakini kwenye simu hizi ni lazima kutumia pia namba ya mtandao muda wote. Kwa kupiga simu ya kawaida kutoka simu ya mkononi ni lazima kutumia muda wote namba ya kieneo hata kama mwenye kupiga yuko mji uleule maana mitandao ni tofauti. tazama pia: Namba za simu Tanzania Marejeo Viungo vya nje Kikokotozi cha nambari ya simu kwa simu za kimataifa Mawasiliano Simu Teknolojia
1208
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiido
Kiido
Kiido ni lugha ya kupangwa. Inafanana sana na Kiesperanto, lakini haizungumzwi na watu wengi kama Kiesperanto. Serufi Nomino (majina) zote zinahitimu kwa kiambishi tawali -o, kwa mfano "arbo" (mti). Wingi wa nomino unahitimu kwa -i (arbi = miti). Vivumishi vinahitimu kwa kiambishi tawali -a, kwa mfano "alta" (-refu). Vitenzi vina viambishi tamati mbalimbali: -ar inatumika kwa vitenzi-jina (kwa mfano "facar" = "kufanya") -as inatumika kwa njeo ya wakati uliopo (kwa mfano "me facas" = "ninafanya" -is inatumika kwa njeo ya wakati uliopita (kwa mfano "me facis" = "nilifanya" au "nimefanya") -os inatumika kwa njeo ya wakati ujao (kwa mfano "me facos" = "nitafanya") -us inatumika kwa hali a masharti (kwa mfano "me facus" = "ningefanya") -ez inatumika kwa hali ya kuamuru (kwa mfano "facez!" = "fanya!"; "il facez" = "afanye") Viungo vya nje http://www.ido.li Wikipedia ya Kiido http://io.wiktionary.org Lugha Lugha saidizi ya kimataifa
1663
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mungu
Mungu
Mungu ni jina lenye asili ya Kibantu linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu. Kati ya wafuasi wa dini hizo, wengi wanaona kuwa Umungu, kwa jinsi ulivyo au unavyofirika, haukubali mgawanyiko. Hasa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu wanasisitiza umoja wa Mungu kuwa ndio msingi wa imani yao. Kwao Mungu ni wa milele, anafahamu yote na kutaka hasa uwepo wa viumbe. Tena kwa hiari yake alipenda kujifunua kwa binadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywa rafiki yake na baba wa waamini wote. Kuna dini nyingine zinazokubali kuwepo kwa miungu mbalimbali (wawili au zaidi). Hasa dini nyingi za jadi zinaamini wingi wa miungu. Dini kubwa duniani inayosadiki miungu mingi ni Uhindu. Pia katika sehemu za Afrika ya Magharibi ibada za miungu mingi zinaendelea hadi leo. Mungu na miungu katika dini asilia za Kiafrika Jamii za Afrika zilikuwa na dini zao ambamo tunaweza kuona imani katika nguvu za kiroho ambazo zinaitwa majina tofauti. Tunaweza kukuta imani ya Mungu Mkuu, pia ya miungu mbalimbali, pamoja na imani ya kuwepo kwa roho za wahenga, mizimu na pepo mbalimbali. Tukijiuliza juu ya uhusiano kati ya mizimu, roho, miungu mbalimbali na Mungu Mkuu, ni lazima kwanza tujue imani za jadi hutofautiana kutoka jamii moja hadi jamii nyingine. Mara ningi imani za Kiafrika humwona Mungu Mkuu mmoja kuwa wa juu na mwenye nguvu zaidi. Yuko kabla ya kila kitu kingine na asili yake haijulikani. Hivyo nguvu hutazamwa kwa ngazi tofauti; Mwenyezi Mungu yuko juu, chini yake kuna roho mbalimbali au hata miungu pamoja na nguvu za asili, na mwishoni binadamu wasio na nguvu nyingi. Wakati mwingine hadithi za uumbaji za Kiafrika zinamwonyesha Mungu akiwa au akienda mbali na watu au hawasiliani nao tena moja kwa moja. Anaacha washughulikiwe na roho au miungu midogo aliyoumba pia. Mungu wa aina hiyo anaonekana mbali sana na mambo ya binadamu; kwa sababu hiyo, mara kwa mara miungu midogo huombwa badala yake ili kupata usaidizi. Katika jamii nyingine wanaamini kwamba mizimu inaweza kuleta mawasiliano baina ya Mungu na binadamu. Vikundi vingine humwona Mungu Mkuu kuwa karibu sawa na miungu mingine, kama mwenyekiti wao au kama mfalme kati ya machifu. Wafon katika Afrika ya Magharibi humwaza Mungu mkuu kama mapacha mawili: Mavu, nguvu ya kike, na Lisa, nguvu ya kiume. Wakitazamwa kama nguvu moja huitwa Mavu pekee. Wameumba watoto ambao hutawala shughuli za dunia na viumbe vyake kama miungu. Dhana za aina hiyo zimeleta majadiliano kati ya wataalamu kuhusu kuainisha dini za Kiafrika kuwa za Mungu mmoja (monotheistic) au za miungu mingi (polytheistic). Wengine huona uainishaji huo hauna maana kwa dini za Kiafrika. Mtaalamu John Mbiti wa Kenya aliona kwamba kimsingi imani katika Mungu mmoja inapatikana kwa namna moja au nyingine katika dini zote za asili. Anaeleza nguvu nyingine za kiroho kama tabia au shughuli za Mungu yeye yule zinazotazamwa pekepeke. Mungu katika Biblia Biblia inaanza kwa kukiri kwamba asili ya uhai wote ni Mwenyezi Mungu: “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwa 1:1). Tena, kwamba Mungu anazidi kushughulikia viumbe vyake, akividumisha na kuviongoza vyote vifikie lengo alilovipangia. “Ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu” (Mdo 17:28). Tunamtegemea pande zote: angetuacha kidogo tungetoweka mara. Yesu alipolaumiwa kwa kuponya watu siku ya pumziko, alijitetea kwamba, “Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi” (Yoh 5:17). "Yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu" (1Pet 5:7). Kutokana na imani hiyo, tunahimizwa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua. “Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je, si bora kupita hao?” (Math 6:26). “Nawe una nini usichokipokea?” (1Kor 4:7). “Nimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?” (Zab 116:12). Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu. “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake” (Rom 1:20). Hivyo tunaweza pia kusema juu ya Mungu kuanzia wema, ukweli na uzuri wa viumbe vyake na kumsifu kiasi chetu kwamba ndiye wema, ukweli na uzuri wenyewe. Lakini tukiri pia kuwa maneno yetu duni hayawezi kutosha kamwe kufafanua fumbo lake. “Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua” (Ayu 42:3). Tungemuelewa, asingekuwa Mungu. Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote. “Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutiki” (Ayu 36:26). “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24). Akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. “Roho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39). Hasa Mungu amejifunua kuwa upendo wenyewe. “Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli” (Kut 34:6). “Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake” (1Yoh 4:16). “Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8). Marejeo Pickover, Cliff, The Paradox of God and the Science of Omniscience, Palgrave/St Martin's Press, 2001. ISBN 1-4039-6457-2 Collins, Francis, The Language of God: A Scientist Presents Evidence for Belief, Free Press, 2006. ISBN 0-7432-8639-1 Miles, Jack, God: A Biography, Vintage, 1996. ISBN 0-679-74368-5 Armstrong, Karen, A History of God: The 4,000-Year Quest of Judaism, Christianity and Islam, Ballantine Books, 1994. ISBN 0-434-02456-2 Paul Tillich, Systematic Theology, Vol. 1 (Chicago: University of Chicago Press, 1951). ISBN 0-226-80337-6 Viungo vya nje Concept of God in Christianity Concept of God in Islam God Christian perspective Hindu Concept of God Jewish Literacy Mystical view of God Relation of God to the Universe Discussion about God in Germany 2009 Mungu Mungu Dini Uyahudi Ukristo Uislamu Teolojia Falsafa
1664
https://sw.wikipedia.org/wiki/Volkeno
Volkeno
Volkeno (pia: volkano au volikano) ni mahali ambako zaha inatoka nje ya uso wa ardhi. Mara nyingi - lakini si kila mahali - volkeno imekuwa mlima. Volkeno huwa na kasoko yaani shimo ambako zaha na gesi zinatoka nje. Asili ya jina Asili ya jina ni mungu wa dini ya Roma ya Kale aliyeitwa "Vulcanus". Kati ya miungu ya Kiroma alihusika na moto, radi na uhunzi; kwa hiyo aliheshimiwa hasa na wote waliotumia moto kwa kuyeyusha metali kama chuma au shaba. Volkeno na ganda la dunia Volkeno ni dalili ya kwamba mahali pake ganda la dunia si nene sana, hivyo joto la ndani linapata njia ya kutoka nje. Volkeno huanza katika tambarare. Zaha hutoka katika hali ya kiowevu; ikipoa haraka inaganda kuwa mwamba na hujenga mlima wa kuzunguka shimo la kasoko yake. Milima ya aina hiyo inaweza kukua sana. Mfano wa volkeno kubwa ni Kilimanjaro. Miamba yake yote ilijengwa na zaha iliyotoka ndani ya dunia. Volkeno nyingi hutokea pale ambako mabamba ya ganda la dunia yanaachana au kusukumana. Hivyo volkeno hutokea hasa kwenye mistari ya kukutana kwa mabamba hayo. Sababu nyingine ya kutokea kwa volkeno ni kuwepo kwa chumba cha magma ndani ya ganda la dunia. Volkeno hai na volkeno bwete Volkeno inaweza kupatikana kama volkeno hai inayoendelea kutema moto, gesi na majivu. Inaweza pia kuonekana kama volkeno bwete inayokaa kama milima mingine bila kuonyesha dalili za moto. Lakini kutokana na umbo na tabia za miamba yake inaonekana mlima huu ulijengwa kwa njia ya kivolkeno. Volkeno bwete inaweza kuamka tena. Mara nyingi kuwepo kwa chemchemi za maji ya moto au kutokea kwa gesi kwenye sehemu fulani ni dalili ya kwamba bado kuna njia kati ya mlima na magma ya chini. Kipindi kati ya milipuko kinaweza kuwa cha miaka mingi. Mlipuko wa volkeno *Angalia makala kuu: Mlipuko wa volkeno Mlipuko wa volkeno ni hatari kwa ajili ya wanadamu na mazingira. Mlipuko unaweza kurusha idadi kubwa ya gesi sumu na mawe ya moto hewani na kumwaga lava nje inayosambaa kama mto wa moto kwa umbali wa kilomita kadhaa. Hiyo hatari ni kubwa zaidi pale ambako volkeno ililala kama volkeno bwete kwa miaka mingi, labda elfu kadhaa. Hapo mara nyingi watu wamevutwa na udongo wenye rutuba kutokana na majivu ya volkeno wajenge makazi na kulima. Kama hapo volkeni inageuka kuwa hai tena hatari ni kubwa. Kuna mifano ya vifo vingi vilivyosababishwa na volkeno. Hasara inategema kama miji iko karibu na volkeno au la, na kama serikali zina huduma za kutazama volkeno na kuonya watu watoke mapema wakati dalili za kwanza zinatokea. Kati ya mifano ya milipuko mikali inayojulikana zaidi ni: mlipuko wa volkeno ya Vesuvio, Italia. Iliharibu miji ya Pompei na Herkulaneo mwaka 79 BK. mlipuko wa volkeno ya Krakatau, Indonesia mwaka 1883. Ilirusha mavumbi mengi angani kiasi kilichoonekana kote duniani mlipuko wa volkeno Nevado del Ruiz, Kolombia mwaka 1985 uliua watu 25.000 kutokana na kuyeyusha theluji na barafu mlimani na kusababisha mafuriko ya ghafla Katika karne ya 21 volkeno ya Nyiragongo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ililipuka mara mara mbili mwaka 2002 na mwaka 2021 na kusababisha vifo katia miji jirani ya Gisenyi na Goma. Ol Doinyo Lengai ni volkeno ndogo iliyolipuka Tanzania kaskazini mwaka 2006. Tazama pia Orodha ya volkeno nchini Tanzania Volkeno
1665
https://sw.wikipedia.org/wiki/Tofaa
Tofaa
Tofaa (pia: tufaha; kutoka kar. تفاح tofah; kwa Kiingereza: apple) ni tunda la mtofaa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Maua nyeupe hutoa tunda lenye umbo mviringo na kipenyo cha sentimita 5 - 9. Asili ya mimea iko Asia. Leo kuna takriban aina 7,500 za matofaa. Mavuno ya kila mwaka hufikia tani milioni 55. Nchi zinazovuna matofaa hasa ni China, Marekani, Uturuki, Ufaransa, Italia na Uajemi. Utangulizi Tufaa ni tunda la mtufaa (Malus pumila), mti wa familia Rosaceae. Ni miongoni ya miti inayokuzwa kwa wingi sana. Mti ni mdogo na wenye kupukutisha majani yake, wenye kufikia urefu wa mita 3 mpaka 12 za kimo, na kushona kwa majani mengi kwelikweli. majani yake yamejipanga kwa namna tofauti tofauti, yakiwa na urefu wa sm 5 – 12 na upana wa sm 3 – 6 kwa upana. Maua mengi huchanua majira ya kuchipua sambamba na kufunguka kwa vichipukizi. Maua ni meupe na alama kidogo za rangi ya waridi ambayo hufifia taratibu. Mfaua hayo huwa na petali tano, na yana upana wa sm 2.5 mpaka 3.5. kwa kipenyo. Matunda hukomaa msimu wa kuchipua, na huwa yamefikia kipenyo cha sm 5 – 9. Katikati mwa tunda huwa na kapeli tano zilizojipanga muundo kama wa nyota tano, huku kila kapeli moja ikiwa na mbegu moja mpaka tatu hivi. Mti huu asili yake ni Asia ya Kati, ambako miti pori ya kale ya tufaa bado inapatikana mpaka leo. Sasa hivi kuna zaidi ya aina ya miti ya tufaa 7,500 inayofahamika inayopelekea kuwa na kila aina ya tabia ya miti ianyotakiwa kwa eneo husika. Aina hizo zinatofautiana kwa mazao yao na ukubwa wa miti yenyewe, hata kama yakipandwa katika shina moja. Zaidi ya tani milioni 55 za matufaa zilizalishwa duniani kote ndani ya mwaka 2005, kwa thamani ya takribani dola za kimarekani bilioni 10. China pekee ilizalisha karibu 35% ya jumla hii. Marekani ni ya pili kwa uzalishajji, kwa zaidi ya 7.5% uzalishaji duniani. Uturuki, ufaransa, Italia na Irani pia wazalishaji wazuri wa tufaa. Aina inayoongoza ni ile ya pori ya "Malus sieverii", inayopatikana huko kati mwa Asia, kusini mwa Kazakstani, Krygyzstani, Tajikistani na Xinjiang, China, na awkati mwingine Malus sylvestris. Historia Mwanzo wa kuchipua kwa jenasi ya Malus ni huko Uturuki Mashariki. Mtufaa pengine ndio ukawa mti wa kwanza kuanza kulimwa na binadamu, na matunda yake yamekuwa yakiboreshwa kwa uchaguzi maalumu kwa miaka maelfu. Mfalme, "Alexander the Great", huonwa ndiye mgunduzi wa miti mifupi ya tufaa huko Asia Ndogo mnamo 300 KK, ambayo baadae ilipelekwa Macedonia. Tufaa za kipupwe, ambazo huchumwa mwishoni mwa msimu wa kuchipua na kuhifadhiwa katika baridi kali, kimekuwa chakula mihimu kwa Asia na Ulaya kwa miaka mingi , hali kadhalika na kwa Marekani na hata huko Argentina. tufaa zilipelekwa Amerika ya kaskazini na wakoloni miaka ya 1600, na mti wa tufaa wa kwanaza huko Amerika ya Akskazini wasemekana kuwa huko Boston, mwaka 1625.mwaka 1900, miradi ya kilimo cha umwagiliaji ilianza kuruhusu kilimo cha matunda kilichogharimu mabilioni, huku tufaa zikiwa ndiyo spishi zinazoongoza. Uzalishaji wa tufaa Kwa kawaida huko msituni tufaa huzaliana kwa mbegu. Hata hivyo, kama yalivyo matunda mengi yanayokua zaidi ya mwaka mmoja, huweza kupanda kwa vichipukizi. Hii ni kwasababu matunda mengi yanayokuzwa kwa mbegu, huweza kuzalisha mmea wenye tabia tofauti kabisa baina yamimea – wazazi, na zinaweza kuwa zenye hasara kubwa. spishi nyingi imara huzalishwa kwa kuchanaganya vizalia vya mimea mbalimbali. Uchavushaji Tufaa lazima zipate uchavushaji kila mwaka ili kuzalisha matunda. Kila msimu wa maua, wakulima wa tufaa lazima waandae wachavushaji kwaajili ya kubeba poleni. Nyuki wa asali hutumika kwa kazi hii, hasa wale wa aina ya Orchard mason bee, na hutumika kwma msaada wa uchavushaji kwenye mashmba ya biashara. Pia wakati mwingine nyuki aina ya "Bumble bee queens" huwepo mashambani kwa kazi hiyo hiyo. Kukomaa na mavuno Aina mbalimbali za tufaa hutofautiana kwa mazao na ukubwa wa miti, hata kama yakikuzwa kwenye shina moja. Kama baadhi ya miti isipopunguzwa hukua na kuwa miti mikubwa kwelikweli, lakini hufanya uvunaji uwe mgumu. Miti ya kawaida iliyokomaa huzalisha kg 40 – 200 za tufaa kila mwaka, japo uzalishaji unaweza kukarubia hata sifuri kwene misimu mibaya. Tufaa huvunwa kwa ngazi tatu zinazofungwa kwenye miti. Miti midogo hutoa karibu kg 10 – 80 za tufa kwa mwaka. Uhifadhi Kibiashara, tufaa huhifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye joto maalumu ili kuratibu kiwango cha kuiva kwa nyakati maalumu kwa kutumia kemikali maalumu. Hutunzwa kwenye chemba zenye kiwango kikubwa cha gesi ya ukaa (kaboni daioksaidi) na hewa iliyochujwa vizuri. Hii huzuia ili kemikali maalumu, ethylene, inayotumika kuivisha matunda isiongezeke na hivyo kuivisha matunda hovyo. Yakiwa nyumbani kwajili ya matamizi, tufaa huweza kuhifadhiwa kwenye jokofu za kawaida kwa majuma mawili hivi, kwenye sehemu zenye baridi hasa chini ya 5 °C. Faida za kiafya Ule msemo “tufaa moja kwa siku, humweka dokta mbali,” huonesha faida za tufaa tangu karne ya 19. Tafiti zinaonesha tufaa hupunguza uwezekano wa mtu kupata kansa ya utumbo mkubwa, tezi ya uzazi (prostate) na hata kansa ya mapafu. ukilinganisha na matunda mengine, tufaa zina kiwangio kidigo cha vitamin C, lakini zina kiwango kikubwa cha kampaundi za antioxidant.Kiwango cha makapi, ambacho ni kidogo kuliko kwenye matunda mw=engine husaidia kuratibu mizunguko ya tumbo na hivyo kupunguza uwezakano wa kansa ya utumbo mkubwa. Husaidia pia kupunguza magonjwa ya moyo, kupunguza uzito, na kiwango cha mafuta kwenye mishipa ya damu na moyo, kwa kuwa na kiasi kikubwa cha kalori kama ilivyo kwa matunda mengi na mbogamboga. Marejeo Matunda
1667
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiazi%20cha%20kizungu
Kiazi cha kizungu
Kiazi cha kizungu, kiazi ulaya, kiazi mviringo au mbatata ni mmea wa chakula uliomo katika familia ya Solanaceae. Chakula ni sehemu nene za mizizi yake (kiazi) yenye wanga, vitamini na madini. Sehemu bichi zinazoonekana juu ya ardhi haziliwi ni sumu. Viazi hivi ni chakula muhimu kimataifa ni chakula kikuu katika nyingi. Asili ya mmea iko Amerika ya Kusini ilipoteuliwa na kukuzwa na Maindio. Wahispania walikikuta Amerika na kuisambaza Ulaya. Hata hivyo wakati mwingine huitwa "kiazi ulaya" au "kiazi kizungu" kwa sababu imefika Afrika kupitia Ulaya. Picha Mnavu na jamaa Mbegu za mimea Mimea ya mazao Chakula
1675
https://sw.wikipedia.org/wiki/Seattle%2C%20Washington
Seattle, Washington
Seattle ni mji wa jimbo la Washington (ncha ya kaskazini magharibi ya Marekani). Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2018, mji una wakazi wapatao milioni 3.87 wanaoishi katika mji huu. Mji uko mita 0-158 juu ya usawa wa bahari. Seattle ni njia kuu ya biashara kati ya Marekani na Asia, ukiwa na bandari ya nne kwa ukubwa katika Marekani Kaskazini kwa kontena, tangu mwaka 2015. Seattle na Mombasa (Kenya) ni miji-ndugu. Seattle ni mji mkubwa zaidi ya yote katika jimbo la Washington na mkoa wa Pacific Northwest katika Marekani Kaskazini na ni mkubwa wa kumi na tano katika Marekani. Katika Julai 2013, Seattle iliongeza haraka zaidi katika miji mikuu ya Marekani. Mji upo ismus kati ya Puget Sound (njia ya Bahari ya Pasifiki) na Ziwa Washington, kilometa 160 (maili 100) kusini mwa mpaka wa Marekani na Kanada. Wamarekani wa asili walikaa eneo la Seattle si chini ya miaka 4,000 kabla ya wakoloni Wazungu kuja kwa mara ya kwanza. Arthur A. Denny na kundi la Wazungu, ambalo liliitwa “Denny Party,” walifika Alki Point tarehe 13 Novemba 1851 katika meli inayoitwa Exact. Walitoka Illinois na walipitia Portland, Oregon kabla ya kufika eneo la Seattle. Walianzisha koloni katika pwani ya mashariki ya Elliott Bay ambayo waliita “Seattle” mwaka 1852 kuheshimu Mtemi Si’ahl wa makabila ya huko yaliyoitwa Duwamish na Suquamish. Sasa, Seattle ina idadi kubwa ya watu kama Wamarekani wa asili, Waafrika na Waasia. Pia, ni mji wa sita kwa kuwa na idadi ya watu wa jamii ya LGBT katika Marekani kwa asilimia. Kiwanda kikuu cha kwanza katika Seattle kilikuwa kukata mbao. Lakini, mwishoni mwa miaka 1800, mji ulibadilika na ulikuwa kituo kikubwa cha biashara na mahali pa kutengenezea meli. Seattle ilikuwa njia kwa watu waliosafiri Alaska wakati wa Klondike Gold Rush. Baada ya vita ya pili ya dunia, Seattle ilikuwa kituo cha kutengenezea ndege, kwa sababu shirika la Boeing lilianzishwa hapo. Tangu miaka ya 80, Seattle imekuwa kituo cha teknolojia na makampuni kama Microsoft na Amazon, ambayo yalianzishwa hapo. Kampuni ya ndege ya Alaska Airlines ilianzishwa katika SeaTac, Washington na ilihudumia uwanja wa ndege wa Seattle, Seattle-Tacoma International Airport. Mji umeona ukuaji wa uchumi kwa sababu makampuni mapya ya teknolojia na mtandao yalileta fedha na rasilimali. Idadi ya watu iliongezeka kwa 50,000 kati ya miaka 1990 na 2000. Seattle na jimbo la Washington lina baadhi ya mishahara mikuu zaidi katika nchi – $15 kwa saa kwa biashara ndogo ndogo na $16 kwa makampuni makuu – kwa sababu idadi ya watu wanaongezeka haraka sana.Seattle ina historia muhimu ya muziki pia. Kati ya miaka ya 1918 na 1951, kulikuwa na karibu  vilabu ishirini na nne vya klabu muziki wa jazz katika mtaa wa Jackson, kutoka wilaya ya Chinatown/International mpaka wilaya ya katikati. Seattle ni mahali pa kuzaliwa ya mwanamuziki maarufu, Jimi Hendrix, na pia makundi ya Nirvana, Pearl Jam, Foo Fighters na harakati za muziki wa mwamba mbadala. Uchumi Mji umejulikana kimataifa hasa kwa sababu hadi 2001 ilikuwa makao makuu ya kampuni ya Boeing inayojenga ndege za abiria na mizigo. Miji ya Marekani Washington
1676
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
Kenya
Jamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi). Kenya ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa. Mji mkuu ni Nairobi. Idadi ya watu imeongezeka sana katika miaka ya karibuni na kufikia milioni 49. Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi aina elfu kadhaa za wanyama pori. Jina la nchi limetokana na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika. Jiografia Kenya ni nchi ya 47 kwa ukubwa duniani ikifuata mara Madagaska ikiwa na eneo la kilomita mraba 580,367 (maili mraba 224,081). Kutoka pwani ya Bahari ya Hindi, nyanda za chini zimeinuka hadi milima ya kati. Milima hii imetenganishwa na eneo la Bonde la Ufa; sehemu tambarare yenye rutuba upande wa mashariki. Milima ya Kenya ni kati ya iliyofaulu kwa kilimo barani Afrika. Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya (na la pili kwa urefu barani Afrika): Mlima Kenya, unaofikia urefu wa mita 5,199 (futi 17,0570) na ni eneo lenye mito ya barafu. Kusini mashariki milima ya Taita ndiyo mwanzo wa tao la Mashariki, safu za milima zenye miaka zaidi ya milioni 100 ambazo zinaenea hasa nchini Tanzania. Upande huohuo wa kusini Mlima Kilimanjaro () huweza kuonekana ukiwa ng'ambo ya mpaka wa Kenya na Tanzania. Halihewa Kenya ni nchi yenye jua kali na nguo za majira ya joto huvaliwa mwaka mzima. Hata hivyo, huwa na baridi usiku na pia asubuhi na mapema. Hali ya hewa ina joto na unyevu sehemu za pwani, joto kiasi sehemu za bara na ni kame katika sehemu za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa nchi. Hata hivyo kuna mvua nyingi kati ya Machi na Aprili, na mvua ya kadiri kati ya Oktoba na Novemba. Halijoto huwa juu zaidi miezi hii yote. Mvua ya masika hunyesha kuanzia Aprili hadi Juni. Mvua ya vuli nayo hunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba. Wakati mwingine mvua hii huwa nyingi na aghalabu hunyesha wakati wa alasiri na jioni. Majira ya joto jingi ni kuanzia Februari hadi Machi nayo ya baridi ni Julai hadi Agosti. Mazingira Kenya ina maeneo makubwa wanapoishi wanyamapori likiwemo Masai Mara, ambapo nyumbu na wanyama wengi walanyasi hushiriki katika uhamaji kila mwaka. Uhamaji huo, hasa uhamaji wa nyumbu, hutokea Juni hadi Septemba na hushirikisha mamilioni ya wanyama. Tukio hili huwavutia sana wapigaji picha za sinema. Takribani nyumbu 250,000 huangamia kila mwaka katika uhamaji huu wa kutafuta lishe wakati wa kiangazi. Wale wanyama wakubwa watano wa Afrika wanapatikana Kenya: simba, chui, nyati, kifaru na ndovu. Wanyama wengine wengi wa pori na ndege hupatikana katika mbuga za taifa na hifadhi za wanyama hawa nchini. Mazingira ya Kenya yanahatarishwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na athari zake. Historia Historia ya awali Mabaki ya mamba mkubwa ajabu wa zamani za Mesozoic Era, ambayo ni miaka milioni 200 iliyopita, yaligunduliwa nchini Kenya katika chimbo zilizochimbwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Utah na Makavazi ya Kitaifa nchini Kenya miezi ya Julai hadi Agosti 2004 katika bonde la Lokitaung, karibu na Ziwa Turkana. Mabaki yaliyopatikana Afrika Mashariki yaonyesha kuwa miaka milioni 20 iliyopita viumbehai mfano wa sokwe waliishi eneo hili. Uchunguzi wa juzijuzi karibu na Ziwa Turkana waonyesha kuwa viumbe aina ya Homo habilis (walioishi miaka milioni 1.8 na 2.5 iliyopita) na Homo erectus (walioishi miaka milioni 1.8 na miaka 350,000 iliyopita) huenda ndio wazazi wa watu wa kisasa homo sapiens walioishi Kenya enzi za barafu kuu kuisha barani. Katika mwaka wa 1984, uvumbuzi uliofanywa na mtafiti maarufu Richard Leakey na Kamoya Kimeu huko Ziwa Turkana ulikuwa wa mifupa ya mvulana iliyohusishwa na Homo erectus wa miaka milioni 1.6 iliyopita. Utafiti wa awali wa viumbe hawa unahusishwa na Mary Leakey na Louis Leakey, ambao ndio waliofanya uchunguzi wa mwanzo wa kiakiolojia huko Olorgesailie na Hyrax Hill. Baadaye utafiti wa Olorgesailie uliendelezwa na Glynn Isaac. Historia kabla ya ukoloni Wakazi wa kwanza wa eneo linaloitwa Kenya walikuwa wa jamii ya Wakhoisan: hadi leo kuna makabila matatu madogo yenye asili hiyo, ingawa yanatumia lugha za Kikushi: Waata, Waawer na Wadahalo. Wakushi kutoka kaskazini waliingia Kenya kati ya miaka ya 3200 KK na 1300 KK. Mwaka 500 KK hivi wazungumzaji wa lugha za Kinilo-Sahara na katika milenia ya kwanza KK wale wa lugha za Kibantu waliingia katika eneo hili, na sasa Waniloti ni 30% ya Wakenya wote. Wafanyabiashara Waarabu walianza kufika pwani ya Kenya karne ya 1 BK. Ukaribu wa Kenya na Uarabuni ulirahisisha ukoloni, hivyo Waarabu na Waajemi walianza kuishi eneo la pwani karne ya 8. Hata hivyo, baadhi ya walioitwa "Waarabu" katika eneo la Afrika Mashariki walikuwa machotara, Waafrika-Waarabu. Pwani ya Kenya imekuwa makao ya jamii ya wahunzi na jamii ya wakulima wadogowadogo, wawindaji na wavuvi ambao walikuwa mhimili wa uchumi kwa kushiriki katika kilimo, uvuvi, utengenezaji chuma, na biashara na nchi za kigeni. Kuanzia karne ya 6 au karne ya 9, Kenya ilijihusisha na shughuli za ubaharia kukuza uchumi ikaanza kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki. Mombasa ulikuwa mji wenye bandari wa nchi ya Kenya katika karne za kati. Bandari hiyo ilitumika kuendeleza biashara na miji mingine yenye bandari Afrika, Uajemi, na wafanyabiashara Waarabu, Yemeni na hata Bara Hindi. Baharia Mreno Duarte Barbosa wa karne ya 15 alidai kuwa "[Mombasa] ni bandari nzuri na yenye shughuli nyingi, mashua nyingi na hata meli kubwa ajabu, ambazo zote hutoka Sofala na nyingine kutoka Cambay, Melinde na nyingine zinazoabiri hadi kisiwani Unguja." Karne kadhaa kabla ya ukoloni, upwa wa Kenya wanakoishi Waswahili ulikuwa sehemu ya eneo la mashariki mwa Afrika lililofanya biashara, hasa ya watumwa na pembe za ndovu na Waarabu na Wahindi. Inasemekana kwamba kabila la Wameru lilitokana na watumwa waliotoroka utumwa Uarabuni miaka ya 1700. Mwanzoni wafanyabiashara wengi walitokea milki za Uarabuni lakini baadaye wengine wakatokea Unguja (kama Tippu Tip). Kiswahili, ambacho ni lugha ya Kibantu iliyokopa misamiati ya Kiarabu, Kiajemi na mingine kutoka Mashariki ya Kati na Asia Kusini, baadaye ilikua ikawa lingua franca ya biashara kwa jamii mbalimbali. Kwa karne nyingi, upwa wa Kenya umekuwa mwenyeji wa wafanyabiashara na wasafiri. Kati ya miji iliyopo kwenye upwa wa Kenya , mji wa Malindi umebakia kuwa makazi muhimu ya Waswahili tangu karne ya 14 na wakati mmoja ulishindana na Mombasa kwa ukuu pande hizi za Afrika Mashariki. Kwa kawaida, Malindi umekuwa mji na bandari ya kirafiki kwa serikali nyingine. Mwaka wa 1414, Sultani Mwarabu wa Malindi alianzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Uchina wa Ming, wakati wa safari za mchunguzi Zheng He. Katika mwaka wa 1498, utawala wa Malindi ulimkaribisha msafiri na mvumbuzi maarufu kutoka Ureno, Vasco da Gama. Chini ya ukoloni Wareno walikuwa Wazungu wa kwanza kuzuru eneo la Kenya ya sasa: Vasco da Gama alikuwa amezuru Mombasa mwaka wa 1498. Safari ya Vasco da Gama ilifaulu alipofikia huko India, na jambo hilo liliwawezesha Wareno kufanya biashara moja kwa moja na Mashariki ya Mbali kupitia bahari na hivyo kutatiza mitandao ya kibiashara ya awali ya nchi kavu na baharini kama njia za biashara ya viungo zilizotumia Ghuba la Uajemi, Bahari Nyekundu na misafara iliyofika hadi eneo la mashariki ya Mediterranea. Jamhuri ya Venisi ndiyo iliyotawala maeneo ya biashara kati ta Uropa na Asia. Baada ya njia za kawaida za nchi kavu hadi India kufungwa na Waturuki wa Ottoman, Ureno ulitarajiwa kutumia njia ya baharini iliyotumiwa kwanza na Vasco da Ghama ili kuvunja ukiritimba wa Venice. Utawala wa Wareno huko Afrika Mashariki ulijihusisha hasa na pwani iliyokaribia Mombasa. Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kulianza rasmi baada ya mwaka wa 1505, wakati manowari za Wareno, zikiongozwa na Don Francisco de Almeida, zilipokishinda Kilwa, kisiwa kilicho katika eneo ambalo sasa ni Tanzania kusini. Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kuliwawezesha kudhibiti biashara katika Bahari ya Hindi, na kulinda njia za baharini zinazounganisha Uropa na Asia. Manowari zao za kivita zilikwamisha biashara za maadui wao magharibi mwa Bahari ya Hindi na walitoza kodi juu ya bidhaa zilizosafirishwa kupitia eneo hilo kwani walitawala bandari zote na njia kuu za meli. Kujengwa kwa ngome iliyoitwa Fort Jesus Mombasa mwaka wa 1593 kulikusudiwa kuimarisha utawala wao katika eneo hilo, lakini ushawishi wao ulikatizwa na kuja kwa Waingereza, Waholanzi na Waarabu wa Omani katika eneo hilo karne ya 17. Waarabu kutoka Omani ndio waliokuwa tishio kuu la utawala wa Wareno Afrika Mashariki na waliizingira ngome ya Wareno, wakazishambulia meli zao za kivita, kisha kuwafukuza Wareno waliobaki kutoka pwani ya Kenya na Tanzania mwaka wa 1730. Kufikia wakati huo, ufalme wa Ureno haukuwa na haja na njia ya bahari ya biashara ya viungo kwani faida yake ilikuwa imepungua sana. Utawala wa Wareno ulibakia tu katika bandari na maeneo ya kusini mwa Msumbiji hadi mwaka wa 1975. Kutawaliwa kwa pwani ya Kenya na Tanzania na Waarabu kutoka Omani kuliifanya miji hii iliyojitawala hapo awali iwe chini ya uangalifu mkali wa wageni kuliko ilivyokuwa katika enzi za utawala wa Wareno. Waarabu wa Omani, kama Wareno waliowatangulia, waliweza kutawala eneo la pwani tu, si eneo la bara. Hata hivyo, kuanzishwa kwa mashamba makubwa ya mikarafuu, kuongezeka kwa biashara ya utumwa na kuhamishwa kwa makao makuu ya Waomani hadi Zanzibar mwaka wa 1839 na Seyyid Said kulisababisha Waomani kuimarisha utawala wao katika eneo hilo. Utawala wa Waarabu katika bandari kuu zote za pwani ya Afrika Mashariki uliendelea hadi Uingereza ilipoamua kumaliza biashara ya utumwa na uanzishaji wa utaratibu wa kufanya kazi kwa malipo ukaanza kushinikiza utawala wa Waomani. Kufikia mwisho wa karne ya 19, biashara ya watumwa katika bahari zote kuu ilikuwa imeharamishwa na Waingereza: Waarabu wa Omani hawakuwa na uwezo wa kupingana na jeshi la wanamaji la Uingereza lililokuwa likitekeleza amri hiyo. Waomani waliendelea kuwepo visiwani Unguja na Pemba hadi mapinduzi ya mwaka wa 1964, lakini kuwepo kwa Waarabu wa Omani nchini Kenya rasmi kulisitishwa wakati Wajerumani na Waingereza walipozidhibiti bandari zote kuu na kuanzisha mahusiano ya kibiashara na viongozi mashuhuri waliokuwa wenyeji miaka ya 1880. Hata hivyo, urithi waliouacha Afrika Mashariki ungali unaonekana kupitia kwa vizazi vyao vipatikanavyo pwani ya Kenya na ambavyo vinaona kuwa asili yao ni Oman. Vizazi hivi hata leo humiliki utajiri mwingi na ndio wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa katika jamii za pwani ya Kenya. Hata hivyo, wanahistoria wengi hushikilia kuwa historia ya ukoloni nchini Kenya ilianza wakati Wajerumani walipoanza kutawala mali ya Sultani wa Unguja iliyo pwani mwaka wa 1885, ikifuatwa na kuja kwa kampuni ya Imperial British East Africa Company mwaka wa 1888. Uhasama wa kwanza baina ya mabepari ulikatizwa wakati Ujerumani ulipouachia Uingereza sehemu ya pwani iliyomiliki. Hii ilifuatia kujengwa kwa reli iliyounganisha Kenya na Uganda. Baadhi ya makabila ya Kenya yalipinga ujenzi huo, hasa Wanandi wakiongozwa na Orkoiyot Koitalel Arap Samoei kwa miaka kumi, kuanzia 1895 hadi 1905 – lakini hatimaye Waingereza waliijenga reli hii. Inaaminika kuwa Wanandi walikuwa kabila la kwanza kuwekwa kwenye maeneo yaliyotengewa Waafrika ili kuwazuia kutatiza ujenzi wa reli. Wakati huo Wahindi wengi wenye ujuzi waliingia nchini ili kuchangia ujenzi. Wakati wa ujenzi wa reli kupitia Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi, Wahindi wengi na wenyeji Waafrika walivamiwa na simba wawili waliojulikana kama “wala watu wa Tsavo”. Wahindi hao na vizazi vyao baadaye walibakia nchini Kenya na kuunda kitovu cha jamii za Wahindi zijulikanayo kama Ismaili Muslim na Sikh. Mnamo Agosti 1914, Vita vya Kwanza vya Dunia vilipoanza, magavana wa British East Africa (kama eneo hilo lilivyojulikana) na German East Africa walifikia makubaliano ili kuepusha makoloni yao machanga na uhasama. Hata hivyo, Luteni Kanali Paul von Lettow-Vorbeck alichukua mamlaka ya majeshi ya Ujerumani, akiwa na kusudi la kutwaa raslimali nyingi iwezekanavyo za Uingereza. Jeshi la Uingereza likiwa limemtenga na Ujerumani, von Lettow aliendesha kampeni iliyofaulu ya vita vya kuvizia, wakila walichopata, wakiteka bidhaa za matumizi za Uingereza, na kuepuka kushindwa. Mwishowe alisalimu amri na akajisalimisha nchini Zambia siku kumi na moja baada ya mapatano ya kusimamisha vita kutiwa sahihi mwaka wa 1918. Waingereza walitumia jeshi la Wahindi kumfukuza Lettow na walihitaji wachukuzi wengi ili kubeba vifaa vya matumizi hadi bara kwa miguu na hivyo kutatua shida kuu ya uchukuzi. Kundi la wanajeshi wachukuzi liliundwa na kuwajumuisha Waafrika 400,000, na kuchangia katika uhamasishaji wao wa muda mrefu kisiasa. Hadi mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya lilijulikana kama Himaya ya Uingereza ya Afrika Mashariki. Mwaka huo, koloni la Kenya liliundwa na kupatiwa jina linalotokana na Mlima KenyaWaingereza walilitamka jina hilo kama ingawa matamshi ya wenyeji na yaliyokusudiwa katika maendelezo asili, Kenia yalikuwa ˈkɛnja. Enzi ya Jomo Kenyatta kuwa rais wa Kenya miaka ya 1960-1969, matamshi ya Kiingereza, yaani yalikubalika na kutumiwa sana kwa sababu jina lake lilidumisha matamshi asilia ya wenyeji. Kumbe saa ya uhuru, mwaka 1963, Jomo Kenyatta alichaguliwa kama rais wa kwanza. Awali alikuwa alishika jina hili kutafakari ahadi yake ya kuikomboa nchi yake na matamshi yake ya jina lake ulisababisha katika matamshi ya Kenya katika Kiingereza kubadilisha nyuma ya makadirio ya awali uliotokea matamshi, Mwanzoni mwa karne ya 20, wakulima Waingereza na Wazungu wengine walituama katika nyanda za juu katika eneo la kati walikoondokea kuwa matajiri kwa kulima kahawa na chai. Kufikia mwaka 1930, takribani walowezi 30,000 waliishi katika maeneo hayo na walikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa sababu ya uwezo wao wa kiuchumi. Maeneo hayo yalikuwa makao ya watu milioni moja wa kabila la Wakikuyu, na wengi wao hawakuwa na ithibati ya kumiliki mashamba kwa mujibu wa Waingereza (ingawa mashamba hayo yalimilikiwa na kabila hilo kabla ya Wazungu kufika), na waliishi kama wakulima wanaohamahama. Ili kuendeleza matakwa yao, walowezi waliwakataza kilimo cha kahawa na kuwalazimisha kulipa kodi ya nyumba, na maskwota walipewa mashamba madogo baada ya kuwafanyia kazi. Wakikuyu wengi walihamia mijini kwani mashamba yao hayangeweza kutosheleza mahitaji yao. Mwaka wa 1951, Horace Hector Hearne akawa mkuu wa sheria nchini Kenya (alitoka Ceylon alikoshikilia wadhifa huohuo) na alifanya kazi katika Mahakama Kuu mjini Nairobi. Alihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 1954 alipoteuliwa kama Hakimu wa Rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Afrika Magharibi. Usiku wa tarehe 5 Februari 1952, wakati Mfalme George VI alipoaga dunia, Hearne alimsindikiza Malkia Elizabeth II na mumewe Filipo mwanamfalme wa Edinburgh, kwa dhifa ya kitaifa hotelini Treetops, ambayo sasa ni kivutio maarufu cha watalii. Hapa ndipo alipouanzia umalkia. Alirudi Uingereza mara moja akiandamana na Hearne. Kuanzia Oktoba 1952 mpaka Desemba 1959, Kenya ilikuwa katika hali ya hatari kufuatia uasi wa Mau Mau dhidi ya utawala wa Uingereza. Gavana aliomba na kupata msaada wa wanajeshi Waingereza na Waafrika, pamoja na King's African Rifles. Mnamo Januari 1953, Meja Jenerali Hinde aliteuliwa kuwa mkuu wa oparesheni ya kuzima uasi. Hali hii haikuimarika kwa kukosa uchunguzi, kwa hivyo Jenerali George Erskine aliteuliwa kuwa kamanda msimamizi wa majeshi ya kikoloni mnamo Mei 1953, akiungwa mkono hasa na Winston Churchill. Kutiwa mbaroni kwa Warũhiũ Itote (aka General China) tarehe 15 Januari 1954, na kuhojiwa kwake kulipelekea Waingereza kuuelewa vyema usimamizi wa Mau Mau. Oparesheni Anvil iliyoanzishwa tarehe 24 Aprili 1954 ilipangwa na jeshi kwa wiki kadhaa baada ya kukubaliwa na kamati kuu ya vita. Wakati wa oparesheni hiyo, mji wa Nairobi ulidhibitiwa na wanajeshi na wakazi wake walihojiwa huku wafuasi wa Mau Mau wakikamatwa na kupelekwa vizuizini. Mnamo Mei 1953, walinzi wa nyumbani walitambulika rasmi kama askari wa usalama. Askari hao wa nyumbani ndio waliounda kikosi cha kupambana na mikakati ya Mau Mau kwani walikuwa Waafrika waaminifu, na si majeshi ya kigeni kama Jeshi la Uingereza na King's African Rifles. Kufikia mwisho wa hali ya hatari, askari hao walikuwa wamewaua Mau Mau 4886, ambao ni asilimia 42% ya waasi wote. Kukamatwa kwa Dedan Kimathi huko Nyeri tarehe 21 Oktoba 1956 kuliashiria kushindwa kwa Mau Mau kukamaliza vita. Baada ya uhuru Utawala wa Kenyatta Waafrika walichaguliwa moja kwa moja katika bunge la uwakilishi kwa mara ya kwanza mwaka wa 1957. Licha ya Waingereza kutamani kuwakabidhi mamlaka wapinzani wasio na siasa kali ya Kiafrika, ni chama cha Kenya African National Union (KANU) kilichoongozwa na Jomo Kenyatta kilichounda serikali punde tu kabla ya Kenya kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963. Tarehe 12 Desemba 1964, Kenya ilipotangazwa kuwa jamhuri, Kenyatta akawa rais wa kwanza. Mwaka huohuo, jeshi la Kenya lilipigana na Vita vya Shifta dhidi ya kabila la Wasomali waliokusudia kuiona NFD imejiunga na Jamhuri ya Somalia. Mashifta walililemea jeshi la Kenya lakini baadaye walishindwa mwaka wa 1967. Kenya ilitia saini mkataba na nchi ya Ethiopia mwaka wa 1969 unaodumu mpaka leo kwa kuhofia mashambulizi kutoka kwa jeshi la Somalia lililokuwa na nguvu zaidi. Eneo la NFD nchini Kenya halijaendelea kutokana na kiangazi na mafuriko. Hata hivyo, wakimbizi wafanyabiashara wa Kisomali waliotajirika wamebadilisha mtaa wa Eastleigh uliokuwa wa mabanda na kuufanya kuwa ngome ya kibiashara katika sehemu kubwa ya mashariki mwa mji wa Nairobi. Utawala wa Moi Mwaka wa 1978, Kenyatta alifariki na Daniel Arap Moi akawa rais. Moi alidumisha urais kwa kuchaguliwa bila kupingwa katika chaguzi za mwaka wa 1979, 1983 (uchaguzi wa dharura) na 1988, zote zikiwa zilifanyika chini ya katiba ya chama kimoja. Uchaguzi wa 1983 ulifanyika mwaka mmoja kabla ya wakati kutokana na njama ya kupindua serikali iliyokosa kufaulu tarehe 1 Agosti 1982. Mapinduzi hayo yaliyotibuka yalipangwa na askari mwanahewa wa cheo cha chini, Bwana Hezekiah Ochuka na kuendelezwa hasa na wanahewa. Jaribio hilo lilizimwa kwa haraka na wanajeshi waaminifu wakiongozwa na Jeshi la Nchi Kavu, General Service Unit (GSU) - kikosi cha polisi wenye hadhi ya kijeshi - na baadaye polisi wa kawaida. Hata hivyo raia kadhaa walijeruhiwa na wengine kuuawa. Tukio hilo lilisababisha kuvunjwa kwa kikosi chote cha wanahewa, huku wengine wakiachishwa kazi na wengine wakishtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi. Katika uchaguzi wa 1988 kura za mlolongo zilianzishwa, ambapo wapigakura walitakiwa kupiga foleni nyuma ya wagombea wanaowapenda, badala ya kutumia kura ya siri Jambo hilo lilionekana kama kilele cha enzi ya ukiukaji mkubwa wa demokrasia likasababisha msukumo mkuu wa mageuzi ya kikatiba. Vipengele vilivyokuwa na utata, kikiwemo kile kilichoruhusu chama kimoja pekee cha kisiasa, vilibadilishwa miaka iliyofuata. Katika uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi wa miaka ya 1992 na 1997, Daniel Arap Moi alichaguliwa tena. Utawala wa Kibaki Kulingana na katiba, mwaka 2002 Moi hakuruhusiwa kuwania urais tena, na Mwai Kibaki wa chama cha upinzani cha "National Rainbow Coalition" — NARC akachaguliwa kuwa rais. Uchaguzi huo ulitambulikana kuwa wa kidemokrasia na wachunguzi wa humu nchini na wa kimataifa na hivyo kuwa chanzo cha mageuzi makubwa ya kidemokrasia nchini Kenya. Mnamo Desemba 2002, Wakenya walifanya uchaguzi uliokuwa wa kidemokrasia na uwazi ambao kwa kiasi kikubwa uliamuliwa kuwa huru na wa haki na wachunguzi wa kimataifa. Uchaguzi wa mwaka huo ulikuwa mwanzo mpya na uliiletea Kenya mabadiliko makuu ya kisiasa yaliyowezesha chama cha Kenya African National Union (KANU), kilichokuwa kimeitawala nchi tangu uhuru, kukabidhi kwa amani mamlaka kwa chama cha National Rainbow Coalition (NARK), uliokuwa muungano wa vyama vingi. Chini ya uongozi wa Rais Mwai Kibaki, muungano wa vyama tawala ulihahidi kushughulikia ukuaji wa kiuchumi, kumaliza ufisadi, kuimarisha elimu na kuandika katiba mpya. Baadhi ya ahadi hizi zimeshatimizwa. Kuna elimu ya msingi ya bure. Mwaka wa 2007 serikali ilitangaza kuwa, kuanzia mwaka 2008 gharama ya masomo ya shule za upili itapunguzwa huku serikali ikilipia gharama zote za mafundisho. Uchaguzi wa 2007 Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 27 Desemba 2007, Rais Kibaki wa chama cha Party of National Unity (PNU) aliwania uchaguzi dhidi ya chama kikuu cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM). Kulingana na wachunguzi wa kimataifa, uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na hivyo kutofikia kiwango kinachokubalika kimataifa. Chama cha ODM kilisambaratika na kupoteza 8 % ya kura zake kwa chama kipya cha Orange Democratic Movement-Kenya (ODM) - kikiongozwa na Kalonzo Musyoka. Kinyang’anyiro kilikuwa kikali kati ya mgombea wa ODM, Raila Odinga na Kibaki wa PNU. Kuhesabiwa kwa kura na Tume ya Uchaguzi ya Kenya kulionyesha Raila akiongoza kwa kura chache na baadaye kwa kura nyingi. Hata hivyo, kura zilipoendelea kuhesabiwa na Tume ya Uchaguzi, Kibaki alimkaribia mpinzani wake kwa kura, kisha akamshinda. Matokeo hayo yalisababisha maandamano na kulaumiwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kumpendelea Kibaki, hivyo Oginga akajitangaza “rais wa watu” na kutaka kura zihesabiwe tena. Maandamano hayo yalibadilika kuwa ghasia zilizosababisha kuharibiwa kwa mali.. Viongozi mashuhuri wa Afrika, wakiongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan walisuluhisha mzozo huo wa kisiasa. Kundi la Annan liliungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Jumuia ya Ulaya, Muungano wa Nchi za Afrika, Serikali ya Marekani na nchi nyingine maarufu ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi rejelea Ghasia nchini Kenya (2007-2008). Annan aliomba usaidizi kwa kamati yake ya upatanishi kutoka kwa shirika la kushughulikia mizozo la Uswisi lijulikanalo kama Kituo cha Mazungumzo ya Kihisani yaani Centre for Humanitarian Dialogue. Serikali ya muungano Tarehe 12 Februari 2008 Kibaki na Odinga walitia sahihi mkataba wa kuunda serikali ya muungano ambapo Odinga angekuwa waziri mkuu wa pili nchini Kenya. Kulingana na mkataba huo, rais angeteua baraza la mawaziri kutoka pande zote mbili za PNU na ODM kulingana na wingi wa wabunge wa kila chama bungeni. Mkataba huo ulieleza kuwa baraza la mawaziri litajumuisha Makamu wa Rais na manaibu wawili wa Waziri Mkuu. Baada ya majadiliano bungeni ilipitishwa kuwa muungano huo utadumu hadi mwisho wa kipindi cha bunge, ama chama kimoja kikijitoa kwenye muungano kabla ya kipindi cha bunge kuisha. Wadhifa huo mpya wa waziri mkuu utakuwa na nguvu na mamlaka kuratibu na kusimamia shughuli za serikali. Vilevile itaongozwa na mbunge aliyechaguliwa ambaye pia atakuwa kiongozi wa chama au muungano wa vyama wenye idadi kubwa ya wabunge bungeni. Ulimwengu ulimshuhudia Annan na kamati yake iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na mwenye kiti wa muungano wa nchi za Afrika Jakaya Kikwete, walipowaleta pamoja wapinzani hawa sugu kwenye sherehe za kutia sahihi mkataba huu. Sherehe hizi zilionyeshwa moja kwa moja kwenya televisheni ya kitaifa kutoka kiingilio cha Jumba la Harambee mjini Nairobi. Wawakilishi wa PNU na ODM walianza majadiliano ya kina kuhusu ugavi wa mamlaka tarehe 29 Februari 2008. Wabunge wa Kenya, kwa pamoja, waliidhinisha mkataba wa ugawaji mamlaka tarehe 18 mwezi wa Machi 2008 ili kuiokoa Kenya iliyoaminika kama mojawapo ya nchi thabiti na iliyoendelea barani Afrika. Mkataba huu uliunganisha PNU iliyoongozwa na Kibaki na ODM ya Odinga kisha kupelekea kuundwa kwa serikali ya muungano, vyama vyote viwili vikiwa na mamlaka sawa. Tarehe 13 Aprili 2008, Rais Kibaki aliitangaza baraza la mawaziri 41 wa serikali hii ya muungano ikijumuisha waziri mkuu na makamu wake wawili. Baraza hili lilijumuisha pia manaibu wa mawaziri 50 na lilitawazwa katika Ikulu ya Nairobi tarehe 17 Aprili 2008 huku Kofi Annan na viongozi wengine mashuhuri wakishuhudia. Tarehe 4 Novemba 2008 ilitangazwa kuwa sikukuu ya kitaifa kusherehekea ushindi wa Barack Obama, ambaye baba yake alikuwa Mkenya, kama rais wa Marekani. Katika sehemu za mashambani, kama wilayani Kisii, visa vya kuchoma watu wakidaiwa kuwa wachawi vinaongezeka. Waathiriwa hasa ni wanawake wakongwe. Mnamo Mei 2008, watu 11 waliuwa na nyumba 30 kuchomwa. Siasa Tazama pia: Orodha ya vyama vya kisiasa nchini Kenya Kwa sasa Kenya ni jamhuri ya kidemokrasia ya kiuwakilishi inayoongozwa na rais, ambaye ndiye mkuu wa taifa na kiongozi wa serikali, na yenye mfumo wa vyama vingi. Serikali ndiyo yenye mamlaka ya juu. Utungaji wa sheria ni jukumu la serikali na la bunge la taifa. Idara ya Mahakama ni huru, na imejitenga na serikali kuu na bunge. Hata hivyo, kulikuwa na kutoridhika kwingi, hasa katika enzi ya rais mstaafu Daniel Arap Moi, kuwa serikali iliingilia sana shughuli za mahakama. Kenya imedumisha uthabiti wa kutosha licha ya mabadiliko katika mifumo yake ya kisiasa na michafuko katika nchi kadhaa jirani. Bunge la mseto wa vyama vingi la 1997 lilianzisha mageuzi yaliyobadilisha sheria za kikoloni zenye dhuluma zilizotumika kuuzuia uhuru wa kuongea na kutangamana. Jambo hilo liliimarisha uhuru wa umma na kuchangia kiasi kuaminika kwa uchaguzi wa Desemba 1997. Kaunti na tarafa Kenya ina kaunti 47, kila moja ikiongozwa na Mkuu wa Kaunti anayechaguliwa na watu ambao wanaishi kwenye hiyo kaunti. Serikali za mitaa huendelezwa kupitia mabaraza ya miji. Maeneo mengi ya mijini huwa ni mji, manisipaa au baraza la mji. Serikali za mitaa katika maeneo ya mashambani huitwa serikali za wilaya. Madiwani wa mitaa hii huchaguliwa katika uchaguzi wa madiwani unaofanywa wakati mmoja na uchaguzi mkuu. Maeneo ya uwakilishi bungeni yamegawanywa kwa sababu ya upigaji kura. Kuna maeneobunge 210 nchini Kenya. Idadi ya watu katika miji muhimu Watu Kenya ni nchi yenye makabila mengi tofautitofauti, hasa ya Kibantu (67%) na ya Kiniloti. Wakenya wengi huzungumza lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili, na asilimia kubwa pia huzungumza lugha mama ya kabila lao. Makundi ya makabila ni kama ifuatavyo: Wakikuyu 22%, Waluyia 14%, Wajaluo 13%, Wakalenjin 12%, Wakamba 11%, Wakisii 6%, Wameru 6%, makabila mengine ya Kiafrika 15%, wasio Waafrika (Wahindi, Waingereza na Waarabu) 1% Kila kundi au kabila lina lugha yake na Kiswahili hutumika kama chombo cha kuwasiliana miongoni mwa makabila tofauti. Dini Upande wa dini, idadi kubwa ya Wakenya ni Wakristo: kulingana na sensa ya mwaka 2019, asilimia 85.5 ya wakazi wa Kenya walikuwa Wakristo (asilimia 53.9 ni Waprotestanti, asilimia 20.6 ni Wakatoliki, asilimia 11.8 ni Wakristo wa madhehebu mengine mbalimbali, wakiwemo Waorthodoksi 621,200), asilimia 10.9 ni Waislamu, asilimia 0.7 ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini (kuna Wahindu takribani 60,000, ambao wameingiliana vyema na Wakenya wengine na huchangia pakubwa uchumi wa nchi), na asilimia 1.6 wanadai hawana uhusiano na dini yoyote ile. Asilimia 60 ya idadi ya Waislamu huishi katika Mkoa wa Pwani, wakiwa asilimia 50 ya jumla ya wakazi wa pale. Wengi wa wanaoishi sehemu ya magharibi mkoani Pwani ni Wakristo. Eneo la kaskazini la Mkoa wa Mashariki ni makazi ya asilimia 10 ya jumla ya Waislamu nchini; hii ndiyo dini ya wakazi wengi wa hapa, na mbali na idadi ndogo ya Wasomali wanaoishi Nairobi, idadi kubwa ya Wakenya wengine ni Wakristo. Utamaduni Kenya ni nchi yenye tamaduni anuwai. Tamaduni zinazotambulika ni pamoja na Waswahili walio katika eneo la pwani, jamii za wafugaji katika eneo la kaskazini na jamii nyingine mbalimbali katika maeneo ya kati na magharibi. Wajaluo wa Kenya ni wazawa wa jamii za wakulima na wafugaji walioishi magharibi mwa Kenya kabla ya ukoloni. Inafahamika kwamba asili ya Wajaluo na makabila mengine ya Waniloti ni kaskazini mwa Kenya, pengine maeneo ya Sudan Kusini ya sasa. Waniloti, kama wanavyoitwa, ni kikundi cha kianthropolojia kilichotoka maeneo ya kaskazini mashariki mwa Afrika. Pengine walihamia kusini kutokana na vita vilivyosababishwa na ukuaji wa Kush na Misri. Waniloti nchini Kenya ni Wajaluo, Waturkana, Wakalenjin na Wamasai. Hili linadhihirika kutokana na kuwepo kwa lahaja zinazofanana kati ya makabila fulani nchini Sudan Kusini leo. Makabila haya ni pamoja na Akoli na Lwo (si sawa na Luo) wanaoishi katika eneo la Darfur. Kuna makabila mengine ya Waniloti yanayoishi nchini Uganda na Tanzania. Hii hasa ni kwa sababu ya Wajaluo kuvutiwa na Ziwa Victoria, ambako wanapatikana katika nchi hizi tatu (Uganda, Tanzania na Kenya). Nchini Uganda, wanajulikana kwa kuanzisha himaya ya Waganda na ya himaya ya Watoro. Wajaluo nchini Kenya walipigana vita na majirani wao, hasa Wakalenjin, ili kulidhibiti ziwa hilo. Leo hii, utamaduni wa Wamaasai unajulikana sana kwa kuangaziwa vilivyo na utalii, hata hivyo Wamaasai ni asilimia ndogo ya idadi ya Wakenya kwa jumla. Wamaasai wanatambulika kwa kujipamba sehemu ya juu ya mwili na kwa vito. Kenya ina utajiri mwingi wa muziki, vituo vya runinga na maonyesho ya sanaa. Elimu Mfumo wa elimu nchini Kenya unajumuisha elimu ya chekechea, ya msingi, ya sekondari na ya vyuo. Elimu ya watoto wadogo aghalabu huchukua miaka mitatu, ya msingi miaka minane, sekondari minne na chuo kikuu miaka minne au sita kwa kutegemea kozi. Shule za chekechea, ambazo ni za watoto wa umri wa miaka mitatu hadi mitano, ni sehemu muhimu ya mfumo huu wa elimu na ni kigezo muhimu kabla ya kusajiliwa katika darasa la kwanza (Gredi ya Kwanza). Mwishoni mwa elimu ya msingi wanafunzi hufanya mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Msingi Kenya (KCPE), ambao huamua watakaojiunga na shule ya sekondari au vyuo vya ufundi. Umri wa shule ya msingi ni miaka 6/7 hadi 13/14. Wale wanaojiunga na shule ya upili hufanya mtihani wa taifa mwishoni mwa kidato cha nne - Mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Shule ya Upili Kenya (KCSE), ambao huamua watakaojiunga na vyuo vikuu, vyuo vya taatuma nyinginezo au kuajiriwa. Baraza Kuu la Usajili (JAB) ndilo lenye jukumu la kuwachagua wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu vya umma. Mbali na shule za umma, kuna shule nyingi za binafsi nchini, hasa katika sehemu za miji. Vilevile, kuna shule kadhaa za kimataifa zinazofundisha mifumo mbalimbali ya elimu ya ng'ambo. Historia ya elimu Mfumo wa kwanza wa elimu nchini Kenya baada ya uhuru uliletwa na wakoloni Waingereza. Baada ya nchi kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963, Tume ya Ominde iliundwa ili kuleta mabadiliko ambayo yaakisi matarajio ya taifa huru la Kenya. Tume hii ilimulika masuala ya usawa na umoja, ambayo yalikuwa muhimu hasa wakati huo. Mabadiliko ya kilichofundishwa katika historia na jiografia yalifanywa ili kuakisi umoja wa kitaifa. Kati ya miaka 1964 na 1985, mfumo wa 7-4-2-3 ulifuatwa (miaka saba masomo ya msingi, miaka minne sekondari ya daraja la chini, miaka miwili sekondari ya daraja la juu, na miaka mitatu masomo ya chuo kikuu). Shule zote zilifuata mtaala mmoja. Mwaka wa 1981, kamati iliyoteuliwa na rais kuratibu namna ya kuanzisha chuo kikuu cha pili nchini Kenya, na pia kuubadilisha mfumo wa elimu kwa jumla, ilianza kazi yake. Kamati hii ilipendekeza kuwa mfumo ule wa 7-4-2-3 ubadilishwe kuwa mfumo wa 8-4-4 (miaka minane shule ya msingi, miaka minne shule ya upili, miaka minne elimu ya chuo kikuu). Jedwali lililo katika Elimu ya Sasa Nchini Kenya linaonyesha muundo wa mfumo wa 8-4-4. Ingawa mfumo wa 7-4-2-3 kinadharia ulifikia kikomo mfumo wa 8-4-4 ulipoanzishwa mwaka wa 1985, kundi la mwisho la mfumo huo wa awali lilihitimu kutoka vyuo vikuu vya Kenya mwaka wa 1992. Elimu nchini Kenya sasa Mfumo wa sasa wa 8-4-4 ilizinduliwa Januari 1985. Ulitilia mkazo masomo ya kiufundi kwa matarajio kuwa, muundo huu mpya utawawezesha wanaoacha shule katika viwango mbalimbali aidha kujiajiri wenyewe au kupata ajira katika sekta ya juakali. Mnamo Januari 2003, Serikali ya Kenya ilitangaza kuanzishwa kwa masomo ya shule za msingi bila malipo. Hili lilipelekea kuongezeka kwa wanafunzi waliojiunga na shule za msingi kwa asilimia 70. Hata hivyo, idadi ya waliojiunga na shule za upili na vyuo haikuongezeka sana kwa sababu malipo bado yalihitajika ili kuhudhuria masomo. Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya msingi nchini Kenya (KCPE) hufanywa katika darasa la nane. Matokeo ya mtihani huu huhitajika ili kusajiliwa katika shule ya upili. Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya shule ya upili nchini Kenya (K.C.S.E.) hufanywa katika kidato cha nne. Wanafunzi hufanya mtihani katika masomo nane. Ukosoaji Mfumo wa elimu wa Kenya 8-4-4 umepitia mengi magumu katika kipindi kirefu ulichodumu. Punde tu baada ya kufuzu kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa mfumo huu mwaka wa 1989, wananchi wengi walijitokeza kuilaumu na kuihukumu serikali kwa kuuanzisha mfumo huu. Wakosoaji hao walidai kuwa waliohitimu hawajaandaliwa vyema na hawangeweza kushindana na wenzao kutoka sehemu nyingine za ulimwengu. Wengine walihoji kuwa waliofuzu kupitia mfumo huu walikuwa aidha wachanga sana au hawajaandaliwa vyema kwa nafasi za kazi zilizokuweko. Serikali haikusikiliza hayo yote pengine kwa sababu uwezekano wa kuubadilisha na kuuunda upya kungeigharimu pesa nyingi. Hata hivyo, kwa miaka mingi waliofuzu kupitia mfumo huu wamewaaibisha walioupinga kwa kufualu katika vyuo vya nchini na ng’ambo. Pia wasomi na wafanyakazi wa afya kuhamia nchi zilizoendelea ni dhihirisho tosha la hali hii. Mkazo uliotiliwa masomo ya ufundi umefifia na mabadiliko ya hivi juzi katika mtaala yanasisitiza teknolojia ya upashanaji habari, sayansi, hesabu na lugha. Kwa vyovyote vile, kazi ya kiakademia na kusisitizwa kwa kupita mitihani iliyoandikwa hakujaacha nafasi kwa useremala, uashi, upishi na mafunzo mengine ya ufundi. Michezo Kenya hushiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo kriketi, mbio za magari, soka, raga na ngumi. Lakini nchi hii inajulikana hasa kwa kutawala katika mbio za masafa ya kadiri na mbio za masafa marefu. Kenya, kwa muda mrefu, imetoa mabingwa wa Olimpiki na michezo ya Jumuia ya Madola katika nyanja mbalimbali, hasa katika mbio za mita 800, mita 1,500, mita 3,000 kuruka viunzi na maji, mita 5,000, mita 10,000 na mbio za masafa marefu. Wanariadha wa Kenya (hasa wa kabila la Wakalenjin) wanaendelea kutawala mbio za masafa ulimwenguni, ingawa ushindani kutoka nchi ya Moroko na Ethiopia umepunguza umaarufu huu. Wanariadha wa Kenya wanaosifika sana ni pamoja na mshindi mara nne wa mbio za masafa marefu za Boston kwa wanawake na mshindi mara mbili wa mbio za dunia Catherine Ndereba, aliyeshikilia rekodi ya awali ya mbio za dunia Paul Tergat, na John Ngugi. Wakati wa michezo ya Olimpiki ya Beijing Kenya ilishinda medali 6 za dhahabu, 4 za fedha, 4 za shaba na kulifanya taifa lililofaulu sana barani Afrika katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Wanariadha wapya walitambulikana, kama Pamela Jelimo, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 kwa wanawake aliyejitahidi na kushinda tuzo la Golden League, na Samuel Wajiru aliyeshinda mbio za masafa marefu kwa wanaume. Bingwa mstaafu wa mbio za Olimpiki na za Jumuia ya Madola, Kipchoge Keino, alisaidia kuanza ubingwa wa mbio za masafa marefu miaka ya 1970 akafuatwa na bingwa wa michezo ya Jumuia ya Madola, Henry Rono, aliyeshikilia rekodi kadhaa za dunia. Hivi majuzi, kumekuwa na mzozo wa wanariadha wa Kenya waliosaliti nchi yao na kuwakilisha nchi nyingine, hasa Bahrain na Qatar. Wizara ya michezo ya Kenya imejaribu kuzuia usaliti huu, lakini umeendelea tu, Bernard Lagat akiwa wa mwisho, akichagua kuiwakilisha Marekani. Usaliti huu, kwingi unatokana na sababu za kiuchumi au kifedha ingawa pia wanariadha wazuri wasioweza kufaulu katika timu nzuri ya taifa huona ni rahisi kufaulu kwa kukimbilia nchi nyingine. Kenya pia imetawala voliboli ya wanawake barani Afrika, huku vilabu na timu ya taifa vikishinda mashindano kadhaa barani Afrika katika mwongo uliopita. Timu ya wanawake pia imeshiriki katika michezo ya Olimpiki na Mashindano ya Ulimwengu ingawa haijafaulu vilivyo. Mchezo wa kriketi ni maarufu na pia ni mchezo wa timu ambao umefaulu sana. Kenya imeshiriki katika Kombe la Dunia la Kriketi tangu mwaka 1996. Timu hii ilishinda baadhi ya timu maarufu ulimwenguni na kufikia semifainali katika mchuano wa mwaka 2003. Walishinda ligi ya kriketi ya dunia daraja la 1 iliyofanyika Nairobi kwa mara ya kwanza, kisha wakashiriki katika mchuano wa ulimwengu wa T20. Nahodha wa sasa wa timu ni Collins Obuya. Kenya imejiundia jina katika muungano wa raga. Mchezo huo ni maarufu nchini hasa kwa sababu ya mchuano wa kila mwaka wa Safari Sevens. Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kila upande ilikuwa nambari ya 9 katika michezo ya dunia ya wachezaji saba IRB katika msimu wa mwaka 2006. Kenya ilikuwa bingwa wa soka katika eneo hili lakini ubingwa huu umefifia kutokana na kutoelewana kwa maafisa wa Kamati ya Soka Nchini. Mizozo hii ilipelekea Kenya kupigwa marufuku na FIFA, lakini marufuku hii iliondolewa mnamo Machi 2007. Kwa upande wa mbio za magari, Kenya ndio waandalizi wa mbio za magari maarufu za Safari Rally zinazotambulika kuwa ngumu zaidi ulimwenguni, na ambazo ni sehemu ya Bingwa wa Mbio za Magari kwa miaka mingi hadi kuondolewa kwake baada ya mbio za 2002 kwa sababu ya matatizo ya kifedha. Baadhi ya madereva maarufu wa mbio za magari ulimwenguni walioshiriki na kushinda mbio hizi ni Bjorn Waldegard, Hannu Mokkola, Tommi Makinen, Shekhar Mehta, Carlos Sainz na Colin McRae. Ingawa mbio hizi bado huendelea kila mwaka kama sehemu ya kutafuta Bingwa wa Mbio za Magari Afrika, waandalizi wanatarajia kuruhusiwa kujiunga tena na Ubingwa wa Magari Ulimwenguni katika miaka michache ijayo. Fasihi Ngugi wa Thiong'o ni mmoja wa waandishi maarufu wa Kenya. Kitabu chake :en:Weep Not, Child ni ufafanuzi wa maisha yalivyokuwa Waingereza walipoitwaa Kenya. Hii ni hadithi kuhusu athari za Mau Mau katika maisha ya Wakenya asili. Kinavyochanganya maudhui - ukoloni, elimu, na mapenzi - kunakifanya kuwa kimojawapo kati ya vitabu bora vya hadithi barani Afrika. Kitabu cha hadithi cha M. G. Vassanji The In-Between World of Vikram Lall kilishinda tuzo la Giller Prize mwaka 2003. Hii ni hadithi ya kubuni ya Mkenya mwenye asili ya Kihindi na familia yake wavyojizatiti na mabadiliko ya kisiasa wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni nchini Kenya. Kuanzia mwaka wa 2003, jarida la fasihi Kwani? limekuwa likichapisha fasihi ya kisasa ya Kenya. Uchumi Baada ya uhuru, Kenya iliendeleza ukuaji wa kiuchumi haraka kupitia kwa uwekezaji wa umma, kuhimiza uzalishaji wa kilimo, na kushawishi uwekezaji wa watu binafsi na wageni katika viwanda. Pato la taifa lilikua kwa asilimia 6.6 kuanzia 1963 hadi 1973. Uzalishaji wa kilimo ulikua kwa asilimia 4.7 kila mwaka kwa kipindi hicho ukiwa umechochewa na ugawaji upya wa mashamba, kuanzishwa kwa kilimo cha mimea iliyoimarishwa, na kuanzisha mashamba mapya. Hata hivyo, kati ya 1974 na 1993 ukuaji wa uchumi wa Kenya ulipungua. Kupungua kwa kilimo kulisababishwa na sera za kilimo zisizofaa, mikopo isiyotosha na vikwazo visiyofaa vya biashara ya kimataifa. Mnamo mwaka wa 1993, Serikali ya Kenya ilianzisha mpango mkuu wa kuimarisha uchumi na kuufanya huru. Waziri mpya wa fedha na gavana mpya wa Benki Kuu ya Kenya walianza mikakati iliyofuatana kuimarisha uchumi kwa usaidizi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa). Kama sehemu ya mpango huu, serikali iliondoa usimamizi wa bei za bidhaa, leseni za uagizaji na uthibiti wa ubadilishaji fedha, kubinafsisha kampuni nyingi zilizomilikiwa na umma, kupunguza idadi ya wafanyi kazi wa serikali na kuanzisha sera madhubuti za kulinda fedha. Kuanzia mwaka wa 1994 hadi 1996 ukuaji halisi wa uchumi wa Kenya ulikadiriwa juu kidogo ya asilimia 4 kwa mwaka. Hata hivyo, kati ya 1997 na 2000, uchumi uliingia kipindi cha kupungua au kutoimarika, kwa sababu ya hali mbaya ya anga na kupungua kwa shughuli za kiuchumi. Mwaka wa 2001 pato la taifa liliimarika kiasi kwani mvua ilirejea kunyesha karibu na viwango vya awali. Ukuaji wa kiuchumi uliendelea kuimarika kiasi mwaka wa 2002 na kufikia asilimia 1.4 mwaka wa 2003, asilimia 4.3 mwaka wa 2004, kisha asilimia 5.8 mwaka wa 2005. Mnamo Julai 1997, Serikali ya Kenya ilikataa kutimiza makubaliano ya awali na IMF kuhusu mabadiliko ya utawala wake. Jambo hili lilisababisha kukatizwa kwa misaada kwa miaka 3, nayo Benki ya Dunia ikaubana mkopo wa dola milioni 90 za mpango wa kuufufua uchumi. Ingawa mabadiliko mengi ya kiuchumi yaliyofanywa kati ya 1993-94 yalibakia, wataalamu wa maswala ya kiuchumi wasiopendelea mabadiliko waliamini kuwa Kenya iliitaji mabadiliko zaidi, hasa ya kiutawala ili kuongeza ukuaji wa pato la taifa (GDP). Serikali ya Kenya ilichukua hatua yakini za mabadiliko, pamoja na kuunda Tume ya Kupambana na Ufisadi (KACA), kuanzisha hatua za kuimarisha uwazi wa katika mikakati ya serikali kupata bidhaa na kupunguza fedha inayotumiwa na serikali kulipia mishahara. Mnamo Julai 2000, shirika la IMF lilitia saini dola milioni 150 za Poverty Reduction and Growth Facility (PRGF), nayo Benki ya Dunia ilifuatia na mkopo wa dola milioni 157 kuimarisha uchumi na kuibadilisha sekta ya umma. Mwezi wa Desemba 2000, iliamuliwa kuwa tume ya kupambana na ufisadi haikuwa ya kikatiba na sehemu za juhudi za mabadiliko kukatizwa mwaka 2001. Shirika la IMF na Benki ya Dunia zilikatiza mipango yao. Juhudi zilizofanywa kuanzisha upya mipango hii katikati ya mwaka wa 2002 hazikufaulu. Chini ya uongozi wa Rais Kibaki, aliyechukua hatamu za uongozi tarehe 30 mwezi wa Desemba 2002, serikali ya Kenya ilianzisha mipango mipya na kabambe ya uimarishaji uchumi na imerejelea ushirikiano wake na Benki ya Dunia na IMF. Serikali mpya ya National Rainbow Coalition (NARC) iliidhinisha Sheria dhidi ya Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi pamoja na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma mnamo Mei 2003 iliyolenga kupiga vita ufisadi katika ofisi za umma. Mabadiliko mengine, hasa katika idara ya sheria, kuagiza bidhaa za umma na kadhalika yamepelekea kurejelewa kwa misaada na matumaini ya kuimarisha uchumi. Kufuatia kupitishwa kwa sheria muhimu za kupambana na ufisadi na serikali mpya, wafadhili walirejelea ufadhili mwezi wa Novemba 2003 na IMF ikaidhinisha msaada wa miaka mitatu wa dola milion 250 ili kupunguza umaskini na kuimarisha uchumi. Wafadhili wakatoa dola bilioni 4.2 kama msaada wa miaka minnne. Kurejelewa kwa ufadhili na kujihusizisha upya kwao kumevutia imani ya wawekezaji. Mswada wa ubinafsishaji umeidhinishwa ingawa kuanzishwa kwa tume ya ubinafsishaji hakujakamilika, mabadiliko katika utendakazi wa umma yametekelezwa na mwaka wa 2007 Kenya ilishinda tuzo la Umoja wa Kimataifa la Utendakazi wa Umma. Hata hivyo, kazi nyingi zinahitajika kufanywa ili kuiwezesha nchi hii kuyafikia mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi, hasa yale ya Mashariki ya Mbali. Changamoto kuu ni pamoja na kuchukua hatua thabiti dhidi ya ufisadi, kupitisha sheria zinazoshughulikia ugaidi na biashara haramu, kutatua upungufu wa ufadhili wa bajeti kisha kurekebisha na kuunda miundo msingi. Inaaminika haya yatasaidia kudumisha sera za kimsingi za kiuchumi, na kuhakikisha ukuaji wa kasi wa kiuchumi uliofikia asilimia 7.2 mwaka wa 2007. Mwaka wa 2007, serikali ya Kenya ilizindua Ruwaza 2030, ambao ni mpango wa kiuchumi wenye matumaini makuu na ambao ikiwa utatekelezwa kikamilifu, una uwezo wa kuifanya nchi hii kuwa katika kiwango sawa na mataifa yaliyoendelea kiuchumi ya Asia. Nairobi inaendelea kuwa kituo muhimu na cha kimsingi kwa mawasiliano na biashara cha Afrika Mashariki. Kinajivuna kuwa na miundo msingi ya uchukuzi na mawasiliano bora zaidi katika eneo hili, na wafanyi kazi wenye ujuzi. Makampuni mengi ya kigeni hudumisha matawi yao katika eneo hili ama ofisi za kuyawakilisha mjini Nairobi. Mnamo Machi 1996, Marais wa Kenya, Tanzania na Uganda waliifufua Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Shabaha za EAC ni pamoja na kusawazisha kodi na ada zinazotozwa bidhaa, utembeaji huru wa watu na kuimarisha miundo msingi katika eneo hili. Nchi hizi tatu za Afrika Mashariki zilitia saini mkataba wa Customs Union Agreement mwezi wa Machi 2004. Utafutaji wa mafuta Mwanzoni mwa mwaka wa 2006 Rais wa Uchina, Hu Jintao, alitia saini kandarasi ya utafutaji wa mafuta na Kenya. Haya ndiyo makubaliano ya hivi punde kati ya mfululizo wa mapatano yaliyopagwa kuelekeza maliasili ya Afrika huko Uchina ambako uchumi wake waendelea kukua kwa haraka. Kandarasi hii iliwezesha kampuni inayoongozwa na taifa la Uchina “offshore oil and gas company” CNOOC Ltd kutafuta mafuta Kenya, ambayo ilianza kuchimba visima vya kwanza mpakani mwa Sudan na Somalia na katika maji ya upwa wake. Tazama pia Orodha ya mito ya Kenya Orodha ya maziwa ya Kenya Orodha ya miji ya Kenya Orodha ya Makabila nchini Kenya Orodha ya Hifadhi za Taifa nchini Kenya Orodha ya benki nchini Kenya Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo Viungo vya nje Serikali Spokeperson serikali Ofisi Mnenaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kenya. Serikali ya Kenya Official site. Kenya Law Reports Legislation Kenya, Uchunguzi Sheria, Official Gazette Notices na kisheria Info. State House Kenya Official site State House, Kenya. Mkuu wa Nchi na Cabinet Members Jumla Maelezo ya nchi (Country Profile) kutoka BBC News Kenya kutoka Encyclopaedia Britannica Kenya kutoka UCB Libraries GovPubs Vyombo vya habari Vyombo vya habari Kenya orodha kutoka Chuo Kikuu cha Stanford Utalii Kenya Tourist Board (Magical Kenya) Historia 1911 Encyclopedia Britannica juu ya Kenya Colony 1911 Encyclopedia Britannica juu wa 1908 Dermacation wa Ethiopia-Kenya Border Nyingine Kenya Coast bibliography. Academic bibliography, hasa kwa Kiingereza, compiled by Jan Hoorweg, Afrika-Studiecentrum, Leiden. Vijijini umaskini katika Kenya (IFAD) Kenya View A photographic mkabala na uzuri wa Kenya. Kenyan Money News Mkusanyiko wa Kazi kutoka kenya. UNESCO Nairobi Office - Sekta ya Elimu Clearinghouse Solar kupikia historia na maendeleo ya hivi karibuni nchini Kenya Plus Size Expert Mkusanyiko wa habari kutoka Kenya. Nchi za Afrika Afrika ya Mashariki Jumuiya ya Madola Jumuiya ya Afrika Mashariki
1677
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mombasa
Mombasa
Mombasa ni mji mkubwa wa pili wa Kenya na wenye bandari muhimu zaidi Afrika Mashariki. Mji huu uko kwenye mwambao wa Bahari Hindi. Baada ya kuundwa kwa serikali ya ugatuzi, Mombasa umekuwa mji mkuu wa kaunti ya Mombasa. Mombasa ni kitovu cha utalii wa pwani ya Kenya. Watalii wengi hufika kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi. Wengine pia husafiri kupitia barabara kutoka Nairobi wakitazama mandhari mbalimbali. Kutoka Nairobi kwenda Mombasa ni takribani kilomita 483.77. Watalii wengi hupenda kuuona mji wa Mombasa kwanza, kisha wanaunganisha ndege hadi Kilimanjaro na sehemu nyingine zilizo na vivutio nchini Tanzania. Kati ya ishara ya mji ni Boma la Yesu na pembe za Mombasa. Mnamo mwaka wa 2016, mji wa Mombasa ulikuwa na idadi ya wakazi takriban milioni moja nukta mbili kwenye kisiwa cha Mombasa pamoja na sehemu zake barani. Wengi wao ni Waislamu. Kiswahili cha Mombasa huitwa Kimvita. Mombasa na Seattle ni "miji-ndugu". Picha Tazama pia Orodha ya miji ya Kenya Viungo vya nje Imombasa Mombasa Online (Kijerumani) Mombasa Polytechnic University College Port of Mombasa Miji ya Kenya Waswahili Kaunti ya Mombasa
1679
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
Togo
Togo ni nchi ya Afrika ya Magharibi inayofikia kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea (bahari ya Atlantiki) ikipakana na Benin upande wa mashariki, Burkina Faso kaskazini na Ghana mashariki. Idadi ya wakazi ilikuwa zaidi ya milioni 8 u nusu mwaka 2022. Mji mkuu ni Lome. Jiografia Togo ni nchi ndogo katika Afrika yenye km² 56,785 pekee kwa umbo la pembenne lenye urefu wa urefu wa kilometa za mraba km 550 na upana wa takriban km 130. Mwelekeo wa eneo la nchi ni kaskazini - kusini. Humo kuna kanda zote za kijiografia za Afrika ya Magharibi kuanzia pwani yenye mchanga na misitu ya minazi kusini, vilima vya nyanda za juu katikati na savana pamoja na maeneo yabisi zaidi ya Sahel kaskazini. Historia Nchi ilianzishwa kama koloni la Togo ya Kijerumani katika pengo kati ya maeneo ya Uingereza na Ufaransa. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia koloni la Kijerumani liligawiwa kati ya majirani hao kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na baadaye ya Umoja wa Mataifa. Mnamo Desemba 1956 wakazi wa Togo ya Kiingereza waliamua kwa kura kubaki na Ghana. Hivyo ni Togo ya Kifaransa pekee iliyopata uhuru mwaka 1960. Rais wa kwanza alikuwa Sylvanus Olympio. Watu Nchini kuna makabila 37; kubwa zaidi ni Waewe (32%). Wazungu hawafikii 1%. Lugha rasmi ni Kifaransa, ingawa kwa kawaida wakazi wanazungumza lugha za kikabila. Upande wa dini, mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa 47.8% ni Wakristo (hasa wa Kanisa Katoliki) 33% wanafuata dini asilia za Kiafrika na 18.4% ni Waislamu (hasa Wasuni). Tazama pia Orodha ya lugha za Togo Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo Bullock, A L C, Germany's Colonial Demands (Oxford University Press, 1939). Gründer, Horst, Geschichte der deutschen Kolonien, 3. Aufl. (Paderborn, 1995). Mwakikagile, Godfrey, Military Coups in West Africa Since The Sixties (Nova Science Publishers, Inc., 2001). Packer, George, The Village of Waiting (Farrar, Straus and Giroux, 1988). Piot, Charles, Nostalgia for the Future: West Africa After the Cold War (University of Chicago Press, 2010). Schnee, Dr. Heinrich, German Colonization, Past and Future – the Truth about the German Colonies (George Allen & Unwin, 1926). Sebald, Peter, Togo 1884 bis 1914. Eine Geschichte der deutschen "Musterkolonie" auf der Grundlage amtlicher Quellen (Berlin, 1987). Seely, Jennifer, The Legacies of Transition Governments in Africa: The Cases of Benin and Togo (Palgrave Macmillan, 2009). Zurstrassen, Bettina, "Ein Stück deutscher Erde schaffen". Koloniale Beamte in Togo 1884–1914 (Frankfurt/M., Campus, 2008) (Campus Forschung, 931). Viungo vya nje Serikali Republic of Togo official site National Assembly of Togo official site Chief of State and Cabinet Members Taarifa za jumla Country Profile from New Internationalist Country Profile from BBC News Togo from Encyclopaedia Britannica Togo from UCB Libraries GovPubs Key Development Forecasts for Togo from International Futures Vyombo vya habari Web Radio Togo official Web Radio Biashara Togo 2012 Summary Trade Statistics Utalii Togo Woezon Tourism Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa jumuiya ya Madola
1686
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani
Pangani
Pangani ni jina la mto, wilaya na mji katika Tanzania. * Mto wa Pangani unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani. * Wilaya ya Pangani ni kati ya wilaya za mkoa wa Tanga. * Mji wa Pangani ni makao makuu wa wilaya ya Pangani iliyomo mkoa wa Tanga ufukoni mwa Bahari ya Hindi na mto wa Pangani. Jina la Pangani hupatikana pia katika miji mbalimbali likitaja eneo au mtaa ndani yake, kwa mfano Pangani katika Nairobi, karibu na Eastleigh. Maana ni "eneo watu walipopanga nyumba zao". Makala zinazotofautisha maana
1696
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mhanga
Mhanga
Mhanga (pia muhanga, fundi-mchanga, kiharara, kukukifuku au loma; jina la kisayansi: Orycteropus afer) ni mnyama wa Afrika aliye spishi pekee ya oda Tubulidentata ambayo inaishi hadi sasa. Wanatokea pande nyingi za Afrika kusini kwa Sahara. Wahanga hula sisimizi na mchwa. Mhanga Wanyama wa Afrika Wanyamapori
1701
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
Wamasai
Wamasai ni kabila la watu wanaopatikana Kenya na Tanzania. Kwa sababu ya mila zao, mavazi tofauti na kuishi karibu na mbuga nyingi za Afrika Mashariki, ni miongoni mwa makabila yanayojulikana zaidi hata nje ya Afrika. Wao wanazungumza Maa, mojawapo ya lugha za familia ya lugha za Kinilo-Sahara inayohusiana na Kidinka na Kinuer. Kwa sababu ya uhamaji, Wamasai ndio wazungumzaji wa Kiniloti wanaoishi kusini zaidi. Pia wameelimika katika lugha rasmi za Kenya na Tanzania: Kiswahili na Kiingereza. Utafiti juu ya DNA yao umeonyesha walivyoathiriwa na urithi wa nasaba mbalimbali, hata kutoka nje ya Afrika, lakini hasa wa jamii ya Wakushi wa Afrika Mashariki. Idadi ya Wamasai wa Kenya ilihesabiwa kuwa 1,189,522 katika sensa ya mwaka 2019 na wale wa Tanzania walikadiriwa kuwa 800.000 katika mwaka 2011 ; kwa jumla inakadiriwa kuwa 2,000.000 Makadirio hayo ya Wamasai katika nchi zote mbili huenda ikawa vigumu kuyathibitisha kwa sababu ya umbali wa maeneo ya vijiji vyao vingi, na asili yao ya uhamaji. Kwa asili walikuwa wafugaji na hivyo walihamahama, na sehemu bado wanaishi maisha ya namna hiyo. Ingawa serikali za Tanzania na Kenya zimeweka mipango kuwahimiza Wamasai kuachana na jadi ya uhamaji ili kuishi maisha ya kisasa, bado wameendelea na desturi hiyo. Wao wanadai haki ya kulisha mifugo katika Hifadhi za Taifa katika nchi zote mbili. Hivi majuzi, Oxfam imedai ni lazima mtindo wa maisha wa Wamasai ukubaliwe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu hawawezi kulima katika majangwa. Historia Kulingana na historia simulizi yao wenyewe, asili ya Wamasai ni kwenye bonde la Nile ya chini, kaskazini kwa Ziwa Turkana (Kenya kaskazini magharibi). Walianza kuhamia kusini karibu na karne ya 15, wakiwasili katika shina la ardhi kutoka kaskazini mwa Kenya na Tanzania ya kati tangu karne ya 17 hadi mwisho wa karne ya 18. Makabila mengine yalilazimishwa kuyahama makazi yao Wamasai walipohamia huko. Eneo la Wamasai lilifikia kilele cha ukubwa wake katikati ya karne ya 19, na kuenea kote katika Bonde la Ufa na pande za ardhi kutoka Mlima Marsabit huko kaskazini hadi Dodoma huko kusini. Wakati huo Wamasai, na vilevile kundi kubwa la waliokuwa wamejiunga nalo, walikuwa wakivamia mifugo hadi umbali wa mashariki ya pwani ya Tanga huko Tanzania. Washambuliaji walitumia mikuki na ngao, lakini walikuwa wamehofiwa kwa kutupa vilabu (orinka) walivyoweza kutupa kwa usahihi kutoka umbali wa mita 100. Mwaka 1852 kulikuwa na ripoti ya msongamano wa wapiganaji 800 wa Kimasai kuhamia nchini Kenya. Mwaka 1857, baada ya kufyeka "Nyika ya Wakuafi" kusini mashariki mwa Kenya, washambuliaji Wamasai wakatisha Mombasa pwani mwa Kenya. Kipindi cha upanuzi ulifuatwa na "Emutai" ya miaka 1883-1902. Kipindi hicho kiliainishwa na uenezi wa magonjwa ya bovin pleuropneumonia, tauni ya ng'ombe na ndui. Kisio la kwanza la mwanajeshi wa Kijerumani huko kaskazini magharibi mwa Tanganyika ni kwamba asilimia 90 ya ng'ombe na nusu ya wanyamapori walikufa kutokana na ugonjwa wa tauni. Madaktari Wajerumani walidai kuwa katika eneo moja "kila sekunde" Afrika kulikuwa na mtoto aliyeugua matokeo ya ndui. Kipindi hicho kiliambatana na ukame. Mvua ilikosa kunyesha kabisa miaka 1897 na 1898. Mtafiti kutoka Austria, Oscar Baumann akisafiri katika nchi ya Wamasai miaka 1891-1893, alieleza makazi huko katika volkeno ya Ngorongoro katika kitabu cha mwaka 1894 durch Massailand zur Nilquelle ("Kupitia nchi ya Wamasai kwenye chanzo cha Nile"): "Kulikuwa na wanawake waliodhoofiwa mno waliotazama ule wazimu wa njaa ... mashujaa waliokuwa wameshindwa kutembea, wakiwa na wazee walioathirika na wasiojali kitu. Vikundi vya tai viliwafuata kutoka juu, wakisubiri waathirika. " Kulingana na kisio moja theluthi mbili za Wamaasai walikufa katika kipindi hicho. Kuanzia mkataba wa mwaka 1904, na kufuatiwa na mwingine wa mwaka 1911, ardhi ya Wamasai nchini Kenya ilipunguzwa kwa asilimia 60 wakati Waingereza walipowafukuza ili kutayarisha mashamba ya wakoloni, na hatimaye kuwalazimu kuishi katika wilaya ya Kajiado na Narok. Wamasai wa Tanzania walifukuzwa kutoka ardhi yenye rutuba kati ya Mlima Meru na Mlima Kilimanjaro, nyanda yenye rutuba iliyo karibu na Ngorongoro katika miaka ya 1940. Ardhi zaidi ilichukuliwa kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori na hifadhi za taifa: Amboseli, Nairobi, Masai Mara, Samburu, Ziwa Nakuru, na Tsavo nchini Kenya; Manyara, Ngorongoro, Tarangire na Serengeti huko Tanzania. Jamii ya Wamasai haijawahi kukubali kamwe usafirishaji haramu wa binadamu, na wote waliotafuta watumwa walikuwa wakiwaepuka Wamasai. Pamoja na kusimama dhidi ya utumwa, waliishi pamoja na wanyama pori wengi huku wakikataa kula wanyama hao wala ndege. Hivyo sasa ardhi ya Wamasai ina Hifadhi za Wanyamapori zilizo bora kabisa kote Afrika Mashariki. Kimsingi kuna jamii kumi na mbili za kabila la Wamasai, kila jamii ikiwa na desturi, muonekano, uongozi na lugha tofauti. Jamii hizo zinajulikana kama Keekonyokie, Daha Besdi, Purko, Wuasinkishu, Siria, Laitayiok, Loitai, Kisonko, Matapato, Dalalekutuk, Loodokolani na Kaputiei. Utamaduni Jamii ya Wamasai inafuata sana mfumo dume: katika desturi yao ni wanaume, pamoja na wazee wastaafu, wanaoamua mambo makubwa zaidi kwa kila kikundi cha Wamasai. Sheria simulizi zinashughulikia masuala mengi ya desturi. Kunyongwa kisheria hakujulikani, na malipo ya kawaida kwa ng'ombe hutosheleza mambo. Kuna mbinu za kutatua migogoro nje ya mahakama kama 'amitu', inayomaanisha 'kufanya amani', au 'arop', ambayo inahusisha kuomba msamaha wa dhati. Wamasai humwabudu Mungu pekee, nao humwita Enkai au Engai. Engai ni Mungu mmoja mwenye asili mbili: Engai Narok (Mungu Mweusi) ana huruma, na Engai Nanyokie (Mungu Mwekundu) ana ghadhabu. "Mlima wa Mungu", Ol Doinyo Lengai, uko kaskazini mwa Tanzania. Mtu mkuu katika mfumo wa dini ya Wamasai ni laibon ambaye anaweza kushiriki katika: uponyaji wa kidini, kuzungumza na Mungu na unabii, kuhakikisha mafanikio katika vita au mvua ya kutosha. Nguvu zozote alizokuwa nazo laibon zilikuwa zimetokana na utu au nafsi yake, si cheo chake. Kwa sasa Wamasai wengi wamekuwa Wakristo, na kwa kiwango kidogo Waislamu. Vifo vingi vya watoto wachanga miongoni mwa Wamasai vimesababisha watoto wengi kutotambuliwa mpaka kufikia umri wa miezi 3, ilapaitin. Kwa utamaduni, mwishoni mwa maisha yao Wamasai huzikwa bila sherehe na maiti wanaachwa nje waliwe na tumbusi Maiti kukataliwa na tumbusi na fisi, wanaojulikana kama Ondili ama Oln'gojine, huonekana kuwa kitu kibaya, na kusababisha jamii ya mfu huyo kulaumiwa. Kwa hiyo haikuwa nadra kupaka miili mafuta na damu ya ng'ombe aliyechinjwa. Mazishi ya zamani yalikuwa yametengwa kwa waheshimiwa wakubwa, kwani iliaminika kuwa mazishi yalidhuru udongo. Maisha ya Wamasai inahusika sana na ng'ombe, ambao huwa msingi wa chakula chao. Kipimo cha mali ya mtu ni idadi ya mifugo na watoto alionao. Kuwa na ng'ombe 50 au zaidi kunaheshimika, na watoto wengi zaidi ni bora. Mtu ambaye anao wengi upande mmoja lakini si upande wa pili anahesabiwa kama maskini. Wamasai huamini kwamba Mungu aliwapa wao ng'ombe wote duniani, kwa hiyo kuchukua mifugo kutoka makabila mengine ni suala la kudai haki yao, lakini zoezi hili limepungua. Katika Bonde la Ufa, ambako kabila hilo liliishi kwa karne nyingi, hakukuwa na malaria, hakuna magonjwa ya ng'ombe, hakuna nzi wanaovamia na kusababisha magonjwa kwa mifugo na ugonjwa hatari kwa watu. Mwanzoni mwa karne iliyopita, wakoloni waliingia Afrika Mashariki. Kabila la Wamasai daima limepinga kwa uthabiti utumwa na kuishi karibu na wanyama wengi wa pori duniani, bila kutaka kula ndege na wanyamapori na ni moja la machache yaliyoweka upinzani mkali kwa wakoloni wa Kiingereza. Kwa takriban miaka kumi (1890-1900), Wamasai walipigania ardhi zao kwa mikuki dhidi ya bunduki za wakoloni. Waliuawa kwa maelfu, na pia ng'ombe, kondoo na mbuzi kuibiwa na kutumika kulisha majeshi yaliyowavamia. Kufikia 1901-1902 kabila la Wamaasai lilishindwa. Mnamo 1904, Waingereza waliwalazimisha Wamasai waliokatishwa tamaa kuondoka kwenye malisho yenye rutuba ya Bonde la Ufa na kuhamia nchi za kusini (eneo la Mbuga ya Masai Mara ya sasa). Waingereza walilazimisha kusainiwa kwa makubaliano, ambayo wao wenyewe walighairi miaka saba baadaye kwa sababu walitaka ardhi zaidi kwa makazi ya Wazungu. Mnamo 1911, makubaliano mengine yalitiwa saini, ambayo wavamizi pia hawakuzingatia. Makazi Kihistoria Wamaasai ni watu wanaohamahama, kwa hiyo tangu jadi wamekuwa wakitumia vinavyopatikana kwa urahisi ili kujenga makazi yao. Nyumba zao za asili ziliundwa kwa ajili ya kuhama mara kwa mara, kwa hiyo hazikujengwa za kudumu. Inkajijik (nyumba hizo) zina umbo la nyota au mviringo, na hujengwa na wanawake. kwa mbao, matawi madogo yaliyochanganywa na matope, vijiti, majani, kinyesi cha ng'ombe, mkojo wa binadamu, na majivu. Mavi ya ng'ombe inahakikisha kuwa paa halivuji, na maji ya mvua yasiweze kupita. Enkaji ni ndogo, kipimo cha mita 3x5 na kimo cha m 1.5 kwenda juu. Ndani ya nafasi hiyo familia hupika, hula, hulala, hupiga gumzo na huweka akiba ya chakula, mafuta na mali nyingine. Mifugo wadogo mara nyingi pia huwekwa ndani ya enkaji. Vijiji huzungukwa na ua (Enkang) lililojengwa na wanaume kwa kutumia miiba ya acacia, mti wa asili. Usiku wote ng'ombe, mbuzi na kondoo huwekwa katikati ya ua hilo, kuwalinda kutokana na wanyamapori. Mpangilio wa jamii Kitengo kati ya jamii ya Wamasai ni umri. Ingawa wavulana hutumwa nje na ndama na kondoo kuanzia utotoni, utoto kwa wavulana ni wakati wa kucheza, isipokuwa kuchapwa viboko kidesturi ili kuthibitisha ujasiri na uvumilivu. Wasichana huwajibika katika kazi ndogondogo kama vile kupika na kukamua ng'ombe, ujuzi ambao hujifunza kutoka kwa mama zao kuanzia umri mdogo. Kila baada ya miaka 15 hivi, kizazi kipya cha Morans au Il-murran (wapiganaji) kitatahiriwa. Hii inahusisha wavulana wengi kati ya umri wa miaka 12 na 25, ambao wamebalehe na si wa kizazi kilichopita. Moja ya sherehe ya kupita ujana hadi upiganaji ni sherehe ya tohara, ambayo inafanywa bila dawa ya kugandisha misuli. Hii tohara hufanywa na wazee, ambao hutumia kisu chenye makali na kigozi cha ng'ombe kufunika jeraha. Neno la Kimasai kwa tohara ni 'emorata'. Kijana lazima avumilie operesheni akiwa kimya. Kuonyesha maumivu huleta aibu, angalau kwa muda. Maneno yoyote ya mshangao yanaweza kusababisha makosa katika operesheni hiyo nyeti, ambayo inaweza kuleta matatizo mengi, majeraha zaidi, na maumivu. Mchakato wa uponyaji utachukua miezi 3-4, wakati ambao kuna uchungu kwenda haja ndogo na wakati mwingine hata hauwezekani, na wavulana lazima wabaki katika nguo nyeusi kwa kipindi cha miezi 4-8. Katika kipindi hicho, wavulana waliotahiriwa wataishi katika "manyatta", yaani "kijiji" kilichojengwa na mama zao. Manyatta hizo hazina nyua za kulinda boma, ili kusisitiza jukumu lao la kulinda jamii. Hakuna ua la mifugo linalojengwa, kwa sababu wapiganaji hawana ng'ombe wala hawana jukumu la kufuga. Ibada za kifungu zaidi zinahitajika kabla ya kufikia hadhi ya mpiganaji mwandamizi, ikifikia upeo katika sherehe ya 'eunoto', yaani "ujio wa umri". Wakati kizazi kipya cha mashujaa kinaanzishwa, waliokuwa ilmoran huendelea kuwa "wazee bila mamlaka", ambao huwajibika kwa maamuzi ya kisiasa hadi wafanywe "wazee wenye mamlaka". Wapiganaji wana jukumu la usalama katika jamii, na hutumia muda wao mwingi wakizuru ardhi yao, pia hupita mipaka yao. Pia wanazidi kushiriki katika biashara ya mifugo kuliko awali, kuendeleza na kuboresha hisa za msingi kupitia biashara na kubadilisha bidhaa. Wavulana wana wajibu wa kuwalinda mifugo wadogo. Katika msimu wa ukame, wote wapiganaji kwa wavulana huchukua jukumu la ufugaji. Wazee ni wakurugenzi na washauri wa shughuli za kila siku. Wanawake wana jukumu la ujenzi wa nyumba, na vilevile kuchota maji, kuokota kuni, kukamua ng'ombe na kupikia familia. Hadithi moja kuhusu Wamasai ni kwamba kila kijana anatakiwa kuua simba kabla atahiriwe. Ingawa simba walikuwa wanawindwa zamani, na uwindaji huo umepigwa marufuku katika Afrika Mashariki, bado simba huwindwa wanapowaua mifugo, na vijana mashujaa wanaohusika katika mauaji hayo hupewa heshima kuu. Kutokana na wasiwasi kuhusu idadi ya simba nchini, kuna mpango wa kulipa fidia wakati simba anapowua mifugo, badala ya uwindaji na kuua simba. Hata hivyo, kuua simba mmoja kuna thamani kubwa na heshima katika jamii. Wasichana pia hutahiriwa ('emorata') wanapobalehe na hupewa maelekezo na ushauri zinazohusiana na majukumu yao mapya, wanasemekana kuwa wamehitimu umri wa wanawake, tayari kuolewa. Ukeketaji nchini Kenya unatekelezwa kwa 38% ya wakazi. Namna ya kawaida ni clitorectomy. Tendo hilo linaweza kusababisha kovu nene ngozini, ambalo linafanya vigumu kwenda haja ndogo, na hii pia umeleta utata. Ukeketaji ni haramu nchini Kenya na Tanzania na huleta ukosoaji mwingi kutoka nje ya nchi zote mbili na hata kutoka kwa wanawake ambao wameupitia, kama vile Mmasai mwanaharakati Agnes Pareiyo. Ni hivi majuzi katika sehemu mbalimbali imebadilishwa na "kukatwa kwa maneno", sherehe kuwashirikisha kuimba na kucheza katika nafasi ya ukeketaji. Hata hivyo, unabakia na thamani kwa utamaduni. Baadhi wanafikiria ni muhimu kwa sababu Wamasai wanaume wanaweza wakakataa mwanamke asiyetahiriwa, eti haoleweki, au sivyo mahari yake itapunguzwa. Tohara hizo ni kawaida kufanywa na 'mtekelezaji' ambaye mara nyingi si Mmasai, kwa kawaida hutoka kwa Wandorobo. Visu vya tohara hutengenezwa na wafua-chuma, 'il-kunono', ambao huepukwa na Wamaasai kwa sababu ya kutengeneza silaha za kifo (visu, panga fupi ('ol alem'), mikuki, n.k.). Sawa na wanaume vijana, wanawake ambao wamekeketewa huvaa nguo nyeusi, hujipaka rangi na alama kwenye nyuso, na kisha kufunika nyuso zao wanapokamilisha sherehe. Wanawake walioolewa wanapokuwa waja wazito huruhusiwa kutofanya kazi nzito kama kukamua ng'ombe na kuokota kuni. Mahusiano ya kingono pia yanapigwa marufuku. Wamasai huoa wake wengi; hii hutendwa ili kukabiliana na vifo vingi vya watoto wachanga na wapiganaji. Kuolewa na wanaume wengi pia kunakubaliwa: mwanamke huolewa si na mumewe tu, lakini umri mzima wa kikundi chake. Wanaume hutarajiwa kumpa mgeni wa rika lake kitanda na mwanamke. Mwanamke anaamua mwenyewe kama atajiunga na mtu huyo. Mtoto yeyote atakayezaliwa ni mtoto wa mume katika utaratibu wa Kimasai. "Kitala", aina ya talaka au kukimbilia, inawezekana katika nyumba ya mke wa baba, kwa sababu ya kumdhulumu mke. Kurudisha mahari, ulinzi wa watoto, n.k. hukubaliwa baadaye. Arusi Wamasai ni watu wa jadi na hawabadili utamaduni wao kwa vikubwa. Hata hivyo, hii inabadilika polepole. Wamasai wanaanza kuvaa mavazi za kisasa pia. Desturi moja ambayo inabadilika ni arusi. Wasichana wanaolewa wakati wapo kati ya umri wa miaka kumi na mbili na ishirini. Lakini, mila hii inabadilika kwa sababu wasichana wanaenda elimu ya juu na hawawezi kuanza famila bado. Siku kabla ya harusi, mume ataleta mwisho wa mahari iliyokubaliwa kwa familia ya msichana. Mahari kwa kawaida ni fedha, ng’ombe, mablanketi, na asali pamoja. Siku hiyo, msichana ananyolewa kichwa chake kama ishara ya mwanzo wake mpya. Hata hivyo, wanawake wa Kimasai wengi hawana nywele na wanaweka kichwa chao. Harusi inaanza na baraka kutoka kwa mzee. Yeye hutoa maziwa karibu na nyumba ya mama wa msichana. Kabla ya msichana kuondoka nyumbani, amefungwa nyasi katika viatu vyake. Hii ni baraka pia kwa sababu nyasi inaashiria wingi kwa Maasai watu. Watu kutoka kijiji cha msichana wanamtembelea kabla ya kuondoka na wanaahidi zawadi. Msichana hufunga fimbo katika mkufu wake kwa kila zawadi. Inaitwa enkariwa na hii inamkumbusha ngapi anavyopaswa kukusanya baada ya harusi. Kisha, sherehe iko katika kijiji cha mtu huyo. Wakati bibi inapofika, yeye anapokea mtoto kuwaonyesha watoto ambao atakuwa nao. Kukabili mashariki, ishara ya mwanzo mpya, wanaarusi hupata baraka za Kimasai kutoka kwa mzee wa Kimasai kutoka kwa jamii. Kisha, wanakula mbuzi na wanacheza muziki. Muziki na ngoma Muziki wa kitamaduni wa Kimasai huwa na sauti kutoka kwaya ya waimbaji huku kiongozi wa nyimbo, 'Olaranyani', huimba kiitikio. Olaranyani kwa kawaida ni yule mwimbaji bora ambaye anaweza kuimba wimbo huo, ingawa watu kadhaa huweza kuongoza wimbo. Olaranyani huanza kwa kuimba mstari kichwa (namba) cha wimbo. Kikundi basi kitajibu kwa kukubali, na Olaranyani ataimba mistari huku kikundi kikiimba. Kila wimbo una namba maalum kulingana na kuita-na-kuitika. Mipangilio ya nyimbo ya kawaida huwa ya 5 / 4, 6 / 4 na 3 / 4 wakati saini. Maneno hufuata maudhui maalumu na hurudiwa mara nyingi baada ya muda. Kutingisha shingo huongozana na kuimba. Wakati wa kupumua kichwa huelekezwa mbele. Kichwa huelekezwa nyuma kwa ajili ya kuvuta pumzi. Kwa ujumla hii hueneza ratiba ya sauti zao. Wanawake huimba nyimbo tulivu, na nyimbo za kuwasifu watoto wao. Namba, ule mfano wa wito-na-majibu, marudio ya misemo isiyokuwa na maana, misemo ifuatayo kila mstari kwa kurudiwarudiwa, na waimbaji kukabiliana na mistari yao ni ishara ya kuimba kwa wanawake. Wakati wanawake wamasai wengi hukusanyika pamoja, wao huimba na kucheza kati yao wenyewe. Wamasai hutumia sauti zao pekee wanapoimba, isipokuwa wanapotumia pembe la Greater Kudu kuwaalika Wamoran kwa sherehe ya Eunoto Kuimba na kucheza wakati mwingine hufanyika katika manyatta, na kuhusisha kutaniana. Wavulana hupiga foleni na kuimba, "Oooooh-yah", kwa kikohozi, pamoja na msukumo wa miili yao. Wasichana husimama mbele ya wanaume na kusokota miili huku wakiimba "Oiiiyo .. yo" katika kuwajibu wanaume. Ingawa miili yao hukaribiana, hawagusani. Eunoto, sherehe ya kubalehe kwa mpiganaji, inaweza kuhusisha siku kumi au zaidi za kuimba, kucheza na ibada. Wapiganaji wa Il-Oodokilani hufanya aina ya mchezo inayoitwa adumu, au aigus, mara nyingine inajulikana kama "ngoma ya kuruka". (adumu na aigus ni vitenzi vinavyomaanisha "kuruka" na adumu humaanisha "Kuruka juu na chini katika ngoma" Wapiganaji hujulikana vizuri, na mara nyingi hupigwa picha, katika ushindani huo wa kuruka. Wapiganaji huingia katika mviringo, na moja au wawili wataingia kati ya mviringo kuanza kuruka, bila kuacha visigino vyao kugusa ardhi. Wajumbe wa kikundi wanaweza kuongeza sauti zao kwa kuzingatia urefu wa wanavyoruka. Washikaji wa Moran ('intoyie') hujitembeza katika nguo maridadi kuvutia wengi wao kama mmojawapo ya eunoto. Mama wa Moran huimba na kucheza kuonyesha heshima kwa ujasiri wa watoto wao. Wanamuziki wa Hip Hop wa kisasa, X Plastaz, kutoka kaskazini mwa Tanzania wamechanganya sauti na midundo ya Wamasai katika muziki wao. Alama mwilini Kutoboa na kunyosha ndewe ni kawaida ya Wamasai. Vifaa mbalimbali hutumika kutoboa na kunyosha masikio, kama vile miiba kwa kutoboa, ukuti, mawe, msalaba, sehemu ya jino la tembo n.k. Idadi ya Wamasai wanaofuata desturi hiyo, hasa wavulana, inazidi kupungua. Wanawake huvaa aina mbalimbali za mapambo katika ndewe la sikio, na mapambo madogo juu ya sikio. Kung'oa jino mojawapo kati ya machonge mapema utotoni ni zoezi ambalo limetiwa kumbukumbu katika Wamasai wa Kenya na Tanzania. Kuna imani kati ya Wamasai kuwa kuhara, kutapika na magonjwa mengine yanayoathiri watoto husababishwa na kuvimba kwa mizizi ya meno, ambayo hufikiriwa kuwa na 'minyoo' au ni 'meno ya karatasi' au 'meno ya plastiki'. Imani hiyo si ya pekee kwa Wamasai. Vijijini Kenya katika kundi la watoto 95 wenye umri kati ya miezi sita na miaka miwili waliotahiniwa mwaka 1991/92, 87% walipatikana kuwa wameng'olewa jino moja au zaidi. Katika kundi la watoto wa umri wa miaka 3-7, 72% ya watoto walikuwa hawana meno ya kusiaga. mchoro Maakuli Kijadi, Wamasai hula nyama, maziwa na damu ya ng'ombe. Utafiti wa ILCA (Nestel 1989) unasema: "Leo hii, chakula kikuu cha Kimasai ni maziwa ya ng'ombe na unga wa mahindi. Wao huyanywa maziwa pekee au katika chai na unga wa mahindi hutumiwa kupika uji au ugali. Unga ulioshikamana unajulikana kama ugali na huliwa na maziwa; na hii inatofautiana na uji, ambayo hutayarishwa na hupikwa na maziwa. Nyama, ingawa ni chakula muhimu, huliwa kwa nadra, kwa hiyo haiwezi kutambulika kama chakula kikuu. Mafuta ya nyama hutumika katika kupika, sanasana uji, mahindi na maharagwe. Siagi pia ni chakula muhimu cha watoto wachanga. Damu hunywewa kwa nadra." Utafiti wa International Livestock Centre for Africa (Bekure et al. 1991) unaonyesha mabadiliko makubwa sana katika mlo wa Kimasai kuelekea bidhaa zisizo za mifugo pamoja na mahindi kuwa asilimia 12-39 na sukari asilimia 8-13; na wastani wa lita moja ya maziwa hunywewa na kila mtu kwa siku. Maziwa hayo hutumika sanasana kama maziwa lala au maziwa-siagi - maziwa yaliyochanganywa na siagi. Maziwa hutumika sana. Mahitaji ya protini huwa yametoshelezwa kikamilifu. Hata hivyo, ugavi wa chuma, niasini, vitamini C, vitamini A, thiamine na nguvu haviwezi kupatikana kikamilifu kwa kunywa maziwa pekee. Kutokana na kubadilika kwa mazingira, hasa msimu wa ukame wa mara kwa mara, wafugaji wengi, pamoja na Wamasai, hutumia nafaka katika maakuli . Wamasai hufuga ng'ombe, mbuzi na kondoo, pamoja na kondoo mwekundu, vilevile ng'ombe waliothaminiwa zaidi. Vipimo vya moyo vilitumiwa kwa wavulana Wamasai 400 na hakukuwa na ushahidi wowote wa ugonjwa wa moyo, upungufu au ulemavu. Utafiti zaidi ulionyesha kuwa wastani wa kiwango cha mafuta moyoni ulikuwa asilimia 50 za wastani wa Wamarekani. Matokeo hayo yalithibitisha afya ya Wamoran, ambayo ilitathminiwa kama "kiwango cha Olimpiki". Supu pengine ni mmojawapo ya matumizi muhimu zaidi ya mimea kwa chakula cha Wamasai. Acacia nilotica ni mmea wa supu unaotumika mara nyingi. Mzizi au shina huchemshwa katika maji na kutumiwa peke yake au huongezwa kwa supu. Wamasai hupenda kuichukua kama dawa, na inajulikana kuwafanya jasiri, wenye nguvu na washindani. Wamasai hunywa supu yenye gome na mizizi inayopunguza mafuta moyoni; Wamasai wanaoishi mijini, ambao hawana mimea hiyo, hupatwa na maradhi ya moyo. Ingawa yanatumiwa kama vitafunio, matunda huwa sehemu kubwa ya chakula cha watoto na wanawake wanaochunga wanyama na pia moran jangwani. Kuchanganya damu ya ng'ombe na maziwa inafanywa kuandaa kinywaji cha kitamaduni katika sherehe za pekee na pia kama chakula kwa wagonjwa. Hata hivyo, kuchanganya damu katika mlo unadidimia kutokana na kupunguka kwa idadi ya mifugo. Hivi majuzi, Wamasai wamekuwa wakitegemea vyakula kutoka maeneo mengine kama vile unga wa mahindi, mchele, viazi, kabichi (zinazojulikana na Wamasai kama majani ya mbuzi) n.k. Wamasai ambao wanaishi karibu na wakulima wameshughulikia kilimo kama msingi wa kujikimu. Katika maeneo hayo, mashamba hayo hayawezi kudumisha idadi kubwa ya wanyama; hivyo Wamaasai hulazimika kulima. Mavazi Mavazi hutofautiana kadiri ya umri, jinsia, na mahali. Vijana wa kiume, kwa mfano, huvaa nguo nyeusi kwa miezi kadhaa inayofuata tohara. Hata hivyo, nyekundu ni rangi iliyopendelewa. Bluu, nyeusi na milia huvaliwa kama zilivyo miundo na rangi za Kiafrika. Wamasai walianza kubadilisha ngozi ya wanyama, ndama na kondoo ili kutumia nguo za pamba katika miaka ya 1960. Mashuka ni vitambaa vinavyozungushwa mwilini, juu ya kila bega, kisha ya tatu juu yao. Hizi kwa kawaida huwa nyekundu, ingawa kuna rangi nyingine (k.m. bluu). Rangi ya waridi, hata yenye maua, haidharauliwi na wapiganaji. Mavazi yanayojulikana kama kanga hupatikana kwa urahisi. Wamasai wanaoishi karibu na pwani huvaa kikoi, aina ya kitambaa inayopatikana katika rangi mbalimbali na nguo. Hata hivyo, mtindo uliopendelewa ni mistari. Wamasai wengi huko Tanzania huvaa makubadhi, ambayo walikuwa mpaka hivi majuzi wakizitengeneza kutoka ngozi ya ng'ombe kulinda nyayo. Siku hizi hutumia gurudumu au plastiki kuyatengeneza. Wanaume na wanawake huvaa vikuku vya mbao. Wamasai wanawake mara kwa mara hufuma marembesho na mikufu ya shanga. Ushanga huwa sehemu muhimu ya urembesho wa miili yao. Ingawa kuna tofauti katika maana ya rangi ya shanga, baadhi ya maana kwa jumla ya rangi chache ni: nyeupe, amani; bluu, maji; nyekundu, mpiganaji / damu / shujaa. Ushanga, unaofanywa na wanawake ina historia ndefu kati ya Wamasai, ambao hujitambulisha katika jamii kupitia mapambo ya mwili na uchoraji. Kabla ya kuwasiliana na Wazungu shanga zilikuwa zikitengenezwa kutoka vifaa vya kienyeji. Shanga nyeupe zilitengenezwa kutoka udongo, pembe, au mfupa. Shanga nyeusi na bluu zilitengenezwa kutoka chuma, makaa, mbegu, udongo, au pembe. Shanga nyekundu zilitengenezwa kutoka mbegu, mbao, maburu, mifupa, pembe, shaba, au chuma. Katika karne ya 19, shanga nyingi zenye rangi mbalimbali zilifika Afrika Mashariki kutoka Ulaya, zikabadilishwa na shanga za jadi na kutumiwa kutengeneza mipangilio bora ya rangi. Hivi sasa, shanga za kioo, bila urembesho hupendelewa. Nywele Kunyoa kichwa ni kawaida katika sherehe za kubalehe, kuwakilisha mwanzo mpya kutoka sura moja ya maisha hadi nyingine. Wapiganaji tu wanaruhusiwa kuwa na nywele ndefu, ambazo huzifuma katika nyuzi ndogondogo. Anapofikisha umri wa miezi 3, mtoto hupewa jina na kichwa hunyolewa safi, isipokuwa kifurushi cha nywele, kinachofanana na kilemba cha jogoo kutoka shingo hadi paji la uso. Ufananishi huu na jogoo humaanisha "hali ya neema" wanayopewa watoto wachanga. Mwanamke aliyepoteza mtoto awali alipokuwa akijifungua ataweka kifurushi hiki cha nywele mbele au nyuma ya kichwa, kutegemea kama alipoteza mvulana au msichana. Siku mbili kabla ya wavulana kutahiriwa, vichwa vyao hunyolewa. Kisha vijana mashujaa huruhusu nywele zao kukua, na hutumia muda mwingi wakisuka nywele. Nywele hizo hupakwa mafuta ya wanyama na mchanga mwekundu, na huhasimiwa juu ya kichwa kwa kipimo cha masikio. Nywele kisha husukwa: inagawanyishwa katika sehemu ndogo na kusongwa kwanza ikiwa imetenganishwa, halafu ikiwa imeunganishwa. Pamba au nyuzi za sufu zinaweza kutumiwa kurefusha nywele. Nywele zilizosukwa huweza zikaachwa zimelegea au zikafungwa pamoja kwa ngozi. Wakati wapiganaji kwenda kupitia Eunoto, na kuwa wazee, nywele zao ndefu zilizosukwa hunyolewa. Vilevile wanaume hunyoa nywele wanapopita kifungu kimoja cha maisha hadi kingine. Bibiarusi pia atanyolewa kichwa chake, na kondoo wawili dume watachinjwa kuzingatia sherehe hiyo. Ushawishi wa dunia ya kisasa Sera za serikali, kama vile hifadhi na utunzaji wa akiba, na kutengwa kwa Wamasai, pamoja na kuongeza idadi, n.k. zimefanya vigumu kudumisha maisha ya Wamasai. Katika kuongezeka kwa umaskini na uhamiaji, mamlaka ya wazee wa jadi wa Kimasai inaonekana kudidimia. Kwa muda, miradi mingi imeanza kusaidia viongozi wa Kimasai kutafuta njia za kuhifadhi mila zao na pia kusawazisha mahitaji ya elimu ya watoto wao kwa dunia ya kisasa. Njia za ajira zinazojitokeza miongoni mwa Wamasai ni kilimo, biashara (kuuza dawa za jadi, biashara ya mikahawa / maduka, kununua na kuuza madini, kuuza bidhaa za maziwa na wanawake, nyuzi), na mshahara wa ajira (kama walinzi wa usalama / wapishi, kuongoza watalii), na wengine ambao wanahusika katika sekta mbalimbali. Wamasai wengi wameacha maisha ya wahamaji na kupata nafasi za kuwajibika katika biashara na serikali. Hata hivyo, licha ya maisha ya kisasa wanayoishi mjini, wengi hurudi nyumbani na nguo za kisasa, na hutoka kwenye familia yao wakiwa wamevalia shuka la kitamaduni (kitambaa cha rangi nyingi), patipati za ngozi ya ng'ombe, na fimbo ya mbao ('o-rinka') - wakihisi huru kwa wenyewe na dunia. Tanbihi Viungo vya nje Kazi kwa haki na kujitegemea kwa jamii kuendeleza Wamasai Watu Mara Triangle Wamaasai Vijiji Association Mtandao wa Change Shirika kwa Wamaasai Wamaasai mawasiliano / info kubadilishana - noc Marafiki Marafiki Kisaru Wamaasai Mradi Massailand Website kuhusu Wamaasai watu na kusaidia miradi. Kujitolea kusaidia miradi katika Maasailand - Kenya Wamaasai Trust Wamasai Makabila ya Kenya Makabila ya Tanzania
