text
stringlengths
1
4.5k
Je kuna haja ya kuendelea kukumbatia uozo huu ambao hauna manufaa kwetu na badala yake unatuumiza?
Bado nasisitiza kuwa kuna haja ya jamii kubadilika na kufanya kazi, tena kwa bidii, ili kujiletea maendeleo na kama ni swala la serikali kutokuweka sera zitakazolinda maslahi ya wananchi wake basi mwaka 2010 sio mbali, tuwaondoe.
Watu wa Musoma wametuonesha kuwa inawezekana, isiishie huko, kama wote tukiamua na kusema basi inatosha, hakika inawezekana.
kazi kuilaumu serikali utafikiri wewe sio sehemu ya serikali. naomba majibu ya maswali ili mada inoge zaidi labda.
Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanziba alikokuwa amelazwa.
Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambpo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi ulipomkuta umauti asubuhi ya leo.
Amina alikua mjini Zanziba kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.
Sikukuu ya Wafanyakazi
Siku ya Kumbukumbu ya Karume
Profesa Thornton ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu alipokutana na Rais John Magufuli kwa ajili ya kujadiliana kuhusu sakata la mchanga wa madini.
Hakuna tatizo tumia fomu yetu ya kupata nywila na kuingiza tena.
Umesahau nywila yako
HABARI NI HABARI NDUGU YANGU: Chadema na ushindi wa kujivunia
@Uwanja wa Jamhuri, Mkoani Dodoma
Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani wanakaribishwa kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka huu ambayo yanatarajia kufanyika kitaifa Mkoani Dodoma. Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ni “Uhuru wetu ni Tunu, Tuudumishe, Tulinde Rasilimali zetu, Tuwe Wazalendo, Tukemee Rushwa na Uzembe”.
KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO MEI 16, 2018
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Commonwealth Secretariet Vacancy Announcement
Rais Magufuli Atoa Wito kwa Nchi Wanachama Kusimamia Vyema Rasilimali Walizonazo.
Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’.
Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:-
Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Mji wa Longido Kupata Majisafi na Salama kwa Asilimia 100
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ametaka wananchi mbalimbali kutenga muda binafsi na kutembelea moja ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia yakifadhiliwa na UNESCO.
Amesema anaamini kuwa kwa wananchi kushiriki watashawishika kuendelea kuishi kwenye maeneo hayo na kuyaenzi.
Amesema kitendo hicho kidhati kitakuwa kimewaunganisha watu na asili na hivyo kuondoa dhana ya zamani ya kuweka maeneo hayo mbali na watu.
“Inaweza kuwa vigumu kuamini sasa, lakini miaka hamsini iliyopita ilidhaniwa kuwa njia bora ya kulinda asili ni kuiweka mbali na watu ...Hii leo, tunajua vyema zaidi kwamba kwa kadri uhusiano baina ya watu na mazingira yao unavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo watu wanavyofahamu zaidi juu ya umuhimu wa asili na viumbe hai, urithi na maji, kwa ajili ya ustawi wao binafsi na kwa ajili ya hali ya baadaye ya sayari yetu.” Alisema.
Mkuu huyo alisema hayo akizungumzia umuhimu na uhifadhi kwa maeneio zaidi ya 2000 duniani ya bayongahewa, maeneo ya hifadhi ya jiolojia ya na maeneo ya Urithi wa Dunia yanayodhaminiwa na UNESCO.
Alisema maeneo hayo pamoja na kuhifadhi urithi wa dunia pia hutoa ajira kwa watu wanaoyazunguka na milango yake iko wazi kwa umma wote.
“Maeneo ya hifadhi ya jiolojia ni vitabu vilivyo wazi vya kihistoria ambavyo huturudisha nyuma mamilioni ya miaka. Hifadhi za Bayongahewa ni mahali ambapo jamii hukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kuunda njia mpya za kijamii na uchumi endelevu. Maeneo ya hifadhi ya jiolojia na hifadhi za Bayongahewa huunganisha uhifadhi na elimu kwa mbinu mpya ya maendeleo endelevu, kama vile utalii wa mazingira na kilimo hai.” alisema katika ujumbe wake kwa dunia.
Aidha alisema vyema kuona eneo la hifadhi ya jiolojia la UNESCO la Tumbler Ridge nchini Canada, na kuogelea katika maziwa ya Alpine yenye maji angavu kama kioo na kulala chini ya nyota.
Pia amewataka kufanya safari ya kutembea kwa miguu katika hifadhi ya Bayongahewa ya Mujib huko Jordan ambayo ipo mita 420 chini ya usawa wa bahari ikiwa karibu wake na Bahari ya Chumvi.
Mkuu huyo wa Unesco ametaka wakazi wa dunia hii wakati wakiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, kutumia ipasavyo maeneo teule ya UNESCO kila mahali kuungana na asili inayowazunguka na inayoleta uzuri, maana na amani katika maisha.
Sifa "Kila kitu kinachoelezewa" kinatangaza Ufaransa Inter kuhusu matumizi ya hidrojeni na matumizi yake ya nishati.
