content
stringlengths 1k
24.2k
| category
stringclasses 6
values |
---|---|
SERIKALI imesema haitakuwa tayari kuona amani na utulivu wa nchi inachezewa huku ikisisitiza uwepo wa umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni wakati akifungua semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha viongozi wa taasisi za Kiislamu, lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao.Naibu Waziri amesema mwelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi na nchi kwa ujumla.“Serikali hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote,” amesema Masauni.Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Alhad Mussa Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo kwa mifarakano kati ya taasisi mbalimbali kama ilivyokuwepo awali huku akisisitiza kuendelea kwa umoja huo ili jamii ipate kuendelea.“Sisi kama Bakwata tunaihakikishia serikali uwepo wa umoja na ushirikiano baina ya baraza na taasisi zingine na tofauti zetu hazipelekei kukoseana au kuvunjiana heshima kwahiyo tunaomba serikali iamini uwepo wa maelewano mazuri tu kwa maendeleo ya nchi hii,” amesema Shehe Alhad.Semina hiyo ya siku mbili imejumuisha viongozi wa taasisi 100 huku mada ya Nafasi ya Taasisi za Kiislamu katika Kuleta Umoja na Kuishi kwa Amani itajadiliwa. | kitaifa |
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesitisha likizo za viongozi wote mkoani humo kutekeleza maazimio ya Jukwaa la Fursa za Biashara la mkoa huo.Mwanri ameagiza kuwa, hata kama kuna likizo zimeidhinishwa zifutwe.Amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Msalika Makungu kuandika barua kwa viongozi kuhusu uamuzi huo na amebainisha kuwa hakushauriwa na mtu, kaamua yeye.“Anayebisha anyooshe mkono, ajifanye angalau anajikuna tu” amesema Mwanri kwenye jukwaa hilo la nane lililomalizika leo.Amewaeleza viongozi wa Tabora kuwa, mambo waliyopanga kuyafanya wakati wa likizo nje ya Tabora wanaweza kuyafanya mkoani humo hivyo wawaite ndugu zao waende mkoani humo.Kiongozi huyo wa Tabora amewaagiza maofisa ugani mkoani humo watoke ofisini wahamie shambani.Viongozi mbalimbali wamehudhuria jukwaa la Tabora akiwemo mwenyekiti wa jukwaa hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Hab Mkwizu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi.Viongozi wengine waliohudhuria jukwaa hilo ni wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, makatibu tawala wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, wakuu wa taasisi na waendai wengine mkoani humo. | uchumi |
SERIKALI imetoa miezi sita kwa taasisi zote za umma ambazo hazitumii mfumo wa GePG katika ukusanyaji wa fedha kufanya hivyo na baada ya hapo itafanya ukaguzi na kuwawajibisha maofi sa masuhuli walioshindwa kutekeleza hilo.Akifungua mkutano wa mwaka wa kwanza wa watumiaji wa mfumo huo jana jijini hapa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Hartibu Kazungu alisema ukaguzi huo ambao utaanza kufanyika Juni mwakani baada ya kipindi kilichowekwa kupita ili kuwabaini maofisa wazembe.Alisema, wizara yake itafanya ukaguzi wa ofisi zote za umma ili kubaini kama kuna fedha zinazokusanywa bila kupitia kwenye mfumo wa GePG na kuwa ofisi itakayobainika kutotumia mfumo huo maofisa masuhuli watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.“Mnifikishie ujumbe wa kuzikumbusha taasisi ambazo hazijaanza kutumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa GePG kufanya hivyo, kwani tunataka hadi kufikia Juni 30, mwaka 2019, kusiwe na fedha yoyote kwenye taasisi ya umma ambayo inakusanywa nje ya mfumo huu,” alisema.Hata hivyo, alisisitiza kuwa utaratibu wa malipo kupitia GePG unawapa fursa ya kuwa na njia nyingi za kulipia zikiwa na lengo la kuwapa walipaji wa huduma za serikali utaratibu rafiki na machaguo mengi ya njia za kufanya malipo.“Nimepewa taarifa kuwa takribani benki kumi na moja (11) na mitandao sita ya malipo kwa njia ya simu za kiganjani zimeshaunganishwa na GePG. “Hii ni kuthibitisha namna mfumo wa GePG umekuwa na fursa nyingi za ulipaji, hivyo kuweka mazingira kwa umma katika kufanya malipo hivyo kuondoa urasimu na ucheleweshaji usiofaa.”Dk Kazungu alisema kuwa mfumo huo ulianzishwa ili kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma pamoja na kupunguza gharama zinazoambatana na ukusanyaji wa fedha za umma.Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi huo Mkurugenzi wa mfumo kutoka wizara hiyo, John Sausi alisema changamoto wanayokuta nayo katika utekelezaji wa mfumo huo uelewa mdogo wa namna ya kutumia.Katika utekelezaji wa mfumo huo tuna changamoto moja kubwa ambayo ni uelewa wa watumiaji wa mfumo kushindwa kutumia vyema mfumo huu vizuri hivyo kulazimika kutumia watu wa operesheni kwa ajili ya kurudia utoaji wa elimu.Alisema changamoto nyingine ni ukosekanaji kwa mtandao katika maeneo ya vijijini hivyo mfumo kushindwa kufanya kazi. “Changamoto ya mtandao tunaangalia namna ya kukabiliana nayo mwaka mzima tangu kuanza kwa mfumo huu, lakini kama wizara tunaamini haiwezi kutusumbua,” alisema. Aidha, Sausi alisema tangu kuanza kutumika kwa mufmo huo hapa nchini hadi sasa taasisi 326 tayari zinatumia mfumo huo katika kutoa huduma. | kitaifa |
KAMPUNI ya mchezo wa kubahatisha ya M-bet imeingia makubaliano ya udhamini na timu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa miaka mitano wenye thamani ya sh Bilioni 1.Akizungumzia udhamini huo jana baada ya kusaini mkataba huo, Meneja Masoko wa Mbet, Allen Mushi alisema sababu ya kuiunga mkono timu hiyo ni baada ya kuvutiwa na kiwango bora walichokionesha timu hiyo tangu msimu uliopita. Alisema kitendo cha kumaliza ligi katika nafasi ya nne bora sio cha mchezo na kwamba hata wanapokuwa uwanjani hucheza soka la kuvutia tofauti na wengine.“Tumeichagua KMC kwasababu tumevutiwa na mambo mengi, kwanza jinsi wanavyojiongoza katika mipango yao ya muda mfupi na mrefu, lakini kingine wanapokuwa uwanjani soka lao ni la kuvutia,”alisema.Alisema wanaweza kuboresha kiwango cha fedha kila mwaka endapo timu hiyo itakuwa inafanya vizuri na hata kuchukua taji la Ligi Kuu. Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta alisema udhamini huo hauzuii fursa mbalimbali kutoka kwa wadau wengine.Alisema fursa za kudhamini timu hiyo zipo na wanategemea wengine watajitokeza kuwaunga mkono kuelekea katika harakati zao za kujenga uwanja wa kisasa wa klabu hiyo.Katika hatua nyingine, Kocha wa KMC Jakson Mayanja alizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Kigali kuwa yanakwenda vizuri. Mchezo huo utafanyika kesho Ijumaa. | michezo |
WATANZANIA wamekumbushwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa kuenzi amani, umoja na kulinda tamaduni za nchi ili kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza, ikiwemo vitendo vya ushoga na matumizi ya dawa za kulevya.Akizungumza wakati wa kutoa heri ya sikukuu hiyo ya Kuzaliwa Yesu Kristo, Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithnasheriya, Shehe Hemed Jalala alisema kuzaliwa kwa Yesu kunalenga kuhubiri na kutangaza amani ulimwenguni. Shehe Jalala alisema licha ya Wayahudi kutilia shaka kuzaliwa kwa Yesu, lakini pindi alipozaliwa alitangaza amani kwake na duniani kote akitaka kila mtu kuishi kwa upendo, amani na umoja.“Jamii yenye amani mara nyingi hupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani, kulinda mila na desturi kwa kupinga vitendo vya ushoga, matumizi ya dawa za kulevya na rushwa. Pia upendo utatawala miongoni mwa majirani, familia na kutokuwa na ukabila,” alisema Shehe Jalala. Pia alisema nchi inayoondoa ujinga, kupambana na maradhi na kuhimiza watu wake kufanya kazi kwa bidii, ina lengo la kudumisha amani hivyo huenda sambamba na ujumbe wa amani aliouacha Yesu.Shehe Jalala alisema amani inaenziwa katika nyanja mbalimbali kuanzia kwa mtu mmoja mmoja, kitaifa na kimataifa na kwamba eneo ambalo kuna uhuru wa kuabudu na mtu kujifanyia mambo yake mwenyewe ni ishara ya uwepo wa amani. “Katika Kitabu Kitakatifu cha Kurani, Mwenyezi Mungu amezungumzia kuzaliwa kwa Yesu na neno la kwanza Yesu (Isa bin Mariam) ni amani iwe kwangu siku niliyozaliwa, kufa na kufufuka nikiwa hai,” alisisitiza.Aliongeza kuwa mambo yote yanayosababisha uvunjifu wa amani yasipewe nafasi badala yake kuendelea kudumisha upendo na amani siku zote. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kikristo ya Outreach Ministries (TCOM), Mchungaji Banza Seleman alisema Yesu alizaliwa baada ya mwanadamu kumuasi Mwenyezi Mungu hivyo alikuja kuwakomboa kutoka dhambini.Alisema kuja kwa mkombozi huo ni upendo mkubwa wa Mungu kwa wanadamu na kwamba lengo ni kuihubiri amani na upendo ili watu waweze kushirikiana na kusaidiana. “Katika Biblia na Kurani, vitabu hivi vinaeleza kuwa Yesu ni mfalme wa amani hivyo tunastahili kulinda amani, kuishi kwa upendo na umoja. Yesu alizaliwa ili aweze kuhubiri amani kwa watu wote,” alisema Mchungaji Seleman. | kitaifa |
Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omary Kopa amesema wasanii nchini hawana umoja, na kwamba, wale wa bongo fleva na watu wengine, wanawaona wa taarabu ni watu wa hali ya chini na masikini.Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, kutokana na mtazamo huo, wasanii wa fani nyingine wamekuwa hawawashirikishi katika mambo yao wale wa taarabu.Amedai kuwa, hata Serikali imekuwa haiwajali wasanii wa taarabu hata inapotokea misiba, na ametoa mfano mfano wa ajali iliyowaua wasanii wengi wa Kundi la Zanzibar Stars Modern Taarabu.Amesema umoja uwe kwa wasanii wote na sio kwa baadhi tu na alilalamika kuwa wamekuwa wakitozwa fedha nyingi wakitaka maeneo ya kurekodia video zao za nyimbo.Katika mkutano huo, muimbaji wa muziki wa dansi nchini, Nyosh El Saadat amesema, amechoka kuwakimbia watu wa Uhamiaji na sasa anataka uraia wa Tanzania baada ya kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 20.Nyoshi alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa wasanii wa fani mbalimbali na wanamichezo walipokutana na mkuu huyo wa mkoa katika viwanja vya Leaders.Nyoshi alimwambia Makonda kuwa amekaa nchini kwa muda mrefu na mara kwa amekuwa akijificha uvunguni ya kitanda au kupanda darini kujificha kuakwepa watu wa Idara ya Uhamiaji kutokana na kutokuwa na uraia.Alisema kuwa sasa wakati umefika kwa yeye kuwa raia wa Tanzania. Naye Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki aliwataka wasanii kupenda na kushirikiana bila ya kujali tofauti ya fani zao.Alitoa masikitiko yake kwa baadhi ya wasanii kutokuwa na ushirikiano miongoni mwao, hivyo aliwataka washirikiane.Nasseeb Abdul au Diamond amesema, mengi yamezungumza ila alipongeza ujenzi wa ukumbi mkubwa utakaoingiza watu 20,000, huku akiwapa shavu wasanii kupigiwa au kuoneshwa bure katika Wasafi Radio na Wasafi TV. | michezo |
Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo aliyasema hayo jana ikiwa ni siku chache baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya mikopo ya viwanja jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyo atoke Dar es Salaam au Kibaha.Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio sababu taasisi hiyo wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali, bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao.“Nafasi ni chache, maana maombi yetu yanafanyika kwa siku ishirini na yameanza Mei 22 hadi Juni 10, na fomu za maombi zinapatikana matawi yote ya taasisi yetu, bila kusahau kupitia B ank of Africa (BOA), ambapo malilipo ya awali yanaanzia Sh 150,000,” alisema.Alisema kukaa mikoani si sababu ya kushindwa kukopa kiwanja kwa sababu wamefungua matawi katika wilaya na mikoa mbalimbali.Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema ukubwa wa viwanja hivyo unaanzia hatua 15 kwa 16, huku thamani yake ikianzia Sh 1,400,000 bila riba. | uchumi |
IDADI ya vifo vya waendesha bodaboda nchini vitokanavyo na ajali imepungua katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu kinachoanzia Januari hadi Machi, ikilinganishwa na idadi ya vifo vya bodaboda kwa kipindi kama hicho kwa mwaka jana. Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Afande Deusi Sokoni akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu alisema kuwa idadi ya waendeshaji bodaboda waliopoteza maisha kwa mwaka huu ni 73 huku majeruhi wakiwa 121.Alisema, kwa mwaka jana kwa kipindi kama hicho waliopoteza maisha walikuwa ni 108 huku waliojeruhiwa ni 214. Sokoni aliongeza kuwa robo ya kwanza ya mwaka huu kwa upande wa waendesha baiskeli waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani walikuwa 23 idadi ambayo ni sawa na ya majeruhi lakini mwaka jana kuanzia Januari hadi Machi, idadi ya waliokufa ilikuwa ni 34 huku waliojeruhiwa wakiwa 30. Alisema pia waendesha mikokoteni tisa wamekufa na wanne wamejeruhiwa huku mwaka jana aliyekufa alikuwa mmoja na 12 walijeruhiwa. Kundi la watembea kwa miguu ambalo ni moja kati ya waathirika wakubwa wa ajali kwa mwaka huu wamekufa 90 na kujeruhiwa 106. Wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 163 na kujeruhiwa 179. Kwa upande wa abiria waliokufa kwa ajali kwa mwaka huu ni 108 na 393 wamekumbwa na majeraha mbalimbali wakati kwa mwaka jana waliokufa walikuwa 191 na majeruhi 575. | kitaifa |
Katika uzinduzi huo, rais amesema kuna haja ya kutafuta majawabu kuhusu namna ya kuongeza maghala ya kuhifadhia mazao kwani kadiri kilimo kinavyoboreshwa mazao yanayozalishwa yanakosa pa kuhifadhiwa.Rais Kikwete aliyasema hayo- Dar es Salaam juzi wakati akizindua kampuni hiyo ambayo itakuwa chini ya Mamlaka ya Soko la Bidhaa Tanzania (CMSA). Alisema uzinduzi wa soko hilo ambalo litaanza kufanya kazi rasmi mwezi Mei, mwakani kwa kuanzia na mazao ya korosho, ufuta, alizeti na mpunga ni muendelezo wa jitihada za serikali katika kuleta mageuzi ya kilimo nchini.“Hii ni habari njema kwa wakulima wa Tanzania kwani katika jitihada zetu za kuleta mageuzi ya kilimo zisingefanikiwa kama Tanzania kusingekuwa na soko la uhakika. Mfumo uliopo sasa unawakandamiza wakulima na kuwanufaisha walanguzi,” alisema Rais Kikwete.Alisema pamoja na kuanzishwa kwa sera ya kilimo kwanza, stakabadhi ghalani, uanzishwaji wa benki ya wakulima na vyama vya ushirika kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo nchini, bado sekta hiyo ilikabiliwa na tatizo la ukosefu wa uhakika wa masoko.Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi wa TMX, Peter Noni alisema kampuni hiyo ilisajiliwa Agosti, mwaka jana kama kiungo muhimu katika mchakato wa kuanzisha soko la bidhaa nchini.Aliwataja wanahisa waanzilishi wa kampuni hiyo kuwa ni msajili wa hazina, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Benki ya Maendeleo (TIB) na Shirika la Vyama vya Ushirika. | uchumi |
KWA mujibu wa vyanzo mbalimbali, Tanzania ina makabila zaidi ya 120, yanayopatikana katika mikoa yote ambayo ndani yake kuna makabila zaidi ya moja. Makala haya leo yataangazia Kabila la Wabende linalopatikana katika Mkoa wa Katavi.Uchunguzi wa makala haya kupitia vyanzo mbalimbali umebaini kuwa, baadhi ya makabila mengine yanayopatikana katika mkoa huo ni pamoja na Waruila, Wapimbwe na Wakonongo. Akiwa Mhifadhi Mila Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa katika Kijiji cha Makumbusho, Wilbard Lema amewahi kunukuliwa akielezea kabila hilo na asili yake.“Kwa asili yao, Wabende ni wawindaji wa wanyama waporini. Maisha yao ni ya kuhamahama kutafuta kitoweo katika mazingira rafiki kwa uwindaji na makazi,” anasema. Mkoani Katavi kabila hilo lipo wilayani Mpanda katika Tarafa za Kabungu, Misunkumilo, Kashaulili na Mwese katika Kata ya Katuma. Watu hawa wana mila na desturi ambazo kwa kiasi kikubwa, zilitengenezwa kutokana na mazingira ya uwindaji wa asili, kilimo tofauti na makabila mengine ya uwindaji.Katika uwindaji wao, hutumia silaha za jadi kama mikuki, mishale, bunduki zilizotengenezwa kwa chuma kilichotokana na kuchomwa hadi kulainika na kuchongwa. Halikadhalika, hutumia upinde na mishale, pamoja na moto wa kupekecha kwenye gogo la mti unaoitwa mlindilindi. Kwa mujibu wa Lema, kwa kawaida Kabila la Wabende halina sifa ya kuwa na waganga wengi wa kienyeji. Hata hivyo, ndilo linaloongoza kwa kuwa na tiba za asili zisizo za ramli. Inaelezwa kuwa, watu hawa hutumia zaidi tiba ya miti shamba kutibu magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunga mifupa iliyovunjika.Anasema: “Kabila hili ndilo linaloongoza kwa kutibu kwa kutumia mitishamba na siyo ramli, na dawa zao za mitishamba ni bora; mkono, mguu au kiungo chochote kilichovunjika, huungwa kwa tiba za mitishamba.” Tiba hizi za asili za Kibende, zinaaminika kutibu kwa muda mfupi kuliko dawa hata kwa waliovunjika mipufa na kimsingi, kabila hili lina msimamo wa kuamini tiba za asili na siyo kupiga ramli kubaini kutafuta wachawi.Mintarafu malezi ya vijana, mtaalamu huyo anasema, kabila hili huwaonya au kuwafunza vijana hasa wanapokuwa kwenye hatua wa awali za kubalehe kwa kupitia sherehe za harusi na misiba ambako huelezea mema na mabaya katika jamii. Mfano, vijana wavivu, wenye lugha chafu, matusi na mambo mengine yanayoleta sifa mbaya kwa jamii, hutengwa na vijana wenzao.Kutengwa huku ni pamoja na kutoshirikishwa katika shughuli za urika kama vile kuchuna mnyama mkubwa kama nyati na wengine kama swala waliowindwa. Kufanya hivyo pamoja na makaripio mengine, hurudisha nidhamu kwa vijana na hivyo, wanaoonyeka kuruhusiwa kuchangamana tena na jambo linaloleta nidhani katika jamii. Kuhusu matambiko wakati wa maafaau njaa, Lema anasema wazee wa kabila hilo hufanya matambiko maafa yatokeapo.Mfano wakati wa njaa, au wadudu waharibifu kama nzige au vifo vya mfululizo vinapotokea kiongozi wa koo, huitishwa kikao cha wazee kujadili tatizo na kisha kufanya matambiko kadiri inavyotakiwa. Matambiko hayo hufanywa lilipotokea tatizo na kama ni wadudu mathalani nzige, hufanya tambiko upande waliokotokea wadudu hao, mathalani Kaskazini au Kusini. Wakati wa kufanya matambiko hayo ngoma za asili hutumbuiza. Ngoma hizo ni pamoja na Maligoligo, Kangungera, Malimba, Nsawaka na Lolomgeni.Chakula cha asili cha Kabila la Wabende ni usali, nyama za pori na asali kwa kuwa kabila hilo ni wafugaji wazuri wa nyuki. Aidha, katika kusisitiza na kuendeleza mila na desturi za kabila hilo, jamii inasisitizwa matumizi ya hadithi, misemo, nahau na soga ambavyo kwa pamoja, vilitumika kufundisha vijana na watoto katika makuzi yao. Katika kabila la Wabende, kiongozi wao huitwa Mwami na msaidizi wake huitwa Ntware.Mwami alisaidiwa kuongoza na jopo la wazee waliotoka katika kila baada ya koo mbili au tatu. Wazee hao husikilizwa sana na wakuu wa kaya pindi linapotokea tatizo au mifarakano ndani ya familia au kaya. Mathalani, ndugu wawili wanapogombana, baba yao aliwaita wazee na kuwaomba wawashauri. Ikiwa muafaka haukupatikana shauri hilo hupelekwa kwa Ntare ambaye ataitisha baraza dogo la wazee kuwajadili, uzuri wa baraza hilo ni kwamba katika shauri hilo hatafutwi mkosaji, bali wote wawili huonywa na kwani kitendo cha kugombana ndugu sio kizuri.Katika Kabila hilo, baba ndiye aliyetoa adhabu kwa kijana aliyekuwa na makosa na ilitakiwa kutekelezwa mara moja adhabu iliyotolewa. Mfano kukata kuni na kuziwasilisha kwa Mwami na Ntware ili kusafisha jina la ukoo. Shughuli za uchumi za Wabende ni uwindaji wa asili, kilimo na urinaji wa asali kwa kutumia misinga ya asili. Kazi kwa kabila hilo ni kipimo cha kukubalika katika jamii na kiini cha kipato katika jamii hiyo. Kila mwanajamii hutakiwa kuwa na shughuli ya kufanya na kuhakikisha anazalisha chakula cha kutosha na kuweka akiba kwa ajili ya nyakati ngumu kwa kutumia vihenge vya asili ambavyo huitwa ntanta. Kabila la Wabende kama yalivyo makabila mengine, wana mtindo wa ujenzi wa nyumba zao.Nyumba za Wabende hujengwa kwa kutumia miti iliyosimikwa na kukandikwa kwa udongo wa kichunguu. Paa lake huezekwa kwa nyasi ndefu zilizokauka vema, nyumba za Wabende hazina madirisha na badala yake, huwekwa matundu madogo yenye ukubwa wa ngumi yaliyozibwa kwa kibuyu kikavu. Lema anasema, mavazi ya asili ya Wabende yanatokana na ngozi za wanyama waliowawinda na magome ya miti aina ya miombo yaliyopondwa pondwa na kulainika. Aidha, Lema anasema kama ambavyo maisha hubadilika, pia utamaduni wa nao unabadilika kulingana na mazingira na kwamba pamoja na kuwepo kwa mila na desturi hizo, lakini hivi sasa baadhi zimebadilika kutokana na mazingira ya sasa.“Utamaduni unabadilika kulingana na mazingira na pia mambo mengine, hivyo hata baadhi ya mila au hata mavazi ya makabila mbalimbali nchini likiwemo hili la Wabende wamebadilika hivi leo tunavaa nguo hatuvai tena magome”, anasema Lema. Ulinzi na usalama Kabila hili lina vingi vya kujivunia ambavyo hadi leo vimehifadhiwa kama mila na desturi nzuri za kuigwa.Baadhi ya vitu hivyo ni suala zima la ulinzi na usalama wa jamii yao. Katika Kabila hilo, kila mkazi wa Ubendeni alitakiwa kuwa mlinzi wa mali na jamii yake wakati wote. Kila alipo Mbende alitakiwa kulinda mali na kutoa taarifa haraka kwa Ntware au Mwami. Taarifa hizo ni kama vile waonapo kundi la tembo, nzige na wageni ambao sio Wabende. Baada ya taarifa inapobainika kuwapo tishio la usalama, jukumu la kupambana na kukabiliana na tishio hilo walipewa vijana walioongozwa na wazee wa rika la kati ambao ndio wenye nguvu. | kitaifa |
MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd amevihimiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini kurejesha ubora wao wa zamani kwa kuhakikisha wanaongoza kufanya vizuri katika michezo ya kitaifa na kimataifa.Kiongozi huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) inayofanyika hadi Machi 9 mwaka huu. Alisema ana imani kupitia michuano hiyo ya Bammata, kiwango cha michezo katika nchi kitapanda na kurudia umaarufu waliojizolea miaka ya zamani.“Sote tunaelewa wachezaji wazuri kitaifa na wawakilishi wetu kimataifa walikuwa wakitoka katika vyombo vya ulinzi na usalama. Hivyo, basi nawaomba msituangushe, na tuna matumaini makubwa mtapeperusha tena bendera ya nchi kimataifa,” alisema. Aliongeza, “Kufanyika kwa michezo hii mwaka huu kunatupa faraja na kwa kweli viongozi wenu wanastahili kupongezwa na wachezaji wote nchini,” alisema.Aliwataka wachezaji kutumia muda wao wa ziada kufanya mazoezi ili kutompa nafasi shetani kuyapeleka mawazo yao katika utumiaji wa dawa za kulevya, ulevi wa kupindukia, ujambazi na mengine yanayofanana na hayo. Pia, aliwaonya wachezaji kama wanataka kufanya vizuri kuacha kutumia vyakula vya makopo na badala yake kula vyakula vya asili vinavyosaidia kujenga mwili. Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alimshukuru balozi huyo kwa kuipa kipaumbele michuano hiyo na kuja kushiriki katika ufunguzi.Aliwashukuru pia, wadhamini wa michuano hiyo na vyombo vya habari kwa kuwaunga mkono na kuwaomba waendelee na moyo huo ili kuendeleza na kudumisha michezo ya Majeshi. Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo alisema wamedhamiria kuendeleza na kukuza michezo katika Majeshi kwa kuhakikisha wanafanya vizuri.Alisema changamoto iliyopo ni ushiriki wa timu hizo katika mashindano ya kitaifa na kimataifa kutofanya vizuri, ndio maana wanataka kutumia michuano hiyo ya Bammata kuibua vipaji. Mwenyekiti wa Bammata, Brigedia Jenerali Suleiman Mzee alisema mashindano hayo yameshirikisha timu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Idara ya Uhamiaji, Magereza na Zimamoto. Alisema uendeshaji wa mashindano hayo unakabiliwa na changamoto ya bajeti kwani yanatakiwa kufanyika kila mwaka lakini miaka mingine hushindwa kutokana na hali hiyo. | michezo |
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewataka wateja waliokuwa na amana zao katika benki iliyositisha huduma zake ya FBME kuwa na subira, huku taratibu za kulipwa fedha zao zikiendelea.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua lini wananchi wenye fedha zao katika benki ya FBME watalipwa fedha zao.Akifafanua zaidi amesema suala la kulipa amana za wananchi mara baada ya benki hiyo kusitisha shughuli zake lipo chini ya Bodi ya Bima ya Amana.Alisema taasisi hiyo imepewa jukumu hilo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye ndiye msimamizi wa taasisi zote za fedha ikiwemo benki.Alisema utaratibu wa kuwalipa amana za wateja unaendelea awamu kwa awamu kulingana na viwango vya fedha za mteja.Alisema wapo wateja wenye akaunti kuanzia Sh milioni 1.5 wamekuwa wakilipwa fedha zao kwa nyakati tofauti na wale wenye kiwango kikubwa zaidi watalipwa fedha hizo baada ya kukamilika kwa mchakato wa ufilisi.''Benki ya FBME imesitisha shughuli zake na sasa ipo katika mchakato wa kulipa madeni ya wateja wake kwa hivyo wananchi ikiwemo walioguswa na kadhia hiyo kuwa na subra,'' amesema.Dk Mohamed alisema serikali inafuatilia suala hilo na kujua hatma yake kwa sababu watu walioathirika wanatoka Zanzibar katika moja ya tawi la benki hiyo.Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, masuala yote ya fedha na sarafu na benki yanasimamiwa na BoT. | uchumi |
MSEMAJI wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abbas amesema waandishi wa habari wanahaki ya kuikosoa serikali lakini hawapaswi kuandika habari za kuzusha na kupotosha.Amesema Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kifungu cha 32 (2) kinatoa haki hiyo ya kila mwandishi kuikosoa serikali na kwamba kifungu cha 52 kinaeleza kwamba haitakuwa kosa kwa waandishi watakaoonesha makosa yaliyopo kwa serikali kwa uthibitisho na sio kuzusha.Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam kwenye semina juu ya jukumu la wanahabari, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mufti wa Tanzania na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.Dk Abbas alisema kwa mara ya kwanza Tanzania imeweka kifungu hicho cha sheria ili kutoa haki ya kitaaluma kwa waandishi wa habari ambao ndio muhimili wa nne wa nchi, hivyo wanapaswa kutimiza wajibu wao katika jamii.Alisema mwandishi aliyefanya utafiti vizuri na kubaini madudu ndani ya serikali na akawa na vithibitisho vyote vyenye ukweli anauwezo wa kuandika habari na kuichapisha kwenye vyombo vya habari na sio kuandika habari za kizandiki."Tunapochukua hatua kali ya kulifungia gazeti kwa kuwa na habari zenye kuhatarisha usalama wa nchi au uzushi wanaharakati wengi wanalalamikia hatua hizo tunasahau kwamba waandishi pamoja na kuwa na haki wana wajibu wa kulinda nchi," alisema Dk Abbas.Aliongeza kuwa waandishi pia wana wajibu wa kuenzi na kulinda amani ya nchi kwa kukataa viashiria vinavyoharibu amani kwa sababu watu wa kwanza kuathirika ni wao wenyewe.Pia alisema kuwa katika mkataba wa Kimataifa wa haki za kisiasa na kiraia unaeleza haki na wajibu wa kitaaluma pamoja na mipaka yake. Alifafanua kuwa kama kutakuwa na habari za kupotosha ndani na nje ya nchi mkataba huo unaelekeza katika kanuni ya kukashifu au kumkejeri mtu, magazeti yatachukuliwa hatua kwa kufikishwa mahakamani."Ni kweli tunao uhuru wa kusema lakini ni wajibu wetu kutoandika habari za kukashifu mtu kwani ni kuvunja kanuni ya mkataba huu. Pia tunapaswa kuzingatia kanuni ya faragha tuandike habari lakini tuwe na ukomo ili kulinda faragha yake," alisisitiza.Dk Abbas alieleza kwamba ni vyema kuangalia usalama wa taifa kwa kuhakikisha kuwa yale mambo yanayohusiana na usalama siri zake zisitolewe kwa sababu zinaathiri ustawi wa nchi.Kwa mujibu wa Dk Abbas, sheria ya huduma za Habari inatoa haki ya kukusanya habari licha ya changamoto zilizopo, uhuru wa kuhariri na uhuru wa kusambaza taarifa hizo.Kwa upande wake, Kiongozi wa Waislamu dhehebu la Shia Ithnasheriya, Shekhe Hemed Jalala alisema wajibu wa mwandishi wa habari ni kuandika habari zenye kufuata misingi ya haki na sheria." Mwandishi wa habari mzalendo ni yule anayeitakia jamii isonge mbele kwa kuenzi mambo mazuri badala ya kuandika habari zinazofitinisha au kuhitilafiana au kuchochea jambo ambalo litaleta chuki baina ya jamii moja na nyingine" alisema Shekhe Jalala.Alibainisha kuwa mwandishi wa habari mzalendo ni lazima ataandika habari kuhusu rasilimali za nchi na maendeleo kwa jamii na kulinda amani, mshikamano na umoja. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake ( TAMWA) , Edda Sanga alisema bado vyombo habari havitoi fursa ipasavyo kwa waandishi wa habari wanawake hasa katika nafasi za juu za uongozi.Alisema vyombo vya habari vina uwezo wa kujenga na kubomoa hivyo vinapaswa kuona nafasi katika jamii kutafuta habari, kuhariri na kusambaza ili watu wengi wanufaike na kupata mabadiliko chanya."Mwaka 2008 ni wanawake watatu pekee ndio waliowahi kushinda kwenye Tuzo za Umahiri wa habari (EJAT) zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), ambao walishinda uandishi wa habari za uchunguzi," alisema Sanga. | kitaifa |