1705
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
Ulaya
Ulaya (asili ya jina ni neno la Kiarabu ولاية, wilaayatun; inaitwa pia Uropa) ni bara lenye eneo la km² 10,600,000 tu, lakini wakazi ni milioni 747 . Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa ukoloni walitawanyika duniani, hasa Amerika, wakiathiri kote upande wa lugha, utamaduni na dini. Utawala Katika karne ya 20, baada ya vita kuu mbili, nchi mbalimbali za Ulaya zilianza kushirikiana kwa njia mbalimbali: Baraza la Ulaya lina nchi wanachama 47 Mkutano wa usalama na ushirikiano katika Ulaya (Marekani na Kanada ni wanachama pia) Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 28 tangu mwaka 2013. Kanda za Ulaya Katika orodha inayofuata kanda zinatajwa katika utaratibu wa Umoja wa Mataifa (UN categorisations/map). Lakini utaratibu huo haukubaliki ndani ya Ulaya kwa nchi za Ulaya ya Kati. Wajerumani, Waaustria, Waswisi, Wacheki, Waslovakia na Wapoland hukubaliana ya kwamba wenyewe si Ulaya ya Magharibi wala ya Mashariki ila Ulaya ya Kati. Kuna majadiliano kuhusu mipaka ya kanda hili yasiyokwisha bado, kwa mfano suala la Hungaria au Latvia. Orodha ya nchi na maeneo Tanbihi 1. Kanda zinazotajwa (Ulaya ya Kusini – magharibi n.k.) zinafuata utaratibu wa Umoja wa Mataifa UN categorisations/map. Nchi kadhaa zinazotajwa hapo chini zinaweza kuhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya na pia bara nyingine (Asia, Afrika, au Oceania). Hii inategemea na namna ya kugawa kontinenti; pia wakazi wenyewe wanaweza kujielewa tofauti na majirani yao. 2. Urusi ni nchi ya kontinenti mbili za Ulaya ya Mashariki na Asia; namba za wakazi na za eneo zimetasjwa kwa ajili ya sehemu ya Kiulaya pekee. 3–5. Guernsey, Kisiwa cha Man, and Jersey ni maeneo ya kujitegemea chini ya Taji la Ufalme wa Uingereza. 6. Namba za Ureno hazijumlishi Visiwa vya Madeira, ambazo ni sehemu ya Ureno magharibi ya Marokko katika Afrika. 7. Namba za Hispania hazijumlishi Visiwa vya Kanari magharibi ya Marokko katika Afrika, wa maeneo ya Ceuta na Melilla ambayo ni sehemu za Hispania kwenye pwani ya Moroko, Afrika ya Kaskazini. 8. Namba za Ufaransa hazijumlishi maeneo yake yaliyopo Amerika ya Kati au Kusini, Bahari Hindi au Oceania. 9. Uholanzi: Idadi ya wakazi ni ya 2004; Amsterdam ni Mji Mkuu lakini Den Haag ni makao makuuy a serikali. 10. Armenia huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki 11. Azerbaijan huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee. 12. Kupro huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Kusini; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu zisozo chini ya Dola ya Kituruki ya Cyprus. 13. Georgia huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee. 14. Uturuki ni nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Kusini; namba zinazotajwa zinahusiana na sehemu ndogo ya Magharibi pakee iliyomo Ulaya hasa jimbo lote la Istanbul. 15. Kazakhstan huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee. Tazama pia Marejeo Bara
1706
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lituanya
Lituanya
Lituanya (au Lituania) ni nchi huru iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Ulaya. Inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Lituania. Inapakana na Latvia, Belarus, Polandi na Russia. Ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Mji mkuu wa Lituania ni Vilnius. Jiografia Lituanya iko kwenye mwambao wa Bahari ya Baltiki. Miji mikubwa Kaunas Vilnius Historia Lituania kuanzia karne ya 13 ilikuwa nchi huru na imara iliyoteka maeneo mengi; kufikia karne ya 15, ikiwa pamoja na Polandi, ilikuwa kubwa kuliko nchi zote za Ulaya. Mwaka 1795 nchi hizo mbili zilifutwa, na Lituania ikawa sehemu ya Dola la Urusi. Mwaka 1918, ikawa tena nchi huru, lakini mwaka 1940 Warusi waliiteka tena. Miaka 1940 - 1990 nchi ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti. Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Lituania ilijitangaza nchi huru. Lituania imekuwa nchi mwanachama ya Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004. Wakazi Wananchi kwa asilimia 84 wanaongea Kilituania ambacho pamoja na Kilatvia ndizo lugha hai pekee za jamii ya lugha za Kibaltiki kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Ndiyo lugha rasmi. Mbali na Walituania asili (86.7%), kuna Wapolandi (5.6%), Warusi (4.8%) na wengineo. Dini ya wananchi ni Ukristo wa Kanisa Katoliki (77.2%), mbali ya Waorthodoksi (4.9%) na Waprotestanti (0.8%). Wasio na dini yoyote ni 6.1%. Tazama pia Wilaya za Lituanya Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Viungo vya nje Serikali The Lithuanian President – Official site of the President of the Republic of Lithuania The Lithuanian Parliament – Official site of the Parliament of the Republic of Lithuania The Lithuanian Government – Official site of the Government of the Republic of Lithuania Chief of State and Cabinet Members Statistics Lithuania – Official site of Department of Statistics to the Government of Lithuania Taarifa za jumla Lithuania from UCB Libraries GovPubs Lithuania from the BBC News Lietuva.lt/en – Lithuanian internet gates Key Development Forecasts for Lithuania from International Futures Heraldry of Lithuania Safari Lithuanian State Department of Tourism Travel Channel movie about Lithuanian – "Essential Lithuania 2010" www.travel.lt – The Official Lithuanian Travel Guide Nchi za Umoja wa Ulaya Mkataba wa Schengen Umoja wa Forodha wa Ulaya Nchi za Ulaya
1707
https://sw.wikipedia.org/wiki/Europa
Europa
Europa ni neno katika lugha mbalimbali lenye asili ya Kigiriki "Ευρώπη" la kutaja bara la Ulaya Europa (mitholojia), binti wa mfalme katika masimulizi ya dini ya Wagiriki wa Kale aliyekuwa mpenzi wa mungu mkuu Zeus Europa (mwezi), mwezi wa pili kati ya miezi ya Mshtarii 52 Europa, asteroidi katika mfumo wa jua Europa (kisiwa), kisiwa ndogo cha Kifaransa katika Bahari Hindi ni sehemu ya Îles Éparses Europa (kombora) ilikuwa kombora la Kiulaya la kurusha vyombo angani kabla ya kupatikaka kwa makombora ya Ariane Kuna pia nyimbo, vitabu, meli, gari na michezo ya kompyuta na makampuni zinazoitwa "Europa" Makala zinazotofautisha maana
1749
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dodoma
Dodoma
Dodoma ni jina la Mji wa Dodoma ambao ni Mji Mkuu wa Tanzania Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Dodoma (mjini na kijijini). Pia ni makao makuu ya chama tawala Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tanzania Makala zinazotofautisha maana
1750
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi
Shilingi
Shilingi ni pesa inayotumika kwa malipo halali katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Somalia. Historia ya Shilingi Asili ya jina ni kitengo cha kihistoria cha pesa katika nchi mbalimbali za Ulaya kama vile Austria, Uswisi, Uingereza, Poland, Denmaki, Norwei na Uswidi. Katika nchi nyingi kati ya hizo pesa hiyo haikutumika tena isipokuwa hadi mwaka 1971 Pauni ya Uingereza ilikuwa na shillings 12 na kila shilling ilikuwa na penny 20. Nchi nyingi zilizorithi mfumo wa pesa kutoka Uingereza walitumia pauni na shilingi hadi kuhamia kwenye pesa ya desimali. Zaidi tena huko Austria "Schilling" ilikuwa pesa rasmi hadi nchi kujiunga na Euro. Shilingi ya Afrika Mashariki Uingereza ilitoa "East African Shilling" kuanzia mwaka 1921 kama pesa ya pamoja kwa ajili ya makoloni yake ya Kenya, Uganda na Tanganyika. Zanzibar ilijiunga na shilingi hiyo mwaka 1935 ilipoacha rupia zake. Baada ya uhuru nchi hizo zilivunja umoja wa kifedha zikaanzisha pesa zao za pekee. Zote zinaitwa shilingi lakini thamani ilianza kutofautiana haraka, ya Kenya ikiongoza na ya Uganda kushika nafasi ya mwisho. Kuna majadiliano ya kurudisha shilingi ya pamoja kwa nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki. Kwanza ilitarajiwa kuanzishwa mwaka 2012, halafu mwaka 2015, sasa mwaka 2024. Picha Tanbihi Pesa Jumuiya ya Afrika Mashariki uchumi wa Kenya uchumi wa Tanzania uchumi wa Uganda uchumi wa Somalia
1751
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro%20%28Volkeno%29
Kilimanjaro (Volkeno)
Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima. Kijiolojia Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730. Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani. Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa. Jina Asili ya jina "Kilimanjaro" haijulikani kikamilifu. Vyanzo vya kimaandishi vinajulikana tangu takriban mwaka 1860 ambapo wapelelezi Wazungu walitumia jina hilo katika taarifa zao wakidai "Kilimanjaro" ni jina la Kiswahili. Pamoja na umbo hili kulikuwa pia na tahajia ya sehemu mbili ama "Kilima-Njaro" au kwa namna ya Kijerumani “Kilima-Ndscharo”. Johann Ludwig Krapf aliandika mnamo 1860 kuwa Waswahili kwenye pwani waliita mlima huo "Kilimanjaro". Alisema pia ya kwamba hao Waswahili walieleza maana yake kuwa ama “mlima mkubwa” au “mlima wa misafara” ingawa mwenyewe hakukubali maelezo hayo. Kwa elezo la mwisho "Kilima" kilimaanisha "mlima" na "Jaro" labda "misafara". Jim Thompson aliandika mnamo 1885 kuwa jina Kilima-Njaro lilichukuliwa mara nyingi kuwa na maana ya "mlima mkubwa" lakini mwenyewe alipendelea maelezo tofauti yaliyosema "mlima mweupe". "Njaro" ni Kiswahili cha Zamani kwa "ng’ara". Vivyo hivyo Krapf aliandika ya kwamba aliwahi kuwatembela Wakamba mnamo 1849 walioita mlima “Kima jaJeu” yaani mlima mweupe Leo hii Wakamba wangesema “Kiima Kyeu” na elezo hili limekubaliwa na watafiti mbalimbali. Wengine huona ya kwamba ni Wazungu wasiojua Kiswahili vema waliochanganya “mlima” na “Kilima”. Wengine wamejaribu kuona msingi wa jina katika lugha ya Kichagga. Hapo wanadai uwezekano kuwa "Kileman" limetokana na neno la Kichagga "kileme" linalomaanisha “kinachoshinda” au neno "kilelema" linalomaanisha "kilichokuwa vigumu, kilichoshindikana". Katika hoja hiyo "Jaro" imetokana na Kichagga “njaare” (aina ya ndege, au kufuatana na wengine chui) au kutoka neno “jyaro” (msafara). Elezo lingine ni kwamba Wachagga walisema mlima huo hauwezi kupandwa "kilemanjaare" au "kilemajyaro" na wapagazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa Wazungu. Tangu miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukaitwa "Kilima-Ndscharo" kwa Kijerumani. Tarehe 6 Oktoba 1889 Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo. Alichagua jina la "Kaiser-Wilhelm-Spitze" ("Ncha ya Kaisari Wilhelm"). Jina hilo lilitumika hadi Tanzania ilipoundwa mwaka 1964, na kilele kubadilishiwa jina kuwa "Uhuru", likiwa na maana ya "Kilele cha Uhuru" Jiolojia ya mlima na tabia za kijiografia Kilimanjaro inapanda hadi mita 4877 juu ya tambarare karibu na mji wa Moshi uliopo miguuni pake. Hii inafanya kilele chake kuwa mita 5895 juu ya uwiano wa bahari. Kilimanjaro ni volkeno ya rusu iliyojengwa na rusu za majivu, zaha na mata nyingine. Ni volkeno ndefu kuliko zote duniani nje ya Amerika Kusini. Vilele vitatu vya kivolkeno juu ya Kilimanjaro ni Kibo iliyo juu zaidi Mawenzi yenye kimo cha mita 5149 Shira yenye urefu wa mita 4005. Vyote vitatu vina kasoko. Mawenzi na Shira ni volkeno zimwe lakini Kibo ni volkeno iliyolala, ila inaweza kuwaka tena. Uhuru ni sehemu ya juu kwenye ukingo wa kasoko ya Kibo. Taasisi ya Tanzania National Parks Authority na UNESCO zinataja kimo cha Uhuru Peak kuwa mita 5895. Kimo hicho kimetokana na upimaji uliofanyika wakati wa ukoloni wa Uingereza mwaka 1952. Tangu upimaji ule kimo cha mlima kimepimwa tena: kinaonyesha kuwa mlima unapungua polepole. Kipimo kilikuwa mita 5892 mwaka 1999 na mita 5891 mwaka 2014. Muundo wa ndani wa Kilimanjaro haujulikani sana kwa sababu hadi sasa haujatokea mmomonyoko mkubwa unaoweza kufunua ndani yake. Shira Kilele cha kale zaidi ni Shira iliyoanza kutema moto takriban miaka milioni 2.5 iliyopita ikaacha miaka milioni 1.9 iliyopita. Wakati ule upande wa kaskazini wa mzingo wa kasoko ulipinduka. Leo hii Shira ina tambarare pana kwenye kilele chake kwenye kimo cha mita 3800; inawezekana hii kiasili ilikuwa kaldera iliyojaa lava. Mabaki ya mzingo wa kaldera yamepungua sana kutokana na mmomonyoko. Kabla ya kutoa moto na kutokea kwa mmomonyoko kimo cha Shira kilikuwa kati ya mita 4,900 na 5,200. Mata yake ni hasa lava pamoja na kiasi cha piroklasti. Mawenzi Mawenzi na Kibo zilianza kulipuka (kutoa moto) takriban miaka milioni iliyopita. Zimetengwa na tambarare ( "Saddle Plateau") kwenye kimo cha mita 4400. Miamba ya kijana kwenye Mawenzi ilitokea miaka 448,000 iliyopita. Mawenzi huwa na mgongo wenye umbo la kiatu cha farasi mwenye ncha kali na kufunguka upande wa kaskazini-magharibi. Mgongo unakatwa na mabonde kadhaa na upande wa mashariki wa mlima umepungua kutokana na mmomonyoko. Mawenzi huwa na kilele cha pili kinachojulikana kwa jina la “Neumann Tower” chenye mita 4425. Kibo Kibo ni pia ya kivolkeno yenye kimo kirefu ikiwa na upana wa kilomita 15 kwenye "Saddle Plateau". Ililipuka mara ya mwisho miaka 150,000 na 200,000 iliyopita na mlipuko huo ulifanya kasoko kwenye kilele cha Kibo cha sasa. Hadi leo gesi inatoka kwenye mashimo ardhini. Kibo huwa na pia kwenye kilele chake chenye umbo kamili. Kuna kaldera yenye upana wa kilomita 2.5 na ndani yake pia iko kasoko ya Reusch. Jina hilo lilitolewa na serikali ya Tanganyika mwaka 1954 kwa heshima ya Mjerumani Gustav Otto Richard Reusch alipopanda mlima mara ya 25. Ndani ya kasoko ya Reusch kuna shimo refu linalojulikana kwa jina la “ash pit” (shimo la majivu). Wakati wa mlipuko wa mwisho uliotokea miaka 100,000 iliyopita sehemu za mzingo wa kasoko ziliporomoka na kuacha pengo kubwa. Kibo huwa na pia za kando zaidi ya 250 ambazo ni mashimo ambako gesi, zaha na piroklasti zilitoka kwenye pande za mlima wakati wa kuwa volkeno hai. Zilitokea miaka 150,000 hadi 200,000 iliyopita . Zinapatikana hadi Ziwa Chala na Taveta upande wa kusini-mashariki na hadi Lengurumani upande wa kaskazini-magharibi. Zaha iliyotoka katika pia hizo za kando ilifunika sehemu kubwa ya pande za mlima. Wamaasai wana kumbukumbu ya kuwa Ziwa Chala upande wa mashariki wa Kibo lilikuwa mahali pa kijiji kimoja kilichoharibika na mlipuko wa volkeno. Maji yatoka mlimani kwa njia ya mito na vijito hasa upande wa kusini unaopokea mvua zaidi hasa juu ya mita 1200. Chini ya kimo hicho maji kwenye mito inapungua kutokana na mvukizo na matumizi ya binadamu. Mito ya Lumi na Pangani inabeba maji ya Kilimanjaro kuelekea mashariki na kusini. Tabianchi Tabianchi ya Kilimanjaro inaathiriwa na kimo cha mlima kinachoruhusu kufika kwa upepo kutoka bahari wenye unyevu mwingi na wakati mmoja pia upepo za juu sana. Tabia nyingine ni hali yake ya kuwa mlima wa juu sana peke yake bila jirani ya karibu sana. Mlima huwa na mfumo wa upepo ambako mchana upepo unaelekea juu na wakati wa usiku kuna upepo unaotelemka kutoka juu. Hii inatokea zaidi upande wa kusini kuliko upande wa kaskazini kwa sababu tako la mlima ni pana zaidi upande wa kusini na mitelemko yake inaelekea zaidi hivyo kuathiri tabianchi zaidi. . Kilimanjaro huwa na majira mawili ya mvua, moja ya Machi hadi Mei na nyingine mnamo mwezi wa Novemba. Mitelemko ya kaskazini hupokea mvua chache kulingana na mitelemko ya kusini. Sehemu za chini za mtelemko wa kusini hupokea milimita za mvua 800 – 900 kwa mwaka. Kiwango hiki kinaongezeka kwa milimita 1,500 hadi 2,000 kwenye kimo cha mita 1,500 na hadi juu ya milimita 3,000 kwenye ukanda wa msitu kwa mita 2,000 hadi 2,300. Juu zaidi usimbishaji unapungua tena hadi milimita 200. Halijoto kwenye kilele ina wastani ya sentigredi -7 yaani jalidi. Halijoto juu ya ngao ya barafu upande wa kaskazini wakati wa usiku huwa na wastani wa sentigredi -9 na wakati wa mchana -4. Viwango vya chini vya -15 hadi -27 vimepimiwa pia. Usimbishaji wa theluji unaweza kutokea wakati wowote lakini kwa kawaida hutokea Zaidi wakati wa majira ya mvua. (Novemba–Desemba na Machi–Mei). Usimbishaji wote kwenye kilele ni hasa theluji au mchnganyiko wa tehluji na mvua kwenye kiwango cha milimita 250 hadi 500 kwa mwaka na kuvukiza haraka. Barafu na barafuto Mlima Kilimanjaro hujulikana kuwa kuwa ni mlima wa Afrika mwenye kofia ya barafu ya kudumu. Pamoja na Kilimanjaro kuna sehemu mbili nyingine tu barani Afrika, ni Ruwenzori na Mlima Kenya. Lakini kiasi cha barafu imepungua kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100. Mwingereza P.C. Spink aliona mwaka 1944 ya kwamba barafu ilipungua sana kulingana na taarifa aliyojua kutoka mpandaji wa kwanza Hans Meyer. Baina 1912 eneo la ngao ya barafu limepungua kutoka kilomita za mraba 12 hadi 1.85 km² kwenye mwaka 2009. Hii inalingana na kupunguzwa asilimia 85%. Sababu kuu ya mabadiliko haya ni kupungukiwa kwa kiwango cha usimbishaji katika mazingira ya mlima tangu mwisho wa karne ya 19. Maana Kilimanjaro ni mlima wa juu vile ya kwamba mvua wote (pamoja na ukungu na usimbishaji mwingine) unaofika kwenye kilele chake utaganda na kuwa theluji. Theluji inayokaa muda mrefu tena katika ganda nene itakuwa barafu. Lakini wakati uleule mishale ya jua zinasababisha kupotea kwa theluji na barafu kwa njia ya uvukizaji. Kwa jumla kuongezeka au kupungukiwa kwa barafu kwenye kimo hiki ni swali la kiasi cha mvua na usimbishaji mwingine zinazofika hapa. Leo hii kuna barafuto kwenye Kibo pekee pamoja na mabaki ya ngao ya barafu kwenye tambarare ya kilele na kwenye mitelemko ya Kibo. http://www.jstor.org/stable/1788958?seq=1#page_scan_tab_contents Hii ngao ya barafu bado iko kwa sababu Kilimanjaro ni mlima usio na vilele vikali unaofika juu ya kimo cha mstari wa jeledi. Kasoko ya Kibo imepita na kukata ngao hiyo. Siku hizi hakuna miendo ya maana inayoonekana kwenye barafuto za kilele kwa sababu unene wao imepungua mno.. Utafiti wa kijiolojia umeonyesha ya kwamba kulikuwa na vipindi vitano vya upanuzi wa barafuto katika miaka 500,000 iliyopita vilivyofuatwa na vipindi vya kupungua. Ngao ya barafu mfululizo ilifunika mlima wote hadi kimo cha mita 3,200 miaka 24,000 – 25,000 iliyopita wakati barafuto kote duniani zilienea sana. Kuna dalili ya kwamba barafu yote mlimani iliwahi kupotea kabisa takriban miaka 11,500 iliyopita kutokana na ukame dunaini wakati ule. Kuongezeka kwa usimbishaji wakati wa Holoseni (miaka 11,500 iliyopita) kumeruhusu kurudi kwa barafu mlimani. barafuto ziliweza kudumisha kipindi cha ukame miaka 4,000 iliyopita. Wakati wa kutembelewa mara ya kwanza katika miaka ya 1880, kilele cha Kibo kilifunikwa kabisa kwa ngao ya barafu yenye eneo la kilomita za mraba 20 hivi na mikondo ya barafuto iliendelea wenye mitelemko ya kando. Isipokuwa pia ya kati, kaldera yote ilifunikwa na barafu. Imetazamiwa ya kwamba barafuto kwenye mitelemko ilirudi nyuma haraka kuanzia 1912 hadi 1953, na polepole zaidi tangu wakati ule. Inaendelea kupungua nah ii inaonyesha ya kwamba bado hakuna uwiano kati ya kiasi cha mvua kinachofika kwenye kilele na uvukizaji nah ii inaonyesha mabadiliko ya tabianachi yanayoendelea. Pamoja na kufunika eneo dogo zaidi, yaani kujikaza, barafuto pia zimepungua unene kutokana na kuyeyuka na uvukizaji. Mabadiliko haya kwenye barafuto za Kilimanjaro zinalingana na mabadiliko yanayoonekana kwenye barafuto kote duniani. At the current rate, most of the ice on Kilimanjaro will disappear by 2040 and "it is highly unlikely that any ice body will remain after 2060". Kama barafu juu ya Kilimanjaro ingepotea kabisa hii isingekuwa tatizo kubwa kwa maji yanayopatikana katika maeneo yanayozunguka mlima. Kiasi cha barafu juu ya mlima ni kidogo sana kuliko kiasi cha maji yanayohifadhiwa na misitu kwenye mitelemko ya mlima chini zaidi. Misitu hii ni chanzo cha maji yanayotiririke chini katika mito na vijito vya mlima mkubwa. Uoto Kuna misitu asilia zinazofunika takriban kilomita ya mraba 1,000 kwenze mlima . Sehemu ya chini hulimwa kwa kupanda mahindi, maharagwe na alizeti, pia ngano upande wa magharibi. Kuna mabaki ya uoto wa savana ya awali yenye miti kama Acacia, Combretum, Terminalia na Grewia. Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu zaidi. Kuanzia kimo cha mita 1000 hadi mita 1800 kuna kilimo cha kahawa kwa namna ya kidesturi ya "Wachaga inayopanda miti na mazao kwa pamoja. Uoto asilia umebaki pekee katika mabonde majkali yasiyoweza kutumiwa kwa kilimo na hapa ni tofauti na uoto kwenye maeneo ya juu Zaidi. Kwenye mitelemko ya kusini penye mvua nyingi kuna misitu ya mvua yenye miti aina ya Ocotea usambarensis pamoja na kangaga na epipythi. Juu zaidi penye ukungu wa kudumu kuna Podocarpus latifolius, Hagenia abyssinica na Erica excelsa pamoja na kuvumwani. Upande wa kaskazini ulio kavu zaidi pana misitu ya mizeituni, Croton-Mlungu-mbago (Calodendrum), Cassipourea (Mugome na Msikundazi) na Juniperus (Mtarakwa) kadri kimo kinaongezeka. Juu zaidi kati ya mita 3,100 na 3,900 hufuata kanda la vichaka vya Erica (mdamba) na juu yake kunamajanimajani tu kama Helichrysum hadi mita 4500. Utafiti kwenye kasoko ya Maundi kwenye kimo cha mita 2780 umeonyesha ya kwamba uoto wa Kilimanjaro ulibadilika katika mwendo wa karne na milenia. Wakati wa baridi kwenye enzi ya barafu miaka 42,000 – 30,000 iliyopita misitu ilishuka chini na kanda la mdamba lilitokea takriban mita 1,500 chini ya hali yake ya sasa.. Wanyama Hakuna wanyama wakubwa wengi waliobaki mlimani. Wanapatikana hasa kwenye misitu na sehemu za chini mlimani. Tembo na nyati wanaweza kuwa na hatari kwa watalii wanaopanda mlima na pia kwa wakulima. Pongo, vinyonga, digidigi, paa, Nguchiro, nyani mbalimbali kama mbega, komba, chui, chozi na ngiri wametazamiwa pia. Punda milia na fisi wanapatikana mara chache kweye tambarare juu ya Shira. Kuna spishi chache zinazopatikana Kilimanjaro pekee hizi ni pamoja na “kirukanjia wa Kilimanjaro” na spishi ya kinyonga kinachoitwa Kinyongia tavetana. Tazama pia Orodha ya volkeno nchini Tanzania Orodha ya milima ya Tanzania Orodha ya milima ya Afrika Orodha ya milima Marejeo Viungo vya nje Mount Kilimanjaro National Park Mount Kilimanjaro National Park NASA Earth Explorer page Weather forecase for Mount Kilimanjaro (19,565 feet) Glacial Recession on Kilimanjaro (pictures of southern icefields) Mount Kilimanjaro live webcam Kilimanjaro flora picture gallery Aerial photographs of Mount Kilimanjaro, 1937-38 How hard is it to climb Mount Kilimanjaro? Field Guide to the Moist Forest Trees of Tanzania Jon C. Lovett, Chris K. Ruffo & Roy E. Gereau, Miti ya milima ya Tanzania Milima ya Tanzania Milima ya Afrika Volkeno za Afrika Mkoa wa Kilimanjaro Volkeno za Tanzania Afrocine 2019-Tanzania
1752
https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius%20Nyerere
Julius Nyerere
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, Mkoa wa Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa Taifa" kwa jinsi alivyoathiri nchi hiyo. Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu." Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais. Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika nchi. Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma lilianza kushughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu". Baada ya hapo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limepokea jukumu la kuratibu mchakato huo pamoja na kesi kuhamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na Nyerere kuishi muda mrefu jijini humo. Maisha yake Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945. Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika). Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika. Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah. Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza. Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi. Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi. Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi. Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu. Mafanikio Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani". Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo). Ukosoaji dhidi yake Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria. Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere katika tafrija ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.” Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake. Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo. Sifa zake Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24. Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama. Heshima na Tuzo Nishani Tuzo 1973: Jawaharlal Nehru Award for International Understanding 1982: the Third World Prize 1983: Nansen Refugee Award 1986: Sir Seretse Khama SADC Medal 1987: Lenin Peace Prize 1988: Joliot-Curie Medal of Peace 1992: International Simón Bolívar Prize 1995: Gandhi Peace Prize 2000: Statesman of the 20th century by the Chama cha Mapinduzi 2009: World Hero of Social Justice by the 63rd President of UNGA, Miguel d'Escoto Brockmann 2011: Tanzania Professional Network Award Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere Freedom and Unity (Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford University Press, 1967)Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968) Ndamo zimo: "The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance"; "The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and "Socialism and development."Freedom & Development (Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford University Press, 1974) Ndani zimo mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi ya uhuru. Ujamaa - Essays on Socialism''' (1977)Crusade for Liberation (1979)Julius Kaisari, Tafsiri ya mchezo wa William Shakespeare unaoitwa Julius CaesarMabepari wa Venisi, Tafsiri ya mchezo mwingine wa William Shakespeare, The Merchant of VeniceUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Mathayo, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya MathayoUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Marko, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya MarkoUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Luka, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya LukaUtenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Yohana, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya YohaneUtenzi wa Matendo ya Mitume, Tafsiri ya kishairi ya Matendo ya Mitume Marejeo Viungo vya nje Taasisi ya Mwalimu Nyerere Contemporary Africa Database - People/ Nyerere http://www.nathanielturner.com/juliuskambaragenyerere.htm Mohamed Said: Mwalimu in 1950s Dar (East African October 12 2008) Nyerere's remarks on Ali Hassan Mwinyi Corrupt practices PBS Interview with Nyerere on the Great Lakes crisis, December 26, 1996 Infed.org article on Nyerere and his views on education in Tanzania Jerry Atkin's Nyerere tribute, from InMotion Magazine SouthCentre Nyerere Memorial Site Mwalimu Neyerere Speeches A translation of Merchant of Venice into KiSwahili Nyerere Obituary from the ANC NPR Weekend Edition reflection on Nyerere Julius Nyerere Fellowship Nyererefoundation Called to greatness MercatorNet, 10 November 2006 Beatification inquiry for Tanzania's Nyerere (from Catholic World News) Is Nyerere's process to sainthood timely? (from IPP Media) The Julius Nyerere Intellectual Festival Week by Gacheke Gachihi, All Africa'', 11 June 2009 The Julius Nyerere Master's Scholarships (University of Edinburgh) Waliozaliwa 1922 Waliofariki 1999 Wanasiasa wa Tanzania Afrocine 2019-Tanzania N N N
1753
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mbege
Mbege
Mbege ni kileo asili cha Wachagga, wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro. Mbege hutengenezwa kwa ndizi mbivu, kimea cha ulezi, na maji. Mara nyingi mbege hutengenezwa na wanawake na hutumika katika sherehe na matukio mbalimbali kama vile harusi, misiba, kipaimara, kuzaliwa kwa mtoto, n.k. Mbege hutumiwa pia kama faini kwenye mahakama za jadi. Utengenezaji wa mbege hufanywa pia kwa biashara. Hapo huuzwa katika vilabu vya pombe na pia nyumbani. Utengenezaji na unywaji Kinywaji hicho hutengenezwa kwa kuchemsha ndizi mbivu kama vile ndizi songea, ndizi uganda, kibungara, kisukari (kama zinapatikana sana) n.k. Ndizi hizo zikishachemshwa huachwa kwa kipindi cha kama tatu au zaidi ili zichache. Baada ya hapo unga wa ulezi hupikwa na kuachwa upoe. Ndizi zilizochemshwa na kuchacha huchanganywa na maji, kisha kukamuliwa ili kupata juisi yake. Juisi hiyo huchanganywa na unga wa ulezi uliopikwa na tunapata (kivuo, kifue, togwa) na kuachwa usiku mzima. Kesho yake mbege huwa tayari kunywewa. Kinywaji hicho kama haitanyewa na kumalizika siku hiyo basi ikilala tunapata kitu kinachooitwa ngera, ambayo ni chachu sana, ila ngera pia huweza kuzimuliwa na kuwa kinywaji kifaacho tena kwa kuchanganya na unga uliopikwa na unga kidogo usiopikwa, ila ngera ikilala tena humwagwa kwani haitafaa kunywea tena. Watengenezaji wengi wa mbege huwa wanaweka gamba la mti wa msesewe (Rauvolfia Caffra), hasa maeneo ya Kibosho, Machame na Rombo ili kuongeza ladha ya uchachu na kupunguza kasi ya mbege kuchacha. Chombo maalum kiitwacho kata hutumiwa kunywea mbege, ila mara nyingi sehemu za mijini hutumia vyombo vya plastiki, vikiwa na ujazo tofauti, navyo huitwa chubuku na kitochi. Katika maeneo ya vijijini mbege hunywewa kijamaa kwa kupokezana kata. Mtu mmoja anakunywa kisha anampatia mwingine anayekunywa na kumpa mwingine. Vinywaji Utamaduni wa Wachagga
1756
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kilimanjaro
Kilimanjaro
Kilimanjaro ni jina la Kiswahili linalomaanisha : Mlima wa Kilimanjaro katika Tanzania ambao ni mlima kubwa kabisa katika bara la Afrika Hifadhi ya Kilimanjaro inayozunguka kilele cha mlima Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa wa Tanzania katika sehemu ya Mlima wa Kilimanjaro Kilimanjaro (Moshi Mjini), kata ya Moshi Mjini Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro kati ya Arusha na Moshi Jina la bidhaa mbalimbali zilizopewa jina la mlima kama vile bia ya aina ya Kilimanjaro Lager au maji ya kunywea katika Tanzania, karatasi za Kilimanjaro (Marekani), au keki ya Kilimandscharo (Ujerumani) Makala zinazotofautisha maana
1757
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nchi%20za%20Maziwa%20Makuu
Nchi za Maziwa Makuu
Nchi za Maziwa Makuu ni nchi zinazopakana na maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya na Uganda. Kati ya maziwa makubwa yaliyoko katika eneo hili kuna Ziwa Nyanza (Viktoria) Ziwa Tanganyika Ziwa Nyasa (Malawi) Ziwa Mwitanzige (Albert]] Ziwa Rutanzige (Edward) Ziwa Kivu Ziwa Turkana Eneo hili ni muhimu kimataifa kutokana na bioanwai kubwa: asilimia 10 ya spishi za samaki wote duniani zinapatikana katika maziwa yake. Maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa hushika robo moja ya maji matamu (yasiyo maji ya chumvi) yaliyopo duniani kote. Marejeo Jean-Pierre Chrétien. The Great Lakes of Africa: Two Thousand Years of History trans Scott Straus Viungo vya nje Afrika Tanzania Rwanda Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kenya Uganda
1758
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fasihi
Fasihi
Fasihi (kutoka neno la Kiarabu فصاحة, fasaha kwa maana ya ulimbi au "literacy" kwa Kiingereza) ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa hadhira husika. Ni ufundi wa kuwasilisha mawazo au ujumbe ulio katika fikra za binadamu.Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha masuala kuhusu maisha ya binadamu na mazingira Vipengele vinavyounda fani ya fasihi ni kama ifuatavyo: fani ni umbo la nje la kazi ya fasihi; maudhui ni umbo lake la ndani. Fani Katika kazi yoyote ya fasihi ni lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji au wasomaji) husika. Ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira huitwa fani, ambayo hujumuisha mambo kama vile: Muundo - ni mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio / visa Mtindo - ni mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine Wahusika - ni watu au vitu vyenye uhai au la ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake Mandhari - ni eneo ambalo fanani hulitumia kujenga matukio na au mtiriko katika kuumba kazi yake au maeneo anayoyatumia fanani kuakisi jamii anayoilenga Matumizi ya lugha - ni lugha anayotumia fanani katika kujenga wasifu wa wahusika kihaiba kazi yake Maudhui Pamoja na fani, kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika huitwa maudhui. Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha: Dhamira Ujumbe/Mafunzo Mgogoro Falsafa/msimamo na Mtazamo Sifa za fasihi Fasihi ni utanzu wa sanaa. Kuna aina tatu za sanaa: sanaa za ghibu, sanaa za maonyesho na sanaa za vitendo. Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika. Fasihi ni maelezo ya fani na maudhui. Fasihi ni ufundi unaotumia lugha ili kulete mguso au hisia fulani za watu katika muktadha fulani. Dhima za fasihi katika jamii Fasihi hufanya kazi mbalimbali katika maisha: Kuelimisha jamii - Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mbalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa kuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi, ubaya wa ufisadi na kadhalika. Kukuza utamaduni - Kupitia fasihi simulizi, tamaduni na mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau na vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika. Kustawisha lugha- Fasihi hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au wasomaji. Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha. Kuburudisha jamii - Pamoja na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika. Kukomboa jamii. Kuonya jamii - Fasihi ina jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii. Kukuza uwezo wa kufikiri-Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika. Kuhifadhi historia ya jamii. Aina za fasihi Fasihi ndiyo aina pekee ya sanaa inayotumia lugha kujitambulisha au kujitofautisha na aina nyingine za sanaa. Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni: Fasihi simulizi - huwasilishwa kwa lugha ya mazungumzo/masumilizi Fasihi andishi - huwasilishwa kwa lugha ya maandishi Fasihi hizi zina dhima sawa katika jamii ingawa ni tofauti. Utofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi hujitokeza katika uwasilishwa wake katika jamii husika. Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya mazungumzo au masimulizi ya mdomo Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya maandishi Fasihi simulizi Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mazungumzo ya mdomo ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Aina hii ya fasihi ndiyo iliyokuwapo tangu zamani kabisa mwanadamu alipoanza kuishi yaani ilianza pale mwanadamu alipochangamana na wenzake katika kufanya mambo mbalimbali mfano,shughuli za biashara,kilimo,na nyinginezo. kuna tanzu nne za fasihi simulizi .ie; 1.utanzu wa hadithi 2.utanzu wa semi 3.utanzu wa ushairi simulizi 4.utanzu wa maigizo 5.utanzu wa mazungumzo Sifa za fasihi simulizi Hutolewa kwa njia ya mdomo. Haitumii gharama Huonyesha uhalisia wa hisia za mzungumzaji Ni mali ya jamii. Hakuna mtu anayeimiliki. Dhima za fasihi simulizi kuburudisha kuelimisha jamii kunasihi kukuza lugha kuunganisha watu Kufanana kwa fasihi simulizi na fasihi andishi Kimsingi fasihi ni moja ingawa imegawanyika katika sehemu kuu mbili, yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Mbali na mgawanyiko huo kuna mambo ambayo yanafanana katika fasihi zote mbili. Mambo hayo ni pamoja na: Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe kwa hadhira husika Zote zina dhima inayofanana katika jamii, yaani, kuelimisha na kuburudisha jamii Zote zina wahusika ambao ni Fanani na Hadhira Zote zina vipengele vya Fani na Maudhui zote zinaweza kukashifiwa na wasanii mbalimbali ikiwa hawajaridhishwa na mbinu za lugha zilizotumika Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi Viungo vya nje blogu ya Eric Ndumbaro kuhusu Fasiki simulizi ya Kiafrika Fasihi Sanaa
1759
https://sw.wikipedia.org/wiki/Intaneti
Intaneti
