text: Wahudumu wa afya Ninawezaje kujilinda na namna gani virusi hivi vinasambaa? Maswali kadhaa yamekuwa yakiulizwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali duniani. Je, barakoa(mask)inasaidia kukinga maambukizi ya virusi vya corona Watu wengi wameanza kuvaa barakoa Kuna ushahidi mdogo sana kuwa barakoa inasaidia kwa namna moja au nyingine. Wataalamu wanasema kuwa usafi wa mara kwa mara wa watu kuosha mikono na kutojigusa mdomoni kunasaidia zaidi. Je, virusi vya corona vinaweza kupatikana katika vitasa vya milango na vinaweza kukaa kwa muda gani? Maeneo mengi wameongeza kasi ya kufanya usafi Kama mtu ana maambukizi na akikohoa katika mkono wake na baadae kushika kitu , je kitu hicho kinaweza kupata maambukizi. Vitasa vya mlango ni mfano mzuri zaidi kuwa kuna hatari kubwa ya kupata maambukizi kama mtu mwenye corona akishika mlango wakati alikoholea mkono wake. Wataalamu wanadhani kuwa virusi vya corona vinaweza kukaa kwa muda wa siku kadhaa. Hivyo namna nzuri ya kukabiliana na jambo hili ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ni kunawa mikono mara kwa mara. Je, nikikutana kingono naweza kupata maambukizi? Haijawa wazi kama watu wakikutana kimwili wanakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya corona. Kwa sasa ni kukohoa na kupiga chapya ndio mambo yanayotajwa kuwa hatari katika maambukizi. Kuna utofauti gani kati ya corona na mafua? Dalili za maambukizi ya virusi vya corona na mafua yanafanana kwa kiasi kikubwa, hivyo inafanya tiba kuwa ngumu bila kupimwa . Dalili za virusi vya corona vinaweza kuanza kwa homa na kukohoa. Mafua mara nyingi huwa yana dalili nyingine kama koo kuwasha, huku watu wenye virusi vya corona huwa wanaweza kuishiwa pumzi kidogo. Je, virusi vya corona vinaambukiza zaidi ya mafua? Ni mapema mno kuweza kulinganisha lakini virusi vyote vinaambukiza. Kwa wastani virusi vya corona vinaweza kuambukiza watu wawili au watatu huku virusi vya mafua huwa ni kama vinatoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine. Ingawa maambukizi yote ya mafua na corona huwa yanasambaa kwa haraka. Je,mtu anaweza kupata virusi vya corona kwa kula chakula kilichoandalia na mtu mwenye maambukizi ya corona? - Mtu mwenye maambukizi ya corona kama amepika bila kuzingatia usafi basi moja kwa moja anaweza kumuambukiza mtu mwingine virusi vya corona. Virusi vya corona vinaweza kusambaa kwa matone ya kikohozi yaliyo kwenye mkono. Kuosha mikono kabla ya kushika na kula chakula ndio ushauri unaotakiwa kuuzingatia. Nichukue tahadhari gani? Kwa watu wanaoishi Italia na maelfu ambao wanasafiri maeneo mbalimbali duniani, wako kwenye hatari ya maambukizi zaidi. Maambukizi yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kwa njia ya matone ya kikohozi. Ni muhimu kwa watu kuzingatia kuosha mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni au dawa ya kuosha mikono(sanitiser). Ni vyema kujizuia kuwa karibu na mtu anayekohoa au mwenye homa. Mtu yeyote anayedhani kuwa amepata maambukizi ya corona ni bora kupigia simu daktari. Baadhi ya mataifa yamepiga marufuku kwa watu kukutana katika mikusanyiko Inawezekana ugonjwa huu kupata chanjo? Kwa sasa hakuna chanjo ya kujikinga na virusi vya corona, ingawa wanasayansi bado wanapambana kutengeneza chanjo ya aina hiyo. Hivi ni virusi vipya ambavyo havijawahi kumpata binadamu kabla. Je, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia athari zinazojitokea katika virusi vya corona? Haijawekwa wazi kama mabadiliko ya hali ya hewa yanachangia maambukizi. Baadhi ya virusi kama vya mafua huwa vinakuja mara nyingi katika wakati wa baridi kali. Je, mtu aliyeugua ugonjwa wa corona anaweza kupata maambukizi tena? Virusi hivi vipya vya corona , vinaweza kukusababisha mtu uugue na wengi ni watu wenye shida ya mapafu. Lakini virusi hivi vipya hakuna ambaye ana kinga dhidi yake. Hivyo haijalishi kama uliugua mwanzo au la. Aidha shirika la afya duniani limesema kuwa kabla ya miezi 18 kupita chanjo ya corona itakuwa imepatikana. Mlipuko wa maambukizi ya corona umeathiri mataifa mbalimbali duniani, na watu wakiwa wanajiuliza swali kuu moja: Maambukizi ya ugonjwa huu yakoje? text: Kazi ya uvuvi , imedhihirika nchini burundi sawa na nchi nyengine duniani kuwa ni wanaume tu ndiyo wanaifanya Mila za kumkataza mwana mke kuingia majini na kuvua samaki zimetokana na nini? BBC imefanya utafiti na kuzungumza na baadhi ya wavuvi wa kwenye ziwa Tanganyika , na baadhi ya wanawake wanao fanya biashara ya samaki karibu na kivuko cha kajaga. Mmoja wa wanawake hao ni Yolanda Hakizimana mwenye umri wa miaka 37,ambaye amejitokeza wazi kuelezea jinsi wanawake wanavyotengwa katika kazi hiyo ya uvuvi. ''Wanaume wavuvi husema mwanamke akiingia katika mtumbwi basi samaki wote majini wana tawanyika'' alisema. Wengine wanasema kuwa mwanamke akiwa katika hedhi au akiwa na mimba changa basi haruhusiwi kukaribia eneo la ziwa. Yolanda anayapuuza madai hayo na kusema kuwa ni dhana iliyopitwa na wakati na kwamba ni ukosefu wa kutojua wa wanaume. ''Inasikitisha kusikia wanaume wanadai mwanamke akingia majini kwa uvuvi samaki wanakimbia na kutawanyika'' ''Sisi tunasafiri kila mara katika mitumbwi kwenda DRC, mbona hakuna hasara ao ajali yoyote imewahi kutokea ?'' anauliza Yolanda. Ameongeza kuwa wakati umewadia na wanawake pia kufanya kazi ya uvuvi bila masharti. Bi Yolanda pia anapendekeza wanawake waruhusiwe kujiunga katika mashirika ya uvuvi kwa wanawake. Wanaume wengi kwenye eneo la ziwa Tanganyika wanapinga kauli hiyo na wanashikilia kuwa wanawake hawawezi kabisa kuwa wavuvi. Wanadai kuwa masuala ya hedhi na uja uzito yanaashiria udhaifu wa mwanamke. Lakini wataalaamu wa masuala ya ki jamii wanasema nini ? Professa Emile Mworoha, ambaye ni pia ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Burundi na mtaalam wa masuala ya Historia anasema kihistoria jamii ya Warundi imezungukwa na mila zinazo kataza mambo kadha wa kadha. Kazi ya uvuvi ni kazi ngumu sana kwa sababu inafanyika usiku, watu wengi wanahoji ikiwa mwanamke una kufanya kazi hiyo akiwa na mtoto mgongoni. "Ni tatizo kubwa haitoshi ukitathmini mila na desturi za Burundi unakuta mambo mengi yamekatazwa'' anasema Profesa Mworoho. Katika mila za kirundi, mwanamke haruhusiwi kupanda juu ya nyumba na kujenga dari, au afanye kazi ya kuuza nyama katia buchari au sokoni. Pamoja na hayo yote katika sekta nyinginezo mwanamke wa Burundi anashiriki katika kazi mbali mbali zinazo hitaji nguvu nyingi kama vile kuhudumu jeshini, polisi, au hata ujenzi wa barabara. Wanawake wengi nchini Burundi wangependelea kuwa wavuvi,Lakini hawaja thubutu kufanya kazi hiyo kutokana na na vikwazo vya kitamaduni. text: Gianluigi Buffon ameshinda Serie A mara kumi Kwenye kikosi hicho, maarufu kama Fifpro World XI, mlindalango Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya Manuel Neuer, naye beki wa AC Milan Leonardo Bonucci akachukua nafasi ya kigogo wa Barcelona Gerard Pique kwenye safu ya ulinzi. Mshambuliaji wa PSG Neymar, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi duniani naye ameingia nafasi ya Luis Suarez katika safu ya mashambulizi. Kikosi hicho kina wachezaji watano kutoka Real Madrid, wawili wa Barcelona, wawili wa PSG, mmoja wa Juventus na mmoja kutoka AC Milan. Hakuna mchezaji hata mmoja wa Ligi ya Premia aliyefanikiwa kujumuishwa katika kikosi hicho. Mkufunzi bora duniani soka ya wanaume Zinedine Zidane amemshinda meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya kuongoza Real Madrid kushinda La Liga msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 2012 na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mtawalia msimu uliopita. Conte alishinda Ligi ya Premia msimu uliopita. Massimiliano Allegri wa Juventus, ambaye aliongoza klabu yake kushinda Serie A na Coppa Italia msimu uliopita alikuwa wa tatu. Mkufunzi bora duniani soka ya wanawake Kocha wa Uholanzi Wiegman aliyeongoza Uholanzi kushinda Euro 2017 nyumbani kwao amechukua taji hilo. Waliwalaza Denmark kwenye fainali. Sarina Wiegman akipokea taji lake Kipa bora zaidi Mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa Serie A mara 10 Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa tuzo ya mlindalango bora duniani mwaka huu. Aliwasaidia Juventus kushinda taji la ligi mara ya sita mtawalia msimu uliopita. Aidha, alicheza dakika 600 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kufungwa. Buffon, 39, amewashinda kipa Keylor Navas, wa Real Madrid na Manuel Neuer wa Bayern Munich. "Ni heshima kubwa sana kwangu kupokea tuzo hii katika umri wangu huu," alisema Buffon. Uchezaji haki Mchezaji wa Togo Francis Kone, ambaye alimfanyia huduma ya dharura kipa wa Bohemians 1905 Martin Berkovec uwanjani wakati wa mechi ya ligi Jamhuri ya Czech mwezi Februari ametunukiwa tuzo ya uchezaji wa haki. Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza kikosi bora cha soka ya wanaume duniani mwaka 2017 ambapo kuna mabadiliko matatu kutoka kwa kikosi kilichotangazwa mwaka 2016. text: Magari zaidi ya 50 aina ya Toyota Prado hayajapatikana Chama tawala kilihesabu magari hayo mwezi mmoja kabla ya kuingia madarakani baada ya kupata ushindi uchaguzini mwezi Desemba. Imekuwa kawaida kwa baadhi ya maafisa wa serikali inayoondoka kutorejesha magari ya serikali, na hulazimu serikali mpya kuyatwaa kwa nguvu nchini Ghama. Waziri mmoja katika serikali iliyoondoka ya John Mahama hata hivyo amesema kuenezwa kwa habari kwamba wenzake walitekeleza uhalifu ni makosa. Aliyekuwa waziri wa usalama Omane Boamah ameambia mwandishi wa BBC Thomas Naadi kwamba hiyo ni "mbinu inayotumiwa na serikali mpya kuipa sababu za kununua magari mapya." Msemaji wa rais Eugene Arhin aliambia wanahabari kwamba maafisa wa serikali mpya walipata magari: Kituo cha redio cha Citi FM nchini Ghana kimeripoti kwamba rais amelazimika kutumia gari aina ya BMW lililoundwa miaka 10 iliyopita kutokana na kutorejeshwa kwa magari hayo. Nana Akufo-Addo (kulia) alimshinda John Mahama (kushoto) mwezi Desemba Alipokuwa anatoa taarifa yake, Bw Arhin alifichua kwamba afisi ya rais ilifaa kuwa na magari zaidi ya 300 lakini hakueleza magari hayo hutumiwa vipi. Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriotic Party alishinda uchaguzi mkuu mwanzoni mwa Desemba na kuchukua hatamu kutoka kwa John Mahama, wa chama cha National Democratic Congress. Serikali mpya nchini Ghana inayatafuta magari 200 yaliyokuwa yakitumiwa na afisi ya rais ambayo yanadaiwa kutoweka, msemaji wa rais amesema. text: Ousmane Dembele na Messi wakishangilia Kufuatia suluhu ya goli 1-1 katika mchezo wa awali, Chelsea walianza kufungwa na Lionel Messi ambaye alikuwa mchezaji bora kwenye mtanange huo hii ikiwa ni dakika ya 3 tokea kuanza kwa mchezo. Mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois hakuwa katika kiwango bora kwenye mchezo huo na kushuhudiwa kuruhusu magoli mepesi. Messi amefikisha magoli 100 kwenye michuano ya UEFA Dakika ya 20 Ousmane Dembele akaiandikia Barca goli la pili kufuatia pasi safi ya Messi baada ya kiungo wa zamani wa Barcelona Cesc Fabregas kupoteza mpira aliokuwa akiumiliki. Messi ambaye aling'ara vilivyo kwenye mchezo huo, akicheza anavyotaka, aliiandikia tena Barcelona goli ya tatu dakika ya 63. Ilishuhudiwa pia mkwaju wa Marcos Alonso ukigonga mwamba baada ya kupiga mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari la Barcelona. Alsonso pia alinyimwa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari na mlinzi kisiki wa Barcelona Gerard Pique. Kwa sasa Barcelona wanaungana na Real Madrid pamoja na Sevilla katika droo itakayofanyika Ijumaa. Kwa upande wa Chelsea wanaungana na Manchester United pamoja na Tottenham kuyaaga mashindano hayo. Chelsea wametupwa nje ya michuano ya klabu bingwa Ulaya katika hatua ya 16 bora, baada ya kupokea kichapo cha 3-0 kutoka kwa Barcelona. text: Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni. Utafiti wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito. Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto. Watafiti wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawafai kuwa na tashwishi yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao. Takriban mimba 225 nchini Uingereza huishia mtoto kuharibika na watafiti wa utafiti huo wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo wanawake wataendea kulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto. Utafiti huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida la Kujifungua ni mkubwa wa aina yake na unathibitisha tafiti ndogo nchini New Zealnd na Australia. Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni. text: Arsene Wenger na mshambuliaji wake Alexis Sanchez Kushindwa kwao kwa 3-0 na Crystal Palace kuliiwacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya sita ,na ponti saba nyuma ya klabu ya Manchester City iliopo katika nafasi ya nne huku ikiwa imesalia mechi nane pekee. Wenger ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu ameiongoza Arsenal katika nafasi nne bora za ligi hiyo katika miaka 20 aliyokuwa mkufunzi wake. Kuhusu timu nne bora, alisema: ''Tunaweza kuwa katika timu nne bora au la''. Raia huyo wa Ufaransa amepewa ombi la kandarasi ya miaka miwili ijapokuwa hajatangaza iwapo ataendelea au la. Kushindwa kwao kwa mechi tano kati ya 10 katika mechi za ligi kuu kumewafanya mashabiki wa Arsenal kumtaka Wenger kuondoka katika klabu hiyo. Alipoulizwa kuhusu hatma yake ya baadaye alisema: kile kitakachoamuliwa na bodi hakinihusu mimi. ''Ninafanya kile nilichoajiriwa kufanya, mchezo mzuri wa timu na kile mashabiki wanachotaka ambacho ni timu iweze kucheza vyema''. The Gunners watacheza dhidi ya Middlesborough siku ya Jumatatu. Wenger amekataa kujibu madai kwamba mshambuliaji Alexis Sanchez amepewa kandarasi mpya ya £300,000 kwa wiki. Arsenal inakabiliwa na changamoto kubwa kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Arsene Wenger ambaye ameongezea kuwa hakuna kilichobadilika kuhusu hatama yake ya siku zijazo. text: Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba shughuli ya kuwachagua mawaziri wake inaendelea "kwa mpango" na kwamba ni yeye pekee awajuaye watu watakaoteuliwa. Mbuneg wa zamani, Mike Rodgers, aliyekuwa akisimamia masuala ya usalama wa taifa katika kundi la mpito amejiuzulu. Kumekuwa na taarifa kwamba alisukumwa nje na shemejiye Bw Trump. Taarifa katika vyombo vya habari zimedokeza kwamba kuna mzozo mkali miongoni mwa maafisa wanaosimamia shughuli ya mpito upande wa Bw Trump, ambao makao makuu yao yamo katika jumba la Trump Tower, New York. Meya wa zamani wa New York, Rudolph Giuliani, ambaye anatarajiwa kupewa wadhifa mkuu, amesema shughuli ya mpito huwa ngumu na ni kawaida kukumbwa na matatizo madogo hapa na pale. Bw Trump ataapishwa kuwa rais 20 Januari mwaka 2017. Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametetea utaratibu wa mpito nchini humo na kusema hakuna mzozo kinyume na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari. text: Siku moja mbele yaani Januari 13, virusi hivyo vikaanza kuwa tatizo la dunia. Mgonjwa wa kwanza alirekodiwa Thailand kisha Japani, Korea Kusini zikafuatia haraka. Katika maeneo mbalimbali ya dunia wakaanza kuongezeka. Kufikia sasa zaidi ya watu zaidi ya milioni 4.8 wamethibitishwa kuugua corona duniani kote kutoka nchi kama Nepal mpaka Nicaragua. Lakini je wakati idadi ya vifo ikiongezeka, na hospitali zikifurika wagonjwa, bado kuna nchi ambazo hazina kabisa wagonjwa wa virusi vya corona? Jibu huenda likakushangaza, NDIO! Kuna nchi 193 ambazo ni wanachma wa Umoja wa Mataifa. Kufikia Mei 14 nchini 13 zilikua hazijaripoti mgonjwa hata mmoja wa virusi vya corona, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Hata hivyo nchi hizo hakuna hata moja iliyopo barani Afrika. Nchi ya Lesotho ilikuwa ya mwisho barani Afrika kupata mgonjwa wa corona, ambaye alithibitishwa siku ya Jumatano Mei 13. Nchini Korea Kaskazini hakujakuwepo mgonjwa aliyeripotiwa pamoja na majaribio zaidi ya makombora Nchi 13 zisizo na Covid-19 Kiribati; Lesotho; Visiwa vya Marshall; Micronesia; Nauru; Korea Kaskazini; Palau; Samoa; Visiwa vya Solomon; Tonga; Turkmenistan; Tuvalu na Vanuatu. Baadhi ya wataalamu wanaafiki kuwa nchi hizi zinaweza kuwa na wagonjwa ambao hawajaripotiwa. Korea Kaskazini kwa mfano, hakuna hata mgonjwa mmoja aliyeripotiwa jambo wataalamu wanamashaka na hilo. Lakini kuna nchi ambazo virusi havijafika. Vingi kati ya visiwa vidogo vyenye wageni wachache - saba kati ya visiwa 10 ambavyo havitembelewi duniani kulingana na data za Umoja wa Mataifa, viko huru na Covid-19. Umbali wake na maeneo mengine - unamaanisha kuwa kanuni ya kutochangamana tayari ndiyo maisha wanayoishi. Hata hivyo rais wa moja ya visiwa hivyo ameimambia BBC kuwa Covid-19 ni jambo la dharura kwao. Nauru, kisiwa kilichopo katika bahari ya Pasfiki, kiko takriban maili 200 (320 km) kutoka eneo lolote jingine - Kisiwa cha Banaba, sehemu ya Kiribati, ni kisiwa kilichopo karibu zaidi. Mji mkubwa uliopo karibu ni Brisbane, ambao upo maili 2,500 kusini magharibi. Kisiwa hiki kina takriban watu 10,000, ikiwa ni idadi ndogo zaidi baada ya ile ya wakazi wa Tuvalu. Ni moja ya maeneo ambayo yanatembelewa na watu wachache zaidi duniani ingawa hakionekani kwenye data za hivi karibu za Umoja wa Mataifa. Mmoja wa wanaoendesha biashara ya utalii nchini humo anasema kisiwa hicho kwa mwaka kinapokea watalii 160 tu. Unaweza kudhani kuwa maeneo hayo ya mbali kiasi hicho hayahitaji kujitenga zaidi. Lakini nchi yenye hospitali moja, bila mashine za kusaidia wagonjwa kupumua na ukosefu wa wauguzi haziwezi kuacha kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi. Sera hiyo, anasema rais Lionel Aingimea, inaitwa "Kuzuiwa kwa Maambukizi". "Tunazuia maambukizi mipakani, anasema rais. "Tunatumia uwanja wetu wa ndege kama mpaka." Wale waliowekwa karantini huchunguzwa iwapo wanadalili kila siku. Pale ambapo baadhi hukutwa na homa hutengwa zaidi na kupimwa ugonjwa wa Covid-19. Mpaka kufikia sasa vipimo vyote vilivyopelekwa Australia, vinaonesha kwamba hakuna mtu mwenye maambukizi. Licha ya kuishi katika kipindi hiki cha janga, wananchi wa kawaida wa Nauru "wako katika hali tulivu", anasema rais. "Tulipoanzisha sera hii ya karantini nilimuomba Mungu na akanipa aya ambayo nimeitunza moyoni mwangu nayo ni Zaburi 147, mstari wa 13 na 14. Hiyo imenitia nguvu wakati tunapopitia hali - kama Biblia inavyosema -hili bonde la mauti." Na huku akijaribu kuizuwia Nauru kupata maambukizi ya Covid-19, anafahamu fika kuwa maeneo mengine ya dunia hayana bahati kama hiyo. "Kila mara tunapoiangalia ramani ya [Covid-19] inaonekana kana kwamba dunia imekumbwa na mlipuko wa surua - kuna alama nyekundu kila mahali,"anasema "Kwa hiyo tunaamini kuwa maombi yetu kama taifa …tunaamini yatasaidia mataifa mengine yanayopitia vipindi hivi vigumu." Kuna madai kwamba taifa la Nauru lililo na umasikini wa kiwango cha juu halitaweza kudhibiti maambukizi hayo Nauru sio kisiwa pekee kidogo kilichoko katika bahari ya Pasifiki kilichotangaza hali ya dharura - Kiribati, Tonga, Vanuatu, na visiwa vingine wamefanya hivyo. Dkt Colin Tukuitonga, kutoka Niue Pasiifik Kusini, ana uhakika kuwa ni sera sahihi. " Kazi yao kubwa bila shaka ni kuhakikisha jinamizi hilo haliingii kwao ," amesema hayo kutoka New Zealand. "Kwasababu likiingia watakua wamepatikana, kusema kweli ." Dkt Tukuitonga ni mtaalamu wa afya ya umma , kamishna wa zamani wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa na sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Auckland Na amesema pia kwamba wakazi wengi wa visiwa vya Pacific tayari wana afya duni. "Maeneo haya mengi yana viwango vikubwa vya visa vya ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo na kifua-yote haya yanahusishwa na dalili mbaya za virusi vya corona ." Wanahitaji kusalia bila kuwa na kisa hata kimoja cha coronavirus. '' Kutengwa kwa visiwa vyao vyenye idadi ndogo ya watu vilivyotengwa sana katika bahari kubwa limekua ni tatizo kwao- lakini kwa sasa tatizo hilo limewakinga," he alisema. Idadi ndogo ya nchi zenye mipaka ya ardhi hadisasa pia havijapatwa na visa vya maambukizi ya coronavirus Ilikua ni Alhamisi tu ambapo Malawi, nchi isiyopakana na bahari yenye watu milioni 18 Mashariki mwa Afrika , iliporipoti kisa chake cha kwanza. Lakini ilikua imejiandaa kwa virusi hivyo. Nchi hiyo ilikua imetangaza "maafa ya kitaifa", ilifunga shulle na kufuta vibali vyote vya safari( Viza) kabla ya tarehe 20 Machi. Pia ilianza kupima anasema Dkt Peter MacPherson, katika taasisi ya mataalamu wa afya ya umma katika taasisi ya Liverpool School ya dawa za magonjwa ya maeneo ya jito, ambaye kazi yake inadhaminiwa na wakfu wa Wellcome anayeishi nchini Malawi. Anasema wiki moja au mbili zaidi "tumekuwa tukijiandaa'' na anaamini kuwa Malawi itakabiliana na virusi. Ramani Maambukizi yaliyothibitishwa duniani Weka taarifa mpya tafadhali Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneo Idadi ya hivi karibuni 1 Desemba 2020, 09:29 GMT +1 "Tumekua tukiathiriwa sana na janga la HIV kwa miaka 30 iliyopita na pia kifua kikuu," anasema. Ushahidi unaonyesha kuwa coronavirus itakwenda katika kila nchi, anasema Dkt MacPherson. Kwa hiyo sio Malawi, ni eneo gani ambalo litakua la mwisho duniani kupata Covid-19 ? "Kuna uwezekano mkubwa kuwa zitakua ni nchi hizo za Pacific Kusini , visiwa vilivyo maeno ya mbali ,ninaweza kubeti kwa pesa kuhusu hilo ," anasema Andy Tatem, Profesa wa masuala ya idadi ya watu na maeneo yao na magonjwa ya majanga katika Chuo Kikuu cha Southampton. "Lakini katika uchumi wetu wa utandawazi, sina uhakika iwapo kuna kokote kutakakoepuka ugonjwa wenye maambukizi wa aina hiyo ." Sheria za kutotoka nje kama -ile iliyowekwa Nauru - zinaweza kuwa na ufanisi, anasema, lakini haziwezi kudumu daima. "Nyingi kati ya nchi hizi zinategemea kiasi Fulani cha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje -ziwe za chakula au bidhaa nyingine pamoja au utalii. Inawezekana kuwa wanaweza kujifungia kabisa, lakini itawaletea athari mbaya-na hatiamae watalazimika kufungua mipaka yake ." Na ameonya kuwa, idadi ya visa haijapanda bado. "Sote tuna hizi sheria za kukaa nyumbani , kwa hiyo bado virusi havijasambaa kwa miongoni mwa watu sanana bado tuna watu wengi ambao hawajapata maambukizi. "Ni vizuri kwa mifumo ya afya, lakini hii ina maanisha kuwa bado tuna watu wengi duniani wanaoweza kupatwa na maambukizi . Tutaishi na virusi hivi kwa muda ." Tarehe 12 Januari chini ya miezi minne iliyopita - virusi vya corona vilikuwa ndani ya Uchina pekee. Hapakuwa na mgonjwa hata mmoja aliyekuwa amepatikana nje ya nchi hiyo ambayo virusi hivyo vilianzia. text: Stena Impero Wamililiki wa meli ya Stena Impero wanasema kwamba wameshindwa kufanya mawasiliano na meli hiyo. Kamati ya dharura ya serikali hiyo, Cobra, inakutana kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo. Bwana Hunt amesema kitendo hicho ''hakikubaliwi kabisa. ''Tunajua wazi kuwa hali hii haitakuwa rahisi kuitatua, kutakuwa na madhara makubwa,'' alisema. Iran yatangaza kukiuka mkataba wa nyukilia Marekani kubuni jeshi la nchi washirika kulinda maji ya Ghuba ''Hatuangalii suluhu ya kijeshi. Tunatafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua hali hii, lakini tunajua tunapaswa kushughulikia.'' Amesema wafanyakazi ndani ya meli walikuwa wa mataifa tofauti tofauti lakini hakuna raia wa Uingereza aliyekuwa akifahamika kuwa ndani ya chombo hicho. Chombo cha kampuni ya Stena Impero kilikuwa kikisafiri majini kikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London. ''Balozi wetu mjini Tehran anfanya mawasiliano na wizara ya mambo ya kigeni wa Iran kutatua hali hii na tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kimataifa,'' alisema. Tukio hili limefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Uingereza, Marekani na Iran. Meli ya Mesdar Jeshi limesema meli hiyo imekamatwa kwa kuvunja kwa sheria tatu: kuzima GPS; kuingia kwenye mpaka kupitia njia ya kutokea badala ya kuingilia; na kupuuza maonyo. Taarifa zinasema hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi na usalama wa wafanyakazi ni jambo la kwanza kwa wamiliki na mameneja. Tarehe 9 mwezi Julai, Uingereza ilieleza tishio la usalama katika maji ya Iran kwenye Ghuba ni ''kubwa''. Wakati huohuo, Marekani imedai kuwa imedungua ndege isiyo na rubani kwenye Ghuba, baada ya Iran kushambulia ndege isiyo na rubani katika eneo hilo mwezi Juni. Raisi wa Marekani Donald Trump amesema atazungumza na Uingereza kufuatia madai kuwa Iran imeikamata meli iliyosajiliwa nchini Uingereza. Stena Impero Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya meli katika maeneo muhimu ya usafirishaji tangu mwezi Mei. Tehran imekana shutuma zote. Mzozo kati ya Marekani na Iran umeshika kasi tangu Marekani ilipoongeza vikwazo dhidi ya Iran baada ya kuamua kujitoa kwenye mkataba wa nyukilia wa Iran wa mwaka 2015 Kutakuwa na 'madhara makubwa''ikiwa Iran haitaachia meli ya mafuta ya uingereza wanayoishikilia, Waziri wa mambo ya kigeni Jeremy Aunt ameeleza. text: "Ndugu wa kambi wa Donald Trump" Lakini hili halijazuia vicheko kwenye mitandao kutokana na picha hii. Wakati picha hii ilitumaa kwa ukurasa wa Facebook wa mchekeshaji na mtangazaji wa redio nchini Marekani Ricky Smiley, mamia ya watu walitoa maoni na maelfu ya wengine kusambaza picha hiyo. Ukweli ni kwamba mtu aliye kwenye picha hii na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo. Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo. Hii ndiyo picha iliyofanyiwa ukarabati ambapo anaonekana akimsalimia mcheza filamu raia wa Ghana Kofi Adu. Picha iliyofanyiwa ukarabati Labda mwenyewe umetambua hivyo. Huyu si ndugu wa kambo wa Donald Trump kutoka Kenya! text: PLO Lumumba Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema amesema hatua hiyo imeliletea aibu taifa hilo. Prof Lumumba, ambaye jina lake kamili ni Patrick Loch Otieno Lumumba, alikuwa atoe hotuba kuhusu ushawishi wa China barani Afrika leo Jumapili katika chuo kikuu cha Eden. Lakini baada ya kuwasili uwanja wa kimataifa wa Keneth Kaunda mjini Lusaka siku ya Jumamosi, alizuiwa kuingia ambapo alilazimika kurudi nchini Kenya. "Serikali kupitia idara ya uhamiaji imemzuia kuingia nchini Prof Patrick Lumumba, raia wa Kenya kutokana na sababu za kiusalama," Waziri wa habari na utangazaji Dora Siliya alisema. Kiongozi wa chama cha upinzani cha United Party for National Development, Hakainde Hichilema amesema hatua hiyo ya kumzuia msomi huyo imeliaibisha taifa hilo. Bw Hichilema alisema kudhalilishwa kwa Prof Lumumba ni thibitisho ya msimamo wa upinzani nchini humo kwamba serikali ya Zambia inaongozwa na 'viongozi wa kiimla'. Alisema kudhalilishwa kwa mtu kama huyo maarufu duniani kunaliharibia sifa taifa hilo. Kwa mujibu wa Bw Hichilema, aliyewania urais dhidi ya Rais Edgar Lungu mwaka 2016, walio hatari kwa Zambia ni wageni ambao wamekuwa wakinyakua ardhi na mali ya umma. China ndiyo mwekezaji mkubwa nchini Zambia na iko pia kwenye nchi kadhaa za Afrika, ikitoa misaada bila masharti na kandarasi nyingi hupewa Wachina. Mjini Lusaka na kote nchini, China iko mbioni kujenga viwanja vya ndege, barabara, viwanda na vituo vya polisi huku miradi mingi ikiwa inafadhiliwa na mikopo kutoka China. Deni la Zambia linakadiriwa kuwa dola bilioni 10.6 lakini kuna shaka kuwa serikali inaficha madeni. Profesa wa sheria na mtoa mihadhara maarufu kutoka Kenya Prof PLO Lumumba alizuiwa kuingia nchini Zambia kutokana na sababu za 'kiusalama' kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo. text: Ngano za kale zinaashiria kuwa baridi huzidisha maumivu - lakini kuna utafiti kidogo unaothibitisha athari za hali ya hewa. Na utafiti huu wa Chuo kikuu cha Manchester wa watu 2,500 uliokusanya data kwa kutumia simu za smartphone, umegundua kwamba maumivu yanazidi kuwa mabaya katika siku za joto, na zenye unyevu. Watafiti wanatumai kuwa matokeo yatasaidia kutoa muelekeo kwa utafiti wa siku za usoni kuhusu kwanini hali inakuwa hivyo. Ukimskia mtu akisema magoti yanamuuma kwasababu ya hali ya hewa ni jambo la kawaida - kawaida kutokana na baridi. wengine husema wanaweza hata kutabiri hali ya hewa kutokana na maumivu wanayoyapata kwenye viungo vya mwili. Lakini kufanya utafiti wa kisayansi kuhusu namna aina tofauti za hali ya hewa zinavyoathiri maumivu umekuwa vigumu. Utafiti wa siku za nyuma umekua mdogo au wa muda mrefu. Katika utafiti huu, ulioitwa 'Cloudy with a Chance of Pain', wanasayansi waliwakusanya watu 2500 wanaougua maumivu ya viungo arthritis, ya kichwa migraine kutoka nchini Uingereza. Walinakili maumivu waliohisi kila siku, kwa kati ya mwezi mmoja hadi miezi 15, huku simu zao zikinakili hali ya hewa waliko. Siku za Unyevu na zenye upepo ziliongeza uwezekano wa kuugua maumivu zaidi kuliko kawaida kwa 20%. Siku za baridi na zenye unyevu pia zilizidisha maumivu. Lakini hapakuwa na uhusiano wa ujoto pekee au mvua. 'Kutabiri maumivu' Profesa Will Dixon, mtaalamu wa yabisi kavu kutoka chuo kikuu cha Manchester, aliyeongoza utafiti huo anasema: "Imedhaniwa kuwa hali ya hewa huwaathiri wagonjwa walio na arthritis tangu [tabibu wa jadi wa ugiriki] Hippocrates. "Karibu robo tatu za watu wanaoishi na yabisi kavu wanaamini maumivu hutokana na hali ya hewa." Dixon anasema iwapo watafiti wengine sasa wanaweza "kutazama kwanini unyevu unahusiana maumivu, hilo litafungua milango kwa matibabu mapya". Na huenda ikawezekana kutengeneza "utabiri wa maumivu" unaoweza kuwaruhusu watu walio na maumivu makali kupanga shughuli zao. Watu walio na matatizo ya afya ya muda mrefu kama vile ugonjwa wa yabisi kavu au arthritis huenda wakahisi uchungu zaidi katika siku zenye unyevu, utafiti umeashiria. text: Spika Job Ndugai aliagiza CAG ahojiwe mwezi Januari akidai kuwa amelidharau Bunge Wabunge wamefikia uamuzi huo baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutaka waridhie mapendekezo yao dhidi ya CAG. Kamati hiyo ilimhoji CAG Januari 21 baada ya kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York mwezi Disemba 2018 ambapo alisema kuwa Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali. "…Kama tunatoa ripoti na inaonekana kuna ubadhilifu halafu hatua hazichukuliwi huo kwangu mimi ni udhaifu kwa Bunge. Bunge linatakiwa liisimamie (serikali) na kuhakikisha kuwa pahali penye matatizo basi hatua zinachukuliwa...Sie kazi yetu ni kutoa ripoti tu na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha lakini ni jambo tunaamini muda si mrefu huenda likarekebishika. Lakini tatizo kubwa tunahisi kwamba bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa," Profesa Assad aliiambia radio ya UN. Spika Job Ndugai alilieleza Bunge mwezi Januari kuwa maelezo ya Assad yalioonesha dharau kubwa dhidi ya mhimili huo na kumtaka aende mbele ya kamati kwa hiyari yake, ama apelekwe kwa pingu. Ripoti ya Kamati Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Maadili ya Bunge, mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema: "Tumejiridhisha CAG Assad amelidhalilisha Bunge na Kamati inamtia hatiani kwa kulidharau Bunge na kudhalilisha shughuli za chombo hiki." Mwakasaka amesema Prof. Assad alikiri mbele ya kamati kuliita Bunge dhaifu lakini alipingana na tafsiri ya neno 'dhaifu' iliyopo kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu inayosema 'goigoi, hafifu, isiyo imara' akisitiza kiuhasibu udhaifu ni 'upungufu'. "Tuliangalia maana ya neno upungufu kwenye kamusi tukabaini ni 'isiyo kamili, isiyo imara', hivyo alidhamiria kulidhalilisha Bunge," amesema Mwakasaka na kuongeza: "Tulimuuliza CAG Assad kama ataacha kulitumia neno udhaifu akasisitiza ataendelea kulitumia na hakujutia kulitumia dhidi ya Bunge. CAG hakuomba msamaha wala kujutia na akasisitiza ataendelea kulitumia neno hilo." Kamati hiyo pia imemtia hatiani mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee ambaye aliunga mkono kauli hiyo ya CAG kuwa Bunge ni dhaifu. Kamati imependekeza Mdee asimamishwe kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge kuanzia leo Aprili 2. Mdee aliiambia kamati kuwa aliunga mkono kauli ya CAG kwani ana uhuru kikatiba wa kutoa maoni yake. "...baada ya kumweleza maana ya neno 'dhaifu' kwa mujibu wa kamusi, alikiri kukosea kulitumia kuunga mkono kauli ya Prof. Assad, lakini hakuonyesha kujutia, hivyo alikuwa na dhamira ovu ya kulidharau na kulidhalilisha Bunge mbele ya umma," inaeleza sehemu ya ripoti hiyo. Hata hivyo, wabunge wa upinzani wamepingana vikali na ripoti ya kamati hiyo ya Bunge. Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amelieleza Bunge kuwa hatua hiyo dhidi ya CAG ni kuminya mawazo ya watu. "Mnataka kuwanyima watu haki na uhuru wa mawazo ilhali Katiba imeruhusu kila mtu, akiwamo CAG ana uhuru wa kutoa mawazo na kueleza fikra zake, kufanya mawasiliano na kutoingiliwa kuhusu taarifa yake...Kamati hii ya maadili haiwezi kutenda haki dhidi ya watu wanaoibua hoja zinazoonekana kutoifurahisha serikali," amesema Mbowe. Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema naye alisimama bungeni na kusema kuwa chombo hicho ni dhaifu. Hapo hapo, Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akaagiza ahojiwe na kamati ya maadili. Baada ya kauli hiyo, wabunge kadhaa wa kambi ya upinzani wakatoka nje ya bunge kuashiria mgomo wao. Kumwondoa kazini CAG Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, CAG huondoka madarakani baada ya kufikisha umri wa kustaafu ama kujiuzulu wadhifa wake. Ibara 144 ya katiba pia inasema CAG anaweza kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Hata hivyo, kuna utaratibu maalumu wa kumwondoa ambapo ibara ya 144 (3) inabainisha kuwa iwapo rais ataona kwamba suala la kumwondoa kazini CAG lahitaji kuchunguzwa, basi atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola. Iwapo Tume itamshauri rais kwamba huyo CAG aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi rais atamwondoa kazini. Wakati wa uchunguzi, rais anaweza kumsimamisha kazi CAG. Lakini uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini. Bunge la Tanzania limeazimia kutokufanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali, (CAG) wa nchi hiyo Prof Musa Assad baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za dharau kwa chombo hicho. text: Karibu watu 1800 wamefariki kutokana na Ebola nchini DRC katika kipindi cha mwaka mmoja uliyopita Jamii ya Kimataifa inajaribu kusaidia kukabiliana na ugonjwa huo lakini hofu na uvumi umewafanya watu kuwashambulia walewanaosaidia kukabiliana na ugonjwa huo - Karibu wafanyikazi saba wa afya wameuawa mwaka huu nchini DRC. BBC imezungumza na madaktari na wauguzi kuhusu hatari wanayokabiliana nayo wakijaribu kuokoa maisha. "Watu wanadhani ni uwongo hakuna Ebola," anasema Dkt Pascal Vahwere, mataalamu wa magonjwa ya kuambukiza anayefanya kazi ya kukabiliana na ugonjwa huo. "Tulishambuliwa kwa kufanya kazi yetu." Dkt Vahwere aliisimulia BBC kilichomkuta alipozingirwa na kundi la watu waliokuwa na hasira mwezi Machi alipokua akiongoza kundi la wafanyikazi wa afya kwenda kutoa chanjo katika kijiji kimoja mkoani Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC). "Ghafla tulishtukia tumezingirwa na kundi la watu waliojihami kwa silaha za moto na mapanga. Hatukujua kwa nini walitaka kutushambulia. Tuliogopa. Tulizungumza nao kupitia viongozi wa kijamii na hatimae waliondoka bila kutudhuru." Kituo cha matibabu ya Ebola kilishambuliwa mjini Butembo Mashariki mwa DRC, ambapo afisa mmoja wa polisi aliuawa na mfanyikazi wa afya kujeruhiwa Wafanyikazi wa umma wanawatambua watu ambao tayari wameambukizwa na kuwaleta katika vito vya matibabu. Pia wanawasidia kuwazika waliofarika. Lakini kwa ni hatari sana kwa wafanyikazi hao kwenda katika vijiji vilivyo na watu walioambukizwa Ebola. Huku maambukizi ya Ebola yakiendelea kusababisha vifo vya watu wengi, wafanyikazi wa afya nchini DRC wanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa na wanamgambo wenye hasira kufuatia uvumi unaosambazwa kupitia makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Karibu wafanyikazi saba wa afya wameuawa mwakahuu peke yake. BBC imezungumza na baadhi ya wale wanaokabiliana na ugonjwa wa Ebola kufahami ni nini kinachofanyika. Uvumi Nadharia ya njama na ukosefu wa mbinu ya kukabiliana na ugonjwa huo inawapandisha ghadhabu watu wanaokabiliwa na hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari. At least seven health workers have been killed this year in DRC "Kusambaa kwa taarifa za uwongo kumewafanya watu kuamini kuwa Ebola ni biashara ya kuwatengenezea pesa wanasiasa," anasema Dkt Vahwere. Anafanya kazi na shirika la Kimataifa la Afya mjini Goma, Mashariki mwa DRC. Mji huo uliripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa huo wiki mbili zilizopita. Kisa cha pili cha Ebola kiligunduliwa mjini humo wiki hii. "Baadhi yao hata wanasema matibabu ya ugonjwa huo yanalenga kuwaua watu," aliongeza. Mashambulio Uvumi huo umechangia ongezeko la mashambulizi hatari. "Kutoka Januari mosi hadi Julai 24 mwaka 2019, mashambulio 198 yameripotiwa dhidi ya vituo vya afya na wafanyikazi wake kama ilivyoratibiwa na WHO imesbabisha vifo vya watu saba na wengine 58 kujeruhiwa DRC," Sakuya Oka, Meneja wa Mawasiliano WHO aliiambia BBC. Richard Mouzoko aliuawa wakati wa shambulio dhidi ya Hospitali ya Chuo Kikuu ya Butembo Orodha ya waliouawa inajumuisha mtaalamu magonjwa yanayosababisha majanga wa ngazi ya juu wa WHO Richard Mouzoko. Aliuawa wakati wakati wa shambulio dhidi ya Hospitali ya Chuo Kikuu ya Butembo Aprili 19. Watu wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio hilo. Mwezi Mei wanavijiji Mashariki mwa DRC waliwashambulia wafanyikazi wa afya na kuiba vifaa katika vituo vya tiba. Tarehe 15 Julai wafanyikazi wawili wa afya walikuwa wakiendesha kampeini ya kukabiliana Ebola waliuawa majumbani mwao katika Mkoa wa Kivu Kaskazini. Kusambaa Visa vya mashambulizi hatari vinaendelea kupungua dhidi ya wale wanaokabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo. Serikali ya Congo imepeleka wanajeshi na polisi kutoa ulinzi kwa wahudumu wa afya Ilichukua takribani siku 224 kwa idadi ya visa vya maambukizi kufika 1,000, lakini ilichukua siku zingine 71 kufikia watu 2,000. "Kufikia (Jumatatu) wiki hii visa 57 vya ugonjwa wa Ebolaviliripotiwa katika kituo cha tiba cha Beni. Hii ni kumaanisha tunakabiliwa na kibarua kigumu kudhibiti hali ya mambo," anasema Dkt Freddy Sangala. Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo. Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi. Hakuna tiba ya Ebola, lakini ugunduzi wa mapema wa dalili zake na kukabiliana na nazo husaidia kuokoa maisha. Chanjo Hivi karibuni chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola imeanza kutumiwa na watu wamekuwa wakipewa chanjo hiyo ilikudhibiti maambukizi ya Ebola nchini DRC. Mhudumu wa afya akipeana chanjo ya Ebola Karibu watu 170,000 waliotangamana na watu waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari wamepewa chanjo. Lakini visa vya mashambulizi dhidi ya wahudumu wa afya vililemaza kampeini ya chanjo, hali iliyochangia kuongezeka na kusambaa zaidi kwa maambukizi mapya. Kutoaminiana na waasi Mlipuko wa Ebola unatokea katika eneo ambalo ni nyumbani kwa makumi ya makundi ya waasi. Baadhi yao wanalaumiwa na serikali kwa kufanya mashambulizi dhidi ya wahudumu wa afya. Baadhi ya wahudumu wa afya walazimika kuvaa mavazi maalum kwa kuhofia kushambuliwa "Cha kusikitisha ni kuwa tuna uwezo wa kiufundi wa kukabiliana na Ebola, lakini hatuwezi kufanya hivyo hadi mashambulizi yakomeshwe, itakuwa vigumu kukabiliana na mlipuko huu," Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliandika katika Twitter yake Mei 10 baada ya wahudumu wa afya kushambuliwa. Katika eneo la Kivu Kaskazini, kundi la waassi linalofahamika kama Mai-Mai linalaumiwa kwa kuhusika na baadhi ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na wafanyikazi wake kwa mujibu wa serikali. Kunsi lengine la waasi ni lile la Allied Defence Forces (Kundi la waasi wa Uganda linalofanya kazi DR Congo) pia linalaumiwa kwa kusababisha wahudumu wa afya kusitisha huduma zao. Kumekuwa na msururu wa maambukizi kutoka kwa kundi lingine lisilojulikana dhidi ya vituo vya tiba ya Ebola. Katika kisa kimoja Mwezi Mei, jamaa wa familia moja waliwavamia wahudumu wa afya waliyokuwa wakiwasaidia kuwazika jamaa zao. Mlipuko wa Ebola uliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umefikia mwaka mmoja leo (Agosti mosi) na umesababisha vifo vya karibu watu 1800. text: Dkt Vicensia Shule anasema ulinzi wa Dkt Magufuli ulimfanya anyamaze Katika kikao hicho Dkt.Vicensia amesema kwamba walijadili namna ambayo itaweza kutatua tatizo la rushwa ya ngono lililopo chuoni humo na mpaka sasa hawezi sema muafaka walioufikia kwa sababu yeye aliwasilisha na kuondoka. Ila anaamini kwamba jukwaa ambalo amepeleka ujumbe wake utafika na kuweza kutengeneza mazingira ambayo wahanga wa tatizo hilo wakapata nafasi ya kulizungumza kwa siri na kupunguza tatizo hilo kwa sababu si rahisi kulikomesha kabisa. Dkt Vicensia alizua mjadala mtandaoni baada ya kudai kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni humo na kuitwa kufika kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho. Barua ya kamati hiyo iliyotiwa saini ya mwenyekiti Prof Evelyne Mbede inamtaka mhadhiri huyo kufika mbele ya kamati hiso Ijumaa saa tisa "ili kamati iweze kulifanyia kazi swala hili kwa haraka." Dkt Vicensia Shule alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba alitaka sana kuufikisha ujumbe wake kwa Rais John Magufuli lakini aliwaogopa walinzi wake. Dkt Magufuli alikuwa amezuru chuo hicho kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) jijini Dar es Salaam. Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati ilijengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika. Dkt Shule alitaka kutumia bango kuufikisha ujumbe kwa rais huyo. Aliandika: "Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli." Alhamisi jioni, aliandika kwenye Twitter kwamba amepigiwa simu na kutakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya UDSM. "Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi," aliandika. "Kwa manusura wa udhalilishaji huu wa kingono, tunakaribia kufika, tutashinda, tutapata ushindi mkubwa!" Ingawa hakueleza ni rushwa ya aina gani iliyokithiri, katika vyuo vikuu vingine kumekuwepo na tatizo la wahadhiri na wanafunzi kutumia ngono katika kutoa alama katika mitihani. Aidha, baadhi ya wahadhiri hutuhumiwa kudai ngono kutoka kwa wenzao ndipo wawapandishe vyeo vyuoni. Tamko lake lilizua mjadala mtandaoni, baadhi wakikubaliana naye na wengine kumwambia angetumia tu ujasiri na kutimiza azma yake. Mtaalamu wa mawasiliano na mtetezi wa haki za wanawake Bi Maria Sarungi amesema Dkt Shule alipotoa kauli yake, pengine alitatarajia angeukwa mkono na baadhi ya viongozi lakini badala yake ameishia kulaumiwa na kushutumiwa. Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Vicensia Shule amehudhuria kikao cha kamati ya maadili cha chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuwaeleza njia ambazo wanaweza kuzitumia ili kuboresha maadili chuoni hapo. text: Hatua hiyo inajiri huku Mbunge huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi usiku kucha ambapo anasubiri kuwasilishwa mahakamani siku ya Alhamisi. Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya, licha ya wabunge wengi kushutumu jinsi ambavyo bwana Jaguar alitoa hoja yake , baadhi yao walikubaliana kwamba kuna swala tata kuhusiana na raia wa kigeni ambalo lilihitaji kuangaziwa. Kulingana na mtandao huo swala hilo liliwasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Uhusiano wa kigeni Katoo Ole Metito katika taarifa yake, akithibitisha kwamba raia wa kigeni hususan kutoka Jumuiya ya Afrika mashariki wana uhuru wa kufanya biashara nchini Kenya. ''Tunashutumu sana matamshi yoyote ya chuki yanayokiuka msimamo huu unaotuleta sisi pamoja kama taifa na kuthibitisha sera ya kuwakaribisha raia wote wa kigeni'', alisema mbunge huyo wa Kajiado kusini. Matamshi yake yaliungwa mkono na mbunge wa Suba Kaskazini John Mbadi ambaye aliwarai wabunge wenzake kutotoa matamshi mbele ya umma kwa lengo la kujitafutia umaarufu na badala yake kuchukua tahadhari. ''Kama bara, tunahitaji kukuza uwiano katika mipaka yetu ili kutafuta ajira; Wakenya wako huru kwenda Tanzania kufanya biashara iwapo biashara hiyo ni halali'', alisema Mbadi. ''Sio sera ya Kenya kuwafukuza Waganda, Watanzania au Wasomali iwapo wako hapa kulingana na sheria na wanafanya biashara halali''. Hatahivyo kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale, ambaye pia alishutumu matamshi hayo ya mbunge huyo wa Starehe alisema kwamba Kenya sio jaa la raia wa kigeni na bidhaa zao, kulingana na mtandao wa Citizen kenya. Kulingana na mbunge huyo wa Garissa mjini, Bunge pamoja na serikali zinafaa kuwalinda wananchi wa kawaida kutopoteza kazi kwa idadi kubwa ya raia wa kigeni waliomo nchini. Mbunge huyo alitaja mfano ambapo wataalam kutoka Kenya kama vile afisa wa kampuni ya Safaricom Sylvia Mulinge alinyimwa fursa ya kufanya kazi katika taifa jirani la Tanzania, akiongezea kuwa Kenya pia inafaa kutokubali maswala mengine. "Lazima ukweli usemwe; Unapoona biashara ya uchuuzi ikichukuliwa na raia wa taifa jingine tuna jukumu la kuwalinda watu wetu. Hawa wabunge hawafai kusahau kwamba kuku wetu walichomwa Tanzania , ng'ombe wetu walipigwa mnada Tanzania'', alisema Duale. ''Leo chini ya utawala uliopo Tanzania Wakenya hawawezi kufanya biashara, kwa nini bidhaa zetu haziingi Tanzania? Kwa sababu wametuwekea kodi ya juu''. Duale aliwataka wabunge kutolichukulia swala hilo na hisia, bali kuchukua tahadhari wanapochukua jukumu lao la kuwalinda raia wa kawaida. ''Kama bunge ni lazima tuamue na kuleta sheria zitakazolinda biashara zetu. Munaweza kumshutumu Jaguar, lakini leo ndiye mbunge maarufu zaidi katika eneo bunge lake'', aliongezea Duale. Naye mbunge wa Ugenya David Ochieng, kwa upande wake aliilaumu idadi kuu ya raia wa kigeni wanaofanya biashara nchini Kenya kwa kushindwa kwa serikali kuidhinisha sera yake. ''Katika uchumi wa leo , ni rahisi kununua bidhaa kutoka mataifa jirani kama vile Tanzania na Uganda na kuleta Kenya. Sio kwamba hatuna sheria, ni swala la utekelezwaji na ufisadi. Tunwaruhusu watu kuingia nchini na kuanza kuuza vitu barabarani. Huwezi kuwalaumu Watanzania kwa kufanya hivyo ni kwa sababu ya mfumo wetu ambao ni dhaifu'', alisema Ochieng'. ''Hatuwakagui watu wanaoingia nchini. Watanzania wanafanya kazi yao, ndio sababu wanaweza kujua kwamba Mulinge hakuhitimu kufanya kazi Tanzania. Hatahivyo Mbunge huyo alishutumu matamshi ya Jaguar , huku akilitaka bunge hilo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wabunge wanaoharibu jina la taifa hilo katika ulingo wa kimataifa. Tayari ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kupitia ukurasa wake wa Twitter imesema mbunge huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kuchochea ghasia. Katika kanda ya video iliosambazwa pakubwa nchini Kenya na katika nchi jirani Tanzania, mbunge huyo alisema hawatokubali watu wa nje waje kuendesha biashara nchini humo. Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles 'Jaguar' Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa. text: Joshua King Dirisha la usajili Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania pia zilifungwa katika saa tofauti tofauti Jumatatu. Hii hapa ni orodha kamili ya mikataba yote ilioafikiwa siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho Ulaya 2021. Uhamisho wa siku ya mwisho Ligi ya Premier 01:00: Joshua King [Bournemouth - Everton] kwa mkopo 01:00: Takumi Minamino [Liverpool - Southampton] kwa mkopo 23:39: Josh Maja [Bordeaux - Fulham] kwa mkopo 22:55: Ainsley Maitland-Niles [Arsenal - West Brom] kwa mkopo 22:00: Ozan Kabak [Schalke - Liverpool] kwa mkopo 20:00: Ben Davies [Preston - Liverpool] kwa pauni milioni 2 18:50: Joe Willock [Arsenal - Newcastle] kwa mkopo 18:00: Okay Yokuslu [Celta Vigo - West Brom] kwa mkopo 16:00: Moises Caicedo [Independiente del Valle - Brighton] kwa pauni milioni 4 Ligi ya Uingereza 00:45: Kieron Freeman [Swindon to Swansea] haijabainika 00:45: Jordon Garrick [Swansea to Swindon] kwa mkopo 00:45: Shane Long [Southampton - Bournemouth] kwa mkopo 00:20: Paul Arriola [DC United - Swansea] kwa mkopo 23:45: Anthony Gordon [Everton - Preston] kwa mkopo 23:45: Diallang Jaiyesimi [Swindon - Charlton] Haijabainika 23:45: Patrick Roberts [Manchester City - Derby] kwa mkopo 23:30: Jacob Mellis [Gillingham - Southend] haijabainika 23:30: Beni Baningime [Everton - Derby] kwa mkopo 23:30: Neeskens Kebano [Fulham - Middlesbrough] kwa mkopo 23:30: Max Sanders [Brighton - Lincoln] Haijabainika 23:20: Nicky Maynard [Mansfield - Newport] kwa mkopo 23:20: Derick Osei Yaw [Oxford - Walsall] kwa mkopo 23:20: Yan Valery [Southampton - Birmingham] kwa mkopo 23:15: Elijah Adebayo [Walsall - Luton] Haijabainika 23:15: Sam Field [West Brom - QPR] kwa mkopo 23:15: George Edmundson [Rangers - Derby] kwa mkopo 23:00: Will Grigg [Sunderland - MK Dons] kwa mkopo 23:00: Brandon Barker [Rangers - Oxford] kwa mkopo 22:55: Oliver Sarkic [Blackpool - Mansfield] kwa mkopo 22:37: Nathaniel Mendez-Laing [Middlesbrough] kwa mkataba 22:30: Josh Doherty [Crawley - Colchester] kwa mkopo 22:30: Cohen Bramall [Colchester - Lincoln] Haijabainika 22:30: James Morton [Bristol City - Gillingham] kwa mkopo 22:30: Jack Vale [Blackburn - Rochdale] kwa mkopo 22:30: Christopher Missilou [Northampton - Swindon] Haijabainika 22:30: Curtis Main [Aberdeen - Shrewsbury] Uhamisho wa bure 22:15: Elliot Embleton [Sunderland - Blackpool] kwa mkopo 22:00: Alex Denny [Salford - Morecambe] kwa mkopo 22:00 Max Melbourne [Lincoln - Walsall] kwa mkopo 21:55: Zak Jules [Walsall - MK Dons] Haijabainika 21:35: Teddy Howe [Blackpool - Scunthorpe] kwa mkopo 21:30: Ollie Crankshaw [Wigan - Bradford] Haijabainika 21:30: David Nugent [Preston - Tranmere] kwa mkopo 21:30: Morgan Whittaker [Derby - Swansea] Haijabainika 21:30: Jack Roles [Tottenham - Stevenage] kwa mkopo 21:15: Dan Batty [Hull - Fleetwood] uhamisho wa bure 21:15: Nathan Wood [Middlesbrough - Crewe] kwa mkopo 21:00: Tom Ince [Stoke - Luton] kwa mkopo 21:00: Jahmal Hector-Ingram [Derby - Stevenage] kwa mkopo 21:00: Ali Crawford [Bolton - Tranmere] kwa mkopo 20:30: Sepp van der Berg [Liverpool - Preston] kwa mkopo 20:30: Calum MacDonald [Blackpool - Tranmere] Haijabainika 20:30: Jonny Williams [Charlton - Cardiff] Haijabainika 20:15: Regan Riley [Bolton - Norwich] Haijabainika 20:00: Marcus Maddison [Charlton - Bolton] kwa mkopo 20:00: Jake Eastwood [Sheffield United - Grimsby] kwa mkopo 19:45: Elliot Lee [Luton - Oxford] kwa mkopo 19:45: Lee Gregory [Stoke - Derby] kwa mkopo 19:30: Liam Lindsay [Stoke - Preston] kwa mkopo 19:30: Conor Grant [Sheffield Wednesday - Rochdale] Haijabainika 19:30: Lewis Wing [Middlesbrough - Rotherham] kwa mkopo 19:30: Will Swan [Nottingham Forest - Port Vale] kwa mkopo 19:15: David Morgan [Southport - Accrington] Haijabainika 19:00: Scott Wootton [Plymouth - Wigan] kwa mkopo 19:00: Luke Matheson [Wolves - Ipswich] kwa mkopo 18:51: Josh Andrews [Birmingham - Harrogate] kwa mkopo 18:30: Ryan Broom [Peterborough - Burton] kwa mkopo 18:00: Fabio Tavares [Rochdale - Coventry] Haijabainika 18:00: George Evans [Derby - Millwall] Haijabainika 17:45: Adam Phillips [Burnley - Accrington] kwa mkopo 17:45: Jamie Proctor [Rotherham - Wigan] kwa mkopo 17:30: Joe Adams [Brentford - Grimsby] kwa mkopo 17:30: Aji Alese [West Ham - Cambridge] kwa mkopo 17:30: Mustapha Olagunju [Huddersfield - Port Vale] kwa mkopo 17:30: MJ Williams [Blackpool - Bolton] uhamisho wa bure 17:15: Callum Wright [Leicester - Cheltenham] kwa mkopo 17:00: Oladapo Afolayan [West Ham - Bolton] kwa mkopo 17:00: Daryl Dike [Orlando City - Barnsley] kwa mkopo 17:00: Serhat Tasdemir [Peterborough - Oldham] kwa mkopo 16:30: Lukas Jensen [Burnley - Bolton] kwa mkopo 16:30: Nnamdi Ofoborh [Bournemouth - Wycombe] kwa mkopo 16:15: George Taft [Bolton - Scunthorpe] uhamisho wa bure 16:00: Teden Mengi [Manchester United - Derby] kwa mkopo 15:30: Taylor Harwood-Bellis [Manchester City - Blackburn] kwa mkopo 15:30: Robbie Willmott [Newport - Exeter] kwa mkopo 15:30: Charles Vernam [Burton - Bradford] Haijabainika 15:00: Dior Angus [Barrow - Wrexham] uhamisho wa bure 15:00: Jamie Pardington [Wolves - Mansfield] kwa mkopo 15:00: Frank Nouble [Plymouth - Colchester] kwa mkopo 14:30: Joe Grayson [Blackburn - Oxford] kwa mkopo 14:00: Josh Earl [Preston - Burton] kwa mkopo 14:00: Keyendrah Simmonds [Manchester City - Birmingham] Haijabainika 14:00: Conor Shaughnessy [Leeds - Rochdale] uhamisho wa bure 14:00: Brendan Wiredu [Charlton - Colchester] Haijabainika 14:00: Troy Parrott [Tottenham - Ipswich] kwa mkopo 14:00: Tristan Abrahams [Newport - Leyton Orient] kwa mkopo 13:40: Harry Pickering [Crewe - Blackburn] Haijabainishwa 13:00 Declan Drysdale [Coventry - Cambridge Utd] kwa mkopo 12:15: Max Clark [Vitesse Arnhem - Hull] uhamisho wa bure 11:30: Jayson Leutwiler [Fleetwood - Huddersfield] uhamisho wa bure 11:00: Terry Taylor [Wolves - Burton] Haijabainishwa 11:00: Matt Smith [Arsenal - Charlton] kwa mkopo 11:00: Winston Reid [West Ham - Brentford] kwa mkopo 10:00: Lenell John-Lewis [Hereford - Grimsby] Haijabainishwa 09:30: Glenn Murray [Brighton - Nottingham Forest] uhamisho wa bure 09:00: Orjan Nyland [ Norwich] Ligi ya Scotland 23:50: Scott Wright [Aberdeen - Rangers] Haijabainishwa 23:34: Jack Simpson [Bournemouth - Rangers] Haijabainishwa 23:19: Florian Kamberi [St Gallen - Aberdeen] kwa mkopo 22:59: Eddie Nolan [Crewe Alexandra - Motherwell] kwa mkopo 22:14: Jordan Roberts [Hearts - Motherwell] kwa mkopo 21:49 Bruce Anderson [Aberdeen - Hamilton] kwa mkopo 21:31: Jonjoe Kenny [Everton - Celtic] kwa mkopo 21:16 Callum Hendry [St Johnstone - Aberdeen] kwa mkopo 21:00: Zech Medley [Arsenal - Kilmarnock] kwa mkopo 20:25: Brandon Pierrick [Crystal Palace - Kilmarnock] kwa mkopo 19:35 Fraser Hornby [Reims - Aberdeen] kwa mkopo 18:05 Charlie Gilmour [Norwich - St Johnstone] Haijabainishwa 14:30 Stevie Mallan [Hibernian - Yeni Malatyaspor] kwa mkopo 13:30 Robbie Crawford [Livingston - Motherwell] kwa mkopo hadi mkataba wa kudumu Kimataifa 23:15: Adama Diakhaby [Huddersfield - Amiens CC] Haijabainishwa 22:50: Olivier Ntcham [Celtic - Marseille] kwa mkopo 22:39: Maxime le Marchand [Fulham - Royal Antwerp] kwa mkopo 22:00: Shkodran Mustafi [Arsenal - Schalke] uhamisho wa bure 21:15: Miguel Angel Guerrero [Nottingham Forest - Rayo Vallecano] Haijabainishwa 18:16: Cenk Tosun [Everton - Besiktas] kwa mkopo 18:00: Gedson Fernandes [Benfica - Galatasaray] kwa mkopo 17:10: Sami Khedira [Juventus - Hertha Berlin] Haijabainishwa 17:00: DeAndre Yedlin [Newcastle - Galatasaray] Haijabainishwa 17:00: Robert Glatzel [Cardiff - Mainz] kwa mkopo 16:15: Miguel Fernandez [Birmingham - CD Guijuelo] kwa mkopo 09:00: Jonas Lossl [Everton - Midtjylland] Haijabainishwa 09:00: Domingos Quina [Watford - Granada] kwa mkopo 09:00: Martin Samuelsen [Hull - Aalborg] kwa mkopo Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho katika Ligi ya Primia na vilabu vya Ligi ya Soka Uingereza ilikuwa ni saa tano usiku Februari mosi, huku vilabu vya Scotland vikiwa na saa moja zaidi ya kukamilisha hatua hiyo. text: Rais John Pombe Magufuli Walikuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa katika hoteli moja mjini Dar es Salaam . Waandalizi wa mkutano huo wanasema kwamba mkutano huo ulikuwa umeitishwa kujadili iwapo wakabiliane na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma za afya. Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki za kibinafsi kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania. Hatahivyo, Sibongile Ndashe anasema kuwa walikuwa hawana haki ya kuwakamata na ameishtumu mamlaka ya Dar es Salaam kwa kuwakamata yeye na wenzake. Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Tanzania. Lazaro Mambosasa , afisa mkuu wa polisi mjini Dar es Salaam aliwaambia maripota kabla ya mawakili hao kukamatwa kwamba walikuwa wakikuza mapenzi ya jinsia moja. Kukamatwa kwao kunajiri kufuatia hotuba ya mwezi Septemba iliotolewa na naibu waziri wa afya Hamis Kingwangala ambaye aliapa mbele ya bunge kukabiliana na makundi yoyote yanayounga mkono wapenzi wa jinsia moja nchini humo, kulingana na chombo cha habari cha AFP. Lakini bi Ndashe aliambia wanahabari hakuna makosa ambayo wangeshtakiwa nayo kwa kuwa mkutano huo haukuwa wa wapenzi wa jinsia moja . Shirika la haki za kibinaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi hilo linaweza kuishtaki serikali ya Tanzania kwa kupiga marufuku vituo vya afya vinavyowauguza wato waliopo katika hatari ya kuambukizwa ukimwi mbali na uagizaji wa kifaa cha mafuta ambayo yanaweza kutumika kujilinda dhidi ya HIV. Bi Ndashe anasema kuwa hatua yao ya kutaka kujua sababu za wao kutimuliwa nchini humo hazikuangaziwa. Kundi hilo sasa limeonya kwenda mahakamani. Tanzania imewafurusha mawakili watatu wa Afrika Kusini waliokamatwa wiki hii wakituhumiwa kwa kukuza mapenzi ya jinsia moja. text: Mamilioni ya watu wamekufa kutokana na ugonjwa huo na wengine wakiwa wanaishi na virusi vya Ukimwi Kadri muda unavyoenda wanasayansi wakiwa wanapambana kupata tiba au hata chanjo ya virusi hivyo, watu wamejifunza jinsi ya kuishi na virusi hivyo. Lakini unyanyapaa bado ni changamoto. Katika jimbo la Wajir kaskazini mwa Kenya ni eneo ambalo utamaduni na dini zimechukua nafasi kubwa na kufanya jamii kuwanyanyapaa zaidi waathirika wa virusi vya Ukimwi. Adhana husikika mara tano kwa siku kuwakumbusha watu kwenda msikitini kwa sala katika mji mzima. Eneo hili ambalo lina wakazi wengi waislamu. Wajir iko karibu na mpaka wa Somalia, wenyeji wa eneo hilo ni wasomali ambao wana ongea lugha moja na wana tamaduni moja. Lakini kuna mengi zaidi ambayo hayafahamiki kuhusu eneo hilo au watu hawayazungumzii. Imesikika kuwa watu wanahangaika sana kimyakimya , kwa sababu ya kuwa na virusi vya ukimwi. BBC imeweza kuzuru katika mji huo na kukutana na baadhi ya watu ambao wameathirika na VVU Vipimo vya ukimwi Saadiya ni miongozi mwao ambaye anaishi katika eneo hili akiwa na watoto watatu. Mtoto wake wa kwanza ambaye anasoma ana umri wa miaka 11. Saadiya hawezi kusimama mwenyewe. Yeye ni muhathirika wa virusi vya ukimwi. Amekuwa akipambana na umaskini peke yake kuwalea watoto. Sijamuona au sijasikia kutoka kwa mume wangu tangu mwaka 2013. Hicho ndicho kipindi ilinibidi nimpeleke mwanangu hospitalini pia. Madaktari walivyompima walimkuta ameathirika pia na virusi vya ukimwi. Walinipima mimi pia na kunikuta nimeathirika. Saadiya anasema kuwa alishtuka sana kusikia hiyo taarifa. Lakini hakuwa amejiandaa kuwa angekutana na changamoto hiyo. Mara tu tatizo hilo linapogunduika kwa umma, anatengwa. Nililazimika kuhama kutoka eneo ambalo nililokuwa ninaishi mpaka kuja kuishi hapa. Majirani zangu walikuwa wanawatukana watoto wangu . Nilikuwa nashindwa kuazima kitu chochote kutoka kwa majirani zangu; hakuna mtu ambaye alikuwa anajali kuwa ninaweza kuishi au kufa. Walikuwa hawawezi kuchangia maji na mimi katika kisima. Hata sasa hapa sio nyumbani kwangu. Wananiongelea sana na walikuwa wanawapiga watoto wangu wakiwaona. Huwa anatumia muda mwingi kukaa peke yake na mara nyingi na huwa anapokea wageni mara chache. Lakini Saadiya anasema alikuwa anakubali kila kitu ambacho kilikuwa kinamkuta. Ni watoto wangu ndio nilikuwa nawahofia. Watoto wangu wanasoma katika shule ya msingi ya umma; mtoto mdogo yuko shule ya awali. Lakini walifukuzwa kuhudhuria masomo ya dini na wanakijiji. Hata watoto wa jirani yangu walikuwa wananitukana sana kila siku kutokana na kile ambacho huwa wanasikia kutoka kwa wazazi na jamii inayonizunguka. Lakini nashukuru kwamba bado wanaruhusiwa kwenda shule. Jamal pia ana virusi vya ukimwi Jamal pia ana virusi vya ukimwi. Yeye anaishi mjini Wajir na yeye alikuwa anakumbana na ubaguzi kutokana na hali yake. Sehemu ya kwanza niliyoishi wakati nilipooa, nilifukuzwa. Walinifukuza hata nyumba niliyoamia baada ya ile . Baada ya miezi miwili au mitatu baada ya kuhamia nyumba mpya, habari kuhusu mimi zilisambaa kutoka kwa watu ambao walikuwa wananijua kabla kuhusu hali yangu. Taarifa zikamfikia mwenye nyumba na kunifukuza. Nilifukuzwa kwa sababu ya hali yangu ya afya. Siwezi kumuomba mtu kitu chochote, si chakula wala malazi yani si kwa chochote. Yani hawataki kusikia hilo neno ukimwi, ninalipa kodi lakini walikuwa hawataki hata pesa yangu. Jamal alilazimishwa kukonda. Alipoteza marafiki zake na familia yake mara tu walipogundua kuwa ana virusi vya ukimwi. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa idadi ya watu ambao wana virusi vya ukimwi nchini Kenya , kuna maambukizi mapya takribani 52 000 kwa watu rika zote. Hii ikijumuisha maambukizi mapya yapatayo 44000 ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 49 . Maambukizi ya watoto wadogo chini ya miaka 14 yalikuwa chini ya 8000 mwaka jana. Licha ya kuwa Wajir kuwa eneo lenye watu wengi nchini humo, bado rekodi zinaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi iko chini kwa 0.2 % . Ingawa kuna hofu kuwa inawezekana kuna watu wameathirika lakini wanshindwa kujitokeza kwa kuogopa unyanyapaa ambao umetawala katika eneo hilo. Mawasiliano yameongezeka na maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezekan. Kuna watu wengi ambao hawajapima na tumewaona, kwa mfano mwezi huu tu tuna rekodi ya maambukizi mapya ya watu nane. Hivyo ukimwi upo katika jamii hii lakini unyanyapa unawafanya watu wasiende kujua hali zao. Uzinzi umekatazwa katika kitabu kitakatifu cha Quran. Katika jumuiya ya kiislamu , waislamu wanahofia kuwa kama wakienda kupima virusi vya uimwina ndugu zao wakawaona, watahusisha kuwa wamefanya uzinzi na unyanyapaa utakuja na jamii kuwatenga. Watu wachache ambao wameweza kuzungumza mbele za watu kuhusu hali zao na kuchukua jitihada za kuelimisha watu kuhusu virusi vya ukimi. Inabidi tujaliane, huwa tunaandika miradi ya kuomba ufadhili ili tuendelee kusaidia wengine. Tunawaeleza kuwa wote sisi ni familia moja. Na katika dunia hii tuna uwezo wa kuishi miaka mingi tukiwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi. Kuna wengi ambao wamenyanyapaliwa lakini bado wapo hai. Hivyo inatupasa kunywa dawa kama tulivyoshauriwa na madaktari. Lakini inaonekana ni rahisi kusema kuliko kutenda. Haswa pale waathirika wengi wanaposhindwa kumudu kununua chakula cha siku. Katika jamii ya wasomali, watu kujitokeza kwa umma kusema hali zao ni jambo la nadra sana. Wafanyakazi wa afya wana kazi ya ziada ili kuwashawishi watu kusema hali yao katika jamii kwa sababu wanakuwa wakali sana. Kila siku kuna simulizi za kutisha kuhusu unyanyapaa wa wagonjwa wa ukimwi katika jamii ya wasomali. Wengine huwa wanatafuta msaada bila mafanikio. Kuna hatua kadhaa zimechukuliwa ilikupunguza ubaguzi dhidi ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi lakini naona hatua hizo zinaenda polepole na safari kuwa ya maumivu makali. Mpaka kila mtu akiwa anauelewa kuhusu virusi vya ukimwi basi wale wenye virusi vya ukimwi inabidi wajitegemee wenyewe. Hii ikimaanisha ishi mwenyewe na upweke. Ni takribani miongo sita sasa tangu virusi vya ukimwi vilipothibitishwa kuepo. Mamilioni ya watu wamekufa kutokana na ugonjwa huo na wengine wakiwa wanaishi na virusi vya Ukimwi. text: Kufikia tarehe 23 mwezi machi , zaidi ya watu 350,000 walikuwa wamembukizwa virusi vya corona katika mataifa 170 duniani huku watu 16000 wakiripotiwa kufariki. Kufikia tarehe 23 mwezi Machi, zaidi ya watu 350,000 walikuwa wameambukizwa virusi vya corona katika mataifa 170 duniani huku watu 16,000 wakiripotiwa kufariki. Na idadi hiyo inaendelea kuongezeka kila uchao. Bila tiba ama chanjo ambayo imeonekana kukabili virusi vya corona madaktari kwa sasa wanaweza kufanya kazi kupunguza makali ya dalili za ugonjwa huo. Kwasababu hiyo , WHO imeanzisha mpango wa mshikamano 'solidarity' ambapo mataifa kumi yatafanyia uchunguzi jinsi dawa nne zinavyoweza kutibu Covid-19. Lengo ni kukusanya data zaidi kwa wakati mfupi ili badala ya kuanza kutengeneza dawa mpya, mchakato unaoweza kuchukua miaka kadhaa, washiriki wa utafiti huo wataona iwapo dawa hizo zinazotumika kukabiliana na magonjwa mengine zitaweza kuzuia makali ya virusi vya corona. Na ijapokuwa baadhi ya dawa hizi zinapatikana sokoni, madaktari wanasisitiza kwamba hazifai kutumiwa bila ya ushauri wa mtaalamu. Nchi za Argentina, Bahrain, Canada, Ufaransa, Iran, Norway, Afrika Kusini, Uhispania, Uswizi na Thailand zimejiunga kufanya utafiti huo ambapo wanatarajia kwamba wagonjwa wengi watashiriki. Virusi vya corona vilianza kusambaa kufikia mwisho wa 2019 "Umuhimu wa utafiti kama huu ni kwamba unaweza kusajili wagonjwa kwa haraka," anaeleza Daktari George Rutherford ambaye ni Profesa wa takwimu za kibaiolojia katika Chuo Kikuu cha Carlifonia nchini Marekani. "Iwapo kwa mfano nilikuwa nikifanyia majaribio haya katika maabara yangu, ningekuwa na wagonjwa wawili au watatu kwa siku, lakini kutokana na ushirikiano wa vituo kadhaa unaweza kuwa na wagonjwa 100 kwa siku,'' ameongezea. Hiyo ni njia bora ya kuweza kufanya kazi kwa haraka. Bi Ana Maria Henao Restrepo, mtafiti idara ya chanjo na kinga ya kibaiolojia kutoka WHO anasema kwamba mradi huo unafanywa kwa haraka zaidi. Kulingana naye WHO inatarajia kuwa na nakala na data ya utafiti huo kuanzia wiki ya mwisho ya mwezi Machi. Profesa Rutherford anasema kwamba iwapo hakuna matatizo ya kimpango, utafiti kama huo unaweza kutoa matokeo katika kipindi cha mwezi mmoja. Kuenea kwa virusi vya corona kumewafanya watu kutotembea Sambamba na utafiti huo wa kimataifa , WHO imesema kwamba wanasayansi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wanafanyakazi ya kutengeneza takriban chanjo 20 za virusi vya corona. Utafiti wa matumaini Ili kuanzisha utafiti huo, jopo la watalaam wa WHO lilichagua tiba nne ambazo wanazithamini kuweza kukabiliana na virusi vya corona. Waliangazia mbinu iliotumika kama vile habari kuzihusu na upatikanaji wake. Tiba hizo zina dawa mchanganyiko ambazo zimetumika kutibu Ebola, Malaria au HIV. Tiba hizo zitatumika bila mpangilio, ikitegemea upatikanaji wake katika kila hospitali kwa wagonjwa wa virusi vya corona. Baada ya tiba kuanza, madatari watachunguza jinsi wagonjwa wanavyoendelea, ikiwemo siku watakazoondoka hospitalini ama iwapo atashindwa kupona. Watu wamelazimika kukaa mbali kwa walau mita moja katika maeneo ya umma Rutherford anasema kwamba katika tafiti kama hizi, lengo ni kuanzisha tiba katika awamu za kwanza za ugonjwa kabla ya mgonjwa kuingia katika chumba cha wagonjwa mahututi. Daktari huyo anaunga mkono mradi huo wa solidarity, lakini anaonya kwamba kufanya kazi na vituo tofauti katika mataifa kadhaa wakati mmoja inaweza kusababisha ugumu fulani. Tiba nne 1.Remdesivir: Licha ya kutengenezwa ili kutibu Ebola dawa ya remdesivir haikuonekana kuwa nzuri. Hata hivyo, inaonekana kuwa na uwezo dhidi ya virusi vya corona kulingana na vipimo vya seli zilizopandwa katika maabara. Pia kuna ripoti zinazoonesha kwamba imekuwa na faida kubwa kwa wagonjwa wa Covid-19, lakini hiyo haitoshi kuthibitisha kuwa dawa hiyo ni nzuri. ''Kati ya dawa zilizojumuishwa katika mradi wa Solidarity, remdesivir inaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na virusi vya corona katika vipimo vya maabara," Stephen Morse, mkurugenzi wa mpango wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Columbia (EE) aliambia BBC. Hakuna tiba wala chanjo thabiti dhidi ya virusi vya corona kufikia sasa 2. Cloroquina/hidroxicloroquina Chloroquine ilitumika kwa miaka mingi kutibu ugonjwa wa malaria hadi pale vimelea ambavyo husababisha ugonjwa huo vilipotengeneza usugu dhidi ya dawa hiyo. "Iwapo inaweza kutibu, haimaanishi kuwa itafanya kazi dhidi ya Covid-19," anasema Rutherford. Dawa hii inaweza kutumika kupitia kinywa lakini pia hutoa athari za maumivu kama yale ya kuumwa na kichwa, kuhisi kizunguzungu, kupoteza hamu ya kula, kuumwa na tumbo, kuhara, kutapika na kutokwa na upele katika ngozi, kulingana na Maktaba ya Kitaifa ya Tiba nchini Marekani. Hatari yake ni kwamba ni rahisi kuipata na muonekano wake katika habari kuhusiana na virusi vya corona umesababisha kesi za sumu kuripotiwa. 3. Ritonavir na lopinavir Mchanganyiko wa dawa hizi mbili umetumika kwa matibabu ya Virusi Vya Ukimwi (VVU). Wataalam waliozungumza na BBC wanakubali kwamba mchanganyiko huu haujaonyesha matokeo ya kutia moyo dhidi ya coronavirus. "Lakini ni busara kujaribu tena," anasema Rutherford. Vita dhidi ya janga la corona ni miongoni mwa vita vigumu zaidi ambavyo wanasayansi wamekabiliana navyo katika historia ya hivi karibuni 4. Ritonavir/lopinavir Tiba ya nne kupimwa na Solidarity ni mchanganyiko wa ritonavir na lopinavir pamoja na interferon-beta, molekyuli ambayo husaidia kudhibiti uchochezi na imeonekana kuwa bora kwa wanyama walioambukizwa na ugonjwa wa kupumua wa Mashariki ya Kati (MERS). Wataalamu wanaonya kuwa ni muhimu kuwa waangalifu wakati zinapotumika kwani; ikiwa zinatumika katika hatua za mwisho mwisho zinaweza kukosa ufanisi au hata kusababisha madhara zaidi kuliko faida kwa mgonjwa. Sasa ni suala la wakati gani matokeo hayo yatapatikana kwa mradi huo wa mshikamano, lakini kulingana na Morse ni "hatua moja kubwa iliyopigwa" . ''Mpango mahsusi wa kuokoa maisha,'' hivi ndivyo Shirika la Afya Duniani WHO linavyoelezea juhudI zake mpya za kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19). text: Jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa Wanasema kuwa msichana huyo alikosa hewa na kufariki baada ya kuwasha moto ili kupata joto. Chini ya tamaduni za Hindu kwa jina Chhaupadi, wanawake walio na hedhi ama ambao wamejifungua huonekana kuwa wachafu. Tamaduni hiyo ilipigwa marufuku na serikali ya Napoli mwaka 2005, lakini bado inaendelea kutekelezwa katika maeneo ya mashambani yaliopo magharibi. Mtaa wa mabanda ambapo wasichana waliotengwa kutokana na kuwa na hedhi hukimbilia ili kuishi Mwili wa Roshani Tiruwa ulipatikana na babake wikendi iliopita katika jiwe na nyumba moja ya matope katika kijiji cha Gajra, Wilayani Accham yapata kilomita 440 magharibi mwa Kathmandu. Baadhi ya jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa. Huku wakiwa wametengwa hunyimwa chakula chao cha kila siku na hawaruhusiwi kunywa maziwa. Maafisa wa polisi huko Nepal wanachunguza kifo cha msichana wa miaka 15 aliyefukuzwa hadi katika mtaa wa mabanda kwa kutokwa na hedhi. text: Mjadala huo ulitokana na kauli iliyotolewa na waziri wa elimu Amina Mohamed, kwamba "Idadi kubwa ya watahiniwa wamejifungua" katika siku tatu za mtihani wa kitaifa wa wanafunzi wa shule ya msingi (KCPE) ambao unafanywa na watoto- waliyo na umri kati ya miaka 13 na 14. Waziri alisema: "Hali hii ikiendelea kujirudia kila mara mwaka mzima, nchi huenda ikatumbukia katika majanga." Kitengo cha BBC cha Reality Check kimechunguza baadhi ya data zilizopo kuhusiana na mimba za utotoni ili kubaini ikiwa hali hiyo inaendelea kuongezeka nchini Kenya. Kitengo hicho kiligundua ujumbe mmoja uliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ukidai kuwa wasichana wa shule wamekuwa wakiwanyonyesha watoto wao wakati wa mtihani. Madai ya uwongo Ujumbe huo umesambazwa kupitia ukurasa wa makundi kadhaa yaliyo na akaunti ya Facebook. Baadhi ya kurasa hizo zinafuatiliwa na watu zaidi ya 150,000. Kila ujumbe uliyosambazwa ulitumia picha aina moja - katika kile kinachoonyesha wanawake wadogo wakiwa wamevalia sare za shule za rangi ya samawati na kila mmoja wao amebe mtoto. Hakuna chochote kinachoonyesha chimbuko la ujumbe huo au taarifa zilizochapishwa. Hata hivyo utumizi wa picha moja katika kila ujumbe uliyosambazwa uliwachanganya na kuwakasirisha watumiaji wa mitandao ya kijamii. Lakini matokeo ya hali hii ni yapi- na Je ina athari gani kwa maadili ya kijamii?" Kuna baadhi ya watu wanatilia shaka ikiwa ujumbe huo ni wa kweli. Takwimu za serikali zinaashiria viwango vya mimba za utotoni vimepungua Picha ya awali katika ujumbe huo ilionekana katika taarifa ya mtandao wa shirika la habari la CNN na haikuwa ya kinamama na watoto wakiwa shuleni nchini Kenya. CNN imethibitisha kuwa picha hiyo ilipigwa nchini Tanzania na ilikuwa ya wanawake wadogo wakiwapeleka watoto wao katka kituo cha mlezi ya mchana. Picha hiyo hatahivyo imeunganishwa na taarifa gushi zinazodai hali ya mimba za utotoni katika shule za Kenya. Baadhi ya taarifa zilizochapishwa ziidai kuwa wanafunzi 19 kati ya 30 walikuwa wakinyonyesha watoto wao. Wengine wakiashiria kuwa ni wanafunzi 21 kati ya 30. Kitengo cha BBC cha Reality Check pia kiligundua kuwa majina ya shule zilizokuwa zikitajwa katika baadhi ya ujumbe huokama vile shule ya upili ya Chabera na Nyanza hazikuwepo. Ukweli kuhusu mimba za utotoni Kenya Mjadala wa hivi karibuni kuhusiana na hali halisi ya mimba za utoto nchini Kenya ''uligubikwa na taarifa ghushi kama hii iliyoangaziwa na kitengo cha BBC Reality Check. Lakini kuna hofu kubwa kuhusiana na suala hili katika jamii za mijini na vijijini. "Mimba za u totoni sio jambo geni nchini Kenya ," asema Elizabeth Muiruri, kutoka shirika la Save the Children. "Hata hivyo taarifa za hivi karibuni katika vyombo vya habari kuhusiana na wasichana wadogo wa shule kujifungua wakati wa mtihani ni za kutia hofu." BBC imefanya mahojiano na waalimu wa shule na maafisa wa afya katika jimbo Kisumu Magharibi mwa Kenya na maeneo yaliyo karibu. Walio hojiwa walisema kumekuwa na ongezeka la idadi ya mimba za utotoni hali ambayo inajumuisha wasichana wa miaka 15. Walisema hali hiyo inachangiwa na umasikini na ukosefu wa elimu ya uzazi na usawa wa kijinsia. Kati ya Julai mwaka 2016 na Juni 2017, wizara ya afya ilirekodi karibu visa 350,000 vya mimba miongoni mwa wasichana wa miaka kati ya 15 na 19. Idadi hiyo ni ya wanawake wajawazito wanaoenda kliniki kutafuta ya uzazi kabla na baada ya kujifungua. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ukilinganisha na mwaka 2014 hali ya mimba za utotoni katika maeneo ya tofauti nchini Kenya imepungua. Upungufu huo umetokana na kuimarishwa kwa elimu ya uzazi shuleni. ambayo imechangia wanafunzi kuwa na ufahamu wa mbini za mpango wa uzazi, asema Fredrick Okwayo mmoja wawashauri wa shirika la UNFPA. Hata hivyo idadi ya wasichana wanaoshirikishwa katika elimu hiyo bado ni dogo. Hali inawafanya baadhi ya wathirika wa mimba za utotoni kupoteza nafasi ya kujiendeleza maishani. Vipi hali ya Kenya iukilinganisha na mataifa mengine? Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia nchi kama Nigeria na Tanzania, zimekuwa na viwango vya juu vya mimba za utotoni. Lakini idadi hiyo imeendelea kupungua katika kipindi cha miaka 30. Afrika Kusini imetajwa kuwa na idadi ya chini ya mimba za aina hiyo. Licha ya ukosefu wa ushahidi wa unaoashiria kuongezeka kwa visa vya mimba za utotoni nchini Kenya ukilinganisha na mataifa mengine barani Afrika, serikali imekuwa mbioni kukabiliana na tatizo hilo. Mjadala umeibuka nchini Kenya kuhusiana na suala la wasichana wadogo wa shule ya msingi kupachikwa mimba. text: Shirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo Ndege hiyo imetua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es Salaam. Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo. Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar es Salaam. Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote". Marubani wa ndege hiyo Ndege hiyo ilikuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo. Bi Mwenifumbo, 24, ambaye alisomea urubani jijini Addis Ababa, Ethiopia amemwambia Munira Hussein wa BBC kwamba alihamasishwa kuwa rubani na baba yake ambaye pia alikuwa rubani. Ndege hiyo uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Mwelekezi pekee wa ndege wa kike uwanja wa JNIA Fatuma Kahabi. Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee. text: Kamera za CCTV zinamuonyesha mwanamume mwenye kofia akiingia studioni akiwa anasindikizwa na polisi waliojihami Bw Nnauye amesema kamati hiyo bado haijamaliza kazi yake na punde itakapofanya hivyo na kukamilisha ripoti husika, wananchi watafahamishwa. "Kuna simu nyingi juu ya ripoti," ameandika kwenye Twitter. "Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!" Waziri huyo wa habari alianzisha uchunguzi baada ya mkurugenzi wa kituo hicho cha habari, Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuambia wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho, akiwa na polisi wenye silaha. Kamera za CCTV katika kituo hicho zinamuonesha mtu anayedaiwa kuwa kamishna wa jiji la Dar es Salaam Paul Makonda akiwa anasindikizwa na polisi waliojihami, akiingia studio. Rais John Magufuli alisema katika hotuba yake Jumatatu alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelee kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye rais wa nchi. Dkt Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini. Waziri wa habari nchini Tanzania Nape Nnauye amewaomba wananchi nchini humo kuwa na subira kuhusu kutolewa kwa ripoti ya uchunguzi wa uvamizi uliotekelezwa katika studio za Clouds. text: Picha hiyo ilizua gumzo mitandaoni huku baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo wakiwakejeli Picha hizo zilipigwa wakati wa mtihani wa kemia katika shule ya upili ya Bhagat mjini Haveri, jimbo la Karnataka. Ziliwaonesha wanafunzi wakiwa wamevalia maboxi yaliokatwa upande mmoja, ili kuwazuia wasiibie kazi ya wenzao. Msimamizi wa shule hiyo ameomba radhi kwa maafisa wa wilaya wa elemu kufuatia kisa hicho. MB Satish aliiambia BBC kuwa waliamua kutumia mbinu hiyo isiokuwa ya kawaida kukabiliana na visa vya udanganyifu wakati wa mtihani. Alisema kuwa shule hiyo ilichukua hatua hiyo kama ''sehemu ya majaribio'' baada ya kusikia inatumika katika maeneo mengine nchini. Maofisa wa shule hiyo wanasema walisikia mbinu hiyo inatumiwa mjini Mumbai Pia alisistiza kuwa wanafunzi wenyewe waliridhia kuvalia maboxi hayo vichwani wakati wa mtihani na kuongeza kuwa walikuja nazo wenyewe. "Hakuna mwanafunzi aliyelazimishwa kuvalia boksi kichwani. Kama unavyoona katika picha hizi kuna baadhi ya wanafunzi ambao hawajazivalia," alisema. "Waliokuwa wamevalia pia baadhi yao walivua baada ya dakika 15, wengine baada ya dakika 20 na hata sisi wenyewe tuliwwambia wazivue baada ya saa moja." Maafisa wa elimu wa kikanda waliripotiwa kufika shuleni hapo kulalamikia hatua hiyo muda mfupi baada ya picha hizo kusambazwa katika mitandao ya kijamii. SC Peerjade, naibu mkurugenzi wa wa bodi ya usimamizi ya shule hiyo alitaja hatua hiyo kuwa ya "kidhalimu". "Nilipopata ujumbe kuhusu kisa hicho, nilitoa agizo kwa usimamizi wa shule kusitisha mpango huo mara moja," alinukuliwa na na gazeti la Times nchini India akisema. Wakuu wa shule wamesema wamekomesha zoezi hilo kufuatia maagizo kutoka kwa bodi ya shule. Maafisa katika shule moja nchini India wameomba msamaha baada ya picha ya kushangaza ya wanafunzi waliovalia maboksi vichwani mwao wakifanya mtihani kusambaa katika mitandao ya kijamii. text: Kundi hilo linalowajumuisha pia Panama ambao watakutana na England Nizhny Novgorod Jumapili. Bao la tano la Ubelgiji lilifungwa na Michy Batshuayi. Tunisia walifungiwa na Dylan Bronn na Wahbi Khazri. Tunisia wanatarajia Panama wawashinde England ndipo waweze kusalia katika michuano hiyo. Hilo lisipofanyika basi Afrika itasalia na mataifa mawili pekee katika michuano hiyo - Nigeria na Senegal. Lukaku amfikia Ronaldo kwa mabao Lukaku sasa ana mabao manne katika Kombe la Dunia, sawa na Cristiano Ronaldo wa Ureno katika kinyang'anyiro cha kushinda Kiatu cha Dhahabu. hazard alikuwa amemkosoa mchezaji huyo mwenzake, waliyecheza pamoja Chelsea wakati mmoja, kwa kutoweka wakati wa kipindi cha kwanza mechi dhidi ya Panama. Lakini leo alitamba mechi yote hadi alipoondolewa uwanjani na nafasi yake akaingia Marouane Fellaini dakika ya 59. Alionekana kuumia kidogo lakini anatarajiwa kurejea mechi dhidi ya England ambayo huenda ikaamua nani atamaliza kileleni kundi hilo. Baada ya mechi ya leo, Hazard amemsifu sana. "Tumeshinda mechi hii, kwa hivyo tuna furaha sana," ameambia BBC. "Tulicheza vyema na kufunga mabao matano. Tumefungwa mawili, lakini tunaweza kujiimarisha. Hata hivyo, sasa tuna siku nne za kupumzika na kisha tucheze na England kushindania atakayemaliza kileleni kwenye kundi. "Ni rahisi sana kucheza na Lukaku, unampa mpira na anafunga kila wakati. Alicheza vizuri sana." Tunisia hawana matumaini Tunisia leo walicheza vyema na kushambulia zaidi ukilinganisha na mechi ya kwanza ambapo walishindwa na England, lakini walitatizika kufunga. Carthage Eagles walishambulia goli mara 16, mara tano makombora yao yakilenga goli, ukilinganisha na mechi dhidi ya England waliposhambulia mara nne na walifanikiwa kulenga goli mara moja pekee. Bila shaka leo hakuna mchezaji wa Ubelgiji atamkosoa Lukaku kwa uchezaji wake Ikizingatiwa kwamba England wanachezaji dhidi ya Panama Jumapili, labda lengo la Tunisia sasa litakuwa kujaribu kuzuia kumaliza wa mwisho katika kundi hilo kwa kumaliza nyuma ya Panama watakapokutana Alhamisi wiki ijayo. 'Tunawaomba radhi mashabiki wa Tunisia' Kocha wa Tunisia Nabil Maaloul amewaomba radhi mashabiki baada ya kushindwa leo. "Kama tulivyotarajia, ilikuwa mechi ngumu sana." "Tokea wakati tulipopangwa kwenye kundi hilo, tulijua Ubelgiji wangekuwa wapinzani hatari. Tungependa kuwaomba radhi mashabiki wa Tunisia waliojitokeza kwa wingi sana uwanjani leo. "Hata hivyo, tulifanya kadiri ya uwezo wetu na tutajaribu kuboresha uchezaji wetu siku za usoni." Takwimu: Lukaku amfikia Diego Maradona Unaweza kusoma pia: Nini kinafuata? Ubelgiji watakamilisha kampeni yao dhidi ya England uwanja wa Kaliningrad Alhamisi, siku ambayo Tunisia nao watakutana na Panama uwanja wa Mordovia Arena, Saransk (mechi zote zitaanza saa tatu usikusaa za Afrika Mashariki). Romelu Lukaku na Eden Hazard walifunga mabao mawili kila mmoja na kuimarisha uongozi wa Ubelgiji dhidi ya England katika Kundi G kwa ushindi wa 5-2 dhidi ya Tunisia Jumamosi. text: Felicia akiendelea na kazi ya uoshaji magari Wasichana wengi katika mtaa huo hujiunga na biashara ya kuchuuza miili yao kwa wanaume, unywaji wa pombe na matumizi ya mihadarati, na wengi wao huwa hawamalizi shule. Bi Felicia alipata mwanawe wa kwanza, baada ya kufanya biashara ya uuzaji wa mwili na hakuweza kukimu maisha yake, mwanawe, na hata familia yake kutokana na fedha duni alizokuwa akipata kutoka kwa kazi ya ufuaji nguo . ''Mimi na familia yangu tulikuwa tumezoea kula chakula cha jioni pekee. Na wakati mwingine tulikuwa tukipata kiamsha kinywa, ambayo ilikuwa ni chai ya mkandaa'' Felicia alikuwa akilipwa shilingi mia tano za Kenya (dola 5 za Kimarekani) na hata wakati mwengine alikuwa halipwi pesa zozote na wateja wake. ''Nilifanya mapenzi na watu wenye umri zaidi ya babangu ilimradi nipate pesa za kujikimu na familia yangu.'' 'Sikutumia kinga kwa miezi kadhaa kwani wakati mwingi nilikuwa sina pesa za kununua mipira ya kondomu, na wateja wengine hawakutaka kutumia mipira hiyo," anasema Bi Felicia. Bi Felicia katika Jumba la TRM Bi Felicia alipata usaidizi kutoka kwa Shirika la Global Communication, ambalo huhudumu chini ya USAID ambalo huwasaidia wasichana kwenye mitaa ya mabanda jijini Nairobi kupata mafunzo anuwai kama vile ushauri nasaha, mbinu za mawasiliano,maadili mema na kuwatafutia nafasi za kazi. Bi Felicia Mkurugenzi wa mradi wa DREAMS bi Betty Adera amesema ni jukumu la mradi huo kuwanufaisha wasichana katika mitaaa ya mabanda jijini Nairobi kuishi maisha bora na kuwa kielelezo bora katika jamii. ''Bi Felicia ni miongoni mwa wasichana 200 tuliowachukua kutoka mtaa wa mabanda wa Majengo na kuwapa masomo ya kujiendeleza kimaisha.Baada ya wiki mbili, kupitia shirika letu la Global Communities,tuliungana na mmiliki wa biashara ya uoshaji magari na akawaajiri wasichana wanne miongoni mwao ni Felicia ambaye anafanya kazi ya uoshaji magari kwenye jumba la kibiashara la TRM kwenye barabara kuu ya Thika.'' Betty alisema. Felicia amesema alikumbana na changamoto nyingi ikiwemo kutoka kwa wateja wakimuona kama msichana asiyeweza kufanya kazi inayodhaniwa kuwa ya wanaume pekee. ''Vifaa vya kazi vilikuwa vizito siku za kwanza, na bado sikuwa nimekubali ningeweza kufanya kazi hiyo ya uoshaji magari.'' Alikabiliwa pia na changamoto kubwa kutoka kwa wafanyikazi wengine, haswa wanaume, waliodhani anatishia kazi yao. Kwa sasa Felicia ni muoshaji wa magari kwenye jumba la TRM, na anatumai kutimiza ndoto yake ya kuwa ....... Hii ni baada ya kufanyiwa mafunzo na kupata ushauri nahasa. Anatumai kufanikisha ndoto yake ya kuwa mhasibu kutokana na mapato anoyoyapata kila siku kwa kazi hiyo ya uoshaji magari. Felicia Onimbo ni mkaazi wa mtaa wa mabanda wa Majengo, jijini Nairobi mwenye umri wa miaka 23. Maisha katika mtaa huo ni ya shida hasa kwa wasichana. text: Alisema hayo baada ya klabu yake kulaza Bournemouth 1-0 Jumatano. United walijikwamua kutoka wka kichapo cha Manchester City wikendi lakini hawakuweza kupunguza mwanya kati yao na City ambao wamo alama 11 mbele yao kwani vijana hao wa Etihad walilaza Swansea 4-0. Romelu Lukaku ndiye aliyewafungia Man United bao hilo la ushindi kipindi cha kwanza. Mourinho alisema: "Mechi hiyo dhidi ya City ilikuwa kubwa, na ukishindwa hilo halisaidii juhudi zako za kujiweka sawa tena - ushindi husaidia, kushindwa hakusaidii. "Bournemouth walikuwa wapinzani wakali na hali ilikuwa ngumu. Kama tungelifunga bao la pili tungetulia. "Nimefurahishwa na alama hizo tatu. Walipumzika siku moja zaidi yetu, walikuwa sawa kutushinda baada ya kupumzika, hata kiakili kwa sababu mechi kubwa huwadhoofisha wachezaji zaidi. "[Mbio za ligi] zitamalizika tu Mei. Kama zingekuwa zimemalizika sasa ningeenda likizo Brazil au Los Angeles." Msimamo wa Mourinho ni tofauti na meneja wa Chelsea Antonio Conte ambaye amekiri kwamba itakuwa vigumu kuwazuia Manchester City. Beki wa Manchester United Luke Shaw alianza mechi kwa mara ya kwanza ligini msimu huu United walikuwa wamecheza mechi 40 nyumbani bila kushindwa hadi walipolazwa na vijana hao wa Pep Guardiola Jumapili. Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema "angelikuwa likizoni Brazil au Los Angeles" iwapo angekuwa anaamini kwamba mbio za Ligi ya Premia msimu huu zimepata mshindi. text: Jean Pierre Bemba Bemba alikutwa na hatia ya kuwahonga mashahidi kwenye kesi ya uhalifu wa kivita. Jean-Pierre Bemba amekuwa gerezani huko Hague kwa kipindi cha miaka 10 na hukumu yake ya kwanza iliyotokana na mashtaka ya uhalifu wa kivita ilikuwa moja ya mafanikio ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC. Ndiyo mara ya kwanza mahakama ya ICC iliangazia suala la ubakaji kuwa silaha ya vita, na mara ya kwanza mshukiwa alihukumiwa kwa makosa ambayo yalifanywa na watu waliokuwa chini ya uongozi wake. Lakini kesi hiyo ilibatilishwa mwezi uliopitaa wakati Bemba aliondolewa mashtaka baada ya kukata rufaa. Mawakili walitambua dosari kwenye kesi iliyohusu uhalifu uliofanywa na wapiganaji wake kutoka kundi la MLC nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mwaka 2007 mawakili wake walikata rufaa kupinga hukumu yake na kuwahonga mashahidi wakidai kulikuwa na dosari katika kesi hiyo. Lakini mwezi Machi mwaka huu rufaa hiyo ilitupiliwa mbali. Mambo Makuu Jean-Pierre Bemba alizaliwa mwaka 1962 kwenye mkoa wa kaskazinia magharibi wa Equateur, Baba yake, bilionea Bemba Saolona alikuwa rafiki wa karibu wa Mobutu Sese Seko. Baba wa watoto watano amemuoa binti wa Mobutu na kusababisha kupewa jina "Mobutu Mdogo" kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na kiongozi huyo wa zamani wa DRC. Novemba mwaka 1998 Bemba alibuni kundi la waasi MLC kwenye mkoa wake wa nyumbani wa Equateur. Vikosi vyake baadaye vilihusika kwenye mzozo kati ya mwaka 2002 na 2003 kwenye nchi jirani ya DRC, vikipagana kwa ushirikiano na vikosi vilivyokuwa watiifu kwa aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ange-Felix Patasse, ambaye alikuwa akipingwa na aliyekuwa mkuu wake wa majeshi wakati huo Francois Bozize. Agosti mwaka 1999, MLC ilisaini mkataba wa amani wa Lusaka ambao ulinuia kufikisha kikomo mapigano nchini DRC. Aligeuza MLC kutoka kundi la waasi na kuwa chama cha kisiasa kufuatia kusainiwa makubaliano ya amani ya mwaka 2002. Bemba alihudumu kama mmoja wa makamu wanne wa rais nchini DRC kwenye serikali ya umoja kati ya mwaka 2003 na 2006. Kama mgombea mkuu wa chama chake aliwania urais mwaka 2006 lakini akashindwa na rais wa sasa Joseph Kabila, kwenye marudio. Mwaka 2007, mapigano kati ya wapiganaji watiifu kwake na jeshi yalizuka mjini Kinshasa na kusababisha vifo vya takriban watu 100. Bemba alikimbilia nchini Afrika Kusini akidai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Baadaye alikimbilia uhamishoni na familia yake. Mwezi Mei mwaka 2008 alikamatwa na mahakama ya ICC mjini Brussels, Ubelgiji kujibu mashtaka ya uhalifu uliotendwa na vikosi vyake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Wengine wanasemaje Mwandishi wa BBC aliye mjini Kinshasa amezungumza na baadhi wa wafuasi wa Bemba ambao wemeelezea hamu yao ya kutaka arudi nyumbani ili apate kuendelea na shughuli zake za siasa. Akizungumzia kufutwa kwa mashtaka ya Bemba, kiongozi wa upinzani nchini DRC ambaye pia anatarajiwa kugombea urais Moise Katumbi, alisema, "kufutwa hukumu hiyo ni ishara kuwa ukweli kawaida hubainika." "Kufutwa kwa hukumu ya Bemba kunaonyesha kuwa ICC haina msimamo, alisema Felix Tshisekedi. Akizungumzia hatma ya kisia ya Bemba, naibu katibu mkuu wa chama cha MLC, Fidele Babala, alisema: "Miaka kumi ya mtu ni mingi sana na atajijenga... ombi letu ni kwamba atarejea shughuli zake alikoachia. Hakuna kitu kitazuia hilo." Matamshi hayo pia yaliungwa mkono na wakili wa Bemba ambaye alisema; "hajakufa moyo katika malengo yake ya kisiasa." Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC itatoa uamuzi wake kuhusu kesi ya aliyekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba leo Jumatano. text: Wanajeshi wa Amisom wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa al-Shabab Muungano wa Afrika umeitaka Burundi kuwaondoa wanajeshi 1000 kutoka kikosi cha AMISOM kufikia mwisho wa mwezi huu hatua ambayo serikali ya Burundi inapinga. Waziri wa ulinzi Emmanuel Ntahomvukiye, amewaambia wabunge kuwa serikali tayari imetoa ilani kwa AU kuhusiana na suala hilo. Mataifa matano ya Afrika yanachangia wanajeshi wao katika kikosi cha kulinda amani cha AMISOM nchini Somalia. Japo kuna hofu kuwa taifa hilo la upembe wa Afrika bado linakabiliwa na tishio kutoka kwa kundi la Al Shabab. Chini ya makubaliano ya umoja wa mataifa zaidi ya wanajeshi 20,000 wa kulinda amani wanatakiwa kuondoka kwa awamu ili kuipokeza majeshi ya Somalia usukani wa ulinzi wa taifa lao. Ufadhili umetajwa kuwa changamoto kubwa kwa vikosi vinavyolinda usalama nchini Somalia. Kila mwezi zaidi ya wanajeshi 20,000 wanaohudumu chini ya jeshi la pamoja la muungano wa afrika AMISOM, wanalipwa zaidi ya dola elfu moja kila mmoja. Mshahara wao umekuwa ukilipwa na Muungano wa Ulaya moja kwa moja kupitia mataifa yao kwa kutumia sarafu za kigeni. Wanajeshi hao hata hivyo hulipwa mishahara yao kwa sarafu ya nyumbani. Serikali ya Burundi haioni kwanini mpango wa sasa wa AU wa kupunguza wanajeshi katika kikosi hicho unalenga wanajeshi wake pekee. Sio mara ya kwanza Burundi kutishia kuwatoa wanajeshi wao kutoka Amisom lakini hatua hii ya sasa huenda ikawa na athari kubwa. Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Mwaka 2017 Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alitangaza kuwa serikali yake itaishtaki Muungano wa Ulaya kuwa kuzuia mshahara wa vikosi vya Burundi vilivyoko nchini Somalia kwa karibu mwaka mmoja. ''Tatizo liliko kwa sasa ni kwamba kikosi cha Amisom hakina ufadhili iliyokuwa nao hapo awali baada ya Muungano wa Ulaya EU kujiondoa sasa mataifa ambayo yanachangi kikosi hicho yanalazimika kkugharamia uwepo wa majeshi yao'' anasema mtaalamu wa masuala ya usalama nchini Kenya George Musamali. Bwana Msamali anasema Uganda pia ilitishia kuondoa wanajeshi wake sawa na Ethiopia ambayo iliondoa wanajeshi wake na kisha kisha kuwarejesha baadae. Hatua hatua ya Burundi inaiacha Somalia katika hali tata hasa ikizingatiwa mzozo wa kidiplomasia uliyoibuka hivi karibuni kati yake na Kenya licha ya kuwa imekuwa mshirika wake mkuu katika juhudi za kupambana na wanamgambo wa Al-shabab. Wapiganaji wa Al shabab ''Somalia haina budi kupambana na hali yao kwasababu hawataishi kwa kutegemea mataifa ya kigeni kuleta majeshi yao na kugharamia ili hali vita dhidi ya Alshabab havionekani kufikia kikomo'' anasema George Msamali. Nini kifanyike kutatua mvutano huu? Muungano wa Afrika umeshauriwa kuepuka na mazoea ya kutegemea ufadhili wa kigeni kutatua changamoto zinazoikabili Somalia. Umoja huo umeshauriwa kukaa meza moja na mataifa wanachama wake kujadili kwa kina hatua zitakazochukuliwa kutatua tatizo la ufadhili katika kikosi cha AMISOM na pia kutafuta suluhicho la kudumu kwa masuala ya usalama nchini Somalia. Burundi imetishia kuondoa wanajeshi wake 5,000 nchini Somalia ambako wamekuwa wakihudumu chini ya kikosi cha kulinda amani cha Muungano wa Afrika, AMISOM kufikia mwisho wa mwezi huu. text: Uwanja huo hupatikana kaskazini mwa Riyadh Mlipuko mkubwa ulisikika karibu na uwanja huo wa ndege. Duru kutoka jeshi la wanahewa la Saudia zimenukuliwa na shirika la utangazaji la serikali ya Al-Arabiya zikisema kombora hilo lilitunguliwa kaskazini mashariki mwa mji huo mkuu. Runinga yenye uhusiano wa waasi wa Houthi kutoka yemen limesema kombora hilo lilikuwa limerushwa kulenga uwanja huo wa ndege. Shirika la habari la serikali la Al-Ekhbariya limesema kombora hilo lilikuwa "ndogo kiasi" na kwamba hakuna uharibifu uliotokea. Kombora hilo la masafa marefu lilikuwa limerushwa kulenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mfalme Khalid, kwa mujibu wa televisheni ya wapiganaji wa Houthi ya Al-Masirah. Yemen imesambaratishwa na vita kati ya wanajeshi watiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa ya Rais Abdrabbuh Mansour Hadi na wapiganaji wa kundi la waasi wa Houthi. Saudi Arabia inaongoza kampeni ya kuwashinda wapiganaji hao wa Houthi. Saudi Arabia imetungua kombora ambalo lilikuwa limerushwa karibu na uwanja mkuu wa ndege mjini Riyadh, taarifa zimesema. text: Behrouz Boochani, raia wa Iran, aliandika kitabu kwa jina- No Friend But the Mountains: yaani ''Hakuna marafiki lakini milima'' - Utunzi kutoka gereza la Manus. Boochani, alitumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kuandika kitabu hicho akiwa gerezani. Boochani ambaye bado anazuiliwa katika gereza la Manus, eneo la Papua New Guinea hajaruhusiwa kuingia nchini Australia kupokea zawadi ya dola 100,000 (£55,000). Gereza hilo tata lilifungwa mwaka 2017 lakini yeye na mamia ya watu wengine walihamishiwa vituo vingine mbadala. Akizungumza na BBC kutoka kisiwa cha Manus, usiku ambao waandishi wenzake walioshinda tuzo walikua wakisherehekea mjini Melbourne, Boochani alisema ushindi huo umempatia "mchanganyiko wa hisia". Behrouz Boochani "Nasikia raha sana kwa sababu tumeweza kuangazia suala ambalo linawagusa watu wengi, bila shaka sasa ulimwengu utafahamu hali ngumu wanayopitia ,hilo ni jambo jema ...lakini kwa upande mwingine sioni haja ya kufurahia kwasababu marafiki zangu wengi wanateseka mahali hapa". Kitabu hicho kiliandikwa kwa lugha ya Farsi kupitia ujumbe katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp, na kutumiwa mtafsiri Omid Tofighian, wakati ambapo Boochani akiwa jela. "WhatsApp ni kama ofisi yangu,"alisema. "Sikuandika kwa karatasi kwasababu wakati huo walinzi walikua wakifanya upekuzi katika chumba chetu kila wiki au mwezi. Nilikua na hofu ya kupoteza kazi yangu, kwa hivyo ilikuwa bora kwangu kuandika na kumtumia mfasiri wangu." Boochani, alizuiliwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya kuingia nchini humo kwa boti kutoka kusini mashariki mwa Asia. Australia ina sera kali dhidi ya wakimbizi wanaowasili chini humo kwa boti kutafuta hifadhi, na imeapa kuwa haitawapatia hifadhi wakimbizi kama hao kwasababu wanahatarisha maisha yao kuingia nchini humo Mwaka jana, Marekani ilikubali kuwapatia hifadhi wakimbizi waliokuwa wakizuiliwa katika jela ya Manus na taifa la kisiwani la Nauru. Zaidi ya wakimbizi 100 wameondolewa lakini Boochani anasubiri taarifa kutoka kwa maafisa wa Marekani baada ya kufanya mahojiano miezi kadhaa iliyopita. Amepewa hadhi ya ukimbizi na Papua New Guinea lakini sawa na wakimbizi wengine hataki kuishi huko. Amesema aliamua kutoroka Iran kufuatia mvutano wa kazi yake ya uandishi na mamlaka ya nchi hiyo: "Nilihofia kufungwa jela nchini Iran kwa hivyo nikaamua kukimbilia Australia na kwa bahati mbaya nilipofika wakanikamata na kunifungia kwa miaka kadhaa." Waamuzi wa tuzo hiyo walielezea kitabu chake kama "kazi ya ajabu ya sanaa na nadharia muhimu ambayo inaibua hisia kwa njia rahisi". Masharti ya kuingia kwa Tuzo ya fasihi ya Australia ni kwamba waandishi lazima wawe raia wa Australia au wakazi wa kudumu. Lakini kituo cha Wheeler Centre, ambacho kinasimamia tuzo hiyo kilikubali ombi la waamuzi na kukubali kushirikisha kitabu cha Boochani katika shindano la kuwania tuzo hiyo. Sera ya wakimbizi ya Australia imeangaziwa sana na vyombo vya habari duniani na kukosolewa na Umoja wa Mataifa makundi ya kutetea haki za binadamu lakini baadhi ya wanasiasa wa Ulaya wamezisifia sana. Lakini Boochani anataka wasomaji wa kitabu chake kuelewa kuwa kumekuwa na njama ya kuwavua wakimbizi "Utambulisho na utu wao". "Sisi sio malaika wala watu wabaya," alisema. "Sisi ni binadamu, watu wa kawaida, hatuna ubaya wowote." Mwezi mmoja umepita tangu alipofungiwa katika gereza la Manus. 'Mimi ni kipande cha nyama kilichotupwa katika eneo lisilojulikana; gereza lenye uchafu na joto kali. Naishi kati ya mamia ya watu wenye nyuso za hasira, wengine wana hofu. Kila wiki ndege moja au mbili zinatua katika uwanja wa ndege wa kisiwa hiki na watu wengi hutolewa na kutupwa ndani ya jela letu ambapo wanachanganyika nasi kama kondoo waliyofikishwa kichinjioni' amesema Boochani. Mkimbizi na mwanahabari aliyezuiliwa kwa miaka kadhaa katika gereza la kisiwa cha bahari ya Pacific, ameshinda tuzo ya fasihi Australia. text: Katika kipindi cha uliopita, zaidi ya watu 1,000 wameokolewa kutoka kwenye vituo vya kidini ambako mara kwa mara watu wamekuwa wakishikiliwa katika hali mbaya Wengi miongoni mwa waliookolewa katika uvamizi wa polisi walikuwa wamefungwa kwa minyororo katika eneo la msikiti, amesema msemaji wa Polisi Gbenga Fadeyi. Katika kipindi cha uliopita, zaidi ya watu 1,000 wameokolewa kutoka kwenye vituo vya kidini ambako mara kwa mara watu wamekuwa wakishikiliwa katika hali mbaya. Polisi inasema baadhi ya waliookolewa katika msikiti huo walikuwa wameishi kwenye kituo hicho kwa miaka kadhaa Wazazi wamekuwa wakiwatuma watoto wanaowasumbua kitabia na vijana wanaoaminiwa kuwa na uraibu wa madawa ya kulevya au wale waliopatikana na makosa madogo katika vituo vya Koran vya kurekebisha tabia. Unaweza pia kusoma: Lakini maafisa wamevifananisha vituo hivyo na vituo vya ukatili ambapo watu wanafungwa minyororo , kufungwa pamoja na kufanyiwa dhuluma. Waliotekwa waliachiliwa Jumatatu jioni baada ya polisi kupewa taarifa na kijana mwenye umri wa maika 17 ambaye alikuwa ametoroka kutoka katika mahabusu nyingine katika eneo hilo. Mmiliki wa mahabusu hiyo na watu wengine wanane wamekamatwa , limeripoti gazeti la Punch nchini humo. Wanawake walikuwa ni miongoni mwa watu waliookolewa mwezi uliopita kutoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia cha kiislamu nchini Nigeria mwezi Oktoba mwaka huu Kamishna wa polisi wa jimbo hilo Bwana Shina Olukolu alinukuliwa akisema kwamba baadhi ya waathriwa wa utekaji huo wamesema wamekuwa wakishikiliwa kwa miaka kadhaa. Hali katika msikiti huo ilikuwa ni mbaya kwa binadamu kuishi na baadhi ya vifo vya waathirika vilivyotokea havikuripotiwa, alinukuliwa akisema. Unaweza pia kusoma: Huu ni mojawapo ya uvamizi wa wa hivi karibuni wa vituo vinavyoitwa ''vituo vya kiurekebisha tabia'' nchini Nigeria ambamo watu wanashikiliwa katika hali mbaya mkiwemo kufungwa na minyororo. Wengi husajiliwa kwenye taasisi hizo na ndugu zao ili kupata usaidizi wa kiroho na kurekebisha tabia kwa wanaotumia madawa ya kulevya. Mwezi uliopita polisi nchini Nigeria waligundua zaidi ya vijana 70 wakiwa wamefungwa katika shule binafsi ya kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mamia ya vijana wametoroka katika shule mbalimbali za dini ya kiislamu katika siku za hivi karibuni. Shule za bweni za kiislamu zinazojulikana kama Almajiris ni maarufu sana kwa waislamu wengi kaskazini mwa Nigeria. Polisi nchini Nigeria imewaokoa watu 259 kutoka katika kituo kisichokubalika kisheria kilichopo ndani ya msikiti katika mji wa Ibadan, uliopo katika jimbo la kusini magharibi mwa nchi hiyo la Oyo, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo. text: Trump amesema anapokea matibabu kupunguza chorestrol Hata hivyo, amedokeza kwamba baada ya kupimwa, imebainika kwamba uzani wake umezidi kiwango na anahitaji kupunguza. Mgombea huyo alitoa muhtasari wa hali yake kiafya kwenye karatasi ya ukurasa mmoja alipokuwa akishiriki katika kipindi cha televisheni cha The Dr Oz Show. Alimwambia mtangazaji kwamba uzani wake ni 236lb (kilo 107.048) na kimo chake ni 6ft 3in, jambo linalomfanya kuwa na uzito kupita kiasi. Amesema anatumia dawa za kupunguza kiwango cha cholesterol kwenye mwili wake, lakini yuko buheri wa afya. Anadaiwa pia kuwa na viwango vya juu kuliko kawaida vya homoni za testosterone. Makala kamili ya mahojiano yake ya mtangazaji huyo itapeperushwa hewani baadaye Alhamisi. Maafisa wake wa kampeni wamesita kufichua yaliyomo kwenye uchunguzi huo. Bw Trump aliambia mkutano wa siasa mjini Canton, Ohio, Jumatano usiku kwamba ana shaka kuhusu iwapo Bi Clinton, aliyezidiwa na kichomi Jumapili na kulazimika kuahirisha mikutano ya kampeni, ana uwezo wa kuongoza moja ya hafla zake. Aliuliza umati: "Mnafikiri Hillary angeweza kusimama hapa kwa saa moja na kufanya hivi? Sidhani, sidhani anaweza." Bw Trump baadaye alisema mgombea huyo wa chama cha Democratic "analala kitandani, akiendelea kupata nafuu". Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema baadaye wiki hii atatoa ripoti ya kina kuhusu hali yake kimwili na kiafya. text: Barcelona yamnunua Coutinho kwa pauni milioni 142 Liverpool watapata malipo ya mapema ya pauni milioni 105 kwa mbrazili huyo kwa miaka 25 huku pesa ambazo zitasalia zikitarajiwa kulipwa baadaye. Coutinho atasaini mkataba wa miaka mitano huko Nou Camp. Alijiunga na Liverpool akitokea Inter Milan kwa pauni milioni 8.5 mwezi Januari mwaka 2013. Pesa alizonunuliwa Coputnho ziko chini ya pauni milioni 200 ambazo Paris St-Germain iliwalipa Barcelona kumnunua Neymar na pauni milioni 165.7 ambazo itagharimu PSG kumununua Kylian Mbappe baada ya kumaliza mkopo wake huko Monaco. Mauzo ghali zaidi ya wachezaji duniani £200m - Neymar (Barcelona kwenda Paris St-Germain) 2017 £165.7m - *Kylian Mbappe (Monaco kwenda PSG kwa mkopo akiwa huru kununuliwa) 2017 £142m - Philippe Coutinho (Liverpool kwenda Barcelona) 2018 £135.5m - Ousmane Dembele (Borussia Dortmund kwenda Barcelona) 2017 £89m - Paul Pogba (Juventus kwenda Manchester United) 2016 Alijiunga na Liverpool akitokea Inter Milan kwa pauni milioni 8.5 mwezi Januari mwaka 2013. Barcelona imemsaini kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho kwa pauni milioni 142, ikiwa ni moja na mauzo ghali zaidi kuwai kufanywa. text: Serikali ya Tanzania inapanga kutumia takriban $14.3 bilioni, katika mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni ongezeko , kutoka shilingi trilioni 32.5 za Kitanzania katika mwaka wa fedha 2017/2018. Waziri wa fedha Philip Mpango, amesema sehemu kubwa ya makadirio hayo ya fedha katika bajeti zitatumika katika kuimarisha miundo mbinu ikiwemo reli barabara na kusambaza umeme katika maeneo ya vijijini. Bajeti ya Kenya, inakadiriwa kuwa dola bilioni 30.2, ambayo ni kubwa kuliko bajeti zote za nchi zingine za afrika mashariki kwa pamoja. Uganda kwa upande wake inakadiria bajeti ya dola bilioni 10.9 huku Rwanda dola bilioni 3.17. Kwa upande wa Uganda, wakosoaji wanaiona nchi hiyo ikiendelea kutingwa na madeni, nakisi ya biashara na kuongezeka kwa kiwango cha umasikini. Hata hivyo viongozi wa serikali ya nchi hiyo wanapinga na kueleza uchumi wa nchi hiyo ni imara na unaendelea kukua. Deni la Kenya limezidi utajiri wake kwa 57%, sehemu kubwa ikitokana na wakopeshaji na wawekezaji wa kimataifa. Kwa upande mwingine takwimu za madeni ya Rwanda, na Tanzania ni chini ya 40% ya pato jumla nchini. Huku mapato yakishuka katika mataifa yote ya Afrika mashariki, inatazamiwa kwamba awamu nyingine ya malipo ya kodi na mikopo yataidhinishwa na mawaziri wa fedha katika bajeti ya mwaka huu. Ina maana gani kwako? Swali kubwa linaloulizwa ni Bajeti hizi zina maana gani kwa raia wa kawaida? Hii ni fursa ya kuelewa serikali imelenga nini katika ugavi wa rasilmali na pia kusaidia kutathmini uzito inayoweka katika masuala ya maendeleo yanayomgusa na kumfaidi mwananchi. Bajeti hizi pia zinatoa ufafanuzi wa iwapo umaskini unapungua katika mataifa. Kipimo kinatokana na kuangalia iwapo mahitaji ya raia masikini yanazingatiwa kwa rasilmali za serikali au iwapo kodi zinazoidhinishwa zinawalemaza zaidi masikini. BBC Swahili imezungumza na baadhi kuhusu matarajio yao katika bajeti ya mwaka huu Afrika mashariki: Noel Shao, Tanzania Kwa maoni yangu sitegemei jambo jipya sana kwa sababu bado historia inaonyesha kwa miaka mingi kumekuwa na ukwamo wa utekelezaji wa bajeti kwa sababu ya uhaba wa fedha. Wizara nyingi zinashindwa kutimiza malengo walio jiwekea kwa sababu fedha wanazo omba hawatimiziwi kwa kiwango kile walicho ainisha. Na ni kwa bahati mbaya sana bajeti yetu kwa asilimia kubwa inategemea wahisani kuliko mapato ya Ndani. Na kwa jinsi hii ni ngumu sana kuwa na bajeti inayo tekelezeka labda hadi Serikali itengeneza mazingira rafiki katika kutegemea vyanzo vyake vya ndani kuliko nje. Kwa uhaba wa fedha Serikalini nategemea kuona uongezeko kubwa la bidhaa hasa mafuta jambo ambalo litasababisha mfumuko wa bidhaa sokoni, hivyo kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi.Ni matamanio yangu kuona makadirio ya fedha kwenye mfuko wa maendeleo ya jamii kuwa kubwa ili kuweza kugusa jamii moja kwa moja. Takwimu tu kwenye karatasi hazitaweza kuondoa na kupunguza changamoto zinazo wakabili wananchi. Vipengele muhimu kwa jamii ni Pamoja na afya, maji na elimu. Hapa ndipo panapo hitaji uangalifu kwani maeneo hayo ni msingi wa maisha hasa kwa wananchi wa kipato cha kati na Chini. Bajeti itakuwa na lugha inayo sikika kama itagusa maeneo hayo. Cornelius Kurgat, Kenya Mimi kama kijana ningependa kuona iwapo serikali imewatengea sehemu kubwa ya bajeti vijana kuwawezesha katika jamii, katika kuunda nafasi za kazi au ajira. Vijana wengi wamemaliza kusoma katika vyuo vikuu, hawana ajira na wanahitaji kitu cha kufanya. Pia tunavyosikia ni kuwa kuna ongezeko la bajeti karibu takriban trilioni tatu na hatujui fedha hizi zitatoka wapi. Hili linatia wasiwasi kwasababu raia hawajuia fedha hizi zitatoka wapi. Raia wana imani hatahivyo, kwamba hatua zitakazoidhinishwa na serikali zitakuwa kwa manufaa ya mwananchi wa chini. Rogers Kigenza, Rwanda Matarajio yangu kwenye bajeti hii yatajikita katika maeneo manne: Kwanza uundwaji wa nafasi za kazi kwa vijana, natarajia kutakuwa na mikakati ya kuwatengea vijana nafasi za kazi katika sekta za uwekezaji na viwanda. La pili ni miundo mbinu, kuimarisha sekta ya kutengeza barabara mpya, kusambaza umeme na hata maji. Unaona miji inapanuka na kuna changamoto za hapa na pale za barabara nzuri zinazohitajika lakini sio tu mijini bali hata vijijini. Kwasababu barabara zinaozunganisha miji na vijiji zinahitjaika. La tatu ni kilimo, tunajua kuwa hii ni sekta kubwa inayotoa kazi kwa watu wengi. Tunataka kuangalia je kilimo kimepewa kipa umbele kiasi gani? La mwisho ni elimu. Tunajua kuna changamoto katika elimu na tunataka tuangalie sekta hiyo imetengewa kiasi gani. Kwasababu ya changamoto zinazoshuhudiuwa mfano vyumba vya madarasa, na pia uboreshaji wa ubora wa elimu inayotolewa katika shule mbalimbali za walimu. Kheri Mbiro, Tanzania Tunategemea kwamba serikali itakuwa imeangalia katika maeneo ya biashara na uwekezaji katika kuimarisha nafasi zote zinazoweza kujitokeza. Kutokana na malalamiko kwamba biashara na hali ya uchumi ya watu wengi imekuwa chini, tunaamini kuwa itawaangalia watu wa chini kwasababu uwekezaji, kilimo, biashara na viwanda unashirikisha asilimia kubwa ya watanzania katika sekta rasmi na zisizio rasmi. Kwahivyo tunategemea kwamba Bajeti itatoa mianya kwa uwekezaji na viwanda sana, na ajira, kusaidia katika ufunguzi wa uchumi na kwa watu binafsi. Pia nategemea kwamba itasaidia kupunguza kodi au katika kuboresha mfumo wa ajira na kuwafanya wafanyakazi wapate unafuu wa maisha hasaa katika wakati huu ambao watu waenalalamika kwamba hali sio nzuri. Suala kubwa zaidi ni bidhaa, hapo ndipo kodi inajikita sana. Na kusababihsa ugumu kwa hali ya maisha hususan kwamba hela imewakimbia wengi, tunategemea kwamba serikali itasoma kodi iliyopunguzwa kwa bidha ambali mbali kuwawezesha Watanzania kupata nafuu ya ununuzi wa bidhaa pamoja na kupunguza makali ya maisha. Leo ni siku ya bajeti kwa nchi za Afrika Mashariki, ambapo mawaziri wa fedha wa nchi hizo watawasilisha bajeti za serikali za nchi zao kwa mwaka wa fedha 2019/2020. text: Malori mengine yanatarajiwa kuwasili baadaye wiki hii. Malori ambayo yamebeba zaidi ya tani 260 za mahindi yaliwasili katika mji wa mpakani wa Moyale leo. Malori mengine yanatarajiwa kuwasili baadaye wiki hii. Malori mengine yanatarajiwa kuwasili baadaye wiki hii. Mahindi hayo yamenunuliwa na Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Kenya. Ethiopia inadaiwa kupata $21.3m kutokana na uuzaji wa mahindi hayo. Gazeti la kibinafsi la Addis Fortune hata hivyo limeshangaa ni kwa nini Ethiopia inauza mahindi nje ilhali kuna maeneo mengine yanayokabiliwa na baa la njaa. Kenya imeanza kuagiza mahindi kutoka taifa jirani la Ethiopia kutokana na uhaba mkubwa wa nafaka hiyo. text: Mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo amesema hawana uhusiano na mtandao huo wa Kenya Mtandao huo wa Tanzania ni maarufu kwa kufichua mambo tofauti na kama jukwaa la watu kutoa maoni haswa wale walio nchini Tanzania na nchi za kigeni. Taarifa zake zimeanza kupatikana katika mtandao wa kenyatalk.com licha ya kwamba mtandao huo bado umefungwa. Waliokuwa wakiutumia mtandao wa Jamii Forums kabla ufungwe, wameanza kutoa maoni kwenye mtandao huo wakifurahia kupata jukwaa jingine la kushiriki kwenye mijadala na kupashana habari mtandaoni. Mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo amesema hawana uhusiano wowote na mtandao huo wa Kenya. Mmoja wa wachangiaji anayejiita Mwifwa ameandika: "Karibu sana mkuu, nafurahi kuwaona mkija na ID zenu za JF kuliko na wale wanaokuja kwa kubadili ID zao." "Na mimi pia nimefurahi, nilikuwa nafikiria sana jinsi gani mtaweza kuja huku naona matumaini yameanza kurejea, washtue basi na jirani zako. Nasikitika sana sikuwa na mawasiliano na watu wengi ya nje ya jamvini isipokuwa tuliishia PM tu." Hata hivyo idadi ya watu ambao wanatembela mtandao huo bado ni ya chini. Jamii Forums hiyo ya Kenya imeibuka siku tatu baada kufungwa nchini Tanzania kufuatia sheria zilizotangazwa na halmashauri ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) ambazo waanzilishi wa Jamii Forums walizioana kama zilizowalenga. Mambo muhimu kuhusu kanuni za mitandao Tanzania Sheria hizo mpya za TCRA ziliwahitaji wachapishaji wa mitandao na wanablogi kufichua wachangiaji na wamiliki kitu ambacho Bw Melo anasema kuwa ni kizingiti kwa kazi yao. Kupitia mtandao wa Kenya wa KenyaTalk, watumiaji wa Jamii Forums waliojiandikisha wanaweza kuchangia maoni yao vile walivyokuwa wanachangia awali. Siku ya mwisho iliyotangazwa na TCRA ya kuwataka wamiliki wa mitandao kujiandikisha na kupata leseni ni Ijumaa tarehe 15 mwezi huu lakini halmashauri hiyo imesema kuwa haitafunga mitando ambayo itakosa kutimizia sheria hiyo hapo kesho. Lakini mitandao hiyo itapigwa mafuruku kuchapisha taarifa zozote mpya hadi ikamilishe shughuli ya kujiandikisha. Mtandao maarufu nchini Tanzania wa Jamii Forums ambao ulisitisha huduma zake kutokana na sheria za serikali za kudhibiti mitandao taarifa zake zimepakiwa na mtandao wa Kenya ambao una sehemu iliyoitwa Jamii Forums. text: Wanambwa waliyozaliwa na mbwa wa amani walitumwa na Kim Jong-un Mbwa huyo anafahamika kama Gomi. Kiongozo wa Kaskazini Kim Jong-un, amemtumia mbwa hao mwenzake wa Kusini Moon Jae-in katika juhudi ya kudumisha amani licha ya msuko suko unaoshuhudiwa katika rasi ya Korea. Gomi, mbwa wa Pungsan anayesifika kwa uwindaji wake hatari alizaa watoto sita, wa kike watatu na wa kiume watatu. Rais Moon aliweka picha ya mbwa hao katika mtandao rasmi wa Twitter wa Blue House siku ya Jumapili. "Ikizingatiwa kuwa mbwa hubeba mimba kwa karibu miezi miwili, huenda, tulikabidhiwa Gomi akiwa na mimba," inaripotiwa aliandika hayo mbwa hao walipozaliwa. "Natumai uhusiano wa Korea mbili utakuwa hivi." Siku kadhaa baada ya mbwa hao kuzaliwa, ndege za kijeshi za Korea Kusini zilitua Pyongyang na shehena ya machenza. Rais Kim Jong Un na wa Korea Kusini, Moon Jae-in Awali Kaskazini ilikuwa imetuma makasha makubwa ya uyoga katika eneo la mpakani wakati wa mkutano kati ya viongozi hao wawili. Gomi na mbwa wengine, Songgang, walisafirishwa Kusini wakiwa na karibu pauni saba ya chakula na kuungana na mbwa wengine wa rais Moon ikiwa ni pamoja na mbwa anayefahamika kama Tory. Bwana Moon amekutana na Kim mara tatu mwaka huu na amekuwa kama mpatanishi kati yake na rais wa Marekani Donald Trump. Mnamo mwezi Septemba , alikuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kusini kuhutubia watu wa Korea Kaskazini wakati wa ziara yake mjini Pyongyang. Rais wa zamani Robert Mugabe 'hawezi kutembea' Alizungumza katika michezo ya Arirang- ambayo inatajwa kuwa shughuli kubwa ya propaganda - ambapo aliwahutubia takriban 150,000. Hivi karibuni rais Moon alisema kuwa anaamini mzozo wa Korea utakomeshwa hivi karibuni. Mapigano yalikomeshwa mwaka 1953 lakini hakuna mkataba wa amani uliotiwa saini. Rais wa Korea Kusini ametoa picha ya kwanza ya watoto wa mbwa waliyozaliwa na mmoja wa mbwa aliyopewa kama zawadi ya amani na kiongozi wa Korea kaskazini. text: Ripoti ilisema kuwa Putin aliamrisha kufanyika kwa udukuzi Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kuwa Urusi imechoshwa na madai hayo. Alisema kuwa ripoti iliyotolewa na mashirika ya ujasusi nchini Marekani kuhudu madai hayo haina msingi wowote. Hayo ndiyo matamshi ya kwanza kutoka Urusi tangu rais mteule Donald Trump akabidhiwe ripoti hiyo. Trump amekuwa akipinga madai ya udukuzi wa Urusi tangu ashinde uchaguzi wa urais mwezi Novemba. Lakini mkuu wake wa jeshi Reince Priebus, amesema kuwa Trump amekubali matokeo ya uchaguzi ambayo yaliwasilishwa kwake na wakuu wa ujasusi. "Hajakana kuwa urusi ilihusika kwenye masuala fulani," Priebus alisema. Hata hivyo hakufafanua ikiwa Trump aliamini ripoti kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa ameamrisha udukuzi huo kufanyika. Bwana Trump alitaja mkutano wa Ijumaa na wakuu wa ujasusi kuwa wenye manufaa, na kusema kuwa ataomba kati kipindi cha ndani ya siku tisini ofisini, kufanyika mpango wa kuzuia udukuzi wa mitandao. Donald Trump alikutana na maafisa wakuu wa ujasusi akiwemo jenerali James Clapper (kulia) Urusi inasema kuwa madai kuwa Marekani iliendesha kampeni ya udukuzi wa mitandao ili kushawishi uchaguzi wa urais nchini Marekani si kweli. text: Paul Lonyangata akiibuka mshindi katika mbio za Paris Marathon Mpinzani wake pia kutoka Kenya katika mbio hizo Stephen Chebogut alikuwa wa pili kwa muda wa saa 2 dakika 6 na sekunde 56 huku Solomon Yego pia wa Kenya akishikilia nafasi ya tatu katika muda wa saa 2 dakika 7 na sekunde 13. ''Nahisi vyema sasa kwa sababu lengo langu lilikuwa kuja hapa na kuibuka mshindi '',alisema. Mtu na mkewe kutoka Kenya washinda mbio za Paris Marathon Huku Paris ikiwa na jua Rionoripo ambaye ni mkewe mshindi wa mbio hizo upande wa wanaume Paul Lonyangata aliibuka mshindi. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 aliweka muda bora wa saa 2 dakika 20 na sekunde 50 na hivyobasi kushinda muda wake binafsi aliouweka kwa zaidi ya dakika 4. Ushindi wa wanandoa hao ulirudisha tabasamu kwa wanariadha Wakenya baada ya habari za kushangaza kwamba bingwa wa mbio za marathon za Olimpiki upande wa wanawake Jemima Sumgong alipatikana ametumia dawa za kusisimua misuli. Mkewe Lonyangata akivuka utepe kushinda mbio za Paris marathon upande wa wanawake Sumgong ni Mkenya wa kwanza mwanamke kushinda medali ya Olimpiki katika mbio za marathon alipoibuka mshindi katika michezo ya Olimpiki ya Rio. Mwanariadha huyo ambaye pia ni bingwa mtetezi wa mbio za london Marathon alipatikana alitumia dawa aina ya EPO baada ya kufanyiwa uchunguzi na IAAF. Lonyangata mwenye umri wa miaka 24 aliamua kuongeza kasi baada ya kilomita 35 akampita Chebogut na hivyobasi kujiongezea mataji aliyoshinda katika mbio za Shanghai marathon 2015 pamoja na Lisbon miaka miwili mapema. Katika mbio za wanawake Rionoripo alifuatwa kwa karibu na Mkenya mwenzake Agnes Barsosio kwa kuweka muda wa saa 2 dakika 21 na sekunde 02 huku Flomena Cheyech akimaliza udhia. Rionoripo alivunja rekodi iliokuwa imewekwa na raia wa Ethiopia Feyse Tadese ya saa 2 dakika 21 na sekunde 06 mwaka 2013 Mkenya Paul Lonyangata alipata ushindi mkubwa wa saa 2 dakika 6 na sekunde 10 katika historia yake licha ya kupoteza muda bora. text: Fernando Hierro alishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu akiwa na Real Madrid Hierro alipewa kazi ya kuwa kocha wa muda baada ya kocha wa taifa hilo Julen Lopetegui kufutwa kazi mkesha wa kuanza michuano hiyo. Hata hivyo, mabingwa hao wa dunia wa mwaka 2010 waliondolewa kwenye michuano hiyo kupitia mikwaju ya penalti na wenyeji Urusi hatua ya 16 bora. Hierro, 50, ameamua kutafuta mambo mengine ya kufanya, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Uhispania. Taarifa imesema mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid amekataa kurejea katika wadhifa wake wa awali kama mkurugenzi wa michezo na kuamua "kuchukua changamoto mpya." Lopetegui alifutwa kazi siku mbili kabla ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Ureno baada yake kutangazwa kuwa meneja mpya wa Real Madrid, wadhifa uliobaki wazi baada ya kujiuzulu kwa Zinedine Zidane. Lopetegui aliteuliwa meneja wa Uhispania mwaka 2016 baada ya kustaafu kwa Vicente del Bosque na alikuwa hajashindwa hata mechi moja kufikia wakati wa kuondoka kwake. Uhispania waliongoza Kundi B chini ya Hierro katika Kombe la Dunia. Hata hivyo, walikuwa wametoka sare ya 3-3 dhidi ya Ureno baada ya kufungwa dakika za mwisho, na walikuwa nyuma 2-1 dhidi ya Morocco kabla ya kusawazisha dakika za mwisho. Baada ya kutupwa nje kwao Urusi, Hierro alisema aliamua kuwajibika kutokana na kushindwa kwao kusonga. "Tulijitolea kadiri ya uwezo wetu lakini hii ni soka," alisema. "Sifikiri unaweza kuzungumzia kuhusu timu kusambaratika au kuporomoka. Kuna mstari mwembamba sana kati ya kushinda na kushindwa." Fernando Hierro, aliyewaongoza Uhispania katika Kombe la Dunia 2018, amejiuzulu wadhifa wake kama kocha wa muda na taarifa zinasema hatarejelea kazi yake ya awali ya mkurugenzi wa michezo. text: Radamel Falcao, Alvaro Morata, Lionel Messi na Paul Dybala Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, kijana mpya wa Chelsea Alvaro Morata na Romelu Lukaku wa Manchester United wako kileleni kwa ufungaji wa mabao. Lakini wako katika kiwango kipi na mawiji wengine wa Ulaya? Wale wanaowania kiatu cha dhahabu barani Ulaya Ni mwezi wa pili wa msimu na wachezaji wawili tayari wamefunga mabao kumi na zaidi. Mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcaoa, amefunga mabao 11 katika mechi saba za Ligue 1, huku Paulo Dybala, akiifunga Juventus mabao 10 kwenye mechi sita za Serie A. Kwenye La Liga, Lionel Messi anaongoza kwa ufungaji kwa mabao tisa katika mechi sita. Ince, Redmond... Ronaldo? Cristiano Ronaldo (katikati) Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Tom Ince wa Huddersfield na Nathan Redmond wa Southampton wana kipi kwa pamoja? Wote wako kwenye kikosi cha wacahwa wanlioana matyzuaia makuwna wangai wa uigumngaji wa mabao Redmond alipiga mikwaju 21 katika mechi sita bila kufunga bao. Ronaldo haonekani kufurahishwa na kasi ya Messi na matatizo yake ya kufunga mabao yanaendelea. Nohodha huyo wa kikosi cha Ureno hajafunga bao hata moja msimu huu licha kujaribu mara 18 ,12 yakiwa kwenye mechi moja. Huku wachezaji watatu wakiwa wamefunga mabao sita kwenye mechi 6, mbio za kushindania kiatu cha dhahabu zinaashiria kuwa zitakuwa mbio kali sana. text: Wanawake 137 huuawa kila siku kote duniani Wanasema nyumbani ndilo eneo ambapo kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa mwanamke kuuawa. Zaidi ya nusu ya wanawake 87,000 waliuawa mwaka 2017 waliripotiwa kufa mikononi mwa watu walio karibu nao. Kati ya idadi hiyo takriban wanawake 30,000 waliuawa na wapenzi wao na wengine 20,000 waliuawa na watu wa familia. BBC 100 walitaka kujua zaidi wanawake waliojipata kwenye takwimu hizi. Tunakupa hadithi kuhusu baadhi ya mauaji haya na jinsi yaliripiotiwa. Zaidi ya nusu ya wanawake waliuawa na wapenzi au jamaa Idadi ya wanaume wanaouawa bado ni ya juu Data iliyokusanywa na UNODC ilionyesha kuwa wanaume kote duniani wako na uwezekano mara nne zaidi kuliko wanawake kupoteza maisha kutokana na kuuliwa makusudi Umoja wa Mataifa unasema kuwa wanaume wanachangia vifo 8 kati ya 10 kote duniani. Pia ripoti hiyo hiyo inasema kuwa zaidi ya vifo 8 kati ya 10 vya muaji yaliyofanywa na wapenzi ni dhidi ya wanawake. Wanawe wako katika hatari zaidi ya kuuliwa na mtu aliye karibu nao Wanawake arobaini na saba, nchi 21, siku moja Takwimu za Umoja wa Mataifa zinachambua matokeo ya mwaka 2017 yanayotokana na takwimu za mauaji kutoka kwa serikali. BBC 100 Women na BBC Monitoring walichukua hatua ya kufahamu zaidi kuhusu wanawake walioathiriwa. Tulifuatilia wanawake waliouawa na watu wengine Oktoba mosi mwaka 2018 kote duniani. Wanawake 47 walihesabiwa kuuliwa kwa sababu zinazohusu jinsia kwenye nchi 21 tofauti na mengi ya mauaji haya bado yanachunguzwa. Hivi ni visa vitano vilivyoripotiwa na vyombo vya habari na kisha kuidhinishwa na mamlaka mabzo BBC iliwasiliana nazo. Judith Chesang Judith Chesang, 22, Kenya Jumatatu 1 Oktoba Judith Chesang na dada yake Nancy walikuwa shambani wakivuna mtama. Judith, mama wa watoto watatu alikuwa ametengana na mume wake Laban Kamuren na kuamua kurudi kwa wazazi wake katika kiji kilicho kaskazini mwa nchi. Mara dada hao walianza kufanya kazi, aliwasili katika shamba la familia akashambulia na kumuua Judith. Polisi wanasema Laban aliuawa na wanakijiji. Wanawake barani Afrika ndio walio kwenye hatari zaidi Afrika ndilo eneo wanawake wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kuuawa na wapenzi wao au na mtu wa familia kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa. Ilifanyika kwa watu 3.1 kati ya watu 100,000. Asia ilikuwa na idadi ya juu zaidi ya wanawake waliouwa na wapinzani au watu wa familia mwaka 2017, kwa jumla wanawake 20,000. Neha Chaudhary Neha Sharad Chaudury, 18, India Neha Sharad Chaudury aliuawa wakati siku yake ya kuhitimiza miaka 18. Alikuwa ameenda kusherehekea na mpenzi wake. Polisi waliiambia BBC kuwa wazazi wake hawakukubaliana na uhusiano huo. Wazazi wake na mwanamume mmoja wa familia wanalaumiwa kwa kumuua akiwa nyumbani usiku huo. Uchunguzi unafanywa na watatu hao wako kuzuizini wakisubiri kushtakiwa. BBC iligundua kutoka kwa wakili anayewakilisha wazazi wa Neha na mwanamume wa familia kuwa wanataka kukana mashtaka hayo. Zeinab Sekaanvand Zeinab Sekaanvan, 24, Iran Zeinab Sekaanvan alinyongwa na mamlaka za Iran kwa kumuua mume mwake. Zeinab alizaliwa kaskazini magharibi mwa Iran kwenye familia moja maskini eneo la Kurdi. Alikimbia nyumbani akiwa msichana kuolewa akiwa na matumaini ya kupata maisha mazuri. Amnesty International inasema mume wake alikuwa anadhulumu na alikataa kumpa talaka na kwamba malalamiko yake yalipuuzwa na polisi. Alikamtwa kwa kumuua mume wake akiwa na umri wa miaka 17. Waliomuunga mkono wakiwemo Amnesty wanasema aliteswa ili akiri kumuua mume wake, akapigwa na polisi na hakupata hukumu yenye haki. Sandra Lucia Hammer Moura Sandra Lucia Hammer Moura, 39, Brazil Sandra Lucia Hammer Moura aliolewa na Augusto Aguiar Ribeiro akiwa na miaka 16. Wanandoa hao walikuwa wametengana kwa miezi mitano wakati mume wake alimuua. Polis huko Jardim Taquari waliiambia BBC kuwa alichomwa kisu shingoni. Walipata video ya mume wakae kwenye simu yake. Kwenye video hiyo alisema Sandra alikuwa na urafiki na mwamamume mwingine na alihisi kuhujumiwa. Pia alisema kuwa hawezi kukamatwa kwa sababu wote watanda kwa Mungu pamoja. Kisha akajinyonga kwenye chumba chao cha kulala. Marie-Amélie Vaillat Marie-Amélie Vaillat, 36, Ufaransa Marie-Amélie alichomwa kisu na kuuawa na mume wake, Sébastien Vaillat. Wanandoa hao walikuwa wametengana baada ya miaka minne ya ndoa. Alimshambulia kwa kisu kabala ya kukiri kwa polisi. Siku chache baadaye alijiua akiwa gerezani. Nje ya mlango wa duka la Marie-Amélie Vaillat eneo la Rue Bichat, wenyeji waliacha maua na kupanga kufanya matembezi kwa heshima kwake. Makumbusho ya Marie-Amélie Vaillat Inagharimu nini kisa cha kuuliwa mwanamke kuripotiwa? Kukusanya ripoti hizi, mtandao ya waandishi wa habari wa BBC Monitoring na watafiti walichambua televisheni, radio, magazeti na mitadao ya kijamii kote duniani, wakiangalia ripoti za wanawake waliouawa tarehe 1 Oktoba mwaka 2018. Walipata jumla ya ripoti 47 za wanawake walioauawa kote dudiani. Tumechapisha baadhi ya visa hivi. Kuna vingine vingi ambavyo nia yao haijulikani au waliotekeleza hawajatambuliwa. Je wanawake 100 ni nini? BBC 100 Women huwataja wanawake 100 wenye ushawishi na wenye kutia moyo kote duniani kila mwaka na tunaangazia hadithi zao. Umekuwa mwaka wenye umuhimu katika masuala ya haki za wanawake kote duniani, kwa hivyo mwaka 2018 msimu wa Wanawake bora 100 wa BBC, utaangazia wanawake waasisi wanaotumia ari, hasira na ghadhabu kushinikiza mageuzi halisi duniani. Jumuika nasi kwenye Facebook, Instagram na Twitter na tumia #100Women Takriban wanawake 137 kote duniani huuawa na waume na pia wape nz i wao au watu wa familia kila siku, kwa mujibu wa data mpya zilizotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu (UNODC). text: Marubani walifuata maagizo yaliopendekezwa na Boeing kabla ya ajali hiyo kulingana na ripoti ya kwanza ya ajali hiyo. ''Licha ya juhudi zao , marubani walishindwa kuidhibiti ndege hiyo'' , alisema waziri wa uchukuzi Dagmawit Moges. Ndege hiyo aina ya ET302 ilianguka baada ya kupaa kutoka mji wa Adis Ababa , na hivyobasi kuwaua watu 157. Ilikuwa ndege ya pili aina ya Boeing 737 kuanguka katika kipindi cha miezi mitano. Mwezi Oktoba mwaka uliopita , ndege aina ya Lion Airflight JT610 ilianguka baharini karibu na Indonesia na kuwaua watu wote waliokuwa wameabiri. ''Wafanyikazi wa ndege hiyo walijaribu kila mbinu walizoelezewa na mtengenezaji wa ndege hiyo lakini walishindwa kuidhibiti'' , bi Moges alisema katika mkutano na wanahabari mjini Adis Ababa. Katika taarifa , afisa mkuu wa Ethiopia Airlines , Tewolde GebreMariam alisema kuwa alifurahishwa na kazi ya marubani hao kujaribu kuidhibiti ndege hiyo. ''Ni bahati mbaya kwamba walishindwa kuidhibiti ndege hiyo kutoangukia pua yake'', ilisema kampuni hiyo ya ndege katika taarifa yake. Waathiriwa ni akina nani? Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian Airlines CEO Tewolde Gebremariam ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na : Wakenya 32 Kenyans, raia wa Canada 18 raia tisa wa Ethiopia , wataliano wanane , Wachina wanane, wamarekani wanane , waingereza saba , Wafaransa saba , Wamisri sita, Wajerumani watano , Wahindi wanne na wanne kutoka Slovakia. Waaustralia watatu, Waswizi watatu, Warusi watatu , Warusi 3, Wakomoro wawili, Wahispania wawili, Wapoland wawili, Waisraeli wawili. Kulikuwa pia na abiria mmoja kutoka nchi za Ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, Togo, Msumbiji, Rwanda, Sudan, Uganda na Yemen. Ndege hiyo ya Boeing 737 Max-8 ilikua ni mpya Boeing ambayo ni kampuni ambayo iliitengeneza ndege iliyoanguka , imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba 'inafuatilia kwa karibu hali' ya mambo. Ndege ya 737 Max-8 ni mpya angani , ikiwa ilizinduliwa kwa mara ya kwanza 2016. Iliongezwa kwenye safari za ndege za Ethiopian Airlines Julai mwaka jana. Boeing imesema ''imesikitishwa sana'' na ajali na imejitolea kutuma kikosi cha wahandisi wake kutoa usaidizi wa kiufundi. Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo , kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia. Ripoti ya uchunguzi kuhusu kuanguka kwa ndege ya Ethiopia Airlines mwezi uliopita inasema kuwa ndege hiyo ilitaka kuangukia pua yake mara kadhaa kabla ya ajali hiyo. text: Neymar, Kylian Mbappe au Kevin de Bruyne huenda siku moja wakarithi nafasi za Cristiano Ronaldo au Lionel Messi Wawili hao wameonyesha uwezo wao wa kuwa wachezaji bora duniani kwa takriban muongo mmoja, wakishikilia mataji yaa mchezaji bora kitu ambacho hakijawahi kufanyika miaka iliopita na hakitafanyika tena katika siku zijazo. Mchezo wao mzuri umewafanya kutuzwa mataji mengi huku Messi anayeichezea Barcelona akishinda mataji matano ya Ballons d'Or, ikiwa ni moja zaidi ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Lakini ni nyota wapi wa soka watakaowarithi wachezaji hao wawili. Tuliwauliza wataalam wa soka wa BBC kutoa uamuzi wao. Nyota ya mchezaji De Bruyne imeanza kung'aa Tangu aanze kuichezea Manchester City mnamo mwezi Septemba 2015, Kevin de Bruyne ametoa pasi nzuri za kusababisha mnagoli zaidi ya mchezaji mwengine yeyote katika ligi ya Ulaya. Mchezaji huyo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne pamoja na mwenzake wa Chelsea Eden Hazard ndio wachezaji katika ligi ya Uingereza wanaopigiwa upato kushindania taji la Ballon d'Or wakati utawala wa Messi na Ronaldo utakapofikia kikomo. De Bruyne, 26, amekuwa mchezaji bora msimu huu na huku mchezaji huyo wa Ubelgiji akiwa hajafikia kiwango cha wawili hao nyota yake imeanza kung'aa Mpinzani wa De Bruyne anaweza kuwa mchezaji mwenza wa Chelsea Eden Hazard, ambaye pia ana umri wa 26, ambaye mchezo wake msimu huu kufuatia uwezo wake wa kuisadia Chelsea kushinda taji la ligi ya Uingereza pia umemfanya kuwa mwananiaji wa tuzo hilo siku zijazo. Mshambuliaji wa City Gabriel Jesus ambaye ana umri wa miaka 20 pia huenda akaonekana kuwa mgombea wa tuzo hilo huku kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba pia akionekana kuudhibiti ulimwengu katika miguu yake. Wachezaji wa Tottenham Harry Kane na kiungo wa kati Dele Alli pia watajiimarisha miongoni mwa wachezaji bora wa Ulaya huku mchezaji wa Liverpool Phillipe Coutinho ,25, akidaiwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa soka duniani. Na iwapo tunaangazia nyota inayoendelea kung'aa ambaye huenda akatawazwa katika siku za usoni ,basi tusimsahau mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah? Ana umri wa miaka 25 na amekuwa mchezaji bora tangu uhamisho wake kutoka Roma wa £34.5m. Neymar anakabiliwa na shinikizo ya kuipatia PSG kombe la vilabu bingwa Neymar alihusishwa na mabao 164 katika mechi 186 alizoichezea Barcelona Tuanze na mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar - ambaye ndiye mchezaji bora wa soka ya Brazill tangu 2011 , na mtu ambaye anaweza kuwa mshindi wa kwanza wa taji la Ballon d'Or kutoka Brazil tangu Kaka 2007. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ndio kiongozi wa timu yake na mchezaji mwenye thamani kubwa duniani. Katika mashindano ya kombe la dunia la 2014 ndio mchezaji ambaye Brazil walimtegemea sana na dunia ilijionea timu yake ilivyocheza vibaya alipotoka katika timu hiyo. Sasa yuko imara zaidi .Lakini ana changamoto kubwa baada ya kujiunga na PSG kwa sababu alinunuliwa ili kuishindia timu hiyo kombe la vilabu bingwa na iwapo atashinda itaonekana kwamba ameshindwa. Iwapo utakiangazia kikosi cha Brazil , hakuna wachezaji wengi kama yeye . Jesus ana uwezo na ana mkufunzi hodari wa kumwezesha kufika katika kiwango cha mchezaji bora kupitia Pep Guardiola lakini hilo huenda lisiafikiwe hivi karibuni. Mchezaji wa Brazil anayefanya vizuri Ulaya kwa sasa ni Ederson-lakini kipa hajawahi kushinda taji hilo tangu Lev Yashin mwaka 1963. Kuna habari nyingi za sifa kumhusu mshambuliaji wa Flamengo mwenye umri wa miaka 17 Vinicius, lakini hajafanya lolote kuthibitisha hilo ijapokuwa ana kandarasi na Real Madrid. Mshambuliaji wa Gremio Luan mwenye umri wa miaka 24 ana kitu tofauti, lakini timu za Ulaya zilikuwa zikimchunguza na kuamua kutomsajili. Iwapo Neymar atashinda taji la Ballon d'Or, atakuwa mchezaji wa kwanza wa Brazil ambaye jina lake halianzi na R- baada ya Ronaldo, Ronaldinho na Ricky Kaka. Mbappe ana uwezo mkubwa wa kuwa mchezaji bora duniani Akiwa na umri wa miaka 18 Kylian Mbappe ndiye mchezaji mwenye umri mdogo aliyefunga mabao 10 katika kombe la vilabu bingwa. Wakati nilipoitembelea klabu ya kwanza ya Kyllian Mbappe, AS Bondy, mapema mwaka huu , wakufunzi wake walianiambia kwamba wamekuwa wakimuita mshindi wa siku zijazo wa Ballon D'Or tangu alipokuwa akiitembelea klabu hiyo katika umri wa miaka saba. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alionyesha umahiri wake msimu uliopita alipoifungia Monaco mabao 26, na sasa ana uwezo mkubwa wa kuwa mchezaji bora duniani. Mwaka ujao , Mbappe atakuwa mchezaji wa pili mwenye thamani duniani wakati Paris St-Germain itakapompatia mkataba wa kudumu na mchezaji atakayekuwa katika nafasi ya tatu - Ousmane Dembele - anaweza kuwa mpinzani wake mkuu katika kipindi cha muongo mmoja ujao. Jeraha la nyuma ya goti limemzuia Dembele, 20, kuwaonyesha mashabiki wa Barcelona kile anachoweza kufanya , lakini alionyesha katika klabu ya Rennes na Borussia Dortmund kwamba ana kila uwezo wa kuwa mchezaji bora duniani. Huu hautakuwa upinzani kati ya Messi na Ronaldo, - Mbappe na Dembele ni marafiki wakubwa na wataichezea safu ya mashambulizi ya Ufaransa katika kipindi kirefu kijacho 'Keita ana siku njema zijazo Katika mechi 31 za Bundesliga msimu uliopita, Keita anayeeleka Liverpool alifunnga mabao manane na kutoa pasi saba za mabao kutoka katikati Iwapo Mwafrika atashinda taji la Ballon d'Or siku zijazo au la itategemea na mkufunzi wa Ujerumani - Jurgen Klopp. Wachezaji wa Afrika wenye thamani ya juu , wale walio na uwezo wa kuimarika watakuwa wakicheza katika kikosi cha Jurgen Klopp na Liverpool katika kipindi cha miaka michache ijayo - mchezaji wa Misri Salah, mchezaji wa Senegal Sadio Mane na mchezaji wa Guinea Naby Keita. Wachezaji wote watatu tayari wameonyesha kwamba wana uwezo mkubwa katika klabu yao. Salah na Mane ambao wote wana umri wa miaka 25 pia wana uwezo wa kuwa viungo muhimu katika timu zao za kitaifa wote wakiwa tayari kuzichezea timu zao katika kombe la dunia msimu ujao. Wote wawili wamebarikiwa na kasi na wanaimarisha uwezo wao wa kufunga mabao -iwapo hilo litaendelea wanaweza kuwa na sifa ya kuwa wachezaji bora duniani. Keita ndiye mchezaji ambaye ameisaidia klabu ya RB Leipzig kuimarika katika ligi ya Bundesliga na anatarajiwa kuimarika katika kikosi bora na katika ligi yenye ushindani mkubwa akiichezea in a stronger squad and in a more competitive league at Liverpool. Iwapo atavaa viatu vya mchezaji wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard, basi atatuzwa duniani. Akiwa na uwezo wa kulinda lango kama vile N'Golo Kante na uwezo wa kufanya mashambulio anaweza kutengeza magoli na kufunga, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ana siku bora za usoni. Kwa wengine ni kitu ambacho hakiaminiki kwamba siku moja soka itaendelea bila ya uwepo wa Ronaldo and Lionel Messi. text: Haijulikani ikiwa serikali ya Afrika Kusini ilimpa Bi Mugabe kinga ya kidiplomasia. Inaeleweka kwamba Grace Mugabe alisafiri pamoja na mumewe leo asubuhi. Wawili hao walikuwa wanahudhuria mkutano wa kikanda Afrika kusini. Haijulikani ikiwa serikali ya Afrika Kusini ilimpa Bi Mugabe kinga ya kidiplomasia. Mwamitindo Gabriella Engels 20, alimshtumu Bi Mugabe kwa kumpiga baada ya kumpata akiwa na watoto wake wawili wavulana ndani ya chumba kimoja cha hoteli huko Sandton, mtaa mmoja wa kifahari kaskazini mwa mji wa Johannesburg Mwamitindo Gabriella Engels Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine. Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye analaumu Bi Mugabe kwa kumgonga, wanasema kuwa mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa. Bi Engels, alionekana kwenye mkutano wa waandishi waahabari siku ya Alhamisi akiwa na bendeji kubwa kwenye uso wake. Grace Mugabe alikataa kufika mahakamani baada ya kushtakiwa wiki jana, akisema kwamba ana kinga ya kidiplomasia. Mamalaka za Afrika kusini zimekanusha madai kwamba Grace Mugabe ana kinga ya kidiplomasia. Vyombo vya habari nchini Zimbabwe zinasema mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe amerejea nyumbani kutoka Afrika kusini licha ya kukabiliwa na mashtaka ya kushambulia mwanamitindo Gabriella Engels katika hoteli moja Johannesburg. text: Mshindi wa Tuzo la BBC World News Komla Dumor Award Tuzo hilo BBC World News Komla Dumor Award, lina lengo la kuendelea kuimarisha uandishi wa habari kuhusu Afrika. Mtangazaji huyu wa kituo cha televisheni cha KTN cha Kenya,alichaguliwa miongoni mwa washiriki wapatao 200. Nancy Kacungira ni mtangazaji habari wa kituo cha televisheni cha KTN Mshindi huyo atakuwa makao makuu ya BBC, mjini London kwa miezi mitatu na pia kutuma taarifa za habari za BBC Televisheni , radio na mtandao kutoka barani Afrika. Tuzo hilo lilianzishwa ili kumuenzi Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41. Bi Kacungira alisema: " nimeshtushwa, lakini pia kufurahishwa sana kwa kupokea habari hizi. Nancy Kacungira, Mtangazaji wa KTN , Kenya ashinda tuzo la BBC Nimepokea kwa unyenyekevu mkubwa ushindi wa tuzo hili". "Hili ni tuzo la bara hili ninalolipenda na ambalo nimejitolea kulihudumia, kwa kutekeleza jukumu langu la kutoa taswira halisi ya bara ambalo kwa muda mrefu taarifa zake zimekuwa zikipotoshwa na kuongezewa chumvi.' "Kuwa sehemu ya kumbukumbu ya Komla ni heshima kubwa, nikama ndoto.'' ''Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu ili kuthibitisha uaminifu niliyoonyeshwa kwa kupewa tuzo hilo.'' 'Pia nitahakikisha kwamba mazao yake hayanifaidi mimi tu". Wahariri wamsifu Mmoja ya waamuzi, Mhariri wa habari, wa Idhaa ya BBC Afrika, Vera Kwakofi,alimsifu bi Kacungira. '' Nancy ni mwerevu sana na ana upeo mpana wa mawazo na ujuzi unaojitokeza mara moja." "Nimefurahi kwamba katika Nancy tumempata mwanahabari mwenye kipaji na ari, ''mtu anayestahili kuwa mshindi wa tuzo tulilolianzisha kwa jina la Komla." Nancy amekulia Uganda ambapo alihitimu kutoka chuo kikuu cha Makerere, mjini Kampala. Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41 Ana ujuzi wa zaidi ya miaka 14 katika fani ya uwanahabari kwani amefanya kazi katika mshirika kadha ya habari nchini Kenya, Uganda na Tanzania. Pia ana shahada ya uzamifu katika mawasiliano kutoka chuo kikuu cha Leeds. Kwa wakati huu yeye ni mtangazaji wa habari za usiku za Kiingereza katika kituo cha televisheni cha KTN na pia ni mhariri wa mtandao wa Kijamii wa shirika hilo. Washiriki wawili waliibuka nambari mbili: Leila Dee Dougan kutoka Afrika Kusini na Paa Kwesi Asare kutoka Ghana. Komla hasahauliki Mshindi wa Tuzo la BBC World News Komla Dumor Award Komla Dumor alikuwa mtangazaji raia wa Ghana mwenye kipaji cha kipekee ambaye katika maisha yake mafupi alikuwa na mvuto wa ajabu nchini Ghana, Afrika na ulimwenguni. Aliwakilisha ule upande wa Afrika wa ujasiriamali na umahiri. Kutokana na uwanahabari wake dhabiti na kipaji chake cha kuelezea habari kwa uweledi mkubwa , Komla alifanya kazi bila kuchoka ili kutoa taswira halisi ya Afrika kwa ulimwengu. BBC inashukuru shirika la Standard Chartered na wahisani wengine kwa misaada yao. Mwanahabari kutoka Uganda, Nancy Kacungira ni mshindi wa Tuzo la kwanza la kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Komla Dumor. text: Kimberley Wadsworth alianza kucheza kamali mwaka 2015 Kimberley Wadsworth aliamua kujiua mara baada ya kumaliza fedha zote katika mchezo wa kamari. Binti huyo alimuomba mama yake fedha za kulipa madeni yake katika mchezo huo lakini mwisho wa siku fedha zote alizichezea tena kamari na kumuacha mama yake bila sehemu ya kuishi. Kimberley ambaye alikuwa na umri wa miaka 32,alianza kucheza kamari katika sehemu za starehe na kwenye mitandao mnamo mwaka 2015. Alianza kupata uraibu wa kamari baada ya kupata sonona mara baada ya kifo cha baba yake na kuwa na ndoa isiyokuwa na furaha. Mtoto huyo alijaribu kumficha mama yake juu ya hali yake ya sonona. Binti huyo alitumia zaidi ya paundi 44,000 katika kamari pamoja na paundi 17,000 kutoka katika urithi wa bibi yake . Bi Wadsworth, mwenye umri wa miaka 65, ambaye ndiyo mama yake alidai kuwa ilimbidi auze nyumba ya familia ili ampe fedha ya kulipa madeni ya kamari ingawa hakuyalipa mpaka alipojiua. "Hakulipa deni hata moja bali aliendelea kucheza kwa muda wa wiki mbili mfululizo hivyo nikabaki bila mahali pa kuishi" alieleza bi.Wadsworth . Mtoto wa Kay Wadsworth's alicheza kamali kwa paundi 36,000 Mama huyo anasema kwamba alijaribu kumtafutia mtaalamu wa afya ya akili ili aweze kupata msaada wa tatizo la uraibu wa kucheza kamari lakini hakwenda. Badala yake aliandika ujumbe " tumechelewa sana mama" kabla hajajiua. Bi.Wadsworth alisema kuwa kama msaada ungetolewa mapema zaidi basi mtoto wake angekuwa hai bado. "Kuna wataalamu ambao wanajua namna ya kukabiliana na watu ambao wana uraibu wa kucheza kamari na wanajua dalili za mtu ambaye ameanza kupata tatizo hilo". "Wataalamu wanajua dalili za watu wenye uraibu wa kamari lakini wanaficha , Wanaendelea kutudanganya kuwa si rahisi kuacha," Wadsworth alisema. Kuna watu ambao wanapata uraibu kwa kiwango kikubwa sana mpaka kuhatarisha maisha yao kwa kujiua. Watu wapatao 340,000 nchini Uingereza wana tatizo kubwa la uraibu wa kamari kwa muhimu wa tume ya mchezo wa kamari. Vituo kadhaa vya afya vimeanzishwa nchini humo ili kuwasaidia watu walioathirika na tatizo la kamari." Uraibu wa kucheza kamari huwa unaongezeka kadri mtu anapozidi kupata fedha nyingi. Kijana mmoja kwa jina la Chris Murphy,alianza kupata uraibu alipopata paundi 350 akiwa na umri wa miaka 17. Tangu wakati huo mpaka alipofika miaka 23, ametumia zaidi ya paundi 100,000 katika kamari Kijana mwenye miaka miaka 33 na ameweza kujizuia kucheza kamari kwa miezi nane. Ukiangalia upande wa matatizo ya kiafya, hali yake sio nzuri na anahitaji msaada. Kwa mujibu wa mtaalamu wa afya anasema kwamba, Jambo la muhimu ni kumtaka yeye mwenyewe kupambana kuacha kucheza mchezo huo wa kamari ambao anadhani kuwa hawezi kuacha. Inawezekana kuacha kucheza kamari ni jambo gumu zaidi ya mtu kuamua kuacha madawa ya kulevya au pombe. Hakuna ubaya kwa mtu kukubali kuwa anahitaji msaada. Ni muhimu watu wanaoanza kupata tatizo hili kutafuta msaada mapema kwa sababu madhara au matokeo yake huwa sio mazuri. Kamari inaweza kumfanya mtu afilisike, kupoteza uhusiano mzuri na wapendwa wake, kupoteza ajira na kupata msongo wa mawazo. Mama mmoja nchini Uingereza alipoteza mtoto wake kwa sababu ya kamari mara baada mtoto huyo kucheza kamari ya kiasi cha fedha cha paundi 36,000 ambayo ni sawa na dola 45,000 . text: Waasi wa kundi la ADF kutoka Uganda wamelaumiwa kwa mauaji ya sasa Vifo hivi ni vya hivi karibuni katika wimbi la miaka miwili la ghasia katika jimbo hilo. Mauji hayo yametokea katika mji wa Eringeti, uliopo kilomita 55 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Beni, mji ambao umekuwa ukikumbwa na misururu ya mashambulio ambayo tayari yamesababisha vifo vya raia 700, kulingana na afisa katika mkoa huo Amisi Kalonda, ambaye amewalaumu waasi kutoka Uganda kwa mashambulio ya hivi karibuni. Bwana Kalonda amesema kuwa wajumbe wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye idadi kubwa ya Waislam wenye itikadi kali kutoka Uganda ambao wamekuwa kwenye kanda hiyo kwa zaidi ya miongo miwili , walivamia mji huo Jumamosi mchana. "ADF wamevamia tena wau wa Eringeti na maeneo yanayozingira mji huo asubuhi ," aliliambia shirika la habari la AFP, kutoka mji mkuu wa Kivu kusini wa Goma. "Jana, waliwauwa raia 10. Miili mingine ya watu kumi na miwili ilipatikana Jumapili katika vijiji vinavyozingira mji ." alisema Bwana Kalonda akiongeza kuwa waathiriwa waliuliwa kwa visu au panga'' Kwa miaka miwili iliyopita eneo linalozingira mji wa Beni limekuwa likikimbwa na mauaji ya kikatili yaliyowauwa mamia ya raia, wengi wao wakichinjwa na kunyongwa hadi kufa. Msemaji wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha shambulio, akisema wanajeshi ''waliwauwa waasi wa ADF " lakini akaongeza kuwa " idadi ya raia waliokufa ni kubwa". Maafisa wa Kongo wamekuwa wakiwalaumu waasi wa ADF kwa mauaji hayo , lakini ripoti kadhaa za wataalam zimekuwa zikisema kuwa makundi mengine, yakiwemo ya wanajeshi wa serikali yalihusika katika baadhi ya mauaji. Msemaji wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha shambulio, akisema wanajeshi ''waliwauwa waasi wa ADF " lakini akaongeza kuwa " idadi ya raia waliokufa ni kubwa". Teddy Kataliki, mkuu wa shirika maarufu la kiraia katika kanda hiyo, pia alisema kuwa waliouawa ni 22. Lakini kasisi wa kikatoliki katika eneo hilo amesema kuwa waliouawa ni watu 27 na idadi inaweza kuongezeka zaidi " kama miili ya waliouawa itabainika katika msitu" unaopakana na mji huo. Wakati mauaji ya kikatili ya Beni yalipofanyika Oktoba 2014, ADF walijibu haraka wakishutumu makundi mauaji hayo kutekelezwa na maafisa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na MONUSCO---Kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, mamlaka za kongo na Umoja wa Mataifa zimeshindwa kuwalinda raia na ADF limesalia kuwa ndilo kundi linalotawala, huku serikali ikisisitiza kuhusu uhusiano wa mauaji hayo na vita vya kidini vya Jihad. Mauaji haya yanatokea huku mahusiano baina ya jamii ya kimataifa na DRC ukiwa mbaya kutokana na hatua ya rais Josep Kabila kukataa kuachia mamlaka, licha ya muhula wake kumalizika taraehe 20 Disemba. Takriban raia 20 wameuawa katika mauaji ya kikatili katika jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kulinga na taarifa zilizotolewa na maafisa Jumapili. text: Serikali inaamini kwamba mashirika yasiokuwa ya kiserikali NGOs hutumia vituo hivyo vya afya kukuza mapenzi ya jinsia moja Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini humo na wanaopatikana na hatia hupigwa faini ya miaka 30 jela. Serikali inaamini kwamba mashirika yasiokuwa ya kiserikali NGOs hutumia vituo hivyo vya afya kukuza mapenzi ya jinsia moja, Kulingana na chombo cha habari cha AP kilichomnukuu waziri wa afya Ummi Mwalimu. Waziri wa afya pia alitangaza kwamba serikali inaongeza takriban vituo 3000 vya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya ukimwi nchini humo, imeongezea AP. AP imeongezea mwezi Septemba kwamba serikali itasimamisha kwa muda huduma ya mipango ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya ukimwi inayolenga wapenzi wa jinsia moja. Serikali ya Tanzania imesitisha huduma za msaada kwa vituo 40 vya matibabu vinavyodaiwa kuwasaidia wapenzi wa jinsia moja kulingana na chombo cha habari cha AP. text: Uchunguzi wa kesi hiyo itasaidia kueleza jinsi binadamu wa atatumika kumueleza. Kesi hiyo pia itatumika kueleza jinsi binadamu wa kwanza alivyoambukizwa virusi ama mlipuko waugonjwa wa bakteria. Uchunguzi wa hali juu wa mfumo wa jeni sasa unawawezesha wataalamu kugundua chimbuko la virusu kupitia wale walioambukizwa. Kupitia uchunguzi wa pamoja, wanasayansi wanaweza kubaini watu wa kwanza ambao huenda walisambaza ugonjwa na hivyo kusababisha mlipuko. Kuwatambua watu hao kunaweza kusaidia kujibu maswali muhimu kuhusu jinsi, lini na kwanini ilianza. Soko la samaki la Huanan lililohusishwa na visa vya awali vya maambukizi ya coronavirus limefungwa Hii inaweza kuwakinga watu zaidi dhidi ya maambukizi kwa wakati huu na magonjwa mengine ya mlipuko siku zijazo. Lakini je tunamjua mgonjwa wa mlipuko wa Covid-19 coronavirus ulionza China?Kwa kifupi jibu ni - la. Mamlaka ya China awali iliripoti kisa cha kwanza cha cha coronavirus kilikuwa Disemba 31 na visa vingi vilionesha dalili zinazokaribiana na homa ya mapafu - ambavyo moja kwa moja vilihusishwa na vyakula vya baharini na soko ya nyama katika mji wa Wuhan, ulipo mkoa wa Hubei. Eneo hilo ni chimbuko la mlipuko wa corona, huku karibu 82% ya visa zaidi ya 75,000-vikiripotiwa China kufikia sasa na vingine vinavyoripotiwa kote duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. (Soma zaidi jinsi ulimwengu unavyopambana na vita dhidi ya coronavirus.) Hata hivyo uchunguzi uliyofanywa na watafiti wa Kichina na ambao ulichapishwa katika jarida la matibabu la Lancet, unadai kuwa mtu wa kwanza alipatilana na Covid-19, Disemba 1 2019 (mapema zaidi) na kwamba mtu huyo "hakukaribiana" soko la Huanan linalouza vyakula vya baharini kwa bei ya jumla. Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi? Wu Wenjuan, daktari wa cheo cha juu hospitali ya Wuhan ya Jinyintan na mmoja wa wachunguzi katika utafiti huo, ameambia idhaa ya Kichina ya BBC kwamba mtu wa kwanza kupatikana na corona, alikuwa mwanamume mzee akiugua ugonjwa Alzheimer. "Aliishi (mgonjjwa huyo) karibu na soko hilo na kwakua ni mgonjwa hakutoka nje ya nyumba," Wu Wenjuan alisema.Pia aliongeza kuwa watu wengine watatu walipatikana na dalili siku zilizofuata na wawili kati yao hawakufika Huanan. Watafiti pia walibaini kuwa watu 27 kati ya wagonjwa 41 waliolazwa hospitali katika awamu ya kwanza ya mlipuko wa ugonjwa walitangamana na watu katika soko hilo. Hatahivyo, watafiti waligundua kuwa watu 27 kati ya wagonjwa 41 waliokuwa wamelazwa hospitali katika awamu ya kwanza ya mlipuko corona "waliwahi kufika katika soko la samaki la Huanan". Matokeo ya uchunguzi wa awali unaashiria kuwa maambukizi yalianza kusambaa kutoka soko hilo na huenda ilitokana na wanyama kabla ya kumuingia binadamu kabla ya maambukizi kuwa kati ya binadamu, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Je mwanadamu anaweza kusababisha mlipuko wa ugonjwa? Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliokumba Afrika magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016 mlipuko uligunduliwa kwanza 1976. Uliwaua zaidi ya watu 11,000 na wengine zaidi ya 28,000,kupata maambukizi kulingana na WHO. Mlipuko huo uliendelea kwa miaka miwili ana ulisambaa hadi mataifa 10, hususan barani Afrika japo visa vya vingine wiliripotiwa Marekani, Uhispania, Uingereza na Italia. Wanasayansi walafikiana kuwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola ulitokana na mtu mmoja - mtoto wa miaka miwili kutoka Guinea - ambaye huenda alipata maaambukizi kwa kucheza karibu na mti uliokuwa makazi ya popo. Mamlaka nchini China pamoja wa wataalamu wa matibabu wako mbioni kutafuta chimbuko la mlipuko unaoendelea wa coronavirus. Ikiwa ni pamoja na utambuzi wa binadamu wa kwanza aliyepata ugonjwa wa corona. text: Hatua yao inakuja wakati ambapo Wizara ya Afya nchini humo inajiandaa kufanya kampeini ya chanjo hiyo katika kipindi cha wiki mbili zijazo. Madaktari hao wanasema hatua ya kupinga chanjo hiyo inazingatia ''utafiti'' ambao unaashiria kuwa chanjo ya HPV ni hatari kwa binadamu. "Chanjo hiyo sio salama kwa mtu yeyote sio watoto pekee. Walioitengeneza hawasemi madhara yake wakati yapo wazi kabisa na ibainike wazi kuwa sio usemi wangu ," Mwenyekiti wa KCDA, Dkt Stephen Karanja, ameiambia BBC. "Hawa watoto sharti walindwe na kila mtu ikiwa ni pamoja na serikali kuhakikisha wanadumisha maadili mema katika jamii." aliongeza Dkt Stephen Karanja, Mwenyekiti wa KCDA, Wataalamu wa ngazi ya juu wanasema madai hayo ''Hayana msingi wowote'' Daktari bingwa wa wanawake katika Hospitali Kuu ya Kenyatta Dkt Alfred Mokomba katika tafiti zake zilizopita amesema chanjo hiyo ni salama na inaweza kutumiwa kwa watoto. Wizara ya Afya itawapatia bila malipo dozi mbili ya chango ya HPV wasichana wa miaka 10 katika hospitali za umma 9,000, za kibinafsi na zile za kidini kote nchini. Shirika la Afya Duniani linapendekeza wasichana wapewe chanjo hiyo na wanawake kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu mara moja kwa mwaka ili kuwapunguzia hatari ya kupata maradhi ya saratani. Siku ya Jumanne maafisa wakuu wa wizara ya Afya nchini Kenya walikutana na washirika wao kujadiliana kuhusu hali ya saratani nchini na kujiandaa kwa mpango wa chanjo ya kitaifa dhidi ya ugonjwa huyo. "Kupata chanjo ya HPV ni njia bora zaidi ya kujikinga na saratani ya shingo ya uzazi na ni salama. Mimi pia ni baba wa watoto wa wasichana na wote wamepata chanjo. Kwa kuwapa chanjo watoto wetu wasichana tunawakinga na ugonjwa huo maisha. Watakuwa vizuri, nakufikia malengo yao maishani," alisema mwakilishi wa WHO nchini Kenya Dr Rudi Eggers. Wizara ya Afya inalenga kupunguza visa vya saratani ya shingo ya uzazi - ambaye ni ya pili baada ya saratani ya matiti nchini Kenya, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la kimataifa la utafiti wa saratani. Ugonjwa huo unaua karibu wanawake saba nchini Kenya kila siku na karibu 3,000 kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu kutoka wizara ya Afya. Kuna karibu visa vipya 40,000 vya saratani ya shingo ya uzazi vinavyoropotiwa duniani kila mwaka. Duniani ni ugonjwa wa nne unaowaathiri zaidi wanawake "Inasikitisha kuwa tunapoteza wanawake saba kila siku kutokana na ugonjwa ambao unaweza kupingwa kupitia chanjo. IUkijikinga dhidi ya maambukizi ya HPV unaweza kujiepusha na saratani ya shingo ya uzazi," alisema mkuu wa chanjo katika wizara ya Afya, Dkt Collins Tabu, katika mkutano wa washika dau wa afya nchini Kenya uliofanyika siku ya Jumanne. Gharama ya matibabu Alisema chanjo hiyo ambayo pia ni mbinu ya kinga ni ya gharama nafuu ikilinganishwa na matibabu ya saratani. "Tunachokifahamu kufikia sasa ni kuwa chanjo hiyo inatoa kinga ya hadi 90% dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi. Tafiti mbili zilizofanywa na KNH zinaonesha kuwa chanjo ya HPV ni bora zaidi katika kukabiliana na aina ya 16 na 18 ya virusi vya HPV- ambavyo vinasadikiwa kusababisha saratani ya shingo ya uzazi," Dkt Mokomba aliliambia Gazeti la Nation. Kwa mujibu wa madaktari wa Kanisa Katoliki, wanasema virusi hivyo kama magonjwa ya zinaa, huwaathiri watu "walio na mienendo ya kufanya ngono kiholela". Wagonjwa na wahudumu wa ugonjwa wa saratani waliandamana jijini Nairobi kuishinikiza serikali kuondoa gharama kubwa ya matibabu ya saratani Sasa wanatoa wito kwa serikali kuhakikisha wazazi wanahamasishwa ili wawezi "kuwalinda watoto wao wasiathiriwe na maovu yanayoendelea katika jamii. Hivi karibuni wagonjwa na wahudumu wa ugonjwa wa saratani waliandamana jijini Nairobi kuishinikiza serikali kuondoa gharama kubwa za matibabu kwa ugonjwa huo. Wagonjwa na wauguzi walioandamana pia walimtaka rais Uhuru Kenyatta atangaze saratani kuwa ni janga la kitaifa. Walisema iwapo hatua hiyo itaidhinishwa basi rasilmali nyingi zitaelekezwa katika kutoa matibabu ya nafuu na yanayowafikia wote nchini pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu na kuweka vifaa hospitalini katika kukabiliana na ugonjwa huo. Hofu dhidi ya chanjo Chanjo zimesaidia kuokoa maisha mamilioni ya watu duniani kote katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, zimekuwa ni hakikisho kwa makuzi salama ya watoto na afya bora kwa watu wazima. Hata hivyo, wataalamu wamebaini hali ya ongezeko la kukataa kutumia chanjo katika baadhi ya maeneo duniani. Shirirka la Afya Dunia (WHO) lipo katika tahadhari kubwa ya hali hiyo kiasi cha kuorodhesha ongezeko hilo kama moja ya mambo 10 yanayohatarisha afya ya ulimwengu kwa mwaka 2019. Hofu dhidi ya chanjo, kwa mfano nchini Marekani ilisababisha mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa ukambi ay surua mika 25 iliopita. Maambukizi ya saratani ya shingo ya uzazi yamedhibitiwa kwa kiwango kikubwa nchini Australia Wakati Kenya inawalenga watoto wasichana kupata chanjo dhidi ya HPV, nchi kama Australia pia inawalenga wavulana katika juhudi ya kutokomeza kabisa virusi hivyo vinavyosababisha saratani. Kwa sababau virusi vya HPV husambazwa kupitia ngono, kuwapa chanjo wavulana kutapunguza kuenea kwa virusi hivyo vinavyohusishwa na na 5% ya maradhi ya saratani. Tafita kadhaa nchini Australia zinzonesha kuwa chanjo ya HPV inatoa ulinzi imara dhidi ya saratani. Uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi nchini Australia inalenga kutokomeza ugonjwa huo kufikia mwaka 2035. Gharama na upatikanaji wa chanjo hiyo hata hivyo bado ni changamoto kubwa nchini Keny. Sio watu wengi wanaoweza kumudu gharama ya kufanyiwa uchunguzi wa mapema wa virusi vya HPV vinavyosababisha saratani ya shingo ya uzazi. Gharama ya utibu saratani ya aina hiyo ni kati ya dolla 1,720 hadi $7,590 ikiwa mgonjwa hatafanyiwa upasuaji nchini Kenya. Na endapo matibabu yatahusisha upasuaji basi gharama hiyo itapanda kwa kati ya dolla 6,720 hadi dolla 12,500 kwa mujibu wa shirika la kudhibiti saratani nchini Kenya . Shirika la madaktari wa Kanisa Katoliki nchini Kenya (KCDA), linapinga mpango wa kuwapa chanjo dhidi ya virusi vya HPV viinayosababisha saratani ya shingo ya uzazi kwa watoto wasichana wa miaka 10. text: Utafiti umebaini kuwa watoto wadogo wana uwezo wa kuhesabu hata kabla ya kufundishwa Watafiti hao kutoka Marekani wanasema kuwa watoto wanaweza kusikia hesabu zinazotamkwa kwa sauti kubwa na kutambua idadi yake. Ikiwa watoto wengi huwa hawaelewi namba hizo huwa zina maana gani mpaka wanapofikia umri wa miaka minne. Wanasayansi sasa wanataka kuona kama uwezo wa watoto kuhesabu wakiwa wadogo huwapelekea na utaalamu wa kuhesabu siku za mbeleni. Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha John Hopkins, watoto kumi na sita ambao walikuwa wanawaangalia wanasesere wanne-huku mbwa mdogo na gari-walikuwa wamefichwa kwenye sanduku. Muda ambao watafiti wlihesabu kwa sauti, wanapodondosha mwanasesere mmoja na husema, angalia - moja, mbili, tatu, nne. Mbwa wanne." Wakati mwingine, watafiti huwa wanasema : Hii, hii ,hii- au hawa mbwa." Wakati wanasesere wamehesabiwa , watoto huwa wanatarajia kuwa ni zaidi ya mwanasesere mmoja ndio anaweza kutolewa kwenye sanduku. "Watoto hawa hawakuweza kuhesabu namba sahihi lakini walikuwa wanakumbuka namba sahihi ambazo wamehesabu", watafiti walisema. Lakini wakati wanasesere hao wakiwa hawahesabiwi, watoto wanahisi kuvurugwa pale watafiti wanapodondosha mdoli mmoja , na kuangalia kama hawaoni kitu kingine chochote. Mtafiti Jenny Wang anasema kuwa wakati wanapowahesabu wanasesere kabla hawajawaficha, huwa wanaonekana kukumbuka wanasesere wangapi walikuepo kabla." Mtafiti anasema kuwa alishangazwa sana kuona namna watoto wachanga wanavyoweza kuhesabu huku watu wengine, kuhesabu huwa sio jambo rahisi". Watafiti wanaamini kuwa watoto wadogo wanaweza kuanza kufundishwa kuhesabu wakiwa wadogo zaidi hata kabla ya umri wa kuanza shule za awali. Timu ya watafiti wanataka kujua kama watoto hao wanao-ongea kiingereza wanaweza kuhesabu kwa lugha za kigeni. Utafiti huu umechapishwa katika jarida la maendeleo ya sayansi. Watoto wadogo wenye umri kuanzia miezi 14 wana uwezo wa kuhesabu hata kabla hawajaanza kuelewa umuhimu wa kujifunza kuhesabu moja, mbili, tatu ; wanasayansi wanasema. text: Madaktari waliofanya mgomo Kenya .Licha ya kuwa mgomo huo umekwisha serikali ya Kenya imeomba usaidizi kutoka Tanzania Madaktari hao walifaa kutumwa Kenya kwa mujibu wa mazungumzo kati ya ujumbe wa Serikali ya Kenya uliiongozwa na Waziri wa Afya Dkt Cleopa Mailu na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli mwezi Machi. Kenya ilikuwa imeomba madkati 500 na Rais Magufuli akakubali ombi hilo. Lakini raia watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi Mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania. Mahakama ilitoa agizo la kuzuia kuajiriwa kwa madaktari hao hadi kesi iliyowasilishwa imalize kusikizwa na hadi sasa agizo hilo bado hilo. "Kwa kuwa hadi tarehe ya taarifa hii Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za Madaktari wa Tanzania nchini Kenya, Rais Magufuli ameamua kuwa, Madaktari hao 258 ambao waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara moja," taarifa kutoka kwa waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu imesema. Wizara hiyo imesema kufikia 27 Machi, jumla ya maombi takribani 496 yaliwasilishwa na kati ya hao waliokuwa wamekidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya walikuwa 258. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Afya kutoka Kenya Dkt Cleopa Mailu mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Madaktari hao walifaa wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili, 2017 muda ambao tayari umepita. " Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari 500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka Madaktari wetu nchini Kenya," amesema Bi Mwalimu. Serikali ya Tanzania imeamua kuwaajiri madaktari waliokuwa wamepangiwa kutumwa Kenya kusaidia kupunguza uhaba wa madaktari nchini humo. text: Conte alionekana kujaribu kutuliza wachezaji wakati wa mfarakano uwanjani tarehe 3 Desemba Chelsea na Manchester City wameshtakiwa kwa kukosa kuwadhibiti wachezaji wao wakati wa mechi kati ya klabu hizo mbili tarehe 3 Desemba. Baada ya visa kadha awali, bodi ya rufaa ya Chama cha Soka England ilikuwa imeonya Chelsea mnamo Julai kwamba karibu utafika wakati ambapo "adhabu pekee itakayotosha ni kupokonywa alama". Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa hilo kutokea, Conte aliwaambia wanahabari: "Unafanya mzaha? Unatania?" Chelsea wametozwa faini mara tano na FA kwa kukosa kuwadhibiti wachezai tangu Februari 2015. Viongozi hao wa EPL awali walitozwa faini ya juu sana ya £375,000 kutokana na mashtaka matatu kutoka kwa mechi ambayo iliisha sare 2-2 wakicheza dhidi ya Tottenham uwanjani Stamford Bridge Mei. Bodi ya rufaa ilipunguza faini hiyo hadi £290,000 lakini ikashutumu Chelsea kwa kuwa na rekodi mbaya ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji. Mara ya mwisho klabu kupokonywa alama kwa sababu ya utovu wa nidhamu ilikuwa Manchester United na Arsenal waliopokonywa alama kutokana na vurugu zilizotokea Old Trafford Oktoba 1990. Kulitolewa kadi 12 za manjano wakati wa mechi kati ya Chelsea na Spurs mwezi Mei Wakati wa kuadhibu Chelsea kuhusu matukio ya Stamford mwezi Mei, tume ya FA ilisema ilitafakari uwezekano wa kupokonya alama Chelsea lakini wazo hilo likaondolewa kutokana na sababu kwamba Chelsea hawakuwa wamepewa onyo la mwisho. Chelsea na Spurs walionywa kuhusu mienendo yao siku za usoni lakini FA haikugusia kamwe "onyo la mwisho". Meneja wa Chelsea Antonio Conte amepuuzilia mbali pendekezo kwamba huenda viongozi hao wa Ligi Kuu ya Uingereza wakapokonywa alama kutokana na utovu wa nidhamu. text: Morsi alikuwa rais wa Misri baada ya Hosni Mubarak kung'olewa madarakani Hatua hiyo ya kijeshi ilifuatia maandamano ya siku kadhaa ya kupinga utawala wake na pamoja na hatua ya Morsi kukupuuza amri ya mwisho ya jeshi ya kumtaka asulihishe mzozo mbaya wa kisiasa nchini humo tangu Hosni Mubarak alipong'olewa madarakani mwaka 2011. Baada ya kuzuiliwa kwa karibu miezi miwili katika sehemu isiyojulikana waendesha mashtaka wa serikali walitangaza mwezi Septemba mwaka 2013 kwamba Morsi atashtakiwa kwa kuwachochea wafuasi wake kumua mwanahabari na wafuasi wawili wa upinzani na kuamurisha wengine kuteswa na kuzuiliwa kinyume cha sheria. Mashataka dhidi yake yalihusiana na makabiliano kati ya waandamanaji wa upinzani na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood nje ya makazi ya rais ya Ittihadiya mjini Cairo mwezi Desemba mwaka 2012. Morsi alishitakiwa pamoja na viongozi wa 14 wa ngazi ya juu wa Muslim Brotherhood Novemba mwaka wa 2013. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake kwa mara ya kwanza, alipiga mayowe kutoka kizimbani akisema kuwa yeye ni mhanga wa "mapinduzi ya kijeshi" na kukataa mamlaka ya mahakama kumfungulia mashtaka. "Mimi ni rais wa Jamhuri kwa mujibu wa katiba ya nchi na nimezuiliwa kwa nguvu ," alisisitiza. Lakini mwezi Aprili mwaka 2015, Morsi na washirika wake walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kuondolewa mashtaka ya uchochezi na kupatikana na makosa ya kuamrisha kuzuiliwa na kuteswa kwa waandamanaji. Morsi pia alifunguliwa mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni kuwaachklia huru wafungwa wakati wa maandamano ya mwaka 2011, kufichua siri za serikali, ubadhirifu pamoja na kutusi mahakama. Mbunge wa kundi la Kiislam Mohammed Morsi alizaliwa katika kijiji cha El-Adwah kilichopo mkoa wa Nile Delta eneo la Sharqiya mwaka 1951. Alisomea uhandisi katika Chuo Kikuu cha Cairo katika miaka ya 1970 kabla ya kwenda Marekani kusomea PhD. Aliporejea Misri alikteuliwa mkuu wa kitengo cha uhandisi katika Chuo Kikuu cha Zagazig. Morsi alishinda uchaguzi kwa tofauti ndogo sana Alishikilia nyadhifa kadhaa katika kundi la Muslim Brotherhood, na hatimae kujiunga na kitengo chake cha kisiasa ambapo aliwania kiti cha ubunge kama mgombea binafsi katika bunge la vuguvugu hilo kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2005 Alipoteza kiti chake cha ubunge nyumbani, kufuatia duru ya pili ya uchaguzi aliyodai ulikubwa na udanganyifu. Akiwa mbunge alisifiwa sana kwa uweledi wake wa luga na kazi , kwa mfano baada ya mkasa wa reli mwa 2002 alipinga madai ya utepetevu kwa upande wa maafisa wa reli hiyo. Morsi aliteuliwa kama mgombea wa uraisi wa kundi la mwezi April 2012 naibu kiongozi wake mfanyibiashara Khairat al-Shater, alipolazimishwa kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho. Japo Morsi hakuonekana kuwa na hulka ya msemaji bora alikuwa mwenyekiti wa chama cha Freedom and Justice Party (FJP). Katika kampeini yake ya uchaguzi, Morsi alijinadi kama mtu atakaeleta mwamko mpya akilinganishwa na viongozi wa zamani kama Hosni Mubarak. Aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo Abdul Fattah al-Sisi aliamuru kuondolewa kwa Morsi madarakani Maandamano mapya Alipoingia madarakani mwezi Juni 2012 baada ya kushinda uchaguzi kibahati, Morsi aliahidi kuunda "serikali ya Wamisri wote". Lakini wakosoaji wake walilalamika kuwa alishindwa kutekeleza wajibu wake wakati wa uongozi wake wa mwaka mmoja uliokumbwa na msukosuko. Walimlaumu kwa kuruhusu makundi yenye misimamo mikali ya Kiislam kuingia katika ulingo wa kisiasa hali iliyoipatia nguvu kubwa kundi la Muslim Brotherhood. Pia walisema, alivuruga uchumi hali iliyomfanya ashindwe kushughulikia masuala yaliyosababisha maandamano yaliyomleta uongozini: na miito ya kupigania haki na usawa katika jamii. Upinzani dhidi ya uongozi wa ulianzamwezi Novemba 2012 wakati, azma yake ya kuhakikisaha makundi ya kiislam yanabata wingi wa viti bungeni ili waweze kukamilisha shughuli ya kuandika katiba mpya ili aweze kujipatia mamlaka zaidi Licha ya maandamano dhidi yake kushika kasi, Morsi alitoa amri ya rais ya kuruhusu vikosi vya usalama kulinda taasisi za kitaifa na maeneo ya kupigia kura hadi kura ya maoni kuhusu katiba mpya ifanyike Disemba 15 mwaka 2012. Wakosoaji walisema amri hiyo ilikuwa sawa na sheria ya kijeshi ndiposa makabiliano yalizuka kati ya wafuasi wake na upinzani ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa. Maandamano makubwa yalifanywa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa utawala wa Morsi, ambapo mamilioni ya watu walijitokeza katika barabara kuu zote nchini Misri. Morsi alihukumiwa kunyongwa, lakini hukumu hiyo baadae ilibatilishwa. 'Mapinduzi' Majeshi yalitoa onyo kwa Morsi kwamba yataingilia mzozo unaokumba utawala wake ikiwa atashindwa kufikia masharti ya raia katika kipindi cha saa 48. Ilipofika jioni ya Julai 3, majeshi yalifutilia mbali katiba na kutangaza kubuniwa kwa serikali ya mpito kabla ya kufanyika upya kwa uchanguzi wa urais. Morsi alipinga hatua hiyo na kuongeza kuwa ni sawa na "mapinduzi". Alikamatwa kufuatia amri iliyotolewa na mkuu wa majeshi - ambaye ni rais wa sasa- Abdul Fattah al-Sisi - na kupelekwa sehemu isiyojulikana na kwa wiki kadhaa bila ya mtu yeyote kujua hali yake. Wafuasi wake waliandamana katika barabara za mji wa Cairo, kushinikiza kuachiliwa kwake na kurudishwa madarakani mara moja. Majeshi yalijibu hatua hiyo kwa kutumia nguvu kuvunja mandamano mnamo Agosti 14 na kuwakamata vingozi wa wakuu wa vugu vugu la Muslim Brotherhood. Karibu watu 1,000 waliuawa katika oparesheni hiyo ambayo utawala wa mpito ulidai kuwa juhudi za kukabiliana na"ugaidi". Miaka iliyofuata baada ya Morsi kuondolewa madarakani, Misri ilishuhudia ongezeko la ghasia na mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam na msako mkali dhidi ya vugu vugu Muslim Brotherhood lilitangazwa rasmi kuwa kundi la kigaidi. Morsi alitoweka machoni mwa umma, na kuishia kuonekana kotini alipofunguliwa mashtaka. Baadae mtangulizi wake Hosni Mubarak aliachililiwa huru kutoka jela - katika hatua ambayo ilionekana na wengi kuwa Misri haikua imeendelea mbele kisiasa licha ya uchaguzi uliomweka Morsi madarakani kwa muda. Mohammed Morsi alikua rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia lakini alisalia madarakani kwa mwaka mmoja kabla ya kutumuliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi tarehe 3 mwezi Julai mwaka 2013. text: Polisi wakituliza ghasia nje ya Bunge la Afrika kusini Wakati akianza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa. Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa, ulifanywa pia na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala. Awali nje ya bunge la nchi hiyo, Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu, ili kuweza kuwasambaratisha. Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa hutuba yake. Bunge la Afrika kusini jana lilijawa na vurugu kuipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma. text: Pogba alifunga goli la kwanza Magoli ya Paul Pogba na Hendrick Mkhitaryan yameipa United sio tu Kombe bali pia nafasi ya kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. Mapema kabla ya mchezo huo kuanza, timu hizo mbili zilitoa heshima zao kwa watu waliopoteza maisha katika shambulio mjini Manchester. Pia wachezaji wa Manchester United walivaa vitambaa vyeusi mikononi kama ishara ya heshima kwa waathirika. Paul Pogba akishangilia bao la kwanza Wakicheza bila ya mfungaji bora wao Zlatan Ibrahimovic, pamoja na mabeki Marcos Rojo, na Luke Shaw, pamoja na Erick Bailly anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu, kikosi cha Mourinho kililazimika kujituma kwenye mchezo huu wa 64 msimu huu. Wakitumia uzoefu, pamoja na jinsi walivyojipanga, waliweza kukisumbua kikosi cha Ajax ambacho kilikuwa na wachezaji chipukizi, wakiwa na wastani wa umri wa miaka 22. Hendrick Mkhitaryan akishangilia goli la pili na Pogba Manchester United sasa wanaungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City katika kucheza Klabu Bingwa Ulaya. Pia ushindi huu utawaingizia kitita cha takriban pauni milioni 50. Hili ni kombe la Pili Mourinho anashinda na United katika msimu wake wa kwanza. United walishinda Kombe la Ligi mwezi Februari. Manchester United wameshinda fainali ya Kombe la Europa kwa kuifunga Ajax Amsterdam kwa mabao 2-0 mjini Stockholm Sweden. text: Wongonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu Huku idadi ya wagonjwa waliopo na waliofariki ikiongezeka, madaktari wamegundua kwamba Covid-19, ugonjwa unaosababisha virusi vya corona ni ugonjwa usiofahamika kwa rahisi zaidi ya ilivyodhaniwa. Ugonjwa huo unaweza kuathiri viungo kama vile ini, figo, utumbo, moyo na ubongo. Tatizo kubwa lakini ni jinsi damu inavyoganda katika mishipa ya wagonjwa wanaopewa dawa za kufanya migando hiyo ya damu kuyeyuka. Migando hiyo ya damu inaweza kufika katika viungo kama vile mapafu, moyo, ubongo na kusababisha mshtuko wa moyo unaoweza kusababisha kifo. Siku chache zilizopita, madaktari katika hopsitali ya Mount Sinai mjini New York walichapisha utafiti unaosema kwamba mgando wa damu hususana katika mapafu unawaathiri vibaya wagonjwa wa Covid-19 walio mahututi. Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona? Wataalamu hao pia walifichua kwamba migando hiyo ya damu inaweza kusababisha ugonjwa wa kiharusi miongoni mwa wagonjwa vijana walioambukizwa virusi vya corona. Madaktari katika mataifa tofauti wameripoti tatizo sawa na hilo. Uchanganuzi wa wagonjwa 183 wa Covid-19 uliofanywa na wanasayansi wa China umebaini kwamba asilimia 71 ya wale waliofariki walikuwa na mgando wa damu. Nchini Uholanzi utafiti uliofanyiwa wagonjwa 184 waliokuwa wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi thuluthi moja ya wagonjwa hao walikuwa na mgando katika damu. Coronavirus inaweza kuathiri sio tu mfumo wa kupumua lakini pia viungo vingine kama vile ini, figo, matumbo, moyo na ubongo Nchini Marekani madaktari wengi wamesema kwamba migando hiyo ndio sababu kuu ya vifo miongoni mwa wagonjwa wa Covid 19. Ijapokuwa migando ya damu sio tatizo lisilo kuwa la kawaida kwa wagonjwa walio katika hali mahututi, maafisa hao wa afya wameshangazwa na idadi ya wagonjwa wa Covid 19 walio na tatizo hilo. Je tatizo hilo husababishwa na nini? Bado hakuna uamuzi wa pamoja kuhusu sababu za migando hiyo ya damu katika mishipa . Kufikia sasa kuna uvumi chungu nzima , alisema Coopersmith mtaalam wa chumba cha wagonjwa mahututi na profesa wa chuo kikuu cha tiba cha Emory University School mjini Atlanta, USA, akizungumza na BBC Brazil.) Anasema kwamba kuna sababu nyingi ambazo lazima ziweko kwa damu kuganda na mwili hushindwa kuamua kati ya kuvuja damu na kuganda kwa damu hiyo. Haijulikani iwapo migando hiyo husababishwa na virusi vya corona ama kinga katika hali yake ya kukabiliana na Covid-19. Wagonjwa wengi huwa wamelazwa hivyobasi inaongeza hatari ya damu kuganda. Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona: Haijulikani iwapo migando hiyo ya damu ni madhara ya kandokado ya mgonjwa ama iwapo migando hiyo inasababisha kufeli kwa viungo mwilini. Kukatwa mguu, mshtuko wa moyo na kiarusi Migando ya damu pia imeonekana miongoni mwa miili ya wagonjwa wengine. Dkt.Gregory Piazza, mtaalamu wa magonjwa ya moyo mjini Birmingham na hospitali ya wanawake mjini Bostona pamoja na kuwa profesa katika chuo kikuu cha tiba cha Havard, anaammbia BC Brazil kwamba pia yeye alianza kugundua migando ya damu miongoni mwa wagonjwa waliokuwa katika cumba mahututi walio na virusi vya corona ambao walikuwa katika hali mbaya. "Katika visa vingine tunagundua migando mikubwa katika mishipa ya damu iliopo karibu na moyo, alisema Piazza''. "Inaweza kuwa katika mishipa ya kupeleka damu katika moyo na hivyobasi kusababisha mshtuko wa moyo au katika mkishipa inayopeleka damu katika ubongo na hivyobasi kusababisha kiarusi ama mara nyengine katika mishipa inayopeleka damu katika miguu na mikono na hivyo usababisha hatari ya mtu kukatwa mguu ama mkono''anasema. Kisa kimoja kilichovutia watu nchini Marekani ni kile cha muigizaji Nick Cordero , 41 ambaye alilazwa hopsitalini mjini New York , aliambia BBC Brazil. Damu kuganda kunaweza kusababisha matatizo kadha wa kadha kwa mgonjwa ikiwemo kifo Wiki iliopita madaktari waliopo katika hospitali hiyo walitoa maelezo kuhusu wagonjwa watano wa virusi vya corona waliougua kiarusi. Walikuwa kati ya umri wa miaka 33 hadi 49, na walikuwa na dalili chache ama hata bila ishara zozote za Covid-19. Baadhi yao hawakujua kwamba wameambukizwa ama hata kubaini walikuwa na kiarusi, na hawakuulizia usaidizi kwa hofu ya kusababisha maambukizi hospitalini. Kulingana na madaktari mgando wa damu katika miguu huonekana mara kwa mara miononi mwa wagonjwa wa Covid-19. Baadhi ya hospitai zimekuwa zikitumia tiba ya kuyeyusha mgando wa damu katika mishipa kwa wagonjwa wote wanaougua Civid-19. Lakini wataalama wanaonya kwamba tiba hiyo inahitaji makini kwa kuwa inaweza kuongeza hatari ya kuvuja damu na kusisitiza kwamba utafiti zaidi unahitajika. Wangonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu hiyo na kufanya tatizo hilo lisilo la kawaida kuwa la kipekee. text: Mchezaji huyo wa Manchester United na Kiungo wa kati wa Manchester City Phil Foden, waliamriwa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Gareth Southgate siku ya Jumatatu. Greenwood alisema: "Ninaweza tu kuomba msamaha kwa aibu niliyoisababisha." Aliongeza: ''Hususani , ninataka kumuomba radhi Gareth Southgate , kwa kumuangusha, wakati alionesha kuniamini kwa kiasi kikubwa. ''Kuichezea England ilikuwa moja kati ya nyakati za kujivunia sana katika maisha yangu na ni mimi pekee ninayepaswa kulaumiwa kwa kosa hili kubwa. ''Ninaiahidi familia yangu, mashabiki, Manchester United na England kuwa hili ni somo nitajifunza.'' Kwa mujibu wa ripoti za Iceland na vyombo vingine, Foden na Greenwood walidaiwa kukutana na wanawake wawili katika sehemu tofauti za hoteli mbali na mahali kikosi cha England kilipokuwa kinakaa. Southgate amewaelezea wachezaji hao kuwa 'wajinga' akiongeza kuwa : ''ni suala kubwa sana na tumelishughulikia namna hiyo na tumechukua hatua haraka sana kadiri tulivyoweza''. ''Tumelishughulikia ipasavyo. Ninatambua umri wao lakini dunia nzima inashughulika na janga hili.'' Mshambuliaji wa kikosi cha England Mason Greenwood amesema '' yeye mwenyewe ndiye wa kulaumiwa'' baada ya kuondoshwa kwa kosa la kukiuka muongozo wa karantini kutokana na virusi vya corona huko Iceland. text: Kwa nini marafiki zangu wa kike hutumiana picha za utupu Picha ya selfi kutoka kwa rafikiye mkuu akiwa utupu inajitokeza. Gita anacheka na kutuma emoji tano za ishara ya moto na ujumbe "On fire girl." akimsifu. Hakuna uhusiano wowote wa kingono kati ya Gita na rafikiye mkubwa. Lakini mara kadhaa kwa wiki wanatumiana picha za utupu. ''Nilianza wakati nilipokuwa bila mpenzi'', anasema Gita mwenye umri wa miaka 26. Nilikuwa nikihisi nimewachwa nje ya watu wanaotumiana ujumbe wa picha za utupu kwa sababu sikuwa na mtu wa kumtumia picha za utupu. Ni njia ya kuwaonyesha marafiki zangu nilivyo na mwili mzuri. Na hivi karibuni nimeanza kuweka mzaha. Ninaweza kutuma picha moja ya selfi ikiwa na titi langu likiwa wazi. Inatufanya tunacheka. Yeye na marafikize sio wao pekee wanaotumiana picha za utupu . Kile ambacho kilikuwa njia ya kuwachochea wapenzi kushiriki katika tendo la ngono sasa kinatumiwa kama ishara ya umoja na kuwezeshana miongoni mwa wanawake. Selfi za utupu ni njia mojawapo ya kupigania imani ya kibinafsi , alielezea mmoja wa marafiki zangu Daisy Walker mwenye umri wa miaka 27 ambaye alikuwa mpiga picha wa fesheni wa zamani . Daisy Walker Imenichukua muda mrefu kukiuka mipaka ya urembo wa mwanamke na kuukubali mwili wangu. Sasa, nina fursa ya kutojali iwapo watu wananitazama kuwa mrembo ama la.Hujiangalia mwili wangu nikiwa uchi na kufikiri, 'Kweli''. Mimi ndiye hupokea picha zake za utupu , ambazo huzituma baada ya kuoga ama wakati anapopiga mswaki na huwa siogopi kuzitazama. Sababu za Daisy kufanya hivyo zinafurahisha. ''Nadhani kwa mwanamke kukuwa katika jamii na kuchukua hatua ya kuukubali mwili wake ni mafanikio na nataka kuwasambazia hilo rafiki zangu'', alisema. Natumai itasambaa kama moto wa msituni. Alianzisha kundi la WhatsApp hususan kwa marafikize kusambaziana picha za utupu. Daisy alianzisha kundi la WhatsApp hususan kwa marafikize kusambaziana picha za utupu. Mmoja wa wanachama anasema kuwa nina picha nyingi za marafiki wangu katika simu. Ni hatua yenye lengo la kusambaziana picha za urembo wetu kati yetu Hatahivyo kutumiana picha za utupu ni hatari, unaweza kuwa rafiki na mtu unayemtumia picha lakini punde urafiki huo unapokatika picha hizo zinaweza kuwafikia watu wengine kwa lengo la kulipiza kisasi. Simu ya Gita's inalia. Anaichukua na mara kwa ghafla picha inajitokeza katika skrini . text: Donald Trump amekuwa akishutumiwa kwa kauli zake Akihutubu katika mkutano wa hadhara Florida, Bw Trump amesema kampeni yake "inafanya vyema sana". Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump kurejea matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi aliyeuawa nchini Iraq. "Ningetaka kuwafahamisha tu kwamba kampeni inaendelea vyema sana," amewaambia watu waliohudhuria mkutano wake eneo la Daytona Beach. Awali, msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul Manaford alikuwa pia amekana taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya kile kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea huyo wa chama cha Republican, zenye kukwaza. ''Kampeni ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga mbele,'' aliiambia kituo cha runinga cha Fox News. Baadhi ya Maafisa wa Kampeni za Trump wamesema ''wanahisi kuwa wanapoteza muda wao''. Hata hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa Trump wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton kwa ripoti hizo Bw Manafort amesema watu wengi bado wana imani na Bw Trump ''Hii ni kauli nyingine ya Clinton ambayo imebebwa na vyombo vya habari, amesema ''Bwana Trump amejitokeza wiki hii kwenye mikusanyiko mikubwa sana ya watu walifurika mpaka mtaani''. Siku ya Jumatano Bw Trump mwenyewe pia aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa ''kuna umoja kwenye Kampeni yangu, pengine mkubwa zaidi kuliko siku zote''. Vita vyake vya maneno na Khizr na Ghazala Khan, wazazi wa Kapteni Humayun Khan aliyeuawa nchini Iraq, vimesababisha watu kutofautiana ndani ya Chama cha Republican. Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hakuna mgawanyiko kwenye kambi yake ya kampeni, licha ya taarifa kudokeza kwamba kuna mzozo mkubwa katika chama hicho. text: Wafanyakazi watano na raia 13 walikuwa miongoni mwa waliofariki , kulingana na vyombo vya waokoji . Ndege hiyo ilikuwa ikifanya mazoezi wakati ilipoanguka na kusababisha moto mkubwa katika nyumba kadhaa. Shahidi mmoja alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa imeshika moto kabla ya kuanguka. Ndege hiyo ya King Air 350 Turboprop ilidaiwa kupiga kona kabla ya kuwasili ilikokuwa ikielekea na baadaye kuanguka. Mji wa Rawalpindi ndio unaomiliki makao makuu ya jeshi Rawalpindi, karibu na mji mkuju wa Islamabad ndio eneo la makao makuu ya jeshi la Pakistan na ndege hiyo inamilikiwa na kitengo cha mafunzo ya angani cha jeshi la Pakistan. Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan alituma risala zake za rambirambi na kuwaombea kupona kwa haraka waliopata majeraha kulingana na ujumbe wa twitter uliotumwa na serikali ya Pakistan. Je ndege hiyo ilianguka vipi? Mashahidi katika eneo la mkasa wamesema kwamba ndege hiyo ilianguka katika nyumba ya familia moja katika makaazi. ''Nilikuwa macho wakati ndege ilipopita mbele ya chumba changu na tayari ilikuwa imeshika moto ikiwa hewani'', alisema mkazi Ghulam Khan''. ''Sauti yake ilikuwa inaogopesha na ilikuwa ndege ndogo. Ilianguka juu ya nyumba ambapo familia moja ilikuwa ikiishi''. Shahidi mwengine , Yasir Baloch, alisema: Mkia wa ndege hiyo ulikuwa umewaka moto na ilichukua chini ya sekunde tatu kabla ya kuanguka kando ya nyumba yangu na kuchomeka. Waombolezaji waloifika katika eneo la tukio Takriban watu 18 wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya ndege ndogo ya kijeshi kuanguka katika makaazi karibu na mji wa rawalpindi nchini pakistan. text: Benny Gantz, mkuu za zamani wa majeshi anakabiliana na Waziri Mku Benjamin Netanyahu kama hasimu mkuu Katika uchaguzi uliopita kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu alikuwa bega kwa bega na Bwana Gantz, na wawili hao sasa wanawania kuunda serikali ya mseto. Miongoni mwa vyama vilivyo katika orodha ya vile vitakavyounda serikali ya mseto ni pamoja na Muungano wa vyama vya waarabu ambavyo vilipata nafasi ya tatu vinavyosema vinataka kumuondoa mamlakani. Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1992 kwa kikundi cha wanasiasa wa kiarabu nchini Israeli kumuidhinisha waziri mkuu Huu ulikuwa ni uchaguzi mkuu wa pili wa mwaka wa Israeli . Baada ya uchaguzi wa kwanza , mwezi April , mazungumzo ya muungano yalivunjika kna uchaguzi ukaitishwa. Muungano wa vyama mseto ukiwasilisha mapendekezo yao kwa Reuven Rivlin Akikabiliwa na mkwamo mwingine wa kisiasa , rais Israel Reuven Rivlin amependekeza kuwepo kwa serikali mpya itakayojumuisha miungano yote ule wa Blue wa Gantz na ule wa White pamoja na chama cha wazri mkuu Bwana Netanyahu cha Likud. Bwana Rivlin amekwishasema kuwa atafanya kila liwezekanalo kuepuka uchaguzi mkuu wa tatu nchini Israeli mwaka huu . Aymen Odeh, kiongozi wa mungano , amemuambia Rivlin kwamba kipaumbele cha muungano wao ni kumzuwia Bwana Netanyahu kuongoza kwa muhula mwingine. Muungano huo wa vyama vya kiarabu una viti 13 bungeni . Bwana Gantz aliidhinishwa na wabunge wote 13 , lakini bado atahitaji viti 61 vinavyohitajika kupata wingi wa viti katika bunge la Israeli lenye viti 120. Huu ni mchakato muhimu wa mamlaka ya kisiasa kwa raia wa Palestina ndani ya Israel Rais Rivlin anashauriana na viongozi wa chama kuhusu ni nani ambaye atamuomba kuongoza nchi baada ya matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao hayakutoa matokeo kamili . Vyaka vya kiarabu vimeonyesha nguvu kwa kuwa namba tatu kwa idadi ya viti vya bunge. Benjamin Netanyahu na Benny Gantz Uungaji mkono wao hautampa wingi wa viti Benny Gantz na muungano wa Blue & White , lakini utamuinua katika mazungumzo kuhusu ni nani atapata nafasi ya kwanza ya kuunda serikali. Kiongozi anayehusika na uundaji wa makundi ya waarabu nchini Israeli , Ayman Odeh, anasema hawamuidhinishi Bwana Gantz na sera zake, lakini wanafanya juhudi za kujaribu kumzuwia Benjamin Netanyahu kupata muhula mwingine madarakani, na vilevile kutuma ujumbe wa wazi kwamba hali ya baadae ya Israeli lazima ijumuishe ushirikishwaji sawa na kamili wa raia wake wa kipalestina. Akizungumza na wafuasi wakati wa kampeni za uchaguzi , Netanyahu alisema: "Sote tumepitia kampeni ngumu ya uchaguzi. "Bado tunasubiri matokeo yenyewe, lakini jambo moja li wazi. Hali nchini Israel ipo katika kiwango cha historia, tumekabiliwa na changamoto nyingi na fursa nyingi." Kwa upande wake bwana Gantz alionekana kuwa na matumaini zaidi alipozungumza na wafuasi wake mapema kidogo. "Bila shaka tutayasubiri matokeo halisi, lakini inavyoonekana ni kana kwamba tumelifikia lengo letu," amesema. "Umoja na utangamano upo mbele yetu." Wabunge Waarabu nchini Israeli wamependekeza kuwa mkuu wa majeshi wa zamani Israeli Benny Gantz ndiye anayepaswa kuwa waziri mkuu wa Israeli. text: Johnson alisitisha vikao vya bunge kwa wiki tano mapema mwezi huu, lakini mahakama imesema ilikuwa ni makosa kuwasitisha wabunge kuendelea na majukumu yao kuelekea Brexit Oktoba 31. Spika wa bunge la wawakilishi, John Bercow amesema wabunge watarudi kwenye vikao Jumatano baada ya uamuzi huo wa kihistoria. Rais wa mahakama ya juu zaidi Lady Hale amesema "athari za msingi wa demokrasia zilivukwa mpaka." Baadhi ya wabunge sasa wanashinikiza waziri mkuu ajiuzulu - Downing Street imesema "kwa sasa inatafakari uamuzi huo". Johnson alilalamika kwamba anataka bunge lisitishe vikao kabla ya hotuba ya Malkia ili aweze kueleza bayana sera zake mpya za serikali. Lakini wakosoaji wanasema alikuwa anajaribu kusitisha wabunge kuchambua mipango yake ya Brexit na hatua hiyo ya kusitisha vikao ilikuwa ndefu mno kusubiria hotuba ya Malkia. Akisoma uamuzi huo rais wa mahakama hiyo ya juu zaidi, Lady Hale, amesema: "Uamuzi wa kumshauri Malkia kulisitisha bunge ulikwenda kinyume na sheria kwasababu iliweza kuchangia kutatiza au kusitisha uwezo wa bunge kuendelea na majukumu yake kikatiba pasi sababu ya maana." Lady Hale amesema uamuzi huo wa pamoja wa majaji 11 unamaanisha kuwa bunge halijasitishwa- Hatua hiyo iliyoidhinishwa haina athari yoyote. Spika Bercow amesema wabunge wanahitaji kurudi "kufuatia uamuzi huo", na aliagiza "maafisa wa bunge la wawakilishi kutayarisha ... kurudi kuendelea kwa vikao vya bunge" kuanzia 11:30 BST Jumatano. Mahakama pia imeshutumu muda wa kusitishwa vikao hivyo, huku Lady Hale akisema haiwezekani kutamatisha, kutokana na ushahidi uliowasilishwa mbele yetu, kwamba kulikuwa na sababu yoyote, kando na kwamba ni sababu nzuri - kumshauri Malkia kusitisha vikao vya bunge kwa wiki tano". Athari imeshatokea Clive Coleman, Mwandishi wa BBC wa masuala ya sheria Hii ni sheria, katiba na bomu la kisiasa. Pengine ni muhimu kushusha pumzi na kutambua uzito wa waziri mkuu wa Uingereza kukutikana na mahakama ya juu zaidi nchini kwenda kinyume na sheria kwa kufunga taasisi huru katika katiba, bunge, katika wakati ambapo kuna mzozo wa kitaifa. Huenda mahakama imekosa tu kutaja kuwa Boris Johnson alikuwa na dhamira isiyo sahihi ya kutatiza ukaguzi wa bunge lakini athari imeshatokea, amekutikana kuchukuwa hatua kinyume cha sheria na kulisitisha bunge kufanya kazi yake pasi kuwepo sababu ya kisheria. Na mahakama imetupilia mbali ushauri wake kwa Malkia na agizo la baraza uliositisha rasmi bunge. Hiyo ina maana bunge halikuwahi kusitishwa na kwahivyo tunachukulia kuwa wabunge wako huru kuingia bungeni. Huu ni mfano wa aina yake wa majaji walio huru, kupitia mfumo wa ukaguzi wa sheria , kusitisha hatua ya serikali kwasababu ilichofanya ni kinyume na sheria. Hata kama u mkubwa kiasi gani, sheria ndio mambo yote - hata iwapo wewe ni waziri mkuu. Hatua ambayo haikutarajiwa, ya aina yake na inayozusha mtikisiko - ni vigumu kukadiria, umuhimu wa kikatiba na kisiasa unaotokana na uamuzi wa leo. Mahakama ilikuwa inatafakari nini? Gina Miller aliwaongoza wanaharakati dhidi ya mpango wa kusitishwa bunge Uamuzi uliotolewa baada ya kusikizwa kwa siku tatu kesi hiyo katika mahakama ya juu zaidi wiki iliyopita iliangazia rufaa za pande mbili - moja kutoka kwa mwanaharakati na mfanyabiashara Gina Miller, na ya pili kutoka kwa serikali. Bi Miller alikuwa amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu Uingereza kuwa kusitishwa kwa bunge ni 'jambo la kisiasa' na sio suala la mahakama. Serikali ilikuwa imekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Uskotchi kuwa kusitishwa kwa bunge ni 'kinyume cha sheria' na hatua hiyo ilitumika 'kulitatiza' bunge. Mahakama iliamua kwa faida ya rufaa aliokata Bi Miller na dhidi ya rufaa ya serikali. Waliohusika na kesi wamepokeaje hatua hii? Mwanachama wa SNP Joanna Cherry amesema msimamo wa waziri mkuu hauwezi 'kutetewa' Akizungumza nje ya mahakama, Bi Miller amesema uamuzi huo unatoa ujumbe mkubwa. "Waziri mkuu huyu ni lazima afungue milango ya bunge kesho. Ni lazima wabunge warudi na wawe wakakamavu katika kuiwajibisha serikali," ameongeza Mwanachama wa SNP Joanna Cherry, aliyeongoza kesi ya Uskotchi amemtaka waziri mkuu Johnson ajiuzulu kufuatia uamuzi huu. "Mahakama ya juu zaidi Uingereza imeamua kwa pamoja kuwa ushauri wake wa kusitisha bunge, ushauri wake kwa Malkia, ni kinyume na sheria,"amesema. "Msimamo wake hauwezi kutetewa na anapaswa kwa mara ya kwanza kufanya lililo sawa, na ajiuzulu." Uamuzi wa Boris Johnson kusitisha bunge Uingereza, ulikuwa kinyume na sheria, mahakama ya juu zaidi nchini humo imeamua. text: Getayawkal Ayele: 'Nabii' wa Ethiopia aliyejaribu kumfufua mfu Tukio hilo lilifanyika katika mji wa Galilee huko Wollega magharibi mwa Ethiopia. Kanda ya video ya 'nabii' huyo ikiita jina la mfu huyo kwa lengo la kumfufua ilisambazwa sana katika mtandao wa facebook. Kanda hiyo ya video inaonyesha 'nabii' huyo akilala kando ya mwili huo na kuita jina la marehemu. Awali alikuwa amekwenda kwa familia ya mfu huyo kwa jina Belay Bifu na kuwahubiria kuhusu habari ya Lazurus, vile Yesu alivyomfufua, muhubiri kutoka mji wa Dhinsa Dabela aliambia BBC. ''Niliona watu wengi wakikimbia kuelekea kule kaburi hilo lilikokuwa wakisema Belay anakaribia kufufuka. Niliwashauri watu kutomuamini nabii huyo lakini walinifukuza wakisema sina imani'', muhubiri huyo alisema. Nabii huyo baadaye aliwafanya watu kuchimba kaburi , na kuchukua kipande cha nguo kilichotumika kumfunga marehemu na kuanza kumwambia Belay amka tena na tena. Baada ya majaribio kadhaa ambayo hayakufanikiwa nabiii huyo aliondoka katika kaburi hilo akisema haiwezekani. Wanachama kadhaa wa familia walikuwa wagonjwa huku wengine karibia wazirai hapo hapo Dhinsa alisema. Watu waliokuwa wakitazama kisa hicho walikasirika na kuanza kumpiga kabla ya polisi kuwasili na kumkamata. Kamanda wa polisi katika eneo hilo Tadese Amenu alithibitisha kwa BBC kwamba nabii huyo anazuiliwa na maafisa wa polisi. Kulingana na kamanda huyo nabii huyo aliyegunduliwa kuwa mfanyikazi wa afisi ya idara ya afya na hakuwa mwanachama wa kanisa lolote. Maafisa wa polisi nchini Ethiopia wamemkamata kijana mmoja anayejiita 'nabii' kwa jina Getayawkal Ayele baada ya kushindwa kumfufua mfu aliyefariki siku nne zilizopita. text: Watu 2,400 wameuawa katika vita dhidi ya mihadarati tangu Rais Rodrigo Duterte aingie madarakani Juni Bw Duterte amesema hayo baada ya Bw Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake. Kiongozi huyo wa Ufilipino alikuwa amemweleza Bw Obama kama "mwana wa kahaba" na kuongeza kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini mwake. Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote. Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani. Hayo yalijiri kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa bara Asia, mjini Laos. Lakini kupitia taarifa, Bw Duterte amesema anajutia matamshi hayo. Amesema wanadiplomasia wa Ufilipino na Marekani wanatarajia kuondoa uhasama na tofauti zilizozuka baina ya nchi hizo mbili. Rais Barack Obama alionywa na Bw Duterte "kuonyesha heshima" Tangu kuingia madarakani, Bw Duterte ameendelea kutumia maneno makali, na kutumia lugha chafu kuwarejelea Papa Francis, maafisa kadha wa Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na balozi wa Marekani nchini Ufilipino. Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema anajutia kwamba amatamshi yake kumhusu kiongozi wa Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi. text: Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32. Fainali itachezwa 15 Julai. Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800. Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa. Ujerumani, waliowashinda Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2014, wanapania kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1962. Hapa ni mwongozo wa makundi yalivyo na mechi zitakavyochezwa hatua ya makundi: Brazil wanatafuta kuweka rekodi nyingine kwa kushinda kombe hilo kwa mara ya sita. Michuano hiyo ya mwezi mmoja inatarajiwa kuwavutia mashabiki nusu milioni kwenda Urusi na kote duniani inatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu. Kuna makundi manane, kila kundi likiwa na timu nne. Timu mbili ambazo zitamaliza juu kwenye kundi ndizo zitakazosonga hadi hatua ya 16 bora. Fainali itachezewa katika uwanja wa Luzhniki ambao hutoshea mashabiki 81,000 mnamo 15 Julai. Nani atashinda Kombe la Dunia? Mabingwa watetezi Ujerumani, mabingwa mara tano Brazil, washindi wa Euro 2016 Ureno, waliomaliza wa pili 2014 Argentina, Ubelgiji, Poland na washindi wa mwaka 1998 Ufaransa ni timu nane ambazo zilikuwa kwenye chungu wakati wa kufanywa kwa droo. Wote wanapigiwa upatu kushinda. Unaweza kusoma pia: Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 inaendelea nchini Urusi. text: Afisa Mtendaji Mkuu wa WTA Steve Simon amedai kuwa muamuzi wa fainali ya Jumamosi ameonesha kiwango kidogo cha ustahimilivu katika mzozo wake na Williams kuliko vile ambavyo angefanya laiti angellikwaruzana na mchezaji wa kiume. Serena ameadhibiwa kwa kukiuka kanuni ya ukufunzi,kutoa matamshi ya matusi na kumuita muamuzi ''mwizi''baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Mashindano ya Wazi ya Marekani (US Open) dhidi ya Naomi Osaka wa Japan. "WTA inaamini kuwa hakuna tofauti katika viwango vya uvumilivu vinavyostahili kuelekezwa kwa hisia zinazotolewa na mchezaji mwanamume au mwanamke,'' amesema Bw Simon katika taarifa yake na kuongeza kuwa haamini suala hilo lilizingatiwa katika uamuzi uliyofikiwa dhidi ya Williams. Simmon pia metoa wito kwa wakufunzi kupewa nafasi katikati ya mchezo kuzungumza na wachezaji. Bondia wa Tanzania ataka pambano na Amir Khan wa Uingereza Mwamuzi Carlos Ramos alimuadhibu Williams baada ya kumuona mkufunzi wake Patrick Mouratoglou,akionyesha ishara ya mkono. Baadaye mkufunzi huyo raia wa Ufaransa alikiri kuwa alijaribu kumuelekeza mchezaji wake. Mkuu wa shirikisho la mchezo wa Tennisi nchini Marekani (USTA) ,Katrina Adams ,amesema "Wachezaji wakiume wamekuwa wakiwakaripia waamuzi wakati wa kubadilishana upande kuchezea na hatuoni chochote kikitokea.". Maoni hayo yanaungwa mkono na mwandishi wa mchezo wa Tennis wa BBC, Sue Barker, ambaye amesema: "Nimekaa mara kadha pembeni ya uwanja na kuwaona wachezaji wakiume wakirusha maneno makali kwa waamuzi na hawakuchukuliwa hatua zozote.'' Kocha wa Serena Williams, Patrick Mouratoglou amekiri kuwa alijaribu kumuelekeza mchezaji wake katikati ya mchezo. Williams, 36, ametozwa faini ya dola $17,000 sawa na euro(£13,100) kwa kukiuka kanuni za mchezo wa Tennis ikiwa ni pamoja na kumuita refa Ramos a "mwongo" na "mwizi". Hata hivyo mchezaji huyo amejishindia dola $1.85m sawia na euro (£1.43m) kwa kufuzu kuingia fainali ya shindano la US Open. Serena Williams ndiye mwanaspoti mwanamke mwenye kipato cha juu zaidi Mizozo iloyopita ya US Open dhidi ya Williams Mwamuzi hakutakiwa 'kumsukuma' Williams - Djokovic Alipoulizwa maoni yake kuhusu mwenendo wa Williams,Novak Djokovic,mshindi mara tatu wa taji la wanaume la US Open siku ya jumapili baada ya kumshinda Juan Martin del Potro, alisema, hatua ya mwamuzi Ramos kuingilia mambo bila sababu za msingi ilibadili mkondo wa mechi."Kwa mtazamo wangu nahis imwenyekiti alimkera Serena kiasi cha yeye kushindwa kustahamili hasa ikizingatiwa ni fainali ya Grand Slam''. Djokovic, ambaye pia ni mshindi mara 14 wa Grand Slam pia amesema anatofautiana na msimamo wa mkuu wa WTA Bw Simon,akiongeza kuwa hakuyaelewa matamshi yake (kuwa Serena kabaguliwa kijinsia) huku akielezea utata huo ni kama hali ngumu kwa muamuzi na kwamba anaungana na muamuzi huyo kipindi hiki kigumu. Chama cha mpira wa tenisi cha wanawa(WTA) kimeunga mkono madai ya nyota wa mchezo huo Serena Williams kuwa amebaguliwa kijinsia. text: kiongozi wa chama cha ACT-wazalando Zitto Kabwe Wamejitoa katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanywa 24 Novemba 2019. ''Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.'' Anasema Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT wazalendo katika mkutano na waandishi wa habari. UnawUnaweza pia kusoma Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa ilikutana hii leo kujadili hali na mwenendo wa uchaguzi huo nchini Tanzania. Lakini pia chama hiko kimedai kutumika vibaya kwa jeshi la polisi la nchini Tanzania kuingia mchakato wa uchaguzi huo. bendera ya chama cha ACT ikipepea ''Kumekuwepo na vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na watendaji wa Serikali kuwabughudhi Wagombea wetu, wanachama na viongozi wetu maeneo mbalimbali nchini. Serikali ya Rais Magufuli isitufikishe kuvuka mstari wa Uvumilivu.'' Anaongeza Zitto Kabwe katika taarifa yake. Mapema leo, Mbunge huyo Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo aliandika katika aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuomba ushauri kwa umma kuwa wachukue hatua gani? katika mchakato unaondelea wa serikali za mtaa? Unaweza pia kusoma: Zitto Kabwe alitoa kauli hiyo mara baada ya chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema kutangaza kuwa kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Aidha serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi imesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ulivyopangwa tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu. Ufafanuzi huo umetolewa mapema hii leo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni, Dodoma ambapo Mbunge wa Singida Kaskazini Justice Monko alitaka ufafanuzi wa serikali hasa baada ya Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kutangaza kujitoa rasmi katika mchakato wa Uchaguzi huo. Chama kingine cha upinzani chenye ushawishi nchini Tanzania kimejitoa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wa nchi hiyo. text: Hii ni mara ya kwanza kwa mmea wa kibaolojia kuchipuwa mwezini, na ni hatua inayofungua njia ya tafiti zaidi za kisayansi mwezini. Chang'e 4 pia ndio chombo cha kwanza kutafiti sehemu ya mbali zaidi ya mwezi, ambayo haitazamani na uso wa dunia. Chombo hicho kilitua mwezini Januari 3 kikiwa kimebeba vifaa vya kuchunguza jiolojia ya eneo hilo. Mimea imekuwa ikioteshwa kwenye kituo cha kimataifa cha anga za juu lakini haijawahi kujaribiwa mwezini. Uwezo wa kuotesha mimea mwezini itakuwa ni sehemu muhimu ya utafiti wa muda mrefu wa mwezi, na pia safari ya kuelekea Mars ambayo inakadiriwa kuchukua miaka miwili na nusu. Hii inafungua milango ya uwezekano wa wanaanga kuweza kuzalisha chakula chao wenyewe wakiwa anga za mbali na kupunguza uhitaji wa kurudi duniani ili kufuata chakula. Chombo hicho cha Uchina kilibeba udongo wenye mbegu za pamba, viazi na hamira. Mimea hiyo imo ndani ya mabakuli yaliyofungwa. Mazao hayo yanatarajiwa kujitengenezea kinga na kujikuza katika mazingira yake itakayojitengenezea. Je mwezi utaathirika? Swali kuu linaloulizwa ni iwapo jaribio hilo la kuotesjha mimea litaleta madhara. Lakini utafiti huo ambao unafanywa kwa ushirikiano wa vyuo 28 vya Uchina unalenga kupata taarifa za namna gani viumbe hai vinavyotumia hewa na kuzalisha nguvu ya baianuwai (hasa mimea) vinaweza kukua mwezini. Mimea hiyo iliyohifadhiwa vizuri imewekewa hewa, maji na virutubisho vingine vitakavyoisaidia kukua. Changamoto kubwa kwa wanasayansi wa Uchina ni kubadilika kwa hali ya hewa mwezini ambapo huwa baina ya -173C and 100C ama zaidi. Wanasayansi wengi wanaamini kuwa uwezekano wa kuathiri mwezi ni mdogo kutokana na utafiti huo. Na pia wanasisitiza kuwa tayari kuna mifuko takribani ya 100 ya uchafu iliyoachwa na binadamu waliotua mwezini na chombo cha Marekani cha Apollo. Fred Watson, mwananga kutoka Australia ameiambia BBC kuwa kuchipua huko kwa mbegu hizo ni habari njema. "Hii inatueleza kuwa yawezekana kusiwe na shida kwa wanaanga kuzalisha chakula chao wenyewe mwezini katika mazingira salama." Mbegu zikiwa ndani ya Chang'e 4 "Kuna umuhimu mkubwa sana katika suala hili, hususani kuutumia Mwezi kama kituo cha kurusha vyombo kwenda sayari ya Mars sababu Mwezi upo karibu na Dunia ," amesema Watson. Profesa Xie Gengxin, ambaye ndiye msanifu mkuu wa utafiti huo amenukuliwa na gazeti moja la Uchina akisema wanalichukulia kwa umuhimu suala la kuishi anga za juu kwa siku za usoni. "Kujifunza namna ambayo mimea inakuwa katika mguvu za mvutano wa asili ndogo kutatuwezesha kuweka msingi wa uwepo wetu wa baadae kwenye anga za juu. Chombo hicho kilichukua siku 20 kutoka Duniani mpaka Mwezini na kimeshapiga picha 170 ambazo zimezituma duniani na zinafanyiwa kazi, shirika la habari la Xinhua linaripoti. Mbegu ambazo zimepelekwa mwezini na chombo cha utafiti wa anga za juu cha Chang'e-4 zimechipua, mamlaka jijini Beijing zimethibitisha. text: Raia 6 wa Urusi ambao waliwahi kuwa chini ya kifungo cha nymbani walizungumza na mwanahabari wa Urusi kuhusu namna ya kuishi maisha ya kujitenga. Muda wa kuanza kutafakari Mwongozaji wa thamthilia Kirill Serebrennikov alihukumiwa kifungo cha nyumbani cha mwaka mmoja na nusu mjini Moscow. Ametengeza video: Namna ya kutoshikwa na kichaa unapokuwa huwezi kutoka nje. Katika maisha ya kawaida kuna mambo mengi , simu unazopigiwa, Instagram na Facebook. Lakini kujitenga kunaweza kukukatizia haya yote. "Ni fursa nzuri ya kujiondolea yote ambayo huenda yanakukera," anasema Kirill Serbrennikov. "Unaweza kujikita katika masuala ya msingi pekee - kama vile kujitambua wewe ni nani na kile unachotaka maishani." Anapendekeza kuwa na kijitabu cha kuandika hata lile jambo dogo kabisa utakalofikiria. Yulia Tsvetkova mtetezi wa masuala ya wanawake na mwelekezi wa filamu za watoto huko Siberia alikuwa chini ya kifungo cha nje kwa miezi minee sababu ni kutetea haki za wanawake na wapenzi wa jinsia moja mtandaoni. Anasema kwamba hiyo ilikuwa ni fursa nzuri ya kutofanya chochote na wala hakuwahi kuhisi vibaya. Tarajia kujihisi mnyonge Sergei Fomin, aliyekuwa kizuizini kwa mwezi mmoja kabla ya kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kifungo cha nyumbani mara tatu kwa kushiriki maandamano mjini Moscow, anakumbuka mipango aliyokuwa nayo baada ya kuachiliwa. "Nilikuwa ninaenda kufanya mazoezi ya aina mbalimbali na kutengeneza ratiba yangu ya kusoma," anasema. Lakini baada ya mwezi mmoja hilo halikuwezekana tena "Sikufanikiwa kufanya kile nilichokuwa nimepanga kila siku. Ningeamka saa 4 asubuhi na kupumzika tu kitandani hadi saa tisa mchana, kisha ningetumia saa tatu bafuni na kurejea tena kitandani." Yulia pia alikuwa na wakati mgumu. "Nilitamani kubadilika na kuwa kiwavi, na kujificha chini ya blanketi na kujitenga na dunia, hilo liliniogopesha," anasema. Mtaalamu wa hesabu Dmitry Bogatov alihukumiwa kifungo cha nyumbani kwa zaidi ya miezi 6 mwaka 2018. Anasema, "Ni vigumu sana kuendeleza ratiba yoyote kwasababu kawaida kuna mambo yanayotupa mwongozo kama muda wa maduka kufungwa na wa kuwa kazini. Lakini hayo yote yanakosa maana." Natalya Sharina, aliyekuwa mkurugenzi wa maktaba ya fasihi Ukraine, alikamatwa 2015 na kupewa kifungo cha nyumbani kwa zaidi ya miezi 18. Baada ya polisi kumvamia, kuhojiwa, kupewa kifungo cha peke yake, na kushtakiwa, akahukumiwa kifungo cha nyumbani lakini kwake hii ilikuwa kama kuwa peponi. Ingawa hilo halikuendelea kwa muda mrefu. "Unafikiria kwamba unaweza kusoma na kusikiliza muziki, lakini ukweli ni kwamba hilo haliwezekani. Ukosefu wa haki, hasa nikifikiria ukweli kwamba sikutenda kosa hilo. Lilinifanya kuwa na hasira sana. Unachukua kitabu ukidhani kwamba utasoma lakini huwezi kumakinika, unafungua televisheni na kila kitu kinaanza kukujia akilini." Muda usiotarajia kwamba utakuwa huru Baada ya kuwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa miezi kadhaa, Natalya aliruhusiwa kwenda hospitali. Alihitaji matibabu ya uti wa mgongo baada ya kupata jeraha akiwa ndani ya gari la polisi. Safari za kumuona daktari kidogo zilianza kumpa matumaini. "Nilienda hospitali lakini kuona wengine wakiendelea na maisha yao ya kawaida kulinifanya nihisi vizuri," anasema. "Wakiniacha nitembee umbali wa mita 500," Yulia Tsvetkova anakumbuka, "Hilo lilikuwa linaibua hisia zangu. Ilikuwa ni kama kupata uhuru kidogo, lakini kwa muda uliosalia siku hiyo, nilikuwa mpweke sana." Sergei alikatazwa kwenda kutembea lakini akavunja sheria mara mbili. "Wakati mwengine saa za usiku, ningevuta kofia ya kwenye jaketi na kujifinika kichwani kisha ninatoka kwenda kununua pombe dukani. Nikitoka nilikuwa ninapata hisia zisizo za kawaida, ni kama vile nimetoroka jela." Zungumza na uwapendao Chini ya kifungo cha nyumbani, mara nyingi mahakama inaruhusu uongee tu na jamaa wako wa karibu. Mume wa Natalya na bintiye walimpa moyo katika kipindi chote alichokuwa amejitenga. Baadaye, akaruhusiwa kuzungumza na simu na kutembelea marafiki. "Wanyama wa nyumba pia nao wanaweza kukufariji," anasema. Mtaalamu wa teknolojia na mwanaharakati wa upinzani Alexander Litreyev alianzisha programu mtandaoni kwa jina De-anonymise kutambua maafisa wa polisi wanaopiga waandamanaji wasiokuwa na hatia. Kifungo chake cha nyumbani ndo kimeanza. Rafiki yake Darya huja kumuangalia kila siku. "Huniletea vitu vitamu vya kula," anasema, "na kunipa moyo." Soma vitabu kupunguza fikira Karibu kila mmoja hutoa ushauri wa kusoma. Kirill Serebrennikov anapendekeza vitabu vya War and Peace, Don Quixote na The Kindly Ones. Pia anapendekeza kuandika mambo mengi tu unayofanya kama kumbukumbu au kujifundisha lugha mpya. Alexander Litreyev ni mtunzi wa mashairi na anapanga vile atakavyoanzisha mradi wake mpya. "Kile kilichoninusuru ni gemu ya draught," anasema Sergei. "Baba yangu alinunua kitabu kinachofunza namna ya kucheza na kushinda mchezo wa draught. Nilikuwa ninatumia muda wa saa tano kwa siku kutengeneza mchezo huo." Kumbuka kuna baadhi ya watu ambao wanapitia changamoto kubwa kuliko wewe Yulia anasema fikiria wafungwa wa kisiasa. "Najua vile mtu anavyohisi ikiwa yeye ni mfungwa wa milele. Karantini siyo kitu cha kuogopesha hivyo ukilinganisha na hicho." Cha msingi zaidi wakati wa kujitenga, anasema Alexei Bushmakov, wakili wa Alexander, ni kufahamu kwamba hauko peke yako na kuwa haijalishi utachukua muda gani kila kitu kitakuwa sawa na utakuwa huru tena. Pia unaweza kutazama: Coronavirus: Kila mgeni atakayeingia Tanzania kufikishwa karantini Je una wakati mgumu kukabiliana na amri ya kutotoka nje? Katika miaka ya hivi karibuni, maelfu ya watu Urusi ( zaidi ya 60,000 kati ya 2013 na 2018) walihukumiwa kifungo cha nyumbani kwa makosa ya kisiasa na mengineo. text: Asmara una wakaazi 500,000 wanaoishi katika mji huo, ambao ukiangazia na mishahara duni, kodi za kiwango cha juu za uingizaji biadhaa na uhaba wa mafuta una maanisha mji huo una magari machache. Na yale utakayoyaona huwa ni makuu kuu ya miaka ya nyuma. Barabara ni tupu hazina magari mengi. Wakaazi wanalalamika kuondoka kwa idadi kubwa ya vijana ambao wameondoka katikamiaka 20 iliyopita kutokana na ugumu wa maisha unaotokana na mizozo na kulazimishwa kulihudumia taifa chini ya serikali ambayo sio kila mtu anakubaliana nayo. Kutokana na hali hiyo, Asmara nimji wenye taswira tofauti na mataifa mengi barani Afrika yaliona msongamano wa magari na foleni zisizokwisha. Hii ikichanganywa na hali ya hewa nzuri, ni mzingira mazuri kwa raia kuendesha basikeli katika mji huo. "Uendeshaji baiskeli ni sehemu ya utamaduni wetu," anasema mwanamume mwenye umri wamiaka 25. Muundo wa ujenzi wa mji wa Asmara unwavutia wengi na hivi karibuni ulitangazwa kuwa kivutio duniani kwa sanaa iliyotumika katika usanifu wa majengo ya mji huo, utajiri ulioachwa katika wakati wa utawala wa kikoloni wa Italia kuanzia 1897 hadi 1943. Madukaya kutengeneza baiskeli yametapakaa kila mahali Asmara. Eritrea ina historia ndefu ya kujitegemea ilioanza wakati wa vita vyake vya kupigania uhuru vya miaka 30 kutoka kwa Ethiopia, baada ya hapo kutengwa kimataifa kumefanya kuwa vigumu na ghali kuingiza vipuri na baiskeli mpya. Vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume nchini humo huendesha "bicicletta", neno linalomaanisha baiskeli katika lugha ya Tigrinya, iliyotokana na lugha ya kiitaliano. Uendeshaji baiskeli pia una umaarufu miongoni mwa raia kutokan na kwamba nijambo lililoidhinishwa na Italia na mashindano ya uendeshaji baiskeli ni fahari kubwa miongoni mwa raia. Timu ya taifa inayomjumuisha Mosana Debesay kwenye picha hii katika mashindano huko Austria Septemba mwaka jana, ina ufanisi mkubwa katika mashindano ya kimataifa. Maridhiano ya hivi karibuni baina ya nchi hiyo na Ethiopia yamewaacha raia wengi Eritrea wakitumaini kwamba uchumi utaimariki kwa kasi, na kurahisisha hali ya maisha Asmara. Imeandikwa na mtaalamu wa masuala ya utu Milena Belloni na mwandishi James Jeffrey Mambo mengi tu ikiwemo mzozo na kutengwa kidiplomasia yamechangia pasi jitihada za makusudi mji mkuu wa Eritrea kuwa pepo ndogo ya uendeshaji baiskeli. text: Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha upinzani (CUF) Julius Mtatiro ,kuhamia CCM Mtatiro ni mwanasiasa ambaye pia ni mchambuzi wa siasa na amekuwa akiandika makala nyingi kuikosoa serikali lakini sasa amehamia huko ambako amekuwa akikukosoa kwa muda mrefu. "Nimejiridhisha kwa hitaji la nafsi yangu kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM" Julius Mtatiro aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya jumamosi,Agosti 11. Mkurugenzi wa habari wa chama cha CUF,Abdul Kambaya amesema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ya chama hicho imesababishwa na Mtatiro. Chama hicho ambacho kimegawanyika katika pande mbili,kuna wale ambao ni wafuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba na wale ambao wako chini ya Maalim Seif. Awali chanzo cha migogoro ya ndani ya chama cha CUF ilidaiwa kuwa ni Profesa Lipumba kutangaza kutengua barua yake ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti aliyoiandika Agosti 2015, wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu. Lakini kwa sasa mgawanyiko wa chama hicho umedaiwa kusababishwa na Julius Mtatiro kutokana na tabia zake za kibabe za kutotaka kusikiliza watu wengine. Inakumbukwa kwamba mwanzoni mwa mwezi Julai,Mtatiro alikamatwa na polisi kutokana na ujumbe alioandika katika mtandao wa kijamii unaomkejeli rais John Magufuli kwa kusema kuwa 'rais kitu gani?' Aidha kujiengua kwa mwanasiasa huyo kumepelekea baadhi ya watumiaji wa mtandao wa kijamii kuanzisha kampeni za kuonesha kupinga au kukasirishwa na uamuzi wake kwa kuwataka watu waache kumfuatila kwenye mitandao ya kijamii kutokana na uamuzi wake kuonekana kuwa wa kisaliti. Katika mtandao wa twitter wameanzisha #unfollowmtatiro na #blockmtatiro Lakini vilevile Mtatiro alikuwa ni kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa anawabeza wanasiasa wengine kuhamia CCM lakini sasa yeye ndiye ameamua kuhamia CCM. Pamoja na kwamba Julius Mtatiro alifahamika kuwa mwanachama wa CUF,ila mwezi julai mwaka huu jumuiya ya vijana za CUF(JuviCUF) ilimtaka Mtatiro kukaa mbali na chama hicho na kuacha tabia ya kuwashambulia viongozi wa juu wa chama cha CUF kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa wao hawamtambui kuwa mwanachama wa chama hicho na aache tabia ya kupotosha umma. Hatimaye sasa kile ambacho chama cha vijana CUF walichokuwa wanakihofia kuwa mwanasiasa huyo sio mwenzao kimeweza kudhihirika wazi. Mtatiro aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF alitangaza kuhamia CCM siku ya jumamosi. Maswali mengi yamezuka mara baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro ,kujivua uanachama wake na kuhamia chama tawala cha CCM. text: Marekani iliwasilisha ombi la mwisho siku ya Ijumaa , siku moja baada ya Giraltar kuiachilia meli hiyo ya Grace 1. Gibraltar imesema kwamba haikuweza kukubali ombi la Marekani kuikamata tena meli hiyo kwa kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina nguvu Ulaya. Meli hiyo tayari imeondoka Gibraltar kulingana na mjumbe wa Iran nchini Uingereza. Tehran imesema kwamba iko tayari kuyapeleka majeshi yake kuisindikiza meli hiyo ambayo jina lalke lilibadilishwa kutoka Grace 1 hadi Adrian Drya 1. Meli hiyo na wafanyakazi wake 29 kutoka India, Urusi, Latvia na Ufilipino ilikamatwa kupitia usaidizi wa wanamaji wa Uingereza tarehe 4 Julai baada ya serikali ya Gibraltar - eneo linalomilikiwa na Uingereza kusema kwamba ilikuwa ikielekea Syria hatua inayokiuka vikwazo vya Muungano wa Ulaya. Hatua hiyo ilizua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Iran , ambao umeendelea katika wiki za hivi karibuni huku Iran nayo ikiikamata meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza Stena Impero katika Ghuba. Mamlaka ya Gibraltar iliiwachilia meli hiyo siku ya Alhamisi baada ya kupokea hakikisho kutoka Iran kwamba haitaipeleka mafuta yake nchini Syria. Idara ya haki nchini Marekani baadaye ikawasilisha ombi mahakamani la kuizuilia meli hiyo kwa msingi kwamba ina uhusiano na jeshi la Iran ambalo imelitaja kuwa kundi la kigaidi. Gibraltar , katika taarifa yake siku ya Jumapili ilisema kwamba haikuweza kukubali ombi hilo kwa kuwa jeshi hilo la Revolutionary Guard sio kundi la kigaidi kulingana na EU ambalo eneo hilo la Uingereza ni mshirika wake. Pia ilisema kwamba vikwazo vya Marekani vya kuzuia uuzaji wa mafiuta wa Iran haviwezi kuidhinishwa na EU ikidai tofauti iliopo kati ya Marekani na EU kuhusu Iran. Hakujakuwa na majibu yoyote kutoka kwa Washington. Balozi wa Iran nchini Uingereza Hamid Baedinejad alituma ujumbe wa twitter siku ya Jumapili kwamba makundi mawili ya wahandisi wa Iran walikuwa wanaelekea Gibraltar na kusema kwamba meli hiyo inatarajiwa kuondoka usiku. Stena Impero, ambayo ilikamatwa na jeshi la Revolutionary Guard tarehe 19 Julai bado ipo mikononi mwa Iran. Uingereza imetangaza kwamba itajiunga na kundi la wanajeshi wa Marekani kulinda meli za biashara zinazosafiri kupitia mkondo wa Hormuz. Meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza Stena Impero ilikamatwa na Iran tarehe 22 Julai Hali ya wasiwasi kati ya Iran na mataifa ya magharibi inatokana na mpango wa kinyuklia wa Iran. Mwaka uliopita, Washington ilijiondoa katika mkataba wa kinyuklia wa Iran wa 2015 ili kuzuia taifa hilo kutengeza silaha za kinyuklia huku kukiwa na wasiwasi kwamba Tehran ilikuwa inajaribu kuunda silaha za kinyuklia , kitu ambacho Iran imekana. Tangu wakati huo , wasiwasi kati ya Marekani na Iran umeongezeka huku taifa hilo likiiongezea vikwazo Iran. Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya yamesema kwamba bado yanaheshimu mkataba huo. Gibraltar imepinga ombi la Marekani kuikamata tena meli ya mafuta ya Iran ambayo ilikuwa ikiizuia tangu mwezi Julai kwa kudhania kwamba ilikuwa ikisafirisha mafuta Syria. text: Millicent sasa hawezi kukaa kwa muda mrefu kutokana na shida ya mgongo na hata kusumbuliwa na misuli Saratani ya mlango wa uzazi inaweza kusababishwa kwa maambukizi ya virusi vya Human Papillomavirus au HPV, na aina hii ya virusi huambukizwa kwa njia ya kujamiiana. Alianza kuhisi kwamba ana tatizo alipojifungua mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 20, ambapo alianza kutokwa na uchafu katika sehemu za siri lakini hakujua ulikuwa ni ugonjwa gani. "Baada ya muda nikaanza kuvuja damu na hapo nilikwenda hospitalini na daktari akasema ''Dada pole unaugua satarani na iko katika kiwango cha nne.'' ''Nilipoteza fahamu na hata wakati huo nilitaka kujitoa uhai na hata watoto wangu wawili kwa sababu ya maisha niliyoyapitia, singependa mtoto wangu apitie hayo''. Bi, Milicent anazungumza akiwa amelala kwenye sakafu kwani hawezi kuketi kwa muda mrefu kutokana na shida ya mgongo na hata kusumbuliwa na misuli. ''Wakati nilipokuwa nimekaa na saratani hiyo kwa muda sikuweza kuzuia haja ndogo au kubwa, nilikuwa navuja damu mara mbili kwa siku kwa dakika tano na nilikuwa nikipoteza zaidi ya lita nne za damu asubuhi na nne jioni''. ''Lakini siwezi kusahau ile siku nilivuja damu kwa siku mbili''. ''Nilitokwa na uchafu ulionuka kutoka sehemu zangu za siri kwa miaka sita, kwa sababu sikujua naugua ugonjwa gani? Nilivumilia kwa sababu niliogopa kubaguliwa na ndoa yangu kuvunjika,''Millicent anasema. Kwa kupitia matibabu haya ya saratani Millicent anasema kwa hivi sasa hawezi kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu au hata kulala kitandani. Iliyobaki analala sakafuni kwa sababu ya maumivu makali mgongoni mwake. Millicent ameongeza kwamba alifika ukomo wa uzazi wa mapema, na hata kuwa mnene kutokana na matibabu hayo. Safari yake ya ugonjwa huo haikukomea hapo, alianza kutengwa akabaki na watoto wake pekee, na hakuna mtu aliyetaka kujihusishwa naye. Jamii yake ilisema kwamba amerogwa, wenine wakasema ni kiboko anachochapwa kutoka kwa maulana na hata wengine wakisema ni laana ya kuzaliwa nayo, kwa jinsi alivyokuwa akivuja damu. ''Kama si matibabu ya kuchomwa na miale ya moto, basi leo hii singekuwa hai,'' Millicent anasema. Millicent alirudi kwa Mungu na kutafuta usaidizi wa kuombewa kanisani Je unaweza vipi kujua unaugua saratani ya mlango wa uzazi? Saratani hii haina dalili hadi inapofika kiwango kikuu. Mara nyingi wanawake hudhani dalili wanazopata ni za kitu kingine, kama vile hedhi ya kila mwezi, maambukizi katika kibofu cha mkojo, au kuvu. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO, hizi ndizo baadhi ya dalili zinazojitokeza kwa muathiriwa: Ni muhimu kwa wanawake wote kufanyiwa ukaguzi wa fuko, au mlango wa uzazi na kupata ushauri wa daktari iwapo baadhi ya dalili zitajitokeza. Kuna saabu nyingi za kukufanya ukavuja damu kupita kiasi na huenda sio saratani ya mlango wa uzazi. Na mambo mengi huzingatiwa katika kulibaini hilo, mfano umri, uzazi, iwapo umejifungua na pia historia ya familia. Kadhalika kuvuja damu baada ya ukomo wa uzazi ni jambo la kawaida, hatahivyo ni vyema kupata ushauri wa daktari wako. Mpiga Picha: David Nthusa Wambundo Millicent Kagonga, ameugua saratani ya mlango wa uzazi kwa miaka 9, na anasema maisha yake hayajakuwa rahisi. text: Taarifa kutoka kwa Jamii Forums inasema Bw Melo alizuiliwa kwa kutotoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo. Alitarajiwa kufikishwa kortini Jumatano lakini hilo halikufanyika. Badala yake, polisi walifika afisi za Jamii Forums kufanya upekuzi kisha wakawahoji wafanyakazi na kuchukua maelezo ya utendaji kazi wao. Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanasema Melo anashikiliwa kinyume cha sheria kwani sheria inataka mtu asishikiliwe na polisi kwa muda unaozidi saa 24 bila kuwasilishwa kortini. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilitoa taarifa Jumatano kulaani kuendelea kuwekwa kizuizini kwa Bw Melo. "Kituo kinalitaka jeshi la polisi kuheshimu katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 1977 inayotoa haki kwa kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru," taarifa ya kituo hicho ilisema. Mwanzilishi wa Jamii Forums akosa kufikishwa kortini Kupitia taarifa, mratibu wa kitaifa wa shirika la watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania (THRDC) Bw Onesmo Olengurumwa aliwataka maafisa wa polisi kumwachilia huru mara moja Bw Melo kwa sababu "wameshindwa kumfungulia mashtaka kortini katika muda unaotakikana kisheria." Aliitaka serikali kuhakikisha Sheria ya Makosa ya Kimtandao haitumiwi kukandamiza uhuru wa kujieleza katika mtandao nchini Tanzania. Wakili wa Melo, Jebra Kambole anasema Ijumaa wana mpango wa kuiandikia Mahakama Kuu ombi la kuiomba iwalazimishe polisi kumpeleka Melo mahakamani hapo afunguliwe mashtaka au aachiliwe Polisi jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa siku nyingine wamekosa kumpelekea mahakamani Maxence Melo, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa Jamii Forums. text: Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano Nikki Haley ametaka kuwepo kwa muda wa dharura wa Baraza la Umoja wa Mataifa utakao jibu majaribio hayo kwa hatua kali. "Vita sio kitu ambacho Marekani ingetaka," alisema. "Hatutaki vita kwa sasa lakini uvumilivu wa nchi yetu hautuzuii." Baadae, kupitia mazungumzo ya simu na Rais Trump, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema atahimiza kuwepo kwa vikwazo vikali kutoka umoja wa nchi za ulaya dhidi ya Pyongyang. Hata hivyo, China imesisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo. Baraza la usalama la umoja wa mataifa mara ya mwisho liliweka vikwazo kwa Korea Kaskazini juu ya bidhaa zake mwezi Agosti Ripoti zinasema kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kwa majiribio mengie ya makombora. Siku ya Jumapili ilifanya jaribio la bomu la chini ya ardhi lililoaminika kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 20 na 120. Kifaa hicho hicho kinaweza kuwa na nguvu mara tatu zaidi ya bomu lililotumiwa kuharibu mji wa Hiroshima mwaka 1945. China haitaki kuwepo nchi yenye silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini na mara kwa mara imeeleza msimamo wake kwa nchi hiyo. Lakini pia haitaki kuona utawala wa Korea Kaskazini ukiondolewa madarakani. Hii itasababisha mamilioni ya wakimbizi kukimbia kwenda China na kuchangia kuungana kwa Korea ambayo itakuwa chini ya ushawishi wa Marekani. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara. text: Isisahaulike kufutwa kwa uchaguzi wa rais nchini Kenya ,kitendo kilichofanyika kwa mara ya kwanza Afrika. Pia tumeripoti kuhusu majanga na ubunifu - lakini hizi ni baadhi ya habari za kushangaza kwa mwaka 2017. 'Githeri Man' Mwanaume mmoja Mkenya aliyepigwa picha akitafuna 'githeri' chakula cha mahindi na maharagwe, wakati wa uchaguzi, alijipatia umaarufu mkubwa. Mwanaume huyu ambaye aliongolewa sana na vyomvo vya habari Kenya Githeriman, ambaye kwa jina lake halisi anaitwa Martin Kamotho, alivuma wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya tarehe nane mwezi wa nane alipoonekana kwenye mitandao ya kijamii akila chakula cha maharagwe na mahindi yakiwa ndani ya mfuko wake wa plastiki. Bw Kamotho anajulikana sana kama "Githeri Man" alivuma sana kwenye mitandao ya jamii; Makampuni makubwa kama vile Safaricom na Maisha Flour Milla yamejitokeza kumsaidia Githeriman na hivi sasa akaunti yake benki imeshiba kutokana na cheki alizoandikiwa na kampuni hizo. Bw.Kamotho alikuwa miongoni ya wananchi 59 waliotunukiwa nishani za heshima na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe za kuidhinisha sikukuu ya jamhuri kwa sababu ya kazi walioifanyia nchi. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, tuzo hiyo ni kwa minajili ya watu ambao "wameonesha uwezo wa hali ya juu, katika uongozi,ujasiri na uzalendo" Hata hivyo baadhi ya Wakenya bado wanapata shida kufahamu ni nini hasa Bwana Kamotho alichofanya ili kupata heshima hiyo. Dk. Shika wa milioni 900 Mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi,ulioharibika nchini Tanzania, iligeuka kumpatia umaarufu mwanaume mmoja kwa jina la Dk. Louis Shika . Dk Shika alijizolea umaarufu baada ya kuibuka kwenye mnada huo na kutaja viwango vya juu vya fedha kuwapiku watu wengine waliojaribu kununua nyumba hizo. Dk Shika aliwashangaza wengi kwa mavazi yake ya kawaida mbazo hazikumuonesha kama mtu ambaye angeweza nunua nyumba za dola za Marekani milion 15 (Sh bilioni 3.2) Lakini baada ya kutolipa asilimia 25 ya fedha zilizohitajika, alikamatwa na polisi kwa shutuma za kuharibu mnada,na kuachiwa baada ya kulipa dhamana. Kwa mujibu ya vyombo vya habari nchini humo, kauli zake katika mnada huo, hasa ya '900 itapendeza' ,ndizo zilizompa umaarufu kiasi cha kupata udhamini wa kampuni tofauti. Baada ya hapo maswali mengi yalivuma kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu ukweli wa hali yake Dk Shika,ambazo zinadai kwamba alikuwa mjasusi wa intelijinsia wa Marekani, CIA, anamiliki mabilioni ya fedha nchini Urusi na Uhispania. Lakini pia ikatokea nafasi ya wengi kutania kuhusu sakata hilo; Msanii maarufu wa Tanzania, Joti, alimtania Dk Shika "Polisi Kinyozi" aliyewaibisha wanawake Mwezi Aprili, taasisi ya usalama barabarani Nigeria, walimuadhibu kamanda aliyepigwa video akiwaadhibu wafanyakazi wa kike kwa kuwakata nywele zao ndefu. Picha zilimuonesha komanda huyo akitumia mkasi kuwakata nywele wakati wa ukaguzi na kuzua hisia za hasira mtandaoni. Inasemekana kuwa wanawake hao walikuwa wamevunja kanuni za mitindo za nywele inayoruhusiwa na taasisi ya usalama barabarani (FRSC) Mwanaume mwenye kofia nyekundu akimkata nywele mwanamke hadharani Msemaji wa FRSC alisema kitendo cha afisa huyo kilikuwa nje ya udhamini wa taasisi hiyo. Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa jamii wa Twitter , Lauretta Onochie, msaidizi wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alikemea kitendo hicho na kukiita "udhalilishaji wa wanawake" Kanisa la Walevi Kanisa jipya nchini Afrika ya Kusini lilifungua milango yao na kuwakaribisha wavuta sigara na wanywaji pombe , ambao kwa kawaida hawapatiwi nafasi katika makanisa ya walokole. Mtandao wa Habari Afrika Kusini ya eNCA, iliripoti kuwa, kanisa la Gobola mjini Johannesburg liliwakaribisha makundi ya watu na chupa za bia wakati wa ibada. Askofu wa kanisa hilo, Tsietsi Matiki alisema kanisa ni "sehemu mwafaka" kwa wanywaji pombe na wavutaji sigara. Lakini, eNCA wanaeleza , baraza la makanisa Afrika Kusini limelipinga kanisa hilo mpya. Kwa mujibu wa mshiriki mmoja wa kanisa la Gobola, pombe inapewa tu kwa waumini waliona umri wa miaka 20 kwenda juu. Vipara Msumbiji Walengwa Mwezi Juni , polisi nchini Msumbiji walionya kuwa wanaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi yanayohusiana na uchawi. Watu wanaamini kwamba mwili wa mtu mwenye kipara una dhahabu , kulingana na kamanda mmoja wa polisi kwa jina Afonso Dias aliiambia BBC mnamo mwezi Juni baada ya misururu ya mauaji yaliyolenga watu wenye vipara. Baadhi ya raia nchini Msumbiji wanaamini kwamba mtu mwenye kipara ana dhahabu Watu watano waliuwauwa wakati tuliporipoti habri hiyo. Polisi pia waliwakamata watuhumiwa wawili walioshiriki katika mauaji hayo ya uchawi. Soma zaidi hapa na hapa Wabunge watwangana makonde Uganda Wabunge nchini Uganda walipigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo Wabunge wa upinzani wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa ni njama za kumuandilia njia Rais Yowei Museveni, mwenye miaka 73, kugombea tena mwaka 2021. Katika kanuni za Katiba, mtu anayewania urais haruhusiwi kuwa na umri zaidi ya miaka 75. Chairs were thrown during the debate in parliament Upande wa Afrika Kusini pia, mzozo huo huo ulitokea mwezi Februari, wakati wabunge wa upinzani wa Economic Freedom Fighters(EFF) walipigana na maafisa wa usalama baada ya wabunge hao kutosikiliza wito wa kutouvuruga hotuba ya taifa ya Rais Jacob Zuma. Vurugu ilitokea kati ya wabunge na maafisa hao, ambao hatimaye walifanikiwa kuwatoa wabunge. Suruali ni Marufuku Sudan Polisi nchini Sudan walivamia sherehe katika mji mkuu wa Khartoum mwezi Disemba na kuwakuta wanawake wakivaa suruali. Wanawake 24 walikamatwa na kushtakiwa kwa kutokuwa na maadili lakini baadaye mashtaka hayo yalifutwa. Shambulio hiyo ilifanywa na idara ya poilisi yenye mamlaka ya kulinda maadili. Wanawake wa Sudan wakiwa Khartoum Kama wanawake hao wangehukumiwa, wangepata adhabu ya mijeledi 40 na kutozwa faini. Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wanakamtwa na kupigwa kwa "kuvaa nguo zisizo na maadili" kila mwaka na kuichapwa mijeledi. Wanasema sheria inayopiga marufuku kuvaa suruali, sketi fupi au ya kubana katika nchi ambayo wengi ni Waislamu, ni ubaguzi dhidi ya Wakristo. Kitamaduni, wanawake wa Sudan wanavaa nguo ndefu zisizobana kama baibui. Soma zaidi hapa #WengerOut Maneja wa timu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenge anaendelea kuwagawana mashabiki wa klabu ya Arsenal, barani Afrika na kwengineko. Mwezi Novemba, wakati Wazimbabwe wengi walikuwa wanatafakari kuhusu jeshi kuchukua mamlaka na maandamano katika mji mkuu wa Harare yaliotaka kumtoa Robert Mugabe mamlakani, wengineyo walichukua muda wao kudai Wenger aachie madaraka. Maada hio ilionekana kuvuma mwaka huu. Picha hapo juu ikionesha maneno "Wenger Out" yaani "Wenger Toka" katika mechi ya soka nchini Ethiopia , siku mbili tu baada ya Arsenal kupoteza mechi dhidi ya Crystal Palace. Maneno hayo pia yalionekana kwenye tamasha la muziki Kenya: "Shahidi Bingwa' Mkenya mmoja amewashangaza weni kwa siku nyingi baada ya kuto shuhuda ya ajali mbili zilizotokea katika maeneo tofauti nchini humo. Picha ya mwanaume huyo alipotokea kwenye vyombo vya habari zilisambazwa sana katika mitandao ya jamii. Mwanaume huyo aliyejitambulisha kama Dennis Muigai alihojiwa na kituo ch habari, Citizen TV baada ya ajali ya helikopta iliyowaua watu watano, tarehe 21 mwezi Oktoba. Na kwa mara nyingine akawashahidi mkuu wakati ajali nyingine iliyotokea mwezi Novemba tarehe 7,huko Murang'a katikati mwa nchi. Ajali hio ilikuwa kilomita 200 kutoka ajali ya kwanza, ambapo gavana wa wa Nyeri alifariki. Aliwaambia kituo cha televisheni, NTV, kuwa alikuwa abiria kwenye gari la polisi wakati ajali hio ilipotokea na akaelezea yaliyotokea kwa undani. Kwa mujibu ya vyombo vya habari vya Kenya, baadaye polisi walikamata kwa shutuma za kumuiga afisa wa polisi,haujulikani nini ilimtokea baada ya hapo. Baada ya yeye kuonekana televisheni, akageuka kuwa mada ya utani, na Wakenya wakaanza mada ya '#WitnessChallenge' kumuiga jinsi ambavyo alivyokuwa pamoja na miwani yake: Matukio mengi ya kukumbukwa yalitokea mwaka 2017 yakiwemo kujiuzulu kwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mabadiliko sambamba katika nchi za Gambia na Angola. text: Patrice Motsepe Anavyofahamika kama mmoja kati ya matajiri barani Afrika, Bwana Motsepe pia ni mwasisi wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini waliokuwa mabingwa wa Afrika mwaka 2016 - lakini je yeye ni nani? Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani amekuwa akimfuatilia kwa karibu: Watu wengi wanafahamu msemo wa "Kuendana na akina Jones", lakini je! Unajua nahau "Kuendelea na Motsepes"? Lazima uwe una ufahamu - kwasababu Patrice Motsepe ni mtu wa tisa tajiri Afrika, kulingana na jarida la Forbes, na miongoni mwa mabilionea weusi nchini mwake. Mwasisi na mwenyekiti wa kampuni ya madini ya African Rainbow Minerals, alikuwa bilionea mwaka 2008 - huku jarida la Forbes likimtaja kuwa mwafrika wa kwanza kuingia katika kundi hilo. Kuongezeka kwa umaarufu na utajiri wake haujapotea katika nchi ambayo sheria za kibaguzi zilifanya wengi kutumbukia katika lindi la umaskini na ukosefu wa fursa za kibiashara kwa miongo mingi. Leo hii mara nyingi utasikia "Mimi sio Motsepe" wa mzazi ambaye hata huwezi kumuomba pesa au usikie utani wa "Mimi ni kijana wa Motsepe" wakiwa na pesa kidogo tu zinazowasumbua. Kwa kifupi, amekuwa mwakilishi wa utajiri na utani na hili linaonesha kuwa uwepo wa Patrice Motsepe una umuhimu mkubwa kwa wengi . Ni ukumbusho wa kile kinachowezekana, sasa basi je Motsepe alifanikiwa vipi kuwa bilionea? Kununua vya rahisi lakini malengo ni ya juu Motsepe alianzisha kampuni yake ya kwanza ya uchimbaji madini mwaka 1994, na kuanza kununua migodi inayozalisha dhahabu kidogo miaka michache baadaye wakati ambapo soko la dhahabu lilikuwa linakabiliwa na changamoto ya kuporomoka na bei yake ikiwa nzuri. Mwaka 2016 klabu yake ya Mamelodi Sundowns ilikua klabu ya pili ya Afrika kusini kushinda kombe la klabu bingwa Afrika Mwaka 2016, klabu ya Mamelodi Sundowns ikawa ya pili kutoka Afrika Kusini kushinda Ligi ya Mabingwa Afrika. Na muda si muda, migodi nayo ikaanza kubadilishwa na kuwa yenye faida. Afueni kubwa kwake inahusishwa na sera za kuwezesha watu weusi kiuchumi nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na tatizo na ukosefu wa usawa ambalo lilikuwepo kwa miongo kadhaa kwasababu ya utawala wa wazungu walio wachache uliofikia ukomo wake mwaka 1994. Kampuni za uchimbaji migodi zilihitajika kuwa na angalau asilimia 26 ya umiliki kabla ya kupatiwa leseni. Na tangu wakati huo, utawala wa migodi wa Motsepe umekuwa ukikua na sasa hivi ana nia ya kuanza kujishughulisha na upatikanaji wa madini ya kobalti, nikeli, madini ya chuma, shaba na makaa ya mawe. Ni mtu aliyejitafutia mali Alizaliwa Januari 28 mwaka 1962. Motsepe alitajwa Patrice Lumumba, waziri mkuu wa kwanza kuteuliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Akiwa kijana, alijifunza ujasiriamali kutoka kwa baba yake Augustine Motsepe, aliyekuwa na familia ya kifalme ya Tswana. Pia alikuwa mmiliki wa duka ambalo ni mmarufu sana Afrika Kusini eneo la Hammanskraal, nje ya mji wa Pretoria. Patrice Motsepe na mkewe Precious wana ushirikiano wa karibu na chama cha ANC Wakati shule zimefungwa, alikuwa akifanya kazi na baba yake na kuanza kujifunza namna ya kufanya biashara. Akasomea uwakili na kuwa mtu wa kwanza mweusi kuongoza kampuni maarufu, Bowman Gilfillan. Baba huyo wa watoto watatu pia ana shahada katika uchimbaji wa madini na anaendesha kampuni ya mawakili kutoka chuo kikuu cha Johannesburg Utajiri wake ukisemekana kuwa dola bilioni 3. Tajiri huyo pia anasaidia miradi kadhaa ya elimu na afya kupitia wakfu wake. Mnamo mwaka 2013, Motsepe alikuwa Mwafrika wa kwanza kutia saini ahadi ya Bill Gate na Warren Buffett ya kujitolea kutoa angalau nusu ya utajiri wake. Motsepe pia yuko karibu sana na watu wenye mamlaka - anavyoonekana hapo mwaka 2018 kati ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama. Mwaka jana, wakfu wa Motsepe uliahidi kutoa randi dola bilioni 1 kusaidia kukabiliana na janga la virusi vya corona Afrika Kusini. Wakati ambapo kila kitu anachoshika Motsepe kinaonekana kubadilika na kuwa dhahabu, amekuwa akilengwa na baadhi ya vyama vya kisiasa ambavyo vinasema kwamba nguvu kubwa iliyo na familia yake inawafanya kupata upendeleo fulani. Lakini amekuwa akikanusha madai hayo na kusema kwamba utajiri wake umepatikana kwa njia halali. Ijumaa, Patrice Motsepe atakuwa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) wakati ambapo raia huyo wa Afrika Kusini atakuwa bila mpinzani kwenye uchaguzi utakaofanyika Morocco. text: Sheria mpya ya udhibiti uzito ya Jumuia ya Afrika Mashariki imelalamikiwa kuikosesha mapato waendesha malori Tanzania Sheria ya udhibiti wa uzito wa magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni zake za mwaka 2017 ilianza kutumika rasmi mwaka huu, huku wadau wakitakiwa kutii sheria hiyo ili kuepuka adhabu kali zinazoweza kutolewa. Sheria inasemaje? Sheria mpya inaeleza kuwa ukomo wa mtaimbo(Axle) wenye matairi mapana utakuwa tani 8.5 badala ya tani 10 za awali. Kuwepo kwa mfumo wa kuweka kumbukumbu za makosa ya msafirishaji na anayezidisha uzito ambao hatimaye unaweza kusababisha gari kufungiwa kufanya usafirishaji kwa muda au moja kwa moja. Adhabu ya malipo ya faini kwa makosa ya usafirishaji hadi dola za Marekani 15,000 au kifungo kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja. Adhabu hizo zinahusu pia watumishi wa mizani wanaoshiriki njama na wasafirishaji ili kukwepa kulipa tozo ya kuzidisha uzito . Gharama za utunzaji gari iliyokuwa na makosa katika maeneo ya mizani baada ya siku tatu ni dola za Marekani 50 kwa siku badala ya dola za Marekani 20 kwa siku kwenye sheria hii mpya. Makamu mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa malori nchini Tanzania, Elias Lukumay amezungumza na BBC, amesema hali ni ngumu mno kwa wafanyabiashara kutokana na sheria hii Nchi wanachama wa SADC kwa kiasi kikubwa hutegemea Bandari ya Dar es Salaam '' Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 70 inategemea nchi za SADC, lakini kwa sasa sheria itatuumiza kwenye soko.'' Tanzania yapoteza matrilioni ya pesa za madini Jeshi la Tanzania limeanza rasmi operesheni ya kuratibu ununuzi wa korosho Kuhusu sababu za kuwa sheria hii kulenga kulinda miundombinu yake ya barabara Lukumay anaona kwamba Serikali za Afrika Mashariki zinapaswa kuchukua hatua ya kuboresha miundombinu ya barabara ambazo nyingi ziliengwa miongo mingi iliyopita. ''Barabara zetu zilijengwa takriban miaka 30 iliyopita ,na barabara hizi wakati zinajengwa zilijengwa kwa makadirio ya kupita magari 10000 kwa wiki , lakini sasa hupita magari takriban 60000 kwa wiki, hivyo matumizi ya barabara yameongezeka. Na kwa miaka yote Bandari ya Dar imekuwa ikitegemea barabara katika usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini.'' ''Wadau waelewe athari za sheria, wenzetu wa Zambia na wa Congo wameanza kuleta mgomo kutumia Bandari ya Dar es Salaam kwa sababu mtu hawezi kutumia gharama zilezile za usafirishaji kwa mzigo mdogo.Magari ya Tanzania yanayokwenda Congo hunyimwa mzigo wakati wa kurudi.'' Kiongozi huyu wa waendesha malori anatoa ombi kuwa Tanzania itazame upya sheria hii waahirishe matumizi yake ili kwanza ufanyike mchakato wa kushawishi nchi za SADC ambazo ni watumiaji wakubwa wa barabara za Tanzania katika kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam watumie sheria hii pia. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe anaona kuna athari kadha wa kadha iwapo sheria hii ya udhibiti uzito wa magari itaendelea kutumika, anasema Tanzania itapoteza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa nchi za SADC zinazotegemea Bandari ya Dar es Salaam. ''Kama malori kutoka Zambia kwa mfano ikiwa hayatafika Tanzania kuchukua mafuta, Tanzania itapata hasara iwapo itatekeleza sheria hii na hasara hii ikiwa ni ukosefu wa ajira kwa watanzania wanaoendesha malori, mabenki yatapata hasara kwasababu wawekezaji wamenunua magari ambayo hayaendi sambamba na sheria hii mpya'' ''Tanzania imepoteza heshima yake kwenye jumuia za kimataifa, Tanzania ingetumia diplomasia yake kushawishi nchi za SADC kuwa na sheria hiyo hiyo ya nchi za Afrika Mashariki na kwa maana hiyo Dar es Salaam ingeendelea kuwa bandari chaguo kwa nchi za Zambia,Malawi na Congo.''Alimalizia Zitto. Wamiliki wa malori nchini Tanzania wamelalamika kuhusu sheria ya udhibiti wa uzito wa magari ya Jumuia ya Afrika Mashariki wakisema kuwa sheria hii inawagharimu kwenye soko text: Mchoro: Kutua kwenye sayari ya Mars lilitarajiwa kuwa jambo ngumu Hii ni baada ya mawasiliano na chombo hicho kukatika. Wataalamu wanasema mawasiliano na roboti iliyo kwenye chombo hicho cha Schiaparelli yalikatika chini ya dakika moja kabla ya wakati ambao chombo hicho kilitarajiwa kutua katika sayari hiyo. Setilaiti zinazoizunguka sayari ya Mars zimejaribu kufanya uchunguzi kubaini hatima ya chombo hicho kilichojaribu kutua, bila mafanikio. Chombo hicho kilikuwa na muda wa chini ya dakika sita kupunguza kasi yake ya kilomita 21,000 kwa saa kiasi cha kukiwezesha kutua salama kwenye sayari hiyo. Moja ya setilaiti za Marekani zilijaribu kuwasiliana na Schiaparelli lakini hakuna majibu yaliyopatikana. Kuna wasiwasi kwamba roboti hiyo ilianguka vibaya kwenye sayari hiyo na kuharibika. Shirika la Anga za Juu la Ulaya hata hivyo bado linasema ni mapema sana na linaendelea kuwa na matumaini. Wahandisi na wataalamu wengine watajaribu kufanya uchunguzi, sana kwenye mifumo yao ya kompyuta, kubaini ni kwa nini mawasiliano yalikatika na kisha wajaribu kuyarejesha. Shughuli hii yote inaweza kuchukua siku kadha. Baadhi ya maelezo muhimu yatatoka kwa chombo mama kilichokuwa kimebeba chombo cha Schiaparelli, ambacho kwa Kiingereza kinaitwa Trace Gas Orbiter (TGO). Chombo cha Schiaparelli kilichokuwa kinaenda kutua, chombo cha TGO kilikuwa kinajiweka sawa katika anga ya Mars. Lakini bado kulikuwa na mawasiliano kati yake na Schiaparelli. Mawasiliano hayo yanaweza kutoa maelezo muhimu kuhusu yaliyojiri chombo hicho kilipojaribu kutua. Wataalamu wa ESA wakishirikiana na wale waliounda Schiaparelli walitathmini data usiku kucha. Mchoro wa roboti ya Schiaparelli Mkuu wa wataalamu waliosimamia mradi huo Paolo Ferri aliambia wanahabari Darmstadt, Ujerumani kwamba: "Watu watakesha wakitathmini data. Nina imani maelezo haya yatatueleza ni nini kilikwama wakati wa kutua na kukatiza mawasiliano. Tutafahamu vyema kesho iwapo chombo hicho kimetoweka kabisa au kama kuna juhudi tunaweza kufanya kufufua mawasiliano." Jaribio la awali la ESA kupeleka chombo katika sayari hiyo lilifanyika mwaka 2003, kwa kutumia chombo cha Uingereza cha Beagle-2. Chombo hicho kilifanikiwa kutua salama lakini kikashindwa kufungua mitambo yake ya kawi ya jua vyema na hivyo mawasiliano yakakatika. Kuchunguza dalili za uhai Chombo Schiaparelli, ambacho kilipaa kutoka duniani mwezi Machi, kilitarajiwa kufanya uchunguzi kubaini iwapo gesi ya Methane ambayo imepatikana katika anga ya sayari hiyo inatokana na shughuli ya kijiolojia au inatokana na viumbe hai. Mambo yote yakienda ilivyopangwa, wataalamu wanapanga baadaye kurusha mtambo wa kusafiri juu ya sayari, kwa kimombo rover, ambao utatumiwa kuchimba chini ya ardhi ya Mars. Mtambo huo, utaunganishiwa nchini Uingereza, unaweza kurushwa mwaka 2018 au ukichelewa mwaka 2020. Uchunguzi wa awali wa setilaiti zinazozunguka dunia na rover ya Curiosity ya Marekani umebaini kuwepo kwa haidrokaboni ingawa za vipimo vya chini sana katika sayari hiyo. Moja ya mambo yanayoweza kuwa yanachangia kuwepo kwa gesi hizo ni shughuli za kijiolojia ndani ya sayari hiyo ambapo maji yanaweza kuwa yanachanganyikana na mawe na kuzalisha gesi ya haidrojeni ambayo baadaye inageuka na kuwa methane. Jambo jingine linaloweza kuwa linasababisha kuwepo kwa gesi hiyo ni kuwepo kwa viumbe hai. Sehemu kubwa ya gesi ya methane duniani hutokana na viumbe hai. Wasiwasi umezidi kuhusu hatiamya chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikuwa safarini kwenda sayari ya Mars, na ambacho kilitarajiwa kutua kwenye sayari hiyo Jumatano. text: Katika mahojiano maalumu na BBC, bwana Ren Zhengfei ameelezea kukamatwa kwa binti yake Meng Wanzhou mwezi Disemba, ambaye ndiye mhasibu mkuu wa kampuni hiyo ni hatua ya kisiasa zaidi. Marekani imeazimia kumfungulia mashtaka bi Meng na kampuni ya Huawei kwa tuhuma za kutakatisha fedha, ubadhirifu wa kibenki na kuiba siri za kibiashara. Kampuni ya Huawei hata hivyo inakanusha madai hayo. "Hakuna namna Marekani inaweza kutuvunja," amesema kwa mara ya kwanza toka mzozo huo uanze. "Dunia haiwezi kututupa kwa sababu tumepiga hatua kubwa. Hata kama watawashawishi baadhi ya mataifa kuwa wasitutumie kwa muda, pia tunaweza kupunguza uzalishaji kidogo." Hata hivyo ameonesha wasi wasi wake kuwa endapo hatua hiyo itatokea basi itakuwa na athari. Je Huawei ni kibaraka wa China? Meng Wanzhou alikamatwa Canada na kupelekwa Marekani Huawei, ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya binafsi China imekuwa ikihusishwa na kutumika na serikali ya China. Marekani na baadhi ya washirika wake wamekuwa wakidai kuwa teknolojia ya Huawei inatumika na mashirika ya ulinzi ya China kuwapeleleza. Kwa mujibu wa sheria ya China, makampuni ya nchi hiyo yanalazimika "kuisaidia serikali katika shughuli za upelelezi wa Taiafa." Hata hivyo Ren amesema kukubali kufanya upelelezi ni hatari ambayo asingeweza kuifanya. "Serikali ya China imeliweka wazi suala hili kuwa haiwezi kufanya jambo hilo. Hatuwezi kufanya kuwakera wateja wetu duniani kote kwa ajili ya kitu kama hiki. Kampuni yetu haiwezi kufanya shuguli za kiupelelezi." Kutengwa na Dunia Wiki iliyopita, waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo ameonya kuwa washirika wake kutumia teknolojia ya kampuni ya Huawei na kudai kuwa itafanya kuwe na shida kwa Marekani kushirikiana nao. Australia, New Zealand na Marekani tayari wameshapiga marufuku ama kuzuia kampuni ya Huawei kusambaza mitambo kwa ajili ya miradi yake ya baadae ya mfumo wa mawasiliano ya intaneti ya simu ya 5G. Huawei imesema hawahatarishi usalama wa nchi yeyote ikiwemo Marekani Wakati huo huo Canada inafanya tathmini kuona iwapo kampuni hiyo ni tishio kwa usalama wake. "Kama taa zitazimwa Magharibi, Mashariki kutaendelea kung'aa. Na kama Kaskazini kutaingia kiza, bado Kusini kupo. Marekani haiwakilishi dunia. Marekani ni sehemu tu ya dunia." Kitengo cha Usalama wa Kimtandao wa Uingereza kimesema kuwa hatari yeyote itakayotokana na kutumia teknolojia ya Huawei inaweza kudhibitiwa. Makampuni mengi ya mawasiliano ya Uingereza wanaitumia Huawei katika maandalizi yao ya kuhamia katika mfumo wa 5G. H Hata hivyo, tathmini rasmi ya serikali inatarajiwa kutolewa mwezi Machi ama Aprili na itawapa muongozo iwapo waendelee kutumia Huawei ama la. Akizungumzia uwezekeno wa kupigwa marufuku Uingereza Bw Ren amesema: "hatutajiondoa nchini Uingereza kutokana na hili. Zaidi tutaongeza uwekezaji wetu maana bado tunaimani na Uingereza na tunaamini Uingereza itaendelea kutuamini zaidi. Na kama Marekani hawatuamini basi tutawekeza Uingereza kwa nguvu kubwa zaidi." Mwanzilishi wa kampuni ya simu ya Huawei amesema hakuna "njia yeyote ambayo Marekani inaweza kuivunja" kampuni hiyo. text: Msemaji wa zamani wa Robert Mugabe amesema kiongozi huyo wa zamani alitaka kuondoka madarakani kwa masharti yake Wakati wa wiki ya mwisho madarakani, Bw Mugabe alikuwa amewekwa kwenye kizuizi kwake nyumbani baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa serikali. Baadaye aliondolewa kikamilifu kutoka madarakani. "Nilianza kufikiria picha sawa na za Muammar Gaddafi," George Charamba, ambaye ni msemaji wa zamani wa Bw Mugabe amesema. Alikuwa anazungumza na tovuti ya kibinafsi nchini Zimbabwe ya Daily News. Huku akikumbuka siku za mwisho za utawala wa Mugabe wa miaka 37, Charamba anasema kiongozi huyo wa miaka 93 alitaka kuondoka madarakani "kwa masharti yake" na kwamba alikuwa ametahadharishwa kuhusu hatari iliyokuwepo baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa nchi na maandamano kuzuka. Mugabe alipokuwa anazuiliwa katika makao yake ya kifahari ya Blue Roof mazungumzo kuhusu mustakabali wake yalikuwa yanafanyika kati ya majenerali, makasisi wa kanisa Katoliki, wasaidizi wake wa kisiasa na wajumbe kutoka Afrika Kusini. Bw Charamba anasema maafisa wa jeshi waliwafahamisha kwamba maelfu ya waandamanaji waliokuwa wanamtaka Mugabe angejiuzulu, kulikuwa na uwezekano, wangetaka kumfikia Mugabe binafsi. "Ingewezekana kwa sababu wanajeshi hao walitwambia 'hatuwezi kuwafyatulia risasi raia ambao wanaandamana dhidi ya rais na kummwaga damu," Charamba amenukuliwa na tovuti ya Daily News. Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi alikamatwa na kisha kuuawa mwaka 2011 baada ya maandamano na maasi ambayo yalifikisha kikomo utawala wake wa miongo minne. Msemaji wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema alikuwa na wasiwasi kwamba raia nchini humo "wangemburura na kumuua" kiongozi huyo kama ilivyotokea nchini Libya. text: Wakaazi wa maeneo ya vijijini Rwanda wamechangamkia kutumia nishati ya umeme inayotokana na miale ya jua Katika kile kinachoelezwa kuwa mapinduzi ya nishati ya umeme, wananchi hasa wa maeneo ya vijijini wamechangamkia kutumia nishati ya umeme inayotokana na miale ya jua. Waanzilishi wa mradi huo wanasema nishati hiyo ni rahisi kwa matumizi, gharama ndogo na hifadhi kwa mazingira. Kenyatta na Trump wataangazia nini White House? Bobi Wine aachiliwa huru kwa dhamana Uganda Ufugaji wa nyuki watunza msitu Zanzibar Katika soko la Kabarondo mashariki mwa Rwanda, wananchi wanajiandikisha kwa wingi kununua vifaa na mitambo ya umeme unaotumia miale ya jua. Malipo pia ni papo hapo kwa njia ya simu inayofahamika kama mobile money. Bwana Ndoramaherezo Pierre amelipia huduma hiyo na anaandamana na fundi wa kusimika vifaa na mitambo ya miale ya jua. Baada ya kumwekea mitambo hiyo sawa sawa, tayari anaanza kutizama runinga. ''Ni furaha ya kupita kiasi kupata vifaa hivi vya umeme.ndoto yangu imetimia.Hii ni hatua kubwa katika maisha yangu na mapinduzi katika kijiji kizima.awali tulikuwa gizani,tukitegemea taa la petrol,sasa naweza kusikiza redio,kuchaji simu yangu lakini hasa kuangalia runinga nakuona dunia nzima maisha yanavyotembea.Kadhalika nataraji kuwa na wageni kwa sababu nina uhakika wanakijiji kila siku watafurika hapa kutizama runinga'' Malipo yanategemea umechukua vifaa gani, mfano daraja la juu kabisa la furushi lenye taa zaidi ya 3 ,runinga na redio linalipiwa franga elfu 14 kama dolla 15 hivi kwa mwezi hadi kipindi cha miaka 3. Katika chumba kimoja wahudumu wanaweza kufwatilia wateja wao popote walipo vijijini na kuzungumza nao mara kwa mara kujua ikiwa wanayo matatizo yanayohitaji mafundi. Mradi huu unaendeshwa na kampuni ya Uingereza ya BBOXX kwa ushirikiano na serikali ya Rwanda. Mahakama yamkuta na kesi ya kujibu kiongozi wa wanafunzi Tanzania Mwakilishi wa kampuni hiyo Bi Monica Keza ameiambia BBC kuwa ni mapinduzi makubwa katika sekta ya nishati ya umeme. Kinachohitajika ni vifaa maalum na wataalamu wa kusimika vifaa hivyo. ''Kuna mabadiliko makubwa kwa sasa,nishati ya umeme tunayozoea lazima utumie vifaa na mitambo kadha wa kadha ili kufanya msimiko nyumbani kwako.Nishati ya miale ya jua haihitaji mambo yote hayo.ni teknolojia ya kisasa ninayoweza kulinganisha na matumizi ya simu za nyumbani za zamani na simu za mkononi za sasa.Teknolojia yetu hii inaendeshwa toka mbali''. Matumizi ya nishati mbadala yanaweza kunusuru uharibifu wa mazingira Tanzania Mwanafunzi aunda gari linalotumia nishati ya jua Kenya Nimeambiwa kwamba mtambo wao unaweza kuhifadhi miale ya jua na hata katika kipindi cha mvua kwa siku kadhaa. Faida za kutumia nishati ya jua: Rwanda imekuwa ikijaribu kutatua tatizo la nishati ya umeme kwa kutumia njia mbali mbali. text: Rais Donald Trump akiwa ameishika karatasi iliyoandikwa makubaliano yake na Mexico Alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akisema kuwa, makubaliano hayo yalikua ''siri''. Lakini alisema hayo huku akiionyesha karatasi ambayo ilikua na maandishi kuhusu makubaliano hayo -ambayo yalipigwa picha na wana habari. Rais Trump amefaya suala la mpaka kati ya Marekani na Mexico kuwa sehemu kubwa ya kampeni yake kwenye makubaliano hayo akitishia kuwekea ushuru Mexico. Trump atishia kufunga mpaka kati ya Marekani na Mexico Marekani yatoa dola $1b kujenga ukuta kati yake na Mexico Kwenye karatasi hiyo kulisomeka maneno kuwa Mexico iliridhia muda uliowekwa kuhakikisha kuwa inafanikiwa kupambana na suala la wahamiaji. Ikiwa Marekani itajihakikishia kuwa hatua zilizochukuliwa ''hazikuzaa matunda'', Mexico italazimika kuchukua hatua kali zaidi za kisheria kushughulikia suala la uhamiaji. Mexico imesema nini kuhusu makubaliano hayo? Waziri wa mambo ya nje wa Mexico, Marcelo Ebrard imethibitisha kuwa Mexico ilikuwa na siku 45 kuonyesha kuwa ina uwezo wa kudhibiti wahamiaji wanaoingia Marekani kwa kuimarisha usalama katika mpaka wake wa kusini. Kwa sasa imepeleka askari 6,000 katika mpaka wake na Guatemala. ''Unapokenda kusini, jambo la kwanza kujiuliza ni: 'mpaka uko wapi?' Hakuna kitu, ''alisema siku ya Jumanne. ''Mpango ni kufanya mpaka wa kusini uwe kama wa kaskazini haraka iwezekanavyo.'' Ikiwa mpango huu hautafanikiwa,waziri wa mambo ya nje amesema, Mexico ilikubali kuwa nchi ya tatu itakayolazimu wanaotafuta hifadhi Marekani kwanza kuomba hifadhi Mexico, mpango ambao Marekani ilipendekeza lakini ulikataliwa vikali na Mexico. Wahamiaji kutoka Honduras wakijaribu kuvuka mto wa Rio Bravo ili kwenda kuomba hifadhi El Paso,Texas Ikiwa Mexico itashindwa kushughulikia suala la uhamiaji katika kipindi cha siku 45, nchi nyingine zitahusishwa kwenye sakata hilo. Mazungumzo yatahusisha pia Brazil,Panama na Guatemala- nchi ambazo kwa sasa hutumiwa kama vituo vya kupitishia wahamiaji.Nchi hizo ambao watagawana jukumu la kushughulikia madai ya watu wanaotafuta hifadhi. Bwana Ebrard pia amesema wapatinishi wa Marekani walitaka Mexico ikomeshe kabisa wahamiaji kuvuka lakini ''mpango huo haukuwezekana''. Rais wa Marekani,Donald Trump kwa bahati mbaya ameweka wazi sehemu ya waraka wa makubaliano kati ya Marekani na Mexico kuhusu uhamiaji. text: Kimbunga Idai kinatarajiwa kuikumba Msumbiji Tufani iliyopewa jina la Idai, ambayo inabeba upepo wenye kasi ya kilomita 225 kwa saa itasababisha kimbunga kikali karibu na bandari ya Beira, mji wenye watu wapatao laki tano. Mvua kubwa iliyonyesha nchini humo tayari imesababisha vifo vya watu 100 nchini Msumbiji na Malawi. Beira ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Msumbiji ambapo bandari yake iko katika mdomo wa mto Pungwe ambao umekwenda mpaka Zimbabwe. Kitengo cha hali ya hewa cha Ufaransa ambacho kinashughulikia maeneo yanayodhibitiwa na Ufaransa katika eneo la Bahari ya Hindi kimeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya kutokana na maji kujaa mengi. Baadhi ya picha zilizotumwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha madhara katika mji huo wa Beira wakati kimbunga hicho kikikaribia kwa miti mingi kuanza kung'oka. Miti iking'oka Msumbiji imekumbwa na vimbunga vingi katika siku za nyuma ikiwemo kimbunga Eline mwaka 2000 kilichoua watu 350 na wengine 650,000 kuyakimbia makazi yao. Na mji wa Beira ndio mara kwa mara unakumbwa na hali hiyo. Msumbiji ni nchi ambayo iko katika hatari ya kuathiriwa zaidi barani Afrika pale hali mbaya ya hewa inapotokea Watu wanaoishi katika mji mkuu wa Msumbiji Maputo wameonywa kutokea kwa hali mbaya zaidi kutokana na kimbunga kikali. text: David Charo alikuwa akipiga mswaki alipoumeza kimakosa Jumapili wiki iliyopita apokuwa anajiandaa kwenda kazini Bamba, Kilifi. Kufikia jana, alikuwa ameanza kupata matatizo ya kupumua. Awali, madaktari walikuwa wamedokeza kwamba angehitaji kufanyiwa upasuaji kuutoa. Lakini Ijumaa asubuhi, madaktari wakiondozwa na Ramadhan Omar wamefanikiwa kuutoa mswaki huo bila kumfanyia upasuaji wa kawaida. Badala yake, wamemfanyia upasuaji wa kutumia matundu madogo. Jumapili, Charo alipokuwa alipoumeza mswaki huo kimakosa, awali ulikwama ndani ya koo kabla ya kutumbukia ndani tumboni. Juhudi za nduguye mdogo Julius Charo za kuutoa hazikufanikiwa na ikalazimu wamkimbize hospitali iliyokuwa karibu. "Tulipompeleka kwenye hospitali hiyo, madaktari walitushauri kumleta katika hospitali hii ya Pwani ambapo alipigwa picha ya x-ray, lakini kwa muda hakufanyiwa matibabu yoyote," Bw Julius aliambia gazeti la Nation. Sima ambayo Charo alikuwa ameila usiku wa kuamkia Jumapili kilikuwa ndicho chakula chake cha mwisho mango kwake kufanikiwa kula. Amekuwa akitegemea vinywaji pekee. "Ninaweza tu kulala au kusimama. Siwezi kujikunja au kuinama. Ninapojaribu kujipinda, nausikia mswaki ukinibana," alisema awali alipokuwa anahojiwa na gazeti la Nation. Mswaki huo ulikuwa umekwama tumboni Akizungumza na gazeti la kibinafsi la Star awali, Bw Charo alikuwa amesema amekuwa akiutumia mswaki huo kupiga mswaki kwa miaka 20. "Ni makosa tu kwamba uliteleza kutoka mikononi mwangu Jumapili. Lakini hali yangu ni nzuri," alisema. Madaktari katika Hospitali Kuu ya Mkoa ya Pwani (CPGH) mjini Mombasa, Kenya wamefanikiwa kuutoa mswaki ambao ulikuwa umekwama tumboni mwa mwanamume mmoja kwa siku sita. text: Kaburi hilo limechimbwa chini umbali wa mita 12 hivi, na juu yake kujengwa jumba kubwa la ghorofa Dkt Anthony Mwandulami mkaazi wa Njombe nyanda za juu Kusini mwa Tanzania ameshaanza kujijengea kaburi lake tayari. Mwandulami ambaye pia ni mganga wa tiba asilia, anasema kaburi hilo ambalo amekuwa akilijenga kwa takriban miaka minane sasa. Alimwambia mwandishi wa BBC David Nkya kwamba sababu kuu inayomfanya kujijengea kaburi hilo ni kuihifadhi historia yake baada ya kifo. Kaburi hili si tu limeleta mshangao kwa wakazi wa eneo la Njombe, lakini pia linawashtua wengi nchini kote. Anthony Mwandulami: Mwanamume anayejiandalia kaburi lake Tanzania Lina urefu wa mita kumi na mbili kwenda chini na limejengwa kwa mfumo wa jengo la ghorofa. Haya ndio makazi ya kudumu ya Antony Mwandulami baada ya kufa. Lakini Waafrika wengi hawana tabia ya kufikiria watazikwa wapi ukiachilia mbali kujijengea makaburi wangali wako hai, kulikoni kwa Mwandulami? "Kaburi hili nimeamua kulijenga, nimeona si vizuri sana kutokana na shughuli zangu nilizozifanya hapa Tanzania na nilivyowasaidia Watanzania, halafu nikapotea tu. Na wakati huo huo nimeona nina uwezo wa kujitengenezea sehemu ya kuhifadhi mwili wangu. Nikaona bora nitengeneze. Kaburi hili nimeliandaa kwa ajili ya kupumzisha mimi na wake zangu," anasema. "Ni muhimu sana kwa sababu siwezi kusahaulika na wajukuu zangu pamoja na watakaozaliwa na familia yangu watakuja kujua kwamba huyu ni nani na alifanya nini kwenye familia yetu. Mwandulami anasema ndani ya kaburi hili, atazikwa yeye pamoja na wake zake watatu. Haya ni makubaliano ambayo wamejiwekea tayari na wake zake. Mke wake mkubwa juu ya suala hili? "Mimi naona ni vizuri amefanya jambo la maana sana, kutengeneza makao yake. Tumelipokea vizuri, tumefurahi. Kwa sababu ameshatengeneza sehemu nzuri anapolala yeye na sisi wake zake tunalala hapo hapo," anasema mkewe kwa jina Damian. Amechimba chini mita 12 na chini kabisa ndiko kunakopatikana makaburi yenyewe. Mwili wake utakaushwa kabla ya kuhifadhiwa, anasema. Utamaduni wa kujijengea kaburi kama hili kabla hujafa ni kitu kigeni kabisa hapa. Lakini kwa mujibu wa Mwandulami, kaburi lake hili linatarajia kugharimu takriban dola 500,000 ambazo ni sawa na Sh1 bilioni mpaka kukamilika kwake. Na kwa viwango vya chini vya maisha kijijini humo, fedha anazotumia ni nyingi sana. Wanakijiji wenzake wameshangazwa na hatua hiyo. Ujenzi bado unaendelea. Licha ya maandalizi haya yote, swali ambalo huenda hata wewe unajiuliza, je ni nini hatma ya ujenzi hasa iwapo kifo chake kitasababisha mwili wake usionekane? Unaweza kusoma pia: Umewahi kujiuliza utazikwa wapi baada ya kufa? Mwanamume mmoja nchini Tanzania ameamua hataki utata kuhusu hatima yake baada ya kufa. text: Rais Donald Trump aonya kujiondoa katika mazungumzo na Kim Jong Un Katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, yeye na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe walisema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti iendelee kwa kukataa kusitisha utengezaji wa silaha za nyuklia. Bwana Abe yuko katika mgahawa wa rais Trump wa Mar-a-Lago resort mjini Florida kwa ,mazungumzo. Mapema , bwana Trump alithibitisha kwamba mkurugenzi wa CIA Mike Pompeo alifanya ziara ya kisiri hadi Korea Kaskazini ili kukutana na Kim Jong Un. Alisema kuwa bwana Pompeo aliweka uhusiano mzuri na bwana Kim ambaye bwana Trump alimuita 'mtu mdogo' na kwamba mkutano wao ulifanyika vizuri. Ziara hiyo iliadhimisha mawasiliano ya juu kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000. Mkutano huo kati ya Trump na bwana Kim unatarajiwa kufanyika kufikia mwezi Juni. Maelezo ikiwemo eneo litakaloandaa mkutano huo bado yanaendelea kufanyiwa kazi. Ni nini kilichosemwa kuhusu mkutano huo? Rais Trump alisema katika mkutano wa pamoja kwamba iwapo anadhani kwamba mkutano huo hautafanikiwa basi hatoshiriki na kwamba iwapo mkutano huo umefanyika na haoni matunda yake basi atasimama na kuondoka. ''Kampeni yetu ya shinikizo itaendelea hadi pale Korea Kaskazini itakapositisha utengezaji wa silaha za Kinyuklia'', aliongezea. Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Donald Trump "Kama nilivyosema awali nyota ya Korea Kaskazini itang'aa wakati taifa hilo litakaposimamisha mpango wake wa kinyuklia .Itakuwa siku kuu kwao na itakuwa siku kuu ulimwenguni." Ni Nini chengine kilichozungumziwa? Kuhusu biashara, viongozi hao wawili walikubaliana kuanza mazungumzo kuhusu biashara huru na isiopendelea upande wowote. Bwana Trump alisema kuwa Marekani itaendelea kupinga hatua ya kujiunga na biashara ya ushirikiano ya Trans Pacific Partnership hadi pale Japan na washirika wengine watakapoweka makubaliano ambayo Marekani haiwezi kukataa. Marekani hatahivyo haikuiondoa Japan katika kuitoza kodi ya vyuma na alminium kama alivyowafanyia washirika wengine wa Marekani. Akizungumzia kuhusu Korea Kaskazini Bwana Abe alisema kwamba amemtaka rais Trump kusaidia kuwachiliwa huru kwa raia wa Japan waliotekwa nyara na Korea Kaskazini miaka ya 1970 na 1980. Korea Kaskazini imekiri kuwateka nyara raia 13 wa Japan ili kuwatumia kuwafunza wapelelezi wake kuhusu forodha ya Japan. Japan inaamini takwimu hizo ziko juu. Swala hilo limeathiri pakubwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili kwa miongo kadhaa. Raia watatu wa Marekani pia wanazuiliwa nchini Korea Kaskazini. Bwana Trump anasema kuwa Marekani itatumia kila njia ili kuhakikisha kuwa raia wa taifa hilo waliotekwa nyara na Japan wanarudishwa nyumbani. Je Mkutano huo utafanyika wapi? Picha zinazoeoonyesha maeneo ambayo mkutanoa huo unaweza kufanyika Rais wa Marekani Donald Trump anasema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un hayazai matunda 'atainuka na kuondoka katika mazungumzo hayo'. text: Uamuzi huo uliopitishwa na mahakama ya kutatua mzozo katika michezo Switzerland, unazima matumaini kwa mwanariadha huyo kurudi mchezoni katika miaka ya hivi karibuni. Mshindi huyo wa mara tatu wa mbio za Boston marathon alishindwa katika rufaa aliyokata kupinga kuongezwa muda wa miaka hiyo miwili uliokuwa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu. Wito wa kuongeza marufuku hiyo ulitolewa katika kesi dhidi yake na shirikisho la kimataifa la riadha IAAF. Rita Jeptoo alipatikana na hatia ya kutumia dawa hizo za kusisimua misuli na shirikisho la riadha Kenya katika uchunguzi aliyofanyiwa mnamo 2014: alipatikana kutumia dawa ya kushinikiza damu EPO. Matokeo yake katika mashindano tangu Aprili mwaka huu yamefutiliwa mbali, ikiwemo ushindi wake katika mashindano ya Boston na Chicago marathon alikoibuka nambari moja. Mwanariadha wa Kenya, Rita Jeptoo ameongezea marufuku ya miaka miwili ya zaidi kutoshiriki mchezo huo kutokana na tuhuma za kutumia dawa za kusisimua misuli. text: Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na mbili na robo asubuhi. Basi hilo la abiria ambalo linamilikiwa na kampuni ya Prince hamida linadaiwa kugongana na treni lilipokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora. Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini. Rais wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kuwtaaka „wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi." "Vyombo husika, chukueni hatua kali kwa wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani," amesema. Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema eneo ilipotokea ajali hiyo hutokea ajali za aina hiyo mara kwa mara. "Nimezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) na tumekubaliana kuwa tuweke kizuizi ( barrier ) Katika eneo hili ambapo reli ikatiza barabara," amesema. „ Hii itasaidia sana kupunguza ajali za namna hii. Mkurugenzi wa TRC Bwana Masanja Kadogosa amekubali ushauri huu ambao Wananchi wengi wa Kigoma Mjini wamekuwa wakiutoa." Watu 10 wamefariki katika ajali iliyotokea baada ya basi la abiria lililogongana na treni eneo la Gungu katika manispaa ya Kigoma Ujiji, kaskazini magharibi mwa Tanzania. text: Alikuwa amekula kiapo kuwa 'Rais wa Kenya' au 'Rais wa Wananchi nchini Kenya'? Muda haukupita kabla ya utata huo kujitokeza katika maelezo kuhusu ukurasa wake wa Twitter @RailaOdinga. Awali, ukurasa huo ulikuwa na maelezo kwamba yeye ni kiongozi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa). Muda mfupi baada yake kukamilisha kula kiapo, maelezo yalibadilishwa na akawa 'Rais wa Jamhuri ya Kenya.' Hapo ndipo utata ulipoanza, kwani Rais Uhuru Kenyatta hujitambulisha pia kama Rais wa Jamhuri ya Kenya. Muda baadaye, alibadilisha na kuwa kiongozi wa Nasa. Baadaye usiku, alibadilika na kuwa "Aliyeapishwa kuwa Rais wa Wananchi mnamo 30/1/2018'. Asubuhi aliondoa maelezo na akabaki tu kuwa 'Mheshimiwa Raila Amolo Odinga'. Wakenya mtandaoni waligundua hilo: Sheria za Twitter huharamisha "kujionesha kuwa mtu mwingine kwa njia ya kukanganya au kuhadaa" na ukurasa kama huo unaweza kufungwa kabisa. "Haufai kujifanya kuwa mtu mwingine, kundi au shirika kwa njia ambayo inanuiwa au inapotosha, kukanganya, au kuwahadaa wengine," zinasema sheria za Twitter. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga alipokuwa kiapo kuwa rais wa wananchi jijini Nairobi Jumanne, mjadala ulizuka kuhusu wadhifa wake. text: Mahujaji zaidi ya 1.7 milioni kutoka nchi mbalimbali wamesafiri kwenda Mecca kwa Hajj Walianza machweo Jumatano kwa kuzunguka Kaaba katika Msikiti Mkuu wa Mecca, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiislamu. Raia wa Iran kwa mara nyingine wanashiriki baada ya kukosa Hajj ya mwaka mmoja kutokana na mkanyagano uliotokea mwaka 2015. Kulikuwa na taarifa za kukinzana kuhusu idadi kamili ya mahujaji wanaohudhuria kutoka taifa jirani la Qatar, ambalo limekuwa kwenye mzozo mkali na Saudi Arabia. Kamati ya Taifa ya Haki za Binadamu, ambayo inafadhiliwa na serikali ya Qatar, imesema ni raia wachache sana wa Qatar ambao wamevuka mpaka, ambao ulifunguliwa wiki mbili zilizopita na serikali ya Saudia kuwawezesha Waislamu kuhiji. Lakini gavana wa Mecca amesema raia 1,564 wa Qatar wanashiriki ibada hiyo ya Hajj, idadi ambayo imeongezeka ukilinganisha na 1,210 mwaka jana. Kwa Waislamu, Hajj ndiyo nguzo ya tano na ya mwisho ya dini ya Kiislamu. Ni ibada ambayo Mwislamu yeyote aliyekomaa anashauriwa kutimiza angalau mara moja maishani mwake iwapo anaweza kulipia gharama na ana nguvu za kimwili kuweza kutimiza abada hiyo. Mahujaji wakipanda Mlima Arafat, 20km (maili 12) mashariki mwa Mecca Jumatano Serikali ya Saudia imesema imechukua tahadhari kuzuia kutokea tena kwa mkanyagano sawa na uliotokea miaka miwili iliyopita. Maafisa wa Saudia wanasema mahujaji karibu 800 walifariki wakati wa mkanyagano huo, lakini takwimu zisizo rasmi zinasema watu zaidi ya 2,400 walifariki. Iran pekee ilikuwa na raia 464 waliofariki na baada ya hapo iliwatuhumu maafisa wa Saudia ikisema wanafaa kulaumiwa kwa vifo vilivyotokea. Maafisa wa Saudia walikanusha tuhuma hizo. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Saudia Meja Jenerali Mansour al-Turki amesema maafisa wa usalama zaidi ya 100,000 wametumwa katika maeneo mbalimbali ya Mecca na Medina kulinda na kuwaelekeza mahujaji. Aidha, kuna kamera nyingi sana za usalama. Mahujaji karibu milioni mbili kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili Saudi Arabia kwa ibada ya Hajj ambayo hufanyika kila mwaka. text: Kijiji kizima kuwajibishwa kwa uharibifu wa miundo mbinu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila aliamuru polisi mkoani humo wakamate wakazi wote wa kijiji hicho siku ya Jumatano, Agosti 15. Wakaazi wa kijiji hicho wanashutumiwa kuharibu miundombinu ya maji yenye thamani ya dola elfu ishirini katika kijiji jirani cha Masheye ambacho kipo katika mkoa huohuo wa Mbeya. Kijiji cha Ngola kipo katika mlima na hakijaunganishwa na huduma za maji safi na salama, hali ambayo inatajwa kuwatia hasira watu 1,600 wa kijji hicho. Mkuu wa mkoa Chalamila ameiambia BBC kuwa kijiji chote lazima kiwajibike kwa ubadhirifu huo. Tayari diwani wa eneo hilo ni miongoni mwa wale waliokamatwa. "Kule kuna watu wenye akili timamu, lakini walishindwa kuzuia uharibifu…baada ya wao kushindwa nikaona ni muhimu kutuma polisi wawakamate wote. Naamini kuanzia sasa wataheshimu na kulinda miundombinu ya umma." Wakuu wa mikoa na wilaya nchini Tanzania wana ruhusa ya kisheria ya kuamuru polisi kukamata mtu na kumuweka rumande mpaka kwa saa 48 kabla ya kumpeleka mahakamani. Polisi mkoani Mbeya nyanda za juu kusini mwa Tanzania wameanza kamatakamata ya watu katika kijiji cha Ngola kwa tuhuma za kuharibu miundombinu ya maji. text: Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) limetoa waraka maalum wa Pasaka Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo. Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi. "Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na ubabe, vurugu, hila, na vitisho", imesomeka sehemu ya waraka huo Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa. Ujumbe huu kutoka baraza la maaskofu wa KKKT umekuja siku chache tu baada ya ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki "Shughuli za kisiasa kama vile maandamano, mikutano ya hadhara, ambayo ni haki ya kila raia, vinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola", inasomeka sehemu ya waraka huo wa Maaskofu wa kanisa Katoliki Maaskofu wa Katoliki waligusia pia kuminywa kwa uhuru wa kutoa na kupokea habari huku wakitaja baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa au kusimamishwa kwa muda. Walionya kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Maaskofu wa KKKT wameasa kwamba roho iliyokuwemo kwa waasisi wa taifa na hata kusaidia kupata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu, inapaswa kuendelea wakati wote "Uhuru ulioletwa kwa majadiliano, utunzwe na kulindwa bila ulazima wa kumwaga damu ya watanzania. Uhuru na Umoja ndizo ngao zetu zilizolitunza taifa kwa zaidi ya miaka 50", wamesema maaskofu wa KKKT Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini. text: Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Korea Kaskazini, imekariri nia ya taifa hilo kubaki na silaha zake za nuklia, ikisema silaha hizo zinalinda heshima na uhuru wa nchi. Matamshi hayo yanasadifiana na mazoezi makubwa ya manuwari za majeshi ya wanamaji, baina ya Marekani na Korea Kusini. Hii ni mara ya kwanza katika mwongo mzima, ambapo manuwari tatu za Marekani zinazobeba ndege, kuhusika katika mazoezi hayo. Akiendelea na ziara yake katika bara la Asia, Rais Trump mara kadha, ameionya Korea Kaskazini, kwamba mradi wake wa silaha za nuklia, ni tishio ambalo halitovumiliwa. Korea Kaskazini imemuelezea Rais Trump kuwa mchafuzi wa amani na utulivu wa dunia, ambaye anatamani vita vya nuklia vitokee. text: Bwana Rudisha alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota V8 siku ya Jumapili alfajiri ambapo tairi lake lilipasuka karibu na mji wa Keroke na hivyobasi kugongana ana kwa ana na basi moja lililokuwa likitokea upande wa pili. Ajali hiyo ya mwendo wa saa nne na nusu ilitokea katika eneo hatari katika barabara kuu ya Kisii Keroka kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya. Bwana Stephen Ole Marai ambaye ni rafiki a Rudisha na jirani alisema kwamba hali ya mwanariadha huyo haipo hataraini na alitibiwa katika hospitali moja iliopo Keroka kabla ya kuhamishwa katika hospitali ya Kilgoris. Katika mitandao ya kijamii Wakenya walimwambia pole Rudisha huku wakiweka picha za gari lake lililoharibika vibaya Bwana Rudisha anatoka eneo la Kilgoris kaunti ya naroko. Rudisha yuko salama , lakini anauguza majeraha. Tunaondoka Kilgoris kueleka kituo cha polisi cha Keroka ambapo atakutana na maafisa wa polisi, alisema bwana Ole Marai akinukuliwa na gazeti la Daily Nation nchini Kenya. Gari la Rudisha lililoharibiwa vibaya pamoja na basi hilo yalipelekwa katika kituo cha polisi cha Keroka. Bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki ametoweka katika riadhaa kwa muda mrefu sasa. Je kwa nini hashiriki riadha? Alitoweka katika riadha huku akikosa misimu miwili mfululizo kutokana na jeraha ambalo alikua akiuguza, lakini hilo halikuwanyamazisha mashabiki wake duniani ambao wametaka kujua hali yake. Mwezi uliopita mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wa facebook uliosema: David Rudisha wacha kunisumbua na watoto wangu. Kwa familia yangu moyo wangu una uchungu siwezi kuvumilia tena. Nawapenda nyote. Ujumbe huo ulionekana kuzua maswali mengi kuhusu familia yake na kutokuwepo kwake katika riadha. Ajenti wa Rudisha Mitchel Boeting alikataa kutoa tamko lolote kuhusu maswala ya kifamilia ya mwanariadha huyo. Aliambia gazeti la The Standard nchini Kenya kutoka Amstaerdam : Siwezi kuzungumzia kuhusu maswala yao ya kifamilia Sijui hata kuhusu chapisho hilo. David huenda asishiriki katika riadha msimu huu. Jeraha lake lilipona na likarudi. Atachalewa kurudi msimu huu na nadhani atarudi msimu ujao. Tunatumaini kwamba kila kitu kitakuwa sawa alinukuliwa na The Standard akisema. Rudisha ambaye ni bingwa wa michezo ya Olimpiki ya 2016 katika mita 800 hajashiriki katika riadha michezo ya almasi ya 2017 iliofanyika mjini Shangahi China. Bingwa wa mbio za mita 800 anayeshikilia rekodi ya dunia David Rudisha anaendelea kupata matibabu kufuatia ajali mbaya ya barabarani ilimuacha akiuguza majeraha . text: Mara ya kwanza alipoifahamisha familia yake kuwa ana jinsia mbili na kwamba angelipendelea kuangazia zaidi jinsia ya kike, swali la kwanza lilikua , "Lakini una nywele nyingi sana mwilini! Utapata tabu sana kuzitoa zote ili upate muonekano wa kike, kwa hivyo achana na wazo hilo." Familia yake iliangazia zaidi nywele nyingi alizokuwa nazo mwilini kiasi cha kumzuia kujitambulisha kwa umma kama mwanamke. ''Watu bado wana uelewa mdogioo kuhusu masuala ya watu waliyozaliwa na jinsia mbili'' alisema Alok Menon. Jamii imetawaliwa na dhana ya kuwa watu waliozaliwa na jinsia mbili ima wanataka kuwa mwanamume au mwanamke lakini haijawahi kutathmini mahitaji mingine ya watu hao linapokuja suala la jinsi wao wanavyotaka kutambulisha jinsia yao kwa hadharani. Alipoamua kuangazia jinsia yake ya kike zaidi japo muonekano wake ni wa kiume alijiunga na kikundi cha watu waliyozaliwa na jinsia mbili kama yeye ili kubadilishana mawazo na pia kupeana motisha kuhusu hali wanazokumbana nazo katika jamii. ''Nimekuwa nikibadilisha mavazi yangu kulingana na hisia zangu wakati mwingine navaa mavazi ya kiume na mara nyingine navalia mavai ya kike, hali hiyo ilikuwa ikiwakanganya watu sana'' alisema. Kwa mfano akivalia rinda, wanawake walikuwa wakimchukulia kama mwanamke mwenzao na umuliza kwa mshangao "Alaa, sasa umekuwa mwenzetu?" Baadhi ya wenzake katika kikundi alichojiunga nacho walimwambia, ni vyema achague moja kati ya jinsia hizo mbili. "Ikiwa unataka watu wabadili msimamo wao kukuhusu kama mtu aliyezaliwa na jinsia mbili basi unahitaji kunyoa nywele zote mwilini na kutafuta ushauri wa kitaalamuli upete matibabu itakayokusaidia kusalia na jinsia moja." Lakini wazo hilo lilimkera sana kwasabau tayari alikuwaakipata ushauri kutoka kwa kila mtu kuhusu maisha yake. Anasema alijiunga na kundi hilo ikidhani kuwa wenzake wataheshimu uamuzi wake. ''Bado kuna dhana kuhusu urembo ambayo ni kigezo kinachoongoza jinsia ya kike - kwamba haiwezekani uwe mwanamke ukiwa na nywele kila mahali mwilini'', alisema Menon. Hata hivyo bado anakabiliana na changamoto ya kujieleza yeye ni nani huku wale wanaomuelewa hasa katika mitandao ya kijamii wakimshauri aachane na juhudi za kutafuta muonekano wa kuwa mwanamke. Wanafanya hivyo kwa kumjali lakini anasema kuwa yeye hujiuliza maswali mengi sana kama vile "Wananitakia nini wakati ni uamuzi wa kibinafsi?" Mara ya kwanza alipogundua kuwa anastahili kuchukia nywele na nyingi mwilini alikuwa na miaka 10. Dada yake mkubwaa mbaye wakati huo alikuwa na miaka 13 alikuwa na nywele kidogo tu zilizomea makwapani. ''Nywele zangu zilipoanza kumea zilinijaa kila sehemu mwilini'', alisema Menon. Anaongeza kuwa alishangazwa na jinsi kila mtu katika familia yake alivyokuwa akijitolea kumnyoa. Ni hapo alianza kuwa kujiuliza maswali kuhusu nywele zake na alipouliza maswali zaidi alifahamishwa kuwa zilitokana na maumbile yake. Nywele ziliendelea kumea kadri alivyokua mkubwa na alihisi uchungu wakati wa kunyolewa hadi baba yake akaamua kuwa asinyolewe tena kutokana na matatizo aliyokuwa akipata. ''Nilimraia baba aniruhusu kunyoa nywele zangu mwilini lakini alikataa kabisa'' Watoto shuleni walikuwa wakimkejeli kwa kuwa na nywele nyingi mwilini, huku wengine wakimfananisha na "mnyama" au uchafu. Alipofikisha miaka 11, kejeli kutoka kwa watu zilizidi kiasi cha wengine kuitenga familia yake wakidai ni ''magaidi'' Alikuwa akiishi na jamaa zake katika mji mmoja jimboni Texas Marekani katika moha ya maeneo yaliokuwa na jamii ya wahindi waliokuwa wachache. Watu walianza kuwaita magaidi na wakati kuna mmoja mtu alimuuliza, "Kwanini watu wako wamekufanyia hivi?" Alipofikisha umri wa miaka 13 hatimae baba yake alimruhusu kunyoa nywele zake mwilini. ''Nakumbuka hiyo siku, nilijihisi vizuri sana kwasababu sasa nitafanana na wasichana wenzangu darasani'', alisema. ''Kwa kweli hatua hiyo ilinisaidia kwasababu kejeli zao zilipungua.'' Alipojiunga na shule ya upili hali ilibadilika kabisa kwani wanafunzi wenzake walishangazwa na uwezo wake wa kufuga ndevu hadi zikawa kubwa kiasi hicho. ''Hata nilijiunga na kundi lililojiita ''ndevu za amani''ambapo tulikua tukijadili masuala kama kujiepusha na ghasia na vurugu shuleni- Nakumbuka nilipewa tuzo kutokana na ndevu zangu nyingi.'' Hatua hiyo ilimfanya ajipende na kujithamini zaidi na ni hapo anasema ''Niliamua kufanya maamuzi yangu mwenyewe kuhusu muonekano unaoniridhisha'' Anasema kuwa na nywele nyingi mwilini hakustahili kuhusishwa na jinsia ya mtu kwasababu kila mtu ana kiwango fulani cha nywele mwilini mwake. ''Sioni kwanini kitu ambacho kinatokana na maumbile yamtu kinaweza kuwafanya watu kumhukumu muathiriwa'' Menon anasema watu wanaofanya biashara ya kuuza wembe na krimu za kuondoa mwele mwili hawangelipata umaarufu kama kila mtu angelizipenda nywele zake mwilini. ''Napenda kuchezea nywele zangu za mwilini kwasababu zinaniliwaza, wakakati mwingine nahisi kana kwamba ni blanketi inayoniongezea joto mwilini'' Anaongezea kusema kuwa anapendelea kuona nywele zake zikichomoza nje ya nguo yake ''Nazichukulia kama sehemu ya urembo wangu'' alisema. Lakini suala la kufuga nywele kwa watu waliozaliwa na jinsia mbili lina madhara makubwa kama vile kunyanyaswa na watu. Wataalau wa tiba kwa watu hao wanasema kufanya hivyo ni kuhatarisha maishakwani popote wanapoenda wanavutia hisia za watu ambao wakati mwingine hufikiria wao ni wapenzi wa jinsia moja. Suala la kutaka kujionesha ndio linachangi wao kuvamiwa hadharani na kutusiwa mitabndaoni kila siku. Utafiti unaonesha watu waliozaliwa na jinsia mbili wanakabiliwa na msongo mkubwa wa mawazo kutokana na kejeli zawatu wengine katika jamii. Alok Menon anasema Pengine maisha yangekuwa tofauti kama ningelinyoa,lakini kwanini iwe hivyo?' Kuwa na nywele mwilini anasema ni sehemu ya maumbile yake na kwamba ni uamuzi wa kibinafsi wa kuuambia ulimwengu, "Niko hapa kuishi!" Picha za zimepigwa na Brian Vu. Alok Vaid-Menon ni mshairi na mwana harakati wa kutetea wanamitindo waliozaliwa na jinsia mbili (kiume na kike) katika mitandao ya kijamii . Lakini mara nyingi watu hukemjeli. text: Mohamed Salah alifungia Liverpool mabao 44 msimu wa 2017-18 Mechi hiyo itachezewa mjini Yekaterinburg na itaanza saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki. Salah, 25, hajacheza tangu alipoumia begani wakati wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mnamo 26 ambapo timu yake ya Liverpool ilishindwa 3-1 na Real Madrid. "Ninaweza kuwahakikishia karibu 100% kwamba atacheza, pengine kutokee mambo yasiyotarajiwa dakika za mwisho," amesema Cuper. "Anaweza kuwa mfungaji mabao bora hapa na mmoja wa wachezaji nyota zaidi." Cuper amesema Salah "anafanya vyema sana" na kwamba alipata nafuu "haraka sana, sana." Aliongeza: "Tunajaribu kumfanya ajiamini zaidi. Madaktari wanampa fursa ya kuamua kama atacheza au hatacheza, lakini namfahamu Salah vyema sana na nina uhakika kwamba hana wasiwasi, hana woga." Beki wao Ali Gabr pia anatarajiwa kuwa sawa kucheza baada ya kuumia usoni wakati wa mazoezi. Uruguay upande wao wanatarajiwa kuchezesha kikosi cha wachezaji wachanga hasa safu ya kati, ambapo watakuwa pia na kiungo wa kati wa miaka 20 Rodrigo Bentancur na Nahitan Nandez, 22. Lakini kwingineko, kikosi chao kina wachezaji wazoefu, na hata zaidi safu ya mashambulizi ambapo wana Luis Suarez na Edinson Cavani. Mataifa hayo mawili yamo Kundi A pamoja na Urusi na Saudi Arabia. Sababu ya wengi kuwapigia upatu Uruguay? Maandalizi ya mechi hii ya leo jioni yamegubikwa na suala la Mo Salah na iwapo atacheza. Alijiunga na kikosi cha Misri Jumatano kwa mazoezi ambapo alipasha misuli moto nao, lakini akamaliza sehemu iliyosalia ya mazoezi pekee. Mechi za leo: Madaktari wa timu walisema baadaye kwamba wanafuatilia hali yake siku baada ya siku. Cuper alipuuzilia mbali umuhimu wa mchezaji huyo na kusema "mbinu zetu hazimzunguki mchezaji huyo pekee." Kuangaziwa zaidi kwa nyota huyo wa Liverpool huenda kukawasaidia Uruguay, ambao wamekuwa hawaangaziwi sana licha ya kuwa wanapigiwa upatu kushinda Kundi A. Wana kikosi chenye wachezaji wazoefu sana, ambapo wachezaji wanne wao wamecheza zaidi ya mechi 100 za kimataifa, na kipa wao Fernando Muslera (97) na mshambuliaji Luis Suarez (98) wanatarajiwa kucheza mechi mia wakifikia hatua ya kumaliza hatua ya makundi. Washambuliaji wao wawili Suarez na Edinson Cavani wamefunga zaidi ya mabao 93 mechi ya kimataifa kwa pamoja. Luis Suarez alihamia Barcelona mwaka wa 2014 Wengi wanatarajia Uruguay washinde. Wanaelekea kwa mechi hiyo wakiwa wameshinda mechi tatu mtawalia. Misri hawajashinda mechi hata moja 2018 na bado hawajashinda mechi yoyote Kombe la Dunia. MAMBO MUHIMU Misri Uruguay Wachezaji Misri Walinda lango: Essam El Hadary (Al Taawoun), Mohamed El-Shennawy (Al Ahly), Sherif Ekramy (Al Ahly). Mabeki: Ahmed Fathi, Saad Samir, Ayman Ashraf (all Al Ahly), Mahmoud Hamdy (Zamalek), Mohamed Abdel-Shafy (Al Fateh), Ahmed Hegazi (West Brom), Ali Gabr (Zamalek), Ahmed Elmohamady (Aston Villa), Omar Gaber (Los Angeles FC). Viungo wa kati: Tarek Hamed, (Zamalek), Shikabala (Zamalek), Abdallah Said (Al Ahli), Sam Morsy (Wigan Athletic), Mohamed Elneny (Arsenal), Mahmoud Kahraba (Al Ittihad), Ramadan Sobhi (Stoke City), Mahmoud Hassan (Kasimpasa), Amr Warda (Atromitos Athens). Washambuliaji: Marwan Mohsen (Al Ahly), Mohamed Salah (Liverpool). Uruguay Walinda lango: Fernando Muslera (Galatasaray), Martin Silva (Vasco da Gama), Martin Campana (Independiente). Mabeki: Diego Godin, Jose Maria Gimenez (both Atletico Madrid), Sebastian Coates (Sporting Lisbon), Maximiliano Pereira (Porto), Gaston Silva (Independiente), Martin Caceres (Lazio), Guillermo Varela (Penarol). Viungo wa kati: Nahitan Nandez (Boca Juniors), Lucas Torreira (Sampdoria), Matias Vecino (Inter Milan), Rodrigo Bentancur (Juventus), Carlos Sanchez (Monterrey), Giorgian De Arrascaeta (Cruzeiro), Diego Laxalt (Genoa), Cristian Rodriguez (Penarol), Jonathan Urretaviscaya (Monterrey). Washambuliaji: Cristhian Stuani (Girona), Maximiliano Gomez (Celta Vigo), Edinson Cavani (Paris St-Germain), Luis Suarez (Barcelona). Unaweza kusoma pia: Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hector Cuper amesema kuna uwezekano wa "karibu 100%" kuwa mshambuliaji Mohamed Salah atacheza mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia mwaka huu leo Ijumaa dhidi ya Uruguay. text: Rais wa Tanzania,Dokta John Magufuli Katika maadhimisho makuu huko mjini Dodoma ya miaka 54 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuunda Tanzania, Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa Muungano wa nchi. Licha ya kwamba kumekuwa na mazungumzo kuhusu maandamano dhidi ya Rais wa Tanzania Dokta John Magufuli ambayo yaliopangwa kufanyika leo, hali imekuwa shwari. Kumekuwa na utulivu wa kawaida katika baadhi ya maeneo nchini licha ya kwamba kumekuwa na mazungumzo kuhusu maandamano dhidi ya kiongozi huyo na utawala wake. Ndani ya mkoa wa kibiashara wa Dar es Salaam, wakaazi wamekuwa wakiendelea na shughuli mbalimbali kama kawaida. Kumekuwa na ukimya katikati mwa mji wa Dar es Salaam wakati siku za kawaida watu hupishana Ulinzi mkali umeimarishwa sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwa tayari kukabiliana na jambo lolote litakalo onekana kuhatarisha amani. Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, mwanaharakati wa kwenye mitandao ya kijamii, mtanzania ambaye makaazi yake ni nchini Marekani amekuwa akiratibu maandamano kupitia ukurasa wake wa Instagram. Mange Kimambi amekuwa akiitisha maandamano nchi nzima dhidi ya rais Magufuli kwa kile anachodai kuwa amekuwa akikiuka haki za binaadam na kudidimiza uhuru wa kisiasa nchini Mara baada ya kuingia madarakani, rais Magufuli alipiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa.Alisema uchaguzi umekwisha sasa ni wakati wa kuchapa kazi. Polisi: Kuhamasisha maandamano kupitia mtandao ni kosa la jinai Tanzania Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza imewatahadharisha raia wake walio Tanzania kuhusu vurumai ambazo huenda zikatokea. Katika maandamano ya mwezi Februari, makabiliano kati ya Polisi na waandamanaji yalisababisha kifo cha mwanafunzi mmoja, baada ya risasi ya risasi ya moto kufyatuliwa. Polisi waliwatia mbarani watu 40 wanaodaiwa kushiriki kwenye maandamano wiki iliyopita nchini Tanzania Kutokana na serikali kuweka kutahadharisha umma dhidi ya maandamano, wengi hawana hakika kama maandamano hayo yatafanyika. Tayari watu kadhaa wamekamatwa wakihusishwa na upangaji wa maandamano hayo. Mwezi uliopita katika mkutano wa hadhara, rais Magufuli ameonya kuwa watakaoandamana watamtambua. ''Kuna watu walioshindwa kufanya siasa za kweli wangependa tufanye maandamano barabarani kila siku. Nimesema acha waandamane na wataona mimi ni nani''. Serikali imekana shutuma kuwa imekuwa ikikandamiza uhuru wa upinzani na uhuru wa kujieleza. Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesisitiza haja ya watanzania kuendelea kudumisha amani na wasikubali kutumika kuivuruga amani ya nchi. text: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya Wafula Chebukati Majaji wa mahakama ya rufaa wamesema mahakama hiyo ya chini ilikosea ilipoamua kwamba wananchi walifaa kushirikishwa katika uamuzi wa kutoa kandarasi hiyo ya thamani ya $24m (£18m) kwa kampuni ya Al Ghurair kutoka Dubai. Mahakama hiyo imesema si lazima kwa taasisi ya serikali inapoamua kutoa zabuni moja kwa moja kushirikisha wananchi katika kufanya uamuzi au hata kufikia uamuzi wenyewe wa kutumia njia hiyo kutoa kandarasi hiyo. Aidha, majaji hao wamesema mahakama ilifaa kuzingatia maslahi ya wananchi na haki yao ya kushiriki katika uchaguzi huru na wa haki. Wamesema ni lazima uchaguzi mkuu ufanyike tarehe 8 Agosti na majaji wa Mahakama Kuu walifaa kuzingatia muda uliopo kwa Tume ya Uchaguzi (IEBC) kujiandaa ili kufanikisha uchaguzi huo. "Walitumia mamlaka yao vibaya bila kuzingatia ratiba iliyopo," majaji hao walisema kwenye uamuzi wao. Kila mhusika ametakiwa kugharimia mwenyewe gharama aliyoingia katika rufaa hiyo pamoja na wakati wa kesi iliyokuwa katika Mahakama Kuu. Mahakama Kuu katika uamuzi wake tarehe 12 Julai ilikuwa imesimamisha uchapishaji wa karatasi za kura za urais na kuitaka IEBC itoe zabuni upya kwa kuwashirikisha wananchi. Upigaji chapa wa karatasi za kura za nyadhifa hizo nyingine ulikubaliwa kuendelea. IEBC Jumanne wiki hii ilipokea sehemu ya kwanza ya karatasi za kura za nyadhifa za ugavana, useneta, ubunge, wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa wadi. Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imebatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu uliokuwa umefuta kandarasi ya kupiga chapa karatasi za kura za urais kufuatia kesi iliyokuwa imewasilishwa na muungano wa upinzani. text: Rais wa Tanzania akiwa na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer Azimio hilo limeeleza namna ambavyo hali ya kisiasa nchini Tanzania inavyokandamiza uhuru wa wananchi kutokana na sheria kali zilizopo dhidi ya asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, vyombo vya habari na vyama vya siasa na huku hofu kubwa ikitanda kwa wapenzi wa jinsia moja. Vilevile wamekemea matukio yote ya chuki na vurugu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Paul Makonda anaacha kuwatishia watu jamii hiyo na haki kutendeka. Hata hivyoserikali ya Tanzania ilijitenga na msimamo wa kiongozi huyo wa Dar es salaam. Bunge hilo limetaka uchunguzi huru kufanyika ili ukweli juu ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia moja, makundi ya watetezi wa haki za binadamu na wanasiasa wa vyama vya upinzani. Azimio hilo limeikumbusha serikali ya Tanzania juu ya majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufuata makubaliano ya kimataifa waliyoyakubali katika kulinda haki na utu wa kila mwananchi wake katika hali yake. Mabadiliko ya sheria Umoja wa Ulaya na nchi wanachama watafanya kila wawezalo ili kuhamamisha nchi zinazoendelea wanawakubali wapenzi wa jinsia moja na unyanyapaa au unyanyasaji dhidi ya watu hao unapungua huku makundi ya watetezi wa haki za binadamu wanakuwa salama. Azimio hilo mpia limezitaka mamlaka za Tanzania kubabili sheria za mtandaoni, mawasiliano ya kielektroniki na posta halikadhalika maudhui ya kwenye mtandao. Huduma za vyombo vya habari kuwa na uhuru wa kujieleza na kufuata viwango vya kimataifa katika kutetea haki za binadamu. Azimio hilo linataka serikali ya Tanzania kufanya mabadiliko ya sheria, sera na kuondoa vipingamizi vyote vya huduma na taarifa kwa wanawake ,wasichana au akina mama wanaojifungua katika umri mdogo . Pia wametaka kauli ya rais Magufuli kukataza msichana yeyote atakayejifungua akiwa shuleni hatoruhusiwa kuendelea na masomo, inapaswa kurekebishwa. Wamemtaka rais wa Tanzania kuiwezesha Tume ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo kufanya kazi yake vile inavyostahili ili kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani nje ya nchi. Wagunge hao pia wanaitaka "Tanzania kuwaachia huru wanasiasa waliopo gerezani." Azimio hilo limesisitiza umuhimu majadiliano hayo ili kuifanya Tanzania kujidhatiti katika kuweka mazingira mazuri kwa kila mtu bila ubaguzi wowote. Inaitaka serikali ya Tanzania "kuacha kutumia mabavu katika kutatua mgogoro uliopo kwa wamasai." Mamlaka za Tanzania ypia zimetakiwa "kulinda haki za asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya na wanaharakati wa kisiasa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania na makualiano ya kimataifa." "Umoja wa Ulaya utaendelea kuwa karibu kuangalia namna ambavyo haki za binadamu zinalindwa nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu kuwa salama." Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yao na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu Tanzania. text: Lissu alishambuliwa na watu wenye silaha za moto mwezi Septemba 2017 ambapo alimiminiwa zaidi ya risasi 30 kwenye gari lake huku 16 zikimpata mwilini. Toka wakati huo, Lissu na viongozi wengine wa upinzani wamekuwa wakilihusisha shambulio hilo na kazi yake ya siasa. Wakati wa shambulio, Lissu hakuwa tu mnadhimu wa kambi rasmi bungeni Tanzania bali pia raisi wa chama cha wanasheria nchini humo. Kwa kutumia kofia zake zote mbili, mwanasiasa huyo machachari alikuwa mwiba mkali wa ukusoaji wa serikali ya Magufuli. Lissu alikuwa miongoni mwa wanansiasa wa upinzani waliopendelea kumuita Magufuli kuwa 'Dikteta Uchwara' ama kwa lugha ya kingereza'Petty Dictator'. Baada ya shambulio hilo, alikimbizwa Nairobi kwa matibabu kisha Brussels Ubelgiji toka mwezi Januari mwaka 2018. Huko kote aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya Magufuli ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake. Lissu amekuwa nje ya Tanzania kwa matibabu toka Septemba 2017, amsema tarejea nyumbani atakaporuhusiwa na madaktari wake. Lissu pia amekuwa akilituhumu bunge chini ya Spika Job Ndugai kwa 'kumtelekeza' na kushindwa kulipia matibabu yake nje ya nchi. Hivi karibuni, Lissu ametoka nje ya Ubelgiji na kufanya mahojiano katika vituo vya televisheni vya kimataifa akianzia BBC katika kipindi maarufu cha Hard Talk na baadae Ujerumani katika telavisheni ya DW. Huko kote, mwanasiasa huyo hakumung'unya maneno juu ya mashambulizi yake kwa serikali ya Magufuli. Akisema mpaka sasa hakuna uchunguzi unaondelea wa kesi yake na hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyetiwa nguvuni na polisi. Gharama za matibabu Spika Ndugai amekanusha madai za Lissu kuwa hajalipwa na Bunge Alhamisi ya wiki iliyopita, Spika Ndugai aliliambia bunge kuwa si kweli kuwa chombo hicho kimtelekeza Lissu. Ndugai alidai dai kuwa hadi mwishoni mwa Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8 milioni pamoja na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu yake na wabunge wenziwe na kufanya jumla kuu ya fedha alizolipwa kuw Sh250milioni. Hata hivyo, Lissu alimjibu Ndugai na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema bunge la Tanzania halijawahi kutoa hata senti moja kugharamia matibabu yake. Lissu amekiri kulipwa Sh43 milioni zilizotolewa na wabunge wenzake kama mchango wao na kwamba kiasi kingine alicholipwa kinachofanya jumla ya fedha hizo kufikia Sh250 ni mishahara na stahiki zake, lakini siyo gharama za matibabu. Uchunguzi wa polisi Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi ameaingia kwenye majibizano na Lissu baada ya mbunge huyo kutoa matamko yake nchini humo, kwa kumtaka Lissu kurejea Tanzania kutoa ushirikiano na polisi. Dk Possi alisema Serikali inafuatilia suala hilo ndiyo maana Rais John Magufuli alishatoa tamko kulaani tukio hilo na kutuma baadhi ya viongozi kumjulia hali jijini Nairobi na hata ughaibuni alipo kwa sasa. "Rais alitoa taarifa ya kulaani tukio hilo na kuagiza uchunguzi wa kina wa haraka. Kwa nyakati tofauti Rais amemtuma makamu wake, Rais mstaafu na viongozi wengine wa Serikali kumtembelea Lissu akiwa hospitali akiwa Dodoma, Nairobi na Brussels," alisema Dk Possi katika tamko lake. Aliongeza kuwa uchunguzi ulishaanza mara tu baada ya kutokea tukio hilo lakini umeshindwa kuendelea kwa sababu ya kutopata ushirikiano kutoka kwa mbunge huyo. Lissu ameimbia BBC na DW kuwa atarejea Tanzania pale tu madaktari wake watakapomruhusu na kudai serikali ya Magufuli itawajibika kumhakikishia ulinzi wake. Akimjibu balozi Possi Lissu amesisitiza kuwa hakuna uchunguzi uliofanyika wa kushambuliwa kwake. Kuhusu kutoa ushirikiano kwa polisi amesema sheria za Tanzania zinaruhusu kuomba msaada wa kupatikana kwa ushahidi iwapo mtuhumia yupo nje ya nchi, na kudai serikali ya Tanzania haijawahi kuwasiliana na serikali ya Kenya na ya Ubelgiji ili kupatiwa msaada wa kuhojiwa yeye na dereva wake. Mbunge wa Singida Mashariki aliyepo kwenye matibabu ughaibuni, Tundu Lissu, ameendelea kuzua gumzo nchini Tanzania juu ya madai yake dhidi ya serikali ya nchi hiyo. text: Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutokea ripoti Marekani na Korea Kusini kwamba simu hizo zilikuwa "zinalipuka" wakati au baada ya kuwekwa chaji. Hilo limejiri wiki moja tu kabla ya mshindani wake mkuu Apple kuzindua simu mpya zaidi ya iPhone. Jumatano, kampuni ya Samsung ilisema imesitisha usafirishaji wa simu hizo kwa kampuni tatu kuu zinazosafirisha simu hizo hadi maeneo mbalimbali duniani ili kufanya uchunguzi zaidi. Mtu mmoja katika YouTube, anayesema anaishi Marekani, aliweka mtandaoni video inayoonesha Galaxy Note 7 ikiwa imeungua na skrini yake kuharibika. Ariel Gonzalez, kwenye video hiyo aliyoweka 29 Agosti, anasema simu yake ilishika moto baada yake kuitoa kutoka kwenye chaja rasmi ya Samsung, chini ya wiki mbili. Picha zaidi za Galaxy Note 7 zilizoungua ziliwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Kakao Story, maarufu nchini Korea, mnamo 30 Agosti. Simu ya Galaxy Note 7 inadaiwa kuungua baada ya kutolewa kwenye chaja Kampuni ya kuunda simu ya Samsung imesema itasitisha uuzaji wa simu maarufu ya Galaxy Note 7 kutokana na matatizo ya betri. text: Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Nyimbo, nyimbo zake iwe ni katika kuchezwa moja kwa moja mtandaoni, kuuzwa kama kanda, kuuzwa mtandaoni au kupakuliwa mtandaoni, ndizo zilizoongoza. David Bowie alikuwa wa pili naye Coldplay wa tatu. Adele, mwanamuziki aliyeuza zaidi 2015, alikuwa wa nne katika orodha ya mwaka 2016 baada ya albamu yake ya 25 kusalia kuwa maarufu mwaka huo wote. Orodha ya shirikisho hilo, ambayo huangazia nyimbo zote za mwanamuziki badala ya wimbo mmoja pekee au albamu moja pekee, pia inajumuisha Justin Bieber, katika nambari tano, ambaye yupo mbele ya Twenty One Pilots na Beyonce. Rihanna, Prince na The Weeknd wanakamilisha orodha ya 10 bora. Ufanisi wa Drake unatokana na mauzo ya albamu yake ya nne, Views, ambayo aliichomoa mwaka jana. Ilikuwa ndiyo albamu ya kwanza nyimbo zake kuchezwa mara bilioni moja katika Apple Music. Wimbo wa One Dance, ulikuwa wimbo wa kwanza kabisa kuchezwa mara bilioni moja katika Spotify. David Bowie alikuwa wa pili, sana kutokana na mafanikio ya albamu yake ya 25 kwa jina Blackstar. Albamu hiyo ilichomolewa siku mbili kabla ya kifo chake Januari 2016. Washindi wa awali ni pamoja na One Direction na Taylor Swift. Mwanamuziki Drake ndiye aliyeuza nyimbo na video nyingi zaidi miongoni mwa wasanii duniani mwaka 2016. text: Trevor amefariki baada ya kushambuliwa na mbwa Trevor alikuwa maarufu sana kwenye kisiwa kidogo cha Niue kutokana na kuwa ndege pekee wa aina yake kuishi kwenye kisiwa hicho. Aliwasili kisiwani hapo mwaka 2018, hata hivyo haijulikani ni kwa namna gani alifika kisiwani hapo. Alikuwa akiishi kwenye dimbwi lililokuwa pembezoni mwa barabara, na alikuwa akihudumiwa na kupewa chakula na wenyeji wa eneo hilo. "Alionekana hapa Niue mwezi Januari 2018 baada ya kutokea gharika kubwa, tunaamini alipaa ama alipeperushwa mpaka kufika hapa," amesema Rae Findlay, mkuu wa chama cha wafanyabiashara wa Niue ambaye pia alifungua ukurasa wa Facebook wa bata huyo . "Inaaminika kuwa ametokea New Zealand lakini kuna uwezekano akawa ametokea Tonga ama kisiwa kingine cha bahari ya Pasifiki. Katika maisha yake mafupi na ya furaha kisiwani Niue, Trevor aliishi kwenye dimbwi. "Hakuna mito, chemchem ama maziwa hapa, hivyo Trevor alichagua kuishi kwenye dimbwi," Bi Findlay ameiambia BBC. Japokuwa ametambulika kama bata mpweke, maisha yake hayakuwa ya kipweke kabisa. Dimbwi la Trevor lilikuwa likikaguliwa mara kwa mara na watu waliokuwa wakimjali. Kikosi cha zimamoto cha kisiwa hicho kilikuwa kikijaza maji dimbwi hilo pale maji yalipokuwa yakikauka. Pale dimbwi la Trevor lilipokuwa likaukiwa na maji... ...kikosi cha zimamoto kilikuwa kikiiingia kazini kwa kujaza maji "Alikuwa kawaida yake kupaa katika maeneo jirani na kula vyakula ambavyo alikuwa akipatiwa, mapeasi, mahindi na shayiri," amehadithia Bi Findlay. Kulikuwa na maoni kutoka baadhi ya watu waliotaka aletwe bata mwingine wa kuishi na Trevor lakini dimbi lake lilikuwa dogo la kumtosha yeye pekee. Hata hivyo alikuwa na urafiki na jogoo, tembe na weka - ndege wa asili wa kisiwa hicho - ambao wote walikuwa wakiishi karibu na dimbi hilo. "Baada ya mwaka mzima wa kuwa na mifuko ya shayiri kwenye begi langu, nitakumbuka kila mara nilipokuwa nasimama kumlisha Trevor nilipokuwa nikienda na kutoka kazini. Alikonga nyoyo za watu wengi, na atakumbukwa sana." Trevor, ambaye alikuwa akifahamika kama bata mpweke zaidi duniani amefariki baada ya kushambuliwa na mbwa kwenye kisiwa kimoja cha mbali kwenye bahari ya Pasifiki. text: Picha hiyo ilizuka katika mtandao rasmi wa meneja huyo kabla ya kuondolewa muda mfupi baadaye Meneja huyo wa zamani wa Paris St-Germain manager anatarajiwa kuzinduliwa rasmi kama mrithi wa Arsene Wenger wiki hii. Klabu hiyo ya London bado haijathibitisha kuwa Emery ndiye kocha mpya. Lakini picha ya Emery iliyoambatana na ujumbe huo na nembo ya Arsenal iliwekwa kabla ya muda mfupi badaye kuondolewa. Haijulikani kama picha hiyo iliwekwa kimakosa au ni kazi ya wadukuzi. Mtandao huo www.unai-emery.com - unaohusishwa na akaunti ya Twitter ya raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 46 - baadaye ulikuwa unaonyesha kuwa na hitilifu kwa waliojaribu kuufungua. Emery aliondoka PSG mwezi huu baada ya kuhudumu kwa miaka miwili ambapo alishinda taji la ligi na vikombe vinee vya mashindano ya nyumbani. Awali aliwaongoza Sevilla kupata ushindi wa mara atatu latika ligi ya Uropa kati ya 2014 na 2016. Wenger aliodnoka Arsenal mwezi huu baadaya kuhudumu kwa miaka 22. Tazama Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano. Mtandao rasmi wa Unai Emery umeweka picha iliyo na ujumbe: "Nasikia fahari kuwa katika familia ya Arsenal." text: Harpreet Kaur alimuandikia barua waziri mkuu ili wabadili jina la kijiji chake "Jina la kijiji changu kinaitwa 'Ganda' maana yake ni chafu au haipendezi," Harpreet Kaur alimuandikia waziri mkuu Narendra Modi mwaka 2016 ili waweze kubadili rasmi jina la eneo hilo. Aliongeza kuwa jina la kijiji peke yake linaweza kuwadhalilisha hata wakazi wa hapo. "Hali ni mbaya sana, yani hata ndugu zetu huwa wanatutania mara kwa mara ," mwanamke mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wanaofanya shinikizo la kubadili jina. Mwaka 2017, mamlaka ilibadilisha jina la kijiji hicho na sasa kinaitwa 'Ajit Nagar' kikimaanisha fahari ya kaskazini mwa jimbo la Haryana,India. Kiongozi wa kijiji Lakwinder Ram, alisema kuwa wamekuwa wakijaribu kwa miaka mingi kuishinikiza serikali kubadili majina bila mafanikio. Licha ya kuwa hakuna mtu ambaye alikuwa hataki kijiji kibadilishwe jina. Wanakijiji wanasema jina la Ganda lilikuja baada ya mafuriko kuharibu eneo hilo miongo kadhaa iliyopita. Na afisa aliyetembelea eneo hilo baada ya janga la mafuriko kutokea ndio alitoa jina hilo, kutokana na uchafu uliokuwa umejaa. Hivyo tangu siku hiyo jina likabaki kuwa ganda yani pachafu. Wawakilishi wengine wa vijiji 50 wameikasirikia serikali ya India kwa kubadilisha jina hivi karibuni. Sababu zao zikiwa kwamba majina mengine yanaonekana kama yana ubaguzi, au ya ajabu na yanaleta aibu kwa wakazi wake. Barua kutoka vijiji 40 zilikuwa zinakubali mabadiliko hao, Krishan Kumar,afisa wa serikali alisema. Miongoni mwa vijiji vilivyobadilishwa ni kijiji kinachoitwa Kinnar yaani mtu mwenye jinsia mbili. Hatua za kubadili jina vijiji sio rahisi nchini humo. Lazima mtu uanze kwa kuishawishi serikali ambayo ndio ina maamuzi ya mwisho. Kwa wakazi wa kijiji cha Lula Ahir kilichopo jimbo la Haryana jina lilikuwa linawakebei watu wenye ulemavu na harakati za kubadili jina hilo limepitia mlolongo wa urasimu mwingi. Waliwahi kuiandikia barua serikalini mwaka 2016 na kuwaeleza jinsi wasivyoridhika na jina la kijiji hicho . Walisubiri majibu kwa miezi sita na kupata majibu ya kukataliwa kwa sababu jina mbadala walilouwa wamelichagua lilikuwa linatumika eneo lingine. Kaskazini mwa nchini India, hivi karibuni vijiji vingi vyenye majina ya kudhalilisha kumekuwa na kampeni ya kuhimiza serikali kubadilisha majina hayo. text: The Blue ilipoteza 2-0 katika ligi ya Uingereza siku ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates na walikuwa na shambulizi moja pekee lililolenga lango. Chelsea imeshinda mara mbili pekee katika mechi tano zilizopita na sasa wako pointi tatu pekee mbele ya Arsenal waliopo katika nafasi ya tano na Man United iliopo katika nafasi ya sita. ''Nimekasirika sana kuhusu mwelekeo tuliochukua'' , Sarri alisema. Ni mwelekeo ambao hatuwezi kukubali. Katika mkutano na vyombo vya habari baada ya timu yake kulazwa, Sarri alisema alitaka kuzungumza kwa lugha ya Kitaliano badala ya Kiingereza kwa sababu alitaka kutuma ujumbe kwa wachezaji wake na alitaka kutuma ujumbe wa wazi. ''Nataka kusema nimekasirika sana, nimekasirika sana'', alisema mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 60, ambaye alimrithi raia mwenzake wa Itali Antonio Conte katika uwanja wa Stamford Bridge. ''Tulishindwa kutokana na mafikra yetu zaidi ya chochote kile. hiki ni kitu siwezi kukubali. Hili kundi la wachezaji hawa ni vigumu kuwasukuma' Hiki sio kikosi kinachojulikana kwa mchezo wake mzuri. Chelsea hivi karibuni ilipoteza katika nusu fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Tottenham Kikosi cha Sarri dhidi ya Arsenal kilishirikisha wachezaji saba ambao walishinda ligi ya Uingereza chini ya ukufunzi wa Conte 2017 kabla ya kumaliza katika nafasi ya tano msimu uliofuata. Raia huyo wa Itali alisema hii sio timu ambayo itajulikana kwa mchezo mzuri lakini tunahitaji kuwa timu ilio na uwezo wa kupambana na mazingira kupata shida kwa kati ya dakika 10 ama hata 15 na baadaye kucheza mchezo wetu. ''Unaweza kujipata katika hali mbaya mara kwa mara lakini tunahitaji kuimarika zaidi ya tulivyofanya siku ya Jumamosi''. Chelsea ilifunga magoli 27 katika mechi 11 za kwanza msimu huu lakini wameishia kufunga magoli 13 katika mechi 13. Mshambuliaji Olivier Giroud na Alvaro Morata wameshindwa kuonyesha umahiri wao na klabu hiyo imehusishwa pakubwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain ambaye Sarri alishirikana naye akiwa klabu ya Napoli. Sarri anasema kuwa fikra ya kikosi hicho inaweza kuimarishwa kupitia kupata mchezaji mpya. ''Ni sharti uwashawishi. Inaweza kuwa ni mchezaji mpya anakuja ama hata mchezaji mmoja wa zamani achukue jukumu'', alisema. ''Mchezaji katika kiwango hiki hawezi kuwa muoga kuchukua majukumu''. Kitu kizuri ambacxho kinaweza kufanyika ni mimi na wachezaji kuzungumza kwa uwazi kuhusu kile kinachofanyika. ''Mimi ndio nimechukua jukumu hili na ni muhimu wao kuwa na tabia hiyo. iwapo hawawezi pengine basi wasicheze katika kiwango hiki''. Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri ameelezea kuwa vigumu sana kuwashawishi wachezaji wake kufuatia kushindwa na Arsenal. text: Wakimbizi wengi nchini Uganda wametoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Sudani Kusini Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Uganda, Joel Boutroue amesema kufikia sasa wana asilimia 9% tu ya fedha jumla wanazotaka katika bajeti yao ya dola milioni 450 walizopanga kutumia mwaka huu. Huenda shughuli za shirika hilo zikakwama kutokana na ukosefu wa fedha kutoka jamii ya kimataifa. Hilo litaathiri pakubwa usaidizi kwa mamilioni ya wakimbizi waliopo Uganda baadhi kutoka Uganda na hivi karibuni wengine wanaoonekana kuwasili nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Wakimbizi Uganda waandaa tamasha la muziki kuwasaidia waathiriwa wa ubakaji Boutroue anasema kwamba kwa sasa wamepokea dola milioni 40 kutoka kwa wafadhili. Na wanatarajia nyongeza ya fungu kutoka Geneva kwani wafadhili wanachagia mfuko wa UNHCR kuendeleza shughuli zao na baadaye inabidi warudishe fedha hizo. Ofisa ya waziri mkuu nchini Uganda inayoshughulika na maswala ya wakimbizi, inaonyesha takwimu za wakimbizi milioni 1.3 kufikia mwisho wa mezi wa nane mwaka 2017. Ikiwa Milioni moja ni kutoka Sudan kusini na wengine kutoka DRC, Burundi, Somalia na mataifa mengine. Wakimbizi wa Burundi waliopo nchini Uganda Mwaka 2012 Shirila la UNICEF katika mradi wa mswala ya binadamu ilitowa ripoti yake kwamba idadi ya wakimbizi nchini Uganda inatarajiwa kuongezeka zaidi kutoka milion 1.4 kufikia milioni 1.8 mwishoni mwa mwezi wa December mwaka 2018. Boutroue ameongeza kusema kuwa Uganda imepokea wakimbizi 100,000 tangu mwezi wa January mwaka huu tokea DRC na Sudani kusini, na hivyo ametowa wito kwa jami ya kimataifa kutowa msaada wa dharura la sivyo watashindwa. 'Kama hatutapata misaada zaidi tuko katika hali ya hatari, nikisema sisi ni wakimbizi na watu wote wanaohusika na katika swala hilo. Maana kama hatutapa fungu jingine mipango yote itaharibika. Hatutaweza kuwalisha, kuwapa elimu na vingine bila ya vitu hivyo tunaweza kufikia katika hali mbaya zaidi. Maandamano yamefanyika nchini Israel kupinga mpango wa kuwaondosha wahamiaji wa Kiafrika kuelekea nchini Uganda Na sioni kwa sababu gani, kwani Uganda ndio mama wa wakimbizi kutoka na sera zake nzuri na. Amesema Joel Boutroue. Kila mkimbizi anyewasili nchini Uganda anapewa kipande cha aridhi futi 50 kwa 50, vifaa vya ujenzi na mgawo wa chakula, na pia wakimbizi wanaruhusiwa kufanya biashara kama ana uwezo wa kufanya biashara popote nchini akiwa na kitambulisho chake cha ukimbizi. Shirika la Umoja wa mataifa la maswala ya wakimbizi UNHCR nchini Uganda limepata wasiwasi wa fungu la fedha la fedha walilonalo la wakimbizi katika mwaka huu wa 2018. text: Bodi ya soka Ulaya itakutana na maafisa wa serikali ya Uingereza na Shirikisho la soka Jumatatu kujadiliana eneo ambalo litatumiwa kucheza fainali hiyo. Chelsea inakabiliana na Manchester City katika fainali itakayochezwa Mei 29. Lakini mashabiki wameonywa kutosafiri baada ya Uturuki kuingizwa kwenye orodha ya waliopigwa marufuku kuingia nchini Uingereza. Kuna mechi ambayo ni lazima ifanyiwe maamuzi huku Wembley ikipangiwa kuwa mwenyeji wa fainali hiyo ya Mei 29. Hata hivyo, inafahamika kuwa EFL itafikiria kuhamisha mechi hiyo ikiwa itaombwa kufanya hivyo na Uefa, na bodi yake itafanya maamuzi ya mwisho. Raia wa Uingereza wanaorejea kutoka nchi zilizopigwa marufuku wanahitajika kuwa karantini katika hoteli zilizoidhinishwa na serikali kwa siku 10. Karantini kama hizo zitaathiri wachezaji ambao watashiriki kombe la Euro 2020 ambalo linaanza Juni 11. Kuhamisha fainali hadi Wembley kunahitaji serikali ya Uingereza kuwa na wepesi wa kukubali mabadiliko kwa kuwaruhusu watu wake kwenda England, kwa kuzingatia washikadau ambao watatarajiwa kuhudhuria. Inaeleweka kuwa moja ya masuala ya kuzingatiwa ni uwezekano wa kuondolewa sharti la kuwa karantini lakini hadi kufikia sasa hakuna kilichofikiwa. Ijumaa, waziri wa usafiri Grant Shapps alisema kuwa nchi zilizopigwa marufuku kwasababu ya ugonjwa wa Covid-19 "hazistahili kutembelewa isipokuwa tu katika hali ambazo haziwezi kuepukika". Aliongeza kuwa serikali iko wazi kuwa mwenyeji wa michezo ya Uingereza. Uefa ilikuwa na matumaini ya kutoa tiketi 4,000 kwa kilabu zote kwa mechi hiyo iliyokuwa imepangiwa kuchezwa uwanja wa Ataturk. Schapps alisema kuwa Shirikisho la Soka lilikuwa linafanya mazunguzo na Uefa kuhusu suala la kubadilisha uwanja mechi hiyo itakapochezwa lakini "huo ni uamuzi wa Uefa". Wafuasi wa Chelsea Trust wamesema kuwa watakutana na Uefa na kuomba kuwa fainali ihamishwe hadi Uingereza huku makundi ya mashabiki wa Manchester City wakisema kuwa watatoa wito mechi hiyo kuchezwa Istanbul. Arsenal 'itafanya nini' baada ya kuondolewa Europa league? Kwingineko kuondolewa kwa Arsenal kutoka mechi za kombe la Europa league kumeirejesha klabu hiyo katika meza ya kupanga upya mikakati yake. "Tumevunjika moyo". Mikel Arteta sio mtu anayependa kuonyesha hisia, lakini unaweza kusema kuwa hii inaumiza. Kushindwa kwa Arsenal kufunga goli moja dhidi ya Villareal katika uwanja wa nyumbani, Emirates siku ya Alhamisi - hatua iliowafanya kuondolewa katika kombe la Yuropa ina madhara. Arsenal iligonga mwamba wa goli mara mbili siku ya Alhamisi Wakiwa katika nafasi ya tisa katika ligi , msimu wa Arsenal unaonekana umekwisha bila chochote cha kuonesha na rekodi yao wanayojivunia ya kushiriki katika michuano ya kimataifa kwa kipindi cha miaka 25 iliopita inaelekea kuangamia. Kutakuwa na maswali mengi kuhusu hatma ya wachezaji wengi, na maandamno ya mashabiki ambayo yalifanyika nje ya uwanja wa Emirates kujaribu kumtimua mmiliki wa klabu hiyo. Hapa katika BBC Sport tunatafuta majibu ya mkufunzi, wachezaji wachambuizi na wengine zaidi ili kujaribu kupima hali ilivyo kufuatia kuondolea kwa Arsenal, na kujiuliza, je klabu hiyo itachukua hatua gani baada ya mechi hiyo. Lazima tuipiganie klabu hii Tulijaribu kila tuwezalo hadi dakika ya mwisho, Arteta aliambia BT Sport baada ya mechi hiyo kukamilika. "Nadhani tulipaswa kushinda mechi hiyo . Tulikuwa na nafasi tatu , na hawakupata chochote lakini ndio walioibuka washindi''. ''Tumevunjika moyo na kweli tumekata tamaa''. Arsenal bila shaka iligonga mwamba wa goli mara mbili kupitia Pierre Aubameyang, huku Emile Smith Rowe na shambulio la Nicolas Pepe likitoka nje ,lakini mashambulizi kama hayo yalikuwa machache katika mechi ambayo haikufurahisha kwa kipindi kirefu. Arteta anahisi kwamba kulikuwa na sababu zilizochangia ikiwemo baadhi ya wachezaji muhimu kukosa mazoezi kwa muda mrefu akiwemo Aubemayeng kufuatia tatizo la Malaria na Kieran Tierney, ambaye alichukua mahala pake Granit Xhaka katika nafasi ya beki wa kushoto baada ya jujeruhiwa katika maandalizi. Arteta ambaye amekiri kwamba kazi ya kila mtu inachunguzwa , alisema: ni vitu kadhaa. Jinsi tulivyoanza Villareal haikuwa vizuri. Hatukuwasili hapa tukiwa katika hali nzuri. Kwa asilimia 90 ya wachezaji wao ilikuwa nusu fainali ya kwanza na hivyobasi lazima tujifunze. Kipa Bernd Leno alikubali kwamba mchezo mbaya walioonyesha Villareal na kushindwa kufunga goli nyumbani ndio chanzo cha kubanduliwa katika michuano hiyo. ''Ni hali ngumu kwetu sote, raia huyo wa Ujerumani aliambia BT Sport. Pia kwa mashabiki, sote tunahuzunika''. ''Pengine msimu ujao huenda tukafanya bora zaidi lakini msimu huu haujaisha na katika mechi zetu nne za mwisho ni sharti tuipiganie klabu na kjuonyesha kwamba tunaipenda klabu hii''. Uefa iko tayari kuamua kufikia Jumatano ikiwa ibadilishe eneo ambalo fainali ya ligi ya mambingwa itachezwa Wembley kutoka Instanbul kwasababu ya masharti ya usafiri. text: Bangi itakayotumwa kwenye soko la Ulaya hata hivyo si kwa matumizi ya starehe kama uvutaji bali ni kwa ajili ya matibabu. Kwa mujibu wa Monitor mainspekta wa bidhaa za matibabu zitokanazo na bangi kutoka Uholanzi walikagua mashamba ya bangi kwenye wilaya za Hima na Kasese kati aya Julai 29 na Agosti 4. Maafisa hao kabla ya kuondoka Uganda waliikabidhi cheti cha kukidhi vigezo kampuni ya Industrial Globus Uganda Ltd kwa kipindi cha Agosti 6, 2019 mpaka Agosti 5, 2020. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benjamin Cadet amelithibitishia gazeti hilo kuwa EU wamewapa idhini ya kuasafirisha bangi Ulaya. "Baada ya EU kuthibitisha bidhaa zetu - usafirishwaji na mnyororo wote wa uzalishaji - kuanzia kupanda mpaka kuvuna kwa bangi utafanyika kikamilifu nchini Uganda na kupelekwa kwenye masoko ya Ulaya," Cadet amesema. Takribani kampuni 50 zimeomba kibali Wizara ya Afya kuungana na kampuni ya Industrial Globus Uganda Ltd ili kuzalisha bangi kwa ajili ya matibabu. Bangi inayozalishwa Uganda katika shamba la wilayani Kasese ina virutubisho vya Cannabinol (CBD) na Tetrahydrocannabinol (THC) ujazo wa 2.7mg THC na 2.5mg CBD mtawalia. Virutubisho hivyo vimepasishwa Ulaya, Marekani na Canada. Uzalishaji na matumizi ya bangi kwa starehe (uvutaji) bado yamepigwa marufuku Uganda Uganda ilishindwa kusafirisha bangi ya thamani ya dola 600 milioni kwenda Canada na Ujerumani mwezi Julai mwaka huu baada ya kampuni ya Industrial Globus Uganda Ltd kutokuwa na cheti kutoka EU. Uganda ndio nchi pekee Afrika Mashariki ambayo imehalalisha uzalishaji wa bangi, japo kwa matumizi ya kiafya. Mwezi Mei mwaka huu, Mbunge wa Kahama mjini nchini Tanzania, Jumanne Kishimba aliitaka serikali kuhalalisha matumizi ya bangi nchini Tanzania kwa mautumizi ya dawa. ''Tunavyozungumza, Uganda imehalalaisha upanzi wa Marijuana kwa matumizi ya dawa'', alisema akitaja ripoti za hivi majuzi kwamba taifa hilo la Afrika mashariki limenunua mbegu kupanda mmea huo. ''Sijui ni kwa nini kitengo cha chakula na dawa hakijachukua sampuli kuelezea serikali kwamba dawa hizo zina bangi ndani yake'', alihoji. Hata hivyo serikali ya Tanzania imepinga uwezekano wowote wa kuhalalishwa kwa mmea huo katika taifa hilo. Wakaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wameidhinisha Uganda kutuma bidhaa za bangi barani Ulaya, gazeti la Daily Monitor linaripoti. text: Mmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake. Ngugu yake, Kalia hata hivyo bado hajapata fahamu. Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha. Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa, Professor Deepak Gupta, ambaye alishiriki katika upasuaji huo aliiambia BBC. Madaktari wanasema pacha hao wako hali nzuri Pacha hao kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus. Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa. Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India. text: Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania lililonukuu mtandao wa Complete Sport.com na Punching.com , Kocha huyo raia wa Nigeria ameamua kuwasilisha malalamishi hayo kwa Fifa ili kutafuta haki yake. Amunike alitimuliwa na shirikisho la soka la Tanzania baada ya tanzania kupata matokeo duni katika kombe la mataifa ya Afrika . ''Nimewasiliana na Fifa juu ya hilo jambo . Sio Swala la kupiga kelele , lakini nina imani watalitazama na kuamua iwapo ni sahihi mtu kutolipwa baada ya kufanya kazi'', Amunike alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema. Kocha huyo ambaye mkataba wake ulivunjwa mwezi Julai mwaka huu amerejea Uhispania ambako makazi yake ya kudumu yapo. Kwa mujibu wa Mwananchi , TFF waliafikia uamuzi huo wa kuvunja mkataba na kocha mchezaji huyo wa zamani wa Nigeria baada ya taifa Stars kuandikisha matokeo mabaya katika fainali ya Afcon 2019 zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19. Katika fainali hizo taifa Stars ilishika mkia kwenye kundi C lililokuwa na Senegal, Kenya, na Algeria baada ya kupoteza mechi zote ta Kushindwa kwao na majirani zao kenya ndio kulikohuzunisha wengi kwa kuwa walipoteza uongozi waliokuwa nao wa 2-0 kufikia kipindi cha mapumziko. Na kufuatia matokeo hayo Amunike alisea kwamba timu hiyo ilihitaji uzoefu wa mashindano makubwa na kwamba wachezaji walihitaji kushiriki katika ligi zenye ushindani mkubwa ili kuweza kuimarika. Kocha huyo ambaye mwenye umri wa miaka 47 ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka klabu ya Sudan ya A; Khartoum mnamo mwezi Machi aliandikisha mkataba wa miaka miwili na taifa hilo la Afrika mashariki akichukua nafasi yake Saulm Mayanga. Amunike alishinda kombe la Afrika akiichezea Super Eagles ya Nigeria 1994 na mshindi wa dhahabu ya Olimpiki miaka miwili baadaye. Katika kipindi chake cha mchezo aliichezea, SC Zamalek, Sporting \lisbon, na Barcelona ijapokuwa majeraha yalimzuia kuafikia ndoto yake mjini Catalonia. Winga huyo wa zamani alianza ukufunzi na timu ya nigeria isiozidi wachezaji wa miaka 17 2014 na kushinda kombe la dunia la kinda hao mwaka mmoja baadaye. Aliyekuwa kocha wa timu ya kandanda nchini Tanzania Emmanuel Amunike amelishtaki shirikisho la soka la Tanzania TFF kwa shirikisho la mchezo huo duniani FiFa akilalamikia kutolipwa haki yake. text: Jiwe hili la amri kumi za Mungu liligunduliwa mwaka 1913 Jiwe hilo ambalo lina urefu wa sentimita 60 limeandikwa kwa lugha ya kiyahudi Liliuzwa katika soko la mnada huko Los Angeles, kwa masharti kuwa litawekwa kwa umma kuliona. Jiwe hilo liligunduliwa mwaka 1913, wakati wa ujenzi wa reli karibu na mji wa Yavneh ulio nchini Israel. Jamii ya Samaria wakiomba mlima Gerizim Wauzaji wanasema kuwa jiwe hilo ni la kutoka miaka ya 300 na 500 AD. Amri ambayo haionekani kwenye jiwe hilo ua "Usitumia jina la Mungu kwa njia isiyostahili" sasa pameandikwa kwa kutoa wito kwa waumini wa Samaria wakitakiwa kujengwa kwa hekalu katika mlima Gerizim, eneo takatifu juu ya mji wa Nablus, ambayo ndio sasa Ukingo wa Magharibi. Jamii ya Samaria ina historia ndefu eneo la Mashariki ya Kati, licha watu hao kutoweka hadi chini ya watu 1000 miaka ya hivi karibuni. Jiwe la kale zaidi lenye amri kumi za Mungu limeuzwa kwenye mnada nchini Marekani kwa dola 850,000. text: SportPesa hudhamini klabu kadha zinazocheza Ligi Kuu ya Kenya Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne, mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa SportPesa Ronald Karauri amesema wamelazimika kujiondoa kwa sababu hawawezi kudhamini michezo kama watatozwa ushuru wa asilimia 35. Miongoni mwa michezo itakayoathiriwa na uamuzi wa SportPesa ni kandanda, ndondi na raga. Kwa upande wa kandanda, kampuni hiyo hudhamini ligi kuu ya Kenya, timu za Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars pamoja na ligi ya Super 8. "Sasa sisi tunaachia serikali mzigo huo wa kudhamini kandanda na michezo mingine. Kama wataweza ama hawataweza ni juu yao,'' anasema Karauri. Pigo kubwa kwa soka Kenya Kampuni hiyo ilipotangaza nia yake mwaka jana, afisa mkuu wa KPL Jack Oguda aliambia BBC kwamba hatua hiyo itakuwa pigo kubwa kwa soka Kenya. Bw Karauri ameambia mwandishi wa BBC John Nene kwamba wamejaribu kila njia kuzungumza na wakuu wa serikali lakini hawakuelewana. Juhudi zao za mahakama kuingilia kati zimeambulia patupu. "Mtu wa mwisho ambaye tunatarajia atatusaidia ni Rais Uhuru Kenyatta. Hivi sasa tunafanya mpamgo tukutane naye tumwelezee kwa undani kuhusu uamuzi wetu,'' anasema Karauri. Licha ya uamuzi huo, Karauri amesema wataendelea kufanya kazi nchini Kenya, na kwamba hawataondoka. Rais wa chama cha ndondi cha Kenya John Kameta amesikitishwa na uamuzi huo wa SportPesa lakini amelaumu serikali kwa kuongeza ushuru hadi asilimia 35. Afisa mkuu mtendaji wa SportPesa Ronald Karauri "Hatuna budi ila kusimamisha ligi ya ndondi msimu huu kwa sababu sisi wenyewe hatutaweza kugharamia ligi yetu, ni pesa nyingi sana zinahitajika na kwa sasa hatuna mdhamini mwingine,'' amesema Kameta. Miongoni mwa sababu za serikali kuongeza ushuru ni kupunguza idadi ya vijana wanaocheza kamari siku hizi. Mazungumzo na serikali Katibu mkuu wa wizara inayosimamia michezo nchini Kenya, Kirimi Kaberia, amesema Ijumaa hii wanakutana na kampuni zote za mchezo wa kamari ikiwemo SportPesa kujadili suala hilo la ushuru kuongezwa kwa asilimia 35 kutoka asilimia 7.5. Kulingana na Kaberia mbali na kampuni za mchezo wa kamari, wahusika wengine watakaohudhuria mkutano huo ni maafisa wa mamlaka ya ushuru na wakuu wa michezo nchini Kenya hasa wale ambao wameathiriwa na uamuzi wa SportPesa kusitisha udhamini wao wa michezo nchini Kenya. Hatahivyo Kaberia hakusema kwa undani kama kuna uwezekano wa serikali kupunguza kiwango cha ushuru huo wa asilimia 35 ambao serikali imeamua kutoza kampuni za mchezo wa kamari nchini Kenya.. Udhamini wa SportPesa kwa klabu za nje ya Kenya hautaathirika. Kampuni hiyo kwa sasa hudhamini klabu za Uingereza, Everton an Hull City. Mwaka jana Sportpesa waliingia Tanzania na kuanza kudhamini Simba, Yanga na Singinda United zinazocheza ligi kuu Tanzania na pia timu ya taifa ya Serengeti Boys. SportPesa ni moja ya kampuni kubwa zaidi za mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi Afrika Mashariki. Uraibu wa kucheza kamari Kodi hiyo ya juu iliidhinishwa na serikali kama moja ya njia za kuzuia watoto na vijana wa umri mdogo kujihusisha na mashindano hayo ya ubashiri wa matokeo. Wakenya waliorodheshwa kuwa miongoni mwa watu wanaoshiriki sana katika mashindano ya bahati nasibu Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na utafiti uliofanywa karibuni. Utafiti huo ulionesha theluthi mbili ya Wakenya wa kati ya miaka 17 na 35 wamewahi kushiriki. Wengi hutumia simu zao za rununu kubashiri matokeo ya ligi za nyumbani na ligi za nje, sana Ulaya. Kumekuwepo na wasiwasi kuhusu athari ya uraibu huo kwa vijana. Wazazi na viongozi wa kidini walikuwa wameiomba serikali kuchukua hatua. Bunge lilikuwa awali limependekeza kodi iwe 50%, lakini rais akapendekeza kodi hiyo ipunguzwe na mwishowe ikafikia 35%. Kampuni ya mchezo wa kamari nchini Kenya, SportPesa, imesitisha udhamini wake wa michezo kutokana na uamuzi wa serikali kuongeza ushuru hadi asilimia 35 kutoka kwa asilimia 7.5. text: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Harisson Mwakyembe Hatua hiyo inajiri wiki mbili tu baada ya maafisa wakuu wa shirikisho la soka nchini humo kushtakiwa na ulanguzi wa fedha. Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Awami hatua hiyo ilitarajiwa. Baraza hilo ambalo linahusika na usimamizi wa michezo nchini humo limetuhumiwa kwa kukosa utendaji. Akilifutilia mbali baraza hilo, waziri wa michezo Harrison Mwakyembe alisema kuwa kushindwa kwao kuimarisha michezo nchini hakutokani na uhaba wa fedha bali uzembe na kutoijali sekta hiyo. Pia ameshutumu operesheni za baraza hilo kwa kutawaliwa na ufisadi, madai ambayo aliyekuwa katibu mkuu wa baraza hilo Mohammed Kiganja ameyakana. "kwanza nataka kusema kwamba hakujakuwa na ufisadi katika baraza hilo.Ufisadi umeshamiri katika michezo kwa jumla. Na ninakubaliana na hilo.Iwapo utaenda katika uchaguzi wa vilabu vya soka kuanzia viwango vya Wilaya hadi kitaifa utaona matatizo haya''. Kuvunjwa kwa baraza hilo kunajiri wiki mbili tu baada ya rais na maafisa wengine wakuu wa shirikisho la soka kushtakiwa kwa ulanguzi wa fedha. Baraza la kitaifa la michezo nchini Tanzania limevunjwa kufuatia madai ya ufisadi. text: Watu wanne wameripotiwa kuuawa katika siku ya kwanza ya mgomo wa kitaifa, kwa mujibu wa madaktari wanaoegemea upande wa upinzani. Wanaharakati wameitisha maandamano ya kupinga utawala huo kuanzia Jumapili, siku kadhaa baada ya msako wa kijeshi uliyosababisha vifo vya makumi ya watu katika mji mkuu wa Khartoum. Wafanyikazi kadhaa wa benki, uwanja wa ndege na pamoja na wa shirika la umeme nchini Sudan wamekamatwa kabla ya mgomo wa kitaifa wa kupinga utawala wa kijeshi, linadai kundi kuu la waandamanaji. Chama cha wataalamu wa Sudan kinasema kuwa wafanyikazi pia wanatishiwa na mamlaka nchini. Baraza la jeshi linalotawala nchi hiyo (TMC) halijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo. Jeshi lilichukua uongozi baada ya kumg'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir mwezi Aprili, na kuahidi kurejesha utawala wa kiraia baada ya kipindi cha mpito. Mwandamanaji aliyejeruhiwa mjini Khartoum, Sudan. Lakini wanaharakati wa kupigania demokrasia wanasema kuwa baraza la jeshi haliwezi kuaminiwa baada kuzuka kwa ghasia ambapo wafuasi wengi wa Upinzani waliuawa mjini Khartoum - na wamekata kufanya mazungumzo ya amani na viongozi wa baraza hilo. Huku hayo yakijiri vikosi vya usalama nchini Sudan vimewakamata viongozi watatu wa upinzani baada ya kukutana na waziri mkuu wa Ethiopia mjini Khartoum ili kusaidia katika mazungumzo ya amani. Hali ikoje mjini Khartoum? Baadhi ya maofisi na biashara zimefungwa na idadi ya magari ni chache barabarani, anasema mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga ambaye anafuatilia matukio nchini Sudan. Kumeripotiwa milio ya risasi huku maafisa wa usalama wakiendelea kushika doria katika baadhi ya sehemu za mji waKhartoum. Idadi ya waandamanaji waliouawa Sudan yaongezeka Viongozi wa maandamano wametoa wito kwa watu kusalia majumbani mwao na kususia kazi kama sehemu ya kupinga utawala uliyopo madarakani. Wanasema maandamano hayawezi tena kufanyika kutokana na msako mkali unaoendeshwa na vikosi vya usalama. "Viguvugu la kususia kazi linaanza Jumapili na litaendelea hadi pale utawala wa kiraia utakapopatikana," taarifa ya SPA ilisema. "Mgomo wa kususia kazi ni hatua ya kisheria na ni silaha hatari sana ambayo inaweza kusambaratisha utawala wowote duniani." Lengo la mgomo ni kuhakikisha serikali inashindwa kuendesha shughuli zake hali itakayoifanya baraza la jeshi kushindwa kutawala, aliongeza mwandishi wetu. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anajaribu kuleta pamoja pande mbili zinazozozana katika meza ya mazungumzo Siku ya Ijumaa , waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alizuru taifa hilo ili kuzipatanisha pande hizo mbili ambazo alikutana nazo katika mikutano miwili tofauti. Lakini saa chache baadaye , habari zilisambaa kuhusu kukamatwa kwa Mohamed Ismat -mwanachama wa muungano wa upinzani na afisa mkuu wa benki kuu nchini Sudan. Baadaye wanajeshi wanadaiwa kumkamata afisa mwandamizi wa SPLM-North Ismail jalab na msemaji Mubarak Ardol. Kiongozi wa chama hicho Yasir Arman pia alikamatwa siku ya Jumatano. Habari za kuzuiliwa kwa viongozi huo zitazua kutoaminika kwa baraza la kijeshi linalotawala. Makundi ya waandamanaji yanapanga kuendelea na kampeni yao siku ya Jumapili. Bwana Esmat na bwana Jalab ni viongozi wakuu wa muungano wa upinzani Freedom for Change , mwavuli wa upinzani unaoshirikisha viongozi wa maandamano na makundi ya waasi. ''Hii ni sawa na baraza la jeshi kusema kwamba linapinga juhudu za mpatanishi waziri mkuu wa Ethiopia ," alisema Khalid Omar Yousef- kiongozi wa muungano wa upinzani akizungumza na shirika la habari la Reuters kufuatia kukamatwa kwa bwana Esmat. Baraza la serikali ya mpito TMC halijatoa tamko lolote. Muhariri wa BBC Mary Harper anasema kuwa hatua hiyo ya hivi karibuni inaonyesha kuwa upatanishi wa waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed haukuchukuliwa na umuhimu mkubwa na jeshi. Baraza hilo linaonekana limepata matumaini ya kisiasa na ufadhili kutoka kwa Saudia , UAE na Misri , mataifa ambayo hayatilii mkazo kuwepo kwa demokrasi nchini humo. RSF, ambalo lilijulikana kama wapiganaji wa Janjaweed lilijipatia umaarufu wake baada ya kutekeleza vitendo vya kikatili katika eneo la Darfur 2003. Wakaazi wa Khartoum wameambia BBC kwamba wanaishi kwa hofu katika mji huo. Baadhi ya wanawake waliokamatwa na RSF waliambia BBC kwamba walipigwa na kutishia kuuawawa. Wanasema kuwa wapiganaji hao waliwataka kunusru maisha yao na baadaye wakawafyatulia risasi. Waathiriwa wengine wanasema walilazimishwa kunywa maji taka ambayo yalikuwa yamekojolewa. Siku ya Alhamisi Muungano wa Afrika ulisitisha uanachama wa Sudan mara moja na kuonya kuichukulia hatua zaidi iwapo mamlaka hayatakabidhiwa raia. Je mgogoro huo unaweza kutatuliwa kidiplomasia? Siku ya Alhamisi Muungano wa Afrika ulisitisha uanachama wa Sudan mara moja na kuonya kuichukulia hatua zaidi iwapo mamlaka hayatakabidhiwa raia. Mwenyekiti wa tume ya Muungano huo Moussa faki mahamat alitaka uchunguzi wa wazi kufanyiwa mauaji yaliotokea. Wakati wa ziara yake mjini Khartoum , waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alizitaka pande zote mbili kuwa na ujasiri na kukubaliana kuhusu hatua zaitakazolipeleka taifa hilo katika demokrasia. Ripoti zinasema alikuwa amependekeza kuanzisha baraza la utawala wa mpito lenye raia wanane na wanajeshi saba huku kukiwa na rais ambaye atakuwa akibadilishwa mara kwa mara. Haijulikani pendekezo hilo lilichukuliwaje. Vikosi vya Usalama nchini Sudan vimerusha mabomu ya machozi na kutumia risasi halisi kuwatawanya waandamanaji mjini Khartoum. text: Baadhi ya wauza nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi. Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa. Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa. Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote. Wateja wa nyama ya mbwa wakibugia vipande vya nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin ya mwaka uliopita Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo. Mwanaharakati mmoja aliambia BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa. Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangiwa kuchinjwa. Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu. text: Baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samata kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Aston Villa. Mbwana Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya Ulaya. Huko mtaani alikokulia Samatta, watu walikusanyika katika uwanja wa mpira ili kufuatilia mechi hiyo kwa pamoja. Hamu kubwa, matarajio na macho ya wengi hapa ni kwa nyota wao Mbwana Ali Samatta Wananchi hawa wametoka mitaa mbalimbali ya eneo la Mbagala mjini Dar es Salaam kuja kuonyesha mapenzi yao makubwa kwa Sammata. Samatta alianzia kucheza soka katika kiwanja hiki wakati anasoma shule ya jirani hapa hadi alipofikia kucheza soka ya kulipwa. Tangu Mbwana Sammata asajiliwe na Aston Villa na kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya England, timu imejipatia umaarufu na kuongeza washabiki nchini Tanzania, kupitia Mbwana Samatta ambaye ameleta matumaini mapya kwa watanzania na mashabiki wa soka Afrika Mashariki. Hii ni mechi ya kwanza Samata kucheza baada ya kusajiliwa na Aston Villa. Ingawa Samatta hakubahatika kufunga magoli katika mchezo huu lakini kwa hapa Mbagala na Tanzania kwa ujumla, Samata anasalia kuwa mfano wa kuigwa na vijana wengi wenye malengo yakufanikiwa katika mpira wa miguu. Mechi kati ya Aston Villa na Leicester city ilikuwa na mvuto wa aina yake nchini Tanzania hapo jana usiku. text: Spika wa bunge la Uingereza John Bercow Mwanachama wa chama cha kihafidhina aliambia BBC kwamba matamshi yake yamesababisha chuki huku mbunge mmoja akisema kuwa hayafai huku wengine wakidai hafai kupendelea upande mmoja. Bw Bercow alisema pingamizi dhidi ya ''ubaguzi wa rangi na ule wa kijinsia'' zinapaswa kuangaziwa sana na wanachama wa bunge hilo. Mbunge wa Marekani Joe Wilson alisema kuwa ni pigo kwa chama cha Trump cha Republican. Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisiasa Eleanor Garnier amesema kuwa ni pigo la kidiplomasia kwamba rais Trump hataruhusiwa kuhutubia bunge la nchi hiyo. Theresa May na Donald Trump Mwezi uliopita waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alisema kuwa rais Trump amekubali mwaliko kutoka kwa malkia wa Uingereza kwa ziara rasmi nchini Uingereza baadaye mwaka huu. Lakini akizungumza bungeni siku ya Jumatatu bw Bercow alisema kuwa anapinga rais Trump kuhutubia mabunge yote kama ilivyo ada na viongozi wengine wa kimataifa. Amesema kulihutubia bunge sio haki bali ni heshima anayopewa kiongozi wa kimataifa. ''Nahisi kwamba pingamizi yetu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na ue wa rangi na haua yetu ya kuunga mkono usawa na uhuru wa mahakama ni muhimu sana na yanapaswa kupewa kipaumbele na wabunge wa Uingereza'', alisema. Spika wa Bunge la Uingereza John Boscow amekosolewa kwa kupinga hatua ya rais Donald Trump kuhutubia bunge la taifa hilo wakati wa ziara yake. text: Katika video yake Bi Denise Nkurunziza anasema ''Wanawake hawakuumbwa kuitwa mama tu. Wana uwezo wa kufanya mambo mengine mengi'' Ukanda wa video wa wimbo huo unaanza kwa picha ya mwanamke anayemkaribisha mume wake nyumbani na kumkaribisha kula chakula cha jioni ambaye anamtemea mate ghafla na kumpiga. "Hauna maanakatika nyumba hii ," asema. "Tumbo lako kila wakati limejaa maharage, huku matumbo ya wanawake wengine yamejaa watoto wachanga." Bi Nkurunziza, mwenye umri wa miaka 49, anaonekana akiingilia kati, akiingia katika sebule ya wanandoa wasio na wa mtoto. Alisikika mwenye akitoa ushauri wa maridhiano, akielezea kwamba: "kusema ukweli unafahamu kuhusu kutokuwa na uwezo wa kuzaa tu baada ya kumuona daktari. "Suala la kutokuwa na uwezo wa kuzaa linaweza kutokea kwa mwanaume au mwanamke ." Katika picha inayofuatia, Mke wa rais, anaonekana akiimba, akidensi na wanenguaji pamoja na wanamuziki wengine. "Wanawake hawakuumbwa kuitwa mama tu. Wana uwezo wa kufanya mambo mengine mengi ," kibwagizo kinaendelea cha wimbo huo Nkurunziza na mkewe wakipanga mstari kwa ajili ya kupiga kura mwaka 2018, wameoana kwa miaka takriban 25 Mke wa Nkurunziza, ambaye ameolewa na rais Pierre Nkurunziza tangu 1994, anawatolea wanaume waliooa kuwasaidia wake zao. " Kutokuwa na uwezo wa kuzaa kunawahusisha watu wawili na kutokuwa na uwezo wa kuzaa hakupaswi kuwa chanzo cha mzozo," anaimba. Nkurunziza na mkewe ambao wana watoto watano pamoja na kuwaasili wengine kadhaa , wanafahamika kuwa ni watu walioshika dini sana na mara kwa mara wamekuwa wakiandaa mikutano ya maombi pamoja. Bi Nkurunziza, ambaye wakati mmoja alifanya kazi kama afisa wa uhamiaji, ni mchungaji aliyetawazwa. Wimba wake huo mpya kwa jina - Umukenyezi Arengeye Kuvyara Gusa (mwanamke ni zaidi ya kuzaa tu ) - ambao ulishirikishwa katika mtandao wa WhatsApp mapema wiki hii inaonekana kuwa ni mara ya kwanza kutoa video ya wimbo usio wa kidini. Bi Nkurunziza amekuwa akionekana wakati mwingine katika nyimbo za kidini, na katika kwaya ya kanisa. Video hiyo ya dakika nne pia imeshirikishwa katika mtandao wa Facebook: Denise Nkurunziza akiimba katika wimbo wake mpya Mke huyo wa rais amepata sifa kutoka kwakatika mitandao ya kijamii kutokana na video yake ya hivi karibuni, ingawa baadhi wamesema wanaume wanaweza pia kukabiliwa na unyanyasaji kutoka kwa wake zao. Katika jamii ya Burundi yenye mfumo dume, wanandoa wanafanywa wajihisi kuaibika pale wanapokuwa hawana watoto - na kutokuwa kwao na kwa kawaida mwanamke huwa ndiye anayelaumiwa pale wanandoa wanaposhindwa kupata mtoto. Baadhi ya wanandoa hulazimika kuachana kutokana wanaposhindwa kuzaa pamoja. Mke wa rais wa Burundi Denise Nkurunziza ametoa wimbo wa kampeni ya kupambana unyanyasaji wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliana nayo. text: Iran iliwanyonga takriban watu 1,000 mwaka uliopita kwa mujibu wa Amnesty international Mkuu wa mashtaka aliyenukuliwa akiongea na kituo komoja cha televisheni amesema kuwa watu hao walihusishwa na mauaji ya watu 20 kwa milipuko na mashambulizi mengine Magharibi mwa Iran. Utawala unasema kuwa watu hao walikuwa sehemu ya kundi moja lenye siasa kali ambalo liliwaua viongozi wa Sunni mwaka 2009. Vyombo vya habari vya dola vinawalaumu kwa mauaji ya wanawake na watoto kati ya mwaka wa 2009 na 2011. Iran, ambayo inaidadi kubwa ya wa-Shia, inadaiwa kuwa imewanyonga takriban watu 977 mwaka uliopita kwa mujibu wa shirika la kupigania haki za kibinadamu la Amnesty International. Mashirika ya kutete haki za kibinadamu yamefutilia mbali madai ya wahanga hao kusikizwa katika mahakama yakidai ilikuwa ni porojo tu. Mashirika hayo yanamtaja Shahram Ahmadi, ambaye wanadai hukumu dhidi yake ilitolewa baada ya kupigwa na kulazimishwa kukiri makosa aliyodaiwa kufanya. Mkuu wa mashtaka Mohammad Javad Montazeri amesema kuwa wakurdi hao walikuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Tawhid na Jihad. China mwaka jana iliwanyonga takriban watu 1000. Mataifa mengine yaliyowanyonga watu wengi ni Pakistan - 326 na Saudi Arabia iliyowatia kitanzi watu 158. Watu 20 wanaoushukiwa kuwa wanachama kwa kile utawala nchini Iran unakitaja kuwa kundi la kigaidi la Sunni wamenyongwa . text: Aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha CCM Abdulrahman Kinana Ameyataja mambo hayo matatu katika sherehe ya kumuaga ilioandaliwa na wabunge hao huku wakimkaribisha rasmi katibu mkuu mpya wa chama hicho Bashiru Ally. Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini Tanzania, anasema kuwa CCM imekuwa na baadhi ya makatibu wakuu walioondoka . ''Nilitumia uwezo wangu wote kujitolea kufanya kazi kwa bidii na kutumia uzoefu wangu ili kuhudumu.Ninyi ndio mahakimu wangu, je nilifanya kama ilivyohitajika? Kinana aliendelea kusema kwamba iwapo kuna matatizo yoyote basi yalikuwa yake. Na iwapo kulikuwa na ufanisi basi ulitokana na ushirikiano wa wanachama wote wa CCM na wabunge. CCM sio chama cha viongozi, ni chama cha wananchi. Chama chetu bado kina nguvu, kinapendwa na kuheshimiwa ndani na nje ya mpaka wetu. ''Chama kiko sawa kilivyo'', Kinana alisema. Amesema kile kilicholeta ufanisi katika chama na kile ambacho kinafaa kuendelea kutekelezwa ni mambo matatu. ''Tunafaa kutekeleza ahadi tulizotoa kwa raia kwa kuwa ziko katika manifesto yetu, kujiandaa kwa chaguzi ndogo na kujiandaa kwa uchaguzi mkubwa. Aliongezea: Iwapo serikali itatekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi , wananchi wataendelea kuiamini. Na iwapo serikali itaangazia matatizo yanayowakumba wananchi watahisi kufarijiwa na mutaendelea kuchaguliwa kwa idadi kubwa. Na mwisho wa siku CCM itaendelea kuongoza. Aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi nchini Tanzania CCM, Abdulrahman Kinana amewaaga wabunge wa chama hicho, huku akiwaachia wasia kuhusu vitu vitatu ambavyo wanafaa kufanya ili kuleta amani miongoni mwa Watanzania. text: Daniel Sturridge's dog Lucci has been safely returned to the former England international Sturridge, 29, alisema yupo tayari kutoa kiwango chochote cha pesa ili kumpata mbwa huyo ambaye alipotea baada ya nyumba yake nchini Marekani kuvunjwa na wezi. Video na picha za mbwa huyo zilichapishwa mitandaoni na baada ya hapo akarejeshwa kwa mmiliki wake halali. "Siamini," Sturridge amesema katika video aliyochapisha kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. "Nataka tu kusema asante kwa kila mtu mitandaoni aliyeniunga mkono na kupaza sauti. Ninashukuru sana." Sturridge hata hivyo hakusema kama alitoa pesa kwa mtu aliyemrejesha. Awali mchezaji huyo alisema tukio hilo limetokea alipokuwa kwenye matembezi Jumatatu usiku. "Tutalipa kiasi chochote kile ili kumpata mbwa wetu," amesema Sturridge. "Yoyote atakayemrudisha mbwa wangu (atapata) elfu 20, elfu 30 (pauni), kiasi chochote kile." Sturridge pia ametuma picha nne za mbwa huyo na pia video zinazoonesha wanaaume watatu waliojifunika uso wakiingia kwenye nyumba hiyo. Sturridge, kwa saasa anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Aston Villa ambayo inarejea EPL msimu ujao utaoanza Agosti. Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge amesema ana furaha isiyo kifani kwa kumpata mbwa wake aliyepotea aitwaye Lucci. text: Askofu Josephat Gwajima amekanusha kuhusika na mkanda wa video ya ngono na kusema hilo ni shambulio dhidi yake. Kwa mujib wa Gwajima, video hiyo imetengenezwa na aliowaita maadui zake ambao wanalenga 'kumnyamazisha'. Akiongea na wanahabari kwenye viunga vya kanisa lake jijini Dar es Salaam, Gwajima amesema msimamo wake na maono juu ya nchi ndiyo yamefanya kusingiziwa kashfa hiyo. "Watu wanafanya haya ili nikose sauti. Wanasema 'tumpige Gwajima ili anyamaze.'" amesema na kuongeza: "Hizi picha zinajaribu kunichafua, lakini hawawezi." Gwajima, ambaye pia amekuwa pia kwa namna moja ama nyengine akihusishwa ama kuhusika na siasa amesema: "Uchaguzi unakuja mwaka kesho (2020) na wanajua nina nguvu, hawataki niwe na sauti yoyote." Hata hivyo, Gwajima hakuwataja kwa majina hao aliowaita kuwa ni maadui zake. Video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya Gwajima inamuonesha akiwa faragha na mwanamke wakifanya tendo la ngono. Na mtu anayedhaniwa kuwa ni Gwajima ndiye alikuwa akiichukua video hiyo kwa kutumia kamera ya mbele ya kifaa ambacho hakionekani. "Ni mwanaume gani ambaye mwenye akili zake timamu anayeweza kujirekodi wakati akifanya tendo la ndoa? Haingii akilini," amejitetea Gwajima na kuongeza, "Zile ni picha za kuunganisha. Wametumia picha yangu moja ya kifamilia nikiwa kifua wazi na kuunganisha na picha nyengine ili wanichafue." "...mkono wa huyo mtu anayejichukua ile video ni mkubwa, ni mkono wa 'baunsa' sio huu mkono wangu mdogo." Gwajima pia amewaambia wanahabari kuwa tayari amesharipoti tukio hilo kwa mamlaka husika na kusema anatumai mtu aliyechapisha picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram atakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Askofu huyo aliambatana na viongozi wenzake wa kanisa lake pamoja na mkewe ambaye ameeleza kuwa ana imani na mumewe. "...mimi ni jasiri kama Simba. Ukweli naufahamu. Mume wangu ninamfahamu na ninamwamini. Mungu akiwa upande wetu hakuna wa kutushinda," amesema Bi Gwajima. Polisi waanza uchunguzi Wakati huohuo, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), wameanza uchunguzi juu ya video ya ngono 'inayomhusisha' Askofu Gwajima. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Mei 8, 2019 na Kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, imeeleza kuwa Mei 7,2019 kuna video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasiojulikana ikionyesha mtu anayefanana na mchungaji huyo akiwa na mwanamke asiyefahamika. "Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limeanza uchunguzi wa video hiyo mara moja na linapenda kuwapa taarifa wananchi (kuwa) Gwajima siyo mtuhumiwa, ni muathirika wa tukio hilo kwani tukio hilo linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa nia ya kutaka kuharibu heshima yake kwa jamii na waumini," amesema Mambosasa. Taarifa hiyo imesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza video hiyo kwa maelezo kuwa ni kosa la jinai na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu kwani uchunguzi unaendelea ili kubaini aliyeisambaza na lengo la kufanya hivyo. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Tanzania, Josephat Gwajima amekanusha kuhusika na video ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii. text: Alafu kuongezea kwamba "Wadukuzi walifanikiwa kuweka mfumo wa uangalizi" na kitengo cha habari cha kampuni hiyo wana kibarua kikubwa mikononi mwao. WhatsApp linasema akaunti kadhaa zililengwa na " mdukuzi mkuu wa mitandao". Lakini iwapo kauli hii imekutia wasiwasi, haya ni baadhi ya mambo unayostahili kufanya kuhakikisha mawasiliano yako yapo salama. Imarisha mfumo wa kinga katika simu yako mara kwa mara Udukuzi huo uligunduliwa kwanza mapema mwezi huu. Wakati huo Facebook, inayomiliki mtandao wa WhatsApp, iliwaambia maafisa wa usalama kwamba lilikuwa : "pengo katika mawasiliano ya sauti ya WhatsApp VOIP [voice over internet protocol] iliyoruhusu udukuzi kupitia vifurushi vya mfumo wa SRTCP [secure real-time transport protocol] vilivyotumwa kwa nambari ya simu ya mlengwa." Sawa. Hebu tulifasiri hilo - ina maana wadukuzi walitumia simu ya WhatsApp kupiga kwa nambari ya mlengwa. Hata kama simu haikushikwa, mfumo huo wa udukuzi uliidhinishwa kutokana na pengo hilo katika mawasiliano ya sauti ambao hauna usalama wa kutosha. Simu pengine ilikatika na haionekani kwenye orodha ya waliopiga simu katika simu yenyewe, kwasababu wadukuzi walikuwa tayari wameidhibiti. Imarisha 'updates' - kwasababu mara nyingi huwa umeimarisha kinga kwa simu yako Hapana, sio kwamba ukiizima simu na kuiwasha utakuwa umetatua tatizo. Siku ya Jumatatu , WhatsApp ilependekeza wateja bilioni 1.5 waimarishe programmu hiyo tumishi baada ya kusambaza mfumo huo mpya ulionuiwa kulinda vifaa vinavyotumia mtandao huo dhidi ya udukuzi. Licha ya kwamba WhatsApp inalinda mawasiliano ya wateja wake, inayomaanisha kwamba ujumbe unaonekana upande wa anayeupokea pekee, mfumo huo wa udukuzi ungemruhusu mshambuliaji aweze kuusoma ujumbe huo. Kwa hivyo ni vyema uimarishe 'updates' - kwasababu mara nyingi huwa umeimarisha kinga kwa simu yako. Usihifadhi taarifa zako kwenye anga la mtandao Licha ya kwamba mawasiliano yanalindwa katika WhatsApp, epuka kuhifadhi taarifa zako kwenye anga la mtandao kama Google Drive au iCloud, hapo kuna tatizo. Anga hilo la mtandao halina usalama kwahivyo mtu yoyote anaweza kuingia na kuyafikia mawaslinao yako yote. Iwapo unajali faragha, basi hilo ni jambo ambalo unapaswa kufikiria kuacha kulifanya. Huenda ukapata ujumbe kwamba hifadhi mawasiliano yako - lakini iwapo unataka kulibadili hilo hivi sasa nenda kwenye eneo la kuhifadhi chati zako yaani Chat Backup, katika eneo la mpangilio wa simu yako - settings. Programu saidizi za kuimarisha ulinzi Kuna programu saidizi za kuimarisha ulinzi, uthibitisho wa mara mbili (2FA) kabla kuingia kwenye mtandao huo ambao ni njia nzuri ya kuweka data yako salama. Ni kama wingu la ziada la usalama kuhakikisha watu wanaojaribu kuingia katika akaunti ya mtandao ni watu asili wanaosemakuwa ni wao. Kwanza, mteja ataingiza jina lake na nywila. Baada ya hapo watahitajika kutoa alama za vidole, au sauti yao au nambari maalum zitakazotumwa na programu hiyo kwenye simu yako ambazo utatumia kufungua na kuingia kwenye akaunti ya Whatsapp na nyinginezo za kijamii. Unaweza kulibadili hilo pia kwenye upande wa mpangilio wako wa simu. Isikukoseshe usingizi Udukuzi huu huenda ni jambo la dharura iwapo wewe ni wakili, mwanaharakati, au mwandishi habari. Kwa mujibu wa kamati ya kuwalinda waandishi habari, huenda hawa ndio watu ambao wamelengwa katika udukuzi huu. Taarifa kwamba "WhatsApp inaweza kudukuliwa" sio jambo ambalo mtumiaji yoyote wa mtandao huo wa kijamii anataka kusikia wala kuona katika kichwa cha habari. text: Kila mtu na imani yake, baadhi ya kina mama huamini kujua jinsia ya mtoto mapema ni kutafuta mikosi. Lakini wengine huamini ni jambo jema kwani inakupa fursa ya kujiandaa na vitu muhimu vya mtoto, kwa mfano mavazi na pia jina la mtoto. Wanawake wa kisasa hupendelea zaidi kujua jinsia ili waweze kuandaa sherehe maalumu inayoitwa Baby Shower. Katika sherehe hii akina mama hawa huweka wazi jinsia ya mtoto kwa kupamba mandari ya pinki kwa mtoto wa kike na buluu kwa mtoto wa kiume. Baadhi hupokea zawadi zenye rangi mbali mbali zisizobagua jinsia mfano rangi nyeupe, kijivu, njano na hata nyeusi na nyekundu. Si wote wanaotafuta kujua jinsia ya mtoto mapema kwa ajili ya sherehe, wengine hutafuta kujua ili wajiandae na mavazi ya mtoto. Baadhi ya kina mama hufurahia zaidi kufanya sherehe ya kumkaribisha mtoto punde wanapo jua jinsia. Katika harakati za kufahamu jinsia ya mtoto kitamaduni kuna mambo mengi sana hufanyika, kwani baadhi hutoa majibu ya jinsia ya mtoto kwa kumwangalia mama mjamzito kwa macho tu. Hawa huamini mwonekano wa mama anapokuwa na mimba unatafsiri amebeba mtoto wa jinsia gani. Mtoto wa kike ana wivu? Baadhi husema mama mjamzito akivimba na kuharibika sura maana yake amebeba mtoto wa kike, kwani mtoto wa kike anawivu. Lakini kama mama mjamzito anapendeza ngozi sura na shepu huyu amebeba mtoto wa kiume kwa sababu watoo wa kiume hawana wivu. Lakini njia inayoaminika zaidi ni kutazama jinsia kwa kutumia kifaa maalumu cha hospitali yaani kufanya Ultrasound. BBC imezungumza na baadhi ya kina mama kufahamu mtazamo wao juu ya kuangalia jinsia ya mtoto. Mama Janeth yeye anaumri kati ya miaka kati ya 55 na 63 anasema hajui lolote kuhusu kuangalia mtoto akiwa tumboni na haaminikuna manufaa ya kufanya hivyo. "Mimi sijawahi kuangalia jinsia ya mtoto, kwanza unaangalia vya nini? Kwa kweli kusema ukweli mimi sijui kabisa kuhusu hicho kitu," anasema mama Janeth. Naye Viola, mama wa watoto watatu, anasema alikuwa na hamu ya kujua jinsia lakini awali hakukubaliana na matokeo ya daktari akataka mpaka ajifungue ndio aamini. "Mimi kikubwa kilichonisukuma ni kwa sababu nilikuwa na wawili wa kiume mmoja wa kike kwa hivyo nafsi yangu nlitamani nizae mwingine wa kike kwa hiyo nikaangalia lakini nlipoambiwa wa kiume sikuamini. Yaani mpaka nikanunua vitu vya mtoto vya rangi zisizobagua basi nilipojifungua kuona kweli wa kiume ndo nikaamini," Violla anaiambia BBC. BBC pia imezungumza na mama wa watoto wa wili Joyce Mbogo yeye anasema mambo yamebadilika sasa. "Watu wanaenda na wakati halafu pia tunapenda kufanya maandalizi ya mtoto. Ujue siku hizi sio kama zamani kipindi mtoto anavaa nguo yoyote ya rangi yoyote, siku hizi nmambo yamebadilika. Kama ni mtoto wa kike aonekane ki-kike zaidi na kama ni wa kiume aonekane kiume zaidi," Joyce anaiambia BBC. Joyce anasema kufahamu jinsia kulimsaidia kujiandaa vyema "Kwa sababu hata mimi nilifanya kwa mtoto wangu wa kwanza, ilinisaidia nikaandaa vitu vya mtoto mvulana, yaani ni kitu kizuri," Wapo wale ambao wanatajiwa jinsia ya mtoto lakini hawakutaka kujua. "Yaani daktari aliponiambia tu mtoto wako wa kiume, nililia kama mtoto kwa sababu mimi hua siamini katika hizo habari. Niache na mimba yangu napokea mtoto yeyote ninayeletewa na mwenyezi Mungu," Aisha ameiambia BBC. Kuna madhara yoyote? Dkt Abdiel Mmile kutoka katika hospitali ya BOCHI jijini Dar es Salaam, anasema hakuna madhara yoyote japo waweza pata changamoto ya kisaikolojia. "Kwa mfano una watoto wawili au watatu wa jinsia moja alafu ukapata majibu mtoto aliye tumboni ni wa jinsia ileile, unaathirika kisaikolojia na kuna uwezekano wa kupuuzia huo ujauzito kidogo," anasema. "Kitaalamu hakuna madhara ila kisaikolojia hii hali ujitokeza." Jokate: Huwezi kunishusha chini kirahisi Daktari anasema kuwa mwanzoni ilitumika X-Ray kubaini jinsia ya mtoto mtoto lakini baadae ikaonekana kwenye mimba changa si salama kwa sababu ya mionzi nururishi. Kwa hivyo ikaja Ultrasound ambayo yenyewe hutumia sauti ya mawimbi badala ya mionzi. Dkt Mmile anasisitiza kuwa umuhimu wa kuangalia jinsia uliongezeka umaarufu wakati ambapo nchi nyingine ziliweka marufuku ya kuwa na mtoto zaidi ya mmoja mfano China. Wakati huo waliruhusiwa kuchagua jinsia ya mtoto wanayemtaka na waliruhusiwa hata kutoa mimba kama ulitaka mtoto wa kike akaja wa kiume. "Kama unaruhusiwa kuzaa watoto idadi yoyote ile hamna ulazima wa kujua jinsia," Dkt Mmile aliambia BBC. Kufahamu jinsia ya mtoto akiwa tumboni kwa kutumia teknolojia ni mtindo ambao umekuwa ukipata umaarufu, lakini pia kuzua mdahalo mkubwa hasa katika nchini za Kiafrika. text: Luteni Generali Salah Abdelkhalek amesema kuwa baraza la jeshi linaweza kukubali kugawana nafasi za uongozi nafasi sawa na raia Luteni generali Salah Abdelkhalek amesema kwamba labda wanaweza kuzingatia kuwapa nafasi sawa za ujumbe katika baraza hilo. Waandamanaji wanaendelea kuandamana kwa kukaa kwa wingi nje ya ofisi kuu ya jeshi la nchini hiyo wakitaka kuachia madaraka. Raisi Omar al-Bashir aliondolewa kwenye madaraka mwezi Aprili tarehe 11 baada ya kutawala Sudan kwa miaka 30. Na Omar al Bashir aliondolewa madarakani na baraza la mpito la jeshi ambalo limechukua utawala kwa raia kwa kipindi cha miaka miwili, jambo ambalo linapingwa na waandamanaji Viongozi wa waandamanaji wamelishutumu jeshi kukataa kufanya majadiliano kwa nia njema na kuhamasisha maslahi ya Bashir. Viongozi wa Jeshi wanasema kuwa wanahitajika kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa wanaongoza na usalama wa taifa hilo. Wajumbe saba wa baraza ambalo linaongozwa na Luteni generali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, ambaye aliiambia BBC mwezi uliopita kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kama watafikia makubaliano na viongozi wa uraia. Viongozi wa upinzani walisema jana kuwa mapendekezo ya nakala ya katiba kwa baraza la jeshi kueleza mapendekezo waliokuwa nayo katika kipindi hiki cha uongozi wa mpito. Wanasema kwa sasa wanasubiri majibu. Nakala ya mapendekezo na majukumu ya baraza jipya haijaainisha nani atakuepo katika baraza. Umoja wa Afrika ilikabidhi utawala kwa viongozi wa jeshi tarehe 15 Aprili na sasa wana siku 60 au kukutana na baraza la uongozi. Makao makuu ya jeshi la Sudan yana muonekano gani? Picha iliyopigwa na satelite ikionyesha makao makuu ya jeshi katika makao makuu ya Khartoum, eneo ambalo waandamanaji walikusanyika na kubaini kuwa limetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuanza kazi ya utawala . Kutoka angani , inaonyesha wazi picha inaonyesha wazi namna majengo ya jeshi yalivyofanana na muundo wa boti na kuonekana kama ndege. Bashir yuko wapi? Kiongozi wa zamani wa Sudan, Bashir mwenye umri wa miaka 75 amehamishiwa katika gereza la Kobar lililopo mji mkuu wa Khartoum baada ya siku kadhaa tangu amekamatwa. Mwendesha mashitaka ametaka rais wa zamani kuhojiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi . Bashir aliondolewa madarakani tarehe 11 Aprili baada ya kuongoza kwa miaka 30. Afisa wa ngazi ya juu wa baraza la jeshi nchini Sudan ameiambia BBC kuwa haitaruhusu raia kuchukua nafasi za juu katika baraza la uongozi nchini humo wakati wa serikali la mpito. text: Maneno aliyoyasema Dangote wakati huo na aliyoyasema jana akiwa Ikulu jijini Dar Es Salaam ni tofauti kabisa, na yawezekana yakaendeleza mjadala wa utofauti baina ya rais wa sasa wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hasssan na mtangulizi wake hayati John Pombe Magufuli. Katika mkutano huo ulioandaliwa na jarida maarufu la habari za biashara, The Financial Times, Dangote ambaye wakati huo alikuwa tayari ameshafanya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha saruji Tanzania alisema sera za uwekezaji nchini humo zinawaogopesha wawekezaji kutoka nje. Dangote pia alimuonya aliyekuwa rais wa Tanzania wakati huo hayati John Magufuli kuwa wakati umefika "kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini humo." Miaka minne baada ya kukosoa vikali sera za uwekezaji Tanzania, Dangote asema atashawishi wawekezaji kurejea nchini humo. "...sheria mpya zinazoundwa Tanzania zinaiweka nchi hiyo kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena," alisema Dangote. Wakati akiyasema hayo, hayati Magaufuli alikuwa yupo katika kile alichokiita vita ya kiuchumi ambapo awali mwaka huo alianzisha uchunguzi wa kina katika sekta ya madini na 'kubaini uhalifu mkubwa' ambao ulisababishwa kuundwa kwa sheria mpya ya madini. Mwisho wa mzozo huo wa madini ukazaa maafikiano na kampuni kubwa ya madini ulimwenguni ya Barrick na kuunda kwa pamoja na serikali kampuni mpya ya kuchimba madini ya Twiga. 'Milango imefunguka' Mara baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu kufuatia kifo cha Magufuli, Rais Samia hakumung'unya maneno kuhusu hali ya uwekezaji nchini humo. Dangote akutana na Rais Samia na kusema mambo yamebadilika Tanzania Katika hotuba zake za mwanzo, alikemea ubabe wanaofanyiwa wawekezaji pamoja na kutotabirika kwa sera za uwekezaji pamoja na kodi. Rais Samia pia alizungumzia suala la kupewa vichocheo (incentives) kwa wawekezaji wakubwa ili walete miradi nchini Tanzania. Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya biashara na uchumi wanaamini kuwa kulikuwa na mvutano baina ya Dangote na serikali ya Magufuli katika utekelezwaji wa vichocheo ambavyo mwekezaji huyo aliahidiwa na aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ndiye alimkaribisha Tanzania. Akiwa Ikulu jana, Dangote amesema kuwa: "mazingira ya kibiashara yamebadilika ghafla na milango imefunguka... na sasa popote pale nitakapokwenda nitainadi Tanzania na kuwaambia watu kuwa mambo yamebadilika na kila mmoja arejee na kuwekeza kwa nguvu." "Nimempongeza (Rais Samia) kwa mabadiliko muhimu anayoyaleta ... Tutaendeea kuwekeza Tanzania ili kuzalisha ajira, mapato ya nchi na kuinua ustawi wa wananchi, nadhani anahitaji kuungwa mkono katika hili na tumemuahidi kuwa tutaendea kuwekeza kwa kiasi kikubwa hapa Tanzania." Mwezi Oktoba mwaka 2017, akiwa katika mkutano mkubwa wa wakezaji jijini London, bilionea wa Nigeria Aliko Dangote alikosoa vikali sera za uwekezaji nchini Tanzania. text: Mlipuko umesababisha uharibifu katika mskiti huko Herat Msemaji wa polisi katika eneo hilo amesema shambulio hilo limetekelezwa na mlipuaji wa kujitoa muhanga. Hakuna kundi linalodai kuhusika. Shambulio dhidi ya Mskiti wa Jawadia limetokea saa mbili usiku wakati mamia ya waumini walipokuwa wanaswali swala ya jioni. Mskiti huo upo katika eneo la mji wa Herat ulio na idadi kubwa ya wasilamu wa madhehebu ya Shia. Afisa wa serikali ameiambia BBC kwamba mlipuaji wa kujitoa muhanga alifyetua risasi ndani ya mskiti kabla ya kujilipua. Herat, mji uliopo karibu na mpaka na Iran, unatazamwa kuwa mojawapo ya miji ya amani Afghanistan. Katika mwaka uliopita, kundi la Islamic State limelenga maeneo ya Shia katika sehemu nyingi nchini. Siku ya Jumatatu kundi hilo limekiri kuhusika na shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya ubalozi wa Iraq katika mji mkuu Kabul. Milipuko na risasi zilizofyetuliwa katika mji uliopo Afghanistan magharibi - Herat imesababisha vifo vya watu takriban 30 na kusababisha wengine wengi kujeruhiwa. text: Waandishi wa BBC Chioma Obianinwa na Nnamdi Agbanelo, pamoja na dereva wao, Ndubuisi Nwafor, walikuwa wameandamana kasisi mwingine wa kanisa katoliki, Father Cajethan Obiekezie na naibu wake Solomon Orakam, kwenda katika kanisa la padri Mbaka jumatano asubuhi. Kasisi Obiekezie alikuwa amepanga mahojiano na Padre Mbaka, lakini mahojiano hayo hayakufanyika kwasababu alikuwa akiongoza ibada. Waandishi wa BBC wakiongozwa na Padre Obiekezie, walienda nyumbani kwa kasisi Mbaka kufanya mahojiano karibu saa kumi na moja jioni. Kasisi Mbaka alipofika nyumbani, waandishi wa BBC waliokuwa wakimsubiri ndani ya gari walipoenda kuongea naye, ghafla walizingirwa na wanaume 20. Kwa mujibu wa Obianinwa wa BBC, wanaume hao walikuwa wamejihami kwa mapanga na walikuwa wanatishia kuwaua kwa kuandika "taarifa mbaya kumhusu Mbaka". "Mbaka alituomba tusubiri hadi mwisho wa shughuli za kanisa ili tufanye mahojiano. Wanaume hao waliokuwa nje ya nyumba yake walisema BBC Idhaa ya Igbo wanaandika taarifa mbaya kumhusu Mbaka na kuanza kuwapiga Nnamdi, Solomon na Ndubuisi. Waliwashambulia kwa makonde mazito mwili mzima'',Obianinwa alisema. Kasisi Mbaka aliwatukana na kuwafokea kwa sauti ya juu waandishi wa BBC Mwandishi huyo wa BBC aidha alisema kasisi Mbaka na kasisi Obiekezie walitoka ndani ya nyumba waliposikia kelele na kisha kasisi Mbaka akaanza kumkaripia na kumnyoshea kidole akiimwita"shatani". "Hatua hiyo iliwachochea wanaume hao kuendelea kuwashambulia huku kasisi Mbaka akiendelea kupiga kelele na kututukana. Aliwaambia wanaume hao kuchukua simu na kamera zetu. Walisema watatuua na hakuna kitu kitafanyika. Walinivua wigi langu na kujaribu kumyonga Nnamdi. Kasisi Obiekezie alikuwa akiwaambia waache kutushambulia lakini yeye pia hakusazwa walimpigwa na kumpokonya simu," alisema. Kasisi maarufu wa Nigeria Ejike Mbaka na baadhi ya waumini wa kanisa lake wamewatukana na kuwashambulia waandishi wa BBC na watu wengine wawili katika jimbo la kusini mashariki la Enugu Jumatano jioni. text: Hotuba ya wazi inayofahamika kutoka kwa Rais Bouteflika ilikua mwaka 2014 Hakuna aliyeamini ilipotangazwa kuwa Abdelaziz Bouteflika anawania awamu ya tano mwezi Aprili-hata mwenyewe hakujitokeza binafsi siku ya Jumapili kujisajili kuwania nafasi hiyo . Waalimu, wanafunzi, wanasheria hata waandishi wa habari waliingia mitaani kuandamana wakiwa na hasira , walionekana kutokubaliana na hatua ya kuongozwa na mtu ambaye haonekani. Wengi wanahofu kuwa kutopatikana kwa mrithi wa Rais Bouteflika, ambaye aliingia madarakani mwaka 1999, kunaweza kusababisha hali ya usalama kuyumba nchini humo. Kiongozi wa kwenye TV Kwa mara ya mwisho alionekana akihutubia Umma mwaka 2014 -hotuba ya shukrani kwa raia wa Algeria kwa kuuamini utawala wake baaa ya kushinda uchaguzi uliokuwa umetangulia. Aliahidi kutekeleza suala la mgawanyo wa madaraka, kuupa nguvu upinzani na kuhakikisha haki za raia zinafuatwa. Baadhi waliona kuwa hii ni ishara ya mabadiliko ya sera katika uongozi , lakini hakua ushahidi wa kuonekana kwake kwa muda mrefu. Rais wa Algeria amtimua Waziri mkuu Miss Algeria 'mweusi' abaguliwa Raia wa nchi hiyo wamekua wakibahatika kumuona mara chache kwenye Televisheni akisalimiana na ujumbe kutoka nchi za kigeni wanaofika nchini Algeria. Au kumuona kwenye ufunguzi wa mkutano mwaka 2016-akionekana amekaa kwenye kiti cha magurudumu, akionekana dhaifu, mwenye uchovu lakini mwenye tahadhari Mpaka mwaka 2018,ikawa wazi kuwa Chama chake kimempendekeza kuwania tena uchaguzi wa mwaka huu. Alikua kwenye ufunguzi wa Msikiti na vituo vya treni za umeme katika mji mkuu wa Algiers.Wiki chache baadae alikua kwenye ziara kutazama ujenzi wa Msikiti mkubwa wa tatu duniani uliogharimu dola za Marekani bilioni mbili. Upinzani Kiongozi huyo alishinda uchaguzi wa mwaka 2014, ingawa hakuwa na Kampeni zozote, mpaka sasa hana wapinzani wenye nguvu Utawala wa Muammar Gaddafi nchini Libya ulionyesha kutoaminiwa baada ya kuruhusu mtu mmoja kutawala Kwa nini sasa chama tawala na upinzani umeshindwa kupata wagombea wanaofaa Upinzani una historia ya kugawanyika.Na chama tawala National Liberation Front kimetawala tangu Algeria ilipopata uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1962 baada ya miaka saba ya vita vya nchini humo. Wachambuzi wa siasa za nchini Algeria wanaona kuwa vijana wenye nguvu wananyang'anywa nguvu zao za uongozi na wazee.,Anaeleza mwandishi maarufu wa vitabu nchini Algeria, James McDougal kutoka chuo kikuu cha Oxford ameiambia BBC. Amesema nchi imekabidhiwa mgombea ambaye ''yu karibu kufa''. Waandamanaji wakionyesha alama inayowakilisha Rais Bouteflika ambaye hutumia kiti cha magurudumu Siku ya Jumapili,Rais Bouteflika kwa mara nyingine aliahidi kutoa nafasi ya kufanyika mazungumzo-na kusaidia mchakato wa mabadiliko ya katiba kwenye suala la duru ya pili ya uchaguzi.Ahadi hiyo ilikuja kwa mtindo wa barua iliyosomwa na mtangazaji kwenye kituo cha Televisheni cha taifa. Kipya katika ahadi zake ni kuwa ataongoza mchakato wa uchaguzi ambao yeye mwenyewe hatashiriki. Hiyo ingetoa fursa kuwahakikishia mbadilishano wa madaraka katika hali ya amani, haraka sana ikizingatiwa hali yake ya kiafya. Lakini Algeria bado ina changamoto nyingi kuliko kile kinachoelezwa na waangalizi wa kikanda kuwa changamoto ni kubwa kuliko matatizo ya kiafya ya rais Bouteflika. Kwa raia wengi wa Algeria ni vigumu kuelewa ni kwa vipi rais wao mwenye miaka 82 ,aliyeugua kiharusi miaka sita iliyopita na kupata shida kwenye kutembea au kuzungumza anaweza kuongoza nchi. text: Kikwete: Viongozi wa upinzani sio maadui wa serikali Afrika Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Afrika Kuhusu uongozi bora na sheria uliofanyika mjini Johannesburg, Kikwete alitoa changamoto kwa vyama vya kisiasa barani Afrika kushirikiana. Alisema badala ya kuuchukulia upinzani kuwa adui, wanafaa kuchukuliwa kuwa washirika katika kuimarisha demokrasia inayoheshimu sheria. Kufuatia taarifa hiyo mchanganuzi wa maswala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha kikatholiki cha Ruaha Prof Gaudence Mpangala alinukuliwa na gazeti la The Citizen nchini Tanzania akisema kuwa taarifa hiyo ya rais Kikwete inafaa kupongezwa. Bwana Mpangala amesema kuwa ni muhimu kwamba taarifa hiyo inatoka kwa kiongozi mwandamizi katika chama cha CCM. ''Tunaunga mkono taarifa ya Kikwete. Kuna tatizo kubwa na tunahitaji kutafuta suluhu ya kukabiliana nalo, Bwana Mpangala alinukuliwa na gazeti la The Citizen nchini Tanzania akisema. Akiongezea: Kuendelea kuwanyima wapinzani haki ya kutekeleza wajibu wao ni sawa na kuwanyima raia haki zao kimaendeleo. Kwa mujibu wa gazeti hilo bwana Mpangala amesema kuwa matatizo mengi yanayokabili Afrika yanatokana na ukandamizaji wa sera za kidemokrasia. Vilevile mwalimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Richard Mbunda amesema kuwa ushauri wa rais Kikwete unaonyesha kitu ambacho alikuwa akifanya katika uongozi wake wa miaka 10 nchini Tanzania. Akizungumza na The Citizen alisema: Tumefanikiwa pakubwa katika kukuza demokrasia na kuheshimu sheria katika miaka ya nyuma lakini sasa tunarudi nyuma. ''Ni lazima turudi katika mwelelekeo unaofaa'', alisema akiongezea :hii tabia ya watawala kuwachukulia wapinzani kama maadui inaufanya upinzani kuitazama serikali kama aduia wake''. Naye mshirikishi wa muungano wa watetezi wa haki za kibinaadamu THRDC bwana Onesmus Ole Ngurumwa amesema kuwa taarifa ya rais Kikwete ni funzo kubwa kwa wanasiasa barani Afrika na husuaan Tanzania. Amewataka viongozi wa zamani kujitokeza hadharani na kuliangazia tatizo hilo huku akiwashauri wapinzani kutoogopa kufanya mazungumzo na rais Magufuli ili kutafiut suluhu ya kudumu. ''Kenya ni mfano mzuri kwetu katika eneo hili.Upinzani unatumia uhuru wa kidemokrasia na imesaidia kundoa hali ya wasiwasi mbali na kuimarisha maenedeleo''.alisema. Wito wa rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa vyama tawala barani Afrika kutowachukulia viongozi wa upinzani kuwa maadui na badala yake kuwafanya kuwa washirika wakuu umeungwa mkono na wengi. text: Bondia Cassius Clay Jr alibadilisha jina lake na kujiita Muhammad Ali wakati alipobadili dini na kuwa mwislamu. Pia walitaka kujua ni majina gani yaliopewa wavulana na wasichana kwa kiwango sawa na iwapo ni lini jina Doris lilikuwa maarufu. Haya hapa majibu yake Je Muhammad ndio jina maarufu miongoni mwa wavulana? Mwanariadha wa mbio ndefu Mo Farah jina lake kamili ni Sir Mohamed Muktar Jama Farah CBE Jina Oliver lilishikilia umaarufu wa kuwa jina lenye umaarufu zaidi miongoni mwa wanaume tangu mwaka 2013, kulingana na ofisi ya takwimu za kitaifa, Idadi kubwa ya wasomaji waliuliza iwapo kuchanganya pamoja herufi za jina Muhammad kutamaanisha kwamba watoto zaidi wangepewa jina hilo badala ya Oliver. Muhammad , ni jina lenye herufi ililopatiwa watoto waliozaliwa 2017, lilikuwa la 10 kwa umaarufu miongoni mwa wavulana kwa jumla. Oliver aliongoza orodha ya 2017 likiwa na watoto 6,259 huku watoto walio na jina Muhammad wakisajiliwa kuwa mara 3,691 bila kuongeza majina yaliongezwa kama vile Muhammad-Ali. Iwapo tutajumlisha herufi 14 tofauti ikiwemo data tutapata wavulana 7,307 ambayo ni zaidi ya 1000 kushinda jina la Oliver. Tofauti ni Muhammad, Mohammed, Mohammad, Muhammed, Mohamed, Mohamad, Muhamad, Muhamed, Mohamud, Mohummad, Mohummed, Mouhamed, Mohammod and Mouhamad. Hatahivyo herufi hizo uhisabika tofauti na inayaoorodhesha tofauti kulingana na jina la mtu linavyojitokeza katika cheti cha kuzaliwa. Kuchanganya herufi za jina fulani kunaharibu orodha hiyo, kwa mfano kujumlisha majina ya Sophie, Sophia na Sofia katika orodha ya wasichana ya 2015 kutaondoa jina la Amelia ambalo ndilo lililokuwa likiongoza kwa umaarufu. Takwimu zinasema kuwa kujumlisha majina yalio na herufi za kufanana kunahitaji mtu kufanya uamuzi mwafaka kuhusu iwapo baadhi ya majina yana tofauti ama la. Kwa mfano watahitajika kuamua iwapo kuchukulia majina ya Sara na Sarah kama majina tofauti licha ya kwamba watu wengi huyatamka tofauti. Je ni jina gani lililo na umaarufu mkubwa katika jinsia zote mbili? Muigizaji Avery Brooks alihusika katika filamu ya Star Trek: Deep Space Nine "Je ni jina gani linalotumiwa na jinsia zote mbili likiwa na idadi sawa ya wavulana na wasichana wanalolitumia . Avery lilikuwa jina maarufu lililotumiwa na jinsia zote mbili likiwa na idadi sawa ya wavulana na wasichana. Kulikuwa na majina 28 katika orodha ya wavulana 6,164 na wavulana 7,508 ambayo yalipatiwa idadi sawa ya jinsia zote mbili. Avery lilikuwa jina maarufu lililopewa jinsia zote 2017 . Lilipatiwa watoto 130 , ikiwemo wavulana 65 na wasichana 65. Jina hilo liliorodheshwa la 851 miongoni mwa wavulana 581 na 637 miongoni wa wasichana mwaka 2017. Ni lini ambapo jina Doris lilikuwa maarufu miongoni mwa wasichana? Wakati Doris Day alipozaliwa nchini Marekani 1992 jina lake lilikuwa miongoni mwa kumi bora nchini Uingereza na Wales Doris lilikuwa miongoni mwa majina kumi bora kati ya mwaka 1904 na1944. Jina hilo liliorodheshwa la tatu 1904 na1914, na kuwa katika nafasi ya saba 1924 na 33rd mwaka 1934. Oliver lilitangazwa kuwa jina maarufu zaidi miongoni mwa wavulana kwa mwaka wa nne mfululizo, lakini baadhi ya wasomaji waliuliza iwapo kuna watoto zaidi walio na jina Muhammad. text: Dereva aliyeruhusu nyani kuendesha basi afutwa kazi India Dereva huyo anafutwa licha abiria hata moja kati ya abiria 30 au zaidi waliokuwa kwenye basi hiyo kutolalamika. Hata hivyo wakati video ya nyani huyo aliyekuwa ametulia huku akiwa usukani kusambaa mitandaoni, waajiri wa dereva huyo walichukua hatua. Maisha ya abiria hayawezi kuwekwa hatarini kwa kuruhusu nyani kushika usukani, msemaji alisema. Hata hivyo hatua hiyo wa waajiri kumfuta dereva haijawafurahisha watumiaji wa mitandao waliofurahishwa na video hiyo. "Vizuri sana, kwa nini mmufute. Angepewa onyo na aambiwe asirudie, mmoaj aliandika katika twitter. Kisa hicho kilitokea siku ya Jumatatu kwa mujibu wa idara ya usafiri wa barabarani ambayo ilikuja kufahammu kuhusu kisa hicho wakati video hiyo ilanza kusambaa. Kwa mujibu wa walioshuhudia, nyani alipanda gari na abiria mwingine lakini akakataa kuketi nyuma bali mbele ya basi. Dereva M Prakash, ambaye alionekana kutotilia maanani sana suala hilo, alimruhusu nyania kuketi kwenye usukani huku wakiendelea na safari. Kulingana ripoti nyania alifika kituo chake akashuka na kumuacha dereva akiendelea na safari yake. Dereva wa basi nchini India amefukuzwa kazi baada ya kumruhusu nyani aendeshe badi lake, text: Kutokana na janga la corona ni mashabiki 1,000 pekee ndio watakuwa na bahati ya kushuhudia pigano hilo katika uwanja wa SSE Arena kumuona Joshua akipigania kuhifadhi taji lake la bingwa wa uzani wa juu mara tatu Japo uwanja huo utakuwa na watu wachache, mamilioni ya watu watakuwa wanafuatilia piano hilo kwenye radio na televisheni huku raia wa Nigeria wakitarajiwa kumshabikia Joshua. Mwana ndondi mwenye umri wa miaka 31- huenda ameshindia Uingereza nishani ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki, lakini ushindi huo unasherehekewa zaidi katika mji wa kusini - magharibi wa Sagamu, Nigeria ambako familia yake inatokea. Alikoanzia Familia ya Joshua inajulikana sana Sagamu ambako mababu walizaliwa. Babu yake mkuu Daniel Adebambo Joshua, tajiri aliyemiliki ardhi na mfanyabiashara anasadikiwa kubatizwa jina lake mwisho baada ya kijiunga na dini ya Kikristo. Daniel alimpelekwa mwanawe wa kiume Isaac Olaseni Joshua kwa msomo nchini Uingereza ambako hatimaye alioana na mwanamke kutoka Ireland na kurudi naye nyumbani Nigeria na kuzaa na kulea watoto saba pamoja. Mmoja wa watoto hao, Robert aliishia kumuoa Yeta Odusanya, pia kutoka Sagamu, ambayeapia ni baba yake Anthony na dada yake Janet. Jina lake la kati kati Olaseni alipewa kwa heshima ya babu yake. Shughuli zake za michezo hivi karibuni zimehakikisha jina la familia linakuwa maarufu sio tu katika mji huo bali pia ndani na nje ya nchi. Kuonesha urithi wake Joshua anajivunia sana chimbuko lake la Nigeria mfano mzuri ukiwa mchoro wa attoo ya Afrika, ikiwa na benders ya Nigeria katika bega lake la kulia. Bendera ya Nigeria huwa inapeperushwa pamoja na bendera ya muung Union Jack ndani ya ulingo wa mapigano. Muziki uliochezwa wakati akiingia ulingoni katika mapigano yake mawili dhidi ya Andy Ruiz Jr. umekuwa wa wasani nyota wa Nigeria kama vile Burna Boy na Femi Kuti, mwana wa kiume wa nguli wa muziki wa Kiafrika Fela Kuti. Mapenzi yake kwa muziki wa Nigeria yanaonekana katika mitandao yake ya kijamiii ambako anyone kana akiweka video yake akiimba nyimbo kutoka nchi hiyo ya Afrika magharibi . Vitu vingine anavyopenda kutoka Nigeria ni vyakula vya kiasili ambavyo pia mara kadhaa hujivunia kuoneshana anavyojua kupika. Upendo wa Joshua kwa Nigeria pia umemfanya kutuma misaada ya chakula Upendo wa Joshua kwa Nigeria pia umemfanya kutuma misaada ya chakula na bidhaa zingine muhimu kwa familia zilizoathiriwa na janga la corona. Hivi karibuni aliandika ujumbe katika mitandao ya kijamii kusimama na vijana waliokuwa wakiandamana kupinga dharma za polisi bnchini Nigeria. Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ni shabiki, wawili hao walikutana mjini London mwezi Januari ambapo Joshua alimpatia mishipi yake. Matukio haya yote yamemfanya kupendwa sana mashabiki wake Wanigeria ambao wanahisi ni mmoja wao kuliko wanandondi wengine wa uzani wa juu waliyokuwa na kizazi cha Nigeria waliyokuwa mbele yake. Henry Akinwande na Samuel Peter wote walishinda mataji WBO na WBC siku zilizopita lakini hakuna hata mmoja wao anayemfikia Joshua kwa umaarufu nchini Nigeria. Kando na hayo, Joshua ana klabubyake ya mashabiki mjini Sagamu ambayo alianzisha mwaka 2017 kabla ya piano lililoimarisha taaluma yake dhidi ya Wladimir Klitschko. "Joshua ameiweka Sagamu kwenye ramani," Azeez Adekunle Okunoren, aka Bwana Naira, mwanzilishi wa klabu ya mashabiki wa Anthony Joshua, aliambia BBC michezo Afrika. "Katika piano lake la mwisho dhidi ya Andy Ruiz, tulionesha piano hilo kwa umma kwenye spring kubwa kwa kutumia projector. "Mashabiki karibu 10,000 walijitokeza kutazama pigano hilo. Baadhi yao walisafiri kutoka miji jirani kujionea. "Hata sasa tumepokea simu nyingi kutoka kwa watu wanaotaka kujua kama tutaonesha pigano la Joshua la leo usiku dhidi ya Pulev." Antony Joshua akiwa na baba yake baada ya kumchapa Carlos Takam Kuangaziwa na vyombo vya habari Televisheni, Radio, Magazeti na Tovuti zote nchini Nigeria zinatoa muda na nafasi kubwa kuhusu mapigano yake na maandalizi kuelekea mapigano hayo Licha ya kwamba Joshua hajawahi kukutana na mashabiki wake na hata ilipozuru Sagamu mwezi Februari mwaka huu na kuamua kukutana na viongozi wa kijamii na kuondoka kimya kimya alivyokuja , watu hakumchukulia vibaya. "Haijalishi. Yeye bado ni mtoto wetu na mwakilishi wetu," anasema Okunoren. "Baba yake, babu yake na babu wa mababu zake wanatoka hapa. Najua pia ana mizizi mjini Watford lakini hakuna namna tutakoza kumuunga mkono. Tunaamini siku moja atatutambua na kutusaidia. "Tutazidi kumuombea apate ufanisi lakini pia tunataka uwepo wake hapa. Tungelipenda avenge nyumba hapa au kuwacha ishara yake hapa. "Iwe ni kituo cha mazoezi ya viungo, au hospitali. Kitu ambacho watu Watson na ambacho kitawakumbusha kumhusu." Usiku wa Jumamosi katika jiji la London, Anthony Joshua ataingia ulingani kwa mara ya kwanza mwaka huu kupigana na Kubrat Pulev wa Bulgeria. text: Rais wa Tanzania Dk John Magufuli Aliingia kwenye moja ya mabehewa ya treni ya TAZARA kwa ajili ya safari ya kuelekea kuweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa kufua umeme katika mto rufiji utakaozalisha umeme wa kilowati 2115 Watu mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti kuhusu hatua ya rais Magufuli kusafiri kwa Treni badala ya usafiri ambao kwa maoni yao wanaona kuwa unamfaa zaidi kwa hadhi yake, wengine wakiona ni jambo jema na kuwataka viongozi wengine ambao hutumia usafiri wa hadhi ya juu kufuata mfano wa rais Magufuli. Awali kabla ya kupanda treni, Rais Magufuli alizungumza na viongozi wa TAZARA na kuwataka kuwasilisha mapendekezo yao juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuboresha usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia TAZARA.Rais Magufuli amesema Serikali inatambua umuhimu wa shirika hilo. January Makamba afutwa uwaziri Tanzania Museveni awasili Chato kumtembelea Magufuli Akizungumza kuhusu changamoto za wafanyakazi rais Magufuli ameutaka uongozi wa shirika hilo kutatua kero za wafanyakazi wa TAZARA kwa mazungumzo ya pande zote mbili. ''Hakikisheni wafanyakazi mnawasaidia hawa wafanyakazi wako frustrated,nimewauliza maswali hawakutaka kuzungumza kwa sababu wameogopa, hawataki kuongea chochote.Si kwamba hawana shida,wana shida kibao, ila wanawaogopa ninyi inawezekana mnawatishia kwamba mtu akizungumza anafukuzwa. Mkae na wafanyakazi mzungumze shida zao mzitatue, zile zinazoshindikana mzilete serikalini''. Alisema Magufuli. Reli ya Tazara yenye urefu wa kilomita 1,860 ina uwezo wa kusafirisha tani milioni tano za mizigo kwa mwaka, lakini kutokana na upungufu wa injini na mabehewa ya kutosha, inasafirisha chini ya tani 300,000 kwa mwaka. Reli hiyo ilijengwa kwa msaada kutoka China, ilianza huduma mwaka 1975 na inamilikiwa kwa ubia wa asilimia 50 kwa 50 wa nchi ya Tanzania na Zambia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza tangu awe rais anasafiri kwa Treni kuelekea Rufiji. text: Watu wanaweza kuombwa wabaki nyumbani kwa muda wa wiki mbili kama walikuwa karibu na watu wenye maambukizi ya virusi vya corona Zaidi ya watu 80 kwa mfano wametengwa nchini Uingereza kwa uchunguzi wa Virusi vya Corona. Hakuna idadi rasmi za watu walioshauriwa kujitenga na watu wengine, lakini hatua ya kujitenga binafsi inaonekana kama njia muhimu ya kupunguza usambaaji wa virusi. Lakini kujitenga mwenyewe inamaana gani na ni vipi unaweza kuhakikisha kujitenga kwako kunakuwa na mafanikio? Ni nani anayepaswa kujitenga? Unahitaji tu kujitenga kama umeambiwa ujitenge na maafisa wa afya. Kwa kawaida wanaoambiwa wajitenge ni wale ambao''wamekua karibuni ama wako karibu'' na watu binafsi ambao walithibitishwa kuwa na virusi- waliobainika kukaa dakika 15 katika umbali wa mita mbili kutoka alipo mtu alieambukizwa. Inakua ni lazima kujitenga na watu hususan kama umesafiri katika maeneo ya ndani ya China, Thailand, Japan, Korea kusini, Hong Kong, Taiwan, Singapore, Malaysia au Macau katika kipindi cha siku 14 zilizopita na una dalili kama vile kikohozi, homa ya mwili na kushindwa kupumua vizuri. Katika hali kama hii, usiende kwa daktari au kituo cha afya. Ukiwa na dalili za virusi vya Corona unashauriwa kujitenga binafsi ili kuepuka maambukizi zaidi Badala yake kaa nyumbani. Unashauriwa kuwasiliana mara moja na maafisa wa afya au hopsitali ili kupata usaidizi wa haraka wa matibabu. Unapaswa kufanya nini unapojitenga kwa ajili ya kutoambukiza watu wengine virusi vya Corona? Ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ni kwamba ''ni jambo la kutumia akili ya kawaida'' jizuwie kukaribiana na watu wengine kadri uwezavyo - kama vile tu ambavyo ungefanya kama ungekua na mafua. Hii ina maana kuwa unapaswa kubakia nyumbani kwa siku 14, na kutoenda kufanya kazi, shule au katika maeneo ya umma. Usiende madukani au sokoni - agiza bidhaa au muombe rafiki akusaidie Unapaswa kukaa kwenye chumba chenye hewa safi ya kutosha chenye dirisha linaloweza kufunguliwa, tofauti na vyumba vya watu wengine nyumbani kwenu. Pia usiwakaribishe wageni kwako. Ni vipi kama unaishi na mtu ambaye amejitenga kutokana na virusi vya Corona? Ingawa inaweza kuwa vigumu kujitenga na mtu kutoka familia yako ama jirani yako kabisa, ushauri ni kuwa na ukomo wa ukaribu na mtu anayeshukiwa kuwa na maambukizi kwa kadri uwezavyo. Ushauri wanaopewa watu wenye uwezekano wa kuugua virusi vya Corona ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni kwa walau dakika 20- hususani baada ya kugusana na mgonjwa au kugusa kifaa au kitu alichokigusa au kukitumia. Inashauriwa usitumie vifaa vya nyumbani na mtu ambaye ametengwa. Pia kama wanachumba tofauti na kama inawezekana wanapaswa kuwa na choo na bafu lao. Inashauriwa pia kuonsha sakafu ya nyumba kila siku, kwa kutumia gloves kama unazo. Uchafu ambao umetoka ama umeguswa na mgonjwa aliyetengwa unapaswa kuwekwa kwenye karatasi ya plastiki ya uchafu na kufungwa na kuwekwa katika karatasi nyingine. Virusi vya Corona: Hospitali iliyojengwa ndani ya siku 10 Watu wengi wanaweza kuwa wataombwa wajitenge na wengine ili kuepuka kueneza virusi vya Corona kutokana na kuenea kwa ugonjwa huo. Lakini unapaswa kufanya nini ikiwa uko hatarini? text: Marufuku hiyo inahusisha maeneo yote ya Tanzania Bara, upande wa pili wa muungano Visiwa vya Zanzibar vinatekeleza marufuku hiyo kwa miaka kadhaa sasa. Tanzania Bara pia imekuwa katika harakati za kupiga marufuku mifuko ya plastiki kwa zaidi ya mwongo mmoja huku harakati hizo zikikwama mara kadhaa. Safari hii serikali ya nchi hiyo imeonekana kujidhatiti kutekeleza marufuku hiyo kama wafanyavyo nchi jirani za Rwanda na Kenya. Marufuku hiyo haitahusisha vifungashio vya plastiki vya bidhaa mbalimbali. Mifuko ya plastiki inalaumiwa pakubwa kwa uchafuzi wa mazingira duniani, na harakati za kukomesha matumizi yake yanalenga kulinda mazingira. Makosa na adhabu Kwa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management Act) serikali ya Tanzania imetunga kanuni za mwaka 2019 za kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Kifungu cha nane cha kanuni hizo kinaorodhesha makosa matano ambayo ni; kuzalisha na kuagiza mifuko ya plastiki, kusafirisha nje ya nchi mifuko ya plastiki, kuhifadhi na kusambaza mifuko ya plastiki, kuuza mifuko ya plastiki na mwisho kumiliki na kutumia mifuko ya plastiki. Kila kosa lina adhabu yake kwa mujibu wa kanuni hizo kulingana na uzito wa kosa lenyewe. Kwa kosa la kwanza la uzalishaji na uagizaji adhabu yake ni mosi,faini isiyopungua TSh milioni 5 na isiyozidi TSh milioni 20, pili kifungo kisichozidi miaka miwili jela, adhabu ya tatu ni mjumuiko wa adhabu zote mbili za awali faini na kifungo. Adhabu za kosa la pili amabalo ni kusafirisha mifuko nje ya Tanzania ni sawa na za kosa la kwanza. Kwa kosa la tatu la kuhifadhi na kusambaza mifuko adhabu zake ni mosi faini isiyopungua TSh milioni 5 na isiyozidi TSh miioni 52, pili kifungo kisichozidi miaka miwili, tatu faini na kifungo kwa pamoja. Ukipatikana na hatia ya kuuza mifuko ya plastiki adhabu ambazo utakumbana nazo ni mosi, faini isiyopungua TSh laki moja na isiyozidi laki tano, pili, kifungo kisichozidi miezi mitatu jela na tatu yawezekana ukahukumiwa adhabu zote mbili za awali kifungo na faini. Ukiendelea kutumia na kumiliki mifuko ya plastiki kuanzia Juni 1 nchini Tanzania, basi jiandae kulipa faini isiyopungua TSh30,000 na isiyozidi laki mbili, kifungo kisichozidi siku saba ama faini na kifungo. Vipi kuhusu shehena zilizopo? Mifuko ya plastiki imelaumiwa kwa kuchangia uchafuzi wa mazingira. Katika kuhakikisha kuwa hakuna anayeonewa ama kuathirika kibiashara na katazo hilo, marufuku ilitangazwa Aprili 10 ili kuwapa watu na wafanyabiashara muda wa kujiandaa. Hivi karibuni, Waziri wa Maazingira wa Tanzania Januari Makamba ametoa mwongozo wa kile kinachotakiwa kufanyika kwa wafanyabiashara ambao watakuwa wangali na shehena kubwa ya mifuko hiyo pale tarehe ya marufuku itakapowadia. Gazeti la Mwananchi limemnukuu waziri huyo akisema mifuko hiyo yaweza kusafirishwa nje ya nchi kwa kibali maalumu ama kubaki nayo hapo hapo ili ibadilishiwe matumizi. "Baadaye utafanyika utaratibu wa kurejerezwa (recycle) na kutengenezwa bidhaa nyingine kama sahani, viti na kadhalika," alisema na kuongeza, "Kwa mfano Sudan hawajakataza mifuko, tutawasaidia wale waliopata soko wasipate hasara lakini kwa kibali maalum na itasindikizwa hadi mpakani kwa gharama za msafirishaji." Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifuko Tayari serikali ya Tanzania imekwisha toa tangazo la katazo ya mifuko kwa wageni wanaotarajia kuingia nchi hiyo kuanzia Juni 1. "Wageni wanaoingia (Tanzania) wanashauriwa kutobeba vifungashio vya plastikivya aina yoyote ile. Katika maeneo ya mipaka ya kuingilia nchini kutakuwa na dawati maalumu kwa ajili ya kutupa mifuko hiyo," ilisema taarifa ya serikali. Serikali ya Tanzania inasema lengo lao si kuwafanya wasafiri kutofurahia safari yao, bali kushiriki katika kutunza mazingira. Namna ukaguzi utakavyofanyika Tanzania kwa mujibu wa serikali ya Tanzania: Mifuko mbadala Waziri Makamba amebainisha kuwa kuna viwanda 70 ambavyo vimejitokeza kutengeneza mifuko mbadala, ambapo kati ya hivyo sita ni vikubwa na 30 vya kati. Umoja wa watengenezaji wa mifuko hiyo nchini Tanzania umebainisha kuwa bidhaa zao zitakuwa zimeshaingia mtaani ifikapo Juni 1. Umoja huo unadai kwa sasa bidhaa zao hazionekani sana kwa sababu bado mifuko ya plastiki imo katika mzunguko mtaani. Kuanzia Juni 1, 2019 itakuwa ni kosa la jinai kutengeneza, kuagiza, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki nchini Tanzania, na wote watakao kaidi marufuku hiyo watakutana na mkono wa sheria. text: IEBC imekuwa ikitangaza matokeo ya awali ya urais mtandaoni, na kwa sasa matokeo hayo yalikuwa yanamuonyesha Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee akiwa mbele na kura 7,795,083 (54.38%) naye Bw Odinga akiwa na kura 6,433,161 (44.76%). Matokeo hayo ni ya kutoka vituo 38561 kati ya vituo 40883 nchini humo. Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 382,705 Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC. Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake. Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia. Bw Odinga, amesema huo ulikuwa "ulaghai wa hali ya juu". Hata hivyo, ametoa wito kwa wafuasi wa muungano huo waendelee kuwa watulivu. Bw Musyoka amesema anawashauri wafuasi wa muungano huo waendelee na shughuli zao za kawaida, ingawa huenda karibuni wakatakiwa kuchukua hatua. Bw Odinga na Kalonzo wamekataa kusema ni hatua gani zaidi watachukua na badala yake wakasema wanasubiri kusikia ufafanuzi kutoka kwa IEBC kuhusu yaliyotokea. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewaambia wanahabari baadaye kwamba wamepata habari kuhusu tuhuma za muungano huo wa upinzani kwamba mitambo yao ya uchaguzi ilidukuliwa. Amesema tume haiwezi kupuuza tuhuma kama hizo na kwamba maafisa wake watafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna ukweli wowote katika madai hayo. Hata hivyo alieleza imani yake kwamba mfumo wa uchaguzi unaotumiwa na tume hiyo ni imara na kwamba ulitumiwa na shughuli zote za awali, na sasa "imesalia shughuli ya mwisho" ya kupeperusha na kutangaza matokeo ya kura. Mgombea urais wa muungano wa upinzani Nasa Raila Odinga amewaambia wanahabari kwamba wamepata habari kwamba mitambo ya Tume ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo halisi kufanyiwa ukarabati. text: Bw. Magufuli alisema hayo mapema siku ya Jumapili alipokuwa akiwahutubia waumini katika kanisa moja jijini Dar es Salaam. Tamko hilo linaashiria kuwa rais amebadili msimamo wake kuhusu ugonjwa wa Covid 19. Kabla ya hapo, kiongozi huyo alisikika akibeza hadharani matumizi ya barakoa akisema nchi yake imefanikiwa kutokomeza maambukizi ya corona. Lakini sasa kauli hiyo inaonekana kubadilika. Akizungumza na mamia ya waumini kanisani, rais ailitoa wito kwa wananchi wenzake kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya, akisisitiza kwamba serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvalia barakoa. Bw. Magufuli pia amewahimizi Watanzania kutumia njia za kiasili kukabiliana na magonjwa ya kupumua ukiwemo ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kujifukiza (kupiga nyungu) Tamko la rais linakuja wakati ambapo Tanzania imeendelea kuripoti vifo vya watu kadhaa mashuhuri miongoni mwao wandani wake wa karibu, japo kilichosababisha vifo vyao hakijawahi kuhusishwa rasmi na ugonjwa wa Covid 19. Ibada ya mazishi ya Katibu Mkuu Kiongozi mhandisi Balozi John Kijazi Leo Jumapili pia ndio siku ya mwisho ya maombi ya siku tatu kwa taifa iliyotangazwa na Rais Magufuli kuomba viongozi wa kidini kufanya sala maalum ya kukinga nchi kutokana na maambukizi ya corona. Huku hayo yakijiri, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuanza kutoa takwimu ya walioambukizwa Covid 19 nchini humo. WHO, linasema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwalinda Watanzania na wale wanaotangamana nao. Pia unaweza kusikiza Magufuli: Unaweza ukafa kwa malaria,unaweza ukafa kwa kansa, ukafa kwa magonjwa mengine Rais wa Tanzania John Magufuli amesema serikali yake haijamzuia mtu yeyote kuvaa barakoa, japo anashauri matumizi ya barakoa zilizotengenezwa nchini akisema anaamini baadhi ya zile zinazoagizwa kutoka nje sio salama. text: Glenn aliibuka mtu mzee zaidi kusafiri anga za juu akiwa na miaka 77 Alikuwa mwanajeshi wa zamani na alihudumu pia kama seneta. Glenn alikuwa amelazwa hospitalini Columbus, Ohio, kwa zaidi ya wiki moja na alifariki akwia amezingirwa na wanawe na mke wa miaka 73. Glenn anafahamika sana kwa kuizunguka dunia mwaka 1962 akiwa na chombo cha anga za juu cha Friendship 7. Ufanisi wake uliashiria wakati ambao Marekani iliufikia Muungano wa Usovieti katika kutumma binadamu anga za juu. Glenn atazikwa katika makaburi ya Arlington, Virginia. Aliporejea duniani, Glenn alichaguliwa seneta wa chama cha Democratic mwaka 1974, ambapo alihudumu kwa miaka 24. Mwaka 1998, miaka 36 baada ya safari yake ya kihistoria anga za juu, aliandika historia tena kwa kuwa mtu mzee zaidi kwenda anga za juu, akiwa na miaka 77. Glenn alizaliwa 1921 Cambridge, Ohio. Rais Barack Obama ameongoza Wamarekani kutoa heshima zao kwa Glenn, ambapo amemtaja kama "rafiki aliyetutoka". Glenn akijiandaa kwa safari yake ya kuizunguka dunia John Glenn akiwa Nasa mwaka 1963 Aliwania kuwa mgombea urais mwaka 1984, lakini akashindwa na Walter Mondale. John Glenn (kushoto), Rais John F Kennedy (kati) na Makamu Rais Lyndon Johnson (kulia) wakikagua chombo cha Friendship 7 Glen alitunukiwa tuzo ya dhahabu kwa Kiingereza, Congressional Gold Medal, tuzo ya juu zaidi inayopewa rais Marekani mwaka 2011. Rais Obama akimpa John Glenn nishani ya Rais ya Uhuru Mwana anga wa zamani John Glenn, ambaye alikuwa Mmarekani wa kwanza kuizunguka dunia kupitia mzingo wa dunia, amefariki dunia akiwa na miaka 95. text: Wanariadha hao walitarajiwa kushiriki kwenye mbio za riadha za Afrika zitakazoanza leo. Jumatano, mjini Asaba, jimbo la Delta, Nigeria. Ingawa mbio hizo zitang'oa nanga leo, matayarisho yalianza mwezi Novemba mwaka wa 2017. Jean Pierre Bemba kurejea nchini Congo Upinzani wadai mgombea wake ameshinda uchaguzi Zimbabwe Kikosi cha Zambia kilichowasili Nigeria siku ya Jumamosi, kilifika uwanja wa mashindano siku ya Jumanne. Mji huu wa Asaba ulitarajiwa kujizolea sifa kwa kuandaa Makala ya 21 ya riadha barani, lakini kuanzia siku ya jumamosi wiki hii, wanariadha kutoka matafa 52 wamekabiliwa na changamoto za uchukuzi na za usimamizi. Wanariadha wa Kenya ndio walioathirika Zaidi huku Zaidi ya wanariadha 40 wakisalia uwanja wa ndege wenzao wakifanya mazoezi uwanjani wa Lagos. Marekani yapiga marufuku nguo kutoka Rwanda Wengine wamegeuza uwanja wa ndege kuwa chumba cha malazi na uwanja wa kupiga jaramba. Wameonekana wakijinyoosha kwenye maeneo ya kuabiri ndege. Tatizo hili limezidi mpaka baadhi ya wanariadha wamelazimika kutumia njia mbadala kama usafiri kwa gari na kuhatarisha usalama wao. Mwanariadha wa Kenya Gilbert Osure alilazimika kusafiri kwa gari "Sikutarajia mhangaiko wa aina hii. Nimesafiri kwa gari kwa Zaidi ya saa mbili hadi hapa. Imekuwa ni safari ndefu na yenye uchovu," alinukuliwa mwanariadha wa Kenya, Gilbert Osure. Wengine waliowasili siku ya jumanne wamekashifu vikali mipango duni ya waandalizi. Afrika kusini kubinafsisha ardhi bila fidia "Sijawahi kuona maandalizi ya aina hii. Nimeshiriki mashindano mengi, lakini hakuna mabaya Zaidi ya tuliyoyapitia hapa Nigeria," alisema mkufunzi wa Algeria, Benid Amar, ambaye kikosi chake kilipitia Paris kufika hapa. Lakini eneo lenyewe lilikuwa na uwezo wa kuandaa mashindano haya? Gavana wa eneo la Delta linalosimamia mji wa Asaba, Ifianye Okowa, amedokeza kuwa awali walikuwa na wasiwasi wa kubeba mzigo wa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kiwango hiki. ''Miezi chache zilizopita, tulipofahamishwa kuwa waandalizi, nilikuwa na woga akilini mwangu," alisema Okowa. Ingawa baraza kuu la riadha barani liliandaa mkutano wake, tatizo hili limetia dosari kwa maandalizi kwa jumla. "Sikuamini Asaba ingeweza kuwa mwenyeji. Nilipozuru uwanja huu mwaka uliopita,nilihisi haungekuwa tayari." Rais wa Riadha barani, Kalkaba Malboum, amesema. Mataifa kama vile Botswana yenye nyota kama vile Nijel Amos waliwasili Jumatatu baada ya kusubiri kwa siku mbili uwanja wa ndege. Mabingwa watetezi Afrika Kusini, walifika Jumanne. Sio kila mmoja ameshangazwa na hali hii. Nyota wa mbio fupi kutoka Nigeria, Blessing Okagbare, amelitetea taifa lake. Biashara ya Benki Tanzania yasuasua kutokana na wateja kutolipa madeni "Linaweza kutokea, lakini ni uchungu kwa mwanariadha" alisema Blessing Okagbare. "Ndio mara ya kwanza tunaandaa mashindano haya na sio rahisi " alizidi. Meneja wa Afrika Kusini John Matiani aliwalaumu waandalizi pia. "Tulikwama Lagos licha ya kuwasili tarehe 28 Julai. Hatuna pasipoti zetu kufikia sasa na hatujui zilipo," alimaliza. Solomon Ogba mwenyekiti wa kamati andalizi Hata baada ya mwenyekiti wa kamati andalizi bwana Solomon Ogba, kujipiga kifua na kujigamba kuwa hakuna shindano bora litakalokuwa kama hili, wanariadha wa Afrika wametishia kujiondoa kutoka mashindano haya. Maafisa hawa wameanza juhudi za kuwasafirisha wanariadha hawa lakini yanajiri saa chache tu kabla ya shindano lenyewe kufunguliwa rasmi. Serikali ya Kenya imeahidi kuingilia kati na kuwasafirisha wanariadha wake, lakini bado wamesalia uwanja wa ndege. Sahihisho 02 Agosti 2018: Taarifa hii awali ilitaja kwamba wanariadha wa Tanzania ni miongoni mwa waliokuwa wamekwama katika uwanja wa ndege Lagos kuelekea kushiriki katika mashindano hayo Asaba. Katibu mkuu wa riadha Tanzania, Wilhelm F. Gidabuday katika taarifa yake amesema timu ya Tanzania ilijiondoa kutoka kwenye mashindano hayo baada ya kushindwa kuondoka nchini mwao kutokana na kucheleweshwa kwa barua ya mwaliko kutoka kwa waandalizi, na sababu za kiusalama. Hawakuwa wameondoka nchini Tanzania. Zaidi ya wanariadha 300 wakiwemo wa kutoka Kenya na kutoka mataifa mengine ya Afrika wamekwama katika uwanja wa ndege wa Murtala Muhammad 2 mjini Lagos Nigeria. text: Zaidi ya watu 100,000 walijitokeza Manchester United walipocheza dhidi ya Real Madrid Michigan mwaka 2014 Uwanja utakaochezewa mechi hiyo bado haujaamuliwa. Mechi hiyo, debi ya kwanza ya Manchester kuchezewa nje ya Uingereza, itachezwa kama sehemu ya michuano ya kila mwaka ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa. City walifaa kukutana na United jijini Beijing, Uchina Julai mwaka jana katika uwanja wa Bird's Nest lakini mechi hiyo ikafutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa. City pia watakabiliana na wapinzani wao wengine kutoka Ligi ya Premia, Tottenham, mjini Nashville 29 Julai kabla ya kukabiliana na miamba wa Uhispania Real Madrid mjini Los Angeles 26 Julai. Spurs pia watakutana na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain, ambao wameshinda michuano hiyo miaka miwili iliyopita, mjini Orlando 22 Julai na Roma ya Italia New Jersey 25 Julai. Kwenye mechi hiyo, kutachezwa pia El Clasico ya pili kuwahi kuchezewa nje ya Uhispania, Real Madrid watakapokutana na Barcelona Miami 29 Julai. Timu hizo zilikutana mara ya mwisho nje ya Uhispania Venezuela mwaka 1982. United pia watakutana na Real Madrid mjini Santa Clara 23 Julai kisha wakutane na Barcelona Washington DC mnamo 26 Julai. Kwenye mechi nyingine za Kombe la Mabingwa wa Kimataifa zitakazochezewa Singapore, viongozi wa Ligi Kuu England Chelsea watacheza dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich 25 Julai na Inter Milan ya Italia 29 Julai. Arsenal watashiriki mechi zitakazochezewa China. Manchester City watakutana na Manchester United katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa kwa msimu nchini Marekani tarehe 20 Julai. text: Baadhi ya watoto walihusika katika uzazi huo walisubiri miaka kadhaa kuthibitisha Vipimo vya vinasaba -DNA vimefichua kuwa Jan Karbaat, aliyefariki dunia miaka miwili iliyopita aliwapa mimba mama zao katika kliniki yake iliyopo katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam. Vipimo hivyo vilithibitishwa Ijumaabaada ya jaji kuruhusu vitangazwe. Mmoja wa watoto , kwa jina Joey, alisema "hatimae amefunga ukurasa " sasa anajua Bwana Karbaat alikuwa ndiye baba yake. "Baada ya uchunguzi wa miaka 11 ninaweza kuendelea na maisha. ninashukuru kwamba hatimae nimeelewa wazi," aliliambia shirika la utangazaji la uholanzi NOS. Tim Bueters, wakili ambaye aliwawakilisha watoto 49, alisema kuwa ameridhishwa na matokeo ya kesi ya baada ya miaka ya kutokuwa na uhakika. "Inamaanisha kwamba hatimaeimekuwa wazi kwa watoto ambao wanafanana," aliliambia shirika la utangazaji la NOS. Wengi wa watoto walizaliwa miaka ya 1980 Bwana Karbaat alipelekwa kwa mara ya kwanza mahakamani mwaka 2017 na kikundi cha watoto wa uzazi wa msaada na wazazi wake baada ya kushuku kuwa walikuwa na uhusiano. Moja ya kesi hizo ilihusu mtoto wa msaada ambaye alifanana kwa maumbile na daktari , makakama ilimsikiliza. Jan Karbaat, aliyefariki dunia mwaka 2017, alikuwa mmiliki wa kliniki ya uzazi wa msaada mali zake zilichukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake Aprili 2017 akiwa na umri wa miaka 89. 'tuhuma kubwa ' mwaka 2017 jaji aliamuru kuwa vipimo vya vinasaba -DNA vinaweza kuchukuliwa na kuhifadhiwa kwa siri hadi matokeo zaidi ya kesi hiyo yatakapotolewa. Mwezi February mwaka huu, mahakama ya Wilaya ya Rotterdam iliamua kuwa matokeo ya vipimo yanaweza hatimae kufichuliwa. Yanaonyesha yanathibitisha "tuhuma kali kwamba Bwana Karbaat alitumia mbegu zake za kiume za uzazi katika kliniki yake ",ilisema taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya kampuni ya sheria ya Rex Advocates. Bwana Karbaat alijiita "muanzilishi katika fani ya uzazi wa msaada ". kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati yalipokuwa madai kwamba alikuwa na data zisizo sahihi, uchunguzi na maelezo ya yasiyo sahihi kuhusu uzazi wa msaada na ruhusa ya kuruhusiwa kuwa na idadi ya watoto sita kwa kila mtoaji wa mbegu za uzazi. Daktari wa uzazi wa kusaidiwa nchini Uholanzi anayeshutumiwa kwa kupandikiza mbegu zake za uzazi kwa waginjwa bila ridhaa yao amethibitishwa kuwa baba wa watoto 49. text: Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92. Ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush. Bi Bush ambaye alikuwa mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 amekuwa akidorora kiafya kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi. Risala za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani. Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani. Barbara Bush na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush Mwana wao George alichaguliwa 2000 na kuhudumu kwa miula miwili kama rais wa 43 wa Marekani. Katika tanzia alisema katika taarifa yake kwamba ''mamangu mpendwa ametuwacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza , lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika. Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92. text: App ya Dalai Lama ni ya bure Kiongozi huyo wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni mwenye umri wa miaka 82, ana akunti ya Twitter iliyo na wafuasi zaidi ya milioni 16. App hiyo ya bure kwa sasa inapatikana kwenye simu za iPhone pekee, na ataitumia kutoa taarifa, video, picha na taarifa nyinginezo China yaionya Botswana kuhusu Dalai Lama Kuna programu nyinge tumishi za kidini zilizozinduliwa, zinazoruhusu viongozi kuwasiliana na wafuasi wao na kuwasiaidia watu kutafuta chakula kinachoambatana na dini zao, wanaposafiri. App hiyo inaitwa, Dalai Lama, haijakaguliwa sana na watumizi. The Dalai Lama Dalai Lama amezindua programu tumishi ya simu kwa wafuasi wake kuweza kufuatilia kwa karibu kuhusu safari na mafunzo yake. text: Visa vya watoto kuambukizwa virusi vya corona imekuwa nadra sana na wataalamu bado wanatafuta majibu Hicho ndo kisa cha kwanza cha mtoto mchanga kupatikana na virusi hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya watu 900 huku wengine 40,000 wakiambukizwa wengi wao wakiwa kutoka Uchina lakini visa vya virusi hivo vimeripotiwa katika nchi zaidi ya 30. Hata hivyo, ni watoto kidogo walioambukizwa. Virusi vya Corona vinasambaa kabla ya dalili kuanza kujitokeza Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ugonjwa huo uliochapishwa katika jarida la Journal of the American Medical Association na kuangazia wagonjwa katika hospitali ya Jinyintan huko Wuhan - mji ambao ni kitovu cha mlipuko huo. Utafiti huo ulibaini kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo ni watu wazima wenye umri wa miaka 40 hadi 59 asilimia 10 pekee ya wagonjwa wakiwa ni chini ya umri wa miaka 39. "Visa vya watoto kuambukizwa virusi vya corona ni kidogo sana," watafiti hao wameandika. Lakini kwanini iwe hivi? Je watoto wana mfumo wa kinga imara zaidi kukabiliana navirusi vya corona? Ni watoto kidogo walioambukizwa virusi vya corona Kuna nadharia nyingi, lakini wataalamu wa afya hawana jibu muafaka kwa nini visa vya watoto kuambukizwa virusi vya corona ni vichache mno. "kwasababu ambazo haziko wazi, watoto wameonekana ama kutopata maambukizi au kuwa nayo lakini kwa kiwango kidogo tu," Ian Jones, profesa wa magonjwa ya maambukizi katika chuo kikuu cha Reading, ameiambia BBC. Hili huenda likamaanisha kwamba watoto wanapata maambukizi kidogo tu na kutofikia kiwango cha kuanza kuonyesha dalili na hatimaye watoto hao hawapelekwi hopsitali kwa vipimo zaidi, kulazwa au hata kuripotiwa kwa visa zaidi. Nathalie MacDermott, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha London, anakubaliana na hilo. "Watoto ambao umri wao ni zaidi ya miaka 5 na vijana wanaonekana kuwa na mfumo wa kinga wa mwili imara kukabiliana na virusi hivyo," anasema. "Henda bado wakaambukizwa lakini maambukizi yao yanakuwa hayana nguvu sana au hata pengine yasioneshe dalili za maambukizi." Pia hii si mara ya kwanza hili linatokea, katika mlipuko wa virusi kama vile wa Sars, ambao pia ulianzia Uchina 2003 na kusababisha vifo kwa watu karibia 800 na pia wakati huo ilibainika kwamba maambukizi ya virusi hivyo kwa watoto yalikuwa ya china. Mwaka 2007, wataalamu kutoka Vituo vya Kudhibiti Maradhi vya Marekani, vilibaini visa 135 vya watoto kuhusiana na virusi vya Sars lakini wakasema kwamba hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa miongoni mwa watoto na vijana." Je kufungwa kwa shule wakati wa sherehe za mwaka mpya wa Uchina kulisaidia kuepusha watoto dhidi ya virusi vya corona Je mwaka mpya wa Uchina kulisaidia kuepusha watoto kuambukizwa virusi vya corona? McDermott pia anafikiria kwamba watoto huenda wasiwe katika hatari kuambukizwa virusi hivyo ikilinganishwa na watu wakubwa - mlipuko huo ulianza wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa Uchina ambapo shule huwa zimefungwa. Karibia majimbo yote ya Uchina yamefunga shule na zingine zitasalia kufungwa katika muda wote wa Februari. "Watu wakubwa mara nyingi wanakuwa kama wauguzi na kuonekana zaidi kulinda watoto wao au hata kuwaondoa kabisa iwapo itabainika kwamba kuna mmoja ambaye ameambukizwa." Kwa hiyo anafikiria kwamba hilo huenda likabadiliko kadiri virusi hivyo vinapoendelea kusambaa na kuongeza uwezekano wa jamii kuwa katika hatari ya kupata maambukizi". Hata hivyo, hadi kufikia sasa kusambaa kwa haraka kwa ugonjwa huo hakujahushishwa sana na kuongezeka kwa visa vya watoto. Kwa mara nyingine tena katika maambukizi ya virusi vya Sars watafiti waliochunguza visa vya watoto walibaini kwamba wale wenye umri wa chini ya miaka 12 wana uwezekano mdogo zaidi wa kuhitaji matibabu hospitalini. Zaidi ya nusu ya idadi ya wale walioambukizwa virusi vya corona wana umri kati ya 40 hadi 59 Je virusi vya corona vina athiri zaidi watu wakubwa kuliko watoto? Ingawa ni watoto kidogo tu waliothibitishwa kuambukizwa, wataalamu wa tiba hawajahitimisha kwamba hili ni kwasababu wao hawawezi kuambukizwi. Maelezo ambayo yanaonekana kujitokeza kwa sasa ni kwamba mlipuko wa virusi vya corona unahusishwa na kuambukiza zaidi watu wazima ikilinganishwa na watoto kama vile ugonjwa wa tetemaji. "Hili huenda lina ukweli zaidi kuliko ile dhana ya kwamba watoto wana mfumo wa kinga imara zaidi kukabiliana na virusi vya corona," Andrew Freeman, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukizwa katika chuo kikuu cha Cardiff, ameiambia BBC. "Huenda ikawa mamlaka haiwafanyii vipimo watoto ambao hawaonyeshi dalili zaidi ya wale wanaonesha dalili kwa mbali," amesema. Christl Donnelly, mtaalamu wa masuala ya takwimu za usambaaji wa magonjwa kutoka chuo kikuu cha Oxford na Imperial College London, anakubaliana na hilo na kutoa mfano wa mlipuko wa ugonjwa wa Sars huko Hong Kong. Hadi kufikia sasa kumekuwa na maelfu ya visa vya ugonjwa wa corona vingi vikiwa ni kutoka Uchina Vipi kwa walio na maradhi tayari? Watu wakubwa wenye maradhi tayari mfumo wao wa kinga una pambanana maradhi mfano, wenye kisukari, ugonjwa wa moyo wanaonekana kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa virusi kama hivi. "Ugonjwa wa matatizo ya kupumua ambao hujitokeza mtu akishapata maambukizi ya virusi vya corona unaathiri sana watu wenye mfumo dhaifu wa kinga kwasababu tayari wako katika hali mbaya ya kiafya," Ian Jones ameelezea. "Hilo linatokea kwa wanaopata mafua makali na matatizo mengine ya kupumua." Ilibainika kwamba karibu nusu ya waathirika waliofanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Jinyintan tayari walikuwa na maradhi mengine. Hakuna ushahidi wa wazi unaoonesha kwanini idadi ndogo ya watoto ndiyo wenye kuambukizwa virusi vya corona Lakini si watoto wanajulikana kwa kusambaza maambukizi ya virusi? Watoto kawaida wanakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi na mara nyingi huchukuliwa kama wasambazaji wakubwa', kulingana na Ian Jones. "Wao husambaza magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vile ambavyo mtu yeyote mwenye mtoto katika shule ya chekechea anavyofahamu," anasema. Kwa hiyo tunaweza kutarajia idadi kubwa ya watoto kuambukizwa - lakini hali ni tofauti kwa sasa. Huenda ikawa watoto wana mfumo imara wa kinga kukabiliana na virusi, au makali ya virusi vyenyewe inakuwa kidogo kwa watoto ikilinganishwa na watu wakubwa, na hivyo basi watoto hawapelekwi kupata matibabu, hawafanyiwi vipimo wala kusajiliwa. Utafiti zaidi unastahili kufanywa ili kupata uelewa wa mlipuko huu dhidi ya watoto. Lakini pia huenda ikawa watoto wametegwa kabisa na kuwa katika uwezekano mdogo wa kupata maambukizi kwa kufunga shule, na kuwekwa katika mazingira mazuri. Na hilo litafahamika watoto wote watakaporejea shuleni nchini uchina. Taarifa za kwamba mtoto aligunduliwa akiwa na virusi vya corona nchini Uchina Februari 5, saa 30 tu kabla ya kuzaliwa, zilisambaa kwa haraka kote ulimwenguni. text: Kwa mujibu wa wasuluhishi, jeshi na upinzani wamekubali kushirikiana katika kuongoza serikali hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu na kisha kusimamia uchaguzi huru na wa haki. Pande hizo mbili zilishindwa kufikia muafaka hapo kabla kutokana na mvutano wa kila upande ukitaka uwe na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye baraza litakalounda serikali hiyo. Lakini sasa wameahidi kuunda serikali huru itakayoongozwa kitaalamu pamoja na kuchunguza ghasia za hvi karibuni zilizosababisha mamia kufariki, Umoja wa Afrika (AU) umesema. Taarifa za makubaliano hayo zilipokelewa kwa shangwe mitaani. Sudani imejikuta ikitumbukia katika lindi la ghasia na suitafahamu toka alipong'olewa madarakani rais Omar al-Bashir kwa mapinduzi ya kijeshi mwezi Aprili. Mapinduzi hayo yalizaliwa baada ya maandamano makubwa ya raia dhidi ya Bashir, ambaye aliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki mwaka 1989. Siku tatu kabla ya makubaliano hayo ya mpito, makundi makubwa ya waandamanaji wakitaka baraza la kiongozi la kijeshi kuachia ngazi na kupisha utawala wa kiraia. Watu saba waliuawa na wengine 181 walijeruhiwa katika vurumai hizo, vyombo vya serikali viliripoti. Mazungumzo ya safari hii yalifanyika jijini Khartoum kupitia usuluhishi ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia na wanachama wa AU. Wamekubaliana nini hasa? "Pande mbili zimekubaliana kuunda baraza huru litakalokuwa na rais wa kupokezana baina ya jeshi na raia kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi," msuluhishi wa AU Mohamed Hassan Lebatt amewaambia wanahabari Ijumaa asubuhi. Uchaguzi utafanyika pale kipindi cha mpito kitakapofikia tamati. "Pia wamekubaliana kuwa na uchunguzi wa wazi, huru na kina juu ya matukio yote ya ghasia yaliyoikumba nchi hiyo katika wiki za hii karibuni," ameongeza. Pia wamekubaliana kuahirisha kuanzishwa kwa baraza la wawakilishi. "Tunaamini kuwa huu ni mwanzo wa zama mpya," amesema Omar al-Degair, kiongozi wa muungano wa wapinzani nchini humo FFC. Naibu kiongozi wa baraza la mpito la jeshi TMC, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, amesema: "Makubaliano haya yatakuwa ni makubwa na hayatamuacha mtu yeyote. "Tunaushukuru Umoja wa Afrika na Ethiopia kwa kutuma wasuluhishi na kuwa wavumilivu." Matukio kabla ya makubaliano Mwezi uliopita, wawakilishi wa waandamanaji walikuwa katika meza ya mazungumzo juu ya nani anatakiwa kuongoza Sudani. Lakini majadiliano yakavunjika baada ya jeshi kushambulia waandamanaji Juni 3 na kuua makumi ya waandamanaji. Jeshi likatangaza kuwa limevunja makubaliano yote na wapinzani baada ya tukio hilo, na uchaguzi ungefanyika ndani ya miezi tisa. Lakini wanaharakati wakasisitiza kuwa serikali ya mpito ya miaka mitatu inahitajika ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki unafanyika. Baada ya mazungumzo kuvunjika, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipaa mpaka Sudani ili kupatanisho pande hizo mbili. Baada ya siku kadhaa za mazungumzo, mwakilishi wa Abiy bwana Mahmoud Dirir, akatangaza kuwa viongozi wa maandamano wamekubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo na wanajeshi. Viongozi wa jeshi nchini Sudani wameafikiana na muungano wa upinzani nchini humo juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito ambayo itaandaa njia kwa kurejeshwa kwa utawala wa kiraia. text: Moja ya Nyumba zilizojengwa na Mgodi wa Buzwagi kama fidia kwa mkazi wa eneo hilo Miongoni mwa migodi hiyo ni Accacia-Buzwagi ulioko kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo viongozi wake wanaeleza kuwa wamekuwa wakijihusisha na shughuli za miradi ya kimaendelo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, hospitali, shule na kulipa kodi inayotumiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Baadhi ya Wananchi wa Mwendakulima wakiwa kwenye kituo cha afya Lakini pamoja na shughuli zote hizo kufanyika katika eneo hilo bado baadhi ya wananchi wanaozunguka mgodi huo wanalalamikia uwepo wa mgodi huo katika kijiji chao. ''..Nina majuto kwanini nimezaliwa Tanzania na kwanini nizaliwe karibu na mgodi hapa Mwendakulima? Kwa sababu mpaka sasa tunapata shida kupata maeneo ya kulima, kwa mfano baba yangu alilipwa milioni saba kwa ekali 23, na ilikuwa mwaka 2008 hivyo, mimi kama mimi siwezi kusema kwamba tumenufaika na mgodi huu kwasababu bado nina maumivu..'' Anasema Simon Mabumba. Pius Mpundi, Mwanasheria kutoka Shirika la kutetea haki za Binadamu "SHIHUDA" anaona kwamba malipo waliyopewa wananchi hawa si ya haki. Kwa kuwa Buzwagi imewafidia kwa kuwajengea nyumba za chumba kimoja, alichofananisha sawa na Msalani. Akisema kuwa maendeleo ya mji huo, hayalingani na faida ambayo mgodi huu wanaupata. Miongoni mwa nyumba zinazojengwa kama fidia na mgodi wa Buzwagi Kwa upande wake, Vicent Ndesekio, Afisa kata wa eneo hilo anasema licha ya Mgodi huo kuwajengea wananchi nyumba nzuri tofauti na walizokuwa nazo awali, bado hawaridhiki. Amesema kwa sasa wanachofanya ni kubadili mtazamo kwamba mgodi unawajibika kuwafanyia kila kitu, kwani nao pia wanapaswa kujiajiri ili waweze kujitegemea. Shule ya msingi ya Mwendakulima iliyojengwa na mgodi wa Buzwagi Asa mwaipopo,Meneja mkuu katika mgodi wa Buzwagi, anasema upande wao wamefata utaratibu wote wa kisheria. ''...Ni kweli kwamba mgodi huu ulipoanza kujengwa ulichukuwa baadhi ya maeneo yaliyokuwa yakimilikiwa na wenyeji. Utaratibu wa fidia ni utaratibu wa kiserikali na ni utaratibu wa kisheria. Ukiwa unafanya kazi na watu wengi kiasi uelewa na tafsiri hutofautiana, lakini utaratibu ulizingatia sheria na taratibu na ulizingatia soko ndio maana wengi waliridhika na wakalipwa. Na kama wangekuwa na madai ya msingi sidhani kama suala hili lingechukua miaka mingi kama hivi...''. Baadhi ya raia nchini Tanzania ambao wanaishi katika maeneo ya migodi,wanalalamikia fidia wanayopewa kutoka kwa wawekezaji, na kudai kuwa hailingani na ardhi iliyochukuliwa. text: Miili ya wataalamu wa UN yapatikana DRC Miili hiyo ilipatikana eneo ambapo raia wa Marekani Michael Sharp na raia wa Sweden Zaida Catalan walitekwa nyara wiki mbili zilizopita. Miili hiyo ni ya mwanamume na mwanamke ambao wote ni wazungu. Kumekuwa na ghasia eneo la Kasai, ambapo pia polisi 40 walipatikana wamekatwa vichwa mwishoni mwa wiki. Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa walikuwa nchini DRC kufuatilia vikwazo vilivyowekwa dhidi DRC, lakini wakati huo walikuwa wakichunguza ripoti za dhuluma eneo la Kasai. Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende, alithibitisha ripoti za kupatikana kwa miili hiyo kwa BBC. Hata hivyo amesema kuwa uchunguzi wa DNA unahitaji kuondoa shaka yoyote kuhusu miili hiyo. Miili ya wataalamu wa UN yapatikana DRC Serikali ya Congo inapigana na kundi la waasi ambalo linahudumu eneo hilo na linaaminiwa kuwateka wataalamu hao. Ghasia eneo la Kasai zimechochewa kufuatia kuuliwa kwa kiongozi wa kitamaduni Kamuina Nsapu, ambaye alikuwa akiongoza upinzani dhidi ya Rais Joseph Kabila Maafisa nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanaamini kuwa wamepata miili ya wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa ambao walitoweka nchi humo. text: Wadukuzi walianza kutumia akaunti hiyo kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu Kundi la wadukuzi linalojiita Chuckling Squad limedai kuhusika na udukuzi wa akauntui ya Twitter ya Jack Dorsey. Akaunti hiyo iliyo wa mashabiki zaidi ya milioni nne ilianza kutumiwa kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu kwa karibu dakika kumi na tano. Twitter inasema mitambo yake haikufikiwa na wadukuzi na badala yake kulaumu kampuni ya mawasiliano ambayo haikutaja jina lake kwa kusababisha hitilafu hiyo. "Nambari ya simu inayohusishwa na akaunti hiyo ilivamiwa kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyosababishwa na kampuni hiyo ya mawasiliano ," ilisema taarifa iliyotolewa na Twitter. "Hali hiyo ilitoa fursa kwa watu wasio na idhini ya kutumia nambari hiyo kuanza kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter." Chanzo cha habari kutoka Kampuni hiyo ilithibitishia BBC kuwa wadukuzi walitumia mfumo unaojulikana kama "simswapping" kuchukua udhibiti wa akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey. Huu ni mfumo ambao inatumiwa kuhamisha nambari halisi ya simu ya Dorsey katika laini nyingine- na kuanza kuitumia. Wadukuzi mara nyingine hutoa hongo kwa wahudumu wa kampuni za mawasiliano au kuwapotosha kupata namabari halisi. Kwa kuchukua udhibiti wa nambari hiyo wadukuzi waliweza kuandika ujumbe moja kwa moja katika akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey. Japo siku hisi watumiaji wengi wa mtandao huo wanatumia programu tumishi kwenye simu zao kutuma ujumbe, awali Twitter ilibuniwa katika mfumo wa kutuma ujumbe mfupi- hali inayoisaidia kudhibiti idadi ya maneno mtumiaji anastahili kuandika. Wadukuzi waliandika nini? Ujumbe wa chuki na wa kibaguzi - ulitumwa moja kwa moja kwa kutumia akaunti ya @jack, na wengine waka sabaza ujumbe huokwa kutumia akaunti zingine. Ujumbe mmoja uliashiria kuna bomu limetegwa katika makao makuu ya kampuni hiyo. Chuckling Squad imedai kuhusika na udukuzi wa Twitter za watu mashuhuri,kama vile mwanablogu wa masela ya urembo James Charles miongoni mwa watu wengine. Japo tukio hilo linaonekana kufanyika nje ya kampuni hiyo, linasalia kuwa aibu kwa mtandao wa kijamii wa Twitter, unaotoa huduma kwa viongozi wenye nguvu zaidi ulimwenguni. Wadukuzi walichukua kwa muda udhibiti wa akaunti ya Twitter ya mwanzilishi wa na mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa Twitter. text: Mashtaka yanahusiana na sheria zinazohusu "utajiri haramu na maagizo ya dharura Mashtaka yanahusiana na sheria zinazohusu "utajiri haramu na maagizo ya dharura ",imesema ofisi ya mwendesha mashtaka, ambayo haikutoa taarifa zaidi. Jeshi lilimuondoa madarakani rais huyo wa muda mrefu mwezi April kufuatia miezi ya maandamano dhidi yake. Msemaji wa jeshi aliesma Alhamisi kuwa makosa yalifanyika wakati majeneraliwalipoamrisha kumalizika kwa mhgomo wa kukaa mbele ya makao makuu ya jeshi ambapo waandamanaji wanadai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo. Ghasia za mwezi Juni zilisababisha vifo vya watu 61, kwa mujibu wa maafisa, au 118,kwa mujibu wa madaktari wanaounga mkono waandamanaji wanaodai demokrasia. Mazungumzo baina ya waandamanaji na baraza la kijeshi la mpito yalivunjika baada ya ghasia. Viongozi wa maandamano baadae waliyaita maandamano kuwa ni ukaidi wa raia , ambayo walisema hayana budi kukoma ili kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani. Baada ya mkutano baina ya Tibor Nagy, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika ,na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan,jeshi lilisema kuwa lina matumaini Marekani inaweza "kuwa na mchango mzuri". Bwana Bashir alipinduliwa na kukamatwa tarehe 11 Aprili baada ya miongo mitatuya utawala wa kiimla nchini Sudan. Hajawahi kuonekana kwa umma tangu alipokamatwa. Mwezi May alishtakiwa kwa makosa ya kuchochea nana kuhusika na mauaji ya waandamanaji. Mashtaka hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa kuhusu kifo cha ddaktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliyosababisha kumalizika kwa utawala wake mwezi uliopita. Hatma ya Bwana Bashir haijawa wazi. Aliripotiwa kutiwa nguvuni mara baada ya kupinduliwa. Mnamo mwezi Disemba, waandamanaji walianza maandamanano dhidi ya uamuzi wa serikali wa kupandisha mara tatu kwa bei ya mkate. Maandamano hayo ghafla yalibadilika kuwa hasira iliyosambaa kote nchini dhidi ya kiongozi huyo ambaye alikuwa mamlakani kwa miaka 30, yakiongozwa na madaktari. Maandamano yalifanyika kwa wiki tano na shahidi mmoja anasema tarehe 17 Januari, vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waandamanaji na kumuua daktari. Waandamanaji walimshinikiza rais Omar Al-Bashir kuachia madaraka Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir uligubikwa na mapigano. Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika zama hizo hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia. Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini. Japo serikali yake ilitia saini makubaliano ya kumaliza vita mwaka 2005, vita vingine vilizuka tena - katika eneo la magharibi mwa Darfur. Bw. Bashir alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo hilo. Licha ya ICC kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake, ameshinda uchaguzi mara mbili mwaka 2010 na 2015, japo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi uliyopelekea ushindi wake. Rais aliyeng'olewa madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir ameshtakiwa kwa kosa la ufisadi. text: Makomandoo wa Afghanstan walidondoshwa kwenye paa la hospitali ya Sardar Daud Makamanda wa Afhanstan tayari wametua kwenye baa la hospitali hiyo ya Sardar Daud na sasa wanapigana na wanamgambo. Kundi la Islamic State(IS) limedai kuhisika na shambulio hilo. Taleban wamekanusha kuhusika, kulingana na ripoti ya vyombo nchini humo. Rais Ashraf Ghani amesema kuwa shambulio hilo kwenye hospitali ya Sardar Daud hospital yenye uwezo wa kuwalaza wagonjwa 400 ni "uvunjaji wa maadili yote ya binadamu". " Katika dini zote, hospitali inachukuliwa kama mahala penye kinga na kuishambulia ni kuishambulia Afghanstan nzima ," alisema . IS wamekuwa wakiendesha harakati zao nchini Afghanistan tangu mwaka 2015 na tayari wamekwisha tekeleza mashambulio kadhaa nchini humo. Ilidai kuwajibika na ulipuaji wa mashambulio ya kujitoa muhanga katika mahakama kuu ya mjini Kabul mwezi uliopita ambapo watu 22 waliuawa. Kundi linalojiita jimbo la Khorasan, ambalo linaunganisha mataifa ya Afghanistan na Pakistan, hivi karibuni limeanza harakati zake katika mataifa yote mawili. Moshi ukifuka kwenye paa la hospitali wakati wa shambulio Wapiganaji wa Taleban pia wamekuwa wakiendesha mashambulio yaliyowauwa watu 16 mjini Kabul katika mashambulio yaliyokuwa ya kujitolea muhanga. Shambulio lilianza saa tatu unusu kwa saa za Aghanstan wakati mwanamgambo alipojilipua katika lango moja la upande wa kusini mwa hospitali- ambayo iko karibu na ubalozi wa Marekani- halafu washambuliaji wengine watatu wa wakaingia ndani ya mazingira ya hospitali hiyo. Wakaingia katika ghorofa la pili na la tatu huku wakiwa na silaha ndogo pamoja na gurunati na kuanza kufyatua risasi. Police wamefunga eneo la tukio Mhudumu mmoja wa hospitali ambaye aliweza kutoka nje alimuona mshambuliaji "akiwa amevalia koti jeupe amesikilia bunduki aina ya Kalashnikov na kumfyatulia risasi yeyote, wakiwemo walinzi, wagonjwa na madaktari". Mhudumu mmoja aliandika kwenye ukurasa wa Facebook: "washambuliaji wako ndaniya hospitali. Tuombeeni." Mmoja wa washambuliaji ameuawa na wengine walikuwa wamejificha chini ya ngazi, alisema msemaji wa wizara ya ulinzi. Askari mmoja pia ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa na wagonjwa wanaokolewa kupitia milango ya kutokea ya dharura. Takriban watu watatu wamekufa na wengine zaidi 60 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa ni wahudumu wa hospitali, amesema waziri wa afya na pia vyombo vya habari. Zaidi ya watu 30 wameuawa, kulinga na maafisa, lakini baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi. text: Armata ni kifaru cha kisasa ambacho kinachukua nafasi ya vifaru vya enzi za muungano wa Usovieti Vifaru hiyo vipya vya Urusi kwa jina Armata T-14 vinaundwa vikiwa na teknolojia ya Kinga Dhidi ya Makombora (APS). Lengo la teknolojia hiyo ni kuwezesha vifaru hivyo kutoharibiwa na makombora mengi yaliyoundwa kukabiliana na vifaru, yakiwemo yale aina ya Javelin yanayoundwa Marekani, ambayo yanatumiwa na jeshi la Norway. Brigidia Ben Barry wa taasisi kuhusu usalama wa kimataifa ya International Institute for Strategic Studies (IISS) mjini London anasema mataifa yanafaa kuanza kufikiria upya mifumo ya kukabiliana na makombora. Anasema mataifa mengi ya Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi (Nato) hayajagundua tatizo linalowakabili. Teknolojia ya APS inatishia kufanya silaha nyingi za kukabiliana na vifaru kutofanikiwa, na mataifa mengi ya Magharibi hayajaanza kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu hatua za kuchukua. Anasema baadhi ya nchi zinafanya utafiti na majaribio kivyake kuweka mfumo huo wa APS kwenye vifaru vya mataifa hayo. "Lakini yanakosa kuzingatia matokeo ya teknolojia hii kwa mfumo wao wa kukabiliana na vifaru," anasema. Norway ni moja ya nchi za kwanza kukumbana na hatari hii. Nchi hiyo inapanga kutumia krona 200-350 milioni (£18.5-32.5 milioni; $24-42 milioni) kubadilisha makombora yake ya Javelin na "kudumisha uwezo wake wa kukabiliana na vifaru". "Kuna haja ya kuwa na makombora ambayo yanaweza kupinga mfumo wa APS." Teknolojia ya APS imebadilisha mambo katika historia ya kuangazia kushambulia na kujilinda wakati wa vita. Katika vipindi fulani, kuna moja ambayo imekuwa mbele. Zamani, vifaru visivyoweza kupenya risasi vilitawala, lakini makombora nayo yakaimarishwa na kumaliza ubabe huo. Tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, vifaru vimeendelea kutawala katika uwanja wa vita. Vifaru hata hivyo, huwa vinaweza kuharibiwa na makombora au mabomu ya vifaru vingine vikiwa karibu. Lakini kulikuwa pia na tishio kutoka kwa silaha nyingine, mfano makombora ya kurushwa kutoka mbali au kutoka kwa ndege, jambo ambalo ndilo teknolojia ya APS imeundwa kukabili. Makombora ya kurushwa kwa kutumia mizinga ya kubeba mabegani yanaweza kuharibu makombora. Hapa, ni mazoezi ya kukabili makombora Korea Kusini, mshirika wa Marekani. Vifaru vya Israel aina ya Merkava huwa na teknolojia ya APS Israel ni miongoni mwa mataifa ambayo yamekuwa yakiongoza katika teknolojia ya kujikinga na vifaru vyake aina ya Merkava hutumia teknolojia hii. Vifaru hivyo vilitumiwa kukabiliana na wapiganaji wa Kipalestina ukanda wa Gaza. Mfumo huo wa Israel pia unachunguzwa na Wamarekani. Uingereza pia imeanza kutafakari uwezekano wa kustawisha teknolojia kama hiyo. Uholanzi imeamua kutumia teknolojia nyingine, pia kutoka Israel, kukinga vifaru vyake. Urusi imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya mfumo wake wa kukabiliana na vifaru wakati wa vita. text: Kiongozi huyo ameombwa kuuwaachia uhuru wa wananchi wazungumze inapowezekana ili kuruhusu demokrasia. Akizungumza kwenye kikao hicho, Mchungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Amani Lyimo amesema, 'Unafanya kazi nzuri sana, lakini baba demokrasia, Watanzania wengi, wana hofu. Hata kama huambiwi na watendaji wako, wengi hawasubutu kuzungumza. Wana hofu. 'Watu hawatachagua maneno watachagua kazi. Na kama ni mpiga kazi, tunaye, kwahiyo kama kuna uwezekano waachie wazungumze'. Rais Magufuli, ameijibu kauli hiyo kwa kutoa hakikisho kwamba Tanzania demokrasia ipo na tena 'ya hali ya juu'. Hatahivyo ameeleza kwamba demokrasia sio kuruhusu maandamano tu na kwamba ina mipaka yake. 'Nyinyi ni mashahidi viongozi wa dini, mumekuwa mukisafiri katika nchi za nje, sina hakika kama mumeshuhudia maandamano na matusi kila mahali, tukienda kwa utaratibu huo, tutashndwa kuitawala nchi, tutashindwa kujenga maendeleo mengine'. Kadhalika rais amefafanua kwamba hakuna aliyezuiwa kufanya mkutano katika maenoe yao ya uwakilishi. Ila kinachozuiwa ni viongozi kwenda kufanya fujo katika eneo la mwingine. 'Kinachozuiliwa ni katika kudhibiti amani ya nchi hii. Mtu anatoka katika jimbo moja kwenda katika jimbo la mwenzake kutukana. Ile ni himaya ya mwingine. Sio mara ya kwanza kwa rais Magufuli kusisitiza umuhimu wa heshima miongoni mwa wanasiasa, aliwahi kumpa salamu hizo Edward Lowassa, kiongozi wa chama cha upinzani Chadema Ametoa wito kwa vyama vya kisiasa kufuata mfano wa namna viongozi wa dini nchini wanavyoheshimiana na kusisitiza kwamba bila ya amani mahali popote hakuna maendeleo. Kuzuiwa kwa mikutano Tanzania Tangu kuingia serikali ya Rais John Magufuli, wabunge na wanasiasa wanaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo wanayowakilisha, na sio vinginevyo na wakati mwengine hata ruhusa hiyo pia huzuiliwa. Hali hii wadadisi wanaona imepunguza kasi ya upinzani kuwafikia wananchi. Kumekuwa na malalamiko kuwa demokrasia imekuwa ikiminywa Tanzania huku baadhi wakihoji kwamba mambo mengine yanafanyika kana kwamba nchi hiyo ni ya chama kimoja ilhali kuna vyama vingi vya kisiasa. Vyama vya upinzani nchini Tanzania vimeshutumu hatua ya polisi nchini humo kupiga marufuku mikutano ya hadhara. Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe akiwa mahakamani Wabunge kadhaa wa upinzani wakishtakiwa kwa makosa mbalimbali akiwemo mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo , Zitto Kabwe. Kwa wakati mmoja hata chama cha Demokrasia na maendeleo - Chadema kilipanga kuzindua msururu wa mikutano ya hadhara nchini walioiita "Operesheni Okoa Demokrasia". Pamoja na mambo mengine operesheni hiyo ililenga kuishitaki serikali ya Rais John Magufuli kwa umma kuhusu maswala kama vile kufungiwa kwa kurushwa moja kwa moja kwa vikao vya bunge na aina ya uongozi wa serikali ya Rais Magufuli. Polisi imewahi kuzuia mikutano ya upinzani katika siku za nyuma nchini humo kwa sababu tofauti ikiwemo usalama, na pia kuzuia ushawishi kwa wananchi kuvunja sheria. Mkutano huo maalum umeandaliwa na rais Magufuli kwa madhumuni ya kukutana, kusikia kauli na kushauriana na viongozi wa kidini na madhehebu mbali mbali, kuhusu masuala wanayoyaona nchini. Viongozi hao wa dini walipata fursa ya kuelezea matatizo yanayoyakabili maeneo kadhaa ikiwemo masuala ya kijamii, kiuchumi na hata yale ya kisiasa. Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wameupongeza na kuhimiza zaidi ushirikiano baina yao na serikali na kueleza kwamba una nafasi ya kuleta ubora katika uongozi wa nchi. Suala la demokrasia na uhuru wa kuzungumza Tanzania limechipuka katika mkutano wa rais John Magufuli na viongozi wa dini zote uliofanyika katika Ikulu mjini Dar es salaam. text: Waziri wa Afya Dorothy Gwajima akionesha jinsi ya kutengeza kinywaji anachodai bila ushahidi kina uwezo wa kuzuia maambukizi wa corona BBC imezungumza na familia moja ambayo inaomboleza kifo cha mume na baba ambaye anadhaniwa kuwa alipata maambukizi ya corona. Hofu iliyopo ni kuwa, japo serikali inakanusha uwepo wa janga, watu wengi wanapoteza maisha kutokana na mlipuko wa virusi hivyo. Peter - si jina lake halisi - alirejea nyumbani akitoka kazini huku akiwa amepoteza ladha ya chakula na kifua kikavu, baada ya wiki moja ya kuugua nyumbani alipelekwa hospitali ambapo baada ya saa chache alipoteza maisha. Peter hakufanyiwa vipimo vya corona. Kuna upimaji wa kiwango cha chini ambao unafanyika Tanzania ukulinganisha na nchi nyengine. Ni vigumu kukadiria ni kwa kiasi gani mlipuko wa corona ulivyopenya Tanzania na ni maafisa wachahce tu wa ngazi ya juu serikalini ambao wanaruhusiwa kuzungumzia hilo. Hata hivyo, kauli mbalimbali ambazo zimetolewa katika siku za hivi karibuni zimetoa taswira ambayo ni tofauti kabisa na uhalisia unaokabiliwa na baadhi ya wananchi, kama mke wa Peter, ambao wanaomboleza kwa ukimya vifo vya wapendwa wao ambao wanadhaniwa kufariki baada ya kuambukizwa virusi hivyo. Maafisa wahamasisha kunawa mikono na mtindo mzuri wa maisha kuzuia maambukizi ya virusi vya corona Familia kadhaa nchini Tanzania zinapitia kipindi kigumu kama familia ya Peter, lakini hata hivyo zimeamua kukaa kimya, zikiogopa madhara ambayo yanaweza kuwakuta kwa kuzungumza. Serikali ya Uingereza imepiga marufuku wasafiri wote kutoka Tanzania, isipokuwa wenye vibali vya kazi, wakati ambapo Marekani imewaonya raia wake dhidi ya kutembelea Tanzania kutokana na corona. Mzozo wa chanjo Toka mwezi Juni mwaka jana ambapo rais John Magufuli alipotangaza Tanzania haina tena corona, yeye pamoja na viongozi wengine wamekuwa mstari wa mbele kukosoa baadhi ya njia za kupambana na corona na kusisitiza kuwa Tanzania haitatumia mbinu hizo. Rais Magufuli pia ameonya - bila kutoa ushahidi - kuwa chanjo za Covid-19 zinaweza kuwa na madhara na badala yake amewarai Watanzania kujifukiza na kutumia dawa za asili, ambazo hakuna hata moja iliyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama tiba dhidi ya virusi vya corona. Ni vigumu kujua kwa nini rais Magufuli amechukua msimamo huo dhidi ya chanjo lakini pia amesema Watanzania wasitumike kama sehemu ya majaribio. "Kama wazungu wangekuwa na kinga, basi kusingekuwa na Ukimwi, kansa na Kifua Kikuu kufikia sasa," ameeleza Magufuli ambaye amejipambanua kama mtu anayepingana na ubeberu. WHO hata hivyo inapinga msimamo huo. "Chanjo zinafanya kazi na naishauri serikali ya Tanzania] kujiandaa na kampeni ya chanjo ya Covid," amesema Dkt Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO barani Africa, na kuongeza kuwa shirika hilo lipo tayari kuisaidia Tanzania. Wizara ya Afya nchini Tanzania imekuwa ikiwashauri raia kujifukiza bila kutoa ushahidi kwamba hatua hiyo inazuia corona Waziri wa Afya Dorothy Gwajima amesisitizia msimamo wa Bw Magufuli juu ya chanjo, akisema kuwa wizara yake "ina taratibu zake za kuagiza dawa na hufanya hivyo baada ya kujiridhisha juu ya ubora wake." Dkt Gwajima aliyasema hayo mwanzoni mwa wiki alipokutana na waandishi wa habari ambapo wizara ya afya ilionesha namna gani ya kutengeneza kinywaji cha asili kwa kutumia tangawizi, vitunguu, ndimu na pilili - mchanganyiko ambao wanadai, bila Ushahidi, kuwa unasaidia kumkinga mtu dhidi ya maambukizi ya corona. Waziri huyo pia amesisitiza juu ya usafi binafsi, kuosha mikono na maji tiririka na sabuni, kujifukiza, kufanya mazoezi, kula lishe bora pamoja na kutumia tiba asili ambazo zimejaa Tanzania. Lakini hatua zote hizo si kwa kuwa Tanzania kuna corona. Waziri ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kuandaliwa kwa kuwa corona ipo nchi jirani. Baadhi ya madaktari hawakubaliani na msimamo wa serikali. "Tatizo ni kuwa serikali inawahakikishia wananchi kuwa tiba asili, ndio suluhisho pekee la kujikinga na corona. Pamoja na faida zake, zinaweza kusaidia kuinua kinga ya mwili na kadhalika, lakini tiba asili si kinga ya corona," daktari mmoja ameiambia BBC kwa sharti la kutotajwa jina na kuwataka wananchi wachukue tahadhari. Hivi karibuni, Kanisa Katoliki lilivunja ukimya na kuwaonya wananchi kuchukua tahadhari zote. "Covid haijaisha, bado ipo. Tusipuuze, inatupasa tujilinde, osha mikono yako na maji na sabuni. Pia inabidi turejee kuvaa barakoa," Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es Salaam Dar es Salaam Yuda Thadei Ruwaichi aliwaambia waumini. Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania Episcopal Conference, Dkt Charles Kitima, ameiambia BBC kuwa kanisa limeshuhudia ongezeko la vifo, hususani mjini. "Tulizoea parokia za miji mikubwa misa ya mazishi moja ama mbili kwa wiki. Sasa kila siku kuna msiba. Tumeona hiki kitu si cha kawaida, kuna kitu hakiko sawa," Padre Kitima aliieleza BBC. Waziri wa Afya hata hivyo alionya kuwa matamko yasiyo rasmi kutoka serikalini yamekuwa yakishtua watu. Lakini kutokuwepo kwa takwimu rasmi kutoka kwa serikali kunafanya hata mjadala wa hali ya mambo ulivyo kuwa mgumu. 'Vaa barakoa - lakini si kwa sababu ya corona' Licha ya serikali kukanusha uwepo wa corona lakini kuna baadhi ya kauli za viongozi ambazo zinajenga picha tofauti. Mwezi uliopita siku moja tu baada ya Kanisa Katoliki kutoa tamko lake na siku chache baada ya Denmark kutangaza kuwa wasfiri wawili kutoka Tanzania wamegundulika kuwa na virusi vipya vya corona, rais Magufuli aliwalaumu baadhi ya Watanzania walioenda kuchanjwa ughaibuni kwa "kuleta corona ya ajabu ajabu." Afisa wa wizara ya Afya Mabula Mchembe Kulia alisema kwamba wagonjwa wanaougua matatizo ya kupumua hawaugua covid -19 Ijumaa, gazeti la Mwananchi nchini Tanzania limemnukuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Mabula Mchembe akisema kuwa uvaaji wa barakoa " si kwa sababu ya corona, kama baadhi ya watu wanavyodhani, lakini ni kwa kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya hewa." Jambo moja ambalo limetia doa msimamo wa serikali ni tangazo kwa umma kutoka chama cha ACT Wazalendo kuwa mmoja ya viongozi wake wakuu, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar pamoja na mkewe na wasaidizi wake kadhaa wamekutwa na maambuzi ya corona. Bwana Magufuli kulia na bwana Hamad wanasalimiana kwa miguu mwezi Machi mwaka uliopita, wiki chache kabla ya Tanzania kuandikisha kisa cha kwanza cha corona Serikali mpaka sasa haijaongelea chochote juu ya hali ya Maalim Seif, pia haijajibu maombi ya BBC ya kutoa maoni yake kuhusu taarifa hii. Januari 21, siku ambayo Peter alianza kuugua, kuna taarifa nyengine kuhusiana na corona iliokuwa ikiendelea mjini Moshi. Uongozi wa shule moja maarufu ya kimataifa ulikuwa ukiomba radhi na kubadili taarifa kuwa moja ya wanafunzi wao alikutwa na corona na kusimamisha masomo ya ana kwa ana. Wakati hali ya mambo ikiendelea kama kawaida nchini Tanzania, mke wa Peter amezongwa na majuto moyoni mwake kwa kuwa kama ilivyo kwa wananchi wengine yeye na mumewe hawakuchukua tahadhari yoyote kujilinda. Kutokujilinda kwao pengine si jambo la kushangaza katika nchi ambayo raisi wake na viongozi waandamizi wamekuwa wakisisitiza kuwa "hakuna corona." Pia unaweza kutazama: Aspera Covid 19 Nyungu, mfumo unaoaminiwa ''kutibu'' corona Kwa miezi kadhaa sasa serikali ya Tanzania imekuwa ikisisitiza kuwa hakuna ugonjwa wa Covid-19 - na hivyo hakuna mipango yoyote ya kuwachanja wananchi wake. text: Rais Donald Trump amekana shutuma kuwa alikuwa na uhusiano na Stormy Daniels Daniels anadai kuwa yeye na Bwana Trump walikuwa na mahusiano tangu mwaka 2006, lakini alikana shutuma hizo. Kwa nini habari hii ni muhimu? Stormy Daniels ni nani? Stormy Daniels alizaliwa Stephanie Clifford, Louisiana mwaka 1979. Alihamia kwenye soko la kucheza filamu za utupu kwanza kama mtumbuizaji, kabla ya hapo mwaka 2004 alikuwa akiongoza na kuandika filamu. Jina lake la jukwaani,Stormy Daniels, limetokana na jina la binti wa mwanamuziki wa kundi la Mötley Crüe, 'Storm' na jina la kinywaji aina ya Whisky , 'Jack Danniels'. Unaweza kumtambua kwenye filamu ya 'The 40-Year-Old Virgin' na 'Knocked Up' na video ya muziki wa kundi la Maroon Five 'Wake up call' . Mwaka 2010 alifikiria kugombea uongozi kwa nafasi ya useneti Louisiana lakini aliahirisha baada ya kusema kuwa ushiriki wake hautiliwi maanani. Stormy Daniels jina halisi ni Stephanie Clifford, anadai alikutana na Donald Trump mwaka 2006 Anadai nini? Mwezi Julai mwaka 2006, Bi Daniels anasema alikutana na Trump kwenye michuano ya hisani ya Golf huko Lake Tahoe, eneo la kujivinjari la kati ya California na Nevada. Katika mahojiano yake na jarida la In Touch Weekly' mwaka 2011 na kuchapishwa mwezi Januari, alisema Trump alimualika chakula cha jioni na kuwa alikwenda kukutana naye kwenye chumba chake cha hoteli. ''Alikuwa amejibwaga kwenye kochi, akitazama televisheni'', alisema kwenye mahojiano hayo, ''alikuwa amevaa nguo za kulalia''. Bi Daniels anasema walifanya mapenzi kwenye chumba cha hoteli (Mwanasheria wa Trump amesema Trump amekana shutuma hizo) Kama madai ya mwanadada huyo ni ya kweli, haya yote yangekuwa yametokea miezi minne tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto wa Trump mdogo, Barron. Donald Trump, Melania Trump na Barron Trump mwezi Januari mwaka 2007 Bi Daniels alisema Trump alimwambia anaweza kumshirikisha kwenye kipindi chake cha Televisheni, The Apprentice. Amedai kuwa aliangalia sinema ya maisha halisi ya Papa na rais huyo ajaye. Michael Cohen anaripotiwa kumlipa Stormy Daniels dola 130,000 mwaka 2016 Baada ya hapo anasema waliendelea kuwasiliana kwa miaka kadhaa, Bi Daniels anasema mara ya mwisho kuwasiliana ilikuwa mwaka 2010, wakati alipoahirisha kugombea useneta. Hata hivyo tetesi kuhusu uhusiano wao zilianza kujionyesha mwezi Novemba 2016 wakati wa uchaguzi wa urais. Jarida la Wall Street liliripoti siku kadhaa kabla ya kura kuwa bi.Daniels alikuwa kwenye mijadala kwenye kipindi cha asubuhi cha televisheni ya ABC ''Good Morning America'' kueleza yote kuhusu mahusiano yake, kabla ya kuyakata ghafla mazungumzo. Kwa nini hii ni habari kwa sasa? Mwezi Januari, Jarida la Wall Street lilichapa makala iliyodai kuwa Wakili wa Trump, Michael Cohen, alimlipa dola za Marekani 130,000 mwanadada huyo mwezi Oktoba mwaka 2016, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi. Jarida linasema pesa hizo zilikuwa ni sehemu ya makubaliano ambayo hayakufahamika,ambayo alisema hakuweza kujadili masuala yake mbele ya Umma. Ripoti nyingi zilitolewa kuhusu hayo lakini shutuma zilikanushwa vikali wakati wakielekea kwenye uchaguzi, maafisa wa Ikulu wameeleza. Rais Trump alighadhabishwa na namna ambavyo Sarah Sanders alikuwa akijibu maswali kuhusu Bi.Daniels Bwana Cohen alikana madai ya kumlipa pesa mwanadada huyo, katika taarifa yake kwenye jarida na kuita shutuma hizo kuwa hazina maana.Na wamekua wakipinga hilo kwa miaka kadhaa. Lakini mwezi Februari alitangaza kuwa alimlipa Bi.Daniels pesa. Katika taarifa aliyoitoa kwa New York Times, Bwana Cohen alisema si kampeni za Trump wala Taasisi yake iliyojua chochote kuhusu malipo,ambayo aliyatoa kutoka mfukoni mwake mwenyewe. Alisema hakurejeshewa pesa. ''Malipo kwa Bi Daniels yalikuwa yamefuata sheria'', haikuwa mchango wa kampeni wala si kwa matumizi ya kampeni. Muda mfupi baada ya makala ya jarida hilo, Bi Daniels alizindua kampeni yake aliyoiita ''Make America Horny Again'' akisafiri kwenda South Carolina kwenye vilabu vya dansi za utupu wakati wa sherehe za maadhimisho ya kuapishwa kwa Donald Trump. Meneja wa klabu,Jay Levy alisema alihitaji huduma yake, hiyo ilikuwa siku moja baada ya Jarida la the Wall Street kuchapisha makala kuhusu malipo ya dola za kimarekani 130,000. Kipeperushi kuhusu sherehe hizo kilikuwa kina mzaha kusu mahusiano. Kikieleza ''alimuona moja kwa moja'' ''unaweza kumuona pia''. Kinachoendelea sasa Bi Daniels siku ya Jumanne alisema anamshtaki Trump, akidai kuwa hakuweka saini makubaliano yao ya kutoyaweka wazi mahusiano yao. Mwanasheria wake, Michael Avenatti, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu mashtaka yakihusishwa na nyaraka zilizowasilishwa kwenye mahakama ya California. Siku iliyofuata, ripoti zilisambaa zikisema Rais Trump alishinda kizuizi dhidi ya Bi Daniels. Amri hiyo ya kizuizi ilimpa marufuku Bi Daniels kutoa taarifa za siri, kuhusu kinachoelezwa kuwa uhusiano wake na Trump. ''Kesi hii ilishafanyiwa suluhisho, kama kitafanyika chochote mbali na hicho, nitafikisha kwa mshauri wa nje wa Rais'' alieleza katibu wa habari wa Ikulu Sarah Sanders siku ya Jumatano. Mwanasheria wa Daniels amesema kuwa kauli hiyo ya Ikulu ni ''kichekesho''. Shirika la habari, CNN liliripoti Alhamisi kuwa Rais Trump amekasirishwa na kauli ya Sanders, kwani ni mara ya kwanza kwa mtu kutoka Ikulu kuashiria kuwa Trump alikuwa kwa namna yeyote akijihusisha na Bi Daniels. Maoni ni yapi kuhusu hayo? Mbunge wa Congress kutoka South Carolina, Mark Sanford ni mmoja kati ya wachache waliotoa maoni, aliliambia gazeti la Washington Post kuwa madai hayo ''yanafedhehesha mno''. Wabunge wa Democrats Ted Lieu na Kathleen Rice, wanaowakilisha jimbo la California na New York wamelitaka shirika la upelelez FBI kuchunguza malipo yaliyofanywa na Cohen kwa Bi Daniels. Ina maana gani kwa Trump? Shutuma hizi zimekuja wakati mgumu kidogo kwa maafisa wa White house, na hazioneshi dalili yoyote ya kuisha. Mbali na kuwepo kwa uchunguzi kuhusu mahusiano yake na Urusi, maafisa wa Trump wamekuwa kwenye kikaango. Hali hii ni kama inaleta kivuli cha aliyekuwa rais wa Marekani. Kumbuka Bill Clinton alikumbwa na tishio la kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye baada ya kusema uongo kuhusu uhusiano wake na staffer Monica Lewinsky. Lanny Davis, mwanasheria aliyekuwa mshauri wa Rais Clinton, siku ya Jumatano aliwashutumu viongozi wa Republican kwa ''kusema uongo'' kwa namna wanavyomtendea Rais Trump tofauti na walivyofanya kwa Clinton. Mcheza filamu za utupu Stormy Daniels anamshtaki Rais Donald Trump kwa kile kinachoitwa ''hush agreement'' ambayo ni makubaliano ya kutozungumzia mahusiano yao. text: Tayari upo uzio unaotenganisha mpaka baina ya Marekani na Mexico Fedha hizo ni za kwanza kutolewa chini ya hali ya tahadhari ya kitaifa iliyotangazwa na rais Donald Trump ambazo hazikupitishwa na baraza la Kongresi na kujenga kizuwizi alichokiahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi. Democrats wameipinga hatua hiyo. Pesa hizo zitatumiwa kujenga uzio wa maili 57. Rais Trump ameitaja hali katika mpaka wa kusini kama "mzozo " na akasisitiza mpaka kizuwizi halisi kinahitajika ili kuwazuwia wahalifu kuvuka mpaka na kuingia Marekani .Wakosoaji wake wanasema amebuni dharura ya mpaka. Taarifa ya Pentagon imesema kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan alikwa "amemuagiza kamanda wa kikosi cha Marekani cha wahandisi kuanza kupanga na kutekeleza usaidizi wa dola bilioni 1 kwa wizara ya usalama wa ndani na udhibiti wa mipaka na forodha". Taarifa hiyo ilielezea sheria ya serikali kuu kwamaba "inaipatia Wizara ya ulinzi mamlaka ya kujenga barabara na uzio na kuweka taa za barabarani kwa ajiliya kufunga mapito baina ya mipaka ya kimataifa na Marekani kama sehemu ya kusaidia kukabiliana dhidi ya shughuli za narcotic chini ya taasisi za usalama ". Pamoja na ukuta huo wenye urefu wa futi 18 "uzio wa wapitanjia ", fedha hizo zitatumika katika ukarabati wa barabara na kuweka taa mpya. Seneta wa Democratic alilalamika kuwa Pentagon haikuomba ruhusa ya kamati husika kabla ya kulifahamisha baraza la Kongresi kuhusu utoaji wa pesa hizo. maelfu ya watu huvuka mpaka kila mwaka wakitafuta maisha mapya nchini Marekani " Tunapinga vikali malengo ya kuhamishwa kwa fedha na pia utekelezaji wa wizara wa kuhamishwa kwa fedha bila kuomba idhini ya kamati za bunge za Kongresi za usalama Kongresi na ukiukaji wa vipengele vya ugawqaji wenyewe wa wizara ya ulinzi ," Waliandika katika barua kwa Bwana Shanahan, limeripoti shirika la CNN. Bwana Trump alitangaza dharura tarehe 15 Februari baada ya Kongresi kukataa ombi lake la kuidhinishwa kwa dola bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta. Kwa kutangaza hali ya tahadhari alipata uwezo wa kutolihusisha baraza la Kongresi na kujenga ukuta kwa pesa za jeshi. Democrats walisema tangazo hilo si la kikatiba. Bunge la Wawakilishi linalodhibitiwa na Democratic lilipitisha azimio la kupinga dharura hiyo mwezi uliopita, na wabunge 12 wa Republican baadae walijiunga na maseneta wa Democratic kuipitisha katika Seneti Hata hivyo, Bwana Trump alitumia mamlaka aliyonayo kupiga kura ya veto dhidi ya maazimio hayo mapema mwezi huu. Kwa sasa Kongresi itahitaji kuwa na theluthi mbili ya walio wengi katika mabunge yote kumpiku , jambo ambalo waandhishi wa habari wanasema huenda lisiwezekane. Wizara ya ulinzi ya Marekani The Pentagon imeidhinisha kuhamishiwa kwa dola bilioni moja ($1bn) kwenye akaunti ya wahandisi wa jeshi kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpaka baina ya Marekani na Mexico. text: George Floyd mara kwa mara aliwaambia maafisa waliomkamata kwamba hawei kupumua George Floyd , 46 alifariki baada ya kukamtwa na maafisa wa polisi nje ya duka moja katika mji wa Minneapolis katika jimbo la Minnesota. Kanda ya video ya tarehe 25 mwezi Mei inamuonyesha afisa wa polisi mzungu , Derek Chauvin , akiwa amepiga magoti katika shingo ya bwana Floyd huku akiwa amezuiliwa chini katikati ya barabara. Bwana Chauvin ,44 kwa sasa ameshtakiwa kwa mauaji. Matukio yaliopelekea kifo cha bwana Floyd yalitokeo katika kipindi cha dakika 30 . Kulingana na walioshuhudia , kanda ya video na taarifa rasmi, hiki ndicho tunachokijua. Ilianza na ripoti kuhusu noti bandia ya $20. Ripoti ilitolewa jioni ya tarehe 25 Mei, wakati bwana Floyd alinunua pakiti ya sigara katika duka la Cup foods. Baada ya kuamini kwamba noti ya dola 20 aliyoitoa Floyd ilikuwa bandia , mfanyakazi mmoja wa duka hilo aliripoti kwa polisi. Bwana Floyd alikuwa akiishi katika mji wa Minneapolis kwa miaka kadhaa baada ya kuhama kutoka Houston katika jimbo la Texas. Alikuwa akifanya kazi kama mlinzi mjini humo, kama mamilioni ya raia wengine wa Marekani, alikuwa amepoteza kazi yake kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Bwana Floyd alikuwa mteja katika dula la Cup Foods . ''Alikuwa rafiki wa duka hilo, mteja mzuri ambaye hakusababisha tatizo lolote'' , mmiliki wa duka hilo Mike Abumayyaleh aliambia chombo cha habari cha NBC. Lakini bwana Abumayyaleh hakuweko kazini siku ya tukio hilo. Katika kuripoti kuhusu noti hiyo bandia, mfanyakazi wake kijana alikua anafuata itifaki za kazi. Baada ya kupiga simu ya 911 mwendo 20.01, mfanyakazi huyo alimtaka Floyd kurudisha sigara hizo , lakini Floyd alikataa kurudisha kulingana na maandishi yaliotolewa na mamlaka. Mfanyakazi huyo alisema kwamba Floyd alionekana kana kwamba amekunywa pombe na hakuweza kujizuia , yalisema maandishi hayo. Muda mfupi baada ya simu mwendo wa 20.08, Maafisa wawili wa polisi waliwasili. Bwana Floyd alikuwa ameketi na watu wengine wawili katika gari ambalo lilikuwa limeegeshwa katika kona moja. Baada ya kulikaribia gari hilo, afisa mmoja wa polisi, Thomas Lane , alitoa bunduki yake na kumuagiza bwana Floyd kuonyesha mikono yake. Wakizungumza kuhusu tukio hilo, waendesha mashtaka hawakuelezea kwa nini bwana Lane aliamua kutoa bunduki yake. Kifo cha Floyd: Wamarekani weusi wasema 'hawako salama' Bwana Lane, waendesha mashtaka walisema walishika mikono ya Floyd na kumvuta nje ya gari hilo. Baadaye bwana Folyd akakataa kufungwa pingu. Baada ya kufungwa pingu, bwana Floyd alikubali kushikwa huku bwana Lane akielezea alikuwa anakamatwa kwa kutoa pesa bandia. Ni wakati maafisa wa polisi walipojaribu kumuingiza wbana Floyd katika gari lao ndiposa mvutano ukatokea. Mwendo wa 20.14, bwana Floyd alikataa na kuanguka chini na kuwaambia maafisa wa polisi kwamba ana tatizo la 'uoga ama hofu', kulingana na ripoti hiyo. Bwana Chauvin aliwasili katika eneo hilo. Yeye na maafisa wengine walihusika katika jaribio jingine kumuingiza bwana Floyd ndani ya gari. Wakati wa jaribio hilo ,20.19, bwana Chauvin alimvuta bwana Floyd nje kutoka katika kiti cha abiria na kumuangusha chini , ripoti hiyo ilisema. Alilala hapo uso wake ukiwa chini bado akiwa amefungwa pingu. Ni wakati huo ambapo mashahidi walianza kumrekodi bwana Floyd, ambaye alionekana kuwa katika hali ngumu. Tukio hilo ambalo lilirekodiwa katika simu nyingi na kusambazwa sana katika mitandao ya kijamii lilikua la mwisho la bwana Floyd. Bwana Floyd alizuiliwa na maafisa , huku bwana Chauvin akimwekea goti lake katikati ya kichwa chake na shingo. 'Siwezi kupumua', bwana Floyd alisema na kurejelea mara kwa mara , akimlilia mamake na kuomba tafadhali, tafadhali ,tafadhali. Kwa dakika 8 na sekunde 46, bwana Chauvin aliweka goti lake katika shingo ya Bwana Floyd , ilisema ripoti ya mwendesha mashtaka. Derek Chauvin anatarajiwa kufika mbele ya mahakama katika mji wa Minneapolis siku ya Jumatatu Dakika sita baada ya tukio hilo, bwana Floyd alikuwa amepoteza fahamu . Katika kanda ya video ya tukio hilo , bwana Floyd alinyamaza huku mashuhuda wakimtaka afisa huyo wa polisi kuchunguza mishipa yake ya damu iwapo bado alikuwa hai. Mmoja wa maafisa hao JA Kueng, alifanya hivyo , akiutazama mkono wa kulia wa bwana Floyd, lakini hakuweza kupata mshipa hata mmoja. Lakini maafisa hao hawakumuachilia. Mwendo wa 20.27 , bwana Chauvin aliondoa goti lake kutoka shingo ya bwana Floyd . Akiwa amepoteza fahamu , bwana Floyd alipelekwa katika kituo cha afya cha Hennepin akiwa ndani ya ambyulansi. Alitangazwa kuwa amefariki saa moja baadaye. Usiku kabla ya kifo chake , bwana Floyd alizungumza na rafikiye mmoja wa karibu , Christopher Harris . Alikuwa amemshauri bwana Floyd kuzungumza na mawakala wa kazi za muda. ''Kughushi , alisema , sio tabia ya bwana Floyd. 'Jinsi alivyofariki ni ukatili mkubwa' , alisema Harris. Aliomba uhai wake. aliomba uhai wake. Unapojaribu kuweka imani kwa mfumo huu, mfumo ambao unajua hakutengenezewa wewe , unapotaka haki mara kwa mara na hauwezi kupata unaanza kuchukua sheria mikononi mwako. Marekani imekabiliwa na maandamano ya kitaifa kuhusu kifo cha M'marekani mweusi aliyekua amekamatwa na maafisa wa polisi. text: Lionel Messi alifunga bao lake la 100 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kusaidia kuwalaza Chelsea 3-0 uwanjani Nou Camp Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1. Mechi ya kwanza uwanjani Stamford Bridge ilikuwa imemalizika 1-1. Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia. "Hatuna majuto," alisema Conte. "Ukiitazama mechi hiyo, utaona kwamba matokeo hayo hayakuwa ya haki." Conte alikiri kwamba Messi - aliyefunga pia bao la Barca mechi ya kwanza Stamford Bridge - ndiye aliyekuwa mwamuzi wa nani mbabe kati ya timu hizo mbili. Bao la pili la mshambuliaji huyo wa Argentina uwanjani Nou Camp lilifikisha 100, idadi ya mabao ambayo ameyafunga Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Lionel Messi akipongezwa na meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya mechi Jumatano Mpinzani wake mkuu kutoka Real Madrid Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi akiwa na mabao 117. Hata hivyo, Messi amefikisha idadi hiyo akiwa amecheza mechi 14 chini ya alizocheza Ronaldo ndipo afikishe mabao hayo. "Tunazungumzia mchezaji bora zaidi duniani," alisema Conte. "Huwa anafunga mabao 60 kila msimu - ni mchezaji mzuri ajabu. Barcelona walikuwa na ufasaha sana wakishambulia." Chelsea waliongoza kwa dakika 13 mechi ya kwanza na waligonga mwamba na mlingoti wa lango mara nne katika mechi zote mbili. N'Golo Kante na Marcos Alonso wote walikaribia kufunga uwanjani Nou Camp, naye Antonio Rudiger alipiga mpira wa kichwa ambao uligonga mwamba wa goli dakika za mwisho. Blues walinyimwa ombi lao la kutaka penalti Alonso alipoanguka eneo la hatari baada ya kukabiliwa na Gerard Pique. "Hatukustahili kushindwa 3-0," alisema Conte. "Tulikosa bahati kiasi. "Tafikiri tulitengeneza naafsi nyingi lakini hatukuzitumia. "NI lazima nijivunie sana wachezaji wangu - walijitolea kabisa na ni lazima tuendelee hivi, nia hii ya kupambana na kupigana vita pamoja uwanjani." Wachezaji wa Chelsea waliotamauka wakiondoka uwanjani baada ya kushindwa Nou Camp Courtois hatarajia kombora la Messi Mlindalango wa Chelsea Thibaut Courtois aliambia BT Sport kwamba anaamini makosa ya wachezaji binafsi yaliigharimu timu hiyo. "Sifikiri kwamba tulifaa kuondolewa, lakini makosa ya wachezaji binafsi yalitugharimu ushindi mechi zote mbili. "Bao la kwanza ... Sikutarajia Lionel Messi angetoa kombora kutokana na pahali ambapo alikuwa na nilichelewa kufunga mwanya kati ya miguu yangu. Hilo lilikuwa kosa langu. "Pahali dhaifu zaidi huwa ni katikati ya miguu ya golikipa. Inaudhi. Siwezi kujificha ndani (ya lango), ni lazima niwe kama mwanamume na kutokea." Antonio Conte atakutana na Leicester Jumapili kupigania nafasi ya kufuzu kwa nusufainali katika Kombe la FA Winga wa Chelsea Marcos Alonso aliambia BT Sport kwamba walifahamu kwamba Barca wana wachezaji wazuri sana. "Na hatuwezi kuwapa nafasi, hata mita moja, kwa sababu wanaweza kuunda nafasi na kufunga." Amesema sasa ni lazima warudi kujiboresha zaidi, kufanya mazoezi na "kujiboresha". Lionel Messi akisherehekea baada ya kuwafunga Chelsea Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki". text: Taasisi ya damu na upandikizaji ya Uingereza inawataka watu waliopona homa ya mapafu, covid-19 kuchangia damu ili waweze kutathimini tiba hii iliyo kwenye majaribio. Matumaini ni kwamba molekyuli walizozitengeneza zitasaidia kupambana na virusi vilivyo kwa wengine. Marekani tayari imeanza mradi mkubwa wa utafiti huu, ikihusisha hospitali 1,500. Mtu anapokuwa na virusi vya corona, mfumo wa kinga hutengeneza molekyuli, ambazo huvishambulia virusi. Kwa kipindi fulani molekyuli hizi zinaweza kupatikana kwenye plazma, sehemu ya majimaji ya damu. Taasisi ya damu na upandikizaji sasa inawasiliana watu waliopona Covid-19 kuona kama plazma zao zinaweza kutolewa na kupewa wagonjwa wengine wanaoumwa ugonjwa huo. Taarifa ya taasisi hiyo imesema: ''tunatafakari uwezekano kwamba hii itatumika awali kama tiba ya Covid-19. ''Ikiwa itaidhinishwa,majaribio yatafanyika kuchunguza kama plazma hizo zitasaidia kuongeza kasi yakuimarisha afya ya mgonjwa aweze kupona haraka. ''Kila majaribio yanapaswa kufuata mchakato wa kuidhinishwa ili kuwalinda wagonjwa na kuhakikisha matokeo ya uhakika yanapatikana. Tunafanya kazi kwa ukaribu na serikali na vyombo vyote vinavyohusika kupitia mchakato wa kupata idhini haraka iwezekanavyo.'' Makundi mengine wanafanya hili? Makundi kadhaa nchini Uingereza yamekuwa yakitazamia kutumia plazma ya damu. Chuo cha kitabibu katika hospitali ya Wales, Cardiff ilitangaza wiki hii kuwa ilitaka kufanyia majaribio teknolojia hii. Profesa Sir Robert Lechler, rais wa shule ya sayansi ya tiba na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la King's Health pia ana matumaini kufanya jaribio jingine dogo. Anataka kutumia plazma kwa wagonjwa walio mahuti ambao hawana namna nyingine ya kupata tiba, wakati ambao jaribio kubwa linaendelea nchini humo. Alisema: ''Ningesikitishwa sana kama tusingeweza kuwaona baadhi ya wagonjwa wakipewa aina hii ya tiba ndani ya majuma kadhaa. Tuwe na matumaini kuwa majaribio yanayofanywa na benki ya kitaifa ya damu yaanze haraka sana.'' Amesema Uingereza imechukua hatua taratibu mno kujaribu tiba hii. ''Ninafikiri kuna namna tofauti ya janga hili tunaweza kutazama na kulisema, ninashangaa kwa nini hatukuharakisha. Ninafikiri suala hili linaweza kuwa moja ya masuala ya kushughulikiwa haraka''. Hali ipoje kwengineko duniani? Duniani kote,majaribio yanaendelea wakitazamia kutumia plazma. Katika kipindi cha majuma matatu pekee, wanasayansi nchini Marekani wamejiunga kwa ajili ya mradi wa kitaifa na karibu wagonjwa 600 wametibiwa mpaka sasa. Profesa Michael Joyner kutoka hospitali ya Mayo, anaongoza kazi hiyo. Kukohoa ni moja ya dalili ya Covid-19 Anasema: ''Kitu tulichojifunza katika juma la kwanza la kazi hii ni kuwa kuwa hakuna tahadhari za kiusalama zilizojitokeza na kuwa tiba hii haijaonekana kuonesha athari ambazo hatukuzitarajia. ''Kuna mengi tussiyoyaelewa kuhusu plazma. Tutajifunza kuhusu plazma nini, vitu gani vinaiunda, na masuala mengine kuihusu kadiri muda unavyoendelea. Ni kwa namna gani njia hii ilisaidia kutibu magonjwa mengine awali? Kutumia damu ya watu waliopona si tiba mpya katika masuala ya kitabibu. Ilishawahi kutumika kabla njia hii zaidi ya miaka 100 iliyopita wakati wa ugonjwa wa mafua ya Uhispania, na zaidi hivi karibuni Ebola na Sars. Mpaka sasa, tafiti ndogo ndogo zimetazama ufanisi wake, na kuna kazi kubwa katika utafiti inayopaswa kufanywa kutazama namna gani ufanisi huu utaonekana dhidi ya virusi vya corona. Lakini nchini Marekani, wanasema hawana upungufu wa watu wanaotaka kusaidia. ''Tuna mamia kwa mamia ya wachangiaji na tumeweza kukusanya damu kiasi cha uniti 1,000 tayari. Inatia moyo kweli kuona kuwa watu walioathirika wanafikiria namna ya kuwasaidia wengine''. Hata hivyo wanasayansi wanasema plazma haiwezi kufanya mazingaombwe. Lakini wakati hakuna namna nyingi za kutibu virusi , kuna tumaini njia hii itasaidia mpaka pale chanjo itakapopatikana. Uingereza inaanza majaribio ya kutumia damu ya waliopona virusi vya corona kuwatibu wagonjwa walio na maambukizi hayo ambao wapo hospitali. text: Uchimbaji wa madini nchini Tanzania Waziri wa habari utamaduni na michezo Dkt Harrison Mwakyembe alilipiga marufuku gazeti hilo katika taarifa iliotolewa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa huduma za habari Dkt Hassan Abbasi siku ya Alhamisi jioni. Abbasi amesema kuwa marufuku hiyo inaanza mara moja. Toleo la gazeti hilo la siku ya Jumatano liliweka picha za marais wa awali wa Tanzania pamoja na habari inayowahusisha na matatizo yanayokumba sekta ya madini nchini Tanzania. ''Nimelazimika kutumia uwezo niliopewa na sheria ya huduma za habari kulipiga marufuku gazeti la Mawio kutochapishwa kwa kipindi cha miezi 24'',ilisema barua hiyo kutoka kwa waziri iliokabidhiwa muhariri wa gazeti hilo. Mbali na uchapishaji, gazeti hilo pia halitaruhusiwa kuendesha toleo lake la kidijitali ama hata katika mitandao ya kijamii. Gazeti la Mawio limeshutumiwa kwa kupuuza agizo la serikali kutoripoti kuhusu marais hao wa zamani. Siku ya Jumatano, rais Magufuli alivionya vyombo vya habari dhidi ya kuwahusisha Mkapa na Kikwete na ripoti za mzozo unaoendelea na kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Acacia. Alitoa onyo hilo baada ya kufanya mazungumzo na mwenyekii wa Barrick Gold Profesa John Thornton katika Ikulu ya rais siku ya Juamatano. ''Vyombo vya habari vinafaa kusita kujiharibia sifa.Vimefanya kazi nzuri katika kutoa huduma katika taifa hili.Tuwawache wapumzike'', alisema rais. Serikali ya Tanzania imelipiga marufuku gazeti la kila wiki la Mawio kutochapishwa kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kuwahusisha marais wa zamani Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na kashfa ya madini nchini humo. text: Mchungaji Alph Lukau (amevaa suti ya samawati) anatuhumu kumfufua jamaa huyu Video iliyosambaa ya mchungaji Alph Lukau inamuonyesha akipiga kelele akisema 'inuka' kwa anayeonekana kuwa maiti ndani ya jeneza ambaye baada ya hapo anainuka nakukaa wima huku waumini na wafuasi wakisherehekea. Kampuni hiyo ya mazishi inasema ilihadaiwa katika kuhusika kwenye tukio hilo. Kioja hicho, kilichofanyika nje ya kanisa la mchungaji Lukau karibu na Johannesburg, kimeshutumiwa na kukejeliwa na watu wengi. "Hakuna miujiza yoyote," tume inayohusika na kuendeleza na kulinda utamaduni, dini na lugha au makabila ya jamii mbali mbali (CRL Rights Commission) imeliambia shirika la habari nchini.. "Hufanywa ili kuwahadaa watu wanyonge watoe pesa." 'Kuzihadaa' kampuni 3 Kampuni tatu za mazishi zinazosema zilihaidawa na 'mpango huo' sasa zinawasilisha kesi kwa kuharibiwa sifa. Kingdom Blue, Kings & Queens Funeral Services na Black Phoenix zimeviambia vyombo vya habari nchini kwamba wawakilishi wa kanisa hilo waliwahadaa katika namna tofuati. "Wanaotuhumiwa kuwa jamaa za maiti" wameiambia kampuni ya Kings & Queens Funeral Services kwamba wamekuwa na "mzozo na kampuni nyingine ya mazishi". Inadaiwa kwamba wateja hao walibandika kibandiko cha nembo ya "Black Phoenix kwenye gari lao binafsi" kuonekana kuwa wa kuaminika kwa Kings & Queens Funeral Services walipokwenda kukodi gari la kusafirisha maiti kutoka kwao. Mjadala wa kitaifa Jeneza hilo, wakurugenzi wa kampuni hiyo ya mazishi wamesema lilipatikana kutoka kwa Kingdom Blue. Kanisa la mchungaji Lukau, Alleluia Ministries International, bado halijajibu ombi la BBC kutoa tamko kuhusu mkasa huu. Mtandao wa The Sowetan unaripoti kwamba kanisa hilo limegeuza kauli yake kuhusu kufufua maiti tangu shutuma zizuke, likieleza kwamba mwanamume "aliyefariki" "yuko hai" alipoletwa kwenye eneo hilo la Kramerville. Mchungaji Lukau "alikamilisha tu, miujiza ambaye Mungu ameanza", Alleluia International Ministries imenukuliwa na mtandao wa The Sowetan. Video hiyo imezusha mjadala wa kitaifa kuhusu wachungaji bandia na ulioshutumiwa na viongozi wa kidini wanoatambulika. Hatahivyo baadhi ya Waafrika Kusini wamelizungumzia suala hilo katika mitandao ya kijamii kwa kutumia hashtag #ResurrectionChallenge katika kudhirisha ucheshi kuhusu suala hilo. Ni mkasa wa hivi karibuni wa kiwango cha juu kuhusu viongozi wa kidini nchini humo wanaotuhumu kufanya miujiuza kwa waumini. Mwaka jana, Mchungaji Afrika kusini alipatakiana na hatia kwa kuwapuliza wafuasi wake kwa dawa ya wadudu ambayo alituhumu kwa uongo kwamba ni tiba kwa saratani na HIV. Kundi la wasimamizi wa mazishi nchini Afrika kusini wanasema watamshtaki mchungaji anayejiita mtume anayedai 'kumfufua maiti'. text: Chanjo ya Urusi imefanyiwa majaribio kwa watu 76 Lakini kwanini inatiliwa shaka? Afisi ya BBC nchini Urusi imesema kwamba nje na ndani ya taifa hilo watalaamu kadhaa na wachambuzi wameonesha hofu kwamba majaribio yake huenda hayakufikia viwango vinavyohitajika duniani - ikiwa ni juhudi za serikali kupata chanjo mbele ya mataifa mengine. Rais wa Urusi aliagiza serikali mwezi Aprili kufanya maamuzi baada ya kubainika kwamba wanasayansi kutoka taasisi ya Gamaleya walijidunga dawa hiyo wakati walipokuwa katika awamu ya kuifanyia majaribio miongoni mwa wanyama. Hatahivyo, mkurugenzi wa Taasisi hiyo Alexander Gintsburg, alielezea kwamba wafanyakazi wa taasisi hiyo walijidunga dawa ya majaribio ili kuweza kuiendeleza bila ya hatari ya maambukizi wakati wa mlipuko, akidai kwamba wanayansi hao hawakupatwa na madhara yoyote. Waziri wa Afya wa Urusi Mikhail Murashko amesema chanjo hiyo "imethibitisha kuwa na ufanisi na salama." Idhaa hiyo ya BBC nchini Urusi inasema kwamba kuna ripoti za hivi karibuni kuwa baadhi ya wanachama wa jeshi la Urusi waliingilia chanjo hiyo mwezi Aprili suala ambalo limepuuzwa na wizara ya Afya. Lakini siku ya Jumanne, rais Putin alithibitisha kwamba mmoja ya watoto wake amepatiwa chanjo hiyo na kwamba anahisi vyema. Watalaamu kadhaa wa kimataifa akiwemo Anthony fauci, pia wametilia shaka kasi hiyo ya Urusi, uwezo wa chanjo hiyo na hatua yake ya kutangaza kampeni kubwa kama hiyo bila kukamilisha majaribio yake. Mtu yeyote anaweza kusema kwamba kuna chanjo na kuitengeneza lakini ni lazima uoneshe kwamba ni salama na ina uwezo, kitu ambacho nina hakika hawajaweza kuthibitisha, fauci alisema mwisho wa mwezi Julai katika mahojiano na BlackPressUSA TV. ''Lazima tuwe makini na watu wanaodai kwamba wanamiliki chanjo'', aliongezea. Mwandishi wa masuala ya sayansi nchini Urusi, Irina Yakutenko pia alihoji ratiba iliochukuliwa, ''kwa kuwa watawadunga watu na kusubiri kuona kitakachotokea ,uchambuzi wa kawaida unaofanywa na ulinganishaji wake hautarajiwi'', alisema katika Telegramu. Kulingana na idhaa hiyo ya Urusi, suali jingine ambalo linasalia kutatuliwa ni uwezo wake iwapo taifa hili litaanzisha uzalishaji wake kwa kiwango kikubwa kabla ya tarehe ilioahidiwa, hususan wakati ambapo miundo mbinu inakabiliwa na changamoto kubwa. Urusi imeidhinisha chanjo ya kwanza ya virusi vya corona duniani. Hatahivyo chanjo hiyo imezua wasiwasi na hofu miongoni mwa washikadau wengi wa afya duniani ikiwemo wataalamu. text: Madaktari walidhani Melissa ataishia kutoona na kwa wakati mmoja walihofia atashikwa na matatizo ya moyo Aliokolewa na mhudumu wa afya aliyemsikia akilia katika taka taka za hospitali nchini Marekani. Hii ni hadithi ya uhai wake, na kuhusu mamake aliyedhani kwamba amekufa. "Nili inukia nikijua kwamba nilizaliwa kabla ya kutimiza miezi 9, na kuwa niliasiliwa," Melissa Ohden, sasa ana miaka 41 anasema. "Kitu ambacho sikujuwa ni kwamba kulikuwana siri kubwa. Kwamba nilitakiwa nife, na badala yake nilizaliwa nikiwa hai." Mnamo 1977, katika hospitali moja nchini Marekani katika jimbo la Iowa, Mamake Melissa aliyekuwa na umri wamiaka 19 aliavya mimba kwa kutumia kemikali kwa zaidi ya siku tano. Melisaa alizaliwa akiwana miezi minane akiwa na kilo 1.3 na akatupwa kwenye taka taka za hospitali. Hapo ndipo nesi mmoja alisikia sauti ya mtoto akilia na kwa kuchungulia akaona mwili ukisogea. Melissa alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo aliponea na kuishi. Melissa na dadake Madaktari walidhani atakuwa hawezi kuona na kwa wakati mmoja walidhani ataugua matatizo ya moyo yasiotibika. Lakini amefanikiwa kusihi maisha yenye afya tele na amelelewana familia iliomuasili. Melissa - ambaye ameandika vitabu kuhadithia maisha yake- anasema aligundua kwamba aliasiliwa wakati alipogombana na dadake kutoka familia iliomuasili. Kwa mara ya kwanza Melissa alichanganyikiwa, lakini wakati fahamu ilipomuingia na alipokaa kuzungumzana wazazi waliomlea hapo ndipo athari ikamjia kwa kuugua matatizo ya kiakili. Uchungu uliendelea kuongezeka, mpaka miaka mitano baadaye - akiwa na miaka 19 - alichukuwa uamuzi wa kijasiri kumsaka mamake aliyetaka kumtoa uhai. Ni shughuli iliyomchukua muda wa karibu muongo mmoja, lakini hatimaye alimpata - na akagundua ukweli ulimshutusha. Melissa akiwa na miaka 14 ndiyo alitambua kwa mara ya kwanza kuwa mamake alijaribu kumuavya "Siri kubwa kweli ni kuwa mamangu alikaa miaka 30 akiamini kwamba nilifariki hospitalini. "Hakuambiwa kwamba nilipona, ilikuwa siri aliofichwa," anasema. Na ndio kwa sababu hiyo walipokutana ana kwa ana miaka mitatau baada ya kutumiana barua pepe , Melissa aliguswa na kwamba mamake alijutia kitendo hicho, kilichomsumbua roho kwa miaka mingi. Lakini mshtuko haukumalizika hapo. Mamake mzazi, Ruth, alimuambia kwamba hakutaka kuitoa mimba , na kwamba aliwekwa katika hali ambayo ni kama alilazimishwa kuitoa mimba hiyo. "Nilichokuja kujua ni kwamba bibi yangu - mamake mamangu - alikuwa mhudumu maarufu wa afya katika jamii, na mtu anayefanya kazi ya kutoa mimba alikuwana rafiki yake. "Kwa pamoja walimlazimisha mamangu kinyume na ridhaa yake kuitoa mimba. Melissa Ohden amekutana na mamake kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 30 Melissa anasema yeye ni "mojawapo ya watu wenye bahati duniani", kwanza kwamba aliweza kupona mkasa huo, na pia kubarikiwa na kuwa na wazazi waliomuasili na mamake mzazi katika maisha yake. Kwa bahati tu, Melissa na mamake mzazi sasa wanaishi mjini Kansas pamoja na mojawapo wa dada zake wa kambo. Akiwa na miaka 14, Melissa Ohden was 14 aliijuwa siri kubwa - mamake alijaribu kumuua akiwa angali tumboni. text: Kulingana na tahadhari hiyo iliochapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa balozi hiyo, kuna uvumi wa mipango ya mashambulizi katika maeneo yanayopendwa sana na raia wa kigeni katika Afrika Mashariki ikiwemo Uganda. Ubalozi huo umesema kuwa ijapokuwa hauna ushahidi wa kutosha kuhusu tishio hilo ama habari kuhusu wakati ambapo mashambulizi hayo yatafanyika umewaonya wakaazi kuchukua tahadhari. "Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari." Umewataka raia kuwa macho wakati wowote katika maeneo wanayozuru, kutahadhari dhidi ya makundi ya watu wengi mbali kufuatilia habari zinazochipuka mara kwa mara . Aidha umewataka raia kuwa macho katika maeneo yanayopendelewa sana na watalii hususan wale wa mataifa ya magharibi. Tahadhari hiyo inajiri siku moja tu baada ya ubalozi huo kutoa tahadhari nchini Tanzania ambayo imewatakaa wakaazi kuchukua tahadhari hususan wale waliopo katika eneo la Masaki. Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo Tahadhari hiyo ilibainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway. Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokuwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo. Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa tahadhari nyingine ya shambulio la kigaidi nchini humo text: Akizungumza katika mkutano maalum alioutishaleo na wafanyabiashara zaidi ya 1,000 kutoka kila kona ya Tanzania Magufuli amesema japo kuna jitihada kubwa zinazofanyika kupambana na rushwa, bado kuna maafisa wa serikali si waaminifu. Magufuli ameyataja maeneo yanayoongoza kwa rushwa ni bandarini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), barabarani pamoja na mipakani. "Jitihada kupambana na rushwa zinaendelea...kuna mfanyabiashara alishawahi kusema kuwa ukitaka kuona rushwa bado ipo, toa kontena bandarini hadi Kariakoo. Sijui kama tumeshafanyia kazi kauli ile..." amesema Magufuli. Magufuli toka alipoingia madarakani amekuwa akijipambanua kwa kuchukia rushwa na kuahidi kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo hilo. Vigogo kadhaa wa serikali wamefutwa kazi na baadhi yao pamoja na wafanyabiashara wakubwa wamefunguliwa mashtaka mbali mbali ya ufisadi. Hii leo, amewaasa wafanyabiashara kwenye mkutano huo wasisite kuwaripoti maafisa wanaowaomba rushwa kwa mamlaka ili wachukuliwe hatua. Magufuli pia amekiri kuwa bado serikali haijaweka mipango endelevu ya kuwaendeleza wafanyabiashara na sekta binafsi kwa ujumla wake ili wachangie zaidi kwenye kuujena uchumi wa nchi yao. "Hapa kwetu tuna zaidi ya wajasiriamali milioni lakini tumeshindwa kuwa na mipango ya kuwatambua, kuwalinda na kuwaongozea tija," amesema na kuongeza: " Mpaka sasa ni watu milioni 2.7 pekee ambao ndio wanaolipa kodi. Wigo kati ya wanaolipa na wasiolipa kodi ni kubwa sana, njia moja ya uhakika ya kutatua hili ni mipango thabiti ya kurasimisha wajasiriamal ili waendeshe uchumi." Magufuli pia ametaja utitiri wa kodi na taasisi za udhibiti kama ni chamgamoto nyengine ya kimfumo inayoathiri ukuaji wa biashara nchini Tanzania. Lakini amesema jitihada za kutatua changamoto hiyo zinafanyiwa kazi na wameanza kwa kufuta tozo a ada zaidi ya 100 kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa upande wa wafanyabiashara, Magufuli amesema wapo ambao si waaminifu wanakwepa kodi kwa kutoa rushwa na wengine kufanya udalali na kujihusisha na makundi ya uhalifu wa kibiashara. Magenge hayo ya kihalifu wa kibiashara amesema yapo katika biashara ya sukari, mafuta ya kula na korosho. "Baadhi yao wamekuwa wakitumia mbinu ya kukwepa kodi kwa kudai marejesho ya fedha ya ongezeko la thamani (VAT) wakati mauzo yaliyofanyika ni hewa ya biashara za nje na kwenye hili nataka niseme wazi nina orodha ya kampuni 17,446 ambazo zimehusika na tuhuma hizo. "Nitawapa copy (nakala) ya kampuni hizo hewa ili mkafanye uchambuzi wenu na kama yalikwepa kitu chochote yakajipange kulipa ndani ya siku 30," amesema Rais Magufuli. Suala la marejesho ya pesa ya makusanyo ya VAT limekuwa kubwa na kugusiwa katika ripoti ya hivi karibuni ya Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ambao wanasema marejesho ambayo hayajafanywa na serikali ni kiasi cha Tsh 2.3 trilioni (takriban dola bilioni 1) kwa kipindi cha miaka 2-3 iliyopita. Rais Magufuli hata hivyo amesema moja ya sababu ya suala hilo kuwa kubwa ni udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara. "...kumekuwa na uongezaji wa marejesho ya fedha ya VAT kwa wafanyabiashara ili waweze kupewa fedha nyingi kutoka serikalini huu ni wizi." Tatizo jengine la wafanyabiashara lilogusiwa na Magufuli ni kubadli matumizi ama kutoendeleza kabisa viwanda ama ardhi walizobinafsishiwa na serikali bila kufuata utaratibu. "Wengine wametumia maeneo hayo kukopa fedha benki kwa ajili ya kazi hiyo na hawajafanya, hiyo ni dhambi na wengine najua mko hapa." "Baadhi ya wafanyabiashara wamejanga viwanda kama gelesha na kuvitumia kupokea bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi stahiki kama vile bidhaa hizo zimetengenezwa nchini." amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema rushwa zinazotozwa na maafisa wa serikali na udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara ni baadhi ya vikwazo vikubwa vinavyoandama ukuaji wa biashara na uchumi nchini Tanzania. text: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kamumusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuizindua kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu. Kushoto ni Balozi wa Kiswahili Afrika, Mama Salma Kikwete. Wapili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Ametoa kauli hiyo alipozungumza na wabunge, viongozi wa Serikali na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. "Serikali inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa nchi yetu na katika kulinda umoja wa kitaifa. Hakika lugha ya Kiswahili ndiyo inayotufanya tuwe Watanzania. Hivyo, tunaithamini na kwetu hii ni lulu na tunu ya Taifa," amesema. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu nakala ya Kamusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuzindua kamusi hiyo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Waziri Mkuu katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake amesema uzinduzi wa kamusi hiyo unaenda sambamba na azma ya Serikali ya kutumia Kiswahili kwenye shughuli zote za kitaifa kama vile mikutano, mijadala, semina na ufundishaji shuleni. Majaliwa amempongeza Rais John Magufuli kwa kuhimiza matumizi ya Kiswahili kwenye mikutano na matukio muhimu ya kitaifa, kama vile dhifa za kitaifa anazowaandalia wageni wake kutoka nje. "Hata alipokuwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, Rais alitumia Kiswahili kuhutubia mkutano huo. Amekuwa akifanya hivyo, hata kwenye mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lengo lake ni kuitangaza lugha hii ya Kiswahili," amesema. Waziri Mkuu , amewasihi wazazi wahakikishe watoto wao wanapata kamusi hiyo kama moja ya nyenzo zao za kujifunza lugha ya Kiswahili."Ninashauri makundi mengine kama vile waheshimiwa wabunge, wanahabari, wakalimani, wafasiri, waandishi na wahariri wa vitabu, maofisa mawasiliano wa kwenye ofisi zetu, muone umuhimu wa kununua kamusi hii ili iwasaidie kujiimarisha kwenye matumizi ya Kiswahili fasaha na sanifu," amesema. Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema Kiswahili ni lugha ya pili inayotumiwa na watu wengi zaidi barani Afrika lakini pia ni lugha ya 10 kati ya 6,000 zinazozungumzwa na watu wengi duniani. Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Dk Seleman Sewangi amesema kazi ya kuandaa kamusi hiyo ilianza Agosti 12, 2011 na kukamilika mwaka 2015 na toleo la kwanza lilichapishwa. Amesema kamusi hiyo imekusanya maneno mengi makuu (vidahizo) kuliko kamusi zilizotangulia na kwamba ya sasa ina maneno 45,500. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali yake inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa taifa na katika kulinda umoja wa kitaifa. text: Ulaji wa vyakula visivyousaidia mwili kiafya mara nyingi huwafamnya watoto wanaoishi maeneo hasa ya mijini kunenepa mwili kupita kiasi na wengine hata kupata maradhi kama vile moyo na kisukari. Mfano Uingereza kuna idadi kubwa ya watoto wenye matatizo ya afya yanayotokana na uzito wa kupita kiasi - lakini mji mmoja nchini humo unaonekana kufanikiwa kuwasaidia watoto kula vyakula vyenye afya. Takwimu zilizotolewa kwenye mkutano kuhusu unene wa mwili wa kupindukia zimeonyesha kuwa wa Leeds imeweza kupunguza viwango vya watoto wanene kupindukia kwa 64% katika miaka ya hivi karibuni. Sehemu muhimu ya mkakati wa mji huo wa kukabiliana na unene wa mwili kupita kiasi ulilenga zaidi shule za chekechea na kuwapatia mafunzo wazazi juu ya nanma ya kuwasaidia watoto wao kuwa wenye afya. Lakini si kila wakati wazazi na walezi wanaelewa somo la chakula . Je ni mambo gani unayoweza kufanya kumshawishi mwanao kula chakula cha afya? Kuwalisha vyakula vya aina tofauti Tina Le anasema watoto wanapaswa kupewa fursa ya kuchagua chakula wanachokipenda miongoni mwa vyakula vyenye afya Tina Le hutoa warsha kama zile ambazo zimekuwa zikifanyika katika mji wa Leeds kwa wazazi mashariki mwa London. Anasema kumpatia mtoto fursa ya kuchagua vyakula wanavyokula wakiwa na umri mdogo , kwa kuwapatia nafasi ya kuchagua vyakula vya afya vya aina mbili, inaweza kusaidia kutoa mwongozo utakaowasaidia kula vema. Baadhi ya dawa "Hii inaweza kuwasaidia kupunguza hatari ya wao kukataa kula kitu chochote kabisa na hujihisi wao ndio wenye kauli ya mwisho ," anasema. "Wakati tunapowanyima watot wetu fursa ya kuchagua chakula wanachokipenda, huwa wanahisi nhawana la kufanya na huwafanya kuwa wenye hasira." Hatua ndogo ndogo Anna Groom, Daktari wa masuala ya lishe ya watoto, anakiri kuwa si rahisi kila mara hasa kama mtoto ni mwenye kupenda kuchagua chakula. Amesema kuanza na mabadiliko ya taratibu ya chakula unachompatia inaweza kupumpunguzia shinikizo ambalo baadhi ya watoto huwa nalo saa za mlo zinapokaribia na kuepusha malumbano wakati wa chakula. " Ni muhimu wawe na chakula ambacho unafahamu kuwa wanakipenda, lakini pia unaweza kuanzisha kitu kipya kwenye sahani yao kwa kiasi kidogo ," anasema. Mwanzoni Belinda alihangaika sana kumshawishi binti yake kula vyakula vya afya Belinda Mould alibaini mbinu ambayo ilikuwa nzuri ya kumshawishi binti yake mwenye umri w amiaka mitatu, ambaye awali akikuwa anakula Soseji tu na maharage ya kuokwa. "Ilikuwa tukimlisha vyakula vingine anavitupa sakafuni au anavip[uuza na matokeo yake hali chochote " aliiambia BBC Lakini anasema kwa kumshawishi kula kiwango kidogo cha chakula kipya mara kwa mara, sasa mwanae anakula karibu kila kitu. "Ninasema , 'Unaweza kumwambia, kula mara moja tu ujaribu na kama hautakipenda , unaweza kula chakula kingine '," anasema Belinda "Unahitaji kuwa mwenye subira ," na kuongeza kuwa . "Kwa hiyo ikiwa watakataa, jaribu tena mara nyingine ." Uwe kielelezo kizuri cha kuigwa Tina anasema kuwa mfano mzuri kwa mtoto tangu aliwa na umri mdogo ni jambo muhimu. " kama unakula chakula cha afya wewe mwenyewe, mtoto wako ana uwezekano mkubwa wa kujifunza kutoka kwako kwa kuiga kile unachokifanya," anasema. Anaongeza kuwa kula pamoja wakati wa chakula au kuwasaidia watoto wadogo kuwaiga tabia ya 'ulaji wa wazazi ' ni muhimu Anna anasema kuwa ni muhimu kwa wazazi kutokizungumzia vibaya au kutoa maoni hasi juu ya chakula ambacho hawakipendi mbele ya watoto wao, kwani wanaweza kushawishi mtizamo wao juu ya vyakula vipya Rewards Tina Le anashauri wazazi watoe zawadi ya kuwapeleka watoto kucheza kuliko kuwazawadia vyakula Kutoa zawadi na kuwasifu watoto kwa kula vyakula vya afya inaweza kuimarisha tabia nzuri ya mtoto , Tina anasema. Hata hivyo, anasisitiza kuwa zawadi haipaswi kuhusiana na chakula, na badala yake mtoto apewe zawadi ya kutembelelea sehemu za michezo , kuchora au kupanga vichezeo vya michoro ya vitu mbali mbali kwa mpangilio unaotakiwa. "Kila mara tunasema epuka kutoa rushwa mwanao ," anasema. "Usiseme kama ukila chakula hiki nitakupa chokoleti au ice cream kwasababu hilo huwafanya kufikiria kuwa chakula cha afya tunachotaka wale kina thamani ndogo kuliko zawadi unayowapatia ." Muonekano wa mwili Hasa kwa watoto wakubwa, chakula na uzito wa mwili huwa ni mada ambayo ina utata kidogo kuizungumzia na hofu juu ya muonekano wa umbo lao la mwili huchangia katika suala la kujiamini. Utafiti wa hivi karibuni ulibaini kuwa unene wa mwili wa kupindukia na afya ya akili vina uhusiano wa karibu sana, huku watoto wanene kupita kiasi wakiwa na uwezekano mkubwa wa kuathirika kisaikolojia mfano kuw na wasiwasi na kujihisi hawana raha wala matumaini. Tinaanapendekeza wazazi wabadili namna wanavyozungumzia chakula kwa kuepuka kuhusisha ulaji wa chakula cha afya na muonekano wa umbo la mwili wa mtoto. "Watie moyo kuwa wenye afyakwasababu inawafanya wajihisi vizuri , badala ya kuwaeleza kuwa chakula wanachokula kitawafanya wawe na muonekano fulani ," anasema. Anna anaafiki kuwa lugha ni muhimu unapozungumzia suala la uzito wa mwili. "Ni muhimu familiazishauriwe kufanya mabadiliko kw aujumla ili mtoto asijihisi kuwa analengwa kw akupewa chakula fulani ," anasema.' Kusema vkauli mfano 'tujitahidi tuwe familia yenye afya' , inamaanisha kuwa mtoto huenda asiwe na wazo kuwa wazazi wana hofia unene wao wa mwili , lakini hilo linaweza kuboresha lishe yao ." Mara kwa mara wazazi na walezi wengi wamekuwa wakihangaika kuwashawishi watoto wadogo kula vyakula vinavyousadia mwili kuwa na afya nzuri kama vile mboga ambavyo wengi wao huwa hawazitaki. text: Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha Chadema amekuwa akipokea matibabu Leuven nchini Ubelgiji tangu kuhamishwa kwake kutoka jijini Nairobi Kenya mwezi Januari. Amekuwa akiishi hospitalini akipokea matibabu. Taarifa ambayo inadaiwa kutoka kwake imesema: "Hello Friends of Me!!! Good afternoon to y'all. Kwa mara nyingine nawaleteeni habari njema. Leo Agosti 7 ni miezi 11 toka siku niliposhambuliwa na watu wanaojulikana sana kama 'watu wasiojulikana." "Septemba 7 mwaka jana sikulala nyumbani kwangu. Agosti 7 ya leo, miezi 11 kamili baadae, nimeamkia nyumbani kwangu ... wote mlikuwa na hofu kubwa kama ningemaliza siku hiyo au siku chache zilizofuata, nikiwa hai. Miezi 11 kamili baadae, professor Dk Wilhelmus Jan mertsemakers daktari wangu tangu nilipokuja University Hospital Leuven, amesema sina sababu ya kitabibu ya kuendelea kukaa hospitali," gazeti la Mwananchi limenukuu taarifa hiyo. Bw Lissu amesema ametakiwa kumuona daktari kila baada ya wiki mbili ingawa atakuwa akiangaliwa na wauguzi nyumbani kwake kila siku kwa muda usiojulikana. Amesema kwamba bado ana chuma kikubwa kwenye paja. "Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuniuguza na kuniponya na chochote mtakachokula au kunywa siku ya leo mnibakishie. Siko mbali," amesema. Bw Lissu aliyekuwa pia rais wa Chama cha Wanasheria (TLS) alipigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mnamo tarehe 7 mwezi Septemba baada ya kuhudhuria vikao vya bunge Dodoma. Alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi. Tundu Lissu: Kushambuliwa kwangu kulichochewa na siasa Tanzania Alipokuwa akizungumza na wanahabari Nairobi kwa mara ya kwanza tangu kuondoka hospitalini Januari mwaka huu, Bw Lissu alisema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma walikuwa na uhusiano na serikali. Mbunge huyo wa Singida Mashariki alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana. "Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawakilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," alisema Lissu. Fatuma Karume: Tutaendelea kuikosoa serikali na kutetea haki Tanzania Serikali imekanusha tuhuma hizo. Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mwezi Novemba mwaka jana alipokuwa ziarani Nairobi. Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa anapokea matibabu Ulaya na sasa ataendelea kupata nafuu akiwa nyumbani. text: Balozi huyo, aliitwa ''mtu mpumbavu'' na rais Trump, baada ya barua pepe hizo kusema utawala wa Trump si stadi''. Ofisi ya mambo ya nje imesifu hatua ya Balozi Kim ''kwa weledi wake''. Balozi huyo amesema anataka kumaliza mzozo uliokuwepo, na kuongeza kuwa kuvuja kwa barua pepe kumefanya utenda kazi wake kuwa ''mgumu''. Katika barua yake kwa wizara ya mambo ya nje Kim alisema: '' tangu kuvuja kwa nyaraka za kiofisi kutoka ubalozi huu kumekuwa na hisia kuhusu nafasi yangu na muda wangu uliobaki kama balozi. Marekani na Uingereza zarushiana cheche za maneno - kunani? Uchunguzi wa Barua pepe zilizovuja dhidi ya utawala wa Trump waanza ''Ninataka nizimalize hisia hizo.'' Akijibu barua hiyo Simon McDonald, mkuu wa masuala ya diplomasia, amesema balozi Kim ametumikia majukumu yake vyema, kwa ustadi na heshima''. Akieleza kuwa kuvuja kwa barua pepe ni tukio la ''hila'' aliongeza Simon: ''Wewe ni bora kwetu.'' Theresa May alisema ilikuwa ''suala la kujutia sana'' kuwa bwana Darroch amejisikia kuwa anahitaji kuachia ngazi, akisema maafisa wanapaswa kuwa na uwezo wa kutoa ''ushauri wa kweli''. ''Kim alijitolea kufanya kazi kutumikia Uingereza na tuna deni la shukrani kwake,'' aliongeza Waziri Mkuu amesema Baraza lote la mawaziri lilikuwa likimuunga mkono wakati wote wa mzozo. Kiongozi wa chama cha Labour, Corbyn aliliambia bunge : ''Kauli zilizotolewa kuhusu yeye si za haki na si sawa. Ninafikiri amefanya utumishi mwema na anapaswa kushukuriwa.'' Balozi Kim alikuwa anatarajiwa kuondoka kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa mwaka. Je Sir Kim Darroch ni nani? Sir Kim anawakilisha malkia wa Uingereza na serikali ya Uingereza nchini marekani. Akiwa mzaliwa wa Kusini mwa Stanley , County Durham mwaka 1954 alisomea chuo kikuu cha Durham University ambapo alisomea elimu ya wanyama. Wakati wa kipindi chake cha miaka 42 kama mwanadiplomasia amekuwa mtaalam wa usalama wa kitaifa na serza muungano wa Ulaya. Mwaka 2007 , bwana Sir Kim alihudumu Brussels kama katibu a kudumu wa Uingereza katika muungano wa Ulaya. Alikuwa balozi wa Uingereza nchini marekani miezi kadhaa kabla ya rais donald trump kuwa rais. Balozi Kim Darroch anayewakilisha Uingereza nchini Marekani, amejiuzulu yakiwa ni matokeo ya kuvuja kwa barua pepe zinazoukosoa utawala wa rais wa Marekani, Donald Trump. text: Rihanna Mwanamuziki huyo ajulikanaye kama The Barbadian singer ametishia kuchukua hatua za kisheria baada ya wimbo wake wa mwaka 2008, unaokwenda kwa jina la Don't Stop the Music, kupigwa katika mkutano wa kisiasa wa raisi Trump huko katika maeneo ya Chattanooga. Rihanna - ajulikanaye pia kama Fenty - timu yake imekwisha tuma barua rasmi katika Ikulu ya Marekani , White House, barua ambayo gazeti maarufu nchini humo Rolling Stone imeishuhudia. Raisi Donald Trump akiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za katikati ya muhula Na inasomeka hivi : "hili limetufikia raisi Trump amekuwa akitumia tungo za muziki za [Rihanna] na rekodi kuu,ikiwemo wimbo wake unaofanya vizuri wa Don't Stop the Music kuhusiana na matukio kadhaa ya kisiasa uliofanyika nchini Marekani. "Kama wewe ni lazima au ujue, Bibi Fenty hakutoa idhini yake kwa Mheshimiwa Trump kutumia kazi zake ama muziki wake kutumiwa katika shughuli hizo. Kuendelea kwa matumizi hayo ni tabia isiyofaa. Miongoni mwa wanamuziki waliothubutu kuzuia kazi zao kutumika katika mikutano ya kampeni za kisiasa , Rihanna anaungana na mamilioni ya wanamuziki hao nchini humo akiwemo Aretha Franklin alizuia wimbo wake wa Amazing Grace wimbo wenye mahadhi ya kidini na baadye ulitumika katika filamu moja baada ya miaka 46 . Mwanamuziki Ri Ri ama mwite Rihanna amekuwa ni msanii wa hivi karibuni kuwa na uthubutu wa wa kutamka hadharani na kumtaka rais wa Marekani Donald Trump kuacha mara moja kutumia tungo zake katika mikutano yake ya kisiasa. text: Katika taarifa yake ya malalamiko, shiriki hilo limeeleza kwamba uwazi na kasi katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo hatari ni muhimu katika kudhibiti mlipuko ambao tayari umetajwa kuwa janga la afya duniani. Katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi, WHO limeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa. Kufikia sasa jitihada zetu za kuifikia serikali ya Tanzania kutoa tamko kuhusu taarifa hii ya WHO hazijafuwa dafu. WHO lilituma kundi la wataalamu kuchunguza kisa cha ugonjwa usiojulikana na ubalozi wa Marekani ulifuatilia hatua hiyo kwa kutoa tahadhari. Hatua hiyo ilisababisha uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba ugonjwa huo hatari umeingia nchini Tanzania. Waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita amesena hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo. Serikali ya Tanzania imesema nini? Serikali ya Tanzania ilifutilia mbali uvumi kwamba kuna visa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo. Waziri wa afya nchini humo bi Ummy Mwalimu aliambia mkutano na wanahabari kwamba hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo. Alisema kwamba taifa hilo limejiandaa kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa na tayari limefanya majarabio ili kujua jinsi ilivyojiandaa huku ikiweka tayari vituo vya kuwatenga waathiriwa. Shirika hilo la Umoja wa mataifa limeendelea kueleza katika taarifa yake kwamba lilifahamishwa mnamo Septemba 10 kuhusu kifo cha mgonjwa kilichotokea mjinia dar es salaam, na kuarifiwa kwa njia isiyo rasmi siku ya pili kwamba mgonjwa huyo alipatikana kuwa na Ebola baada ya kufanyiwa vipimo. Kadhalika WHO linaeleza kwamba liliarifiwa kuhusu visa vingine viwili vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo. Mmoja kati yao, alikutikana kutokuwa na Ebola baada ya vipimo na hapakuwa na taarifa zozote kuhusu mgonjwa wa pili, imeeleza taarifa hiyo. ''Nataka kuwahakikishia kwamba idara ya afya ilichukua sampuli na matokeo yake ni kwamba wawili hao hawakuwa na ugonjwa wa Ebola. Hakuna Ebola Tanzania na watu hawafai kuwa na wasiwasi'', alisema waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita kuhusu uvumi wa visa hivyo. Kufanya vipimo tena vya homa ya Ebola katika maabara inashauriwa sana ili kuthibitisha matokeo ya vipimo na hivyo kubaini aina ya virusi Ebola . WHO linasema kuwa limewapatia maafisa wa Tanzania ushauri huu. Mgonjwa huyo ambaye inaarifiwa ni mwanamke alifariki tarehe 8 Septemba kwa mujibu wa WHO. Msururu wa matukio ya mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na Ebola Tarehe 10 Septemba 2019, Shrika la Afya duniani WHO lilipokea ripoti ya taarifa ya kisa cha mambukizi ya Ebola mjini Dar es Salaam, Tanzania. Kisa hicho kinachoshukiwa kilimhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa akisomea nchini Uganda. Aliwasili nchini Uganda akitokea nchini Tanzania tarehe 08 Agosti 2019. Taarifa hiyo inasema kwa kuanzia tarehe 08 hadi 22 Agosti, alikuwa katika eneo la kati la Uganda, akiishi katika hosteli ya kibinafsi karibu na mji mkuu Kampala. Ebola ni nini? Ebola ni kirusi ambacho mwanzo husababisha joto la mwili na kudhoofisha misuli na uvimbe kooni. Kisha mgojwa huanza kutapika, kuharisha na kuvuja damu ndani na hata nje ya mwili. Watu huambukizwa wanapogusana moja kwa moja kupitia michubuko ya mwili, au mdomo na pua, huku damu, matapishi, kinyesi au kugusa majimaji ya mwili ya mgonjwawa Ebola Wagonjwa huwa wanakufa kutokana na ukosefu wa maji mwilini na kuharibika kwa viungo vya ndani vya mwili. Tazama pia: Je inawezekana kuangamiza virusi vya Ebola? Shirika la afya duniani limelalamikia ukosefu wa ushirikiano kutoka serikali ya Tanzania katika utoaji taarifa kuhusu visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola nchini. text: Papa Makiti (kati) akiwa na viongozi wenzake wa kanisa hilo Walikuwa wakilia na kuimba "Mama, Mama". Walijitetea kwamba nao pia walikuwa na haki ya kumuomboleza mtu waliyemuenzi sana. Kiongozi wao alikuwa amevalia mavazi ya kidini. Hakuwa mwingine ila Papa Makiti kiongozi wa kanisa jipya nchini Afrika Kusini ambalo limekuwa likiwashangaza wengi. Kanisa hilo linalofahamika kwa jina Gobola (yaani nipe Ulevi ninywe kidogo kwa Lugha ya Kitswana, moja ya lugha rasmi nchini humo) lina mwaka mmoja hivi tangu lianzishwe. Mwasisi wa kanisa hilo ni Tsietsi D Makiti, 53, ambaye kwa sasa anajiita Papa Makiti. Hujieleza kama papa wa kwanza mweusi kutoka bara la Afrika. Alilianzisha kanisa hilo katika baa moja, na kanisa hilo hufanya ibada zake katika baa na vilabu. Aliambia mwandishi wetu wa Afrika Kusini Omar Mutasa kwamba kanisa la Gobola na ulevi, vyote ni vya Mungu na ni wajibu wake kuwapa nasaha bora walevi wote waliofukuzwa kwenye makanisa mengine. Kanisa hilo lina wafuasi wanawake pia Kanisa kuu la Gobola limo ndani ya baa inaitwa Freddie's Tarvern na mwenye baa hiyo Askofu Freddie Mathebula ndiye naibu wa Papa Makiti, husaidia kuongoza mahubiri na ibada wakati mwingine. Tangu kuanzishwa kwake, kanisa hilo limekuwa likipata umaarufu na inakadiriwa kwamba kwa sasa lina waumini kati ya 500 na 2,000, ingawa idadi yenyewe ni vigumu kuithibitisha. 'Huu ni ukumbi kwa watu kuja pamoja kwa jina la Mungu bila kuaibishwa kwa kuwa walevi," anasema. 'Pombe si mbaya, watu ndio wabaya' Mwezi Machi mwaka huu, wakati akitawazwa kuwa papa, aliandika katika Facebook: "Ni kwa nini watu wanalichukia kanisa la Gabola, kana kwamba ndilo lililoleta pombe duniani, na kuanzia wakati huo kwamba pombe ikawepo? "Ninataka kukariri kwamba hakuna chochote kibaya kuhusu pombe au unywaji pombe, iwapo mtu ana tatizo akiwa mlevi, ni mtu huyo mwenye tatizo si pombe, msiilaumu pombe. "Mnasema kwamba pombe husababisha vita, ajali, watu kupigana nyumbani na uzinzi, si kweli hata kidogo. Mambo haya yote huwatokea hata watu wasiokunywa pombe…wapita njia hugongwa na magari, baadhi (ya madereva) huwa si walevi, watu kupigana na mizozo mingine hivi vyote vipo hata katika makanisa yasiyotumia pombe kama kanisa la Gabola." Kanisa la Gobola lina watu wa tabaka mbali mbali wanaume kwa wanawake na ndani yake kuna vyeo sawa na ilivyo kwenye makanisa na madhehebu mengine. Mfano wamo mapasta, makasisi na maaskofu lakini hakuna kadinali. Kila siku ya Jumapili ndipo wasaidizi wa Papa Makiti wanapovalia rasmi mavazi yao ya upadri. Tulipomwuliza Papa Makiti idadi ya baraza la wasaidizi wake hao alisema wapo wengi tu na kila jumapili yeye huwatawaza wanachama wa kanisa la Gobola kuwa makasisi na mapadri na kuwavalisha majoho meusi. Lakini mwenyewe anasema siyo hoja kujuwa wapi walikosomea mafunzo ya dini ya Kikristo kuweza kupewa vyeo hivyo jambo ambalo Baraza kuu la makanisa Afrika Kusini huwa linalisisitiza kwamba ni muhimu katika kanisa lolote lile. Baraza hilo lenye makao yake mjini Johannesburg halikubaliani kabisa na mafundisho ya kanisa la Gobola na limesema kwamba ni njia moja ya kuwapotosha wafasi wa dini ya Kikristo. Papa TD Makiti naye amekua akiwalaumu viongozi wa baraza la makanisa kusini mwa Afrika kuwa hawana mamlaka ya kumshutumu wala kumhukumu kwa anayoyafanya. Amesema mwenye uwezo wa kumhukumu ni Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba ni dhambi kubwa kwa hao wanaomtuhumu na adhabu yao watakwenda motoni. Sherehe ya ubatizo Wakati Papa Makiti akisema hayo, wakati tukimhoji, wafuasi wake wanamshangilia kwa vifijo na nderemu na kusema 'Haleluya kanisa la walevi lidumu'. Kwa mujibu wa katiba ya Afrika Kusini, kila mtu ana haki ya kuabudu anavyotaka na ndipo kila kukicha nchini Afrika Kusini kunaibuka makanisa mapya kama uyoga ili mradi mtu mhusika asiingilie dini za watu wengine. Sherehe inayo wafurahisha wengi katika kanisa la Gobola ni Papa TD Makiti anapoanza kuwabatiza wanachama wapya wa Kanisa la Gobola. Huwa anawapaka kileo usoni mwao huku akiwausia siku zote walitetee kanisa la Gobola. Mapadri na wahubiri wa kanisa hilo pia hutawazwa kwa kutumia kileo, kila mmoja kwa kileo akipendacho. Miongoni mwa wanachama wapya wa Kanisa la Gobola (ambalo wakati mwingine huandikwa Khabula) ni Bi Lydia mke wa Papa Makiti. Yeye alikataa kunywa ulevi isipokuwa soda ya Coca Cola. Wanachama wa Kanisa la Gobola wote ni wachangamfu, wacheshi na wenye maneno mengi mazuri na mabaya na siyo rahisi kiongozi wao Papa Makiti kuwanyamazisha wanapoanza kupiga gumzo na kupiga kelele ndani ya baa hiyo iliogeuzwa kuwa Kanisa kuweza kuwaleta pamoja walevi wote kuwa na msimamo mmoja. Wakati mwengine imekuwa ikimlazimu Pope Makiti hata kuwapiga makofi kama watoto wadogo na kuwambia wanyamaze huku akiamrisha hata wengine watolewe nje ya Kanisa la Gobola kutokana na utovu wa adabu. Kuwatia adabu waumini Mmoja ya wanachama wa Kanisa la Gobola alikuwa akipiga makelele na kusema ovyo ovyo baada ya kunywa kileo kwa wingi, ndipo Pope Makiti akamzaba makofi na kuamrisha atolewe nje ya Kanisa. Mwandishi wetu Omar Mutasa alimfuata nje kusemezana naye. Mwumini huyo alisema inashangaza kumuona papa mzima, mtu wa Mungu anapiga watu makofi bila sababu. "Tangu lini papa wapige watu makofi kanisani? Papa Makiti amenivunjia heshima na uhuru wangu wa kuabudu na njia peke ni kumshitaki polisi Papa Makiti kwa kosa la kumpiga makofi mtu mzima," alilalamika. Wanaojidai kuwa manabii wanahubiri dini? Hatukufuatilia kubaini iwapo alifika kwa polisi, lakini ikizingatiwa kwamba alisema hayo akiwa amelewa, msomaji unaweza kujiamulia mwenyewe yaliyotokea baadaye. Papa Makiti anasema Kanisa la Gobola halitaki kutegemea sana misaada kutoka kwa wahisani na ndio mana wanawahimiza wanachama wao kununua pombe kwa wingi, kutoka duka lao lililopo ndani ya kanisa na hivyo kulifanya kanisa la Gobola kulipa kodi ya serikali. Nabii Tito na wenzake: Wanaojidai kuwa manabii wanahubiri dini? Katika kanisa hilo, watu huwa hawatoi sadaka, mapato hutoka kwa mauzo ya bia na vileo vingine. Kwa upande mwengine Kanisa la Gobola halina tofauti na makanisa mapya yanayoanzishwa Afrika Kusini kila kukicha kama kitega uchumi, viongozi wao kutajirika sana na wengine kumiliki hata ndege za kibinafsi. Wana pia nyimbo zao walizotunga wenyewe, miongoni mwake Gabola Mpepe unaosema 'Ninapoonja kidogo, huwa na lewa lewa, hii haina maana kwamba huwa sifuati njia iliyonyooka'. Papa TD Makiti anasema yeye bado ni mwanajeshi wa jeshi la Afrika Kusini (SANDF) akiwa na cheo cha Kapteni na alikuwa Jamhuri ya DRC akihudumu katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa. Anasema akiwa huko ndipo alipowasaidia wanawake wa DRC kwa kuwajengea Kanisa waweze kuhishimu na kuzingatia dini ya Kikristo ili kuacha biashara ya kuuza miili yao (ngono). Juhudi zetu za kutaka kuthibitisha iwapo Papa Makiti bado ni mwanajeshi, amefukuzwa jeshi au alistaafu hazikufua dafu. 'Walevi wote ni wanachama' Kwa sasa Kanisa la Gobola lipo na linatarajiwa kuendelea kuwepo na wengi wa wanywaji pombe, bia na vileo vikali ukizungumza nao kuhusu kanisa hilo wanakwambia ni mpango mzuri walevi nao wajihisi wana kundi la kuwatetea. Kanisa la Gobola linasema kila mlevi nchini Afrika Kusini ni mwanachama wa kanisa hilo na wala haina haja ya kujua kuna idadi ya walevi wangapi walio nchini humo. Wote wanakaribishwa kwa mikono miwili ya Papa Makiti mkono wa kulia ukiwa na chupa ya kileo na mkono wa kushoto ukiwa na kitabu cha Biblia. Ili kuwa mwanachama kamili lazima Papa Makiti akubatize kwa pombe unayoipenda zaidi, inaweza kuwa Johnnie Walker Red Label, Guinness, Smirnoff na kama ingekuwa Afrika Mashariki pengine Serengeti, Castle, Tusker au hata Konyagi. "Iwapo wewe hunywa bia, basi unabatizwa kwa bia," Papa Makiti anasema. "Vile vile kwa wale wanaokunywa cider na vileo vingine." Wakati wa kumuomboleza mwanaharakati aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Winnie Mandela, siku moja, kundi la waumini walioonekana kulewa walizua kioja. text: Mchezaji filamu wa Hollywood Julia Roberts anawakilishwa na jina la wakala sawa na James Maddison wa Leicester City, huku wakakilishi wa Samuel L Jackson - ICM Partners - pia wakiwa wamenunua hivi karibuni katika wakala wa soka. Mendes ni wakala wa Doherty. Na wakala wa meneja wa klabu zote - Jose Mourinho na Nuno Espirito Santo. Mmiliki wa Wolves Fosun, wakati huo huo ana hisa ya 20% katika wakala wa Mendes maarufu sana dunaini kwa jina la Gestifute agency. Mwaka 2018, Ligi ya soka iliwachunguza wakala wa Mendes kuhusiana na Wolves na ikasema walitimiza sheria. Kwingineko katika biashra ya mawakala wa soka, hatahivyo, kuna madai mengi ya utendaji mbaya. Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa , limeapa kuingilia kati na kudhibiti - ikisema kuwa inataka "kumaliza au walau kupunguza matumizi mabaya na utendaji wa kupita kiasi " katika soka. "Tunalenga kwa na mfumo wenye uswa na unaofaa wa udhibiti, badala ya sheria za zinazowalinda walio na uwezo ambazo kwa sasa zipo, huku kukiwa na mzozo wa maslahi na malipo ya kupita kiasi 'ya malupulupu' yakitolewa kushoto na kulia ," ilisema. Kwa maelezo hayo, mawakala wa Marekani ambao huwatafuta nyota wakuu wa filamu duniani-ambao huenda wangetaka kulinda majina na makampuni yao - huenda wangetaka kuepuka kile kinachoonekana kama mazingira msitu wa wanyama pori. Ukweli ni kwamba hawafanyi hivyo. Mwaka jana, Shirika la Creative Artists lilinunua wakala wa soka -Base Soccer, na kuunganisha mashirika yanayofuatilia kazi miongoni mwa mwake, wakiwemo mameneja wa nyota wa Hollywood Roberts Carlo Ancelotti na Jose Mourinho pamoja na mshambuliaji wa Leicester Maddison. Okotba 8 , wakala mwingine wa vipaji wa Marekani - ICM Partners - aliinunua Stellar katika mkataba mkubwa hata zaidi wa mamilioni ya dola. Samuel L Jackson ICM ambao ni wakala wanaotafuta nyota wa soka kama Samuel L Jackson na Ellen DeGeneres. Stellar - mawakala wa Jonathan Barnett- walifanya mazungumzo na Gareth Bale kuhusu kurejea kwake katika Tottenham kutoka Real Madrid. "Tunafahamu vizuri masuala hasi kuwahusu mawakala wa soka ," anasema Mkurugenzi mkuu wa ICM Chris Silbermann. "Ninafahamu mtazamo wa watu na ninafahamu kuwa watu wanaona mawakala wakitengeneza pesa nyingi na baadhi katika mchezo wanalilalamikia hilo. Ni biashara mbaya - lakini sina tatizo na hadhi za watu ninaowashughulikia ." Mbali na mtazamo wa ubaguzi wa mawakala unaosababishwa na wateja wao wanaowasukuma kufanya uhamisho ambao unawapatia faida, Silbermann anasema ukweli wa mashirika kama yake ni tofauti sana "Tunafahamu kuwa mamlaka ya mtu maarufu na kile yanachomaanisha ," Silbermann anasema. "Njia ya kupanua umaarufu wake ni kufanya kazi na wachezaji kwasababu ni watu maarufu duniani kuliko ilivyowahi kutokea miaka ya nyuma''. "Mawakala wanaowakilisha watu maarufu duniani kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo kokote. Tunaweza kufungua milango." Silbermann hajawahi kukutana na Bale. Kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish Barnett ataendelea kutoa utaalamu wa soka na kuilinda kazi ya wateja wa Welshman na Stellar , ikiwa ni pamoja na kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish na mlinda lango wa Everton Jordan Pickford. "Kazi yangu ni kuhakikisha mchezaji anastaafu na pesa za kutosha kama wanataka kuendelea kufanya kazi, kwasababu wanataka kufanya hivyo, na si kwamba wanalazimika kufanya hivyo," anasema Barnett. "Tumetumia pesa kuwasaidia jamaa hawa kufikia wanakotaka kufika. Tuna wafanyakazi wa kudumu kwasababu hatutaki wapotee tu na kufanya kazi hii peke yao ." Barnett anasema kuwa hatawaingiza baadhi ya mawakala hasimu wenye mikakati ya kuharibu juhudi za kuwapatia wateja wake mikataba bora, lakini anadai '' ili mradi wanafuata sheria na maadili haina shida". Anahisi kuna matatizo ambayo sekta ya mawakala inahitaji kuyatafutia ufumbuzi, na hafuhrahishwi hasa kuhusu idadi ya wachezaji ambao kwa sasa wanatunzwa na ndugu zao. Barnett anasema amesikitishwa pia na namna Fifa inavyoshugulikia suala hilo. Mwezi Januari, alijiunga na Mendes na Mino Raiola - ambao wanamuwakilisha Midifilda wa Manchester United Paul Pogba - katika mkutano wa mawakala wa kujadili hali yao. Kuhusu Mendes, anasema: " amefanya kazi nzuri sana kwa ajili ya Wolves, na katika maeneo mengine amefanya kazi nzuri pia ." Hadi sasa, hapajawa na mazungumzo kuhusu mageuzi . Alhamisi, Fifa iliainisha mapendekezo yake, ambayo ni pamoja na malupulupu ya mawakala kwa kiasi cha 3% kitakachokatwa kutoka kwenye mshahara wa mchezaji Barnetthajafurahia hilo . Anaamini Fifa inajaribu kujinadi na kupata mtizamo chanya kutoka kwa umma kwa kuwalenga bila usawa ambao wanaweza kulengwa kwa urahisi na kuongeza kuwa bila kubadili mbinu yake kesi itapelekwa mahakamani. "Ningependa pinafsi na mawakala wengine kadhaa kukaa chini ana kwa ana na Fifa Fifa tukiwa tujadili suala hili upya pamoja ," alisema. " Ninaamini tunaweza kufanya kitu kizuri na cha maana zaidiambacho kitamsaidia kila mtu'' Kwa mfano, kuhusu nafasi ya Jorge Mendes katika uhamisho wa mlinzi wa Jamuhuri ya Ireland Matt Doherty kutoka Wolves kuelekea Tottenham kwa garama ya pauni milioni 15 mwezi Agosti . text: Alvaro Morata na Alexandare Lacazette walikuwa miongoni mwa wachezaji waliobeba matumaini ya wengi sio? Ni sawa. Hakuna kati yetu anaweza kutabiri hali ya siku zijazo. Mara nyengine hata wakufunzi wazuri hukataa uhamisho ambao mara nyengine wanasalia wakijilaumu , ama mara nynegine mambo huenda mrama. Hii hapa ni baadhi ya mifano ambayo huenda ingebadili historia ya ligi ya Uingereza. Kaka kuelekea Manchester City Mwaka 2009, kikosi kipya cha Manchester City kilikuwa kikitaka kutumia kitita kikubwa cha fedha kumsajili mchezaji wa Brazil Kaka. Klabu ya AC Milan na Kaka walivutiwa na dau la City la £108m walilowasilisha .Kilikuwa kitita cha juu zaidi ambapo miaka 10 baadaye kilipitwa na uhamisho wa Neymar na Kylian Mbappe kuelekea klabu ya PSG pekee. Shabiki mmoja wa City alikuwa ana uhakika kwamba makubaliano hayo yatafanyika na hivyobsi akaweka tatoo ya mchezaji huyo katika kifua chake. Lakini mwishowe, mshindi huyo wa taji la Ballon d'Or 2007 aliamua kwamba haukuwa wakati mzuri na kukataa fursa hiyo ya kujiunga na Manchester City na hivyobasi kumwacha afisa mkuu wa City akiwa amekasirika na kusema kuwa AC Milan imemkosea. Steven Gerrard kuelekea Chelsea Mwaka 2005, baada ya kushinda kombe la vilabu bingwa Ulaya, Steven Gerrard aliwashangaza wengi katika uwanja wa Anfield kwa kuwasilisha ombi la uhamisho. Mkufunzi mpya kwa jina Mourinho alikuwa ana hamu ya kumsajili mchezaji huyo kwa mradi wake wa Stamford Bridge. Kulikuwa na hisia kali na tisheti zikachomwa , lakini baadaye kama Jammie Caragher anavyosema , Gerrard aligundua kwamba kuridhika na taji moja akiwa Anfield ni zaidi ya kushinda mataji matatu ama manne Stamford Bridge. Bahati mbaya kwa wachezaji wote wawili ni kwamba Chelsea imeshinda mataji manne ya ligi ya Uingereza huku Liverpool ikisubiri. Robert Lewandowski kuelekea Blackburn Kabla apate umaarufu kama mmojawapo wa washambuliaji bora duniani, Kijana Robert Lewandowsky alikuwa mpango wa mkufunzi Sam Allardyce katika klabu ya Blackburn Rovers . Klabu hiyo ya Lancashire iliwasilisha ombi la £4m kwa mchezaji huyo wa Poland mwaka 2010. Hatahivyo majivu ya Volcano yaliweka wingu jeusi angani Iceland na kukatiza usafiri wa ndege na kumzuia Lewandowsky kusafiri kuelekea Blackburn. Kufikia sasa amekiri kwamba Rovers ilikuwa timu yake ya pili alioipenda baada ya Borussia Dortmund , lakini pengine wikendi moja na Big Sam ingemshawishi kusalia. Rivaldo kuelekea Bolton Wanderers Mwaka 2014, Bolton Wanderers walikuwa na ufanisi mkubwa wakiwa ndoto ya kucheza Ulaya. Sam Allardyce aligonga vichwa vya habari alipoulizia uwezo wa mshambuliaji wa Brazil Rivaldo, 32 ambaye alikuwa akiichezea AC Milan. Rivaldo alitoa taarifa iliosema: Nataka changamoto ya kutaka kuifikisha Bolton katika michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yake, ni wakati mzuri. Mwishowe, alikuwa na mabadiliko ya kimawazo na kwenda Olympiakos. Bolton ilimaliza msimu huo ikiwa sawa kwa pointi na Liverpool , ikiwa pointi tatu nyuma ya viongozi wanne wa ligi. Msimu uliopita walifunga bao la dakika za lala salama katika mechi yao ya mwisho kuzuia kushushwa daraja. Andriy Shevchenko kuelekea West Ham Harry Redknapp karibu amsajili mmojawapo wa washambuliaji wazuri zaidi duniani wakati huo akiwa West Ham 1994. Harry anakumbuka kwamba alikuwa na Shevchenko akimchunguza kwa siku nne katika kikosi cha pili cha Barnet. Hatahivyo uzoefu wake wa kusajili wachezaji kutoka mashariki mwa Ulaya kulimfanya kumwacha Sheva. ''Hakungo'a miti lakini alikuwa na nidhamu ya kutosha''. ''Lakini huo ni wakati ambapo nilikuwa na matatizo na wachezaji kutoka Romania na nikafikiria kwamba kitu cha mwisho ningetaka ni kumsajili raia wa Ukrain''. Na ni kupitia maamuzi kama hayo ambapo mchezaji wa haiba ya Sheva aliponyoka. Zlatan Ibrahimovic kuelekea Arsenal Mwaka 2000, Arsene Wenger alimwalika kinda raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kukutana na kikosi chake cha wachezaji kilichojaa vijana. Alimpatia tisheti iliokuwa na nambari tisa mgongoni na kila kitu. Kila kitu kilikuwa kikiendelea vizuri hadi pale Wenger alipomwambia kufanya majaribio. Na kama Zlatan alivyoelezea: ''hapana Zlatan harajibiwi''. Fikiria timu hiyo ikiwa na Zlatan, lo! Sio vibaya kukubali, Kabla ya msimu uliokwisha kuanza , Mohammed Sala hakujulikana na timu uipendayo , je ni kweli? text: Mwanamke huyo anadaiwa kuiba zawadi za thamani ya maelfu ya dola na pesa kutoka kwa wanandoa wapya wanaooana Mwanamke huyo ambaye hajatambuliwa amekuwa akishutumiwa kujitokeza kwenye harusi, bila mwaliko, walau katika harusi nne tangu mwezi Disemba. Polsi pia wameushirikisha umma picha ya mwnamke huyo akiwa dukani akijaribu kutumia kadi ya zawadi ambayo awali ilitumiwa na wanandoa waliofanya harusi karibuni. Zawadi ya dola 4,000 (sawa na pauni 3,300) imetangazwa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake. "Tusiache aharibu siku maalum ya mtu yeyote na tumlete mvamizi huyu wa harusi za watu mbele ya sheria ," imesema taarifa ya ofisi ya mkuu wa polisi wa kaunti ya Comal - Texas. Bodi ya maandalizi ya harusi katika eneo hilo imekiambia kituo cha habari cha CBS kuwa inatambua sura za watu waliopiga picha za harusi "tumekuwa na harusi za wazi msimu huu wa mahira ya joto ambao tumewaona wakizurura wakitafuta watu wanaouza bidhaa na kumbi za haruri," amesema Rhonda Hollon, rais wa kampuni wa kampuni ya maandalizi ya harusi ya - New Braunfels Wedding Chamber. Bwana mmoja na mewe waliliambia shirika la habari la NBC kuwa waligundua kwa mara ya kwaza kuwa wameibiwa zawadi wakati walipokuwa katika fungate yao . "ninafikiri tulipogundua kwa mara ya kwanza , lilikuwa ni jambo la kusikitisha , lililotufanya tufikirie kwamba kwamba hili limetokea," alisema rittany Flores. Yeye na mumewe Andy wanasema pia wallimtambua mwanamke mwizi, na wanaamini aliibamamia ya dola fedha taslimu na maelfu ya hundi za dola na kadi za zawadi. Lakini wanandoa hao wanasema wanatumaini polisi wataweza kumpata muhusika wa uhalifu huoculprit. "ninafikiri hilo ndilo tunalobaki nalo kutokana na hili, sio kuchacha tu yaishie hapa ... Mvamizi wa harusi, kwa jina lolote wanalomuita, muondoshe katika siku yetu ," alisema Bi Flores. "hawezi kuiba penzi letu Polisi wanamsaka mwanamke ambae amepachikwa jina la " mvamizi wa harusi " ambaye amekuwa akishutumiwa kuiba zawadi kutoka kwenye harusi kadhaa kusini mwa jimbo Texas nchini Marekani. text: Ritchie (kushoto) katika mapambano yake ya mwisho na Tim Tszyu mwezi Agosti Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27, na baba wa watoto watatu alikuwa ana mapambano na Michael Zerafa huko Melbourne. "Ni maskitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanamisumbwi Dwight Ritchie ambaye amefariki akiwa anafanya kitu ambacho anakipenda," alisema promota wake Jake Ellis. Ritchie alishindwa mara mbili katika mapambano 21, Hivi karibuni alipigana na Tim Tszyu wakiwa wanawania michuano ya uzito wa juu nchini Australia mnamo mwezi Agosti. Kifo cha bondia huyo kimetokea mwezi mmoja baada ya kifo cha bondia wa Marekani kutokea. Bondia wa Marekani alikufa baada ya kupata jeraha kwenye ubongo mara baada ya kupigana na bondia Charles Conwell. "Dwight atakumbukwa katika ulimwengu wa ndondi kutokana na kipaji chake na jinsi alivyokuwa akishiriki mchezo huo kwa namna ya kipekee na hata mfumo wake wa maisha." Ritchie aliposhindwa mchezo uliopita ndio sababu iliyomfanya kurejea kupambana na Tommy Browne. Kifo chake kimepokelewa na salamu nyingi katika mitandao ya kijamii wakieleza sifa zake na kuonyesha majonzi yao. Tazama pia Lulu Kayage,bondia muuza matunda Bondia mmoja wa nchini Australia, Dwight Ritchie amefariki mara baada ya kutoka kwenye mazoezi. text: Maelfu ya wakimbizi kutoka DRC wamvuka mpaka kuingia nchini Uganda Katika mkutano maalum mjini Geneva Uswizi, Umoja wa Mataifa ulikuwa unatarajia kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinaadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 5 wamelazimika kuyatoroka makazi yao kwasababu ya mapigano katika sehemu tofauti za nchi hiyo kubwa. Lakini serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo wa ufadhili ikisema kwamba hali inafanywa kuwa mbaya wakati ni kinyume. Umoja wa Matiafa umejibu kwa kutangaza majanga ya kibinadamu nchini humo kuwa kiwango cha tatu - kiwango cha dharura cha juu zaidi. "Hali imefikia kiwango cha Yemen na Syria kwa namna ambavyo watu wanahitaji msaada, ameeleza Jan Egeland, mkuu wa zamani wa Ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya dharura ambaye sasa anaongoza baraza la wakimbizi la Norway pia hivi karibuni alikuwa DRC. Janga la DR Congo kwa takwimu Chanzo: Umoja wa Mataifa Mkutano huo umedhamiria kuchangisha dola bilioni 1.7 kupunguza uzito wa inachotajwa na Umoja wamataifa kuwa ni janga kubwa la kibinaadamu nchini Congo. Mpaka sasa serikali ya DRC haijajibu mwaliko wa Umoja wa mataifa ikisema taasisi hiyo kuu imetilia chumvi hali halisi nchini na ukubwa wa tatizo lililopo. Mashirika ya misaada yanasema watu milioni tano wamelazimika kuyatoroka makazi yao kutokana na ghasia, mapigano, njaa na ukosefu wa utulivu na kwamba maelfu ya raia wa Congo wamelazimika kutafuta hifadhi magharibi mwa Uganda. Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu ndani ya DRC wamekumbwa wasiwasi kutokana na hatua hiyo ya serikali kususia mkutano huo mkuu mjini Geneva. Kumeshuhudiwa ghasia na maandamano nchini kumshinikiza rais Joseph Kabila aondoke madarakani Wasiwasi wa aina hiyo pia umetolewa na baadhi ya raia wanaosema kwamba wataendelea kuteseka bila ya msaada wa jumuia ya kimataifa. Je kuna hasara gani kwa serikali hiyo kukataa kuhudhuria mkutano wa Geneva? Mashirika ya misaada yanasema DRC inateseka katika janga kubwa lenye uzito la kibinaadamu lililosahaulika kwa muda mrefu. Kuna watu milioni 13 wanaohitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2 wanaugua utapia mlo mbaya, na watu milioni 4.5 wamepoteza makazi yao. Lakini tathimini hii ya mashirika ya misaada imeiudhi serikali ya DRC. Inatizama kiwango cha daraja la tatu kilichowekwa cha hali ya janga hilo kuwa kama tusi. Mashirika ya misaada yanasema watu milioni 13 wanahitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2 Na ndio sababu ikachukua hatua hii ambayo haikutarajiwa ya kususia mkutano wa Geneva. Hata hivyo,maafisa wa Umoja wa mataifa wanatumai kwamba wanadiplomasia wa Congo watabadili uamuzi wao na wahudhurie mkutano huo leo. Ni wazi kwamba mkutano wenyewe utaendelea licha ya chochote kile kitachotokea, wanaharakati wanasema maisha ya mamilioni ya watu yamo hatarini. Serikali ya Congo imekataa kuhudhuria mkutano huo wa kuchangisha fedha za msaada kwa janga linaloshuhudiwa nchini ikisema Umoja wa mataifa umetilia chumvi ukubwa wa tatizo lililopo. text: Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wote wameshinda mara tano tuzo ya Ballon d'Or Lakini zinapo wakutanisha wachezaji wawili bora duniani - Lionel Messi na Cristiano Ronaldo - ambao wamekubaliana kukaa chini pamoja na kupata mlo wa jioni, hugeuka kuwa kitu kingine tofauti. Kulikuwa na ucheshi baina ya kiungo wa mbele wa Juventus Ronaldo na mwenziwe wa Barcelona Messi walipotaniana na kuchekeshana wakiwa wamekaa karibu pamoja. Ilikuwa vigumu hata kuwafikiria wawili hao kwamba waliwahi kuwa mahasimu wakuu katika kipindi cha miaka 9 ya Ronaldo akiwa Real Madrid katika muongo mmoja uliopita wa kura ya kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya mchezaji bora duniani wa soka. "Tumekuwa katika jukwaa hili pamoja kwa miaka 15 years. Sijui kama hilo limewahi kufanyika katika siku za nyuma - watu hao hao wawili katika jukwaa hili wakati wote," Ronaldo amesema. "Bila shaka tuna urafiki mzuri. Hatujawahi kula meza moja, lakini natarajia hilo litafanyika katika siku zijazo. "Tulikuwa na ushindani huo Uhispania. Nilimshinikiza na yeye akanishinikiza mimi pia. Kwahivyo ni vizuri kuwa sehemu ya historia ya soka." Kwa mapenzi kama haya , nani anayeweza kuthubutu kusema kwamba kuna uhasama kati ya wawili hawa? Virgil van Dijk awabwaga Lionel Messi na Cristiano Ronaldo Enzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi za kutawala tuzo za mpira zinaendelea kusukumwa ukingoni, na usiku huu beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk amewaangusha. Van Dijk amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa bara Ulaya kwa mwaka 2018/19 Van Dijk baada ya kuingoza safu ya ulinzi ya Liverpool kuchukua Champions League msimu uliopita. Van Dijk amekuwa baraka kwa Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Southampton na amekuwa kiungo muhimu kuisaidia kushinda Champions League msimu uliopita na pia kuisaidia kuwania taji la Ligi ya Premia dhidi ya Manchester City hadi mwisho. Kwa kawaida droo za mechi na hafla za tuzo huenda zikajivuta kwa hotuba ndefu na kukosa msisimko. text: Dkt. Jan Karbaat alijiita "muasisi wa fani ya uzazi wa kutunga mimba kwa kupandikiza mbegu ". Jan Karbaat anashukiwa kuwa baba wa watoto wapatao 60 katika kituo cha afya alichomiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam. Vipimo sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake mwezi Aprili, akiwa na umri wa miaka 89. Wakili wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo. Jan Karbaat alijiita "muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa". Kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati kulikuwa na taarifa kwamba alidaiwa kugushi data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiumena kuzidisha idadi inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za uzazi. Katika kesi ya mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba visa vinavyoshukiwa vinajumuisha mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wakeambaye anasura inayofanana na daktari. Taarifa za vinasaba DNA zitasalia kuwa siri hadi pale watoto watakapoonyesha kuwa kuna sababu za kuamini daktari alikuwa baba yao, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan, ambaye alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Rotterdam. Hatimae, kama taarifa za vinasaba-DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya 1980s, kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba hawangepaswa kuwepo, ameongeza Anna Holligan. Joey, ambaye anaamini Jan Karbaat huenda ni baba yake ameiambia BBC: " Ina maana kubwa kwangu ... Tunatumai kupata majibu ." Wakili wa familia ya Karbaat anapinga kufanyika kwa vipimo vyovyote vya vinasaba DNA. Wakati wa uhai wake, daktari mwenyewe alikataa kufanya vipimo hivyo. Hata hivyo, mwezi uliopita,kijana yake Jan Karbaat alitoa vinasaba vyake DNA vipimwe ambavyo vilionyesha kuwa daktari anaweza kuwa babawa watoto 19, waliozaliwa kwa njia ya uzazi wa kutungishwa mbegu kwa lugha ya kitaaamu IVF, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP. Mahakama moja nchini Uholanzi imeidhinisha ombi la familia zinazotaka vipimo vya vinasaba DNA vichukuliwe juu ya mmiliki wa kliniki ya uzazi ya daktari anayeshutumiwa kutumia mbegu zake za kiume katika makumi kadhaa ya kesi. text: Ndovu waliokwama wanusuriwa Tanzania Ndovu wanne wakiwemo watoto wawili waliokolewa lakini ndovu mmoja mkubwa alifariki kutokana na ukosefu wa maji kulingana na chombo cha habari cha China Xinhua. Kulingana na duru kutoka kwa kampuni ya Sinohydro, baadhi ya wakaazi wa manyoni eneo la Singida waliwaita wafanyikazi wa kampuni hiyo kuwasaidia tembo hao yapata kilomita 40 kutoka katika hifadhi hiyo. Saa moja baadaye, waokoaji hao wa China waliwasili katika eneo hilo na kuanza uokoaji baada ya kupata ruhusa kutoka kwa gavana wa eneo hilo na wasimamizi wa hifadhi hiyo. Ndovu wavamia chuo kikuu cha Dodoma Tanzania Kulingana na Xhinua wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa wanyama hao walianguka katika shimo hilo walipokuwa wakitafuta maji. Shimo hilo lilikuwa dogo na kuwalazimu ndovu hao kuanza kusukumana kwa hofu. Baada ya saa tano za kazi ngumu ya kuwanusuru, ndovu mmoja mkubwa na watoto wake walikuwa wa kwanza kutolewa katika shimo hilo. Ndovu wengine wawili walifuatia baadaye lakini mmoja mkubwa akaaga dunia. Kampuni ya ujenzi ya China Sinohydro imewapeleka wahandisi wake na tingatinga katika eneo la kuhifadhi wanyama pori la Rungwe katikati ya Tanzania ili kuwaokoa tembo watano waliokwama katika shimo. text: Kama huna maelewano na bosi wako ni jambo gumu zaidi. ''Niliipenda sana kazi yangu lakini kama kuna bosi ambaye anachukia unachokifanya au anajaribu kukushusha thamani, inakuvunja moyo sana'' amesema Craig. Mara ya kwanza alimpenda sana meneja wake lakini alianza kumchukia pale alipomuona anamgombeza msaidizi wake kwenye simu. Na kuanzia hapo mambo yaliendelea kuwa mabaya. Alikuwa anamgombeza sana ofisini na kumdhihaki kwenye mkusanyiko wa watu. ''Kwanza yalianza maneno ya dharau'' ameeleza. ''Kidogo kidogo vitu vikaanza kubadilika kufikia kiasi cha kusema maneno ya shari, uadui na kujiona bora kuliko wengine.'' Ameongeza ''ilikuwa inaumiza sana kwenda kazini kila siku. Mahusinano yako na watu wa karibu yanakuwa yanaharibika kabisa.'' ''Ukifanya kazi na bosi mbaya , mtu ambaye haoni thamani yako, inakufanya na wewe ujione mtu wa kiwango cha chini sana. Unakuwa hauwezi kufanya kazi kwenye kiwango kinachotakiwa, unakuwa hauna furaha, na hautaki kabisa ujitume zaidi.'' Tafiti zinasema kuwa uhusiano mbaya kazini husababisha tabia za wizi Tatizo hili kwa Craig sio la kushangaza. Uchunguzi uliofanywa na kampuni ya '' Chartered Institte of personnel ad Development (CIPD) umeonesha asilimia 7 ya watu wanasema hawaelewani na mabosi wao. Ben Willmott ni kiongozi wa sheria za umma amesema katika kesi nyingi wafanyakazi huwalalamikia mabosi wao kwa sababu ya kupewa kazi nyingi au ukosefu wa haki wa muda mrefu. ''Ni mara nyingi sana, vitu vidogo vidogo ndivyo vinasababisha matatizo'' ameendelea kusema. Kuepuka haya anawashauri waajiriwa wawe wazi na mabosi wao kuhusu tatizo lolote, kama wakijisikia huru kufanya hivyo. ''bosi anaweza kuwa hajui jinsi gani tabia yake inawaathiri watu wengine na hivyo kumwambia inaweza kuwa kitendo cha kumfanya abadilishe matendo yake,'' amesema Bw Willmott. Lakini, anapelekea kwenye matatizo makubwa zaidi kama vile kudhihaki na kumuabisha mtu, ambazo zinatakiwa kushughulikiwa na afisa (HR) ama meneja mwingine. Damian Beelay anasema kuwa alikua akinyanyaswa sana na bosi wake Hata hivyo Damian Beeley ambaye ni mtaalamu wa uhusiano wa umma, aliwahi kuwa na matatizo na bosi wake, anasema kuwa kama jambo lina uhusiano binafsi basi ni bora uache kazi na kutafuta sehemu nyingine. Lakini anasema kuwa ni tatizo ambalo anaweza kuwa nalo meneja kuliko mwajiri. ''Kama meneja kuna watu hawatokupenda lakini inabidi ufikirie kwanini hawakupendi,'' amesema. ''lakini kama wewe ni muajiriwa na unamchukia bosi wako , hiyo ni hali mbaya sana kuwa nayo''. ''Unakuwa huwezi kufanya kazi kwenye kiwango kinachotakiwa, unakuwa hauna furaha, na hautaki kabisa ujitume zaidi.'' text: Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania. Ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini Tanzania. Pia anakuwa rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar, wa kwanza akiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 10 kutoka mwaka 1985 mpaka 1995. Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Tanzania kufiwa na rais akiwa madarakani na makamu wake kuchukua nafasi. Lakini je, Mama Samia ni nani? Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, msafara wa aliyekuwa mgombea mwenza wa CCM, Samia Hassan Suluhu, ulikuwa na wasanii wengi mashuhuri nchini. Awali, wengi walimwogopa kwa sababu ya heshima yao kwake - lakini kuvunja mipaka, akaomba jambo moja kwao; wamwite Mama. Tangu hapo, ukuta kati yao ukavunjika na kampeni zake zikawa na msisimko na hamasa kubwa - tofauti na ilivyozoeleka kwenye matukio ya wagombea wenza. Kwa Watanzania wengi, jina la Samia Hassan Suluhu (61) lilipata umaarufu zaidi wakati alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba lililoteuliwa mwaka 2014. Tanzania ilikuwa inaelekea kutengeneza Katiba mpya - baada ya kukamilika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kupitia Tume ya Jaji Warioba na Mama Samia alikuwa amepewa jukumu la kuongoza mchakato huo kupitia Bunge la Katiba. Kwa sababu bunge lile lilikuwa likionyeshwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na Watanzania wengi wakiwa na kiu kubwa ya kujua nini kinaendelea - sura ya Samia ilianza kuzoeleka kwenye macho ya wengi na uwezo wa kuongoza ukionekana dhahiri. Lakini hiyo ilikuwa taswira yake ya hadharani. Katika duru za kisiasa bungeni wakati ule, Samia alikuwa akifahamika kwa uwezo wa kuonyesha utulivu - hata katika nyakati ambazo hali ya hewa katika bunge hilo ikiwa imechafuka na pia kuzungumza na wote. Muundo wa bunge hilo ulitaka viongozi wake wa juu watoke katika pande mbili za muungano na kwa vile mwenyekiti wa bunge hilo alikuwa ni hayati Samuel Sitta kutoka Tanzania Bara, nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliangukia kwa Mzanzibari Samia. Hata hivyo, wengi hawakutarajia kwamba angetangazwa na aliyekuwa mgombea urais wa chama cha mapinduzi mwaka 2015, John Magufuli, kuwa mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi huo. Ingawa wakati huo tayari alikuwa na uzoefu wa uwaziri wa takribani miaka 15; kujumlisha na uzoefu wake huo katika Bunge la Katiba- si watu wengi walimwona yeye kama mmoja wa watu wanaoweza kupewa wadhifa huo. Wakati CCM iliposhinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 - unaotajwa kuwa mgumu kuliko yote kwa chama hicho tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini - Samia aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu kuanzishwa kwa taifa la Tanzania. Siri ya mafanikio ya Samia Sifa moja kubwa ambayo watu waliowahi kufanya naye kazi wanaisema na ambayo si watu wengi wa nje wanaifahamu ni uwezo wake mkubwa wa kiuongozi. Mbunge wa jimbo la Bumbuli (CCM), January Makamba, anasema Samia ni miongoni mwa wanasiasa wenye uwezo mkubwa aliowahi kufanya kazi nao na ni bahati mbaya tu kwamba wengi wa Watanzania hawajapata fursa ya kuliona hilo. Makamba alifanya kazi kwa karibu na mama Samia katika kipindi cha kati ya mwaka 2015 hadi 2020 wakati akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - ambapo alikuwa akiripoti kwa mama huyo moja kwa moja. "Mama Samia amedunishwa. Ana uwezo mkubwa wa kufanya aonekane ni mwanasiasa wa kawaida lakini ukweli ni kwamba uwezo wake ni mkubwa sana na hili sijasimuliwa na mtu bali nimeliona kwa kufanya naye kazi kwa karibu," alisema. Samia Suluhu Hassan: Fahamu maisha na majukumu ya makamu wa rais wa Tanzania Mama Samia anaelezwa kama mwanasiasa anayependa kufanya maamuzi kupitia kusikiliza kila mmoja na si mtu wa kuamua mambo kwa pupa au kwa kuonea wengine. Samia pia anaelezwa kuwa mwanasiasa jasiri na asiyeyumbishwa kwenye jambo analoliamini na kulikuwa na maneno kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM kumfanya yeye kuwa mgombea mwenza wa Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kulitokana pia na kufahamu sifa yake hiyo. Kwa vile Magufuli ni mtu anayeamini katika kusukuma mambo kwa haraka na wakati mwingine bila kujali athari za kisiasa au kisaikolojia kwa uamuzi huo, CCM ilitaka Makamu atakayekuwa na uwezo wa kumwambia ukweli bila kumwogopa badala ya kukubali kila kitu. Mfano mmoja wa tabia za Samia ni kitendo chake cha kwenda kumjulia hali aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alipokuwa amelazwa nchini kenya. Katika mojawapo ya matukio ya kutisha kwenye historia ya Tanzania, Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba mwaka 2017 akiwa jijini Dodoma alikokuwa anahudhuria vikao vya bunge. Samia alikuwa ndiye kiongozi wa juu wa kwanza wa serikali - na pekee, kwenda kumuona mwanasiasa huyo mashuhuri. Historia ya Samia kwa ufupi Mama Samia aliolewa na mumewe, Hafidh Ameir, mnamo mwaka 1978 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata watoto wanne. Mtoto wake maarufu zaidi - Wanu, ni mbunge wa bunge Tanzania. Samia ni msomi wa kiwango cha shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza na ni mhitimu pia wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alikosomea masuala ya utawala. Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar mwaka 1977 na akapanda ngazi hadi kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988. Alihudumu pia kama meneja wa mradi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Zanzibar kati ya 1985 na 1997, na pia kama meneja mkurugenzi wa Mwamvuli wa NGO 1998 hadi 1999. Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa. ''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija. Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia. Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa ni mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki Jumatano Machi 17. text: Stena Impero ilishutumiwa kwa kuvunja sheria ya kimataifa ya baharini Mmiliki wa meli ya Stena Impero ambaye ni raia wa Sweden amesema kuwa ipo safarini kutoka bandari ya Bandar Abbas , ambapo ilikuwa imeegeshwa tangu mwezi Julai. Meli hiyo ilikamatwa na wanajeshi wa Iran katika mkondo wa Hormuz baada ya kuishutumu kwa kuvunja sheria za baharini. Maafisa wanasema kwamba iliondoka na kuelekea katika maji ya kimataifa saa moja unusu saa za Afrika mashariki siku ya Ijumaa alfajiri. Erik Hanell, afisa mtendaji wa Stena Bulk amesema kwamba meli hiyo itaelekea Dubai ambapo wafanyakazi wake watazungumziwa na kufanyiwa vipimo vya matibabu. ''Familia za wafanyakazi wa meli hiyo zimeelezwa kwamba kampuni hiyo kwa sasa inafanya mipango ya kuwarudisha makwao wafanyakazi wake haraka iwezekanavyo'', alisema katika taarifa. Kukamtwa kwa meli hiyo tarehe 19 mwezi Julai kunajiri wiki mbili baada ya meli moja ya Iran kuzuiwa Gibraltar kupitia usaidizi wa wanamaji wa Uingereza. Footage released by Iran's Revolutionary Guard-affiliated Fars news agency appears to show Stena Impero being seized Meli hiyo ilituhumiwa kukiuka vikwazo vya muungano wa Ulaya nchini Syria , lakini liachiliwa mwezi Agosti. Operesheni dhidi ya Sterno Impero ilionekana kama kisasi cha jukumu la Uingereza katika kusaidia kuikamata meli hiyo ya Iran madai ambayo Iran imekana. Kwa nini meli hiyo ilikamatwa? Tukio hili limefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Uingereza, Marekani na Iran. Jeshi limesema meli hiyo imekamatwa kwa kuvunjwa kwa sheria tatu: kuzima GPS; Kuingia kwenye mpaka kupitia njia ya kutokea badala ya kuingilia; na kupuuza onyo. Taarifa zinasema hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi na usalama wa wafanyakazi ni jambo la kwanza kwa wamiliki na mameneja. Tarehe 9 mwezi Julai, Uingereza ilieleza tishio la usalama katika maji ya Iran kwenye Ghuba ni ''kubwa''. Meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza sasa inaondoka nchini Iran baada ya kukamatwa kwa zaidi ya miezi miwili. text: Redoine Faid alisaidiwa na watu kadhaa waliojihami ambao walitengeneza mwanya katika lango la jela hiyo huku helikopta hiyo ikitua katika uwanja karibu na jela hiyo. Ndege hiyo ilipaa hadi eneo la Gonessa lililopo karibu na jela hiyo ambapo ilipatikana na maafisa wa polisi. Faid 46, amekuwa akihudumia kifungo cha miaka 25 kwa jaribio la wizi wa mabavu lililotibuka ambapo afisa mmoja wa polisi aliuawa. Hii ni mara yake ya pili kutoroka jela: Mwaka 2013 alitoroka jela baada ya kuwatumia walinzi wanne kama ngao huku akilipua milango kadhaa kwa kutumia kilipuzi. Alifanikiwa kutoroka chini ya nusu saa baada ya kuwasili katika jela hiyo iliopo kaskazini mwa Ufaransa. Mwaka 2009 Faid aliandika kitabu kuhusu uzoefu wake katika mitaa ya Paris iliojaa uhalifu na kuwa mtu aliyekukuwa akivunja sheria mara kwa mara. Alidai kuwacha uhalifu lakini mwaka mmoja baadaye alihusika katika jaribio la wizi lililotibuka ambapo alipelekwa jela ya Réau katika jimbo la Seine-et-Marne. Faid na washirika wake walitorokea katika uwanja huo wa jela ambao haukuwa na ulinzi mkali, bila ya kumjeruhi yeyote kulingana na chombo cha habari cha Ufaransa Europe1. Watu waliokuwa wamejihami kwa risasi walimchukua mfungwa huyo katika chumba cha kuwatembelea wageni kabla ya kumpeleka katika helikopta hiyo na kutoroka naye kulingana na duru za usalama zilizonukuliwa na chombo cha habari cha reuters. Ripoti zinadai kwamba rubani wa helikopta huenda alikuwa ametekwa nyara. Usakaji wa maafisa wa polisi unaendelea katike eneo lote la Paris. Hatua zote zinafanywa kumtafuta mtoro huyo , kulingana waziri wa maswala ya ndani. Akiwa amezaliwa 1972, Faid alilelewa katika maeneo ya uhalifu mwingi ya mitaa ya Paris kabla ya kuanza maisha ya uhalifu Miaka ya tisini , alikuwa akisimamia genge lililohusika na uhalifu wa kujihami na ulafi ktika mji mkuu wa Paris. Alikuwa akisema kwamba maisha yake yalipata msukumo wa filamu za uhalifu za Hollywood, ikiwemo Al Pacino na Scarface. Mwaka 2001 alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa uhalifu Maafisa wa polisi wa Ufaransa wanaamini kwamba Faid aliongoza uhalifu ambapo afisa wa polisi aliuawa, lakini akahukumiwa kwa uhalifu aliotekeleza mnamo Aprili. Alikuwa amerudishwa jela 2011 kwa kukiuka masharti ya msamaha yanayohusiana na makosa ya awali. Mwaka 2013, alitoroka katika jela ya kaskazini mwa Ufaransa ya Sequedin nje ya Lille, kwa kuwateka nyara walinzi wawili, lakini akakamatwa tena wiki sita baadaye Mwaka uliopita, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kutoroka jela 2013 Jambazi sugu ametoroka jela kwa kutumia ndege aina ya helikopta katika jela moja mjini Paris , mamlaka ya Paris imesema. text: Urusi inakana kuunda silaha zinazokiuka mkataba huo Bwana Trump amesema amekuwa akizungumza na na nchi hizo mbili kuhusu wazo hilo na wote "walilifurahia sana sana". Kauli zake Trump zinakuja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba muhimu wa nyuklia na urusi , ikielezea juu ya aina mpya ya silaha. Enzi ya Vita Baridi mkataba wa zana za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Mkataba huo (INF) ulipiga matrufuku matumizi ya zana za masafa ya kati yanayopiga kilomita 500 hadi 5,500 (310-3,400 miles). Kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba huo Ijumaa kumefuatia shutuma za marekani kwamba Urusi ilikuwa imekiuka mkaataba huo kwa kuunda mtambo mpya wa mfumo makombora . Moscow imekanusha haya. Akijibu maswali juu ya ni vipi ataepuka silaha za nyuklia kufuatia kuvunjika kwa mkataba wa INF , Bwana Trump amesema utawala wake umekuwa ukizungumza na Urusi Russia "kuhusu mkataba wa nyuklia, ili waachane na baadhi ya silaha, waachane na baadhi ". "Tutahitaji kwa vyovyote vile kuijumuisha Uchina wakati fulani ,"aliongeza. Bwana Trump amesema mkataba wa aina hiyo unaweza kuwa "kitu cha kizuri kwa dunia " na kwamba anaamini hili litatekelezwa. "Uchina ilifurahia sana, sana kuhusu kuzungumzia juu ya suala hili na ilikuwa hivyo hivyo kwa Urusi . Kwa hiyo ninadhani tutakuwa na mkataba wakati fulani ", Trump aliwambia waandishi wa habari Ni kwanini Trump alijiondoa kwenye mkataba ? Marekani zimeishutumu Urusi kukiuka mkataba kwa kumiliki aina mpya ya silaha, kwa kutengeneza makombora kadhaa ya 9M729 - yanayofahamiwa na Nato kama SSC-8. Shutuma hizi pia ziliwasilishwa kwa washirika wa Marekani katika muungano wa Nato, ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani. "Urusi inawajibika kwa kuvunjika kwa mkataba'', amesema waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo katika taarifa aliyoitoa Ijumaa. "Kwa uungaji mkono kamili wa washirika wetu wa Nato, Marekani imeamua kuwa Urusi ndio imesababisha kuvunja mkataba, imekuwa ikikiuka mara kwa mara wajibu wake chini ya mkataba ,"aliongeza. --------------- Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake Nato imesema inajiweka kando na mvutano kuhusu silaha mpya na Urusi, Katibu Mkuu wake ameeleza, baada ya Marekani kujiondoa rasmi kutoka kwenye mkataba wa nyukilia na Urusi. Rais Donald Trump mnamo Februari ametangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2. Rais wa Urusi Vladimir Putin amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye. Kuna hatari gani? "Breki ya thamani katika vita vya nyuklia" inaeleka kupotea, ameonya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres. "Huenda hili likaongeza na sio kupungua tishio la makombora," aliongeza, na kuomba pande zote kutafuta "makubaliano mapya ya mtazamao wa pamoja ya udhibiti wa silaha kimatiafa". Wachambuzi wanahofia kwamba kutibuka kwa makubaliano hayo ya kihistoria huenda kukachangia ushindani mpya wa silaha kati ya Marekani, Urusi na China. "Kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo sasa, tutashuhudia utengenezaji na utumiaji wa silaha mpya," Pavel Felgenhauer, mchambuzi wa zana za Urusi ameliambia shirika la habari la AFP. "Urusi tayari ipo tayari." Mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameiambia BBC kuwa makombora ya Urusi - ambayo alisema kuwa ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba huo" - zina uwezo wa nyuklia, ambayo ni magumu kutamabua na yanaweza kufika katika miji ya Ulaya katika muda wa dakika. Mkuu wa ujasusi Marekani ajitenga na utawala wa Trump. Uturuki yaikaidi Marekani kwa kujihami na makombora ya Urusi. "Hili ni jambo zito," aliongeza. " Mkataba wa INF umekuwa jiwe la msingi katika udhibiti wa silaha kwa miongo kadhaa, na sasa tunashuhudia kuvunjika kwa mkataba huo ." Ameongeza kwamba hakujakuwepo "ishara zozote" kuwa Urusi itatii na makubaliano hayo na kwamba "ni lazima tujitayarishe kwa ulimwengu usiokuwa na mkataba wa INF na ulio na makombora zaidi ya Urusi". Stoltenberg pia alisema kuwa uamuzi wowote wa Nato kuhusu namna gani ya kujibu utatolewa baada ya kupita muda huo wa mwisho uliotolewa. Aina mpya ya makombora ya nyuklia inayodaiwa na Marekani kuuundwa na Urusi nato haina mpango wa kutuma makombora yake ya ardhini Ulaya lakini makombora ya angani na ya ulinzi, ya mazoezi na utayari wa vikosi vyake na mipango mipya ya udhibiti wa silaha huenda yakawa ni sehemu ya jibu lake. Mkataba wa (INF) ni nini? Ulisainiwa na Marekani na uliokuwa Muungano wa Sovieti mnami 1987, mkataba huo ulipiga marufuku silaha zote za nyuklia na makombora yasio ya nyuklia ya masefu marefu na ya wastani isipokuwa ya baharini. Marekani ilikuwa na wasiwasi kuhusu kutumwa kwa kombora la SS-20 la Sovieti mnamo 1979 na ilijibu kwa kuweka makombora ya masafa mafupi ya ardhini Ulaya - hatua iliyozusha maandamano makubwa. Kufikia 1991, takriban makombora 2,700 yaliharibiwa. Mataifa hayo mawili yaliruhusiwa kukagua hifadhi za taifa mwenza. Mambo yaliharibika wapi? Mnamo 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kuwa mkataba huo haushughulikii maslahi ya Urusi. Hilo lilifanyika baada ya rais wa Marekani George W Bush, mnamo 2002, kuitoa Marekani katika mkataba wa kupinga makombora ya masafa ya juu, uliopiga marufuku silaha zilizoundwa kuzuia makombora ya aina hiyo. Mnamo 2014, rais wa wakati huo Marekani Barack Obama aliishtumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo wa INF baada ya kutuhumiwa kufanya majaribio ya kombora la ardhini. Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka mkataba mpya wa nyuklia usainiwe na Russia na China kwa pamoja. text: Ulemavu huu wa ngozi husababishwa na ngozi kushindwa kutengeneza viini vya melanin vinavyohusika kwa kiasi kikubwa na utengenezaji wa rangi ya ngozi ya kila binadamu Licha ya kuwa baba na mama yake Grace Nzomo ni watu wenye rangi nyeusi , Grace alizaliwa akiwa na ngozi nyeupe , lakini sio weupe wa kawaida , ila ni ule wa ulemavu wa ngozi . Kuishi na hali hii kulingana na Grace kumekuwa na changamoto kubwa sana , mojawapo wa changamoto hizi ni unyanyapaa na mtazamo ambao jamii inawapa watu kama Grace; kuna jamii hadi leo zinatazama albino kama soko tayari la kafara inayoleta 'bahati nzuri' katika maisha ya watu. Grace alisema " Imani potofu zinaendelea kutiliwa mkazo na itikadi za kitamaduni , zinazosababisha binadamu wanaoishi na ulemavu wa ngozi kuwa kwenye hatari ya dhuluma na unyanyapaa , inaonekana kana kwamba sisi wenye ualbino tunadhamana kuu tukiwa wafu kwa sababu tunapozaliwa tunafichwa , na tunapofika utu uzima tunawindwa ili sehemu za mwili wetu ziuzwe " Matamshi ya Grace yaliibuka pale alipoanza kufikiria kuhusiana na upeo au mtizamo ambao jamii imewapatia watu kama yeye , kwa kiasi kuwa kila siku katika maisha ya mtu mwenye kuishi na ulemavu wa ngozi anapambana kuishi kwa kuwa mwangalifu zaidi kuliko mtu mwingine. "kuishi katika sehemu nyingi barani Afrika , kuna hatari chungu nzima , lakini kila siku watu kama sisi tunapigana kudhihirishia ulimwengu urembo na nguvu tulionayo katika maisha haya "Grace aliongezea kusema Grace Nzomo alizaliwa miaka 26 iliyopita, yeye ni mtoto wa kwanza katika jamii yake, ana dada yake kwa jina Martha Nzomo mwenye miaka 22 ambaye anamfuata, ambaye pia alizaliwa na hali hiyo hiyo , haikuwa rahisi kwa jamii yake Grace kuwa wazazi wake walijifungua watoto wawili waliofuatana wakiwa na ugonjwa ambao unatizamwa na jamii kwa njia tofauti kabisa . Ila kwa wazazi wake Grace walipambana kwa hali na mali kuwalea mabinti wao kwa mapenzi na pia kwa kuwafahamisha kuwa walikuwa ni watu tofauti na watoto wengine kutokana na ulemavu wao wa ngozi. "Nilipozaliwa na nikafikisha wakati wa kwenda shuleni , waalimu na wanafunzi hawakuwa na ufahamu wa hali kama yangu , kwa hiyo hawakujua hata jinsi ya kunichukulia , lakini kwa kuwa mamangu mzazi alikuwa mwalimu alisaidia sana kuhamasisha waalimu na pia wanafunzi kuhusu hali yangu wakati huo mambo yalikuwa mepesi kwangu " Grace alisema Kulinganana Grace mamake alikuwa ni msaada mkubwa kwake kutokana na kuwa alikuwa mwalimu katika shule ya msingi alikokuwa anasoma , mmojawapo wa changamoto zake Grace ni kuwa mcho yake yalianza kuwa na matatizo ya kuona , akiwa mbali na maandishi ya mwalimu Grace alipata matatizo ya kuona kabisa , na ililazimu walimu wke kuandika kwa herifu kubwa zaidi , hii ni hali ambayo inawaa changamoto wau wengi wanaoishi na hali ya albino kuwa na shida ya macho , hususan wanapokuwa katika mazingira ya mwanga au jua Changamoto iliwadia alipoingia shule ya sekondari , na waalimu wa somo la Jeografia , chemia walipendekeza kuwa Grace aachishwe masomo kwa kuwa alikuwa na mattaizo ya mcho , na ilipendekezwa kuwa aingie shule ya watu wasiokuwa na uwezo wa kuona ilikusoma , kupitia BRAILE , Braile ni maandishi rasmi ya watu vipofu , hali hii Grace anasema ilimpotezea muda mwingi na pia kumkosesha nafsi ya kusomea taaluma za udakitari na kadhalika Lakini Grace hakukata tamaa licha ya kuwa na changamoto ya kuona , alihitimu n ahata kuingia chuo kikuu kimoja nchini Kenya aliposomea Saikolojia Grace pia anashiriki sana kama mwanamitindo na maonyesho ya ulimbwende ambapo anachukua nafasi ya hali yake kudhihirishia ulimwengu changamoto zinazoandamana na watu wenye ulemavu wa ngozi ''Mimi hushiriki katika maonesho ya mavazi na urembo , kwa kuwa nina Imani kuwa unapokuwa na ujasiri wa kujitokeza kimsomaso licha ya muonekano wako uwa kimwili , basi unadhihirishia ulimwengu kuwa wewe umejikubali , na hauhitaji mtu mwengine kukueleza wewe ni nani '' Grace alisema Grace anasema kuwa wakati wake wa ziada yeye hujipumbaza na densi za mtindo wa kilatino, kuogelea . Grace ana maono makubwa kwake yeye na kwa watu ambao wanaishi na ulemavu maishani. Ya kuwa licha ya changamoto nyingi ambazo zinawazunguka wanajizatiti kuyafikia malengo yao kama binadamu wengine duniani Grace Nzomo hayuko pekee yake katika Kuishi na changamoto za ngozi Wakati Bi Elizabeth Wangui mwenye miaka 26 pia kutokana nchini Kenya alipogundua alama nyeupe usoni , Alikuwa wa haraka Mno kupuuza tu , lakini ikawa hofu kwani alama hiyo haikwisha. "Nilikuwa kidato cha Pili , nilidhani ni alama ya chaki ya mwalimu nilipoifuta niligundua ilikuwa ndani ya Ngozi yangu " alisema Wangui Ilibidi niombee ruhusa shuleni kutafuta matibabu , Alipata matibabu na kupona na akarejea shule, punde tu alama nyingine nyeupe ikatokea mgongoni , wakati huu ilienea kwa kasi Mno , na alipotafuta matibabu ndipo aliambiwa kuwa ana ugonjwa wa ngozi wa Vitiligo. Kila siku alama ile ilipanuka kwenye ngozi yake. Hali hii ilisababisha muonekano wa sura yake kubadilika Mno. Hivyo basi maisha yake kukumbwa na changamoto nyingi . Uso wake uliathirika kwa kiasi kikubwa na kuanza kuwa na madoa meupe na Meusi. Anataja kuwa wengine wamemfananisha na ngozi ya wanyama kama ngombe, na kudhihirisha unyanyapaa mkubwa kutoka kwa jamii kuhusu hali ya Vitiligo " wengine husema kuwa niliungua na wengine pia kusema kuwa ni ishara ya bahati mbaya maishani , Yaani kila mtu ana maoni yake kuhusu muonekano wangu " alisema Wangui Wangui anasema kuwa wakati mwingine baadhi ya watu hukataa kumsalimia kwa kuhofia kuwa akiwashika mikono yao au kuwakumbatia wataambukizwa hali anayoishi nayo. Je wataalamu wa ngozi wanasema nini kuhusu vitiligo? Grace Maria Nzomo ni Mwanamke wa miaka 26 kutoka Nairobi Kenya, anayejivunia mengi katika maisha yake hususan kwa kuwa yeye alizaliwa na ulemavu wa ngozi . text: Suala hilo limeangaziwa katika ripoti iliyowasilishwa bungeni leo Ijumaa. Zaidi ya Waganda 40,000 wanafanya kazi Oman - taifa ambalo halina makubaliano yoyote ya kibiashara. Serikali ya Uganda imekuwa ikijaribu kuwafikia raia wake ambao ni wahamiaji wanaofanya kazi Mashariki ya Kati baada ya kupokea simu za kutafuta usaidizi kutoka kwa raia hao wanaofanya kazi za ndani. Wengi wao ni wanawake ambao wamekosa nafasi ya ajira chini mwao na kuamua kutafuta kazi katika mataifa ya Uarabuni. Lakini mpango wa ajira kwa wahamiaji umekumbwa na madai ya unyanyasaji wa kingono pamoja na dhulma wanazopitia wafanyikazi wa ndani kutoka kwa waajiri wao. Wengi wao wamekuwa wakinasa kanda za video na kuzisambazwa katika mitandao ya kijamii wakiomba jamaa na marafiki wawasaidie kurudi nyumbani. Katika kisa cha hivi karibuni mwanamke wa umri wa makamo waliyekuwa akifanya kazi Jordan, alidai kuuzwa kama mtumwa kwa dola 3000. Alimpigia simu mbunge mmoja nchini Uganda ambaye baadae aliwasilisha kisa chake katika bunge la nchi hiyo. Licha ya changamoto zinazowakabili raia wake ugenini, serikali ya Uganda imesema kuwa haitasitisha mpango wa kuwapeleka watu wake kufanya kazi nje ya nchi. Madhila ya mayaya wanaotafuta kazi katika nchi za kiarabu Serikali inasema hatua yakuweka marufuku ya muda kwa mpango huo mwezi Januari mwaka 2016, ilichangia ongezeko lavisa vya ulanguzi wa binadamu. ''Kuondoa marufuku hiyo kulituwezesha kujadiliana na mataifa husika na kufikia mkataba wa kibiashara, pia ilituwezesha kuzuru mataifa hayo kubainisha kama watu wanaolalamikia visa vya unyanyasaji ni raia halisi wa Uganda. Ukweli ni kwamba tulipochunguza walikotoka watu hao nchini Oman tulibaini kuwa ni raia wa Uganda.'' aliongeza waziri huyo wa leba. Pia ameongeza kuwa wamefingua mfisi za kushughulikia amslahi ya wafanyikazi wa uganda waliopo Ughaibuni. Waziri wa leba amesema serikali inajaribu kufanya rasmi mkataba wa ajira na Oman, ili kuhakikisha haki ya Waganda wanaofanya kazi nchini humo zinalindwa. Mkataba kama huo tayari umeumetiwa saini kati ya Uganda na mataifa ya Saudi Arabia, Jordan na Falme za Kiarabu, UAE. Karibu kampuni 200 zipepewa leseni ya kuwa mawakala wa kuwatafutia kazi ng'ambo raia wa Uganda. Kampuni sita tayari zimefutiwa leseni kufuatia madai hayo ya unyanyasaja. Uganda imelezea hofu yake kuhusu hali ya raia wa nchi hiyo wanaofanya kazi Oman ikidai kuwa huenda ni wahanga ''ulanguzi'' wa binadamu. text: Lakini mwingine atasema ni yule dada niliyemuona kwenye filamu za kiswahili kutoka Tanzania, bado yupo atakaye sema yule mwenye kampuni ya kidoti, au aliyekuwa na mahusiano na Ali Kiba. Huku huyu akisema ni yule aliyekuwa anatangaza kwenye vipindi vya televisheni kama vile The one show ya TV1 na Top ten Most ya Chanel O. Ni kweli Jokate Mwegelo ni mkuu wa wilaya pekee mwenye majina ama vyeo mbali mbali nchini Tanzania. Kwa ufupi tu ni Mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti, Mwanamitindo, mfanyabiashara, mshereheshaji, mwigizaji, mwimbaji, mtangazaji wa televisheni nk. Baadhi wamekuwa wakitilia shaka uwezo wake wa kuhudumu katika wadhifa huo lakini mwenyewe anasema hilo halimnyimi usingizi. "Huwezi kunishusha chini kirahisi, najiamini sana na kile Mungu amenipa nafanyia kazi vipaji vyangu na nafanyia kazi taaluma yangu kwa nguvu zote na nina imani thabiti juu ya kile nina fanya kwa jamii yangu" Jokate anaiambia BBC Jokate Urban Mwegelo, aliteuliwa majuzi na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe iliyopo katika mkoa wa Pwani Tanzania. Ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 31. Alizaliwa Marekani mahali ambapo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi. Lakini amesoma elimu ya msingi, sekondari na chuo kikuu Tanzania. Waswahili husema nyota njema huonekana asubuhi, alikuwa kiongozi tangu sekondari. Akiwa katika shule ya Loyola Dar es Salaam Jokate Mwegelo alipata nafasi ya uongozi na kuwa Dada mkuu wa shule. Alipotoka shule akajiingiza katika maswala ya urembo. Safari yake ya urembo ndiyo iliyozaa fursa mbali mbali katika uigizaji na kupelekea kupata tunzo ya mwigizaji bora wa kike kupitia filamu ya Chumo kwenye Zanzibar International Film Festival mwaka 2011, ambapo katika mashindano hayo hayo mwaka 2014, alipata tunzo ya mwigizaji bora wa kike katika filamu za Kiswahili kupitia filamu ya Mikono salama. Mbali na uigizaji mwaka 2012 Jokate Mwegelo alifungua kampuni yake ya Kidoti Loving ambayo ina dili na bidhaa mbali mbali za urembo na hasa Nywele. Kampuni yake ilifanya vizuri sana na kuanza kuzalisha bidhaa zingine kama mabegi ya shule na ndala. Mafanikio hayo yalipelekea mwaka 2017 Jokate kupata tunzo ya malkia wa nguvu katika kipengele cha ubunifu wa biashara. Na mwaka huo huo alialitajwa kuwania tunzo ya Mjasiriamali wa mwaka katika tunzo za Africa Youth Awards. Baadhi wanajiuliza anaweza kuongoza? Jokate ana shahada ya sanaa katika sayansi ya Siasa na falsafa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Na ameingia katika siasa kupitia chama tawala akiwa mmoja wa vijana wa UVCCM. Baadaye alipata fursa ya kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM). Jokate pia alikuwa miongozi mwa wanachama 450 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Pamoja na kuchukua fomu jokate hakufanikiwa kupata fursa hiyo. Mwaka 2018 haukuanza vizuri sana katika shughuli zake za kisiasa kwani aliondolewa katika wadhfa wa kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM). Na hii ni baada ya kuwapo kwa mzozo juu ya wadhifa huo tangu alipopata fursa hiyo. Kupingwa kwake katika harakati za kisiasa si jambo geni, hasa baada Watanzania kuwa na maoni tofauti baada ya Bi Mwegelo kutangazwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe. Wapo walio mpongeza na walioona huwa hakustahili. BBC imefanya majungumzo na mkuu huyo mpya wa wilaya ya Kisarawe anasema hasumbuliwi na wanao mpinga. "Binadamu tunatofautiana sio? Wapo ambao watafikiria A na wengine watafikiria B. Hatuwezi wote tukafikiria sawa sawa, ni maoni yao nayaheshimu lakini mimi najua Jokate mwegelo ana talanta zipi ana vipaji vipi na ana record gani. Nadhani with time na wao watakuja kuelewa zaidi na watabadilisha maoni yao," anasema Jokate. Hata hivyo anaongeza kuwa ni Mungu tu ndiye anayemsaidia kumpitisha katika mapito mbali mbali ambayo ameyapitia na kumpa nguvu ya kuweza kupigana kila siku kwani akiona vijana wenzie wanavyo hangaika hujifunza na kutambua kuwa ni sehemu ya maisha. "Maisha si lelemama maisha si kwamba kila siku itakuwa ni chokoleti na pipi kuna siku zingine itakuwa tafrani, lakini ndiyo sehemu ya maisha. Wanasema hakuna mafanikio bila changamoto," anaiambia BBC. Je unadhani ni wewe pekee huamini kama Jokate ameteuliwa na Rais kuwa mkuu wa wilaya? Si wewe tu, kwani hata Jokate hakuwahi kufikiria kama anaweza kuteuliwa na Rais. Yeye alikuwa akiwaza nafasi zingine kama kuwa mwakilishi wa wananchi katika bunge lakini si nafasi hiyo ya kuteuliwa ndani ya serikali. Ataendeleza kazi yake ya uanamitindo na uigizaji? Hata hivyo Jokate amezungumza na BBC juu ya hatma ya harakati zake za uanamitindo, uigizaji na muziki. "Dhamana niliyopewa ni kubwa na imani niliyoonyeshwa ni kubwa pia, na deni ambalo inabidi nililipe ni kubwa pia. Kwa hiyo niseme tu kwamba sasa hivi kipaumbele changu ni kutumikia wananchi wa Kisarawe, mengine yote yatafwata," ameiambia BBC. Kama binti wa kike aliyekutana na vikwazo mbali mbali ikiwemo kukataliwa katika harakati za kisiasa anasema watoto wa kike wasikubali kuyumba, wajue kuna changamoto nyingi hasa ukiwa mtoto wa kike. "Wengine hawataangalia vigezo ambavyo vinakufanya uwe kiongozi, wataangalia labda urembo wako, wataangalia au unavaa mavazi ya hivi, wataangalia historia yako. Wataangalia vitu ambavyo havina maana. Wataacha kuangalia vyeti vyako vya kimasomo hivyo mabinti wawe thabiti," Jokate anasisitiza. Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu walikua wakisambaza picha zake na video zake za zamani. Hali iliyopelekea baadhi ya watu maarufu na hasa wanawake kupitia mitandao yao ya kijamii kukemea kitendo hicho. Hata hivyo siku chache zilizo pita Jokate mwegelo alifuta picha zake zote katika mtandao wake wa Instagram. "Ni mwanzo mpya na utawala mpya, ni mimi mwenyewe maamuzi yangu, kunavitu lazima uviheshimu ili uweze kufungua ukurasa mpya, Jokate ameiambia BBC. Kuwatetea wanawake Jokate ameonekana kujikiza sana na masuala ya kuwatetea na kuwahamasisha wanawake. Kipindi hiki ambacho ulimwengu unaadhimisha Wiki ya Kunyonyesha Watoto, ameandika ujumbe wa kuwahamasisha wanawake kuhakikisha wanawanyonyesha watoto wao. "Muda na njia sahihi ya kunyonyesha mtoto maziwa ya mama, humpa afya, humfanya akue vizuri. Mama anaenyonyesha ale vyakula bora, kwa afya bora ya mtoto," ameandika kwenye Twitter. "Nimewapongeza wamama wa @KisaraweMpya na wote Duniani kwa kujali afya za watoto. Karibuni Kisarawe." Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu aliandika: "Siku ya wanawake duniani haipaswi kuishia kuwa ya matamasha au kuandika matamanio yetu ya namna mambo yanavyopaswa kuwa pekee. Tufanye kidogo tulichojaaliwa na kubadilisha maisha ya mmoja-mmoja." Unaposikia jina la Jokate Mwegelo, akilini vinakuja vitu tofauti tofauti kwa kila anayemfahamu. Yupo anayemfahamu kama mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika mashindano ya urembo ya miss Tanzania mwaka 2006. text: Tangu Solskjaer apewe rasmi usukani wa kuinoa klabu hiyo mwezi Machi, Man United wameshinda mara tano tu katika mechi 18. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, anapigiwa upatu kuwa miongoni mwa makocha wawili wa ligi ya Primia waliopo kwenye hatari ya kupoteza ajira zao muda wowote pamoja Marco Silva wa Everton . "Mimi mwenyewe sina wasiwasi, kama sitajiamini mwenyewe basi dunia yote itakosa imani nami" amesema kocha huyo. United inatarajia kucheza na Arsenal usiku wa leo baada ya kupoteza mechi ya nyumbani dhidi ya Crystal Palace na ugenini dhidi ya West Ham katika msimu huu. Klabu ipo nyuma ya vinara Liverpool kwa pointi 13 na kuwa na pointi tatu tu mbele ya Aston Villa iliyopo nafasi ya 18, ambayo ndipo mstari wa kushuka daraja huchorwa. "Tulikuwa na mjadala mkubwa sana, lakini tunaamini kile tunachokifanya," alisema Solskjaer said. Mechi dhidi ya Arsenal inakuja siku chache baada ya kuondoka kwa kocha wa walinda mlango Emilio Alvarez. Alvarez, ambaye alikuwa na uhusiano mzuri wa kazi na David de Gea tokea klabu ya Atletico Madrid, alipoteza nguvu yake baada ya klabu hiyo kumleta Richard Hartis kuwa kocha mkuu wa magolikipa hivi karibuni. Hartis, alishawahi kufanya kazi klabuni hapo kwa mwongo mmoja na awali alifanya kazi na Solskjaer huko Molde na Cardiff. 'Kuna umuhimu gani kuwa na wachezaji ambao hawataki kuwa katika klabu hiyo?' Siku ya Jumanne, Makamu Mwenyekiti wa Man United Ed Woodward alisema kuwa Solskjaer atapewa muda kuweka mipango yake katika utekelezaji. Hii ikiwa inamaanisha kuwa wataendelea kuwa na Solskjaer ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo hata kama watashindwa kumaliza katika nafasi nne za juu kwa msimu wa pili mfululizo. Hata hivyo Solskjaer, haoni kama timu yake itakosa vigezo vya kushiriki michuano ya ligi kuu. "Timu mbili zilizokuwa zinaongoza zilikuwa mbali zaidi yetu," alisema. "Lakini nadhani msimu huu tutakaribia. Chelsea pia inakabiliana na changamoto kama yetu ya kujijenga. Kuna sisi ,Arsenal, Tottenham na Leicester. "Kuna timu nyingi zinataka hizo nafasi na hapo ndipo na sisi tunataka kuwa." United imehangaika sana kufunga magoli msimu huu mpaka sasa. Toka walipoifunga Chelsea goli nne katika mechi ya ufunguzi wa msimu, wameshindwa kufunga zaidi ya goli moja katika mechi saba zilizofuata. Majeraha waliyoyapata Anthony Martial na Marcus Rashford ambayo yatawafanya waukose mchezo dhidi ya Arsenal kumemfanya kinda Mason Greenwood, 17, kuwa mshambuliaji kinara wa United. Greenwood alifunga mara mbili dhidi ya Astana na Rochdale - lakini wapo wanaohoji kuwa inakuwaje mzigo huo mkubwa kupewa mchezaji wadogo na kuhoji maamuzi ya kutolewa kwa Romelu Lukaku na Alexis Sanchez kwenda Inter Milan, ambapo tayari wote wamefunga. "Rom hakutaka kubaki hapa ,kuna umuhimu gani kuwa na wachezaji ambao hawataki kuwa hapa?"amesema Solskjaer. "Kuna washambuliaji wengine wengi lakini sio hao ndio tunawahitaji. Kama washambuliaji tunaowataka wangekuepo tungewasajili". "Kuondoka kwa Rom na Alexis , sio lazima mtu uwe mwanasayansi wa roketi kuona kuwa tunatafuta ubunifu na magoli" alisema kocha huyo. Ole Gunnar Solskjaer anasisitiza kwamba yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza Manchester United, licha ya kwamba timu yake ipo alama tatu tu juu ya mstari wa kushuka daraja. text: Serikali imesema marufuku hiyo itasaidia kulinda mazingira. Juhudi za watengenezaji wa bidhaa kuomba muda zaidi kabla ya kutekelezwa kwa marufuku hiyo kortini ziligonga mwamba Ijumaa baada ya ombi la kuchelewesha marufuku hiyo kukataliwa na mahakama kuu. Yeyote anayepatikana akitengeneza, kuuza au kutumia mifuko hiyo ya plastiki anaweza kupigwa faini ya hadi dola 40,000 au kufungwa jela hadi miaka minne. Serikali imesema marufuku hiyo itasaidia kulinda mazingira. Lakini watengenezaji wa bidhaa wamesema marufuku hiyo itasababisha kupotea kwa nafasi 80,000 za kazi. Wakenya hutumia takriban mifuko 24 milioni ya plastiki kila mwezi, kwa mujibu wa takwimu za serikali. Nchi nyingine kadha za Afrika zimepiga marufuku mifuko hiyo zikiwemo Afrika Kusini, Rwanda na Eritrea. Tanzania pia imekuwa ikifanya juhudi kupiga marufuku mifuko hiyo ingawa hatua hiyo imekuwa ikiahirishwa. Mifuko ya plastiki kuwa marufuku Kenya Hili ni jaribio la tatu la kupiga marufuku mifuko hiyo nchini Kenya katika kipindi cha miaka kumi. Ingawa wengi Nairobi wamekuwa wakiunga mkono marufuku hiyo, kuna shaka kuhusu jinsi Wakenya watazoea maisha bila mifuko hiyo ambayo hutolewa bila malipo madukani wateja wanaponunua bidhaa. Serikali imekuwa ikihimiza wateja kuanza kutumia mifuko mbadala ambayo haijaundwa kwa kutumia plastiki. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Mazingira Kenya, wasafiri wanaopakiwa bidhaa walizonunua katika maduka yasiyotozwa kodi watalazimika kuiacha mifuko hiyo ya plastiki uwanja wa ndege kabla ya kuruhusiwa kuingia. Mahakama Kuu iliamua kuwa maslahi ya mazingira yanazidi maslahi ya kibiashara Serikali ilikuwa imetoa muda wa miezi sita kwa wadau kujiandaa kabla ya kuanza kutekelezwa kwa marufuku hiyo. Watengenezaji bidhaa wanaotumia mifuko ya plastiki kupakia bidhaa viwandani hata hivyo hawajaathiriwa na marufuku hiyo. Serikali ya Kenya imeanza kutekeleza marufuku ya mifuko ya plastiki nchini humo baada ya juhudi za miaka mingi za kutaka kuipiga marufuku bila mafanikio. text: Lionel Messi alimefunga jumla ya magoli 48 katika msimu wa mwaka 2017/2018 Mkwaju wa penati wa Mchezaji huyu,30 na nyota wa Barcelona haukuleta madhara mbele ya mlinda mlango Hannes Halldorsson na kufanya timu hizi mbili kutoka sare ya 1-1 Messi alikuwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema akitazama matokeo ya hasimu wake wa siku nyingi Cristiano Ronaldo hasa mabao matatu aliyoyafunga siku ya ijumaa dhidi ya Uhispania. ''Tumepata uchungu kwa kukosa alama tatu, kuanza kwa ushindi ni muhimu sana wakati wote, sasa tunapaswa kufikiria kuhusu Croatia''. ''tutajitahidi kuhakikisha hili linapita haraka''. Messi alisema mbinu ya Iceland ilifanya mchezo ukawa mgumu ''hawakutaka kucheza'' lakini alikiri kuwa walijihami kwa ''kiasi kikubwa'' Messi akipiga Penati katika mchezo ambao uliishia kwa sare ya 1-1 kati ya Iceland na Argentina Kocha wa Argentina Jorge Sampaoli alimsifu Messi namna alivyocheza katika mchezo huu mgumu ''kutathimini kazi aliyoifanya Messi ni ngumu kwa sababu haikuwa mechi nzuri kwake''. ''Iceland walicheza kwa kujihami sana, wakifunga nafasi zote lakini tulifanya kila tuwezalo ili kushinda.Leo anajitoa kwa Argentina''. ''Mara zote huwa trunakuja kushinda, ndio maana kumekuwa na hali ya taharuki''. Argentina itakabiliana na Croatia siku ya Alhamisi katika uwanja wa Nizhny Novgorod. Mlinda mlango wa Iceland Hannes Halldorsson alikuwa mchezaji nyota wa mchezo huo Mlinda mlango wa Iceland Hannes Halldorsson ameeleza jitihada alizofanya kuhakikisha anapangua mipira ya Messi. Anasema alitazama penati nyingi za Messi na kutafuta mbinu ya kuzikabili. ''Ni ndoto iliyotimia kuishinda penati, hasa kwa kuwa imetusaidia kupata alama moja ambayo ni muhimu katika kufuzu hatua ya makundi''. Lionel Messi amesema inamuumiza sana baada ya Penati yake dhidi ya Iceland kuokolewa wakati Argentina ilipokutana na Iceland. text: Rais amekutana na Bw Wafula Chebukati katika afisi ya Bw Kenyatta katika jumba la Harambee, Nairobi. Mwenyekiti huyo wa tume alikuwa amekutana na mgombea wa upinzani Bw Raila Odinga Ijumaa. Bw Odinga alijiondoa kutoka kwenye uchaguzi huo wa Alhamisi akisema hana imani uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki. Uchaguzi huo wa 26 Oktoba unaandaliwa baada ya Mahakama ya Juu kufuta uchaguzi wa kwanza uliofanyika tarehe 8 Agosti ikisema kulikuwa na kasoro nyingi. Bw Chebukati wiki iliyopita alikuwa ameitisha mkutano wa wagombea wote wa urais lakini baadaye akauahirisha na baadaye akakutana na Bw Odinga kivyake. Alidokeza kwamba anapanga kuwakutanisha Bw Odinga na Bw Kenyatta baadaye baada kukutana na rais huyo. Taarifa kutoka ikulu imesema Rais Kenyatta amemwambia mwenyekiti huyo kwamba yuko tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na hana masharti yoyote kwa tume hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Naibu Rais William Ruto pia amehudhuria mkutano huo. "Tumeweka wazi kwamba hatuna masharti wala matakwa yoyote kwa kuhusu suala hili. Tumetoa fedha za kutumiwa na IEBC kufanya kazi yake. Sasa wanafaa kfuanya kazi hiyo," amesema Rais Kenyatta. "Tunasisitiza tu kwamba uchaguzi ufanyike tarehe 26 Oktoba, huo ndio wakati uliowekwa na IEBC kwa mujibu wa matakwa yaliyoambatana na kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti." Odinga: Hakutakuwa na uchaguzi Kenya 26 Oktoba Mahakama ya Juu, kwenye uamuzi wake ilikuwa imeagiza uchaguzi mpya ufanyike kwa kufuata katiba na sheria kikamilifu katika muda wa siku 60. IEBC awali ilikuwa imetangaza uchaguzi mpya ufanyike tarehe 17 Oktoba lakini baadaye ikaahirisha tarehe hiyo hadi 26 Oktoba baada ya moja ya kampuni zilizokuwa zikitoa huduma muhimu kwa ajili ya uchaguzi huo kusema hazingekuwa tayari wakati huo. Bw Odinga amekuwa akiitaka IEBC kuahirisha uchaguzi huo na ametangaza kwamba tarehe hiyo "hakutakuwa na uchaguzi". Kumekuwa na utata kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo hasa baada ya kujiuzulu kwa mmoja wa makamishna wa tume hiyo Dkt Roselyn Akombe wiki iliyopita. Dkt Akombe alisema anaamini tume hiyo haina uwezo wa kuandaa uchaguzi huru na wa haki Alhamisi. Lakini maandalizi ya uchaguzi huo yamekuwa yakiendelea. Shehena ya kwanza ya karatasi za kupigia kura iliwasili Jumamosi na shehena nyingine inatarajiwa kufika Nairobi baadaye leo. Wakuu wa IEBC Mwenyekiti: Wafula Chebukati Naibu Mwenyekiti: Consolata Nkatha Maina Makamishna: Afisa Mkuu Mtendaji/Katibu: Ezra Chiloba Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilimtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, akiwa mbele ya mpinzani wake Raila Odinga wa muungano wa upinzani Nasa kwa zaidi ya kura 1.4 milioni. Bw Odinga alipinga matokeo hayo mahakamani na Mahakama Kuu ikaamua ulijaa kasoro nyingi na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku sitini. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) huku uchaguzi wa marudio ambao umekumbwa na utata ukiendelea kukaribia. text: Mukhtaar Roobow anayejulikana pia kama Abu Mansur Mukhtaar Roobow anayefahamika pia kama Abu Mansur, alijitoa katika kundi la Alshabaab mnamo 2012 lakini alijisalimisha kwa serikali ya Somalia mnamo Agosti mwaka jana. Atawania urais wa jimbo la ksuini magharibi mwa Somalia katika uchaguzi wa kieneo mwezi ujao. Je ni kweli Al shabaab ina mfumo bora wa kutoza kodi? Kiongozi wa zamani wa al-Shabaab ajisalimisha Somalia Mukhtar Robow amesema uamuzi huo kuingia katika siasa ni kufuatia wito wa wananchi, wafuasi wake katika jimbo hilo la kusini magharibi. Amedhihirisha kwamba yupo tayari iwapo atashinda, kuidhinisha uhusiano thabiti na serikali ya shirikisho katika mji mkuu Mogadishu, ambayo imekuwa katika mzozo na tawala za baadhi ya majimbo. Mukhtaar Roobow ni kiongozi wa juu zaidi katika kundi la al-Shabab kuwahi kujitoa kutoka kundi hilo na kujisalimisha, licha ya kuwa mojawapo ya waasisi wa kundi hilo. Mwanaume mmoja akihuzunika karibu na maiti katika eneo ambapo bomu lililipukia jijini Mogadishu Oktoba 14, 2017 Je Roobow ana nafasi gani ya kupata uongozi serikalini? Mwandishi wa BBC Bashkas Jugosdaay anasema kuna mgawanyiko. Kuna kundi linalomtazama na sura ya uovu unaotekelezwa na Alshabaab uliochangia vifo vya maelfu ya watu. Hilo ni donda ambalo daima kovu yake itasalia na kwa hivyo huenda ikawa vigumu kwake kupata uungwaji mkono kikamilifu. Na kuna upande wa pili ambao wanatazama faida inayotokana na kujisalimisha kwake na kutoa ushirikiano kwa serikali kuu ya Somalia katika kusaidia kupambana na kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu. Hivyobasi matumiani ni kwamba huenda faida ikaongezeka na pengine ndio anastahili kupata uongozi huo. Na kama anavyoeleza mwenyewe Roobow, wapo watu waliomshinikiza kuwania uongozi, pengine ndio hakikisho la uungwaji mkono wake. Mukhtaar Roobow Robow ni nani? Mnamo Juni mwaka jana , kufuatia taarifa kwamba Robow anashirikiana na serikali ya Somalia, Wizara ya mambo ya nje ilimuondoa katika orodha ya magaidi na kufutilia mbali kitita cha dola milioni 5 iliyokuwa imeahidi kwa yoyote atakayesaidia katika kukamatwa kwa Robow. Rais Mohamed Abdullahi Farmaajo Usalama bado ni mtihani mkuu kwa utawala wa Somalia Miezi michache baada ya kutwaa urais wa Somalia kutoka uwanja wa ndege kwa kuhofia mashambulio ya Al Shabaab, Mohamed Abdullahi alitoa ahadi yake kwa wananchi wa Somalia. Alisema, 'Lengo langu ni kuwashinda Al Shabaab kwa miaka miwili ijayo. Natumai kwamba tukifanya kazi pamoja, tutaleta Amani na utulivu nchini Somalia'. Congo na Somalia ni miongoni mwa nchi kumi hatari kwa wanawake Kijana Msomali afunga ndoa na wanawake wawili wakati mmoja Lakini uongozi wake umeshuhudia mashambulio, na Mogadishu ingali mojawapo wa miji hatari zaidi duniani. Je majeshi ya Somalia yako tayari kulinda usalama wa nchi hiyo? Hassan Sheikh, mchambuzi wa masuala ya usalama anasema, 'Kwa sababu ni wapiganaji, wanaweza kupenya kirahisi katika maeneo ya umma na ya kibinafsi, na wana athari kubwa katika mfumo wa jamii kisiasa, kiuchumi na kijamii. 'Muhimu zaidi ni kuwa walisababisha uoga, na uoga huu huwasaidia kwani ni vigumu sana kuwakamata au kuwashinda'. Wachanganuzi wanaamiini kuwa jinamizi la Al Shabab ni gumu kuliangamiza. Aliyekuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo wa kiislamu nchini Somalia, Alshababaab ametangaza kuwa anawania uongozi serikalini. text: Neil Gorsuch alisema hawezi kupima maamuzi aliyowahi kuyatoa kwa mujibu wa uzito Neil Gorsuch ameambia kikao cha bunge la Seneti kwamba hakuna mtu yeyote aliyemtaka kutoa ahadi kuhusu jinsi atakavyofanya maamuzi yake pindi atakapoidhinishwa kuwa jaji katika mahakama hiyo. Amesema angekataa uteuzi huo iwapo Bw Trump angemtaka kubatilisha uamuzi wa kihistoria wa mahakama katika kesi Roe v Wade ambao ulihalalisha utoaji wa mimba. Bw Gorsuch pia alishutumu vikali hatua ya Trump kuwashambulia kwa maneno majaji wa mahakama mara kwa mara na kusema "inavunja moyo". Februari, rais huyo alimweleza jaji aliyebatilisha marufuku yake ya usafiri dhidi ya raia wa nchi saba kama "mtu huyo anayeitwa jaji". Bw Gorsuch faraghani aliwaambia maseneta kwamba hilo lilikuwa na maana kwamba iwapo kungetokea shambulio la kigaidi katika ardhi ya Marekani, basi jaji huyo ndiye angekuwa lawamani. "Mtu yeyote anapokosoa uaminifu na maadili au nia ya jaji wa mahakama, hilo linavunja moyo. Nafikiri linatamausha - kwa sababu naujua ukweli," alisema. Alipoulizwa iwapo hilo linamhusu pia rais, alijibu: "Mtu yeyote ni mtu yeyote." Msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer baadaye aliandika kwenye Twitjer kwamba Bw Gorsuch alikuwa akizungumza "kwa mapana" na kwamba hakumtaja mtu kwa jina." Maandamano dhidi ya Neil Gorsuch 15 Machi Wakati wa kikao chake cha kwanza kuhojiwa na maseneta, Gorsuch, ambaye ni jaji wa Colorado aliulizwa maswali mengi kuhusu msimamo wake. Maseneta wa Democrat walisisitiza kuhusu baadhi ya mambo yenye utata, lakini alisisitiza mara kwa mara kwamba ingekuwa makosa kwake kueleza angetoa uamuzi wa aina gani katika kesi yoyote hilo. Alisema huo ungekuwa ndio "mwanzo wa mwisho" wa mahakama huru. Bw Gorsuch, amependekezwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Jaji Antonin Scalia miezi 13 iliyopita. Jaji aliyependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kujaza nafasi iliyo wazi katika Mahakama ya Juu nchini humo, amesema hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria, hata Rais Trump aliyependekeza uteuzi wake. text: Vyama vyote vikuu vya kisaiasa vimeiambia BBC kuwa wapinzani wao walihusika na kusambazwa kwa habari hizo. Rais Muhammadu Buhari, anayegombea muhula wa pili madarakani kwa tikiti ya chama cha Progressives Congress (APC), na mpinzani wake mkuu Atiku Abubakar, wa chama cha People's Democratic Party (PDP), wameshambuliwa kwenye video zilizo na taarifa za ghushi katika mitandao ya kijamii. "Kampeni za chama cha PDP zimekuwa zikitumia mbinu ya kusambaza taari za uwongo ili kuwapotosha watu," anasema Tolu Ogunlesi, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya dijitali wa rais Buhari. Vyama vyote viwili vimenasema havina ufahamu kuhusu watu wanaosambaza taarifa za uwongo ndani ya vyama vyao. "Chama cha APC kinaendesha taarifa za propaganda - kiasi cha kufanyia ukarabariti picha na maneno kufikia lengo lao," anasema Paul Ibe, mshauri wa mawasiliano wa Bw. Atiku Abubakar. Madai ambayo chama cha APC imepinga vikali huku ikiilaumu PDP kwa kusambaza taarifa za ghushi. Kitengo cha BBC Reality Check kimekusanya baadhi ya taarifa ghushi zilizotolewa dhidi ya wagombea wawili wakuu wa urais katika uchaguzi wa Nigeria. Wasichana wa Dapchi walisafirishwa hadi Abuja kwandege ya kijeshi Kutoweka kwa wasichana wa Dapchi Taarifa ghushi zilianza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii siku chache kumhusu msichana Leah Sharibu, wa miaka 15 aliyekuwa ametekwa na wanamgambo wa Boko Haram kwa kukataa kujiunga na na dini ya Kiislam Zaidi ya wasichana 100 walitekwa kutoka kijiji cha Dapchi, Kaskazini mwa Nigeria, lakini wote waliachiliwa. Taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya WhatsApp na Facebook, zilidai kuwa Leah amefariki - nalilisambaa kwa kasi sana mitandaoni. Mtu asiyejulikana na aliyedaiwa kuwa "jamaa wake" alithibitisha kifo cha msichana huyo, kwa mujibu wa taarika kwenye mitandao ya kijamii. Kujibu madai hayo serikali ilitaja kuwa ''Taarifa feki'' na bw. Ogunlesi, kutoka kampeni ya rais Buhari anasema taarifa hiyo ilitumika dhidi ya serikali. Pesa za bure? Taarifa nyingine inahusiana na madai kuwa mgombea wa upinzani Atiku Abubakar alipanga njama ya kupeana pesa na chakula katika moja ya kampeni zake. Taarifa hii iliwekwa mtandaoni na msaidizi wa rais Buhari, aliyeweka picha ya vyombo vya chakula vilivyofungwa kwa kutumia sarafu ya noti ya Nigeria katika jimbo la Sokoto. "Wafanye masikini, kisha wahonge kwa pesa - Atiku alisema hayo jana mjini," aliandika. Zifahamu changamoto kuu za Nigeria katika ramani 9 Kampeni ya Buhari imekanusha kuhusika na taarifa hiyo. Ilibainika kuwa picha hiyo ilipigwa mika miwili iliyopita katika hafla ya wakfu wa Kokun dhidi ya Njaa. Mshauri wa kampeni ya Atiku ameiambia BBC Reality Check: "Atiku hawezi kumpatia hongo mtu yeyote." Kuididimiza zaidi Nigeria? Video nyingine ni ile inayodai Atiku Abubakar amefikia mkataba na Boko Haram kwa kuwapa ardhi na mafuta. Video hiyo ilitizamwa zaidi ya mara 200,000, ilisambazwa na kundi linalojiita ''Make Nigeria Worse Again''. Lakini haina maelezo kuhusi ni lini na wapi kampeni ya Atiku ilitangaza mpango huo. Maafisa wa kampeni ya Atiku wameiambia BBC Reality Check kwamba hawana mpango wowowte kama huo - "hakuna kitu kama hicho". Buhari alipopiga kura 'dhidi ya Nigeria' Taarifa nyingine ya uwongo inayosambazwa mitandaoni ni ile inayodai kuwa Muhammadu Buhari alikuwa akiwapendelea watu wa jamii yake alipokuwa mkuu wa majeshi miaka ya 1980. Taarifa hiyo inahusiana na hatua ya bw. Buhari kutomuunga mkono mgombea wa Nigeria katika wadhifa wa katibu mkuu Muungano wa Afrika. Badala ya kuangazia kwanini aliamua kuchukua hatua hiyo, taarifa iligeuzwa kuwa alimuungha mkono mgombea wa nchi jirani ya Niger Taarifa hiyo ilipingwa vikali na msemaji wa rais, Garba Shehu. Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Nigeria zinatarajiwa kukamilika rasmi leo Alhamisi lakini mitandao ya kijamii imelaumiwa pakubwa kwa kuchangia kusambaa kwa taarifa za kughushi. text: Kwa mashabiki wa mpira Afrika Mashariki, kundi lilolomo midomoni wao zaidi ni C, na wengi yamkini wakilitazama kundi hilo kama gumu zaidi kwenye micguano hiyo. Kundi hilo linaundwa na timu jirani na hasimu za Tanzania na Kenya pamoja na timu zenye uzoefu na wachezaji wakubwa kimataifa za Senegal na Morocco. Lakini je, kundi hilo ni gumu kiuhalisia ama ni hisia tu za wapenzi wa kandanda wa Kenya na Tanzania? Kwa wafuatiliaji wa kandanda na wachambuzi, kundi hilo linaonekana kuwa ni la kawaida, huku Senehal yenye wachezaji wakubwa kama Sadio Mane na Khalidou Koulibaly na Algeria yenye wachezaji kama Riyad Mahrez zikipigiwa upatu kusonga mbele. Iwapo Tanzania na Kenya itaifunga timu yoyote kati ya hizo matokeo hayo yatachukuliwa kama ya kushangaza kwenye ulimwengu wa kandanda. Kama kundi C siyo gumu, basi kundi lipi ni gumu ama kundi la kifo kama ifahamikavyo kwenye lugha za kimichezo? Mauritania wamefuzu kwa mara ya kwanza michuano hiyo Wachambuzi wanaamini kuwa kundi D lenye timu za Ivory Coast, Morocco, Afrika Kusini na Namibia. Timu tatu katika hizo ukiacha Namibia washawahi kunyakua ubingwa wa Afcon hapo kabla. Na ukiangalia uhalisia timu ya Namibia haipigiwi upatu kupenya kwenye kundi hilo. Swali ni timu zipi mbili katika mabingwa hao wa zamani watafuzu kwa hatua ya mtoano ya michuano hiyo? Kwa mujibu wa takwimu za ubora wa timu zinazotolewa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni Fifa, Morocco ndiyo timu yenye kiwango cha juu zaidi kwenye kundi hilo ikishika nafasi ya 47 duniani, ikifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 62, Afrika Kusini nafasi ya 72 huku Namibia ikiachwa mbali katika nafasi ya 113. Je Mbwana Samatta atawika mbele ya Senegal na Algeria? Ni vyema kuwa na tahadhari lakini kuwa, si mara zote takwimu za nje ya uwanja huwa na uhalisia uwanjani. Mwaka 2012, timu ya taifa ya Zambia ambayo haikuwa wachezaji wenye majina makubwa iliushangaza ulimwengu wa kandanda kwa kuchukua kombe hilo ikiifunga kwa mikwaju ya penati timu ya Ivory Coast ambayo inatajwa kuwa ni kizazi cha dhahabu cha taifa hilo. Ivory Coast ya wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Didier Drogba, pamoja na nyota wengine kama ndungu Yaya na Kolo Toure, Solomon Kalou, Didier Zokora na Gervinho. Lakini walishindwa kuwafunga Zambia ya akina Stophira Sunzu, Christopher Katongo, Rainford Kalaba, Emmanuel Mayuka na wengineo. Kundi ambalo linaonekana kufuatia kwa ugumu ni F lenye timu za Benin, Cameroon, Ghana na Guinea Bisau. Kwa macho ya kawaida, Cameroon na Ghana wanapigiwa upatu kupita kwenye kundi hilo. Cameroon ndio mabingwa watetezi wa kombe la Afcon Cameroon ni mabingwa mara tano wa michuano huku Ghana wameshinda mara nne kombe hilo. Hata hivyo timu zote za kundi hilozinatokea katika ukanda wa Afrika Magharibi na zinajuana vilivyo katika sampuli zao za uchezaji. Kundi A pia linaonekana jepesi kwa mwenyeji wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Misri ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo. Hata hivyo kutakuwa na kipute kigumu si haba baina ya mataifa ya DRC, Zimbabwe na Uganda. Yote kwa yote, hesabu za makundi zitatimia pale michezo hiyo itakapoanza kutimua vumbi Ijumaa. Si ajabu Kenya ama Tanzania zikafuata nyayo za Zambia katika kuangusha timu kubwa kama ilivyotokea mwaka 2012. Zimesalia siku tatu pekee kabla ya michuano ya kandanda ya Mataifa ya Afrika kuanza nchini Misri - lakini swali swali ni, lipi kundi gumu zaidi kati ya sita yaliyopo? text: Kwa muda mrefu sasa amekuwa akionyesha hisia zake wazi wazi za kumsifu Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter na mahojiano mbali mbali. Hata hivyo amekuwa akiwakosoa wanaomkemea kwa kuwataka wamwache awe na uhuru wa mawazo yake. Kanye West alialikwa katika ikulu ya Marekani kwa ajili ya chakula cha mchana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mageuzi katika magereza, ajira na masuala ya wamarekani weusi. Ni mjadala uliojaa vioja vingi kutokana na ukweli kwamba Trump na Kanye wote ni wazungumzaji sana na hutumia zaidi mtandao kuweka wazi hisia zao. Hata hivyo uongeaji wa Kanye West pia ulitengeneza habari. Katika majadiliano hayo yaliyolenga siasa, mageuzi na uzalishaji, West alinukuliwa akisema "wamejaribu kunitisha, marafiki zangu kuhusu kuvaa hii kofia, lakini hii kofia inanipa nguvu". Kanye West aliweka wazi hisia zake za kumkubali sana Rais wa Marekani Kanye alienda mbali zaidi na kusema kofia hiyo iliyoandikwa "Make America great again" maneno yanayowakilisha kauli mbiu ya utawala wa donald Trump inamfanya anajionea fahari sana na anajiona kama Superman na aliongeza kuwa Trump ametengeneza kofia shujaa kwa ajili yake. Hata hivyo kauli za Kanye hazikupokelewa vizuri na baadhi ya watu Shule hazivutii Hata hivyo alitoa hoja zake mbali mbali ikiwemo kwa sasa shule zina upweke zaidi na sio kama simu "Mara nyingine watu wanasema mtoto huyu hana uwezo wa kusikiliza kwa makini, Hauna huo ugonjwa, shule imejaa upweke, sio ya kufurahisha kama hii," anasema Kanye huku akionyesha simu yake ya mkononi. Pia alimtaka Rais Trump ajenge viwanda katika mji alipozaliwa wa Chicago na alimpongeza Donald kwa kufanikiwa kusimamisha vita na Korea kaskazini. "Umesitisha vita, tumetatua tatizo letu kubwa zaidi," Kanye alimwambia Trump. Taarifa za Kanye kukutana na Trump zilisambaa sana huku zikiwa zimeambatana na video mbalimbali zinazo mwonyesha Kanye akimkumbatia Rais huyo wa marekani. Lakini pia baadhi ya video hizo zimemwonyesha akiwa katika mazungumzo ambapo alisikika akimsifia sana Rais huyo wa Marekani kuwa anampenda. Hata hivyo mkutano huo umekuwa gumzo mtandaoni huku watu mbali mbali wakionyesha kukerwa na kitendo cha Kanye West kukutana na Trump lakini pia maneno aliyozungumza. Baadhi ya wasanii maarufu ambao awali pia walikuwa ni marafiki wa Kanye west wameonyesha kukerwa na kitendo hicho cha Kanye. Huku baadhi wakitamka wazi wazi kuwa Kanye anaitia aibu jamii ya wamarekani weusi. Kupitia kurasa mbali mbali za mitandao ya kijamii, wasanii hao wamerusha madongo yao wazi wazi akiwemo P. Didy, TI, 50 Cent na wengine wengi. Hii ni mara ya kwanza kwa Kanye West kutembelea Ikulu ya Marekani Kanye West aliwahi kumtembelea Donald Trump huko Manhattan mwaka 2016 mwezi mmoja baada ya Trump kushinda, lakini hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutembelea ikulu ya Marekani. Mke wake Kim Kardahian amewahi kwenda mara mbili katika Ikulu hiyo maarufu kama White House. Si jambo la kushangaza kusikia Kanye West mmoja kati ya wasanii maarufu zaidi duniani katika miondoko ya kufoka foka amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump. text: Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9. Hii inafuata ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Jumapili ilioanguaka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157. Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800. Hatahivyo, huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa. Ndege kama hiyo ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189. Katika taarifa rasmi iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter ya mkurugenzi mkuu katika shirika hilo la usafiri wa ndege Rwanda, Silas Udahemuka, RCAA limesema kwamba marufuku hiyo imeanza kufanya kazi mara moja. "Shirika la usafiri wa ndege Rwanda kwa uwezo uliopewa katika kifungu cha 16 cha sheria za usafiri wa ndege nchini inaagiza marubani na kampuni za ndege zinazohudumu ndege za Boeing 737 - 8 Max na Boeing 737 - 9 Max, zisiendeshe usafiri wowote wa ndege hizo katika anga ya Rwanda mara moja," inasema taarifa hiyo. Marekani ni nchi ya hivi karibuni kusitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo. Boeing 737 Max yasitisha matumizi ya ndege aina hiyo 'hadi angalau Mei' Ndege zote za Boeing 737 Max 8 na 9 zimepigwa marufuku kuhudumu hadi angalau Mei baada ya ajali hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia, Shirika la kitaifa la usafiri wa ndege nchini Marekani (FAA) limesema. Ndege hizo hazitohudumu hadi mfumo wake wa uhudumu uimarishwe na uidhinishwe, FAA limesema. Mkasa huo wa ndege nje kidogo ya mji mkuu Addis ulisababisha vifo vya watu 157 kutoka mataifa 35. Ni ajali ya pili ya aina hiyo ya ndege ya 737 Max katika muda wa miezi mitano. Baadhi ya watu wamegusia ufanano wa mikasa hiyo, huku baadhi ya wataalamu wakitaja data ya satelaiti na ushahidi kutoka eneo la mkasa kuonyesha uhusiano wa ajali ya ndege ya Ethiopia na ile ya iliyotokea Indonesia ya Lion Air mwaka jana. Maafisa wanasema ni shughuli inayohitaji umakini mkubwa Wachunguzi nchini Ufaransa wamepokea jukumu la kisanduku kinachonakili data ya safari hiyo ya ndege maarufu 'black boxes' wakijaribu kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo ya Boeing 737 Max. Huenda ikachukua muda kupata data ya awali, lakini mengi itategemea hali ya kisanduku hicho. Shirika la usafiri wa ndege Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 ana 9 katika anga ya Rwanda. text: Endapo Uganda itashinda mchezo huo, itaandika historia ya pili katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon). Siku ya Jumamosi Uganda iliandika historia kwa kushinda mchezo wake wa kwanza wa Afcon, ikiwaadhibu jirani zao DR Congo goli 2-0. Mwaka 2017 Uganda ilishiriki Afcon lakini ilishindwa kuandika ushindi walau kwenye mchezo mmoja. Leo hii wanavaana na Zimbabwe, Uganda wanahitaji ushindi kwa hali na mali ili wafuzu moja kwa moja hatua ya mtoano. Katika mechi ya kwanza dhidi ya DRC Uganda hawakupigiwa sana upatu kuondoka na ushindi. DRC kwa takwimu za ubora wa viwango ipo juu ya Uganda, ina wachezaji wenye uzoefu zaidi na ni mabingwa mara mbili wa kombe hilo. Lakini magoli ya Patrick Kaddu katika dakika ya 14 na Emmanuel Okwi katika dakika ya 48 yalitosha kuzamisha jahazi la DRC. Wenyeji Misri pia wapo kwenye Kundi A, na mchezo wa kwanza walipata ushindi mwembamba wa goli moja dhidi ya Zimbabwe. Japo Zimbabwe wanaonekana ni vibonde katika kundi hilo, kufungwa goli moja na wenyeji Misri inaonesha kuwa si timu ya kubeza. Tayari kocha wa Uganda, Sebastien Desabre amekanusha kuidharau Zimbabwe na kusema anatarajia mchezo mgunu hii leo. Kwa Uganda, wakishindwa kupata ushindi, walau sare itawafaa katika kujiimarisha na hesabu za kufuzu kwa hatua ya mtoano. Katika mpambano mwengine hii leo, wenyeji Misri watacheza na DRC. Mchezo huo utapigwa kuanzia saa tano usiku. Misri, itataka kuonesha kiwango bora zaidi kulinganisha na mechi dhidi ya Zimbabwe, na kupata ushindi utakaowavusha mpaka hatua ya mtoano. DRC wao wanataka kuonesha kuwa bado ni timu nzuri ambayo kwa kiwango chao hawawezi kufungwa mechi mbili mfululizo. Uganda inashuka dimbani saa mbili usiku wa leo dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa pili wa Kundi A. text: Meli hiyo iliondoka Gibraltar siku ya Ijumaa Naibu waziri wa maswala ya kigeni Miltidias Varvitsiotis aliambia chombo cha habari cha ANT 1 kwamba taifa lake haliko tayari kuisaidia Meli hiyo inayodaiwa kuelekea Syria. Hatua hiyo inajiri baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo kutishia vikwazo dhidi ya taifa lolote ambalo litaisaidia meli hiyo. Adrian Darya 1 iliondoka Gibraltar siku ya Jumapili na kusema kwamba inaelekea katika bandari ya Ugiriki ya Kalamata. Mamlaka katika taifa hilo linalomilikiwa na Uingereza iliizuia meli hiyo mwezi Julai. Awali ilijulikana kama Grace 1. Licha ya ombi la dakika za mwisho la Marekani , Gibraltar iliiwachilia meli hiyo siku ya Ijumaa na meli hiyo ikaondoka na kuelekea mashariki mwa bahari ya Mediterenea. Iran ilinukuliwa ikisema kwamba iko tayari kutuma wanamaji wake ili kuisindikiza meli hiyo na sasa iko kaskazini mwa bandari ya Algeria ya Oran. Je Ugiriki imesemaje? Kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo, bwana Varvitsiotis alithibitisha kwamba Marekani imeitaka kutoisaidia meli hiyo. Iran haijawasiliana na serikali ya Ugiriki, alisema. Hatahivyo meli hyo ya Adrian 1 ambayo inabeba mapipa milioni 2 ya mafuta ghafi ni kubwa mno kwa bandari yoyote ya Ugiriki kuiegesha, alisema bwana Varvitsiotis. Alipoulizwa je Ugiriki itachukua hatua gani iwapo meli hiyo itaegesha katika maji ya taifa hilo, alijibu iwapo hilo litatokea tutaona la kufanya. Marekani inaamini Adrian Darya-1 ina uhusiano na jeshi la Iran la Revolutionary Guard - tawi la jeshi la taifa hilo ambalo limetajwa kuwa kundi la kigaidi na Marekani. ''Tunataka kuwanyima njia za kuendeleza kampeni yao ya ugaidi'' , bwana Pompeo aliambia maripota. ''Tumesema wazi kwamba mtu yeyote atakayeisaidia , yeyote atakayeiruhusu kuegesha katika bandari yake atakuwa katika hatari ya kupokea vikwazo vya Marekani'', alisema akiongezea Marekani itachukua hatua inayoweza kuizuia meli hiyo kuwasili Syria. Je meli hiyo inaelekea wapi? Adrian Darya-1 bado imesema kwamba inaelekea katika bandari ya Kalamata Samir Madani, mwanzilishi wa tovuti ya maswala ya baharini TankerTrackers.com, ameambia BBC kwaba meli hiyo ilikuwa inajaribu kurudi nyumbani kupitia rasi ya Suez Canal. Italazimika kupakua mapipa milioni moja kwa meli nyengine ambayo itakuwa ikipeperusha bendera ya Iran kwa kuwa meli hiyo imebeba uzani mkubwa, alisema. Kuelekea Syria pia itakuwa vigumu kwa kuwa imebeba mafuta mengi mno kupakua bila usaidizi katika bandari ya Baniyas. Meli hiyo ilichukua njia ya mviringo kuelekea Mediterrenia , ikisafiri kwa kuizunguka Afrika badala ya kuchukua njia fupi ya rasi ya Suez canal. ''Sio lazima wazunguke njia yote hiyo ili kuwasili Syria'', alisema bwana madani. Wachanganuzi wanaamini kwamba meli hiyo inaelekea katika maji ya Syria kama eneo salama , na kutokea hapo watapakua mafuta kwa meli ndogo ndogo kupeleka katika maeneo ya Meditereania. Inaweza kuwa wanunuzi wa kusini mwa Ulaya kwa mfano , alisema. Je kuna mgogoro gani wa meli hiyo ya mafuta? Meli hiyo na wafanyakazi wake 29 kutoka India, Urusi, Latvia na Ufilipino ilikamatwa na wanamaji wa Uingereza tarehe 4 mwezi Julai baada ya serikali ya Gibraltar - eneo linalomilikiwa na Uingereza kusema kwamba inaelekea Syria swala ambalo ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya. Hatua hiyo ilizua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Iran ambao uliendelea kwa wiki kadhaa huku nayo Iran ikilipiza kisasi kwa kuikamata meli ya Sweden iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza Stena Impero katika Ghuba. Stena Impero bado ipo katika maji ya Iran ikiendeleza kuzuiliwa. Kumekuwa na uvumi kwamba meli hiyo itaachiliwa iwapo Adria Darya itaachiliwa licha ya maafisa kukana habari hizo. Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni alisema siku ya Jumatatu kwamba walikuwa wakisubiri agizo la mahakama kabla ya meli hiyo kuachiliwa lakini wakasema kwamba hakuna uhusiano wowote wa meli hizo mbili. Greece imekataa kuisaidia meli ya mafuta ya Iran ambayo hivi majuzi ilizuiliwa Gibraltar kwa tuhuma ya kusafirisha mafuta kuelekea Syria. text: Rais Trump akiwa ziarani Uingereza Ameliambia gazeti la Sun kuwa mpango wa huo wa waziri mkuu utaua mipango ya kibiashara ya Uingereza na Marekani,ambapo lengo la Marekani ni kufanya biashara na Uingereza pekee bila kuhusisha umoja wa Ulaya,na ameongeza kuwa Uingereza inapaswa kutoshirikiana kabisa na umoja huo ili kuweza kuiamini na kushirikiana nayo kibiashara. Bi.Theresa May amekuwa akijitahidi kutumia ziara hii ya kwanza ya Trump kumshawishi biahsra huru kati ya mataifa hayo mawili akisisitiza kwamba suala kujiotoa katika umoja wa Ulaya ni fursa ya kukukuza uchumi wa Marekani na Uingereza. Katika hatua nyingine rais Trump amemsifia aliyekuwa waziri wa mambo wa nje alijiuzuru Boris Johnson na kudai kuwa anafaa hata kuwa waziri mkuu lakini wamempoteza. Ameongeza kuwa kile kinachoendelea kwa sasa katika Uingereza kujitoa katika umoja huo wa Ulaya ni tofauti kabisa na kile kilichopigiwa kura na wananchi. Trump amesema kuwa alimshauri Bi.May njia nzuri ya kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya lakini hakumsikiliza,hatuwezi kuwa tayari kuwa na mashirikiano ambayo ndani yake kuna umoja wa Ulaya. Mhariri wa BBC wa masuala ya siasa Laura Kuenssberg, amesema kauli hii ya Trump inatupilia mbali madai ya Bi May ambaye amekuwa akisema Uingereza bado inaweza kuwa na makubaliano imara ya kibiashara na dunia pamoja na kuwa na ushirikiano kwa namna moja na umoja wa Ulaya. Rais Trump akiwa na mwenyeji wake Bi Theresa May. Naye mbunge kutoka chama cha Labour Phil Wilson, anayeunga mkono kura ya wananchi kujitoa katika umoja huo amesema maoni ya rais Trump yanaonyesha wazimpango wa waziri mkuu Bi Theresa unazidi kuonekana mbaya mbaya kila kukicha. Leo siku ya ijumaa Bi May na Trump watakwenda makao makuu ya kijeshi kushuhudia mazoezi ya pamoja ya kikosi maalumu cha kukabiliana na ugaidi kinachoundwa na muungano wa Marekani na Uingereza. Rais Donald Trump amesema Uingereza huenda haitapata mikataba ya kibiashara na Marekani iwapo itaendelea mpango wake wa kwa mfumo wa sasa juu ya namna ya kujitenga na Umoja wa Ulaya. text: Katika umri wa miaka 37 Jacinda Ardern anataraji kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini New Zealand Bi Ardern amekuwa kiongozi wa upinzani kwa miezi mitatu sasa. Katika umri wa miaka 37 anataraji kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini New Zealand tangu mwaka 1856. Chama chake cha Lebour kilichukua nafasi ya pili mwezi Septemba ambapo hakuna chama kiliweza kupata wingi wa kura. Sasa kinatarajiwa kuingia madarakani baada ya chama kidogo cha New Zealand First party kukubali kujiunga na serikali. Muungano huo mpya pia utaungwa mkono na chama cha Green Party. Katika umri wa miaka 37 Jacinda Ardern anataraji kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini New Zealand Jacinda Arden tayari ameonyesha kuwa anaweza kufanya kampeno nzuri na kufanya mikataba ya kisiasa lakini bado anakabiliwa na chamgamoto mpya. Kwanza ni kuwashawishi watu nchini New Zealand ambao hawakumpigia kura kuwa chama hicho ambacho kilichukua nafasi ya pili kitaongoza. Pia kuna uhusiano wa kujengwa na serikali ya Australia ambayo ilikilaumu chama cha New Zealand Labour party kwa upinzani dhidi yao wakati wa suala ya uraia mara mbili. New Zealand inajiandaa kwa serikali ya Muungano ambayo itaongozwa na kiongozi wa chama cha Labour, Jacinda Ardern text: Wanaakiolojia hao wanakadiria kwamba mji huo ulikuwepo kuanzia karne ya 10 na ulikuwa kitovu cha biashara katika eneo hilo. Kugunduliwa kwa mabaki ya mji huo wa Harlaa kumefichua kuwepo kwa vitu, bidhaa na vifaa kutoka maeneo ya mbali kama vile Misri, India na China. Miongoni mwa vitu vilivyogunduliwa eneo hilo ni msikiti ambao inakadiriwa ulijengwa karne ya 12, pamoja na makaburi ambayo yalitumiwa na Waislamu waliokuwa wanaishi eneo hilo. Mwanaakiolojia mkuu anasema muundo wa msikiti huo unafanana sana na misikiti iliyogunduliwa kusini mwa Tanzania na maeneo ya Somaliland, na ni ishara kwamba kulikuwa na uhusiano na mawasiliano kati ya jamii za Waislamu barani Afrika. Wataalamu hao pia wamegundua sarafu za fedha na shaba za karne ya 13 kutoka Misri, pamoja na vito kutoka Madagascar, Maldives, Yemen na China. Wakulima katika eneo hilo wamekuwa wakipata vitu vya ajabu, vikiwemo sarafu kutoka China katika mashamba yao, jambo ambalo lilichangia kuenea kwa dhana kwamba eneo hilo huenda lilikuwa makao ya majitu. Wanakiolojia hao hata hivyo wanasema hawakupata ushahidi wowote kwamba kulikuwa na majitu eneo hilo. Kumepatikana pia vito na mapambo kutoka maeneo ya mbali Watachimbua zaidi na kutafiti katika eneo hilo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao. Watachunguza pia mabaki ya miili ya watu 300 iliyozikwa katika makaburi yaliyogunduliwa, kubaini walikuwa wanala nini walipokuwa hai. Vitu vilivyofukuliwa kutoka eneo hilo vitawekwa katika kituo cha turathi eneo hilo na katika makavazi ya taifa mjini Addis Ababa. Kumepatikana pia vyungu Wataalamu wa mambo ya kale wamegundua mabaki ya mji wa kale ambao ulikuwa umesahaulika mashariki mwa Ethiopia. text: Jumba la kumbukumbu za Wamarekani weusi lafunguliwa Marekani Obama amesema kuwa jumba hilo la utamaduni na historia ya Wamarekani weusi litatoa historia ya Marekani ambayo haijatambuliwa na wengi. Mtindo wa Jumba hilo ulichorwa na raia wa Uingereza David Adjaye. Huku baadhi ya vitu vilivyopo katika jumba hilo vikionyesha wakati wa utumwa, vyengine vinaonyesha utamaduni wa watu weusi ambao umeingia katika utamaduni wa Marekani. Wanaharakati wa haki za watu weusi nchini Marekani walipendekeza kujengwa kwa jumba hilo mwaka 1915. Rais wa Marekani Barrack Obama amefungua rasmi jumba la kumbukumbu za Wamarekani-weusi mjini Washington DC. text: Waliongoza kikundi kilichofahamika kama 'Panya Road' kilichotikisa Jiji la Dar es salaam kwa uhalifu. Lakini leo wameamua kuachana na vitendo vya uhalifu kwa hiari na kuanzisha kijiwe chao cha kuosha magari na kupata fedha za kuendesha familia zao. Salum Kilango ni miongoni mwa vijana hao zaidi ya 30. Yusuph Mazimu amemtembelea anapofanya shughuli na wenzake, katika eneo la Gongolamboto kando kando ya jiji la Dar es salaam Kilango,anasimulia jinsi alivyoishi maisha ya hatari alipokuwa akijihusisha na uhalifu Ilikua ama zake ama za anayemkaba na kumuibia. Kwa zaidi ya miaka 10, yeye na wenzake walikua wahalifu wa kuogopwa na jamii, lakini sasa ametubu: ''Baada ya kukutana na wenzangu majanga yaliyowakuta watu waliochomwa na moto waliingia jela kwa kweli ilinibidi ninyooshe mikono juu''. Anaeleza Kilango. Kilango hivi sasa anafanya shughuli mbalimbali za kijamii katika mtaa anaoishi kwake na hata majirani zake ikiwa ni njia ya kurejesha uaminifu katika jamii yake ambayo ilikuwa ikimtenga au kumuogopa kutokana na historia ya maisha yake aliyoyaishi hapo kabla. Vijana wameamua kujiajiri kujikimu na familia zao ''Sehemu nyingine napata ajira lakini nashindwa kuaminika na jamii kutokana na sura yangu, wale wote, jamii iliyokuwa pale mimi sifanani nao''. Alieleza Kilango Lakini kutokana na changamoto ya ajira vijana kama Kilango wapatao 30 wameanzisha biashara ya kuosha magari, kazi ambayo huwapatia kipato si haba kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya familia zao. Uhasama na Polisi haupo tena kwani ni sehemu ya wateja wao, anaeleza mmoja wa vijana hao. ''Hapa tupo kwa ajili ya kutafuta pesa, tunaaminika hata polisi wanatuachia magari yao tunaosha kuna vitu kama simu Flashi na vitu vingine vya thamani''. Hivi sasa vijana hawa wanafanya kila jitihada kurejesha uaminifu kwa jamii yao Bi Maryam ni mke wa Kilango, yeye alifichwa na mumewe kuhusu kazi anayofanya, alikuwa mtu wa kusikia mtaani tu, lakini kwa sasa ni familia moja yenye watoto wawili na yenye furaha sana. ''Mwanzoni sikujua lakini baadae tulipozoeana nikajua shughuli zake nikachukulia kawaida tu, nilikuwa na wasiwasi mwanzoni kutokana na maisha tuliyokuwa tunaishi, lakini kwa sababu nilimpenda nilichukulia kawaida. Kujikwaa si kuanguka, Swali hapa ukianguka unachukua hatua gani? Miaka 3 mpaka 10 iliyopita walikua vijana hatari, waliokuwa na uwezo wa kufanya uhalifu wowote, bila woga; kama kuiba, kukaba, kupora mpaka kuua. text: Mradi huo unafadhiliwa na mkopo wa dola bilioni 17 kutoka Japan na utatoa huduma kati ya miji ya Ahmedabad na Mumbai. Mradi huo unafadhiliwa kwa mkopo wa dola bilioni 17 kutoka Japan na utatoa huduma kati ya miji ya Ahmedabad na Mumbai. Wakati mradi huo utaanza kutoa huduma katika kipindi cha miaka mitano, safari ya kilomita 500 inatarajiwa kupunguzwa hadi masaa matatu kutoka masaa manane ya kawaida. Bw. Abe anafanya ziara ya siku mbili nchini India ambayo ni mshirika mkuu wa Japan. Japan ndiye mwanzilishi wa treni za mwendo kasi "Rafiki yangu waziri mkuu Narendra Modi ni kiongozi mwenye kuona mbali. Alifanya uamuzi miaka miwili iliyopita kuleta treni ya mwendo kasi nchini India na kujenga India mpya," alisema baada ya kuweka jiwe la msingi leo Alhamisi. "Nina matumani ya kufurahia mandhari mazuri ya India kupitia kw\ madirisha ya treni wakati nitarudi hapa miaka michache inayokuja". Treni hiyo ya viti 750 inatarajiwa kuanza kuhudumua kuanzia Agosti mwaka 2022. Mifumo ya usafiri wa treni nchini India husafirisha zaidi ya watu milioni 22 kwa siku na baadhi ya treni zimepitwa na wakati hali ambayo huchangia ajali za mara kwa mara. Mifumo ya usafiri wa treni nchini India husafirisha zaidi ya watu milioni 22 kwa siku na baadhi ya treni zimepitwa na wakati hali ambayo huchangia ajali za mara kwa mara Waziri mkuu wa Japan shinzo Abe amezindu mradi wa kujengwa kwa treni ya kwanza ya mwendo kasi katika jimbo la nyumbani mwa waziri mkuu wa wa India Narendra Modi la Gujarat. text: Rais Trump alianza kurejesha vikwazo dhidi ya Iran tangu mwezi Mei Ikulu ya Marekani imesema "hivi ni vikwazo vigumu kuwahi kuwekwa na utawala huu" dhidi ya Tehran. Inalenga Iran na mataifa yanayofanya biashara na Iran Hata hivyo, mataifa manane yamepewa muda mfupi kuendelea kuingiza mafuta kutoka Iran. Mataifa ya bara ulaya yanayounga mkono mkataba huo wa nuklia yamesema yatalinda kapuni za ulaya zinzaofanya biashara ''halali"na Iran. Rais DonaldTrump alijiondoa kutoka kwa mkataba wa wa nuklia wa Iran mwezi Mei, na kutaja makubaliano hayo ya kupunguza shughuli za kinyukila za Iran uliofakiwa mwaka 2015 kama mbaya zaidi kuwahi kuafikiwa. Siku ya Ijumaa Trump aliandika katika mtando wake wa Twitter akisema "Vikwazo vinakuja," Marekani imekuwa ikiregesha pole pole vikwazo dhidi ya Iran, lakini hatua hii ya sasa ni muhimu kwa sababu inalenga sekta kuu ya uchumi wa Iran. Makubaliano ya awali yaliifanya Iran kupunguza shughuli zake tata za nuklia ili vikwazo dhidi yake vilegezwe. Barack Obama, rais wa Marekani wakati huo, alihoji makubaliano hayo yalilenga kuzuia Iran kusitisha uundaji wa silaha za nuklia. Uingereza, Ufaransa, Ujerumani Urusi na Uchina pia ziliunga mkono mkataba huo wa nyuklia wa Iran na kuendelea kuudumisha. Kwa nini Marekani ikajiondoa? Rais Donald Trump alitangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia wa Iran mwezi Mei na kuuita mpango uliooza na kero kwa raia wote wa Marekani. Alisema mpango huo unaifaidi tu na kuiongeza nguvu Iran. Hatua gani zitachukulia? Vikwazo hivyo Marekani dhidi ya Iran vitaanza kutekelezwa tena kuanzia Jumatatu Novemba 5, na vitakuwa na athari kwa sekta ya kawi na ile ya uchukuzi wa majini nchini Iran bila kusahau bishara ya mafuta, na biashara kati ya taasisi za kifedha za kigeni na benki kuu ya Iran.usafiri wa meli, fedha na nishati. Sekta ya mafuta ya Iran inakabiliwa na vikwazo vipya Iran imejibu vipi hatua hiii mpya ya Marekani? Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran,Bahram Qasemi amekiambia kituo cha kitaifa cha runinga ya nchi hiyo kwamba ''tuna habari kuhusiana na vikwazo hivyo lakini tuna uwezo wa kukabiliana na masuala ya kiuchumi ya taifa letu'' Alisema kuwa''hakuna uwezekano''wa Marekani ''kufikia malengo yake ya kisiasa kupitia vikwazo kama hivyo'' Vikwazo hivyo ni vipi? Bwana Trump alitia saini agizo kuu ambalo lilirudisha vikwazo dhidi ya taifa hilo siku ya Jumanne. Vikwazo hivyo vinalenga: Ununuzi wa noti za Marekani unaofanywa na Iran. Biashara ya dhahabu na vyuma vingine Graphite, aluminium, chuma, mkaa na programu zinazotumiwa katika sekta ya viwanda Ubadilishanaji wa fedha unaohusishwa na sarafu ya Iran Vitendo vinavyohusishwa na ulipaji madeni ya Iran Utawala wa Trump umerejesha vikwazo vyote vya Marekani vilivyokuwa vimeondolewa chini ya mkataba wa nuklia uliyofikiwa mwaka 2015. text: Machafuko nchini Burundi yalizidi mwezi Mei mwaka 2015 baada ya kutokea jaribio la mapinduzi ya serikali Eloge Willy Kaneza na wanahabari wenzake walipata njia bora za kukabiliana na ukandamizaji kwa kutumia mfumo ya teknolojia za kimitandao, waandalizi wa tuzo za Peter Mackler za wanahabari wakakamavu na wenye maadili walisema. Bw Kaneza Eloge,34, ni kioo cha muungano wa wanahabari wa SOS nchini Burundi, uliobuniwa baada ya vituo vingi vya habari kufungwa mwezi Mei mwaka 2015 baada ya kutekelezwa kwa jaribio la mapinduzi ya serikali ya Rais Pierre Nkurunziza. Wanahabari hao walitumia simu za rununu aina ya Smartphone, na kufanya kazi katika hali ngumu ili kuwa chombo cha habari kwa raia waliokuwa ndani na nje ya Burundi, waandalizi walisema. Mwanahabari wa Burundi ameshinda tuzo la kimataifa la kwa kuwa mwanahabari mkakamavu na jasiri. text: Kutangazwa kwa hali ya dharura kumechangia maandamano Kesi hiyo imewasilishwa katika mahakama ya wilaya ya kaskazini katika jimbo la California. Inajiri siku kadhaa baada ya Trump kuidhinisha hali ya dharura, inayompa nguvu kulivuka bunge na kujipatia fedha kwa ujenzi huo - ambayo ni ahadi kubwa aliyotoa wakati wa kampeni yake. Democrats wameapa kupinga hatua hiyo "kwa kutumia njia zozote zilizopo". Mkuu wa sheria katika jimbo hilo la California Xavier Becerra amesema wanampeleka Trump mahakamani "kuzuia matumizi mabaya ya nguvu za rais". "Tunamshtaki Trump kumzuia dhidi ya kuiba pesa za mlipa ushuru, zilizotengwa kisheria na bunge kwa watu wa majimbo yetu. Kwa wengi wetu, ofisi ya rais sio eneo la vioja ," aliongeza Kesi hiyo iliyowasilishwa Jumatatu inaanza kwa kusikizwa awali ombi la kutaka kumzuia Trump ashughulikie dharura hiyo aliyoitangaza, wakati kesi ikiendelea kotini, gazeti la Washington Post linaripoti. Ukuta huo wa Trump unaarifiwa utakuwa na paneli za kunasa miale ya jua ili kutengeza kawi ya bei rahisi Trump alitangaza mpango huo baada ya bunge kukataa kufadhili ujenzi wa ukuta. Kesi ya kwanza iliwasilishwa mara moja siku ya Ijumaa. Kundi la kutetea haki, Public Citizen, liliwasilisha kesi kwa niaba ya hifadhi asili, na wamiliki watatu wa ardhi katika jimbo la Texas ambao wamearifiwa huenda ukuta huo ukajengwa kwenye ardhi yao. Trump alitangaza vipi hali hiyo ya dharura? Akitoa tangazo hilo katika ikulu ya White House siku ya Ijumaa, rais amesema hali hiyo itaruhusu kupata takriban dola bilioni 8 kwa ujenzi wa ukuta huo wa mpakani. Hiki ni kiwango kilicho chini ya gharama ya jumla ya dola bilioni 23 zinazohitajika kujenga ukuta huo wenye urefu wa maili 2000 wa mpakani. Trump alikubali kwamba angeshtakiwa kwa hatua hiyo, na alitabiri kwamba kutangaza kwa hali hiyo ya dharura kutasababisha hatua za kisheria ambazo zina uwezekano mkubwa kuishia katika mahakama ya juu zaidi. "Tutakabiliana na mzozo wa usalama wa kiatiafa katika mpaka wetu wa kusini ," alisema. "Kila mtu anafahamu kwamba ukuta unafanya kazi." Hatahivyo, rais pia alisema kwamba hana haja ya kutangaza hali ya dharura lakini alifanya hivyo kutokana na matumaini ya kupata fedha kwa haraka zaidi, lakini wachambuzi wanasema kauli hii huenda ikamtia mashakani katika kujitetea kisheria. Kumeshuhudiwa maandamano ya kupinga azma hiyo ya Trump kujenga ukuta mpakani Dharura ya kitaifa ni nini? Sheria ya hali ya dharura ya kitaifa imenuiwa kwa nyakati ambapo kunashuhudiwa majanga ya kitaifa. Trump amebaini kwamba kuna janga la uhamiaji katika mpaka wa kusini wa taifa hilo - tuhuma inayopingwa pakubwa na wataalamu wa uhamiaji. Idadi kubwa ya wahamiaji wanaoingia Marekani kila mwaka ni wale wanaoishi nchini baada ya viza zao kumalizika muda. Kutangaza hali ya dharura kutampa nguvu maalum rais ambazo zitamruhusu kuuvuka mpangilio wa kisiasa, na ataweza kuelekeza fedha kutoka kwenye ufadhili wa sasa kwa jeshi, au bajeti ya kukabiliana na majanga ili kuulipia ujenzi wa ukuta huo. Kwa mara nyingi katika tawala zilizopita, hali hiyo ya dharura iliidhinishwa kukabiliana na mzozo wa sera za kigeni - ikiwemo kuzuia ugaidi - mashirika yanayohusishwa kuzuia kupokea ufadhili, au kuzuia uwekezaji katika mataifa yanayohusishwa na ukiukaji wa haki za binaadamu. Muungano wa majimbo 16 nchini Marekani yakiongozwa na California yameushtaki utawala wa Rais Donald Trump kuhusu uamuzi wa kutangaza hali ya dharura ili kukusanya fedha za ujenzi wa ukuta wa mpakani na Mexico. text: China ni moja ya nchi zinazodai kumiliki maeneo ya kusini mwa bahari ya China Akiongea katika mkutano wa kiusalama huko Singapore, Bwana Mattis amesema kwamba hatua ya Uchina ya kutengeneza visiwa bandia na kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika bahari ya kimataifa unahatarisha amani katika eneo hilo. Hata hivyo amesema ugomvi kati ya Marekani na Uchina unaweza kuepukika, na akaipongeza Uchina kwa juhudi zake za kukabiliana na mgogoro unaotokana na uundaji wa zana za kinyuklia nhini Korea Kaskazini. Waziri wa ulinzi wa Marekani Gen Mattis Matamshi hayo yanatolewa muda mfupi baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia majaribio kadha ya makombora mwaka huu. Baraza hilo liliunga mkono kwa wingi vikwazo hivyo baada ya mazungumzo ya majuma kadha kati ya Marekani na China Ramani ya kusini mwa bahari ya China Marekanai hautakubali China kuweka wanajeshi kwenye visiwa ilivyojenga Kusini mwa bahari ya China, waziri wa ulinzi wa Merekani James Mattis ameonya. text: Mochi: Chakula kitaamu lakini kinachowaua watu Japan Chakula hicho kinaonekana kutokuwa na madhara yoyote , lakini kila mwaka kimewaua watu kadha, na kusababisha onyo kutolewa kwa umma. Mochi ni chakula gani? Keki zinazoitwa mochi ni nzuri zinazopikwa kutoka kwa mchele. Kwanza kabisa mchele huchemshwa na kisha kupondwa na kukorogwa. Kwanza kabisa mchele huchemshwa na kisha kupondwa na kukorogwa. Kile kitokanacho na kupondwa kwa mchele hufinyangwa na kisha kuokwa au kuchemshwa. Huua kwa njia gani? Keki za mochi hunata. Kutokana na ukubwa wake zinahitaji kutafunwa sana kabala ya kumezwa. Yeyote ambaye hawezi kukitafuna kwa njia inayostahili kwa mfano watoto au watu wazee hupata keki hizo vigumu kula. Kile kitokanacho na kupondwa kwa mchele hufinyangwa na kisha kuokwa au kuchemshwa. Ikiwa keki hizo haziwezi kutafunwa vizuri zinaweza kukwama kwenye koo na hata kusababisha kifo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Japan asilimia 90 ya wale waliokimbizwa hospitalini wakati wa sherehe za mwaka mpya walikuwa ni watu walio na miaka 65 na zaidi. Ni njia ipi salama ya kula chakula hicho? Tafuna, Tafuna, Tafuna. Kama hilo haliwezekani keki hizo zinastahili kukatwa vibande vidogo. Kila mwaka mamlaka huwanonya watu hasa wazee na watoto kula mochi zikiwa zimekatwa vibande vidogo. Licha ya onyo hilo kutolewa, kila mwaka hutokea vifo vinavyosababishwa na chakula hicho. Watu wawili wamefariki nchini Japan huku wengine wakiwa katika hali mbaya baada ya kusakamwa na chakula cha kitamaduni maarufu kama (mochi) ambacho ni keki zilizopikwa kutoka kwa mchele, wakati wa shere za kuukaribisha mwaka. text: Erick Kabendera anakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa kiuchumi Tanzania Orodha inayochapishwa kila mwezi na One Free Press Coalition, iliidhinishwa na muungano wa mashirika kadhaa likiwemo TIME kwa lengo la kuwalinda waandishi habari wanaoshambuliwa kutokana na kazi zao. Orodha ya mwezi huu Septemba imewatambua waandishi habari kutoka mataifa ya Tanzania, Saudi Arabia, Mexico, Colombia na India miongoni mwa mataifa mengine duniani waliofungwa gerezani, walionyanyaswa kwa kazi zao na wengine hata kuuawa. Mwaka jana Time iliwatambua waandishi wanne na shirika moja la habari kwa kazi zao wakati wakikabiliwa na tishio dhidi ya uhuru wa habari. Jamal Khashoggi, mwandishi habari maarufu aliyeangazia taarifa kubwa kwa mashirika tofauti nchini Saudia na ambaye alidaiwa kuuawa ndani ya ubalozi wa Saudia nchini Uturuki mnamo 2018, ni miongoni mwa waandishi waliotambuliwa na amejumuishwa pia katika orodha ya mwezi huu. Wanaharakati waliidhinisha kampeni katika mitandao ya kijamii Tanzania kuonesha kumuunga mkono Kabendera kufuatia taarifa za kukamatwa kwake Kabendera anakabiliwa na mashtaka gani? Katika nafasi ya tatu ya orodha hiyo ni mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera kutoka Tanzania ambaye anazuiwa gerezani nchini humo kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa kiuchumi. Kabendera alipandishwa kizimbani Agosti 5 na kusomewa mashtaka matatu. Katika mashtaka hayo, Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini Tanzania, shtaka la pili ni la kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za kitanzania. Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini. Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani. Makosa yote hayana dhamana na Kabendera anaendelea kusota rumande. Wengine kwenye orodha hiyo mwezi huu ni : Azory Gwanda ametoweka tangu Novemba 2017 na hajaonekana nchini mpaka hivi sasa Azzory bado hajulikani alipo Na katika nafasi ya tano kwenye orodha hiyo ni mwandishi habari mpekuzi kutoka Tanzania Azory Gwanda ambaye tangu Novemba 2017 hajaonekana nchini mpaka hivi sasa. Hii ni mara ya pili Azory kujumuishwa kwenye orodha ya One Free Press Coalition. Mnamo Mei mwaka huu, muungano huo wa uhuru wa vyombo vya habari duniani uliangazia tena habari za mwanahabari huyo kwa lengo la kuishinikiza mamlaka kuwajibika kwa kutoweka kwake. Mwandishi huyo wa Tanzania alikuwa akiifanyia kazi kampuni ya Mwananchi wakati alipotekwa katika mazingira ya kutatanisha. Alikuwa akiripoti kesi za mauaji ya kiholela katika eneo la kibiti katika mwezi uliopelekea kupotea kwake. Serikali imedai kuchunguza kesi yake na za watu wengine waliotoweka lakini hakuna kilichoafikiwa hadi sasa. Kuna shinikizo kutoka kwa makundi ya haki za kibinaadamu , waandishi na mashirika ya habari kama vile kamati ya kuwalinda wanahabari CPJ zikitoa wito kwa mamlaka ya Tanzania kuipatia kipau mbele kesi ya Gwanda na kutoa majibu kuhusu hatma yake kupitia hashtag WhereIsAzory na hashtag MrudisheniAzory zikisambazwa katika mitandao ya kijamii. Kesi yake hivi karibuni imewasilishwa katika majukwaa ya umma kuhusu haki za raia na 2018 alishinda tuzo ya 'Daudi Mwangosi' bila ya yeye kuwepo ili kuheshimu kazi yake na ujasiri. Waandishi habari kutoka nchini Tanzania Erick Kabendera na Azory Gwanda wametajwa kuwa miongoni mwa visa kumi vya dharura vya tishio kwa uhuru wa vyombo vya habari duniani. text: Kituo cha kamari cha Resorts World Manila kimewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kisa hicho Wengi wa waliofariki inaaminika wamefariki kutokana na kukosa hewa safi kutokana na moshi uliotanda mwanamume huyo alipowasha moto meza za chumba hicho cha kamari. Mwanamume huyo alianza kwa kupiga risasi skrini za TV katika chumba hicho cha Resorts World Manila mapema Ijumaa. Polisi wanasema baadaye alijiteketeza. Kisa hicho kimesababisha kuanzishwa kwa operesheni kali ya kiusalama. Maafisa awali walisema hakuna aliyekwua ameumia kutokana na kisa hicho, lakini sasa inabainika kwamba wamepataa miili ya watu wakikagua chumba hicho. Polisi wanasema kisa hicho kinaonekana kuwa kisa cha kawaida tu cha wizi, na kwamba hakikuhusiana na ugaidi. Watu zaidi ya 50 wamepelekewa hospitalini wakiuguza majeraha. Mwanamume huyo alionekana kwenye kamera za CCTV ndani ya chumba hicho Shambulio lilitekelezwa vipi? Maafisa wanasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijatajwa kufikia sasa, aliingia ukumbi wa kituo hicho na kuanza kufyatulia risasi skrini za runinga mwendo wa saa sita usiku. Watu waliokuwemo ndani walianza kukimbia. Pia alichoma moto meza za kamari na kujaza mkoba wake na vipande vya kuchezea kamari vya thamani ya peso milioni 113 za Ufilipino (£1.7m, $2.3m). Baadaye alikimbia na kuingia upande wa kituo hicho wenye hoteli, akaacha mkoba wake, na kuingia chumba cha hoteli. "Humo, alilala kitandani, akajifunika kwa blanketi aliyokuwa ameimwagilia mafuta ya petroli na kisha akajiwasha moto," mkuu wa polisi wa taifa Ronald Dela Rosa alisema Ijumaa. Resorts World Manila wamesema katika taarifa kwamba alijipiga risasi kabla ya kujiwasha moto, na kwamba alipatikana akiwa amefariki mwendo wa saa moja asubuhi saa za Ufilipino. Maafisa wanasema taarifa zinaonesha mwanamume huyo alikuwa na matatizo ya kiakili. Watu 36 wameuawa katika kituo cha kuchezea kamari mjini Manila, Ufilipino baada ya mtu mwenye silaha kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwemo humo. text: Ramirez alikuwa anatetea haki za Wapalestina na wakomunisti Tayari anatumikia vifungo viwili vya maisha jela kwa kutekeleza visa kadha vya mauaji, akidai alikuwa anatetea haki za Wapalestina na wakomunisti. Carlos, ambaye jina lake kamili ni Ilich Ramirez Sanchez, alipewa jina hilo alipokuwa mmoja wa magaidi waliotafutwa sana duniani. Alikaa miaka kadha akiwa mtoro kabla ya kukamatwa mwaka 1994 nchini Sudan. Anashtakiwa nini? Ramirez, 67, alifikishwa mbele ya majaji watatu mahakamani Paris leo Jumatatu kuhusiana na shambulio la guruneti lililotekelezwa katika jumba moja la kibiashara mtaa wa Latin Quarter mjini Paris Septemba 1974. Watu wawili waliuawa na wengine 34 wakajeruhiwa wakati wa shambulio hilo. Ramirez amekanusha mashtaka hayo na wakili wake, Isabelle Coutant-Peyre, amesema kesi hiyo ni kupoteza wakati wa pesa bure. Ni mara ya tatu kwa Ramirez kushtakiwa Ufaransa "Kuna maana gani kumfikisha kortini muda mrefu hivyo baada ya matukio kutekelezwa?" alishangaa. Lakini Georges Holleaux, wakili wa waathiriwa, amesema jamaa za waathiriwa wanasubiri sana na wangefurahia kumuona akiwa kizimbani. "Waathiriwa wamesubiri sana kumuona Ramirez akishtakiwa na kuhukumiwa. Vidonda vyao havijawahi kupona," amesema. Katika mahojiano na gazeti moja, Ramirez anadaiwa kusema alitekeleza shambulio hilo kuishurutisha Ufaransa kumwachilia huru mwanaharakati wa kikomunisti kutoka Japan. Carlos the Jackal ni nani hasa? Ramirez alipewa jina la utani Carlos the Jackal na wanahabari, kutokana na mhusika gaidi katika riwaya ya 1971 iliyoandikwa na Frederick Forsyth kwa jina The Day of the Jackal. Riwaya hiyo baadaye iligeuzwa na kuwa filamu ambayo ilivuma sana. Alizaliwa Venezuela, na alichukuliwa kuwa mmoja wa magaidi hatari zaidi wa kisiasa miaka ya 1970 na 80. Akiwa na miaka 24, alijiunga na kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP) na akaanza kupokea mafunzo kama mwanamgambo mwanamapinduzi. Miaka michache baadaye, alitekeleza shambulio lake la kwanza dhidi ya Joseph Edward Sieff, aliyekuwa rais wa maduka maarufu ya Marks and Spencers jijini London. Sieff, Myahudi maarufu, alinusurika jeraha la risasi kichwani. Ramirez alikuwa mhusika mkuu katika kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine Alipatikana na makosa ya kutekeleza mashambulio manne ya mabomu Paris na Marseille mwaka 1982 na 1983, yaliyoua watu 11 na kujeruhi wengine 150. Alipatikana na hatia mara ya kwanza kortini Ufaransa mwaka 2011 na tena 2013. Akipatikana na makosa ya mauaji, basi huenda akahukumiwa kifungo cha tatu cha maisha jela. Ramirez alikamatwa mjini Khartoum na maafisa wa usalama wa Ufaransa mwaka 1994, miaka 20 baada yake kutekeleza shambulio lake la kwanza. Carlos the Jackal, gaidi kutoka Venezuela, anayedaiwa kuhusika katika mashambulio kadha Ufaransa miaka ya 1970 na 80, ameshtakiwa tena kuhusiana na shambulio lililotekelezwa katika duka moja. text: Filamu ya mauji ya Eve na afisa wa kijasusi Eve anayeigiza nafasi ya Sandra Oh, inaangazia mchanganyiko wa mambo yanayofanyika katika jamii ya sasa. Makala hiyo inaendelea kuvutia hisia mseto kutokana na ustadi wa wahusika wakuu katika masuala ya upelelezi. Baadhi ya watazamaji wanauliza ni vipi wanawake wanaweza kuwa hatari jinsi hiyo. Hayo ni yale yaliyoigizwa katika filamu lakini je, kuna wanawake hatari kama hao duniani? Mata Hari (1876-1917) Alikuwa mchezaji densi za kiajabu aliyekiuka maadili ya jamii yake kwa kuigiza filamu za Marekani zinazofahamika kama Hollywood. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipaji chake kusakata densi, iliyompatia nafasi ya kushiriki katika filamu maarufu ya Mata Mari mwaka 1931 . Jina lake halisi ni Greta Garbo, mzaliwa wa Holland. Alifahamika kama Margaretha Geertruida MacLeod katika filamu ya Mata Hari. Margaretha alikuwa mke wa kapteni wa jeshi aliyekuwa akimnyanyasa sana. Siku moja alimpiga hadi akapoteza ujauzito wa mtoto wake, ukatili uliyomfanya kubadilisha mtazamo wake kuhusu wanaume. Sawa na "Mata Hari, alikuwa mchezaji densi katika miji ya Milan na Paris, na alitumia kazi yake kukwepa sheria ya ustaarabu kwa kutambulisha maonyesho ya densi yake kama ''densi takatifu'' Alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume mashuhuri. Mmoja wa wapenzi wake alimpeleka Ujerumani kumpatia fedha na taarifa kuhusu washirika wake. Wakati huo wa vita vya kwanza vya dunia vilikuwa vinaendelea. Inadaiwa kuwa alipewa jukumu la kuchunguza mienendo ya vikosi vilivyokuwa vikikabiliana na Ujerumani, hatua iliyomfanya kupata kazi ya ujasusi wakati wa vita vya kwanza vya Dunia. Mata Hari nembo ya udanganyifu wa wanawake na sliti wa kisiasa Japo hakumua mtu yeyote lakini inasemekana kazi yake ya ujasusi ilichangia kuawa kwa wanajeshi 50,000. Ufaransa ilimshuku kwa kuhusika na mauaji hayo na baadaye alikamatwa mjini Paris Februari 1917. Aliuawa na kikosi cha 'firing squad' mwezi Oktoba mwaka huo huo. Tangu kuuawa kwake zaidi ya miaka mia moja iliyopita, kumekua na mjadala iwapo alikuwa na hatia au la. Lakini ukweli ni kwamba amekuwa sura ya wanawake wanaotumia mapenzi kusaliti jamii kisiasa . Charlotte Corday (1768-1793) Jina lake halisi lilikuwa Marie-Anne Charlotte de Mademoiselle Corday . Kitu cha kushangaza kumhusu mwanamke huyu ni kwamba alihusika moja kwa moja na mapinduzi ya Ufaransa. Lakini alikuwa na tabia ya kumleta karibu mwanamume aliyetaka kumuangamiza. Charlotte Corday akiwa gerezani, baada ya kukamatwa Muathiriwa wake, Jean-Paul Marat , alikuwa kiungo mashuhuri katika kundi pinzani la Jacobin. Jacobins walikuwa wafuasi wa sera ya magauzi ya siasa kali ambayo baadaye yaligeuka na kutibua mapigano makali yaliyosababisha mauaji ya watu 16,500. Corday alishtakiwa kwa mauaji ya Marat japo wakati wa kujitetea alisema kuwa "nimemuua ili kuyaokoa maisha ya maelfu ya watu". Hata hivyo alihukumiwa kunyongwa, kwa kosa la mauaji. Alifariki akiwa na umri wa miaka 24. Shi Jianqiao (1906-1979) Alifahamika kama Shi Gulan, lakini wandani wake walimbatiza jina la Shi Jianqiao kumaanisha 'Upanga' unaoashiria ahadi yake ya kulipiza kisasi kifo cha babake aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na kiongozi Sun Chuanfang, mwaka 1925. Shi Jianqiao alitumia miaka 10 kulipiza kisasi kifo cha babake. Miaka kumi baada ya Sun Chuanfang kustaafu, Shi Jianqiao, alimvizia na kumuua kwa kumpiga risasi kichwani akiwa anaomba katika hekalu la kibudha . Badala ya kutoroka eneo la tukio, Shi Jianqiao, aliamua kuwasmulia wapita njia kuhusu kitendo chake. Inadaiwa hatua hiyo ilikuwa njama ya kuvutia vyombo vya habari na kutafuta huruma ya watu. Alifikishwa mahakamani na kusamehewa mashtaka mwaka 1936 , kwa sababu kosa lake lilionekana kama kitendo cha kuwaheshimu ya wazazi wake. Shi Jianqiao alifariki mwaka 1979. Brigitte Mohnhaupt (Alizaliwa 1949) Alifahamika kama mwanamke katili zaidi nchini Ujerumani. Alikuwa mwanachama wa kitengo mashuhuri cha jeshi la Red Army Brigitte Mohnhaupt alihusishwa na mtandao wa ugaidi uliyofahamika kama 'Autumn German' mwaka 1977. Wanamgambo wa kundi hilo walisumbua utawala wa Ujerumani kwa kutekeleza visa vya utekaji nyara,mauji na mashambulizi ya mara kwa mara ya miaka ya 1970. Mohnhaupt hakuwahi kujutia makosa yake. Mohnhaupt alikamatwa mwaka 1982, na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani pamoja na kifungo kingine cha miaka 15 kwa kuhusika moja kwa moja na mauaji ya watu tisa ikiwemo moja ambapo alionekana akimpatia mhasiriwa shada la maua kabla ya kumpiga risasi na kumuua. Licha ya kutojutia makosa yake Mohnhaupt, aliachiliwa huru mwaka 2007 katika hatua iliyozua mjadala mkali kote nchini Ujerumani. Mohnhaupt yuko hai mpaka leo. Ajenti Penelope (miaka haijulikani) Alikuwa ajenti wa wa wapelelezi wa Israel, Mossad aliyefahamika kwa jina la "Penelope". Alihusishwa na jaribio la mauaji dhidi Ali Hassan Salameh, kiongozi wa kundi la Black Septemba nchini Palestina ambalo liliwateka nyara na kuwaua wanariadha 11 wa Israel wakati wa michezo ya olimpiki ya Munich mwaka1972. Katika hatua ya kujibu mauaji hayo, Waziri Mkuu wa Israel, wakati huo, Golda Meir aliidhinisha "Operesheni ya Ira de Dios" ambapo mawakala wa Mossad waliwatesa wanachama wa Black Septemba waliohusika na mauaji ya wanariadha hao. Kufuatia majaribio matano ya mauaji dhidi yake yaliyotibuka ,Salameh hatimaye alifariki akiwa pamoja na walinzi wake wanne na wapita njia wawili baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka nje ya nyumba yake mjini Beirut mwaka 1979. Inadaiwa ajenti Penelope ndiye aliyelipua bomu hilo. Makala mpya ya BBC inayofahamika kama "Killing Eve'' ambayo inasimulia mateso wanayopitia wahusika kama vile Villanelle anayejulikana kama Jodie Comer, text: Vijana nchini Misri kupigania haki ya usawa kwa uendeshaji baiskeli Si kawaida kumuona mwanamke akiendesha baiskeli nchini Misri, na wale wachache ambao hupeleka husumbuliwa na wapiti njia. Lakini wasichana watano wanajaribu kubadili dhana hiyo. Wamebuni kundi kwa jina 'hakuna tofauti'' ili kuwaimarisha uendeshaji kama njia mbadala kwa wanawake wanaosafiri, kutokana na ongezeko kubwa la bei ya texi na mabasi madogo tangu serikali walipopunguza ruzuku ya mafuta. Hafla ya kwanza, ilikuwa uendeshaji wa baiskeli iliyo jumuisha watu wengi katika mji wa pwani uliowavutia wanawake na wanaume.'' Tunataka kuonyesha kuwa hakuna tofauti kati ya wanaume na wasichana ,'' Isra Fayed mmoja wa waandalizi alisema hayo kupitia kituo cha televisheni cha serikali cha Al -Qanal. ''Wasichana wana uwezo wa kupeleka baiskeli,na lengo letu la kwanza ni kumahamasisha jamii kuzoea kuwaona wanawake kwenye baiskeli.'' Mradi huo umeungwa mkono na kundi la kutetea haki za wanawake la Kahilah. Muanzilishi wa kundi hilo Enas al-Maasarawy amesema mamia ya vijana wamejiunga na kampeni hiyo ya undeshaji wa baiskeli. ''Kumeshuhudia kiwango kikubwa cha watu.Ni mwanzo wa mabadiliko, Enas al-Maasarawy aliiambia BBC. Kumekuwa na pongezi nyingi katika ukurasa wa Facebook wa mradi huo, ambapo msichana mmoja kati ya walioshiriki alisema wameungana kwa lengo moja: kuihamasisha jamii kuamini kwamba uendeshaji wa baiskeli ni jambo la kawaida,na hakuna sababu ya kuona haya. Kumekuwa na maswala mengi kuhusiana na haki za wanawake nchini misri kwa miaka ya hivi karibuni baada ya maswala ya unyanyasaji wa kijinsia na vita dhidi ya wanawake kufuatia mageuzi ya mwaka 2011. Adhabu kali zilianzishwa mwaka 2014 ikiwemo kifungo jela cha hadi miaka mitano. Wasichana kaskazini mwa Misri wamezindua kampeini ya uendeshaji baiskeli, kupinga maoni potuvu miongoni wanawake wanaoendesha baiskeli. text: Ng'ombe nchini India ni wanayama watakatifu na kuna sheria dhidi ya ulaji na uchinjai wa mnyama huyo. Maafisa wa Polisi siku ya Jumanne walisema kuwa vipimo walivyochukua katika nyama iliopatikana katika hoteli hiyo ya Hayat Rabbani mnamo mwezi Machi vilionyesha kwamba sio nyama ya ng'ombe, bali kuku kulingana na gazeti la Hindustan Times. Ng'ombe ni wanyama watakatifu miongoni mwa jamii ya Hindu nchini India na kuna sheria kali dhidi ya uchinjaji na ulaji wa wanyama hao katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo ikiwemo Rajasthan. ''Kuanzia siku ya kwanza ,nimekuwa nikisema kuwa ni kuku lakini hakuna mtu mmoja aliyenisikiza'', alisema Naeem Rabbani. ''Ripoti hiyo pia ilithibitisha madai dhidi yetu ni ya uwongo''. Hoteli hiyo ilifungwa baada ya kundi moja la kulinda ng'ombe kufanya maandamano mbele ya hoteli hiyo kwa saa kadhaa mnamo mwezi Machi, wakiimba nyimbo za kitaifa. Mmiliki mmoja wa hoteli katika jimbo la Rajasthan nchini India ameonyesha masikitiko yake baada ya hoteli yake kufungwa kwa madai ya uwongo kwamba aliuza nyama ya ng'ombe. text: Bango hilo liliharibiwa baada ya Wakenya mtandaoni kulalamika kuhusu tangazo hilo lililokuwa limeandikwa kila kitu kwa Kichina. Ni nambari za simu ambazo zilikuwa zimeandikwa kwa herufi za Kilatini ambazo ziliweza kusomeka. Mabaki ya bango hilo baada ya kuharibiwa Wakenya mtandaoni walilalamika ni vipi bango hilo 'lisiloeleweka' na wenyeji liliidhinishwa kuwekwa kwenye barabara hiyo bila kutafsiriwa kwa Kiingereza au Kiswahili. Baadhi waliwaomba maafisa wakuu serikali wawasaidie kutafsiri: Mtangazaji huyu alisema matangazo yanafaa kuwa kwa Kiingereza na Kiswahili na kupendekeza liondolewe. Baadhi hata hivyo walitetea bango hilo wakisema huenda aliyeliweka aliwalenga Wachina pekee. Miongoni mwa waliolalamika ni Shirikisho la Watumizi wa Bidhaa na Huduma Kenya (Cofek). Nani aliweka tangazo hilo? Tangazo hilo liliwekwa na kampuni ya ujenzi ya Yunnan International. Tangazo hilo lilisema nini? Tafsiri iliyofanywa na Idhaa ya Kichina ya BBC inaonesha linasema: Yunnan International Kituo cha huduma zote za ujenzi Nambari ya simu ya moja kwa moja: 0708 848 008 Kampuni ya kuaminika na ya kusifika Yenye kufanya kazi kwa utaalamu na njia bora zaidi Huduma ya kiwango na ubora wa juu Baadhi ya Wakenya mtandaoni waliingiza utani: Bango la matangazo ambalo lilikuwa limeandikwa kwa Kichina na kuweka katika barabara kuu ya Mombasa kwenda Nairobi limeharibiwa na watu wasiojulikana. text: Mwanamke aliyebakwa na kaka yake, anasema amekuwa akiishi na maumivu ya kimwili na kisaikolojia Ingawa walikuwa na watoto wachanga migongoni mwao, miongoni mwao hakuna yeyote ambaye ana umri wa kujifungua, jambo ambalo lingemfanya yeyote kuwa na shauku ya kujua ni nini walikuwa wanaongea kati yao. Tulikwenda kuzungumza nao kwenye makazi. Ana umri wa miaka 23. Ni vigumu kumtambua ni nani hasa kwa kumtazama. Ni mpole. Alipokuja kwenye makazi haya, miaka iliyopita, hakuja kutafuta kazi. Bali kutafuta maficho dhidi ya maumivu ya mwili na ya kisaikolojia aliyoyapitia baada ya kubakwa na kaka yake. Anakumbuka kuwa alikua ameanza kuwa na uoga wa watu baada ya magumu aliyoyapitia na kwamba asingeliweza kumtazama wala kuongea na mtu yoyote. "Nilikuwa na maisha magumu na ya huzuni " anasema huku akikumbuka kipindi kilichopita. Licha ya kwamba maumivu yake yalikuwa mazito anashukuru walau anajihisi walau anaweza kuendelea kuishi, anasema kwamba kutembea akitizama mbele wakati mwingine alihisi kana kwamba wakati mwingine haiwezekani. Nyumba iliyompatia hifadhi baada ya tukio la kubakwa , 'Refuge for Women and Children' ndiko anakofanya kazi. Huwashirikisha watu wengine habari yake ya maumivu, kwani anaamini kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kama mfano wa kuwanusuru wasichana wanaoweza kukabiliana na unyanyasaji wa kingono. Kaka yake mkubwa ambaye alimpeleka mjini na kumuahidi kuwa atampleka shule alikuwa polisi. Alikuwa na umri wa miaka 16 wakati huo na wote waliishi kwenye nyumba moja ambayo ilikodishwa na kaka yake. "Kwasababu nilikuwa mdogo, sikujua mengi na sikuweza hata kuongea wazi. Nilipokuwa nikiwaona watu, nilifikiri wangenidhuru pia", alielezea masaibu ya kisaikolojia aliyoyapitia. Alikuwa akifikiria kwamba watu watagundua siri yake kwa kumtizama tu. Kwa hiyo taratibu akaacha kwenda shule. Katika kipindi chote cha miaka 5 walichoishi pamoja, kaka yake alikuwa akimbaka. Katika kipindi hicho alipata uzauzito na kutoa mimba mara kadhaa. Vitisho kutoka kwa kaka yake, umri mdogo na maumivu havikumuwezesha kuongea neno hata moja juu ya hili kwa yeyote, anasema. Hata hivyo, anaeleza kwamba siku walipohamia nyumba nyingine alipata fursa aliyokuwa akiitaka. Muda mfupi baada ya kuhamia kwenye nyumba yao mpya, mwenye nyumba aligundua namna alivyokuwa hapendi kuongea na akamuuliza "Ni kwanini wewe ni muoga sana wa kuwasogelea watu? Wewe ni ndugu yake?" Maswali yote yalikuwa ni magumu kwake kuyajibu. Kwasababu alikuwa anatafuta njia za kutoroka ili kulinda utu wake hakutaka kumdanganya mwanamke , lakini kumuambia ukweli lilikuwa ni tatizo jingine lililomuelemea. Baada ya kufikiria na kuupiga moyo konde alipata nguvu ya kumueleza mwenye nyumba. Baada ya kusikia habari yake mwenye nyumba ambaye alishitushwa na aliyoyasikia kutoka kwa binti huyo alimpeleka mara moja kwenye kituo cha karibu cha polisi. Baada ya kuhojiwa katika kituo cha polisi alichukuliwa kwenye nyumba ambako wanawake wenye matatizo kama yake hupelekwa na kupewa mahala salama na usaidi wa kisheria. Msichana aliyebakwa an kaka yake anasema jamii huwalaumu na kuwashutumu wanawake kwa ubakaji wanaofanyiwa Kesi ilipofika mahakamani, familia ambayo ilifahamishwa kuhusu hali ya mambo walimgeuka " Hawezi kufanya jambo kama hilo, anaongea hivi kwasababu ni mtoto" walisema, hawakumuamini . "Kila mtu katika familia yangu, isipokuwa mama yangu walikasirishwa sana na mimi " alieleza namna alivyogeuka na kuwa mwenye makosa ili hali akiwa yeye ndie muathiriwa. Pia anasema kuwa kutokana na kwamba kawaida kituo vcha polisi hakipokei wanawake wenye matatizo kama yake, ni jambo lililomuongezea uwoga. Anasema hawakuwa watu wa kumsikiliza na bila huruma walimuuliza maswali mabaya "Ulikuwa unafanya nini mpaka leo hii" wakimaanisha kuwa hakujitokeza mapema vya kutosha. Hii ndio hali inayowakumba wanawake wengi. Wengi wanalazimishwa na jamii kuamini kuwa ni makosa yao. Watu wanaowazingira huwalaumu kwa mambo waliyofanya, mambo ambayo wangepaswa kufanya na mengine mengi, hivyo kuwalazimisha wengi kuendelea kujificha na kutosikika. Katika hifadhi alipata maficho ambayo kwa sasa yamekuwa mahala pake pa kazi, na sasa amekutana na wanawake ambao waliwahi kubakwa na kaka zao, baba zao n ahata babu zao. Anaeleza kuwa wote walilaumiwa na jamii kwa kuwa chanzo cha ubakaji wao. "Sifahamu mengi juu ya mfumo wa sheria. Lakini kwa yale niliyoyashuhudia, naweza kusema mfumo wa sheria ni mbaya "Anasema. Mara nyingi wabakaji hutembea huru. Anasema tangu alipompeleka kaka yake mahakamani hakuna matokeo yoyote aliyoyapata kutokana na kesi na kaka yake anatembea huru. " Nilipata maumivu makali sana na nikasimama mahakamani bila mafanikio. Afadhali nisizungumzie hili " aliongeza. "Tunahitaji kuwa tayari kusaidiwa" Kutokana na uaviaji mimba wa mara nyingi alioupitia alihitaji kupitia matibabu mbali mbali. Baada ya haya yote "niliumia zaidi kisaikolojia. Hasa kwa namna familia yangu ilivyopokea taarifa ya kubakwa kwangu iliniuma sana" anasema. Alipokuwa nyumbani, hakuweza kula wala kumuamini yeyote aliyekuwa karibu nae. Alikuwa na ndoto moja tu na ilikuwa ni ya kujiua na kujimalizia maumivu yote mara mara moja . Amesema aliweza kuyashinda majaribu kwa msaada wa kufuatiliwa kwa karibu kisaikolojia. Alipopata tena matumaini alianza kufanya masomo mbali mbali. Makazi hayakumpatia tu ujuzi mbali mbali ili kuwezesha kuwa mtu anayejitegemea tu, bali yalimuwezesha kujiamini kupitia mafunzo ya Taekwondo ambayo pia yalimnufaisha. Wakati watu wanapoumizwa hawahitaji mengi. Mara nyingi huwa hawataki kusikia wala kuwa tayari kuelewa chochote "licha ya kwamba kuna watu wengi walio tayali kutoa msaada wao, tunahitaji kuwa tayari kusaidiwa" anasema. Ili kuondoka katika maumivu ya kimwili na kisaikolojia anasema alipata nguvu mwenyewe "Nilijiamini mwenyewe na niliamini ninaweza kujitatulia mwenyewe tatizo la maisha yangu yaliyotawaliwa na huzuni ." Anasema kwamba licha ya kwamba wanawake wengi hawazungumzi wazi, anadhani wameweza kukabiliana na mambo mengi mabaya kuliko aliyoyapitia. Anaongeza kwamba anaamini kuwa kama jamii isingewapuuza wanawake hawa wengi wangejifunza kutokana na uzoefu wa aina hiyo. "Tunapowaona wanawake wamevaa vitambaa na kutembea kana kwamba uzito wa dunia uko kwenye mabega yao, ninadhani pia wanaishi maisha yangu" kwa hiyo anasema huwa anawafuata na kuongea nao , kuwasikilizana kuwakumbatia. Anasema anaamini kwamba jamii inahitaji kujifunza kuwahusu wanawake na masaibu wanayoyapitia ili kuwasaidia na kuwasaidia wanawake ambao wamejipata katika hali kama yake. Anaongeza kuwa kwasababu hii itawezesha kuzuwia mashambulio sawa na hayo. Familia zinapaswa kufahamu kuwa mavazi, chakula na masomo ambayo watoto wao wanapokea havitoshi, anasema wanahitaji kutambua kuwa wanaweza kuwa katika hali ya hatari kokote wanapoenda. "Ni nani angependa kuwa nami sasa?" Makazi yanajitahidi kufanya kazi na wanawake waliopitia hali sawa na yangu, wanaamini kwamba hawatakiwi na jamii na mara nyingine hupanga kujiua. Makazi yamekuwa yakiwasaidia wanawake kisheria na kisaikolojia kwa miaka 15 sasa. Maria Munir, muasisi wa makazi hayo alililieleza jarida la 'Temsalet Gets' nchini humo kwamba hakuna chochote kinachompatia furaha kuliko kuwaona wanawake ambao awali walitaka kujiua wakifanya vizuri shuleni na hata kitaaluma. Makazi hayo yameweza kuwawezesha wanawake kuwa Wahandisi, Viongozi na katika Nyanja nyingine kupitia mafunzo wanayopata mjini Addis Ababa, Dessie na vituo vingine. Mwanamke mdogo aliyetushirikisha habari yake kwa sasa ni mkufunzi na anacheo cha meneja. Wakiishi katika maeneo tulivu ya wilaya ya Megenagna mjini Addis Ababa, wasichana 7 au 8 wanaonekana wakiondoka kwenye makazi yaliyofungwa wakiwa wamewabeba watoto wachanga. text: Mataifa kadhaa ikiwemo marekani yamependekeza kwamba raia wake wavalie barakoa wanapotoka nje Shirika la Afya Duniani WHO limesisitiza siku ya Jumatatu kwamba kunapaswa kuwa na ushahidi kwamba utumizi wa mask au barakoa, pamoja na maelezo mengine unasaidia kupunguza mlipuko huo. Hakuna jibu la moja kwa moja , wala kiini macho. 'Mask' pekee haziwezi kuzuia mlipuko huo , alisema mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus , akitoa wito kwa maelezo mengine kama vile yale ya kuosha mikono kuendelea kutekelezwa. Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa nchini Marekani CDC kilisema kwamba kulingana na utafiti wa hivi karibuni , walipendekeza kujilinda uso katika maeneo ambayo watu wanakaribiana zaidi . CDC inapendekeza matumizi ya barakoa za vitambaa kujilinda uso katika maeneo ya umma ambapo maagizo mengine ya kutokaribiana ni vigumu kutekeleza, ilisema taasisi. Barakoa iliotengenzwa kwa kitambaa Katika maeneo ya umma kama vile kwenye maduka ya jumla , ama yale ya kuuza dawa inaweza kua vigumu kutekeleza agizo la kutokaribiana hivyobasi kuna hatari ya maambukizi miongoni mwa watu. Hatahivyo kupitia mask ama barakoa zilizotengenezwa nyumbani ama hata kupitia barakoa zilizothibitishwa na maafisa wa afya , kuna maelezo ambayo iwapo yatapuuzwa yanadhoofisha utumiaji wa vifaa hivyo. Kununua mask wakati huu sio rahisi kwa kuwa mahitaji yake yapo juu sana. Hatahivyo lazima uangalie makosa yanayofanyika sana wakati wa matumizi yake kulingana na CDC na WHO. Dhana ya kuwa barakoa ni kinga ya kiwango cha juu Mojawapo ya onyo kutoka mamlaka za Afya sio kudhania kwamba barakoa iliotengenezwa kwa kitambaa ina uwezo wa kukulinda kama ile ya N95 katika matumizi ya kimatibabu. Kimatibabu N 95 ni vifaa vinavyohitaji kutumiwa na maafisa wa Afya, hivyobasi hazifai kutumiwa na raia wa kawaida ili kuzuia uhaba. Barakoa zilizotengezwa na vitambaa kulingana na CDC hupunguza kasi ya virusi vya corona na husaidia watu ambao huenda wameambukizwa kutowaambukiza wengine. Barakoa zilizothibitishwa na maafisa wa afya kama ile ya N95 hazifai kuvaliwa na watu wengine ili kuzuia uhaba Kwa upande mwengine, barakoa za N95 ambazo zimeidhinishwa kimatibabu ni vifaa vinavyohitajika kutumiwa na maafisa wa Afya, hivyobasi hazifai kutumiwa na raia wa kawaida ili kuzuia uhaba wake. Kutoosha mikono na kukaribiana na watu wengine WHO na CDC zinakubaliana kwamba matumizi ya kinga hii ni mojawapo ya maelezo ambayo kila mmoja anapaswa kufuata ili kuzuia maambukizi. Kutokaribiana, kuzuia mikutano ya zaidi ya watu 10 pamoja na kuosha mikono kwa mara kwa mara kunasalia kuwa nguzo ya CDC katika kinga ya kibinafsi hata iwapo mtu amaevalia barakoa. Kufunika mdomo pekee Kosa jingine linalofanywa na watu wengi wakati wa utumizi wa barakoa ni kufikiria kwamba wanaweza kuziba mdomo pekee. Maeneo yoyote yanayotumika kupumua mwilini yanafaa kufinikwa , hivyobasi barakoa zilizotengenezwa na vitambaa zinafaa kuziba mdomo na pua kwa kuwa ndizo zinazotumika kwa maambukizi. Vilevile barakoa hizo hazifai kuwekwa karibu na watoto chini ya umri wa miaka 2 ama watu wenye matatizo ya kupumua ama watu ambao hawawezi kuzivua bila usaidizi, imeonya CDC. Kutoosha barakoa zilizotengenezwa na vitambaa baada ya matumizi. Barakoa zilizotengenezwa nyumbani kwa kutumia vitambaa zinaweza kutumika kwa mara nyengine iwapo maelezo ya usafi wake yatatimizwa. Kutoziosha baada ya matumizi kunaweza kusababisha maambukizi. CDC inasema kwamba kuziosha na kuzikausha inatosha. Barakoa zilizoidhinishwa kimatibabu hazifai kutumika mara ya pili. Kushika barakoa bila kuosha mikono Kwa kuwa barakoa huwa na vimelea wakati zinapotumika , ni muhimu kutozishika na iwapo hilo litafanyika ni muhimu kuosha mikono. Vievile kabla ya kuvaa na kuvua pia unapaswa kuosha mikono yako. Wakati ambapo haitumiki barakoa iliotenegenzwa kwa kutumia kitambaa inafaa kuwekwa mahala pasafi, ndani ya mfuko uliofungwa. barakoa zinazotumia vitambaa zinaweza kutengezwa kwa kutumia mashine za kushona Katika vita dhidi ya virusi vya corona , kuna suala ambalo linazidi kuibua mjadala kuhusu iwapo raia wanapaswa kujifunika uso na pua kwa kutumia barakoa? text: Amesema taifa hilo limeendelea kuilaghai Marekani, ilhali inazidi kupokea mabilioni ya dola ya msaada, hasa katika miaka ya hivi karibuni. Bw Trump amesema Pakistan imepokea jumla ya dola bilioni 33 katika miaka 15 iliyopita "na hawajatusaidia kwa chochote ila uongo na ulaghai, wakiwafikiria viongozi wetu kuwa wapumbavu". Akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Bw Trump amedai kuwa, Pakistan inawapa hifadhi magaidi, ambao wanatafutwa na wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan. Marekani inadhamiria kuendelea kuzuilia zaidi ya dola milioni 250 ya msaada kwa Pakistan, ambayo ilichelewesha makusudi kuwashilishwa kwa taifa hilo la bara Asia, tangu mwezi Agosti mwaka jana. Wakati huo, Wizara ya nchi za kigeni nchini Pakistan, iliahidi kuwa itazidisha juhudi zake za kimataifa za kupambana na magaidi. Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumu Pakistan na kusema imekuwa ikiihadaa na kuidanganya Marekani kwa muda mrefu. text: Chloroquine, hydroxychloroquine au placebo zitatolewa kwa wafanyakazi wa afya zaidi ya 40,000 kutoka Ulaya, Afrika, Asia na Amerika ya kusini. Washiriki wote ni watumishi wa afya ambao wanahudumia wagonjwa wa Covid-19. Rais Donald Trump alikosolewa baada ya kusema kuwa ametumia dawa ya malaria iitwayo hydroxychloroquine, licha ya angalizo kuwa inawezekana si salama kutumia dawa hiyo kwa ajili ya corona. Mshiriki wa kwanza, Uingereza katika jaribio la kwanza la kimataifa imesema siku ya Alhamisi katika hospitali ya Brighton na hospitali ya chuo kikuu cha Sussex pamoja na hospitali ya John Radcliffe mjini Oxford. Watapewa dawa ya hydroxychloroquine au placebo kwa kipindi cha miezi mitatu. Wakati Asia, washiriki watapewa chloroquine au placebo. Mipango ya awali ni katika majimbo 25 ya Uingereza na matokeo yanatarajiwa mwishoni mwa mwaka. Jaribio hilo liko wazi kwa yeyote ambaye anatoa huduma moja kwa moja kwa wagonjwa wenye virusi vya corona nchini Uingereza, ikiwa kama bado hawajapata maambukizi ya virusi vya corona. Jaribio hili litaangalia kama dawa hizo zitaweza kuzuia wafanyakazi wa afya kupata maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa wagonjwa. 'Ina manufaa au ni hatari' Utafiti mmoja wa Prof Nicholas White kutoka chuo kikuu cha Oxford alisema: "Kiukweli hatufahamu bado kama chloroquine au hydroxychloroquine kama ni kinga au zina madhara dhidi ya Covid-19." Lakini alisema, utafiti wa maeneo mbalimbali kama huu , ambapo si mshiriki au mtafiti anafahamu kuwa kupewa dawa hiyo ndio namna nzuri ya kujua umuhimu wa dawa husika. "Chanjo ambayo ni salama na yenye uhakika itachukua muda mrefu kupatikana," alisema Prof Martin Llewelyn kutoka Brighton na chuo cha afya cha Sussex, ambaye pia anaongoza utafiti huo. "Kama dawa za malaria za chloroquine na hydroxychloroquine zinaweza ,kupunguza urahisi wa mtu kuambukizwa virusi vya corona, basi itakuwa jambo bora zaidi ambalo litasaidia." Dawa hizo zinaweza kupunguza homa na maambukizi na kuweza kutumika pia kwa ajili ya kuzuia na kutibu malaria. Rais Trump alizungumzia kabla kuhusu matumizi ya dawa hizi kwa ajili ya Covid-19 Kituo cha kujitolea cha Lupus nchini Uingereza na Marekani kimetoa wasiwasi wake kuhusu ongezeko la uhitaji wa dawa hiyo kwa ajili ya virusi vya corona kunaweza kuhatarisha hali za wagonjwa ambao wanazitegemea tayari, kama zitapungua wagonjwa wa malaria watapata shida kuzipata ili kutibiwa. Dawa hizo zimepata umaarufu baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa dawa hizo zinaweza zikasaidia katika janga hili la corona, na wiki hii alitumia dawa ya hydroxychloroquine ili kujizuia kupata maambukizi ya corona. Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani ilitoa angalizo dhidi ya matumizi ya dawa hizo nje ya hospitali, wakati wakitoa ruhusa ya dawa hizo kutumika katika kesi kadhaa au majaribio ya kitabibu. Wakati chuo kikuu cha Oxford kikifanya jaribio la kuzuia maambukizi katika mazingira ya huduma za afya, shirika la afya duniani limetoa angalizo kuwa baadhi ya watu ambao wanajitibu wenyewe wanaweza kupata madhara makubwa. Hazijaonekana kuwa salama na zenye uhakika wa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona bali kuna hatari ya kupata matatizo makubwa ya moyo. Utafiti huo umejumuisha watafiti kutoka Uingereza, Thailand, Vietnam, Laos, Cambodia na Italia. Jaribio la matumizi ya dawa za malaria kuona kama zinaweza kuzuia ugonjwa wa Corona limeanza nchini Uingereza katika mji wa Brighton na Oxford. text: Kazi ya DJ katika klabu ni kuwatumbuiza wateja kwa kucheza mziki waupendao Dax J ni mzaliwa wa London na ameshtakiwa kwa kosa la kukosea maadili ya umma, lakini uamuzi huo ulitolewa wakati ambapo alikuwa tayari ameshatoroka Tunisia baada ya kuomba msamaha. Klabu aliyocheza muziki huo ilifungwa baada ya kanda ya video kuonesha akicheza mziki uliochanganywa na Adhan . Watu walionyesha kukerwa katika mitandao ya kijamii. Msemaji wa mahakama alikiambia kituo cha habari cha AFP kuwa mashtaka dhidi ya mmiliki wa klabu na wale walioandaa hafla hiyo yametupiliwa mbali. Hafla hiyo ilikuwa mojawapo ya tamasha ya Orbit, huko Nabeul na ilikuwa na DJ wawili wa Kiingereza. Muziki huo ulijumuisha aina ya densi iliyochanganywa na Adhan, wito wa Waislamu kwa ibada, mara tano kwa siku. "Hatutaruhusu mashambulizi dhidi ya hisia za kidini" alisisema gavana wa Nabeul Mnaoaur Ouertani. Waandalizi wa tamasha hilo la Orbit waliomba msamaha katika ukurasa wao wa facebook, lakini walisema kuwa hawatokubali kosa la kuchezwa kwa muziki wa kupotosha. DJ "hakujua kwamba mtindo wake utawaudhi waliohudhuria, wengi ambao wanatokaa nchi ya Kiislamu kama hii yetu," walielezea katika ujumbe wao katika mtandao wa kijamii kwa lugha ya Kifaransa. Dax J, aliyecheza Adhan, aliomba msamaha kwa yeyote yule aliyekerwa na muziki alioucheza katika tamasha hilo la Orbit. "Haikuwa kupenda kwangu kumkasirisha mtu yeyote," alisema. Dax J amecheza muziki katika tamasha na vilabu mbalimbali kote duniani ikiwemo tamasha la techno la Awakenings huko Uholanzi na Glastonbury, Uingereza. Anaendesha studio mjini Berlin ambako pia anafanya kazi kama mhandisi wa sauti. Mahakama moja ya Tunisia imetoa amri ya DJ wa Uingereza kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kucheza muziki uliyochanganywa na Adhan klabuni. text: Msikiti wa zamani zaidi nchini Uingereza Utawala katika tarafa ya Nyarugenge kunakopatikana jamii kubwa ya Waislam nchini humo umebainisha kuwa kumekuwepo muafaka wa kubadili mbinu za kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa kuwasumbua wananchi. Kulingana na mwandishi wetu mjini Kigali John Gakuba wito huo wa Waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa wananchi. Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo. Wito huo wa mamombi miongoni mwa jamii za Waislamu kote duniani hutumia vipaza sauti na hufanyika mara tano kwa siku. Licha ya utawala wa eneo hilo kudai kwamba kumekuwa na mwafaka kutoka pande zote mbili baadhi ya Waislamu waliohojiwa wametoa hisia tofauti. Kulingana na katibu mtendaji wa tarafa hiyo ya Nyarugenge, amri hiyo iliagizwa yapata miaka maiwili iliopita lakini ikapuuziliwa mbali. ''Pengine wakati ule sababu ambazo watu hawakupokea vyema ujumbe ilikuwa hakuwa umeelezewa sawa sawa ,lakini leo baadhi ya makanisa yalilazimika kufunga milango baada ya kushindwa kutimiza kanuni za ujenzi huku misikiti yenye vipaza sauti na makanisa yenye kengele tukiyataka kutotumia mtindo huo. Mtu aliye lala akiishi jirani na kengele hiyo inampigia kelele. Kwa hiyo ni uamzi unaohusu pande zote nna ni matarajio yetu kuwa hakuna aliyenyimwa haki.'' Naye mshauri wa Mufti wa Rwanda shekh Mbarushimana Suleinam alisema kuwa hatua hii ya kuzuiliwa kwa matumizi ya adhana misikiti inafuatia operesheni inayoendela ya kufungwa kwa makanisa na vigango Zaidi ya mia saba ambavyo viliripotiwa kuwa havijatimiza kanuni za ujenzi na amri ilitolewa kwanza kutimiza matakwa ili zipewe tena idhini ya kufanya kazi. Marufuku ya matumizi ya adhana{ Wito kwa Waislamu kuhudhuria maombi} katika tarafa moja ya mji wa Kigali nchini Rwanda imepingwa vikali na baadhi ya Waislamu jijini humo. text: Bobi Wine aliachiwa kwa dhamana Jumatatu wiki hii baada ya kuwekwa kizuizini na jeshi la Uganda ambapo inaripotiwa aliteswa. Mmoja wa mawakili wake Tonny Kitara anasema kuwa Bobi Wine bado amelazwa katika hospitali moja mjini Kampala kufuatia majeraha aliyopata wakati alipokamatwa na wanajeshi. Mwanamuziki huyo anatarajiwa kusafirishwa kwa matibabu ijapokuwa haijulikani anatarajiwa kupelekwa wapi. Watu 25 waliokuwa wameshtakiwa pamoja naye katika mahakama ya hakimu mkuu mjini Gulu waliwasili mahakamani humo kaskazni mwa Uganda kulingana na bwana Kitara. Jumla ya watu 33 wameshtakiwa na uhaini kufuatia madai kwamba waliupiga mawe msafara wa rais Yoweri Museveni. Baadhi ya washukiwa hao hawakuonekana mahakamani kwa sababu ya hali mbaya ya kiafya ama mkanganyiko wa siku ya kusikizwa kwa kesi hiyo . Stakhabadhi zao za dhamana kwa makosa zilisema kuwa wanatarajiwa kuwasili mahakamani Septemba 30 na sio Agosti 30. Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe mosi Oktoba. Baadhi ya washitakiwa wanaendelea kupata matibabu hospitalini na huenda wakashindwa kuhudhuria mahakamani ambapo watawakilishwa na mawakili wao. Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi ni mwakilishi wa eneo bunge la Kyadondo Mashariki na ni msanii maarufu wa muziki nchini Uganda. Alikamatwa wiki mbili zilizopita kwa tuhuma za uvamizi wa msafara wa Rais Museveni mjini Arua na kupokea kipigo kikali yeye na wenzie 32 kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Dereva wa Bobi Wine alipigwa risasi na kuuawa katika purukushani hizo. Watuhumiwa hao waliwekwa chini ya ulinzi wa jeshi huku Bobi Wine awali akipandishwa katika mahakama ya kijeshi kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria. Rais Yoweri Museveni alijitokeza na kukanusha taarifa kuwa Bobi Wine ameumizwa vibaya na kuvishutumu vyombo vya habari kwa kueneza taarifa za uongo. Baada ya kelele za upinzani kupazwa ndani na nje ya Uganda pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, kesi yake mbele ya mahakama ya kijeshi ilifutwa na kuachiwa huru kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka ya uhaini katika mahakama ya kiraia. Jumatatu wiki hii, Bobi Wine na washukiwa wengine wote waliachiwa kwa dhamana. Mbunge wa Uganda na msanii Bobi Wine hakuhudhuria kikao cha mahakama hii leo kuhusiana na kesi ya uhaini iliowasilishwa dhidi yake na serikali. text: Idadi ya twiga imepungua sana maeneo mengi Afrika Idadi ya twiga duniani imeshuka kutoka 155,000 mwaka 1985 hadi 97,000 mwaka 2015 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi wa mambo asilia (IUCN). Idadi ya wanyama hao imepungua sana kutokana na kuharibiwa kwa maeneo wanamoishi, uwindaji haramu na migogoro ya kisiasa katika maeneo mengi Afrika. Baadhi ya aina wa twiga, sana maeneo ya kusini ya Afrika, wanaongezeka hata hivyo. Hadi kufikia sasa, IUCN hawakuwa wameorodhesha twiga kuwa miongoni mwa wanyama walio hatarini. Hata hivyo, kwenye orodha yao mpya ya wanyama walio hatarini, mnyama huyo ameorodheshwa kuwa "hatarini", baada ya idadi ya wanyama hao kushuka kwa zaidi ya asilimia 30. Kwa mujibu wa Dkt Julian Fennessy, mwenyekiti wa kundi la IUCN linaloshughulikia twiga, wanyama hao "wanaangamia kimya kimya." "Ukienda kwenye safari, twiga wapo kila mahali," aliambia BBC News. "Ingawa kumekuwepo na wasiwasi kuhusu ndovu na vifaru, twiga wamesahaulika. Ni jambo la kusikitisha kwamba idadi yao imeshuka sana na ni jambo la kushangaza, kwamba wamepungua hivyo katika kipindi kifupi." Twiga hupenda sana kupeleleza na hili huwafanya kuwindwa kwa urahisi na majangili na wapiganaji Ongezeko kubwa la idadi ya watu limesababisha maeneo mengi ya misitu kuharibiwa kwa ajili ya kilimo, jambo ambalo limepunguza maeneo wanamoishi twiga. Vita katika baadhi ya maeneo Afrika pia vimeathiri idadi yao. "Katika maeneo haya yenye vita na migogoro, hasa kaskazini mwa Kenya, Somalia na Ethiopia katika mpaka wake na Sudan Kusini, twiga ambao ni wanyama wakubwa wanaliwa." Twiga wamepungua sana duniani katika kipindi cha miaka 30 iliyopita na kwa sasa wanakabiliwa na hatari ya kuangamia. text: Mila hiyo inafahamika kama 'gukuna' hufanywa na shangazi wa mtoto wa kike au mamake mwenyewe. Lengo hasa ni kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa. Mila hii imeanza kutoweka kwa vijana wa kizazi kipya hasa sehemu za mijini, Lakini inaonekana kushamiri kwa wanawake ambao hawakuitekeleza wakiwa watoto Shangazi ambaye anaishi katika mji wa Rubavu na ambaye hakutaka jina lake kamili litajwe anasema kuwa yeye huwasaidia wanawake na wasichana wanaotaka kurefusha sehemu zao za siri. Anasema kuwa yeye hutumia dawa ya mimea inayochanganywa na mafuta ya ngombe ambayo hutumiwa na wasichana wa kati ya miaka12 hadi 20. ''Anasema hii ni kazi aliyofanya kwa miaka mingi nchini Rwanda na sasa amepanua soko lake hadi nchi jirani ya Congo ambako anaweza kulipwa hata dolla 100 kwa mtu anayetaka huduma hiyo. Anasema kwamba kwa wale wanaotekeleza mila hii ya Kinyarwanda makusudio yao ni kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa. Hatahivyo baadhi ya raia wasiopendelea utamaduni huo wanasema kuwa ndoa nyingi huporomoka kutokana na kutekeleza utamaduni huo. Wanasema kuwa utamaduni huo una madhara hususan wakati wa kujifungua. Lakini kulingana na Bwana Mutabazi Leon ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, utamaduni huo hauathiri kivyovyote njia ya uzazi wakati wa kujifungua. ''wakati mwanamke anapojhifungua sisi huangalia njia ya ndani ya uzazi kwa hivyo utamaduni huo hauna athari zozote kwa wanawake wajawazito''. Huku nchi nyingi za Afrika zinapofanya mila ya ukeketaji wa wanawake,nchini Rwanda hali ni tofauti,sehemu nyeti haikatwi badala yake hurefushwa hadi kufikia urefu wa kidole cha katikati. text: Rais Trump amesema kwamba Iran sio nchi ileile aliyoikuta alipoingia madarakani Maamuzi hayo yanakuja mara baada ya waziri wa mambo ya nje alipofanya ziara fupi bila kutangaza katika mkutano wa matifa makubwa 7 yenye nguvu duniani siku ya jumapili. Mahusiano kati ya Iran na Marekani yamezidi kuwa mabaya tangu Washington ilipojitoa mwaka jana katika makubaliano ya mwaka 2015 ya kudhibiti matumizi ya nyuklia ya Iran. Licha ya kwamba, siku ya Jumatatu Trump alisema kwamba ana matumain chanya juu ya matarajio ya mpango mpya wa nyuklia na Iran . "Iran sio nchi ileile miaka miwili na nusu iliyopita wakati nilipoingia madarakani," aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa G7 akiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron . "Nina imani kuwa Iran litakuwa taifa zuri... lakini hawapaswi kuwa na silaha za nyuklia," alisema," lazima kuwa lazima wawe wachezaji wazuri kabla hajakubali katika mkutano. Mapema siku ya jumatatu, bwana Rouhani alisema kuwa yuko tayari kukutana na yeyote kama ataona kuwa itakuwa ni kwa manufaa ya Iran. "Kama sina uhakika kuwa kuhudhuria mikutano hiyo hakutasaidia kuendeleza nchi yangu au kutatua matatizo ya watu wa nchi basi sitasita kufanya hivyo," alisema. Trump alitoa hotuba ya kuhitimisha mkutano wa G7- mkutano ulioudhuriwa na viongozi kutoka Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani. Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na moto wa Amazon , maendeleo ya Ukraine, Libya na Hong Kong. Wamefikaje hapo? Mvutano dhidi ya Iran ulirefushwa kwa sababu Marekani ilijitoa katika mpango wa nyuklia wa mwaka 2015, na kuweka tena vikwazo . Makubaliano mengine yalikuwa ya Uingereza, Ujerumani, Urusi na Uchina walijaribu kuokoa mpango wa nyuklia. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alisema kuwa alikuwa na mazungumzo mazuri na washirika wa Ufaransa na Macron, pembeni ya mkutano wa G7 huko Biarritz. Macron ambaye alichukua jukumu la kujaribu kuokoa makubaliano, alisema kuwa alikuwa amemfahamisha Bw Trump kuhusu mpango wake wa kumualika Bwana Zarif, baada ya majadiliano na maafisa wa Iran ili kutafuta uvumbuzi. Alisema kuwa anaamini kuwa vigezo vya mkutano kati ya Trump na Rouhani ndani ya siku chache zijazo umechapishwa . "Hakuna ambacho kimewekwa wazi na bado mambo si shwari, lakini mazungumzo yao yameanza kuonyesha maendeleo fulani," alisema na aliongeza kumwambia Rouhani kuwa "kama utakubali kukutana na Trump nina imani kuwa makubaliano yataafikiwa tu". Mpango Mpya utafananaje? Makubaliano ya mwaka 2015 yalihusisha Iran kupunguza kwa matumizi ya nyuklia kutoka miaka 10 mpaka 15 na kurejesha kwa vikwazo. Mpango huo uliikataza Iran kutotumia rasilimali zake za nyuklia bila ukaguzi kutoka kimataifa . Iran alielezea vigezo hivyo kuwa havikubaliki. Katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana Trump alisema mpango mpya kuwa alikuwa anataka kusiwe na silaha za nyuklia kwa muda mrefu zaidi . Haijafahamika kama Iran itakubali vigezo hivyo vipya" TV ya Iran iliripoti kupinga kwa mazungumzo hayo kuwa hayataweza kufikia makubaliano bila kunukuu aliyesema. Kwa sasa Macron alisema kuwa kunahitajika kuhakikisha kuwa Iran haitapata silaza za nyuklia na itaweza kusaidika kiuchumi kama itatekeleza hilo. Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na rais wa Iran Hassan Rouhani chini ya makubaliano sahihi. text: Bendera ya Somalia Mwaka 1985 alichaguliwa kuwa katibu wa kwanza katika ubalozi wa Washington DC. Mwaka 1989, aliondoka na kujipatia shahada yake ya historia katika chuo kikuu cha Buffalo mjini New York . Wakati huo Farmajo alitafuta hifadhi ya kisiasa nchini Marekani baada ya serikali ya Somalia kuanguka 1991. Aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Buffalo na kujipatia shahada ya uzamili katika somo la sayansi ya siasa pamoja na mahusiano ya kimataifa. Rais Sharif Ahmed wa Somalia alimchagua Farmajo kuwa waziri mkuu mnamo mwezi Oktoba 2010 ili kumrithi Omar Abdirashid Sharmake ambaye alijiuzulu katika wadhfa wake kufuatia mgogoro. Farmajo alijiuzulu katika wadhfa wake mnamo mwezi Juni 2011 baada ya shinikizo ya jamii ya kimataifa miongoni mwa makubaliano ya Kampala kati ya rais Ahmed na spika wa bunge Aadan ambapo makubaliano ya kamati hiyo ya mpito yaliongezwa hadi mwezi Agosti 2012. 2011 Farmajo alianzisha chama kipya cha Somali Justice and Equality kwa jina maarufu Tayo. Farmajo ni katibu mkuu wa Tayo ambacho kinaongozwa na mwenyekiti Mariam Qasim,aliyekuwa waziri wa maswala ya wanawake. Tayo ni chama cha kwanza cha kisiasa nchini Somalia kinachoongozwa na mwanamke. Farmajo anazungumza lugha ya Kisomalia na Kiingereza na ana uraia wa Somalia na Marekani. Mwaka 2012 Mohamed alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi huo ambapo aliangushwa katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo. Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo alizaliwa 1962 mjini Mogadishu kutoka katika familia ya Gedo kusini magharibi mwa Somalia. text: Eric Murangwa Eugene akipigania Rwanda kwenye uwanja wa Nakivubo katika mji mkuu wa Uganda. Alipokuwa na umri wa miaka 18, kipa huyo mchanga aliweka kifo usoni wakati mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu nchini Rwanda yalipoanza nyumbani kwake Aprili 1994. Zaidi ya miaka 25 kuendelea, kurudi Rwanda aliiambia BBC hadithi yake jinsi alivyonusurika katika tukio moja lenye sura zenye damu na kutisha zaidi katika historia ya bara hilo. Aliokolewa na picha Eric Murangwa Eugene akirudi nyumbani kwake nchini Rwanda ambapo alitoroka kuuawa akiwa ameokolewa na picha za yeye akicheza mpira. "Kikosi cha askari kilikuja, kilipiga kelele, kilipiga kelele. Walikuja kutuua," Eric alijadili shida na BBC alikaa kwenye sofa ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi. "Ilikuwa inatisha sana. Bado naweza kusikia mayowe yao hivi sasa", Alilazimishwa kusema uongo sakafuni, Eric na mfanyakazi mwenzake walingojea mwisho ufike - kabla ya bahati kucheza mkono. "Askari walikuwa wakizunguka nyumba wakitupa vitu juu na chini na kutuita kila aina ya majina," aliendelea. "Mojawapo ya mambo yalitokea kuwa albamu ya picha. Ilivutia umati wa mmoja wa wauzaji na akaniuliza 'watu gani kwenye hizo picha?' Nilisema 'ni wachezaji wenzangu'. Niliona uso wake ukibadilishwa mara tu atagundua mimi ni nani. " Sio tu kwamba Eric alikuwa mchezaji anayecheza mpira wa miguu, pia aliichezea Rayon Sports, timu maarufu nchini Rwanda. "Kwa dakika 10 zilizofuata tulikuwa tunazungumza juu ya mpira wa miguu. Dakika chache mapema niliogopa kwa kweli kwa maisha yangu. Kwa kweli picha ziliokoa maisha yangu." Kabla ya mauaji ya kimbari Kipa ambaye alinusurika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994 anatumia mpira wa miguu kuunganisha nchi. Mzaliwa wa Kigali, mji mkuu wa Rwanda, Eric alijiunga na Rayon Sports akiwa na umri wa miaka 14, haraka kuwa kipa wa kwanza wa timu hiyo. Mwezi mmoja kabla ya mauaji ya kimbari alianza alishiriki katika mchezo katika uwanja wa kitaifa wa Amahoro ambao umeteremka katika historia ya mchezo wa Rwanda kwani Rayon Sports ilikabili Al Hilal ya Sudan katika mechi ya Kombe la Washindi wa Kombe la Shirikisho Afrika. Kuingia kwa bao 1-0 baada ya mguu wa mbali, timu ya nyumbani ilishinda 4-1 kufikia mzunguko wa pili."Ninakumbuka jinsi wakati huo ulikuwa mzuri. Uwanja ulijaa uwezo," alikumbuka. "Jamii ya Wanyarwanda ilikuwa imevunjika kimsingi. Lakini tuliposhinda mchezo huo watu walisahau tofauti yoyote walionayo na walisherehekea ushindi wetu kama watu moja."amani haingedumu. Kuanza kwa mauaji ya Kimbari Eric Murangwa Eugene (kulia kulia) na kikosi cha Rwanda Katika siku 100 tu karibu watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda na kabila la Wahutu. Wakitiwa moyo na serikali, walilenga washiriki wa jamii ndogo ya Watutsi, wahutu wastani na wapinzani wao wa kisiasa, bila kujali kabila lao. Watutsi walipewa jina la "mende" kukomeshwa. Familia ya Eric walikuwa Watutsi. "Wakati ulianza ni kitu ambacho kilipangwa na kufanywa na vikosi vya serikali na wanamgambo, lakini ndani ya wiki chache watu wa kawaida walihimizwa kuwa sehemu ya mashine ya mauaji ya kimbari," alielezea. "Tulifukuzwa na majirani na marafiki na katika visa vingine familia walikuwa na mahali pa kujificha." Wakati huo, kadi za kitambulisho zilikuwa na kabila la watu juu yao, kwa hivyo wanamgambo waliweka vizuizi vya barabarani na kujipanga na machete na vilabu. "Kila mtaa ulibidi uwe na kizuizi cha barabara," Eric alikumbuka alipokuwa amesimama karibu na kona katika kitongoji chake cha zamani huko Kigali ambacho kimejaa pikipiki zilizojaa maegesho. "Mmoja wa majirani, mtu anayeitwa Tifu, aliongozwa na watu wawili ambao sikujua. "Alishtakiwa kuwa adui wa serikali. Niliangalia vitendo vya kwanza kisha nikagundua kile kinachotokea na kisha nikaenda zake. "Mahali hapo, tangu siku hiyo, ikawa uwanja wa mauaji." Ndugu wa Eric wa miaka saba, Irankunda Jean Paul, alikuwa mmoja wa wale waliopoteza maisha pamoja na watu wapatao 70 wa familia yake. Kwa kushangaza, Eric anajiona kuwa na bahati kwa sababu wengi wa familia yake wa karibu walinusurika. Kutafuta pakujificha Mlinzi wa zamani wa Rwanda Eric Murangwa Eugene katika siku zake za kucheza mpira Safari ya Eric mwenyewe ya kuishi ilimwona akimbilia katika maeneo mengi kwenda Kigali ikijumuisha Hoteli ya Mille Collines ambayo iliokoa na ilitumika kuwahifadhi maelfu ya watu. Mnamo 2004 hadithi yake iligeuzwa kuwa sinema inayoitwa Hotel Rwanda. Masharti yalikuwa mbali na anasa. Bwawa la kuogelea lilitumika kama chanzo cha maji ya kunywa kwa zaidi ya wakazi 1,000. "Kila chumba kilikuwa na chochote kati ya watu watano na 20", Eric alifunua baada ya kuingia ndani ya chumba kama kile alichokaa ndani kwa wiki kadhaa. "Mapazia yalifungwa kila wakati. Hatukuweza kuangalia nje kwa sababu tuliogopa kupigwa risasi." Kabla ya kukaa katika hoteli hiyo, Eric alikuwa amewageukia wenzi wake wa timu ya Rayon Sports kupata ulinzi katika nyumba zao. Mmoja wao, Longin Munyurangabo, alitoka kumsaidia Eric. "Kunaweza kuwa na ujumbe unaosema kuna tukio, wanamgambo au askari akitembea chini kwa hiyo ningekimbia, kuruka juu (uzio) na wewe ukaanguka upande mwingine, kaa hapo kwa dakika chache," alielezea. "Basi wakati wowote hatari inapokuwa wazi mtu angekupa ishara halafu unarudi. "Nilihitaji msaada, nilihitaji msaada, nilihitaji mtu wa kuonyesha kuwa ananijali kwa sababu hali yangu ilikuwa imeniacha kabisa." Longin asingeweza kuishi kwa mauaji ya kimbari. Inafikiriwa aliuawa akijaribu kukimbia na rafiki yake wa kike wa Tutsi. Mwishowe Eric alihamishwa kutoka Kigali na askari wa Umoja wa Mataifa kabla ya mauaji ya kimbari kumalizika mnamo Julai 1994. Baada ya mauaji ya kimbari Eric Murangwa Eugene na wenzi wenzake wa Rwanda wanajiandaa kwa mechi Pamoja na serikali kupinduliwa, mzozo huo ulienea zaidi ya mipaka ya Rwanda - haswa ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - kama Wahutu milioni mbili walikimbia nchi. Lakini wanamgambo wa Wahutu aliyeitwa Interahamwe bado walitaka kuwafuta Watutsi. Washirika wake wakati mwingine waliiba kurudi Rwanda kufanya mauaji. Eric aliambiwa jina lake likiwa kwenye moja ya orodha yao. "Niliogopa kidogo ni nini kinaweza kuwa huko nje, wangapi kati yao," akaongeza. "Ingawa nilikuwa nimenusurika na vita vilikuwa vimemalizika sikuwa katika hali ambayo ningejisikia salama kweli." Kwa hivyo, akiwa njiani kurudi kutoka kucheza katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Tunisia mnamo Juni 1996, Eric alikimbia na kudai hifadhi, kwanza huko Ubelgiji na kisha Uingereza. Hivi sasa ameishi London kwa miaka 23, kuanzisha hisani yake mwenyewe, taasisi ya Ishami, kusaidia waathirika wa mauaji ya kimbari. Mnamo 2018 alifanywa MBE. "Siku zote nadhani nilinusurika kwa sababu na sababu hiyo ni kujaribu na kutumia uzoefu wa mateso kujenga maisha bora na salama kwa jamii yangu, nchi yangu na ulimwengu kwa jumla," aliendelea. Eric sasa anatumia mpira kujaribu kuponya mgawanyiko uliosababishwa na mauaji ya kimbari - na kuzuia kutokea tena. "Mpira wa miguu kwangu ni kifaa chenye nguvu kuleta mabadiliko kwa watu, kushawishi watu kwa dhati na ninaitumia kuhakikisha kuwa watoto wangu na watoto wa marafiki na majirani wataelewa hatari ya mgawanyiko. "Sio kitu ambacho unaweza kumaliza katika muda wa miaka mitano, 10 au hata 20 lakini nimefurahishwa na yale ambayo tayari yamepatikana." Watu wakati mwingine kuna muda wanaona ni utani wa mpira wa miguu kuwa suala la maisha na kifo "lakini kwa nahodha wa zamani wa Rwanda Eric Murangwa Eugene MBE, taarifa hiyo sio jambo la kuchekesha. text: Tangazo hilo lilifanywa na wapatanishi moja kwa moja katika runinga siku ya Jumatatu usiku na kuthibitisha ripoti kutoka siku ya Ijumaa kwamba pande hizo mbili ziliafikiana. Serikali hiyo itakua na mawaziri 66. Hao ni pamoja na waziri mkuu Sylvestre Ilinkumba ambaye alichaguliwa na bwana Kabila. Mawaziri 42 watatoka katika chama cha kabila huku 23 wakitoka katika muungano wa bwana Tshisekedi. Majina ya watakaoshikilia nyadhfa hizo bado hayajatolewa. Hatua hiyo inajiri miezi saba baada ya muungano wa bwana Tshisekedi kwa jina CACH kushinda uchaguzi huo. Maswali yaliulizwa wakati huo kuhusu matokeo hayo huku kukiwa na madai kwamba bwana Tshisekedi alifanya makubaliano ya kugawana mamlaka na bwana Kabila kabla ya uchaguzi huo. Duru zinaelezea kwamba huenda Rais Tshisekedi atamteua waziri wa mambo ya ndani, waziri wa mambo ya nje, yule wa bajeti na uchumi na gavana wa benki kuu, huku Joseph Kabila akiteua waziri mkuu, wizara ya ulinzi, sheria, fedha na akiba. Mgombea aliyechukua nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi huo Martin Fayulu alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kutotambua matokeo hayo na kutishia kufanya maandamano. Taarifa yake ilijiri baada ya ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha ushindi wa mgombea mwengine wa upinzani , Felix Tshisekedi . Muungano wa Afrika ulisema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa. Bwana fayulu sio mgombea pekee ambaye anaamini kwamba yeye ni muathiriwa wa wizi wa kura huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi. Mahakama ya kikatiba nchini humo iliidhinisha ushindi wa uchaguzi huo Ilikataa ombi la rufaa iliowasilishwa na Martin Fayulu . Licha ya uamuzi wa mahakama hiyo, bwana Fayulu alisema kuwa yeye ndio mshindi wa uchaguzi huo wa urais. Bwana Fayulu pia alihoji kwamba jamii ya kimataifa haitambui matokeo rasmi ya uchaguzi huo. Mahakama ilisemaje? Mahakama ilisema kuwa bwana Fayulu alishindwa kuthibitisha kuwa tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo bandia. Iliendelea na kumtanagaza Felix Tshisekedi kuwa rais aliyechaguliwa kwa wingi wa kura. Ghasia zimetokea kila kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi katika taifa hilo. Lakini thibtisho la matokeo rasmi ya uchaguzi huenda likaonyesha kubadilika kwa uongozi kihalali tangu DR Congo ijipatie uhuru wake kutoka kwa taifa la Ubelgiji 1960. Bwana Fayulu alihoji kwamba Bwana Tshisekedi alikuwa amefanya makubaliano ya kugawana mamlaka na rais Joseph Kabila, hatahivyo upande wa Tshisekedi umekana hilo. Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamekubaliana kuunda serikali ya muungano. text: Aretha Franklin afariki akiwa na umri wa miaka 76 Mwanamuziki huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2010 na alitangazwa kuwa anaumwa hapo mwaka jana wakati akistaafu katika muziki. Ni kwa nini China inataka kuubomoa msikiti huu mpya Mambo muhimu kuhusu ugonjwa wa zinaa unaozua wasiwasi duniani Muziki wake ambao ulijulikana zaidi ulikuwa ni 'Respect and Think' ambao ulikuwa katika nyimbo 20 bora zilizopendwa zaidi nchini Marekani kwa miongo saba. Aretha Franklin alifanya onyesho lake la mwisho mwaka 2010 Aretha aliweza onyesho lake la mwisho mwezi novemba katika gala iliyoko mjini New York akiwa amesaidiwa na taasisi ya Elton John ' Elton John Aids Foundation' Aretha alizaliwa Memphis na alianza kuimba kama muimbaji wa dini na mpiga kinanda na alikuwa muhubiri katika sherehe za ubatizo. Franklin alianza kufundishwa katika umri mdogo kuwa nyota wa mziki wa dini kama ilivyokuwa kwa Mahalia Jackson na Clara Ward. Aretha Franklin akiimba wakati wa tamasha za Tribeca Film Festival Opening Gala premiere mwaka 2017 Franklin aliweza kuhangaika kupata umaarufu katika umri mdogo akiwa chini ya rekodi za Columbia ambazo zilijitahidi kuondoa aibu aliyokuwa nayo na kuiweka sauti yake inayovutia kuweza kung'ara duniani. 'Utalii wa Kenya umekomaa kushinda Tanzania' Mwanamuziki Elton Jon ameandika salamu zake za pole katika ukurasa wa insagram na kusema kifo cha Aretha Franklin kimeshtua kila mmoja anayependa muziki wa kweli. Franklin aliwavutia mamilioni ya watu Muziki kutoka moyoni ,kwenye nafsi na kanisani. "Sauti yake ilikuwa ya kipekee,jinsi alivyokuwa anapiga piano kwa ufanisi...nilimpenda na nilithamini talanta yake .Mungu ambariki na salamu zangu za pole kwa familia"Elton. Aretha Franklin ni malkia wa muziki wa taratibu 'queen of soul' na alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika Rock na Hall of Fame amefariki dunia huko Detroit akiwa na umri wa miaka 76. text: Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari hii leo Oktoba 20 kuwa kuachiwa kwa Mo ni mwanzo wa kuwanasa wahalifu hao na kjuahidi kuwapata wakiwa wazima au wamekufa. "Mbio ukizianza sharti uzimalize. Huu ni mwanzo tu. Hao wahalifu wanaotaka kuchafua jina la nchi yetu lazima tuwatie nguvuni." Sirro amesema upelelezi umeimarishwa kwa kushirikiana na mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol. "Nataka niwaambie (wahalifu) yawezekana wananisikiliza hivi sasa kuwa, popote watakapoenda tutawanasa. Wakienda Afrika Kusini tunao, Kenya tunao, Uganda tunao hata Msumbiji, popote pale tutawakamata maana tayari tunaushirikiano na wenzetu." IGP Sirro amesema taarifa za kiupelelezi alizozitoa jana juu ya gari lilotumika kumteka Mo Dewji Alhamisi ya wiki iliyopita na dereva aliyekuwa analiendesha lilipoingia Tanzania limesukuma watekaji hao kuogopa na kumwachia huru Mo. "Tayari tunamjua dereva, tunamjua mmiliki wa gari...tumeweka wazi picha za gari. Wkaona hawana namna zaidi ya kumwachia tu. Lakini kama nilivyosema nitawapata na kuwagonga na sheria wakiwa wazima au wametangulia mbele ya haki (wamekufa)." Kuchoma gari moto Jana kamanda Sirro alionesha picha za gari aina ya Toyota Surf akisema wanaamini ndilo lilitumika kumteka Mo kutokana na picha za CCTV. Gari hilo lilikuwa na namba za usajili za AGX 404 MC, BBC ilifanya uchunguzi na kugundua ni nambari za usajili za nchi ya Msumbiji iliyopo kusini mwa Tanzania. Kwamujibu wa polisi gari hilo tena hii leo lilitumika kumtoa Mo kwenye eneo ambalo alikuwa anashikiliwa mpaka eneo la Gymkhana ambapo walimtelekeza mishale ya saa nane usiku. Mo inadaiwa alitumia simu ya moja ya walinzi katika eneo la karibu kumpigia simu baba yake na kufuatwa kisha kutoa taarifa polisi. Sirro amesema mara baada ya kumuachia, wahalifu hao walijaribu kuharibu ushahidi kwa kulichoma gari hilo lakini ilishindikana. "Mkienda pale eneo la tukio mtaliona hilo gari, kuna madumu ya mafuta, walijaribu kuliwasha moto lakini ikashindikana." Polisi wanaarifu kuwa walikuta ndani ya gari hilo bunduki moja na bastola tatu zilizokuwa na jumla ya risasi 32. Watekaji walitaka pesa Sirro pia amewaambia waandishi wa habari kuwa waliomteka Mo Dewji walifanya hivyo kwa lengo la kujipatia pesa. Sirro amesema bilionea Mo aliwapa nambari ya simu ya baba yake mzazi mzee Gulam ili waongee nae juu ya hilo lakini hawakupiga simu wakihofia kunaswa na polisi. "Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana..." amesema Sirro na kuongeza, "...walimwambia wanataka pesa, alipowauliza shilingi ngap ihawakusema. Aliwapa nambari ya simu ili waongee na baba yake lakini waliogopa kwa sababu wanafahamu ulinzi wetu ni imara na tungewakamata." Utata waibuka gari alilotekewa Mo Dewji Kamanda Sirro amesema watu hao waliokuwa wakimshikilia Mo walikuwa watatu, wawili walikuwa wakiongea Kingereza na mmoja akiongea Kiswahili kidogo. Mkuu wa polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa awali alisema Mo alibainisha kuwa lafudhi za watu waliokuwa wakimshikilia ni kama za watu wa mataifa ya kusini mwa Afrika. Polisi nchini Tanzania wamesema watafanya kila wawezalo kuwatia nguvuni watu waliomteka na kumshikilia bilionea Mohammed Deji, Mo, kwa siku tisa. text: Serena Williams alirudi katika tenisi mwezi Februari baada ya likizo ya mwaka ,mmoja ambapo alimzaa mwanawe wa kwanza. Bingwa huyo mara 23 wa taji la Grand Slam alitoa madai hayo katika ujumbe wa twitter baada ya maafisa wa kukabiliana na dawa za kusisimua misuli kumtembelea. Raia huyo wa Marekani alikuwa ameonyesha kukerwa kuhusu kiwango cha vipimo anavyofanyiwa mapema mwezi huu. "Kati ya wachezaji wote imethibitishwa kuwa mimi ndio nafanyiwa vipimo vingi zaidi, Ubaguzi nadhani,'' alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36. Taarifa iliochapishwa na tovuti ya Deadspin mwezi Juni ilibaini kwamba Williams amepimwa licha ya kutokuwa katika mashindano na shirika la kukabiliana na utumizi wa dawa za kusisimua misuli la Marekani katika matukio matano 2018. Pia limedai kwamba mchezaji huyo hakuwepo wakati maafisa wa Usada walipomtembelea nyumbani mnamo tarehe 14 mwezi Juni -mtu anayefanya vipimo hivyo aliwasili nyumbani kwake saa 12 mapema zaidi ya muda walioafikiana. Baadaye vipimo hivyo viliorodheshwa kuwa 'vipimo ambavyo havikufanyika-vitatu kati ya hivyo vilikiuka vipimo vya Usada . Wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hiyo ya Deadspin, Williams alifanyiwa vipimo mara mbili zaidi ya wachezaji wengine nyota -ikiwemo wanaume na wanawake-pamoja na bingwa wa taji la US Open Sloane Stephens na dadake Venus Williams. Williams aliulizwa kuhusu matokeo ya ripoti hiyo wakati wa mashindano ya Wimbledon mapema msimu huu wa joto. "Sikujua kwamba nilifanyiwa vipimo mara nyingi zaidi ya mchezaji mwengine yeyote yule'' , alisema bingwa huyo mara saba ambaye alipoteza kwa Mjerumani Angelique Kerber katika fainali. Serena Williams amesema kuwa yeye ni mwathiriwa wa ubaguzi kwa kuwa ndiye mchezaji anayefanyiwa vipimo vya mara kwa mara vya matibabu ikilinganishwa na mchezaji mwengine yeyote yule katika mchezo wa tenisi nchini Marekani. text: Baadhi wa wananchi wakikimbia kimbunga Matthew Bw Scott ametoa wito kwa wakazi wa jimbo hilo kujiandaa kuhama makwao zoezi ambalo ndilo litakalokuwa kubwa zaidi katika historia ya jimbo hilo. Msongamano mkubwa wa magari na watu umetokea katika barabara huku watu wakihamia maeneo ya bara. Wakazi katika jimbo la Carolina Kusini pia wametakiwa kuhama maeneo yaliyo hatarini. Gavana Nikki Haley amesema watu 250,000 watahamishwa kutoka maeneo ya pwani. Rais wa Marekani Barack Obama amesema kimbunga hicho kinaweza kuwa hatari sana na kuwataka wakazi wa eneo hilo kufuata ushauri unaotolewa na mamlaka. Shule zimefungwa na wagonjwa wametolewa katika baadhi ya hospitali. Kimbunga kikubwa cha mwisho kukumba jimbo la Florida kilikuwa ni Katrina miaka 10 iliyopita. Mkazi wa Florida akijiandaa kuhama Kimbunga Matthew tayari kimepiga mataifa ya Haiti na Cuba. Watu kumi wamethibitishwa kufariki nchini Haiti lakini hali halisi ya uharibifu na maafa yaliyotokea badi haijajulikana. Watu wanne wamefariki katika Jamhuri ya Dominika. Gavana wa jimbo la Florida nchini Marekani, Rick Scott ameonya kuwa uharibifu utakaotokea utakuwa mkubwa sana ikiwa kimbunga Matthew kitapiga jimbo hilo. text: Bw Trump aliushangaza ulimwengu Aprili alipotangaza kwamba amekubali mwaliko wa kukutana moja kwa moja na Bw Kim. Wawili hao awali walikuwa wamerushiana matusi na vitisho. Ufanisi huo ulitokea baada ya mazungumzo ya kihistoria kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini. Trump ametangaza hilo saa chache baada yake kuwakaribisha nyumbani Wamarekani watatu ambao wamekuwa wakizuiliwa na Korea Kaskazini ambao waliachiliwa huru na kuruhusiwa kurejea nyumbani. Waliachiliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo mjini Pyongyang kupanga na kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mkutano huo wa Trump na Kim Jong-un. Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Singapore tarehe 12 Juni. text: Uhaba wa vitu muhimu majumbani Uganda, uliwafanya wafanyabiashara kutaka usafiri bora wa kuvusha bidhaa kama sukari na chumvi, masafa ya kilomita moja hivi kutoka Kenya, eneo la Busia. Boda Boda ikazalika. Kama biashara ndogo ya faida, bodaboda inavutia vizito na mabepari kwa mikopo;. Kwa wingi wake, inavutia wenye vyeo na vyama; kwa wepesi wake, inavutia wahalifu. Kwa hesabu za mwaka 2013, Uganda ilitumia zaidi ya $30m kuagiza pikipiki, siku hizi zinaundiwa nchini. Huku 70% ya Waganda wakitegemea uchukuzi wa umma, teknolojia ya kurahisha usafiri ikizidi kusasishwa, mustakabali wa bodaboda ni mzuri, licha changamoto za utovu wa sheria barabarani, ajali, na uhalifu. Tangu bodaboda izinduliwe, kama mfumo wa uchukuzi miaka 47 iliopita, sasa ni ya pili kwa ajira, baada ya kilimo. Kama kiserema katika kilimo, mwanzo duni wa bodaboda, ulikuwa Baskeli. Neno Boda Boda limetoka wapi? Asili ya neno bodaboda, mwasisi wa mfumo huo, Pascali Bwire, anasema, ilikuwa utashi wa wafanyabiashara kuvuka kienyeji masafa ya maili moja, kati ya mpaka wa Uganda na Kenya kwa baskeli, kubeba bidhaa kama sukari, chumvi, unga na sabuni mwaka 1972. Biashara 'nzuri' wakati huo. Leo bodaboda ime-sasishwa, toka kengele na magurudmu mawili ya spoki, hadi Pikipiki; na si mpakani tu. Imesambaa mijini na vijijini Uganda. Inakisiwa nusu milioni ziko ndani na kuizunguka Kampala peke yake. Ni uchukuzi wa uzito na haraka zaidi, kupita njia ya vichochoro, panda na shuka vilima, inafika gari zisikofika. Maelfu ya wapanda bodaboda, wendeshaji, hasa vijana wanaume, wanapata ajira: kama mwajiriwa, au mshirika, au mfanyabiashara pekee, kama huyu Kasibante. Yeye anajitegemea; anatumia mfumo wa tangu zamani kupata wateja: watu wamjuaye, simu ya mkononi, na kuota njiani. Teknolojia imeingilia. Huduma hii mpya, bodaboda za kuitwa, unaendeshwa na mashirika mfano Taxify, Safeboda, Uber. Inakisiwa zaidi ya bodaboda 10,000 ni wanachama wa mashirika hayo, yakielezwa kama salama, haraka, bei nafuu na ni mustakabali wa bodaboda. Ingawa yasemwa, kiingiacho mjini si haramu, kampeni ya upinzani, chini ya kundi la Bodaboda Industry Uganda (au BIU) inadai, mpango wa Taxify, Safeboda, Uber na wengineo, kutumia simusmati na app, ni wa kuwatapeli wendeshaji. Katika Uganda, 85% ya wendeshaji bodaboda, ni waajiriwa, huwategemea matajiri au wako chini ya shirika. Mwanzoni bodaboda ilibaini mgawanyo wa kijamii, si tu kiajira lakini pia kiabiria, kama usafiri wa watu wa chini. Mwimbaji na mtangazaji mashuhuri wa zamani, hayati Elly Wamala, aliyakisi hayo katika wimbo wake, boda-boda: Ubeti unasema, 'bodaboda hutoza pesa sahili, ili asikukamue na kukufanyia ngumu. Na katika wimbo kusema, hawa ni watu wa manufaa sipendi watetwe; sisi akina-yahe hatumudu gari mpya, bodaboda hakika zimetufaa kabisa; sisi makabwela zimetuponya…' Ukweli wa mambo, hata wenye vyeo na vyao siku hizi wanapanda bodaboda, kama si kwa lolote jengine, asichelewe endako. Licha ya kutanuka tasnia ya bodaboda nchini Uganda lakini bado wadadisi wanasema uchumi wa bodaboda unatoa mchango kidogo tu katika ukuaji wa uchumi. Hilo ni la kuvaliwa njuga na wakuu. Chimbuko ya bodaboda ni utashi wa wajasiriamali kuvuka mpaka wa Uganda kwenda Kenya, mwaka 1972 - muda mfupi baada ya Idi Amin kuipundua serikali ya Milton Obote katika 1971. text: Uganda Cranes watakuwa nyumbani kuvaana na Taifa Stars ya Tanzania siku ya Jumamosi katika mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Afcon 2019. Kocha mpya wa Taifa Stars ya Tanzania mchezaji maarufu wa zamani wa Niigeria Emmanuel Amunike atakuwa na kibarua kigumu katika mechi ya kwanza kutokana na rekodi safi ya Uganda maarufu The Cranes. The Cranes ndio timu pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki kushiriki mashindano hayo miaka miwili iliyopita nchini Gabon. Timu hizo mbili zipo katika kundi L linaloongozwa na Uganda yenye pointi tatu baada ya kuifunga Cape Verde inayoshika mkia. Tanzania na Lesotho wote wana pointi moja baada ya kutoka sare jijini Dar es Salaam. Uganda watakuwa wanamtegemea mshambuliaji wao Emmanuel Okwi ambaye anachezea klabu ya Simba ya Tanzania. Okwi alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Tanzania msimu wa 2017/18. Taifa Stars kwa upande wao wanamtegemea nahodha wao Mbwana Samatta ambaye anang'ara na klabu ya Genk ya Ubelgiji. Taifa Stars itamtegemea Mbwana Samatta anayekipiga kwenye klabu ya Genk ya Ubelgiji kuongoza mashambulizi dhidi ya Uganda Cranes. Historia inaibeba zaidi Uganda ambayo imeshinda mara 29 kati ya mechi 53 baina ya timu hizo mbili. Tanzania imeshinda mechi 10. Taifa Stars na Cranes wametoka sare mara 14. Kenya vs Ghana Nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama ataukosa mchezo dhidi ya Ghana kutokana na sababu za kiafya. Kwa upande wa Kenya watashuka dimbani Moi Kasarani bila nahodha wao Victor Wanyama anaekipiga ligi ya England na klabu ya Tottenham Hotspurs. Wanyama amekuwa majeruhi kwa muda mrefu na hivi karibuni ameripotiwa kuanza kufanya mazoezi. Kenya maarufu kama Harambee Stars ina mtihani mgumu zaidi baada ya kushangazwa na Sierra Leone kwa kufungwa 2-1 katika mchezo wa awali wa kundi F. Ghana, wanaofahamika kama Black Stars walianza kampeni yao kwa kuwabamiza Ethiopia kwa goli 5-0. Mara ya mwisho Kenya kukutana na Ghana ilikuwa mwaka 2005 katika mechi ya kirafiki iliyomalizika kwa sare ya 2-2. Kwa namna yeyote ile mchezo wa kesho ni wa kufa na kupona kwa Kenya katika harakati za kutafuta nafasi ya kutinga fainali za mwakani zitakazopigwa nchini Cameroon. Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa mwaka 2005 katika mechi ya kirafiki iliyomalizika kwa sare ya 2-2. Timu mbili za juu katika makundi yote ndizo zitakazofuzu kwenye mashindano ya Afcon 2018. Katika michezo mingine, Burundi itaminyana na Gabon Jumamosi pia. Siku ya Jumapili Rwanda watavaana na Ivory Coast huku DRC wakicheza dhidi ya Liberia. Vumbi litatimuka Jumamosi jijini Kampala ambapo mataifa jirani ya Tanzania na Uganda wataminyana kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2019. text: Bwana Bensalah atakuwa kaimu rais wakati kipindi cha mpito ambapo uchaguzi mpya utaandaliwa. Lakini yeye sio maarufu na waandamanaji ambao walikongamana katika maandamano hayo makubwa ambayo yalimngatua mamlakani bwana Bouteflika. Kwa nini maandamano yamefanyika licha ya tangazo Wanamchukulia bwana Bensalah kuwa mwandani wa rais huyo aliyeoindolewa madarakani. Na dakika chache baada ya tangazo la uteuzi wa Bensalah waandamanji walirudi barabarani mjini Algiers. Abdelaziz Bouteflika alijiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchini mwake. Tayari alikuwa amefutilia mbali mpango wa kugombea muhula mwingine kutawala kutokana na kukuwa kwa upinzani. Bouteflika alitangaza kutowania muhula mwengine Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari aliondoa mipango yake ya kusaka awamu ya tano madarakani, wakati upinzani dhidi ya serikali yake ukiongezeka. Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi. Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma. Chama tawala na jeshi viliunga kuondolewa kwake madarakani Chama tawala nchini Algeria FLN kiliunga mkono kuondolewa madarakani kwa rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye ametajwa kuwa mgonjwa na hivyobasi kutoweza kuongoza. Uamuzi huo wa FLN ulijiri siku moja baada ya mkuu wa jeshi nchini humo Luteni Ahmed Gaed Salah kusema kuwa uamuzi wa kikatiba unafaa kufanywa kumuondoa afisini rais huyo. Bouteflika ambaye yuko chini ya shinikizo kali baadaye alikubali kujiuzulu baada ya marekebisho ya kikatiba kupitishwa. Awali Abdelaziz Bouteflika, amepeleka mbele uchaguzi wa urais uliotakiwa kufanyika tarehe 8,april na kusema kuwa hatagombea tena, Nia ya kugombea kwake ilizuia maandamano ya nchi nzima kwa wiki kadhaa sasa. Ameongoza Algeria kwa miaka 20 sasa, lakini hajaonekana muda mrefu katika maeneo ya wazi , kutokana na ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2013. Bunge la Algeria limemteua spika wa bunge kuu Abdelkader Bensalah, kumrithi rais Abdelaziz Bouteflika ambaye alilazimishwa kustaafu baada ya kuhudumu kwa miaka 20. text: Picha ya mshukiwa Wayne Rooney baada ya kukamatwa na polisi wa Wilaya ya Loudoun Mchezaji huyo wa zamani wa England alifanya hivyo akiwa safarini kwenye ndege. Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United alikamatwa 16 Desemba katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles jimbo la Virginia akirejea kutoka safari ya siku moja nchini Saudi Arabia. Rooney, 33, alishtakiwa na akalipa faini ya $25 na gharama ya kesi ya $91 mnamo 4 Januari kwa mujibu wa nyaraka za mahakama kutoka Mahakama ya Hakimu ya Wilaya ya Loudoun. Taarifa ya msemaji wa mchezaji huyo imesema : "Akiwa safarini kwenye ndege Wayne alimeza tembe alizokuwa ameagizwa na daktari kuzinywa na akachanganya na pombe jambo ambalo lilimfanya kuchanganyikiwa alipowasili uwanja wa ndege. "Polisi alimpata katika hali hiyo na akamkamata kwa kosa dogo la uvunjifu wa amani. "Alipokezwa faini ya moja kwa moja ya kawaida na akaachiliwa huru muda mfupi baadaye katika uwanja huo wa ndege. Kisa hicho sasa kimehitimishwa. "Wayne angependa shukrani zake kwa jinsi kisa hiki kilishughulikiwa na wahusika wote zipokelewe." Rooney, anayechezea klabu ya DC United inayocheza Ligi Kuu ya Marekani na Canada alishtakiwa kosa la ngazi ya 4 ambazo adhabu yake ya juu zaidi ni faini ya $250. Rooney alikuwa amepigwa marufuku kutoendesha magari kwa miaka miwili Septemba 2017 baada yake kukiri kwamba alikuwa ameendesha gari akiwa mlevi eneo la Cheshire, Uingereza. Mshambuliaji huyo alihamia Marekani Juni 2018 baada ya kutia saini mkataba wa miaka mitatu na nusu na DC United. Wayne Rooney alivyofunga bao dhidi ya Gor Mahia Rooney aliongoza klabu hiyo kufika hatua ya mechi ya muondoano wa baada ya msimu msimu punde baada ya kujiunga nao, ambapo walishindwa mechi yao ya kwanza, mchezaji huyo wa zamani wa Everton akipoteza mkwaju wa penalti dhidi ya Columbus Crew. Taarifa kutoka DC United imesema: "Tunafahamu kuhusu taarifa zinazodokeza kwamba Wayne Rooney alikamatwa Desemba. "Tunafahamu hamu ya vyombo vya habari kutaka kujua zaidi kuhusu suala hili lakini tunaamini hili ni suala la faragha kwa Wayne ambalo DC United italishughulikia kwa mifumo ya ndani. Hatuna jambo jingine la kusema kuhusu hili." Wayne Rooney alikamatwa baada ya kupatikana akiwa amelewa na "kukanganyikiwa" baada ya kunywa dawa za kupa usingizi na pombe kwa pamoja, msemaji wake amesema. text: Mangi Meli (kushoto) pichani na wake zake alinyongwa na Wajerumani mwaka 1900 Mangi Meli alinyongwa baada ya kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni na baadae kichwa chake kukatwa na kupelekwa Ujerumani. Fuvu lake yawezekana kuwa ni moja kati ya mafuvu mengi yaliyopo kwenye makumbusho moja kubwa jijini Berlin. Wanaharakati wanataka fuvu hilo lirejeshwe ili lipate mazishi ya heshima anayostahili kama shujaa nyumbani kwao Moshi, kaskazini ya Tanzania. Isaria Meli, mwenye miaka 87 ni mjukuu wa Chifu huyo wa jamii ya Wachaga amezitaka serikali za Tanzania na Ujerumani kushirikiana ili kuwezesha kupatikana na kurejeshwa kwa fuvu hilo. Isaria Meli, 87, ni mjukuu wa Mangi Meli na anatamani kuona fuvu la babu yake likirudishwa. Isaria alifanyiwa vipimo vya DNA jijini Berlin baada ya kukaribishwa na Wakfu wa Urithi wa Utamaduni wa Prussia (maarufu kama SPK) ambao unahifadhi mabaki ya mafuvu yalichukuliwa na wakoloni wa Kijerumani. SPK tayari imeorodhesha mafuvu sita ambayo yanaaminika kutokea Moshi na yalihifadhiwa katika kipindi ambacho Chifu huyo aliuawa. Mafuvu yote hayo yameandikwa "Dschagga/Wadschagga" ikimaanisha Wachaga, ambalo ndilo kabila la Mangi Meli. Watafiti wataangalia kama vinasaba vya DNA vya Isaria vitaendana na moja ya mafuvu hayo. Majibu yanatarajiwa kupatikana ndani ya miezi sita ya mwanzo ya mwaka ujao, 2019. Ujerumani na mafuvu kutoka Afrika Mwanzoni mwa karne iliyopita, maelfu ya mafuvu kutoka makoloni ya Mjerumani ya Afrika yalipelekwa Berlin. Mafuvu hayo yalikuwa ni sehemu ya utafiti wa kibaguzi ambao hivi sasa unalaaniwa. Baada ya kupitia katika mikono tofauti ya umiliki, mafuvu hayo 5,500 ikiwemo 200 kutoka Tanzania yalikabidhiwa kwa SPK mwaka 2011. Wakfu huo sasa unachunguza sehemu hasa mafuvu hayo yalipotokea. Mpaka sasa bado ni kitendawili kujua hasa ni nini kilitokea kwa fuvu la Mangi Meli ambalo limepotea. Mangi Meli ni shujaa kwa watu wake kwa kupambana na utawala wa kikoloni wa Kijerumani Ukiachana na harakati za mjukuu huyo, Mtanzania mwengine, Mnyaka Sururu Mboro amekuwa katika harakati za kulisaka fuvu hilo kwa miaka 40 sasa. Amesema ni muhimu kwake "kulirudisha fuvu hilo kwa watu wake ambao bado wanahuzunika na kifo cha Mtemi wao." Hata hivyo baadhi ya wanaharakati wanamatumaini madogo juu ya kufanikiwa kwa kipimo hicho cha DNA. Mafuvu sita yanayotarajiwa kufanyiwa vipimo yalipelekwa Ujerumani na Luteni Kanali Moritz Merker ambaye aliuwa moja ya maafisa wakuu wa jeshi la Wajerumani mjini Moshi wakati Mangi Meli akinyongwa, mwanaharakati Konradin Kunze ameiambia BBC. Lakini Kanali Merker hakusema kama ana fuvu lolote la Chifu katika rekodi zake, ameongeza Kunze. Isaria Meli amejiandaa pia kupokea habari za kuwa hakuna fuvu lililoendana na vinasaba vyake lakini anaimani kuwa fuvu la babu yake litapatiikana akiwa bado yu hai. Mjukuu wa Mangi Meli, amefanyiwa vipimo vya kinasaba vitakavyosaidia kusaka fuvu la chifu huyo aliyenyongwa na wakoloni wa Kijerumani mwaka 1900. text: Abu Bakr al-Baghdadi Ikiwa ni ukweli utakuwa ni ujumbe wa kwanza kutoka kwake katika kipindi cha mwaka mmoja, na huenda ukamaliza uvumi kuwa aliuawa. Sauti hiyo inawataka watu nchini Iraq kulinda mji wa Mosul dhidi ya jeshi la Iraq, ambao linajaribu kuukomboa kutoka kwa wanamgambo wa Islamic State. Mahala alipo Baghdadi hapajulikani. Baadhi ya maafisa wanasema kuwa huenda yuko ndani ya mji wa Mosul pamoj na wapiganaji wa Islamic State. Jeshi la Iraq linashirikiana na vikosi vingine kuteka mji wa Mosul Haijabainika ikiwa saudi hiyo ni ya Baghdadi. Kuna uvumi kuhusu kuuawa kwake miaka iliyopita, ikiwemo mwaka uliopita wakati jeshi la Iraq lilisema kuwakuwa lilishambulia msafara wake. Mosul ambayo ni ngome ya mwisho ya Islamic State nchini Iraq ndio mji Baghadadi alitangazia kujitawala miaka miwili iliyopita. Mosul, the last IS urban stronghold in Iraq, is where Baghdadi declared a caliphate two years ago. Abu Bakr al-Baghdadi au nee Ibrahim Awwad Ibrahim al-Badri, alizaliwa mwaka 1971 kwenye familia ya kusinni eneo la Samara nchini Iraq. Kundi la Islamic State limetoa kanda ya sauti ambayo linasema kuwa ni kutoka kwa kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi. text: Shirikisho la soka barani Afrika Caf laongeza zawadi za fedha katika mashindano yake Washindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika watapata dola milioni 4,wakati ambapo Ivory Coast ilizawadiwa dola milioni 1.5 iliposhinda taji hilo mwaka 2015. Mshindi wa kombe la vilabu bingwa Afrika atajishindia dola milioni 2.5 badala ya dola milioni 1.5 ambazo Mamelodi Sundowns walijishindia mwezi uliopita. Orodha ya fedha ambazo zitazawadiwa washindi Wakati huohuo fedha za mshindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika upande wa wanawake zitaongezwa na kufikia 80,000 mwaka 2019 kutoka dola 50,000 mwaka huu. Fedha hizo ni chache mno ikilinganishwa na zile inazopewa timu iliomaliza ya mwisho katika kombe la bara Afrika upande wa wanaume. Shirikisho la soka barani Afrika Caf limeongeza kitita cha fedha zinazozawadiwa washindi katika michuano yote kuanzia mwaka 2017 kueleka 2020. text: Katika baadhi ya mataifa elimu ya bure inakabiliwa na changamoto zikiwemo uhaba wa bidhaa msingi kama walimu wa kutosha, vitabu, madawati na hata vyoo Tangu mwaka 1993, wazazi wamekuwa wakilipa walimu ada ya mafunzo na hivi sasa serikali imeamua kuwalipa mishara. Lakini baadhi ya walimu mpaka sasa wana shaka kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo mpya ya serikali. Ndani ya darasa moja katika shule ya msingi ya KILIMANI, iliopo mjini Kinshasa mwalimu anawafunza watoto vokali sita za alpabeti ya lugha ya kifarnsa. Mijinga ni mzazi aliyefika katika shule hii kumuandkisha mtoto wake wa umri wa miaka sita, kama wazazi wengi. 'Nimekuja kumwandikisha mtoto wangu hapa, lakini alikuwa anasoma kwenye shule ya serikali. Kipya ni kwamba sitalipa tena pesa, kwa sababu watoto walikuwa hawasomi tena vizuri, walikuwa wakifukuzwa kila wakati ikiwa sijalipa. 'Nashukuru rais Felix Tshisekedi kwa kile anachotenda kwa sisi raia wa kongo' anasema mzazi huyo. Mwalimu Nsumbu Coneil anafundisha katika shule ya msingi ya Kilimani kwa muda wa miaka kumi na mitano sasa lakini anapokea ada ya $60 kila mwezi kutoka kwa wazazi. Lakini amejumuishwa katika orodha rasmi ya wanfanyakazi wa serkali, mpaka sasa anasema ana shaka na serikali kutekeleza hatua ya kuwalipa mishahara. Kwa mujibu wa Godé Moju mkurugenzi wa shule ya Kilimani, Kwa sasa watoto wengi wameeanza kukaa sakafuni kutokama na ukosefu wa viti na madarasa yamekuwa madogo kuweza kupokea idadi inayoongezeka ya wanafunzi . Hali ambayo anaeleza huenda ikachangia 'watoto kusoma katika mazingira mabovu'. 'Licha ya watoto sasa kuwa wengi, walisema tupokee watoto wote, hivi nimeweka kila darasa wawili wawili, watoto wengi sasa wameanza kukaa chini sababu tu wafundishwe'. Mpango wa elimu bila malipo Tanzania umefanikiwa? Walimu wanatishia kuanza mgomo ikifika tarehe ishinirini mwezi huu ikiwa serkali haitawalipa mshara wa kutosha. 'Amechukuwa (Felix Tshisekedi) hatua hio ya kusema wazazi wasilete tena pesa, sisi tumemunga mkono, hapa kwani nina walimu ambao hawajawahi kupokea pesa kutoka kwa serkali, nadhani ni muhimu kulipa walimu ,kama walimu hawatalipwa haraka, itakuwa athari sana' amesema Moju. Gharama ya elimu ya bure kwa watoto wa shule ya msinigi ni kama 40% ya bajeti ya nchi ambayo ni ya dola za Marekani karibu bilioni sita. Wachambuzi wa uchumi wana shaka iwapo hatua hio ya serikali itafanikiwa lakini rais Felix Tshisekedi ana matumaini mengi. "Itakuwa hatua ambayo itakamilishwa katika miezi michache ijayo. "Mpango huu tumeukuta lakini hakukuwa na bajeti. Hili ndilo nitakalolipa kipaumbele. Congo ina uwezo wa kuongeza mshahara kugharamia elimu na tutalipa" amesema rais Felix tshisekedi. Serikali mpya ilihiadi kufuatiliwa kwa karibu pia uamuzi huu wa rais wa kutoa elimu ya bure kwa watoto wa shule za msingi. Katika taifa la Burundi shule kadhaa zimejengwa chini ya utawala wa rais Nkuruzinzana alitangaza elimu ya bure punde tu alipoingia madarakani lakini viwango vya elimu bado havijaridhisha Funzo gani kutokana na mifano ya kieneo? Congo inafuata mifano ya mataifa mengine katika eneo la Afrika mashariki kama Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi katika kutoa elimu ya bure katika shule za msingi. Katika miongo kadhaa ya nyuma, elimu ya bure katika shule ya msingi iliidhinishwa katika baadhi ya mataifa kusini mwa jangwa la Sahara kama sehemu ya jitihada za kufufua mfumo wa elimu ambao umekuwa ukidorora, na kukabiliana na idadi ndogo ya wanafunzi wanaojiunga shuleni, linaripoti shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni - UNESCO. Hatua hiyo hatahivyo imekabiliwa na changamoto katika utekelezaji wake tangu kuanzishwa katika vipindi tofuati kwenye mataifa hayo, ikiwemo kucheleweshwa kutolewa kwa ufadhili kutoka kwa serikali, uhaba wa walimu wa kuwafunza idadi kubwa ya watoto, uhaba wa vifaa vya kufundisha pamoja na usimamizi mbaya wa miradi hiyo. Katika taifa la Burundi kwa mfano, shule kadhaa zimejengwa chini ya utawala wa rais Nkuruzinzana alitangaza elimu ya bure punde tu alipoingia madarakani lakini viwango vya elimu bado havijaridhisha. Swali kubwa sasa wakati mpango huu unaidhinishwa leo Congo, Je ni vipi hatua hii inaweza kuendelezwa ipasavyo nchini humo? Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo leo inaidhinisha elimu ya bure katika shule za msingi za umma kwa lego la kutekeleza yaliomo katika katiba ya mwaka 2005, ambao inasisitiza elimu ya bure kwa watoto wa shule za msingi. text: DRC wana uzoefu na kiwango kikubwa zaidi ya Uganda Kipute cha kwanza cha namna hiyo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kitatokea siku ya Jumamosi, ambapo majirani Uganda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wataumana kwenye mchezo wa pili wa Kundi A. Nani ataibuka mbabe wa mechi hiyo? Si rahisi kupata jibu kabla ya 90, lakini yawezekana takwimu zinaweza kusaidia kutatua fumbo hilo. Uganda imekuwa na kiwango bora kwa siku za hivi karibuni kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilikuwa timu pekee iliyoshiriki michuano hiyo miaka miwili iliyopita kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata Hivyo waliishia kwenye hatua ya makundi na kuambulia alama moja. Kikosi cha Uganda kinaongozwa na nanodha na mlinda mlango Denis Onyango, anayecheza kandanda la kulipwa nchini Afrika Kusini na ni moja kati ya makipa bora barani Afrika kwa kizazi kilichopo. Onyango pamoja na kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Sebastien Desabre wanaamini wanaweza kushinda mchezo huo. "Yawezekana hatuna kiwango sawa lakini tunaweza kuwahimili uwanjani. Kushinda mchezo wetu wa kwanza litakuwa jambo kubwa sana kwetu. Mashindano yaliyopita yalikuwa magumu kwetu...lakini sasa tuna wachezaji wenye uzoefu," amesema Onyango. Mlinda mlango wa Uganda Denis Onyango anaamini wanaweza kupata ushindi dhidi ya DRC Lakini je, mawazo ya nahodha na kocha wa Uganda yana uhalisia kwa kiasi gani. DRC ni moja ya miamba ya soka barani Afrika, washawahi kufuzu Kombe la Dunia na ni mambingwa mara mbili wa michuano ya bara la Afrika, mwaka 1968 na 1974. Wakati Uganda ikiishia raundi ya kwanza AFCON 2017, DRC ilifika hatua ya robo fainali na kutolewa na Ghana baada ya kufungwa goli 2-1. Miaka miwili nyuma, 2015, DRC ilimaliza mashindano ya AFCON katika nafasi ya tatu, walifanya hivyo pia mwaka 1998. Hata kwa kiwango cha mchezaji mmoja mmoja, DRC wamewaacha mbali Uganda. Ni dhahiri kuwa, kiwango na historia vipo upande wa DRC dhidi ya Uganda. Na endapo historia itajirudia, basi huenda DRC wakafika mbali kwenye mashindano haya. Mara ya mwisho kuchukua kombe hilo mwaka 1974, DRC ilifanya hivyo nchini Misri, na mwaka huu mashindano yamerejea Misri. Timu hizo zipo Kundi A, ambalo linaunda pia na wenyeji Misri na Zimbabwe. Ni rahisi kutabiri kuwa Misri na DRC watamaliza kwenye nafasi mbili za juu. Lakini mpira hudunda, na matokeo ya dakika 90 aghlabu hushangaza wengi. Kipute cha Kombe la Afrika Mashariki na Kati kimewadia, na kuna mechi zinazokutanisha mataifa jirani ambazo ukali wake hauishii kwenye viwanja na wachezaji 22 wanaopambana. text: Mataifa matano ya Afrika yatafuzu kwa kombe la dunia la 2022 nchini Qatar The indomitable lions ya Cameroon imeiwakilisha Africa mara saba katika kombe la dunia, huku Ivory Coast ikishiriki katika kombe hilo mara tatu. Makundi mengine mawili yanashirikisha timu mbili ambazo zimeiwakilisha Afrika katika kombe la dunia. Ghana na Afrika Kusini zitakutana katika kundi G pamoja na Zimbabwe na Ethiopia huku Misri na Angola pia zikikutana katika kundi F pamoja na Gabon na Libya. Misri ilikuwa miongoni mwa wawakilishi watano wa Afrika katika kombe la dunia pamoja na Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia - na zote zinaamini kwamba zina fursa nzuri ya kufika katika raundi ya tatu na ya mwisho mnamo mwezi Novemba 2021. Katika kundi B, Tunisia itakutana na Zambia, Mauritania na Equitorial Guinea huku Nigeria ikikutana na Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya kati na Liberia katika kundi C. Kundi H Senegal itakabiliana na Congo, Namibia na Togo huku Morocco ikichuana na Sudan, na Guinea pamoja na Guinea Bissau katika kundi I. Raundi ya kwanza ya mechi hizo za kimakundi itaanza Oktoba 2020 na kukamilika Oktoba 2021 kabla ya kufanyika kwa michuano ya muondoano Novemba 2021. Ni washindi wa makundi hayo 10 pekee watakaosonga mbele katika mechi za muoandoano ambapo awamu mbili zitaamua wawakilishi watano wa kombe la dunia kutoka Afrika. Mechi za kufuzu zilitarajiwa kuanza mwezi Machi lakini shirikisho la CAF likaahirisha michuano ya Afcon kutoka mwezi Juni hadi Januari. Raundi ya kwanza ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia za Afrika ziliyafanya mataifa yanayoorodheshwa chini kushindana katika awamu mbili huku mshindi akisonga mbele na kujiunga na mataifa mengine 26 ambayo yataendelea katika raundi ya pili. Cameroon au Ivory Coast haitashiriki katika kombe la dunia 2022 nchini Qatar baada ya timu hizo kuwekwa katika kundi moja katika raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia. text: Mwandishi aliyejeruhiwa asaidiwa na wengine wakati wa maandamano Venezuela Idadi hiyo ipo juu zaidi ya ilivyoshuhudiwa 2017, lakini haipo juu sana kama viwango vilivyoshuhudiwa katika miaka ya nyuma wakati mzozo katika mataifa ya Iraq na Syria yalikuwa yakitokota. Kiwango kikubwa cha vifo vya waandishi habari kilichowahi kunukuliwa ni waandishi 155 mnamo mwaka 2006. Takwimu hizi zinajumuisha yoyote anaefanya kazi katika kiwango chochote katika shirika la habari. Kifo cha mwandishi kilichoigusa dunia mnamo 2018 kilikuwa cha mwandishi habari wa Saudia Jamal Khashoggi. Aliuawa Oktoba baada ya kwenda katika ubalozi wa Saudia nchini Uturuki. Mkasa huo ulizusha mzozo wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili na shutuma kali za kimataifa. Na mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana aliyepigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani, baada ya mwanasiasa kuitisha adhabu dhidi yake. Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra. Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana. Ni sehemu gani ilio hatari zaidi? Afghanistan inasalia kuwa nchi ilio hatari zaidi kuishi kama mwandishi habari, kukishuhudiwa vifo vya waandishi 16 mwaka jana. Waandishi 9 walifariki kwa wakati mmoja nchini Afghanistan katika mji mkuu Kabul, baada ya kufika katika eneo la shambulio la bomu kuripoti kuhusu kilichotokea. Kumelipuliwa bomu la pili na mlipuaji aliyesemekana kujifanya kuwa mwandishi habari. Na katika eneo la mashariki mwa Afghanistan, mwandishi wa BBC Ahmad Shah aliuawa katika mojawpao ya mashambulio hayo katika jimbo la Khost. Waandishi habari walifariki Marekani pia mwaka jana. Watano walipigwa risasi katika shambulio dhidi ya ofisi za gazeti la Capital Gazette huko Maryland, lililotekelezwa na mwanamume anayearifiwa alijaribu kulishtaki gazeti hilo miaka kadhaa nyuma. Kutoweza kuvumilia taarifa za habari zinazo chapishwa, umaarufu, pamoja na rushwa na uhalifu ni vigezo muhimu sasa linasema IFJ. Wanachangia "mazingira ambapo kuna waandishi zaidi wa habari wanauawa kwa kuangazia masaibu kwa jamii zao, mijini na hata mataifa, kuliko kuripoti matukio katika maeneo yanayokumbwa na mizozo". Kamati ya kuwalinda waandishi habari (CPJ) huwapiga picha waandishi wa habari waliofungwa gerezani mwanzo wa mwezi Desemba kila mwaka. Takwimu hizi hujumuisha yoyote anayefanya kazi kama mwandishi habari, aliyefungwa kwa shughuli zinazohusiana na kazi yake. Mataifa yenye idadi kubwa ya waandishi waliofungwa mnamo 2018 ni pamoja na: Uandishi habari na demokrasia Umoja wa mataifa mwaka huu unaangazia jukumu kuu la uandishi huru wa habari kwa demokrasia hususan wakati wa uchaguzi. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres anasema katika taarifa yake kwamba "hakuna demokrasia iliokamilika pasi kuwepo habari za wazi na za kuaminika." Courtney Radsch, kutoka kamati ya kuwalinda waandishi habari CPJ, anasema kauli za kupinga uandishi habari zimeongezeka katika nchi nyingi akitaja zaidi Ufilipino na Marekani. Anaamini mitandao ya kijamii na intaneti kwa jumla zimechangia katika masaibu yanayowakabili waandishi habari. Katika faharasha yake ya mwaka huu - katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari , kundi la waandishi wasio na mipaka (RSF) wanaitaja hali Marekani kuwa ni 'tatizo'. Marekani imeshuka kwenye orodha ya RSF katika uhuru wa waandishi habari mwaka huu na ni kama ilivyo kwa India na Brazil. Lakini wanaongeza kwamba mataifa yalioshuhudia kiwango kibaya cha uhuru wa vyombo vya habari - kama Venezuela, Urusi na China - zimezidi kudidimia chini mwaka huu. Takriban waandishi habari 95 wameuawa mwaka jana wakiwa kazini, kwa mujibu wa shirikisho la waandishi habari wa kimataifa (IFJ). text: Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Ana ndugu mkubwa aliyezaliwa mjini Landon na wadogo zake waliozaliwa Mjini ,Manchester. Familia yake inadaiwa kuwa na mizizi nchini Libya. Wameishi katika maeneo tofauti mjini Manchester ikiwemo jumba lililopo barabara ya Elsmore katika eneo la Fallowfield ambalo lilivamiwa na polisi siku ya Jumanne. Majirani wamesema vile familia hiyo imekuwa ikipeperusha bendera za Libya katika nyakati tofauti za mwaka. Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 22 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kwenye mulipuko huo ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki. Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi. Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London. Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima. Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi. Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria. Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo. Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga. Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa wanaume, ndio ukumbua mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua watu 18,000 Barabara ya ukumbi huo unuangana na kituoacha treni cha Victoria kati kati mwa mji. Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Ukumbi huo hutumiwa kuandaa tamasha za manyota wakuu kama Ariana Grande nyota wa runinga mwenye umri wa miaka 23 ambaye sasa ni nyota wa muziki wa pop. Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza Mshukiwa wa shambulio la Manchester ametajwa kuwa ,Salman Abedi, ambaye ni mzaliwa wa Manchester mwenye umri wa miaka 22. text: Wanajeshi hao wapya watatoka Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan na Uganda Rais Salva Kiir alichukua hatua hiyo baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Bw Kiir alikuwa awali amekataa kutumwa kwa wanajeshi hao 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini. UN iliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi waaminifu kwa Bw Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Dkt Riek Machar mwezi Julai mjini Juba. Kikosi hicho cha ziada kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho kimekuwa kikihudumu nchini humo. Rais wa Sudan Kusini hatimaye amekubali kikosi cha ziada cha wanajeshi wa kulinda amani kitumwe nchini humo. text: Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili. Gaby mwenye umri wa miaka 28 anasema kuwa ameamua kutangaza jinsia yake ili kuhamasisha watu kuhusu watu wenye jinsia mbili mbali na kutoa hamasa kwa jamii. Ni miongoni mwa wanamitindo wa hadhi ya juu kuzungumzia kuhusu jinsia yake. Watu wenye jinsia mbili hawana viungo vya ndani ama vya nje vinavyowatambulisha moja kwa moja kuwa na jinsia ya kiume ama ile ya kike. ''Nimefikia wakati katika maisha yangu ambapo nimeamua kutangaza jinsia yangu'', alisema Hanne. ''Ni wakati wa watu wenye jinsia mbili kujitokeza, kuondoa uoga na kuzungumzia maswala ambayo yalitukumbuka tukiwa watoto''. Hanne ameshiriki katika kuuza mitindo ya Chanel na Prada na pia amekuwa katika kampeni za Mulberry na Balenciaga. Katiika kanda za video zilizochapishwa katika mtandao wake wa Instagram ,anaelezea kwamba licha ya kuzaliwa na jinsia mbili hajashindwa kupigania kazi yake katika sekta ya mitindo. Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili. text: Watafiti nchini Canada wanasema wamepata ushahidi kwamba wanaume hutatizwa zaidi ya mafua ya kawaida na si kwamba huwa wanajifanya kwamba wamezidiwa. Mtafiti mkuu Dkt Kyle Sue amesema wanaume huenda wana mfumo dhaifu kidogo wa kinga mwilini dhidi ya virusi vinavyosababisha mafua wakilinganishwa na wanawake. Hilo huenda likawa huchangia kulemewa kwao na dalili za mafua kuliko wanawake. Dkt Sue anadokeza kwamba wakati umefika pengine kwa wanaume "kutengewa au kutengenezewa maeneo mahsusi, yaliyo na televisheni na viti vizuri, ambapo wanaweza kuuguza mafua yao hadi wapate nafuu bila usumbufu." Matokeo ya utafiti huo huenda yakafurahiwa sana na wanaume wengi wanaotatizwa na mafua ambao wamehisi kwa muda mrefu kwamba hakujakuwa na watu wa kuwaelewa. Lakini huenda yasiwafurahishe wanasayansi wengi - na wake pengine - ambao bado wana shaka kuhusu iwapo ni kweli kuna 'mafua ya wanaume' au huwa tu katika fikira za wanaume. Utafiti mpya unaashiria kwamba ni kweli wanaume hutatizwa na mafua zaidi ya wanawake, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa dhana kwamba huwa kuna mafua ya wanaume. text: Issa Kapande `Chef Issa' Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu. Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya. Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania. Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande. Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto. "Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara. Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu. Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013."Tulilazimika kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje. Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta. Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania. Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush. Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi. Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa', umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia. text: Ujumbe kutoka kwa mashabiki wa Maradona wakimtakia heri apone haraka Maradona, aliliongoza taifa lake katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 1986,. Alifanikiwa kufanya upasuaji katika ubongo ili kuondoa kuganda kwa damu, mapema mwezi huu. Hata hivyo , tatizo la utegemezi wa pombe limemfanya akae hospitalini kwa muda mrefu. "Jambo zuri ni kuwa Diego yuko sawa sasa," alisema wakili wake, Matias Morla. Wiki iliyopita, Maradona alilazwa katika kliniki ya Ipensa huko Buenos Aires , akiwa anasumbuliwa na anaemia . Rafiki zake wachache tu ndio waliruhusiwa kumtembelea hospitalini. Wakili wake amesema Diego amepitia kipindi kigumu zaidi katika maisha yake na ilikuwa kama miujiza kukuta damu imeganda katika ubongo wake na angeweza hata kupoteza maisha yake. Mchezaji mkongwe Diego Maradona ametolewa hospitali siku ya Jumatano, na kuelekea kliniki ya kurekebisha tabia ili kuacha kutegemea pombe. text: Carles Puyol (kulia) na Pep Guardiola Licha ya kukubali kushiriki kwenye kipindi cha kutangaza mechi ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Iran, na hata kuwasili Iran, Puyol alilazimika kusalia kwenye hoteli baada ya kunyimwa ruhusa kutangaza mchuano huo. Puyol alitarajiwa kushirki kipindi hicho spesheli kwenye kituo cha IRTV 3 akiwa na mtangazaji Adel Ferdosipour. "Namna mnavyojua, nilitarajiwa kuwa na Carles Puyol studioni leo, lakini yuko hotelini kwa sasa. Licha ya juhudi zangu zote, hatukufanikiwa. Tunaomba radhi,"Ferdosipour alisema. Bwana Puyol alifahamishwa na idhaa ya taifa ya IRIB hangeweza kushiriki kwenye kipindi kwani nywele zake zilikuwa ndefu. Idhaa ya taifa ya Iran haina sheria juu ya mtindo wa nywele lakini mambo yanayokinzana na mafunzo ya Kiislamu huzuiwa. Aidha, sheria za shirikisho la soka la Iran zinawazuia wachezaji dhidi ya kuwa na mtindo wa nywele 'unaoeneza mitindo ya kigeni' na wachezaji huonywa dhidi ya kuwa na mitindo ya nywele inayokatazwa. Hii sio mara ya kwanza hali kama hii kushuhudiwa kwenye runinga ya Iran. Miaka miwili iliyopita, kipa wa timu ya taifa ya soka ya ufuo Peyman Hosseini, alizuiwa kushiriki kipindi cha televisheni kwa sababu ya nywele zake. Aidha, alikataa pia kuzifunika. Uamuzi wa kumzuia Puyol unajiri wiki chache tu baada ya mkurugenzi wa IRTV3's Ali Asghar Pourmohammadi, kuondolewa na nafasi yake kupewa afisa mwenye misimamo mikali ya kidini. Hata hivyo naibu mkuu wa idhaa ya taifa (IRIB), Morteza Mirbaqeri amenukuliwa Jumamosi akipinga madai hayo. Shirika la Jam-e Jam daily linalomilikiwa na IRIB, limemtaja bwana Mirbaqeri akisema "Idhaa ya taifa inapinga madai hayo asilimia 100% ". Beki wa zamani wa Barcelona na Uhispania Carles Puyol amepigwa marufuku kushiriki kipindi cha kombe la dunia nchini Iran kwa kuwa na nywele ndefu. text: Kanda ya video ya kiongozi wa genge la majambazi hao kwa jina Gaza akijigamba kuhusu uhalifu aliotekeleza imesambaa katika mitandao ya kijamii na kuwawacha wengi vinywa wazi Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya kiongozi huyu wa genge ambaye polisi wanamtambua kwa jina Seba alias Johnnie alionekana katika kanda hiyo ya video akijigamba kwamba bado yeye ndiye mfalme wa uhalifu nchini Kenya na kwamba hakuna kile ambacho polisi wataweza kufanya. Katika video hiyo Seba ambaye alikuwa akitekeleza operesheni zake kutoka eneo la Mlango Kubwa jijini Nairobi anasikika akiwatishia maafisa wa polisi kwamba atawashambulia na visu. Kiongozi huyo wa genge ambaye kwa sasa anadaiwa kutekeleza uhalifu wake kutoka kaunti ya Tana River anaendelea kujigamba kwamba kufikia sasa ameweza kuiba simu 86 kutoka kwa raia na kwamba maafisa wa polisi walifanya makosa kwa kudai kwamba ameiba simu 46 pekee. Seba ambaye alikuwa ameandamana na wenzake wanne katika video hiyo amewaonya raia wanaopeleka ujumbe kwa polisi kwamba atawashambulia kwa visu iwapo wataendelea kufanya hivyo. Mitandao ya kijamii Wakenya katika mitandao ya kijamii wamewataka polisi kumtafuta Seba na kundi lake wakidai kwamba wameyafanya maisha ya wakaazi wa Nairobi kuwa magumu. ''Maafisa wa polisi wanatakiwa kuchukua hatua za haraka kabla ya kutekeleza vitisho vyao'', Robert Jakoriw aliandika katika mtandao wa facebook. ''Je DCI kinoti yuko wapi, hawa vijana wanafaa kuchukuliwa hatu'' , alisema Frank Rapemo mtumiaji mwengi wa mtandao wa Facebook. Uhalifu Eneo la Kayole jijini Nairobi limesemekana kuwa nyumbani kwa wanachama wa Genge hilo la Gaza , ambalo ni mojawapo ya megenge yanayoogopwa sana eneo la Eastaland. Wakaazi wengi katika eneo hili wanaishi chini ya dola moja kwa siku , hatua inayowashinikiza vijana wengi kujiingiza katika uhalifu. Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya genge hilo la Gaza linaaminika kutekeleza idadi kadhaa ya mauaji na uhalifu katika eneo hilo lakini operesheni zake hazijulikani. Wanachama wake hutumia visu na bunduki kama vifaa vya biashara yao. Genge hilo pia linadaiwa kuanzisha genge jingine la Yakuza ambalo uhusika na uhalifu wa hali ya juu kama vile wizi wa benki na ule wa barabara kuu. Mapema mwaka huu, maafisa wa polisi walikiri kwamba kundi hilo limekuwa likiwatishia wakaazi lakini wamesema kuwa wanatumia kila njia kuimarisha usalama wa wakaazi wa eneo hilo. Raia wa nchini Kenya wamewataka polisi nchini humo kumtafuta mtu ajulikanaye kwa jina Seba na kundi lake na kuchukua hatua dhidi ya genge lao. text: G kwenye tarakimu hizi inawakilisha 'Generation', yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu. Hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu. Lakini wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi. Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991. Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G. Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa chini... Kisha 2G ikaja na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi au arafa Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi. Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service). Na pia simu za wakati huo zilikuwa na teknolojia ya GSM, GPRS, EDGE kama hizi zilizo hapa chini. Kupiga simu kwa video kuliwezekana 2001 3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya smartphone zilianza kuuzwa madukani. Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya. Angalau ilikuwa hatua fulani. Na watu waliweza kupiga simu za video. Ili kufahamu kasi yake au mwendo wake wa upole ulivyokuwa, iwapo ungetaka kupakua filamu ya ucheshi ya David Brent: Life on the Road kutoka kwenye iTunes, ingekuchukua saa tano kupakua faili hiyo ya 4.26GB. 2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu. Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G. Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea. Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa. 5G ndiyo mwendo kasi? Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa. Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee. Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda? Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini? text: Mshambuliaji huyo wa Barcelona amempiku mchazaji mwenza katika klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye ana thamani ya pauni milioni 149. Mshambuliaji huyo wa Barcelona amempiku mchazaji mwenza katika klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye ana thamani ya pauni milioni 149. Mchezaji wa pekee kutoka Uingereza aliyeorodheshwa miongoni mwa wachezaji 10 walio na thamani ya juu duniani ni mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane mwenye thamani ya pauni 122 na Dele Alli mwenye thamani ya pauni milioni 96. Paul Pogba ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United kwa rekodi ya kitita cha pauni milioni 89 ana thamani ya pauni milioni 136.4. Utafiti huo umefanywa na kundi moja la wasomi kutoka CIES. Walitafuta thamani hiyo kupitia viwango vya uchezaji wa wachezaji hao, kama vile umri na urefu wa kandarasi. Cristiano Ronaldo, mshindi wa taji la mchezaji bora duniani yuko katika nafasi ya saba akiwa na thamani ya pauni milioni 111, huku kiungo wa kati wa Real Madrid Gareth Bale akiwa katika nafasi ya 14 na thamani ya pauni milioni 73.8. Pogba ni mchezaji wa pekee aliyeko miongoni mwa 5 bora ambaye hachezei klabu ya Uhispania huku Antoine Griezman akiwa katika nafasi ya tatu na thamani ya pauni milioni 132 naye mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez akiwa wa tano na thamani ya pauni milioni 127. Kuna wachezaji 42 wa klabu za ligi ya Uingereza miongoni mwa 100 bora akiwemo Eden Hazard wa Chelsea mwenye thamani ya pauni milioni 89, Anthony Martial wa Manchester United mwenye thamani ya pauni milioni 81, Raheem Sterling wa Manchester City mwenye thamani ya pauni milioni 75 na Jamie Vardy wa Leicester City mwenye thamani ya pauni milioni 45. Kiungo wa kati wa West Ham Michail Antonio anafunga orodha ya wachezaji 100 wenye thamani ya juu akiwa na thamani ya pauni milioni 31. Neymar ndio mchezaji mwenye thamani ya juu barani Ulaya akiwa na pauni milioni 216 kulingana na utafiti mpya ambao pia unatoa thamani ya wachezaji kumi walio na thamani ya Yuro milioni 100. text: Mchezo huo ulianza kwa Lazio kuwatangulia Juve katika dakika 59, Juve wakasawazisha kupitia Canselo dakika ya 74 na Ronaldo kupiga msumari wa pili na wa ushindi dakika mbili kabla ya mchezo. Ronaldo alisajiliwa kwa dau la pauni milioni 99.2 mwaka jana, na tayari ameshaifungia Juventus magoli 17. Mechi hiyo ilionekana kama Juve wataipoteza, na ingekuwa kipigo cha kwanza msimu huu kwa miamba hiyo. Timu hiyo inayonolewa na Massimiliano Allegri sasa inaonekana dhahiri kunusa ubingwa wa Serie A kwa mara nane mfululizo baada ya timu inayowafukuzia ya Napoli kutoka sare na AC Milan. Tottenham yaangukia tena pua Tottenham wamejikuta wakitupwa nje ya makombe mawili ndani ya siku nne tu. Jana wametandikwa goli mbili kwa sifuri na Crystal Palace katika mzunguko wa nne wa michuano ya FA katika uga wa Selhurst Park. Goli hizo zilifungwa ndani ya dakika 35. Alhamisi iliyopita, Spurs waling'olewa kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Carabao kwa kuchapwa kwa mikwaju ya penati na Chelsea. Spurs walikosa nafasi ya wazi baada ya Kieran Trippier kukosa mkwaju wa penati muda mfupi kabla ya mapumziko. Timu hiyo inayonolewa na Mauricio Pochettino sasa wamepoteza mechi tatu katika nne walizocheza hivi karibuni. Palace wamtwanga kigogo mwengine Palace ilipoteza michezo yake mitano iliyopita dhidi ya Spurs Palace inayonolewa na Roy Hodgson sasa imeshawafunga Manchester City na Tottenham msimu huu na pia imeenda sare na Arsenal na Manchester United. Kubakia kwenye Ligi ya Premia ndio kipaumbele cha kwanza kwa Palace na Hodgson anaamini kiwango chao cha sasa kitawaongoza kufikia malengo. Goli la dakika ya 88 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Cristiano Ronaldo umeifanya Juventus kujisimika kileleni kwa tofauti ya alama 11. text: Ana Brnabic alaumiwa kwa kushindwa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja Ripoti zinasema kuwa mama aliyejifua anayefahamika kama Milica Djurdjic pamoja na mtoto aliyepewa jina la Igor wote wana afya nzuri. Bi Brnabic mwenye umri wa miaka 43 amekuwa ni mwanamke wa kwanza ambaye anajihusisha katika mapenzi ya jinsia moja kuwa waziri mkuu mwaka 2017 mwezi Juni. Kuchaguliwa kwake kuliwashangaza wengi kwa sababu taifa hilo halitambui ndoa za watu wa jinsia moja. "Ana Brnabic ni waziri mkuu wa kwanza ambaye mwenza wake amepata mtoto wakati akiwa madarakani na vilevile ni mahusiano ya kwanza ya jinsia moja duniani kote kupata mtoto," AFP iliripoti. Bi Djurdjic ambaye ambaye anafanya kazi kama daktari, alipata ujauzito kwa njia ya kupandikiza na sio asili. Serbia ni nchi ambayo inafuata mila na desturi na ubaguzi ni jambo ambalo lipo kwa wingi. Katiba ya nchi hiyo imeweka wazi kuwa ndoa inayokubalika ni ya mwanaume na mwanamke na mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja hayatambuliki kitaifa. Wapenzi wa jinsia moja nchini humo wamezuiwa kuasili watoto, ingawa mtu ambaye hajaoa au kuolewa anaweza kuasili mtoto. Nchi hiyo ina sheria ambazo zinawabagua wapenzi wa jinsia moja hivyo kukabiliana na changamoto za kauli za chuki, kukosa haki licha ya wanaharakati wamekuwa wakipinga ukiukwaji huo wa haki. Wakosoaji wamedai kuwa Bi Brnabic hajafanya lolote kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja. Na hajawahi kusema kama atapenda kuhalalishwa kwa ndoa za jinsia moja nchini Serbia. Mpenzi wa jinsia moja wa waziri mkuu wa Serbia Ana Brnabic amejifungua mtoto wa kiume. text: Kutoka New York mpaka Los Angeles na kutoka Washington mpaka Florida, vifaa hivyo viliripotiwa kuwa ni jambo ambalo sio la kawaida na vilitumwa katika bahasha ambazo zinafanana. Hakuna kifurushi hata kimoja ambacho kililipuka na shirika la kijasusi wameanza kufanya uchunguzi. Shirika hilo la kijasusi limeanza msako eneo la Miami, wakati ambao wachunguzi wanajaribu kuona ni nani anahusika na vilipuzi hivyo. Vifaa hivyo vimetumwa kwa watu 8 mashuhuri akiwemo rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na muigizaji Robert De Niro. Maafisa ambao hawakujitambulish majina yao waliviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa wachunguzi wanaamini kuwa inaaminika kuwa kifurushi kimoja kilitumwa kutoka Florida. Vifurushi vya aina hiyohiyo vilitumwa kwa makamu wa rais wa zamani Joe Biden na katibu wa taifa hilo Hillary Clinton, Shirika la kijasusi FBI haijatoa ripoti yeyote kuhusu uchunguzi wanaoufanya. Na haya ndio tunayafahamu. Walengwa ni akina nani? Kifaa cha kwanza kuonekana katika sanduku la barua karibu na nyumba ya bilionea mfanyabiashara Soros huko New york mwezi Oktoba tarehe 22. Bwana Soro ,mfadhili wa chama cha Democratic , amekuwa mara kwa mara akikosolewa kwa kuwa upande wa upinzani. Kifaa hicho kiligunduliwa na mfanyakazi mmoja na baadae kifaa hicho kiliharibiwa na maafisa. Polisi wanasema kuwa vifurushi hivyo vilikuwa vinajumuisha unga wa poda inayolipuka na imetengenezwa na vitu vinavyotengenezwa na bomu. Kamishina wa polisi mjini New York, James O'Neill (katikati), Meya wa New York Bill de Blasio (kushoto) na msaidizi wa mkurugenzi wa FBI William Sweeney (kulia) akiongea na waandishi wa habari Siku iliyofuata idara ya huduma za siri iligundua kuwa kifurushi kilichotumwa kwa bi.Hillary Clinton ambaye alikuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic na katibu wa zamani wa Marekani. Imeripotiwa kuwa uchunguzi wa barua hizo zilizotumwa alimshirikisha mume wake ambaye ni rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton huko Chappaqua, New York. Afisa wa Marekani aliwaambia waandishi wa habari kuwa kilikuwa ni kifaa kinachoweza kulipuka. Kifurushi cha tatu ambacho kilitumwa kwa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, kilitumwa tarehe 24 mwezi oktoba mjini Washington Dc. Vifurushi hivi vilikuwa vinapelekwa katika maeneo ambayo yalilengwa, tamko lililotolewa na idara ya huduma ya siri ilielezea matukio yote mawili. Waandamaji hawakupata vifurushi hivyo wala kupata vitisho vya kupokea vifurushi vipi, idara hiyo iliongeza. Tukio lingine lilitokea katika ofisi za CNN mjini New York ziligunduliwa siku ya jumatano asubuhi baada ya kudhania kuwa kuna bomu lilitumwa katika chumba chao barua. Ilielezwa kuwa mkurugenzi wa zamani wa CIA John Brennan,ambaye huwa anamkosoa rais Trump, alikuwa amepangwa kuonekana katika kipindi cha The network. Polisi wanasema kuwa walikuta bahasha iliyokuwa na unga mweupe wa poda katika kifaa hicho ambacho pia kinafanyiwa uchunguzi. Kipindi kilikuwa hewani wakati kifurushi hicho kilipobainika na kengele ya tahadhari iliposikika, wakati watangazaji wakijadili stori. Baadae siku hiyohiyo, ripoti ziloonyesha kuwa wakili mkuu wa zamani Eric Holder alikuwa ametumiwa kifaa kinacholipuka. Na taarifa nyingine kuwa kuna kifaa kingine kilitumwa kwa Maxine Waters ambaye ni mshirika wa Democratic kimeonekana katika eneo la kupokea barua karibu na mji wa Washington, DC. Kifurushi kingine ambacho kilishukiwa na kiliandikwa jina lake kilionekana Los Angeles. Vifaa vinavyosadikiwa kuwa ni vilipuzi vilikutwa katika sanduku la barua nje ya nyumba ya bwana Soro huko Bedford, New York Siku ya alhamisi, Kifurushi kingine kilitumwa katika mgahawa ambao unamilikiwa na muigizaji Robert De Niro. Baadae FBI walidhibitisha kuwa kuna vifaa vingine ambavyo vilitiliwa shaka vilivyotumwa kwa makamu wa raisi wa zamani Joe Biden huko Delaware. Tunafahamu nini kuhusu vifurushi hivyo? Hakuna kifurushi hata kimoja ambacho kililipuka au kusababisha madhara yeyote mpaka sasa. Vifurushi vyote vilikuwa vimefungwa katika bahasha ya manila, zikiwa zimeandikwa kwa maandishi ya kompyuta na mtumaji akiwa ameandikwa Debbie Wasserman Schultz, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama cha Democratic ingawa jina hilo lilikuwa halijaandikwa kiusahihi. Mwanamke huyo mwanasiasa kutoka Florida ameeleza masikitiko yake kwa jina lake kutumika. Kifaa hicho kilisadikiwa kuwa ni bomu . Kifaa kilichotumwa katika ofisi za CNN ambazo picha yake inaonyesha kifaa hicho kilizungushiwa gundi ya karatasi ya rangi nyeusi. Wakala wa Shirika la kijasusi la FBI Bryan Paarman aliwaambia waandishi wa habari kuwa kifaa hiki kilikuwa kinafanya kazi. Maafisa hawakusema kama vifurushi hivyo vilikuwa ni bomu na wachunguzi wanafanyia kazi kuhakikisha hilo Uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa vifaa hivyo vinavyosadikiwa kuwa ni vilipuzi vilikuwa vinafanana. Kifurushi kilichotumwa katika ofisi ya shirika la utangazaji la CNN mjini New York Hatua gani zimechukuliwa? Matukio hayo yameshukiwa kuwa ni ya kisiasa. Chama cha Conservatives kudai kuwa Democrats wamelenga kuhamasisha chuki kwa kuweka vitisho vya bomu. Rais Trump ameviambia vyombo vya habari kuacha kutoa taarifa zinazohamasisha chuki baada ya tukio hilo kutokea. Lakini kauli yake ilikosolewa na kudaiwa kuwa huwa anatumia lugha ambazo sio nzuri kwa wapinzani na waandishi wa habari. Raisi wa shirika la habari la kimataifa CCN Jeff Zucker alidai White house imekosa kuwa waelewa kabisa na haizingatii suala ya mashambulizi katika vyombo vya habari. Vifurushi kadhaa vinavyodhaniwa kuwa ni vifaa vya vilipuzi ambavyo rais Donald Trump alivikosoa vinaendelea kuchunguzwa na mamlaka nchini Marekani. text: Samatta tayari ameshafunga goli moja kwenye michuano ya Champions League Genk, itakuwa nyumbani Ubelgiji katika dimba la Luminus Arena ikiwakaribisha miamba kutoka Italia klabu ya Napoli. Katika mchezo wake wa kwanza Genk iliangushiwa kichapo kizito cha goli 6-2 ugenini dhidi ya RB Salzburg, huku Samatta akifunga goli moja la kufutia machozi. Katika mchezo huo, Samatta aliweka rekodi binafsi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Champions League na kufunga goli. Napoli wao walianza kwa kuwafunga mabingwa watetezi Liverpool goli 2-0. Hivyo, Genk hii leo watakuwa tena na kibarua kizito cha kuwazuia Napoli. Hata hivyo, japo Genk haijawahi kupata ushindi hata mechi moja ya Champions League katika mara zote tatu walizoshiri michuano hiyo, wamefungwa mechi moja tu nyumbani kati ya sita walizocheza na kutoka sare tano. Napoli pia hawajapata ushindi wakiwa ugenini kwenye hatua ya makundi ya Champions League katika mechi sita zilizopita. Hivyo, japo si ya kutumainia, historia inaweza kuwabeba Genk na kupata walau sare. Kalidou Koulibaly alimkaba Samatta vilivyo Senegal ilipoifunga Tanzania 2-0 kwenye micuano ya Afcon. Mechi ya leo pia itawakutanisha tena Samatta na beki kisiki Kalidou Koulibaly raia wa Senegal. Wawili hao waliminyana kwenye michuano ya Afcon Juni 23mwaka huu ambapo Senegal ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania. Je, Samatta ataweza kumpita Koulibally leo na kufunga goli baada ya kushindwa kufurukuta mbele yake Afcon? Mechi hiyo itapigwa kuanzia saa mbili kasoro dakika tano za usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Tottenham yapigwa 7, Real Madrid yaponea chupuchupu Serge Gnabry alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Tottenham. Katika michezo ya Champions League iliyopigwa jana usiku, klabu ya Tottenham ilipokea kipigo kizito cha 7-2 wakiwa nyumbani jijini London dhidi ya miamba ya Ujerumani Bayern Munich. Kipigo hicho ni anguko kubwa kwa Tottenham ambao msimu uliopita walifika fainali ya michuano hiyo na kufungwa 2-0 na Liverpool. Tottenham ndio walianza kupata bao katika mechi hiyo kupitia mshambuliaji Son Heung-Min ktika dakika ya 12, lakini Joshua Kimmich alisawazisha baada ya dakika tatu tu, Robert Lewandowski akaitanguliza Bayern katika dakika ya 45 na kipindi cha kwanza kuisha kwa matokeo ya 2-1. Kipindi cha pili kilikuwa kichungu mno kwa Tottenham, na mshambuliaji Serge Gnabry alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya wenyeji. Gnabry amecheka na nyavu za Spurs mara nne, na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga idadi hiyo ya magoli katika kipindi cha pili kwenye michuano ya Champions League. Magoli yake alipachika katika dakika za53,55,83, 88. Bao la pili la Tottenham lilipachikwa kwa mkwaju wa penati na nahodha Harry Kane. Lewandowsi alipachika bao lake la pili na la sita kwa Bayern katika dakika ya 87. Katika dimba la Santiago Bernabeu, Real Madrid waliponea chupuchupu kufungwa mechi ya pili mfululizo na kufanikiwa kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Club Bruges ya Ubelgiji. Mshambuliaji kinda wa Nigeria Emmanuel Dennis ameichachafya safu ya ulinzi ya Madrid. Mshambuliaji wa Nigeria Emmanuel Dennis aliitanguliza Club Brugges kwa magoli mawili ya kipindi cha kwanza (dakika ya 9 na 39). Kipindi cha pili Real Madrid wakapata bao la kwanza katika dakika ya 55 kupitia Sergio Ramos, na dakika tano kabla ya mchezo kuisha, Casemiro akaisawazishia timu yake na kufanya matokeo kuwa 2-2 mpaka mwisho wa mchezo. Kwa matokeo hayo, Madrid wanasalia mkiani mwa kundi A wakiwa na alama 1, hali inayoendelea kuuweka mustakabali wa kocha wao Zinedine Zidane katika wakati mgumu. Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa leo akiwa na klabu yake ya KRC Genk anatarajiwa kushuka dimbani kwa mchezo wake wa pili wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Champions League) dhidi ya Napoli. text: Bejing imekuwa ikivibadilisha visiwa hivyo kuwa kambi zake za kijeshi Akizungumza nchini Singapore, Jenerali Mattis alisema kuwa vitendo vya Beijing vinazua maswali mengi kuhusu malengo yake. Pia alisema kuwa swala la vikosi vya kijeshi vya marekani nchini Korea Kusini halitazungumziwa katika mkutano wa mwezi huu kati ya rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Marekani imetaka mataifa ya rasi ya Korea kusitisha kabisa mipango ya kinyuklia, aliongezea. Waziri wa Uinzi nchini Korea Kusini Song Young-moo pia aliambia mkutano wa usalama wa Shangri-La Dialogue kwamba majeshi ya Marekani nchini Korea Kusini ni swala tofauti na lile la mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini. Kuna takriban wanajeshi 28,500 wa Marekani Korea Kusini. Bwana Mattis aliambia mkutano huo wa usalama kwamba Beijing ilipeleka silaha ikiwemo zile za kushambulia meli ,makombora ya kudungua ndege katika maeneo yaliopo katika bahari ya kusini mwa China. ''Licha ya madai ya China kukana, silaha hizo zimewekwa tayari kwa matumizi ya moja kwa moja ya kijeshi kwa lengo la kutishia na kuwashurutisha majirani zake'' , alisema Jenerali Mattis. Jenerali Mattis alisema kuwa utawala wa rais Trump ulitaka uhusiano mzuri na China lakini utashindana na taifa hilo kwa hali na mali iwapo utahitajika kufanya hivyo. Ramani ya Visiwa vya bahari ya kusini mwa China Alisema kuwa Marekani inatambua kwamba China ina jukumu katika eneo hilo. Bahari hiyo ya Kusini mwa Korea ambayo ni njia muhimu ya kibiashara inagombaniwa na mataifa sita. China imekuwa ikijenga visiwa vidogo na vipengee vyengine katika eneo hilo. Mwezi uliopita China ilisema kuwa kwa mara ya kwanza iliwasilisha makombora katika kisiwa cha Woody na kisiwa cha Paracel na hivyobasi kupata onyo kutoka kwa Marekani kwamba inaleta wasiwasi wa kiusalama katika eneo hilo Kisiwa cha woody, kinachoitwa Yongxing na China pia kinapiganiwa na Vietnam pamoja na Taiwan. China inapeleka silaha katika eneo la bahari ya kusini mwa nchi hiyo ili kuwatishia na kuwashurutisha majirani zake, waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amesema. text: App hiyo ya tbh app imepakuliwa zaidi ya mara 5 milioni katika kipindi cha wiki tisa App hiyo kwa jina tbh, ambayo ni ufupisho wa "to be honest" (kuwa mwaminifu/mkweli) imekuwepo kwa wiki tisa tu, lakini tayari imepakuliwa zaidi ya mara 5 milioni. Waliounda programu hiyo wamesema inasalia kuwa programu ya kujitegemea lakini sasa watakwua na rasilimali zaidi kutoka kwa Facebook. "Tulivutiwa na njia ambazo wangeweza kusaidia kutimiza ruwaza ya tbh na kuifikisha zaidi kwa watu," tbh wamesema. Kwa mujibu wa tovuti ya TechCrunch, Facebook walinunua programu hiyo kwa "chini ya $100m", na wafanyakazi wanne waliokuwa wanaifanyia kazi tbh sasa watakuwa waajiriwa wa Facebook. tbh wamesema ufanisi wa app hiyo unaonesha kwamba vijana wanapenda zaidi kuwa na uhusiano mwema na wa manufaa mtandaoni. App hiyo ina kiwango fulani cha usiri. Baada ya anayetaka kutumia app hiyo kujiandikisha, huwa anaulizwa maswali mazuri na pia kupewa fursa ya kuchagua mmoja kati ya marafiki wanne. Wanaotumia hufahamishwa kwamba wamechaguliwa, lakini maelezo kuhusu nani aliwachagua hubaki siri. Facebook sasa inatumiwa na watu 2 bilioni duniani tbh inaonekana kufuata mtindo uliotumiwa na Facebook nyakati za mwanzo - ilikuwa inatumiwa na kundi ndogo la wanafunzi chuoni, kisha ikawa inapatikana kwa watu wa majimbo kadha. Watu walipashana habari kwa maneno hadi ikaenea shule mbalimbali. "Asilimia arobaini ya wanafunzi shuleni waliipakua siku ya kwanza. Siku iliyofuata, shule tatu zaidi na siku ya tatu shule zikafika 300," alisema mmoja wa wahusika. Snapchat kwa sasa unaonekana kuwa mtandao unaowavutia zaidi vijana Marekani, ambao umri wa wastani kwa wanaotumia mtandao huo ni miaka 16. Facebook walijaribu kununua Snapchat mwaka 2013 kwa $3bn. Snap, kampuni inayomiliki Snapchat, kwa sasa ina thamani ya $19bn. Kampuni ya Facebook imenunua programu tumishi inayowalenga vijana wa chini ya miaka 19 na kuwahimiza wawe na wema wanapohusiana. text: Rais wa Marekani Donald Trump Ikulu ya whitehouse imesema kuwa hatua hiyo inajiri baada ya miaka kadhaa ya mazungumzo yalioshindwa kupata suluhu kuhusu wala hilo. Vikwazo hivyo vitashirikisha ushuru na masharti mengine. Mpango huo umezua hofu kuhusu vita vya kibiashara. Ikulu ya whitehouse iliripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuweikea ushuru wa kati ya $30bn-$60bn kwa mwaka pamoja na masharti ambayo yatazuia uwekezaji . Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamishi yake kwa shirika la biashara duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara. Mpatanishi mkuu wa biashara nchini Marekani Robert Lighthizer aliambia wabunge wa Congress siku ya Jumatano kwamba Marekani inafaa kuiwekea China shinikizo kali na shinikizo ya chini watumiaji wa Marekani. Bwana Lighthizer amesema kuwa kulinda ubunifu ni muhimu kwa uchumi wa Marekani. ''Ni swala mushimu sana'' , alisema bwana Lighthizer. ''Nadhani kitakuwa kitu muhimu ambacho kitafanyika katika kuleta usawa wa kibiashara''. Je nini kilichoshinikiza kuwekwa kwa ushuru huo? Afisa wa biashara nchini Marekani ambaye alizungumza na wanahabari alisema kuwa Marekani ina ushahidi kwamba China inataka kampuni za Marekani kuingia katika ushirikiano na kampuni za China ili kuingia katika soko la taifa hilo kwa lengo la kuzishinikiza kampuni hizo kuhamisha teknolojia yao. Rais Xi-Jinping wa China na mwenzake Donald Trump wa Marekani Marekani pia iligundua kwamba China inawekeza katika kampuni muhimu za Marekani na kufanya mashambulio ya mitandao. Matokeo hayo yanatoka katika uchunguzi ulioagizwa na rais Trump mwezi Agosti kwa jina 301. Katika kipengee cha 301 cha sheria ya biashara, serikali imejipatia uwezo wa kuwekea vikwazo mataifa ambayo inahisi hayafanyi biashara kwa usawa. Bwana Trump mara kwa mara amekuwa akilalamika kuhusu ukosefu wa usawa kibiashara kati ya Marekani na China. Je hatua hiyo inaungwa mkono na wengi? Kuna wasiwasi mkubwa nchini Marekani kwamba China inatafuta teknolojia ambayo wanaweza kuitumia kijeshi. Bunge la Congress pia linapanga kupitisha sheria ambayo itaipatia serikali uwezo wa kubadilisha mikataba ya biashara za kigeni kutokana na vitisho vya kununua viwanda vya Marekani. Lakini wanasiasa na viwanda ikiwemo watumiaji wameonyesha wasiwasi kwamba huenda China ikalipiza kisasi. Bwana Lighthizer amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa China ikalipiza kisasi akidai kwamba Kilimo cha Marekani huenda kikaathiriwa , lakini akasisitiza kwamba hatua hiyo haitaizuia Marekani kuchukua hatua. Iwapo watalipiza kisasi basi Marekani italazimika kuwalinda wakulima wake. Je China imesema nini? China imesema kuwa hakutakuwa na mshindi yeyote katika vita vva kibiashara. Siku ya Jumanne , siku ya mwisho ya kikao cha kila mwaka cha chama tawala cha taifa hilo, kiongozi wa China Le Keqiang amesema kuwa ombi lake ni kwamba pande zote mbili zinafaa kutulia. Pia alisema kuwa anatumai kwamba Marekani itapunguza masharti kuhusu bidhaa za kiteknolojia zinazoingia China. Utawala wa rais Trump unapanga kutangaza vikwazo dhidi ya China siku ya Alhamisi baada ya kubaini kwamba taifa hilo linashinikiza wizi na uhamisho wa ubunifu kutoka biashara za Marekani. text: Kwa mujibu wa chapisho la Jilu Evening, limeandika kuwa Liu alikuwa anaendesha gari siku ya jumatatu katika jimbo la Shandong na huku akiwa anajikuna wakati anapita katika kamera ya trafiki. Ghafla alipokea ujumbe unaomwambia kuwa amevunja sheria barabarani kwa kuendesha gari huku anaongea na simu. Picha ya kosa ambalo alikuwa amelifanya liliambatanishwa katika ujumbe huo wa kuvunja sheria. Aliambiwa kuwa ataondolewa pointi mbili katika leseni yake na vilevile alitakiwa kulipa dola saba kama faini. "Huwa nawaona watu mitandaoni wakiwa wamekatwa kwa kosa la kuendesha huku wamewashika watu wengine labda miguu lakini mimi nimekamatwa kwa kujishika mwenyewe ndio nimeonekana kuwa nimevunja sheria, inashangaza'!" Mshitakiwa huyo amesema kuwa anajaribu kuongea na mamlaka ili kupata suluhisho ya tatizo lake . Liu aliweka picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii Gazeti la Global Times limesema kuwa trafiki polisi wamefuta risiti ya makosa waliomwandikia na kumwambia kuwa kamera yao huwa inarekodi mwendo wa dereva moja kwa moja, ndio maana kunikuna kwake uso kulimweka matatani na kuonekana kama anaongea na simu. Picha yake imezua gumzo mtandaoni huku wengine wakiwa wakiwa wanaweka kejeli ya kesi yake na wengine kutoa maoni juu ya namna faini zinavyotolewa . "Mfumo huo unahaibisha sana, watu wanakuwa hawana faragha." "Je, hakuna umuhimu kwa wachina kuwa na faragha?" mtu mwingine aliuliza. Kamera zaidi ya milioni 170 zipo nchini China na nyingine milioni 400 zinatarajiwa kuwekwa mwakani. Kamera hizo zimewekwa huku zikiwa na teknolojia inayoweza kutambua muonekano wa watu na kujua umri , jinsia na eneo walilotoka. Mwanaume mmoja kutoka mashariki mwa China amepigwa faini mara baada ya kamera ya trafiki kumpiga picha akiwa anajikuna usoni. text: Je tunastahili kurauka ili tuimarishe afya yetu? Hatari ya kifo cha mapema, matatizo ya akili na magonjwa yanayotokana na kupumua ndio mambo yaliogunduliwa katika utaifiti huo, uliounga mkono tafiti nyingine zinazoashiria watu wanaolala kuchelewa wamo katika hatari ya kuugua magonjwa hayo. Lakini je kulala na kuamka kuchelewa kuna hatari gani kwako na je ina maana kuwa baadhi yetu tunapaswa kulala mapema na kuamka mapema ili tuziimarishe afya zetu. Uchofu wa wiki nzima' Ni taswira inayofahamika vizuri na wafanyakazi wengi katika wiki. Baada ya kuutafuta usingizi kwa saa nyingi na kuishia kulala kuchelewa, ghafla unaamshwa na kengele ya saa ya kukuamsha. Ikifika mwishoni mwa juma unakuwa taabani na unaishia kulala saa zaidi ya kawaida yako unavyolala Jumatatu hadi Ijumaa ili kupatiliza usingizi ulio ukosa. Huenda unaona hili ni jambo la kawaida, lakini ni ishara sio tu ya kwamba hupati usingizi wa kutosha lakini pia una uchofu wa wiki nzima. Tofuati ya saa unayo lala katika wiki nzima ikilinganishwa na unavyo lala wakati wa wikendi ndio kigezo kikuu wakati tuna uhuru wa kulala na kuamka kwa wakati tunaotaka. Utafiti unaonyesha watu walio na uchofu mkubwa wa wiki huishia kuwa katika hatari zaidi ya kuvuta sigara na kulewa. Kila unapokuwa na uchofu zaidi ndio unajiweka katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa kama ya moyo na mengine yanayohusu mfumo wako wa kusaga chakula. Hayo ndiyo yanayotoa msukumo wa utafiti huo hususan kwa watu wanaoamka kuchelewa - wanaoonekana kuwa katika hatari zaidi ya kuwa na afya mbaya ikilinganishwa na watu wanaorauka asubuhi, kwa mujibu wa Till Roenneberg, mhadhiri katika kitengo cha utafiti wa afya wa magonjwa ya akili katika chuo kikuu cha Ludwig-Maximilian mjini Munich. Na iwapo utawalazimisha watu wanaorauka kufanya kazi na kuishia kulala kuchelewa pia watakabiliwa na matatizo ya afya anasema Russell Foster, mkuu wa maabara ya Nuffield katika taasisi ya Circadian Neuroscience. 'Ni biolojia ya binaadamu' Basi wafanye nini watu wanaoamka kuchelewa? Je wanastahili kuamka mapema wikendi badala ya kulala kupita saa yao ya kawaida? Hilo sio jambo jema," anasema Mhadhiri Roenneberg, anayeamini kwamba hakuna kitu kilicho na hatari kwa afya kuhusu kuamka kuchelewa. "Kama hujalala kutosha kwa siku tano , ni afadhali upatilize uzingizi wako kwa wakati muafaka kwako." Je watu wanaomka kuchelewa wanastahili kuamka mapema wikendi? Hii ni kwasababu muda tunaotaka kuala au kuamka sio tabia tu wala maadili. badala yake inatokana na shinikizo la jinsi miili yetu ilivyoundwa, ambapo 50% inatokana na jini zilizomo ndani ya miili. Mengine yanatokana na mazingira, umri , huku miaka 20 ikiwa ndio umri unaoonekana kuwa juu kwa watu kulala na kuamka kuchelewa na kadri tunavyozeeka ndio wengi hushia kuwa waraukaji. Huenda uziweze kugeuza mienendo inayotokan an jini zako mwilini ka kuamua tu kuamka mapema ,badala yake unaweza kujinyima usingizi ambao tayari huupati wa kutosha katia wiki, wataalamu wanasema. Wakati utafiti wa hivi karibuni ulipokagua tofuati za kiafya kati ya watu wanaoamka kuchelewa na wanaorauka, ulikonekana kuonyesha hali sio nzuri sana kwa wanaoamka kuchelewa. text: Costa alifungia Chelsea mechi yao ya mwisho, fainali Kombe la FA walipolazwa na Arsenal Mhispania huyo wa miaka 28 amehusishwa na kuhaam klabu hiyo baada ya kufahamishwa na meneja Antonio Conte kwamba hayupo kwenye mipango yake. Costa hakujiunga na wenzake kwa mazoezi Jumatatu. "Iliafikiwa kati yake na klabu kwamba anafaa kuchukua siku zaidi kupumzika," taarifa kwenye klabu hiyo ilisema. Costa anatarajiwa kutohudhuria mazoezi wiki hii. Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji pekee ambaye hakufika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham kando na Antonio Rudiger, ambaye alijiunga na klabu hiyo Jumapili. Costa aliwajulisha wanahabari kwamba Conte alikuwa amemwandikia ujumbe wa simu kwamba hakuwa kwenye mipango yake mwezi jana, na inaarifiwa kwamba msimamo wake haujabadilika. Duru zimeeleza BBC kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania anakaribia kuihama klabu hiyo. Costa alifungia Chelsea mabao 20 katika mechi 35 za Ligi ya Premia msimu uliopita na kuwasaidia kutwaa ubingwa wa ligi. Amehusishwa na kurejea Atletico Madrid, licha ya klabu hiyo kuzuiwa kununua wachezaji wapya hadi Januari. Costa alizaliwa Brazil na alikaa misimu minne Atletico kabla ya kujiunga na Chelsea kwa £32m mwaka 2014. Mshambuliaji Diego Costa amepewa muda zaidi wa kumpumzika na Chelsea, hatua iliyozidisha uwezekano kwamba huenda akaihama klabu hiyo majira haya ya joto. text: Waliuawa wakiondoka harusi yao wakitumia helikopta Will Byler na Bailee Ackerman Byler walikuwa wote wanafunzi kwenye chuo cha Sam Houston . Vifo vyao viliripotiwa kwanza na gazeti la wanafunzi. Ajali hiyo ilitokea karibu na Uvalde karibu kilomita 135 magharibi mwa San Antonio. Kwenye mitandao ya kijamii walioshuhudia harusi walichapisha rambi rambi kwennye mitandao ya kijamii pamoja na picha za harusi. "Nimehusunika sana sana!" aliandika rafiki mmoja kwenye mtandao wa Facebook, akiongeza kuwa rubani wa helikopta pia naye aliuawa. Rafiki mwingine aliondoka kwenye mtandao wa Instagram kuwa: Nina amani ndani yangu kuwa mliondoka duniani mkiwa mmejawa furaha na mapenzi. Itakuwa vyema kufanyia fungate zenu kwa Yesu. "Tunashukuru tuliweza kuwa nanyi siku hizi chache za maisha yenu. Roho zetu zimeumia lakini tunajua hii haitakuwa daima." Wawili hao walikuwa mume na mke kwa karibu saa moja kabla ya helikopta yao kuanguka kusini mwa Texas. Kulinga na gazeti la nchuo the Houstonia, Will Byler aliukuwa anasomea uhandisi wa kilimo. Bailee Ackerman Byler alikuwa akisomea mawasiliano ya kilimo. Wote walikuwa mwaka wao wa mwishoi chuoni. Kulingana na bodi ya kitaifa ya usafiri jali hiyo ilihusu ndege ya helikopta aina ya Bell 206B. Mabaki ya helikopta hiyo yaligunduliwa siku ya Jumapili asubuhi. Polisi walisema kulikuwa na vifo kadhaa lakini bado waliofariki hawajatajwa. Rubani wa ndege hiyo naye pia ametambuliwa kama mmoja wa waliokufa. Binti yake wa kambo aliiambia ABC kuwa alikuwa kampteni wa jeshi na alihudumu nchini Vietnam. Wanandoa wachanga kutoka Texas walifariki wakati helikopta iliyokuwa ikiwasafirisha kutoka harusi yao ilianguka siku ya Jumatatu usiku kwa mujibu wa maafisa. text: Sergio Aguero na Leroy Sane City walikwea zaidi kileleni baada ya kuichapa Arsenal 3 - 1 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ethiad siku ya Jumapili kabla ya Manchester United kupoteza dhidi ya Chelsea, City kwa sasa ni kama hawazuiliki Alan Shearer anaamini kinachozinyima usingizi timu nyingine kwenye mbio hizo za ubingwa ni namna ambavyo City wameimarika toka walipomaliza msimu uliopita wakiwa nyuma ya mabingwa Chelsea kwa alama 15 kwenye msimu wa kwanza wa kocha Pep Guardiola kukinoa kikosi hicho. City wanazidi kusonga mbele wakiwa na magoli 38 kutoka kwa michezo 11 ambayo wameshacheza msimu huu wanonekana kuimarika sana katika safu ya ushambuliaji na ulinzi. Katika mchezo na washika mitutu wa London golikipa Ederson aliokoa mkwaju wa Aaron Ramsey ambao ulikuwa unatokomea kimiani, wachambuzi wanasema msimu uliopita wakiwa na golikipa Claudio Bravo bila shaka mkwaju huo ungekuwa goli Na kama ungetinga wavuni ingekuwa 1-1 badala ya 1-0 na matokeo hayo yangeweza kabisa kubadili hali ya mchezo Inaonekana Pep Guardiola amejifunza kutokana na makosa waliyoyafanya msimu ulipita kiasi cha kuwa tishio kwa vilabu vingine msimu huu Alan Shearer anasema ailipokuwa Blackburn, Manchester United walikuwa wakiongoza kwa alama 12 baaada ya michezo 16 ya msimu wa 1993 - 94 lakini walilipambana na kuwafikia kufikia mwezi Aprili. Lakini tatizo kwa timu nyingine ni kwamba Shearer haoni udhaifu wowote kwa City, walipocheza na Arsenal kwa kifupi msimu huu wamo kwenye kiwango kizuri sana. Katika misimu miwili iliyopita City walizanza vizuri pia, lakini wakati wa kipindi cha baridi walitetereka, pengine kutokana na majeruhi na mpangilio wa ratiba lakini Guardiola anajua hawezi kuruhusu hilo lifanyike tena. Ameshinda mataji akiwa Uhispania na Ujerumani kama mwalimu anajua nini chakufanya, kwa sasa ana kikosi kamili ata akiwa na majeruhi ana mbadala wa kutosha kuliko timu nyingine yoyote msimu huu. Aguero asipokuwepo, wana Jesus Sergio Aguero akiumia wana Gabriel Jesus wakati Chelsea bila Alvaro Morata wata yumba Tottenham bila Harry Kane, Manchester United bila Romelu Lukaku watashuka. Utangulizi wao kwa alama nyingi unatisha klabu nyingine. Manchester city wameshinda michezo 15 mfululizo kwenye mashindano yote msimu huu, wakiongoza ligi ya Uingereza kwa alama nane. text: Prof Sergio Canavero ameiambia BBC amepata watu kadhaa kutoka Uingereza waliojitolea kufanyiwa. Upasuaji huo utahusisha kichwa cha mgonjwa kubandikwa katika mwili wa mtu aliojitolea. Licha ya kuwa ni taswira ya kuogofya, Prof Canevero ana imani kwamba sasa teknolojia hiyo inaweza kufanikishwa. "Itategemea lakini iwapo kutapatikana mtu wa kufaa atakayejitolea ubongo. "Ilichukuwa miezi kadhaa kufanikisha upandikizaji wa mwisho wa uso uliofanyika, kwasababu hapakuwa na mtu wa kufaa aliyejitolea, lakini teknolojia itakuwepo." Canavero ameiambia BBC. Prof Canavero hatofanya tena majaribio kwa kutumia ndizi Licha ya hatari kubwa katika upasuaji huo, Dakatari huyo anasema amepata watu wengi waliojitolea kufanyiwa upandikizaji huo. Mgonjwa Valery Spiridonov anataka kufanyiwa upandikizaji wa kichwa Valery Spiridonov ana miaka 31 na anaugua tatizo la kulika misuli, lililomsababisha kuishia kwenye kiti cha magurudumu. Akizungumza kwenye televisheni ya ITV Uingereza, anasema yuko radhi kichwa chake kipandikizwe kwenye mwili tofuati. "Maisha yangu leo ni magumu, na ninategemea mno watu kunisaidia kila siku - saa nyengine hata mara mbili kwa siku, kwasababu nahitaji mtu anitoe kitandani, na aniweke kwenye kiti. "Inanifanya ninategemea watu sana. "Iwapo kuna namna ya kulibadili hili, naamini tunapaswa kujaribu na kuitumia njia hiyo." Vipi upandikizaji wa kichwa utakavyofanikishwa? Daktari anadai upandikizaji huo utahitaji wahudumu 150 wa afya, na saa 36 kufanya upasuaji huo. Anasema hatua ya kwanza itakuwa ni kukigandisha kichwa na mwili kuuzuia mwili usife. Baada ya hapo shingo itakatwa na mipira iunganishwe na mishipa tofuati ya mwili. Alafu inawadia sehemu iliyo ngumu,, kuukata uti wa mgongo. Utakatwa na kisu maalum kilichotengenezwa kwa almasi kutokana na nguvu za jiwe hilo. Baadaye kichwa kinaunganishwana mwili na uti wa mgongo unashikanishwa pamoja kwa gundi maalum. Misuli, mishipa na sehemu za ndani ya mwili zinarudishwa na ngozi inashonwa upya. Kuifanyia Sayansi majaribio Profesa Canavero anasema kutakuwa na majaribio kwa watu waliojitolea walio na ubongo usio fanya kazi. Wataalamu wengi wa afya wanasema uvumbuzi wake hauna uhalisi na upandikizaji wa kichwa hauwezekani kabisa. Lakini Profesa Canavero ameiambia BBC kuwa ana imani anaweza kufanikisha upasuaji huo. Profesa Canavero anasema 90% ina maana kuwa mgonjwa atainuka pasi kuwa na madhara yoyote na ataweza kutembea katika muda wa mwezi mmoja. Kwa sasa anasema lengo lake ni kuleta matumaini kwa watu waliovunjwa moyo na madawa ya mataifa ya magharibi. Daktari wa upasuaji anayetaka kufanya upandikizaji wa kwanza wa kichwa kuwahi kufanyika anasema upasuaji huo unaweza kufanyika kuanzia mwaka ujao. text: Ms Suu Kyi, a Nobel Peace Prize laureate, has been criticised for inaction Ilikuwa hotuba yake ya kwanza kwa nchi kuhusu ghasia katika jimbo la Rakhine ambazo zimesababisha zaidi ya watu 400,000 wa jamii ya Rohingya kuvuka mpaka na kuingia nchini Bangladesh. Bi Suu Kyi amelaumiwa vikali kuhusu jinsi alishughulikia suala hilo. A new wave of Rohingya Muslims has been pouring into Bangladesh since 25 August Lakini amesema kuwa waisilamu wengi hawajakimbia jimbo hilo na kwamba hali imetumia Kwenye hotuba yake kwa bunge la Mynammar, Aung San Suu Kyi alisema amuhusuniswa na kuendelea kutaabika kwa watu wote katika mzozo huo na kwamba Myanma imejitolea kutatua suala hilo kwa jamii zote nchini humo. BBC reporters witnessed burning Muslim villages in Myanmar Bi Suu Kyi ambaye ameamua kutohudhuria mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa mjini News York badaye wiki hii, alisema kuwa alikuwa anataka jamii ya kimataifa kufahamu kile kilichokuwa kikifanywa na serikali yake. Kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi amesema kuwa serikali yake haina hofu ya kuchunguzwa kuhusu njia inashughulikia suala la watu wa Rohingya. text: Mpiga mbizi mfaransa akiogelea juu ya mabaki ya iliyokuwa ndege ya Marekani ya USAAF P-47 Thunderbolt (Warthog) Shirika la (DPAA) limekuwa likisaidiwa na jeshi la Ufaransa kutafuta mabaki ya ndege. Uchunguzi wa DNA kwa mabaki yaliyogunduliwa utasaidia kutambua marubani wa Marekani ambao wameorodheshwa kuwa waliotoweka wakiwa vitani. Picha hizi zinaonyesha wapiga mbizi wa jeshi la Ufaransa kutoka FS Pluton M622 wakiogelea juu ya mabaki ya USAAF P-47 Thunderbolt ambayo ilianguka mwaka 1944. Picha hizi zinaonyesha wapiga mbizi wa jeshi la Ufaransa kutoka FS Pluton M622 wakiogelea juu ya mabaki ya USAAF P-47 Thunderbolt ambayo ilianguka mwaka 1944. Mbiga mbizi Mfaransa wa kikosi cha FS Pluton M622 akiogelea juu ya mabao ya ndege Lengo la DPAA ni kuwatafuta wamarekani kutoka kwa mizozo iliyopita kuanzia Vita vya Pili vya Dunia. Lengo la DPAA ni kuwatafuta wamarekani kutoka kwa mizozo iliyopita kuanzia Vita vya Pili vya Dunia. Lengo la DPAA ni kuwatafuta wamarekani kutoka kwa mizozo iliyopita kuanzia Vita vya Pili vya Dunia. Lengo la DPAA ni kuwatafuta wamarekani kutoka kwa mizozo iliyopita kuanzia Vita vya Pili vya Dunia. Wapiga mbizi wafaransa na DPAA pia walikusanya mabaki kutoka kwa ndege kuyachunguza. Wapiga mbizi wafaransa na DPAA pia walikusanya mabaki kutoka kwa ndege kuyachunguza. Wapiga mbizi wafaransa na DPAA pia walikusanya mabaki kutoka kwa ndege kuyachunguza. Wapiga mbizi wafaransa na DPAA pia wanakusanya mabaki kutoka kwa ndege ya USAAF P-47 Thunderbolt kuyachunguza. Wapiga mbizi wakiogelea juu ya mabaki ya ndege ya USAAF P-47 Thunderbolt (Warthog) . Wapiga mbizi kutoka jeshi la wanamaji wa Ufaransa wanashirikiana na shirika moja la Marekani wa kutafuta mabaki ya marubani wawili wa Marekani wa vita vya pili vya Dunia mashariki pwani mwa kisiwa cha Ufaransa cha Corsica. text: Maandamano hayo ambayo yalikuwa yanaratibiwa na jumuiya ya vijana ya chama hicho. Lengo la maandamano hayo ni kushinikiza Bunge la Tanzania kufuta azimio lake la kutokufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa nchi hiyo, Prof Mussa Assad. Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma ambapo ndipo Bunge la Tanzania hukaa, Gilles Muroto jana alionya hatua kali zingechukuliwa kwa yeyote abaye angeingia mtaani na kuandamana. 'Wale wote waliopanga kufanya maandamano mnamo Aprili 9, 2019 wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa," alitahadharisha Muroto. Awali ACT walipinga vikali kauli hiyo na kutaka "ikemewe na kila Mtanzania maana ni kauli ya vitisho dhidi ya haki za kikatiba." Pili vijana hao wakandelea kushikili msimamo wao wa kuendelea na maandamano: "Maandamano yapo kama yalivyopangwa na yanafanyika kwa mujibu wa katiba na wajibu wa polisi ni kuyalinda na si kuyazuia au kuwatisha wananchi, wasitekeleza wajibu wao." Hata hivyo, baadae usiku kupitia ukurasa wao wa mtandao wa twitter, umoja huo wa vijana ulitangaza kuahirisha kwa muda maandamano hayo wakinukuu barua ya polisi kutoka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya Dodoma, M.J Makanja. Katika barua hiyo, polisi wametoa sababu tano za kuzuia maandamano hayo ikiwemo za kisheria. Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, maandamano kama hayo yanabidi yaripotiwe saa 48 kablahuku barua ya ACT ikiwafikia polisi saa 22 kabla ya siku tukio. Pia imewataka ACT na vyama vingine vya upinzani vyenye uwakilishi bungeni kuhoji na kukosoa juu ya suala hilo la CAG ndani ya bunge na si vinginevyo. "Ngome ya vijana imeazimia kuyasogeza mbele maandamano haya na kushughulikia hoja namba mbili iliyotolewa kwenye barua ya polisi (kuhoji bungeni) kisha kuyarudisha tena maandamano haya katika siku za usoni hasa endapo tarifa ya CAG haitajadiliwa Bungeni na pia bunge kuondoaazimio lake la kutofanya kazi na CAG," sehemu ya taarifa ya chama hicho imeeleza. Mzozo wa Bunge na CAG CAG Prof Mussa Assad Mnamo tarehe mbili mwezi huu, Bunge la Tanzania liliazimia kutofanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali, (CAG) wa nchi hiyo Prof Musa Assad baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za dharau kwa chombo hicho. Wabunge waliafikia uamuzi huo baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutaka waridhie mapendekezo yao dhidi ya CAG. Kamati hiyo ilimhoji CAG Januari 21 baada ya kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York mwezi Disemba 2018 ambapo alisema kuwa Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali. Marufuku ya mikutano na maandamano Mara baada tu ya kuingia Ikulu ya Magogoni, Rais John Magufuli aliweka wazi msimamo wake kuwa hatopenda kuwaona wanasiasa wakizunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara. Hoja yake kubwa ni kuwa "watu waachwe wafanye kazi na kulijenga taifa" na wanasiasa wasubirie kampeni za Uchaguzi wa 2020 ili kuzunguka nchi kujinadi. Marufuku hiyo pia imejumuisha maandamano na migomo dhidi ya serikali Vyama vya Upinzani na wanaharakati wa haki za binaadamu kama ilivyotarajiwa walipinga vikali katazo hilo. Chama kikuu cha upinzani cha Chadema kilitangaza operesheni ya kupinga kile walichokiita Udikteta Tanzania (UKUTA) na kudhamiria kufanya maandamano ya nchi nzima mwaka 2016, lakini waliisitisha kabla ya kuanza. Mwaka 2018, mwanaharakati Mtanzania anayeishi Marekani, Bi Mange Kimambi aliitisha maandamano makubwa ya nchi nzima ambayo yalikuwa yafanyike Aprili 26, 2018. Mjini Dodoma kamanda Muroto alitahadharisha kuwa wanaotaka kuandamana kuwa "watapata tabu sana" na wangepokea "kipigo cha mbwa koko". Maandamano hayo hayakufanyika nchini Tanzania. Baadhi ya Watanzania wanaoishi ughaibuni waliandamana katika balozi za nchi hiyo. Chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo kimetangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Dodoma hii leo. text: Takriban raia 535 waliuawa kati ya tarehe 16 na 17 mwezi Disemba katika vijiji vitatu vya Yumbi , eneo la mashambani magharibi mwa DR Congo ukingoni mwa mto Congo yapata kilomita 350 kaskazini mwa Kinshasa. Mauaji ya kikabila yalifanyika kwa siri kubwa mara ya kwanza kwa sababu yaliendeshwa siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa urais. Siku kadhaa zilipita na habari zikaanza kuchipuka na ilichukua takriban mwezi mmoja kabla ya kiwango cha muaji hayo kubainika. "kile kilichotokea katika eneo la Yumbi mnamo mwezi Disemba sio kitu cha fahari kwa taifa langu'', alisema waziri wa mashirika ya haki za kibinadaamu nchini DRC Marie-Ange Mushobekwa ambaye kwa sasa yuko mjini Geneva. "Wanasiasa na maafisa wa utawala walihusika katika mauaji hayo , na kusababisha ndoto mbaya tunayozungumzia kwa sasa," alisema Mushobekwa akidai kwamba mauaji hayo yanahusishwa na mzozo wa ardhi. Mauaji yalifanyika lini? Mauaji hayo yalihusisha kukatwa mapanga kwa wanawake wajawazito pamoja na kunyofolewa sehemu zao za siri, alisema. Waziri huyo alikuwa akizungumza katika mkutano wa baraza la Umoja wa mataifa kufuatia kuchapishwa kwa ripoti ya Uchunguzi wa Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 hadi 26 mwezi Januari. Matamshi ya waziri huyo yanajiri huku wanaharakati wa haki za kibinaamu nchini humo wakishinikiza kuwasilishwa mahakamani kwa watuhumiwa wa mauaji hayo haraka iwezekanavyo. Mwanaharakati wa haki za kibinaadamu Jean Claude Katende anasema kuwa mashirika hayo yanataka kujua ni akina nani waliohusika kupanga mauaji hayo upande wa serikali pamoja na upande wa raia. ''Tunataka kujua kwa nini walifanya hivyo hatujui walitaka kuzuia uchaguzi ama sijui kwa malengo yapi. Kwa sasa tunasubiri ripoti ya makundi ya haki za kibinadamu juu ya mauaji hayo'', alisema bwana Katende Je mauaji hayo yaliopangwa? Wakati wanahabari wa shirika la AFP walipotembelea eneo hilo baadaye mwezi Januari, duru ziliarifu kuwa mauaji hayo yalikuwa yamepangwa kwa siri na watu wa jamii ya Batende dhidi ya watu wa jamii ya Banunu. Shambulio hilo lilitekelezwa kwa matumizi ya mbinu za kijeshi huku washambuliaji wakionekana kuvaa magwanda ya kijeshi , kulingana na vyanzo hivyo vya habari. Duru hizo ziliwatuhumu baadhi ya maafisa wa jeshi na maafisa wa utawala wa eneo hilo katika mauaji hayo. Baada ya umwagikaji huo wa damu, serikali iliwabadilisha maafisa waliokuwepo ikiwemo maafisa wa polisi na wakuu wa ujasusi , wanajeshi na maafisa wa serikali ya Utawala. Wachunguzi wa Umoja wa mataifa UN wiki iliopita walisema kuwa wamegundua kwamba visa vya kufanana vya ghasia vilitokea baada ya mazishi ya chifu wa utamaduni wa jamii ya banunu. Ripoti hiyo ilielezea visa vya kutisha ikiwemo kisa cha mtoto wa miaka miwili aliyetupwa katika shimo la maji taka huku mwanamke mmoja akibakwa baada ya mumewe kuuawa huku mtoto wao wa miaka mitatu akikatwa mikono. Uhalifu wa kivita Shambulio hilo linaweza kuorodheshwa miongoni mwa mashtaka ya uhalifu wa kivita ,kulingana na wachunguzi hao. Uchunguzi huo hatahivyo ulishindwa kubaini iwapo serikali ilihusika na mauaji hayo. Lakini jukumu la serikali linahusishwa baada ya uchunguzi huo kubaini kwamba utawala wa kitaifa na ule wa mkoa ulionywa kuhusu hatari ya ghasia hizo lakini haikuchukua hatua zozote za kuzuia kitendo hicho, ulisema uchunguzi huo. Mushobekwa alisema kuwa rais mpya wa DR Congo Felix Tshisekedi , aliagiza uchunguzi kuhusu kile kilichotokea na ripoti yake itatumwa kwa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha siku chache zijazo. "Wale waliotekeleza mauaji haya watakamatwa na kuwasilishwa mahakamani ili kujibu majukumu yao. Tunajua kwamba bila haki hakutakuwa na amani ya kutosha nchini DR Congo''. Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imekiri kwa mara ya kwanza kwamba maafisa wa serikali walitumika katika mauaji ya mamia ya watu mwezi Disemba mwaka jana. text: Mshambuliaji wa manchester United Zlatan Ibrahimovic Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Manchester United akiwa mchezaji huru kutoka Paris-St Germain kwa kipindi cha msimu mmoja huku akiwa na nafasi ya kuongeza kandarasi yake. Raia huyo wa Sweden amefunga magoli 26 katika mechi 38 msimu huu,zikiwemo bao mbili katika ushindi wa kombe la EFL dhidi ya Southampton. ''Sote tunataka asalie na tunaamini atafanya hivyo kwa msimu mwengine mmoja'', alisema mkufunzi huyo. Ibrahimovic alibeba kombe lake la 32 katika kipindi chake chote cha soka baada ya kufunga bao la dakika 87 katika uwanja wa Wembley . Katika kipindi hicho Manolo Gabiadiani aliifungia Saints mabao mawili baada ya Jesse Lingard kuiweka Red Devils ikiwa inaongoza kwa 2-0. Mourinho aliongezea: Sipendelei kum'bembeleza mchezaji kutia saini kandarasi mpya ama kunichezea.Wakati Zlatan alipoelekea Barcelona kutoka Inter Milan nilihisi vibaya sana.Lakini iwapo anahitajika mashabiki wanaweza kwenda hadi mlangoni kwake kupiga kambi usiku kucha. Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anamtaka mshambuliaji wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mwengine mmoja. text: Nancy ni mgombea pekee mwanamke anayewania nafasi ya urais akiwa mgombea binafsi. Kama ilivyokuwa kwa mgombea binafsi mwingine kijana John katumba ndivyo ilivyo kwa Nancy Kalembe mwenye umri wa miaka 40 akiwakilisha vijana wanawake katika taifa hilo wenye nyota hafifu ya kung'ara katika majukwaa ya kisiasa kila unapowadia uchaguzi mkuu. Duru za kisiasa nchini humo zinaonesha mchuano mkali upo kwa wagombea wawili wenye ushindani mkubwa Yoweri Museveni na Robert Kyagulanyi, lakini kuibuka kwa mgombea mwanamke katikati yao kunafanya kinyang'anyiro hicho kutia fora huku maelfu ya wapigakura wakiwa na hamu na ghamu ya kuamua mshindi siku ya upigaji kura tarehe 14 Januari mwaka 2021. Je, ni nani huyu Nancy Kalembe? Mwaka 2003 alishiriki mashindano ya urembo Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la The Independent limemuelezea Nancy Kalembe kuwa alizaliwa kwa wazazi George Patrick Bageya na Aida Cissy Kubaaza. Alipata elimu yake hadi kidato cha nne St. Mary's College na kidato cha tano na sita alisoma shule ya Juu ya Mariam. Shahada ya kwanza alihitimu katika Chuo Kikuu Makerere mwaka 2007. Awali mwaka 2003 alishiriki mashindano ya urembo, baadaye aliajiriwa na kituo cha redio Sanyu F.M. Januari 8, mwaka 2008 alishiriki kipindi cha runinga cha Apprentice Africa kilichoongozwa na Donald Trump na kushika nafasi ya sita kati ya washiriki 16. Kipindi hicho kilifungulia njia ya kupata ajira katika Benki ya PHP nchini Nigeria. Mwaka 2009 alirudi Uganda kufanya kazi na Benki ya Orient hadi alipojiuzulu mwaka 2010 ili kusimamia biashara zake ikiwemo kampuni ya kufanya usafi ya Mbalimbali Limited iliyoweka makao yake huko Nakawa. Amewahi kufanya kazi katika televisheni ya UTV na Shirika la mawasiliano la Uganda. Mgombea huyo ana sera zipi kwa wapigakura? Anasisitiza uongozi wa kulinda maadili, kuzalisha ajira kwa vijana, huduma bora za afya kwa wananchi wote, kuboresha mitaala ya elimu, kuboresha sekta ya michezo, kupinga ubaguzi miongoni mwa watoto na watu, kufanya mabadiliko ya mifumo ya vyombo vya dola, kuimarisha umoja wa kitaifa,kulinda uchumi na wawekezaji na kudhibiti ushawishi wa vyombo vya habari vya nje. Hivi karibuni gazeti la New Vision lilieleza kuwa mgombea huyo alifanya tukio la kipekee kwa kufanya kampeni katika jukwaa moja na wagombea chama cha NUP katika Kata ya Goma Manispaa ya Mukono. Wagombea hao wa nafasi tofauti alioshirikiana nao ni Mchungaji Peter Bakaluba Mukasa, Hanifer Nabukeera na Betty Nambooze. Akiwa katika mkutano huo aliwaambia wafuasi wa Bob Wine kuwa hana tatizo na mgombea mwenzake huyo kwa sababu wote wanapigania jambo moja la ustawi wa wananchi na taifa. Je, 'Mission 56' ni nini? Ni kauli mbiu ya ilani anayotumia kuwasiliana na wapigakura kote nchini humo. Mission 56 ina maana ya makabila 56 yaliyoko nchini Uganda. Mission 56 imekusudia kuwaunganisha Waganda bila kujali itikadi zao za kisiasa, na haki sawa kwa wananchi wa makabila yote nchini humo na kuwafanya wafanye kazi pamoja. Katika kauli mbiu hiyo lipo neno la nyongeza, "Leaving No One Behind", kwamba hakuna atakayeachwa nyuma. Akizungumza na mwandishi wa makala haya kwa njia ya simu kutoka jijini Kampala mgombea huyo anafafanua sera yake kuwa inalenga kujenga msingi wa umoja miongoni mwa raia wa Uganda. Anasema akishinda urais suala la umoja litakuwa ajenda nyeti, hivyo kuomba Waganda kuwa naye bega kwa bega. "Tupo makabila 56 hapa Uganda lakini kwa miaka mingi hatuna umoja. Kwanza zama za ukoloni ziliweka mipaka na kutugawa kijiografia, na kisha tugawanywa kwa misingi ya dini na itikadi za siasa. Masuala ya rasilimali, uongozi na maendeleo vikawa vitu adimu katika makabila yetu na kuendelea kufukarisha watu wetu. Mipango niliyonayo sasa ni kuhakikisha makabila yote 56 yanasimamia ajenda na mwelekeo mmoja wa kitaifa,kuzikubali tofauti zetu kiitikadi na dini kwa madhumuni ya kuchochea maendeleo ya taifa. Tofauti hizo zisiwe kikwazo cha umoja wetu na kufaidi rasilimali zetu bila ubaguzi," Aidha, anasema kampeni zake zilizinduliwa katika uwanja wa Kakiundu jijini Jinja mnamo Novemba 12 mwaka huu wa 2020, kisha akaelekea miji mingine, ambapo anatarajia kufunga kampeni hizo ifikapo Januari 12 mwaka 2021 jijini Jinja nchini humo. Nani anafadhili kampeni zake? Anasema kuwa bajeti za kampeni zake zinatokana na michango ya hali na mali kutoka kwa wafuasi,wadau na wapenzi wa mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Hivyo basi kama walivyo wengine naye amekuwa akitoa matangazo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuomba michango ya hali na mali kwa ajili ya kuendesha kampeni zake. Wachangiaji wanatakiwa kuchangia kwa njia ya akaunti ya benki au simu ya mikononi. Ikumbukwe harambee ni miongoni mwa vitu muhimu kwa mgombea bila kujali mgombea binafsi au anatoka chama cha siasa. Nafasi za wanawake katika jumuiya Wakati Tanzania ikifanya uchaguzi wake Oktoba 28 mwaka 2020 ilikuwa na wagombea wawili kati ya 15 wanawake katika nafasi ya urais, Queen Cathbert Sendinga wa chama ADC na Cecilia Augustiono Mwanga kutoka chama cha Demokrasia Makini. Upande wao Kenya jumla ya wagombea 8 walichuana katika uchaguzi wa mwaka 2017 nchini, lakini hakukuwa na mgombea mwanamke. Mataifa ya Afrika mashariki kama yalivyo mengine ya bara la Afrika ni nadra kwa wanawake kugombea ama kutia nia kwa nafasi za juu za uongozi. Matarajio ya nchi za kusini mwa Jangwa Sahara ni kuhakikisha usawa katika vyombo vya uamuzi na ushiriki kwenye masuala ya uendeshaji jamii na taifa kwa ujumla. Umoja wa Afrika unasisitiza ajenda ya hiyo na kwamba ifikapo mwaka 2050 bara la Afrika liwe na limepiga hatua kubwa kwenye suala la haki sawa. Uganda inaonekana kuwa nyuma kwenye ushiriki wa demokrasia, kujitokeza mwanamke mmoja kuwania nafasi ya urais akiwa mgombea binafsi huku vyama karibu vyote vikiwa na wagombea wanaume ni ishara ya suala la jinsia kupigwa teke, licha ya matumaini yaliyopo siku zijazo. Ingawa matumaini yangalipo kuwainua wanawake, lakini wanasisitizwe na kushiriki kwenye vyombo vya uamuzi na siasa za ushindani kuliko kusubiri nafasi za kuteuliwa. Miaka mitano baada ya kuzaliwa Nancy Linda Kalembe ndipo Yoweri Museveni alitwaa uongozi nchini Uganda kutoka msituni akiwa na miaka 42. text: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka uchunguzi ufanyike akisema ametamaushwa na ripoti kuwa maafisa walifyatua risasi hospitalini. Marekani na Uingereza zimesema ni ''tukio la kikatili''. Sudan imekua chini ya utawala wa kijeshi tangu Rais Omar al-Bashir alipopinduliwa mwezi Aprili. Viongozi walioongoza vuguvugu la kutaka utawala wa kiraia kuongoza nchi hiyo, wamesema wamesitisha mawasiliano na serikali ya mpito ya kijeshi na kufanya mgomo. Vikosi vya usalama vilifika maeneo ambayo watu walikua wakiandamana, mapema Jumatatu na sauti za risasi zilisikika kwenye picha za video. Katika taarifa yake iliyosomwa kwa njia ya televisheni ya taifa, Jeshi limeeleza masikitiko yake kwa namna hali inavyozidi kuwa mbaya na kusema kuwa operesheni ilikua imewalenga ''wanaotia dosari hali ya usalama na wahalifu''. Jeshi limesema kuwa limekuwepo kwa ajili ya kulinda raia. Awali, wanaharakati wamesema vikosi vya usalama waliizunguka hospitali moja mjini Khartoum na kufyatulia risasi hospitali nyingine. Kamatikuu ya madaktari wa Sudan, walio karibu na waandamanaji wamesema watu 30 akiwemo mtoto wa miaka minane wa,meuawa, na idadi ya waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka. Mamia ya watu wamejeruhiwa. Baadhi ya wakazi wamekilaumu kikosi cha Rapid Support Forces, kilichokuwa kikipambana kumsaidia Bwana Bashur kubaki madarakani na kushiriki kwake kwenye mzozo wa Darfur magharibi mwa Sudan ulioanza mwaka 2003. Wakati huo wakifahamika kwa jina ''Janjaweed'', wanamgambo hawa walitekeleza mauaji. Nini kilifuata? Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka mamlaka za Sudan kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya wale waliohusika. Taarifa yake imelaani matumizi ya nguvu kuwatawanya waandamanaji, na kushtushwa na ripoti kuwa vikosi vya usalama kufyatua risasi kwenye hospitali. Shirika la habari la Sudan limesema mwendesha mashtaka ameunda kamatai kufanyia uchunguzi matukio hayo. Ramadhan 'inavyoimarisha' maandamano Sudan Waandamanaji wakata ushirikiano na jeshi Sudan Chanzo ni nini? Waandamanaji wamekua wakikita kambi nje ya jengo la makao makuu ya jeshi tangu tarehe 6 mwezi Aprili, siku tano kabla ya kuangushwa kwa utawala wa Bashir. Mwezi uliopita, waandaaji na majenerali watawala walikubaliana kuhusu muundo wa serikali mpya na muda wa mpito wa miaka mitatu kuelekea kwenye utawala wa kiraia. Hawajaweza kuamua kuhusu ni upande upi hasa kati ya raia au jeshi kuchukua nafasi nyingi zaidi. Jeshi la nchini Sudani limekemewa kutokana na mashambulizi yake dhidi ya waandamanaji mjini Khartoum, hatua iliyosababisha watu 30 kupoteza maisha. text: Mamia ya wazima moto wamekuwa wakikabiliana na moto huo Moto mkali unaoshambaa kutokana na upepo mkali umesababisha uharibifu mkubwa katika kijiji kilichoko ufukweni mwa bahari Mati, na kuyaharibi magari na nyumba katika eneo hilo. Waokozi wameyapata miili ya watu 26 na watoto ambao wanaonekana kukumbatiana walipokuwa wanafariki, wakiwa wamekwama katika moto huo uliozuka mita chache chache kutoka baharini. Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto, wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo, huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema watafanya lolote linalowezekana kibinadamu kuhakikisha wanaokoa maisha ya watu. Watu wakijaribu kujiokoa na magari Hata hivyo waziri huyo amelazimika kukatisha ziara yake ya Bosnia ili kusaidia uratibu wa hali hiyo,ambayo vikozi vya uokoaji vinasema ni mbaya kuwahi kutokea. Msemaji wa serikali Dimitris Tzanakopoulos amethibisha kuwa watu 20 wamekufa kutokana na moto huo, amefafanua kuwa wale waliokwama upande wa baharini takribani kilomita 40 kaskazini mashariki mwa mji wa Athens ndiyo waliokufa wakiwa nyumbani kwao na wengine kwenye magari. Watu 104 wamejeruhiwa kati yao 11 wakiwa katika hali mbaya, lakini watoto 16 nao wamejeruhiwa. Waziri mkuu Tsipras amesema hali ya hatari imetangazwa katika Attica karibu na mji wa Athens. Nchi za Italia, Ujerumani, Poland na Ufaransa wametuma misaada ya ndege, magari na watalaamu wazima moto. Wengi wa waliofariki walikuwa katika mji wa pwani wa kitalii wa Mati, kaskazini mashariki mwa Athens Huu ndio moto mbaya zaidi wa nyikani kukumba Ugiriki tangu mwaka 2007 pale watu kadha walippouawa na moto rasi ya Peloponnese kusini mwa nchi hiyo. Wakazi wametakuwa kuhama nyumba zao Waziri Mkuu Alexis Tsipras amesema wazima moto wote wameitwa kukabiliana na moto huo Nyumba nyingi zimeharibiwa na moto huo Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 60, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo ulio janga baya kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja. text: Kiongozi wa upinzani nchini Kenya akijiapisha kuwa ''Rais wa Wananchi'' Marekani pia imeishutumu serikali kwa kufungia vituo vinne vya habari nchini humo ambavyo viliadhibiwa baada ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo ya upinzani. Umoja wa Afrika na Muungano wa Ulaya pia wameshutumu hatua hiyo ya Bw Odinga. Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema taifa hilo linaamini mizozo yoyote ile inafaa kutatuliwa kwa njia zifaazo kisheria. "Tunakataa vitendo vyovyote ambavyo vinahujumu Katiba ya Kenya na utawala wa sheria. Uhuru Kenya alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya mnamo Oktoba 26, 2017 katika uchaguzi ambao uliidhinishwa na Mahakama ya Juu," taarifa hiyo iliyotumwa na msemaji wa wizara hiyo Hearther Nauerth imesema. "Umoja wa Afrika unakataa vitendo vyote amabvyo vinahujumu mfumo wa kikatiba na utawala wa sheria. Mwenyekiti wa Tume (Moussa Faki Mahamat) anatoa wito kwawahusika wote kujiepusha na vitendo kama hivyo ambavyo pia vinatia hatarini uthabiti wa kisiasa Kenya," taarifa ya Tume ya Umoja wa Afrika imesema. Bw Odinga, mgombea urais wa muungano wa National Super Alliance (NASA) uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambao matokeo yake yalibatilishwa baada ya kesi iliyowasilishwa naye Mahakama ya Juu, alisusia uchaguzi huo wa marudio na amesema hamtambui Rais Kenyatta kama rais halali wa taifa hilo. Jumanne, alikula kiapo kuwa Rais wa Wananchi katika hafla iliyohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wake uwanja wa Uhuru Park, Nairobi. Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, ambaye ni makamu wa rais wa zamani, hakuhudhuria sherehe hiyo ingawa walikuwa wameahidi kuapishwa wote wawili kwa pamoja. Wafuasi wa Bw Odinga wakisherehekea Kisumu baada yake kula kiapo Uhuru Park, Nairobi Bw Musyoka baadaye alisema alipokonywa walinzi wake na hivyo kuzuiwa kuondoka nyumbani kwake kwenda kuhudhuria sherehe hiyo. Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo alisema Bw Musyoka angeapishwa baadaye. Jumatano, mbunge wa upinzani Tom Joseph Kajwang' anayewakilisha eneo bunge la Ruaraka, Nairobi alikamatwa na akashtakiwa kwa makosa ya kuhudhuria mkutano haramu na kushiriki katika kulishwa kiapo kwa Bw Odinga kwa njia ya kudai kumfunga Bw Odinga "kutekeleza kosa la jinai la uhaini". Bw Kajwang', ambaye ni wakili, alikuwa amevalia sare za uwakili na kwa pamoja na mshauri wa zamani wa Bw Odinga, Miguna Miguna, walikuwa karibu na Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo. Matukio makuu mzozo wa kisiasa Kenya Ijumaa, polisi walimkamata pia mshauri wa zamani wa Bw Odinga, Miguna Miguna, ambaye ndiye aliyetia saini hati ya kiapo cha Bw Odinga. Kufungiwa kwa vituo vya habari Marekani imesema imesikitishwa sana na vitendo vya serikali kwa "kufunga, kutisha na kuminya vyombo vya habari". "Uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na kwa wanahabari, ni muhimu sana kwa demokrasia, na umelindwa kwenye Katiba ya Kenya," taarifa ya Marekani imesema. "Tunaihimiza serikali na Wakenya wote kuheshimu uhuru wa kujieleza na kutii agizo la mahakama na kuvifungulia vituo hivyo vya televisheni." Mahakama ilikuwa imeamuru vituo hivyo vya Citizen, Inooro, NTV na KTN vifunguliwe Alhamisi lakini kufikia Ijumaa asubuhi, agizo hilo lilikuwa bado halijatekelezwa. Ingawa Marekani imewasifu polisi na vikosi vya usalama kwa jinsi walivyosimamia hafla hiyo ya kuapishwa kwa Bw Odinga Jumanne, wamesema visa vya kukamatwa na kushtakiwa kwa washukiwa vinafaa kutekelezwa kwa kufuata sheria kikamilifu. Marekani imewahimiza viongozi wa kisiasa Kenya kufanya mazungumzo kwa lengo la kuimarisha uwiano na utangamano na kutatua matatizo ya muda mrefu nchini humo. Serikali ya Marekaniimesema imesikitishwa na hatua ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ya kujiapisha Jumanne wiki hii. text: Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya makombora manne Waziri wa maswala ya kigeni Wang Yi alisema kuwa kwa makubaliano hayo Marekani na Korea Kusini zitasitisha mazoezi ya kijeshi ya pamoja ambayo yanakasirisha Korea Kaskazini. Ombi hilo linajiri baada Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora yake manne siku ya Jumatatu na kukiuka vikwazo vya kimataifa. Ili kujibu hatua hiyo, Marekani imeanza kuweka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini. Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Thaad. Akizungumza kando kando ya mkutano wa kila mwaka wa bunge, bwana Wang alisema kuwa mgogoro huo wa Korea ni kama treni mbili zinazokwenda katika barabara moja huku zote zikikataa kutoa nafasi kwa mwengine kupita. "je pande hizi mbili ziko tayari kugongana?,aliuliza. ''Usitishaji wa operesheni za kijeshi baina ya mataifa haya utakuwa hatua ya kwanza katika kumaliza wasiwasi na kuanzisha majadiliano'',alisema. China imependekeza kwamba Korea Kaskazini ipige marufuku majaribio yake ya makombora pamoja na teknolojia yake ya nyuklia ili kuzima wasiwasi unaoendelea. text: Mwanamuziki wa nyimbo za kufoka Lil Wayne Mtandao wa wasanii wa TMZ umesema mwanamuziki huyo wa nyimbo za kufoka, 34, anayeugua ugonjwa wa kifafa, ameangushwa na ugonjwa huo mara kadhaa na alipoteza fahamu pindi tu alipowasili huko A&E. Alitarajiwa kuwatumbuiza mashabiki wake huko Las Vegas siku ya Jumapili usiku. Nyota huyo, ambaye kwa jina lake rasmi Dwayne Michael Carter Jr, alipokea matibabu mwaka uliopita baada ya kupoteza fahamu mara mbili lakini kwa kiasi kidogo. Miaka minne iliyopita Lil Wayne alikuwa akipokea matibabu kwa siku kadhaa katika hospitali moja huko Los Angeles. Baada ya kupata fahamu, mwanamuziki huyo aliambia kituo cha redio cha Power 106 kwamba, anaugua ugonjwa wa kifafa na yuko katika hatari za kukosa fahamu mara kadhaa. Alimwambia DJ Felli Fel: ''Hiyo haikuwa mara yake ya kwanza, pili, tatu, nne , tano, sita au saba … nimepatwa na kifafa mara kadhaa, ni vile huwa hampati habari hizo.'' Lil Wayne amesema hupoteza fahamu baada ya kupatwa na msongo wa kiakili, kutopumzika na kufanya kazi kupita kiasi. Mashabiki waliokuwa na wasiwasi wamekuwa wakituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kupitia #prayforweezy baada ya kisa cha mwanamuziki huyo kuripotiwa. Mzaliwa huyo wa New Orleans, alianza taaluma hiyo akiwa na umri wa miaka 9, alipokuwa msanii mdogo kusajiliwa na rekodi ya Cash Money. Tuzo zake tano bora za Grammy zinajumuisha tuzo ya albamu bora ya nyimbo za rap mwaka 2008 kwa albamu yake ya Tha Carter III na utumbuizaji bora wa rap kwa wimbo wake wa No Problem akiwa na Chance the Rapper & 2 Chainz. Mwanamuziki Lil Wayne amekimbizwa hospitalini baada ya kuanguka kutokana na kifafa na kupatikana akiwa hana fahamu katika chumba cha hoteli alimokuwa huko Chicago. text: TCRA Hatua hii imekuja ili kudhibiti maudhui mitandaoni ikiwa ni matakwa ya sheria mpya ambayo ilionekana kuwa na mkanganyo. Ikiwa sehemu ya usajili, wachapishaji wote wa kwenye mtandao kwa maandishi, video na sauti wanapaswa kulipa dola 1000. Aidha wachapishaji wa mtandao huo wanatakiwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote ambavyo wanatakiwa kuainisha ikiwa ni pamoja kuweka mfumo wakukagua taarifa zisozoruhusiwa katika mitandao na kuweka rekodi ya watumiaji wote, vikiwemo vitambulisho vyao na anuani za wasambazaji wa intaneti. Atakaye kiuka vigezo muhimu vilivyowekwa atapata adhabu ya kulipa faini isiyopungua dola 2000 au kufungwa jela kwa muda usiopungua mwaka mmoja au adhabu zote kwa pamoja. Wanaharakati wengi, watumiaji wa mtandao na wamiliki wa mitandao hiyo wameona serikali imeamua kutumia mwanya huo ili kubana uhuru wa kujieleza. Lakini serikali ya Tanzania inasema imeamua kuchukua maamuzi hayo ili kulinda taifa na maudhui kutoka nje au ndani ya nchi ambayo hayahitajiki katika jamii. Hata hivyo mwenyekiti wa wamiliki wa blogu ndugu Johakimu Mushi anasema wao kama Tanzania bloggers hawana tatizo kabisa na suala la kujisajili maana wanajua umuhimu wa kusajiliwa ni kuonekana kwamba wanatambuliwa na kazi wanazozifanya na itasaidia kuangalia maadili. Changamoto iliyopo kwa wamiliki hao wa mitandao wanasema inakuja kwenye ulipaji wa tozo. "Suala tata ni kuhusiana na tozo zilizowekwa maana sio bloggers wote wanafanya biashara sana kuna wengine wanatoa elimu tu ya afya au michezo na hakuna faida yeyote wanayopata hivyo itakuwa ngumu kwa wao kuendelea kuchapisha kwenye mtandao,tunataka kutoa ushirikiano wa dhati lakini kiuhalisia ni ngumu hivyo inabidi TCRA watoe elimu kwanza," Jonathan aeleza. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA ) imewapa muda wa wiki mbili wamiliki wa mitandao ya kijamii ya 'blogs', tovuti na aina nyingine ya vyombo vya habari vya habari vinavyochapisha kwenye mtandao kujisajili nchini Tanzania. text: Bi Grace Mugabe Phyllis Chikundura ,msemaji wa tume ya kukabiiana na ufisadi nchini humo alithibitisha kuwa kulikuwa na uchunguzi uliokuwa ukiendelea. ''Tumethibitisha kuwa kuna ripoti kama hiyo na kwamba kuna uchunguzi kama huo pia'', alisema. Bi Mugabe alidaiwa kupata Shahada hiyo baada ya miezi kadhaa ya masomo 2014. Gazeti la serikali The Herald liliripoti wakati huo kwamba kutoweka kwa Bi Mugabe kulifanywa kwa lengo la kubadilisha hali ya jamii na kazi ya familia. Inadaiwa kwamba alifanya utafiti kuhusu nyumba za watoto wa Zimbabwe. Bi Mugabe yeye mwenyewe alituzwa shahada hiyo na aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe ambaye alikuwa chansela wa chuo kikuu cha Zimbabwe. Alipongezwa wakati huo na maafisa wengine wa serikali waliotetea shahada hiyo yenye utata. Bi Mugabe alitumai kumrithi mumewe kama kiongozi, lakini akachokoza upande mmoja wa chama cha Zanu-Pf ambacho hatua iliosababisha mgawanyiko ndani ya chama hicho. Jeshi baadaye lilingilia kati na kumlazimisha rais Mugabe kuondoka madarakani baada ya kipindi cha miaka 37 na kumuweka mamlakani aliyekuwa makamu wake Emmerson Mnangagwa kuwa rais. Mamlaka ya kukabiliana na ufisadi nchini Zimbabwe imeanzisha uchunguzi kuhusu shahada ya udaktari iliopewa mkewe Robert Mugabe, Grace Mugabe kulingana na ripoti ya AFP. text: Tunisia imefuzu katika robo fainali ya michuano ya Afcon bila kushinda mechi katika dakika 90 Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban. Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa ziada Rami Bedoui kujifunga kupitia kichwa dakika za lala salama alipogusa mpira kwa mara ya kwanza. Wakati huohuo Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Mali 1-0 ili kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon. Mshambuliaji huyo wa Crystal Palace ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal aliufukuza mpira wa adhabu uliopigwa na Sylvain Gbohouo na kuupata kabla ya kipa Djigui Diarra. Mali ilikuwa imepoteza nafasi chungu nzima kupitia Moussa Marega na Moussa Djenopo, wote wakikosa nafasi nzuri baada ya pasi safi. Ivory Coast sasa itacheza dhidi ya Algeria katika mechi ya robo fainali siku ya Alhamisi. Ndovu hao wameibuka washindi wa komnbe hilo mara mbili mwaka 1992 na 2015 lakini walisonga mbele katika raundi ya muondoani wakiwa katika nafasi ya pili baada ya kushindwa 1-0 na Morocco. Tunisia ilikuwa inaongoza kupitia goli la mshambuliaji wa IsmailiaTaha Yassine Khenissi aliyepata krosi nzuri kutoka kwa Wajdi Kechrida. Mshambuliaji wa Leeds Ekuban ndiye mchezaji wa pekee aliyekosa mkwaju wake katika penalti hizo huku Ferjan Sassi akifunga goli la ushindi. Tunisia sasa itakabiliana na Madagascar iliopo katika nafasi ya 108 duniani siku ya Alhamisi licha ya kutoshinda mechi hata moja katika dakika 90. Mwewe hao walitoka sare mechi zao zote tatu kabla ya mikwaju hiyo ya penalti dhidi ya Ghana. The Black Stars walitawala kipindi cha mwanzo cha mchezo huku shambulio la kichwa la Nuhu Kassim likigonga mwamba wa goli. Walipata bao la kwanza lakini likakataliwa . Thomas Partey alimpigia pasi Jordan Ayew ambaye naye alitoa pasi murua kwa nduguye Andre na kufunga kupitia kisigino. Refa aliamuru kwamba Partey alikuwa ameunawa huku refa wa kutumia Video VAR akitarajiwa katika mechi za robo fainali, lakini kiungo huyo wa Atletico alikuwa ameuzuia mpira huo kwa kifua. Tunisia ilitawala mechi wakati Wahbi Khazri ambaye alikuwa na jeraha alipoingia kunako dakika ya 68. Muda mfupi baadaye kona yake iligonga mwamba wa goli kupitia kichwa cha Khenissi. Hatahivyo bahati ya Tunisia ilisimama wakati Khazri alimpigia pasi ya kisigino Kechrida ambaye krosi yake ilifagiliwa hadi wavuni na Khenissi. Shambulio la kiungo wa Ghana Mubarak Wakaso lilipanguliwa kabla ya kuchangia katika bao la kusawazisha. Beki Bedoui aliingia katika nafasi ya Khenissi katika dakika ya mwisho ili kuongeza ulinzi-lakini alifunga mkwaju wa adhabu wa Wakaso hadi wavuni mwa goli la Tunisia. Pande zote mbili zilikuwa na fursa dakika za lala salama -lakini zilishindwa kuzitumia hivyobasi mechi ikaishia kuamuliwa kupitia mikwaju ya penalti. Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar. text: Rais wa zamani wa Afrika Kusini,Jacob Zuma Mara baada ya Bwana Zuma kuwasili katika mahakama kuu huko Durban hapo jana kwa kipindi cha dakika 15,kesi yake ilihairishwa mpaka tarehe 8 mwezi Juni. Bwana Zuma ambaye anakabiliana na mashtaka 16 ya ufisadi,rushwa ,udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha. Bwana Zuma alilazimika kuachia madaraka yake mwezi februari licha ya kukataa kuhusika na kosa lolote. Wafuasi wake walisambaa mjini wakiandamana kwa ajili yake huku wapinzani wake walilalamika kwamba mahakama inachukua muda mrefu kutoa hukumu. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa,Bwana Zuma aliwahutubia mkusanyiko wa watu waliomsindikiza mahakamani kutoka nyumbani kwake. "Sijawahi kuona mtu anashtakiwa kwa uhalifu, alafu mashtaka yake yanafutwa lakini baada ya miaka kadhaa ,mashtaka hayohayo yanarejeshwa" ,Zuma alisema. "Hizi ni njama za kisiasa" Wafuasi wa Zuma nje ya mahakama Baada ya hapo Bwana Zuma aliongoza nyimbo na kucheza pamoja na wafuasi wake. Mamia ya askari pia yalikuwa yanalinda Mpango wa silaha ulikuwa ni upi? Mpango wa silaha ulifanyika mwaka 1999 mwaka ambao bwana Zuma alihama kutoka mkuu wa jimbo kuwa makamu wa rais. Anashtakiwa kwa kukubali kuchukua malipo yasiyokuwa halali 783 Mshauri wake wa mambo ya fedha ,Schabir Shaikh alikutwa na hatia kwa kujaribu kuomba rushwa kwa niaba ya bwana Zuma kutoka katika kampuni ya silaha za Ufaransa na kosa hilo lilipelekea akafungwa jela mwaka 2005. Kesi dhidi ya bwana Zuma ilifutwa muda mfupi kabla hajawania nafasi ya uraisi mwaka 2009. Rais wa zamani wa Afrika Kusini anayeshtakiwa kwa makosa ya rushwa inayohusishwa na mpango wa silaha wa mwaka 1990. text: Mwanasiasa huyo wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema anafahamu kwamba Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshi. Ameongeza kwamba alikuwa hana kwingi kwa kwenda kutafuta hifadhi baada yake kudaiwa kumdhalilisha mwanamitindo Afrika Kusini jambo lililomaanisha kwamba hawezi kuwa salama huko. Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa na jeshi. Kwenye taarifa rasmi kwenye runinga ya taifa awali, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alihakikishia taifa hilo kwamba rais na familia yake walikuwa salama na usalama wao ulikuwa umehakikishwa. Taarifa hiyo ilionekana kuashiria kwamba huenda familia ya rais ilikuwa inazuiliwa kwa pamoja nyumbani kwao Harare. Nick Mangwana, mwakilishi wa chama tawala cha Zanu-PF nchini Uingereza ameambia BBC kwamba mwenyewe pia amepokea taarifa kwamba Grace hayupo tena nchini Zimbabwe. Lakini Bw Mangwana amesema katika siasa za Zanu-PF, Bi Mugabe ni mtu wa chini sana na hana usemi wowote. Amesema ana mamlaka tu kwa sababu ya kuwa ni mke wa Rais Mugabe. "Alichukua wadhifa wa juu kuliko ule anaostahiki kuwa nao," amesema. Bi Mugabe amekuwa akitaka kuwa makamu wa rais, na sasa kwa sababu ameongoka, chama hicho kinaweza kufanya mkutano wake mkuu bila kuingiliwa. Amekiri kwamba si kawaida kwa jeshi kuchukua mamlaka katika nchi inayoongozwa kidemokrasia lakini kwamba hali haijakuwa ya kawaida Zimbabwe. "Tuna rais wa miaka 93, na hilo si jambo la kawaida, na hatuna sarafu yetu pia," amesema. Lakini amesema kirasmi Rais Mugabe bado yumo kwenye usukani kwani jeshi halijasitisha utekelezwaji wa katiba na kwamba taifa hilo bado lina serikali ya kiraia. Amesema rais Mugabe aliongoza mkutano wa baraza la mawaziri jana jioni kama kawaida. Grace Mugabe ni nani na mbona kuinuka kwake kunakumbwa na utata? Mbunge wa upinzani nchini Zimbabwe Eddie Cross ameambia BBC kwamba anaamini mke wa Rais Mugabe, Grace, ametorokea Namibia. text: Vita kusababisha maafa zaidi Sudan Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na kuzuia mauaji ya watu wengi, Adama Dieng amesema zaidi ya watu elfu 52 wamekimbilia nchini Uganda katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita pekee na wamekuwa wakizungumzia mauaji ya raia, uharibifu wa nyumba na unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa wakati wa mapigano hayo. Amesema binafsi ameshtushwa na hali ilivyo katika mji wa Kajo -keji ulioko kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Juba, ambako kikosi cha Walinzi wa Usalama wa Umoja wa Mataifa walifika huko siku ya Jumapili. Baada ya kupata uhuru wake mwaka 2011 Sudan ya kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 na kusababisha watu takriban milioni tatu kuyakimbia makazi. Zaidi ya watu milioni sita, nusu ya idadi ya watu wa nchi hiyo inasemekana wanahitaji msaada wa haraka. Umoja wa Mataifa umeonya juu ya mapigano yanayoendelea Sudan kusini kuwa yanaweza kusababisha maafa zaidi. text: Wanajeshi maalum wa Ufilipino wanakabiliana na wanamgambo wa Kiislamu Marawi Jeshi hilo limesema wanamgambo hao kwa sasa wanadhibiti maeneo machache sana ya mji huo wa kusini mwa Ufilipino. Bado kuna taarifa za mapigano kuendelea na maelfu ya raia wamekwama katika mji huo. Raia 19 wamethibirishwa kufariki, baadhi wakipatikana kwenye korongo wakiwa na majeraha ya risasi vichwani. Wapiganaji wanaoegemea kundi la Islamic State waliingia katika barabara za mji wa Marawi na kuanza mapigano baada ya jeshi kujaribu kumkamata mmoja wa viongozi wakuu wa kundi hilo. Wengi wa wakazi walitoroka baada ya vita kuzuka, lakini afisa mmoja wa serikali anasema kuna watu 2,000 ambao hawakufanikiwa kutoroka maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji hao. Msemaji wa Majeshi ya Ufilipino Brigidia Jenerali Restituto Padilla alsiema wanajeshi "wanaudhibiti mji wote ila maeneo machache sana" ambayo bado yanadhibitiwa na kundi la Maute. Alisema kuna wapiganaji kati ya 40 na 50 waliosalia katika mji huo, lakini hawa huenda wakaongezeka baada ya wapiganaji kuachilia wafungwa karibu 100 kutoka kwenye jela moja. Jenerali Padilla alsiema wanajeshi 18 wameuawa na zaidi ya wapiganaji 61 wa Maute kuuawa kwenye mapigano hayo. Taarifa zinasema wapiganaji hao bado wanashikilia mateka watu kadha, akiwemo kasisi na Wakristo kadha. Wanamgambo wa Maute waliweka bendera nyeusi sawa na za IS katika maeneo ya mji huo Raia wengi wa Ufilipino ni Wakristo, lakini maeneo ya Waislamu, hasa Mindanao yamekuwa yakipigania kujitenga. Mji wa Marawi hufahamika kama 'Jiji la Kiislamu' nchini Ufilipino kutokana na idadi kubwa ya Waislamu huko. Jeshi la Ufilipino limesema limepiga hatua kubwa katika kuukomboa mji wa Marawi kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu, huku makabiliano yaliyosababisha vifo vya watu 100 yakiendelea. text: Sharlene Cartwright-Robinson (kulia) ni waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Turks & Caicos Mwezi Disemba taifa hilo ambalo ni koloni ya zamani ya Uingereza, lilipata waziri mkuu wa kwanza mwanamke, Sharlene Cartwright-Robinson. Wanawake pia wanashikilia nyadhifa za naibu gavana, mkuu wa sheria, jaji mkuu, mkuu wa mashtaka na makatibu wengine watano wa kudumu, miongoni mwa nyadhifa zingine. Kufuatia wanawake kuwalemea wenzao wa kiume, sasa jitihada zinafanywa kuwapa motisha vijana wa ili wajeza kupigania nao nyadhifa za juu. Waliofanikiwa Wanawake nchini Turks & Caicos walipataje mafanikio kama hayo ambayo wengi wana ndoto ya kutapata? Waziri wa elimu Josephine Connolly (kushoto) akiwa na "wanawake wenye maona mazuri siku za usoni pamoja na wanaume" Bi Cartwright-Robinson ambaye chama chake cha PDM kilipata ushindi mkubwa tarehe 15 kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba anasema kuwa alikuwa "mwanamume bora kwa kazi hiyo" Akifanya kampeni kwa manifesto ya haki za jamii na serikali yenye uwazi, aliwashinda wagombea wengine 52 kupata wadhifa huo. Ushindi wake ulifikisha kikomo uongozi wa chama cha PNP wa miaka 13, wa waziri mkuu Michael Misick ambaye anakabiliwa na kesi ya ufisadi. Anaamini kuwa wanawake hufanya kazi kwa njia inayobora. "Wanawake huwa waaangalifu zaidi. Tunashikilia nyadhifa ambazo hatujawai na ukweli ni kwamba tunaziendesha kwa njia nzuri," Bi Cartwright-Robinson alisema. Rhondalee Braithwaite-Knowles aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza mkuu wa sheria nchini TCI mwaka 2014 Mwezi Februari mwaka 2014 Bi Braithwaite-Knowles, aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza mkuu wa sheria nchini humo baada ya kufanyika uchaguzi huru kote nchini. Kwa sasa kati ya wanafunzi 17 kutoka TCI ambao wamepata mafunzo nchi za kigeni 14 ni wanawake. Nyadhifa nyingi za juu za sheria nchini TCI zinashikiliwa na wanawake "Hakuna vizuizi" Mkuu huyo wa sheria anasema kuwa kile ambacho kitakuwa ni changamoto ni kujaribu kutekeleza majukumu ya kimaisha kama mama kwa mtoto wake wa miaka 7 na mke. Anasema kuwa kwa wanawake kupata nyadhifa kama hizo, wanastahili pongezi. Anasema ni vyema kuonyesha kuwa wamepata nyadhifa hizo kwa njia iliyo ya haki. BiConnolly, Bi Cartwright-Robinson na naibu Spika Karen Malcolm wana baadhi ya nyadhifa za juu nchini humo Naibu Gavana Williams anakubaliana na hilo. Wajibu wake ambao ni pili kutoka ule wa London wa John Freeman, pia ulikuwa wazi kwa wagombea kote duniani. Naibu Gavana Anya Williams aliapishwa kwa mara ya pili Desemba 21 Wajibu wa Bi Williams unahusu kusimamia idara ya wafanyakazi wa umma iliyo na wafanyakazi 1700. Aliapishwa na kujiunga na baraza la mawaziri kwa mara ya pili tarehe 21 mwezi Disemba. Anaiambia BBC kuwa wanawake wameishikia nyadhifa za juu kwenyr nchi hiyo ya watu 35,000, hasa katika nyanja za elimu, afya, siasa na serikali. Wanawake wengi bado hawajapata fursa ya kuchukua nyadhifa za juu katika nchi nyingi, lakini hiyo ni kinyume kwa Taifa la Caribbean la Turks & Caicos au TCI. text: Theo Martins Jackson Victor Mlotshwa alikuwa akizungumza nje ya mahakama ya mji wa kaskazini mashariki wa Middelburg ambapo waliotaka kumshambulia waliwasilishwa katika mahakama. Theo Martins Jackson and Willem Oosthuizen ''Nilidhani wataniua'',alisema. Kanda ya video ya dakika 20 iliorekodi kisa hicho imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini. Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani huko Middelburg anasema kuwa ndani ya mahakama hiyo ,washtakiwa hao ,Theo Martins Kackson na Willem Oosthuizen,walisimama wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini huku waandishi wa habari na raia wakichukua picha zao. Victor Mlotshwa Wameshtakiwa kwa kumteka nyara na kumshambulia kwa lengo kumjeruhi vibaya.Hawajakubali ama kukana mashtaka hayo. Wawili hao wanazuiliwa hadi tarehe 25 Januari huku waendesha mashtaka wakisema kwamba walihitaji muda zaidi kuchunguza ,ikiwemo kuthibitisha video hiyo. Victor Mlotshwa akisikiliza kesi mahakamani Mamake bw Mlotshwa alijawa na hasira na kushindwa kujizuia wakati wa kusikizwa kwa kwesi hiyo.Nje ya mahakama kulikuwa na kelele za wafuasi wa vyama vikuu nchini humo huku #RacismMustFall ikisambazwa katika mitandao ya kijamii. Mamake Mloshwa alishindwa kujizuia wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo Mtu mweusi nchini Afrika Kusini ambaye alidaiwa kulazimishwa kuingia katika jeneza na wakulima wawili weupe kwa kupita katika shamba lao amesema kuwa anahofia maisha yake. text: Hata hivyo, teknolojia ya uzazi wa kusaidiwa kwa upandikizaji wa mbegu za kiume katika yai la uzazi la mwanamuke na maarufu IVF, umelainisha mtizamo wa kitamaduni na hivyo kuwachochea wanawake wengi kupata watoto wakiwa na umri mkubwa jambo lililofanya uzazi wa njia ya kumbebea mimba mwanamke mwingine kuongezeka. Katika miongo miwili iliyopita, limekuwa ni jambo la kawaida duniani. Hakuna idadi kamili inayofahamika kuhusu idadi ya watot wanaozaliwa kwa njia hiyo lakini mwaka 2012 sekta ya uzazi wa kubeba mimba kwa niaba ya mwanamke mwingine ilikuwa na thamani ya dola takriban Bilioni 6 kwa mwaka. Nchini Uingereza pekee, idadi ya wazazi walioagiza wanawake kuwabebea mimba za watoto wao wana watoto mapacha watatu kuanzia 121 hadi 368 kufikia mwaka 2018 lakini idadi kamili ya matukio ya uzazi huu inaweza kuwa ni ya juu zaidi, kwani sio lazima kwa mtu kutuma maombi ya kufanya hivyo Kim Kardashiananatarajia kupata mtoto wa nne, wapili alipatikana kwa kubebewa mimba na mwanamke mwingine Aina za kupata mtoto kwa kusaidiwa na mwanamke unayemchagua Watoto wanaopatikana kwa njia ya mwanamke kujifungua kwa niaba ya mwanamke mwenzake huja kwa aina mbili - aina ya kwanza ni ile inayofahamika kama gestational, ambapo mama wa kujitolea hupandikizwa yai na mbegu ya uzazi ya mwanamume na ya pili iliyoanza kutumika tangu zamani ambapo yai la mwanamke anayejitolea kumzalia mwenzake hutumika. Mchakato huu unaweza kuleta faida kubwa, hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kupata watoto kwa njia ya kawaida, kwa kuwaruhusu watu binafsi na wanandoa kuwa na watoto wao ''wenyewe'' bila kupitia mchakato mrefu wa kuasili. Katika matukio mengi, mchakato huu hufanyika bila matatizo, Lakini uzazi huu ambao umekuwa maarufu umekuja kwa gharama za uanadamu na hadithi za uwezekano mateso wanayofanyiwa watoto wanaozaliwa kwa njia hii zimekuwa zikigonga vichwa vya habari katika miaka ya hivi karibuni. Mtoto mchanga Gammy na mama aliyesaidia kumpata Pattaramon Chanbua, ambaye amemlea na kumkuza Kwa mfano, kisa cha baby Gammy kilichotisha ulimwengu, wakati ilipodaiwa kuwa wazazi waliogiza azaliwe kupitia mama mwingine walimuacha makusudi Gammy, ambaye alikuwa na matatizo ya afya ya ubongo -Down's syndrome, nchini Thailand, huku wakimchukua pacha wake msichana Pipah nyumbani kwao Australia. Kizungumkuti cha kujaliwa watoto wenye jinsia mbili Mahakama baadae iliamuru kuwa hakuwa ametelekezwa, ingawa ilibainika kuwa baba aliyemuagiza awali alikuwa amepatikana na hatia ya makosa ya ubakaji wa watoto , jambo lililowafanya wengi wahofie maisha ya watoto hao wa uzazi wa kusaidiwa. Baby Manji alizaliwa kupitia mama wa India baada ya wazazi kutoka Japan kuagiza apandikizwe Hofu ya kwanza juu ya maslahiya watoto, kuna pia mifano ya wanawake wanaosaidia uzazi wa kuwabebea mimba wenzao wanaotumiwa vibaya na wakala na kutunzwa katika hali mbaya kinyume na ubinadamu. Wanawake wenye matatizo ya kifedha na kijamii wanaweza kulengwa kwa kazi ya kuwakutumiwa kuzaa watoto kwa ajili ya wanawake wenzao, na vile vile baadhi huvutiwa na pesa nyingi kufanya hivyo. Wazazi waliyo na watoto walemavu Zanzibar washauriwa kutowaficha majumbani Hata hivyo kumekuwa na taarifa za mateso yanayofanywa na akina mama wanaosaidiwa kupata watoto kwa watoto wanaowapata kwa njia hiyo ,huku baadhi wakikataa kuwalipa wakina mama waliowasaidia kuwazalia watoto pale wanaposhindwa kupata masharti yao au hata mimba zinapotoka kwa bahati mbaya. Hofu hizi zimesababisha nchi nyingi kufunga huduma yao ya awali ya kuwasaidia akina mama kupata watoto kwa kusaidiwa na wanawake wenzao huku mwaka jana Umoja wa mataifa ukionya kuwa uzazi wa kusaidiwa na mwanamke mwingine wa malipo kawaida ni sawa na kumuuza mtoto. Ukrainekimekuwa ni maarufu kwa uzazi wa ksaidiwa kupitia mwanamke anayelipwa Kuhusu taarifa hii Hii ni tathmini iliyoagizw ana BBC kutoka kwa wataalamu wanaofanya kazi nje ya shirika. Watoto wenye ulemavu wa ngozi walia ukiwa HIV yatumika kuwaponya watoto Daktari Claire Fenton-Glynn ni mwalimu katika Chuo kikuu cha Cambridge kitivo cha sheria ambako amebobea katika maswala ya hali za watoto, sheria ya familia na sheria ya kimataifa ta haki za binadamu Kujifungua mtoto au watoto kwa niaba ya mwanamke mwingine soi jambo geni. Kwa miaka maelfu kadhaa wanawake wamekuwa wakiwachagua wengine kujifungua watoto wa niaba yao. text: Wazazi hao wanasema hatua ya binti wao kukosa cheti cha kuzaliwa itaweza hatarini kutambuliwa kwa uraia wake. Wizara ya afya ya umma katika jimbo hilo ilikataa kumpa msichana huyo wa umri wa miezi 22 cheti cha kuzaliwa kwa sababu ya jina lake. Elizabeth Handy na Bilal Walk wanasema haikubaliki kwamba sasa mtoto wao ameachwa kirasmi akiwa hana jina. Lakini maafisa wa serikali katika jimbo hilo wanasema jina la ukoo la mtoto huyo - ZalyKha Graceful Lorraina Allah - linafaa kuwa Handy, Walk au majina yote mawili. Allah ni jina la Mungu kwa Kiarabu. Shirika la Haki za Raia Marekani (ACLU) tawi la Georgia limewasilisha kesi kwa niaba ya familia hiyo katika mahakama kuu ya wilaya ya Fulton. Babake msichana huyo aliambia gazeti la Atlanta Journal-Constitution kwamba aliamua kumpa jina Allah kwa sababu ni jina "adilifu". "Huu ni ukiukaji wazi wa haki zetu," Bw Walk alisema kuhusu hatua ya jimbo hilo kukataa kutambua jina hilo. Hata hivyo, mawakili wa Wizara ya Afya ya Umma ya jimbo hilo wanasema sheria za Georgia "hutaka jina la ukoo la mtoto liwe la baba au mamake mtoto kwa ajili ya hati ya kwanza rasmi ya kuzaliwa (kwa mtoto)." Kwenye barua kwa familia hiyo, maafisa wa serikali walisema jina la ukoo la ZalyKha linaweza kubadilishwa baadaye kupitia ombi kwa mahakama kuu ya jimbo hilo. Hata hivyo, hilo linaweza kufanyika tu baada ya cheti cha kwanza cha kuzaliwa kwa mtoto huyo kutolewa. Serikali kuvuka mipaka? Kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa kwa niaba ya familia hiyo, wanandoa hao ambao hawajafunga ndoa rasmi wana mtoto wa kiume aliyepewa jina Masterful Mosirah Aly Allah. ACLU wanasema bila kupata cheti cha kuzaliwa, itakuwa vigumu kwa wazazi hao kupata nambari rasmi ya utambulisho kwa ajili ya kupokea huduma kutoka kwa serikali. Wanahofia kwamba huenda utambulisho wa msichana huyo, pamoja na haki zake kama raia wa Marekani zikatiliwa shaka. ACLU wamesema hatua ya jimbo hilo kukataa kutimiza maombi ya familia hiyo ni mfano wa serikali kuvuka mipaka na kutofuata katiba. "Wazazi ndio huamua jina la mtoto," twakili wa familia hiyo Michael Baumrind amesema. "Sio jimbo. Ni suala rahisi sana." Wanandoa wawili katika jimbo la Georgia nchini Marekani wamewasilisha kesi mahakamani baada yao kuzuiwa kumpa mtoto wao jina Allah. text: Ushirikiano mwingi uliokuwepo katika enzi za uliokuwa muungano wa Sovieti ulikatizwa baada ya kuanguka kwa Muungano huo, lakini wakati uhusiano na magharibi ukififia kwa mara nyingine, Kremlin imeidhinisha uhusiano wa kutosha kiuchumi, kiusalama na kisiasa na Afrika. Moscow itajaribu kuimarisha zaidi uhusiano huu wakati wa mkutano wa kwanza baina ya Urusi na Afrika unaofanyika mjini Sochi kuanzia leo tarehe 23 hadi kesho Oktoba 24. ratiba ya mkutano huo ni kujadili nishati, madini na ushirikiano wa kijeshi. Kufikia 2018, biashara ya Urusi na bara la Afrika ilikuwa na thamani ya dola bilioni 20.4, iliyoongezeka mara nne zaidi ya ilivyokuwa 2010. Kumekuwa na tuhuma nyingi kuhusu Urusi kupanua kwa siri uwepo wake kijeshi kwa kuwatumia mamluki katika baadhi ya mataifa ya Afrika na pia kuwatuma wawakilishi na kusambaza taarifa zisizo sahihi katika kampeni ya kushawishi siasa za dai ya nchi. Moscow imeshuhudia ziara rasmi zinazoongezeka, huku viongozi 12 wa mataifa ya Afrika wakifika katika mji mkuu Moscow tangu 2015. Mkutano huo unafanyika chini ya uenyekiti wa rais Vladimir Putin na kiongozi mwenzake wa Misri ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Abdel Fattah el-Sisi. Biashara ya silaha Mkutano huo unatoa fursa kwa Urusi kujadili mikataba ya silaha na ushirkiano wa kijeshi. Licha ya kwamba soko la silaha za Urusi ni Asia, Moscow imefanikiwa kujikita Afrika pia. Kwa mujibu wa taasisi ya utafiti - Stockholm International Peace Research Institute (SIPRI), Asia hununua kiasi ya nusu ya silaha zote zinazosafirishwa kutoka Urusi, huku Afrika ikinunua 30% mnamo 2018, huku wateja wakuu wakitoka Afrika kaskazini - yaani Algeria na Misri - ikijumuisha 95% ya mauzo yote ya silaha za Urusi barani Afrika mnamo 2018. Urusi pia imeziuzia silaha Angola, Burkina Faso, Cameroon, Equatorial Guinea, Mali, Nigeria, Sudan kusini na hata Sudan. Mnamo Septemba 2018, mkuu wa idara ya huduma kwa jeshi Dmitry Shugayev amesema mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara yaliagiza silaha zenye thamania ya zaidi ya dola bilioni 3. Nigeria imeeleza kutaka kusaini ushirkiano wa kijeshi mwezi huu Oktoba, gazeti la Urusi Izvestia limeeleza. Rais Muhammadu Buhari anatarajiwa kukutana na Putin kando kando mwa mutano huo kukamilisha makubaliano yatakayoisaidia serikali kupambana na wanamgambo wa Boko Haram, Balozi wa Nigeria mjini Moscow amesema. Mnamo Agosti mwaka huu, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema mazungumzo yanaendelea kuanzisha utaratibu katika bandari Eritrea " kuidhinisha biashara ya pande mbili". Mradi huo pia utaiweka Urusi karibu na kambi ya kijeshi ya Marekani katika nchi jirani ya Djibouti. Mamluki Televisheni nchini Urusi ilikana uwepo wa mamluki wa Kirusi barani Afrika Suala moja ambalo litasalia kimya kima ni taarifa za uwepo wa mamluki wa Urusi barani Afrika. Waandishi watatu wa Urusi waliuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka mmoja uliopita wakiwa wanachunguza ripoti kuwa kampuni binafsi ya kijeshi inayoitwa Wagner ipo nchini humo. Inaarifiwa kuwa Wagner ina uhusiano na mfanyabiashara anayehusishwa na Kremlin Yevgeny Prigozhin. Kwa mujibu wa Bloomberg, Wagner ipo katika mataifa mengine kadhaa zikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Sudan, Libya, Madagascar, Angola, Guinea, Guinea-Bissau, Msumbiji, na Zimbabwe. Hivi karibuni, mwezi huu Oktoba, The Times iliripoti kuwa mamluki wapatao 200 wa Urusi waliwasii Msumbiji kuisaidia serikali kupambana na wapiganaji jihadi. Kremlin ilikana uwepo wa wanajeshi wa Urusi katika taifa hilo. Kampeni za ushawishi wa kisiasa Kumekuwa na taarifa pia kwamba Urusi imekuwa ikijaribu kushawishi siasa katika baadhi ya mataifa ya Afrika kupitia operesheni za mfanyabiashara huyo Prigozhin. Mfano, Kremlin inatuhumiwa kujaribu kushawishi uchaguzi wa urais wa Malagasy mwishoni mwa 2018. Mnamo Mei mwaka huu Urusi ilituhumiwa kuwahiribia jina viongozi wa upinzani Afrika kusini Julius Malema na Mmusi Maimane. Duru za kutoka Kremlin zimetoa taarifa mwezi huu zikipuuzilia mbali kuwa Prigozhin aliuawa katika ajali ya ndege huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mradi wa uchunguzi - The Dossier Centre, unaofadhiliwa na mkosoaji wa serikali ya Urusi, Mikhail Khodorkovsky, umedai kuwa mfanyabiashara huyo Prigozhin alihusika pia katika mipango ya Urusi kumuunga mkono kiongozi wa Sudan wa zamani Omar al-Bashir. Mnamo Desemba 2018, Al-Bashir alikuwa kiongozi wa kwanza wa jumuiya ya nchi za kiarabu kuizuru Syria tangu kuzuka vita nchini humo. Alipigwa picha akisalimiana na rais Assad mbele ya ndege ua Urusi ambayo inaarifiwa ndio iliomsafirisha kwenda Damascus. Mafuta na Gesi Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alifanya ziara kwenda Moscow mnamo Agosti Kampuni kubwa za mafuta Urusi Rosneft na Lukoil zimehusika katika uchimbaji wa mafuta na gesi barani Afrika. Rosneft imehusika katika utafutaji gesi nchini Msumbiji na inashikilia 20% ya hisa katika mradi huo. Inamiliki hisa pia katika miradi kama hiyo nchini Misri na Algeria, licha ywa kwamba kumekuwana taarifa kwamba Urusi inatazamai kuuza hisa zake hapo baadaye. Lukoil ina miradi nchini Cameroon, Ghana, Nigeria, kwa mujibu wa gazeti la biashara la kila siku Kommersant. Mnamo Juni mwaka huu, iliarifiwa kuwa Lukoil inaelekea kukamilisha ununuzi wa 25% ya hisa ya mradi wa mafuta Marine XII katika Jamhuri ya Congo, gazeti la Urusi Vedomosti limeandika. Nyuklia Nishati ya nyuklia inatarajiwa kuwa mada kuu katika mkutano huu wa Sochi. Imeripotiwa kuwa Putin huenda akajadili ujenzi wa rusi wa kinu cha kwanza cha nyuklia huko El Dabaa nchini Misri. Ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwakani, huku Urusi ikijitolea mkopo wa dola bilioni 25 kwa Misri kufadhili mradi huo. Katika mahojiano na shirika la habari Urusi RIA Novosti, balozi wa Nigeria mjini Moscow Steve Ugbah amesema rais Muhammadu Buhari alinuia kujadili uwezekano wa Urusi kuhusika katika ujenzi wa vinu viwili vya nyuklia nchini mwake. Kwa mujibu wa RIA Novosti, Ethiopia pia inatumai kutumia mkutano huu leo kusaini makubaliano na Urusi kuhusu ujenzi wa kinu cha nyuklia. Kwa sasa Urusi ina ushirkiano wa miradi ya nyuklia na Rwanda, Uganda na Sudan. Bwawa Ethiopia Mkutano wa Sochi pia unatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo yanayolenga masuala matupu kuhusu Afrika. Mfano Misri na Ethiopia zinatarajiwa kutafuta azimio la mkwamo kuhusu mradi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance katika mto wa Blue Nile nchini Ethiopia. Cairo inasema linaweza kusababisha uhaba wa maji nchini Misri. Katika miaka michache iliyopita, Urusi imerudi upya kama nguvu ya kutambuliwa katika bara la Afrika. text: Katika video hiyo, iliotolewa ili kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan , kiongozi huyo alizungumza kwa lugha ya Kiarabu na kuonekana kutatizika kuona, kutokana na vile alivyokuwa akipata matatizo ya kusoma maandishi yake. Katika ujumbe wake kiongozi huyo alipinga demokrasia na kutetea sera za kundi hilo za chuki dhidi ya elimu ya dunia na chochote kinachohusiana na utamaduni wa magharibi. Hakuna lolote jipya isipokuwa wakati ambao kanda hiyo imetolewa ni muhimu na huenda inatuma ujumbe wa moja kwa moja kwa serikali ya Nigeria. Lengo la kanda hiyo ya video Rais Muhammadu Buhari aliapishwa kwa muhula wa pili wiki iliopita huku taifa hilo likiwa miaka 20 tangu kurudi kwa demokrasia- mfumo wa serikali ambao kundi la Boko haram limekuwa likijaribu kuupindua ili kuweka sheria ya kiislamu. Inonekana kwamba bwana Shekau anajaribu kutoa ishara kwamba yeye na kundi lake bado wapo licha ya kwamba kundi la Boki haram linaloshirikiaa na wapiganaji wa islamic State IS ndilo linaloonekana kutekeleza mashambulio mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria. Shekau ambaye ameliongoza kundi la Boko haram kwa muongo mmoja , alianzisha ushirikiano na IS 2015, akiliita kundi hilo Islamic State mkoa wa Afrika magharibi (iswap). Ujumbe huo unaonekana kulilenga jeshi ambalo hivi karibuni lilisema kuwa mashambulizi yake yalilishinda kundi la Boko Haram, ijapokuwa limekiri kwamba kundi la Iswap ni changamoto kubwa. Kundi la Iswap latoa changomoto kwa Boko Haram Lakini mwaka uliofuata, kundi hilo lilivunjika baada ya IS kumfuta kazi Shekau, kwa kutekeleza mashambulizi bila kujali raia wakiwemo Wislamu , wanawake na watoto. Shekau na kundi lake la Boko Haram waliendelea kufanya mashambulizi yao tofauti na kundi la Iswap. Uasi wa miaka 10 wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria - na nchi nyingine kadhaa - umewaua zaidi ya watu 20,000 na kulazimisha mamilioni ya wengine kutoroka makaazi yao. Kiongozi wa kundi la Boko haram nchini Nigeria Abubakr Shekau , amejitokeza katika video mpya ikiwa ni ya kwanza baada ya kipindi cha mwaka mmoja. text: Vyombo vya habari vilionyesha picha hiiiliyoonyesha Kim Jong-un akizindua kiwanda cha mbolea Ijumaa Shirika la habari la KCNA limeripoti kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskanzini alikata utepe katika ufunguzi wa kiwanda cha mbolea. Liliongeza kuwa watu katika kiwanda hicho '' walimshangilia shangwe kubwa" alipojitokeza siku ya Ijumaa. Taarifa za kuonekana kwake-mara ya kwanza tangu alipoonekana katika tukio kwenye vyombo vya habari vya taifa hilo tarehe 12 Aprili- zinakuja huku kukiwa na tetesi kote duniani kuhusu afya yake. Taarifa za hivi punde kutokavyombo vya habari vya taifa la Korea Kaskazini hazikuweza kuthibitishwa. Vyombo vya habari baadae vilitangaza picha ambazo zilionyesha Bwana Kim akikata utepe nje ya kiwanda. Alipoulizwa kuhusu taariofa za kuonekana kwa Kim, rais wa Marekanai Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa asingetaka bado kuzungumzia lolote juu ya taarifa hizo. Je rip[oti ya vyombo vya habari vya taifa inasemaje? Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa- Korean Central News Agency (KCNA), Bwana Kim aliambatana na maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini, mkiwemo dada yake Kim Yo Jong. Kiongozi wa Korea Kaskazini akakata utepe katika sherehe iliyofanyika katika kiwanda, katika jimbo la kaskazini mwa nchi la Pyongyang, na watu waliohudhuria tukio hilo " walimshangilia kwa shangwe kubwa ' kiongozi huyo wa ngazi ya juu ambaye anawaamuru watu wote kwa ujumla kutimiza jukumu zuri la mafanikio ", KCNA ilisema. "Kelele za shangwe kubwa '" zilisikika wakati kiwanda kilipofunguliwa, kwa mujibu wa KCNA Bwana Kim alisema kuwa ameridhishwa na mfum wa uzalishaji wa kiwanda, na akakisifu kwa kuchangia katika maendeleo ya viwanda vya kemikali na uzalishaji wa chakula, liliongeza shirika hilo Ni nini kilichoibua tetesi kuhusu afya yake? Tetesi kuhusu afya ya Kim zilianza baada ya kukosa katika sherehe za maadhimisho ya sikuuu ya kuzaliwa ya babu yake, muasisi wa taifa Kim Il Sung tarehe 15 Aprili. Kumbukumbu hiyo ni moja ya matukio makubwa katika kalenda ya Korea Kaskazini, na Bwana Kim kwa kawaida huadhimisha siku hii kwa kutembelea katika eneo la makumbusho yenye mnara ambako babu yake amezikwa. Bwana Kim hajawahi kukosa kuhudhuria tukio hili. Madai kuhusu kuugua kwa Bwana Kim, yaliandikwa katika tovuti ya muasi wa Korea Kaskazini. Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kufahamika kiliiambia Daily NK kuwa "wana taarifa kuhusu matatizo yake ya kiafya langu mwaka jana mwezi Agosti, lakini tatizo limezidi kuwa kubwa baada ya kurudia kutembelea mlima Paektu". Hii imevifanya vyombo vingine vya habari vya kimataifa kuripoti kwa kutegemea chanzo kimoja. Wakala wapya wa habari wakaanza kuja na madai kuwa ndio hicho walichokuwa nacho mpaka ripoti kutoka kikosi cha ujasusi kilichopo Korea Kusini na Marekani kufuatilia madai hayo. Lakini wakaja na kichwa cha habari cha taharuki zaidi kutoka vyobo vya habari vya Marekani kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini yuko kwenye hali ya mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Kim Jong-un hajawahi kukosa kuhudhuria kumbukumbu za siku ya kuzaliwa ya babu yake awali Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alikuja kuongeza chumvi tetesi hizo kwa kusema hadharani tarehe 29 Aprili kuwa hawajamuona Bwana Kim hivi karibuni. Ingawa taarifa kutoka serikali ya South Korea na taarifa kutoka wana intelijensia wa China alizungumza na wakala wa habari- Reuters - kusema kuwa hakuna ukweli wowote katika hilo. Je Kim Jong-un aliwahi kutoonekana kwa muda hapo awali? Ndio bwana Kim aliwahi kupotea kwa muda wa siku 40 mnamo Septemba 2014, baada ya kuhudhuria tamasha. Na akaonekana tena katikati ya mwezi Oktoba akiwa anatumia fimbo. Chombo cha habari cha taifa hilo hakikuwahi kuelezea alikuwa wapi. Lakini kikosi cha ujasusi cha South Korea kilisema kuwa labda walikuwa anafanyiwa operesheni ya goti lake ambalo lilipata shida. Bwana Kim Jong-akiwa anapanda mlima Paektu Uchambuzi Na Laura Bicker Mwandishi wa BBC Seoul Tahadhari huwa inawekwa katika kuripoti taarifa kuhusu North Korea. Chanzo cha habari ni kidogo, na tetesi ndio zinakuwa zinavuma zaidi na kusababisha vichwa vya habari kuhusu Kim Jong-un kuwavutia watu wengi. Ni ngumu sana kupata ripoti sahihi kutokana na usiri wa taifa hilo. Ukweli na vyanzo vya habari ni ngumu kupatikana haswa tangu taifa hilo kuwa limefungwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona. Serikali ya South Korea ilikuwa wazi kusema kuwa imebaini kuwa Nort Korea haifanyi shughuli zake kama kawaida. Seoul huwa ina kitengo cha majasusi wazuri kutoka Pyongyang. Lakini hata wao wamekuwa wakikosea hapo nyuma.Tuwe wazi kuwa Kim Jong-un alikuwa anaugua au alifanyiwa upasuaji wiki mbili zilizopita. Au alikuwa mapumzikoni akiicheka dunia kwa utabiri wao mbaya. Kutoonekana kwake kwa siku 20 bila maelezo yoyote bado kuna maswali mengi kuhulizwa kuhusu mridhi wake na mipango yake ni ipi kama chochote kikitokea kwake. Lakini kuna jambo moja ambalo halipo katika haya yote, North Korea ni zaidi ya mwanaume mmoja .Ni taifa ambalo lina watu milioni 25 ambao wamekuwa wamefungiwa. Leo Bwana Kim kutoonekana ilikuwa kama mmea ambao uliorutubishwa kunyauka. Vichwa vya habari vikasababisha kurejea kwake lakini alikuwa wapi na je vita vitaweza kusaidia taifa lake kukomboka katika uhaba mkubwa wa chakula. Ninawahakikishia kuwa watu wa North Korea sasa hivi, kuwa hilo ni jambo muhimu zaidi ya kujua kiongozi wao alikuwa wapi. Kim Jong-un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya siku 20, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema. text: Sasa Ufaransa inazindua ripoti ya kutoa wito wa kutaka maelfu vinyango kutoka Afrika vilivyo kwenye makavazi yake kurudishwa Afrika. Shaba za Benin Kinyago cha shaba kutoka Benin Shaba za Benin ni mkusanyiko wa vinyago vya thamani kubwa vilivyokuwa kwenye kasri la kifalme la Oba, Ovonramwen Nogbaisi, katika ufalme wa Benin. Vilichongwa kutoka kwa pembe za ndovu, shaba na kutoka kwa miti. Vingi vilichongwa kwa madhabahu ya wafalme za zamani na malkia. Mwaka 1897 Waingereza waliendesha uvamizi dhidi ya Benin kujibu shambulizi dhidi ya wanadiplomasia wa Uingereza. Kando na vinyago vya shaba, vifaa vingi vilichukuliwa na sasa vinasambazwa kote duniani. Vinyago hivi vya shaba kutoka Benin vilirudishwa Nigeria mwaka 2014 kutoka Uingereza. Makavazi mjini London yanasema kuwa vifaa kutoka Benin viliwasilishwa kwake mwaka 1898 na ofisi ya mashauri ya nchi za kigeni. Mwezi Oktoba makavazi makubwa ya barani Ulya yalikubali kutoa kwa mkopo vinyago kwenda nchini Nigeria kwa makavazi yake mapya yanayopangwa kufuguliwa mwaka 2021. Simba wala watu Sanamu ya simba wawili kutoka Tsavo zilinyakuliwa na kupelekwa Chicago, Illinois Hawa ni simba wawili maarufu wala watu kutoka eneo la Tsavo nchini Kenya, Afrika Mashariki ambao waliwaua na na kuwala wafanyikazi wa reli kutoka nchini Uingereza waliokuwa na asili ya Kenya -Uganda mwishoni mwa karne ya 19 . Wafanyikazi hao walikuwa wakijenga reli kati ya Mombasa na ziwa Victoria kwa miezi tisa mnamo mwaka 1898. Luteni kanali John Patterson mmoja wa simba aliyemuua Simba hao walipigwa risasi na kuawa na mhandisi wa Ungereza Luteni kanali John Patterson. Sanamu ya simba hao ilinunuliwa kutoka kwa Patterson na makavazi ya historia ya Marekani iliyopo mji wa mwaka 1925 na kuhifadhiwa kama vituo asilia vya kudumu. Luteni kanali Patterson aliripoti kuwa simba hao waliwaua na kuwala takribani wafanyikazi 135 wakiwemo waafrika weusi, Lakini makavazi inayohifadhi mabaki yao baadaye ilisema watu waliouawa walikuwa karibu 35. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi wao. Makavazi ya kitaifa ya Kenya sasa inataka mabaki ya simba hao kurejeshwa nyumbani. Jiwe la Rosetta Jiwe la Rosetta katika makavazi ya Ungereza ya Bloomsbury Oktoba October 14, 2016 mjini London Jiwe hilo la Rosetta la urefu wa mita 1.12 kwenye makavazi ya Uingereza likitokea nchini Misri. Ni sehemu ya jiwe kubwa lenye maandishi juu yake ambayo yamewasaidia watafiti kujifunza jinsi kusoma kuhusu mifumo ya kuandika nchini Misri uliotumia picha na ishara. Haijulikani vile jiwe hilo liligunduliwa mwezi Julai mwaka 1799 lakini kuna imani kuwa liliguduliwa na wanajeshi waliopigana na kiongozi wa jeshi la Ufaransa Napoleone Bonaparte wakati wakijenga kwenye mji wa Rashid. Wakati wa Napoleon, Waingereza walichukua umiliki wa jiwe hilo chini ya makubaliano yaliyofahamika kama Treaty of Alexandria mwaka 1801. Malkia Bangwa Mchongo wa malkia Bangwa Queen kwa sasa unamilikiwa na wakfu wa Dapper mjini Paris, Ufaransa Hii ni sanamu maarufu la kuchongwa la Malkia Bagwa kutoka inayojulikana sasa kama Cameroon mwishoni mwa karne ya 19. Sanamu hilo lenye urefu wa inchi 32 au (sentimita 81) linaashiria madaraka na afya ya watu wa Bangwatall Bangwa. Ni moja ya sanamu maarufu zaidi Afrika na ina umuhimu mkubwa kwa watu nchini Cameroon. Sanamu zilichongwa na kupewa majina ya wake wa wafalme au wanaufalme na kuitwa Malkia wa Bangwa huko Bangwa. Sanamu ya Malkia wa Bangwa labda ilipewa au kuibwa na wakoloni wa Ujerumani karibu mwaka 1899 kabla ya eneo hilo kutawaliwa na wakoloni. Vito vya thamani vya Maqdala Taji la Maqdala Vito vya thamani ya Maqdala ni pamoja na taji la karne ya 18 na nguo ya harusi vilivyochukuliwa kutoka Ethiopia na jeshi la Uingereza mwaka 1868. Wanahistoria wanasema ndovu 15 walihitajika kubeba vifaa vilivyoibwa kutoka Maqdala. Waingereza walivamia Maqdala kupignha kutwalia kwa ubalozoi wao wakati uhusiano kati ya pande hizo ulidorora. Nguo hii ya miaka ya 1860 inaaminiwa kuwa ya malkia Woyzaro Terunesh Ndege wa Zimbabwe Ndege wa Zimbabwe Vinyago nane wa ndege wa Zimbabwe waliibwa kutoka mahame ya mji wa zamani. Ni ndege nane waligunduliwa. Walikuwa kwennye kuta za mji wa kale uliojengwa kati ya karne ya 12 na 15 na wahenga wa watu wa Shona. Saba kati ya vinyago hao walikuwa nchini Zimbabwe tangu mwaka 2003 wakati mmoja alirudishwa kutoka Ujerumani. Picha zote zina hakimiliki Wakati wa utawala wa ukoloni barani Afrika, maelfu ya vinyago viliharibiwa. Nchi za Afrika zinataka virudi na makavazi makubwa zaidi kote ulaya yamekubali kutoa vinyago maarufu vya shaba vya Benin kwa mkopo kwenda Nigeria. text: Madaktari watapata ujuzi wa kung'amua mapema maradhi ya saratani na kuyashughulikia ipasavyo Hii ni sehemu ya mpango ulioandaliwa na taasisi Uingereza ya British Council kwa ushirikiano na chuo cha kitabibu cha Uingereza cha Royal School of Physicians, serikali za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda, na kudhaminiwa na benki ya maendelea ya Afrika mashariki. Mradi huo unalenga kuongeza idadi ya madaktari wanaoweza kushughulikia visa vya saratani vinavyoendelea kuongezeka. Nchini kenya pekee, takriban watu 28,000 hupatikana na maradhi ya saratani kila mwaka. Wengi wao hutambua kuwa wana ugonjwa huo wakati ukiwa umefikia kiwango cha juu. Lakini mpango huu mpya ulioanzishwa kwa madaktari unatarajiwa kuongeza idadi ya madaktari wenye ujuzi wa kung'amua mapema maradhi ya saratani na kuwahudumia ipasavyo. Madaktari hao 600 watachaguliwa kutoka hospitali za serikali zanye ukosefu wa madaktari bingwa na ambazo ziko mbali na miji. Baada ya mafunzo madaktari hao watatakiwa kuhakikisha wanarejea kwenye hospitali walikoajiriwa na kufanya kazi kwa walau miaka mitano. Mara kwa mara wagonjwa wengi wa saratani katika kanda ya Afrika mashariki hulazimika husafiri nje ya nchi kwa matibabu kutokana na ukosefu wa ujuzi muhimu wa kitabibu, ukosefu wa teknolojia na dawa. Madaktari 600 wanaofanyia kazi katika nchi za Afrika mashariki watapata mafunzo maalum juu ya saratani na magonjwa mishipa mjini London kwa kipindi cha miaka minne . text: Bw Osinbajo amesema wasichana wote wamo buheri wa afya. Rais Muhammadu Buhari yumo kwenye ziara rasmi nchini Ujerumani. Afisa wa usalama ameambia BBC kwamba wasichana hao waliachiliwa huru karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon. Amesema waliachiliwa kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana, ambapo wafungwa wanne wa kundi la Boko Haram waliachiliwa huru na serikali. Lakini serikali imekanusha madai hayo kwamba makamanda wane wa Boko Haram waliachiliwa huru ndipo kundi hilo likubali kuwaachilia huru wasichana hao. Kundi hilo liliwateka zaidi ya wasichana 250 kutoka kwenye shule ya Chibok Aprili mwaka 2014, kisa kilichoshutumiwa vikali na jamii ya kimataifa. Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ni miongoni mwa walioshiriki kampeni ya kutetea kuachiliwa huru kwa wasichana hao iliyokuwa na kitambulisha mada #BringBackOurGirls. Wasichana 21 waliotekwa na kundi la Boko Haram miaka miwili iliyopita, ambao waliachiliwa huru jana, wamekutana na makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo. text: Madaktari na wauguzi wamekuwa wakigoma tangu mwezi Disemba Maafisa wa chama cha madaktari walikuwa wamepewa vitisho kuwa watafungwa ikiwa mgomo huo haungeisha leo. Madaktari wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara. Wamekataa mshahara walioongezewa na serikali wa asilimia 40 wakisema kuwa ni wa chini kuliko ule walioafikiana mwaka 2013. Karibu madaktari na wauguzi 5000 kutoka hospitali 2000 za umma, walianza mgomo wiki ya kwanza ya mwezi Disemba na wagonjwa wamekuwa wakikosa matibabu. Jaji katoka mahakama ya ajira amesema kuwa siku hizo tano sio za mazungumzo bali za kumaliza mgomo. Mahakama nchini Kenya imewapa madkatari wa wauguzi muda wa siku tano kumaliza mgomo wao. text: Raia huyo wa Jamaica mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kucheza mechi ya mazoezi katika ya klabu hiyo na timu ya taifa ya Norway ya wachezaji wa chini ya miaka 19 baadaye wiki hii katika klabu hiyo. Bolt, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za 100m na 200m, tayari amefanya mazoezi na Borussia Dortmund ya Ujerumani na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. "Pengine kuna klabu itaona jambo zuri kwangu na kunipa nafasi," alisema Bolt ambaye anajiandaa kwa mechi ya hisani. Atakuwa nahodha wa timu inayowajumuisha watu nyota na wachezaji nyota wa sasa na waliostaafu katika mechi ya Soccer Aid kwa ajili ya kuchangisha pesa za kutumiwa na Unicef 10 Juni uwanjani Old Trafford, Uingereza. Kutakuwa na timu ya England na timu ya watu kutoka nje ya England (Dunia XI) "Yeye ni mchezaji mzuri, vinginevyo hangekuwa akishiriki mazoezi nasi," mkurugenzi wa uchezaji wa Stromsgodset Jostein Flo alisema. Flo amesema Bolt amepewa jezi nambari 9.58 - rekodi yake katika mbio za mita 100m. Kuwasili kwake Stromsgodset kuliwashangaza wachezaji. Wachezaji wa timu zitakazokabiliana mechi ya Soccer Aid England Robbie Williams, Olly Murs, Mo Farah, Paddy McGuinness, Michael Owen, Ben Shephard, Mark Wright, Wes Brown, Joe Wicks, David Seaman, Lee Mack, Phil Neville, Freddie Flintoff, Danny Murphy, Myles Stevenson, Jamie Redknapp na Robbie Fowler. Wachezaji wa timu ya dunia (Dunia XI) Usain Bolt, Clarence Seedorf, Robert Pires, Gordon Ramsey, Brendan Cole, Yaya Touré, Kevin Pietersen, Jaap Stam, Dan Carter, Patrick Kluivert, Edwin van der Sar, Eric Cantona na Ashley Fongho. Flo, mchezaji wa zamani wa Sheffield United alisema: "Tuliwafahamisha kwamba kuna mchezaji ambaye angefika kufanya mazoezi na kwamba ana kasi ajabu - mlango ulifunguliwa, na Bolt akaingia. Wengi wao walipatwa na mshangao, hawakuamini." "Yeye ni mmoja wa wanariadha nyota zaidi katika historia, na bila shaka tunaweza kujifunza mengi sana kutoka kwake. "Uwepo wake hapa bila shaka utawatia moyo wachezaji, wakufunzi na klabu yote." Bolt alistaafu kutoka kwenye riadha Agosti mwaka 2017 baada ya mashindano ya ubingwa wa dunia jijini London. Mwanariadha huyo ni shabiki sugu wa klabu ya Manchester United ya Uingereza na amekuwa akizungumzia hamu yake ya kutaka kucheza kandanda. Bolt alitia saini mkataba na kampuni ya mavazi ya Ujerumani ya Puma ambao pia ni wadhamini wa Sundownd akiwa bado mdogo mwaka 2003. Usain Bolt akifanya mazoezi na Mamelodi Sundowns Amekuwa akiashiria hamu yake ya kuwa mwanakandanda baada yake kustaafu riadha, na anaamini kwamba anaweza kuwa sawa kiasi cha kuchezea timu ya taifa ya Jamaica. Bolt alifanya mazoezi wiki moja na klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund mwezi Machi mwaka huu. Amekuwa akisema tangu akiwa mdogo alikuwa na ndoto ya kucheza kandanda. Bingwa wa Olimpiki mara nane Usain Bolt anafanya mazoezi na soka na klabu inayocheza ligi kuu ya Norway, Stromsgodset. text: Ramil Shamsutdinov ambaye amekamatwa - huenda alikuwa akiugua tatizo la kiakili , wanasema. Tukio hilo lilifanyika katika kitengo cha kijeshi nambari 54160 katika kijiji cha Gorny , sio mbali na mji wa Chita, siku ya Ijumaa jioni. Uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea. Je ni nini kinachojulikana kuhusu shambulizi hilo? Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa kumi na mbili na robo , kulingana na kamati ya uchunguzi ya Urusi. Wizara ya ulinzi mapema ilisema kwamba risasi zilifyatuliwa wakati wa kubadilishana zamu katika eneo la Transbaikal. Bwana Shamsutdinov , kurutu, aliwaua maafisa wawili na wanajeshi wenzake sita. Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti kwamba mshukiwa huyo aliwalenga waathiriwa katika vichwa. Tume maalum inayoongozwa na naibu waziri wa ulinzi Andrey Kartapolov inaelekea katika eneo hilo ili kuchunguza mauaji hayo. Kitengo hicho cha jeshi nambari 54160 kinahifadhi makombora. Kina makombora ya Iskander ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vya kinyuklia. Huduma za jeshi ni lazima nchini Urusi kwa wanaume wote walio kati ya umri wa miaka 18-27. Wao uhudumu kwa miezi 12 , na baadaye wanaweza kusaini kandarasi za kitaalam ili kuendelea kuhudumu katika jeshi. Katika miaka ya 2000, makundi ya haki za kibinadamu yaliripoti ghasia na unyanyasaji kwa jina ''dedovshchina'' dhidi ya makurutu wapya katika jeshi la Urusi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, Urusi inajivunia kuliimarisha jeshi lake na kuondoa unyanyasaji. Mwanajeshi mmoja wa Urusi amewapiga risasi wanajeshi wenzake wanane na kuwajeruhi vibaya wengine wawili katika kambi ya kijeshi iliopo mashariki, kulingana na maafisa. text: Wakati wa kikombe cha chai katika jumba la "urafiki wa kimataifa" Aidha, mara kwa mara taarifa za raia wa nchi za Magharibi kukamatwa na kufungwa jela huripotiwa. Lakini sasa kuna mwanafunzi Mwingereza ambaye anaamini wengi hawajalifahamu vyema taifa hilo. Badala ya kuitenga Korea Kaskazini, anaamini wakati umefika kwa watu kufanya urafiki na taifa hilo. "Tumekuwa wepesi wa kuibandika Korea Kaskazini manenokama vile 'marufuku' 'taifa lenye usiri mkubwa', 'dhiki', 'ukatili' na kadhalika, lakini nataka kuondoa dhana hiyo, angalau kwa dakika moja, tuitazame Korea Kaskazini katika ngazi ya utu,2 anasema Benjamin Griffin, 24. Kabla yake kufanya ziara yake ya kwanza nchini humo miaka minne iliyopita, ufahamu wake kuhusu nchi hiyo anasema ulitokana na "makala moja pekee aliyokuwa ameitazama na video fupi za YouTube." Lakini alipata nafasi ya kusafiri taifa hilo kwa kutumia shirika lakitalii la Juche Travel Services (JTS), safari iliyomfumbua macho. "Nilipoiona Pyongyang kwa mara ya kwanza mwaka 2013, nilitarajia kuwaona wanajeshi kila nilikoenda. Ni kana kwamba sikuwa nawatazama kama watu halisi," anasema. Lakini ukweli ni kwamba tuliwaona watu wakitembea kwenda kazini, kwenda madukani na kucheza ngoma katika bustani. Kwa kiasi fulani, nilishangazwa na maisha hayo ya kawaida. "Ukweli ni kwamba, katika maisha ya kila siku ya raia wa Pyongyang, huwa hawana wasiwasi kuhusu njia gani bora ya kukabiliana na ubabe wa Marekani au maovu ya mfumo wa ubepari. Wanachokijali zaidi ni, 'Nitaenda wapi dukani kununua bidhaa? Nimefikia wapi katika kazi yangu? Binti yangu ataolewa?" Mwaka uliofuata, akiwa na miaka 21, aliyejea huko kama mwalimu wa kujitolea wa somo la Kiingereza katika chuo cha utalii cha Pyongyang. Griffin akiwa na wanafunzi chuo cha utalii Baadaye, alihitimu na kuwa mwelekezi wa watalii wa TJS na sasa ameanzisha mpando wa kuwasaidia watu kila tabaka au asili wanaotaka kwenda kukaa chuo kikuu cha Kim Il-sung mwezi Julai. Washiriki watalala katika mabweni ya chuo na kujifunza Kikorea kwa saa nne kila siku. Muda huo mwingine watautumia kwa kutembea kujionea mji na vivutio mbalimbali, na kisha kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile kuogelea, kucheza ngoma asili na kucheza mchezo wa kandadna wa wachezaji watano kila upande. Kutakwua pia na fursa ya kukutana na baadhi ya raia wa Korea Kaskazini, ingawa raia hao watakwua wamechunguzwa kikamilifu. "Hatuwezi kamwe kusahau matatizo yaliyopo Korea Kaskazini, lakini tunafaa kwua na uelewa fulani. Utalii wa elimu unasaidia hilo. "Sitaki kuacha kuuliza mazwali lakini ni muhimu pia kuifahamu nchi hiyo kikamilifu, watu wake na thamani na maadili yao. "Ni kweli kuna siasa - wana majaribio yao ya silaha za nyuklia, na ukiukabi wa haki za kibinadamu - lakini ni muhimu kuangazia uhusiano wa binadamu mmoja na mwingine." Kim Jong-un alisomea fizikia chuo kikuu cha Kim Il-sung Ben akiwafunza wanafunzi chuo cha utalii Watu wakicheza ngoma za asili Pyongyang Benjamin Griffin akiwa nje ya kaburi la Kim Il-sung Korea Kaskazini inapotajwa, linalotokea akilini mwa wengi sana huwa ni majaribio ya makombora na silaha za nyuklia, pamoja na kiongozi wake Kim Jong-un. text: Tatizo la umeme Zimbabwe lamponza waziri Nafasi ya waziri huyo amepewa naibu waziri wa usafirishaji na miundo mbinu Forune Chasi. Gumbo sasa amepewa wadhifa wa kuwa waziri katika ofisi ya rais ,kufuatilia utendaji na utekelezaji wa idara za serikali. Kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali amesema siku ya jumatatu kuwa umeme ambao umekuwa ukikatika kwa saa tano au nane kutokana na upungufu wa maji katika mtambo mkubwa wa uzalishaji umeme. Zimbabwe imekuwa ikipata tatizo la ukataji umeme tangu mwaka 2016 Siku ya jumatatu , kampuni ya uzalishaji umeme inayomilikiwa na serikali ilitangaza kuwa umeme utakatika kwa saa tano mpaka nane. Vilevile machimbo ya migodi yatahathirika na kukatika huko kwa umeme. Mamlaka inalaumu kuzimika au kukatika kwa umeme huo kutokana na mtambo wa uzalishaji umeme kuzalisha umeme kwa kiwango kidogo kutokana na ukame ambao umesababisha maji kupatikana kwa kiwango kidogo. Baadhi ya nchi jirani wamedai kuwa umeme kwao umewahi kukatika kwa muda mrefu zaidi hadi saa 10. Aidha serikali ya Zimbabwe imepanga kuagiza nishati kutoka nchi jirani ya Msumbiji na Afrika kusini. Kabla ya mwaka 2016, tatizo hilo la umeme limezua gumzo katika mitandao ya kijamii tangu wakati huo mpaka sasa . Awali raia wengi wa Zimbabwe walikuwa wanawaonea huruma majirani zao wa Afrika Kusini kwa kukatikiwa umeme mara kwa mara lakini sasa tatizo limerudi kwao. Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemfukuza kazi waziri wa nishati, Joram Gumbo kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara tangu mwaka 2016. text: Wafanyazi hao huonekana ni watu wa tofauti kwenye jamii, huku wakikabiliwa na changamoto mbalimbali na wengine kufikia hatua ya kutengwa na jamii wakiwaogopa. Katika kukabiliana na changamoto hizo sasa baadhi ya hosptali nchini humo zimeanza kutoa mafunzo maalumu kwa wafanyakazi hao ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Watu 103 wakamatwa katika maandamano Uganda Ukosefu wa mafunzo ya awali umewasababisha wafanyakazi hao kuchukuliwa tofauti na jamii, huku changamoto mbalimbali zikiwaandama na hata kuonekana kuwa si watu wa kawaida na wengine kutengwa. Lakini sasa mtazamo umebadilika, haswa baada ya kuanza kutolewa mafunzo hayo na kazi yao kuonekana kuwa ni rasmi. Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza, imeanzisha mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti. Dokta Kahima Jackson, Mkuu wa Idara ya Maabara katika hospitali ya Buganda akitoa mafunzo Dokta Kahima Jackson, Mkuu wa Idara ya Maabara katika hospitali ya Buganda na Mkufunzi wa mafunzo hayo, ana sema lengo la kuanzishwa ni kutokana na watumishi wengi waliokuwepo kutokuwa na taaluma hiyo. 'Tuliamua kuanzisha baada ya kubaini kwamba watumishi wengi wa chumba cha maiti walikuwa wakitolewa mitaani na kwamba watu hawa hawana elimu inayohusiana na utunzaji wa maiti.' Amesema Dakta Kahima. Je, njia za kisasa za uzazi wa mpango zina madhara? Licha ya kuhusika na utunzaji wa maiti, moja ya kazi yao pia ni kushirikiana na Daktari, pale uchunguzi unapohitajika kujua kiini ama sababu za kifo. Dokta Kahima anasema uchunguzi unafanywa kwa lengo la kusaidia masuala ya kisheria, pale penye utata. Theophilda Ngojani mojawapo ya wanafunzi wakifuatilia kwa makini mafunzo Kusaidia madaktari na uchunguzi wa kitaalamu na pia kuna baadhi ya watu hutaka kujua sababu zilizosababisha kifo cha ndugu yao. Mafunzo haya yanatarajia kusaidia kwa kiasi kikubwa wafanyakazi kama Shija kutoka katika hospital ya Nyamagana jijini Mwanza. Kabla ya kupokea mafunzo hayo, Mhoja alikuwa akifanya kazi yake bila ya utaalamu, hali ambayo ilimsababisdhia madhara. '' Nilichojifunza ni ule uchanganyaji wa dawa inayotumiwa kuhifadhi mwili, kule nilikokuwa nilikuwa nikiitumia bila ya kuchanganya, ni kali sana ilikuwa ikinichoma kwenye macho, inaniingia puani....'' Amesema Mhoja. Je ni kweli Adui wa Mwanamke ni Mwanamke? Kwa upande wake mwanamke pekee katika mafunzo hayo Theophilda Ngojani anasema watu walikuwa wakimchukulia kama mtu aliyechanganyikiwa kutokana na kufanya kazi hiyo. 'Hii kazi ndio iliyotuweka mjini utakuta wote tunapanga foleni kutafuta mkate'. Amesema Theophilda. Wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika hosptali nyingi nchini Tanzania wamekuwa wakifanya kazi kwenye mazingira magumu bila ujuzi wowote. text: Wataalam wa kijeshi walitumwa kuchunguza kisa hicho na kugundua mashimo makubwa katika meli hizo. Hakuna ushahidi uliotolewa kuonyesha Iran ilihusika. Mataifa yalioathiriwa bado hayajatoa lawama zozote. Kisa hicho kimeongeza hali ya wasiwasi kati ya Iran , ambayo iko karibu na mpaka wa Hormuz na Marekani. Kiwango kikubwa cha mafuta yanayotumika duniani hupitia katika eneo hilo la mpakani . Mwezi uliopita , Iran ilitishia kuufunga mpaka huo iwapo ingezuiwa kutumia mkondo huo wa maji. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Marekani kuondoa msamaha wa vikwazo kwa wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran. Kundi hilo la wachunguzi wa Marekani liligundua mashimo makubwa katika meli zote nne zilizoathiriwa na wanaamini uharibifu huo ulisababishwa na vilipuzi, kulingana na AP, likinukuu maafisa ambao hawakutajwa. Hawakuelezea ni vipi uhairibifu huo ulihusishwa na Iran. Chombo cha habari cha CBS kilikuwa na ripoti kama hiyo kikiwanukuu mafisa ambao hawakutajwa. Je tunajua nini kuhusu hujuma hiyo? Maelezo machache yametolewa kuhusu kisa hicho , ambacho kinadaiwa kufanyika mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri siku ya Jumapili katika maji ya milki za kiarabu UAE katika Ghuba ya Oman , mashariki mwa Fujairah. Wizara ya maswala ya kigeni UAE ilisema kuwa meli nne za biashara zililengwa katika shambulio la hujuma karibu na Bandari ya Fujairah, ikiwa ni nje ya eneo la Hormuz Maboti ya wanamaji wa UAE yamepigwa picha karibu na Al Marzoqah, meli ya mafuta ya Saudia ambalo lilihujumiwa Hakukuwa na majeraha lakini Saudia inasema kuwa meli zake mbili ziliathirika pakubwa. Waziri wa kawi wa Saudia , Khalid al-falih alisema kuwa mojawapo ya meli hizo za mafuta ilikuwa inaelekea kujazwa mafuta ya Saudia ambayo yalitarajiwa kupelekewa wateja nchini Marekani. Meli nyengine ya mafuta ilikuwa na usajili wa taifa la Norway huku ya nne ikidaiwa kuwa na bendera ya UAE. Kampuni ya meli ya Norway Thome Ship ilisema kuwa meli yake moja ilishambuliwa Runinga ya Saudia ilionyesha picha za meli zilizoharibiwa, huku picha iliotolewa na UAE ikionyesha meli ya Norway yenye bendara kwa jina Andrea ikiwa na uharibifu mkubwa upande wa chini. Kampuni ya usimamizi wa meli ya Thome Ship management kutoka Norway ilisema katika taarifa kwamba iliharibiwa na kifaa kisichojulikana katika eneo la chini lililopo majini. Ni jaribio la makusudi kuongeza wasiwasi? Ukilinganisha na shambulio la hapo awali dhidi ya meli mashariki ya kati - meli za USS Cole mwaka 2000, ile ya mafuta ya Limburgh 2002 na hivi majuzi mashambulio ya Yemen, uharibifu uliofanywa kwa meli nne katika pwani ya UAE siku ya jumapili ni mdogo. Hakujaripotiwa kumwagika kwa mafuta , hakuna moto na hakuna majeraha. Lakini wakati ambapo tukio hilo lilifanyika ni hatari na kutilia shaka kubwa. Yeyote aliyetekeleza shambulio hilo lazima alikuwa ana ufahamu kuhusu hali ya wasiwasi katika Ghuba , huku Marekani ikipelekea vikosi vya ziada katika eneo hilo. Inaonekana kwamba aliyetekeleza kitendo hicho alitaka kuchochea wasiwasi na hata kusababisha mzozo. Huku Saudia na UAE zikionekana kumlaumu adui, maafisa wa , Iran, Marekani wamesema kwamba hapo ndipo ulipo wasiwasi wao. Lakini Iran imeshutumu mashambulizi hayo kuwa mabaya huku msemaji wa bunge la nchi hiyo akisema kuwa Iran inaishuku Israel. Iran imesema nini? Iran imetaka uchunguzi wa kisa hicho unachokitaja kuwa cha kutia wasiwasi kufanywa . Katika Ikulu ya Whitehouse siku ya Jumatatu , rais wa Marekani Donald Trump alitoa onyo kwa Iran. Iwapo watafanya chochote itakuwa makosa makubwa ..iwapo watafanya chochote watakiona cha mtema kuni. Lakini rais wa Iran Hassan Rouhani alikuwa moja kwa moja , akisema kuwa taifa hilo ni kubwa sana kutishiwa na mtu yeyote. ''Mungu akipenda tutapita kipindi hiki kigumu kwa ushindi na kuwashinda maadui'' , alisema katika mkutano na viongozi wa dini siku ya Jumatatu. Maelezo machache, lakini maswali maengi Mtandao wa maswala ya baharini dunini umehoji maelezo kuhusu kisa hicho. Orodha yenye ushawishi ya Lloyds List Maritime ya ujasusi ililaumu mamlaka kutokana na maelezo machache. Ikinukuu kampuni ya usalama wa majini Dryad Global, ilisema: Kushindwa kwa Saudia kutoa ,malezo na ushahidi pamoja na vile ilivyoripoti kisa hicho kunazua maswali mengi kuhusu shambulio hilo. Mtandao wa Fleetmon ulisema: Ni nini kilichotokea haswa, je milipuko hiyo ilikuwa mibaya kwa kiwango gani iwapo kuna yoyote ilioshuhudiwa. Je ni yapi matukio ya awali? Marekani hapo awali ilionya kwamba Iran ama washirika wake huenda ikazilenga safari za majini katika eneo hilo na katika siku za hivi karibuni kupeleka meli za kivita kukabiliana na tishio kutoka kwa taifa. Kaimu waziri wa ulinzi Patrick Shanahan ameweka wazi mipango ya serikali ya Iran kuvishambulia vikosi vya Marekani , kulingana na New York Times. Rais Hassan Rouhani amesema kuwa Iran ni kubwa sana kutishiwa Wachunguzi wa Marekani wanaamini kwamba Iran ama makundi inayoyaunga mkono yalitumia vilipuzi kuharibu meli nne karibu na milki za kiarabu UAE siku ya Jumapili, vyombo vya habari vimeripoti. text: James Almond Gumzo na mfungwa mmoja kuhusu kandanda lilisababisha James Almond kuvunja sheria mwenyewe. Akiwa mfanyakazi wa gereza wakati huo, alikuwa akifanya mazungumzo na mfungwa kuhusu klabu yake anayopenda ya Manchester United, wakati mfungwa aliyekuwa akizungumza naye alimuomba ampelekee simu ambayo ni marufuku ndani ya gereza. "Alikuwa akiniuliza kila siku," Almond alisema. Huo ulikuwa mwaka 2014 wakati alikuwa ameajiriwa katika gereza moja eneo la Rutland. Almond mwenye umri wa miaka 33 kisha akakubali kupeleka simu na kafanya hivyo kwa wiki kadha kabla ya kupatwa na kusababisha yenye mwenye kufungwa. Sasa anasimulia hadithi yake ili wengine wapate kuelewa shinikizo alililokumbana nalo kutoka kwa mfungwa. Kesi yake inaangazia tatizo la ufisadi miongoni mwa wafanyakazi wa magereza nchini Uingereza na Wales. Simu za mkononi ni kitu cha thamani kwa sababu huwawezesha wafungwa kuwasiliana na familia na wahalifu wengine James Almond hakutarajia hilo wakati akianza kufanya kazi katika gereza hilo lililo na wafungwa 670 wa kiume, wengi wanaotumikia vifungo vya makosa ya ghasia. "Nahisi nilijipata kimakoaa katika hali hiyo kwa sababu nilikuwa na msongo wa mawazo baada ya kifo cha babangu. "Na hili ndilo wafungwa hugundua kwa haraka sana," anasema Almond. Uingizaji wa bahasha Mfungwa Almond alifanya mazungumzo naye, kisha akaanza kumtisha kuwa angeidhuru familia yake ikiwa hangeitikia kupeleka simu. Alinitisha sana hasa wakati alisema kuwa aliwafahamu wapwa wangu. Jamaa huyo alikuwa gerezani kwa wizi wa kutumia nguvu na sikujua kile alikuwa na uwezo wa kufanya. Vitisha hivyo vilisababisha Almond kukubali kupeleka simu kwa wafungwa. Simu za mkononi ni kitu cha thamani kwa sababu huwawezesha wafungwa kuwasiliana na familia na wahalifu wengine walio nje. Almond alitekeleza hilo kwa kuchukua bahasha kutoka kwa mtu ambaye hakumfahamu na kuiweka kwa mfuko wake na kisha kupita nayo kwenye milango ya gereza bila kutambuliwa. "Ilikuwa ni hatua hatari sana hadi siku moja waliamua kuwakagua wafanyakazi wa gereza," anasema hakukaguliwa kwa kipindi cha miezi sita alifanya kazi. Anasema alilipwa pauni 500 kwa kila bahasha, na alifanya hivyo mara mbili kwa wiki. John Podmore, ambaye amefanya kazi katika idara ya magereza kwa miaka 25 anaamini kuwa mshahara kidogo na kutokuwepo mafunzo mema ni baadhi ya masuala yanayochangia wafanyakazi kuingiza bidhaa gerezani. Ndege zisizokuwa na rubani au drones, zimekuwa maarufu kwa kutumiwa kupeleka madawa ya kulevya na simu za mkononi ndani ya magereza, lakini hata hivyo wafanyakazi wa magereza kuwapelekea wafungwa simu pia ni njia nyingine maarufu. text: Zaidi ya watu 1,000 wameondoka kutoka makaazi yao kwa mujibu wa rais Cyril Ramaphosa ambaye ametembelea maeneo yaliyoathiriwa. Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika maeneo ya Kusini na Mashariki ya nchi hiyo siku chache zilizopita. Mafuriko zaidi na upepo mkali unatarajiwa katika maeneo ya pwani huku onyo likitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa. Mafuriko hayo makubwa yaliharibu biashara na nyumba za watu pamoja na vyuo vikuu viwili - huku mamia ya watu wakifurushwa makwao. Watu wamekua wakifarijiana huku wakitathmini uharibifu uliyosababishwa na mafurok ahayo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amezitembelea familia zilizopoteza wapendwa wao katika mafuriko hayo. Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko anaarifu kuwa rais aliweka shada la maua katika eneo ambalo watu wanane wallifarika. Pia alionekana akiwasukuma walinzi waliokuwa wakiwazuia watu kusema nae. "Ni muhimu kuja kuona kile kilichofanyika au kilichotokea na kuomboleza na familia zilizopoteza wapendwa wao katika janga hili. Kupoteza maisha sio jambo rahisi, hasa maafa yakitokea ghafla," alisema Bw. Ramaphosa. Watu kadhaa wafariki baada ya kuzikwa na maporomoko ya tope Siku ya Jumatano, alitoa taarifa ya kusema kuwa: "Hali hii inatuhitaji sote kuja pamoja kama taifa kufikia jamii zilizosthirika." Huku hayo yakijiri, waziri wa utawala wa mkoa Nomusa Dube-Ncube ameiambia maafisa wa kituo cha radio cha SAFM kwamba bado wanaendelea kutathmini kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mkasa huo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Siku zijazo watu watalazimika kuhamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika, alisema. Watu kadhaa wamepelekwa hospitali huku shughuli ya kuwatafuta manusura waliyozikwa chini ya vifusi vya majengo yalioporomoka Maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 60, katika mikoa ya Durban na KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, maafisa wanasema. text: Wahalifu wenye silaha za moto na mabomu walivamia viunga vya hoteli hiyo Jumanne saa 9 alasiri. Gazeti hilo lenye makao makuu yake nchini Marekani limechapisha picha za marehemu wakionekana dhahiri kuwa na matundu ya risasi kwenye miili yao na kulowa damu. Rais Kenyatta 'Magaidi wote wameuawa' Wakenya walimimina hasira na kukirihishwa kwao kwa hatua hiyo ya NYTimes kwa kuandika ujumbe katika mitandao ya kijamii ikwemo Twitter. Baadhi hata walilinganisha namna walivyoripoti matukio ya uhalifu nchini Marekani tofuati na walivyofanya kwa mkasa huu Kenya. Wameeleza kwamba hatua ya gazeti hilo ilikosa heshima. AU, Marekani walaani shambulio la Riverside Baada ya shutuma hizo kushika kasi, uongozi wa gazeti hilo ulitoa taarifa ya kujitetea wakisema lengo lao ni "kuonesha uhalisia wa tukio zima japo picha zinaweza kuwa za kuogofya." Wameendelea kufafanua kwamba wao hufanya vivyo hivyo wanaporipoti matukio kama hayo kwengineko duniani. Gazeti la New York Times limeshutumiwa vikali kwa kuchapisha picha za miili ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi. text: Mapigano Sudan kusini yamedumu kwa miaka minne hivi sasa Hii ikiwa ni jitihada ya hivi karibuni kusitisha mapigano ya kiraia yaliodumu zaidi ya miaka minne mpaka kufikia sasa. Kituo hicho cha utangazaji kinasema ujumbe wa serikali ulitaka zaidi ya wajumbe watatu wahudhurie kikao hicho. Pande hizo mbili zinatarajia kufufua makubaliano ya amani ya mwaka 2015. Duru tofauti mjini Addis Ababa zimeiambia Radio Tamazuj kwamba ujumbe wa serikali uliamua kususia kikao cha leo mchana kwasababu walitaka zaidi ya wajumbe watatu kuhudhuria. "Serikali inataka wajumbe zaidi ya watatuu wahuhudhurie lakini IGAD inaruhusu watau pekee," mmoja wao alisema. Kikao cha pili leo mchana kinafafanua kuhusu ajenda ya awamu ya pili ya mpango wa kufufua makubaliano ya amani ya mwaka 2015. Mazungumzo hayo yanajiri katika wakati ambapo kunajumuiya ya imatiafa inazidi kushindwa kuuvumili utawala wa kisiasa na kijeshi wa taifa hilo changa barani Afrika. Wajumbe wa Sudan Kusini walipewa ujumbe mkavu muda mfupi kabla ya kutarajiwa kaunza kikao hicho. Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, aliwaambia kwamba wanahusika kwa jinamizi wanalolishuhudia hivi sasa raia wa Sudan kusini. Sudan kusini ilijipatia uhuru mnamo 2011 Makubaliano ya mwisho ya kusitisha mapigano yalitiwa saini mkesha wa Krismasi na ulidumu kwa saa kadhaa. Katika miaka minne iliyopita, maelfu ya watu wameuawa katika mapigano na kiasi ya thuluthi moja ya raia nchini wameachwa bila ya makaazi. Marekani iliunga pakubwa mkono uhuru wa Sudan kusini mnamo 2011. Lakini wiki iliyopita Marekani iliidhinisha vikwazo vya silaha na hivi karibuni mkuu wa muungano wa Afrika ameitisha kuidhinisha vikwazo dhidi ya wanaorefusha mzozo huo. Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa Sudan kuisni nchini Ethiopia yamegonga mwamba kwa baada ya wajumbe kususia kikao hicho, Radio Tamazuj inaripoti. text: Bi Jemimma, 32, alikuwa anahitaji kiasi cha pauni 10,194 ili kumalizia mwaka wa pili na wa mwisho wa masomo yake ya uzamili. Baada ya kuchangiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, amefanikiwa kupata pauni 11,160 ambayo ni pauni 966 zaidi ya lengo. Alifikia lengo siku ya Jumamosi na kuanzia jana amesitisha kupokea michango. "Sihitaji taji tena mchango. Sikuwahi kufikiria kuwa ipo siku ningsema hivi, lakini sasa ninaacha kupokea mchango. Nina bahati sana. Nawashukuru sana kwa msaada wenu madhubuti," ameandika bi Jemmimah katika ukurasa wake wa mtandao wa Go Fund Me Page ambao alikuwa akiutumia kwa kampeni yake. Mchango huo umetolewa na watu takriban 170, ambao waliguswa na kisa cha bi Jemmimah cha kujioa mwenyewe. Ndoa mbili batili kufadhili elimu Uganda Ukiacha mchango wa fedha, pia amepokea ufadhili wa tiketi za ndege kwa kipindi kilichobaki cha masomo yake baina ya Uingereza na Uganda. "Siyo tu nimepata pesa ya ada, kwa sasa sina haja ya kuwa na hofu yeyote ya kuhamisha fedha katika benki, usafiri wa ndege na pesa ya kuombea viza," ameongeza bi Jemimmah. Kwa nini alijioa Licha ya mafanikio ya kielemu kwa kujiunga na chuo maarufu duniani, anasema watu waliendelea kumuuliza swali moja ambalo kwa miaka kadhaa hakuwa analifurahia. Swali lenyewe ni anapanga kuolewa lini, ili aanzishe familia na kupata watoto. "Hawaamini kuwa kinachonifanya kuwa macho usiku sio hofu ya uwezekano wa kutopata bahati ya kutembea altarini kwenda kufunga ndoa." "Nikiwa na miaka 16 baba yangu aliandika hotuba yake kwa ajili ya kuisoma siku ya harusi yangu. Kila nilipokuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa mama yangu alikuwa akiniombea, na kwa miaka ya karibuni maombi yake yalikuwa pamoja na kupata mume bora, ambaye atanifaa," amesema Bi Jemimah. Kutokana na hali hiyo, Jemimah anasema aliamua kuchukua uamuzi wa kuwatuliza; "Nilipotimiza miaka 32 nikaamua kujioa. Naamini mimi nitajitunza na kujipa amani." Harusi yake ilimgharimu kiasi cha dola 2 tu ambazo ni gharama yake ya usafiri. Aliazimisha gauni la harusi kwa rafiki, vito kutoka kwa dada yake na keki ya harusi iliokwa na kaka yake. Waalikwa walitakiwa kujinunulia chakula na vinywaji kwa pesa zao wenyewe. Kampeni ya ada Lengo la bi Jemimah ni kuionesha jamii yake kuwa inawezekana kufikia malengo kimaisha bila ya msaada wa mume. Hata baada ya kujioa mwezi Agosti mwaka huu jijini Kampala Uganda, Bi Jemimah alikuwa anachangamoto moja ya kutafuta ada ya kumalizia masomo yake. Alitumia ndoa yake hiyo, ambayo baadhi ya watu, wanaiona kama kituko kufanya kampeni mtandaoni ili kupata usaidizi wa kulipa ada hiyo. Katika mwaka wake wa mwanzo wa masomo Bi Jemimah anasema alikumbana na changamoto nyingi za kifedha zilizomfanya aishi katika mazingira magumu. Mambo ya kushangaza kuhusu tendo la ndoa duniani Licha ya kuchangiwa na watu kadhaa, alishawahi kulala maktaba kutokana na kukosa pesa ya kodi ya chumba. Anasema haikuwa dhamira yake kuomba msaada lakini hofu ya kufutwa chuo kutokana na kukosa fedha imemlazimu afanye hivyo. "Nimepata bahati ya kuwa katika chuo bora chenye wanafunzi makini na walimu wenye weledi mkubwa...Nimefikia hapa kutokana na msaada wa marafiki na watu nisiowafahamu. Kwa mara nyingine tena naomba msaada wenu," aliandika mtandaoni kabla ya kuanza kuchangiwa. Mwanamke aliyejioa nchini Uganda, Lulu Jemimmah, hatimaye amepata ada ya kusoma chuo maarufu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza. text: Waanndamanaji walifika kwenye eneo ambalo polisi wanaohusika na mauaji wanadhaniwa kufanya kazi Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na waandamanaji walirusha mawe na kupulizia mapambo ya graffiti kwenye magari ya polisi. Kilichotokea kwenye maandamano Walianza siku ya Jumanne jioni, wakati mamia ya watu walipofika katika eneo ambalo tukio lilitokea, Jumatatu jioni. Waratibu walijaribu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuzingatia masharti ya kukaa mbalimbali, waandamanaji waliimga ''siwezi kupumua,'' na ''ingeweza kuwa mimi''. Bango lililoandikwa jina la mwanaume aliyeuawa Mmoja wa waandamanaji Anitha Murray aliliambia gazeti la Washinton Post: ''inaogopesha kuwa hapa wakati wa janga la corona, lakini kwa nini nijiweke mbali?'' Kundi la mamia ya watu baadae waliandamana mpaka kwenye idara ya polisi 3rd Precinct, ambapo maafisa waliohusika na kifo hicho walikuwa wakifanya kazi. Mtu mmoja alikiambia chombo cha habari cha CBS: ''Hii ni mbaya sana. Polisi lazima watambue kuwa hali hii wameitengeneza wenyewe.'' Polisi wamesema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi lakini taarifa za kina hazijatolewa kuhusu tukio hilo. Video ya tukio hilo la Minneapolis iliwekwa kwenye mtandao wa kijamii Maafisa wanne wa polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani wamefutwa kazi kufuatia kifo cha mtu mweusi ambaye alikuwa amekamatwa na kuonekana akizuiliwa chini kwa kushikwa shingo. Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo Medaria Arradondo amesema kwamba maafisa hao wanne sasa ''sio wafanyakzi wa kikosi hicho''. Kanda ya video inaonesha, mtu huyo kwa jina George Floyd , akilia na kuwaambia maafisa hao weupe ''siwezi kupumua''. Kisa hicho kinafanana na kile cha Eric Garner, mtu mweusi aliyefariki akikamatwa na polisi mjini New York mwaka 2014. Shirika la ujasusi nchini Marekani FBi lilisema litachunguza kisa hicho cha Minneapolis kilichofanyika Jumatatu jioni. George Floyd aliwaambia polisi mara kadhaa kwamba hawezi kupumua Maafisa wa polisi wa Minnesota walisema kwamba Floyd mwenye umri wa miaka 46 , ambaye alikuwa anafanya kazi kama afisa wa usalama katika mkahawa mmoja alifariki akifanyiwa matibabu kufuatia malumbano na maafisa wa polisi. Siku ya Jumanne, Meya Jacob Frey alithibitisha kwamba maafisa hao wanne waliohusishwa na kisa hicho wamefutwa kazi. ''Huu ndio uamuzi tuliochukua''. Katika mkutano na vyombo vya habari mapema, bwana Frey alikitaja kisa hicho kama cha kushangaza. ''Ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango chochote kile'' , alisema. ''Kuwa mtu mweusi nchini Marekani hakustahili kuwa hukumu ya kifo''. Ni madai ya hivi karubuni ya unyanyasaji unaotekelezwa na maafisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi. Visa maarufu vya hivi karibuni vinashirikisha afisa mmoja wa eneo la Maryland ambaye alimpiga risasi mtu mmoja akiwa ndani ya gari la kupiga doria. Kisa hicho cha Minneapolis kilianza baada ya ripoti kwamba mteja mmoja alikuwa anajaribu kutumia noti bandia ya dola 20 katika duka moja. Afisa huyo alimuona mshukiwa akiwa ndani ya gari lake, mtu huyo alikataa kukamatwa kulingana na maafisa wa polisi. Waliambiwa kwamba mtu huyo ambaye hajatambulika alikuwa ameketi juu ya gari la rangi ya buluu na alionekana kana kwamba ametumia kishawishi fulani. Waandamanaji wakimuombea George Floyd, ambaye kifo chake kimezua mjadala wa ukatili wa polisi Marekani Baada ya kuagizwa kuondoka na kusimama kando ya gari hilo , jamaa huyo alikataa kukakamtwa lakini maafisa walifanikiwa kumfunga mikono yake kwa pingu na akaonekana kana kwamba alikuwa anaugua tatizo la tiba., taarifa hiyo iliongezea. Katika kanda hiyo ya dakika 10 iliochukuliwa na shahidi , mtu huyo aliwekwa ardhini na afisa huyo na katika wakati mmoja alisikika akisema ''musiniue''. Shahidi mmoja alisikika akimwambia afisa huyo kuondoa goti lake katika shingo ya mshukiwa huyo, akidai kwamba alikuwa hayumbi. Mwengine alisema pua yake inatoka damu, huku mwengine akiomba ''ondoka katika shingo yake''. Mtu huyo anaonekana ametulia kabla ya kuingizwa katika ambulansi na kuondoka naye. Maafisa wa polisi wanasema kwamba hakuna silaha iliotumika wakati wa kisa hicho , na kwamba picha zimepelekwa katika shirika la ujasusi la kukabiliana na uhalifu la Minnesota, ambalo linachunguza kesi hiyo. Siku ya Jumanne jioni maafisa walitumia vitoa machozi kutawanya maandamano ya umma nje ya kituo cha polisi mjini Mineapolis , kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo. Mwandishi mmoja wa gazeti la The Star Tribune alituma ujumbe wa twitter kwamba alikuwa amepigwa na risasi bandia iliofyatuliwa na polisi. Ripota mmoja wa runinga ya KTSV alituma ujumbe wa Twitter akisema kwamba waandamanaji walivunja vioo katika kituo hicho na kuchora maandishi machafu katika gari moja la polisi. Maafisa wa polisi walisema katika taarifa yao awali kuhusu kifo cha Geore Floyd: Baada ya kupata habari zaidi, imebainika kwamba shirika la ujasusi nchini Marekani FBI litashirika katika uchunguzi huo. Akizungumza kwa vyombo vya habari vya Marekani siku ya Jumanne, Afisa mkuu Arradondo alisema kwamba sera za kikosi cha polisi kuhusu kumdhibiti mshukiwa zitachunguzwa kama mojawapo ya uchunguzi huo. Kulingana na chombo cha habari cha AP, maafisa wa polisi wa Minneapolis wanaruhusiwa kupitia sera ya kutumia nguvu kuweka magoti yao katika shingo ya mshukiwa iwapo kitendo hicho hakitaathiri njia za kupumua za mshukiwa. Alipoulizwa kuhusu uchunguzi huo wa FBI Arradondo alisema , aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kupokea habari zaidi kutoka chanzo kimoja cha kijamii. Kumekuwa na vurugu na mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minneapolis nchini Marekani baada ya kifo cha mwanaume mmoja mweusi akiwa mikononi mwa polisi text: Gwaride la kijeshi la Korea Kaskazini Taifa hilo limesema hivyo wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amehudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang, akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo. "tumejiandaa kwa vita kamili'' ,alisema Choe Ryong-hae, anayeaminika kuwa mu wa pili mwenye uwezo mkubwa katika taifa hilo. ''Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia''. Jeshi la Korea Kaskazini likiwa katika gwaride la kijeshi Huku kukiwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa kukamilisha silaha za Kinyuklia, Gwaride la Jumamosi ilikuwa fursa kwa bwana Kim kuonyesha uwezo wa kijeshi wa taifa hilo. Vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza vilikuwa vile vilivyotajwa kuwa manuwari za Pukkuksong ,makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda kwa takriban kilomita 1000. Wachanganuzi wa vifaa vya kijeshi pia wanasema kuwa kuna makombora mawili mapya yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine, lakini haijulikani iwapo yamefanyiwa majaribio. Kulikuwepo na sherehe za kawaida, kama vile mamia ya wanajeshi kupiga gwaride na msafara wa magari ya kivita huku yakiwa yamebeba silaha kama vile makombora. Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini Maonyesha ya silaha nyingi yanaendelea nchini humo wakati ambapo kuna hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani kufuatia mazoezi ya makombora ya kinyukilia yanayoandaliwa na Korea Kaskazini. Hali ya wasiwasi imekumba eneo la Korea kwa ujumla kufuatia majaribio kadhaa ya makombora ya kisasa na Korea Kaskazini na mapema Jumamosi shirika la habari la taifa hilo lilionya Marekani kusitisha kiherehere chake cha vitisho vya kijeshi. Marekani imetuma meli kadhaa za kivita katika Rasi ya Korea. Hiyo jana waziri wa mashauri ya kigeni wa Uchina alionya kuwa vita vyovyote kati ya Korea Kaskazini na Marekani havitamfaidi ye yote. Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia mshambulio ya kinyuklia. text: Richard Huckle, mwenye umri wa miaka 33, kutoka eneo la Ashford, Kent, nchini Uingereza aliwalawiti watoto hadi 200 Mnamo mwaka 2016, alihukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani baada ya kukiri makosa 71 ya ubakaji wa watoto waliokuwa na umri wa miaka kati ya sita na 12 kati ya mwaka 2006 na 2014. Inafahamika kuwa alishambuliwa siku ya jumapili alipokuwa katika mahabusu ya gereza la Full Sutton karibu na York, na kisu kinachotumiwa jikoni. Polisi waliitwa majira ya saa sita usiku na kuanza uchunguzi kuhusina na kifo hicho ambacho wanakishuku. Katika kesi dhidi ya Huckle mwaka 2016 wapelelezi waliochunguza kpmpyuta yake walibaini zaidi ya picha na video zaidi ya 20,000 za aibu za matukio yake ya ulawiti wa watoto. Alizishirikisha kwa walawiti wengine kote duniani kupitia wavuti wa siri uliofahamika kama wavuti wa giza. Huckle, ambaye alifanyakazi kama mpigapicha wa kujitegemea , alijaribu kutumia unyanyasaji huo wa kingono kwa kuuza picha hizo . Alikuwa akikusanya picha za vitendo hivyo wakati alipokamatwa mnamo mwaka 2014. Katika mwisho wa kesi yake , Judge Peter Rook alisema kuwa hukumu ya Huckle inaonyesha " kero la umma " kuhusu "kampeni yake ya ubakaji ". Alisema "Ni nadra sana kwa jaji kumuhukumu mtu mmoja kwa makosa ya ubakaji kwa kiwango hiki ." Wakazi wakiandamana kupinga mpango wa kupanua gereza la Full Sutton Huckle alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataiofa wa Gatwick Airport nchini Uingereza na maafisa wa kukabiliana na uhalifu mwezi Disemba 2014, baada ya kupewa taarifa na maafisa wa Australia. Alijitambulisha kama mkristo na kwamba alitembelea Malaysia kwa mara ya kwanza kama mwalimu alipokuwa na umri wa miaka 18 au 19. Baadae alikuwa akiwasaidia watoto kukuza vibaji vyao huku akifanya kazi ya kujitolea. Katika jumbe zake za mtandao, Huckle alituma ujumbe wa mzaha uliosema : "Watoto maskini ni rahisi sana kutongoza kuliko watoto wa kipato cha kati katika nchi za magharibi" Akielezea kumhusu mmoja wa waathiriwa wa unyanyasaji, alijisifu akisema "Nilimharibu msichana wa miaka 3 ambaye alikuwa amenipenda kama mbwa wangu na hakuna yeyote aliyejali ." Mwaka jana BBC ilianda kipindi maalum kumuhusu Huckle, kilichofichua uhalifu wake miongoni mwa watoto nchini Cambodia, India na Uingereza. Mwanamme Muingereza aliyekuwa akitumikia kifungo gerezani kwamakosa kadhaa ya uhalifu wa kingono dhidi ya watoto wa malasia amepatikana akiwa amedungwa kisu hadi kufa gerezani. text: Upungufu wa mazoezi ni hatari kwa afya ya mwanadamu Ripoti ya shirika la afya duniani linakadiria kwamba zaidi ya robo moja ya watu duniani- biliioni 1.4 - hawafanyi mazoezi ya kutosha , takwimu ambayo haijaimarika tangu 2001. Ukosefu wa mazoezi kunaongeza hatari ya kuugua matatizo ya afya, kama matatizo ya moyo, kisukari na pia baadhi ya saratni. Na imegunduliwa kwamba kati ya kundi hilo, wanawake ndio wasiojishughulisha na mazoezi isipokuwa katika bara la Asia. Inaarifiwa huenda inatokana na masuali tofuati, ikiwemo majukumu ya kuwalea watoto, na mila na tamaduni katika baadhi ya jamii zilizofanya kuwa vigumu kwao kufanya mazoezi. Faida kwa wanaoishi katika nchi kama Uganda: Utafiti huo umebaini hatahivyo kwamba kwa watu wanaoishi katika mataifa yenye kipato cha chini wana faida au ahueni. Wengi katika nchi kama Uganda au Msumbiji kwa kawaida hulazimika kujishughulisha wakiwa kazini, wanapotembea kwenda kazini au hata kuabiri magari ya uchukuzi wa umma ambayo kwa kiasi fulani kunahesabika kama kufanya mazoezi. Wataalamu wanasema tofauti katika mataifa yalio tajiri ambapo watu wengi hutafuta kazi zisizo na shughuli nyingi za mwili, mfano kukaa tu ofisini, pamojana kuongezeka kwa matumizi ya usaifiiri wa magari binfasi, huenda inaeleza viwango vikubwa vya ukosefu wa mazoezi miongoni mwao. Nchi zenye kiwango kikubwa cha watu wasiofanya mazoezi: Nchi zenye kkiwango kidogo cha watu wasiofanya mazoezi: 'Wasiwasi mkubwa' Utafiti uliofanywa na WHO na kuchapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet Global Health, ambalo lilichambua data iliyotolewa na washiriki milioni mbili umebaini kuwa kuna jitihada kidogo imefanyika kati ya 2001 na 2016. Shirika hilo limeendelea kutanabahisha kuwa asilimia arobaini ya raia wanaosihi katika mataifa yalioendelea, mfano Uingereza na hata Marekani hawajishughulishi na afya zao na kwamba hali hii ni mbaya zaidi katika nchi ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia na Iraq. Kazi za kukaa ofisini zina madhara na kuchangia kwa kosefu wa mazoezi, wataalamu wanaonya. Muongozo wa mazoezi kwa walio na umri wa kati ya 19 - 64 Kiasi gani? Je mazoezi ya wastani ya aerobic ni gani? Je mazoezi ya uzito ni gani? Ni mazoezi gani yanayoimarisha misuli? Chanzo: NHS Wataalamu wametoa wito kwa serikali kutoa na kuimarisha miundo mbinu inayohimiza michezo na kushinikiza kutembea au kuendesha baiskeli kama mbinu za usafiri. Waandishi wa ripoti wameonya kwamba kwa hali ilivyo, huenda azimio la WHO kupunguza viwango vya watu kutofanya mazoezi kufikia 2025 kwa 10% lisifikiwe. Shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa mabaya, kutokana na sababu ya kutotaka kujishughulisha na afya zao. text: Rais Mugabe na mkewe Grace Mugabe walisusia sherehe ya kuapishwa kwa Emmerson Mnangagwa Sababu kuu ilioteolewa ni kwamba bwana Mugabe alikuwa amechoka. Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kujiuzulu kama rais kufuatia shinikizo kutoka kwa jeshi na raia. Hatua hiyo inajiri baada ya Mugabe na mkewe kufumta kazi rais huyo mpya wakati alipokuwa makamu wa rais kwa madai kwamba alikuwa akipanga njama za kutaka kumuondoa madarakani rais Mugabe Aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa amewataka raia wa Zimabwe kusalia watulivu na kuweka amani na kutolilipiza kisasi. Umati mkuwa wa takriban raia 60,00 wa Zimbabwe wakiwemo viuongozi wa kimataifa na wanadplomasia walihudhuria sherehe ya kumuapisha Mnangagwa katika uwanja wa michezo wa mj9ini harare. Upinzani umemtaka rais mpya kukabiliana na ufisadi.wakati rais Mugabe alipolazimishwa kuondoka madarakani siku ya Jumanne baada ya jeshi kuchukua mamlaka kulikuwa na sherehe matika maeneo tofauti ya taifa hilo. Robert Mugabe na mkewe Grace walikosa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Emmerson Mnangagwa baada ya wananiasa hao kukubaliana kwamba Mugabe anaweza kupumzika. text: Mnyama huyo ambaye alikuwa mgonjwa alifunikwa kabisa na kupe hao, na alikutwa ndani ya bwawa la kuogelea katika eneo la Gold Coast jimboni Queensland. Mtaalamu wa kunasa nyoka alimtoa nyoka huyo kwenye bwawa na kumkimbiza katika hospitali ya wanyama kwa matibabu. Madaktari wa wanyama waliondoa kupe zaidi ya 500 kutoka kwenye mwili wa nyoka huyo. Tony Harrison, ambaye ndiye alimnusuru nyoka huyo ameiambia BBC kuwa inatarajiwa nyoka huyo atapona kabisa. 'Kama kubeba begi la marumaru' Bw Harrison anaamini kuwa nyoka huyo alikuwa akijaribu kuwazamisha kupe hao kwenye maji ili ajinusuru. "Bila shaka [chatu huyo] hakuwa na raha kabisa," amesema. "Uso wake wote ulikuwa umevimba na ulikuwa umefunikwa na kupe waliokuwa wakimnyonya." Amesema kumyanyua nyoka huyo ilikuwa ni kama "kubeba begi la marumaru ambazo zilikuwa zikitembea kwenye mkono wangu". Nyoka kwa kawaida huvamiwa na kiasi kidogo cha kupe na wadudu wengine mwituni, amesema Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Queensland. Hata hivyo, mtaalamu huyo anasema kuvamiwa na kundi kubwa la wadudu hao inaashiria kuwa nyoka huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi yaliyotokana na joto kali ama ukame. "Ni dhahiri kuwa alikuwa anaumwa mpaka akashindwa kujilinda kabisa. Sidhani kama angelipona iwapo asingeliokolewa na kupelekwa kupatiwa matibabu," Profesa Fry ameeleza. Mwokozi wake, Bw Harrison baadae akaeleza kuwa nyoka huyo aliyepewa jina la Nike alipata maambukizi japo sasa "anaendelea vyema". "Nike leo kiasi amekuwa mchangamfu," amesema Bw Harrison katika video iliyopakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa wakamata nyoka wa Gold Coast na Brisbane . "[Hata hivyo] ataendelea kulazwa kwa muda mrefu kidogo [katika kitua cha uhifadhi na matibabu ya wanyama cha Currumbin Wildlife Sanctuary] mpaka hali yake itakapotengemaa na kurudishwa mwituni." Wakamata nyoka nchini Australia wamemnusuru chatu ambaye alikuwa amevamiwa na mamia ya kupe. text: Wanandoa Susan Njogu Eling na Phillip Eling Wengi hudai alifanya uamuzi huo kutokana na tamaa ya pesa, jambo ambalo kamwe anasema halikumuingia akilini. Erin, 28, ameishi na Phillip Eling kama mume na mke kwa miaka miwili sasa. Uamuzi huo ni jambo ambalo linalozungumziwa zaidi na baadhi ya marafiki zake wa karibu. 'Sikutarajia itakuwa gumzo' Kiini kikuu hasa kimelenga maumbile ya mume wake kwani sio kama ya mwanamume wa kawaida. Mume wake anaishi na ugonjwa ambao unaathiri misuli na viungo vyake. Hali hii inajulikana kama Bethlem Myopathy - na kwa kweli hali hiyo imeashiria kuwa mume wake ana ulemavu kwa kiasi kikubwa. Mume wake anaishi na ugonjwa ambao unaathiri misuli na viungo vyake Bwana Phillip hawezi kutumia mikono yake wala miguu yake na hata sehemu ya shingo lake. Mume wake hawezi kutembea, kuinua chochote wala hata kujihudumia mwenyewe kwa mfano kula chakula au hata kuchana nywele zake mwenyewe. Kimsingi ni kuwa maisha ya mume wake yanazungukia kukaa kwa muda mwingi katika kiti cha magurudumu. "Sikudhani kuwa uamuzi wangu wa kibinafsi kumpenda mume wangu ungekuwa gumzo mitaani," anasema. "Maoni yaliouma zaidi ni yale yalioelekea kuwa nilikubali kuolewa na Phillip kwa sababu yeye kutoka asili ya kizungu na ana fedha nyingi." Kwa mtu anayekutana na Susan na mume wake Phillip kwa mara ya kwanza atagundua kuwa wachumba hawa wawili wanamapenzi ya ajabu. Haipiti dakika nyingi kwa wapenzi hawa wawili kabla hawajakumbatiana na kupeana busu. Susan analitaja kama jambo la kawaida katika maisha ya wanandoa hawa wawili. Ila safari ya ndoa yao kwa upande mwengine ni kielelezo chanya katika jamii hasa wakati unapokutana na mwanamke ambaye hana matatizo yeyote ya maumbile na anakubali kumpenda na kumtunza mume mwenye ulemavu mkuu maishani mwake. Kukutana kwa njia isiyo ya kawaida "Sikudhani kuwa uamuzi wangu wa kibinafsi kumpenda mume wangu ungekuwa gumzo mitaani" Susan alisafiri kutoka kaunti ya Nakuru nchini Kenya hadi nchini Austalia akitafuta masomo maalum katika fani ya matibabu. Alipofika nchini humo alibadilisha kusudi lake na kuanza masomo spesheli ya kuelewa maisha ya watu wanaoishi na ulemavu. Baada ya kuhitimu, aliamua kutafuta ajira katika kampuni moja iliyokuwa inashughulika na maswala ya walemavu. Aliandika maombi ya kazi na kuyatuma. Siku mmoja aliitwa kwenye usaili na hapo ndipo alipokutana na mume wake mara ya kwanza akiwa mmoja wa wale waliokuwa kwenye jopo la kumhoji kikazi. Baada ya hafla hio Susan alirejea nyumbani kusubiri uamuzi. Baada ya siku mbili hivi alipokea barua pepe ya kibinafsi kutoka kwake Philiph iliyokuwa inakusudia kumwalika kwa mkutano wa kirafiki. Kukutana kwao katika ukaribu mkuu na hapo ndipo penzi lilianza kuota na kukolea kati ya wapenzi hawa wawili. Bwana Philiph hawezi kutumia mikono yake wala miguu yake na hata sehemu ya shingo yake "Kusema ukweli tangu nikiwa binti nilikuwa najipata nikiwa na umakini sana nilipokuwa karibu na watu waliokuwa wanaishi na ulemavu. Nilijipata nikitaka kuwa wa msaada au kuwafanyia mema watu waliokuwa na upungufu wa mwili sehemu yoyote nilipokuwa," anakumbuka Susan Na kwa hio sio ajabu kuwa urafiki wake na Phillip haukukumbwa na changamoto hiyo ya yeye kujiuliza ni vipi wataishi kama mume na mke na mtu ambaye alikuwa kila wakati anaishi kwenye kiti cha magurudumu. Baada ya muda Phillip alikuwa amemtambulisha kwa jamaa zake na pia alikuwa tayari alikuwa amemuomba wafunge ndoa. Kufunga ndoa Susan hakuwa na budi ila kuwaeleza jamaa zake nchini Kenya mpango wake. Alitaka sana kujua iwapo baba na mama mzazi wangemkubali afunge ndoa na mtu aliyekuwa anaishi na ulemavu. "Kwa bahati nzuri nilipowaeleza wazazi wangu hawakupingana na chaguo langu , wala hakuna siku walinidunisha kutokana na uamuzi wangu ila walinipa ushauri wa kuendelea mbele ikiwa mimi na mchumba wangu wakati huo tulikuwa tumefanya uamuzi," Susan anakumbuka Mwaka wa 20018 Susan na Phillip walifunga ndoa na wachumba hawa wawili walionekana kujawa na furaha na msisimko mkuu wa kuwa pamoja. Tangu Susan Njogu Eling alipoamua kufunga ndoa, amekuwa akishambuliwa na wengi kutokana na uamuzi wake. Kushambuliwa katika mitandao ya kijamii Kizazaa kilianza pale walipoweka picha zao kwenye mtandao wa kijamii kila aina ya semi na jumbe zilifurika kwenye mitandao yao. Wengi walilenga kumdunisha na kumyooshea kidole cha lawama kwa kuchukua hatua ya kuolewa na 'mlemavu'. "Mtandao wa kijamii ulifurika na mambo ambayo yalinishangaza mno, kwa mfano kuna wale waliosema bila aibu kuwa mimi nilikubali kufunga ndoa kama tiketi ya kupata fedha na pia viza ya kuishi Australia. Wengine nao walikuwa wanasema kuwa niliingia kwenye ndoa hio kwa lengo la kumuua mume wangu kwani yeye anahitaji usaidizi wa hali ya juu kutoka kwa watu waliokaribu naye,"Susan anakumbuka Siku za kwanza baada ya kufunga ndoa, zilikuwa za wawili hawa kujenga mikakati ya kukabiliana na maoni ya uchochezi na matusi yaliyokuwa yanaibuliwa kutoka mitandao wa kijamii. "Maoni kwenye mitandao ya kijamii yalinisukuma kujiuliza iwapo niliufanya uamuzi wa busara au la, ila kila wakati nilipokuwa na mtizama mume wangu nilihisi amani na furaha. Nilipiga moyo konde na kuamua kufunga masikio yangu na macho yangu iliniweze kuishi kwa ndoa yangu bila uchochezi wa watu ," Susan anasema Kulingana na Susan kueleza mapenzi aliyonayo kwa mume wake Phillip kwa dunia sio jambo ambalo atafaulu kulifanya - ila yeye anahisi kuwa hakuna kizingiti chochote ambacho kinaweza kumtenganisha na mume wake. "Wengi ni wale ambao huniuliza maswali mengi kuhusu chaguo langu, wameniuliza maswali kama ikiwa nilikuwa timamu nikifanya uamuzi wa ndoa , ila kwa watu wa jamii yangu na pia kwa upande wa mume wangu hakuna aliyenyoosha kidole cha lawama kwetu," Susan anasema Mwanadada huyu anasema kuwa ndoto na pia azma walizonazo pia zimeongezea ladha ya ndoa yao kwani kwa upande mmoja Susana anafanya kazi na watu wanaoishi na ulemavu nchini Austalia. Mumewe Phillip naye amekuwa balozi anayetetea maswala mbalimbali yanayohusu walemavu nchini humo. Kuelewa matatizo Susan anasema kuwa alifahamu alichokuwa amechagua tangu alipokubali kuchumbiwa na mume wake - hali anayoishi nayo Phillip Bethlem myopathy - humfanya muathirika kuzidi kupoteza nguvu ya misuli na pia kuathiri viungo vya mwili kwa kiasi kuwa kila kuchao huzidi kuwa vigumu mno. Kwa mfano utapata kuwa mikono yake mumewe haina uwezo wa kufunguka au kunyooka vyema. Vivyo hivyo sehemu za miguu yake. Kwa hivyo inahitaji Susan kuhakikisha kuwa anamsaidia mumewe kila kuchao katika shughuli kama kupiga mswaki, kuchana nywele na pia kumpa chakula. "Ninaposikia watu wakizungumza kuhusu maisha yangu na Phillip mimi husikia uchungu mno kwa kuwa Phillip ni mume hodari mno licha ya mapungufu yake mimi nimejitolea kuhakikisha kuwa changamoto za ugonjwa anaoishi nao zimepungua," anasema Susan. Mwanadada huyu amesema kuwa alikutana na mume wake akiwa tayari anapambana kuishi na hali hiyo, na aliona jinsi familia yake ilivyokuwa imemtunza kwa kila hali. Susan anasema kuwa kwa kuishi karibu na Phillip anaelewa na kung'amua matatizo ya walemavu. Hasa anasema kuwa kumuona mumewe na uchungu humpa machozi na kamwe anasema kuwa hatachoka kumpenda na kumhudumia licha ya maswali na maneno ya watu . Susan na Phillip pia waliamua kudhihirishia ulimwengu jinsi wanavyoishi kwa kufungua akaunti katika mtandao wa YouTube. Huwa wanaangazia matukio na masuala mbalimbali kuhusu maisha yao hapo. Tangu Susan Njogu Eling alipoamua kufunga ndoa, amekuwa akishambuliwa na wengi kutokana na uamuzi wake. text: Watafiti kutoka chuo kikuu cha Glasgow waliangalia rekodi za karibu wanawake 4,000 wa Uskochi wenye ugonjwa wa kisukari. Walibaini kuwa viwango vya juu vya sukari mwilini miongoni mwa wanawake wajawazito wenye maradhi ya kisukari walikuwa na "uwezekano wa hatari " ya kupata watoto njiti. Kiwango cha unene wa mwili (BMI) cha mwanamke mwenye ugonjwa wa kisukari pia ni sababu kubwa, utafiti ulibaini. Watafiti pia walibaini kuwa theluthi tatu ya watoto wa aina hiyo wanaozaliwa kwa wanawake wenye ugonjwa wa kisukari hutokea wanapomaliza muhula kamili. Kujifungua mapema Dr Sharon Mackin, ambaye alifanya utafiti huo, amesema kuwa: "Ni muhimu kwamba sisi kama wataalamu wa huduma ya afya , tutafute njia bora za kuwasaidia wanawake wakati wanapokuwa na umri wa kupata ujauzito kudhibiti uzito wao na viwango vya sukari mwilini, ili wanapokuwa wajawazito iwe kwa kupanga au kwa kutopanga , wawe wamejiandaa na kupunguza hatari za matokeo mabaya. "Ni muhimu kwa wanawake wenye kisukari wawe watu wenye kujali hili, na wawe na uwezo wa kupata ushauri nasaha wa awali kabla ya kupata ujauzito, hata kama ikiwezekana wapange ujauzito. "Wanawake wenye ugonjwa kisukari pia wanapaswa kuwasiliana na kliniki zao za kisukari mapema iwezekanavyo mara wanapotambua kuwa ni wajawazito ili tuweze kuwaona na kuwasaidia mapema ." Uvumbuzi ambao "haukutarajiwa " wa utafiti ulikuwa ni kwamba watoto njiti walikuwa ni kiume zaidi kuliko wa kike miongoni mwa wanawake wenye aina ya 2 ya kisukari Utafiti ulibaini kuwa kujifungua mapema kunaweza kuangaliwa kama "chaguo linalowavutia wengi " lakini kwamba utafiti zaidi unahitajika kabla ya kuidhinisha hilo kwa kuwa muda wa kujifungua mapema unatakiwa kupangwa. Dr Mackin amesema kuwa swali la kujiuliza "linapaswa kuwa ni ikiwa kujifungua mapema kwa wanawake wote wajawazito wenye ugonjwa wa kisukari kunaweza kuwazuwia kujifungua watoto njiti ". Amesema: "hatufahamu jibu kuhusu hili . Muda sahihi wa kujifungua wa nujauzito wa aina hiyo haujulikani." Utafiti ulibaini kuwa watoto wachanga 5,392 walizaliwa kwa akina mama 3,847 wenye kisukari katika Uskochi mwenzi Aprili 1998 hadi Juni 2016. Akina mama wenye aina ya 1 ya kisukari walikuwa na uwezekano mara tatu wa kupata watoto njiti, huku wale wenye aina ya 2 walikuwa na uwezekano wa kuwapata watoto hao mara nne Viwango vya watoto njiti vilikuwa ni watoto 16.1 kati ya wazazi 1,000 miongoni mwa wanawake wenye aina ya 1 ya ugonjwa wa kisukari na watoto 22.9 kwa wanawake 1,000 miongoni mwa wanawake wenye aina ya 2 ya ugonjwa huo ililinganishwa na 4.9 kwa wanawake 1,000 miongoni mwa wanawake wote kwa ujumla. Utafiti umebaini kuwa "kwa ujumla juhudi za kuboresha viwango vya sukari mwilini kabla na wakati wa ujauzito ni suala muhimu Wanawake wenye aina ya 1 ya ugonjwa wa kisukari waliokuwa na uzazi wa watoto njiti walikuwa na kiwango cha juu ya wastani wa sukari katika damu yao kwa kipindi chote cha ujauzito wao, huku viwango vya kabla ya ujauzito vikiwa muhimu sana katika ubashiri wa uzazi wa watoto njiti miongoni mwa wale waliokuwa na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari. Watoto wachanga wenye uzito wa juu au wa chini walikuwa na uwezekano zaidi wa hatari ,ulibaini utafiti uliochapishwa na jarida maalumu linaloandika kuhusu ugonjwa wa kisukari- Diabetologia journal. Dr Emily Burns, mkuu wa mawasiliano ya utafiti katika kituo cha utafiti wa ugonjwa wa kisukari nchini Uingereza -Diabetes UK, amesema : "Wanaweki wengi wenye ugonjwa wa kisukari wana ujauzito wenye afya na watoto wachanga wenye afya, lakini utafiti huu unahimiza umuhimu wa kuwasaidia wanawake kudhibiti viwango vyao vya sukari katika damu zao pale wanapopanga kupata ujauzito, ili kupunguza hatari ya matatizo kadri wawezavyo. "Utafiti huo pia umeonyesha kuwa kupunguza uzito wa ziada, kwa wanawake wenye aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari ambao wana uzito wa mwili kupita kiasi, wanaweza kusaidia kupunguza hatari pia Unaweza pia kutazama: Umuhimu wa maziwa ya mama: Wanawake wachangia akiba ya maziwa kuokoa vichanga Kenya "Tunahitaji utafiti kubaini njia bora zaidi za kubashiri ni nani yuko katika hatari ya kupata matatizo wakati wa ujauzito, kuhakikisha usaidizi unatolewa kwa wale wanaouhitaji zaidi''. Wanawake wenye ugonjwa wa kisukari wana uwezekano mara nne wa kujifungua watoto njiti na hivyo kutoweza kuishi kuliko wasio na ugonjwa huo , umebaini utafiti text: Mkuu wa wilaya ya Ukerewe,Kanali Lucas Magembe amesema waliokolewa wakiwa salama ni watu 37, watu 32 wako hospitalini kwa ajili ya matibabu. Juhudi za uokoaji ziliendelea mpaka majira ya saa mbili usiku ambapo zoezi hilo lilisitishwa kutokana na hali ya giza ambayo ilikuwa kikwazo kutekeleza zoezi hilo. ''Sababu nyingine ni kuwa nguvu kubwa inahitajika na inahitaji ushiriki wa jamii na watu wengi walikuwa wameshachoka, hasa wale wenye mitumbwi ambao walikuwa wakifika pale kubeba miili'' alieleza Kanali Magembe. Taarifa za awali zinaeleza kwamba kivuko hicho kilikuwa kimebeba mamia ya abiria. Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima ameeleza kwamba maafisa kadhaa kutoka eneo hilo wakiwemo polisi na jeshi la majini wanaelekea kujiunga katika jitihada za uokoaji. ''Hatuijui hali halisi tunakwenda kuikagua kwanza halafu baadaye tutatoa tamko rasmi. Malima ameeleza kwamba maboti ya polisi na jeshi yatashirikiana katika zoezi hilo. ''Tunaomba mungu atupe subira kwa wakati huu, na tusishuhudie idadi kubwa ya vifo' Mkasa huo umewashutusha wengi nchini kama mwanamke mmoja aliyeshuhudia mkasa huo ambaye alionekana kujawa na hisia. ''Tazama Tazama.. Kivuko kile pale kimezama …….miili inaelea, imezama sasa hivi''. Umati mkubwa wa watu umeshuka ufukweni kutazama jitihada za uokozi Mikasa ya vivuko kuzama Tanzania Tanzania ina historia ya ajali za vivuko kuzama, kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kilikuwa mnamo Mei 1996, wakati MV Bukoba ilipozama kutoka Mwanza katika ziwa lilo hilo Viktoria kaskazini magharibi mwa Tanzania na kusababisha vifo vya takriban watu 1000. Rekodi rasmi hata hivyo iliopo ni watu 894 waliofariki. Kumewahi kushuhudiwa pia mikasa mingine kama vile Mv Skagit kivukio kilichozama mnamo 2012 wakatikikiwa kimebeba abiria 290 wakiwemo watalaii 17 kutoka pwani ya Zanzibar. Mwanza ni mji muhimu wenye bandari Tanzania katika ziwa Viktoria, inayopokea bidhaa kama pamba chai, kahawa zinazotoka magharibi mwa nchi hiyo. Ziwa viktoria ni la pili kwa ukubwa duniani baada ya ziwa Superior Amerika kaskazini. Miili ya watu 44 imeopolewa kutoka Ziwa Victoria baada ya kivuko kilichokuwa kimebeba mamia ya abiria kuzama jijini Mwanza Kaskazini magharibi mwa Tanzania. text: Meli ya mafuta na ya mizigo zagongana China watu 32 hawajulikani waliko Meli ya mafuta ya Sanchi yenye usajili wa Panama ikibeba tani 136,000 za mafuta kutoka Iran ilishika moto baada ya kugongana. Wizara ya uchukuzi nchini China ilisema kuwa watu ambao hawakulinai wali ni wahudumu wa meli wakiwemo 30 raia wa Iran na wawili kutoka Bangladesh. Wahudumu 21 wa meli ya mizigo wameokolewa. Picha iliyochapishwa na kituo cha taifa cha CGTN, ilionyesha moto mkubwa na moshi ukitoka kwenye meli ya mafuta. Ajali hiyo ilitokea karibu kilomita 296 kutoka pwani ya Shanghai. Meli nane za China zimetimiwa kwa oparesheni ya uokoaji kwa mujibu wa shirika la Xinhua nchini China. Korea Kusini nayo imetuma meli ya walinzi wa pwani na helikopta kusaidia katika uokoaji. Meli ya mizigo ya usaljili wa Hog Kong CF Crystal ilikuwa imebeba tani 64,000 za nafaka kutoka Marekani kwenda mkoa wa Guangdong kusini mwa China. Meli ya mafuta na ya mizigo zagongana China watu 32 hawajulikani waliko Watu 32 hawajulikani waliko baada ya meli ya mafuta na ile ya mizigo kugongana mashariki mwa pwani ya China Jumamosi jioni. text: Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuhudhuria ibada hiyo, polisi walilazimika kufunga barabara zote ambazo zinaelekea kwenye kanisa hilo. Safu ya waombolezaji imeongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la nchi hiyo Job Ndugai. Mapema asubuhi saa tatu kanisa lilikuwa limejaa, na nje pia kulikuwa pamefurika. Baadhi ya waombolezaji walipata nafasi ya kuaga mwili ndani ya kanisa lakini ilifika mahala hatua hiyo ilisitishwa ili ibada na hotuba zitolewe. Mwili ulitolewa kanisani kwa safari ya mwisho ya makaburini saa tisa na nusu. Na shughuli za mazishi zilikamilika saa 11 na nusu. Familia yatoa neno Mke wa Mengi Jacquiline akiwa pamoja na watoto katika ibada ya mwisho ya mazishi ya mume wake Mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu Mengi, Abdiel, amesema kwa niaba ya familia wanashukuru na wameguswa na upendo waliooneshwa. "Sisi kama familia tumeguswa sana na upendo ambao umeoneshwa kwa baba yetu. Mengi mazuri kuhusu mzee wetu mmeyasema. Mapenzi yao yamemgusa mzee wetu, hili ni uthibitisho kuwa muda na nguvu zake ambazo aliziwekeza kwa watu hawa hazikupotea bure. " Abdiel amemzungumzia baba yake kuwa ni mtu ambaye alipenda kufanya mambo mengi na kujaribu na alikuwa na mipaka yake pia. "Lakini hakuwa na mpaka kwenye kupambana na umasikini. Alikuwa na mtoto wa masikini lakini hakuna aliyeweza kumzuia kupambana na umasikini na kujikwamua. Pia hakukubali mpaka wa kuambiwa yeye kama mwekezaji mzawa basi hawezi fanya hili ama lile nchini. Hilo alilipinga kwa nguvu zote." Marehemu Mengi ameacha mjane, ambaye ni mlimbwende maarufu nchini humo Jacqueline Ntuyabaliwe na watoto wanne. Umauti ulimfika usiku wa Jumatano ya wiki iliyopita jijini Dubai, Falme za Kiarabu ambapo alienda kwa ajili ya matibabu. Mengi ni nani? Mengi alizaliwa wilayani Machame, Kilimanjaro, Tanzania mwaka 1942, akiwa mmoja wa watoto saba wa Bw Abhraham Mengi na Bi Ndeekyo Mengi. "Familia yetu ilikuwa masikini sana, kila siku ilikuwa ni vita ya kupambana na umasikini. Tulimiliki sio zaidi ya ekari moja tukiishi kwenye vibanda vya udongo tukichanganyika na ng'ombe wachache na kuku. Ninaporudisha fikra na kutazama nyuma ni vigumu napatwa na ugumu wa kufikiri namna tulivyoweza kuishi katika hali ile," alipata kusema kwenye uhai wake. Alianza safari yake kielimu shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Kwa ufadhili wa Chama cha Ushirika kilichokuwa na nguvu ya kifedha ushawishi KNCU Mengi alisomeshwa masomo yake ya shahada ya kwanza ya uhasibu nchini Uingereza. Baada ya masomo ughaibuni, Mengi alirudi Tanzania 1971 na kuajiriwa na kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ( sasa PricewaterhouseCooper) mpaka mwaka 1989 alipoamua kujikita kwenye ujasiriamali. Baada ya kuachana na ajira, Mengi aliiboresha kampuni yake ya Industrial Projects Promotion Limited na baadae kufahamika zaidi kama IPP Limited. Kupitia IPP Limited Mengi alaianzinza kampuni mbalimbali na kufanya biashara kadha wa kadha kuanzia uzalishaji wa sabuni, soda, maji ya kunywa, madini, mafuta, gesi asilia na kilimo. Hata hivyo, umaarufu mkubwa wa Mengi ni kutokana na kumiliki vyombo vya habari, kuanzia magazeti, vituo vya runinga na redio. Mwaka 2014, jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes lilikadiria utajiri wa Mengi kuwa unafikia dola milioni 560. Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi. text: Chupa moja tu ya bia inaweza kukuletea madhara ya kiafya Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe. Watafiti wamekubali kwamba kunywa kwa kiasi kunaweza kumlinda mtu dhidi ya ugonjwa wa moyo lakini waligundua kwamba kuna hatari ya mtu kupata saratani na kukosa kinga ya magonjwa mengine Mwandishi wa utafiti huu alisema matokeo aliyoyapata yalikuwa ya muhimu sana kwa sasa kwa sababu ya mambo mengi yaliyozingatiwa Je! unywaji wa pombe unasababisha hatari kubwa kwa kiasi gani? Bilauri moja ya mvinyo sio nzuri kiafya Utafiti uliofanywa na 'Global Burden of Disease'unaangalia kiwango cha pombe na madhara yake kiafya kwa mataifa 195 ikiwemo Uingereza katika miaka ya 1996 mpaka 2016. Utafiti uliangalia umri kuanzia miaka 15 hadi 95,mtafiti alilinganisha watu ambao wanakunywa pombe hata chupa moja kwa siku na wale ambao hawanywi kabisa. Na kubaini kwamba watu wasiokunywa kati ya 100,000 ni watu 914 tu ndio wanasumbuliwa na matatizo ya kiafya kama saratani au kusumbuliwa na majeraha yeyote. Lakini watu wanne zaidi wanapata madhara kama wanakunywa pombe hata chupa au bilauri moja kwa siku. Imethibitishwa kwamba hakuna pombe iliyo na manufaa kiafya Kwa watu ambao hunywa chupa mbili za pombe kwa siku,Watu 63 kati yao uanza kupata mabadiliko ya kiafya na wale ambao hutumia chupa tano kwa kila siku kuna ongezeko kubwa la watu wapatao 338 ambao hupata madhara ya kiafya. Kiongozi wa tafiti hiyo Dr Max Griswold kutoka Taasisi ya Health Metrics and Evaluation (IHME) katika chuo cha Washngton alisema kwamba utafiti wa awali ulibaini kwamba kuna hatari kubwa za kiafya ambazo zinahusishwa na uongezekaji wa uywaji wa pombe. Uhusiano mkubwa wa matumizi ya pombe na hatari ya kupata saratani pamoja na magonjwa ya kuambukiza inaondoa kinga ya ugonjwa wa moyo katika utafiti. Je, unakunywa pombe kiasi gani? Ingawa hatari ya matumizi ya pombe huanza polepole hukua kwa haraka kwa watu ambao hunywa pombe kwa kiwango kikubwa. Mwaka 2016 ,serikali Uingereza iliweka kiwango ambacho watu wnapaswa kutumia kwa wanawake na wanaume ili kupunguza athari ya ongezeko la ugonjwa huo. Habari mbaya kwa wale ambao huwa wanafurahia na kufikiri kwamba bilauri moja ya mvinyo kwa siku ni nzuri kwa kiafya. text: Rais Rouhani wa Iran ahsinda muhula wac pili wa urais nchini Iran Huku ikiwa kura zote zimehesabiwa Bwana Rouhani alikuwa amejishindia asilimia 56 hatua iliozuia awamu ya pili ya uchaguzi dhidi ya mpinzani wake mkuu Ebrahim Raisi. Rais Rouhani aliripotiwa kuongoza kwa kura millioni 14 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ebrahim Raisi mwenye kura millioni 10 kufikia sasa. Asilimia 70 ya waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura zao. Awali Ibrahim Raisi alitoa malalamishi akidai kumekuwa na dosari katika uchaguzi huo. Raisi, ambae anaungwa mkono na kiongozi wa kidini nchini humo , Ayatollah Khamenei, amekuwa akikosea sera za rais Rouhani akisema ameruhusu mwingilio wa nchi za kigeni kuathiri Iran huku kukiwa pia na usimamizi mbaya. Bw. Rouhani kwa upande wake ametetea sera zake akisema zilimwezesha kuuchipua uchumi kwa kufanikiwa kushawishi kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vilivyokuwa vimewekewa taifa hilo kwa miaka mingi. Na pia kufanikisha mkataba wa kinuklia jambo ambalo limepunguza uhasama na mataifa ya nje. Kituo cha Televisheni kinachomilikiwa na serikali ya Iran kimempongeza rais anaetetea kiti chake katika uchaguzi wa sasa Hassan Rouhani kwa ushindi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Ijumaa. text: Teknolojia hiyo ilifanyiwa majaribio Las Vegas mapema mwaka huu Gari hilo lililokuwa limewabeba abiria kadha liligongwa na lori lililkuwa katika mwendo wa chini. Hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa ajali hiyo ambayo maafisa wanaema ilitokana na hitilafu ya dereva wa lori. Basi hilo ndilo la kwanza la aina yake kutumiwa kwenye barabara za umma. Ajali hiyo ilitokea siku moja baada ya Waymo - inayomilikiwa na kampuni ya Google, Alphabet, kutangaza kuwa inazindua teksi zinazojiendesha huko Phoenix, Arizona. Basi hilo linawabeba hadi wau 15 na lina kasi ya hadi kilomita 45 kwa saa lakini kawaida mwendo wake ni kilomita 25 kwa saa. Msemaji wa mji wa Las Vegas aliiambia BBC kuwa ajali hiyo ilkuwa ni kidogo na kwamba basi hilo litarudi barabarani Alhamisi baada ya majaribio ya kawaida. Lori la mizigo lilikuwa likitoka kupakia mizigo. "Basi likafanya kile linastahili kufanya na kusimama. Kwa bahati mbaya dereva wa lori hakusimama, alisema afisa wa mawasiliano Jace Radke. Ajali za magari yanayojiendesha zimeripotwa awali, lakini karibu ajali hizo zote zimesababishwa na makosa ya wanadamu. Basi linalojiendsha huko Las Vegas lilihusika kwenye ajali wakati wa siku yake ya huduma. text: Utafiti mkubwa duniani uliochunguza mtazamo wa watu kuhusu chanjo unaonyesha ni watu wachache walio na imani na chanjo duniani. Uchambuzi wa wakfu wa Wellcome Trust unajumuisha majibu ya zaidi ya watu 140,000 katika mataifa 140. Haya yanajiri wakati shirika la afya duniani WHO likiwa limeorodhesha ususiaji chanjo kama mojawapo ya tishio kumi kuu dhidi ya afya duniani. Unahitaji mtandao wenye JavaScript kutazama. Je watu wanaamini chanjo nchini mwako? Tafuta Nchi: Tafuta Nchi: Watu waliulizwa iwapo wanakubali, wanakataa, hawakubali au kukataa au hawana maoni kuhusu kauli hizi Chagua kauli kuona matokeo Huenda idadi isifike 100% kutokana na makadirio Utafiti huo umewauliza watu maoni yao kuhusu masuala ya sayansi. Wellcome imetathmini majibu ya maswali matano makuu na kukagua 'imani kwa wanasayansi' kwa imani ya kiwango cha juu, wastani na chini. Chanzo: Wellcome Global Monitor, Gallup World Poll 2018 Samahani hakuna data ya eneo hili Intaneti haifanyi. Jaribu tena Wellcome Global Monitor lilitekeleza utafiti uliokuwa na uwakilishi wa kitaifa katika nchi 142. Mada za utafiti zilijumuisha: imani kwa sayansi, taarifa ya afya; kiwango cha uelewa na shauku kwa sayansi na afya na mitazamao ya watu kwa chanjo. Utafiti huo wa kimataifa unafichua kwamba idadi kubwa ya watu wanasema wanaamini kwa kiasi kidogo chanjo. Walipoulizwa iwapo chanjo ni salama: Walipoulizwa iwapo wanaamini chanjo zinafanya kazi: Kwanini ina umuhimu? Kuna ushahidi mwingi tu wa kisayansi kuwa chanjo nikinga bora dhidi ya maambukizi hatari kama surua au ukambi. Chanjo huwalinda mabilioni ya watu duniani. Imefanikiwa kuangamiza kabisa ugonjwa wa - smallpox - na zinakaribia kuangamiza magonjwa mengine kama polio. Lakini baadhi ya magonjwa kama surua, yanazuka upya na wataalamu wanasema watu wanaosusia chanjo, hatua inayotokana na hofu na kuenea kwa habari za uongozo kuhusu chanjo hizo ni mojawapo wa sababu. Dkt Ann Lindstrand, mtaalamu wa chanjo katika shirika la afya duniani amesema hali iliopo sasa ni nzito sana. "Kususia chanjo kuna uwezo kwa baadhi ya maeneo kutatiza pakubwa hatua zilizopigwa duniani katika kudhibiti magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo. "Visa vyovyote tunavyoviona vya kuzuka upya kwa magonjwa ni hatua isiyokubalika ya kurudi nyuma." Surua/Ukambi umerudi Mataifa yaliokaribia kuangamiza ukambi yameshuhudia milipuko mingi ya ugonjw ahuo. Data zinaonyesha ongezeko la visa katika takriban kila sehemu duniani, huku kukiwa na 30% ya visa zaidi vilivyoshuhudia mnamo 2017 ikilinganishwa na 2016. Uamuzi unaotokana na sababu yoyote ile ya kususia chanjo ni hatari sio tu kwa wengine, lakini kwa mtu binfasi kurudiwa na maambukizi. Iwapo watu wa kutosha watapata chanjo, inasitisha ugonjwa kutosambaa katika umati wa watu - jambo ambalo wataalamu wanaliita "herd immunity"au kinga ya wengi. Mifano ya ufanisi Watu wengi wanaoishi katika maeneo masikini wapo salama. Kiwango kikubwa kipo Asia kusini ambako 95% ya watu wanakubali, ikifuatiwana Afrika mashariki ambako 92% ya watu wanaziamini chanjo. Bangladesh na Rwanda zina makubaliano yanayokaribiana kuwiana kuhusu usalama na ufanyaji kazi wa chanjo na zimefanikiwa kupata kiwango kikubwa cha watu waliopewa chanjo licha ya changamoto nyingi katika kuzifikisha chanjo kwa watu. Rwanda ilikuwa nchi ya kwanza ya kipato cha chini duniani kuhakikisha wanawake kote wanapata chanjo ya HPV inayotoa kinga dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi. Kwanini kuna imani ndogo? Baadhiya watu wanaoishi katika maeneo mengine yalio ya kipato cha juu ni miongoni mwa wanaoamini kwa uchache kuhusu usalama wa chanjo Nchini France - nchi mojawapo miongoni mwa nyingine za Ulaya ambazo sasa zinashuhudia mlipuko wa surua - mtu mmoja kati ya watatu haamini kuwa chanjo zi salama. Hicho ni kiwango kikubwa kwa asilimia kwa taifa lolote duniani. Raia wa Ufaransa pia ni miongoni mwa walio n auwezekano mkubwa kukataa kwamba chanjo zinafanya kazi, 19%, na wanakataa kuwa chanjo ni muhimu kwa watoto 10%. Serikali ya Ufaransa sasa imeongeza chanjo nane za ziada za lazima kwa tatu zilizopo ambazo watoto nchini humo hupewa. Nchi jirani Italia - 76% wanakubali kuwa chanjo ni salama - hivi maajuzi ilipitisha sheria inayoruhusu shule kuwapiga marufuku watoto ambao hawajachanjwa, au inawatoza faini wazazi baada ya takwimu za wanaopokea chanjo kushuka pakubwa. Uingereza bado ingali kufika kiwango hicho lakini waziri wa afya Matt Hancock amesema sio ajabu kukaidhinishwa chanjo za lazima ikibidi. Kumeshuhudiwa pia milipuko ya surua nchini Marekani - mlipuko mkubwa kuwahi kutokea nchini humo katika muongo mmoja huku kukishuhudiwa visa 980 katika majimbo 26 katika mwaka 2019 kufikia sasa. Imetengenezwa na Becky Dale na Christine Jeavans; ubunifu wa Debie Loizou; utengenezaji wa Scott Jarvis na Katia Artsenkova Imani ndogo kutoka kwa umma dhidi ya chanjo duniani inaathiri na kurudisha nyuma vita dhidi ya magonjwa hatari yanayoweza kuzuilika, wataalamu wanaonya. text: Mtoto huyo anapata matibabu hospitalini Abhinandan Singh amewaambia wanahabari kuwa mtoto huyo alipatikana na mwanakijiji aliyekuwa ameenda kumzika mtoto wake aliyefariki baada ya kuzaliwa. Mtoto huyo aliyekuwa amewekwa ndani ya chunguu na kuzikwa katika shimo la futi tatu, amekimbizwa hospitali ambako anapokea matibabu. Polisi imeanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho. "Tunajaribu kutafuta wazazi wa mtoto huyo kwani tunashuku huenda hatua hiyo ilifikiwa kutokana na idhini yao," Bw. Singh aliwaambia wanahabari katika jimbo la Uttar Pradesh. Kwa mujibu wa mkuu huyo wa polisi, mwanakijiji mmoja wlimpata mtoto huyo alipokuwa akifukua kaburi la kumzika mwanawe aliyefariki baada ya kuzaliwa. "Walipokuwa wanaendelea na shughuli ya uchimbaji kaburi kijiko cha kutoa mchanga katika shimo liligonga chungu kilichokuwa kimezikwa fiti tatu. walilopokitoa walipata ndani kuna mtoto," Bw Singh alieleza. "Polisi walimpeleka mtoto huyo katika hospitali iliyo karibu ambako anaendelea kupokea matibabu." Suala La kijinsia nchini India linatajwa kuwa katika hali mbaya zaidi duniani. Wanawake mara nyingi hubaguliwa katika jamii hukiu watoto wa kike wakichukuliwa kama mzigo wa kiuchumi, hasa katika jamii masikini. Wanaharakati wa kutetea usawa wa kijinsia wanasema watoto wa kiume wanapendelewa zaidi kuliko wa kike. Japo mimba za watoto wakike mara nchini hutolewa baada ya wazazi kubaini jinsia ya mtoto kupitia kiliniki zilizopigwa marufuku, visa vya watoto wa kike kuawa baada ya kuzaliwa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara. Mtoto mchanga wa kike amepatikana akiwa amezikwa hai katika kaburi la kina kifupi kaskazini mwa India, mkuu wa polisi afichua kisa hicho. text: Mkutano huo wa Januari 9 utaangazia kutafuta njia ya wachezaji wa Korea Kaskazini kushiriki michezo hiyo itakayoandaliwa Korea Kusini Februari. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema wiki hii kwamba atawatuma wawakilishi katika michezo hiyo na kusema hiyo itakuwa "fursa nzuri ya kuonyesha umoja" miongoni mwa raia wa Korea Kaskazini. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Panmunjom, mpakani. Eneo hilo linalofahamika kama kijiji cha amani linapatikana katika eneo lisiloruhusiwa kuwa na wanajeshi mpakani, na ni hapo ambapo mazungumzo kati ya nchi hizo yamekuwa yakifanyika tangu zamani. Panmunjom imetajwa kama pahala ambapo maafisa wa nchi hizo mbili wanaweza kukutana Kwa mujibu wa afisa kutoka afisi ya rais wa Korea Kusini, mkutano huo utaangazia zaidi michezo hiyo itakayofanyika Pyeongchang. Hata hivyo, aliambia shirika la habari la Yonhap la Korea Kusini kwamba anaamini kutakuwepo pia na "mazungumzo kuhusiana na kuboresha uhusiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini baada ya kuthibitishwa kwa ushiriki wa Kaskazini katika michezo hiyo." Hayo yatakuwa mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya juu kufanyika kati ya nchi hizo mbili tangu Desemba 2015. Haijabainika ni nani watashiriki mazungumzo hayo. Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alikuwa awali amesema anatazama michezo hiyo kama fursa mwafaka ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Mapema wiki hii, Korea Kaskazini ilirejesha mawasiliano ya simu maalum kati ya nchi hizo mbili, kufanikisha mazungumzo hayo. Hata hivyo, afisa wa wizara ya Korea Kusini kuhusu kuunganishwa kwa mataifa hayo mawili alisema Korea Kaskazini ilikubali mwaliko wa kushiriki mazungumzo hayo kupitia kipepesi. Korea Kaskazini imekubali kushiriki mazungumzo ya ngazi ya juu wiki ijayo kuhusu kushiriki kwa wachezaji wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, Korea Kusini imesema. text: Maji hayo yaligunduliwa kilomita 3 chini ya ardhi kwenye mgodi Canada Maji hayo yamegunduliwa katika mgodi uliopo nchini Canada. Wanasayansi walikuwa wamegundua maji mengine mwaka 2013 eneo hilo yaliyokadiriwa kuwa ya kutoka miaka 1.5 bilioni iliyopita lakini sasa wanasema maji waliyoyagundua karibuni ni ya zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita. Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Toronto waliwasilisha matokeo ya utafiti wao katika mkuano wa wataalamu wa fizikia ya dunia mjini San Francisco. Profesa Barbara Sherwood Lollar, aliyeongoza wataalamu waliofanya ugunduzi huo aliambia BBC: "Watu wanapofikiria kuhusu maji haya, wanafikiri labda ni matono ya maji yaliyokwamba ndani ya jiwe. "Lakini haya ni maji yanayotiririka. Yanatoka kwa kasi ya lita kadha kila dakika - ni maji mengi sana kuliko watu wanavyotarajia." Maji ya awali yaliyoaminika kuwa ya kale zaidi yalipatikana 2.4km chini ya ardhi katika mgodi wa shaba nyekundu, zinki na fedha. Wachunguzi waliendelea kufanya utafiti kadiri mgodi ulivyoendelea kuchimbwa. Maji hayo yaliyogunduliwa sasa yalipatikana karibu 3km chini ya ardhi. Mgodi huo unaendelea kuchimbwa Maji hayo ya kale yanawapa wanasayansi fursa nadra ya kuchunguza historia ya sayari ya dunia, na pia kutoa vidokezo kuhusu viumbe walioishi wakati huo. Watafiti hao wamegundua kemikali ambazo wanaamini zilitokana na viumbe wa seli moja ambao waliishi kwenye maji hayo. Wanasema kuchunguza maeneo yenye maji kama hayo ya kale duniani kunaweza kuwadokezea iwapo kunaweza kuwa na uhai katika sayari nyingine katika Mgumo wa Jua. Wanasayansi nchini Canada wamegundua maji yanayoaminika kuwa ya kale zaidi duniani, ambayo wanaamini yamekuwepo angalau kwa miaka bilioni mbili. text: Utalipa dola 250,00 kulala gereza alimofungwa Mandela? Shirika moja linafanya mnada huo wa kuanzia dola 250,000 kuruhusu watu 67 kulala kwa siku moja ndani ya gereza la ulinzi mkali ambapo Mandela alifungwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 ya kifungo chake. Warsha hiyo inaandaliwa na kundi linalofahamika kama CEO Sleepout, kuadhimisha siku ambayo Mandela ambaye alifariki mwaka 2013 akiwa na miaka 95 angefikisha miaka 100. Linasema kuwa mnada huo utafungwa usiku wa manane tarehe 17 Julai siku moja kabla ya kuadhimishwa siku yake ya kuzaliwa. Kisiwa cha Robben sasa ni kituo cha kitalii Mandela aliachiliwa kutoka gerezani mwaka 1990 wakati Afrika Kusini ulikuwa unaupigia kwaheri ubaguzi wa rangi, jambo lililofikia kikomo mwaka 1994 wakati alichaguliwa kama rais wa kwanza mweusi nchini humo. Baadhi ya pesa ambazo zitapatikana kutoka kwa mnada huo zitapewa kundi moja la kimarekani linalowasaidia wafungwa kupata elimu cha chuo kikuu. Maisha ya Nelson Mandela miaka 27 gerezani "Nilienda likizo ndefu ya miaka 27," Nelson Mandela wakati mmoja alisema kuhusu miaka yake gerezani. Maneno kwanza ya mlinzi wa gereza wakati Nelson Mandela na wenzake wa ANC walifika yalikuwa ni: "Hiki ni kisiwa, Hapa ndipo mtafia." Walipitia maisha mabaya kwenye gereza hilo jipya lililojengwa kuwazuia wafungwa wa kisissa. Kila mmoja alikuwa na chumba chake ya futi saba mraba na kilizungukwa na ua uliojengwa waka saruji. Kwanza hakuruhusiwa kusoma chochote. Maisha katika kisiwa cha Robben yalikuwa magumu Walivunja mawe kwa nyundo kutengeneza kokoto na walilazimishwa kufanya kazi kwa timbo lililokuwa na mwangaza mkali. Mfungwa mwenzake Walter Sisulu alingumza kuhunu kuibuka kwa uongozi wa Mandela miongoni mwa wafungwa kauanzia uasi kwenye matimbo. Mfungwa nambari 46664 jinsi alivyofahamika - mfungwa wa 466 kuwasili mwaka 1964 - akawa wa kwanza kuasi kupinga kutendewa vibaya na mara nyingine alitenganishwa na wafungwa wengine kama adhabu. Wakati wa miaka ya kwanza kwanza, kutengwa ilikuwa kawaida. Tulihukuiwa kwa makosa madogo na kutengwa, aliandika kwenye kitabu chake, The Long Walk to Freedom. Mamlaka ziliamini kuwa kutengwa ilikuwa jibu kwa uasi wetu. Chuo ndani ya gereza Baada ya miezi michache ya kwanza kwenye kisiwa cha Roben, maisha yalirudi kuwa ya mpangilio. "Maisha ya gerezani na mpangilio: kila siku ni sawa na iliyopita, kila wiki ni sawa na iliyotangulia na hivyo miezi na miaka huingiliana, Mandela aliandika. Muda ulivyopita na kulingana ni alikuwa akisimamia gereza, mambo kadhaa yaliruhusiwa. Wale waliotaka walituma maombi ya kusoma. Lakini masomo mengine kama ya siasa na historia ya jeshi vilikuwa haramu. Robben Island ikaja kufahamika kama "chuo ndani ya gereza." Wakati Mandela alizungunzia maisha yake huko Robben baada ya kurudi huko mwaka 1994 alisema: "Vidonda ambavyo havionekani, ni vichungu sana kuliko vile vinavyoweza kuonekana na kutibiwa na daktari. Moja ya nyakati zenye husuni zaidi wakati wa miaka yangu gerezani ulikuwa wakati wa kifo cha mama yangu. Wakati mwingine ni wakati wa kifo cha mtota wangu wa kwanza wa kiume aliyefariki kwenye ajali ya barabarani." hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi yote hayo. Mnada unafanyika nchini Afrika Kusini wa kutoa fursa kwa watu kuweza kulala kwa siku moja kwenye jela alimofungwa rais wa kwanza mweusi nchini humo Nelson Mandela huko Robben Island. text: Roboti yagundua mafuta ya nuklia katika kinu cha Fukushima Viwango vikubwa vya vitu vinayoonekana kama mawe vimeonekana katika kinu chake cha tatu. Ikiwa itathibitisshwa itakuwa mafanikio makubwa kati oparesheni ya kusafisha kinu hicho. Roboti yagundua mafuta ya nuklia katika kinu cha Fukushima Kinu hicho kulikumbwa na tsunamni mwaka 2011 na kusababisha ajali mbaya zaidi ya kinu cha nuklia tangu ile ya Chernobyl. Zaidi ya watu 200,000 walilazimika kuhama makwao kutokana na uchafuzi uliotoakana nakinu hicho. Baadhi ya maeneo yaliyoharibiwa bado yana uchafu mbaya wa nuklia na toboti hutumiwa kuyasafisha. Roboti yagundua mafuta ya nuklia katika kinu cha Fukushima Ugunduzi huo ulifuatia uchunguzi wa siku tatu wa kutumia roboti ndogo ya chini ya maji inayoitwa Little Sunfish. Zaidi ya watu 18,500 waliuawa au kutoweka wakati tetemeko la ardhi lilisababisha tsunami kubwa ambayo ilisababisha ajali katika kinu cha Fukushina. Roboti yagundua mafuta ya nuklia katika kinu cha Fukushima Roboti ya chini ya maji imenasa picha zinazoaminika kuwa za kwanza kabisa ya mafuta ya nuklia yaliyoyeyuka ndani ya kinu cha Japan kilichoharibiwa cha Fukushima. text: Mkuu wa Tesla Elon Musk ameahidi kuwa betri hiyo itaundwa kwa siku 100 Betri hiyo inatarajiwa kulikinga jimbo la Australia Kusini dhidi ya mgogoro wa kawi sawa na uliosababisha kukatizwa kwa umeme kabisa katika jimbo hilo Septemba 2016 baada ya kutokea kwa tufani mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 50, waziri mkuu wa jimbo hilo Jay Weatherill. Watu zaidi ya 1.7 milioni huishi katika jimbo hilo ambalo ni kubwa mara 40% zaidi ya jimbo la Texas. Jimbo hilo lina ukubwa wa zaidi ya kilomita mraba 980,000 (maili mraba 380,000). Mkuu wa kampuni ya Elon Musk amethibitisha kwamba kampuni hiyo itaunda betri hiyo katika kipindi cha siku 100, na ikishindwa kufanya hivyo basi itaunda betri hiyo bila malipo. Betri hiyo itakuwa na uwezo wa megawati 100 (megawati 129 kwa saa), na inatarajiwa kuanza kutumiwa mwaka huu. "Bila shaka kuna changamoto kadha, kwa sababu itakuwa betri kubwa zaidi duniani kwa mbali," Musk alisema akiwa Adelaide Ijumaa. Aliongeza kuwa "betri inayoifuata hiyo kwa ukubwa ina uwezo wa megawati 30". Betri hiyo mpya ya Tesla, ambao wameshirikiana na kampuni ya nishati ya upepo ya Neoen, itakuwa ikifanya kazi bila kuzimwa na itatoa umeme zaidi hasa wakati wa dharura. "Itakabilisha kabisa jinsi kawi mbadala inavyohifadhiwa, na pia kuimarisha mfumo wa kusambaza umeme wa jimbo la Australia Kusini," Weatherill alisema. Umeme ulikosekana jimbo lote la Australia Kusini mwaka jana kutokana na tufani Siku 100 alizoahidi Musk zitaanza kuhesabbiwa baada ya mkataba kutiwa saini rasmi. Tesla wamekuwa wakipanua biashara yao ya uundaji wa betri sawa na uundaji wa magari ya umeme. Betri kubwa zaidi ya lithium duniani itaundwa na kuwekwa nchini Australia, kupitia makubaliano kati ya kampuni inayounda magari ya kutumia umeme ya Tesla na kampuni ya kawi ya Australia Neoen. text: Vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaripoti kuwa Charles Kanyi Njagua maarufu kama Jaguar amekamatwa mchana huu akiwa anatoka kwenye viwanja vya bunge. Tayari ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kupitia ukurasa wake wa Twitter imesema mbunge huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kuchochea ghasia. Katika kanda ya video iliosambazwa pakubwa nchini Kenya na katika nchi jirani Tanzania, mbunge huyo alisema hawatokubali watu wa nje waje kuendesha biashara nchini. ''Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine. Raia wa Pakistan wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote'', alinukuliwa akisema. Licha ya Serikali ya Tanzania kuwaomba raia wake kuwa na utulivu na serikali ya Kenya kujitenga na matamshi ya mbunge huyo, bado gumzo linaendelea katika mitandao ya kijamii huku baadhi wakimtaka mbunge huyo aombe radhi kwa matamshi yake. Jaguar hii leo kwa kutumia mtandao wake wa Twitter amedai kuwa matamshi yake hayo yametafsiriwa vibaya. "Nataka amani kwenye nchi na biashara ziendelee bila kuingiliwa na wageni wote wanakaribishwa nchini mwetu," ameandika Jaguar kupitia mtandao wa Twitter. Soko kubwa la mitumba la jijini Nairobi la Gikombaa lipo ndani ya jimbo la Starehe. Matamshi hayo yameibua mzozo wa kidiplomasia, huku Tazania ikimuita balozi wa Kenya nchini humo Dan Kazungu kujieleza juu ya kauli hiyo. Waziri Mkuu wa Tanzania aliliambia Bunge kuwa Kenya imeihakikishia serikali ya Tanzania kuwa matamshi hayo ya chuki si msimamo wa serikali na kuwa Watanzania wataendelea kuwa salama nchini Kenya. ''Sisi kama Watanzania tuendeleeni kuishi na amani na Wakenya hatuna matatizo nao,'' alisema Majaliwa. Tayari serikali ya Kenya kupitia msemaji wake kanali mstaafu Cyrus Oguna imetoa taarifa yake ikisema kuwa matamshi ya mbunge huyo ni ya kibinafsi na kwamba sio msimamo wa serikali ya Kenya. '' Tungependa kusema kuwa huo sio msimamo wa serikali ya Kenya na tunashutumu matamshi hayo yaliotolewa katika kanda hiyo ya video. Matamshi hayo hayafai katika ulimwengu wa sasa'', alisema Oguna. ''Wakenya ni wapenda amani ambao kwa miaka mingi wameishi na raia wengine wa kigeni bila tatipo lolote. Hii ni thamani ambayo tunajivunia kama taifa na ni lazima tuendelea nayo'', ilisema taarifa hiyo iliotiwa saini na msemaji huyo wa serikali. Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda waliopo jijini Nairobi. text: Rais Yoweri Museveni sasa anaweza kuwania urais tena mwaka 2021 Baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini kutokana na kuupinga muswada. Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu. Wabunge wa Uganda Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023. Ni pengine kutokanana malalamiko kuwa kuondolewa kwa ukomo wa umri kunaweza kumfanya Bwana Museveni kuwa Rais wa milele. Wafuasi wa Museveni wanadai ni waganda ndiyo wanaweza kumwondoa madarakani kwa Kura. Upande wa upinzani waliweka pingamizi kuzuia mswaada huo usipite lakini idadi yao katika bunge ni ndogo, kiongozi wa wabunge wa upinzani Winne Kiiza amesikitishwa na kupitishwa mswaada huo. Lakini upande wa chama tawala ulitumia kila mbinu kuona kwamba mswaada huo unapita ili Rais Museveni kuendelea kutawala . Kupitishwa mswaada huo kunampatia tena Rais Museveni kutawala miaka mingine 14 kulingana na mswaada huo, lakini raia wa Uganda wengi walikuwa hawaungi mkono kubadilishwa kwa katiba kumuongeza Rais Museveni kutawala baada ya kutawala zaidi ya miongo mitatu. Wabunge wa Uganda wameyapitisha mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita. text: Wataalamu wa afya wanasema kujitoa uhai ni ugonjwa na siyo hatia. Kukabiliana na changamoto hiyo, jamii zinaombwa kushirikiana pamoja na kuzuia watu wengi kujiua. Takwimu zinaonyesha kwamba vifo vingi miongoni mwa vijana kati ya umri wa miaka 15- 29 vinasababishwa na kujitoa uhai. Sababu kuu ya watu kujitoa uhai imetajwa kama matatizo ya kiakili, kumpoteza mpendwa au kupata hasara ya aina moja au nyingine. Wataalamu wa afya wanasema kujitoa uhai ni ugonjwa na siyo hatia. Hii ni kwa sababu katika baadhi ya mataifa ya Afrika kujitoa uhai ni hatia kisheria. Hali hii pamoja na unyanyapaa unaowaandama wanaojaribu kujitoa uhai imewafanya wengi ambao ni wagonjwa kutotafuta matibabu. Roselyne Omondi kutoka Kenya ameambia BBC kwamba alijaribu kujiua mara nne. ''Nilikunywa dawa nyingi kwa mpigo nikitaka kulala milele kwenye mauti. Nilihisi kwamba nilikuwa mzigo kwa wazazi na wanangu ambao walikuwa wadogo.Nilikata tamaa ya maisha.Licha ya kuponea kifo mara ya kwanza, nilijaribu tena kujiua mara tatu.Mara ya mwisho nilijipata katika chumba cha wagonjwa mahututi,'' wakati huu wote hakuwahi kumuambia yeyote wakiwemo wanawe ambao kwa sasa ni watu wazima. ''Niliona aibu sana, sikutaka mtu hata mmoja kujua hali yangu. Nilihofia kuhukumiwa na watu ambao wangefahamu kwamba nilijaribu kujitoa uhai''. Jamii nyingi barani Afrika zinaendelea kuwalaani wale wanaojitoa uhai pamoja na kuzitenga familia zao. Wale wanaojaribu kujitoa uhai pia hawaepuki ghadhabu hiyo. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya akili watu wengi hawachukulii hali hiyo kama ugonjwa huku baadhi ya watu wakichukulia kama hatua ya kumkosea Mungu na kwamba ni dhambi kubwa. Wale wenye dhana hizi katika harakati ya kumtafutia matibabu muathiriwa huamua kumpeleka kwa viongozi wa kidini ili wapate kuombewa. Jamii pia huchukulia matatizo ya kiakili kama laana na jamaa ya muathiriwa hufanya kila juhudi kuficha ukweli kuhusu kile anachougua mpendwa wao. Nini kinachangia mtu kutaka kujiua? Wanasikololojia wamefanya utafiti na kugundua kuwa baadhi ya watu huchukulia wazo la kujitoa uhai kama kitendo cha kulipiza kisasi kwa mtu,yeye binafsi au kwa mtu mwingine. Mtu aliye na mawazo ya kujitoa uhai mara nyingi hutingwa na mawazo ya kujiona mkosaji. Kwa mfano huenda akajishutumu kwa kujisababishia maisha magumu pengine kwa kushindwa kukabiliana na changamoto zinazomkabili maishani. Kuna yule pengine anadaiwa na ameshindwa kulipa deni,hali ambayo imemfanya kushindwa kukidhi mahitaji ya familia na kutokana na hali hiyo anaishi kwa tabu. Kwa upande wa jamii mtu mwenye mawazo ya kutaka kujitoa uhai,anahisi kuwa yeye ndiye chanzo cha masaibu yanayomkabili,kwa mfano anaona aibu kwa kushindwa kufikia malengo ya maisha,hivyo basi hapendwi na watu na wala hawamjali. Hali hizi humfanya muathiriwa kupata msongo wa mawazo na hatimaye kujihisi mpweke. Jamii inaweza vipi kuzuia watu kujitoa uhai? -Kufahamu dalili ambazo zinaweza kumfanya mtu akajitoa uhai. -Kuwaonyesha upendo wale ambao wana matatizo ya akili. -Kuhamasisha wale ambao hawajaelewa kwamba huu ni ogonjwa na siyo laana, au hatia. -Kusitisha suala la unyanyapaa dhidi ya kujitoa uhai. Kando na unyanyapaa unaowakabili watu wanaojaribu kujitoa uhai changamoto nyingine ni sheria kali ambayo inawafanya wagonjwa kutotafuta matibabu. Hata hivyo Bi Omondi, ambaye amejaribu kujitoa uhai mara nne,anasema alipoanza kuzungumzia wazi wazi hali yake alipata faraja baada ya kuona kwamba si yeye peke yake aliyekuwa anakumbwa na tatizo hilo. Jamii ina jukumu la kumsaidia mtu aliye na mawazo ya kujitoa uhai kwa kumpeleka kwa mshauri ambaye atamsaidia kujieleza bila kuhijihisi kwamba ataeleweka visivyo. Nchi nyingi barani Afrika zinaharamisha jaribio la kujitoa uhai Wataalamu wa afya sasa wanasema wakati umewadia kwa mataifa kubadilisha sera dhidi ya kujitoa uhai. Dk Catherine Mutisya,daktari wa magonjwa ya akili nchini Kenya anasema,''Kenya ukijaribu kujiua utakuwa umevunja sheria na utashitakiwa.Utapitia mchakato mzima wa sheria hadi pale hakimu au jaji atakapoamua kwamba wewe unastahili matibabu.'' Dk Catherine pia anasema watu walioshtakiwa kwa madai ya kujaribu kujitoa uhai huwapewi matibabu kama wagonjwa wa kawaida bali hupelekwa huspitali kama wafungwa wenye matatizo ya kiakili. anasema ipo haja ya kufanyia marekebisho kifungu cha sheria inayoangazia afya ya akili ili kuondoa kipengele cha uhalifu katika sheria hiyo. Takwimu zinaonyesha kuwa nchi masikini na zile zinazoendelea hususan barani Afrika ndizo zilizo na idadi kubwa ya watu wanaojitoa uhai. Nchi hizo pia zinakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo uhaba wa vifaa na watalaamu wa kushughulikia watu wanaohitaji matibabu. Shirika la Afya Duniani (WHO) sasa linaonya kwamba kujitoa uhai ni changamoto ya dunia. text: Montagner alikuwa akirekodi kisa cha 'soap opera' iliyopewa jina Velho Chico Montagner alikufa maji mtoni eneo ambalo yeye na wahusika wengine walikuwa wakirekodi kisa kimoja cha filamu hiyo. Montagner aliigiza kama mhusika mkuu katika filamu hiyo ya Velho Chico, iliyopewa jina la mto huo wa Sao Francisco katika jimbo la Sergipe, kaskazini mashariki mwa nchini hiyo, ambapo alifariki. Mwigizaji huyo wa umri wa miaka 54 alikuwa ameenda kuogelea na mwigizaji mmoja wa kike baada ya kurekodi siku nzima mkasa huo ulipotokea. Mwigizaji mwenzake Camila Pitanga anasema Montagner alisombwa na mawimbi makali. Anasema alijaribu kuita wenyeji wafike kumsaidia lakini walichelewa kuchukua hatua kwani mwanzoni walidhani wawili hao walikuwa wanaigiza kisa cha mtu kufa maji mtoni. Kwenye filamu hiyo, Montagner aliigiza mkulima ambaye mara kwa mara alikabiliana na wavamizi wenye silaha. Katika moja ya kisa, alipigwa risasi mara kadha na kuonekana kuzama katika mto Sao Francisco, lakini akatokea wiki chache baadaye. Taarifa zinasema mtu mmoja mmoja hufa maji kila mwaka eneo hilo tangu 2005. Mtangazaji wa runinga Angelica Huck aliandika kwenye Instagram: "Siamini - alikuwa mwigizaji mzuri na mtu mwema pia." Saa nne baada ya kisa hicho, maafisa wa uokoaji waliupata mwili wa Montagner ndani ya maji, mita 300 (984ft) kutoka eneo ambalo alizama. Montagner alizaliwa Sao Paulo na alifanya kazi kama mwanasarakasi kabla ya kuwa mwigizaji wa televisheni mwaka 2008. Hii ilikuwa mara yake ya 12 kuigiza kama mwigizaji mkuu filamu ya runingani. Filamu yake ya kwanza ya televisheni ambayo alishiriki ilikuwa mwaka 2011, na aliigiza kwenye filamu za kawaida 2012. Montagner alikuwa amemuoa mwigizaji Luciana Lima kwa miaka 14 na kujaliwa watoto watatu. Filamu yake ya karibuni zaidi, Um Namorado Para Minha Mulher (Mpenzi wa Kiume wa Mke Wangu), ilizinduliwa wiki mbili zilizopita. Mmoja wa waigizaji nyota wa filamu za televisheni nchini Brazil, Domingos Montagner, amefariki akiigiza moja ya filamu mashuhuri sana za televisheni, ambazo hufahamika kama 'soap operas', nchini humo. text: Costa mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 14 na kusaidia kutengeza mabao 5 msimu huu Raia huyo wa Uhispania hajashiriki mazoezi kwa siku tatu na hajasafiri na viongozi hao wa ligi ili kushiriki mechi dhidi ya bingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Leicester. Habari hizo zinajiri huku kukiwa na ripoti kwamba anashirikishwa na uhamisho nchini China wenye thamani ya pauni milioni 30 kwa mwaka. Costa mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 14 na kusaidia kutengeza mabao 5 msimu huu. Chelsea hatahivyo imekataa kutoa tamko lolote. Inaeleweka kwamba mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich hataki kumwachilia katika kandarasi yake inayokamilika 2019, na hafurahii mpango wa kushinikizwa kufanya hivyo. Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amewachwa nje katika kikosi cha Chelsea dhidi ya Leicester baada ya mgogoro na kocha kuhusu uzima wake. text: 62.4% ya watu wa Escobares, katika jimbo la Texas ni masikini Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku. "Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu," anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani. Débora Hernández,mkaazi wa Escobares. Bi. Debora hajui kusoma na kuandika, anasema alijifungua watoto saba lakini ni mmoja kati yao aliyebakie wengine wote wamefariki. Alipoulizwa nini kilichosababisha vifo vyao alisema "Sijui, na wala sikuambiwa kilichowasibu". Alipokuwa mdogo alipelekwa katika shule ya wanafunzi wanaohitaji huduma maalum. Japo alikamilisha masomo ya msingi hakujifunza lolote. Licha ya hayo yote Debora amekuwa akiishi na mume wake ambaye hana kazi kwa miaka mitatu sasa. Paa la nyumba yao linavuja kukinyesha na hali yao ya maisha kwa jumla inamfanya mtu kujiuliza ikiwa siku moja mabo yatabadilika. "Inabidi utoke hapa kila siku kutafuta kibarua vinginevyo utalala njaa" Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha. "Wale waliyo na stakabadhi zinazohitajika, wanafanya kazi katika eneo la kaskazini," anasema Homero Rosales. Homero Rosales, mkaazi wa Escobares "Cha kusikitisha ni kuwa lazima utengane na familia yako kwa miezi kadhaakwenda kutafuta ajira la sivyo wapendwa wako watakufa kwa njaa." Homero ambaye ni baba wa watoto wanne anafanya kazi ya kujenga mabomba ya mafuta katika mji wa Pecos uliyopo Texas magharibi. "Mwanangu mkubwa alilazimika kuacha shule ili kufanya kazi na mimi". Wale ambao hawafanyi kazi ya ujezi wa mabomba ya mafuta wanafanya vibarua katika miji mingine au wanategea msaada wa serikali kwa jamii kununua chakula. "Watu wanaoishi maeneo ya kusini mwa Marekani wanakabiliwa na viwango vya juu vya umasikini,"Rakesh Kochhar, mtafiti katika kituo cha utafiti cha Pew mjini Washington, aliiambia BBC. Kituo hicho kinasema kiwango cha umasikini nchini Marekani kimefikia 12.3%, na takriban watu milioni 40 wameathiriwa. 12.3% ya watu nchini Marekani ni masikini hii inamaanisha takriban watu milioni 40 hawana uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya msingi Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya "Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,"anasema mtafiti, Rakesh Kochhar. Miaka 13 iliyopita mji wa Escobares haukuwepo lakini mwaka 2005 ulitambuliwa kuwa moja ya miji nchini Marekani, kabla ya hapo watu waliyoishi sehemu hiyo hawakua chini ya mamlaka yoyote ya mji. Baada ya Marekani kusikia kuwa mji wa karibu unaofahamika kama Rome ulikuwa na mpango wa kunyakuwa sehemu ya mji wa Escobares mambo yalibadilika. Nyumba za trela ni maarufu sana mjini Escobares 98% ya watu wanaoishi Escobares wanatokea taifa jirani Mexico Baadhi yao walizaliwa mjini humo na wengine wamepewa urai wa Marekani lakini kuna wale ambao hawana "stakabdhi rasmi" waliyotoroka mauaji na utekaji nyara katika jimbo la Tamaulipas.Ukiwa mgeni katika mji wa Escobares ni vigumu kubaini kuwa ni moja ya miji masikini nchini Marekani. Hakuna visa vya watu kuishi mitaani kama vile vinavyoshuhudiwa mjini Los Angeles, au kukutana na watu wanaoishi katika hali ngumu kutokana na ubaguzi wa rangi katika miji ya Detroit na Baltimore. Lakini watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Mji wa Escobares katika mpaka Mexico na Marekani haujawahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani lakini wakaazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku. text: Hydroxicloroquine ni dawa ya gharama ya chini abayo imetumika kutibu magonjwa kama vile ya malaria Rais huyo anaamini kwamba dawa hii inaweza kuleta tofauti kubwa duniani katika vita dhidi ya virusi vipya vya ugonjwa wa covid-19 katika mwili wa mwanadamu. ''Inaonekana kuwa na matumaini baada ya kutoa matokeo mazuri. Na tutahakikisha kwamba dawa hiyo inapatikana kila mahali mara moja'', alisema katika mkutano na vyombo vya habari wiki iliopita. ''Nafikiria huenda ikaleta manufaa na pengine hata kushindwa lakini nadhani inaweza., kutokana na kile ninachoona inaweza kubadilisha mambo''. ''Dawa hiyo ina uwezo mkubwa , ina uwezo mkubwa'' , aliongezea. Ijumaa iliopita alisisitiza uwezo wake na kusema kwamba idara ya chakula na dawa ilikuwa ikiifanyia majaribio. Na siku ya Jumamosi alisisitiza kupitia mtandao wake wa Twitter ' Hydroxychloroquine na azithromycin zikitumika kwa pamoja zinaweza kuleta mafanikio makubwa katika historia ya tiba. Idara ya chakula na dawa FDA imefanya kitu muhimu na natumai zote mbili zitaanza kutumika mara moja. Watu wanafariki , harakisheni na Mungu ambariki kila mmoja, aliandika. Rais huyo alisema kwamba, tayari dawa hiyo imeidhinishwa na Idara hiyo ya chakula na dawa na kwamba kwa kuwa ni maarufu inaweza kutengenezwa kwa urahisi. Hatahivyo idara hiyo ya chakula ilitoa taarifa ambapo ilisema kwamba dawa hiyo inafanyiwa majaribio katika maabara hivyo basi matumizi dhidi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona hayajaruhusiwa. Dawa hiyo imetumika kwa miongo kadhaa katika tiba ya ugonjwa wa malaria. Rais Trump amekuwa na matumaini makubwa ya matumizi ya ya dawa ya hydroxychloroquine kutibu cirusi vya corona Idara ya dawa nchini Marekani FDA inaamini kwamba ijapokuwa dawa hiyo ina uwezo mkubwa dhidi ya virusi vipya , ni lazima ifanyiwe majaribio ili kubaini iwapo ndio dawa inayoweza kukabiliana na virusi hivyo ambavyo tayari vimesababisha zaidi ya vifo 10,000 duniani. ''Ni dawa ambayo rais huyo ametaka kuiangazia kwa karibu ili kuona iwapo matumizi yake yanaweza kupanuka na iwapo itawasaidia wagonjwa'', alisema kamishna wa FDA Stephen Hahn. Na wametoa wito wa dawa hiyo kutotumika bila ushauri wa mtaalam kwa kuwa tayari imeripotiwa kwamba baadhi ya waliotumia walitumia kiwango cha juu. Mtu mmoja alifariki tarehe 23 mwezi Machi baada ya kutumia dawa inayotumiwa kutibu vidimbwi vya maji ambayo imechanganywa na chloroquine phosphate, na ina viungo vya dawa ya hydroxychloroquine. Visa vingine vya watu kutumia dawa hiyo kwa kiwango cha juu pia vimeripotiwa nchini Nigeria. Je, hydroxychloroquine ni nini? Hydroxychloroquine ni dawa ya kulinda kinga ambayo imetumika kwa miongo kadhaa katika kutibu malaria, hatua inayoifanya kujulikana kama dawa ya kukabiliana na malaria. Pia inatumika kutibu yabisi. Huitwa kwa kiungo chake cha chloroquine , licha ya kwamba dawa zote mbili zina kemikali na matumizi ya kimatibabu ambayo hayafanani kabisa. Hydroxychloroquine hupatiwa wagonjwa kupitia ushauri wa madaktari Pia hutumiwa kutibu erythematosus na arheumatoid kwa wagonjwa ambao hawajaimarishwa na matibabu mengine. Matumizi yake ni ya kutumia mdomo na inadhibitiwa na maagizo yaliyotolewa na madaktari. "Kwa sababu imetumika kwa muda mrefu, usalama wake na wasifu wake unajulikana, tayari imeidhinishwa na FDA na EMA (Shirika la Dawa la Ulaya)," anasema Morse. Walakini, matumizi ya chloroquine na hydroxychloroquine pia yana athari mbaya kwa wagonjwa wengine. Hii ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuhisi kisunzi , kupoteza hamu ya kula, kuharisha ,kutapika, na kuwa na upele katika ngozi. China ilianzisha utengenezaji wa dawa ya chloroquine baada ya kipindi cha miaka 15 Je, inaweza kutibu Virusi vya corona? Daktari George Rutherford, na profesa katika chuo kikuu cha California , San Francisco anaelezea BBC kwamba ijapokuwa dawa hiyo ina uwezo wa kutibu magonjwa kama vile Covid 19 ulimwengu unafaa kusubiri kupata matokeo muafaka. "Unapoifanyia majaribio dhidi ya virusi vya corona huzuia virusi hivyo kutoingia katika seli na kusababisha metaboliki mwilini hatua inayozuia uwezo wa virusi hivyo kuongezeka'' , anasema. Hatahivyo anasema kwamba inapofanya kazi dhidi ya malaria haimaanishi kwamba inaweza kufanya kazi dhidi ya Covid-19 . Na kwamba hata ijapokuwa inafanya kazi vizuri katika majaribio haimaanishi kwamba itafanikiwa katika mwili wa mwanadamu, anaongezea. Mtaalamu huyo anasema kwamba dawa hiyo inafaa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kuelewa jinsi inavyoweza kufanya kazi vyema hatua inayoweza kuchukua kati ya mwezi mmoja hadi mwaka mmoja. Ripoti kutoka gazeti la The New York Times na Washington Post zinasema kwamba dawa hiyo imefanyiwa majaribio miongoni mwa wagonjwa nchini Marekani huku chombo cha habari cha Xinhua kikiripoti kwamba imetumika katika hospitali kumi mjini Beijing na mikoa mingine miwili. Swali la kujibiwa ni kwamba ni katika hatua gani ya ugonjwa huo ambapo mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi vya corona anaweza kusaidika? Kwa kuwa athari yake haiwezi kuwa sawa mwanzoni katikati ama katika hatua za mwisho. Morse hatahivyo anasema kwamba WHO haijaidhinisha matumizi ya hydroxychloroquine na chloroquine kama tiba ya virusi vya corona. Utafiti unaweza kuchukua muda wa kati ya mwezi mmoja hadi mwaka ikitegemea idadi ya wagonja wanaofanyiwa vipimo Jina lake ambalo ni gumu kulitamka limekuwepo katika kinywa cha rais Trump, mara kwa mara rais huyo wa Marekani alitaja dawa aina ya hydroxychloroquine. text: Bintu Bitrus, Mama wa Godiya, binti aliyetekwa nyara akisali na wazazi wengine Wazazi wa wasichana wanahofu kuwa kuna nguvu isiyoonekana kwa macho, zaidi ya Boko Haram ambayo imekua chanzo cha masumbufu waliyoyapitia katika kipindi cha miaka mitano tangu watoto wao walipochukuliwa shuleni Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Zaidi ya wasichana 200 walitekwa wakiwa kwenye mabweni tarehe 14 mwezi Aprili mwaka 2014, 107 wakiwa wameokolewa au kuwekwa huru baada ya mazungumzo na Serikali ya Nigeria na wanamgambo wa kiislamu huku wengine zaidi ya 100 wakiwa hawajulikani walipo. ''Kuna kitu kinatufuata kwa namna moja au nyingine,'' anaeleza Yakubu Nkeki, Mwenyekiti wa Umoja wa wazazi wa watoto waliotekwa nyara na ambaye mpwawe alikua miongoni mwa kundi la mwisho la wasichana walioachiwa mwezi Mei mwaka 2017. Boko Haram wameshindwa? Mfahamu rais wa Nigeria Muhammadu Buhari Mwezi Aprili mwaka jana, wazazi wa baadhi ya wasichana walioachiwa huru ghafla walipata ajali.Walikua wakisafiri pamoja wakielekea mkutanoni katika Chuo Kikuu mjini Yola ambako mabinti zao walidahiliwa kwenye masomo ambayo yalifadhiliwa na Serikali.Mzazi mmoja alipoteza maisha papo hapo huku wengine 17 wakipelekwa hospitali kutokana na majeraha waliyoyapata. Mwezi Januari mwaka huu, ndugu 18 wa wasichana ambao bado hawajulikani walipo, ambao wanafadhiliwa na kituo cha msaada, walikua wakirejea shuleni wakati chombo cha moto walichokuwa wamekodi kupata ajali. Wanane kati yao walipata majeraha, pia aliyejeruhiwa vibaya Zannah Lawan, Katibu wa umoja wa wazazi, aliyekuwa akiwasindikiza wanafunzi shuleni. Kukua kwa chuki Majuma kadhaa baadae, mwezi Machi, watoto waliokuwa wamejeruhiwa walikua tayari kurudi kwenye masomo yao.Bwana Nkeki aliongozana nao kwenda shule, akawashusha na kuwarejesha nyumbani.Gari alilokodi ambalo alikua akisafiri nalo likapata ajali. ''Gari ilipinduka lakini sikujeruhiwa,'' alisema, lakini akaongeza, ''Mambo haya si ya kawaida.'' Rifkatu Galang, alitekwa akiwa na miaka 17, bado hajapatikana Wanachama wa umoja wa wazazi 34 wamepoteza maisha baada ya mabinti zao kutekwa nyara na sasa, kutokana na ajali, maradhi, na zaidi mashambulizi ya Boko Haram. Bwana Nkeki pia ana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa chuki miongoni mwa jumuia ya wazazi.Mikutano imekua ikimalizika kwa malumbano, wazazi wakijaribu kupigana wenyewe kwa wenyewe. Mwaka jana, baadhi ya wazazi wa watoto waliopotea walitishia kuzuia msafara wa mabasi unaowachukua watoto walioachiwa huru kupelekwa Yola, baada ya mapumziko ya majira ya joto.Walikua wakihisi kuwa kuachiwa kwa baadhi ya wasichana na kurudi kwao shuleni kumefanya umakini wa kuwafikiria wengine ambao bado wanashikiliwa umeondoka kabisa. ''Sipendi kuwaalika wote kwa wakati mmoja kwenye mikutano,'' Alisema bwana Nkeki. ''Wakati mwingine nachagua watu wachache ambao husikilizana vizuri na kupeleka ujumbe kwa wengine.'' Wakati huohuo, tishio la Boko Haram ni tukio la kweli kwa watu wa Chibok-ambapo mchanganyiko wa watu wa imani ya kikristo na kiislamu wanaishi.Pamoja na mafanikio ya jeshi kudhibiti eneo hilo kutoka mikononi mwa wanamgambo. Majuma kadhaa yaliyopita, Boko Haram walifanya uharibifu katika vijiji saba wakiharibu makazi yakiwemo ya watu ambao watoto wao waliachiwa huru na kuendelea na masomo katika chuo kikuu cha Yola. Baadhi ya walioachiwa wanasoma chuo kikuu cha Amerika huko Yola ''Kinachoendelea Chibok ni kibaya sana,'' alisema Nkeki.''Watu wengi hawako majumbani mwao.'' Wazazi wa Chibok wanatazama kutekwa kwa watoto wao ni moja ya mfululizo wa matukio ya bahati mbaya kukumba watu na jamii yao. Kutafuta miujiza Katika kumbukumbu ya miaka mitano ya vitendo vya kutekwa nyara kwa wasichana, ambavyo viliishitua dunia na kuanzisha kampeni ya #BringBackOurGirls sasa wazazi wanaomba msaada wa kiimani. Mchungaji TB Joshua Mwanzoni mwa mwezi huu, wawakilishi wa jumuia ya wazazi walisafiri zaidi ya saa 48 kwa barabara kutoka Chibok kwenda Lagos kukutana na mchungaji maarufu TB Joshua. Ni mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi, Kanisa la mataifa yote (SCOAN), Muhubiri mashuhuri nchini Nigeria. Maelfu ya watu hufika makao makuu ya kanisa hilo kutoka ulimwenguni kote kufuata miujiza na kushuhudia shuhuda mbalimbali. ''Sababu ilifanya twende kumuona tumeona nguvu ya wizara ya wanawake, serikali ya Nigeria na watu wengine wengi, mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kuhusu wasichana,'' alisema Yana Galang, mmoja kati ya wazazi 12 waliofika katika kanisa la SCOAN na ambaye binti yake Rifkatu anashikiliwa mpaka sasa. ''Hakuna anyetuambia habari zozote kuhusu wasichana.Ndio maana tumefika kukabidhi jambo hili kwa Mungu.'' Wasichana walichukuliwa kutoka shule ya bweni ya Dapchi, jimbo la Yobe, Mwezi Februari Miongoni mwa waliokuwa kwenye safari ni mlezi wa Leah Sharibu, binti wa miaka 14 ambaye mwezi februari mwaka 2018 alichukuliwa na wanamgambo akiwa na wasichana wengine zaidi ya 100 kutoka kwenye shule nyingine-hii Kaskazini -Mashariki mji wa Dapchi. Baadhi ya wasichana wa Dapchi walipoteza maisha wakiwa kwenye safari na Boko Haram wengine wakirejeshwa mwezi mmoja baadae baada ya mazungumzo kati ya Boko Haram na Serikali ya Nigeria.Lakini Leah alibaki nyuma kwa kuwa alikataa kubadili dini. Pamoja na ahadi ya Serikali kuhusu kuachiwa kwake, alitumia kumbukumbu yake ya miaka 15 ya kuzaliwa akiwa ameshikiliwa.Wazazi wake wote wako na hali mbaya kiafya, hivyo walimtuma ndugu yao wa karibu awawakilishe wanapokutana na TB Joshua. Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari, Garba Shehu amesema jitihada zinaendelea kuhakikisha wasichana waliobaki wanaachiwa. Katika mfululizo wa barua kutoka kwa waandishi wa kiafrika, Mwandishi wa Nigeria Adaobi Tricia Nwaubani anasema wazazi wa wasichana wa Chibok waliopotea, wamekosa matumaini ikiwa ni miaka mitano baada ya mabinti zao kutekwa nyara. text: Jo Cameron hahisi maumivu Yeye ni mtu wa pili duniani kuwa na hali hii ya mabadiliko ya kijenetiki ambayo hutokea kwa nadra sana. Ina maanisha kuwa Jo Cameron huwa hahisi maumivu kabisa, hana wasiwasi wala huwa hapati hofu. Hali ilikua hivyo mpaka alipotimiza miaka 65, ndipo alipogundua kuwa yuko tofauti-pale madaktari waliposhindwa kuamini kuwa hahitaji dawa za kuondoa maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa. Kwa nini wasichana huchomwa moto matiti yao Afrika magharibi Papa kutibu binadamu saratani na 'uzee' Alipofanyiwa upasuaji kwenye mkono wake, madaktari walimtahadharisha kuwa ategemee kupata maumivu baada ya upasuaji. lakini bi Cameron hakuhisi maumivu yeyote, Daktari wake wa dawa za usingizi Devjit Srivastava alimpeleka kwa wataalamu wa masuala ya maumbile na jenetiki katika chuo cha London na Oxford. Baada ya vipimo, walibaini kuwa ana mabadiliko kwenye vinasaba vyake vinavyomfanya asihisi maumivu kama ilivyo kwa watu wengi. 