Hayo yalisemwa na Rais wa TCCIA, Peter Chisawilo, hivi karibuni mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe kufungua mkutano mkuu wa mwaka na wa uchaguzi wa chama hicho mkoa wa Morogoro.Chisawilo alisema pamoja na kuunga mkono hatua ya serikali ya awamu ya tano kuhusu kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, pia alishauri kuwekwa mazingira mazuri ya kulinda viwanda vya ndani licha ya kuvutia wawekezaji wa nje kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.“TCCIA Taifa imepokea, inakubaliana na inaunga mpango wa Rais Magufuli wa kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, lakini serikali pekee haiwezi kujenga viwanda bali yenyewe inaweka mazingira mazuri ya kuifanya sekta binafsi pamoja na TCCIA wajikite katika uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vya aina mbalimbali,” alisema.Mbali na hayo alisema, Serikali inapaswa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kuimarisha viwanda vya ndani vya uzalishaji wa sukari nchini kwani kwa sasa uwezo wao ni mdogo kutosheleza mahitaji ya sukari nchini. | uchumi |
Rais John Magufuli amemteua Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo anachukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.Taarifa ya Ikulu iliyosambazwa mapema leo Jumamosi (Juni 8, 2019) imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA).Mahede anachukua nafasi ya Charles Kichere ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Kabla ya uteuzi huo, Mahede alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.Uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda utafanywa baadaye, taarifa hiyo imeeleza. Kutokana na mabadiliko hayo, Kichere ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe.Kichere anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Erick Shitindi ambaye amestaafu. Mababdiliko haya yamefanyika baada ya Rais Magufuli kukutana na wafanyabiashara kutoka wilaya mbalimbali hapa nchini. Kikao hicho kilitawaliwa na lawama zilizoekelezwa kwa vyombo ya serikali kama TRA na mamlaka nyingine za udhibiti. | kitaifa |
JESHI la Polisi linamshikilia mkazi wa Madale Mivumoni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ernest Alias (19) kwa tuhuma za kushiriki katika mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Mgaya(21).Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo. Alisema katika upelelezi wa awali, baada ya kuhojiwa kwa mtuhumiwa huyo alikiri kumchoma kisu mwanafunzi huyo na kumuibia pochi, simu aina ya Tecno, Sh 8,000 na kadi zake za utambulisho. Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuzitupa kadi hizo na pochi huku akiiuza simu hiyo.Kwa mujibu wa Mambosasa, mtuhumiwa alimuelezea marehemu jinsi alivyokuwa amevaa siku ya tukio ambao alidai kuwa alivaa shati jeusi, suruali ya jeans na kofia nyeusi. Tukio hilo lilitokea Juni 16, mwaka huu katika kampasi ya KIU iliyopo eneo la Gongolamboto, Manispaa ya Ilala Dar es Salaam.Kamanda huyo alisema bado jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kuweza kuwakamata watuhumiwa wengine watakaohusishwa na mauaji hayo. Mpaka sasa watuhumiwa 31 wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo. | kitaifa |
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Joseph Iha, alisema huduma hiyo imezinduliwa wakati muafaka kipindi ambacho wateja wa benki hiyo wanazidi kuongezeka tangu kufunguliwa kwa benki hiyo hapa nchini.Alisema kwa kuzingatia ubora katika utoaji wa huduma, uongozi wa benki hiyo uliona vyema kuja na huduma hiyo ili kuwaondolea usumbufu wateja wake wa kufuata huduma katika matawi yake au sehemu za kutolea fedha (ATM).“Huduma hii imelenga kuhakikisha mteja anaendelea kutekeleza majukumu yake ya kawaida wakati wote huku akipata pia akipata huduma za kifedha kupitia simu yake bila kujali muda na mahali alipo. Kikubwa cha kufanya ni kupakua ‘APP’ katika simu yake,” amesema Iha.Amesema benki kupitia ‘EazzyBanking’ imezidi kujipanua kwa kuwafikia wateja wake waliopo katika maeneo mbalimbali nchini na mawakala wake zaidi ya 1600 waliopo nchini kote.Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa imezidi kuwajengea ubora katika utoaji wa huduma.“Tunawasihi wananchi wote kupaukua ‘APP’ hiyo katika simu zao kuondokana na usumbufu usio wa lazima unaoweza kujitokeza kipindi mteja anapotaka kupata huduma ikiwemo misururu ya wateja wanaofika benki kupata huduma,” amesema Iha.Amesema mteja wa benki hiyo ana fursa ya kutuma na kupokea fedha kwa kutumia ‘APP’ hiyo nchini au nje ya nchi na kuomba mkopo kuanzia Sh 10,000 hadi Sh milioni tatu kulingana na takwimu za miamala ya kifedha. | uchumi |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka washiriki wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili mambo ya nyuklia, kuhakikisha usalama wa watu, mazingira na mfumo wa ikolojia yanazingatiwa katika eneo la SADC kwa mujibu wa sheria.Alitoa mwito huo jana jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa mionzi kutoka nchi za kusini mwa Afrika.Waziri Mkuu alisema watu, mazingira na mfumo wa ikolojia lazima vilindwe dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na kuchimbwa, kusafishwa, kuchakatwa pamoja na kusafirishwa kwa madini ya urani.Alisema kuwa usafirishaji wa nyuklia au malighafi za mionzi ni suala linalogusa ulimwengu mzima na siyo tu suala la nchi moja, hivyo ni muhimu kwa SADC kuwa na mwongozo wa pamoja kuhusu usalama na ulinzi wa malighafi za nyuklia kwa ajili ya kulinda afya za watu, mazingira na mfumo wa ikolojia kwa upana wake.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kikubwa cha madini ya urani kinachokadiriwa kufikia tani 58.5 katika maeneo mbalimbali ikiwemo Namtumbo (Mkuju), Bahi, Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Ziwa Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba na Nachingwea.“Japo Bodi nyingi za Nyuklia barani Afrika zimeanzisha mifumo ya uthibitisho, ukaguzi na utekelezaji wa udhibiti wa nyuklia na malighafi nyingine za mionzi, bado kuna kazi ya kufanya katika kuimarisha miundombinu ya udhibiti wa kitaifa kwa usafirishaji wa urani na malighafi za mionzi,”alisema Majaliwa.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu pia amefungua maabara ya kisasa ya kwanza katika ukanda wa Afrika iliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 8.4 iliyojengwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya(EU).Alisema lengo la serikali la kujenga maabara hiyo ni kuimarisha zaidi udhibiti wa mionzi na pia kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia nchini na katika mataifa haya ya mashariki na kusini mwa Afrika.Pia aliitaka Tume ya Atomiki (TAEC) kuacha urasimu na kukwamisha upimaji wa bidhaa za wafanyabiashara kwa haraka ili kuondoa malalamiko kwa wafanyabiashara wanaohitaji kupata uhakiki wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali ya mipaka na mengineyo.Alisema TAEC ni miongoni mwa Taasisi inayolalamikiwa sana na wafanyabiashara kutokana na urasimu wa ucheleweshwaji wa upimaji ikifuatiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Alisema urasimu katika taasisi hizo umekuwa ukilalamikiwa na wafanyabiashara na serikali imekuwa ipokea malalamiko kuhusu urasimu huo hivyo alitoa rai tatizo hilo liishe mara moja ikiweko TBS na TFD.“Serikali imejenga maabara hii ili kuhakikisha usalama wa nyuklia unakuwa salama kwa nchi na tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuhakikisha maabara hii inajengwa nchini kwani ni ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC)pamoja na Bara la Afrika.Alisisitiza TAEC kufungua maabara maeneo mbalimbali za kimkakati ili kupunguza urasimu na kumsisitiza Mwenyekiti wa Bodi ya Taec, Dk Najat Mohamed kuwapandisha vyeo wafanyakazi watatu ambao ni Patrick Simpokolwe, Mchibya Matulanya na Artanas Kalolo.Wafanyakazi hawa waliokataa rushwa maeneo ya mipakani wapandishwe vyeo na kuongezewa fedha badala ya Sh milioni moja hadi Sh milioni 3 kutokana na uzalendo walioonesha kwa kukataa rushwa na kukataa bidhaa zisizopimwa ubora wake kuingia nchini.Imeandikwa na Matern Kayera na Veronica Mheta. | kitaifa |
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa NBS, Ephraimu Kwesigabo, alisema jana kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Juni imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwezi Mei.Hata hivyo, Kwesigabo alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 148.98 kwa mwezi wa Juni kutoka 140.00 Juni 2013. Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi umepungua hadi asilimia 8.1 Juni kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa Mei mwaka huu.Mkurugenzi huyo alisema badiliko la Fahirisi za bei za bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani, imepungua hadi asilimia 8.7 kutoka asilimia 9.3 ilivyokuwa Mei wakati badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula, limeongezeka hadi asilimia 4.8 Juni kutoka asilimia 4.1 Mei mwaka huu.Akizungumzia mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi, Kwesigabo alisema umepungua kwa asilimia 0.6, ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.4 kama ilivyokuwa Mei.Fahirisi za bei katika kipindi hicho, pia zimepungua hadi 148.98 mwezi Juni kutoka 149.89 Mei mwaka huu. Kupungua kwa fahirisi hizo, kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula.Alitaja baadhi ya bidhaa za vyakula, zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele asilimia 3.0, mahindi asilimia 12.3, unga wa mahindi asilimia 3.5, muhogo kwa asilimia 8.9. Bidhaa zingine ni viazi vitamu asilimia 9.1, dagaa kwa asilimia 4.1, matunda jamii ya machungwa asilimia 14.4, mboga asilimia 1.2 na vitunguu maji kwa asilimia 2.5.Kuhusu thamani ya Shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma kutoka mwezi Septemba 2010, alisema imeongezeka hadi Sh 67 mwezi Juni kutoka Sh 66 na senti 72 Mei, mwaka huu.Mkurugenzi huyo alisema fahirisi za nishati na mafuta na fahirisi za vyakula na vinywaji baridi, zimekuwa na mwenendo wa juu kwa kipindi chote, zikilinganishwa na fahirisi nyingine."Kundi la nishati na mafuta limeonesha pia kuwa na mwenendo wa fahirisi usio imara ikilinganishwa na makundi mengine kwa kipindi husika," alisema Kwesigabo.Aliongeza kuwa fahirisi za bidhaa zisizo za chakula na fahirisi za bidhaa zisizojumuisha chakula pamoja na nishati, zimeonesha mwenendo wa bei ulio imara. | uchumi |
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ameanza operesheni maalumu ya kuzibana Taasisi ambazo ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Dara es Salaam kwa kutembelea ofisi moja hadi nyingine ili zilipe madeni yao katika muda uliopangwa.Katika ziara hiyo taasisi sita kati ya saba alizotembelea zimeahidi kulipa zaidi ya Sh bilioni 4.5 ifikapo Desemba, mwaka huu.Alitembelea taasisi hizo juzi ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisha wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi wanalipa madeni yao kabla ya hatua za kuwafikisha kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya wale watakaokaidi kulipa ambapo adhabu yake ni kulipa ama kupigwa mnada kwa mali za taasisi husika kufidia deni la kodi ya pango la ardhi.Taasisi alizotembelea Naibu Waziri huyo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalodaiwa SH bilioni tatu, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Sh bilioni 1.4, EPZA Sh milioni 200, Shirika la Reli Tanzania (TRC) Sh bilioni 2.5, Shirika la Masoko Kariakoo Sh milioni 249 pamoja na Chuo cha Taifa cha Utalii Sh milioni 26.8.Akiwa katika Shirika la Masoko Kariakoo, Naibu Waziri Mabula alishangazwa na Shirika hilo kudaiwa zaidi ya Sh milioni 200 huku likiomba kulipa deni lake katika kipindi cha miaka miwili jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za ulipaji madeni ya kodi ya pango la ardhi ambazo humtaka mdaiwa kulipa nusu ya deni.Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, Hetson Kipsi katika barua yake, Shirika lake liliahidi kulipa kwa awamu deni hilo katika kipindi cha miaka miwili kwa kutoa milioni saba kila mwezi jambo lililokataliwa na Naibu Waziri aliyeeleza kuwa Shirika hilo linapaswa kulipa nusu ya deni kwanza ndipo liingie makubaliano ya kulipa kiasi kilichobaki kwa awamu. Hata hivyo Shirika la Masoko Kariakoo lilikubali kutoa Sh milioni 100 ifikapo Julai 29, mwaka huu na kukamilisha kiasi kilichobaki Desemba, mwaka huu.Kwa upande wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mkurugenzi Mtendaji wake, Masanja Kadogosa alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi kuwa Shirika lake halipingi kulipa deni inalodaiwa bali inachofanya ni kuhakiki upya deni hilo kwa kuwa kumekuwa na uhamisho wa umiliki wa mali za TRC kwenda TBA tangu mwaka 1999 sambamba na baadhi ya nyumba za Shirika kuuzwa kwa wananchi huku baadhi ya mali za TRC zikiwa hazina hati.Kadogosa alisema kiasi cha Sh bilioni 2.4 wanachodaiwa ni kikubwa na hakilingani na uhalisia wa deni la TRC na kubainisha kuwa uhakiki utakapokamilika ana imani deni hilo litapungua kwa kiasi kikubwa.Mabula alimueleza kuwa, Shirika lake linapaswa kulipa robo ya tatu ya deni hilo wakati uhakiki ukiendelea na iwapo itaonekana deni limepungua basi kiasi cha fedha kilichozidi kitarudishwa, hata hivyo, Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TRC alikubali kulipa kiasi cha Sh milioni 400 kwa awamu hadi kufikia Oktoba, mwaka huu wakati kazi ya uhakiki wa deni hilo unaohusisha wataalamu wa shirika hilo na wizara ukiendelea. | kitaifa |
KOCHA wa Nigeria, Gernot Rohr ameibuka na kusema kuwa hapingi mfumo wa teknolojia ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) baada ya timu yake kushinda mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kuisni juzi katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).Mfumo wa VAR, ambao umeanza kutumika katika hatua ya robo fainali ya Afcon 2019 na umetumika kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo, umeingilia maamuzi ya mshika kibendera, Bongani Zungu ukidai kuwa mfungaji aliotea. “Ilibidi tusubiri kwa dakika tano, kujua goli au sio goli, na jambo hilo lilikuwa gumu kwa tuimu yangu,” alisema Kocha alipozungumza na waandishi wa habari. “Bao la pili halikuingia na uliona ule mpira wa adhabu, na uamuzi huu wa VAR una walakini kwani huwezi kujua nini kitatokea katika mpira wa adhabu.”Rohr pia alikipongeza kikosi chake kwa kutoka nyuma kwa 2-1 na kuibuka na kuifunga Cameroon kwa mabao 3-2 katika raundi iliyopita na kupata ushindi wa dakika za mwisho katika mchezo huo wa Jumatano. “Sasa tumeimarika kimawazo na tunaweza kurejea,” alisema. “Tabia ya wachezaji wangu ni ya ajabu...kama kuwa na uhusiano na kila mmoja.” Rohr alikumbuka wakati Nigeria ilipofungwa 2-0 na Afrika Kusini nyumbani wakati wa mechi za kufuzu kwa fainali hizo miaka miwili iliyopita, ukiwa mchezo wake wa kwanza akiifundisha timu hiyo.“Tulikuwa na timu changa lakini timu hii inaendelea kufanya kazi na matokeo haya labda yametusaidia kuifunga Cameroon katika mchezo uliofuata, ambao walikuwa mabingwa wa Afrika, 4-0 kwenye uwanja huo huo (katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la dunia, hivyo tumejifunza kutoka katika mechi hii,” aliongeza. | michezo |
Akizungumza kwenye uzinduzi wa vilainishi hivyo vya magari jana katika kituo kipya cha mafuta ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo nchini, Phillipe Corsaletti alisema promosheni hiyo itafanyika kwa wiki kadhaa.“Castrol inaongoza duniani katika ubora wa utengenezaji, usambazaji, matangazo ya vilainishi, grisi na huduma zinazohusiana na bidhaa hizo zitumikazo katika magari, viwanda, meli, ndege na katika uchunguzi na uchimbaji wa mafuta ghafi. “Puma na Castrol tuna mkakati wa pamoja na malengo sawa ya kukuza biashara yetu katika maeneo mbalimbali barani Afrika. Hivyo tega masikio na chunguza kwa makini alipo ‘Puma Man’ na ulizia ofa maalumu ambazo tunazitoa kwenye bidhaa zetu za Castro GTX 20W50 & GTX Diesel 15W40, katika kipindi hiki cha uzinduzi,” alisema Corsaletti.Puma Energy ni moja ya kampuni inayokua kwa kasi duniani, ikijishughulisha na usafirishaji, usambazaji wa mafuta vituoni na kwa watumiaji wakubwa wa mafuta. Puma Energy inafanya kazi zake katika nchi za Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, na Amerika ya Kusini.Puma ilianzishwa mwaka 1997 ikiwa na lengo la kuanzisha mtandao mkubwa unaojitegemea wa kuhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta. Puma ipo katika nchi zaidi ya 35 duniani likiwa na ofisi za kanda katika nchi za Afrika Kusini, Singapore, Australia na Estonia.Puma Energy inatoa ajira kwa zaidi ya watu 6,000 duniani na wengine zaidi ya 20,000 wakipata ajira katika vituo vya mafuta.Trafigura Group ambao ni miongoni mwa wachuuzi wakubwa wa bidhaa mbalimbali duniani, wanamiliki asilimia 50 ya hisa za Puma Energy. Sonangol kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Angola inamiliki asilimia 30 ya hisa za Puma Energy.Asilimia 50 ya hisa za Puma Energy Tanzania zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania, wakati asilimia 96 ya wafanyakazi wake 154 ni Watanzania wazawa. Aidha inatengeneza ajira kwa takribani watu 405 wanaofanya kazi kwenye vituo vya mafuta. | uchumi |
['Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale anakaribia kuondoka katika klabu hiyo kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Zinedine Zidane. ', 'Mchezaji huyo wa taifa la Wales aliwachwa nje wakati Real Madrid ilipolazwa 3-1 na Bayern Munich nchini Marekani.', 'Akizungumza baada ya mechi hiyo, Zidane alisema: Tunatumai ataondoka karibuni. Itakuwa vyema kwa kila mmoja wetu. ', 'Tunaandaa uhamisho wake kwa timu nyengine. Sina ubinfasi wowote dhidi yake , lakini inafikia wakati ambao lazima mambo yafanyike. ', 'Bale ambaye ana miaka mitatu iliosalia katika kandarasi yake ameshinda kombe la mabingwa Ulaya mara nne tangu uhamisho wake wa £85m kujiunga na Madrid kutokaTottenham mwaka 2013 - ambapo ulivunja rekodi ya dunia mwaka huo.', 'Akijibu matamshi ya Zidane ajenti wa Bale Jonathan Barnetta aliambia AFP: Zidane ni aibu hana heshima kwa mchezaji ambaye ameifanyia makubwa Real Madrid. ', 'Majeraha yamerudisha nyuma harakati za mchezaji huyo wa Wales akiichezea Real Madrid mara 79 pekee katika misimu minne. ', 'Alicheza mechi 42 msimu uliopita nusu ya mechi hizo akiwa mchezaji wa ziada. ', 'Bale alizomwa na mashabiki wa nyumbani msimu uliokwisha , ijapokuwa ajenti wake alisema mnamo mwezi Machi kwamba mchezaji huyo alitaka kumaliza kipindi chake cha mchezo katika uwanja wa Bernabeu.', "''Lazima tufanya uamuzi lazima tubadilishe'', aliongezea Zidane. ''Uamuzi wa kuondoka ni wa Mkufunzi na mchezaji ambaye anaelewa hali ilivyo. Hali itabadilika sijui baada ya saa 24 ama 48, lakini itabadilika, na ni vyema kwa kila mtu''. ", 'Bale alikuwa mchezaji wa ziada msimu uliopita huku Real ikikamilisha kampeni yake mbaya zaidi nyumbani katika kipindi cha miaka 20, ikishinda mara 12 kujipatia pointi 68 na kumaliza katika nafasi ya tatu alama 19 nyuma ya mabingwa wa ligi Barcelona. ', 'Pia walibanduliwa katika kombe la mabingwa na Ajax katika hatua ya muondoano. Zidane alirudi katika uwanja wa Bernabeu mnamo mwezi Machi na kuwa kocha wa tatu wa klabu hiyo msimu huu.', 'Wakati huo Barnett aliambia BBC kwamba usajili wa Zidane ulikuwa habari mbaya kwa kuwa hakupenda kufanya kazi na Bale na kwamba wawili hao wametofautiana kuhusu mbinu ya mchezo. ', 'Siku ya Jumapili Barnett aliambia BBC Wales kwamba tunafanya mambo fulani. ', "''Gareth Bale ni mchezaji wa Real Madrid lakini iwapo atakubali kuondoka utakuwa uamuzi wake mwenyewe, sio wa Zidane''. ", 'Mbali na mataji manne ya ligi ya mabingwa, Bale ameshinda taji la la Liga , Copa del Ray na mataji matatu ya Uefa mbali na lile la klabu bingwa duniani akiichezea Real Madrid.', 'Amewafungia mabingwa hao wa Uhispania zaidi ya magoli 100 lakini amepewa jina la utani la The Golfer na wachezaji wenzake na kipa wa Real Thibaut Courtois pia alisema kwamba Bale alikosa chakula chake cha jioni kwa kuwa hakutaka kukosa kulala wakati wake wa kawaida.'] | michezo |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imetaifi sha mali zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 93.16 sawa na Dola za Marekani milioni 41 zilizotokana na uhalifu.Mali zilizotaifishwa ni madini, nyumba, magari, fedha za upatu, mbao na maliasili kwa kipindi cha mwaka 2013 hadi 2019 zilizotokana na uhalifu wa kupangwa, utakatishaji fedha, kughushi na wanyamapori.Akifungua Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Taasisi zinazokabiliana na Uhalifu kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (ARINSA), jana jijini Dar es Salaam, Samia alisema miongoni mwa mali walizotaifisha ni madini yenye thamani ya Sh bilioni 32.Samia alisema mafanikio yaliyopatikana yametokana na marekebisho makubwa katika sheria za nchi, ikiwemo Sheria ya Utakatishaji wa Mali zinazotokana na Uhalifu na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu ili kuhakikisha zinakuwa na ufanisi unaotakiwa katika kupambana na mbinu mpya za kihalifu hasa unaovuka mipaka.Alieleza kuwa pamoja na kuwepo wapelelezi na waendesha mashitaka wachache waliopata mafunzo kupitia umoja huo, wamechangia kutaifishwa kwa mali hizo. Alisema hatua ya kutaifisha mali imerudisha heshima kwa kuhakikisha kuwa maliasili za Tanzania zinawanufaisha Watanzania na ni matokeo ya ARINSA inayohakikisha malengo yanafikiwa.“Niwahakikishie tutaendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za nchi wanachama wa umoja huu katika kufikia malengo yake ili kuhakikisha kuwa nchi za ukanda huu zinakuwa salama kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wake,” alisema Samia.Aliongeza kuwa umoja huo umetanua wigo wa ushirikiano katika masuala ya upelelezi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kiupelelezi zinazosaidia kuharakisha kukamilika kwa maombi ya ushahidi nje ya nchi na upatikanaji wa mali zinazohusiana na uhalifu. Samia alisema makosa mengi ya kupangwa na mbinu za utendekaji wake wa kisasa kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hususani Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).Pia alisema kupitia programu za wapelelezi na waendesha mashitaka wameweza kujengewa uwezo kwenye makosa ya kifedha, wanyamapori na misitu na ufadhili wa ugaidi, ikiwa ni pamoja na kufuatilia mali walizozipata wahalifu au kuzitumia kutenda uhalifu ili kuzitaifisha. “Nimeambiwa kuwa mkaa nao unachangia uhalifu kwani wapo baadhi ya watu wanauza mkaa nje ya nchi na kufadhili uhalifu.Kama msimamizi wa mazingira, tutahakikisha kuwa miti haikatwi kwa mkaa,” alifafanua. Alisema nchi wanachama zimefaidika kupitia programu za mafunzo kwa kurekebisha sheria mbalimbali zilizokuwepo au kutunga sheria mpya ili kurahisisha utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu na kuhakikisha nchi zinaendelea kuwa salama.Aidha, alizitaka nchi wanachama kuhakikisha kuwa kila mali inayotaifishwa kwenye nchi yao, asilimia kidogo ya fedha inayopatikana inaingia kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashitaka na kupelekwa ARINSA ili iweze kujitegemea na kuendeleza nchi mbalimbali za Afrika.Kwa upande wake, Rais wa ARINSA, Biswalo Mganga alisema kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2019 umoja huo umeweza kutaifisha mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.406. Mganga ambaye ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), alisema mwaka huu pekee mali zilizotaifishwa ni Dola za Maarekani milioni 700 na kwamba mali zinazoshikiliwa zinathamani ya dola za Marekani 594.23 na maombi ya kutaifisha mali ni 142.Alisema changamoto wanazokabiliana nazo ni kupoteza thamani ya mali zinazokamatwa na kukaa muda mrefu kwenye vituo vya polisi na baadhi zinaharibiwa na wahalifu wenyewe. Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga alisema ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii hauwezi kutimia endapo hakuna amani kwa watu na mali zao kwenye nchi wanachama. Aliwataka wawakilishi kutoka nchi 16 za ARINSA kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kujifunza na kufurahia uwepo wao hapa nchini. | kitaifa |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema serikali ipo mbioni kuweka utaratibu utakaowalazimisha waingizaji na wazalishaji wa chupa za plastiki kuziondoa kwenye soko kunusuru mazingira.Makamba ameyasema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha Paper Craft International kinachomilikiwa na Kampuni ya Said Salim Bakhresa Group kinachojihusisha na uzalishaji wa vifungashio vya karatasi.Alisema serikali haijapiga marufuku chupa za plastiki kwa sababu zina uwezo wa kurejelezwa, lakini baadhi ya chupa ambazo zinakinywaji cha kuongeza nguvu ‘energy drink’ zikiwemo zile zinazozalishwa na Kampuni ya Azam na Melt hazina soko na hivyo zimekuwa zikiharibu mazingira kwani zimejazana kwenye mitaro na pembezoni mwa bahari.“Hatupigi marufuku chupa za plastiki, lakini natoa wito kwa watu wote wazalishaji na waingizaji wa vinywajji vya chupa za plastiki na kama itahitajikaaidha waanzishe au washiriki katika urejelezaji wa chupa za plastiki, tunafanya vizuri kwenye vifungashio lakini chupa za plastiki ni changamoto... mwezi ujao tutalazimisha watu wanaozalisha chupa za plastiki kuziondoa kwenye mazingira aidha kwa kuziondoa au kuzirejeleza,” alisema.Waziri Makamba alisema chupa hizo za Energy Drink zenye rangi nyeusi zinazozalishwa na Azam hazina soko kwa vile bei zake ni ndogo kilo ni Sh 80 wakati chupa za maji ni Sh 400 hivyo watu hawaziokoti, hivyo kuna umuhimu wa kutazama mbinu mbadala ya namna ya kutumia malighafi ambayo itafanya zikusanywe kama ilivyo kwenye chupa za maji.Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa Uhusiano wa Said Salim Bakhressa, Hussein Sufian alisema wameshaanza mazungumzo ya ushirikiano na baadhi ya makampuni mengine ambao ni wazalishaji wa vinywaji baridi namna ya kuandaa mchakato wa ukusanyaji wa chupa ili zitengeneze bidhaa mbadala kwa kushirikiana na Afrika Kusini na kwamba mchakato huo utafanyika nchini nzima.Kuhusu kiwanda hicho, Makamba alisema endapo kitaanza kuzalisha vifungashio hivyo kwa ajili ya soko la ndani itarahisisha upatikanaji mkubwa wa bidhaa hiyo, hasa baada ya serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia mwezi uliopita.“Wakati tunatafuta namna ya kukidhi soko, wakati tunatafuta mifuko mbadala, kazi ya upigaji marufuku limejaribiwa takribani miaka 10 lakini tumekuwa tukihairisha kwa vile hatukuweza kukidhi soko. Wapo ambao walisubiri wakidhani tutahairisha tena,” alisema Makamba.Alisema ingawa serikali imepiga marufuku lakini bado hatukidhi uwezo wa kuzalisha kwa wingi vifungashio, mifuko yenye ubora na bei nafuu na hivyo serikali iliona faraja kuona kuna kiwanda kikubwa kama Craft International kinazalisha vifungashio ingawa pia hakizalishi kwa uwezo wake hasa soko la ndani.“Nimezungumza na waziri wa viwanda na biashara, sisi watu wa mazingira tungependa mifuko ya karatasi ndio ijaze soko kama mbadala ya plastiki, lakini changamoto imekuja kuwa mifuko ambayo ndio ipo sokoni kwa sasa kama mbadala ni ya kitambaa lakini chenye plastiki ambayo nayo si salama kwa mazingira,” alisema.Alisemaa kwa vile ni kipindi cha mpito serikali isingeweza kukataza watu kuzalisha ndio maana iliweka kiwango ambacho ni uwezo wa kurejelezwa ambao ni ya uzito wa gramu 70.Meneja Uhusiano wa makampuni ya Bakhresa Hawa Bayumi alisema namna ambavyo wanaweza kutumia fursa kufikia soko kutokana na mabadiliko ya kutunza mazingira na kubainisha kuwa awali kiwanda kilikuwa kwenye mfumo wa EPZ, kwa ajili ya kuzalisha vifungashio kwa ajili ya soko la nchi za nje, lakini sasa wanaangalia namna ambayo wanaweza kuzalisha vifungashio kwa ajili ya Tanzania na masoko ya nje.“Kwa sasa kiwanda kipo kwenye mfumo wa EPZ ama Kanda Maalumu ya uchumi, tunangalia namna ya kuamisha kwenye mfumo ambao utakua soko moja la ndani la Afrika Mashariki, lakini kwa sasa ni changamto katika sheria,” alisema Bayumi na kuongeza kuwa iwapo sheria hiyo ya EPZ itabadilishwa basi wataweza kuleta ushindani katika soko la ndani na Afrika Mashariki kwa ujumla. | kitaifa |