Pakua faili (usajili wa jarida inaweza kuhitajika): Ufaransa-Inter: kila kitu kinafafanuliwa juu ya hidrojeni
Taswira: Ziara ya Msajili wa Vyama Jaji Mutungi Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kaskazini
Jaji Mutungi amesema kuwa ANAPENDELEA KUWA KARIBU NA VYAMA VYA SIASA YEYE KAMA MLEZI jambo ambalo litasaidia kujua uhitaji wa vyama Vya Siasa na hata kutoa ushauri kwao.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi akizungumza na viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini katika ofisi ya Kanda eneo la Ngarenaro Jijini Arusha
Taswira: Ziara ya Msajili wa Vyama Jaji Mutungi Of...
Baada ya Kushika Nafasi ya Kwanza Kwa Usafi, Jiji ...
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Aamuru Wananchi wa Kijiji Kizima Wakamatwe na Kuwekwa Ndani…..RPC Mbeya Tayari Keshatuma Polisi
Kampuni ya Uber yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya. Dara Khosrowshashi, mmarekani mwenye asili ya Iran amekuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni ya usafiri ya Uber.
Khosrowshashi ambaye alikuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za usafiri mtandaoni ya Expedia, Jumanne iliyopita alithibitisha kuwa angekubali nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Uber.
Khosrowshashi alitangaza nia yake ya kuchukua uongozi wa kampuni ya usafiri ya Uber yenye makao makuu yake huko San Francisco alipofanya mahojiano na Wall Street Journal na Bloomberg.
Bodi ya wakurugenzi wa Uber walipiga kura Jumapili usiku kumpendekeza Khosrowshashi.
Mwaka huu wa 2017, Uber imehusishwa na kashfa kuhusiana na madai ya watendaji wake kuunga mkono utawala wa Rais Donald Trump na mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia katika makao makuu ya kampuni hiyo.
Ushirikiano wa Uber na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Trump, Travis Kalanick, uliacha kampuni hiyo mwezi Juni katika wakati mgumu.
Lakini Kalanick atabaki kwenye bodi ya Uber na anamiliki kiasi kikubwa cha hisa za kampuni hiyo. Kwa sasa ameshtakiwa na mwanachama mwingine wa bodi ya Uber, Benchmark Capital Partners, ambaye anamshtaki kwa udanganyifu.
Kupitia jarida la Los Angeles Times, Msemaji wa Kalanick ametupilia mbali madai hayo , akisema kuwa mashtaka hayo hayakuwa ya ukweli na yamejaa uongo.
Ingawa Uber imepunguza hasara kwa kipindi cha robo ya mwaka, lakini imepoteza dola 645 milioni kwa mapato ya dola 1.75 bilioni wakati wa robo ya pili ya mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma.
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ipo katika maandalizi ya mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unatarajiwa kufanyika Oktoba 2014 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na usimamizi wa uchumi na mipango hapa nchini.
Mkutano huu ambao ni wa kitaalamu unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango ambao hukutana kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.
Mkutano huu unatoa fursa kubwa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Pia hutoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. Mkutano huo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, mkutano wa mwaka huu utajikita katika kujadili masuala yafuatayo;
Mkutano utajadili fursa, na changamoto zilizopo katika kuleta maendeleo katika nchi. Huko nyuma kada hizi zilikuwa zinaratibiwa na iliyokuwa Wizara ya Mipango Uchumi na Uwezeshaji. Kwa sasa watakuwa chini ya uratibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Hatua hii itarahisisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya nchi.
Utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16) unaendelea na tayari Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango imeanza kufanya mapitio ya utekelezaji wake ili kujua mafanikio na changamoto. Hivyo, katika mkutano huo wapanga mipango wanaandaliwa waweze kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Mpango wa Pili wa Maendeleo (2015/16 – 2020/21).
iii) Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma;
Serikali imeandaa mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika sekta ya Umma, lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo.
iv) Jinsi ya Kujiandaa na Uchumi wa Gesi
Mkutano utajadili ni kwa jinsi gani Tanzania inajipanga kufaidika na rasilimali ya gesi asilia. Kwa kifupi masuala ya yanayohusu uwekezaji katika gesi asilia, usimamizi na jinsi ya kutumia rasilimali na menejimenti ya mapato yatokanayo na gesi, pamoja na ushiriki wa wananchi katika fursa mbalimbali zinazotokana na ujio wa gesi hiyo. Utayarishaji wa wataalam katika eneo hilo la gesi husani vyuo vya ufundi, vyuo vikuu na kadhalika.
Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Mkutano wa mwisho wa mwaka wa maafisa mipango ulifanyika mkoani Morogoro tarehe 12 Machi 2010 ambapo uliandaliwa na Wizara ya Fedha. Mada nne zilizowasilishwa na kujadiliwa zilikuwa ni;
i. Wajibu wa wataalamu wa mipango katika Maendeleo ya Uchumi: Mipango ya Kiuchumi, Utekelezaji na Uandaaji wa Taarifa;
ii. Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki;
iii. Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Wafanyabiashara Wadogo na Wakati; na
iv. Ufanisi wa Uwekezaji kutoka nje katika Uchumi wa Tanzania
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukichanja mbuga kutokea jijini Tanga kuelekea jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Umati wa wakazi wa mji wa Muheza.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake leo Septemba 29, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Swahili Time: Katika Hifadhi ya Wanyama Mikumi
Hii ndio picha iliyopata like nyingi Instagram kwa siku moja
Tazama picha ambayo imeweza kupata umaarufu mkubwa sana katika kurasa ya Instagram kwa muda wa siku moja.
Imepata like zaidi ya milioni 8 na comment zaidi ya laki 4.
Mpaka sasa imekaa kwa muda wa siku moja.
Hii ni picha inayomuonesha mwanadada maarufu duniani kwa kazi yake ya muziki pia ni mke wa rapa Jay Z; Anaitwa Beyonce. Hii ndio picha inamuonesha akiwa na ujauzito wa watoto mapacha ambao dunia inataji kuwapokea.
KILIMO CHA MKATABA KUONGEZA UZALISHAJI WA PAMBA
WAKULIMA wa pamba nchini, wamehimizwa kujiunga na kilimo cha mkataba kwa kuwa kina faida na mafanikio kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), James Shimba, alisema kilimo cha mkataba kimesaidia kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba na matumizi ya mbegu bora aina ya UK M08.
Pia, alisema kilimo hicho kimesaidia katika usambazaji na matumizi ya viuadudu na upatikanaji wa huduma za ugani.
“Kilimo cha mkataba kimewafanya wakulima wa ukanda wa Magharibi unaojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Tabora, Singida, Kagera na Kigoma, kupata usimamizi mzuri wa sheria na sera za kilimo kupitia maofisa ugani walioko kwenye halmashauri zao za wilaya.
“Kilimo hicho pia kimesaidia kuongeza eneo la uzalishaji wa pamba, matumizi makubwa ya mbegu za kupanda, ingawa bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuhakikisha wakulima wengi zaidi wanajiunga na kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba.
“Kwa sasa pamoja na kwenda vizuri, kuna changamoto ambayo bodi ya pamba inaendelea kukabiliana nayo kwa kutoa elimu ya kilimo cha mkataba ambapo tunawaelimisha namna ya kulima kwa kuzingatia vipimo na maelekezo yanayopendekezwa na wataalamu.
“Lakini pia, tunawahimiza wang’oe na kuchoma moto miche ya pamba baada ya kuvuna kwa kuwa wakiiacha inakuwa mazalia ya wadudu waharibifu wa pamba.
“Hivyo basi, lazima iwepo mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji kwa kushirikiana na wakulima, wachambuaji wa pamba, viongozi wa ngazi ya wilaya na Serikali Kuu,” alisema.
Kanuni hizi zipo kila kituo cha polisi, kama kuna wengine hawazisomi huko naomba wasome hapa. Kanuni za maadili za Jeshi la Polisi Kamanda wa Polisi wa Arusha anazijua, Mkuu wa Polisi wa wilaya anazijua, na Mkuu wa Upepelezi ambaye kwa namna ya pekee alinikasirikia nisihojiane naye bila shaka naye anazijua.
Haya si maneno yangu, ni ya baadhi ya wakazi wa Arusha, pamoja na hao ambao nimewataja hapo juu. Wanahoji utendaji wa Jeshi la Polisi jijini Arusha lilivyojiaibisha. Lilivyotumika kisiasa bila kutumia akili yake.
Sisi askari wa upande wa polisi jamii wenye nia na mapenzi mema kwa nchi yetu turudie kuzisoma kanuni hizi na maadili yao.
Kanuni hizi zinasema: “Nikiwa ofisa wa polisi nina wajibu wa kutekeleza sheria, wajibu wangu ni kuwahudumia watu, kulinda maisha na mali.
“Kuwalinda wasio na hatia dhidi ya udanganyifu, dhaifu dhidi ya ugandamizaji au vitisho na utulivu dhidi ya vurugu au fujo, kuheshimu haki za kikatiba za raia wote katika uhuru usawa na haki.
“Nitatunza heshima yangu binafsi kama mfano kwa wote, kuwa jasiri wakai wa utulivu na wakati wa hatari. Sitakuwa na dharau au dhihaka, kuwa na uvumilivu na kujali ustawi wa wengine.
“Nitakuwa mwaminifu kimawazo na kimatendo katika maisha yangu binafsi na ya kijamii. Nitaonyesha mfano wa kufuata sheria za nchi na kanuni ya idara yangu. Chochote nitakachoona au kusikia ambacho ni siri au ambacho nimeaminiwa kutokana na wadhifa wangu kitakuwa siri isipokuwa tu pale itakapobidi kufichuliwa katika kutekeleza wajibu wangu.