Intaneti (kutoka Kiingereza Internet) ni mfumo wa kushirikiana kwa tarakilishi nyingi unaowezesha watu mbalimbali duniani kuwasiliana baina yao. Kupitia mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe. Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya tarakilishi inayotumia itifaki inayokubalika ya intarnet Suite (TCP/IP). Intaneti hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za wavuti wa ulimwengu mzima (www) na miundombinu ya kusaidia barua pepe. Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za rununu na runinga, zimeundwa upya kutumia teknolojia za tovuti, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia tovuti (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika tovuti, ubadilishanaji maoni, na kupatikana habari zinapotokea tu. Intaneti imewezesha au kuharakisha uundaji wa aina mpya za mafungamano za kibinadamu kupitia ujumbe mbashara, majukwaa ya tovuti na mitandao ya kijamii. Kuna mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta wavuti (kama google) au kwa kamusi elezo kama wikipedia. Asili ya intaneti ina mizizi katika miaka ya 1960 wakati Marekani ilifadhili miradi ya utafiti wa makala zake za kijeshi na kujenga mitandao iliyosambaa ya tarakilishi ambazo zina uwezo wa kustahimili mabadiliko na ni vumilivu kwa makosa. Kipindi hiki cha utafiti na ufadhili wa raia wa Marekani wa uti mpya wa mgongo uliofanywa kwa msingi wa kitaifa wa sayansi, ulisababisha dunia yote kushiriki katika maendeleo ya teknolojia mpya. Pia ulisababisha ufanyajibiashara wa tovuti za kimataifa katikati ya miaka ya 1990, na kusababisha kujulikana kwa zana nyingi karibu kila uwanja wa maisha ya kisasa ya binadamu. Kufikia mwaka wa 2009, wastani wa robo ya idadi ya watu duniani hutumia huduma ya tovuti. Istilahi Maneno intaneti na mtandao wa ulimwengu mzima mara nyingi hutumika bila tofauti kubwa. Hata hivyo, intaneti na mtandao wa ulimwengu mzima si kitu kimoja, wala hazina maana sawa. Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mawasiliano ya data. Ni miundombinu ya vifaa na programu ambayo huwezesha mawasiliano kati ya kompyuta. Kwa kulinganisha, mtandao ni mojawapo ya huduma inayowasilishwa na intaneti. Ni mkusanyiko wa nyaraka zilizounganishwa na rasilimali nyingine, zilizoshikanishwa na viungo na URL. Historia Uzinduzi wa Sputnik na USSR ulichochea Marekani kuanzisha shirika la utafiti wa juu wa miradi, iliyojulikana kama ARPA, katika mwezi Februari 1958 ili kuongoza kiteknolojia. ARPA ilitengeneza ofisi ya teknolojia za kuchambua habari (IPTO) ili kuendeleza utafiti wa programu inayojitekeleza ya mazingira ya chini (Sage), ambayo iliunganisha mifumo ya rada za nchi nzima kwa mara ya kwanza. J. C. R Licklider alichaguliwa kuwa kiongozi wa IPTO. Licklider alihama kutoka maabara ya masomo yanayochunguza jinsi ubongo wa binadamu unavyofasiri sauti katika Chuo Kikuu cha Harvard MIT mwaka 1950, baada ya kuvutiwa na teknolojia ya habari. Akiwa MIT, alikuwa kwenye kamati iliyoanzisha Maabara ya Lincoln na kufanya kazi ya mradi wa Sage. Mwaka wa 1957 akawa Makamu wa Rais katika BBN, ambapo alinunua kompyuta ya kwanza ya PDP-1 na kuongoza maonyesho ya kwanza ya ugawanaji muda. Akiwa IPTO, Licklider alimleta Lawrence Roberts ili aanzishe mradi wa kutengeneza mtandao, na Roberts alikita msingi wa teknolojia katika kazi ya Paulo Baran, ambaye alikuwa ameandika masomo kamili kwa Wanajeshi wa waangani wa Marekani akipendekeza ubadilishaji pakiti (badala ya ubadilishaji mzunguko) ili kupata mtandao bora unaobadilika na unaoweza KUstahimili janga. Profesa wa UCLA Leonard Kleinrock alikuwa ametoa msingi wa nadharia ya pakiti za mitandao mwaka 1962, na baadaye, katika mwaka 1970, wa upitishaji wa kiviwango, dhana ambazo zimekuwa msingi wa maendeleo ya intaneti ya leo. Baada ya kazi nyingi, sehemu mbili za kwanza ambazo zingekuwa ARPANET ziliunganishwa kati ya Shule ya Uhandisi na Sayansi Tumikizi ya UCLA na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti ya Stanford (SRI) katika bustani ya Menlo, California, tarehe 29 Oktoba 1969. ARPANET ilikuwa moja ya mitandao tangulizi ya mtandao wa intaneti ya leo. Kufuatia maonyesho kuwa ubadilishaji pakiti ulifanya kazi kwa ARPANET, kituo cha posta cha Uingereza, Telenet, TRANSPAC na DATAPAC zilishirikiana kuunda mtandao wa kwanza wa huduma ya ubadilishaji pakiti. Nchini Uingereza, hii ilikuwa inajulikana kama huduma ya kimataifa ya ubadilishaji pakiti (IPSS), mwaka 1978. Mkusanyiko wa mitandao yenye msingi wa X.25 ilikua kutoka Ulaya na Marekani na kutanda Kanada, Hong Kong na Australia kufikia mwaka 1981. Sheria ya ubadilishaji pakiti ya X.25 ilitengenezwa katika CCITT (sasa inaitwa ITU-T) mwaka 1976. X.25 ilikuwa huru kutoka itifaki ya TCP/IP ambayo iliinuka kutokana na kuwa kazi ya majaribio ya DARPA kwenye ARPANET, mtandao wa Pakiti za Redio na Mtandao wa Pakiti ya Setilaiti wakati mmoja. Vinton Cerf na Robert Kahn walitengeneza maelezo ya kwanza ya itifaki ya TCP mwaka 1973 na kuchapisha karatasi kuhusu mada hii katika mwezi Mei 1974. Matumizi ya neno "Internet" kuelezea mtandao mmoja wa kiulimwengu wa TCP/IP yalianza katika mwezi Desemba 1974 na uchapishaji wa RFC 675, yakiwa maelezo kamili ya kwanza ya TCP iliyoandikwa na Vinton Cerf, Yogen Dalal na Carl Sunshine, waliokuwa katika Chuo Kikuu cha Stanford. Katika miaka tisa iliyofuata, kazi iliendelea kurekebisha itifaki hizo na kuzitekeleza katika mifumo ya oparesheni ya aina mbalimbali. Mtandao wa Kwanza wenye upana mkubwa wa msingi wa TCP / IP ulikuwa ukifanya kazi kufikia tarehe 1 Januari 1983 wakati ambapo viwekaji vyote vya ARPANET vilibadilishwa kutoka itifaki za hapo awali za NCP. Mwaka 1985, Wakfu wa Sayansi wa kitaifa Marekani (NSF) uliamuru ujenzi wa NSFNET, uti wa mgongo wa mtandao wa chuo kikuu wenye kasi ya kilobaiti 56 kwa sekunde kwa kutumia kompyuta zilizoitwa "fuzzballs" na mvumbuzi wake, David L. Mills. Mwaka uliofuata, NSF ilifadhili ubadilishaji hadi mtandao wenye kasi ya juu zaidi ya megabaiti 1.5 kwa sekunde. Maamuzi muhimu kutumia itifaki za DARPA TCP/IP ulifanywa na Dennis Jennings, aliyekuwa msimamizi wa programu ya kompyuta zenye nguvu huko NSF. Ufunguzi wa mtandao huo kwa maslahi ya kibiashara ulianza mwaka wa 1988. Baraza ya Mitandao ya Kimajimbo Marekani ilikubali ushikanishaji wa NSFNET na mfumo wa barua wa MCI katika mwaka huo, kiungo kilifanywa katika msimu wa joto wa mwaka wa 1989. Huduma zingine za kielektroniki za kibiashara zilishikanishwa zikiwemo: OnTyme, Telemail na Compuserve. Katika mwaka huo, watoaji wa huduma ya Intanet watatu waliundwa: UUNET, PSINet na CERFNET. Muhimu, mitandao tofauti iliyotoa viingilio, na baadaye kuungana na Intanet ilikuwa BITNET na Usenet. Mitandao mingine ya kibiashara na elimu kama Telenet, Tymnet, Compuserve na JANET iliunganishwa na Intanet iliyokuwa ikikua. Telenet (iliyoitwa Sprintnet baadaye ) ulikuwa mtandao mkubwa wa kompyuta wa kitaifa uliofadhiliwa kibinafsi, wenye upigaji simu ya intaneti burekatika miji, kote Marekani na uliyokuwa ukifanya kazi tangu mwongo wa 1970. Hatimaye, mtandao huu uliunganishwa na mingine katika mwongo wa 1980 wakati ambapo itifaki ya TCP / IP iliendelea kuwa maarufu zaidi. Uwezo wa TCP/IP kufanya kazi kwa karibu mtandao wowote wa mawasiliano uliruhusu ukuaji rahisi, ingawa ukuaji wa haraka wa Intanet ulikuwa juu ya upatikanaji rahisi wa safu ya vielekezi vya kibiashara kutoka makampuni mengi, upatikanaji wa vifaa vya kibiashara vya Ethanet ya mitandao ya mitaa, na kuenea kwa utekelezaji na uwekaji sheria mkali wa TCP / IP katika UNIX na karibu kila mfumo mwingine wa oparesheni. Ingawa vifaa msingi na miongozo vinavyofanya uwezekanaji wa intanet vimekuwepo kwa karibu miongo miwili, mtandao huo haukupata kuona nyuso za umma mpaka mwongo wa 1990. Tarehe 6 Agosti 1991, CERN, shirika ya Ulaya ya utafiti wa chembe, ulieleza umma kuhusu mradi mpya wa matandao wa dunia nzima. Mtandao ulizuliwa na mwanasayansi waKiingereza Tim Berners-Lee mwaka wa 1989. Kivinjari cha mtandao kilichokuwa cha kwanza na chenye umaarufu sana kilikuwa ViolaWWW, iliyofuata mtindo wa HyperCard na kujengwa kwa kutumia mfumo wa X Window. Hatimaye ilichujwa na umaarufu wa tovuti ya Mosaic. Mwaka wa 1993, Kikao kikuu cha zana za kompyuta zenye nguvu katika Chuo Kikuu cha Illinois ilitoa aina ya kwanza 1.0 ya Mosaic, na mwisho wa mwaka wa 1994 hamu ya umma iliongezeka Intanet ambayo hapo awali ilikua ya taaluma na ufundi. Kufikia mwaka 1996 matumizi ya neno Intaneti yalikuwa kawaida, na kwa hiyo, hata matumizi yake kama kisawe cha mtandao wa ulimwengu mzima. Muongo huo ulipoendelea, intaneti ilifanikiwa kushughulikia mitandao mingi binafsi wa awali (ingawa baadhi ya mitandao, kama FidoNet, vimebaki tofauti). Katika miaka ya 1990, ilikuwa inakadiriwa kwamba intaneti ilikua kwa asilimia 100 kila mwaka, na kipindi kifupi cha mwaka wa 1996 na 1997 ukuaji wake ulilipuka. Ukuaji huo ulitokana na ukosefu wa utawala mkuu, ambao unaruhusu ukuaji wa kikaboni wa mtandao, na pia ukosaji ubinafsi na huru katika itifaki za intaneti, ambao unahamasisha ubadilishaji wauzaji na kuzuia kampuni yoyote kuwa na udhibiti mkubwa wa mtandao. Makadirio ya idadi ya watumiaji wa internet ni bilioni 1.67 kufikai 30 Juni 2009. Teknolojia Itifaki Ugumu wa miundombinu ya mawasiliano ya Intanet unahusisha vipengele vya vifaa vyake na sehemu za mfumo wa progamu inayodhibiti tabaka mbalimbali za usanifu. Ingawa vifaa vinaweza kutumika kusaidia mifumo mingine ya programu, ni urasimu na mifumo ya sheria za usanifu wa programu zinazoainisha Intanet na hutoa msingi wa ukubwa wake na mafanikio yake. Wajibu wa urasimu wa usanifu wa mifumo ya programu za Intanet umepewa tume ya uhandis wa Intanet (IETF). IETF huongoza makundi ya kuweka sheria, wazi kwa mtu yeyote, kuhusu masuala mbalimbali ya usanifu wa Intanet. Majadiliano yanayotokea na amri za mwisho huchapishwa katika mfululizo wa machapisho, iitwayo Kuomba kwa Maoni (RFC),ipatikanayo bure kwenye tovuti ya IETF. Mbinu muhimu za utengenezaji wa mitandao zinazowezesha Intanet ziko katika RFC teule yenye sheria za Intanet. Sheria hizi hueleza msingi unaojulikana kama Itifaki ya Intanet. Hii ni kielelezo cha usanifu unaogawanya huduma kuwa visehemu katika itifaki ya mfumo(RFC 1122, RFC 1123). Visehemu hivi vina uhusiano na mazingira au upeo ambao huduma zao hufanya kazi. Sehemu ya juu ni Sehemu ya zana, nafasi iliyotengwa kwasababu ya mbinu za utenegnezaji mitandao zinazotumika katika zana za programu, mfano, kivinjari. Chini ya sehemu hii ya juu, kuna sehemu ya Usafiri iunganishayo zana katika kompyuta tofauti kupitia mtandao (mfano, client-server) na mbinu sahihi za kubadilishana takwimu. Chini ya sehemu hizi ndipo kulipo na msingi wa teknolojia ya mitandao, linalojumuisha sehemu mbili. Sehemu ya Intanet inayowezesha kompyuta kutambuana kupitia anwani za Itifaki ya internet(IP), na huziwezesha kuungana pamoja kwa kutumia mitandao zilizo karibu. Mwisho, chini ya usanifu huu, ni sehemu ya programu , na sehemu ya uunganishaji, ambayo huwezesha kuungana kwa kompyuta zilizo katika kiunganishi sawa wa mtandao ya mtaa , kama vile mtandao wa eneo(LAN) au uunganishi wa kupiga. Mfano huu, ujulikanao pia kama TCP / IP, ni iliyoundwa isitegemee vifaa inavyotumia, kwa hivyo mfano huu hauna haja ya kujishughulisha na maelezo yoyote. Mifano mingine vimeundwa, kama vile mfano wa mifumo ya kiunganishi kilichofunguka (OSI) , lakini si sawa katika maelezo ya ufafanuzi, wala utekelezaji, lakini kufanana kupo n itifaki ya TCP / IP hujumuishwa katika majadiliano ya mitandao ya OSI . Sehemu maarufu zaidi ya picha simamizi ya Intanet ni Itifaki ya Intanet (IP) ambayo hushughulikia upeanaji wa (anwani za IP) kwa kompyuta zilizo katika Intanet. IP inawezesha ushikanishaji wa mitandao na kimsingi hujenga Intanet yenyewe. Toleo ya 4 ya IP (IPv4) ni toleo lililotumiwa katika kizazi cha kwanza cha Intanet ya leo na bado yatumika vikubwa. Iliundwa kushughulikia hadi watumiaji billioni~ 4,3 (10 9) wa intanet. Hata hivyo, kulipuka kwa ukuaji wa Intanet umesababisha kuisha kwa anwani za IPv4 ambayo inakadiriwa kuingia hatua yake ya mwisho katika takriban mwaka wa 2011. Toleo ya itifaki mpya, IPv6, iliundwa katikati ya mwongo wa 1990. Toleo hili linauwezo mkubwa wa kupeana anwani na mbinu bora zaidi ya uelekezaji wa trafiki ya Intanet. IPv6 kwa sasa ipo katika awamu ya kuachiliwa kibiashara duniani mashirika ya kuweka anwani za intanet(RIR) yameanza kuwahimiza mameneja wote wa rasilimali kupanga uchukuzi na uongofu wa haraka. IPv6 haishirikiani kikazi na IPv4. Kimsingi toleo la IPv6 hutengeneza toleo "sambamba" la Intanet ambalo halipatikani moja kwa moja na IPv4. Hii ina maanisha uboreshaji wa Programu au vifaa vya ukalimani ni muhimu kwa kila kifaa cha mtandao ambacho linahitaji kuwasiliana kupitia Intanet ya IPv6. Mifumo ya kuendesha kompyuta ya kompyta za kisasa tayari vimebadilishwa ili vifanye kazi na toleo zote za itifaki ya Intanet. Miundombinu ya mtandao , hata hivyo, bado yamebaki nyuma katika maendeleo hayo. Mbali na tata za viungo vinavyotengeneza miundombinu yake, Intanet imewezeshwa na mikataba ya kibiashara (mfano, mkataba wa kujitakia), na kwa ufundi maalum au itifaki zinazoeleza jinsi ya kubadilishana data kwa kupitia mtandao. Hakika Intanet ina ainishwa na viungo vyake na sheria za uelekezaji. Muundo Muundo wa Intanet na sifa za matumizi yake vimekuwa vikisomwa kwa undani. Imedhamiria kuwa muundo wa uelekezaji katika Intanet ya IP na viungo vya hypertext vya mtandao wa dunia nzima ni mifano ya mitandao isiyo na kipimo. Sambamba na jinsi watoa huduma, wa kibiashara za Intanet huwasiliana kwa kupitia sehemu za ubadilishanaji habari, mitandao ya utafiti kwa kawaida huunganishwa kupitia mitandao mikubwa kama GEANT, GLORIAD, Internet2 (halifa wa Mtandao wa Abilene ), na mtandao wa utafiti na kitaifa na elimu wa Uingereza, JANET. Mitandao hii imeundwa kutoka kwa mitandao mingine midogo (pia tazama orodha ya mashirika ya kiakademia ya mitandao ya kompyuta). Wanasayansi wengi wa Kompyuta huelezea Intanet kama "mfano halisi wa mfumo uliyo mkubwa, wenye uhandisi wa hali ya juu lakini changamano zaidi.". Intanet ina tofauti nyingi mno, kwa mfano, kiwango cha kuhamisha data na sifa za kiumbo za uunganishaji vinatofautiana sana. Intanet inaonyesha "tukio ibuka" linalotegemea muundo wake mkubwa. Kwa mfano, takwimu za viwango vya kuhamisha data vinaonyesha kufananakwa muda. Kanuni za mbinu za uelekezaji na utoaji anwani kwa trafiki katika Intanet zinarejelea asili yake katika mwongo wa 1960 wakati ukubwa na umaarufu wa mtandao haukuweza kutarajiwa. Kwa hivyo, uwezekano wa kujenga miundo mbadalia unachunguzwa. Utawala Internet ni mtandao uliyosambaa duniani ulioundwa na mitandao mingi tofauti iliyoshikanishwa. Hufanya kazi bila kitengo cha serikali kuu. Hata hivyo, ili kudumisha uwezo wa mifumo tofauti kufanya kazi pamoja, nyanja zote za kifundi na sera ya msingi wa miundombinu na nafasi za jina kuu husimamiwa na Shirika la Intanet linalotoa majina na nambari (ICANN), lililo na makao makuu huko Marina del Rey, California. ICANN ndiyo yenye mamlaka ya kusitiri utaratibu wa utoaji wa vitambulisho vya kipekee kwa matumizi ya Intanet, pamoja na majina ya vikundi, anwani za Itifaki ya Intanet (IP), nambari ya vipenyezo katika itifaki ya usafiri, na takwimu zingine nyingi. Nafasi ya iliyounganishwa ya majina ya ulimwengu, ambapo majina na nambari za kipekee hutolewa, ni muhimu kwa mataifa katika kupata huduma za Intanet. ICANN huongozwa na halmashauri ya wakurugenzi wa kimataifa wanaotolewa kutoka jamii za, ufundi wa Intanet, biashara, elimu, na mengine yasiyo ya kibiashara. Serikali ya Marekani inaendelea kuwa na jukumu la msingi katika kuidhinisha mabadiliko katika shina la DNslililoko katika kitovu cha mfumo wa eneo la majina. Jukumu la ICANN katika kuratibu zoezi la utoaji vitambulisho vya kipekee hulitofautisha kama shirika la kipekee lenye madaraka ya kuratibu Intanet ya kimataifa. Tarehe 16 Novemba 2005, Mkutano wa Dunia juu ya Jamii ya Habari, uliofanyika Tunis, uliunda Fora ya Utawala wa Intanet (IGF) kujadili masuala yanayohusiana na Intanet. Matumizi ya kisasa Intaneti inaruhusu mabadiliko makubwa katika masaa na maeneo ya kufanyia kazi, hasa kwa kuenea kwa viunganishi vya kasi visivyopimwa na zana za mtandao. Intaneti kwa sasa yaweza kupatikana karibu popote kwa njia mbalimbali, hasa kupitita vifaa vinavyobebwa mkononi. Simu za mkononi, kadi za data, michezo ya video na vielekezaji vya mkononi vinaruhusu watumiaji kujiunganisha na intanet kutoka popote pale walipo na mtandao usiotumia waya unaoruhusu teknolojia ya kifaa hiki. Ndani ya mipaka inayowekwa na skrini ndogo vifaa vingine pungufu kama vifaa vya mfukoni, huduma za Intanet, pamoja na barua pepe na mtandao, huweza kupatikana. Watoa huduma za Intanet huweza kuzuia huduma zinazotolewa na malipo ya usafirishaji wa data bila kutumia nyaya yaweza kuwa ya juu zaidi kuliko mbinu zingine za kupata intanet. Intaneti pia imekuwa soko kubwa kwa makampuni; baadhi ya makampuni makubwa leo yamekua kwa kuchukua faida ya gharama nafuu ya matangazo na biasharakwa kupitia Intanet, pia inajulikana kama biashara kupitia intaneti (e-commerce). Ni njia ya haraka sana katika kueneza habari kwa idadi kubwa ya watu kwa ujumla. Intaneti pia imebadilisha ununuzi - kwa mfano, mtu anaweza kuagiza CD kupitia intaneti na kuipokea katika barua baada ya siku kadhaa, au kuitoa kwa mtandao moja kwa moja katika baadhi ya kesi. Intaneti pia imewezesha uuzaji wa kibinafsi ambao unaruhusu kampuni kuuza bidhaa kwa mtu fulani au kundi maalum la watu, zaidi ya njia zingine za matangazo. Mifano ya uuzaji binafsi hujumuisha jamii zilizo katika Intanet kama vile MySpace, Friendster, Orkut, Facebook, na nyingine yznye maelfu ya watumizi wa Intanet ambao hujiunga kujitangaza wenyewe na kufanya urafiki kupitia Intanet. Wengi wa watumiaji hawa ni vijana na waliobaleghe wenye kati ya miaka 13-25. Kwa upande mwingine, wakati wanapojitangaza wao wenyewe hao pia hutangaza maslahi na mazoea yao, ambayo makampuni ya uuzaji katika Intanet yanaweza kutumia kama habari ili kujua kile ambacho watumiaji hawa watanunua kupitia Intanet, na kutangaza bidhaa za makampuni kwa watumiaji hao. Gharama ya chini na ubadilishanaji wa haraka wa mawazo, maarifa, na ujuzi vimefanya kazi shirikishi kuwa rahisi sana, kwa msaada wa programu shirikishi. Makundi hayawezi tu kuwasiliana kwa bei ya chini, bali upana wa Intanet unaruhusu makundi kama hayo kujiunda kwa urahisi. Mfano wa makundi hayo ni harakati ya programu za bure, ambazo zimetengeneza, miongoni mwa programu nyingine, Linux, Mozilla Firefox, na OpenOffice.org. "Kuongea" kupitia intaneti, iwe katika fomu ya vyumba vya kuongea vya IRC, au kupitia mfumo wa ujumbe wa moja kwa moja , kunaruhusu mfanyikazi na wenzake kuwasiliana kwa njia rahisi sana wakati wanapofanya kazi katika kompyuta zao wakati wa mchana. Ujumbe unaweza kubadilishwa kwa njia ya haraka na inayofaa zaidi kuliko barua pepe. Maongezo katika mifumo hii huweza kuruhusu ubadilishanaji wa faili, michoro ya "ubao mweupe" au mawasiliano ya sauti na video kati ya wanachama wa timu moja. Mifumo ya kudhibiti toleo unaruhusu timu zinazoshirikiana kufanya kazi kwa seti za hati zenye umiliki mmoja, bila ajali ya kufuta kazi za timu nyingine au wanachama kusubiri hadi kupata hati "zilizotumwa" ili kuweza kutoa michango yao. Biashara na timu za miradi zinaweza kushirikiana katika kalenda vilevile nyaraka na taarifa nyingine. Ushirika kama huo hutokea katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utafiti wa kisayansi, maendeleo ya programu, kupanga mikutano , wanaharakati wa kisiasa na uandishi wa bunifu. Ushirikiano wa kijamii na kisiasa pia unaenea wakati upatikanaji wa Intanet na idadi ya watu waliosoma kompyuta inapoongezeka. Kutoka 'matukio' ya makundi yanayoundwa haraka na watu mwanzo wa miaka ya 2000 na matumizi ya mitandao ya kijamii katika maandamano ya uchaguzi wa 2009 huko Iran, Intanet inaruhusu watu kufanya kazi pamoja kwa ufanisi zaidi na kwa njia nyingi zaidi kuliko iwezekanavyo bila Intanet. Intanet inaruhusu watumiaji wa kompyuta kufikia kompyuta zingine, na habari huhifadhiwa kwa urahisi, popote walipo duniani. Wanaweza kufanya hivi pamoja na, au, bila matumizi ya usalama, kujitambulisha na teknolojia za kuficha, kutegemea na mahitaji yao. Hii inahimiza njia mpya ya kufanya kazi kutoka nyumbani, kushirikiana na kubadilishana habari katika viwanda vingi. Mhasibu aliyeketi nyumbani anaweza kukagua vitabu vya kampuni iliyo katika nchi nyingine, kupitia kitumishi kilicho katika nchi nyingine ya tatu, ambayo inahifadhiwa na wataalamu wa IT katika nchi ya nne. Akaunti hizi zinaweza kuwa ziliundwa na waweka vitabu wafanyao kazi nyumbani, katika maeneo mengine, kwa kuzingatia habari-e waliyopata kupitia barua pepe waliyotumiwa kutoka ofisi za duniani kote. Baadhi ya mambo haya yalikuwa yanawezekana kabla ya kuenea kwa matumizi ya Intanet, lakini gharama ya laini binafsi ya kukodisha ingefanya mamboo hayo yasiweze kufanyika. Mfanyakazi wa ofisi akiwa mbali na dawati lake, labda upande mwingine wa ulimwengu katika safari ya kibiahsara au likizo, anaweza kufungua kikao katika kompyuta yake binafsi iliyoko ofisini mwake kwa kupitia mtandao binafsi wenye usalama (VPN) kwa kupitia Intanet. Hii inampa mfanyakazi upatikanaji kamili wa faili zake zote za kawaida na data, pamoja na barua pepe na zana nyingine za matumizi , wakati akiwa mbali na ofisi. Dhana hii pia inajulikana na baadhi ya watu wa usalama wa mitandao kama mtandao binafsi wa kidhahania wenye ndoto za kutisha, kwa sababu inapeleka mzunguko salama wa mtandao wa shirika ndani ya nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo. Huduma Habari Watu wengi hutumia maneno Intaneti na mtandao wa ulimwengu mzima (au Web tu ) kama visawe, lakini, kama tulivyojadiliana awali, maneno haya mawili yana maana tofauti. Mtandao wa Dunia Nzima ni seti ya nyaraka, picha na rasilimali nyingine, zinazotazamwa na kushikanishwa na kitafuta rasilimali sawa (URL) na viungo. URL hizi huruhusu watumiaji kuvipatia anwani vijakazi vya mtandao na vifaa vingine vinavyohifadhi rasilimali hizi na kuvipata vinapohitajika kwa kutumia HyperText Transfer itifaki ya kupelekea hati (HTTP). HTTP ni itifaki ya kipekee ya mawasiliano inayotumika katika mtandao wa Intanet. Huduma za mtandao huweza pia kutumia HTTP kuruhusu mifumo ya programu kuwasiliana ili kuweza kushiriki na kubadilishana mantiki ya biashara na data. Bidhaa za programu zinazoweza kupata rasilimali za Mtandao mara nyingi huitwa ajenti wa matumizi. Katika matumizi ya kawaida, tovuti za mtandao, kama Internet Explorer, Firefox, Opera, Apple Safari, na Google Chrome, huwaruhusu watumiaji kuvuka kutoka kurasa ya mtandao mmoja hadi nyingine kupitia viungo vya hyper. Hati kwenye mtandao huweza kuwa na mchanganyiko wowote wa data ya kompyuta, zikiwemo, picha, sauti, maandishi, video, mchanganyiko wa picha na sauti na mambo yanayomhusisha mtumiaji wa Intanet kama michezo, zana ofisi na maonyesho ya kisayansi. Kupitia utafiti wa Intanet unaoendeshwa na maneno maalum kwa kutumia mitambo ya utafutaji kama Yahoo! na Google, watumiaji duniani kote huweza kupata habari nyingi, kwa urahisi na moja kwa moja kutoka kwa Intanet. Ikilinganishwa na kamusi elezi zilizochapishwa namaktaba za kawaida, Mtandao wa Dunia Nzima umewezesha kusambaa ghafla kwa habari na data. Kwa kutumia mtandao, pia ni rahisi kuliko awali kwa watu binafsi na mashirika kuchapisha mawazo na habari kwa watazamaji wengi wanaotarajiwa. Kuchapisha kurasa ya mtandao, kibadilishanaji maoni - blogu, au kujenga tovuti inahusisha gharama ndogo za awali na huleta kupatikana kwa huduma nyingi zisizo na gharama. Kuchapisha na kudumisha idadi kubwa ya, mitandao ya kitaalamu yenye kuvutia, habari tofauti na ya moja kwa moja bado ni swala gumu na ghali, hata hivyo. Watu wengi na baadhi ya makampuni na vikundi-vitumizi hutumia mitandao ya ubadilishanaji maoni au blogu ambayo hutumika kama jarida zenye urahisi wakati wa kuongeza habari. Baadhi ya mashirika ya kibiashara huwahimiza wafanyakazi kuwasilisha ushauri katika maeneo yao maalum katika matumaini ya kuwa wageni watafurahishwa na maarifa ya mtaalam na habari za bure, na kuvutiwa kwa shirika hilo kama matokeo. Mfano mmoja wa zoezi hili ni Microsoft, ambayo watengenezaji bidhaa zake huchapisha mitandao ya ubadilishanaji binafsi katika blogu ili kuvutia umma kwa kazi zao. Mikusanyo ya kurasa binafsi za mtandao zilizochapishwa na watoa huduma wakubwa hubakia maarufu, na imeendelea kuwa ya kipekee. Ingawa oparesheni kama vile Angelfire na GeoCities zimekuwepo tangu siku za mwanzo wa Tovuti, oparesheni mpya, kwa mfano, Tovuti Facebook na MySpace kwa sasa vina wafuasi wengi. Oparesheni hizi mara nyingi hujionyesha kama mtandao ya huduma za kijamii kuliko viwekaji vya kurasa za mtandao. Kuweka matangazo katika kurasa za tovuti pendwa huwa na faida, biashara-e (biashara ya mtandao)(e-commerce) au uuzaji wa bidhaa na huduma moja kwa moja kupitia tovuti inaendelea kukua. Katika siku za mwanzo, kurasa za mtandao kwa kawaida zilitengenezwa kama seti za faili za nakala kamilifu na zilizo peke za HTML zikihifadhiwa kwenye tovuti ya huduma. Hivi karibuni, tovuti hutengenezwa kwa kutumia kisimamizi cha yaliyomo au kifaa ororo cha wiki, ambacho huwa na maudhui machache sana mwanzoni. Wachangiaji wa mifumo hii, ambao wanaweza kuwa wafanyakazi wanaolipwa, wanachama wa klabu au shirika zingine au wanachama wa umma, hujaza vihifadhi-data na maudhui kutumia kurasa zilizoundwa kwa kusudi hilo, ilhali wageni huangalia na kusoma yaliyomo katika ombo lake la mwisho la HTML. Kuna uwezekano wa kuwa au kutokuwa na mifumo ya uhariri, kibali na mifumo ya usalama iliyojengwa katika mchakato wa kuchukua maudhui mpya iliyoingizwa na kuifanya ipatikane na wageni wanaolengwa. Mawasiliano Barua pepe ni huduma muhimu ya mawasiliano inayopatikana kwenye Intanet. Dhana ya kutuma ujumbe wa kielektroniki wa maandishi kati ya wahusika kwa njia iliyosawa na kutuma barua au memo ilitangulia utengenezaji wa Intanet. Leo inaweza kuwa muhimu kutofautisha kati ya Intanet na mifumo ya kindani ya barua pepe. Barua pepe ya Intanet inaweza kusafiri na kuhifadhiwa kimaandishi katika mitandao mingine mingi na mashine zilizo nje ya udhibiti wa mtumaji na mpokeaji. Kwa wakati huu kunauwezekano wa yaliyomo kusomwa na kubadilishwa na mhusika wa tatu, ikiwa kuna mtu yeyote anayefikiri kuwa una umuhimu wa kutosha. Mifumo ya barua za kindani, ambapo habari haipaswi kamwe kutoka nje ya mtandao wa kampuni au shirika , ni salama zaidi, ingawa katika shirika lolote kutakuwa na wafanyikazi wa IT na wafanyakazi wengine ambao kazi yao inahusu ufuatiliaji, na mara chache kufikia, barua pepe za wafanyikazi wengine ambazo hawajatumiwa hao. Picha, nyaraka na faili nyingine zinaweza kutumwa kama viungo vya barua pepe. Barua pepe zinaweza kutumwa kwa anwani nyingi za barua pepe. Telefoni ya intaneti ni huduma nyingine la mawasiliano ya kawaida iliyowezekana kwa uundaji wa a Intanet. VoIP husimamia itifaki ya kupitisha sauti kupitia Intanet, ikirejelea itifaki msingi ya mawasiliano ya Intanet. Wazo hili lilianza mwanzo wa mwongo wa 1990 na zana zilizofanana na simu za polisi za kompyuta binafsi. Katika miaka ya hivi karibuni mifumo mingi ya VoIP imekuwa rahisi kutumia na kuwa na manufaa kama simu ya kawaida. Faida ni kwamba, Intanet inapobeba trafiki ya sauti, VoIP inaweza kuwa bure au kuwa na gharama ndogo sana kuliko upigaji simu wa jadi, hasa juu ya umbali mrefu na hasa kwa wale wenye viunganishi vinanvyowaka wakati wowote kama vile Cable au ADSL. VoIP inapevuka na kujitokeza kama mshindani mbadalia wa huduma za simu za jadi. Uwezo wa kubadilishana ujumbe kati ya watoa huduma mbalimbali imeboreshwa na uwezo wa kupiga au kupokea simu kutoka kwa simu ya jadi unapatikana. Vibadilisha mtandao vya VoIP ambavyo ni rahisi na vya bei nafuu vinapatikana na vinaondoa haja ya kuwa na kompyuta binafsi. Ubora wa sauti unatofautiana kutoka wito moja hadi mwingine lakini mara nyingi ni sawa, na huweza hata kuzidi ule wa simu za jadi. Matatizo yaliyobakia kwa VoIP hujumuisha upigaji simu kwa nambari ya dharura na utumainikaji. Hivi sasa, watoa VoIP wachache hutoa huduma ya dharura, lakini haipatikani na wote. Simu za jadi huwezeshwa na nguvu za laini na hufanya kazi wakati stima zinapopotea; VoIP haifanyi hivyo bila chanzo kingine cha nguvu kwa vifaa vya simu na vifaa vya upatikanaji wa Intanet. VoIP pia imekuwa maarufu kwa zana za michezo , kama njia ya mawasiliano kati ya wachezaji. Wateja wa VoIP wanaojulikana katika michezo ni kama vile Ventrilo na Teamspeak. Wii, PlayStation 3, na Xbox 360 pia hutoa sifa za VoIP za kuongea kupitia mtandao . Kuhamisha data Kugawana failini mfano wa uhamishaji wa kiasi kikubwa cha data kupitia Intanet. Faili ya kompyuta inaweza kutumwa kwa kutumia barua pepe kwa wateja, waenzi na marafiki kama kiungo. Inaweza kuwekwa kwenye tovuti au tumishi ya FTP kwa upakuaji rahisi na watu wengine. Inaweza kuweka ndani ya "eneo lenye wamiliki wengi" au ndani ya tumishi ya failikwa ajili ya matumizi ya haraka na washikadau. Mzigo wa upakuaji mzito kwa watumiaji wengi unaweza kupunguzwa na matumizi ya "vioo" vya huduma au mitandao ya viwango aina moja. Katika hali hizi zote, upatikanaji wa faili unaweza kudhibitiwa na kujitambulisha kwa watumiaji, usafiri wa faili katika ya Intanet unaweza kuborongwa kwa kupewa maana fiche, na hongo ya pesa yaweza kutumiwa ili kuzipata faili. Bei inaweza kulipwa kutoka eneo tofauti kwa njia isiyokuwa wazi, kwa mfano, kutoka kwa kadi ya deni(krediti) ambayo maelezo yake hupitishwa pia - kwa kawaida hupewa maana fiche kabisa- kupitia Intanet. Asili na dhibitisho la faili iliyopokewa inaweza kuangaliwa kupitia saini za dijitali au kwa MD5 au aina nyingine ya ujumbe. Sifa hizi rahisi za intanet, juu ya msingi wa dunia nzima, zinabadilisha uzalishaji, mauzo, na usambazaji wa kitu chochote ambacho kinaweza kupunguzwa na kuwa faili ya kompyuta kwa usafirishaji. Hii ni pamoja na kila namna ya machapisho ya magazeti , bidhaa za programu, habari, muziki , filamu, video, picha, grafiki na sanaa zingine. Hili kwa upande mwingine limesababisha mabadiliko katika kila moja ya viwanda ambavyo awali vilidhibiti uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizi. Utabakishaji wa vyombo vya habari unahusu kitendo ambacho watangazaji wengi wa redio na televisheni wanatumia kukuza lishe ya Intanet ya habari za moja kwa moja kutumia sauti, na tabaka za video (kwa mfano, BBC). Wanaweza pia kuruhusu maonyesho na usikilizaji kulingana na mabadiliko ya wakati kama kuangalia mbele, picha klasiki na sifa za kusikiliza tena. Watoaji huduma hawa wameungwa na anuwai ya "watangazaji" halisi wa Intanet ambao kamwe hawakuwa na leseni za kutoa habari moja kwa moja. Hii ina maanaisha kuwa kifaa kilichounganishwa na intanet, kama vile kompyuta au kitu kingine maalum, kinaweza kutumika kupata vyombo vya habari vilivyounganishwa na Intanet kwa njia ile ile kama ilivyowezekana tu na mpokezi wa televisheni au redio. Aina ya matini ni pana sana, kutoka kwa ponografia hadi tovuti za ufundi na utaaluma wa juu. Podcasting ni aina fulani katika mada hii, ambapo - kwa kawaida ni sauti- matini zinapakuliwa na kuchezwa tena kwenye kompyuta au kubadilishwa kwenye chombo cha habari kinachobebeka ili kisikilizwe matu anapotembea. Hizi mbinu za kutumia vifaa rahisi vinaruhusu mtu yeyote, aliye na udhibiti ufichaji au udhibiti wa leseni, kutangaza picha , muziki na video kote ulimwenguni. Kamera za mtandao zinaweza kuonekana kama ongezeko ya chini ya bajeti ya jambo hili. Ingawa baadhi ya kamera za mtandao zinaweza kutoa video za kiima kizima, picha huwa ndogo au hujiongeza pole pole. Watumiaji wa intanet wanaweza kuangalia wanyama waliyozunguka kidimbwi cha maji huku Afrika, meli katika kipisho cha Panama, trafiki katika mzunguko wa barabara za mtaa au kufuatilia wanapoishi katika muda halisi. Vyumba vya kuongea vya video na mikutano ya video pia ni maarufu, matumizi mengi yakipatikana ya kamera kibinafsi za mtandao, zilizo na, au zisizo na sauti inayotamba pande zote mbili. YouTube ilianzishwa tarehe 15 Februari 2005 na sasa ni tovuti inayoongoza kwa maonyesho ya video za bure pamoja na idadi kubwa ya watumiaji. Inatumia mtandao wenye msingi wa kichezaji cha flashi kuonyesha faili za video. Watumiaji waliojiandikisha huweza kuongeza idadi isiyo na kipimo ya video na kutengeneza vitambulishi vyao binafsi. YouTube inadai kuwa watumiaji wake hutazama mamia ya mamilioni, na huongeza mamia ya maelfu, ya video kila siku. Upatikanaji Lugha ya iliyoenea katika mawasiliano ya Intanet ni Kiingereza. Hii inayotumika zaidi katika intaneti ni Kiingereza. Hili latokana na kuwa ndiyo lugha asilia ya intanet na pia nafasi yake kama lingu-franca = lugha sambazi. Pia inaweza kuhusiana na upungufu wa utendaji wa kompyuta za awali, kiasi kikubwa zikitoka Marekani, kushughulikia maandishi mengine kuliko yale ya lahaja ya Kiingereza ya alfabeti ya Kilatin. Baada ya Kiingereza (asilimia 29 ya wageni wa Tovuti) lugha zilizohitajika zaidi katika Tovuti ya Dunia Nzima ni Kichina (asilimia 22), Kihispania (asilimia 8), Kijapani (asilimia 6), Kifaransa (asilimia 5), Kireno na Kijerumani (kila moja asilimia 4 ), Kiarabu (asilimia 3) na Kirusi na Kikorea (kila moja asilimia 2 ). Katika kanda, asilimia 42 ya watumiaji wa intaneti duniani wana makao Barahindi, asilimia 24 Ulaya, asilimia 15 Amerika ya Kaskazini, asilimia 11 Amerika Kusini na Caribbean zikichukuliwa kwa pamoja, asilimia 4 Afrika, asilimia 3 Mashariki ya Kati na asilimia 1 Australia / Oceania. Teknolojia za Intanet zimeendelea ya kutosha katika miaka ya hivi karibuni, hasa katika matumizi ya Unicode, kwamba vifaa vizuri vinapatikana kwa maendeleo na mawasiliano katika lugha zinazotumiwa kwa wingi. Hata hivyo, baadhi ya matatizo kama mojibake (uonyeshaji usiosahihi wa maandishi ya lugha za kigeni , pia inajulikana kama kryakozyabry) bado hubakia. Njia za kawaida za kupata Intaneti nyumbani ni kwa kupiga, laini za broadband (kupitia waya za koax, nyuzinyuzi za optiki au waya za shaba), Wi-Fi, setilaiti na teknolojia ya rununu ya 3G. Maeneo ya umma kwa matumizi ya Intaneti ni maktaba na mikahawa ya Intaneti, ambamo kompyuta zilizounganishwa na Intaneti hupatikana. Pia kuna sehemu za kupata Intaneti katika maeneo mengi ya umma kama vile kumbi za uwanja wa ndege na maduka ya kahawa, katika baadhi ya sehemu hizi kwa matumizi mafupi wakati umesimama. Maneno mbalimbali hutumiwa kama vile "kiosk za umma za interneti", "pahala pa upatikanaji intaneti pa umma", na "simu za kulipia za Mtandao". Hoteli nyingi sasa pia huwa na pahala pa umma, ingawa hizi hulipiwa kulingana na matumizi. Sehemu hizi hutumika kwa matumizi mbalimbali kama ununuzi tiketi , amana za benki, malipo kupitia mtandao nk. Wi-Fi hutoa upatikanaji usiotumia waya wa mitandao ya kompyuta, na kwa hiyo yaweza kufanya hivyo kwa Intanet yenyewe. Sehemu moto zinazotoa upatikanaji kama huo hujumuisha mikahawa ya Wi-Fi, ambapo watumiaji hupaswa kuleta vifaa vyao visivyotumia waya kufikia Intaneti kama vile Kompyuta za pajani au PDA. Huduma hizi huweza kuwa bure kwa wote, bure kwa wateja tu, au waliolipishwa. Eneo moto halina haja ya kuwa finyu katika eneo ndogo. Kampasi nzima au bustani, au hata mji mzima unaweza kuwezeshwa. Juhudi za mashinani zimesababishamitandao ya kijamii isiyotumia waya. Huduma za Wi-Fi za kibiahsara zinazofunika maeneo ya miji mikubwa zinapatikana London, Vienna, Toronto, San Francisco, Philadelphia, Chicago na Pittsburgh. Intanet huweza kupatikana kutoka sehemu hizo kama kiti cha bustani. Mbali na Wi-Fi, kumekuwa na majaribio na mitandao ya simu ya kibiashara isiyotumia waya kama Ricochet, huduma mbalimbali za kasi za data kupitia mitandao ya simu za mkononi na, huduma zisizotumia waya zisizobadilika. Simu za mkononi za hali ya juu kama vile smartphone kwa ujumla huja na upatikanaji wa Intaneti kwa kupitia mtandao wa simu. Vivinjari cha mitandao kama vile Opera hupatikana katika simu hizi za mkononi zilizoendelea, ambazo pia huweza kutekeleza aina nyingie tofauti ya programu za Intaneti. Simu nyingi za mkononi huweza kupata Intanet kuliko PC ingawa hii haitumiki kwa upana. Kinachotoa huduma za upatikanaji wa Intaneti na muundo wa mfanyiko wa itifaki hutofautisha mbinu zinazotumika kupata Intaneti. Taathira za kijamii Intaneti imefanya kuwe na uwezekano mkubwa kabisa wa aina mpya za mahusiano ya kijamii, shughuli na upangaji, kutokana na sifa zake msingi kama vile kuenea katika matumizi na upatikanaji. Tovuti za kijamii kama vile Facebook na MySpace vimetengeneza aina mpya ya ufahamianaji na mwingiliano. Watumiaji wa tovuti hizi huweza kuongeza vitu mbalimbali kwa kurasa zao binafsi, kuonyesha maslahi yao ya kawaida, na kuungana na watu wengine. Inawezekana kupata mzunguko mkubwa wa marafiki, hasa kama tovuti inaruhusu watumiaji kutumia majina yao halisi, na kuruhusu mawasiliano kati ya makundi makubwa ya watu waliomo. Tovuti kama meetup.com zipo ili kuruhusu matangazo mapana ya makundi ambayo yanaweza kuwepo hasa kwa mikutano ya ana-kwa-ana, lakini ambayo inaweza kuwa na mahusiano mbalimbali madogo katika tovuti ya kundi lao katika meetup.org, au tovuti zingine zenye kufanana. Kizazi cha kwanza kwa sasa kinakuzwa na upatikanaji ulioenea wa kujiunga na Intaneti, unaosababisha utovu wa faragha, utambulisho, na wasiwasi wa kimiliki. "Wenyeji wa dijitali" hukumbwa na wasiwasi tofauti ambao haukuwa na vizazi vya mwanzoni. Katika jamii za kidemokrasia, mtandao umepata uhusiano mpya kama chombo cha kisiasa, kupelekea udhibiti wa Intaneti na baadhi ya nchi. Kampeni ya urais wa Howard Dean mwaka 2004 huko Marekani ulikuwa mashuhuri kwa uwezo wake wa kutoa michango kupitia Intaneti. Makundi mengi ya kisiasa hutumia interneti ili kufanikisha utaratibu mpya wa kujiandaa , ili kutimiza wanaharakati wa Intaneti. Baadhi ya serikali, kama zile za Iran, Korea ya Kaskazini, Myanmar, Jamhuri ya Watu wa China, na Saudi Arabia, zinaudhibiti wa juu wa yale watu katika nchi zao wanayoweza kupata kwenye Intanet, hasa maudhui ya kisiasa na kidini. Hii inakamilishwa kwa kupitia programu inayoficha makundi na maudhui ili yasipatikane kwa urahisi bila mbinu ya kitaaluma zaidi. Nchini Norway, Denmark, Finland na Uswidi, watoa huduma za Intaneti kwa hiari yao(pengine kuepuka mpangilio kama huo kuwa sheria) walikubali kudhibiti upatikanaji wa tovuti zilizotajwa na polisi. Ingawa orodha hii ya URL haramu inapaswa kuwa na anwani za tovuti zinazojulikana zenye kuonyesha ponografia ya watoto, yaliyomo katika orodha hii ni siri. Nchi nyingi, ikiwemo Marekani, zimepitisha sheria zinazofanya umiliki au usambazaji wa nyenzo fulani, kama vile ponografia ya watoto, iliyoharamu, lakini hazitumii programu ya kuficha. Kuna programu nyingi za bure na zinazouzwa ziitwayo, programu za udhibiti wa maudhui, na ambazo mtumiaji anaweza kuchagua kuzuia tovuti zinazokera katika kompyuta binafsi au mitandao, kama kuzuia uwezekano wa mtoto kupata habari za kimapenzi au vurugu. Intaneti imekuwa chanzo kikuu cha burudani tangu kabla ya mtandao wa dunia nzima, kukiwa na majaribio ya kijamii yanayofurahisha kama vile MUD na MOOyaliyofanywa katika vitoa nhuduma vya vyuo vikuu, ambapo makundi ya Usenetya vichekesho yalipokea kiasi kikubwa cha trafiki kuu. Leo, majukwaa mengi ya Intaneti yana sehemu ya michezo na video za kuchekesha; katuni(vibonzo) fupi katika mfano wa sinema za flashi pia ni maarufu. Zaidi ya watu milioni 6 hutumia vibadilishanaji maoni (blogu) au mbao za ujumbe kama njia ya mawasiliano na kwa ajili ya kubadilishana mawazo. Viwanda vya sinema za watu wazima na kamari vimechukua faida kamili ya mtandao wa dunia nzima, na mara nyingi hutoa chanzo muhimu ya mapato ya matangazo kwa tovuti zingine. Ingawa serikali nyingi zimejaribu kuweka vikwazo katika matumizi ya Intaneti katika viwanda hivi, zilishindwa kupunguza kuenea umaarufu wa viwanda hivi. Eneo moja kuu la burudani kwenye interneti ni Michezo yenye wahusika wengi. Aina hii ya burudani inajenga jamii, kuwaleta watu wa umri fofauti na asili zote kufurahia mwendo wa kasi wa ulimwengu wa michezo ya wahusika wengi. Hii inaanza kutoka MMORPG hadi mfyatua risasi wa kwanza , kutoka michezo ya kusawiri mhusika hadi kamari ya Intaneti. Hii imebadilisha njia ambayo watu wengi huweza kuingiliana na jinsi wao wanvyoweza kutumia muda wao wa bure katika Interneti. Wakati michezo ya Intaneti imekuwapo tangu mwongo wa 1970, aina ya kisasa ya michezo ya Intaneti ilianza na huduma kama GameSpy na MPlayer, ambayo wachezaji wa michezo kwa kawaida walijiunga nayo. Wasiyojiunga walikubaliwa kucheza baadhi ya aina za mchezo iliyochezwa au baadhi ya michezo. Wengi hutumia Intaneti kwa kupata na kuchukua muziki, sinema na vitu vingine kwa starehe zao na utulivu. Kama ilivyojadiliwa hapo awali, kuna vyanzo za kulipia na vya bure kwa haya yote, kwa kutumia vitoa huduma vikuu na teknolojia za viwango vinavyolingana. Baadhi ya vyanzo hivi hujali zaidi haki za wasanii wa awali na juu ya sheria za kimiliki kuliko wengine. Wengi hutumia mtandao wa dunia nzima kupata habari, taarifa za michezo na hali ya hewa na, kupanga likizo na kujua zaidi kuhusu mawazo na maslahi yao. Watu hutumia maongezi kupitia mtandao, utumaji wa ujumbe na barua pepe kuwasiliana na marafiki duniani kote, wakati mwingine kwa njia sawa na jinsi baadhi ya watu awali walivyokuwa na marafiki ambao walifahamiana kwa barua tu. Mitandao ya kijamii kama MySpace, Facebook na mingineo, pia huwasaidia watu kuwasiliana kwa starehe zao. Intaneti imeshuhudia kuongezeka kwa idadi ya kopyuta binafsi za mtandao, ambapo watumiaji wanaweza kupata faili zao, folda, na masharti kupitia Intaneti. Matumizi ya Intaneti yamesababisha upungufu mkubwa kwenye rasilimali ya kampuni; mfanyikazi wastani wa Uingereza hutumia dakika 57 kwa siku akipitia mtandao wa dunia nzima wakati akifanyakazi, kulingana na utafiti wa mwaka wa 2003 uliofanywa na Huduma za Kibiashara za Peninsula. Hatari za Intaneti Wavuti wa Webmd umesema kuwa mtu aliyepatwa na ashiki ya kuwa kwa mitandao kila wakati (addicted) huenda akawa na maswala mengine ya kiafya kwa ubongo (mental health issues). Wavuti pia umefanya watu wawe na uchu wa kuangalia filamu za ponografia kwa sababu hili hufanyika kwa urahisi. Vijana wengi pia wamejipata kwa hatari baada ya jumbe katika vyombo vya habari vya kijamii (social media) baada ya kutapeliwa au hata kutekwa nyara na watu waliojifanya marafiki. Kumekuwa pia na michezo mibaya iliyowafanya vijana kujiua kama vile Blue Whale challenge ambapo wachezaji walikuwa wakishawishiwa wajitoe uhai baada ya kushiriki katika mchezo. Kumekuwa pia na michezo ya kamari (online betting) ambapo watu wapoteza pesa na hata kugeukia kuwa wezi ili waweze kuendelea kucheza michezo ile. Jinsi ya kudhibiti intaneti kama mzazi Wazazi wana jukumu la kuhakikisha kuwa wanao hawaingii katika wavuti baya za ponografia, ugaidi, zinazofunza itikadi kali au zinazohimiza au kuwashawishi watoto kushiriki katika tabia mbovu. Wanaweza kufanya hivi kwa kuweka "rotating proxies" ambazo hudhibiti kinachoonwa kwa wavuti ile. Pia wanafaa waongee na watoto na kuwaambia madhara ya mitandao. Kama una uraibu wa Intaneti, inafaa uchukue likizo usitumie mitandao ili uweze kuongea na watu moja kwa moja. Tazama pia Blogu Wiki Tovuti Uhuru wa habari Tanbihi Marejeo Rehmeyer, Julie J. 2007. Mapping a medusa: Intaneti inasambaza mizizi yake Science News 171 (23 Juni) :387-388. Inapatikana http://www.sciencenews.org/articles/20070623/fob2.asp . Castells, M. 1996. Rise of the Network Society. 3 vols. Vol. 1. Cambridge, MA: Wachapishaji wa Blackwell . Castells, M. (2001), “Lessons from the History of Internet”, in “The Internet Galaxy”, Ch. 1, ukurasa 9-35. Uchapishaji wa Chuo Kikuu cha Oxford. RFC 1122, Requirements for Internet Hosts—Communication Layers, IETF, R. Braden (Ed.), Oktoba 1989 RFC 1123, Requirements for Internet Hosts—Application and Support, IETF, R. Braden (Ed.), Oktoba 1989 Viungo vya nje Orodha ya maneno ya tarakishi ya mradi wa Kilinux kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kwa Kiingereza Intanet (Wakfu wa sayansi wa Kitaifa) "Miaka 10 iliyobadilisha dunia" - Wired anaangalia nyuma mageuzi katika Intanet kwa miaka 10 iliyopita Makao ya Intanet na jamii ya Berkman yaliyo Harvard Hifadhi za Dijital za CDC-Uzushi wa umri wa Intanet Jinsi Intanet ilikuja kuwa jinsi ilivyo. Kurasa ya nyumbani ya tovuti la Shirika la Intanet. RFC 801, Upangaji wa ubadilishanaji katika TCP/IP Kutayarisha masuala ya dijitali ya usoni ya Ulaya - i2010 Upitiaji tena wa kati ya muhula Manjoo, Farhad - The Unrecognizable internet of 1996 - Slate No cure no pay zoekmachine optimalisatie Media Freedom Internet Cookbook ulioandikwa na Mwakilishi wa OSCE kuhusu uhuru wa vyombo vya habari huko Vienna mwaka wa 2004 First Monday Jarida lililochunguzwa na wasomi wa kiwango kimoja katika Intaneti. How Much Does The Internet WEIGH? ulioandikwa na Stephen CASS, Discover 2007 Fixing ‘DNS Probe Finished No Internet’ Error Intaneti Habari Mawasiliano Teknolojia
1760
https://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu
Blogu
Blogu ni teknolojia mpya inayowezesha watu binafsi kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao wa tarakilishi maarufu kama wavuti au intaneti. Blogu inaweza kuchukuliwa kama ni shajara pepe. Neno la Kiswahili "blogu" linatokana na neno la Kiingereza, "blog", ambalo limetokana na neno lingine, "weblog". Kimsingi, blogu ni aina ya tovuti ambayo huandikwa mara kwa mara na kwa mpangilio wa mambo mapya kutokea ukurasa wa mbele kuendana na tarehe na mwezi. Aina za blogu Katika blogu za binafsi, waandishi hutoa mawazo yao kuhusu masuala ibuka katika jamii na kwa njia hii kuanzia mazungumzo katika intaneti. Wasomaji wanaweza kuchangia na kuendeleza katika mawazo haya kwa kupeana maoni yao yanayoweza kukubaliana na yale ya mwenye blogu au hata kutofautiana. Mawazo haya ya wasomaji huwekwa kwa komenti ambazo huwa pale chini ya blogu. Wanablogu wanaweza kuchochea hisia nzito katika jamii kama zile za uanaharakati au siasa. Ili kuwa na blogu yako binafsi, wafaa kuwa unajua kutumia intaneti na pia uwe na jambo la kuwafahamisha watu au kuwafunza ili upate wasomaji. Wafaa pia uwe na mtindo. Blogu za kampuni huwa na lengo maalumu ya kuwafahamisha wasomaji kuhusu bidhaa mbali mbali za kampuni. Wenye kampuni huzitumia pia kuwafahamisha wateja na wasomaji kuhusu mambo mapya katika kampuni. Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano, blogu za maandishi, blogu za mkononi, blogu za picha, blogu za sauti, na blogu za video. Blogu ya mradi wa Global Voices inaandika muhtasari wa majadiliano na habari zinazojitokeza katika blogu mbalimbali duniani, hasa nje ya Marekani. Mradi huu una wanablogu katika nchi mbalimbali duniani ambao wanaandika juu ya masuala muhimu yanayojitokeza katika blogu za nchini mwao au katika bara lao. Blogu za sauti Tofauti na blogu za maandishi ambapo mwenye blogu huwa na mtindo wa kuandikaandika katika shajara hiyo yake, blogu za sauti huwa na sauti za mwenyewe akiongea au akihoji watu. Wanaomfuata huja na kusikiza sauti zile. Blogu za video au vlogu Kando na blogu ambayo huwa na maandishi na picha pekee, pia kuna vlogu ambayo huwa na video. Mwenye vlogu huchukua video akifanya mambo kama mafunzo, kuoka mikate, kupika, kutengeneza simu na watu hufuata vlogu yake ili waweze kusoma.Unapokuwa na blogu ya aina hii, lazima uwe na kamera nzuri ya kuchukua video zako na pia uwe na uwezo wa kurekebisha video. Viungo vya nje Tovuti ya kuanzisha blogu bure Historia ya blogu toka 1994-2018 Mwongozo wa kisheria kwa wanablogu toka Electronic Frontier Foundation Mradi wa Global Voices Masomo kwa wanablogu wapya Azimio la Dodoma Jumuiya ya Wanablogu Tanzania Maadili ya wanablogu yaliyoandikwa na Tim O'Reilly Mtandao wa Wanablogu wa Afrika Mchango wa blogu katika demokrasia Computer Law and Security Report Volume 22 Issue 2, Pages 127-136 blogs, Lies and the Doocing by Sylvia Kierkegaard (2006) Law Library Legal Blawgs Web Archive from the U.S. Library of Congress Teknolojia Blogu Uandishi wa Raia
1773
https://sw.wikipedia.org/wiki/Jua
Jua