WABUNGE wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kurudisha zana za wavuvi zilizochukuliwa na kukamatwa wakati wa Operesheni Nzagamba II na wale walioziingiza nchini nyavu zenye saizi hizo ndogo wachukuliwe hatua.Wakichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa na Waziri Luhaga Mpina, wabunge wamesema nyavu zilizoharibiwa haziwezi kurudishwa, lakini injini za boti zinaweza kurudishwa.Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Christina Ishengoma alisema operesheni hiyo ya kutokomeza uvuvi haramu, ilisaidia kuongeza samaki, lakini akaomba waliohusika kuingiza nyavu zenye matundu madogo nchini wachukuliwe hatua.Alisema elimu pamoja na nyavu kuchomwa ni sawa, lakini akaomba walioingiza nchini nyavu hizo wachukuliwe hatua kutokana na kuwatia wavuvi hasara.Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (CCM) alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa ajili ya kulinda rasilimali hizo za nchi, lakini sera na sheria zilizokuwapo ziliathiri maisha ya wananchi kutokana na kuteketeza nyavu hizo.Alisema wananchi walinyang’anywa mashine na injini walizopata kwa jasho, hivyo inatakiwa warudishiwe mashine hizo ili waendelee na uvuvi na kulinda rasilimali za nchi kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.Alisema wizara inatakiwa kwenda mbali zaidi badala ya kuzuia kwa kuangalia saizi ya nyavu, zuio hilo linatakiwa kutolewa kwa vipindi, kuruhusu miezi kadhaa na kukataza mingine kuvua samaki.Alisema zuio limekuwa likifanyika nchini katika Ziwa Victoria, lakini nchi jirani za Kenya na Uganda, zimekuwa zikiendelea kuvua samaki ambao wanasafiri kutoka eneo moja hadi lingine na Tanzania kuendelea kupata hasara.Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) alitaka kujua wale waliochomewa nyavu zao katika operesheni hiyo serikali imeweka mkakati gani wa kuhakikisha wanafidiwa.Lakini pia alisema vifaa ambavyo bado vimeshikiliwa kama injini wanatakiwa kurudishiwa ili kuendelea kufanyia kazi.Mbunge wa Mtwara Mjini, Naftaha Nachuma (CUF) amesema operesheni hiyo ilisababisha nyavu za wavuvi wengi kuchomwa, lakini waliozileta nchini hawajachukuliwa hatua.Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba (CCM) alisema operesheni iliwahusu wananchi wake takribani asilimia 90, hivyo anaunga mkono serikali kupiga vita uvuvi haramu, lakini haungi mkono njia zilizotumika katika kufanya operesheni hiyo ambayo haikuzingatia sheria za nchi.Amesema operesheni hiyo ilihusisha pia vitendo vya rushwa kwani baadhi ya watendaji walitumia mwanya huo kupokea rushwa.Mbunge wa Viti Maalumu, Jacqueline Msongozi (CCM) alisema uvuvi haramu umeleta shida katika maeneo mbalimbali nchini. | kitaifa |
POLISI wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa inamshikilia William Sokoni (33) akidaiwa kumtukana matusi ya nguoni, mama yake mzazi, Clemensia Wangabo (77) na kumsababishia umauti.Mwanaume huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtenga inadaiwa alighadhabika baada ya mama yake mzazi kumtaka amlipe kiasi cha Sh 50,000 alizomkopesha muda mrefu.Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, wilaya ya Nkasi kwa masharti ya mtoaji taarifa kutoandikwa majina yake gazetini kwa kuwa sio msemaji wa jeshi hilo zimethibitisha kutokea kwa mkasa huo uliotokea Juni 10, mwaka huu katika kijiji cha Mtenga, Kata ya Mtenga wilayani humo.Diwani wa Kata ya Mtenga, Pacras Maliyatabu akizungumza na gazeti hili kuhusu mkasa huo katika mji mdogo wa Namanyere, alisema kuwa maziko ya mama huyo yalifanyika juzi kijijini humo.“Mama huyo kwa muda mrefu alikuwa akimdai mwanawe, William na kumtaka kiasi cha Sh 50,000 alizomkopesha... mke wa William alimsihi mumewe amlipe mama yake na kweli mumewe alikubali na kumpatia apeleke,” alieleza. Aliongeza kuwa baada ya mke wa William kufika nyumbani kwa mama mkwe wake ili alipe deni hilo, ghafla William alitokea nyumbani hapo na kuanza kumporomoshea matusi mama yake mzazi.“Alimtusi mama yake kuwa heri yeye William angenyonya maziwa ya mbwa kuliko ya mama yake huyo, ndipo ghafla mama huyo akaanguka na kupoteza fahamu mbele ya mwanawe huyo na mkewe,” alieleza Malyatabu.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mtenga, Daina Namfukwe alisema kuwa Clemensia alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika zahanati hiyo. | kitaifa |
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafi sadi imemhukumu raia wa Nigeria, Christian Ugbechi (28) kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafi risha pipi 56 za dawa za kulevya aina ya heroin hydrochloride.Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji Sirrilius Matupa alisema upande wa mashitaka katika kesi hiyo umethibitisha pasipo kuacha shaka kupitia mashahidi wake 11 na vielelezo 22 waliofika mahakamani hapo kuthibitisha mashitaka hayo.Aidha, mahakama imeamuru dawa za kulevya alizokutwa nazo mshitakiwa ziteketezwe kwa mujibu wa sheria. Jaji Matupa alisema mahakama imemhukumu mshitakiwa kutumikia miaka 30 gerezani na siyo kifungo cha maisha kwa sababu imeona inayo mamlaka ya kumpa mshitakiwa adhabu kwa jinsi yenyewe inavyoona kutokana na mkanganyiko uliopo kwenye kifungu cha sheria cha 15(1) (a) na 15(1).Alisema sheria hizo mbili zilikuwa na madhumuni tofauti kutokana na matumizi ya maneno ambayo yako kwenye kifungu cha 25(1)(a) na kifungu cha 15(1). Kabla ya kutolewa kwa adhabu, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai kuwa hawana kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa hivyo wanaomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, upande wa utetezi ukiwakilishwa na Jeremiah Ntobesya aliomba mahakama kumpunguzia adhabu mteja wake kwa sababu ana mke na watoto wawili wanaomtegemea.Pia alidai mshitakiwa huyo anasumbuliwa na matatizo ya moyo na kwamba alipokuwa gerezani kwa mwaka mmoja na nusu alikuwa na tabia njema. Katika ushahidi, askari wa upelelezi kutoka Kituo cha Uwanja wa Ndege namba G 1782 D/C Peter alidai kuwa aliandika maelezo ya mshitakiwa huyo na katika mahojiano alimueleza kuwa amemeza pipi za dawa za kulevya.Alidai baada ya kueleza hayo alimweka mahabusu ili azitoe na kwamba hadi Januari 30, 2018 saa 10:30 jioni alitoa pipi 23 alizomeza. Pia alidai walichukua kielelezo hicho na pipi nyingine zilizokutwa kwenye begi na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali ambapo kwa pamoja zilikutwa na uzito wa gramu 947.17. “Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa pipi zote zilikuwa ni dawa za kulevya ambazo ni heroin hydrochloride zilizochanganywa na paracetamol metronidazole na papavirine,” alidai Peter.Mkuu wa Kituo cha Uwanja wa Ndege, Inspekta Dickson Haule alidai siku ya tukio saa 08:00 mchana akiwa ofisini alijulishwa na askari huyo wa upelelezi kuwa kuna mtuhumiwa amekamatwa na dawa za kulevya. Haule alidai baada ya taarifa hiyo alienda Ofisi ya Polisi Interpol walipokuwa na alishuhudia mtuhumiwa akipekuliwa ndipo aliona begi dogo la mgongoni kuna pipi 56 zikiwa zimeviringishwa ndani ya soksi mbili nyeusi. Inadaiwa Januari 28, mwaka jana maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, alisafirisha dawa hizo zenye uzito wa gramu 947.57. | kitaifa |
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inaridhishwa na misaada inayotolewa na taasisi za fedha za kimataifa, ikiwemo Benki ya Dunia.Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia uliofanya ukaguzi wa miradi ya Mfumo wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kwa upande wa Unguja.Amesema Zanzibar ipo makini katika matumizi ya fedha za mfuko huo kuona kwamba zinawafikia kutokomeza umasikini.Alisema familia nyingi zilizoingizwa katika mpango huo zimetumia vizuri fedha za Tasaf, huku wengine wakitaka kuondoshwa na kuingizwa walengwa wapya ili wafaidike na fedha hizo.“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaridhishwa na utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini ambao umezifikia kaya masikini huku ikiwezesha familia hizo kupeleka watoto wao shule na kupata matibabu kwa wakati,” amesema.Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika mradi wa Tasaf, Muderius Abdillahi ameihakikishia Zanzibar kwamba taasisi hiyo itaongeza nguvu zake za uwezeshaji na utoaji wa taaluma katika kuona miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wananchi inapata mafanikio.Alisema uongozi wa juu wa Benki ya Dunia unaosimamia mradi wa Tasaf umefurahishwa na utekelezaji wa miradi ya Tasaf kwa upande wa Zanzibar kwani malengo yote yaliyowekwa yamefikiwa.“Benki ya dunia inaihakikishia Zanzibar kuendelea kuunga mkono katika utekelezaji wa mradi wa Tasaf ambao matunda yake yameonekana kwa wananchi wenyewe kutamka kufaidika na mpango huo,” alisema.Ujumbe wa Benki ya Dunia ulikuwepo Zanzibar kukagua na kufanya tathmini ya miradi ya Tasaf. | kitaifa |
Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Woiso Original Products, Leornad Mtei, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.Alisema baadhi ya wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ya utengezaji wa ngozi, wamekuwa wakishindwa kutengeza bidhaa zenye ubora zaidi ya bidhaa zinazotoka nje, kutokana na kushindwa kuwa na mashine nzuri.Alisema wapo wajasiriamali wengi wenye ujuzi, lakini wanashindwa kufanya vizuri kutokana na kutokuwa na miundombinu za kuwawezesha kuonesha ujuzi wao.“Serikali ni kama imetupa kisogo sisi wajasiriamali, ukiangalia nchi kama Ethiopia Serikali yao inawasaidia sana na wametuzidi mbali sana, serikali yao inawakopesha vitendea kazi na kufanya kazi yao kuwa bora,” alisema Mtei.Aliongeza kuwa serikali ingeweza kuwakopesha mashine za kuchanganyia ngozi, ingeweza kuwasaidia wao kutengeneza viatu vyenye ubora sawa na vile vya kutoka nchini Italia ambavyo vinaaminika kuwa imara.Serikali isiposhikamana nao hawataweza kufika mbali katika ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.“Tutaweza kufika mbali zaidi kama serikali itatubeba,” aliongeza. Aidha, alisema wafugaji pia bado hawana elimu nzuri ya kutosha kuhusiana na matunzo ya ngozi za mifugo hivyo kushindwa kujitengenezea kipato kizuri kutokana na ngozi hizo. | uchumi |
Yanga ilimtambulisha mshambuliaji Ibrahim Ajib iliyemsajili kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika. Singida United imemsajili mshambuliaji Pastory Athanas aliyedumu miezi sita tangu ajiunge kutoka Stand United Shinyanga.Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga Jangwani na alikabidhiwa jezi namba 10 aliyokuwa akivaa Antony Matheo ambaye hatakuwepo tena Yanga msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika Jezi namba 10 ndiyo ilikuwa ikivaliwa na mshambuliaji wa zamani, Jerry Tegete.Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema Ajibu hajapotea bali ameenda mahali sahihi. Alimtaka aoneshe jitihada kubwa kutimiza malengo yake. “Ajib ni kijana wangu, hapa hajapotea.Nimwombe tu kwamba aonyeshe jitihada, nidhamu na pia kiwango bora,” alisema. Mkwasa alisema Ajib akionyesha juhudi na kupata timu zinazomuhitaji nje ya nchi, watamwachia aende kujaribu bahati yake.Katika hatua nyingine, Klabu hiyo imesema inatarajia kuwapima afya wachezaji wote kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya soka Tanzania bara kuanzia Jumatatu ijayo. Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe alisema Kocha George Lwandamina ameagiza wachezaji wapimwe afya ili kujua hali zao waanze maandalizi wakiwa na nguvu.Alisema baadhi ya wachezaji waliokuwa likizo wanawasili leo. Hao ni Thaban Kamusoko na Donald Ngoma wa Zimbabwe. Awali Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo alisema Pastory amesaini kujiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili.Amesema usajili huo ni pendekezo la Kocha wao Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm anayemhusudu kutoka Stand United. Sanga ni mchezaji wa pili kuondoka Simba baada ya Ibrahim Ajib kusaini pia mkataba wa miaka miwili na mahasimu, Yanga SC | michezo |
WATU watano wakiwa ndugu wa kiume wa familia moja waliopigwa risasi na askari wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na kulazwa kwa matibabu katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Katavi, wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu ya kibingwa, ikiwamo kuwatoa risasi kwenye miili yao.Wanaume hao ni wakazi wa Kijiji cha Ikongwe kilichopo katika Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mpanda ambao walituhumiwa na askari hao wa TFS kuwa walikuwa wamevamia Hifadhi ya Misitu Msaginya, ambao unahifadhiwa na kumilikiwa na TFS na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo.Kutokana na kujeruhiwa vibaya na risasi za moto katika sehemu mbalimbali za miili yao, watano hao walikimbizwa na kulazwa kwa matibabu katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Katavi iliyopo katika Mji wa Mpanda. Watano hao ni Filbert Patrick (40) aliyejeruhiwa mguuni na wadogo zake watatu Joseph Patrick (27) amejeruhiwa kifuani, Geoffrey Patrick (39) aliyejeruhiwa mkono wa kushoto na Januari Patrick (22) aliyejeruhiwa begani.Mwingine ni Nkuba Sai aliyejeruhiwa mkono wa kushoto. Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa watano hao wamelazimika kuhamishiwa Mbeya kwa matibabu ya kibingwa baada ya madaktari wa Hospitali Teule ya Katavi kushindwa kutoa risasi zilizomo ndani ya miili yao ambayo imeharibu pia mifupa kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya x-ray hospitalini hapo.Baadhi ya ndugu wa majeruhi hao kwa masharti pia ya kutoandikwa majina yao, wamekiri majeruhi wote watano tangu juzi wamesafirishwa jijini Mbeya kwa matibabu ya kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Akizungumzia hilo, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Richard Mbogo alithibitisha kutokana na Hospitali Teule ya Mkoa wa Katavi kutokuwa na x-ray, majeruhi hao wamelazimika kuhamishiwa Mbeya ili wapatiwe huduma za kibingwa.Alieleza kusikitishwa kwake na kitendo kilichofanywa na askari wa TFS huku akisisitiza hawakuwa na sababu yoyote ya kutumia nguvu kubwa kiasi hicho kuwapiga risasi wananchi ambao hawakuwa na silaha zozote zile. “Eneo hili linalodaiwa na TFS lilipimwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2002 na kuwa eneo la wananchi ili waishi na kufanyia shughuli za kibinadamu ...isitoshe waliopima eneo hilo mwaka huu ilikuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kabla ya kuanzishwa kwa Halmashauri ya Nsimbo,” alisema Mbogo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda juzi alikiri kuokota ganda la risasi lililotumika katika bunduki aina ya shotgun katika eneo hilo la tukio ambao inadhaniwa kutumika na askari hao wa TFS. Pia alikaririwa akisema ameagiza askari wote wa TFS waliohusika wasakwe na wakamatwe ili wahojiwe na watakaobainika wafikishwe mahakamani, lakini jana alipohojiwa hakuwa tayari kuthibitisha kama wameshawakamata au wanaendelea kusakwa.Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Sitalike, Adamu Cherehani, kiini cha shambulio hilo ni askari hao wa TFS kufyeka mahindi katika shamba la wanakijiji ambao baadaye kama 10 walijitokeza na kuanza kuwazomea, na wakati wakiondoka katika gari lao, askari hao walianza kuwashambulia wananchi hao kwa kuwapiga risasi za moto na watano kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao wanne kati yao ni ndugu. | kitaifa |
KAMPUNI ya ndege Tanzania (ATCL) imesema haijaajiri wazee kutoa huduma kwenye ndege na pia wote wanaofana kazi hiyo wana sifa za kitaaluma kwa kuwa utaratibu wa kuwapata, umezingatia matakwa ya kimataifa yanayohusiana na kazi hiyo na si urembo wao.Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema jijini Dar es Salaam kuwa, kimsingi wahudumu wa ndege hizo, wameajiriwa kutokana na sifa sambamba na kuwa na viwango vinavyotambuliwa na Mamlaka ya Usalama Anga (TCAA).Amesema, ATCL ina wahudumu wa kike na wa kiume, na wote urefu wao haupungui futi 5.2 na kwamba urefu huo ni kwa mujibu wa sheria, kanuni na aina ya ndege zao na kwa kuzingatia sheria za kimataifa.Kwa mujibu wa Matindi kuhudumia ndani ya ndege ni taaluma yenye vigezo na masharti na kwamba, ATCL inazingatia hilo"Kwa hiyo tunapozungumzia uzuri ni ule uwezo wa kufanya ile kazi, kwangu ndiyo definition (maana) ya uzuri, uwezo wa kufanya ile kazi na ile haiba ambayo tumeieleza sie, urefu wa chini futi 5.2, uzito upo umeelezwa kabisa body mass index yaani uwiano wa urefu na uzito wa mtu, upo umeelekezwa na hii ni kwa sababu aweze kufanya kazi zake bila matatizo sio awe aende akafanye catwalk, siajiri catwalkers, hapana." amesema MatindiAlisema ATCL inatekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Chicago, unaoelezea viwango mbalimbali wanavyohitajika kuwa navyo watoaji wa huduma za ndege, huku ikizingatia viwango vya urefu vya wahudumu hao na mafunzo waliyopata tayari, kukabiliana na hali yoyote inayoweza kujitokeza wakati wa safari.“Mhudumu anayepaswa kufanya kazi hizi, kwanza anapaswa kuwa mwenye uwezo wa kumiliki vifaa vyote vya usalama ndani ya ndege mbali na uzoefu wa kuogelea, kwa kuwa jukumu lake ni kuhakikisha anamsaidia msafiri kwa hali yoyote pale majanga yanapotokea,” alisema Matindi.Kauli ya Mkurugenzi huyo, imekuja siku chache tangu kutolewa hoja na mmoja wa wabunge bungeni, aliyesema kuwa wahudumu wa ndani ya ndege za kampuni ya ATCL, hawana mvuto kutokana na kutokuwa warembo, ikilinganishwa na mashirika mengine ya ndege na hivyo kuzua mjadala."Tuna experienced cabin crew na lazima uwe na experience hiyo, unajua kutengeneza hao mabinti wazielewe kazi, kuwe na nidhamu kwenye ndege na kila kitu kwa hiyo ni taaluma, ni taaluma yenye masharti na vigezo, kuna kigezo cha uzuri kinazungumzwa, mimi uzuri siwezi nikau-define, sijui nyie waandishi kama mnajua, nani mzuri kati yenu hapa ajitokeze aseme uzuri ni mimi, ukitaka kuajiri ukisema uzuri ni mimi"amesema Matindi.Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye alitoa ufafanuzi kwa mbunge huyo, kwa kueleza kuwa suala la wahudumu wanaohitajika kufanya kazi katika ndege hizo, linasimamiwa zaidi na taaluma na siyo urembo wao.Akisisitiza majibu hayo, Mkurugenzi huyo wa ATCL alisema kama mahitaji ya wahudumu wa ndege hizo, yangekuwa yanahusu urembo wao, wangeweza kuwaajiri washiriki wa mashindano ya urembo, kufanya kazi katika ndege hizo.Lakini, siyo hivyo, ndiyo maana wamewaajiri wahudumu wenye vigezo vinavyotambuliwa kimataifa.Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alisema tangu kuanzishwa kwa safari za ndege kwenda mkoani Katavi, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa abiria na kuifanya ndege hiyo inayofanya safari mara moja kwa wiki kujaa kila wakati.Alisema kutokana na hatua hiyo, wanatarajia kuongeza safari za ndege hiyo ifikapo Desemba mwaka huu baada ya kuwasili kwa ndege zingine mbili kati ya mwezi huu na Desemba. | uchumi |
Serikali ya Kenya imetangaza kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa ndani katika miji mikubwa kufi kia Shilingi za Kenya 13,500, ambayo ni sawa na zaidi ya 300,000 za Tanzania .Lakini, kwa upande wake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema katika kuhakikisha mishahara inapanda katika sekta za umma na binafsi baada ya kukaa kwa zaidi ya miaka mine, wameunda tume maalum kwa ajili ya kuchambua sababu za kutaka mishahara kupanda. Tume hiyo itaangalia namna ya kupanda mishahara kwa wafanyakazi wote, wakiwemo wa ndani, kwa kuongeza kima cha chini cha sasa cha Sh. 100,000. Kwa Kenya, wizara inayoshughulikia masuala ya ajira imetaka waajiri katika miji mikubwa, kuwalipa wafanyakazi wa kazi za ndani kiwango hicho cha mshahara, hasa kwa wanaoishi miji mikubwa ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.Aidha, wale wanaoishi katika Manispaa na Halmashauri za miji watawalipa wafanyakazi wao mishahara ya Shilingi za Kenya 12,522, sawa na Shilingi za Tanzania 284,586 au Shilingi za Kenya 600 sawa na 13,600 kwa siku . Hatua hiyo imetokana na wafanyakazi wa ndani kuandamana katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika Viwanja vya Uhuru Park. Wafanyakazi watakaonufaika na malipo hayo mapya ni wafanya usafi, wasimamizi wa bustani, waangalizi wa watoto, wasaidizi wa kazi za ndani, walinzi na wahudumu.Marekebisho hayo yamesainiwa na Waziri wa Kazi, Ukur Yattani Desemba 19. Alisema agizo hilo jipya la mishahara, litaongezwa katika posho ya nyumba kwa wafanyakazi. Pia waajiri wanatakiwa kutoa michango katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mwezi. Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya akizungumza na gazeti hili , alieleza mikakati ya shirikisho hilo ni kutaka mishahara katika sekta zote kupanda, tofauti na ilivyo sasa ambapo kima cha chini ni Sh.100,000. “ Kima cha chini hiki kimekaa muda mrefu na sasa tumeunda kamati ya wataalamu kutoka vyuo vikuu na taasisi zisizo za kiserikali, kutusaidia kuangalia hoja zitakazosaidia nia yetu kufanyiwa kazi”alisema Alisema kamati hiyo inatarajia kuwapelekea mapendekezo mwezi ujao ili kuweza kufanyia kazi na kuwasilisha wakati wa Sikukuu ya Mei Mosi na utekelezaji wake ufanyike kuanzia mwezi Julai mwaka huu. | kimataifa |
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeongeza udhibiti biashara haramu ya nyara za serikali, pembe za ndovu, madini, dawa za kulevya na vitu vinavyopita viwanja vya ndege.Hatua hiyo ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Hamad Masauni alipofanya ziara ya kukagua hali ya usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal 1, Terminal 2 na Terminal 3.Masauni alisema madini ya dhahabu kilo 35.34 kusafirishwa kupitia viwanja vya ndege vya Mwanza na Kilimanjaro na kukamatiwa Kenya, kumewatia aibu, hivyo wamechukua hatua madhubuti kudhibiti biashara hizo haramu. Alisema vyombo vyote vya ulinzi na usalama na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) vitashirikiana kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi kutumia viwanja hivyo.“Lengo la ziara yangu ni kuangalia usalama wa viwanja vya ndege nchini na leo nimeanzia hapa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambao ndiyo mkubwa,” alisema.“Kitendo cha dhahabu yetu kukamatwa nje ya nchi kimetutia aibu kwa kweli, Mheshimiwa Rais John Magufuli anapambana sana kulinda rasilimali za nchi yetu ziwanufaishe wananchi, hivyo tutafanyia kazi upungufu na changamoto zote jambo hili lisijirudie,” alieleza Masauni.Alizitaja baadhi ya changamoto zinazovikabili viwanja vya ndege ni ushiriki madhubuti wa vyombo vya ulinzi na usalama na TAA, jambo ambalo alisema linafanyiwa kazi ili vyombo hivyo vifanye kazi kwa pamoja kwa ufanisi. Alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kupeleka askari wa kutosha uwanjani hapo wenye vigezo na uwezo kubaini vitu vinavyotoroshwa kama madini, dawa za kulevya na nyara za serikali na vitu vingine.Pia alimwagiza IGP Sirro kuongeza idadi ya askari mbwa wenye ubora na sifa ya kubaini vitu vya uhalifu hasa jengo jipya la Terminal 3. Alisema kitengo cha mbwa wa Polisi katika viwanja vya ndege lazima kiimarishwe na atafuatilia kama maagizo hayo yametekelezwa. Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Jeremia Shila alisema wamejipanga kimfumo, kimaadili na kiushirikiano ili kuhakikisha hakuna kitu chochote kibaya kinachoweza kuingia nchini au rasilimali yoyote ya nchi kutoroshwa kupitia viwanja hivyo.Ofisa wa Polisi wa Kikosi cha Mbwa Uwanjani hapo, Inspekta Omary Lunyombe alimweleza Waziri Masauni kwa sasa wana mbwa wanne na wanahitaji waongezewe mbwa 12 kukidhi mahitaji.Alisema mbwa wazuri, wenye ubora na uwezo wanapatikana Marekani au Ulaya. “Uwanja huu ni bora Afrika kutokana na teknolojia ya kisasa iliyofungwa. Mifumo ya kukagua abiria na mizigo iko imara na inafanya kazi vizuri. Tuna kamera za kutosha za usalama na watu wa usalama wanafanya kazi vizuri,” alisema Meneja wa Terminal 3, Burton Komba.Akiwa Terminal 2, Ofisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), John Badika alimwonesha Naibu Waziri kupitia kompyuta yake namna wanavyoweza kubaini vitu vya uhalifu vilivyofichwa kwenye mzigo wa abiria. | kitaifa |
KOCHA Mkuu wa Simba, Patric Aussems amedai kutoridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo Simba walishinda kwa mabao 2-1.Simba ilitwaa taji hilo ikiwa ni mara yake ya nne, wakati wapinzani wao Yanga wakilitwaa mara tano tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2001.Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha huyo amesema dakika 25 za kipindi cha kwanza timu yake haikucheza mpira mzuri na kutoridhishwa na mbinu ya mipira mirefu ambayo ilitumiwa na wachezaji wake na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo.“Tumeonesha uwezo mzuri,lakini sikufurahishwa na kiwango cha wachezaji kukaa na mipira, walikuwa wakitumia mipira mirefu na natakiwa kulifanyia kazi kwa mchezo ujao, mimi nina aina yangu ya uchezaji, sitaki kutumia mipira mirefu kwa sababu wachezaji wangu hawana uwezo wa kuitumia,” amesema Aussems.Amesema timu yake ina wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu na katika hilo alisema anataka kumiliki mpira kwa viungo wake kupiga pasi za mwisho zenye uhakika na sio mipira mirefu.Katika mchezo huo, Kiungo Hassan Dilunga na Emanuel Okwi waliumia na kutolewa nje, ambapo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons, Kocha huyo alisema atapokea ripoti ya madaktari kujua hali zao kiafya. | michezo |
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman ameitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kurekebisha sheria zilizopitwa na wakati ambazo baadhi hazifanyi kazi tena.Suleiman alisema hayo wakati akiagana na wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Mazizini kutokana na kutenganishwa kwa wizara na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.Alisema katika kipindi cha miaka mitatu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya kazi kubwa ya kuzifanyia marekebisho sheria zilizopitwa na wakati. Alizitaja sheria zilizofanyiwa marekebisho katika kipindi chake ni pamoja na sheria ya ushahidi ambayo ilikuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu.“Mafanikio yangu makubwa katika kipindi cha miaka mitatu nilipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria ni kufanyiwa marekebisho kwa sheria ya ushahidi ambapo sasa ushahidi wa mtoto unatambuliwa,” alisema.Aliyataja marekebisho mengine yaliyofanyika katika sheria zilionekana kikwazo katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ni Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2017.Alisema sheria hizo kwa kiasi kikubwa zimeleta mabadiliko makubwa na kudhibiti matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na kutambua ushahidi unaotolewa na mtoto ambaye hajafikia umri wa miaka 18.“Naipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa kazi kubwa ya kuzifanyia marekebisho sheria zilizopitwa na wakati ambazo ni kikwazo katika kutekeleza majukumu ya wananchi,” alisema.Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hassan Said Mzee alisema wataendelea kuzifanyia marekebisho sheria zilizopitwa na wakati ambazo hazina maslahi kwa jamii.“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu moja ya vipaumbele vyetu ni kuzifanyia marekebisho sheria zilizopitwa na wakati ambazo hazina tija kwa jamii,” alisema.Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Jaji Bakari Mshibe alisema zipo sheria ambazo zinahitaji marekebisho makubwa zikiwa na lengo la kuleta mabadiliko ya sheria.“Miongoni mwa kazi tunazotarajiwa kuzifanya ni kurekebisha sheria zilizopitwa na wakati na kutunga mpya ili kuleta mabadiliko makubwa ya wakati uliopo,” alisema. | kitaifa |
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limebuni mkakati maalumu utakaotoa fedha kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu, watakaoibuka washindi kwa kuandika mapendekezo bora ya kibiashara yanayohusu utalii, kilimo, nishati mbadala na masuala ya mazingira.Mkakati huo wa NEEC wanaoshirikiana na Ubalozi wa Uholanzi utawalenga zaidi vijana wa umri kati ya 18 na 35, katika kuanzisha na kuendeleza biashara watakazozifanya ambazo siku zijazo zitaweza kuwaajiri vijana wengine ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana.Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa amesema jijini Dar es Salaam kuwa, kwa kuanzia, vijana watakaojitokeza wataanza na programu maalumu ya mafunzo itakayowalenga vijana 50 kutoka vyuo vikuu nchini kuwapa ujuzi na kuwawezesha.“Vijana tutaowachukua ni wale ambao ndiyo kwanza wametoka vyuoni, lakini pia wale ambao walihitimu masomo yao miaka mitano iliyopita pia wanakaribishwa kuhudhuria programu hiyo ambayo itawawezesha wao kuanza na kukuza biashara mbalimbali watakazokuwa nazo,” amesema.Amesema vijana wanaotaka kuhudhuria programu wanapaswa waandike pendekezo la biashara kwenye maeneo ya utalii, kilimo, nishati mbadala au mazingira.Mtaalamu huyo wa masuala ya uchumi aliongeza kuwa kwenye mafunzo hayo, programu ya wiki moja ya ujasiriamali itafanyika na itawasaidia vijana kupata mbinu za kijasiriamali ikiwemo kujua jinsi gani ya kuendesha biashara kisha wataandika pendekezo ambalo litashindanishwa kwenye mashindano.“Vijana ambao watachaguliwa kwa ajili ya kozi ya wiki moja, wataandaa pendekezo kwa ajili ya kushindana na washindi watatu watapewa zawadi. Mshindi wa kwanza atapata Sh milioni 10, wa pili atapewa Sh milioni saba wakati wa tatu atajishindia milioni tano,”amesema.Aidha, amesema kuwa washiriki wengine watanufaika na mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na ujuzi wa masuala ya biashara.Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul alisema kuwa programu hiyo itasaidia vijana kwenye masuala ya kuongeza ujuzi kwenye ujasiriamali na hivyo kupunguza tatizo la ajira. | uchumi |
