[INST] Mradi wa Kuzidisha Ubora wa Chakula cha Siku zijazo (AVCD) nchini Kenya- Kitengo cha Mifugo [/INST] Mwongozo wa Nyanjani wa magonjwa ya mifugo kwa kutegemea dalili zao katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya [INST] Dibaji [/INST] Magonjwa ya mifugo hupunguza kiwango cha ufugaji na biashara za mifugo, hasa katika maeneo ya ufugaji ambako huduma za tiba ya mifugo ni adimu. Mifumo mipana ya ufugaji inayotumiwa maeneo haya- kama vile ufugaji wa kuhamahama, uhamaji wa kila msimu na mifumo-mseto ya ufugaji na ukuzaji wa mazao kwa pamoja- inazua changamoto zaidi kutokana na ulishaji wa pamoja wa mifugo, uhamaji wa kila mara na mwingiliano kati ya mifugo na wanyamapori. Tafiti za hivi majuzi katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya (miongoni mwa jamii za Waborana, Warendille, Waturkana, Wasomali na nyingine za wafugaji) zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuambukiza kama vile Homa ya Mapafu inayosambaa haraka, ugonjwa wa mapafu ya mifugo, sotoka ya wanyama wa kucheua (PPR), kimeta, ugonjwa wa vinundu vya ngozi na ugonjwa wa miguu na midomo hutokea kila mara. Tafiti hizo, kadhalika, zinaonyesha kuwa jamii hutumia kiwango kikubwa cha dawa za tiba ya mifugo kudhibiti magonjwa haya lakini tiba nyingi hutumika bila ushauri wa kitaalamu. Kwa hivyo, kuna uwezekano kwamba nyingi ya tiba hizi hazifai. Muhimu zaidi ni kuwa, kipindi cha baada ya matumizi ya dawa hizo ni kifupi kuliko inavyotakiwa, hali inayozua hofu kuwa bidhaa za mifugo waliopewa dawa hizo zina kiwango kikubwa cha mabaki ya dawa, hivyo basi, upo uwezekano kuwa hali hii inachangia mifugo kuwa sugu kwa dawa. Idara ya Huduma ya Afya ya Mifugo, kwa ushirikiano na mashirika ya kimaendeleo ya humu nchini na kimataifa, imetekeleza mikakati mseto ya kufuatilia na kukabiliana na magonjwa katika eneo la kaskazini mwa Kenya. Hata hivyo, hatua hizi zinapaswa kutekelezwa na wadau wote katika sekta hiyo ili zifanikiwe. Wamiliki wa mifugo, kwa mfano, wanao mchango mkubwa katika uhamasishaji/ ufundishaji kuhusu magonjwa kwa kutoa ripoti zinazohusu mikurupuko ya magonjwa. Usahihi wa taarifa zinazotolewa unaweza kuimarishwa kupitia mafunzo kuhusu dalili za magonjwa ambayo wafugaji wanakumbana nayo mara kwa mara. Mwongozo huu utatumiwa kuwapa mafunzo wafugaji wa kieneo, watoaji wa taarifa za magonjwa katika kiwango cha kijamii, matabibu/wahudumu wa kibinafsi wa afya ya wanyama, wauzaji wa dawa, wafanyabiashara na wadau wengine husika kuhusu magonjwa na mbinu za kuyadhibiti magonjwa ya kieneo ili kuimarisha uwezo wao wa kusaidia kufaulisha harakati za utekelezaji wa mikakati ya ufuatiliaji na ukabilianaji na magonjwa hayo. Muundo wa Mwongozo huu umechochewa na Mwongozo wa Nyanjani wa Magonjwa ya Wanyama unaotegemea Dalili (yaani A Field Manual of Animal Diseases by Syndromes) - uliochapishwa mwaka wa 2013 na Mradi wa Viwango, Mbinu na Taratibu za Afya ya Wanyama (yaani Standards Methods and Procedures in Animal Health -SMP-AH) kama sehemu ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, Ukanda wa Afrika Mashariki; Ofisi ya Umoja wa Afrika, Interafrican, kuhusu Rasilimali za Wanyama; Idara ya Marekani ya Kilimo - Kitengo cha Kilimo cha Kigeni; na Chuo Kikuu cha Georgia, Athens nchini Georgia. Hata hivyo, mwongozo huu ni sehemu ya jozi/awamu tatu za miongozo inayoangazia magonjwa ya kieneo ambayo huathiri hasa ng’ombe, kondoo, mbuzi na ngamia katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya. Hii ni tofauti na mwongozo wa SMP-AH uliokarabatiwa mahsusi kwa ajili ya magonjwa yanayoathiri biashara za mifugo. [INST] Utaratibu wa mwongozo wa ngamia [/INST] Mwongozo huu wa ngamia umewasilishwa kama Awamu ya 3 inayoangazia magonjwa ya ngamia. Magonjwa hayo yameanishwa katika makundi tisa kulingana na dalili zayo kuu; kama vile, kuathiriwa kwa mfumo wa kupumua, maambukizi na uvamizi wa ngozi, madonda ya miguu na midomo, ukosefu wa utulivu, kuharibika kwa mimba/ujauzito, kuhara/mharo, magonjwa ya kutokwa na damu ghafla, mkojo mwekundu na magonjwa mengine ya kieneo yanayoambukiza ngamia. Mada zilizoangaziwa chini ya kila ugonjwa ni majina ya wenyeji, umri wa ngamia wanaoathiriwa, uambukizaji, idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi, idadi ya wanaokufa, msambao, hali hatari zinazochangia maambukizi, dalili za ugonjwa, wanyama waliokufa/mizoga, udhibiti na uzuiaji/kinga. Mwongozo huu ni nakala inayoweza kuimarishwa baada ya muda kutegemea michango ya wadau mbalimbali watakaohusishwa. [INST] Shukrani [/INST] Watu wengi walichangia katika utayarishaji wa mwongozo huu. Wanajumuisha maafisa wa afya ya wanyama kutoka kaunti za Turkana, Marsabit, Isiolo, Garissa na Wajir walioshiriki katika warsha za mafunzo; Michael Baariu, Dabasso Barako, Changayo Orkhobeshe, Ehele Haile, Stephen Mutahi, Boku Bodha, Adano Umuro, Dennis Mwongela, Joseph Muriira, John Koskei, Siyat Onle Takal, Abubakar Siraj, Job Ronoh, Jane Akale, Daud Abukar na Anthony Ngugi. Joseph Mathooko kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo pia alishiriki. [INST] Marejeleo yaliyopendekezwa [/INST] Bett, B., Kihu, S., Wamwere-Njoroge, G. and Kiara, H. 2019. Field manual for livestock diseases in pastoral areas in northern Kenya based on syndromes. Camel diseases (Volume 3). Accelerated Value Chain Development (AVCD) Program - Livestock Component. Nairobi, Kenya: ILRI. Bett, B., Kihu, S., Wamwere-Njoroge, G. na Kiara, H. 2019. Field manual for livestock diseases in pastoral areas in northern Kenya based on syndromes. Camel diseases (Volume 3). Mpango wa Accelerated Value Chain Development (AVCD) - Livestock Component. Nairobi, Kenya: ILRI. [INST] Magonjwa ya maambukizi na uvamizi wa ngozi kwa jumla [/INST] Sehemu hii inahusu magonjwa ambayo dalili zake hujidhihirisha kupitia maambukizi ya ngozi. Yanajumuisha upele unaowasha (ambao huathiri aina zote za mifugo), majipu, mapunye na tetekuwanga (Camel pox) ya ngamia. [INST] Mifugo wote [/INST] Picha 1.1.1 Ngamia aliyeathirika na upele unaowasha hupoteza manyoya na ngozi kujikunjakunja(wrinkles). [INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama aliye mzima kiafya hupata ugonjwa huu kwa kugusana na mwenzake aliyeambukizwa au kwa kujisugulia mahali ambapo wanyama wagonjwa walijisugulia. Upele wa Kuwasha husababishwa na wadudu wanaopenyeza na kukaa kwenye ngozi. Wadudu hao huweza kuishi katika mazingira hayo kwa hadi muda wa wiki mbili. [INST] Idadi inayoambukizwa katika kundi la wanyama [/INST] Hadi asilimia 20 ya wanyama katika kundi moja huambukizwa ila hii hutegemea ubora wa mbinu zinazotumika kuudhibiti ugonjwa huu. [INST] Kutoka manyoya katika sehemu za ngozi zilizoathirika [/INST] Huanzia sehemu yoyote iliyogusana na mnyama mgonjwa/ mnyama aliyeathirika na kuenea katika sehemu nyingine za mwili [INST] Epuka kuchanganya makundi ya wanyama [/INST] Tenganisha wanyama wageni, uwatibu kwa kufuata ushauri wa afisa wa tiba ya mifugo ndipo uwachanganye na wengine [INST] [Ni mifugo wepi wengine wanaothirika] [/INST] Picha 1.2.1 Majipu pembeni mwa jicho Picha 1.2.2 Jipu hatari kwenye kiwiko cha kushoto [INST] Uambukizaji [/INST] Majipu yanaweza kutokana na maambukizi kwenye sehemu zilizokwaruzwa au majeraha, kiwewe (trauma), au kutumia sindano chafu kumdungia mnyama mwingine. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu hausababishi vifo isipokuwa iwapo viini vimeingia ndani ya damu na kusababisha maambukizi. [INST] Majipu haya yanaweza kupasuka na kutoa usaha wenye rangi ya manjano isiyokolea [/INST] Hutokea mahali popote mwilini lakini mara nyingi huwa kwenye tezi, kichwa, shingo, kifua, mgongo na miguuni. [INST] Wanyama wote huambukizwa [/INST] Picha 1.3.1 Sehemu ya madonda ya mviringo iliyoathiriwa na mashilingi (mapunye) kwenye shavu la mguu wa ngamia [INST] Uambukizaji [/INST] Mgusano wa moja kwa moja baina ya Wanyama wagonjwa na wazima kiafya. Wanyama hao pia wanaweza kushikwa na mapunye kwa kujisugulia mahali ambapo mnyama aliyeambukizwa alijisugulia. [INST] Idadi ya Wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Wanyama wachanga kiumri ndio hasa huambukizwa, na wengi wa wanyama (hasa wanaofugwa pamoja) huambukizwa. [INST] Hakuna [/INST] Picha 1.4.1 Vipele vya tetekuwanga (Camel pox) sehemu ya mdomo Picha 1.4.2 Vipele sehemu ya chini ya mkia [INST] Uambukizaji [/INST] Ni ugonjwa wa kuambukizana sana wa ngozi unaosababisha vipele, na unaosambazwa kupitia migusano baina ya wanyama wagonjwa na wasio wagonjwa. [INST] Idadi ya wanaoathirika kwenye kundi [/INST] Huathiri zaidi wanyama wachanga, hasa wenye umri usiozidi miaka mitatu (wanyama waliozaliwa baada ya mkurupuko wa mwisho wa upele huo). Ikiwa wakomavu wataathirika, fahamu kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu hausababishi vifo lakini panapotokea mkurupuko hatari, kati ya ngamia 10 wachanga walioathirika 3 wanaweza kufa; wale wa kike huavya mimba, na kiwango cha maziwa kuvurugwa. [INST] Vipele na vidonda kutokea kwenye pua, mdomo, macho na chini ya mkia [/INST] Picha 1.4.3 Vidonda vingi vigumu kwenye mdomo Picha 1.4.4 Vidonda vigumu katika sehemu kadhaa za mwili wa ngamia [INST] Magonjwa yenye dalili za kukosa utulivu/kiwewe [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa yenye dalili za kukosa utulivu kama vile kuzungukazunguka kila mara, kufinyilia kichwa kwenye kitu miongoni mwa nyingine. Magonjwa yaliyoangaziwa katika sehemu hii yanajumuisha kichaa cha mbwa na maji kujaa kwenye moyo. [INST] Uambukizaji [/INST] Maambukizi hutokea baada ya mnyama aliyeambukizwa kumuuma mwingine, hasa mbwa na wanyamapori wa jamii ya mbwa. [INST] Ndogo zaidi--- mara nyingi huwa ni mnyama mmoja tu katika kundi [/INST] Idadi ya vifo [INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Mnyama anaweza kuwashambulia wanyama wengine, watu na vitu vilivyo katika mwendo lakini mashambulio hayo huwa hayajakusudiwa. [INST] Mbwa kuchanjwa [/INST] Mfungie mnyama aliyeathiriwa mahali na upige ripoti iwapo kisa chochote cha kichaa cha mbwa kimetokea. [INST] Maji kujaa kwenye moyo [/INST] Hakuna jina la wenyeji kwa ugonjwa huu wa ngamia. Ugonjwa huu uligunduliwa na kuripotiwa kwa mara ya kwanza miongoni mwa ngamia mnamo mwaka 2016. [INST] Uambukizaji [/INST] Viini vinavyosababisha ugonjwa huu hupitishwa na kupe, hasa wenye rangi nyingi. Kupe huyo huchukua viini hivyo wakati akimfyonza damu mnyama aliyeambukizwa. Viini hivi hukua ndani ya kupe huyo na baadaye kupitishwa hadi kwa mnyama mwingine anayefyonzwa damu na kupe huyo huyo. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathiriwa [/INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika hutofautiana kutegemea eneo husika kulingana na idadi ya kupe, wanyama kuwahi kuambukizwa hapo awali, na mbinu zinazotumika kuudhibiti ugonjwa huu. Mkurupuko wa mwisho wa ugonjwa huu miongoni mwa ngamia nchini Kenya, uliripotiwa kuchangia vifo vya ghafla vya ngamia vilivyozidi kwa mbali vifo vyote vilivyowahi kushuhudiwa na wafugaji hapo awali. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ya wanyama wanaokufa baada ya kuambukizwa ni ya juu katika maeneo yanayoshuhudia ugonjwa huo kwa mara ya kwanza. [INST] Usambaaji [/INST] Ingawa ugonjwa huu unapatikana katika kaunti zote, kaunti ya Marsabit ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa huu wa maji kwenye moyo. [INST] Kifo cha ghafla [/INST] Dalili za kukosa utulivu na uthabiti kama vile kushindwa kutembea vizuri, kuchomoza ulimi nje, kuinua miguu juu zaidi wakati wa kutembea, kujizungusha na mwili kutetemeka. [INST] Wanyama waliokufa/Mizoga [/INST] Maji mengi yenye rangi kwenye moyo, sehemu inayohifadhi moyo na kwenye chemba ya tumbo (abdominal cavity) [INST] Magonjwa yanayosababisha mimba kuharibika [/INST] Magonjwa yanayohusiana na kuharibika kwa mimba kama vile Homa ya Rift Valley (RVF) na Ugonjwa wa Mimba Kutoka (Ugonjwa wa Maziwa na Nyama kwa binadamu) yameangaziwa katika sehemu hii. [INST] Uambukizaji [/INST] Mbu hupata virusi kutoka kwa mnyama mgonjwa anapomfyonza damu. Kisha husambaza virusi hivyo kwa mnyama asiye mgonjwa baadaye anapomfyonza damu mnyama mwingine. Watu huambukizwa ugonjwa huu kwa kugusa damu, majimaji ya mwili na sehemu nyingine za mwili wa mnyama aliyeambukizwa. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Homa ya Rift Valley huathiri wanyama wengi hasa baada ya msimu wa mvua nyingi na ya kipindi kirefu, ambapo mbu wengi huwa wanazaana na kukua. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu unaweza kuua karibu asilimia 10 hadi 50 ya wanyama wenye umri mdogo. Wanyama waliokomaa wanaweza kuambukizwa lakini ni wachache (asilimia 10) ambao hufa. [INST] Hutokea hasa baada ya kunyesha kwa mvua kubwa na ya kipindi kirefu inayosababisha mafuriko [/INST] Visa vichache pia vinaweza kutokea nyakati za mvua ya kiwango cha kawaida, lakini visa hivi ni vigumu kutambuliwa. [INST] Uambukizaji [/INST] Njia kuu ya uambukizaji wa ugonjwa huu ni ulaji wa lishe au unywaji wa maji yaliyochafuliwa na vijusi/vitoto na uchafu mwingine kutoka kwa ng’ombe au ngamia walioambukizwa. Njia nyingine zinazoweza kuchangia hili ni kama vile dume aliyeambukizwa anapomtungisha mimba ngamia jike. Watu wanaweza kupata ugonjwa huo kutoka kwa wanyama walioambukizwa kupitia unywaji wa maziwa yasiyochemshwa, ulaji wa chakula kisichopikwa vizuri na kushika sehemu za mwili wa mnyama aliyeambukizwa. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ndogo ya wanyama hufa kwa kuathiriwa na minyoo, ingawa ndama wanaoathiriwa na minyoo wanaweza kufa kuliko wanyama waliokomaa. [INST] Uambukizaji [/INST] Ulaji wa chakula kilichoambukizwa na viini vinavyosababisha tatizo hili kama vile rotavirus na bakteria wengine wanaosababisha mharo huo. Unywaji wa maziwa kupindukia pia husababisha kuhara. [INST] Idadi ya Vifo [/INST] Idadi ya vifo hutofautiana, na athari ya matibabu huwa hafifu. Kiwango cha vifo cha karibu asilimia 25 kimewahi kuripotiwa. [INST] Ndama kunyonya maziwa mengi kupindukia [/INST] Ndama wanaozaliwa na majike wachanga wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huu kuliko wanaozaliwa na majike waliokomaa kiumri [INST] Uambukizaji [/INST] Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu hubebwa kwenye pumzi ya wanyama walioambukizwa (kwa njia ya matone). Pia hubebwa kwenye mate, uchafu unaotoka mdomoni na puani, na kwenye kinyesi. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Asilimia kubwa (hadi 80%) ya wanyama walioambukizwa hufa. Kifo kinaweza kutokea ghafla lakini wakati mwingine huwa kati ya siku 2 — 8 baada ya dalili za kwanza kuonekana. [INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu hutokea hasa katika msimu wa mvua, na wakati mwingine unahusishwa na unywaji wa maji ya mafuriko. Mara nyingi hutokea ghafla na kuua wanyama haraka. Unaathiri wanyama wanaoonekana kuwa na hali nzuri kiafya hasa walioanza kukomaa na ndama wanaoanza kula nyasi. [INST] Shingo iliyofura [/INST] Tezi (limfu) iliyofura na yenye uchungu hasa pembeni ndani ya mashavu na chini ya shingo (tezi au limfu ni kiungo kinachobeba majimaji yenye kinga ya mwili) [INST] Uambukizaji [/INST] Kimeta husababishwa na bakteria wanaoweza kuishi kwenye udongo kama viini kwa muda wa hadi miaka 60 na ni sugu au hustahimili joto jingi na ukame. Ugonjwa huu unaweza kuzuka katika maeneo ambayo wanyama hukusanyika, kwa mfano, mahali pa kunywa maji na pa kuramba udongo wa magadi. Mnyama huingiza bakteria hawa mwilini anapokula nyasi zilizo katika udongo wenye maambukizi. Watu wanaweza kupata kimeta kwa kugusana na mnyama au uchafu wake ulio na maambukizi moja kwa moja au vinginevyo. [INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Usiwahi kumchinja mnyama aliyekufa kutokana na kimeta. Mzoga wake haujikazi (kushikamana au kukakamaa) kama inavyotarajiwa kwa mnyama mfu. [INST] Weka katika karantini/watenganishe wanyama wanaougua na wasiougua [/INST] Hakikisha mzoga wenye kimeta na vifaa vilivyoambukizwa vimezikwa vizuri kwenye shimo refu (futi sita) WEKA BANGO LENYE MAANDISHI ‘USIENDELEE KUNA HATARI’: USIPASUE MZOGA WA MNYAMA ALIYEKUFA KUTOKANA NA KIMETA. [INST] Idadi inayoathirika kwenye kundi [/INST] Kifo cha ghafla cha ngamia hutokea kwa wingi wakati wa mikurupuko ya maradhi ambayo huambukiza wanyama wengi kwa wakati mmoja [INST] Idadi ya vifo [/INST] Wanyama wachache kwenye kundi hufa, lakini huwa na athari kubwa ya kiuchumi kwa sababu vifo huwaathiri wanyama wenye thamani kubwa. [INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Kifo cha ghafla cha ngamia hutokea kwa kiwango kikubwa hasa miongoni mwa ngamia waliokomaa, wa kike wajawazito na wanaonyonyesha, madume ya kuzalisha na kubeba mizigo, wenye uzani mwingi na/au walio na afya nzuri. [INST] Kifo katika muda usiozidi saa moja baada ya kuanguka. [/INST] Hakuna dalili zinazoweza kutoa tahadhari kabla ya mnyama mgonjwa kuanguka. Wanyama kwenye kundi moja hufa mmoja mmoja kwa muda fulani kisha wanaacha. [INST] Uambukizaji [/INST] Maambukizi ya ugonjwa huu yanatokana na kugusana kwa wanyama walioathirika na wazima kiafya. Wanyama hawa wazima kiafya huwa kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu wanapogusa vidonda vya wanyama walioambukizwa. Maambukizi haya mara nyingi hufanyika kupitia kwa majeraha yaliyo kwenye ngozi ya mnyama yaliyosababishwa na kuchubuka/kudungwa wakati akila nyasi ngumu au mimea yenye ncha kali. Virusi vya ugonjwa huu vinaweza kudumu kwenye vidonda hivyo kwa muda mrefu hasa katika misimu ya kiangazi. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathiriwa kwenye kundi [/INST] Wengi wa wanyama hao hasa wachanga huathirika. Maambukizi mapya baada ya kupona ni ya kawaida kwa sababu ugonjwa huu haujengi kinga thabiti mwilini. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu kwa kawaida hauui bali majeraha yanayotokea kwenye midomo yanaweza kuwazuia kula hasa wanyama wachanga. Vidonda hivi pia vinaweza kupata viini na kuzua maambukizi hatari zaidi yanayoweza kusababisha kifo. [INST] Vidonda hivyo hutokea kwenye mdomo na wakati mwingine kwenye pua. [/INST] Vidonda hivyo hugeuka kuwa upele mbaya kwenye mdomo na wakati mwingine husambaa hadi ndani ya mdomo, sehemu ya chini ya miguu, na hata kwenye matiti ya mnyama anayenyonyesha. [INST] Dalili nyingine [/INST] Ugonjwa huu mara nyingi hudumu kwa wiki nne hadi sita kisha baadaye mnyama huyo huanza kupona polepole. [INST] Safisha maboma ya wanyama kwa dawa za kuua viini [/INST] Osha mikono kwa sabuni baada ya kushika vidonda vya ugonjwa huu kwa sababu virusi hivyo vinaweza kumshika binadamu. [INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Ng'ombe, kondoo, na mbuzi ingawa panaweza kuwapo tofauti za aina ya vimelea vinavyoambukiza kila jamii ya mnyama. [INST] Uambukizaji [/INST] Ngamia wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu kupitia kwa mbung'o au nzi wanaouma yaani pange/kipanga walio na viini (pange au kipanga wanajulikana kisayansi kama Tabanids au Stomoxys) [INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika kwenye kundi [/INST] Hadi thuluthi moja (yaani mmoja kati ya watatu) ya ngamia wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwenye kundi lakini idadi hii hutofautiana zaidi kutegemea idadi ya mbung'o na nzi wa kuuma walio katika eneo hilo. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Karibu ngamia wote walio na ugonjwa huu hufa ikiwa hawatatibiwa. Huwa wanaugua kwa muda mrefu. Kwa kawaida, karibu asilimia 3 hivi ya ngamia hufa kutokana na ugonjwa huu. [INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unapatikana katika maeneo yote ambayo yana mbung'o. Nzi wanaouma huongeza hatari katika eneo hilo, hasa ikiwa kuna mnyama aliye na ugonjwa huo mwilini. [INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Wanyama waliokufa huwa wamedhoofika sana. Ugonjwa huu hausababishi vidonda kwenye viungo vya ndani ya mwili. [INST] Kinga [/INST] Angamiza mbung'o na nzi wanaouma kwa kutumia dawa za kuua wadudu, kama ulivyoagizwa na afisa wa tiba ya mifugo. [INST] Mbuzi na twiga. [/INST] Picha 7.2.1 Hatua ya awali ya ugonjwa wa kupinda shingo isiyokuwa hatari Picha 7.2.2 Hatua hatari ya ugonjwa wa kupinda shingo kwa ngamia [INST] Mradi wa Kuzidisha Ubora wa Chakula cha Siku zijazo (AVCD) nchini Kenya-Kitengo cha Mifugo [/INST] Mwongozo wa Nyanjani wa magonjwa ya mifugo kwa kutegemea dalili zao katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya [INST] Dibaji [/INST] Ufugaji ni mbinu kuu ya kujipa riziki miongoni mwa jamii za wafugaji katika ukanda wote wa Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika. Jamii hizi nchini Kenya huishi katika kanda za malisho ya mifugo ambazo hupata huduma duni sana za tiba ya mifugo na miundomsingi hafifu inayohitajika kwa ufugaji bora wa mifugo na biashara yao. Kadhalika, mitindo ya maisha inayofuatwa eneo hili kama vile ufugaji wa kuhamahama, uhamaji wa kila msimu na mifumo mseto ya kilimo, yaani, ufugaji na ukuzaji wa mazao, kwa pamoja, huimarisha mwingiliano baina ya wenyeji, mifugo yao na wanyama-pori. Uhusiano huu, mbali na kuchangia katika kuzuka kwa migogoro baina ya binadamu au mifugo na wanyama-pori, pia huchangia katika uambukizanaji wa viini vya magonjwa ya aina nyingi miongoni mwao. Tafiti za hivi majuzi zaidi katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya zilidhihirisha uwepo mkubwa wa viini vya kila mara vya magonjwa ya kieneo pamoja na kuibua ushahidi wa kina wa uzukaji na uibukaji mpya wa viini vya maradhi yanayoathiri mfumo wa kupumua ya Mashariki ya Kati, virusi vya Korona, virusi vya Homa ya Rift Valley (RVF), homa ya Q n.k. Kwa hivyo, matumizi ya dawa za tiba ya mifugo katika maeneo hayo yameongezeka kila kukicha katika juhudi za wafugaji hao kukabiliana na matatizo ya kiafya ya wanyama wao. Kutokana na changamoto hizi za kipekee katika maeneo kame nchini Kenya, jitihada nyingi zimetekelezwa ili kuzidisha ufuatiliaji na ukabilianaji na magonjwa haya. Jitihada hizo hufanikishwa kupitia kwa harakati za uhamasishaji wa jamii na ukumbatiaji wa mifumo bora ya kuripoti matukio, inayochangia mafanikio ya viwango mbalimbali. Takwimu kuhusu utokeaji wa magonjwa haya mashinani hufuatiliwa na kurekodiwa na maafisa wa nyanjani wa afya ya mifugo wanaoshirikiana na watoaji taarifa za magonjwa katika kiwango cha kijamii. Mfumo huu huwa unafaulu zaidi unapotekelezwa kama mradi wa kukabiliana na magonjwa makuu ya mkurupuko yanayoweza kubainishwa ambayo hutokea katika eneo kubwa, lakini ufanisi wake hauwi mkubwa iwapo unahusu aina nyingi za magonjwa ya kieneo ambayo hasa husababisha hasara kubwa ya uzalishaji katika eneo lililoathiriwa. Mwongozo huu unakusudiwa kuzidisha maarifa kuhusu magonjwa na mbinu za kuyadhibiti miongoni mwa wafugaji wa kieneo, watoaji wa taarifa za magonjwa katika jamii, matabibu/wahudumu wa kibinafsi wa afya ya mifugo, wauzaji wa dawa, wafanyabiashara na wadau wengine husika. Lengo hapa ni kuimarisha ufanisi wa juhudi za kukabiliana na kufuatilia magonjwa, zinazobuniwa na Idara ya Huduma za Afya ya Mifugo. Muundo wa Mwongozo huu unafanana na wa Mwongozo wa Nyanjani wa Magonjwa ya Wanyama unaotegemea Dalili (yaani A Field Manual of Animal Diseases by Syndromes) uliochapishwa mwaka wa 2013 na Mradi wa Viwango, Mbinu na Taratibu za Afya ya Wanyama (Standards Methods and Procedures in Animal Health -SMP-AH) kama mkakati wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Ofisi ya Umoja wa Afrika, Interafrican, kuhusu Rasilimali za Wanyama, Idara ya Marekani ya Kitengo cha Kigeni cha Kilimo, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Georgia, Athens nchini Georgia. Maboresho muhimu kutokana na toleo la SMP-AH yalijumuisha (i) kuangazia ng'ombe, kondoo, mbuzi na ngamia wanaofugwa katika eneo lengwa, (ii) magonjwa mbalimbali pamoja na magonjwa yanayovuka mipaka ya kimaeneo ambayo mwongozo wa awali uliangazia, (iii) mbinu zinazoweza kutumika kudhibiti kila aina ya ugonjwa, na (iv) kutafsiriwa katika lugha za wenyeji ili kuwawezesha wengi kuusoma katika ngazi ya kieneo. Dalili kuu za ugonjwa na viungo vya wanyama vilivyobainika kuathiriwa, pia vimechapishwa kwenye picha/michoro. Mwongozo huu ni nakala inayoweza kuboreshwa hatua kwa hatua kulingana na michango ya wahusika mbalimbali watakaohusishwa. [INST] Utaratibu [/INST] Mwongozo huu unaangazia magonjwa ya ng'ombe. Magonjwa haya yameainishwa katika makundi tisa kulingana na dalili kuu ambazo magonjwa hayo yanaonyesha, kwa mfano: kupumua, maambukizi ya ngozi/uvamizi wa viini, vidonda vya miguu na midomo, ukosefu wa utulivu, mimba kutoka, mharo/kuendesha, ugonjwa wa kuvuja damu ghafla, mkojo mwekundu na magonjwa mengine ya kieneo. Mada zinazozungumziwa chini ya kila magonjwa hayo zinajumuisha, majina ya wenyeji, mifugo iliyoathirika, uambukizaji, idadi ya wanyama walioathirika kwenye kundi, idadi ya vifo, msambao, dalili za ugonjwa, dalili za magonjwa katika wanyama wafu (uchunguzi wa mizoga) na kinga. [INST] Shukrani [/INST] Watu wengi walichangia katika utayarishaji wa mwongozo huu; wanajumuisha maafisa wa afya ya mifugo na maafisa wengineo katika Kaunti za Turkana, Marsabit, Isiolo, Garissa na Wajir; walioshiriki katika vikao vya mafunzo: Michael Baariu, Dabasso Barako, Changayo Orkhobeshe, Ehele Haile, Stephen Mutahi, Boku. Bodha, Adano Umuro, Dennis Mwongela, Joseph Muriira, John Koskei, Siyat Onle Takal, Abubakar Siraj, Job Ronoh, Jane Akale, Daud Abukar na Anthony Ngugi. Dk Joseph Mathooko wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Kilimo na Chakula pia alishiriki. Waandishi hawa mahiri pia wanatambua mchango wa Maafisa Waratibu wa Nyanjani wa AVCD LVC (Haret A. Hambe (Garissa), Adan A. Kutu (Isiolo), Abdisemed Osman (Wajir), Simon Chuchu (Marsabit) na Viola Chemis (Turkana)) katika kaunti zinazolengwa, ambao waliboresha mwongozo huu, kwa kujumuisha maoni yaliyotolewa na maafisa wa kwanza wa nyanjani katika kaunti, watoaji wa ripoti za magonjwa katika ngazi ya kijamii na wafugaji katika ngazi ya kijiji. [INST] Marejeleo [/INST] Bett, B., Kihu, S., Kiara, H. and Wamwere-Njoroge, G. 2018. Field manual for livestock diseases based on syndromes in pastoral areas in northern Kenya: Cattle diseases. Accelerated Value Chain Program (AVCD) program-Livestock Value Chain Component, Nairobi, Kenya: ILRI. [INST] Magonjwa yanayobainika kwa namna ya kupumua [/INST] Magonjwa yaliyoangaziwa katika sehemu hii ni yale ambayo dalili zake kuu hugunduliwa kwa kuangalia jinsi mnyama anavyopumua. Maradhi hayo yanajumuisha Homa ya Mapafu na Ndigana Kali almaarufu East Coast Fever (ECF). [INST] Uambukizaji [/INST] Ng'ombe walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu, huambukizwa kwa kuvuta ndani ya mwili pumzi kutoka kwa mnyama aliyeathirika. Pia ugonjwa huu unaweza kuambukiza kupitia matone ya mkojo kutoka kwa mnyama anayeugua. Maambukizi hayo yanaweza kutokea hata ikiwa ng’ombe asiye mgonjwa yuko mita 20 hadi 200 kutoka kwa yule aliyeathirika. Mchoro 1: Kielelezo cha jinsi homa ya CBPP inavyosambazwa — mnyama aliyeathirika na ugonjwa wa CBPP husambaza kiini cha ugonjwa huo kupitia kwa matone ya pumzi yanayomtoka anapokohoa (mchoro wa kushoto). Mnyama mzima kiafya au dhaifu anapovuta ndani matone hayo, huambukizwa na kuendeleza ugonjwa huo (mchoro wa kulia). [INST] Idadi inayoathirika kwenye kundi [/INST] Katika maeneo ambayo hayajawahi kushuhudia ugonjwa huu, hadi asilimia (%) 100 ya wanyama huathirika. Katika maeneo ambayo hushuhudia ugonjwa huu mara kwa mara, kati ya 10%—%60 huathirika. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Katika maeneo ambayo hayajawahi kushuhudia maambukizi haya, ugonjwa huu huua zaidi ya 50% ya wanyama. Katika maeneo ambayo maambukizi hutokea mara kwa mara, chini ya 10% ya wanyama hao ndio hufa kutokana na ugonjwa huu. [INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Mwili kujivuta nyuma kisha mbele anapopumua, pamoja na sauti ya kunguruma kutokana na maumivu —upumuaji wa juujuu na wa haraka [INST] Kikohozi kikavu anaporukaruka [/INST] Ng’ombe kupinda mgongo kwa juu akiwa amesimama, visugudi au viwiko vikiwa nje huku kichwa na shingo vimerefushwa [INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu huambukizwa kupitia kwa kupe wa kahawia wa masikioni. Kupe hawa hubeba viini vya ugonjwa huu kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa wanapomfyonza damu yake. Halafu kupe hao huambukiza mnyama anayefuatia wanapomnyonya/kufyonza damu.. Kupe hawa wanaweza kuishi na viini hivyo kwenye malisho kwa miaka miwili. Idadi kubwa ya mifugo inaweza kuathirika kulingana na wingi wa kupe hao walioambukizwa. Mchoro 1.5: Kielelezo cha jinsi ugonjwa wa ECF unavyoambukizwa—kupe wa kahawia wa masikioni hubeba viini vinavyosababisha ECF. Kupe hao hupata viini hivyo kutoka kwa wanyama aliyeambukizwa na kuvisambaza kwa wanyama wazima kiafya wanaponyonya damu yao. [INST] Idadi inayoathiriwa kwenye kundi [/INST] Inategemea idadi ya kupe walioambukizwa katika eneo hilo pamoja na afya ya mnyama. Miongoni mwa ng'ombe wa kiasili (Zebu, Borana), maambukizi yanaweza kufika 100%, lakini kwa kawaida vifo huwa vichache. Lakini kwa ng'ombe wa kigeni, vifo vinaweza kufika 100% ikiwa ugonjwa huo hautakabiliwa mapema. [INST] Magonjwa ya maambukizi na mavamizi ya ngozi kwa jumla [/INST] Sehemu hii inashughulikia magonjwa ambayo maambukizi au uvamizi wa ngozi ndio dalili kuu. Haya yanajumuisha Vinundu vya Ngozi na Upele Unaowasha/Ukurutu ambao huathiri kila aina ya mifugo. [INST] Ugonjwa huu husambazwa kupitia kwa angalau njia tatu kuu: [/INST] Wanyama wasio wagonjwa wanapogusana na walioathirika, wanapata viini vya ugonjwa huu hasa kupitia kwa mate. Nzi wa kuuma (pange/vipanga) na mbu wanaweza kupata viini kutoka kwa mnyama anayeugua wanapomfyonza damu na kuvihamisha hadi kwa wanyama wazima kiafya. Wanyama wazima wanaweza kupata ugonjwa huu kwa kunywa maji yaliyochanganyika na mate ya mnyama aliyeathirika. [INST] Idadi ya wanyama wanaoathiriwa [/INST] Hii hutofautiana sana, na hutegemea iwapo mnyama huyo aliwahi kuugua ugonjwa huo hapo awali au la. Kati ya asilimia 3-80 ya mifugo wanaweza kuambukizwa. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Wanyama wachache hufa, mara nyingi chini ya 5% ya wale walioathirika. Ni nadra sana idadi ya vifo vya wanyama wanaoathirika kufika 20%. [INST] Zuia migusano kati ya mifugo wa makundi tofauti (k.m. katika maeneo ya kunywa maji, malishoni) [/INST] Epuka kutumia wanyama (ndume), vifaa, magari, na wafanyakazi kutoka mashamba mengine katika kipindi cha ugonjwa huu. [INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama mzima hupata ugonjwa huu kwa kugusana na aliyeathirika, au iwapo ataegemea sehemu zilizotumiwa na wanyama wagonjwa kujisugua, na/au kulala katika maeneo yaliyotumiwa na mnyama anayeugua ugonjwa huu. Unasababishwa na vimelea ambacho hujipenyeza hadi ndani ya ngozi. Kiroboto hicho kinaweza kuishi kwa hadi wiki mbili ardhini. Mchoro 2.2: Jinsi Upele Unaowasha unavyotoka kwa wanyama walioathirika hadi kwa wazima kiafya. Kielelezo hiki kinaonyesha wanyama walioathiriwa wajisugua kwenye miti kisha kuacha chembe za ngozi zenye viini vya upele huo, vinavyoweza kuganda kwa wanyama wasiokuwa wagonjwa wanapoegemea miti hiyo. [INST] Idadi inayoathirika katika kundi [/INST] Kwa kutegemea unavyowalisha, kuwatunza na ubora wa mbinu za kuyadhibiti maradhi haya, ni hadi 20% ya wanyama katika kundi moja wanaoathiriwa. [INST] Epuka kuchanganya mifugo katika eneo la kuwanywesha maji na malishoni [/INST] Watenge/kuwaweka katika karantini na kuwakagua kwa umakinifu wanyama wapya — tafuta usaidizi wa afisa wa tiba ya mifugo [INST] Magonjwa ya vidonda vya miguu na midomo [/INST] Sehemu hii inafafanua magonjwa yanayosababisha vidonda kwenye midomo na miguuni: ugonjwa huu huathiri wanyama wote wenye kwato zenye mwanya katikati, na mwozo wa miguu hasakwato. [INST] Wanyama wengine wanaoathiriwa [/INST] Wanyama wote wenye kwato zenye mwanya huathiriwa na FMD. Mara nyingi ng’ombe huathirika zaidi kuliko kondoo na mbuzi. Nguruwe hunya virusi zaidi kuliko ng'ombe, kondoo au mbuzi lakini makali ya ugonjwa huo hutegemea aina ya virusi na uthabiti wa afya ya nguruwe hao. [INST] Uambukizaji [/INST] Wanyama wazima kiafya hupata ugonjwa huu wanapogusana na uchafu unaotoka mwilini, k.m. mate, mkojo, maziwa, kinyesi au mbegu za kiume/manii kutoka kwa wanyama walioathirika. Ugonjwa huu husambaa kwa kugusana na wanyama walioathirika, vitu vilivyoambukizwa (vifaa vilivyoambukizwa) au magari. Ugonjwa huu pia unaweza kuenezwa kupitia kwa hewa pale mnyama mzima anapovuta pumzi iliyotolewa na mnyama aliyeambukizwa. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Husambaa kwa kasi miongoni mwa wanyama walio katika hatari ya kupata ugonjwa/wadhaifu kiafya. Pia kuna uwezekano wa wanyama wote kwenye kundi kuathirika. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu hauui sana wanyama waliokomaa kwa sababu wengi huwa na uwezo wa kupona. Wanyama wachache wachanga hufa kutokana na matatizo ya moyo. Ndama wenye umri wa chini ya miezi 3 wanaweza kufa zaidi. [INST] Uambukizaji [/INST] Kukaa kwenye unyevu kwa muda mrefu au kuumia mguuni huwezesha viini vinavyoishi hasa katika ngozi kuingia miguuni/kwatoni, hivyo basi kusababisha ugonjwa huu. [INST] Dalili za ugonjwa huu kwa wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Uchelewaji wa matibabu unaweza kuzidisha maambukizi hadi kwenye mifupa ya ndani, tando laini za viungo, na kupunguza uwezekano wa kupona. [INST] Magonjwa yenye dalili za Kuhangaika [/INST] Sehemu hii inashughulikia magonjwa yenye dalili za kukosa utulivu kama vile kuzungukazunguka, kufinyilia kichwa mahali na kadhalika. Magonjwa makuu yanayoangaziwa hapa ni Maji kujaa kwenye Moyo na Kichaa cha Mbwa (T9), ambayo huathiri aina nyingi za mifugo. [INST] Uambukizaji [/INST] Viini vinavyosababisha ugonjwa huu husambazwa na kupe, hasa kupe wa Kusini mwa Afrika (bont-. Kupe hubeba bakteria wa ugonjwa huu wanapowafyonza/kunyonya damu wanyama walioambukizwa. Bakteria hawa hukua zaidi kwenye kupe hao na kuambukiza mnyama asiyeugua wakati kupe huyo anapomnyonya damu. [INST] Idadi inayoathirika kwenye kundi [/INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika hutofautiana kutegemea eneo, idadi ya kupe, maambukizi ya awali ya bakteria hao na mbinu zinazotumika kuangamiza kupe. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ya wanyama wanaofariki baada ya kuambukizwa iko juu. Idadi ya vifo hufika 80% kwa mifugo (kundi la wanyama) wadhaifu kiafya. [INST] Sehemu ya chini ya Mashavu/Taya kuvimba [/INST] Kukosa utulivu, kushindwa kusimama imara, ulimi kutoka nje, kuinua miguu sana wakati wa kutembea, kufinyilia kichwa mitini au ukutani, kuzungukazunguka,, kiwewe na hisia kali kupita kiasi hadi anapozirai. [INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Wanyama wote walio na damu moto wakiwemo kondoo, mbuzi, punda na ngamia wako katika hatari ya kuambukizwa kichaa cha mbwa. Pia huathiri wanadamu na mbwa. [INST] Uambukizaji [/INST] Maambukizi hutokana na kuumwa na mnyama aliyeathirika, hasa mbwa au wanyamapori wa jamii ya mbwa. Binadamu anaweza kuambukizwa kwa kuumwa au kukwaruzwa na mnyama aliyeathirika kama vile mbwa au kutokana na mate ya mnyama aliye na ugonjwa huu. [INST] Kutoka mate kwa wingi [/INST] Kushindwa kutoa sauti anapojaribu kuroroma au wakati mwingine kukoroma mfululizo hadi kupooza/kulemaa [INST] Magonjwa yanayosababisha mimba kutoka [/INST] Magonjwa yanayohusiana na uharibikaji wa mimba k.m. Homa ya Rift Valley na Ugonjwa wa Kutupa Mimba, yanaangaziwa katika sehemu hii. [INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unapatikana sana katika Kaunti ya Garissa, maeneo ya Pwani, Kati ya Kenya, na kaskazini mwa Bonde la Ufa (Naivasha, Baringo, Uasin Gishu na Trans Nzioa). [INST] Uambukizaji [/INST] Mbu hupata virusi hivi kutoka kwa mnyama mgonjwa wanapomnyonya damu. Kisha virusi hivi hupitishwa kwa mnyama mwingine, asiye na ugonjwa huo wakati anaponyonywa damu na mbu hao. Watu hupata ugonjwa huu kwa kugusa damu na majimaji mengine ya mnyama aliyeathirika wanapomchinja, au wanapomsaidia kuzaa au kugusa vitoto/vijusi na uchafu wa vijusi hivyo. Watu wanaweza pia kuugua kwa kula nyama na viungo vya wanyama wagonjwa ambavyo havijapikwa vizuri, au wakiumwa na mbu. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Kwa wanyama wachanga, ugonjwa huu unaweza kuua kati ya asilimia 10-50 ya wanyama hao. Wanyama waliokomaa wanaweza kuambukizwa lakini ni wachache (karibu 10%) hufa. [INST] Uzuiaji wa ugonjwa huu kwa binadamu [/INST] Ikiwa kuna mkurupuko, mizoga ya wanyama wafu, uchafu wanaoutoa, na vitoto vilivyokufa tumboni, vinafaa kuzikwa kwa njia salama [INST] Uambukizaji [/INST] Kula nyasi, maji na lishe nyingine iliyochanganyika na vijusi na uchafu mwingine wa ng’ombe aliyeambukizwa. Maambukizi haya pia yanaweza kutokea dume anapomtungisha jike mimba. Utungishaji wa mimba kwa mbinu ya kisayansi inayotumia mbegu za kiume/manii yaliyo na ugonjwa huu pia unaweza kusambaza bakteria wanaosababisha ugonjwa huu. Mchoro 15: Mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa wa kutupa mimba. Vijusi vilivyoharibika na tando za vijusi hivyo kutoka kwa wanyama walioambukizwa husambaza viini vya ugonjwa huo kwenye malisho. Wanyama walio katika hatari ya kuambukizwa/wadhaifu kiafya humeza bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanapokula malishoni na kusababisha maambukizi mapya. [INST] Kupanuka na kufura kwa korodani (kende) moja au zote (miongoni mwa madume) [/INST] Kukosa kutoka kwa baadhi ya viungo vya kuwalinda watoto wanapokuwa tumboni mwa mama (kwa mfano kondo au mfuko wa mimba) [INST] Uwezekano wa binadamu kuambukizwa [/INST] Binadamu anaweza kuupata ugonjwa huu kutoka kwa wanyama walioambukizwa kwa kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa na kushika vijusi au viungo vya vijusi viliyoathirika. Ili kuzuia binadamu kuambukizwa, chemsha maziwa, pika nyama vizuri na kuepuka kugusana na viungo/tishu zilizoathirika. Wakati wa kusaidia wanyama kuzaa, unafaa uvae mavazi ya kinga. [INST] Unyonyaji wa maziwa mengi [/INST] Ndama, vifungua mimba (waliozaliwa na ng’ombe jike aliye mchanga kiumri), wako katika hatari kuu ya kuambukizwa kuliko waliozaliwa na ng’ombe aliyewahi kuzaa hapo awali [INST] Mifugo hupata minyoo hii kutokana na ulaji wa nyasi zilizo na mayai au mabuu ya minyoo hiyo. [/INST] Mchoro 17: Maambukizi ya minyoo hiyo hutokea ikiwa mifugo/wanyama watakula lishe iliyo na kinyesi kilicho na minyoo au mabuu/viluwiluwi hivyo [INST] Maradhi ya kuvuja/kutokwa na damu [/INST] Magonjwa yanayosababisha umwagikaji/uvujaji mkubwa wa damu, yakiwemo maambukizi ya damu, kimeta na ugonjwa wa chambavu (donda kubwa kwenye paja hasa la mguu wa nyuma), yanaangaziwa katika sehemu hii. [INST] Uambukizaji [/INST] Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu huwa kwenye mate yanayotoka mdomoni na puani, na katika kinyesi. Huenea kupitia kwa malisho yaliyoambukizwa na mnyama anayeugua au anayebeba viini hivyo mwilini bila kuonyesha dalili. Kupe na nzi wanaouma/pangevipanga, wameripotiwa kuwa wasambazaji wa bakteria hawa. Mchoro 7.1: Maambukizi ya Damu kutokana na kikohozi, malisho yaliyoambukizwa kwa mate au kinyesi. Wanyama wengi hufa kutokana na ugonjwa huu ikiwa watakosa kutibiwa. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Mara nyingi huathiri wanyama wachache kwenye kundi, na unapatikana sana katika maeneo yenye mafuriko ya maji. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Asilimia kubwa (hadi 80%) ya wanyama wagonjwa hufa. Vifo hivi vinaweza kutokea ghafla lakini wakati mwingine hutokea siku 2—8 baada ya dalili za mwanzo kuonekana. [INST] Hali hatari zinazochangia maambukizi [/INST] Ugonjwa huu huzuka katika msimu wa mvua. Hasa kutokana na msongo wa mawazo unaohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa k.m. mvua ya ghafla inayotokea punde baada ya kiangazi. [INST] Dalili za ugonjwa huu kwa wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Viungo vya ndani kufura na kugeuka vyekundu, majimaji kwenye mapafu, majimaji yasiyo na rangi kupatikana ndani ya ngozi na mapafu yaliyoathirika. [INST] Mifugo wengine wanaoambukizwa [/INST] Kimeta ni ugonjwa wa wanyama wenye damu moto (kama vile mamalia) wakiwemo ngamia, kondoo, mbuzi na swara n.k. Wanadamu wanaweza pia kupata ugonjwa huu kwa kugusana na damu, viungo vya ndani, na vitu kutoka kwa wanyama walioambukizwa, kuvuta hewa yenye seli za bakteria,kushika au kugusa bidhaa za wanyama hao na ulaji wa nyama iliyoathirika. Kwa hivyo, unahimizwa kuwa mwangalifu sana unapowahudumia wanyama wagonjwa na mizoga ya wanyama. [INST] Uambukizaji [/INST] Kimeta husababishwa na bakteria/kiini kinachoweza kuishi udongoni kwa muda mrefu (hadi miaka 60) na sugu/ konachostahimili joto, ukame, baridi kali na kemikali za kuua viini. Ugonjwa huu unaweza kuzuka katika maeneo ambayo wanyama hukusanyika, kwa mfano, mahali pa kunywa na pa kuramba magadi ya udongoni. Huambukizwa kupitia kwa malisho na vyakula vilivyoambukizwa viini hivyo. Nzi na wadudu wengine wanaweza kusambaza ugonjwa huu kutoka kwa mnyama mmoja hadi mwingine. Mchoro 18: Uambukizaji wa kimeta hutokea wanyama wanapomeza viini vya kimeta vinavyoishi udongoni wakati wanapokuwa malishoni. Ugonjwa huu husababisha kifo cha ghafla; Damu nyeusi hutoka kwa wingi hasa mdomoni na kitakoni mwa wanyama waliokufa. Mizoga hiyo isipozikwa na kufukiwa vizuri, bakteria walio katika viungo vya mizoga hiyo huingia kwenye malisho na udongoni. Hiki huwa chanzo cha maambukizi kwa wanyama wanaolishwa kwenye malisho hayo. [INST] Utupaji/uzoaji mbovu wa mizoga [/INST] Wanyama wanaweza kupata kimeta kwa kugusana moja kwa moja au vinginevyo na wanyama walioathirika au bidhaa zao. [INST] Mara nyingi, wanyama wanaoonekana kuwa wenye afya katika kundi huambukizwa [/INST] Mara moja moja, mnyama mgonjwa huonyesha dalili za ugonjwa huo kwa mara ya kwanza licha ya kuwahi kuugua maradhi haya bila kuonyesha dalili hapo awali: kupepesuka, kupumua kwa shida, kutetemeka, kuanguka, kuzirai na kupigapiga miguu (degdege kama mtu wa kifafa), damu kutoka kwenye sehemu za mwili zilizo na uwazi, na kifo. [INST] Dalili za ugonjwa huu kwa wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Damu nyeusi, isiyoganda na kutoka kwa wingi katika viungo vyote vya mwili vilivyo na uwazi (mdomoni, puani na kitakoni) bila kukoma Mzoga haukakamai yaani haujikazi na kuwa mgumu (yaani rigor mortis) kama inavyotarajiwa kwa mnyama aliyekufa. [INST] Kinga [/INST] Wafahamishe maafisa wa tiba/afya ya mifugo kuhusu visa vyovyote vinavyoshukiwa kuwa kimeta na vifo vyovyote vya ghafla Wanyama wanaoshukiwa kufa kutokana na kimeta hawafai kuchunwa ngozi au viungo vyake kufunguliwa wazi, kwani hewa huwasaidia bakteria kuunda utando au ukingo unaowalinda Maboma ya wanyama hayafai kutumiwa hadi wanyama wote walio kwenye hatari wachanjwe, na mizoga yote kuzikwa na kufukiwa kwenye shimo refu au kuchomwa Hakikisha kwamba mizoga yoyote ya wanyama waliokufa kwa kimeta na vitu vilivyoambukizwa vinazikwa (vinafukiwa) kwenye shimo refu la angalau futi 6. [INST] Kukabiliana na kimeta miongoni mwa wanadamu [/INST] Kuna aina tatu kuu za kimeta zinazoambukiza wanadamu kulingana na njia ya kuingia kwa bakteria wake mwilini. Kwa kawaida, kimeta huingia mwilini kupitia kwa ngozi (kimeta ya ngozi), ya mapafu (kimeta ya kupumua), au mfumo wa utumbo (kimeta ya utumbo). Aina hizi zote za kimeta hatimaye zinaweza kusambaa katika mwili wote na kusababisha kifo ikiwa hazitatibiwa kwa dawa za kuua vijasumu (antibiotics). [INST] Uambukizaji [/INST] Uambukizaji hutokea pale mnyama anapomeza nyasi zilizo na bakteria wanaosababisha ugonjwa huu; viini hivi huishi kwenye udongo na njia ya chakula ya mnyama. Miongoni mwa kondoo, ugonjwa huu hasa hutokea baada ya mnyama huyo kupata jeraha. Mchoro 19: Chambavu hutokea pale mnyama anapomeza bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanaoishi kwenye udongo. [INST] Kulemaa kwa miguu/kushindwa kutembea [/INST] Uvimbe mwekundu na mchungu katika nyama ya sehemu iliyoathirika, kisha baadaye kupoa na uchungu kuondoka [INST] Damu kuganda haraka [/INST] Sehemu iliyovimba hugeuka kuwa nyeusi, viungo vya ndani hubadilika rangi na kutoa harufu mbaya na viputo vya hewa (air bubbles). [INST] Magonjwa yanayotambulika kwa mkojo mwekundu [/INST] Sehemu hii inaangazia dalili za ugonjwa wa Mkojo Mwekundu (Babesia, yaani homa ya kupe), ugonjwa unaotambuliwa kwa mnyama kukojoa mkojo mwekundu. [INST] Uambukizaji [/INST] Kupe wa bluu/samawati wa kike waliokomaa (wanaojulikana kisayansi kama Rhepicephalus Boophilus) hupata viini kutoka kwa mnyama aliyeathirika. Kisha huvisambaza kwa vizazi vyao kupitia kwa mayai. Kisha mabuu (au kupe wachanga) huvisambaza wanapowafyonza/wanapowanyonya wanyama wengine damu. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Utokeaji wa ugonjwa huu kwenye kundi hutofautiana, kulingana na sababu kadhaa. Katika maeneo ambayo ugonjwa huu hutokea kwa kawaida, dalili chache sana za ugonjwa huu huonekana. Mikurupuko ya ugonjwa huu inaweza kutokea ikiwa ndama ambao hawajawahi kuathiriwa na kupe wakiwa wachanga zaidi, watapelekwa kwenye eneo lililoathiriwa na/au ikiwa kupe walioambukizwa watavileta viini hivyo katika eneo lisilo na kupe. [INST] Magonjwa mengine ya kieneo [/INST] Magonjwa ya kieneo hupatikana sana katika maeneo ya ufugaji wa ng'ombe kwa wingi. Sehemu hii itaangazia ugonjwa wa malale (Nagana), ndigana baridi na kititi/ugonjwa wa kiwele [INST] Uambukizaji [/INST] Ng’ombe wanaweza kuupata ugonjwa huu kwa kuumwa na mbung'o au wadudu wengine wanaouma kama vile nzi wa kumma yaani pange kipanga (kisayansi wanaitwa Tabanids na Stomoxys mtawalia). Mchoro 23: Uambukizaji wa malale kupitia kwa mbung'o waliomuuma mnyama aliyeambukizwa hadi kwa yule aliye katika hatari ya kuambukizwa. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika [/INST] Tafiti zinaonyesha kwamba hadi thuluthi moja (1/3) ya wanyama kwenye kundi hupata ugonjwa huu, lakini hili hutofautiana kulingana na idadi ya mbung'o na nzi hao wengine wa kuuma. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Karibu wanyama wote walio na ugonjwa huu hufa ikiwa hawatatibiwa. Maradhi haya hukaa sana kabla ya kusababisha kifo. Katika hali za kawaida, hadi 3% hufa kutokana na ugonjwa huu. [INST] Hupatikana sana katika maeneo ya wanyama wengi wa porini. [/INST] Wanyama wengi huugua punde msimu wa mvua unapoisha kutokana na kuongezeka kwa mbung'o na nzi wa kuuma. [INST] Uambukizaji [/INST] Kupe husambaza viini/vimelea hivyo kutoka kwa wanyama walio na ugonjwa huo mwilini hadi kwa wanyama wazima wanapowafyonza damu. Ugonjwa huu unaweza pia kusambazwa kupitia kwa nzi wanaouma. [INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Kulingana na idadi ya kupe walioathirika katika eneo, na aina ya ng’ombe walioathirika. Ng’ombe wa aina za kiasili kama vile Zebu na Boran hawaathiriwi sana kwa sababu ya ustahimilivu wao wa maambukizi ya kupe. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Ng'ombe wa umri wa kati ya mwaka mmoja na miwili huonyesha ghafla dalili za ugonjwa huu, ambazo hujitokeza kama homa/joto mwilini, kukataa chakula, kupumua kwa juujuu na kwa haraka, kusita kutembea na tando za kamasi kubadilika rangi, lakini kifo si rahisi. Ng'ombe wa maziwa walioathirika pia hupunguza kiwango chao cha maziwa. Ng'ombe wanaozidi miaka miwili huonyesha dalili za ugonjwa huu ghafla kisha kufa kwa ghafla. Mara nyingi wanyama hawa hupatikana wamekufa. Idadi ya vifo inaweza kuanzia asilimia 30 — 50 kwa wanyama wanaozidi miaka miwili ambao wameonyesha dalili za ugonjwa huu. Wanyama walioambukizwa huendelea kuwa na ugonjwa huu mwilini maishani mwao na ndio huambukiza wengine kwenye kundi. [INST] Hali hatari zinazochangia maambukizi [/INST] Kuleta ng’ombe mgeni aliyeathirika kwenye kundi na uwepo wa wadudu wanaoambukiza (kupe na nzi wa kuuma) [INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Mara nyingi wanyama huwa hawaonyeshi dalili yoyote ya ugonjwa huu. Hata hivyo, kwa nadra dalili huwa: [INST] Dhibiti kupe [/INST] Tafuta usaidizi wa Afisa wa Afya ya Mifugo na kutibu ugonjwa huo haraka iwezekanavyo punde dalili zinavyojitokeza [INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu husambazwa kutoka kwa mnyama mmoja hadi mwingine kupitia kwa mikono iliyoambukizwa na kutodumisha usafi kwenye maboma ya mifugo. Mchoro 25: Maambukizi ya bakteria wanaosababisha kititi. Hii hutokea mtu asipozingatia usafi wakati wa kukama.Husambaa hasa unapomkama ng’ombe aliyeambukizwa, kabla ya kuwakama wanyama ambao hawajaambukizwa. Bakteria wanaosababisha kititi huhamishwa kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa hadi kwa yule aliye hatarini kwa kutozingatia usafi. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Kifo kinaweza kusababishwa na kititi kipevu (hatari) kinachotokana na bakteria wenye sumu ndani ya damu [INST] Ng’ombe wanaotoa maziwa mengi wako kwenye hatari zaidi [/INST] Matumizi ya mbinu zisizo za kawaida za kukama kama vile kutumia mkojo na mate kulainisha matiti unapokama. [INST] Kiwele (robo moja au zaidi) kufura, kuwa kigumu, na moto, kikishikwa kinaweza kugeuka chekundu [/INST] Rangi yake kubadilika, kiwango cha maziwa kupungua na maziwa yasiyokuwa ya kawaida (kuwa na damu au kugeuka rangi ya manjano) [INST] Mradi wa Kuzidisha Ubora wa Chakula cha Siku zijazo (AVCD) nchini Kenya - Kitengo cha Mifugo [/INST] Mwongozo wa nyanjani wa magonjwa ya mifugo kwa kutegemea dalili zao katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya [INST] Awamu ya 2: Magonjwa ya wanyama wadogo wa kucheua [/INST] Dibaji Magonjwa ya mifugo hupunguza kiwango cha ufugaji na biashara za mifugo, hasa katika maeneo ya ufugaji ambako huduma za tiba ya mifugo ni adimu. Mifumo mipana ya ufugaji inayotumiwa maeneo haya- kama vile ufugaji wa kuhamahama, uhamaji wa kila msimu na mifumo-mseto ya ufugaji na ukuzaji wa mazao kwa pamoja- inazua changamoto zaidi kutokana na ulishaji wa pamoja wa mifugo, uhamaji wa kila mara na mwingiliano kati ya mifugo na wanyamapori. Tafiti za hivi majuzi katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya (miongoni mwa jamii za Waborana, Warendille, Waturkana, Wasomali na nyingine za wafugaji) zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuambukiza kama vile Homa ya Mapafu inayosambaa haraka, ugonjwa wa mapafu ya mifugo, Sotoka ya Wanyama wa Kucheua (PPR), kimeta, ugonjwa wa vinundu vya ngozi na ugonjwa wa miguu na midomo hutokea kila mara. Tafiti hizo, kadhalika, zinaonyesha kuwa jamii hizi hutumia kiwango kikubwa cha dawa za tiba ya mifugo kudhibiti magonjwa haya lakini tiba nyingi hutumika bila ushauri wa kitaalamu. Kwa hivyo, kuna uwezekano kwamba nyingi ya tiba hizi hazifai. Hata muhimu zaidi ni kuwa, kipindi cha baada ya matumizi ya dawa hizo ni kifupi kuliko inavyotakiwa, hali inayozua hofu kuwa bidhaa za mifugo kama hao zina kiwango kikubwa cha mabaki ya dawa. Idara ya Huduma za Afya ya Mifugo (DVS), kwa ushirikiano na mashirika ya kimaendeleo ya humu nchini na kimataifa, imetekeleza mikakati mseto ya kuhamasisha na kuzuia magonjwa katika eneo la kaskazini mwa Kenya. Hata hivyo, hatua hizi zinapaswa kutekelezwa na wadau wote katika sekta hiyo ili zifanikiwe. Wamiliki wa mifugo, kwa mfano, wanao mchango mkubwa katika ufuatiliaji wa matukio ya magonjwa kwa kutoa ripoti kuhusu mikurupuko ya magonjwa hayo. Usahihi wa taarifa zinazotolewa unaweza kuimarishwa kupitia ufundishaji wa wafugaji kuhusu dalili na ishara za magonjwa wanayokumbana nayo mara kwa mara. Mwongozo huu utatumiwa kuwapa mafunzo wafugaji wa kieneo, watoaji wa taarifa za magonjwa katika kiwango cha kijamii, matabibu/wahudumu wa kibinafsi wa afya ya wanyama, wauzaji wa dawa, wafanyabiashara na wadau wengine wahusika kuhusu magonjwa na mbinu za kuyadhibiti magonjwa ya kieneo ili kuimarisha uwezo wao wa kusaidia kufaulisha juhudi za utekelezaji wa mikakati ya ufuatiliaji na ukabilianaji na magonjwa hayo. Muundo wa Mwongozo huu umechochewa na Mwongozo wa Nyanjani wa Magonjwa ya Wanyama unaotegemea Dalili (yaani A Field Manual of Animal Diseases by Syndromes) - uliochapishwa mwaka wa 2013 na Mradi wa Viwango, Mbinu na Taratibu za Afya ya Wanyama (yaani Standards Methods and Procedures in Animal Health -SMP-AH) kama sehemu ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, Ukanda wa Afrika Mashariki; Ofisi ya Umoja wa Afrika ya Inter-African kuhusu Rasilimali za Wanyama; Idara ya Marekani ya Kilimo - Kitengo cha Kilimo cha Kigeni; na Chuo Kikuu cha Georgia, Athens nchini Georgia. Hata hivyo, mwongozo huu ni sehemu ya jozi/awamu tatu za miongozo inayoangazia magonjwa ya kieneo ambayo huathiri hasa ng’ombe, kondoo, mbuzi na ngamia katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya. Hii ni tofauti na mwongozo wa SMP-AH uliokarabatiwa mahsusi kwa ajili ya magonjwa yanayoathiri biashara za mifugo. [INST] Utaratibu wa mwongozo huu [/INST] Mwongozo huu umewasilishwa katika awamu tatu; Awamu hii ya 2 inaangazia magonjwa ya wanyama wadogo wa kucheua. Magonjwa hayo yameanishwa katika makundi tisa kulingana na dalili zayo kuu; yaani, kuathiriwa kwa mfumo wa kupumua, maambukizi/uvamizi wa ngozi, madonda ya miguu na midomo, ukosefu wa utulivu, kuharibika kwa mimba/ujauzito, kuhara/mharo, magonjwa ya kutokwa na damu ghafla, mkojo mwekundu na magonjwa mengine ya kieneo. Mada zilizoangaziwa chini ya kila ugonjwa huo ni; majina ya wenyeji, wanyama wanaoathiriwa, uambukizaji, idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi, idadi ya vifo, usambaaji/msambao, hali hatari zinazochangia maambukizi, dalili za ugonjwa, wanyama waliokufa/mizoga, na kinga. Mwongozo huu ni nakala inayoweza kuimarishwa baada ya muda kwa kutegemea michango kutoka kwa wadau mbalimbali watakaohusishwa. [INST] Shukrani [/INST] Watu wengi walichangia katika utayarishaji wa mwongozo huu. Wanajumuisha maafisa wa afya ya wanyama kutoka kaunti za Turkana, Marsabit, Isiolo, Garissa na Wajir walioshiriki katika warsha za mafunzo; Michael Baariu, Dabasso Barako, Changayo Orkhobeshe, Ehele Haile, Stephen Mutahi, Boku Bodha, Adano Umuro, Dennis Mwongela, Joseph Muriira, John Koskei, Siyat Onle Takal, Abubakar Siraj, Job Ronoh, Jane Akale, Daud Abukar na Anthony Ngugi. Joseph Mathooko kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo pia alishiriki. Pia tunatambua michango ya Waratibu wa Nyanjani wa AVCD (Adan A. Kutu (Isiolo), Abdisemed Osman (Wajiri), Simon Chuchu (Marsabit) na Viola Chemis (Turkana) katika kaunti lengwa walioboresha mwongozo huu kwa kutegemea maoni yaliyotolewa na maafisa wa nyanjani katika kaunti, Watoaji Taarifa kuhusu Magonjwa katika Jamii (CDRs) na wafugaji katika ngazi ya kijiji. [INST] Marejeleo yaliyopendekezwa: [/INST] Bett, B., Kihu, S., Wamwere-Njoroge, G. Hambe H. and Kiara, H. 2019. Field manual for livestock diseases based on syndromes in pastoral areas in northern Kenya. Small ruminant diseases (Volume 2). Accelerated Value Chain Development (AVCD) Livestock Component. Nairobi, Kenya: ILRI. [INST] Magonjwa yanayoathiri Mfumo wa kupumua [/INST] Magonjwa yanayoangaziwa katika sehemu hii hubainika kwa kuangalia jinsi mnyama anavyopumua kama dalili kuu ya ugonjwa. Homa ya mapafu (CCPP) miongoni mwa mbuzi ndio ugonjwa maarufu zaidi unaoangaziwa katika sehemu hii . [INST] Mifugo wengine wanaoathirika [/INST] Ugonjwa huu hasa huambukiza mbuzi. Hata hivyo, unaweza kuathiri kondoo wanaochanganywa na mbuzi wagonjwa. [INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama mgonjwa anaweza kuusambaza ugonjwa huu kupitia matone ya pumzi (droplets) yake anayopumua nje kisha mbuzi mzima kiafya kuyavuta ndani ya mwili wake anapopumua. Wanyama wazima kiafya wanaogusana au kusogeana karibu na mnyama aliyeambukizwa huwa katika hatari kuu ya kuupata ugonjwa huu. Mchoro 1.1.1 Unaonyesha jinsi ugonjwa huu wa mapafu (CCPP) unavyosambazwa. Mnyama aliyeathiriwa husambaza kiini kinachousababisha kupitia matone (droplets) yanayomtoka anapokohoa. Wanyama walio hatarini ambao wako karibu naye huvuta ndani kiini hicho kilichoingia hewani (kwenye matone), na kuongeza hatari ya kusababisha maambukizi. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Karibu wanyama wote kwenye kundi ambao hawajawahi kuambukizwa viini hivi wanaweza kuupata ugonjwa huu. Hata hivyo, ni takribani nusu yao huonyesha dalili za ugonjwa huo. [INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unapatikana katika maeneo yote ya wafugaji na huenea polepole katika maeneo yote ambayo wanyama hao huhamishiwa. [INST] Kufadhaika/kiwewe [/INST] Kuwepo wa wanyama wadhaifu kiafya (ama kwa sababu hawajawahi kuambukizwa viini hivyo au hawajachanjwa). [INST] Kiwango cha juu cha joto/homa [/INST] Kiwango cha vifo hutofautiana (kiko juu katika maeneo ambayo hayajawahi kuushuhudia, na katika wanyama wachanga kiumri) [INST] Magonjwa yenye maambukizi na uvamizi wa ngozi kwa jumla [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa ambayo dalili yake kuu ni maambukizi ya ngozi. Haya yanajumuisha upele unaowasha ambao huathiri jamii zote za mifugo, pamoja na tetekuwanga ya kondoo na mbuzi [INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama mzima kiafya hupata ugonjwa huu kwa kugusana moja kwa moja na mnyama aliyeathiriwa, au kujisugulia katika sehemu ambazo wanyama wenye ugonjwa huu walijisugulia. Pia wanaweza kuupata wanapolala katika sehemu ambazo wanyama walioambukizwa walilala. Husababishwa na vimelea (aina fulani ya viroboto) vinavyojipenyeza ndani ya ngozi. Vimelea hivyo vinaweza kuishi katika mazingira kama hayo kwa muda wa hadi wiki mbili. Mchoro 2.1.1 Unaonyesha jinsi upele unaowasha unavyosambazwa kutoka kwa wanyama walioathiriwa hadi kwa wanyama wazima kiafya. Mchoro huu, aidha, unaonyesha wanyama walioathiriwa wakijisugulia kwenye miti (kama mfano). Katika harakati hii ya kujisugua, wanaacha hapo chembechembe za ngozi zilizo na vimelea vya upele ambao unaweza kuwaambukiza wanyama wazima kiafya wanaojisugulia kwenye miti iyo hiyo. [INST] Idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi [/INST] Kwa kutegemea mfumo wa ufugaji na mbinu za kuudhibiti zinazotumika, thuluthi (mmoja kwa watatu) ya wanyama kwenye kundi huathiriwa. [INST] Katika aina fulani ya upele unaowasha, uvimbe hutokeza kwenye ngozi [/INST] Sehemu zilizoambukizwa huanza kuwasha na kusababisha mnyama kuanza kujiuma na kujisugulia kwenye kuta, miti n.k [INST] Tumia dawa inayofaa kulingana na ushauri wa afisa wa tiba ya mifugo [/INST] Picha 2.12 (b) Mbuzi anayeugua upele unaowasha akionekana kupoteza manyoya, kuwa na mabaka magumu ngozini na kujisugua sehemu iliyoathiriwa kutokana na mwasho [INST] Uambukizaji [/INST] Mate na majimaji mengine kutoka kwenye ngozi hubeba virusi. Madonda au mabaka ya ngozi pia yanaweza kusababisha maambukizi mapya hata baada ya muda mrefu. Madonda hayo yanaweza kudumisha virusi hivyo katika kivuli kwa hadi miezi sita. Wanyama wazima kiafya wanaweza kugusana na wale walioathiriwa na hivyo kuambukizwa. Kondoo wanaweza kuwaambukiza kondoo wengine pekee tetekuwanga ya kondoo huku mbuzi nao wakiwaambukiza mbuzi wenzao pekee. Maambukizi yanaweza kusambazwa kupitia hewani wakati wa kulisha kundi la wanyama. Nzi wanaouma pia wanaweza kusambaza virusi vya tetekuwanga. Mchoro 2.1.3 Waonyesha jinsi tetekuwanga ya kondoo na mbuzi inavyosambaa kupitia migusano au hewa kutoka kwa wanyama walioambukizwa hadi kwa wale wazima kiafya wakati wanapolishwa pamoja. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Katika maeneo yanayoshuhudia ugonjwa huu, wanyama wachache, karibu asilimia 5-10 hufa. Wana wa mbuzi na kondoo huwa katika hatari kuu ya kufa. Hata hivyo, katika maeneo ambayo hayajawahi kushuhudia ugonjwa huu, wanyama wengi, hadi asilimia 100, hufa. [INST] Magonjwa yenye madonda miguuni na midomoni [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa yanayodhihirika kupitia madonda makuu kwenye mdomo na kwato. Maradhi haya yanajumuisha mwozo wa kwato unaoweza kuwaathiri mifugo wote, ugonjwa wa miguu na midomo (FMD), unaoathiri wanyama wote wenye kwato na vidonda vya kuambukizana (orf) ambavyo vinaweza kuathiri mbuzi. [INST] Uambukizaji [/INST] Kuzoesha mnyama kwenye unyevunyevu kwa kipindi kirefu kunaweza kusababisha maambukizi ya bakteria wanaokaa ngozini au katika mazingira kwa muda mrefu. Bakteria hao hujipenyeza ndani ya ngozi na kusababisha ugonjwa huu., Pia bakteria hao wanaweza kujipenyeza katika jeraha la kwato na kusababisha kwato kuoza(copy from Cattle Manual). Picha 3.1.1 Inaonyesha kondoo na mbuzi waliofungiwa katika maboma yenye tope/unyevunyevu yanayowaweka katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa mwozo wa kwato. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Wanyama walioathiriwa kwa kawaida huwa hawafi. Hata hivyo, kiwango cha maziwa katika mbuzi wa kukamwa pamoja na uzito wa nyama ya mbuzi walioathiriwa hupungua kutokana na shida ya kutembea na hivyo kupunguza ulaji wa chakula. [INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa katika kundi [/INST] Wanyama wote wenye mwanya katika kwato zao wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu. Kondoo na mbuzi wanaweza kuathiriwa na FMD lakini hili ni nadra unapolinganisha na ng’ombe. [INST] Uambukizaji [/INST] Wanyama wenye afya hupata ugonjwa huu wanapogusana au kukaribiana na majimaji yanayotoka mwilini kama vile mate, kamasi, mkojo, maziwa, kinyesi au mbegu za kiume (manii) za mnyama aliyeambukizwa. Virusi vinavyosababisha ugonjwa huo vinaweza kubebwa na upepo; nao wanyama walio katika hatari ya kuambukizwa wanaweza kuathiriwa wanapovuta ndani hewa iliyoambukizwa na virusi hivyo. Vivyo hivyo, virusi hivi vinaweza kuishi kwenye mazingira haya kwa siku kadhaa, hasa katika msimu wa unyevunyevu. Msimu huu huwa ndio kiini cha maambukizi kwa wanyama wadhaifu kiafya. [INST] Idadi ya wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Husambaa haraka miongoni mwa wanyama wadhaifu kiafya na kuna uwezekano mkubwa kuwa wanyama wote katika kundi kama hilo wanaweza kuambikizwa. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Miongoni mwa wanyama waliokomaa, ugonjwa huu si hatari kwa kuwa wengi wa wanyama hawa hufanikiwa kupona wanapoambukizwa. Hata hivyo, wanyama wachache wachanga hufa kutokana na matatizo ya moyo. [INST] Uhamishaji au usafirishaji ama utembezaji wa wanyama [/INST] Kutumia eneo moja kuwanyweshwa maji, malisho ya pamoja au maeneo mamoja ya kuramba udongo wenye magadi Msimu wa kiangazi huzidisha utembeaji wa wanyama kwa kuwa visima vyenye maji ya kuwanywesha huwa vichache. Malisho ya pamoja pia huchangiamaambukizi. [INST] Mifugo wengine wanaoambukizwa [/INST] Mbuzi na kondoo wote wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu, lakini huathiri mbuzi zaidi. Ngamia pia wanaweza kuathiriwa hasa wale wachanga. [INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu huambukiza wanyama wazima kiafya kutoka kwa wanyama wagonjwa kupitia kwa kugusana. Wanyama wazima kiafya huwa kwenye hatari ya kuambukizwa wanapojigusisha kwenye madonda au kugusana na wanyama walioathiriwa. Mara nyingi maambukizi huenea kupitia majeraha kwenye ngozi pale wanyama wanapokula nyasi au matawi yenye ncha kali au magumu. Virusi vya ugonjwa huu vinaweza kudumu kwenye vidonda kwa muda mrefu katika maeneo kame. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Wengi wa wanyama, hasa wachanga, huathiriwa. Ugonjwa huu huathiri sana mbuzi kuliko kondoo. Maambukizi yanayotukia mara ya pili baada ya mnyama kupona huweza kutokea kwa sababu ugonjwa huu huwa haujengi kinga thabiti mwilini (kinga ya daima). [INST] Idadi ya vifo [/INST] Upele wa mdomoni wa kuambukizana kwa kawaida hauui, lakini majeraha yanayozuka kwenye mdomo yanaweza kumzuia mnyama mwathiriwa kukosa kula, hasa miongoni mwa wanyama wachanga. [INST] Vidonda huzuka kwenye mdomo na pua ya mnyama (Picha 3.4) [/INST] Vidonda hivyo hugeuka kuwa madonda magumu kwenye mdomo (Picha 3.5), ingawa wakati mwingine madonda haya yanaweza kuenea hadi ndani ya mdomo, (sehemu za chini ya miguu, na matiti ya majike yanayonyonyesha). [INST] Mipasuko sehemu zilizoathiriwa [/INST] Ugonjwa huu mara nyingi hudumu kwa majuma manne hadi sita, halafu mnyama huyo huanza kupona polepole mwenyewe [INST] Nyunyiza dawa ya kuua viini katika maboma au maeneo ambako wanyama hukaa [/INST] Osha mikono kwa sabuni baada ya kugusa/kushika madonda ya orf kwa kuwa virusi vyake vinaweza kuambukiza hata binadamu [INST] Magonjwa yenye dalili za kuhangaika/kiwewe [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa yanayodhihirika kwa dalili za ukosefu wa utulivu kama vile kujizungusha, kufinyilia kichwa mahali n.k. Magonjwa makuu yanayoangaziwa hapa ni maji kujaa kwenye moyo na kichaa cha mbwa (T9). Magonjwa haya yote huathiri jamii nyingi za wanyama. [INST] Uambukizaji [/INST] Viini vinavyosababisha ugonjwa huu husambazwa na kupe, hasa wenye rangi mbalimbali. Kupe wasiokuwa na viini hivi huvipata kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa wakati wanapomnyonya/kumfyonza damu yake. Viini hivyo hukua vikiwa kwenye kupe huyo na kisha kusambazwa wakati kupe huyo anapomnyonnya damu mnyama mwingine. [INST] Picha 4.11 Kupe wenye rangi mseto wanaosambaza viini vinavyosababisha maji kujaa kwenye moyo [/INST] Picha 4.1.2 Inaonyesha mzunguko wa maambukizi ya viini vinavyosababisha ugonjwa wa maji kujaa kwenye moyo. Kupe hawa wenye rangi mbalimbali) huvipata viini hivyo kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa wakati anapomnyonya damu na kuvisambaza hadi kwa mnyama mwingine anapomnyonya damu pia. [INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika katika kundi [/INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika hutofautiana kulingana na wingi wa kupe, maambukizi ya hapo awali na mbinu zinazotumika kukabiliana na ugonjwa huo. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ya wanyama wanaokufa baada ya kuambukizwa ugonjwa huu huwa juu katika maeneo ambayo haujawahi kushuhudiwa. [INST] Kifo cha ghafla [/INST] Kukosa utulivu huongezeka muda unavyosonga, hali inayosababisha ukosefu wa uthabiti wa kutembea, utoaji ulimi nje, uinuaji miguu zaidi ya kawaida wakati wa kutembea, ufinyiliaji kichwa mahali na kujizungusha. Mwishowemnyama mgonjwa huanguka na kuanza kupigapiga miguu (degedege). [INST] Uambukizaji [/INST] Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu hutokana na kuumwa na mnyama aliyeathiriwa, hasa mbwa na wanyamapori wa jamii ya mbwa. Mate yanayotoka kwa mnyama huyo aliyeathiriwa huwa na virusi ambavyo huingia mwilini mwa mnyama anayeumwa. Mchoro 4.2.1 Unaonyesha mzunguko wa maambukizi ya kichaa cha mbwa, ambao ni ugonjwa wa virusi unaoweza kuambukiza pia binadamu. Mnyama mwenye kichaa hiki kama vile mbwa au mbuzi humuuma mwenzake, na katika hali hiyo kusambaza virusi hivyo kupitia kwa mate yake. Ugonjwa huu ni hatari kwa wanyama. Iwapo mwanadamu ataumwa, osha jeraha haraka kwa kutumia maji yenye sabuni kisha utembelee kituo cha afya kilicho karibu kwa matibabu ya haraka. [INST] Kukosa kula au kunywa [/INST] Utembeaji usiokuwa wa kawaida na kupungua kwa hisi; kupungua kwa hisi sanasana huathiri miguu ya nyuma. [INST] Kabiliana na idadi ya mbwa koko [/INST] Wanyama walioambukizwa wanafaa kuuawa kitaalamu (ambako hakuna uchungu) ili kupunguza maambukizi zaidi [INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Mifugo wote wanaweza kuathiriwa, lakini ugonjwa huu ni maarufu sana miongoni mwa kondoo na mbuzi. Ugonjwa huu unasababishwa na minyoo wachanga (viluwiluwilu/mabuu) wa tegu miongoni mwa mbwa na wanyama wengine wala-nyama. [INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] [INST] Magonjwa yanayosababisha mimba kutoka [/INST] Mabaki ya tegu yanapatikana katika ubongo au uti wa mgongo. Mabaki hayo huwa na urefu wa angaa sentimita tano. [INST] Uambukizaji [/INST] Magonjwa yanayohusisha mimba kutoka k.m Homa ya Rift Valley (RVF) na ugonjwa wa maziwa (ugonjwa wa kutupa mimba), yameangaziwa kwa kina katika sehemu hii. [INST] Picha 5.1.1 Mbu wa Aedes ametambuliwa kama msambazaji mkuu wa viini vya RVF [/INST] Mbu hupata virusi vya ugonjwa huu anapomnyonya damu mnyama aliyeambukizwa. Kisha humwambukiza mnyama mzima kiafya anapomnyonya damu. Mbu wa jamii ya Aedes hutambuliwa kama mbebaji wa viini vya ugonjwa huu huku mbu wale wengine kama vile culex, anopheles, na nzi wa kuuma/pange wakitajwa kama wasambazaji wa raundi ya pili ya maambukizi. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Watu huambukizwa ugonjwa huu kwa kugusa damu na majimaji ya mwili wa wanyama walioambukizwa wakati wanapowachinja, au wanapowasaidia kuzaa au wanapogusa vitoto/vijusi vilivyofia tumboni na viungo vyao. Binadamu pia wanaweza kuambukizwa kwa kula nyama au viungo vya wanyama walioambukizwa visivyopikwa vizuri au kwa kuumwa na mbu. Picha 5.1.2 Mzunguko huu unaoonyesha jinsi maambukizi ya virusi vya homa ya Rift Valley yanavyofanyika. Huwa wanasambaza virusi hivyo kwa mifugo wakati wanapowanyonya damu. Pia wanaweza kuambukiza binadamu virusi hivyo, lakini visa vingi vya homa ya Rift Valley miongoni mwa wanadamu hutokana na mgusano wa moja kwa moja na wanyama wanaougua ugonjwa huo. Hili hutokea binadamu anapomsaidia mnyama anayetupa mimba au wakati wa kuchinja wanyama walio wagonjwa. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Huathiri wanyama wengi, hasa baada ya msimu mrefu wa mvua kubwa wakati ambapo mbu wengi huzaana na kukua. [INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unaweza kuua karibu asilimia 10-50 ya wanyama wachanga. Wanyama waliokomaa wanaweza kuambukizwa lakini wengi wanaoambukizwa hawafi (karibu asilimia 10 pekee ndio hufa). [INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu hutokea hasa baada ya msimu mrefu wa mvua kubwa na ya mafuriko. Visa vichache pia hutokea wakati wa mvua ya kawaida, lakini mara nyingi visa vinavyotokea katika hali kama hii hukosa kubainishwa. Ugonjwa huo nchini Kenya hutokea hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki, pwani, Kati ya Kenya, na kaskazini mwa Bonde la Ufa (Naivasha, Baringo, Uasin Gishu na Trans Nzoia). [INST] Uzuiaji wa ugonjwa wa maziwa miongoni mwa binadamu [/INST] Chanzo kikuu cha kusambaa kwa ugonjwa wa maziwa ni ulaji wa lishena unywaji wa maji yaliyoambukizwa kutokana na wanyama walioathirika. viini . Watu wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu kutokana na unywaji wa maziwa mabichi yaliyoambukizwa au vijusi na kondo/tando zinazolinda vijusi hivyo tumboni. [INST] Uambukizaji [/INST] Kuhakikisha binadamu anakunywa maziwa yaliyochemshwa, upikaji bora wa nyama na kuepuka kugusana moja kwa moja na viungo vya wanyama walioambukizwa. Harakati ya kumsaidia mnyama kuzaainafaa itekelezwe kwa kutumia mavazi ya kujikinga mwili. [INST] Idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi [/INST] Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu hutoka na kinyesi, au kutokea katika mate na machozi ya wanyama walioambukizwa. Wanyama wazima kiafya hupata ugonjwa huu kwa kugusana moja kwa moja na kinyesi chenye virusi. Aidha, ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kupitia majimaji ya hewani pale wanyama walioambukizwa wanapowekwa pamoja au kwa karibu na wazima kiafya. Mchoro 6.1.1 Ukionyesha jinsi virusi vya PPR vinavyoambukizwa kupitia kwa kikohozi kutoka kwa wanyama walioambukizwa hadi wanyama wazima kiafya. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Miongoni mwa wanyama walio hatarini, wengi wao huambukizwa. Kiwango cha maambukizi mapya hasa huwa chini katika maeneo ambayyo ugonjwa huu hutokea mara kwa mara. Wanyama wachanga huathiriwa zaidi ya wanyama waliokomaa. [INST] Kutembea au kusafirishwa kwa wanyama [/INST] Wengi wa wanyama walioathirika, hasa miongoni mwa wale wachanga, hufa. Wanyama waliokomaa huweza kustahimili ugonjwa huu kwa muda mrefu hadi wanapopona hatimaye. [INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Kipindi kirefu cha kiangazi kinachochangia wanyama wengi kujazana katika maeneo machache yenye maji na malisho. [INST] Uambukizaji [/INST] Majimaji yasiyo na rangi kutokea puani katika hatua za awali za ugonjwa huu. Baadaye majimaji hayo huanza kuwa mazito katika hatua za baadaye [INST] Idadi ya vifo [/INST] Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu huuenea kupitia pumzi ya wanyama walioambukizwa. Pia huunea kupitia kwa mate, majimaji mengine yanayotokea mdomoni, puani na katika kinyesi. Usambaaji wake hufanyika kupitia kwa lishe iliyoambukizwa au kupitia kwa wanyama wagonjwa au wanyama wanaoubeba mwilini. [INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Asilimia kubwa (hadi asilimia 80) ya wanyama wagonjwa hufa. Kifo kinaweza kutokea ghafla lakini wakati mwingine hutokea siku 2 hadi 8 baada ya kuonekana kwa dalili za mwanzo. [INST] Uambukizaji [/INST] Kimeta ni ugonjwa wa wanyama wa damu moto wanaojumuisha ngamia, ng’ombe, swara n.k. Wanadamu pia wanaweza kuupata ugonjwa huu kwa kugusa damu, viungo, na bidhaa nyinginezo za wanyama walioambukizwa, au kuvuta hewa yenye bakteria wakati wa kushughulikia bidhaa za wanyama walioambukizwa na ulaji wa nyama ya wanyama hao walioathiriwa. [INST] Hali hatari zinazochangia maambukizi [/INST] Kimeta husababishwa na chembechembe ya bakteria ambayo inaweza kuishi katika udongo kwa kipindi kirefu na huwa sugu kwa joto, kiangazi, baridi kali na kemikali za kuua viini. Ugonjwa huu unaweza kutokea katika maeneo ya kukusanyika kwa wanyama kama vile mahali wanapokunywa maji na penye udongo wa magadi ya kuramba. Huwa unaambukiza kupitia ulaji wa malisho yaliyoambukizwa bakteria hao. Nzi na wadudu wengineo wanaweza kuueneza ugonjwa huu kutoka kwa mnyama mmoja hadi kwa mwingine. Picha 7.2.1 Uambukizaji wa kimeta hufanyika kwa wanyama wanapomeza chembechembe za bakteria wa kimeta wakiwa malishoni. Ugonjwa huo husababisha kifo cha ghafla na damu iliyokolea weusi humtoka mnyama aliyekufa hasa kupitia mdomoni na kitakoni. Wanyama wafu wasipozikwa na kufukiwa, bakteria walio miilini mwao husambaa katika malisho na udongo; hiki huwa chanzo cha maambukizi kwa wanyama wengine. Visa vya kimeta miongoni mwa wanadamu huhusishwa na mgusano wa moja kwa moja au vinginevyo na wanyama walioambukizwa au bidhaa zao.. [INST] Mara nyingi wanyama wenye hali nzuri kiafya katika kundi huambukizwa [/INST] Ugonjwa huu huhusishwa na msimu mrefu wa mvua kubwa baada ya kiangazi cha muda mrefu, mafuriko, hali ya hewa yenye joto la wastani na uharibifu wa udongo. [INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Mara moja moja, mnyama aliyeathiriwa anaweza kuonyesha dalili hizi hata iwapo hakuna ushahidi wowote wa kuwahi kuugua ugonjwa huo hapo awali. [INST] Karantini [/INST] Damu nzito, nyeusi hutoka kwa wingi kwenye viungo vilivyo wazi mwilini (mdomo, pua, kitako) bila kuganda [INST] Wanyama wengine wanaoambukizwa [/INST] Hakikisha kuwa mzoga wa kimeta pamoja na vitu vyote vilivyoambukizwa vinavizikwa katika shimo la kina kirefu (futi sita) Usiwahi kumchinja mnyama aliyekufa kutokana na kimeta. Mzoga wake haujikazi (kukakamaa) kama inavyotarajiwa. [INST] Uambukizaji [/INST] Ng’ombe na ngamia. Ugonjwa huu hutokea mara kwa mara miongoni mwa kondoo na mara chache miongoni mwa mbuzi, na nadra sana katika ng’ombe. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Bakteria fulani walio na sumu, ambao huishi katika utumbo, huzaana na kisha kuingia kwenye mishipa ya damu. Katika hali ya kawaida, wanyama hula lishe iliyoambukizwa kupitia kwa kinyesi, kisha bekteria hao huingia kwenye mfumo wa kusaga/kumeng’enya chakula lakini huwa hawasababishi ugonjwa huo hadi hali inapokuwa shwari kwa maambukizi. Mchoro 7.3.1 Unaonyesha malisho yaliyoambukizwa bakteria hao wenye sumu. Malisho hayo huambukizwa kupitia kwa kinyesi kilicho na viini hivyo kisha kuambukiza wanyama. Dalili zinazojitokeza zinajumuisha mnyama kukosa hamu ya kula na kifo cha ghafla cha wanyama wanaoonekana kuwa na afya nzuri. [INST] Uambukizaji [/INST] Mkurupuko unaweza kuathiri kundi zima la wanyama. Ugonjwa huu hasa huathiri wanyama wanaoonekana kuwa na afya nzuri. [INST] Picha 8.1.1 Ni kupe wa bluu anayesambaza viini vinavyosababisha ugonjwa wa mkojo mwekundu [/INST] Uambukizaji wa ugonjwa wa mkojo mwekundu hutokea pale kupe wa kike wakomavu wa rangi ya bluu (samawati), wanaotoka kwa mnyama aliyeathirika, wanapojipenyeza ngozini mwa mnyama asiyeathirikakisha wakamwambukiza mnyama huyo viini vya ugonjwa huo. Kupe hao huwa wanawarithisha watoto wao viini hivyo kupitia kwa mayai. Halafu viluwiluwi/mabuu (au watoto hao wa kupe) nao husambaza viini hivyo wanapomnyonya damu mnyama mzima kiafya. [INST] Idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi [/INST] Picha 8.1.2 Mchoro unaoonyesha maambukizi ya homa ya kupe kutokana na kupe waliobeba viini katika malisho yaliyoambukizwa viini hivyo. [INST] Kukosa hamu ya chakula [/INST] Hutofautiana pakubwa - katika maeneo yanayoshuhudiwa ugonjwa huu mara kwa mara, visa vya maradhi hayo huwa vichache sana. [INST] Wengu (spleen) iliyofura, nyeusi, na rahisi kukatika [/INST] Uwezekano mkubwa wa wanyama walioathiriwa kujitenga na wenzao, kuwa wadhaifu, kuhangaikana kusita kutembea [INST] Mifugo wengine walioathiriwa katika [/INST] Kibofu cha mkojo kinaweza kuwa na mkojo mwekundu wenye weusi au wenye rangi ya chokoleti (hudhurungi) [INST] Uambukizaji [/INST] Ngamia na ng’ombe, ingawa kuna uwezekano ipo tofauti za aina za viini zinazoambukiza kila jamii ya mnyama [INST] Picha 9.1.1 Inaonyesha nzi wa kuuma (Pange) na Mbung’o [/INST] Mbuzi na kondoo wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kuumwa na mbung’o au nzi wa kuuma (pange). Maambukizi ya viini hivi yameonyeshwa hapa chini katika Picha 9.1.2. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Picha 9.1.2 Inaonyesha maambukizi ya malale kupitia kwa mbung’o, kutoka kwa mnyama aliyeathiriwa hadi kwa mnyama aliye hatarini kuambukizwa. [INST] Idadi ya vifo [/INST] Tafiti zinaonyesha kuwa hadi thuluthi (mmoja kati ya watatu) ya kondoo na mbuzi kwenye kundi wanaweza kupatwa na ugonjwa huu, lakini hilo hutofautiana sana kutegemea idadi ya mbung’o na nzi wa kuuma waliopo. [INST] Usambaaji [/INST] Karibu kondoo na mbuzi wote wanaougua ugonjwa huu hufa iwapo hawatibiwi. Wanyama walioambukizwa huugua kwa muda mrefu. Katika hali za kawaida, hadi asilimia tatu ya kondoo na mbuzi katika kundi hufa kutokana na ugonjwa huu. [INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu hutokea katika maeneo ambapo mbung’o hupatikana. Nzi wa kuuma huzidisha usambaaji wa ugonjwa huu, hasa iwapo kuna maskani/makazi yao eneo hilo. [INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Kupe husambaza viini vinavyosababisha ugonjwa huu wakati wa kunyonya damu ya wanyama wasiokuwa wagonjwa. Ugonjwa huu pia unaweza kuambukiza kupitia kwa nzi wa kuuma/pange. Picha 9.2.1 Jinsi maambukizi ya ndigana bari yanavyoenezwa na kupe wa bluu waliovamia eneo la malisho ya wanyama. [INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Kwa kawaida, ugonjwa huu hauonyeshi dalili za wazi miongoni mwa kondoo na mbuzi. Wanyama wachache huambukizwa katika tukio lolote lile la ugonjwa huu.