Jua (alama: ) ni kitovu cha mfumo wa Jua wenye sayari nane, sayari vibete na magimba mengi madogo. Dunia ni sayari ya tatu katika mfumo huu. Jua ni nyota iliyo karibu na Dunia yetu kuliko nyota nyingine zote. Umbo la Jua Umbo la Jua linakaribia kuwa tufe kamili. Maada yake ni utegili yaani gesi ya joto sana inayoshikamanishwa na nguvu ya graviti. Kipenyo cha Jua ni takriban kilomita 1,392,684 ambayo ni mara 109 kipenyo cha Dunia yetu. Masi yake ni mara 330,000 ya masi ya Dunia. Kwa ujazo Jua ni kubwa mara milioni moja kuliko Dunia. Kikemia masi ya Jua ni hasa hidrojeni (73%) na heli (25%). Kiasi kinachobaki ni elementi nzito zaidi, kama vile oksijeni, kaboni, chuma na nyingine. Ingawa elementi nzito ni asilimia ndogo tu za masi ya Jua, kutokana na ukubwa wa Jua, elementi nzito zinalingana mara 5,000 na masi ya Dunia Muundo wa Jua Muundo wa Jua hufanywa na kanda tatu: Kiini ambako atomi za hidrojeni zinayeyungana kutengeneza heli kutokana na hali ya shinikizo na joto kubwa mno; Ukanda wa myuko (convection zone) ambako joto la kiini linaendesha mizunguko ya utegili inayopeleka nishati kutokana kiini kwenda angahewa ya Jua Ukanda wa angahewa ya Jua. Sehemu yake kubwa inaitwa tabakanuru (photosphere). Tabakanuru ni asili ya nuru na joto tunazopokea duniani. Sehemu ya nje ya angahewa ni "korona" inayoonekana tu wakati wa kupatwa kwa Jua. Historia ya Jua Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Jua lilitokea takriban miaka bilioni 4.57 iliyopita katika wingu kubwa la molekuli za hidrojeni. Kama nyota zote Jua linapitia ngazi mbalimbali katika maisha yake. Wataalamu wengi hukadiria kwamba baada ya miaka bilioni 5 ijayo akiba ya hidrojeni katika kitovu cha Jua itapungua. Halafu Jua litapanuka sana na kuwa jitu jekundu. Katika hali hii inaweza kuenea hadi njia ya obiti ya Zuhura na hakuna nafasi tena kwa uhai kwenye Dunia kutokana na joto kali. Wataalamu wanatofautiana katika makadirio yao kama upanuzi huu utasababisha pia kupotea kabisa kwa sayari za Utaridi, Mirihi na Dunia zikimezwa na kuingia ndani ya Jua. Baada ya miaka bilioni kadhaa ya kuwaka kama jitu jekundu, masi yake itakuwa imepungua itajikaza na kuendelea kwa muda usio mrefu kama nyota ndogo na hafifu. Kuna uwezekano mkubwa wa kwamba Jua litaendelea baadaye kama nyota kibete nyeupe (White Dwarf) itakayoendelea kuzimika polepole. Mnururisho na upepo wa Jua Jua linatoa mwanga, joto na mnururisho mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la chembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kama upepo wa Jua. Masi ya upepo wa Jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde. Asili ya nishati hii ni mchakato wa myeyungano wa kinyuklia ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heliamu. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heliamu inaachisha nishati inayotoka kwenye Jua kwa njia ya mnururisho. Nishati ya mnururisho huu ni msingi wa maisha ya mimea na viumbe hai katika dunia. Nuru ya Jua inabadilishwa na mimea kwa njia ya usanisinuru kuwa nishati ya kikemia inayojenga miili yao itakayokuwa lishe tena ya mimea na wanyama. Mambo yanayo athiri tabia ya nchi ya afrika mashariki Jua la utosi,upepo,mwinuko,mvua,uoto,bahari na maziwa ni mambo yanayoathiri tabia ya nchi ya Afrika Mashariki. Jua la utosi Dunia yetu ina mistari ya kubuni inayowezesha kutambua maeneo mbalimbali kwa urahisi,mistari hiyo ni pamoja na mstari wa Ikweta,tropiki ya kansa na tropiki ya Kaprikoni Mstari wa Ikweta unaigawa dunia katika sehemu nbili za kaskazini na kusini,mstari huu una nyuzi 0 na unapita eneo la Afrika mashariki katika nchi za Kenya na Uganda.Mstari wa Tropiki ya kansa upo upande wa kaskazini mwa Ikweta. Mstari wa tropiki ya Kaprikoni Upo Kusini mwa Ikweta. Kipindi ambacho jua la Utosi lipo Tropiki ya kansa ,eneo La Kizio cha Kaskazini Huwa na joto,kwa kuwa hewa ikipata joto hutanuka hivyo huwa na mgandamizo mdogo wa hewa.Pepo huvuma kuelekea huko. Upepo Pepo hizi huvuma kutoka kusini-mashariki kuanzia mwezi desemba wakati jua la utosi linapokuwa tropiki ya kaprikoni kipindi hiki kizio cha kusini huwa na joto na Pepo huvuma kutoka kusini-mashariki.Pia hali hiyo husababisha mabadiliko ya upatikanaji wa mvua na hali ya joto katika eneo la Afrika Mashariki. Maeneo ya Ikweta yana tabia ya Kiikweta ya kuwa na mvua nyingi na joto jingi.Kusini na Kaskazini mwa eneo lenye tabia ya Kiikweta kuna tabia ya kitropiki yenye majira mawili makuu ya mwaka.Majira hayo ya mwaka ni masika na kiangazi.Lakini katika maeneo ya pwani majira ya mwaka hugawanyika katika sehemu nne ambazo ni vuli,kipupwe,masika na kiangazi. Mwinuko Afrika Mashariki ina mwinuko wa meta 0 kutoka usawa wa bahari hadi kufika meta 4600.Maeneo ya pwani mwinuko wake ni kuanzia meta 0 hadi meta 500 kutoka usawa wa bahari. Wastani wa jotoridi ni nyuzi za sentigredi 26.Joto hupungua kadiri unavyoelekea bara.Meta 1500 Kutoka usawa wa bahari ni nyuzi za sentigredi 22 ambapo ni wastani wa joto linalopatikana katika maeneo ya Tabora.Maeneo ya mlima mrefu kama kilimanjaro wenye urefu wa meta 5895 huwa na jotoridi la chini ya nyuzi za sentigredi 0 Maziwa na bahari Maeneo yaliyo kandokando ya maziwa na bahari huwa na unyevunyevu na mvua nyingi.Mara nyingi maeneo yanayozunguka bahari na maziwa mfano Ziwa Viktoria na Bahari ya Hindi yana tabia ya nchi ya aina moja.Maeneo hayo kwa kawaida hupata mvua nyingi. Uoto wa misitu Maeneo yenye misitu hupata mvua nyingi kwani mawingu huweza kufanyika kwa urahisi.Misitu hiyo pia huifadhi unyevu usipotee ardhini kwa urahisi kwa njia ya mvukizo. Pepo Pepo za msimu za Kaskazini-mashariki Huleta Mvua kidogo katika eneo kubwa la kenya na kaskazini mwa Tanzania. Pepo huvuma sambamba na pwani.Pepo hizi pia huvuma kutoka sehemu kubwa ya nchi kavu katika nchi ya Ethiopia na Sudani kabla ya kufika eneo la Afrika Mashariki. Tanbihi Viungo vya Nje Nasa SOHO (Solar & Heliospheric Observatory) satellite National Solar Observatory Astronomy Cast: The Sun A collection of spectacular images of the Sun from various institutions (The Boston Globe) Satellite observations of solar luminosity Sun|Trek, an educational website about the Sun The Swedish 1-meter Solar Telescope, SST An animated explanation of the structure of the Sun (University of Glamorgan) Animation – The Future of the Sun Solar Conveyor Belt Speeds Up – NASA – images, link to report on Science NASA 5-year timelapse video of the Sun Sun in Ultra High Definition NASA 11 January 2015 Album of images and videos by Seán Doran, based on SDO imagery Nyota Mfumo wa jua
1774
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wachagga
Wachagga
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu (lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi) wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi yao ni watu 2,000,000. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara, kilimo na kazi za ofisini. Vikundi vya Wachagga Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame). Wachaga ni kama vile Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndiyo inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kufuatana na vijiji hivyo. Wengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha. Lugha ya Kichagga Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mlima Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo (ambacho nacho kinatofautiana kadiri unavyotoka eneo moja hadi jingine; mfano Kiseri, Kimashati, Kimkuu, Kimengwe, Kimahida), Kimachame, Kivunjo, Kimarangu, Kioldimoshi, Kingassa, Kiuru, Kikibosho, na Kisiha. Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makundi hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Kioldimoshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, hivyo lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo. Koo za Kichagga Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi au Moshi, Mmasy, Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena n.k. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo, Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Moshi, Kombe, Njau wanatoka Old Moshi na Vunjo. Majina mengine ya Old Moshi ni kama yafuatayo: Saria, Mmari, Macha, Machange, Mshiu, Kyara, Moshi, Massamu, Kimambo, Mboro, Mlngu, Saule, Tenga, Njau, Malisa, Maro, Maeda, Ringo,Olomi, Ngowi, Lyatuu na mengine mengi. Kavishe, Mrosso, Bongole, Mariki, Moshi, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Mushi, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Masue, Maleto, Mramba, Kauki, Kiwango na Kyauke wanatoka Rombo. Mchaki, Masawe, Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau, Saria, Mtei wanatoka Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba, Foya, Munishi, Kilawe, na kadhalika hutoka Kibosho. Ukoo wa akina Teri wako Mamba, Chami, Chuwa, Kiria Owoya na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha. Utawala wa jadi wa Wachagga Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Akina mangi walihodhi mashamba, ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa jadi. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Shangali (wa ukoo wa Mushi) kutoka Machame, Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho na Mangi Horombo wa Keni - waliojulikana kwa uhodari wao wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao, na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Mangi Meli alikuwa mangi wa Waoldmoshi ambaye alipigana na Wajerumani na aliishia kukatwa kichwa; mpaka sasa fuvu lake lipo Ujerumani, alizikwa kiwiliwili tu baada ya kunyongwa; mti aliyonyongewa upo mpaka sasa sehemu ya Oldmoshi bomani karibu na Kolila Sekondari. Alinyongwa kwa sababu alikataa kuwa kibaraka wa kutumika na Wajerumani. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hao wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hao pia wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao wamekaa kuhesabu mali zao. Hii ni desturi ya watawala, hasa wafalme kote ulimwenguni. Elimu kati ya Wachagga Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa katika uwanja wa elimu, hususani katika masomo ya sayansi na hisabati. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila namba moja lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa (elimu ya juu) na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa huo una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania. Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule. Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote. Ni vema pia kusema kuwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu. Ardhi Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula, pamoja na biashara nyingine. Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa mbalimbali. Kilimo na chakula Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu. Ndizi za Wachagga na upishi wa samaki Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika. Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea kinywaji maarufu kiitwacho mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi. Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au kinywaji kingine. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto. Wachagga na muhogo Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu. Ulaji kiti-moto Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe kwa ajili ya biashara kwani nyama ya nguruwe hupendwa sana na watu na huuzwa sana kwenye baa na hoteli mbalimbali mijini hasa katika jiji la Dar es Salaam. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwapendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani na Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wengi wao ni Waislamu, kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasio Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa". Maoni juu ya Wachagga Kipato cha Wachagga ni kikubwa kulingana na cha makabila mengine. Wanawake wa Kichagga (hasa kutoka Machame) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Mama wa Kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani, hivyo wanakuwa nyumbani na mayaya au peke yao. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za biashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Ingawa wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Kilimanjaro) kufuga ng'ombe na kufanya kazi za shambani. Kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongoni mwao. Pia baadhi ya kina mama wa Kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Ili kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri, tofauti na chakula walichoandaliwa watoto, japo ni chakula kilekile. Pia Wachagga wamekuwa na desturi ya kuwaenzi wazee wao waliotangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanaporudi nyumbani mwezi Desemba. Hilo limekuwa suala la kawaida sana. Wengi wao huwa wanarudi na magari, ndiyo sababu utaona ya kwamba kila mwaka ufikapo mwezi Desemba foleni za magari zimekuwa zikiongezeka katika mji wa Moshi kutokana na Wachagga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. Wengi wao wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi. Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Pia imekuwa kama desturi wanaukoo kukaa pamoja na kujadiliana mambo jinsi yalivyokwenda katika kipindi kizima cha mwaka na wakati mwingine inakuwa sehemu ya kwenda kuwatambulisha watoto kwa bibi na babu zao, hasa wale waliozaliwa mijini. Ni kipindi chenye shangwe na furaha sana: hakuna kaya utakayokuta haina furaha kwa sababu hata kama huna sherehe kuna mialiko mbalimbali ambao haihitaji kadi au michango. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wamepokea sana dini (imani) ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa mwaka mzima. Sababu kuu za Wachaga wengi kwenda kwao mwisho wa mwaka Kupumzika, hii ni baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima bila kwenda, biashara asubuhi, jioni mahesabu, kwao Desemba ni mwezi wa kutulia tu na familia ndugu na jamaa Kuchinja mbuzi, hapa kuna za matambiko na za kula na kufurahia tu. Matambiko hayo ni kushukuru wazee wao waliokufa mapema kwa baraka walizopata kwa kipindi chote cha mwaka mzima Sherehe mbalimbali: sherehe za wafu, maadhimisho ya ndoa mbalimbali, Krismasi, Ubatizo, Kipaimara, Komunyo, kutoa watoto jandoni na Mwaka mpya wenyewe. Kila inayoitwa sherehe hufanyika kipindi hiki, kuanzia tarehe 25 Desemba kufika tarehe 1 Januari ni shughuli tu, kula kunywa kusaza. Utambulisho mbalimbali kwa wazee, jamaa wa nyumbani kama vile mke, mchumba, mume, gari jipya, nyumba mpya, watoto n.k. Kukutana na watu mbalimbali ambao hamuonani baada ya kipindi hicho kama, marafiki, majirani, ndugu na jamaa. Hii ni kwa wale wanaofanya kazi mikoa tofauti (huyu Morogoro yule Mwanza mwingine katoka Dar es Salaam) Utekelezaji wa miradi mbalimbali hapo nyumbani kama ujenzi au ukarabati wa nyumba, njia pana za magari na kukagua mashamba n.k. Si wote wanakwenda kwa sababu hizo zote bali lazima sababu mojawapo ihusike. Kutokana na sababu hizo wanaokwenda ni watu wote wa dini zote. Ukienda tofauti na kipindi hiki huwezi kukuta watu wengi sana. Kwanza baada ya kipindi hicho kupita kila mtu anashughulika na mambo yake (kutafuta pesa). Kama umekwenda na huna chochote, utakumbana na ubaguzi na manyanyaso makubwa. Tanbihi Marejeo Viungo vya nje Historia ya Kilimanjaro Kisa: Kumuona Mchagga Mkoa wa Kilimanjaro Makabila ya Tanzania Wachagga
1775
https://sw.wikipedia.org/wiki/Djibril%20Diallo
Djibril Diallo
Dakta Djibril Diallo ni mzaliwa wa Senegal. Amewahi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa, mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mkutano wa kimataifa wa haki za binadamu. Tena alikuwa waziri nchini Mali. Hivi sasa anahudumia ofisi ya Umoja ya Mataifa inayojihusisha na miradi ya kuleta amani kwa kutumia michezo. Diallo pia ni msemaji wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wanasiasa wa Senegal Wanasiasa wa Mali Viongozi wa Afrika
1776
https://sw.wikipedia.org/wiki/Abedi%20Amani%20Karume
Abedi Amani Karume
Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi. Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964. Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amani Abeid Karume, ambaye ni mtoto wa Sheikh Karume, alikuwa rais wa Zanzibar tangu mwaka 2000 hadi 2010. Waliozaliwa 1905 Waliofariki 1972 Wanasiasa wa Tanzania
1777
https://sw.wikipedia.org/wiki/Orodha%20ya%20vyama%20vya%20siasa%20Tanzania
Orodha ya vyama vya siasa Tanzania
Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992. Chama tawala ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimetokana na muungano kati ya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shiraz Party (ASP) ya Zanzibar. Vyama vingine vya siasa Tanzania ni Civic United Front (CUF), Tanzania Labour Party (TLP), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), National Convention for Constitution and Reconstruction-Mageuzi (NCCR-Mageuzi), National League of Democracy (NLD), Democratic Party (DP), na Demokrasia Makini. Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Orodha kamili ya vyama vya siasa nchini Tanzania] Vyama Vyama
1778
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nelson%20Mandela
Nelson Mandela
Nelson Rolihlahla Mandela (18 Julai 1918 - 5 Desemba 2013) alikuwa mwanasiasa nchini Afrika Kusini, kiongozi wa mapambano dhidi ya siasa ya ubaguzi wa rangi (Apartheid), mfungwa jela kwa miaka 27 halafu rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi yake. Alikuwa mwanasheria na mwanachama, baadaye kiongozi wa chama cha ANC kilichopigania haki za binadamu wote nchini Afrika Kusini. Maisha Utoto na ukoo Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai 1918 katika familia ya kabila la Waxhosa kwenye kijiji cha Mvezo karibu na Umtata iliyokuwa kwenye Jimbo la Rasi. Alipewa jina la Rolihlahla linalomaanisha "anayevuta tawi la mti" kwa maana ya "mwenye kuleta matata" katika lugha ya Kixhosa. Baadaye alijulikana kwa jina la ukoo wake "Madiba". Jina la Nelson alilipokea kutoka kwa mwalimu wake siku alipoanza kwenda shule. Alitoka katika familia ya kifalme. Baba wa babu yake Ngubengcuka alikuwa mfalme wa Wathembu katika maeneo ya Transkei wa jimbo la kisasa la Rasi Mashariki la Afrika Kusini. Baba yake Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa chifu na mshauri wa mfalme tangu mwaka 1915 hadi 1926. Mama yake Nelson, Nosekeni Fanny, alikuwa mke wa tatu. Miaka ya kwanza aliishi kijijini alipojifunza mila na desturi za Waxhosa na kutunza mifugo pamoja na wavulana wengine. Baba aliaga dunia Nelson alipokuwa na umri wa miaka tisa. Alibatizwa katika Kanisa la Kimethodisti akawa Mkristo wa kanisa hilo hadi kifo chake. Baada ya kifo cha baba, mama alimpeleka kwa chifu mkuu wa Wathembu aliyemlea kama mtoto wake. Pamoja na wazazi wake wapya alihudhuria ibada za kanisani kila Jumapili zilizoimarisha imani yake ya Kikristo. Akaendelea kusoma katika shule ya Kimethodisti aliposoma Kiingereza, Kixhosa, historia na jiografia. Katika ikulu ya chifu alisikia masimulizi mengi kuhusu historia ya Waafrika kutoka wageni waliokuja kumwaona baba wa kambo. Elimu Mwaka 1925 babake alimtuma kusoma shule ndogo ya Kimethodisti alipofanyikiwa vema. Baada ya kifo cha baba aliishi kwa chifu wa Watembo na hapo kwene umri wa miaka 16 alishiriki katika sherehe ya jando alipotahiriwa na kupokea jina Dalibunga. Baadaye aliendelea kusoma kwenye shule ya sekondari ya „Clarkebury Boarding Institute“ huko Engcobo iliyokuwa shule ya bweni kubwa kwa ajili ya vijana kutoka Wathembo. Hapa alianza mazoezi ya michezo na kupenda kazi ya bustani aliyoendelea kwa maisha yote. Baada ya miaka miwili alipokea cheti kidogo cha elimu ya sekondari. Mwaka 1937 kwenye umri wa miaka 19 aliendelea kwenye chuo cha Wamethodisti huko [[Fort Beaufort. Hapo alikuwa mara ya kwanza rafiki na kijana nje ya kabila lake aliyekuwa Msotho akaathiriwa na mwalimu mpendwa Mxhosa aliyevunja mwiko kwa kumwoa mke kutoka kwa Wasotho Mandela alitumia muda mwingi huko Healdtown kwa kufuata michezo ya kukimbia na bondia. Tangu 1939 alianza masomo kwa shahada ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Fort Hare, chuo kwa ajili ya wanafunzi Waafrika katika jimbo la Rasi Mashariki. Masomo yake yalikuwa Kiingereza, anthropolojia, siasa na sheria. Wakati ule alitaka kuendelea kuwa mfasiri au afisa katika Idara ya Shughuli za Wazalendo (kitengo cha serikali ya Kizungu kwa maeneo ya Waafrika katika Afrika Kusini). Katika bweni lake alikuwa rafiki wa Kaiser Matanzima na Oliver Tambo aliyeendelea kuwa rafiki yake kwa miaka mingi ijayo. Pamoja na kupenda michezo Mandela alijifunza dansi ya Kizungu , alishiriki tamthiliya kuhusu about Abraham Lincoln, akatoa darasa la Biblia katika kanisa. Harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano au sera ya amani baina yake na watu weupe nchini Afrika Kusini, jambo ambalo watu wengi hawakulitegemea. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani ambayo ni tuzo ya nadra kutolewa duniani. Baada ya kutengana na mke wake, Winnie Madikizela, alimuoa Graca Machel aliyewahi kuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel. Marejeo Kujisomea Waliozaliwa 1918 Waliofariki 2013 Wanaharakati wa Afrika Kusini Marais wa Afrika Kusini Viongozi wa Afrika Tuzo ya Nobel ya Amani Nelson Mandela
1781
https://sw.wikipedia.org/wiki/Rosa%20Parks
Rosa Parks
Rosa Louise McCauley Parks (4 Februari 1913 – 24 Oktoba 2005) anakumbukwa kwa uamuzi wake wa kukataa kumpisha kiti Mmarekani Mweupe kama alivyodaiwa na dereva wa basi. Uamuzi wake huo hapo mwaka 1955 ulipelekea mzozo uliosababisha Mgomo wa Mabasi wa Montgomery na kuchangia katika Vuguvugu la Haki za Kiraia Marekani. Baada ya kitendo chake cha kukataa kumpa mtu mweupe kiti ndani ya basi na Mgomo wa Montgomery uliodumu kwa mwaka, Mahakama ya Marekani ilitamka kuwa sheria za ubaguzi ndani ya mabasi huko Alabama na Montgomery zilikiuka katiba. Viungo vya nje Makumbusho na Maktaba ya Rosa Parks Taasisi ya Maendeleo Binafsi ya Rosa Raymond Parks Picha na mahojian ya Rosa Parks Waliozaliwa 1913 Waliofariki 2005 Wanaharakati wa Marekani Wamarekani Weusi Wanawake wa Marekani
1782
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kwame%20Nkrumah
Kwame Nkrumah
Kwame Nkrumah (21 Septemba 1909 - 27 Aprili 1972) alikuwa Rais wa kwanza wa Ghana na mmoja wa viongozi wenye nia ya kujenga Muungano wa Afrika, tena mchochezi wa falsafa ya Umajinuni. Maisha Miaka ya kwanza katika Ghana Kwame Nkrumah alizaliwa mnamo mwaka 1909 katika kijiji cha Nkroful kwenye koloni la Gold Coast (leo Ghana). Nkrumah mwenyewe aliandika ya kwamba tarehe ilikuwa 18 Septemba 1909 iliyokuwa siku ya Jumamosi. Hii inalingana na jina "Kwame" ambalo katika utamaduni wa Waakan ni jina la mwanamume aliyezaliwa siku hiyo. Ila tu aliposoma Marekani alijulikana kwa jina la Francis Nwia Kofi Nkrumah na "Kofi" ni jina la mwanamume aliyezaliwa siku ya Ijumaa. Baba yake, ambaye jina lake halikuhifadhiwa, alikuwa na kazi ya fundi dhahabu. Mama yake aliitwa Nyanibah akaishi hadi kifo chake na kwa muda alitunza kaburi la mwanawe. . Mtoto alilelewa kijijini pamoja na watoto wengine wa babake na ukoo. Mama alimsomesha katika shule ya msingi ya misioni ya Kanisa Katoliki. . Alipita madarasa kumi katika muda wa miaka minane. Mnamo 1925 alikuwa Mkristo aliyebatizwa akafundisha katika shule yake kama mwalimu msaidizi. Kutoka hapo alikaribishwa na mchungaji Alec Garden Fraser, mkuu wa chuo cha ualimu cha serikali mjini Accra kujiunga na masomo huko. Huko makamu wa mkuu Kwegyir Aggrey aliyewahi kusoma Marekani alimweleza mafundisho ya Marcus Garvey na W. E. B. Du Bois. Aggrey, Fraser na walimu wengine wa chuo walifundisha ya kwamba ushirikiano wa watu wa rangi zote ni shabaha kwa maendeleo ya Gold Coast. Lakini Nkrumah alifuata mwelekeo wa Marcus Garvey akiamini ya kwamba ni lazima nchi yake itawaliwe na Waafrika wenyewe. Baada ya kumaliza masomo yake mwaka 1930 Nkrumah aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi ya Kikatoliki huko Elmina na baada ya mwaka 1 alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya Axim. Huko alianza kushiriki katika majadiliano ya kisiasa akaanzisha "Nzima Literary Society". Mwaka 1933 aliendelea na kuwa mwalimu kwenye seminari ya Kikatoliki mjini Amissa. Marekani Alipokuwa mwanafunzi wa chuo Nkrumah alisikia hotuba ya mwandishi Nnamdi Azikiwe (baadaye alikuwa rais wa Nigeria). Alikutana naye, na Azikiwe alimpa ushauri kuendelea na masomo yake huko Marekani kwenye chuo cha Lincoln College alikowahi kusoma mwenyewe an kilichokuwa chuo kwa Waamerika Weusi. Nkrumah angependelea kusoma London (Uingereza) lakini alishindwa mitihani ya kuingia. Hivyo kwa msaada wa mjomba tajiri alisafiri Pennsylvania na kuanza masomo huko Lincoln kwenye Oktoba 1935.. Hakuwa na pesa nyingi, hivyo alifanya kazi ndogo kama kusafisha vyombo hotelini. Siku za Jumapili alisali katika makanisa ya Weusi mjini Philadelphia na New York. Mwaka 1939 alimaliza masomo akapokea digrii ya bachelor katika fani ya uchumi. Chuo kikampa nafasi ya mhadhiri msaidizi kwa masomo ya falsafa akaendelea kusoma teolojia akachukua BA mwaka 1942. Alisoma pia Chuo Kikuu cha Pennsylvania alipomaliza digrii za master katika falsafa na ualimu.. Wakati huohuo alishirikiana na mwanaisimu William Everett Welmers kutunga kitabu cha sarufi ya Fante iliyokuwa lugha yake ya kwanza. Wakati wa likizo Nkrumah alipenda kwenda Harlem (New York) iliyokuwa kitovu cha kiutamaduni kwa Waamerika Weusi. Hapa alienda kuzunguka mitaani na kusikiliza wahubiri wa barabarani. Chuoni Nkrumah alikusanya wanafunzi kutoka nchi za Afrika na kuanzisha "African Students Association of America and Canada" akichaguliwa kuwa mwenyekiti wake. Katika majadiliano ya kundi hili alisisitiza haja ya nchi zote za Afrika kushikamana baada ya uhuru, si kufuata shabaha za pekee kwa kila koloni. Nkrumah alishiriki pia katika Mkutano wa Umoja wa Afrika mjini New York wa mwaka 1944 uliosisitiza Marekani kusaidia nchi za Afrika kufikia uhuru baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Katika kipindi chake nchini Marekani Nkrumah alikutana pia na wafuasi wa Umarx, hasa wa mwelekeo wa Trotzki. Hasa C.L.R. James kutoka Trinidad alikuwa na athira juu yake. Nkrumah aliandika baadaye ni Johnson aliyemfundisha namna gani kufanya kazi ya kisasa kwa siri kama ni lazima.. Wakati Nkrumah alitaka kurudi Afrika baada ya vita kwenye mwaka 1945, James alitunga barua ya kumtambulisha kwa marafiki huko London akiandika: "Huyu kijana anakuja sasa kwenu. Si mtu mwelekevu mno, lakini fanyeni mnachoweza kumsaidia; anataka kuwafukuza Wazungu kutoka Afrika". London Nkrumah alfika London mwezi wa Mei 1945 akajiandikisha kwenye chuo cha London School of Economics kama mwanafunzi wa PhD katika anthropolojia. Aliacha baada ya mhula mmoja, akajiandikisha kwenye chuo kikuu kwa shabaha ya kufuata PhD ya falsafa lakini hakuendelea. Mwishoni alijaribu masomo ya sheria. Profesa wa falsafa Alfred Ayer hakumwona Nkrumah kuwa mwanafalsafa bora. Alisema juu yake: "Nilimpenda nikafurahi kujadili naye. Lakini kwangu hakuonekana kuwa na akili ya mchambuzi. Alitafuta majibu ya harakaharaka. Labda sehemu ya matatizo yake ilikuwa ya kwamba hajajikazia kuendeleza thesis yake. Kwake ilikuwa njia tu ya kupita muda hadi aliweza kurudi Ghana" Nkrumah alitumia nguvu nyingi kupanga mikutano ya siasa. Alikuwa kati ya waratibu walioandaa mkutano wa Pan-African Congress mjini Manchester (15-19 Oktoba 1945). Wajumbe wa mkutano huu walipatana kuelekea kwa Shirikisho la Maungano ya Madola ya Afrika na kujenga utamaduni mpya kwa Afrika bila ukabila na siasa itakayounganisha usoshalisti au ukomunisti na demokrasia. Kati ya wajumbe waliohudhuria walikuwa mzee W.E.B. Dubois pamoja na Waafrika walioendelea kuwa viongozi wa nchi zao baada ya uhuru kama vile Hastings Banda wa Nyasaland (Malawi), Jomo Kenyatta wa Kenya, Obafemi Awolowo wa Nigeria na C.L. R. James. Kurudi Ghana Baada ya kurusi Gold Coast, Nkrumah kwenye mwaka 1947 alikuwa katibu mkuu wa chama cha United Gold Coast Convention (UGCC). Mwaka 1948 kulitokea ghasia ya "Accra Riots"; askari Waafrika wa jeshi la Kiingereza walioachishwa baada ya vita kuu walidai malipo waliyoahidiwa. Nkrumah alihutubia mkutano wao; baada ya maandamano yao kuvunjwa na polisi na watu kufa katika ghasia iliyofuata, polisi ilikamata viongozi wa chama cha UGCC. Mwaka 1949 Nrumah alitoka katika UGCC akaunda Convention People’s Party (CPP) iliyokuwa na madai makali zaidi. Mwaka 1951 CPP ilipata kura nyingi katika uchaguzi baada ya kudai uhuru mara moja. Nkrumah aliyekuwa tena mbaroni aliruhusiwa kugombea, alipata asilimia 98,5 za kura mjini Accra akaachwa huru. Mwaka 1952 alichaguliwa na Halmashauri ya Kisheria kuwa waziri mkuu wa koloni. Aliendelea kuongoza serikali na mwaka 1957 wakati wa uhuru alibadilisha jina la nchi kuwa Ghana. Hii ilikuwa koloni la kwanza kupata uhuru katika Afrika ya Magharibi, baada ya Liberia. Mwaka huohuo alifunga ndoa na Fathia Helen Ritzk, Mkristo wa Kikopti kutoka nchi ya Misri. Baada ya uhuru Nkrumah alianzisha mipango mingi ya kuendeleza Ghana kiutamaduni, kielimu na kiuchumi. Pamoja na Haile Selassie wa Ethiopia aliunda Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU). Alikaribia nchi za kikomunisti na kuajiri washauri na wahandisi kutoka Urusi na China. Alijipatia maadui kati ya machifu waliokuwa na mamlaka kubwa wakati wa ukoloni lakini sasa wengi waliachishwa au kupinduliwa na serikali kama hawakufuata maagizo yote kutoka juu. Alipata pia maadui kati ya wakulima tajiri wa kakao kwa sababu aliongeza sana kodi wakati bei ya zao hili kwenye soko la dunia ilipanda juu. Mnamo mwaka 1960 bei za kakao zilishuka sana na hapo alikosa pesa kwa miradi mingi aliyoanzisha wakati mapato ya kakao yalikuwa juu. Gharama za miradi kubwa zililipiwa kwa kukopa pesa nje ya nchi. Deni la taifa lilikua haraka. Baada ya bidhaa kadhaa kuwa haba, serikali ilijaribu kuongoza uchumi kwa mfano wa nchi za kikomunisti. Upinzani kati ya wananchi ulitazamwa kama uasi na watu wengi walikamatwa. Kodi zilipandishwa. Inasemekana ya kwamba pia huduma za siri za CIA (Marekani) na MI5 (Uingereza) zilichochea wapinzani wa Nkrumah waliopanga kumpindua. Mwaka 1966 alipokwenda safari ya kutembelea China na Korea ya Kaskazini kamati ya siri ya upinzani pamoja na jeshi la ulinzi na polisi ya kitaifa ilipindua serikali. Nkrumah alishindwa kurudi. Kwa miaka kadhaa alikaa Guinea. Baada ya kugonjeka alihamia kwa tiba huko Romania alipoaga dunia mwaka 1972. Vitabu vilivyoandikwa na Kwame Nkrumah "Negro History: European Government in Africa", The Lincolnian, 12 April 1938, p. 2 (Lincoln University, Pennsylvania) - see Special Collections and Archives, Lincoln University Ghana: The Autobiography of Kwame Nkrumah (1957). ISBN 0-901787-60-4 Africa Must Unite (1963). ISBN 0-901787-13-2 African Personality (1963) Neo-Colonialism: the Last Stage of Imperialism (1965). ISBN 0-901787-23-X "The essence of neo-colonialism is that the State which is subject to it is, in theory, independent and has all the outward trappings of international sovereignty. In reality its economic system and thus its political policy is directed from outside." (Introduction) Axioms of Kwame Nkrumah (1967). ISBN 0-901787-54-X African Socialism Revisited (1967) Voice From Conakry (1967). ISBN 90-17-87027-3 Dark Days in Ghana (1968). ISBN 0-7178-0046-6 Handbook of Revolutionary Warfare (1968) - first introduction of Pan-African pellet compass. ISBN 0-7178-0226-4 Consciencism: Philosophy and Ideology for De-Colonisation (1970). ISBN 0-901787-11-6 Class Struggle in Africa (1970). ISBN 0-901787-12-4 The Struggle Continues (1973). ISBN 0-901787-41-8 I Speak of Freedom (1973). ISBN 0-901787-14-0 Revolutionary Path (1973). ISBN 0-901787-22-1 Marejeo Soma pia Defense Intelligence Agency, "Supplement, Kwame Nkrumah, President of Ghana", 12-January-1966. Viungo vya nje Kwame Nkrumah Mausoleum and Museum at Nkroful, Western Region Kwame Nkrumah Memorial Park & Museum, Accra Ghana-pedia Dr. Kwame Nkrumah Ghana-pedia Operation Cold Chop: The Fall Of Kwame Nkrumah Dr Kwame Nkrumah Excerpt from Commanding Heights by Daniel Yergin and Joseph Stanislaw Timeline of events related to the overthrow of Kwame Nkrumah The Kwame Nkrumah Lectures at the University of Cape Coast, Ghana, 2007 Kwame Nkrumah Information and Resource Site Ghana re-evaluates Nkrumah by The Global Post Dr Kwame Nkrumah's Midnight Speech on the day of Ghana's independence – 6 March 1957. Waliozaliwa 1909 Waliofariki 1972 Viongozi wa Afrika Marais wa Ghana Historia ya Ghana
1783
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ghana
Ghana
Jamhuri ya Ghana ni nchi ya Afrika Magharibi inayopakana na Côte d'Ivoire (Ivory Coast) upande wa magharibi, Burkina Faso upande wa kaskazini, Togo upande wa mashariki, na Ghuba ya Guinea upande wa kusini. Kabla ya ukoloni Ghana ilikaliwa na idadi ya watu wa kale, hasa wa Falme za Akan, wakiwemo Waakwamu upande wa mashariki, Ufalme wa Ashanti ya bara na falme kadha wa kadha za Kifante, pia falme zisizo za Kiakan kama Waga na Waewe waliokuwa pwani na bara. Biashara na nchi za Ulaya ilistawi baada ya kukutana kwao na Wareno katika karne ya 15, na Waingereza walianzisha nchi ya Gold Coast, chini ya himaya ya Uingereza mwaka wa 1874. Nchi ya Gold Coast ilijinyakulia uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1957, ikawa taifa la kwanza la Afrika Kusini mwa Sahara (Sub-Saharan Africa) kufanya hivyo Ghana ni mwanachama wa mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Mataifa. Ghana ni nchi ya pili baina ya nchi zinazozalisha mmea wa kakao ulimwenguni kote, pia ni kiambo cha Ziwa Volta, ambalo ndilo ziwa kubwa zaidi ulimwenguni kuundwa na binadamu. Vilevile, Ghana ni nchi inayojulikana sana katika ulimwengu wa soka. Tarehe 16 Oktoba 2009, Ghana lilikuwa taifa la kwanza la Kiafrika kushinda Kombe la Dunia la FIFA kwa walio chini ya umri wa miaka 20 (FIFA U-20 World Cup) kwa kushinda nchi ya Brazil kwa mabao 4 kwa 3 kupitia mikwaju ya penalti. Asili ya jina Neno Ghana lina maana ya "Shujaa Mfalme", na lilikuwa jina la heshima walilopewa wafalme wa Himaya ya Ghana nyakati za kale za Afrika Magharibi.. Limekuwa chimbuko la jina “Guinea” (kupitia kwa Kifaransa Guinoye), ambalo limetumika kurejelea pwani ya Afrika Magharibi (na ambalo linatumika katika Ghuba ya Guinea). Jina hilo lilichaguliwa kwa taifa jipya ili kuashiria himaya ya kale ya Ghana, ambayo kwa wakati mmoja ilienea katika sehemu kubwa ya Afrika Magharibi, ingawa kijiografia, Himaya ya Ghana inakadiriwa ilikuwa kilomita 800 kaskazini na magharibi mwa Ghana ya kisasa, na ilitawala majimbo katika eneo la Mto Sénégal na mashariki kuelekea Mto wa Niger, katika maeneo ya sasa ya Senegal, Mauritania na Mali. Ghana lilichaguliwa kuwa jina rasmi la nchi ya Gold Coast nchi hii iliponyakua uhuru mnamo tarehe 6 Machi 1957; hata hivyo, Ghana haikuweza kutangaza uhuru wake kamili kutoka kwa Uingereza hadi tarehe 1 Julai 1960 ambapo nchi ilianza kujulikana kama Jamhuri ya Ghana. Jiografia Nchi hii ina eneo la kilomita mraba 238,500 (maili mraba 92,085). Eneo hili limezungukwa na Togo kwa upande wa mashariki, Cote d’Ivoire upande wa magharibi, Burkina Faso upande wa kaskazini na Ghuba ya Guinea (Bahari ya Atlantiki) upande wa kusini. Ghana ni nchi ambayo inapatikana katika Ghuba ya Guinea, nyuzi chache kaskazini mwa Ikweta, jambo ambalo linaipa nchi hii hali ya joto. Vilevile mstari wa Greenwich Meridian hupita ndani ya Ghana, katika jiji la viwanda la Tema. Hivyo kijiografia Ghana iko karibu zaidi ya sehemu ya “katikati” mwa ulimwengu kuliko nchi yoyote ile, ingawa sehemu halisi ya katikati, (0°, 0°) inapatikana katika Ghuba ya Guinea, katika Bahari ya Atlantiki, kwa makadirio kilomita 614 (maili 382) kusini mwa Accra, Ghana. Nchi hii ina maeneo tambarare, vilima vya chini na mito michache. Nchi ya Ghana inaweza kugawanywa katika maeneo matano tofauti ya kijiografia. Eneo la pwani ni sehemu ambayo ni ya chini na iliyo na ufuo wa mchanga huku ikipakana na koko na kukingamana na mito na vijito kadha wa kadha huku sehemu ya kaskazini ikiwa na maeneo ya juu yaliyo tambarare. Eneo la kusini magharibi na kusini ya kati mwa Ghana ni sehemu iliyoinuka sawa na pana yenye misitu ikiwa na vilima vya Ashanti na eneo sawa na pana (plateau) la Kwahu na safu ya vilima vya Akuapim-Togo vinapatikana kwenye mpaka wa mashariki mwa nchi. Bonde la Volta linachukua eneo la kati mwa Ghana. Sehemu ya juu zaidi nchini Ghana ni Mlima Afadjato ulio na urefu wa mita 855 (futi 2,904) na unaopatikana kwenye safu ya vilima vya Akwapim-Togo. Hali ya hewa ni ya hari. Kanda ya pwani ya mashariki ni ya joto na iliyokauka (angalia Dahomey Gap); pembe ya kusini magharibi, huwa na joto jingi na unyevu hewani; huku sehemu ya kaskazini ikiwa yenye joto jingi na iliyokauka. Ziwa Volta, ziwa lisilo la asili kubwa zaidi ulimwenguni, linaenea kupitia katika mafungu makubwa mashariki mwa Ghana na ndicho chanzo kikuu cha vijito vingi kama vile vya Oti na Afram. Kuna misimu miwili mikuu nchini Ghana, masika na kiangazi. Kaskazini mwa Ghana huwa na msimu wa masika kutoka Machi hadi Novemba huku sehemu ya kusini, ukiwemo mji mkuu wa Accra, ikiwa na masika kutoka Aprili hadi Novemba katikati. Kusini mwa Ghana kuna misitu ambayo daima ni ya kijani kibichi na ile ambayo hupoteza majani yake wakati fulani wa mwaka ikiwa na miti kama mikangazi, odumu na mipingo. Sehemu hii inayo pia mingi ya mitende ya mafuta na mikoko. Miti ya Shea, mibuyu na mikakaya hupatikana kwa kawaida katika maeneo ya Volta na kaskazini mwa nchi. Maeneo kiutawala Ghana imegawiwa katika mikoa 16, ambayo yamegawiwa zaidi katika wilaya 275, kila moja ikiwa na Bunge la Wilaya (District Assembly). Chini ya wilaya kuna aina kadhaa za mabaraza, yakiwemo mabaraza 58 ya miji au maeneo, mabaraza 108 ya kanda na mabaraza 626 ya maeneo. Kamati za vitengo 16,000 huwa katika daraja ya chini zaidi. Mikoa hiyo 16 ni: Idadi ya wakazi katika majiji makubwa Historia Historia ya kale Kuna ushahidi kutoka kwa maarifa ya mambo ya kale ambao unaonyesha kwamba watu wameishi katika eneo linalojulikana siku hizi kama Ghana kutoka karibu miaka ya 1500 KK (Kabla ya Kristo). Licha ya hayo, hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa wakazi hao wana uhusiano na wale wa eneo hili kwa sasa. Kwa mujibu wa mapokeo simulizi, mengi kati ya makabila ya Ghana, leo kama vile watu wa chimbuko la makabila kadhaa kama Waakan, Waga na Waewe, walifika Ghana mnamo karne ya 13. Mengi ya maeneo ya Ghana yanajumuisha eneo lililokuwa la Himaya ya Ashanti, mojawapo ya falme zilizokuwa na ushawishi mkubwa katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara kabla ya enzi za ukoloni. Wahamiaji Waakan walihama kuelekea kusini na kuanzisha mataifa kadhaa, likiwemo lile la kwanza la himaya kuu ya Akan ya Wabono, ambayo kwa sasa inajulikana kama eneo la Brong Ahafo nchini Ghana. Sehemu kubwa ya eneo la sasa la kusini na kati mwa Ghana ilikuwa imeungana chini ya Himaya ya Ashanti ya Waashanti, tawi la Waakan wa karne ya 16. Utawala wa Waashanti ilihudumu mwanzoni kama mtandao mlegevu kabla ya kuwa ufalme ulioungana huku ukiwa na urasimu ulioendelea na wenye uchanganuzi mkubwa uliokuwa na makao yake Kumasi. Inasemekana kuwa katika kilele chake, Waasantehene wangeweza kutuma askari 500,000 vitani na kuwa na ushawishi wa kijeshi wa kiwango fulani juu ya majirani wake wote. Thuluthi moja ya Waashanti wote walikuwa watumwa. Waga walianzisha muungano wenye ufanisi mnamo 1500 na Wagonja, Wadagomba na Wamamprusi, pia walipigania uwezo wa kisiasa katika miaka ya 1620. Mwanzo wa ukoloni Mawasiliano ya awali na Ulaya kutoka kwa Wareno, walioingia Ghana mnamo 1419, yalizingatia upatikanaji wa dhahabu. Wareno walitua kwanza katika jiji la pwani lililokuwa makazi ya ufalme wa Wafante na kuliita eneo hili Elmina, jina ambalo linamaanisha “mgodi” kwa Kireno. Mwaka wa 1481, Mfalme John II wa Ureno aliagiza Diogo de Azambuja kujenga Kasri ya Elmina, ambayo ilikamilishwa mwaka uliofuata. Lengo lao lilikuwa kufanya ubadilishanaji wa dhahabu, pembe za ndovu na watumwa, ili kuimarisha mamlaka yao yaliyokuwa yanakua kwa kasi katika eneo hilo. Kufikia mwaka wa 1598 Waholanzi walikuwa wameungana nao, na kujenga ngome katika maeneo ya Komenda na Kormantsi. Mwaka wa 1637, waliiteka Kasri ya Elmina kutoka kwa Wareno na vilevile Axim mwaka wa 1642 (Ngome ya Mtakatifu Antoni). Wafanyabiashara wengine kutoka Ulaya walijiunga nao kufikia miaka ya kati ya karne ya 17, hasa Waingereza, Wadenmarki na Waswidi. Wafanyabiashara Waingereza, waliovutiwa na rasilimali katika eneo hilo, waliliita Gold Coast, (Pwani ya Dhahabu), huku nao wafanyabiashara Wafaransa, wakivutiwa na mapambo waliyokuwa wakivaa watu wa pwani, wakiliita eneo la sehemu ya magharibi “Côte d'Ivoire", au Ivory Coast (pwani ya pembe za ndovu). Zaidi ya ngome na kasri thelathini zilijengwa na wafanyabiashara Wareno, Waholanzi, Waingereza na Wadenmarki. Eneo la Gold Coast lilijulikana kwa karne nyingi kama ‘Kaburi la Mtu Mweupe’ kwa sababu wengi kati ya Wazungu walioenda huko kutoka Ulaya walikufa kutokana na malaria na magonjwa mengine ya eneo la hari. Baada ya Waholanzi kuondoka mwaka wa 1874, Uingereza iliiweka Gold Coast chini ya himaya yake. Kufuatia ushindi wa Uingereza mwaka wa 1896, hadi unyakuzi wa uhuru mnamo Machi 1957, eneo la Ghana ya sasa ghairi ya sehemu ya Volta Region (British Togoland), lilikuwa likijulikana kama Gold Coast. Vita vingi vilitokea baina ya utawala wa kikoloni na baadhi ya mataifa ya eneo hilo vikiwemo Vita vya 1806 vya Ashanti-Fante na mapambano ya kudumu ya Waashanti dhidi ya Waingereza, ambayo yalikoma baada ya Vita vya Tatu baina ya Waashanti na Waingereza (the third Ashanti-British War) (1900-1901).. ] Hata chini ya utawala wa kikoloni machifu na watu wao walipinga mara kwa mara sera za Waingereza; hata hivyo, ushawishi wa kupinga ukoloni ulikolea baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Mwaka wa 1947 chama kipya cha United Gold Coast Convention (UGCC) kilitoa wito wa “utawala wa kujitegemea katika wakati mfupi iwezekanavyo.” Kuelekea uhuru Baada ya kuongezeka kwa maandamano mnamo 1948, wanachama wa chama cha United Gold Coast Convention walikamatwa, akiwemo Waziri Mkuu na Rais wa baadaye, Kwame Nkrumah. Baadaye, Nkrumah aliunda chama chake mwenyewe, the Convention People's Party (CPP) ambacho kiliongozwa na usemi ‘serikali ya kujitegemea sasa’ (self government now). Alianzisha kampeni ya ‘Vitendo Chanya’ na kupata ufuasi wa watu wa sehemu za mashambani na wa daraja la wafanyakazi. Kwa mara nyingine Nkrumah alishikwa na kuzuiliwa kwa kuwa msimamizi wa chama ambacho kilisababisha ususiaji, migomo na vitendo vingine vya uasi wa raia. Hata hivyo, baada ya kushinda wingi wa viti katika Bunge ya Kuunda Sheria mnamo 1952, Kwame Nkrumah aliachiliwa na kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa Masuala ya Serikali. Baada ya uhuru Baada ya mazungumzo na Uingereza, hatimaye tarehe 6 Machi 1957 saa sita usiku, Kwame Nkrumah alitangaza Ghana kuwa “huru milele”. Bendera iliyokuwa na rangi nyekundu, dhahabu, kijani kibichi na nyota nyeusi ilikuwa bendera mpya mnamo 1957. Bendera hiyo iliundwa na Theodosia Salome Okoh, na rangi nyekundu inawakilisha damu iliyomwagwa ili kupata uhuru, rangi ya dhahabu inawakilisha ukwasi wa madini wa Ghana, ile ya kijani kibichi inaashiria utajiri wa kilimo na ile nyeusi ni ishara ya Uhuru wa Waafrika. Huku ikiundwa kutoka kwa muungano wa maeneo ya Gold Coast na British Togoland kufuatia matokeo ya kura ya maoni ya watu yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa mnamo 1956, Ghana ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika Kusini mwa Sahara kunyakua uhuru mnamo 1957. Kwame Nkrumah, Waziri Mkuu wa kwanza na baadaye Rais wa nchi ya sasa ya Ghana, hakuwa tu kiongozi wa Kiafrika wa kupigana dhidi ya ukoloni ila alikuwa pia mtu aliyekuwa na ndoto ya muungano wa Afrika ambayo haingejipata katika ukoloni mamboleo. Alikuwa kiongozi wa serikali ya kwanza Afrika kukuza Muungano wa Waafrika (Pan-Africanism), wazo ambalo alilipata wakati wa masomo yake katika Chuo Kikuu Cha Lincoln lililoko Pennsylvania (Marekani), wakati ambapo Marcus Garvey alikuwa anapata umaarufu kwa harakati zake za “Back to Africa Movement." Aliunganisha ndoto za Macus Garvey na zile za mwanachuo mashuhuri Mmarekani Mweusi W.E.B. Du Bois ili kuandaa Ghana kisasa. Kanuni za Ghana za uhuru na haki, usawa na elimu ya bure kwa wote, bila kujali kabila, dini au mila, zinatokana na utekelezaji wa wazo la Pan-Africanism. Ingawa lengo lake la muungano wa Afrika halikuwahi kuafikiwa, Osagyefo Dr. Kwame Nkrumah, kama ajulikanavyo sasa, alishiriki kwa kiwango kikubwa katika kuzinduliwa kwa Shirika la Umoja wa Afrika, ambalo lilifuatwa mnamo 2002 na Umoja wa Afrika (African Union). Ingawa Nkrumah aliheshimika sana ng’ambo, hakuwa akipendwa katika masuala ya ndani ya nchi. Hakufeli tu kuanzisha uchumi wa viwanda, ila hata sera zake hukusu uchumi ziliishia kuifanya nchi ya Ghana kuwa maskini kuliko ilivyokuwa wakati wa kupata uhuru. Mafanikio yake yalikuwa kutambuliwa na raia wa Ghana wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa Centenary wake na siku aliliweka kama likizo umma nchini Ghana. Hatimaye Nkrumah aliondolewa madarakani na jeshi alipokuwa ng’ambo mnamo Februari 1966, na mabadiliko hayo yalikaribishwa na wengi wa wakazi wa Ghana. Inaaminika na wengi wa wachanganuzi wa masuala ya kisiasa kwamba shirika la Marekani la Central Intelligence Agency (CIA) lilihusika na mapinduzi hayo, lakini wazo hilo halijawahi kuthibitishwa. Mfululizo wa baadaye wa mapinduzi kati ya 1966 na 1981 uliishia kwa kuingia madarakani kwa Liuteni wa Jeshi la Wanahewa (Flight Lieutenant) Jerry Rawlings mwaka wa 1981. Mabadiliko hayo yalisababisha kusimamishwa kwa katiba ya nchi mnamo 1981 na kupigwa marufuku kwa vyama vya kisiasa. Uchumi ulishuka sana punde baadaye, na Waghana wengi walihamia nchi zingine. Ingawa wengi wa Waghana waliohama walienda Nigeria, serikali ya Nigeria iliwarudisha Ghana karibu Waghana milioni moja mwaka wa 1983. Punde baadaye, Rawlings aliafikiana na shirika la International Monetary Fund juu ya mkataba wa mpango wa maendeleo (structural development plan) na kubadili sera nyingi za awali za uchumi na hivyo uchumi ukaanza kukua. Katiba mpya iliyorudisha mfumo wa siasa za vyama vingi ilitangazwa mwaka wa 1992, na Rawlings alichaguliwa kuwa Rais na tena mwaka wa 1996. Katiba ya mwaka wa 1992 ilimzuia kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu, kwa hivyo chama chake, National Democratic Congress, kilimchagua Makamu wake wa Rais, John Atta Mills, kuwania urais dhidi ya vyama vya upinzani. Huku akishinda uchaguzi wa mwaka 2000, John Kufuor wa chama pinzani cha New Patriotic aliapishwa kama Rais mnamo Januari 2001, na kumshinda tena Mills mwaka wa 2004; hivyo kuhudumia kama Rais kwa mihula miwili. Mwaka wa 2009, John Atta Mills alichukua mamlaka huku kukiwa na tofauti ndogo sana ya kura 40,000 ambazo ni 0.46% kati ya chama chake, National Democratic Congress, na kile cha New Patriotic Party, tukio hili likiwa la pili la ubadilishanaji wa mamlaka kutoka kwa kiongozi mmoja aliyechaguliwa kihalali kwa mwingine, na hivyo kuimarisha hadhi ya Ghana kama demokrasia iliyo imara. Serikali na siasa Kwa mujibu wa Fahirisi ya Mataifa Yaliyoanguka (Failed States Index), Ghana inaorodheshwa katika nambari ya 53 baina ya mataifa ambayo hayajaanguka huku likiorodheshwa kwa nafasi ya pili baina ya mataifa ya Afrika baada ya Mauritius. Taifa la Ghana liliorodheshwa katika nafasi ya 124 baina ya nchi 177 katika fahirisi hii na liliainishwa kama taifa la wastani. Vilevile, nchi ya Ghana imo katika nafasi ya 7 baina ya nchi 48 za Afrika zilizo Kusini mwa Sahara katika fahirisi ya mwaka wa 2008 ya Ibrahim Index of African Governance ambayo ilitokana na hakiki za mwaka wa 2006. Fahirisi ya Ibrahim ni kipimo chenye uchanganuzi mwingi kuhusu maswala ya utawala barani Afrika, kinachotokana na maswala ya mabadiliko tofautitofauti ambayo huashiria kufuzu kwa serikali wakati wa kutoa huduma muhimu za kisiasa kwa wananchi wao. Serikali Taifa la Ghana lilianzishwa kama demokrasia ya bunge wakati wa kupata uhuru mnamo mwaka wa 1957, ikifuatiwa na ubadilishanaji wa serikali za kijeshi na za kiraia. Mnamo Januari 1993, serikali ya kijeshi iliondoka na kuipisha Jamhuri ya Nne baada ya uchaguzi wa urais na ubunge mnamo mwisho wa mwaka wa 1992. Katiba ya 1992 inagawa mamlaka kati ya Rais, Bunge, Baraza la Mawaziri, Baraza la Taifa na mahakama huru. Serikali huchaguliwa na upigaji kura wa haki kwa wote; ingawa bunge halina uwiano kabisa kwani wilaya zilizo na watu wachache hupata wawakilishi wengi kwa kila mtu zikilinganishwa na wilaya ambazo zina idadi ya juu ya wakazi. Mfumo wa Mahakama Mfumo wa kisheria unatokana na ule wa Uingereza yaani British common law, sheria za kimila (kitamaduni), na katiba ya mwaka wa 1992. Daraja za mahakama hujumuisha Mahakama Kuu ya Ghana (mahakama ya juu zaidi), Mahakama za Rufaa na Mahakama Kuu za Kisheria. Chini ya mahakama hizi kuna mahakama za kuzunguka, mahakama za hakimu, na mahakama za kitamaduni. Taasisi zingine zisizo chini ya sheria ni pamoja na mahakama za umma. Tangu unyakuzi wa uhuru, mahakama zimekuwa huru kwa kiwango fulani; uhuru huu unaendelea chini ya Jamhuri ya Nne. Mahakama za chini zinadhahirishwa na kupangwa upya chini ya utawala