FAMILIA ya Naomi Marijani, mwanamke anayedaiwa kuuawa na mumewe Khamis Luongo kisha kuchomwa moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, imesema bado haina imani kama ndugu yao huyo kuteketezwa kwa moto wa mkaa.Kauli yao hiyo imekuja baada ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kigamboni, Thobias Walelo kubainisha kuwa Naomi ameuawa na mumewe huyo ambaye baada ya tukio hilo alichimba shimo na kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia mkaa magunia mawili.Walelo alisema, Jeshi la Polisi lilimhoji Luongo aliyekiri kutekeleza mauaji hayo na kuwa aliuchomea mwili nyumbani kwake Gezaulole Kigamboni, hatua iliyowafanya wataalamu kutoka Jeshi la Polisi kufuatilia mabaki ya mwili wa marehemu Kigamboni ili kuchukua mabaki ya mwili kwa uchunguzi ili kubaini ukweli kama mabaki hayo ni mwili wa Naomi.Jana gazeti hili liliwasili nyumbani kwa dada wa marehemu, Salma Marijani aishiye, Mbweni- Ubungo, Dar es Salaam na kuzungumza na Msemaji wa familia Wiseman Marijani ambaye alibainisha kuwa hawana imani kama ndugu yao amechomwa moto kweli. Hata hivyo alisema kuwa familia itaendelea kusubiri majibu ya Polisi. Alisema mtuhumiwa huyo amedanganya wanafamilia kuwa ndugu yao amesafiri nje ya nchi baada ya kupata mwanaume mwingine huku akijua fika kuwa amemuua. | kitaifa |
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) inatarajia kuendesha kampeni maalumu ya mfano, kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika eneo la mpaka wa Namanga unaoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.Kampeni hiyo inatarajiwa kuwa na matokeo chanya na kujenga uwezo wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko hasa kwa nchi hizo mbili.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Jumuiya ya Afrika Mashariki ilieleza kuwa kazi hiyo itafanyika kwa siku nne kuanzia Juni 11 hadi 14 mwaka huu.Kampeni hiyo itakayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kuwahusisha wadau 250 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wanaohusika na afya ya wanyama, afya ya binadamu, mazingira, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, waandishi wa habari, wananchi na viongozi wa kijamii.Wananchi wanafanya shughuli zao katika mpaka wa Namanga wilaya ya Longido Kaskazini mwa Tanzania na upande wa Kajiado nchini Kenya wameombwa kuwa watulivu kwa kipindi cha siku nne za majaribio na kutokuwa na hofu.Mwakilishi wa Shirika la GIZ, Dk Irene Lukassowitz alisema kama watu watakuwa na taarifa sahihi watajua jinsi magonjwa ya milipuko yanaambukizwa hivyo ni rahisi kujikinga.Alisema, “Hicho ndicho tulichojifunza kuhusu ugonjwa wa ebola huko Afrika Magharibi. Tunatakiwa kuunganisha nguvu na kufanya kazi pamoja ili kupambana na magonjwa haya, na ndio maana tunawaleta watu pamoja ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko,” alisema Dk Lukassowits.Katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuna magonjwa mengi ya kuambukiza yanayoathiri wanyama na binadamu kama vile homa ya bonde la ufa, ebola, kipindupindu na kichaa cha mbwa na ndio sababu jumuiya hiyo inaona upo umuhimu wa wadau mbalimbali kutoka eneo hilo kuunganisha nguvu kuyadhibiti.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Michael Katende alisema mpango huo unafuatia makubaliano ya mawaziri wa afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofikiwa mwaka 2015 ya kudhibiti magonjwa ya milipiko kwenye maeneo ya mipakani.Magonjwa hayo ya milipuko yanatajwa kuzikumba nchi nyingi hasa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara na kuua maelfu ya watu, kuathiri mifugo, makazi pamoja na uchumi. | kitaifa |
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amewataka baadhi ya wanasiasa nchini wanaobeza majadiliano yaliyofanywa baina ya Rais John Magufuli na viongozi wa madhehebu ya dini Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni kutubu kwa kitendo hicho.Aidha, amewaonya wanasiasa nchini kuacha kuropoka hovyo, mambo yanayochochea chuki miongoni mwa jamii, kwa vile maneno ni sumu itakayowagharimu na kuwaangamiza kisiasa.Ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye Ibada ya pili kanisani hapo, huku akiwaambia waumini wake kuwa ni jambo la kusikitisha, kuona baadhi ya wanasiasa wanawatukana viongozi wa dini walioalikwa Ikulu hivi karibuni kuzungumza na Rais Magufuli.“Ni jambo la kusikitisha sana kuona baadhi ya wabunge wa Chadema ambao wana nafasi kwneye chama hicho wanawatukana viongozi wa dini kwenye mitandao kuhusu mazungumzo yao na Rais Ikulu, wanatubeza, mambo waliyoyataka wao sisi hatukuyasema, sasa ni vyema wakatubu vinginevyo, watatumbukia kwenye shimo refu na hawatainuka tena,” amesema Askofu Kakobe huku akishangiliwa na waumini wa kanisa hilo.Akizungumzia hilo kwa undani, alisema mkutano wa viongozi wa dini na Rais Magufuli Ikulu, ulikuwa wa kipekee kuwahi kutokea nchini na ulikuwa na baraka na furaha kwa viongozi wote na pia uliwafanya viongozi wote kuwa wamoja licha ya imani zao tofauti.“Ni mkutano wa ajabu, ulikuwa baraka na furaha sana, viongozi wote wa dini tulifurahi na haijawahi kutokea, na huo ulikuwa mwanzo mzuri wa kujadili mambo mengine yahusuyo nchi yetu, cha ajabu ni baada ya kumalizika, huko mitandaoni wakaibuka wabunge wa Chadema na kuanza kuwashambulia viongozi wa dini kwa kebehi na matusi, na hakuna kiongozi wa chama hicho aliyesimama na kuwaonya, hii sio sawa,”alisema Askofu Kakobe.Alisema ni lazima watubu hadharani, kama ambavyo wameandika kwenye mitandao ya kijamii vinginevyo hawatakuwa na mustakabali mzuri kisiasa.Alisema ni vyema wakatambua nguvu ya viongozi wa dini na kwamba matusi ya wabunge hao, yamewaumiza viongozi wote wa dini si yeye pekee na kuvitaka vyama vya siasa nchini kurejea kwenye kanuni ya zamani ya vyama, kuwapika makada wao ili wajifunze maadili na jinsi ya kuzungumza badala ya kuropoka.“Vyama vya siasa jifunzeni enzi za zamani kulikuwa na vyuo vya kuwatengeneza makada na walipikwa vyema wakawa wepesi wa kusikia na si kusema, pia walijua hasara za kauli za wanasiasa iwapo zitatolewa haraka haraka,”alisema.Katika hatua nyingine, Askofu huyo alisema, ni agizo la Mungu kuwaombea viongozi wa nchi kama Rais na Wafalme na kwamba yeye kama kiongozi wa kanisa na mtumishi wa kiroho, ana jukumu la kumuombea Rais na kuheshimu mamlaka yake.“Mnapaswa kutambua mamlaka ya Rais na kuitii, na hili ni la wote vyama vya siasa, wanasiasa na wengine, na sisi watumishi wa Mungu tulipewa fursa ya kuzungumza na Rais na hata hatujaenda hatua ya pili, wanasiasa wanaleta maneno,sasa kwa maneno hayo ya ovyo hamuwezi kupata ufumbuzi wa mkwamo wenu wa kisiasa,”alisisitiza.Aliongeza,” Zamani nilikuwa simuelewi Rais, hata pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa kupokea ndege yetu, niliongea na Rais kuhusu fursa ya kukutana na viongozi wa siasa na yeye aliniambia unawezaje kukutana na watu wanaokutukana kila siku , leo ndio nimemuelewa,”alisema Kakobe.Alisisitiza ni vigumu kukutana na watu wanaokutukana kwa majina tofauti kila siku na kuwataka wabadilike, vinginevyo kwa staili hiyo haiwezi kuleta suluhu ya siasa nchini na mwisho wa siku wataachwa wapambane na hali zao wenyewe.“Tubuni mmeyataka wenyewe, vinginevyo pambaneni na hali zenu sisi tunakula bata Ikulu,” alisema Askofu Kakobe.Hata hivyo, aliwakumbusha wanasiasa kuwa watambue kuwa Tanzania si nchi yenye asili ya vurugu na kama walitarajia kufanya hayo, hawatafanikiwa huku akiwataka warejee mpango wao wa Aprili 26, mwaka jana ambao ulikwama.“Jifunzeni ,Watanzania si watu wa asili ya vurugu, kama mlitarajia hilo hamtafanikiwa, kumbukeni mpango wenu wa Aprili 26, mwaka jana (maandamano yaliyoandaliwa kwa kushinikizwa na baadhi ya Watanzania waishio nje), hamkufaninikiwa, jifunzeni,”alisisitiza.Wakati huo huo, muungano wa vyama 10 vya upinzani vya siasa umeipongeza serikali kwa kupokea maoni yao na kuyaingiza katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.Viongozi wa vyama hivyo wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, walisema Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imepokea maoni yao na kuyafanyia kazi hivyo hawana budi kupongeza, lakini pia kuendelea kuomba mabadiliko zaidi katika yale yaliyoachwa ambayo wao wanaona kuna umuhimu wa kuyabadili.Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu, alisema kuwa yapo mambo ambayo walipigia kelele yamepokelewa na Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.“Yapo mambo ambayo tulipigia kelele, kuyalalamikia, yamesikilizwa, kamati imesikiliza kilio chetu na imeyapokea tunapongeza kwa hilo,” alisema Mwalimu akitoa tamko kwa niaba ya vyama vya Chadema, ACT Wazalendo, CHAUMMA, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR Mageuzi, CCK, DP, UPDP, NLD na ADC. | kitaifa |
BODI ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali imetakiwa kuhakikisha miradi inayotekelezwa na mashirika hayo inazingatia mipango na vipaumbele vya serikali na wananchi katika eneo husika.Hayo yameleezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati wa kufunga mafunzo ya wajumbe wa bodi hiyo yaliyofanyika jijini hapa.Alisema ili kusaidia utekelezaji wa pamoja wa afua mbalimbali na hivyo kuharakisha juhudi za kuwaletea maendeleo ya wananchi wa Tanzania, ni lazima bodi kuzingatia kwa umakini vipaumbele na mahitaji ya wananchi na serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.“Katika eneo la kisheria ambalo napenda bodi izingatie kwa umakini ni eneo la vipaumbele na mahitaji ya wananchi na serikali katika kutekaleza miradi ya maendeleo,” alisema na kuongeza: “Kwa kuimarisha uratibu, serikali itaweza kuwa na utambuzi wa maeneo yenye uhitaji wa huduma za kijamii, hivyo kupunguza mrudikano wa shughuli za NGOs katika eneo moja na kuacha maeneo mengine yenye uhitaji mkubwa wa huduma za jamii”.Alisema uratibu imara utaiwezesha serikali kujipima na kutathimini utekelezaji wa mipango na mikakati yake ya maendeleo kwa kuhusisha juhudi zilizofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali, jambo ambalo litawezesha serikali kutumia rasilimali za umma kwa ufanisi kwa kuandaa bajeti inayozingatia mahitaji halisi ya wananchi. Bodi hiyo mpya ambayo ni ya nne chini ya uwenyekiti wa Dk Richard Sambaige imepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika sheria juu ya miongozo ya uendeshaji wa NGOs nchini.Naye, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk John Jingu alisema kuanza kazi kwa bodi mpya hiyo kutasaidia mabadiliko chanya kwenye sekta ya NGOs nchini hasa katika suala zima la uwazi na uwajibikaji kwa wananchi wanaowahudumia. Naye, Kaimu Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Neema Mwanga alisema baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo kutasaidia baadhi ya NGOs kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, kanuni za uwazi na uwajibikaji kwani kinyume chake chombo hiki kitawachukulia hatua. | kitaifa |
SIMBA tayari imemaliza kazi moja na inatarajia kuanza nyingine mpya kabisa. Ndiyo, wamemaliza vyema safari ya kupambana na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika! Simba imeingia hatua hiyo baada ya kucheza mechi nne za kimataifa na sasa inatembea kifua mbele ikitamba kila kona, si wachezaji wala viongozi.Siyo mashabiki wala wanachama lakini pia hata watanzania wenye mapenzi ya kweli na soka la nyumbani wamekuwa na msisimko wa kutosha kwa Simba kufika hatua hii. Si kwamba wekundu hao wamebahatisha kupata mafanikio hayo kidogo ambayo ni makubwa kwa sasa ukilinganisha na mara ya mwisho timu za Tanzania kufika hatua hiyo. Nitakwambia kwa nini? Ila kwa faida yako mara ya mwisho Tanzania kufikia hatua hii ilikuwa 2003 na Simba hii ndiyo ilipindua meza kibabe.Kwanza, ilimnyoosha bingwa mtetezi wa wakati huo, Zamalek ya Misri na kutinga hatua ya makundi na sasa imerudia tena makali yake hayo baada ya kupita miaka 15 bila Tanzania kuonekana katika hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu Afrika. Turejee kwa nini Simba haikubahatisha kufanya hivyo. Msingi wa timu hiyo, tangu inaanza kufanya mabadiliko ya uongozi, wimbo wao mkubwa ulikuwa ni kufika hatua kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.Bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’ambaye ni mwekezaji mwenye hisa asilimia 49 kwa klabu hiyo alipambana kwa kila namna pamoja na viongozi wengine wa timu hiyo kuhakikisha wanakuja wachezaji wakali na wanapata wanachokihitaji ili mambo tu yaende sawa. Haikuishia hapo, benchi la ufundi la timu hiyo lilipigwa msasa wa kutosha kama siyo kusafishwa vyema ili tu apatikane mtu sahihi atakayewaongoza kufika nchi ya ahadi ambayo sasa Simba ipo.Ilianza mtihani wake wa kwanza kwa timu ngumu ya eSwatini, Mbabane Swallows ingawa safari hii ilionekana kuyumba na Simba ikatumia mwanya huo bila ya kupoteza muda na kuifumua mabao 4-1 katika mechi ya kwanza ailiyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao yalifungwa na John Bocco, Clatous Chama na Meddie Kagere. Katika mechi ya pili iliyopigwa kwenye ardhi ya Mfalme Mswati, Simba iliamua kufanya maajabu hukohuko ugenini kwa kuwabubujua wapinzani wao kwa mabao 4-0.Katika mechi hii, Chama aliweka mabao mawili murua na kisha Emmanuel Okwi na Kagere wakakandamiza moja kila mmoja. Hatua iliyofuata, wakakutana na Nkana FC kutoka Zambia. Hapa haikuwa shughuli nyepesi na hapa ndipo Simba ilipoonesha kwa kiasi gani ilikuwa na kiu ya mafanikio ya kufika katika hatua ya makundi. Ilianza kwa kipigo kule Kitwe, Zambia kwa kuchapwa mabao 2-1.Licha ya Simba kukukuruka na kupambana kutengeneza nafasi nyingi lakini Nkana walisimama imara katika ardhi yao ya nyumbani na mwisho Simba ikaondoka Zambia kichwa chini. Hazikuwa hisia nzuri kwa watanzania hasa mashabiki wa Simba, waliamini hawana chao na shughuli ndiyo imeishia hapo. Historia ya Nkana dhidi ya Simba haikuwa nzuri hata kidogo. Hapo awali Simba haikuwahi kukutana na Nkana na ikatoka salama na mara zote wamekuwa wakizidiwa bao moja tu katika matokeo ya jumla mwisho kutupwa nje ya mashindano.Lakini safari hii, historia haikufanya kazi na hisia mbaya pia hazikuwa na nguvu zaidi ya matumaini na mapambano ya kweli yaliyojaa mioyoni mwa wachezaji wa timu hiyo, ndicho kilichoirejesha Simba kwenye ramani ya soka la Afrika. Mechi ya pili iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa z utata huo. Maelfu ya mashabiki walijitokeza kuipa nguvu timu yao ingawa mapema walianza kukatishwa tamaa na kuamini hawana chao baada ya dakika ya 17 ya mchezo, Walter Bwalya kuipatia Nkana bao la kuongoza na kuifanya mechi kuwa ngumu zaidi. Katika mechi hiyo, Simba ilihitaji ushindi wa bao 1-0 pekee ili isonge mbele kwa kuwa walikuwa wakilindwa na lile bao moja la ugenini walipofungwa 2-1.Lakini kwa bao la Bwalya, Sasa Simba ilihitaji ushindi wa mabao kuanzia matatu huku wakiwa hawajaruhusu jingine ili ikate tiketi ya kuingia makundi. Simba ilijitutumua na kuamini bado wana nafasi. Jonas Mkude aliyelelewa na kukulia katika timu ya vijana ya Simba kwa muda mrefu akiwa hajaifungia bao timu hiyo, siku hiyo ndiyo ilikuwa wakati wake wa kulipa fadhila kwa kupiga shuti nje ya 18 na kumzidi mlinda mlango wa Nkana na mpira kujaa wavuni dakika ya 29. Shangwe zenye matumaini finyu zililipuka na Simba wakacharuka wakitandaza kabumbu huku wakilisakama lango la wapinzani hao na zikiwa zimesalia sekunde chache kwenda mapumziko, Kagere akaiandikia Simba bao la pili.Kazi ikawa imelainika lakini ikahitajika shughuli ya ziada ili kuwa na uhakika juu ya hilo. Baada ya vuta nikuvute, wengi wakiamini mshindi ataamuliwa kwa matuta kama ilivyotokea mwaka 2003 wakati Simba inaingia hatua ya makundi kwa mara ya mwisho, Clatous Chama akaiandikia Simba bao la tatu dakika ya 88. Lilikuwa bao safi, litakalobaki kwenye kumbukumbu ya watanzania wengi kwa miaka mingi kuliko unavyofikiri. Alifunga kwa kisigino chepesi akiwahadaa kipa na beki wa Nkana baada ya kupokea pasi ndani ya 18 kutoka kwa Hassan Dilunga.Huo ukawa mwisho wa Nkana katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ukawa mwanzo mpya kwa Simba katika michuano hiyo. Jana ndiyo droo ilitarajiwa kupangwa mjini Cairo, Misri. Timu zilizofuzu hatua hiyo ni Al Ahly ya Misri, TP Mazembe (Congo DR), Wydad AC (Morocco), Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates (Afrika Kusini).AS Vita Club (Congo DR), CS Constantine na JS Saoura (Algeria), Ismaily SC (Misri), Lobi Stars (Nigeria), FC Platinum (Zimbabwe), Horoya SC (Guinea), CA African (Tunisia), Asec Mimosas (Ivory Coast) hizi ndiyo timu zinazotarajia kuumana na Simba katika makundi. Hakuna timu ya kubeza hapo. Hakuna timu nyepesi, wote hawa ni wazoefu na wamejipanga kila kona kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ‘ndoo’.Hiki ni kipimo halisi cha Simba yenye malengo na inayojitutumua kuandika kwa wino mwekundu jina lake katika ramani ya soka la Afrika. Inawezekana popote na muda wowote kama kweli Simba itayavaa mashindano hayo kikamilifu na kuendeleza kile ilichoanza kukifanya tangu katika mechi za awali. Simba hii ina kikosi kipana na chenye kutafuta matokeo kwa machozi, jasho na damu. Inaweza kupambana kwa ajili ya nembo yao kubwa lakini pia ikiiweka begani Tanzania na kudhihirisha Afrika Mashariki sio ya kinyonge! Kila la heri Simba katika mapambano yenu, ni wakati wenu kuudhihirishia ulimwengu wa soka juu ya nini Simba imedhamiria kufanya, inataka kuonesha nini na imepanga kulitawala soka la Afrika. | michezo |
Kwa matokeo hayo, Yanga imerejea katika nafasi ya pili na kuendelea kumfukuza mnyama kimya kimya kwa kufikisha pointi 43 ikizidiwa pointi tatu na Simba huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara 20. Jadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilikuwa suluhu na kuwafanya mashabiki wa Yanga kuwa na hofu wakihofia timu yao huenda ikalazimishwa sare.Kipindi cha pili kilikuwa na neema kwa Yanga, ambapo mnamo dakika ya 53, Ibrahim Ajibu alifunga bao la kwanza kwa njia ya penalti, baada ya beki mmoja wa Kagera Sugar kuunawa mpira katika eneo la hatari. Yanga iliendeleza makali katika kipindi cha pili na katika dakika ya 77 ya mchezo huo, 77, Emmanue Martin alifunga bao la pili baada ya kupata pasi ya Chirwa na kufanya timu hiyo kuwa mbele kwa mabao 2-0.Kazi nzuri ya Mhilu ilizidi kuzaa matunda tena, ambapo katika dakika ya 88, Godfrey Taita alijifunga, kufuatia kazi nzuri ya Mhilu aliyepiga shuti kali lilisababisha mchezaji huyo wa Kagera kujifunga. Yanga sasa ina pointi 43 ikiwa nafasi ya pili, huku Simba ina alama 46, na Azam imeshuka hadi nafasi ya tatu ikiwa na alama zake 41. Yanga imeibuka na ushindi huo baada ya Jumanne kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa. | michezo |
Timu za taifa za Para Taekwondo na Taekwondo zilizoondoka nchini mwishoni mwa wiki na kwenda Morocco kwa ajili ya mashindano hayo ya Afrika ya Taekwondo.Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Machi 28-30 wakati yale ya Para Taekwondo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu, itaanza siku moja baadaye.Rwanda ambao walikuwa wenyeji wa mashindano ya Para Taekwondo mwaka jana, walimaliza kileleni katika msimamo wakiwa na medali sita, zikiwemo mbili za dhahabu tatu za fedha na moja ya shaba.“Baada ya miezi mitatu ya mazoezi ya nguvu, sasa tuko tayari kwa ajili ya kusaka medali nchini Morocco," alisema Bagire siku moja kabla timu haijaondoka kwenda Morocco.Aliongeza kusema: “Wachezaji wangu wana uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa ambao nina uhakika utatuongoza sisi katika ushindi. Tutacheza dhidi ya baadhi ya wachezaji bora Afrika lakini sisi ni mabingwa watetezi wa Para Taekwondo na tunatakiwa kuonesha kuwa ushindi wetu wa mwaka jana hatukubahatisha.Ikishika nafasi ya nane katika ubora wa mchezo huo Afrika, kwa mujibu wa Shirikisho la Dunia la Taekwondo (WTF), Rwanda itakuwa ikisaka mafanikio ya kutetea taji lao la Afrika walioutwaa mwaka jana mjini hapa.Katika mashindano hayo ya Afrika, Rwanda itakuwa na timu iliyokamilika ya wachezaji 14, nane katika taekwondo na sita katika Para Taekwondo. Wapambanaji wa Rwanda watakutana na ushindani mkali kutoka kwa wenyeji Morocco, Misri, Algeria, Tunisia na Gabon.Timu kamili: Para Taekwondo: Jean de la Croix Nikwigize, Consolee Rukundo, Jean Claude Niringiyimana, Jean Marie Vianney Bizumuremyi, Parfait Hakizimana na Jean Pierre Manirakiza Taekwondo: Benoit Kayitare (captain), Savio Nizeyimana, Vincent Munyakazi, Moussa Twizeymana, Delphine Uwababyeyi, Raissa Umurerwa, Aline Ndacyayisenga na Benise Uwase. | michezo |
.Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa licha ya idara ya mahakama nchini kuendelea kufanya kazi nzuri bado inakabiliwa na upungufu wa watumishi.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ikiwa ni mwanzo wa kuanza kwa shughuli za mahakama, Jaji Mkuu amesema kuwa mahitaji ya idara hiyo ni watumishi 10, 351 lakini waliopo sasa ni 5, 947 tu.Jaji Mkuu ameongeza kuwa idadi ya watumishi wa mahakama imekua ikiendelea kupungua mwaka hadi hadi mwaka, ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Disemba mwaka 2019 watumishi 258 waliondoka kazini kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kustaafu, kuhama na vifo.Kufuatia hali hiyo, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ameiomba Serikali kuajiri watumishi zaidi wa idara ya mahakama ili waweze kufanya kazi katika mahakama mbalimbali zinazoanzishwa hapa nchini na hivyo kutoa haki kwa wakati kwa wananchi.Kaulimbiu ya siku ya mahakama kwa mwaka huu ni Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau kuweka Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji. | kitaifa |
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mohamed Said Dimwa wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliokuwa wakijadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016.Alisema ni kweli soko la mwani limekuwa likiyumba ambapo wafanyabiashara wa ndani wananunua kwa bei yao wanayotaka huku wakulima wakilalamika kuwa ni ndogo na imepitwa na wakati.Alifahamisha kwamba suala la bei ya mwani linafuatiliwa kwa karibu sana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kwa mujibu wa agizo la Serikali lilivyowataka kufanya kazi hiyo.“Wizara mbili hizi zinafanya kazi kama zilivyoagizwa na Serikali ya kutafuta muafaka wa bei ya mwani katika soko la nje kufuatilia malalamiko ya wakulima kwamba bei ni ndogo sana,” alisema.Aidha alisema Wizara ipo katika mchakato wa kuona zao la mwani linaboreshwa zaidi kwa kuweza kutumika kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali katika matumizi ya kawaida ya ndani.Zanzibar inashika nafasi ya tatu kwa uzalishaji wa mwani kwa wingi katika Bara la Afrika ambapo kilimo hicho hulimwa kwa wingi zaidi na wanawake katika maeneo ya mwambao wa pwani.Dimwa alisema Wizara imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba inazalisha wataalamu wengi zaidi katika masuala ya kupata madaktari wa mifugo waliobobea katika taaluma hiyo.Alisema juhudi kubwa za wizara zimechukuliwa katika kuwaendeleza vijana kupata mafanikio katika fani ya udaktari wa mifugo lakini kwa bahati mbaya wanafunzi wanane waliopelekwa katika baadhi ya Vyuo Vikuu vya Tanzania Bara walifeli mitihani yao na kurudishwa nyumbani.“Tunasikitika sana Serikali imechukua juhudi kubwa katika kusomesha vijana katika fani ya udaktari wa mifugo lakini kwa bahati mbaya walifeli vibaya mitihani yao,” alisema. | uchumi |
MWANAFUNZI bora matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, Hope Mwaibanje (18) wa Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Arusha, amesema anataka kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu.Kwenye matokeo hayo, Mwaibanje ameibuka kuwa mwanafunzi bora akiwa ana alama za 1.7 ikimaanisha kuwa amepata alama ya A kwenye masomo yake yote saba. Mwenyewe ameweka wazi kuwa anapenda masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia, kwa kuwa ndiyo yatakayomwezesha kuwa daktari.Anasema anajiona mwenye wajibu mkubwa wa kusaidia jamii za Tanzania hasa za maeneo ya vijijini, ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto kwenye upatiwaji wa huduma bora za afya. Akizungumzia siri ya kufanya vema kwenye matokeo hayo, alibainisha jana kuwa anapenda kusoma na alikuwa akilazimika- 5hata kuamka usiku kujisomea, huku akiwasumbua walimu na rafiki zake kumfundisha, kama kuna kitu hakukielewa wakati kikifundishwa.Aliongeza “Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kushinda na kuwa mwanafunzi bora, kwa kweli mimi nilikuwa najisomea tu na sikujua kuwa ningeibuka kuwa bora, ila kwa uwezo wa Mungu amenifanya kuwa mwanafunzi bora wa mwaka na mimi lazima nikaitumikie jamii”. Alisema msaada wa walimu na mazingira bora ya kujisomea shuleni ni moja ya sababu za kufanya vema kwenye matokeo hayo.Aliwataka wanafunzi wengine nchini, kuongeza bidii katika masomo. Akihojiwa kwa njia ya simu jana, Mkuu wa shule hiyo ya Ilboru, Dennis Otieno, alibainisha kuwa nidhamu ni moja kati ya siri za ushindi wa mwanafunzi wake huyo, ambapo alisema ana nidhamu ya hali ya juu na anapenda kusoma na kushirikiana na wenzake kwenye masomo.Alisema alikuwa akifanya vema tangu akiwa kidato cha kwanza, alikuwa akifanya kazi zake za darasani kwa wakati na alipenda kujisomea mara kwa mara. Akizungumzia hali ya matokeo na ufaulu kwenye shule hiyo kwa mwaka jana, alibainisha kuwa wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza ni 99, daraja la pili 29, la tatu 10 na daraja la nne mmoja na hakuna sifuri. Alieleza sababu za ufaulu huo mzuri kuwa ni ukarabati wa shule uliofanywa na serikali, ambapo madarasa, vyoo na mabweni, yamekarabatiwa kwa kiwango cha juu.Alisema wanafunzi wamevutiwa na mazingira hayo, kiasi cha kujikuta wakipenda kusoma na kuipenda shule. Alisema pia walimu waliweka utaratibu wa kuwa na muda wa kuwasaidia wanafunzi masomo yao. Mama mzazi wa kijana huyo, Ikupa Kapendile alisema amefurahishwa na matokeo hayo mazuri ya mwanawe, kwa kuwa ameiletea heshima kubwa familia yake.Alisema kuwa familia itaendelea kumtunza zaidi. Alibainisha kuwa mwanawe amefanya vema kutokana na kujituma, kuwa na nidhamu na kupenda masomo. Alisema Cosmas alihitimu masomo yake ya elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Lyoto iliyopo Mbeya. Ni mtoto wa tano kuzaliwa kwenye familia ya watoto sita ya Mzee Cosmas Mwaituka na mama, Ikupa Kapendile. | kitaifa |
BAADA ya Mbwana Samatta (pichani) kuangushiwa lawama na mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kuwa hajitumi anapokuwa na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, hatimaye mwenyewe amefunguka kuhusiana na tuhuma hizo.Awali, kulikuwa na maneno ya chini chini kuwa Samatta ambaye ni nahodha wa Stars kuwa hajitumi anapokuwa na jezi za Tanzania tofauti akiwa na kikosi cha klabu yake ya Genk ya Ubelgiji kabla ya hivi karibuni mashabiki hao kueleza kinagaubaga mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Stars dhidi ya Libya.Katika mechi hiyo ya kuwania kushiriki Afcon 2021, Stars iliyokuwa ugenini ilipoteza kwa mabao 2-1. Samatta ndiye aliyefunga bao hilo moja kwa mkwaju wa penalti lakini haikutosha kumlinda dhidi ya lawama hizo.Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Samatta alieleza kuwa amepata jumbe mbalimbali za kuhusiana na yeye kutojituma katika mechi za timu ya taifa, lakini akasisitiza kufurahia kuelezwa ukweli na atayafanyia kazi maoni hayo.“Nimepata ujumbe na maoni kutoka kwa watu kadhaa kuwa hawajaelewa kiwango nilichoonesha katika mechi za timu ya taifa, ukweli nimefurahi kuona watu wanasema ukweli. “Sichukulii binafsi bali nachukulia kama chachu itakayonifanya nijitume zaidi ili niweze kuwa bora zaidi, haina kufeli,” aliandika Samatta. | michezo |
Akihutubia Jumuiya ya Sekta Binafsi nchini Kenya juzi, mkuu huyo wa IMF alisema hadhani kwamba EAC iko tayari kwa utekelezaji wa mpango huo na inahitaji kwanza kushughulikia masuala muhimu ndani ya nchi zao kabla ya kuunganisha fedha zao, kwa mujibu wa habari zilizorushwa na Radio Capital FM ya Kenya.Lagarde aliwasili Kenya Jumapili kwa ziara ya siku tatu kujadili uhusiano kati ya IMF na Kenya kwa kukutana na wadau mbalimbali.Nchi wanachama wa EAC imeshaanza kutekeleza itafaki za Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja na bado hawajaanza kuonja matunda ya hatua hiyo. Hatua ya tatu ni ya Umoja wa Fedha na ya nne na ya mwisho ni Shirikisho la Kisiasa.Miongoni mwa changamoto ambazo mkuu huyo wa IMF alizitaja ni pamoja na kuongezeka kwa vikwazo visivyo vya kodi, tofauti ya uchumi miongoni mwa nchi wanachama na tofauti za kodi ndani ya nchi hizo.‘Nikiwa mjumbe wa Umoja wa Fedha wa Ulaya, ninawajibika kuwaeleza kuwa huu ni mradi wenye kuleta hamasa sana, lakini ni mradi ambao Aristotle (mwanafalsafa wa Ugiriki) alipata kusema unatakiwa kutekelezwa kwa taratibu. Msiharakishe,’’ Lagarde alinukuliwa na Capital Radio akisema.Alisema Kenya ikiwa mstari wa mbele kupigia debe mtangamano wa kiuchumi, inatakiwa pia kuongoza wanachama wenzake wa Jumuiya hiyo kuhakikisha makosa yaliyofanywa na jumuiya kama hizo katika umoja kama huo, hayarudiwi. Rais Uhuru Kenyatta ndiye Mwenyekiti wa sasa wa EAC.‘’Hakikisheni mnajifunza kutokana na makosa yetu na Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki unaweza pia kuwa funzo kwa ule wa Ulaya juu ya kuutekeleza kwa njia sahihi,’’ Lagarde alisisitiza.Itifaki ya Umoja wa Forodha wa EAC ilisainiwa na wakuu wa nchi wanachama mwezi uliopita mjini Kampala, Uganda, ukiwa umeanzisha rasmi mchakato wa kuwa na sarafu moja katika kipindi cha miaka 10 ijayo.“Kuna uzoefu mwingi, uwe wa Umoja wa Fedha wa Ulaya, Umoja wa Visiwa vya Caribbean, Umoja wa Afrika Magharibi na umoja mwingine mahali kwingine duniani. Yapo makosa, mapengo, upungufu ambavyo vinaweza kutumika kujifunza,” alisema.Sarafu moja inalenga kuboresha biashara katika eneo hili la Afrika na pia kuimarisha ushirikiano uliopo.“Utangamano umefungua masoko mapya, umesaidia kuanzishwa kwa wafanyabiashara wa kati, na kuwezesha mahitaji ya ndani kuwa chachu ya maendeleo. Mchakato huo unapaswa sasa kuimarishwa,” alielezea.Wakati huo huo, aliitaka Kenya kuja na sera nzuri ambazo zitawezesha utekelezaji mzuri wa mabadiliko ambayo alisema ndiyo changamoto kubwa katika uchumi wa nchi hiyo.Mfanyabiashara Chris Kirubi baadaye alielezea msimamo wa Lagarde juu ya Umoja wa Fedha kama ushauri ambao umekuja kwa wakati mwafaka.“Huu ni ushauri uliokuja kwa wakati mwafaka kabisa, kutoka kwa Mkuu wa IMF. Umoja wa Fedha unapaswa kuwa kitu cha mwisho kabisa Kenya kuingia. Tusiruhusu kitu ambacho kitatugawa,” Kirubi alisema kwa njia ya simu kutoka Dubai. | uchumi |
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara ,Yanga tayari wamewasili mkoani Shinyanga kuwafuata Stand United kwa ajili ya mchezo ujao utakaochezwa kesho. Jumla ya kikosi cha wachezaji 18 kikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Samwel Lukumay kilitua kwa ndege Mwanza jana, kisha kwenda Shinyanga kwa basi.Akizungumzia mchezo huo wa kesho, beki wa Yanga Juma Abdul alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kupata pointi tatu zitakazozidi kuwaimarisha kileleni. “Tumejipanga vizuri kushinda, tunawaomba mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono ili kuamsha morali na kujitahidi kupambana kupata matokeo mazuri,” alisema.Alisema mashabiki walioko karibu na mkoa wa Shinyanga hawana budi kujitokeza kuwaunga mkono akiamini ni njia pekee itakayowasaidia kupata matokeo. Yanga tangu imeanza ligi imekuwa kwenye kiwango bora ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja baada ya kucheza michezo 19, kushinda 17 na sare mbili ikiwa na pointi 53.Timu hizo zitakutana kesho kwenye Uwanja wa CCM, Kambarage Shinyanga zikiwa na kumbukumbu ya kukutana raundi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kushinda mabao 4-3.Stand United haiko katika nafasi nzuri inashika nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 22, kushinda sita, sare nne na kupoteza 12 ikiwa na pointi 22. Timu hiyo imetoka kupoteza mchezo uliopita baada ya kufungwa na Biashara United ya Mwanza bao 1-0.Bila shaka mchezo wa kesho Stand inahitaji matokeo mazuri ili kujiepusha kuingia kwenye hatari ya kushuka daraja. | kitaifa |
BARAZA la Utendaji la Chama cha Mahakimu na Majaji Afrika Mashariki (EAMJA), litafanya kikao chake kuanzia leo hadi kesho kutwa, mwaka huu jijini Arusha.Katika kikao hicho, Mahakimu na Majaji watajadili Sera ya Jinsia ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuzalisha sheria ambazo zinawawezesha wanawake kupata haki mahakamani bila kukwazwa na mapingamizi yanayotokana na ufundi haba wa kisheria unaowakabili.Kikao cha Baraza hilo kitakuwa chini ya uenyekiti wa, Rutazana Angeline, ambaye pia ndiye Rais wa EAMJA.Wajumbe kutoka Tanzania katika Kikao hicho ni Wilberforce Luhwago, Jaji Robert Makaramba, Jaji Sophia Wambura na Angelo Rumisha.Vyama vinavyounda EAMJA ni Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Chama cha Majaji na Mahakimu Kenya (KMJA), Chama cha Majaji na Mahakimu Uganda (UJOA), Chama cha Majaji na Mahakimu Zanzibar, na Mahakama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.Dhima ya EAMJA ni kukuza, kuimarisha na kulinda utawala wa sheria, na upatikanaji wa haki kwa watu wote, kwa njia ya kuwianisha mifumo ya sheria na kujenga uwezo wa maofisa wa Mahakama katika Afrika Mashariki.Rais wa Chama cha Mahakimu na Majaji nchini, Wilberforce Luhwago alisema jana kuwa kwa mujibu wa Katiba ya hicho, Baraza Tendaji hukutana mara 4 kwa mwaka, na mikutatano ya baraza hilo na mikutano mikuu hufanyika kwa mzunguko ambapo kila nchi mwanachama wa huwa mwenyeji wa vikao vya Baraza Tendaji na Mkutano Mkuu. Rais wa chama hicho juzi alisema:“Baraza Tendaji litapokea na kufanya tathmini ya maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu huko Zanzibar.”Aliongeza: “Baraza pia litafanya shughuli zake za kawaida za baraza kwa mujibu wa Katiba, kama vile kupokea taarifa za maendeleo ya vyama vinavyounda chama, maendeleo au shughuli zilizofanywa na vyama hivyo tangu baraza hilo lilipokutana mara ya mwisho Machi, mwaka huu, Kigali, Rwanda. | kitaifa |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mshitakiwa wa pili, Alloycious Mandago anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni mbili pamoja na wenzake, kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).Mbali na Mandago, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Mohamed Yusufali, aliyetajwa na Rais John Magufuli kuiibia serikali Sh milioni saba kila dakika na Isaac Kasanga ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 39. Wakili wa Takukuru, Leonard Swai alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa. Alidai kuwa wapo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuandaa maelezo ya mashahidi, lakini wanaomba kumhoji mshitakiwa Mandago akiwa gerezani.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliridhia mshitakiwa huyo kuhojiwa akiwa gerezani na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Machi 2, 2010 na Aprili 26,2016 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam, walikula njama kwa kughushi, kukwepa kulipa kodi na kutakatisha fedha.Katika mashitaka ya pili, linalomkabili mshtakiwa wa tatu, Kasaga, anadaiwa katika ofisi za Wakala wa Usajili (Brela) zilizoko Manispaa ya Ilala, aliwasilisha nyaraka ya uongo yenye Fomu Namba 128 ya Mei 2, 2016 akionyesha kuwa Machi 4, 2012 wakurugenzi wa kampuni ya Superior Financing Solution Limited ni Mohamed Mustafa Yusufali, Izack Kassanga na Maria Barnett.Katika mashitaka mengine inadaiwa kati ya Marchi 4, 2011 na Aprili 13, 2016, akiwa mmiliki na Mkurugenzi wa kampuni ya Superior Financing Solution Limited, walijihusisha na muamala wa kiasi cha Sh bilioni 2.9, wakijua fedha hizo zinatokana na zao la pesa haramu. | kitaifa |
['Ulikuwa uhamisho ambao ulimfanya Neymar kuondoka katika kivuli cha nyota wa Barcelona Lionel Messi. ', 'Hatahivyo raia huyo wa Brazil amegonga vichwa vya habari kwa sababu tofauti tangu alipojinasua kutoka katika mabingwa hao wa Uhispania na kuelekea PSG. ', 'Amefunga magoli 34 kati ya mechi 37 ili kuwasaidia kushinda taji la ligi ya daraja la kwanza. ', 'Lakini pia amepigwa marufuku kutoshiriki mechi tatu kwa kumkaripia shabiki mmoja baada ya PSG kubanduliwa katika kombe la ligi ya Ufaransa, alidaiwa kushiriki katika kizazaa kilichotokea katika chumba cha maandalizi na wachezaji wenzake na atakaosa kushiriki katika mechi tatu za Yuropa kwa kuwatusi maafisa. ', 'Na tayari amepokonywa unahodha wa timu ya taifa ya Brazil kabla kuanza kwa kombe la Copa America nchini Brazil. ', 'Huku ikiwa hajamaliza hata miaka miwili tangu aliponunuliwa kwa dau la juu zaidi duniani la £200m , huenda huduma zake katika uwanja wa Parc des Princes zinakaribia kikomo. ', "''Sitaki kuchezea tena PSG nataka kurudi nyumbani kwangu, ambapo nisingeondoka'', alidaiwa kumwambia rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi katika ujumbe , kulingana na gazeti la Uhispania la Mundo Deportivo. ", 'Sasa ataelekea wapi? Barcelona? ama pengine aelekea kaika ligi ya Uingereza? ', 'Akizungumza na BBC Radio 5 waandishi Tim Vickery , Miguel Delaney na Ben Haines wanazungumzia kuhusu hatma ya mchezaji huyo.', 'Vickery: Wachezaji wakuu wa kikosi cha Barcelona wangefurahia sana kumkaribisha Neymar. ', 'Yeye ana uhusiano mzuri na Messi, Suarez na Gerald Pique-Wachezaji watatu ambao ndio nguzo ya Barcelona na nadhani hilo linampatia fursa. ', 'Sidhani kama kuna mchezaji ambaye alichukiwa zaidi ya Neymar na naweza kuelewa hilo. ', 'Ni mchezaji ambaye anaponekana kana kwamba ameharibika lakini nadhani pia kuna upande mwengine wake mzuri. ', 'Cha kushangaza ni kwamba wachezaji wenzake hususan katika klabu ya Barcelona na wale wa timu ya Brazil wamekuwa na uhusiano mzuri naye-wakimpenda sana.', 'Delaney: Nilikuwa nikizungumza na jamaa mmoja ambaye ametumia wakati wake mwingi na Neymar siku moja. ', 'Walisema licha ya anavyochukuliwa , unapokutana naye moja kwa moja ana upande wake mzuri. ', 'Ni mtu ambaye ni rahisi kumpenda na anaweza kukusaidia. lakini swala hapa ni vipi anachukuliwa kama mtoto na watu wake , akiwemo babake. ', 'Hilo linaweza kutoa ubaya wake kama tulivyoona akiichezea PSG.', 'Vickery: Kuna uamuzi unaochukuliwa na watu wake wa karibu ambapo huwezi kujua iwapo ni yeye anayefanya uamuzi huo au la.', 'Lakini unashangaa iwapo uhusiano wake na babake anafaa kuupa kisogo ili kujisimamia. Ningependa kumuona akilivua joho la kuwa Neymar mdogo na badala yake kuwa mtu mzima.', 'Delaney: Sasa amegundua kwamba uhamisho wa kuelekea PSG ulikua makosa makubwa', 'Baada ya kuzungumza na watu wachache ambao wameshirikiana na Neymar ama watu wake wa karibu, kuna wasiwasi kuhusu kule ambako mchezo wake unaelekea. ', 'Kuna madai mengi kwamba pia hafanyi mazoezi. ', 'Kwamba amejishirikisha sana katika klabu ya PSG hadi kiwango cha mchezo wake kimeshuka. ', 'Baadhi ya wale walio na wasiwasi zaidi wanasema kuwa kipindi chake cha mchezo kipo hatarini kuangamia. Nadhani hiyo ni mojawapo ya sababu ambazo anahitaji kuondoka katika mazingira hayo.', 'Vickery: Niko tayari kukosolewa lakini nadhani kulikuwa na lengo fulani katika uhamisho wa mchezaji huyo kuelekea PSG. Pengine lengo la kutaka kushinda taji la mchezaji bora duniani. ', 'Wachezaji wengi wa Brazil walishinda taji hilo la Ballon d Or miaka ya nyuma . Je angelishinda vipi taji hilo wakati ambapo amekuwa akicheza chini ya kivuli cha Lionel Messi .', 'Nadhani alikuwa na lengo la kuelekea PSG ili kuwa kiongozi wa timu hiyo. Bahati mbaya ni kama kana kwamba kandarasi yake katika klabu hiyo haijaanza. ', 'Alisajiliwa kwa kitu kimoja pekee. Kuisaidia timu hiyo kusonga mbele katika awamu ya kimakundi katika kombe la ligi ya mabingwa. ', 'Kufikia sasa amecheza mara moja kutokana na majeraha swala ambalo sio kupenda kwake.', 'Vickery: Ana nafasi chache kuhusu ligi atakayojiunga nayo. Kwa sababu ni wapi anaweza kuelekea? Kitu ambacho hatujakitaja ni ligi ya Uingereza. ', 'Ligi hiyo ni mojawapo ya ligi yenye ushindani mkali duniani na klabu zilizo na uwezo wa kumnunua-lakini je watahatarisha fedha zao? ', 'Je umewahi kufikiria Neymar akijiunga na ligi ya Uingereza? Unaweza kufikiria ghadhabu atakazopata atakapojiangusha kama ilivyo kawaida yake? ', 'Sasa Real Madrid wamempata Eden Hazard je watamuhijitaji Neymar pia?', 'Delaney: Sidhani. wamemnunua mchezaji Luca Jovic hivyobasi wametatua tatizo lao la safu ya mshambulizi. ', 'Nadhani inaonekana kwamba Neymar alikuwa mchezaji wa pili ama wa tatu kwa ubora duniani katika kipindi cha miaka michache iliopita na Madrid hawana haja naye tena. ', 'Nakumbuka kusikia mwaka mmoja uliopita vile rais wa Real Florentino Perez alivyokuwa akisaka saini ya mchezaji huyo na hilo limekwisha hali ya kwamba unaweza kumsikia Neymar pekee akilizungumzia badala ya mtu yeyote kutoka Madrid. ', 'Meli imeondoka na sasa itategemea iwapo atarudi Barcelona kwa sasa.'] | michezo |
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku makamanda wa polisi wa mikoa nchini, kuyazuia mabasi yanayotoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa, kusafiri muda wa usiku kwa kisingizio cha kuhofia kuvamiwa na majambazi.Amesema hawana mamlaka ya kupanga ratiba ya mabasi kusafiri wasambaratishwe na wakamatwe kama kuku.Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo imara na kamwe haliwezi kucheka na majambazi wala kuwaonea huruma na kuanza kuwapangia wananchi muda gani mabasi yasafiri na yasisafiri.Ametoa msimamo huo katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Namibu Kata ya Neruma Jimbo la Mwibara Wilayani Bunda mkoani Mara jana.Lugola aliagiza kuwa mabasi yanayosafiri kutoka Kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam, yasizuiwe Morogoro na yanayotoka Dar es Salaam kwenda Kanda ya Ziwa yasizuiwe Shinyanga kwa sababu zinazodaiwa za kiusalama.“Mimi ndiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hatuwezi kupangiwa ratiba ya kusafiri na majambazi, Serikali ya Rais John Magufuli ipo imara, na Polisi ipo imara, hivyo agizo hili ambalo pia niliwahi kulitoa lizingatiwe ipasavyo, niliagiza majambazi wote wasambaratishwe, asakwe mpaka jambazi wa mwisho, akamatwe kama kuku,” alisema Lugola.Aliongeza, “Taarifa ya uhalifu zinaonesha Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu na hasa uhalifu wa majambazi, na niliwahi kuagiza kipindi hiki si cha kuwa na huruma na majambazi, ni kipindi cha kuwashughulikia ili wananchi waishi kwa amani.”Lugola alifafanua kuwa, nchi haiwezi kupangiwa na majambazi muda wa kusafiri na kufanya biashara, hivyo maelekezo aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi liendelee kupambana na majambazi popote walipo nchini.“Nimeelekeza magari yanayosafiri yasizuiwe Morogoro yanapopita muda wa usiku saa nne usiku na kuendelea, yasizuiwe Shinyanga, ili majambazi wajue popote walipo wapo imara wamejipanga vizuri na mimi waziri wao nipo imara, kuhakikisha Jeshi la Polisi linawashughulikia majambazi mmoja baada ya mwingine ili kuwafanya wananchi katika nchi yao waendelee kushughulika na masuala ya kujijengea uchumi ili serikali ya Rais Magufuli, iweze kuwa na uchumi wa kati na majambazi wote wakamatwe kama kuku,” alisema Lugola. | kitaifa |
WAVUVI wa soko la Msasani jijini Dar es Salaam, wameanza kunufaika na matokeo ya vita dhidi ya uvuvi haramu kwa kupata idadi kubwa ya samaki, hasa aina ya jodari.Gazeti hili limefuatilia undani wa suala hilo kwa siku mbili kwa kutembelea sokoni hapo na kukuta idadi kubwa ya wavuvi wakitokea baharini kuvua. Likiwa sokoni hapo saa 12 asubuhi hadi saa 1.30, gazeti hili lilishuhudia idadi kubwa ya samaki ikipakiwa kwenye gari dogo la kubeba mizigo, aina ya kirikuu.Kwa siku ya kwanza lilishuhudia samaki wakiwa wamejaa kwenye kirikuu kimoja huku siku ya tatu ya ufuatiliaji wake, ambayo ni jana iliona kirikuu kimoja kimejaa na kingine kikiwa kimepelea kidogo.Katibu wa Chama cha Wavuvi sokoni hapo, Ujeje Mamboleo, katika mazungumzo yake, alibainisha kuwa kwa mwaka jana wote wavuvi wameshuhudia mabadiliko chanya kwenye sekta hiyo ya uvuvi. Alisema tofauti na miaka kadhaa iliyopita, kwa mwaka jana wavuvi walikuwa wakivua idadi kubwa ya samaki na wengine ni samaki ambao ni adimu kupatikana.Alisema kukosekana kwa samaki baharini, kulisababishwa na ongezeko la matukio ya uvuvi haramu, ambapo kulikuwa na wavuvi waliokuwa wakivua kwa kutumia mabomu. Alisema wavuvi hao walisababisha samaki kutoweka, kwa kuwa walikuwa wakiua samaki huku wakiharibu na vyakula vyao vya majini.Alisema baada ya msisitizo wa Rais John Magufuli wa kukabiliana na uvuvi wa aina hiyo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikiongoza operesheni kwa kushirikiana na wavuvi katika kukabiliana na uvuvi haramu huo. Alibainisha kuwa kwenye eneo la usawa wa soko hilo la Msasani ambako wavuvi huingia na kuanza kusaka samaki kumekuwa na operesheni ya kukabiliana na wavuvi haramu ambao wapo waliokamatwa na kuchukuliwa hatua. | kitaifa |
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema fedha za mfuko wa jimbo ni za wananchi wa jimbo la uchaguzi na sio za mwakilishi hivyo zinatakiwa kutumika ili kuleta maendeleo yao.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed ametoa msimamo huo wakati anajibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotaka wajumbe wa Viti Maalumu kupewa fedha za mfuko wa jimbo.Mwakilishi wa Viti maalumu, Mwantatu Mbaraka aliwasilisha hoja binafsi inayoitaka serikali kutoa fedha hizo kwa Wawakilishi wa Viti maalumu ambao hufanya kazi za kuwahudumia wananchi.Alisema katika muundo wa mfuko wa jimbo, Mwakilishi wa jimbo ni Mwenyekiti tu na si mtu wa mwisho wa maamuzi ya matumizi ya fedha.Amesema anachojua katika hoja binafsi ni uwepo wa mabadiliko katika muundo wa mfuko huo ikiwemo kuingizwa Wajumbe wa baraza hilo wa Viti Maalumu kama sehemu ya mfuko huo.''Tunaweza kuwaingiza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Viti maalumu kama sehemu ya mfuko wa jimbo na sio kuanzisha mwingine,'' amesema.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akijibu hoja alisema Zanzibar inayo bahati kuwa na mifuko miwili katika jimbo moja ikiwemo Mfuko wa Mbunge na Mwakilishi.Alisema kinachotakiwa ni viongozi hao wawili kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzipatia ufumbuzi kero zilizopo katika jimbo la uchaguzi.''Wenzetu Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwahi kulalamika kwanini Zanzibar wana mifuko miwili ya jimbo, wa Mwakilishi na Mbunge huku majimbo yao yakiwa na idadi ndogo ya watu na eneo,'' amesema.Aboud aliwakumbusha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kusema kwamba kazi za kisiasa ni za kujitolea zenye uzito mkubwa ikiwemo kuwa tayari kuwahudumia wananchi wakati wowote.''Hizo ndiyo kazi za kisiasa zinahitaji kujitolea na kuwa tayari kuwatumikia wananchi wakati wowote huku kiongozi ukitumia fedha binafsi, '' amesema. | kitaifa |
TIMU ya Mwadui FC imefunguka kuwa wameshajikamilisha vilivyo kukabiliana na wapinzani wao Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 33 baada ya kushuka uwanjani mara 14, Mwadui wapo nafasi ya 16 baada ya kushuka uwanjani mara 24 na kupata pointi 24. Mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu ambapo Simba wanataka kujiwekea mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wao kwani kama itashinda viporo vyake vyote tisa itakuwa sawa na Yanga ambayo inaongoza ligi huku Mwadui akihitaji kujiondoa katika sehemu mbaya ya kukumbwa na rungu la kushuka daraja mwishoni mwa msimu.Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Mwadui, Ramadhan Kilao alisema kuwa katika michezo ya Simba iliyopita ukiwemo dhidi ya Al Ahly ambao walikubali kipigo cha mabao 5-0 wamegundua madhaifu mengi ya timu hiyo hali iliyowafanya wapate mbinu nyingi za kuwamaliza. Alisema kuwa mbinu hizo wameshazifanyia kazi na wachezaji wamezielewa vizuri na wanawasubiri Simba kama wataingia wazimawazima basi watawamaliza mapema kirahisi.“Kikosi kipo tayari kwa ajili ya kucheza na Simba na tumeshayajua mapungufu yote ya wapinzani wetu hao, mbinu tutakazozitumia katika mchezo huo kwa sasa tumeona tuzifanye siri maana tukiziweka wazi wapinzani wetu wazifahamu ila tunahakika tunaweza kuibuka na ushindi. “Kikosi chetu kipo hapa Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo tunachokiangalia ni kupata pointi tatu ili kujitengenezea mazingira ya kujiweka sehemu salama ya msimamo wa ligi,” alisema Kilao. | michezo |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, alisema mwishoni mwa wiki kuwa ni vizuri wafanyabiashara mkoani humo na Watanzania kwa ujumla wake, wakachangamkia fursa hizo na kuufanya mkoa huo eneo la kuvutia wawekezaji.“Dodoma ya leo siyo ya miaka ishirini iliyopita, kwani ina mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii pia ni kitovu cha elimu, hivyo mna kila sababu ya kujipanga nakuangalia ni namna gani mnaweza kuifanya Dadoma kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji hapa nchini,” alisisitiza.Akizindua Baraza la Biashara la Mkoa huo (RBC), Gallawa alisema Baraza kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, linapaswa kutangaza vivutio vilivyopo Dodoma kwa lengo la kupata wawekezaji ili kupiga hatua kiuchumi.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi alisema amefurahishwa kwa mwitikio mkubwa wa wadau katika ufunguzi wa baraza hilo na kuwataka kutumia uwepo wa baraza katika kujadiliana juu ya fursa zilizopo na namna ya kuboresha mazingira ya biashara.Alisema umuhimu wa baraza hilo ni kutatua matatizo yanayowakabili wafanyabiashara hivyo ni jukumu la sekta za umma na binafsi kukaa pamoja na kujitathmini ili kufikia lengo la kukuza uchumi wa mkoa na maendeleo kwa ujumla. | uchumi |
NCHI wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinafi kiria kugeukia kilimo cha mianzi kama moja ya vyanzo vya fedha za kigeni kutokana na soko la bidhaa hiyo kuongezeka kwa kasi duniani.Kwa sasa, bidhaa zitokanazo na mianzi zinatajwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 7 (zaidi ya Sh trilioni 15.4 za Tanzania kwa mwaka) kote duniani. Ni kutokana na ukweli huo, baraza la kisekta linaloshughulikia kilimo na usalama wa chakula, limeshauri nchi za EAC kufanya utafiti kabla ya kugeukia moja kwa moja katika kilimo hicho kinachoziingizia fedha nyingi nchi za Asia-Pasifiki.Soko la mianzi linakua kwa kasi kutokana na kufaa kwa uzalishaji chakula, utengenezaji wa karatasi, mbadala wa mbao, kazi za sanaa za mikono, mkaa, ujenzi wa nyumba na vibanda vya kisasa, mabomba ya maji, mapambo, chakula, pombe, dawa, nyuzi za kutengenezea magodoro na kadhalika. Katika kikao kilichomalizika hivi karibuni cha mawaziri wa kilimo, pia imeziagiza nchi wanachama wa EAC kulinda vyanzo vya maji kwa kupanda mianzi katika kingo zake na pia matumizi mengine yenye manufaa kwa jamii.Maazimio hayo yamechangiwa pia na ripoti ya EAC iliyotokana na Mafunzo ya Teknolojia ya Mianzi ya mwaka 2018 yaliyofanyika kati ya Aprili na Juni huko Hangzhou, China. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Mianzi China (CBRC) na kudhaminiwa na Wizara ya Biashara ya China yalikusanya washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Argentina, Brazil, Colombia, Peru, Thailand, Timor Mashariki na Sekretarieti ya EAC. Taasisi ya Future Market Insights ya London, Uingereza itatabiri kuwa, takribani tani milioni 63 zitauzwa kote duniani ifikapo mwaka 2027 na kutoa mapato ya zaidi ya Dola bilioni 10 (sawa na Sh trilioni 22 za Tanzania). | kitaifa |
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Martin Ngoga amesema, Bunge hilo ni taasisi inayotafakari na kuchukua hatua muafaka kwa mujibu wa matakwa ya nchi sita wanachama wa jumuiya kutekeleza majukumu iliyojipangia.Ngoga ameyasema hayo alipozungumza na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Chukwani mjini Unguja.Ngoga amefika Zanzibar kuomba ruhusa kufanya vikao vya Bunge hilo Zanzibar Februari mwakani.Amesema zipo changamoto katika uwajibikaji wao.Amesema wabunge wa Eala wamekuwa wakishiriki vyema vikao vya maamuzi yenye kuleta ustawi na mwelekeo unaozingatia hatma ya wananchi wake. ''Nawapongeza kwa dhati wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa ushiriki wao vizuri katika Bunge hili ambao unatokana na maslahi ya nchi zao na wananchi,'' amesema.Balozi Iddi amesema Bunge hilo likiwa na sauti moja katika maamuzi yake kwa kiasi kikubwa litaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo kwa faida ya nchi wanachama.Alisema wananchi wa nchi za EAC matarajio yao makubwa baada ya kuundwa kwa jumuiya ni kuona mabadiliko ya kiuchumi sekta mbalimbali.''Hayo ndiyo matarajio makubwa ya wananchi wa nchi za Afrika Mashariki....mabadiliko ya uchumi na maendeleo yanafikiwa kwa faida ya wengi”, amesema.Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki kutoka Zanzibar, Makame Hasnuu amesema wakati umefika kwa Serikali za Afrika Mashariki kubadilisha mfumo wa Bunge litumie Kiswahili.'’Kiswahili kinatumiwa na wananchi wote wa nchi sita za EAC na njia pekee ya kupata umaarufu zaidi ni Bunge kutumia lugha hiyo, '' amesema. | kitaifa |
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi ameahidi kutoa raha katika tamasha la Simba linalotarajiwa kufanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba hufanya tamasha lao Agosti 8 ya kila mwaka ambapo hucheza hutambulisha jezi watakazotumia msimu mzima, wachezaji na mwisho hucheza mechi ya kirafiki na timu kutoka nje ya nchi.Katika ujumbe wake alioutuma jana akiwa kwenye kambi ya maandalizi ya msimu na timu yake Uturuki, Okwi alisema wanaendelea vizuri na mazoezi kuhakikisha wanatoa burudani ya kipekee siku hiyo.“Tuko poa, mambo yanakwenda vizuri kwa ajili ya tamasha la Simba, tunajipanga kupambana ili kutoa burudani kwa mashabiki wetu kabla ya kuanza kwa msimu,” amesema.Okwi amesema chini ya Kocha mpya Patrick Aussems anaamini watafanya vizuri kwani wachezaji wanaonekana kuwa na morali ya hali ya juu tayari kwa burudani. Kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili nchini kuanzia Agosti 5, mwaka huu tayari kwa tamasha hilo.Hivi karibuni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara alisema tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti na misimu mingine wakipania kulifanya liwe kubwa na lenye kuvutia kwa burudani mbalimbali. | michezo |
KAMPUNI ya Vodacom katika mwaka huu wa fedha ulioishia Machi 31, imefanikiwa kuongeza mapato yake ya huduma hadi kufikia Sh trilioni moja, sawa na ongezeko la asilimia 5.4.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi, ongezeko la mapato hayo limetokana na mapato kukua katika huduma za M-Pesa, huduma za data na SMS.Akizungumza na waandishi wa habari jana mkurugenzi huyo alisema kampuni hiyo imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika utoaji wa huduma za mawasiliano na fedha nchini.Alieleza kuwa Vodacom imefanikiwa kufikia wateja milioni 14.1 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 9.6, ikiongeza nafasi yake katika soko, hadi kufikia asilimia 32.4.“Kukua kwa huduma ya M-Pesa kumeendelea kuwa chachu ya uvumbuzi wenye kuboresha ujumuishi katika huduma za kifedha kupitia mifumo kama vile ‘Lipa kwa Mpesa’ ambayo inarahisisha malipo na kuwawezesha Watanzania kujipatia kipato,” alieleza.Alisema katika mwaka uliopita, upanuzi wa huduma za M-Pesa umewezesha wateja wapya 620,000 kufanya miamala kwa njia ya simu.Huu ukiwa ni ukuaji chanya wa wateja kwa asilimia 9.7 wanaotumia huduma hiyo.Alifafanua kuwa mapato yatokanayo na huduma ya MPesa yalikua kwa asilimia 14.5 na kufikia Sh bilioni 333.5.5.“Uhodari wetu kama mtoaji huduma za kifedha kwa njia ya simu ukifika asilimia 38.6 sawa na watumiaji milioni saba wa M-Pesa wanaofanya miamala inayofikia Sh trilioni 4.1 kwa mwezi.”Hendi alisema kupitia M-Pesa, Vodacom imekuwa ikiunga mkono jitihada za serikali katika kujenga uchumi imara wenye ushindani na hivyo kuweka rekodi kubwa ya wafanyabiashara 11,000 waliofanya miamala kufikia Sh trilioni 1.1 katika mwaka uliopita.Ukuaji pekee wa asilimia 186.0. Alisema kukua kwa mawasiliano kumewaleta watu pamoja na kuifanya kampuni hiyo ya Vodacom kuweka huduma za kidigitali katika maisha yao na kuwawezesha kujenga maisha bora ya baadaye.“Hii imedhihirishwa kupitia data ya mapato yaliyokua kufikia Sh bilioni 167 sawa na ukuaji wa asilimia 17.9 huku hatua za kudhibiti kushuka kwa mapato ya sauti zimeendelea kuonesha mafanikio,” alisema.Alifafanua kuwa, ingawa ukuaji wa mapato katika data yanatia hamasa, lakini ili kuweza kutoa mchango katika Pato la Taifa (GDP) na sekta ya afya kwa ujumla, ni muhimu kushughulikia gharama za data kutokana na kiwango cha sasa cha data kuwa cha gharama ya chini.Alisema Tanzania ndio nchi inayoongoza kuwa na data zenye gharama ya chini. Hali hiyo inaifanya kampuni hiyo ishindwe kuwekeza katika miundombinu na teknolojia katika kuendelea kuwaunganisha watanzania.“Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Takwimu (NBS), kufikia mwaka 2030, asilimia 50 ya idadi kamili ya watanzania watakuwa wenye umri chini ya miaka 18. Mgawanyo huo wa idadi ya vijana ni kiashirio kwa Vodacom kuendelea kuwekeza katika mtandao wake,” alieleza.Mkurugenzi huyo alisema mwaka huu, kampuni hiyo ilifanya uwekezaji mahususi wa kiasi cha Sh bilioni 171.4 kukuza uchumi wa nchi na kuwawezesha wateja kupata huduma ya 4G na 4G+ katika majiji makubwa, kuimarisha na kuboresha mtandao ili kuwawezesha wateja kufurahia data. | uchumi |