wa Jamhuri ya Nne. Siasa Vyama vya kisiasa vilihalalishwa katikati mwa mwaka wa 1992 baada ya kupigwa marufuku kwa miaka kumi. Kuna vyama vingi vya kiasisa chini ya Jamhuri ya Nne; hata hivyo vile vikubwa ni National Democratic Congress kilichoshinda uchaguzi wa urais na ubunge mnamo 1992, 1996 na 2008; New Patriotic Party, chama kikubwa cha upinzani kilichoshinda uchaguzi wa mwaka wa 2000 na ule wa 2004; People’s National Convention, na Convention People’s Party, ambacho kilichukua mahali pa chama cha awali cha Kwame Nkrumah kilichokuwa na jina lilo hilo. Mahusiano ya Kigeni Tangu unyakuzi wa uhuru, Ghana imefuata kwa dhati mwelekeo wa kutojiunga na upande wa kibepari au ule wa kikomunisti (nonalignment) na pia siasa zinazopendelea siasa za umoja wa Afrika (Pan-Africanism); mawazo ambayo yanahusishwa na rais wa kwanza, Osagyefo Dr. Kwame Nkrumah. Nchi ya Ghana inapendele31ushirikiano wa kimataifa na wa kikanda wa kisiasa na wa kiuchumi, na ni mwanachama mwenye mashuhuri wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Wanadiplomasia na wanasiasa wengi Waghana wana vyeo katika mashirika ya kimataifa. Hawa ni pamoja na mwanadiplomasia Mghana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Akua Kuenyehia, na rais wa zamani Jerry Rawlings, ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (Economic Community of West African States). Wakazi Nchi ya Ghana ina idadi ya watu inayokadiriwa kuwa milioni 27. Makabila Ingawa Ghana ni kiambo cha zaidi ya makabila 70 tofauti, haijashuhudia migogoro ya kikabila kama ile ambayo imesababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi nyingi za Afrika. Makabila nchini Ghana ni ya Waakan (ambalo linajumuisha Fante, Akyem, Ashanti, Kwahu, Akuapem, Nzema, Bono, Akwamu, Ahanta na makabila mengine) 47.5%, Wamole-Dagbon 16.6%, Waewe 13.9%, Waga-Adangbe (likijumuisha Ga, Adangbe, Ada, Krobo na makabila mengine) 7.4%, Wabassare 5.9%, Wakonkomba 5.7%, Waguan 3.7%, Wagurunsi 2.5%, Wakusasi 2.2%, Wabissa 1.1%, mengine (Wahausa, Wazabarema, Wafula) 1.4% (sensa ya 2010). Lugha Lugha rasmi ni Kiingereza; hutumika sana katika masuala ya serikali na biashara. Lugha hiyo vilevile ndiyo inayotumika katika mafundisho ya elimu. Kifaransa pia kinajulikana sana na kiko mbioni kufanywa lugha rasmi ya pili. Hata hivyo, Waghana wengi pia huzungumza kwa kiasi lugha moja ya kikabila. Ingawa wataalamu wengine wanasema nchini Ghana huzungumzwa zaidi ya lugha na lugha ndogo 250, Ethnologue inaziorodhesha 79 tu (angalia pia orodha ya lugha za Ghana). Lugha za asili za Ghana zimegawanywa katika jamii mbili ndogo kutokana na jamii ya lugha za Kiniger-Kongo. Lugha za jamii ndogo ya Kwa zinapatikana zaidi katika maeneo ya kusini mwa Mto Volta, huku zile za jamii ya Gur zikipatikana katika eneo la kaskazini. Kikundi cha Kwa, lugha ambayo huzungumzwa na takribani 75% ya wakazi wa nchi, kinajumuisha lugha za Akan, Ga-Dangme na Ewe. Kikundi cha Gur kinajumuisha lugha za Gurma, Grusi, na Dagbani. Lugha kumi na moja zina hadhi ya kuwa lugha zinazodhaminiwa na serikali: Akuapem Twi, Ashanti Twi, Fante, Nzema, Dagaare/Wale, Dagbani, Dangme, Ewe, Ga, Gonja na Kasem. Ingawa si lugha rasmi, Kihausa ndiyo lugha ya mawasiliano inayozungumzwa na Waislamu wa Ghana. Dini Kwa mujibu wa sensa ya serikali ya 2010, mgawanyiko wa kidini ni: Wakristo 71.2% (hasa Waprotestanti 46.7% na Wakatoliki 13.1%), Waislamu 17.6%, dini asilia za Kiafrika 6.2%. Afya Kufikia mwaka wa 2009, matarajio ya urefu wa maisha (life expectancy) wakati wa kuzaliwa ni takriban miaka 59 kwa wanaume na 60 kwa wanawake huku makisio ya vifo vya watoto wachanga yakiwa 51 kwa watoto 1000 waliozaliwa hai . Hesabu ya watoto wanaozaliwa pia ni takriban watoto wanne kwa kila mwanamke. Kuna takriban madaktari 15 na wauguzi 93 kwa watu 100,000. Asilimia 4.5 ya Pato la Taifa lilitumika kwa masuala ya afya mwaka wa 2003. Watu na Utamaduni Ghana ni nchi iliyo na makabila mbalimbali; kwa hivyo ni mchanganyiko wa tamaduni wa makabila yake yote, Ashanti, Fante, Akyem, Kwahu, Ga, Ewe, Mamprusi na Dagomba, baina ya mengine. Jambo hili linadhihirika katika upishi, sanaa na desturi ya mavazi ya Ghana. Maadhimisho ya tamasha nchini Ghana ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Ghana na kuna tamasha nyingi kama vile Homowo, Odwira, Aboakyer, Dodoleglime na Sandema baina ya zingine. Ibada na mila kadha wa kadha hufanywa wakati wote wa mwaka katika sehemu mbali mbali za nchi, zikiwemo zile za kuzaliwa, ibada za mpito maishani kama vile kubalehe, ndoa na kifo. Michezo Soka ndiwo mchezo ulio na umaarufu zaidi nchini. Timu za kitaifa za soka ya wanaume zinajulikana kama The Black Stars, the Black Satellites na the Black Starlets na timu hizi hushiriki katika michuano mingi ikiwemo ile ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Kombe la Dunia la FIFA na Kombe la Dunia la FIFA kwa walio chini ya miaka 20. Timu ya the Black Satellites ilishinda Kombe la Dunia la FIFA kwa walio chini ya miaka 20 mnamo 2009 baada ya kushinda timu ya Brazili ya Seleção. Kuna timu za soka kadhaa nchini Ghana za kutajika zaidi zikiwa Accra Hearts ya Oak SC na Asante Kotoko baina ya zingine. Baadhi ya wachezaji wa soka wa Ghana wanaojulikana katika daraja ya kimataifa au waliopata ufanisi katika soka ya Ulaya ni Abedi Pele, Ibrahim Abdul Razak, Tony Yeboah, Anthony Annan, John Paintsil, Asamoah Gyan, Samuel Osei Kuffour, Richard Kingston, Sulley Muntari, Laryea Kingston, Stephen Appiah, Andre Ayew, Emmanuel Agyemang-Badu, Dominic Adiyiah na Michael Essien. Desturi ya Mavazi Kufumwa kwa vitambaa ni kitengo muhimu cha utamaduni wa Ghana. Vitambaa hivi hutumika kutengeneza mavazi ya kiasili na ya kisasa. Michoro na rangi tofauti humaanisha vitu tofauti. Pengine Kente ndicho kitambaa mashuhuri zaidi baina ya vitambaa vyote vya Ghana. Kente ni kitambaa cha sherehe cha Waashanti ambacho kinatengenezwa kwa mkono kwenye kitanda cha mfumi. Vipande vya takribani inchi nne kwa upana hushonwa pamoja ili kuwa vitambaa vikubwa zaidi. Vitambaa hivi huwa katika rangi, ukubwa na namna tofautitofauti na huvaliwa wakati wa hafla muhimu sana za kijamii au kidini. Katika muktadha wa kitamaduni, kitambaa cha kente kina umuhimu zaidi ya vazi tu. Ni uwakilishi wa kuonekana wa historia, na pia aina ya lugha iliyoandikwa kwa kufuma. Neno Kente lina mizizi yake katika neno la Kitwi kenten ambalo lina maana ya kikapu. Wasusi wa kwanza wa kente walitumia nyuzi za ukindu kufuma vitambaa vilivyoonekana kama kenten (kikapu); na hivyo vilikuwa vinaitwa kenten ntoma; kumanisha kitambaa cha kikapu. Jina la kiasili la Kiasante la kitambaa hiki lilikuwa nsaduaso au nwontoma, kumaanisha “kitambaa kilichotengenezwa kwa mkono kwenye kitanda cha mfumi”; hata hivyo neno kente ndilo hutumika zaidi na watu wengi siku hizi. Aina nyingi tofauti za vipande vyembamba vya vitambaa vinavyofanana na kente hufumwa na makabila mengi tofauti nchini Ghana kama Ewe, Ga na mengine ya Afrika. Kente pia hupendwa na Waafrika wanaoishi katika nchi za ng’ambo. Muziki Nchi ya Ghana ina aina nyingi ya muziki wa kitamaduni na wa kisasa. Midundo hii hutofautiana kutoka kabila moja hadi jingine na eneo moja hadi lingine. Muziki wa Ghana unajumuisha aina nyingi tofauti za vyombo vya muziki kama vile ngoma za talking drum ensembles, zeze ya goje na kinubi cha koloko, muziki wa jumba la mfalme, ikiwemo miziki ya Waakan wa Atumpan, wa Waga wa mitindo ya Kpanlogo, na marimba ya gogo itumikayo katika muziki wa Waasonko. Aina za muziki ambazo zinajulikana zaidi kutoka Ghana ni Afro-jazz ambayo ilifumbuliwa na msanii Mghana Kofi Ghanaba. na aina ya awali zaidi ya muziki wa kidunia inayoitwa Highlife. Highlife ni muziki uliochimbuka katika miaka ya mwisho ya 1800 na miaka ya mwanzo ya 1900 na kuenea kote Afrika Magharibi hasa Sierra Leone na Nigeria. Katika miaka ya 1900 aina mpya ya muziki ilizinduliwa na vijana huku ikiunganisha jinsi za Highlife, Afro-reggae, Dancehall na Hiphop. Mchanganyiko huu huitwa Hiplife. Wasanii wa Ghana kama vile mwimbaji wa R&B na Soul Rhian Benson, mwimbaji wa Highlife Kojo Antwi na msanii wa rap Tinchy Stryder (Kwasi Danquah) wamekuwa na ufanisi wa kimataifa. Ngoma Ngoma (densi) ya Ghana ina tofauti mithili ya muziki wake. Kila kabila lina ngoma zake za kitamaduni na kuna ngoma tofauti tofauti kwa hafla tofauti tofauti. Kuna ngoma za mazishi, sherehe za maadhimisho, usimulizi wa hadithi, sifa na kuabudu na kadhalika. Baadhi ya ngoma hizi ni: Bamaya Ngoma hii huchezwa na watu wa eneo la kaskazini mwa Ghana. Inasimulia hekaya ya wakati wa ukame mkubwa. Miungu iliwaambia watu kuwa ukame huo ulikuwa umeletwa na jinsi wanaume walikuwa wakiwakandamiza na kuwatweza wanawake. Ilisema pia kwamba ukame ungeondolewa tu pale wanaume wangejizusha na kuchukua majukumu waliyokuwa wamewatwika wanawake kwa kuvaa marinda na kushiriki katika ngoma hii. Wanaume walipofanya hivi, mvua ilianza kunyesha. Kwa sasa ngoma hii huchezwa wakati wa mavuno katika eneo la kaskazini magharibi mwa Ghana na wanaume pamoja na wanawake wa Dagbani. Adowa Ngoma ya watu wa Ashanti wa Ghana. Ngoma hii inatajika hasa kwa madaha na weledi wa mzunguko wa wachezaji. Upigaji ngoma pia unasifika kwa weledi wa mfuatano wa sauti zinazochanganyika na ngoma mbili za atumpan ambazo zinatumika kama ngoma za kuongoza au ngoma simamizi. Ngoma hii ilikuwa awali ikichezwa katika mazishi, lakini kwa sasa inachezwa pia katika tamasha za kila mwaka na mikusanyiko ya kijamii. Kpanlongo huchezwa na watu wa Ga wa Ghana. Ngoma hii ya Kpanlongo ambayo mara nyingi huitwa “ngoma ya vijana,” ilianza kuchezwa punde tu baada ya unyakuzi wa Uhuru wa Ghana kama aina ya muziki wa burudani jijini Accra. Kpanlongo huchezwa kwa sasa kwa matukio yanayohusu maisha, tamasha na mikutano ya kisiasa. Klama Huu ni muziki na ngoma ambayo inahusishwa na ibada za kubalehe kati ya watu wa Krobo wa Ghana. Inasisitiza kusonga kwa madaha kwa mikono na miguu. Huku wakipiga hatua ndogo kuambatana na muziki na wakigeuza vichwa kwa utaratibu kuangalia chini, wacheza ngoma huwa mfano wa madahiro tulivu. Tofauti baina ya hatua za wachezaji zinanuiwa kuonyesha uzuri wa wacheza ngoma. Mara kwa mara, wachumba wanaotazama ngoma hii kutoka pembeni huzuru jamii ya msichana baada ya sherehe kwa madhumuni ya kumposa msichana huyo. Vyombo vya Habari na Burudani Vyombo vya habari vya Ghana ni mojawapo ya vile vilivyo na uhuru zaidi barani Afrika. Hapo awali, vilikuwa vimewekewa vizuizi vingi wakati wa mfululizo wa mapinduzi ya serikali na viongozi wa jeshi. Sura ya 12 ya katiba ya 1992 ya Ghana inatoa hakikisho la uhuru na kujisimamia kwa vyombo vya habari huku Sura ya 2 ikizuia uthibiti. Baada ya kujinyakulia uhuru, serikali na vyombo vya habari vimekuwa mara kwa mara vikiwa na uhusiano ulio na mvutano, huku mashirika ya kibinafsi yakifungwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi na sheria kali ili kuzuia ukosoaji wa serikali. Uhuru wa vyombo vya habari ulirejeshwa mnamo mwaka wa 1992, na baada ya uchaguzi wa 2000 wa John Kufuor mivutano kati ya vyombo vya habari vya kibinafsi na serikali ilipungua. Kufuor alikuwa mtetezi mkubwa wa uhuru wa vyombo vya habari na alifuta sheria ya masingizio, ingawa alisisitiza kuwa ni lazima vyombo vya habari vifanye kazi kwa uwajibikaji. Vyombo vya habari vya Ghana vimeelezwa kuwa “baadhi ya vile visivyo na uthibiti mkubwa na serikali mwingi” barani Afrika, huku vikifanya kazi vikiwa na masharti machache mno kwa vyombo vya habari vya kibinafsi. Vyombo vya habari vya kibinafsi mara kwa mara hukosoa sera za serikali. Vyombo vya habari vilifanya kazi kwa bidii wakati wa uchaguzi wa rais wa Ghana wa mwaka wa 2008, na Chama cha Wanahabari wa Ghana (Ghanaian Journalists Association (GJA)) kilimpongeza John Atta Mills kwa ushindi wake, huku kikinuia kukuza uhusiano mwema baina ya vyombo vya habari na serikali. Elimu Kiwango cha kujua kusoma na kuandika kwa watu wazima kilikuwa 65% mnamo 2007, huku wanaume wakiwa 71.7% na wanawake wakiwa 58.3%. Nchi ya Ghana ina mfumo wa elimu ya msingi wa miaka 6 kuanzia umri wa miaka sita, na, chini ya mageuzi ya elimu yaliyotekelezwa mnamo 1987 na kurekebishwa mnamo 2007, watoto huingia katika mfumo wa miaka mitatu wa elimu ya upili ya daraja la chini. Mwishoni mwa mwaka wa tatu katika shule ya upili ya Junior High, kuna mtihani wa lazima unaojulikana kama Basic Education Certificate Examination (BECE). Wale wanaoendelea na masomo ni lazima wamalize masomo ya miaka mitatu ya shule ya upili ya daraja ya juu (senior high school - SHS) na kufanya mtihani wa kukubaliwa kuingia katika masomo ya chuo kikuu au taasisi yoyote ile. Kwa sasa, Ghana ina shule za msingi 21,530, shule za upili za daraja ya chini 8,850, shule za upili za daraja ya juu 900, vyuo vya mafunzo vya umma, 52, vyuo vya mafunzo vya kibinafsi, 5 vyuo vya elimu ya sanaa, 5 taasisi za umma ambazo si vyuo vikuu, 4 zisizo chuo kikuu Msingi umma taasisi, 8 vyuo vikuu 4 na zaidi ya taasisi za kibinafsi 45. Wengi baina ya Waghana wanaweza kupata huduma za elimu ya msingi na ya upili kwa urahisi. Idadi hizi zinaweza kutofautishwa na zile za chuo kikuu kimoja tu na shule chache tu za upili na za msingi zilizokuwepo wakati wa kujinyakulia uhuru mnamo 1957. Gharama ya nchi ya Ghana kwa elimu imekuwa kati ya asilimia 28 na 40 ya bajeti yake ya mwaka katika mwongo mmoja uliopita. Mafunzo yote hufanywa kwa lugha ya Kingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya Ghana, na hufanywa na walimu Waghana waliohitimu. Masomo yanayofunzwa katika Shule ya Msingi au ya Mwanzo ni pamoja na Kingereza, Lugha na Utamaduni wa Ghana, Hisabati, masomo ya masuala ya Mazingira, Masomo ya Kijamii na Kifaransa kama lugha ya tatu, yakiongezwa masomo ya Sayansi Jumuishi au ya Ujumla, masomo ya mwanzo ya Ustadi wa Ufundi (Pre-vocational Skills and Pre-technical skills) Elimu ya Dini na Maadili na shughuli za utendaji kama vile Muziki, Ngoma na Elimu ya Mazoezi ya Viungo. Mtaala wa daraja la upili la Senior High una masomo ya Lazima na yale ya Kuchagua. Wanafunzi wanapaswa kuchukua masomo manne ya lazima ya Lugha ya Kingereza, Hisabati, Sayansi ya Ujumla (yakiwemo masomo ya Sayansi, Kilimo na Masomo ya maswala ya Mazingira) na Masomo ya Kijamii (uchumi, jiografia, historia na serikali). Wanafunzi wa shule ya upili vilevile hufanya masomo matatu ya kuchaguliwa kati ya matano yafuatayo: Mtaala wa Kilimo, Mtaala wa Kijumla (chaguo la Sanaa au Sayansi), Mtaala wa somo la Biashara, Mtaala wa Ufundi (Vocational Programme and Technical Programme). Mbali na shule za msingi na za upili zinazofuata mfumo wa elimu wa Ghana, kunazo shule za kimataifa kama vile Ghana International school, Lincoln Community School na SOS-Hermann Gmeiner International College ambazo hufuata mfumo wa International Baccalaureat, Advanced Level General Certificate of Education na International General Certificate of Secondary Education (IGCSE). Huku ikiwa na asilimia 83 ya watoto wake shuleni, kwa sasa nchi ya Ghana ni baina ya nchi zilizo na viwango vya juu zaidi vya uandikishaji shuleni katika eneo la Afrika Magharibi. Uwiano wa wasichana na wavulana katika ujumla wa mfumo wa elimu ni 1:0.96, ambao kwa nchi ya Afrika Magahribi, ni mafanikio makubwa. Kadiri ya watoto 500,000 hawaendi shuleni kwa sababu ya ukosefu wa mapato ya kuwezesha ujenzi wa shule, kutoa vitabu vya kusoma vya kutosha na kutoa mafunzo kwa walimu wapya. Chuo Kikuu cha zamani zaidi nchini Ghana, Chuo Kikuu cha Ghana, ambacho kilianzishwa mnamo mwaka wa 1948, kilikuwa na takriban jumla ya wanafunzi 29,754 katika mwaka wa 2008. Tangu unyakuzi wa uhuru wa Ghana, nchi hii imekuwa mojawapo ya vitovu vya elimu katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara na imekuwa mwenyeji wa watu maarufu kama vile Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Alhaji Sir Dauda Jawara wa The Gambia na Cyprian Ekwensi wa Nigeria baina ya wengine. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, ambacho ndicho chuo kikuu cha pili kuanzishwa nchini Ghana, ndicho chuo cha kwanza cha masomo ya sayansi na teknolojia nchini humo na katika ukanda wa Afrika Magharibi. Uchumi Ikiwa imejaliwa sana na maliasili, nchi ya Ghana ina mapato yanayokadiriwa kupata kila mtu (per capita output) yaliyo mara mbili yakilinganishwa na yale ya nchi zilizo maskini zaidi za Afrika Magharibi. Hata hivyo, Ghana imebakia kutegemea kwa kiwango fulani biashara na usaidizi wa kimataifa na vilevile shughuli za uwekezaji kutokana na Waghana wanaoishi nchi za ng’ambo. Karibu 28% ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa kimataifa wa umaskini wa dola za kimarekani 1.25 kwa siku, na kwa mujibu wa wa Benki ya Dunia, kisio la mapato ya kila mtu (per capita income) ya Ghana yamekuwa mara dufu lakini kwa shida kwa miaka 45 iliyopita. Nchi ya Ghana, ikijulikana kwa dhahabu yake katika enzi za ukoloni, bado ni kati ya wazalishaji wakuu ulimwenguni wa dhahabu. Mauzo yake mengine nje ya nchi kama vile kakao, mbao, umeme, almasi, bauxiti, na manganisi ni uzalishaji mkuu wa fedha za kigeni. Kiwanja cha mafuta kinachoripotiwa kuwa na hadi pipa bilioni 3 (480,000,000 m3 za mafuta mepesi kiligunduliwa mnamo mwaka wa 2007. Utafutaji wa mafuta bado unaendelea na kiasi cha mafuta kinaendelea kuongezeka. Bwawa la Akosombo, ambalo lilijengwa juu ya Mto Volta mnamo mwaka wa 1965 linatoa umeme unaozalishwa na maji kwa nchi ya Ghana na nchi zinazoizunguka. Nguvukazi ya Ghana katika mwaka wa 2008 ilikuwa jumla ya watu milioni 11.5. Uchumi unaendelea kutegemea sana kilimo ambacho huchangia 37% ya Pato la Taifa na kutoa ajira kwa kwa 56% ya watu wanaofanya kazi, hasa wenye ardhi ndogo. Sekta ya viwanda ni sehemu ndogo tu ya uchumi wa Ghana iliyochangia kwa ujumla 7.9% ya Pato la Taifa mnamo 2007. Sera za kiuchumi zisizofaa za serikali za kijeshi zilizopita na masharti ya vikosi vya kulinda usalama katika maeneo ya kanda vimechangia mfumuko katika fedha za nakisi, kushuka thamani kwa Sidi, na kuongezeka kwa kutoridhika kwa umma katika maswala ya hatua za kupunguza ugumu wa maisha. Hata hivyo, Ghana inabakia kuwa mojawapo baina ya nchi za Afrika nzima ambazo zina ustawi wa kiuchumi. Mnamo Julai 2007, Benki ya Ghana ilianzisha shughuli ya kugeuza sarafu, kutoka kwa Sidi (¢) hadi kwa sarafu mpya, Sidi ya Ghana (GH¢). Kiwango cha ubadilishanaji ni Sidi moja ya Ghana kwa kila Sidi 10,000. Benki ya Ghana ilizindua kampeni kabambe katika vyombo vya habari ili kuelimisha umma juu ya mageuzo haya. Sarafu mpya ya Sidi ya Ghana iko imara kwa kiwango kikubwa na katika mwaka wa 2008 ilibadilishwa kwa ujumla kwa thamani ya dola moja ya marekani kwa Sidi 1.1 ya Ghana. Kodi ya Ongezeko la Thamani ni kodi ya matumizi itozwayo nchini Ghana. Utaratibu huu wa kodi ambao ulianza mnamo 1998 ulikuwa wa kiwango kimoja lakini tangu Septemba 2007 utaratibu wa viwango kadhaa ulizinduliwa. Mnamo 1998, kiwango cha kodi kilikuwa ni 10% na na kilirekebishwa mnamo mwaka wa 2000 na kuwa 12.5%. Hata hivyo baada ya kupitishwa kwa Sheria ya 734 (Act 734) ya mwaka 2007, kodi ya usawa ya 3% (a 3% VAT Flat Rate Scheme (VFRS) ) ilianza kufanya kazi kwa sekta ya usambazaji wa rejareja. Hii inawezesha wauzaji wa rejareja wa bidhaa zinazotozwa ushuru chini ya Sheria ya 546 (Act 546) kotoza ushuru wa pambizoni wa 3% kwa mauzo yao na kuhesabu ushuru huu pamoja na ule wa VAT. Hii inanuia kurahisisha utaratibu wa uchumi na kuongezeka kwa maafikiano. Cheo katika Ngazi za Kimataifa Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Jumuiya ya Madola Umoja wa Mataifa Uchukuzi nchini Ghana Tanbihi Viungo vya nje Serikali Tovuti rasmi ya Ghana Tovuti rasmi ya Bunge la Ghana Tume ya Kitaifa ya Utamaduni Mkuu wa serikali na Wanachama wa Baraza la Mawaziri Habari za ujumla Maelezo ya nchi (Country Profile) kutoka BBC News Ghana kutoka Encyclopaedia Britannica Ghana kutoka UCB Libraries GovPubs Tovuti ya African Activist Archive Project ina picha za mkutano wa All Africa People's Conference uliofanyika Accra, Ghana, 5-13 Desemba 1958 ikiwemo ile ya Kwame Nkrumah, Waziri Mkuu wa Ghana , akiuhutubia mkutano, ujumbe wa American Committee on Africa ukikutana na Nkrumah, na ya Patrick Duncan na Alfred Hutchinson wa Afrika Kusini katika mkutano huo. Vyombo vya habari Shirika la Utangazaji la Ghana (Ghana Broadcasting Corporation) Utalii Utalii nchini Ghana (Ghana Tourism) Tovuti Rasmi ya Utalii wa Ghana Picha za Ghana katika Bigfoto.com Picha za Ghana katika City photos Usafiri nafuu kwenda Ghana Ghana Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Jumuia ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi Nchi na maeneo yanayozungumza Kiingereza Jumuiya ya Madola
1788
https://sw.wikipedia.org/wiki/Carola%20Kinasha
Carola Kinasha
Carola Daniel Amri Kinasha (alizaliwa Longido, Mkoa wa Arusha, Tanzania, mnamo Machi mwaka 1962) ni mwanamuziki wa kike wa kitanzania. Baada ya kumaliza masomo ya elimu ya msingi huko Longido, alihamia jijini Dar Es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari na ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Carola amekuwa akijihusisha na masuala ya muziki tangu mwaka wa 1988. Ameshiriki katika miradi na matamasha mbalimbali ya kimuziki, ndani na nje ya Tanzania.Pia amekuwa mtetezi wa haki za binadamu kwa ujumla akiweka msisitizo zaidi kwenye haki za wasanii wa Tanzania. Anaamini kuwa ili tasnia ya sanaa ya Tanzania iweze kukua na kujulikana kimataifa ni muhimu kurejesha elimu ya sanaa kwenye shule zetu. Pia kuwa na sehemu za kufanyia shughuli za sanaa kwenye kila kitongoji. Viungo vya nje Tovuti ya Women's Voice Wanamuziki wa Tanzania
1789
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia
Wikipedia
Wikipedia ni kamusi elezo huru ya lugha nyingi katika mtandao wa wavuti. Inalenga kukusanya elimu nyingi iwezekanavyo na kuisambaza kwa njia ya intaneti. Inatumia taratibu za wikiwiki. Ni bure kabisa, na inaweza kusomwa, kuandikwa, na kuhaririwa na mtu yeyote, popote pale. Yaani kila mtu anaweza kuchangia makala akiwa na uhuru wa kuboresha makala zilizopo kwa kuzihariri. Kamusi hii inajengwa kwa utaratibu huria ambao unategemea falsafa ya ushirikiano ambako watu wengi hushirikiana kwa kujitolea bila kupokea malipo yoyote. Falsafa hii inaonekana katika vuguvugu la programu huria ya tarakilishi, mikutano huria, demokrasia huria, n.k. Wikipedia inaweza kusomwa pia nje ya mtandao kwa kutumia programu huria ya Kiwix. Historia Wikipedia ilianzishwa kwa Kiingereza mwezi Januari mwaka 2001. Mwaka 2003 kamusi elezo hii ilianzishwa katika lugha ya Kiswahili. Wikipedia imeshachukua nafasi za kamusi elezo mashuhuri kama Encyclopedia Britannica zilizotazamwa kuwa mkusanyo wa elimu ya Dunia kabla ya kutokea kwa intaneti. Kwa lugha za Kiafrika kama Kiswahili ni mara ya kwanza ya kwamba jaribio la kukusanya elimu za fani mbalimbali limeanzishwa. Hadi mwaka 2018 wachangiaji wa Wikipedia walishirikiana kuunda zaidi ya makala milioni 47 kwa lugha 300. Wikipedia kubwa zenye makala zaidi ya milioni mbili zilikuwa kwenye Novemba 2018: Wikipedia ya Kiingereza (makala 5,758,502), ya Kicebuano (makala 5,379,917), ya Kiswidi (makala 3,764,225), ya Kijerumani (2,243,097) na ya Kifaransa (makala 2,060,362). Kwa jumla kulikuwa na Wikipedia zenye zaidi ya makala milioni moja kwa lugha 15. Taasisi ya Wikimedia Foundation Kisheria maudhui yote ya Wikipedia si mali ya mtu yeyote kwa kuwa ni maudhui huria. Seva za wikipedia na programu zake zinatunzwa na taasisi ya Wikimedia Foundation ambayo ni shirika lisilo la kiserikali lililoandikishwa chini ya sheria za jimbo la Kalifornia, Marekani. Taasisi hii inapokea mapato yote kutoka kwa wafadhili wa kujitolea kote duniani. Taasisi ya kitaifa na makundi ya watumiaji Katika nchi mbalimbali kuna shirika za kitaifa zinazojumuisha wanawikipedia ama kwa umbo la taasisi au kwa umbo la makundi ya watumiaji (Wikimedia User Groups). Nchini Tanzania kuna kundi la Wikimedia Community User Group Tanzania. Kundi la Jenga Wikipedia ya Kiswahili ni jumuiya ya wachangiaji kutoka nchi mbalimbali wanaoangalia maendeleo ya Wikipedia ya Kiswahili. Tazama pia Wikipedia ya Kiafrikaansi Wikipedia ya Kifaransa Wikipedia ya Kihispania Wikipedia ya Kiingereza Wikipedia ya Kiingereza Rahisi Wikipedia ya Kijerumani Wikipedia ya Kiswahili Wikipedia ya Kiyoruba Wikimedia Kamusi elezo
1790
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dar%20es%20Salaam
Dar es Salaam
Kwa maana nyingine, tazama Mkoa wa Dar es Salaam Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la mkoa wake. Dar es Salaam ni mji mkongwe na wenye watu wengi zaidi katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika Tanzania ndio mji wenye vitega uchumi vingi na ndio mji unaoangaliwa na watu wengi. Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania (kinadharia tangu mwaka 1973). Mpango wa kuhamishia serikali mjini Dodoma unaendelea kwa kasi chini ya rais John Magufuli, japokuwa bado ofisi kadhaa za serikali, ikiwa ni pamoja na Ikulu, zipo Dar es Salaam. Mji una wakazi wapatao 5,383,728 kwa hesabu ya sensa iliyofanyika katika mwaka wa 2022. Jina Jina la Dar es Salaam linatoka katika Kurani ambako linamaanisha mahali patulivu au hata paradiso. Surah Al-Anam (Korani 6:127) ina maneno لَهُمْ دَارُ‌ السَّلَامِ عِندَ رَ‌بِّهِمْ lahum dāru as-salāmi `inda rabbihim yanayomaanisha "Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao." . Jina linafanywa na maneno mawili ya Kiarabu; دار dar inayomaanisha "nyumba, jengo, makazi, eneo", "es" ni silabi ya kuunganisha sehemu za jina linalounganishwa na maneno mawili, سلام salaam inamaanisha "amani, raha, usalama". Mara nyingi jina limetafsiriwa kama "Bandari ya Amani" lakini hii ni kosa kutokana na kuchanganya maneno ya Kiarabu دار "dar" (nyumba) na بندر "bandar" (bandari) maana kwa matamshi ya Kiswahili tofauti ya tahajia katika Kiarabu haitambuliki. Jina la Daressalaam limetumiwa kwa maumbo tofauti kwa mahali mbalimbali katika mazingira ya Kiislamu, kwa mfano huko Brunei Darussalaam, Dar El Salam (Misri), Dar os Salam (Iran), pia kama majina ya taasisi mbalimbali. Historia Jiji hili zamani lilikuwa kijiji na kuitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar aliamua kujenga ikulu ya pili barani kando la Mzizima akachagua jina "Dar es Salaam". Hadi leo kuna majengo mawili yaliyobaki ya vyanzo hivi ambayo ni Boma la Kale na Nyumba ya Atiman House. Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka 1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya Uingereza. Utawala Utawala wa Dar es Salaam uliona mabadiliko kadhaa ambapo mwanzoni mji ulitawaliwa na halmashauri yake na baadaye serikali ya kitaifa ilichukua utawala mikononi mwake au kuukabidhi kwa tume ya serikali. Mwaka 2000 eneo la jiji liligawanywa kwa mamlaka tofauti ambazo mwanzoni zilikuwa nne, ambazo zilikuwa manisipaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Baadaye Ubungo na Kigamboni zilikuwa manisipaa za pekee, kila moja na halmashauri yake. Kwa jiji lote Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliundwa. Kwa hiyo hadi 2021 Dar es Salaam ilikuwa na Halmashauri 6. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Kwenye Februari 2021 Halmashauri ya Dar es Salaam ilivunjwa na serikali, na Ilala ilibadilishwa jina kuwa Dar es Salaam. Wakazi na uchumi Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ikulu, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k. Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k. Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika manisipaa za Temeke, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo. Wakazi na uchumi Dar es Salaam ni mji unaosemekana kuwa mkubwa kuliko yote kwa sababu ya maendeleo mbalimbali ya viwanda, uwepo wa bahari, uwepo wa sehemu mbalimbali za kihistoria n.k. Huduma za jiji Huduma ya maji Dar es Salaam imekuwa na tatizo kubwa katika kudhibiti mfumo wa maji taka katika mkoa wa Dar es Salaam kwa muda mrefu. Tangu shirika la maji DAWASCO (Dar es Salaam Water Supply Company) lilipowekwa rasmi kama shirika husika katika kuratibu utaratibu mzima wa mfumo wa maji safi na maji taka, kumekuwa na nafuu kidogo tu, lakini baada ya muda, liliibuka tatizo la kuibiwa kwa mabomba na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vya maji. Elimu Kwenye suala hili la elimu vijana wanatakiwa kupewa elimu; hasa vijana wa mitaani wasioingiza kipato inabidi wapewe elimu kwa kazi fulani ili waweze kuajiriwa na kulipa faida taifa kwa kuingizia kipato na kukuza uchumi wa taifa. Mfano wa kazi hizo ni kama ujenzi wa nyumba n.k. Picha Marejeo Viungo vya nje DAR ES SALAAM CITY PROFILE Mohamed Said: Mwalimu in 1950s Dar (East African October 12 2008 - inasimulia maisha ya Nyerere Dar es Salaam pamoja na habari nyingi za jiji wakati wa miaka ya 1950) Dar es Salaam kwenye Wikipedia commons Miji ya Tanzania Tanzania Miji Mikuu Afrika
1791
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bahari%20ya%20Hindi
Bahari ya Hindi
Bahari ya Hindi ni bahari ya tatu kwa ukubwa duniani ikiwa imechukua asilimia 20 ya uso wa dunia na kuzungukwa na mabara manne. Upande wa kaskazini imepakana na Asia ya Kusini; magharibi imepakana na Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Shamu na Afrika; mashariki imepakana na Ghuba ya Malay, visiwa vya Sunda (Indonesia), na Australia; na upande wa kusini imepakana na Bahari ya Kusini. Bahari hii ni njia muhimu ya usafiri na usafirishaji kwa meli kati ya Asia na Afrika. Jiografia Mipaka Mipaka ya Bahari Hindi imeelezwa na Shirika la Kimataifa la Hidrografia kama ifuatayo: upande wa magharibi (Atlantiki) ni mstari unaoelekea kusini kutoka Rasi Agulhas (Afrika Kusini) kwenye longitudo ya 20° mashariki upande wa mashariki ni mstari unaoelekea kusini kutoka sehemu ya kusini zaidi cha Tasmania (Australia) kwenye longitudo ya 146°55'E kati ya Australia na Asia ni mstari wa visiwa vya Indonesia upande wa kaskazini ni pwani za Asia na Afrika upande wa kusini imeamuliwa kutumia latitudo ya 60°S kama mpaka wa Bahari Hindi na Bahari ya Kusini inayozunguka bara la Antaktiki. Kwa hiyo eneo lote la uso wa bahari hii ni kilomita za mraba 70,560,000 km²; kina cha wastani ni mita 3,741 ilhali kina kikubwa kinafikia mita 7,906. Mjao wake ni kilomita za ujazo 264,000,000 km³ inayolingana na asilimia 19.8% ya mjao wa bahari zote duniani. Jiolojia Chini ya Bahari Hindi kuna mabamba ya gandunia mbalimbali yanayopakana hapa: Bamba la Antaktiki, Bamba la Afrika, Bamba la Uarabuni, Bamba la Uhindi na Bamba la Australia. Kama kawaida, pale ambako mabamba yanaachana kuna nafasi inayoruhusu kupanda juu kwa joto na magma kutoka kiini cha dunia na kutokea kwa volkeno pamoja na safu za milima chini ya maji. Tetemeko la ardhi na tsunami ya 2004, iliyosababisha uharibifu na vifo katika sehemu za kaskazini za Bahari Hindi, ilisababishwa na mwendo wa ghafla la bamba la Australia juu ya bamba la Uhindi. Bahari za pembeni Bahari za pembeni, ghuba na hori za Bahari Hindi ni pamoja na: Bahari ya Uarabuni Ghuba ya Uajemi Bahari ya Shamu Ghuba ya Oman Ghuba ya Aden Mlangobahari wa Bab-el-Mandeb (kati ya Bahari ya Shamu na Bahari ya Uarabuni) Hori ya Katch Hori ya Khambat Mlangobahari wa Palk (kati ya Hori ya Bengali na Bahari ya Uarabuni) Hori ya Bengali Bahari ya Andamani Mlangobahari wa Malakka Mfereji wa Msumbiji Hori Kuu ya Australia Bahari ya Timor Ghuba ya Mannar Bahari ya Lakadivi Tabianchi Kwa jumla Bahari Hindi ina halijoto ya juu kulingana na bahari kubwa nyingine za dunia. Tofauti na Atlantiki na Pasifiki haina maeneo makubwa kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia hivyo haipokei baridi kutoka Aktiki. Upande wa kazkazini wa ikweta kuna monsuni; upepo kutoka kazkazini-mashariki uko kuanzia Oktoba hadi Aprili, kinyume chake upepo kutoka kusini unaendelea kuanzia Mei hadi Oktoba. Badiliko hili linafuata utaratibu wa kila mwaka na lilikuwa msingi kwa usafiri na biashara katika bahari hii maana iliwezekana kutumia upepo kwa jahazi tangu kale. Wakati wa badiliko la monsuni dhoruba kali zinaweza kutokeas hasa katika Bahari ya Uarabuni na Hori ya Bengali. Nchi zinazopakana na Bahari Hindi Asia Israel na Jordani (kupitia Ghuba ya Akaba na Bahari ya Shamu), Ufalme wa Uarabuni wa Saudia, Yemen, Omani, Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Iraq, Iran, Pakistan, India, Bangladesh, Myanmar, Uthai, Malaysia, Indonesia na Timor ya Mashariki. Australia Australia Afrika Afrika Kusini, Msumbiji, Tanzania, Kenya, Somalia, Jibuti, Eritrea, Sudani na Misri (kupitia Bahari ya Shamu). Nchi za visiwani Ndani ya Bahari Hindi kuna mataifa huru ambayo ni nchi za visiwani pamoja na Bahrain (Ghuba ya Uajemi), Komori, Madagaska, Maldivi, Morisi, Shelisheli na Sri Lanka. Indonesia na Timor ya Mashariki ni nchi za visiwani zinazopakana na Bahari Hindi. Visiwa katika Bahari Hindi Agalega, Anjouan, Bahrain, Cargados Carajos, Visiwa vya Cocos (Keeling), Diego Garcia, Kilwa Kisiwani, Kirimba (visiwa), Kisiwa cha Mafia, Komori, Kisiwa cha Krismasi, Lamu (kisiwa), Morisi, Madagaska, Mahore, Mahé, Maskarena, Mayotte, Moheli, Msumbiji (kisiwa), Mwali, Ngazija, Pamanzi, Pate, Pemba (kisiwa), Rodrigues (kisiwa), Réunion, Shelisheli, Sokotra, Unguja, Îles Éparses, Tanbihi Kujisomea | Bahari
1792
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nairobi
Nairobi
Nairobi ni mji mkuu wa jamhuri ya Kenya na vilevile mojawapo ya kaunti za Kenya. Kulingana na sensa ya mwaka 2019, Nairobi ina wakaaji 4,397,073 katika eneo la km2 696 (sq mi 269). Pamoja na vitongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Afrika. Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkarenairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi." Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili pamoja na Sheng. Eneo la jiji la Nairobi Nairobi yenyewe iko ndani ya eneo la jiji la Nairobi (kwa Kiingereza: Greater Nairobi Metropolitan region) lililoundwa na kaunti 4 kati ya jumla ya 47 za Kenya. Kaunti hizo ni: Source: Kenya Census Eneo hilo linazalisha asilimia 60 za pato la taifa. Mazingira na hali ya hewa Nairobi iko kilomita 150 upande wa kusini ya ikweta kwenye nyanda za juu za Kenya kando la mto Nairobi. Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya mto Athi inaanza kupanda juu hadi milima ya Ngong na vilima vingina vinyvyofanya ukuta wa mashariki wa Bonde la Ufa. Kitovu cha Nairobi kiko zipatao m 1624 juu ya UB. Sehemu za mashariki za jiji ziko bado kwenye tambarare, na sehemu za magharibi ziko kwenye mtelemko unaopanda hadi mita 1800 kwenye mpaka wa jiji na mita 2000 juu ya UB kwenye nje ya jiji huko Limuru. Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5°C mwezi wa Machi, na 16,8°C mwezi wa Julai. Wakati wa Juni na Julai usiku unaweza kuwa baridi halijoto ikishuka chini ya sentigredi 10. Mvua nyingi hunyesha mwezi Machi (mm 199), kiangazi kina mm 14 tu wakati wa Julai. Historia ya Nairobi Chanzo kwenye kambi la reli Nairobi ilianzishwa na Waingereza mwaka 1899 kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Njia ya reli ilikuwa imefika kutoka Mombasa ikaonekana ya kwamba kuanzia hapa kasi ya ujenzi itachelewa kutokana na ugumo na eneo la Bonde la Ufa na mitelemko yake mikali. Mahali palikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji pakaonekana panafaa kwa kituo njiani. Hasahasa ilionekana tabianchi ya nyanda za juu ilifaa kiafya kwa Waingereza walioteswa na joto la pwani na kwenye nyanda za chini. Kitangulizi cha Nairobi kilikuwa kituo kidogo kilichoanzishwa mwaka 1896 kando ya mto Nairobi na wakala Mwingereza wa reli kwa kusudi la kuajiri wafanyakazi wazalendo kwa ujenzi wa reli. Mwaka uliofuata 1897 wakaguzi walioandaa njia ya reli walipiga kambi karibu naye. . Mji mkuu wa koloni Njia ya reli ilifika kwenye kambi tarehe 30 Mei 1899. Hapo idadi ya wafanyakazi - hasa Wahindi - iliongezeka sana na kambi lilikuwa kubwa ya mahema na ghala za vifaa vya ujenzi. Mwezi wa Juni mizigo ya mabati ilifika kutoka Mombasa - tayari kwa reli - na majengo ya kudumu yalianza kutengenezwa katika mazingira ya eneo la kituo cha reli cha leo. Mwezi wa Agosti kamishna Mwingereza wa jimbo la Ukamba aliamuliwa kuhamisha makao makuu yake Nairobi kutoka Machakos akajenga boma lake kwenye eneo la Moi Avenue, mbali na reli jinsi inavyoonekana hadi leo kwenye majengo ya polisi ya kihistoria yanayotazama Bustani ya Jivanji. Barabara kuu ya kwanza ilikuwa "Station Road" kandokando ya Mtaa wa Tom Mboya wa leo iliyoitwa Victoria Street ikawa mahali pa maduka na hoteli za kwanza zilizoendeshwa na Wazungu na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya Haile Selassie na Harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa huko kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano. Pale mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuhusu chaguo la mahali; baada ya mvua kali sehemu ya mahema na vibanda vilipatikana katikati ya ziwa la matope. Magonjwa yalisambaa na baada ya epidemia ya tauni soko la Wahindi Lilichomwa na kuhamishwa sehemu nyingine. Majaribio ya kukausha kinamasi yaliendelea kwa miaka kadhaa hadi kufaulu. Kutokana na usumbufu wa matope maafisa wa ngazi ya juu walijenga nyumba zao kwenye kilima cha karibu kilichojulikana kama Nairobi Hill. Mwaka 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ikawa hivyo makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa, baadaye Kenya Colony). Uchumi wa mji ulitegemea pale mwanzoni hasahasa mahitaji ya utawala wa serikali na reli na utalii; matajiri wengi kutoka pande zote za dunia waliFIka kwa kusudi la kuwinda wanyama wakubwa wakivutwa na wingi wa wanyama kwenye nyanda za juu na usafiri rahisi kwa reli. Baadaye ardhi katika mazingira ya mji ilitolewa kwa walowezi Wazungu na kilimo cha biashara kilianza kuchangia. Kiasili Nairobi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Wazungu wa reli na serikali pamoja na Wahindi; Waafrika hawakupewa makazi isipokuwa mabweni ya wanfanyakazi wa reli na vibanda vya wafanyakazi wasaidizi kandokando ya nyumba za mabwana wao. Lakini Waingereza waliajiri askari kutoka Sudan na Somalia katika jeshi na polisi, na hao walifuatwa na wafanyabiashara kutoka kwao. Wapagazi na askari kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki walifika Nairobi kikazi na wengine waliamua kubaki. Mitaa ya vibanda iliota haraka nje ya mji wenyewe, mingine ilibomolewa haraka, mingine iliweza kubaki. Mnamo 1921 kulikuwa na Waafrika 12,000 waliokaa katika mitaa ya Waafrika iliyoitwa Mombasa, Masikini, Kaburini, Kariokor, Kibera, Pumwani na Pangani. Tangu uhuru Mwaka 1963 ikawa mji mkuu wa nchi huru ya Kenya ikaendelea kukua haraka. Nairobi ya leo Nairobi imeibuka kuwa mmojawapo kati ya miji mikubwa katika bara la Afrika. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya mashirika haya ni ofisi za tawi la Umoja wa Mataifa (United Nations), UNEP. Kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbalimbali duniani. Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa Nairobi hawakutegemea kuwa utatanuka hivyo. Wataalamu wengi wametoa maonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji huu na uwezo wake wa kuwahudumia wakazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka. Nairobi imewavutia wakazi wengi, wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. Ijapokuwa wapo wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakaachwa bila pesa au hali ya kujikimu. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wakazi wa maeneo yasiyotengwa wananchi, maarufu kama 'slums' kwa Kimombo. Eneo kubwa zaidi jijini Nairobi ni Kibera. Eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakazi takribani milioni moja. Eneo hili halina mipango yoyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule. Kunayo pia matatizo ya ujambazi na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa Nairobi. Maeneo bunge Kaunti ya Nairobi imegawanywa katika maeneo bunge 17 na kata 85,. Tazama pia Orodha ya miji ya Kenya Marejeo Kujisomea Red Strangers: The White Tribe of Kenya, by Christine Stephanie Nicholls, Timewell Press, 2005 (via google books, imetazamiwa Aprili 2 Viungo vya nje Tovuti rasmi ya Nairobi Chuo Kikuu cha Nairobi Miji ya Kenya Miji Mikuu Afrika Kaunti ya Nairobi Kaunti za Kenya
1797
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara%20la%20Antaktiki
Bara la Antaktiki
Antaktiki ni bara lililopo kwenye ncha ya kusini ya dunia, kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Jina "Antaktiki" linatokana na lugha ya Kigiriki likimaanisha "kinyume cha Aktiki", ambapo Aktiki ni eneo karibu na ncha ya kaskazini. Bara hili lina eneo la kilomita za mraba milioni 14 na eneo hili limefunikwa karibu kabisa, yaani kwa asilimia 98% za eneo na theluji na barafu. Eneo lake ni kubwa kushinda Ulaya lakini hakuna mti hata mmoja. Bara hili linajulikana kama jangwa baridi. Kwa sababu ya baridi kali katika bara hilo, ni bara pekee ambako binadamu hawaishi kwa namna ya kudumu, isipokuwa kuna watu 5,000, hasa wanasayansi, wanaokaa kwa muda katika vituo vyao. Uvumbuzi Bara la Antaktiki halikujulikana hadi karne ya 19, lakini wataalamu wa jiografia waliwahi kuhisi tangu zama za kale ya kwamba eneo kubwa la nchi kavu liko kwenye sehemu ya kusini ya dunia. Kuanzia Aristoteli wataalamu waliamini ya kwamba dunia ilipaswa kuwa na uwiano fulani, hivyo kuwepo kwa bara kubwa ingekuwa lazima kulingana na mabara ya nusutufe ya kaskazini. Nchi hii isiyojulikana kwa muda mrefu ikaitwa kwa jina la Kilatini "terra australis" yaani "nchi ya kusini" na pia kuchorwa kwenye ramani za dunia zilizoanza kutengenezwa tangu safari za wavumbuzi Wareno waliozunguka dunia nzima kwa mara ya kwanza. Ila tu ramani hizi za kwanza zilikuwa kama njozi tu. Kundi la kwanza la watu kufika kusini kwa kutosha na kuona kona ya barafu ya Antaktiki lilikuwa mwaka 1820 msafara wa kisayansi wa nahodha Fabian von Bellingshausen (Mjerumani Baltiki katika utumishi wa Tsar wa Urusi) akifuatwa mwaka uleule na nahodha Edward Bransfield wa Uingereza na tena Mmarekani Nathaniel Palmer. Ila tu hakuna uhakika kama wavumbuzi hao walitambua tayari ya kwamba waliona bara jipya. Pamoja na taarifa za mabaharia wengine waliopita kwenye pwani bado haikueleweka kama huko karibu na ncha ya kusini kulikuwa na visiwa mbalimbali au nchi kavu kubwa zaidi. Ni misafara ya Wafaransa na Wamarekani mnamo mwaka 1840 iliyoweza kuthibitisha ya kwamba ncha ya kusini ilipatikana ndani ya bara jipya. Sasa shauku ya upelelezi ilififia kwa sababu haikueleweka kuna nini katika bara jipya. Tangu mwaka 1890 Shirika la Kifalme la Jiografia (Royal Geographic Society) nchini Uingereza lilianza upya kusisitiza umuhimu wa utafiti wa Antaktiki iliyokuwa sehemu ya mwisho wa dunia isiyochunguliwa bado kabisa. Hapo misafara mbalimbali kutoka nchi tofauti ilifuatana na kupeleleza Antaktiki: Mwaka 1907 ncha sumaku ya kusini ilifikiwa na msafara wa Mwingereza Ernest Shackleton Mwaka 1910 misafara miwili kutoka Norwei na Uingereza ilishindana kufika ncha ya kusini ya kijiografia. Mnorwei Roald Amundsen alikuwa wa kwanza kufika nchani tarehe 14 Disemba 1910 akarudi salama kwa meli yake. Kundi la Mwingereza Robert Scott likachelewa siku 33 likakuta bendera ya Norwei na hema la Amundsen. Kwenye njia ya kurudi Scott alikuta hali ya hewa mbaya akaishiwa chakula chote akafa pamoja na wenzake katika barafu. Katika miaka iliyofuata idadi ya misafara iliongezeka. Tangu mwaka 1929 eropleni zilitumika pia katika upelelezi. Ni hasa Mmarekani Richard Byrd aliyeongoza misafara kadhaa akitumia ndege akaweza kuweka msingi wa ramani kamili ya Antaktiki. Jiografia Bara la Antaktiki lina takriban umbo la duara isiyo kamili ikizunguka ncha ya kusini. Pande zote inapakana na bahari: ni mahali ambako maji ya kusini ya Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi yanakutana. Kwa namna nyingine inawezekana kusema inazungukwa na Bahari ya Kusini. Eneo lake ni zaidi ya kilomita za mraba milioni 14, hivyo ni bara la tano duniani kwa ukubwa. Umbali kutoka pwani hadi pwani uko baina ya kilomita 4,500 na 5,600. Pwani ina urefu wa kilomita 17,968. Sehemu za Antaktiki Safu ya Milima ya kuvukia Antaktiki (kwa Kiingereza Transantarctic Mountains) inagawa bara katika sehemu mbili za Antaktiki Magharibi na Antaktiki Mashariki. Mpaka huu unalingana takriban na longitudo ya 180. Antaktiki Magharibi ni upande mdogo zaidi. Ndani yake inagawiwa kwa rasi kadhaa kwa hiyo ina athira ya tabianchi kutoka bahari. Hata kama sehemu kubwa inafunikwa na barafu halijoto haishuki chini mno jinsi ilivyo upande wa mashariki. Rasi kubwa ni Rasi ya Antaktiki (ing. Antarctic Peninsula) Antaktiki Mashariki inafanana zaidi na nusutufe, hakuna rasi au hori kubwa. Kwa hiyo tabianchi ni zaidi ya kibara. Uso unafunikwa na ganda la barafu lenye unene wa kilomita 1.6 au zaidi. Halijoto ya duni inayojulikana ilipimika mwaka 1983 kuwa sentigredi 89,4 chini ya sifuri. Visiwa Visiwa kadhaa vinahesabiwa kuwa sehemu za Antaktiki. Baadhi ya visiwa hivyo viko ndani ya maji ya bahari. Vingine vinafunikwa na barafu ya kudumu na hivyo haionekani mara moja ya kwamba kuna kisiwa, maana sehemu nyingi ngao nene ya barafu ya kudumu inaingia baharini nje ya pwani. Visiwa hivi ni pamoja na Kisiwa cha Alexander ambacho ni kisiwa kikubwa cha Antaktiki; kina upana wa kilomita 200, urefu wa kilomita 378 na eneo la km² 49,070. Kinatengwa na bara kwa mfereji wa bahari mwenye upana wa kilomita 24-60, lakini yote inafunikwa kwa barafu ya kudumu ila tu sehemu ya pwani inaiongia katika maji ya bahari. Kisiwa cha Berkner ambacho ni kisiwa kikubwa cha pili chenye urefu wa 320 km, upana wa 135 km na eneo la km² 43,873. Kinafunikwa kabisa na ngao ya barafu, hakionekani hata kutoka baharini. Visiwa vya Joinville, Roosevelt, Ross na kadhalika. Milima Milima mingi ni sehemu ya Safu ya Milima ya kuvukia Antaktiki (au: milima transaktiki) ambayo ni safu ndefu yenye urefu wa kilomita 3,500 na kufikia kimo cha mita 4500 na zaidi. Ncha za milima yake mirefu zinaonekana juu ya uso wa ngao ya barafu inayofunika bara lote. Mlima mrefu katika safu hii ni Mlima Kirkpatrick wenye urefu wa mita 4528 juu ya UB. Pale ambako Rasi ya Antaktiki inaanza kuna safu ya milima ya Ellsworth na huko uko mlima mrefu kabisa wa bara: ni Mlima Vinson wenye mita 4,892 juu ya UB. Kuna pia volkeno kadhaa, nyingine zimelala, nyingine ziko hai. Volkeno hai ndefu inayotema moto barani ni Mlima Erebus wenye kimo cha mita 3,794: iko kwenye kisiwa cha Ross. Ngao ya barafu ya kudumu Tabia ya pekee ya Antaktiki ni ngao ya barafu inayofunika karibu uso wote wa nchi yake pamoja na sehemu za bahari ya karibu. Ngao ya barafu hii ni mkusanyiko mkubwa wa barafu duniani. Unene wake (yaani kimo juu ya ardhi) unafikia hadi mita 4,500. Ngao ya barafu inajumlisha asilimia 90 ya barafu yote duniani asilimia 70 ya maji matamu yote duniani Ni asilimia 2-3 za eneo lote la bara zisizofunikwa na barafu, yaani km² 280,000 tu. Ngao hiyo ilianza kutokea miaka milioni kadhaa iliyopita. Uzito wake ni mkubwa na inaaminiwa ya kwamba bara lote lilishuka chini kiasi na kama siku moja ngao ya barafu itapotea litapanda tena juu mita kadhaa. Barafu hii inashika maji mengi kiasi kwamba kama barafu yote itayeyuka siku moja uwiano wa bahari duniani kote itapanda juu takriban mita 61. Mito, maziwa na barafuto Tabia ya pekee ya Antaktiki ni pia uhaba wa mito. Mito yote inayotokea ni ya maji ya barafu ya kuyeyuka wakati wa "majira ya joto" katika miezi ya Februari na Machi. Katika sehemu nyingine ya mwaka mito yote inaonekana kama kanda la barafu. Mto mkubwa ni Onyx unaofikia urefu wa kilomita 30 ukiishia katika Ziwa Vanda. Mito haina samaki, lakini katika ile mikubwa zaidi kuna mikrobi na algae. Kuna maziwa kadhaa chini ya ngao ya barafu. Hata kama jotoridi yake ni chini ya sentigredi 0 baadhi yanaweza kuwa na maji ya kiowevu kwa sababu shinikizo kubwa ya ngao ya barafu linashusha halijoto ya kugandisha maji, hasa kama maji ni ya chumvi. Barafu ya ngao haikai kimyakimya lakini yote ina mwendo ikifuata mtelemko wa uso wa nchi. Katika sehemu kadhaa barafu ina mwendo wa haraka zaidi na sehemu hizi zinaitwa "mito ya barafu" na ni aina ya barafuto. Mito ya barafu hii iko yenye urefu hadi kilomita mia kadhaa, upana wa 50 km na unene wa kilomita 2. Mwendo unafikia hadi mita 1.000 kwa mwaka. Pale inafikia kwenye ufuko wa bahari inajenga ulimi wa barafu inayosukumwa katika maji. Hali ya kisiasa Antaktiki si nchi wala dola na hakuna wenyeji au wananchi. Lakini madola mbalimbali yalitangaza madai ya kutawala sehemu za eneo lake. Madai haya hayalingani na mara kadhaa kuna mataifa mbalimbali yanayodai sehemu ileile. Mataifa yanayodai kutawala sehemu za Antaktiki ni pamoja na Argentina, Australia, Chile, Ufaransa, New Zealand, Norwei na Ufalme wa Maungano. Tangu mwaka 1961 kuna Mkataba wa Kimataifa kuhusu Antaktiki unaosimamisha madai yote ya utawala bila kuyafuta. Mataifa yote yana haki ya kuwa na vituo vya kisayansi. Mapatano ya kando yaliweka masharti makali kwa shughuli za kiuchumi na hadi sasa imewezekana kuzuia migodi na uchimbaji wa madini. Mengineyo Mtoto wa kwanza kuzaliwa barani huko alizaliwa mwaka 1984. Kwa sasa kuna shule kadhaa na kanisa moja la Waorthodoksi Warusi. Marejeo Viungo vya nje Antarctic Place-names Commission of Bulgaria L.L. Ivanov et al, Topographic map of Livingston Island and Greenwich Island British Services Antarctic Expedition 2012 Antarctic Treaty Secretariat, de facto government British Antarctic Survey (BAS) U.S. Antarctic Program Portal Australian Antarctic Division South African National Antarctic Programme – Official Website Portals on the World – Antarctica from the Library of Congress NASA's LIMA (Landsat Image Mosaic of Antarctica) (USGS mirror) The Antarctic Sun (Online newspaper of the U.S. Antarctic Program) Antarctica and New Zealand (NZHistory.net.nz) Journey to Antarctica in 1959 – slideshow by The New York Times Listen to Ernest Shackleton describing his 1908 South Pole Expedition The recording describing Shackleton's 1908 South Pole Expedition was added to the National Film and Sound Archive's Sounds of Australia registry in 2007 Map of Antarctican subglacial lakes Video: The Bedrock Beneath Antarctica Antaktika Bara