KUTOKANA na mabadiliko ya wakati, kuongezeka kwa biashara ya silaha na matukio ya kigaidi duniani, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaunga mkono mabadiliko ya Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa kwa faida ya usalama wa nchi.Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam wa kutoa maoni kuhusu uboreshaji wa Muswada huo wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyma vya Siasa, jana jijini Dar es Salaam.Lubinga amesema jamii yoyote duniani, taasisi, kabila au familia ina mfumo wake wa kuendesha shughuli zake kulingana na mazingira yake, hivyo Tanzania kama nchi huru na inayofuata mfumo wa kidemokrasia, ina utaratibu wake wa kuendesha mambo yake ili wananchi wake waishi kwa amani na kujiletea maendeleo.Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni serikali ya kidemokrasia, iliyochaguliwa na wanachama wa CCM na Watanzania kwa ujumla, hivyo ina wajibu wa kuwaletea wananchi maendeleo.Alifafanua kuwa chama cha siasa ni kundi la watu wachache ndani ya jamii, ambalo linaoongozwa na itikadi yao wakiwa na kusudi na lengo la kukamata hatamu za dola, ambayo ndiyo kazi kubwa ya chama cha siasa. Baada ya kuanzishwa kwa vyama vya siasa nchini mwaka 1992, alisema Msajili wa Vyama vya Siasa aliwekwa kwa lengo la kusimamia na kuendesha utaratibu wa vyama vya siasa kulingana na hitajio lililopo ambalo hitajio hilo hubadilika kulingana na mazingira.Kwa mantiki hiyo, Lubinga alisema CCM inaunga mkono muswada huo, ambao pamoja na mambo mengine unamtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kujua fedha za vyama vya siasa zinatoka wapi na kwa lengo lipi.“Muswada unasema fedha zote za vyama vya siasa zinazotoka nje, lazima msajili ajue, mafunzo yanayotolewa katika Vyama vya Siasa, lazima Msajili ajue; kwa mfano, ukichelewa kuoa au kuolewa una bahati kwa sababu unaona waliokutangulia mahali walipokwama na sababu iliyowakwamisha, hivyo una nafasi ya kujifunza.“Maana yangu ni kwamba, Tanzania tumechelewa kuingia kwenye matatizo yanayotokea duniani, wenzetu wanavyouana, iwe fundisho kwetu kwamba kila tunachokifikiri au kukifanya lazima tuwe imara, leo hii Nairobi wamelipuliwa, maana yake ni kwamba kikiungua kijiji cha jirani, wewe lazima pia ujiandae” alieleza.Alisema marekebisho hayo makubwa ya Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, yana lengo la kuifanya Tanzania kujiandaa kukabiliana na matukio kama hayo.Alisema siku hizi kuna fedha zinazotoka nje kwenda kwenye vyama vya siasa kwa ajili ya kutoa mafunzo.Kwa mujibu wake, mfumo wa uchumi duniani nyakati hizi umebadilika hasa kuhusu masuala ya silaha.Alisema zamani kulikuwa na uzuiaji wa utengenezaji wa silaha, ambao kwa sasa haupo, badala yake uchumi wa dunia leo umeelekezwa kwenye viwanda vya kutengeneza silaha, ambao unadaiwa kuwa na faida zaidi ya viwanda vya kutengeneza vifaa vya kijamii.Alisema hayo ndiyo matokeo ya baadhi ya nchi ikiwemo Libya, Iraki na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujikuta kwenye matatizo na silaha zinauzwa kwa wingi.Alisema kwa kuwa Tanzania haijachukua hata nusu ya bajeti yake kununulia silaha, jambo hilo haliwafurahishi wengi, hivyo wanaiona Tanzania kama keki kwenye biashara ya silaha.Kutokana na sababu hiyo, Msajili wa Vyama vya Siasa ana wajibu wa kufuatilia mambo hayo kisheria ndiyo maana ya Muswada huo kuletwa ili utolewe maoni ya kuuboresha kwa faida ya nchi.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, alisema muswada huo utaviwezesha vyama vya siasa ambavyo ni taasisi za umma kuwa imara na madhubuti, kuvifanya vyama kutambua kuwa umoja wa kitaifa ni muhimu kuliko tofauti zao za kiitikadi pamoja na kutambua ulinzi na usalama wa nchi ni muhimu katika ujenzi wa maendeleo.Alisema vyama vya siasa vina wajibu wa kuweka mifumo thabiti ya kidemokrasia ndani ya vyama vyao ikiwemo mfumo wa kushiriki na ushirikishwaji wa wanachama, utaratibu mzuri wa kupata viongozi ndani ya vyama, utaratibu mzuri wa mapato na matumizi ya fedha za vyama ambazo ama zinatoka serikalini au kwenye vyanzo vingine.Upungufu wa Muswada Kwa kuwa sheria ya vyama vya siasa haijafanyiwa marekebisho kwa miaka 10 tangu mwaka 2009, Polepole alisema pamoja na mambo mengi mazuri yaliyomo kwenye muswada huo ambao CCM inayaunga mkono, lakini kuna upungufu mchache.Polepole alisema katika muswada huo kuna pendekezo kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa atoe elimu ya uraia katika vyama, lakini CCM wanapendekeza msajili asimamie utoaji wa elimu katika vyama vya siasa na siyo kutoa elimu.Alisema Msajili anapaswa kujiridhisha kuhusu elimu inayotolewa ndani ya vyama hivyo.Alisema pia maofisa katika Ofisi ya Msajili, hawapaswi kuhojiwa wanapotekeleza majukumu yao kwa nia njema kama ilivyo kwa wabunge na majaji wanapotekeleza majukumu yao wanapokuwa bungeni au mahakamani, ila Ofisi ya Msajili inaweza kuhojiwa kama itakiuka taratibu kama vile kukifuta chama bila kuhojiana nao kwanza.Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kheri James alisema wanapendekeza Kifungu cha 6(a) kifanyiwe marekebisho.Kifungu hicho kinataka wazazi wa mtu anayetaka kusajili chama cha siasa, lazima wawe raia wa Tanzania.Kwa mujibu wa James, kila raia wa Jamhuri ya Muungano apewe haki ya kusajili chama cha siasa bila kuangalia uraia wa wazazi wake, lakini pia Wasajili Wasaidizi katika Ofisi ya Msajili waendelee kuitwa Wasajili Wasaidizi na siyo wakurugenzi kama muswada unavyopendekeza.Mjumbe wa NEC, Mariam Ngula alisema CCM inapendekeza Kifungu cha 17 cha muswada kinachotaka vyama vya siasa kuungana ndani ya siku 21 kabla ya kufanya uteuzi wa wagombea wao, kibadilishwe na badala yake viruhusiwe kuungana wakati wowote kabla ya uteuzi wa viongozi hao. | kitaifa |
“Tawi letu hili la kipekee litatumika kuhudumia wateja wetu wote wakubwa na kukidhi matakwa yao kikamilifu kwa kutoa huduma zote za kibenki za kipekee katika eneo maalumu. Jitihada hizi zinaenda pamoja na dhamira ya Benki ya Exim ya kutoa huduma bora kwa wateja wake katika nyanja zote,” alisisitiza.Manek alisema kuwa tawi hilo mkoani Arusha lina wataalamu wa kutosha walio tayari kutoa ufumbuzi mbali mbali za masuala ya kibenki ili kukidhi matakwa ya wateja wakubwa.Alisema benki yake imejikita katika mkakati madhubuti unaolenga kuiwezesha benki hiyo kuwa benki inayoongoza katika utoaji wa huduma bora za kifedha Tanzania na zaidi.“Ikiwa ni sehemu ya mkakati wetu, tumejikita katika mkakati wa kutanua huduma zetu kupeleka bidhaa na huduma zetu bora kwa wateja wetu Tanzania nzima pamoja na matawi yetu mengine nje ya nchi.“Tuna imani kuwa tawi letu litasaidia katika shughuli za kiuchumi hapa mkoani Arusha, ikiwa ni pamoja na shughuli za misitu, maendeleo ya wiwanda, madini, ukanda wa kilimo-uchumi, maliasili na wanyamapori pamoja na maendeleo ya makazi,” aliongeza.Alisema katika mkakati huo, benki yake inalenga kufikisha jumla ya matawi 50 nchi nzima pamoja na machine za kutolea fedha (ATM) 100 ifikapo 2016,” alisema.Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa tawi hilo jipya, Hamad Said wakati wa hafla hiyo alisema kuwa tawi hilo litaendelea kutoa huduma kwa wakati na kumpa mteja uzoefu wa kipekee.“Wateja wetu wakubwa sasa wataweza kufaidika na huduma zetu mbali mbali katika sehemu moja ambazo zitatosheleza kikamilifu mahitaji yao yote. Tunajiamini kuwa wateja wetu wataona faida zake na kutumia fursa hii kikamilifu,” alisema.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo wakati wa hafla hiyo aliwaasa umekuja katika muda muafaka ambapo mkoa huo unatarajia kupata miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya miundombinu.“Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litakuwa chachu ya maendeleo mkoani Arusha. Natoa fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara mkoani hapa kuchangamkia fursa hii,” alisema.Hata hivyo, Mulongo alitoa changamoto kwa benki hiyo kutoa huduma bora siyo tu kwa wateja wakubwa bali hata wateja wadogo (SMEs) kwa kuwa wana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa. | uchumi |
TANZANIA na Kenya zimekubaliana kuimarisha uhusiano ma ushirikiano hasa katika masuala ya kiuchumi, sambamba na kujenga uwiano wa kibiashara wenye maslahi ya pande zote mbili.Hayo yamebainishwa na Rais John Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta kufuatia mazungumzo ya faragha baina yao katika kijiji cha Mlimani kabla ya Rais Uhuru kuruka katika uwanja wa ndege wa Chato, mkoani Geita akiwa amekamilisha ziara yake binafsi ya siku mbili ya kumtembelea Rais Magufuli.Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya hususani katika masuala ya kiuchumi na kutaka biashara baina ya nchi hizo ikuzwe zaidi pamoja na kujenga uwiano wa kibiashara wenye maslahi kwa pande zote.Ras Magufuli alisema kwa kuzingatia kuwa Kenya imefanya uwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania ikilinganishwa na uwekezaji wa Tanzania nchini Kenya, wamekubaliana kuwa kampuni za Kenya zijielekeza kuongeza thamani ya bidhaa kwa kuanzisha viwanda vitakavyosindika mazao na kuchakata bidhaa mbalimbali hapa hapa Tanzania badala ya kusafirisha malighafi kwenda Kenya.Aliongeza kuwa wamekubaliana kuwa Kenya itanunua gesi ya Tanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya Bara la Afrika kwa kuwa Tanzania imejaaliwa gesi nyingi na wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kukutana na kujadili namna Kenya itavyonunua gesi hiyo.Hali kadhalika kuhusu Ziwa Victoria ambalo kwa asilimia 51 lipo Tanzania na asilimia tano lipo Kenya, Rais Magufuli alisema wamekubaliana kuwa Mawaziri wa nchi hizo wahakikishe meli za Tanzania na Kenya zinaimarishwa na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha meli hizo kufanya kazi ya kukuza biashara katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zinazunguka ziwa hilo.Katika hatua nyingine, Rais Uhuru alimshukuru Rais Magufuli kwa mapokezi mazuri aliyoyapata Chato na upendo mkubwa uliooneshwa na wananchi wa Chato kwake na ujumbe wake na kuongeza kuwa huo ni uthibitisho wa uhusiano mzuri, undugu na urafiki wa karibu kati ya Wakenya na Watanzania.Alisema pamoja na kuimarisha zaidi uhusiano wa Tanzania na Kenya uliojengwa na Waasisi wa Mataifa hayo Hayati Julius Nyerere na Hayati Jomo Kenyatta, wamekubaliana kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na amani na kuheshimu mkataba wa kukabiliana na uhalifu unaosema Mtanzania atakayekamatwa kwa uhalifu nchini Kenya anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Kenya na Mkenya atakayekamatwa kwa uhalifu nchini Tanzania anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.Rais Uhuru alisisitiza kuwa wakenya na watanzania hawana sababu ya kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi bali kuhakikisha uchumi unakua, biashara inaongezeka na uhusiano na ushirikiano katika maeneo mbalimbali unaimarika zaidi.Wakati huo huo Rais Magufuli na Rais Uhuru wamekubaliana kuwakutanisha wake wa waasisi wa Mataifa ya Tanzania, Kenya na Uganda ambao ni Mama Maria Nyerere, Mama Ngina Kenyatta na Mama Miria Obote kwa siku tatu Jijini Dar es Salaam ili wapate muda wa kujadiliana pamoja na kukumbuka misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa hayo.Akiwa nyumbani kwa Rais Magufuli katika Kijiji cha Mlimani, wilayani Chato Rais Uhuru aliweka shada la maua katika makaburi ya familia ya Rais Magufuli na pia alimtembelea tena Mama Mzazi wa Rais Magufuli, Suzana Magufuli ambaye baada ya kupatiwa matibabu ya kiharusi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam, anaendelea kupata matibabu hayo akiwa nyumbani.Mbali na kumshukuru kwa kumtembelea nyumbani kwake Chato, Rais Magufuli alitoa zawadi ya ndege wanne aina ya Tausi kwa Rais Uhuru ili akawafuge na kuweka kumbukumbu nyingine ya uhusiano mzuri wa Tanzania na Kenya. | uchumi |
KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) inazindua safari ya kwanza kwenda Johanesburg, Afrika Kusini kesho. Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hatua hiyo ni mafanikio ya mpango mkakati wao ulioanza mwaka 2017, waliojiwekea kuhakikisha shirika hilo linapata mafanikio kwenye usafiri wa anga kwa kufungua vituo vingi vya biashara nje ya nchi.Matindi alisema safari katika ruti hiyo itahusisha ndege mpya za kisasa za Air- bus A220-300. Uzinduzi wa tiketi kwa ajili ya safari hiyo ulifunguliwa rasmi mwezi mmoja uliopita. “Nitoe mwito tu kwa Watanzania na wasafiri wote wanaokwenda kwenye majiji ya Johannesburg, Mumbai, Comoro, Zimbabwe na nchi nyingine tulikozindua safari zetu, wapande ndege za ATCL watafurahia huduma na bei zetu nafuu,” alisema Matindi.Alisema kufunguliwa kwa kituo cha ndege za ATCL, jijini Johannesburg na kingine kitakachozinduliwa mwezi ujao Mumbai, India kunafanya idadi ya vituo vya biashara nje ya nchi kwa ndege hizo kufika saba. Vituo hivyo ni Zam- bia, Zimbabwe, Uganda, Comoro, Burundi, Johannes- burg na Mumbai.Mapema mwezi uliopita, Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini India, ilitoa kibali kwa ATCL kuanzisha safari zake nchini humo ambapo Julai 17, mwaka huu kampuni hiyo itazindua safari zake kwenda Mumbai, India, huku dirisha la tiketi likiwa limeshafunguliwa. Hata hivyo, safari za nje ya nchi kwa ndege za ATCL zilichelewa kuanza kutokana na mambo ya msingi yaliyokuwa yakifanywa, ikiwemo nchi kurudishwa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA).“Tulipanga kuzindua mapema safari za nje, ila tulichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA) ambayo kwetu kwa sasa tumeshafikia mwisho,” alisema Matindi.Kwa sasa ndege za ATCL zinafanya safari za kwenda Zambia, Zimbabwe na Uganda na ruti za ndani ya nchi kwenye mikoa kadhaa ikiwemo Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Mbeya na Zanzibar. Wakati huo huo, maan- dalizi ya kwenda safari nyingine za nje ya bara la Afrika ikiwemo Thailand, China kwa ndege ya Dream- liner na Airbus 220-300 yanaendelea. | kitaifa |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Waislamu nchini waendeleze utulivu, amani na uadilifu waliouonesha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kwa kufanya hivyo, watasaidia kukuza umoja wa kitaifa, uchumi na kuboresha huduma za jamii.Amesema ni vema Waislamu wakatambua uadilifu waliouonesha wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni silaha muhimu kuimarisha maendeleo na kudumisha haki, umoja, usawa, upendo na utulivu nchini.Waziri Mkuu, Majaliwa alitoa kauli hiyo juzi kwenye Baraza la Idd el Fitr katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, jijini Tanga. “Nawasihi kuyaenzi mema yote mliyoyafanya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,’’ amesema.Kadhalika, Waziri Mkuu alizipongeza taasisi za Kiislamu na imani nyingine ambazo zimejenga shule ili kuchangia maendeleo ya elimu kitaifa.Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza shule nyingine na vyuo zaidi pamoja na kuziboresha zilizopo ili kusaidia jitihada za Serikali kuboresha huduma za jamii nchini.Alisema licha ya juhudi inazozichukua, serikali peke yake haina uwezo wa kueneza huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji kila pembe.Alisema, inapotokea taasisi za Kiislamu au madhehebu mengine yakaweka mikakati ya kueneza huduma hizo, Serikali itaziunga mkono juhudi hizo na kuchangia ufanisi wake.Wakati huo huo, alilitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) lichukue hatua kuhakikisha huduma nyingi za maendeleo na za kijamii zinaifikia mikoa mingi ya pembezoni.“Huu ni wakati muafaka kutafakari ni namna gani Watanzania wa maeneo mengine nao watanufaika na uwepo wa huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na nyinginezo,” alisema.Mufti wa Tanzania, Shehe Mkuu Aboubakar Zubeir bin Ally alitumia fursa hiyo kuwataka Waislamu wote nchini wabadilike na waache mazoea ili wasonge mbele kielimu na kiuchumi.Alisema ni vema kwa Waislamu wakajiimarisha kiuchumi kwani kutawaondolea changamoto za kuendesha shughuli zao mbalimbali na hivyo watajiletea maendeleo na kuboresha maisha yao.Mbali na wito huo pia aliwataka Waislamu wote wahakikishe wanatii mamlaka yaliyo juu yao, viongozi walio madarakani, wa kiserikali na dini kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Diwani Athuman alisema ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu na usalama Watanzania wote hawana budi kuungana kupiga vita vitendo vya rushwa.“Rushwa ni dhambi kubwa na hukumu yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni moto kwa sababu rushwa ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo. Hivyo tuungane kupinga rushwa ndani ya nchi yetu kama Rais John Magufuli anavyotuongoza,” Diwani aliwaasa Waislamu.Dk Shein awafagilia WawakilishiKatika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameeleza kuridhishwa na michango inayotolewa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kikao cha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.Amesema michango ya wawakilishi imelenga kuzipatia ufumbuzi kero na matatizo ya wananchi katika majimbo yaoa ya uchaguzi.Alisema hayo katika Baraza la Iddi el Fitr lililofanyika katika ukumbi wa Shehe Idriss Abdull Wakil. Alisema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanafanya kazi waliyotumwa na wapiga kura katika majimbo ya uchaguzi.Alisema kazi kubwa ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni kupokea kero za wananchi na kuziwasilisha kwa serikali kufanyiwa kazi.Aliwataka kuongeza bidii ya kuibua hoja mbalimbali na kuziwasilisha serikali kwa mawaziri husika waliomo katika Baraza la Wawakilishi ili zipatiwe ufumbuzi wake.‘’Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid nimeridhika na kazi kubwa unayoifanya kuliendesha Baraza la Wawakilishi zaidi kuisimamia serikali na kuona inatekeleza majukumu yake kwa wananchi,’’ alisema.Dk Shein aliwataka wananchi kusubiri bajeti ya serikali yake mwaka wa fedha 2019/2020 ambayo inatarajiwa kuwasilishwa barazani hapo na Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa Juni 20, 2019.Alisema bajeti imejipanga ikiwa imekusanya mambo mengi ya ustawi wa jamii kuimarisha huduma za afya na shule, pamoja na kujikita katika kuleta maendeleo na miundombinu.Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinaendelea Chukwani mjini Unguja ambapo tayari jumla ya bajeti za wizara 11, zimewasilishwa mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kujadiliwa. Imeandikwa na Ikunda Eric, Dar, na Suleiman Khatib, Zanzibar. | kitaifa |
KATIKA kuhakikisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inafanikisha vyema miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia bajeti, ilipunguza kutegemea fedha za nje kutoka Sh bilioni 775.8 ya mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Sh bilioni 547.38 ya mwaka wa fedha 2018/2019.Aidha serikali iliongeza fedha zake za ndani kwenye miradi ya maendeleo kutoka Sh trilioni 4.35 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Sh trilioni 4.89 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kwa mujibu wa taarifa za bajeti za miaka miwili ya fedha iliyomalizika (2017/18 na 2018/190, Serikali imejikita katika kupunguza utegemezi wa fedha za nje lakini pia kuongeza fedha za maendeleo kwa kutumia fedha za ndani ambazo zinatokana na kodi za wananchi. Katika mwaka wa fedha wa 2017/18, Serikali ilipanga kutumia Sh trilioni 31.71 lakini ilifanikiwa kutoa jumla Sh trilioni 21.68 sawa na asilimia 68.4 ya lengo.Katika fedha hizo zilizotoka ilifanikiwa kutoa Sh trilioni 5.12 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Sh trilioni 4.35 zilikuwa ni fedha za ndani na Sh bilioni 775.8 ni fedha za nje. Kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 Serikali ilipanga kutumia Sh trilioni 32.48 ambapo serikali ilifanikiwa kutoa jumla ya Sh trilioni 22.19 ya lengo husika.Katika kuhakikisha inaongeza nguvu kwenye shughuli za maendeleo, Sh trilioni 5.44 zilitolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo Sh trilioni 4.89 ni fedha za ndani wakati Sh bilioni 547.38 ni fedha za nje.Fedha zilipoendana na mafanikio yake Katika kipindi cha miaka miwili ya fedha serikali ilijikita kwenye maeneo yafuatayo; Kwa mwaka wa 2018/19, miongoni mwa maeneo ya kimkakati ambayo yalipatiwa fedha katika kipindi hicho yalikuwa ni Mradi wa kufua umeme utokanao na nguvu za maji katika Mto Rufiji ambapo kiasi cha shilingi bilioni 723.6 zilitolewa.Shilingi bilioni 616.9 zilitolewa kwaajili ya kugharamia elimu ya msingi bila ada pamoja na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Pia mwaka huu ulioisha, Sh bilioni 269.3 zilitolewa kwa ajili ya Awamu ya Tatu ya Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Alkadhalika Serikali ilitumia Sh bilioni 238.8 katika ununuzi na uendeshaji wa ndege mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL). Sambamba na miradi hiyo ya maendeleo, Sh bilioni 27.6 zilitumika kuendeleza ujenzi wa meli mpya katika maziwa makuu.Kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, Serikali ilifanikiwa kutekeleza yafuatayo katika kipindi cha Julai 2017 hadi Aprili 2018; Kwanza ilitoa jumla ya Sh bilioni 59.0 kwa Halmashauri za Wilaya 110 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya, na Sh bilioni 24.1 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali za mikoa 24.Aidha, jumla ya shilingi bilioni 125.7 zilitolewa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama, serikali ilitoa Sh bilioni 156.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini.Pia ilitoa Sh bilioni 409.9 kwa ajili ya miradi ya nishati vijijini, umeme wa jotoardhi, uzalishaji wa umeme katika vyanzo mbalimbali na usambazaji wa gesi asilia Aidha Serikali ilitimiza sehemu ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutoa Sh bilioni 618.0 kwa ajili ya elimu msingi bila ada na kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.Kwa mwaka huo wa 2017/18, Serikali ilitoa Sh trilioni 1.87 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miundombinu ili kupanua fursa za uchumi, kilimo, biashara na viwanda ikiwemo kujenga barabara zinazounganisha mikoa na nchi jirani, barabara zinazopunguza msongamano katika majiji, barabara za vijijini, reli, viwanja vya ndege, na bandari. | kitaifa |
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani linalishikilia basi la kampuni ya Smart kwa kubeba nguo zinazodhaniwa kuwa hazijalipiwa ushuru.Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mombasa lilikamatwa likiwa na nguo hizo likitokea Mombasa kwenda Dar es salaam.Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 10 majira ya saa 11 alfajiri wilayani Kibaha wakati askari wakiwa doria na kulikuta basi hilo lenye namba za usajili T 819 CAW likiwa na mzigo huo. “Basi hilo lilikuwa limebeba nguo za aina mbalimbali zikiwa zimewekwa kwenye buti na nyingine zikiwa ndani vitu vingine zikiwemo nazi, mchele na mafuta ya kupikia huku likiwa na abiria tisa tu,”alisema Nyigesa. Alisema kuwa mzigo huo unadhaniwa kuwa umeibwa au haujalipiwa ushuru na haukustahili kubebwa kwenye basi la abiria.Naye Meneja wa TRA, Euvansia Lwiwa alisema basi hilo lilibeba mzigo huo lakini haukuwa na taarifa za kutosha. Lwiwa alisema kuwa wanawasiliana na timu inayohusika na udhibiti wa magendo kupitia Kamishna wa Ushuru na Forodha ili kubaini kama haujalipiwa ushuru ili hatua zichukuliwe.Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mosi Nzero alisema kuwa walifanya ukaguzi kwenye basi hilo na kugundua kuwa mbali ya ubebaji mizigo pia gari hilo lilikuwa bovu.Nzero alisema kuwa ubebaji wa mizigo kwenye basi la abiria ni kosa kisheria na wamekiuka sheria ya usalama barabarani. Dereva wa basi hilo, Shaban Mbwana alisema kuwa mzigo waliobeba ni halali na wahusika wa mzigo huo walipanda magari mengine. | kitaifa |
Yanga ilirejea Dar es Salaam Alhamisi, ikitokea Zanzibar baada ya kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi hatua ya nusu fainali dhidi ya URA kwa mikwaju wa penalti 5-4. Jumatano ijayo wanatarajiwa kucheza mchezo wa raundi ya 13 wa Ligi kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili, Nsajigwa alisema kikosi kitaanza mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo muhimu kwao katika mbio za kutetea taji la ligi. “Tunautazama mchezo huo ni muhimu kwetu kupata matokeo, kama unavyojua kwenye ligi hakuna timu ndogo, ni lazima tupambane kupata matokeo mazuri,” alisema.Alisema Mwadui ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri hivyo, iwapo wataibeza inaweza ikawaumbua. Yanga huenda ikalipiza kisasi kwa Mwadui kwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri baada ya mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbao FC kuchapwa mabao 2-0 huko jijini Mwanza.Kutokana na matokeo hayo yaliyopita Yanga ilibaki na pointi 21 ikishika nafasi ya nne kabla ya michezo ya jana, ikiwa nyuma ya Singida United yenye pointi 23. Iwapo itaruhusu kupoteza mchezo huo kuna uwezekano wa kuendelea kushuka | michezo |
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga ilitawala katika kipindi chote cha kwanza na ndipo ilipopata mabao hayo mawili. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 46 sawa na vinara Simba wanaoongoza kwa uwiano mzuri wa mabao wakiwa na mechi moja kibindoni. Simba sasa italazimika kushinda mechi yake ijayo inayotarajiwa kuchezwa wiki ijayo.Yanga ilipata bao la kuongoza katika dakika ya sita likifungwa na Yusuph Mhilu aliyeunganisha mpira wa krosi kabla ya mpira kumgonga beki wa Stand United na kujaa wavuni. Dakika sita baadaye Ibrahim Ajibu alifunga bao la pili baada ya kupewa pasi na Gadiel Michael kabla ya kuujaza mpira wavuni. Kipindi hicho cha kwanza Yanga walimiliki mpira kwenye idara zote na Stand United wakionekana ‘kutii’ kila wanachotaka mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu.Kipindi cha pili, Stand walibadilika na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara hali iliyowafanya wachezaji wa Yanga kurudi nyuma muda mwingi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza. Juhudi zao zilizaa matunda katika dakika ya 85 walipopata bao lililofungwa na Tariq Seif aliyemalizia vizuri krosi ya Ally Ally.Hata hivyo, bao hilo halikudumu kwani dakika moja baadaye Obrey Chirwa aliandika bao la tatu kwa Yanga baada ya kupokea mpira mrefu wa Martin akiwa ndani ya 18 na kuachia shuti lililojaa moja kwa moja wavuni. Matokeo hayo si mazuri kwa Stand United iliyo nafasi ya 13 kwenye msimamo, kwani sasa inachungulia ukanda wa kushuka daraja na isipojitahidi katika mechi zinazofuata, safari inaweza kuwakuta. | michezo |
WATU wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na polisi wakati wakiwa kwenye majibizano ya risasi ndani ya msitu wa Kisanga Kijiji cha Kisanga Tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro huku wengine 19 wakishikiliwa.Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa alisema kuwa tukio hilo ni Mei 16 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri katika pori hilo lililipo Kijiji cha Kisanga wilaya ya kipolisi ya Ruhembe.Kwa mujibu wa kamanda huyo, polisi wakiwa wanafuatilia matukio ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyokuwa yamefanyika katika maeneo tofauti ya tarafa za Mang’ula na Ifakara wilaya ya Kilombero, walipata taarifa kuwa watuhumiwa waliojihusisha na matukio hayo, walikimbilia kwenye pori lililo karibu na Kijiji cha Kasanga kujificha ili wasikamatwe.Kwamba baada ya kupata taarifa zao, polisi waliwafuata na kukuta kundi la watuhumiwa hao, lakini wao baada ya kuwaona askari, walielekea walipo na kuanza kuwavyatulia risasi. Kufuatia shambulizi hilo, askari walilazimika kujibu mashambulizi hayo, huku wakiwa kwenye tahadhari wasidhuriwe.Hata hivyo katika majibizano hayo, watuhumiwa wanne walijeruhiwa kwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Wengine walitokomea porini na hawakupatikana. Kamanda Mutafungwa alisema watu hao wanne walikufa, baada ya kuvuja damu nyingi wakiwa njiani kupelekwa hospitalini kupatiwa matibabu.Alisema watu hao walikutwa na bunduki mmoja aina ya shortgun double barrow yenye namba 107735, iliyokatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili na ganda moja la risasi. Kwamba watu hao walihusika kwenye matukio mbalimbali ya uporaji na ujambazi katika tarafa ya Mang’ula.Mbali na kuuawa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi, Polisi waliendesha msako na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine 19, wakiwemo wapangaji wa matukio hayo ya ujambazi, ambao ni wakazi wa miji ya Ifakara, Man’gula, Kiberege na Ruaha. Mutafungwa alisema watuhumiwa wote wanaoendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. Miili ya waliouawa imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. | kitaifa |
RAIS John Magufuli amesema mgogoro wa ardhi wa vijiji 33 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kati ya wananchi na wawekezaji, utapatiwa ufumbuzi hivi karibuni, kwa kuwa ripoti ya Tume ya mawaziri wanane aliyoiunda, imeshakabidhiwa serikalini.Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilikuja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kumweleza kuwa kazi aliyowatuma wameshaimaliza na tayari ripoti wameikabidhi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye pia na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Kwa mujibu wa Lukuvi, wakazi wa vijiji hivyo 33 walipaswa kuondolewa kupitia Tangazo la Serikali Namba 28 kutokana na vijiji hivyo kuwa ndani ya hifadhi.Hata hivyo, uamuzi huo ulisitishwa na Rais Magufuli na kuamua kuunda Tume ya Mawaziri wanane ili kufuatilia suala hilo ili uamuzi wa haki, utolewe kwa upande wa wananchi na upande wa serikali.Lukuvi alimweleza jana Rais Magufuli kwenye mkutano wake wa hadhara na wananchi wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuwa kazi ya kupitia upya maeneo, taarifa mbalimbali na sheria kuhusu mgogoro huo wameshaikamilisha. Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, Tume hiyo imeshakabidhi ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawiziri ili iweze kujadili katika Baraza la Mawaziri chini ya uenyekiti wa Rais Magufuli na kisha kutolewa uamuzi wa ama kuwaondoa wananchi katika vijiji hivyo 33 au la.“Kazi tumeimaliza, tumepata taarifa ya mkoa, tumezungumza na viongozi na wananchi hawa, Baraza la Mawiziri litaketi chini yako na kukushauri na ikikupendeza uamuzi wa vijiji hivi 33 na vijiji vingine vilivyokuwa na matatizo kama hapa Mbarali uweze kutolewa, kwa hiyo Wanambarali suala ya GN 28 limekwisha, msubiri matokeo yakayotolewa na vikao halali,”alieleza Lukuvi.Kuhusu mgogoro wa mashamba ya Kapunga na Highland, Lukuvi alisema nao umeshafanyiwa kazi. Alisema mashamba hayo yalibinafsishwa na serikali kwa mujibu wa sheria na wanunuzi walipatikana. Alisema shamba la Kapunga lilinunuliwa na Kampuni ya Tanzania Export Trading Company ya Patel, wakati shamba la Highland lilinunuliwa na Mbunge wa Mbarali wa sasa, Haroon Mulla Pirmohamed.Baada ya hayo yote, Lukuvi alisema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, iliamua kufunga ekari 4,675 zilizokuwa zimeingizwa kwa mwenye shamba wakati zilitakiwa kuwa za wananchi na kuongeza kuwa kazi ya kuzirudisha ilikamilika mwaka 2016 wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa Abbas Kandoro.“Baada ya mgogoro kati ya vijiji 11 na mmiliki wa shamba la Highland, tulifanya uhakiki ili kujiridhisha kama kweli shamba hili liliingia kwenye mipaka ya wananchi, baada ya uhakiki, ekari 1,352 zilikatwa kutoka shamba hili na kurudishiwa wananchi na mwaka 2018 Highland alipewa hati nyingine ambayo ina pungufu ya eneo la awali kwa ekari 1,352, na shamba namba 77 na 78 pia limerudishwa ambazo ni eakari 1,375,”alieleza Lukuvi.Bonde la Mto Ruaha Kuhusu uharibifu wa Bonde la Mto Ruaha, ambalo pia hujulikana kama Bonde la Usangu ni moja ya mabonde manne makubwa hapa nchini likiwemo Bonde la Mto Kilombero na Rufiji chini, alisema Bonde hilo lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 85,554 sawa na asilimia 47 ya Bonde la Rufiji. Alisema vijiji 33 katika eneo hilo, viliathirika kutokana na Tangazo Namba 28 la Serikali ambapo kabla ya tangazo hilo, eneo hilo lilikuwa na ukubwa wa hekta 10,000, lakini baada ya tangazo likaongezwa na kuwa hekta 20,000.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, katika hilo, kuna mambo ambayo serikali ilikosea na kuna mambo ambayo wananchi nao pia walikosea. Alisema kwa upande wa serikali wakati inatoa tangazo hilo la kufuta vijiji 33 vilivyokuwa na wakazi takribani 40,000, haikuelezwa wananchi hao wataenda wapi. Lakini, pia alihoji ni kweli kwamba serikali ilikuwa inalihitaji eneo lote hilo. Kwa kuwa Mto Ruaha Mkuu unaundwa na mito tisa, matumizi ya maji yaliyofanywa na wananchi wa eneo hilo kwa kilimo cha umwagiliaji, ulitishia uhai wa mto huo ambao ni muhimu kwa uzalishaji wa umeme kwa mabwawa ya Mtera na Kidatu na maporomoko ya Mto Rufiji ya Stiegler’s Gorge.Mbali na shughuli hizo za kilimo, wananchi pia walikuwa wakikata miti hovyo, kuingiza mifugo holela na shughuli holela za uchimbaji madini, ambavyo vyote viliathiri ustawi wa mto huo. Alisema kwenye miaka ya 1960, maji ya mto huo yalikuwa yakimiminika wakati wote. Lakini, kwa sasa maji hukatika hata kwa miezi sita na kusababisha vifo vya wanyama wakiwemo viboko na samaki.Kijiji cha Machimbo Kuhusu wananchi wa Kijiji cha Machimbo kutaka kulipwa fidia, Rais Magufuli alisema wananchi hao walishalipwa fidia ya Sh milioni 800 na waliobaki wanatakiwa kulipwa Sh milioni 31 tu. Alisema wananchi hao baada ya kuchukua fidia hiyo, hawakuhama na waliendelea na shughuli zao, hivyo hawatalipwa na wanatakiwa kuondoka.Alisema kama watabaki, watatakiwa kurudisha fedha hizo. “Kuna mradi mmoja uligharimu zaidi ya shilingi bilioni 20, baadaye mradi huo ukagawiwa kwa wananchi na kila mmoja alipata hekta 1 ili walime, lakini wananchi wale wakaanza kuuza maeneo yao kwa wafanyabiashara na waliowauzia wanajulikana, baada ya kuwauzia yakaenda kwenye mikono ya wajanja na wajanja hao wakaanza kuwakodishia wananchi kwa shilingi milioni 1,” alisema Rais Magufuli.Kuhusu ekari 4,675 na ekari 1,300 alizoagiza zirudi kwa wananchi, Rais Magufuli alitaka kujiridhisha kuhusu hilo na kuwaagiza Waziri wa Ardhi, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, wampatie orodha ya watu waliopewa ekari hizo kwa sababu zinaweza kuwa ekari hewa. Rais Magufuli pia alisema Mwekezaji wa Shamba namba 77 na 78, alipewa kihalali na aliamua kukodisha mashamba hayo kwa wananchi kwa gharama ya Sh 2,295 kwa ekari, lakini madalali waliyauza maeneo hayo kwa kuyakodisha kwa Sh 600,000 hadi Sh 700,000, hivyo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ahakikishe madalali hao wanatafutwa. | kitaifa |
Mkurugenzi wa Idara ya vyama vya ushiriki Daud Simba alisema hayo wakati alipozungumza na wanachama wa Elimu Saccos katika mkutano wa kufanya tathmini ya maendeleo ya Saccos hiyo.Simba alisema sheria nambari 4 ya vyama vya ushirika imeweka mikakati na malengo mazuri ya kuhakikisha vyama vya ushirika vinaleta tija kwa kuimarisha uchumi na kupambana na umasikini.Alisema tayari jumla ya vyama vya ushirika 60 vimesajiliwa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wanachama wake Unguja na Pemba,hatua ambayo ni moja ya dalili nzuri ya kuimarika kwa vyama vya ushirika na Saccos nchini.“Idara ya vyama vya ushirika imefurahishwa na mwamko mkubwa wa wananchi walioitikia kwa ajili ya kuimarisha na kufufua vyama vya ushirika Unguja na Pemba kama njia pekee ya kukuza uchumi na kupambana na umasikini,” alisema.Mapema Mwenyekiti wa Elimu Saccod Ahmed Mohamed alisema wamepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwa Saccos hiyo ambayo imekuwa tegemeo kwa Jumuiya ya Walimu na wanachama wake.Kwa mfano alisema Elimu Saccos imefanikiwa kutoa zaidi ya mikopo kwa wanachama wake wapatao 12,000 na kutumia zaidi ya Sh milioni 120 ambayo wanachama wameitumia kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi na miradi mingine. | uchumi |
SHIRIKA la Kimataifa la Uhifadhi Viumbe Baharini na Wanyama (WWF Tanzania) wilayani Kilwa mkoani Lindi litatumia Sh 424,361,857.00 kwa ajili ya mradi wa kuboresha zao la pweza katika kijiji cha Songosongo, utakaokamilika muda wa miaka miwili.Mwakilishi wa Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Matrida Simfukwe alisema hayo juzi kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo uliohudhuriwa na viongozi wa serikali, halmashauri ya wilaya, wadau wa sekta ya uvuvi katika kijiji cha Songosongo. Alisema muda huo wa miaka miwili ni kipindi cha majaribio katika kijiji hicho cha Songosongo wilayani Kilwa na kuwa mradi huo upo katika nchi tatu ikiwemo Tanzania na Kenya.Simfukwe alisema dhamira kuu ni kuhakikisha zao hilo linavunwa na kuhifadhiwa katika mazingira mazuri wakiwa na ubora wake mpaka mlaji anapata ubora wa zao hilo la pweza, wakati akihitaji. Alisema uhifadhi utakapokuwa mzuri ni rahisi kuokoa pweza wanaoharibika au kubanikwa kwa kuni ili wasiharibike na kusababisha mazingira kuharibiwa. Mwakilishi huyo alisema utafiti wa shirika la chakula duniani ulibaini kuwa chakula kinachotoka baharini huaribika kwa asilimia 90 kila wakati na kuongeza kuwa jamii inakosa chakula bora cha lishe na kusababisha kuwapo hasara kwani hata soko lake halipo kutokana na kukosa ubora unaoatakiwa.Mratibu wa mradi huo Dk Modesta Merdad aliwaaeleza wajumbe hao kuwa kuna changamoto za mavuno madogo na wanaopatikana pweza ni wadogo. Alisema sanjari na kupoteza zao hilo la pweza kwa kuharibika na jamii nayo imeendelea kuwa masikini wakati ina fursa za kiuchumi kupitia zao hilo lenye soko nchi za Ulaya na kuongeza kuwa kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kitasaidia kuweka miundombinu ya kuhifadhia zao la pweza ambapo mlaji atahakikishiwa kuwa anapata chakula bora chenye viwango. Dk Merdad alisema mbali na kutoa mafunzo kwa wavunaji wa zao hilo jinsi ya kuhifadhi itasaidia kuongeza kipato cha wavunaji na kunyanyua uchumi wao. | kitaifa |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) imepanga ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, FA ambapo timu kongwe za Simba na Yanga zitaanzia Dar es Salaam.Kwa mujibu wa ratiba hiyo ya raundi ya tatu itakayoshirikisha timu 64 iliyotolewa na shirikisho hilo Dar es Salaam jana, Simba itaanza na AFC ya Arusha na Yanga itacheza na Iringa United ya Iringa, timu hizo zote zipo ligi daraja la kwanza. Mechi za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 20 na 24 mwaka huu.Bingwa wa michuano hiyo anaiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mara kadhaa Simba iliyotwaa ubingwa msimu wa mwaka 2016/17, huishia njiani kwenye michuano hiyo kwa kutolewa mapema. Iliwahi kutolewa kwenye hatua hiyo na Mashujaa na Green Worriers.Yanga iliwahi kuwa bingwa wa michuano hiyo msimu wa mwaka 2015/16, msimu uliopita iliishia nusu fainali baada ya kutolewa na Lipuli ya Iringa. Mabingwa watetezi Azam FC watacheza na African Lyon kwenye uwanja wake wa nyumbani ulipo Chamazi, Dar es Salaam.Timu mbili zenye historia kubwa na soka la Tanga, African Sports na Coastal Union zimepangiwa kukutana kwenye hatua hii mchezo ambao unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini. Ratiba ya mechi zingine inaonesha kuwa Mwadui FC itacheza na Mkamba Rangaer, Migombani na Mbeya City, Polisi Tanzania watavaana na Top Boys.Mechi zingine Tukuyu Stars itacheza na Singida Utd, Mbuni FC na KMC, Alliance na Transit Camp, Ndanda FC na Cosmopolitan. Mirambo FC na Ruvu Shooting, Mbao FC na Stand Utd, Nyamongo FC na Biashara Utd, Mpwapwa FC na Kitayosa Utd, Mawenzi na Mtwivila, Talinega na Friends Rangers, Ihefu na Kasulu Red Stars.Toto Africans na Gipco, Mighty Elephant na Mashujaa, Jeshi Worriors na Dodoma FC, Majimaji FC na Pamba FC, Panama FC na Area C Utd, Gwambina FC na Mbeya Kwanza, Pan African na Geita Gold. | michezo |
['Mchezo wa kamari unaendelea kuenea barani Afrika haswa miongoni mwa mashabiki wa soka. Ni biashara sasa iliyo na thamani ya mabilioni ya dola kwa kampuni zinazoendesha biashara hii, lakini si vile kwa wanaocheza, amebaini mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi.', ' Alipotembelea Katika chumba kimoja katikati mwa jiji la Nairobi, aliwapata vijana kadhaa wakiwa wamesimama wakitizama televisheni kwa umakini, huku wakiwa wameshilia risiti mikononi. Walikuwa ndani ya chumba cha kucheza kamari, kwa ajili ya kujaribu bahari yao. ', ' Mara nyingi mchezo wa kamari huchezwa kwa timu za kandanda za bara Ulaya , lakini kwa sasa msimu uko likizoni. Katika televisheni ni michezo ya kandanda bandia iliyotengenezwa kwa kompyuta, ambapo wachezaji wanakuwa ni vibonzo, lakini bado wanakamari wanacheza kutambua mshindi baina ya timu mbili bandia. ', 'Katika televisheni nyingine kuna mashindano ya vibonzo vya mbwa , lakini wachezaji hawajali, wanaendelea kubahatisha, anasema Omondi ambaye alitembelea kituo kimoja cha Kamari jijini Nairobi.', " Dommie, ni kijana ambaye hana kazi hufika kwenye kituo cha kamli kujaribu bahati yake: ''Sisi kama vijana tunajaribu kutafuta kazi hatuna, tumekuja kupata pesa ya rahisi hapa, sio eti nanajua nitapata nini, hii ni kubashiri tu'' ", ' Ahadi ya kupata ushindi mkubwa ndio kivutio kikubwa Zaidi kwa wachezaji hawa. Utafiti uliofanywa na kampuni ya Geopoll unaonyesha kwa taifa la Kenya ndilo linaloongoza barani afrika kwa wachezaji kamari. Asilimia 75 ya wakenya walio na umri wa chini ya miaka 35 wamewahi kucheza kamari. ', 'Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zinazoongoza kwa mujibu wa utafiti huo. Wengi wanacheza kwa urahisi kwa njia ya simu. Mmoja wao ni Justin Sanyo, ambaye anasema kuwa, japo ni mwanasayansi aliye na mshahara wake, hawezi akakosa kutenga kiasi cha mshahara wake kucheza kamari.', " ''Baadhi yetu wamechukua mchezo wa kamari kama kazi, na kwa wengine ni tabia ya kila siku. Ila tunafahamu kwamba kamari ni biashara, na wenye makampuni wanataka tupoteze fedha ili wapate faida. Kwa hivyo tahadhari ukiwa unacheza, uchague kwa makini sana timu utakazofanya nazo kamari''.", "Kwa kuwa uwezekano wa kupoteza pesa ni mkubwa kuliko wa kuzipata, kwa wasio na kazi kama Dommie, ni kuhatarisha hela zao kidogo walizo nazo. Alipoulizwa ikiwa ataweza kuuacha mchezo huo alisema: '' Huu ni mchezo ambao nimejiingiza, lakini usipende mtoto wako ajiingize kwenye mchezo huu, au mtu wako. Mimi nimesoma niko na vyeti vyangu vimelala nyumbani, wakinipatia kazi mimi nitaacha, lakini sasa nitaachacje mchezo huu wakati ninakuja kubahatisha''. ", 'Wachezaji kamari wameufanya mchezo huu kuwa biashara ya thamani ya mabilioni ya dola Afrika na ulimwenguni. Sasa serikali pia zinataka haki zao kwa njia ya kodi. ', 'Nchini Kenya makampuni ya kamari hutozwa asilimia 30 ya mapato kama kodi, lakini katika bajeti ya nchi iliyosomwa hivi karibuni, serikali imeongeza kodi nyingine ya asilimia kumi kwa kila hela ilayowekwa kama kamari ama dau. ', 'Kumaanisha kuwa mchezaji atatozwa hata kabla hajashinda chochote. Ikiwa hatua hii itawavunja moyo wachezaji au la, ni swala la kusubiriwa.'] | michezo |
MIKAKATI ya uboreshaji wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) umezidi kushika kasi baada ya kukamilika kwa ripoti ya pili ya upembuzi yakinifu.China imesema iko tayari kutoa fedha za kuboresha reli hiyo na kinachosubiriwa sasa ni mchakato unaoendelea baina ya Tanzania na Zambia kuhusu namna bora ya kuiboresha reli hiyo.Tazara inatarajia kupokea vipuri vya kuboresha reli hiyo kabla ya kufanyiwa marekebisho ya jumla walivyonunua kutokana na Sh bilioni 10 zilizotolewa na serikali ya Tanzania kuwasili mwezi huu.Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tazara, Timothy Kayani amesema katika uboreshaji, Tanzania na Zambia waliiomba China kuwasaidia kupata kampuni ya kufanya utafiti ili kubaini matatizo na mwongozo utakaotumika kuboresha.Alisema, China iliiteua kampuni ya Railway Survey and Design Institute (TSDI) iliyofanya upembuzi huo kwa mwaka mmoja na kuwasilisha ripoti ambayo baada ya Zambia na Tanzania kujadili ilikuwa na mapungufu na kuomba China kupitia upya.Amebainisha kuwa, kampuni hiyo iliendelea na mchakato na sasa wameishakabidhi ripoti ya pili ambayo itajadiliwa na pande zote ikifikiwa mwafaka itafanyiwa kazi na uboreshaji kuanza.“China imekubali kuboresha reli hii, lakini bado kuna makubaliano yanatakiwa kufikiwa na Tanzania, Zambia na China kwa kutumia ripoti hii ili uboreshaji kuanza,”alisema.Kayani alisema katika fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania Sh bilioni 10 kuboresha reli hiyo zimenunua vipuri vinavyotarajiwa kuwasili mwezi huu.Alieleza kuwa, fedha kama hizo zinatakiwa kutolewa pia na Zambia kwa kuwa ni makubaliano katika kuboresha reli hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi hizo mbili.Awali, Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa kumbukumbu ya raia wa China waliokufa wakati wa ujenzi wa Tazara wiki hii kuwa nchi yake iko tayari kuboresha reli hiyo ambayo ni alama ya ushirikiano kati ya China na Afrika.Alisema wanasubiri kukamilika kwa majadiliano na michakato baina ya Zambia na Tanzania kuhusu uboreshaji huo ili kuanza kazi.Mei mwaka jana, Tanzania ilitoa Sh bilioni kumi kwa ajili ya kuboresha reli ya Tazara nchini ili iweze kujiendesha kwa kusafirisha mizigo na abiria kati ya Tanzania na Zambia, kuzalisha faida na kuchangia ukuaji wa uchumi na pato la taifa kwa nchi mbili. | uchumi |
TANZANIA imeweka rekodi ya dunia kwa ukusanyaji wa mapato, yatokanayo na sekta ya uchimbaji wa madini, hatua inayotokana na usimamizi mzuri wa rasilimali hiyo, ikichangiwa na mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na serikali katika sekta hiyo hivi karibuni.Hayo yalielezwa jana na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk Hassan Abbas katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.Alisisitiza kuwa hatua hiyo, imetokana na utendaji kazi wa ‘kisayansi’ wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli. Dk Abbas alisema katika kipindi cha miezi 11 kuanzia Julai, 2018 hadi juzi, serikali imeweza kuingiza Sh bilioni 302.63 za mapato hayo, ikiwa imesalia mwezi mmoja mwaka kukamilika.Alisema katika kipindi cha mwaka 2017 na 2018, kiasi cha Sh bilioni 301 za mapato hayo zilikusanywa ikiwa ni pungufu kwa wastani wa Sh bilioni moja zilizopatikana hadi sasa kwa mwaka huu unaoishia Juni.Aidha, alisema mwaka 2015/2016 kiasi cha Sh bilioni 210 zilipatikana kwa kipindi hicho ikilinganishwa na Sh bilioni 302 za msimu huu, suala alilosema kuwa kwa kiasi kikubwa limeonesha mafanikio katika sekta hiyo. Alisema kukusanywa kwa kiasi hicho cha fedha, kabla ya hata kukamilika kwa mwaka, kunatokana na usimamizi mzuri wa serikali katika sekta hiyo muhimu, ulioendana na kuanzishwa kwa masoko ya madini, miezi mitano tangu Rais Magufuli aagize uanzishwaji wake.Alisema hadi sasa kuna jumla ya masoko 24 ya madini, yaliyoanzishwa ndani ya kipindi cha miezi mitano, ambayo kimsingi yameonekana kufanya vyema katika ukusanyaji wa mapato hatua inayotoa matumaini. | kitaifa |
['Real madrid inajiandaa kumtoa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,30, kwa pauni milioni 70 kubadilishana na mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling ,24. (Sky Sports)', 'Chelsea wana mshambuliaji wa Crystal Palace na mchezaji wa timu ya taifa Ivory Coast Wilfred Zaha,26 huku mshambuliaji wa RB Leipzig Tino Werner, 23, akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu wanaowawinda ikiwa marufuku dhidi yao itaondolewa. (Express)', 'Meneja wa Chelsea Frank Lampard, atakuwa na mpaka pauni milioni 150 kwa ajili ya dirisha dogo la usajili mwezi Januari ikiwa klabu hiyo itaruhusiwa kusajili wachezaji tena baada ya kuzuiwa kufanya hivyo.(Telegraph)', 'Manchester United na Liverpool wamehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Werner lakini klabu hizi za England zimeieleza RB Leipzig kuwa hazina nia ya kumfanya mshambuliaji huyo kuicha klabu yake.(Mirror)', 'Manchester United imemfanya kiungo wa pembeni wa West Ham Declan Rice,20, kuwa mchezaji wanayemtolea macho kwa kipindi kijacho cha majira ya joto. Lakini huenda akafikishwa kwenye klabu hiyo mapema mwezi Januari (Goal)', "Chelsea imeingia katika kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele,23, huku mchezaji huyo wa zamani wa Celtic macho yake yakiwa Manchester United.(Mail)", 'Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho angependa kuifundisha Bayern Munich, kwa mujibu wa kiungo Bastian Schweinsteiger.', 'Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 04.11.2019', "Wachezaji wa Barcelona 'kusaidia usajili' wa Neymar ", 'Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ni miongoni mwa walio kwenye orodha ya Bayern ya kushika nafasi ya Kocha wa zamani Niko Kovac, aliyeondoka kwenye klabu ya mabingwa hao wa Ujerumani.(Guardian)', 'Manchester United will itabaki bila kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba, 26, kwa karibu majuma mengine manne kwa sababu ya jeraha la kifundo cha mguu. (ESPN)', 'Wolves wanaandaa ofa ya kitita cha pauni milioni 13 kumnasa kiungo Dejan Kulisevski,23, ambaye pia amehusishwa na klabu za Manchester City na Arsenal.(Sport Witness)', 'Manchester United imekataa ofa ya pauni milioni 13 kutoka Roma kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling.(Star)', 'Tottenham imempa ofa mpya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Japhet Tanganga, 20, ili kumzuia asiondoke baada ya mkataba wake kukamilika majira yajayo ya joto.(Football Insider)', 'Wolves imeingia kwenye mbio sambamba na Watford na Newcastle zikimuwinda mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Royal Antwerp, Aurelio Buta 22.(Birmingham Mail)', 'Leicester imeanzisha mazungumzo na Club Bruges kuhusu uhamisho muhimu wa mshambuliaji Emmanuel Dennis,21, wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Leicester Mercury)', 'Leicester, Wolves na Everton wanamuwania winga wa Burnley Dwight McNeil, 19.(Teamtalk)', 'Newcastle na Leicester wanataka kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal Habib Diallo,24, kutoka klabu ya Metz ya Ufaransa. (Express)'] | michezo |
MKAZI wa kijiji cha Mkwapa kata ya Namatutwe wilayani Masasi mkoani Mtwara, Sandali Omari (40) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili (jina linahifadhiwa) anayesoma Shule ya Msingi Mkwapa, baada ya kumdanganya kumpa kilo moja ya korosho.Akizungumza na gazeti hili jana kijijini hapo, Mtendaji wa Kijiji cha Mkwapa, Mohamedi Dadi alisema tukio hilo ni la Novemba 17, mwaka huu saa saba usiku nyumbani kwa kijana huyo, ambaye alimchukua mwanafunzi huyo na kwenda naye kwake, akimdanganya kuwa atakwenda kumpa kilo moja ya korosho.Siku ya tukio, mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kwao akiwa na wenzake na kwenda kwenye sherehe ya unyago katika nyumba jirani, ambako lilikuwa linapigwa disko la kunogesha sherehe hiyo.Wakati mwanafunzi huyo akicheza disko, alikutana na mtu huyo ambaye alimshawishi kwenda naye nyumbani kwake mara moja ili akampe korosho, zimsaidie kupata fedha za matumizi ya shule na kwamba wangerejea baadaye kucheza disko.Kwa sasa bei ya korosho huko ni Sh3,300. Mtendaji huyo wa kijiji alisema baada ya mtuhumiwa huyo kufanikiwa kudanganya, mwanafunzi huyo alikubali kwenda naye, lakini alipofika chumbani kwake alimtishia kwa kitu chenye ncha kali na hatimaye kumbaka."Wakati mbakaji akiwa na mwanafunzi, pale disko baadhi ya vijana walishuhudia tangu alipokuwa amesimama karibu naye na kuanza kumdanganya kuwa anakwenda naye nyumbani kwake ili akampe korosho na wakati anaondoka naye na wao walimfuatilia na kugundua baadaye kuwa alikuwa anambaka," alisema Dadi.Baada ya kugundua hivyo, walikwenda Shule ya Msingi Mkwapa anakosoma mwanafunzi huyo na kumueleza tukio hilo mwalimu mkuu, ambapo naye alikwenda nyumbani kwa Mtendaji wa Kijiji na kumuelezea mkasa mzima.Alisema baadaye kwa pamoja viongozi wa kijiji, mwalimu mkuu na mgambo walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kumkuta akiwa amelala kitandani, akiwa tayari ameshamtoa mwanafunzi huyo baaada ya kumaliza kumbaka.Alisema walifanikiwa kumkamata usiku huo huo na kumfungia katika ofisi ya kijiji na asubuhi walikwenda naye Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Masasi, ambako anashikiliwa hadi sasa.Baba mzazi wa mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa), akizungumza na gazeti hili baada ya tukio hilo, aliiomba serikali kulishughulikia kwa mujibu wa sheria. "Mwanangu bado ni mdogo sana halafu amefanyiwa kitendo cha kinyama, kwa vile tumeshafika hospitali na kuthibitisha kuwa na michubuko ya kuingiliwa, mimi naisubiri serikali kutenda haki juu ya hili, napongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtuhumiwa," alisema Mahmudu.Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi, alikiri kupokea taarifa hizo na kuvitaka vyombo vya sheria kuchukua hatua za kisheria kwa mhusika. | kitaifa |
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji hili, Juma Idd wakati alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, miundombinu ya soko hilo kwa sasa imechakaa na imefikia mwisho wa uhai wake.Idd alisema, soko hilo halifai kukarabatiwa hivyo hatua iliyopo ni kubomolewa na kujengwa soko jipya litakalokuwa na miundombinu bora kuliko ilivyo sasa.Alisema wanamalizia uboreshaji wa miundombinu ya Soko la Shuma lililopo kata ya Elerai ambalo kuanzia sasa litakuwa likitumika kushushia bidhaa zote zikiwemo matunda, samaki na vitunguu, na wafanyabiashara watakuwa wakitumia magari madogo kubeba bidhaa zao hadi soko la Kilombero.Mkurugenzi huyo alisema, magari yote ya mizigo ya biashara hayaruhusiwi kushusha wala kupakia mizigo ndani ya soko la Kilombero na hayo ni maandalizi ya kulibomoa soko hilo ili lijengwe upya.Akijibu swali la kuondoa harufu ya maji taka na uchafu inayotoka kwenye chemba za kusafirishia maji taka na kusambaa maeneo mbalimbali ya jiji, alisisitiza kuwa hilo ni jukumu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Arusha (AUWSA).Alisema AUWSA inapochelewa kushughulikia uondoaji wa maji taka Halmashauri ya Jiji imekuwa ikiwatoza faini ambayo ni adhabu kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao.Aliongeza kuwa, AUWSA imekamilisha mchakato wa kupata mkopo wa fedha Sh bilioni 200 kwa ajili ya kukarabati miundombinu yake ikiwemo usafirishaji wa maji taka, kuhamisha mabwawa ya maji taka kutoka eneo la Lemara kuyapeleka Terat kwenye eneo lililotengwa. | uchumi |
WAKATI Yanga ikiingia kimya kimya jijini Tanga kwa ajili ya mechi yake na Coastal Union katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wapinzania wao wamesema, wamejiandaa kupambana na kuwafunga vinara hao.Ikitumia njia ya barabara, Yanga iliingia saa nne usiku jijini Tanga kimya kimya na kufikia katika hoteli ya Tanga Beach Resort moja ya hotel zenye gharama kubwa jijini hapa iliyopo eneo la Sahare pembezoni mwa ufukwe wa Bahari ya Hindi.Kama kawaida yake ikija Tanga kwa njia ya barabara, timu hiyo imekuwa ikisimama katika matawi yake ya Korogwe, Hale, Muheza na Pongwe jijini hapa, na kupata nafasi ya kusalimiana na wanachama wake.Katika matawi yote ,Tawi la Muheza ndiyo tawi ambalo hutegemewa na timu hiyo katika maandalizi yote ya timu hiyo inapokuja Tanga. Jana Jumamosi asubuhi timu hiyo ilifanya mazoezi yake katika Uwanja wa shule ya Sekondari Galanos na jioni ilitarajia kufanya kwenye Uwanja wa Mkwakwani.Akiongea na Mwandishi wa gazeti hili Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda alisema kuwa kikosi chake hakina majeruhi na wamejipanga kupambana na Yanga kuhakikisha wanatoka na ushindi.“Kikosi changu kimejipanga kucheza na Yanga na hakuna mchezaji yoyote majeruhi na tumejipanga kupambana na Yanga na kushinda, “alisema.Katika mchezo huo wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo Coastal Union watakuwa wenyeji ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, walifungwa.Yanga ambayo kwa muda sasa inaongoza msimamo wa ligi hiyo, haitakubali kupoteza mchezo mwingine wa Ligi Kuu baada ya ule wa mwisho kufungwa 1-0 na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kabla ya kusonga mbele katika Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Biashara United kwa penalti 5-4 jijini Dar es Salaam. | michezo |
MREMBO na mfanyabiashara wa Uganda, Zari Hassan ‘The Boss Lady’, amejinunulia zawadi ya nyumba nchini Afrika Kusini anakoendesha maisha yake kwa sasa katika kumbukizi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari ambaye ni mama wa watoto watano, wawili akiwa amezaa na mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Nassib Abdul maarufu Diamond Platinumz ameandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa kuongeza miaka.Ujumbe huo umepokewa kwa maoni tofauti katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakimpongeza mwanamke huyo na kumtakia maisha marefu na yenye furaha. Katika ujumbe wake huo, Zari aliandika: “Asanteni kwa wote ambao mmeniletea zawadi kuelekea Birthday yangu, nimejizawadia mwenyewe nyumba mpya, nashukuru kwa baraka za kuona naongeza mwaka mwingine, sina cha kukulipa Mungu. Asante kwa neema zako”. Miaka 39 iliyopita, Septemba 23, ndiyo siku mwanamama huyo mwenye asili ya Uganda alizaliwa na jana Septemba 22 aliwaalika ndugu, jamaa na marafiki katika sherehe za awali kwa ajili ya kupata chakula na vinywaji nchini humo. | michezo |