1798
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ubaguzi%20wa%20rangi
Ubaguzi wa rangi
Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha kuthamini au kutenga binadamu kwa misingi ya rangi za ngozi. Ubaguzi wa rangi ulikuwa maarufu sana katika nchi kama Afrika Kusini kwa jina la "apartheid" na Marekani kwa jina la "segregation" ambapo huko Waafrika walikandamizwa kutokana na rangi yao katika kupata huduma mbalimbali za kijamii na kimaendeleo. Wakati wa ukoloni, rangi ilitumika kama msingi wa utoaji huduma muhimu mfano: shule, matibabu na haki nyingine za kibinadamu. Rangi nyeusi ilipewa hadhi ya chini zaidi. Siku hizi katika karibu nchi zote, sheria zinapinga ubaguzi wa rangi. Lakini katika nchi nyingi bado kuna wabaguzi wachache ambao wanavunja sheria kwa kuendelea kubagua. Kwa mfano, kuna wabaguzi wanaobagua Watu weusi nchini Marekani, nchini China, nchini India na katika nchi za Ulaya. Viungo vya nje Mkutano wa Kimataifa Dhidi ya Ubaguzi
1799
https://sw.wikipedia.org/wiki/Utumwa
Utumwa
Utumwa ni mfumo unaotoa fursa kwa binadamu kummiliki binadamu mwenzake kama mali yake. Binadamu anayemilikiwa anakuwa na hadhi sawa na chombo au kifaa chochote kinachoweza kuuzwa. Mfumo huu ulianza kabla ya uandishi kubuniwa, ukawa maarufu hasa kabla ya harakati za ukoloni duniani, mathalani kuanzia karne ya 15, ambapo watumwa walihitajika katika shughuli za kilimo na uchimbaji madini katika sehemu mbalimbali za ulimwengu, hasa Amerika, ingawa katika sehemu nyingine, hasa Uarabuni, walitafutwa hasa watumwa wanawake kwa ajili ya uasherati. Mfumo huu huunda matabaka ya "mabwana" ambao humiliki watumwa na "watwana" ambao ni watumwa wenyewe. Utumwa tofautitofauti Katika historia zilitokea aina mbalimbali za utumwa. Kulikuwa na utumwa wa muda (yaani mtu huwa mtumwa kwa miaka kadhaa) au kwa maisha yote. Kulikuwa na utaratibu ambao watoto wa mtumwa walikuwa watumwa tena, hivyo kuzaliwa watumwa; kulikuwa pia na utaratibu wa kwamba watoto wa watumwa walitazamiwa kama watu huru. Kulikuwa na jamii ambako watumwa hawakuwa na haki kabisa, yaani mabwana waliweza kuwatendea jinsi walivyotaka, hata kuwaua; lakini kulikuwa pia na jamii zilizojua haki fulani za watumwa: hapo watumwa waliweza kuwa na mali ya binafsi na kwa njia hii hata kununua uhuru wao kutoka kwa mabwana. Watumwa katika utumishi wa watawala waliweza kupata nafasi muhimu katika jamii; mfano ni Wamameluki wa Misri waliokuwa watumwa wanajeshi wakatawala nchi hiyo kwa karne kadhaa. Chanzo cha utumwa Chanzo cha utumwa kilikuwa mara nyingi ama vita ama madeni. Vitani waliotekwa wakauzwa kama watumwa wakihesabiwa kama sehemu ya uwindo wa washindi. Sababu kuu nyingine ilikuwa madeni ya watu waliokamatwa na kuuzwa ili madeni yalipwe kwa njia hii. Mahitaji ya kiuchumi ya kupata watumwa wengi yalisababisha biashara ya watumwa. Uchumi wa Roma ya Kale ulitegemea watumwa waliokamatwa na kusafirishwa kutoka pande zote za mazingira ya Bahari Mediteranea. Milki za makhalifa wa Uislamu ziliendelea kutegemea watumwa. Waosmani walichukua watoto wa Kikristo, hasa kutoka nchi za Balkani, na kuwapeleka kama watumwa katika sehemu za kusini za milki yao kama Misri walipofanya kazi kama wanajeshi. Biashara ya Waarabu kuhusu watumwa ilidumu miaka 1,300, na kupeleka mamilioni ya Waafrika upande wa Asia. Mahitaji ya uchumi wa kimataifa tangu karne ya 15 yalisababisha kuongezeka kwa biashara ya watumwa hasa kutoka Afrika; mamilioni walikamatwa na watawala wa milki kwenye pwani za Afrika au Waarabu na kuuzwa kwa wafanyabiashara Wazungu waliowapeleka Amerika walipohitajika kwa kazi kwenye mashamba makubwa ya miwa na pamba. Biashara hii ilianza kupingwa zaidi tangu mwisho wa karne ya 18. Mkutano wa Vienna (1814-1815) ulikuwa mapatano ya kwanza ya kimataifa yaliyolenga kukataza biashara ya watumwa kutoka Afrika. Hata hivyo iliendelea kwa miaka kadhaa hasa upande wa bahari Hindi ambako wanafayabiashara Waislamu kama Tippu Tip waliendelea kukamata watumwa na kuwapeleka pwani na Zanzibar kulikokuwa na soko la watumwa kubwa kuliko yote. Ukoloni ulimaliza kwa kiasi kikubwa biashara hiyo Afrika pia, ingawa Mauritania ilifanya utumwa kuwa kosa la jinai mwaka 2007 tu. Tangu karne ya 20 utumwa na pia biashara ya watumwa zimepigwa marufuku katika mapatano ya kimataifa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Lakini miaka ya hivi karibuni imeona biashara mpya inayotumia nafasi za usairi wa kisasa; hata kama duniani hakuna utumwa kisheria tena, ni hasa wanawake na mabinti wanaouzwa kwa kazi haramu ya ukahaba kati ya nchi na nchi. Uislamu na utumwa Uislamu ulikubali utumwa, hivyo katika nchi zinazofuata dini hiyo utumwa ulichelewa zaidi kufutwa. Lakini Waislamu walifundishwa masharti fulani kama kuwatendea watumwa vizuri. Walifundishwa pia kwamba ni tendo jema mbele ya Mungu (Allah) kumwacha huru mtumwa. Ukombozi wa watumwa Tazama makala kuu Wendo wa ukomeshaji wa utumwa Katika historia ndefu za utumwa, kulitokea juhudi za kukomboa waliotekwa, hasa kwa kuwanunua ili kuwaacha huru. Kati ya Wakatoliki yalianzishwa hata mashirika maalumu ya kitawa kwa lengo hilo, kwa mfano Watrinitari na Wamersedari. Ukristo na utumwa Kwa muda mrefu utumwa ulikuwa utaratibu wa kijamii katika sehemu nyingi za dunia. Habari za kwanza za kimaandishi juu ya Afrika Mashariki (karne ya 2 K.K.) zilisema: "wanaleta kutoka pwani ile ndovu, dhahabu na watumwa". Kule Ulaya kuna kundi la mataifa linaloitwa tangu zamani "Waslavi" (kama vile Warusi, Wapolandi, Waserbia n.k.). Kumbe neno "slavi" kiasili linamaanisha "watumwa": watu wa mataifa yale walikamatwa zamani na kuuzwa kama watumwa katika sehemu nyingine za Ulaya, Asia na pia Afrika Kaskazini. Hali hiyo ni mbaya sana, hailingani kabisa na utu na heshima ya kibinadamu, wala haipatani na Ukristo unaokiri na kulenga udugu wa watu wote. Lakini watu walioishi zamani katika mazingira yenye utumwa walikuwa wamezoea hali hiyo. Habari za watumwa tunaweza kuzisoma hata katika Biblia. Ilikuwa jambo la kawaida katika mazingira ya Israeli ya Kale. Mtu aliweza kukamatwa na kuuzwa utumwani ili kulipia madeni yake. Mara nyingi watumwa walikuwa watu waliokamatwa vitani. Kwa mfano wakazi wote wa Yerusalemu walifanywa watumwa baada ya mji huo kutekwa na wanajeshi Waroma mwaka 70 B.K. Wakati wa Biblia asilimia 20 hivi za wakazi wa Dola la Roma walikuwa watumwa. Lakini katika nchi ya Israeli hali ilikuwa tofauti. Sheria ya Musa ilimwacha mtumwa awe huru baada ya miaka 7 (Kut 21:2). Kwa sababu hiyo hawakuwapo watumwa wengi katika Israeli. Labda ndiyo sababu Yesu hakufundisha juu ya utumwa kwani walikuwa wachache sana katika mazingira yake. Mtume Paulo aliishi zaidi nje ya eneo la Israeli. Katika miji mikubwa kama Antiokia, Korintho, Efeso au Roma watumwa walikuwa wengi. Paulo alifundisha ni wajibu wa mabwana Wakristo kuwatendea watumwa wao vizuri. Kwa nini hakupinga utumwa? Wataalamu wengi hudhani kwamba Paulo alitegemea kurudi kwake Yesu na mwisho wa dunia kuwa karibu sana, hivyo hakuona umuhimu wa kubadilisha taratibu za kijamii. Lakini alisititiza kwamba ndani ya Kanisa ni marufuku kutofautisha kati ya watumwa na walio huru. Ukristo uliweza kuvuta watumwa wengi, kwani uliwakubali kuwa binadamu wenye utu na heshima kamili. Wapinzani wa Ukristo waliuita "Dini ya watumwa". Walau mtumwa mmoja alichaguliwa kuwa Askofu wa Roma. Kanisa Katoliki linamkumbuka kama Mtakatifu Papa Kalisti I. Baada ya uenezaji wa Ukristo utumwa ulipungua sana Ulaya. Vilevile walimu wengi Wakristo walipinga utumwa wenyewe. Hatimaye mabadiliko ya uchumi yaliondoa faida ya kutumia watumwa. Hali hii ilibadilika baada ya kuanzishwa kwa ukoloni Amerika. Wareno na Wahispania walioteka nchi za huko walivutwa na tamaa ya dhahabu. Mataifa ya Ulaya yalipeleka ng'ambo mara kwa mara wafungwa wao kwa nia ya kusafisha jamii zao na kupunguza gharama za magereza. Watu waliona kule mbali hawawezi kusababisha hasara. Kumbe hawakujali hali ya wenyeji walioteswa na wale wakorofi walioona nafasi ya kujitajirisha. Hata maafisa wa serikali za kikoloni walishindwa kuwadhibiti vizuri kwani waliwategemea katika kuwatawala wenyeji ambao hawakunyamaza kwa hiari. Ndipo wamisionari walipojitahidi kupambana na ukorofi uliokuwepo, lakini kiasi: jinsi mapato kutoka makoloni yalivyokuwa muhimu kwa makisio ya serikali za Ulaya, haikuwa rahisi kupambana na unyonyaji katika makoloni ya mbali. Kanisa Katoliki halikukubali rasmi biashara ya watumwa, lakini Mapapa waliona hawana nguvu ya kuizuia. Walijaribu zaidi kuweka masharti jinsi ya kuwatendea watumwa. Mataifa kadhaa yalifuata mafundisho ya Kanisa: k.mf. Hispania na Ufaransa zilikataa kuwa na soko la watumwa lakini zilifunga macho raia wao wakiendesha biashara hiyo nje ya mipaka yao. Wengine kama Wareno hawakuona tatizo kufanya biashara hiyo. Watumwa wa kwanza kutoka Afrika waliingia Ureno wakati Mfalme wa Ureno alipokubali kupokea kutoka kwa Waarabu wa Moroko watumwa kadhaa kama malipo ya madeni. Wapelelezi Wareno walioanza kuzunguka pwani za Afrika walileta tena na tena wafungwa kama watumwa. Lakini mpaka wakati ule walikuwa wachache kwani Ulaya soko lilikuwa dogo. Kumbe baada ya kuanzishwa kwa makoloni Amerika watumwa walitafutwa sana kwa ajili ya kulima mashamba makubwa na kuchimba madini kule. Hivyo ukoloni Amerika ulisababisha kukua kwa mahitaji ya watumwa. Hapo utaratibu wa kale wa utumwa ulipanuka kuwa mbaya sana kuliko awali. Milioni nyingi za Waafrika waliuawa katika vita vya kukamata watumwa na nyingine nyingi wakapelekwa wamefungwa kule Amerika katika hali ya kutisha. Vurugu iliyoharibu jamii nyingi za Kiafrika ndiyo iliyosababisha vilevile uharibifu wa misheni za Kikristo katika karne za 16-18. Uharibifu wa taratibu za kijamii ulikuwa mbaya zaidi katika maeneo ya pwani yaani kulekule walipoingia wamisionari. Si ajabu kwamba Waafrika wengi walishindwa kutambua tofauti kati ya wamisionari Wareno na wafanyabiashara ya watumwa kutoka taifa lilelile. Hali ilikuwa mbaya zaidi wamisionari wenyewe walipojiingiza katika mambo ya utumwa kama walivyofanya wengine. Kwa jumla ni aibu kubwa kwamba Wakristo wengi walitumia muda mrefu mno kutambua kwamba Ukristo na utumwa havipatani. Mwanzoni awamu mpya ya utumwa haikuonekana kwa watu wengi kule Ulaya, maana uliendeshwa hasa Afrika na Amerika. Lakini habari zake zilienea. Mara walijitokeza waliopinga utumwa au waliojaribu kupunguza nguvu yake. Lakini wakati ule katika nchi mbalimbali za Ulaya hata wakulima wengi hawakuwa huru kweli (ingawa si watumwa). Katika karne ya 17 kule Uingereza Wakristo wa madhehebu ya "Marafiki" (waliitwa pia "Quakers") waliamua kwamba utumwa haupatani na Ukristo, hivyo mwenye watumwa anajitenga nayo. Polepole wengine wakaunga mkono hoja hiyo hata likajitokeza tapo la kufuta utumwa. Wakristo wa tapo hilo walimshtaki Mwingereza mlowezi katika Visiwa vya Karibi aliyetembelea Uingereza akiwa na mtumwa. Mwaka 1772 hakimu aliamua si halali kuwa na watumwa katika nchi hiyo. Wapinzani wa utumwa wakaendelea kusukuma Bunge la Uingereza. Lakini matajiri wa Liverpool (waliofaidika na utumwa kama wenye meli au kwa sababu waliendesha biashara ya watumwa wenyewe) walitetea vikali hali halisi. Katika karne ya 19 polepole utumwa na biashara ya watumwa vilikomeshwa katika sehemu nyingi za dunia. Mtawanyiko ndani ya Kanisa ulikuwa jambo wa kusikitisha sana. Kumbe hapa tumepata mfano jinsi Mungu alivyotumia vikundi vidogovidogo kuelimisha Wakristo wote. Maana madhehebu makubwa yalikosa nguvu ya kupinga vikali utumwa kwa kuwa karibu mno na serikali, tena matajiri. Ni Wakristo wa madhehebu madogo kama Marafiki au Wamethodisti waliotangulia na kusaidia Wakatoliki, Waanglikana na Wareformati kutambua ukweli. Hali nyingine iliyosaidia kukomesha utumwa ni mabadiliko ya uchumi. Umuhimu wa kazi ya watumwa ulipungua sana kutokana na njia mpya za kuzalisha mali. Si tena wafanyabiashara ya "Biashara kati ya Amerika, Ulaya na Afrika" (Triangular trade) waliokuwa na pesa nyingi (hivyo na athari pia) katika jamii ya Uingereza. Waliopata uzito zaidi ni mabepari ambao waliendesha viwanda wakitumia wafanyakazi huru na si watumwa. Hivyo ubepari ulibadilisha mkazo ndani ya jamii mbalimbali. Tazama pia Ukomeshaji wa Biashara ya Watumwa Sarah Baartman Suema Akumboke Yosefina Bakhita Marejeo Ya jumla Bales, Kevin, Disposable People: New Slavery in the Global Economy (1999) Campbell, Gwyn, Suzanne Miers, and Joseph C. Miller, eds. Women and Slavery. Volume 1: Africa, the Indian Ocean World, and the Medieval Atlantic; Women and Slavery. Volume 2: The Modern Atlantic (2007) Davis, David Brion. The Problem of Slavery in the Age of Revolution, 1770-1823 (1999) Davis, David Brion. The Problem of Slavery in Western Culture (1988) Drescher, Seymour. Abolition: A History of Slavery and Antislavery (2009) highly regarded history of slavery and its abolition, worldwide Finkelman, Paul, ed. Encyclopedia of Slavery (1999) Gordon, M. Slavery in the Arab World (1989) Greene, Jacqueline. Slavery in Ancient Egypt and Mesopotamia, (2001), ISBN 0-531-16538-8 Joseph, Celucien L. Race, Religion, and The Haitian Revolution: Essays on Faith, Freedom, and Decolonization (CreateSpace Independent Publishing Platform, 2012) Joseph, Celucien L. From Toussaint to Price-Mars: Rhetoric, Race, and Religion in Haitian Thought (CreateSpace Independent Publishing Platform, 2013) Miers, Suzanne, and Igor Kopytoff, eds. Slavery In Africa: Historical & Anthropological Perspectives (1979) Morgan, Kenneth. Slavery and the British Empire: From Africa to America (2008) Postma, Johannes. The Atlantic Slave Trade, (2003) Rodriguez, Junius P., ed., The Historical Encyclopedia of World Slavery (1997) Rodriguez, Junius P., ed. Slavery in the United States: A Social, Political, and Historical Encyclopedia (2007) Shell, Robert Carl-Heinz Children Of Bondage: A Social History Of The Slave Society At The Cape Of Good Hope, 1652–1813 (1994) Westermann, William Linn The Slave Systems of Greek and Roman Antiquity (1955), ISBN 0-87169-040-3 Vyanzo visivyotajwa Hogendorn, Jan and Johnson Marion: The Shell Money of the Slave Trade. African Studies Series 49, Cambridge University Press, Cambridge, 1986. The Slavery Reader, ed. by Rigas Doganis, Gad Heuman, James Walvin, Routledge 2003 Marekani Baptist, Edward E. The Half Has Never Been Told: Slavery and the Making of American Capitalism. Basic Books (2014). ISBN 046500296X Berlin, Ira. Many Thousands Gone: The First Two Centuries of Slavery in North America (1999), most important recent survey Blackmon, Douglas A. Slavery by Another Name: The Re-Enslavement of Black Americans from the Civil War to World War II Doubleday (March 23, 2008), ISBN 0-385-50625-2 ISBN 978-0-385-50625-0 Boles, John. Black Southerners: 1619–1869 (1983) brief survey Engerman, Stanley L. Terms of Labor: Slavery, Serfdom, and Free Labor (1999) Genovese Eugene D. Roll, Jordan Roll (1974), classic study Richard H. King, "Marxism and the Slave South", American Quarterly 29 (1977), 117–31, a critique of Genovese Parish, Peter J. Slavery: History and Historians (1989) Phillips, Ulrich B. American Negro Slavery: A Survey of the Supply, Employment and Control of Negro Labor as Determined by the Plantation Regime (1918; paperback reprint 1966), southern white perspective Phillips, Ulrich B. Life and Labor in the Old South (1929) Sellers, James B. Slavery in Alabama (1950). Sydnor, Charles S. Slavery in Mississippi (1933) Stamp, Kenneth M. The Peculiar Institution: Slavery in the Ante-Bellum South (1956), a rebuttal of U B Philipps Vorenberg, Michael. Final Freedom: The Civil War, the Abolition of Slavery, and the Thirteenth Amendment (2001) Weinstein, Allen, Frank O. Gatell, and Lewis Sarasohn, eds., American Negro Slavery: A Modern Reader, third ed. (1978) Nyakati zetu Jesse Sage and Liora Kasten, Enslaved: True Stories of Modern Day Slavery, Palgrave Macmillan, 2008 ISBN 978-1-4039-7493-8 Tom Brass, Marcel van der Linden, and Jan Lucassen, Free and Unfree Labour. Amsterdam: International Institute for Social History, 1993 Tom Brass, Towards a Comparative Political Economy of Unfree Labour: Case Studies and Debates, London and Portland, OR: Frank Cass Publishers, 1999. 400 pages. Tom Brass and Marcel van der Linden, eds., Free and Unfree Labour: The Debate Continues, Bern: Peter Lang AG, 1997. 600 pages. A volume containing contributions by all the most important writers on modern forms of unfree labour. Kevin Bales, Disposable People. New Slavery in the Global Economy, Revised Edition, University of California Press 2004, ISBN 0-520-24384-6 Kevin Bales (ed.), Understanding Global Slavery Today. A Reader, University of California Press 2005, ISBN 0-520-24507-5 Kevin Bales, Ending Slavery: How We Free Today's Slaves, University of California Press 2007, ISBN 978-0-520-25470-1. Mende Nazer and Damien Lewis, Slave: My True Story, ISBN 1-58648-212-2. Mende is a Nuba, captured at 12 years old. She was granted political asylum by the British government in 2003. Gary Craig, Aline Gaus, Mick Wilkinson, Klara Skrivankova and Aidan McQ­ e (2007). Contemporary slavery in the UK: Overview and key issues, Joseph Rowntree Foundation. ISBN 978-1-85935-573-2. David Hawk, The Hidden Gulag - Slave Labor Camps in North Korea, Washington DC: Committee for Human Rights in North Korea, 2012, ISBN 0-615-62367-0 Somaly Mam Foundation Thomas Sowell, The Real History of Slavery, in: Black Rednecks and White Liberals, San Francisco: Encounter Books, 2005. ISBN 978-1-59403-086-4. Viungo vya nje Zamani Slavery Resource Guide, from the Library of Congress Digital Library on American Slavery African Holocaust Emory and Oxford College The West African Sqron and slave trade Slavery – PBS Understanding Slavery Slavery http://www.ull.ac.uk/specialcollections/archives/slaveryarchivesources.shtml Archives on slavery held by the University of London] (archive) Mémoire St Barth (archives & history of slavery, slave trade and their abolition), Comité de Liaison et d'Application des Sources Historiques. Archives of the Middelburgsche Commercie Compagnie (MCC) 'Trade Company of Middelburg' (Inventory of the archives of the Dutch slave trade across the Atlantic) Nyakati zetu news-politics, modern-slavery Modern Slavery - slideshow by The First Post Slavery – PBS Walk Free Foundation – Global Slavery Index 2013 | Explore the Index Uchumi Siasa Utumwa
1800
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukoloni
Ukoloni
Ukoloni ni mfumo wa taifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja za uchumi, utamaduni na jamii. Maeneo hayo yanaweza kuitwa makoloni ya kawaida au maeneo lindwa tu. Jina Neno "koloni" linatokana na Kilatini colonia (kupitia Kiingereza colony). Ni kwamba Roma ya Kale ilipanua eneo lake kwa kuanzisha miji mipya ya nje kwa kuteua raia na kuwapa ardhi kwa ajili ya mashamba huko. Hiyo iliitwa koloni. Milki nyingine za kale zilitumia mtindo huohuo kama vile Wagiriki wa Kale na Wafinisia. Neno hilo la Kilatini lilitumiwa baadaye kwa ajili ya kutaja makazi mapya ya watu kutoka eneo moja katika eneo la mbali. Ilhali hatua hii ilimaanisha mara nyingi pia upanuzi wa utawala wa eneo mama, neno likataja baadaye pia eneo linalotawaliwa na nchi ya mbali. Historia Ukoloni ni hasa ule wa kipindi tangu karne ya 15 ambako Ureno na Hispania zilianza kueneza himaya zao Afrika na Amerika ya Kusini na kudumu pengine hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Lakini kulikuwa na vipindi vya ukoloni pia zamani katika historia kama vile ukoloni wa Roma ya Kale, ukoloni wa Waarabu na wengine. Ukoloni kwa maana hii unaweza kuwa tofauti na kuundwa kwa koloni katika vipindi mbalimbali vya historia ambapo maeneo bila wakazi au yenye wakazi wachache sana yaliingiliwa na watu kutoka sehemu nyingine. Ukoloni mamboleo ni aina ya nchi au kundi la nchi fulani kutawala nchi nyingine kinyemela kwa kuweka vikwazo na masharti yatakayowafanya watawaliwa waendelee kuwa na uchumi tegemezi ili watajirishe zaidi hao wanaowatawala kinyemela. Utawala wa kikoloni Utawala wa kikoloni ni utawala ulioanzishwa hasa na Wazungu kwa lengo la kunyonya na pengine kuwabagua Waafrika na watu wengine wenyeji wa Asia, Oseania na Amerika. Utawala huo ulitegemea hali ya taifa husika pamoja na hali ya jamii zilizokuwa zinatawaliwa. Baada ya kuanzisha utawala huo wakoloni walibadilisha utawala wa jadi na kuufanya utawale kwa masilahi ya wakoloni; pia utawala huo uliharibu hadhi ya utawala wa jadi na misingi ya jadi. Muundo wa utumishi Muundo wa utumishi katika utawala wa kikoloni ulikuwa wa kibaguzi na kinyonyaji: (a) Kazi katika ngazi za juu zilifanywa na Wazungu, hasa kazi zilizohitaji ujuzi. (b) Kazi katika ngazi za chini zilifanywa na wenyeji kama vile ukarani, utarishi, ufagizi na ukorokoroni. (c) Wakoloni walitoa elimu duni kwa wenyeji ili waendelee kuwaajiri katika ngazi za chini. Makoloni yaliyokuweko Afrika Nchi za Afrika ziliwekwa rasmi chini ya ukoloni wa nchi za Ulaya mara baada ya Mkutano wa Berlin wa 1885 ulioitishwa na chansella wa Ujerumani Bismarck mwaka 1884-1885. Nchi zilizojenga ukoloni huo Afrika zilikuwa Uingereza, Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Uhispania, Italia na Ubelgiji. Uholanzi karne za nyuma ilikuwa na Afrika Kusini. 1. Ubelgiji ilikuwa na maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda ya leo 2. Uingereza ilikuwa na Afrika Kusini, Botswana, Cameroon ya Kiingereza, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Misri, Nigeria, Shelisheli, Sierra Leone, Somaliland, Sudan, Swaziland, Tanganyika, Uganda, Zanzibar, Zambia, Zimbabwe na sehemu nyingine kwa muda. 3. Ufaransa ilikuwa na Algeria, Benin, Cameroon, Chad, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jibuti, Komoro, Gabon, Guinea, Madagaska, Mali, Mauritania, Moroko, Niger, Senegal, Togo, Tunisia na sehemu nyingine kwa muda. 3. Ujerumani ilikuwa na Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani (leo Namibia), Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (tangu 1922 Burundi, Rwanda na Tanganyika), Kamerun na Togo, lakini baada ya vita vikuu vya kwanza ilinyang'anywa kila mojawapo; zilikuwa maeneo ya kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa na kuweka chini ya Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika Kusini. 4. Italia ilikuwa na Eritrea, Libya na Somalia ya Kiitalia; pia Ethiopia kwa miaka mitano tu (1936-1941). 5. Ureno ilikuwa na Angola, Cape Verde, Guinea-Bissau, Msumbiji, Sao Tome na Principe 6. Hispania ilikuwa na Guinea ya Ikweta, sehemu za Moroko na Sahara Magharibi. Tazama pia Koloni nyakati za kale Koloni Vitabu Maria Petringa. Brazza, A Life for Africa (2006). ISBN 978-1-4259-1198-0 Historia ya Afrika Ukoloni
1841
https://sw.wikipedia.org/wiki/Burundi
Burundi
{| border="1" cellpadding="2" cellspacing="0" align="right" width="330px" style="margin-left:15px; border-collapse:collapse; border-color:#f2f2f4" |+<font size="+1">Republika y'u Burundi (Kirundi) République du Burundi (Kifaransa)Jamhuri ya Burundi</font> | align="center" colspan="2" | |---- | Lugha rasmi || Kifaransa, Kirundi, Kiswahili |---- | Mji Mkuu || Gitega au Bujumbura |---- | Serikali || Jamhuri |---- | Rais || Évariste Ndayishimiye |---- | Eneo || km² 27,834 |---- | Eneo la Rwanda Kazembe || km² 123.553 |---- | Idadi ya wakazi || 10,395,931 (2014) |---- | Wakazi kwa km² || 373.4 |---- | Pesa || Burundi franc |---- | Wimbo wa Taifa || Burundi Bwacu (Burundi yetu) |---- | colspan="2" align="center"| |---- | colspan="2" align="center"| |}Jamhuri ya Burundi (iliyojulikana zamani kama Urundi') ni nchi ndogo ambayo iko katika eneo la Maziwa Makubwa ya Afrika. Burundi imepakana na Rwanda upande wa kaskazini, Tanzania upande wa mashariki, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi. Burundi ni mwanachama wa Umoja wa Afrika na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jina Jina lenyewe la nchi hii, limetokana kwa msingi na kutanuka kwa lugha ya Kirundi ambacho ni lugha ya Kibantu kama vile Kiswahili ambacho pia kinatumika sana. Jiografia Burundi ni kati ya nchi ndogo zaidi zilizomo barani Afrika. Eneo lote ni km² 27,834 pekee. Wakazi milioni 10 ni wengi kulingana na eneo dogo la nchi, msongamano wa watu ni wakazi 314.3 kwenye kila kilomita ya mraba. Ingawa Burundi haina bahari, sehemu ya mpaka wake eneo la mashariki unaishia kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika. Eneo lote ni nyanda za juu zenye kimo cha mita 1700 juu ya UB kwa wastani. Sehemu ya juu zaidi ni kilele cha mlima Heha chenye mita 2685 juu ya uwiano wa bahari uliopo katika safu ya milima inayopakana na bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Sehemu ya magharibi ya nchi ni sehemu ya bonde la ufa yenye kimo cha mita 760-850 juu ya uwiano wa bahari. Sehemu ya kusini ya bonde la ufa katika Burundi imejaa maji ya Ziwa Tanganyika. Upande wa mashariki wa safu ya milima inayopakana na bonde la ufa kuna chanzo cha mto Ruvyironza (pia: Luvironza) unaoishia katika mto Kagera na hivyo huhesabiwa kati ya vyanzo vya mto Naili. Hali ya hewa ni ya kitropiki: kuna vipindi viwili vya mvua. Joto linapungua kutokana na kimo cha nchi. Kuna mvua kwa wastani wa milimita 1,000 kwa mwaka. Matumizi ya ardhi ni kwa ajili ya kilimo au mifugo. Msongamano wa watu umesababisha kuenea kwa ukataji wa misitu, mmomonyoko wa ardhi na kupotea kwa ardhi yenye rutuba. Eneo la misitu lililobaki ni kilomita cha mraba 600 pekee linalopungua kwa kasi ya asilimia 9 kwa mwaka. Kuna hifadhi mbili za taifa ambazo ni Hifadhi ya Taifa ya Kibira kwenye kaskazini-magharibi (inapakana na Msitu wa Nyungwe huko Rwanda), na Hifadhi ya Taifa ya Ruvubu upande wa kaskazni-mashariki karibu na mto Rurubu (pia Ruvubu au Ruvuvu). Hifadhi zote mbili zilianzishwa mwaka 1982 kwa shabaha ya kuhifadhi wanyamapori. Watu Idadi ya watu ni takriban milioni 10 na nusu. Asilimia 46 kati yao hawajamaliza miaka 15. Umri wa wastani ni miaka 16.7 hivi. Idadi ya watoto wanaoaga dunia mapema, ni 62 kati ya 1000 wanaozaliwa (mwaka 2007). Kwa umri wa kifo kwa wastani ni miaka 54 tu. Takriban 1.2% za wananchi wana UKIMWI. Familia ni imara kuliko zile za nchi zote za Afrika. Wanawake wanazaa kwa wastani watoto 6: hii nafasi ya juu ya tano duniani kote. Jamii ya Burundi ni jamii ya vijijini, ni asilimia 13 pekee wanaoishi katika miji. Vikundi kati ya wakazi ni hasa Wahutu (~80%), Watutsi (~14%) na Watwaa (mbilikimo) (chini ya 1%). Wote wanatumia lugha ya Kirundi. Pamoja na hayo, kuna Warundi wachache wanaojinasibu kuwa wao si Watutsi wala Wahutu bali ni Waswahili (~5%). Hilo kabila lilikuwepo toka enzi za tawala za kifalme nchini humo, na ndio wenyeji wa jiji la Bujumbura, waliomsaidia Mwanamfalme Louis Rwagasore katika harakati za kutafuta uhuru wa Burundi. Dini Upande wa dini, Wakristo ni 80-90% kati ya wakazi wote, hasa Wakatoliki (65%), halafu Waprotestanti (26%). Asilimia 5 wanafuata dini za jadi na 3 Uislamu. Historia Historia ya awali Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo. Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Ufalme wa Burundi Dola la kwanza katika eneo hili lilikuwa Ufalme wa Burundi. Katika mapokeo ya wenyeji ulianzishwa katika karne ya 17 na mtu kwa jina la Cambarantama aliyefika ama kutoka Rwanda ama kutoka Buha katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania ya leo. Ufalme huo ulitawaliwa na kundi la Watutsi waliokuwa wafugaji wa ng'ombe na kutawala wenyeji waliokuwa wakulima Wabantu. Watutsi walikuwa tabaka la kikabaila. Mfalme au mwami alikuwa mkuu wa makabaila hao ambao walitazamiwa kama mabwana wa ardhi iliyolimwa na watu wa kawaida. Hao wakulima waliruhusiwa kulima nchi wakipaswa kutoa huduma na sehemu ya mavuno kwa mabwana waliopaswa kuwatetea dhidi ya maadui. Ufalme huo ulienea katika karne zilizofuata. Mwami Ntare IV Rutaganzwa Rugamba aliyetawala tangu mwaka 1796 hadi 1850 aliweza kupanua mipaka ya ufalme wake hadi kushika sehemu kubwa ya eneo la leo. Ukoloni Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa wapelelezi Waingereza Richard Burton na John Hanning Speke mnamo mwaka 1854. Lakini habari za falme kwenye eneo kati ya maziwa makubwa hazikuenea sana. Wakati wa Mkutano wa Berlin 1885 Wajerumani hawakujua ya kwamba falme za Burundi na Rwanda zilikuwepo ndani ya eneo waliotegemea kutwaa. Waliitambua baadaye tu. Mwaka 1894 Mjerumani wa kwanza alipita Burundi aliyekuwa Oskar Baumann. Wakati ule Ujerumani uliwahi tayari kuanzisha koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini Wajerumani walichelewa kufika kaskazini-magharibi mwa maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao. Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo 1896 wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika mji mkuu Gitega ambaye hakuhusika na mambo ya utawala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "Urundi". Hapa sawa na Rwanda na Bukoba Wajerumani walitumia mbinu ya eneo lindwa ingawa walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni lao. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa Ubelgiji kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa lililoitwa Ruanda-Urundi. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwachia mtemi mamlaka kubwa. Waliweka Ruanda-Urundi chini ya serikali ya Kongo ya Kibelgiji. Lakini baadaye walianza kuingilia zaidi, na ilhali wakati ule walipendelea Watutsi, karibu machifu wote walikuwa Watutsi, na Wahutu walipotea katika nafasi za uongozi kimahali. Tangu mwaka 1946 Shirikisho la Mataifa lilikwisha na Ubelgiji ilipokea wito wa kutawala Ruanda-Urundi na Umoja wa Mataifa. Uhuru Mwaka moja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi ya UM na chama mshindi kilikuwa UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore aliyemwoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na ukabila. Mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urundi uhuru kamili, lakini kila nchi pekee. Baada ya uchaguzi wa 1965 mapigano yalitokea kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali kilichukua serikali. Mwaka 1966 mwami alipinduliwa na mwanasiasa Michel Micombero aliyejitangaza kuwa rais na nchi kuwa jamhuri. Kuanzia hapo wanasiasa na watumishi wakubwa walio Wahutu walifukuzwa, kukamatwa au kuuawa. Hali ya nchi kijamii na kisiasa Burundi ilundwa kama ufalme ulioongozwa na Watutsi waliotawala Wahutu. Lakini kabla ya ukoloni mipaka kati ya makundi hayo haikuwa imara mno; Wahutu matajiri katika utumishi wa mwami waliweza kupanda ngazi na kuwa Watutsi na pia Watutsi maskini waliweza kushuka ngazi na kuhesabiwa kati ya Wahutu, hasa baada ya kuoa au kuolewa na mtu wa upande mwingine. Uhusiano wa makundi hayo ulifanana zaidi na ule wa matabaka si wa makabila tofauti, pia kwa sababu lugha ilikuwa moja kwa wote. Utawala wa kikoloni uliimarisha mipaka kati ya makundi hayo mawili maana kila mtu aliandikishwa na kupangwa katika moja kati ya makundi hayo. Pia Wabelgiji walipendelea Watutsi na kuangalia wapate nafasi zote za uchifu ambako walipaswa kutoa kibali. Kuhamia katika kundi lingine kulikwisha. Uhusiano kati ya makundi ulianza kufanana zaidi na ukabila. Mwishoni mwa ukoloni Wabelgiji walibadilisha msimamo na kupendelea Wahutu. Katika hali hiyo Burundi ilikaribia uhuru. Vyama vya siasa viliundwa vilivyofuata ugawaji wa kimbari kati ya Watutsi na Wahutu. Mapigano ya kwanza kati ya Wahutu na Watutsi yalitokea mwaka 1959 kabla ya uhuru yakakomeshwa na Wabelgiji. Baada ya uhuru katika Burundi, kinyume na Rwanda, utawala ulibaki upande wa Watutsi kwa sababu jeshi lilikuwa mikononi mwao. Vipindi vya mashambulio kati ya vikundi vilifuata. Mwaka 1972 malaki ya Wahutu waliuawa na jeshi la Kitutsi waliolenga hasa Wahutu wenye elimu. Mwaka 1993 uongozi wa Kitutsi ulikubali tena uchaguzi huru ambako Mhutu Melchior Ndadaye alichaguliwa kuwa rais. Alipouawa na wanajeshi Watutsi malaki ya Watutsi waliuawa na Wahutu wakali. Kipindi kilichofuata kilikuwa cha Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika sehemu mbalimbali za nchi. Tangu mwaka 1995 Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zilijitahidi kujenga mapatano kati ya vikundi. Marais na wanasiasa walioshiriki katika jitihada hizo walikuwa pamoja na Julius Nyerere, Boutros Boutros-Ghali, Nelson Mandela, Thabo Mbeki na rais wa Marekani Bill Clinton. Mapatano yalifikiwa na kusainiwa mwaka 2000 na washiriki karibu wote huko Arusha. Majadiliano yaliendelea hadi mwaka 2003 hatimaye vita ilisimamishwa. Mapatano yaliyofikiwa yanasema ya kwamba Watutsi pamoja na Watwa, ambao ni asilimia 15 za wananchi, watakuwa na asilimia 40 ya nafasi kwenye bunge na ya kwamba jeshini kila upande utashika asilimia 50 za nafasi. Pia kwenye senati ya bunge kila upande utakuwa na asilimia 50. Rais atachaguliwa na wananchi wote lakini mapatano yalisema rais wa kwanza atachaguliwa na bunge. Siasa Mwaka 2005 uchaguzi wa kwanza wa bunge baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ulifanyika. Chama cha CNDD-FDD kilipata kura nyingi na kiongozi chake Pierre Nkurunziza alichaguliwa na bunge kuwa rais wa taifa. Vyama vya UPRONA na FRODEBU vilivyotangulia kuongoza serikali ya mpito vilipata kura chache kwa sababu vilishtakiwa kuwa na rushwa na upendeleo wa kindugu. Chama tawala kinajaribu kufuata siasa ya mapatano ya ndani, lakini ina uvumilivu mdogo tu kwa upinzani na mawazo yanayopinga siasa yake. Mwezi Aprili 2009 chama cha Palipehutu FNL hatimaye kilisimamisha upinzani kwa silaha kikakubaliwa kama chama cha kisiasa cha FNL. Nkurunziza alichaguliwa tena kwa kura ya wananchi wote mwaka 2010. Chama cha upinzani FNL kilikataa kukubali ushindi wa CNDD-FDD. Mwaka 2015 rais Nkurunziza alipendekezwa kugombea tena urais katika uchaguzi akakubali. Hatua hiyo ilisababisha upinzani mkali wa wananchi walioandamana wakiona hii inavunja mapatano ya amani ya Arusha. Tarehe 13 Mei jenerali Godefroid Niyombare alitangaza kufukuzwa kwa Nkurunziza kutoka urais wakati huyo alikuwa safarini Tanzania, lakini uasi huu wa kijeshi ulikandamizwa. Nkurunziza alirudi na kutangaza ya kwamba kura inatakiwa kufanyika jinsi ilivyopangwa tarehe 26 Mei 2015 kwa bunge na tarehe 26 Juni kwa urais. Taasisi ya kimataifa na nchi jirani walitamka wasiwasi kuhusu mwelekeo wa hali ya kisiasa katika Burundi. Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa kamati tendaji ya Umoja wa Afrika, aliomba kuahirishwa kwa kura nchini Burundi hadi hali iwe imetulia. Tarehe 24 Julai 2015 Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Nkurunziza mshindi wa uchaguzi kwa 69.41% za kura. Agathon Rwasa alishika nafasi ya pili kwa 18.99% ingawa alikuwa amehimiza wananchi wasipige kura. Kilichofuata kimesababisha wananchi 200,000 wakimbie, huko rais akikataza Umoja wa Afrika usitume askari kulinda amani na haki nchini, wakati wanajeshi wanaendelea kuua na kunyanyasa Watutsi wakielekea mauaji ya kimbari. Utawala Burundi imegawiwa katika mikoa 17 (kwa Kifaransa province, kwa Kirundi: IProvense) inayoitwa kufuatana na miji yenye makao makuu ya utawala. *Angalia Mikoa ya Burundi Mikoa imegawiwa kwa wilaya inayoitwa "communes" na hii imegawiwa kwa "collines" (vilima). Tazama pia Orodha ya miji ya Burundi Orodha ya mikoa ya Burundi Orodha ya Marais wa Burundi. Kandanda nchini Burundi Waandishi wa Burundi Muziki wa Burundi Mawasiliano nchini Burundi Mahusiano ya kimataifa ya Burundi Jeshi la Burundi Usafiri nchini Burundi Uislamu nchini Burundi Ukristo nchini Burundi Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Tanbihi Marejeo Mambo mengi ya Burundi yamepatikana kutoka CIA World Factbook 2000 na 2003 U.S. Department of State website. Burundi: Ethnic Conflict and Genocide'' Reni Lemarchand and Lee H. Hamilton Viungo vya nje Serikali Tovuti ya serikali ya Burundi Habari Agence Burundaise de Presse (ABP) Habari za Burundi toka tovuti ya habari ya allAfrica - Burundi Radio Isanganiro Radio binafsi nchini Burundi kwa Kifaransa na Kirundi na Kiswahili. umuco.com Habari kuhusu Burundi kwa Kifaransa Burundi Réalités Habari na Uchambuzi kwa Kiingerenza na Kifaransa. Overviews BBC News - Country Profile: Burundi CIA World Factbook - Burundi Maendelezo Open Directory Project - Burundi directory category Stanford University - Africa South of the Sahara: Burundi directory category University of Pennsylvania - African Studies Center: Burundi directory category Yahoo! - Burundi directory category Vinginevyo Burundian Human Rights Organisation "Ligue Iteka" - with up-to-date news in English and French Campaign for the prosecution of FNL leader Agathon Rwasa Human Rights Watch reports on Burundi Woodrow Wilson Center Reports on Burundi Human Rights Watch special report on the August 2004 Gatumba massacre Links to political analyses from 1998 on by the International Crisis Group Reuters Alertnet - Burundi humanitarian news Updated humanitarian news from the United Nations Office for the Coordination of Humanitarian Affairs Umoja wa Afrika Nchi za Afrika Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa Jumuiya ya Afrika Mashariki
1843
https://sw.wikipedia.org/wiki/Eritrea
Eritrea