MIPANGO madhubuti inayoendana na utendaji bora, utoaji huduma bora kwa wananchi, na ukusanyaji mapato umeifanya serikali ya awamu ya tano kufufua na kuimarisha mashirika ya umma ambayo yalikuwa goigoi na sasa yanatoa gawio kwa serikali.Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas alisema serikali ya awamu ya tano ndani ya kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2015 ilipoingia madarakani, imefanya mageuzi na mabadiliko na yaliyokuwa ndoto kutimia.Amezitaja baadhi ya taasisi na kampuni za umma ambazo zimeinuka na kujiendesha zenyewe na nyingine kutoa gawio kwa serikali ni TRA, Tanesco, Bodi ya Mikopo, Benki ya TIB na Wakala wa Ununuzi serikalini.Kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Abbas amesema imeendelea kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya kodi nchini.“Kwa mujibu wa takwimu za hadi Desemba 31, mwaka jana, ambayo ni nusu ya mwaka wa bajeti, ilikusanya shilingi trilioni 7.99 sawa na ongezeko la ukuaji wa asilimia 2.01. Mwezi Desemba pekee mwaka jana, TRA ilivunja rekodi ya mwaka mzima kwa kukusanya Sh trilioni 1.63,” amesema.Dk Abbas amesema miaka michache iliyopita Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilisifika kwa gharama kubwa za uendeshaji na kutegemea ruzuku, lakini tangu serikali hii iingie madarakani limeanza kuwa na ufanisi.“Kati ya mwaka 2014 na 2015, Tanesco ilikuwa ikipokea shilingi bilioni 354 na bilioni 163 mtawalia. Lakini umakini wa serikali ya sasa wa kukata mizizi ya ufisadi ikiwemo kuzima mitambo ya kutumia umeme ghali wa mafuta hatimaye tangu 2016/17 haipokei fedha zozote za serikali,” amesema Dk Abbasi.Amesema mwaka 2015, serikali ilitoa Sh bilioni 354 kwa ajili ya kuendesha shirika hilo na mwaka 2016 fedha zilipungua hadi bilioni 163, lakini hadi sasa shirika hilo halitegemei ruzuku ya walipa kodi kujiendesha. | uchumi |
['Manchester City imeanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa kimataifa wa England Raheem Sterling, 24. (Mirror)', 'Mkufunzi wa Leipzig, Julian Nagelsmann na Jose Mourinho wanapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino, aliyefutwa kazi kama mkufunzi wa Tottenham. (Star)', 'Wengine ambao wamejumuishwa katika orodha hiyo ni Eddie Howe wa Bournemouth na Carlo Ancelotti wa Napoli ambao huenda wakapata kazi katika uwanja wa Tottenham Hotspur. (Sun)', 'Fidia itakayolipwa na Tottenham kwa kumfuta Pochettino na wafanyikazi wake huenda ikafikia £19.6m kiwango ambacho Manchester United ilimlipa Jose Mourinho na timu yake mwezi Disemba 2018. (Mirror)', 'Pochettino alifutwa kazi kufuatia malumbano kati yake na wachezaji katika chumba cha kubadilisha nguo hali ambayo ilifikia kiwango cha kuathiri utendakazi wake. (Mail)', 'Pochettino alikataa ombi la Daniel Levy la kumtaka ajiondoe hatua ambayo ilimfanya mwenyekiti wa Spurs chairman kumfuta kazi siku ya Jumanne. (Telegraph)', 'Red Devils huenda wakalipa hadi £85m kumsaini mshambuliaji wa Salzburg na Norway mzaliwa wa Leeds-Erling Braut Haaland, 19. (Standard)', 'Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Reading Danny Loader, 19, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)', 'Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, amepuuzilia mbali tetesi kuwa alitoa wito kwa Blues kutomsajili mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero kabla ahamie Manchester City. (Mirror)', 'Swansea na Stoke zinamtaka winga wa Celtic wa miaka 32- Jonny Hayes mkataba wake unapoelekea kukamilika. (Scottish Sun)', 'Robert Moreno anatarajiwa kutoa kauli yake kuhusu hatma yake kama kocha wa Uhispania baada ya hatua ya mkataba wake kuvunjwa. (AS - in Spanish)', 'Wachezaji wa Manchester United wameombwa kutotoka nje kwa zaidi ya dakika kumi watakaposafiri kucheza na FC Astana katika ligi ya Europa kutokana na hali ya baridi kali nchini Kazakhstan. (ESPN)'] | michezo |
LICHA ya vyombo vya Habari vya Tanzania kuibuka kinara kwa kuwa nchi ya kwanza kuripoti matukio ya kupinga ukatili wa kijinsia katika nchi mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), bado imekumbwa na changamoto kubwa za kutafsiri sera.Hayo yalielezwa jana katika jukwaa la Protokali la Jinsia na Maendeleo kwa nchi za SADC lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kutathmini mikataba mbalimbali ambayo nchi 15 wanachama wa jumuiya hiyo wameridhia katika upande wa sera na mipango mbalimbali ambayo nchi imeweza kujidhamini kuwa itatekeleza.Akizungumza kwenye jukwaa hilo, mmoja wa majaji kutoka Gender Links, Dk Geofrey Chambua alisema lengo ni kutambua jitihada za makundi au watu binafsi katika kuendeleza usawa wa kijinsia Tanzania, hatua ya kwanza ilishafanyika kupitia asasi za kiraia ambapo walipitia madodoso mbalimbali ikiwemo ya maeneo ya uchumi, afya, mazingira, tabia nchi na maeneo mengine.Alisema changamoto kubwa kwa Tanzania ni kutafsiri sera katika rasilimali na kwamba mwaka 2017 na 2018 walitengeneza mkakati kuondoa ukatili wa wanawake na watoto unaoisha mwaka 2022 Chambua alisema changamoto kubwa ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake, rasilimali zake zinatakiwa kutoka serikali za mtaa, hata hivyo haijapangiwa bajeti ya kutosha.“Nchi yetu imeshajigeuza kimfumo kutoka kwenye uchumi wa chini hadi wa kati, ukisikia kauli mbiu ya kimataifa kupitia maendeleo endelevu mtu yeyote asiachwe nyuma, bado kundi la wanawake na watoto wanaachwa nyuma,”alisema Chambua.Alisema kundi hilo la wanawake limeachwa nyuma kutokana na kulimbikiziwa majukumu mengi ya nyumbani yanayofanya washindwe kushiriki katika fursa za kiuchumi.“Ufikiaji wa rasilimali kutokana na mfumo dume uliojikita kwenye nchi yetu kwa muda mrefu, wanawake wamekuwa na changamoto ya kufikia rasilimali kama mitaji, ajira, ngazi za amuzi, mikopo hata katika uchumi mkubwa ni changamoto ambayo tunahitaji kuifikia,” alisema. | kitaifa |
WAZIRI wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amezitaka kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kuongeza michango ya fedha na huduma kwa jamii inayozunguka mapori ya akiba nchini.Akizungumza na watendaji wa Taasisi ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) inayomiliki kampuni za uwindaji wa kitalii, katika maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Simiyu, Dk Tizeba amesema kuna kampuni zinapata fedha nyingi lakini uchangiaji jamii ni ndogo."Nyie najua mnafanya vizuri lakini wenzenu katika maeneo mengine hadi wamefikia hatua ya kuwachagulia miradi wananchi," amesema.Ofisa Uhusiano wa FCF, Clarence Msafiri amesema kampuni zilizo chini ya taasisi hiyo zimekuwa zikitoa kwa jamii asilimia 20 ya mapato yao kila mwaka.Alisema kampuni zao ikiwepo Mwiba Holding na TGTS na walizowekeza wilayani Meatu pori la Akiba la Maswa na Makao, licha ya kutoa michango ya kijamii pia kwa mwaka wanatoa kwa vijiji zaidi ya Sh milioni 610 kama kodi ya pango.Meneja ujirani Mwema wa kampuni ya Mwiba Holdings, Alfred Mwakivike alisema kampuni hiyo kabla ya kusaidia miradi imekuwa ikipata maelekezo ya halmashauri.Alisema miradi wanayoitekeleza ina thamani zaidi ya Sh bilioni mbili na yote imeidhinishwa na Halmashauri ya Meatu.Taasisi ya Friedkin inashiriki Maonesho ya Nanenane kwa mara ya kwanza kuhamasisha uhifadhi, kupiga vita ujangili na pia kuonesha umuhimu wa uhusiano wa uhifadhi na kilimo. | uchumi |
BAADA ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa na timu nne kwenye michuano ya klabu Afrika, Simba imesema ilikuwa siku ya kihistoria kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuongeza alama ambazo zimeiwezesha nchi kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2019/2020. Kwa mujibu wa TFF, Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limethibitisha kuwa pointi 12 ambazo zimepatikana zimesaidia nchi kuongezewa timu mbili hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa hivyo zitakwenda Simba na Yanga huku shirikisho zikienda Azam FC na KMC. Simba wameweka ujumbe kwenye mtandao wa Instagram, ikionesha kumbukumbu ya siku walipoitoa AS Vita na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliosomeka “Ilikuwa siku ya kihistoria kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuongeza alama ambazo zimeiwezesha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2019/2020”. Ujumbe huo ulimalizika kwa maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ambayo ni “SIMBA IKISHINDA, TANZANIA IMESHINDA”. Naye mwekezaji wa Simba ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri Afrika, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa “Tunajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa, na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa kimataifa kwa maslahi ya klabu na nchi yetu. Hongera kwa Wanasimba kwa kazi kubwa tuliyoifanya, tunastahili pongezi”. Timu mbili zitashiriki katika Ligi ya Mabingwa na timu mbili nyingine zitashiriki Kombe la Shirikisho na nafasi hiyo kwa Tanzania imekuja baada ya kuwa katika nafasi 12 bora kwenye viwango vya ubora vya CAF.Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu zilizofanyiwa marekebisho na Kamati ya Utendaji baada ya kupatikana nafasi nne (4), timu za Tanzania zitakazowakilisha kwenye mashindano hayo ni Simba na Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa (CAF CL), Azam FC na KMC Kombe la Shirikisho (CAF CC). KMC itawakilisha Kombe la Shirikisho kwa mujibu wa kanuni hiyo, ambayo inatamka kama timu iliyomaliza nafasi ya tatu itakuwa ndio bingwa wa Kombe la FA, basi mshindi wa nne anapata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho kwa sababu bingwa wa FA anaiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo. Tayari CAF imefungua dirisha kwa mashirikisho kusajili timu kupitia mtandao wa CMS na mwisho wa usajili ni Juni 30 ambapo TFF inatakiwa iwe imesajili timu zitakazoshiriki kwenye mashindano ya Kimataifa msimu wa 2019/2020. | michezo |
['Vioja vya shabiki sugu wa timu ya taifa Tanzania katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika - Bongo Zozo amewaacha wengi hoi katika mitandao ya kijamii nchini humo baadhi wakiguswa na ushabiki wake kwa timu hiyo.', ' Ametoa matumaini kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo licha ya kipigo cha 2-0 walichopokea Taifa Stars katika mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri dhidi ya Senegal siku ya Jumapili.', 'Bongo Zozo, kama anavyojiita katika mitandao ya kijamii ikiwemo You Tube, anaonekana katika mojawapo ya kanda ya video iliosambaa mitandaoni akitembea mjini Cairo akiwa amevaa jezi huku akipeperusha bendera ya Tanzania huku akizungumzwa kiswahili na mashabiki wengine wa Tanzania.', 'Nchini kwenye Tanzania kwenyewe, picha zake zimesambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwemo hata makundi ya Whatsapp.', 'Baadhi wakifurahia namna Bongo Zozo anavyozungumza kiswahili na kuimba wimbo wa taifa.', 'Ni swali wanaloniuliza watu wengi "Mzungu mswahili ametuzidi uzalendo" baadhi wakiandika katika mitandao ya kijamii.', 'Bongo Zozo - ambaye jina lake halisi ni Nick Reynolds - alizaliwa Zimbabwe na kuwahi kuishi Tanzania kabla ya kuhamia Uingereza.', 'Ameeleza kwamba anazipenda Tanzania na Zimbabwe mataifa yalio karibu sana moyoni mwake.', '"Mimi ni shabiki wa timu mbili Ya Zimbabwe na timu ya Tanzania\'', 'Anasema anaishabikia Zimbabwe sababu ndiko alikolizaliwa Zimbabwe, na Tanzania kwa upendo alio nao kwa taifa hilo. ', "'Napenda na navutiwa sana na mpira wa Afrika lakini sanasana mpira wa Tanzania, sababu kuna fujo isiyoumiza. Yaani watu tuna kelele sana kuliko (mashabiki wa timu nyingine) watu.'", 'Hatahivyo anaongeza kuwa Kenya pia ni timu anayoishabikia kwasababu zote ni timu za Afrika mashariki kiashiria cha kwamba watu wote ni wamoja.', '"Nimeishi Tanzania kwa muda wa miaka kumi na minane tangu mwaka 98 hivi, nilikutana na mwanamke nikamuoa alafu basi nimekuwa Mtanzania," amesema.', 'Anasema anafurahia sana Tanzania kufuzu katika mashindano ya kombe la mataifa mwaka huu baada ya kusubiri kwa miaka 39."', 'Je kura anaitupa wapi katika mpambano wa Alhamisi wa Taifa stars dhidi ya Harambee stars ya Kenya?', "'Tanzania lazima tuwakung'ute (Kenya)'.", "'Sema nitalia machozi hata ya damu kama ni droo - sababu kama tunashindwa kuwafunga Kenya, naombeni mutufunge sababu ikiwa droo basi hatufuzu sisi (Tanzania) na Kenya haiwezi kufuzu' anaeleza Nick."] | michezo |
CHIPUKIZI wa Azam FC, Shaban Idd ‘Chilunda’ anaondoka katika timu hiyo lakini kocha wa Azam, Hans van Pluijm amesema hakuna tabu kwa kuwa tayari yupo Mzimbabwe, Donald Ngoma. Chilunda anaondoka baada ya kuchukuliwa na timu ya Tenerife ya Hispania.Timu hiyo imeshawishika kumtwaa mchezaji huyo kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha msimu uliomalizika wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Kagame akiisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.Pluijm ambaye amejiunga na Azam akitokea Singida United, alisema kuwa Chilunda anaondoka akiwa bado mdogo na anahitajika Azam, kitu ambacho ni kizuri kwa mchezaji huyo lakini haina budi kwenda kuendeleza kipaji chake akiwa ameacha pengo katika timu hiyo.Hata hivyo, amepiga moyo konde na kusema uwepo wa mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Ngoma aliyetua akitokea Yanga atarekebisha kila kitu na mambo yatakuwa sawa kwa kuwa uwezo wa mshambuliaji huyo unafahamika.“Chilunda ni mchezaji mzuri mno, anapambana na anajua kufunga. Ameondoka wakati timu bado inamuhitaji lakini hata hivyo wakati yeye anaondoka, kuna ujio wa Ngoma ambaye naye ni mzuri pia na kila mmoja anafahamu shughuli yake, kwa hiyo nafikiri kazi itaendelea kama kawaida,” alisema Pluijm.Pluijm ametua na upepo mzuri katika kikosi hicho baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kutetea ubingwa wa Kombe la Kagame kwa kuifunga Simba mabao 2-1. Bao moja lilifungwa na Chilunda. | michezo |
RAIS John Magufuli amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu ya dini nchini katika kutoa huduma za jamii kwa wananchi, ikiwemo elimu na afya.Hayo yamebainishwa jijini Mwanza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana aliyemwakilisha Rais Magufuli kwenye Ibada ya Misa Takatifu ya Kumsimika Mhashamu Renatus Nkwande kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.Kabla ya kuja Mwanza, Askofu Mkuu huyo alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda na Baba Mtakatifu Francis amemteua kuendelea kuwa Msimamizi wa Jimbo hilo.Akisoma hotuba hiyo ya Rais, Waziri Mkuu alisema serikali na madhehebu ya dini hayana budi kwenda kwa pamoja katika kutoa huduma za jamii kwa Watanzania licha ya viongozi hao wa dini kuwa na majukumu ya ziada ya kiroho.“Ukitaka kwenda haraka tembea peke yako, lakini ukitaka kwenda umbali mrefu, tembea na wenzako, hivyo kwa upande wetu kama serikali tunahitaji kutembea kwa pamoja na madhehebu ya dini kwa lengo la kufikia mafanikio mbalimbali ya kijamii,” alieleza Majaliwa.Kuhusu kudumisha amani nchini, Waziri Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa dini kupitia mafundisho yao wahakikishe wanadumisha amani na utulivu kwenye nyumba za ibada, jamii na taifa kwa kuwa haitarajiwi viongozi hao kuwa chanzo cha migogoro na vurugu za aina yoyote.Aliwapa wito wa kuendelea kuhubiri huruma, msamaha na upendo kwa watu.Alisema mbali na kuhubiri neno la Mungu, viongozi wa dini pia wanapaswa kuwasisitiza waumini wao na Watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua na umasikini.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, serikali itayafanyia kazi makatazo yaliyotolewa na Askofu Mkuu Nkwande kuhusu kupambana na vitendo vya ushoga na utoaji mimba bila kusita na kuongeza kuwa wananchi wanatakiwa kutoa taarifa wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.Akizungumza awali, Nkwande aliwataka Watanzania kutokuiiga mambo ya hovyo ukiwemo ushoga na utoaji mimba.Alisema kuna baadhi ya taasisi zinazohamasisha mambo hayo na wakati mwingine serikali ikisita kuchukua hatua ya kuyadhibiti.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alichangia mifuko 400 ya saruji na Sh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa Kuu na makazi mapya ya Askofu Nkwande unaoendelea katika eneo la Kawekamo.Nkwande anakuwa Askofu wa tano wa Jimbo Kuu la Mwanza lakini pia ni Askofu Mkuu wa tatu wa jimbo hilo akitanguliwa na Hayati Anthony Mayala na Askofu Mkuu Mwandamizi, Yuda Thadeus Ruwa’ichi aliyehamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. | kitaifa |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amewataka wanawake nchini kujitokeza wenyewe kuzitumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo za uongozi na kutosubiri kupelekwa jambo linaloleta mafanikio kitaifa na hata kijamii kwa ujumla.Alisema tafiti mbalimbali zinabainisha kuwa kampuni au taasisi zilizofanikiwa ni kwa sababu ya wanawake kushika nafasi za juu za uongozi, wakijitahidi kutatua migogoro isiyo na tija kazini na hata kuondokana na matatizo ya wafanyakazi.Mhagama alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 pamoja na mahafali ya pili ya programu ya mwananke wa wakati ujao ulioandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE).Mkutano huo ni moja ya jitihada za kuhakikisha idadi ya wanawake katika nafasi za juu za uongozi inazidi kuongezeka pia wanawake kuwa na idadi kubwa ya uwakilishi katika bodi za wakurugenzi na makampuni mbalimbali.Wanawake 25 kutoka kampuni na taasisi 16, wamepewa mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo katika kuongoza kwenye nafasi za juu na kuleta matokeo makubwa katika maeneo yao pasipo kuathiri majukumu binafsi.Kuhusu uwezo wa wanawake, Mhagama alisema ni vyema wanawake wakatambua nguvu yao kitaifa na hata kijamii hivyo wajitokeze wenyewe pindi wazionapo fursa katika nyanja tofauti tofauti.“Tumieni fursa zilizopo, ziwe kubwa ama ndogo, usingoje kupelekwa kwa kila fursa inayojitokeza kwani unaposubiri wanaokwenda kwa wingi ni wanaume,” alisema Mhagama na kuongeza kuwa kiongozi mwanamke ni mwenye sifa ya kuthamini kazi yake pamoja na wenzake lakini pia wakiweza kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja.Alisema ni muhimu wanawake wakaaminiwa kuwa wanaweza kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kiwango kikubwa, kwani anapokuwa na madaraka huwa na ndoto kubwa lakini pia wakiweza kumudu hali yoyote ya kikazi mahali popote | kitaifa |
WASANII wakiwemo mwigizaji Wema Sepetu, Msaga Sumu, Juma Nature wanatarajiwa kumuaga beki na nahodha mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro ' katika bonanza la michezo litakalofanyika Agosti 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.Akizungumzia bonanza hilo Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema kutakuwa na mechi itakayochezwa saa 8.00 mchana kati ya timu ya wanawake ya Yanga Princess dhidi ya Kombaini ya Morogoro itakayosimamiwa na mhamasishaji Sepetu.Alisema saa 10:00 jioni kutakuwa na mechi kati ya Yanga dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Kwanza ya Mawenzi yenye wachezaji wengi waliowahi kucheza na Canavaro, akiwemo Abdi Kassim 'Babi' na wengine."Tumealika wasanii mbalimbali kama Billnas, Lulu Diva, Gigy Money, Mr. Bluu, Msaga Sumu, Doro Richeon kutoa burudani ya kumuaga Canavaro. Tunawaomba wanachama na mashabiki kujitokeza kwa wingi kusherehekea, "amesema na kuongeza kuwa, mechi hiyo itakuwa pia ni sehemu ya maandalizi ya ligi na michuano ya kimataifa.Amesema siku hiyo itajulikana mchezaji mrithi wa jezi ya Canavaro namba 23. Viingilio vya mchezo huo ni Sh 10, 000 kwa VIP na 5,000 kwa viti vya kawaida. | michezo |
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema wanarudi nyumbani kujifunza na kuendeleza vipaji vya soka vilivyopo.Stars ilikuwa mjini hapa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, Afcon na kupoteza mechi zote tatu za kundi lake. Ilianza kufungwa na Senegal mabao 2-0 kabla ya kufungwa na Kenya 3-2 na kufungwa na Algeria 3-0.Akizungumza baada ya mechi ya Algeria juzi, Amunike alisema watarudi Tanzania kujifunza makosa yao na kujipanga upya. “Mechi ilikuwa nzuri, tulipata nafasi lakini hatukuzitumia na tulifanya makosa ambayo Algeria waliyatumia kutuadhibu,” alisema. “Uzoefu ni muhimu sana kwenye mashindano ya aina hii, kwenye soka wakati mwingine kuna nafasi huna mara moja kila la heri Algeria katika hatua zinazofuata”.Stars imeshiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39. Amunike alisema Tanzania haikuwa tayari kushindana kwenye fainali hizi licha ya kufuzu. “Tulikuwa tayari kufuzu maana hapa hatukuja kama waalikwa tumekuja kwasababu tumefuzu lakini hatukuwa tayari kushindana”.Baada ya mechi za juzi, timu zilizofuzu hatua ya mtoano ni Misri, Uganda, Algeria, Senegal, Madagasca, Nigeria, Morocco na Ivory Coastal. Timu nyingine zilitarajia kujulikana baada ya mechi za jana usiku ambapo pia timu nne zitakazoingia hatua ya mtoano kama best loser pia zilitarajia kujulikana. | michezo |
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ataufanyia marekebisho makubwa uwanja wa ndani wa Taifa ili uwe wa kisasa zaidi na uendane na hadhi ya nchi yetu.Hayo aliyasema wakati akifunga mashindano ya mpira wa kikapu ya vijana ya Kanda ya Tano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa. Mashindano hayo yalianza Juni 17 na kumalizika Juni 22.Rwanda ndio waliibuka wababe wa mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Dunia, Fiba, kwa vijana hao wenye umri huo.Mshindi wa pili aliibuka Uganda kwa wavulana na wasichana na mshindi wa tatu Tanzania, huku Sudan ikishika nafasi ya nne, wachezaji bora ni Kazeneza Emil na Ofeastine Mwizera kutoka Rwanda.Timu nne za Tanzania, Uganda, Rwanda na Sudan ndizo zilizoshiriki fainali hizo za vijana zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini.Akizungumza Dar es Salaam, Mwakyembe alisema kuna kazi kubwa ya kufanya juu ya mapinduzi ya michezo nchini, kwani kila taifa nje na ndani ya Afrika linatamani kuleta michezo nchini, lakini miundombinu sio rafiki.Aidha, alisema wao kama Wizara wameliona hilo na baada ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti watakaa na kuanza kulifanyia kazi hasa hili la viwanja vya mpira wa kikapu kwa kuanza na kuukarabati uwanja huo wa ndani wa Taifa na kuanza kujenga vingine vipya.“Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini (TBF) mmejitahidi sana kwa maandalizi na hatua mliyofikia licha ya timu zetu kufanya vibaya na kushindwa kutwaa vikombe, lakini mmeonekana uzalendo mkubwa, sisi Wizara tuko tayari kuwasaidia, “alisema Mwakyembe.Hatahivyo, Rais wa Fiba Kanda ya Tano ya Afrika, Zobe Hasheem Al Hariri alisema amevutiwa na mwamko ulionekana kwa vijana juu ya mchezo wa kikapu licha ya kufanyika kwa mara ya kwanza.Alisema baada ya Tanzania kuandaa vizuri mashindano hayo, sasa wakati umefika kwa Fiba Kanda yaTano kuleta mashindano ya wakubwa katika ukanda huo.Rais wa TBF, Phares Magesa alisema wanashukuru wadau wote waliowaunga mkono kufanikisha maandalizi ya fainali hizo akiwemo Waziri Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Hasheem Thabit, Saintary Hospital, Diaspora, Jumuiya ya Waliosoma India na Kampuni ya rangi nchini, Kiboko.Aliwataka wadau wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi kusaidia kuendeleza mchezo huo, kwani wao wamejipanga vizuri kuhakikisha mchezo huo unasonga mbele. | michezo |
NCHI za Kiafrika zimeiomba China kuhakikisha kuwa ufadhili ama mikopo inayotoa kwa nchi hizo inalenga katika miradi ya kikanda itakayoziunganisha na kuzinufaisha nchi hizo kiuchumi.Tanzania imeitaka China kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inayowekeza nchini iwe ya manufaa kwa pande zote mbili.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi aliyasema hayo Beijing, China katika mkutano wa waratibu wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika (FOCAC) alipopata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo.Alisema endapo China itazisaidia kwa ufadhili ama kwa mikopo nafuu kuwekeza katika miradi hasa ya miundombinu itakayoziunganisha nchi za kiafrika kwa kiasi kikubwa itazisaidia nchi hizo kufanya biashara zenyewe kwa zenyewe itaziwezesha kupiga hatua za kimaendeleo na kiuchumi na hivyo kujitegemea.Aliongeza kuwa mkutano huo wa FOCAC umekuwa ni wa manufaa kwa kuwa nchi zenyewe za kiafrika zimepata fursa ya kutaja baadhi ya miradi ya kipaumbele kutokana na uhitaji wa nchi husika huku akiitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji kwa kuwa nchi nyingi za Kiafrika bado zina vyanzo vingi vya maji vinavyoweza kuzalisha umeme ambao utakuwa ni wa bei nafuu na kusaidia katika ujenzi wa viwanda.Aidha katika mkutano huo wa siku mbili nchi 53 za Kiafrika zimeitaka China pia kuhakikisha inasaidia ama kufadhili katika kuinua uwezo wa kitaaluma utakaowawezesha vijana kwa Kiafrika kujiajiri na kupata wataalamu wabobezi katika masuala mbalimbali kutokana na uwekezaji hasa wa viwanda na miundombinu utakaofanywa kwa pamoja na China na nchi za Kiafrika.Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Profesa Kabudi alisema Tanzania imesisitiza kuwa katika miradi ya uwekezaji ya misaada ama ile ya mikopo nafuu inayoelekezwa Tanzania iwe ni ile yenye manufaa kwa pande zote mbili kama anavyosisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli. | kitaifa |
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kirando, Dk Gideon Msaki alisema iliwachukua zaidi ya saa sita kuokoa maisha ya Joyce kufuatia huduma ya dharura ya upasuaji waliyomfanyia ikiwa ni pamoja na kumuongezea uniti nne za damu."Naendelea vizuri....nampenda sana mtoto wangu,” anasema kwa taabu Joyce Kilinda (32) anayesadikiwa kurarua tumbo lake kwa ‘wembe’ na kumtoa mtoto wa kike akiwa hai, wakati alipoulizwa na mwandishi kuhusu hali yake juzi. Mwanamke huyo amehamishiwa hospitali Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga kwa matibabu zaidi. Kuendelea kuimarika kwa hali ya mwanamke huyo kumetokana na juhudi kubwa za saa sita za kuokoa maisha yake zilizofanywa katika kituo cha afya Kirando baada ya kumpokea akiwa hajitambui na kupoteza kiasi kikubwa cha damu. Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Boniface Kasululu, mzazi huyo alifikishwa katika Kituo cha Afya Kirando huku sehemu ya utumbo ukiwemo mfuko wa uzazi na kondo la nyuma vikiwa nje. Aliongeza kuwa godoro alilobebewa mwanamke huyo kutoka nyumbani kwake hadi kituoni lilikuwa limelowa damu huku mwenyewe akiwa amezimia ambaye amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Rukwa mjini hapa na kupokewa Alhamisi saa tano usiku. Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kirando, Dk Gideon Msaki zaidi ya saa sita kuokoa maisha ya Joyce kufuatia huduma ya dharura ya upasuaji waliyomfanyia ikiwa ni pamoja na kumuongezea uniti nne za damu kwa kuwa alikuwa amepoteza damu nyingi. Joyce na mwanawe wamelazimika kusafirishwa umbali wa kilometa 160 kutoka Kituo cha Afya Kirando hadi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini hapa, huku hali yake na mwanawe vikielezwa kuimarika. Dk Kasululu anakiri kuwa hadi sasa bado uchunguzi wa kitabibu haujabaini nini hasa kilichomsibu mwanamke huyo kujirarua tumbo lake na kumtoa mtoto akiwa hai. “Isitoshe swali jingine ambalo halijapatiwa majibu ni kwamba hajathibitishwa kama ni yeye mwenyewe aliyejirarua tumbo lake na kumtoa mtoto nje au kuna mtu mwingine aliyemfanyia hivyo,” alisisitiza. Timu ya ufuatiliaji ya wataalamu wa afya ngazi ya mkoa na wilaya ikiongozwa na Dk Kasululu imejiridhisha kuwa huduma za dharura za upasuaji wa kuokoa maisha ya mwanamke huyo zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Kuonesha kuimarika kwa afya yake, Joyce ambaye amelazwa katika chumba maalumu cha uangalizi, mwandishi wa gazeti hili alipomtembelea aliweza kuinuka na kuketi kitandani kwa msaada wa muuguzi, Veronica Wambura. Kituo cha Afya Kirando ambacho kiko umbali wa kilometa 160 kutoka Sumbawanga mjini ni miongoni mwa vituo vya afya tisa ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano imevifanyia upanuzi na ukarabati kwa zaidi ya Sh bilioni 4 vikiwa na uwezo wa kukabiliana na huduma za upasuaji wa dharura. | kitaifa |
MCHEZAJI wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars na Klabu ya Defaa El Jadidi ya Morocco, Simon Msuva amemuomba rais wa Shirikisho la Soka nchini, Wallace Karia kuwekeza kwenye soka la vijana.Nyota huyo alisema jana, hadi alipofikia sasa anajivunia mchango mkubwa alioupata kwenye vituo vya soka alivyolelewa hivyo anaishauri TFF kuwekeza kwa vijana kama wanataka kunufaika.Akizungumza na gazeti hili, Msuva alisema licha ya mazingira ya nchi kuwa magumu, lakini lazima wajitahidi kuwapa morali vijana kwa kuwalea kimpira ili wavune wachezaji wenye vipaji kwa ajili ya timu ya taifa.“Nchi yetu inachanga moto kubwa ikiwemo ukosefu wa vifaa kama viatu na viwanja vibovu ambavyo vinawafanya wachezaji kushindwa kuendana na malezi ya soka la kisasa nawaomba TFF, kwa kushirikiana na jopo lao kufanya kazi bila kuchoka kuwasaidia vijana ambao ni hazina kubwa kwa taifa,” alisema Msuva.Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji ameshawasili kwa ajili ya kambi ya Taifa Stars inayo- tarajia kushiriki michuano ya kombe la mataifa Afrika nchini Misri mwezi ujao. | michezo |