Eritrea ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Mashariki na Kusini-Mashariki Eritrea ina pwani ndefu katika Bahari ya Shamu. Upande wa Magharibi imepakana na Sudan, upande wa Kusini imepakana na Ethiopia, na Kusini-Mashariki kuna nchi ya Djibouti. Eneo hili lote hujulikana pia kama Pembe ya Afrika. Jina Jina la nchi limetungwa mnamo mwaka 1890 na wakoloni wa Italia kutokana na neno la Kigiriki "erythraîa" linalomaanisha “bahari nyekundu” – kwa Kiingereza “Red Sea”. Hii ni kwa sababu Bahari ya Shamu iliitwa "Sinus Erythraeus" na mabaharia Wagiriki au “Mare Erythraeum” kwa Kilatini na Waroma wa kale – maana yake ni "bahari nyekundu". Jiografia Eritrea iko katika eneo la Pembe la Afrika na ina Bahari ya Shamu upande wa kaskazini mashariki. Kwa mchanga wa pwani ulio eneo kame pahali pa kutega samaki ni Funguvisiwa la Dahlak. Eneo ambalo liko kwa milima kusini si kame vile, lakini hali ya hewa ni poa. Mlima wa juu zaidi ni Soira, ambao uko kati ya nchi, mita 3018 juu ya bahari. Miji Mji mkuu wa Eritrea ni Asmara na miji mingine ni kama vile mji wa bandari Assab kusini mashariki, na pia miji kama Massawa na Keren. Eneo Eritrea imegawiwa katika maeneo 6: Kati (Maekel) Anseba Kisini ziwa lekundu (Debubawi-Keih-Bahri) Kaskazini ziwa lekundu (Semienawi-Keih-Bahri) Kusini (Debub) Gash-Barka Historia Hadi karne ya 19 maeneo ya Eritrea yalikuwa sehemu ya Ethiopia. Pwani ilikaa karne nyingi chini ya utawala wa Uturuki au baadaye Misri kama nchi zenye nguvu kwenye Bahari ya Shamu. Historia ya Eritrea kama eneo la pekee jinsi ilivyopata uhuru mwisho wa karne ya 20 ilianza na ukoloni wa Italia. Mwanzo wa ukoloni wa Italia Mnamo Novemba 1869 kampuni ya biashara ya Kiitalia ya Rubattino ilinunua bandari ya Assab kutoka kwa sultani wa Afar. Ilikuwa inatafuta kituo kwa meli zake zilizoanza kupita katika bahari ya Shamu baada ya kufunguliwa kwa Mfereji wa Suez mwaka uleule. Serikali ya Misri ilipinga mapatano hayo kwa sababu ilidai eneo lilikuwa chini ya amri yake. Makubaliano hayakufikiwa hadi 1882, serikali ya Italia ilipochukua moja kwa moja mali ya kampuni kama koloni lake la kwanza katika Afrika. Tangu kuporomoka kwa utawala wa Misri nchini Sudan, baada ya vita vya Al-Mahdi, Misri ilijiondoa pia katika pwani ya kusini mwa bahari ya Shamu. Italia ilitumia nafasi hiyo na tarehe 5 Februari 1885 ilipeleka wanajeshi mjini Massawa na kuitangaza kuwa koloni lake. Waitalia waliendelea kuunganisha maeneo yao ya Assab na Massawa. Baadaye walijaribu kupanua utawala wao kutoka tambarare za pwani hadi nyanda za juu zilizokuwa chini ya Dola la Ethiopia. Negus Yohanne IV hakufurahia kufika kwa Italia kwa sababu aliamini ya kwamba Massawa iliahidiwa kwake baada ya kuwasaidia Wamisri kujiokoa mbele ya jeshi la Al-Mahdi. Hivyo upanuzi wa Italia katika nyanda za juu ulikutana na upinzani. Tarehe 26 Januari 1887 jeshi la Waitalia 587 walioelekea kaskazini lilishambuliwa karibu na Massawa kwenye kijiji cha Dogali na kushindwa na Ras Alula aliyekuwa mtemi chini ya Negus ya Ethiopia. Waitalia walipaswa kuongeza wanajeshi 13,000 ili kuhakikisha utawala wao. Mkataba wa Wuchale na mapigano ya Adowa Baada ya Yohanne IV kufariki katika mapigano na jeshi la Al-Mahdi, Waitalia walichukua nafasi hiyo ya kuziingia nyanda za juu za Tigray na kujenga vituo vyao huko. Mfalme mpya Menelik II tarehe 2 Mei 1889 aliutia sahihi mkataba wa Wuchale uliokubali utawala wa Italia juu ya kanda ya pwani pamoja na maeneo kadhaa ya nyanda za juu za Tigray. Waitalia walijaribu kumdanganya Negus katika mkataba huo kwa kuingiza maneno katika nakala ya Kiitalia yaliyosema "Ethiopia itakuwa chini ya ulinzi wa Italia". Menelik baada ya kuelewa haya alikana mkataba. Italia ilijibu kwa kuvamia Ethiopia kwa jeshi kubwa. Jeshi hilo lilishindwa na Waethiopia katika mapigano ya Adowa tarehe 1 Machi 1896. Italia ilipaswa kukubali uhuru wa Ethiopia katika mkataba wa amani tarehe 26 Oktoba 1896. Ethiopia ilikubali mamlaka ya Italia juu ya koloni lake katika kaskazini. Koloni la Eritrea Baada ya kumaliza mashindano na Ethiopia, Italia tarehe 1 Januari 1890 iliunganisha maeneo yake yote katika koloni lililoitwa Eritrea kufuatana na jina la kale "Bahari ya Eritrea". Katika kipindi hiki cha utawala wa kikoloni Eritrea ilitokea kama jamii na eneo la pekee. Koloni la Eritrea liliunganisha maeneo matatu yenye tabia za pekee: kanda la pwani lililokuwa na historia ndefu ya biashara na mawasiliano na Uarabuni ng'ambo ya Bahari ya Shamu kanda la Sahel katika kaskazini-magharibi lililowahi kuwa sehemu ya Sudan kanda la nyanda za juu liliwahi kuwa sehemu ya utamaduni wa Watigray Wakristo Italia ilianzisha miradi ya kufanya Eritrea chanzo cha malighafi kwa ajili ya uchumi wa Italia. Kijiji cha Asmara katika nyanda za juu kilikuwa mji mkuu wa koloni na kupanuliwa kuwa mji kwa ajili ya walowezi Waitalia. Asmara ilipambwa na majengo mazuri ya kisasa. Katika miaka ya 1930 idadi ya motokaa zilizoendeshwa Asmara ilishinda idadi ya magari ya binafsi mjini Roma. Urithi huo wa majengo umekuwa sababu ya kuingiza Asmara katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO. Waitalia walipanga na kujenga miji mingine kama vitovu vya biashara, mabandari, vituo vya kijeshi au vya kiuchumi. Idadi ya wakazi wote ilikadiriwa kuwa takriban 200,000 mwaka 1890. Idadi hiyo iliongezeka haraka kufikia zaidi ya 600,000 mnamo 1939. Mabadiliko makubwa yalitokea hasa katika nyanda za juu ambako walowezi Waitalia walianzisha mashamba yao na miji mikubwa zaidi ilijengwa. Idadi ya wasemaji wa Kitigrinya iliongezeka kutoka asilimia 35 mwaka 1905 kuwa asilimia 54 mwaka 1939. Mwisho wa vita kati ya vikundi mbalimbali na kupatikana kwa huduma za kiafya pamoja na kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula, vyote vilichangia katika kuongezeka kwa idadi ya watu. Kati ya mabadiliko makubwa ulikuwa ujenzi wa barabara na reli kati ya Massawa, Asmara, Keren na Agordat. Viwanda kadhaa vilianzishwa, pia migodi ya kuchimba mawe au madini. Sehemu za Waeritrea waliingia katika maisha ya ajira ya kibepari. Hivyo maarifa ya wakazi wa Eritrea hasa katika nyanda za juu yalikuwa tofauti na wenzao katika Ethiopia yenyewe walioendelea kuishi chini ya utaratibu wa kikabaila. Waeritrea walisukumwa katika maisha ya kisasa na uchumi wa fedha. Hadi mwaka 1940 Eritrea ilikuwa tayari na tabaka la wafanyakazi wa viwandani na katika miji pia tabaka la wasomi wenye elimu ya kisasa. Baada ya Mussolini kushika serikali, siasa ya Italia ilibadilika. Wafashisti walidharau Waafrika na kuanzisha siasa ya ubaguzi wa rangi. Wenyeji walipewa tu shughuli duni kabisa katika utumishi wa serikali. Italia ya kifashisti ilifanya mipango ya kulipizia kisasi mapigano ya Adowa ikiandaa vita dhidi ya Ethiopia. Vita vilianza mwaka 1935 kutoka ardhi ya Eritrea. Silaha mpya za Italia (zikiwemo za kikemikali) zilishinda jeshi la Negus, hivyo Ethiopia yote ikawa koloni la Italia kwa miaka michache. Waitalia walishindwa katika Vita Vikuu vya Pili mwaka 1941, ambapo Waingereza waliteka Ethiopia pamoja na Eritrea. Baada ya vita vikuu vya pili Waingereza walitawala Eritrea hadi 1952. Mwaka huo Umoja wa Mataifa ulikabidhi Eritrea kwa Ethiopia kama eneo la pekee lenye serikali na bunge lake katika shirikisho. Mfalme wa Ethiopia, Haile Selassie hakupendezwa na utaratibu huoː alilenga kuunganisha tena Eritrea na Ethiopia na kwa mbinu mbalimbali alipata kura ya bunge la Eritrea ya kujivunja na kuwa jimbo la Ethiopia (1962). Vita vya kupigania uhuru Baada ya tukio hilo vikundi vya wanamgambo walienda porini kupigania kwa silaha uhuru wa Eritrea. Vita vilitapakaa mwaka 1974 baada ya ufalme kupinduliwa na Umaksi kuingia na rundo la Jeshi lililoitwa Derg kuchukuwa mamlaka, na baadaye kuvamia Eritrea. Ukorofi wa serikali ya Mengistu Haile Mariam ulifanya mengi kuongeza waliotumaini uhuru wa Eritrea katika miaka ya 1980. Ukombozi wa Eritrea ulitegemea rundo la Eritrean Liberation Front (ELF), ambayo pia inaitwa "Jebha", na Eritrean People's Liberation Front (EPLF), ambaye pia inaitwa "Shaabia". ELF ilikuwa na Waislamu wengi wa pwani na wahifadhi wa tedo za wananchi, na EPLF wengi Wakristo kutoka nyanda za juu za Tigrayi waamini wa Umaksi-Ulenin. ELF ilisaidiwa na wafadhili Waarabu, na EPLF kutoka nchi za kikomunisti zilizokuwa upande wa Urusi, lakini baadaye nchi hizo zikapinduka na kusaidia Derg ya Mengistu Haile Mariam. ELF na EPLF hazikuweza kufanya kazi pamoja na kwa hiyo EPLF ikaimaliza ELF na kuendelea kutafuta uhuru. Vita vya uhuru vilikwisha mwaka 1991, ambapo Waeritrea na waasi Waethiopia kutoka Tigray walishinda jeshi la Ethiopia na kuteka Addis Ababa; serikali ya Derg ikaanguka miaka miwili baadaye. Eritrea huru Baada ya kura ya wakazi wa Eritrea kukubali karibu kwa kauli moja, uhuru wa nchi ulitangazwa tarehe 24 Mei 1993 na kukubaliwa kimataifa. Tangu hapo nchi inaendeshwa na chama kimoja bila uchaguzi. Awali uhusiano na serikali mpya ya Ethiopia ulikuwa mzuri, lakini baada ya miaka ya kwanza ulizorota. Mwaka 1998 kulitokea vita kati ya Eritrea na Ethiopia vilivyokwisha na ushindi wa Ethiopia. Wanajeshi la kulinda amani la UM wanajaribu kutunza hali ya kutopigana. Kiongozi wa EPLF, Isaias Afewerki, akawa Rais. Eritrea (EPLF or Shaebia), ikawa chama pekee kinachotawala Eritrea kwa sheria na kubadilisha jina People's Front for Democracy and Justice (PFDJ). Mwaka 1998, vita vya mpaka na Ethiopia vilileta kifo kwa wanajeshi wengi kwa nchi zote mbili, na Eritrea uchumi wake ukafifia na wananchi wakahangaika sana. Umma wa nchi ukanza kuhama na uchumi kukosa maendeleo. Eritrea ni nchi moja ya Afrika ambapo kuna shida ya mabomu ya ardhi. Serikali ya Ethiopia iliwafukuza WaEritrea ambao waiishi Ethiopia ama watu waliokuwa na utamaduni wa Eritrea baada ya vita na Eritrea. Hii iliwaletea Waeritrea shida na uhamaji. Hata baada ya kuonyesha maendeleo kidogo kwa uchumi na siasa, serikali ya Eritrea inanyanyasa magazeti na waandishi na pia watu kwa siasa. Serikali yenyewe hata haijaweza kuweka Katiba mpya na kuleta kura ya kidemokrasia. Baadaye, serikali ya Eritrea imeweza kusisitiza desturi ya ukoloni wa Waitalia ambayo inadai Kanisa na Dini kujiandikisha kwa serikali na kupewa ruhusa wa kuhubiri. Dini zilizopewa ruhusa na serikali ni Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea, Kanisa Katoliki, Kanisa la Mekane Yesus (Walutheri) na Uislamu. Nyingine zote, hasa zenye itikadi kali zimebanwa kote nchini. Vita vya Eritrea na Ethiopia viliisha mwaka 2000 kwa mashauriano yanayojulikana kama Mapatano ya Algiers. Mojawapo ya makubaliano lilikuwa kuanzisha Muungano wa kimataifa wa kuweka amani, ambao unajulikana kama Muungano wa Kimataifa wa misheni ya Eritrea na Ethiopia (UNMEE); Walinda amani 4,000 wa UM wamebaki kutoka mwezi Agosti 2004. Makubaliano mengine ya Algiers yalikuwa kuanzisha usawazisho wa mwisho wa mpaka uliyobishaniwa kati ya Eritrea na Ethiopia. Komisheni iliyokuwa na madaraka kutoka kwa UM, iliyoitwa Komisheni ya Mpaka wa Ethiopia na Eritrea (EEBC), baada ya mashauriano mrefu, ilikata maamuzi ya mwisho mnamo Aprili 2002, lakini maamuzi yao yakakataliwa na Ethiopia. Kutoka Oktoba 2005 bishano la mpaka bado lilibaki kuwa suala nyeti, na wanajeshi wa kulinda amani wa UM walijaribu kutunza hali ya kutopigana. Hatimaye mwaka 2018 waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed alimaliza mgogoro huo. Kumbe mwaka 2020 Eritrea ilimuunga mkono dhidi ya Jimbo la Tigray lililotaka uhuru na kulivamia. Siasa Bunge la Taifa la viti 150, liliyotekezwa mwaka 1993 baada ya Uhuru, lilimchagua Rais wa sasa, Isaias Afewerki. Kura za nchi huwa zinapangwa na kupanguliwa. Shina za taarifa madaraka za kutangaza habari kwa siasa za nyumbani Eritrea haziko; na Septemba 2001 serikali ilifunga vyombo vya habari vya binafsi, na watu wanaopinga serikali hufungwa bila kushtakiwa. Hii yote ni kutoka taarifa ya washufu wa ulimwengu, kama Waangalizi wa haki za Kibinadamu (Human Rights Watch) na Wakombozi wa Kimataifa (Amnesty International). Mambo ya nje yanahusu vita na Ethiopia, Sudan na Jibuti. Baada ya wajumbe wa serikali ya Eritrea wa Idara ya mambo ya kigeni kuenda Sudan, ushirikiano umeanza kuwa wa kawaida. Bishano na Ethiopia bado ni wazo kubwa la chuki ambalo limemfanya Rais kuuambia Umoja wa Mataifa ichukue hatua. Uagizaji huu umeelezwa kwa barua kumi na moja za Rais. Watu Wakazi wa Eritrea walikadiriwa kuwa 6,380,803 mwaka 2014. Makabila makubwa ni Watigrinya (55%) na Watigre (30%), ambao wote wawanazungumza lugha za Kiafrika-Kiasia. Nchi haina lugha rasmi ili kuheshimu sawasawa lugha zote. Hata hivyo Kitigrinya, Kiarabu na Kiingereza vina nafasi za pekee. Serikali inatambua rasmi Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea, Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri pamoja na Uislamu. Makadirio yanatofautiana: Wakristo kwa jumla ni 50-68%, Waislamu 36-48%. Mwaka 2004 Idara ya taifa ya Marekani (U.S. State Department) iliamua kwamba Eritrea ni Nchi mahsusi ya kufuatiliwa (Country of Particular Concern, au CPC) kwa kufinya uhuru wa dini. Tazama pia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Orodha ya mito ya Eritrea Tanbihi Nchi za Afrika Umoja wa Afrika Bahari ya Shamu Pembe ya Afrika
1848
https://sw.wikipedia.org/wiki/Umoja%20wa%20Mataifa
Umoja wa Mataifa
Umoja wa Mataifa (UM) (Kiingereza: United Nations, UN) ni shirika la kiserikali ambalo malengo yake ni kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa, na kuwa kituo cha kuoanisha matendo ya mataifa. Ni umoja wa nchi zote duniani isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa dola huru. Umoja huo ulianzishwa na nchi washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kuchukua nafasi ya Shirikisho la Mataifa (1919 - 1946). Makubaliano yalifikiwa tarehe 24 Oktoba 1945 huko San Francisco, California. Mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka 2017 kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali ya Ukulu mtakatifu (Vatikani) na Palestina ambazo zinashiriki kama watazamaji wa kudumu, zikiwa na haki karibu zote isipokuwa kupiga kura. Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia sheria na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama usalama, amani, maendeleo ya jamii na ya uchumi, haki za binadamu, uhuru, demokrasia n.k. Toka mwanzo makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako Manhattan, New York City, New York nchini Marekani na hayako chini ya mamlaka ya nchi hiyo. Ofisi nyingine ziko Geneva (Uswisi), Nairobi (Kenya) na Vienna (Austria). Lugha rasmi za UM ni sita: Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Kihispania, Kiingereza na Kirusi. Katibu Mkuu wa UM anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni António Guterres kutoka Ureno, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka 2016 akichukua nafasi ya Ban Ki-moon. Muundo wa UM UM una vyombo vitano: Mkutano Mkuu wa UM (United Nations General Assembly) Baraza la Usalama la UM (United Nations Security Council) Ofisi Kuu ya UM (United Nations Secretariat) Mahakama Kuu ya Kimataifa (International Court of Justice) Baraza la Uchumi na Ustawi wa Jamii la UM (ECOSOC = Economic and Social Council) Cha sita kilikuwa Baraza la Wafadhili la UM (Trusteeship Council), ambacho kimesimama mwaka 1994. Baraza la Usalama linaamua kutuma walinzi wa amani wa UM penye maeneo ya ugomvi. Mashirika ya pekee ya UM UNICEF (United Nations Children's Fund) - Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa WHO (World Health Organization) Taasisi ya Afya ya Ulimwengu FAO (Food and Agriculture Organization) - Taasisi ya Chakula na Kilimo UNESCO (United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization) - Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni ILO (International Labour Organization) Taasisi ya Kimataifa ya Kazi IMF (International Monetary Fund) - Mfuko wa Fedha wa Kimataifa UNCTAD (United Nations Conference on Trade and Development) - Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara na Maendeleo ITC (International Trade Centre (UNCTAD/WTO) - UNDCP (United Nations Drug Control Programme) - Taasisi ya Kimataifa ya Mpango wa Kusimamia Madawa UNDP (United Nations Development Programme) - Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo UNIFEM (United Nations Development Fund for Women) Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Wanawake UNV (United Nations Volunteers) UNEP (United Nations Environment Programme) Mpango wa Kimataifa wa Mazingira UNFPA (United Nations Fund for Population Activities) UNHCR (Office of the United Nations High Commissioner for Refugees) UN-HABITAT (United Nations Human Settlements Programme) UNRWA (United Nations Relief and Works Agency for Palestine Refugees in the Near East) IAEA (Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia) inashirikiana na UM na kutoa taarifa kwa Baraza la Usalama hata kama si chini ya katiba ya UM UNDIO ( United Nations Data and Information Organization) Viungo vya nje Tovuti rasmi United Nations UN Works UN Chronicle Magazine About the United Nations United Nations Charter United Nations Security Council Resolutions United Nations Webcasts United Nations Volunteers Universal Declaration of Human Rights UN Organisation Chart Global Issues on the UN Agenda World Map of UN websites and locations Journal of the United Nations: Programme of meetings and agenda. High-level Panel on United Nations Systemwide Coherence The United Nations Regional Information Centre (UNRIC) Tanbihi Mashirika ya kimataifa
1855
https://sw.wikipedia.org/wiki/Marijani%20Rajab
Marijani Rajab
Marijani Rajabu (3 Machi 1955 - 23 Machi 1995) alikuwa mwanamuziki maarufu katika miondoko ya muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Historia yake na muziki Historia ya gwiji huyu ilianzia siku alipozaliw,a tarehe 23 Machi mwaka 1955, katika eneo la Kariakoo. Mama yake alikuwa mama wa nyumbani wakati baba yake alikuwa anafanya shughuli za uchapishaji. Maisha yake ya utoto yalikuwa ya kawaida ila alikuwa akipenda sana uimbaji wa Tabu Ley na mwimbaji mmoja wa Guinea Sorry Kandia. Alisoma shule ya Msingi ikiambatana na elimu ya Madrasa. Mwaka 1970 Akiwa bado shuleni, utaona umri wake ulikuwa miaka 15 tu, alijiunga na STC Jazz, ikiwa chini ya mpiga gitaa maarufu wakati huo Raphael Sabuni, kabla ya hapo bendi hii ilikuwa ikijulikana kama The Jets. Katika bendi hii Marijani aliweza kutoka nje ya Tanzania kwa mara ya kwanza ambapo alikwenda Nairobi na kurekodi nyimbo zilizotoka katika label ya Phillips. Hili jambo la mwanafunzi kusafiri na bendi likaleta shida na kwa vile (STC) ilikuwa mali ya umma akaachishwa kazi na mwaka1972 alijiunga na The Trippers ya David Mussa ambayo kwa wakati huo ilikuwa inapiga zaidi nyimbo za hoteli na za kukopi na muimbaji wao kiongozi wakati huo alikuwa Ali Rajabu. Marijani akiwa na The Trippers Hapa ndipo ubora wake ulifunguka haswa na kuweza kuinyanyua Trippers, ambayo sasa ilibadili jina na kuwa Safari Trippers kutokana na msimamo wa serikali wakati huo wa kutaka majina ya nyumbani yatumike bala ya yale ya kigeni na kuwa moja ya bendi maarufu za wakati huo. Waliweza kutoa vibao vilivyopendwa mfululizo na kuweza kuzunguka nchi nzima. Vibao kama Rosa Nenda Shule, Georgina, Mkuki Moyoni, viliweza kuuza zaidi ya nakala 10,000 za santuri na hivyo kuwezesha bendi kuwa na vyombo vyake vizuri. Bendi wakati huo ikiwa na wanahisa wanne, ambao kwa bahati mbaya wakati bendi ndio iko juu, wakakosa kuelewana na ukawa ndio mwisho wa bendi hiyo. Marijani alishiriki kutunga, kuimba nyimbo karibu zote za Trippers sanjari na kupiga gitaa kwa baadhi ya nyimbo. Mfano wimbo Olila ambao alipiga rhythm na kuimba. Marijani na DAR International Mwaka 1976, Marijani na baadhi ya wanamuziki wa Trippers waliamua kuihama bendi na kwenda baadaye kuasisi Dar es salaam International chini ya umiliki wa Mzee Zakaria Ndabemeye. Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja na Abel Baltazar kutoka Msondo, Kassimu Mponda kutoka Trippers, Abdallah Gama, Joseph Mulenga, Haruna Lwali na George Kessy Omojo waliokuwa wanapiga muziki Magot pale, Said Mohamed kutoka Polisi Jazz, Cosmas Chidumule kutoka Urafiki, Belesa Kakere kutoka Biashara Jazz, Joseph Bernard kutoka Trippers, Ali Rajabu kutoka Trippers, na King Michael Enock kutoka Dar es Salaam Jazz. Akiwa Dar Inter alishiriki kutunga nyimbo mbili, Betty na Sikitiko. Hata hivyo kama waswahili wanavyosema mafahari wawili hawakai zizi moja ndivyo ilivyotokea kati yake na Abel Balthazal kiasi cha hatimaye Marijani kufukuzwa ndani ya bendi kutokana na ubishi kuhusu wimbo aliotunga Marijani, kuna maelezo kuwa wimbo ulionekana unafanana na wimbo fulani toka Kongo na hivyo Marijani akatakiwa aubadilishe na ndipo ugomvi ukaanza. Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 1978, Marijani alirejeshwa tena kundini kutokana na rundo la wanamuziki wa Dar Inter kuihama bendi kwa kishindo kikubwa na kwenda kuifungua bendi mpya kabisa ya Orchestra Mlimani Park. Aliporejeshwa Marijani alikuja na wanamuziki wengi wapya wakati huo kama akina Christopher Kasongo, Mohamed Tungwa, Mafumu Bilal, Hamis Milambo, Athuman Momba, Mzee Alex Kanyimbo na wengine na kuja na mtindo wa Super Bomboka. Katika kudhihirisha hasira zake kwa Abel, Marijani alimtungia Abel wimbo wa kumnanga ukiitwa Kidudu Mtu ambao hata hivyo RTD waliukataa kuurekodi, jambo lililokuwa kawaida enzi hizo kwa redio kukataa wimbo. Sifa nyingine ambayo Marijani alikuwa nayo ni kuibua wanamuziki chipukizi kama alivyofanya mwaka 1983 alipomuibua kutoka Tanga kijana Mkuu Waziri Kungugu Kitanda Milima almaaruf Fresh Jumbe ambaye kwa hakika kabisa Marijani hakujutia kumchukua kijana huyo. Alimuamini kupita maelezo kiasi kwamba wakati mwingine alikuwa akimuachia bendi aongoze na yeye anapumzika nyumbani. Mbali na Fresh, wanamuziki wengine ni kama vile Tino Masinge, Mohamed Mwinyikondo, Juma Choka na wengine kibao. Baada ya kurekodi Zuena na Mwanameka na nyimbo nyingine katika album hiyo alichoambulia ni malipo ya nauli toka RTD ya sh 2500/- tu. Kilichosikitisha zaidi ni kuwa nyimbo zao tisa ziliuzwa kwa kampuni ya Polygram bila ridhaa yao. Hata hivyo safari ya Dar International ilikoma mwaka 1987 kutokana na sababu za kawaida za kufa kwa bendi lakini kubwa ni uchakavu wa vyombo. Hata hivyo Marijani aliendelea kufanya muziki na kwa kipindi kifupi amewahi kucheza na Kurugenzi ya Arusha na Mwenge Jazz ambayo alirekodi nayo wimbo mmoja wa Ukimwi na hata kupitia bendi ya Watafiti ambayo hatimaye ilikuja kuwa 38.. Mwaka huohuo wa 1987 Marijani na Muhidin Maalim Gurumo waliliongoza kundi la wanamuziki zaidi ya 50 kutunga nyimbo maalum hasa kwa maadhimisho ya miaka 10 ya CCM na 20 ya Azimio la Arusha. Kundi hilo lilijulikana kwa jina la Tanzania All Stars. Aidha mwaka 1994 aliwahi kurekodi zong zing na marehemu Eddy Sheggy. Bendi yake ya mwisho ilikuwa ni Africulture ama Mahepe Ngoma ya Wajanja, iliyokuwa mali ya Rogers Malila, alikokuwa na wanamuziki kadhaa kama akina Hassan Kunyata, Mgosi na wengine. Bado Marijani ataendelea kukumbukwa na wapenda muziki kote nchini na hata Afrika kwa ujumla kwa nyimbo zake zenye mafundisho na tamu huku akienzi utamaduni na ngoma za kwao Kigoma. Tazama pia Shaw Hassan Fresh Jumbe DAR International Waliozaliwa 1955 Waliofariki 1995 Wanamuziki wa Tanzania Muziki wa dansi
1856
https://sw.wikipedia.org/wiki/Uchoraji
Uchoraji
Kuhusu nyota angalia hapa Mchoraji (kundinyota) Uchoraji ni sanaa ya kuweka alama au picha kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kuchorea, kama vile kalamu ya wino au ya risasi, burashi, penseli za rangi ya nta, crayoni, makaa, choko, pastels, aina mbalimbali za erasers, markers, styluses, metali mbalimbali (kama silverpoint) na siku hizi hata elektroniki au kitu kingine cha kuandikia au kupaka rangi katika karatasi, kitambaa, ubao, metali, mwamba, kadi, plastiki, ngozi, canvas, na bodi au penginepo. Michoro ya muda mfupi inaweza kufanywa katika ubao mweusi au mweupe. Tokeo la uchoraji huitwa mchoro au picha. Mara nyingine picha huchorwa kwa ustadi mkubwa sana. Upatikanaji mpana wa vyombo vya kuchora hufanya uchoraji kuwa moja ya shughuli za kawaida za kisanii. Ni sanaa wakilishi maana inaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kwa jamii, hivyo imekuwa njia maarufu na ya msingi ya kujieleza kwa umma katika historia ya binadamu. Ni njia rahisi na yenye ufanisi zaidi ya kuwasiliana mawazo ya kuona. Mbali na namna zake zaidi za kisanii, kuchora mara nyingi hutumiwa katika biashara, usanifu, uhandisi na ufundi. Msanii anayeshughulikia au anafanya kazi katika kuchora kiufundi anaweza kuitwa pia mchoraji. Hata hivyo kuna aina tofauti za uchoraji. Hii inategemea mchoraji mwenyewe anapenda aina gani ya uchoraji: wakati mwingine sanaa hii ya uchoraji si ya kuwakilisha ujumbe tu, bali pia kumvutia mtazamaji kwa rangi za kupendeza bila kujali ujumbe uliobebwa na picha hiyo. Wakati mwingine inawezekana picha isiwe na ujumbe kabisa, lakini ikawa imechorwa kwa ustadi mkubwa na kupakwa rangi za kuvutia sana, mpaka mtazamaji kumvutia na kumfanya apende kuendelea kuitazama picha husika. Maelezo ya jumla Kuchora ni moja ya aina kuu za kujieleza ndani ya sanaa za kuona. Kwa ujumla ni wasiwasi na kuashiria mistari na maeneo ya toni kwenye karatasi / vifaa vingine, ambapo uwakilishi sahihi wa ulimwengu wa kuona unaonyeshwa juu ya uso wa ndege. Mchoro wa jadi ulikuwa monochrome, au angalau alikuwa na rangi kidogo, wakati michoro za kisasa za rangi za penseli zinaweza kufikia au kuvuka mipaka kati ya kuchora na uchoraji. Katika istilahi ya Magharibi, kuchora ni tofauti na uchoraji, ingawa mara nyingi vyombo vya habari vinavyoajiriwa katika kazi zote mbili. Vyombo vya kavu, vinavyohusishwa na kuchora, kama vile choko, vinaweza kutumika katika uchoraji wa pastel. Kuchora kunaweza kufanywa kwa kati ya kioevu, hutumiwa na maburusi au kalamu. Msaada sawa pia unaweza kutumika: uchoraji kwa ujumla unahusisha matumizi ya rangi ya kioevu kwenye tani iliyopangwa tayari au wakati mwingine, lakini wakati mwingine kutengeneza chini hutolewa kwanza kwa msaada huo huo. Kuchora mara nyingi huchunguza, kwa msisitizo mkubwa juu ya uchunguzi, kutatua matatizo na utungaji. Kuchora pia hutumiwa mara kwa mara katika maandalizi kwa ajili ya uchoraji, na kuendelea kuifanya tofauti yao. Michoro iliyoundwa kwa madhumuni haya inaitwa masomo. Kuna makundi kadhaa ya kuchora, ikiwa ni pamoja na kuchora takwimu, kuchora, kuchora, mkono wa bure na shading. Pia kuna mbinu nyingi za kuchora, kama vile kuchora mstari, kusonga, shading, njia ya surrealist ya entopic graphomania (ambayo dots hufanywa kwenye maeneo ya uchafu katika karatasi tupu, na mistari hufanyika kati ya dots), Na kufuatilia (kuchora kwenye karatasi inayojitokeza, kama vile kufuatilia karatasi, karibu na muhtasari wa maumbo yaliyomo ambayo yanaonyesha kupitia karatasi). Historia Picha za kale kabisa zinaonyesha uchoraji kwenye miamba katika mapango. Katika Afrika ni Wasan au watu waliokuwa karibu nao waliochora wanyama kwenye kuta za mipango walipopumzika. Picha zao zinapatikana kote katika Afrika ya Kusini hadi Tanzania ambako kuna mifano mbalimbali karibu na Kondoa. Mifano ya uchoraji wa aina hii imepatikana pia Ulaya, Asia na Australia. Hatujui mengi kuhusu namna nyingine za uchoraji wa kale kwa sababu vifaa vingine vilivyotumiwa havikudumu. Kutoka ustaarabu wa juu kama wa Misri, bonde la Indus au China tunajua mifano mingine ya uchoraji inayoonyesha hali ya juu zaidi. Katika ustaarabu wa madola ya kwanza wachoraji walikuwa tayari watu waliokuwa na nafasi ya kufuata sanaa yao bila haja ya kuwinda au kulima wenyewe, kwa sababu mtu mkubwa kama mfalme au kuhani aliwapatia riziki ya maisha. Katika makaburi ya Nubia, Ufalme wa Kush kuna picha zilizohifadhiwa ukutani. Makaburi ya Wamisri yalijengwa mara nyingi kwenye jangwa, kando ya bonde la Naili. Ukavu wa mazingira pamoja na giza vilitunza rangi vema. Wamisri wa Kale walichora watu bila kutofautisha mandharimbele au mandharinyuma. Wati muhimu waliochorwa wakubwa kuliko wale waliokuwa na cheo kidogo. Mwili ulionyeshwa mara nyingi kwa mbele lakini kichwa na uso kwa kando. Katika Ugiriki wa Kale uchoraji na wasanii wake waliheshimiwa sana. Philostrates aliandika mnamo mwaka 300 KK ya kwamba uchoraji ulibuniwa na miungu. Kuna taarifa juu ya picha lakini ni machache tu yaliyohifadhiwa kwa sababu ya hali ya hewa na kwa sababu picha nyingi zilichorwa juu ya ubao au matofali. Waroma wa Kale walituachia mifano mingi ya uchoraji wa ukutani; nje ya makaburi ni hasa nyumba za miji ya Pompei na Herkulaneo zilizofunikwa na majivu ya volkeno Vesuvio ambako picha nzuri zimehifadhiwa tangu mwaka 79 BK. Wakati ule wasanii walitofautisha tayari kati ya mandharimbele na mandharinyuma. Uchoraji wa China uliendelea sana kufuatana na utamaduni wake; mnamo mwaka 600 kuna picha za mandhari zinazoonyesha nchi na milima; msanii wa kwanza anayejulikana alitumia mbinu hii alikuwa Zhan Ziqian. Viungo vya nje On Drawing, an essay about the craft of drawing, by artist Norman Nason. Archived from the original on April 25, 2012. Leonardo da Vinci: anatomical drawings from the Royal Library, Windsor Castle, exhibition catalog fully online as PDF from The Metropolitan Museum of Art (a great drawing resource). Leonardo da Vinci, Master Draftsman, exhibition catalog fully online as PDF from The Metropolitan Museum of Art (a great drawing resource). Drawing in the Middle Ages A summary of how drawing was used as part of the artistic process in the Middle Ages. Sanaa Uchoraji
1857
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi%20elezo
Kamusi elezo
Kamusi elezo (pia: ensaiklopidia kutoka Kiingereza: encyclopedia) ni kitabu kinachokusudiwa kukusanya ujuzi wa binadamu kadiri iwezekanavyo kulingana na wingi wa kurasa zake. Siku hizi, Wikipedia ni kamusi elezo kubwa zaidi duniani lakini si kitabu cha karatasi, ni mkusanyo wa habari kwa umbo dijitali katika intaneti. Zamani (kabla ya kuja kwa Wikipedia) Encyclopedia Britannica ilikuwa kati ya kamusi elezo kubwa zaidi iliyokuwa ikitolewa kama vitabu vilivyochapishwa. Historia Katika historia yalikuwepo majaribio mbalimbali ya kukusanya ujuzi wote wa dunia. Mfano bora wa kale ni kamusi ya Yongle kutoka China iliyotungwa na wataalamu 2000 katika karne ya 14 na kuandikwa kwa mkono katika vitabu 1100. Lakini kamusi elezo au ensaiklopedia zimekuwa na athari kubwa sana tangu Johannes Gutenberg na kupatikana kwa uchapaji wa vitabu ulioshusha kabisa bei ya vitabu kwa watu wengi. Ensaiklopedia ya kwanza ya kisasa iliyokuwa na athira kubwa sana ilikuwa "Encyclopédie ou Dictionnaire raisonné des sciences, des arts et des métiers" iliyokusanywa na Denis Diderot pamoja na Jean Baptiste le Rond d’Alembert pamoja na waandishi zaidi ya 130 katika karne ya 18 huko Ufaransa. Kamusi elezo hii ikawa moja kati ya vyanzo vya harakati ya Zama za Mwangaza. Elimu
1858
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngoma
Ngoma
Neno ngoma lina maana mbalimbali: Ala ya muziki inayotumika sana barani Afrika. Muziki unaochezwa kwa kupiga ala hiyo. Muziki wa aina yoyote. Kucheza na muziki wa ngoma au wa aina yoyote. Katika lugha ya mitaani, ngoma inaweza kumaanisha virusi vya UKIMWI au Ukimwi wenyewe. Neno hili limetokana na methali ya Kiswahili isemayo, Ngoma ikivuma sana, mwishowe hupasuka. Ngoma (Ukerewe) ni kata ya wilaya ya Ukerewe kwenye mkoa wa Mwanza (Tanzania). Wilaya ya Ngoma iko mkoa wa Mashariki (Rwanda). Viungo vya nje Music
1859
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ellen%20Johnson-Sirleaf
Ellen Johnson-Sirleaf
Ellen Johnson-Sirleaf (alizaliwa 29 Oktoba 1938 nchini Liberia) amekuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika baada ya kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2005. Johnson-Sirleaf ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na katika mashirika ya kimataifa. Baada ya kumaliza masomo katika chuo kikuu cha Harvard, alifanya kazi katika serikali ya Rais William Tolbert mwaka wa 1970 akiwa ni Waziri wa Fedha. Johnson amekuwa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika. Hata hivyo yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Malikia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi yake kwa miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. Ruth Perry ni mwanamke wa kwanza Afrika kuwa mkuu wa nchi pale alipokuwa mwenyekiti wa urais wa pamoja wa jamhuri ya Liberia toka mwaka 1996 hadi 1997. Johnson-Sirleaf alihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela mwaka 1985 baada ya kushutumu utawala wa kijeshi nchini humo katika kampeni zake za kugombea ubunge. Alitumia kifungo hicho kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa na baadaye kukimbilia uhamishoni hadi aliporudi mwaka 1997 akiwa anafanyia kazi Benki ya Dunia na Citibank. Johnson-Sirleaf alimuunga mkono Charles Taylor wakati wa mapinduzi yake dhidi ya Jenerali Samuel Doe lakini baadaye alikuja kuwa mpinzani wake mkubwa na hata kugombea urais dhidi yake mwaka 1997. Taylor alimwandana na hata kumpeleka mahakamani kwa madai ya kuhusika na hujuma za kihaini. Uchaguzi wa urais mwaka 2005 ulirudiwa baada wagombea urais kutopata kura za kutosha. Katika raundi ya kwanza Johnson-Sirleaf alikuwa wa pili, wa kwanza alikuwa ni mpinzani wake mkubwa George Weah. Katika raundi ya pili ya uchaguzi, Johnson-Sirleaf alitangazwa kuwa mshindi. Hata hivyo, George Weah amepeleka mashtaka mahakama kuu akidai kuwa uchaguzi haukuwa wa haki. Mnamo Desemba 2021, James Sirleaf mmoja wa wana wa Ellen Sirleaf alikufa katika makazi yake huko Liberia chini ya hali isiyojulikana. Wasifu Ellen Johnson Sirleaf alizaliwa mjini Monrovia, mji mkuu wa Liberia, na elimu ya wazazi. Kabila lake ni nusu Gola kutoka upande wa baba yake, na robo Kru na robo Kijerumani kutoka upande wa mama yake. Babake Sirleaf Jahmale Carney Johnson, alikuwa mzaliwa wa Liberia wa kwanza kuweza kukaa katika mbunge la taifa. Sirleaf alisoma maswala ya uchumi na akaunti katika Chuo Afrika Magharibi mjini Monrovia. Aliolewa na James Sirleaf akiwa na miaka 17 tu na kuhamia Marekani katika mwaka wa 1961 ambapo aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Colorado na kuhitimu na shahada ya digri. Alisomea maswala ya uchumi na sera za umma katika chuo Chuo Cha Maswala Ya Serikali ya John F. Kennedy, mjini Harvard katika miaka ya 1969 na 1971 na kupata shahada ya maswala ya serikali. Kisha alirudi Liberia na kufanya kazi chini ya rais William Tolbert. Alikuwa naibu waziri wa fedha kati ya mwaka wa 1972 na 1973. Alikuwa waziri wa fedha toka mwaka wa 1979 hadi Aprili 1980. Aliweza kuwa naibu mwenyekiti wa benki ya CitiBank mjini Nairobi, Kenya kutoka mwaka wa 1983-1985. Aliwahi kufungwa mafungo ya nyumbani na Samule Doe aliyepindua serikali kwa kutangaza nia ya kugombea urais. Baadaye alienda uhamishoni. Kati ya miaka ya 1986-1992 alikuwa makamu wa rais na mwanachama wa bodi ya benki ya Equator, Washington, DC. Kati ya miaka ya 1988-1999 alikuwa mbunge wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Synergos. ALigombea urais kwa tiketi ya chama ya maungano(Unity Party) katika mwaka wa 1997 na kuwa Urais Ndiye rais wa sasa wa Liberia. Alimshinda alikuwa mwanasoka mashuhuri George Weah na zaidi ya asilimia ishirini katika uchaguzi wa mwaka wa 2005. Uzinduzi ulifanyika tarehe 16 Januari 2006 na ulihudhuriwa na wageni mashuhuri wakiwemo aliyekuwa waziri ya maswala ya kigeni wa Marekani, Condeleeza Rice, Laura Bush na Mitchelle Jean. Katika mwaka wa 2005 alianzisha tume ya ukweli na maridhiano ambayo ilitoa ripoti yake katika mwaka wa 2009. Hatamu za Uongozi 1972–1973:: Naibu Waziri wa Fedha wa Liberia 1979–1980: Waziri wa Fedha wa Liberia 1982-1985: Makamu wa Rais wa Kanda ya Afrika Ofisi ya Citibank, Nairobi 1986-1992: Makamu wa Rais na mwanachama wa bodi ya beni ya Ikweta, Washington, DC 1988-1999: Mbunge wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Synergos 1992-1997: Mkurugenzi wa Mpango wa Maendeleo ya Umoja wa mataifa Ofisi za bara Afrika 1997: Rais mgombea wa chama cha Umoja(Unity Party) 2004-2005: Mwenyekiti wa Tume ya Mageuzi ya Utawala Bora 2005:Mgombea urais kwa tikiti ya chama ya umoja 2006 hadi leo: Rais wa Liberia Nyadhifa nyingine zilizotangulia Mwanachama mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa kwa Wanawake katika uongozi wa kisiasa Mwanachama wa bodi ya ushauri wa kisasa wa Kukuza Uchumi na Uwekezaji Afrika Kampuni Afisa mwandamizi wa mkopo wa Benki ya Dunia Liberia
1860
https://sw.wikipedia.org/wiki/George%20Weah
George Weah
George Weah (alizaliwa Monrovia, 1 Oktoba 1966) ni rais wa Liberia kuanzia mwaka 2017. Kabla ya kuwa mwanasiasa aliwahi kuwa mwanakandanda mashuhuri duniani. Maisha Utoto, familia na kabila Weah ni wa kabila la Kru ambalo linatoka upande wa kusini-mashariki mwa Liberia kwenye Kaunti ya Grand Kru, ambayo ni moja ya maeneo maskini sana nchini humo. Wazazi wake walikuwa William T. Weah, Sr. na Anna Quayeweah. Alilelewa zaidi na bibi yake upande wa baba, Emma Klonjlaleh Brown. Weah alikulia jijini Monrovia katika kitongoji cha maskini cha Clara. Alihudhuria shule ya msingi katika shule ya Muslim Congress and sekondari katika shule ya Wells Hairston High School. Weah amemuoa Clar Weah, mwenye asili ya Visiwa vya Karibi. Wana watoto watatu: George Weah Jr, Tita na Timothy. Huyo, baada ya majaribio na timu ya Chelsea mwaka 2013, alijiunga na timu ya Paris Saint-Germain mwaka 2015. Timothy anaichezea pia timu ya taifa ya Marekani ya chini ya umri wa miaka 18. Binamu yake Weah, Christopher Wreh aliwahi pia kucheza soka la kulipwa kwenye timu ya Arsenal. Weah aliwahi kubadili dini toka Ukristo kwenda Uislamu na baadaye akarudi tena kwenye Ukristo. Hivi sasa ni muumini wa Ukristo wa Kiprotestanti. Elimu Kielimu, Weah ana Shahada ya Kwanza ya Uendeshaji Michezo toka Chuo Kikuu cha Parkwood, London, Uingereza. Hata hivyo baadhi ya watu wanatilia shaka shahada hii kwakuwa chuo hiki kinajulikana kwa kutoka shahada bila kusoma hapo. baadaye alipata shahada ya Usimamizi wa Biashara toa Chuo Kikuu cha DeVry, Miami nchini Marekani. Mwaka 1999 alipata shahada ya Udakitari ya Heshima toka Chuo Kikuu cha A.M.E Zion nchini Liberia. Katika soka Kabla ya kujiunga na soka la kulipwa, Weah alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Liberia kama fundi simu. Mwaka 1995 Weah alipewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) tuzo ya kuwa Mwanasoka Bora Duniani. Yeye ni mwanasoka pekee toka Afrika aliyewahi kupewa tuzo hiyo. Mwaka huohuo alichaguliwa pia kuwa Mwanasoka Bora Ulaya na Mwanasoka Bora Afrika. Miaka 1989, 1994 na 1995 alichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika na mwaka 1996 alichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Karne wa Afrika. Mwaka 2004, Pelé alimchagua kwenye orodha ya FIFA ya wachezaji bora ambao wako hai. Weah alianza safari yake ya soka katika timu Incincible Eleven ya Liberia na Tonnerre Yaounde ya Cameroon. Baada ya hapo alikwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya mwaka 1988. Alijiunga na timu ya Monaco ambayo ilikuwa ikifundishwa na Arsène Wenger ambapo aliiongoza kushinda kombe la Ufaransa mwaka 1991. Baadaye alijiunga na Paris Saint Germain mwaka 1992-95. Aliiongoza timu hii kuchukua kombe la ligi ya Ufaransa mwaka 1994. Akiwa hapo aliweza kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA Champions League) mwaka 1994–95. Mwaka 1995-2000 alikuwa akiichezea timu ya AC Milan ambayo ilishinda ligi ya Italia mwaka 1996 na 1999. Mwaka 2000 aliondoka AC Milan na kujiunga na Chelsea, baada ya muda mfupi alijiunga na Manchester City na baadaye Marseille mwaka 2001. Alimaliza soka la kulipwa akiwa na timu ya Al JAzira ya Falme ya Nchi za Kiarabu. Kwa ujumla alicheza soka la kulipwa kwa miaka 14. Weah aliichezea pia timu ya taifa ya Liberia na aliiwakilisha nchi yake katika Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili. Weah amekuwa akitoa misaada kwa wananchi wa Liberia. Mwaka 2004 alipewa Tuzo ya Ujasiri ya Arthur Ashe kwa juhudi zake za kusaidia kujenga nchi yake. Katika siasa Kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2005, Weah alishindwa kwenye raundi ya pili na rais wa kwanza mwanamke Afrika, Ellen Johnson Sirleaf. Uchaguzi uliofuata mwa mwaka 2011, Weah alipigania kiti cha umakamu wa rais kama mgombea mwenza wa Winston Tubman. Mwaka 2014, Weah alishinda kiti cha useneti kupitia chama cha Congress for Democratic Change kwenye Kaunti ya Montserrado. Mwaka 2017 alishinda uchaguzi wa urais wa Liberia. Aliongoza kwa kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 10 2017. Hata hivyo, alishindwa kupata asilimia zaidi ya asilimia 50. Kwenye raundi ya pili ya uchaguzi hapo 25 Desemba 2017 alimshinda Joseph Boakai aliyekuwa makamu wa rais aliyetangulia Ellen Johnson Sirleaf. Weah alipata asilimia 61.5 za kura.. Tanbihi Viungo vya nje Ukurasa rasmi wa Twita wa George Weah Kuhusu George Weah kwenye tovuti ya UNICEF Tovuti ya chama cha George Weah cha Congress for Democrats Waliozaliwa 1966 Watu walio hai Wanasiasa wa Liberia Wachezaji mpira wa Liberia Marais wa Liberia
1861
https://sw.wikipedia.org/wiki/Monrovia
Monrovia
Monrovia ni mji mkuu wa Liberia. Eneo uliko mji huu mwanzoni liliitwa Cape Mesurado na Wareno katika miaka ya 1560. Eneo hili lilianzwa kujenga mji mwaka 1822 na chama cha American Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchini Marekani. Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa Marekani James Monroe. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2003, Mji huu una wakazi wapatao 572,000. Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vile saruji, mafuta, matofali, vigae, samani, na kemikali zinatengenezwa Monrovia. Historia Wakati mabaharia Wareno walipowasilia Monrovia na kuuita mji huu "Cape Mesurado" tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo. Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katika Kisiwa cha Sherboro nchini Sierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia. Mkutano wa kutunga katiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845. Liberia Miji ya Liberia Miji Mikuu Afrika
1864
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ngoma%20%28muziki%29
Ngoma (muziki)
Ngoma inaweza kumaanisha muziki unaochezwa na ala ya muziki inayoitwa ngoma pia. Ngoma ni muziki na lugha ya pekee inayotumika kwa kuelezea utamaduni na historia ya nchi fulani, tunatumia lugha ya ngoma katika kuelezea hali mbalimbali za maisha yetu, kama vile huzuni, furaha, mapenzi, faraja, vitisho, shukurani na ushindi. Tangu zamani Waafrika walikuwa na lugha hii ya ngoma ambayo ilirithishwa kwa mapokeo. Ngoma pia ilitumika na jamii mbalimbali kama njia ya kuita watu kwenye kusanyiko muhimu, kama vile vita, mikutano n.k. na ilipigwa kwa milio tofauti kulingana na tukio. Fasihi muziki
1869
https://sw.wikipedia.org/wiki/Bombwe%20%28sanaa%29
Bombwe (sanaa)
Bombwe ni sanaa ya urembo wa kuchora mwilini, kama kuchora kwa hina na kuchora kwa piko, sanaa hii hutumika zaidi na wanawake. Tanbihi Sanaa Utamaduni
1870
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togwa
Togwa
Togwa ni kinywaji baridi kinachotengenezwa kwa nafaka au maji ya matunda. Namna ya kutengeneza ni sawa na pombe ya kawaida ila tu haikubadilika bado kuwa na alikoholi. Togwa ndiyo itakuwa pombe ikikaa. Kwa mfano, togwa ya ulanzi ni utomvu kutoka mianzi baada ya masaa kadhaa, na ulanzi wenye pombe ni utomvu uleule kutoka mianzi baada ya siku mbili hivi. Nafaka zinazotumika kutengenezea zaidi huwa ni mtama au mahindi. Jinsi ya kutengeneza togwa la mtama Kwanza chukua mtama mkavu uoshe na uuweke kwenye chombo kikavu alafu uufunike kwa muda wa siku 2,ukifunua utakuta umeanza kuota(kimea) chukua mtama mwingine uloweke kwa siku moja alafu uusage,unga wake pika uji wa saizi ya kati si mzito si mwepesi.Uache ule uji upowe,ukisha poa chukua kile kimea(mtama ulioanza kuota) usage kidogo ili kubakia na chenga chenga.Alafu mimina zile chenga chenga za kimea kwenye ule uji.Tia sukari unaweza kunywa baada ya nusu saa na kuendelea. Vinywaji
1871
https://sw.wikipedia.org/wiki/Liberia
Liberia
Liberia (yaani Nchi ya watu huru kwa Kilatini) ni nchi iliyoko Afrika ya Magharibi. Imepakana na nchi za Ivory Coast, Guinea, na Sierra Leone. Ni mojawapo ya nchi za Afrika ambazo hazikutawaliwa na Wazungu. Hata hivyo watu wa Liberia huongea Kiingereza sana. Historia Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili nchini humo na wahamiaji Weusi toka Marekani na Karibi (5%), mbali na machotara wa aina mbalimbali. Wamarekani Weusi hao walikuwa watumwa waliopata uhuru ambao kwa kushirikiana na chama cha American Colonization Society waliunda taifa hili na kutangaza uhuru wa nchi hiyo tarehe 26 Julai 1847. Wamarekani Weusi hao waliichukulia nchi hiyo kama nchi ya ahadi kutokana na asili yao kuwa Afrika, ambako ndiko mababu zao walikotokea kabla ya kupelekwa utumwani Marekani. Hata hivyo, wahamiaji hao waliendelea kujitambulisha kama Wamarekani na hawakujenga mahusiano ya karibu na wenyeji. Alama za taifa hili (bendera, kauli mbiu, na nembo) na hata muundo wa serikali vilikuwa vikionyesha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili. Liberia ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya miaka 1989-1996 na 1999-2003. Hivi karibuni umefanywa kwa mara ya pili uchaguzi kwa amani na kuweza kumchagua George Weah kushika nafasi ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika, Ellen Johnson-Sirleaf. Watu Lugha rasmi ni Kiingereza, ambacho kinatumiwa na asilimia 15 za wakazi. Lugha za taifa ni 4: Kiingereza cha Kiliberia, Kikpelle, Kimeriko na Krioli. Upande wa dini, wakazi kwa asilimia 85.5 ni Wakristo, hasa Waprotestanti, halafu Wakatoliki (5.8%). Waislamu ni 12.2%. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% tu. Tazama pia Orodha ya lugha za Liberia Orodha ya nchi kufuatana na wakazi Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa Demografia ya Afrika Marejeo Wilton Sankawulo, Great Tales of Liberia. Dr. Sankawulo is the compiler of these tales from Liberia and about Liberian culture. Published by Editura Universitatii "Lucian Blaga"; din Sibiu, Romania, 2004. ISBN 973–651–838–8. Sundown at Dawn: A Liberian Odyssey by Wilton Sankawulo. Recommended by the Cultural Resource Center, Center for Applied Linguistics for its content concerning Liberian culture. ISBN 0-9763565-0-3 Victoria Lang, To Liberia: Destiny's Timing (Publish America, Baltimore, 2004, ISBN 1-4137-1829-9). A fast-paced gripping novel of the journey of a young Black couple fleeing America to settle in the African motherland of Liberia. Godfrey Mwakikagile, Military Coups in West Africa Since The Sixties, Chapter Eight: Liberia: 'The Love of Liberty Brought Us Here,' pp. 85–110, Nova Science Publishers, Inc., Huntington, New York, 2001; Godfrey Mwakikagile, The Modern African State: Quest for Transformation, Chapter One: The Collapse of A Modern African State: Death and Rebirth of Liberia, pp. 1–18, Nova Science Publishers, Inc., 2001. Elma Shaw, Redemption Road: The Quest for Peace and Justice in Liberia (a novel), with a Foreword by President Ellen Johnson Sirleaf (Cotton Tree Press, 2008, ISBN 978-0-9800774-0-7) Helene Cooper, House at Sugar Beach: In Search of a Lost African Childhood (Simon & Schuster, 2008, ISBN 0-7432-6624-2) Viungo vya nje Serikali ya Liberia Chief of State and Cabinet Members Liberia from UCB Libraries GovPubs. Liberia profile from the BBC News. "Liberia Maps", Perry-Castañeda Library, University of Texas at Austin. Nchi za Afrika Umoja wa Afrika
1873
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ruth%20Perry
Ruth Perry
Ruth Fahnbulleh Perry (16 Julai 1939 - 8 Januari 2017) alikuwa kiongozi wa Liberia toka 3 Septemba 1996 hadi 2 Agosti 1997. Aliongoza nchi hiyo kama mwenyekiti wa Baraza la Taifa ambalo liliongoza nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa Sajenti Samuel Doe na mwisho wa urais wa Amos Sawyer. Perry alikuwa mwanachama wa chama cha National Democratic Party cha Liberia. Baada ya uchaguzi wa Urais hapo Julai 1997, Perry alimwachia madaraka Charles Taylor. Wanasiasa wa Liberia
1875
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwai%20Kibaki
Mwai Kibaki
Mwai Kibaki (1931-2022) alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kuanzia mwaka 2002 hadi 2013 akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na rais wa pili Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley . Maisha Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. Akiwa mwanafunzi Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya, Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani. Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African National Union. Kibaki, licha ya kuwa mbunge, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mgongano na Rais Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya. Mwaka 1991 Kibaki aliondoka chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 alikuwa wa pili. Uchaguzi wa urais 2002 Katika uchaguzi wa 2002 Kibaki alishinda na kutangazwa kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa mgombea wa maungano wa vikundi vingi vya upinzani vilivyoshirikiana kwa jina la "NARC". Kibaki ameweka historia mwezi Novemba 2005 baada ya kuwa Rais wa kwanza nchini Kenya kuondoa baraza lote la mawaziri kufuatia kura ya maoni ambayo ilikuwa inahusu katiba mpya ya Kenya. Kibaki alikuwa upande wa kundi lililokuwa likiunga mkono katiba hiyo kambi ya ndizi. Kundi lililokuwa likiipinga katiba hiyo kambi ya machungwa lilipata ushindi. Uchaguzi wa urais 2007 Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani,ODM , na watazamaji wa kimataifa kuwa matokeo hayo hayakuwakilisha matakwa ya Wakenya. Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi Kamati ya Uchaguzi iliposimamisha kuhesabu; baada ya kuendelea na matanganzo Kibaki alionekana kuwa mbele. Kulikuwa na hofu ya kwamba matokeo ya majimbo ya uchaguzi kadhaa yalibadilishwa yakiegemea upande wake kwa kumwongezea kura. Hisia hizi zilisababisha ghasia kuibuka Nairobi, Kisumu, Eldoret, Kericho, Mombasa na sehemu zinginezo nchini. Kibaki aliapishwa upya kuwa rais wa Kenya masaa machache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi; hafla ilifanywa katika Bustani ya Ikulu ya Nairobi mbele ya waalikwa wachache walioruhusiwa kushuhudia. Kamati iliyobuniwa tutathmini ukweli wa mambo katika uchaguzi huo wa urais, iliyoongozwa na jaji mstaafu kutoka Afrika Kusini Johann Kriegler, iliripoti kwamba mshindi katika uchaguzi huo wa urais wa 2007 hangeweza kujulikana. Hii ni kwa sababu wizi wa kura ulifanyika katika sehemu nyingi nchini na ulitekelezwa kule mashinani na wafuasi wa wapinzani wote katika kinyang'anyiro cha Urais. Kriegler pia alielekeza lawama kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kutowajibika katika utendakazi, na ripoti hiyo ya Krieger ilipendekeza tume hiyo ivunjwe na ibadilishwe na ingine iliyo huru. Kinyume cha uchaguzi wa rais uchaguzi wa Bunge la Kenya 2007 uliendelea bila matatizo makubwa. Serikali ya Januari 2007 Baada ya kutangazwa kuwa rais mpya Kibaki aliteua mawaziri 17 kama awamu ya kwanza ya serikali akiacha nafasi nyingine serikalini kando kwa muda. Makamu wa Rais na waziri wa mambo ya ndani: Stephen Kalonzo Musyoka Waziri wa utawala wa mikoa na usalama wa ndani katika Ofisi ya Rais: George Saitoti Waziri wa ulinzi katika Ofisi ya Rais: Yussuf Mohamed Haji Waziri wa mipango maalumu katika Ofisi ya Rais: Dr. Naomi Namsi Shaban Waziri wa utumishi wa serikali katika Ofisi ya Rais: Asman Abongotum Kamama Waziri wa fedha: Amos Muhinga Kimunya Waziri wa elimu: Sam Ongeri Waziri wa mambo ya nje: Moses Wetangula Waziri wa serikali ya mitaa: Uhuru Kenyatta Waziri wa habari na mawasiliano: Samuel Lesuron Poghisio Waziri wa maji na umwagiliaji: John Munyes Waziri wa nishati: Kiraitu Murungi Waziri wa barabara na kazi za umma : John Njoroge Michuki Waziri wa sayansi na teknolojia: Noah M. Wekesa Waziri wa sheria na mambo ya katiba: Martha Karua Waziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki: Dr. Wilfred Machage Waziri wa usafiri: Chirau Ali Mwakwere Kifo Rais Kibaki alifariki tarehe 21 Aprili 2022 akiwa na umri wa miaka 90 na kifo chake kutangazwa na rais wa nne wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kupitia televisheni za taifa. Mnamo tarehe 25 Aprili 2022, mwili wake ulipelekwa katika majengo ya bunge kwa mazishi ya kitaifa. Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta waliongoza Wakenya kuuona mwili wake. Ibada ya mazishi ilifanyika tarehe 29 Aprili 2022 katika uwanja wa Nyayo na ilihudhuriwa na wageni mashuhuri pamoja na baadhi ya ma rais wa sasa. Hatimaye alizikwa nyumbani kwake Othaya, iliyopo katika Kaunti ya Nyeri tarehe 30 Aprili 2022 huku Kanisa Katoliki likiadhimisha misa. Marejeo Viungo vya nje Wanasiasa wa Kenya Marais wa Kenya Waliozaliwa 1931 Waliofariki 2022 1lib1ref 2023