'Hii si hali ya kawaida' Jo aliiambia BBC kwa madakrari hawakumuamini alipowaambia hahitaji dawa ya kuondoa maumivu baada ya upasuaji. Alisema:''Tulizungumza kabla ya kwenda kwenye chumba cha upasuaji na nikawahakikishia kuwa sitahitaji dawa za kuondoa maumivu. ''Alipogundua kuwa sikuwahi kumeza dawa za maumivu, alitazama historia yangu ya kitabibu na kugundua kuwa sikuwahi kutumia dawa za kuondoa maumivu.'' Ndio sababu hata akapelekwa kwa wataalamu nchini Uingereza. Jo,akiwa na mume wake na mama yake. Ilipobainika, Jo alijua kwamba kumbe hakuwa na'' afya njema'' sana kama ailivyokua akiamini. Alisema:''Nikikumbuka huko nyuma, nikagundua sikuwahi kuhitaji dawa za kuondoa maumivu,lakini kama huzihitaji huwezi kuhoji kwa nini huhitaji. ''Wewe ni wewe ulivyo mpaka pale mtu mwingine atakapobaini vinginevyo.Nilikua mwenye furaha ambaye sikubaini kama kuna tofauti yoyote mwilini mwangu.'' Hakuwahi kupata maumivu hata wakati anajifungua, akikumbuka:''halikua jambo la kawaida, lakini sikuwa na maumivu. kwa kweli niliifurahia hali hii.'' Jeni zenye kuleta furaha Madaktari waliamini kuwa Jo atakua na uwezo wa kupona haraka sana kuliko kawaida.Jeni zake pia zinamfanya asahau na asiwe mwenye hofu ''Inaitwa jeni zenye kuleta furaha au zinazosahau.Nimekuwa nikiwaudhi wengine kwa kuwa na furaha na mwenye kusahau maisha yangu yote-Nina sababu sasa,'' alieleza. Jo alisema hivi karibuni alikua na uvimbe mdogo baada ya kujigonga akiwa kwenye gari, lakini hali hiyo ambayo wengi wangeiona mbaya sana, haimkumshtua hata kidogo. ''Sina adrenalini.Lazima uwe nayo ili iweze kukupa tahadhari kuhusu hali ulionayo, ni sehemu ya hali ya kuwa binaadamu,lakini siwezi kubadili hali hii.'' Dereva mwingine, alisema, ''Alikua akitetemeka kwelikweli'',lakini aliweza kutulia baadae.''Mimi hali hii hainitokei...si kuwa mimi ni mwerevu, ni kwamba hali ya hofu haijitokezi.'' Watafiti wanasema inawezekana kuna watu wengine kama Jo. ''Mmoja kati ya wagonjwa wawili baada ya upasuaji hupata maumivu kidogo au maumivu makali, pamoja na kuwepo kwa uboreshwaji wa dawa za kuondoa maumivu. alisema Dokta Srivastava. Aliyoyapitia Jo yamo kwenye maandiko ya utafiti wa British Journal of Anaesthesia, ulioandikwa na Dokta Srivastava na Dokta James Cox Jo Cameron aligundua kuwa ngozi yake inaungua mpaka anaponusa harufu ya kuungua kwa ngozi yake.Mara nyingi mikono yake huungua kwenye jiko la kuokea, lakini hahisi maumivu ya kumpa tahadhari kuwa yuko hatarini. text: Utafiti huo uliofanywa na Chuo cha Imperial cha London na Shirika la Afya Duniani uliangazia umri wa kuishi katika mataifa 35 yaliyostawi kiviwanda. Utafiti huo unaonesha watu watakuwa wakishi miaka mingi kuliko sasa kufikia mwaka 2030 na pengo kati ya wanaume na wanawake litaanza kufutika katika mataifa mengi. Watafiti hao wanasema matokeo ya utafiti wao ni changamoto kwa hazina za malipo ya uzeeni na vituo vinavyowatunza wazee. "Korea Kusini imefanya mambo mengi kwa njia ifaayo," Prof Majid Ezzati aliambia BBC. "Wanaonekana kuwa na mazingira yenye usawa na mambo yao mengi yamewafaa watu kwa juma - elimu, lishe - watu wengi wamenufaika. "Na kufikia sasa, wanafanya vyema katika kukabiliana na shinikizo la damu na wana viwango vya chini zaidi vya unene duniani." Takwimu hizo pia zinakadiria kwamba Japan, ambayo zamani ilifahamika kwa raia wake kuishi maisha marefu, inaendelea kushuka. Kwa sasa, ina kiwango cha juu zaidi cha umri ambao wanawake huishi, lakini itapitwa hivi karibuni na KOrea Kusini na Ufaransa, utafiti huo unadokeza. Umri wa wanaume kuishi Japan nao utashuka kutoka kuwa wa nne miongoni mwa nchi zilizochunguzwa hadi nambari 11. Marekani yabaki nyuma Marekani pia haijafanya vyema kwa mujibu wa utafiti huo na huenda ikawa na kiwango cha chini zaidi cha umri wa kuishi miongoni mwa mataifa tajiri kufikia 2030. Utafiti huo unabashiri kwamba kiwango cha wastani cha umri wa wanaume kuishi Marekani kitakuwa miaka 80 kwa wanaume na 83 kwa wanawake, karibu sawa na Mexico na Croatia wakati huo. Marekani pia itakuwa imepitwa na Chile, ambapo wanawake watakaozaliwa 2030 watatarajia kuishi miaka 87 na wanaume 81. Kati ya 2015 na 2030, umri wa kuishi Uingereza utapanda kutoka 79 hadi 82 kwa wanaume na 83 hadi 85 kwa wanawake. Wanaume wanapanda Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la Lancet, unaonesha pengo kati ya umri wa kuishi kati ya wanawake na wanaume linapungua. Prof Ezzati alisema: "Wanaume kawaida waliishi maisha yasiyo ya afya, na hawaishi muda mrefu ukilinganisha na wanawake. Walikunywa pombe na kuvuta sigara zaidi, na waliuawa sana nyumbani au kufa kwenye ajali barabarani. Hata hivyo, mtindo wa maisha kati ya wanaume na wanawake sasa unakaribia kufanana. Hivyo, umri wa wanaume kuishi unaonekana kuongezeka." Wanawake nchini Korea Kusini watakuwa wa kwanza duniani kuwa na umri wa kuishi wa zaidi ya miaka 90, utafiti unaonesha. text: Waziri wa ulinzi Mark Esper aliambia wanahabari kwamba wanajeshi hao wataelekea katika taifa hilo ili kuimarisha ulinzi . Hatahaivyo idadi yao bado haijajulikana. Waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema kwamba walihusika na mashambulizi ya visima viwili vya mafuta wiki iliopita. Lakini Saudia na Marekani zimelaumu Iran kwa mashambulizi hayo. Siku ya Ijumaa , rais Trump alitangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran huku akisema kwamba alipendelea kuzuia mgogoro wa kijeshi. Vikwazo hivyo vipya ambavyo rais Trump alivitaja kuwa vya kiwango cha juu vitalenga benki ya Iran na mali yake iliopo ugenini. ''Nadhani kujizuia ni muhimu'' , aliambia afisi ya White House. Lakini siku ya Jumamosi. Kamanda wa jeshi la Iran Revolutionary Guard IRGC alisema kwamba taifa hilo litamuangamiza mchokozi yeyote. ''Tahadharini '', alisema Meja Jenerali Hossein Salami katika runinga ya taifa hilo. ''Tuko tayari kumuadhibu mtu na tutaendelea hadi kuwaangamiza wachokozi''. Je Pentagon imesemaje? Saudi Arabia imesema kwamba UAE iliomba msaada, kulingana na bwana Esper. Amesema kwamba vikosi vya Marekani vitaangazia kupiga jeki wanajeshi wake wa angani mbali na kujilinda dhidi ya silaha za angani na kwamba itapeleka silaha kwa nchi zote mbili. Waziri wa ulinzi wa marekani Mark Esper, left, na mkuu wa majeshi ya Marekani Joseph Dunford walitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa Mwenyekiti wa wanajeshi jenerali Joseph Dunford aliunga mkono upelekeji wa wanajeshi hao akidai kwamba hatasema idadi yao. hatahivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu aina ya vikosi hivyo vitakavyotumwa. Kulingana na gazeti la New York Times , wakati maripota walipomuuliza bwana Esper iwapo mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran yalikuwa yanapatiwa kipau mbele alijibu: Kwa sasa hatujafikia uamuzi huo. Je ni nini kilichotokea Saudia Mashambulio yaligonga visima vya mafuta vya Abqaiq na kile cha Khurais nchini Saudia wiki moja iliopita na kuathiri usambazaji wa mafuta duniani. Siku ya Jumatano , wizara ya ulinzi ya ufalme huo ilionyesha mabaki ya ndege zisizo na rubani na silaha ikithibitisha kwamba Iran ndio iliohusika. ''Taifa hilo lilikuwa linafanya uchunguzi kujua ni wapi mashambulio hayo yalitekelezwa'', alisema msemaji. Marekani pia imesema kwamba Iran ndio iliohusika . Maafisa waandamizi wameambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba wana ushahidi kwamba mshambulizi hayo yalitekelezwa kusini mwa Iran. Iran imekana kuhusika katika mashambulio hayo , huku rais Hassan Rouhani akiyataja kuwa kisasi cha raia wa Yemen. Marekani haiamini kwamba waathiriwa wa vita vya Yemen vya miaka 4 na nusu hawawezi kutekeleza mashambulio kama hayo. Siku ya Jumatano waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani aliyataja mashambulio hayo kama kitendo cha vita. Bwana Zarif alionya katika mtandao wake wa Twitter kwamba ''Iran haipendi vita lakini hatutasita kujilinda''. Wakati huohuo kampuni ya mafuta ya Saudia , Aramco imesema kwamba inatarajia kiwango cha mafuta kurudi kufikia kiwango cha kabla ya shambulio kufikia mwezi Septemba. Marekani kuzipa mwanya wa ulinzi wa Saudia Na mchanganuzi Frank Gardner. Mshamabulizi kadhaa ya ndege za rubani dhidi ya hifadhi za mafuta za Saudia yameonyesha uwezo wa Saudia kiulinzi. Kwa sasa Marekani ambayo ndio mshirika wake wa kimkakati imejitolea kuziba mwanya. Meli ya kijeshi ya Marekani The Destroyer imeegeshwa kaskazini mwa Ghuba ili kuzuia makombora yanayotoka upande huo. The Pentagon pia imetangaza upelekaji wa vikosi zaidi Saudia ili kusaidia kuimarisha ulinzi wake dhidi ya makombora. Vifaa zaidi ya kujilinda vinatumwa kote Saudia na UAE kufuatia hali ya wasiwasi na jirani yao Iran. Lakini kuwepo kwa kambi za vikosi vya Marekani Saudia kumezua utata katka siku za nyuma. Licha ya kwamba vilialikwa na mfalme wa Saudia, uwepo wao ulitumika na Osama bin Laden kuwavutia wapiganaji wa kijihadi kupinga kile alichokitaja kuwa uvamizi wa rasi ya Arabuni. Ni nini chanzo cha yote hayo? Waasi wa Houthi mara kwa mara wamerusha makombora na ndege zisizo na rubani katika maeneo yanayokaliwa na raia nchini Saudia. Wanapigana dhidi ya vikosi vya muungano wa Saudia ambavyo vinamuunga mkono rais ambaye waasi hao walimtimua wakati mgogoro huo wa Yemen ulipochacha mnamo mwezi Machi 2025. Iran ndio mpinzani wa Saudia na ndio mpinzani mkuuu wa Marekani ambayo iijiondoa katika makubaliano ya kinyuklia ya Iran baada ya Trump kuchukua mamlaka. Wasiwasi kati ya Marekani na Iran umezidi mwaka huu. Marekani ilisema kwamba Iran ilihusika na mashambulio ya meli mbili za mafuta katika Ghuba mwezi juni na Julai , pamoja na meli nyengine nne mwezi Mei. Tehran ilipinga madai hayo katika visa vyote viwili. Marekani imetangaza mipango ya kutuma vikosi vya kijeshi nchini Saudia kufuatia mashambulizi dhidi ya hifadhi za mafuta za taifa hilo. Marekani kutuma wanajeshi Saudia text: Caster Semenya alishinda nishani ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki mjini Londo 2012 Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 28 hawezi kushiriki katika mbio za mita 800 bila kutumia dawa za kupunguza homoni za kiume mwilini mwake sheria mpya ilioidhinishwa na shirika la riadha duniani IAAF. Hatua hiyo inamaanisha kwamba hawezi kutetea ubingwa wake wa mita 800 mjini Doha mwezi ujao - ijapokuwa bado anapigania kubadilishwa kwa sheria hiyo kupitia mahakama. Kwa sasa amejiunga na klabu ya soka ya wanawake iliopo Gauteng kwa jina JVW. Bingwa huyo mara tatu ambaye alitangaza mwezi Julai kwamba hatotetea ubingwa wake katika mbio za mita 800 kwa kuwa hawezi kuanza kuichezea JVW hadi msimu wa 2020, baada ya kujiunga na timu hiyo nje dirisha la uhamisho. ''Ninatazama kuanza safari mpya , nashukuru mapenzi na uungwaji mkono niliopata kutoka kwa timu hii'', Semeya aliambia mtandao wa klabu hiyo. JVW FC, ilibuniwa 2013 na nahodha wa timu ya taifa ya wanawake nchini Afrika Kusini Janine van Wyk, akitaka kuwatambua, kuwaimarisha na kuwafichua wachezaji wa kike. Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu kubwa katika ligi katika mkoa wa Gauteng - ligi kuu ya wanawake nchini Afrika Kusini imegawanyika katika makundi manane ya kimkoa. Mmiliki wa klabu hiyo van Wyk aliambia BBC kwamba Semenya hajawacha kukimbia. Alisema: Yuko katika mapumziko kwa wakati huu ndio maana ana muda wa kufanya kitu tofauti. Ameshiriki mazoezi mara mbili na timu hii na unaweza kuona kwamba anajua kucheza soka lakini bado ni sharti kumsaidia kidogo kwa kuwa uchezaji ni tofauti na riadha. Kumuona katika ligi hii ni jambo jema na nadhani wasichana wadogo watapata msukumo mkubwa kutoka kwa Caster. Semenya sio mwanariadha wa kwanza kujiunga na kandanda - baada ya kustaafu 2017 , Usain Bolt alifanya mazoezi na klabu moja ya Norway Stromsgodset na nyengine ya Australia Central Coast Mariners, lakini hakupata kandarasi. Semenya pia anafuata nyayo za Maria Mutola wa Zambia ambaye alijiunga na kandanda baada ya riadha. IAAF iliamua kuweka sheria hiyo kwa madai kwamba wanariadha wanawake walio na homoni nyingi za kiume wana uwezo zaidi ya wenzao wa kike. Wanariadha hao wametakiwa kutumia dawa ili kupunguza viwango vya homoni hizo ili kuweza kushiriki katika mita 400 hadi 1500 la sivyo waingie katika mbio nyengine ndefu. Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mbio za mia 800 Caster Semenya amejiunga na timu ya soka ya wanawake nchini Afrika Kusini. text: Kikao cha Rais Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kati) na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba pamoja na wafanyabiashara Septemba 28 kilitazamiwa kumaliza sakata la ununuzi Siku 11 zilizopita, Rais wa Tanzania John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikutana na wanunuzi wa zao hilo baada ya kutokea mgomo wa wakulima kuuza korosho zao kwa wanunuzi hao. Mwaka jana zao hilo liliuzwa kwa wastani wa Shilingi za Tanzania 4,000 kwa kilo lakini mwaka huu bei ikaporomoka mpaka wastani wa Sh1,900 mpaka Sh2,700 kwa kilo. Mgomo wa wakulima hao uliungwa mkono na Serikali ambapo tarehe 28 Septemba kwenye kikao baina yao na Magufuli na Majaliwa wafanyabiashara hao walikubali kununua zao hilo kwa bei isiyopungua Sh3,000 kwa kilo. Serikali pia ilikubali kwa upande wake kuondosha baadhi ya tozo na vikwazo vilivyopelekea wafanyabiashara kushusha bei. Hata hivyo, wafanyabiashara hao wanaounda kampuni 35 wanaripotiwa kutonunua korosho hiyo kama ilivyotarajiwa na hali hiyo imechukuliwa na serikali kama mgomo baridi. Leo hii Waziri Mkuu Majaliwa amekuja na onyo la mwisho; waseme ndani ya siku nne zijazo watanuanua tani ngapi na lini ama wafutiwe leseni zao za biashara. Kwanini hekalu la shetani linawashtaki waliounda sanamu ya Sabrina "Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale wote ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidodo, wahakikishe ndani ya siku hizo nne kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24," amesema Majaliwa. "Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua wakionesha kiwango wanachokihitaji. Zaidi ya hapo serikali haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena." Katika kikao cha Septemba 28, Rais Magufuli alinda mbali kwa kuwaambia wafanyabiashara hao kuwa serikali yake ipo radhi kuzinunua korosho zote kwa bei inayowafaa wakulima na kuziuza katika masoko ya kimataifa nchini Marekani na Uchina. Rais Magufuli amesema yupo tayari kutumia jeshi kununua korosho kwa bei ambayo inakubalika na wakulima. "…nipo tayari hata kutumia majeshi yetu kununua korosho na tutatafuta masoko ya uhakika ili tuuze kwa bei nzuri" amesisitiza Rais Magufuli. Jana Alhamisi Majaliwa alitangaza bungeni kuwa serikali pia inajadiliana na wanunuzi kutoka nje ya nchi ili kuwavutia kununua zo hilo ambalo ndilo mhimili mkuu wa kiuchumi kwa wakaazi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania. Wafanyabiashara wa korosho wakimsikiliza Rais Magufuli Septemba 28 Mapema mwezi Mwezi Juni mwaka huu kulikuwa na mnyukano bungeni ambapo wabunge bila kujali tofauti zao za kisiasa walikuwa wakiyapinga mapendekezo ya serikali katika Sheria ya Fedha wa mwaka 2018 kwa kuchukua asilimia 100 ya tozo za mauzo ya korosho nje ya nchi (Export levy) kupelekwa mfuko mkuu wa fedha za serikali. Awali, asilimia 65 ya tozo hiyo ilikuwa ianenda kwenye mfuko wa zao hilo na baadae kurejeshwa kwa wakulima kupitia pembejeo. Hoja ya wabunge wakiongozwa na kamati ya bajeti ilikuwa, hatua ya kuchukua fedha zote ingeleta athari kubwa kwa maendeleo ya zao hilo na wakulima wake. Korosho zazua gumzo Tanzania, kwa nini? Mjadala ukawa mkali lakini hoja ya serikali ikapita. Baadae, Rai John Magufuli akasema hakupendezwa na namna ya wabunge wa CCM hususani wa mikoa ya kusini kwa namna walivyolijadili suala hilo, na akatishia kuwa laiti wangeliandamana basi angetuma askari wawaadhibu. Msimu wa mwaka jana, serikali ya Tanzania iliingiza kiasi cha dola 209 milioni za Marekani kutokana na zao la korosho. Sakata la korosho nchini Tanzania lianendelea kufukuta na sasa serikali ya nchi hiyo imewapa wafanyabiashara siku nne za mwisho kununua zao hilo. text: China huendesha karibu shughuli zote za uchimbaji wa madini ya kipekee inayopetikana duniani Madini hayo kutoka China ni malighafi kuu ambayo hutumiwa na kampuni nyingi za Marekani kutengeneza vitu kama magari yanayotumia nguvu za umeme, simu na bidhaa nyengine nyingi za kielektroniki. Mwaka jana utafiti uliofanywa na shirika la Jiolojia la Marekani uliorodhesa madini hayo kama yenye umuhimu mkubwa katika uchumi na ulinzi wa taifa la Marekani. "China inatathmini hatua ya kuthibiti usafirishwaji wa madini hayo ya kipekee nchini Marekani," Gazeti la kitaifa la Global Times, liliandika katika mtandao wake tweeter wiki hii. Madini hayu ni yapi? Madini hayo adimu, ambayo hufahamika kwa lugha ya Kingereza kama rare earths ni kundi la madini 17 yanazotumiwa kwa utengenezaji na ukuzaji wa vitu kadhaa katika sekta mbalia mbali, ikiwemo nishati mbadala, bidhaa za kielektroniki, bidhaa za kutengeneza mafuta na pia hutumika kutengeneza vioo. Japo madini hayo husemekana ''hayapatikani'' kwa urahisi, utafiti uliyofanywa na Shirika la Jiologia la Marekani umebaini kuwa yanapatikana kwa wingi katika ukoko wa dunia Hata hivyo kuna sehemu chache sana duniani kunakopatikana migodi inayotoa madini hayo. Uchimbaji wake ni mgumu sana na umetajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira. China ndio kinara wa uzalishaji wa madini hayo kwa kutoa asilimia 70. Myanmar, Australia, Marekani na mataifa mengine pia huchimba madini hayo kwa kiasi kidogo. Katika kuchakata makinikia ya madini hayo, China inaongoza zaidi. Mwaka jana karibu 90% ya uchakatwaji wa makinikia yake ulifanyika nchini China. Kampuni moja ya Australia inayoendesha shughuli zake nchini Malaysia ilichakata kiasi kilichobaki. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kiwango cha uzalishaji wa madini hayo ya kipekee kilichosafirishwa nje ya China kiliongezeka mara mbili zaidi kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na nchi hiyo. Marekani inaitegemea China kwa kiwango gani? Marekani inaagiza karibu 80% ya kundi la madini hayo 17 ya kipekee kutoka China, takwimu za serikali ya Marekani zinabainisha. Estonia, Ufaransa na Japan pia zinaiuzia Marekani madini hayo japo kwa uchache. Kampuni pekee inayosafisha madini hiyo nchini Marekani hutuma malighafi yake Uchina kusafishwa - na tayari imeathiriwa na nyongeza ya kodi ya 25% iliyowekwa na China. Marekani inaweza pia kuagiza madini hayo kutoka Malaysia, lakini sio kwa kiwango kitakachokidhi mahitaji yake. Serikali ya Malaysia imetishia kupiga marufuku uchakatwaji wa madini hayo kutokana na sababu za kimazingira. Mgodi wa madini China Je, Marekani ina uwezo wa kuanzisha kampuni yake ya kusafisha madini hayo ya kipeke ambayo ni vigumu kupatikana? Hilo bila shaka linawezekana , lakini itachukua muda kwasababu itakabiliwa na changamoto ya kupata malighafi ikiwa China itaondolewa katika mnyororo wa uzalishaji wa bidhaa hiyo kwenda Marekani. Hadi mwaka 1980, Marekani ilikuwa ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini hayo. China ishawahi kudhibiti usafirishaji wa madini hayo hapo kabla. Mwaka 2010, walichukua hatua hiyo dhidi ya Japan, kufuatia mzozo wa kimaeneo. China ikiidhinisha hatua ya kudhibiti uuzaji wa madini yake, kampuni nyingi za Marekani zinazotegemea madini hayo kuendesha biashara zao zitapoteza matrilioni ya dola. China imekuwa ikionesha dalili kwamba huenda ikadhibiti usafirishwaji wa madini yake ya kipekee na adimu kwenda Marekani kipindi hiki mzozo wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili ukizidi kufukuta. text: Wengi katika mitandao ya kijamii wanasema jinsi sera hiyo ilivyoidhinishwa kuchelewa Tangazo hilo limetolewa baada ya data ya sensa kuonesha kushuka vibaya kwa viwango vya watu kuzaana. Baadhi yao - hasa vijana wa sasa - wanauliza jinsi tangazo hilo la Jumatatu ambalo pia linalenga kuchelewesha umri wa kustaafu litakavyotekelezwa. Wengine walitoa wito kwa jamaa zao kufidiwa kutokana na usumbufu wa kiakili waliopata kutokana na hamu ya kutaka kuwa na zaidi ya mtoto mmoja miaka ya nyuma. Chini ya sera kali ya kuwa na mtoto mmoja iliyoanzishwa nchini China mwaka 1979, familia zilizokiuka sheria hiyo zilipigwa faini, kupoteza kazi na hata wakati mwingine kulazimishwa kutoa mimba. Wanaharakati wanasema pia ilisababisha maswala kama mauaji ya watoto wachanga wa kike, kutoripotiwa inavyostahili kuzaliwa kwa watoto wa kike. Maelezo kadhaa ya jinsi familia zilivyoteseka wakati huo sasa yameibuka mtandaoni kujibu sera hiyo mpya. 'Kila mtu amekuwa data' Mtu mmoja katika mtandao wa kijamii wa Weibo huko China alidai mama yake alilazimishwa kutumia mbinu ya mpango wa uzazi (IUD) baada ya kumzaa kama mtoto wa pili, akiongeza kuwa mpaka leo anakabiliwa na athari zake. "Sera hii mpya ni ishara ya kutojali - haiangazii usumbufu wa kimawazo iliyosababishia watu. Kila mtu amegeuzwa kuwa data, badala ya watu kuonekana na kuheshimiwa," aliandika katika mtandao wa Weibo akitumia akaunti ya siri inayojulikana kama Chillsyrup. Watu wengi walikumbuka kisa cha Feng Jiamei ambaye alilazimishwa kutoa mimba ya miezi saba kwasababu alishindwa kulipa faini ya kuzaa mtoto wa pili. Maafisa wa jiji waliomba msamaha baada ya picha inayomuonesha Bi Feng na mtoto wake aliyetolewa tumboni kabla ya muda wake wa kuzaliwa kufika, kuwashangaza watumiaji wa mitandaoni. Mwingine anayefahamika kama Jia Shuai aliandika....kuwa mtoto haramu aliyelelewa vijijini, anakumbuka alivyoruka kwenye kidimbwi kujificha asionekane na maafisa wa uzazi wa mpango. "Ukishindwa kulipa faini, baadhi ya maafisa wangelichukuwa vitu kwenye nyumba yenu au kuondoka na mifugo wenu. Ni kumbukumbu ya kustaajabisha" aliandika. Mtumiaji mwingine wa ntandao alidai kuwa dada yake mdogo bado yuko hai kutokana na huruma ya daktari ambaye alimwachia mama yake atoroke hospitali, baada ya kuagizwa aende akatoe mimba ya miezi nane. Huku hayo yakijiri mtengenezaji filamu Zhang Yimou na mke wake- ambao walipigwa faini kubwa ya dola milioni 1.2m (£842,850) mwaka 2014 kwa kukiuka sera ta nchi hiyo ya kuwa na mtoto mmoja - pia alitoa kauli yake kuhusu tangazo hilo jipya. Muandaaji Filamu wa China Zhang Yimou, ambaye ana watoto watatu, alitozwa faini ya dola milioni 1.2m mwaka 2014 kwa kuvuja sera ya nchi ya kuwa na mtoto mmoja.. "Tulikamilisha wajibu kabla ya muda," wanandoa hao waliandika kwenye mtandao wa Weibo, wakiambatanisha na emoji ya kunyoosha mikono. Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema sera hiyo, sawa na iliyotangulia, bado inakiuka haki ya kingono na ya uzazi. "Serikali haina mamlaka ya kudhibiti idadi ya watoto watu wanatakiwa kuwa nao. Badala ya 'kudhibiti' sera yake ya uzazi, China inatakiwa kuheshimu maisha ya watu na kukomesha njia yoyote ya kuwaamulia watu jinsi ya kupanga familia zao," alisema mkuu wa shirika hilo nchini China, Joshua Rosenzweig. Kizazi kilichojipata katika njia panda' Lakini wengi wanaokosoa sera hii mpya ni vijana wa kizazi cha sasa, ambao walilalamikia "kuchanganyikiwa" kizazi ambacho kimejipata katikati njia panda kuhusu ya sera hiyo. "Kwa wale tuliozaliwa baada ya miaka ya 1980 na 1990 - hatupumui. Serikali inatuhamasisha tuzae watoto, lakini bado wakati huo huo inataka tufanye kazi kwa muda mrefu. Haya ni maisha gani?" Mmoja aliuliza. Kwa zaidi ya miongo minne, umri wa kustaafu nchini China haujabadilishwa, miaka 60 kwa wanaume na 55 kwa wanawake. Lakini siku ya Jumatatu China ilisema itachelewesha kwa awamu miaka ya kustaafu, ijapokuwa haikutoa maelezo. "Sitaki hata mtoto mmoja, itakuwa watatu ," Mwingine wanandika. Kwanini wanawake wa China hawataki watoto zaidi? Hadi maelezo zaidi yatakapotolewa, baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wanatilia shaka kubadilishwa kwa sera hiyo kutachangia ongezeko la watoto wanaozaliwa. Wakati China ilipofutilia mbali sera yake ya kuwa na mtoto mmoja mnamo 2016 na kuruhusu watu kuwa na hadi watoto wawili, ilishindwa kubadili msimamo wa watu juu ya suala hilo. "Kama kulegeza sera ya uzazi ingelikuwa na ufanisi, sera ya sasa ya watoto wawili ingelikuwa imeonesha ufanisi wake pia," Hao Zhou, mchumi mwandamizi wa Commerzbank, aliliambia shirika la habari la Reuters Jumatatu.wa. Uamuzi wa China wa kuruhusu watu kuwa na hadi watoto watatu umeendelea kuibua gumzo mitandaoni baadhi yao wakihoji ikiwa hatua hiyo huenda imechelewa. text: Castro amewahi kusema kwamba hakuzaliwa akiwa mwanasiasa Mzee huyo, aliyetawala kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 50, hajaonekana hadharani kwa miezi mingi na bado haijabainika iwapo atajitokeza leo. Ingawa Cuba imebadilika sana tangu kakake Raul achukue hatamu miaka minane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba. Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshirika wa karibu wa Cuba, amewasili Havana kushiriki katika sherehe hizo. Fidel Castro amekuwa akirejea chuo alichosomea na kutoa mihadhara Mtengenezaji sigara maarufu raia wa Cuba ametayarisha msokoto mrefu zaidi wa sigara duniani kwa heshima ya Castro. Msokoto huo una urefu wa mita 90. Kiongozi mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake. text: Kupitia taarifa, Melania Trump amesema amekuwa akitii sheria na kanuni za uhamiaji "wakati wote" Bi Trump hata hivyo bado hajafafanua alitumia viza ya aina gani alipopigwa picha za uanamitindo jijini New York mwaka 1995. Amekuwa akisema alianza kufanya kazi kama mwanamitindo Marekani mwaka 1996, lakini picha zake za utupu zilizochapishwa na gazeti la udaku la New York zinaashiria kwamba huenda zilipigwa mwaka 1995 zikikusudiwa kutumiwa katika jarida moja la Ufaransa ambalo kwa sasa halichapishwi. Mwandishi wa BBC jijini Washington Gary O'Donoghue anasema kasoro hiyo imeibua maswali kuhusu hali Melania wakati huo na iwapo alikuwa na kibali cha kufanya kazi Marekani. Bw Trump amekuwa na msimamo mkali kuhusu wahamiaji haramu katika kampeni yake. Kufikia sasa, maafisa wake wa kampeni wbado hajasema wazi Bi Trump alitumia viza gani na alipewa wakati gani. Madai ya kwamba huenda mwanamke huyo alivunja sheria yamejiri katika wiki ambayo imekuwa na misukosuko kwa tajiri huyo kutoka New York. Kuna taarifa za mgawanyiko mkubwa kutokea katika uongozi wa chama cha Republican kutokana na matamshi yenye utata ambayo yamekuwa yakitolewa na mgombea huyo. Kampeni ya Donald Trump imekumbwa na misukosuko wiki hii Mmiliki wa mojawapo wa mawakala wa uanamitindo waliotumiwa na Melania, Paolo Zampolli, anasema alimdhamini Bi Trump na kumuwezesha kupata viza ya kufanyia kazi ya ngazi ya H1B mwaka 1996. Melania amekuwa akisema alilazimika kurejea Slovenia, nchi yake ya kuzaliwa, mara kwa mara baada ya miezi kadha kufanya upya viza yake, jambo ambalo sana huhitajika kwa watu wanaotumia viza za kitalii au biashara na wala si za kufanya kazi. Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amekanusha madai kwamba huenda alivunja sheria za viza alipoanza kufanya kazi kama mwanamitindo jiji New York, Marekani. text: Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155. Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita. Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayona ni kwa nini. Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani. Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19. Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani. text: Poulsen akisherehekea na wenzake baada ya kufunga dhidi ya Peru Hii ni baada ya mchezaji ambaye babake ni Mtanzania, Yusuf Yurary Poulsen, kufanya vyema akiichezea timu ya taifa Denmark katika Kombe la Dunia Urusi. Poulsen alifunga bao pekee wakati wa mechi hiyo dhidi ya Peru Jumamosi na baadaye akatawazwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Fifa. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Yusuph Singo, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuweka utaratibu wa kutambua wachezaji kama hao. Singo alisema shirikisho hilo ndilo lenye dhamana ya kujua idadi ya wachezaji wenye asili ya Tanzania wanaocheza Ulaya ambao watawekewa utaratibu na Serikali ili kuitumikia timu ya taifa. "Serikali hatuwezi kujua kila mchezaji anayecheza Ulaya ndio maana kuna taasisi (TFF) ambayo pamoja na mambo mengine ya kiutendaji, inatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kutambua wachezaji wetu wanaocheza nje ya nchi," amenukuliwa na gazeti hilo. "Kwa mfano huyu Mtanzania anayecheza Denamrk hatukuwa tukimfahamu, kama vyama vyetu vya michezo vingekuwa na utaratibu mzuri wa kujua wachezaji gani wanacheza nje ingekuwa rahisi." Anapocheza soka ya kulipwa, mchezaji huyo hutumia jina lake la Kidenmark, Poulsen, lakini katika timu ya taifa hutumia jina la babake, Yurary. Kumekuwa na mjadala mtandaoni kuhusu iwapo anafaa kuchukuliwa kama Mtanzania au kama raia wa Denmark, ikizingatiwa kwamba kwa sasa sheria ya Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili. Poulsen ndiye mchezaji wa kwanza wa asili ya Tanzania kucheza fainali za Kombe la Dunia na pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa asili ya Tanzania kufunga bao. Mchezaji mwingine wa asili ya Tanzania Patrick Mtiliga aliwahi kujumuisha kikosi cha Kombe la Dunia lakini hakuingia uwanjani kucheza. Poulsen, ambaye babake alitokea Tanga, amewahi kuzuru Tanzania mara kadha. Kwenye mahojiano na vyombo vya habari awali, alisema hakupokea ombi lolote la kuichezea Tanzania ingawa kwa sasa hajui jibu lake lingekuwa gani. "Kwanza ilikuwa faraja kwangu kucheza timu iliyokuwa daraja la kwanza Denmark mwanzoni na kucheza kwa msimu mzima, kuhusu kwani nini sikucheza timu ya taifa ya Tanzania? ni swali zuri lakini kiukweli sikupokea ofa kutoka Tanzania ya kucheza timu ya taifa lakini pia sijui ingekuwaje kama ofa ingekuja," alisema alipohojiwa na Ayo TV Julai mwaka jana. Hata hivyo, alikiri kwamba hawezi kusema iwapo angelipokea ofa kama hiyo, uamuzi wake ungekuwa gani. "Nimecheza timu zote za vijana za taifa za Denmark na sasa timu ya wakubwa lakini sikuwahi kufikiria kama ningepata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya wakubwa ya Denmark hadi nilivyoitwa lakini nimezaliwa na kukulia Denmark kama nilivyosema awala kama ofa ya Tanzania ingekuja sijui ningechagua kucheza timu gani". Ndoto ya Patrick Mtiliga Kombe la Dunia Yussuf Poulsen amezidi ufanisi wa mchezaji mwingine mwenye asili kama yake, Patrick Jan Mtiliga ambaye kwa sasa amestaafu soka. Mtiliga alizaliwa 28 Januari 1981 ambapo babake alikuwa Mtanzania. Alikuwa beki na alichezea timu ya taifa ya Denmark mechi sita na alikuwa ameteuliwa kikosi cha wachezaji 23 wa kucheza Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini. Hata hivyo hakufanikiwa kucheza. Denmark waliondolewa kwenye michuano hiyo hatua ya makundi baada yao kumaliza nafasi ya tatu kundi lao. Katika soka ya kulipwa, Alichezea klabu kadha za Denmark na Uholanzi kabla ya kuhamia Malaga ya Uhispania mwaka 2009. Mwanzoni mwa mwaka 2010, aliumizwa kwneye pua na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid jambo lililomfanyakutocheza wiki tatu. Aliondoka Malaga Juni 2011 baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na FC Nordsjælland ya Denmark ambapo alimalizia uchezaji wake mwaka 2015 baada ya kuwachezea mechi 150 na kufunga mabao 5. Afisa mmoja mkuu serikalini Tanzania amesena taifa hilo la Afrika Mashariki linafaa kutathmini na kujua idadi ya wachezaji wenye asili ya taifa hilo ambao wanacheza katika mataifa ya nje. text: Taarifa katika vyombo vya habari nchini zinaeleza kwamba ndege hiyo ilianguka Jumapili mwendo wa saa mbili usiku katika eneo la Turkana. Inaarifiwa kwamba Kapteni Mario Magonga amefariki pamoja na abiria wengine wanne. Polisi inasema helikopta hiyo imeanguka katika eneo la Labolo, kisiwa chenye milima ya volcano katikakati ya ziwa Turkana - Central Island National Park kaskazini magharibi mwa Kenya. "Taarifa zilizopo zinaashiria kwamba ndege mbili zilitua mapema katika kambi ya Lobolo katika kisiwa hicho kilichopo kwenye mbuga ya kitaifa, hatahivyo moja ndio iliyofanikiwa kutua salama katika eneo hilo," idara ya polisi imesema katika taarifa yake rasmi. Inaarifiwa kwamba vikosi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo katika kusaidia kwenye jitihada za kuondosha miili na masalio ya ndege hiyo. Kufikia sasa, chanzo cha ajali bado hakijajulikana. Kapteni Magonga ni nani? Alikuwa rubani wake naibu rais wa Kenya William Samoei Ruto. Aliwahi kuwa rubani katika jeshi la Kenya. Ni mzawa wa Nyamataro, Kitutu Chache kusini, kaunti ya Kisii - kusini magharibi mwa Kenya. Babake ni mwanajeshi mstaafu; Brigedia (rtd) Magonga. Alikuwa rubani mkuu wa helikopta za kampuni ya KIDL helicopters - inayotoa huduma za usafiri binafsi katika eneo zima la Afrika mashariki. Alikuwa mkufunzi aliyehitimu wa helikopta. Alipokea mafunzo kutoka kikosi cha ulinzi Kenya KDF. Ana uzoefu wa kuendesha ndege kwa zaidi ya saa 5500 kwenye ndege za injini moja na injini zaidi ya moja. Kwa waliofahamu, wanamueleza kuwa rubani aliye na taaluma na uzoefu mkubwa, na aliheshimika pakubwa. Rubani wa naibu rais William Ruto amefariki katika jali ya ndege baada ya helikopta aliyokuwemo kuanguka nchini Kenya. text: Maandamano ya k,upinga ziara ya Trump Ubelgiji yalifanyika Brussels Trump anatarajiwa kukutana na maafisa wa Ulaya leo Alhamisi. Amekuwa mkosoaji wa NATO na Muungano wa Ulaya. Baada ya kuwasilia mjini Brussels, Bwana Trump alikutana na mfalme na malkia wa Ubelgiji huku maelfu ya watu wakiandamana kupinga kuwepo kwake mjini Brussels. Mapewma Trump alikutana kwa muda mfupi na Papa Francis huko Vatican. Baada ya kuwasili mjini Brussels, Bwana Trump alikutana na mfalme na malkia wa Ubelgiji Bwana Trump amewalamua wanachama wengine wa NATO kwa matumizi ya chini kwa ulinzi kuliko kiwango kilichoafikiwa cha asilimia mbili ya pato la nchi. Kabla ya mkutano wa leo Alhamisi , waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Rex Tillerson aliwaambia waandishi wa ahabriu kuwa Trump anataka kuwashinikiza wanachama wa NATO kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Bwana Tillerson alisema kuwa Rais Trump ambaye ameshinikizwa na mataiafa ya Ulaya kuunga mkono mkataba kuhusu hali ya hewa wa Paris, bada hajafanya uamuzi ikiwa Marekani iatajiondoa kwenye makubaliano hayo. Rais wa Marekani Donald Trump yuko mjini Brussels kwa kile kinachotajwa kuwa mazungumzo magumu na wanachama wa Nato. text: Wafanyakazi wa kiwanda cha Coca-Cola wamekataa kuhusishwa kama wachunguzi wa chanzo cha mihadarati hiyo Dawa hiyo iliyokuwa imefichwa kwenye mifuko ya kuuzia juisi ya machungwa , ilifika kwenye shehena kutoka Amerika Kusini Uchunguzi unaendelea katika kijiji cha Signes, kilichopo kusini mwa Ufaransa. Kukamatwa kwa kilo 370kg za kokeini kunafanya kiwango hicho kuwa kikubwa zaidi kuwahi kupatikana kwenye ardhi ya Ufaransa. Mwendesha mashtaka mjini Toulon, Xavier Tarabeux, amesema kuwa bei ya mtaani ya dawa hiyo ya kulevya ni "Euro milioni 50" na kwamba ni tukio baya sana la kushangaza". Wafanyakazi wa kiwanda cha Coca-Cola wamekataa kuhusishwa kama wachunguzi wa chanzo cha mihadarati hiyo . " Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wafanyakazi wa kiwanda hizo hawahusiki kwa vyovyote vile ," alieleza rais wa kikanda wa Coca-Cola Jean-Denis Malgras, Mwezi Aprili 2015, maafisa wa forodha wa Ufaransa walisaidia katika kuwamakata wanaume wawili waliokamatwa walipokuwa wakijaribu kuendesha manuari iliyokuwa imesheheni kilo 250 za kokeini hadi Uingereza. Kokeini yenye thamani ya bei ya mtaani kiasi cha Euro 50 m imegundulika katika kiwanda cha a Coca-Cola kilichopo kusini mwa Ufaransa. text: Barabara nyingi zimezibwa na mawe makubwa Wengine 163 wamelazwa hospitali, 20 wakiwa na majeraha yanayohusiana na mvua kubwa. Wanne wana majeraha mabaya. Watu wapatao 300 wanadaiwa kukwamba katika hori ya Romero, mashariki mwa mji wa Santa Barbara. Polisi wamesema eneo lililokumbwa na maporomoko hayo linafanana na "uwanja wa vita wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia". Mawe makubwa yalimeguka kutoka milimani na kuziba barabara Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani umbali wa maili 30 (48km). Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda. Maafisa wa Kikosi cha Ulinzi Baharini wametuma ndege kadha kusaidia juhudi za uokoaji na wametahadharisha umma dhidi ya kutumia ndege zisizo na marubani kwani zitatatiza juhudi za uokoaji. Maelfu ya wakazi wa California waliamrishwa kuondoka makwao Jumatatu, mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwa sababu ya moto, wakati huu ni kwa sababu ya mvua. Mbwa wa polisi akiwatafuta manusura eneo la Montecito Watu 13 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mwa jimbo la California, Marekani, maafisa wamesema. text: Alexis Ohanian na mpenzi wake Serena Williams Nyota akiwemo Beyonce, Kim Kardashian na Eva Longoria walikuwa katika harusi hiyo iliofanyika katika eneo la New Orleans siku ya Alhamisi. Sherehe hiyo ilikuwa na wageni 200 katika orodha ya wageni kulingana na vyombo vya habari. Eneo moja kubwa la mji lilifungwa kwa sherehe hiyo ambayo ilifanyika katika kituo cha Contemporary Arts Center. Wageni wengine ni pamoja na nyota Caroline Wozniack, Kelly Rolland ,Ciara, La La Anthony na muhariri wa jarida la Vogue Anna Wintour kulingana na gazeti la daily mail. Eneo lililofungwa ili kuruhusu haruasi hiyo kufanyika Limeripoti kwamba harusi hiyo iligharimu dola milioni 1 huku wageni wakiagizwa kutoingia na simu zao kutokana na mkataba na jarida la Vogue. Mkufunzi wake Patrick Mouratoglu alimtakia serena ''siku njema ya harusi'' katika mtandao wake wa Instagram. Wanandoa hao walitangaza fungate yao manmo mwezi Disemba mwaka uliopita baada ya kuchumbiana kwa miezi 15. Walitangaza habari yao ya kuwa pamoja baada ya kusambaza shairi katika Reddit kwa jina: ''Nilikubali''. Serena na mwanawe Serena alijifungua mtoto wao wa kwanza wa kike Alexis Olympia, miezi miwli iliopita. Serena Williams amefunga ndoa na mwanzilishi mwenza wa Reddit Alexis Ohanian katika harusi kubwa iliojaa mbwembwe za aina yake ya mwaka huu. text: Wahadhiri na wanafunzi wamekuwa kwenye mgomo Rais alisema amechukua hatua hiyo "kuhakikisha usalama wa watu na mali." Chuo kikuu hicho kilikuwa kimekumbwa na vurugu kutokana na mgomo wa wahadhiri na wanafunzi. Chama cha wahadhiri Jumatatu kiliamua kuendelea na mgomo hadi wahadhiri walipwe marupurupu ya miezi minane ambayo yamefikia Sh32bn (dola 9.2 milioni za Marekani). Wanafunzi walijiunga na mgomo Jumanne, na walitaka kukutana na Rais Museveni badala ya mwenyekiti wa baraza simamizi ya chuo chini ya uenyekiti wa Dkt Charles Wana-Etym. Naibu chansela wa chuo hicho Prof Ddumba Ssentamu wiki iliyopita alikuwa amewasihi wahadhiri wakubali kurejea kazini huku suluhu ya kudumu ikiendelea kutafutwa. Wanafunzi wameanza kuondoka kutoka Chuo Kikuu cha Makerere baada ya Rais Yoweri Museveni kutangaza kifungwe mara moja Jumanne jioni. text: Papa Francis ameonesha kusikitishwa na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Mmishenari kutoka Uhispania kuhusu wito wa kidini. Mahojiano hayo ni sehemu ya kitabu kinachoandikwa na mmishenari huyo. Papa amesema mahusiano ya jinsia moja ni jambo la "fasheni", na ametaka makasisi kutii viapo vyao vya utawa (kutojihusisha na mapenzi). Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia limechapisha sehemu ya mahojiano hayo katika mtandao wake juzi Jumamosi. Papa Francis amesema kanisa katoliki linapaswa kuwa "imara" wakati wa kuchagua watu watakaokua makasisi. "Hili suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni kubwa sana," amesema Papa na kusisitiza kuwa wale wote wanaohusika na mafunzo kwa makasisi wahakikishe kuwa wanafunzi wao "wamekomaa kibinaadamu na kihisia" kabla ya kuwapatia Sakramenti ya Upadre (upadrisho). Papa Francis alaani vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto "Kwa sababu hiyo, Kanisa linawataka watu wenye tabia hizo (wapenzi wa jinsia moja) wasikubaliwe katika maisha ya ukasisi." Agizo hilo pia linawahusu wanawake ambao wanataka kuwa watawa wa kanisa hilo. "Katika jamii zetu, sasa inaonekana kuwa suala hili la mapenzi ya jinsia moja limekuwa fasheni. Mawazo kama hayo sasa yanaanza kupata ushawishi nadani ya kasnisa," amesema papa na kuongeza: "suala hili katu halina nafasi katika maisha ya watawa wetu." Mahojiano hayo yalifanyika mwezi Agosti Mwaka 2013, Papa alisisitiza juu ya msimamo wa kanisa hilo kuwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni dhambi. Papa Francis awatahadharisha watawa kuhusu matumizi ya mitandao Kuhusu mahusiano binafsi ya Mungu na mtu mwenye kujihusisha na vitendo hivyo alijibu; "Kama mtu ni shoga na anataka ukaribu na Mungu na ana nia njema, mimi ni nani wa kuhukumu?" "Nguvu ya Utumishi", ni kitabu kilichotungwa na padre Fernando Prado,baada ya mahojiano ya saa nne na Papa kuhusu changamoto za kuwa kasisi. Kinatarajiwa kuchapishwa wiki ijayo. Papa Francis amesema mapenzi ya jinsia moja kwa makasisi ni "jambo kubwa" na ambalo linampa "hofu". text: Rais wa Marekani Donald Trump ameutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel Rais huyo pia ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati. Trump amesema uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za dhati za kuleta amani ya kudumu bali inataka kutafuta suluhu ya mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina ambao .Marekani haifungaman na upande wowote na kuingilia mipaka ya Israel na mamlaka zake ,na hatuko tayari kuingilia katika migogoro yao ,hayo ni mambo yao wenyewe. Huku kwa upande wake Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesikitishwa na maamuzi ya rais Trump na kudai kuwa Marekani imepoteza haki ya kusimamia hatua ya kupatana kwa amani ambayo imekuwa ikitafutwa miongo kadhaa iliyopita. Huku waziri mkuu wa Israel ,Benjamin Natanyau ameonekana kuunga mkono hatua ya rais Trump kwa kuelezea kuwa ni maamuzi ya kihistoria licha ya kuwa wapalestina wamemkosoa na huku Uingereza na nchi nyingine wanachama wa baraza la usalama wa umoja wa mataifa wameitisha kikao cha dharura ili kujadili maamuzi yaliyofanywa na rais Trump. Rais Trump amefanya maamuzi ya kihistoria ya kuipindua sera za miaka mingi ya Marekani kwa kuutambua mji wa Yerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel. text: Je wajua uwezo wa simu yako? Wanasayansi kutoka California waligundua chembechembe za kafeini pamoja, dawa za kupunguza msongo wa mawazo na vipodozi vya ngozi kwenye simu 40 walizozichunguza. Utafiti unaonyesha kuwa hata kunawa mikono mara kwa mara hakutazuia kusambaa kwa chembechembe hizo katika vitu vingine. Watafiti kutoka chuo kikuu cha California kilichopo mjini San Diego, wamefanya tafiti za sampuli 500 kutoka kwenye simu 40 za watu wazima na mikono yao. Dkt Amina Bouslimani ambaye ni mwanasayansi msaidizi katika utafiti huo alisema matokeo yalionyesha kuwa inawezekana kupata maelezo ya kina kumhusu mtu kutoka kwenye simu, ''Kwa kuchunguza chembechembe zilizoachwa kwenye simu zao...tunaweza kubaini iwapo mtu ni mwanamke, na anatumia vipodozi, na kupaka rangi nywele zake, anakunywa kahawa na, anapendelea bia kuliko divai, anapenda kula vizuri, anatibiwa msongo wa mawazo, anaikinga ngozi na jua, kupulizia marashi, mara nyingi hupenda kutumia muda wake mwingi nje ya nyumba …. na vitu vingine kama hivyo,'' alieleza. Mara nyingi Chembechembe hizo zinaweza kutoka kwenye ngozi na jasho la mikononi kwenda kwenye simu za watu. Dawa za mbu na zile za kuzuia miali ya jua zimekuwa zikidumu kwa muda mrefu kwenye ngozi na kwenye simu hata kama hazijatumiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja. Tafiti zilizopita zilizofanywa na watafiti haohao zinaonyesha kuwa hata kama mtu hajanawa kwa siku tatu hivi, bado ataonekana kuwa msafi na mrembo. Utafiti unaonyesha uchunguzi wa simu unaweza kutumiwa: Mtafiti anataka kujua zaidi juu ya wingi wa bakteria walioko kwenye ngozi zetu na wanaanisha nini kuhusu sisi. Mwandishi mkongwe prof Pieter Dorrestein amesema kuwa mwili wa binadamu una bakteria ambao si chini ya 1000 tofauti tofauti katika sehemu mbalimbali za mwilini. Chembechembe zinazopatikana kwenye simu za mikononi zinaweza kuashiria kiwango cha afya na maisha ya mmiliki, ikiwemo matibabu na aina ya chakula anachopendelea. text: Bw Trump hupenda sana kuwakumbusha wapiga kura kwamba anafadhili kampeni yake binafsi Jarida hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw Trump ni $3.7bn (£2.7bn). Forbes wanasema kushuka huko kwa thamani ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi' kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la New York. Bw Trump, ambaye wakati mmoja liandika kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa Midas: Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa kuwa dhahabu), amekuwa akisema kwamba rais wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu mwenye busara katika biashara na majadiliano. Wakati wa mdahalo wa urais Jumatatu, alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati umefika kwa taifa hili kuwa na mtu anayefahamu mengi kuhusu pesa." Mapema mwaka huu, hoteli mpya ya Trump ilifunguliwa Washington DC, karibu na White House Alipoteza vipi $800m? Forbes, ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu, wanasema hilo limetokana na kudorora kwa soko la nyumba, afisi na ardhi New York. Kati ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo jumba maarufu la Trump Tower linalopatikana Manhattan. Jumba lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach, Florida, pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes. Lakini majumba saba ya Trump, likiwemo jumba la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda thamani. Ametumia pesa ngapi kwenye kampeni? Inakadiriwa kwamba amewekeza $50m, pesa zake binafsi, kwenye kampeni kufikia sasa. Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye mashirika makubwa kama vile NBC Universal, Univision na Macy's. Ivana na Donald Trump mwaka 1989 Utajiri wake kamili? Utajiri wake kamili haujulikani. Alipowasilisha taarifa zake za kifedha kwa Tume ya Dola ya Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni kumi." Lakini Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn, Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao Fortune wanasema ana $3.9bn. Moja ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw Trump pia huhesabu thamani ya jina lake, ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni karibu $3.3bn. Trump na mkewe Melania na watoto wao wakati wa mkutano wa kampeni Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa jarida la Forbes. text: Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais Trump Agizo hilo la jaji wa wilaya Judge Derrick Watson katika jimbo la Hawaii, ni pigo jipya kwa marufuku hiyo. Jaji huyo alisema kuwa marufuku hiyo haikuelewa vizuri agizo la mahakama ya juu . Uamuzi huo uliotolewa mwezi uliopita, uliidhinisha kwa uchache marufuku hiyo dhidi ya wakimbizi na wanaozuru taifa hil kutoka kwa mataifa sita ya kiislamu. Ulisema kuwa wale walio na familia zao wataruhusiwa kuingia Marekani. Lakini utawala wa Trump uliamua kwamba uamuzi huo haukuhusisha bibi na babu pamoja na wajukuu, mashemeji ,wajomba, mashangazi, mpwa wa kiume na wa kike na binamu. Jaji huyo alishutumu uelewa wa serikali kuhusu watu wa karibu wa familia. Ukweli ni kwamba, kwa mfano watu wa karibu wa familia wanashirikisha bibi na babu. Bibi na Babu ndio chanzo cha watu wa karibu wa familia,aliandika. Mahakama ya juu bado inaangazia jaribio la kuwazuia raia wa Iran,Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kuingia nchini Marekani. Mahakama iliamuru marufuku ya muda kutekelezwa mnamo mwezi Mei. Bwana Trump anasema kuwa vikwazo hivyo vinahitajika ili kuimarisha usalama wa Marekani dhidi ya mashambulio ya kigaidi. Hatahivyo wakosoaji ikiwemo majimbo na makundi yanayopigania makundi ya wakimbizi yamesema kuwa marufuku hiyo inawabagua Waislamu. Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais Trump , jaji mmoja ameamuru. text: Mji huo mpya utajengwa kando ya mji wa Riyadh Mji huo ambao utakuwa na ukubwa wa kilomita 334 mraba ambao utakuwa sawa na mji wa Las Vegas, utatoa huduma za kitamaduni, michezo na mambo mengine ya burudani. Inaripotiwa kuwa mji utakuwa wa aina yake duniani. Ujenzi wa mji huo utataanza mapema mwaka ujao na awamu ya kwanza kukamilika mwaka 2022. Katika malengo ya mwaka 2030 uliotangazwa na naibu mfalme Mohammad Bin Salman mwaka mmoja ulipita, una lengo la kuboresha uchumi na kuzuia kutegemea mafuta kwa taifa hilo. Mji huo ambao ni kama sehemu moja ya tano ya mji wa Riyadh, ndio mradi wa hivi punde kutangazwa. Utawala unasema kuwa matumaini ni kuwa utawavutia wageni, kuboresha uchumi na ukawa wa burudani na furara kwa wale wataishi mji mkuu Riyadh. Mji huo mpya utajengwa kando ya mji wa Riyadh Saudi Arabia imeanzisha mipango ya kujenga mji wa burudani kando mwa mji wa Riyadh ambao utakuwa mkubwa mara 50 zaidi ya himaya ya Uingereza ya Gibraltar. text: Haki za wanawake wengi nchini Sudan hukiukwa "Leo tulikata rufaa kwenye mahakama ya rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini," wakili wake Al-Fateh Hussein aliliambia shirika la AFP Alhamsi. Mahakama ya Sudan ilimpata na hatia Bi Hussein kwa kuua makusudi mapema mwezi Mei baada ya familia ya mumewe kukataa kufidiwa fedha. Hatma ya Bi Hussein ambaye sasa yuko miaka 19, ilizua maoani kote duniani na hata kuanzisha kampeni #HakikwaNoura Baba yake Bi Hussein alimalazimisha kuolewa akiwa na miaka 16 na alikua amejaribu kukimbia. Baada ya ya familia kumkabidhi kwa mume wake, Bi Hussein alisema mume wake aliwaita binamu zake waliomshika huku akimbaka. Alimdunga kisu na kumua mumewe wakati alijaribu tena kumbaka siku iliyofuati. Mahaka ya sharia ilimhumu kifo kwa kunyongwa. Wakati huo huo kundi la wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu la Equality Now limesema kuwa litamwandikia rais Omar al-Bashir kumuomba amuonee huruma. Shirika la Amnesty International limesema kuwa hukumu ya mwanamke ya kifo ambaye alikuwa akijitetea inaangazia uzembe wa serikali kukabiliana na ndoa za watoto , ndoa za lazima na ubakaji katika ndoa. Msichana raia wa Sudan Noura Hussein ambaye alihukumiwa kifo kwa kumuua mume wake kutokana ya madai kuwa alimbaka amekata rufaa. text: Manuwari ya Marekani iliokamatwa na China China iliikamata manuwari hiyo katika maji ya kimataifa siku ya Alhamisi. Haijasema ni kwa nini ilichukua hatua hiyo na kuishutumu Marekani kwa kulifanya jambo hilo kuwa kubwa. Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameishutumu China kwa kuiiba meli hiyo ,huku akisema: Tunafaa kuiambia China kusalia na manuwari hiyo walioiba, aliandika katika mtandao wake Twitter. Kisa hicho ni miongoni mwa visa vibaya zaidi vya makabiliano ya kijeshi kati ya mataifa hayo yenye uwezo mkubwa wa kijeshi katika kipindi cha miongo kadhaa. Trump aitaka China kuhifadhi manuwari ya Marekani Pentagon imesema kuwa manuwari hiyo inayojulikana kama UUV ilikuwa ikitumika kubeba utafiti wa kisayansi wakati ilipokamatwa na kutaka irejeshwe mara moja. Imeionya China kutochukua hatua kama hiyo katika siku zijazo. Lakini msemaji alisema siku ya Jumamosi kwamba mataifa hayo mawili yameafikiana. ''Kupitia mazungumzo na mamlaka ya China,tumeafikiana kwamba China itarejesha chombo hicho kwa Marekani '',alisema msemaji wa Pentagon Peter Cook katika taarifa. Wizara ya ulinzi nchini China imesema kuwa meli hiyo itarudishwa katika njia ilio sawa. Haijulikani ni lini hatua hiyo itatekelezwa. Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon imesema kuwa imeafikiana na China kwamba itairejesha manuwari iliopatikana katika bahari ya kusini mwa China. text: Kabla ya mkasa huo, Claudia alikuwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo, ndoto ambayo amehakikisha ameitimiza licha ya kuwa na makovu usoni. "Tulipokuwa kwenye hoteli tukiwekewa chakula, jiko la gesi lililipuka na mafuta yakanimwagikia usoni. Nilianza kukimbia nikitafuta maji". Alichukuliwa kisha akapelekwa hospitalini. Alikuwa ameungua kwa asilimia kumi na nne usoni. Alikaa hospitalini kwa muda wa miezi mitatu. Hali hii ilifanya maisha yake kubadilika sana, hata kukosa marafiki. "Baada ya kuungua, watoto ambao walikuwa wadogo kuniliko kwa umri, walikuwa wananiogopa, na wale ambao walikuwa wa rika langu, walikuwa wananicheka, wananitania. Nikiwa shuleni, nilikuwa napata barua za matusi na mwalimu akitupatia zoezi la kufanya kwa makundi, hakuna mtu alikuwa ananikubali tufanye naye pamoja," anasema. Claudia Wanjiru: Mimi bado mrembo na makovu yangu Hali hii ilipelekea Claudia kukumbwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya jinsi ambavyo watu walimtendea na kumsema. "Watu walisema kwamba nilijaribu kubadilisha rangi ya ngozi yangu lakini dawa hizo zikakataa kufanya kazi. Wengine wakasema kwamba niko na Ukimwi. Nilikuwa najipendekeza kwa watu ili nipate marafiki, na mtu ambaye alikuwa anakubali kuwa rafiki yangu ana lengo fiche." Wakati alipokosa marafiki, upweke ulimzidi, na ikamlazimu kutafuta njia za kujipunguza machungu. "Nilihisi hakuna mtu ananipenda, wazazi wangu na dada yangu mdogo pekee ndio walionipenda na ambapo wazazi wa mtu lazima wampende, hata ukimuuwa mtu, mzazi wako bado atakupenda tu." Msongo wa mawazo ulipomzidia, Claudia akaiga tabia ya kujikata kutoka kwa filamu ambayo anasema kuwa ilikuwa na msichana ambaye alikosa marafiki, na akawa anajikata ili kutoa machungu ya upweke. Machungu ambayo yanamuathiri hadi leo, kwani aliyasimulia kwa machozi. "Nilianza kujikata kata kwenye mikono na miguu, kwa sababu nilikuwa natafuta njia yoyote ya kusaidiwa, nilifikiria wazazi wakiona wataniuliza eeh Claudia nini inaendelea?.. ama walimu ama mtu yeyote tu. Lakini walimu wangu walipoona, wakasema kwamba mimi nimeingia kwenye ushirikina na mambo ya kishetani. Watu ambao nilifikiria watanielewa, wao ndio hawakunielewa kabisa". Kujaribu kujitoa uhai "Nilijaribu kujitoa uhai kwa kuweka jiko katika chumba changu na kufunga mlango na madirisha, lakini sikufa, nikajua Mungu ameniokoa. "Nilijua kwamba mungu amenipatia nafasi nyingine na kuwa kama Mungu ananipenda si lazima nipendwe na mtu kwa kuwa yeye ndiye aliyenipatia maisha haya, ni yeye ndiye aliniweka huku duniani." Aliponusurika baada ya kujaribu kujitoa uhai, mwanafunzi huyu wa chuo kikuu cha JKUAT akaamua kujikubali na kujitahidi kuafikia ndoto yake ya kuwa mwanamtindo. "Nikaanza uwanamitindo, ili niwasaidie wasichana wengine ambao pengine wanazuiwa kushiriki katika uwanamitindo kwa sababu ni wanene ama ni wafupi, atakaponiona kisha asome historia yangu atajua kwamba kuna matumaini kwa kuwa nimeafikia ndoto yangu licha ya yale nimepitia." Amejaribu kwenda katika mashindano ya uwanamitindo lakini kila wakati mawakala humbagua. "Kuna wakati ambapo nilienda kujisajili katika mashindano ya uanamitindo lakini wakala huyo akanizuia mlangoni na kuniambia "ni ya wanamitindo pekee walioruhusiwa kuingia," anasema. Alijua ni kwasababu ya makovu yake. Licha ya kukataliwa na mawakala, Claudia ambaye pia anajitambulisha kama 'Vanilla Afrika' kwa jina lake la kisanii, hakukata tamaa na kwa usaidizi wa wanafunzi wenzake, yeye hupigwa picha katika mazingira tofauti na kuziweka katika mtandao wa Instagram. Makovu yao pia yamemkosesha mchumba, kwa sababu hajui malengo yao huwa gani. "Mvulana ambaye nilikuwa namchumbia, kila wakati tukikosana, ananikumbusha juu ya alama zangu usoni ananiambia anavumilia kuwa na mimi kwa sababu hakuna mtu mwingine anayeweza kunipenda na alama hizo." Hata hivyo msichana huyu anaelezea urembo kulingana na anavyotambua. "Urembo ni tabia, ni kumsaidia mtu, kumheshimu mtu, urembo ni utu... Hii ndiyo maana ya urembo, kwasababu mtu anaweza kuwa na sura ya kupendeza, lakini hana tabia za kupendeza. "Kama mimi mwenyewe niko na hizi alama, najiambia kwamba mimi ni mrembo, kwasababu si alama zinanipatia jina, alama ni ngozi tu, kila mtu anayo." Claudia Wanjiru ni mwanamtindo mwenye makovu usoni. Makovu hayo aliyapata baada ya kunusurika mkasa wa moto akiwa mwanafunzi wa darasa la saba. text: Refa akionesha kadi nyekundu Maafisa wa polisi na wale wa huduma ya ambyulansi waliitwa ili kuingilia kati. Refa huyo kwa jina Satyam Toki, 28 anafanya uamuzi wa kuwasilisha mshtaka mahakamani. Klabu hiyo ya Sporting de Mundial inasema kwamba mchezaji huyo ameondolewa katika klabu hiyo na kwamba atapatiwa matibabu ya kiakili. SatyamToki ni mkufunzi na refa ''Tunashutumu kitendo hicho cha kutisha'', waliongezea katika mtandao wao wa Twitter. Toki alisema kwamba alimuomba mchezaji huyo mara kadhaa kutumia lugha nzuri na kuwacha kulalamika, kabla ya kumuonya. Alianza kutoka na kuelekea katika eneo la wachezaji wa ziada wa timu yake na alipokuwa akiondoka alinitishia kwamba ataniona baada ya mechi, Toki alisema. ''Ni wakati huo ndiposa nilimpatia kadi nyekundu na kunipiga ngumi usoni''. ''Karibu anasisababishie upofu kwa sekunde chache, na baadaye nilianza kutokwa damu. Kushambuliwa kwa Satyam Toki kulinaswa na kamera ya uwanjani Toki anasema kwamba ana wasiwasi kwamba iwapo atamshtaki mchezaji aliemshambulia, huenda akapoteza kazi yake, lakini akaongozea: kwa upande mwengine, iwapo sitamshtaki, katika siku za usoni huenda akamfanyia kitendo hicho refa mwengine. Refa mmoja amepigwa ngumi usoni katika mechi ya kandanda ya kirafiki baada ya kumpatia kadi nyekundu mchezaji wa klabu ya Sporting de Mundial mjini London siku ya Jumapili. text: Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo Taarifa kuhusu mahala au tarehe ya kifo cha Hamza Bin Laden bado haijawa wazi katika ripoti ya chanzo hicho cha habari. Mwezi Februari, Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo. Hamza Bin Laden, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa ujumbe mbalimbali wa sauti na video akitoa wito wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani na nchi nyingine. Ripoti zilitolewa kwanza na mashirika ya habari ya NBC na New York Times. Hamza Bin Laden aliwatolea wito wapiganaji wa jihadi kulipiza kisasi mauaji ya baba yake aliyeuliwa na kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan mnamo mwezi Mei 2011. Kadhalika alikuwa amewatolea wito watu wa rasi ya Arabia kulipiza kisasi. Saudi Arabia ilimyang'anya uraia mwezi Machi. Aliaminika kuwa katika kifungo cha nyumbani nchini Iran lakini ripoti nyingine zilisema kuwa huenda alikuwa akiishi katika mataifa ya Afghanistan, Pakistan na Syria. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kuwa nyaraka zilizokamatwa katika uvamizi wa mwaka 2011 katika nyumba ya baba yake ya Abbottabad, Pakistan, zinaonyesha kuwa Hamza Bin Laden alikuwa anaandaliwa kuchukua utawala wa al-Qaeda. Vikosi vya Marekani pia viliripotiwa kubaini video hii ya harusi yake akimuoa binti wa afisa mwingine wa ngazi ya juu wa al-Qaeda ambayo ilidhaniwa kufanyika nchini Iran: Baba mkwe wake alikuwa ni Abdullah Ahmed Abdullah au Abu Muhammad al-Masri, ambaye anatafutwa kwa madai ya kuhusika katika mashambulio ya ugaidi ya mwaka 1998 dhidi ya balozi za Tanzania na Kenya. Al-Qaeda lilikuwa ni kundi lililotekeleza mashambulio mabaya ya ugaidi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani, lakini hadhi yake kwa sasa imeshuka katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita baada ya kuibuka kwa umaarufu wa kundi la Islamic State. Alikuzwa katika misingi ya kuichukia Marekani Ni ishara ya jinsi taarifa chache kumuhusu Hamza Bin Laden kiasi kwamba maafisa hawakuweza kuthibitisha umri wake. Katika miezi ya hivi karibuni walisema kuwa huenda alikuwa nchini Afghanistan, Pakistan au Iran. lakini hawakuweza hata kusema ukweli hasa ni nchi gani mmoja wa watu ambao Marekani ''inawatafuta sana'' anaishi. Zawadi ya dola milioni moja kwa yeyote atakayetoa taarifa kumuhusu ilikuwa ni hatua si tu ya uwezekano wa hatari anayoweza kusababisha lakini pia ilikuwa ni ishara ya umuhimu kwa al-Qaeda na propaganda yao. Hamza alikuwa ni mtoto pekee aliyekuwepo wakati baba yake aliposaidia kupanga njama za mashambulio ya Septemba 11 lakini, kwa mujibu wa wakuu wa kundi hilo lenye itikadi kali, alikuwa pamoja naye wakati wa mashambulio hayo. Kwa mtoto wa kiume ambaye alikuwa akifundishwa kuichukia Marekani, kukwepa mauaji ya ulipizaji kisasi mikononi mwa kikosi maalumu lingekuwa ni jambo ambalo lingesalia akilini mwa watu. Katika miaka ya hivi karibuni alituma ujumbe mtandaoni akitoa wito kwa mashambulio dhidi ya Marekani na washirika wake. Al-Qaeda: Taarifa muhimu Osama Bin Laden akiwa karibu na Kabul mwaka 2001 Hamza Bin Laden, mwana wa mwanzilishi wa kundi la al-Qaeda Osama Bin Laden, aliuawa katika shambulio la angani , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani vikinukuu maafisa wa ujasusi. text: Baktash na nduguye Ibrahim walikamatwa mjini Mombasa mwaka 2014 wakiwa pamoja na raia kutoka Pakistani na mwingine wa India. Ndugu hao wa Akasha wanatuhumiwa kutumia ghasia, mauaji na kutoa hongo kulinda biashara yao. Wanatuhumiwa kupanga mauaji ya mhalifu raia wa Afrika kusini anayefahamika kwa jina moja pekee 'Pinky'. Hukumu hiyo inatarajiwa leo wakati taarifa zinaeleza kuwa afisa wa zamani katika idara ya upelelezi nchini DCI, majaji kadhaa na maafisa wengine wa serikali huenda wakahamishwa kupelekwa Marekani kukabiliwa na mashtaka yanayohusu ulanguzi wa madawa ya kulevya. Gazeti la Nation nchini Kenya linaripoti kuwa duru zinaarifu kwamba serikali ya Marekani tayari imeifahamisha kuhusu nia hiyo ya kuwashtaki washukiwa katika mahakama za Marekani. Hatua inayomaanisha kwamba huenda katika siku zijazo kukashuhudiwa kuwasilishwa kwa washukiwa kwa maafisa wa usalama Marekani. Athari ya madawa ya kulevya kwa vijana Mombasa Mji wa Mombasa katika pwani ya Kenya unapitia madhara mengi ya dawa za kulevya, huku familia hiyo ya Akasha ikilaumiwa kuchangia janga hilo pakubwa. Mwandishi kutoka eneo hilo Francis Ontomwa anaeleza kwamba unapolitaja jina la Akasha mjini Mombasa, linaibua uoga na wasiwasi mwingi. Kwa miaka kadhaa, familia ya Akasha iliendesha na kujenga himaya ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, kutoka kitovu cha Mji huo wa Mombasa, kufikia Afghanistan, Ulaya na hata nchini Marekani. Madhara ya biashara hiyo yanaonekana wazi katika mji huo wa pwani ya Kenya. Salma Hemed ni mwanaharakati wa kutetea haki za ibnaadamu kutoka shirika la Haki Afrika ambalo limekuwa likijishughulisha na harakati za kupambana na madhara biashara hiyo haramu miongoni mwa vijana. 'Kwa wale wenye kuuza wanahitaji vijana wa kutoka nyanjani tofuati. Na katika kuonja mihadarati, inawafanya wao waanze kuwa watumiaji wakuu na pia kutegema pakubwa (waraibu) na kuanza kuwa watumiaji mihadarati'. Takriban watu wanane wamejeruhiwa baada ya vijana waliojihami kwa mapanga kuushambulia mtaa wa Kisauni mjini Mombasa. Uhalifu uliokithiri Kisauni Kisauni ni sehemu mojawapo ya mitaa maskini Mombasa. Ni eneo linalokabiliwa na uhaba mkubwa wa usalama. Wiki iliyopita watu wanane walijeruhiwa vibaya na gengi la majambazi. Utumiaji mihadarati umekithiri pakubwa miongoni mwa vijana katika mktaa huo. 'Sisi letu kubwa ilikuwa ni kuwakanya na kuiambia serikali kwamba wale ambao wanahusikana mambo kama haya wasiwahurumie' anasema mkaazi mmoja. Ni miongo miwili tangu babayao ndugu wawili wanaosubiri kuhukumiwa leo - kuuawa huko Amsterdam nchini Uholanzi. Kuuawa kwa mzee Akasha kunahusishwa na biashara ya ulanguzi wa mihadarati. Baadhi ya wakaazi wanadai kuwa familia ya Akasha imlifanikiwa kukita mizizi na kujenga himaya yao Mombasa, kutokana na rushwa na kuhongwa kwa maafisa wa idara za sheria na haki. Baktash mwenye umri wa miaka 42 anatarajiwa kuhukumiwa leo na mahakaman ya wilaya ya kusini New York na nduguye Ibrahim anatarjiwa kuhukumiwa Novemba 8 baada ya wote kukiri mashtaka yaliowasilishwa dhidi yao. Hukumu ya anayetajwa kuwa mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya Baktash Akasha inatarajiwa kutolewa baadae leo mjini New York nchini Marekani. text: Mwana mfalme huyo ameamua kufuata nyayo za mama yake, Princess Diana ambaye mwaka 1997 alitembelea maeneo hayohayo na kutaka kuondoa mabomu yaliochimbwa ardhini. Picha za ziara yake zilipendwa na wengi duniani kote. Eneo hilo hatari bado linaendelea kumaliza maisha ya watu wengi katika nchi nyingi. Je, sehemu hizo ziko katika maeneo gani duniani na hatua gani zimechukuliwa? Jinsi Prince Harry anavyofuata nyayo za mama yake Princess Diana alijulikana sana kwa kujitolea kwa wahitaji ingawa mafanikio yake hakuyaweka hadharani. Kwa mfano Diana alifungua kliniki ya kwanza Uingereza kwa ajili ya waathirika wa virusi vya ukimwi mwaka 1987, na kuweza kufanikiwa kubadili tabia za waathirika Kuhamasisha uwelewa juu ya mabomu yaliyochimbwa ardhini, ni miongoni mwa kosa kubwa lililosababisha apewe talaka na mume wake Prince Wales mwaka 1996. Kwa miongo kadhaa mabomu ya ardhini yalikuwa yamaetumika katika migogoro mingi. Mabomu mengi ambayo hayajalipuka yaliachwa wakati wa vita, kipindi ambacho mauaji ya watu yalifanyika kwa wingi au yalilipuka bila kutarajiwa. Picha inaonyesha namna wakazi wa Angola walivyoathirika na vilipuzi hivyo. Wakati wa ziara yake Prince Harry ameelezea mabomu hayo yaliyochimbiwa ardhini ni kovu la vita lisilopona . Vilipuzo hivyo vimesababisha mauaji ya watu wa ngapi na wangapi wameumia? Mabomu hayo ambayo yaliyofukiwa ardhini huwa yanalipuka kwa makubaliano fulani au bila kulipuka bila kutarajiwa. Kuna aina mbili ya mabomu: Mabomu yaliyofukiwa yakiwa yanalenga kujeruhi watu au kuwauwa na aina ya pili ya mabomu yametengenezwa kwa ajili ya kuteketeza magari. Vilipuzi hivyo vilitumika katika vita ya kwanza ya dunia, lakini yalianza kulipuka kuanzia mwaka 1960 na kuendelea. Kuchimbia mabomu ardhini ilikuwa miongoni mwa mbinu za kivita zilizotumika, na kusababisha madhara katika maisha ya wengi. Nchi kama 60 bado zinakabiliwa na changamoto za mabomu hayo yaliyofukiwa ardhini. Utafiti umebaini kuwa watu zaidi ya 120,000 waliuwawa au kujeruiwa na mabomu hayo ya ardhini kati ya mwaka 1999-2017. Karibu nusu ya waathirika ni watoto, asilimia 84 ni watoto wa kiume. Nchi zipi zina mabomu yaliyofukiwa ardhini? Maelfu ya mabomu hayo yaliyofukiwa ardhini yapo duniani kote. Angola ikiwa ni miongoni mwa taifa lililoathirika zaidi duniani kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1975 mpaka 2002. Asasi ya kusaidia wahitaji ya Halo inasema kuwa sio rahisi kujua ni mabomu mangapi yamefukiwa katika nchi hiyo lakini ni zaidi ya 100,000 yamelipuka tangu mwaka 1994. Mamlaka ya uchibaji madini nchini Angola imesema kuwa mabomu hayo yalikuwa kama 1200. Kuondoa migodi ni gharama na kazi ya hatari.Kwa sasa , inaweza kuchukua miaka mia moja kukabiliana na hali hiyo duniani kote. Maeneo mengine ambayo yana vilipuzi vilivyofukiwa kwa wingi ni Chad, Afghanistan, Cambodia, Thailand, Azerbaijan, Bosnia-Herzegovina, Croatia, Uturuki, Iraq, Yemen na magharibi mwa jangwa la Sahara. Jitihada gani zimefanyika kukabiliana na changamoto hiyo? Princess Diana alitaka duniani kote kupiga marufuku watu kufanya uchimbaji wa madini katika maeneo ambayo yalifukiwa mabomu. Mwaka 1997, miezi mitatu tu baada ya kifo chake, nchi 122 zilisaini mkataba wa Ottawa, ambao ulikataza kutumiwa wa maeneo ambayo yalikuwa yamefukiwa mabomu. Nchi hizo zilipewa jukumu za kutokomeza mabomu yote yaliyofukizwa ardhini kwa kipindi cha miaka 10 na miaka minne ya kuteteteza. Sasa ni nchi zaidi ya 164 ambazo zimesaini mkataba huo, Uingereza ikiwa miongoni mwa nchi hizo. Ingawa Marekani, China, India na Urusi - ni miongoni mwa nchi 32 ambazo hazikusaini makubaliano hayo. Mataifa mengi hayakufikia makubaliano hayo kwa wakati na mengine bado yanafukia mabomu ardhini. Mabomu hayo ya ardhini yameripotiwa Myanmar ambayo haikusaini makubaliano hayo. Vilevile makundi mengine ya wanamgambo yasiyokuwa ya serikali kama Boko Haram wamekuwa wakiyatumia kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2014. Katika sehemu ya ziara yake kusini mwa Afrika, Mwana mfalme Harry ametembelea nchini Angola ili kuendeleza jitihada za kuondoa mabomu yaliyo ardhini. text: Rais Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt Hafez Ghanem walifanya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk Ghanem alisema benki hiyo inatoa fedha kwa ajili ya wasichana wote bila kujali hali zao, hivyo kuwatenganisha kwa kigezo cha ujauzito . Dk Ghanem amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema: "Mradi wa Tanzania haujajadiliwa. Lakini kwa mazungumzo tuliyofanya, utajadiliwa Serikali itakapotimiza masharti tuliyokubaliana. Baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, Rais John Magufuli alisema benki imekubali kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, nyumba za walimu na vifaa vya kufundishia. Awali chanzo ndani ya benki hiyo kiliiambia BBC Swahili kuwa sababu kuu mbili za zuio hilo zilikuwa ni mosi, uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua. Rais Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt Hafez Ghanem walifanya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam Pili, maboresho ya Sheria ya Takwimu yaliyopitishwa na Bunge la Tanzania Septemba 10 ambapo pamoja na mengine, inakataza usambazaji wa takwimu zinazolenga kupinga, kupotosha au kukinzana na takwimu rasmi za serikali. Adhabu ya kufanya hivyo ni faini ya Dola 6,000 au kwenda jela miaka mitatu. Vilevile, Dk Ghanem alisema walizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Takwimu na wameishauri Serikali kuhakikisha wadau wake wanakuwa huru kukusanya na kutumia takwimu. Siku ya Ijumaa Rais Magufuli alisema pesa hizo "hazijafyekelewa mbali" kama baadhi ya watu "wasiotutakia mema walivyosema." Rais Magufuli alinukuliwa akisema kuwa Ghanem alikwenda Tanzania kuthibitisha kuwa Benki ya Dunia haitaiacha nchi hiyo. Rais Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt Hafez Ghanem walifanya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam "Namshukuru Dkt. Hafez Ghanem na Benki ya Dunia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Tanzania, hizo Dola Milioni 300 ambazo baadhi ya watu wasiotutakia mema walisema zimefyekelewa mbali, anasema zitaletwa, na pia Benki ya Dunia imetoa Dola Bilioni 5.2 ambazo zinafadhili miradi mbalimbali ya elimu, nishati, barabara, kilimo, afya na maji, ni miradi mikubwa na mingi. Kwa hiyo amekuja kututhibitishia kuwa Benki ya Dunia haitatuacha." alisema Rais Magufuli. Mazungumzo kati ya Magufuli na Ghanem yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Tanzania Bi. Bella Bird. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Dk Hafez Ghanem amesema kuna masharti wamekubaliana kabla Tanzania haijapewa mkopo wa Dola 300 milioni za Marekani kwa ajili ya kuboresha elimu nchini. text: Watafiti wamesema ni muhimu kufanya mazoezi kwa kiwango cha wastani. Wanaume ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati , mbegu zao huwa na afya njema, kulingana na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi. Watafiti wamesema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani , kwa sababu mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume. Utafiti umebaini kwamba wale wanaoshiriki katika michezo kama vile ya uendeshaji baiskeli wanauwezo wa kupunguza kiwango cha mbegu zao za uzazi. Mbinu za kuongeza mbegu za kiume: Wanaume wote 261 waliosajiliwa katika majaribio hao hawakuwa na matatizo yoyote ya kiafya au shida ya uzazi. Walikuwa na kiwango sawa cha bengu za uzazi na zilizokuwa na afya, na walioishi maisha bila kufanya mazoezi. Wanaume hao walishirikishwa kwenye mradi mmoja kati ya miradi minne ikiwemo: Mafunzo ya mazoezi yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi zilizo na afya Mafunzo ya mazoezi yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi zilizo na afya huku waliofanya mazoezi yaliowastani walipata matokeo bora zaidi. Wanaume wote katika makundi matatu walipunguza uzani wao na walipata matokeo bora ikilinganishwa na wanaume ambao hawakufanya mazoezi kwa wiki 24 katika kipindi cha majaribio. Watafiti wamesema manufaa waliopata wanaume hao ni kutokana na kupunguza uzani katika makundi matatu ,wote walipunguza kiwango cha mafuta kutoka kwa miili yao. Watafiti tayari wamebaini kwamba unene kupita kiasi unaweza kusababisha shida za uzazi. Robo tatu ya wanaume hao walikuwa na uzani kupita kiasi. Huduma ya kwanza ya kuimarisha mbegu za uzazi ni gani? Kile kitu ambacho hakijajulikana ni iwapo mazoezi huchangia kuimarisha mbegu za uzazi. Hili ni jambo ambalo watafiti wanahitajika kuchunguza zaidi kwenye mahabara kuchunguza iwapo mazoezi huchangia katika ongezeko la mbegu za uzazi. Mtafiti mkuu Behzad Hajizadeh Maleki amesema, '' kulingana na matokeo hayo yamebaini kwamba kufanya mazoezi inaweza kuwa mbinu rahisi, na bora ya kuimarisha mbegu hizo za uzazi kwa wanaume ambao wanachangamoto za uzazi.'' ''Hi bayana kukiri kwamba wanaume wengine hawapati watoto si kwa sababu ya ukosefu wa viwango vya mbegu zao za kiume. Shida za uzazi kwa wanaume zinaweza kuwa kubwa na iwapo wanaume wataweza kubadili njia zao za kuishi zinaweza kukabiliana na shida hizo kwa urahisi.'' kwa mujibu wa Prof. Allan Pacey wa chuo kikuu cha Sheffield. Uingereza umewasihi watu wazima kufanya mazoezi kwa dakika 150 , kama vile kuendesha baiskeli , au kutembea kwa haraka, ama dakika 75 ya mazoezi yanayotumia nguvu kama vile kukimbia kila wiki. Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa wanasayansi text: Wenger akisherehekea Arsenal kufunga dhidi ya Burnley Alishuhudia vijana wake akicharaza Burnely 5-0 Jumapili. Alianza kazi 1996 kwa ushindi wa 2-0 Ewood Park dhidi ya Blackburn Rovers. Matumaini yake ya kuondoka na kikombe msimu wake wa mwisho yalizimwa Alhamisi waliopoondolewa na Atletico Madrid kutoka michuano ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League hatua ya nusu fainali. Jumapili, baada ya ushindi mkubwa wa Arsenal, ulikuwa ni wakati wa kutafakari kuhusu ufanisi wa Wenger katika klabu hiyo aliyoiongoza kwa miaka 22. Uwanja wa Emirates, mashabiki walibeba mabango ya kumsifu Wenger na kumshukuru. Kulikuwa na bango kubwa lililosema "Merci Arsene" (Asante Arsene) nje ya uwanja kwa Kifaransa. Wenger ni Mfaransa. Fulana za rangi nyekundu zenye ujumbe sawa na tarehe ziliwekwa kwenye kila kiti kati ya viti vyote 60000 vya uwanja huo. Wachezaji wa Arsenal na Burnley waliandaa gwaride la heshima kumkaribisha Wenger uwanjani. Meneja wa Burnley Sean Dyche alikuwa miongoni mwa walioandaa gwaride hilo. Arsenal wamefunga mabao 53 ya Ligi ya Premia msimu huu - mabao mengi zaidi tangu 2004/05 (54) Kumekuwa na kupanda na kushuka na shutuma kutoka kwa mashabiki lakini zaidi wengi waliangazia ufanisi wa mataji matatu ya Ligi ya Premia, pamoja na ufanisi mkubwa wa msimu wa 2003-04 walipomaliza msimu bila kushindwa. Wenger ameshinda pia vikombe saba vya FA. Wenger alimpatia shabiki mmoja tai yake baada ya kikao cha baada ya mechi Wakati wa Wenger kuzungumza, kwanza alimtakia uponaji wa haraka mpinzani wake mkuu wa muda mrefu Sir Alex Ferguson. Wenger alikuwa amepewa zawadi na Sir Alex siku saba zilizopita uwanjani Old Trafford, lakini sasa Sir Alex yupo hospitalini akiwa hali mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye ubongo wake. Akihutubu, mashabiki walikaa kimya. 'Nitawakosa sana' Wenger alikabidhiwa kikombe cha dhahabu kilichopewa klabu hiyo msimu wa 2003-04 baada ya kumaliza msimu bila kushindwa Wenger, huku bendera kubwa yenye picha yake ikipepea, alizungumza kwa upole na kwa kuonyesha hisia na kusema: "Nitawakosa sana." Wenger alisemaje? Baada ya mechi, Wenger alisema: "Haiwezekani kutohisi chochote, labda uwe wewe ni roboti. "Imekuwa ni miaka 22 ya kujitolea kikamilifu na ya umoja. Kwa jumla, ningependa kuwashukuru yote. Nilikuwa na bahati ya kufanya kazi hii kwa miaka 22 katika klabu moja na nashukuru sana kwa hilo. "Ni vigumu kutathmini msimu huu kwa yale ambayo timu hii imefanya. Nyumbani umekuwa uchezaji wa kushinda ligi, lakini ugenini uchezaji haujatosha. Tulifika pia fainali Kombe la Ligi na nusu fainali Europa League. "Mashabiki huenda wakaona mambo yakiwa tofauti msimu ujao, lakini watakuwa na meneja mpya na wanaweza kuendelea na kazi kwani msingi wa kila kitu upo." Wenger alisema pia kwamba atasalia kuwa shabiki wa Arsenal. "Mimi ni shabiki zaidi ya yote, na nitasalia kuwa shabiki," alisema. Shabiki kupewa tai Shabiki mmoja mtoto alitimiziwa matamanio yake baada ya kukaa adhuhuri yote akiwa ameinua bango bango kubwa lenye ujumbe: "Arsene - unaweza kunipa tai yako?" Wenger atahitimisha kazi yake Arsenal kwa mechi ugenini dhidi ya Huddersfield Town wiki ijayo. Mmoja wa wachezaji 83 waliofanikiwa kupanda kutoka kwa akademi hadi kwenye timu kubwa alitawazwa mchezaji bora wa mechi Wenger: Nataka mashabiki wafurahi Kabla ya mechi, Wenger alikuwa amesema: "Nilijaribu kujitolea kwa miaka mingi sana, kuwafanya watu wengi wafurahi na natumai kwamba watu wanaopenda klabu hii wataendelea kufurahi siku zijazo na kupata matamanio yao na wanayoyapenda. "Nimekutana na watu ambao kwao mimi ndiye meneja pekee wa Arsenal wanayemfahamu, kwa hivyo sasa ni fursa nzuri kwa klabu kuwa na watu wapya na mawazo mapya ya kuendelea kusongeza mbele klabu, jambo ambalo ndilo nimejaribu kulifanya maisha yangu yote." "Arsenal imekuwa klabu ambayo hufanikiwa kuunganisha utamaduni na kupiga hatua. Nilipofika hapa changamtoo kuu ilikuwa kupigisha hatua klabu na kuheshimu utamaduni. Nilipotua, Liverpool na Man United silikuwa ndizo klabu bora zaidi, na zilikuwa na wachezaji wazuri sana. Na hiyo ndiyo changamoto niliyokumbana nayo." "Ninajivunia kwamba kwa miongoni iliyopita, tulifanikiwa kudumisha utambulisho wa wachezaji wetu. Wachezaji wetu wana uhusiano wa kipekee na klabu. Sehemu ya maisha ya mchezaji na kukumbana na pahala maalum pa kipekee, na hapo ni Arsenal." Wenger, pia alisema hatachangia kuamua mrithi wake. "Sihusiki katika kuamua mrithi wangu atakuwa nani, hiyo si kazi yangu, lakini ninachoweza kumwambia ni kwamba anafaa kufanya analofikiria ndilo sahihi kwa klabu. Nimeongozwa na hilo maisha yangu yote hapa." Takwimu muhimu kuhusu Wenger London kaskazini Nini kinafuata? Arsenal watasafiri Leicester Jumatano nao Burnley wawe wenyeji wa Bournemouth Jumapili. Mechi ya mwisho ya Arsenal msimu huu itakuwa dhidi ya Huddersfield Town. Arsene Wenger aliaga uwanja aliosaidia kuujenga wa Emirates kwa ushindi, sawa na alivyofanya alipoanza kazi kama meneja wa Arsenal siku 7,876 zilizopita. text: Usiuchome mkate hadi ukawa na rangi ya hudhurungi Badala yake, wanasema zinafaa kupikwa hadi viwe na rangi ya manjano iliyokolea dhahabu. Wanasema hilo litapunguza ulaji wa kemikali ambayo huenda inachangia saratani. Acrylamide huzalishwa wakati vyakula vyenye wanga vinapochomwa au kukaangwa kwa muda mrefu katika kiwango cha juu sana cha joto. Wakala wa Viwango vya Ubora vya Chakula Uingereza (FSA) anapendekeza wapishi wafuate vyema maagizo wakati wa kupika na wasiache chakula kipate rangi ya kahawia. Shirika la kukabiliana na kansa la, Cancer Research UK, linasema hata hivyo kwamba uhusiano wa moja kwa moja kati ya Acrylamide na saratani miongoni mwa binadamu haujathibitishwa. FSA wanasema pia kwamba viazi na mboga aina ya karoti ziitwazo parsnips hazifai kuhifadhiwa kwenye friji. Hii ni kwa sababu viwango vya sukari kwenye mboga huongezeka zinapohifadhiwa kwenye viwango vya chini sana vya joto (mazingira baridi) na hivyo kuongeza kiasi cha Acrylamide inayozalishwa chakula kinapopikwa. Acrylamide hupatikana katika vyakula vingi na huzalishwa chakula kinapopikwa. Viwango vya juu vya kemikali hiyo hupatikana wakati wa mapishi, vyakula vyenye viwango vya juu vya wanga kama vile viazi, vibanzi (chipsi), mkate na parsnips, vinapookwa, kuchomwa au kukaangwa katika viwango vya juu sana vya joto. Viwango vya juu vya acrylamide hupatikana kwenye vyakula vyenye kiwango cha juu cha wanga vinapopikwa viwandani kwa joto ya zaidi ya nyuzi joto 120C, kama vile kaukau, mkate, biskuti, keki na kahawa. Aidha, huzalishwa nyumbani wakati wa kupika vyakula vyenye viwango vya juu vya wanga kama vile viazi, chipsi, mkate na pasnips kwa kuoka, kuchoma au kukaanga katika kiwango cha juu sana cha joto. Mkate unapochomwa na kutengeneza tosti, kwa mfano, hilo huzalisha acrylamide zaidi. Kadiri rangi ya tosti inavyokolea hudhurungi (kahawia), ndivyo kiwango cha acrylamide kinavyokuwa juu. Wakati wa chakula kubadilika rangi na kuwa cha hudhurungi, sukari, amino asidi na maji kwenye mkate hushikana na kutengeneza rangi na acrylamide - pamoja na ladha tamu na harufu nzuri. FSA wanasema hawana uhakika binadamu anafaa kula kiasi gani cha acrylamide bila kupata madhara. Hata hivyo, wanasema wanaamini kwamba binadamu kwa sasa wanakula chakula chenye kiwango cha juu cha acrylamide kupita kiasi. Watu wanashauriwa: Cancer Research UK wanasema kaukau (crisps), chipsi na biskuti huwa sana na acrylamide Mkate, chipsi na viazi pamoja na vyakula vingine havifai kuchomwa au kupikwa hadi kupata rangi ya hudhurungi, wataalamu wameonya. text: Madaktari wamekuwa kwenye mgomo wa siku 100 wakitaka serikali iwaongezee mishahara Hii ni baada ya mgomo wa madaktari nchini kenya, ambao umedumu siku mia moja na kuathiri vibaya huduma za afya nchini humo. Chama cha madaktari kikiongozwa na mwenyekiri wake Oroko Samuel, kuliungana na waziri wa Afya Cleopha Mailu kwenye ofisi za magavana wakati wa kutiwa sahihi makubaliano hayo. Makubaliano hayo yalitiwa sahihi mbele ya viongozi wa kidini. Katibu wa chama cha madaktari Ouma Oluga Awali kulikuwa na hofu wakati madaktari walikataa kuingia ofisi ambapo makubaliano hayo yangetiwa sahihi, wakilalamikia utata wa vipengee fulani. Madaktari walianza mgomo huo wakidai kuwa serikali imeshindwa kutimiza makubaliano waliyoafikiana, ya nyongeza ya mishahara yao na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya kazi. Wiki iliyopita rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alitangaza kuwa madaktari wangechukuliwa hatua iwapo hawangemaliza mgomo wao. Serikali ya Kenya pamoja na madaktari nchini humo, hatimaye wametia sahihi makubaliano ya kurudi kazini. text: Shughuli za baharini zilizofungwa ni pamoja na uvuvi, safari za meli na vyombo vyengine vya usafiri baharini, kuanzia na kulingana na tangazo la tahadhari shughuli hizo zimefungwa '' kuanzia Aprili 24, 2021 saa tatu (3:00) asubuhi, mpaka itakapotolewa taarifa nyengine na mamlaka zinazohusika, ikiwa ni sehemu ya tahadhari ya kutokea kimbunga kilichopewa jina la 'Jobo'. Uvuvi ni mojawapo ya shughuli za baharini zilizositishwa Zanzibar kufuatia tahadhari ya kimbunga ''jobo'' Wakati huo huo taarifa ya Mamlaka ya Hali ya hewa nchini Tanzania kuhusu mwenendo wa kimbunga jobo katika Ppwani ya Tanzania imewashauri kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza. Kulingana na Mamlaka hiyo mwenendo wa kimbunga "Jobo" kilichopo bahari ya Hindi kwa sasa kipo umbali wa kilomita 200 mashariki mwa kisiwa cha Mafia. Imesema kimbunga hicho kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani. ''Hivyo, "Jobo" kwa sasa ni kimbunga hafifu'', imesema Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika taarifa yake. Uwepo wa kimbunga hafifu baharini, unatarajiwa kusababisha mawimbi makubwa Kimbunga jobo kinachosafiri kwa kasi ya kilometa 18 kwa saa baharini, kinatarajiwa kusababisha vipindi vya mvuakubwa katika maeneo machache hususan ya ukanda wa Pwani kadri kinavyosogea nchi kavu kwa siku ya leo tarehe 24 na kesho 25 mwezi Aprili, 2021 Uwepo wa kimbunga hafifu baharini, unatarajiwa kusababisha mawimbi makubwa. Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani (ikiwemo kisiwa cha Mafia), Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesitisha shughuli zote za baharini kuanzia Jumamosi ikiwa ni sehemu ya tahadhari ya kutokea kwa kimbunga kilichopewa jina ''jobo'' text: Raisi wa Rwanda Paul Kagame amekana shutuma kuwa anadukua simu za wapinzani wake Akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali siku ya Ijumaa, raisi Kagame amesema anatamani angekuwa na uwezo wa kununua teknolojia hiyo ''kujua zaidi'' kuhusu adui zake. Raia wa Rwanda anayeishi nchini Uingereza aliiambia BBC juma lililopita kuwa anaamini kuwa alikuwa muathiriwa wa udukuzi uliofanyika kwa WhatsApp. Faustine Rukundo alisema yeye na wafuasi wenzake wa chama cha Rwanda National Congress- kundi linaloipinga serikali ya Rwanda walikuwa wanalengwa kwa kutumia huduma za ujumbe. Maabara ya Citizen, kundi la utafiti katika Chuo Kikuu cha Toronto, imethibitisha kuwa alikuwa anafuatiliwa. WhatsApp imeishutumu Kampuni ya NSO Group kwa kuweka programu kwenye simu karibu 1,400 kwa nia ya kufanya upelelezi. Programu yake ya Pegasus inaweza kufanya kazi hiyo hata ikiwa mbali. Idadi kubwa ya watu wanaofuatiliwa wanadaiwa kuwa raia wa Rwanda. Kampuni ya NSO Group imekana madai dhidi yao, ikisema kuwa programu ya Pegasus imekuwa ikiuzwa kwa wateja waliohakikiwa na si wenye nia mbaya. WhatsApp ni moja ya mitandao mikubwa duniani inayotumia programu tumishi ya kutuma na kupokea ujumbe papo kwa kwa papo Kilichotokea kwa Rukundo Kwa miezi kadhaa Rukundo aliamini yeye na wenzake walikuwa kati ya watu karibu 1,400 waliokuwa wamelengwa na wadukuzi kupitia WhatsApp. Lakini ilithibitishwa juma lililopita baada ya kupokea simu kutoka maabara ya Citizen mjini Toronto. Kwa miezi sita, shirika lilikuwa likifanya kazi na Facebook kuchunguza udukuzi na kubaini walioathirika. Watafiti wanasema ''Katika uchunguzi maabara ya Citizen imegundua visa 100 vya udhalilishaji vilivyowalenga watetezi wa haki za binaadamu na waandishi wa habari katika nchi karibu 20 dunani. Bwana Rukundo aliyejipambanua kwenye ukurasa wake wa WhatsApp ni mkosoaji wa utawala wa Rwanda, sambamba na wengine wa kaliba yake walikuwa walengwa. Mtandao wa udukuzi ulijengwa na kuuzwa na kampuni moja yenye makao makuu yake nchini Israel NSO na kuuza kwa serikali mbalimbali duniani. Faustin Lukundo amedai kudukuliwa kupitia mtandao wa WhatsApp Wadukuzi walitumia programu za kuwapeleleza waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binaadamu, lakini tukio hilo kwake liliifanya familia yake kuogopa mno. ''Kwakweli , hata kabla sijathibitiha hili, tulipigwa na butwaa na kuingiwa na hofu. Inaonyesha kuwa walikua wakiifuatilia simu yangu kwa karibu majuma mawili na waliweza kufikia kila kitu,'' aliiambia BBC. ''Si tu shughuli zangu wakati huo lakini historia za mawasiliano yangu ya barua pepe na watu ninaowasiliana nao na kuzungumza nao.Kila kitu kilikua kinanaswa, Kompyuta, simu zetu, hakuna kilichokuwa salama.Hata tulipokua tukiongea, huenda walikua wanasikiliza pia.Bado ninahisi siko salama.'' Bwana Rukundo alitoroka Rwanda mwaka 2005 baada ya wakosoaji wa serikali kukamatwa na kutupwa gerezani. Alipambana ili mke wake aachiwe baada ya kutekwa na kushikiliwa kwa miezi miwili. Facebook, mmiliki wa WhatsaApp, anajaribu kuishtaki kampuni ya NSO. NSO imekana shutuma dhidi yake. Programu hiyo ya simu inatumiwa na watu karibu bilioni 1.5 katika nchi 180. Unaweza kusoma zaidi Raisi wa Rwanda Paul Kagame amejibu shutuma kuwa amekuwa akiwapeleleza wapinzani wake kupitia simu zao, amesema teknolojia inayohitajika kufanya hivyo ni ghali sana. text: Zanzibar, Tanzania Aliyetoa ripoti hiyo kwa niaba ya serikali alikuwa katibu kiongozi, Abdulahamid Yahya Mzee baada ya kupokelewa na Rais wa Zanzibar Dr Ali Muhammed Shein Novemba 30 mwaka jana kutoka kwa Jaji Abdulhakim Ameir aliyeongoza jopo la watu 10. Yahya akielezea sababu zilizogunduliwa na tume kuwa chanzo cha kuzama kwake ni kujaza abiria kupita kiasi, mizigo kuwekwa vibaya, matatizo ya kiufundi yaliofanya kiwango cha upakizi kisijulikane, kuingia maji na uzembe wa nahodha kutoomba msaada. Pia imetoa hesabu ambayo sasa itakuwa rasmi ya watu waliopotea na waliozama ambapo inasimama kuwa 1370. Tume imesema abiria waliopakiwa katika meli hiyo walikuwa 2,470 wakati uwezo wake ulikuwa ni watu 620 ikiwa ni karibu kidogo ya mara nne zaidi ya uwezo wake. Tume imesema ubovu wa meli hiyo ulijulikana tokea mwezi Julai, miezi miwili kabla ya kuzama kwake kutokana na ukaguzi uliofanywa na taasisi ya usalama wa bahari Sumatra, lakini bado meli hiyo ilipewa leseni. Maiti za watu waliofariki kwenye ajali ya MV Spice Islander Taarifa imesema kuna mnyororo mrefu sana wa watu waliokuwa na dhamana lakini walishindwa kufanya wajibu wao kuanzia maafisa wa meli hiyo, maafisa wa bandari na pia maafisa kama vile wa polisi na taasisi ya kukusanya mapato TRA, ambao wanatuhumiwa kupokea fedha na kupenyeza abiria. Tume hiyo imependekeza watu kadhaa washtakiwe na imetaja makosa iliyoona yanawahusu na polisi waliwatia mbaroni watu kadhaa sku ya Jumatano katika kutekeleza hilo. Watu muhimu watakaoshtakiwa ni pamoja na Abdula Muhammed mrajis wa meli, Haji Vuai Ussi mkurugenzi wa usafiri wa baharini, Juma Seif mkaguzi wa meli na wamiliki watano wa kampuni za Visiwani Shipping na Al Gubra Marine Services. Pia nahodha Abdullah Kinyaiite anatakiwa kushtakiwa lakini serikali alikiri katibu kiongozi hajulikani alipo na tume haikusema yuhai au la. Jana polisi ilitia kishindo mji wa Zanzibar kwa kamata kamata ya watuhumiwa hao, lakini haikujulikana iwapo leo walipelekwa mahakamani au la au ni lini taratibu zitakamilika na kusomewa mashtaka yao. Mwandishi wetu wa Zanzibar Ally Saleh amesema ripoti hiyo pia inataja orodha ya watu ambao wameonekana wanafaa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mmoja wao ni mkurugenzi wa shirika la bandari Mustafa Aboud Jumbe ambaye kama wengine wataondoshwa sehemu zao za kazi mara moja. Waliojiokoa kwenye ajali Zanzibar Kwa bahati meli hiyo ilikuwa imewekewa bima isipokuwa bima hiyo haitahusu mizigo kwa sababu eneo hilo halikuwa limekingwa, lakini bima hiyo itasaidia kulipa jamaa za watu waliofariki dunia na tume imependekeza angalau kiwango cha shs 10,000,000 kwa kila mtu aliyefariki dunia kwa maana ya pia waliopotea. Pia serikali imesema itazigawa kwa waathirika na jamaa waliofiwa fedha zote zilizokusanywa ikiwa ni michango mara taratibu zitapokamilika lakini kazi hiyo sasa ni rahisi kwa vile orodha kamili na iliyohakikiwa imeshapatikana. Serikali imesema ripoti hiyo itachapishwa kwa uwazi na ukamilifu na kuweza kusomwa na kila mtu ikiwa na pamoja na kwenye mtandao. Serikali ya Zanzibar leo imetoa ripoti ya uchunguzi wa kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hapo Septemba 10, 2011 eneo la Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja. text: Luteni Malick Jatta alikuwa anatoa ushahidi mbele ya tume ya ukweli na maridhiano TRRC inayochunguza maovu yaliotekelzwa chini ya utawala wa miaka 22 ya Jammeh. Hapo awali alikiri kuhusika katika mauaji ya mwandishi Deyda Hydara mnamo 2004 kwa agizo la kiongozi huyo wa zamani Gambia. Jammeh - ambaye sasa anaishi uhamishoni huko Guinea ya Ikweta - amekana kuhusuika katika vifo vya wahamaiji na mwandishi habari huyo. Deyda Hydara alikuwa muasisi mwenza na mhariri msimamizi wa gazeti la The Point nchini humo. Jatta alisema alilipwa $1,000 kutekeleza maujai hayo, licha ya kwamba ni mpaka siku ya pili ambapo aligundua kwamba alikuwa amemuua Hydara. Jammeh alitorokea Guinea ya Ikweta mnamo 2017 baada ya kushindwa katika uchaguzi. Waathiriwa wa utawala wa jammeh sasa wanapata fursa ya kuzungumza Gazeti la the Point, ambako Hydara alikuwa akifanya kazi kablaya kuuawa mnamo 2004, limeangazia kwamba imechukua miaka 15 kutambua nani aliyemuua mwandishi huyo. Katika mtandao wake, gazeti hilo limeweka bango tangu wakati huo lililoambatana na swali, "Ni nani aliyemuua Deyda Hydara?". Gazeti hilo halikutoa tamko jingine kuhusu taarifa hii ya sasa. Hydara aliwahi pia kulifanyia kazi shirika la habari la AFP na waandishi wasiokuwa na mipaka. Kukiri kwa Luteni Jatta kunawiana na matokeo ya wanaharakati wa haki za binaadamu kama Human Rights Watch. Ripoti yake imesema wahamiaji wa Afrika magharibi waliokiuwa wanaeleeka Ulaya walikamatwa na kuuawa baada ya boti walilokuwa wamepanda nchini Senegal kuishia nchini Gambia. Yahya Jammeh ni nani? Mwandishi wa Sierra Leone- na Gambian Ade Daramy anasema raia wa Gambia wanajaribu kupokea maovu yaliotekelezwa wakati wa utawala uliokuwepo. Lakini anaeleza kwamba kuna kitu ambacho kinawaondolea raia hao wa Gambia tabasamu, vikao vya tume hiyo ya ukweli na maridhiano (TRRC). Tume ya TRRC iliundwa kubaini "Rekodi ya historia ya hali, sababu na kiwango cha ukiukaji wa haki za binaadamu uliotekelezwa katika kipindi chaJulai 1994 hadi Januari 2017" - kipindi maalum kinachojumuisha utawala wa miaka 22 wa kiongozi huyo aliye uhamishoni sasa. Daramy anafichua kwamba kilichobainika kutoka kwenye kikao hicho na kinachoendelea kuficguka ni kuchambuliwa gamba la maovu na muamko usiovutia vile kwa tiafa - unaolilazimu kujitathmini kwa mtazamo mpya na pengine mkali. Mwanajeshi mmoja nchini Gambia amekiri kuhusika katika mauaji ya wahamiaji wapatao 50 mnamo 2005 kutokana na agizo la rais Yahya Jammeh, anayearifiwa kuwa alihofia kwamba wanaume hao walikuwa na nia ya kumpindua. text: Vitu kumi ambavyo huenda hauvijui kuhusu Google Chochote unachokitafuta liwe jina la kitu fulani au jinsi ya kuandika jina fulani au jina la eneo fulani bila shaka ni lazima utafute kwenye Google. Kwa kukadiria Google hushughulikia karibu mambo 40,000 kwa sekunde moja, hiyo ni sawa na mambo bilioni 3.5 kwa siku. Google sasa imegeuka kuwa sio eneo tu la kutafuta majina lakini pia sehemu muhimu kwa matangazo na mkusanyaji wa taarifa za watu. Kila wakati unapofanya kitu fulani, Google inajua kuhusu tabia zetu. Lakini wewe unafahamu mambo yapi kuhusu Google? Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukushangaza. 1. Jina Kuliandika vibaya jina kati ya marafiki Google ni nini? kwa kweli neno Google halimaanisha chochote. Lilitokana na kuandikwa vibaya kwa jina la 'googol' Kuna madai kadhaa kuhusu labda vile mhandisi au mwanafunzi aliweza kuibuka na jina hilo. Makosa hayo ya uandishi yalichangia kupatikana nene hilo, na mengine ni historia. 2. 'Backrub' Awali waalipa Google jina jina 'Backrub'. Waanzilishi wa Google Larry Page na Sergey Brin awali waliipa Google jina jina 'Backrub'. Haikumaanisha kisugua mgongo lakini ilimaanisha mfumo wa kuorodhesha vitu. 3. Mchezo Usishangae hamna tatizo lolote na macho yako Google haihusu tu biashara. Kuna mchezo pia. Andika jina "askew" kwa Google na ujionee... 4. Mbuzi Kuna lishe kwa mbuzi huko Google Google inasema inaunga mkono mazingira kwa hivyo moja ya njia ni kubadilisha mashine za kufyeka na mbuzi. Bustani kubwa za makao makuu ya Googleplex huko Mountain View, California, zinahitaji watu wa kuzitunza kila wakati, kwa hivyo kile unachokiona ni karibu mbuzi 200 wanaozunguka huku wakitafuta lishe. 5. Biashara inayokua Google imekuwa ikinunua kampuni kila wiki tangu mwaka 2010. Baada ya kuunda kampuni za GMail, Google Maps, Google Drive, Google Chrome...Google imekuwa ikinunua kampuni kila wiki tangu mwaka 2010. Hautajua lakini kampuni kama Android, Youtube, Waze na AdSense zinamilikiwa na Google na kuna zingine 70. 6. Nembo Nembo ya kwanza ya Googe au Doodle ilikuwa na nia ya ujumbe wa tarehe 30 Agosti mwaka 1998. Nembo ya kwanza ya Google au Doodle ilikuwa na nia ya ujumbe wa tarehe 30 Agosti mwaka 1998. Hilo liliamuliwa wakati Larry na Sergey walikwenda huko Nevada kwa warsha moja iliyofahamika kama (Burning Man Festival) ndipo wakataka watu wafahamu kuwa hawakuwa karibu kuwahudumia. Tangu wakati huo imekuwa kawaida kwa Google kufanya hivyo kila mara kuashiria siku fulani au watu fulani. 7. Fursa iliyopotezwa lakini si kwa Google Mgao katika soko Mwaka 1999 Larry na Sergey walijaribu kuiuza Google kwa dola milioni moja lakini hakuna mtu aliyetaka kuinunua hata licha ya bei kushushwa. Google kwa sasa ina thamani ya dola bilioni 300. Kuna mtu anajutia sana. 8. Kauli mbiu 'Usiwe muovu' ilikuwa moja ya kauli mbiu ya kwaza ya kampuni hiyo. 'Usiwe muovu' ilikuwa moja ya kauli mbiu ya kwanza ya kampuni hiyo. Iwapoa kampuni imedumisha hilo au la ni wewe uamue. 9. Chakula ni muhimu sana Kuna chakula kila wakati huko Google Kulingana na jarida la Forbes, mwanzilishi wa Google Sergey Brin aliamua mapema kuwa hakuna ofisi ya Google inaweza kuwa umbali wa mita 60 kutoka mahala kuna chakula. Kuna uvumi kuwa siku za mwanzo chakula bora kwenye kampuni hiyo kilikuwa ni kitu kilikuwa kinaitwa "Swedish Fish", lakini siku hizi wafanyakazi wa Google, (ambao ni mimi na wewe) wanaweza kupata vyakula vizuri kama kahawa ya kiwango cha juu. 10. Rafiki mkubwa wa Google. Mbwa na rafiki mkubwa wa Google Wafanyakazi wa Google au wasio wafanyakazi huruhusiwa kupeleka mbwa wao kazini lakini wawe wamefunzwa vizuri wasije wakachafue ofisi. Unakumbuka maisha kabala ya Google? ulifanya nini wakati ulihitaji kutafuta taarifa fulani kwa haraka? text: Alijizolea tuzo mbalimbali enzi za uhai wake Muigizaji huyo veterani alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kufariki kwake. Taarifa ya ikulu imesema King Majuto amefariki dunia majira ya saa 1:30 Jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Tayari watu maarufu ndani na nje ya Tanzania wametuma salamu za rambirambi kwa familia yake kupitia mitandao ya kijamii, miongoni mwao Rais wa Tanzania John Magufuli. Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo. "King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake," amesema Rais Magufuli. Kiongozi huyo wa nchi alimjulia hali msanii King Majuto alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam 31 Januari, 2018. Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma-Ujiji Zitto Kabwe amesema: "Nimepokea Taarifa ya msiba wa Mzee Majuto kwa masikitiko makubwa sana. Tumshukuru Mola kwa uwezo wake na kuwaombea wafiwa kwa mola awape subra." Msanii maarufu wa bongo fleva Naseeb Abdul akijulikana zaidi kama Diamond Platnumz, ameandika kuwa Mzee Majuto ni mfalme ambae ataishi mioyoni mwa wengi daima. Msanii Ali Kiba naye ameandika: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika Mzee Wetu Amri Bin Athuman (King Majuto) yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na dhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu. Amin." Vanessa Mdee ni miongoni mwa walioandika ujumbe wa kumuomboleza kwenye mitandao ya kijamii Akiwa kama mfalme wa tasnia ya maigizo ya uchekeshaji nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mzee Majuto aliweza kujizolea umaarufu mkubwa kupitia namna ambavyo alikua akiigiza na kuwa miongoni mwa watu wenye mvuto mkubwa miongoni mwa wasanii. Aliweza kuvaa kila aina ya uhusika Afya ya Mzee Majuto ilizorota zaidi kuanzia mwaka 2018 ambapo awali alipelekwa nchini India kwa matibabu baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli na wapenzi wa sanaa ya Mzee Majuto kumchangia ili kunusuru uhai wake kabla ya baadae kurejea nchini Tanzania. Wiki chache zilizopita taarifa za uongo za kifo chake zilisambaa mitandaoni kabla ya familia yake kukanusha mara kwa mara. Majuto aliyezaliwa mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania mwaka 1948 alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka tisa. Amecheza kwa mafanikio makubwa kwenye tamthiliya kama vile Mama Nitilie, Kondakta na nyinginezo nyingi zilizompa umaarufu mkubwa. Akiwa na waziri wa sanaa Tanzania Harisson Mwakyembe ambaye alikua mstari wa mbele kupigania maslahi yake Kabla ya kifo chake tayari alikwisha wasamehe baadhi ya waandaaji na wasambazaji ambao inasemekana walikua wakimdhulumu mamilioni ya fedha baada ya waziri anayehusika na sanaa nchini Tanzania Harisson Mwakyembe kutishia kuwashitaki watu hao. Atabaki kuwa nembo ya tasnia ya uigizaji wa vichekesho nchini Tanzania hata baada ya kifo chake. Msanii mkongwe na maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefariki dunia wakati akipokea matibabu kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Dar es Salaam Tanzania. text: Mashambulizi ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani nchini Yemen yalianzishwa na Rais Obama Hata hivyo jeshi la Marekani linasema kuwa kamando wake mmoja, aliuwawa, na wengine watatu walijeruhiwa, katika shambulio dhidi ya makao makuu ya al-Qaeda nchini Yemen. Ndege ya jeshi la Marekani iliyotumika katika shambulio hilo, ilielezewa kuwa ilitua kwa kishindo, na kujeruhi wanajeshi zaidi. Helikopta aina ya Apache ya jeshi la Marekani Jeshi linasema wapiganaji 14 waliuwawa, katika shambulio hilo lilofanywa alfajiri, katika jimbo la al-Baida. Lakini watu wa huko, wanasema idadi ya waliouwawa ilikuwa kubwa zaidi, na wanasema raia kadha pia waliuwawa. Wadadisi wanasema, shambulio hilo la kwanza la aina yake, tangu Rais Donald Trump kuapishwa, litaonekana kama ishara ya lengo lake la kutumia nguvu zaidi dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Kiislamu. al-Baida Yemen Ripoti kutoka Yemen, zinaeleza kuwa shambulio, lililofanywa na makamando wa Marekani, limeuwa watu kama 30, wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Qaeda na raia. text: Maafisa wanasema wamewapata watu 163 baada ya boti hilo kuzama kutoka pwani ya Misri Boti hilo lilikuwa limewabeba kati ya wahamiaji 450 na 600 lilipozama kilomita 12 kutoka mji wa bandari wa Rosetta. Lilikuwa linawasafirisha raia wa Misri, Syria, Sudan, Eritrea na hata wahamiaji wa Somalia. Maafisa wanasema kiasi ya watu 163 wameokolewa lakini walionusurika wameiambia BBC kuwa mamia wengine huenda wamezama. Boti linalozama katika picha kutoka operesheni ya uokozi ya Umoja wa Ulaya - takriban watu 30 walizama Wanasema wasafirishaji haramu wa binaadamu walimlazimisha yoyote aliyetaka makoti ya kuelea majini kulipa pesa zaidi . Washukiwa wanne wamekamatwa na polisi kwa kushukiwa kwa mauaji yasio ya makusudi na usafirishaji haramu wa binaadamu, maafisa wa Misri wanasema. Boti hilo lililo ondolewa kutoka pwani kwa siku tano wakati wahamiaji zaidi walipoletwa, linasemekana kuzama baada ya kundi la mwisho la watu 150 kujazwa ndani. Mkasa huo unatokea wakati shirika la kulinda mpaka wa Umoja wa Ulaya limeonya kuwa idadi inayoongezeka ya wahamiaji wanaoelekea Ulaya wanatumia Misri kama eneo la kuondoka. Zaidi ya watu 10,000 wamefariki wakivuka bahari ya Mediterrania kuelekea Ulaya tangu 2014, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Idadi ya miili ya watu iliopatikana baada ya boti la wahamiaji kuzama kutoka pwani ya Misri Jumatano imefika 162, huku operesheni ya kutafuta miili zaidi ikiendelea. text: Kim Jong Nam, marehemu kwa sasa Nao polisi nchini Malysia wamesema kwamba Kim Jong Nam alishambuliwa siku ya Jumatatu wakati alipokuwa akitarajia kuabiri kuelekea Macao. Kabla hajafariki dunia wakati akipelekwa hospitalini, alitoa maelezo kuwa alivutwa kutoka kwa nyuma na kumwagiwa kitu kioevu usoni mwake. Uchunguzi wa kitabibu utafanywa ili kuweza kubaini chanzo cha kifo, huku kukiwa na tetesi kuwa huenda kimiminika alichomwagiwa usoni huenda ikawa ni sumu. Chanzo kutoka katika serikali ya Marekani kinasema kwamba wanaamini kwa dhati kuwa Bw Kim, aliyekuwa anaishi uhamishoni, aliuawa na mawakala kutoka Korea Kaskazini. Mwaka 2001 Kim alikamatwa akijaribu kuingia Japan akitumua pasipoti bandia. Aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kuzuru eneo la burudani la Disneyland mjini Tokyo. Kim alikwa akionekana kama mtu ambaye angemrithi babake lakini kitendo hicho kilisababisha wao kutofautiana. Kim Jong-nam alitumia muda wake mwingi nje ya Korea Kaskazini Kim Jong-nam ndiye mtoto wa kwanza wa kiume wa Kim Jong-il, ambaye aliitawala Korea Kaskazini kuanzia mwaka 1994 hadi wakati wa kifo chake mwaka 2011. Baada ya nduguye mdogo wa kambo kuchukua uongozi wa Korea Kaskazini wakati babake alifariki mwaka 2011, Kim Jong-nam hakuoneka saana na alitumia muda wake mwingi nje ya nchi hasa Macau , Singapore na China. Aliyekuwa ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, inaarifiwa kuwa chanzo cha kifo chake ni mauaji dhahiri yaliyotokea katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia. text: Hasunga amewasili leo mkoani Mtwara mara baada ya kuapishwa na rais John Magufuli jana Ikulu jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Charles Tizeba aliyefutwa kazi kutokana na kadhia ya korosho. Rais Magufuli jana alitangaza rasmi kuwa serikali itazinunua korosho zote kwa kupitia benki ya kilimo na uratibu wa jeshi baada ya wafanyabiashara kuonekana wakisuasua. "Hatima ya wafanyabiashara wa korosho labda wasuburi tukishanunua hizi korosho ndio tutakaa nao tuamue. Tulishakaa nao vikao vingi, tukakubaliana na bei elekezi, wao hawakutaka kuzingatia. Wanadhani serikali labda hatuwezi ndio maana tunanua wenyewe sasa, halafu ndio tufikirie sasa namna ya kushirikiana nao," amesema Hasunga na kuongeza: "Tunajua kuwa wanaumuhimu, lakini si umuhimu wa kuringa ama kutaka kununua kwa shilingi 1,500 au 2,000..." Hasunga pia amesema maamuzi ya serikali yanalenga kuongeza kipato kwa mkulima, kutoa ajira mpya kwa kuzibangua korosho ndani ya nchi na pia kuliongezea thamani zao hilo kwa kulifungasha kabisa kabla ya kusafirisha nje ya nchi na kuongeza pato la taifa. Waziri huyo amesema kuwa wanajeshi wanatarajiwa kuwasili muda wowote hii leo kuanza kuratibu mfumo mpya wa manunuzi ya zao hilo. Hali imepoa kidogo leo Mtwara hakuna kazi Awali, wanawake wajasiriamali wanaoshughulika na kubangua korosho nchini Tanzania wameulalamikia mpango mpya wa ununuzi uliotangazwa. Wanawake hao wanasema kuwa hatua hiyo itawanyima fursa ya ununuzi wa kiwango cha kawaida kwa lengo la biashara ndogo ndogo kwani, wana wasiwasi kwamba huenda jeshi likabadili kabisa mfumo wa uuzaji korosho tofauti na walivyozoea.Hapo jana ikiwa ni kabla ya muda uliowekwa kwa wafanyabiashara kujiorodhesha ili wanunue korosho ya wakulima mkoani Mtwara, rais alibadili mawazo yake na kuamua kwamba wafanya biashara hao hawatanunua tena korosho hiyo, akihoji kwamba walikuwa wapi. "Yani huu mpango ambao rais ameuweka katika uuzaji wa korosho Mtwara kusimamiwa na jeshi, sisi wafanyabiashara wadogo kiukweli wametuangusha", amedai mmoja wa wanawake ambaye ni maarufu kwa biashara hiyo. "Mimi ni mjasiriamali mdogo ambaye nnanunua gunia moja au mbili katika kipindi cha msimu wa korosho , nabangua na kuuza. Sasa wameweka usimamizi wa jeshi , nitanunua wapi? Nina miaka 15 ninafanya hii shughuli nnaendesha maisha na nnasomesha watoto"... amelalamika mjasiriamali mwingine mwanamke. Leo ni siku ya pili Baada ya serikali ya Tanzania kukabidhi Jeshi la nchi hiyo, kuratibu shughuli za ununuzi wa korosho katika mkoa ulioko Kusini mwa nchi hiyo, Mtwara. Hatua hiyo inafuatia Rais John Magufuli kusitisha mpango wa makampuni kununua zao hilo kwa kile alichodai wamekuwa na bei hazina tija kwa wakulima . "Kiukweli nimevurugwa kwa msimamo huu uliowekwa, kwa sababu sisi ni wajasiriamali wadogo ambao hatuna uwezo wa kununua tani moja, tani mbili ..tunajikwamua tu kidogo kidogo. Wanasaidiwa wakulima lakini sisi wajasiriamali wadogo wadogo tutaishije?" Kwa sasa korosho zinauzwa kwa gharama ya shilingi 3,300 badala ya shilingi 3000 za kitanzania ambayo ni sawa na dola 1.43. Jumamosi, Rais Magufuli aliwatimua mawaziri wawili katika baraza lake, Waziri wa Kilimo Charles Tizeba na Waziri wa Biashara Charles Mwijage. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Rais amesema anataka kuhakikisha maelfu ya wakulima wanapata faida kwa mazao yao na kuhakikisha kipato kutokana na usafirishaji wa korosho katika mataifa ya nje. Lakini wakosoaji wanasema huenda ni hatua ya kujaribu kutafuta uungwaji mkono katika eneo la Mtwara, eneo lililo ngome ya upinzani. Mwansiasa wa upinzani Zitto Kabwe amesema serikali inastahili kupata ridhaa ya bunge kununua korosho hizo. Kadhalika rais Magufuli ameivunjilia mbali bodi ya usimamizi wa zao la korosho Tanzania na kutegua uteuzi wa mwenyekiti wake, Anna Abdallah. Waziri mpya wa Kilimo nchini Tanzania Japhet Hasunga ameiambia BBC kuwa serikali itafikiria hatima ya wafanyabiashara wa korosho mara baada ya kumaliza ununuzi wa zao hilo. text: Mende wa Diploptera puncata hujifungua Wamegundua kwamba chembe za protini za maziwa kwenye mende zina virutubisho "vingi ajabu”. Wanasema vinasema kutumiwa kama tembe ama chakula chenye virutubisho vya protini kwa kiwango cha juu. Wanasayansi katika taasisi ya sayansi ya seli katika mji wa Bengaluru, wamefanya ugunduzi huo baada ya kutafiti muundo wa chembe za protini zinazopatikana katika utumbo wa aina ya mende wajulikanao kama Diploptera puncata, ambao ndio pekee hujifungua. Ingawa mende wengi kwa kawaida hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera puncata huwa wanatengeneza aina fulani ya maziwa yenye protini kwenye utumbo, ambayo hutumiwa kulisha watoto wake. Chembe moja ya protini hiyo inakadiriwa kuwa na kiwango mara tatu cha nguvu ya mwili ikilinganishwa na kiasi sawa cha maziwa ya nyati. Aidha, chembe hizo zina nguvu mara nne kushinda maziwa ya ng’ombe. “Ni chakula kamili, unapata protini, mafuta na sukari,” amenukuliwa mmoja wa watafiti waliohusika, Sanchari Banerjee, na gazeti la The Times of India. Mende huliwa katika maeneo mengi duniani hasa Mashariki ya Mbali Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la International Union of Crystallography. Ramaswamy anasema kwa kutumia ufahamu wao wa muundo wa protini hizo, wanaweza kutumia hamira kuzalisha chembe kama hizo kwa wingi kwenye maabara. Isitoshe, anasema muundo wa chembe hizo unaonesha matumaini kwamba zinaweza kuundwa na kutumiwa katika vidonge vya dawa. Wengi huenda wakawa hawawezi kuwavumilia mende, hata kuwatazama pekee, lakini wanasayansi nchini India wanasema huenda mende wakatoa tumaini kwa binadamu, katika lishe. text: Park Geun-hye Msemaji wa serikali amesema kuwa takriban dawa 400 zinazotumiwa kutibu tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume zilinunuliwa kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na tofauti ya hali ya anga Afrika mashariki,ijapokuwa dawa hizo hazikutumika. Hayo yanajiri huku kukiwa na shutuma kwamba kiongozi huyo wa Korea Kusini aliruhusu urafiki mrefu kushawishi maamuzi yake kuhusu maswala ya kitaifa na kile rais huyo alichovaa. Waandamanaji wakipinga uongozi wa rais Park Geun Hye Afisi ya rais imethibitisha ilinunua dawa 364 za viara na dawa nyengine kama hizo ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika ziara ya Afrika mashariki,ijapokuwa dawa hizo hazikutumika. Mwandishi wa BBC Evans aiyepo mjini Seoul anasema kuwa ugunduzi huo utazidisha lawama zinazomkabili rais huyo . Wakorea wengi wanaamini kwamba bi Park anaishi katika maisha tofauti swala ambalo litaongeza shinikizo za kisiasa kwa yeye kujiuzulu. Dawa za Viagra zilizonunuliwa na afisi ya rais huyo wa Korea Kusini Uvumi wa awali miongoni mwa raia wa Korea unadai kuwa bi Park huenda alihusika na ibada ya kimila na rafikiye bi Choi. Bi Choi ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa bi Park ni mwana wa Choi tae-min kiongozi wa kidini ambaye alihusishwa na babake bi Park aliyekuwa rais Park Chung -hee. Ushahidi uliobaini kwamba dawa hizo zilinunuliwa Kashfa nchini Korea Kusini inayohusisha maisha ya faragha ya rais Park Geun-hye imechukua mwelekeo usio wa kawaida huku ikidaiwa kuwa afisi yake ilinunua dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume Viagra . text: Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia Wawili hao, raia wa Indonesia na Vietnam wanakabiliwa na hukumu ya kifo, kwa mauji ya Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar. Malaysia inasema, Bwana Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu aina ya , VX, ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa Mataifa. Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uwanja wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu. Wamesema kuwa walidhani walikuwa wakifanya mzaha katika filamu. Watashtakiwa chini ya sheria ambapo iwapo watapatikana na hatia watanyongwa. Hatahivyo hakuna hatua iliochukuliwa kuhusiana na kumshtaki raia wa Korea Kaskazini ambaye pia anazuiliwa kwa muaji hayo. Wanawake hao ni Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia na ni miongoni mwa washukiwa 10 waliotambuliwa na Malaysia kwamba huenda walihusika na mauaji hayo. Washukiwa hao ni pamoja na afisa mkuu katika ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Kuala Lumpur pamoja na mfanyikazi mmoja wa kampuni ya ndege ya taifa hilo. Korea Kusini inaamini kwamba washukiwa wanne ni wapelelezi wa Korea Kaskazini. Mwanasheria mkuu wa Malaysia, anasema wanawake wawili wanaodaiwa kumuua ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un watashtakiwa kwa makosa ya mauaji. text: Kikosi cha TP Mazembe Mchezo huo wa robo fainali umepigwa jijini Lubumbashi nchini Congo ulikuwa ni wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa jijini Dar es Salaam wikendi iliyopita. Simba walishindwa kufurukuta wiki iliyopita wakiwa nyumbani na kulazimishwa sare tasa. Awali Simba walionekana kama wanaenda kuvunja mwuko wao wa unyonge ugenini kwa kuuanza mchezo wa leo vyema. Straika wa Simba Emmanuel Okwi aliwanyamazisha mashabiki wa Mazembe kwa kuitanguliza timu yake katika dakika ya pili ya mchezo. Mazembe ambao ni mabingwa mara tano wa michuano hiyo walusawazisha katika dakika ya 23 ya mchezo kupitia beki Kobaso Chongo. Meshack Elia ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Simba aliwaandikia Mazembe goli la pili katika dakika ya 38. Kikosi cha wachezaji wa Simba Kipindi cha pili kilianza kwa Mazembe kuendelea kujiamini na walifunga bao lao la tatu kupitia kiungo fundi Tresor Mputu katika dakika ya 62. Msumari wa mwisho kwenye jeneza la Simba uligongelewa na Jacob Muleka katika dakika ya 74. Matokeo ya leo ni muendelezo wa kiwango hafifu ambacho Simba imekuwa ikikionesha wanapokuwa ugenini. Kufuzu kwa Simba kwenda robo fainali ni matokeo ya kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani. Simba wamefungwa mechi tano kati ya sita za ugenini walizocheza kwenye michuano hiyo. Na katika mechi sita walizocheza nyumbani wameshinda tano na kutoka sare mmoja. Timu pekee ambayo Simba imeifunga nyumbani (4-1) na ugenini (0-4) ni Mbabane Swallows ya eSwatini katika raundi ya kwanza kwa jumla ya goli 8-1. Raundi ya pili Simba ilicheza na Nkana ya Zambia na kufungwa ugenini 2-1 kabla ya kuwatoa kwa ushindi wa nyumbani wa magoli 3-1. Kwenye makundi Simba ilifungwa goli 5 mara mbili nchini DRC na Vita na nchini Misri na Al Ahly. Simba pia ilifungwa 2-0 na JS Soura nchini Algeria. Mara ya mwisho kwa Simba kufikia hatua ya robo fainali ilikuwa mwaka 1994, ambapo walitolewa na klabu ya Nkana ya Zambia kwa jumla ya magoli 4-3 baada ya kucheza michezo miwili. Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa Simba kufika robo fainali, mara ya kwanza ilikuwa miaka 45 iliyopita mnamo 1974 ambapo walisonga mpaka kufikia hatua ya nusu fainali na kutolewa na Ghazl Al-Mahalla ya Misri kwa mikwaju ya penati 3-0. Klabu ya Simba ya Tanzania imekubali kichapo cha goli 4-1 kutoka kwa TP Mazembe ya DRC na kung'olewa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika. text: Mali yake imeshuka thamani kutoka $3.5bn (£2.5bn) hadi $3.1bn. Jarida hilo limesema kushuka kwa utajiri wa Trump kumetokana zaidi na kushuka kwa thamani ya nyumba na vipande vya ardhi New York na pia kushuka kwa mapato kutoka kwa viwanja vyake vya kuchezewa mchezo wa gofu. Anayeongoza orodha ya matajiri wa kupindukia ni mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos. Utajiri wa Bezos umepanda na kufikia $112bn kutoka takriban $39.2bn mwaka jana. Kuimarika kwa utajiri wa Bw Bezos ndiko kwa juu zaidi katika historia. Amemuondoa mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kutoka uongozini kwenye orodha hiyo. Utajiri wa Gates unakadiriwa kuwa $90bn mwaka huu kutoka $86bn, na ndiye anayeshikilia nafasi ya pili. Bw Gates ameongoza orodha hiyo kwa miaka 18 kati ya miaka 24 iliyopita. Forbes wanasema kuna mabilionea 2,208 (kwa kutumia dola za Marekani) ambao walishirikishwa katika orodha ya 32 ya kila mwaka ya jarida hilo. Matajiri hao kwa pamoja wana utajiri wa $9.1 milioni. Miongoni mwao, kuna mabilionea 259 wapya ambao walijipatia utajiri wao kutoka wka biashara za aina nyingi zikiwemo nguo za harusi, wanasesere wa kuchezewa na watoto na magari yanayotumia umeme. Mwekezaji mmarekani Warren Buffett ndiye wa tatu utajiri wake ukiwa $84bn. Utajiri wake umepanda kutoka $75.6bn mwaka uliotangulia. mtu tajiri zaidi Ulaya ndiye wa nne kwenye orodha hiyo, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya bidhaa za kifahari ya LVMH, Bernard Arnault, ambaye utajiri wake ni $72bn. 'Kupanua pengo' Marekani ndiyo nchi iliyo na mabilionea wengi duniani, ambapo ina mabilionea 585, ikifuatwa na China. Jimbo la California pekee lina mabilionea 144, zaidi kushinda mataifa yote isipokuwa Marekani na China. Ujerumani ndiyo nchi inayoongoza Ulaya ikiwa na mabilionea 123. India ina mabilionea 119 nayo Urusi mabilionea 102. Kuna mabilionea 53 kutoka Uingereza kwa mujibu wa Forbes na idadi hiyo imeshuka kutoka 54 mwaka 2017. Luisa Kroll na Kerry Dolan kutoka kwa Forbes Media alisema: "Watu matajiri kupindukia wanazidi kupanua mwanya kati yao wenyewe, na pia kati yao na watu wengine." Orodha ya mabilionea ya Forbes inatumia takwimu za kufikia Februari 9, 2018. Jarida hilo hutumia bei ya soko la hisa na ubadilishanaji wa fedha za kigeni ya siku hiyo kutoka kila pembe duniani kuandaa orodha hiyo. Rais wa Marekani Donald Trump ameshuka nafasi 222 katika orodha ya kila mwaka ya watu tajiri zaidi duniani ambayo hutolewa na jarida la Forbes. text: Mwanzo wa kupatwa kwa mwezi katika mji wa San Diego , California Wakati wa tukio hilo mwezi huo unaojulikana kama 'Super Blood Moon', hubadilika na kuwa mwekundu , huku ukionekana kuwa na mwangaza mwingi na ulio karibu na dunia zaidi ya ilivyo siku za kawaida Tukio hilo lilikuwa likionekana kutoka Kaskazini na marekani kusini, pamoja na magharibi mwa Ulaya. Nchini Uingereza, mawingu mengine yalizuia kuonekana kwa mwezi huo vizuri. Kupatwa kwa mwezi kunatarajiwa katika kipindi cha miaka miwili, mnamo tarehe 26 mwezi Mei 2021 Walter freeman , naibu profesa katika chuo kikuu cha Syracuse University mjini New York state, alisema: "mwanga mdogo wa jua hutolewa na dunia na kufika katika mwezi, ukijipinda kando kando ya dunia. Kiwango hiki cha rangi nyekundu huangazia mwezi vya kutosha kwa binadamu kuweza kuona. Kupatwa kwa mwezi kama ilivyokuwa mjini Madrid. Muda mzuri wa mwezi kupatwa ulikuwa mwendo wa 05:12 GMT Tukio hili hujiri wakati dunia inapopita katikati ya Jua na mwezi. Katika hali hii, jua huwa nyuma ya dunia huku mwezi ukizunguka katika kivuli cha dunia. Kupatwa kwa mwezi kulianza mwendo wa 02:35 GMT siku ya Monday na kukamilika saa 07:49 GMT, lakini kipindi ambacho mwezi wote ulikuwa mwekundu ilikuwa mwendo wa 05:12 GMT. Awamu tofauti za mwezi uliobadilika na kuwa mwekundu mjini Panama Tukio hilo lisili la kawaida hupata jina 'Super' kutokana na swala kwamba mwezi utakuwa karibu mno na dunia- ambapo utaonekana mkubwa angani zaidi ya ilivyo kawaida. Nalo Jina "wolf" linatokana na majina yanayopewa miezi mikubwa mwezi Januari "wolf moons". Tukio hilo lilionekana katika mji wa Uingereza wa Liverpool, lakini baadaye ulizimbwa na mawingu. Mwezi huo ulionekana mjini Dresden Ujerumani Wachunguzi wa anga wamekuwa wakitafuta tukio lisilo la kawaida la kupatwa kwa mwezi ambalo lilianza siku ya Jumapili usiku. text: Tumbili wamekuwa janga katika kunti ya Muranga Kaunti hiyo imetangaza vita vikali dhidi ya wanyama hao na imeanza mpango kwa jina 'Tafuta Tumbili' kuwakabili wanyama hao. Lakini huku wakulima hao wakiwa na matumaini kwamba sasa wataweza kuvuna mazao yao baada ya wanyama hao kukamatwa, baadhi ya wakaazi katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakilidharau wazo hilo. Katika mtandao wa kijamii Peter Kamau alielezea hatua hiyo ya serikali ya kaunti kuwa ya majuto wakidai kuwa ni njia ya utumizi mbaya wa fedha kwa kuwa haikujadiliwa na bunge la kaunti. ''Serikali ya kaunti inapaswa kujua kwamba licha ya kilimo kugatuliwa inafaa kuweka muda wao mwingi katika kukamilisha mradi wa kiwanda cha maziwa na kuwacha jukumu la kukabiliana na wanyama kwa wataalamu wa shirika la wanyama pori la KWS'', alisema Kamau. Zaidi ya tumbili 10,000 wanalengwa katika mradi huo ambao utaendelea hadi mwezi Machi 24 kufuatia ombi la wakulima kwa kaunti hiyo wakilalamikia uharibifu wa chakula na nyasi za mifugo unaotekelezwa na wanyama hao. Operesheni hiyo ilianza siku ya Jumamosi mjini Gatanga ambapo takriban tumbili 125 walikamatwa kupitia mitego na wengine kuuawa. Serikali hiyo ya kaunti imetoa nambari ya simu kwa wakaazi wa kaunti hiyo ili kuwasaidia kuwakamata tumbili hao. Tumbili hao waliodaiwa kupelekwa katika msitu jirani na watu wasiojulikana miaka kadhaa iliopita wamekuwa wakiharibu mimea mbali na kuwanyanyasa wanawake na watoto. Anastasia Mugure , mkaazi wa kijiji cha Ngangaini village, anasema kuwa wanawake wanalazimishwa kutembea na silaha ili kujitetea iwapo watashambuliwa na wanyama hao. ''Hawaogopi hata kuingia jikoni na kuchukua chakula kutoka kwa sufuria hadi pale kunapokuwa na mwanamume kwa nyumba'' , alisema akiongeze kwamba wanalazimika kununua chakula baada ya wanyama hao kuharibu mimea yao kwa misimu miwili mfululizo''. Serikali ya kaunti ya Muranga imeshutumiwa kwa kutenga fedha za kukabiliana na tumbili wavamizi katika kijiji cha Gatunyu huko Gatanga. text: Sheria hiyo inadaiwa kulenga kuwanyamazisha wanahaari nchini humo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imewataka watu ambao wamekuwa wakitoa imetoa ilani kwa wahudumu wote ambao bado hawajapata leseni kukoma kutoa huduma hizo kuanzia leo. Mamlaka hiyo imesema wahudumu hao wana hadi Ijumaa wiki hii kuhakikisha wamejipatia leseni la sivyo watachukuliwa hatua. TCRA imesema wanaoathirika ni wamiliki wote wa blogu, majukwaa ya mitandaoni, redio na televisheni. Wameandika kwenye mtandao wao: "Kutokana na notisi iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo Juni 10, 2018 inayotoa muda mfupi wa kututaka kusitisha utoaji huduma mara kabla ya Juni 11, 2018, tunalazimika kutii mamlaka na hivyo huduma hii haitapatikana kwa muda wakati tukifanya jitihada za kuhakikisha huduma inarejea. "Kwa wateja wetu walio nchi nyingine, huduma hii itarejea mapema zaidi lakini kwa walio Tanzania kurejea kwa huduma kutategemeana na matokeo ya hatma ya jitihada za wawakilishi wetu walio Tanzania. "Tunasikitika kuwa tunalazimika kufikia hatua hii ghafla lakini ni matumaini yetu kuwa wateja wetu mtaendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki." Ujumbe wa mwisho kutoka kwa jukwaa hilo kwenye Twitter ulipakiwa usiku wa manane, na ulikuwa wa kutangaza taarifa hiyo kutoka kwa TCRA. Mwanablogu Carol Ndosi ni miongoni mwa walioathiriwa na kuanza kutekelezwa kwa sheria hizo, mwanzoni aliomba ufafanuzi kuhusu wanaotakiwa kusitisha kuchapisha taarifa mtandaoni. Baadaye, aliandika kwamba amelazimika kusitisha uandishi wa taarifa mtandaoni. Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ni miongoni mwa walioshangazwa na hatua ya sheria hiyo kuanza kutekelezwa na Jamii Forums kulazimika kufunga huduma zao kwa muda. Wamiliki wa huduma za mitandaoni Tanzania walikuwa wamepewa muda wa wiki mbili kujisajili baada ya serikali kushinda kesi iliofunguliwa na wadau wa habari kupinga kanuni za maudhui mitandaoni 2018. Wanablogu ambao wataopatikana na hatia ya kutoheshimu sheria hizo mpya watakabiliwa na faini ya hadi milioni 5 ama kifungo kisichopungua miezi 12 ama zote mbili kulingana na sheria hizo mpya, ilisema taarifa hiyo. Mike Mushi, mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums alikuwa awali ameambia BBC kwamba kanuni hizo, ambazo zinawataka wachapishaji wa taarifa zenye maudhui mtandaoni kuhifadhi maelezo ya wachangiaji kwa miezi 12 huenda zikaathiri mtandao wa Jamii Forums. "Sheria hizi zinaenda kinyume na jinsi sisi huendesha shughuli zetu. Huwa twawaruhusu watumiaji wetu kuandika ujumbe bila majina yao kutambulishwa, hivyo itatulazimu kufikiria kwa kina iwapo tutaweza kuendeleza kuendesha shughuli zetu." Alisema mtandao huo kufikia Aprili ulikuwa na watumiaji 3.7 milioni kwa mwezi na walikuwa wanapokea ujumbe takriban 20,000 kila siku. Wanablogu Rais Magufuli alitoa agizo la kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayechapisha habari za uongozi kuhusu serikali katika mitandao ya kijamii. Idadi ya watumiaji wa mitandao nchini Tanzania ilipanda hadi asilimia 16 (watu 23 milioni) mwaka 2017. Hiyo ni sawa na asilimia 44 ya raia wa Tanzania. Wengi hutumia simu kupata huduma za mtandao. Jukwaa maarufu nchini Tanzania Jamii Forums limekuwa miongoni mwa watoaji huduma za maudhui mtandaoni ambao wameathiriwa na kuanza kutekelezwa kwa sheria mpya za mtandaoni. text: Jeneza lenye mwili wa Peres limekuwa nje ya majengo ya bunge Jerusalem Kuna ulinzi mkali katika eneo ambalo litatumika kwa mazishi yake, katika maeneo ya makaburi ya kitaifa mlimani Herzl mjini Jerusalem. Waombolezaji watajumuisha Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama na Rais wa zamani Bill Clinton, aliyefanya kazi na Bw Peres katika mkutano wa mwafaka wa amani wa Oslo mwaka wa 1993. Viongozi kadhaa wa Kipalestina pia watahudhuria mazishi hayo akiwepo Rais Mahmoud Abbas na mpatanishi mkuu wa zamani Saeb Erekat. Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010. Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bunge la Israeli, Knesset. Shimon Peres (kulia) na Mahmoud Abbas na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri Amr Moussa picha iliyopigwa 29 Desemba, 1993 Ulinzi mkali umewekwa Jerusalem Peres aliacha maelezo ya kina kuhusu utaratibu wa mazishi yake Barack Obama akiabiri Air Force One Alhamisi kuelekea Israel Polisi wa Israel wamesema maafisa 8,000 wanatumiwa kudumisha usalama. Mazishi hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika Israel tangu mazishi ya waziri mkuu Yitzhak Rabin, aliyeuawa na Myahudi 1995. Bw Peres alifariki Jumatano baada ya kuugua kiharusi kwa muda wa wiki mbili. Wageni mashuhuri: Who was Shimon Peres? Viongozi mbalimbali duniani wanajiandaa kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi ya kiongozi shupavu wa Israeli marehemu, Shimon Peres, aliyefariki Jumatano wiki hii. text: Watalii wengi hutembelea mlima wa volkano wa Erta Ale Dereva wake pia alijeruhiwa wakati wa tukio hilo, ambalo lilifanyika katika jimbo la Afar, karibu na mpaka wa Eritrea. Ripoti zanasema raia huyo wa Ujerumani alikuwa miongoni mwa kundi la watalii ambao walikuwa kwenye ziara ya volkano ya Erta Ale - kivutio kikubwa kwa watalii wanaozuru Ethiopia. Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema hadi kufikia sasa haijabainika ni nani hasaa aliyetekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Ethiopia inasema inachunguza mauaji hayo. Serikali pia inasema vikosi vya usalama vimetumwa kuimarisha usalama huko. Eneo hilo la mpakani linatumika sana na kundi la waasi linalotaka kujitenga na Ethiopia. Mnamo mwaka 2012, watalii watano waliuawa na wengine wanne kutekwa nyara baada ya wapiganaji kuwashambulia katika eneo hilo. Kundi lililojihami la Afar Revolutionary Front lilidai kuhusika kwenye shambulio hilo. Mtalii mmoja kutoka Ujerumani amepigwa risasi na kuuawa kaskazini mashariki mwa Ethiopia. text: Watafiti wanaonya kwamba huenda malengo ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza maambukizi ya HIV yasifikiwe Walitathmini tafiti za mwaka mzima za WHO zilizofanywa katika nchini 127 kati ya mwaka 2012 na 2014 huku utafiiti huo ukiuliza uwezo na matumizi ya vipimo vya damu vinavyochunguza hali ya HIV na afya. Watafiti walibaini uhaba wa kutisha katika uchunguzi huo. Wanaonya kwamba huenda malengo ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza maambukizi ya HIV yasifikiwe. Malengo hayo yanasema kufikia mwaka 2020, asilimia 90% ya watu wote wanaoishi na virusi vya ukimwi -HIV-watakua wanapata dawa za -antiretroviral -zinazopunguza makali ya Ukimwi na kwamba asilimia 90% ya watu hao wanapaswa kuwa wanapata "dawa ya kudumaza virusi hivyo". Vipimo vya maabara ni muhimu kuweza kufikia malengo haya. Lakini Vincent Habiyambere na wenzake wanasema katika jarida la kitabibu la PLoS kwamba baadhi ya nchi zenye kipato cha chini na cha wastani, zikiwemo zile za mataifa ya Afrika ambako maambukizi ya HIV ni kero kubwa, haziko tayari kwa changamoto hiyo. Hata hivyo upimaji wa HIV umekuwa ukiongezeka kwa miaka, lakini bado kuna mapungufu katika baadhi ya maeneo ya dunia. Ukosefu wa vipimo vya virusi vya HIV vinavyosababisha maradhi ya ukimwi unaweza kuzorotesha juhudi za dunia za kubaini na kuwatibu watu wenye maambukizi ya HIV, wameonya wataalam kutoka Shirika la Afya Duniani. text: Watu 11,300 walifariki wakati wa mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi 2014-15 Mlipuko huo uliathiri sana nchi za Liberia, Sierra Leone, na Guinea na operesheni kubwa ya kibinadamu iliendeshwa kuwasaidia waathiriwa na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Jumla ya $100m (£76m) pesa taslimu zilitolewa kwa mashirika ya Shirika la Msalaba Mwekundu katika mataifa hayo matatu na Shirikisho kuu la Msalaba Mwekundu mjini Geneva. Nchini Liberia, $2.7m (zaidi ya £2m) zilitoweka kwa njia ya ulaghai kupitia kuongezwa chumvi kwa vitu vilivyouziwa shirikisho hilo. Kadhalika, nyingine zilitoweka kupitia mishahara iliyolipwa kwa wafanyakazi hewa. Nchini Sierra Leone, wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu walikula njama na benki moja kupora zaidi ya $2m. Na nchini Guinea, ambapo uchunguzi bado unaendelea, takriban $1m zilitoweka kupitia kutumiwa kwa risiti feki za ulipaji wa kodi. Shirika la Msalaba Mwekundi limesema linaomba radhi kutokana na kupotea kwa fedha hizo na likaongeza kwamba limeweka mikakati zaidi ya kifedha kuzuia ufujaji kama huo wa pesa siku za usoni. Aidha, shirikisho hilo limeahidi kuwaadhibu wafanyakazi ambao itagunduliwa walihusika. Shirika la Msalaba Mwekundu ni moja ya mashirika yanayoaminika sana duniani na ufichuzi huo huenda ukaathiri sifa zake. Wakaguzi wa hesabu katika Shirikisho la Msalaba Mwekundu wamefichua kwamba mamilioni ya dola ambazo zilikuwa zimetolewa kama msaada wakati wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola zilifujwa. text: Polisi wanaamini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 71 alianguka mnamo 2016. Wanatuhumu kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 47 alishindwa kumhudumia vizuri mamake aliyefariki "siku chache baadaye" kutokana na athari ya kuanguka huko. Masalio ya mwili wa marehemu yalipatikana kwenye sakafu ya chumba kimoja. Binti yake na mjukuu wake marehemu walilala katika chumba cha pili katika nyumba hiyo. Mjukuu wa marehemu alikuwa na miaka 15 wakati akiishi na maiti ya bibi yake. Na kutokana na hilo, mamake ameshtakiwa kwa 'kumdhuru mtoto' wa chini ya miaka 15. Mjukuu huyo sasa anatazamwa na jamaa zao na anapokea usaidizi kutoka kitengo cha kuwalinda watoto. Huenda mamake akakabiliwa na hadi miaka 20 gerezani na faini ya hadi $10,000. Polisi wanasema marehemu bibi huyo aliheshimika katika jamii kwenye eneo hilo, na alifanya kazi kama karani na mwalimu msaidizi katika mojawapo wa shule katika eneo hilo kwa miaka 35. Alipostaafu, alikuwa akifanya kazi ya kukusanya tiketi katika sherehe za michezo huko Seguin. Mwanamke mmoja jimboni Texas, Marekani amekamatwa baada ya masalio ya maiti ya mamake inayooza kugunduliwa nyumbani wanakoishi pamoja. text: Waziri wa maswala ya nchi za kigeni Kenya Amina Mohammed Balozi Amina ambaye alipoteza wadhfa huo kwa mpinzani wake kutoka Chad Moussa Faki Mahamat alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone na wale wanaozungumza kizungu Anglophone. Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake. Bendera za mataifa ya Afrika mashariki ''Baadhi ya majirani zetu hawakutuunga mkono, walisikika wakizungumzia swala hilo'', Amina alisema bila ya kutaja majina.Nadhani hofu kwamba pengine Kenya ingeshinda ndio iliowafanya kutotuunga mkono''. ''Nadhani sisi Wakenya ni watu waaminifu sana kwa hivyo ni vigumu kushirikiana na watu wanaohadaa.kwa hivyo nadhani walijiondoa''. Tukisonga mbele ni funzo zuri kwetu sisi. Katika raundi ya tano ya kura hizo Amina alikuwa anaongoza kwa kura 27 dhidi ya za Mahmat 25'',aliongezea Amina. Taifa moja halikupiga kura. Ni wakati huo ambapo mataifa mawili kutoka shirika la IGAD yaliamua kumpigia kura mpinzani wa Amina na hivyobasi kumpatia kura 28 zaidi ya 26 zilizohitajika ili mgombea kuibuka mshindi. Mgombea wa wadhfa wa mwenyekiti kutoka Kenya katika tume ya Umoja wa Afrika AU Amina Mohammed ametaja usaliti miongoni mwa mataifa jirani ya Afrika Mashariki kuwa sababu ya yeye kutoshinda wadhfa huo. text: The Reds walipata ushindi wa mapema kupita Mohamed Salah katika dakika ya nne kutoka kwa pasi fupi kutoka kwa Andy Robertson. Lakini hakuna bahati yoyote katika ushindi wao pale Sadio Mane alipofunga bao la pili baada ya Salah kukosa nafasi hiyo. Majogoo wa Jiji Liverpool, waliweza kuweka mwanya huo wa alama 13 baada ya wapizani wake wa karibu Leicester na Manchester City kujipatia ushindi katika mechi za mwaka mpya. Mohamed Salah alifunga dhidi ya timu 22 kati wapinzani 25 wa ligi ya Premia aliopambana nao kama mchezaji wa Liverpool, na kushindwa kufunga bao dhidi ya Manchester United, Swansea na Aston Villa Upande huo unaogozwa na Jurgen Klopp ulishuka kwa alama mbili wakiwa na alama 58 badala ya alama 60 msimu huu. Kwa upande wa Chris Wilder ulikuwa umeshidwa kwa mara ya pili mfululizo , lakini wamesalia wakakamavu na kuwa nambari sita katika jeduali ya ligi ya Premia na alama 29. Ushindi wa Liverpool dhidi ya Sheffield United umeweka historia ya kuwa miongoni mwa timu ambazo hazijafungwa kwa mwaka mmoja katika ligi kuu Uingereza. The Reds wameshiriki mechi 37 bila kupoteza na wakajizolea alama 101 wakati huo ambapo walipoteza kwa magoli 2-1 msimu uliopita kwa mabingwa wa Champions Manchester City walipokutana tarehe 3 mwezi Januari mwaka 2019. Upande wa meneja Jurgen Klopp ndio timu inayoshiriki ligi ya Premia kuweza kukamilisha mwaka mmoja bila kushindwa. Arsenal ambao walishiriki michezo 49 katika msimu wa mwaka 2003-04 na Chelsea kutoka mwezi wa oktoba 2004 hadi Novemba 2005 ni miongoni mwa timu ambazo zimeweza kucheza mechi bila kushindwa kwa mwaka mmoja. Jordan Henderson amkubatia mkufunzi wao Jurgen Klopp baada ya mechi yao dhidi ya Sheffield United Liverpool ilishindwa nyumbani dhidi ya Wolves katika kombe la FA mwezi Januari mwaka jana. Pamoja na timu yao ya vijana chipukizi kupoteza kwa Aston Villa katika kombe la Carabao mwezi uliopita. Liverpool imepoteza mara mbili katika ligi ya Champions dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya mkondo wa kwanza kabla ya mkondo wao wa pili dhidi ya Napoli mwaka huu katika hatua ya makundi. Licha ya kutofungwa, Liverpool haikushinda kombe lolote la nyumbani mwaka 2019. Mafanikio yao yalikuwa katika mechi za kimataifa, kuwa klabu ya kwanza ya Uigereza kupata ushindi wa kombe la Champions, Uefa Super Cup waliolipata Agosti baada ya kuichapa Chelsea kwa mikwaju ya penati na katika michuano ya kombe la Fifa. Liverpool,imeshikilia uongozi wa ligi kuu ya England kwa mwaka mzima bila kufungwa baada ya Sheffield United kugaragazwa uwanjani Anfield. text: Picha zilizoachwa karibu na White House wakati wa maandamano ya Januari 21 Akaunti yao ramsi ya twitter ilitangaza habari za mpango huo. Ilijumuisha picha inayosema "siku isiyo na wanawake" Mgomo huo unafuatia maandamano makubwa katika historia ya Marekani mjini washington tarehe 21 mwezi Januari huku mamilioni ya watu wakiandamana kwa uzalendo kote duniani. Mgomo mwingine tayari ulikuwa umepangwa nchini Marekani tarehe 17 mwezi Februari na kundi linalojiita Strike4Democracy kumpinga Trump. Terehe ya mgomo huo wa wanawake ilitangazwa baadaye. Waandalizi wanasema pia kuwa wanaunga mkono majaribio ya makundi mengine kugoma yakitumia nguvu za kiuchumi. Maandamano ya wanawake mjini Washington Kipi kitatokea wakati wanawake watagoma? Hatua ya wanawake kugoma ina historia yake ya kuangazia kutokuwepo usawa kwenye majukumu ya nyumbani. Wanawake wa Iceland waligoma mwaka 1975 na kuwaacha waume zao wakiwatunza watoto, wakipika na kufanya usafi. Miaka mitano baadaye nchi hiyo ilimchagua kiongozi mwanamke wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia. Mwaka uliopita wanawake nchini Poland nao waligoma kupinga sheria za utoaji mimba zilizopendekezwa na serikali. Waandalizi wa maandamano ya wanawake wa mji wa Washington ya kumpinga Rais Donald Trump, wanapanga mgomo wa wanawake. text: Jamaa za abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wameanza kufika kituo cha huduma za dharura uwanja wa ndege wa Jakarta Ndege hiyo safari nambari JT-610 iliyokuwa imewabeba abiria 188 ilikuwa safarini kutoka mji huo mkuu wa Indonesia kwenda Pangkal Pinang, jiji linalopatikana katika visiwa vya Bangka Belitung. Iitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari. Katika kikao na wanahabari, maafisa wamesema ndege hiyo, ambayo ni ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX 8, ilikuwa imewabeba abiria 178 watu wazima, watoto watatu, marubani wawili na wahudumu watano wa ndege. Yusuf Latif, msemaji wa shirika la huduma za uokoaji na kuwatafuta manusura amewaambia wanahabari: "Imethibitishwa kwamba ndege hiyo imeanguka." Maafisa wa uokoaji wakiwa eneo ambalo ndege hiyo ilianguka Afisa wa shirika hilo la ndege ameiambia BBC kwamba bado hawajui chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo. Afisa mkuu mtendaji Edward Sirait ameambia shirika la habari la Reuters: "Hatuwezi kusema chochote kwa sasa. Tunajaribu kutafuta maelezo na data zaidi." Ndege moja ya Lion Air ikiwa Palu (picha ya maktaba) Vyombo vya habari Indonesia vimemnukuu afisa wa bandarini Tanjung Priok akisema kwamba maafisa wa boti la kusindikiza meli wameripoti kwamba wameviona vifusi vya ndege hiyo kwenye mai. Suyadi, ambaye hutumia jina moja pekee kama raia wengi wa Indonesia, amesema vyombo vingine vya baharini vimefunga safari kuelekea eneo hilo. Ndege hiyo safari namba JT-610 iliondoka Jakarta saa 06:20 saa za huko Jumatatu asubuhi (23:30 GMT Jumapili). Baada ya kusafiri kwa muda mfupi, ilitarajiwa kutua Pangkal Pinang saa moja baadaye. Ndege hiyo inadaiwa kuwa Boeing 737 MAX 8, muundo wa ndege ambao umetumiwa kuanzia 2016. Tovuti ya kufuatilia safari za ndege ya Flightradar24 inasema ndege hiyo iliwasilishwa kwa Lion Air mwezi Agosti. Mtaalamu wa masuala ya uchukuzi wa ndege Gerry Soejatman ameambia BBC kwamba ndege hiyo aina ya MAX 8 imekuwa ikikumbwa na hitilafu tangu ilipoanza kutumiwa, saidi katika kupaa kwa utaratibu ufaao. Ndege hii ya Lion Air ilipaa baharini Bali mwaka 2013, lakini abiria wote walinusurika Indonesia, taifa kubwa la mkusanyiko wa visiwa, hutegemea sana uchukuzi wa ndege, lakini ina historia ya ajali nyingi za ndege. Lion Air ni shirika la safari nafuu za ndege. Mwaka 2013, ndege ya Lion Air safari nambari 904 ilianguka baharini Bali ikijaribu kutua uwanja wa ndege wa Ngurah Rai. Abiria wote 108 waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika. Mwaka 2004, ndege nyingine ya Lion Air safari nambari 538 kutoka Jakarta ilianguka na kuvunjika vipande vipande ilipokuwa inatua mjini Solo na kuwaua watu 25. Ndege ya kuwabeba abiria ya shirika la Lion Air aina ya Boeing 737 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Jakarta, maafisa wa Indonesia wamesema. text: Gari la kim jong un Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote . Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka. Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji. Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri. Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi. Mwisho-mlinzi mmoja huchunguzwa familia yake na vizazo vyake vilivyopita . Maafisa wengi wa wapiganaji hao wana uhusiano na familia ya Kim Jong Un ama familia kubwa za Korea Kaskazini. Wanapokubalika kuwa walinzi { huwezi kukataa kazi hiyo} hufanyiwa mafunzo ya kiwango cha juu .Walinzi hao hufunzwa kuwa na ujuzi maalum. Hufunzwa kwa kutumia bunduki, mbinu za uvamizi, judo, karate , kung fu na taekwndo . Walinzi hao humzunguka kiongozi hiyo wakimlinda na wanaweza kuona kwa kuzunguka digree 360 kuwatazama watu walio karibu naye na walipo. Wanaotembea , mbele yake ni kati ya walinzi watatu hadi watano akiwemo mkurugenzi wa agfisia hiyo ya wapiganaji. Pamoja naye , ni walinzi wanne hadi sita , wawili ama watatu wakiwa upande wake wa kulia . Kuna wengine wanne ama watano nyuma yake. Ili kuonyesha uwezo wao katika utawala huo, ndio raia pekee wanaokubaliwa kubeba bunduki zilizo na risasi karibu na kiongozi wa taifa lao, sana sana huwa bunduki zinazodaiwa kuwa automatic pamoja na silaha nyengine. Walinzi hao walioonekana wakikimbia kandokando ya msafara wa rais Kim wakati mkutano wa mataifa ya Koreamwezi Aprili Licha ya kubeba silaha, ulinzi mkubwa wanaompatia rais Kim jong un ni ujuzi walio nao katika kuwachunguza watu walio karibu na kiongozi huyo na kukabiliana na tishio lolote kwa kutumia mikono yao na mwili. Wakati Kim Jong il alipokuwa hai mlinzi mmoja alikuwa akiwalinda maafisa wakuu wawili anaondamana nao. Walinzi wa Kim Jong Un ikilinganishwa na wale wa babake ni wachache na hawaonekani mara kwa mara. Walinzi hao huvalia suti za magharibi kama wanavyoonekana nchini Singapore . Dereva wa Kim Jong un huvalia glavu za plastiki ama za ngozi kushika usukani. Pia hutumia mawasiliano ya redio kupitia hedifoni. Hatahivyo mbinu zao za mawasiliano ni za zamani. Kitengo hicho cha afisi ya wapiganaji kina takriban kati ya maafisa 200-300, ambao nusu yao ni walinzi na waliosalia ni madereva na wafanyikazi wa kiufundi. Huku baadhi ya walinzi wa viongozi hao wakiwa watu walio na uzoefu mkubwa , wengi wao huwa wamefanya kazi kwa miaka 10. Pombe , chakula na sigara Uchunguzi wa hivi karibuni na ripoti kuhusu ziara ya Kim nchini Singapore zimebaini kwamba ndege tatu ziliwasili katika mji mkuu wa Pyongyang . Walinzi wa Kim Jong un walikuwa ndani ya ndege hizo. Wanaume hao na wanawake uhusishwa na usaidizi wa Kim. Wao husimamia laini za simu ambazo zitatumiwa na kiongozi huyo mbali na kumpatia tarakilishi yoyote anayotumia. Mbali na hilo wana kinywaji , chakula na sigara zozote ambazo bwana Kim atataka kutumia wakati wa ziara yake Singapore na watachunguza chakula chochote ama kinywaji kabla ya kupakuliwa. Pia wana idara ya matibabu ambapo daktari wake wa maungo na maafisa wa matibabu na wawili kati ya maafisa hao wako naye ziarani Singapore. Kuhusu ulinzi binafsi wa Kim, idara ya GC's #2 huweka ulinzi mkali wa karibu na huangazia pale bwana Kim anapofanya kazi , anapoishi na kutembea. Maafisa wa usalama wa Korea Kaskazini wanaonekana nje ya hoteli ya bwana kim nchini Singapore Iwapo unataka kuona eneo analokaa rais huyo katika hoteli ya St Regis nchini Singapore bila shaka utakutana nao. Ulinzi wa aina hiyo haiujawahi onekana kwengine kokote. Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore. text: Maafisa wamesema vitisho vyovyote vinavyotolewa kupitia mitandao ya kijamii vinafaa kuchunguzwa. Karius, 24, na familia yake wamekuwa wakipokea vitisho baada ya makosa mawili kutoka kwake kuwasaidia Real Madrid kupata ushindi wa 3-1. "Tunachukulia ujumbe huu wa vitisho kwenye mitandao ya kijamii kwa uzito sana. Visa hivi vitachunguzwa," polisi wamesema. "Maafisa wa polisi wanafahamu kuhusu ujumbe kadha na vitisho vilivyotolewa kupitia mitandao ya kijamii. "Polisi wa Merseyside wangependa kuwakumbusha wanaotumia mitandao ya kijamii kwamba makosa yooyte yakiwemo kutoa mawasiliano yenye hila na kutumia vitisho, haya yote yatachunguzwa." Mjerumani huyo alimpa mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema bao rahisi la kwanza mjini Kiev. Baadaye, alimruhusu Gareth Bale kufunga bao la tatu la Real kutoka mbali alipojaribu kuzuia kombora lake lakini likapita mikono yake na kutumbukia wavuni. Hilo liliwawezesha Real kushinda taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu mtawalia. Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, mlinda lango huyo alionekana kusikitika na kutokwa na machozi. Baadaye, aliwaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo ya Anfield. Loris Karius alifanya makosa mawili kwenye fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Liverpool wana nyenzo za kumsaidia Karius - Mignolet Mlinda lango mwenzake Liverpool Simon Mignolet amemtetea Karius na kusema atajikwamua kutoka kwa masaibu hayo ya fainali hiyo ya Uefa. "Iwapo anataka kuzungumza, bila shaka nitakuwepo," alisema Mbelgiji huyo aliyekuwa kwenye benchi wakati wa mechi hiyo. "Kila kipa anamuelewa. "Nimewahi kujipata katika hali kama hii mwenyewe awali na hayo ni mambo ambayo huwa unakumbana nayo. "Kitu pekee nilichomwambia ni kwamba kuna sababu iliyotufanya kufika fainali, na kuna sababu yetu kucheza kwenye fainali, hivyo fikiria hilo. "Lakini bila shaka, ni jambo ngumu sana kumwambia chochote na kumwacha atulie na kuelewa. "Liverpool husimamia umoja, Liverpool husimamia 'sote kwa pamoja'. Nafikiri hilo halitakuwa tu kwamba ndilo jambo bora kwa Liverpool, bali imekuwa ndiyo historia yao na itasalia hivyo sku za baadaye." Mkufunzi wa makipa wa Liverpool John Achterberg alijaribu kumliwaza Karius baada ya mechi hiyo. "Bila shaka kilichotokea hakikuwa kitu kizuri. Ilikuwa mkosi kwake kwamba ilitokea wakati wa mechi hii," alisema Mholanzi huyo. "Nilijaribu kuinua kichwa chake na kumuonesha kwamba tunafaa kusonga mbele. Ni vigumu lakini hayo ndiyo maisha katika soka." Beki Dejan Lovren alisema haitakuwa na faida yoyote kumlaumu karius. Ni rahisi sana kumlaumu mtu, lakini tupo kwenye meli hii pamoja na kila mtu alitoa maneno mazuri kwake kadiri tulivyoweza. Atajikwamua," Lovren alisema. "Msiandike hadithi kubwa na ndefu kuhusu hilo. Ni kweli kwamba ni kubwa kwa sababu ilikuwa fainali, lakini hakuna asiyefanya makosa." Loris Karius alihamia Liverpool kutoka Mainz ya Ujerumani kwa £4.7m Mei 2016 Karius mwenyewe amesema "anaomba radhi bila kipimo" baada ya makosa yake. "Najua kwamba nilikosea sana kwa makosa yangu hayo mawili na niliwavunja moyo nyote," aliandika kwenye mitandao ya kijamii. "Kusema kweli, sijapata usingizi hadi sasa," aliandika baada ya mechi. "Yaliyotokea bado yanapitia kichwani mwangu tena na tena. "Nawaomba radhi bila kipimo wachezaji wenzangu, nanyi mashabiki, na kwa wafanyakazi wote wa klabu. "Ningelipenda sana kusongeza nyuma mshale wa saa lakini hilo haliwezekani. "Inauma zaidi kwani sote tulihisi kwamba tungewalaza Real Madrid na tulikuwa tunacheza vyema kwa muda mrefu. "nawashukuru sana mashabiki waliofika Kiev na kuniunga mkono, hata baada ya mechi. "Sitalisahau hilo na kwa mara nyingine tena lilinionyesha jinsi tulivyo kama familia moja kubwa. Asanteni, na tutaerejea tukiwa na nguvu zaidi." Ninamuonea huruma sana - Klopp Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, ambaye bado hajashinda kikombe tangu ajiunge na Liverpool 2015 amesema anamuonea huruma sana karius. "Kosa hilo la pili lilitokea kwa sababu ya lile la kwanza. Ni vigumu sana kuzifuta fikira hizo mbaya kutoka akilini mwako," alisema. "Loris anajua hilo, kila mtu anajua. Ni aibu sana kutokea katika mechi kama hii, katika msimu kama huu. "Namuonea huruma sana. Yeye ni mchezaji mzuri." 'Tukishinda tunashinda kama timu, tukishindwa, kama timu pia' Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson alikataa kulaumu makosa ya Karius kwa kushindwa kwa Liverpool kwenye fainali hiyo. Liverpool walikuwa pia wameshindwa fainali Kombe la Ligi Uingereza na Europa League 2016. Ushindi wao wa mwisho fainali ulitokea jijini Cardiff kwa mikwaju ya penalti fainali ya Kombe la Ligi Uingereza 2012. "Si makosa yaLoris Karius, tulifika fainali kama timu na tulishindwa kama timu. Ni kuhusu kila mtu. Uchezaji wetu haukutosha siku hiyo." 'Itamchukua miezi mitatu hivi kusahau' Mwnaasaikolojia wa michezo Dkt Steve Peters, ambaye amewahi kufanya kazi na timu ya taifa ya England anasema Karius atahitaji muda kuyasahau makosa yake. "Hii ni michezo na siku moja mambo wakati mwingine huenda mrama. Jambo muhimu zaidi ni kukubali kwamba hajapoteza kipaji chochote au uwezo wowote. Ni makosa kadha tu, kwa hivyo vyema zaidi huwa kukubali ukweli. Huenda asiwahi kurudia makosa hayo tena. "Kwa kawaida, itamchukua miezi kama mitatu hivi kwake kukubali kwamba hayo yalipita. Hatujui ni kwa sababu gani huchukua muda kama huo - akili huchukua muda kutafakari na kulikubali jambo. Kwa usaidizi wa wataalamu, hili linaweza kufanikiwa hivi kwamba mwishowe unatokea ukiwa hata na nguvu zaidi badala ya kukudhoofisha." Kipa wa zamani wa Ray Clemence, aliyeshinda Kombe la Ulaya akiwa na Liverpool kati ya 1977 na 1981, anasema kipindi cha mapumziko ya majira ya joto kitakuwa kirefu sana kwa Karius ambaye hakutajwa kikosi cha Kombe la Dunia cha Ujerumani. "Alifanya makosa mawili makubwa wakati muhimu kwenye mechi na itamulazimu kuishi na hilo maisha yake yote," kipa huyo wa zamani wa England Clemence aliambia BBC Radio 5. Polisi wa eneo la Merseyside, Uingereza wamesema wanafahamu kuhusu vitisho vya maisha ambavyo vimetolewa dhidi ya mlinda lango wa Liverpool Loris Karius baada ya kuchezwa kwa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi. text: Waraka wa kanisa Katoliki umetolewa wa wakati wapenziwa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao Mwongozo huo wenye kurasa 31 za mafundisho, umetolewa ukiwa na kichwa cha taarifa ''Mungu aliumba Mke na mume'' Mwongozo huo unazungumzia "mzozo wa mafundisho" na kuongeza kuwa mjadala wa sasa kuhusu jinsia unaweza "kupotosha dhana asilia " ya jinsia na kuyumbisha familia. Waraka huo ambao umetolewa wa wakati wapenziwa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao , umekosolewa mara moja na makundi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadilisha jinsia zao LGBT. Kanisa katoliki limesema jinsia ya mtu haimriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee na kwamba maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili , kazi ya mwanamme na mwanamke Waraka huo wa kanisa katoliki umetolewa na kongamano la Katoliki la Elimu kama mwongozo wa mafunzo kwa wale wanaohusika na masuala ya watoto. Waraka huo haukutiwa saini na Papa Francis mwenyewe, lakini uliinukuu kauli yake na maandiko ya biblia kuhusiana na jinsia zilizoumbwa na Mungu kulingana na kanisa katoliki. Waraka unasemaje? Waraka unatoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo, lakini unatoa mwongozo juu ya masuala kadhaa yakiwemo yanayohusu jamii ya watu wanaobadilisha jinsia yao. Unakosoa vikali uelewa wa kisasa kuhusu jinsia na kulifanya suala la jinsia kuwa gumu kuliko ilivyo kawaida ambapo kuna wanaume na wanawake. Waraka huo umeendelea kusema kuwa nadharia za kisasa "zinapinga maumbile halisi " na badala yake " linakuwa ni swala la hisia za binadamu ". Waraka huo unasema pia kwamba utambulisho wa jinsia "mara nyingi hauna msoingi wowote isipokuwa ni dhana potofu ya mkanganyiko wa uhuru wa hisia za mtu na vile anavyotaka yeye kuonekana na kutambulika ". Mwongozo wa umetolewa wakati wapenzi wa jinsia moja wakisherehekea mwezi wa kujivunia jinsia yao Waraka huo unaendelea kusema kuwa jinsia haiamriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee: " Maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili , kazi ya mwanamme na mwanamke ." Wapenzi wa jinsia moja Waraka huo unasema kuwa taasisi zinapaswa kufundisha jamii kwa usawa juu ya "asili ya kweli ya wanadamu"kwa kuzingatia "elimu ya historia na tabia ya maendeleo ya binadamu kwa uwazi na kwa njia inayoaminika ". Wapenzi wa jinsia moja katika moja ya matembezi ya kujivunia jinsia zao. Matembezi haya hufanyika kila mwaka katika nchi mbali mbali hususan za magharibi Hata hivyo, waraka huo unasema kwamba waoto na vijana wanapaswa kufundishwa kumuheshimu kila mtu ili asiwepo hata mmoja atakayeumizwa na matusi au ubaguzi wa aina yoyote ile Kundi la New Ways, lenye makao yake nchini Marekani ambalo linatetea wapenzi wa jinsia moja Wakatoliki, limeelezea waraka huo wa kanisa katoliki kama '' zana hatari'' ambayo itatumiwa "kuwadunisha na kuwadhuru watu waliobadilisha jinsia zao, pamoja na wapenzi wa jinsia moja wakike na wakiume ". Mkurugenzi New Ways- Francis DeBernardo, amepinga vikali dhana kuwa watu "huchagua jinsia zao". Katika taarifa iliyojibu waraka wa kanisa katoliki ,Francis DeBernardo , alisema kuwa waraka huo ''utawakanganya wale wanaohangaika kutafuta jinsia yao " na akaelezea kuwa Vatican imekuwa "katika kipindi cha giza " kuhusiana na suala la utambulisho wa jinsia. Uongozi wa makao makuu ya kanisa katoliki umetoa waraka wa mwongozo unaopinga dhana ya kisasa juu ya utambulisho wa jinsia. text: Ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake, tayari Magufuli ameshafukuza kazi mawaziri tisa kati ya 19 aliowateua Desemba 10, 2015. Akizungumza leo Ikulu katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wapya, Rais Magufuli amesema ataendelea kufanya mabadiliko ya baraza lae pale patakapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo. "…hii ni kama safari, sio lazima wote tufike. Inawezekana hata mie kiongozi nisisfike lakini lengo letu lazima litimie," amesema Magufuli. Mawaziri wapya walioapishwa leo ni Japhet Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo na Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Ambao wametimuliwa katika nafasi hizo ni Dkt. Charles Tizeba na Charles Mwijage mtawalia. Mawaziri hao wawili wamekuwa wahanga wa sakata la korosho lakini kwamujibu wa Magufuli utendaji wao wa kazi ulikuwa unamkwaza siku nyingi. Charles Tizeba (kushoto) ametimuliwa katika nafasi yake ya uwaziri wa kilimo. Magufuli 'alipovamia' mkutano kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na wanunuzi wa sekta binafsi tarehe 28 Septemba aligundua 'madudu' mengi ambayo yangeweza kutatuliwa na wizara hizo mbili na bodi ya korosho lakini hawakufanya hivyo mapema. "Kwenye mkutano ule nilikuta bodi ya korosho imetoa bei elekezi ya Sh1,500, iliniumiza sana...lakini mwisho wa yote unajiuliza wizara ya kilimo ipo wapi? Au Mwijage nae alikuwa tu na viwanda akasahau wafanyabiashara ya korosho." Katika mkutano wa Oktoba 28, Magufuli na wafanyabiashara walikubaliana bei elekezi ya Sh3,000 lakini utekelezaji wake ulisuasua. "Sikuona tamko lolote kutoka kwa Waziri wa Kilimo au Biashara kukemea kile ambacho kilikuwa kinaendelea, mpaka ikabidi nimtume Waziri Mkuu awape wanunuzi siku nne tu wafanye maamuzi." 'Kila Kitu Waziri Mkuu' Magufuli pia ameiambia hadhara iliyokuwepo ikulu kuwa alishawahi kumwambia Waziri Mkuu kuwa atamfanya kuwa Waziri wa Kilimo kutokana na kutatua changamoto nyingi za wiazara hiyo. "Kulipokuwa na shida ya bei ya kahawa mkoani Kagera, ilibidi Waziri Mkuu aende akalimaliza ndani ya moda mfupi. Sasa najiuliza Mwijage hakuliona hili na yupo karibu, lakini kahawa nizao la kilimo hawakuchua hatua pia." Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa walipokutana na wanunuzi wa korosho Oktoba 28 Waziri Majaliwa alienda Kagera mwezi Oktoba na kutangaza mfumo mpya wa minanda ya kahawa na kumaliza sakata hilo. Changamoto nyengine ilikuwa ya kiwanda cha chai cha Mponde Tanga ambacho kilikuwa hakifanyi kazi kwa zaidi ya miaka mitano lakini Majaliwa akamaliza mgogoro wake mapema mwezi huu. "Sio kama siwapendi, nampenda Tizeba nataniana na Mwijage lakini katika hili nimeona siwezi tena kuwasukuma, nitawavunja miguu. Wacha hawa wapya waje waendane na spidi." Mawaziri Waliotoswa Mwezi Mei 2016, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga alifutwa kazi kwa tuhuma za kuingia Bungeni akiwa amelewa. Mawaziri wawili Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini) George Simbachawene (Ofisi ya Rais) walifutwa kazi kufuatia sakata la mchanga wa madini (makinikia) wa kampuni ya Acacia. Julai mosi mwaka huu Mwigulu Nchemba alitolewa kwenye nafasi ya uwaziri wa Mambo ya Ndani. Rais Magufuli alitaja sababu 13 kumwondoa Mwigulu ikiwemo ajali za barabarani na matumizi mabaya ya fedha za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. Mwezi Machi 2017 Nape Nnauye aliyekuwa Waziri wa Habari alitimuliwa kazi. Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia Kituo cha Televisheni cha Clouds akiwa na askari wenye silaha akitaka kipindi anachotaka yeye kirushwe hewani. Je Paul Makonda anapendelewa na serikali Tanzania? Nape akiwa kama waziri mwenye dhamana, akaitisha uchunguzi huru wa tukio hilo. Ripoti ya uchunguzi huo ilimtia lawani Makonda. Nape aliahidi kuifikisha ripoti hiyo kwa Rais, lakini hatimaye alifutwa kazi, na badala yake Magufuli, mbele ya hadhara akamsihi Makonda " piga kazi" na kusema yeye Rais hapangiwi nini cha kufanya. Mawaziri wengine waliotimuliwa kazi ni Prof Jumanne Maghembe (Maliasili na Utalii) na Gerson Lwenge (Maji na Umwagiliaji). Rais wa Tanzania John Pombe Magfuli amesema hatachoka kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri kila itakapohitajika. text: Mpaka kufikia leo, Jumatano jioni bado haijulikani ni akina nani waliomteka na wapi walipomficha na lipi hasa kusudio la kumteka mfanya biashara huyo maarufu kama Mo. Mo alikwapuliwa na watu wasiojulikana nje ya hoteli moja jijini Dar es Salaam alipokuwa akienda kufanya mazoezi. Toka hapo, giza nene limetanda juu ya tukio hilo, licha ya hatua kadhaa ambazo mamlaka za nchi na familia imezichukua. Mwenendo wa uchunguzi Toka siku ya kwanza ya tukio polisi kupitia Kamanda wa Dar es Salaam wamekuwa wakiuhakikishia umma kuwa ulinzi umeimarishwa na uchunguzi unafanyika kwa kasi na weledi. Maeneo yote ya kutoka na kuingia jiji la Dar es Salaam ikiwemo fukwe za bahari zinakaguliwa. Hatahivyo, si wote wanaoonekana kuridhishwa na kasi ya uchunguzi. Mathalan, suala la picha za kamera za CCTV zilizonasa tukio hilo ni kizungumkuti. Polisi wanasema kamera za hoteli hazikunasa tukio hilo ipasavyo na kuwapa ugumu wa kung'amua undani wa tukio hilo. Hata hivyo, waziri kivuli wa mambo ya ndani na mbunge wa upinzani Godbless Lema ameonesha wasiwasi wake juu ya kauli za mamlaka akitaka picha hizo ziwekwe wazi ili wananchi wasaidie katika utambuzi wa watekaji na magari yaliyotumika. Watanzania waendelea na harakati za kuomba kurejeshwa kwa Mo Dewji Gazeti la Mwananchi la leo Jumatano Oktoba 17 pia limeandika kuwa licha ya uwepo wa kamera za CCTV hotelini hapo, majengo mengi yanayoizunguka hoteli hiyo na barabara ambayo yadaiwa kutumiwa na watekaji imesheheni kamera za CCTV. Upinzani na watumiaji wa mitandao Tanzania pia wamekuwa wakiomba serikali ikaribishe mashirika ya upelelzi ya nje kama FBI na Scotland Yard kuja kusaidia kutatua fumbo hilo lakini serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola na naibu wake Hamad Masauni wote kwa nyakati tofauti wametupilia mbali ombi hilo wakisema vyombo vya ndani vya ulinzi vinauwezo wa kutosha. Jumla ya watu 26 walikamatwa kutokana na tukio hilo na mpaka jana Jumanne 19 waliachiwa kwa dhamana. Donge nono Licha ya familia kutangaza zawadi nono bado bilioneo huyo hajapatikana. Baada ya kukaa kimya kwa siku nne, familia ya Mo ilijitokeza siku ya Jumatatu na kutangaza kuwa watatoa zawadi ya Shilingi za kitanzania bilioni moja kwa yeyote atakayewapatia taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa Mo. Msemaji wa familia hiyo, Azim Dewji amesema familia inapitiakipindi kigumu na wanashukuru kwa dua na faraja wanayopewa na Watanzania. Matajiri sita waliotekwa Afrika mwaka 2018 Licha ya kutangazwa kwa dau hilo siku tatu zilizopita, bado mpaka sasa hajapatikana. Mo anakisiwa kuwa na utajiri wa $1.5 bilioni kwa mujibu wa jarida la masuala ya fedha la Forbes na kumfanya kuwa tajiri namba moja Afrika Mashariki na bilionea mwenye umri mdogo zaidi Afrika. Tukio la kutekwa bilionea Mohammed Dewji, 43, Alhamisi ya wiki iliyopita bado limesalia kuwa ni fumbo lisilokuwa na jibu. text: Karl Kreile (kushoto) na Bodo Mende, kutoka Berlin, wameishi pamoja kwa miaka 38 Wanaume wawili mjini Berlin ambao wamekuwa pamoja kwa miaka 38 walikuwa wa kwaza kufunga ndoa. Wapenzi wa jinsia moja nchini Ujerumani wamekuwa wakisajili uhusiano wao tangu mwaka 2001, lakini ni kuanzia tu mwisho wa mwezi Juni ndipo bunge lilipiga kura ya kuwepo usawa wa ndoa. Kufunga ndoa kutawaruhusu wapenzi wa jinsia moja kunufaika na ulipaji kodi, kupanga watoto kama ndoa za kawaida kati ya mwanamume na mwanamke. Ndoa za wapenzi wa jinsia moja zimefanyika kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani. text: Neymar amekana madai kamba alimbaka Najila Trindade mjini Paris Najila Trindade aliambia runinga ya SBT nchini Brazil kwamba kisa hicho katika hoteli moja ya Paris mnamo tarehe 15 mwezi Mei kilikuwa cha unyanyasaji pamoja na ubakaji. Neymar amekana madai hayo , akituma ujumbe wa Whats App ili kujaribu kuonyesha kwamba hana hatia. Aliichezea kwa muda mfupi timu yake ya Brazil siku ya Jumatano katika mechi aliyodai kuwa ngumu katika kipindi chote che uchezaji wake. Neymar alipata jeraha baada ya dakika 20 ya mechi hiyo dhidi ya Qatar mjini Brasilia na sasa atakosa kushiriki katika michuano ya kombe la Copa America 2019 nchini Brazil akiwa na jeraha la mguu. Ni nini kilichosemwa katika mahojiano? Bi Trindade anasema kuwa alivutiwa na mchezaji huyo wa PSG na Brazil na alitaka kushiriki ngono naye. Anasema alisafarishwa kwa ndege hadi mjini Paris na kulipiwa katika hoteli ,moja ya mjini Paris. Bi Trindade alikuwa mtu wa kawaida- mwanamitindo na mwananfunzi wa mitindo , mtoto na mama. Aliyekuwa akimuhoji alimuuliza Bi Trindade iwapo kile kilichotokea ulikuwa ubakaji na bi Trindade alimjibu kwamba ulikuwa unyanyasaji wa kingono na ubakaji. Anasema kwamba wakati walipokutana na Neymar alikuwa mtu wa fujo ''mtu tofauti na yule niliyemjua katika ujumbe''. Bi Trindade alikua amejiandaa kushiriki ngono lakini akataka watumie mipira ya kondomu. Anadai kwamba Neymar alikataa akaleta fujo na kumbaka. Anasema kwamba alimwambia kuacha kufanya hivyo lakini akakataa. SBT ilichapisha baadhi ya mahojiano hayo katika mtandao wa Twitter { kwa Kireno). Video imepatikana. Je inaonyesha nini? Kanda ya Video inaonyesha mtafaruku kati ya bi Trindade katika chumba kimoja cha hoteli-ikidaiwa kuchukuliwa na bi Trindade. Wawili hao wanaonekana wakiwa wamelala katika kitanda ambapo baadaye mwanamke huyo anasimama na kuanza kumpiga mwanamume aliyelala kitandani ambaye anajikinga na miguu yake. Mwanamke huyo anasema nitakupiga, unajua kwa nini kwasababu umenipiga , mtafaruku huo ukionekana kuwa mkutano wao wa pili . Neymar amesema kuwa yeye na bi Trindade walikutana mara mbili. Katika mahojiano hayo ya Runinga ya SBT , Bi Trindade alisema kuwa alianza kuelewa kila kitu kilichofanyika baada ya mkutano wao wa kwanza ulipokamilika na kwamba alirudi ili kuthibitisha kitendo kilichofanyika huku akitaka haki kufanyika. Kanda hiyo ya Video ilionyeshwa katika kituo hicho cha Brazil. Je Neymar amesema nini? Neymar hajatoa tamko lolote kufikia sasa kuhusu mahojiano hayo ya runinga. Babake Neymar dos Santos , alihojiwa na TV Record kuhusu kanda hiyo ya video iliochukuliwa katika chumba cha hoteli na alisema kuwa ,mwanawe alikuwa ametegwa na kwamba Neymar alikuwa hana hatia. Katika taarifa ya mapema , Usimamizi wa Neymar uliziita shutuma hizo kuwa zisizo na haki na kusema kuwa mchezaji huyo alikua mwathiriwa wa jaribio la kumlaghai. Neymar alirudia madai hayo ya ulaghai katika ukurasa wake wa Instagram kwa dakiika saba. Akizungumza kwa lugha ya Kireno , mchezaji huyo alisema: Kile kilichotokea siku ile ni mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamume na mwanamke ndani ya chumba kama inavyokuwa kati ya wapenzi wawili. Na siku iliofuatia hakuna kubwa lililotokea. Tuliendelea kutumiana ujumbe . Aliniomba zawadi ya mtoto wake . Katika kanda hiyo ya video , mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alionyesha kile alichokitaja kuwa msururu wa ujumbe wa WhatsApp kati yake na Trindade , ikiwemo picha za kimapenzi naye." Anasema kwamba alilazimika kuziweka wazi ili kuonyesha kwamba kulikuwa hakuna na mno. katika mahojiano hayo bi Trindade alikana kujaribu kumlaghai bi Trindade akisema kuwa . Nataka haki na sio kulipwa fidia ya kifedha. Rais wa Brazil Jair Bolsonaro alimtembelea Neymar hospitalini baada ya mchezaji huyo wa kandanda kupata jeraha siku ya Jumatano ''akimtakia kupona kwa haraka'' ,bwana Bolsonaro alisema awali. ''Yuko katika hali ngumu lakini namuamini''. Je hali ya kisheria ikoje? Mawakili waliomwakilisha bi Trindade wanasema kuwa malalamishi yake ya kwanza yalikuwa ya uchokozi ama kupigwa na Neymar. Wanasema kwamba walikuwa wamekubaliana jinsi ya kutatau swala hilo na mawakili wa Neymar lakini baadaye mawakili hao walikataa. Mawakili wa pande zote mbili walitofautiana kuhusu ni nani haswa aliyeitisha kikao hicho. Baadaye Trindade aliwasilisha mahakamani madai yake siku ya Ijumaa mjini Sao Paulo. Neymar pia huenda akakabiliwa na uchunguzi kuhusu kuchapisha picha za Trindade bila ruhusa yake ka kuwa kitendo hicho huenda kikakiuka sheria za kulinda faragha ya mtu. Mwanamke aliyedai kubakwa na mchezaji wa soka nchini Brazil Neymar amejitokeza hadharani na kumshtumu mchezaji huyo katika runinga moja ya Brazil text: Mnangagwa akichukua kiapo cha kuwa rais Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla. Emmerson Mnangagwa, kwa jina la utani The the crocodile", ameanza hotuba yake kama rais wa Zimbabwe. ''Nahisi furaha sana kwa uamuzi wa chama cha Zanu PF kunialika kuhudumia taifa letu la Zimbabwe kama rais na kamanda mkuu wa majeshi kuanzia leo''. ''Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabil''a. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu . Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa. ''Kwangu mie bado ni rafiki mkubwa''. amesema kuwa jukumu lake halitatekelezwa kupitia hutuba. Raia wakimshangilia rais Mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Wafuasi wa rais mpya wa Zimbabwe Lazima nianze kazi.... Tutaanza kazi kwa haraka kutoka pale alipowachia aliyekuwa rais wetu Robert Mugabe. Hatuwezi kubadili yaliopita, kuna mengi ambayo tunaweza kufanya kwa sasa ili kulipatia taifa letu mwelekeo mpya. Hatuwezi kukubali kuwa watumwa wa yaliopita. Amesema kuwa mabadiliko ya umiliki wa ardhi yalifanyika na hayawezi kubadilishwa kwa kuwa huo utakuwa ukiukaji mkuu wa upiganiaji wa Uhuru. Lakini rais huo mpya ameahidi kuwalipa wakulima waliopoteza mashamba yao katika sera tata iliotekelezwa na utawala wa rais MUgabe. Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ameapishwa katika uwanja michezo wa Harare. Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke . Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe. Raia wa Zimbabwe akiwa amevalia kiatu cha muundo wa mamba, kama ishara ya kumuunga mkono rais mpya Emmerson Mnangagwa anayejiita ''Mamba''. Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa. Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari. Rais Mugabe alishutumiwa kwa kumuandaa mkewe Grace kuchukua wadhfa wa urais Bwana Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu Jumapili, na haifahamiki wako wapi . Alhamis , taarifa zilielezea kuwa Bwana Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa. Televisheni ya taifa imesema kuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bwana Munangagwa. Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare wenye viti 60,000- huku waandalizi wakiwataka waZimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo. lhamisi Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini (MDC ) alitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kisiasa ili kuondoa masuala yaliyoweka madarakani kwa muda mrefu utawala wa Bwana. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement fo Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai Bwana Munangagwa alikimbilia nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita- na kurejea nchini Jumatano wiki hii ambapo alipokelewa kama shujaa. Bwana Mnangagwa aliahidi kubuni ajira ambapo baadhi wanakadiria kuwa 90% ya watu hawana ajira. "Tunataka kukuza uchumi wetu, tunataka amani, tunataka kazi, kazi, kazi ," aliuambia umati wa watu uliomshangilia mjini Harare. Jumatano chama tawala cha ZANU PF kilisema kitafanya mageuzi kuondoa sheria zilizomfanya Mugabe kuwepo madarakani kwa muda mrefu. Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa. text: Shambulizi hilo lililenga harusi iliyokuwa ikiendelea ambapo takribani watu hamsini waliuawa Amri hiyo inakuja huku kukiwa na taarifa kwamba majeshi ya Uturuki yanajiandaa kushikilia mji wa mpakani wa Jarablus ambao upo mikononi mwa I-S . ''Tutapigana kuipinga Islamic State na taasisi nyingine za kigaidi mpaka mwisho. Tutaendelea kuunga mkono nchi zote zinazopambana na vikundi hivyo. Kama unavyojua wapiganaji wa upinzani wamefanikiwa kutekeleza mashambulizi kadhaa AL-Rai na mpakani kwetu. Kwa hakika, mikoa iliyo mipakani lazima iwaondoe kabisa wapiganaji wa IS. Kwa kipindi hiki tutaendelea kutoa ushirikiano ili kuwaondoa wapiganaji wa IS kutoka katika maeneo'' Wanamgambo wa Islamic state wanashutumiwa kutelekeza shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotokea mwishoni mwa juma lililopita katika mji wa Gaziantep uliopo kusini mwa Uturuki. Makaburi yakiwa tiyari kwa maziko Shambulizi hilo lililenga harusi iliyokuwa ikiendelea ambapo takribani watu hamsini waliuawa ,wengi wao wakiwa ni watoto. Uturuki imeshambuliwa mara kadhaa mwaka huu huku shambulizi la juma lililopita likitajwa kuwa baya zaidi. Wafiwa wakiomboleza kwa uchungu Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kundi la Islamic state linatakiwa kuondolewa kabisa kutoka mikoa ya kaskazini mwa Syria. text: Amina Okuyeva na mumewe walipigana dhidi ya makundi yanayoiunga mkono Urusi Adam Osmayev alijeruhiwa lakini anaweza kuishi baada ya gari alilokuwa akilitumia kumiminiwa risasi kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya ukrain. Wizara hiyo ilisema kuwa mke wake Osmaye, Amina Okuyev aliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji cha Hlevaha. Mwaka 2012 maafisa nchini Urusi walisema kuwa Bw. Osmayev alikuwa sehemu ya njama ya wanamgambo kumuua Bwa Putin. Vyombo vya habari vya Urusi viliripoti wakati huo kuwa watu walipanga kutega mabamu kwenye barabara ya Kutuzovsky mjini Moscow, inayotumiwa na Bw Putin kila siku. Ukrain Urusi baadaye iliitaka Ukrain kumsalimisha Bw. Osmayev lakini mamlaka nchini Urusi zikakataa kufanya hivyo, zikisema kuwa zilitaka kungoja hadi mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya kuamua kuhusu ombi lake la kupinga kusalimishwa kwa Urusi. Mwezi Juni alinusurika jaribio la kumuua mjini Kiev. Mshambuliaji kisha akapigwa risasi na kujeruhiwa na Bi Okuyeva. Hakuna mtu aliyedai kuhusika kwenye shambulizi la siku ya Jumatatu. Hii inakuja chini ya wiki moja baada ya mbunge wa Ukrain kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu kwenye mji mkuu Kiev. Mlinzi wa Ihor Mosiychuk na mtu mwingine waliuawa wakati wa mlipuko huo. Bi Okuyeva wakati moja alifanya kazi kama mshauri wake. Mwamamue moja kutoka Chechenia ambaye analaumiwa kwa kupanga kumuua rais wa Urusi Vladimir Putin amejeruhiwa na mke wake kuuliwa wakati wa shambulizi karibu na mji mkuu wa Ukrain Kiev. text: Disemba, 1987: Meli ya mafuta inachomeka katika mkondo wa Ormuz wakati wa vita kati ya Iran-Iraq Tumekuwa hapa siku za nyuma: Miaka 28 iliopita, Marekani na Iran zilipigana katika maji hayohayo. Meli zilishambuliwa , na wafanyikazi wakauawa na wengine kujeruhiwa. Kabla ya vita hivyo kuisha, ndege ya abiria ya Iran ilishambuliwa na kuanguka kwa bahati mbaya. Je hayo yanaweza kutokea tena? Vita vya meli za mafuta vilisababisha wasiwasi mkubwa wa kimataifa wakati wa vita vya miaka minane kati ya Iran na Sadam hussein wa Iraq. Mataifa hayo mawili yalishambuliana visima vya mafuta wakati wa miaka ya katikati ya 80. Na mara meli ambazo hazikuwa zikihusika zilianza kushambuliwa huku mataifa yakiendeleza shinikizo pande zote mbili. Meli za mafuta za Kuwait zilijipata katika hali mbaya. Marekani chini ya uongozi wa rais Ronald Regan haikutaka kujihusisha. Lakini hali iliokuwa ikiendelea katika Ghuba ilikua inaendelea kuwa hatari- ikithibitishwa wakati meli ya Marekani ya kivita , USS Stark iliposhambuliwa na kombora lililorushwa na ndege ya kivita ya Iraq -ijapokuwa maafisa wa Iraq baadaye walidai kwamba ilikuwa bahati mbaya. Kufikia mwezi Julai 1987, meli za mafuta za Kuwait zilizosajiliwa upya , zikipeperusha bendera ya Marekani zilisindikizwa katika Ghuba na meli za kivita za Marekani. Wakati huo ndio uliokua msafara mkubwa wa wanamaji tangu vita vya dunia vya pili. Oktoba 1987: Ndege ya Marekani ikisindikiza meli ya mafuta ya USS Guadalcanal katika Ghuba ya Persia Wakati huo kama sasa Marekani na Iran walikuwa katika mgogoro. Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Khomeini, alikuwa akiita Marekani 'shetani mkubwa' tangu mageuzi ya Iran ya 1979. Washington ilikua bado ikiuguza pigo ililopata kufuatia kutekwa nyara kwa wanadiplomasia wake 52 mjini Tehran kwa siku 444 kutoka 1979 hadi 1981. Na ijapokuwa Iran na Iraq ndio waliokuwa wakizozana, vita vya mashambulizi dhidi ya meli za mafuta vilikuwa mojawapo ya mgogoro wa muda mrefu kati ya Iran na Marekani. Ni vita ambavyo havijaisha na ambavyo vimezuka upya kufuatia uamuzi wa rais Donald Trump kuweka shinikizo kali baada ya kujiondoa katika mkataba wa kinyuklia wa Iran wa 2015. Kwa wakati mwengine tena maji ya mkondo wa bahari wa Hormuz yamekuwa eneo ambalo mgogoro huo unapiganiwa. Je mambo yamebadilika? Pande zote mbili zimepanua uwezo wao , kulingana na Dkt. Martin Navias , mwandishi wa kitabu cha vita vya meli za kubebea mafuta. Iran anasema ina uwezo mkubwa wa kutumia mabomu ya kutegwa ardhini , manuwari na maboti yenye kasi kushambulia na kuharibu meli za kibiashara na hata zile za kivita. Na sio tu vita baharini: Uwezo wa Iran wa kushambulia ndege za ujasusi za Marekani unaonyesha mwelekeo mpya wa vita hivyo. Jeshi la marekani lilitambua ndege hiyo kuwa wanamaji wa marekani RQ-4A Global Hawk Je Marekani na Iran zinaweza kushambuliana? Iwapo mashambulizi dhidi ya meli za mafuta yataongezeka , tunaweza kuona tena meli za mafuta zikipeperusha bendera za Marekani na kusafirishwa na meli za kivita za taifa hilo katika mkondo wa Hormuz. Mnamo tarehe 24 mwezi Julai 1987 , meli ya mafuta ya Kuwait iliokuwa ikipeperusha bendera ya Marekani ili kuilinda dhidi ya maadui iligonga bomu la ardhini la Iran katika msafara wa kwanza wa Marekani. Marekani ilipeleka meli zaidi za kivita katika eneo hilo. Pande hizo mbili sasa zinalumbana . Mnamo mwezi Septemba, ndege za Marekani zilishambulia meli ya Iran baada ya kuiona ikitega mabomu usiku kucha. Katika miezi iliofuatia, meli zaidi za mafuta na moja ya kivita ya Marekani zilishambuliwa. Wanajeshi wa Marekani walijibu kwa mashambulizi makali, wakiharibu kambi za jeshi la Iran na kushambulia meli za Iran za kivita. Vita hivyo vikaisha lakini baadaye kombora la Marekani kuiangusha ndege ya abiria ya Iran iliodhani kuwa ndege ya kivita na kuwaua abiri wote ndani yake. In 1988, a US warship shot down an Iranian airliner over the Persian Gulf killing 290 Ripoti rasmi kuhusu kisa hicho inasema kuwa huenda uharibifu wa data ndio uliosababisha shambulio hilo. Wanamaji wa Marekani waliwekeza pakubwa katika teknolojia na mafunzo ili kuzuia makosa kama hayo katika siku za usoni. Lakini mchanganuzi wa jeshi la wanamaji katika taasisi ya kimkakati Nick Childs anasema kuwa mazingira ya sasa ambapo wapinzani wanatumiana cheche kali za maneno katiika mitandao ya kijamii inazua mazingira ya hofu. Sekta ya habari imebadilika , anasema. Watu wanakuwa na hofu na kwamba kila upande unafikiria vibaya kuhusu mpinzani wake. Donald Trump na Hassan Rouhani wote wanasema kuwa hawataki vita. Wale wenye misimamo mikali kutoka pande zote mbili wanaelewa mambo tofauti. Why does the Strait of Hormuz matter? Mbali na vitisho vyote vilivyotokea 1987 na1988, ni meli chache za mafuta ambazo zilizamishwa huku uchukuzi wa meli katika mkondo wa bahari wa Hormuz ukiendelea bila tatizo lolote. N sasa miaka 30 baadaye , Marekani haitegemei sana mashariki ya kati kwa mafuta . Iran ndio itakayoathirika pakubwa iwapo mkondo wa bahari wa Hormuz utafungwa. Kwa sasa vita vya meli za mafuta sio rahisi kutokea lakini kwa kuwa pande zote mbili hazitaki vita sio kwamba vita haviwezi kutokea. Mazingira yaliopo yanaweza kuzua lolote. Meli za mafuta zinazochomeka katika Ghuba. Meli za kivita za Marekani zinaingilia kati. Matamshi ya uchochezi yanazua hofu ya mgogoro mkubwa. text: Mabegi yaliyojaa dawa za kulevya aina ya cocaine yenye kiwango cha Pauni milioni 50 yalipatikana katika fukwe mbili tofauti, Uingereza Zaidi ya kilo 360 ya mihadarati hiyo ilipatikana imesombwa hadi katika ufukwe wa Hopton, karibu na Great Yarmouth na ufukwe mwingine ulioko hapo karibu wa Caister. Mwananchi mmoja alifahamisha maafisa wa polisi wa kituo cha Norfolk, baada ya kugundua mabegi yaliyokuwa na dawa hizo za kulevya katika ufukwe wa Hopton. Maafisa wa usalama waendelea kutafuta madawa zaidi Polisi na maafisa wa mamlaka hiyo kuu ya kupambana na uhalifu wanaendelea kusaka maeneo hayo. Matthew Rivers, kutoka mamlaka hiyo kuu (NCA), na askari wa kulinda mipaka ya nchi, anasema kuwa: "tunafanya kazi pamoja na kikosi cha kulinda mpaka, idara ya polisi wa pwani, na maafisa wa polisi wa kituo cha Norfolk, ili kubaini namna mifuko hiyo ilifikishwa hapo, hata hivyo ni jambo la kutamausha ikiwa kweli madawa hayo yallikuwa yakifikishwa Uingereza. "Bila shaka hii ni shehena kubwa Zaidi ya dawa za kulevya kupatikana, na kupotea kwake ni pigo kubwa kwa magenge ya uhalifu yanayohusika." Wapelelezi hawaamini madawa hayo yalikuwa yakipelekwa katika eneo la Norfolk Superintended Dave Buckley, kutoka jimbo la Norfolk Constabulary, anasema: "Huku tukiamini kuwa tumepata shehena yote, raia yeyote akipata dawa zingine, tunaomba atufahamishe mara moja. "Tunao maafisa wa ziada watakaosalia katika eneo hilo ili kuendesha uchunguzi na kufuatilia taarifa zozote ambazo zinaweza kuchipuka." Dave Buckley alisema Mamlaka kuu ya kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza, imesema kuwa dawa ya kulevya aina ya Cocaine, yenye kiasi cha pauni milioni 50, imepatikana ikiwa imesombwa na maji hadi katika ufukwe wa Norfolk, Nchini Uingereza. text: Kwa usaidizi wao tutaangazia masuala tofuati, ikiwemo kutumia ghadhabu kushinikiza hatua kuchukuliwa, na kuwafichua wanawake ambao hawakuangaziwa katika hostoria. Wakiwa ni baina ya umri wa miaka 15 hadi 94, na kutoka zaidi ya mataifa 60, Msimu wa Wanawake 100 bora wa BBC inawajumuisha viongozi, wahamasishaji na mashujaa wa kila siku. Baadhi watakuwa wakitueleza katika Pakacha la Uhuru - kikapu chetu cha kidigitali kuhusu masuala yote ambayo wanawake wanahisi yanawazuia kujiendeleza. Wengine watatuletea hadithi za ufanisi dhidi ya vikwazo - kuanzia Mwanamke wa Uingereza aliyetumia kifungo chake kuanzisha biashara, hadi msichana wa Afghanistan ambaye nusra abadilishwe akifikiriwa kuwa ni mvulana. Juliet Sargeant, 53 - Mbunifu wa kurembesha bustani, Tanzania. Juliet Sargeant ametuzwa kwa harakati zake za kutaka utangamano katika kilimo cha maua Juliet Sargeant amezaliwa nchini Tanzania na ni mbunifu anayerembesha bustani. Juliet ni daktari pia ambaye sasa anajihusisha na kutengeneza bustani ili watu 'wahisi vizuri wanapozitembelea kama kwa mfano wa uzuri unaoonekana'. Alituzwa kwa kulipangia bustani iliyodhihirisha na kuhamasisha kuhusu utumwa mambo leo. Bustani hiyo ilijumuisha milango kadhaa na mti wa Mwaloni - iliyodhihirisha kukamatwa, na mti ambao William Wilberforce alikaa chini alipo apa kusaidia kumaliza biashara ya utumwa. Bustani hiyo ilibuniwa kuadhimisha siku ambayo bunge Uingereza lilipitisha sheria ya 2015 ya kupambana na utumwa wa mambo leo. "Nilitaka kusisitiza kwamba ni uhalifu wa kufichwa, nyuma ya milango iliyofungwa , kwahivyo ndani ya bustani kuna milango iliyo na rangi za kung'ara, iliyo na utepe katika pande nne," amesema Juliet. Kwa mujibu wa Bi Sargeant kuna matumaini makubwa katika mti huo wa Mwaloni kwasababu " ni chini ya mti kama huo ambapo William Wilberforce alisimama alipojitolea maisha yake kusitisha utumwa". Wengine kwenye orodha ya wanawake bora 100 wa BBC Abisoye Ajayi-Akinfolarin, 33 - Mjasiriamali katika masuala ya kijamii, Nigeria. Abisoye ni muasisi wa GirlsCoding, shirika lisilo la serikali linalowafunza wasichana namna ya kupamba na kuunda tovuti zinazosaidia kutatua matatizo katika jamii. Nimco Ali, 35 - Mwandishi na mwanaharakati, Somaliland. Nimco ametuzwa kwa harakati zake za kupambana na ukeketaji. Noma Dumezweni, 49 - Muigizaji eSwatini (Iliyokuwa Swaziland). Noma ni mwanamke wa kwanza kumuigiza Hermione Granger katika filamu ya Harry Potter and The Cursed Child, inayoonyeshwa katika ukumbi wa West End London na Broadway, New York. Shrouk El-Attar, 26 - Mhandisi wa Electroniki, Misri. Shrouk ni mkimbizi ambaye anafanya kazi ya uhandisi, anayenengua viuno kuhamasisha na kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Msiri. Raghda Ezzeldin, 26 - Mpiga mbizi, Misri. Raghda ameweka rekodi ya kupiga mbizi katika kina kirefu cha maji pasi kutumia vyenzo vya kumsaidia kupumua akiwa ndani ya maji. Mamitu Gashe, 72 - Mhudumu mkuu/Daktari wa upasuaji wa fistula, Ethiopia. Mamitu sasa ni daktari anayetambulika kimataifa wa upasuaji kurekebisha tundu linalojitokeza katika sehemu za siri au Fistula, baada ya kutibiwa kwa tatizo hilo mwenyewe. Thando Hopa, 29 - Mwanamitindo,Wakili, Mwanaharakati, Afrika kusini. Thando ni wakili anayetetea uwakilishi sawa na utangamano. Yeye ni mtu wa kwanza mweusi kuangaziwa katika chapisho la kalenda ya Pirelli 2018, Afrika kusini. Hindou Oumarou Ibrahim, 35 - Mwanamazingira na mteteaji haki za watu wa asili na wanawake, Chad. Hindou ni mwanamke wa asili nchini Chad, anayetetea kulindwa kwa mazingira na haki za watu wa asili katika kiwango cha kimataifa. Ruth Medufia, 27 - Mfuaji Vyuma, Ghana. Ruth ni mfuaji vyuma mwanamke anayeishi katika mitaa ya mabanda mjini na anatazamia kuwa mfano mwema kwa wasichana katika sekta ya ujenzi. Amina J Mohammed, 57 - Naibu katibu mkuu Umoja wa mataifa, Nigeria. Amina aliwahi kuwa waziri wa mazingira Nigeria na aliwahi pia kuwa mshauri maalum kwa katibu mkuu wa Umoja huo zamani, Ban Ki-moon. Helena Ndume, 58 - Daktari wa macho, Namibia. Helena amefanya upasuaji wa kurekebisha macho ya raia 35,000 nchini Namibia, bure bila ya malipo - baadhi kubwa ya wagonjwa aliowatibu sasa wanamuita "Daktari wa miujiza Namibia". Olivette Otele, 48 - Mhadhiri wa Historia katika chuo kikuu cha Bath Spa, Cameroon. Olivette ni mwanahistoria na msomi anayeshughulika na historia ya ukoloni wa Ulaya na tawala za uongozi wa baada ya utawala wa kikoloni. Brigitte Sossou Perenyi, 28 - Mzalishaji makala ndefu ya televisheni, Ghana. Brigitte ameshinda tuzo katika uzalishaji vipindi kwenye televisheni, aliyesimulia hadithi yake ya kuwa Trokosi nchini Togo - utamaduni wa kuwatumia wasichana kama watume kwenye mahekalu kama njia ya 'kutakasa madhambi' ya jamaa zao kwenya familia. Fatma Samoura, 56 - Katibu mkuu wa FIFA, Senegal. Fatma ni mwanamke wa kwanza na Muafrika wa kwanza kushikilia wadhifa wa katibu mkuu katika shirikisho la soka duniani Fifa. Bola Tinubu, 51 - Wakili, Nigeria. Bola ni wakili wa kibiashara aliyeanzisha huduma ya kwanza ya bure ya nambari za simu za usaidizi kwa watoto nchini Nigeria. Je wanawake 100 ni nini? BBC 100 Women huwataja wanawake 100 wenye ushawishi na wenye kutia moyo kote duniani kila mwaka na tunaangazia hadithi zao. Umekuwa mwaka wenye umuhimu katika masuala ya haki za wanawake kote duniani, kwa hivyo mwaka 2018 msimu wa Wanawake bora 100 wa BBC, utaangazia wanawake waasisi wanaotumia ari , hasira na ghadhabu kushinikiza mageuzi halisi duniani. Jumuika nasi kwenye Facebook, Instagram na Twitter na tumia #100Women BBC imetangaza orodha ya wanawake 100 bora wenye ushawishi kutoka kote duniani kwa mwaka 2018. text: Willian ajiunga rasmi na Arsenal The Blues ilitoa ofa yake mpya kwa mchezaji huyo lakini haikuwa tayari kufikia kile ambacho the Gunners imempa. "Naamini ni mchezaji ambaye kweli anaweza kutufanyia mabadiliko makubwa," amesema kocha wa Arsenal Mikel Arteta. "Tulikuwa tumedhamiria kabisa kuimarisha upande wa kushambulia wa kuingo wa kati na nafasi ya winga." Willian alishiriki michezo 339 kwa Chelsea baada ya kusajiliwa kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa pauni milioni 30 mwaka 2013. "Ni mchezaji ambaye tunaweza kumbadilisha badilisha, Anaweza kucheza nafasi tatu au nne tofauti," Arteta ameongeza. "Ana tajriba ya kila safu ya uwanja wa soka lakini bado ana nia ya kuja hapa kuchangia kuweka klabu katika nafasi inayostahili kuwa. "Nimefurahishwa sana na mazungumzo yangu nae na jinsi alivyokuwa anataka kujiunga nasi." Kiungo wa kati wa Brazil Willian, 32, kusaini mkataba wa miaka mitatu na Arsenal Arsenal ilimaliza ya nane katika Ligi ya Premia msimu uliopita, huku Chelsea ikimaliza ya nne na kupata nafasi ya kushiriki katika kombe la klabu bingwa Ulaya. Hata hivyo, Gunners iliwashinda mahasimu wao wa Uingereza katika fainali ya kombe la FA mechi ambayo Willian hakucheza kwasababu ya jeraha - ili kuhakikisha inajipatia nafasi katika mechi za Ligi ya Ulaya. Highlights: Arsenal beat Chelsea 2-1 to win FA Cup Willian anafuata nyayo za mlinzi David Luiz aliyehama Chelsea na kujiunga na Arsenal Agosti mwaka jana. Mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya Arsenal Edu alisema: "Namfahamu vizuri sana, kwa kipindi kirefu kwasababu tumekuwa tukifanyakazi pamoja katika timu ya taifa ya Brazil. "Anasifa nyingi nzuri yeye binafsi na pia kama mchezaji wa kandanda." Arsenal imemsajili kiungo wa kati wa Brazil Willian kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mkataba wa mchezaji huyo, 32, kukamilika. text: Trump amewataka wafuasi wake wahakikishe "timu yake inasalia ilipo" kwa miaka minne zaidi. Rais huyo anayetokana na chama cha Republican alitangaza uamuzi wake huo mbele ya maelfu ya wafuasi wake kwenye mkutano wa hadhara Florida, huku akilitaja jimbo hilo "makazi yake ya pili." Trump alitumia mkutano huo kueekeza mashambulizi kwa chama cha Democrats, akiwatuhumu wanachama wake kwa kujaribu "kuichanachana vipande nchi." Hata hivyo, kura za maoni za awali zinaonesha kuwa Trump yupo nyuma ya wagombea kadhaa ambao wanaweza kusimamishwa na chama cha Democrats. Aliungana jukwaani na mkewe bi Melania, ambaye amesema kuwa atakuwa mwenye furaha kuendelea kuwa Mke wa Rais mpaka mwaka 2024. "Leo hii nasimama mbele yenu kuzindua kampeni zangu za awamu ya pili kama rais wa Marekani," Trump amewaambia wafuasi wake. " Nawahakikishia kuwa sitawaangusha." Florida ni moja ya majimbo magumu ya kisiasa na Trump lilinyakua kwa ushindi mwembamba mwaka 2016. "Tutaendelea kuifanya Marekani kuwa imara zaidi," amesema kwenye mkutano huo uliofanyika Jumanne usiku kwa saa za Marekani. Baadhi ya wafuasi wake walikuwa wakisubiria kumuona kwa siku moja kabla. Maandamano ya kumpinga Trump yalifanyika katika eneo karibu na alipofanya uzinduzi wake wa kampeni. Trump amesema nini? Katika hotuba yake ya dakika 80, Trump alirejelea baadhi ya mambo ambayo yalimhakikishia ushindi katika kampeni za mwaka 2016. Ameendelea kuahidi kubana mbavu uhamiaji haramu, siku moja baada ya kuchapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa mamlaka za uhamiaji hivi karibuni zitawarudisha makwao mamilioni ya wahamiaji haramu. "Tunaamini nchi yetu inatakiwa kuwa ni sehemu salama kwa wananchi wafuatao sheria, sio kwa wahamiaji haramu wahalifu." Pia amewashutumu viongozi wa Democrats kwa kutaka kuwahalalisha wahamiaji haramu ili kuongeza idadi ya wapiga kura wao na kusema "wanataka kuharibu nchi yetu." Trump amewaita wapinzani wake kama genge la wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kushoto. "Kumchagua kiongozi yeyote wa Democrat mwaka 2020 ni kuchagua kunyanyua siasa kali za kijamaa na kusambaratisha ndoto ya Marekani," aliiambia hadhara. Pia amesifu ukuaji wa uchumi, akaukashifu uchunguzi dhidi yake maarufu kama Ripoti ya Muller, amabo uliangalia iwapo alishirikiana na Urusi kwenye kampeni zake za mwaka 2016, na kusema taarifa za habari kuhusu uchunguzi huo zilikuwa ghushi. Nini kilitokea kabla ya hotuba yake? Maelfu ya wafuasi walikusanyika nje ya eneo , wengine waliweka kambi eneo la Amway huko Orlando tangu mapema Jumatatu asubuhi. Trump mwenyewe alidai kuwa idadi ilikua ni maelfu siku mbili kabla hata hajafika katika eneo hilo. Wafuasi wa Trump wakimsubiria Chombo cha habari cha CBS kimetoa taarifa kuwa wapiga kura wengi waliokua katika foleni, wametaja suala la uchumi na uhamaiaji kama mambo makuu ambayo Trump anatakiwa kuyaongelea wakati wote wa kampeni zake. Waandamanaji pia walihudhuria baada ya kufanikiwa kwa harambee yao kupitia tovuti ya GoFundMe, pulizo linaloakisi muonekano wa Trump akiwa mtoto lilielea katika anga ya London pia wakati wa ziara ya hivi karibuni ya umoja wa ulaya lilionekana. Video katika mitandao ya kijamii kutoka eneo la tukio zimewaonesha kundi la msimamo mkali la mrengo wa kulia wakizuiwa na polisi walipotaka kuingilia maandamano ya wanaompinga Trump Mtihani wa Trump kuwasawishi Wamerekani Na Anthony Zurcher Mwandishi wa BBC Amerika Kaskazini Siku ya jumanne jioni huko Orlando, Florida, Donald Trump alianza Rasmi kampeni zake za kugombania muhula wa pili wa Urais. Hakuna mtu aliyeshangazwa, tayari watu walijua kuwa atagombea muhula wa pili, alijaza fomu yake ya 2020 mara baada ya kuapishwa Januari 2017 na tangu hapo amekua akipiga kampeni zake mara kwa mara katika majimbo mbalimbali. Wapinzani wa Trump Na siku ya Jumanne huko Florida, moja ya jimbo kubwa la ushindani wa uchaguzi,jimbo ambalo ni lazima Rais ashinde uchaguzi wa 2020, siku hiyo ilikua sio kuhusu kutoa taarifa yake ya kugombea muhula wa pili bali ilikua ni kwa namna gani ataweza kushinda. Tukio lilikua ndio mara ya kwanza Trump anatoa taarifa yake wazi wazi ya kugombea muhula wa pili katika uwanja wa unao beba watu elfu ishirini, mbele ya kundi la Maelfu ya wafuasi waliokua wakishangilia kwa kelele za hali ya juu huku wakiwa wamevalia kofia nyekundu. Mgombea wa Demokratiki Bernie Sanders alituma ujumbe Twitter uliosema kuwa ''trump anaishi katika ulimwengu wa kufikirika'' ''kazi yetu ya msingi ni kuhakikisha tunamshinda Rais hatari Zaidi katika historia ya nchi hii'' alisema Bernie Sanders. Rais wa Marekani Donald Trump ameazindua rasmi kampeni za kutetea kiti chake cha urais katika uchaguzi utakaofanyika mwakani 2020. text: Bw Mark Zuckerberg Kwenye orodha ya mabilionea waliopo duniani, Forbes wanasema kati ya mabilionea 2,208 ni 63 pekee ambao ni wa chini ya miaka 40. Idadi hiyo hata hivyo imeongezeka kutoka 56 mwaka 2017. Kati ya matajiri wa umri mdogo waliopo kwa sasa duniani, 34 ndio waliojitafutia utajiri wao ambapo 26 wamejizolea utajiri kupitia uwekezaji katika sekta ya teknolojia. Baadhi wamepata utajiri wao kupitia kuunda mitandao yao ya kijamii na huduma za biashara kwa kutumia simu na mtandao. Wengine wameunda kampuni za kuwawezesha watu kutumia bidhaa na huduma kwa pamoja, mfano kukodisha nyumba kwa kipindi ambacho mtu amesafiri. Mabilionea wote wa chini ya miaka 40 ambao walijizolea utajiri wao kupitia kuwekeza ni wanaume. Wanawake wote 16 mabilionea wa chini ya miaka 40 walirithi utajiri wao. Kwa jumla, mabilionea wote wa chini ya miaka 40 wanamiliki mali ya thamani ya $265 bilioni, idadi ambayo imeongezeka kutoka $208 bilioni. Mabilionea wa umri mdogo zaidi duniani Kwa mwaka wa tatu mtawalia, mabilionea wa umri mdogo zaidi ni wanawake wawili kutoka Norway - Alexandra na Katharina Andresen walio na miaka 21 na 22 mtawalia. Baba yao Johan H. Andersen aliwapa umiliki wa kampuni ya familia kwa jina Ferd mwaka 2007. Wawili hao wana utajiri wa dola $1.4 bilioni kila mmoja. Katharina Andresen aligonga vichwa vya habari Aprili 2007 aliposimamishwa na polisi Aprili 2017 akiendesha gari lake la kifahari aina ya Audi Q3 karibu na kituo kimoja cha kutelezea kwenye barafu akiwa mlevi. Alikuwa amepitisha kiwango kilichoruhusiwa mara tatu. Majaji walimpiga faini ya $32,000 na leseni yake ya kuendesha magari ikasimamishwa kwa miezi 13. Bilionea wa umri mdogo zaidi ambaye amejitafutia utajiri wake ni John Collison, 27, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Stripe. Alianzisha kampuni hiyo kwa pamoja na nduguye Patrick Collison, 29, ambaye pia yumo kwenye orodha ya mabilionea wa umri mdogo zaidi. Kampuni ya wawili hao Novemba 2016 ilikadiriwa kuwa na thamani ya dola 9.2 bilioni. Wote wawili utajiri mali yao ni $1 bilioni kila mmoja. John Collison ni mdogo kidogo wa umri kwa mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Snap inayomiliki mtandao wa Snapchat ambaye pia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo Evan Spiegel. Utajiri wa Evan ni $4.1 bilioni. Mwaka uliopita, aliongoza mpango wa kuuboresha mtandao wa kijamii wa kampuni hiyo wa Snapchat. 'Zuckerberg wa Urusi' Mtu mgeni katika orodha ya mabilionea hawa ni Pavel Durov ambaye amekuwa akifahamika kama Mark Zuckerberg wa Urusi. Yeye ndiye mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa pili kwa ukubwa Urusi, mtandao wa Vkontakte. Wote wawili wana miaka 33. Aliuanzisha mtandao huo akiwa na miaka 22 mwaka 2007. Mtandao wake wa kijamii una watumiaji zaidi ya 400 milioni. Durov alianzisha mtandao wa Telegram Yeye pia ndiye mmiliki mkubwa wa mtandao wa Telegram ambao unatumiwa na watu zaidi ya 100 milioni duniani. Lynsi Snyder ni tajiri mwingine ambaye kwa sasa ana miaka 35 na utajiri wa $1.2 bilioni. Alirithi sehemu ya biashara ya hoteli za familia yake ya In-N-Out nchini Marekani. Babu na bibi yake Harry na Esther Snyder walianzisha biashara hiyo mwaka 1948. Bilionea tajiri zaidi wa umri mdogo Bilionea tajiri zaidi miongoni mwa walio na chini ya miaka 40 ni Mark Zuckerberg ambaye anawazidi wengine pakubwa. Utajiri wake ni $71 bilioni. Bilionea wa pili tajiri zaidi wa umri mdogo ni Yang Huiyan ambaye ni mrithi katika kampuni kubwa ya uwekezaji katika nyumba na ardhi yenye makao yake China. Ana miaka 36 na utajiri wake unakadiriwa kuwa $21.9 bilioni. Yang humiliki asilimia 57% ya hisa katika kampuni ya Country Garden Holdings ambao ni urithi kutoka kwa babake Yeung Kwok Keung alioupokea 2007. Watu kumi matajiri zaidi duniani wa chini ya miaka 40 10. Mark Zuckerberg, 33, Utajiri wake: $71 bilioni Marekani, Facebook 9. Dustin Moskovitz, 33 Utajiri wake: $14 bilioni Marekani,Facebook 8. Julio Mario Domingo III, 32 Utajiri wake: $2.2 bilioni Marekani, Pombe 7. Ginia Rinehart, 31 Utajiri wake: $1.3 bilioni Australia, Madini 6. Patrick Collins, 29, Utajiri wake: $1 bilioni Ireland, Stripe 5. Bobby Murphy, 29 Utajiri wake: $4.2 bilioni Marekani, Snapchat 4. John collison, 27 Utajiri wake: 1 bilioni Ireland ,Stripe 3. Evan Spiegel, 27 Utajiri wake: $ 4.1 bilioni Marekani, Snapchat 2. Katharina Andresen, 22 Utajiri wake: $1.4 bilioni Norway, uwekezaji 1. Alexandra Andresen,21 Utajiri wake: $1.4 bilioni Norway, uwekezaji Mabilionea wengi walio na umri mdogo duniani, ambao hawakurithi mali kutoka kwa wazazi wao, walijipatia utajiri wao kupitia uwekezaji katika sekta ya teknolojia, kwa mujibu wa jarida la Forbes. text: Mkurugenzi Mtendaji wa (LHRC), Bi. Anna Henga katika uzinduzi wa ripoti ya Haki za Binadamu 2018 Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliopewa jina "Ukatili wa Kingono: Tishio kwa Haki na Ustawi wa Mtoto Tanzania", iliowasilishwa na mwakilishi wa LHRC Fundikila Wazambi, haki ya kwanza kuvunjwa ni haki dhidi ya Ukatili. "...Mambo yaliyoathiri haki za binadamu Tanzania kwa mwaka 2018 ni pamoja na Sheria kandamizi, Ukatili dhidi ya watoto, hasa matukio ya mauaji na ulawiti wa watoto... " ameeleza Fundikila ambaye pia ni mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo. Imani za kishirikina zimetajwa kuchochea ukatili dhidi ya watoto huku watoto wenye ulemavu bado wakibaguliwa na kukabiliwa na ukatili...ikiwemo kufichwa. Janga la mauaji ya watoto katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo mkoani Njombe, kusini magharibi Tanzania bado limegubika vyombo vya habari nchini tanzania tangu mapema mwaka huu. Mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu Tanzania ilitikiswa na mauaji ya watoto chini ya miaka 10 katika mikoa ya Njombe na Simiyu. Haki 5 za binaadamu zilizovunjwa zaidi Tanzania 2018 Katika visa vyote hivyo, imani za kishirikina zimekuwa zikihusishwa kuwa ni chanzo kikuu na tayari mamlaka nchini Tanzania zimewakamata washukiwa kadhaa. Kadhalika, haki za kujieleza na kukusanyika pia zinaarifiwa kukiukwa Tanzania na hilo LHRC inasema limeendelea kuathiri kukua kwa vyama vya siasa nchini. Ripoti hiyo iliyoandikwa na LHRC kwa upande wa Tanzania bara, na ZLSC kwa upande wa Zanzibar, imeeleza kwamba uhuru wa kujieleza umezidi kudorora ikiwa imechangiwa na sheria mbalimbali ikiwemo ya sheria ya makosa ya mtandaoni, hususan kanuni zake za mwaka 2018 na nyinginezo ambazo zinatajwa kuchangia sana kudorora kwa uhuru na haki hii. Ripoti hiyo ya mwaka huu imegusia haki za kisiasa, kiraia , kijamii na makundi ya watu walio katika hatari. Ripoti ya LHRC 2018 imetolewa wakati ambapo mashirika yasio ya serikali 38 nchini Tanzania, barani Afrika na kimataifa yametoa wito kupitia barua iliyochapishwa kwa wanachama wa baraza la haki za bnaadamu katika Umoja wa mataifa kuchukua hatua kuhusu hali nchini Tanzania. Katika barua hiyo yanaeleza kwamba nafasi imeendelea kupungua kwa watetezi wa haki za binaadamu, mashirika ya kiraia, waandishi habari, wamiliki blogu, wapenzi wa jinsia moja, upinzani na sauti jumla zinazoikosoa serikali. Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbas ameipongeza ripoti hiyo na kusema hiyo ni sehemu ya demokrasia kwa sababu inazungumza tatizo ambalo lipo katika jamii. Watoto wanakumbana na matukio mbalimbali ya ukatili hivyo ni wito kwa wanajamii kama wazazi, walezi kutimiza wajibu wetu katika ngazi ya familia, mtaa na taifa. "Serikali imetimiza wajibu wake kwa kuweka mfumo wa kumtetea mtoto kisheria" Dkt.Abas aeleza. Aidha Dkt Abas amesisitiza kuwa ameisoma ripoti hiyo na kuona kuwa kuna mikanganyo katika uwasilishaji wake jambo ambalo siku za mbeleni inabidi waboreshe. Kwa kugusia eneo la uhuru wa habari kuwa wamepima vipi huo uhuru, ukosoaji wa serikali na kuna mambo mengine wametaja matukio ambayo yalishatolewa mahamuzi na mahakama je iweje ripoti inachapisha masuala hayo kuwa kukiukwa kwa haki za binadamu. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Augustine Mahiga amewahi kusema kutofautiana kwa mitazamo na baadhi ya mataifa hayo kuhusiana na suala la haki za binadamu kunatokana na utofauti wa tafsiri ya misingi ya haki za binadamu. "Mara nyingi watu wanapozungumzia suala la haki za binadamu wanapiga picha kwa mara moja bila kutazama mazingira yote, bila kutazama limetokana na nini na limetokea wapi na kwa nini suala hilo limezungumzwa? Hapa katikati kumekuwa na masuala mbalimbali ambayo hayakufafanuliwa vizuri, misingi ya haki za kibinadamu huwezi kuchanganya na utamaduni wa nchi, huwezi kuchanganya na sheria za nchi na kuchanganya na misimamo ya kidini na Imani za watu." Mahiga ameieleza BBC. Visa vya mauaji ya kutoweka kwa watu Tanzania Serikali ya Marekani katika ripoti ya haki za binaadamu ya mwaka 2018, imeeleza kwamba licha ya serikali ya Tanzania kuchukua hatua kuwashtaki maafisa ambao wamekiuka haki za binaadamu, lakini impunity imesambaa katika idara ya polisi na vitengo vingine vya usalama na vya kiraia ndani ya serikali. Ripoti hii ya LHRC imetokana na mkusanyiko wa matukio yalioripotiwa ya ukiukaji wa haki za binaadamu tangu mnamo 2018 kupitia vyombo vya habari na pia kwa kutathmini nyaraka mbali mbali ambapo kumekuwepo ripoti za wanasiasa wa upinzani na wakosoaji wa serikali waliokamatwa, kushambuliwa na wengine hata kuuawa na watu wasiojulikana. Zaidi ya visa 6000 vya ukatili au unyanyasaji dhidi ya watoto ikiwemo ukatili kiongono viliripotiwa mnamo 2018, kimebainisha Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) katika ripoti yake mpya iliyozinduliwa leo. text: Guzman alikuwa mkuu wa genge la walanguzi la Sinaloa Hata hivyo, Guzman anaweza akakata rufaa uamuzi wa kumpeleka Marekani na mawakili wake wanasema watapigana vita hadi mwisho. Anakabiliwa na mashtaka kadha nchini Marekani yakiwemo ulanguzi wa dawa na mauaji. Kiongozi huyo wa genge la Sinaloa anazuiliwa katika gereza la Ciudad Juarez, karibu na mpaka wa Mexico na Marekani, chini ya ulinzi mkali. Alikamatwa mwezi Januari miezi sita baada yake kutoroka gerezani kwa kupitia njia ya chini ya ardhi iliyochimbwa hadi kwenye seli yake gerezani. Alikuwa tayari ametoroka kutoka gereza la ulinzi mkali mara moja awali, na akakaa miaka 13 akitafutwa sana na maafisa wa usalama. Kamishna mkuu wa usalama wa Mexico Renato Sales Heredia amesema kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga kwamba Mexico inatarajia kumhamishia Marekani mshukiwa huyo "Januari au Februari". Lakini wakili Jose Refugio Rodriguez, amesema kuna kesi nyingi za rufaa ambazo uamuzi wake unasubiriwa na kwamba hilo haliwezi kufanyika haraka. "Muda huo hautoshi," Bw Rodriguez amesema na kudokeza kwamba njia pekee ya kumpeleka Guzman Marekani mapema mwaka ujao ni kwa kutumia nguvu pekee. Mexico inapanga kumkabidhi mlanguzi hatari wa mihadarati Joaquin "El Chapo" Guzman kwa maafisa wa Marekani mwezi Februari, kwa mujibu wa afisa mmoja mkuu nchini Mexico text: Forbes ilikadiria utajiri wa Kylie Jenner kukaribia dola bilioni 1 Ni mafanikio ambayo watu wachache sana wanaweza kuyapata. Kulikuwa na watu 5,700 kote duniani waliokuwa na utajiri unaozidi dola milioni 500 mwaka uliopita kulingana na ripoti kutoka kwa Global Wealth Report. Mabilionea halisi hata hivyo ni wachache. Lakini mtu anahitaji nini hadi kuitwa bilionea? 1. Anzisha kampuni yako Ukiangalia watu matajiri duniani kwa mfano Jeff Bezos wa Amazon, Mark Zuckerberg wa Facebook, Amancio Ortega wa Zara na Jack Ma wa Alibaba ndio wanatawala. Forbes inawatambua watu thuluthi mbili ya mabilionea 2,208 kuwa waliojizolea utajiri wao na idadi hiyo inazidi kuongezeka. Ni kweli kuwa neno utajiri wa kujizolea linaweza kuwa na ugumu kulielezea. Hatua ya Forbes kumtaja Kylie Jenner - ambaye amezaliwa katika familia tajiri kama aliyejipatia utajiri ilizua maoni mengi kwenye mtandao. Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon, ndiye mtu tajiri zaidi dunaini 2. Kurithi pesa Karibu thuluthi moja ya watu walio katika orodha ya Forbes walirithi pesa zao. Hao ni pamoja na watu saba wa familia ya Walton, warithi wa maduka wa Walmart na Francoise Bettencourt-Meyers ambaye familia yake ilianzisha kampuni ya L'Oreal. Urithi ni muhimu hasa barani Ulaya kutokana na kuwa umechangia kwa karibu nusu ya mabilionea kulinda na takwimu za Forbes za mwaka 2014. Kuna sababu kadhaa zilizochangia watu ambao walirithi mali kuzidi kuongezeka. Sababu moja ni kuwa thamani ya mali kama hisa imeongezeka kwa haraka kuliko mali nyingine miaka ya hivi karibuni. 3. Kuwa na mfuko wa uwekezaji Kuna zaidi ya watu 140 katika sekta ya fedha walio na utajiri unaozidi dola blioni 2.5 kwenye orodha ya watu matajiri kwenye jarida la Forbes mwaka 2018. Wengi wao ni kutoka nchini Marekani ambapo asilimia 25 ya mabilionea hupata utajiri wao kutoka sekta ya fedha. Lakini usidhani kuwa ni rahisi kupata mafanikio hayo. Mkuu wa kampuni ya JP Morgan Chase boss Jamie Dimon ni baadhi ya mabilionea wachache waliochukua mkondo huo. Abigail Johnson, ambaye anaismia mfuko wa uwekezaji wa babu yake wa Fidelity Investments, ni kati ya wanawake walio kwenye Forbes Na wafadhili wengi karibu asilimia 20 ya watu matajiri zaidi ya 143 wana uhusiano na mifuko ya uwekezaji. 4.Hama Uingereza. Idadi ya mabilionea nchini Uingereza ilishuka mwaka uliopita ambalo ni eneo tu duniani hali kama hiyo ilishuhudiwa kwa mujibu wa Forbes, Eneo linaloshuhudia kuongezeka kwa watu matajiri duniani ni la Asia Pacific. Karibu asilimia 29 ya watu mabilionea wapya mwaka uliopita walitokea eneo hilo kwa mujibu wa jarida la WealthX linalokadiria kuwa kuna mabilionea 2,750 duniani idadi iliyo juu kuliko ile ya Forbes. China pekee ina mabilionea 29 kati ya 259 mabilionea wapya, idadi ya juu kuliko ua nchi yoyote. Licha ya hatua zilizopigwa sehemu zingine duniani, Marekani inasalia nchi yenye mabilionea wengi zaidi ikiwa na mabilionea 585. Mwanzilishi wa Alibaba Jack Ma ni mmoja wa watu maajiri zaidi nchini China 5. Usiwe na wasi wasi wa kufuata sheria Mabilionea si wageni kwa kesi mahakamani. Kwa mfano Bill Gates, anawez kujulikana kama mtu tajiri wa kutoa misaada lakini historia yake si safi vile. Mnamo miaka ya tisini Marekani iliishtaki kampuni ya Microsoft kwa kutumia mbinu zinazozuia ushindani. Serikali ya Marekani ilishinda na Microsoft ikakata rufaa. Kesi hiyo iliishia makubaliano. Tume ya Ulaya nayo ishaipiga faini kampuni ya Microsoft. Baddhi ya kampuni ambazo pia zimepigwa faini ni pamoja na Google na Samsung na piazile zisizo za teknolojia kama ya kamari ya Las Vegas Sands. Forbes ilizua maoni mengi wiki hii wakati ilisema kuwa nyota wa mitandao ya kijamii Kylie Jenner amepata utajiri wa karibu dola bilioni 1 text: Zimbabwe imepuuzilia mbali madai hayo. Waziri wa habari Nick Mangwana anasema Marekani haina ushahidi wa kuthibitisha madai yake na kuongeza kuwa Washington "imepotoshwa au kuhadaiwa kuhusu"suala hilo. Eneo la Marange mashariki mwa Zimbabwe linakadiriwa kuwa na hifadhi kubwa ya madini ya almasi duniani. Madini hayo ni yanasemekana kuwa kiungo muhimu sehemu katika ukuaji wa uchumi wa Zimbabwe. Maaekani inasema nini What? Marekani imetaja mfumo wa kuajiri watu katika migodi hiyo imezungukwa na ulaji rushwa na kwamba watu wanaotaka kufanya kazi mahali hapo wanalazimika kulipa hongo kabla ya kuruhusiwa kufika migodini. Wanapofika, kwa mujibu wa kampuni ya Brenda Smith, wafanyikazi hawaruhusiwi kuoka na wale wnaokaidi amri hiyo wanachukuliwa hatua ya kupigwa/kunyanyaswa kimapenzi ai kukamatwa. Serikali ya Marekani inasema kuwa ushahidi "umenakiliwa vililivyo". Wanajeshi na walinzi wa kibinafsi wanadhibiti migodi ya almasi ya Marange Ushahidi ni upi? Wanahabari na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamedhibitiwa kufika maeneo hayo, lazima wawe na idhini maalum. Kundi linalochunguza mfumo wa ajira katika migodi ya Marange diamond limekusanya ushahidi kuhusu ajira ya lazima. Menyekitiwa Bocha Diamond Trust, Moses Mukwada, aliiambia BBC kumekuwa na visa vya wanavijiji kukamatwa na kulazimishwa kufanya kazi katika migodi ya alamasi. Makundi mengine hata hiyo yalichelea kuzungumzia suala hilo. Kituo cha kusimamia mali asili (CNRG), shirika la kutetea haki za wachimbaji madini katika eneo hilo, linaasema dhulma dhidi ya wachimbaji madini vinatokana na kufanyishwa kazi kwa lazima. "Kama shirika hatujapuuza suala la watu [kulazimishwa kazi], lakini taarifa [kutoka kwa serikali ya Marekani]na tungependelea kujua ni nani anamlazimisha nani," Simiso Mlevu, msemaji wa CNRG. Marekani imepiga marufuku uagizaji wa almasi kutoka Zimbabwe mapema mwezi huu kwa kuhofia watu wanalazimishwa kufanya kazi katika migodi ya madini ya taifa hilo. text: Feri hiyo husafirisha watu kupitia mto Gambia hadi mji mkuu wa Senegal Dakar Adama Barrow alishinda uchaguzi na kuapishwa kwake kunapangwa kufanyika siku ya Alhamisi. Lakini Rais Yahya Jammeh aliyakataa matokeo hayo na amesema kuwa hataondoka madarakani hadi pale mahakama ya juu itakaposikiliza kesi. Adama Barrow apewa makao Senegal Wasifu wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow Bunge limekutana kwa kikao cha dharura. Huku sababu ya kikao hicho ikiwa haijulikani, mwandishi wa BBC mjini Banjul anasema kuwa bunge huenda likaombwa kuongeza muhula wa bwana Jammeh. Bwana Barrow atabaki nchini Senegal hadi siku ya kuapishwa kwake. Gambia, nchi yenye watu wasiozidi milioni mbili inazungukwa pande tatu na Senegal, ambayo inasema kwa inatathmini kuchukua hatua za kijeshi kumuondoa bwana Jammeh madarakani. Mfanyakazi katika kivuko kikuu cha feri nchini Gambia, ameiambia BBC kuwa maelfu ya watu wanaikimbia nchi kila siku wakihofia kutokea vita. text: Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani. Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika. Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya. Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu. Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa. Hebu tuwafahamu zaidi. Nyoka mdogo aina ya pit viper Je ni kweli? Nyoka hawatambai kwenye mawe na kamba Wanaweza kutambaa juu na hata chini ya mawe, kwenye miti na majengo. Nyoka hupenda kujificha ardhini. Ni rahisi kwao kujificha chini ya vichaka, na vigumu kutambaa chini ya mawe madogo kwenye bustani. Ni vyema kuzikata nyasi ziwe ndogo na uondoshe masalio yoyote ya nyasi zilizokatwa au majani makavu yalioangukana kujikusanya. Kadhalika ni vymea uondoshe sehemu za mti zilizoanguka juu ya paa au zinazoning'inia kutoka nyumba yako. Ukiona mtoto wa nyoka na familia nzima i papo Iwapo nyoka huzaa watoto au kutaga mayai, kawaida anapojifungua huwaondokea watoto na kuwaacha kivyao. Iwapo utamuona nyoka mkubwa karibu na mdogo basi huenda ni sadfa tu. Wao hutawanyika punde wanapojifungua. Eyelash viper Nyoka huteleza Kawaida, watu ambao hawajawahi kumgusa nyoka hudhani kwamba wanyama hao huteleza ukiwagusa. Ngozi ya nyoka huonekana kuwa kavu, lakini kwa kuigusa ni nyororo. Nyoka ni wakali Nyoka wanaogopa binaadamu zaidi ya binaadamu wanavyowaogopa. Kwa kawaida huwa wana haya au aibu sana na iwapo wangekuwa na nafasi anaweza kutoroka asionekane. Ni iwapo tu amekwama au ametishiwa, kama ilivyo kwa kiumbe chochote, nyoka hushambulia kujilinda. Lakini mara nyingi baadhi huona afadhali kutoroka kuliko kushambulia. Nyoka wote hutaga mayai Licha ya kwamba reptilia wengi hutaga mayai, sio nyoka wote wanaotaga. Baadhi ya nyoka kama wa aina ijulikanayo kama Oriental Vine, huzaa nyoka wadogo. Wasukuma na utamaduni wao wa kuwafuga nyoka Tanzania Mfahamu zaidi Nyoka Kwa kawaida nyoka hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika. text: Polisi wa Malaysia wakishika doria nje ya hospitali unakohifadhiwa mwili wa Kim Jong-nam Mkurugenzi mkuu wa afya Noor Hisham Abdullah amewaambia wanahabari kwamba hawajapata ushahidi wowote wa kutokea kwa mshtuko wa moyo au vidonda vilivyotokana na kudungwa mwilini. Amesema uchunguzi kwenye maabara pia haukuweza kuutambia mwili huo. Kim Jong-nam anadaiwa kuwa mwanamume aliyefariki wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, baada ya kuonekana kana kwamba alipewa sumu. Pyongyang imetilia shaka utambulisho wa mwili huo na imeitaka Malaysia kusalimisha mwili huo kwa maafisa wa Korea Kaskazini. Jumatatu, Malaysia ilimuita nyumbani balozi wake kutoka Korea Kaskazini huku mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ukiendelea kutanda. Kuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasia Maafisa wa Malaysia wamesema wanahitaji kupata vinasaba kutoka kwa jamaa za Kim Jong-nam ndipo waweze kuutambua mwili huo kikamilifu. Ulinzi mkali umewekwa katika hospitali ambapo mwili huo unahifadhiwa. Kuna taarifa kwamba huenda mwanawe Kim Jong-nam, Kim Han-sol, amesafiri Malaysia kuuchukua mwili huo. claim the body. Jumanne, maafisa wa polisi waliokuwa na silaha kali walifika katika hospitali hiyo ya Kuala Lumpur, na baadaye wakafuatwa na maafisa wa usalama waliokuwa katika magari yasiyokuwa na utambulisho rasmi. Mwanawe Kim, Kim Han-sol amekuwa akiishi Macau. Mwanamke mmoja alikamatwa kuhusiana na mauaji hayo, na alisema alidhani ulikuwa mchezo wa kuigiza Raia wanne wa Korea Kaskazini wanasakwa na wachunguzi wa jinai kuhusiana na kifo cha Kim Maafisa wa serikali ya Malaysia wamesema bado hawajabaini nini kilisababisha kifo cha ndugu wa rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. text: Mwanamke wa China anayefanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo. Matilda Ho alizungumza katika mkutano wa Teknonoljia, utumbuizaji na mitindo kuhusu umuhimu wa kusambaza ujumbe wa chakula chenye afya. Anaunga mkono vyakula ikiwemo vile vilivyo na protini kutoka kwa viwavi. China ina tatizo la ukuwaji kutokana na kunenepe kupitia kiasi na ugonjwa wa kisukari. ''China ina asilimia 20 ya watu duniani lakini ni aslimia 7 pekee ya ardhi yake ilio na rutba'', alisema bi Ho. Mtu mmoja kati ya raia wanne wa Uchina anaugua ugonjwa wa kisukari na mmoja kati ya watu wanne amenenepa kupita kiasi. Wadudu kwa jina Silkworms anaofanya kampeni kwa Wachina kuwala Bi Ho alianza kukabiliana na swala hilo kupitia soko la mtandao la wakulima ambalo sasa linatoa bidhaa 240 kutoka kwa walkulima 57. Mtandao huo umepata wateja 40,000 tangu uzinduliwe miezi 18 iliopita. ''Nilitaka kutumia teknolojia ili kupunguza pengo lililopo kati ya wakulima na wanunuzi'', bi Ho aliambia BBC. ''Ni haki yako kujua kule chakula chako kinakotoka na kuwahamasisha wateja''. Chakula hicho husambazwa kwa wateja kupitia magari ya kielektroniki na maboksi. Mfanyibiashara mmoja wa Uchina anafanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo. text: Mfumo huo umetumika na Israel tangu 2011 Mfumo huo unaotumia rada na kutungua makombora kwa lengo la kukabiliana na tishio lolote umekuwepo tangu 2011. Idara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa mfumo huo utatumika kufanya majaribio huku ikitafuta mahitaji ya muda mrefu ya jeshi lake. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametaja mauzo hayo kuwa mafanikio makubwa ya taifa lake. ''Hili ni dhihirisho jingine la kuimarika kwa ushirikiano wetu thabiti na Marekani, na onyesho kwamba Israel inazidi kupandisha hadi yake duniani, "taarifa yake iliendelea. Ufanisi wake Mfumo huo wa Iron Dome hufanya kazi kwa kufuatilia tishio lolote la shambulio kwa muda mfupi kupitia rada yake , kisha inachambua data kuhusu eneo litakaloathirika - kabla ya kuamua kurusha kombora litakalotungua shambulio hilo. Maafisa wa Israel wanasema kuwa mfumo huo wa makombora unaoweza kufanya kazi katika mazingira yoyote mbali na kusafirishwa kutoka eneo moja hadi jingine una mafanikio ya hadi asilimia 90. Unasemekana kuwa na uwezo wa kulinda mji mzima dhidi ya tishio lolote la angani na umetumiwa sana kutungua makombora yaliorushwa na wapiganaji wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza. Mfumo huo umetumika na Israel tangu 2011 Utengenezaji wa mfumo huo Ilichukua miaka kadhaa kuunda mfumo huo na ulitengezwa na kampuni ya ulinzi nchini Israel Rafael Advanced Defence Systems. Marekani ilichangia sana katika uundaji wa mfumo huo, na baadhi ya vifaa vyake vinatoka kwa makampuni ya Marekani. Katika taarifa, idara ya ulinzi nchini Israel ilisema kuwa ununuzi huo ulifanyika kutokana na mahitaji yake ya dharura ya jeshi la Marekani. Ripoti zilivuja kuhusu ununuzi huo mwezi uliopita. Kanali Patrick Seiber wa jeshi la Marekani amesema kuwa mfumo huo unachunguzwa na kujaribiwa ili kuwalinda wanajeshi wa Marekani waliotumwa katika mataifa ya kigeni. Huku mfumo huo wa Iron Dome ukiwa umetumika na wanahewa wa Israel tangu 2011 na kuthibitisha uwezo wake katika vita, ilazima ibainike kuwa jeshi la Marekani litauchunguza kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa siku zijazo wa kujilinda , taarifa iliotolewa siku ya Jumatano ilisema. Jeshi la Marekani limetangaza mipango ya kutaka kununua na kujaribu mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa Israel kwa jina Iron Dome. text: Waombolezaji waliovaa nguo nyeusi na nyekundu wamejaa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Accra ambako unaweza kupokea takriban watu 4000. Watu wengine zaidi wamekaa katika ukumbi mwingine nje ya ukumbi mkuu wakitazama kupitia televisheni shughuli zinavyoendelea. Wageni waheshimiwa kutoka kote duniani wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wamataifa akiwemo rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast pamoja na katibu mkuu wa sasa Antonio Gutterrez. Viongozi wa kitamaduni, walizunguka jeneza la Annan Waombolezaji wamekuwa wakiimba nyimbo na kumkumbuka Annan akiwemo mkewe, wakili nchini Sweden Nane Maria Annan. Katika hotuba yake, ameeleza jinsi Annan daima alivyotazamia kurudi nyumbani, na ameishukuru Ghana kwa kumleta duniani mtu wa aina yake. Alimaliza kwa kusema: "Ataendelea kukumbukwa kupitia wakfu wake na kupitia kwetu sote." Katibu mkuu wa sasa wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amewaambia waombolezaji, wakiwemo baadhi ya viongozi wa Afrika na viongozi wa zamani kwamba wakati Annan akizungumza: Nukuu ya ujumbe huo: ''Dunia hutegemea kusikiza na tulifaidika kutokana na busara yake." Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake Annan umekuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu. Viongozi tofuati duniani wanahudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra. Mjane wa aliyekuwa rais wa kwanza afrika kusini Nelson Mandela - Bi Graca Machel na Gro Harlem Brundtland ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu nchini Norway ni miongoni mwa wanaohudhuria mazishi ya Annan Mojawapo ni Graça Machel, mke wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrika kusini, Nelson Mandela Nukuu ya ujumbe wake: ''Daima alitetea amani , na kuwapatia watu kipa umbelekatika mchango wake duniani. Ninampenda kwa dhati, ni kakangu na kwa kweli nilazima niseme, bado sijakubali kwamba ameondoka." Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006. Leo inahitimisha kilele cha wiki kadhaa ya maandalizi ya mazishi yake, ambaye ni mmoja wa wana diplomasia wanaoheshimika duniani. Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Accra anasema kuwa, ngoma za maombolezo zilisikika mfululizo kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Accra, sehemu ambayo mwili wake ulikuwa ukiagwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Wachezaji ngoma wa jamii ya Ashanti wakati wa ibada iliyofanyika Jumatano Miongoni mwa waombolezaji hao ambaye tayari amewasili mjini humo ni aliyewahi kuwa mke wa Rais wa kwanza wa Afrika kusini Nelson Mandela, Bibi Graca Machel. Marais na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo Ivory Coast, Ethiopia na Zimbabwe watahudhuria shughuli hizo za mazishi, wakiwemo pia marais wa zamani kutoka nchi za Ujerumani, Finland na Uswizi. Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete anamkumbuka vipi marehemu Kofi Annan? Shughuli hizo za kumuaga marehemu zitafuatiwa na mazishi yatakayofanywa kwa ndugu wa karibu na kwa heshima zote za kijeshi. Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan inafanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra. text: Bwana Kichere na watumishi wengine walioteuliwa mwishoni mwa juma lililopita wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa Assad ambaye ameitumikia nafasi hiyo kwa miaka mitano. Kabla ya wadhifa huu mpya, Kichere alikuwa katibu tawala wa Mkoa wa Njombe. Akizungumza baada ya kumuapisha, Raisi Magufuli amesema ofisi ya CAG si safi kama inavyofikiriwa. ''Usije ukaenda huko ukajifanya wewe ni mhimili, mihimili ni mitatu tu, na umeiona hapa, mahakama, kuna bunge na sisi wengine wa serikali na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza nafasi yako ni mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa hiyo mwenye serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri za ukaguzi, unapopewa maagizo na mihimili mingine kama bunge katekeleze, usibishane nao ukipewa maagizo na mhimili kama mahakama katekeleze, wewe ni mtumishi''. Alisema Raisi Magufuli. Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Tanzania Profesa Assad amesema nini? Kuhusu jambo hili amesema ni vyema watu wengine wakilifafanua jambo hili watu wengine kuhusu hatua hiyo kisheria kuliko kulieleza yeye mwenyewe kwa kuwa linamuhusu moja kwa moja. Bwana Assad amesema anatarajia leo kupatiwa barua yake rasmi kwa kuwa uteuzi ulifanyika mwishoni mwa juma na haikua wakati wa kazi, hivyo wataichanganua na Kuhusu namna alivyopokea uamuzi huu ameiambia BBC kuwa alitegemea uwezekano wa kuwepo kwa uamuzi wa Dokta Magufuli. ''Jambo hili si la kisiasa ni jambo la kisheria, lakini nasema riziki anayo mwenyewe Mwenyezi Mungu na kwake haiishi kwa hiyo sikupata wasiwasi, kuna vitu chungumzima vya kufanya Inshallaah Mungu atatufanyia na kila kitu kitakwenda vizuri.'' alisema Profesa Assad. Charles Kichere ni nani? Alisomea elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na chuo kikuu cha Tumaini, mjini Dar Es Salaam. Kichere aliwahi kuwa naibu kamishna mkuu wa TRA. Mnamo tarehe 25 Machi mwaka 2017, aliteuliwa na rais Magufuli kuwa kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). Aliipokea nafasi hiyo kutoka kwa Alphayo Kidata ambaye aliteuliwa wakati huo kuwa katibu mkuu ikulu Tanzania. Charles Kichere alihudumu kama kamishna wa TRA kuanzia Machi 2017 hadi Juni mwaka huu 2019, wakati aliondoshwa katika mamlaka hiyo ya TRA, katika mageuzi ya rais Magufuli aliyotoa ikulu mjini Dar es Salaam kupitia taarifa rasmi ya mkurugenzi wa mawasiliano ya rais. Kichere aliteuliwa badala yake kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Yuko kwenye bodi ya Benki ya CRDB Tanzania. Zamani alikuwa mkaguzi mkuu wa shirika la Kitaifa la barabara, mweka hazina na pia mkaguzi mkuu wa hesabu katika kampuni ya majani chai ya Unilever nchini Kenya na Tanzania. Siku ya Jumamosi taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ikulu ya rais, ilisema kuwa walioteuliwa ni Mathias Kabunduguru ambaye sasa ndiye mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Hussein Katanga aliyeteuliwa kuwa balozi. Wengine walioteuliwa ni Godfrey Mweli kuwa naibu katibu mkuu Tamisemi anayeshughulikia elimu. Kabla ya uteuzi huo Mweli alihudumu kama mkurugenzi wa mipango katika wizara ya katiba na Sheria. Hashim Abdallah Komba naye ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya Uteuzi huo Komba Komba alikuwa akihudumu kama katibu tawala mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ilioachwa na Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Vilevile kiongozi huyo wa taifa amemteua Hassan Abbas Rungwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nachingwea. Anachukua mahala pake bakari Mohammed Bakari ambaye ameondolewa na huenda akapatiwa kazi nyingine. Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtaka CAG mpya Charles Kichere kutojifanya mhimili, badala yake awe mtiifu kwa mihimili anapoagizwa kutekeleza majukumu. text: Asilimia 61 ya wafanyakazi wanaona kuwa msongo umewafanya waugue Anasema kwa hakika kabisa kutokana na utafiti alioufanya kwa miongo kadhaa, nchini Marekani na duniani kwa ujumla Profesa Pfeffer kutoka shule ya biashara ya Chuo cha Stanford na mwandishi na mwandishi msaidizi wa vitabu 15 kuhusu muundo wa kampuni na masuala ya uongozaji rasilimali watu, ametoa hoja katika kitabu chake cha hivi karibuni kiitwacho , ''Kufa kwa ajili ya Mshahara'' Jinsi mifumo ya kazi inavyoathiri na hata kusababisha kukatisha maisha ya watu. Katika kitabu hicho anazungumzia tuko la Kenji Hamada, mwenye miaka 42 aliyekufa kwa mshtuko wa moyo akiwa kwenye dawati lake kazini jijini Tokyo.Nilifanya kazi saa 72 kwa wiki na ilikua inanichukua saa mbili kufika kazini. Kabla ya kifo chake, alifanya kazi siku 40 mfululizo bila kupumzika na mjane wake anasema Kenji alikuwa na msongo mkubwa Huu ni moja kati ya mifano iliyokuwa kwenye chapisho lake, ambapo mwandishi anaeleza madhara ya mfumo wa kazi ambao wakati mwingine ''si ya kibinaadamu'' kutokana na majukumu makubwa ya kazi. Kwa mujibu wa ushahidi uliowekwa na Pfeffer,nchini Marekani, asilimia 61 ya wafanyakazi wanaona kuwa msongo umewafanya waumwe na asilimia 7 wanasema walilazwa kutokana na sababu zinazohusiana na kazi. Makadirio yake ni kwamba msongo una uhusiano na vifo vya wafanyakazi 120,000 wa Marekani. Wafanyakazi hupoteza maisha kutokana na majukumu mengi ya kazi Kwa mtazamo wa kiuchumi, msongo umewagharimu waajiri zaidi ya dola za Marekani 300,000 kwa mwaka nchini Marekani. Katika kitabu chako umeeleza kuwa kuna mfumo wa ufanyaji kazi unaowaua watu.Ni ushahidi gani ulionao kuhusu hili na ni kwa jinsi gani mfumo wa kisasa wa ufanyaji kazi unawaathiri waajiriwa? Kuna ushahidi wa madhara ya kiafya.Saa nyingi za kufanya kazi,kupunguzwa kazi, kukosa bima ya afya, masuala ya kiuchumi, migogoro kwenye familia na maradhi. Kazi sasa imekua si ya kibinaadamu.Kwa upande mwingine, makampuni yameacha kuwajibika kwa ajili ya wafanyakazi wao. Lakini changamoto za kiuchumi zimeongezeka, hofu ya kukosa ajira pia inaongezeka. Katika Benki za uwekezaji, kwa mfano, kuna namna ya ufanyaji kazi, unakwenda nyumbani kwako kuoga na kurejea ofisini. Katika mfumo huo, waajiriwa wengi huingia katika uraibu wa madawa, kwa sababu wanaishia kutumia Cocaine na madawa mengine ili wawe macho. Mfanyakazi wa kiwanda, rubani wa ndege, mwendesha lori, wana idadi ya saa za kufanya kazi. Lakini kuna kazi nyingine hakuna saa maalumu za kazi. Nchini Marekani, sababu ya tano ya vifo ni sehemu ya kazi. Siku ya kimataifa ya kufurahi: Njia 5 za kujipa furaha Uhusiano wa ubongo na maradhi yanayotokana na 'mshtuko' Lakini nani anawajibika kwa vifo hivi? Waajiri na serikali zinawajibika kwa kutochukua hatua yoyote kuhusu suala hili. Ni kazi kubwa tunapaswa kufanya kitu kwa ajili ya kukomesha hili.Lakini hatutaweza kufanya chochote kama mtu mmojammoja. Kama unataka kutatua tatizo yapaswa kuwa katika utaratibu ambao utatoka kwa mtindo wa sheria. Mazingira mabaya ya kazi husababisha maradhi kama vile sukari na shinikizo la damu. Lakini tukizungumzia gharama,makampuni yanaweza kuleta hoja kuwa kufanya mabadiliko katika mfumo wa kazi kutaathiri kipato cha kampuni. Hii si kweli, anasema Profesa Pfeffer.''Tunajua kuwa watu walio katika msongo wa mawazo wako katika nafasi kubwa ya kuacha kazi''.Tunajua kuwa wafanyakazi wasio sawa kisaikolojia hawawezi kuizalishia kampuni inavyopaswa''. Alitolea mfano kuwa inafahamika kuwa Marekani na Uingereza zaidi ya 50% ya siku za kazi hupotea kwa sababu ya wafanyakazi kutokuwepo kutokana na msongo wa kazi. Hivyo kuna athari kubwa kwa mfanyakazi mgonjwa anayekwenda kazini na asifanye kazi kama anavyotakiwa.Hali hii huigharimu kampuni. Wafanyakazi wanapaswa kuzijali afya zao Wafanyakazi wanapaswa kujijali Kwa upande wa wafanyakazi, Profesa ameandika kuwa watu wajijali.Lakini ameulizwa swali kuwa itakuwaje ikiwa muajiriwa akadai kuboreshewa mazingira ya kazi na kuna uwezekano akaishia kufukuzwa? Je mazingira ya kazi yatabadilishwaje? Profesa anasema, kwanza waajiriwa wanapaswa kujali afya zao. Ikiwa unakwenda kazini, mahali ambapo huwezi kuoanisha maisha ya kazi yako na familia, unapaswa kuacha kazi hiyo. Jambo jingine ni kwamba watu wanapaswa kuhakikisha kua sheria zinafuatwa. Jeffrey Pfeffer anaposema kuwa ''kazi zinawaua watu na hakuna anayejali,'' hasemi kwa njia ya mafumbo text: Muhtasari wa ripoti haukuelezea ikiwa Bwana Trump alizuia utekelezwaji wa sheria - lakini pia haikumuhusisha rais na madai hayo. Ripoti hiyo iliwekwa kwa muhtasari kwa ajili ya Congresi na Mwanasheria Mkuu, William Barr. Trump alituma ujumbe wa twitter kujibu muhtasari wa ripoti yake akisema: " hakuna ushirikiano, hakuna kuzuia sheria." Rais Trump, ambaye mara kwa mara aliuelezea uchunguzi kama ''uwindaji wa kichawi'', alisema Jumapili kwamba "ni aibu kwamba nchi ililazimika kupitia hili", akiuelezea uchunguzi dhidi yake kuwa "kuangushwa kwa jambo lililo kinyume cha sheria ". Ripoti hiyo inakamilisha uchunguzi wa miaka miwili wa Bwana Mueller, ambapo wakati wa uchunguzi huu washirika wa karibu wa rais walishitakiwa, na wakati mwingine hata kufungwa. "Japo ripoti hii haionyeshi kuwa rais alifanya uhalifu, haimuweki huru ,"Bwana Mueller aliandika katika ripoti yake. Kile kilichomo kwatika muhtasari wa ripoti Barua ya muhtasari wa ripoti hiyo ya Bwana Barr inaainisha matokeo ya uchunguzi unaohusiana na juhudi za Urusi za kushawishi matokeo ya uchaguzi wa 2016. Bwana Barr alihitimisha ripoti yake kwa kusema: "Mchunguzi maalum hakumpata Trump, mtu yeyote wa Marekani au afisa wa kampeni ya Trump na hatia ya kushirikiana au kwa kufahamu kuratibu ushirikiano wowote na Urusi ." Sehemu ya pili ya barua hiyo ilizungumzia suala la kuzuwia utendaji wa sheria . Muhtasari wa Bwana Barr unasema ripoti wa mchunguzi mkuu "Hatimae haimuweki katika nafasi ya kushtakiwa ". Uchunguzi wa Robert Mueller umechukua takribani miaka miwili "Kwa hiyo baraza la uchunguzi halikutoa hitimisho - kwa njia moja au nyingine- juu ya ikiwa mienendo iliyochunguzwa ilikuwa ni ya kuzuwia utendaji wa kisheria ,"ilielezea barua hiyo. Bwana Barr anasema kuwa ushahidi haukutosha "kubaini kwamba rais alitenda kosa la kuzuwia utendaji wa washeria ". Bwana Barr alikamilisha barua yake kwa Congresi kwa kusema kuwa atafichua mengi zaidi katika ripoti kamili , lakini akasema baadhi ya yanazuwiwa kutangazwa. "Kutokana na masharti hayo , mpango wa mchakato wa ripoti hiyo utategemea kwa upande mmoja juu ya namna wizara ya mambo ya nje itakavyoweza haraka kubaini yaliyopendekezwa na jopo kuu la mahakama ambayo kw amujibu wa sheria hayapaswi kutangazwa kwa umma ," aliandika. " Nimeomba msaada wa mchunguzi mkuu katika kutambua taarifa zote zilizomo kwenye ripoti haraka iwezekanavyo ." Walichosema wanasiasa wa marekani kuhusu Muhutasari wa ripoti Mjumbe wa Congresi Jerry Nadler, ambaye ni mwenyekiti wa tume ya sheria wa Democratic katika bunge la wawailishi, alisisitiza kuwa mwanasheria mkuu hakusema moja kw amoja kwamba Trump alizuwia utendaji wa sheria . "Barr anasema kwamba rais huenda alizuwia uutekelezwaji wa sheria, lakini kupatikana na hatia hiyo , 'serikali itahitaji kutoa ushahidi wa kutosha kwamba mtu alifanya hivyo kwa kukusudia, au kuhusika katika mwenendo wa kuzuwia utekelezwaji wa sheria'." Seneta wa Democratic Richard Blumenthal, ambaye ni mjumbe wa kamati ya Seneti ya sheria, alisema kwamba japo ushahidi ulikosa wa "kushtakiwa kwa uhalifu wa kushirikiana ", bado maswali yanabakia juu ya ikiwa Bwana Trump alihusika. Katika taarifa ya pamoja , Spika wa bunge kutoka chama cha Democratic Nancy Pelosi na kiongozi wa wabunge wa Democratic katika seneti Chuck Schumer walisema barua ya Bwana Barr '' inaibua maswali mengi kama inavyoyajibu'' na wakatoa wito wa ripoti kamili kutolewa. "kwa rais kusema yuko huru kabisa inakwenda kinyume kabisa na maneno ya Bwana Mueller na maneno yake hayapaswa kuchukuliwa kuwa ni ya kuaminika ," ilisema taarifa yao. Afisa habari wa ikulu ya White House Sarah Sanders alielezea matokeo ya uchunguzi huo kuwa "ya kumuweka huru kwa jumla rais". Wakili wa Trump, Rudy Giuliani, alisema ripoti "ilikuwa bora kuliko nilivyotarajia ". Nae Seneta wa Republican Mitt Romney aliafiki "habari njema ", akituma ujumbe wake wa twitter kwamba ''Ni wakati wa taifa kusonga mbele ". Kampeni iliyoendeswa na raiswa Marekani Donald Trump 'haikushirikiana na Urusi wakati wa uchaguzi wa 2016, kwa mujibu wa muhtasari wa ripoti ya ya mwanasheria mahususi Robert Mueller iliyowasilishwa kwenye bunge la Congress Jumapili. text: Muhubiri mmoja nchini Rwanda amesema kuwa wanawake ''ni chanzo cha uovu'' wote duniani Muhubiri hiyo wa kanisa la Seventh Day Adventist Nicolas Niyibikora aliwambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu wakati wa matangazo ya idhaa ya redio ya Amazing Grace mwezi Januari akionya kuwa ''hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa wanawake''. ''Unaposoma Biblia , ni nani aliyeleta dhambi duniani''? Aliuliza akiongeze, ''sio mwanamume''. Tayari mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneneo kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa , kulingana na gazeti la Rwanda la New Times. Kundi la kutetea haki za wanawake liliwasilisha malalamishi yake katika tume ya udhibiti wa vyombo vya habari ambayo inatarajiwa kukutana ili kuzungunmzia kuhusu swala hilo wiki ijayo. Afsa mkuu Emmanuel Mugisha aliambia gazeti la New Times kwamba kuna uwezekano idhaa hiyo italazimika kujieleza. Kanisa la Seventh Day nchini Rwanda limefanya juhudi za kujitenga na Niyibikora, ambaye wanasema aliipgwa marufuku kwa miaka ,mitano. Muhubiri mmoja wa Rwanda huenda akajapata mashakani mbele ya vyombo vya habari baada ya kuwaita wanawake ''chanzo cha uovu'' katika mahubiri ya redio. text: Jaribio lililotekelezwa Ijumaa linaaminika kuwa kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na Korea Kaskazini Jaribio hilo la Ijumaa lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini. Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio Punggye-ri ambalo linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote. Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya jaribio hilo la Ijumaa na hali ya wasiwasi na uhasama imeongezeka. Jumapili, mmoja wa maafisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na shirika la habari la taifa hilo Yonhap akisema kwamba nchi hiyo ina mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza shambulio la kinyuklia. Bado kuna shaka kuhusu uwezo wa Korea Kusini kuweka mabomu ya nyuklia kwenye makombora ya masafa marefu, kuiwezesha kutekeleza shambulio, lakini wataalamu wanasema hatua zilizopigwa na taifa hilo zinazua wasiwasi. Jumatatu, shirika la Yonhap lilimnukuu afisa mmoja wa serikali akisema dalili zinaonesha Korea Kaskazini imekamilisha maandalizi ya kutekeleza shambulio jingine milimani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Korea Kaskazini hutekelezea mashambulio yake Punggye-ri Maafisa wa korea kusini wametahadharisha kwamba huenda Korea Kaskazini ikafanya jaribio jingine la bomu la nyuklia wakati wowote, baada ya kutekeleza jaribio jingine la bomu la nyuklia Ijumaa. text: Bw Juan Manuel Santos Rais Santos aligonga vichwa vya habari baada ya kufanikiwa kupata makubaliano ya amani na waasi hao jambo ambalo lilifikisha kikomo vita vilivyodumu kwa karibu miaka hamsini. Mkataba huo ulitiwa saini na Bw Santos na kiongozi wa waasi hao kamanda Rodrigo Londono, anayejulikana vyema kwa jina Timochenko mjini Cartagena tarehe 27 Septemba. "Colombia inasherehekea, ulimwengu unasherehekea kwa sasa kuna vita vimemalizika duniani," alisema wakati huo. "Tutatimiza malengo yote, tutazidi nguvu changamoto zote na kugeuza nchi hii kuwa taifa ambalo tumekuwa tukitaka liwe, taifa la amani." Watu 260,000 waliuawa kwenye vita hivyo na wengine milioni sita kuachwa bila makao. Mapatano hayo na kundi la waasi la Farc yalikataliwa na raia katika kura ya maoni iliyoandaliwa Oktoba 2. Rais wa Colombia Santos, kushoto na kiongozi wa waasi ajulikanaye kama Timochenko wamepeana mikono baada ya kutia saini mkataba huo. Wakosoaji wanasema kuwa mkataba huo wa amani unawapa waasi wa Farc fursa ya kukwepa haki kwa makosa waliyofanya. Lakini rais Santos kwa upande wake anasema kuwa hayo ndiyo mapatano bora zaidi yanayoweza kufanywa kwa niaba ya Colombia. Baadhi ya wanachama wa FARC, pamoja na maafisa wa kijeshi na polisi walipangiwa kufikishwa mbele ya mahakama maalumu kujibu mashtaka kwa makosa ambayo wametekeleza katika vita nchini humo chini ya mkataba huo. Kundi la Farc, ambalo lilianza kama wanamgambo wa Chama cha Kikomunisti mwaka 1964, linatarajiwa kuacha vita na kuingia katika siasa za amani. Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2016 licha ya kuvunjika kwa mkataba wake wa kusitisha vita na waasi wa Farc nchini humo. text: Alexei Navalny (kushoto) aliitisha maandamano kupinga ufisadi ndani ya serikali Bwana Navalny alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliokamatwa kwa kuhusika kwenye mikutano kadha kote nchini. Mahakama mjini Moscow mapema ilimpiga faini ya karibu dola 350 kwa kupanga maandamano yaliyoharamishwa. Leo Jumatatu, serikali ya Urusi iliulaumu upinzani kwa kuchochea kuvunjwa kwa sheria na uchokozi. "Baadhi ya vijana walilipwa kushiriki maandamano," msemaji wa polisi alisema. Baadhi ya waandamanaji walibeba bata au mabango ya bata Bwana Navalny baadaye alimshutumu tena Dmistry Medvedev kwa kuhusika kwenye ufisadi. Bwana Navalny alifikishwa mahakamani ya kukamatwa siku ya Jumapili na kushinda korokoroni. Licha ya kukwepa kifungo kwenye mashtaka ya kwanza, alihukumi kifungo cha siku 15 jela kwa kumpuuza afisa wa polisi. Wakili wa bwana Navalny Olga Mikhailova, aliliambia shirika la Reuters kuwa, aliitarajia hukumu kama hiyo na kuwa atakata rufaa. Kabla ya hukumu kutolewa leo Jumatu, bwana Navalny mwenye umri wa miaka 40, aliandika kwenye mtandao wa akiwa mahakamani akisema , "Hello kila mmoja, ni kutoka mahakama ya Trerskoy. Wakati utawadia tutawaweka hukumuni." Alidai kuwa bwana Medvede ndiye anastahili kushtakiwa kama mwandalizi mkuu wa maandamano, kwa sababu ya vitendo vyake vya ufisadi vilivyochangia watu kuingia mitaani katika miji 99 nchini Urusi. Alexei Navalny alikamatwa Jumapili Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, amehukumiwa kifungo cha siku 15 jela kwa kukiuka amri za polisi wakati wa maandamano makubwaa siku ya Jumapili. text: United walitozwa faini ya euro 15,000 (£13,203) kutokana na kuchelewa kuanza kwa mechi yao na Valencia uwanjani Old Trafford mwezi Oktoba. Kadhalika, walifika kuchelewa kwa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Juventus, ambapo Mournho alilazimika kutembea. "Taarifa tulizo nazo ni kwamba mambo ni mabaya kuliko wakati huo mwingine," amesema Mourinho. "Tunakaa katika hoteli iliyo mita kadha tu kutoka uwanjani. Mambo [ya foleni] yasipoimarika, basi nitatembea [kwenda Old Trafford]." Man Utd wanakabiliwa na shinikizo? Kando na matatizo ya jinsi ya kufika uwanjani kwa mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, United wamekuwa wakiandikisha matokeo mseto wakiwa uwanja wao wa Old Trafford. Wameshindwa mechi tatu katika mashindano yote msimu huu. Jose Mourinho Mourinho amepuuzilia mbali madai kwamba huenda wachezaji wanashindwa kuhimili shinikizo za kuchezea nyumbani. "Kama waihisi presha, basi salia nyumbani utazame mechi kwenye TV," aliongeza. "Iwapo unahisi presha ya kuchezea nyumbani ambapo watu hujitokeza kukuunga mkono, aisee. Huwa sihisi presha nikiwa nyumbani. Ukaniuliza mimi kama ningelipenda kurudi Bern (Uswizi) au kuchezea nyumbani, daima nitasema kwamba ningependa nyumbani zaidi. "Ninachokitaka ni timu kuanza vyema mechi, sio kusubiri tu na baadaye kuanza kucheza baada ya kufungwa. "Pengine mnafikiria kwamba Jose aliwaambia waanze kwa mwendo pole, wacheze bila kujisumbua sana na kutazama jinsi mechi itakavyoendelea. Ni kinyume kabisa. Ninawataka waanze kwa ukali na kushambulia tokea mwanzo." Majeraha ya Lindelof Mourinho amethibitisha kwamba mchezaji wa kimataifa wa Sweden Victor Lindelof anatarajiwa kutocheza kwa muda baada ya kuumia akicheza dhidi ya Crystal Palace Jumamosi, mechi ambayo ilimalizika kwa sare tasa. Victor Lindelof ameanza mechi katika mechi saba za karibuni zaidi Manchester United. Eric Bailly na Luke Shaw wako sawa kucheza hata hivyo. Beki wa Ivory Coast Bailly hajacheza tangu alipoondolewa uwanjani dakika ya 19 katika mechi ambayo mashetani hao wekundu waliwalaza Newcastle 3-2 mnamo 6 Oktoba. Eric Bailly Shaw amekuwa akitumikia marufuku kutokana na kulimbikiza kadi tano za manjano katika ligi za nyumbani. Beki huyo wa England amekuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi katika mechi zote walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu. United wakifanikiwa kuandikisha ushindi leo, basi watafuzu kwa hatua ya muondoano iwapo Valencia hawatafanikiwa kuwashinda Juventus mjini Turin. Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema atatembea kutoka hotelini kwenda uwanjani kwa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Young Boys iwapo tatizo la foleni litajirudia. text: Eneo ambalo kaburi la mwana wa Pharao lilipatikana Wizara ya mambo ya kale imesema kuwa kaburi hilo lililopo katika eneo la kifalme la Dahshur Kusini mwa Cairo lilikuwa na sanduku la mbao lililochongwa. Ndani ya sanduku hilo kulikuwa na mitungi iliojaa nguo za mapambo vikiwemo viungo vya marehemu ambaye ni mwana wa kike wa mfalme Emnikamaw. Piramidi hiyo ya mfalme ina urefu wa mita 600 kutoka kwa kaburi hilo. Mwezi uliopita watalam wa vitu vya kale wanaochunguza mabaki ya jengo hilo walipata afueni kwa kupata picha za mabaki hayo zilizokuwa na jina la Emnikamaw. Pia waligundua mabaki ya makaburi ya mawe. Sanduku la vitu vya kulinda Viungo vya mwana wa Pharaoh Dahshur ni eneo ambalo mfalme Sneferu wa awamu ya nne alijenga piramidi ya kwanza yenye urefu wa futi 341 iliokuwa na upande mmoja ambao ulikuwa umelainishwa takriban miaka 4000 iliopita. Pia alijenga piramidi ya awali iliokuwa na urefu wa mita 105 ambayo mteremko wake ulikuwa na ngazi zilizobadilishwa kutoka pembe yenye digree 54 hadi 43. Mfalme Sneferu alirithiwa na mwanawe Khufu anayejulikana sana kwa kujenga Piramidi kubwa katika eneo la Giza ambayo ilikuwa na urefu wa mita 138 ambayo ilikuwa maajabu ya dunia wakati huo. Kaburi la miaka 3,700 la mwana wa kike wa Pharaoh linaamika kupatikana karibu na mabaki ya piramidi iliogunduliwa Misri. text: Milima ya Golan ina umuhimu wa kisiasa Katika chapisho la Twitter , bwana Trump alitangaza kwamba milima hiyo ni muhimu sana katika usalama wa Israel na uthabiti wa eneo la mashariki ya kati. Israel iliunganisha milima hiyo na taifa lake hatua ambayo haikuungwa mkono na jamii ya kimataifa. Syria ambayo imekuwa katika harakati za kuikomboa milima hiyo haijatoa tamko lolote. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye ameonya kuhusu Iran kuingilia vita vya Syria alituma ujumbe wa shukran kwa bawana Trump kupitia mtandao wa twitter. ''Katika wakati ambapo Iran inataka kuitumia Syria kama eneo la kuikabili Israel, Bwana Trump aliitambua Israel kama mmiliki rasmi wa milima ya Golan. Richard Haass, afisa mwanadamizi katika wizara ya kigeni nchini Marekani ambaye ndiye rais wa baraza la uhusiano wa kigeni alisema kuwa hakubaliani na bwana Trump. Alisema kuwa hatua ya kuitambua Israel kuwa mmiliki wa milima hiyo ni ukiukaji mkubwa wa azimio la Umoja wa Mataifa , ambalo linapinga unyakuzi wa eneo moja kupitia vita. Uamuzi huo wa rais unajiri wakati ambapo Netanyahu anakabiliwa na ushindani mkali katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu tarehe tisa mwezi Aprili mbali na msururu wa madai ya ufisadi. Mwaka 2017, bwana Trump aliitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kuagiza kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani katika mji wa Tel Aviv. Uamuzi huo ulishutumiwa na Palestina ambayo inataka mashariki mwa Jerusalem kuwa mji mkuu wa taifa la Palestina na Umoja wa mataifa unataka kufutiliwa mbali. Cha kushangaza kuhusu Trump Je ujumbe wa twitter wa rais Trump uliwashangaza hata wandani wake wa karibu? Vyombo vya habari vilivyokuwa vikisafiri na waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo vilikuwa vikisubiri nje kwa waziri mkuu Netanyahu kusikia kutoka kwa viongozi wote wawili, wakati bwana Trump alipofanya uamuzi huo. Wawili hao walichelewa sana mpaka wanahabari wakahisi kana kwamba walikuwa wakishindwa kutoa tamko la pamoja. Lakini iwapo tangazo hilo liliwashangaza wengi , lilimshangaza zaidi bwana Netanyahu -Nimefurahi zaidi , ni maneno yake ya kwanza alipotoka. Israel imepata uungwaji mkono katika ikulu ya Whitehouse na baadhi ya wanachama wa bunge la Congress kwa kuhoji kwamba Iran inaitumia Syria kama kambi ya kushambulia Israel huku milima hiyo ya Golan ikiwa eneo la mbele la Vita. Lakini utambuzi huo haubadilishi chochote katika eneo hilo, Israel tayari ilikuwa imejihami vilivyo katika milima hiyo ikiwa na ushawishi mkubwa. Hivyobasi wakosoaji wamesema kuwa hilo ni jaribio la wazi kumpiga jeki Netanyahu katika uchaguzi ulio na ushindani mkali. Iwapo hilo ndio lengo basi ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa wanasema. Bwana Trump ameunga mkono unyakuzi wa eneo fulani hivyobasi hana maadili kuilaumu Urusi kwa kutekeleza kitendo kama hicho katika eneo la Crimea nchini Ukraine. Je milima ya Golan ina muhimu gani? Eneo hilo liko yapata kilomita 60 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Syria na lina ukubwa wa kilomita 1,200 mraba. Israel ililiteka eneo hilo kutoka kwa Syria mwisho mwisho wa vita vya mashariki ya kati , na kuzuia jaribio la Syria kulikomboa eneo hilo wakati wa vita vya 1973. Mataifa hayo mawili yalikubaliana kuweka eneo lisilo na wanajeshi kati yao litakalopigwa doria na wanajeshi wa Umoja wa mataifa .Lakini bado mataifa hayo mawili yanasalia kuwa katika hali ya kivita. Syria haitakubali makubaliano ya amani na Israel hadi itakapoondoka katika milima hiyo Mwaka 1981, bunge la Israel lilipitisha sheria ya usimamizi na umiliki wa milima hiyo ya Golan hatua ilioonyesha kulichukuwa na kuliunganisha eneo hilo na taifa lake. Lakini jamii ya kimataifa haijatambua hatua hiyo na kusisitiza kuwa milima hiyo ya Golan inamilikiwa na Syria. Azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilitangaza hatua hiyo kuwa haramu. Miaka mitatu iliopita wakati aliyekuwa rais Barrack Obama alipokuwa afisini , Marekani ilipiga kura ya kuunga mkono azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likionyesha wasiwasi kuwa bwana Netanyahu hatorejesha milima hiyo kwa Syria. Syria imekuwa ikisistiza kwamba haitakubali kuweka amani na Israel hadi pale itakapoondoka katika milima hiyo. Mazungumzo ya mwisho ya amani yalioongozwa na Marekani mwaka 2000 yalivunjika huku Uturuki ikiingilia kati na kuanzisha mzungumzo hayo 2008 ambayo pia hayakufua dafu. Kuna zaidi ya makaazi 30 ya Israel katika milima hiyo ya Golan ambayo ni nyumbani kwa raia 20,000. Makaazi hayo yanatumbulika kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa , ijapokuwa Israel inapinga hilo. Wakaazi hao wanaishi pamoja na raia 20,000 wa Syria wengi wao wakiwa Waarabu wa kabila la Druze ambao hawakutoroka wakati milima hiyo ilipotekwa. Rais Donald Trump amebadilisha sera ya miongo kadhaa ya Marekani kwa kusema kuwa ni wakati kuitambua Israel kama mmiliki halisi wa milima ya Golan ambayo iliiteka kutoka kwa Syria 1967. text: Baadhi ya watumiaji wa Twitter waliwaambia wenye ndevu hao kuwacha kuangalia juu kwa sababu picha hizo zilikuwa zinatisha. Picha hizo zilianza kusambazwa baada ya mtumiaji mmoja wa twitter kutuma ujumbe akisema wanaume wenye ndevu wanapoangalia juu tazama. Mwandishi huyu naye pia hakusita kupiga picha hiyo na kuweka mtandaoni Watu walijiunga na wengine kuchora nyuso za watu ili kuongezea. Dan alituma picha zake za ndevu alizopiga picha. Ilijibiwa mara kumi ya maelfu. Kieron alikuwa wa kwanza kujiunga. Nikiwa ripota wa kipindi cha Newsbeat mwenye ndevu nyingi pia nilijipata nimepiga picha Huku picha hizo zikisambazwa haraka na kwa wetu wengi kwa mufda mfupi kama ilivyo ada katika mtandao wa twitter, watu walianza kumwambia mtu wa kwanza kupiga picha hiyo kuongeza mapambo katika picha hiyo Scott alituma ujumbe wa twitter akimtaka Dan kuchora uso katika shingo zao na wengine wakakubliano kwamba huo ndio mwelekeo. Baadhi ya watu waliongezea macho na emoji na mtu mmoja akachora uso wake na kalamu. Na wengine waliigiza na kuweka picha hizi Sio kila mtu alifurahia picha hizo zilizosambazwa , kuna wengine wanahoji ni nini haswa kinachowavutia katika picha hizo. Watu wenye ndevu wamekuwa wakijipiga aina ya selfie kutoka chini na wamekuwa wakiwaogopesha watumiaji wa mitandao ya kijamii. text: Wasichana wengi wamekuwa hawaridhishwe na muonekano wa uke wao Huduma hiyo inapatikana kwenye mtandao wa masuala ya afya ya uzazi na ngono wa Brook, ambao unatoa mifano kwa kutumia video na kutoa ushauri kuhusu jinsi sehemu za siri za mwanamke hubadilika wakati anapobalehe au kuvunja ungo. Lengo kuu ni kuwahamasisha wasichana kujikubali walivyo. Watafiti wa afya waliotengeneza mtandao huo wamesema wana matumaini kwamba wasichana wataanza kujiamini zaidi na kuwafanya kutotaka ''upasuaji wa urembo'' wa sehemu zao siri. Upasuaji wa aina hiyo haustahili kufanyiwa kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18. Upasuaji huo wa urembo wa sehemu nyeti maarufu kama- labiaplasty - unaofanywa kuongeza au kupunguza sehemu hizo hutekelezwa na madaktari binafsi ambao hutoza maelfu ya mapauni. Kwa mara nyingi, operesheni hiyo huweza kufanywa na mamlaka ya huduma ya afya -NHS iwapo sehemu nyeti za msichana zina kasoro, iwapo inamsumbua au inamwathiri kiafya. Madaktari wa afya hawastahili kutoa uamuzi kwamba wasichana wafanyiwe upasuaji kwa sababu ya urembo pekee. Kulingana na takwimu za NHS, 2015-16 zaidi ya wasichana 200 chini ya miaka 18 walifanyiwa upasuaji wa sehemu zao za siri na zaidi ya 150 ya wasichana hao walikuwa chini ya miaka 15. Picha ya sehemu za siri Bi Louise Williams, ambaye ni muuguzi katika chuo kikuu cha University College Hospital na kiongozi wa mradi huu, amesema: "Elimu hii itawasaidia wasichana kuelewa sehemu zao za siri na jinsi inavyokomaa wakati wanapovunja ungo, haswa wakiwa na wasiwasi jinsi wanavyojitizama au kijihisi. "Tuna matumaini kwamba tutawahakikishia wasichana kwamba sehemu zao za siri ziko na maumbo tofauti na ukubwa fulani na iwapo wanahitaji usaidizi na mawaidha , wanaweza kujua pale watakapopata ujumbe huu.'' Dkt Naomi Crouch kutoka chuo cha taasisi cha Royal College cha Madaktari wa uzazi na wataalamu wa afya ya uzazi na shirika la Uingereza la watoto pia walihusika kwenye utafiti huo. Alisema: "Hakuna utafiti wowote wa kisayansi ambao unaounga mkono upasuaji wa sehemu za siri na iwapo una athari zozote za kimwili au kisaikolojia hasa kwa vijana ambao bado wanakuwa. "Tunatumai kwamba ujumbe huu utawapatia wasichana ufahamu zaidi kwa kwamba sehemu zao za siri ni maalumu na hubadilika wanapokua maishani na ni kawaida." Upasuaji kwenye uke unaweza kusababisha madhara Upasuaji huo unaweza kusababisha: Kunaweza kuwa na matatizo mengine madogo: Wasichana nchini Uingereza wanahimizwa kutumia huduma ya mtandaoni ili kuwasaidia kuangalia iwapo maumbile ya uke wao ni ya kawaida. text: Mahakama imeelekeza kwamba Wema Sepetu azuiwe kwa siku 7 wakati ikisubiriwa kutoa hukumu katika kesi ambapo alishtakiwa kwa kusambaa kwa kanda ya video ya mahaba kati yake na mwanamume mmoja katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania. Wiki iliyopita mahakama ilitoa agizo la kukamatwa kwa nyota huyo aliyekuwa malkia wa urembo nchini. Waranti ya kukamatwa kwake ilitolewa baada ya mshtakiwa pamoja na mdhamini wake kutofika mahakamani walipohitajika wakati wa kusililizwa ushahidi wa kesi hiyo. Wakili wa Wema, Ruben Simwanza alieleza kuwa mteja wake alikuwemo mahakamani, lakini aliugua na akalazimika kuondoka - ufafanuzi ambao haukuiridhisha mahakama. "Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa ninikutoa taarifa mahakamani", alisema hakimu. Wema amewahi kushtakiwa katika kesi nyingine kwenye mahakama hiyo ya Kisutu mnamo 2017 kwa mashtaka ya umiliki wa mihadarati. Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari 2017, Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika eneo la Kunduchi Ununio. Mahakama ilimpata na hatia Juali 2018 na kumpiga faini ya shilingi milioni mbili za Kitanzania. Maafisa wa polisi nchini Tanzania walianzisha msako dhidi ya watu maarufu baada ya baadhi yao kuhusishwa na ulanguzi wa mihadarati. Mahakama ya kisutu imeagiza msanii maarufu nchini Tanzania Wema Sepetu azuiwe mahabusu hadi Juni 24 baada ya kukiuka masharti ya dhamana katika kesi inayomkabili. text: Katibu mkuu wa chama cha LDP Toshihiro Nikai, mnamo mwezi Septemba, alizungumza na wanahabari Chama cha Liberal Democratic (LDP) kilipendekeza wabunge wanawake washuhudie bodi ambayo ina wanaume tu namna wanavyoendesha mkutano wao. Hawaruhusiwi kuzungumza wakati wa mkutano - lakini wanaweza kutoa maoni yao baadaye. Wanawake nchini Japani kwa kipindi kirefu wamekuwa wakijitenga na ushiriki wa kisiasa na kiuchumi. Nchi hiyo imeorodheshwa kuwa ya 121 kati ya nchi 153 kulingana na kipimo cha Jukwaa la Kiuchumi Duniani mwaka 2020 cha tofauti la kijinsia Duniani. Wanawake wawili sasa hivi ndio wanaoshiriki katika bodi ya watu 12 ya chama cha LDP ambacho kimekuwa madarakani karibu kila wakati tangu mwaka 1955. Toshihiro Nikai, 82, katibu mkuu wa chama cha LDP, amezungumza na wanahabari Jumanne kwamba anataka kukaribisha wanawake katika mkutano huo. Alisema anafahamu ukosoaji unaoendelea dhidi ya wanaume kutawala bodi ya chama hicho na ilikuwa muhimu kwa wanachama wa kike wa chama hicho kufuatilia mchakato wa maamuzi unavyoendeshwa, alinukuliwa na shirika la habari la Reuters "Ni muhimu kuelewa majadiliano yanavyoendelea. Kutazama na kufuatilia," alisema. Chombo cha habari nchini Japani kimesema wanawake watano huenda wakaruhusiwa kuketi na kufuatilia mkutano wa bodi inayofanya maamuzi lakini hawataruhusiwa kuzungumza. Wanaweza kuwasilisha maoni yao baadaye kwa Sekretarieti. Sasa hivi wanasiasa 46 kati ya 465 nchini Japani ndio waakilishi wa wanawake - hiyo ikiwa ni takriban asilimia 10 ikilinganishwa na asilimia 25 kote duniani. Ubaguzi wa kijinsia Japani Maoni ya Mariko Oi, BBC News Kama mwanamke wa Kijapani, ubaguzi wa kijinsia kwa bahati mbaya ni jambo ambalo limezoeleka kwa miaka mingi. Inawezakana ukatokea katika mikutano ya kibiashara, wakati wafanyakazi wanakunywa vivywaji vyao baada ya kazi au mikutanoni. Nyakati kama hizo, wengi wetu hucheka tu na kujifanya hatukusikii kilichotokea na kusonga mbele. Hiyo ndio sababu matamshi ya Bwana Mori hayakunishangaza, na uamuzi wa chama tawala wa kuruhusu wanawake kwenda katika mkutano wao mradi tu wasizungumze ni mbinu ambayo tunaifahamu. Chini ya utawala uliopita wa Shinzo Abe, serikali iliweka lengo lake la kuongeza idadi ya viongozi wanawake kufikia mwaka 2020. Na baada ya kushindwa kufikia lengo hilo, taratibu ikasongeza lengo hilo kwa mwongo mmoja. Kwa kipindi kirefu wakosoaji wamekuwa wakisema badala ya kuongeza idadi ya wanawake basi tu, kile Japani inachohitaji ni mabadiliko kuanzia elimu hadi utamaduni wa kuajiri. Kipi kilichotokea katika mzozo wa Olimpiki? Yoshiro Mori, 83, alisema katika majadiliano juu ya kuongeza idadi ya wanawake katika bodi, kwamba "lazima tuhakikishe muda wao wa kuzungumza unadhibitiwa - wanakuwa na wakati mgumu kumaliza mazungumzo." Baada ya matamshi hayo kusababisha hasira miongoni mwa wananchi, alijiuzulu kwa kile kilichodaiwa ni "matamshi yasiofaa". Wafadhili wakubwa wa mashindano ya Olimpiki ya Tokyo walikosoa matamshi hayo ikiwemo kampuni ya Toyota. Kundi la wabunge wanawake walivaa nguo za rangi nyeupe na kufanya maandamano dhidi ya matamshi hayo na gavana wa Tokyo Yuriko Koike akasema hatahudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa maafisa wa Olimpiki. Baadhi ya watu 400 inasemekana walifuta mambi yao ya kujitolea katika michezo ya Olimpiki, ambayo imepangwa kufanyika baadaye mwaka huu. Siku kadhaa baada ya mkuu wa michezo ya Olimpiki nchini Japani kulazimishwa kujiuzulu kwasababu ya maneno yake ya kudhalilisha wanawake, chama chake kimeamua kualika wanawake kuhudhuria mikutano muhimu - mradi tu wasiseme neno. text: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano ya msaada wa vyakula hivyo kutoka nchini Burundi yamefanyika mpakani mwa Tanzania na Burundi katika eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga wilayani Ngara ambapo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakati Burundi iliwakilishwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye. Akikabidhi vyakula hivyo, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa Serikali ya Burundi na Warundi wote walipatwa na mshtuko mkubwa na majonzi baada kusikia taarifa ya maafa yaliyowatokea ndugu zao wa mkoani Kagera."Kwa Kirundi tunasema, "Umubanyi niwe muryango" ikimaanisha jirani yako ni ndugu yako, kwa maana hiyo imekuwa ni wajibu kwa Serikali ya Burundi kuagiza wawakilishi wake ili waweze kufika hapa nchini Tanzania mkoani Kagera kuwaona ndugu zetu Watanzania na kuwapa pole". Waziri Bi. Leontine aliendelea kusema "Ndio maana tumekuja na kifurushi kidogo tu ili tuweze kuwaliwaza ndugu zetu waliofikwa na matatizo hayo" alisema Waziri Bi. LeontineWaziri Bi. Leontine alivitaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na mchele tani 100, mahindi tani 50, sukari tani 30 na majani ya chai tani 3. Akizungumzia suala la mahusiano ya Tanzania na Burundi, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa udugu uliojengeka baina ya nchi hizo mbili na wananchi wake ni wa kihistoria, si wa leo au wa jana na kusema Serikali yake inadhamira ya kuendeleza udugu huo vizazi na vizazi huku akiamini Tanzania nayo ina dhamira hiyo hiyo. Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba ameishukuru Serikali ya Burundi kwa msaada waliotoa kwa Tanzania na kuongeza kuwa msaada waliotoa ni kielelezo cha mahusiano ya karibu na ya kidugu baina ya nchi hizo mbili na watu wake. Pia Naibu Waziri Dkt. Suzan amewataka viongozi wa Serikali ya Burundi wafikishe salamu na shukrani za dhati za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza na kuwathibitishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambao ndio umeathirika na tetemeko hilo Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye pia ni Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa mkoa huo ameihakikishia Serikali ya Burundi kuwa msaada walioutoa utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.Msaada huo uliotolewa na Burundi umekuwa ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na nchi za Afrika Mashariki kwa Tanzania kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu na kuathiri mikoa ya kanda ya ziwa. Burundi imeungana na nchi za Uganda na Kenya kwa kutoa misaada kwa waathirika wa tetemeko hilo ambapo September 17 mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki 2 ambazo ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania milioni 437 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera. Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa tani 183 za vyakula mbalimbali kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya kuwafuta machozi waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoni Kagera mapema mwezi huu na kuathiri maisha ya wakazi wa mkoa huo. text: Martin Olsson akipigania mpira na Marco Marin wa Ujerumani wakati wa mechi ya kimataifa ya kirafiki ya Uefa U21 uwnajani Malmoe, Ujerumani 2007 Lakini katika kikosi kinachowakilisha taifa hilo la Ulaya, kuna mchezaji aliye na uhusiano wa karibu sana na Kenya, kimsingi ni raia wa Kenya ikizingatiwa kwamba uraia pacha unaruhusiwa Kenya chini ya katiba ya sasa. Mchezaji huyo si mwingine ila ni Martin Tony Waikwa Olsson mwenye miaka 30 anayechezea klabu ya Swansea City ya Uingereza. Aliwahi kuchezea pia klabu za Blackburn Rovers na Norwich City. Olsson amewakilisha timu za taifa za vijana za Sweden na amekuwa katika timu kuu ya taifa tangu mwaka 2010. Amekuwa kwenye benchi katika kikosi cha Sweden kufikia sasa. Sweden wanacheza dhidi ya Mexico Jumatano jioni. Waliwashinda Korea Kusini 1-0 mechi yao ya kwanza 18 Juni lakini wakashindwa na Ujerumani 2-1 dakika za mwisho kupitia bao la Toni Kroos. Mchezaji huyu alizaliwa 17 Mei 1988 mjini Gavle, Sweden. Babake ni raia wa Sweden lakini mamake Maggie Olsson alikuwa Mkenya ingawa kwa sasa ni marehemu. Alitokea Nanyuki, karibu na Mlima Kenya. Familia yao ni ya wachezaji kwani ndugu yake ambaye ni pacha Marcus Jonas Munuhe Olsson ni mchezaji kandanda na sawa na Martin yeye pia ni mkabaji wa upande wa kushoto uwanjani ambaye pia hucheza safu ya kati. Dada yao Jessica Olsson, ambaye ni mkubwa wao, ameolewa na mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Ujerumani Dirk Nowitzki ambaye huichezea Dallas Mavericks katika NBA. Wawili hao wana watoto watatu, na wa kwanza na msichana pekee alipewa jina Malaika. Wawili hao walifanya harusi Kenya na nchini Ujerumani na hata akalipa mahari Kiafrika. Marcus Olsson (kushoto) ameichezea Derby mechi 67 tangu ajiunge nao kutoka Blackburn 2016, akikabiliana na Jesse Lingard wa Manchester United Martin na Marcus wana majina ya Kiafrika kwenye majina yao rasmi - Waikwa na Munuhe. Martin Olsson alianza uchezaji soka kwa kujiunga na timu cha wachezaji chipukizi katika klabu ya Hogaborgs BK ya Sweden na baadaye akahamia klabu ya Blackburn Rovers ya Uingereza. Baada ya kupanda ngazi Blackburn Rovers alijiunga na timu kuu ya klabu hiyo mwaka 2007 na kuwachezea mechi yao ya kwanza wakati wa mechi za kufuzu kwa michuano ya ubingwa Ulaya msimu wa 2007/08. Martin alicheza mechi yake ya kwanza Ligi ya Premia 30 Desemba 2007 dhidi ya Derby County. Baadaye alitia saini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo mwaka 2008 na kuwafungia bao lake la kwanza dhidi ya Everton Septemba mwaka huo. Alihamia Norwich City kwa mkataba wa miaka minne Julai 2013. Martin Olsson alijiunga na Swansea City Januari mwaka jana kwa uhamisho wa thamani ya $ 5.54 milioni na akawafngia bao la kwanza dhidi ya Leicester City 12 Februari 2017. Katika timu ya taifa, alicheza vikosi vya wachezaji wa chini ya miaka 19 na 21 kabla ya kujiungana kikosi kikuu mwaka 2010. Martin Olsson alianza uchezaji wake Hogaborgs BK, Sweden Amewachezea Sweden mechi 41 na kuwafungia mabao matano. Katika kipindi ambacho amekuwa na timu ya taifa ya Sweden, amecheza na wachezaji nyota wa Sweden. Alikuwa na wachezaji kama vile Seb Larsson na Mikael Lustig chini ya nahodha Zlatan Ibrahimovic katika Euro 2012 na 2016. Kujivunia kuwa Mkenya Katika mahojiano na mtandao wa Wales Online, Martin alisema anajivunia sana asili yake. "Ninajivunia sana asili yangu, mamangu alifariki miaka michache iliyopita na tulilelewa katika utamaduni huo na najivunia kuwa raia wa Sweden na Mkenya pia," alisema. "Nina jamaa wengi sana huko, huwa twajaribu kutembea na kuzuru, dadangu husafiri huko mara nyingi kwa sababu ya ratiba yangu hapa. Nilikwenda huko miaka kadha iliyopita na nilifurahia kuwaona jamaa zangu." Anasema alifurahia kuona kwamba mtindo wa maisha ni tofauti, watu huwa wametulia, na "kila mtu huwa hazungumzi kwa simu." "Napenda maisha sana huko na hali ya afya ni nzuri." "Tuna jamaa Nairobi na Mombasa. Nairobi ndiko tulikozoea kuishi, na tuna jamaa Nanyuki pia, mwendo wa saa mbili hivi kutoka mji huo mkuu." "Binamu zangu wako huko na hutazama mechi kupitia runinga, kwa hivyo Swansea wana mashabiki Kenya." Kikosi kamili cha Sweden Kombe la Dunia Walinda lango: Robin Olsen (Copenhagen), Karl-Johan Johnsson (Guingamp), Kristoffer Nordfeldt (Swansea). Mabeki: Mikael Lustig (Celtic), Victor Lindelof (Manchester United), Andreas Granqvist (Krasnador), Martin Olsson (Swansea), Ludwig Augustinsson (Werder Bremen), Filip Helander, Emil Krafth (both Bologna), Pontus Jansson (Leeds United). Viungo wa kati: Sebastian Larsson (Hull), Albin Ekdal (Hamburg), Emil Forsberg (RB Leipzig), Gustav Svensson (Seattle Sounders), Oscar Hiljemark (Genoa), Viktor Claesson (Krasnador), Marcus Rohden (Crotone), Jimmy Durmaz (Toulouse). Washambuliaji: Marcus Berg (Al Ain), John Guidetti (Alaves), Ola Toivonen (Toulouse), Isaac Kiese Thelin (Waasland-Beveren). Katika kikosi cha timu ya taifa ya Sweden kinachocheza katika Kombe la Dunia Urusi ni vigumu kufikiria kuna uhusiano wowote kati ya kikosi hicho na Kenya. text: Gina Haspel anadaiwa kukasirishwa na kuvuja kwa ripoti ya CIA Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa bi Haspel atakutana na viongozi wa bunge la Seneti baadae leo Jumanne. Mkurugenzi huyo hakuwepo wiki iliyopita wakati mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi walipofanya mazungumzo na viongozi wa Seneti, kitendo ambacho kiliwakasirisha baadhi ya wajumbe wa bunge hilo. Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme Mohammed bin Salman. Vyombo vya habari vya Marekani pia vimeripoti kuwa ripoti ya CIA juu ya mkasa huo inaonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa bin Salman aliamuru mauaji hayo. Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman. Vyombo vya habari nchini Marekani pia vinaripoti kuwa CIA wana ushahidi unaonesha kuwa bin Salman aliwasiliana kwa wa ujumbe nfupi wa simu ya mkononi na Saud al-Qahtani ambaye inadaiwa ndiye aliyeendesha operesheni ya mauaji ya Khashoggi. Hiki ndicho kikosi 'kilichomuua' Khashoggi Waziri wa mabo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na waziri wa ulinzi James Mattis waliwaambia maseneta wiki iliyopita kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha bin Salman na mauaji hayo. Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa mstari wa mbele kumtetea bin Salman akidai kuwa ripoti ya CIA haikuhitimisha kinagaubaga kuwa mwanamfalme huyo aliamuru Khashoggi auawe. Bi Haspel pia anadaiwa kukasirishwa na kuvuja kwa ripoti ya CIA kwa vyombo vya habari. Msimamo wa Seneti Maseneta wengi, kutoka vyama vyote vya Republican na Democrats hawafurahishwi na msimamo wa Trump juu ya mauaji hayo, na hasira zao ziliongezeka zaidi baada ya bi Haspel kutohudhuria mahojiano ya wiki iliyopita. Kuonesha hasira zao, maseneta hao walipiga kura 63 kwa 37 mpango wa kusitisha usaidizi wa Marekani kwa Saudia na washirika wake kwenye vita nchini Yemen. Mpango kama huo uliwasilishwa bungeni mapema mwaka huu lakini ulitupiliwa mbali. Trump atakiwa kutoa majibu kuhusu mauaji ya Khashoggi "Ni wakati sasa kuwatumia salamu Saudia kwa namna ambavyo wanavunja haki za binaadamu na kutengeneza janga kubwa nchini Yemen," amesema Seneta Bob Mendez wa Democrat. Seneta wa Republican Lindsey Graham amesema hatapiga kura kwenye muswada wowote mpaka pale bi Haspel atakapolieleza bunge la seneti ukweli wa mambo. "Namna ambayo utawala huu umelishughulikia suala la Khashoggi haikubaliki kabisa," amesema na kuongeza: "Mahojiano (ya wiki iliyopita) hayakunisaidia hata kidogo kuelewa mchango [wa bin Salman] katika mauaji ya Khashoggi." Jamal Khashoggi ni nani? Akiwa mwanahabari mashuhuri, aliripoti habari kubwa kama uvamizi wa Usovieti nchini Afghanistan na kufanya mahojiano na Osama Bin Laden. Jamal Khashoggi alienda Istanbul kushughulikia mchakato wa ndoa yake Kwa miongo kadhaa alikuwa na ukaribu na familia ya kifalme ya Saudia na pia aliwahi kuhudumu kama mshauri wa serikali. Hata hivyo alijitenga na utawala wa sasa na kuwa mkosoaji kisha kukimbilia nchini Marekani akihofia maisha yake mwaka jana. Akiwa Marekani alikuwa akiandika makala kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo aliendeleza harakati zake za kumkosoa Mohammed bin Salman. Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani Bi Gina Haspel atafanya mahojiano na wajumbe wa bunge la Congress juu ya mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi. text: Video hiyo ilionesha genge la vijana lililoonekana kuwateka wasichana katibu 10 katika jingo moja ambalo halijamalizwa kujengwa huku wakiwapiga kwa ukatili kwa viboko vingi mfulurizo na kuwachapa mateke. Wasichana hao ambao wanakadiriwa kuwa na miaka kati ya kumi na minane na zaidi ya 20, walionekana wakipiga mayowe na kulia kwa huzuni kubwa, huku wakiwaomba watesaji wao wawahurumie. Waathiriwa wameombwa na polisi kufika kwenye kituo cha polisi kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwakamata na kuwashitaki wahusika. Polisi imelaani ukatili huo na kuapa kuwasaka wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria. Video ilionesha nini? Video ilionesha kikundi cha vijana wadogo wakiwachapa kikundi cha wasichana Katika vido hiyo iliyoangaliwa na BBC, vijana hao wanaonekana wakiwapiga wasichana huku wakipiga kelele. Wakati mwingime wasichana walionekana wakiomba msamaha huku wakilia kwa uchungu, lakini vijana hao waliendelea kuwapiga viboko na hakuna aliyejaribu kuwazuia. Baadhi ya watazamani wa video hiyo walihesabu idadi ya viboko alivyopigwa kila msichana na kufikia hadi viboko 10 na kugeuzwa tena upande wa pili na kutandikwa vingine zaidi. Msichana mmoja aliyejaribu kutoroka alipigwa viboko katikati ya miguu yake, huku mwingine akisiskika akipiga mayowe "Toka kwenye masikio yangu, usinishike hapa". Polis waliongeza kuwa baada ya genge la vijana hao kuwachapa wasichana, walinyoa nywele zao kwa wembe, kuwatukana matusi makubwa na kuwadhalilisha. "Watu wetu tayari wameanza uchunguzi, na vijana hawa watakamatwa hivi karibuni na kupelekwa mbele ya sheria . "Ukiukaji wa aina hiyo wa haki za binadamu ni jambo la kusikitisha, ni jambo la ubaguzi wa jinsia ," ilisema taarifa ya polisi. Iliongeza kuwa : "Kila mwanamke anayo haki ya kuishi kwa heshima-na kuhisi kuwa hana uoga, kutukanwa au kuteswa, na tutahakikisha kwamba kikosi cha jimbo la Bauchi kinahakikisha mambo kama haya yanashugulikiwa kulingana kisheria . " Wasichana walifanya nini? Taarifa zinasema kuwa genge la vijana hao liliwafanyia ukatili wasichana kwa kuwashuku kuwa walikua wazururaji katika kile kinachofahamika jimboni humo kama "jioni njema," katika eneo la Dumi Gate . Hata katika video hiyo wanasikika wakiwaonya wasichana kwamba wanaadhibiwa kwa makossa waliyoyafanya. Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bauchi waliozungumza na BBC wanasema eneo hilo ni maarufu sana kwa vitendoi vya ukatili. Wameithibitisha kuwa kamati sasa imeundwa kwa ajili ya kutatua tatizo la usalama wa raia katika eneo hilo. Lakini watu wanahoji juu ya ikiwa vijana wana haki ya kuwahukumu vijana wenzao wa kike kwa makossa wanayowatuhumu?. Chini ya sheria ya Nigeria, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kujichukuli sheria mkononi kwa uhalifu wowote ule aliofanya mtu. Uwavera Omuzuwa pia alishambuliwa na genge la wanaume nchini Nigeria alipokuwa kanisani mwaka jana Nchini Nigeria, tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi mara nyingi husababisha hata watu kupoteza maisha yao. Mwaka jana pia Wanageri waligadhabishwa na mauaji ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22, Uwavera Omozuwa aliyeuawa kanisani. Kampeni ya hashtag #JusticeForUwa au # HakiKwaUwa ilienea kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, huku familia yake ikiomba msaada wa kumtafuta aliemuua. Uwavera alikua anajisomea katika kanisa "tulivu" karibu na nyumbani Benin City wakati alipouawa, dada yake, Judith, aliiambia BBC idhaa ya Pidgin. Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi alikufa hospitalini, siku tatu baada kushambuliwa. Polisi katika jimbo la Nigeria la Bauchi imesema kuwa imeanza uchunguzi juu ya video iliyosambaa na kuibua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii iliyoonesha jenge la vijana waliokua wakiwatesa wasichana. text: Vyuo vitano vimefungiwa nchini Tanzania Hata hivyo, Baraza hilo, limesema limelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya vyuo hivyo kushindwa kuwa na sifa stahiki za kuendelea kutoa mafunzo katika ubora unaohitajika. Miongoni mwa vyuo vilivyoathiriwa na hatua hiyo ni Taasisi ya Wanyamapori Pasiansi iliyopo jijini Mwanza ambapo Dr. CUthbert Nahonyo ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya ushauri katika Chuo hicho anakosoa hatua hiyo na kusema kuwa ni baraza lenyewe ndio lenye makosa kwa kuwa usajili wao uliisha tangu mwaka 2012 na wamekuwa wakifuatilia kupata usajili mpya kwa muda mrefu bila kupata majibu. Ama kwa upande wa vyuo vilivyofutiwa usajili ni Chuo cha Zoom Polytechnic College kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo mmiliki wa chuo hicho bwana Syeta Malimi anaona zoezi hilo limeharakishwa bila ya wao kushirikishwa.Japo kuwa NACTE waliwahi kuwatembelea na kuwataka waboreshe mazingira ya kusomea kama vile kuwa na maktaba na kukarabati jengo,lakini gharama ikawa kubwa hivyo wakaona ni bora kukiamisha chuo hicho katika eneo lingine ambalo wataweza kumudu gharama,na barua ya kutoa taarifa juu ya kuhama kwao rasmi tayari walishaituma baraza. Pamoja na kwamba chuo hicho kimefutwa lakini BBC ilipokitembelea ilikuta wanafunzi wanaendelea na masomo yao kama kawaida, ingawa hawakuficha hisia zao juu ya kushtuliwa na taarifa za kufutwa kwa chuo chao hasa ikizingatiwa kwamba hatua hii imechukuliwa wakati ambapo baadhi ya wanafunzi walikuwa tayari washalipa ada na wengine wanakaribia kumaliza muda wao wa masomo, hivyo taarifa hiyo imewafanya kutojua mustakbali wao na hata wazazi wao watakuwa katika nafasi gani ya kuwasaidia kuendelea na masomo yao. Baadhi ya Wanafunzi wakiendelea na masomo Utaratibu wa kawaida Hata hivyo Baraza hili limesema,huu ni utaratibu ambao upo mara kwa mara ili kuboresha elimu ya ufundi nchini Tanzania. Twilumba Mpozi ni kaimu mkurugenzi wa usajili na ithibati ya vyuo anasema zoezi hili huwa linafanyika mara kwa mara haswa wakati huu wa usaili ili wanafunzi na wazazi waweze kujua vyuo ambavyo vimesajiliwa na vina ubora. Na hatua hiyo imekuja baada ya kipindi cha miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania, kumekuwa na utitiri wa vyuo ambavyo baadhi havikidhi kiwango, hivyo kushusha kiwango cha elimu. Baadhi ya wamiliki na wadau wa elimu wamelalamikia Baraza la Elimu ya ufundi nchini Tanzania kuvifutia usajili vyuo vitano huku vingine arobaini na moja vikifungiwa kuendesha mafunzo. text: Alikuwa mkuu wa jeshi la wanahewa Perence Shiri akila kiapo Rais huyo aliwaondoa mawaziri kadha ambao alikuwa ametangaza kuwateua awali. Miongoni mwa aliotupa nje ni waziri wa elimu ambaye alikuwa anahudumu chini ya mtangulizi wake Robert Mugabe. Baadhi ya watu walipinga kuteuliwa tena kwake. Mawaziri wengine waliwatupa nje baada ya kugundua uteuzi wao ulikuwa unakiuka katiba, anasema mwandishi wa BBC mjini Harare Shingai nyoka. Kwa jumla, mawaziri 21 wamekula kiapo ambao ni mchanganyiko wa wanasiasa ambao wamekuwa uongozini kwa muda mrefu pamoja na wakuu wa kijeshi. Wakosoaji wanasema uteuzi wa baraza hilo la mawaziri unaonesha jinsi jeshi lilivyodhibiti serikali. Waziri mpua wa ardhi ambaye alikuwa mkuu wa jeshi la wanahewa Perrance Shiri amepuuzilia mbali madai hayo. "Nilipokuwa jeshini nilikuwa chini ya wizara ya ulinzi ambayo ni sehemu ya serikali. Na nani amesema wanajeshi hawawezi kuwa wanasiasa? Mimi ni raia wa Zimbabwe na nina haki ya kushiriki katika siasa za nchi hii," ameambia BBC. Mwanajeshi mwingine, Meja Jenerali Sibusiso Moyo ambaye alitangaza kwamba jeshi lingechukua udhibiti wa serikali ameapishwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa. Amesema atahakikisha "uchumi na diplomasia" vinaifaa nchi hiyo. Rais Emmerson Mngangagwa ameahidi kufanikisha enzi mpya ya ustawi kwa kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo na nchi za magharibi - ambao ulikuwa umedorora chini ya Bw Mugabe - pamoja na uhusiano wake na wawekezaji kutoka nje ya nchi hiyo. Bw Mnangagwa alikuwa ametangaza mawaziri ambao wangeteuliwa mapema wiki iliyopita, lakini aliwabadilisha wengine baada ya kugundua kwamba alikuwa amewateua baadhi ambao si wabunge kinyume na maagizo ya katiba. Baadhi wanasema hiyo ni ishara kwamba rais huyo alikuwa "anawasikiliza wananchi" au kwamba "aliharakisha kufanya jambo hilo muhimu sana." Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameliapisha baraza lake la kwanza la mawaziri baada ya kuchukua uongozi nchini humo wiki mbili zilizopita. text: Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya ni mshindi wa mbio za Olympic mita 800 Mshindi wa mbio za Olympic mita 800 Caster Semenya, mwenye umri wa miaka 28, anapinga nia ya Shirikisho la kimataifa la Riadha (IAAF) juu ya mpango kuweka masharti ya viwango vya testosterone miongoni mwa wanariadha wa kike. Umoja wa mataifa imeitaja mipango hiyo kama "isiyo na umuhimu , ya udhalilishajia na yenye mathara ". IAAF imesema kuwa muswada uliopatiwa Umoja wa Mataifa unajumuisha "kauli zisizo sahihi". Umoja wa Mataifa wazitaka bodi za michezo kuacha kuandaa na kutekeleza sera zinazowasukuma wanariadha wanawake na wasichana kupitia tiba zisizo za lazima Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone anatakiwa kukimbia na wanaume au kushiriki mashindano ya watu waliobadilishwa mpaka apate tiba ya kupunguza viwango hivyo. Sheria hizo zinawahusu wanawake wanaokimbia mbio za mita 400 na maili moja na inawapasa wanariadha hao kuhakikisha viwango vya testosterone vinakuwa chini kulingana na kiwango kilichowekwa. "kwa walau miezi sita kabla ya mashindano ". Suala hilo lilijadiliwa na kikao cha 40 cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa cha mwezi Machi, ambapo wajumbe waliomba ripoti yenye maelezo ya kina juu ya suala hilo iandaliwe kwa ajili ya mkutano ujao. Kabla ya hayo, baraza hilo lilielezea "hofu zake " juu ya mapendekezo ya IAAF. Baraza hilo limesema bodi za utawala hazinabudi "kuacha kuandaa na kutekeleza sera na utendaji ambao unalazimisha , kushurutisha au kuwasukuma wanariadha wanawake na wasichana kupitia , udhalilishaji na mathara ya upasuaji wenye madhara wa kimatibabu usio wa lazima kama njia ya kuruhusiwa kushiriki katika matukio mashindano ya michezo ya wanawake". Katika taarifa yao iliyochapishwa katika jarida la matibabu la Uingereza, hivi karibuni wataalamu walidai kuwa sheria za IAAF zinaitia katika hatari ya "kuweka viwango visivyo vya kisayansi kwa matukio mengine ya faida za maumbile ". IAAF ilitaka kuweka sheria mpya tarehe 1 Novemba 2018, lakini ikakabiliwa upinzani wa kisheria uliolazimisha kusheleweshwa kwa utekelezwaji wake hadi Mahakama ya utatuzi wa migogoro ya michezo (Cas) itakapoamua juu ya suala hilo. Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa tarehe 26 Machi, lakini Cas iliiahirishahadi mwezi ujao. Ushindi kwa Semenya utamfanya awe huru kuendelea kushiriki mashindano kama ambavyo amekuwa akifanya, lakini iwapo atashindwa kwenye kesi hiyo itamaanisha kuwa mwanariadha huyo wa Afrika Kusini anaweza kutoshiki mashindano, kushindana na wanaume au kulazimika kutumia dawa za kushusha viwango vyake vya homoni Awali Semenya aliagizwa na wakuu wa riadha afanyiwe vipimo vya jinsia, lakini hakuna matokeo ya vipimo hivyo yaliyotangazwa rasmi kwa umma. Testosterone ni homoni inayoongeza ukubwa wa misuli, nguvu za mwili na chembechembe nyekundu za damu,ambayo hathiri uwezo wa nguvu za mwili. Semenya ashinda dhahabu mbio za 800m London Jibu la IAAF kuhusu muswada wa Umoja wa Mataifa. Katika taarifa iliyotolewa kwa BBC kitengo cha Spoti IAAF ilisema "ni wazi kwamba mwandishi wa ripoti hakuwahi kuona maelezo ya sheria za IAAF wala maelezo taliyowasilishwa hivi karibuni katika Mahakama ya utatuzi wa migogoro ya michezo. " Kuna kauli ambazo si sahihi zilizomo kwenye muswada uliowasilishwa katika baraza la Haki za binadamu la umoja wa Mataifa kwa hiyo ni vigumu kujua ni wapi pa kuanzia. " Tunalokubaliano sote ni kwamba tunaamini ni muhimu kuzingatia usawa katika mashinda ya michezo ya wanawake ili wanawake wawe huru kushiriki katika mashindano ya kitafa na kimataifa ya michezo . " Kufanya hili ni muhimu ili kuhakikisha mashindano yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake yanalindwa, jambo linalohitaji shertia na masharti ili kulilinda, vinginevyo tunajiweka katika hatari ya kupoteza kizazi kijacho cha wanariadha wanawake, kwani hawataona njia ya mafanikio katika michezo ya kike." Mipango ya kuwatenga wanariadha wa kike kulingana na viwango vyao homoni za testosterone "Ni ukiukaji wa haki Kimataifa za biadamu " linasema Baraza la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. text: Simu zaidi ya 100 zilizokuwa zimeibiwa zilipatikana Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My iPhone kufuatilia simu zao. Simu hizo zilikuwa zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo la California, polisi wamesema. App hiyo huonesha ilipo simu ya mtu, na baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kupiga ripoti kwa polisi, maafisa walifuatilia kwa kutumia app hiyo hadi wakamnasa mshukiwa. Walipata zaidi ya simu 100 zikiwa kwenye mfuko wa mshukiwa huyo wa wizi. Baadhi ya simu zilirejeshewa wenyewe papo hapo. Nyingine zimekabidhiwa kwa wasimamizi wanaokusanya mali na bidhaa zilizopotea wakati wa tamasha hilo. Polisi walikuwa tayari wametumwa kwa wingi katika tamasha hilo baada ya visa vya wizi wa simu kuongezeka, anasema afisa wa polisi Dan Marshall, akinukuliwa na mtandao wa Gizmodo. Lakini wenye simu ndio waliosaidia kunaswa kwa mshukiwa. Wanaohudhuria tamasha hilo wameshauriwa: Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhones amekamatwa nchini Marekani. text: Dkt Tatu Kamau anasema sheria inayoharamisha ukeketaji wa wanawake na wasichana inakiuka utamaduni katika jamii nyingi za Kiafrika. kadhalika, amesema ni ubaguzi dhidi ya wanawake ikizingatiwa kwamba upashaji tohara wa wanaume unakubalika kisheria. Daktari huyo anataka pia bodi ambayo iliundwa nchini humo kukabiliana na upashaji tohara wa wanawake ivunjiliwe mbali. Aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama Kuu mjini Machakos, mbele ya jaji David Kemei. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mwezi ujao. Dkt Kamau, akizungumza na wanahabari baada ya kuwasilisha kesi yake, alisema wanawake wote, sawa na watu wazima popote pale, wanafaa kuruhusiwa kufanya uamuzi kuhusu miili yao wenyewe bila kuwekewa vikwazo na sheria. Amesema ukeketaji ni neno ambalo lilitetwa na watu kutoka nchi za Magharibi Lakini sasa amesema raia wa nchi za Magharibi wanafanya jambo sawa na ukeketaji, kufanya upasuaji kwenye uke kurekebisha maumbile. "Upashaji tohara ulikuwa sehemu ya utamaduni wa Waafrika kabla ya kufika kwa wakoloni na haifai kuharamishwa," amesema. "Punde tu itakapohalilishwa, tutaweza kufanya tohara kwa njia iliyo bora Zaidi, mojawapo ikiwa njia ya hospitali. Tukifanya hivyo basi itakuwa salama kabisa. Na njia hii ni mojawapo wa upasuaji wa kawaida duniani kote." Wanawake wakiandamana dhidi ya ukeketaji wa wasichana Nairobi awali Anasema wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa wa dola au hata kufungwa jela kwa sababu ya ukeketaji. "Ingawa tunataka sana kumlinda mtoto msichana, kuna wanawake wengi sana ambao wamekamatwa na kufungwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita," anasema. "Unapokuwa mtu mzima, hakuna sababu yoyote ya kuzuia kufanya uamuzi (iwapo ungependa kupashwa tohara)" alisema. Takwimu muhimu kuhusu ukeketaji Kenya Chanzo: Takwimu ya Utafiti kuhusu Afya na Watu Kenya ya mwaka 2014 Dkt Kamau alisema jamii nyingi zimekuwa zikifanya upashaji tohara kwa njia nyingi na kwamba si aina zote za tohara hiyo ambayo ina madhara kwa mwanamke. Alisema sawa na jinsi watu huonywa dhidi ya athari za uvutaji sigara au ungwaji pombe, kampeni ya kuwahamasisha watu kuhusu madhara ya ukeketaji inafaa kuendelea lakini wale wanaoamua au wangependa kupashwa tohara wanafaa kuruhusiwa. Mamilioni ya wanawake duniani wamekeketwa Dkt Kamau ameshutumu hatua ya Bunge nchini Kenya la kupitisha sheria ya kuharamisha ukeketaji akisema Bunge lilivuka mipaka na kuingilia masuala ya utamaduni. "Iwapo wanaweza kuharamisha utamaduni, kesho wataharamisha dini au kitu kingine. Dada anastahili kutetewa akifanya maamuzi yake, na wala si kulazimishwa kufanya mambo mengine," amesema. Makundi yanayokabiliana na ukeketaji yameshutumu hatua ya Dkt Kamau. Mwenyekiti wa bodi ya kukabiliana na ukeketaji Bernadette Loloju amesema ukeketaji hupingwa kwa sababu ya madhara yake kwa wanawake, hasa wakati wa kujifungua. Amesema kampeni hiyo imefanikiwa kupunguza visa vya ukeketaji kutoka asilimia 37 mwaka 2008 hadi 21 mwaka 2014 kwa mujibu wa takwimu za serikali. Kwa sasa hata hivyo, ukeketaji hutekelezwa kisiri. Watoto wamekuwa pia wakipashwa tohara wakiwa wadogo kinyume na zamani ambapo ulifanywa wasichana wakibalehe. Wasichana takriban 140 milioni wamekeketwa maeneo ya Afrika, Mashariki ya Kati na Bara Asia. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo pia zimeathiriwa pakubwa na ukeketaji wa wasichana. Inakadiriwa kwamba nchini Tanzania, wasichana na wanawake 7.9 milioni wamekeketwa. Kwa nini imekuwa vigumu kukabiliana na ukeketaji? Katika baadhi ya jamii Afrika Mashariki, ni utamaduni unaoathiri hadhi ya mwanamke katika jamii. Baadhi ya jamii, mwanamke haruhusiwi kuolewa au kutangamana na wasichana wengine wa rika lake iwapo hatapashwa tohara. Katika jamii ya Wamaasai kwa mfano, mwanamke huwa na wakati mgumu kuthibitisha kwamba yeye ni mwanamke kamili iwapo hajapashwa tohara. Aidha, watoto wake huchukuliwa na jamii kama wasiokubalika. Sherehe ambazo huambatana na upashaji tohara na wazazi wa msichana kutambuliwa kama wazee katika jamii iwapo binti mabinti wao wamepashwa tohara huwafanya kutaka sana mabinti wao wakeketwe. Daktari mmoja nchini Kenya amewasilisha kesi mahakamani akitaka upashaji tohara wa wanawake ambao hufahamika pia kama ukeketaji uhalalishwe. text: Waendeshaji wa programu hii tumishi wanahitaji filamu 14 kila juma lakini sasa wanapata fiilamu moja pekee yenye ubora. Na katika kuinua ufanisi wa kazi hiyo waendeshaji wanakiri kuwa changamoto bado ni kubwa lakini wameanza jitihada kadhaa kuzifanyia kazi. "Bado kuna changamoto katika uandaaji wa filamu za kiswahili lakini tuna mipango thabiti ya kuhakikisha kuwa na filamu zenye taswira zenye ubora zaidi na tuna uhakika baada ya muda mfupi swahiliflix itakuwa ni sehemu ambayo mtu akitaka kuangalia kitu chenye ubora wa juu anakuja kwetu"Maximilian Rioba ni mkurugenzi wa programu hiyo. Raymond Kigosi, msanii wa Bongomovie Hadi sasa zaidi ya watu elfu kumi na tano wameanza kufaidi matunda ya mfumo huo wa lugha ya Kiswahili ikiwa ni chachu ya kueneza lugha ya kiswahili. "Soko la filamu limetawaliwa na lugha ya kiswahili Afrika mashariki na kati" Kwa muda sasa soko la filamu nchini Tanzania limekuwa likiporomoka lakini wadau wa filamu za Kiswahili wanasema huenda jukwaa hili likarejesha matumaini . Swahiliflix kunadi filamu za kiswahili kimataifa "Tuna matumaini kuwa tunafikia kiwango cha kimataifa kutokana na filamu nilizoziona humo" "Sio lazima kwenda kununua mkanda wa video au kuazima mikanda, popote nilipo ninaweza kuangalia filamu kwenye simu yangu au komputa na kufurahia sinema". Wasanii wa filamu wanasema ujio wa programu hii ni mwanzo mpya na wanajizatiti kuwekeza Zaidi "Watu walikuwa hawafanyi kazi zaidi kwa sababu walikuwa hawajui wanazipeleka wapi hizo filamu lakini sasa sehemu ya kuzipeleka ipo,"msanii wa bongo movie Raymond Kigosi aeleza Huenda sasa jina Bongo Movie nalo likapenya kwenye rubaa za kimataifa na kuchuna vyema katika soko la filamu ulimwenguni. Swahiliflix imeanzishwa wakati kampuni maarufu ya Netflix, inayotoa huduma za video mtandaoni moja kwa moja, imezinduliwa katika mataifa karibu yote duniani na kuzua msisimko mkubwa. Sekta ya burudani pia haikuachwa nyuma katika kutumia Kiswahili hususan kupitia kutafsiri kazi zao kwa lugha hiyo ili kuwalenga takriban watu milioni 200 wanaoizungumza. Kunao wanaoamini itatoa ushindani kwa zinazotoa huduma za runinga, filamu na video kwa malipo. Wengi wanaitazama kama njia ya kuwawezesha kupata video, ambazo awali walikuwa hawawezi kuzipokea, kwa urahisi na kwa bei nafuu. Mahitaji ya lugha ya kiswahili yameongezeka duniani huku baadhi ya vyuo vikuu vikianzisha lugha hiyo pamoja na vitivo kamili. Katika jitihada za kukuza soko la filamu nchini Tanzania, wasanii nchini humo wameanzisha programu tumishi inayojulikana kama Swahiliflix, ikiwalenga zaidi wapenzi wa filamu hizi walioko maeneo mbalimbali duniani. text: Wiki mbili zilizopita ofisi hizo zilitoa tamko la pamoja juu ya kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania." Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria. "Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo. Jumatano jioni, ofisi hizo mbili tena kwa kupitia mitandao ya kijamii zilitoa ujumbe kuwa wanaendelea kufuatili kesi ya Kabendera. "Tunaendelea kufuatilia kesi ya Erick Kabendera. Haki za kisheria ni haki ya raia wot, na kuhakikisha upatikatnaji wa haki hiyo ni wajibu wa serikali zote," unaeleza ujumbe ambao umechapishwa katika kurasa za twitter za Ubalozi wa Marekani na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke. Kabendera anakabiliwa na mashtaka gani? Kabendera alipandishwa kizimbani Agosti 5 na kusomewa mashtaka matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi . Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini Tanzania, shtaka la pili ni la kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za kitanzania. Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini. Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani. Makosa yote hayana dhamana na Kabendera anaendelea kusota rumande. Alifikishwa tena mahakamani Jumatatu wiki hii, lakini kesi ikaakhirishwa mpaka Agosti 30 baada ya upande wa mashtaka kudai hawajakamilisha upelelezi. Kumekuwa na wasiwasi ndani na nje ya Tanzania kuhusu namna ambavyo amekamatwa, na taswira inayotokana na hatua hiyo kwa uhuru wa yombo vya habari nchini humo. Pia baadhi ya wanaharakati wameonyesha kushangazwa na kubadilika kwa yaliominika kuwa ndio makosa anayotuhumiwa nayo. Awali maafisa wa polisi na wale wa idara ya uhamiaji walisema anachunguzwa kuhusu utata wa uraia wake. Baadaye mawakili wake walitoa taarifa wakieleza mteja wao atashtakiwa kwa kuhusika na ripoti iliyochapiswha katika jarida la The Economist, lakini mahakamani kibao kikageuka tena na kuwa kesi ya ubadhirifu wa kiuchumi. "Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake, kama ilivyotambua kwamba ni haki ya msingi na kuridhia kwenye mikataba mbali mbali ya haki za kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa, miongoni mwao ikiwemo azimio la kimataifa la haki za kirai na kisiasa," inaeleza sehemu ya tamko la awali la Marekani na Uingereza juu ya wasiwasi huo. Ofisi za ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini Tanzania zimeendelea kumulika kesi ya mwanahabari maarufu wa uchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera. text: Kevin Odour Kevin amesema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Afya cha BBC juu ya safari yake ndefu inayostaajabisha na kusisimua lakini jambo kubwa anajivunia maisha yake. ''Safari yangu ya kuishi na virusi ilianza nilipozaliwa lakini nilianza kumeza dawa za virusi nikiwa na umri wa miaka sita wakati ambapo nilianza kuugua mara kwa mara na kulazwa hospitalini,'' Kevin alieleza. Aliongeza kusema kuwa wakati alipoanza kulazwa mara kwa mara hospitalini na kumeza dawa za kifua kikuu alikuwa hafahamu kama ameathirika. Dawa za virusi vya ukimwi "Baada ya kufanyiwa uchunguzi walinipatia dawa lakini hawakuniambia zilikuwa ni za nini na hata mama yangu pia hakuniambia lakini kila siku nilikuwa nikijuuliza hizi dawa ni za nini na kwa nini nakunywa kila siku? Nilipofika darasa la sita nikamuuliza mama yangu; mbona dada yangu hamezi hizi dawa lakini ni mimi na wewe tu? Akaniambia kwamba muda ukifika ataniambia , alisisitiza kwamba nikiendelea kukua atanieleza lakini na nikaendelea kumeza dawa hizo huku nikiendelea na masomo yangu. Nilipofika umri wa miaka tisa niliamua kutomeza dawa hizo na hapo ndipo nilipoanza kuugua sana. Virusi vya ukimwi Baadae niliamia katika nyumba ya watoto wadogo waliozaliwa na virusi vya Ukimwi na wale wasio na wazazi. Huku ndipo nilikutana na watoto wengine kama mimi wakimeza dawa nilizokuwa nikimeza hapo awali lakini swali la kwa nini ninameza dawa hizi bado lilikuwa akilini mwangu. Maswali haya yote yalifika kikomo pale ambapo mtawa mmoja alipotutembelea katika nakazi yetu na akiongozana na nesi mmoja na kutuuliza iwapo tunafahamu kuhusu hali zetu? Nilijiangalia na nikajiuliza ni hali gani hiyo? Basi nesi huyo hakuficha akatuuliza iwapo tunafahamu kama tuna virusi vya ukimwi? Habari hiyo ilinishtua sana nakujiuliza kuwa hizi dawa ambazo nimekuwa ninameza kila siku ni za Ukimwi. Kwa familia yetu mimi peke yangu ndio nilikuwa nimezaliwa na virusi hivyo vya Ukimwi. Baada ya kusikia hayo ikawa ni mara ya pili ninaapa kuwa "sitakunywa tena dawa hizo". Lakini baada ya kupata taarifa hiyo ambayo ilinishtua nikaamua kumuuliza mama yangu iwapo yeye pia ana virusi vya ukimwi? Alishtuka lakini akakiri kwamba ana virusi vya ukimwi na hiyo ndio siku aliamua kufunguka kuniiambia kuhusu hali yake na yangu. Niliweza kubaini kuwa mama yangu ana saratani lakini vilevile anaishi na virusi vya Ukimwi. Kisa hicho cha mama yangu kilinifanya nimuhakikishie kuwa sitaacha tena kumeza dawa, nitaishi na kujenga familia. Nilipitia unyanyapaa nilipokuwa nakua , marafiki zangu walikataa hata kucheza mpira na mimi wakidhani kuwa nitawaambukiza. Wengine waliogopa kucheza na mimi kwa hofu ya kuambukizwa na taratibu nikajitenga nao. Kevin Odour Ndoto yangu ilikuwa ni kuwa na familia, nilikutana na msichana ambaye nilimpenda ingawa ilinichukua muda kumwambia kutokana na hali yangu. Sikuwa na matumaini kuwa atanikubali kama nikimwambia hali yangu lakini cha kushangaza alinikubali huku akijua hali yangu ya kiafya. Mke wangu hakuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi mpaka sasa hana virusi hivyo. Miaka saba iliyopita ndipo nilimwambia kuhusu hali yangu mbele ya daktari na akanihakikishia ataiishi nami na alimshukuru kwa kumwambia mapema. Na tangu hiyo siku nilimuahidi kutomuacha maishani kwangu. Baada ya miaka kadhaa mke wangu alipata uja uzito na kujifungua mtoto msichana ambaye hana virusi vya ukimwi pia," Kevin alisimulia. Kulingana na wataalam mtoto anastahili kufahamisha hali yake akiwa kati ya umri wa miaka 6 hadi 9. Kevin odour mwenye umri wa miaka 24, alizaliwa na virusi vya ukimwi na sasa ameweza kupata mtoto asiye na virusi hivyo. text: Mabao mawili aliyofunga Aubameyang katika mechi ya Arsenal dhidi ya Burnley imemaanisha amepata kujiunga na Salah na chezaji mwenzake wa Liverpool Mane, aliyeitinga Wolves, kwa mkusanyiko wa mabao 22. Salah alishinda tuzo hiyo msimu uliopita. Ni ushindi wa chini wa taji hilo tangu 2010-11, wakati Dimitar Berbatov na Carlos Tevez waliposhinda pamoja tuzo hiyo ya Golden Boot inayopewa mfungaji mabao mengi kila mmoja akiwa amefunga mabao 20. Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Gabon Aubameyang aliyefunga mara mbili baada ya kipindi cha mapumziko huko Turf Moor amesema: "Napokea taji hili na wachezaji wengine wawili ninaowapenda, g wachezaji bora na Waafrika. Tunaiwakilisha Afrika, ni vizuri. "Ninafurahi tumeshinda, na napokea tuzo hii [Golden Boot] tna watu nnaowapenda. wachezaji wenzangu walijua kuhusu tuzo hii. Mimi sikusema kitu. Sikutaka wacheze wakinilenga mimi. Mimi napneda kushirikiana na wenzangu." Salah amekuwa mchezaji wa sita kushinda taji hilo la Golden Boot katika misimu inayofuatana 'Wote ni wachezaji wangu' Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameeleza mshtuko na furaha kwa mchezaji huyo wa zamani wa kiungo cha mbele wa Dortmund aliyemsajili kutoka Saint-Etienne mnamo 2013, alipokuwa anakiongoza kikosi huko Westfalenstadion. "Auba pia? wapewa tuzo tatu? Ni vizuri. wote ni wachezaji wangu" amesema. Salah, mwenye umri wa miaka 26, amefunga mabao 32 msimu uliopita. Idadi hiyo ni rekodi ya mabao mengi zaidi katika kampeni ya mechi 38. Amekuwa mchezaji wa sita kushinda taji hilo katika misimu inayofuatana. Harry Kane wa Tottenham mchezaji wa mwisho kulizuia taji hilo la ligi kuu ya Engalnd baadaya kulishinda mnamo msimu wa 2015-16 na 2016-17, alimaliza kwa mabao 17 baada ya kujruhiwa katika msimu. Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang wafunga mabao ya fanali na kufanikiwa kutuzwa kwa pamoja na Mohamed Salah wafungaji mabao bora katika ligi kuu ya England. text: Kipigo cha 4-0 didi ya Leicester ilikuwa ni ishara tosha kuwa LIverpool haitanii msimu huu. Hawawezi kusema hadharani, ama kuonesha furaha yao kwa sasa, kwa kuwa katika miaka hiyo 30 kumekuwa na vipindi ambavyo walikaribia kunyakua kombe lakini likawaponyoka. Lakini yaonekana mwaka huu hadithi ni tofauti, ubora wa kikosi ni wa hali ya juu, yawezekana ikawa sahihi kusema kikosi hiki cha sasa ndiyo bora zaidi kuliko vyote katika miongo mitatu iliyopita. Nuru ya ushindi iling'ara zaidi kwa vijana hao wanaonolewa na Mjerumani Jurgen Klopp baada ya kuichapa Leicester City inayoshika nafasi ya pili kwa goli 4-0 siku ya Boxing Day. Ushindi wa Liverpool uliambatana na kiwango safi cha umiliki wa kandanda, Leicester ambayo watu walikuwa wakiipigia chapuo la kuizuia Liverpool na kufanya maajabu ya kuchukua ubingwa kama mwaka 2016 walikuwa zaidi ya wanyonge katika mchezo huo uliopigwa dimbani kwao. Kwa matokeo hayo, Liverpool ikafikisha alama 52, na kuifanya ikae kwenye usukani wa ligi kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya Leicester yenye alama 39. Ijumaa Disemba 27, ikawa siku njema pia kwa Liverpool japo hawakushuka dimbani, mabingwa watetezi Manchester City ambao wapo nafasi ya tatu wakapoteza mchezo wao dhidi ya Wolves kwa goli 3-2. Kwa matokeo hayo, pengo baina ya Livepool na Man City yenye alama 38 ni pointi 14. Pep Guardiola akiri kuwa Man City haiwezi kuifikia kasi ya Liverpool msimu huu Ikumbukwe pia kuwa Livepool ana mchezo mmoja mkononi hivyo endapo ataushinda mchezo huo atakuwa na alama 55. Baada ya mchezo dhidi ya Wolves, kocha wa Man City Pep Guardiola alikiri kuwa safari ya ubingwa kwao imefikia tamati. "Pengo ni kubwa sana...ni kitu kisicho na uhalisia kwa sisi kuanza kuwafikiria Liverpool. Kwa sasa tunawapigia hesabu Leicester, tunaamini tunaweza kurudi katika nafasi ya pili," amesema Guardiola. Kwa upande wa kocha wa Leicester, Brendan Rodgers pia itakuwa ni vigumu sana kuwazuia Liverpool. "(Liverpool) Ni timu nzuri sana. Kiwango chao cha kujiamini kipo juu. Wamekuwa ni wazoefu wa kushinda na hawajapoteza michezo mingi katika miezi 18 iliyopita. Sasa wana wachezaji wa kutosha, uzoefu na ubora wa kuwafanya wamalize kazi mapema." Klopp: Hakuna kilichoamuliwa Kocha wa Liverpool kwa upande wake anaonekana kukagua kila neno analoliongea kuhusu mustakabali wa ubingwa. Naam, uhalisia ni kuwa bado kuna mechi 20 zinawasubiri kabla ya kumaliza msimu huu. Nusu yao ya ligi, sawa na michezo 19 itakuwa kesho dhidi ya Wolves. Mpaka sasa Liverpool wameshinda mechi 17 na kutoka sare mchezo mmoja tu dhidi ya mahasimu wao Man United. "Bado hakuna chochote kilichoamuliwa, sisikii maamuzi yeyote kwenye masikio yangu. Sisi tunajitahidi kufanya kila tuliwezalo kujiandaa na mechi zetu zinazofuata," anadai Klopp. Klopp: Mipango yetu ni kujiandaa na michezo yetu ijayo Licha ya kauli hiyo ya Klopp, uhalisia ni kuwapengo baina yao na timu zinazowafukuza katika msimamo wa ligi ni kubwa. Si jambo linaloyumkinika kuona Liverpool ambayo haijafungwa michezo ya ligi 34 iliyopita kudondosha alama 14 mpaka msimu utakapokamilika mwakani. Toka mwaka 2019 uanze Livepool imefungwa mchezo mmoja tu wa ligi. Ili ubingwa uwaponyoke msimu huu, basi watalazimika kufungwa michezo mitano kati ya 20 ijayo, huku wapinzani wao wa karibu, Man City na Leicester washinde michezo yao yote. Hakika hizo zitakuwa hesabu ngumu kutimia. Mpaka sasa Man City washapoteza mechi tano kati ya 19 (mzunguko wa kwanza wa ligi). Msimu uliopita walipoteza mechi nne katika mechi zote 38. Uongozi huu wa ligi wa Liverpool, kwa alam nyingi kama hizo kufikia siku ya 'Boxing Day' mara ya mwisho ulishikiliwa na Manchester United miaka 26 iliyopita msimu wa 1993-1994, ambapo United walinyakua ubingwa. Kwa namna yeyote ile, Liverpool ni bingwa mteule wa ligi ya Primia msimu wa 2019/2020. Mara yao ya mwisho kuchua taji hilo ilikuwa ni miaka 30 kamili iliyopita, msimu wa 1989/1990. Japo wenyewe hawasemi, ama yawezekana hawataki kunukuliwa wakisema, miaka 30 ya kushindwa kuchukua taji la Ligi ya Primia kwa Liverpool hatimaye inaelekea kufika kikomo. text: Thamani ya Naira imeshuka sana Amesema hayo siku moja tu baada ya Afrika Kusini kutwaa tena nafasi ya taifa lenye uchumi mkubwa barani Afrika. Nigeria ilikuwa imeshikilia nafasi hiyo kwa miaka miwili baada ya kutathmini upya uchumi wake. Afrika Kusini iliipita Nigeria baada ya kutumiwa kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha dhidi ya dola ya Marekani. Sarafu ya rand ya Afrika Kusini imeimarika pakubwa ilhali naira ya Nigeria imeshuka sana. Kwa sasa, thamani ya uchumi wa Afrika Kusini ni $301bn (£232bn) nao uchumi wa Nigeria $296bn. Mataifa yote mawili hata hivyo si thabiti kiuchumi. Bw Buhari Akiongea mjini Abuja, Bw Buhari alisema: "Umekuwa mwaka mgumu sana kwa Nigeria. Kabla yetu kuingia madarakani, mafuta yaliuzwa $100 (£77) kwa pipa. Bei hii ilishuka hadi $37, na sasa ni kati ya $40 na $45 kwa pipa." "Ghafla, tumekuwa taifa maskini, lakini kujitolea kwetu kuhakikisha uwazi na uwajibikaji kunazuia wananchi kuhisi kwamba kuna upungufu mkubwa katika uchumi." Bw Buhari alichukua mamlaka mwaka jana baada ya kushinda uchaguzi wa urais. Aliahidi kukabiliana na ufisadi na kuinua uchumi wa Nigeria. Kiongozi wa Nigeria Muhammadu Buhari amelalamika kwamba taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika limekuwa maskini ghafla. text: Matukio ya uonevu shuleni yamekuwa yakiendelea katika shule mbalimbali za bweni hususani za Umma Waliosoma shule nyingi hususan za umma katika nchi za Kiafrika zikiwemo za Afrika mashariki hali huwa ni tofauti kutokana na uonevu ambao baadhi ya wanafunzi huwa wanakabiliana nao kutoka kwa wanafunzi wenzao, na hata waalimu wao. Uonevu huu hufanyika kwa njia tofauti, ikiwemo kudhalilishwa, kutukanwa, kuibiwa au kufichwa kwa mali zao, wakati mwingine hata kupigwa na kujeruhiwa. Matukio ya aina hii yamekuwa yakiendelea, huku baadhi yakijulikana na mengine kutojulikana kutokana na wanaoonewa kunyamaza kwa hofu ya kushambuliwa zaidi au hata kufukuzwa shule. Wiki iliyopita karibuni Wanafunzi 10 Umbwe Sekondari nchini Tanzania walisimamishwa masomo, kutokana na vurugu zilizotokea katika shule hiyo, na hii ilisababisha wanafunzi. Tukio hilo lilikemewa na Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa Seleman Jafo akililitaja tukio hilo kama ubaguzi na mateso kwa wanafunzi, na kubainisha kuwa Serikali haitavumilia walimu wakuu wanaotajwa kuwa na tabia hizo, na akaagiza uchunguzi ufanyika juu ya wahusika. Mwanasaikolojia Perpetual Wanyugi, anasema mwanafunzi au mtoto anayewafanyia ukatili wenzake binafsi huwa hajiamini na huenda pia alipitia ukatili katika familia yake Miongoni mwa watu waliopitia uonevu wa aina hii katika shule za sekondani ni Bwana Nickson R. Mlang'a alipokuwa akisomea shule ya sekondari ya Nyamongo . Licha ya kwamba vurugu hizi zilikuwa ni kati ya makundi mawili-kutokana na malumbano ya vidato vya chini na vidato vya juu, binafsi aliathirika kwa kiasi kikubwa: ''Vurugu zilikuwa ni kati vidato vya juu yaani cha tano na cha sita ambao walikuwa wanataka wanafunzi wa vidato vya kwanza, cha pili hadi cha nne, ni lazima tuwaheshimu na kuwafanyia kazi zao ...Kidato cha nne kikaingilia kati na kusema hilo halitawezekana ndio kukatokea malumbano na vurugu''. Alikumbuka Mlang'a katika mahojiano na BBC. Anasema: ''Zilikuwa ni wiki mbili kabla tuanze mitihani ya Moko iliniuma sana...kutokana na vurugu tukaambiwa tutoke shuleni mara moja ...Tukaambiwa tumepangiwa kwenda shule nyingine, yaani ilikuwa ni kututawanya...sijui shule gani! , Nilikuwa Nyamongo nikahamishiwa kiboriloni, kwa hiyo hatukuwa na muda wa maandalizi ya mtihani wa Moko. Kuhamia shule nyingine kuizowea na kuzowea masomo iliniathiri sana...hili lilinitoa kabisa katika mawazo ya masomo'', anasema Mlang'a na kuongeza kuwa vurugu hizo zilichangia kuathiri ufaulu wa masomo yake. Matukio haya ya uonevu na mateso dhidi ya wanafunzi wanaosoma katiks shule za mara nyingine huwa ya kutisha. Mfano nchini Kenya kisa cha mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15- aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya 'Nairobi School' aliyedaiwa kushambuliwa kikatili kiasi cha kuuharibu ubongo wake, jambo lililoibua hisia kali miongoni mwa Wakenya. Taarifa hiyo iliyotangazwa kwa mara ya kwanza na televisheni ya kibinafsi nchini Kenya, iliashiria ukubwa tatizo hili katika shule za umma nchini humo. Mara nyingi wanafunzi waonevu huwalenga wenzao wanaowaona kuwa dhaifu kwao , wapole, na wanaokaa peke yao Sababu ya uonevu wa ukatili shuleni ni zipi? Kulingana na Mwanasaikolojia wa watoto waliofikia umri wa barehe, Perpetual Wanyugi, mtoto anayewafanyia uonevu ima ukatili wenzake kwanza kabisa binafsi huwa anajiona kama mtu ambaye hafai, na kutekeleza uonevu ili kujiaona kama anayefaa:'' Mtoto wa aina hii huwa kwanza anajidharau na hufanya hivyo kutokana na kwamba huenda yeye pia amedhalilishwa, kupigwa au kufanyiwa ukatili wa aina fulani ambao unamfanya ajidharau , anaona kwa kufanya hivyo basi hata yeye anatambulika'', amefafanua Bi Wanyugi katika mazungumzo na BBC. Mara nyingi mtu humshambulia mtu ambaye anaona ni dhaifu kwake kumshinda ,na watoto kama hawa huwalenga watoto ambao ni wapole, wanaokaa peke yao na ambao hawawezi kuripoti kwa waalimu au kwa wazazi wanaofikiri kuwa wakiwaambia waalimu basi watauliwa, anasema Bi Wanyugi. Kwa ujumla watoto walioathiriwa na uonevu wanahitaji ushauri wa wazazi na walezi , ambao kwanza itawabidi waelewe ni nini chanzo cha wao kuwa na tabia ya uonevu wa ukatili kwa wenzao. Na iwapo hali itakuwa mbaya zaidi mtoto wa aina hiyo anahitaji matibabu ya kisaikolojia, anashauri Wanyugi. Uonevu una athari mbaya: Uonevu huathiri watoto wa shule na hivyo kushindwa kuwa makini wawapo darasani na baadae katika maisha yao Mwanasaikolojia Perpetual Wanyugi anashauri iwapo mtoto wa shule atabainika kuwa na uonevu wa ukatili unaorudia rudia anahitaji kufundishwa nidhamu, apewe msaada wa nidhamu ya wazazi na hata majirani na pale inapozidi atafutiwe msaada wa kisaikoloji Wakati wazazi wanapowapeleka watoto wao katika shule za sekondari za bweni ,wengi wao kama si wote, huwa wanategemea kuwa maisha yao yatakuwa mema, salama na watatunzwa vema, lakini haiwi hivyo kwa baadhi. text: Alikamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini. Wine alikamatwa upya na kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa. Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda. Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala. Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru. Wengi nchini Uganda wanatazama kesi hii kama jitihada za kumnyamazisha mkosoaji mkuu wa serikali aliyechaguliwa kuwa mbunge mwaka jana tu. Mawakili wa jeshi wameeleza mahakama kuwa mashtaka dhidi ya Wine yameondolewa na kwamba mwanasiasa huyo akabidhiwe kwa polisi ili akabiliwe na mashtaka ya uhaini pamoja na na wabunge wengine waliokamatwa . Wakili wake Wine Medard Segona ameiambia mahakama kwamba licha ya kuwa wameridhishwa na hatua ya mahakama ya kijeshi , anapinga hatua ya sasa ya mteja wake kuhamishwa katika mahakama ya kiraia kukabiliwa na mashtaka mapya. Alitaka mbunge huyo aachiwe huru ili aweze kupelekwa kupokea matibabu. Mahakama iliamua kuwa Bobi Wine yu huru, iwapo hakuna mashtaka mengine yatakayowasilishwa dhidi yake. Mambo matano tunaweza kujifunza kutoka kwa sokwe kuhusu siasa Jeshi Uganda laomba radhi baada ya waandishi kupigwa Wakati huo Wine alionekana akilia na kupangusa machozi huku hukumu hiyo ikisomwa. Alitoka nje ya mahakama akiwa anatemba kwa magongo na kuonekana kuwa na maumivu makali. Nchini Kenya raia walimiminika katika mji mkuu wa Nairobi leo kushinikiza kuachiwa kwa Bobi Wine Hapo ndipo alipokamatwa upya. Shinikizo kubwa kutaka Wine aachiwe Jitihada za kumshtaki Bobi Wine mbele ya mahakama ya kijeshi zimekabiliwa na shutumA kubwa kimataifa na hata miongoni mwa makundi ya kutetea haki za binaadamu. Nchini Kenya raia walimiminika katika mji mkuu wa Nairobi leo kushinikiza kuachiwa kwa mbunge huyo wa upinzani Uganda. Mjini Kampala Polisi imemkata kiongozi mkuu wa upinzani Kizza Besigye. Besigye amakamatwa mara kwa mara katika jitihada za maafisa wa utawala kuzuia maandamano ya kuipinga serikali kufanyika. Kizza Besigye: Upinzani Afrika usishurutishwe kukubali matokeo kwa kusingizia utulivu Besigye alikamtwa mapema leo alipojaribu kuondoka nyumbani kwake Kasangati; na inaarafiwa amefikishwa katika kituo cha polisi cha Naggalama Uganda. Awali polisi walizingira makaazi yake. Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa. Trump; sihusiki na makosa ya Cohen Mzozo wa kidiplomasia waibuka kati ya China, Taiwan na Swaziland Waraka huo umeanzishwa na Rikki stain aliekua msimamizi wa zamani wa mawamuziki fella kuti ambae alikua mkosoaji mkubwa wa serikali ya Nigeria Anasema kuwa likua akipigwa hata kwa kuzungumza. Zaidi ya watu 80 akiwemo mwandishi mkongwe whole soyinka na wanamuziki wa kundi la U2 bassist Adam Clayton, muambiaji kiongozi Chrissie Hynde na Genesis Peter Gabriel. Zaidi ya wasanii 80 wanataka Bobi wine aachiwe Huru akiwemo Chris Martin (kustoto), Angelique Kidjo (katikati) na Damon Albarn (kulia) Bobi Wine ni nani? Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili. Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati. Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC). Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia. "Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki...Ninataka siasa zitulete pamoja... jinsi muziki ufanyavyo." Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ameshtakiwa kwa uhaini nchini. text: Mchoro wa Yesu Salvator Mundi au (Mkombozi wa Dunia) umeuzwa dola milioni 450 Marekani Mchoro huo unajulikana kama Salvator Mundi (Mkombozi wa Dunia). Ndio mchoro wa bei ya juu zaidi kuwai kuuzwa kwa mnada. Leonardo da Vinci alifarika mwaka 1519 na kuna chini ya 20 ya michoro yake iliyobaki. Ni huo mmoja tu unaoaminiwa kuwa mikononi mwa mtu ambao unaamimiwa kuwa ulichorwa baada ya mwaka 1505. Mchoro huo uliuzwa kwenye mnada Picha hiyo inamuonyesh Yesu akiwa ameunua mkono mmoja huku mwingine ukishika kioo. Mwaka 1958 mchoro huo uliuzwa kwenye soko la mnada mjini London kwa Dola 60. Wakati huo mchoro huo uliaminiwa kuwa kazi ya mfuasi wa Leonardo na wala haukuwa wa Leonardo mwenyewe. Miaka minne iliyopita mchoro huo ulinunuliwa na raia wa Urusi kwa dola milion 127.5 lakini wakati huo hakuuzwa katika mnada. Mchoro wa miaka 500 wa Yesu unaoaminiwa kuchorwa na Leonardo da Vinci, umeuzwa mjini New York kwa kima cha dola milioni 450. text: Muimbaji huyo anasema kuwa kwa mara ya kwanza hakuelewa ni kwanini baadhi ya watu waliyaona maneno ya mistari ya nyimbo zake kama "uchochezi wa ubakaji". Lakini baadae alibaini kwamba "kuna wanaume wanaotumia lugha inayofanana na hiyo kuwadhalilisha kingono wanawake ". Wimbo huo unaojulikana kama Blurred Lines (Mistari iliyofichwa) katika nyimbo zake ilikosolewa na baadhi ya watu ambao walidai kuwa maneno hayo yalichochea ngono bila muafaka. Nyimbo hizo zilipigwa marufuku katika vyuo vikuu kadhaa na tangazo la biashara lililokuwa na wimbo na walioigiza katika video yake kupigwa marufuku kuchezwa katika vipindi vya mchana vya televisheni mwaka 2013. Pharrell alishirikiana na Robin Thicke katika mistari ya wimbo iliyofichwa uliotolewa mnamo mwaka 2013 Katika mahojiano na jarida la GQ, Pharrell, mwenye umri wa miaka 46, alisema kuwa alizaliwa ''katika enzi tofauti " na baadhi ya mambo mengine ambayo yaliokuwa yanaruhusiwa wakati huo "hayawezi'' kufanyika wakati huu. Alitoa mfano wa matangazo ya kibiashara "yaliomuonesha mwanamke kama chombo" na "maudhui ya nyimbo ". "Baadhi ya nyimbo zangu za zamani, siwezi kamwe kuziandika au kuziimba leo hii''. "Ninaaibishwa na baadhi ya nyimbo hizo. Ilinichukua muda mrefu na kukua ili kufikia mahali pale." Alisema kuwa mistari iliyofichwa ilimsaidia kupanda kimuziki lakini akakiri kuwa mwanzo "hakuelewa"ni kwanini nyimbo hizo zilipingwa kiasi kile na baadhi. Wimbo - ambao aliuimba kwa ushirikiano na Robin Thicke -ulijumuisha mistari kama vile "Ninachukia sana mistari hii iliyofunikwa, ninajua mnaitaka " na " Lazima ninataka kuwa mbaya". Mlimbwende Emily Ratajkowski alipata na kuwa nyota baada ya kuonekana kwenye video ya Blurred Lines Muimbaji huyo alisema kuwa aliwaona baadhi ya wanawake waliupenda wimbo huo na wangeweza kuimba maneno hayo wakati wowote "Na kisha nikagundua kuwa kuna wanaume ambao hutumia lugha hiyo hiyo kuwadhalilisha wanawake, na haijalishi hiyo sio tabia yangu. Au jinsi ninavyofikiria mambo. "Ni muhimu kuelewa jinsi inavyowaathir wanawake. Na nikasema sasa nimeelewa Ni vizuri " Aliongeza kuwa "Niligundua kwamba tunaishi katika nchi ambayo ina wabaguzi . Sikuwa nimegundua hilo . Sikutambua kwamba baadhi ya nyimbo zangu zilikuwa na mwelekeo huo ." Wimbo wake ulikuwa namba moja kwenye chati za muziki za Uingereza kwa wiki kadhaa na awali Pharrell aliitetea mistari ya nyimbo hizo. Katika mahojiano na Pitchfork alisema "Unapomuangalia vizuri katika wimbo mzima, ujumbe ni kwamba ni msichana mzuri, na hata wasichana wazuri wanataka kufanya mambo na hapo ndipo mistari inafichwa. "Anaponesha hisia zake katika mtindo wake wa densi kwasababu ni msichana mzuri. Watu wanakasirika tu wanataka tu kuwa wendawazimu na ninayakubali maoni" Pharrell na Robin Thicke pia wamekuwa na matatizo mengine kuhusu nyimbo hizo. Waliambiwa walipe faini ya dola milioni 5 baada ya familia ya Marvin Gaye' kudai kuwa wimbo huo ni nakili ya wimbo wa gaye wa mwaka 1977 uliojukana kama Got to Give It Up. Pharrell Williams anasema kuwa utata uliozingira maneno ya mistari ya nyimbo zake ulimfanya abaini kuwa baadhi ya nyimbo zake "ziliendeleza" utamaduni wa ubaguzi wa kijinsia. text: Mkurugenzi wa FBI James Comey atazungumzia tuhuma za uhusiano kati ya Urusi na maafisa wa kampeni wa Trump Pia, watatoa ushahidi kuhusu tuhuma kwamba kulikuwa na ushirikiano na mawasiliano kati ya Urusi na maafisa wa kampeni wa Rais Donald Trump. Kadhalika, wataangazia tuhuma zilizotolewa na Bw Trump kwamba simu zake zilidukuliwa na mtangulizi wake Barack Obama. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la FBI James Comey na mkuu wa Idara ya Taifa ya Usalama Mike Rogers watatoa ushahidi katika kikao nadra sana cha wazi cha kamati ya bunge kuhusu ujasusi. Bw Trump ametaja uchunguzi huo kuwa usio wa haki. Urusi imekanusha tuhuma kwamba lijaribu kuingilia uchaguzi wa urais Marekani. Madai yaliyotolewa Januari, mashirika ya ujasusi ya Marekani ,yalisema kuwa wadukuzi waliosaidiwa na Urusi, walidukua akaunti za barua pepe za maafisa wa vyeo vya juu wa chama cha Democrat na kufichua taarifa za aibu, ili kumsaidia bwana Trump kumshinda Hillary Clinton. Ripoti ya mashirika ya CIA,FBI na NSA ilisema kuwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin, aliamrisha kufanywa kampeni ya kushawishi uchaguzi huo. Tangu wakati huo Trump amekumbwa na lawama kuwa timu yake ya kampeni ilikuwa na ushirikiano na maafisa wa Urusi. Davin Nunes(kulia) mwenyekiti wa kamati ya ujususi pamoja na afisa wa Democrat Adam Schiff, Afisa wa Republican Davin Nunes, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ujasusi pamoja na afisa wa Democrat Adam Schiff, wanaongoza uchunguzi wa madai hayo. Bwana Nunes siku ya Jumapili, alisema kuwa hajaona ushahidi wowote unaoonyesha kuwa Urusi iliingilia kampeni ya Trump. Naye mkurugenzi wa zamani wa idara ya kitaifa ya ujasusi James Clapper, naye amesema kuwa hakuna ushahidi wowote kuonyesha kuwa Urusi ilihusika. Wakuu wa mashirika mawili makuu ya ujasusi Marekani wanatarajiwa kutoa ushahidi kwa kamati za Bunge la Congress kuhusu madai kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani mwaka jana. text: Watafiti kwa kutumia mfumo wa vinasaba wa papa hao wamebaini pingili ambazo zinawalinda samaki hao dhidi ya saratani na magonjwa mengine. Wanasayansi wanaamini kuwa utafiti zaidi unaweza kusaidia kutimia matokeo hayo katika kutibu magonjwa yatokanayo na umri mkubwa kwa binaadamu. Aina hiyo ya papa wanaweza kujitibu vinasaba vyao katika namna ambayo haiwezekani kwa vinasaba vya binadamu. Utafiti huo umefanyika katika chuo kikuu cha Nova Southeastern Florida, Marekani. Jeni, au sehemu ya vinasaba inayorithisha tabia au maumbile fulani, ambazo si thabiti za binaadamu ndizo ambazo hufanya watu kupata maradhi ya saratani na mengine ambayo huendana na uzee. Papa hao wapo baharini kwa zaidi ya miaka milioni 16 sasa, dahari na dahari kabla ya uwepo wa binadamu, na hufikia mpaka urefu wa futi 20 na ukubwa wa uzito wa tani tatu. Vinasaba vya papa ni vikubwa kwa mara moja unusu zaidi ya binadamu, hiyo ina maana kuwa kuna vitu samaki hao wanaweza kuvifanya ambayo binadamu hawawezi. Na wanasayansi sasa wanatazamia kufumua siri hizo ili kutatua maradhi hayo kwa binadamu. Pia papa hao wanatazamiwa kusaidia matibabu ya kuzuia damu kuvuja sababu wana uwezo mkubwa wa kupona majeraha hatari. Utafiti huu sasa utaongeza umaarufu wa samaki hao ambao ni moja ya wanyama wanaoogopwa zaidi kutokana na meno yao makubwa na makali. Mpiga picha Kimberly Jeffries hivi karibuni ameiambia BBC kuwa hakujihisi kuwa kwenye hatari alipoogelea na moja ya papa mkubwa zaidi wa jamii hiyo afahamikaye kama Deep Blue. "Ni fursa adimu..." amesema bi Kimberley na kuonya watu hata hivyo kutowakaribia wanyama hao. "Hawa ni wawindaji wenye nguvu, hivyo inabidi waheshimiwe." Papa hao huwinda jamii nyengine za samaki hususani wale ambao ni walegevu. Tafiti pia zinaonesha kuwa papa ni muhimu kwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa viumbe wanaowawinda zaidi ni wale ambao huchafua zaidi hewa baharini. Papa aina ya 'great white' inawezekana wakawa wanashikilia siri za kutibu saratani na maradhi mengine yanayoambatana za uzee. text: Moshi mkubwa ukifoka kutoka kwenye ghala la tume ya uchaguzi DRC mapema mwezi huu, mashaka yaeemendelea kutanda iwapo uchaguzi wa Congo utafanyika kwa haki Kura hiyo ambayo ilitakiwa kupigwa Disemba 23 mwaka huu iliahirishwa kwa wiki moja mpaka Disemba 30, yaani Jumapili ijayo. Hata hivyo uchaguzi huo tayari umeshacheleweshwa kwa miaka miwili sasa, huku wapinzani na wanaharakati wakimlaumu rais amalizaye muda wake Joseph Kabila kwa kutafuta visingizio kusalia madarakani. Mgombea wa chama tawala Ramazani Shadary ni mshirika mkubwa wa Kabila na inatarajiwa ataendelea kulinda maslahi ya Kabila akiingia madarakani. Maeneo hayo matatu ambayo yanaonekana kuwa ni ngome za upinzani ni Beni na Butembo kwa upande wa mashariki ambayo yamekuwa yakipambana na milipuko ya ugonjwa hatari wa Ebol toka mwezi Agosti mwaka huu. Eneo la tatu ni Yumbi lilopo magharibi mwa nchi ambapo watu zaidi ya 100 wameuawa wiki iliyopita katika makabiliano ya kikabila. Shughuli za uchaguzi katika sehemu nyengine zote zilizobaki za nchi hiyo kubwa zitaendelea kama ilivyopangwa siku ya jumapili. Matokeo ya uchaguzi wa maeneo hayo matatu hayataathiri mbio za urais kwa sababu mshindi atatangazwa Januari 15 na kuapishwa Januari 18. Katika taarifa yake, tume ya uchaguzi (CENI) imesema hatua hiyo inatokana na kusambaa kwa Ebola katika maeneo ya Beni na Butembo pamoja na kudorora kwa amani katika maeneo hayo. Mikutano yote ya Kampeni imepigwa marufuku jijini Kinshasa saa chache kabla mgombea wa upinzani Martin Fayulu kuhutubia wafuasi wake. Katazo hilo la wiki iliyopita bado halijaondolewa. Tayari hatua hiyo imeshaibua upinzani mkali nchini Congo. Mapema leo kabla ya kutangazwa rasmi kwa uamuzi huo, mgombea kinara wa upinzani Martin Fyulu alionya kuhusu hilo kupitia mtandao wake wa tweeter. "Kisingizio cha Ebola ni cha uongo sababu kampeni zimefanyika katika maeneo hayo. Hiui ni mbinu nyengine ya kuteka nyara ukweli wa kura," ameandika Fayulu. Maaskofu wa Kanisa Katoliki ambao wamekuwa mstari wa mbele kupambana ili uchaguzi ufanyike wanatarajiwa kukutana ili kutoa tamko la pamoja kutokana na hatua hiyo mpya. "Kuahirisha uchaguzi eneo hilo haiwezi eleweka wakati walikubali kampeni ifanyike licha ya uwepo wa Ebola. Mimi binafsi kama raia nawaza kuwa kuna kitu wanaficha. Tunasubiri kwanza sisi Maaskofu tukutane (kabla ya kutoa taarifa rasmi)," amesema Donatien Shole, Katibu Mkuu wa Kanisa Katoliki DRC. CENI kikaangoni Mashine hizi za kupigia kura zimekuwa vikipingwa na upinzani Wakati huo huo wagombea saba wa urais kutoka upinzani nchini DRC wameituhumu tume ya huru ya uchaguzi nchini humo kuwa na njama kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu ujao. Wagombea hao wametoa tuhuma kadha ikiwemo matumizi ya mashine za kielektroniki jambo ambalo wanasema ni kinyume cha sheria. Pili ni kuweko na taarifa za kuongeza kwa orodha ya wapiga kura kwenye daftari la wapiga kura. Katika tamko lao ambalo limetiwa saini na wote saba pia wagombea hao wanawataka waangalizi wa kimataifa kutenda haki na kuamua kwa maslahi mapana ya Raia wa DRC. "...Raia wa DRC wataenda kupiga kura kwa lengo la kuadhibu wale waliokuwa madarakani. Tunapenda mambo yawe wazi na hatutaki siku watakayotangaza matokeo watangaze kile ambacho si matarajio ya Wacongo," amesema Marie Ifoku ambaye ni mgombea pekee mwanamke katika kinyang'anyiro hicho. Mustakabali wa uchaguzi nchini Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) wazidi kuingia dosari baada ya tume ya uchaguzi leo Disemba 26 kutangaza kuahirishwa upigwaji kura katika mikoa mitatu mpaka mwezi machi 2019. text: Aliambia bunge siku ya Jumatatu kwamba mataifa mengine manne ya Afrika tayari yemahalalisha Marijuana kutumiwa kutengeneza dawa. Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania mbunge huyo anasema kuwa ni vyema kama taifa kuanza kufikiria kuhusu fursa hiyo mapema. ''Tunavyozungumza, Uganda imehalalaisha upanzi wa Marijuana kwa matumizi ya dawa'', alisema akitaja ripoti za hivi majuzi kwamba taifa hilo la Afrika mashariki limenunua mbegu kupanda mmea huo. ''Sijui ni kwa nini kitengo cha chakula na dawa hakijachukua sampuli kuelezea serikali kwamba dawa hizo zina bangi ndani yake'', alihoji. Kulingana na gazeti hilo ,bangi kama inavyojulikana ni haramu nchini Tanzania na inavutia hukumu kali jela na faini kubwa. ''Tuna bangi lakini kile kinachoonekana kila siku ni maafisa wa usalama kuharibu mmea huo. Bangi imetumika kwa miaka kadhaa kutengeneza dawa''. Bangi hutumika kutengeneza dawa Alisema kwamba Lesotho na Zimbabwe zilihalalisha utumizi wake akiongezea kwamba amewahi kuona kiwanda kinachotengeneza dawa kwa kutumia bangi. Aliongezea kuwa gunia moja la bangi linauzwa kati ya Sh4 million na Sh4.5 millioni huku likiuzwa Sh20 millioni nchini Zimbabwe na Lesotho. WebMD, Mtandao unaotoa habari za kiafya unasema kuwa ushahidi mkubwa kuhusu mmea wa bangi ni uwezo wake wa kupunguza maumivu, kichefuchefu na kutapika baada ya mgonjwa kupatiwa tiba ya kutumia kemikali {chemotherapy}. Kulingana na The Citizen Tanzania Uganda inatarajiwa kuuza bangi inayotumika kama dawa yenye thamani ya Shilingi bilioni 600 billion mwezi Juni kwa taifa la Canada na Ujerumani ikilinukuu gazeti la The Daily Monitor nchini Uganda. Imani ya Rastafari Imebainika kwamba mnamo tarehe 7 mwezi Disemba Uganda iliuza bangi, na mauwa yenye thamani ya $10,000 kwa kampuni moja ya Afrika kusini. Muungano wa Rastafari nchini Tanzania ni mojawapo wa mashirika ambayo yanashinikiza wazo la kuhalalishwa kwa bangi katika taifa hilo. Rasta wanaamini kwamba mmea wa 'Tree of Life' uliotajwa katika bibilia ni ule wa bangi. Mbali na imani za wengi , Rasta hushutumu matumizi ya marijuana kwa lengo la ulevi. Wale wanaounga mkono wazo la mmea huo kuhalalishwa nchini Tanzania ni pamoja na mbunge wa Geita mashambani muheshimiwa Joseph Msukuma. Katika kikao cha bunge Msukuma alisema kuwa hajawahi kusikia ama kuona utafiti wowote wa kisayansi uliopata bangi na miraa kuwa na tatizo lolote. Alisema kuwa hatua ya serikali kuharamisha mimea hiyo haina msingi wowote. Msimamo wa Serikali Hatahivyo serikali ya Tanzania imepinga uwezekano wowote wa kuhalalishwa kwa mmea huo katika taifa hilo. Mnamo mwezi Februari 2016, naibu waziri wa afya Dkt. Hamis Kigwangalla alipinga kuhalalishwa kwa bangi na miraa ahihusisha utumizi wake na matatizo ya kiakili . ''Tafiti kadhaa zimethibitisha kwamba matumizi ya marijuana yanasababisha matatizo ya kiakili na hivyobasi serikali haiwezi kuhalalisha matumizi yake'', alisisitiza Kigwangalla. Lakini mwenyekiti wa Rastafari United Front Thau-Thau Haramamba anasema kuwa matatizo ya kiakili yanayowakabili watumizi wa bangi hayatokani na matumizi ya bangi badala yake uchanganyaji wa bangi na vitu vileo vingine. Anahoji kwamba hakuna utafiti umewahi kupata matumizi ya mmea huo kushirikishwa na tatizo la Kiakili. Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba anataka serikali kuhalalisha matumizi ya bangi ama marijuana nchini tanzania kwa mautumizi ya dawa. text: Inaarifiwa kwamba City na Arsenal walikuwa wamefikia makubaliano, kwa masharti hata hivyo, kuhusu kuhama kwa Sanchez, 28, hadi Etihad. Ada ya uhamisho wake ilikuwa £55m, na vikolezo vya £5m, lakini ilitegemea kufanikiwa kwa Arsenal kumpata mchezaji wa kujaza nafasi yake. Mchezaji waliyemtaka zaidi alikuwa winga wa Monaco Thomas Lemar ambayo inadaiwa alikataa kuhamia Arsenal. Monaco walikuwa wamekubaliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa Lemar, 21, ambaye huchezea timu ya taifa ya Ufaransa kwa £90m. Sanchez alitaka kujiunga na City ambapo angeunganishwa tena na meneja wake wa zamani alipokuwa Barcelona Pep Guardiola. Mchezaji huyo wa Chile anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na kuna uwezekano mkubwa kwamba ataondoka majira yajayo ya joto bila kulipwa ada yoyote. Mchezaji aliyendoka Emirates siku ya mwisho ni mshambuliaji Lucas Perez, ambaye alijiunga nao msimu uliopita kwa £17.1m. Perez alirejea klabu yake ya awali Deportivo La Coruna kwa mkopo baada ya kufunga mabao saba katika mechi 21 alizowachezea Gunners. Uchanganuzi Kiungo wa kati wa Stoke Charlie Adam akizungumza na BBC Radio 5: Arsenal wanamhitaji Alexis Sanchez zaidi ya wanavyohitaji £60m. Bila yeye, hawana nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Baada ya kumalizika kwa kipindi cha kuhama wachezaji, atatulia na kujitolea tena kwa msimu mwingine. Kiungo wa kati wa zamani wa Aston Villa, Chelsea naJamhuri ya Ireland Andy Townsend: Arsenal wamo taabani. Ningemwacha Sanchez aende. Ishara alizoonyesha baada ya Arsenal kushindwa 4-0 na Liverpool hazikuwa nzuri. Amechoka na fikira zake ziko kwingine. Sidhani atayasahau yote na kurejea haraka kuwachezea kama kawaida. Mwanachama wa bodi ya mashabiki, Arsenal Supporters' Trust Akhil Vyas: Naomba arudi kuangazia tena timu na kujitolea kabisa, jambo ambalo hufanya akiwa uwanjani, kwa msimu huu angalau. Dirisha la kuhama wachezaji limefungwa kwa masikitiko, iwapo hatumnunui mchezaji mwingine, basi ilikuwa lazima tusalie na Alexis. Sanchez aliwachezea Arsenal mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili Kuhama kutoka Barca Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili. Sanchez alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban £35m na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita. Mapema mwezi huu meneja wa Arsenal Arsene Wenger alisema Sanchez anataheshimu uamuzi wake wa kutaka kusalia naye mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake. Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na England Danny Murphy amesema Arsenal hawawezi kuthubutu kumwachilia. "Wakimwacha aende watakuwa katika matatizo chungu nzima. Bado wako kwenye matatizo makubwa kwa kiasi fulani tayari. "Alifanya kazi kwa bidii sana (mechi dhdii ya Liverpool) lakini mechi ilipoanza kuwalemea Arsenal, ungemuona alionekana kukata tamaa. Awali, Arsenal walikuwa wamekataa majaribio yoyote ya kutaka kumchukua Sanchez kufikia na iliaminika kwamba wangefurahia sana iwapo Raheem Sterling angekuwa kwenye sehemu ya mkataba wake wa kuhamia City. Meneja wa City Pep Guardiola hata hivyo alitaka kumnunua Sanchez, 28, moja kwa moja. Hata hivyo, hatua ya kumnunua ingewezaweza kutilia shaka mustakabali wa Raheem Sterling katika City. Sterling, 22, anayechezea timu ya taifa ya England amechezea City mechi zao zote tatu za kwanza ligini msimu huu. Lakini hangehakikishiwa nafasi ya kuanza mechi Etihad hasa baada ya kuwasili kwa Bernardo Silva kutoka Monaco. BBC ilikuwa imefahamu kwamba Sterling anaweza kufurahia kwenda Arsenal na kurejea jijini London iwapo angekuwa kwenye sehemu ya mkataba wa kumchukua Sanchez. Juhudi za klabu ya Manchester City kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez ziligonga mwamba siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji baada ya Gunners kukosa mchezaji wa kujaza nafasi yake. text: Bi Mghwira aliwania urais mwaka 2015 kupitia chama cha ACT Wazalendo Bi Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye aliacha kazi. Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Bibi Anna Elisha Mghwira kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa Kilimanjaro bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa, dini, makabila na kanda wanazotoka. Alisema anaamini mwanasiasa huyo ana uwezo wa kutekeleza majukumu yanayoambatana na kazi hiyo. "Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi," amesema Dkt Magufuli, baada ya kumuapisha katika Ikulu jijini Dar es Salaam. Bi Mghwira amemshukuru Rais kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa. "Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong'ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo" amesema Bi Mghwira. Bi Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015. Amekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, chama kichanga zaidi Tanzania kilichoundwa 2014. Mghwira, 56, anatoka mkoa wa Singida. Babake alikuwa diwani na kiongozi chama cha Tanu na baadaye CCM. Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemuapisha aliyekuwa mgombea urais mwaka 2015 Bi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kusema anaweza kuitekeleza kazi hiyo. text: Mchezaji anayelengwa kusajiliwa na Arsenal katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari Malcom anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu katika klabu ya Bordeaux. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alionyeshwa katika mitandao ya kijamii akicheka na kufanya utani pamoja na wachezaji wenza Cafu na Otavio baada ya timu yao kushindwa na klabu ya Caen siku ya Jumanne. Bordeaux waliomsajili mchezaji huyo wa Brazil kutoka Corinthians 2016 ilisema kuwa wachezaji hao walionyesha ukosefu wa ukomavu, umoja na heshima kwa taasisi hiyo. Klabu hiyo ilisema kuwa inashutumu vikali kanda ya video na kwamba mashtaka ya kuwachukulia adhabu yataanzishwa. Malcolm amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal kutoka Bordeaux ambapo amefunga magoli 18 katika mechi 80. Hatahivyo makubaliano yoyote yataafikiwa iwapo mshambuliaji wa Gunners Theo Walcot atajiunga na Everton. Arsenal pia inamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang na haiwezekani kwamba watawasajili wachezaji wote watatu. Mchezaji anayelengwa kusajiliwa na Arsenal katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari Malcom anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu katika klabu ya Bordeaux. text: Vikosi vya zimamoto katika harakati za kuzima moto uliotokana na mashambulizi ya ndege ya alfajiri ya leo. Mashambulizi ya alfajiri ya Jumatatu ni makubwa zaidi tangu mapambano yaanze wiki moja iliyopita. Israeli inasema imeshambulia majengo yanayomilikiwa na wanamgambo wa Hamas pamoja na nyumba kadhaa za makamanda wa kundi hilo, hata hivyo barabara kuu kadhaa na nyaya za umeme pia zimeharibiwa. Mashambulio hayo yanatokea wakati jumuiya ya kimataifa ikitaka pande zote mbili katika mgogoro huo kusitisha mashambulizi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilifanya mkutano wa dharura jana Jumapili na Katibu Mkuu wa UN António Guterres ameonya kuwa mapambano zaidi "yanaweza kusababisha hali mbaya ya kiusalama na kibinaadamu." Guterres pia ametaka mapambano hayo "mabaya" yasitishe haraka iwezekanavyo. Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameeleza leo Jumatatu kuwa nchi yake "imepiga hatua kubwa katika kutafuta kusitishwa kwa mapambano...na matumaini bado yapo." Lakini mpaka sasa hakuna dalili za hilo kutokea huku mapambano makali yakiingia wiki ya pili. Ghasia hizo ni zao la wiki za hamaki na wasiwasi baina ya Israeli na Palestina katika eneo la Jerusalemu Mashariki ambapo hali hiyo iliishia katika mapambano katika eneo takatifu kwa Waislamu na Wayahudi. Kundi la Hamas, ambalo linaongoza Ukanda wa Gaza, likaanza kurusha makombora ya roketi baada ya kuionya Israeli iondoke katika eneo hilo la Jerusalemu, na hapo ndipo Israeli ilipoanza kufanya mashambulizi ya anga ya kulipiza. Jeshi la Israeli linasema zaidi ya ndege 50 za kivita zimefanya mashambulizi ya dakika 20 muda mfupi kabla ya alfajiri ya leo. Ndege vita hizo zimepiga na kuteketeza "maeneo ya kigaidi" 35 na kuharibu zaidi ya kilomita 15 za mfumo wa mahandaki yanayomilikiwa na Hamas, linadai jeshi la Israeli. Jeshi hilo pia linadai kuwa limezipiga nyumba tisa za makamanda "wa ngazi ya juu" wa Hamas. Hata hivyo hakujakuwa na idadi rasmi kufikia sasa ya watu waliofariki na kueruhiwa, lakini mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Gaza zinasema kuwa mashambulizi hayo yamesababisha umeme kukatika katika maeneo mengi na kuharibu mamia ya nyumbana majengo mengine. "Hakujawahi kuwa na mashambulizi ya ukubwa huu," mkaazi mmoja wa Gaza ameliambia shirika la habari la kimataifa la AFP . Mad Abed Rabbo, 39, amesema alihisi "woga mkubwa na kutishika" wakati mashambulio hayo yakiendelea. "Nilikuwa najiandaa kufariki dunia. Ilibidi nikubaliane na hali hiyo," Najla Shawa, mtoa misaada ya kibinaadamu na mama wa watoto wawili ameiambia BBC. Mkaazi mwengine wa Gaza, Sarah Mahmoud, ameiambia BBC: "Bado tungali hai, lakini hatupo salama. Ndege zimeharibu barabara nzuri zaidi ya Gaza." Kabla ya mashambulizi ya alfajiri ya leo, maafisa wa Palestina walitangaza kuwa mashambulio ya jana Jumapili yaliyosababisha vifo vya watu 40 ndiyo yalikuwa mabaya zaidi. Kuufikia sasa idadi ya waliofariki katika Ukanda wa Gaza imefikia 200, ikiwemo watoto 59 na wanawake 35 huku waliojeruhiwa ni 1,305, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Hamas. Israeli inasema wapiganaji 130 wa Hamas ni miongoni mwa waliouawa. Israeli imefanya mashambulizi kadhaa alfajiri ya leo katika Ukanda wa Gaza, baada ya wanamgambo wa Palestina kurusha makombora ya roketi katika miji iliyopo kusini mwa Israeli. text: Fionn, Luna na Roby wakiwa kituoni wamiliki wao walipoenda kupiga kura Cumbria Na punde si punde, watu walianza kugundua kwamba wanyama hao walikuwa wengi sana ajabu, na kitambulisha mada cha #DogsAtPollingstations (Mbwa vituo vya kupigia kura) kikaanza kuvuma mitandaoni. Kando na mbwa, kunao watoto, paka na hata nungunugu walionekana na kuvutia watu vituoni. Phoebe alisubiri nje ya kituo cha kura Manchester Wengi walipakia picha za mbwa wao mtandaoni Alhamisi asubuhi na katika kipindi cha saa mbili za kwanza baada ya vituo kufunguliwa, ujumbe 8000 kuhusu mbwa ulikuwa umepakiwa mtandaoni. Mtindo kama huo ulionekana katika uchaguzi wa mitaa mwezi uliopita, kura ya maoni kuhusu kujiondoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya na wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Mwaka huu, Twitter hata walitoa kibonzo cha mbwa akiwa amevalishwa bendera ya Uingereza. Twitter walishirikiana na wakfu wa The Dogs Trust kutetea kuwepo kwa mazingira bora ya mbwa kwenye vituo vya kupigia kura. Otto na Ava wavumilia kibaridi kikali asubuhi katika kituo cha kupigia kura Hampshire Max akiwa Tamworth, Staffordshire alionekana kutatizwa na upweke kiasi Si mbwa pekee waliofika vituoni kwa njia ya kipekee. Hapa mbwa Finlay & Ivy wanasubiri nje ya kituo cha polisi wakiwa na watoto wawili, Lexi wa miaka miwili na Owen wa mwaka mmoja katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Whinstone, Ingleby Barwick. Skye alihakikisha kwamba mpiga picha anapata picha yake nzuri eneo la Essex Lakini Hugo aliyekuwepo kituoni Nottingham alionekana kutatizwa na mwasho... There was an interruption when an unexpected guinea pig popped up. Nungubandia buyu kwa jina Sergeant Pepper, anayefahamika pia kama 'The Wig' alihakikisha nungubandia pia hawaachwi nje. Lakini mbwa bado walikuwa ndio wengi. Deli wa aina ya dachshund akiwa London magharibi alihakikisha anamwacha mmiliki wake apige kura kwa faragha Two-year-old Romanian rescue Marlowe wa asili ya Romania na mwenye miaka miwili alikuwa kituoni Canterbury, Kent Digby almaarufu Mr Woofs alifika Leicester kutekeleza majukumu yake mbele ya umma kwa kuwa nadhifu na 'mstaarabu' Mtazame hapa Bruce wa aina ya Dalmatian aliyesubiri mmiliki wake kwa hamu Derbyshire Ped mbwa wa aina ya Lurcher alionekana kuangazia zaidi kucheza na kujigaragaza juu ya nyasi Surrey. "Mbona mwaingia huko?" anaonekana kushangaa Mavis akiwa Bury, Lancashire Baadhi ya mbwa aina ya Pooch hawakuweza kufika vituoni, lakini wanaonekana kutotaka kuachwa nje: Wamiliki wa Sirius The Dog eneo la Knockbain, Scotland walipiga kura yao mapema kupitia posta. Lakini hawakutana kuachwa nje katika kusambaza picha za mbwa Kuliwepo hata hivyo na wanapaka, na kitambulisha mada ya #catsatpollingstations (paka vituoni) pia kilivuma kiasi. Paka hutu alionekana Clare Bowyer eneo la Colburn, North Yorkshire. Hakukuwepo na mbwa karibu. Hata nungunungu huyu kwa jina Friday alitaka kushiriki Hemel Hempstead. Nungunungu kwa jina Friday katika kituo cha kura Hemel Hempstead Na farasi je? Walikuwepo pia. Sunset Skye akiwa Sussex Magharibi Na mwisho kabisa kulikuwa na kondoo na mwanakondoo wake kituo cha kura cha Melness, Sutherland. Wapiga kura walipokuwa wanafika vituoni kupiga kura Uingereza, mbwa wa kila aina hawakuachwa nyuma. text: Nyuki wa jasho mara nyengine huwarukia watu ili kunywa jasho Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 , aliyejulikana kama bi He, alikuwa aking'oa mizizi wakati nyuki hao walipoingia katika macho yake. Daktari Hong Chi Ting wa chuo kikuu cha hospitali ya Fooyin aliambia BBC kwamba alishangazwa wakati alipowatoa wadudu hao kwenye macho. Bi He ametolewa hospitalini na anatarajiwa kupona kabisa. Nyuki wanaofuata jasho huvutiwa na jasho na mara nyengine huwarukia watu ili kunywa jasho. Pia hunywa machozi ili kujipatia protini kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha kansas kuhusu wadudu. 'Wote walikuwa hai' Bi He alikuwa akipalilia makuburi ya watu wa jamii yake wakati nyuki hao waliporuka na kuingia katika jicho lake la kushoto. Wakati upepo ulipompiga usoni mwake alidhani kwamba ni uchafu uliokuwa umeingia , aliambia maripota. Alikuwa akitembelea kaburi hilo kuadhimisha sherehe ya ufagiaji wa kaburi la Qing Ming ambayo huadhimishwa kwa kufagia makaburi ya watu unaowaependa. Lakini saa chache baadaye macho yake yalikuwa yamefura yakiwa na uchungu mwingi, swala lililomshinikiza kwenda hospitalini ili kupata matibabu kusini mwa Taiwan. ''Hakuweza kufunga jicho lake kabisa'' . ''Niliatazama kwa kutumia darubini na kuona kitu cheusi kilichofanana na mguu wa mdudu'', Daktari Hong ambaye ni profesa aliyesomea magonjwa ya macho katika hospitali hiyo aliambia BBC. ''Niliushika mguu huo na polepole nikamtoa nyuki mmoja , na baadye nikamuona mwengine , na mwengine na mwqengine. Wote walikuwa wazima''. Picha za nyuki hao zilionyeshwa katika runinga ya Taiwan. Dkt. Hong aliongezea kuwa nyuki hao huenda walipeperushwa ndani ya jicho lake na upepo uliochanganyika na vumbi na kusalia ndani ya jicho la mwanamke huyo. Nyuki hawa huwa hawashambulii binadaamu lakini wanapenda kunywa jasho, hivyobasi ndio wakapewa jina hilo, aliongezea. Dkt Hong aliongezea kwamba bi He alikuwa na bahati kwamba hakufuta macho yake wakati nyuki hao walipoingia ndani. ''Alikuwa akivaliia miwani inayoshikana na macho hivyobasi kuweza kuharibu miwani hiyo. Iwapo angejaribu kujikuna jicho angewafanya wadudu hao kutoa sumu , pengine angekuwa kipofu''. Nyuki hao bado ni wazima kwa sasa Dkt huyo anasema na watafanyiwa utafiti . Hii ni mara ya kwanza nchini Taiwan kitendo kama hicho kufanyika. Mwanamke mmoja nchini Taiwan alipatikana na nyuki wanne wa sukari waliokuwa wakiishi ndani ya jicho lake , kikiwa ni kisa cha kwanza katika kisiwa hicho. text: Kushikana mikono kumekuwa ni jambo gumu kulingana na tamaduni zetu ila kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa unaoendelea duniani kuna njia mbalimbali ambazo zinaelezewa na James Jaffrey. Ule utiifu wa kupeana mikono ulionekana kuwa kama njia rahisi ya kusalimiana kati ya watu wawili ambao hawafamianiani au kutofahamiana au ikawa ishara ya kuagana. Ila kushikana mikono inaweza kukubaliana katika mikataba mbalimbali yenye thamani ya mabillioni ya fedha Kati ya wafanyabiashara wakubwa duniani. Kuna mitazamo mbalimbali ambayo inaelezea chimbuko la kupeana mikono au kusalimiana kwa mikono ,chimbuko lake linasemekana kutokea Ugiriki miaka mingi iliyopita ambapo ilikuwa kama ishara ya kupeana amani kati ya watu wawili, ambapo inaonekana kama kila mmoja hajabeba silaha. Au pia kupeana mikono au kusalimiana kwa mikono kuna wezekana kuwa chimbuko lake limetokea Ulaya eneo la Medieval ambapo wapiganaji mashujaa walikuwa wakiwapa mikono wengine ili kuondoa silaha walizokuwa wamezificha kwa siri. Kwenye upande wa dini , miaka ya nyuma walikubali zaidi kushikana mikono kuliko kitendo cha kuinama. Pamoja na historia inaonesha miaka elfu moja nyuma iliyopita, kushikana mikono au kusalimiana kwa mikono inaweza ikawa ni siyo jambo la rahisi kuliacha kwa haraka. "Ukweli ni kwamba tulipotoka kwenye njia ya kusalimiana kwa kuinama kama mbadala ilionyesha umuhimu wa kushikana mikono, hatukutaka kupoteza ukaribu pale ambapo tunashikana mikono,"alisema Professa Legare. Uhusiano wa kibaiolojia unaopelekea kushika au kushikwa pia unaonekana kwa wanyama wengine pia kwenye miaka ya 1960,mwanasaikologia wa Marekani Harry Harlow,aliezea namna mahusiano ya kushikana mikono inaweza kuathiri ukuwaji wa nyani wadogo. Kushikana mikono au kusalimiana kwa mikono ni"kile kitendo cha binadamu kukubaliana na kitu au kuwa karibu n kitu".Ni ishara ya binadamu kujiingiza kiundani zaidi kwenye mambo ya kijamii , alisema haya Cristine Legare ni profesa wa Saikolojia katika chuo kikuu Cha Texas kilichopo Austin. Kumekuwa na upingamizi siku za hivi karibuni kuhusu kushikana mikono, kwamba utaratibu wa kabla ya mlipuko wa homa kali ya mapafu umebadilika: mnamo 2015, hospitali ya UCLA lilianzisha eneo huru la kushikana mikono katika kitengo cha dharura (sera hiyo ya UCLA ilidumu miezi sita tu). Wakati huohuo, wanawake wengi wa Kiislamu duniani kote hawakubali kushikana mikono kwa misingi ya dini. Lakini licha ya kutoridhishwa na hali hiyo ya wale wanaokataa dhamiri kushikana kwa mikono kwa dhamiri, karne ya 20 ilipoendeleza ishara hiyo ilibadilika kuwa ishara ya karibu na isiyowezekana ya salamu za kitaalam. Uchunguzi wa kisayansi wa ibada hiyo umegundua umuhimu wa kushikana mikono katika sehemu ya ubongo ambayo husindika aina zingine za kichocheo cha thawabu kama vile chakula kizuri, vinywaji na hata ngono. Wakati ujao bila kushikana mikono? Kuna majimbo kadhaa huko Marekani yanaanza kupunguza hatua za kufungia watu ndani, hali ya kuendelea kutokushikana mikono bado haijulikani. "Sidhani kama tutawahi kushikana mikono tena, kiukweli sifahamu," Dkt Anthony Fauci, mjumbe muhimu wa kutoka katika kamati maalumu ya kupambana na homa kali ya mapafu ya Ikulu ya Marekani, alisema tena mnamo Aprili. "Sio tu kuwa nzuri kuzuia ugonjwa wa corona; labda itapunguza matukio ya mafua makubwa katika nchi hii." Miongozo ya kutengwa kwa jamii inaweza kukaa mahali kwa muda mrefu ujao, kulingana na miongozo ya serikali ya Marekani ya kufungua upya nchi, haswa kwa watu walio katika mazingira hatarishi kama wazee na wale walio na matibabu na uangalizi maalumu kama ugonjwa wa mapafu, ugonjwa wa kunenepa sana na ugonjwa wa sukari. Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona: Hii inaweza kutoa sababu ya Stuart Wolf, mtaalamu wa sayansi na dawa anasema iwapo jamii ingegawanywa kwa wale ambao wanaweza kugusa na kuguswa, na wale ambao lazima wabaki wa pekee. Hiyo inaweza kuunda athari mbaya za kisaikolojia, Dkt. Wolf anasema. "Tayari tunaweka jitihada kwa vijana ambao ni nguvu kazi katika jamii, tofauti ipo kwa wazee na watu ambao wana afya dhaifu na hofu ipo kuwa labda ugonjwa utawaathiri watu wengine sana." Kuhimiza kufikia - kwa mwili - kuna waya sana ndani yetu. Kuna sababu ya rais wa Amerika inakadiriwa kushikana mikono na watu 65,000 kwa mwaka. "Tabia hufa kwa bidii," anasema Elke Weber, profesa wa saikolojia na mambo ya umma katika Chuo Kikuu cha Princeton ambaye anasoma jinsi watu huchukua tahadhari. "Kwa upande mwingine, tabia na mila ya kijamii inaweza kubadilika kutokana na sababu za kijamii na kiuchumi na, katika kesi hii, muktadha wa afya unabadilika, [fikiria] kufunga mguu nchini China, ambayo pia ilikuwa utamaduni kutoka miaka ya nyuma. Tayari kuna njia nyingi zisizo za mawasiliano ya kusogeleana, kwa mfano, tayari tekeleza sana ulimwenguni kote kwa kutumia teknolojia- Thailand tayari imesifiwa kwa kuwa na vifo vichache sana. Alafu kuna kupunga mkono, kutikisa kichwa, kutabasamu na ishara nyingi za mikono ambazo hazihusishi kuwasiliana kimwili. Lakini Prof Legare anabainisha kuwa moja ya ujinga wenye nguvu wa Covid-19 ni kwamba ni sawa wakati wanadamu wanakabiliwa na hali zenye kusumbua ambazo hutegemea kugusa kwa mwanadamu. "Fikiria njia tunazojibu wakati watu wanaomboleza baada ya kifo au kitu kibaya kilichotokea, ni kwa kumkumbatia, au inaweza kuwa amekaa kando ya mtu na kugusa bega." Masuala ya usafi kwa kuhamishia salamu kwenye kiwiko hakuwezi kuvunja ukaribu wa binadamu. Wakati wowote zinapotokea kila wakati kuna maarifa kamili ya ndani ya jinsi wanavyopingana na nafaka ya urafiki wa hali ya juu, anabainisha Steven Pinker, Profesa wa Familia ya Chuo Kikuu cha Harvard cha John Psychology, katika nakala ya gazeti la The Harvard Gazette, tovuti rasmi ya habari ya chuo kikuu. "Hiyo inaelezea kwa nini, angalau katika uzoefu wangu, watu wanafuatana na ishara hizi kwa kucheka kidogo, kana kwamba tunahakikishiana kuwa maonyesho ya nguvu zaidi ni makusanyiko mapya katika wakati unaoambukiza na kutolewa kwa nia," Prof Pinker anasema. Kutokana na kazi yake katika afya ya umma, pamoja na magonjwa ya kuambukiza, Delana Garcia alikuwa tayari akikwepa kupeana mikono na watu wengi. Lakini tabia zingine ni ngumu kuvunja kuliko zingine. "Mimi ni mtu anayependa sana kukumbatiana," anasema Bi Garcia, kutengana na mama yake wa miaka 85 imekuwa ngumu sana. "Yeye yuko karibu sana, na mimi nataka tu kwenda kwake na kumsafisha uso wake mdogo na kumpa busu na kumwambia ninampenda." Mhimizo huu wenye nguvu unaibuka na wasiwasi juu ya maambukizi, na kusababisha "ngoma mbaya" kati ya hao wawili, anasema. "Hata kama anavyokaribia, naweza kuhisi mwenyewe kuwa na wasiwasi - ni nini ikiwa nitamfanya mgonjwa?" Bi Garcia anasema. "Kwa hivyo najiondoa, lakini ikiwa ataanza kuondoka, mimi hufuata. Ninahitaji kujihakikishia lakini bado siwezi kumruhusu aondoke. Tunapendana kama vile miti sawa kwenye sumaku." Vigumu kama vile siku zijazo bila mikono au kugusana kunaweza kuwa, ni bora kuliko mbadala, Prof Weber anasema. "Sidhani watu wanaweza kubadilika katika hatua hii, tofauti kabisa." "Kupona au kujaribu kukaa hai ni njia nyingine muhimu ya msingi ya wanadamu. Njia mbadala ni kurudi kwenye maisha kama tulivyoijua na kupuuza ukweli kwamba idadi kubwa ya wazee, watu wenye tabia mbaya watakufa hadi tutakapoanzisha kinga ya kundi , ambayo itachukua muda mwingi. " Lakini usikate tamaa kwa kushikana mkono bado. Wakati wa kuzuia magonjwa ni sehemu muhimu ya kuishi kwa wanadamu, ndivyo maisha ya kutimiza na magumu ya kijamii, anasema Arthur Markman, profesa katika idara ya saikolojia katika Chuo Kikuu cha Texas huko Austin. "Labda tunaanza kwa kuzingatia zaidi kunawa mikono, vitakasa mikono, na mikakati ya kuzuia kugusa uso wako kuliko kutoa kabisa kugusa," anasema. "Wasiwasi wa kweli ni kwamba tutakua na hali mpya ambayo haina mawasiliano ya kugusana, na kwa hivyo hatutagundua kile tunakosa kwa kutokuwa na mawasiliano yoyote na watu kwenye mtandao wetu wa kijamii." Binadamu duniani kote wamekuwa wakipata shida kuacha mazoea waliokuwa nayo tangu jadi, mazoea hayo ni kutokuwa na mikusanyiko na pia kushikana mikono. text: Jay-Z na mke wake Beyonce Amekiri hilo kwa mara ya kwanza alipokuwa akihojiwa kuhusiana na maisha yao na jarida moja. Aliambia jarida la Style la gazeti la The New York Times kwamba alijiwekea vizuizi kutokana na matatizo aliyokumbana nayo alipokuwa mtoto, jambo ambalo lilimfanya kujifungia na kuwa uzinifu. ''Kitu kigumu ni kuona uso wa mtu uliojaa huzuni uliosababishwa na wewe, alisema Jay -Z." Wanandoa hao walikuwa wamedokeza kuhusu Jay-Z kutokuwa mwaaminifu kwenye nyimbo zao. Mwanamuziki huyo amesema kwamba wangetalikiana lakini alipata ushauri nasaha ili kumsaidia kukabiliana na matatizo yake ya hapo awali. Kama unavyofahamu, watu wengi hutalikiana, na visa vya kutalikiana ni takriban asilimia 50 mambo kama haya yanapotokea. Mwanamuziki wa rap Jay -Z na Beyonce Mwaka wa 2013, kulikuwa na uvumi kwamba mwanamuziki huyo wa nyimbo za rap hakuwa mwaminifu kwa mke wake na ilichochewa na kitambulisha mada cha #elevatorgate pale Solange Knowles alipomshambulia Jay -Z, huku Beyonce akionekana kunyamaza kimya. Albamu ya hivi majuzi ya Jay -Z ya 4:44 ilizungumzia yeye mwaminifu. Aliandika :''Naomba radhi / kwa kutoka nje ya ndoa/aliyemfanya mtoto wangu kuzaliwa kupitia kwa macho ya mamake.'' Mwaka mmoja kabla ya albamu hiyo ya 4:44 kuzinduliwa , Beyonce aliimba kuhusu ''Becky with good hair (Becky mwenye nywele nzuri)'' kwenye albamu yake ya Lemonade. Familia ya Jay-Z ''Yeye hunihitaji wakati sipatikani, heri ampigie Becky ambaye ana nywele ndefu.'' Jay -Z na Beyonce walikuwa wamepanga kutoa albamu ya pamoja badala yake wakaishia kufanya nyimbo kila mmoja yake. ''Tunatumia sanaa kujiliwaza. Tulianza kutunga nyimbo zetu pamoja. Na nyimbo alizokuwa akibuni wakati huo zilikuwa mbele sana. ''Kwa hivyo albamu yake ilizinduliwa kinyume na matarajio ya kuwa albamu hiyo ingekuwa imewashirikisha wanandoa hao. Pia Jay-Z hakuzungumzia kuhusiana na ndoa yake pekee, pia alizungumzia kuhusiana na mahusiano yake na Kanye West. ''Nilizungumza na Kanye wakati mmoja, kumwambia yeye ni kama kakangu. Nampenda Kanye. Kwa kweli. Ni mahusiano tata kati yetu. Alikubali kwamba hawajakuwa na uhusiano rahisi. Kanye West aliripotiwa kuacha kazi katika kituo cha umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki ya Jay Z, Tidal ,kuhusiana na mzozo wa kifedha. ''Niko na uhakika anahisi nimemfanyia mambo kadhaa pia yeye. ''Natumai tutakapofika umri wa miaka 89, tutaangazia haya baada ya miezi sita au wakati wowote na kutafurahia haya yote.'' Mwanamuziki wa rap Jay -Z amekiri kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine akiwa bado kwenye ndoa yake na Beyonce. text: Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza Abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo ya shirika la Uingereza, walikuwa tayari wameingia ndani ya ndege hiyo wakati lilitolewa tangazo kuwa ingechelewa. Carly, ambaye alikuwa ndani ya ndege, alisema kuwa mhudumu alitangaza, "walisema kitu kisicho cha kwaida kimetokea" Panya Kisha mhudumu huyo akasema wameambiwa ndege nyingine imepatikana lakini abiria wangesubiri saa kadhaa ili kuanza safari. Kisha safari nyingine ikaanza saa nne baadaye. Shirika la ndege la Uingereza lilisema; "Tunaelewa kuwa karibu kila mtu anataka kusafiri nasi hadi San Francisco, lakini wakati huu kulikuwa na mteja mdogo ambaye lazima tungemtoa. "Kila mmoja aliye na miguu miwili kwa sasa yuko safarini kuenda California, na tunaomba radhi kwa kuchelewa." Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza Safari ya ndege kutoka uwanja wa Heathrow hadi San Francisco, ilichelewa kwa saa kadhaa baada ya panya kuonekana ndani ya ndege. text: Huo sio ubakaji chini ya sheria za Uingereza na Wales lakini mwanzilishi wa utafiti mpya kuhusu swala hilo pengine anasema unafaa kuwa ubakaji. Baadhi ya wasomi watakerwa ba habari hii Dkt Siobhan Weare wa chuo kikuu cha sheria cha Lancaster alifanya utafiti wa kwanza kuhusu mwanamume kulazimishwa kushiriki tendo la ngono mwaka 2016-7 na kukusanya habari kutoka kwa zaidi ya wanaume 200 kupitia utafiti uliofanyika kupitia mitandao. Utafiti wake wa hivi karibuni uliochapishwa wiki hii kutokana na mahojiano ya ana kwa ana na wanaume 30 kati ya mwezi Mei 2018 hadi Julai 2019-unaonyesha kwa maelezo ya ndani jinsi ngono ya lazima inapofanyika, madhara yake pamoja na sheria inavyosema. Wote walioshiriki hawakutajwa majina lakini nitamuita mmoja wao kwa jina John. John anasema kwamba ishara ya kwanza kwamba mambo hayakua shwari ni wakati mwenzake alipoanza kujiumiza . Baada ya kisa cha kutisha alimkimbiza kwa matibabu. Wapenzi hao wawili walijadiliana kuhusu uwezekano wa sababu za kisaikolojia. Takriban miezi sita baadaye badala ya kujiumiza mwenyewe alimlenga John. ''Nilikuwa nimeketi sebuleni na alikuja kutoka jikoni , na kunipiga ngumi kwa nguvu katika pua yangu na kukimbia akicheka'', John anasema. Ugomvi ukaanza polepole na kuendelea mara kwa mara. Alijaribu kupata usaidizi kutoka kwa GP, John anasema. Alipatiwa ushauri nasaha na kuambiwa amuone dkt wa saikolojia . Hatahivyo hakwenda. ''Angeweza kuja nyumbani kutoka kazini na kutaka kushiriki ngono kwa nguvu'', anasema. ''Yeye angetumia nguvu na ikafikia wakati ambapo nilikuwa nikichukia anaporudi kutoka kazini''. Wakati mmoja John aliamka na kugundua kwamba mpenzi wake alimfunga kamba mkono wake wa kulia na kitanda. Na baadaye akaanza kumgonga katika kichwa na spika kubwa akamfunga mkono mwengine na kitanda na kujaribu kumlazimisha kushiriki ngono naye. Akiogopa mamumivu aliokuwa nayo John alilazimika kufanya anachotaka - baadaye alimpiga tena na kumwacha amefungwa kwenye kitanda kwa nusu saa kabla ya kurudi na kumfungua. Baadaye alikataa kuzungumzia yaliojiri. Muda mfupi baada ya visa hivyo akapata ujauzito na mgogoro aliokuwa nao ukapungua. Lakini miezi michache baada ya mtoto kuzaliwa ,John aliamka usiku mmoja na akajipata kwamba mpenzi wake amemfunga mkono wake wa kulia katika kitanda. Baadaye anasema mpenzi wake akamlazimisha kula dawa ya Viagra. hakuna kitu ningeweza kufanya , anasema. Baadaye nilienda kuoga sijui kwa dakika ngapi ....nilishuka chini. Kitu cha kwanza alichoniuliza wakati nilipoingia katika chumbani ni tutakula nini jioni? Wakati John anapoanza kuwaambia watu kuhusu kisa hicho anasema kwamba wanashangaa. ''Nimekuwa nikiulizwa ni kwa nini niliondoka nyumbani? Ndio ni nyumba yangu ambayo niliwanunulia watoto wangu''. Madai ya habari ya John yamerejelewa katika baadhi ya visa vya wanaume wengine ambao Dkt Weare aliwahoji. Mojawapo ya mambo aliyogundua ni kwamba mshukiwa katika uingiliaji wa lazima ni mwanamke . Utafiti wake unaangazia uingiliaji wa lazima miongoni mwa wanaume na wanawake na kwamba visa hivyo huwa moajwapo ya sababu za migogoro nyumbani. Tatizo la watu kutomuamini mwanamume anapozungumza kuhusu vitendo kama hivyo pia vilitajwa na baadhi ya waliohojiwa. ''Ungefurahia ama umeripoiti mapema sana'', mwanamume mmoja aliambiwa na afisa wa polisi. Mshiriki mwengine alisema: Tunaogopa kuzungumzia na tunapozungumzia hatuaminiki kwa kuwa sisi ni wanaume. Ni vipi mwanamume anaweza kudhulumiwa kwa njia hiyo? mwangalie ni mwanamume." Kitu kimoja ambacho utafiti wa Weare unapinga ni kwamba tendo la ngono kwa lazima haliwezekani kwa kuwa wanaume wana nguvu ukilinganisha na wanaume. Chengine ni kwamba wanaume hulitazama tendo la ngono na wanawake kama fursa kubwa. Weare anasema kwamba msisimuko wa mwili wa mwanamume hutokana na kichocheo. Anasema kwamba wanaume wanaweza kupata msisimuko wa mwili na kusalia nao hata iwapo wamekasirika ama ni waoga. Pia kuna utafiti unaosema kwamba wanawake wanaweza kusisimka wakati wanapobakwa kwa kuwa mili yao husisimka kimaungo. Hili ni swala la waathiriwa wanaume na wanawake ambalo huwa halijadiliwi vya kutosha lakini kuna ushahidi kulihusu. Mmoja ya waliohojia katika utafiti huu mpya alielezea kwamba walienda nyumbani na mwanamke baada ya ya kutoka katika klabu ya burudani na kulala baada ya kupewa dawa. Anasema kwamba baadaye alilazimishwa kushiriki katika tendo la ngono bila ya yeye kujua Weare anasema kwamba wengi wa wale walioshiriki katika utafiti huo mpya walidai kwamba visa vya wao kulazimishwa na wanawake kushiriki tendo la ngono vilikuwa ubakaj na kwamba wengine walikasirishwa na swala kwamba huenda sio ubakaji chini ya sheria za Uingereza na Wales. Kuna mafadhaisho kwamba jamii ya Uingereza huenda wasiijumuishe kama ubakaji. Wakati mwanamume anapofanya tendo la ngono na mwanamke bila ruhusa yake ,huo ni ubakaji. Lakini je inakuwaje wakati mwanamke anapomlazimu mwanamume kushiriki ngono naye bila ruhusa yake? text: Katika kitabu hicho, Becoming, Bi Obama amefichua kwamba alitokwa na ujauzito na akalazimika kutumia mbinu ya IVF ambapo mayai ya wapendanao huchanganywa nje na baadaye kuwekwa katika kizazi cha mwanamke kupitia sindano. Bi Obama aliambia kituo cha ABC Good morning America kwamba alihisi 'amepotea na mpweke' baada ya kupoteza uja uzito miaka 20 iliopita. Pia alimkosoa rais Donald Trump kwa kuweka usalama wa familia yake hatarini . Bi Obama na mumewe , aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama walilazimika kufanyiwa vikao vya ushauri , na pia alifichua kwamba kwa mara ya kwanza katika kitabu chake chenye kurasa 426 kitakachotolewa siku ya Jumanne. Kufuatia kuchapishwa kwa kitabu hicho Bi Obama atatembelea miji 10 ikiwemo London. Alipokuwa mjamzito Bi Obama , wakili wa zamani na msimamizi wa hospitali aliambia ABC kwamba baada ya kupoteza uja uzito, nilihisi kwamba nimefeli kwasababu sikujua takwimu za kumwagika kwa uja uzito. ''Tunajitenga tukiwa na uchungu'', alisema akiongezea kuwa ''ni muhimu kuzungumza na akina mama wachanga kuhusu ukweli kwamba uja uzito unaweza kukutoka''. Alisema kwamba alipokuwa na umri wa miaka 34, aligundua muda wa kibaiolojia upo na kwamba uzalishaji wa mayai ni mdogo swala lililomshinikiza kutafuta mbinu ya IVF. ''Nadhani ni kitu kibaya zaidi tunachofanyiana sisi kama wanawake kwa kutoambiana ukweli kuhusu miili yetu na vile inavyofanya kazi'', bi Obama alimwambia mwandishi wa ABC Robin Roberts katika kipindi cha Good Morning America. Kuhusu ndoa yake Bi Obama alifichua kwamba ndoa yao ilikumbwa na misukosuko mara nyengine , hususan baada ya mumewe kujiunga na bunge la jimbo hilo , na hivyobasi kumwacha nyumbani ambapo alilazimika kutumia sindano za IVF mwenyewe. ''Ushauri katika ndoa yetu kwetu sisi ulikuwa mojawapo ya njia ambapo tulijua kushughulikia tofauti zetu'', aliambia ABC. ''Najua wanandoa wengi wachanga ambao wanakabiliwa na changamoto na nadhani kuna makosa wanayofanya, Na nataka wajue kwamba bi Michelle na Barrack Obama ambao wamekuwa na ndoa nzuri na ambao wanapendana sana, pia huketi chini na kuimarisha ndoa yao. na tunapata usaidizi wa ndoa yetu tunapohitaji''. Pia alielezea vile alivyopendana na bwana Obama wakati mmoja mjini Chicago. ''Punde tu nilipojiruhusu kumhisi Barrack'', aliandika, hisia zilikuja kwa wingi za kumpenda. familia ya Obama na watoto wao nchini Indonesia 2017 Kuhusu Trump Katika kitabu hicho cha in Becoming, Bi Obama anasema hatomsamehe tena rais Trump kwa kusema kuwa mumewe sio mzaliwa wa Marekani wakati wa kampeni yake ya urais kulingana na habari zilizochapishwa katika vituo vya habari. Swala lote la alikozaliwa Obama lilikuwa la kukera. Je ingekuwaje iwapo mtu ambaye hana akili timamu angechukua bunduki na kuelekea Washington ? Je iwapo mtu huyo angekwenda kuwatafuta wana wetu?. ''Trump na tabia zake alikuwa akiweka familia yangu hatarini''. Anasema kuwa alishangazwa sana na ushindi wa rais Trump. Aliyekuwa mke wa rais wa Marekani Michelle Obama ametoa kumbukumbu ambapo amefichua matatizo aliyopitia katika ndoa yake na uja uzito wa watoto wake wawili. text: Virusi hivyo kwa jina Covid-19 vimeripotiwa kuwauawa watu 53,160 kote duniani huku wengine 1.016,401 wakiambukizwa. Virusi hivi ni vinatoka katika familia ya coronavirus - maambukizi ya kawaida yanayosababisha Flu na dalili za homa ya kawaida , joto mwilini, kikohozi na matatizo ya kupumua. Watu wengi wanaoambukizwa virusi hivi hupata dalili hafifu na wengi wanatarajiwa kupona kabisa. Lakini kama Sars na Influenza , virusi hivi vipya vinaonekana kuwa hatari zaidi miongoni mwa watu wazee na wale wanaougua magonjwa mengine. Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi? Hakuna tiba, sawa na jinsi hakuna tiba ya homa ya kawaida. Ni nini kinachotokea hospitalini? Wale wanaopelekwa hospitalini hupatiwa tiba kwa kukabiliana na dalili walizonazo huku kinga yao ikijaribu kukabiliana na virusi hivyo. Mgonjwa anapokuwa hospitalini pia ni njia muhimu ya kuzuia virusi hivyo kusambaa, kulingana na Jonathan Ball mtaalam wa virusi katika chuo kikuu cha Nottingham. Anapokuwa katika hali mbaya, virusi hivyo vinaweza kusababisha homa ya mapafu au uvimbe katika mapafu. Katika hali hiyo mgonjwa hulazimika kupata usaidizi ili kupumua, amesema profesa Ball. Wagonjwa hupatiwa Oxygen na katika hali mbaya kabisa huwekwa katika vifaa vya kuwasaidia kupumua. Kisa kimoja kati ya visa vinne duniani hudaiwa kuwa kibaya zaidi. Mgonjwa aliyeanza matatizo ya kupumua kama huyu anahitaji kuwekewa mashine ya kumsaidia kufanya hivyo "Iwapo mgonjwa anaonesha dalili za kushindwa kupumua wanamsaidia kupumua .Iwapo kuna shinikizo katika baadhi ya viungo vya mwili watausaidia mwili wake kukabiliana na shinikizo hiyo," kulingana na Profesa Ball. Wakati mgonjwa anakabiliwa na dalili hafifu, wagonjwa hupata shida kudumisha shinikizo la damu na hivyobasi hupatiwa dawa kudhibiti tatizo hilo. Mgonjwa pia hutiwa maji mwilini iwapo anaharisha na dawa aina ya ibuprofen hutolewa kumaliza maumivu. Zhang Dingyu, mkuu wa hospitali ya Jinyintan mjini Wuhan , aliambia chombo cha habari cha China CCTV kwamba wagonjwa waliopona katika eneo hilo walikuwa 'katika hali nzuri'. ''Wengine huwa na matatizo ya mapafu'' , alisema , lakini nina matumaini kwamba watapona . Je dawa za HIV zinasaidia? Ijapokuwa hakuna chanjo dhidi ya virusi vya corona , vipimo vinaendelea China kuona iwapo dawa mbili za kukabiliana na virusi zinazotumiwa kutibu HIV -lopinavir na ritonavir - zinaweza kuwa tiba nzuri. Dawa hizi zimeonekana kusaidia kukabiliana na virusi vya Sars mwaka 2003, baada ya ushahidi kuonesha kwamba wagonjwa wa HIV ambao walikuwa wakitumia dawa na ambao pia wana virusi vya Sars walikuwa na matokeo mazuri. ''Matumaini ni kwamba virusi vya Sars na vile vya corona vinafanana kwa dawa hiyo kuweza kuwa na mafanikio ya kutosha'', profesa Ball alisema. Iwapo kuna dalili za mapema inaweza kufanya kazi, kwa kuwa dawa hiyo imethibitishwa kukabiliana na dalili kama hizo. Matumizi ya huruma ni iwapo dawa ambazo hazijaidhinishwa kutibu ugonjwa fulani zinatumika chini ya masharti makali kwa wagonjwa walio katika hali mbaya ama walio katika hali hatari. Watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona wanatibiwa hospitalini - lakini je ni tiba gani wanayopata na imefanikiwa kwa kiwango gani? Je ni v i rusi gani hivi? text: Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyikazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki kwenda nyumbani na kupata wakati bora wa kujamiana na wapenzi wao. Aliambia BBC lengo kuu lilikuwa kuimarisha uhusiano baina ya watu. ''Ni jina la herufi tatu{Sex} , ''Bw Muskos aliposema mwezi Februari , akipuzulia mbali pendekezo la kwamba anaingililia maisha ya watu binafsi. Lakini wanachama wa baraza hilo ambao ni wahafidhina walipinga wazo hilo. Meya wa Övertorneå, Tomas Vedestig, alihitimisha kwa kusema maisha ya kibinafsi ya wafanyikazi yanastahili kuwachwa vile yalivyo. ''Si kazi ya baraza kuingililia,'' aliambia SVT. Bw Muskos alitumai kwamba kichwa cha mpango wa unyakuaji ungeongeza idadi ya watu katika mji wake ambao kwa hivi sasa idadi hiyo imezidi kushuka. Mji wa Övertorneå kwa hivi sasa ni eneo ambalo lina watu 4,500 lakini wengi wao ni mwenye umri wa wastani. ''Vijana wengi huondoka mji huo pindi tu wanapo kamilisha masomo yao ,''Kasela amesema. Pia anadhani kwamba kutenga saa moja kwa wiki kutawasaidia wanandoa ambao hawana wakati na wapenzi wao. ''Watu wana vitu vyengine vingi vya kufanya ,'' alisema. Ukiwa nyumbani watu wako kwenye mitandao, unahitajika kuwapeleka watoto kushiriki katika michezo ya soka na mpira wa magongo ya barafu , watu hawana wakati wa kulinda kila mmoja na kuwa na wakati bora bila watoto. Iwapo wafanyikazi wa 550 wa baraza wamekasirika, itakuwa afueni kupata njia ya kutoa hasira katika hali hiyo mbaya: kwa sasa wana saa moja kwa wiki kushiriki katika michezo tofauti. Madiwani katika baraza la mji mdogo wa Sweden wamepinga muswada wa pendekezo la kuwapa wafanyikazi wa manispaa wanaolipwa, 'mapumziko ya kufanya tendo la ngono' text: Wabunge hao walitaka mbunge wa Wajir Mashariki Rashid Amin kukamatwa kwa kumpiga mbunge mwakilishi wa wanawake wa jimbo la Wajir Fatuma Gedi. Tukio hilo lilijiri wakati bunge liliporejelea kikao cha mchana cha usomaji wa bajeti. Wabunge hao walisikika wakiimba nyimbo za kumtaka mbunge Rashid na kiongozi wa wengi bungeni kujiuzulu Aden Duale. Wanawake hao walimlaumu Duale kwa kushindwa kuwatetea viongozi wanawake bungeni. Spika wa Bunge la Kenya, Justin Muturi, alilazimika kuwaita maafisa wa ulinzi wa Bunge kuwatoa nje wabunge waliokuwa wakizua vurugu mda mfupi kabla ya kusomwa kwa makadio ya Bajeti ya mwaka 2019/2020. "Walinzi wa bunge watoeni wabunge wote wanaopiga mayowe katika ukumbi wa bunge," alisema Bw. Muturi . Lakini viongozi hao waliokuwa na hasira waliendelea kupiga mayowe wakisama "Hatutanyanyaswa na wanaume, tumechoka'' hadi pale agizo la Spika lilipotekelezwa. Inaripotiwa kuwa Bw. Rashid alimshambulia Bi Fatuma katika eneo la kuegesha magari baada ya wao kutofautiana vikali kabla ya kumzaba makofi mbele ya walinzi wao . Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa Rashid alitaka kujua kwa nini Bi Gedi - ambaye ni mwanachama wa kamati ya bajeti - hakuitengea mgao wa fedha eneo bunge la Wajir Mashariki wakati kamati ya bejeti ilipozuru eneo hilo hivi karibuni. Mwakilishi wa wanawake wa Homabay Magharibi mwa Kenya Gladys Wanga amethibitisha kushuhudia tukio hilo kwani alikuwa akiandamana na Bi Gedi. Katika picha iliyosambazwa, Gedi anaonekana akitokwa na machozi kadhalika kuonekana kuwa na matone ya damu mdomoni. Kisa hicho kimezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini Kenya huku wengi wamuelekezea Bw. Rashid ghadhabu zao. Kwa kutumia hushtag #JusticeForFatumaGedi katika mtandao wa kijamii wa Twitter Wakenya wamekua wakishinikiza mbunge Fatuma Gedi. Tayari mbuge Fatuma Gedi amewasilisha rasmi ripoti kwa polisi kuhusiana na kisa hicho. Mbunge, Rashid Khasim anazuiliwa katika kituo cha polisi. Purukushani hilo ambalo lilichukua karibu nusu saa lilitulia baadae na wabunge hao wakarejea bungeni. Wabunge wanawake nchini Kenya wamesusia kikao cha kusomwa kwa bajeti kulalamikia hatua ya mwenzao kudaiwa kushambuliwa katika majengo ya Bunge na mbunge wa kiume. text: Kuna hofu kwamba mfumuko wa bei huenda ukatikisa tena bara Ulaya Uchumi katika maeneo ya Jumuiya ya Ulaya yanaendelea kukua lakini kwa mwendo wa kobe sana na kukosa kuongezeka kwa bei za bidhaa kumetajwa kama sababu mojawapo inayozuia kufufuka kwa uchumi. Kuongezeka kwa bei za bidhaa barani Ulaya kumekua kwa kiwango cha chini mno, takwimu zikionesha kuwa bei ya bidhaa iliimarika kwa asilimia 0.5. Iwapo bei za bidhaa nchini humo zitaporomoka zaidi, kuna uwezekano mkubwa kuwa wanunuzi watachelea kulipia bidhaa zao wakisubiri bei ishuke zaidi ili wanufaike kwa faida ya juu. Kushuka kwa bei za bidhaa pia kunaweza kuvuruga mipango ya kulipa madeni. Benki Kuu ya Jumuiya ya Ulaya inatazamia kuyaepusha mataifa shirika na tatizo hilo la kiuchumi kwa kupunguza kiwango cha riba inachotoza. Benki hiyo pia, inatazamia kupunguza faida inayopatikana kwa wale wanaoweka pesa zao kwa akiba hivi kwamba, watanufaika zaidi iwapo watawakopesha wawekezaji mtaaji wa biashara . Aidha benki hiyo inapania kutekeleza sera hizo miongoni mwa zingine madhubuti kuhakikisha kuwa mikopo ya mtaaji ni nafuu zaidi kwa wawekezaji . Banki Kuu ya Muungano wa Ulaya inatarajiwa kuchukua hatua kadhaa Alhamisi, kushughulikia hofu kuwa mataifa wanachama wa Ulaya huenda yakakabiliwa na mfumuko wa bei. text: Wapiganaji wa M23 waliondoka kuelekea nyumbani katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo Wapiganaji hao walioandamana na jamaa zao kumi wamesafirishwa kwa ndege ya Umoja Mataifa kutoka uwanja wa Entebbe hii leo kuelekea nchi yao. Walioigiza kuwa rais wa Kenya wakamatwa Hatua ya kuwarejesha nyumbani imechukuliwa chini ya mpango wa utekelezaji wa makubaliano yaliofanyika mwaka 2013 ukiwa moja kati ya mikakati ya kutatua mzozo wa vita katika eneo la maziwa makuu. Wapiganaji wa kikundi cha M23 walionekana kuwa na shauku ya kurudi nyumbani DRC Mwandishi wetu wa Kampala anasema wafuasi hao wa M23 walionekana wenye nyuso za furaha huku wakiimba kuonyesha kwamba wako tayari kurudi katika nchi yao kwa hiari . Kushuka kwa thamani ya shilingi ni uchungu kiasi gani kwa watanzania? Walimuhakikishia balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Uganda Jean Pierre Massala kuwa wako tayari kurudi nyumbani. Wapiganaji wa M23 waliambatana na familia zao walipokuwa wakirejea nyumbani DRC Kundi hilo limekubali kurudi makwao chini ya mpango wa kuwarudisha nyumbani waliokuwa wapiganaji unaohusisha pia wapiganaji wa kundi la FDLR maarufu kama Interahamwe, linaloshutumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda. Balozi Robert Masolo ni afisa wa ngazi za juu Uganda aliyeongoza shughuli ya kuwakabidhi Wakongo hao 57 pamoja na jamaa zao 10 kwa serikali ya DRC. Wapigajani hao wameishi Uganda miaka mitano lakini wenzao wengi ambao idadi yao haikufichuliwa bado hawajakubali kurudishwa nyumbani chini ya mpango huo. Wapiganaji wa M23 waliwahakikishia maafisa kuwa wako tayari kurejea nyumbani Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 26.02.2019 Wapigajani hao wamesafirishwa kwa ndege ya Umoja Mataifa. ''Watakapofika DRC watarejeshwa tena katika maisha ya kawaida'', amesema balozi wa DRC nchini Uganda Jean Pierre Massala Bado kuna wapiganaji wengine wa zamani wa kundi la M23 eneo la Bihanga magaharibi mwa Uganda na haijulikani ni lini ni lini watarejea nyumbani kwa hiari. Wapiganaji 57 waliokuwa wajumbe wa kundi la waasi wa M23 wamekabidhiwa kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na serikali ya Uganda. text: Rais Duterte ametishia kurejesha takataka nchini Canada Nchi hiyo imewasilisha mara kadhaa malalamiko yake kidiploamasia kupinga hatua ya Canada ya kutuma tani za uchafu nchini Ufilipino kati ya mwaka 2013 na 2014. Wiki hii rais Duterte alitishia kurejesha takataka hizo nchini Canada. Canada inasema "ina nia sana" ya kutatua swala hilo na itashirikiana na Wafilipino kufanya hivyo. Rais Duterte aliikosoa Canada juu ya mzozo huo wa muda mrefu wa kidiplomasia , akisema imeibadilisha nchi yake saying it is kuwa "dangulo la kutupa uchafu". "Kuhusiana na taka za Canada , ninataka maboti yaandaliwe," alisema Jumatatu, na kuongeza kuwa: "ni bora wavute hicho kitu nje ya nchi yetu au nipeleke meli za uchafu wao huko''. "Ngoja tupambane na Canada. Nitatangaza vita dhidi yao." Rais Duterte anafahamika kwa mtindo wake wa kutoa kauli za wazi na mara nyingi hutumia lugha na kauli kali zenye utata. Uchunguzi ulibaini kuwa baadhi ya makontena yalikuwa na chupa za plastiki na mifuko, takataka za nyumbani na nepi za watu wazima zilizotumiwa (diapers) Kauli zake za Jumatatu zilihusu kontena zilizotumwa kwa meli katika mji mkuu Manila, na kampuni ya kibinafsi ya Canada kwa ushirikiano na wadau wau wa Ufilipino. Serikali mjini Manila inasema makontena hayo yaliyowasili katika bandari ya kimataifa ya Manila, yaliwekwa utambulisho gushi, ambapo yaliandikwa kuwa yalikuwa na plastiki ambazo zingetumiwa kutengeneza bidhaa nyingine , lakini ukweli ni kwamba yalikuwa yamesheheni vifaa vikuukuu mbali mbaloi vya nyumbani. Uchunguzi ulibaini kuwa baadhi ya makontena yalikuwa na chupa za plastiki na mifuko, takataka za nyumbani na nepi za watu wazima zilizotumiwa (diapers). Uchunguzi mwingine iwa kontena zilizosalia 2015 ulibaini kuwa zilikuwa na uchafu mwingine usio hatari, zikiwemo taka za nyumani na mitaani. Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau (kushoto) akiwa pamoja na rais wa Ufilipino Lodrigo Duterte Maafisa wa Ufilipino walitoa malalamiko yao kwa Canada kwa mara ya kwanza 2014. Serikali inasema makontena hayo yamesababisha mlundikano katika bandari na ni hatari kwa afya ya umma. Baadhi yamesalia kwenye magala katika bandari ya Manila na mengine yametupwa kwenye dangulo la wazi. Mnamo mwaka 2016, mahakama ya Ufilipino iliamuru uchafu huo urejeshwe kwa meli hadi Canada kwa garama ya aliyeyatuma. Mwaka huo huo, Canada ilifanya mabadiliko ya sheria zake juu usafirishaji wa takataka hatari ili kuzuwia jambo kama hilo kutokea tena. Mapema mwaka huu, muungano wa makundi ya mazingira katika nchi zote mbili ulimuandikia waraka waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau ukitaka uchafu huo urejeshwe kwa aliyeuleta. Maafisa wa pamoja wa masuala ya kiufunzi kutoka nchi zote mbili kwa sasa wanachunguza "masuala yote yanayohusiana na kuondolewa kwa taka hizo ", ilisema taasisi ya Mazingira ya Canada katika taarifa yake kwa BBC iliyotolewa Jumanne. Changamoto ya uchafu wa dunia - na kule unakotiupwa imekuwa ikiendelea kuongezeka kote duniani. Chinailianzisha marufuku kwa " taka za kigeni" kama hatua ya kuboresha sekta ya taka katika kipindi ch amwaka mmoja tu uliopita. Kiwango cha plastiki kinachochukuliwa na Uchina kilishuka kwa 94% baina ya mwaka 2016-17 na 2017-18, huku Malaysia, Uturuki Poland na Indonesia zikipunguza kiwango cha taka kutoka nje. Umoja wa Mataifa unasema soko la taka za dunia kuanzia ukusanyaji wake hadi pale zinapotumika kutengeneza bidhaa nyingine hugharimu $410bn (£316bn). Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameifokea nchi ya Canada kwa kushindwa kuchukua hatua juu ya takataka ilizosafirisha hadi katika nchi yake iliyopo kusini mashariki mwa Asia miaka kadhaa iliyopita. text: Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu. Maandamano hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano. Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji. Jeshi liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais , akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi. Waandamanaji wakiunga mkono jeshi Bwana Mugabe , mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980. Jeshi limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi karibuni. Mkutano wa siku ya Jumamosi unaungwa mkono na jeshi na wanachama wa chama cha Zanu -PF. Waandamanaji wakimtaka rais Mugabe kujiuzulu wengi wakibeba mabango yakumtaka ang'atuke mamlakani Wapiganiaji wa uhuru ambao hadi kufiki mwaka uliopita walikuwa watiifu kwa rais Mugabe pia wanasema kwamba rais Mugabe anafaa kung'atuka mamlakani. Kiongozi wa shirika hilo amewataka raia kuelekea katika makao ya rais Mugabe. Nje ya ikulu ya rais kuna baadhi ya watu walioketi chini ili kuonyesha pingamizi yao mbele ya majeshi, huku kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai akihutubia umati mkubwa. Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu. text: Mfumo huu wa urembo ni biashara kubwa China Bidhaa hizo zinazokadiriwa kuwa za thamani ya karibu dola milioni 4.3 zinajumuisha sindano za kuongeza makalio bandi na zile za kuongeza vitamin C miongoni mwa bidhaa zingine. Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa na mtandao wa wafanyibiashara haramu kwa kipindi cha miezi sita. Mamlaka imewafungulia mashataka watu watano waliyokamatwa katika msako huo. Bidhaa bandia za urembo zinasadikiwa kuuzwa katika miji mbali mbali nchini China. Mara ya kwanza mamlaka kubaini ukubwa wa biashara hiyo ilikuwa mwezi Septemba baada ya kufanywa kwa msako wa kushutukiza katika maduka kadhaa ya urembo mjini Changde. Bidhaa zinazouzwa katika maduka ya urembo ziligunduliwa kuwa za mfanyibiashara mmoja aliyepo mkoa wa Jilin - kwa jina la Zuo -ambaye anaziuza kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat. Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa Polisi walivamia bohari la bwana Zuo ambapo chupa 2,300 za kemikali ya aina ya hyaluronic acid -ambayo hutumiwa sana kutengenezea mafuta ya kupaka na bidhaa zingine bandia za urembo. Rekodi ya usafirishaji bidhaa za bwana Zuo zinaonesha kuwa bidhaa hizo tayari zimetumiwa wateja 10 katika mikoa tofauti. China ni moja ya soko kubwa la upasuaji wa urembo duniani na pia imekuwa na ongezeko la watu wanaotafuta matibabu mbadala. Serikali ya China imekuwa na wakati mgumu kuwaonya raia wake kuhusu hatari inayotokana na matumizi ya bidhaa feki za urembo. Hii ni baada ya watumiaji wa bidhaa hizo kujipata hospitali wakipigania maisha yao kufuatia upasuaji wa uremboo uliyotibuka. Kumeshuhudiwa visa kadhaa vinavyohususishwa utumiaji holela wa bidhaa bandia za urembo ambazo huagizwa kutoka nje. Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandia Korea Kusini pia inakabiliwa na tatizo la urembo bandia Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila unapotembea katika mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia. Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii. Kwenye treni na mitaani, unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'' Upasuaji mwingine ni wa ''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''. Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake. Nchini Venezuela pia kumekuwa na ripoti za wanawake kutumia kemikali haramu kuongeza ukubwa wa makalioyao na kujiletea madhara makubwa ya kiafya Hii ni kutokana na mtindo ambao unaonekana na wengi nchini humo kwamba mwanamke mwenye makalio makubwa ndiye anayependeza zaidi Wanawake wengi sasa wanahatarisha afya zao kwa kutaka kuwa 'warembo' Polisi nchini China imefanya msako mkali dhidi ya bidhaa bandia za urembo. text: Medali ya tuzo ya Nobel Lakini katika sayansi , tayari tuzo za mwaka huu zimetangazwa na wengi katika jamii ya wanasayansi wanaona hakuna usawa kuhusu washindi. Hathaivyo jamii ya wanasaynsi ilibaini kwamba washindi wa tuzo hiyo mwaka huu walikuwa na ulinganifu fulani. wanawake 100 Makala ya wanawake 100 ya BBC huwataja wanawake 100 walio na ushawishi mkubwa dunia kila mwaka. Mwaka 2017, tuliwapatia changamoto ya kukabiliana na maswala yanayowakabili wanawake hii leo kama vile ukosefu wa elimu miongoni mwa wanawake, unyanyasaji katika maeneo ya uma na kuwatenga wanawake katika michezo. Huku tuzo zikitolewa kila mwaka ama hata miongo baada ya kuwatuza ni fursa kwa sherehe kwa makundi yaliohusika. Mwanaanga, Marytin Rees alisema kwamba wanafizikia watatu waliotuzwa na kamati ya tuzo ya Nobel walikuwa watu imara ambao mchango wao ni tofauti na wa kipekee Lakini licha ya kufurahishwa na hatua hiyo wanahisi kwamba mabadiliko ni muhimu. Ni wanawake 17 pekee ambao wametuzwa tuzo za nobel katika orodha tatu za sayansi tangu tuzo hizo zianze mwaka 1909. Hakujawai kuwa na washindi weusi wa sayansi . Kati ya washindi 206 wa fizikia waliotambulika, wawili wamekuwa wanawake-Marie Curie[1903] na Maria Goeppert Mayer[1963] Kuna wanaume wengi wanaoitwa Robert katika orodha ya washindi wa kemia ikilinganishjwa na washindi wa tuzo hilo upande wa wanawake. Baadhi ya watafiti katika Twitter walilalamikia vigezo vilivyotumika kuwatuza washindi hao. Kila Tuzo haiwezi kugawanywa na zaidi ya washindi watatu , washindi hawateuliwi na orodha za walioteuliwa huwekwa katika siri kwa miaka 50. Vera Rubin, Lise Meitner na Jocelyn Bell Burnell walionekana kuwa watu waliokuwa na uwezo wa kushinda tuzo hiyo katika miaka ya nyuma. Kifo cha Rubin 2016 kinamaanisha kwamba kazi yake kuhusu Mata nyeusi inayodaiwa kuwepo katika eneo kubwa la sayari ya mass sasa ina uwezo wa kutambulika. Otto Hahn alituzwa tuzo ya nyuklia fishon 1944, ambayo hakuigawanywa , licha ya kuteuliwa katika miaka iliopita na miaka mingine Burnell na Chien -Shiung Wu ,wote wanafizikia pia waliona taasisi zao zikishinda kwa utafiti walioufanyia kazi lakini hawakushirikishwa. Ukiangazia umuhimu wa mda mrefu wa kushinda taji la Nobel, tuzo hiyo ni muhimu kwa kupiga jeki kazi yoyote ya utafiti .Mtu anayewania anaweza kupata ufadhili katika sekta ambayo ina ushindani mkubwa kupata ufadhili. lakini kwa wanawake waliopo katika fizikia na kemia, kuna wachache waliopo kifua mbele. Sekta ya matibabu hatahivyo ina afadhali ikiwa na wanawake 12 walioshinda tuzo hiyo. Tuzo nyengine kama vile fasihi huwa na usawa wa kijinsia ,huku washinda waliopita akiwemo Alice Munroe, Doris Lessing na Toni Morrison. Mwaka huu, tuzo hiyo ya fasihi imemwendea mwandishi mwenye asili ya Kijapan na Uingereza kazuo Ishuguro. Huku harakati za kupigania usawa wa kijinsia zinazopigiwa upato na masharika kama vile Athena Swana na Stemettes zikiendelezwa ,tuzo za Nobel zinasalia kuwa kiwango cha juu zaidi katika ulimwengu wa sayansi. Ikiwa miongoni mwa chanagmoto za wanawake 100 mwaka huu,kundi moja huko Sillicon valley , ambapo wanawake wana nafasi moja kuu kati ya 10 litaangazia njia za kukabiliana na changomoto hiyo. Watatoa matokeo yao tarehe sita Ijumaa. Msimu wa Nobel wa 2017 unaendelea huku tuzo za amani , uchumi zikitarajiwa kutangazwa text: Iceland waliwashinda Croatia na Uturuki na kufuzu kutoka Kundi I Iceland, ambao walifika robofainali Euro 2016, baada ya kuwaondoa England hatua ya 16 bora, ni taifa la raia 335,000 pekee. Ndiyo nchi ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia ikiwa na idadi ya watu ambao ni chini ya milioni moja. Gylfi Sigurdsson wa Everton na Johann Gudmundsson wa Burnley ndio waliofungia taifa hilo Jumatatu. Sigurdsson aliwapa matumaini kwa kufunga muda mfupi kabla ya mapumziko na kisa akamsaidia Gudmundsson kufunga bao la kuwahakikishia ushindi. Iceland sasa wameshinda mechi saba kati ya 10 Kundi I la kufuzu kwa Kombe la Dunia. Mataifa madogo zaidi kuwahi kufuzu kwa Kombe la Dunia Mkufunzi alihofia sherehe zingewaathiri Mkufunzi wa Iceland Heimir Hallgrimsson alikuwa na wasiwasi kwamba angetatizika kuwapa motisha wachezaji wake baada ya kufana sana Euro 2016 nchini Ufaransa. "Bia ya kwanza baada ya sherehe huwa si nzuri. Jambo ngumu zaidi lilikuwa kuendeleza ufanisi baada ya sherehe yetu kubwa kutokana na ufanisi Ufaransa," alisema. "Na isitoshe, tulikuwa kwenye kundi lenye ushindani mkali lililokuwa na Croatia, Uturuki, Ukraine na Finland, nchi ambazo zinatuzidi kwa viwango vya soka. "Ufanisi huu si mwisho bali ni safari ndefu ya kuelekea hadi kwenye mwisho wa safari." Meneja wa Kosovo Albert Bunjaki amesifu sana Iceland kwa ufanisi wao na kusema kuwa hilo litatia moyo mataifa madogo. "Naipongeza timu yote ya Iceland," amesema Bunjaki, ambaye taifa lake la Kosovo lina watu mara sita zaidi ya Iceland. "Ni mfano mwema kwa mataifa madogo kama nchi yetu ambao hulenga kuwa na timu nzuri, yenye mpangilio mzuri, siku za usoni." Iceland imekuwa nchi ndogo zaidi kuwahi kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kuwalaza Kosovo 2-0 na kumaliza kileleni kundi lao la kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Urusi 2018. text: Hawa ni bakteria wanne ambao husababisha magonjwa makali ya zinaa ambayo yanaweza kuleta tishio la afya ya jamii. 1. Neisseria meningitides Neisseria meningitidis, pia hufahamika kama meningococcus husababisha uvimbe hatari wa tando za uti wa mgongo na ubongo. Lakini, bakteria huyo sasa anapata umaarufu zaidi kwa kusababisha maambukizi kwenye maungo ya uzazi. Utafiti mmoja uliofanywa miaka ya 1970 ulibainisha ni kwa namna gani dume moja la sokwe alihamisha bakteria hao hatari kutoka mdomoni na puani kwenda kwenye uume wake baada ya kujilamba sehemu zake nyeti. "Mnyama huyu (sokwe) mara kwa mara hujilamba uume wake," waandishi wa utafiti huo walibaini. Takribani asilimia 10 ya watu wazima wana bakteria aina ya Neisseria katika makoo na pua zao. Tafiti zinabainisha kuwa wanaweza kuhamisha bakteria hao kupitia mabusu makali yahusishayo ndimi, ama kunyonya sehemu za siri za watu ambao hawana bakteria hao. Watafiti hata hivyo hawana hakika ni kwa nini bakteria hao wamesambaa kwa kasi na kuzuz ugonjwa hatari kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja barani Ulaya, nchini Marekani na Canada. Hata hivyo, utafiti mmoja juu ya uwasho mkali wa mrija wa kupitisha mkojo toka kweye kibofu unaosababishwa na bakteria huyo ulibainisha kuwa wanaume waliopata maambukizi hayo kupitia ngono ihusishayo mdomo. Wanasayansi wanaamini kuwa, maambukizi makali ya bakteria huyo yaliyokumba kwa nguvu miji kadhaa ya Marekani mwaka 2015 yalichochewa na vinasaba vya karibu vya bakteria wa familia mojaNeisseria gonorrhoeae, ambaye husababisha ugonjwa mwengine wa zinaa wa kisonono. Ukaribu wa bakteria ha ulisababisha kusambaa kwa haraka kwa maambukizi hayo hatari. Kuna aina tano ya bakteria hatari wa Neisseria meningitidis duniani, lakini kwa bahati nzuri kuna chanjo za aina mbili ambazo zinapatikana na zinakinga dhidi ya aina zote za bakteria hao. 2. Mycoplasma genitalium Mycoplasma genitalium ni hatari sana kwa mfumo wa uzazi kwa wanawake Mycoplasma genitalium, moja ya bakteria wadogo zaidi wanaofahamika, wanapata umaarufu mkubwa zaidi ya maumbo yao kwa kusabisha maambukizi hatari ya ugonjwa wa zinaa. Bakteria huyo aligunduliwa miaka ya 1980, na leo hii anaambukiza asilimia moja mpaka mbili ya watu hususani vijana. Maambukizi ya Mycoplasma genitalium ambayo kwa kawaida hayana dalili, wakati mwengine hufanana na dalili za kisonono na kaswende kwa kuwashwa mfululizo kwa mrija wa mkojo kwa wanaume na mlango wa kizazi kwa wanawake. Kutokana na kuweza kusamabisha maumivu makali ya nyonga kwa wanawake, bakteria huyo anahusishwa pia ugumba, kuharibika kwa mimba, kuzaliwa watoto njiti na hata kufariki watoto tumboni kwa mama. Ijapokuwa kondomu inaweza kuzuia maambukizi yake, watafiti wanatoa tahadhari juu ya usugu wa bakteria huyo kutibika na dawa za antibaotiki za azithromycin na doxycycline. 3. Shigella flexneri Shigella flexneri hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao. Shigellosis husababishwa kwa kugusa moja kwa moja au kwa njia moja au nyengine kinyesi cha binadamu. Maambukizi ya bakteria ho hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao. Ijapokuwa ugonjwa huo umekuwa ukionekana zaidi kwa watoto na wasafiri kwenye nchi zenye uchumi mdogo na wa kati, watafiti walianza kupokea kesi za ugonjwa huo kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja toka miaka ya 1970. Ugonjwa huo, wanasayansi wanaamini, umechukuwa njia mpya ya maamukizi kwa kutumia ngono ya kinyume na maumbile na ngono inayohusanisha midomo na kusabisha maambukizi kadhaa ya gonjwa hilo la zinaa kwa miongo minne sasa. 4. Lymphogranuloma venereum (LGV) Magonjwa mengi ya zinaa yanaweza kuepukwa kwa kutumia kondomu LGV mwanzo hutokea kama kipele ama lengelenge na kisha kushambuli mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kupelekea uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi. Ugonjwa huu pia husababisha maambukizi katika njia ya haja kubwa na pia kusababisha maumivu makali ya tumbo. Katika miaka 10 iliyopita, kumekuwa na maambukizi makubwa ya LGV barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini hususani kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Kutumia kondomu kunaweza kupunguza uwezekano wa maambukizi, na kutibu ugonjwa huu kunahitaji walau matibabu ya wiki tatu na kunywa antibaotiki kama doxycycline. Magonjwa mapya huibuka kila uchao, na magonjwa yaambukizwayo kwa ngono nayo ni miongoni mwao. text: David de Gea aliichezea Sweden baad aya kuachwa kwenye benchi dhidi ya Norway wiki iliopita Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alionekana kuumiza msuli wake wa paja wakati wa mechi ya kufuzu taifa lake katika mashindano ya Euro 2020 dhidi ya Sweden. Kepa Arrizabalaga wa Chelsea alilazimika kuichukuanafasi yake baada ya saa moja huku upande wake ukifungwa 1-0. Bao la lala salama la Rodrigo lilisawazisha na mechi kuishia kwa sare ya 1-1 na kuipa fursa Uhispania kujikatia tiketi kwa mashindnao hayo ya Euro 2020. Jeraha la De Gea halikutokana na hali ya kuumizwa - alijishikilia nyuma ya mguu ghafla baada ya kupokea pasi ya nyuma kutoka kwa mchezaji mwenzake. Alikaa chini kwenye lango lake kabla ya kusaidiwa kuondoka uwanjani na wahudumu wa afya. United ipo katika nafasi ya 12 kwenye Premier League na haijafanikia kupata ushindi katika mchi tatu zilizopita za juu. Itakabiliana na Liverpool inayopania kupata ushindi wa 18 katika ligi hiyo, jumla itakayo kuwa sawa na rekodi inayoshikiliwa na Manchester City. De Gea alikosoa mchezo wa timu yake msimu huu baada ya mechi ya mwisho iliyoishia kwa kufungwa 1-0 na Newscastle - akisema: "Msimu mzima haukubaliki kwetu. "Tuna wachezaji waliojeruhiwa lakini hicho sio kisingizio. Sisi ni Manchester United. Tunahitaji kufanya mazoezi sana ili kuweza kuendelea kupambana na turudi kushinda mechi." Iwapo De Gea hatoweza kushiriki mechi Old Trafford mwishoni mwa juma, Argentine Sergio Romero - aliyeshirikishwa katika ligi ya Uropa na kombe la Carabao msimu huu - huenda akawekwa kuichukua nafasi yake. Kipa wa man United David de Gea anatiliwa shaka kushiriki katika mechi ya ligi kuu England au Premier League dhidi ya Liverpool Jumapili baada ya kujeruhiwa katika kibarua huko Uhispania. text: City waliweka mwanya wa alama 11 kileleni Ligi ya Premia kati yao na United walipowalaza Jumapili Hata hivyo, amesema hawezi kuomba radhi eti kwa sababu Jose Mourinho alikereka. Mourinho alirushiwa maziwa nje ya chumba cha kubadilishia mavazi baada yake kwenda kulalamikia jinsi City walivyokuwa wakisherehekea baada ya kushinda debi ya Manchester Jumapili. "Iwapo tuliwakera United - sio mchezaji mmoja, au Jose - Manchester United, basi naomba radhi," amesema Mhispania huyo. Mourinho amesema matukio hayo baada ya ushindi wa City wa 2-1 yalikuwa "tofauti ya kitabia, na kielimu". Kisha, alikamilisha kikao chake na wanahabari Jumanne kwa kudokeza kwamba kuendelea kuangaziwa kwa matukio hayo kunaashiria kutowaonea heshima Bournemouth, ambao watacheza dhidi ya United baadaye Jumatano. Chama cha Soka cha England kimezipatia klabu hizo mbili za Manchester hadi Jumatano kujibu kuhusu yaliyotokea wakati huo. Hata hivyo Guardiola amesema wachezaji wana haki ya kusherehekea, hasa baada ya ushindi huo kuwafanya kuwa alama 11 mbele ya United. "Ni lazima tufurahie haya. Iwapo watu hawaelewi, basi pole. Tulishinda debi," alisema. "Iwapo hatukuwa sahihi, basi nawaomba radhi Manchester United. Nia yetu haikuwa hiyo. Nia yetu ilikuwa kusherehekea ndani ya chumba cha kubadilishia mavazi." Uhasama Mourinho alikimbia uwanjani Nou Camp kusherehekea baada ya Inter Milan kuwalaza Barcelona nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2010 Mourinho na Guardiola walifanya kazi pamoja Barcelona, Mourinho akiwa msaidizi wa wakufunzi na Pep mchezaji, lakini uhusiano wao umedorora. Alipoondoka Chelsea 2007, Mourinho anadaiwa kuhojiwa na wakuu wa Barcelona kuhusu kazi ya umeneja lakini badala yake Guardiola ambaye hakuwa na uzoefu mwingi kama yeye akapewa kazi hiyo Frank Rijkaard alipoondoka. Miaka miwili baadaye, Mourinho alikimbia uwanjani Nou Camp kusherehekea baada ya Inter Milan kuwalaza Barcelona nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2010. Guardiola alibaki kushangaa. Akiwa Real Madrid, Mourinho alimwelekezea kidole jichoni msaidizi wa Guardiola Tito Vilanova na kudokeza kwamba Barca walikuwa wanapendelewa na waamuzi na maafisa wa Uefa. Guardiola alipoondoka Barca na kuchukua likizo kutoka kwa soka 2012, Mourinho alisema ni hatua ambayo "haiwezi kufikirika". "Yeye ni mdogo wangu, lakini mimi sijachoka," alisema. Guardiola akisherehekea na wachezaji wake Jumapili Guardiola naye amesema kuwa anapotazama na kuzipima timu zinazosimamiwa na Mourinho huwa hataki kujifunza kutoka kwa 'vituko' vya Mourinho pembeni mwa uwanja. Wote wawili walipewa kazi Manchester majira ya joto 2016 na walikutana mara tatu msimu uliopita, City wakashinda ligini Old Trafford Septemba, United wakashinda Old Trafford mechi ya Kombe la Ligi na mechi ya ligi ya Etihad Aprili ikaisha kwa sare tasa. Kabla ya mechi ya Jumapili, Mourinho alidokeza kwamba wachezaji wa City hujiangusha na kufanya makosa ya kiufundi ili kufaidi kwenye mechi. Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema anaomba radhi kwa Manchester United iwapo sherehe za City baada ya kuwashinda mahasimu hao wao wa jiji ziliwakera. text: Paul Whelan was held in December after taking a group on a tour of the Kremlin museums Akizungumza na BBC, Bwana Mr Whelan, ambaye pia ni raia wa Uingereza, Canada na Ireland, amesema kuwa rafiki yake alikuwa amemuwekea kifaa cha kunasa sauti kwenye mfuko wake bila yeye kujua. Kesi ya rufaa ya Whelan mwenye umri wa miaka 48- ya kupinga kufungwa kwake mahabusu ilikataliwa na mahakama ya Moscow. Waendesha mashtaka walisema kuwa ''alikamatwa akifanya ufasusi '' na maafisa wa ujasusi wa taifa la Urusi mwaka jana. Uchunguzi sasa umemalizika, na mawakili wa Bwana Whelan wameanza kuchunguza ushahidi dhidi ya mteja wao. Kwasababu ni kesi ya ujasusi, taarifa zote kuhus mashtaka yanayomkabili zinafichwa. Balozi wa Marekani mjini ambassador ametoa wito kwa Urusi kuacha "kufanya mzaha " na kesi . Paul Whelan amesema nini? Bwana Whelan ana uraia wa Marekani , Uingereza, Canada na Ireland Katika mazungumzo ya muda mfupi kupitia vioo vya kizimbani alipokuw amahakamani, Bwana Whelan alielezea hadithi yake kwa mara ya kwanza. Mwandishi wa BBC mjini Moscow Sarah Rainsford anasema Alimwambia kuwa alikuwa amefanyiwa hila , na kwamba hakutekeleza uhalifu wowote . "Mtu alikuja katika chumba changu cha hoteli na kuweka kitu ndani ya mfuko wangu, halafu nikakamatwa " Alisema Bwana Mr Whelan. "Mtu huyo alikuwa ni afisa wa huduma za usalama za Urusi FSB . Mtu ambae nilimfahamu kwa miaka 10. Hapakuwa na sababu kabisa ya mtu yule kuwepo chumbani kwangu . Hakuna sababu ya wao kunipatia kifaa hicho(flash drive)." Alipoulizwa na BBC ikiwa kulikuwa na siri za taifa kwenye kifaa hicho , kama waendeshamashtaka walivyosisitiza , Bwana Whelan alisema kuwa "hakufahamu ". "Sikukiangalia kifaa chenyewe . Sikujua kuwa nilikuwa nacho mpaka nilipokamatwa . Huu ni uchokozi asilimia 100% na ni mbaya sana ," alisema. Wakili mtetezi wa mshtakiwa ladimir Zherebenkov pia aliielezea kesi hiyo kama ''uchokozi'' , na kuongeza kuwa hakuona ushahidi hadi sasa wa kumweka mteja wake hatiani Bwana Whelan ameendelea kupata mkanganyiko na ni wazi kuwa amekanganyikiwa , anasema mwandishi wa BBC Jaji alirejea kusoma hukumu dhidi yake - na kusema kuwa anapaswa kuwekwa mahabusu, kabla ya kufanyika kwa kesi dhidi yake na ndipo Bwana Whelanalipopaza sauti kupinga kesi yake akiitaja kama "takataka". Bwana Whelan, ambaye amesema kuwa aliumizwa na daktari na kukataa matibabu , pia amezitaka serikali zote za mataifa yake kumsaidia. Ni kwanini alikamatwa ? Bwana Whelan aliwasili Urusitarehe 22 Disemba kuhudhuria harusi na alikuwa na mpango wa kutembelea St Petersburg pamoja na Moscow kabla ya kurejea nyumbani tarehe 6 Januari, kulinga na maelezo yaliyotolewa na kaka yake alipozungumza na BBC. Akikamatwa mjini Moscow baada ya kuchukua kikundi cha wageni waliokuwa wakihudhuria harusi katika matembezi kwenye makumbusho ya Kremlin Maafisa wa huduma za ujasusi za Urusi FSB wanasema alikamatwa "wakati alipokuwa akifanya kitendo cha uchunguzi wa ujasusi ". Whelan ni nani ? Bwana Whelan alizaliwa nchini Canada na wazazi wake walikuwa Waingereza lakini akahamia Marekani alipokuwa mtoto . Kwa sasa ni Mkuu wa usalama wa kampuni ya Michigan automotive components supplier BorgWarner. Kaka yake anasema Bwana Whelan amekuwa akitembelea Urusi kwa shughuli za kibiashara na za burudani tangu mwaka 2007. Bwana Whelan alijiunga na kikosi cha wanamaji cha Marekani mwaka 1994 na kupanda hadi cheo cha Sajenti mwama 2004. Alihudumu nchini Iraq kwa miezi kadhaa katika miaka ya 2004 na 2006. Mwanajeshi wa zaman wa kikosi cha majini cha Marekani Paul Whelan, ameishutumu Urusi kwa kufanya upelelezi wa kijasusi na akasema yeye sio jasusi ila alipangiwa njama na rafiki yake Mrusi. text: Rais Magufuli baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika ibada iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mnamo 31 Desemba Kuanza kwa mwaka huu, katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, kuna mambo ambayo tayari yamegusa hisia za wengi. Takriban idadi kubwa ya nchi hizi zinaonekana hazijaanza mwaka vizuri. Mathalan, kule nchini Kenya, ajali ya basi baada ya kugongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo vya takriban watu 40 na wengine kujeruhiwa. Haikuwa habari nzuri kwa ajali hiyo ambayo imetokea siku moja tu kabla ya kuanza mwaka huu. Msiba huu mbali na kugusa nyoyo za wengi, lakini pia ilimgusa rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta ambaye alituma salamu zake za rambirambi kwa taifa lakini zaidi kwa wafiwa. Kana kwamba hiyo haitoshi, nako nchini Uganda, tumeshuhudia kifo cha polisi, hii ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya namna hiyo ambayo yamekuwa yakilenga askari nchini humo. Maandamano dhidi ya Kabila Nchini DRC nako, waliamua kuukaribisha mwaka kwa namna yake, nayo haikuwa nyingine bali kufanya maandamano yanayopinga kuendelea kwa Rais Joseph Kabila kuwepo madarakani. Maandamano hayo yalisababisha vifo vya watu wanane. Nchini Tanzania hali ilikuwa tofauti kidogo. Viongozi wa dini nchini humo, kwa pamoja waliamua kutumia sikukuu ya Krismasi na ile ya Mwaka Mpya, kuhutubia amani lakini zaidi kuinyooshea kidole serikali kwa maana ya kuikosoa katika baadhi ya mambo. Aliyefungua ukurasa huo si mwengine, bali ni askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe ambae amenukuliwa akiitaka serikali itoe fursa kwa vyamba vya upinzani kutekeleza wajibu wake. Watu 36 walifariki katika ajali iliyohusisha lori la basi la uchukuzi wa abiria eneo la Migaa barabara ya kutoka Nakuru kwenda Eldoret nchini Kenya Hii ni baada ya serikali kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa vyama vya kisiasa. Hatua ambayo, wengi wanaiona kama ni ukandamizwaji wa demokrasia. Hata hivyo, kauli za viongozi hawa wa dini kwa serikali haikupokewa vizuri. Serikali kuwaonya viongozi wa kidini Inaonekana tayari kumeibuka mvutano baina ya serikali na baadhi ya viongozi wa dini ambao kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakionyesha kuwa na mtizamo tofauti na serikali, hasa katika suala zima la kuikosoa katika baadhi ya mambo. Serikali ya Tanzania imewatahadharisha viongozi hao wa dini kwa kuwa wanaingilia siasa. Hivyo kuwataka wakae mbali kabisa masuala ya kisiasa. Kauli hii ya serikali inaonekana kuzua mjadala mkali nchini, huku baadhi wakihoji ni ipi mipaka ya dini na siasa? Au ni wapi au ni wakati gani ambapo viongozi wa dini wanaruhusiwa kuzungumzia siasa na ni wakati gani ambapo hawaruhusiwi? Tayari, baadhi wameshuhudia wakati fulani wanasiasa wakikimbilia kwa viongozi wa dini na kuwataka wazungumze na wafuasi wao baadhi ya mambo ya siasa. Na sio hivyo tu, baadhi ya wanasiasa wameonekana mara kadhaa wakikimbilia katika nyumba za ibada hasa wanapoona mambo yamewafika kooni, aidha kwa kutaka kuombewa au kuwaomba viongozi wa dini kutumia ushawishi wao kwa wafuasi wao ili wawapigie kura. Ni kwa sababu hiyo, ndio maana msimamo wa serikali dhidi ya viongozi wa dini unaonekana kupokelewa kwa hisia tofauti. Ingawa wapo wanaoungana na serikali kwa kuona kwamba viongozi wa dini jukumu lao ni la kiroho zaidi hivyo wajikite katika masuala kama vile ya ndoa, kutoa sadaka na kuhimiza watu kufanya ibada. Maalim Seifn anaamini viongozi wa kidini wana haki kuikosoa serikali Lakini pia wapo wasiokubaliana na fikra hiyo. Kwa mfano, Maalim Seif ambaye ni katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ameshauri viongozi hao waachwe wazungumze kwa sababu bila shaka watakuwa wameona kasoro za kiutendaji serikalini. Akinukuliwa na moja wa gazeti maarufu nchini Tanzania, Maalim ambaye pia amewahi kuwa makamu wa rais wa kwanza Katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar amesema viongozi wa dini bila shaka itakuwa wamehisi kuna kasoro ndani ya serikali ndiyo maana wameamua kutoa dukuduku. Ni mara ya kwanza? Hata hivyo, ikumbukwe kwamba, hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini kuibuka na kuanza kuinyooshea vidole serikali iliyopo madarakani. Hayo yametokea katika awamu zote, ikiwemo serikali ya awamu ya nne ambayo ndio imetoka madarakani. Mara kadhaa viongozi wa dini walionyesha kutoridhishwa kwao kwa jinsi mambo yanavyokwenda. Na hii pia sio mara ya kwanza kwa mjadala wa viongozi wa dini kulaumiwa kwa misingi ya kuchanganya dini na siasa kuibuka. Ingawa wapo wanaoamini kwamba, viwili hivi katu haziwezi kuepukika kwani uhusiano wake ni wa karibu sana, aidha kimoja kipo kwa mwengine, au kingine kimemmeza mwenzake. Siasa katika mahubiri Pierre Whalon, ambaye ni askofu wa mkusanyiko wa makanisa katika nchi za Ulaya anasema, kwa mara kadhaa amekuwa akifuatwa na watu na kuambiwa aache kuingiza siasa katika mahubiri yake. Hata hivyo, anasema, muhimu ifahamike katika historia ya binadamu kwamba siasa na dini ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutenganishwa. "Kwa maana hiyo, haiwezekani kutenganisha dini na siasa, na yeyote anayejaribu kufanya hivyo, aidha anadanganya au hajafikiria vizuri," anasema mchungaji huyo katika moja ya makala zake yenye kichwa, 'Religion and Politics Are Inseparable: Get Over.' (Dini na Siasa haziwezi Kutenganishwa: Kubali hayo). Suala la dini na siasa ni la muda mrefu sana, na halijazua mjadala katika nchi za Kiafrika pekee, bali hata katika zilizoendelea ambazo wengi wanaamini kwamba ndipo kwenye ukomavu wa demokrasia. Swali hili pia limejitokeza katika kitabu kiitwacho, Religious Convictions and Political Choice (Itikadi za Kidini na Uamuzi wa Kisiasa), kilichoandikwa na Kent Greenawalt. Swali hilo hilo, limejibiwa katika kitabu cha zaidi ya kurasa 200, lakini mwisho wa siku, imeonyesha dhahiri kwamba, siasa na dini vina ukaribu mkubwa sana, na imani ya dini siku zote ina ushawishi mkubwa sana hata kwa wanasiasa wenyewe. Mwaka 2018 hatimaye umeanza. Wengi wamekuwa wakiusubiri kwa hamu wakidhani kwamba, huenda kuanza kwa mwaka mpya kunaweza kuleta mambo mapya au afueni katika baadhi ya mambo ambayo kwao pengine yalikuwa na ugumu kwa mwaka uliopita. text: Kumekuwa na mjadala ikiwa Ali Bongo ni mwana wa Omar Bongo ikizingatiwa kuwa mama yake alikuwa mja mzito miezi 18 kabla ya kuolewa madai ambayo Ali Bongo amekuwa akipinga. Aidha, wakati wa kuzaliwa kwake mamake alikuwa na miaka 15. Baada ya kusomea uwanasheria Ali Bongo alijitosa katika siasa za Gabon ambapo alijiunga na chama PDG mwaka 1981 na muda mfupi baadae aliteuliwa katika kamati kuu ya chama mwezi Machi mwaka 1983. Baadae aliteuliwa kumwakilisha baba yake katika chama hicho nafasi ambayo ilimwezesha kujiunga na asasi kuu ya uongozi wa chama katika uamuzi ambao ulifikiwa katika kongamano maalum ya PDG mwaka 1986. Ali Bongo ni mwana wa kiume wa rais Omar Bongo, ambaye aliongoza Gabon kiimla kutoka mwaka 1967 hadi alipofariki dunia mwaka 2009. Ali Bongo amemuoa mzaliwa wa Ufaransa Sylvia, ambaye hapa anaonekaa akiwa na watoto wao wanne Wakati wa utawala wa baba yake Ali Bongo aliwahi kuhudumu kama waziri wa mambo ya nje wa wa Gabon kati ya mwaka 1989 na 1991. Pia aliwahi kuhudumu kama naibu kiongozi wa bunge la kitaifa kuanzia mwaka 1991 hadi 1999. Wakati wa uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2005 alifanya kazi kama mshirikishi wa vijana katika kampaini ya baba yake. Baada ya uchaguzi huo alipandishwa cheo na kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Gabon kuanzia Januari 21 mwaka 2006 huku akiendelea kushikilia wadhifa wa waziri wa ulinzi. Rais Ali Bongo wa Gabon Alishikilia wadhifa huo hadi mwaka 2009. Ali Bongo alitarajiwa kuwa mrithi wa baba yake Omar Bongo ikizingatiwa kuwa alimteua katika nyadhifa muhimu katika utawala wake. Hata hivyo uungwaji mkono wa Ali Bongo ndani ya uongozi wa chama cha PDG ulihojiwa na vyombo vya habari na kulikuwa na maoni kwamba raia wengi wa Gabon walimchukulia kama ''mtoto aliyedekezwa na kwamba hawezi kuwasiliana kwa lugha asilia ya nyumbani kwasababu alizaliwa Congo-Brazzaville, kulelewa nchini Ufaransa. Kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa madarakani kwa miaka 41, alichaguliwa kuendelea na uongozi wa taifa hilo mwezi Agosti mwaka 2009. Siku chache baada ya uchaguzi uliyofanyika Agosti 30 mwaka 2009 alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata 42% ya kura. Matokeo ya uchaguzi huo yaliidhinishwa mara moja na mahakama ya kikatiba. Upinzani ulipinga matokeo hayo rasmi ya uchaguzi ukidai kuwa ulikumbwa na udanganyifu. Hatua ambayo ilisababisha maandamano makubwa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Gabon. Nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi alizuru Gabon mwaka 2015 Ili kujibu madai hayo mahakama ya katiba iliamuru kuwa kura za uchaguzi wa uraisi zihesabiwe upya. Ali Bongo aliibuka tena mshindi baada ya kupata 41.79% ya kura zote zilizopigwa wakati wa uchaguzi uliyofanyika oktoba 12 mwaka 2009. Aliapishwa kuwa raisi wa Gabon oktoba 16 katika hafla iliyohudhuriwa na marais kadhaa wa mataifa ya Afrika. Rais Ali Bongo ana mke na watoto wanne. Ali Bongo Ondimba alizaliwa Februari 9 mwaka 1959 mjini Brazzaville na alifahamika kama mwana wa Alain Bernard Bongo (ambaye baadaye alifahamika kama Omar Bongo Ondimba) na Josephin Kama (baadaye Patience Dabany). text: Kwa mujibu wa utafiti mpya uliyofanywa nchini Uingereza, wananawake wanastahili kupewa ushauri sawa na wanaume na pia kupewa ushauri wa kuachana na uvutaji sigara. Watafiti wanatoa wito kwa madaktari kusaidia katika harakati ya kuwatambua wanawake waliyo katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo. Hata hivyo watafiti hao wanasema wanaume bado wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo mara tatu zaidi ya wanawake. Utafiti huo uliyofanywa na watafiti wa chuo kikuu cha Oxford ulijumuisha karibu watu 500,000 waliyo na miaka kati ya 40-69 ambao wameorodheshwa katika data ya afya ya Uingereza. Watafiti walibaini kuwa watu, 5,081 waliyofanyiwa uchunguzi walikabiliwa na mshuko wa moyo zaidi ya miaka saba na wengi wao ni wanawake. Japo hatari ya kupata mshtuko wa moyo kwa wanawake iko chini kuliko wanaume wa miaka yote, kuna baadhi ya sababu zinazowafanya waopi kuwa katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo. Wanawake wanaovuta sigara wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo kuliko wale ambao hawavuti sigara. Wanaume wanaovuta sigara wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo mara mbili zaidi. Shinikizo la damu linaongeza hatari ya wanawake kupata mshtuko wa moyo kwa 83%. Utafiti pia umebaini kuwa aina ya kwanza na ya pili ya kisukari zinawaweka wanawake katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo kuliko wanaaume Watafiti wanasema sababu za kibayolojia huenda zikachangia hali hiyo. Kwa mfano aina ya pili ya kisukari,ambayo mara nyingi inahusishwa na mtindo wa maisha ya mtu binafsi huenda ikaathiri zaidi moyo wa mwanamke kuliko ule wa mwanamume. Hata hivyo utafiti unasema kuwa wanawake hawana ufahamu kwamba wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na huenda wakawa wanapokea matibabu yasiyofafaa. Watafiti aidha wanasema wanaume pia huenda wakawa katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo lakini ugonjwa huo umechangia pakubwa vifo vya wanawake nchini Uingereza. Dalili za mshtuko wa moyo Kwa mujibu wa mtandao wa huduma ya kitaifa ya afya nchini Uingereza mtu anastahili kutafuta ushauri wa kimatibabu akijipata na dalili hizi. Japo kuumwa na kifua huwa ni dalili mbaya zaidi, baadhi ya watu huenda wakahisi maumivu kidogo kifuani na katika visa vingine huenda mtu asiumwe na kifua kabisa. Dalili hizo sana sana zimeelezewa kuwapata wanawake, wazee na watu wanaougua kisukari. Jinsi ya kuboresha afya ya moyo wako: Dkt Elizabeth Millett, mtafiti mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Afya kutoka chuo Kikuu cha Oxford, amesema ugonjwa wa moyo pia una waathiri wanawake na kwamba hilo linastahili kutiliwa maanani. "Wanawake wanatakiwa kujua kuwa wako hatarini, lakini licha ya kampeini nyingi kuhusiana na ugonjwa huo bado baadhi yao hawajalitilia maanani. Ameongezea kuwa siku zijazo idadi ya wanawake wanaofariki kutokana na ugonjwa itakuwa sawa na ya wanaume. Wanawake wanaovuta sigara, wanaougua kisukari au waliyo na tatizo la shinikizo la damu wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo. text: Polisi waliwatia mbarani watu 40 wanaodaiwa kushiriki kwenye maandamano mwezi uliyopita nchini Tanzania Polisi jijini Dar es Salaam imethibitisha kukamatwa kwa watu kumi na moja kwa tuhuma za kushiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima yenye lengo la kupinga utawala wa Rais John Pombe Magufuli. Hayo yamethibitishwa na kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamanda Lazaro Mambosasa. "Wawili walikuwa ni wanafunzi wa chuo cha diplomasia na watu tisa walikamatwa katika mtaa wa Samora. Mmoja wao amekutwa akiwa amevaa koti, ambalo ndani yake lilikuwa na bango na alikuwa na tisheti iliyokuwa inashiria kuwa alikuwa akitaka kufanya maandamano.Tukikamilisha upelelezi watafikishwa mahakamani. Hali ya jiji kwa sasa hivi ni shwari." 'Mitaa meupe' Maandamano hayo yaliandaliwa na mwanaharakati wa kisiasa kwenye mitandao ya kijamii, aliyopo Marekani, Mange Kimambi. Katikati ya mji wa Dar es Salaam eneo la Posta: ndipo mahali ambapo palisemekana waandamanaji wangekutana, lakini hakuna kilicho tokea Wakati huo huo, sehemu kubwa ya nchi hasa mijini, ilibaki kimya huku vikosi vya usalama vikionekana kushika doria katika miji mikubwa, hali inayoelezewa kuleta hofu miongoni mwa wananchi. Kumekuwa na ukimya katikati mwa mji wa Dar es Salaam wakati siku za kawaida watu hupishana Siku Jumanne watu 7 walikamatwa kuhusiana na maandamano ya Aprili 26 Tanzania mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania. Bi Mange Kimambi amekuwa akifanya juhudi za kuandaa maandamano kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwa zaidi ya mwezi mmoja. 'Onyo Kali' Serikali iliwajibu kwa onyo kali. Mitandao ya kijamii yalivuma na picha na video za vikosi vya askari wakiwa na silaha nzito wakipiga doria katika miji mikubwa Tanzania. Mkuu wa polisi wa mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto aliwaambia waandishi wa habari kuwa wale waliopanga kufanya maandamano leo wangeshughulikiwa vilivyo. Gilles Muroto Rais Magufuli mwenyewe, katika maadhimisho ya muungano kati ya Tanganyika na Zanizibar hakusema lolote kuhusu maandamano hayo, bali kusisitiza Watanzania kuendelea kudumisha amani na wasikubali kutumika kuivuruga amani ya nchi. 'Watu wachache' Bi Kamambi alishiriki katika maandamano siku ya Jumatano, nje ya ubalozi wa Tanzania mjini Washington, akiwa pamoja na watu wengine waliokuwa wanaomuunga mkono. Waandamanaji Ujerumani Watu wachache walijitokeza katika baadhi ya miji ya Ulaya pamoja na nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini. Maandamano hayo yalilenga kuipinga serikali ya Magufuli ambayo imeshutumiwa kuzidi kuuminya uhuru wa kujieleza tangu alipoingia madarakani zaidi ya miaka miwili iliyopita. Maoni Maoni Maoni Je, kukosa kwa maandamano kufanyika kuna maana gani? Mchambuzi wa masuala wa siasa Rashid Chilumba, anasema hakutegemea kwa watu kujitokeza kwa wingi kuandamana dhidi ya serikali sababu ya historia ya Watanzania na maandamano. Anasema watu nchini Tanzania wanatabia ya kuandamana kukiwa na jambo lililowakera katika wakati huo huo, na wakati huo huo wakapata hamasa ya kutoka na kuonyesha makovu yao. Pamoja na hayo, vitisho vya serikali kusema wangeshughulikia waandamanaji kikamilifu na vikosi vya jeshi kupiga doria iliwatia watu hofu. Maandamano ya kitaifa yaliyopangwa nchini Tanzania, hayakufanikiwa kutokea leo baada ya Polisi kuwaonya waandamanaji kutoingia barabarani. text: Tumeangalia baadhi ya data zinazoangazia hali ya uhalifu na haki nchini Marekani, kubaini zinasema nini kuhusu maisha ya Wamarekani weusi linapokuja suala la utekelezaji wa haki na sheria. 1. Wamarekani weusi wako katika hatari ya kuuawa kwa kupigwa risasi ramani inayoonyesha mauaji ya risasi na idadi ya watu kulingana na jamii Takwimu zilizopo zinaonesha katika visa ambapo polisi wamepiga risasi na kuua, idadi ya Wamarekani weusi inakadiriwa kuwa juu ikilinganishwa na watu wa jamii zingine nchini Marekani. Inasadikiwa kuwa, mwaka 2019, japo Wamarekani weusi walichangia asilimia 14 ya idadi jumla ya watu nchini Marekani (kwa mujibu wa sensa rasmi), walikadiria zaidi ya asilimia 23 ya vifo 1,000 vilivyotokana na kupigwa risasi na polisi. Na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka tangu mwaka 2017, wakati idadi ya Wamarekani weupe walioathiriwa ikiendelea kupungua kutoka wakati huo 2. Wamarekani weusi wengi wanakamatwa kwa utumizi wa dawa za kulevya Idadi ya Wamarekani weusi wanaokamatwa kutokana na utumizi wa dawa za kulevya iko juu kuliko ya Wamarekani weupe, japo uchunguzi unaonesha viwango vya matumizi ya dawa za kulevya kati ya jamii hizi viko sawa. Mwaka 2018, karibu watu 750 kati ya kila Wamarekani weusi 100,000 walikamatwa kwa kosa la utumizi wa dawa za kulevya, ikilinganishwa na karibu watu 350 kati ya kila Wamareekani weupe 100,000. Tafiti zilizopita za kitaifa kuhusu utumizi wa mihadarati zinaonesha watu weupe wanatumia dawa za kulevya kwa viwango sawa, lakini Wamarekani weusi wanaendelea kukamatwa kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano, utafiti uliofanywa na Muungano wa Uhuru wa Raia wa Marekani, ulibaini kuwa Wamarekani weusi walikuwa katika hatari ya kukamatwa mara 3.7 wakipatikana na bangi ikilinganishwa na Wamarekani weupe, japo matumizi yao ya bangi ni sawa. 3. Wamarekani weusi wanafungwa zaidi Wamarekani wenye asili ya Kiafrika wanakabiliwa na tishio la kufungwa mara tano zaidi ikilinganishwa na Wamarekani weupe mara miili zaidi ya Wamarekani wenye asili ya Kihispania, kwa mujibu wa data za hivi karibuni. Mwaka 2018, Wamarekani weusi walikadiria 13% ya idadi ya watu Marekani, lakini karibu thuluthi moja ya idadi ya wafungwa nchini humo ni wao. Wamarekani weupe wanakadiriwa kuwa karibu 30% ya wafungwa licha ya idadi yao kuwa zaidi ya 60% ya watu wote nchini Marekani. Hii inamaanisha kuna zaidi ya wafungwa 1,000 kwa kila Wamarekani weusi 100,000, ikilinganishwa na wafungwa 200 kwa kila Wamarekani weupe 100,000. Ghasia zimeibuka katika miji tofauti nchini Marekani kufuatia kifo cha George Floyd, raia wa nchi hiyo mwenye asili ya kiafrika ambaye alikuwa amekamatwa na polisi. text: Jamii ya Wakristo wa Iraq ni moja ya jamii za kale zaidi duniani katika hojtuba aliyoitoa mjini London, Askofu Rev Bashar Warda alisema kuwa Wakristo wa Iraq sasa wanakabiliwa na hatari ya kutoweka baada ya miaka 1,400 ya kuuawa. tangu majeshi ya marekani yalipovamia Iraq na kuuondoa madarakani utawala wa Saddam Hussein mnamo mwaka 2003, amesema, jamii ya Wakristo imepungua kwa 83%, kutoka watu milioni 1.5 hadi watu 250,000. "Ukristo nchini Iraq," amesema , "ambao ni moja ya makanisa ya kale, kama si ya kale zaidi duniani, unakaribia kutoweka. Wengine wetu tuliobakia lazima tuwe tayari kukabiliana na kufia dini ." Alikuwa anazungumzia tisho kubwa la hivi karibuni kutoka kwa wapiganaji wa jihadi wa Islamic State (IS) kuwa ni "vita vya mwisho vya wakristo", kufuatia mashambulizi ya awali ya kundi hilo mnamo mwaka 2014 yaliyowasambaratisha wakristo 125,000 kutoka makazi yao asilia. Akamatwa Uhispania kwa 'kufadhili wapiganaji wa IS' Kiongozi wa IS 'ajitokeza baada ya miaka 5 mafichoni' Marekani yawaondoa wafanyakazi wake Iraq "Wanaotutesa wanamaliza uwepo wetu ," alisema, "huku wakitaka kupangusa historia yetu na kuangamiza maisha yetu yajayo. Nchini Iraq hakuna fidia kwa wale waliopoteza mali zao, nyumba wala biashara. maelfu kwa maelfu ya wakristo hawana la kuonyesha kuhusu maisha yao ya kazi, katika maeneo ambapo familia zao zimeishi, labda kwa miaka elfu moja. Islamic State wanaofahamika katika ulimwengu wa kiarabu kama Daesh, walifukuzwa kutoka ngome yao ya mwisho ya Baghuz nchini Syria mwezi machi baada ya kushambuliwa na wanajeshi wengi wa mataifa mbali mbali na kusema kuwa ulikuwa ndio mweshi wa "mtawala wa kiislamu". Kabla ya hapo, kundi la Islamc State lilikuwa limefukuzwa kutoka mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq wa Mosul mwezi wa Julai 2017. Lakini makanisa , majengo ya kidini na nyumba za familia za Wakristo zimekuwa zikiangamizwa na maelfu ya familia hazijarejea tena. Wiki hii Askofu mkuu ameonya juu ya kile alichosema kuwa ni ongezeko la makundi yenye itikadi kali yanayoamini kuwa mauaji ya Wakristo na Wayazidi yalisaidia kueneza Uislamu. 'Usahihi wa kisiasa' Askofu huyo aliendelea kuwashutumu viongozi wa kikristo wa Uingereza kwa kile alichokitaja kuwa ni "usahihi wa kisiasa" juu ya suala - jambo ambalo alisema ni kushindwa kulaani itikadi kali "saratani ", akisema hawazungumzii kwa sauti ya kutosha kutokana na hofu ya kushutumiwa kwa kuwa na ubaguzi dhidi ya Uislamu. "Utaendelea kukubali uovu ambao hauishi, mauaji ya kupangwa dhidi yetu ?"alisema. "Wakati wimbi lijalo la ghasia linaanza kutupiga, kuna hata mmoja wenu ambaye atachukua jukumu la kuitisha maandamano na kuonyesha ishara zinazosema 'Sote ni wakristo'?" Wakristo wa Iraqi wamekuwa wakilengwa kwa mashambulizi na wanamgambo wa Kiislamu wakiwe IS Maoni yake juu ya usahihi wa kisiasa yanaungwa mkono kwa kwa upande mmoja na Analogy wa Truro, Rt Rev PhilipFC Mounstephen, mbaye ni mwenyekiti wa ofisi huru ya udhibiti wa mauaji ya Wakristo Katika mataifa ya kigeni duniani. "Ninadhani Askofu anasema ukweli kwamba utamaduni wa"usahihi wa kisiasa" umeyazuwia mataifa mataifa ya magharibi kuzungumza juu ya mauaji ya Wakristo," alisema. " Ninadhani hata hivyo hii hasa inasababishwa na hali ya kusita sita kuchukua hatua kutokana na majuto ya baada ya ukoloni ." Askofu Mounstephen anasema kwamba mauaji ya Wakristo yanapaswa kuangaliwa kwa mtizamo mpana wa kidunia na yanatokana na sababu mbalimbali. "Tukiangalia tu kwa mtizamo wa wanamgambo wa kiislamu ," tutawaacha watu wengine ambao wanapaswa kuwajibika kwa mauaji." Ukiangalia kwa mtizamo wa kihistoria, Askofu mkuu wa Irbil alilalamikia ukweli kwamba kwa karne nyingi kulikuwa na kipindi cha furaha cha ushirikiano uliozaa matunda miaka ya nyuma baina ya Waislamu na Wakristo nchini Iraq. Wakati mwingine wanahistoria waliuelezea wakati huo kama Kipindi cha Dhahabu cha Uislam. "Mababu zetu Wakristo walishirikiana na Waislamu Waarabu fikra za kitamaduni na filosofia," anasema Askofu Warda. "Walizungumza na nao katika mazungumzo yenye heshma kuanzia karne ya 8. "Aina ya mazungumzo ya maelewano, na ambayo yalifanyika tu kwasababu ya viongozi wakuu wa dini ya kiislamu walivumilia Jamie za walio wacheche.Wakati uvumilivu ulipokwisha ,utamaduni na utajiri uliotokana nao pia ukaisha." 'Wakati wa ukweli' Kwingineko katika Mashariki ya katika Mashariki ya Kati kuna picha tofauti kwa Wakristo mwaka 2019. Wakoptiki wa Misti, ambao ni asilimia 10 ya raia zaidi ya milioni 100 wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa Mara kutoka kwa wanamgambo wa jihadi ambao walilipua makanisa yao na kujaribu kuwafurusha nje ya kaskazini mwa Sinai, lakini Februari Papa Francis alifanya ziara ya kihistoria ya siku tatu katika Falme za kiarabu iliyokuwa ya kwanza ya Papa kuwahi kuifanya katika rasi ya kiarabu ambayo ilihudhuliwa na Wakristo wanaokadiriwa kuwa 135,000 wengi wao wakiwa ni wahamiaji.Na nchini Saudi Arabia ambako Uislam ulizaliwa, ibada ya Kwanza ya Wakristo wa dhehebu la Coptic iliruhusiwa mwezi Disemba.Nchini Syria, Wakristo ambao ni wachache walihisi kwa tisho kubwa kutoka kwa makundi ya hususan y'all waasi wa Kiislamu. Huku vikosi vya rais Assad vikiwa vinakaribia kuondoka, kutokana na baadhi ya mashambulio ya kikatili, Wakristo wa Syria huenda wanapumua kutokana na ishara ndogo za amani. Hata hivyo nchini Iraq hali ya Wakristo bado ni tete. Uhasama baina ya Wasunni na Waislamu wa Kishia umeendelea kushamiri, na bado kuna wapiganaji wasiojulikana wa IS wanaojificha katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi. Askofu mkuu ameziaonya nchi za magharibi kutoshiriki makosa kwa kutochukua hatua Askofu mkuu wa Warda ameelezea mambo ya kusikitisha juu ya hali ya baadae.Marafiki, tunaweza kuwa tunakabiliana na mwisho wetu katika ardhi ya mababu zetu. Tunabaini holiday. Katika mwisho Wetu, dunia nzima, inakabiliwa na kipindi cha ukweli. '' Je watu wa amani, wasio na hatia wataruhusiwa kuuawa na kuangamizwa kwasababu ya imani yao? Na kwa ajili ya kutozungumza ukweli kwa wauji, dunia itakuwa inashiriki katika kutumaliza?" Askofu mkuu wa Irbil, mji mkuu wa jimbo la Iraq la Kurdistan, amewashutumu viongozi wa kikristo wa uingereza kwa kushindwa kufanya juhusi za kutosha kuilinda jamii ya inayotoweka ya Wakristo wa Iraq. text: Ndege aina ya Tupolev Tu-160 iliyotua uwanja wa Simón Bolívar Jumatatu Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumattau katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho ni sawa na "serikali mbili fisadi kufuja mali ya umma." Serikali ya Urusi imesema maneno yake hayo "hayafai hata kidogo." Ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja wa ndege wa Simón Bolívar viungani mwa mji mkuu wa Venezuela, Caracas, zikiandamana na ndege nyingine mbili za Urusi. Venezuela na Urusi zimekuwa marafiki kwa muda mrefu na ndege hizo mbili za kivita ziliwahi kutumwa tena taifa hilo mwaka 2008, zikiwa pamoja na manowari moja yenye uwezo wa kurusha makombora. Ndege hizo zilifika tena Venezuela mwaka 2013. Waziri wa ulinzi wa VenezuelaVladimir Padrino (wa pili kushoto, mstari wa mbele) aliwalaki Warusi hao Kitendo cha sasa kimetokea siku chache tu baada ya rais Maduro kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow. Waziri wa Ulinzi wa Venezuela Vladimir Padrino alisema ndege hizo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Venezuela na mshirika wake Urusi. "Hili tunalifanya kwa pamoja na marafiki zetu, kwa sababu tuna marafiki duniani ambao hutetea na kuheshimu uhusiano wa usawa." Njia zinazotumiwa na raia wa Venezuela baada ya kuondoka nchini mwao "Tunajiandaa kuilinda Venezuela hadi hatua ya mwisho ikilazimu," alisema waziri huyo akionekana kurejelea tuhuma za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ya nchi hiyo kwamba yapo mataifa yanayotaka kupindua serikali ya nchi hiyo. Rais Maduro alisema Jumapili kwamba kuna juhudi zinazoendelea kwa sasa "zikiratibiwa moja kwa moja kutoka White House (Marekani) za kuvuruga maisha ya kidemokrasia Venezuela na kutekeleza mapinduzi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kikatiba, kidemokrasia na iliyo huru ya taifa letu." Bw Pompeo alishutumu kitendo cha kutumwa kwa ndege hizo za Urusi kwenye Twitter. Msemaji wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, Dmitry Peskov, amesema tamko la Pompeo si la kidiplomasia hata kidogo. Bw Pompeo hakuwa afisa pekee wa Marekani aliyeshutumu kitendo hicho cha Urusi. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Kanali Rob Manning alisema hivi majuzi, Marekani ilituma meli ya jeshi la wanamaji inayotumiwa kama hospitali Amerika Kusini kutoa msaada wa kimatibabu kwa mamilioni ya raia wa Venezuela ambao wameikimbia nchi yao kutokana na mfumko mkubwa wa bei ya bidhaa na huduma na uhaba mkubwa wa bidhaa, chakula na dawa nchini mwao tangu mwaka 2014. Maelfu ya raia wa Venezuela wamekuwa wakiyakimbia maisha magumu nchini mwao "Hii ni tofauti sana na Urusi, ambao hatua yao kutatua mgogoro huu wa kibinadamu Venezuela ni kutuma ndege za kuangusha mabomu badala ya msaada wa kibinadamu," amesema Kanali Manning kwa mujibu wa kituo cha habari cha NBC. Lakini Urusi siyo pekee iliyotuma ndege za kivita katika taifa au mataifa mengine. Mmoja wa marubani wa kijeshi waliosafiri na ndege hizo za Urusi Marekani pia ilituma ndege za kivita nchini Ukraine, moja ya washirika wake, baada ya uhusiano wake na Urusi kudorora hasa baada ya Urusi kumega eneo la Crimea mwaka 2014. Urusi ilichukulia hatua ya Marekani na mataifa ya Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato) ya kujenga ushirikiano wa karibu na Ukraine kwama tisho kwake. Ndege aina ya Tu (Tupolev)-160 ni za aina gani? Unaweza kusoma pia Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. text: Matokeo ya awali yanakaribiana mno kati ya Benjamin Netanyahu na Benny Gantz Muungano wa chama cha mrengo wa kati Blue and White alliance cha aliyekuwa mkuu wa jeshi Benny Gantz kinatabiriwa kushinda kati ya viti 32 na 34 bungeni na chama cha Likud cha mrengo wa kulia chake waziri mkuu Benjamin Netanyahu kikitabiriwa kujishindia kati ya viti 30 hadi 33. Huenda kiongozi wa chama cha Yisrael Beiteinu, Avigdor Lieberman akabaini mshindi wa siku. Netanyahu aliitisha uchaguzi huo wa dharura baada ya kushindwa kuunda serikali ya muungano kufuatia uchaguzi mnamo Aprili. Majadiliano ya kuunda serikali mpya ya muungano yanatarajiwa kuanza punde baada ya matokeo ya awali yatakapotangazwa leo Jumatano. Akizungumza na wafuasi mapema leo, Netanyahu amesema: "Sote tumepitia kampeni ngumu ya uchaguzi. "Bado tunasubiri matokeo yenyewe, lakini jambo moja li wazi. Hali nchini Israel ipo katika kiwango cha historia, tumekabiliwa na changamoto nyingi na fursa nyingi." Kwa upande wake bwana Gantz alionekana kuwa na matumaini zaidi alipozungumza na wafuasi wake mapema kidogo. "Bila shaka tutayasubiri matokeo halisi, lakini inavyoonekana ni kana kwamba tumelifikia lengo letu," amesema. "Umoja na utangamano upo mbele yetu." Matokeo yanaonyesha nini? Matokeo ya baada ya kufungwa vituo vya kura yaliotolewa na shirika la utangazaji Israel Kan mapema Jumatano yanaonyesha kuwa chama cha Blue and White huenda kingejinyakulia viti 32 na chama cha Likud kikajipatia viti 31 kati ya jumla ya viti 120 bungeni. Katika nafasi ya tatu ni chama cha Israeli Arab Joint List kilichojinyakulia viti 13; kikifuatwa kwa chama cha Lieberman, Yisrael Beitenu kilichojinyakulia viti 9; Vyama vya Shas na cha umoja wa Torah Judaism vikijinyakulia viti 9 kila mmoja; cha mrengo wa kulia Yamina viti 7, na cha mrengo wa kushoto Labour-Gesher na Democratic Union alliances vikijanyakulia viti vitano na sita mtawalia. Channel 12 News kimeviweka vyama vya Blue and White na cha Likud kujinyakulia viti 32 kila mmoja huku matokeo yaliobadilishwa ya Channel 13 News yakitabiri kuwa chama cha Blue and White kitashinda viti 32 huku cha Likud kikijinyakulia 30. Kulikuwa na ukimya katika makao makuu ya chama cha Likud mjini Tel Aviv wakati matokeo hayo yakitangazwa ya baada ya kufungwa vituo vya kupiga kura. Huenda chama cha Netanyahu cha Likud kikaishia kuwa dhaifu zaidi kuliko ilivyokuwa baada ya uchaguzi wa Aprili Mamia ya viti vya wafuasi vilikuwa havina watu wakati wanaharakati wakiambiwa wasubiri nje ya ukumbi na viongozi wakitafakari matokeo hayo. Mkurugenzi wa mambo ya nje wa chama cha Likud amesema kwamba matokeo hayo ya baada ya kufungwa vituo vya kura yamekoseka katika siku za nyuma. Mara ya mwisho makadirio ya chini yalitolewa kwa kura ilizojinyakulia Likud na pia kwa baadhi ya vyama vya kidini vilivyo washirika wa Netanyahu. "Hakuna maana ya kuanza kutafuta serikali ya muungano kwa kutumia matokeo haya kwasababu yatabadilika," Eli Hazan amesema. Lakini chama cha Blue and White kimekuwa na matumaini kwa uangalifu kwamba Israel itapata uongozi mpya, msemaji Melody Sucharewicz ameliambia gazeti la Times of Israel. Kura zitahesabiwa usiku kucha. Lakini huenda ikachukua wiki kadhaa za majadiliano ya kuunda serikali ya muungano kabla ya serikali mpya na waziri mkuu mpya kuibuka. Uchaguzi huo umekuwa ni kura ya maoni kwa utawala wa miaka kumi ya mwisho kwa Benjamin Netanyahu. Katika ngome za upinzani mjini Tel Aviv mhariri wa masuala ya mashariki ya kati wa BBC Jeremy Bowen, anasema kulishuhudiwa misururu mirefu ya wapiga kura waliokuwa wakisubiri kwa matumaini kusitisha uongozi wake wa kisiasa. Kama kawaida yake Netanyahu alifanya kampeni nzuri tu hata kushirikishwa katika matangazo yake ya kumtangaza. Ujumbe wake ni kwamba yeye ndiye mtu pekee - aliye na marafiki wenye nguvu kama Donald Trump - kuwalinda raia Israel dhidi ya Iran na Palestina. Mwandishi wa BBC Bowen anasema wakati akizunguka mjini Tel Aviv, amekutana na Avigdor Lieberman, ambaye anaweza kuwa mwanasiasa anayeogopewa na waziri mkuu wakati majadiliano ya kuunda serikali ya muungano yatakapoanza. Chama chake Yisrael Beiteinu huenda ndicho kikaleta mshindi wa siku. Jambo moja muhimu ni kwamba licha ya kwamba alikuwa mshirika wa karibu wa waziri mkuu huyo , sasa ni wapinzani na pengine hata maadui. Baada ya matokeo hayo baada ya kufungwa kwa vituo vya kupiga kura, wafuasi wa Lieberman ndio waliokuwa wakisherehekea peke yake. Iwapo matokeo yatathibitishwa mwisho wa siku - kwasababu matokeo huwa mara nyingi sio sahihi - basi huenda enzi ya utawala wa Netanyahu katika siasa za Israel inamalizika. Nini kinachoweza kufanya baada ya hapa? Mwandishi wa BBC Tom Bateman, anasema iwapo matokeo ya kura yatathibitishwa, Netanyahu atakuwa hana njia rahisi kuingia serikalini. Kwa hakika takwimu hizo zinamuweka katika nafasi dhaifu kuliko aliyokuwa baada ya uchaguzi wa Aprili wakati mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano yalipotibuka, anaongeza. Huenda Gantz akaibuka kiongozi wa chama kikubwa, lakini huenda akawa na kibarua kigumu zaidi kuunda serikali. Lieberman, ambaye ni mshirika aliyegueka kuwa hasimu mkubwa wa waziri mkuu, huenda akawa kiungo muhimu katika maamuzi ya nani atakayeingia uongozini. Alimzuia Netanyahu kuunda serikali ya muungano baada ya uchaguzi uliopita lakini alikataa kurudi nyuma kuhusu mzozo wa muda mrefu na vyama vya kisiasa kuhusu mswada unaotoa msamaha kwa vijana wa kiothodoxi kuingia jeshini. Avigdor Lieberman anataka "serikali pana, huru ya kitaifa" Avigdor Lieberman anataka "serikali pana huru ya kitaifa" Katika mkutano wa kisiasa mjini Jerusalem Jumanne usiku, Lieberman alisisitiza wito wake aliotoa wakati wa kampeni wa serikali ya muungano. "Tuna uamuzi mmoja tu," aliwaambia wafuasi. "Serikali pana huru ya kitaifa inayojumuisha vyama vya Yisrael Beiteinu, Likud na Blue and White." Mwandishi wetu anasema muungano huo unawezekana iwapo tu bwana Netanyahu atapinduliwa kama kiongozi wa Likud, wakati makundi ya upinzani yameapa kutokaa na yeye uongozini. Uwezekano mwingine unaweza kutokea, ikiwemo uchaguzi mwingine, unaotatizwa kwa kesi dhidi ya Netanyahu kuhusu tuhuma za ufisadi. Waziri mkuu huyo anakana kufanya makosa yoyote Iwapo matokeo hayo hayatatoa mshindi, itakuwa ni jukumu la rais Reuven Rivlin kuamua ni nani anayepata jukumu la kujaribu kuunda serikali. Atakayechaguliwa atakuwa na muda wa siku 28 kufanya hivyo huku kukiwepo uwezekano wa kuongezwa muda usizidi wiki mbili baada ya hapo. Matokeo ya awali baada ya uchaguzi mkuu wa pili Israel unaofanyika katika muda wa miezi mitano yanaonyesha kuwa matokeo ya kura yanakaribiana mno kuweza kupata mshindi wa wazi. text: "Muombeeni [Trump] kwa sababu wakati Mungu anapoweka watoto wake katika nafasi fulani, wakati mwingine jehanamu hufanya kila kitu kumwangamiza mtu huyo," alisema Mchungaji wa Nigeria Chris Oyakhilome, muhubiri maarufu wa televisheni, mwezi Juni. Pia alitahadharisha kuwa wakosoaji wa rais wa Republican ambaye anatafuta kuchaguliwa tena mwezi Novemba wanawachukia wafuasi wake. Wana hasira na Trump kwa kuwaunga mkono Wakristo, lazima mfahamu. Hivyo wanaowachukia kweli ni nyinyi mlio Wakristo,'' alisema mchungaji huyo ambaye matangazo yake ni maarufu sana duniani, ikiwemo Marekani. Rais Trump amekuwa mtu wa kutatanisha ulimwenguni kote lakini ni maarufu katika nchi za Kiafrika kama Nigeria na Kenya, kulingana na utafiti wa Pew uliotolewa mnamo mwezi Januari, ambapo wafuasi hawaonekani kuwa na wasiwasi kuwa kutokana na kuzitaja nchi za Kiafrika kuwa "chafu "mnamo 2018. Nigeria na Kenya ni nchi zinazofuata mikondo ya kidini . Makanisa ya Mega yanaenea Kusini mwa Nigeria - taifa lenye watu wengi barani Afrika - na nchini Kenya wanasiasa wengi huenda kwenye mahubiri ya kanisa kuhutubia wafuasi wao, huo ndio umaarufu wao. Makundi mengi ya Kikristo ya Kiinjili barani Afrika, ambayo ni zaidi hupinga kuavya mimba, vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na hupinga mkono wa Israel, hayakuwa na nia na mtangulizi wake wa Democrat Barack Obama, licha ya kuwa na mizizi ya Kenya. "Utawala wa Obama ulikuwa unashinikiza ajenda ya ukombozi hapa Afrika na ajenda hiyo ilikuwa ya wasiwasi kwa baadhi yetu viongozi wa Kikristo. Ilikuwa faraja kwamba wakati wa Trump alikuwa amerudi nyuma kidogo," Richard Chogo, mchungaji katika Kanisa la Deliverance katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, liliambia BBC. Aliusifu utawala wa Trump kwa kuondoa ufadhili kwa baadhi ya mashirika kama vile Marie Stopes, ambayo hutoa huduma za uzazi wa mpango na uavyaji mimba salama katika nchi kadhaa barani Afrika. Shirika hilo lilikosoa marufuku ya ufadhili wa Marekani wa mwaka 2017, likisema kwamba "inaweka maisha ya wanawake hatarini". Lakini Mchungaji Chogo anakubaliana na sheria nchini Kenya ambapo utoaji mimba ni haramu isipokuwa iwapo afya ya mama iko hatarini, akisema kwamba kuhalalisha utoaji mimba ni sehemu ya "ajenda ya kudhibiti idadi ya watu". Bwana Trump amejuvuna kwamba amewafanyia mambo mengi mazuri Wamarekani weusi ''Black Lives Matter''Mjadala kuhusu utoaji mimba umekuwepo katika siasa za nchini Marekani kwa karibu miongo minne. Wainjilisti weupe wameungana kuhusu suala hilo na kugeuza harakati zao za kupambana na utoaji-mimba kuwa nguvu ya kisiasa yenye ushawishi. Baada ya uamuzi wa kihistoria wa 1973 Roe v Wade na Mahakama kuu ya Marekani kuhalalisha utoaji mimba, wainjilisti weupe, ambao wakati huo hawakuwa na uhusiano wowote kisiasa na moja ya vyama kuu viwili, walimuunga mkono Ronald Reagan wa Republican katika uchaguzi wa urais wa 1980 dhidi ya kiongozi wa Democratic wa wakati huo Jimmy Carter Wainjilisti weupe tangu hapo wamekuwa kambi muhimu ya kupiga kura kwa Chama cha Republican na wameongeza ushawishi wao ulimwenguni. Hii ni licha ya waprotestanti weusi nchini Marekani kuwa wengi wa Democrat na kukosoa rekodi ya Bw Trump, kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa Pew, Emeka Ezeji, mchungaji na shemasi mkuu katika Kanisa la Kimishenari la Kianglikana katika jimbo la Enugu Kusini Mashariki mwa Nigeria, anasema maoni yake ya kisiasa yamedhamiriwa tu "na yale maandiko yanasema". "Imani ni kitu binafsi, yangu ni ya kuunga mkono maisha ... Wakristo wa Kiafrika wanaamini kuwa rais wa Republican ni bora kwa Marekani na ulimwengu," alisema. Amekuwa akimuombea Bw Trump kumshinda mgombea wa Chama cha Democrat Joe Biden mwezi Novemba, na kutenga muda kila siku kumwombea rais apone wakati alikuwa hospitalini hivi karibuni baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona. Kama Mchungaji Chogo, yeye pia anaamini kwamba "udhaifu" wa Bw Trump haupaswi kufunika yaliyo"mazuri " kwetu. Kwa mfano, anatupilia mbali harakati za black lives matter(BLM), ambayo Bwana Trump ameitaja kama "ishara ya chuki", akisema "imetekwa nyara kwa maono yake". Licha ya kutoa matamshi ya dharau kuhusu Afrika, Rais wa Marekani Donald Trump amevutia wafuasi waumini wa Kikristo wengine barani. text: Sanamu hilo linalofananana na marehemu Aaliyah limekuwepo mahali hapo kwa siku tano tu-lakini baadhi wamekuwa wakipigwa picha wakiongezea urembo wao zaidi kwenye sanamu hilo. Twitter rasmi ya Aaliyah' imeitaja tabia hiyo kama "isiyofaa na isiyokubalika". Muimbaji huyo aliyetunukiwa tuzo mbalimbali za muziki alifariki katika ajali ya ndege mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 22. Sanamu hilo lililotengenezwa kwa nta limeonyeshwa kwa umma kwa ajili ya maadhimisho ya 18 tangu kifo chake. Ukurasa wa Twitter wa mwanamuziki huyo pia ulituma ujumbe kutoka kwa Madame Tussauds Las Vegas ukisema wana wahudumu kwenye wavuti wao kila sikuambao "hupanga upya " namba na kuhakikisha "zinaonekaba bora zaidi". Akaunti ya Aaliyah ilituma ujumbe huu uliosema: "Ni aibu kwamba baadhi ya watu hawana heshima". Aaliyah alikuwa nani ? Aaliyah Haughton - ambaye alifahamika zaidi kwa jina lake la kwanza - alikuwa Muimbaji wa muziki wa R&B, mchezaji filamu na mwanamitindo wa Marekani. Akizaliwa mwaka 1979 mjini New York na kukulia Detroit. Kaka yake Aaliyah Rashad Haughton, alihusika katika mchakato wa utengenezaji wa sanamu iliyotengenezwa kwa nta Albamu yake ya kwanza ya muziki iliyokuwa na wimbo Age Ain't Nothing But a Number ilirekodiwa akiwa na umri wa miakma 14 kwa usaidizi wa msahuri wake R Kelly. Baadae aliteuliwa kwa tuzo mbali mbali za Grammys, na kushinda tuzo mkiwemo tuzo za MOBO na za Muziki wa Marekani. 'Try Again' ulikuwa ni moja ya nyimbo zake maarufu. Alitengeneza filamu yake akicheza kama 'Romeo Must Die' sambamba na sanamu ya 'Jet Li'. Aaliyah aliolewa na R Kelly alipokuwa na umri wa miaka 15 na Kelly akiwa na umri wa miaka 27 Aaliyah aliolewa na R Kelly alipokuwa na umri wa miaka 15 na Kelly akiwa na umri wa miaka 27, katika sherehe ya siri. Ni nadra sana kuelezea mahusiano yao. Tarehe 25 Agosti 2001 Aaliyah alikuwa anarejea Marekani baada ya kuchukua video ya filamu ya muziki katika visiwa vya Abaco vilivyoko Bahamas wakati alipokufa katika ajali ya ndege. Watu wengine wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pia walikufa. Familia ya Aaliyah imeomba kuwepo na "heshima" baada ya watu kuonekana wakiongezea kupaka lipstiki sanamu la mwanamuziki huyo wa pop lililopo katika eneo la Madame Tussauds mjini Las Vegas. text: Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza". Mzozo huo unaibuka wakati Bi Park anaitwa kuhojiwa kufuatia kutajwa kama mshukiwa kwenye sakata kubwa ya ufisadi ambayo ilichangia kuondolewa kwake madarakani. Alitimuliwa wiki iliyopita wakati mahakama ya katiba ilidumisha uamuzi wa kuondolewa kwake madarakani. Korea Kusini itafanya uchaguzi wake wa urais tarahe 9 mwezi Mei. Bi Park ndiye rais wa kwanza aliyechagulia kidemokrasia kuondolewa madarakani. Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza". Mwishoni mwa wiki Bi Park aliondoka ikulu ya rais ambayo inafahamika kam Cheong Wa Dae na kuelekea nyumbani kwake kwenye mtaa wa kifahari mjini Seoul. Mbwa wake tisa hawakuwa miongoni kwa vitu alivyoandamana navyo. Kundi la kupinga unyanyasaji wa wanyama linasema kuwa alikiuka haki za wanyama kwa kuwaacha nyuma. Msemaji wa ikulu alikana madai kuwa Bi Park aliwatelekeza mbwa wake na kuliambia shirika la Reuters kuwa mbwa hao waliachwa nyuma kwa sababu haingekuwa vyema wao kuondolewa kwenye makazi yao. "Aliwaambia wafanyakazi wa ikulu kuwa wawatunze mbwa hao na wawatafutia makao ikiwa itawezekana," msemaji wake alisema, Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza". Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza". Korea Kusini imekuwa ikiongozwa na waziri mkuu Hwang Kyo-ahn tangu bunge lipige kura ya kumuondoa madarakani mwezi Disemba. Tarehe ya uchaguzi wa rais ilitangazwa wakati wa mkutano wa mawaziri siku ya Jumatano Wakati wa mkutano huo bwana Hwang alisema kuwa hatawania urais, hatua ambayo ilikuwa pigo kwa chama cha Conservative. Makundi ya kutetea haki za wanyama yamemlaumu rais wa Korea Kusini aliyeondoka madarakani Park Geun-hye, kwa kuwatelekeza mbwa wake wakati aliondoka ikulu text: Baadhi ya Wapwani wanategemea madafu kwa kipato chao, mmoja wao ni Mzee Mwajita Khamis ambaye anauza madafu yake barabara ya Digo karibu na soko la Mackinnon ama Marikiti ukipenda. ``Mimi nimeuza madafu tangu mwaka wa 1984, hii ni kama ofisi yangu na hapa ndio mategemeo ya kila kitu,'' anasema Mwajita. ``Madafu ni zao kubwa ambalo tunategemea sisi Wapwani, halafu haya madafu ni tiba kubwa sana kwa sababu maji ya madafu kazi yake ni kuosha mwili wa mwanadamu sehemu ya figo huwezi pata shida hapo.'' Huku nami nikiwa nanywa madafu nikizungumza na Mwajita, mteja wake wa kila siku Musa Zimbwe anaunga mkono asemayo Mwajita kuhusu madafu kuosha mwili. ``Madafu yanasaidia mwili, hasa haja ndogo na kwa upande wetu yanatusaidia kwa nguvu za kiume, ng'ome inaimarika tu sana ukinywa madafu,'' anasema Zimbwe ``Mimi kila siku sikosi hapa kwa Mzee Mwajita, nimetumia madafu kwa zaidi ya miaka hamsini, nimezaliwa nikiyaona, kuna madafu ya kunywa pekee, na madafu mengine yana nazi changa hivi ndani watafuna.'' Mwajita anasema biashara ya madafu ni ya familia anayofanya akisaidiwa na wanawe wa kiume. ``Hii ni kama royal family, inanifaidisha, nalea na ndio kila kitu kwa maisha yangu yetu. Sisi Wadigo madafu mhimu kwetu, hapa ni kama kiwanda chetu. Mimi mwenyewe mbali na kuuza nanywa madafu kama tano ama sita kila siku. Ukiniangalia mimi mbali na nywele nyeupe nina nguvu na ngozi yangu laini kwa sababu ya madafu.'' Utafiti ambao nimeiufanya kwa mtandao unathibitisha asemayo Mwajita kuhusu umuhimu wa maji hayo ya nazi changa. Pamoja na kulainisha ngozi, madafu ni tiba ya figo, yanasafisha uchafu mwilini, husaidia wanawake waja wazito na kupunguza presha mwilini miongoni mwa manufaa yake. Mtaalam wa lishe Joe Lewin ameambia BBC madafu yana umuhimu sana kwa mwili wa binadamu na kwamba uzuri wake kiwango chake cha sukari kiko chini tofauti vinywaji vingine kama vile soda na juici. Lewin hatahivyo anasema hamna ukweli wa madai kwamba madafu husaidia wana riadha kufanya vyema zaidi, na isitoshe ingekua hivyo basi maji hayo yangewekwa kundi moja na dawa zingine za kuongeza nguvu zilizopigwa marufu na shirikisho la kimataifa, IAAF. Mtaalam huyo wa lishe hatahivyo anasema madafu husaidia moyo wa binadamu na madini ya potassium. Utafiti uliofanywa kwa kutumia panya unaonyesha unywaji wa madafu unashusha kiwango cha cholesterol lakini Lewin anaeleza bado hakuna ushahidi wa kutosha kwa upande wa binadamu. Kwa upande wa kuimarisha nguvu za kiume kama anavyosema Musa Zimbwe wa Mombasa hilo ni suala la kibinafsi lakini ni dhahiri kwamba madafu ni kinywaji mhimu sana pwani ya Kenya. Madafu ni kinywaji maarufu sana pwani ya Kenya hasa mjini Mombasa. Kuanzia wenyeji mpaka watalii wote wanapenda madafu, maji ya nazi ambayo haijakomaa. text: Wafula Chebukati amewalaumu wanasiasa Mkutano huo ulikuwa umepangiwa kufanyika saa nane unusu adhuhuri lakini tume hiyo imetoa taarifa na kusema umeahirishwa. Uchaguzi mpya umepangiwa kufanyika Alhamisi wiki ijayo. Hata hivyo, ingawa Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza yuko tayari kwa uchaguzi huo na utaendelea, mgombea wa upinzani Raila Odinga alijiondoa wiki iliyopita. Jana, Bw Odinga, ambaye ni mgombea wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) alitangaza kwamba siku hiyo badala ya kushiriki uchaguzi, wafuasi wake watafanya maandamano makubwa kote nchini. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati siku ya Jumatano alikuwa amewalaumu wanasiasa wa kusababisha kuwepo kwa mazingira yanayoifanya vigumu kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Alisema alikuwa anawapa "kadi ya manjano". Bw Chebukati alikuwa ameahidi kuhudumu kama mpatanishi kati ya wanasiasa hao. Tume hiyo Jumatano ilipata pigo baada ya mmoja wa makamishna Dkt Roselyn Akombe kutangaza kujiuzulu akiwa Marekani na kusema hana mipango yoyote ya kurejea Kenya hivi karibuni. Kenyatta kupinga mazungumzo Rais Kenyatta today alionekana kupinga mkutano Jumatano alipotangaza kwamba hatafanya mazungumzo yoyote na upinzani. Akihutubu Saboti, Trans Nzoia magharibi mwa nchi hiyo, alisema wale ambao hawataki kushiriki uchaguzi wa 26 Oktoba hawafai kuwazuia watakaotaka kushiriki uchaguzi huo kupiga kura. "Vile hakuna anayelazimisha mtu kushiriki uchaguzi wa 26 Oktoba, vile vile hakuna aliye na haki ya kuzuia wengine kushiriki," alisema. Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilimtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, akiwa mbele ya mpinzani wake Raila Odinga wa muungano wa upinzani Nasa kwa zaidi ya kura 1.4 milioni. Bw Odinga alipinga matokeo hayo mahakamani na Mahakama Kuu ikaamua ulijaa kasoro nyingi na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku sitini. Tume ya uchaguzi ilitangaza tarehe mpya ya uchaguzi kuwa 26 Oktoba lakini Bw Odinga alijiondoa wiki iliyopita akisema mageuzi ambayo yalifaa kutekelezwa kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki hayajatekelezwa. Tume ya Uchaguzi Kenya imeahirisha mkutano ambao ulikuwa umepangwa kufanyika leo kati ya mwenyekiti wa tume hiyo na wagombea wa urais. text: Mitaa ya mji wa Bugarama uliopo katika kati ya nchi tatu: Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi Makahaba katika mji wa Bugarama wanasema ukahaba siyo kazi tena kama ilivyokuwa zamani kutokana na kuwa wanawake wengi sasa wanajiingiza katika shughuli hiyo ambayo imekuwa ni njia rahisi ya kujipatia kipato. Katika ukumbi wa burudani mjini Bugarama makahaba hufurika kwa wingi wakisubiria wateja wao pembezoni mwa lango kuu, anasema mwandishi wa BBC nchini Rwanda Yves Bucana. '' Ukahaba nilianza nikiwa na miaka 14 , hivi naeneza miaka 25, toka miaka 14 hesabu sijui nimelala na wanaume wangapi na bado ningali nawapata. Nimelala na wanaume wengi sana, inatoikana na jinsi wanavyopatikana kwa usiku mmoja kama wakipatikana hata 10 unaweza kulala nao. Wakikosekana utapata wawili watatu, inatokana na wakati wa pesa, kama kuna pesa unapata wanaume wa kutosha.'' alisema kahaba mmoja. Wanaume Kutoka DRC wanaaminika kwa kutoa malipo mazuri kwa makahaba wa Bugarama zaidi ya wanaume kutoka nchi nyingine ''Siwezi kuwahesabu nijue ni wangapi, ni wengi, usiku unaweza kupata wanaume hadi watano. Tunapata wanaume wanyarwanda, wakongo na wachina''. Alisema kahaba mwingine huku akitabasamu. Upande wa malipo wanasema wateja wao nambari moja ni wanaume kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambao wanaaminika kumheshimu zaidi mwanamke: '' Wakenya anaweza hata kukupa dola 50, Wakongo ndio wanalipa vizuri na hakuna tatizo , na hataleta kelele, ukiamka asubuhi atakulipa pesa yako, jinsi mlivyoelewana, Wakongo wanaheshimu sana wanawake, Wakongo ndio wanalipa vizuri wanalipa kwa dola, Wakongomani wanawathamini wanawake.'', Alisisitiza kahaba huku akitazama huku na kule kuangalia ikiwa anaweza kumpata mteja. BBC ilibaini kuwa wateja wengi wa makahaba nchini Rwanda hivi karibuni hutembea na mashine za kujipima wenyewe ugonjwa wa ukimwina ujauzito. Ukahaba haukubaliki na ni kosa la jinai Rwanda Hata hivyo bei ya kutumia mipira ya kondomu na kutoitumia hutofautiana wanasema makahaba, Bei ya kutumia kondomu ni dola ishirini na bei ya kutovaa kondomu ni dola hamsini, wanasema. ''Leo wikendi kuko show yaani napata raha yaani napataga wa teja wa kujiheshimia Alhamdulillah,wazee, mabwana wa kujiheshimia, ukiona bwana unasema Alhamdulillah yaani kesho sitakuwa na njaa.''Anasema mwanamke huyu ambaye alikuwa akipokea simu za wateja wakati wa mahojiano. Ukahaba haukubaliki na ni kosa la jinai Rwanda. Makahaba wanasema kazi yao kwa sasa haina tija ikilinganishwa na zamani kwa sababu siku hivi karibuni idadi ya makahaba wanaoingia Bugarama kutoka nchi maeneo mbali mbali ya Rwanda na mataifa jirani imeongeza. Mji wa Bugarama kusini magharibi mwa Rwanda uliopo kwenye mpaka wa nchi tatu Rwanda,Burundi na DRC umekuwa kitovu cha ukahaba. text: Lucas Moura alifunga bao la ushindi katika dakika ya 96 na kuisaidia timu yake kutoka nyuma na kuilza miamba ya Uholanzi Ajax Amsterdam 3-2 na kutinga fainali dhidi ya Liverpool. Wakiwa nyuma 1-0 kutoka mkondo wa kwanza, Spurs ilianza na mkosi mbaya mjini Amsterdam baada ya nahodha Matthijs de Ligt kuruka juu na kufunga kichwa kizuri kufuatia kona . Hatahivyo Tottenham iligonga mwamba wa goli kupitia Son Heung kabla ya Hakim Ziyeck kufunga goli la pili na hivyobasi kuiweka Ajax kifua mbele baada ya pasi nzuri kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Southampton Dusan Tadic. Bao hilo lilivunja matumaini ya Spurs katika nusu fainali nyengine , lakini katika kipindi cha pili kikosi hicho cha Mauricio Pochettino kilifunga magoli mawili katika muda wa dakika tano. Moura alipunguza pengo hilo kupitia bao zuri kabla ya mchezaji huyo wa Brazil kusawazisha katika usiku ulioiwacha Tottenham ikitafuta bao moja la ushindi ili kutinga fainali. Na katika mashambulizi ya mara kwa mara ya Tottenham, Vertonghen alipiga kichwa kilichogonga mwamba wa goli kabla ya Moura kufunga goli lake la tatu kwa kutumia guu lake la kushoto akiwa maguu 16 kutoka kwa goli katika dakika ya sita ya lala salama. Itakuwa fainali ya pili inayoshirikisha timu za Uingereza baada ya Manchester United kuilza Chelsea katika mikwaju ya penalti katika fainali iliochezewa mjini Moscow 2008. Ni usiku usio sahaulika kwa Tottenham Kocha wa Tottenham Maurico Pochettino hakuweza kuzuia hisia zake baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa ambapo alidondokwa na machozi huku akionekana kusherehekea bila kujali na wachezaji wake. Raia huyo wa Argentina ambaye ataadhimisha mwaka wake wa tano akiifunza Tottenham baadaye mwezi huu alikuwa katika magoti baada ya usiku kama ule ambao Liverpool ilitoka nyuma na kuilaza Barcelona siku ya Jumanne. Harry Kane ambaye anaendelea kuuguza jeraha , alijiunga na wenzake uwanjani kusherehekea mbele ya mashabiki wao 2500. Spurs ilionekana kana kwamba imevunjika nguvu wakati Ziyeck alipounga goli lao la tatu kwa jumla kabla ya kipindi cha kwanza lakini walijikusanya na kutinga fainali ya kombe la klabu bingwa. Hatahivyo ni mchezaji Lucas Moura aliyerudisha matumaini ya mashabiki wa Tottenham , akitoa pasi tatu nzuri , ya tatu baada ya kichwa cha mchezaji wa zamani wa Ajax Vertonghen kugonga mwamba wa goli kutoka maguu manne huku ikiwa zimesalia dakika nne za muda wa kawaida. Bao la tatu ambalo ndilo lililobainisha mbivu na mbichi lilijiri wakati alipochukua mpira kufuatia shambulio la Delle Ali ambalo lilipanguliwa na kipa Onana. Kilikuwa kiunzi muhimu kwa Tottenham kuruka Walikuwa wamepoteza mechi tatu za nusu fainali ikiwemo mikwaju ya penalti dhidi ya Chelsea katika kombe la Carabao. Baada ya kuwasili katika uwanja mpya uliogharimu £1bn mwezi uliopita , huu ni wakati muhimu wa Spurs wanaowania kushinda kombe la kwanza katika kipindi cha miaka 11. Na huku akiwa tayari wamefanikiwa kutinga nne bora katika ligi ya EPL wamesalia na ushindi mmoja pekee kutawazwa mabingwa wa Ulaya. Mtumaini ya Ajax Ulaya yasitishwa ghafla Ajax imekuwa timu nzuri kuitazama ikicheza katika michuano yote ya klabu bingwa ilioanza tarene 25 mwezi Julai katika raundi ya pili ya muondoano dhidi ya timu ya Austria Sturm Graz. Wamepata mashabiki wengi wapya wakati wa michuano hiyo ambayo iliondoa miamba ya La Liga Real Madrid na ile ya Seria A Juventus ili kutinga nusu fainali. Ijapokuwa mabingwa hao mara nne wa Ulaya watahitajika kujipa moyo baadaye baada ya kunyimwa fainali yao ya kwanza tangu 1996 katika dakika za mwisho. Wakiwa kifua mbele kwa magoli matatu kufikia kipindi cha kwanza , mashabiki wao walikuwa wakisherehekea kabla ya miujiza ya Tottenham kufanyika. Bao la mapema la nahodha mwenye umri wa miaka 19 De Ligt kutoka kona muda mfupi baada ya kipa Hugo Lloris kuzuia shambulio la Tadic lilifuatiliwa na bao jingine la Ziyeck na hivyobasi kuipatia Tottenham mlima wa kupanda. Lakini hawakujua kitakachowapata baada ya Spurs wakiongozwa na Moura kubadilisha mambo. Mchezaji bora -Luca Moura Tottenham Klabu ya Tottenham imetoka nyuma na kuwashangaza wenyeji wao Ajax katika mechi ya pili ya nusu fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya. text: Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner John Barnett anasema uchunguzi umebaini kuwa hadi robo ya mfumo wa oksijeni una hitilafu na kwamba huenda ikakosa kufanya itakapohitajika. Pia anadai kuwa vipuri vya ndege vilivyo na kasoro vimewekwa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikiundwa katika kiwanda cha Boeing. Boeing imepinga madai hayo ikisema kuwa ndege zake zote zinaundwa kwa kuzingatia viwango vy usalama vya hali ya juu. Kampuni hiyo imejikuta mashakani siku za hivi karibuni baada ya ajali mbili mbaya zilizohusisha ndege yake ya 737 Max -iliyokuwa ya shirika la ndege la Ethiopia na kupata ajali mwezi Machi na ajali ya Lion Air ya Indonesia mwaka jana. Bwana Barnett, ni injinia wa zamani wa udhibiti wa ubora, aliyefanya kazi na Boeing kwa miaka 32, hadi alipostaafu kwa misingi ya afya yake mwezi March mwaka 2017. Kutoka mwaka 2010 aliajiriwa kama meneja anayesimamamia masuala ya ubora wa viwango vya uundaji ndege katika kiwanda cha Boeing cha North Charleston,Kusini mwa jimbo la Carolina. John Barnett injinia wa zamani wa udhibiti wa ubora, katika shirika la Boeing Kiwanda hicho ni moja ya viwanda vilivyohusika na uundaji wa 787 Dreamliner, inayotajwa kuwa ndege ya kisasa ya aina yake ambayo hutumika sana kwa safari ndefu kote duniani Licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa baada ya kuanza huduma zake ndege hiyo ilivutia mashirika kadhaa ya ndege kuimiliki, na imekuwa chanzo cha faidi kwa mashirika hayo. Lakini kwa mujibu wa Bw. Barnett, 57, kinyang'anyiro cha ununuzi wa ndege hiyo mpya ilisababisha uundaji wake kuharakishwa, hali ambayo huenda ilifanya viwango vya usalama wake kutozingatiwa kikamilifu. Shirika la Boing limepinga kauli hiyo na kusisitiza kuwa "usalama, ubora na uadilifu ni msingi wa utendakazi wa Boing". Mwaka 2016, anaiambia BBC, kuwa aligindua tatizo la kiufundi katika mfumo wa oksijeni ambayo inastahili kuwasaidia abiria na marubani kupata hewa endapo ndege itakumbwa na hitilafu ikiwa angani kutokana na sababu yoyote. Mirija ya kupumulia hewa safi inatarajiwa kuning'inia kutoka juu ya ndege, ambayo inasaidia kupata hewa ya oksigeni. Bila mfumo kama huo, abiria watashindwa kupumua. Ndege ikiwa inapaa umbali wa futi 35,000, kutoka ardhini au juu ya bahari abiria watazirai kwa chini ya dakika moja. Ndege ikiwa inapaa umbali wa futi 40,000, hali hiyo inaweza kujitokeza katika kipindi cha sekunde 20. Wakati huo ubongo utaathiriwa na huenda abiria wakafariki. Ndege ya aina ya Boeing 737-700 ya shirika la ndege la Southwest ikiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Philadelphia baada ya kulazimika kutua ilipokumbwa na hitilafu katika injini yake April 17, 2018. Bwana Barnett anasema wakati alipokuwa anarekebisha mfumo wa hewa ndani ya ndege ulioharibika aligundua kuwa baadhi ya mitungi ya kusambaza hewa ya oksijeni ilikuwa haifanyi kazi kama inavyostahili. Alipokuwa akifanyia marekebisho mfumo huo aliifanyia majaribio kwa kutumia utafiti wa Boeing yenyewe ili kuiunda upya. Uchunguzi huo ulifanywa kwa kutumia vifaa ambavyo "havitumiki" na vilivyoharibika, ulitengenezwa ili kuiga jinsi zitakavyotumika ndani ya ndege ikiwa safarini, kwa kutumia umeme kama kichocheo. Anasema mifumo 300 ilifanyiwa majaribio na 75 kati ya hizo hazikufanya kazi vyema, kwa asilimia 25%. Bwana Barnett anasema juhudi yake ya kushughulikia hitilafu hiyo ilipingwa na mameneja wa Boeing. Ndege ya Boeing aina ya Dreamliner ikifanya safari yake ya kwanza mwaka 2009 na kutoka wakati huo ndege zaidi ya 800 zimenunuliwa na mashirika ya ndege tofauri duniani Mwaka 2017,aliwasilisha suala hilo kwa Utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA), kwamba hakuna hatua iliyochukuliwa kurekebisha hitilafu hiyo. Lakini FAA, hatahivyo ilisema kuwa haiwezi kuthibitisha madai hayo, kwasababu Boeing ilisema itashughulikia suala hilo wakati huo. Boeing yenyewe imepinga kauli ya Bw. Barnett. Ilikubali kuwa mwaka 2017 "iligundua kuwa baadhi ya mikebe ya oksijeni waliyopokea kutoka kwa wasambazaji wao zilikuwa hazifanyi kazi vizuri. Tuliondoa chupa hizo katika kiwanda chetu cha kuunda ndege na hata zile zikuwa zimetumiwa wakati wa uundaji wa ndege zilizotanzgulia na kuwasilisha malalamiko yetu kwa wasmbazaji hao". Lakini pia ilisema kuwa "mfumo wa hewa ya oksijeni ya kila abiria iliyowekwa katika ndege yetu imefanyiwa uchunguzi mara kadhaa kabla ziwasilishwe ili kuhakikisha zinafanya kazi vyema, na lazima zipite uchunguzi huo kabla kuwekwa kwenye ndege." "Mufumo huo pia unafanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara hata baada ya ndege kuanza kuhudumu," ilisema. Jengo la Utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) Haya sio madai pekee yaliyoelekezwa kwa Boeing kuhusu kiwanda chake cha kuunda ndege cha South Carolina, hatahivyo. Bw. Barnet pia anasema kuwa Boeing ilikosa kuzingatia mwongozo wake binafsi, ambao unalenga kufatilia ubora wa vipuri vya ndege zake wakati zikiundwa, hali ambayo inaruhusu vipuri vilivyo na kasoro "kupita". Anadai kuwa wafanyakazi walio katika presha ya kufikia malengo ya kampuni wanaishia kutumia vipuri vya viwango vya chini kutoka katika jaa la taka ambalo liko karibu na eneo la kuundia ndege mpya. Katika kisa kimoja hata afisa wa ngazi ya juu alijua kitu kama hicho kinafanyika. Anasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuokoa muda, kwa sababu "kiwanda cha Boeing cha South Carolina kinaeneshwa kwa ratiba na gharama ya uundaji wa ndege mpya". Kuhusu suala la vipuri kupotea, mapema mwaka 2017 uchunguzi uliofanywa na Utawala wa safari za anga nchini Marekani ulithibitisha hofu ya Bw. Barnett. Tangu wakati huo, kampuni hiyo inasema kuwa, "ilitatua kikamilifu matokeo ya FAA kuhusu ufuataji wa vipuri na kutekeleza mapendekezo yote ya ukarabati wa ndege ili kuzuia hitilafu kutokea tena". Haikutoa mailezo zaidi kuhusu uwezekano wa vipuri vilivyo na kasoro kutumiwa kuunda ndege mpya- japo vyanzo kutoka ndani ya kiwanda hicho cha North Charleston vinasema huenda hilo linafanyika. Kiwanda cha Boeing cha North Charleston mjini South Carolina ni moja ya viwanda vilivyounda 787 Dreamliner Bw Barnett kwa sasa amechukua hatua za kisheria dhidi ya Boeing, ambayo analaumu kwa kumharibia sifa na kusambaratisha taaluma yake kutokana na masuala aliyofichua, na hatimae kushurutisha kustaafu mapema. Kampuni ilijibu hoja hiyo kwa kusema kuwa injinia huyo alikuwa na mpango wa kustaafu kwa muda mrefu na kwamba alifanya hivyo kwa hiari. Inasema kuwa "Boeing haijaathiri kwa vyovyote uwezo wa bwana Barnett kuendelea na kazi yoyote aliyotaka kufanya hata baada ya kuondoka katika kampuni hiyo". Mfichua siri wa Boeing amedai kuwa abiria katika ndege ya 787 Dreamliner huenda wakaachwa bila hewa ya oksijeni ndege hiyo iwapo ikipata hitilafu ya kiufundi ghafla. text: Aidha amezungumzia uchezaji wa klabu za Afrika katika Kombe la Dunia. Kuhusu hatua yake kukata nywele zake, amesema hilo halikuwa jambo la ajabu sana kwake. "Ni jambo nililokuwa nimelifanya miezi kama saba hivi iliyopita, lakini nafikiri mimi si mzuri sana katika kuweka mambo mitandao ya kijamii - huwe siwezi selfie za kutosha," amesema. "Kwa hivyo, ninajua ni jambo watu wengi hawajalizoea, kwa sababu nilikuwa na nywele ndefu kwa miaka mingi - lakini kuwa bila nywele ndefu si jambo geni." Amesema hata hivyo kwamba "huwa inarahisisha mambo." "Kwa sababu sasa huwa situmii muda mwingi kwenye bafu," amesema Drogba akihojiwa na BBC. 'Afrika hawachezi kama timu' Mataifa ya Afrika hayajapata matokeo ya kuridhisha Kombe la Dunia isipokuwa Senegal na Nigeria ambao wameshinda mechi moja kila mmoja. Misri na Morocco tayari zimeyaaga mashindano na matumaini ni finyu kwa Tunisia baada yao kushindwa 5-2 na Ubelgiji mechi yao ya pili. Drogba anasema Nigeria, mechi yao dhidi ya Iceland, walicheza jinsia anavyotaka kuona nchi za Afrika zikicheza "kwa kushambulia, kutumia kasi na nguvu, na kushambulia goli mara nyingi." Anasema hilo halikuwepo walipochapwa na Croatia mechi yao ya kwanza. "Walikuwa wanacheza wenyewe - kujiweka sawa, kujilinda bila kushambulia, na kwa kutoa pasi sehemu moja ya uwanja hadi nyingine," amesema. "Wakati huu (dhidi ya Iceland) walicheza kushinda. Walikuwa na washambuliaji wawili na walikuwa na kasi sana na ukali wakishambulia kiasi kwamba Iceland waliingiwa na asiwasi. Walikuwa hawatabiriki kwa mashambulizi na walivutia sana. "Nilitarajia wacheze hivi Kombe la Dunia - na ndio maana wakashinda mechi hiyo," anasema. Anaongeza kuwa mataifa ya Afrika yakicheza Kombe la Dunia yanafaa kudumisha utambulisho wao kama time, na anasema ni Senegal pekee waliokuwa wamefanikiwa kufanya hivyo kabla ya Nigeria mechi yao ya pili. "Ni muhimu kwao kuendelea kufanya hivyo - na Nigeria pia - ili wafike hatua ya 16 bora. Wakiamua kucheza mchezo wa kujilinda na kuanza kuogopa kufungwa, watarudi nyumbani." 'Namuelewa Mo Salah, yalinitokea 2010 Afrika Kusini' Drogba amesema pia anafahamu mambo yalivyokuwa kwa Mohamed Salah kutokuwa sawa wakati wa Kombe Dunia. "Namfahamu vyema kutoka kwa wakati wetu Chelsea, ambapo alikuwa kama kaka mdogo kwangu, na najua anachoongeza kwenye timu ya Misri," anasema. Anaeleza kwamba Misri pia hujihisi wako salama akiwa uwanjani. "Nimeyapitia kama hayo nilipovunjika mkono kabla ya Kombe la Dunia 2010. Kama salah, nilicheza - lakini sikuwa karibu asilimia 100 kuwa sawa wakati Kombe la Dunia unahitaji kuwa sawa asilimia 120". Ingawa Morocco wanarudi nyumbani, anasema walijaribu mechi yao dhidi ya Ureno. Amekubaliana hata hivyo na kocha wa England Gareth Southgate kwamba la Tunisia ni ngumu mno. Anasema tangu mwanzo alitarajia Ubelgiji na England wasonge hadi hatua ya muondoano. 'England, Croatia na Ubelgiji' Drogba anasema ingawa anawapenda England, na alifurahishwa na uchezaji wao dhidi ya Tunisia, ni mapema sana kwao kupigiwa upatu. Anasema amependezwa piana Croatia, na viungo wao wa kati - Ivan Rakitic, Luka Modric na Ivan Perisic - waliocheza vyema sana dhidi ya Argentina. Lakini anapendezwa zaidi na Ubelgiji kufikia sasa. Sababu ya kwanza ni kwamba ana marafiki wengi kikosi hicho, lakini anasema wana ustadi mwingi na uzoefu na wanacheza vizuri sana. "Sijui ni kwa nini watu wengi hawawaangazii kama wanaotarajiwa kushinda," anasema. 'Mshambuliaji ni kujituma' Drogba anasema ingawa tumeshuhudia mataifa mengi yanayodhaniwa kutokuwa stadi kwa mpira yakiwaangusha miamba, kilichompendeza zaidi ni uchezaji wa kushambulia. Anasema amefurahishwa zaidi na uchezaji wa Cristiano Ronaldo wa Ureno aicheza dhidi ya Uhispania ambapo alifunga mabao matatu, na Ahmed Musa wa Nigeria aliyefunga mawili dhidi ya Iceland. "Wote wawili walikuwa na nia ya kujaribu, na hawakuwa na wasiwasi wa kukosa," anasema. Anaeleza pia kwamba amefurahishwa na teknolojia inayowasaidia waamuzi, maarufu kama VAR ambayo imechangia uamuzi wa kutoa penalti mara kadha. "Mnaweza mkafikiria nazungumza kama mshambuliaji wa zamani hapa - lakini kusema kweli imewafaa mabeki pia. Inapunguza makosa pande zote mbili." Anaamini alifikiri mara ya kwanza kwamba Neymar alifaa kupewa penalti dhidi ya Costa Rica, lakini uamuzi uliotolewa ulikuwa sahihi kwa sababu hakukuwa na nguvu za kutosha kumwangusha. "Ni maamuzi kama haya ambayo yanaathiri mechi ambayo ni muhimu sana kuwa sahihi." "Kuwa na VAR katika Kombe la Dunia la sasa umekuwa ni uvumbuzi na uboreshaji bora zaidi katika soka ya sasa - ni mabadiliko muhimu sana katika mchezo huu." Didier Drogba alikuwa akizungumza na mwandishi wa BBC Sport Chris Bevan mjini Moscow. Mchezaji wa zamani wa Ivory Coast na Chelsea Didier Drogba amesema watu hawafai kushangazwa sana na hatua yake kunyoa nywele ingawa amekiri maisha yake yameimarika. text: Raia waliruhusiwa kulitazama kombe hilo likiwa ndani ya sanduku la kioo katika ikulu, Nairobi siku ya Jumatano. Wengi walitumia simu zao kupiga picha, kujiwekea kumbukumbu. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alilipokea rasmi kombe hilo la dhahabu katika ikulu ya Nairobi Jumanne. Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa pekee nchini Kenya. Kando na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao huruhusiwa kuligusa. Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni nchini Urusi. Ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil. Mwaka 2010, lilipokelewa na rais wa wakati huo Mwai Kibaki ambaye alistaafu mwaka 2013. Kenya ni ya 21 mwaka huu kuwa mwenyeji wa kombe hilo mwaka huu kati ya mataifa 51 yanayotarajiwa kulipokea kabla ya Juni. Kombe hilo ambalo lina uzani wa kilo 6.1 limeelekea Maputo, Msumbiji. Wakati wa kuwasili kwa kombe hilo Jumanne, wacheza ngoma waliovalia mavazi ya kitamaduni ya jamii ya Wamaasai walikuwepo kuwatumbuiza wageni. Baadhi walitumia fursa hiyo kupiga picha zao kwa kutumia simu. Picha/AFP, Getty na PSCU Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili. text: Ancelotti, 60, ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na AC Milan ametia saini mkataba wa kuwanoa Everton mpaka mwaka 2024. Kocha huyo mwenye mafanikio lukuki anaichukua timu hiyo ikiwa nafasi ya 15 kwenye jedwali la Ligi ya Primia, wakiwa na alama nne tu juu ya mstari wa kushuka daraja. "Champions League ni mpango wetu wa muda mrefu," amesema na kuongeza. "Hakuna kisichowezekana katika mpira wa miguu." Everton hawajamaliza katika nafasi nne za juu toka mwaka 2005, na kabla ya hapo ilikuwa mwaka 1988. Klabu pekee ambazo Ancelotti amefundisha na kukosa uwiano wa ushindi wa kufikia 50% ni klabu za Italia za Reggiana na Parma mwishoni mwa miaka ya 1990. Ancelotti amesema kilichomvutia kujiunga na klabu hiyo ni: "Historia na utamaduni wa klabu. Ni moja ya klabu kubwa zaidi England." Ancelotti ameshinda Champions League mara tatu kama kocha - mara mbili akiwa na AC Milan na mara moja na Real Madrid. Pia ametwaa ubingwa wa Ligi ya Primia na Kombe la FA akiwa na Chelsea mwaka 2010 na ametwaa mataji wakiwa na Bayern Munich na Paris St-Germain. Ancelotti ametua Everton siku chache baada ya kutimuliwa katika klabu ya Napoli ya nchini kwao Italia. "Ni kweli nimefunza klabu kubwa," amesema, "Mipango ya Paris St-Germain ilikwa mizuri. Naamini itakuwa hivyo na hapa pia. Nimeenda uwanja wa mazoezi jana. Mambo yalikuwa mazuri. Mipango ya klabu kujenga uwanja mpya inaonesha kuwa klabu inataka mafanikio. "Kukusanya mapato ni jambo kubwa katika mpira wa kisasa. Everton wanataka uwanja wao mpya ili uwasaidie kukusanya mapato na kuwa na ushindani mkubwa. "Kwangu, itakuwa ni jambo zuri kuwepo hapa wakati uwanja mpya ukifunguliwa." Kuigeuza Everton kuwa klabu ya kugombea nafasi ya kucheza Champions League si jambo ambalo halitawezekana, anaeleza kocha mpya wa klabu hiyo Carlo Ancelotti. text: Brazil waliondolewa hatua ya robofainali baada ya kulazwa na Ubelgiji. "Nilikuwa ninaomboleza, nilikuwa na huzuni sana, lakini uzuri huzuni huondoka siku zinavyosonga," amesema mchezaji huyo wa Paris St-Germain. "Nina mwanangu wa kiume, familia yangu, marafiki zangu na hawapendi kuniona nikiwa nahuzunika na kujisikitikia nyumbani." Mchezaji huyo wa miaka 26 pia amezungumzia tetesi ambazo zimekuwa zikimhusisha na kuhamia Real Madrid akisema huo ni "uvumi tu". Neymar alihamia PSG kwa uhamisho wa £200m kutoka Barcelona ambao uliweka rekodi mpya ya dunia mwaka jana. Amefunga mabao 28 katika mechi zote alizochezea klabu hiyo ya Ufaransa. Mbrazil huyo alishutumiwa sana wakati wa Kombe la Dunia kwa kudaiwa kuigiza kila alipoguswa au kukabwa na wapinzani, lakini amesema kwamba alifaa kulindwa zaidi na waamuzi. "Watu walikuwa wepesi sana wa kukosoa aliyekuwa anachezewa visivyo badala ya yule aliyefanya madhambi," Neymar ameambia AFP. Neymar ameshutumiwa kufanya udanganyifu uwanjani "Nilikwenda Kombe la Dunia kucheza, kuwashinda wapinzani, na si kugongwa kila wakati. Ukosoaji dhidi yangu ulitiwa chumvi, lakini mimi ni mwanamume sasa, nimezoea kukumbana na mambo kama haya." Neymar amesema kuwa watu wana nia ya kumuangusha kimchezo "Siwezi kuwa mwamuzi na niwe nacheza wakati upo huo, lakini kuna nyakati huwa natamani kama naweza kufanya hivyo." Mshambuliaji wa Brazil Neymar amesema hakutaka "kuuona mpira wowote karibu naye" au hata kutazama mechi zilizosalia za Kombe la Dunia baada ya taifa lake kuondolew akwenye michuano hiyo. text: Ramos amekuwa akishutubiwa baada ya nyota wa Liverpool na Misri Mohamed Salah kuumia begani walipokabiliana wakati wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya. Ramos pia aligongana na kipa wa Liverpool Loris Karius na inadaiwa kwamba huenda tukio hilo lilimduwaza kwa kumsababishia mtikisiko wa ubongo jambo ambalo pengine lilichangia makosa ya kushangaza aliyoyafanya kipa huyo. Makosa yake mawili yalichangia mabao mawili ya Real Madrid ambao walishinda mechi hiyo 3-1. Akinfenwa ameandika kwenye Twitter kwamba daima atakuwepo kuwasaidia na kuwaunga mkono Liverpool wakitishiwa. Amepakia video kwenye mtandao huo wa kijamii akionesha nguvu zake kwa kuvuta buti kwa kutumia mikono yake mwenyewe. Klabu yake inatokea High Wycombe eneo la Buckinghamshire, England na inacheza ligi ya daraja ya tatu kwa sasa. 'Mnyama' Akinfenwa - ambaye jina lake la utani ni The Beast (Mnyama) - amekiri kwenye video hiyo yake kwamba pengine hatawahi kukutana na Sergio Ramos uwanjani. "Tazama kama, sitawahi kucheza dhidi yako kwa sababu klabu yangu haitawahi kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na una bahati." Mashabiki wa Liverpool wameonekana kumshukuru sana mchezaji huyo. Ramos mwenyewe amejitetea na kusema hafai kulaumiwa, akisema hatua ya Mohamed Salah kumshika mkono kwanza ndiyo iliyosababisha mchezaji huyo wa Liverpool kuumia. Ramos, 32, aliambia jarida la michezo la AS la Uhispania: "Upuuzi mtupu, wamemwangazia Salah sana. Sikutaka kuzungumza kwa sababu kila kitu kimeongezwa chumvi." "Kitu pekee sijasikia ni Roberto Firmino akisema kwamba alipata mafua kwa sababu aliangukiwa na jasho langu," amesema Ramos kwa kutania. Ramos pia amedai kwamba Salah angeendelea kucheza mechi hiyo "iwapo angedungwa sindano kipindi cha pili". "Nautazama mchezo vyema, anaushika mkono wangu kwanza na ninaanguka upande mmoja, na jeraha lilitokea kwenye mkono ule mwingine na wanasema kwamba nilishika mkono na kuukatalia kama mchezaji wa judo. Baada ya hapo, kipa wao anasema nilimduwaza kwa kumgonga. "Niliwasiliana na Salah kupitia ujumbe, alikuwa vyema. Angeendelea kucheza iwapo angedungwa sindano kipindi cha pili. Nimefanya hivyo mara kadha lakini wakati ni Ramos alifanyajambo kama hilo, linakwamilia zaidi. "Sijui kama ni kwa sababu umekuwa (nimekuwa) Madrid kwa muda mrefu na umeshinda kwa muda mrefu sana kiasi kwmaba watu hulitazama tofauti." Akinfenwa ni nani? Saheed Adebayo Akinfenwa ni mchezaji aliyezaliwa 10 Mei 1982. Anafahamika sana kutokana na nguvu zake za mwili na unene na misuli yake. Kimo chake ni futi tano na inchi 11. Amewahi kuwachezea Swansea City na Northamptom. Alikuwa anachezea klabu ya AFC Wimbledon kabla ya kuhamia Wycombe. Utotoni, alikuwa anaishabikia sana Liverpool na mchezaji aliyempenda zaidi alikuwa John Barnes. Babake ni Mwislamu lakini mamake ni Mkristo. Alikuwa Mwislamu na hata alikuwa akifunga mwezi wa Ramadhan alipokuwa mdogo lakini siku hizi ni Mkristo. Anafahamika zaidi kwa kuorodheshwa kuwa mchezaji mwenye nguuv zaidi katika mchezo wa video wa FIFA. Mwaka 2014 alihudhuria uzinduzi wa FIFA 15 akiwa pamoja na wachezaji wengine nyota na watu mashuhuri kama vile Rio Ferdinand, George Groves na Lethal Bizzle. Akinfewa uzani wake unadaiwa kuwa kilo 101 na anaweza kuinua kilo 200, ambao ni karibu mara mbili uzani wake. Ana kampuni ya mavazi ya Beast Mode On, ambapo hutumia sifa zake kama mtu mwenye nguvu kama za mnyama. Salah alianguka vibaya na kuumia kwenye bega wakati wa kipindi cha kwanza dhidi ya Real. Licha ya kuumia, ametajwa kwenye kikosi cha Misri kitakachocheza Kombe la Dunia nchini Urusi. Inaaminika kwamba ingawa huenda asichezee Misri mechi yake za kwanza Urusi, huenda akashiriki mechi za baadaye. Wengi wa mashabiki wa Liverpool wanamlaumu Ramos kutokana na kuumia kwa Salah, tukio ambalo mwamuzi hakutoa adhabu yoyote. Sergio Ramos aliwaongoza Real Madrid kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara ya nne katika miaka mitano Ombi limeanzishwa kuwataka Fifa na Uefa kumwadhibu mchezaji huyo wa Uhispania. Wakili mmoja nchini Misri amewasilisha kesi ya kutaka Ramos atakiwe kulipa fidia ya £874m kwa madhara na hasara aliyowasababishia raia wa Misri "kimwili na kiakili." Mshambuliaji wa klabu ya Uingereza ya Wycombe Wanderers Adebayo Akinfenwa ametoa onyo kali kwa nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos. text: Wavuvi wavuta maboti yao ufukweni mwa bahari wakati moshi mkubwa umetanda angani kutokana na volkano Maafisa Indonesia wameongeza kiwango cha hatari na kupanua zaidi eneo linalokaribiana na mlima huo wa vokano unoendelea kuchemka linalotarajiwa kuathirika. Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa. Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3400 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza. Hatari kwa ndege baada ya Volkano Bali Hofu ya kulipuka volkano katika kisiwa cha kitalii cha Bali Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja. Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama eneo hilo na kwenda kwingine. Maafisa wanasema mlma huo wa volkano umekuwa ukitoa moshi mkubwa mfululizo Mlima huo wa volkano ulionekana ukitoa moshi na sauti za milipuko zilisikika kwa umbali wa kilomita 12 kutoka juu ya mlima huo. "Miale ya moto inazidi kutizamwa usiku kucha. Hii inaashiria uwezekano wa mlipuko mkubwa zaidi ," imesema taarifa ya bodi ya kitafa ya usimamizi wa majanga Indonesia, katika ukurasa wake wa Facebook. Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600. Takriban watu laki moja karibu na mlima Agung kisiwani Bali wametakiwa kuhama wakati maafisa wanahofia mlima huo wa volkano kulipuka pakubwa. text: Samatta amefunga zaidi ya magoli 30 msimu huu akaiwa na klabu ya Genk. Samatta, maarufu kama Samagoal, amedokeza kuwa kuna vilabu sita vya Ligi ya Primia ambavyo vinapigana vikumbo kumsajili. "Kwa sasa sipo katika nafasi nzuri ya kuelezea ni klabu gani lakini pia kuna klabu nyingine mbili kutoka Hispania ambazo zimekuwa zikiisaka saini yangu. Hata hivyo, mimi ndoto zangu ni kucheza katika Ligi Kuu ya England," Samatta ameliambia gazeti la Mwananchi. Hii si mara ya kwanza kwa Samatta kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Ligi ya Primia, lakini inaonekana kuwa safari hii mambo yameiva. "Ndiyo, nitaondoka mwishoni mwa msimu huu...(klabu ya England) moja inanifukuzia sana na imekuwa ikipiga simu kwa wakala wangu kila siku," amesema Samatta. Samatta amechezea klabu ya Genk kwa misimu mitatu sasa. Katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari mwaka huu, klabu ya Cardiff ilituma ofa ya Pauni milioni 13 kumng'oa Genk, lakini uhamisho huo ukakwama. Klabu ya hata hivyo Cardiff imeshuka daraja. Ukiachana na Cardiff, vyombo vya habari vya Uingereza mwaka jana viliripoti klabu nyengine tatu za nchini humo amabazo zilikuwa zikihusishwa na kutaka huduma ya ushambuliaji kutoka kwa Samatta. Klabu hizo ni Everton, WestHam na Burnley. Kipenzi cha mashabiki Genk Samatta ameendelea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Genk msimu huu baada ya kuongoza safu ya ushambulizi wa timu hiyo na kunyakuwa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuukosa kwa miaka nane. Streka huyo mwenye miaka 26, ameifungia Genk magoli 23 na kumaliza kama mshambuliaji bora wa ligi. Pia ameifunga magoli 9 kwenye michuano ya ligi ya Europa. Jina la Samatta limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Genk, na wamekuwa wakimuomba mshambuliaji huyo kusalia klabuni hapo kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya. Samatta ameiambia Mwananchi kuwa moyo wake upo England japo kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa ni kitu cha kutamanisha pia. Samatta alipohamia KRC Genk 2016 Hata akihamia England, bado atakuwa ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kufanya hivyo. Pia amekuwa Mtanzzania wa kwanza kucheza Ligi ya Europa. "Hawa jamaa (Genk) hawajacheza Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2011 enzi za akina (Kevin) De Bruyne, najua wanataka nicheze msimu ujao lakini Ligi Kuu ya England ina heshima yake...ni ligi ambayo tayari imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na Ligi Kuu ya Ubelgiji. Ni ligi ambayo inapendwa na watu wengi duniani, Ligi inayoonekana sehemu kubwa duniani. Yaani kwa vitu vingi iko mbali." Mbwana Samatta: Kauli ya 'Haina Kufeli' imenifaa maishani na katika kandanda Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20. Amesalia na miezi 12 kabla ya mkataba wake kumalizika. Samatta alihamia Ubelgiji mwaka mmoja baada ya kutawazwa mchezaji bora wa mwaka Mwafrika aliyekuwa anacheza ligi za barani Afrika mwaka 2015. Alishinda vikombe sita vikuu akiwa na TP Mazembe ikiwa ni pamoja na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015 kabla ya kuondoka. Samatta aliichezea Simba kabla ya kujiunga na TP Mazembe mnamo mwaka wa 2011. Mshambuliaji nyota wa mabingwa wa ligi ya Ubelgiji klabu ya Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta huenda akatua Ligi Kuu ya England (Primia) msimu ujao. text: Hatua hiyo inajiri baada ya waliohudhuria mnada huo kushindwa kuafikia bei iliowekwa. Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, mnada huo ulifanyika katika eneo la ndani la kuweka makasha ICD chini ya usimamizi wa wakala Yono Auction Mart ambaye amepewa kandarasi na mamlaka ya ushuru nchini Tanzania TRA kuchukua jukumu hilo. Baadhi ya bidhaa zilizopatikana katika makasha hayo ni pamoja na samani za afisini kama vile viti, meza na kabati. Kulingana na ripoti iliowekwa wazi kwa umma na Makonda, bidhaa hizo ziliagizwa na marafikize kutoka nchini Marekani ili kukabidhiwa shule za mjini Dar es Salaam. Ripoti kutoka eneo la mnada huo zinasema kuwa waliotaka kununua vitu hiyo walitoa kati ya sh.15 milioni na sh.30 milioni fedha zilizokuwa chini ya bei iliotolewa ya Sh60 million. Mmoja ya wanunuzi hao amesema kuwa bei ya vitu hivyo ni ghali mno. Maswali mengi pia yaliibuka juu ya mzigo huo wa samani baada ya kusambaa mtandaoni kwa barua iliyokuwa ikionesha Paul Makonda kuomba msamaha wa kodi ambao halikuridhiwa mpaka sasa. Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria sambamba na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi. "Kwa mujibu wa sheria ya Madeni, Dhamana na Misaada Namba 30 ya mwaka 1974 (kama ilivyorekebishwa na sheria namba 9 ya mwaka 2003) kifungu cha 3, 6, 13 na 15, Waziri wa Fedha na Mipango ndiye mwenye mamlaka ya kukopa nje na ndani, kutoa dhamana na kupokea misaada kwa niaba ya Serikali. Kwa msingi huo, hakuna mtu yoyote mwenye mamlaka ya kukopa, kutoa dhamana na kupokea misaada kwa niaba ya Serikali bila mtu huyo kukasimiwa mamlaka hayo na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa sheria hiyo" amesisitiza Rais Magufuli. BBC imefanya mazungumzo na mtaalamu wa masuala ya siasa Goodluck Ng'ingo, ambae anasema kila kitu ambacho kinachozua mjadala sheria yake ipo wazi. "Waziri Mpango anasimamia sheria na kanuni na Mkuu wa Mkoa anaonekana kuweka siasa." Kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Afrika Mashariki, Mtu anaweza kusimama kama taasisi au kusimama kama mtu binafsi katika kusafirisha mzigo ukiwa unaonesha ni wa nani na umetokea wapi? Mchambuzi huyo pia ameendelea kusema kuwa asasi za kiraia na taasisi za dini peke yake ndio zina msamaha wa kodi tena kwenye bidhaa ambazo zinahusu afya na elimu lakini vilevile msamaha huo upo kwenye bidhaa ambazo hazizalishwi nchini. Kisheria hakuna msamaha kwa mtu mmoja na kwa vitu vinavyotengenezwa ndani ya nchi, ameongeza kusema Goodluck. Jaribio la tatu la kupiga mnada makontena 20 yalioingizwa nchini Tanzania na kamishna wa jimbo la Dar es Salaam Paal Makonda yamekosa mnunuzi siku ya Jumamosi. text: Mwigizaji Mwingereza Joshua Sasse na mwanamuziki wa Australia Kylie Minogue Minogue, 48, na mwigizaji Mwingereza Joshua Sasse, 28, walitangaza uchumba wao mapema mwaka huu. Wawili hao wamekuwa wakitetea haki sawa za kufunga ndoa nchini Australia. Serikali nchini humo imependekeza kuandaliwa kwa kura ya maamuzi kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja Februari 2017. Kylie Minogue akiwa amevalia fulana yenye ujumbe "Say I Do Down Under" ya kuunga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja kufunga ndoa Bw Sasse amesema angependa wafunge ndoa mjini Melbourne lakini hawatafanya hivyo "hadi sheria hii ipitishwe nchini Australia". Amesema alishangaa sana alipogundua kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja hazikubaliwi kisheria nchini humo. Kura hiyo ya maamuzi itagharimu jumla ya A$160m (£95m; $120m) ambazo zinajumuishwa pia pesa za kufadhili kampeni za wanaounga mkono na wanaopinga. Mchumba wa mwanamuziki maarufu kutoka Australia Kylie Minogue amesema wameahirisha harusi yao hadi pale ndoa za jinsia moja zitakapohalalishwa nchini Australia. text: Helicopter footage of the maiden flight of the world's longest aircraft. Hatua hiyo inakuja baada ya sampuli ya awali ya Airlander 10 yenye thamani ya pauni milioni 32 - ambayo ni mjumuiko wa ndege na meli inayopaa - kustaafishwa rasmi baada ya kufaulu majaribio ya mwisho. Kutokana na mafanikio hayo, kampuni iliyobuni ndege hiyo ya Hybrid Air Vehicles (HAV) yenye maskani yake Bedford, Uingereza imepewa ruhusa na mamlaka ya usafiri wa anga wa kiraia wa nchi hiyo Civil Aviation Authority (CAA) kuanza uzalishaji wa aina hyo ya ndege. Kampuni hiyo awali mwezi wa Oktoba 2018 ilipewa kibali cha usanifu kutoka kwa mamlaka ya usalama wa usafiri wa kiraia barani Ulaya European Aviation Safety Agency (Easa). Airlander 10 baada ya kuanguka Novemba 18, 2017 wakati wa safari ya majaribio Stephen McGlennan, ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya HAV amesema mwaka 2018 ulikuwa mzuri sana na kusema kibali cha Easa kilikuwa ni ishara kubwa. Amesema kwa sasa azma ya kampuni yake ni kutengeneza ndege aina ya Airlander 10 kwa ajili ya biashara na kupakia abiria. "Sampuli ya awali imetimiza kazi yake kwa kutusaidia kupata takwimu na taarifa muhimu tulizokuwa tukizihitaji ili kuvuka kutoka hatua ya sampuli mpaka utengenezwaji wa ndege halisi," amesema. Kwa sasa matarajio ni kwamba ndege ya kibiashara itakamata mawingu ikiwa na abiria waliolipia safari yao miaka ya mwanzoni ya 2020. Sampuli ya awali ya Airlander iikiwa katika majaribio HAV ilitenga kitita cha pauni milioni 32 baada ya sampuli ya awali kudondoka, na kuwaarifu wanahisa wake kuwa hiko ndicho "kiwango cha juu zaidi cha bima". Vibali kutoka kwa CAA na Easa sasa vinaipa kampuni hiyo "nafasi imara ya kuanza uzaishaji". HAV ilifanya majaribio ya awali ya Airlander 10 kutoka katika eneo lake la awali la uwanja wa ndege wa Cardington mwezi Agosti 2016 lakini walihama eneo hilo Juni mwaka jana. Mwezi Julai wakatangaza mipango yao ya kutoa "huduma za kifahari" pale ambapo majaribio yote yatakapomalizika kwa mafanikio. Ndege ndefu zaidi duniani ipo tayari kwa ajili ya kuanza kutengenezwa kibiashara na kupakia abiria. text: Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya ni mshindi mara mbili wa Olimpiki umbali wa mita 800 Sheria, ambazo zitaanza kutumika tarehe 1 mwezi Novemba,zitawahusu wanawake wanaokimbia kuanzia mita 400 mpaka maili moja Mshindi wa mbiao za mita 800 kwenye michuano ya Olimpiki, Caster Semenya ni miongoni mwa watakaoathirika Mkimbiaji wa Afrika Kusini awali alitakiwa kufanyiwa kipimo cha kubaini jinsia na wakuu wa shirika hilo laini majibu hayakuwekwa hadharani. ''Sheria hizo si kuhusu udanganyifu, ni kuhakikisha kunakuwa na michuano ynayofanyika kwa haki na umaana''Rais wa IAAF Lord Coe alieleza akizungumza baada ya kushinda mbio za mita 800 na mita 1500 kwenye michuano ya jumuia ya madola mwezi Aprili,Semenya alisema atakimbia umbali mrefu zaidi Sheria inasemaje? Wanariadha wanawake wanaotaka kushindana wanalazimika kupata dawa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kuingia mashindanoni, na kuhakikisha kuwa kiwango cha homoni hizo kinashuka. Ikiwa mwanariadha wa kike hatataka kutumia dawa, wanaweza kushindana kwenye: Wanaotaka kushiriki michuano hawatakiwi kufanyiwa upasuaji . Taarifa ya IAAF imesema sheria hizo ''hazina lengo la kuwahukumu au kuhoji jinsia ya mwanariadha''. Katika utafiti wa hivi karibuni imeonekana kuwa wanawake wenye mchanganyiko wa homoni za kiume wana uwezo mkubwa wa kukimbia zaidi ya wasio nazo. Semenya ashinda dhahabu mbio za 800m London Semenya aingia fainali 800m Baadhi ya wakimbiaji wa kike wenye homoni nyingi za kiume watatakiwa kukimbia dhidi ya wanaume au kubadili mashindano mpaka pale watakapopata matibabu, hizi ni sheria mpya zilizotolewa na chombo cha riadha duniani. text: Rais Putin alitarajiwa kufanya ziara nchini Ufaransa baadaye mwezi huu Alitarajiwa kukutana na Rais wa Ufaransa Francois Hollande na kufungua kaniss jipya la Orthodox baadaye mwezi huu. Lakini baada ya serikali ya Ufaransa kusema kuwa mazungumzo yataegemea zaidi suala la Syria ziara hiyo ilifutwa. Ufaransa ina wasi wasi na mashumbulio yanayoungwa mkono na Urusi mjini Aleppo Siku ya Jumatatu Hollande alipendekeza kwamba Urusi inafaa kushtakiwa kwa uhalifu wa kivita kutokana na mashambulio ya mabomu yanayotekelezwa na ndege za kivita za Urusi mjini Aleppo, Syria. Bwana Hollande aliiambia runinga moja ya Ufaransa kwamba taifa hilo linafaa kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Alidokeza pia kwamba huenda angekataa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, wakati wa ziara hiyo "Hawa ni watu ambao ni waathiriwa wa uhalifu wa kivita. Wanaotenda haya wanafaa kuwajibishwa, hata kama ni katika mahakama ya ICC," Bw Hollande aliambia TMC. Urusi imekanusha madai kwamba inashambulia raia na badala yake imekuwa ikisisitiza kwamba inawashambulia magaidi. Wiki iliyopita, Urusi ilitumia kura ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa urushaji mabomu Aleppo. Azimio hilo lilikuwa limewasilishwa na Ufaransa na Uhispania. Urusi imekanusha madai kwamba inashambulia raia na badala yake imekuwa ikisisitiza kwamba inawashambulia magaidi. Urusi na Syria si wanachama wa ICC. Rais wa Urusi Vladimir Putin amefuta ziara yake nchini Ufaransa wakati unaendelea kushuhudiwa mzozo kuhusu Syria. text: Mwanaharakati Nabeel Rajab UN inasema kuwa hukumu ya Nabeel Rajab ilifanyika kinyume cha sheria na ilikiuka uhuru wake binafsi wa kujieleza. Hadi sasa Nabeel amekwisha tumia miaka mingi tu gerezani tangu alipokuwa akiongoza harakati zake za kidemokrasia mwaka 2011.Lakini serikali kwa upande wake inasema kuwa mashitaka ya Rajab yalitolewa katika mfumo wa uhuru na uwazi. Nabeel Rajab, mkuu wa kituo cha haki za binadamu cha Bahrain Center for Human Rights (BCHR) na makamu katibu mkuu wa taasisi ya kimataifa ya haki za binadamu ya International Federation of Human Rights (FIDH), amekuwa akishikiliwa tangu june mwaka 2016. Mwezi Februari mwaka huu alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kutokana na kutoa ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter ulikuwa ukipinga kile kinachodaiwa kuwa ni mateso wanayoyapata wafungwa wa Bahrain na vitendo viovu vya jeshi la Saudia wakishirikiana na muungano wa wapiganaji wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Yemen Hata hivyo hukumu hiyo ilikuja huku akiwa anatumikia kifungo cha awali cha miaka miwili gerezani baada ya kukutwa na makossa ya kueneza habari zinazodaiwa kuwa ni za uongo. Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa taarifa kutoka kwa wanafamilia wa Rajab,zinasema kuwa anaishi katika mazingira magumu,anafungiwa katika chumba kichafu,chenye wadudu ambacho ukubwa wake si zaidi ya futi kumi,lakini pia afya yake imedhoofu na anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi ambapo anahitaji matibabu. Bodi ya umoja wa mataifa UN,imetaka kuachiliwa huru kwa mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahraini Nabeel Rajab aliyefungwa kwa madai ya kufanya makosa ya kueneza habari za uongo na kukashifu mamlaka za kiserikali. text: Polisi wa Queensland walipakia picha hiyo mtandaoni mara ya kwanza Jumatatu Ingawa walipigwa na butwaa mwanzoni, walitumia fursa hiyo kupiga picha na chatu huyo. Picha ya mmoja wa polisi hao ilipakiwa mtandaoni na imezua hisia si haba. "Nyoka huyo alikuwa na urefu wa zaidi ya mita tano, na kusema kweli si kiumbe ambaye unaweza kutafuta utepe useme utampima," polisi hao waliambia BBC. Picha hiyo iliyopakiwa na polisi hao kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa imetazamwa mara zaidi ya milioni mbili, na kutolewa maoni mara 10,000. "Huwa hatufanyi mambo ya upweke," waliandika polisi hao. "Huwa huwezi kujua utakutana na nini ukiwa kwenye zamu." Polisi hao walikutana na nyoka huyo karibu na Wujul Wujul, karibu 345km (maili 210) kaskazini mwa jiji la Cairns. Chatu aina ya Scrub, ambao huwa ndio nyoka warefu zaidi Australia, wanaweza kufikia urefu wa hadi 7m (futi 23). Maafisa wawili wa polisi katika jimbo Queensland nchini Australia walipigwa na butwaa walipokumbana na chatu mkubwa wakipiga doria. text: Philippe Coutinho amesema uhamisho wake kwenda Barcelona ni ndoto iliyokamilika Kiungo huyo alieleza hisia zake za kutimiza ndoto yake alipokuwa akipigwa picha katika uwanja wa Nou Camp wakati klabu yake mpya ilipokuwa ikicheza na Levante. "Mashabiki wa Barcelona tayari nipo hapa, ndoto zimekuwa kweli natumani tunaonana kesho, " alisema Coutinho kupitia video fupi aliyoiweka katika mtandao wa Twita. Coutinho anatarajiwa kutambulishwa leo kuwa mchezaji mpya wa Barcelona baada ya klabu yake ya Liverpool kukubali kuuza kiungo huyo kwa dau la pauni milioni 142. Nyota huyu atasaini mkataba wa miaka mitano na klabu itayotaka kumnunu mchezaji huyo italazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 355. Kiungo wa kibrazil Philippe Coutinho amesema uhamisho wake kwenda Barcelona ni ndoto iliyokamilika. text: Maradona alimlaumu refa wa mechi hiyo kwa kuipendelea Uingereza dhidi ya Colombia. Akizungumza katika programu yake ya kila jioni ya katika idhaa ya televisheni ya Telesur inayomilikiwa Venezuela, Maradona aliongeza, ''Ukimchunguza, au kumfanyia utafiti, utagundua kuwa hastahili kusimamia mechi. Utakuta ni raia wa Marekani, ni kinaya''. Maradona alihisi kuwa Geiger angemwadhibu Harry Kane kwa kumchezea rafu kiungo wa Colombia Carlos Sanchez lakini badala yake aliipa Uingereza penalty iliyomruhusu Kane kuiweka Uingereza kifua mbele. Lakini leo ameandika kwenye mitandao ya kijamii kuomba radhi. "Niliyasema mambo kadha na, nakiri, baadhi yalikuwa hayakubaliki," ameandika. "Ninaiheshimu sana kazi - ambayo si rahisi - ambayo taasisi hiyo (Fifa) na waamuzi huifanya," ameongeza. Nahodha wa Colombia Radamel Falcao pia ameungana na Maradona kueleza kuwa walionewa kwenye mechi hiyo na refa Geiger. Falcao anahoji kuwa maamuzi yote yaliegemea upande wa Uingereza. "Ni aibu," alisema Falcao. Geiger alionekana kuwa na kazi ngumu alipokuwa akisimamia kipute hicho mjini Moscow, kabla ya Uingereza kushinda kupitia penalti. "Hali nzima ilituathiria na mabo yalikuwa dhidi yetu," alizidi Falcao. Maradona alipigwa picha kwenye mechi hiyo akiwa amevalia jezi ya Colombia na pia alinaswa baadaye akisherekea goli la kusawazisha mechi la beki Yerry Mina. Colombia walipinga uamuzi wa mwamuzi kuwapa England penalti ambayo Harry Kane alifunga na kuwapa uongozi Shirkilisho la soka la Fifa limelaani tamko la Maradona na kulitaja kuwa ''lisilofaa''. Fifa imeongeza kuwa imestajaabishwa kusikia kauli hizo kutoka mchezaji aliyechangia historia ya soka duniani. "Fifa inapinga vikali shtuma dhidi ya utendakazi wa maafisa wa mechi ulioonekana chanya katika mechi ngumu na yenye hisis nyingi. Timu ya taifa ya soka ya Uingereza ikijiandaa kwa mechi ya robo fainali, siku ya Jumamosi, mchezaji wa zamani wa Argentina Diego Maradona amesema kuwa ushindi wao dhidi ya Colombia mechi ya hatua ya mchujo ni ulaghai. text: Katika ibada ya kuamkia leo Papa Francis aliwahimiza waumini wasiwapuuze wahamiaji na maskini. Katika ibada ya kuamkia leo Papa Francis aliwahimiza waumini wasiwapuuze wahamiaji na maskini. Ametoa ujumbe huu ukienda sambamba na shughuli wa kuwaoa zaidi ya watu 5,000 kutoka ngalawa mbovu zilizopatikana zikielea katika Ufuo wa Bahari ya Libya na Italia. Papa Francis pia anatarajiwa kuzungumzia umuhimu wa mashauriano kati ya Madhehebu mbalimbali. Matamshi hayo yanaonekana kulenga milipuko iliyotokea katika Kanisa la Coptic nchini Misri siku chache zilizopita. Misa pia zilifanyika katika makanisa ya Coptic nchini Misri ambapo mashambulizi ya wiki iliyopita yalidaiwa kutekelezwa na Islamic State yaliwaua watu 45. Maelfu ya wamehudhuria misa Papa Francis akiwa St Peter's Square Ulinzi ulidumishwa Misa pia zilifanyika katika kanisa la Coptic nchini Misri Maelfu ya mahujaji wamekusanyika Roma kushuhudia Papa Francis akiongoza ibada ya pasaka katika eneo la St Peter's Square. text: Wanawake wenye watoto wanne na zaidi kusamehewa kodi Hungary Waziri mkuu wa nchi hiyo Viktor Orban ameyasema hayo wakati akizindua mipango iliyobuniwa kwa ajili ya kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa. Amesema hiyo ni njia ya kulinda mustakabali wa Hungary bila ya kutegemea Wahamiaji. Katika hatua hizo zinazochukuliwa pia, wanandoa vijana watakuwa wanapewa mkopo usio na roba wa dola elfu 26, ambao utafutwa watakapofikisha watoto watatu. Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban Wanasiasa wa mrengo wa kulia nchini humo wamekuwa wakipinga uhamiaji unaofanywa na Waislamu. Idadi ya watu nchini Hungary imekuwa ikipungua kwa elfu 32 kwa mwaka na wanawake nchini humo wana watoto wachache kushinda wastani wa Umoja wa Ulaya.Waziri mkuu huyo wa Hungury amesema kwa nchi za magharibi jibu la kupungua kwa watoto wanaozaliwa kwa Ulaya ni Wahamiaji. ''...kwa kila mtoto anayepungua lazima mwengine aje, halafu idadi itakuwa sawa...Watu wa Hungary wanafikiri tofauti, hatuhitaji idadi tunataka watoto wa Hungary...'' alisema. Waziri Mkuu huyo wa Hungary amekuwa akichukua hatua kali dhidi ya wahamiaji, hali ambayo mara kwa matra imefanya kutofautiana na wenzake wa Ulaya. Ufaransa ni nchi inayoongoza kwa mwanamke kuzaa watoto wengi nchi za Umoja wa Ulaya kwa wastani wa 1.96 huku Hispania ikiwa na kiwango cha chini kabisa cha 1.33. Niger nchi iliyoko Afrika magharibi ndiyo inayoongoza kwa mwananmke kuzaa watoto wengi duniani kwa watoto 7.24 kwa mwanamke mmoja. Wanawake nchini Hungary wenye watoto wanne na zaidi watasamehewa kulipa kodi ya mapato maishani mwao. text: Mashambulizi ya makombora yamethibitisha umuhimu wa mfumo huo Tangu Jumatatu, Wapiganaji wa Hamas wamerusha makombora 1000 katika ardhi ya Israel mengi yakilenga mji mkuu wa Tel Aviv na maeneo yake nao wanajeshi wa Israel wakifanya mashambulizi ya mabomu katika ukanda wa Gaza na kuwauwa makumi ya raia. Lakini Israel ina kinga yenye uwezo mkubwa kujilinda dhidi roketi zinazorushwa na Hamas kutoka Gaza , kwa jina 'Iron Dome'. Kama ilivyoripotiwa na jeshi la Israel, kati ya roketi 1050 zilizorushwa, 850 zilitunguliwa na mfumo huo wa kutungua makombora. Picha kadhaa na kanda za video zimeonyesha uwezo wake , ikiweza kuharibu makombora kadhaa angani na kuyazuia kuanguka katika makao ya raia. Hatahivyo kama mifumo mingine ya ulinzi , silaha ya Iron Dome ina mapungufu yake na wataalamu wanaonya kwamba mashirika yenye uwezo mkubwa yanaweza kuathiri uwezo wake. Mwanamume akitazama kombora lililotunguliwa Jinsi mfumo wa Iron Dome unavyofanya kazi. Mfumo huu ni mojawapo ya mifumo ya kulinda anga ya Israel. Lengo lake kuu ni kulinda taifa hilo dhidi ya silaha za masafa marefu, roketi na vitisho vingine. Mfumo huo uliundwa na kampuni ya Rafael Advanced Defence System Ltd, kampuni ya kibinafsi inayoshirikiana kwa ukaribu na jeshi la Israel ambayo pia hutengeza mifumo ya kinga ya baharini na majini ya taifa hilo. Kampuni hiyo pia inafadhiliwa na Marekani kwa takriban US $ 200m. Mtengenezaji wake anahakikisha kuwa ni mfumo unaotumiwa sana kutungua makombora angani duniani na kwamba umefanikiwa kufanya kazi katika matukio asilimia 90. Betri za mfumo huo hutengenezwa kwa kutumia makombora ya kutungua makombora, Rada na mifumo inayochambua ni wapi kombora la adui litaanguka. Teknolojia ya Rada inatofautisha kati ya makombora ambayo yanaweza kufika katika miji na yale yanayokosa lengo lake. Mfumo huo baadaye unaamua ni kombora gani linafaa kutunguliwa. Silaha hiyo ya kutungua makombora hurushwa wima kutoka kwa mfumo huo. Baadaye hutungua makombora hayo angani. Makombora yatunguliwa angani Je ni kwanini mfumo huo uliundwa? Chanzo cha mfumo huo wa Iron Dome ni mzozo wa 2006 nchini Israel dhidi ya kundi la Hezbollah, wapiganaji wa Lebanon. Hezbollah wakati huo ilirusha maelfu ya roketi , na kuwaua makumi ya Waisraeli na kusababisha uharibifu mkubwa. Hatahivyo juhudi za Israel kujenga mfumo wa kinga ya makombora ulianza miongo mitatu iliopita na ni kutokana na ushirikiano kati ya jeshi la Marekani na Israel. Mwaka 1986, Israel ilitia saini kandarasi na Marekani ili kufanya utafiti kuhusu mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya masafa marefu, mradi ulioanzishwa na utawala wa rais Ronald Reagan wa Marekani. Miaka mitano baada ya makubaliano hayo , viongozi wa Israel walisukuma juhudi za kujenga mfumo huo wakati rais wa Iraq Saddam Hussein alipoagiza kurushwa kombora la Scud nchini Israel wakat wa vita vya kwanza vya Ghuba. Kufikia mwanzo wa 2010, silaha ya Iron Dome ilikuwa imefanikiwa kupita majaribio yaliofanywa na jeshi la Israel. Mwezi Aprili 2011, mfumo huo ulijaribiwa katika makabiliano ya kijeshi kwa mara ya kwanza wakati ilipoangusha kombora lililorushwa katika mji wa Beersheba , kusini mwa taifa hilo. Mfumo wa kukabiliana na makombora Israel Mapungufu ya 'Iron Dome' Tangu siku ya Jumatatu , ving'ora vya makombora yanayorushwa kutoka Gaza vimesikika vikilia katika miji kadhaa ya Israel , kama vile Tel Aviv , Ashkelon, Modiin na Beeresheba. Wapiganaji wa Kipalestina wamekuwa wakijaribu kurusha makombora mengi kwa mpigo. Mtaalamu wa masuala ya usalama na ulinzi Anna Ahnronheim wa gazeti la Jerusalem Post nchini Israel aliambia BBC kwamba inatia hofu kusikia makumi ya silaha zilizotunguliwa na makombora yakianguka karibu na mfumo huo. Idadi ya mashambulizi ya roketi iliongezeka baada ya nyumba mbili kuangushwa na mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza siku ya jumanne. Israel ilisema kwamba ilikuwa ikilenga vituo vya kurushia roketi hizo, majumba marefu , makaazi na ofisi zinazotumiwa na Hamas katika eneo la Gaza siku ya Jumanne huku ikiongezea kwamba ilikasirishwa na hatua ya Hamas kushambulia makaazi ya raia. Baadhi ya watalamu wanahoji matumizi ya Iron Dome Awali , mfumo wa Irone Dome uliripotiwa kuangusha kati ya asilimia 85-90 ya makombora yaliorushwa na Hamas. Ufyatulianaji wa makombora kati ya vikosi vya Israel na wapiganaji wa Palestina unaendelea huku Umoja wa Mataifa ukihofia 'vita vikali vaidi'. text: Mkahawa wakataa kuwahudumia wanawake waislamu Ufaransa Katika kanda hiyo,iliosambazwa sana katika mitandao ya kijamii ,mwanamume anamwambia mwanamke aliyevaa Hijab :''Magaidi ni Waislamu na Waislamu wote ni Magaidi''. Kisa hicho kilitokea katika mkahawa wa Le Cenacle,Tremblay-en-France siku ya Jumamosi usiku. Siku ya Jumapili,mtu huyo aliomba msamaha kwa kundi lililokongamana nje ya mkahawa huo. Waandamana kupinga hatua ya mkahawa mmoja kukataa kuwahudumia wanawake Waislamu Ufaransa Anasema kuwa alijisahau na kutoa matamshi hayo kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo kuhusu vazi la Burkini katika fukwe za bahari za Ufaransa,na kwamba ana rafikiye aliyefariki katika shambulio la mjini Paris katika eneo la Bataclan mnamo mwezi Novemba. Kanda ya video mjini Paris ilioonyesha mkahawa mmoja ukikataa kuwahudumia wanawake wawili Waislamu imezua hisia kali nchini Ufaransa. text: Nchi za Korea kuifanya rasi ya Korea kuwa eneo la amani Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alitangaza kuwa nchi yake itaacha mpango wake wa zana za kinuklia.Trump amesema mambo yalikuwa mazuri. ''Tumepiga hatua nzuri kuhusu Korea kaskazini. Awali kabla ya kuwa rais ilionekana kana kwamba tutaingia vitani na Korea Kaskazini na sasa tumepiga hatua sana. Tumerejeshewa wafungwa wetu, tunarejeshewa mabaki ya wapiganaji wetu,lakini la muhimu hakuna tena majaribio ya makombora, majaribio ya silaha za nuklia. Sasa wanataka kuomba kuhodhi mashindano ya olimpiki, sasa tuna mambo mengi mazuri yanayoendelea,'' alieleza. Trump amerejelea kauli yake kuwa utawala wake umekuwa chachu ya kuleta mazingira tulivu yanayoonekana sasa. ''Kumbuka hili, kabla ya kuwa rais watu wengi walifikiri kuwa tunakwenda vitani lakini sasa mahusiano mazuri yamejengwa, nawaambia kwa mawazo yangu, mahusiano ni mazuri, hali imekuwa ya utulivu, kwa sasa tunapoongea hali imetulia, amekuwa mtulivu, nimekuwa mtulivu hivyo tutaona mambo yatakavyokuwa'' Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesema makubaliano hayo yanalenga kumaliza historia ya matukio ya makabiliano na kuifanya rasi ya Korea kuwa ardhi ya amani bila kuwepo kwa vitisho wala silaha silaha za nyuklia. Rais wa Marekani, Donald Trump ameunga mkono makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wawili wa Korea katika mkutano uliofanyika mjini Pyongyang. text: Wataalamu wanasisitiza kwamba ni lazima mtu ale mayai kwa njia ifaayo, na mtu awe anakula lishe bora yenye afya, ndipo aweze kupata manufaa hayo. Lakini bado wasiwasi kwamba ulaji wa mayai mengi unaweza kudhuru afya ya binadamu kwa sasa unaonekana kupungua. "Mtu anaweza kufikiria zaidi kuhusu tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu wa lishe, lakini kilichobainika kutoka kwa utafiti huu wa China ni kwamba kula angalau yai moja kwa siku hakuongezi hatari ya kuugua maradhi ya moyo, na badala yake kuna faida," anasema Prof Nita Forouhi, wa Chuo Kikuu cha Cambridge. Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la masuala ya moyo la Heart, ulifanywa baada ya miaka mingi ya watu kuonyesha dhidi ya ulaji mayai. Watu walikuwa wakitahadharishwa kwamba kula mayai kunaweza kuwasababisha kuambukizwa viini vya salmonella na pia kwamba yana kiwango cha juu cha cholesterol. Mayai mangapi bora? Siku hizi, wengi wa madaktari huwa hawashauri watu kutokula mayai, kwani ni miongoni mwa vyakula vyenye virutubisho na madini mengi zaidi ya manufaa kwa mwili. Yana protini ya kiwango cha juu pamoja na Vitamini A, D, B na B12, na pia madini ya lutein na zeaxanthin ambayo yanaweza kuzuia mtu kupata matatizo ya macho atakapozeeka. "Moja - hata mawili - kwa siku ni sawa kabisa," anasema Dkt Frankie Phillips, kutoka kwa Chama cha wataalamu wa Lishe Uingereza. "Watu hawafai kuwa na wasiwasi wa kula mayai mengi." Dkt Phillips anasema onyo pekee watu wanafaa kuzingatia ni kwamba kula chakula cha aina moja pekee kwa wingi kuna maana kwamba "watu wanakosa madini na virutubisho ambayo hupatikana kutoka kwa vyakula vingine." Na ingawa mayai yana protini, Dkt Phillips anasema kawaida mwili hupata protini za kutosha kutoka kwa vyakula vingine, na kula protini kupindukia kunaweza "kuwa mzigo kwa figo". Wakfu wa Moyo Uingereza (BHF) uliondoa ushauri wake wa kuwataka watu wasile mayai zaidi ya matatu kwa wiki mwaka 2007 kutokana na kutokea kwa utafiti mpya kuhusu cholesterol. Cholesterol Kwa mujibu wa ushauri wa Huduma ya Taifa ya Afya Uingereza (NHS), "ingawa mayai yana cholesterol, kiwango cha mafuta kutoka kwa mafuta na vyakula vingine tunavyovila huathiri zaidi kiwango cha chorestrol kwenye damu kuliko kinavyoathirika kutokana na ulaji wa mayai." Kimsingi, mayai sio chanzo cha matatizo ya kuwepo na kiwango cha juu cha chorestrol kwenye damu. Ni mafuta tunayoyatumia. Kwa mujibu wa Heart UK, yai la kawaida (58g; 2oz) huwa na mafuta 4.6g. Lakini ni robo pekee ya mafuta hayo huwa mafuta mabaya, yaani yale yanayoongeza kiwango cha chorestrol. Siagi na jibini hali ni tofauti. Mayai yanavyotumiwa huwa na manufaa kwa mwili Yapikweje? Kwa kuangazia jinsi tunavyopika mayai, mayai ya kuchemshwa ndiyo bora zaidi. Wataalamu wengi wa lishe hupinga kukaangwa kwa mayai kwa sababu mara nyingi mafuta hutumiwa na hivyo kiwango cha cholesterol anachokula mtu huongezeka. Mayai mabichi au yalivyopikwa kidogo tu pia ni sawa, mradi tu yawe yalitokana kwenye mazingira safi. Mayai yaliyopikwa ndiyo njia bora zaidi ya kujikinga na maambukizi. Usinunue mayai ambayo yamevunjika kwani yanaweza kuwa yameingia uchafu au bakteria. Wengi bado wanakumbuka jinsi ya kutumia maji kwenye bakuli kubaini iwapo yai limeharibika au la. Iwapo litazama, ni bora na lisipozama limeharibika. Mayai mengi huwa katika kiwango kizuri kwa siku 28 tangu yanapotagwa. Utafiti ambao uliwashirikisha watu laki tano nchini China unadokeza kwamba kula yai moja kwa siku kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo na kiharusi. text: Emilie Telander (kulia) anasema ana uchovu mwingi kwa vile amerejea muda wa kawaida wa kufanya kazi Muuguzi kwenye makao ya watu wazee Emilie Telander, mwenye umri wa miaka 26 anasema hajafurahia kuona muda huo ukifika kikomo, tena ameambiwa kufanya kazi tena muda wa masaa nane. "Ninahisi kuwa mchovu zaidi kuliko nivyokuwa awali, anasema kuwa sasa ana muda mfupi nyumbani kupika na kusoma na bintiye mwenye umri wa miaka minne. Gothenburg umekuwa ukifanyia majaribio muda wa kufanya kazi wa saa nane Wakati wa kipindi cha majaribio, wafanyakazi wote walikuwa na nguvu. Niliweza kuona kuwa kila mtu alikuwa na raha. Bi Telander alikuwa kati ya wauguzi 70 ambao masaa yao yalikuwa yamepungua wakati wa majaribio hayo. Baada ya kubuniwa kuboresha sekta ambayo ina changamoto za kupata wafanyakazi wa kutosha kuwaangalia watu wazee nchini humo, wauguzi zaidi waliajiriwa ili kusaidia muda uliopunguzwa. Makao ya watu wazee ya Svartedalen Watafiti huru nao walilipwa kuwasoma wafanyakazi ambao waliiendelea kufanya kazi muda wa kawaida. Ripoti ya mwisho inaratajiwa kutolewa mwezi ujao, lakini takwimu zilizotolewa zinaunga mkono maoni yake Telander. Wakati wa miezi 18 ya majaribio wauguzi ambao walifanya kazi saa chache waliomba likizo chache, na walifanya kazi kwa asilimia 85 zaidi kama vile kuwatembeza wagonjwa na kuimba nao. Huenda muda wa kawaida wa saa nane wa kufanya kazi ukasalia Hata hivyo mradi huo ulipata kukosolewa na wale waliokuwa na wasi wasi kuwa gharama yake ilikuwa ya juu kuliko manufaa. Wapinzani wa kati-kulia, walipeleka mswada wakati manispaa ya Gothenburg wakitaka kuusitisha mradi huo mapema mwezi wa tano, wakidai kuwa haikuwa vyema kuwekeza pesa za walipa kodi katika mradi ambao haukuwa na manufaa ya kiuchumi. Utafiti zaidi unafanyiwa mfumo wa kupokezana kazi nchini Sweden Sweden imekuwa ikifanyia majaribio muda wa masaa sita, huku wafanyakazi wakipata saa chache za kufanya kazi, sasa majaribio hayo ya miaka miwili yamekamilika na yote yanaonekana kuenda salama text: Virgil van Dijk na Vivianne Miedema ni wachezaji wa kwanza kutoka nchi moja kushinda tuzo ya PFA pamoja. Wote ni raia wa Uholanzi. Sterling, 24, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu inayotelwa na chama cha Waandishi wa Kandanda (FWA). Tuzo hiyo kwa upande wa wachezaji wanawake imenyakuliwa Nikita Parris, wote wawili wanatokea Manchester City. Van Dijik ambaye ni beki kisiki wa Liverpool kwa upande wake ameshinda tuzo inayotolewa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) nchini humo. Kwa wanawake tuzo hiyo imenyakuliwa na Vivianne Miedema anayekipiga klabu ya Arsenal. Beki huyo amekuwa wa kwanza kushinda tuzo ya PFA toka iliponyakuliwa na John Terry katika msimu wa 2004/05 alipokuwa akikipiga na Chelsea. Van Dijik pia amemrithi mshambuliaji wa klabu yake ya Liverpool Mohammed Salaah amhaye alishinda tuzo hiyo msimu uliopita. Klabu ya Liverpool inaendelea kuminyana vikali na Manchester City kuwania ubingwa wa Primia. Timu hizo zinatofautiana alama moja tu na City wameketi kileleni kukiwa na mechi mbili za kucheza kabla msimu kuisha. Van Dijik ambaye amejiunga na Liverpool Januari 2018 anatajwa kuwa mwamba kwenye safu ya ulinzi wa klabu hiyo. Liverpool wamecheza michezo 19 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa katika mechi 36 walizocheza mpaka sasa msimu huu huku van Dijik akiongoza safu ya ulinzi. Beki huyo amefunga magoli matatu na kutengeneza magoli mawili kwa timu yake. "Hii ni tuzo kubwa kwa mchezaji, kuchaguliwa kuwa wewe ni bora na wachezaji wenzako unaocheza dhidi yao kila wiki," amesema van Dijik na kuongeza, "ni kitu cha kipekee na ninajivunia kukipokea." Katika mbio za ushindi van Dijik amewapiku Raheem Sterling, Bernardo Silva, Sergio Aguero, Sadio Mane na Eden Hazard. Hata hivyo Sterling pia ameshinda tuzo za PFA kwenye kipengele cha mchezaji kinda. Raheem Sterling na Nikita Parris wameng'ara na Manchester City msimu huu Nyota ya Sterling imeendelea kung'ara msimu huu japo amekumbwa na visa kadhaa vya kubaguliwa kwenye ligi ya Primia na hata kwenye ligi ya klabu bingwa Ulaya. Zaidi ya waandishi 400 ambao ni wanachama wa FWA walipiga kura huku Sterling akimshinda Van Dijik kwa zaidi ya kura 100. Wachezaji wengine ambao walipata kura japo hawakushinda ni pamoja na Harry Kane, Eden Hazard, Alexandre Lacazette, Bernardo Silva na David Silva. Sterling anakuwa mchezaji wa kwanza wa City kushinda tuzo hiyo kwa miaka 50 toka iliponyakuliwa na Tony Book mwaka 1969. "Sterling ni mfano bora wa mchezaji kwenye kipaji ambaye waanzilishi wa tuzo hii walitaka kumtuza walioianzisha mwaka 1947," amaesema mwenyekiti wa FWA Carrie Brown. "... tuzo hii pia ni kielelezo cha kuthamini ujasiri alionao Sterling katika kupambana na ubaguzi wa rangi, jambo ambalo litaacha alama kwa vizazi vijavyo kwenye mpira na jamii kwa ujumla," amesema Bi Brown. Raheem Sterling na Virgil van Dijik wameibuka wachezaji bora wa msimu Ligi ya Primia kwa 2018/19 wa ambao upo ukingoni. text: Hatua hiyo inaweza kuzifanya nchi tajiri zinazotoa msaada kutoa fedha zaidi kukabiliana na ugonjwa huo. Lakini shirika hilo limesema hatari ya ugonjwa huo kusambaa nje ya Congo si kubwa. Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya watu 1,600 nchini humo. Juma hili ugonjwa ulibainika mjini Goma, kuliko na wakazi zaidi ya milioni moja. ''Sasa ni wakati wa kuchukua tahadhari, ''Mkuu wa WHO Adhanom Ghebreyesus amewaambia wana habari mjini Geneva siku ya Jumatano, siku ambayo hali ya dharura ilitangazwa. Amesema amekubali mapendekezo yaliyotolewa kwamba kusiwe na zuio la watu kusafiri au kwa ajili ya kufanya biashara wala kuwapima abiria katika bandari au viwanja vya ndege. Shirika la msalaba mwekundu limeunga mkono mapendekezo hayo. ''Ingawa haibadili ukweli wowote kwa waathirika na washirika wanaosaidia kupambana na Ebola, tuna matumaini kuwa itafanya jumuia ya kimataifa kulichukulia kwa uzito unaotakiwa.'' Taarifa ya shirika hilo ilieleza. Hali ni mbaya kiasi gani nchini humo? Mlipuko wa Ebola ni ugonjwa wa pili kwa ukubwa katika historia ya nchi hiyo, ulianza mwezi Agosti na inaathiri majimbo mawili nchini DRC, Kivu Kaskazini na Ituri. Zaidi ya watu 2500 wameathiriwa na ugonjwa huo na theluthi mbili kati yao wamepoteza maisha. Ilichukua siku 224 kwa idadi ya walioathirika kufika 1,000 , lakini ndani ya siku 71 zaidi idadi ilifika 2,000. Watu takribani 12 huripotiwa kupata ugonjwa huo kila siku. Kwanini ugonjwa huu haujadhibitiwa? Wafanyakazi wa afya wamekua wakipata vikwazo vya kutoaminika na machafuko nchini humo. Watu wengine hawawaamini watoa huduma za afya, hivyo hufanya watu wenye dalili za ugonjwa huo kukwepa matibabu, hali hii inawia vigumu kuzuia kuenea kwa virusi vya ebola. Ingawa zaidi ya watu 1,300 wamepoteza maisha tangu mwezi Agosti, Shirika la misaada la Oxfam linasema linakutana na watu kila siku ambao hawaamini kama kuna virusi vya ebola. Tangu mwezi Januari kulikua na matukio 198 ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, na kusababisha majeruhi 58. Shirika la afya duniani WHO, limesema kuwa hatari ya kusambaa zaidi si kubwa sana, lakini inawezekana ugonjwa huo kuingia nchi jirani. Ebola ni nini? ◾Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo. ◾Kisha mgonjwa hutapika, kuharisha na kutoka damu. ◾Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola ◾Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi. Shirika la afya duniani, WHO limetangaza ugonjwa wa Ebola nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa ni ''dharura ya kiafya inayohitaji jumuia ya kimataifa kuitazama''. text: Akizungumza na wataalamu wa ujenzi hii leo amesema kuwa ana uhakika kuwa sauti zile zilikuwa zao lakini amefikiria na kuwasamehe. "Siku za hivi karibuni kuna watu walinitukana na kuthibitisha kuwa sauti zile ni zao, nikawa nakaa nafikiriaa, nikasema hawa wakipelekwa katika kamati ya siasa, adhabu itakuwa kubwa nikasema ngoja ninyamaze lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha... Nilijiuliza... kila siku mimi huwa naomba msamaha kwa Mungu , kwa ile sala ya "tusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe wengine", nikaona hawa waliokuja kuniomba msamaha nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa hivyo nikaamua kuwasamehe. Hawa waliokuja kuniomba msamaha na kutoa kweli katika dhamira yao ni Januari Makamba na William Ngereja. Niliwasamehe na kusahau" Magufuli aeleza. Rais Magufuli akiwa na mbunge wa Bumbuli, January Makamba mwaka 2015 Januari Makamba ambaye ni mbunge wa CCM jimbo la Bumbuli na William Ngereja ambaye ni mbunge wa Sengerema kupitia chama hicho ni miongoni mwa viongozi ambao sauti zao zilisikika mitandaoni zikimzungumzia vibaya rais Magufuli. Rais Magufuli akimsikiliza Ngereja Hata hivyo Magufuli hajasema lolote kwa wengine ambao sauti zao zilidaiwa kusikika kama amewasamehe au bado. January Makamba, aliyehudumu katika nafasi ya Waziri wa Mazingira na Muungano nchini Tanzania toka kuingia madarakani kwa Rais John Pombe Magufuli ametimuliwa kazi mara baada ya sauti yake kuvuja mitandaoni ikisikika kumsema vibaya. Kupitia mtandao wa Twitter, Makamba ameandika: "Ni kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo." Huku akiambatanisha maneno hayo na picha yake na rais msaafu Ally Hassan Mwinyi wakiwa wanaangua kicheko. Rais Magufuli amesema amewasamehe wabunge January Makamba na William Ngeleja baada ya sauti zinazodaiwa zao kusambaa mitandani wakiwa wanamzungumzia vibaya rais. text: Kwa mujibu wa tafiti iliyochapishwa nchini Marekani, mwezi Aprili, mlo wa asubuhi unaweza pia ukaokoa maisha yako. Kutokupata kifungua kinywa kunahusishwa na hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa moyo na hatimaye kupelekea kifo. Matokeo ya utafiti huo ulisimamiwa na jopo la madaktari kutoka vyuo vikuu mbali mbali nchini Marekani. Walichakata matokeo kutoka kwa watu 6,550 kati ya umri wa miaka 45 na 70 ambao walifanyiwa utafiti kati ya mwaka 1988 na 1994. Watu hao walikuwa wakiripoti ni mara ngapi hawapati kifungua kinywa. Kwa jumla, 5% ya washiriki waliripoti kuwa hawali kabisa mlo wa asubuhi, 11% hula mara chache na 25% walisema hula bila kukosa. Watafiti baada ya hapo wakatathmini rekodi ya vifo vya washiriki mpaka mwaka 2011. Washirirki 2,318 walikuwa wameshafariki kufikia mwaka huo, na watafiti wakaangazia uhusiano baina ya vifo na kifungua kinywa. Baada ya kutoa sababu nyengine kama kuvuta sigara na unene, wataalamu wakabaini kuwa watu ambao walikuwa hawali mlo wa asubuhi walikuwa na hatari ya asilimia 19 kufa kwa magonjwa megine na asilimia 87 ya kufa kwa magonjwa ya moyo. Angalizo Tafiti za kitabibu tayari zimeshathibitisha kuwa kuacha kifungua kinywa kuna athari kwa afya, lakini wanasayansi bado wanaendelea kufanya tafiti kwenye eneo hilo. Mamlaka ya Afya Uingereza (NHS) imesema utafiti huo bado "hauwezi kuthibitisha kwa yakini kuwa kuacha mlo wa asubuhi kunapelekea kifo kutokana na ugonjwa wa moyo." "Watu ambao walikuwa hawapati kufungua kinywa (kwenye tafiti) inawezekana walikuwa wavuta sigara, walevi wa kiwango cha juu, wavivu, hawakuwa na lishe bora na ufinyu wa kipato kuliko wale ambao walikuwa wanapata kifungua kinywa," chapisho la NHS limeeleza. "Tafiti imeangalia kipengele cha kifungua kinywa kwa wakati mfupi, hali ambayo yawezekana si tabia ya mtu kwa wakati wote wa maisha yake. Pia haiwezi kutubainisha kifungua kinywa kina maana gani kwa watu tofauti." "Mfano, watu wengi hupata kifungua kinywa, lakini hutofautiana sana katika vile wanavyokula. Kuna ambao wanapata mlo kamili saa 2 asubuhi na wengine huonja tu kipande cha nyama au sharubati kwenye saa nne au tano asubuhi." Hata hivyo, Dkt. Wei Bao, ambaye ni profesa msaidizi katika chuo kikuu cha Iowa na mwandishi mkuu wa matokeo ya utafiti huo ametetea kazi yao. "Tafiti nyingi zimebainisha kuwa kuacha kupata kifungua kinywa kuna hatarisha kupata kisukari, shinikizo la damu na kolestro," Bao amesema. "Utafiti wetu mwishowe unashauri kuwa, kupata kifungua kinywa ni njia nyepesi ya kutatua matatizo ya ugonjwa wa moyo." Magonjwa ya moyo pamoja na kiharusi ni chanzo kikubwa cha vifo duniani. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) watu milioni 15.2 walipoteza maisha kutokana na matatizo hayo. Mlo wa asubuhi ama kifungua au kiamsha kinywa wataalamu huuita "mlo wa muhimu zaidi wa siku". text: Trump amesisitiza kwamba aliambiwa na Comey kwamba hachunguzwi na FBI Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Comey heri "atumai kwamba hakuna kanda zozote kuhusu mazungumzo yetu". Bw Comey, ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi kuhusu uwezekano wa ushirikiano kati ya maafisa wa kampeni wa Bw Trump na serikali ya Urusi alifutwa kazi Jumanne. Bw Trump baadaye alisema aliambiwa na Bw Comey kwamba yeye mwenyewe hakuwa anachunguzwa. Bw Trump amesema kwamba alikuwa amehakikishiwa mara mbili na Bw Comey, mara moja wakati wa dhifa ya jioni na mara ya pili kwa njia ya simu kwamba hakuwa anchunguzwa. Rais huyo amesema: "Nilisema: 'Ikiwezekana, unaweza kunifahamisha: je ninachunguzwa?' Alinijbu: 'Hauchunguzwi.'" Bw Trump alisema wiki hii kwamba alichukua hatua ya kumfuta Bw Comey mwenyewe. Wakati wa kumfuta, alimweleza kama mtu asiye wa kuaminika na mtu mwenye kujitakia sifa. Hilo lilionekana kwenda kinyume na tamko la maafisa wa uatawala wake kwamba Bw Comey alifutwa kutokana na mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu jeff Sessions na naibu wake Rod Rosenstein. Mstari wa kwanza wa barua ya Bw Trump ya kumfuta Bw Comey inarejea barua iliyoandikwa na Bw Rosenstein na inasema: "Nimekubali mapendekezo yao." Katika ujumbe mwingine kwenye Twitter Ijumaa, Bw Trump alizungumzia tofauti hizo, na kusema: "Mimi ni Rais mwenye shughuli nyingi na shughuli nyingi zinafanyika, haiwezekani kwa watu wangu kusimama jukwaani na kusema jambo kunihusu kwa ufasaha kabisa!" Aliongeza: "pengine, njia bora zaidi kwangu kufanya inaweza kuwa kwangu kufuta "vikao vya kuwapasha wanahabari" na badala yake niwe nikitoa ujumbe ulioandikwa kwa ajili ya kufanya mambo yote yawe sahihi???" Bw Trump alipuuzilia mbali uchunguzi unaofanywa na FBI na akasema wafuasi wa Democratic wanatumia "taarifa za uongo" kutuhumu maafisa wake wa kampeni kwamba walikuwa na uhusiano na maafisa wa Urusi. Aliandika katika ujumbe mwingine: "James Clapper mwenyewe (mkuu wa zamani wa Idara ya Taifa ya Ujasusi), na karibu kila mtu aliyekuwa na ufahamu kuhusu kisa hiki cha kuwinda maafisa wangu, aliposema hakukuwa na uhusiano wowote, ni lini haya yataisha?" Mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey Lakini mrithi wa Comey, kaimu mkuu wa FBI Andrew McCabe, alisema Alhamisi kwamba uchunguzi huo unasalia kuwa "uchunguzi muhimu". Akitoa ushahidi mbele ya kamati ya Seneti kuhusu ujasusi, aidha, alitilia shaka madai ya ikulu ya White House kwamba Bw Comey alikuwa amepoteza imani machoni pa wafanyakazi wake. "Ninaweza kuwaambia kwa imani kwamba wengi wa wafafanyakazi wana uhusiano wa ndani na uliokolea na Mkurugenzi Comey," Bw McCabe alisema. Rais wa Marekani Donald Trump amemtahadharisha mkuu wa shirika la uchunguzi wa jinai FBI aliyefutwa kazi James Comey dhidi ya kufichua habari kwa vyombo vya habari. text: Mji wa Raqqa umeharibiwa sana Wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF), wanaoungwa mkono na Marekani walitwaa udhibtii wa Raqqa wiki iliyopita. Kundi hilo hujumuisha wapiganaji wa Kikurdi na wa Kiarabu. Picha na video zinaonyesha mji wa Raqqa umebaki magofu, na Urusi imefananisha kuharibiwa kwa mji huo na kuharibiwa kwa mji wa Dresden, Ujerumani na majeshi ya nchi za Magharibi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Muungano huo unaoongozwa na Marekani umesema ulijaribu kabisa kupunguza maafa kwa raia. Urusi yenyewe imetuhumiwa kutekeleza makosa ya uhalifu wa kivita kwa kuangusha mabomu Aleppo mwaka jana. Wachunguzi wa makosa ya uhalifu wa kivita wa Umoja wa Mataifa mwezi Juni walisema "raia wengi walifariki" Raqqa. Wanaharakati watetezi wa haki Syria wanasema raia kati ya 1,130 na 1,873 waliuawa na kwamba wengi wa raia waliofariki ni kutokana na mashambulio ya mabomu ya kutoka angani yaliyokuwa yakiangushwa na Marekani kuwasaidia wapiganaji hao wa Kikurdi na Kiarabu kusonga vitani. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi amelinganisha uharibifu huo na uharibifu wa Dresden. "Raqqa imerithi hatima ya Dresden 1945, kufutwa kabisa kutoka kwa uso wa dunia kwa mabomu ya Wamarekani na Waingereza," Meja Jenerali Igor Konashenkov amesema. Amesema nchi za Magharibi sasa zinaonekana kuharakisha kutuma msaada wa kifedha Raqqa kama njia ya kuficha makosa yao ya kivita. Mabaki ya mji wa Dresden mwaka 1945 Muungano wa Marekani umesema ulifuata taratibu zote katika kuamua maeneo ya kushambulia na kwamba walijaribu kadiri ya uwezo wao kupunguza madhara kwa raia. SDF walitangaza kukomboa Raqqa wiki iliyopita baada ya vita vya miezi minne dhidi ya IS waliokuwa wameudhibiti kwa miaka mitatu. Wamesema pia kwamba wametwaa udhibiti wa kisima cha mafuta cha al-Omar, chanzo kikuu zaidi cha mapato kwa IS. Vita vya SDF dhidi ya IS sasa vinaandazia ngome yao ya mwisho Syria katika mkoa wa Deir al-Zour mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi la Syria, likisaidiwa na ndege za kivita za Urusi pamoja na wanamgambo wanaosaidiwa na Iran, limekuwa pia likishambulia IS. Urusi imedai majeshi ya muungano ulioongozwa na Marekani ni kama yaliufuta mji wa Raqqa nchini Syria kutoka kwenye uso wa dunia wakati wa vita dhidi ya kundi la Islamic State. text: Magoli kutoka kwa bernand Silva na leroy sane yaliipatia City ushindi wa 2-0 dhidi manchester United na kupanda juu ya Liverpool juu ya jedwali la ligi. City italihifadhi taji hilo iwapo watashinda mechi tatu zilizosalia. ''Bado hatujakuwa mabingwa huku ikiwa imesalia mechi tatu'', alisema Guardiola, ambaye amewataka wachezaji kuwa watulivu baada ya mechi hiyo ya debi iwapo wanataka kulihifadhi taji Pogba aorodheshwa katika kikosi bora cha mwaka Uingereza Wachezaji sita wa Manchester City ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Liverpool ambao wameorodheshwa katika kikosi bora cha mwaka cha ligi ya Uingereza -lakini ni kushirikishwa kwa wachezaji waliosalia ambako kumezua hisia. Licha ya msimu wenye matokeo mabaya kiungo wa kati wa timu ya Manchester United Paul Pogba amejipata katika kikosi hicho cha wachezaji 11 bora, akiwa ni mchezaji wa pekee ambaye hatoki katika klabu mbili za kwanza katika ligi hiyo ya EPL. Kikosi hicho kilipigiwa kura na achezaji wa ligi ya Uingereza. Lakini je, Paul Pogba alistahili kushirikishwa katika kikosi hicho? Na iwapo hapana ni nani aliyefaa kushirikishwa? Solskjaer awataka wachezaji wake kubadili mwenendo Wachezaji wa Manchester United wanafaa kubadili tabia zaidi ya kila mtu iwapo wanataka kupunguza pengo dhidi ya Manchester City, kulingana na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer. United, ambao walipoteza 2-0 dhidi ya City katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford siku ya Jumatano wako katika nafsi ya sita wakiwa pointi 25 nyuma ya viongozi hao wa ligi. Matokeo mabaya katika mechi ya debi ni yao ya saba katika mechi tisa katika mashindano yote. ''Kipindi cha kwanza tulicheza mchezo wa kuridhisha'', alisema Solskjaer. Hatahivyo tulifungwa magoli rahisi ambayo tungeyazuia. Unai Emery: Arsenal itatinga nne bora Arsenal iliopo katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi ya Uingereza inaweza kujikwamua na kupanda hadi nafasi nne bora licha ya kupoteza mechi mbili mfululizo, kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Unai Emery. Magoli kutoka Ruben Neves , Matt Doherty na Diogo Jota aliisaidia Wolves kushinda 3-1 dhidi ya Arsenal, ambayo ilifunga bao la kufutia machozi kupitia kichwa cha Sokratis. Ilikuwa ni mechi ya pili kupoteza katika kipindi cha siku nne baada ya kupoteza 3-2 dhidi ya Crystal palace nyumbani. Huku ikiwa imesalia mechi tatu Arsenal iko alama nne nyuma ya majirani zao Tottenham waliopo katka nafasi ya tatu na wana pointi moja chini ya Chelsea walio katika nafasi ya nne. Wachezaji wa Manchester City watalazimika kuwa watulivu baada ya mechi yao ya debi iwapo wanataka kulihifadhi taji la ligi ya Uingereza. text: Mtambo wa Marekani wa kuangamiza makombora unaolindwa na kikosi cha majini USS Donald Cook, uko kwenye bahari ya Mediterranian Msemaji wa Ikulu ya White House Sarah Sanders amewaambia wandishi wa habari kuwa hakuna ushahidi wa mwisho uliokwisha chukuliwa juu ya mashambulio ya kijeshi. Lakini amesema Marekani inaziwajibisha Urusi na Syria kwa tukio hilo. Tayari rais Donald Trump ameionya Urusi "kuwa tayari" kwa mashambulio ya makombora nchini Syria Baraza la Kitaifa la Usalama la Marekani litakutana Alhamisi, huku waziri mkuu wa Uingereza PM Theresa May akiitisha mkutano wa baraza la mawaziri kujadili tukio hilo la Syria. Wanaharakati, wahudumu wa uokozi na madaktari wanasema makumi ya watu walikufa katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Douma Jumamosi. Lakini serikali ya Bashar al-Assad -ambayo inapata uungwaji mkono wa kijeshi kutoka Urusi- imekanusha kutekeleza shambulio hilo. "Rais ana maamuzi mengi ya kujibu shambulio na mengine yanajadiliwa ," Alisema Bi Sanders wakati wa kikao na waandishi wa habari Jumatano . "Bado hatujaainisha ni hatua gani hasa tunapanga kuchukua ,"aliongeza Bi Sanders. Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May(kushoto) na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwapamoja wameahidi kushirikiana na Marekani kujibu shambulio la'' kemikali'' la Syria Kauli hizo zinaonekana kama kusisitizia onyo la awali lililotolewa na rais Donald Trump awali aliposema kuwa Urusi hainabudi "kuwa tayari" kwa mashambulio ya makombora nchini Syria. " Jitayarishe Urusi, kwasababu watakuja, wazuri na wapya 'watanashati!'" Bwana Trump alisema katika ujumbe wake wa mapema asubuhi kwneye ukurasa wake wa Twitter jana Jumatano. Pia alimuita kiongozi wa Syria "mnyama anayeua kwa gasi". Marekani, Uingereza na Ufaransa wamekubaliana kushirikiana na wanaaminiwa kujiandaa kwa mashambulio ya kijeshi ili kujibu shambulio hilo linalodaiwa kuwa la kikemikali la mwishoni mwa juma. Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis anasema Marekani bado inatathmini shambulio la kemikali, lakini akaongeza kuwa jeshi liko tayari "kuchukua hatua za kijeshi ikiwa zitafaa kama rais alivyobainisha.'' Ikulu ya White House imesema kuwa rais hajaainisha ratiba ya hatua maalum zitakazochukuliwa. Mtambo wa kuangamiza makombora unaolindwa na kikosi cha majini cha Marekani , USS Donald Cook, yuko katika bahari ya Mediterranean. Picha ya video ambayo haijulikani ilichukuliwa na nani inaonyesha watoto walioshambuliwa wakipata matibabu Ni kipi kilichotokea Jumamosi? Muwakilishi wa Ufaransa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alisema gesi ya sumu ilitumiwa kwa makusudi kwasababu inaweza kusambaa hadi sehemu za chini za majengo hadi. Marekani ,ufaransa na Uingereza wameongoza kampeni ya kimataifa ya kulaani shambulio hilo linalodaiwa kuwa la kemikali, huku serikali ya Syria na waungaji mkono wao Urusi wakikana kuwajibika kwao kokote na tukio hilo. Marekani inasema kuwa "tayari ana maamuzi mengi'' za kujibu shambulio linaloshukiwa kuwa la kikemikali nchini Syria, huku viongozi wa magharibi wakiendelea kupima hatua za kijeshi. text: Meli hii ya The Lighthouse Winmore ilidaiwa kubeba mafuta kupeleka Taiwan lakini safari yake hakuishi eneo hilo, imedaiwa Katika Ujumbe wa twitter, bwana Trump alisema kuwa China ilionekana ''hadharani'' ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini. Amesema hakuwezi kuwa na suluhu ya kirafiki katika mgogoro wa Korea Kaskazini iwapo mafuta yataruhusiwa kusafirishwa hadi Pyongyang. China mapema ilikana kwamba kumekuwa na ukiukaji wowote wa azimio la Umoja wa mataifa la mafuta kati ya China na Korea Kaskazini. Wiki iliopita , Beijing iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90. Ujumbe wa twitter uliochapishwa na rais Donald Trump Vikwazo hivyo vikali ni jaribio jipya kuzuia majaribio ya silaha yanyotekelezwa na Pyongyang. Matamshi hayo ya rais Trump dhidi ya China yanajiri baada ya gazeti moja la Korea Kusini Chosun IIbo kuripoti kwamba meli za China zimekuwa zikisafirisha mafuta kwa siri kupitia baharini kuelekea Korea Kaskazini. Likiwanukuu maafisa wa serikali ya Korea Kusini, limesema kuwa usafirishaji huo unaenda kinyume na sheria kutoka meli moja hadi nyingine ulipigwa picha na Satellite za Marekani za ujasusi takriban mara 30 tangu mwezi Oktoba. Maafisa wa Marekani hawakuthibitisha ripoti hiyo lakini afisa ya idara moja ya serikali aliyenukuliwa na reuters alisema kuwa usafirishaji huo huenda unaendelea. Usafrishaji wa mafuta kutoka meli moja hadi nyingine unaendelea kuleta wasiwasi ikiwa miongoni mwa njia za Korea Kaskazini kukwepa vikwazo hivyo. China ambayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa taifa la Korea Kaskazini , imesema kuwa inatekeleza vikwazo vyote vilivyowekwa na UN dhidi ya Korea Kaskazini. Kiongozi wa korea Kaskazini Kim Jong un amepuuzilia mbali shinikizo za kimataifa Alipoulizwa maswali kuhusu ripoti za usafirishaji wa mafuta kutoka meli moja hadi nyingine, msemaji wa wizara ya ulinzi nchini China Ren Guoqiang aliambia maripota kwamba: hali ulioitaja haipo. Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani Michael Cavey alisisitiza kuhusu wito wa mataifa yote kusitisha uhusiano wa kiuchumi na Korea Kaskazini. ''Tunatoa wito kwa China kusitisha uhusiano wowote wa kiuchumi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Korea Kaskazini ikiwemo utalii pamoja na uuzaji wa mafuta ama bidhaa za mafuta'', alisema. Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amevunjwa moyo na China kufuatia ripoti kwamba iliruhusu mafuta kusafirishwa hadi nchini Korea Kaskazini. text: Kombora kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea Inategemea ni upande upi wa mzozo huo mataifa yanaunga mkono. Mataifa yanayo unga waasi wanaopambana na utawala wa rais wa Syria Bashar al Assad, yameunga mkono shambulio hilo. Baadhi ya watoto walioathirika na kemikali,Syria Uturuki imepokea vizuri ufyetuaji makombora hayo, wakati afisa wa wizara ya mambo ya nje wa Saudia amemsifu rais Trump kwa ukakamavu wake na Uingereza imejitolea usaidizi kikamilifu. Waziri mkuu wa Israel amesema ujumbe wa wazi umetumwa unaopaswa kusikika sio tu Damascus lakini pia Iran na Korea kaskazini. Kwa upande wake Iran ambayo kama Urusi inaunga mkono serikali ya Syria imeshutumu shambulio hilo. Serikali ya Putin anasema kiongozi huyo amepokea kwa utulivu taarifa hiyo Moscow imetaja mashambulio hayo kama uchukozi mkali dhidi ya taifa huru. Msemaji wa rais Putin (Dmitry Peskov) amesema kwamba kando na kukiuka sheria za kimataifa , Washington imesababisha uharibifu mkubwa katika uhusiano na Moscow. Wizara ya mambo ya nje imetangaza kusitishwa kwa makubaliano na jeshi la Marekani yalioundwa kuzuia mashambulio ya angani anga ya Syria. Katika taarifa kwenye televisheni Jeshi la Syria limesema watu 6 wameuawa na mali kadhaa kuharibiwa kutokanana shambulio hilo la makombora. Kumekuwa na shutuma na uungwaji mkono wa makombora iliyofyetuwa Marekani dhidi ya Syria. text: Paul Pogba hana raha Old Trafford kulingana na kocha wa Ufaransa Didier Deschamps Mshambuliaji huyo amekuwa si mtu mwenye furaha na kuonekana hapendwi katika uwanja wao wa Old Trafford. Pogba yupo katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Colombia na Urusi alionekana kutopendezwa kwa kufanyiwa madadiliko na timu yake ya Manchester United katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Brighton . Didier amesema mengi atayasikia kuhusu hilo kwa Pogba ni hali ambayo haifai, United watakuwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Swansea tarehe 31 Machi. United itarudi katika mechi za ligi ya Uingreza dhidi ya Swansea mnamo tarehe 31 Machi. Pogba alianzishwa katika kikosi cha United dhidi ya sevilla katika mechi ya vilabu bingwa Jumanne iliopita baada ya kukosa kushirikishwa katika mechi ya ushindi dhidi ya Liverpool kutokana na tatizo la jeraha. Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps ''Sijui kwa nini iwe hivyo, aliongezea Deschamps. Ni kwa nini mambo yalifikia kiwango hicho, lazima kuna sababu''. ''Mimi huzungumza sana na wachezaji katika kambi ya mazoezi ili kujua hisia zao . Sio Pogba pekee''. Pogba alijiunga na United mwaka 2016 kwa ada ya pauni milioni 89 na mpaka sasa ameisaidia United kushinda Kombe la ligi na Europa League msimu uliopita. Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema kwa sasa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Paul Pogba hana furaha text: Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wamekuwa wakijibizana vikali kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kuendelea kustawisha silaha za nyuklia na pia kufanyia majaribio makombora, jambo ambalo taifa hilo haliruhusiwi na Umoja wa Mataifa. Marekani ilituma kundi la meli zake za kivita karibu na Korea Kaskazini, jambo ambalo liliikera Korea Kaskazini. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili haujakuwa mzuri tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Hata hivyo wiki iliyopita uhasama ulizidi na kufikia kiwango cha juu kuliko awali. Jumatatu - Meli za kivita za Marekani Rais Trump aliagiza kundi la meli za kivita za Marekani pamoja na meli moja yenye uwezo wa kubeba ndege na pia kutumiwa na ndege hizo kupaa na kutua, zielekee upande wa Korea Kaskazini. Taifa hilo limetekeleza majaribio kadha ya silaha za nyuklia na hilo halijaifurahisha Marekani. Rais Trump alisema Marekani imejiandaa kuchukua hatua kivyake, bila usaidizi wa China, kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini. Jumanne - Kim amjibu Trump Kim Jong-Un hakufurahishwa na hayo na alimjibu vikali Bw Trump. Wizara yake ya mambo ya nje ilinukuliwa ikisema hatua hiyo ya Marekani ni ya "kipumbavu" na ikaahidi kujilinda "kwa nguvu zote za kivita." China, ambao ni mshirika wa karibu zaidi wa Korea Kaskazini, walionya kwamba wataingilia kati na kutoa adhabu kali zaidi za kifedha kwa Korea Kaskazini iwapo taifa hilo lingefanya majaribio zaidi ya makombora. Jumatano - China yazungumza Vyombo vya habari vya China vilisema rais wa taifa hilo alimpigia Rais Trump kutuliza hali. Rais Trump mwenyewe aliandika kwenye Twitter kwamba alikuwa amewasiliana na Rais Xi Jinping. Bw Xi alidaiwa kumwambia Trump kwamba anataka amani na utahibiti eneo hilo na kwamba anaunga mkono pia juhudi za kumaliza silaha za nyuklia katika rasi ya Korea. Alhamisi- Gwaride la wanajeshi Korea Kaskazini ilizindua mpango wake mpya wa ujenzi wa nyumba za makazi na biashara mjini Pyongyang. Ulionekana kuwa mpango wa kawaida tu, lakini ilikuwa pia fursa ya taifa hilo kuonyesha nguvu zake. Waandishi wa habari wa mashirika ya kigeni walialikwa kushuhudia wanajeshi wakifanya gwaride na kutembea kwenye barabara za mji huo. Donald Trump hakufurahishwa na hilo. Aliandika tena kwente Twitter kwamba Marekani iko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini. Ijumaa- Onyo la China China ilitahadharisha kwamba mzozo mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini "unaweza kutokea wakati wowote". Ilizionya nchi zote mbili kukoma kurushiana vitisho, na kusema hakuwezi kuwa na mshindi katika vita. Hayo yakijiri, Korea Kaskazini ilikuwa inakamilisha maandalizi ya gwaride kubwa na maonyesho ya kijeshi Jumamosi. Jumamosi - Vifaru barabarani Korea Kaskazini iliadhimisha miaka 105 tangu kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung. Vifaru zilitolewa barabara za Pyongyang. Serikali ya Korea Kaskazini pia ilionyesha hadharani kwa mara ya kwanza makombora yanayoweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine, na pia makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka kwenye nyambizi. Maafisa wa serikali ya Korea Kaskazini waliionya Marekani dhidi ya kuchukua hatua zozote, wakisema nchi hiyo iko tayari kwa vita. Walisema watajibu kwa "mashambulio ya nyuklia". Hayo yakijiri, Makamu wa Rais Mike Pence alielekea Korea Kusini kujadiliana na washirika wa Marekani kuhusu njia bora zaidi za kukabiliana na Korea Kaskazini. Jumapili - Jaribio la makombora Marekani ilidai kwamba Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora, lakini likalipuka sekunde chache baada ya kupaa angani. Inasadikika kwamba lilikuwa kombora la masafa marefu, ambalo hupaa juu anagani kwanza na ambalo huelekezwa, lakini baadaye huanguka hadi pahali ambapo panalengwa kutokana na mvuto wa dunia. Umoja wa Mataifa umeipiga marufuku Korea Kaskazini kufanya majaribio kama hayo. Rais Trump atachukua hatua gani? Ni yeye mwenyewe pekee ajuaye jibu - au labda mwenyewe binafsi amekanganyikiwa! Ukafuatilia matukio, mijadala na ujumbe katika mitandao ya kijamii, unaweza kudhani Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia vinakaribia. text: Wyclef Jean ashukiwa kimakosa kuwa mwizi Los Angeles Mwanamuziki huyo raia wa Haiti, alichapisha video yake kwenye mtandao wa twitter akisimama karibu la gari la polisi baada ya kufungwa pingu. Alidai kuwa polisi wa Los Angeles walimfunga pingu bila ya sababu yoyote lakini idara hiyo ya polisi ilikana kufanya hivyo. Wyclef Jean anafahamika vyema kuwa moja wa waanzilishi wa kundi la rap la Fugees na ameshirikiana na wanamuzi kama Shakira, Timbaland na Lil' Kim. Anasema alikuwa kwenye sudio na mwanamuziki T-Baby wakati kituo cha mafuta kilipopowa, na kudai kuwa alisimamishwa na polisi baadaye kwa sababu alikuwa mtu mweusi ambaye alikuwa amefunga bandana iliyokuwa ikifanana na mtu aliyepora kituoa cha mafuta. Akiongea na BBC msemaji wa idara ya polisi wa Los Angeles alisema kuwa Wyclef Jean, alikuwa kwenye kiti cha abiria kwenye gari lililokuwa likifanana na lile lilotumika kwenye wizi. Polisi walisema kuwa walimwachilia bila ya kumfungulia mashtaka. Mwanamuziki Wyclef Jean amewalaumu polisi huko Los Angeles, Marekani, kwa kumshuku kuwa mwanamume ambaye aliiba kutoka kituoa cha mafuta kilichokuwa karibu. text: Wawili hao wamekuwa kizuizini toka mwezi uliopita kupisha polisi kufanya uchunguzi wa kifo cha mfanyabiashara Monica Kimani, aliyeuawa kwa kukatwa shingo Septemba 19 katika nyumba yake jijini Nairobi. Baada ya uchunguzi wa wiki tatu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya Noordin Haji ameagiza wawili hao kufikisha Mahakama Kuu mara moja na kufunguliwa mashtaka ya mauaji. "Baada ya kupitia kupitia ushahidi uliokuwepo kwa kina nimejiridhisha kuwa unajitosheleza kuendesha mashtaka ya jinai kwa kosa la mauaji kinyume cha kifungu cha 203 na 204 cha Kanuni ya Adhabu," ameeleza haji katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Irungu maarufu kama Jowie inasemekana alikuwa na mahusiano na Bi Kimani na yadaiwa kuwa walikutana kabla ya tukio hilo la mauaji. Mwili wa marehemu ulibainiwa na kaka yake George bafuni huku ukiwa mikono imefungwa na kamba na shingo ikiwa imekatwa na na kitu chenye ncha kali. Bi Kimani alizikwa Septemba 29 huku familia yake ikiomba haki itendeke na wahusika wachukuliwe hatua. Je wazazi hukwamisha vipaji vya watoto? Polisi wamehoji watu 15 wakiwemo washukiwa hao wawili juu ya mkasa huo wa mauaji. Jowie awali alidai kuwa alipigwa risasi saa chache baada ya mauaji ya Kimani. Hatahivyo, wapelelezi wamebaini kuwa Jowie alijipiga risasi chumbani kwa Maribe. Haijafahamika bado iwapo Jowie alitaka kujitoa uhai ama alitaka kupoteza ushahidi katika mkasa uliomfika bi Kimani. Awali ilidhaniwa kuwa Jowie ndiye angekumbana na shtaka kuu la mauji na Maribe angeshtakiwa kwa kutoa usaidizi, lakini yaonekana waendesha mashtaka wanataka kuichia mahakama mamlaka ya kuamua ni kwa kiwango gani wawili hao walishiriki ama hawakushiriki katika tuhuma hizo zinazowakabili. Trump amwomba radhi Jaji Kavanaugh Polisi wanashuku kuwa mauji hayo yamechochewa na masuala ya fedha. Wapelelezi walibaini kuwa Jowie alitumia silaha ya Brian Kassaine kujidhuru. Kissaine ni rafiki na jirani wa Maribe na Jowie, awali nae aliwekwa kizuizini lakini inaarifiwa kuwa atapanda kizimbani akiwa kama shahidi wa upande wa mashtaka. Maribe alikamatwa na kuwekwa kizuizini Septemba 30 huku Jowie akishikiliwa siku tano kabla yake. Jowie ni mlinzi kwenye kampuni binafsi katika nchi ya Falme za Kiarabu. Mwandishi wa habari wa runinga ya Citizen ya Kenya Jackie Maribe na mchumba wake Joseph Irungu sasa watapandishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji. text: Tom Makui, maarufu kama Junior, 27, alifanya sherehe hiyo ya harusi Jumanne wiki hii. Ameambia Mwandishi wa BBC Anne Ngugi kwamba sasa watu wameanza kumbandika majina ya ajabu. "Nimeitwa Simba na hata Dume," amesema. Makui anatokea kwenye familia ambayo ndoa za wake wengi ama mitala ni jambo la kawaida. Hata hivyo kuoa wake wawili kwa mpigo ni jambo ambalo halikuwahi kusikika katika jamii ya Kimaasai ambayo wanandoa hao wametokea. Wapo wanaume wanaowaoa wake wengi lakini si kwa wakati mmoja. Katika harusi hiyo ambayo ilipambwa vilivyo katika kitongoji cha Kisaju, Mako aliwaoa Elizabeth Silamoi, 25, na Joyce Tikoyo, 23. Wote wawili ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenya Assemblies of God mjini Kitengela, si mbali sana na eneo Kisaju anakoishi Tom. Huhudhuria masomo na kurejea nyumbani jioni. Wamekuwa pamoja kwa mwaka mmoja, na sherehe ya Jumanne ilikuwa ya kurasmisha ndoa kati ya kitamaduni. Ana wasiwasi kuhusu kutosheleza mahitaji ya wawili hao? "Nina uhakika kuwa nitaweza kuwatosheleza wake wangu wawili, najua wana umri ambao kila mwanamke anahitaji mume wake, lakini mimi sijichanganyishi na vileo wala sigara au madawa ya kulevya kwa hivyo nitaweza kazi zote kuwaridhisha wake wangu," anasema Makui. "Mambo ya kule ninakoishi sana sana mimi ninaamua jioni nitakapolala, hakuna siku nimegawanya wala nini, mimi hupiga simu na kumueleza mke mmoja kuwa siji kwake na ninakwenda kwa mwenzake wako majirani ndani ya boma langu." Mako alikutana na Bi Silamoi miaka miwili iliyopita wakati akichunga ng'ombe wake karibu na nyumabni kwa mwanamke huyo. Mwaka jana akakutana na Bi Tikoyo pia akiwa anachunga ng'ombe karibu na kwao. Katika mila za Kimasai, mahari ya ng'ombe hutolewa kabla ya kufungwa kwa ndoa, na bwana harusi Makui alikamilisha hilo ipasavyo. Mako aliwaoa wakeze kimila japo wote walivalia mavazi ya kimagharibi. Makui alivalia suti ya rangi ya samawati na wakeze wakivaa mashela meupe. Wote pia walivalia urembo wa Kimaasai. "Nataka kuliweka sawa hili, harusi yangu ilikuwa ya kimila na haikuwa na mahusiano yoyote na kanisa. Kuna watu wanatuma habari za kupotosha mitandaoni kuwa ndoa yangu ilisimamiwa na wachungaji," Makui, ambaye ni mfanyabiashara, awali aliambia gazeti la kibinafsi la Star la nchini Kenya. Amesema amewaoa wanawake hao kwa sababu wote wanampenda na hakutaka kumsononesha yeyote kati yao. "Huu ni ujumbe ninaoutuma kwa waume wa kisasa wanaojifanya kuwa wanampenda mwanamke mmoja na huku wakiwalaghai kwa kuingia kwenye mahusiano na wengine pembeni," amesema. "Nimekuwa muaminifu kwa wake zangu kwa sababu sitakuwa na sababu ya kuongeza mke mwengine. Ninaamini wawili watanitosheleza." Wake hao wawili wanapendana? Bi Silamoi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye penzi na Makui, na kusema kabla ya kuja kwa mwenzake wawili hao walijadiliana kwa kina na kukubaliana. "Ninampenda. Nilimpa Baraka zangu kuongeza mpenzi. Nampenda (mke mwenzake) pia." Mke wa pili Bi Tikoyo alipoulizwa na BBC kuhusu kuingia kwake kwenye uhusiano huo, alisema: "Hapa mimi sijakuja kuharibu ndoa , tulisikilizana wote na mke mwenza hakuwa na matatizo yeyote na mimi, mimi nilipenda mumewe wangu tu nilipomuona na sina wasiwasi wakuwa tuko wawili " Naye Mke wa Kwanza alipoulizwa ikiwa hana wivu kuwa ana mwenza, alisema: "Ndio wivu lazima uwepo kwa kuwa sisi ni binadamu lakini kwa kuwa ninampenda mume wangu nimekubali tu, ndio ndoa ina changamoto nyingi lakini kwa yote ninamtumainia Mungu." Bi Tikoyo, amesama wote wamekubaliana kuwa katika mahusiano ya aina hiyo na wazazi wake walikubali hilo kwa sababu wanamuamini Makui. Wazazi wa bwana harusi, Bw Makui Busabus na Bi Sintiyio, wamesema hawakuamini mwanzoni mtoto wao alipowaambia anataka kuoa wake wawili kwa siku moja, na sherehe moja. Lakini hilo limepita. "Kwa umri wangu wa miaka 90 sijawahi kuona kitu kama hiki huku umasaini. Kwa kawaida, mtu anayetaka kuongeza mke husubiri kwanza walau baada ya mwaka au miaka miwili toka alipofunga ndoa ya kwanza," amesema Busabus. Mamorani wengine pamoja na wageni waliohudhuria harusi hiyo wanamchukulia Makui kama shujaa kwa kufanya jambo ambalo halikuwahi kufanyika kabla Umasaini. Baadhi wanasema ameonyesha ukomavu, na hata anafaa kugombea wadhifa wa diwani na baadaye hata awe gavana wa jimbo. Baada ya harusi, watatu hao wamekuwa wakiendelea na maisha yao. Hapa wanaonekana wakiwa myumbani kwao Alhamisi Wakiwa nyumbani kwao Alhamisi Ingawa Bi Silamoi na Bi Tikoyo wanatokea ukoo mmoja, hawajatokea familia moja. Bi Silamoi (kushoto) na mke mwenza wake Bi Tikoyo Unaweza kusoma pia: Picha zote zina hakimiliki Morani mmoja katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya ameacha watu midomo wazi baada ya kufunga ndoa na wanawake wawili kwa mpigo. text: Hapa ni katika ufukwe wa Nungwi visiwani Zanzibar, Tanzania. Watu hawa wanaonekana kuwa tayari sana kuukaribisha mwaka mpya wa 2018. Yogyakarta, Indonesia, fataki zilitanda angani mshale wa saa ulipogonga saa tisa usiku Hapa ni katika Bandari ya Victoria nchini Hong Kong Jumba refu sana la Petronas Towers nalo liliangazwa kwa fataki Kuala Lumpur, Malaysia Tukirudi Indonesia tena, taa zenye puto ziliwashwa na kupeperushwa angani katika hekalu la Borobudur Na katika jumba la ghorofa la 123 la Lotte World Tower, Seoul, Korea Kusini, hali haikuwa tofauti sana Cairo nchini Misri, Santa Claus alipiga kengele sokoni kutangaza kufika kwa mwaka mpya Mjini Jakarta, eneo la katikati mwa jiji fataki zilirushwa kila pahali Nchini Singapore, Marina Bay ndicho kilichokuwa kitovu cha sherehe Marekani wakazi walikuwa miongoni mwa watu wa mwisho kuukaribisha Mwaka Mpya. Katika Times Square, New York, wawili hawa walivumilia baridi kali kuusubiri Mwaka Mpya Sydney Harbour, maonesho haya ya fataki maarufu sana yalikuwa miongoni mwa matukio ya kuukaribisha mwaka ambayo yalioneshwa kwenye runinga pande mbalimbali duniani Na mbali kidogo kusini mashariki Melbourne pia walisherehekea Mabuddha katika hekalu la Kelaniya nchini Sri Lanka waliomba kuukaribisha Mwaka Mpya Mjini Istanbul nchini Uturuki wakazi walijitokeza barabarani kusherehekea wakisubiri kuvuka mwaka Champs-Élysées mjini Paris watu walifurika kama siafu Jijini London saa ya Big Ben ililia mshale wake wa saa ulipogonga saa sita usiku, licha ya kwamba bado inafanyiwa ukarabati mkubwa Na katika ufukwe maarufu wa Copacabana, Rio de Janeiro, wengi walikusanyika kuburudika na kuukaribisha mwaka mpya kwa shangwe . Ulimwengu unapoendelea kusherehekea kufika kwa mwaka mpya wa 2018, sherehe za aina yake zimekuwa zikifanyika miji mbalimbali mashariki hadi magharibi. Picha hizi ni za jinsi hali ilivyokuwa miji mbalimbali. text: Rais Robert Mugabe be amekuwa mamlakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400- walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa "inayofaa" kufanya hivyo. Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake. Malumbano ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana kuendelea kudhoofika zaidi. Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka. Mwaka 2006 alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008. Licha ya hayo aligombea na kushinda katika uchaguzi uliokuwa na ghasia ambao matokeo yake yalibishaniwa. Kwa hivyo haijawa wazi ni lini , kama kweli Rais Mugabe ataondoka madarakani. Mnamo mwishoni mwa juma kamati za kikanda za chama tawala cha, Zanu-PF zilimuidhinisha kama mgombea wake katika uchaguzi wa 2018, ambapo atakuwa na umri wa miaka 94. Chama hicho kitaidhinisha uamuzi huo katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi ujao. Kwa hiyo kwa sasa haionekani kama kweli anaangalia uwezekano wa kustaafu. Utawala wa Mugabe umekuwa ukikumbwa na maandamano huku wanaharakati na raia kwa ujumla wakimtaka rais Mugabe aachie mamlaka. Maandamano ya kulalamikia hali mbaya ya uchumi Zimbabwe Utawala wa rais Mugabe umekuwa ukikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa sarafu ya nchi hiyo. Hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira vilisababisha maandamano makubwa kote nchini humo, wanaharakati na raia kwa ujumla wakimtaka rais Mugabe aachie mamlaka. Hata hivyo Mugabe amekuwa akiyazima maandamano hayo na kuwatia nguvuni wapinzani wake anaosema kuwa wanachochewa na mataifa ya kigeni. kutokana na vikwazo kutoka mataifa ya magharibi. Mugabe amekuwa akikosolewa kwa kukandamiza upinzani. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo. text: Hata kama hujawahi kusikia kuhusu illuminati , kuna uwezekano kwamba umeshawahi kuona ishara zinazohusishwa nazo. Mbuzi, jicho linaloona kila kitu - 'the all seeing eye' linaloonekana kwenye noti za Marekani. Katika kanda za video za muziki, baadhi ya mistari iliyokatwa pia huhusishwa na hilo kama kibao cha Rihana S&M kilichoonyesha kichwa bandia cha habari kinachomtaja yeye kuwa mwanamfalme wa illuminati. Basi kwanini wanamuziki na wasanii wanapenda kufanya mzaha kuhusisha illuminati? Mwandishi habari na muandishi vitabu, David Bramwell anasema kwa ufupi ni kujifurahisha. Jay-Z ni mmoja wa wasanii mashuhuri duniani ambao wamedaiwa kuonyesha ishara ya Illuminati Wengi wanavutiwa na hadithi hizo kama baadhi yetu tunavyovutiwa. 'Nakumbuka uvumi uliosambazwa mnamo 1966 kwamba Paul McCartney wa kundi la the Beatles alifariki katika ajali ya gari alipokuwa akielekea nyumbani baada ya kurekodi muziki. Na kwamba alibadilishwa na DJ mmoja wa Canada ambaye alifanana mno na yeye ambaye alijifunza kwa haraka, kuimba na kupiga gita kama yeye'. Bramwell anaeleza kwamba McCartney mwenyewe hajawahi kukana fikra hiyo. Na kama ilivyo kwa Mccartney na Jay Z na Rihanna, wengineo pia wanafurahishwa na taarifa hiyo. Ishara inayohusishwa na illuminati Iluminati ni nani? Ni kweli kwamba Illuminati ni vivuli vya watu wanaoidhibiti dunia? Illuminati kwa ufahamu uliopo, walikuwa ni jamii yenye usiri kutoka Bavaria iliyoundwa katika karne ya 18. Jamii hiyo ilipinga mazingaombwe, ushawishi wa kidini na uongozi wa taifa. Waliunda kitabu cha sheria kilichosema kuwa lengo kuu ni kusitisha matumizi ya mashine ya wanaodhulumu watu, na kuwadhibiti bila ya kuwatawala. Punde si punde jamii hiyo ya Bavaria ikaishia kutokuwa na maana. Na halihusiki kwa namna yoyote na fikra zilizopo leo kuhusu Illuminati. Fikra inayofahamika leo inatokana na vuguvugu la Discordian - wanaomini kwamba vurugu ni muhimu kama utulivu. Inaelezwa kwamba vuguvugu hilo lilianzishwa mnamo 1965 katika ofisi ya wakili mmoja jimboni texas Marekani. Wanafunzi wawili waliosoma shule moja, Greg Hill na Kerry Thornley walitumia mashine ya kutoa kopi kuchapisha nakala za waraka ulioidhinisha vuguvugu hilo. Waraka huo uliendekeza fikra kwamba 'vurugu au ghasia ni muhimu kama ilivyo kwa utulivu'. Na vuguvugu hilo lilishika kasi katika miaka ya 60 na 70 huku wanafunzi hao wawili wakizidi kusambaza utundu na taarifa za uongo. Mwanafalsafa Ujerumani Johann Adam Weishaupt muasisi wa jamii ya siri ya Illuminati Lengo lao lilisambazwa zaidi na raia wawili wengine wa Marekani. Mwandishi Robert Anton Wilson aliyeliandikia jarida la PlayBoy na rafiki yake Robert Shea. Wawili hao Bramwell anaeleza waliamua kuandika riwaya inayojumuisha fikra zote hizo na kukiita kitabu Illuminatis. Walihisi kwamba itakuwa ni jambo la kufurahisha kujaribu kusambaza vurugu na taarifa za uongo kwa makusudi kuhusu illuminati na walifanikiwa kwa kuandika barua kwa vyombo vya habari, lakini pia kupitia sehemu ya barua ndani ya jarida hilo la Playboy. Waliandika barua za urongo kutoka kwa wasomaji wasiokuwepo, waliosema kwamba illuminati sio wa kweli au wengine walioonekana kutokuwa na msimamo kamili kuhusu suala hilo. Kilichokuwa na uzito ni kwamba watu wote hao waliokuwa wamezusha gumzo kuhusu illuminati na fikra ilikuwa ni kwa lengo kwamba msomaji atauliza maswali, kulihoji suala hilo na kuuliza iwapo 'ni kweli kuna illuminati?' Dhana hiyo ilisambaa pakubwa, na kitabu hicho kilizusha maswali kama kwa mfano 'ni nani aliyempiga risasi John F. Kennedy?' Licha ya kwamba ukubwa wa fikra hizo zinazojitokeza katika kitabu hicho ni za uongo, zimechanganyika na ukweli wa kiasi fulani kuzifanya kukubalika. Kitabu hicho kilipata umaarufu kiasi cha kugeuzwa mchezo wa kuigiza wa muda wa saa nane ulioigizwa katika jukwaa Liverpool. Jarida hilo la miaka ya 70 la utamaduni kwa sasa halipatikani katika kizazi cha intaneti, lakini uvumi kuhusu illuminati bado unaendelea katika mitandao kadhaa ambapo watu wanaomaini hubadilishana mawazo, fikra na ushahidi wa uwepo wa illuminati. Mwisho wa siku uamuzi ni wako wewe kuamini iwapo kuna illuminati au la. Je Jay Z ni mfuasi wa Ilimunati? Donald Tump, Katty Perry na hata Beyonce wameshutumiwa kuwa wafuasi wa Illumanti. Kundi la siri linalo arifiwa kuwajumuisha watu wenye nguvu na udhibiti duniani. text: Juventus wana matumaini kuwa Manchester United watamruhusu kiungo wa kati Paul Pogba, kurejea Turin kwa mkopo mwezi ujao. (Sunday Mirror) United tayari wamekataa mpango wa kubadilishana na Juve wakiwahusisha winga Douglas Costa, 30, na kiungo wa kati wa Barcelona Miralem Pjanic,30, ili kumnasa Pogba. (Calciomercato) Baba wa Erling Braut Haaland- mchezaji wa zamani wa Leeds Alf-Inge- amesema kuwa mshambuliaji wa Norway ana furaha sana akiwa Borussia Dortmund hivi sasa, lakini anaweza kuendelea mbele siku za usoni. (Tuttosport - in Italian) Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hajamkataa mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil anayechezea kikosi cha washika bunduki kabla ya mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 32 kumalizika msimu huu. (Star on Sunday) Wolverhampton Wanderers walishindwa uhamisho wa pauni milioni 19 kwa beki wa kushoto wa Manchester City Oleksandr Zinchenko msimu huu, lakini wako tayari kutoa zabuni nyingine kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine katika dirisha la uhamisho la Januari. (Star on Sunday) Kocha wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amesema kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 23, hakufanya "chaguo nzuri" kujiunga na Old Trafford. (Ziggo Sport - in Dutch) Chelsea wanajitahidi kutafuta wanunuzi wa kipa Kepa Arrizabalaga, 26, beki wa kushoto Mhispania Marcos Alonso, 29, na mlinzi wa Kidenmark Andreas Christensen, 24, ambao wote watapatikana mwezi Januari. (Sunday Express) Mwenyekiti wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy yuko tayari kuidhinisha mkataba wa mkopo wa miezi 18 kwa kiungo wa England mwenye umri wa miaka 24 Dele Alli, ambaye anataka kuondoka klabuni hapo mwezi Januari ikielezwa kuna uwezekano anaelekea Paris St-Germain. (90min) Wolves wanafikiria kumchukua kiungo wa kati wa Mainz Marlon Roos-Trujillo, 17, ambaye amewakilisha Ujerumani kwa wachezaji wa chini ya umri wa miaka 19. (Bild - in German) West Bromwich Albion wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 anayekipiga Newcastle United Dwight Gayle, ambaye mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Birmingham Live) Arsenal wamepanga kumfanya mlinzi wa Ufaransa 19 William Saliba mwenye umri wa miaka 19 apatikane mwezi Januari, akiwa na mashaka juu ya utayari kwa Soka la Primia . (Football London) Kocha wa Middlesbrough Neil Warnock anamtaka winga wa Uingereza Duncan Watmore mwenye umri wa miaka 26 kutia saini mkataba mpya wakati vilabu vingine vikimhitaji. (Sun on Sunday) Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameghairi chakula cha mchana wakati wa sikukuu ya Krisimasi kwa sababu ya hofu ya Covid-19. (Sunday Mirror) Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, amedokeza kuwa nafasi ya yeye kuondoka Paris St-Germain itategemea ridhaa ya wazazi wake. (Copa 90, via Sun on Sunday) text: Vifaru na silaha nyingine za Marekani vikiwasili Ujerumani wiki iliyopita Wanajeshi hao watapelekezwa taifa hilo la Ulaya kama sehemu ya hatua za Rais Barack Obama kuwahakikishia washirika wake katika muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi (Nato) kwamba imejitolea kukabiliana na tishio kutoka kwa Urusi. Kuwasili kwa wanajeshi hao kunajiri siku chache kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump kuwa rais mpya. Bw Trump ameashiria kwamba anataka uhusiano kati ya Marekani na Urusi uimarike. Operesheni ya sasa ndiyo kubwa zaidi kwa Marekani kupeleka wanajeshi Ulaya katika kipindi cha miongo kadha. Tayari zaidi ya vifaru 80 na mamia ya magari ya kivita vimewasilishwa Ujerumani na sasa vinasafirishwa hadi mashariki mwa Ulaya kwa barabara na reli. Wanajeshi wa Marekani watashiriki mazoezi ya kijeshi katika mataifa ya bahari ya Baltic. Hii inatazamwa na wengi kama hatua ya Rais Obama kujibu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kuwahakikishia washirika wake Nato. Mpango wa sasa ni wa kuwabadilisha wanajeshi watakaokuwa huko kila baada ya miezi tisa. Kuchaguliwa kwa Donald Trump hata hivyo kumeibua maswali kuhusu iwapo mpango wa sasa wa jeshi la Marekani utaendelea. Waziri wa ulinzi aliyependekezwa na Bw Trump, Jenerali James Mattis, huenda akaulizwa kuhusu mtazamo wa utawala wa Trump kwa urusi atakapokuwa anahojiwa na kamati ya ya bunge la Seneti baadaye Alhamisi. Marekani itatuma vifaru na magari ya kivita pamoja na wanajeshi 3,000 nchini Poland kuanzia Alhamisi. text: Mtindo huo mpya wa maisha umezua gumzo katika jamii huku baadhi ya watu wakihoji hatima ya siku zijazo za utamaduni wa kulipa mahari. BBC imetembelea kijiji hicho na kuzungumza na wanawake, wanaume, viongozi wa kijiji na baadhi ya wahusika ili kufahamu zaidi kwa nini utamaduni huo unazidi kupata umaarufu. Kaitesi Lilian mmoja wa kina mama wa kijiji hicho anasema "Mvulana anapokuja kumposa msichana wako unajua kwamba mambo yameiva, lakini ndoa ikikaribia unaskia kwamba amemgeuka na kumwambia kwamba ndoa haitawezekana ikiwa hatapewa pesa za mahari". Alipoulizawa mbona wanawake wengine wameolewa bila kufuata utaratibu huo alifafanua kwa kusema"Wakati huo binti alikuja na kuangua kilio huku akinishinikiza niuze kila kitu hata mabati au shamba ilimradi yeye apate pesa ya kumpa mchumba wake. Tofauti na maeneo mengine ya nchi ambapo mwanaume ndio hutoa posa kwa familia ya mwanamke, utamaduni huu mpya unawashinikiza wasichana kumlipa pesa mwanamume. Inasadikiwa kuwa pesa hizo ni kama dola 1500 na huongezeka kulingana na uwezo wa familia ya msichana. Waliyoshuhudia wanasema pesa hizo lazima zipatikane kwa udi na uvumba. Lakini ni nini kinacho wafanya vijana kugeuza utamaduni uliopo? Katika tamaduni za wanyarwanda mahari lazima itolewe tena na bwana harusi mtarajiwa. Hata kama mahari haijakamilika kwa wakati huo familia husika zinakubaliana jinsi itakavylipwa, na hatimae harusi hufanyika. Katika mkoa wa msgharibu nchini Rwanda pesa hizo zikikosekana hakuna harusi tena. Kaibanda Bernard ameiambia BBC kuwa vijana "Wanafanya hivyo wakisema idadi ya wasichana sasa hivi ni kubwa sana'' Wasichana wengine wameshindwa kuvumilia, ambapo msichana akitinga umri wa miaka kumi na tano hivi anatafuta pesa kwa nguvu ili aweze kumnunua bwana. Vijana wenyewe wanaona ni ishara ya ushirikiano katika familia mpya kutokana na hali ya maisha ilivyo ghali siku hizi. John Gatera anasema mmoja wa watu wanaounga mkono mtindo huo wa maisha anasema "Zamani kutoa mahari ilikuwa ni kitu rahisi sana ni ngombe labda na kiwanja lakini sasa hata kupalilia sehemu ya ujenzi lazima ulipe pesa''. Anasema yeye binafsi akifikisha umri wa kuoa lazima msichana amlipe pesa la sivyo harusi haitafanyika. Baadhi ya watu katika kijiji cha Nyamashekhe wanataka serikali kuingilia kati suala hilo. Mmoja wao ni mzee Kaihura ambaye anasema''Kijana hawezi kupata heshima katika jamii ikiwa hatatoa mahari''. Utamaduni huu mpya umepokelewaje? Sio mara ya kwanza Mkoa huo wa Magharibi ambao ndio mkubwa kuliko mikoa mingine kuzua gumzo kuhusiana na masuala ya kijamii. Kabla ya mtindo huu wa sasa wa vijana kutaka walipwe pesa na wasichana ili wawaoe, kulikuwa na wakati inadaiwa kuwa mvulana akimtembelea mchumba wake kwao sharti achinjiwe jogoo. Katika kijiji cha Nyamashekhe kilichopo mkoa wa magharibi nchini Rwanda kumekithiri utamaduni wa wanawake kulipa pesa kwa mwanaume ili waolewe. text: Mugabe ameongoza Zimbabwe tangu 1980 Pasta Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi ameambia wanahabari. Alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa "Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo," Bw Mtisi aliambia AFP. "Awali alishtakiwa kwa kudunisha na kukosea heshima mamlaka ya rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa kuwatusi watu wa asili fulani au dini fulani." Pasta Mugadza, ambaye huhudumu katika mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo, aliandaa kikao na wanahabari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Mugabe angefariki Oktoba 17 mwaka huu. Kumfanyia mzaha Rais Mugabe au kutoa unabii au ubashiri kumhusu ni jambo hatari nchini Zimbabwe. Patrick Mugadza amekamatwa mara kadha na polisi Zimbabwe Nchini humo kuna sheria ambayo huharamisha "kudunisha mamlaka ya au kumtusi rais." Mwaka 2015, Mugadza alikamatwa na kuzuiliwa kwa karibu mwezi mmoja baada ya kujitokeza hadharani na bango lililokuiwa na ujumbe uliomwambia Mugabe kwamba watu wamekuwa wakiteseka chini ya utawala wake. Siku ya maadhimisho ya uhuru mwaka jana, alitoa mahubiri akiwa amejifungia kwenye boriti ya taa nje ya duka kubwa zaidi la kibiashara mjini Harare, akisema hiyo ilikuwa ishara ya raia kukandamizwa Zimbabwe. Maandamano ya kupinga uongozi w arais Mugabe Zimbabwe Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu 1980. Kumekuwa na uvumi kuhusu afya yake na mara kwa mara husafiri mataifa ya Asia kwa matibabu. Bw Mugabe amekataa kumtaja mrithi wake na chama chake cha ZANU-PF kimekuwa kikiyumbishwa na makundi ya watu wanaotaka kumrithi. Mwishoni mwa mwaka uliopita, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani waliandamana kupinga utawala wake. Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu. text: Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga dhidi ya klabu ya Villareal uwanjani Bernabeu Mshambuliaji huyo wa Ureno amefunga magoli tisa katika mechi sita za vilabu bingwa lakini amefunga bao nne katika mechi 14 za la Liga msimu huu. Kulingana na ripoti , Ronaldo amekuwa na mgogoro wa kandarasi na klabu hiyo na amehusishwa na uhamisho wa kurudi Manchester United. Lakini Zidane alisema: Mimi hupendelea kusema kitu hicho hicho kwamba sioni Real Madrid bila Cristiano Ronaldo. Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 yuko katika kandarasi hadi 2021 na alishinda taji lake la tano la Ballon d'Or mwezi uliopita, mbali na kufunga bao la pekee katika mechi ya fainali ya klabu bingwa duniani dhidi ya Gremio. Licha ya kuonyesha mchezo mzuri katika mechi za vilabu bingwa, wako katika nafasi ya nne katika ligi ya La liga baada ya kushindwa nyumbani na Vilareal siku ya Jumamosi. Tangu kujiunga na Real Madrid kutoka Man United ambapo alivunja rekodi ya £80m 2009, Ronaldo ameifungia timu yake mabao 422 katika mechi 418, lakini meshindwa kufunga katika mechi tatu za ligi. Zidane alisema: Tunajua kilichojadiliwa , lakini kile Cristiano anachofaa kufanya ni kufikiria kucheza kama kawaida. Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 yuko katika kandarasi hadi 2021 na alishinda taji lake la tano la Ballon d'Or mwezi uliopita 'Ningependa kuzungumza kuhusu mchezo wake kwa sasa na kile anachoweza kuchangia katika timu akiwa uwanjani''. ''Cristiano ni mmoja wa klabu hii, ambapo yupo. Klabu, mashabiki na kila mtu anampenda. Upande wake wa mchezo ndio nilio na hamu nao. Sitaki kuzungumzia kandarasi yake na vitu kama hivyo''. Baada ya kushinda mechi mbili kati ya saba za ligi, Real wako na pointi 19 nyuma ya viongozi Barcelona wakiwa na mechi ambayo hawajacheza. Alipoulizwa kuhusu hatma yake ya siku za usoni , Zidane alisema: Sifikirii kuhusu hilo.Nafanya kazi kulingana na siku ilivyo na siwezi kubadilisha hilo. Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anaamini kwamba mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo atasalia katika klabu hiyo na haoni sababu za yeye kuondoka katika klabu hiyo ya Uhispania. text: Lakini siku mbili baada ya mtoto wangu kuzaliwa, maziwa yalikuwa yakitoka kidogo kidogo. Nilijaribu kuyakanda, nilikula vyakula vya mafuta, nilikunywa maziwa ya ng'ombe magaloni kwa magaloni. Lakini siku ya tatu, mkunga alinishauri nirudi hospitali: mtoto wetu alikuwa na njaa. Ni ngumu Niliposhauriwa kuanza kutumia pampu ya maziwa hospitalini, damu ilitoka badala ya maziwa. ''Nina matatizo gani? Mwili wangu unakataa hali ya kuwa mama?'' nikajiuliza. Mtoto wangu alikuwa akinyonya maziwa kwa nguvu ili aweze kupata maziwa kiasi chuchu zangu zilipata vidonda. Laiti ningejua kuwa suala la kunyonyesha haliji tu lenyewe. ni mchakato wa kupanda na kushuka. Unaweza kufanikiwa kwa kujaribu mara kwa mara, kwa kuwa si rahisi mara zote, ni mchakato ambao unaweza kuumiza. Je, kuna wazazi wanaologa watoto kisa mali? Kwanini utapia mlo unakithiri Mpwapwa? Ni upweke Baada ya kufanikiwa mtoto wangu alianza kupata maziwa, nilikuwa na muda mfupi sana wa kulala, kuoga hata muda wa kujitazama kwenye kioo. Kutoka halikua jambo jema kwangu: ''Nilifikiri majirani wataonaje? maarafiki watafikiri nini?'' Maeneo niliyopenda kuyatembelea sikwenda tena kwa kuwa sikuwa nikipendelea kunyonyesha hadharani. Nilikuwa nikiamka usiku wa manane, pekeyangu na mtoto, nikijisikia mpweke nje ya ulimwengu, nilikuwa na msongo sikuwa na mtu wa kunisaidia. Bora ningejua kuwa kujitunza mwenyewe ni muhimu pia kama ilivyo kwa kumtunza mtoto. Mama mwenye afya njema na aliyepata muda wa kupumzika ni bora zaidi kuliko aliye na wasiwasi mwingi na mwenye sonona Mtoto wangu kwanza walimpatia maziwa ya unga hospitali, alilala kwa saa kadhaa. Nakumbuka niliwahi kuwaza mwenyewe kuwa kama nitahitaji kulala, nitaweza kumpa maziwa ya kopo badala ya kumnyonyesha. Haikunichukua muda kuanza kujiona mwenye hatia. Maziwa ya kopo yakaanza kuacha mabaki kama utando kwenye ulimi- ilikuwa na harufu mbaya na yakaonekana hayana uhalisia. Ilikuwa kama nilikuwa namlisha mtoto wangu vyakula visivyo na faida kwenye mwili wake. Kila wakati nilikuwa nikijiambia kuwa : ''Ningejaribu zaidi.Kwa kweli sikuwa nahitaji muda zaidi wa kulala.'' Laiti ningejua kuwa hali ya kujisikia mwenye hatia haiishi. Lakini ni jambo ambalo halina utetezi, kila mtu atafanya kile ambacho anaona kinamfaa- kunyonyesha au la. Pata msaada Unyonyeshaji ni suala la gharama kubwa, kwa kila changamoto, kuna gharama ya fedha kwa kila ufumbuzi wenye kuleta nafuu. Niligundua kwenye duka nililokuwa nimeenda kutafuta tiba nikaziona za kila namna. Lakini tiba muhimu kwangu ilikuwa ni kwenda kwenye madarasa yanayotoa elimu kuhusu unyonyeshaji na kupata msaada kutoka kwa wataalamu na watu wenye uzoefu. Laiti ningalijua kuwa sikuwa peke yangu, nami ni miongoni mwa watu wengi wanaopata shida kwenye suala la kunyonyesha. Kuna msaada unaopatikana, na kuomba msaada ni jambo zuri zaidi unaloweza kufanya. Unyonyeshaji ni kuchagua. Nafikiri uwe ni uchaguzi wa mtu mwenyewe, lakini kushindwa au kutotaka kunyonyesha hakukufanyi kuwa mama mbaya. Nilikwenda kwenye madarasa ya uzazi, ninunua sidiria za kuvaa wakati wa kunyonyesha- Nilikuwa tayari kabisa kuwa mama mnyonyeshaji. text: Msichana huyo alibakwa mara kadhaa na babake wa kambo na anatarajiwa kujifungua katika kipindi cha miezi minne ijayo Sheria ya India haikubali utoaji mimba baada ya wiki 20, ila tu ikiwa maisha ya mwanamke mja mzito yamo hataraini. Sheria hii kali ilipitishwa ili kuwezesha usawa wa jinsia zote, kiume na kike. Kumekuwa na mila na desturi India ambapo wanawake wengi wamekua wakitoa mimba punde wanapogundua wanabeba mimba ya mtoto msichana. Katika miezi ya karibuni, Mahakama ya Juu ilipokea maombi ya wanawake kadhaa waliodai kupata mimba baada ya kubakwa. Wanawake hao walitaka kutoa mimba zilizopita wiki 20. Mahakama imekua ikituma maombi haya kwa jopo la wataalamu wa afya. Kesi ya sasa kutoka jimbo la Haryana, madaktari wanakutana kuamua ombi la familia ambayo inataka mtoto wao wa miaka kumi kutoa mimba. Habari za mimba hii zilitolewa na mamake msichana huyo ambaYe alimpeleka mwanawe hospitalini baada ya kulalamika maumivu ya mwili. Duru zinasema msichana huyo amekua akiishi nyumbani wakati mamake akiwa kazini ambapo ni kijakazi. Alimuambia Mamake kwamba babake wa kambo amekua akimbaka kila mara na kumtisha asiseme lolote. Mwanamume huyo amekamatwa na anazuiliwa korokoroni baada ya mkewe ku Jopo la madaktari linakutana India kuamua iwapo mtoto wa miaka 10 aliyebakwa na babake wa kambo anaweza kuruhusiwa kutoa mimba. text: Maafisa wa afya walikusanya visodo vya vitambara vilivyotumika kutoka kwa wanakijiji Lakini hilo ndilo walilofanya wahudumu wa afya katika vijiji katika jimbo la magharibi India Maharashtra - ili kutambua uwezekano wa wanawake kuugua saratani ya kizazi. Zaidi ya robo ya wagongwa wa saratani ya kizazi wanatoka India. Hatahivyo kuna sababu nyingi kwanini wanawake hawaendi kufanyiwa ukaguzi wa vizazi- ukosefu wa miundombinu na taasisis katika maeneo ya mashinani pamoja na gharama kubwa, na kukerwa na fikra ya kufanyiwa ukaguzi wa ndani ya mwili. "Wanawake wa mashambani wana haya, wanaogopa ukaguzi huo na huona haina maana," wanasema watafiti walioandika katika jarida la Ulaya kuhusu kuzuia saratani. Zaidi ya 90% ya wanawake wa mashambani India hutumia vitambara wakati wa hedhi na sio visodo vya kuuzwa madukani. Watafiti kutoka Tata Memorial Centre na taasisi yakitaifa ya utafiti kuhusu afya ya uzazi India wamegundua kuwa kwa kukagua visodo vilivyotumika wanaweza kutambua uwepo wa kirusi cha human papilloma virus (HPV), kinachosababisha saratani ya kizazi. "Kizingiti kikuu ya kuidhinisha kwa ukubwa mpango huu wa ukaguzi wa saraatani ya kizazi ni hatari ya kupungua kwa wanawake wanaoshiriki." amesema Dkt Atul Budukh, mtafiti mkuu wa taasisi hiyo. Kutokana na hilo madakatari wanasema wagonjwa wengi wa saratani hiyo hutambuliwa wakati saratani imekomaa au wakati wakifika hospitali kwa matatizo mengine ya kiafya. Wanasayansi India wanakagua sampuli za visodo katika maabara Zaidi ya wanawake 500 wameshiriki utafiti huo wa kati ya umri wa miaka 30 na 50, ambao hawana historia ya saratani wana afya nzuri ya akili na mwili na hupata hedhi zao kama kawaida. Waliwasilisha visodo walivyotumia kwa utafiti huo wa miaka miwili. Vitambara vya hedhi vilivyokusanywa vilihifadhiwa katika mazingira ya baridi kali na vilitumwa katika taasisi ya ukaguzi kukaguliwa. Chembechembe za DNA zilitolewa kutoka damu iliokauka na kukaguliwa. Wanawake 24 waligunduliwa kuwana kirusi hicho cha HPV na walitambuliwa kupokea matibabu zaidi, alisema Dkt Bhuduk. Wanawake wachache katika maenoe ya mshinani India hutumia visodo vya kuuzwa. Watafiti pia walinakili historia yao ya afya ya uzazi wao, vyoo wanavyotumia na vifaa wanavyotumia wakati wa hedhi. Utafiti huo uligunduwa haja kubwa ya kutoa elimu kuhusu afya na usafi wa sehemu za siri. Dr Budukh anasema: "kutokana na hali mbaya ya vyoo au ukosefu wa vyoo, wanawake katika maeno ya mashamabni hawana faragha ya kujiosha sehemu zao za siri." Usafi duni wa sehemu za siri ndio chanzo kikuu cha kuzuka saratani ya kizazi na matumizi ya visodo vilivyotengenezwa na vitambara na kutumika zaidi ya mara moja, inaongeza hatari, utafiti unaonyesha. Hedhi ni jambo lisilozungumziwa India, kwa hivyo hebu fikiria hisia dhidi ya fikra ya kukusanya visodo vilivyotumika na wanawake wakiwa katika hedhi. text: Lionel Messi scored his first hat-trick in World Cup qualifying matches Brazil walikuwa tayari wamefuzu. Luis Suarez alifunga mabao mawili kuwawezesha Uruguay kulaza Bolivia 4-2 na kufuzu pia. Colombia pia wamesonga mbele baada ya kutoka sare 1-1 ugenini Peru. Peru walimaliza wa tano katika michuano ya kufuzu Amerika Kusini na sasa watakutana na New Zealand katika mechi mbili za muondoano za kufuzu. Lakini nyota wa Arsenal Alexis Sanchez na taifa lake la Chile wako nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa 3-0 ugenini Brazil. Argentina walianza siku wakiwa nambari sita na kwenye hatari ya kutofuzu kwa mara ya kwanza tangu 1970. Aidha, walianza vibaya katika mechi hiyo iliyochezewa mji ulio nyanda za juu wa Quito. Wenyeji walijiweka kifua mbele baada ya sekunde 38 kupitia bao la Romario Ibarra, bao la kasi zaidi ambalo Argentina wamewahi kufungwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia. Hata hivyo, Argentina, waliomaliza wa pili Kombe la Dunia nchini Brazil 2014, walijikwamua wakisaidiwa sana na ustadi wa Messi. Alisawazisha baada ya dakika 12 aliposhirikiana vyema na nyota wa zamani wa Manchester United Angel di Maria. Bao lake la pili alilipata dakika nane baadaye na kisha akafunga la tatu na la ushindi kipindi cha pili. Msiba kwa Chile Alexis Sanchez hatacheza Kombe la Dunia 2018 Chile, ambao wameshinda Copa America katika michuano miwili ya karibuni zaidi, walikuwa wanapigania kufuzu kwa mara yao ya tatu mtawalia baada ya kufuzu na kufika hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014. Walianza mechi za mwisho wakiwa nafasi ya tatu lakini walifungwa mabao mawili na Brazil katika kipindi cha dakika tatu kipindi cha pili kutoka kwa Paulinho na Gabriel Jesus. Baada ya Peru kufunga bao la dakika ya mwisho la kusawazisha dhidi ya Colombia, Chile walihitaji kufunga kujipatia nafasi ya kucheza mechi za muondoano za kufuzu. Dakika za mwisho, walicheza kwa kikosi chao chote akiwemo kipa Claudio Bravo, kwenye nusu ya uwanja ya Brazil. Hata hivyo, Brazil walishambulia na Jesus alipata lango likiwa wazi baada ya mchezaji mwenzake wa Manchester City Claudio Bravo kukwama uwanjani na hivyo safari ya Chile kwenda Kombe la Dunia ikafikia tamati hapo. Lionel Messi alifunga mabao matatu na kuiwezesha Argentina kutoka nyuma ugenini dhidi ya Ecuador na kuwalaza 3-1 na kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi. text: Maelfu ya watu hufariki kutokana na malaria kila mwaka kutokana na vimelea vya Plasmodium falciparum -aina ambayo ilifanyiwa uchunguzi na watafiti - akichangia visa vingi. Sokwe ndio waliokuwa 'wakibeba' vimelea hiyo. Lakini mabadiliko yaliyotokana na maumbile miaka elfu 50 iliyopita iligeuka kuwa tishio kwa wanadamu, wataalam wamegundua. kuumwa na mbu Matokeo ya utafiti uliochapishwa katika jarida la PLoS Biology, huenda ikavumbua njia mpya ya kukabiliana na malaria, watafiti wa Taasisi ya Wellcome Sanger wanatumai. Malaria husababishwa na Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vijidudu kitaalamu viitwavyo Plasmodium Husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au wanyama baada ya kuumwa na mbu jike wanaokuwa wakitafuta damu kwa ajili ya chakula. Mtu anapoumwa huugua homa kali. Kuna aina tofauti ya vijidudu hivyo na moja kati ya vile vinavyoathiri binadamu peke yake ni Plasmodium falciparum. Ilihama kutoka kwa sokwe mtu na wakati sawa na ule ambao binadamu walihama kutoka Afrika, miaka kati ya 40,000 hadi 60,000 iliopita, watafiti wanasema. Vijidudu hivyo huathiri seli kwenye ini na chembechembe nyekundu za damu, na kusababisha dalili nyingine ikiwemo upungufu wa damu. Hatimaye ugonjwa huathiri mwili mzima, ikiwemo ubongo na unaweza kuua. Takriban watu 435,000- wengi wao watoto- hufa kutokana na malaria kila mwaka. Uchunguzi wa jeni za kale za vijidudu tofauti vinavyosababisha malaria, uliangazia zaidio jeni moja iliofahamika kama rh5 - sehemu muhimu ya chembe chembe ya vinasaba DNA ambayo huwezesha malaria kushambulia celi nyekundu katika mwili wa binadamu. Ni moja ya tafiti ambazo madaktari wanatumia kutengeneza chanjo mpya ya malaria. Watafiti wanaamini maelfu ya miaka iliopita, aina mbili za vimelea vya malaria vilitokea kuambukiza sokwe na wakabadilishana vitu vya maumbile kati yao. Plasmodium falciparum ilichagua jeni aina ya rh5. Mmoja wa watafiti hao Dr Gavin Wright anasema: "Hii ilikuwa tukio ambalo sio la kawaida ambayo ilichangia ongezeko la vifo kwa binadamu. "Tumeshangazwa sana na matokeo hayo. Ilikuwa na matokeo chanya kwasababu inashabihiana na tafiti zingine zilizofanywa na na wenzetu . Ilibainisha maelezo kuhusu jinsi vijidudu hivyo vilivyooka kwa sokwe na kuingia kwa binadamu. "Rh5 kwasasa ni chanjo muhimu katika kiwango cha damu cha mtu ambaye anaweza kupata malaria kwa hio tukipata maelezo zaidi kuhusu jeni hii, inaweza kutusaidia katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu." Alisema uwezekano wa vijidudu hivyo kuendlea kuzaana muda mfupi baadae ni "kidogo sana", japo hilo kihalisia inasemekana kuna uweze kano huo. Karibu nusu ya watu duniani wanakabiliwa na tisho la kupatikana na malaria. Vifo vingi vinavyotokana na malaria hasa kwa watoto katika eneo la Jangwa la Sahara barani Afrika husababishwa na Plasmodium falciparum. Msururu usio wa kawaida wa matukio uliibua aina hatari ya malaria kutoka kwa sokwe "kuhama" na kuanza kushambulia binadamu, kwa mujibu wa wanasayansi. text: Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Sam wa ukweli Sam alitamba sana na kazi zake kama vile Sina Raha alioutoa katika ya mwaka 2009 na 2010, Usiniache, Lonely na Hata kwetu wapo. Hapo kati kati alipotea mpaka mwishoni mwa mwaka 2017 alipoibuka na kibao kingine kwa jina Kisiki na baadaye mwanzoni mwaka huu wa 2018 akauachia Wimbo Ni Wewe. Ingawa ni mtu wa Singida Sam wa Ukweli amekulia Kiwangwa jirani na mji wa Dar es Salaam ambako amelelewa na Bibi yake mzaa mama. Kwa mujibu wa aliyekuwa Meneja wa msanii huyo, Abdulmalik Mohamed , mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mipango ya mazishi inaendelea katika eneo la Tandale lakini Maziko yatafanyika Alhamis hii Kiwangwa mkoani Pwani. Aidha meneja huyo amesema chanzo cha kifo cha msanii huyo ni Malaria na UTI (Urinary Tract Infection) ya muda mrefu. Sam alikuwa akiandaa nyimbo zake mpya kabla ya kuanza kusumbuliwa na Tumbo akiwa Studio. Ameacha mke na mtoto mmoja wa kike. Msanii wa Bongo Fleva, Salum Mohamed aliyetamba kwa jina la Jukwaani kama Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2018. text: Angelina Jolie aliasili binti kutoka Ethiopia mwaka 2005 Ethiopia ni miongoni mwa nchi ambazo ni vyazo vikuu vya watoto wanaoasiliwa na raia wa Marekani kwa kiwango cha kufiki asilimia 20 kwa kwa ujumla. Watu maarufu kama Brad Pitt na Angelina Jolie ni miongoni mwa walioasili watoto kutoka Ethiopia. Hata hivyo, mwaka 2013, wanandoa wawili kutoka marekani walishtakiwa kwa kumuua binti mmoja wa Ethiopia waliyekuwa wamemuasili. Kesi ambayo ilileta mjadala mkali nchini Ethiopia. Mchakato mzima wa kuasili watoto nchini Ethiopia umekumbwa na maswali mengi asasi za kutetea haki za binadamu wakisema kuwa unawanufaisha wafanyabiashara wanaosafirisha binadamu. Miaka miwili iliyopita , Denmark ilisitisha kuasili watoto kutoka Ethiopia. Watunga sheria wa nchi hiyo wanasema kuwa yatima na watoto wote wasiojiweza wanatakiwa kutunzwa chini ya msaada utakao patikana nchini Ethiopia kwa ajili ya kuwalinda. Ingawa baadhi ya wabunge wanasema nchi hiyo bado haina huduma bora inayoweza kuwapa uangalizi mzuri watoto hao wenye uhitaji. Tangu mwaka 1999, watoto zaidi ya 15,000 wameasiliwa Marekani kutoka Ethiopia. Wengine wengi wakiwa wanapelekwa katika nchi za ulaya kama Hispania, Ufaransa na Italia. Serikali ya Ethiopia imekataza raia wa kigeni kuasili watoto wa Ethiopia kwa madai kuwa watoto hao hunyanyaswa na kutelekezwa wakiwa ughaibuni. text: Wanasayansi hao wanataka kuunda taifa anga za juu ambalo litaitwa Asgardia Taifa hilo litaundwa katika anga za juu, eneo. Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu huzunguka dunia. Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa mwaka ujao. Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa. Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai umiliki wa maeneo anga za juu. "Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa hata pasipoti, anasema Lena de Winne, mmoja wa maafisa wakuu wa mradi huo ambaye alifanya kazi kwa miaka 15 katika Shirika la Anga za Juu la Ulaya (EPA). Maelfu ya watu tayari wameonyesha nia ya kutaka kujiunga na taifa hilo Mradi huo unaongozwa na shirika la Aerospace International Research Center, ambalo lilianzishwa na mwanasayansi Mrusi, ambaye pia ni mfanyabiashara, Dkt Igor Ashurbeiyli. Mashindano yanaandaliwa kuamua bendera na wimbo wa taifa wa nchi hiyo mpya. Profesa Sa'id Mosteshar, mkurugenzi wa Taasisi ya Sera na Sheria za Anga za Juu ya London, amesema itakuwa vigumu kwa Asgardia kutambuliwa kama taifa ikizingatiwa kwamba haitahusiana na taifa lolote linalojitawala duniani, na pia 'raia wake' wengi watakuwa ardhini. Tayari zaidi ya watu 50,000 wamewasilisha maombi mtandaoni kutaka kuwa raia wa taifa hilo. Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia. text: Wanawake wakishangili baada ya matokeo nchini Mexico Mexico imechagua idadi sawa ya wanawake na wanaume bungeni katika mabunge yote mawili, hatua inayodhihirisha kuwa nchi hiyo imepiga'' hatua kubwa''. Serikali ya Uhispania, ilichaguliwa mwezi Juni, ni ya kwanza tangu nchi hiyo ilipokuwa ya kidemokrasia kwa kuwa na wanawake wengi kuliko wanaume kwenye baraza la mawaziri Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern alijifungua mtoto wa kike tarehe 21 mwezi Juni na kuwa mwanamke wa pili pekee kuwa na mtoto akiwa madarakani,baada ya waziri mkuu Benazir Bhutto mwaka 1990. Je mwaka 2018 ni mwaka wa wanawake kushika nyadhifa mbalimbali? Mwaka mmoja baada ya Hillary Clinton kushindwa nafasi ya urais nchini Marekani, kumekuwa na wanawake ambao wanawania nafasi mbalimbali nchini humo kuliko ilivyokuwa zamani. Mgombea wa chama cha Democrat Alexandria Ocasio-Cortez alimshinda mwanasiasa mkongwe Joe Crowley mwenye miaka 56, jijini New York mwezi Juni. Binti huyo mwenye miaka 28 aliwashangaza wengi kwa kuwa hakuwa na historia ya kuwa kwenye siasa, lakini alipambana na mtu aliyetumika kwenye siasa kwa awamu 10. Muigizaji Cynthia Nixon (kulia) , Alexandria Ocasio-Cortez (kushoto)- Nixon anawania nafasi ya ugavana New York Profesa Farida Jalalzai, mkuu wa idara ya sayansi ya siasa katika Chuo cha Oklahoma, anaamini kuwa uthubutu wa wanawake kuwania nafasi mbalimbali ni kwa sababu pia hawapendezwi na Donald Trump Anasema kuwa wanawake wanafanya vizuri sana mwaka huu kwenye bunge la Congress.Lakini kuna safari ndefu bado kwa kuwa kuna 20% pekee kwenye bunge la wawakilishi Vipi kuhusu Ulaya? Wanawake wako mpaka 30% kwenye mabunge ya mataifa ya ulaya ikiwemo (Monaco). Mwaka 2017 idadi kubwa ya wanawake ilijitokeza kwenye chaguzi duniani, lakini hakukuwa na mafanikio makubwa.Ulaya ilipata wanawake wengi waliokuwa na uwakilishi bungeni, lakini wengi walikosa nafasi hizo. Baraza la mawaziri la Uhispania lina wanawake 11 kati ya 17 Karibu kila nchi duniani imerekodiwa kuwa na ongezeko la idadi ya wabunge wanawake tangu mwaka 1997 baada ya umoja wa mabunge(IPU) kukusanya matokeo Miongo miwili iliyopita Sweden,Norway,Finland,Denmark na Uholanzi zilikuwa na zaidi ya 30% ya wabunge wanawake-huku Sweden ikiongoza kwa 40.4%. Miaka 21 baadae, nchi zinazoongoza sambamba na nchi za Scandnavia zimepitwa na Rwanda na nchi kadhaa za America ya kati na kusini , Bolivia, Grenada, Mexico, Nicaragua, Costa Rica na pia visiwa vya Caribbean kama vile Cuba, pia ni miongoni mwa nchi 10 zenye zaidi ya 40% ya wabunge wanawake. Lakini Zeina Hilal, ambaye ni kiongozi wa masuala ya mpango wa jinsia ndani ya IPU, anasema maendeleo katika kuhakikisha kuwa kuna usawa kati ya wanawake na wanaume katika uwakilishi yanaonyesha kuzorota katika kipindi cha miaka miwili au mitatu. ''Tunasikitika kwa kuwa miaka michache iliyopita ilikuwa ongezeko la kiasi cha 0.6% kwa mwaka 2016 na 2017, kwa miaka miwili mfululizo tumefikia uwiano wa 0.1% hii inaogofya''. Ikiwa uwiano huu utaendelea, IPU inakisia kuwa itachukua miaka 250 kufikia usawa wa jinsia kwenye mabunge. Nchi nyingi duniani hazina viongozi wanawake.kwa sasa kuna viongozi wajuu wanawake 11 duniani-ukijumuisha marais idadi inafika 21 Angela Merkel ni kiongozi pekee aliyehudumu muda mrefu kwenye serikali ya Ujerumani, amekuwa kiongozi tangu mwaka 2005 Jacinda Ardern, mwnza wake Clarke Gayford, na binti yao Neve Mbali na Sheikh Hasina Wajed wa Bangladesh, ambaye kwa sasa yuko kwenye muhula wa tatu,wanawake wengine walio viongozi wa serikali wamekuwa kwenye nafasi hizo kwa miaka mitano au chini ya hapo.Jacinda Ardern wa New Zealand, Kiongozi wa Iceland Katrin Jakobsdottir na Ana Brnabic wa Serbia wote walichaguliwa mwaka 2017. Erna Solberg alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Norway mwaka 2013.Nchini Namibia Saara Kuugongelwa aliingia madarakani mwaka 2015, Theresa May akawa waziri mkuu wa pili mwanamke mwaka 2016, mwaka sawa na aliochaguliwa Aung San Suu Kyi nchini Myanmar. Viorica Dancila ni mwanamke wa kwanza katika historia kuwa waziri mkuu, alichaguliwa Januari mwaka 2018. Rwanda inaongoza kwa kuwa na wawakilishi wanawake IPU imeorodhesha nchi tatu zenye mambunge madogo zenye uwakilishi wa zaidi ya 50% wa wanawake nazo ni Rwanda, Cuba na Bolivia.Ingawa Mexico ina kiasi cha 48.6%. Rwanda inaongoza kwa kuwa na uwiano mkubwa wa wanawake katika bunge kuliko nchi nyingine yeyote Mabadiliko ya katiba mwaka 2003 imeruhusu 30% ya viti kuwa vya wanawake bungeni.Tangu wakati huo wanawake wamekuwa wakijitokeza katika chaguzi mbalimbali Mabadiliko hayo yalikuja baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994 ambapo watu 800,000 wengi wanaume walipoteza maisha, wanawake walilazimika kufanya majukumu mapya mengi ili kuijenga upya nchi yao. Rwanda hivi sasa ni moja kati ya nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika ingawa Rais Paul Kagame amekuwa akikosolewa kuwa amekuwa akiwabana wapinzani. nchi nyingine iliyo na uwiano mzuri wa jinsia ni pamoja na Bolivia na Mexico Nchi gani ina wawakilishi wachache wanawake bungeni? Miongoni mwa nchi zilizo na rekodi mbaya kwa uwakilishi wa wanawake bungeni ni Yemen,Oman,Haiti,Kuwait,Lebanon na Thailand-nchi zote zikiwa na 5% ya uwakilishi au chini ya hapo. Kuna visiwa kadhaa ambavyo havina uwakilishi wa wanawake kabisa kama vile Vanuatu, Micronesia na Papua New Guinea na nchi nyingine kama El Salvador na Sierra Leone ambayo idadi ya uwakilishi wa wanawake haifahamiki. Yingluck Shinawatra aliweka historia ya kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Thailand mwaka 2011. Yingluck Shinawatra Wakati huo alikuwa mmoja kati ya wawakilishi wanawake kwa 16% bungeni-namba kubwa katika bunge la Thailand-lakini mwaka 2015 alishtakiwa kwa shutuma za ufisadi na kutoroka nchini humo. tangu wakati huo idadi imeshuka mpaka kufikia 5%. Nchini Yemen kuna mwanamke mmoja tu aliyechaguliwa bungeni kati ya wabunge 301.Mpango wa kuhakikisha kunakuwa na uwakilishi wa angalau 30% haukufanikiwa. Professor Franceshet anasema anaamini hali itabadilika ikiwa wanawake wataendelea kuweka msukumo kwa vyama vya kisiasa na kwa viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kuwapa nafasi zaidi wanawake. Rekodi ya idadi ya wanawake wanaowania nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi duniani inabadili uso wa siasa na kuchochea uwepo wa usawa wa jinsia katika mabunge text: Mshambuliaji wa Wales Bale aliachwa nje ya kikosi cha wachezaji 24 katika mechi inayotarajiwa kuchezwa Ijumaa nchini England Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alianza mechi 14 katika mashindano yote msimu wa 2019-20 na amecheza mara mbili tangu kandanda kurudi nchini Uhispania mwezi Juni. ''Yalikuwa mazungumzo binafsi baina yetu. Aliamua kutocheza'', alisema Zidane. Yaliyosalia ni kati yangu na yeye lakini ni kwamba alisema asingependelea kucheza. BBC inaelewa Bale aliamua kutosafiri hadi Manchester kwasababu alijua kwamba hana nafasi ya kushirikishwa katika mechi hiyo. City ilishinda 2-1 katika awamu ya kwanza nchini Uhispania mnamo mwezi Februari kabla ya mlipuko wa corona hatua iliyofanya mashindano hayo kusitishwa kwa takribani miezi mitano. Manchester City walioshinda mechi hiyo watacheza dhidi ya Lyon au Juventus katika robo fainali. Bale ambaye alitarajiwa kuhamia katika ligi kuu nchini China na kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning msimu uliopita kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba amekuwa mtu tofauti katika wiki za hivi karibuni , ikiwemo kujifanya kwamba alikuwa amelala wakati Real Madrid ilipokuwa ikicheza mechi yake ya mwisho iliyowafanya kutawazwa kuwa mabingwa wa Uhispania. Alipoulizwa iwapo hatma ya Bale ipo mikononi mwa Madrid , Zidane alisema: Sijui. Kwasasa ni mchezaji wa Real Madrid . Hilo halijabadilika. bado yeye ni mchezaji wetu, naheshimu hilo na namuheshimu yeye, kama mtu mwingine yeyote. ''Aliamua kutocheza. Hicho ndio kitu ambacho naweza kusema.'' Gareth Bale hakutaka kucheza katika mechi ya marudio ya kufuzu kwa robo fainali ya klabu bingwa Ulaya katika mechi dhidi ya Manchester City , kulingana na kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane. text: Conte aliwasaidia kutwaa mataji ya ligi ya Premiea msimu wake wa kwanza pamoja na Kombe la FA. Kufikia sasa, klabu hiyo imekataa kufunguka kuhusu hatma ya meneja huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 48 lakini inafahamika kwamba amefutwa kazi na hata wachezaji wa Chelsea wamekuwa wakimtakia heri na kumshukuru kwa muda aliokaa Chelsea.. Conte aliwasaidia kutwaa mataji ya ligi ya Premia msimu wake wa kwanza pamoja na Kombe la FA. Licha ya Conte kuwaongoza wachezaji mazoezini wiki hii, hatma yake imekumbwa na taharuki huku mkufunzi wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri akitarajiwa kujaza pengo lake. The Blues wa Chelsea tayari wamefikia makubaliano ya kuwasili kwa Sarri mwenye umri wa miaka 59. Iwapo usajili wa Sarri utadhibitishwa, atakuwa mkufunzi wa tisa wa Chelsea tangu Mrusi Roman Abramovich aliponunua timu hiyo 2003. Licha ya kutoinua taji lolote na Napoli miaka mitatu aliyowaongoza, Sarri amerudisha hadhi ya Napoli na kuwawezesha kumaliza nafasi ya pili, tatu, na pili nyuma ya Juventus msimu uliomalizika wa 2017-18. Aidha, Sarri, kocha wa zamani wa Empoli, alitajwa kocha bora wa mwaka Serie A, msimu wa 2016-17. Aslimia ya ushindi wa Conte mechi za Premier League ni bora kuliko wakufunzi wote waliowahi kuinoa timu hiyo. Hata baada ya kubeba Kombe la FA mwezi Mei kwa kuizamisha Manchester United, mustakbali wa Conte ulizidi kutapatapa. Hakupoteza matumaini na aliweza kurudi kuinoa timu hiyo wakati ikijiandaa kwa msimu ujao. Isitoshe, dalili za kuondoka kwake ziliongezeka kuanzia mwisho wa msimu uliopita baada ya Blues kukosa kufuzu kwa Champions League kwa kumaliza nafasi ya tano Premier League. Hata ubingwa wa Chelsea mwezi Mei Kombe la FA ilimaanisha kuwa Conte - aliyeifunza Juventus kutoka 2011 hadi 2014 - hajawahi kuondoka mikono mitupu katika misimu mitano iliyopita ambapo alihudumu kuwa meneja. Lakini mambo yalibadilika msimu uliopita na Chelsea ilimaliza alama 30 nyuma ya Manchester City, mabingwa wa Premier League pamoja na kutemwa nje ya Champions League, hatua ya mchujo baada kufungwa 4-1 na Barcelona katika mechi za mikondo miwili. Matokeo hayo yalizamisha ufanisi wa klabu hiyo ya London Magharibi huku Conte akilaumu msongamano wa mechi kwenye ratiba katika msimu wa Krismasi. Mnamo mwezi Oktoba, Blues walidhalilishwa na Crystal Palace ambayo hata haikusajili pointi moja katika mechi saba na kumchochea Conte kujitetea dhidi ya kuwepo kwa mgomo baridi kutokana na mbinu zake za mazoezi. Baada ya Krismasi, Chelsea ilifungwa mechi nne - mbili mfululizo - mwanzo dhidi ya Bournemouth na Watford, kabla ya kudunishwa na timu za Manchester City na Manchester United. Hata baada ya kufufua fomu yake baadaye kwa kushinda mechi nne mfululizo msimu ukikaribia kukatika, haikuiwezesha Chelsea kumaliza kati ya timu nne za kwanza. Kasoro ya Conte ni kukosa kuwasajili mastaa? Miezi miwili tu baada ya kuiongoza Chelsea kutwaa taji la ligi ya Premier 2016-17, Conte alizidisha mkataba wake ikiwemo kurefusha muda wake Stamford Bridge miaka miwili zaidi. Lakini alionywa dhidi ya kufuta rekodi yake kwa kumuiga Mourinho ambaye, msimu mmoja tu baada ya kuisaidia Chelsea kunyakua ligi 2015-16, aliwarudisha nyuma kwa kumaliza nafasi ya 10 kwenye jedwali msimu uliofuata. Msimu wa 2017 ulikumbwa na kuondoka kwa viungo muhimu wa timu hiyo akiwemo nahodha John Terry aliyeitumikia Chelsea miaka 22, na Diego Costa aliyefahamishwa kupitia arafa kuwa hakuoana na mipango ya Conte. Hali hiyo ilipelekea Costa kujiunga na to Atletico Madrid ambapo walibeba Kombe la Europa League msimu uliokamilika 2018. Uhamisho huo wa Chelsea uliendelea huku ikiagana na kiungo mkabaji wake Nemanja Matic na kumpiga bei kwa mahasimu wake Manchester United kwa kitita cha pauni milioni £40. Chelsea ilijaribu kuokoa chombo kwa kumsajili Alvaro Morata, lakini haikufanikiwa kumshawishi nyota wake wa zamani Romelu Lukaku, kujiunga nao. Lukaku aliishia kutua Old Trafford. Sakata hizi zilipelekea kuibuka kwa maswali kuhusu kusalia kwa Conte klabu hiyo na tangu mwezi Januari mwaka huu, maswali haya yalizidi. Conte hakukosa kuyajibu na kila alipoulizwa, alisisitiza kuwa alikuwa mwenye furaha huku akitaka klabu hiyo imuunge mkono na kumhakikishia uwepo wake kiti cha Ukufunzi. Chelsea inatarajiwa kuweka wazi uamuzi wake wa kutengana na Conte baada ya kuwatumikia kwa miaka miwili hivi karibuni. text: Barcelona iliishinda Real Madrid 5-1 katika uwanja wa Nou Camp msimu uliopita Mechi hiyo ya Ligi ya La liga ilitarajiwa kuchezwa tarehe 26 mwezi Oktoba lakini iliahirishwa kutokana na hofu za maandamano ya raia. Timu zote mbili zina pointi 35 lakini Barca inaongoza jedwali kupitia toafuti ya magoli. ''Katika mechi kama hizi ni muhimu kuonyesha uwezo wako katika dakika zote 90'', alisema Zidane. Mechi hiyo imecheleweshwa kwa miezi miwili kufuatia maandamano yaliofanyika Barcelona baada ya viongozi 9 wa Catalan wanaopigania kujitenga kwa jimbo hilo kuhukumiwa kwa kufanya uasi kufuatia hatua yao katika kura ya maoni na kupewa kifungo jela cha kati ya miaka tisa na 13. La liga iliwasilisha ombi la kuiahirisha mechi hiyo kutokana na sababu ambazo zilikuwa haziwezi kuepukika kwa kuwa maandamano zaidi yalikuwa yakitarajiwa Barcelona katika siku ya mechi hiyo. Klabu zote mbili hazikukubaliana kupeleka mechi hiyo Real Madrid lakini zitatumia hoteli moja kabla ya kuchezwa kwa mechi ya leo na kusafiri wakati mmoja saa mbili kabla ya mechi kuanza kutokana na sababu za kiusalama. Zidane alisema: Hicho ni kitu tofauti kwetu, tumeambiwa kwamba ni muhimu sisi kuishi pamoja na hilo ndilo tunalolifanya . Hakuna chengine cha kuelezea . Kitu muhimu ni kwamba mechi hiyo itaendelea. Mkufunzi wa Barcelona Ernesto Valverde aliongezea: Nadhani tungecheza mechi hii siku iliokuwa imepangwa na hakuna sababu ya kutocheza mechi hii siku ya Jumatano. ''Sio rahisi katika hali kama hii kwamba wachezaji watakutana kabla ya mechi, hivyobasi sitakutana na Zidane, lakini ninamuheshimu sana''. Ushindani kati ya timu zote mbili: Barcelona imeshinda mechi nyingi zaidi katika ligi ya La Liga dhidi ya Real Madrid zaidi ya timu nyengine yeyote ile katika mashindano hayo (72), huku Real Madrid ikiwa imeishinda Barcelona mara nyingi zaidi katika mashindano hayo (72). Barcelona inaweza kuweka rekodi ya kushinda mechi nyingi zaidi ya Real Madrid kwa mara ya kwanza katika historia ya El Clasico. Barcelona imepungua goli moja kufikia magoli 400 katika ligi hiyo katika mashindano yote na magoli manne kabla ya kusawazisha Magoli 403 ya Real Madrid kwa jumla. Real Madrid imecheza mechi sita za La liga bila kupata ushindi wowote dhidi ya Barcelona ikiwa ndio msururu mbaya zaidi katika mechi zao za El Classico tangu Disemba 2011 wakati walipokuwa na saba. Barcelona Lionel Messi amefeli kufunga ama kutoa usaidizi katika mechi zake tatu dhidi ya Real Madrid katika mashindano yote. Raia huyo wa Argentina hajawahi kucheza mechi nne dhidi ya Real Madrid bila kupata bao ama kutoa pasi itakayosababisha goli. Luis Suarez anaweza kuwa mchezaji wa tatu wa Barcelona kufunga magoli 10 na zaidi dhidi ya Real Madrid katika historia ya La liga. Baada ya magoli 18 ya Lionel Messi na 12 ya Cesar Rodriguez. Sergio Roberto ametoa pasi sita zilizosababisha magoli katika mechi nane dhidi ya Real Madrid katika la Liga huku pasi tano kati yazo zikifungwa na Luis Suarez. Wameshirikiana kwa magoli mengi ya La Liga katika El Clasico zaidi ya wachezaji wawili wowote katika karne ya 21{5} Real Madrid Nahodha wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos ana fursa ya kuwa mchezaji aliyshiriki mechi nyingi za El Clasico [43] akiipiku rekodi iliowekwa na Manola Sanchis , Francisco Gento na Xavi wote wakishiriki mechi 42. Zinedine Zidane jahawahi kushindwa katika mechi nne akiwa mkufunzi katika mechi zote na atakuwa mkufunzi wa kwanza wa Real madrid kutoshindwa katika mechi tano za ugenini za Clasicos. Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kwamba ni muhimu kuwa na matumaini kwamba mechi ya Jumatano ya El Classico dhidi ya wapinzani wao wa jadi Barcelona itaendelea kama ilivyopangwa. text: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro (katikati)pamoja na maafisa wengine kabla ya ndge kuondoka kuelekea Tanzania Shirika la ndege hiyo imeandika katika ukurasa wake wa Tweeter kuwa safari za ndege hiyo kuelekea Afrika kusini zitarejea siku ya ijumaa. Mwisho wa Twitter ujumbe, 1 Mapema leo Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja. Mwandishi wetu wa Afrika Kusini Nomsa Maseko anasema kuwa utaratibu wa kuiachia ndege hiyo kurejea Dar es Salaam kutoka uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg unaendelea. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzania imeridhishwa na uamuzi wa mahakama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzania imeridhishwa na uamuzi wa mahakama. Mkulima ambaye alipeleka shauri hilo mahakamani Hermanus Steyn na kupata kibali cha kushikiliwa ndege hiyo, hakuridhishwa na hukumu ya awali na kukata rufaa. Mwandishi wa BBC Maseko anaripoti kuwa Bw Steyn amedondoshwa pia kwenye rufaa yake na kutupiliwa mbali na mahakama. Jaji Twala M L akisoma hukumu yake mapema leo na kuamuru ndege ya Tanzania kuachiwa Dkt Ndumbaro ambaye pia ni wakili amesema kama Steyn bado ana madai yeyote, inafaa arudi kwenye mahakama za Tanzania na kusikilizwa. "Oh, niamini, raisi (John Magufuli) tayari ameshapewa taarifa (ya hukumu)," mwandishi wa BBC aliyepo mahakamani anamnukuu Dkt Ndumbaro akisema. Ndumbaro pia amesisitiza kwa kuwa serikali ya Tanzania imeshamlipa Steyn dola milioni 20, maana yake wapo tayari kumalizia bakaa ya deni, lakini mkulima huyo "anatakiwa kurudi katika mahakama za Tanzania, na aache kuihusisha Afrika Kusini." Baada ya ya kushindwa kwa kesi ya awali na hatimaye rufaa, wakili wa Steyn ameiambia BBC kuwa uamuzi wa mahakama: "Ni kushindwa moja kwa moja kwa haki, na mteja wangu anaona kuwa ameonewa. Bw. Steyn amepoteza kikomboleo cha mali na hii inamaanisha kuwa hawezi kukata rufaa bila ya ndege kuwa imezuiliwa." Jaji aliyesikiliza rufaa amesisitiza kuwa Afrika Kusini haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) ya kuliamulia jambo hilo. Kwa nini ndege ilizuiliwa? Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 ilikuwa imeshikiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg kwa amri ya mahakama. Hermanus Steyn alifungua kesi ya fidia dhidi ya serikali ya Tanzania. Steyn alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali nyingi ambazo zilitaifishwa na serikali ya Tanzania miaka ya 1980. Ilipofika miaka ya 1990 walikubaliana fidia atakayolipwa, kwa ujumla wake dola milioni 33 na tayari ameshalipwa dola milioni 20 kati ya hizo. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Tanzania, kwa mujibu wa mkulima huyo imeacha kulipa deni hilo, na hatua ya kuomba ndege kushikiliwa ilikuwa moja ya harakati zake za kutaka kumaliziwa deni. Ndege ya Air Tanzania imetua nyumbani Tanzania mwendo wa saa mbili unusu usiku huu baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya Afrika Kusini. text: Messi amehusishwa na kuhamia Manchester City na Paris St-Germain Barcelona ilikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hizo. Kwa mujibu wa El Mundo, mkataba wa Messi wa miaka minne ulikuwa wa thamani ya takriban euro 555,237,619 hadi Juni 30, 2021. Hii inamaanisha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa anapokea pauni milioni 123 kwa msimu. Barcelona imesema katika taarifa iliyotoa kuwa "inasikitishwa na uchapishaji wa maelezo hayo". Na kuongeza kuwa: "FC Barcelona haihusiki kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hiyo na itachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya gazeti la El Mundo, kwa uharibifu wowote ule ambao huenda umetokea kwasababu ya taarifa hiyo. "FC Barcelona imeonesha kumuunga mkono Lionel Messi, hasa katika jaribio lolote la kumdhalilisha na kuharibu uhusiano wake katika klabu hiyo ambako amefanyakazi na kuwa mchezaji bora duniani na katika historia ya soka." Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina Messi alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 lakini akatuma ombi la kutaka aruhusiwe kuhamia kwingineko mnamo mwezi Agosti. Bado haijafahamiki ikiwa atabaki katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika. Messi ni mchezaji wa Barcelona aliyeweka rekodi katika ufungaji wa magoli mengi na ameshinda makombe 10 ya La Liga, Ligi ya mabingwa mara nne na tuzo ya Ballon d'Or - alipewa tuzo mara sita ya mchezaji bora duniani. Ombi lake la kutaka kuondoka Barcelona lilifuatiwa na kutoelewana kati yake na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu, aliyeacha kazi hiyo mnamo mwezi Oktoba. Messi, anayeelezea utawala wa Bartomeu kama "janga", alisema mnamo mwezi Desemba "Bado sijajua nitakachofanya." Barcelona imesema kuwa itachukua "hatua za kisheria" dhidi ya gazeti la Uhispania la El Mundo baada ya kuchapisha maelezo kuhusu mkataba wa mshambuliaji, Lionel Messi wa pauni milioni 492. text: Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Msemaji wa umoja huo alikataa ombi hilo akisisitiza taarifa ya katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Gutierrez ambapo amewataka viongozi wa Kenya kusuluhisho mgogoro wowote wa uchaguzi huo katika taasisi zinazofaa kikatiba. Umoja huo umesema kuwa utatazama mpango mpya wa Raila Odinga ambao anapanga kutangaza siku ya Jumatano. Wiki iliopita kiongozi huyo wa Nasa alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kukagua matokeo hayo ya uchaguzi uliokamilika. Akizungumza na gazeti la Financial Times bwana Odinga alisema kuwa ana ushahidi wa kuthibitisha kwamba uchaguzi huo wa urais ulifanyiwa udanganyifu. ''Tutaonyesha ulimwengo ule mchezo uliochezwa, Kile tunachotaka ni Umoja wa Mataifa kubuni jopo la wataalam ambalo litatusaidia kutathmini matokeo hayo''. Kiongozi huyo wa upinzani alisema kuwa tume ya uchaguzi nchini IEBC ilikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa maafisa wa serikali inayoongozwa na rais Kenyatta. Antonio Gutterres ''Kufuatia mauji ya mtaalam wa maswala ya kiteknolojia katika tume hiyo Chris Msando, wafanyikazi wengine waliogopa''. ''Kile kilichotokea kimeshinikizwa na serikali. Sio kuhusu mimi, Sio Kuhusu Raila Odinga sitokuwa mgombea tena. Tunataka Wakenya kujua kilichofanyika, kile ambacho dunia nzima haielewi kinafanyika''. ''Hakuna haja ya watu kwenda kupanga milolongo mirefu ya kupiga kura kwa saa kadhaa ama kufanya kampeni na huku kompyuta moja katika tume ya IEBC inatumiwa kuchakachua matokeo hayo''. Umoja wa Mataifa umekataa ombi la kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kukagua matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti. text: Uvumi wa kuvunjika kwa penzi lao la miaka minne ulisambaa katika mitandao ya kijamii kabla ya Omondi mwenyewe kuthibitisha rasmi katika mtandao wake wa Instagram. Tukio hilo linajiri wakati ambapo mchekeshaji huyo anazidi kuvutia mashabiki wengi katika sekta hiyo ya uchekeshaji huku wengi wakihoji ni nini haswa kilichosababisha kuvunjika kwa mahaba yao. Katika chapisho lake refu katika mtandao huo wa Instagram, Omondi ameandika kwamba anamtakia heri Grazioli huku akiendelea na awamu yake mpya ya maisha bila yeye huku akisisitiza kuwa mwanadada huyo alibadilisha maisha yake. ''Nilikutana nawe ukiwa na umri wa miaka 19.... Nimekuwa kwa miaka minne na nusu....tuliishi na kuwa na wakati mzuri zaidi katika maisha naye. Ulibadilisha maisha yangu kabisa....wakati unapoanza maisha yako mapya na mimi au bila mimi nakutakia heri mpenzi wangu. Njia iliotuleta pamoja sasa inatupeleka maeneo tofauti na unapoenda njia tofaut nakutakia heri katika maisha'', aliandika. Na kutokana na visa vingi vya uhalifu wa kimapenzi...Eric Omondi alitoa ushauri wa bure kwa wanaume kuhusu jinsi wanavyotakiwa kufanya kufuatia kuvunjika kwa mahusiano yao na wapenzi wao. ''Kwa wale vijana wanafikiria kuuana baada ya mapenzi kuisha , nataka hili liwe funzo kweny nyote. Hauwezi kum'miliki mpenzi wako na mara nyingine mambo huenda visivyo. Alielezea kwamba wote wako salama, baada ya kuwa marifiki mwanzoni. ''Nakuombea mungu kwamba atakulinda. Namuomba akuongoze.... nataka kukwambia kwamba...nitakuwepo kila utakaponihitaji wakati wowote na muda wowote. Unapoelekea mpenzi wangu nakuombea ung'are kama kama malaika ulivyo. Ntakuenzi kila mara...kila wakati. Wewe ni kitu bora zaidi katika maisha yangu!! Na kwa wale wadau wadaku, Mimi na Chantal hatuna tatizo . Sisi tulikuwa marafiki kabla ya kuwa wapenzi na urafiki wetu utasalia kwa maisha.." Na baada ya ujumbe huo mmoja wa mashabiki wake katika mtandao wa instagram walianza kutoa mawazo yao kufuatia hatua hiyo ya Eric Omondi Shabiki wake kwa jina Akotheekenya: Nakupenda kwa kweli , ndugu yangu , wapenzi wengi wanafaa kujua kwamba penzi haliishi na iwapo unampenda mwanchilie.... nalia machozi ya hisia tofauti. Mwengine kwa jina kansiime alisema: unafanya mapenzi kuwa mazuri zaidi Wengine walimwamba kwamba amekuwa akimpenda mwanadada huyo zaidi ya anavyompenda. Mchekeshaji maarufu Afrika mashariki Eric Omondi amewachana na mpenzi wake wa siku nyingi Chantal Grazioli. text: Ryan Mason akiwa chini baada ya kugongana kichwa na beki wa Chelsea Gary Cahill Mason aligongana kichwa na beki wa Chelsea Gary Cahill, katika dakika ya kumi na tatu ya mchezo wa ligi kuu England, na alipelekwa katika hospital ya St Mary's Hospital iliyoko jijini London, alikofanyiwa upasuaji huo. Taarifa iliyotolewa na klabu ya Hull City kiungo huyu ataendelea kuwa chini ya usimamizi wa madaktari kwa siku kadhaa Nahodha wa Hull City Michael Dawson, daktari wa timu Mark Waller, mkuu wa kitengo cha matibabu cha timu Rob Price, pamoja na mwenyekiti wa timu Matt Wild walimtembelea mchezaji huyo hospitalini. Nao wachezaji wa Chelsea Gary Cahill, John Terry, na kocha msaidizi wao msaidizi Steve Holland alikwenda kumjulia hali mchezaji huyo. Mchezaji kiungo wa Hull City Ryan Mason afya yake imeimarika na anaweza kuongea baada ya jana kufanyiwa upasuaji wa fuvu la kichwa. text: Ni wageni 200 pekee huruhusiwa kufika kisiwa hicho kila mwaka Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kiasi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema. Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi. Jopo maalum liliwasilisha pendekezo kwa Unesco watambue rasmi kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu mwezi Mei. Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini. Madhabahu hayo yalijengwa karne ya 17. Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema. Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigwa marufuku. Wageni wa kiume pia hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa. Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudiwa wakiwa kwenye kiswa hicho. "Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kitaorodheshwa kuwa turathi," anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii. Zamani, hata kabla ya madhabahu kujengwa, kisiwa cha Okinoshima kilikuwa kikitumika kwa matambiko na mabaharia na pia kilihusika katika mashauriano ya kibiashara kati ya watu wa Korea na watu wa China. Maelfu ya vitu vya kale, vilivyowekwa katika kisiwa hicho kama zawadi kutoka maeneo ya mbali, vimepatikana katika kisiwa hicho ikiwa ni pamoja na pete za dhahabu kutoka rasmi ya Korea, gazeti la Japan Times linasema. Kisiwa hicho kwa sasa hupokea wageni siku moja pekee, 27 Mei, na sheria za kale bado hufuatwa. Idadi ya wageni wanaoruhusiwa kufika kisiwa hicho kwa mwaka ni 200 pekee. Na lazima watimize matambiko yote baharini, na lazima wawe wanaume. Madhabahu ya Okitsu yalijengwa karne ya 17 na hutumiwa na mabaharia kufanya maombi Bado hakuna uwezekano kwamba marufuku dhidi ya wanawake itaondolewa. "Msimamo wetu kuhusu jinsia hautabadilika hata kama kitaorodheshwa kuwa Turathi ya Ulimwengu," afisa wa Munakata Taisha aliambia gazeti la Mainichi Daily, awali. "Tutadhibiti watu wanaozuru kisiwa hicho." Kisiwa cha Okinoshima nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kimetambuliwa kama Turathi ya Ulimwengu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Unesco. text: Mwezi wa Europa ni moja ya maeneo ambayo wanasayansi wanatafuta iwapo kuna viumbe wanaoishi anga za juu Wanasayansi waliripoti mara ya kwanza kuhusu kuwepo kwa maji katika mwezi huo kwa jina Europa mwaka 2013 baada ya kuufuatilia kwa karibu kwa kutumia darubini kwa jina Hubble. Sasa, wamethibitisha hilo baada ya kuitumia Hubble kuchunguza mwezi huo ulipokuwa unapita mbele ya sayari ya Jupiter (Mshtarii). Walitumia darubini hiyo kuchunguza nguvu za mionzi ya jua kuona ikiwa ilikuwa inamezwa na kitu chochote kutoka kwa mwezi huo. Walichunguza mara kumi, na mara tatu wakafuailia kilichoonekana kama "vidole vyeusi' vilivyokuwa vikitoka kwa Europa. Mtaalamu aliyeongoza uchunguzi huo William Sparks, anasema hawezi kufikiria kitu kingine kinachoweza kusababisha jambo kama hilo kando na maji. Michirizi hiyo ya inayoaminika kuwa ni ya maji ilionekana eneo ambalo miaka kadha iliyopita, wanasayansi waliokuwa wakitumia Hubble, waligundua oksijeni na haidrojeni, viungo vinavyounda maji. Ni hatua muhimu kwa sababu Europa, sehemu yake kubwa imefunikwa na bahari ya maji, na ni moja ya maeneo ambayo inaaminika huenda kukawa na viumbe wanaoishi anga za juu kando na dunia. Wanasayansi wanakadiria kwamba huenda wakaweza kuchota maji hayo na kuyafanyia uchunguzi kwa kupitisha chombo cha anga za juu kwenye michirizi hiyo. Njia nyingine, ambayo inausisha kupeleka chombo ambacho kitatua katika mwezi huo na kuchimba kilomita nyingi ndani ya barafu ili kufikia maji, huenda ikawa na changamoto nyingi sana. Michirizi ya maji ambayo ilionekana katika mwezi kwa jina Europa Michoro kwenye sehemu ya juu ya mwezi wa Europa, ambao umefunikwa pakubwa na barafu Michirizi ya maji imewahi kuonekana katika mwezi wa Enceladus, mwezi wenye barafu wa sayari ya Saturn (Sarteni). Chombo cha anga za juu cha Cassini kwa sasa kinazunguka sayari hiyo na tayari kimepitia katika michirizi hiyo kufanya uchunguzi. Hata hivyo, vifaa vya chombo hicho havina uwezo wa kuchunguza uwepo wa viumbe hai. Wanasayansi wanasema wamepata ushahidi kuwa mojawapo ya miezi inayozunguka sayari ya Jupiter imekuwa ikimwaga maji mengi anga za juu. text: Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote Bilionea huyo wa Nigeria awali alikuwa ameonyesha hamu yake ya kutaka kuinunua klabu hiyo ya kaskzini mwa London. Dangote anasema kwamba kwa sasa anaangalia maslahi mengine , lakini analenga mwaka ujao kuzindua ombi lake la kuinunua klabu hiyo kulingana na gazeti la Miror Uingereza. Mwezi Januari , alisisitiza, malengo yake akisema: Ni klabu ambayo kweli ningependa kuinunua siku zijazo, lakini kile ninachosema ni kwamba tuna miradi yenye thamani ya dolla bilioni 20 na hilo ndio ninaloaangazia kwa sasa. ''Ninajaribu kumaliza kujenga kampuni hiyo , halafu baada ya kumaliza pengine mwaka 2021 tutawasilisha ombi. Sitainunua Arsenal hivi sasa , nitainunua Arsenal nitakapomaliza miradi yote hii kwa sababu najaribu kuinua kampuni hiyo hadi kiwango chengine'', alisema Na sasa Dangote ameambiwa atakavyogharamika kuinunua klabu hiyo ya Premia na Bob Ratcliffe, ndguye mmoja wa watu matajiri zaidi nchini Uingereza Sir Jim Ratcliffe. Sir Jim amehusishwa na ununuzi wa klabu ya Chelsea kwa miaka kadhaa sasa, lakini mwezi Agosti uliopita kampuni yake Ineos ilikamilisha makubaliano ya kuinunua klabu ya Nice badala yake. Nduguye Bob, ambaye ndiye mkuu wa soka katika Ineos amefichua itagharimu fedha ngapi kuinunua klabu ya ligi ya Premia. Bob aliamnbia gazeti la Financial Times kwamba ununuzi wa klabu sita kuu utagharimu sio chini ya £2bilioni. Thamani ya Aliko Dangote Katika ripoti ya Forbes 2020 mfanyabiashara tajiri nchini Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa kwa mara ya tisa mfululizo, kuwa mtu tajiri zaidi barani Afrika . Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara ya Simiti, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1. Wakati huohuo , ununuzi wa timu nyenegine nje ya ligi ya Premia utagharimu kati ya £150m na £350m. Aliongezea: 'vyote vinauzwa'. Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote hatimaye amepatiwa bei ya kuinunua klabu ya Ligi kuu ya England Arsenal. text: Kim Jong-un mapema Januari alisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na Korea Kusini Matamshi ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Taro Kono huko Canada, yanakuja huku Korea Kaskazini na Kusini wakijadili mipango ya Korea Kaskzini kushiriki mashindano ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini. Mawaziri 20 wa mashauri ya nchi za kigeni huko Vancouver walikubaliana kuongeza shinikizo didi ya Korea Kaskazini. Lakini waliunga mkono mazungumzo yanayoendelea kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Kwa miaka miwili iliyopita Korea Kaskazini kwa haraka iliboresha programu yake ya makombora licha ya kuwepo vikwazo vya kimataifa. Jaribio la mwisho la kombora la masafa marefu la tarehe 28 Novemba lilizua awamu mpya ya vikwazo kutoka kwa Umoja wa Mataifa ambavyo vililenga uagizaji wa mafuta na usafiri. Lakini kiongozi wa Korea Kim Jong-un mapema Januari alisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na Korea Kusini na kupendekeza kutuma timu kwa mashindano huko Pyeongchang mwezi ujao. Japan yaonya kuhusu urafiki ambao umeonekana kutoka Korea Kaskazini Japan imeuambia mkutano wa kimataifa kuhusu Korea Kaskazini kuwa dunia isifumbwe macho na urafiki amabo umeanza kuonekana kutoka kwa Korea Kaskazini. text: Kiongozi wa kamati hiyo ya maandalizi ya michezo hiyo itakayofanyika mwaka 2024 anasema kutambulisha mashinda ya kucheza muziki katika mtindo wa 'breakdance' pamoja na mchezo wa kuteleza na kuruka,utafanya mashindano hayo kuvutia zaidi. Mwanzo wa muziki wa 'breaking' Aina hiyo uchezaji huu ilianza mwaka 1970 huko New york. Muziki huu una midundo ambayo yanawavutia vijana na ina asili ya Latino. Mchezo huu ambao unahitaji mtu kutumia viungo vyake kucheza na nguvu pia hutumika. Wachezaji wa 'Breakdancers' New York City, 1981 Miondoko hii ya muziki ambayo imedumu tangu miaka ya 1980 na kuendelea kupendwa mpaka sasa. Namna gani uchezaji wa breaking unaweza kufanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki? Kama kamati ya kimataifa ya Olimpiki itakubali kuwa mashindano ya mwaka 2024 , mchezo huu unaopendwa na vijana unaweza kuleta mafanikio makubwa. Mashindano ya mwaka 2018, uligawa wachezaji wanawake na wanaume pamoja na kuchanganya wachezaji wanawake wanaume na wanaume. Taarifa nyengine kuu: Majaji wataangalia nini? Vigezo ambavyo mashindano ya Olimpiki wataangalia ubora wa mchezaji na uchezaji wake. Mashindano ya kucheza muziki aina ya 'breakdance' yatakuwa miongoni mwa michezo iliyopendekezwa na kamati ya kimataifa ya Olimpiki. text: Muonekano wa kituo cha Hotan kupitia uzio wa waya Mamia ya watu pia wanazuiliwa katika kambi kubwa huku mpango wa kujenga shule ya bweni ukiendelea. Kulingana na stakabadhi za umma zilizofuatiwa na mahojiano kadhaa ya familia zinazoishi ughaibuni BBC, imepata ushahidi mkubwa kufikia sasa kuhusu kile kinachofanyiwa watoto katika eneo hilo. Rekodi zinaonesha kuwa watoto 400 wametenganishwa na wazazi wao iwe ni kufungiwa katika kambi au jela. Ukaguzi unafanywa kubaini ikiwa watoto hao wanahitaji ''uangalizi maalum". Shule ya chekechea ya Hotan sawa na zingine hupewa ulinzi Kutokana na udhibiti mkali wa salama wa eneo la Xinjiang,wanahabari wa kimataifa wanafuatiliwa saa 24 hali ambayo inakuwa vigumu kusema na wahasiriwa. Lakini baadahi yao wanapatikana nchini Uturuki. Katika ukumbi mmoja mkubwa mjini Istanbul, makumi ya watu wanapanga foleni wakiwa wameshikilia picha za watoto wao zinazosimulia jinsi walivotoweka nyumbani. "Sijui ni nani anawatunza," mama mmoja alisema huku akionesha picha ya binti zake watatu wadogo, "hauuna mawasiliano kabisa." Mama mwingine aliyekuwa ameshikilia picha ya watoto wake watatu wa kike na mmoja wa kiume analia akisema: "INasikia kuwa wamepelekwa katika kituo cha kulea watoto," Katika mahosjiano 54 tofauti wazazi wamesimulia jinsi watoto wao zaidi ya 90 walivyopotea Xinjiang. Wote ni wanatokea jamii ya Uighurs - na wengi wao ni waumini wa dini ya kiislamu ambao wamekuwa na ushirikiano mkubwa wa kidini na taifa la Uturki Maelfu yao wako nchini humo kwa masomo, kufanya biashara, kutembelea familia zao au wametoroka sera ya Uchina ya uzazi wa mpango na ukandamizaji wa kidini. Lakini miaka mitatu iliyopita wamejikuta mashakani baada ya China kuanza kuwakamata mamia ya watu wa jamii ya Uighur na kuwazuilia katika kambi maalum. Mamlaka za China zinasema kuwa watu wa jamii ya Uighurs wanapewa elimu katika "vyuo vya kiufundis" ili kukabiliana na itikadi kali za kidini. Lakini ushahidi unaonesha kuwa wengi wao wanafungiwa katika vituo hivyo ili kuwazuia kufuata muongozo wao wa kidini kama vile kusali na kuvaa nguo zinazoashiria misimamo yao ya kidini au kuwazuia kusafiri mahali kama Uturuki. Kutokana na hali hizo kwa watu wa Uighurs, kurudi nyumbani kunamaanisha kwenda kuzuiliwa katika vituo hivyo. Nambari zao za simu zimenakiliwa - kumaanisha hata kuzungumza na jamaa wako aliye nje ya nchi ni hatari katika mji wa Xinjiang. Mtu mmoja ambaye mke wake amefungiwa aliiambia BBC kuwa anahofia huenda watoto wake wanane wako mikononi mwa serikali. "Nadhani wanasomeshwa katika vituo hivyo" alisema. Utafiti mpya uliofadhiliwa na BBC unaangazia kile wanachofanyiwa watoto hao na maelfu ya wengine. Dr Adrian Zenz ni mtafiti wa Ujerumani ambaye alisifika sana kwa kufichua jinsi China imekuwa ikiwazuilia waumini wa dini ya Kiislamu mjni Xinjiang. Kulingana na maelezo yalio wazi kwa umma na ripoti yake inaashiria kuna mpango wa kupanua shule katika eneo la Xinjiang. Jimbo hilo limekua likiimarisha juhudi zake ili kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya watoto wanaozidi kuongezeka. Katika kipindi cha mwaka mmoja idadi ya watoto wanaojiunga na shule za chekechea katika Jimbo la Xinjiang imeongezeka kwa zaidi ya nusu milioni. Watoto kutoka jamii ya Uighur na waislamu wengine wanakadiria 90% ya ongezeko hilo. Kutokana na hilo kiwango cha watoto wanaojiunga na shule hizo imeongezeka na kupita kiwango kilichowekwa na serikali. Katika eneo la Kusini mwa Xinjiang, amabko kuna idadi kubwa ya watu wa Uighur, mamalaka imejenga vituo vipya vya watoto kwa thamani ya dola bilioni $1.2. China imekuwa ikiwatenganisha kimakusudi watoto wa Kiislamu na familia zao, dini na lugha yao katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa utafiti mpya. text: Santillan alikuwa bingwa wa zamani wa uzani wa feather Bondia huyo mwenye umri wa miaka 23 alizirai katika ukumbi siku ya Jumamosi baada ya pigano lake la ukanda wa WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu nchini Argentina kuisha kwa sare. Alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini akafariki siku ya Alhamisi. ''Lala kwa amani, Hugo Santillan'' ,alisema afisa wa ukanda wa WBC katika ujumbe wake wa Twitter. Santillan ni bondia wa pili kufariki kutokana na majeraha aliyopata katika ulingo wa ndondi wiki hii baada ya kifo cha Dadashev kuthibitishwa siku ya Jumanne. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 alipelekwa hospitalini akitokwa na damu katika ubongo baada ya pigano lake la IBF ukanda wa Welterwieght dhidi ya Subriel Matias kusimamishwa mwisho wa raundi ya 11 Ijumaa iliopita. Alifanyiwa upasuaji wa dharura lakini ukafeli. Bondia wa Argentina Hugo Santillan amefariki kutokana na majeraha aliyopata katika pigano , siku chache baada ya kifo cha bondia wa Urusi Maxim Dadashev. text: Barabara za Mogadishu mara nyingi zina magari mengi Waandishi wa habari wanasema kuwa shule nyingi na maofisi yamesalia yamefunguliwa lakini watu walilazimika kutembea ili kufika maeneo yao. Wabunge watakusanyika kwenye uwanja wa ndege siku ya Jumatano kumchagua rais mpya,. Kumekuwa na hofu kuwa kundi la wanamgambo la al-Shabab ambalo limeendesha mashambulizi mengi mjini Mogadishu, huenda likavuruga uchaguzi huo. Uwanja wa ndege unaonekana kama eneo salama zaidi kwenye mji mkuu wa Mogadishu na uchaguzi ulihamishiwa huko kutoka kwa taasisi ya polisi kutokana na wasi wasi wa kiusalama. Hatua za kiusalama za siku ya Jumatano zinahusu marufuku kwa safari za ndege kutoka uwanja wa Mogadishu. Zaidi ya wagombea 20 wanawania wadhifa wa Rais. Rais wa sasa Hassan Sheikh Mohamud, anawania tena na wadadisi wanasema kuwa ni mmoja wa wale watakaosonga mbele kuwania katika duru zingine, Marufuku ya magari imetangazwa kwenye barabara kuu za mjini Mogadishu nchini Somalia, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais kesho Jumatano. text: Shirika la ndege ya Air Tanzania lilitakiwa kuwa safari zake zitarejea siku ya Ijumaa tarehe 6 kuelekea Afrika Kusini mara baada ya ndege yake iliyozuiliwa Agosti 23, 2019 kuachiwa kwa amri ya mahakama na kurudi Tanzania. Lakini kutokana na hali ya usalama nchini humo kutokuwa nzuri, safari hizo zimesitishwa kwa muda. "Tutasitisha kwa muda usafiri wa ndege hadi serikali itakapofanya mawasiliano na nchi hiyo kwa maandishi kuhakikisha usalama wa abiria na chombo chetu. Hatuwezi kuwapeleka abiria kwenye nchi yenye fujo. Tutawapa taarifa hali itakapotulia," amesema Kamwelwe katika gazeti la Mwananchi. Hatua hiyo inajiri baada ya Afrika Kusini kufunga ubalozi wake nchini Nigeria , huku nalo taifa hilo likifunga vituo vyake vya biashara vilivyopo Afrika Kusini Waziri wa maswala ya kigeni nchini Afrika Kusini alitaja ghasia hizo kuwa aibu kwa taifa lake. "Serikali yetu inajutia ghasia dhidi ya maduka yote yanayomilikiwa na wageni ama Waafrika katika mataifa mengine wanaoishi nchini Afrika kusini, kilisema chombo cha habari cha SABC kikimnukuu waziri Naledi Pandor. Alikuwa ameagiza kufungwa kwa ubalozi wa taifa lake katika mji mkuu wa Abuja na Lagos kufuatia vitisho vilivyowalenga wafanyikazi wake wa kidiplomasia , bi Pandor aliambia Reuters. Nchini Zambia , kituo maarufu cha redio kimesema kuwa hakitapiga tena muziki wa Afrika kusini kupinga mapigano ya ubaguzi ambayo yanaendelea Afrika Kusini . "Hot FM imesitisha kupiga muziki aina yoyote ulioimbwa na msanii wa Afrika Kusini," Kituo hicho kimeandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Facebook. "Mataifa yote ya Afrika yalisimama mstari wa mbele kuisaidia Afrika Kusini walipokuwa na shida," redio hiyo ilisema ikinukuu Umoja wa Afrika. Wakati wa mapigano dhidi ya ubaguzi wa rangi , makao ya chama tawala cha Afrika Kusini(ANC) yalikuwa Zambia . "Afrika ni moja ingawa sasa wenzetu Afrika Kusini ndio wameamua kuleta ubaguzi tena, Tunapinga uvamizi wa chuki za kibaguzi dhidi ya ndugu zetu unaoendelea katika katika nchi hiyo ." Siku ya Jumatano , maduka kadhaa katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka yalifungwa wakati wanafunzi walipoingia barabarani kuandamana kupinga vurugu zinazoendelea Afrika Kusini, Chama cha mpira wa miguu kilisitisha mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini ambayo ilitarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi mjini Lusaka. Mara baada ya vurugu hizo kutokea Afrika Kusini imefunga ubalozi wake katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja na kufunga vituo vyake vya biashara vilivyopo Afrika kusini Raia wa Nigeria ndio walihusishwa zaidi katika ghasia za ubaguzi wa wageni mara baada ya ghasia za ubaguzi zilipoanza mjini Johanesburg. "Baada ya kupata taarifa za vitisho kutoka kwa wanaijeria , hivyo tuiamuka kufunga kwa muda mpaka hali itakaporejea kuwa shwari," AFP ikimnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lunga Ngqengelele Mpango wa kidiplomasia ulimalizika siku ya jumatano, waziri alisema. Takriban watu 423 wamekamatwa kufuatia ghasia za uporaji kote mjini Johannesburg a na jimbo hilo , kwa mujibu wa maafisa. Raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini wamepewa ofa ya ndege za bure kurejea nyumbani kukwepa vurugu za kibaguzi zinazoendelea Afrika Kusini. Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeri imesema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa. "Wote watakaotaka huduma hiyo wanashauriwa kuwasiliana na Ubalozi wa Nigeria jijini Pretoria na ofisi ndogo za ubalozi jijini Johannesburg jwa matayarisho muhimu," taarifa ya wizara imeeleza. Huko Jamuhuri ya Kidemokrasi ya kongo pia maandamano yanafanyika mjini Kinshasa kupinga ghasia za uporaji dhidi ya raia wa kigeni. Raia hao wa DRC wanasema kwamba kile kinachoendelea Afrika Kusini sio kitu kizuri kabisa ndio maana wamea mua kwenda kwenye ubalozi wa nchi hiyo kuonyesha hisia zao. "Si kweli kwamba ndugu zetu wanaoishi Afrika Kusini wanaoiba kazi zao, hiyo sio kweli kabisa. Tunawaomba waache wanachokifanya sisi wote ni ndugu. Sheria yao inaruhusu watu wafanye kazi kwao, hawapasi kutufanyia sisi hivyo sisi ni ndugu na tuliwasaidia sana Afrika Kusni wakati wanapambana na ubaguzi wa rangi, nchi zote za Afrika zilisaidia, kwa nini sasa iwe hivi..." alisema raia mmoja wa DRC. Maandamano Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mwaka 2007 baadhi ya raia wa Kisomali walijihami dhidi ya uvamizi wowote wa Wageni mjini Pretoria katika eneo la Marastabad nchini Afrika Kusini. Kundi hilo lilikuwa linakabiliana na kundi jingine la raia wa Afrika kusini lililoongoza ghasia dhidi ya wahamiaji. Makundi ya wahamiaji waliiojihami nchini Afrika Kusini Hatahivyo maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwatimua kwa kutumia ndege aina ya helikopta pamoja na risasi za mipira. Makundi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini Takriban watu wawili walijeruhiwa na risasi hizo za mipira wakati polisi walipokuwa wakitawanya maandamano dhidi ya wageni nchini humo. Mpiga picha mmoja alipigwa risasi mbili za mipira mgongoni alipokuwa akirudi nyumbani kutoka shule. Maafisa wa polisi wawatawanya waandamanaji Afrika Kusini Licha ya Bwana Mashaba kusema kuwa ghasia hizo hazina nafasi katika taifa hil,o wanaharakati wa shirika hilo wanadai kuwa matamshi yake kwamba wahamiaji nchini humo ndio wanaohusishwa na uhalifu ndio yaliosababisha ghasia hizo. Serikali ya Tanzania imesitisha kwa muda huduma ya usafiri wa ndege zake nchini Afrika Kusini hadi hali ya usalama nchini humo itakapotengamaa. text: Chatu anaweza kuwa hadi urefu wa mita 10 Licha ya visa kama hivyo kuwa vichache hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha mtu kuliwa na chatu nchini Indonesia kwa takriban mwaka mmoja. Ni kipi kilimpata mwanamke huyo? Wa Tiba, 54, alitoweka Alhamisi iliyopita wakati akiwa kwenye shamba lake la mboga katika kisiwa cha Muna mkoa wa Sulawesi. Shughuli kubwa ya kumtafuta ilifanywa na wakaazi wa eneo hilo. Viatu vyake na upanga vilipatikana siku moja baadaye huku chatu aliyekuwa na tumbo lililofura akipatikana mita 30 kutoka eneo hilo. Wenyeji walishuku kuwa nyoka huyo alimuua, kwa hivyo wakamuua na kumtoa shambani. Tumbo la nyoka huyo lilipasuliwa na mwili wa mwanamke huyo ukapatikana ndani. Picha za kutisha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Indonesia zikionyesha mwili wa mwanamke huyo ukitolewa tumboni mwa chatu huyo mbele ya umati mkubwa. Chatu wanashambuaje? Chatu wa sulawesi wanaweza kukua hadi urefu wa miaa 10 na wana nguvu sana, Wanashambulia kwa kuvizia, wakijifungia kwa windo lao na kulivunja kwa kufinya hadi kuua. Chatu anaweza kuwa hadi urefu wa mita 10 Wakati unapowadia kuwala binadamu, kizuia huwa na mabega ambayo hayawezi kuvunjika. Mary-Ruth Low mtunzaji wa mbuga za wanyamapori huko Singapore ni mtaalamu wa chatu aliambia BBC. Wanakula wanyama wakubwa? Kawaida chatu hula panya na wanyama wengine wadogo, lakini mara wanapofikia ukubwa fulani hukosa hamu ya kula panya tena kwa sababu ni wadogo sana. Sasa wao huanza kuwalenga wanyama wakubwa kama nguruwe au hata ng'ombe. Mwili ukitolewa kwenye tumbo la chatu Mwaka uliopita mwanamume mmoja mkoani Sumatra nchin Indonesia alifanikiwa kumshinda nguvu chatu mwenye urefu wa mita 7.8 ambaye alikuwa amemshambulia kwenye shamba lake. Alinusurika na majeraha mabaya. Mwanamke mmoja nchini Indonesia ameuawa na kumezwa mzima mzima na chatu mwenye urefu wa mita 7. text: Uchaguzi wa Marekani utafanyika siku ya Jumanne ya Novemba 8, 2016 Amesema kuwa matamshi ya wagombea wote wawili wakati wa midahalo yote ni ushahidi wa uvunjifu wa thamani ya binadamu nchini Marekani. Ameonya kudhibiti siasa nchini Iran dhidi ya makubaliano ya moja kwa moja na Marekani kwa jambo lolote. Katika hotuba tofauti Rais Hassan Rouhani ameelezea kuwa chaguo lililombele ya raia wa Marekani kuwa ni baya na chafu. Na aliyekuwa Rais wan nchi hiyo Akbar Hashemi Rafsanjani amemuelezea Donald Trump kuwa ni mtu hatari. Wairani wanaona kwamba kama Trump atashinda basi itakuwa ni vilio kuhusu makubaliano ya Nuklia na nchi zenye nguvu duniani, na kuanzishwa tena kwa vikwazo. Kiongozi mkuu wa Irani Ayatollah Ali Khamenei, amedharau mwenendo wa kampeni za urais Marekani. text: Kanda ya video iliomuonyesha mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles Kanyi maarufu Jaguar akitishia kuwafukuza raia wa kigeni aliowatuhumu kuchukua biashara za Wakenya ilisambaa katika mitandao ya kijamii nchini humo siku ya Jumanne. ''Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine. Raia wa Pakistan wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote'', alinukuliwa akisema. Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, matamshi hayo hayakupokelewa vyema katika bunge la Jamhuri ya Tanzania, huku Mbunge wa Rufiji kupitia chama cha CCM Mohammed Mchengerwa akimtaka spika kutoa uongozi kuhusu umuhimu wa serikali ya taifa hilo kutoa taarifa kuhusu usalama wa raia wa Tanzania ambao wanaishi na kufanya kazi pamoja na biashara nchini Kenya. Gazeti hilo lilimnukuu spika wa bunge hilo akiagiza serikali kutoa taarifa kuhusiana na hilo huku waziri mkuu Kassim Majaliwa akisema kuwa serikali ililichukua swala hilo na umuhimu mkubwa na kumtaka balozi wa Kenya nchini Tanzania kujieleza. ''Tulimuita mjumbe wa Kenya nchini Tanzania. Pia tulizungumza na mjumbe wa Tanzania nchini Kenya. Mwanadiplomasia huyo wa Kenya alisema kuwa lilikuwa tamshi la kibinafsi ambalo halikuhusishwa na msimamo wa serikali ya Kenya. Aliahidi kwamba serikali itamuhoji mbunge huyo kuelezea kile alichomaanisha katika matamshi yake'', alisema Majaliwa. Huku akiwataka raia wa Tanzania kuwa watulivu kufuatia ombi la mwanadiplomasia huyo wa Kenya , bwana Majaliwa alisema kuwa taarifa hiyo pia ilikosolewa na wabunge wa bunge la Afrika mashariki ambao walikuwa wakifanya kikao mjini Arusha. ''Sisi kama Watanzania tuendeleeni kuishi na amani na Wakenya hatuna matatizo nao'', alisema. Kulingana na gazeti hilo bwana Majaliwa aliwataka raia wa Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi pamoja na Sudan Kusini kutokubali kutoa matamshi ambayo yanakiuka makubaliano ya umoja wa Afrika mashariki. Tayari serikali ya Kenya kupitia msemaji wake kanali mstaafu Cyrus Oguna imetoa taarifa yake ikisema kuwa matamshi ya mbunge huyo ni ya kibinafsi na kwamba sio msimamo wa serikali ya Kenya. '' Tungependa kusema kuwa huo sio msimamo wa serikali ya Kenya na tunashutumu matamshi hayo yaliotolewa katika kanda hiyo ya video. Matamshi hayo hayafai katika ulimwengu wa sasa'', alisema Oguna. ''Wakenya ni wapenda amani ambao kwa miaka mingi wameishi na raia wengine wa kigeni bila tatipo lolote. Hii ni thamani ambayo tunajivunia kama taifa na ni lazima tuendelea nayo'', ilisema taarifa hiyo iliotiwa saini na msemaji huyo wa serikali. Taarifa hiyo imesema kuwa serikali ya Kenya inachukulia yaliomo katika kanda hiyo na umuhimu mkubwa na tayari imeanza kuchukua hatua kali za kisheria. Aidha serikali ya Kenya imewahakikishia raia wote wa kigeni na wale walio na hamu ya kutaka kuwekeza nchini humo kuhusu usalama wao pamoja na mali yao. Awali gazeti la The Citizen nchini Tanzania liliandika kwamba wabunge walitoa matamshi dhidi ya mbunge huyo wa Kenya huku wakisubiri serikali kutoa msimamo wake rasmi na wakati mmoja spika wa bunge Job Ndugai alisema kuwa matamshi hayo ya Jaguar hayawezi kuwa msimamo wa serikali ya Kenya. ''Tusilichukulie hili kuwa sawa''. ''Iwapo kuna taifa katika jangwa la sahara barani Afrika ambalo raia wake wanapatikana kwa wingi katika kila taifa na zaidi , basi taifa hilo ni Kenya'', alisema kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe. Karibu kila mbunge ambaye alijadili swala hilo alimkosoa Jaguar, akisema matamshi yake hayafai na kwamba serikali ya Kenya ilihitajika kutoa taarifa ya kumshutumu. Serikali ya Tanzania imewarai raia wake kuwa watulivu kufuatia matamshi ya mbunge mmoja wa Kenya aliyewatishia wageni wanaoishi nchini humo ikiwemo raia wa Tanzania. text: Odion Ighalo aliondoka Watford na kwenda China mwaka 2017 Makubaliano ya kumsajili mchezaji wa kimataifa Ighalo, 30, Old Trafford inakuwa haina chaguo jengine zaidi ya kumnunua. Ighalo, ambaye bado yuko China anatarajiwa kusafiri kwenda Uingereza ndani ya siku chache zijazo, alifunga mabao 39 katika mecho 99 alizocheza Watford kati ya mwaka 2014 na 2017. "Odion ni mchezaji mwenye tuzoefu mkubwa," amesema mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer. "Ataingia na kuongezea idadi ya washambuliaji tulionao katika kipindi kifupi atakachokuwa nasi.'' "Mchezaji mahiri sana katika kazi yake, atakuwa na manufaa makubwa hapa." alisema Solskjaer. Odion Ighalo ni nani? Ighalo alijunga Super League ya China mwaka 2017, kwanza akiwa na timu ya Changchun Yatai. Baada ya misimu miwili, akajiunga na timu ya Shanghai Shenhua na kufunga mara 10 katika mechi 19 ambazo alishiriki. Aidha,Odion Ighalo alikuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la Afrika kwa kufunga mabao 7 kabla ya kufunga matano katika mashindao ya msimu wa joto. Inafahamika kwamba klabu za ligi nyengine za Premier pia zilikuwa zimeonesha nia ya kumsajili Ighalo lakini mwenye alitaka kucheza na United. Ighalo ni mchezaji wa waknza kusajili kwa mkopo wa aina hiyo tangu kuwasilis kwa Radamel Falcao kutoka Monaco mwaka 2014. Ighalo (kushoto) alipigwa picha akiwa amevalia fulana ya Manchester United wakati akiwa mtoto Mapema Ijumaa, United ilifunga mpango wake wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth, Josh King badala yake ikamchukua mlinda lango Nathan Bishop kwa kima cha pesa ambacho hakikuwekwa wazi. United kumkubali Ighalo haku wendani na sera ya United ya kusajili wachezaji kwa muda mrefu kama vile Bruno Fernandes, aliyahamia Old Trafford kutoka Sporting Lisbon Alhamisi. Hata hivyo, hatua hii imechukuliwa ili kuziba pengo la Marcus Rashford aliyepata jeraha na United haingeweza kumaliza msimu bila ya kutafuta mtu atakayechukuanafasi yake. Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Rashford, 22, amekuwa nje kwasababu ya jeraha alilopata mgongoni baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba wakati wa Kombe la FA dhidi ya Wolves Januari 15. Mwaka uliopita, Odion Ighalo alikataa ofa ya Barcelona Mwandishi wa BBC John Bennett: Mwaka 2015 baada ya timu ya Watford kupandishwa daraja, Ighalo aliulizwa iwapo angependa kujiunga na timu gani katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi ya Premier. Bila kusita: "Old Trafford. Itakuwa ni ndoto iliyotimia iwapo nitakuja kucheza dhidi ya Manchester United, timu niliyokuwa naishabikia nikiwa kijana". Hakuwa na ufahamu wa kile kitakachotokea miaka 5 baadae. Odion anajishirkisha kwa kiasi kikubwa tu na masuala ya kusaidia wengine nchini Nigeria na bado ni mshambuliaji mwenye kipaji. Hatua iliyochukuliwa na United sio ya kawaida na nina uhakika kwamba mumesoma na kusikia mambo mengi yenye mtazamo hasi na ili kuwa na uwiano acha na mimi niwape yenye mtazamo chanya: Ighalo ni mchezaji namba 9 kwa kipaji cha kizaliwa na mfungaji magoli mwenye kasi na nguvu. Barcelona ilijaribu kumsajili miezi 12 iliyopita kwasababu walitaka mchezaji wa aina hiyo lakini akakataa ofa yao. Odion Ighalo ni mchezaji mahiri na mwenye kuhimili changamoto. Nchini Nigeria alikosolewa vikali baada ya kukosa nafasi za kufunga kama mchezaji wa Super Eagles ambapo timu hiyo ilibanduliwa na Argentina katika mashindano ya kombe la Dunia mwaka jana lakini alipita jaribu hilo na kulimaliza akiwa mshindi zaidi baada ya kuwa mfungaji bora sio tu kwa Mashindano ya Kombe la Afrika bali pia katika mchezo wenyewe na kuwapiku wachezaji wengine mahiri kama vile Sadio Mane, Mohamed Salah na Riyad Mahrez. Bila shaka ni mchezaji atakaye pambana kuhakikisha anakuwa na mafanikio makubwa ndani ya United. Pia, kujiunga kwake United ni sawa na kurejea nyumbani kwasababu familia ya Ighalo imekuwa ikiishi Manchester. Na hatua hii ni historia kubwa kwa mashabiki wa United kutoka Lagos. Sasa wakati umewadia wa kuona ikiwa kwa mara ya kwanza katika taaluma yake, atadhihirishia umma kuwa anaweza. 'Ni shabiki wa United tangu akiwa mtoto Mwandishi wa Nigeria Oluwashina Okeleji: Miaka 5 baada ya mashabiki wa soka Nigeria kushuhudia kushindwa kwa mchakato wa kumsajili John Mikel Obi katika timu ya Manchester United, raia wa nchi hiyo hatimaye wana fursa ya kumshuhudia mchezaji wao mwenyewe akichezea timu ya Red Devil. Akiwa na umri wa miaka 30, Odion Ighalo amekuwa mchezaji wa kwanza wa timu ya Super Eagle kujiunga na Old Trafford. Ighalo akiwa alizaliwa katika eneo maskini la, Ajegunle, amekuwa shabiki wa United tangu akiwa mtoto. Mashabiki wa taifa hilo la magharibi mwa Afrika, wanafuatilia kwa karibu Ligi ya Premier, ambayo imesajili baadhi ya wachezaji wazuri kutoka bara la Afrika. Manchester United imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Watford Odion Ighalo kutoka Shanghai Shenhua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. text: uchaguzi huo umetazamwa kote duniani Wakati wa kipindi cha miaka minne iliopita , uhusiano wa Marekani na ulimwengu ulibadilika ghafla. Wanahabari wa BBC duniani , kutoka Beijing hadi Berlin , wanaelezea jinsi habari za ushindi wa Joe Biden zilivyopokelewa na maana yake kwa mahusiano muhimu ya Marekani. Joe Biden anatoa changamoto mpya kwa serikali ya China aliandika mwandishi John Sudworth mjini Beijing. Unaweza kufikiria kwamba Beijing ingelifurahia sana iwapo Donald Trump angeshindwa. Alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele kuikashifu China mara kwa mara na kuiwekea vikwazo kadhaa mbali na kuilaumu kwa virusi vya corona. Lakini wachambuzi wanasema kwamba uongozi wa China huenda sasa unahisi kutofurahishwa na kushindwa kwake , Sio kwasababu wanampenda bali kwasababu alikuwa anaiharibu Marekani kwa kuwa mgawanyaji nyumbani na kuharibu uhusiano wake na mataifa mengine. China ilidhani kwamba muhula mwengine wa Trump ungeliporomosha uchumi wa Marekani na kusababisha kuanguka kwa uwezo wake. Mizizi ya Kamala Harris ni chanzo cha majivuno kwa India ;lakini Narendra Modi huenda akawa na uhusiano usio mzuri na Joe Biden ikilinganishwa na mtangulizi wake anasema. Rajini vaidnathan kutoka Delhi. India imekuwa mshirika mkubwa wa Marekani na kwamba uhusiano huo hautabadilika chini ya Uongozi wa Biden Hatahivyo uhusiano kati ya viongozi hao wawili huenda ukachukua mweleko usio wa kawaida. Bwana Trump amekuwa akizuia kuzikosoa sera zenye utata za Modi ambazo wengi wanasema zimekuwa zikiwabagua Waislamu. Lakini bwana Biden amekuwa wazi , Tovuti yake ya kampeni imekuwa ikitaka haki kupatiwa raia wa Kashmir . Korea kaskazini ambayo kuna wakati ilimuita Joe Biden 'mbwa koko', lakini sasa Kim jong un atalazimika kufanya hesabu zake vizuri kabla ya kumchokoza rais huyo mpya kulingana na mwandishi Laura Bicker mjini Seoul. Ni wazi kwamba Kim angependelea tena muhula mwengine wa miaka minne ya rais Donald Trump. Mikutano ya viongozi hao wawili ilileta picha za kihistoria lakini hakuna kikuu kilichoafikiwa. Hakuna hata pande moja iliopata kile ilichokuwa ikitarajia. Korea Kaskazini imeendelea kujenga silaha za kinyuklia na Marekani imeendelea kuiwekea vikwazo. Badala yake Joe Biden ametaka Korea kaskazini kuonyesha kwamba ipo tayari kuwacha utengenezaji wa silaha za kinyuklia kabla ya kufanya mikutano yoyote na Kim Jong un. Wachambuzi wanasema kwamba iwapo rais Biden hatoanzisha mazungumzo ya haraka na kiongozi huyo huenda hali ya chuki kati ya mataifa hayo mawili ikarejea. Kim jong un huenda akataka kuilazimisha Marekani kurudi katika meza ya mazungumzo kupitia majaribio ya makombora yake. Moscow inahofia kwamba Biden ataiwekea shinikizo na vikwazo zaidi . Huku mgombea wa Democrat akiingia Ikulu ya Whitehouse je ni wakati wa kulipa kisasi cha Urusi kuingilia uchaguzi wa 2016? Ushindi wa Biden unaweza kuirudisha Iran katika meza ya majadiliano anaandika mwandishi wa BBC Persia Kasra Naji. Wiki chache kabla ya uchaguzi wa Marekani , rais Trump alisema kwamba atakapochaguliwa kwa muhula wa pili simu ya kwanza atakayopokea itakuwa kutoka kwa Iran ikitaka waanze mazungumzo mapya kuhusu mipango yake ya kinyuklia. Hatahivyo mazungumzo yoyote na rais Trump yasingefanyika . Chini ya uongozi wa Trump vikwazo vya Marekani vimeiwacha Iran kukaribia kuanguka kiuchumi. Pia aliagiza kuuawa kwa jenerali Qasem Soleimani rafiki wa karibu wa kiongozi wa kidini wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei. Kuna matumaini ya mabadiliko ya kisera za rais Donald Trump katika eneo la mashariki ya kati. Anaandika mwndishi Tom Bateman mjini Jerusalem. Rais Trump aliwapendelea sana washirika wake katika eneo hilo huku akiitosa Iran. Rais Mteule Biden atajaribu kurudisha sera za Marekani katika eneo hilo ilivyokuwa wakati akiwa makamu wa rais wa Marekani chini ya rais Obama. Akipunguza shinikizo kali dhidi ya Iran na kurudisha makubaliano ya amani ya nyuklia yaliofutiliwa mbali na Trump miaka miwili iliopita. Hali hiyo itaikasirisha Israel na mataifa ya mashariki ya kati kama vile Saudia na UAE. Waziri mmoja wa Israel alisema akijibu ushindi wa Biden kwamba sera hiyo itaisha na vita kati ya Israel na Iran kwasababu 'tutalazimika kuchukua hatua'. Baada ya siku kadhaa za hali ya wasiwasi , Joe Biden ameshinda uchaguzi wa Marekani. text: Kifedha msanii huyo wa muziki wa bongo anamiliki mali Tanzania mbali, biashara zilizofanikiwa, na ameteuliwa na kushinda mataji kadhaa ya kimataifa kama vile BET na MTV. Ushawishi wa msanii huyo unaweza kupimwa na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii: Kwa mfano ana mashabiki milioni 4.8 katika mtandao wa Instagram, milioni 2.5 katika mtandao wa facebook na milioni 1.3 katika mtandao wa Youtube mbali na wafuasi elfu 574 katika mtandao wa Twitter. Na hivi majuzi msanii huyo wa wimbo 'Iyena' na 'sikomi' alichapisha orodha ya watu waliokuwa kiungo muhimu katika ufanisi wake. Alimuorodhesha mamake Sanura Kassim, AY TID, Dully Sykes, Jay Z , P Diddy, Usher Raymond miongoni mwa wengine kama watu waliochangia sana katika kukuwa kwa muziki wake. Sanura Kassim Mamake Diamond Platinumz AY Ambwene Allen Yessayah, kwa jina maarufu A.Y. ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania . Alizaliwa tarehe 5 mwezi July, 1981, mjini Mtwara, Kusini mwa Tanzania. Alianza usanii na kundi kwa jina S.O.G. mwaka 1996. Mwaka 2002 aliamua kufanya muziki akiwa pekee. Amewahi kushinda mataji kama vile Channel O Music Video Awards, Pearl of Africa Music Awards Vilevile amewahi kuteuliwa kuwania mataji ya MTV Africa Music nyimbo bora ya Hip Hop. Aligonga vichwa vya habari baada ya kanda ya video ya wimbo wake 'Zigo' alioimba na Diamond Platinumz kupigwa marufuku nchini Tanzania. Video hiyo ilipogwa marufuku kutokana na picha zake za utupu. TID Ni mwanamuziki wa Tanzania ambaye jina lake kamili ni Khalid Mohamed. TID ina maana ya 'Top In Dar es Salaam' mjini anakoishi. Anajulikana sana kwa nyimbo zake 'Zeze' na 'siamini'. Alianza kuimba mwaka 1994 na kundi kwa jina Black Gangsters. Alianza kuimba pekee miaka mitano baadaye akiwa na umri wa miaka 21 baada ya kuandikisha mkataba na Poa Records. Wimbo wake wa kwanza 'Mrembo' ulitolewa 2002. Aliwahi kuigiza katika filamu ya Girlfriend. Dully Sykes Msanii huyo anayejulikana kikamilifu kama Abdul Sykes alizaliwa tarehe 4 mwezi Disemba 1980. Ni msanii wa Tanzania anayejulikana kuwa miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa bongo fleva nchini humo. Pia akijulikana kuwa Mr Misifa ama Mr Chicks amezuru Uingereza na ni mmoja wa waanzilishi wa muziiki wa kiswahili wa dance Hall katika maeneo ya maziwa makuu. Ni maarufu kwa nyimbo zake Julieta, Salome, Historia ya Kweli na Leah. Mr. Blue Khery Sameer Rajab alizaliwa tar. 14 Aprili 1987. Ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mr. Blue. Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki wa muziki, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue' ambapo baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii. Mr Blue alikuwa gumzo wa wimbo 'Mr Blue' kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na ujanja wa ala ya muziki wenyewe. Q Chila Eric Shigongo Eric Shigongo ni mjasiriamali ambaye alijikita katika uandishi wa vitabu. Amezaliwa mnamo tarehe 10- 8-1969. Mpaka sasa ana vitabu vingi kamaː Malkia wa Masokwe, Damu na Machozi, Raisi Anampenda Mke Wangu, Siri Iliyotesa Maisha Yangu na mwisho Maisha ya Mike. Jay-Z Akijulikana kwa jina Shawn Corey Carter (alizaliwa mnamo tarehe 4 mwezi Disemba1969) akijulikana kama Jay-Z . Ni mwanamuzi wa wa aina ya Rap , mtunzi, mwandishi, mtayarishaji na mfanyibiashara. Ni miongoni mwa wasanii ambao muziki wao umeuzwa sana duniani na mmoja wa wanamuziki wakubwa wa mtindo wa Rap. Ameshinda tuzo 21 za Grammy Awards, pamoja na Kanye West.. Joseph Kusaga Ni mkurugenzi wa Cloud Media nchini Tanzania Joseph Kusaga ni mjasiriamali mwenye mawazo makubwa na ujuzi aliyependa muziki. Awali Joe aliwahi kuwa DJ na alishiriki katika hafla tofauti za muziki katika maeneo mengi nchini Tanzania akicheza muziki. P Diddy, Kwa jina Sean John Combs (alizaliwa mwezi Novembea 4, 1969), kwa jina maarufu kama Puff Daddy, Puffy, P. Diddy, Diddy. Ni msanii wa Marekani , mwimbaji, mtunzi, muigizaji, mtayarishaji na mfanyibiashara. Alizaliwa mjini New York na kulelewa katika eneo la Mount Vernon, mjini New York. Alifanya kazi kama mkurugenzi wa vipaji katika kampuni ya Uptown Records kabla ya kuanzisha kampuni yake ya Bad Boy Entertainment 1993. Albamu yake ya kwanza No Way Out (1997) iliuza mara milioni saba Usher Raymond Usher Raymond IV (alizaliwa mnamo mwezi Oktoba tarehe 14, 1978). Ni msanii wa Marekani , mwandishi na mchezaji densi. Alizaliwa mjini Dalls, Texas ma kulelewa katika eneo la Chattanooga, Tennessee hadi alipoelekea Atlanta, Georgia. Akiwa na umri wa miaka 12, alimuigiza katika shindano la kuimba kabla ya kuvutia kampuni ya muziki ya A&R kutoka LaFace Records. Alitoa albamu yake, Usher (1994) lakini alipata umaarufu miaka ya 90 alipotoa albamu yake ya pili My Way (1997). Shah Rukh Khan Shah Rukh Khan (alizaliwa na kupewa jina Shahrukh Khan; tarehe 2 mwezi November 1965). Akijulikana kama SRK, ni muigizaji wa filamu na mtayarishaji. Akijulikana katika mtandao kama "Badshah of Bollywood", "King of Bollywood", "King Khan", ameigiza katika takriban filamu 80 na kushinda mataji kadhaa ikiwemo lile la 14 Filmfare Awards. Khan ana ushabiki mkubwa barani Asia pamoja na nchini India. Ametajwa kuwa mmojawapo wa waigizaji waliofanikiwa zaidi duniani. Said Bakhresa Said Salim Awadh Bakhresa (alizaliwa 1949 in Zanzibar). Ni mfanyibiashara wa Tanzanian . Ndio mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni za Bakhresa Group Of Companies. Ni mfanyibishara nchini Tanzania na kisiwa cha Zanzibar . Iwapo unazungumzia kuhusu fedha, kuhusu muziki bora, tuzo na ushawishi basi Diamond ndio mwanamuziki mwenye ufanisi Afrika mashariki. text: Msichana huyo alipiga sarakasi ya nyuma nchini Afrika Kusini katika moja ya maeneo ya michezo katika mji wa Alexandria Johannesburg alipokuwa shule Jumanne Mwanasarakasi Phaphama Nxumalo akionekana siku hiyo hiyo akionyesha wenzake umahiri wake wa kujirusha hewani Huko huko Johannesburg, mwanamieleka akiwa mbele ya mashabiki wake Jumamosi.. Shabiki wa mieleka wa Afrika kusini hapa wakiwa katika maombi mwanamitindo mzaliwa wa Somalia na mjasiliamali Iman akiingia katika zulia jekundu katika tamasha la kimataifa la filamu la Venice International Nchini Italia Jumatano Katika tamasha hilo hilo alikuwepo mwanamitindo wa Afrika Kusini Candice Swanepoel hapa akiwa tayari kupigwa picha Nyota wa Afrobeats Mnaigeria D'banj aligonga vichwa vya habari kwa shoo yake katika Brixton Academy mjini London Jumapili . Mapema wiki hiyo , aliiambia BBC kuwa yeye na mkewe wanatarajia kupata ,mtoto mwingine , mwaka mmoja baada ya mtoto wao wa kwanza kufariki Siku ya Alhamisi mjini Abidjan, Ivory Coast, watu wakishiriki katika sherehe za kitamaduni za "Fatchue" Tamasha hilo ni kilele cha shughuli ya kitamaduni ya kuwapa majukumu ya uongozi wa kijamii vijana mwanamuzi wa Uganda aliyegeuka kuwa mwnasiasa mbunge MP Bobi Wine akibarikiwa na makasisi wa kikatoliki Jumapili katika tukio la kampeni . Kiongozi huyo wa upinzani anapanga kugombea dhidi ya rais wa muda mrefu Yoweri Museveni katika uchaguzi wa mwaka 2021 Katika eneo la kati mwa kenya siku ya Ijuma, walinzi wa wanyamapori walimsindikiza faru mweupe aliyesalia ili kutoa mayai yake ya uzazi . Inatumainiwa kuwa mayai hayo ili kuendeleza kizazi chao. Picha kutoka Reuters, EPA, Getty Images, AFP, Redferns na SOPA Images Baaadhi ya picha bora zilizochukuliwa kutoka maeneo mbali mbali ya bara la Afrika na kwingineko , wiki hii : text: Inapunguza nusu ya muda unaotumika kutoka Casablanca hadi Tangi Mfalme Mohammed VI na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron waliipanda treni hiyo katika safari ya uzinduzi kutoka Tangier hadi katika mji mkuu Rabat. Rais wa Ufaransa Eammanuel Macron amealikwa katika uzinduzi wa treni ya kasi Morocco Takwimu kuu kuhusu treni ya kasi Afrika: Afrika inatazamia kuimarisha miundo mbinu ya usafiri kushinikiza biashara, uwiano na utangamano wa kieneo. Mataifa ya Afrika yanakumbatia mfumo wa reli ya mwendo kasi katika kujaribu kushinikiza na kukuza uchumi na kuimarisha kasi za kusafirisha bidhaa baina ya mataifa kibiashara. Raha na karaha ya treni ya SGR Katika miaka 20 iliyopita jitihada za kufufu mfumo wa reli umechangi baadhiya maatifa kuamua kubinafsisha huduma hizo hususan katika mataifa ya magharibi na mashariki ya Afrika. Reli ya kisasa ya SGR nchini Kenya Kenya: Mradi wa reli mpya ya kisasa nchini Kenya SGR umefadhiliwa na serikali ya China ambao unaunganisha mji wa pwani wa Mombasa na Nairobi ulifadhiliwa kwa mkopo wa kima cha $3bn kutoka kwa benki ya China ya Exim katika kipindi cha miaka 15. Reli hiyo ya SGR ni miongoni mwa miradi muhimu ilioahidiwa na rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wake, ukizinduliwa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa urais uliopita. Awamu ya kwanza ya reli Kenya ilianza kazi mnamo Juni 2017. Tanzania: Jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge liliwekwa na rais John Pombe Magufuli mnamo Aprili 2017. Mradi huo umenuiwa baadae kuziunganisha nchi za Rwanda na Burundi pia. Katika awamu hii ya kwanza, ujenzi utakuwa wa reli yenye urefu wa kilomita takribani 300, ambayo itatoka jijini Dar es Salaam na kuishia mkoa wa jirani wa Morogoro. Ni reli ya kisasa, na ya kwanza Afrika Mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nguvu ya umeme. Reli hiyo inajengwa kwa awamu ya kwanza na kampuni kutoka nchi mbili, Uturuki na Ureno kwa gharama ya takriban dola bilioni 1.2 za Kimarekani. Dkt Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma. Ethiopia Reli mpya ya aina yake inayounganisha mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na mji mkuu wa Djibouti imezinduliwa Oktoba 2016. Reli hiyo mpya ina urefu wa kilomita 752 na inatoka Addis Ababa hadi bandari ya Doraleh katika mji wa Djibouti, kwenye ghuba ya Aden. Inasafirisha abiria na mizigo. Sehemu kubwa ya reli hiyo imo Ethiopia, Kilomita 652 kutoka Addis Ababa hadi Dewale mpakani, na sehemu iliyosalia Djibouti. Reli hiyo inaunganisha Addis Ababa na mji wa Djibouti Gharama ya ujenzi wa reli hiyo ni dola 4 bilioni za Marekani. Ufadhili umetoka kwa benki ya serikali ya China ya Exim & Import (70%) na sehemu iliyosalia kutoka kwa serikali ya Ethiopia. Benki ya maendeleo ya Afrika inataja kwamba katika ubinfasishaji ufadhili bora, muongozo wa sheria na utaalamu ni mambo muhimu. Mradi wa mtandao wa reli za kasi Afrika, ni sehemu ya ajenda ya Umoja wa Afrika 2063 na umenuia kuimarisha mifumo iliyopo sasa ya kitaifa ya reli. Morocco imezindua treni inayokwenda kwa kasi zaidi barani Afrika - itakayopunguza nusu ya muda unaotumika kusafiri katika miji ya kibiashara na kiviwanda Casablanca na Tangi text: Toure amehusishwa na kuhamia China Toure, 33, anahudumu miezi sita ya mwisho ya mkataba wake Etihad na yuko huru kuanza kuwasiliana na klabu nyingine. Lakini amesema: "Kwa sasa naangazia City. Siku za usoni zipo lakini kwa sasa ligi bado haijamalizika." Raia huyo wa Ivory Coast alirejeshwa kucheza Novemba baada ya kuwekwa kwenye baridi kwa miezi mitatu kutokana na matamshi ya wakala wake. Meneja wa City Pep Guardiola alikuwa ameapa kutomchezesha Toure hadi wakala wake Dimitri Seluk aombe msamaha kwa kusema Toure aliaibishwa kwa kutojumuishwa kikosi cha City kinachocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Toure aliomba msamaha kwa niaba ya Seluk mwezi Novemba na amekuwa kiungo muhimu katika timu yake. Aliwafungia mabao mawili ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace tarehe 19 Novemba. Yaya Toure amesema hatatafuta klabu ya kuhamia kipindi cha kuhama kwa wachezaji mwezi Januari na badala yake ataangazia kusaidia klabu yake ya Manchester City. text: Mwizi huyo alivalia kama mtawa na kuibia duka la kubadilishana sarafu Kenya Kasi ya wizi huo imewashangaza wachunguzi. Duru karibu na wachunguzi zimeilezea BBC kuwa mwanamke huyo aliyevalia kama mtawa aliingia katika duka la kubadilishia sarafu kabla ya muhudumu kumpa pesa za sarafu 15 mbalimbali. Picha za kamera za CCTV kutoka kwenye duka hilo zinamwonyesha mwanamke huyo akielekea hadi kwenye sehemu ya kuhudumiwa kama mteja baada ya kukaguliwa kwenye mlango. Kisha anazungumza na muhudumu kabla ya kukubaliwa kuingia eneo ambalo pesa huwekwa kupitia mlango salama wa chuma. Baada ya muda kidogo wa mazungumzo, muhudumu anamfungulia kasha la chuma ambapo pesa zilikuwa kabla ya kuanguka kwenye kiti. Wizi wote ulichukua chini ya dakika kumi na mlinzi wa langoni hakugundua kilichokuwa kikiendelea. Wachunguzi wanashuku kulikuwa na ushirikiano kutoka kwa wafanyikazi wa duka hilo na tayari wamemkamata mhudumu aliyehusika. Mwezi Novemba mwaka jana, wezi walichimba handaki lenya urefu wa mita thelathini na kuiba dola alfu mia tano kutoka kwa benki moja mjini Thika, kilomita 40 Kaskazini Mashariki mwa Nairobi. Kasi ya wizi huo imewashangaza wachunguzi. Duru karibu na wachunguzi zimeilezea BBC kuwa mwanamke huyo aliyevalia kama mtawa aliingia katika duka la kubadilishia sarafu kabla ya muhudumu kumpa pesa za sarafu 15 mbalimbali. Picha za kamera za CCTV kutoka kwenye duka hilo zinamwonyesha mwanamke huyo akielekea hadi kwenye sehemu ya kuhudumiwa kama mteja baada ya kukaguliwa kwenye mlango. Kisha anazungumza na muhudumu kabla ya kukubaliwa kuingia eneo ambalo pesa huwekwa kupitia mlango salama wa chuma. Baada ya muda kidogo wa mazungumzo, muhudumu anamfungulia kasha la chuma ambapo pesa zilikuwa kabla ya kuanguka kwenye kiti. Wizi wote ulichukua chini ya dakika kumi na mlinzi wa langoni hakugundua kilichokuwa kikiendelea. Wachunguzi wanashuku kulikuwa na ushirikiano kutoka kwa wafanyikazi wa duka hilo na tayari wamemkamata mhudumu aliyehusika. Mwezi Novemba mwaka jana, wezi walichimba handaki lenya urefu wa mita thelathini na kuiba dola alfu mia tano kutoka kwa benki moja mjini Thika, kilomita 40 Kaskazini Mashariki mwa Nairobi. Maafisa wa polisi nchini Kenya wameanzisha msako dhidi ya mwanamke aliyevalia kama mtawa na kufanikiwa kuibia duka la kubadilisha sarafu takriban dola 35,000. text: Erdogan amesema hayo alipokua akiwahutubia wabunge chama tawala nchini Uturuki. Amesema Uturuki ina ushahidi mkubwa wa kuthibitisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa na kutekelezwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2. Erdogan pia anataka washukiwa wafunguliwe mashtaka mjini Istanbul. Picha ya Jamal Khashoggi na Recep Tayyip Erdogan Anataka Saudi Arabia kutoa majibu kuhusu ulipo mwili wa Khashoggi na ni nani aliyeamuru oparesheni hiyo. Ufalme wa Saudia umetoa taarifa ya kutatanisha kuhusiana na kile kele kilichomkuta mwandishi huyo baada ya kusshiilia kwa wiki kadhaa kwamba alikua hai sasa mamlaka imekiri kuwa aliuawa katika opaeshenio ya kikatili. Tamko la rais Recep Tayyip Erdogan linakuja huku kongamano la waekezaj likianza nchini Saudi Arabia licha ya baadhi ya serikali na viongozi wakuu wa kibiashara wakijiondoa. Raisi wa Uturuki amesema nini? Rais Erdogan amethibitisha kuwa watu 18 wamekamatwa nchini Saudi Arabia kutokana na kesi hiyo japo hajatoa maelezo zaidi kuhusiana na ushahidi uliotolewa Hakuzungumzia rekodi ya sauti au video ambayo imetajwa katika ripoti ya vyombo vya habari baada ya kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi. Jamal Khashoggi alikwenda kwenye ubalozi wa Saudia mjini Istanbul kupata nyaraka za udhibitisho wa talaka aliyompa aliyekuwa mke wake Rais Erdogan pia amesema kuwa kundi la watu 15 wanaosadikiwa kuwa raia wa Saudia waliwasili mjini stanbul kwa kutumia ndege tofauti siku kadhaa kabla ya mauaji yake. Siku moja kabla ya mauaji ya Khashoggi ,baadhi ya watu kutoka kundi hilo walisafiri hadi msitu wa Belgrad, karibu na ubalozi wa Saudia mjini Istanbul. Amesema maafisa wa polisi wa Uturuki wamekua wakitafuta mwili wa marehemu katika eneo hilo tangu wiki iliyopita. Pia ameongeza kuwa watu hao waliondoa kamera za usalama kutoka jengo la ubalozi wa Saudia kabla Khashoggi kufika mahali hapo. Akizungumza na wabunge wa chama tawala cha AK, Bwana Erdogan amesema "Nataka watu 18 waliokamatwa kufunguliwa mashataka mjini Istanbul.'' Aidha amesema wale wote waliyohusika na mauaji hayo waachukuliwa hatua. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa. text: Tume ya IEBC imeanza kuwasajli Wakenya wanaoishi nchi wanachama wa EAC na Afrika Kusini Idadi hiyo ni asilimia 62 ya jumla ya wapiga kura 6 milioni ambao tume hiyo ililenga kuwasajili katika kipindi hicho. Shughuli ya kuwasajili kwa wingi wapiga kura ilitarajiwa kumalizika Februari 14 lakini mahakama ikaongeza muda wa siku tano hadi Jumapili Februari 19. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati ameambia wanahabari kaunti iliyoongoza kwa idadi kubwa ya wapiga kura kujitokeza kati ya waliolengwa ni Kajiado, kusini mashariki mwa Kenya, ambapo asilimia 240 walijitokeza. Kaunti ya Mandera kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ilifuata kwa asilimia 116 kujitokeza. Kwa jumla ya idadi ya wapiga kura waliojitokeza, jiji la Nairobi linaongoza kwa wapiga kura 461,346 likifuatwa na kaunti ya Kiambu (225,995) na jimbo la Nakuru likawa la tatu na wapiga kura 175,756. Bw Wabukati amesema tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2013, idadi ya wapiga kura waliojitokeza sasa imefikia 5.2 milioni. Baadhi ya wanaume wakisajiliwa kama wapiga kura nchini Kenya kufuatia kuanzishwa kwa shughuli hiyo siku ya Jumatatu Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, wapiga kura 1 milioni waliwasilisha maombi ya kubadilisha vituo vyao vya kupigia. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IEBC Marjan Hussein Marjan ameambia BBC kwamba suala la kuchukua kura na kuipiga huwa ni hiari na kwamba hatua ya watu kutojiandikisha ilivyotarajiwa siyo sababu raia hawana imani na taasisi yake. Kwa sasa tume hii inatarajia kuanza kuwasajili raia wa Kenya wanaoishi katika mataifa ya Afrika Mashariki, sambamba na katika magereza kote nchini Kenya. Nje ya nchi, usajili unafanyika Dar es Salaam, Arusha, Kampala, Kigali, Bujumbura na Pretoria. Macho yote sasa yanaelekea katika mchujo wa vyama vya kisiasa ambapo kumezuka mjadala wa kitaifa hususan baada ya chama tawala Jubilee kuomba tume hiyo kusimamisha mchujo huo. Katiba inakubalia tume kusimamia shughuli hiyo, lakini wasi wasi wa sasa ni ikiwa hali hii huenda ikaweka dosari uhuru wa tume ya uchaguzi. Aidha tume hii inakumbwa na changamoto ya kuanza kandarasi mpya ya kuchapisha makaratasi ya kura baada ya mahakama moja nchini Nairobi kubatilisha kandarasi iluiyotolewa hapo awali. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema IEBC imeanza utaratibu wa kutoa kandarasi na kwamba tume yake itakua tayari kuendesha uchaguzi huru na haki. Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kenya (IEBC) imetangaza kwamba ilifanikiwa kuwasajili wapiga kura 3.8 milioni katika kipindi cha mwezi mmoja wa kuwasajili kwa wingi wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwezi Agosti. text: Dikina Muzeya anasema wanafunzi wa kiume wanafaa kuangazia vitabu wala si miguu ya wanafunzi wa kike Chuo kikuu cha Zambia kimeweka matangazo kwenye maeneo ya maktaba kikiwataka wanafunzi wa kike kuvaa vizuri. ''Tumebaini kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanavaa nusu utupu wakiwa maktaba, hali inayosumbua wanafunzi wa kiume.'' lilieleza tangazo hilo ''Hivyo tunawashauti wanafunzi wa kike kuvaa vizuri wanapokuwa kwenye maeneo ya chuo. Mavazi ya niqab na burka yapigwa marufuku Austria Mavazi ya naibu gavana benki kuu Nigeria yazua mjadala mkali mitandaoni Baadhi ya wanafunzi wa kike hawakubaliani na amri hiyo ''Kama nia yako ni kwenda maktaba kusoma, kwanini uanze kuangalia vitu vingine kama miguu ya wasichana?'' Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Dikina Muzeya ameiambia BBC. ''Zingatia vitabu vyako, basi.'' Moja ya matangazo Chuo kikuu cha Zambia kinachowataka wanafunzi kuacha kuvaa nusu utupu Lakini Killion Phiri, mwanafunzi wa kiume anakubaliana na uamuzi wa mamlaka. ''Unajua jinsi miili ya wanawake inavyovutia.Utawezaje kuzingatia kusoma wakati mtu anaingia amevaa sketi fupi au nguo ya kubana.Utaanza kufikiria kuhusu vitu vingine na hautaweza kuwa makini. Moja kati ya vyuo vikuu vya juu nchini Zambia kimewaonya wanafunzi wa kike kutoingia maktaba wakiwa ''nusu utupu''kwa sababu vitendo hivyo vinawafanya wanafunzi wenzao wa kiume kutokuwa makini. text: Farouk Miya (kulia) alifangia Uganda bao la pekee Jumapili Ushindi wao wa 1-0 uliwawezesha kufuzu kwa fainali zitakazochezewa Gabon mwaka ujao kama mojawapo wa mataifa mawili bora yaliyomaliza ya pili katika makundi. Wapinzani wao Kundi D Burkina Faso pia walifuzu kwa ushindi wa dakika za mwisho wa 2-1 dhidi ya Botswana, ushindi uliowawezesha kuongoza kundini. Tunisia na DR Congo pia zilifuzu baada ya kuongoza katika makundi yao. Mataifa 16 yatashiriki michuano hiyo itakayoandaliwa 14 Januari hadi 5 Februari. Waliofuzu ni viongozi wa makundi yote 13, mataifa mawili bora yaliyomaliza ya pili hatua ya makundi, na wenyeji Gabon. Algeria, Cameroon, Egypt, Ghana, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Mali, Morocco, Senegal na Zimbabwe walijihakikishia nafasi kabla ya mechi za Jumapili. Katika kufuzu, Uganda pia walifikisha alama 13, kupitia bao la dakika ya 35 la Farouk Miya mjini Kampala, lakini wakaorodheshwa wa pili kwa sababu walilemewa na Burkina Faso klabu hizo mbili zilipokutana. Mara ya mwisho Uganda kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika ilikuwa miaka 38 iliyopita ambapo walimaliza wa pili baada ya kushindwa fainali an Ghana. Uganda imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza katika fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1978 baada ya kulaza Comoros Jumapili. text: Eneo ambalo ndege ilianguka Kusini-Mashariki mwa Addis Ababa. Miongoni mwa waliopoteza maisha ni raia 32 wa Kenya, 18 Canada, 9 Ethiopia na 7 raia wa Uingereza,hii ni kwa mujibu wa orodha ya abiria iiyochapwa na maafisa wa Ethiopia. Abiria kadhaa wanaaminika kuwa na uhusiano na Umoja wa Mataifa. Uganda Polisi nchini Uganda wanaomboleza kifo cha kamishna wa polisi nchini Uganda Alalo Christine ambaye alikua akifanya kazi na kikosi cha kulinda amani cha AMISOM nchini Somalia akitumiakia nafasi ya kamishna wa polisi msaidizi. Alikua anarejea kutoka Italia kuelekea Mogadishu,Somalia akiwa mmoja kati ya abiria wa ndege hiyo iliyoanguka siku ya Jumapili. Kamanda wa polisi alifikisha taarifa hizo kwa familia yake na kuratibu taratibu za kuhakikisha mweili wa Bi Alalo unarejea nyumbani Kenya Captain Yared (kulia) ana asili ya Kenya na Ethiopia Kapteni Mulugeta Gatechew,ambaye ana asili ya Kenya na Ethiopia, alikua rubani mkuu kwenye ndege namba 302. Amekua akifanya kazi na Shirika la ndege la Ethiopia tangu mwezi Novemba mwaka 2007. Ni ''mwenye kusifika kwa utendaji wake'' akiwa ametumia zaidi ya saa 8,000 angani, Kampuni imeeleza. Rafiki wa Kapteni Yared anasema ''nywele zake zilimsimama'' aliposikia kuwa amepoteza maisha. Katika mahojiano na BBC kwa lugha ya Amharic, Hassan Katende amesema alipata taarifa za ajali kwenye mitandao ya kijamii. ''Siwezi kulala.Imenishtua sana.Ni vigumu kuamini, huwezi kuamini kwa kweli,'' alieleza. Cedric Asiavugwa Miongoni mwa waliopoteza maisha ni Cedric Asiavugwa, Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya sheria chuo cha Georgetown. Alikua akisafiri kwenda Nairobi kuhudhuria mazishi ya nduguze, ripoti zimeeleza. ''Familia ya Georgetown imepoteza mwanafunzi wake kinara, rafiki wa wengi, na mahiri kwenye taaluma yake ya sheria Afrika Mashariki na duniani,'' alieleza mkuu wa idara ya Sheria chuo cha Georgetown, William Treanor. Bwana Asiavugwa ametumia taaluma yake ya masuala ya haki za jamii, hasa haki za wakimbizi na makundi ya jamii zisizo na utetezi, kilieleza chuo hicho. Pia alianya utafiti katika mada mbalimbali kuhusu amani, usalama wa chakula nchini Kenya, Uganda, Tanzania na Sudani Kusini. Hussein Swaleh, Mwamuzi wa mchezo wa soka, pia amepoteza maisha kwenye ajali hiyo, Shirikisho la Soka Afrika limeithibitishia BBC. Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya ameandika kwenye ukurasa wa twitter kuwa ''ni siku ya huzuni kwa wapenda soka'' Inaelezwa Swaleh alikua akirejea nyumbani baada ya kuchezesha mchezo wa ligi ya kilabu bingwa Afrika, huko Alexandria,Misri.CAF imeeleza kwenye taarifa yake. Salamu za rambirambi zimeendelea kumiminika kutokana na kifo cha Mwanahabari Anthony Ngare 49, aliyepoteza maisha kwenye ajali ya ndege. Bwana Ngare alikua akiwakilisha Kenya kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Paris na alikua akielekea Nairobi. Alikua Mhariri wa Standard Group na pia kwenye shirika la serikali. Kabla ya kifo chake alikua akifanya kazi na UNESCO kama Mkurugenzi msaidizi wa mawasiliano. Tume ya Taifa ya UNESCO Kenya imemtaja Bwana Ngare kuwa ''mmoja kati ya Nyota zinazong'ara''. Canada Pius Adesanmi Canada imethibitisha kuwa mmoja kati ya watu waliowatambua ni Profesa Pius Adesanmi, mzaliwa wa Nigeria, Mkuu wa Taasisi ya taaluma ya masomo ya Afrika, Chuo cha Carleton ''Mchango wake chuoni ni mkubwa,'' alisema kiogozi wa idara ya Sanaa na Sayansi ya jamii, Pauline Rankin. ''Alifanya kazi bila kuchoka kuijenga taasisi ya masomo ya Afrika, akishirikiana vizuri na wanafunzi.Alikua mkufunzi na mwalimu wa kaliba ya juu ambae ameacha alama chuon Carleton.'' Kifo chake kimewashtua, wasomi na waandishi wa habari. Profesa Adesanmi alikua akisafiri kuelekea Nairobi kushiriki mkutano ulioratibiwa na Umoja wa Afrika, ripoti zimeeleza. Danielle Moore Danielle Moore,24 ,alikua akisafiri kwenda Nairobi kuhudhuria mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa. Tarehe 9 mwezi Machi aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook : ''Ninafurahi sana kuwashirikisha kuwa nimechaguliwa kuhudhuria na niko njiani nakwenda kwenye mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa jiini Nairobi Kenya .'' ''Wiki ijayo nitapata nafasi ya kujadili masuala ya mazingira, kushirikishana habari na kukutana na vijana wengine na viongozi kutoka duniani kote.Ninafurahia fursa hii na ningependa baadae kuwashirikisha wengine nikirejea nyumbani.'' Bi Moore alikua mwanafuzi wa chuo kikuu cha Dalhousie baadae Taasisi ya Sayansi ya bahari Bermuda mwaka 2015. Ethiopia Sara Gebre Michael alikua Kiongozi wa wahudumu wa ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines namba 302. Msanii maarufu nchini Ethiopia ambaye alikua jirani yake Tesfaye Mamo, ameiambia BBC kuwa alikua mama anayejali, na atakumbukwa sana. Amemuacha mume na watoto watatu. Tesfaye pia ameweka picha za Sara Gabre Michael kwenye ukurasa wake wa facebook. Joseph Waithaka Joseph Waithaka,55, ana uraia pacha wa Uingereza na Kenya.Mtoto wake Ben Kuria, amesema alipata mshtuk baada ya kusikia kuwa baba yake ambaye alihamia Uingereza mwaka 2004, alikua ndani ya ndege hiyo. Bwana Kuria amemuelezea baba yake kuwa ni mtu ''aliyependa haki'' Abiria kutoka kwa zaidi ya mataifa 30 walikua kwenye ndege ya Ethiopian Airlines kutoka Addis Ababa kuelekea Nairobi iliyoanguka na kugharimu maisha ya watu 157 siku ya Jumapili. text: Bw Kim amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) Wamesema jina lake ni Kim Sang-duk, lakini pia amekuwa akifahamika kamaTony Kim. Mhadhiri huyo ambaye ni Mmarekani wa asili ya Korea amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) kwa wiki kadha kabla ya kukamatwa kwake. Chuo kikuu hicho hata hivyo kimesema masuala yaliyopelekea kukamatwa kwa Bw Kim hayana uhusiano wowote na chuo hicho. Bw Kim alikamatwa alipokuwa anajiandaa kuondoka Pyongyang. Maafisa wa Korea Kaskazini bado hawajasema sababu iliyochangia kukamatwa kwake. Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap limesema Bw Kim, ambaye umri wake ni miaka hamsini hivi, alikuwa anashiriki katika mipango ya kutoa misaada na alikuwa Korea Kaskazini kufanya mashauriano kuhusu juhudi za kusaidia watu wasiojiweza. Shirika hilo limesema Bw Kim aliwahi kuwa profesa katika chuo kikuu cha Yanbian nchini China. Chansela wa chuo kikuu cha PUST, Park Chan-mo, amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema Bw Kim "alikuwa anajihusisha na shughuli nyingine nje ya PUST kama vile kusaidia kituo cha mayatima." Raia wa tatu wa Marekani kuzuiliwa Bw Kim amezuiliwa kipindi ambacho wasiwasi umekuwa ukiongezeka katika rasi ya Korea huku meli za kivita za Marekani zikielekea eneo hilo. Korea Kaskazini imetishia kuzishambulia meli hizo. Marekani kwa muda imekuwa ikiituhumu Korea Kaskazini kwa kuwakamata na kuwazilia raia wake kisha kuwatumia kama rehani. Bw Kim sasa ni raia wa tatu Mmarekani kuzuiliwa na Korea Kaskazini. Mwezi Aprili mwaka jana, Kim Dong-chul, 62, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 na kazi ngumu baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi nchini humo. Alikuwa amekamatwa Oktoba mwaka uliotanguliwa. Mwanafunzi Mmarekani Otto Warmbier, 21, naye alikamatwa Januari mwaka jana akijaribu kuiba bango la propaganda hotelini alipokuwa ziarani Korea Kaskazini. Alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kazi ngumu kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola Machi mwaka 2016. Chuo kikuu kimoja nchini Korea Kaskazini kimesema raia wa Marekani aliyekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa nchi hiyo Jumamosi alikuwa mhadhiri katika chuo hicho. text: Mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 32, anaondoka City baada ya kuhudumu kwa miaka 10 ambapo aliongoza ufungaji wa magoli akiwa na mabao 260 katika mechi 390. Mechi yake ya mwisho ilikuwa mechi ya fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya aliposhiriki kama mchezaji wa ziada ambapo timu yake ilipoteza kwa Chelsea. Aguero atahudumu Barcelona akizuiwa na kifungu cha kuondoka cha £86m katika klabu hiyo ya Catalan. Aguero aliyeshinda mataji 15 katika kipindi chake akiichezea Manchester City , atajiunga na rafiki yake wa karibu Lionel Messi katika uwanja wa Nou Camp huku klabu hiyo ya Catalan ikijaribu kujiimarisha kutoka nafasi ya tatu. Walimaliza nyuma ya Atletico Madrid na Real Madrid baada ya kumuuza Luis Suarez kwa klabu hiyo kwa Yuro 5.2m mwanzo wa msimu huu. Barca iliondolewa katika michuano ya klabu bingwa Ulaya katika raundi timu 16 bora na PSG , lakini walifanikiwa kuilaza Atletico Bilbao 4-0 ili kushinda kombe la Copa Del Rey mwezi Aprili. Messi ndiye aliyefunga magoli mengi katika michuano yote akiwa na magoli 38 , huku mshambuliaji mwenza Antoine Griezman akiwa na magoli 20 naye Ousmane Dembele akipachika mara 11 . Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Aguero atajiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa mwezi Juni. text: Gael, ni mgonja katika hospitali ya utafiti wa watoto ya St Jude na mamake Matokeo ya utafiti huo uliofanyika katika hospitali ya Tennesee yalichapishwa katika jarida la matibabu la Uingereza. Watoto hao waliozaliwa bila kinga sasa wana kinga imara mwilini. Watoto walio na tatizo hilo na ambao hawajapatiwa matibabu huishi katika hali mbaya na mara nyingi hufariki wakiwa wachanga. Matibabu hayo ya jeni hushirikisha kukusanya uboho wa watoto hao na kusahihisha tatizo lililopo katika jeni muda mfupi baada ya kuzaliwa. David Vetter, aliyejulikana kama Bubble Boy miaka ya sabuini Jeni sawa iliotumika kusahihisha tatizo hilo iliingizwa katika toleo la mabadiliko ya moja ya VVU, virusi vinavyosababisha UKIMWI. Watafiti wanasema kuwa watoto hao walitoka na kwenda nyumbani baada ya mwezi mmoja. Dkt. Ewelina Mamcarz wa hopsitali ya St Jude , mwanzilishi wa utafiti huo, alisema katika taarifa ya hospitali hiyo: Hawa wagonjwa ni watoto ambao wanaitikia chanjo na wana mifumo ya kinga ya kufanya seli zote za kinga ambazo zinahitajika kuimarika ili kuulinda mwili kutokana na maambukizi kwa lengo la kuishi maisha ya kawaida. "Mafanikio haya ni ya kwanza kwa wagonjwa walio na SCID-X'', aliongezea akitaja aina ya kawaida ya SCID. Wagonjwa hao walitibiwa katika hospitali ya utafiti wa watoto ya St Jude mjini Memphis na Hopsitali ya watoto ya UCSF Benioff mjini San Francisco. Je huu ni ugonjwa gani? Kisa cha David Vetter pengine ndio kilichochulikana sana cha ugonjwa huo wa ukosefu wa kinga mwilini (SCID), ugonjwa ambao ulimzuia kushirikiana na ulimwengu Ukipewa jina la utani la "Bubble Boy", Vetter alizaliwa mwaka 1971 akiwa na ugonjwa huo na kufariki akiwa na umri wa miaka 12 baada ya kufeli kwa upandikizaji wa uboho Katika sekunde 20 za kwanza za kuzaliwa kwake katika hospitali ya watoto ya Texas mjini Houston alitengwa na kuwekwa ndani ya plastiki ambapo aliishi hadi kufikisha umri wa miaka sita ambapo alipewa nguo maalum ya plastiki iliotengezwa na Nasa , shirika la anga za juu la Marekani. Wazazi wake tayari walikuwa wamempoteza mtoto mmoja kutokana na ugonjwa huo kabla ya yeye kuzaliwa. Je kuna tiba mbadala? Kwa sasa tiba bora ya ugonjwa wa SCID-XI ni upandikizaji wa uboho na mfadhili wa tishu aliye na uhusiano wa karibu nawe. Lakini kulingana na hospitali ya watoto ya St Jude , zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa hukosa wafadhili hao hivyobasi hulazimika kutegemea seli za damu kutoka kwa wafadhili wengine. Mchakato huo huponya ugonjwa wa Bubble boy na husababisha madhara makubwa baada ya tiba hiyo. Tafiti nyengine za matibabu ya jeni zilitoa tiba mbadala ya upandikizaji wa oboho , lakini tiba hizo mara nyengine hushirikisha tiba ya kemikali na huwa na matokeo ya magonjwa mengine mengi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya damu na seli mundu. Wanasayansi wa Marekani wanasema kuwa wametumia HIV kutengeza matibabu ya jeni ambayo yaliwaponya watoto wanane waliokuwa na ukosefu wa kinga imara mwilini kwa jina ''Bubble boy''. text: Mwanamke amtia nyoka katika ndewe yake Ashley Glawe alichapisha picha yake katika mtandao wa facebook akiwa hospitali. Aliandika: Kilikuwa kisa cha kushangaza sana katika maisha yangu baada ya nyoka wangu kuingia katika tundu ya sikio langu . Alichapisha katika ujumbe huo katika mtandao akisema anamshikilia nyoka huyo kwa jina Bart baada ya kuingia katika ndewe yake ya sikio. ''Lilikuwa tukio la haraka hadi sikuweza kujitetea''. Nyoka aliyeingia katika ndewe na kukwama Anasema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu nyoka wake lakini hakuna tatizo lolote kufikia sasa. Aliwaambia marafiki zake mtandaoni kwamba madaktari walidunga sindano sikio lake na kulituliza, wakapanua ndewe hiyo kabla ya kumtoa nyoka huyo. Nyoka huyo kwa sasa anadaiwa kuwa kati hali nzuri. Mwanamke mmoja kutoka jimbo la Oregon alifanikiwa kumuingiza nyoka wake katika ndewe kabla ya nyoka huyo kukwama. text: Hata hivyo shughuli hiyo katika eneo hilo kwa sasa inaenda kombo kutokana na uhaba wa samaki kwenye ziwa Tanganyika huku baadhi ya wavuvi wakiamini kuachwa kwa mila na desturi ni moja ya sababu inayochangia uhaba wa samaki. Jitihada ni kubwa, mavuno madogo, wanawake wamefika ufukweni asubuhi na mapema kuchuuza samaki lakini upatikanaji ni adimu. Miezi kadhaa iliyopita wavuvi walikuwa wakipata zaidi ya ndoo ishirini za samaki, lakini kwa sasa mambo ni tofauti. Wanawake wamefika ufukweni asubuhi na mapema kuchuuza samaki lakini upatikanaji ni adimu. Wavuvi wengine wameamua kuachana na kazi hii na kuingia kwenye kilimo huku baadhi yao wanaona kuzipa kisogo mila na desturi ndio huchangia uhaba wa samaki katika ziwa hili. Dunia Rashid ni mvuvi katika eneo hili anasema: 'Tunaweza kuchukua mwaka mzima tunavuwa samaki kama dagaa na samaki wakubwa wakubwa. 'Basi wale waliokuwepo, wazee wametoweka wengine, wamebaki vijana wadogo, shughuli hawawezi kuzifanya.' Wazee wa kimila wanasema asiyesikia la mkuu huvunjika mguu, wananyooshea vidole teknolojia kama chanzo cha vijana wengi kuachana na mila na desturi ambazo huamini ndio njia pekee ya mafanikio. 'Machifu walikuwa wanafanya matambiko, wanaomba dua kwa MwenyeziMngu kutumia mambo ya asili, na kweli MwenyeziMngu alikuwa anatoa jibu. Moshi Haruna ambaye ni mvuvi, anawaelemisha wavuvi wenzake dhidi ya kuamini kuwa mila ndio husababisha uhaba wa samaki Mboga zilikuwa zinavulika na kupatikana,' anasema mzee Muhsini Mmbanga. Katika mkusanyiko ulio mfano wa kanisa ila sio kanisani, Moshi Haruna, mvuvi mwingine katika eneo hili anawaelemisha wavuvi wenzake dhidi ya kuamini kuwa mila ndio husababisha kushindwa kupata mavuno ya samaki. 'Wale wanaoendekeza mila, wanaamini kwamba bila ya mila hawawezi kupata. Ila sisi ambao hatuamini mila tunaamini, Mungu anatoa kulingana na vile anaona awalisheje binaadamu. Kwa wa mila wanakula, na sisi ambao hatuamini mila tunakula na tunaishi' anaeleza Haruna. Mamlaka za serikali zinazoshughulikia uvuvi katika ziwa hili, zinasema uhaba wa samaki kwa msimu huu sio jambo lakiimani. Edimund kajuni-ni afisa wa uvuvi Kigoma: 'Kwa uhalisia ni kwamba katika ziwa Tanganyika tuna misimu mitatu ya uvuvi'. 'Kuna kipindi ambacho ni msimu mb'aya, ambao ndio msimu tuliopo hivi sasa unaoanza mwezi wa tano Mei hadi wa saba Julai' anaeleza Edimund, afisa uvuvi Kigoma. Uvuvi katika Ziwa Tanganyika Imani potofu, dhana duni za uvuvi ni moja ya sababu zinazotajwa kurudisha nyuma sekta ya uvuvi nchini Tanzania. Baadhi wanaona jitihada zaidi zinahitajika kuifanya sekta hii iweze kuinufaisha jamii na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa. Nchini Tanzania uvuvi hunufaisha zaidi ya watu milioni nne, huku wakaazi wa mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania wakiutegemea kama shughuli kuu inayoendesha Maisha yao kiuchumi. text: Jumapili, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby alikuwepo katika kanisa la Kiangilikana la All Saints, Nairobi. Alikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga. Tamasha ya kutubu na kufurahia iliadhimishwa nchini Ivory Coast siku ya Jumamosi... Jamii ya N'zima wanashiriki tamasha hii iitwayo Abissa au tamasha ya kuuliza swali. Inaitwa hivi kwa sababu wao hujiuliza: Je, jamii ya N'zima inastahili kuuona mwaka mpya?... Mfalme na mwanawe wanabebwa mjini Grand Bassam... Wakiwa wamevalia mavazi ya waliowadhulumu mwaka uliopita, wanacheza kwa sauti za chombo cha mziki aina ya tam-tam. Punde makosa yote yamesamehewa, wanafurahia mwaka mpya. Siku iyo hiyo, Lamoj ambaye ni mwanamziki wa muziki wa Afrobeat alicheza katika maonyesho ya kibiashara jijini Lagos, Nigeria. Siku ya Jumapili, wakazi wa Zimbabwe wanacheza ngoma katika mkutano wa injili ulitumika kama mkutano wa siasa iliyofanyika mjini Harare... Wengi wa waliohudhuria walikuwa wakristo wa tabaka mbali mbali... Mrengo wa vijana wa chama tawala Zanu-PF nao walipanga mkusanyiko huu ili kuonyesha uaminifu wao kwa mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe... Alikuwepo na mumewe mwenye miaka 93, Rais Robert Mugabe. Bi Mugabe alitoa hotuba kali huku akionekana kuendeleza juhudi za kutaka kuchukua usukani kutoka kwa mumewe. Jumanne, Moustafa, 15, anabeba nyuzi katika kiwanda kilichosalia pekee katika eneo nzee la mji wa Cairo, Misri... Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7 wakati wa utawala wa mfalme Farouk aliyesemekana kuwashika wanaume wote ambao hawakuwa wanafanya kazi. Sasa zaidi ya miaka 70 baadaye kiwanda hiki ndicho kimesalia pekee eneo la kale la Cairo. Nyuzi hizi hutumiwa kutengeneza kamba za viatu na migodoro. Salama, 76, mmiliki wa kiwanda hiki alianza kufanya kazi hii akiwa miaka 7. Wavuvi nchini Libya wanatia nanga katika bandari ya Tripoli, Novemba 3, 2017. Samaki wauzwa katika soko la samaki mjini Tripoli, Libya Novemba 3, 2017 Picha hii ilipigwa Alhamisi, taipureta iliyo katika maonyesho yaliyofanyika katika jumba la makumbusho la polisi mjini Cape Town, Afrika Kusini. Jumba hili la makumbusho pia linaonyesha mfano wa jinsi maafisa walivyokuwa karne ya 1913-1957. Images courtesy of AFP, EPA, PA and Reuters Mkusanyiko wa picha za kuvutia zaidi kutoka Afrika na kuwahusu Waafrika pande mbalimbali duniani. text: Rais Edgar Lungu wa Zambia na mwenzake wa Tanzania Pombe Magufuli Uamuzi huo umetangazwa jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Zambia Edgar Lungu amefanya ziara ya kikazi ya siku tatu. Taarifa ya pamoja imesema kuwa viongozi wa mataifa hayo mawili wanashawishika kwamba mabadiliko hayo ya kisheria yataliokoa shirika hili la reli kutoka hali ya maututi inayolikabili hivi sasa. Sheria zinazoliongoza shirika hilo zinasema kwamba Mkurugenzi Mkuu wa shirika anapaswa kutoka Zambia huku makamu wake akitoka Tanzania. Tazara imeshuhudia kuporomoka katika uwezo wa kuendesha shughuli zake ambapo kwa mujibu wa Rais John Magufuli, mwaka 1976 wakati wa uanzishwaji wake lilikuwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani milioni 5 kwa mwaka wakati hivi sasa lina uwezo wa kubeba tani Laki moja na elfu 28 tu. Rais wa Zambia amesema kuwa shirika hilo linapaswa kuendeshwa kibiashara zaidi,ili liweze kurudisha faida ya uwekezaji ambao watu wa Zambia na China walifanya. ''Kinachotokea hivi sasa ni kwamba tunafungwa na matakwa ya kisheria kwamba uongozi wa juu wa shirika uundwe kwa mujibu wa sheria zilizopo.Lakini tumedhamiria sasa kwamba tunataka shirika hilo liendeshwe kibiashara zaidi, ili lirudishe faida ya uwekezaji ambao watu wa Zambia na China waliufanya''. Mbali na kuporomoka kwa idadi ya mizigo inayosafirishwa na TAZARA, miaka ya hivi karibuni shirika hilo limezongwa na mlolongo wa migomo ya wafanyakazi waliokuwa wakidai malimbikizo ya malipo yao Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema: "Ukizungumza na uongozi wa TAZARA kwa vyovyote vile watakwambia kwamba wanahitaji mtaji, lakini ukweli tatizo ni uongozi. Kwasababu kama ni mtaji, walikuwa nao mwaka 1976, lakini huo mtaji umeshuka hata sasa hauonekani kama ni mataji tena" Mambo mengine ambayo Rais Magufuli na mwenzake Rais Lungu waliyajadili ni pamoja na kupunguzwa kwa vizuizi vya barabarani katika usafirishaji wa mizigo lakini pia upanuzi au uboreshaji wa usafirishaji wa mafuta na gesi kutoka Tanzania kwenda Zambia kupitia bomba la mafuta la TAZAMA Tanzania na Zambia wamekubaliana kubadilisha sheria ili kuruhusu mkurugenzi mkuu wa shirika la reli la TAZARA kupatikana kutoka nje ya nchi hizo mbili. text: Bara la Afrika ndilo lenye idadi kubwa ya watu wenye idadi kubwa ya utapiamlo, na tatizo hili huanzia utotoni Kiwango cha njaa kimepanda karibu katika maeneo yote ya Afrika, na kulifanya bara la Afrika kuwa kanda yenye idadi kubwa ya watu wenye utapiamlo, kwa takriban asilimia 20, ikifuatiwa na Asia ambako zaidi ya asilimia 12 ya wakazi wa bara hilo wana tatizo hilo. Asilimia 7 ya watu wa Amerika Kusini na Caribbean pia wameathiriwa na utapiamlo. Kuna watoto zaidi ya milioni 40 wenye uzito wa mwili wa kupindukia duniani ,hili kikiwa ni ongezeko la watoto milioni 10 wenye tatizo hilo tangu mwaka 2000. Japo idadi ya watoto idadi ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 waliodumaa, imepungua kwa ujumla duniani, bado watoto milioni 149 au asilimia 21.9 ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wamedumaa. Hata hivyo Afrika bado ina kiwango cha juu kuliko mabara mengine cha watoto waliodumaa katika ukuaji. Mnamo mwaka 2018, mabara ya Africa na Asia ayalikuwa na kiwango cha tisa kwa kumi cha watoto wote waliodumaa duniani (sawa na asilimia 54.9 kwa Afrika na asilimia 39.5 kwa Asia). Mabadiliko ya hali ya hewa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ukosefu wa chakula barani Afrika, unasema Umoja wa mataifa Kiwango hicho kinafanya idadi ya waathiriwa wa ukosefu wa usalama wa chakula kufikia zaidi ya watu bilioni mbili. Tathmini ya kipekee kuhusu kuongezeka kwa uzito wa mwili inaonyesha kwamba kuna ongezeko la haraka la uzito wa mwili miongoni mwa watoto wa shule na watu wazima katika maeneo yote ya Afrika. Sababu za njaa utapiamlo Afrika Kulingana na Umoja wa Mataifa watoto wa shule hawali matunda na mboga za kutosha, mara kwa mara hula vyakula vyenye kutia nguvu na joto mwilini , na mara nyingi hula vyakula vinavyotengenezwa haraka kama vile vibanzi na vinywaji vya sukari nyingi kama vile soda, na hawafanyi mazoezi ya mwili. Mazowea haya mabaya , yanaweza kuwa yanachangia kwa sehemu fulani, kuongezeka kwa uzito wa mwili miongoni mwa watoto wa shule, inasema ripoti. Tatizo hilo linachangiwa, kwa sehemu moja na kuongezeka kwa masoko ya vyakula vilivyopitia mchakato wa viwandani na upatikanaji wake, pamoja na viwango vya chini vya mazoezi ya mwili. Kudorola wa chumi za dunia pamoja na kufungwa kwa biashara kuu za dunia kumeelezewa kuchangia kwa ukosefu wa hivi karibuni wa usalama wa chakula pamoja na ukosefu wa virutubisho vya mwili unaoendelea, pamoja na na ukosefu wa sera za muda mfupi na mrefu ambazo ni muhimu katika kulinda usalama wa chakula, iwe nyakati za matatizo ya kiuchumi au katika kuandaa sera hizo. Ukosefu wa mboga na matunda ya kutosha katika mlo wa watoto wawapo shuleni ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa utapiamlo barani Afrika Mabadiliko ya hali ya hewa pia yamechangia kuathiri kilimo na kusababisha kupungua kwa idadi ya wakulimana shughuli za kilimo . "haya yote yamesababisha mabadiliko ya namna chakula kinavyozalishwa, kugawanywa na kuliwa kote duniani - na kujitokeza kwa changamoto mpya za usalama wa chakula na afya ." wanasema wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa. Wakizungumza kuhusiana na baa la njaa, wakuu hao wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wameapa kuandaa mikakati ya kukabiliana na baa la njaa duniani. " Matendo yetu ya kukabilana na hali ya njaa inayotatiza dunia yatakuwa thabiti," Walisema viongozi hao wa Umoja wa Maraifa. na kuongeza kuwa: "Lazima tukabiliane na umaskini na kuandaa muundo wa mikakati ya mabadiliko inayoshirikisha ikiwalenga watu na kushirikisha jamii zilizozo katika hatari ya kuathirika kiuchumi na kujipanga wenyewe ili kumaliza njaa, kuweka usalama wa chakula na kukabiliana na aina zote za utapiamlo." Wanasema maafisa wa Umoja wa mataifa. Umoja wa mataifa unasema kuwa kasi ya mafanikio katika kukabiliana na kudumaa kwa mtoto na kupungua kwa idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa na uzito wa chini wa mwili ni ya kiwango cha chini sana, na hivyo kupunguza fursa za kufikia mafanikio malengo mengine ya kudumu. Umoja wa Mataifa unasema kuwa licha ya kwamba kiwango cha kudumaa kwa watoto kimepungua duniani kwa asilimia 10 katika kipindi cha miaka sita, bado mafanikio ni ya taratibu sana kulingana na malengo ya 2030 ambapo kiwango cha watoto wanaodumaa katika ukuaji kinatarajiwa kupunguzwa kwa asilimia 50. Unaweza pia kutazama: Wakazi wa maeneo ya kaskazini magharibi mwa kenya bado wanakabiliwa na baa la njaa Zaidi ya watu milioni 820 au 10.8% duniani bado wanakabiliwa na njaa, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa wakati dunia ikiadhimisha siku ya njaa siku ya njaa. text: Messi, 33, aliwasilisha ombi la uhamisho tarehe 25 Agosti lakini Ijumaa iliyopita alisema kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo kwasababu "haiwezekani " kwa timu yoyote kulipia kipengele kinachomruhusu kuondoka. Ni mara ya kwanza kwa Muargentina huyo kufanya mazoezi katika klabu hiyo tangu kuwasili kwa meneja mpya Ronald Koeman. Barcelona inaanza mechi dhidi Villarreal kutoka La Liga tarehe 27 Septemba. Messi alifanya mazoezi peke yake kama alivyofanya Philippe Coutinho, huku wachezaji wenzake wakifanya mazoezi pamoja. Messi alishindwa kuhudhuria kupima Covid-19 na wachezaji wenzake tarehe 30 Agosti na hakuhudhuria mazoezi tangu alipotuma ujumbe akiifahamisha klabu hiyo juu ya nia yake ya kutekeleza kipengele katika mkataba wake ambacho anaamini kitamruhusu kuondoka bila malipo mara moja. Barcelona na La Liga kwa pamoja zinasisitiza kwamba kipengele hicho si halali tena - na kwamba klabu yoyote inayotaka kumnunua itatakiwa kulipia garama ya Euro milioni 700 za kipengele cha kumuachilia. Rais wa La Liga Javier Tebas alisema kuwa katika uzinduzi wa msimu wa La Liga wa 2020-21 Jumatatu "hakuwa na wasiwasi mkubwa kabisa " kwamba Messi angeliondoka Barcelona msimu huu. "Tunataka Messi awe nasi. Ni mchezaji bora katika historia ya soka na tunataka amalizie mchezo wake katika La Liga," Tebas alisema. "Amekuwa nasi kwa miaka 20 na tunafarijika sana anaendelea kuwa nasi na haendi katika ligi nyingine ." Mchezaji maarufu aliyeifungia Barcelona magoli mengi, Lionel Messi amerejea mazoezini kufuatia kushindwa kwa jaribio lake la kulazimisha kuondoka katika klabu hiyo. text: Taifa hilo limeeleza kuwa linaweza kujibu shinikizo lolote kwa kuchukua hatua kubwa zaidi,mmoja wa maafisa wa juu ambaye jina lake alifahamiki alisema." Khashoggi, ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia alitoweka Oktoba 2 katika mazingira ya kutatanisha baada ya kutembelea ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki. Rais wa Marekani Donald Trump alidai kuiadhibu Saudi Arabia kama itabainika kuwa nchi hiyo imehusika kumuua mwandishi huyo. Aidha mamlaka ya Istanbul inaamini kwamba Khashoggi aliuawa alipokuwa anajadiliana na watu kutoka Saudi Arabia hivyo kukataa malalamiko hayo ni uongo. Kupotea kwa mwandishi huyo kumepelekea Uingereza na Marekani kukataa kuhudhuria mikutano mikubwa ya kimataifa iliyofanyika Saudi Arabia mwezi huu. Uchumi wa Saudi Arabia una ushawishi mkubwa duniani Jamal Khashoggi,mwandishi aliyepotea Saudia Arabia ambayo imekuwa na shinikizo kubwa la kimataifa juu ya kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari imejibu kukataa kupokea vitisho vyovyote ambavyo vinatokana na msukumo wa kisiasa au kiuchumi. Nchi hiyo imedai kujibu hatua yeyote itakayochukuliwa kwa kuchukua hatua kubwa zaidi. Mwanadiplomasia James Landale ameiambia BBC kuwa Katibu wa Hazina wa Marekani Steve Mnuchin na Katibu wa Biashara wa Kimataifa wa Uingereza Liam Fox wamekataa kuhudhuria mkutano mkuu wa uwekezaji ambao utafanyika mwezi ujao huko Riyadh, unajulikana kama "Davos in the desert". Mwanamfalme Mohammed bin Salman amekosolewa kuhusiana na kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi Tukio hilo ambalo limeandaliwa na mwana wa mfalme Mohamed bin Salman kwa lengo la kuhamasisha ajenda ya marekebisho. Wadhamini kadhaa na vyombo vya habari wameamua kujitoa . Taarifa inayothibitisha kwamba bwana Khashoggi aliuawa na watu kutoka Saudi inajadiliwa na wanadiplomasia wa Marekani na Ulaya. Rais Trump alisema nini kuhusu kutoweka kwa Jamal Khashoggi Rais Donald Trump wa Marekani alihaidi kuiadhibu Saudi Arabia na kama hawataadhibiwa na Marekani basi Urusi au China itawaadhibu. "Hatuwezi vumilia vitendo kama hivyo kutokea kwa waandishi ama kwa mtu awaye," Trump. Jamal Khashoggi ni nani? Khashoggi ni mwandishi wa habari mashuhuri ambaye amewahi kuangazia, taarifa za jinsi Sovieti ilivyovamia Afghanistan na kuibuka kwa Osama Bin Laden. Amefanya kazi katika mashirika kadhaa ya habari nchini Saudi Arabia. Aliwahi kuwa afisaa wa ngazi ya juu wa Saudi Arabia, lakini baadaye akatofautiana na serikali. Mwaka jana alikimbilia uhamishoni nchini Marekani ambako amekuwa akiandika makala ya kila mwezi katika gazeti la Washington Post. Katika makala yake ya kwanza ya gazeti hilo, Bw Khashoggi alisema kuwa anagopa kukamatwa kwa kukosoa wazi wazi utawala wa nchini Saudi Arabia. Siku tatu kabla ya kutoweka kwake Khashoggi, aliambia BBC kuwa "Watu wanao kamatwa si wapinzani wa serikali na kwamba wana uhuru wa kujielezabali wanajieleza. Saudi Arabia imekataa kupokea "vitisho vya kisiasa na kiuchumi" juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, idara ya habari ya Saudi Arabia imeharifu. text: Baadhi ya makontena yaliyobeba vyakula katika bandari ya Oman Meli kadhaa zikiwa zimebeba vyakula na bidhaa mbalimbali zimeonekana zikielekea Qatar kutokea bandari mbili zilizopo Oman. Qatar inategemea uingizwaji wa chakula kutoka nje. Saudi Arabia, Bahrain na muungano wa Falme za Kiarabu zilizuia uingizwaji wa bidhaa kwenda Qatar wiki chache zilizopita kwa shutuma kuwa nchi hiyo inaunga mkono vitendo vya kigaidi. Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amewasili mjini London na kisha Paris kujadili mgogoro huo. Wakati hatua ya kuitenga Iran ilianza wiki iliyopita kulikuwa na ripoti za watu kununua chakula kwa wingi wakihofia kuwepo upungufu. Qatar huagiza asilimia kubwa ya chakula chake kutoka nchi za nje Lakini mwishoni mwa wiki bidhaa kutoka Uturuki zilianza kuwasili katika maduka na ndege tano lizosheheni matunda na mbona nazo ziliondoka nchini Iran. Meli tatu zilizosheheni tani 350 za chakula pia zinatarajiwa kuondoka nchini Iran kuelekea Qatar. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar anasema kuwa asilimia 16 ya chakula chake kilikuwa kinasafirishwa kupitia Saudi Arabia ambayo ilifunga mpaka wake. Nchi ya Qatar imefungua huduma za usafiri wa meli kutokea Oman kwa lengo la kukabiliana na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na majirani zake. text: ''Mtu'' huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana Mwili huo - unaoaminiwa kuwa wa mwanamume - ulipatikana umeanguka katika bustani ya Clapham siku ya Jumapili. Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi. Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua. Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake. Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa. Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesema: "Ndege hii huchukua saa 8 na dakika 50 kukamilisha safari yake. Inasikitisha kuwa mtu alipoteza uhai wake baada ya kuingia ndege yetu kisiri. "Kenya Airways inashirikiana na mamlaka husika mjini Nairobi na London katika uchunguzi wa tukio hili." Sio mara ya kwanza kifo kama hiki kimeripotiwa katika ndege inayoelekea uwanja wa Kimataifa wa Heathrow. Mwezi Juni mwaka 2015, mtu mmoja alipatikana akiwa amefariki katika paa la makao makuu ya Notonthehighstreet.com katika barabara ya Kew Road, Richmond, huku mwingine akipatikana katika hali mahututi baada ya kuning'inia katika ndege ya British Airways kutoka mjini Johannesburg. Mwezi Agosti mwaka 2012, mwili wa mwanamume ulipatikana kwenye buti ya ndege iliyokuwa ikitoka mjini Cape Town Afrika Kusini, ilipotua katika uwanja wa Kimataifa wa Heathrow. Mwili wa mtu anayeshukiwa kuabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' umeanguka ndege hiyo ikielekea kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London. text: Kiongozi wa upinzani nchini DRC Etienne Tshisekedi Upinzani umehusika katika maandamano ya umma ukimtaka rais kabila kujiuzulu kwa sababu katiba inamzuia kusalia madarakani baada ya mwezi huo. Hatahivyo ,maafisa wa uchaguzi wanasema kuwa uchaguzi unaotarajiwa mwezi Novemba utacheleweshwa kutokana na ugumu wa kuwasajili wapiga kura katika taifa la takriban watu milioni 30. Akizungumza baada ya mkutano wa siku tatu wa muungano wa vyama vya upinzani katika mji mkuu wa kinshasa,Tshisekedi alisema kuwa tume ya uchaguzi inafaa kuvunjwa kwa kushindwa kuafikia mahitaji ya kikatiba ya kuitisha uchaguzi mwezi Novemba. Takriban watu 17 waliuawa katika makabiliano na vikosi vya usalama mnamo tarehe 19 baada ya upinzani kufanya maandamano ya kutaka kusitishwa kwa utawala wa Kabila mnamo mwezi Disemba. Tshisekedi alisema: Mnamo tarehe 19 mwezi Octoba,tutampatia kadi ya njano.Na iwapo hatakuwa amejiuzulu kufikia mwezi Disemba tutamuonyesha kadi nyekundu. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ataonyeshwa kadi nyekundu iwapo atasalia mamlakani mnamo mwezi Disemba kulingana na kiongozi wa Upinzani Etienne Tshisekedi text: Kwa mujibu wa taarifa kutoka Safaricom, Collymore amefikwa na umauli asubuhi ya leo Jumatatu Juni Mosi 2019 nyumbani kwake jijini Nairobi. Mwenyekiti wa kampuni hiyo Nicholas Ng'ang'a amesema kuwa afya ya Collymore ilikuwa mbaya majuma ya hivi karibuni. Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani .Alirejea Kenya mwezi Juni mwaka jana. Gazeti la Standard media nchini Kenya limeripoti. Marehemu ameacha mke na watoto wanne. Collymore alianza kuongoza gurudumu la Safaricom mwaka 2010 kutoka kwa Michael Joseph ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo, pia mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Kenya Airways. Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha. Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya kampuni hiyo. Kuna Masuala 'yanayogubika' uhusiano wa Kenya na Tanzania? Wamiliki simu za Huawei 'wahaha' kufuatia marufuku ya Google Viongozi kadhaa wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta wametuma salamu za rambirambi kwa familia kutokana na kifo hicho. Uhuru amesema nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa. ''Ni huzuni kuwa asubuhi hii nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Safaricom bwana Bob Collymore baada ya miaka kadhaa ya kupambana na saratani.Nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa,'' alisema Rais Uhuru Kenyatta. Rais Uhuru Kenyatta atuma Salamu za rambirambi ''Ni huzuni kuwa asubuhi hii nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Safaricom bwana Bob Collymore baada ya miaka kadhaa ya kupambana na saratani.Nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa,'' alisema Rais Uhuru Kenyatta. Rais Kenyatta amesema Bob Collymore alikuwa kiongozi ambaye aliiongoza Safaricom katika nafasi kubwa ya kuwa kampuni yenye matunda makubwa zaidi Afrika Mashariki. Ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu,marafiki na wafanyakazi wa Safaricom, Mbali na kutumikia nafasi yake akiwa Safaricom, amesema Collymore alitoa ujuzi wake wa kiutawala katika kutekeleza ajenda ya maendeleo ya taifa. Mbali na Rais Kenyatta, viongozi wengine wa kisiasa wameendelea kutoa salamu za rambirambi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa zaidi ya mawasialiano ya simu Afrika Mashariki Safaricom, Bob Collymore ameaga dunia, kampuni hiyo imethibitisha. text: Rais wa Tanzania John Magufuli "Kutumbua majipu" ni neno ambalo limekuwa maarufu katika vinywa vya wengi baada ya kiongozi huyo kuwafukuza kazi watendaji pale ambapo anaona mambo hayaendi sawa. Mfano hivi karibuni, Rais Magufuli amewaachisha kazi wakurugenzi wawili mkoani Kigoma mara tu baada ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kumkabidhi ripoti ambayo ilikuwa na matokeo mabaya katika eneo hilo. Lakini haya chini ni orodha ya marufuku aliyoyatoa Rais Magufuli yanaoathiri sekta mbali za serikali ya Tanzania tangu aingia madarakani; Maandamano na mikutano ya Kisiasa Polisi wamekuwa wakitahadharisha juu ya maandamano mara kwa mara Rais Magufuli amenukuliwa akisema shughuli za siasa ikiwa ni pamoja na maandamano na mikutano ya hadhara isimame hadi uchaguzi ujao mwaka 2020. Amedai baada ya uchaguzi uliopita, "sasa ni wakati wa kazi tu" Vyombo vya usalama vimekuwa vikitahadharisha mara kwa mara kuwa hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo. Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania. Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi. Shughuli za siasa, ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ni haki ya raia kwa mujibu wa katiba ya Tanzania. Usafirishwaji wa madini nje ya nchi Rais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini alipofanya ziara ya kushtukiza Machi 2017 Mwaka jana, Rais Magufuli alipiga marufuku usafirishwaji wa madini yasiyo chenjuliwa mpaka pale kodi za nyuma ziwe zimelipwa. Serikali hiyo iliweka mpango wa utaratibu utakaowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia yaani Smelter, hapa nchini ili kudhibiti upotevu wa mapato na kutengeneza mapato kwa watanzania. Waliopata mimba shuleni wasirejee shule Wanafunzi watakaopata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleni Rais Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wanafunzi wa kike ambao watakaopata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleni. Aidha Magufuli alikumbusha kwamba sheria inasema mwanaume ambaye atapatikana na hatia ya kumpa mimba mtoto wa shule, atafungwa jela miaka 30. Magufuli aliongeza kwamba mwanaume huyo atapata fursa ya kutumia nguvu alizotumia kumpachika mimba msichana huyo, kufanya kilimo akiwa gerezani. Nchini Tanzania kuna takriban wasichana 8,000 ambao huacha shule kila mwaka kutokana na kuwa wajawazito, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch. Usajili wa meli mpya Miongoni mwa meli za kigeni zilizosajiliwa Tanzania Miongoni mwa mambo ambayo yamepigwa marufuku nchini Tanzania tangu rais Magufuli aingie madarakani ni pamoja na kusitisha usajili wa meli mpya nchini humo 'mpaka itakapotangazwa vinginevyo'. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli aliagiza utoaji wa vibali na usajili usimame hadi hapo uchunguzi kina ufanyike kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa Tanzania na zinapeperusha bendera ya Tanzania. Agizo hilo lilikuja baada ya taarifa za kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha huku zikiwa zinapeperusha bendera ya Tanzania. Mbali na marufuku hizo ambazo zimetolewa na yeye mwenyewe zipo nyingine ambazo zimetajwa wakati wa utawala wake. Shisha shisha Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini humo na kulitaka jeshi la polisi kufanya kila juhudi kutokomeza uraibu huo. Uvutaji wa shisha ni marufuku Tanzania Katazo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Paulo makonda lilifuatiwa na lile la Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambapo alitoa agizo na kusema uvutaji shisha umekuwa ukichangia katika kudorora kwa maadili miongoni mwa vijana, na kuwapunguzia uwezo wa kiakili na kimwili wa kufanya kazi. Viroba Kenya wakiteketeza pombe haramu 2015 Mapema mwaka jana,pombe zilizokuwa zinauzwa kwenye mifuko midogo ya plastiki zimepigwa marufuku kuuzwa katika maeneo yeyote nchini humo. Serikali yapiga marufuku viroba Tanzania Rais wa Tanzania,John Magufuli ameonekana kuwa ni kiongozi anayetoa maamuzi ya haraka kwa kutoa marufuku ya jambo au kuwaachisha kazi watendaji katika nyadhifa zao. text: Zidane aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa. Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate pia yuko kwenye orodha hiyo baada ya kuwaongoza kufika nusufainali Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990. Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, Jurgen Klopp wa Liverpool na kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez wameorodheshwa pia. Kocha wa timu ya kinadada ya Chelsea Emma Hayes yupo kwenye orodha ya makocha wa kike. Chini ya Southgate, England walifikia kiwango cha juu zaidi walichowahi kufika wakicheza Kombe la Dunia wakiwa ugenini. Guardiola naye alishinda Ligi ya Premia na kuweka rekodi ya kushinda mechi nyingi zaidi msimu mmoja ligi hiyo. City walikuwa klabu ya kwanza kufunga mabao 100 katika ligi kuu. Gareth Southgate aliwaongoza England kufika nusufainali Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu 1990 Klopp aliwaongoza Liverpool kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo walishindwa na Real Madrid mwezi Mei, huku naye Martinez akiwasaidia Ubelgiji kuandikisha matokeo yao bora zaidi Kombe la Dunia kwa kumaliza wa tatu baada ya kuwashinda England. Ubelgiji walikuwa wamewatoa Brazil robofainali. Ufaransa walishinda Kombe la Dunia miaka miwili baada ya kumaliza wa pili Euro 2016 Kocha wa Ufaransa Deschamps aliibuka wa tatu (baada ya Mario Zagallo na Franz Beckenbauer) kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha pia. Upigaji kuwa utafungwa saa sita usiku 10 Agosti, na sherehe ya kutoa tuzo itafanyika London mnamo 24 Septemba. Emma Hayes aliwaongoza Chelsea Ladies kushinda ligi yanyumbani na kombe la ligi msimu uliopita Hayes kushinda tuzo ya wanawake Hayes, 41, aliwaongoza Chelsea Ladies kushinda Kombe la FA na Kombe la Ligi Kuu ya Wanawake siku chache kabla yake kujifungua mtoto mvulana. Kwenye orodha hiyo yupo pia kocha wa zamani wa Chelsea Ladies Mark Parsons, ambaye sasa anaongoza Portland Thorns ya Marekani. Orodha hiyo ya makocha wanne iliandaliwa na jopo la wataalamu wa Fifa ambalo lilimjumuisha nyota wa zamani wa Marekani Mia Hamm. Aliyekuwa meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa aliyeshinda Kombe la Dunia Didier Deschamps ni miongoni mwa wakufunzi 11 walioorodheshwa kushindania tuzo ya Fifa ya Kocha Bora wa Mwaka 2018 duniani. text: Mkuu wa polisi Tanzania, Simon Sirro Hii inafuatia mauaji ya watoto 10 katika maeneo ya Njombe na Simiyu mwishoni mwa Januari mwaka huu. Mkuu wa polisi , Simon Sirro amethibitisha kuwa waganga 45 wa tiba za jadi wamekamtwa katika eneo la Simiyu na wengine 20 katika eneo la Njombe. "Kuna sababu nyingi ambazo huenda zilichangia mauaji hayo lakini wao wanatuhumiwa kutokana na kuhusishwa kwao na imani za kishirikina.'' alisema bwana Sirro. Ameongeza kuwa washukiwa hao wanahojiwa kuhusiana na mauaji ya watoto yaliyosababisha mjadala wa kitaifaTanzania. Baadhi ya waganga wa kienyeji wa Njombe walikutana wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni mapema mwezi Februari na kujitetea kuwa hawakusuka na matukio hayo. Mkuu huyo wa polisi aidha amesema kuwa msako mkali dhidi ya waganga hao ambao ni washukiwa wakuu wa mauaji hayo yamekuwa yakiendelea tangu wiki moja iliyopita. 'Nimetoa amri kuwa kila mganga wa tiba za jadi waliyosajiliwa na wale ambao hawajasajiliwa wachunguzwe na wale watakaoshukiwa kuwa wahalifu wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria'' Alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Polisi inawalenga wanaganga wa jadi ambao hawajasajiliwa rasmi kuendesha shughuli zao. 'Mapema mwaka huu watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 katika maeneo ya Njombe na Simiyu walipatikana wamefariki katika mazingira ya kutatanisha. Serikali ya Tanzania iliahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji hayo ya kikatili. Watu waliyo na ulemavu wa ngozi ni miongoni wahasiri wa mauji yanayohusishwa na imani za kishirikina ambapo sehemu za miili yao hutumiwa kufanyia matambiko Waganga wa tiba za jadi wilayani Njombe hata hivyo wamejitenga na tuhuma kuwa wanachochea mauaji ya watoto wilayani humo. Polisi nchini Tanzania imewakamata waganga 65 wa tiba za jadi wanaoshukiwa kuhusika na mauji ya kikatili ya watoto kusini magharibi mwa taifa hilo. text: Lissu amekuwa nje ya Tanzania kwa matibabu toka Septemba 2017, amsema tarejea nyumbani atakaporuhusiwa na madaktari wake. Uchaguzi huo mdogo ulikuwa ufanyike Julai 31, mwaka huu, kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu kuvuliwa ubunge. Afisa wa uchaguzi wa Wilaya ya Ikungi, Jonal Katanga amemtangaza Mtaturu Ijumaa jioni na baada ya kutowekewa pingamizi lolote. Mtaturu amekabidhiwa cheti cha ubunge wa jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na Tundu Lissu tangu mwaka 2010 hadi Juni 28, 2019. Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi Mbunge huyo mteule alirejesha fomu jana kabla ya saa kumi jioni, muda ambao wagombea wote waliochukua fomu walitakiwa kuwa wamezirejesha. Wagombea wengine waliochukua fomu ni Hamidu Hussein (ADA-Thadea), Tirubya Mwanga (UPDP), Ameni Npondia (CCK), Amina Ramadhan (DP), Ayuni John (UDP), Amina Mcheka (AAF), Maulid Mustafa (ADC), Selemani Ntandu (CUF), Feruzy Fenezyson (NRA), Abdallah Tumbo (UMD), Donald Mwanga (TLP) na Masalio Kyara (SAU). Uchaguzi katika jimbo hilo ulikuwa umepangwa kufanyika Julai 31, 2019 kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lissu aliyepoteza sifa za kuwa mbunge kutokana na kutojaza fomu za mali na madeni na utoro bungeni. Fomu ya Mtaturu ilibandikwa katika ubao wa matangazo wa ofisi ya halmashauri ya Ikungi ili kutoa fursa ya watoa pingamizi hadi leo saa kumi jioni.(Saa za Afrika Mashariki) Lissu yupo nje Tanzania tangu Septemba 7, 2017 akitibu majeraha ya risasi alizomiminiwa akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea. Mwanasiasa huyo mwandamizi wa upinzani nchini Tanzania, hivi karibuni aliiambia BBC kuwa anapanga kwenda Mahakama Kuu nchini Tanzania kupinga kuvuliwa ubunge. Spika Ndugai Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, alitangazia bunge la nchi hiyo Ijumaa Juni 28 kuwa ameiandikia tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuileleza kuwa jimbo la Singida Mashariki, lililokuwa likishikiliwa na Lissu kupitia chama kikuu cha upinzani Chadema lipo wazi. Mwanasiasa huyo pia ameiambia BBC kuwa yeye si mtoro bungeni na yungali anapokea matibabu barani Ulaya. "Mimi si mtoro bungeni na sijawahi kuwa mtoro. Kilichonikuta kinajulikana, nilipigwa risasi 16 nikiwa natoka bungeni Septemba 7, nikaletwa nje kwa matibabu. Tangu hapo nipo nje natibiwa," amesema Lissu na kuongeza, "Kwanza walionishambulia mpaka sasa hawajulikani, hakuna aliyekamatwa. Leo inasemwa sijulikani nilipo navuliwa ubunge... kinachoendelea si ajabu, kuna watu hawana maarifa tena, walichobaki nacho ni mabavu tu." Japo inafahamika kuwa mwanasiasa huyo alilazimika kusafirishwa nje ya Tanzania awali nchini Kenya na kisha Ubelgiji kwa matibabu baada ya shambulizi dhidi yake, kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya kutokuwepo kwake bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Hivi karibuni ikiwa yungali ughaibuni amezuru nchi za Marekani, Ujerumani na Uingereza, kote huko, amehojiwa na vyombo vya habari za kutoa mihadhara kwenye vyuo vikuu juu ya hali ya haki za binaadamu Tanzania. Hali hiyo iliibua hoja miongoni mwa wakosoaji wake kuwa tayari amepona na anastahili kurudi Tanzania. Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Miraji Mtaturu, amepita bila ya kupingwa katika hatua za awali za matayarisho ya uchaguzi mdogo ambao ungefanyika kwenye Jimbo la Singida Mashariki, baada ya wagombea 12 wa vyama vya upinzani kutorejesha fomu. text: Mabaki ya wapenzi wa jinsia moja waliokufa wakiwa wameshikana mikono yapata miaka 1500 iliyopita Masalio ya mabaki hayo yalijulina kama 'Lovers of Modena'. Watafiti hawakuweza kugundua jinsia za mabaki hayo wakati walipoyagundua nchini Italia mwaka 2009 kwa sababu walikuwa hawajahifadhiwa vizuri. Lakini njia mpya ya utafiti wa utafiti wa protini katika meno, umeweza kubainisha jinsia zao. Uhusiano wa mabaki haya ya watu wa kale ya karne ya 4 mpaka 6 bado haujafahamika. Watafiti wanasema kuwa wanaume hawa walizikwa wakiwa wameshika mikono. Baadhi ya watafiti walihusisha mabaki hayo kwa kudai kuwa walikuwa ndugu au wanajeshi waliokufa pamoja katika vita. Watafiti hawa wanahusisha vita kwa sababu makaburi mabaki hayo yalipatikana katika makaburi ya vita. Watafiti wamebaini kuwa mabaki ya miili ya watu wa kale waliokuwa wameshikana mikono yaliyopatikana Roma , Italia , wote walikuwa wanaume. text: Furaha ya ushindi ya wana Liverpool City walianza vizuri wakati walipojaribu kulipa deni la 3-0 walizofungwa katika mechi ya kwanza. Ilikuwa dakika ya pili tu ya mchezo ambapo Raheem Sterling alimwanzishia Gabriel Jesus aliyeitumia nafasi hiyo kupachika bao la kuwapa matumaini Man City. Hata hivyo baada ya tukio la vurugu kabla ya muda wa mapumziko lililoisha kwa Meneja Pep Guardiola kuondoshwa katika eneo la benchi la ufundi, City hawakuweza kuyafikia matamanio yao. Tukio lenyewe lilianzia pale ambapo Bernardo Silva alikuwa amepiga mkwaju kuelekea lango la Liverpool, huku Liverpool ikiwa katika shinikizo zito, mpira ukamkuta Leroy Sane ambaye aliukwamisha wavuni na kuwafanya City kudhani wamefanikiwa kupata goli la pili. Lakini hali ilikuwa tofauti kwani mwamuzi Antonio Mateu Lahoz alilikataa goli hilo kwa madai kuwa limepatikana katika mazingira ya kuotea yaani offside, jambo ambalo limemkera Pep Guadiola aliyeingia uwanjani kumkabili mwamuzi Antonio Mateu Lahoz, na hivyo meneja huyo wa City kuambulia kufukuzwa katika eneo lake la ufundi hali iliyomfanya kulazimika kuitizama kipindi cha pli akiwa katika viti vya mashabiki. City wakijaribu kupambana katika mazingira ambayo mwalimu wao yuko mbali, wakapoteza mwamko na kuwapa nafasi wageni Liverpool kupitia Mohamed Salah akajipatia bao lake la 39 la msimu baada ya mbio za nguvu kutoka kwa Sadio Mane mnamo dakika ya 56. Goli zuri la Robert Firmino dakika 13 kabla ya kumalizika kwa mchezo, limekuwa msumali wa mwisho katika jeneza la Man City na hivyo kuwahakikishia Liverpool kusonga mbele. Sasa Liverpool wanasubiri kuwajua wapinzani wao katika nusu fainali wakati droo itakapochezeshwa Ijumaa [12:00 BST] huko Nyon, Uswisi. Liverpool imefika katika nusu fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka 10 baada ya kujikokota na kuishinda Manchester City kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 yaliyoleta ushindi wa jumla wa Liverpool 5-1 Man City. text: Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake watatu waliweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti Wakenya wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara ya huru wa mahakama. Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day. Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa wanachama wa kanisa hilo. Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya ya siku ya Sabato kuisha. Matamshi ya Jaji Maraga Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo. Aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake. Jaji Maraga mwenye umri wa miaka 66, alifuzu kama wakili miaka 40 iliopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kibinafsi. Alichaguliwa jaji 2003 na kujiunga na mahakama ya rufaa 2012. Ameoa na ana watoto watatu. Mwaka uliopita kufuatia kustaafu kwa jaji mkuu Willy Mutunga, aliwashinda majaji wengine 10, mawakili na wasomi kuteuliwa jaji mkuu. Hatahivyo mapema mwaka huu aliripotiwa kumkemea mtu aliyemchagua, rais Uhuru Kenyatta. Wakati akifanya kampeni nyumbani kwa jaji Maraga rais Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanafaa kumpigia kura kwa sababu alimpatia kazi ''mwana wao''. Hatahivyo jaji mkuu kupitia idara ya mahakama JSC alisema kuwa yeye sio mradi wa serikali. Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini Kenya Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alikuwa amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama , ijapokuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya. Hatahivyo baadaye alisema kuwa majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine''. ''Maraga na wahahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi. Sasa mimi sio tena rais mteuliwa bali rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba sasa mimi ni rais anayehudumu''. Licha ya vitisho hivyo , rais hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70. Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake watatu waliweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti. text: Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani wanadai kwamba wameunda programu ya kompyuta ambayo inaweza kuangalia uso wa mtu na maumbile yake na kutofautisha kati ya wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wengine. Programu hiyo inaweza kutambua mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyabaini, wanasema. Lakini watetezi wa haki za mashoga wameshutumu utafiti huo na kusema ni "hatari" na "sayansi isiyo na manufaa". Lakini wanasayansi wanaohusika wamesema wanaopinga programu hiyo hawajaielewa vyema. Maelezo ya kina kuhusu mradi huo yatachapishwa katika jarida moja kuhusu sifa za watu na saikolojia ya kijamii. Kuangalia utaya Katika utafiti huo, wataalamu waliunda programu kwa kutumia picha za wanaume 14,000 wazungu kutoka kwa tovuti ya kutafuta wapenzi. Walitumia picha kati ya moja na tano za kila mtu na kurekodi msimamo wa mtu kimapenzi kama alivyojitangaza katika tovuti hiyo ya kuchumbiana. Wataalamu hao wanasema programu waliyoiunda ilionekana kuwa na uwezo wa kuwatofautisha wanaume na wanawake wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja. Katika jaribio moja, programu hiyo ilipopatiwa picha mbili ambapo moja ilikuwa na basha na nyingine ya mwanamume wa kawaida, ilifanikiwa kuwatofautisha mara asilimia 81. Kwa wanawake, ilifanikiwa asilimia 71. "Wapenzi wa jinsia moja huonekana kufanana. Wanaume wapenzi wa jinsia moja huwa wana jaya jembamba na pua ndefu, nao wanawake wapenzi wa jinsia moja wana taya kubwa," wanasema watafiti hao. Lakini wakati mwingine, programu hiyo haikufanikiwa sana, mfano wakati wa majaribio mengine ilipopewa picha za wanaume mabasha 70 na wanaume 930 wapenzi wa kawaida. Ilipotakiwa kuwachagua wanaume 100 ambao wana uwezekano mkubwa wa kuwa mabasha, iliwakosa 23. Watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja wanahofia huenda ikatumiwa katika kamera za kisiri (CCTV) za kufanya upelelezi Gazeti la Economist ambalo lilikuwa la kwanza kuchapisha utafiti huo limesema miongoni mwa upungufu wa programu hiyo ni kwamba imeangazia zaidi Wazungu na pia imetumia picha kutoka kwa mitandao ya kuchumbiana, ambazo mara nyingi huwa zinaashiria msimamo wa watu. Mashirika mawili ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja yametoa taarifa kushutumu utafiti huo na kusema kwamba unaweza kutumiwa kuwadhuru wapenzi wa jinsia moja. Utafiti ambao unafanyia majaribio teknolojia inayodaiwa kuwa na uwezo wa kutofautisha watu wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja umezua mzozo mkali kati ya waliotayarisha teknolojia hiyo na watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja. text: Kwa kawaida siku hii huwa ni fursa ya kuchukua hatua, kufanya mabadiliko, kushinikiza, kuhimiza na kuwawezesha wanawake wa nyanja zote kujitambua uwezo wao. Licha ya kwamba wanawake wanachangia ukuaji wa uchumi kote Afrika, ukandamizaji unatatiza nafasi wanazoweza kuwa nazo. Kutokana na kuendelea kukithiri kwa umaskini, wanawake wengi wanajipata katika ajira zenye vipato vya chini na wanakuwa na nafasi finyu ya kujiendeleza. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, ili kuyatimiza, malengo ya maendeleo endelevu kama sehemu ya ajenda ya mwaka 2030, kuna haja ya kulisaidia bara la Afrika katika kushinikiza ustawi endelevu wa kiviwanda na unaojumuisha kila mtu. Na hiyo ni kumaanisha hakuna atakaye achwa nyuma, hususan wanawake. Baadhi ya mataifa ya Afrika yanapania kuwa na nchi zilizoendelea kiviwanda, lakini kwa mara nyingi idadi kubwa ya wanawake wanaonekana kususia kujitosa katika sekta hiyo. Je ni kwanini? Tumezungumza na wanawake watatu kutoka Afrika Mashariki ambao ni miongoni wanawake wengi waliolivuka daraja hili na kupata ufanisi. Siri yao ni gani? Bertilda Niyibaho, mmiliki wa kiwanda kinachozalisha unga unaotokana na uyoga Bertilda Niyibaho - Mjasirimali nchini Rwanda: Bi Niyibaho Bertilda ni mjasiriamali aliye na kiwanda kinachozalisha unga unaotokana na uyoga kufwatia mradi kabambe alioanzisha wa kuimarisha lishe bora miongoni mwa jamii. Biashara yake imepanuka na kuvuka mipaka ya Rwanda. Huku akionyesha kiwanda chake, ambayo sehemu kubwa ni maabara na sehemu nyingine inatumiwa katika kurutubisha zao la uyoga, anasema akianza alikuwa mkulima tu wa kawaida: "Nilianza shughuli zangu nikitengeneza pombe ya kienyeji itokanayo na ndizi, lakini nikaja kuona kwamba mabaki ya ndizi na mabaki ya mazao mengine yanatupwa tu kiholela ilhali yangeweza kuzalishwa mambo mengine yakawa na manufaa kwa jamii, basi nikajitosa katika kulima uyoga." Sehemu ya kiwanda cha bi Niyibaho inatumiwa katika kurutubisha zao la uyoga Kiwanda chake kilikua na akaanza kutengeneza unga wa uyoga na mazao mengine. Biashara yake imekuwa kadri muda ulivyosogea na imepanuka na kuvuka mipaka. Kwa sasa yeye husafirisha bidhaa zake hadi Tanzania, Kenya, Uganda na hata Burundi. Licha ya ufanisi huu anasema hakukosa changamoto: "Shida niliyo nayo ni kwamba, bidhaa zangu zikifika huko mfano Uganda zinabandikwa leseni ya kwamba zilitengenezwa Uganda! "Binafsi nilifuatilia nikatembelea wale wanaolangua bidhaa zangu nikashangaa nilipokuta kwamba wameandika eti 'Made in Uganda!' Changamoto nyingine anasema ni kukosa uungwaji mkono wa serikali na kupata leseni ya ubora wa bidhaa kumwezesha kupenya katika masoko ya Ulaya na Marekani. Jennifer Bash - Tanzania Mkurugenzi wa kampuni ya Alaska Jennifer Bash ni mkurugenzi wa kampuni ya Alaska nchini Tanzania. Kampuni yake imejikita katika kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo yanayo zalishwa na wakulima wa Tanzania, wengi wao wakiwa ni wanawake. Kampuni hii pia inajishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za vyakula kama mayai, mchele, mafuta ya Alizeti, unga wa sembe na dona. Je ni ipi siri ya ufanisi wake katika sekta ya viwanda? Jenifer anaamini kwamba mtaji sio kikwazo kwa kuwa wazo ndio mtaji. 'Mara nyingi watu wanakua na mawazo makubwa lakini washindwa kuyafanyia kazi wakidhani wanahitaji mtaji mkubwa kufanyia kazi wazo lao. 'Ubunifu ni muhimu' Wakati kuwaza makubwa ni vyema, lakini tukubali kuanza na kidogo ili kufikia makubwa kulingana na mazingira yanayotuzunguka'. Jennifer anasema ubunifu wa uendeshaji wa biashara ni jambo muhimu kwenye kufanikisha biashara yeyote ili kupata wateja. Alaska Tanzania imebuni soko lake kwa kujikita kwenye programu iitwayo 'Mama Alaska" ambayo inamuwezesha mama ntilie (Mama Lishe) kupata bidhaa za Alaska kwa urahisi na bei nafuu. Pia inawawezesha wakulima kupata elimu ya kukuza biashara yao na kuona thamani ya kile wanachokifanya kwa kuboresha huduma zao na kutengeneza mnyororo mpya wa thamani. Lorna Rutto - Kenya Mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Ecopost Lorna Rutto ni mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa EcoPost, kampuni ambayo imekuwa ikitumia taka za plastiki kuunda bidhaa mbalimbali zikiwemo boriti za kutumiwa kwenye nyua na mabango. Kampuni yake huunda pia bidhaa mbalimbali za kutumiwa katika ujenzi. Lorna amepokea tuzo nyingi Kenya na kimataifa na alikuwa miongoni mwa wanawake vijana 20 wenye nguvu Afrika walioorodheshwa na jarida la Forbes. Alipokuwa anaanzisha Ecopost, alikumbana na changamoto nyingi hasa katika kutafuta mtaji. "Tulitazamwa kama biashara iliyo na hatari nyingi tukilinganishwa na biashara nyingine sokoni. Benki zilitaka taarifa za akaunti za benki kuthibitisha kwamba biashara yetu ilikuwa inafanya vyema ilhali tulikuwa tu ndio tunaanza," anasema. "Tulitakiwa pia tunatakiwa kutoa dhamana ya mkopo lakini hatukuwa na chochote." Waliwasilisha maombi katika mpango wa Enablis- uliofadhiliwa na Wakfu wa Safaricom na wakashinda na hapo wakafanikiwa kupata mtaji. Kando na fedha, walikabiliwa pia na tatizo la mitambo ya kutumia ambayo walihitajika kuiagiza kutoka nje ya nchi, pamoja na wafanyakazi wenye ufundi uliohitajika kuendesha mitambo hiyo. Gharama ya uzalishaji ilikuwa pia juu - gharama ya umeme, malighafi, kulipia leseni na kadhalika. "Hatukupokea pia usaidizi kutoka kwa serikali na wanaounda sera. Wajasiriamali hasa walio katika sekta ya viwanda wanahitaji kichocheo na usaidizi pamoja na mazingira mahsusi ili kufanikiwa," anasema Bi Rutto. Anasema amegundua kwamba "fursa zipo kila pahali". "Niliigundua fursa yangu katika kutumia tena taka. Taka si taka hadi zitupwe. Kazi yote pia ni ya heshima. Nimejifunza pia kwamba ni muhimu kuwa mbunifu, kuvumbua na kuendelea kujiboresha kila wakati," anasema. "Safari yangu haijakuwa rahisi lakini nimejifunza kutokata tamaa kamwe. Nimegundua pia kwamba kuomba usaidizi inapobidi ni muhimu," anasema Bi Rutto. 'Ni muhimu kuomba usaidizi' "Wanawake wengi hufikiria kwamba kuomba usaidizi ni dalili ya udhaifu; ukweli ni kwamba ni ishara ya nguvu. Kupata washirika wafaao ni muhimu pia. Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali, shirikiana na wengine." Ushauri wake kwa wanawake ambao wangependa kufanikiwa katika viwanda ni kwamba lazima utafute soko la bidhaa zako kwanza. "Ningewahimiza wanawake wawe wabunifu na kuvumbua mambo na pia kuingia katika sekta ambazo zimetawaliwa na wanaume kwa muda mrefu mfano viwanda wakiona kuna fursa. "Usiige tu wengine au kuchagua biashara iliyo rahisi. Soko limejaa wahusika wengi na kuna changamoto katika kutafuta nafasi ya ukuaji." Baadhi ya watu huogopa kutofanikiwa lakini Bi Rutto anasema ni muhimu kujiamini mwenyewe. "Kuwa na ujasiri na anza bila kukawia. Usizuiwe na chochote, usizuiwe hata na mtaji. Ningewashauri wanawake kuacha na fedha walizo nazo na kuzitumia vyema." Anasema katika kuanzisha biashara au kiwanda, ni vyema kufikiria mchango wa biashara hiyo kwa jamii. "Moja ya yaliyosaidia ukuaji wa Ecopost ni nia yetu ya kutaka kuleta mabadiliko katika jamii, tukihifadhi mazingira pia." Haki na usawa kwa ndio mambo makuu yanayoshinikizwa duniani wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake wiki hii. text: Shinikizo katika baadhi ya timu zimesababisha kufutiliwa mbali kwa wakufunzi hao ama hata kupewa onyo la kufutwa iwapo misururu ya matokeo mabaya itaendelea kushuhudiwa. Hivi majuzi klabu ya AC Milan ilimteua Stefano Pioli kama meneja wake mpya, kufuatia kufutwa kwa Marco Giampaolo siku ya Jumanne baada ya miezi mitatu akiifunza timu hiyo. Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia msururu mbaya wa matokeo. Lakini sio timu hiyo pekee ambapo meneja alikabiliwa na shinikizo kali na hatimaye kufutwa. Kabu ya Olympique Lyonnais ya Ufaransa wiki hii imemfuta kazi kocha wake Sylvinho baada ya kuwa na matokeo mabovu toka walipompa kazi miezi michache iliyopita. Ijapokuwa hawajapigwa kalamu wakufunzi kama vile Zinedine Zidane wa Real Madrid ,Pochettino wa Tottenham na Marcos Silva wa Everton pia wapo chini ya shinikizo kufuatia matokeo mabaya. Katika klabu ya Everton , aliyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes anapigiwa upatu kuchukua mahala pake Silva huku Jose Mourinho akitarajiwa kumrithi Zinedine Zidane iwapo atapigwa kalamu. Silva huenda akaachishwa kazi baada ya timu yake kushindwa kupata ushindi wa ligi tangu siku ya kwanza ya mwezi Septemba licha ya kununua wachezaji wapya. Klabu hiyo ilimuunga mkono na zaidi ya £100m msimu uliokwisha lakini kumekuwa na ishara chache za timu hiyo kuimarika uwanjani. Mourinho ni miongoni mwa wakufunzi waliokumbwa na kipindi kigumu katika klabu ya Man United kufuatia matokeo mabaya yanayodaiwa kusababishwa na mbinu yake ya uchezaji, uhusiano mbaya kati yake na wasimamizi wa bodi ya timu hiyo pamoja na wachezaji na kadhalika. Ni nini kilichojiri? alipigwa shoka na mahala pake kuchukuliwa naye mkufunzi wa sasa Ole Gunnar Solskjaer ambaye ni mmojawapo wa wachezaji wa kikosi cha United kilichoshinda kombe la mabingwa Ulaya 2008. Je ni wakati kwa Ole Gunnar kuiaga Man United? Baada mkufunzi huyo kuanza na mguu mzuri, kwa kushinda mechi 14 kati ya 19 akiwa kaimu mkufunzi aliandikisha kandarasi ya miaka mitatu. Lakini tangu hapo kocha huyo ameshindwa kuinoa timu hiyo licha ya kupewa fursa ya kusajili wachezaji wakati wa dirisha la uhamisho lililopita. Na kufikia sasa timu hiyo ipo katika nafasi ya 12 na pointi 9 baada ya kucheza mechi nane huku ikishinda mara mbili kushindwa mara tatu na kutoka sare mara tatu. Wachanganuzi wanatabiri kwamba timu hiyo itajipata katika eneo la kushushwa daraja baada ya mechi dhidi ya Liverpool na Norwich hatua ambayo huenda ikaamua hatma ya kocha Olegunnar Solskjaer. Matumaini pekee ya United kujizolea pointi ni kucheza katika uwanja wa Old Trafford, lakini hilo pia halijaizuia United kupoteza mechi kufikia sasa, Kocha huyo ameshinda mechi mbili pekee kati ya 13 na hivyobasi kuwa mara ya kwanza kwa United kuanza vibaya katika ligi ya England katika kipindi cha miaka 30. Amedaiwa kuwaambia wachezaji wake kwamba kazi yake ipo hatarini baada ya klabu hiyo kushindwa na Newcastle mbali na kuwasisitizia wachezaji hao kwamba hatma zao hazijulikani iwapo hawataimarika , huku meneja mpya akitarajiwa kuchukua mahala pake. ''Ningependa kuomba msamaha kwa mashabiki kwa sababu hatushindi mechi , lakini hilo litanatokana na kuanza upya kujijenga, hivyobasi tumejipatia jukumu kubwa la kuweza kufaulu katika timu sita bora, bila kujali timu nne bora. Hivi sasa tunahitaji matokeo ili tuweze kwenda mbele'', alinukuliwa akisema. Je anahitaji muda zaidi Kocha huyo amekuwa akiomba kupewa muda zaidi na usimamizi wa timu hiyo kuwa na subra naye. Man United imejikuta imewekeza pakubwa na sio tu kwa kandarasi ya miaka mitatu aliyopewa kocha huyo. Mabadiliko ya kuwanunua Harry Maguire na hususan Aaron wan Bissaka pamoja na Dan James yamepokelewa vyema. Ukweli kwamba wachezaji hao watatu wameanza vyema ni swala ambalo limemshawishi Ed Woodward kwamba klabu hiyo ipo katika mwelekeo mwema. Tatizo ni kwamba Woodward na Man United wataendelea kulimbikiziwa lawama iwapo watahisi kuendelea kumuunga mkono Solskjaer. Hatahivyo baada ya kuruka kutoka mkufunzi mmoja hadi mwengine tangu alipostaafu Sir Alex Furguson kuna kiu cha mkufunzi ambaye ataendelea kuifunza timu hiyo . Ufutaji wa David Moyes, Louis Van Gaal hadi Jose Mourinho haukuwa mzuri na athari zake zilikuwa ghali mno. Lakini mapendekezo yoyote kwamba hilo pekee ni sababu kwa Solskjaer kusalia katika wadhfa huo - baada ya msururu wa matokeo ambayo yameleta ushindi mara 2 katika mechi 13 za ligi ya England - ni kutoeleweka kwa jukumu la mkufunzi katika klabu ya kisasa. Solskjaer anazungumzia kuhusu kuimarisha utamaduni wa klabu hiyo na ni swala linalovutia kwa kweli ,lakini Sera kama hizo zinawezekana bila yeye kuwepo. United haimuhitaji mkufunzi huyo kutilia mkazo sera ya kuleta wachezaji vijana na wale walio na kiu katika kikosi hicho. Lengo lake ni kuimarisha timu hiyo uwanjani na kutumia raslimali zilizopo kwa lengo la kupata matokeo mazuri - kupitia mbinu nzuri ya mchezo. Lakini hali ilivyo ni kwamba ameshindwa na hana rekodi yoyote ya kumshawishi mtu yeyote kwamba atafanya lolote isipokuwa kuendelea kufeli katika siku za usoni. Ni msimu mwengine ambao wakufunzi walioshindwa kuzisaidia timu zao kuvuka viwango fulani wamepata shinikizo kali kutoka kwa bodi simamizi za timu wanazofunza mbali na mashabiki wa timu hizo. text: Liverpool inacheza na Leicester leo 26 Desemba kisha dhidi ya Wolves 29 Desemba Majogoo wa Jiji Liverpool, wanaminyana na Leicester siku ya Alhamisi, na baada ya hapo kucheza na 'Wolves' siku ya Jumapili, lakini timu zingine zimepata siku moja tu ya kupumzika kabla ya kuingia tena uwanjani. Liverpool itakuwa imecheza michezo tisa ndani ya mwezi huu Disemba, baada ya kushinda kombe la klabu la dunia nchini Qatar na kushindwa katika kombe la Carabao. ''Sio sawa kabisa'' amelalama Klopp. ''Na bado tuna mechi. Hakuna meneja hata mmoja aliyekuwa na tatizo la kuwa na mechi katika siku ya ''Boxing Day'' lakini kucheza tarehe 26 na 28 ni uhalifu.'' ''Tunaweza kusema chochote tunachokitaka lakini hakuna mtu yoyote anayejali, lakini kila mwaka kitu hicho kinajirudia kwa makocha wanaoshiriki.'' Kombe la klabu la dunia ni taji la pili kwa Liverpool msimu huu na wana alama 10 juu ya chati ya Ligi ya Primia wakiwa na mechi moja ya kiporo mkononi. Taji lao la kwanza lilikuwa kombe la Uefa Super Cup waliolipata Agosti baada ya kuichapa Chelsea kwa mikwaju ya penati. Nusu fainali na fainali nchini Qatar ziligongana na kwa robo fainali za kombe la Carabao dhidi ya Aston Villa, kitendo ambacho kiliwafanya watume timu nyingine kushindana katika mashindano hayo. Vijana wa Klopp, ambao wanaikimbiza nafasi ya kwanza kwa Liverpool ndani ya miaka 30 kushinda Ligi ya Primia, watakuwa na siku mbili tu za kupumzika katikati ya mechi za ligi katika msimu huu wa sikukuu , lakini klabu 14 zitakuwa na siku moja tu ya kupumzika kati ya mechi nyingine. "Hakuna sababu ya kutoa saa chini ya 48 kwa timu kucheza mechi nyengine katika ligi," Klopp ameongeza. "Sayansi ya michezo haikupi kitu cha kukabiliana nacho, mwili unahitaji muda fulani kupumzika. Ni rahisi. Hiyo ni sayansi. Lakini hilo linapuuzwa kabisa." Crystal Palace inayonolewa na Roy Hodgson inacheza na West Ham nyumbani Alhamisi hii saa 18:00 (Saa za Afrika Mashariki) na saa 48 baadaye itakipiga na Southampton ugenini Jumamosi saa 18:00 (Saa za Afrika Mashariki). "Nilifurahia mazoezi, mechi zenyewe ni kidogo na nafikiri kwamba kucheza kwa kiwango tunachocheza ukilinganisha na muda tunaopumzika haviendani," amesema Hodgson. "Si jambo gumu kutatuliwa. Silifurahii kwa kweli na najua huu ni wakati hatari sana - kunaweza kuwa na majeruhi, pamoja na uchovu. Na ghafla utajiona unaangalia juu ya jwedwali badala ya chini." Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ni uhalifu mkubwa kwa timu za Ligi ya Primia kucheza mechi mbili ndani ya siku tatu katika msimu huu wa Sikukuu. text: Skauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya Alhamisi Mashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0 Huyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon. Mechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa). Wacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana. Mwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua kwa huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano. Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili. Hali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini Morocco Familia hii ni moja kati ya maelfu ya watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea Uganda Siku ya Jumatatu, wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra Leone Uchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP) Nchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi. Kikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti. Mkusanyiko wa picha nzuri zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika maeneo mbalimbali duniani wiki hii. text: Rais Nkurunziza akiidhinisha marekebisho ya katiba Ametoa tangazo hilo akiwa eneo la Bugendana, Gitega ambapo alikuwa anaidhinisha katiba mpya ya nchi hiyo. Mwezi uliopita, raia nchini humo walipiga kura na kuunga mkono kwa wingi marekebisho ya katiba ambayo yalifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo kubadilisha muhula wa rais kutoka miaka mitano kuwa saba. Mwandishi wa BBC Bujumbura Ismail Misigaro amesema kwa sasa wengi wanatarajiwa kutakuwa na mabadiliko katika baraza la mawaziri karibuni. Wengi waliamini Bw Nkurunziza ndiye aliyeshinikiza kufanyika kwa kura hiyo ya maoni ili kumpa fursa ya kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034. Matokeo yaliyotolewa na tume hiyo yalionesha waliokuwa wanaunga mkono marekebisho hayo walikuwa 73.6%. Waliokuwa wanapinga walikuwa19.3% ilhali kura 4.1% ziliharibika. Asilimia 3.2 ya wapiga kura hawakuunga mkono upande wowote. Wapiga kura zaidi ya 98% ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo hawakushiriki shughuli hiyo. Rais wa Burundi walikuwa wanaamua iwapo muda wa muhula wa rais uongezwe kutoka miaka mitano hadi miaka saba, yenye kikomo cha mihula miwili. Marekebisho hayo ya katiba yanamruhusu Nkurunziza kuwania uchaguzi wa mwaka 2020 na angeweza kuwania kwa mihula mingine miwili chini ya katiba mpya, kwani kuhesabiwa kwa mihula kungeanza tena baada ya mwaka huo. Aliwania kwa muhula wa tatu mwaka 2015 hatua iliyozua utata na kusababisha msururu wa ghasia na jaribio la mapinduzi ya serikali. Mamia ya watu walifariki na wengine 400,000 kukimbia nchi hiyo na kutorokea mataifa jirani. Burundi imebadilisha katiba yake mara kadhaa miaka ya hivi punde. Burundi ina historia ya machafuko tangu miaka ya 60, mabaya zaidi yakiwa ya miaka ya 90 ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 300,000. Mkataba wa Amani uliotiwa sahihi Arusha ndio ulimaliza vita hivyo na kumwezesha Pierre Nkurunziza kuwa rais. Alitarajiwa kuondoka madarakani mwaka 2015 lakini akaamua kuwania kwa muhula mwingine. Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kwamba hataomba kuchaguliwa tena baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2020. text: Hivi ndivyo msanii Evans Yegon alivyomchora Bwana Trump Afrika Kusini- na Pumza Fihlani Afrika kusini imeweza kujiweka katika hali ya nchi ambayo haihitaji misaada bali mshirika mwenye uwezo na anayejiamini kibiashara . Lakini mazungumzo magumu na Marekani kuhusu makataba wa fursa ya ukuaji wa kiuchumi wa Afrika (AGOA) mwishoni mwa mwaka jana huenda yalikuwa ukumbusho kwa nchi zinazoendelea kuhusu mahala halisi zilipowekwa kiuchumi na Marekani. Baaadhi ya wakosoaji wa Mapatano ya AGOA wanasema Afrika kusini, kama mataifa mengi ya Afrika, ilikuwa ngao thabiti katika kukubali masharti ambayo hayainufaishi kwa minajili tu ya kupata mshirika thabiti. Bwana Trump ana sifa ya kuwa mfanyabiashara maarufu, na huku haijawa wazi ni sera gani aliyo nayo kwa Afrika kusini, baadhi nchini humo wana hofu kuwa huenda uhusiano mzuri iliyokuwa nayo nchi yao na Marekani ukavunjika. Wanasema utawala wa mfanyabiashara huyo huenda ukaitaka Afrika Kusini kuonnyesha ni kwa nini inafaa kuwa katika kikosi cha Bwana Trump. Nigeria - na Naziru Mikailu Tangu kuchaguliwa kwa rais Muhammadu Buhari mwaka jana , Nigeria imeboresha uhusiano na Marekani uliotiwa dosari kubwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya jeshi la Nigeria, hususan katika vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram . Jeshi la Nigeria lilipata mafunzo na zana kutoka kwa utawala wa Obama na bila shaka itataka kuendeleza uhusuiano huu ulioboreka. Nigeria pia itataka uhusiano wa kibiashara na taifa lililoimarika zaidi kiuchumi duniani. Hivi ndivyo magazeti ya Kenya yalivyoripoti ushindi wa Trump Kwa upande mwingine nchi hizi mbili zinaweza kujikuta katika uhasama ikiwa Bwana Trump ataamua kuwatambua waasi wanaotaka kujitenga wa Biafra. Pia inasemekana kuna raia wa Nigeria zaidi ya milioni moja wanaoishi nchini Marekani , na baadhi wanahofu kwamba sera za uhamiaji za Bwana Trump zinaweza kupelekea maelfu yao kurejeshwa nyumbani. Uganda - na Catherine Byaruhanga Serikali ya Marekani hutoa msaada wa dola milioni mia saba ($700m) kwa Uganda kila mwaka. Mingi kati ya misaada hiyo huelekezwa katika mipango ya kuboresha afya, hususan dawa utoaji wa dawa za bure za HIV/Aids kwa wale wanaozihitaji. Kiasi cha pesa kisichojulikana pia hutolewa kwa ajili ya msaada wa jeshi. Hakuna maelezo yanayotolewa lakini kutokana na kwamba Uganda imeongeza kikosi cha askari wake wa kulinda amani katika mataifa ya kigeni, ikiwemo Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, serikali ya Washington imekuwa mfadhili wake mkuu. Marekani pia imekuwa ikitoa msaada wa mafunzo kwa wanajeshi. Katika barua ya hivi karibuni kwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni, maafisa wa mpito wa Bwana Trump walihoji kuhusu shughuli hizi. Hofu ya Uganda ni kwamba utawala mpya utasitisha ama kupunguza msaada huu .Kwa upande mwingine baadhi ya wapinzani wamedai kuwa wafadhili wa kimataifa hawakuipatia serikali msaada unaofaa. Katika sekta ya afya , kupunguzwa kwa msaada kunaweza kuwaacha wengi mashakani. Kenya and Somalia - na David Wafula Takriban theluthi moja ya Wakenya 90,000 wanaoishi Marekani ni wahamiaji haramu, kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Pew . Hii inamaaninsha kuwa zaidi ya watu 30,000 wanaweza kurejeshwa nchini Kenya kama Donald Trump atatekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwarejesha makwao wahamiaji haramu. Hii itaathiri kwa kiasi kikubwa kipato chao wanachotuma nyumbani kinachokadiriwa kuwa dola milioni sitini ($60m ) kutoka Marekani na Canada mwaka 2015. Walipokuwa wakitathmini uhusiano baina ya Marekani na Kenya pamoja na Afrika kwa ujumla maafisa wa mpito wa Bwana Trump walielezea hofu yao kuhusu hali ya baadae ya ushirikiano huo. Walihoji ni kwanini Marekani imekuwa ikipigana na al-Shabab kwa muongo mzima bila kushinda vita hivyo. Na walihoji ikiwa pesa ambazo Washington inatoa kama msaada kwa nchi mbali mbali za Afrika zinatumiwa kwa kwa umakini. Zimbabwe - na Shingai Nyoka Serikali ya rais Robert Mugabe imesema inatumaini mabadiliko ya hali iliyowezoweleka yanaweza kuisasidia kurejesha uhusiano baina yake na Washington. Bwana Mugabe, baadhi ya maafisa wake na baadhi ya makampuni yanayomilikiwa na serikali yanakabiliwa na vikwazo vya kusafiri nchini Marekani na kiuchumi tangu wakati wa utawala wa rais George W Bush' kufuatia mnadai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Bwana Mugabe anaamini vikwazo hivyo vinakiuka sheria. Hata hivyo bado Trump hajatoa tamko lolote kuhusu Zimbabwe ama Bwana Mugabe na hakuna ishara yoyote kwamba msimamo wake kwa Zimbabwe utatofautiana na ule waliokuwa nao watangulizi wake. Donald Trump alishinda urais baada ya kusema kuwa atafanya mabadiliko makubwa kuhusu mahusiano ya nchi yake na nchi nyingine duniani. Je kuingia kwake katika ikulu ya White House kuna maana gani kwa nchi tofauti za Afrika ? text: Warmbier alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu Wazazi wa Otto Warmbier wanasema kuwa waliambiwa wiki iliyopita kuwa alikuwa hali mahututi. Walisema kuwa walitaka ulimwengu ujue ni kwa njia gani wao na mtoio walivyohangaishwa na Korea Kaskazini, Mamlaka za Korea Kaskazini zinasema kuwa alipewa tembe ya usingizi baada ya kuwa mgonjwa Bwana Warmbier alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu, baada ya kukiri kuwa alijaribu kuiba bango lenye ujumbe wa propaganda. Mamlaka za Korea Kaskazini zinasema kuwa alipewa tembe ya usingizi baada ya kuwa mgonjwa muda mfupi baada ya hukumu yake na tangu wakati huo hajaamka. Watu wengine watatu raia wa Marekani bado wanaaminiwa kufunngwa nchini Korea Kaskazini. Mwanafunzi raia wa Marekani ambaye aliachiliwa kutoka gerezani nchini Korea Kaskazini, amepelekwa hospitalini nchini Marekani. text: Kifaru cha Urusi kikielekea kwa mazoezi ya kijeshi ya Zapad Mazoezi hayo ni moja ya mazoezi makubwa kabisa ya kijeshi kuwahi kufanywa na Urusi tangu ilipotwaa rasi ya Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi 12,700 wanashiriki, lakini wataalamu wa Nato wanatarajia kwamba idadi itakuwa juu zaidi ya hiyo. Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika ndani na maeneo ya karibu na belarus na yanashirikisha vifaru, ndege za kivita na manowari. Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameonya kuwa Zapad-2017 (jina ambalo maana yake kwa Kirusi ni "Magharibi") huenda ikawa ni hatua ya mwisho kabla ya kuivamia Ukraine. Kiev imeimarisha ulinzi wake mpakani. Makundi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi wanadhibiti maeneo makubwa ya mashariki mwa Ukraine na wameendelea kukabiliana na wanajeshi wa serikali. Bomu la nyuklia la USSR lililoishangaza dunia Hii ni licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha mapigano Februari mwaka 2015 mjini Minsk. Nato imeituhumu Urusi kwa kuwapa waasi hao silaha kalikali pamoja na wanajeshi. Urusi imekanusha tuhuma hizo, lakini imekiri kwamba kuna baadhi ya raia wa Urusi "wanaojitolea" wanaowasaidia waasi hao. Nato imetuma wanajeshi jumla ya 4,350 Poland, Estonia, Latvia na Lithuania, nchi ambazo zinapakana na Belarus na Urusi. Nchi 29 wanachama wa Nato pia zinashika doria angani katika mataifa ya eneo la Baltic. Kinachofanyika wakati wa mazoezi ya sasa ya kijeshi ya Zapad-2017 ni kuigiza hali dhahania ya maasi nchini Belarus ikiongozwa na "wasaliti" na "magaidi" wanaoungwa mkono na nchi dhahania kwa jina "Veishnoria". Wanajeshi wa Urusi wanatumwa Belarus kuisaidia kumaliza maasi hayo. Lengo kuu ni jinsi ya kuunganisha makao makuu ya kijeshi ya mataifa hayo mawili wakati wa vita. Belarus imetuma wanajeshi 7,200 na Urusi imetuma wanajeshi 5,500, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema. Jimbo la Urusi la Kaliningrad - ambalo lipo katikati ya Poland na Lithuania ambazo ni nchi wanachama wa Nato - limeshirikishwa katika mazoezi hayo ya kijeshi. Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ana uhusiano wa karibu na Urusi, ingawa kumekuwepo na mzozo wa mara kwa mara kati ya serikali yake na Urusi kuhusu biashara. Urusi na Belarus zimeanza mazoezi makubwa ya pamoja ya kijeshi, ambayo yamepewa jina Zapad-2017, na ambayo yamezitia wasiwasi nchi jirani wanachama wa shirika la kujihami la nchi za Magharibi la Nato. text: Picha za barafu hiyo iliyopigwa na satelaiti ya Suomi NPP inayomilikiwa na NASA Jiwe hilo kubwa la barafu linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilomita mraba 6,000, ukubwa sawa na wa eneo la Wales nchini Uingereza. Kipande hicho cha barafu kina ukubwa mara 50 kushinda kisiwa cha Manhattan, Marekani Satelaiti ya Marekani ilionesha jiwe hilo kubwa likiwa limemeguka ilipokuwa inapitia eneo la barafu lifahamikalo kama Larsen C Jumatano. Wanasayansi walikuwa wanatarajia hilo. Wamekuwa wakifuatilia ufa mkubwa katika barafu ya Larsen kwa zaidi ya mwongo mmoja. Larsen C ndiyo sehemu kubwa ya barafu iliyo kaskazini zaidi mwa dunia eneo la Antarctica. Watafiti walikuwa awali wamesema iwapo eneo hilo lingepoteza kipande hicho cha barafu basi sehemu yote yenyewe itakuwa hatarini ya kupasuka tena siku za usoni. Eneo la barafu la Larsen C lina kina cha mita 350. Barafu hiyo huelea maeneo ya pembeni Antarctica Magharibi na kuzuia mito ya barafu ambayo huisaidia kukaa imara. Watafiti wamekuwa wakifuatilia Larsen C baada ya kumeguka kwa sehemu ya barafu ya Larsen A mwaka 1995 na kisha kupasuka ghafla kwa sehemu ya barafu ya Larsen B mwaka 2002. Wataalamu wanakadiria kwamba iwapo barafu yote kwenye sehemu hiyo ya bahari ya Larsen C itayeyuka na kuwa maji na kuingia baharini, viwango vya maji baharini vitapanda kwa sentimeta 10. Ufa uliokuwa kwenye eneo hilo la barafu kabla ya kipande hicho kumeguka Picha zilizopigwa Novemba mwaka jana zikionyesha ufa uliotokea Kwa sasa ni katikati mwa majira ya baridi Antarctic. Ufa kwenye barafu hiyo ulipigwa picha majira ya joto yaliyopita. Kipande kikubwa zaidi cha barafu kuwahi kuonekana duniani kimemefuka kutoka kwenye eneo la Antarctica. text: Romelu Lukaku Raia huyo wa Ubelgiji wa miaka 24 alifunga mabao 26 katika Ligi ya Premia msimu uliopita. United, wamekuwa wakimtafuta Lukaku kwa kipindi kirefu majira haya ya joto. Baada ya kumpata mshambuliaji huyo, sasa hawana haja tena ya kumtafuta Alvaro Morata wa Real Madrid. Mazungumzo kuhusu kuhama kwa Lukaku hayahusiani na mazungumzo kuhusu uwezekano wa mshambuliaji wa United Wayne Rooney kurejea Everton. Klabu hiyo ya Jose Mourinho ina matumaini kwamba itakamilisha usajili wa Lukaku kwa wakati kumuwezesha kujiunga na kikosi cha timu hiyo kitakachosafiri kucheza mechi za kabla ya msimu nchini Marekani Jumapili. Mshambuliaji huyo alikuwa miongoni mwa orodha ya wachezaji ambao Mourinho aliwasilisha kwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kwamba alitaka kuwanunua kabla ya msimu kumalizika. Awali, ilidhaniwa Lukaku angerejea katika kalbu yake ya awali Chelsea, ambayo alijiunga nayo kutoka Anderlecht mwaka 2011. Mshambuliaji huyo aliuziwa Everton kwa £28m na Mourinho mkufunzi huyo kutoka Ureno alipokuwa katika kipindi chake cha ukufunzi Chelsea mwaka 2014. Lukaku ni mteja wa wakala Mino Raiola, ambaye pia huwasimamia Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan - wachezaji watatu walionunuliwa na United majira ya joto msimu uliopita. Mbelgiji huyo alikataa ofa ya juu sana kutoka Everton Machi na kusema: "Sitaki kusalia katika kiwango sawa. Ninataka kujiboresha na najua ni wapi nahitaji kwenda kutimiza hilo." Manchester United wameafikiana na klabu ya Everton kulipa £75m kumchukua mshambuliaji Romelu Lukaku. text: Hadi sasa, chanjo mbili dhidi ya virusi vya rotavirus zimekuwa zikitumika kuzuwia maambukizi hayo, lakini zote ni ghali na lazima ziwekwe kwenye friji Upatikanaji wa chanjo hii umeonekana kama mafanikio makubwa pale itakapofika kwenye masoko kwa kuwa inatarajiwa kuuzwa kwa bei nafuu kuliko chanjo nyingine zilizopo na haihitaji kuwekwa ndani ya friji. Matokeo ya majaribio ya chanjo hiyo yaliyofanyika nchini Niger yamechapishwa katika jarida la tiba la Uingereza. Inakadiriwa kuwa watoto 1,300 hufa kila siku kutokana na kuhara kunakosababishwa na rotavirus. Hadi sasa , chanjo mbili zimekuwa zikitumika kuzuwia maambukizi hayo, lakini zote ni ghali na lazima ziwekwe kwenye friji. Watoto wengi katika jamii zenye kipato kidogo ambazo hazina huduma ya umeme hushindwa kupata chanjo hiyo. Lakini sasa , shirika la madaktari wasio na mpaka - MSF -linasema kuwa chanjo mpya iliyofanyiwa majaribio nchini Niger inaweza kusaidia kuokoa maisha ya watoto wanaoihitaji zaidi. Dawa hiyo mpya inaweza kutibu aina ya virusi vya rotavirus vinavyopatikana katika nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika. Inatarajiwa kugharimu chini ya dola mbili unusu kwa kila mtoto. Lakini kabla kutengenezwa ama kusambazwa chanjo zilizokuwepo kulihitaji kwanza idhini ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Chanjo mpya dhidi ya maradhi hatari ya virusi vya rotavirus - yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya utotoni imethibitishwa kufaa na salama. text: Rais Trump akiwa katika mkutano wa kampeini jimbo la Indiana siku moja kabla ya kura ya katikati ya muhula Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa kwenye Pwani ya Mashariki huku vyama vya Republican na Demoratic vikipania kuchukua udhibiti wa mabunge ya uwakilishi na Seneti. Uchaguzi huu wa katikati ya muhula unakuja wakati rais Trump amefikia nusu ya muda wa uongozi wake madarakani. Uchaguzi huo pia unatarajiwa kubaini ikiwa Trump ana uwezo wa kuongoza Marekani katika kipindi cha miaka miwili ijayo. Shauku ya upigaji kura inatarajiwa kuchochea watu wengi zaidi kushiriki zoezo hilo. Viti 435 katika bunge la waakilishi na viti 35 kati ya 100 katika Seneti vinakabiliwa na ushindani mkubwa. Siku za hivi karibuni rais Trump amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwasilisha hoja ambazo zinaonekana kuzua hisia mseto katika juhudi ya kuimarisha uungwaji mkono wake. Aliyekuwa mtangulizi wake, Barack Obama - amekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeini za chama cha Democratic - amesema "hulka ya taifaletu iko katika sanduku la upigaji kura". Ni masuala gani muhimu katika uchaguzi huu? Wakati wa kampeini zake za mwisho katika majimbo ya Ohio, Indiana na Missouri, bwana Trump alirejelea masuala muhimu yaliyomsaidia kushinda uchaguzi wa mwaka 2016 akisisitiza kuwa Democrats watasambaratisha uchumi na kwa kuruhusu uhuamiaji haramu. Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama Wagombea wa Democratic kwa upande wao wameamua kujiepusha na makabiliano ya moja kwa moja na wapinzani wao na badala yake kuangazia masuala ibuka kama vile ya afya na ukosefu wa usawa katika mambo ya uchumi. Chama hicho kunatumai kuwa wapiga kura vijana na wale wanaotokea katika makundi ya wachache waliyotengwa watavutiwa na kura hiyo kama hatua ya kupinga msimamo wa rais Trump dhidi ya masuala yanayo wagusa wao na wenzao moja kwa moja. Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutokana na lugha yake ambayo inadaiwa kuwagawanya watu. Upigaji kura wa mapema ulianza Novemba 4 katika majimbo ya Los Angeles na California Watafiti wa kura ya maoni wanabashiri kuwa Democrats huenda wakashinda viti 23 wanazohitaji kuongoza bunge la waalikilishi , na viti vingine zaidi kama 15 za ziada. Hata hivyo Democrats wanatarajiwa kupoteza viti viwili kupoteza nafasi hiyo ambayo itawawezesha kuchukua udhibiti wa bunge la Seneti. Nini kitakachofanyika wakati wa uchaguzi? Baada ya miezi kadhaa ya kampeni, uvumi na mabilioni ya dola zilizotumika kwenye matangazo, wapiga kura hatimae watakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi yao ya mwisho siku ya Jumanne. Watu milioni 35 tayari wameshapiga kura na katika jimbo la kusini mwa Texas, idadi ya watu waliojitokeza mapema kupiga kura, tayari imepita jumla ya waliopiga kura katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Magavana pia chatachaguliwa katika majimbo 36 kati ya 50 Stacey Abrams anapania kuandikisha historia ya kuwa gavana wa kwanza mwanamke Marekani Uchaguzi huu unamaanisha nini? Uchaguzi wa katikati ya muhula utaamua ni nani atakayechukua udhibiti wa mabunge yote mawili ambayo yanatunga sheria ya nchi. Ikiwa Republicans watafanikiwa kuendelea kuongoza mabunge ya seneti na ya uwakilishi, huenda wakaimarisha ajenda ya chama na ile ya rais Trump. Lakini Democrats wakiwapokonya jukumu hilo huenda wakabadilisha mipango ya bwana Trump. Katika mahojiano na runinga ya ABC siku ya Jumatatu, rais Trump alisema anataka kupunguza makali ya matamshi yake katika kipindi kilichosalia cha uongozi wake. "Nahisi kwa kiwango fulani, sina chaguo, nadhani nilitakiwa kupunguza makali ya matamshi yangu kuanzia mwanzo." Wamarekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa wa katikati ya muhula ambao unaonekana kama kura ya maoni kuhusu urais wa Donald Trump. text: Rais huyo aliwapa mwaliko wa kukutana naye ikulu, ambapo mkutano ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Picha zilizotolewa na ikulu hata hivyo zinaonesha Bw Kikwete hakuhudhuria mkutano huo. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kukutana na viongozi hao wakuu wastaafu na taarifa ya ikulu imesema lengo lilikuwa "kupokea ushauri na maoni yao juu ya uendeshaji wa Serikali na mustakabali wa Taifa". Dkt Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim Magufuli akisalimiana na Spika Mstaafu Anne Makinda. Aliyeketi karibu na Bi Makinda ni Spika Msaafu Pius Msekwa Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Dkt Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume kabla ya kikao Picha ya pamoja ya viongozi waliohudhuria Ni miaka miwili na nusu sasa tangu serikali ya Awamu ya Tano yake Rais Magufuli ilipoingia madarakani. Bw Lowassa aliwania urais mwaka 2015 dhidi ya Dkt Magufuli lakini akamaliza akiwa wa pili. Miongoni mwa waliofika kulikuwa na rais wa zamani Benjamin Mkapa. Waziri Mkuu Mstaafu John Samwel Malecela akizungumza katika mkutano huo Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli ametumia fursa hiyo pia kuwaeleza viongozi hao juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali yake ambapo ni pamoja na uongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali ambao amesema umeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 800 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.3 kwa mwezi. Aidha, kuna kuanza ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma utakaogharimu Shilingi Trilioni 7.26, kujenga mradi wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers' Gorge) utakaozalisha Megawati 2,100 za umeme, kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo na kuongeza mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Unaweza kusoma pia: Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amekutana na marais wa zamani pamoja na viongozi wengine wa zamani walioshikilia nyadhifa mbalimbali serikali. text: Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton Rob Goldstone ambaye alipanga mkutano huo wa Juni mwaka 2016, aliandika hayo kupitia barua pepe. Bwana Trump Jr alitetea hatua ya kuhudhuria mkutano huo akisema kuwa ahadi ya taarafa potovu aliyopewa haikuwepo. Trump Jr amekana kutoa habari za kukanganya kuhusu mkutano huo wa mwaka uliopita. Pia amesema kuwa lilikuwa jambo la kawaida kupata taarifa kuhusu wagombea pinzani. Maafisa nchini Marekani wanachunguza madai yanayohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani. Mkwe wa Trump Jared Kushner na aliyekuwa mkuu wa kampeni Paul J Manafort, walikuwa pia katika mkutano huo na Natalia Veselnitskaya. Jared Kushner hajazungumza kuhusu taarifa ya Donald Trump Jr Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton, ambaye alikuwa mshindani wa babake katika kiti cha urais. Mkutano huo ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower, wiki mbili baada ya Donald Trump kupata uteuzi wa Republican. Unaaminiwa kuwa mkutano wa kwanza wa siri kati ya raia wa Urusi na watu waliokuwa karibu na Bwana Trump. Baada ya New York Times kuripoti mara ya kwanza kuhusu mkutano huo siku ya Jumamosi, Bwana Trump Jr alitoa taarifa iliyothibitisha kuwa mkutano huo ulifanyika lakini haikutaja ikiwa ulihusu kampeni ya kuwania urais Mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump, Donald Trump Jr , aliambiwa kuwa taarifa kumhusu Hillary Clinton ambayo angepewa na wakili wa Urusi, ilikuwa sehemu ya jitihada za Urusi kumsaidia babake katika kampeni ya uchaguzi text: De Bruyne alichechemea na kuondoka uwanjani baada ya kuonekana kuumia dakika tatu kabla ya mechi kumalizika. Nyota wa mechi hiyo alikuwa kinda Mhispania Brahim Diaz ambaye alifunga bao moja kila kipindi, dakika ya 18 na 65, hayo yakiwa mabao yake ya kwanza kufungia timu kubwa ya Manchester City. City sasa watakutana na mshindi wa mechi kati ya Leicester na Southampton kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo hufahamika kama Kombe la Carabao. Mbelgiji De Bruyne mwenye miaka 27 alikuwa ameanza mechi kwa mara yake ya pili pekee msimu huu tangu alipopata jeraha kwenye kano za goti lake la kulia mwezi Agosti. "Anachunguzwa na madaktari," alisema meneja wa City Pep Guardiola baada ya mechi. "Hatujafahamu kufikia sasa iwapo hakuna kitu chochote kibaya kimemtendekea au kama ni kitu kibaya." De Bruyne alikuwa amecheza vyema sana na kuonekana kujituma uwanjani lakini aliondoka uwanjani akiwa anagusa goti lake la kushoto, na moja kwa moja akaelekea chumbani kupokea matibabu. Viongozi hao wa Ligi ya Premia kwa sasa walikuwa wamefanya mabadiliko 10 kwenye kikosi chao kilicholaza Tottenham Jumatatu lakini bado waliwazidi nguvu Fulham waliotumia kikosi chao cha kwanza, walikuwa na makombora 27 yaliyolenga goli wakilinganishwa na wageni wao waliolenga goli mara tano pekee. Debi ya Manchester City watafahamu klabu watakayokutana nayo robo fainali mnamo 27 Novemba mechi kati ya Leicester na Southampton - iliyoahirishwa kutokana na ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha mmiliki wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha na watu wengine wanne wakiondoka uwanjani Jumamosi - itakapochezwa. Ustadi wa De Bruyne na juhudi zake vilionekana wazi uwanani Etihad na alitamba safu ya kati na kwenye mashambulizi kuhakikisha City wanaidhibiti mechi. Kevin de Bruyne hakucheza kwa miezi miwili msimu huu kutokana na jeraha la goti Alikuwa amecheza dakika 150 pekee kwa jumla msimu wa 2018-19 kabla ya mechi hiyo na hakuonekana kuwa na uchovu. Alishambulia mara kwa mara na alionekana kujizatiti kuupata mpira tena kila City walipopokonywa. Alikabili wapinzani na kushinda mpira mara saba, na akazuia mpira mara tatu. "Ni kawaida kwa watu kusema mchezaji ameonyesha kiwango cha kuwa stadi zaidi duniani, lakini hautakuwa unaongeza chumvi ukisema kuhusu uchezaji wa De Bruyne," Pat Nevin aliyekuwa akichambua mpira katika BBC Radio 5 alisema. Huku kukiwa na mechi nyingine tano za kuchezwa Novemba, ambapo miongoni mwake kuna mechi ya debi dhidi ya Manchester United uwanjani Etihad, Guardiola atatumai kwamba De Bruyne hakuumia sana. Brahim Diaz alikuwa anachezea Manchester City mechi yake ya 14, lakini ilikuwa mara yake ya tatu kuanza mechi Nini kinafuata? Mkimbio wa City kucheza mechi tano katika kipindi cha siku 13 utaendelea kwa mechi ya nyumbani Ligi ya Premia dhidi ya Southampton Jumapili. Watarejea tena uwanani Etihad Stadium Jumatano wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Fulham, wanaotafuta ushindi wao wa kwanza ligini tangu 26 Agosti, watarejea kusaka ushindi watakapokuwa wageni wa Huddersfield wanaoshika mkia ligini Jumatatu. Fulham wanashikilia nafasi ya 18 kwenye jedwali. Manchester City walifanikiwa kuwalaza Fulham 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Ligi iliyochezwa Alhamisi lakini wameingiwa na wasiwasi kuhusu kiungo wao nyota Kevin de Bruyne. text: Diamond Platinum aanzisha biashara ya kuuza njugu karanga Msanii huyo alizindua bidhaa ambayo sasa iko madukani nchini Kenya. Huku wasanii wengi wakitumia muda wao mwingi kuuza tisheti, Diamond alianzisha manukato ya Chibu ambayo ni bidhaa ya kipekee. Msanii huyo baadaye alifanya kile ambacho wengi hawakutarajia kwa kuzindua njugu karanga siku ambayo alimkaribisha Rayvanny nchini Tanzania. Hivi ndivyo alivyoandika katika chapisho lake la akaunti yake ya facebook siku ya Alhamisi: USISEME KARANGA SEMA DIAMOND KARANGA!!!!...Habari njema kwa Vijana wenzangu wote, sasa unaweza kujipatia Mtonyo wa ChapChap kupitia @diamondkaranga ambapo utaweza kununua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa boksi moja lenye pakiti Mia moja (100) ndani ambazo ukiuza unapata faida ya elfu kumi fanya mawasiliano sasa na mawakala walio karibu yako. Msanii wa muziki wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platinums sasa amepanua biashara yake katika harakati za kuwafurahisha mashabiki na wateja wake. text: Jina la mbwa huyu lilimuweka matatani mmiliki wake kwa mujibu wa gazeti maarufu nchini humo Beijing News, mmiliki wa mbwa mwenye umri wa miaka karibu 30 aliyetambulika kwa jina la kifamilia kama Ban anayeishi katika jimbo la mashraiki la Anhui Province aliitwa na polisi Jumatatu, baada ya kutuma picha ya mbwa wawili kupitia messenger WeChat kwa njia ya simu yake wakiwa na majina Chengguan na Xieguan Majina hayo yaliibua utata kwasababu yalikuwa ni majina ya wafanyakazi wa huduma za serikali na kiraia wanaoheshimiwa. "Chengguan" ni maafisa waliajiriwa katika maeneo ya mijini kukabiliana na uhalifu mdogo na "Xieguan" ni wafanyakazi wasio rasmi wa jamii kama vile wasaidizi wa maafisa wa usalama barabarani. Gazeti hilo linasema Bwana Ban aliwapatia mbwa wake majina kwa ajli ya ''kujifurahisha'' lakini maafisa hawaoni mzaha wowote katika lolote. Polisi wa Yingzhouwanasema wameanzisha uchunguzi mara moja juu ya mwanamume huyo, ambaye wanasema alikuwa ametoa taarifa za matusi dhidi ya wahudumu wa usalama. Wameongeza kuwa, "kulingana na vipengele husika vya sheria ya wa watu wa Uchina kuhusu usalama wa umma ", lazima awekwe kwenye kituo cha mahabusu ya utawala iliyopo Xiangyang kwa siku 10. Amesababisha madhara Bwana Ban lazima awekwe lumande kwa siku 10 kwa kuwaita mbwa wake majina yenye utata Afisa wa polisi aliyetambuliwa kwa jina lake la ubini kama Li aliliambia gazeti la Beijing News kwamba Bwana Ban amekuwa akiendeleza uchokozi kwenye akaunti yake ya WeChat, na kuongeza kuwa hatua zake "zimesababisha madhara makubwa kwa taifa na kwa utawala wa jiji hasa upande wa hisia ". Bwana Ban anasema anajutia matendo yake huku gazeti la Beijing New likimnukuu akisema "Sikujua sheria, sikujua hii ilikuwa ni kinyume cha sheria ." Huku baadhi wakisema kuwa alikuwa ''anajitafutia matatizo ", kukamatwa kwake kumewashtua watumiaji wengi wa mtandao maarufu wa Sina Weibo microblog. Watumiaji wengi wameonyesha hofu yao juu ya mazingira anamoshikiliwa Bwana Ban . "Unaweza kunieleza ni sheria gani inasema kuwa mbwa hawawezi kuitwa Chengguan?" mtumiaji mmoja wa blogi hiyo aliuuliza, na mwingine aliuliza : "Ni maneno gani mengine yanaweza kukufanya ufungwe?" Baadhi ya watumiaji wamekuwa wakitania kuwa Bwana Ban ameshikiliwa kwasababu "kushukiwa kuupinga utawala wa taifa" au "kutoa siri za taifa", ikimaanisha kuwa, chengguan ni mbwa halisi. Unaweza pia kutazama: Mbwa kutambua ugonjwa wa Malaria kwa kunusa Mwanamume mmoja wa uchina amefungwa mashariki mwa Uchina kwa kuwapatia mbwa wake majina ''yasiyokubalika'' kisheria, imeripotiwa. text: Ni sabubu ya China asema Trump Kupitia ujumbe wa Twitter alisema hakuna sababu ya kutoendelea tena na mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini ambayo yamekuwa yakiikasirisha Korea Kaskazini. Siku zilizopita waziri wake wa ulinzi alisema mazoezi ya kijeshi yanaweza kuendelea. China imeikosoa Marekani kwa kuilaumu kuhusu uhusiano wake na Korea Kaskazini. Mkutano kati ya Bw Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi Juni ulikamilika kwa ahadi kutoka Korea Kaskazini kufanya kazi katika kuharibu silaha za nyuklia kwenye rasi na Korea. Baadaye Trump alitangaza kuwa hakukuwa tena na tisho kutoka Korea Kaskazini. Lakini tangu wakati huo waangalizi wengi wanasema kuwa Korea Kaskazini haifanyi hima katika kuharibu maeneo yake ya kurushia makombora. Trump alisema tatizo limetatuliwa baada ua mkutano na Kim Jong-un ,mwezi Juni. Kwa nini anailaumu China? Kwenye matamshi yake kupitia Twitter, Bw Trump anasema Korea Kaskazini iko chini ya shinikizo kutoka China kwa sababu ya mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na serikali ya China. China ndiyo mshirika pekee wa Korea Kaskazini na inatajwa kuwa na ushawishi mkubwa kwenye maamuzi yake. China pia ndiye mshindani mkubwa wa Marekani na wa muda mrefu eneo hilo. Marekani na China ziko kwenye mvutano mkuwa wa kibiashara na kila upande umeziwekea ushuru bidhaa za mwingine. Hatua gani zimepigwa katika kuharibu silaha za nyuklia? Tangu mkutano wa Juni, Korea Kaskazini imesitisha majaribio yake ya nyuklia, ikidai kuharibu kituo cha kufanyika majaribio ya nyuklia na ikarudisha mabaki ya wanajeshi wa Marekani waliouawa wakati wa vita vya Korea kati ya mwaka 1950-53. Bw Trump ameilaumu Korea Kaskazini kwa kile amekitaja kuwa kutokuwepo hatua katika makubaliano yake ya kuharibu silaha za nyuklia. Ripoti ya hivi majuzi ya Vox ilisema Korea Kaskazini ilijikokota kusonga mbele baada ya Trump kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa Bw Kim, kuwa angeweka sahihi mukubaliano ya kumaliza vita vya Korea. Baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kupata kuwa Korea Kaskazini ilikuwa inandelea na mipango yake ya nyuklia, Marekani iliitaka jamii ya kimaifa kudumisha vikwazo vya kiuchumi na Korea Kaskazini. Korea Kaskazini ilifanya majaribio kadhaa ya makombora mwaka 2017 Mazoezi ya kijeshi yatarudi? Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea yameikasirisha kwa siku nyingi Korea Kaskazini. Kufuatia mkutano wa Juni Bw Trump alisimamisha mazoezi hayo ya kijeshi. Katika ujumbe wake wa hivi majuzi, rais wa Marekani alisisitiza kuwa uhusiano wake na Kim ulibaki kuwa mzuri na hakukuwa na sababu ya kuanzisha tena mazoezi ya kijeshi na Korea Kaskazini. Lakini aliongeza kuwa ikiwa yataanza yatakuwa makubwa kuliko yoyote yale. Wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini wakifanya mazoezi Tangu kumalizika vita vya Korea, wakati Marekani ilishirikiana na Korea Kusini kuipiga vita Korea Kaskazini, Marekani imekuwa na wanajeshi wake nchini Korea Kusini. Karibu wanajeshi 29,000 wa Marekani wako nchini Korea Kusini chini ya makubaliano ya ulinzi yaliyofikiwa mwaka 1953. Rais wa Marekani Donald Trump ameikosoa China kwa kuhujumu jitihada zake na Korea Kaskazini, wakati kuna malalamiko kuhusu maendeleo ya kuharibu silaha za nyuklia za Korea Kaskazini. text: Chama tawala cha NRM kimekuwa madarakani tangu 1986. Taarifa ya pamoja imeashiria kwamba baada ya mashauriano kati ya viongozi hao wawili, wamekubaliana kuhusu masuala kadhaa wakati wanapokuja pamoja kushirikiana kisiasa dhidi ya rais Museveni, Daily Monitor linaripoti. Hapo jana akizungumza na waandishi habari Kyagulanyi maarufua Bobi Wine alisema wamekuwa wakishauriana katika mikutano kadhaa na vyama tofuati vya kisiasa nchini kikiwemo cha Democratic Party maarufu DP bloc na hivi karibuni na kiongozi wa People's government, Dkt Kizza Besigye. "Tunaungana na vikosi vingine vya kutaka mageuzi, tunajua kwamba kumaliza haya (struggle) mapambano, ni muhimu kwetu kukaa pamoja," amesema Bobi Wine. Katika mkutano na waandishi habari hii leo wasemaji wa People Power, kundi linaloongozwa na Bobi Wine, Joel Ssenyonyi na Betty Nambooze, msemaji wa 'People's Government' ambayo ni kambi ya Dkt Besigye, wametangaza kwamba pande hizo mbili zitatakeleza shughuli zao za kisiasa kwa pamoja katika kutafuta njia za kumtoa madarakani Rais Museveni. Kiongozi wa upinzani na hasimu mkubwa wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Bw Kizza Besigye amewahi kusema kwamba miaka mingi ya Bw Museveni kusalia madarakani ndiyo chanzo cha ukosefu wa usalama na mauaji ya watu mashuhuri nchini humo, hasa katika mji mkuu Kampala. Ushirikiano wa Bobi Wine na Besigye una maana gani kwa utawala wa Museveni? Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Uganda Tumusime, anasema ushirikiano kati ya Bobi Wine na Kizza Besigye sio tishio kwa serikali ilioko madarakani. Anaeleza utofuati wa sera na maslahi kati ya viongozi hao wawili ambayo anasema inafanya kuwa vigumu kwa muungano au ushirikiano wa aina hiyo kuwa thabiti. "Kila mtu ana nia yake, malengo yake, wameamua kukubaliana au kufanya jambo pamoja lakini wakati ukifika wa kusema tuchague mgombea wa muungano wetu, watu wataanza kupata mawazo tofuati," anasema Tumusime. Ameongeza kwamba ushirikiano huu hauna uzito wowote kwa kutazama pia tofauti na uhasama uliokuwepo katika siku za nyuma kati ya viongozi wa upinzani na wafuasi wa vyama vyao. Tumusime anakiri kwamba siasa nchini Uganda imebadilika kadri miaka ilivyosogea lakin imaslahi ya kibinafsi ni tatizo linaloendelea kuwepo kati ya viongozi wa kisiasa. Kizza Besigye ni nani? Kanali (Mstaafu) Dkt Kizza Besigye Kifeefe alizaliwa mwaka 1956 katika wilaya ya Rukungiri, magharibi mwa Uganda. Besigye alifuzu kama daktari baada ya kusomea Chuo Kikuu cha Makerere, mjini Kampala. Alijiunga na chama cha Museveni cha Uganda Patriotic Movement muda mfupi baada ya kuondolewa madarakani kwa Idi Amin 1978. Mwaka 1982, alijiunga na Museveni vitani baada ya kuzuiliwa miezi miwili katika hoteli moja mjini Kampala akituhumiwa kushirikiana na waasi. Baada ya Museveni kuingia uongozini, alimteua Dkt Besigye, wakati huo akiwa na umri wa miaka 29, kuwa waziri wa nchi aliyesimamia masuala ya ndani na masuala ya siasa za taifa. Dkt Besigye alipanda cheo jeshini na kufikia cheo cha kanali. Alistaafu muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2001, miezi michache kabla ya kujitokeza na kutangaza kwamba angewania urais. Besigye aliwahi kukimbilia uhamishoni Afrika Kusini Alipata asilimia 28 ya kura zilizopigwa akilinganishwa na mshindi, Museveni, aliyepata asilimia 69. Baada ya kushindwa, Besigye aliwasilisha kesi Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya uchaguzi. Alishindwa kesi hiyo na akakimbilia uhamishoni Afrika Kusini akilalamikia kudhulumiwa kisiasa. Alirejea Novemba 2005 na kuongoza chama cha FDC kwenye uchaguzi wa februari. Hata hivyo alikamatwa wiki chache baadaye na kufunguliwa mashtaka kadhaa yakiwemo uhaini na ubakaji. Aliachiliwa huru wiki mbili baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi. Besigye husifiwa sana kutokana na moyo anaoonyesha anapotoa hotuba zake na wengi wamemsifu kwa kusimama na kupinga utawala wa Museveni. Hata hivyo, wakosoaji wake humshutumu wakisema hana uchu wa madaraka na baadhi husema hawezi kufanikisha mabadiliko yoyote kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Museveni. Mbunge wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi na mwanaharakati wa kisiasa na mpinzani Dkt Kizza Besigye wameahidi kushirikiana kukiondosha madarakani chama tawala National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni. text: Kazi ya uchunguzi wa kijiolojia wa mlima huo ipo chini ya taasisi ya uangalizi wa volkano ya Goma, ambayo ilikatiwa ufadhili wa kifedha na Benki ya Dunia kutokana na kukithiri kwa madai ya ufisadi katika taasisi hiyo. Dalili za kulipuka kwa volkano hiyo katika maiaka ya hivi karibuni zilikuwa zipo wazi. Mwaka jana mkurugenzi wa uangalizi wa mlima huo wa Volkano, Katcho Karume, aliiambia BBC kuwa ziwa la lava ya volcano limekuwa likijaa haraka na hivyo kuongeza uwezekano wa kulipuka katika miaka michache ijayo. Lakini alionya kuwa tetemeko la ardhi linaweza kusababisha maafa mapema. Katika ripoti ya Mei 10 mwaka huu, waangalizi walionya kwamba mitetemo ya chini ya ardhi katika mlima Nyiragongo ilikuwa imeongezeka. Sasa kwa nini tahadhari haikutolewa kwa jamii mpaka mlipuko ukatokea na wananchi ikawalazimu kujihami kwa kukimbia makaazi yao bila maelekezo ya kitaalamu? BBC Swahili leo imezungumza na Bwana Kasereka Mahinda Celestine afisa mwandamzi wa taasisi ya volkano ya Goma ambaye amekiri kuwa ukata wa kifedha umeathiri kazi zao kwa kiwango kikubwa, japo anakiri bado tahadhari ingeweza kutoka mapema. Fahamu jinsi volcano inavyojitengeneza na kulipuka "Kulikuwa kuna dalili, lakini kuna kipindi tumepita bila ya matumizi (ya pesa), takribani kwa miezi sita mambo hayatembei vizuri kwa kazi juu ya ukosefu wa pesa...Baada ya kupata msaada na kuanza kazi tukaona hiyo dalili na kuandaa ilani kumbe (hatari) ilikuwa mbele zaidi (ya hali ya ilani)...baada ya kutoa tahadhari viongozi wanatakiwa kutoa mpango kwa wakaazi lakini inaonekana kuwa hatukusisitiza (hali ya hatari) katika ripoti yetu ya kila baada ya wiki mbili kwa viongozi," amekiri bwana Mahinda. Mlima huo wa volkano uliopo kilomita 10 (maili sita) kutoka Goma, ulilipuka mara ya mwisho mwaka 2002 na kusababisha vifo vya watu250 huku watu wengine 120,000 wakiachwa bila makazi. Mlipuko wa volkano uliosababisha vifo zaidi ulitokea mwaka 1977, ambapo watu 600 waliuawa. Profesa Mike Burton, mtaalamu wa masuala ya volkano katika Chuo Kikuu cha Manchester, England aliiambia BBC kuwa lava katika Mlima Nyiragongo ni ya kimiminika na ina uwezekano wa kusonga haraka. Picha iliyochukuliwa kwa ndege ikionesha uharibifu wa nyumba viungani mwa mji wa Goma Idadi ya vifo Takriban watu 15 wamethibitishwa kufariki kutokana mlipuko wa volkano uliotokea katika Mlima wa Nyiragongo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) lakini huenda idadi ya vifo ikaongezeka wakati maafisa wakiyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi. Volkano ililipuka katika mlima Nyiragongo una kumwaga ujiuji wa moto ama lava uliolifanya anga kuwa jekundu Jumamosi, lakini lava hiyo haikuhfika katika mji wa Goma unaokaliwa na watu milioni mbili kusini mwa mlima huo. Wakazi wa vijiji vya karibu na mlima huo pamoja na mji Goma ambao waliyakimbia makaazi yao kwa hofu ya mlipuko huo wameanza kurejea huku wengi wao wakiwasaka jamaa zao waliopotea. Watu tisa miongoni mwa waliothibitishwa kufa, walipoteza maisha katika ajali za barabarani wakati watu walipokuwa wakihaha kukimbia ili kuokoa maisha yao. Wanne walikufa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani huku wawili wakiungua hadi kufa, alisema msemaji wa serikali Patrick Muyaya Jumapili. Zaidi ya watoto 170 wanahofiwa kupotea na wengine 150 wametengana na familia zao, kulinga na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) ambalo linasema litaweka vituo vya kuwapokea watoto watakaopatikana wakiwa peke yao. Lava iliishia karibu na wilaya ya Buhene, viungani mwa mji wa Goma na kuangamiza mamia ya nyumba na hata majengo makubwa. Ukarabati unatarajiwa kuchukua miezi kadhaa. "Nyumba zote zilizopo katika wilaya ya Buhene zimeungua," Innocent Bahala Shamavu aliliambia shirika la habari la kimataifa la Associated Press. Wakazi wamekuwa wakipekua kusaka mabaki katika nyumba zao zilizoangamizwa Maafisa nchini Rwanda wamesema zaidi ya watu 3,000 wamevuka mpaka kutoka Goma. Baadhi walianza kurejea Goma Jumapili. Wengine walikwenda kwenye maeneo ya milimani magharibi mwa mji wa Goma. Mkazi mmoja wa Goma, Richard Bahati, alisema kuwa alikuwa ndani ya nyumba wakati aliposikia watu wakipiga mayowe na akaingia wasiwasi mkubwa alipoona anga limegeuka kuwa jekundu nje. "Niliishi kwa shida na volkano hii mwaka 2002. Volkano iliharibu nyumba na mali zetu zote," alisema. Shughuli za kujenga upya nyumba zilizoharibiwa zitachukua miezi Kwengineko, lava ilikatiza katika moja ya barabara kuu inayounganisha Goma na mji wa Beni, ambayo ni njia muhimu ya usambazaji wa misaada. Hata hivyo, uwanja wa ndege wa wa mji wa Goma haukuguswa na lava, kinyume na ripoti za awali kwamba uliathiriwa. Mitikisiko ilisikika baada ya kulipuka kwa volkano hiyo, alisema Bw Muyaya. "Watu wanashauriwa kuendelea kuwa macho, kuepuka safari zisizo za lazima, na kufuata maelekezo," ulisema ujumbe wake wa Twitter. Wakazi wa Goma walianza kuzikimbia nyumba zao kabla serikali kutangaza mpango wa namna ya kuondoka katika mji huo. Umati wa watu ulionekana usiku ukiondoka kwa miguu huku baadhi yao wakiwa wamebeba magodoro na mali zao nyingine. Mwaka 2002, volkano hiyo ililipuka na kuua watu 250 Mfanyabiasha mkazi wa Goma, Kambere Ombeni, alikuwa miongoni mwa wale waliorejea kwenye eneo la tukio wakati vifusi vya nyumba vilipokuwa bado vinafuka moshi. "Tulitazama eneo lote linalozingira Nyiragongo likiungua na kufuka moshi. Moto ulitoka hapa. Hata sasa bado tunaona lava ," alisema. Mkazi mwingine, Irene Bauma, alisema watu watahitaji msaada kutoka serikalini kuyajenga upya maisha yao. "Kuna ardhi, watu ambao wamepoteza kila kitu, labda pia kuna vifo, nani anayejua? Tunaiomba serikali kuja na kuwasaidia manusura wa mlipuko huu ." Tom Peyre-Costa, kutoka Baraza la Wakimbizi la Norway mjini Goma -Norwegian Refugee Council, aliiambia BBC jinsi tukio la mlipuko wa volcano lilivyotokea. Mfanyabiasha mkazi wa Goma, Kambere Ombeni, alikuwa miongoni mwa wale waliorejea kwenye eneo la tukio wakati vifusi vya nyumba vilipokuwa bado vinafuka moshi. "Tulitazama eneo lote linalozingira Nyiragongo likiungua na kufuka moshi. Moto ulitoka hapa. Hata sasa bado tunaona lava ," alisema. Mkazi mwingine, Irene Bauma, alisema watu watahitaji msaada kutoka serikalini kuyajenga upya maisha yao. "Kuna ardhi, watu ambao wamepoteza kila kitu, labda pia kuna vifo, nani anayejua? Tunaiomba serikali kuja na kuwasaidia manusura wa mlipuko huu ." Tom Peyre-Costa, kutoka Baraza la Wakimbizi la Norway mjini Goma -Norwegian Refugee Council, aliiambia BBC jinsi tukio la mlipuko wa volcano lilivyotokea. Mlima Nyiragongo ambao wikendi hii umelipuka ni mojawapo ya volkano zilizo hai zaidi dunani na kumekuwa na hofu kwamba ume kuwa hauchunguzwi ipasavyo hali iliyopelekea tahadhari ya mlipuko wa sasa kutokutolewa mapema. text: Yawezekana ndio sababu mwanamuziki huyu Kala Jeremaiah ameonekana kuwa wa tofauti na hata kuwa miongoni mwa watu 16 waliotunukiwa tuzo ya mabingwa wa mabadiliko nchini Tanzania. Katika sehemu ya maadhimisho yanayoendelea ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini Tanzania, Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (WiLDAF) na Umoja wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI), kwa Ufadhii wa Shirika la Umoja Wa Matafa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania, waliandaa hafla ya kusherehekea Mabingwa 16 wa Mabadiliko na miongoni mwao ni watu binafsi ambao wanafanya kazi nchini humo kila siku kutetea na kulinda haki za wanawake na wasichana kuwawezesha kuishi maisha bila ukatili na unyanyasaji wa kijinsia. Uteuzi wa mabingwa 16 uliotokana na mamia ya majina ni njia ambayo inatoa motisha ya kuleta mabadiliko ili kuondoa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na mila kandamizi nchini Tanzania. Kwa upande wake Kala Jeremiah anadhani mabadiliko yanaanza na yeye kwasababu; "Mtu yeyote mwenye nafasi ya kusikilizwa na kusikika ana fursa kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii yake," hayo ni maneno ya Kala Jeremiah ambaye ni mwanamuziki nchini Tanzania. Jeremiah anasema sanaa yake inaambatana na kusaidia watu wengine. "Huwa sifikiriii kuimba wimbo kama wimbo bali huwa nafikiria kutoa mafunzo, kumuinua yule aliyekata tamaa na kumpa burudani. Kwa karma yangu naamini nimegusa maisha ya watu wengi. Wimbo wa 'wanandoto' ambao unayahusu maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu unatoa nafasi ya kumkumbusha msikilizaji wa wimbo yangu kuwa yule mtoto aliyeko barabarani hakufika pale kwa kupenda bali naye ana ndoto ya kuishi maisha mazuri. Wimbo mwingine ambao Kala Jeremiah anajivunia maudhui yake ni wimbo wa 'kijana' anasema ametumia nafasi yake kama kijana ili kumuonesha na kumuelimisha kijana mwingine juu ya maisha na uwajibikaji. Kala Jeremiah anasema ameamua kutoa huduma kupitia muziki wake hivyo hafanyi biashara katika muziki huo ili kuwapa fursa watu waweze kuelimika na kuburudika kupitia muziki. "Muziki wangu sio biashara bali ni jukwaa la elimu bure," anasema Kala Jeremiah." Joyce Kiria maarufu kama dada wa 'Wanawake Live' Kwa zaidi ya miaka 10, anasema amekuwa katika harakati binafsi za kujitoa kwa ajili ya jamii yake. "Kama mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia niliamua kuanzisha wanawake live kupaza sauti za wanawake kupigania haki zao. Naamini kuwa Mabadiliko yanaanza na mimi , hivyo niliamua kujitoa maisha yangu ili kuleta mabadiliko.…kazi hii inanifanya nitoe utu wangu na heshima katika jamii." Kupitia kipindi chake cha Wanawake live anasema anakuwa anajaribu kuibua matukio ya kijamii. "Kwa kuonesha matukio ya ukatili ambayo yanatokea katika jamii mfano kama mume amemchoma mkewe kisu…. na kuna kesi nyingi za kutisha na kustaajabisha katika jamii zinaweza kuleta mafunzo katika jamii kabla ya madhara kutokea kwa upande wao" Aidha ameeleza kuwa haijawa kazi rahisi kwake kwa kuwa amekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wanawake wenzangu. Joyce alikuwa anafanya kazi za ndani yaani 'housegirl' lakini sasa ameamua kuanzisha kituo maalum kwa ajili ya kuwatetea katika ajira. Janeth Mawinza Yeye anatembea nyumba kwa nyumba kuibua unyanyasaji katika jamii inayomzunguka. Katika kampeni ya nyumba kwa nyumba tunakutana na kesi ya ubakaji, ulawiti na kupigwa. Mfano kuna unyanyasaji wa msichana kung'atwa meno na mwajiri wake kwa zaidi ya miezi mitatu mfululizo na kisa kingine cha msichana mwingine kuwa anachomwa na pasi na mwajiri wake. "Nyumba yangu huwa ni hifadhi wahanga wa unyanyasaji na jeshi la polisi huwa msaada wangu wa karibu pamoja na serikali za mtaa. Hali ngumu ya wasichana wengi ilimpa hamasa kuweza kusaidia wasichana hao wanaonyanyaswa,"anasema Janeth. Rhobi Samweli Rhobi anatokea maeneo ya Serengeti ana taasisi yake inayoitwa 'Hope For girls' inayokabiliana na ukatili wa kijinsia kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni, uonevu kwa wajane na nyinginezo. Kikubwa anachofanya Serengeti mkoani Mara , ni kutoa elimu kwa jamii dhidi ya ukatili wa kijinsia. "Mbinu tunazozitumia kufanya majadiliano katika jamii ni Kuwa na road shows, kuonesha filamu na kuwahifadhi wasichana katika 'safe house' yaani nyumba salama." Nyumba hizo salama zina uwezo wa kuhifadhi watu 55 lakini wako watu 107 kwa sasa. Huo ni mipango wa jinsi ya kumtetea mhanga wa ubakaji, ndoa za utotoni, Ukeketaji. Njia nyingine inayowasaidia ni kutumia Ramani au 'Mapping' kutafuta wahanga wa ukatili. Katika nyingine ya ulinzi wa mama na mtoto ,kuna wamama 87 ambao tunawaita digital champion. Wamama hao 87 wanapewa Smart phone kuwapa motisha na kusaidia kurahisisha kazi yao ya kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia vijijini. Mpaka sasa Rhobi anasema wameweza kuokoa maisha ya wasichana zaidi ya 1000 dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia. Selemani Kipunguni Katika mwaka unaogawanyika na mbili kama huu 2020, huwa ndio msimu maalum wa ukeketaji . Na kama mtoto alieenda kukeketwa akikutwa ameanza kufanya ngono , basi mzazi anapewa faini kwa kushindwa kutoa malezi bora. Faini huwa ni ng'ombe na fedha. Sulemani anasema sababu kubwa ya kufanyika kwa ukeketaji ni kuonesha thamani katika jamiii kwa kutaka kuolewa. "Kama mwanaume natambua nafasi ya mwanamke kwa kiasi kikubwa sana. Nilipokuwa mdogo mtu wa kwanza niliyemuamini alikuwa mama. Hivyo hata kama changamoto wanazozipitia licha ya kuwa hazinifikii moja kwa moja ila ninajua madhara na ubaya wa unyanyasaji wa jinsia. Jambo la ukeketaji linalofanyika katika jamii ninayoishi huwa linaonekana kuwa jambo la kawaida yaani kama shughuli nyingine yeyote. Tangu mwaka 2010 ninaona wasichana wakikeketwa na tunaalikwa; tunakula na kunywa kama shughuli nyingine, sawa kabisa na kwenda harusini. Faraja ya wengi huwa ni ndoa. Hivyo mimi huwa natumia mbinu ya kuamsha mjadala miongoni mwao kuhusu jambo hilo na mwisho wa siku wanapata jibu wenyewe kuwa thamani ya ndoa si ukeketaji. Harakati shirikishi inanisaidia kutatua matatizo yao kiurahisi bila kuvutana. Wakati naanza harakati za kupinga ukeketaji maeneo ya kipunguni na kitunda jijini Dar es Salaam nilifanya utafiti halisia kwa kushiriki kwenye sherehe za ukeketaji ambapo watoto wa kike waliokeketwa hupitishwa barabarani wakitokea kwa ngariba wakishangiliwa na ndugu huku wakiwa wamevalishwa mavazi ya kiume . Mtu asiyefahamu hawezi kugundua kwamba hao ni watoto wa kiume au wa kike." Ni nadra sana kukuta mwanamuziki wa kizazi kipya kuimba nyimbo za maudhui tofauti na mapenzi. text: Beji Caid Essebsi alilazwa hospitali Jumatano usiku Alikuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani. Alilazwa hospitali Jumatano lakini maafisa hawakueleza kwanini alipelekwa kupokea matibabu. Essebsi alishinda uchaguzi huru wa kwanza Tunisia mnamo 2014 kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu. Alilazwa hospitalini mwezi uliopita baada ya kukabiliwa na maafisa wanachotaja kuwa hali mbaya ya afya. Hawakutoa ufafanuzi zaidi wakati huo. Waziri mkuu Youssef Chahed, aliyemtembelea hospitalini, aliwaomba watu kuacha kusambaa habari za uongo kuhusu hali yake. Essebsi ni muasisi wa chama cha Nidaa Tounes Mapema mwaka huu, Essebsi alitangaza kwamba hatogombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba. Aliwaambia wajumbe wa chama chake tawala Nidaa Tounes katika mkutano kwamba kijana anahitajika kuchukua uongozi. Alisema muda umewadia "kuwafungulia mlango vijana". Beji Caid Essebsi ni nani? Aliyekuwa rais wa Tunisia Zine el-Abedine Ben Ali alitimuliwa madarakani mnamo 2011 baada ya kuhudumu kwa miaka 23 madarakani. Tangu hapo , Tunisia imeshinda sifa kama taifa la pekee lililoibuka kutoka mapinduzi na kuingia katika demokrasia baad aya vuguvugu katika nchi za kiarabu. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, taifa hilo limekabiliwa na mashambulio utoka kwa wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu na matatizo ya kiuchumi, huku ukosefu wa ajira ukikithiri. Kiongozi aliyechaguliwa kwa huru rais Beji Caid Essebsi amefariki akiwa na miaka 92, ikulu ya nchi hiyo imeeleza. text: Viboko wageuka magaidi kwa wakazi pwani ya Kenya Kwa kawaidia viboko hao huwavamia usiku kwani wakati huo macho yao huona zaidi ya vile yanavyoona mchana. Kulingana na mzee wa kijiji, Safari Kadenge Karisa, idadi ya viboko imeongezeka na kuwa zaidi ya mia nne, hivyo basi wengi wao ikifika usiku huvamia wenyeji kwenye makaazi yao. "Tumechoka na uvamizi huu wa viboko,'' asema Karisa. "La kusikitisha ni kwamba kila mara tunapopiga ripoti kwa watu wa shirika la huduma la wanyama pori wanachelewa sana kuwasili kutuhudumia tunapovamiwa. Tumeamua endapo KWS hawatatusaidia tutavichinja viboko tupate chakula.'' Spika wa wodi ya Sabaki, Stembo Kaviha anasema: "Tangu lini wanyama wakatawala maisha ya binadamu? Ni binadamu ambaye anatawala lakini sasa wakaazi wa Sabaki tumekuwa watumwa wa viboko. Kufikia saa kumi na mbili za jioni sote tuko ndani ya nyumba na hamna kutoka nje maanake viboko wanazunguka kwenye nyumba zetu. Tumeamua sasa ni vita vya binadamu na wanyama. Na KWS wasiingilie. Kaviha anasema viboko wamekuwa na magaidi hatari zaidi kwao "Hapa Kenya tuna janga la Al Shabaab lakini sasa imekua ni Al Kiboko!, wale wengine ni magaidi wa kimataifa lakini hawa viboko ni magaidi wa hapa nyumbani. "Kuna haja gani watu wa KWS wawe huko Marine Park, kilomita kama kumi na tano kutoka Sabaki. Mbona wasije hapa karibu na viboko wao badala ya kutuachia sisi tuwafanyie kazi yao. Ofisi zao ziko mbali sana.'' Kwa hivi sasa wakaazi wa Sabaki wanaomboleza kifo cha mmoja wao, Kennedy Kenga Charo, aliyeuawa na kiboko kwake nyumbani. Tukio hili limewaudhi zaidi, na wanasisitiza watachukua sheria mkononi mwao kwa kuwaua viboko hao. Mjane wa marehemu Kennedy Charo Kenga, Sidi Mzungu kwake kijiji cha Sabaki. Mzee Kenga amemuacha mjane, Sidi Mzungu, na watoto wanane. Mama huyo anawaza na kuwazua jinsi atawalea watoto hao wote, wengine wakiwa bado wako shule ya chekechea. Mama Mzungu anatueleza jinsi mumewe alivamiwa kwake nyumbani na kiboko. "Bwanangu alitoka nje aliposikia ng'ombe anapiga kelele, kumbe ni kiboko alimvamia.Kiboko huyo alipomuona bwanangu akamvamia na kumuangusha chini, akamuuma paja na meno yake marefu ya mbele. Alitoa damu nyingi sana hadi akafa. Mimi nadai malipo ya kiwango cha juu cha kuniwezesha kulea hawa watoto wangu maanake sina mtu mwingine wa kunisaidia.'' Mtoto wake mkubwa, Emmanuel Kenga, anasema huenda ikambidi aache shule (yuke sekondari sasa) amsaidie mamake. "Tumeachwa na mzigo mzito sana, na kufikia sasa hawa KWS hawajasema lolote vile watatusaidia. Tuko njia panda hatujui tuanzie wapi. Yote haya ni kwa sababu wa viboko.'' Kahindi Safari ni mmoja ya waathiriwa waliovamiwa na viboko lakini kwa bahati nzuri hakumalizwa kabisa. Safari anatusimulia zaidi: "Mimi nilikua navuka mto Sabaki sehemu ambayo haina maji mengi nikilisha mifugo yangu, ndio nikavamiwa na viboko wawili. Niliamua kujikinga kwa kuingia ndani ya maji, wakanifuata na kunikanyaga kabisa. Naumia sana kwa maumivu ya tumbo, figo, mgongo, shingo na kichwa. Sijapata matibabu ya kutosha. Hata usiku silali kwa sababu ya maumivu." Mkuu wa shirika la huduma la wanyama pori kaunti ya Kilifi, Jane Gitau, anasema wanajaribu wawezavyo kuwafidia waathiriwa waliovamia na viboko huko Sabaki. "Kwanza twatoa rambi rambi zetu kwa familia ya mzee Kenga aliyeuliwa na kiboko wetu. Sote tumesikitika mno na tayari tumeanza kushugulikia malipo yake. Tukifuata sheria tutamlipa shillingi milioni tano za Kenya. "Ni kiwango kidogo kweli lakini hizo ndizo pesa twatoa kuwapa pole waliouliwa na viboko. Hatahivyo twaweza kumsaidia zaidi kulingana na uwezo wetu. Serikali ya kaunti nayo pia itashugulikia familia ya marehemu.'' Hata hivyo baadhi ya waathiriwa wanasema hawajafidiwa na serikali tangu wavamiwe na viboko hao, wakilaumu shirika la huduma la wanyama pori kwa kutilia maanani maslahi ya viboko zaidi ya binadamu. Jane Gitau amekanusha madai ya wakazi wa Sabaki kwamba wamezembea kwa kuwahudumia ipasavyo. "Sio kweli tumezembea sisi kama KWS. Tunaelewa shida inayowakabili watu wa Sabaki, na ndio kwa maana kila siku tuko huko. Tatizo ni uchache wa watu wetu wa kazi lakini tutawadumia kikamilifu wakaazi hao.'' Mkuu huyo anasema wanafikiria suluhu ya kudumu kama vile kujenga ua ambalo litawazuia viboko kutoka nje na kuvamia watu kwenye makaazi yao. Kiboko mkubwa kwa kawaida huwa ana uzani wa kati ya kilogramu 1000 hadi 1,600. Meno yake mawili ya mbele ni makali sana na ndiyo wanayatumia kung'ata wakaazi wa Sabaki. Kiboko ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi duniani. Wakazi wa eneo la Sabaki kaunti ya Kilifi pwani ya Kenya wamelalamika vikali kuhusu viboko ambao wanawavamia mpaka nje ya nyumba zao, na kuharibu mashamba pamoja na kuingilia mifugo yao. text: Mjadala wa tatu wa urais kati ya Clinton na Trump Ukweli:Hii inahusishwa na kanda za video zilizotolewa na mradi wa mwanablogu wa mrengo wa kulia James O'Keefe. Kanda za kamera zilizofichwa zinaonekana zikionyesha kampuni zinazounga mkono kampeni ya Hillary Clinton pamoja na kamati ya kitaifa ya chama cha Democrat zikizungumza kuhusu kuwafunza watu waliojitolea kuhudhuria mikutano ya Trump na kuzua ghasia. Mmoja wao ,Scott Foval,anasikika akisema haikuchukua muda mwingi kuchochea ghasia miongoni mwa mashabiki wa Trump kwa sababu wana matatizo ya kiakili. Wengine wanaonyeshwa wakijigamba kuzua fujo nje ya mkutano wa Trump mjini Chicago. Foval alifutwa kazi kama mkurugenzi wa kitaifa wa maswala ya mashinani katika kampeni ya Clinton siku ya Jumatatu kutokana na kanda hizo. Robert Creamer mwanakandarasi mwengine wa Democrat ambaye alihusika katika mpango huo wa hila chafu,madai,licha ya kusema kuwa mazungumzo kama hayo hayakufanyika. Kampeni ya Clinton imekana kuwaweka waandamanaji na kuzua ghasia kwa makusudi katika mikutano ya Trump. Huku mradi huo ukidaiwa kutoa kanda ya video isio sahihi,baadhi ya mbinu zilizotumika katika video hiyo zina tatiza licha ya mpango huo kutofanyika,alisema Zac Petkanas,msemaji wa kampeni ya Clinton katika taarifa yake. ''Tunaunga mkono hatua ya kamati ya kitaifa ya Democrat katika kutatua swala hili na tutaendelea kufanya kampeni yenye mawazo endelevu'' Lakini shabiki wa Trump Jeffrey Lord aliambia CNN kwamba mrengo wa kushoto wa Marekani una tabia kama hizo na hilo halikubaliki kabisa. Donald Trump Trump amekuwa akisema mara kwa mara kwamba rais wa Urusi Vladimnir Putin amekuwa akimsifu. Ukweli:Hili halionekani kuwa ukweli. Mwaka 2015,Putin alitumia neno 'Yarkii' kumtaja mgombea huyo wa Republican kuwa mwerevu. Putin mwenyewe ,alikana neno ''kipaji'' mnamo mwezi Juni katika mahojiano na CNN. ''Ulitoa matamshi fulani kuhusu mgombea wa urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump''.ulimtaja kuwa bora na mwenye ''kipaji', mwandishi wa CNN fareed zakaria alisema. Matamshi hayo yaliripotiwa dunia nzima. ''Nilikuwa nataka kujua ni nini kilichokuvutia kutoa uamuzi huo, na je bado unashikilia msimamo huo''? ''Kwa nini kila mara unabadilisha ninachokisema''? Putin alijibu kupitia mkalimani. ''Nilisema pekee kwamba ni mwerevu,wadhani si mwerevu''?,ndiye.Sikusema lolote jingine kumhusu''. Hillary Clinton naye anatetea uamuzi wake wa sheria ya kudhibti bunduki nchini humo kwa kusema kuwa nchini Marekani kuna vifo takriban 33,000 vinavyosababishwa na bunduki kila mwaka. Ukweli: Takwimu za Clinton zinatoka katika kituo cha kudhibiti magonjwa na uzuiaji wa vifo.Takwimu hizo ni za mwaka 2014,ambazo ni za hivi karibuni kutolewa. Ili kusawazisha asilimia 33 ya vifo vya mauaji,asilimia 63 ikiwa ni watu wanaojiua. Donald Trump mara kwa mara amekuwa akitumia Chicago kama mji ambao una visa vingi vya ghasia ambazo haziwezi kudhibitiwa. Ukweli:Viwango vya mauji ya Chicago viko juu zaidi ikilinganishwa na miji mingine kama vile New York na Los Angeles. Kufikia sasa mwaka huu zaidi ya watu 600 wameuawa,ikiwa ni ongezeko la asilimia 24 ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka uliopita. Trump amekuwa akidai kwa siku kadhaa sasa kwamba mfumo wa upigaji kura umefanyiwa udanganyifu mbali na kukabiliwa na maswala ya ufisadi,na kwamba udanganyifu miongoni mwa wapiga kura ni jambo la kawaida. Ukweli:Trump ananukuu kutoka kwa utafiti wa mwaka 2012 uliofanywa na shirika moja lisilopendelea upande wowote Pew, ambalo linakadiria kwamba takriban watu milioni 24 ama mmoja kati ya kila wanane sio halali tena na kwamba kuna makosa. Kati yao,ripoti hiyo inasema ,wapiga kura milioni 1.8 walifariki. Lakini ripoti hiyo ya Pew, haisema kwamba watu miloni 1.8 waliofariki walishiriki katika upigaji kura. Ilisema kuwa makosa yaliopo ni ushahidi wa kuimarisha mfumo wa usajili wa wapiga kura. Watafiti wengine wanasema kuwa udangayifu katika upigaji kura unaohusisha masunduku ya kupiga kura kuhusu kura zilizopigwa na watu waliofariki ni jambo lisilo la kawaida. UKweli: George W Bush alipunguza kodi miongoni mwa watu wanopokea mapato ya hali ya juu kutoka asilimia 39.6 hadi 35. Chini ya mpango wa Trump,kodi ya watu wanaopata mapato ya juu itapunguzwa kutoka asilimia 39.6 hadi 33. Trump anamshambulia Clinton kuhusu rekodi yake ya kuwa mamlakani,akimwambia: Wakati ulipokuwa waziri wa maswala ya kigeni ,takriban dola milioni 6 zilitoweka ,pengine ziliibwa....hakuna anayejua. Ukweli:Ni madai ambayo yametolewa na Trump hapo awali ..na madai ambayo yamethibitishwa kuwa ya uongo. Donald Trump anadai kwamba Bi Clinton anaunga mkono uavyaji mimba ,akidai unaweza kufanyika siku mbili au tatu kabla ya mtoto kuzaliwa. Ukweli:Hii inatokana na matamshi yaliotolewa na Clinton wakati wa kampeni za chama cha Demokratic aliposema kuwa uavyaji wa mimba kubwa unatokana na ''mahitaji ya kimatibabu''. Alimwambia Trump wakati wa mjadala: Hicho sio kinachofanyika wakati huo.Na anasema ukweli-kwamba uavyaji wa mimba kubwa unaotajwa na Trump una visa vichache sana. Data iliopatikana kutoka kwa taasis ya Guttmacher inaonyesha kwamba uavyaji mimba mwingi hufanyika mapema. Hillary Clinton Ni aslimia 1.2 ya visa vya uavyaji mimba nchini Marekani, ambavyo ni 12,000 kwa mwaka,hutokea baada ya wiki 21. Baadhi ya majimbo 43 tayari yanapinga uavyaji mimba katika kiwango fulani ,kwa hivyo uavyaji wa mimba kubwa umepigwa marufuku katika maeneo mengi ya taifa hilo. Madai: Donald Trump anasema kuwa ghasia katika baadhi ya mikutano yake ikiwemo ule wa Chicago zilisababishwa na kampeni ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton na rais Barrack Obama. text: Romelu Lukaku alijiunga na United kutoka Everton kwa dau la £75m mwaka 2017 Mkufunzi wa United Mourinho alitaka kupewa heshima na vyombo vya habari baada ya kukasirika katika mkutano na wanahabari baada ya timu yake kupoteza 3-0 nyumbani dhidi ya Tottenham mwezi Agosti. Lakini Lukaku anasema kuwa raia huyo wa Ureno ni mtu wa familia , ''huwafanya wachezaji kucheka na anawapigania'' , hivyobasi anahitaji heshima. ''Watu wanajua kwamba ana upande unaomfanya kuwa mshindi'', alisema Lukaku. ''Lakini kile ninachompendea hawezi kuficha hisia zake. Wakati anapokasirika utajua amekasirika, anapofurahi utajua anafurahi''. ''Sijui kwa nini watu hawapendi ukweli kumuhusu. Wakati anaponikasirikia najua kwamba amenikasirikia hivyobasi najaribu kufanya anachotaka hatua inayomfanya kufurahi tena. Katika mahojiano na Dion Dublin , mshambuliaji huyo wa Ubelgiji pia amezungumnzia kuhusu mafunzo aliopata kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Ufransa na Arsenal pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba , mbali na uhusiano wake na mkufunzi wa zamani wa Everton Ronald Koeman huku akitaka kumaliza kazi yake bila majuto yoyote. 'Mourinho anependwa na kila mtu' United ilimaliza ya pili katika jedwali la ligi ya Uingereza msimu uliopita lakini ilipoteza mechi mbili za kwanza kati ya nne katika kampeni yao. Lukaku ,25, anasema kuwa Mourinho hatosita kuingilia kati iwapo hafurahii wachezaji wanavyocheza ama timu yote kwa jumla. ''Mara nyengine wachezaji tunakuwa laini sana'' , aliongezea Lukaku. ''Ninapowasikiliza wachezaji wa zamani na wa sasa , mkufunzi hawezi kusema anachotaka kutoka kwa mchezaji kwa sababu unahisi anakushambulia''. ''Lakini sihisi ananishambulia, kwasababu hivyo ndivyo nilivyo-mimi sio laini, lakini huwezi kupata nguzo kama hiyo katika soka -ninakotoka ndivyo tulivyo''. ''Uhusiano wangu naye ni mzuri . Ananichekesha , anawafanya wachezaji kucheka ni mtu anayependa familia''. Lazima watu waheshimu kwamba anataka kujihifadhia heshima yake. Hapa anataka tuimarike . Ni mtu wa kawaida, tuna uhusiano mzuri naye anapendwa na kila mtu. Jose Mourinho hadanganyi na hawezi kuficha hisia zake kama wakufunzi wenzake katika ligi ya Uingereza , kulingana na mshambulijia wa United Romelu Lukaku. text: mwandishi wa habari wa kujitegemea Phocus Ndayizera kutoka nchini Rwanda ajikuta matatani Msemaji wa idara ya polisi ya upelelezi nchini humo amesema kwamba mwandishi huyo anatuhumiwa makosa ya ugaidi. Mwandishi huyo alifanyia kazi vyombo vya habari mbali mbali na mara kwa mara amekuwa akiripotia BBC Idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi yeye amesema kwamba hajui kwa nini anazuiliwa. Mwandishi wa BBC aliyeko Kigali, Yves Bucyana, amesema Phocus Ndayizera wakati alipoonekana mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya idara ya polisi inayohusika na upelelezi alikuwa amevalishwa pingu na hali yake ilionesha alikuwa mchovu. Phocus Ndayizera akiwa amefungwa pingu Mwandishi huyo alifahamika katika vyombo vya habari mbali mbali na mara kwa mara aliifanyia kazi BBC idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi kama mwandishi wa kujitegemea. Mara ya mwisho kwa Phocus Ndayizera kuendelea kuiripotia idhaa ya BBC ilikuwa mwezi wa Juni mwaka huu. Alipotakiwa na polisi kuwambia waandishi wa habari tuhuma dhidi yake, Bwa Ndayizera amesema kwamba hana habari yoyote kuhusu mashitaka dhidi yake akisisitiza tu kwamba na yeye anasubiri upelelezi kukamilika. Amesema kwamba alikamatwa katika mtaa wa Nyamirambo jijini Kigali alipokwenda kumuona jamaa yake na kupelekwa sehemu isiyojulikana kabla ya kujikuta katika mahabusu ya polisi kituo cha Remera. Msemaji wa idara ya upelelezi Modeste Mbabazi amewambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi Polisi wa upelelezi wamekiri kuwa ndio waliokuwa wanamshikilia mwandishi huyo kwa wiki nzima. Msemaji wa idara ya upelelezi Modeste Mbabazi amewambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi na pia kukutwa na vifaa vya vilipuzi. Kwa mujibu wa msemaji huyo, walikuwa na taarifa za mipango ya watuhumiwa kutumia vilipuzi kuhatarisha usalama wa nchi ya Rwanda. vifaa alivyokutwa navyo Phocus Ndayizera Msemaji wa Polisi amesema walisubiri siku kadhaa kutangaza kumshikilia mwandishi huyo kutokana na kwamba makosa ya ugaidi yanafwatiliwa kwa njia ya kipekee tofauti na makosa mengine. Haijafahamika ni lini mwandishi huyo na wengine wanaotuhumiwa pamoja watakapofikishwa mahakamani. Mwandishi wa habari wa kujitegemea Phocus Ndayizera ameonyeshwa mbele ya vyombo vya habari na polisi wa upelelezi nchini Rwanda wiki moja baada yake kutoweka. text: Matokeo hayo yanauweka uongozi wa mkufunzi Sarri katika hali mbaya , huku United ikijibu baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza chini ya ukufunzi wa Ole Gunna Solskjear na kuweka tarehe na Wolveshampton katika robo fainali ya kombe hilo. Ander Herrera alifunga krosi iliopigwa na Paul Pogba ili kuipatia United uongozi kunako dakika ya 31 kabla ya Pogba kufunga bao la pili kupitia kichwa na kuipatia timu yake fursa nzuri baada ya krosi iliopigwa na Marcus Rushford. Huku Chelsea wakishindwa kwa mara nyengine , mashabiki wao walimshutumu Sarri. Waliwazoma wachezaji wa ziada walioingizwa uwanjani na mkufunzi huyo mbali na kufanyia mzaha filosofia yake, na kutaka kurudi kwa Frank Lampard kama mkufunzi wa timu hiyo huku wakishirikiana na mashabiki wa United kuimba ''utafutwa alfajiri''. ''Tulicheza kana kwamba tumekanganyikiwa katika kipindi cha pili lakini katika kipindi cha kwanza tulionyesha mchezo mzuri''., alisema Sarri. ''Nina wasiwasi kuhusu matokeo haya lakini sio kuhusu mashabikikwa sababu naelewa hali yao. Ninawaelewa mashabiki wetu kwasababu matokeo hayo sio mazuri na tumetolewa katika kombe la FA''. ''Nilikuwa na wasiwasi mkubwa nilipokuwa katika ligi ya daraja la pili nchini Itali lakini sio sasa''. Solskjaer hakuwa na matatizo hayo baada ya kufurahia sifa alizokuwa akimwagiwa na mashabiki wa United baada ya kuongeza ushindi mwengine licha ya kutokuwepo kwa Jesse Lingard na Anthony Martial ambao wanauguza majeraha. ''Mchezo wetu ulikuwa mzuru sana leo , mbinu zetu zilizaa matunda'' ,alisema kamimu mkufunzi huyo wa United. 'Historia inaonyesha kazi ya Sarri ipo hatarini' Mashabiki wa klabu hiyo walioimba jina la mkufunzi huyo hawatakuwa na kura ya kupiga wakati uamuzi kuhusu mkufunzi mpya utakapotolewa, lakini walionyesha hisia zao katika usiku mwengine muhimu kwa mtu ambaye anatumai kumrithi Jose Mourinho kwa kandarasi ya kudumu. Solakjaer amekabiliwa na msururu wa mitihani muhimu tangu aliporudi katika klabu ya Old Trafford baada ya kufutwa kazi kwa Mourinho katikati ya mwezi Disemba. Mtihani wa kwanza ilikuwa jinsi angejibu matokeo duni yaliowachwa na mtangulizi wake. Sarri anapoteza umaarufu Mkufunzi Sarri alianza kazi yake vizuri katika wiki za mapema za msimu huu huku Chelsea ikionekana kushindana na Manchester City na Liverpool huku kukiwa na matumaini kwamba raia huyo wa Itali alionyesha sifa nzuri katika soka ya Uingereza. Lakini huku muda ukiyoyoma , Sarri alikabiliwa na hasira zote za Stamford Bridge huku wasiwasi ukizidi kuhusu hali ya matokeo duni ya Chelsea. Kulikuwa na wito wa kurudi kwa Frank Lampard ambaye kwa sasa anaifunza Derby County. Ulikuwa usiku ambao mashabiki walikosa subira huku, watu wakitoa maoni yao huku Sarri akithibitishiwa kwamba anaendelea kupoteza umaarufu miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo. Klabu hiyo itakabiliana na Manchester City katika fainali ya kombe la Carabao siku ya Jumapili na itakuwa uamuzi muhimu kwa klabu hiyo kumfuta kazi siku chache kabla ya mechi hiyo. Bado vigumu kumuona Sarri akiponea shoka hilo. Mchezaji bora wa mechi - Paul Pogba (Man Utd) Pogba alishiriki katika bao la kwanza na akafunga la pili Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri alisema kuwa timu yake ilichgeza mchezo wa 'Kunganyika' baada ya Man United kupata ushindi katika uwanja wa Stamford Bridge ili kufika katika robo fainali ya kombe la FA. text: Mnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno. Baada ya kutenguliwa, subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye ilifikia kikomo. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake. Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa. Amekanusha kuhusika wowote katika mauaji hayo na kuilaumu jeshi. Hata hivyo, hamna matumaini kuwa vitendo vya kukiuka wa haki za binadamu vitasitishwa chini ya utawala wake. Wakosoaji wake wanasema Mnangagwa ana damu mikononi mwake. Anajulikana kama "mamba" sababu ya kizimu cha jamii yake; jina ambalo linaokenana kumfaa.Kwa maana hiyo, wafuasi wake hufahamika kama "Lacoste" Emmerson Mnangagwa ni nani? •Anajulikana kama "mamba" sababu ya kizimu cha jamii yake. , wafuasi wake wanafahamika kama "Lacoste" •Alipata mafunzo ya jeshi nchini China na Misri •Aliteswa na vikosi vya Rhodesia baada ya mashambilizi yake ya kiaina •Alisaidia kuongoza kupigania uhuru nchi ya Zimbabwe miaka ya 70 •Alikuwa mjasisi wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa. •Anaojulikana lama muunganishi baina ya jeshi, idara ya ujasisi na chama cha Zanu- PF •Anatuhumiwa kwa kuwa nyuma ya mashambilio dhidi ya wafuasi wa upinzania baada ya uchaguzi wa 2008 Walipigania uhuru Zimbabwe miaka ya 1970 wametawala siasa za nchi hiyo Wale waliopigana katika vita ya miaka 70, kama Bw Mnangagwa, wamehodhi madaraka kwa muda mrefu nchini Zimbabwe,huku wakiogopa kupoteza vyeo vyao kama Grace Mugabe angemritihi mume wake,kwa hio waliingilia kati. Wakati rafiki wake wa karibu , Jenerali Constantino Chiwenga alionya dhidi ya 'vitendo vya vinavyolenga kuwatoa wanachama waliopiginia uhuru wa taifa' ilikuwa wazi kwamba alikuwa akizungumzia kufukuzwa kazi kwa Mngangagwa. Uhusiano na Congo Bw Mnangagwa alizaliwa mkoa wa kati wa Zvishavane na anatokea jamii ya Karanga iliyo jamii kubwa zaidi katika kabila ya Washona. Wakaranga ni wa kundi kubwa la Washona na wengi wanahisi ni zamu yao kuingia madarakani kufuatia miaka 37 ya kutawaliwa na kundi la Zezuru atokaye Mugabe. Wanajeshi wa Zimbabwea waliingilia kati mzozo DR Congo kuisaidia serikali Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa wa mwaka 2001, Bw Mnangagwa alionekana kama 'mhandisi wa shughuli za kuingiza fedha za Zanu-PF.' Hii kwa kiasi kikubwa inahusisha operesheni za jeshi la Zimbabwe na wafanyabiashara katika Jamuhuri Ya Kidemokrasia ya Congo. Majeshi ya Zimbabwe yaliingilia mzozo wa Congo kwa upande wa serikali, kama ilivyo nchi nyingine, wametuhumiwa kuutumia mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo kuiba utajiri wa maliasili wa nchi hiyo kama vile Almasi, dhahabu a madini mengine. Lakini licha ya mchango wa kukipatia chama fedha, Bwana Mnangagwa, ambaye ni mwanasheria aliyekulia Zambia, sio mtu anayependwa sana na watu wenye vyeo na wasio na vyeo katika chama chake. Mmoja wa Maveterani wa vita nchini Zimbabwe, ambaye alifanya naye kazi kwa muda mrefu, anaweka wazi kwa kumuelezea kuwa ni mtu katili. Mnangagwa alijipatia sifa zake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya 1980 kati ya chama cha Zanu chake Robert Mugabe (kushoto) na Zapu chaJoshua Nkomo (kulia) Afisa mwingine wa ZANU PF aliuliza swali lenye mvuto, wakati alipotaka kujua kuhusu mtazamo wa Bwana Mnangagwa '' Unadhani kuwa Mugabe ni mbaya. Lakini ulifikiri kuwa yoyote atakayekuja badala yake anaweza kuwa mbaya zaidi?'' Mgombea wa upinzani ambaye ambaye alimshinda Bwana Mnangagwa katika kampeni za ubunge mwaka 2000, katika eneo la Kwekwe, Blessing Chebundo anaweza pia kukubaliana kwamba mpinzani wake siye mtu wa amani. Wakati wa Kampeni kali, Bwana Chebundo alinusurika kifo baada ya vijana wa chama cha ZANU-PF, ambao walimteka na kummwagia petroli, lakini hata hivyo hawakufanikiwa kumchoma. Ukatili Sifa za kutisha za Bwana Mnangagwa zilianza wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka miaka ya 80 kati ya chama cha Rais Mugabe cha Zanu na kile cha Joshua Nkomo cha Zapu. Kama Waziri wa Usalama wa Taifa wa Zimbabwe, Bwana Mnangagwa alikuwa akihusika na Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo ilikuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na jeshi kukikandamiza chama cha Zapu. Maelfu ya raia wasio na hatia, wengi wakiwa kabila la Ndebele, ambao ndio walioonekana kama wafuasi wa Zapu, waliuawa kabla ya vyama hivyo viwili kuungana na kuunda Zanu-PF. Mnangagwa hapendwi sana na watu wanaofuata sera za Zanu-PF Miongoni mwa mambo ya ukatili yaliyofanyika ni pamoja na wanavijiji kulazimishwa kucheza huku wakiwa wamenyooshewa bunduki, wakati wa mazishi ya jamaa zao na maneno ya kumuunga mkono Mugabe. Licha ya makubaliano ya umoja yaliyofikiwa mwaka 1987, bado majeraha ya maumivu yangali yapo. Na watu wa Kabila la Matebele pengine wanaweza kukaidi kumuunga mkono Mnangagwa katika kinyang'anyiro cha Urais. Amepata Mafunzo China Bw Mnangagwa ana wafuasi wengi ya waliokuwa katika wakiongoza kampeni ya vita dhidi ya wakulima weupe na wapinzani kutoka mwaka 2000. Zimbabwe ilipigana vita vya msituni kabla ya kujipatia uhuru 1980 Grace Mugabe (kulia) anaonekana kukumbana na kisiki akikabiliana na Bw Mnangagwa Wanamkumbuka kama mmoja wapo wa wanaume, ambaye baada ya mafunzo ya kijeshi China na Misri, alioongoza vita vya kupigania uhuru. Maelezo rasmi ya Bw Mnangagwa ni kwamba alikuwa mhanga wa ukatili uliotekelezwa na serikali iliyoongozwa na Wazungu katika taifa la zamani la Rhodesia mwaka 1965. Hii ni baada ya yeye na 'kundi la mamba' alilokuwa analiongoza walisaidia kulilipua treni iliokuwa karibu na eneo la Fort Victoria(ambayo sasa ni Masvingo). Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais. text: Uvalishanaji pete Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya miaka 13 kwa zaidi ya watu laki tisa ambao wana matatizo aina tatu ya moyo, umebaini kwamba wanandoa wenye kiwango kikubwa cha lehemu wana asilimia 16 ya kuishi kuliko wale ambao hawako kwenye ndoa. Wale anaougua maradhi ya kisukari na presha pia walikuwa katika hali nzuri. Watafiti wanaamini, ingawa hawawezi kuthibitisha, kwamba wanandoa wenye furaha wanaweza kukushajiisha kuishi vizuri. Utafiti nchini Uingereza umebaini kwamba ndoa inaleta afya ya moyo. text: Waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono wakishiriki katika somo la uchoraji katika kituo kimoja Mogadishu, Somalia Kulingana na sheria hiyo atakayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 gerezani. Sheria hiyo pia inapiga marufuku mpango wa kusuluhisha kesi za unyanyasaji wa kingono kupitia njia za kitamaduni. Spika wa bunge la Somaliland Bashe Mohamed Farah ameambia BBC kwamba visa vya ubakaji vimekuwa vikiongezeka lakini anatumai kwamba sheria hiyo itazuia hilo sasa. Ubakaji utachukuliwa kama kosa la uhalifu badala ya tatizo la kijamii au kitamaduni. Njia za kitamaduni, ambazo mara nyingi humfaa mbakaji, pia zimeharamishwa. Awali, wabakaji wangetakiwa kuwaoa waathiriwa wao, na familia zingeuka mkono hilo kuepuka kubaguliwa na aibu ya kufahamika kwamba mtoto wao alibakwa. Sheria hiyo mpya imepitishwa baada ya juhudi za miaka mingi za watetezi wa haki za wanawake na watoto. Faisa Ali Yusuf wa Wakfu wa Ajenda ya Wanawake ameambia BBC kwamba wameisubiri sheria hiyo kwa miaka mingi. Somaliland inataka pia kuonekana kimataifa kama taifa la kidemokrasia lenye mifumo ya kidemokrasia inayofanya kazi. Hata hivyo, kutekeleza sheria kama hiyo katika jamii iliyojikita sana katika utamaduni itachukua juhudi zaidi. Nchini Somalia, hakuna sheria dhidi ya ubakaji. Bunge katika eneo la Somaliland lililojitangazia uhuru wake limepitisha sheria mpya dhidi ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono. text: Kanisa katoliki DRC limetoa wito kwa raia kuandamana kwa amani kote nchini kushinikiza mageuzi Rais Joseph Kabila, alifikia makubaliano na vyama vya upinzani kuandaa uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka 2017. Na kufikia mwisho wa mwaka huo, rais Kabila alikuwa tayari ashafika kikomo cha utawala wake wa mihula miwili kikatiba. Kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu: Hatua ya tume ya uchaguzi kuahirisha kwa mara nyingine uchaguzi mkuu hadi Aprili mwaka 2019 baada ya kuahirisha awali hadi mwishoni mwa mwaka jana 2017 uliongeza ghadhabu iliopo. Corneille Nangaa, kiongozi wa tume ya uchaguzi nchini, CENI, amesema ilikuwa ni muhimu kuuharisha uchaguzi huo kutokana na kuzuka ghasia katika eneo la Kasai ya kati, hali inayotatiza usajili wa wapiga kura. Kabila alitarajiwa kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2016 wakati muhula wake ulipomalizika Mahakama ikatoa uamuzi baada ya hapo kwamba rais Kabila anaweza kusalia madarakani hadi pale uchaguzi mwingine utakapoandaliwa. Tangu wakati huo, waandamanaji wamekuwa wakimiminika barabarani, na watu kadhaa wameuawa. Kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo limetoa wito kwa raia kuandamana kwa amani kote nchini kushinikiza mageuzi hayo ya uongozi. Haya ni licha ya serikali kupiga marufuku maandamano kufanyika tangu Septemba 2017 wakati maandamano ya kupinga utawala wa Kabila yalipokabiliwa na vurugu. Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linasema watu takriban milioni 7 wanahitaji usaidizi wa dharura wa kibinaadamu kutokana na mapigano ya kujihami nchini. Ghasia katika sehemu nyingi za DRC zimesababisha wengi kuishia kuhitaji msaada wa dharura Utawala wa Kabila: Katika muda wa utawala wake, kuna hisia kuwa rais Joseph Kabila amejitenga na demokrasia na kuiweka Congo katika hali iliyokosa utulivu. Hilo sasa linazusha hofu, hata kwa jamii ya kimataifa kuwa ongezeko la ghasia zinazoshuhudiwa kisiasa linaweza kuitumbukiza DRC katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hasira inaonekana kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo dhidi ya rais Joseph Kabila tangu akatae kuondoka madarakani wakati muhula wake ulipomalizika Desemba 2016. text: Borussia Dortmund iliwafunga wapinzani wao Schalke 4-0 huku wachezaji wakisherehekea magoli hayo kwa kugongana visukusuku Ligi ya taifa la Korea Kusini ilianza wikendi iliopita , huku ligi ndogo ndogo kama ile ya Belarus na Nicaragua zikiendelea bila wasiwasi. Je mechi zilichezwaje mwezi Mei 2020- zilichezwa bila mashabiki mbali na masharti ya kutokaribiana- je ilikuwaje? Vipimo vya kuchunguza joto, huku mabasi kadhaa na mipira ikinyunyiziwa dawa za kuuwa virusi. Video hii katika klabu ya RB Leipzig iliwataka watu kuosha mikono Timu ziliwasili katika mabasi kadhaa ili wachezaji wasikaribiane wakati wa safari ya kuelekea uwanjani . Wachezaji na wafanyikazi walikuwa wamewekwa katika karantini katika hoteli za timu hizo wiki yote na mara kwa mara walifanyiwa vipimo vya virusi vya corona. Wakati walipokuwa wakiondoka katika basi walivalia barakoa wakielekea uwanjani. Watu wengine waliokuwa wakihudhuria mechi hiyo , ikiwemo vyombo vya habari , walichunguzwa kwa vipimo vya joto kabla ya kuruhusiwa kuingia. Mashabiki hawakuruhusiwa kuingia kutazama mechi viwanjani hivyobasi hakuna mashabiki waliowasili katika uwanja. Ni watu 213 pekee walioruhusiwa uwanjani - 98 kandokando ya uwanja , - kama vile wachezaji , makocha na wavulana wanaorudisha mpira uwanjani na watu 115 katika maeneo ya mashabiki kama vile maafisa wa usalama , maafisa wa afya na wanahabari. Watu wengine 109 wakiwemo walinda amani na wasimamizi wa Video zinazomsaidia refa VAR waliruhusiwa kandokando ya uwanja. Mipira ilinyunyiziwa dawa ya kuuwa virusi na vijana wanaotumika kuingiza mipira uwanjani kabla na wakati wa kipindi cha mapumziko. Kulikuwa na mipira 30 ilioandaliwa kwa mechi , kila mmoja ukiwa umenyunyiziwa dawa na vijana wakurudisha mipira uwanjani na kuwekwa katika eneo moja badala ya kuwapatia wahezaji. Wachezaji wa ziada kutokaribiana walikokaa Wachezaji wote wa ziada walikaa katika viti huku kukiwa na umbali wa mita moja na nusu katika yao Wachezaji wa ziada na makocha walivalia barakoa na kukaa mbalimbali katika viti vyao. RB Leipzig ambayo ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Freiburg iliwawekea ngazi wachezaji waende katika viti vyao katika standi zao. Makocha waliruhusiwa kuingia bila barakoa ili kuweza kutoa maelezo kwa wachezaji wao. Wachezaji wa ziada walitoa barakoa zao ili kupasha misuli na wakati wa mabadiliko wachezaji waliokuwa wakitoka walipatiwa barakoa kabla ya kukaa katika viti vyao. Walisalimiana kwa kutumia visukusuku vya mikono badala ya kukumbatiana Baadhi ya magoli ylisherehekewa bila wachezaji kukaribiana ... lakini wengine walishindwa kufuata masharti ya kutokaribiana mna waliweza kusherehekea kwa pamoja Mchezo wenyewe haukuwa tofauti na ule wa kawaida huku wachezaji wakikabiliana na kukabana mbali na ufungaji wa magoli 16 katika mechi zote sita zilizochezwa siku ya Jumamosi. Lakini wachezaji hawakukaribiana wakati wa kusherehekea magoli yaliofungwa kama ilivyo kawaida - ambapo wachezaji hukumbatiana . Walisalimiana kwa kutumia viwiko vya mikono yao badala ya kukumbatiana. Hatahivyo baadhi ya magooli hususan yale yaliofungwa na wachezaji wa Hertha Berlin katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Hoffenheim yalisherehekewa kama kawaida. Hertha Berlin haitaadhibiwa kwa kuwa ligi hiyo ya Ujerumani ilitoa agizo hilo kama muongozo na sio sheria. Huku ikiwa ni watu wachache pekee wanaopiga kelele katika viti, watazamaji wa runinga waliweza kuwasikia wachezaji na wakufunzi wao wakizungumza pamoja na sauti ya mpira ukipigwa na kupiga wavu. Timu ziliruhusiwa kutumia wachezaji watano wa ziada katika mechi moja - kitu ambacho ligi nyengine zitalazimika kufaya zitakaporudi . Hivyobasi klabu ya Schalke , katika mechi yao dhidi ya Borrusia Dortmund walioshindwa 4-0 , waliweza kufanya mabadiliko mawili wakati wa mapumziko na wengine watatu baada ya mapumziko hayo. Wachezaji baadaye walipongeza standi tupu bila mashabiki Wachezaji wa Borussia Dortmund walikwenda hadi katika standi ya mashabiki wao na kusherehekea ushindi wao Baada ya kipenga cha mwisho wachezaji wa Borussia Dortmund walienda katika standi ya mashabiki wao kusherehekea mbele ya standi zisizo na mashabiki hao inayojulikana kama ukuta wa manjano inayobeba mashabiki 25,000. Wachezaji wa Wolfsburg walisalimiana na marefa wa mechi hiyo kwa kugongana miguu baada ya mechi Wachezaji wa Wolfsburg waligongana viatu na marefa na manaibu wao , badala ya maamkuzi ya kawaida kufuatia ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Augsburg. Wachezaji na maneja walihojiwa na maripota wa runinga wakiwa mbali huku mahojiano baada ya mechi yakifanywa kupitia mikutano ya video . Mshambuliaji wa RB Leipzig Yussuf Poulsen alihojiwa akiwa mbali Je mashabiki walisusia mechi? Police made sure fans could not congregate outside Sababu mojawapo ya mechi za ligi ya premia kuchezeshwa katika viwanja visivyopendelea upande wowote ni kujaribu kuzuia mikutano ya mashabiki nje ya viwanja vyao wakati wa mechi. Lakini hilo halikuonekana kuwa suala nyeti nchii Ujerumani siku ya Jumamosi. Iwapo huwezi kusherehekea kila kitu hakifurahishi. Baada ya sare ya bila magoli na Paderborn , mkufunzi wa klabu ya Fortuna Dusseldorf Uwe Rosler alisema: Siku haikuwa ya kawaida. ''Mimi ni mtu wa hisia , napenda kumkumbatia mchezaji mikononi mwangu kitu ambacho nilishindwa kufanya hii leo''. Mkufunzi wa Dortmund Luvcien favre alisema: hakuna kelele. Unashambulia goli, unapiga pasi nzuri, unafunga na hakuna kinachotokea. Ni kitu cha kushangaza kwa kweli. Ligi ya kandanda nchini Ujerumani iliendelea siku ya Jumamaosi na kutoa ishara za jinsi ligi ya Premia na ligi nyengine kuu zitakavyochezwa wakati zitakaporejea. text: Makala mpya ya filamu hizo itatolewa katika kipindi cha miezi saba ijayo. Mpiga picha Katie Lee anasema aliamua kuchukua hatua hiyo kujikumbusha kuhusu filamu hizo azipendazo sana. "Nilijua kwamba lingekuwa jambo ngumu kufanikisha, nikiwa bado nahakikisha kwamba inakuwa harusi ya kufana," aliambia BBC. Kulikuwa hata na mbweha - mbwa aliyepambwa kufanana na mbweha - kukamilisha muonekano wa Game of Thrones. Katie alihamasishwa zaidi na wahusika awapendao zaidi Daenerys Targaryen na Sansa Stark. Erin Foley aliyehusika katika mitindo na mavazi katika harusi hiyo anasema ndiyo yake aliyoifurahia zaidi na kwamba anajivunia pongezi ambazo amekuwa akipokea. Lindsay Pizzuti alihusika katika kupamba nywele za bi harusi na bwana harusi Bila shaka, Game of Thrones haiwezi kukamilika bila mbweha. "Nilitaka sana kuongeza mbweha," anasema Katie. "Nilijua ingeboresha picha za harusi zaidi." Walimtafuta mbwa kwa jina River katika kituo cha kutunza mbwa walioteswa na wamiliki wao na kutelekezwa. Harusi hiyo ilifanyika katika jumba la Smithmore ambalo linapatikana katika shamba la eka 121 katika mlima wa Blue Ridge, mashariki mwa Marekani. Keki ilikuwa na sifa za zimwi, kwa heshima ya Daenerys, Mama wa Mazimwi. Mashabiki sugu wa mwendelezo wa filamu za Game of Thrones waliamua kupiga hatua zaidi katika ushabiki wao kwa kufanya harusi ambayo iliiga filamu hiyo. text: Jaji Mkuu David Maraga akila kiapo Jaji Maraga atakuwa jaji wa pili kuhudumu nchini Kenya tangu kuanza kutekelezwa kwa katiba ya sasa nchini Kenya, ambayo ilifanyia mabadiliko mfumo wa mahakama, mwaka 2010. Ameapishwa baada ya kuidhinishwa na bunge siku ya Jumanne. Moja ya shughuli muhimu anazotarajiwa kutekeleza ni kuwaapisha wanachama wa jopo la kuteua makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Kenya inapoendelea kujiandaa kwa uchaguzi mkuu Agosti mwaka ujao. Kama jaji mkuu, atakuwa pia Rais wa Mahakama ya Juu ambayo husikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi za matokeo ya uchaguzi wa urais. Jaji Maraga anatazamwa na wengi kama mhafidhina. Wakati wa kuhojiwa kwake na Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), kabla ya jina lake kupendekezwa kwa rais, alikuwa amedokeza kwamba hawezi kufanya kazi siku ya Jumamosi ambayo ni siku ya kupumzika kwa mujibu wa dini yake ya Kiadventisti. Hata hivyo, ameonekana kusisitiza umuhimu wa kutumiwa kwa njia mbadala za kutatua mizozo katika jamii. Jaji David Maraga ameapishwa kuwa Jaji Mkuu mpya wa Kenya baada ya kustaafu kwa jaji mkuu wa awali Dkt Willy Mutunga. text: Kim alishambuliwa alipokuwa anasubiri kuabiri ndege kuenda Mshukiwa mmoja mwanamke raia wa Indonesia na mwanamume raia wa Malaysia ambaye anakisiwa kuwa mpenzi wake wote walikamatwa leo Alhamisi. Mwanamke mmoja maabye alikuwa na hati ya kusafiri ya Vietnam naye amekamatwa. Kim alifariki siku ya Jumatatau kutokana na kile kinachaoimiw akuwa aliwekeka simu wakati akisubiri kuabiri ndeg mjini Kuala Lumpur. Polisi wanasema kuwa wamemaliza kuufanyia uchunguzi mwili wake Kim licha ya matokeo kutotangazwa Picha hii ya CCTV imepeperushwa nchini Korea Kusini na Malaysian Washukiwa hao wawili wa wamezuiwa rumande kwa siku saba. Kuna uvumi unaoenea kuwa Korea Kaskazini ilihusika na mauaji hao. Picha moja kutoka kwa kamera za usalama ambayo imepepeshwa nchini Korea Kusini na Malaysia, inaonyesha mwanamke mwenye fulana nyeupe yenye jina "LOL". Inaaminiwa kuwa Kim alishambuliwa kwenye ukumbi wa kuabiri ndege kwenye uwanja wa ndege na wanawake wawili waliotumia aina fulani ya kemikali Kim Jong-nam na ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Leo Alhamisi Korea Kaskazini inasherehekea kile kinachotajwa kuwa miaka 75 ya kuzaliwa kwa Kim Jong-il, mareheu kiongozi wa zamani na baba wa Kim Jong-nam na Kim Jong-un. Familia inayoongoza Korea Kaskazini Washukiwa wawili zaidi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong-nam, ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Malaysia. text: Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010. Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa serikali na kudunisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Amekuwa akiongoza ukosoaji wa rais Paul Kagame huku akiongezea kuwa hukumu yake ilishinikizwa kisiasa. Bwana Kagame amepongezwa kwa kurekebisha uchumi wa Rwanda lakini pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Kuwachiliwa huru kwa bi Ingabire na wafungwa wengine 2,140 kulitangazwa na seriikali kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri. Taarifa ilisema kuwa bwana Kagame aliwaonea huruma chini ya uwezo wake kama rais. Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa kwa miaka 10, 2015 kwa kupanga njama za kumuua rais Paul Kagame. Alipokuwa akitoka jela, bi Ingabire alimshukuru rais Kagame, akisema huu ndio mwanzo wa kufunguka kwa sehemu ya kisiasa nchini Rwanda, kulingana na shirika la AFP. Lakini waziri wa haki Johnston Businge alipuuzilia mbali umuhimu wa kuachiliwa kwa bi Ingabire. ''Hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kuachiliwa kwake-na hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kufungwa kwake'', aliambia Reuters. Lakini Je Ingabire ni nani? Bi Ingabire alirudi kutoka jela nchini Uholanzi 2010 ili kushiriki katika uchaguzi wa urais. Alikamatwa na kuzuiliwa kuwania urais na amekuwa akihudumia kifungo jela tangu wakati huo. Bi Ingabire , ambaye ni mwanachama wa kabila la Hutu, alikuwa akihoji ni kwa nini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda ya 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Hutu. Wengi wa watu 800,000 waliouawa walikuwa watu wa Kabila la Tutsi lakini Wahutu wenye msimamo wa kadri pia waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali. Chama cha Rwanda Patriotic Front cha Rais Kagame kinachotawaliwa na Watutsi wengi kilimaliza mauaji hayo. Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu. text: Soko la kitaifa la uuzaji wa bangi lilifunguliwa saa sita usiku kuamkia Jumatano huku kukiwepo maswali kuhusu madhara kwa afya , sheria na usalama wa umma. Matayarisho ya kuhalilishwa matumizi ya mihadarati hiyo ilijumuisha kutumwa kwa sanduku la posta sheria kwa wakaazi milioni 15 inayoeleza sheria mpya na kampeni ya uhamasisho wa umma. Lakini wasiwasi bado unasalia, ikiwemo utayari wa idara ya polisi kukabiliana na visa vya uendeshaji magari, madereva wakiwa wamelewa bangi. Majimbo na manispaa nchini Canadian yamekuwa yakijitayarisha kwa miezi kadhaa kuelekea kumalizika kwa sheria inayopiga marufuku bangi nchini. Wanunuzi wa kwanza kufika bangi halali muda mfupi baada ya saa sita usiku Tawala za kieneo zinatarajiwa kutoa muongozo kuhusu sehemu ambazo bangi itauza na inapoweza kutumiwa. Hili limezusha kazi kubwa kisheria nchini huku idara zikichagua mifumo isiyobana uuzaji na matumizi ya bangi. Nduguye mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya afariki Coca-Cola yenye bangi italewesha? Maduka yalifunguliwa ilipofika saa sita usiku na katika baadhi ya maeneo tayari kulikuwa na misururu ya watu waliosubiri kuhudumiwa. Katika baadhi ya maeneo tayari kulikuwa na misururu ya watu waliosubiri kuhudumiwa. Ontario, jimbo lenye idadi kubwa ya watu nchini Canada litaanza kufunguwa maduka ya kuuza msimu ujao wa machipuko, licha ywa kwamba wateja wataweza kununua bangi kupitia maduka ya mitandaoni. Baadhi ya maduka ambayo yamekuwa yakiuza bangi kiharamu ambayo yameshamiri katika miaka ya nyuma tangu kupendekezwa kwa sheria hiyo huenda pia yakasalia wazi. Fahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa Haijulikani wazi iwapo Polisi itawasaka mara moja au iwapo itawapuuzia tu na kuwaruhusu waendelee na shughuli hizo. Prime Minister Justin Trudeau announced plans to legalise cannabis prior to the 2015 federal election Ni kwanini Canada imehalilisa bangi? Kuhalilishwa kwa bangi kunatimiza ahadi aliyotoa waziri mkuu Justin Trudeau, katika kampeni ya uchaguzi mnamo mwaka 2015. Kiongozi huyo wa chama tawala cha ki Liberali ameeleza kwamba sheria za jadi za nchi hiyo dhidi ya matumizi ya bangi hazifanyi kazi, ukizingatia kwamba raia nchini humo ni miongoni mwa wanaotumiwa kwa kiasi kikubwa bangi duniani. Ameeleza kuwa sheria hiyo mpya imeundwa kuwaondolewa watoto bangi karibu, na kuondosha faida wanayoipata wahalifu. Serikali ya shirikisho inakadiria pia itapata $ milioni 400 kwa mwaka katika tozo la kodi katika mauzo ya bangi. Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi Umiliki wa bangi ulikuwa haramu kwa mara ya kwanza Canada mnamo 1923 lakini matumizi yake kwa misingi ya dawa ilihalilishwa tangu 2001. Canada inafuata nyayo za Uruguay, iliyokuwa nchi ya kwanza duniani kuhalilisha uuzaji wa bangi kwa starehe mnamo 2013. Baadhi ya majimbo nchini Marekani tayari yamepiga kura kusitisha marufuku hiyo. Matumizi ya bangi kwa manufaa ya dawa yamekuwa yakikithiri pia katika nchi nyingi za Ulaya. Canada imekuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalilisha uuzaji, umiliki na matumizi ya bangi kwa starehe. text: Bernard mwenye miaka 40, alihukumiwa kwa makosa ya mauaji mwaka 1999 alipokuwa kijana mdogo, na alikuwa mhalifu mdogo kuhukumiwa na serikali katika kipindi cha miaka karibu 70. Bernard aliiambia familia ya wenza aliowaua kuwa anaomba msamaha, kabla ya kuuawa kwa kuchomwa sindano siku ya Alhamisi. Hukumu nyingine nne za vifo zimepangwa kutekelezwa kabla Donald Trump hajaondoka madarakani. Ikiwa yote matano yatafanyika, Bwana Trump atakuwa amesimamia hukumu zaidi za kifo katika kipindi cha zaidi ya karne moja. Na kufanya idadi yake kufikia 13 tangu mwezi Julai. Maneno yake ya mwisho kabla ya kifo Bernard alitangazwa kuwa amekufa saa 21:27 za huko siku ya Alhamisi sawa na saa 11 siku ya Ijumaa katika gereza la jela la Terre Haute. Kabla ya hayo alielekeza maneno yake ya mwisho kwa familia ya walioathirika, akizungumza kwa utulivu kwa zaidi ya dakika tatu. ''Ninaomba radhi. Haya ni maneno pekee ninayoweza kusema kuelezea namna ninavyojisikia sasa na namna nilivyojisikia siku hiyo,'' alisema, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press. Utekelezaji wa hukumu ya kuuawa ulicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili baada ya mawakili wa Bernard kuitaka Mahakama kuu kusitisha- lakini ombi hilo lilikataliwa. Kesi ya Brandon Bernard Bernard alipewa adhabu ya kifo kwa kuhusika kwake katika mauaji ya Todd na Stacie Bagley mnamo Juni 1999. Alikuwa mmoja wa vijana watano wanaotuhumiwa kuwaibia wawili hao na kuwalazimisha kuketi nyuma ya gari lao huko Texas. Walipigwa risasi kwenye gari na mwenzao wa miaka 19 Christopher Vialva kabla ya Bernard kulichoma moto gari. Mawakili wa utetezi wanasema wote wawili walifariki kabla ya gari kuchomwa moto. Mchunguzi huru aliyeajiriwa na upande wa utetezi alisema Stacie alikuwa amekufa kabla ya moto. Walakini, ushuhuda wa serikali wakati wa kesi hiyo ulidai kwamba ingawa Todd Bagley alikufa papo hapo, Stacie alikuwa na masizi katika njia yake ya hewa, akiashiria kwamba alikufa kutokana na kuvuta pumzi ya moshi na sio jeraha la risasi. Mawakili wa Bernard wanadai aliogopa nini kingetokea kwake ikiwa atakataa kufuata maagizo ya Vialva, ambaye aliuawa mnamo Septemba. Wengine waliohusika katika tukio hilo walipewa vifungo vya gerezani kwani walikuwa chini ya miaka 18 na kuhesabiwa kama vijana. Mawakili wa Bernard walisema kwamba anapaswa kupewa kifungo cha maisha gerezani bila msamaha, kwani, kwa muda wote wa gerezani, amehifadhi rekodi nzuri na alifanya kazi na mipango ya kuwafikia watu ili wasijihusishe na uhalifu. Nani alimtetea? Mwendesha mashtaka wa ambaye alipinga hukumu ya kifo ya Bernard alikuwa ametaka Bernard atumikie kifungo gerezani. Katika kipengele cha maoni kilichochapishwa katika jarida la Indianapolis Star, Angela Moore aliandika: "Baada ya kujifunza mengi tangu mwaka 2000 kuhusu kukomaa kwa ubongo wa mwanadamu na kuona Brandon akiwa mtu mzima mnyenyekevu, mwenye majuto anayeweza kuishi kwa amani gerezani, tunawezaje kusema ni miongoni mwa kundi dogo la wahalifu ambao lazima wauawe? " Mawakili watano kati ya wanasheria tisa walitaka Bwana Trump abadilishe hukumu ya kifo ya Bernard. Maelfu ya watu wengine walimsihi rais ampe huruma Bernard, pamoja na maseneta Richard J Durbin na Cory Brooker. Siku ya Alhamisi, mawakili wanaoongoza Allen Dershowitz na Ken Starr pia walijiunga na timu yake ya utetezi. Nyota wa runinga Kim Kardashian West alituma ujumbe kadhaa katika mtandao wa twitter kuhusu kesi ya Bernard kwa wafuasi wake wakati wa kuelekea kunyongwa, akiwataka wajiunge kupinga hukumu hiyo. Kardashian West anasomea kuwa wakili huko California na hapo awali amesaidia utetezi katika kesi za uhalifu. Mwezi Machi alitembelea Ikulu akiwa na wanawake watatu ambao hukumu yao ya kifungo cha gerezani ilikatishwa na Rais Trump. Hukumu ya kifo ya mfungwa Brandon Bernard imetekelezwa jimboni Indiana baada ya ombi la dakika za mwisho kutenguliwa kwa hukumu kukataliwa na Mahakama kuu ya Marekani text: Fataki hapa zinaonekana London Eye ambapo zilirushwa angani kwa dakika 10 hivi katikati mwa London "Yellow Vest", waandamanaji wanaovalia fulana za rangi ya manjano nchini Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokuwa wanaandamana karibu na Champs-Elysees jijini Paris Hapa, fataki zinaonekana juu ya sanamu ya Quadriga katika lango maarufu la Brandenburg Gate, Berlin Wanandoa hawa nao wanaonekana wakikoleza upendo wao kama sehemu ya sherehe za kuulaki Mwaka Mpya eneo la Red Square, Moscow Jijini Nairobi, fataki zinaonekana zikirushwa angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya Na hapa, mwanaulimbwende anaonekana akipamba nywele ya mmoja wa watu waliojitokeza mjini Ahmedabad, India kwa sherehe za kuulaki mwaka mpya Maelfu walikusanyika pia Pyongyang, Korea Kaskazini kwa maonesho ya fataki katika uwanja wa Kim Il Sung Hapa ni fataki zikirushwa na watu ufukweni Gangneung, katika mkoa wa Ganwon, Korea Kusini Katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, Dubai, fataki zilikuwa tele pia Ufilipino, huyu aliamua kuvalia miwani ya 'kumsaidia kuuona vyema' Mwaka 2019 katika sherehe iliyofanyika katika eneo la Metro Manila, jijini Quezon Waumini wa Kibuddha nao hapa wanaonekana wakiwasha mishumaa kuukaribisha Mwaka wa Nguruwe kwa mujibu ya miaka ya nyota ya Kichina katika hekalu la Jogyesa jijini Seoul, Korea Kusini Hapa watu wanaonekana wakijaribu kupiga picha fataki zilizorushwa kwenye jengo refu maarufu la Taipei 101 nchini Taiwan Anga ya Hong Kong pia ilipambwa kwa fataki watu wakiukaribisha mwaka 2019 nchini China Sherehe ya Mwaka Mpya pia ilifanyika Beijing, China Na Marina Bay, Singapore kulikuwepo uhondo zaidi Huko Sydney Harbour Bridge nchini Australia, maonyesho ya fataki yalidumu dakika 12 Unaweza kusoma pia: Njia bora ya kutimiza malengo yako ya Mwaka Mpya Upinzani waazimia 'kudai demokrasia' Tanzania 2019 Apandikizwa uso mpya baada ya kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi Picha zote zina hakimiliki. Shangwe, vifijo, nderemo zilisheheni miji mbalimbali watu wakisherehekea kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2019 katika majiji mbalimbali duniani, fataki nazo zikatanda angani . text: Seneta wa Australia Larissa Waters amekuwa mwanasiasa wa kwanza kunyonyesha katika bunge la taifa hilo. Bi Waters kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha Green Party alimnyonyesha mwanawe wa miezi miwili Alia Joy wakati wa kura siku ya Jumanne. Bunge mwaka uliopita lilijiunga na seneti kuruhusu kunyonyesha, lakini hakuna mbunge ambaye alikuwa amewahi kufanya hivyo. Hatua hiyo inajiri baada ya Kelly O'Dwyer, waziri wa serikali 2015 kutakiwa kutoa maziwa ili kutokosa vikao vya bunge. ''Tunataka wanawake zaidi na wazazi bungeni'', bi Waters alisema katika mtandao wake wa facebook. ''Na tunahitaji mazingira bora katika maeneo ya kazi kwa uangalizi mzuri wa watoto kwa kila mtu''. Seneta wa Leba Katy Gallagher alisema kuwa wakati huo unapaswa kutambuliwa. ''Wanawake wamekuwa wakinyonyesha katika mabunge tofauti duniani'', aliamba chombo cha habari cha Skynews Australia. '''Wanawake wataendelea kuwa na watoto na iwapo wanataka kufanya kazi zao na wawe kazini na kuangalia watoto wao...basi bila shaka ukweli ni kwamba tutalazimika kuwapatia haki yao''. Hadi kufikia mwaka uliopita, wabunge katika bunge dogo walikuwa wanaweza kuwabeba watoto wao na kuingia katika afisi za bunge pekee ama maeneo ya uma. Wanasiasa wameruhusiwa kunyonyesha katika bunge la seneti tangu 2003. Wazo hilo ni swala tata katika mabunge mengi duniani. Mnamo mwaka 2016, mbunge wa Uhispania Carolina Bescansa kutoka chama cha Podemos alikosolewa na kupongezwa wakati huohuo kwa kumpeleka mwanawe bungeni na kumnyonyesha. Seneta wa Australia Larissa Waters amekuwa mwanasiasa wa kwanza kunyonyesha katika bunge la taifa hilo. text: Kwa saa kadhaa sasa toka matokeo ya uchaguzi yaanze kutangazwa, amekuwa nyuma ya mshindani wake Joe Biden. Hata hivyo mbio za ushindi bado hazijafikia kikomo, na msamiati wa kushindwa ni adimu kabisa katika kamusi ya Trump. Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na alikuwa tangu mwanzo amesema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani na hata kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Trump ni tajiri anayemiliki majumba mengi na mahoteli, na hata kabla ya kushinda urais miaka minne ilopita alikuwa maarufu kwa kuendesha kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga. Kwa wafuasi wake, yeye ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani. Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani. Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri. Lakini kwa wakosoaji wake, Trump anaonekana ni mbaguzi na mfitini, mfidhuli mkubwa ambaye hakustahili toka awali kuwa kiongozi wa taifa lenye nguvu zaidi duniani. Je, urais wake umekuwaje? Trump, akiwa mgeni kabisa kwenye ulimwengu wa siasa alistaajabisha dunia Novemba 2016 kwa kumuangusha mwanasiasa mkongwe Hillary Clinton. Alipata kura za wajumbe 278, Bi Clinton akiwa na 218. Mshindi alihitajika kupata kura 270 za wajumbe. Kinyume na matarajio ya wengi, ndoto ya kisiasa ya Trump ikatimia. Lakini miaka minne ya urais wa Trump imeendaje mpaka sasa? Kama ilivyokuwa kwenye kampeni yake ya awali, urais wake pia umejaa mambo ambayo baadhi wameyatafsiri kama ni viroja. Mwezi wake wa kwanza madarakani, Januari 2017, Trump alitia saini amri yake ya kwanza, kuzuia wasafiri kuingia Marekani kutoka mataifa saba ambayo mengi ni ya wenye raia wengi Waislamu. Japo uamuzi huo umetafsiriwa na wengi kama ni wa kibaguzi, Mahakama ya juu zaidi ya Marekani ilitoa hukumu ya kumuunga mkono Trump. Baada ya hapo, akaishangaza Marekani kwa kumtimua kazi Mkurugenzi wa Shirika la Ukachero la FBI James Comey. Kufutwa kazi kwa Comey kulitafsiriwa ni kama sehemu ya njama ya kuficha ukweli kuwa Urusi ilisaidia Trump kuingia madarakani. Hata hivyo uchunguzi rasmi wa tuhuma hizo ulionesha kuwa hakukuwa na njama yoyote ya kijinai baina ya kampeni ya Trump na Urusi. Trump huwa anaamini sana atashinda katika mambo mengi ayafanyayo Baada ya hapo zikaja tuhuma kwamba Trump ameishinikiza serikali ya nchi moja kuchunguza tuhuma ambazo zingeweza kumpaka matope mpinzani wake Joe Biden. Tuhuma hizo zikafanya Trump apigiwe kura ya kutokuwa na imani na Bunge la Congress ambalo lina wajumbe wengi wa Democrats, hata hivyo, Bunge la Senate lenye wajumbe wengi kutoka chama chake cha Republican wakamsafisha na kusalia madarakani. Trump na mkewe wa sasa Melania wakati wa kongamano la chama cha Republican mjini Cleveland Julai Licha ya yote, Bwana Trump ameweza kusalia na umaarufu wake na ushawishi katika maeneo ambayo walimchagua toka awali, hilo ni kutokana na kutekeleza ahadi za kampeni ambazo alizitoa. Bila shaka, jambo alofanya Trump ambalo litaendelea kudumu nchini humo na kuathiri juu ya mustakabali wa sera za nchi hiyo ni uteuzi wake wa majaji watatu wa mrengo wa kihafidhina katika Mahakama ya Juu Zaidi ya nchi hiyo. Uchaguzi wa mwaka huu umetawaliwa na janga la virusi vya corona na katika suala hilo, Trump amekosolewa vikali namna alivyolishughulikia. Marekani inaongoza duniani kwa idadi ya maambukizi na vifo. Kampeni yake ilibidi isimame kwa muda baada ya yeye mwenyewe kuambukizwa virusi hivyo. Kwa sasa, kura zimeshamalizwa kupigwa, na mchakato wa kuzihesabu unaendelea ili kuona kama Wamarekani wamemrejesha katika Ikulu ya White House kwa miaka mingine ama wamemtoa na kumpa nafasi hasimu wake Joe Biden. Failia ya Trump Donald Trump ameo mara tatu, Ivana na Marla Maples, mke wa kwanza na wa pili mtawalia ambao wote ametalikiana nao. Mke wake wa sasa ni Bi Melania. Bwana Trump ana watoto watoto watano, watatu wa kiume Donald Trump Jr, Eric, Barron na watoto wawili wa kike Ivanka na Tiffany. Rais huyo wa 45 wa Marekani alizaliwa Juni 14 mwaka wa 1946, mjini New York, akiwa mtoto wa tano kati ya watoto sita. Babake Fred alikuwa tajiri aliyemilki majumba na babu zake Trump walikua wahamiaji kutoka Ujerumani. Mamake Mary alikuwa mzaliwa wa Scotland. Tangu utotoni, Trump alikuwa mtundu na wazazi wake walimpeleka shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi mjini New York. Baadaye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, kitivo cha elimu ya biashara mwaka wa 1968. Alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha kadiri, viungani mwa New York. Hata hivyo Donald Trump alikuwa na ndoto ya kufanya biashara nje ya makaazi ya Queens na Brooklyn. Donald Trump akiwa na mkewe Ivana mwaka 1989 Aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyowekwa na utawala wa Reagan miaka wa 1980. Kuna tofauti kuhusu utajiri hasa wa Trump. Aliwahi kuambia tume ya uchaguzi kwamba anao utajiri wa kima cha dola bilioni 10. Hata hivyo jarida la Forbes limenadi kwamba utajiri wa Trump haufikii juu ya bola bilioni 4.5. Lakini unapotembea barabara kuu za Manhattan, kampuni ya Trump imeweka mabawa yake kwa majumba ya kifahari yaliyofuatana. Yapo mahoteli, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai nembo yake ikiwa ni Trump. Ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking'aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, "The Apprentice," katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico. Donald Trump, Rais wa Marekani, kwa sasa yupo katika mpambano mkali wa kuzuia kuwa rais wa kwanza wa taifa hilo kwa takriban miongo mitatu kuongoza kwa kipindi kimoja tu cha miaka minne. text: Hali ilivyo kwenye eneo la jangwani ambapo barabara ya Morogoro imefunikwa na maji yaliyofurika. Kampuni ya Mabasi ya mwendo kasi (Udart) imelazimika kusitisha huduma zake usafiri kwa mabasi yanayotumia barabara kuu ya Morogoro eneo la Jangwani na barabara ya Kawawa katika Bonde la Mkwajuni kuelekea Morocco. Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Udart, Deus Bugaywa imeeleza kuwa safari zilizositishwa ni kati ya Kimara -Kivukoni, Kimara - Gerezani, Morocco - Kivukoni na Morocco -Gerezani kuanzia mapema alfajiri ya leo Jumatatu. "Huduma zinazotolewa sasa ni kati ya Kimara - Mbezi, Kimara -Magomeni Mapipa, Gerezani - Muhimbili, Kivukoni - Muhimbili na Gerezani - Kivukoni" amesema Buyagwa. Eneo la Jangwani linafahamika kwa kujaa maji mengi barabarani kipindi cha mvua. Udart wameomba radhi wateja wao na kuongeza kuwa wanaendelea kufuatilia hali ya maji Jangwani na kwamba yakipungua huduma zitaendelea kutolewa. Baadhi ya watu wamekua wakitoa ushauri kwa wenzao walioshindwa kufika sehemu zao za kazi kutokana na changamoto ya usafiri ya kati kati ya mji kutumia usafiri mbadala. Wengine waliamua kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter kufanya hivyo. Ukiachana kutatizika kwa usafiri wa mwendokasi, wakaazi wengine wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wamekubwa na adha kubwa ya foleni kutokana na mvua hizo kuharibu ama kuziba baadhi ya barabara muhimu. Mamlaka zaonya mvua kubwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (MET) tayari imeshatoa tahadhari juu ya uwepo wa mvua kubwa ambayo itaupiga ukanda wa pwani wa nchi hiyo kwa siku tatu mfululizo kutokea leo Jumatatu Mei 13 mpaka Jumatano Mei 15. MET wametahadharisha kuwa mvua hizo zitakuwa na madhara makubwa ikiwemo: "Baadhi ya makazikuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kijami. Kuanguka kwa kwa majani na matawi ya miti. Kuathirika kwa usafiri wa baharini na uvuvi." Mamlaka hiyo pia imetahadharisha kuwa kwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii, ukanda huo wa pwani ya Tanzania utakabiliwa na upepo mkali. Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika mji wa Dar es Salaam, Tanzania imeathiri huduma ya usafiri wa umma huku idara ya hali ya hewa ikitoa tahadhari. text: Alicia Keys ameipakia video hiyo katika ukurasa wake wa Twitter ulio na wafuasi 31 milioni, na kuambatisha ujumbe: "Look at this beautiful soul!! / Hebu tazama kiumbe huyu alivyo mzuri" Amani mwenye miaka 13 alikuwa akiuimba wimbo kwa jina This Girl is on Fire na anasema aliuimba kama shukrani kwa mtalii aliyekuwa amempa yeye na watoto wenzake pipi. Anasema hiyo ilikuwa ndiyo zawadi pekee ambayo angeweza kumpa mtalii huyo. Video yake iliwekwa mtandaoni na mtalii huyo na mara moja ikawavutia wengi na kusambaa kwa kasi. Amani anatoka mtaa wa Githurai Kimbo, Kiambu karibu na jiji la Nairobi. Mtazame hapa: Msichana Mkenya aliyegusa nyoyo za wengi kwa kipaji chake. Wanaomfuatilia Alicia Keys kwenye mtandao wa Twitter wamevutiwa sana video hiyo baadhi wakimsifu na pia kumshukuru msanii huyo kwa kuisambaza video hiyo. Baadhi wamemtaka Keys kumfunza uimbaji au hata kuwa mdhamini wake na wengine wakashangaa kama ni yeye aliyemfunza uimbaji. Mandela Onchwati ameandika: "Natumai atafanikiwa, siku za usoni, tunaweza kuwa na hadithi ya ufanisi kutoka Githurai Ghetto Kenya. Nyota anayeibukia." Huyu alitaka kutambuliwa, lakini Bob Marley alituacha zamani. Huyu anamuomba Alicia Keys amsaidie msichana huyo, lakini anasema ni miongoni mwa watu wenye vipaji kutoka Afrika wanaobanwa na sera za muda mrefu za kuibagua na kuifanya Afrika kusalia maskini. Unaweza kusoma pia: Video ya msichana Mkenya kwa jina, Gracious Amani, kutoka eneo maskini nchini Kenya ambayo ilipata umaarufu kutokana na alivyouimba wimbo wa nyota wa muziki Alicia Keys hatimaye inaonekana kumfikia msanii huyo. text: Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakikabiliana na polisi mtaa wa Mathare na Kibera jijini Nairobi na eneo la Kisumu Mpinzani mkuu wa Bw Kenyatta, Bw Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi mkubwa wa kura. Seneta James Orengo ameiambia BBC kuwa chama chake, kinachoongozwa na Bw Raila Odinga, hakitapinga matokeo ya uchaguzi mkuu mahakamani, huku akisema kuwa Uhuru Kenyatta tayari ametoa vitisho kwa majaji. Kufikia sasa watu 11 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu, ambazo zilianza mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kushinda kutangazwa mshindi kwa muhula wa pili mnamo usiku wa kuamkia Jumamosi. Tume ya taifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya, imetoa orodha ya juu ya wahasiriwa wa ghasia hizo huku ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao wameuwawa katika visa vinavyohusiwa na uchaguzi huo, huku ikiongeza kuwa polisi wanatumia nguvu kupita kiasi. Uhuru Kenyatta kushoto) na Mpinzani wake Raila Odinga (kulia) Kaimu Waziri wa usalama wa ndani, Fred Matiangi, amewataja waandamanaji kama "wahalifu". Kiongozi mmoja mkuu wa chama cha upinzani, Bwana Johnson Muthama, amesema kuwa polisi wanajaribu kuwalazimisha watu "wakubali matokeo hayo." Ghasia zilitokea pia mtaa wa Kibera, Nairobi Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya, ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na maandamano wenye nia ya kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo "feki" ya uchaguzi mkuu. text: Baadhi ya yatima,ambao sasa ni watu wazima, hawajui walikua wakiitwa majina gani Oswald hajui chochote kuhusu maisha yake kabla ya kuokotwa na mwanamke mmoja akiwa kwenye rundo la miili jijini Kigali, akijaribu kunyonya matiti ya mwanamke aliyepoteza maisha. Inakadiriwa alikua na umri wa miezi kati ya miwili na mitatu, hakuna anayejua kwa hakika. Kwa uhakika ni kuwa ni mmoja wa watoto wengi waliopoteza majina yao, miaka ya kuzaliwa na historia zao wakati wa siku 100 za machafuko yaliyoikumba Rwanda, yaliyoanza tarehe 7 mwezi Aprili, miaka 25 iliyopita. Giti: Eneo pekee Rwanda ambalo haikuathirika na mauji ya kimbari Wapiganaji 57 M23 waliokuwa Uganda warejea nyumbani DRC Wakati Rwanda ikiadhimisha kumbukumbu ya mauaji hayo, Oswald na vijana wengine wa kiume na wakike kama yeye wamejikuta peke yao, wadogo sana kuweza kukumbuka maisha yao ya zamani, wamekua wakiangalia watu waliokusanyika wakijiuliza kama familia zao zitakua zimesimama miongoni mwa watu walionusurika, au ni miongoni mwa watu 800,000 wahutu na watutsi waliopoteza maisha. ''Kwa asilimia hamsini nafikiri wazazi wangu walifariki, asilimia 50 nina matumaini kuwa nitawapata,'' Oswald alisema, akionyesha matumaini ambayo yanaonekana kushangaza baada ya miaka mingi kupita. Oswald ni miongoni mwa watoto 95,000 wanaoaminika kuwa yatima kutokana na mauaji ya kimbari, ambayo yalianza saa kadhaa baada ya ndege iliyokua imembeba rais wa wakati huo Juvenal Habyarimana kushambuliwa, kuanguka tukio lililogharimu maisha ya kila mtu aliyekua kwenye ndege hiyo. Kuna kitu kimepungua Mwanamke mmoja wa kabila la Hutu aliyemuokota, Josephine, alimpoteza mumewe wakati wa mauaji ya kimbari.Aliuawa na wanamgambo wakati akijaribu kuwasaidia watutsi Alipitia madhila ya kubakwa na wanamgambo wa Interhamwe ambao walitekeleza mauaji dhidi ya watu wengi, kisha akaambukiwa virusi vya ukimwi. Pamoja na shida hiyo, aliweza si tu kumtunza Oswald, lakini pia watoto wengine, akawatunza kama wakwake. Lakini kadiri Oswald alipokua akikua, alianza kuhisi kuwa kuna kitu kimekosekana. ''Niliwaona watoto wengine na baba zao, na nikaanza kufikiria kuhusu wazazi wangu'', aliiambia BBC. Kujaribu kujua wewe ni nani wakati unacho kidogo kukufanya usonge mbele ni vigumu sana Unicef inasema watoto 95,000 walikua yatima wakati wa mauaji ya kimbari Kwa Jean Pierre, kutafuta kwake majibu kumefanyika kwa kutambua nyuso mitaani ''Nikimuona mtu anayefanana na mimi, ninahisi ni ndugu yangu,'' anasema Jean Pierre ambaye anaamini ana umri wa miaka 26 japo hana uhakika. Njia hii, anaamini, inaweza kuzaa matunda: hivi karibuni alikutana na mwanamke mmoja anayefanana naye, kisha akamfuata ili aweze kumjua vizuri. Ikabainika kuwa mwanamke huyo alipoteza kaka yake wakati huo, kijana mdogo ambaye kwa sasa angekua na umri sawa na Jean Pierre. Jean Pierre alikimbia kwenda kukutana na mama. Kusaidiana ''Nilipokutana na Mama Asalia, niliguswa,'' alisema.''Nilihisi ni mama yangu kabla hajatambulishwa kwangu.'' Wawili hao huwa wanawasiliana karibu kila siku, ingawa hawana ushahidi kuwa wana undugu, Vipimo vya vinasaba DNA ni ngumu kupatikana sababu ya gharama. Lakini itakuwaje kama siye? akionyesha mashaka.Ataweza kuishi , hata hivyo ameishi miaka 25 imepita. Oswald na Jean Pierre, na rafiki yao Ibrahim, waliamua kufanya jambo.Hivyo waliunda kundi kwa ajili ya kuwasaidia yatima wenzao. Jean Pierre (kushoto), Ibrahim (katikati) na Oswald wameamua kuwasaidia yatima wa mauaji ya kimbari Ibrahim amewasikiliza marafiki zake wawili wakisimulia.Kama wao, hafahamu ana umri gani hasa;Labda 25, anahisi. Hajui majina ya wazazi wake-Kitu ambacho huwa anakumbushwa kila mara anapojaza fomu za kiofisi. Si kama Oswald na Jean Pierre, haamini kama wazazi wake wako hai kutokana na namna alivyookotwa akiwa mdhaifu sana. Wakati fulani ilikua karibu aipate familia yake:Miaka michache iliyopita,alialikwa kukutana na familia ambazo zilikua zikitafuta watoto wa kiume waliopotea wenye umri kama wake. Ikaishia kuwa kumbukumbu mbaya kwake,yenye kuvunja moyo. Watu ambao walikua watoto kipindi cha mauaji ya kimbari, inawawia vigumu kuwapata ndugu zao. Hajakata tamaa, hana kazi na ndoto zake za kufika elimu ya juu ziliyeyuka.Anajiona mtu asiye na msaada, aliyetengwa, hisia ambazo marafiki zake wamezieleza pia. ''Hatuna msaada wa kutufanya tuweze kusonga mbele,'' Jean Pierre anaeleza. ''Hatuna namna ya kutufanya tuishi maisha mazuri.'' Walichonacho ni urafiki wao, na kupitia umoja wao 'Tumaini kwa familia ijayo' wamekubaliana kushirikiana kwa kila walichonacho. Wakati tunaondoka, kuna swali moja la kuuliza linalokwenda kwa Oswald: Josephine, mwanamama aliyemlea kwa mapenzi atajisikiaje akijua kuwa ameipata familia yake? Anatabasamu ''Itakuwa jambo jema kwetu sote.'' Miaka 25 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, baadhi ya yatima kwa shauku kubwa wanaendelea kutafuta historia yao ambayo ilipotea. text: Rooney aliongoza England kushinda mechi dhidi ya Scotland Ijumaa Nahodha huyo alihudhuria sherehe hiyo ya harusi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa inakaa wakicheza mechi ya kimataifa. Nahodha huyo amesema kupitia taarifa kwamba picha hizo "hazifai". Amesema ingawa picha hizo zilipigwa wakati wake wa kupumzika, "hazifai kwa mtu wa hadhi" yake. Gazeti la The Sun la Uingereza lilichaisha picha hizo ambazo zinamuonesha Rooney, 31, akiwa kwenye sherehe usiku wa Jumamosi baada ya mechi ya England ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland. England walishinda mechi hiyo. Chama cha Soka cha England (FA) kimesema kitathmini upya sheria kuhusu mambo ambayo wachezaji wanaruhusiwa kufanya wakati wao wa kupumzika. Gazeti la The Sun linadai FA imechukua hatua hiyo kwa sababu wachezaji 10 wa England walikaa kwenye kilabu cha usiku hadi saa 04:30 GMT Jumapili. Rooney hakucheza mechi ambayo England walitoka sare 2-2 na Uhispania Jumanne kwa sababu ya jeraha ndogo kwenye goti. Wayne Rooney amemuomba radhi kaimu meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate baada ya picha kutolewa zikimuonesha akiwa mlevi wakati wa sherehe ya harusi. text: Bwana Botha an umri wa miaka 51 na baba wa watoto watano kutoka mkoa wa Limpopo nchini Afrika Kusini. Mtandao wa anaripotiwa kupigwa risasi wakati alimuinua Theunis Botha akitumia pembe yake kabla ya kuanguka na kufariki huku akimlalia na kumuaa bwana Botha. Amekuwa akiongoza kundi la wawindaji karibu na mbuga ya Hwange nchini Zimbabwe wakati alifariki. Mbuga hiyi ndiko simbna Cecil aliuwawa na muwindaji mmarekani mwezi Julai mwaka 2015 na kuzua shutuma kote duniani. Mtandao wa Botha unasema kuwa alikuwa na ujuzi wa kuwinda Simba na Chui. Bwana Botha an umri wa miaka 51 na baba wa watoto watano kutoka mkoa wa Limpopo nchini Afrika Kusini. Mtandao wa Botha unasema kuwa alikuwa na ujuzi wa kuwinda Simba na Chui. Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vilisema kuwa bwana Botha alikuwa rafiki wa muwindaji mwingine Van Zyl, ambaye mabaki yake yalipatikana ndani ya mamba mwezi uliopita. Mtaalamu mmoja wa uwindaji ameuwawa baada ya kulaliwa na ndovu ambaye alikuwa amepigwa risasi text: Tahadhari hiyo iliyotolewa Jumanne jioni na kuchapishwa kwenye tovuti ya ubalozi na mitandao ya kijamii ya ubalozi huo inaendelea kuonya raia wan chi hiyo waliopo Tanzania na hususani jijini Dar es Salaam kuendelea kuchukua tahadhari. Hatua hiyo inakuja wiki moja toka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania kumuita na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani Bi Imni Peterson juu ya tahadhari zilizotolewa hapo awali. Katika taarifa iliyotolewa na serikali baadaye ilieleza kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Wilbert Ibuge alieleza masikitiko yake juu ya namna Ubalozi huo umekuwa ukitoa tahadhari zake. Suala kuu ambalo wizara ililalamikia ni juu ya ubalozi kudai kuwa hospitali nyingi jijini Dar es Salaam (bila ya kuzitaja hospitali hizo) zimefurika wagonjwa wa COVID-19 jambo ambalo serikali inasema si kweli. Juu ya suala hilo la kuelemewa kuwa, katika tahadhari hii mpya, ubalozi umeeleza: "Vituo vya afya Tanzania vinaweza kuelemewa kwa haraka katika janga la kiafya. Kumekuwa na nyakati ambazo wakati wa mlipuko wa COVID-19 ambapo hospitali jijini Dar es Salaam zilifikia ukomo kwa kupokea wagonjwa wengi wa COVID-19." Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dkt Elisha Osati hivi karibuni aliimbai BBC kuwa mfumo wa afya nchini humo haujaelemewa na corona. Kama ilivyokuwa awali, tahadhari mpya imeeleza kuwa takwimu mpya za ugonjwa wa corona ikiwemo vifo hazijatolewa nchini Tanzania toka Aprili 29. Hata hivyo, serikali ya Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa kasi ya ugonjwa wa corona imepungua. Kutokana na hali hiyo Rais John Pombe Magufuli ameruhusu kwa baadhi ya shughuli zilizokuwa zimefungwa awali kama ligi kuu ya kandanda, masomo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kidato cha sita kurejea. Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu Jumatatu wiki hii alieleza kuwa "kuna wagonjwa wanne tu wa corona ambao bado wamelazwa hospitali kwa Tanzania Bara." Tahadhari hiyo inaonya raia wa Marekani kuwa kuna uwezo mdogo wa hospitali nchini Tanzania ambao unaweza kusababisha ucheleweshwaji wa huduma na kuhatarisha Maisha yao. Ubalozi huo katika tahadhari iliyopita ya Mei 25 ilieleza kuwa hakukuwa na mpango wa karibuni wa kuleta ndege ya kuwaondosha raia wake nchini humo. Katika tahadhari mpya, umeeleza raia wake kuwa kutokana na serikali ya Tanzania kuruhusu ndege za abiria za kimataifa kurejesha safari zake tayari kuna mashirika ya ndege ambayo yameanza huduma toka Juni 1. Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari mpya ya afya na kusisitiza kuwa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona bado ipo juu jijini Dar es Salaam. text: Harvey Weinstein ni mwandaaji filamu maarufu Bw Weinstein alikuwa anachanga fedha nyingi kwa chama cha Democratic. Kampuni yake ilimfuta kazi Jumapili kutokana na tuhuma hizo. Binti wa rais huyo wa zamani, Malia, alifanya kazi kama mkurufunzi katika kampuni ya Weinstein majira yaliyopita ya joto. Mwandaaji huyo wa filamu ametuhumiwa kuwabaka wanawake watatu. Baadhi ya waigizaji nyota Hollywood wamejitokeza na kudai kwamba walidhalilishwa kingono pia ni Weinstein wakiwemo Angelina Jolie, Mira Sorvino na Gwyneth Paltrow. Produsa huyo amekanusha tuhuma hizo na kusema kwamba alishiriki tendo la ngono na wanawake hao kwa hiari yao. Angelina Jolie (kushoto) na Gwyneth Paltrow ni miongoni mwa waliomtuhumu Weinstein Mke wake Georgina Chapman ametangaza kwamba atamwacha. Chapman, 41, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya mitindo ya mavazi ya Marchesa, na Weinstein, 65, wana watoto wawili. Jolie aliandika kwenye barua pepe: "Nilikuwa na kisa cha kusikitisha sana kati yangu na Harvey Weinstein wakati wa ujana wangu, na kwa sababu yake, niliamua kwamba singefanya kazi naye tena na nilikuwa nikiwatahadharisha wengine wakifanya kazi naye. "Tabia hii dhidi ya wanawake katika fani yoyote haikubaliki katika taifa lolote lile." Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, na mkewe, Michelle, wamesema wameshangazwa sana na tuhuma za udhalilishaji wa kimapenzi wa wanawake ambazo zinamkabili mwandaaji wa filamu wa Hollywood Harvey Weinstein. text: Rais Magufuli akitete na Dkt Willem Jacobs kutoka Barrick Kampuni hiyo ambayo ni mmiliki wa kampuni ya Acacia ambayo iliingia kwenye mzozo na serikali ya Tanzania juu ya usafirishwaji wa mchanga wa madini au makinikia na kukwepa kodi. Acacia imeendelea kukana tuhuma zote dhidi yake lakini mzozo huo ukiendelea kufukuta, uongozi wa Barrick chini ya mwenyekiti wake Prof John Thornton walijitosa kwenye mazungumzo na serikali ya Tanzania. Mwezi Oktoba 2017, pande hizo mbili ziliafikiana kuwa kampuni hiyo kuilipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa asilimia hamsini ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka migodi 3 inayoimiliki.. Barrick pia walikubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo. Makubaliano hayo hata hivyo hayajatekelezwa, na kulishughulikia hilo, hii leo Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Barrick anayeshughulikia Africa na Mashariki ya Kati Dkt Willem Jacobs amekutana na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Waziri wa Katiba wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi mbaye ndiye aliyeongoza mazungumzo ya suluhu amesema wanatarajia utekelezwaji wa makubaliano hayo kufikia mwishoni mwa mwezi Machi 2019. "…sasa ni kwa kila upande kwenda kwenye vyombo vyake vinavyohusika kufanya maamuzi ya mwisho ili utekelezaji ufanyike," amenukuliwa Prof Kabudi kwenye taarifa ya Ikulu. Hata hivyo kwa upande wake, kampuni ya Barrick katika taarifa yao hawajataja ni lini hasa maafikiano hayo yatafanyiwa kazi. Katika taarifa yao wamesema kuwa watawasilisha makubaliano yao kwa "wakurugenzi huru" wa Acacia hivi karibuni ili wayafanyie kazi. Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Barrick Mark Bristow amenukuliwa kwenye taarifa hiyo akisema kuwa mzozo huo umekuwa na athari kubwa kibiashara na wanaamini kuwa utekelezwaji wa makubaliano hayo utakuwa na tija kwa pande zote. Kampuni ya Barrick Gold na Serikali ya Tanzania leo Jumatano Februari 20 wamefanya mazungumzo juu ya utekelezwaji wa makubaliano ambayo pande hizo mbili waliingia mwaka 2017. text: Bw Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita, amesema katika kipindi hicho kunafaa kufanyika marekebisho ya katiba kuchunguza upya mamlaka ya rais. Kiongozi huyo ambaye ameanza ziara nchini Marekani alisema yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu marekebisho ya kikatiba ambayo anasema yanahitajika kupunguza hatari ya kuzuka kwa fujo kutoka kwa makundi ya jamii za wachache ambao wanajiona kwamba wametengwa. Bw Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba akiwa na kura 7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa. Waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo ni asilimia 39 ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo. Uchaguzi huo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga, kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambapo Bw Kenyatta alikuwa ametangazwa mshindi akiwa na asilimia 54 ya kura. Mahakama ya Juu ilisema uchaguzi huo wa mwanzo ulikumbwa na kasoro nyingi. Bw Odinga alisusia uchaguzi wa marudio akisisitiza lazima mageuzi yafanywe katika Tume ya Uchaguzi (IEBC). Alisema hakuna na imani kwamba uchaguzi huo wa marudio ungekuwa huru na wa haki. Wafuasi wa Bw Odinga wamekuwa wakiandamana mara kwa mara tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kwanza. Watu zaidi ya 50 wameuawa katika makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani. "Mfumo halisi wa utawala wa urais unaendeleza ukabila kwa sababu kila kabila linahisi kwamba haliko salama ikiwa mtu kutoka kabila hilo si kiongozi," aliambia Reuters kwenye mahojiano. Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi Katiba mpya iliyoanza kutekelezwa mwaka 2010 iligatua baadhi ya mamlaka ya serikali kuu kwa kuunda serikali za majimbo 47 zinazoongozwa na magavana. Serikali hizo huwa na uwezo wa kujiendeshea shughuli nyingi lakini bw Odinga anasema mamlaka mengi bado yamebaki kwenye serikali kuu na hilo linafaa kubadilika. "Tulipata katiba mpya mwaka 2010; Tunafikiri kwamba wakati umefika tuiangalie upya," amesema. Alieleza kuwa marekebisho ya Katiba hiyo yanafaa kuimarisha taasisi huru za serikali mfano tume ya uchaguzi na kupunguza mamlaka ya rais. "Tunafikiri kwamba pengine miezi sita itatosha kufanikisha marekebisho haya ambayo tunayahitaji katika taifa hili," alisema. Bw Kenyatta, baada ya kutangazwa mshindi, alisema hatafanya mazungumzo na upinzani hadi umalize njia zote za kisheria za kupinga matokeo ya uchaguzi. Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na IEBC Bw Odinga, siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi alitangaza kwamba atageuza muungano wake wa National Super Alliance (Nasa) kuwa vuguvugu la kupinga serikali. Majuzi, muungano wake uliwahimiza wafuasi wake kususia bidhaa na huduma za kampuni tatu kuu ambazo alisema zimekuwa zikiisaidia serikali ya Rais Kenyatta. Kesi mbili ziliwasilishwa kupinga ushindi wa Bw Kenyatta Jumatatu katika Mahakama ya Juu. Mahakama hiyo ina siku 14 kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi hizo. Upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa marudio na badala yake kusema uchaguzi mpya unafaa kufanyika katika kipindi cha siku 90. Nasa hata hivyo hawajawasilisha kesi ya kupinga matokeo hayo mahakamani. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amependekeza serikali ya muda iundwe nchi humo na kutawala kwa muda wa miezi sita kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo. text: Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema, Freeman Mbowe yupo rumande tango Novemba baada ya kufutiwa dhamana. Vyama vya ACT-Wazalendo, CUF, UMD, NLD, Chadema, TLP, NCCR-Mageuzi na Chauma vilijadili na kupitisha makubaliano yaliyobatizwa jina la Azimio la Zanzibar. Azimio hilo la mwaka 2018 limebebwa na kauli mbiu ya 'kurudisha demokrasia' ambayo inadaiwa kuminywa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa. Si lengo la makala haya kueleza makubaliano yaliyofikiwa bali kuchambua kile ninachoona namna gani vyama hivi vinatakiwa kusonga mbele baada ya makubaliano hayo. Inakubalika kuwa ushirikiano miongoni mwa vyama katika siasa za ushindani. Ni njia mojawpao ya kujenga demokrasia na mshikamano miongoni mwa viongozi,wafuasi na wanachama. Mazingira ya siasa Chama cha siasa kinatakiwa kukumbushwa na kujikumbusha kuwa haki yake kisiasa ndio matunda ya ushiriki wa wanachama wake katika sekta hiyo. Chama cha siasa kinatakiwa kukumbushwa kuwa hata siku moja bakuli la uji likiwa mezani haliendi mdomoni pasipo kutumia mkono kuinyanyua au mkono kutumia kijiko kunywa uji huo. Kwamba vyama vya siasa vifahamu kuwa katika mazingira ya utawala huu visitegemee kuletewa haki mlangoni kama mgeni mtoka mbali. Vyama vyetu vya siasa vinatakiwa kuwa na msingi wa hekaheka katika kutafuta haki zao kisiasa na wananchi kushiriki siasa kwa uhuru. Mwaka 2019 unaelekea kuwa wa hekaheka za kutafuta haki ya kidemokrasia katika kila eneo ambalo limefifishwa au haki zake kudhoofishwa. Kwa sababu haijawahi kutokea kokote duniani kuwa serikali iliyopo madarakani ikashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake kwa sababu ya kuwepo kwa mikutano ya hadhara. Maalim Seif: Yanayotokea chini ya Magufuli, hatujawahi kuyaona Tanzania Rais wa nchi yoyote hashindwi kuzindua mradi kwa sababu nchi yake inafanya mikutano ya hadhara ya kisiasa. Chama kinachotawala katika nchi Tanzania hakishindwi kutekeleza ilani yake kwa sababu vyama 15 vya Tanzania vitakuwa vinafanya mikutano ya hadhara au ndani pamoja na wanachama wake. Mikutano ya hadhara ni sehemu ya kuwakutanisha wananchi na kuwaelimisha elimu ya uraia,haki na wajibu wao kwa nchi na binafsi. Ni sehemu ya kuwapa maarifa juu ya siasa kuwa ni maisha,elimu,uchumi, utamaduni, michezo na burudani. Siasa hugusa karibu kila kitu hata kupanda kwa bei ya bidhaa sokoni. Kwahiyo siasa hii inatakiwa kuzalishwa kupitia mikutano ya hadhara. Ikumbukwe mikutano ya ni sehemu ambayo wananchi wanatumia kusikiliza na kujifunza juu ya sera na kufanya maamuzi ya kuunga mkono chama chochote, kutambua wajibu, kupata elimu ya uraia na kadhalika. Ndiyo kusema, azimio la Zanzibar kama sehemu ya ukuzaji wa demokrasia ni muhimu sana kuhakikisha mikutano ya hadhara inakuwa katika mipango yao ya kuzungumza na wananchi pamoja na kuwa sehemu ya kutafiti masuala ya haki, sheria na maendeleo. Nadharia Viongozi wa upinzani na wanaharakati baada ya kupitishwa kwa Azimio la Zanzibar 2018. Kama ni kweli wamedhamiria kutekeleza mipango yao kisiasa kwa kufanya mikutano bila woga basi wanapaswa kufahamu kuwa wanasiasa thabiti husimamia hoja zao na hawatetereki kwa sababu wameambiwa "watafanywa hivi au vile". Kwanini? Hakuna nadharia yoyote inayosema kuwa mikutano ya hadhara ni chanzo cha nchi kuwa na maendeleo duni. Hakuna nadharia yoyote inayosema kuwa mikutano ya hadhara ni chanzo cha kuchelewesha miradi ya maendeleo kwa wananchi. Hakuna nadharia inayokubali kuwa mikutano ya hadhara ni chanzo cha umasikini wa wananchi. Kwa kipindi cha miaka 24 ya uongozi wa Mwalimu Nyerere hapakuwa na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, je umasikini wetu ulipungua au kuongezeka? Pamoja na kutokuwapo kwa mikutano ya hadhara (kwa sababu hapakuwa na vyama vya upinzani baada ya kufutwa) bado hatujaondoka kwenye lindi la umasikini mbali ya hatua zetu kama taifa tulizozifikia. Umasikini sio sifa ya uzalendo. Msingi mkuu ni kwamba vyama vyote 15 vinatambua haki ya kulilinda taifa la Tanzania. Vinatambua kuwa kuharibika kwa taifa hili ni hasara kwa watanzania na watunza nia ya amani. Ili kuwe na amani ni muhimu kuwa huru kimawazo na ushirikiano. Ili mtanzania awe mzalendo ni muhimu kuhakikisha anapata mahitaji yote ikiwemo 'kupumua' (kukutanika na kuzungumza na wengine kwenye mikutano ya hadhara). Ni mwaka wa hekaheka? Tafsiri tunayopata ni kwamba vyama vya upinzani nchini vinataka kuufanya mwaka 2019 kuwa wa hekaheka za kisiasa. Mwaka huu kutafanyika chaguzi za serikali za mitaa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Vilevile vyama vya upinzani vinaweza kuufanya kuwa mwaka wa hekaheka za kisheria kutafsiri sheria mbalimbali ili wapate haki zao. Kushindwa kesi ni sehemu ya mchakato, lakini kufungua kesi ni njia mojawapo ya kushiriki siasa halali. Viongozi na wanachama wa vyama wanatakiwa kutumia fursa ya mahakama zilizopo kufafanua sheria katika maeneo mbalimbali; kuhusu dhamana, kesi za kisiasa, kuzuiwa mikutano ya hadhara kwa kisingizio cha intelijensia,udhalilishaji wa wafuasi na wanachama wao,mamlaka za wakuu wa wilaya na mikoa katika kuadhibu watumishi wa umma na raia wengine pamoja na viongozi na sheria za kuwaweka ndani kwa saa 48. Inawezekana ukawa mwaka hekaheka za kisiasa. Ni mwaka ambao utakuwa unawaweka kwenye mizani ya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020. Hekaheka za madai mbalimbali ya kisiasa, sheria na haki vinaweza kuwa vitu vitakavyotengeneza taswira ya upinzani. Intelijensia: tafakuri ya pamoja Lowassa: Kuna dalili za ‘udikteta’ serikali ya Magufuli Tanzania Mikutano mingi ya vyama vya siasa nchini iwe ndani au hadhara imekuwa ikizuiwa. Kuna mikutano ya ndani ya vyama vya siasa ambayo ni kama vile vikao vya taasisi zozote zile za kitaaluma, siasa na kadhalika. Chama cha siasa ni taasisi, na kinatakiwa kuheshimiwa kwa uTaasisi wake. Mara kadhaa vyama vinazuiwa kufanya mikutano kwa sababu zinazoitwa za Kiintelijensia; je kama wenye mamlaka wamebaini hilo, wanatumia mbinu gani kuzuia? Intelijensia ni pamoja na kuhakikisha inaondoa matishio yote na kuwapa nafasi za kufanya mikutano ya kuzungumza na wafuasi na wanachama wao. Ni muhimu kwa vyama kutorudi nyuma au kukaa chini na kulalamika, badala yake vinatakiwa kuchukua hatua juu ya hiki kitu 'Intelijensia', na kukifikisha kwenye vyombo vya sheria. Ni muhimu Mahakama ikatakiwa kufafanua 'Intelijensia ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa' inavyochukuliwa na wajibu wa wanaohofia 'taarifa za kiintelijensia' katika kuzuia madhara. La pili, ni vile vyama vya siasa vinavyokubaliana na 'intelijensia' hii kama sehemu ya kufifisha aria yao. Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania walikutana mwishoni mwa mwaka 2018 visiwani Zanzibar kwa mwaliko wa mwanasiasa mkongwe Maalim Seif Sharrif Hamad. text: Baadhi ya wadadisi wa bidhaa walikuwa awali wamesema Note 7 ilikuwa simu bora zaidi ya Android kuwahi kuundwa Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya kampuni hiyo ya Korea Kusini kutangaza kwamba ingesitisha uundaji na uuzaji wa simu hizo kutokana na kuongezeka kwa visa vya simu hizo kushika moto au kulipuka. Mamlaka inayosimamia bidhaa na matumizi nchini Rwanda imesema hatua ya kupiga marufuku simu hizo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama. "Kwa sababu za kiusalama, wateja ambao huenda walinunua simu hizi binafsi nje ya nchi wanatakiwa kuzizima na kuzirejesha eneo walizozinunua," imesema taarifa ya kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Meja Jenerali Patrick Nyirishema. Baadhi ya simu za Note 7 zimekuwa zikishika moto Samsung pia imewashauri walio na simu hizo kuzizima na kutozitumia tena. Serikali ya Rwanda imepiga marufuku uagizaji na usambazaji wa simu za kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7. text: Mamba wakubwa na wadogo wote waliuawa Mauaji hayo yalikuwa ni ya kulipiza kisasi kifo cha mwanamume mmoja ambaye aliuawa na mamba mmoja eneo hilo. Maafisa na polisi wanasema kuwa hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka dhidi ya waliohusika. Kuuawa kwa wanyama wanaolindwa ni hatia na adhabu yake inaweza kuwa kifungo jela nchini Indonesia. Mwanakijiji huyo aliuawa siku ya Ijumaa asubuhi wakati akitafuta mboga eneo la kuzalia mamba. Mfanyakazi mmoja alisikia mtu akiitisha msaada na alipofika huko aliona mamba akimshambulia mtu. Baada ya mazishi siku ya Jumapili, wanakijii mamia kadha wenye hasira walielekea eneo la makao ya wanyama wakiwa wamejihami kwa visu, chuma, nyundo na sururu. Vyombo vya habari vinasema kuwa wanakijiji waliishambulia ofisi kwenye makao ya wanyama na kisha kuwachinja mamba wote 292. Kundi la wanakijiji limewaua karibu mamba 300 kwenye makao ya wamyama katika mkoa wa West Papua nchini Indonesia. text: Polisi wa Ujerumani wametoa picha za Anis Amri Amri alipigwa risasi na kuuawa hiyo jana na polisi nchini Italia. Bethany Bell ametutumia taarifa ifuatayo kutoka Berlin. Kuna hali ya utulivu nchini Ujerumani ambapo watu wametambua kuwa Anis Amri si hatari tena nchini humo. Lakini kama anavyosema Angela Merkel, kesi hii inazusha maswali mengi sana. Maafisa wa Ujerumani wanasema kuwa wapelelezi wa tukio hilo wanataka kujua iwapo Amri alikuwa na mtandao wa wafuasi. Watataka pia kujua kwa nini ilikuwa vigumu yeye kuondolewa nchini licha ya amri nyingi kutolewa na kwa nini maafisa wa usalama walikoma kumfuatilia licha ya kufahamu kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na wanachama kadhaa wa Waislamu wenye itikadi kali. Licha kutangazwa kuwa yeye alikuwa mshukiwa mkuu katika shambulio la Berlin, aliweza kusafiri kusafiri katika mataifa kadhaa ya Ulaya. Bi Merkel alisema kuwa taifa lake litachukua hatua kambambe kuimarisha usalama. Yeye na Serikali yake wametiliwa shinikizo kutekeleza ahadi hiyo. Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, ameitisha taarifa kamili juu ya kesi inayomhusu Anis Amri, raia wa Tunisia aliyekuwa akitakikana nchini Ujerumani kwa kushambulia soko la Krismasi jijini Berlin. text: Ahmad Bahaa alionekana katika kipindi cha Runinga ya Misri Mhandishi Bahaa amesema katika kipindi cha runinga ya Al-Nahar TV kuwa ameshafanya matangazo ya simu na vinywaji laini akiwa ni mhusika kama Mo Salah pamoja na kampeni za kuacha madawa ya kulevya. ''Nimefanya matangazo mengi na Salah", alisema Ahmed Bahaa. katika matangazo aliyofanya Bahaa anaonekana akiwa katika picha za mbali na sio za ukaribu sana na kuonesha sura. Je unaona mapacha? hapo ni Mo Salah na Ahmad Bahaa ''Salah kwa kweli hawezi kukaa na kufanya tangazo moja kwa muda mrefu,'' Bahaa alielezea. ''Ninachukua muda mwingi kurekodi matangazo hapa na nitaenda pia Uingereza kumalizia kurekodi naye Salah, hii ni kuharakisha mambo kwa sababu yeye hana muda mwingi wa kufanya matangazo'' Taarifa hii iliwashtua sana watu katika mitandao ya kijamii, baadhi walitumiana video inayomuonesha Bahaa katika mtandao wa Twitter. Shabiki mmoja alishangazwa na kudhani kuwa huenda Bahaa hucheza katika michuano ya Misri akishiriki kama Mo Salah. ''Yeye ni mtu mwenye mambo mengi na Misri kila siku inafungwa huenda huyu ndo anacheza na sio Mo Salah'' Misri alikua mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Afrika lakini ilishindwa kufika Robo fainali. Ahmad Bahaa anafanana sana na mshambualiaji wa Liverpool na Misri Mohamed salah, na ameigiza katika matangazo mbalimbali ya televisheni. text: Baadhi ya waliojeruhiwa walipelekwa katika kliniki iliyokuwa karibu kupokea matibabu Hofu ilitanda katika eneo la Bamburi Jumatatu usiku baada ya kundi la vijana wapatao 30 waliojihami kwa mapanga, visu na silaha nyingine butu kulivamia eneo hilo na kuanza kuwashambulia wakaazi waliopita njia. Polisi iliarifiwa na wakafika katika eneo hilo - lililogeuka kuwa enoe la makabiliano baina ya maafisa wa usalama na wahaifu hao na palishuhudiwa ufyetulianaji risasi. Washukiwa watatu wamekamatwa na maafisa wa usalama wanasema uchunguzi umeidhinishwa. Picha za kuogofya zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii baada ya mkasa huo, zilizoonyesha baadhi ya manusura wakiwa na majeraha mabaya katika sehemu tofuati za mwili baada ya baadhi kupigwa kwa mapanga au kuchomwa visu. Baadhi walifikishwa katika kliniki iliyokuwa karibu na eneo hilo, kabla ya kuhamishwa na kupelekwa katika hospitali kuu ya mkoa, Coast General kupokea matibabu zaidi. Wakali Kwanza ni nani? Kwa mujibu wa Johnston Kipara, kamanda wa polisi mjini Mombasa aliyezungumza na BBC, anasema ni kundi la vijana wahalifu. 'Lengo lao ni kuweka uoga na kutekeleza uporaji katika jamii' amefafanua. Kwa baadhi ya wakaazi, Wakali Kwanza ni moja ya makundi mawili ya uhalifu yanayohudumu katika eneo hilo la pwani na yanafahmika kwa kujihusisha katika biashara haramu na matumizi ya madawa ya kulevya, uporaji na wizi wa mabavu. 'Jukumu letu ni kuhakikisha mji wa Mombasa unabaki salama na wanaohusika hatua zinachukuliwa wanapopatikana' amesema kamanda wa polisi Kipara. 'Inatusaidia kupanga mipango yetu kwa haraka na kuhakikisha kwamba tunakuwa macho kila wakati' ameongeza. Mchambuzi wa masuala ya usalama Isaac Mwendwa, anayehusika na kampeni dhidi ya itikadi kali na ugaidi nchini Kenya anasema shambulio la Jumatatu usiku ni ushindani baina ya makundi hasimu ya uhalifu kila moja likitaka kujionyesha nguvu. Amefafanua kuwa ni kuonyesha ushindani baina ya makundi hasimu yanayotaka kuonekana kuwa na ushawishi katika uhalifu kama biashara ya madawa ya kulevya, wizi na kadhalika. Tathmini yake ni kwamba serikali haijaonesha kutilia uzito wa kutosha hatari ya inayotokana na magengi hayo japo ni madogo. Amekosoa mbinu inayotumika na maafisa wa utawala anayosema hairidhishi. Amefafanuwa kwamba kuna haja ya kuwepo jitihada endelevu na za ushirkiano mkubwa wa pamoja na jamii katika Pwani ya Kenya ili kutatua kikamilifu changamoto hiyo na sio tu kwa kuwakamata wahalifu. Wasiwasi wa jamii Taarifa zilisambaa kwa kasi na baadhi ya raia waliingia katika mitandao ya kijamii kuelezea wasiwasi na hofu walionayo kutokana na uhalifu wa magengi hayo ya vijana. Kuna na baadhi waliojipata katikati ya shambulio hilo wakati lililpotokea jana usiku na kutumia mitandao ya kijamiikuelezea kilichowakuta. Serikali ilitoa makataa kwa wafuasi wa magengi hayo ya uhalifu kujisalimisha. Aliyekuwa mkuu wa polisi katika kaunti hiyo Nelson Marwa, amesema makundi hayo ya vijana hufadhiliwa na baadhi ya matajiri wenye ushawishi katika eneo hilo la pwani. Uchunguzi sasa unaangazia kwanini yamefanyika, na uhalifu ulitekelezwa kwa ushirikiano wa nani. Maswali ambayo pia yameulizwa na baadhi katika mitandao ya kijamii, kwamba dhamira ya mashambulio hayo dhidi ya Wakenya wasiokuwa na hatia ni ipi? na ni nani mfadhili wa makundi hayo? Takriban watu wanane wamejeruhiwa baada ya vijana waliojihami kwa mapanga kuushambulia mtaa moja katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya katika kinachojitokeza kuwa ni uhasama baina ya makundi mawili hasimu ya magengi ya uhalifu. text: Kulingana na taarifa tahadhari hiyo ya Uingereza mtu mmoja alifariki dunia nchini Tanzania mwezi wa Septemba 2019. Imeongeza kuwa inaonekana kuwa huenda kifo chake kilikuwa huenda kina uhusiano na Ebola. Serikali ya Uingereza kupitia wavuti wake pia imewaarifu raia wake kuwa shirika la afya duniani WHO clinaendelea kuchunguza na limetoa taarifa. ''Ubalozi wa Uingereza jijini Dar es Salaam inawasiliana na maafisa wa Tanzania na mashirika ya afya ya kimataifa, tahadhari hii itafanyiwa marekebisho pale taarifa mpya zitakapopatikana. ''Mnapaswa kufuatilia taarifa mpya kuhusu mabadiliko yoyote kwenye Mtandao wa Afya kuhusu safari na kituo na mitandao ya WHO'', imeongeza taarifa hiyo. Tahadha hii ya Uingereza imekuja baada ya taifa la Marekani pia mwishoni mwa juma kuwaonya raia wake kuchukua tahadhari ya kiwango cha juu wakati wanapozuru nchini Tanzania kufuatia wasiwasi wa ugonjwa wa ebola, ikiitaka nchi hiyo ya Afrika mashariki kutoa habari kuhusu visa vya ebola nchini humo kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. ''Wanaozuru Tanzania wanapaswa kuwa waangalifu sana'' , idara ya maswala ya kigeni ilisema siku ya Ijumaa katika tahadhari yao ya usafiri kufuatia kifo kinachohusishwa na ugonjwa huo mjini Dar es salaam. Tanzania ilikana ripoti hiyo ikisema kuwa hakuna visa vya ebola vilivyoripotiwa, lakini kwa sasa serikali hiyo ipo katika shinikizo kali kutoa ufafanuzi kulingana na chombo cha habari cha Reuters. Chini ya kanuni za Afya za Kimataifa, makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama, nchi zinalazimika kuiarifu WHO mara tu zitakapokuwa na milipuko ya magonjwa makubwa ya kuambukiza ambayo yanaweza kuwa hatari kwa majirani zao na ulimwengu mpana. Serikali za Afrika mashariki pamoja na zile za Afrika ya kati zimekuwa katika tahadhari ya kiwango cha juu kutokana na uwezekano wa maambukikizi ya ugonjwa huo kutoka DR Congo ambapo takriban watu 2,100 wamefariki kufuatia mlipuko wa ebola. Mataifa ya Tanzania na DR Congo yanapakana na mto ulioyatenga. Katika hatua isio ya kawaida, Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki iliyopita lilisema kwamba, kinyume na kanuni za afya za kimataifa, Tanzania ilikuwa ikikataa kutoa maelezo ya watuhumiwa. Siku chache mapema, mkuu wa Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa alisafiri kwenda Tanzania kwa agizo la waziri wa Afya wa Marekani Alex Azar, ambaye pia alikuwa amekosoa nchi hiyo kwa kutotoa habari. WHO ilisema kwamba, licha ya kwamba ina wasiwasi kuhusu ukosefu wa uwazi, haina ushahidi wa kuwepo kwa Ebola nchini Tanzania, lakini ilikatiza hatua za adhabu na kusisitiza kwamba ilitoa ushauri wa kutosafiri nchini humo mbali na vikwazo vya kibiashara. Siku ya Jumanne Tanzania ilifanya mazungumzo na mwakilishi wa ndani wa shirika la afya duniani WHO kuhusu madai yake. Katikati ya mwezi Septemba, waziri wa afya alisema serikali ilichunguza kesi mbili za ugonjwa usiojulikana , lakini hawakupata ugonjwa huo. WHO ilisema nini? Shirika la afya duniani lililalamikia ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa serikali ya Tanzania katika utoaji taarifa kuhusu visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola nchini. Katika taarifa yake ya malalamiko, shiriki hilo limeeleza kwamba uwazi na kasi katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo hatari ni muhimu katika kudhibiti mlipuko ambao tayari umetajwa kuwa janga la afya duniani. Katika taarifa hiyo iliyotolewa WHO limeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa. WHO lilituma kundi la wataalamu kuchunguza kisa cha ugonjwa usiojulikana na ubalozi wa Marekani ulifuatilia hatua hiyo kwa kutoa tahadhari. Hatua hiyo ilisababisha uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba ugonjwa huo hatari umeingia nchini Tanzania. Waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita amesena hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo. Serikali ya Tanzania imesema ilisema nini? Serikali ya Tanzania ilifutilia mbali uvumi kwamba kuna visa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo. Waziri wa afya nchini humo bi Ummy Mwalimu aliambia mkutano na wanahabari kwamba hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo. Alisema kwamba taifa hilo limejiandaa kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa na tayari limefanya majarabio ili kujua jinsi ilivyojiandaa huku ikiweka tayari vituo vya kuwatenga waathiriwa. Shirika hilo la Umoja wa mataifa limeendelea kueleza katika taarifa yake kwamba lilifahamishwa mnamo Septemba 10 kuhusu kifo cha mgonjwa kilichotokea mjinia dar es salaam, na kuarifiwa kwa njia isiyo rasmi siku ya pili kwamba mgonjwa huyo alipatikana kuwa na Ebola baada ya kufanyiwa vipimo. Kadhalika WHO linaeleza kwamba liliarifiwa kuhusu visa vingine viwili vinavyoshukiwa kuwa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo. Mmoja kati yao, alikutikana kutokuwa na Ebola baada ya vipimo na hapakuwa na taarifa zozote kuhusu mgonjwa wa pili, imeeleza taarifa hiyo. 'Nataka kuwahakikishia kwamba idara ya afya ilichukua sampuli na matokeo yake ni kwamba wawili hao hawakuwa na ugonjwa wa Ebola. Hakuna Ebola Tanzania na watu hawafai kuwa na wasiwasi'', alisema waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu wiki iliyopita kuhusu uvumi wa visa hivyo. Kufanya vipimo tena vya homa ya Ebola katika maabara inashauriwa sana ili kuthibitisha matokeo ya vipimo na hivyo kubaini aina ya virusi Ebola . WHO linasema kuwa limewapatia maafisa wa Tanzania ushauri huu. Mgonjwa huyo ambaye inaarifiwa ni mwanamke alifariki tarehe 8 Septemba kwa mujibu wa WHO. Msururu wa matukio ya mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na Ebola Tarehe 10 Septemba 2019, Shrika la Afya duniani WHO lilipokea ripoti ya taarifa ya kisa cha mambukizi ya Ebola mjini Dar es Salaam, Tanzania. Kisa hicho kinachoshukiwa kilimhusu mwanamke mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa akisomea nchini Uganda. Aliwasili nchini Uganda akitokea nchini Tanzania tarehe 08 Agosti 2019. Taarifa hiyo inasema kwa kuanzia tarehe 08 hadi 22 Agosti, alikuwa katika eneo la kati la Uganda, akiishi katika hosteli ya kibinafsi karibu na mji mkuu Kampala. Ebola ni nini? Ebola ni kirusi ambacho mwanzo husababisha joto la mwili na kudhoofisha misuli na uvimbe kooni. Kisha mgojwa huanza kutapika, kuharisha na kuvuja damu ndani na hata nje ya mwili. Watu huambukizwa wanapogusana moja kwa moja kupitia michubuko ya mwili, au mdomo na pua, huku damu, matapishi, kinyesi au kugusa majimaji ya mwili ya mgonjwawa Ebola Wagonjwa huwa wanakufa kutokana na ukosefu wa maji mwilini na kuharibika kwa viungo vya ndani vya mwili. Tazama pia: Je inawezekana kuangamiza virusi vya Ebola? Serikali ya Uingereza imetoa tahadhari kwa raia wa nchi hiyo wanaosafiri kuelekea nchini Tanzania juu ya ''uwezekano'' wa kuwepo Ebola katika taifa hilo la mashariki mwa Afrika text: Serikali inasema imekuwa ikipoteza shilingi bilioni 400 kwa mwaka kutokana na mkataba wa TTMS Taarifa kutoka Ikulu imesema Bw Simba amesimamishwa kazi kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS). Bodi ya TCRA imekuwa ikiongozwa na Prof Haji Semboja. Taarifa hiyo inasema hatua hiyo ilisababisha Tanzania kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka. Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu tarehe 22 Machi, 2013. Kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), kwa mujibu wa serikali. Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja. Aidha, amewataka Waziri Prof Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa. “Nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili,” amesema Rais Magufuli. Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt Ally Yahaya Simba. text: Neymar alishinda vikombe tisa misimu minne aliyokaa Barcelona Ununuzi huo wa mchezaji huyo wa miaka 25 umevunja rekodi ya awali iliyowekwa Paul Pogba aliporejea Manchester United kutoka Juventus kwa £89m Agosti 2016. Atakuwa analipwa euro 45m (£40.7m) kwa mwaka - euro 865,000 (£782,000) kila wiki - kabla ya kutozwa ushuru katika mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano. Hiyo ni jumla ya £400m. Neymar amesema amejiunga na "mojawapo ya klabu zenye ndoto kuu zaidi Ulaya". "Ndoto kuu ya Paris St-Germain ilinivutia kujiunga na klabu hiyo, pamoja na kujitoleza kwao na nguvu zinazotokana na hili," amesema. "Najihisi niko tayari kuanza kazi. Kuanzia leo, nitafanya kila niwezalo kuwasaidia wachezaji wenzangu wapya." Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa imepanga kuwa na kikao na wanahabari mwendo wa saa 12:30 BST Ijumaa (saa nane unusu Afrika Mashariki). Neymar baadaye atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa PSG Jumamosi wakati wa mechi yao ya kwanza kabisa ya msimu mpya, ambayo itakuwa nyumbani uwanja wa Parc des Princes dhidi ya Amiens. Neymar akiwa na Lionel Messi na Luis Suarez na watoto wao baada ya kushinda Copa del Rey Neymar alikuwa amefika kituo cha mazooezi cha Barcelona Jumatano akiandamana na babake na mwakilishi wake na kufahamisha klabu hiyo ya Uhispania kwamba angetaka kuondoka. Alipewa ruhusa na meneja wa Barca Ernesto Valverde kwenda "kupanga mustakabali wake". Nchini Uhispania, kifungu cha kumwachilia mchezaji kutoka kwa mkataba wake kinaweza tu kufunguliwa kwa mchezaji kulipa pesa yeye binafsi. Neymar alipofika na pesa Alhamisi kulipa hata hivyo, maafisa wa La Liga walikataa malipo hayo. Kulitokea majibizano kati ya maafisa wa La Liga na wasimamizi wa Ligue 1. La Liga wanaamini PSG huenda wanakiuka sheria za uchezaji haki kifedha (FFP) kwa kumnunua mchezaji huyo wa Brazil. Baada ya kushindwa kulipa pesa hizo kwa La Liga, wawakilishi wa Neymar walilipa euro 222m (£200m) katika afisi za Barca badala yake. Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 na akashinda mataji mawili ya La Liga na moja la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. PSG wameorodheshwa wa 11 kwa thamani duniani na Forbes lakini ni mara yao ya kwanza kwao kuvunja rekodi ya dunia katika kumnunua mchezaji. Neymar ni nani? Neymaralifunga bao la kasi zaidi historia ya Olimpiki sekunde 14 pekee baada yamechi ya nusufainali dhidi ya Honduras kuanza Olimpiki Rio 2016 The top 10 most expensive deals (fees as reported in sterling at the time) before Neymar Paris St-Germain wamekamilisha kumnunua mshambuliaji wa Brazil, Neymar, kwa ada iliyoweka rekodi mpya ya ununuzi wa mchezaji ya euro 222m (£200m) kutoka Barcelona. text: Polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji Mkusanyiko mkubwa upo katika mji wa Moscow ambapo shinikizo ni kumtaka waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev kujiuzulu. Wanaharakati wanasema kuwa hadi sasa watu 800 wanashikiliwa na Polisi. Maandamano haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi ya yale yaliyowahi kutokea nchini Urusi kwa miaka mingi, ambapo wanadai kuwa waziri mkuu wao Dmitry Medvedev amekuwa akutumia fedha za umma katika mambo yake binafsi kwa kujenga majumba kifahari, kununua boti za kifahari, mashamba ya mvinyo na jumba la kufugia bata. Maandamano makubwa yalikuwa katika mji wa Moscow Katika viunga vya Pushkin mjini Moscow, kuna kundi kubwa la waandamanaji waliokusanyika, mmoja wao amesema kuwa fedha za serikali zinaibiwa. Marekani imeilaumu Urusi kwa hatua yake ya kuwashikilia mamia ya waandamaji kwa madai kuwa wanavuja haki dhidi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa haki za binadamu. Maelfu ya raia wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini Urusi wakiandamana kupinga kile wanachodai matumizi mabaya ya fedha za umma. text: Dkt Stella Nyanzi amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa mtandaoni Nyanzi alipatikana na hatia ya unyanyasaji wa kimtandao pamoja na mawasiliano ya udhalilishaji dhidi ya rais Yoweri Museveni na familia yake. Dr. Nyanzi alikataa kumsikiliza hakimu akisoma hukumu dhidi yake na badala yake kufanya vurugu kwa kuvua nguo na kuonesha sehemu ya mwili wake. Mwanaharakati huyo hakuwa mahakamani lakini hukumu dhidi yake ilitolewa kupitia video link kutoka jela. Wakati kesi ikiendelea Bi. Stela alikataa kuomba dhamana na amekuwa katika gereza kuu la Uganda la Luzira kwa miezi minane. Sasa atazuiliwa gerezani kwa miezi tisa zaidi. Bi Nyanzi alishtakiwa kwa kumtusi rais Yoweri Museveni, na mkewe Janet Museveni pamoja na marehemu mama yake Museveni, Bi Esteri Kokundeka kupitia Facebook Nchini Uganda Uganda, Bi Nyanzi amekua sura na sauti ya matumizi ya lugha chafu katika upinzani dhidi ya kile anachokiita serekali mbaya. Haoni haya ya kuandika maneno ambayo wengi wanayaona kama ni ya aibu. Nyanzi ni mtafiti wa masuala ya jamiina msomi na kabla ya kuanza kampeni yake ya matusi kupitia kwenye mitandao ya kijamii aliwa ni mwalimu katika chuo kikuu cha umma nchini Uganda cha Makerere. Mashtaka hayo chini ya ya sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta ni jaribio la utekelezwaji wa sheria ya uhalifu wa mtandaoni inayokosolewa. Wengi miongoni mwa washukiwa wa unyanyasaji wa mtandaoni, wamekuwa hata hivyo wakishutumiwa kwa kumshambulia rais Museveni. Kufikia sasa karibu watu 15 wamekamatwa kwa madai ya kumkasirisha rais Museveni tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2016. Dr Stella Nyanzi, Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda Wengine waliokamatwa Watu wengine waliokamatwa ni pamoja na Raymond Soufa, maarufu Peng Peng, Nasser Mugerwa pamoja na Jane Kuli, ambao walizuiliwa na polisi kwa kukiuka sheria hiyo. Andrew Mwenda, Mmiliki wa jarida la kibinafsi, aliyepata umaarufu miaka ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa kukosoa utawala wa Rais Museveni kwa kukandamiza vyombo ya habari anasema Waganda wana haki ya kumkosoa rais. Bw aliandika katika mtandao wake wa Twitter: "Kukamatwa kwa Joseph Kabuleta kwa "kumkasirisha Rais" ni ushamba na hatua iyo haina nafasi katika ulimwengu wa sasa! Waganda wana kila sababu ya kumkosoa Rais. Wamemchagua awahudumie. Wanatakiwa wawe huru kumwelezea kero lao ikiwa hawajaridhishwa na jinsi anavyoongoza nchi!" Mwaka jana, Mbunge wa Manispaa ya Mukono MP Betty Nambooze alikamatwa na kuzuiliwa kwa kukiuka sheria ya kutumia vibaya mitando ya kijamii. Inadaiwa ujumbe aliyochapisha katika mitandao ya kijamii kabla na baada ya kupigwa risasi na kuuawa kwa mbunge wa Arua Ibrahim Abiriga na ndugu yake Saidi Butele Kongo ulikua wa kichocheza. Januari 2019: Polisi katia wilaya ya Gomba walimkamata mtu wa miaka 19 kwa kumtusi Rais Museveni. Mamlaka zilisema,Joseph Kasumba, mkaazi wa Kanoni, alimtukana rais Museveni, majina ya kumdhalilisha. Juni 18, 2019: Andrew Mukasa, ambaye pia anafahamika kama Bajjo, alishitakiwa kwa kuchochea ghasia thidi ya utawala wa rais Museveni na kuvunja sheria ya mawasiliano. Novemba 2017: Wakurugezi watano wa na wahariri watatu wa gazeti la Red Pepper washitakiwa kwa makosa saba ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa sheria ya utumizi wa kompyuta, kutia dosari sifa ya rais Museveni na kumsumua kiakili ndugu yake mdogo Jenerali Henry Tumukunde. Mwanaharakati msomi wa Uganda Dkt. Stella Nyanzi amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela. text: Libya imekumbwa na mapigano tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi Kuna wapinzani wawili nchini Libya kwa sasa: Umoja wa Mataifa ilitambua serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Serraj, na kuna utawala uliongozwa na vikosi vya waasi chini ya Jenerali Khalifa Haftar. Wiki hili pekee, pande mbili zilikuwa zimekubaliana kusitisha mapigano baada ya shinikizo kutoka kwa Urusi na Uturuki. Lakini wengi walitarajia kwamba, hilo lingemalizika baada ya siku chache tu, hasa baada ya Jenerali Haftar alipokataa kuweka rasmi makubaliano ya kusitisha vita, na kurejesha nchi hiyo katika enzi za wasiwasi wa kutokea kwa machafuko. Lakini ilikuwaje hadi Libya ikafikia hapo ? Ahadi za haraka Urusi na Uturuki zinatakuwa kuwa na ushawishi nchini Libya katika siku za baadaye Makubaliano hayo yanalenga kusitisha vita vilivyodumu kwa miezi tisa ambavyo vilianza wakati vikosi vya Jenerali Haftar vilipoanza kufanya mashambuli mapya. Zaidi ya mizi 6 iliyopita peke yake, karibia watu 2,000 wameuawa huku 146,000 wakitoroka makazi yao. Berlin ndiyo mwenyeji wa mkutano wa Amani utakaofanyika Januari 19, japo haijafahamika iwapo matokeo ya hivi karibuni huko Libya yataathiri mkutano huo. Lakini kupata uhalisia wa kwa nini ni vigumu kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita, kinachohitajika kufanywa ni kurejelelea chimbuko la mapigano. Tulifikaje hapo? Kama ilivyotokea kwa Syria, ilianza tu kwa maandamano ya wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya Arabuni 2011. Vikosi vinavyoungwa mkono na Nato vilipindua utawala wa muda mrefu wa Muammar Gaddafimwaka huo, huku raia wakiwa na matumaini mengi tu si raia wa Libya pekee badi hata jamii ya kimataifa. Libya imekuwa katika vita tangu kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi, 2011 Tangu wakati huo, nchi hiyo imekuwa katika vita vya wenywe kwa wenyewe. Baada ya miaka kadhaa ya mapigano, Umoja wa Mataifa ilisaidia kuanzishwa kwa utawala ulioongozwa na waziri mkuu Serraj. Serikali yake ya Muungano wa Kitaifa ilikuwa mjini Tripoli na ilitarajiwa kuunganisha nchi hiyo. Japo siyo kila mmoja aliyeunga mkono makubaliano hayo na Jenerali Haftar alitaka kuwa nguvu zaidi ya madaraka. Aliunda jeshi lake la taifa mashariki mwa nchi hiyo kwa kuzingatia miji ya Tobruk na Benghazi. Pia alidai kwamba anaweza kurejesha usalama na kupiga vita kile alichokiita ugaidi wa makundi ya kiislamu. Vikosi vya Jenerali Haftar vimekuwa vikiingia kuelekea mji mkuu wa Tripoli tangu April 2019. Mwezi huu, vilifanikiwa kuteka mji wa kimkakati wa pwani wa Sirte. Lakini ili kuchanganya mambo zaidi, wanamgambo wapo katika miji mbalimbali, wakipigana vita vyao na wakati hayo yakiendelea, kundi linalojiita Islamic State limejitokeza na kuendeleza shughuli zake katika maeneo mbalimbali ya jagwani. Kina nani wanaochochea vita Vita vya Libya kwa kiasi kikubwa vinafanan na vya Syria: makundi hasimu hayatokei tu nchiniLibya. Pande zote za mgogoro wa Libya umevutia washirika wenye nguvu wa eneo na kimataifa. Gen Haftar has recruited powerful regional allies to his side UAE na Saudi Arabia wanasema kwamba wanataka kumaliza makundi ya Kiislam katika eneo hilo. Kwa kujitokeza kama adui wa makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali, Jenerali Haftar alifanikiwa kuvutia nchi hizi upande wake. Pamoja na Jordan, UAE imekuwa ikitoa silaha na usaidizi wa anga kwa Jeshi la taifa la Libya, na Umoja wa Mataifa imelaumu UAE kwa kusambaza silaha za kijeshi ambako kulisababisha mauaji ya raia wengi wakati Jenerali Haftar alifanya mashambulizi. Misri, majirani wa Libya upande wa mashariki, wanamuunga mkono Jenerali Haftar na pia imekuwa ikiisaidia kwa masuala ya usafiri. Na kwa wakati huu Urusi ambayo pia inatafuta kuwa na ushawishi pia imeingia kwenye vita hivyo. Inasemekana kwamba mamluki wa Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya Jenerali Haftar ingawa Urusi imekanusha madai hayo. Wabunge wa Uturuki walipiga kura ya upande mmoja kutuma vikosi vya Uturuki Libya Upande mwengine Uturuki, imetuma vikosi vyake kumuunga mkono waziri mkuu Serraj. Kama ilivyo kwa Urusi, Uturuki pia inataka kuwa na ushawishi sku zijazo na kuonekana kama wenye nguvu katika eneo hilo. Serikali ya Uturuki imesema kwamba vikosi vyake vimepelekwa Tripoli kutoa mafunzo na ushauri. Lakini chanzo katika serikali ya Haftar kimeithibitishia BBC kwamba vikosi vya Uturuki ni pamoja na wapiganaji wa waasi wa Syria wanaungwa mkono na Uturuki. Kulingana na mwanahabari wa BBC Jonathan Marcus, nia ya Uturuki huenda ikawa inataka raslimali za baharini. Kwa mara nyengine tena, Libya imetumbukia kwenye mapigano huku juhudi za kimataifa za kupatikana kwa amani zikiendelea kati ya makundi hasimu. text: Japo matamasha kadhaa ya muziki huo yamezuiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, jitihada za serikali kuupiga marufuku kabisa zimegonga mwamba. Sababu marufuku ya serikali imeshindikana, Putin anataka mamlaka zifanye kazi ya ziada kuudhibiti. "Wizara ya Utamaduni itatafuta namna bora ya kusimamia matamasha ya vijana," amesema Putin. Kauli ya Putin inakuja siku chache baada mwanamuziki wa maarufu wa rap nchini humo anayefahamika kama Husky kukamatwa baada ya matamasha yake kufutwa. Awali mwezi huu wa Disemba mamlaka katika jiji la kusini la Krasnodar zilizuia tamasha la Husky kwa kile walichokiita "msimamo mkali". Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Dmitry Kuznetsov - alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kutumbuiza kutoka juu ya gari. Hata hivyo alikamatwa na kufungwa jela kwa siku 12 kwa kitendo hicho. Mwanamuziki wa Rap nchini Urusi Dmitry Kuznetsov maarufu kama Husky amekuwa akikabiliana na mamlaka kila uchao Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Utamaduni na Sanaa katika jiji la St Petersburg, rais Putin amesema "tatizo hili linapaswa kutatuliwa kwa umakini mkubwa". "Kile ambacho ninakubaliana nacho ni kuwa, kama ni ngumu kuuzuia (muziki wa rap), basi inabidi uongozwe kwa namna yake," amesema. Putin ameelezea khofu yake juu ya matumizi ya mihadarati kwa vijana. "Rap na aina nyengine za kisasa za sanaa zimejikita katika nguzo tatu- ngono, mihadarati na maandamano," amesema Putin na kuongeza:"Ninaogopa zaidi mihadarati, maana hiyo ndio njia ya kuangamiza taifa." Putin amelalamikia lugha chafu inayotumika kwenye rap, na kusema amezungumza suala hilo na mtaalamu wa lugha. Japo mtaalamu huyo alimwambia kuwa matusi ni "sehemu ya lugha yetu", Putin alifananisha suala hilo na mwili wa binadamu, huku akitania kuwa "tuna viungo vya kila aina, lakini hatuvuachi wazi kila wakati". Serikali ya Urusi imekuwa na mahusiano ya kutatanisha na muziki kwa muda mrefu. Bendi ya muziki ya Pussy Riot ambayo ni maarufu kwa kuukosoa utawala wa Putin imedai kuwa shirika la ujasusi la nchi hiyo lilimdunga sumu mwana bendi hiyo Pyotr Verzilov mwezi Septemba mwaka huu. Pyotr Verzilov akipelekwa mahakamani baada ya yeye na wanabendi wenzie wa Pussy Riot kuvamia uwanja kwenye fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwezi Julai 2018. Chini ya Usovieti, aina za muziki za Magharibi kama pop na rock zilikuwa ni marufuku na baadhi ya wanamuziki wa Kirusi waliofanya aina hizo za muziki walikabiliana na mkono wa sheria. Hata wale waliofanya muziki wa asili pia waliingia kwenye migogoro na serki. Mwanamuziki Dmitri Shostakovich alipigwa marufuku mara mbili chini ya utawala wa Joseph Stalin. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameitaka serikali yake "kuchukua uongozi" wa muziki wa kufoka foka ama rap. text: Kimbunga hicho kimepungua katika saa chache zilizopita lakini utabibiri wa hali ya hewa unategemea kuwa kutakuwa na mvua kubwa ambayo itasababisha mafuriko. Idara ya kuthibiti majanga nchini Msumbiji imesema watu elfu thelathini wamehamishwa katika makazi yao ambapo dhoruba la kimbunga linaweza kupiga tena. Mwezi uliopita Kimbunga Idai kilisababisha vifo vya mamia ya watu nchini humo. Watu zaidi ya 900 walikufa wakati ambapo mvua kubwa ilipopiga maeneo ya Mozambique, Malawi na Zimbabwe. Watu wapatao milioni tatu walikuwa wanapata msaada wa kibinadamu. Utabiri wa hali ya hewa unatarajia kimbunga kupiga tena eneo la Idai. Jambo gani jipya? Kimbunga Kenneth kilipiga kwa kasi kubwa ya upepo wenye kasi ya kilimota 220 kwa saa sawa na tufani ya awamu ya nne na kuwasili kaskazini mwa Pemba. Shughuli za uokoaji wa lazima kwa familia unafanyika na utaendelea kufanyika mpaka watu wote wafikishwe kwenye eneo salama. Watu zaidi ya 680,000 wapo hatarini na kimbunga, afisa mmoja wa utawala nchini Msumbiji aeleza. Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa tahadhari juu ya mvua kubwa katika eneo hilo kwa siku kadhaa. Safari za ndege zimesitishwa tayari na shule zimefungwa nchini Msumbiji kwa kuhofia dhoruba hiyo kupiga. Wakazi wa kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Mtwara walitengewa eneo maalum kwa ajili ya kujikinga lakini tahadhari hiyo imesitishwa na watu wamerudi katika makazi yao. Njia ya kimbunga imebadilika kusini, hii ikiwa ina maana kuwa janga kubwa halitarajiwi tena eneo hilo na ndio maana wamewaruhusu watu waendelee na shughuli zao za kawaida, Kamishna wa kikanda Gelasius Byakanwa aliwaambia waandishi wa habari. Wananchi wa Mtwara, Tanzania wakirejea katika makazi mara baada ya kutangaziwa kuwa njia ya kimbunga imebadilika Kimbunga Keneth kimepiga kisiwa cha Comoro kwa mvua kubwa na upepo na mamlaka ya nchi hiyo imesema watu wapatao watatu wameuwawa. Kimbunga Kenneth tayari kimefanya uharibifu kaskazini mwa Msumbiji, huku bado nchi hiyo inatarajia dhoruba nyingine kubwa. text: Kuwepo kwa TV katika chumba cha kulala cha mtoto kunaweza kumsababishia kutopata usingizi wa kutosha na kuwa na tabia ya ulaji usiofaa Watafiti walibaini kuwa watoto wasichana kadri wanavyokaa muda mrefu wakitazama TV, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano mkubwa wa uzito wao wa mwili kuongezeka. Watafiti wanasema kuna haja ya haraka sasa ya kuchunguza uwezekano huo kwa watumiaji wa vipakatanishi (laptops) na simu za mkononi (mobiles). Wataalam wanasema wakati watoto wanapotumia muda mefu kutazama TV hupata madhara mengi ya kiafya. Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa kuhusu Unene wa kupindukia (International Journal of Obesity) ulitathmini data kutoka kwa watoto wadogo zaidi ya 12,000 nchini Uingereza. India: Ujumbe wa dhihaka wamsaidia polisi kutibiwa India: Ujumbe wa dhihaka wamsaidia polisi kutibiwaIndia: Ujumbe wa dhihaka wamsaidia polisi kutibiwa Je nguo za kubana zina madhara kwa mwili wa binaadamu? Wanasayansi hao walibaini kuwa zaidi ya nusu ya watoto waliokuwa na TV katika vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa miaka saba. Wazazi waliulizwa kueleza ni kwa kiwango cha saa ngapi kwa siku watoto wao hutazama TV kwa ujumla . Baadae , watoto hao walipofikia umri wa miaka 11, watafiti walipima viwango vya uzito wao wa mwili kulingana na kimo chao cha urefu kwa kuangalia asilimia ya mafuta ya mwili waliyonayo. Wasichana waliokuwa na TV ndani ya vyumba vyao vya kulalawakiwa na umri wa miaka saba walipatikana na asilimia 30% ya uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia wanapofika umri wa miaka 11, wakilinganishwa na watoto wenzao ambao hawakuwa na TV vyumbani mwao. Kwa wavulana, hatari hiyo iliongezeka kwa asilimia 20%. Mtafiti Dr Anja Heilmann, alisema: "utafiti wetu unaonyesha kuwa kwamba kuna ushahidi wa wazi wa uhusiano baina ya kuwana TV chumbani kwa mtoto na kuongezeka kwa uzito wa mwili kwa mtoto miaka michache baadae." Watafiti wanajiuliza ikiwa matumizi ya simu za mkononi (mobiles) pia yana uhusiano na kuongezeka kwa unene wa mwili wa kupindukia Watafiti wanasema hawawezi kuwa na uhakika juu ya nini kinachosababisha uhusiano baina ya kutazama TV na kuongezeka kwa mwili, lakini wanasema huenda sababu ikawa ni watoto wenye TV vyumbani kusinzia kwa muda mfupi wakitumia muda mrefu kuitazama katika vyumba vyao vya kulala ama ulaji wa kiholela wanapotazama TV. Watafiti wanatoa wito wa kuandaliwa kwa mikakati ya uzuwia unene wa kupindukia miongoni mwa watoto kwa kuangalia njia za kukabliana na tatizo hili. Katika waraka wao kwenye jarida, wanasema : "wakati screen za TV zikiendelea utengenezwa kuwa vyembamba zaidi, watoto wetu wanakuwa na unene zaidi ." tabia ya Ulaji usiofaa Na kuna baadhi ya matokeo ya uchunguzi yaliyobaini kuwepo kwa uhusiano baina ya muda wasichana wanaoketi mbele ya TV na kuongezeka kwa uzito wa mwili husababishw ana kwamba wasichana hufanya mazoezi ya mwili kidogo kuliko wavulana wenye umri sawa na wao. Profesa Russell Viner, kutoka chuo cha tiba na afya ya watoto cha Royal College (RCPCH) anasema matokeo ya utafiti huo yanapaswa kuchukuliwa kwa umakini zaidi. Prof Viner anasema utafiti huo unaunga mkono haja ya kuzuwia ulaji wa vyakula visivyo na virutubisho vya mwili pamoja na matangazo ya TV yanayonadi vyakula hivyo Watoto wenye TV katika vyumba vyao vya kulala wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito wa kupindukia kuliko wale ambao hawana, utafiti katika chuo cha wanasayansi cha London London kinasema. text: When Greece declined, mathematical progress in China achieved new heights Safari ya uvumbuzi wa hesabu ilianzia Misri, kisha Mesopotamia na Ugiriki, lakini baada ya dola hizo kuanguka, maendeleo ya hesabu nayo yakaanguka ka umande wa Magharibi. Lakini kwa upande wa Mashariki mambo yalikuwa tofauti na hatua kubwa zilikuwa zikipigwa. China ya kale, hesabu ndio kilikuwa kiungo tegemezi cha kusimamisha Ukuta Mkuu ambao mpaka leo ni moja ya maajabu ya dunia. Na namba zilikuwa muhimu hata katika kupangilia maisha katika nyumba ya ufalme. Mpangilio wa hesabu za mapenzi Kuwa mfalme kulihitaji mtu awe na nguvu za kutosha Kalenda na mwenendo wa sayari ndio vilichangia maamuzi yote ya mfalme, mpaka namna maisha yake ya mchana - na usiku - yalivyopangiliwa. Washauri wa mfalme walitengeneza mfumo ambao ulimuwezesha mfalme kulala na idadi kubwa ya wanawake walokuwa chini ya milki yake. Mfumo hou wa kijiometriki, ulimuwezesha kulala na wanawake 121 ndani ya siku 15 tu, ambao ni; Kila kundi ni kubwa mara tatu zaidi ya kundi la awali. Kutokana na mfumo huo, wataalamu wa hesabu walimuwezesha mfalme kuwa na kalenda ambayo ilimfikia kila mwanamke aliyekuwa katika milki yake. Nguvu ya mfalme Si nyumba ya mfalme tu ndio ambayo ilitegemea hesabu, bali mambo yote ya utawala wa nchi. Usiku wa kwanza ulitegwa maalumu kwa malkia. Usiku wa pili kwa wapenzi wake wakuu watatu. Wakeze tisa usiku wa tatu, baada ya hapo wakeze wadogo 27 walilala nae kwa siku tatu tisa kwa usiku mmoja. Baada ya hapo katika kipindi cha siku 9 zilizofuata, watumwa 9 tofauti walikuwa wakilala na mfalme kila siku. Mfumo huo uliwekwa maalumu ili wanawake wenye wadifa mkubwa zaidi walale nae katika kipindi ambacho mwezi huangaza zaidi, kipindi ambcho yin au nguvu zao zipo katika kiwango cha juu ili zikabiliane na yan au nguvu za mfalme za kiume. Kuwa mfalme kulihitaji mtu awe na nguvu za kutosha, lakini malengo yalikuwa wazi - kuzaa wanamfalme wengi inwezekavyo ili kuwezesha ufalme uendelee. Si nyumba ya mfalme tu ndio ambayo ilitegemea hesabu, bali mambo yote ya utawala wa nchi. Kuvutiwa na hisabati China ya kale ilikuwa na eneo kubwa ambalo lilitawaliwa kwa sheria kali, zikiwemo za kodi, vipimo vya uzani na pesa. China ya kale ilikuwa na eneo kubwa ambalo lilitawaliwa kwa sheria kali, zikiwemo za kodi, vipimo vya uzani na pesa. Dola hiyo ilikuwa ikitumia mfumo wa desimali miaka 1000 kabla ya nchi za Magharibi kuanza kutumia. Wachina walikuwa wanamifumo ya hisabati ambayo haikuonekana katika nchi za Magharibi mpaka mwanzoni mwa karne ya 19. Kulingana na ngano za kale, mtawala wa kwanza wa China aitwaye Mfalme wa Njano, alitengezewa hisabati na moja ya miungu yake mwaka 2800 kabla ya kuzaliwa Kristo akiamini kuwa fani hiyo ina nguvu kubwa. Mpaka leo, Wachina wanaamini katika nguvu hizo za ajabu za nambari. Namba tasa zinachukuliwa kuwa ni za kiume na shufwa ni za kike. Namba nne huepukwa na nguvu zote, wakati namba nane huleta bahati nzuri. Kuanzia kupiga hesabu ya nyakati mpaka kuvuka bahari, hesabu ndio utaalamu ambao falme na ustaarabu wa watu wa kale waliutegemea. text: Magufuli akizungumza na wananchi katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma Jumapili Kiongozi huyo alisema mikopo inayochukuliwa na taifa hilo ina manufaa na itachochea ukuaji wa uchumi. Dkt Magufuli alikuwa akihutubu alipokuwa anaifungua rasmi barabara ya lami ya Iringa - Migoli - Fufu yenye urefu wa kilometa 189. Barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma na Barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya kuanzia Cape Town nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri (The Great North Road). Ujenzi wa barabara hiyo uligharimu Shilingi Bilioni 207.457 ikiwa ni ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa asilimia 65.9, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa asilimia 21.3. Serikali ya Tanzania ilitoa asilimia 12.8. Tanzania imekuwa ikikopa kutoka kwa mashirika ya kimataifa kufadhili miradi mingi ya miundo mbinu ikiwemo miradi ya barabara na reli. Ripoti ya mwaka wa kifedha wa 2016/2017 ripoti ya Bank Kuu ya Tanzania inaonesha deni la taifa hilo limefikia Dola 23.78 bilioni (zaidi ya Sh52.29 trilioni). Deni hilo liliongezeka kwa asilimia 9.1 katika mwaka huo ulianza Juni 2016. Hata hivyo, serikali imesisitiza kwamba kiwango hicho cha deni badi hakijapita kiwango kinachokubalika kimataifa. Deni hilo ni sawa na asilimia 48.9 ya pato la Taifa, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya BOT. Sehemu kubwa ya deni hilo ni kutoka kwa wakopeshaji wa nje ambao wameikopesha Tanzania dola za Marekani bilioni 18.5. Kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 8.9 ukilinganisha na kiwango cha deni mwaka uliodangulia ambapo deni lilikuwa dola za Marekani bilioni 16.4. Baadhi ya wachanganuzi wameikosoa hatua ya serikali kukopa kiasi kikubwa cha fedha lakini Dkt Magufuli amesema hakufai kuwa na wasiwasi wowote. Akihutubu Iringa, Rais huyo alisema na fedha hizo hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa muda mrefu, na kwamba ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kuchochea uchumi. Wakati wa kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, kiongozi huyo alieleza matumaini kwamba uchumi wa Tanzania utatengemaa. "Taifa letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 4," alisema. Baadaye alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinumwi Adesina. Taarifa iliyotolewa na ikulu ilisema Dkt Adesina alimpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuimarisha uchumi wa Tanzania na kusema wamejadiliana mambo kadhaa yakiwemo namna benki hiyo ilivyosaidia juhudi za maendeleo za Tanzania tangu mwaka 1971 na inavyoendelea kusaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Alitaja baadhi ya maeneo ambayo AfDB itatoa ufadhili kuwa ni uzalishaji na usambazaji wa nishati, uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Jiji la Dodoma hasa barabara. "Yote kwa yote nimemhakikishia Rais Magufuli kuwa AfDB itamuunga mkono katika mipango yake na maono yake ili tuweze kuisaidia Tanzania kukua zaidi, nimefurahi kuzungumza na Mhe. Rais na naona Tanzania ipo katika njia sahihi," alisema Dkt Adesina kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ikulu. Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, AfDB imefadhili miradi ya maendeleo yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.457 (sawa na Shilingi Trilioni 7.78 Tanzania) zikiwemo fedha za miradi 25 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2017 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.986 (Shilingi Trilioni 4.47 Kitanzania). Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka raia nchini humo kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa sana. text: Polisi wa kupambana na ugaidi walivamia nyumba eneo la Montpellier Wanaume watatu na msichanawa umri wa miaka 16 walipatikana na bidhaa za kutengeneza bomu na kikosi cha kupambana na ugaidi, wakati wa uvamizi kweye nyumba moja kusini mwa mji. Vilipuzi vya kutengezewa nyumbani sawa na vile vilivyotumiwa wakati wa shambuliki la mji wa Paris Novemba 15 vilipatikana. Ripoti zinasema kuwa msichanna alikuwa ameandika ujumbe wa itikadi kali mtandaoni. Tangu mwanzo wa mwaka 2015, takriban watu 230 wameuawa kwenye mashambulizi nchini Ufaransa. Ufaransa Wiki iliyopita mwanajeshi mmoja alipata majeraha madogo, wakati mwanamme moja aliyekuwa na panga alipojaribu kuingia makavazi ya mjini Paris. Mwanamume huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 29 Abdullah Hamamy, alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya Ripoti za awali zilisema kuwa mmoja wa washukiwa wa Montpellie, huenda akawa mshambuliaji wa kujitoa mhanga. Shirika moja la habari la Ufaransa lilisema kuwa watu hao wanne, walikuwa wakipinga kushambulia eneo wanakotembea watalii mjini Paris, lakini taarifa za polisi zililiambia shirika la habari la Reuters kuwa uchunguzi haujabaini hasa ni wapi walikuwa wamelenga kushambulia. Polisi walivamia nyumba moja ambapo walipata vifaa vya kutengeneza mabomu Njama ya kufanya shambulizi nchini Ufaransa umetibuliwa huku washukiwa wanne wakikamatwa eneo la Montpellier, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani Bruno Le Roux. text: Greenwood mwenye umri wa miaka 18 aliwasawazishia wenyeji baada ya goli lililofungwa na Junior Stanislas kuishangaza Man United kunako dakika ya 15 kabla ya kuifungia United goli lake la nne baada ya kipindi cha kwanza . Marcus Rashford alikuwa ameiweka United 2-1 juu kutoka mkwaju wa penalti kabla ya Anthony Martial kufunga bao zuri kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika. Katika mechi ilioja mbembwe za kila aina , Joshua King aliifungia timu yake goli la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika nne baada ya kipindi cha mapumziko. Kikosi hicho cha Edie Howe , kilifunga goli la kusawazisha ambalo lilikataliwa kwa kuwa la kuotea. Wakati huohuo Arsenal iliishangaza klabu ya Wolves ugenini na kuimarisha matumaini yake ya kufuzu katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuwalaza wenyeji wao 2-0 katika uwanja wa Molineux. Kinda wa Gunners Bukayo Saka, ambaye alitia saini kandarasi mpya siku ya Jumtano alianza kuifungia klabu yake . Adama Traore aliharibu nafasi bora zaidi ya kusawazisha , kabla ya Alaxandre Lacazette kuingia kama mchezaji wa ziada na kufunga bao la ushindi. Arsenal ilipanda hadi katika nafasi ya saba huku ikiwa pointi tatu nyuma ya Wolves. Mason Greenhood alifunga mara mbili katika ligi ya premia kwa mara ya kwanza huku Man United ikitoka nyuma na kuilaza Bournemouth 5-2 na kuongeza matatizo ya klabu hiyo inayokaribia kushushwa daraja. text: Gari la Katanka lilivumbuliwa na Kwadwo Sarfo Kwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya Katanka na mbaye pia ni kiongozi wa dini alionyesha gari alilotengeza aina ya V8, pikipiki za magurudumu matatu, mashine za roboti za kuchomelea vyuma miongoni mwa vinginevyo. Kwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya Katanka na rais wa Ghana kulia Nana Akofu Ado Rais Nana Akofu-Addo, ambaye alihudhuria maonyesho hayo amesema serikali yake itaangazia kuhusu elimu ya sayansi na teknolojia ili kuimarisha maendeleo ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Joy News. Magari ya kantanka Bw Sarfo ambaye ni babake mbunge mmoja amesema kuwa uvumbuzi wake unaonyesha uwezo mkubwa wa mtu mweusi katika sekta ya teknolojia na uvumbuzi. Alitengeza gari lake la kwanza mwaka 1998 na tangu wakati huo chapa yake ya Kantanka imetoa magari kadhaa ikiwemo magari yenye magurudumu manne na SUV. Gari la magurudumu matatu lililotengezwa Mvumbuzi mmoja wa Ghana ameonyesha kile anachotaja kuwa uvumbuzi wake wa hivi karibuni unaoshirikisha magari katika maonyesho ya Kiteknolojia katika mji mkuu wa Accra. text: Antonio Conte anakaribia kuongoza Chelsea kushinda taji la ligi msimu wake wa kwanza Stamford Bridge Inter wamemfuta kazi meneja wao Stefano Pioli. Taarifa nchini Italia zinasema klabu hiyo ya Serie A, inapanga kumuahidi Conte ujira wa £250,000 kwa wiki iwapo ataondoka Chelsea, klabu ambayo ameiongoza kwa msimu mmoja pekee. Pioli alifutwa kazi Jumanne miezi sita baada yake kuteuliwa kuwa mkufunzi mkuu. Mkufunzi huyo wa miaka 51 alikuwa amejaza naafsi ya Frank de Boer mwezi Novemba na alikuwa ametia saini mkataba wa kuwa meneja hadi Juni 2018. Conte, 47, ambaye alikuwa meneja wa timu ya taifa ya Italia, alihudumu kama meneja wa mahasimu wakuu wa Inter, Juventus kati ya 2011 na 2014. Inter, wakiwa wamesalia na mechi tatu za kucheza msimu huu, wamo nafasi ya saba Serie A, alama tatu nyuma ya AC Milan ambao wanashikilia nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League. Pioli amewahi kuwa mkufunzi klabu 11 zikiwemo Lazio, Parma na Bologna Inte Milan hawajashinda mechi hata moja katika mechi saba walizocheza karibuni ligini.Mkufunzi wa timu ya vijana Stefano Vecchi amepewa majukumu ya kuongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu. Pioli alikuwa meneja wa tisa Inter tangu kuondoka kwa Jose Mourinho mwaka 2010. Klabu ya Inter Milan ya Italia imekataa kuzungumzia taarifa kwamba inapanga kuwasilisha ombi kumtaka meneja wa Chelsea Antonio Conte ajiunge nao. text: Daktari wa maradona alitoa mahojiano yaliyowaliza watu baada ya kifo cha nyota wa kandanda Polisi mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo- Leopoldo Luque huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona. Maradona ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupona baada ya kufanyiwa upasuaji. Dokta Luque bado hajashitakiwa. Anakana kufanya kosa lolote. Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana na kujganda kwa damu , uliofanikiwa mapema mwezi wa Novemba na amekuwa akipata matibabu kutokana na uraibu wa pombe. Binti yake alikuwa amesisitizia kupata taarifa zaidi kuhusu matibabu ya baba yao. Je uchunguzi unalenga nini hasa? Polisi wapatao 30 walivamia makazi ya daktari dokta Luque Jumapili asubuhi - huku wengine 20 wakienda katika kliniki yake iliyopo katika mji mkuu Buenos Aires. Uvamizi huo uliagizwa na Waendesha mashitaka wanaojaribu kujenga picha kwamba kuhusu siku zamwisho za maisha ya Maradona nyumbani kwake. Walichukua kompyuta, simu za mkononi na taarifa za matibabu, wanasema maafisa. Maafisa wanaangalia rekodi za matibabu ya mchezaji nyota wa soka Wanashuku kwamba nyota huyo wa soka aliruhusiwa kwake kwenda nyumbani hakukutimiza vigezo vya kumruhusu atoke hospitalini, ikiwemo kupewa wauguzi au nesi wa kumuhudumia saa 24 "wataalamu wa uraibu ",kupewa daktari anayeweza kumuita wakati wowote na gari la kubebea wagonjwa lenye vifaa vya kumsaidia kupumua. Maafisa wanataka kufahamu kuhusu uhusika wa daktari Luque katika mipango ya kupona kwa Maradona katika nyumba ya nyota huyo. Dokta Luque anajitetea vipi? Katika mkutano na waandishi wa habari uliokgubikwa na hisia Jumapili , Dkt Luque - ambaye alielezewa kama daktari wa kibinafsi wa Maredona -aliangua kilio, akisema kuwa alifanya kile alichoweza kuyanusuru maisha yake ya rafiki yake. Alisema kuwa Maradona alikuwa ni mwenye huzuni katika siku za hivi karibuni . Wakati mmoja daktari aliwakaripia waandishi wa habari : " Mnataka kujua ni upi wajibu wangu ? Kwa kumpenda, kwa kumhudumia , kwa kurefusha maisha yake , kwa kuyaboresha mpaka mwisho ." Daktari alisema kuwa alifanya " chochote ambacho, hadi kile ambacho hakikuwezekana ". Akizungumzia masuala ambayo maafisa wanataka kuyachunguza , dokta Luque alielezea iliyokuwa kazi yake . ''Ukiniuliza mimi, mimi nilikuwa daktari wa upasuaji wa ubongo na kazi yangu iliisha . Nilikuwa nimemalizana ," alisema akizungumzia upasuaji aliomfanyia mwezi Novemba - na akasisitiza kuwa kuruhusiwa kwa Maradona kwenda nyumbani haukuwa wajibu wake. Diego Maradona "ataishi mioyoni mwetu daima" "Maradona angepaswa kwenda kwenye kituo cha kurekebisha tabia. Hakutaka kufanya hivyo," Dokta Luque alisema,akimtaja marehemu nyota huyo kama mtu ambaye "ilikuwa vigumu kufikiria ni mtu wa aina gani ". Anasema hajui ni kwanini hakupewa gari la ambiolansi lenye vifaa au ni nani alihusika na kutopelekwa kwa gari hilo nje ya nyumba ya Maradona. Na aliongeza kuwa : Diego "alikuwa mtu mwenye huzuni , na alitaka kuwa peke yake, na sio kwasababu hakuwapenda binti zake , familia yake au wale waliomzingira". Waendesha mashitaka nchini Argentina wanamchunguza daktari wa Diego Maradona kwa uwezekano wa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea siku nne zilizopita . text: Rose Marie Bentley aliishi na hali hiyo isiokuwa ya kawaida kwa miaka 99 Rose Marie Bentley, alifariki mwezi Oktoba mwaka 2017, lakini alikua amewapatia idhini watafiti wa Chuo Kikuu cha Oregon kufanyia uchunguzi mwili wake. Wanafinzi wa sayansi ya viungo vya mwili mara ya kwanza waligundua ya kwamba viungo vyake vingi havikuwa mahali vilipostahili kuwa. Licha ya kufanyiwa upasuaji mara kadhaa, hali yake haikufahamika. Madaktari walishanga jinsi Bi Bentley alivyoweza kuishi maisha marefu bila matatizo ya kiafya licha ya hali ya viungo vyake. Wataalamu wanasema alikua na hali inayofahamika kama ''situs inversus'', iliyomaanisha kuwa ini, utumbo na viungo vingine vya sehemu ya chini ya tumbo vilikuwa mahali pasipo stahili kuwa ima viungo hivyo vilikua upande wa kushoto au kulia. Moyo wake hata hivyo ulikuwa upande wa kushoto wa mwili kama ilivyokawaida. Picha inayoonesha viungo vya ndani vya mwili wa Bi Bentley vilivyokuwa katika sehemu zisizofaa Hali hiyo si ya ''kawaida kabisa'', alisema Dkt Cam Walker, mmoja wa maprofesa waandamizi wa sayansi ya viungo katika chuo cha Oregon cha sayansi ya afya, ambaye aliwasaidia wanafunzi wake kubaini maajabu ya kimaumbile ya mwili wa Bentley. Dkt Walker ameimbia BBC kuwa utafiti huo ulianza wakati wanafunzi wake walipokua wakifanyia upasuaji wa mshipa mkubwa wa kusafirisha damu mwilini lakini wakashindwa kufikia mshipa huo. Ni hapo walipobaini kuwa mwili wa Bi Bentley ulikuwa tofauti na watu wengine. Ni mtu mmoja kati ya watu 22,000 ambao huzaliwa na hali kama hiyo duniani. Hali hiyo mara nyingi huhusishwa na maradhi hatari ya moyo au magonjwa mengine. Dkt Walker anakadiria kuwa ni mtu mmoja kati ya watu milioni 50 wanaozaliwa nha hali ya viungo vya mwili kuwa katika sehemu zisizostahili ambao huishi hadi utu uzima. Yeye na wenzake wanaamini kuwa Bentley ni mtu wa kwanza kuwahi kuishi na hali hiyo kwa miaka mingi. Wanasayansi wametafiti matukio mawili ya wagonjwa walioishi na hali hiyo hadi miaka 70. "Hakuna hata mmoja wa wafanyakazi wenzangu aliyewahi kuona mtu aliye na ''situs inversus'' japo wengi wao walikuwa wamefunza kuhusu hali hiyo kwa mika 30," Dkt Walker alisema. "Sijawahi kuona kitu kama hiki." "Wanafunzi, nadhani, hawatawahi kusahau," alisema Dkt Cam Walker na Dkt Mark Hankin waliyofanyia uchunguzi mwili wa Bi Bentley Louise Allee, mmoja wa watoto wa Bw na Bi Bentley, alikiambia chuo kikuu cha sayansi cha Oregon kuwa mama yake angelifurahia sana jinsi hali yake ilivyoangaziwa. "Mama angelichukulia suala hili kuwa ni wazo zuri sana", Bi Allee alisema. Watoto wa Bentley walikiambia chuo hicho kuwa mama yao aliishi maisha ya kawaida licha ya hali aliyopitia. Alifanyiwa upasuaji mara tatu na wakati huo madaktari walitoa kongosho baada ya kubaini ilikua upande ambao haikustahili kuwa. Mwanamke mmoja nchini Marekani ameishi na viungo vya mwili katika sehemu zisizofaa hadi akafariki dunia akiwa na miaka 99. text: Felix Tshisekedi raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Raisi Tshisekedi ameahidi kukutana na tume ya uchaguzi na maafisa wengine mwanzoni mwa wiki ijayo, inaarifiwa kuwa raisi pia alimhimiza mwendesha mashitaka wa serikali kufungua uchunguzi dhidi ya viongozi hao. Haijafahamika dhahiri muda wa kuapishwa kwa maseneta wapya, Uchaguzi wa magavana pia umeahirishwa kwa muda usiojulikana. Naye Waziri wa Mambo ya Ndani Basile Olongo wa DRC, alizungumza na BBC kufuatia mkutano aliohudhuria pamoja na raisi Felix Tshisekedi, wakiwemo maafisa kutoka tume ya uchaguzi nchini humo, pamoja na maofisa wengine wa serikali. Magavana hao walitarajiwa kuchaguliwa Machi 27 na wabunge wa mkoa huo ambao wameshutumiwa kwa kuuza shahada za kupigia kura kabla ya uchaguzi . Raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Matokeo ya muda mrefu yanaonyesha kuwa rais Kabila alishinda viti vingi katika Seneti, na hivyo kuipa kambi yake nguvu ya kuongoza pande zote ikiwemo utoa kambi yake ya udhibiti wa bunge na hivyo kuwa na ushawishi mkubwa. Wafuasi wa raisi Tshisekedi waliingia mtaani mwishoni mwa juma lililopita kushutumu tamko la uwepo wa "rushwa mbaya" katika mchakato wa kuwapata magavana na maseneta ingawa wagombea saba wa nafasi hizo walijiengua wenyewe kwenye mchakato, kabla ya kupiga kura kuwashtaki Wabunge wa mkoa kwa hadaa ya kunua shahada za wapiga kura kwa shahada moja kiasi cha dola za kimarekani elfu 50,000. Tume ya uchaguzi nchini humo ilikataa ombi kutoka kwa mwanasheria mkuu wa erikali ya Kongo kusimamisha zoezi la upigaji kura ili kuruhusu polisi kufanya uchunguzi juu ya madai hayo. Muungano wa wanashria wa raisi Tshisekedi i wa ushirikiano wa Tshisekedi walisema wataweka malalamiko kwa mahakama dhidi ya wabunge wao wa mkoa wanaoshukiwa kuwa wanahusika katika sakata la rushwa. Kwa sheria, Mahakama ya Katiba nchini humo ina muda mpaka kufikia mwishoni mwa juma hili kutangaza matokeo ya wazi ya uchaguzi wama seneta. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, raisi Felix Tshisekedi ameamuru ufungaji wa sherehe dhidi ya maseneta wapya waliochaguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia shutuma dhidi yao kutoka kwa umma juu ya ununuzi wa kura. text: Kulingana na taarifa liliotuma kwa vyombo vya habari na shirikisho hilo limeanza kujiandaa kwa mwechi za ligi hiyo kufuatia hatua ya rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli kupendekeza kundelea kwa ligi hiyo. Akizungumza katika hafla ya kumuapisha waziri mpya wa maswala ya katiba siku ya Jumapili Mwigulu Nchemba nyumbani kwake huko Chato, Magufuli alisema kwamba amewasilisha pendekezo hilo kwa washauri wake ambao wanakutana kujadiliana jinsi mashindano hayo yatakavyoanza. Hatahivyo aliongezea kwamba mashabiki watalazimika kutazama mechi hizo katika runinga ili kuzuia uwezekano wa maambukizi ya virusi vya corona. Katika taarifa yao TFF na TPLB wamesema kwamba wanaendelea na mchakato wa ndani kuelekea kurejea kwa ligi. Hatahivyo taarifa hiyo imeongezea kwamba kurejea kwa ligi hiyo hatahivyo kutetegemea uamuzi wa serikali ambayo itatangaza muda mwafaka wa kurudi kwa ligi hiyo. Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba kwa sasa mchakato huo ni wa ndani na kwamba wanachama wa shirikisho hilo wanapaswa kutekeleza agizo la awali la kuepuka mikusanyiko. Wamesema kwamba watatoa muongozo mwengine baada ya kupata muongozo wa serikali. Akizungumzia kuhusu kurejea kwa ligi hiyo rais Magufuli alisema: Napendekeza kwamba tuanzishe mechi za ligi yetu ya soka , lakini watu wataruhusiwa kutazama katika runinga. Nasubiri ushauri wa wataalam ili ligi iendelee'', alisema katika hotuba ilipeperushwa moja kwa moja kutoka nyumbani kwake Chato Geita. Tanzania iliripoti kisa chake cha kwanza cha Covid-19 tarehe 16 mwezi Machi. Tangu wakati huo, idadi hiyo imeongezeka maradufu hadi 480. Kati ya visa hivyo wagonjwa 167 wamepona na wameruhusiwa kujiunga na familia zao nyumbani huku watu 16 wakiripotiwa kufariki. Tarehe 16 mwezi Machi, taifa hilo lilitangaza kufungwa kwa shule kuanzia zile za chekechea hadi fomu 6 kwa siku 30. Akizungumzia kuhusu soka, rais Magufuli amesema kwamba hakuna ushahidi kwamba wale wanaofanya mazoezi wanaweza kuathiriwa na mlipuko wa Covid-19. 'Inawezekana kwamba tutaishi na Covid-19 kama vile ambavyo tumekuwa tukiishi na virusi vya ukimwi na magonjwa mengine'', alisema. Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF pamoja na bodi ya ligi hiyo TPLB zinajiandaa kuendelea na ligi ya mchezo huo nchini licha ya kuwepo kwa virusi vya corona. text: Baadhi ya timu za wanaume, kama vile Jersey Bulls na Vauxhall Motors, tayari zilikuwa zimefaulu kupandishwa daraja hadi hatua ya 5 ya vilabu ambavyo haviko kwenye ligi lakini hilo limefutiliwa mbali Baadhi ya wabunge pia wameziambia klabu hizo kuwa wataiandikia Idara ya Digitali, Utamaduni, Mawasiliano na Michezo wakitaka iingilie kati katika kile ambacho wamekieleza kama moja ya uamuzi wenye kukatisha tamaa. Wiki iliyopita ilitangazwa kwamba mashindano yote chini ya madaraja matatu ya juu ya England yanasitishwa mara moja huku matokeo ya mechi zilizochezwa tayari yakiufutwa. Hii inamaanisha kwamba hakuna timu itakayopanda wala kushuka daraja katika ligi 91. Hatua sawia na hiyo itatekelezwa katika ligi ya wanawake. Hata hivyo umauzi huo bado haujaidhinishwa na Baraza la FA. Michezo imeathirika vibaya na janga la virusi vya corona huku mechi ambazo zilikuwa zimepangwa zikiahirishwa mapema mwezi huu. Ijumaa ya wiki hii klabu zinazoshiriki Ligi ya Primia zinatarajiwa kukutana na kujadili mustakabali wa ligi hiyo iliyosimamishwa mpaka Aprili 30. Barua hiyo inasema: "Wasiwasi wetu ni kuhusu uamuzi uliochukuliwa kwa haraka bila ya majadiliano ya kina ama kushauriana na klabu zilizoathirika. "Uamauzi huo pia hauzingatii mamilioni ya pauni ya wawekezaji na muda uliotumika ambavyo vyote vimekuwa na athari mbaya ya kifedha. "Kuandika barua hii ya pamoja, tunatambua kwamba uamuzi wa kufuta matokeo ya msimu wa 2019-20 bado kunategemea kuidhinishwa na Baraza la FA. "Hatahivyo, tunaamini kwamba kupitishwa kwa uamuzi kama huu ni jambo lisilokubalika. Tunaomba kufanya mazungumzo haraka iwezekanavyo na FA lengo likiwa ni kutaka uamuzi huo upitiwe tena." BBC imekuwa ikifuatilia mawasiliano kati ya vilabu na wabunge wao wa eneo wameashiria kwamba wameandika au wataiandikia Idara ya Digitali, Utamaduni, Mawasiliano na Michezo kuhusu suala hili. Barua hiyo inasema kwamba ikiwa hakuna makubaliano yatakayofikiwa na vilabu hivyo, watachukua mkondo wa kisheria". Katika taarifa, Shirika la FA limesema: Uamuzi uliochukuliwa kutamatisha msimu wa mwaka 2019- 20, Ligi ya taifa, ligi ya wanawake na mashindano mengine ya eneo ulifanyika kupitia wawakilishi wa kamati za ligi husika na kuungwa mkono na bodi ya FA na bodi ya Wanawake ya FA. "Kwa sasa barua hiyo itaenda katika Baraza la FA ili kuidhinishwa. Tunaunga mkono uamuzi unaotolewa wakati wa changamoto hizi na hatua ambazo hazijawahi kuchukuliwa kabla katika soka ya Uingereza." Zaidi ya klabu 100 ambazo hazishiriki kwenye ngazi za juu za ligi nchini England zimetuma barua ya wazi kwa Shirikisho la Mprira (la nchi hiyo) FA na kulitaka kufikiria tena uamuzi wake wa kufuta misimu yao. text: Mji wa Aleppo ulivyokuwa ukionekana mwaka 2006 Umesema kuwa kumekuwepo mapigano mkali baina ya majeshi ya serikali na makundi ya waasi ambayo yamewaacha zaidi ya watu milioni mbili bila ya Pia tahadhari kuhusu usambazwaji wa chakula na dawa upo katika hatari kufuatia kutengwa na wakazi wa maeneo hayo. Mji wa Aleppo unavyoonekana hivi sasa Katika siku za karibuni waasi walifukuzwa na majeshi ya serikali yaliyopo mjini Aleppo. Shirika la habari la serikali la Syria limeripoti kuwa majeshi ya serikali yamefanikiwa kurudisha majimbo yaliyokuwa mikononi mwa waasi katika mji wa kusini magharibi mwa mji iliyokaliwa na waasi. Umoja wa mataifa umetaka kusitishwa kwa haraka mapigano yanayoendelea katika mji wa Alleppo nchini Syria. text: Wanaotoa lugha za dhihaki dhidi ya Rais wa Tanzania ,John Magufuli waendelewa kushitakiwa Yuston Emmanuel mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mkaAzi wa Ngara mkoani Kagera,Tanzania amehukumiwa kwa kosa a ambalo mwendesha mashtaka alidai kwamba alikuwa amekwenda kinyume na kifungu cha 89(1) (a) cha kanunu ya adhabu iliyorekebishwa na kuna umuhimu wa adhabu kali kutolewa ili iwe fundisho kwa wengine. Raia huyo ni miongoni mwa watu wasiopungua kumi wa nchi hiyo, idadi ambayo inajumuisha viongozi wa upinzani na raia wa kawaida walioshitakiwa kwa kosa la kumdhihaki au kumtusi rais Magufuli tangu aingie madarakani. Mwezi Juni mwaka 2016, Mulokozi Kyaruzi ni miongoni mwa raia wa Tanzania ambaye alishtakiwa chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni baada ya kudaiwa kumtusi Rais John Pombe Magufuli . Mbunge wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Halima Mdee mwezi agosti 2017 alishtakiwa kwa kosa la kumtusi rais na aliachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni kumi za Tanzania . Muhadhiri mmoja pia alishtakiwa katika mahakama moja nchini Tanzania kwa kumtusi rais wa taifa hilo chini ya sheria ya uhalifu iliowekwa mwaka uliopita. Halima Mdee aliwahi kushtakiwa kwa kumdhihaki rais na kuachiwa kwa faini Kulingana na afisi mkuu wa polisi wa eneo la kusini magharibi mwa Tanzania, alidai shtaka hilo ni hatia na mtu anaweza kufungwa hadi miaka mitatu jela ama kupigwa faini ya dola 3,000 ama zote. Mhadhiri huyo alikana mashtaka hayo. Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Osmund Mbilinyi, mnamo tarehe 26 Februari alihukumiwa kifungo cha miezi mitano na mahakama ya hakimu mkazi Mbeya kwa kupatikana na kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli. Hatia ya mashtaka imesema maneno waliyoyatamka yalienda kinyume na Sehemu 89(1) a ya Sheria za jinai ambayo inaharamisha kutumiwa kwa lugha ya matusi. Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Osmund Mbilinyi Maneno hayo, hati za mashtaka zinasema, yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani. Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanza kutekelezwa mwaka uliopta. BBC ilifanya mahojiano na wakili Jebra Kambole ambaye alisema adhabu hizo zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 89 ambapo kifungo huwa ni miezi sita au faini ambayo hutolewa kwa kuangalia uwezo wa mtu mwenyewe. "Sheria ipo lakini sheria hii ni tishio la uhuru wa mtu kujieleza na demokrasia kwa pamoja kwa sababu inawezekana kuwa tafsiri za maneno zikatofautiana na hii sheria inawagusa hata kwa mtu kwa mtu sio kwa viongozi peke yake,labda ni wakati sasa watetezi wa haki za binadamu nao waingilie kati suala hili",Jebra alieza. Licha ya kuwa watu kadhaa wamekamatwa katika siku za nyuma kwa kuchapisha ujumbe katika mitandao ya kijamii ambayo mamlaka inadai inaingilia kisiasa. Mamlaka inaamini kwamba inafuata sheria na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba hakuna ''migogoro yoyote miongoni mwa wananchi'' nchini Tanzania. Raia mwingine nchini Tanzania amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi sita au kulipa faini ya sh.200,000 kwa kosa la kutumia lugha ya kumdhihaki rais Magufuli. text: Lakini kuna wasiwasi unaoongezeka Uganda kuhusu athari yake kwa jamii. Serikali imetangaza udhibiti mpya katika biashara hiyo, ulionuiwa kuzuia shughuli za kampuni za kamari za mataifa ya nje. "Vijana Uganda wamekwama katika mzunguko wa michezo ya kamari, wanatoa mishahara kidogo wakitarajia watashinda mali nyingi," amesema waziri mdogo wa fedha David Bahati, akizungumza katika hafla aliyoihudhuria kwa niaba aya rais Yoweri Museveni. "Kuanzia sasa, hakuna kampuni mpya itakayopewa kibali. Kampuni zilizosajiliwa hazitopewa vibali vipya wakati walivyonavyo vikimalizika muda." Kwa hivyo, je ni kweli kuwa vijana ndio wanaocheza kamari zaidi na je kuna tataizo linalokuwa kubwa kutokana na uchezaji kamari? Kukuwa kwa michezo ya kamari Afrika mashariki Katika miaka kadhaa iliyopita, kampuni mpya za uchezaji kamari zimeibuka katika eneo la Afrika mashariki. Michezo mingi ya kamari huwa kwenye simu, huku michezo kama soka ya ligi kuu ya England yakiwa na umaarufu mkubwa. Wengi wanatumia simu kuweka dau Serikali imeyahimiza makampuni haya yanayoingiza kipato cha kodi na inayooekeza katika ligi za soka. Lakini rais Museveni, ambaye awali aliyahimiza, makampuni hayo yalioshamiri, sasa anaonekana kubadili kauli yake na kuelezea kwanini ana wasiwasi nayo. Zaidi ana wasiwasi kuhusu makampuni kukusanya faida nje, badala ya kuekeza upya nchini Uganda. "Wanachofanya ni kukusanya pesa tu kutoka kwa raia wa Uganda, alafu wanazitoa nje ya nchi," amesema. Alipoulizwa bungeni kuhusu uwepo wa makampuni hayo ya nchi za nje ya kamari, Bahati amesema: "Kwa kutazama nafasi ndogo iliopo, ni makampuni ya Uganda pekee yatakayoruhusiwa." Je ni kweli vijana ndio wanaocheza kamari zaidi? Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, umegundua kwamba wengi walioshiriki kamari walifanya hivyo kupata kipato, kujikimu maisha na sio kwasababau za starehe. Utafiti huo wa taasisi ya Economic Policy Research Centre, imeashiria kwamba 45% ya wanaume Uganda walio na umri wa kati ya miaka 18-30 walijihusisha zaidi na aina fulani ya kamari, ikilinganishwa na takriban robo ya watu wazima wote. Utafiti huu, umegundua kwamba "wanaocheza kamari kukabiliana na umaskini wana uwezekano mkubwa wa kuwa waraibu kuliko wale wanaocheza kwa starehe". Kwa mujibu wa EPRC, ni mchezo unaowavutia zaidi wanaume, huku chini ya 4% ya wanawake walioitikia katika utafiti huu wakisema wamewahi kucheza kamari. Ripoti hiyo pia imekadiria kwamba wanaocheza kamari, wanatumia takriban 12% ya mishahara yao kila mwezi katika michezo ya kamari. "Hamu ya kutaka akupata pesa haraka kutoka kamari inawashinikiza vijana kujiingiza katika kamari kiasi kwamba baadhi wanatazama mchezo huo kama njia ya kujikimu kimaisha badala ya kutafuta ajira," watafiti wamesema. Pato la kodi laongezeka Kuongezeka kwa haraka kwa pato la kodi katika miaka michache iliyopita kutoka sekta ya kamari ni kipimo cha wazi kwamba uchezaji kamari umeongezeka miongoni mwa raia Uganda. katika miaka minne iliyopita (ikiwemo 2017-18), data ya serikali inaashiria ongezeko la zaidi ya mara nne katika pato la kodi. Iwapo serikali ya Uganda itaendeleza mipango yake kukatiza uchezaji kamari, ni wazi kwamba hatua hiyo itaathiri pato la nchi. Baadhi wameelezea kushtushwa kwao kwamba serikali imechukua hatua hii, hasaa kwa kutazama faida inayopokea sasa kutokana na biashara ya kamari. Je wasiwasi ni upi wa kijamii? Shutuma zilizoelekezwa kwa biashara hiyo zinazidi kuongezeka, huku kukiwa na lawama kwamba inaathiri maisha ya vijana sio tu Uganda lakini katika eneo zima. Afisa katika duka la michezo ya kamari mjini Kampala, Patrick Lubaale, anadokeza kwamba maelfu ya watu wanategemea ajira katika biashara hiyo. Na anasema kampuni za michezo ya kamari zimekuwa zikihimiza watu wacheze kwa uwajibikaji. "Iwapo rais analalamika kuhusu athari mbaya kwa vijana," anasema Lubaale, "tayari tumekuwa tukihamasisha watu kuhusu athari za kutowajibika katika mchezo huu, na watu wanalifahamu hilo - lakini hilo halipaswi kuwa sababu ya kupiga marufuku biashara hiyo." Lakini suala la uraibu wa mchezo wa kamari miongoni mwa watu walio na kipato kidogo linazidi kuulizwa Uganda. Waziri wa fedha, Matia Kasaija ametaka liwe kwa kipimo. "Hautoingia katika matatizo. Utaishiwa na pesa, hautokuwa na chakula, mahali pa kulala, na kitakachofuata sasa ni uhalifu wa kuibia watu." Hatahivyo, licha ya ahadi ya serikali kutotoa vibali vipya hakujakuwa na ishara ya wazi ambayo makampuni ya kamari Uganda yatafahamu, ni vipi na lini yatakaathirika. Michezo ya kamari inaongezeka Afrika mashariki - kwa simu, kwa kompyuta na katika maduka ya kamari. Ni biashara kubwa na inaleta mapato ya kodi yanayohitajika pakubwa kwa serikali. text: Ngozi ya samaki kwa rangi nne tofauti "Mara 200 ya kwanza tulitengeneza supu ya samaki iliyokuwa na harufu kali," alisema. Bi Gunnsteinsdóttir ni meneja wa mauzo wa kampuni ya Atlantic Leather kutoka Iceland ambayo inajihusisha na biashara ya bidhaa za samaki Barani Ulaya. Tangu mwaka 1994 kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza ngozi kutokana na samaki wa aina kadhaa kama vile salmon, perch, na cod. Shughuli ya kutengeneza ngozi hiyo huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu, na wafanyikazi 19 wanaweza kutengeneza karibu tani moja ya ngozi ya samaki kwa mwezi. "Harufu ya samaki hubadilika katika awamu ya kwanza ya utengenezaji wake, na baadaye hubadilika na kunukia kama ngozi ya kawaida," anaongeza Bi Gunnsteinsdóttir. Ngozi ya samaki inaendelea kupata umarufu wa kutengenezewa vibeti vya wanawake Kampuni hiyo inapata malighafi yake kutoka Iceland, Norway na visiwa vya Faroe. Tofauti na utengenezaji wa ngozi inayotokana na ng'ombe ambayo inasemekana kuwa hatari kwa mazingira utengenezaji wa ngozi wa samaki ni salama kwa mazingira. Atlantic Leather pia inatumia 'dye' ya kawaida na ile isiyo na athari kwa mazingira kutengeneza ngozi kutokana na samaki Bei ya ngozi inategemea aina ya samaki kwa mfano ngozi inayotokana na samaki aina ya salmon inauzwa kwa dola $12. Kipochi kilichotengenezwa kutokan na ngozi ya samaki Bidhaa zao zinaagizwa sana na kampuni maarufu za mitindo kama vile Jimmy Choo, Dior na Ferragamo, na Bi Gunnsteinsdóttir anasema kumekuwa na dhana kuwa ngozi inayotokana na samaki sio dhabiti na inaweza kuchanika kwa urahisi. "Ngozi ya samaki ni imara mara kumi zaidi ya ngozi ya ng'ombe" anasema. "Hii ni kwasababu ngozi ya samaki inapitana pitana bada ya kwenda juu na chini... hali ambayo inaifanya kuwa thabiti zaidi hasa kwa utengenezaji wa mishipi, viatu na vibeti vya wanawake." Japo ngozi inayotokana na samaki inachangia chini ya 1% ya mauzo ya ngozi duniani, shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa zinahamasisha ukuzaji zaidi wa ngozi hiyo ili kuwaongezea kipato wafanyibiashara wa smaki duniani. Wafanyikazi wa kiwanda cha ngozi cha Victorian Foods nchini Kenya "Tunadhani ngozi ya samaki ndio njia bora ya kuimarisha maisha ya watu bila kuhatarisha usalama wa chakula ," anasema Jackie Alder,ambaye ni afisa wa kitengo cha uvuvi wa shirika la FAO Ongezeko la upatikanaji wa ngozi ya samaki litapunguza uhitaji wa ngozi ya nyoka na wanyama wengine ambao wakabiliwa na hatari ya kuangamia duniani Utumiaji wa ngozi ya samaki pia siku zijazo huenda ikapunguza uhitaji wa ngozi ya ng'ombe ambayo mfumo wake wa utengenezaji sio salama kwa mazingira. Viwanda vya utengenezaji ngozi inayotokana na ng'ombe imehusishwa moja kwa moja na ongezeko la ulaji nyma. Kiwango cha sasa cha ulaji nyama na ngozi ya ng'ombe kinakadiriwa kuchangia tani milioni ya uchafuzi wa mazingira kila mwaka.Tangu mwaka 2005, makundi ya kampuni zinazojihusisha na utengenezaji ngozi ambayo wanachama wake ni pamoja naAdidas, Nike na Primark -yanasema yamekuwa yakishinikiza umuhimu wa kutunza mazingira. Victorian Foods inapata malighafi yake kutoka kwa wavuvi 300 Kampuni ya Kenya inayofahamika kama Victorian Foods pia kwa ushirikiano na Jackie Alder na kundi lake wanatumia samaki kutoka ziwa Turkana kutengeneza ngozi. Afisaa mkuu mtendaji wa Victorian Foods' James Ambani anasema katika kipindi cha miaka mitatu cha utendakazi wake kampuni hiyo sasa inatengeza kilo 400 za ngozi kwa wiki ambayo inauzwa kwa dola tano kwa mraba. Kampuni hiyo imewaajiri wanawake 10 na imekuwa ikiwapa mafunzo makundi ya watu wanaojihusisha na biashara ya utengenezaji ngozi inayotokana na samaki. Ngozi ya samaki huenda ikapunguza uhitaji wa ngozi ya mamba Mwanamitindo wa mavazi mzaliwa wa Kenya Deepa Dosaja hivi karibuni alitumia ngozi ya samaki kutengeneza vibeti vya wanawake.. "Hii ni fasheni ya hali ya juu na inapendeza sana - najivunia kuimarisha taaluma yangu," anasema. Steinunn Gunnsteinsdóttir anakiri kuwa iliichukua familia majaribio ya mara kadhaa kuweza kutengeneza ngozi kutokana na samaki. text: Wanaharakati wanaounga mkono itumiaji wa bangi walionekana wakisheherekea uamuzi huo wa mahakama Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi. Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi wamesheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Akitoa hukumu hiyo Naibu jaji Mkuu, wa Afrika Kusini, Raymond Zondo, amesema sheria inayopiga marufuku watu wazima kutumia bangi ilikuwa kinyume cha katiba. Serikali ya Afrika kusini bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na na uamuzi huo. Watumiaji watatu wa bangi walikuwa wanakabiliwa na mashtaka walijitetea mbele ya mahakama hiyo wakisema '' mashataka dhidi yao yaliingilia uhuru wao'' Naibu jaji mkuu Raymond Zondo alisema: "Sio hatia kwa mtu mzima kutumia au kugusa bangi akiwa katika eneo la faraghani hasa ikiwa anafanya hivyo kwa maatumizi yake ya kibinafsi'' Licha ya uamuzi huo, ni hatia kwa mtu kuvuta au kuuza bangi hadharani. Bunge litatatoa uamuzi ni kiwango gani cha bangi watu wanastahili kuwa nacho Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini limeunga mkono uamuzi wa mahahakama dhidi ya matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho. Jeremy Acton, kiongozi wa chama cha Dagga, ambacho kinaendesha kampaini ya kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi pia kimepongeza uamuzi huo wa mahakama ya katiba kimesema uamuzi huo pia ungelijumuisha kuhalalisha ubebaji wa bangi hadharani. Bangi hutambuliwa kama "dagga"nchini Afrika Kusini. Je unazifahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa? Lesotho Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho. Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini. Afrika Kusini Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa. Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi, vivyo hivyo kwa makampuni kutengeneza bidhaa zitokanazo na bangi na mawakala kusambaza bidhaa. katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma, wale walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha bangi wameleta maendeleo makubwa kufungua milango katika uzalishaji wa bangi kwa ajili ya dawa. Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi Ghana Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi . kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya. Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika. pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao. Korea Kaskazini Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni. wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria. Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho. Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha. text: Farah Khalek ni mwanamke mwenye miaka 33 ambaye ana ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama 'Scleroderma' Licha ya kuwa anakabiliana na ugonjwa wa ngozi ambao umebadilisha muonekano wake wa sura kabisa. Ugonjwa huu unajulikana kama Scleroderma. Farah Khalek hakuzaliwa akiwa na sura aliyo nayo kwa sasa, alikuwa ni mtoto mwenye muonekano wa kawaida kama wengine. Farah Khalek ni binti pekee kati ya ndugu wanne, hapo alikuwa na miaka mitano Farah ni msichana wa pekee kati ya ndugu watatu kwa wazazi wake, hivyo anahisi kuwa alipata malezi ya kupendwa zaidi kaatika familia. "Wazazi wangu na ndugu zangu walinidekeza tangu nikiwa mtoto mdog , kwa hiyo mimi nilikuwa katika mazingira ambayo nilihisi upendo na kukubalika" alisema Farah. Farah anaeleza kuwa akiwa na miaka 17 hali yake ilianza kubadilika wakati akiwa katika masomo yake ya sekondari. Anasema kuwa ugonjwa huo ulianza na dalili za mikononi, ambapo mikono yake ilianza kuwa migumu sana huku kucha zake zikibadilika rangi na kuwa bluu inayokaribia nyeusi. Fahamu ugonjwa wa Scleroderma uko vipi? Wakati huo anasema kuwa hisia za kero na machungu zilimjia asijue la kufanya. "Nilikuwa na hasira nao sana, wakati huo nakumbuka kuwa nilikuwa nagombana na mama yangu sana nikawa napigana na mamangu kila wakati huku nalia tu kwa kuwa sura yangu ilikuwa inanitisha hata mimi mwenyewe " Faraha alisimulia. Farah anasema kuwa kila uchao mwili wake ulichukua muonekano usiokuwa wa kawaida na binadamu wengine, ngozi nayo ikaendelea kuwa ngumu na viungo vya mwili vilikuwa vigumu mno . Walipoenda hospitalini nchini Kenya, Farah anasema kuwa wazazi wake walishauriwa watafute matibabu nje ya nchi, na hapo ndipo wazazi wake waliamua kwenda nchini India. Ndipo walipogundua kuwa ana ugonjwa ambao hauna kinga unaojulikana kama 'scleroderma' baada ya kufanyiwa uchunguzi. Farah ameiambia BBC kuwa tangu akiwa na miaka 17 mpaka sasa ana miaka 33 mwili wake umepitia mabadiliko mengi. Farah Khalek alianza kuwa na dalili za ugonjwa akiwa na miaka 17 Muonekano wake wa zamani na sasa si rahisi kuweza kugundua kuwa ni mtu mmoja kwani hali ambayo anaishi nayo ya Scleroderma imembadilisha sana sura. Athari nyingine za mwili ni kutokanana ugumu wa viungu vya mwili kwa mfano mikono yake ina ulegevu kiasi kuwa hawezi kuchana nywele zake kwa kutumia kichanuo wala kifaa chochote . Shughuli ambazo binadamu huzichukulia kuwa za kawaida kama kusimama , kuinama , kuandika kwa kalamu, sio mambo ya kawaida kwake Farah . "Mambo ya kawaida kama kuchana nywele zangu siezi, kwa kuwa viungo vyangu vya mkono vimekuwa vigumu na kushikana, kwa hiyo inabidi mamangu anisaidie kila siku "Farah alisimulia. Pia Farah anaeleza kuwa changamoto kuu ya kuishi na hali hii ni kutokana na jamii akila mara akiwa nje ya nyumba yake watu humtizama sana, na watoto walikuwa wanamuogopa sana kwa sababu ya sura yake kuwatishia licha ya yeye mwenyewe kujaribu kuwapa tabasamu lakini bado wanamuogopa. "kwa kweli siku hizi mimi hucheka tu watu wanaponikodolea macho njiani, kwani sina la kufanya " Farah anakiri kuwa ilichukua muda kwake kukubali kujiangalia kwenye kioo. Sura yake imepelekea watu kumuita majina ya ajabu, wakati mmoja anasema kwenye mitandao ya kijamii kunao watu ambao walimuita jina la 'sura mbaya' , lakini pamoja na yote anasema kuwa amekubali sasa kwani alianza kujipenda na kujiamini licha ya muonekano wake. Je nini kinachompa nguvu ya kuendelea na maisha licha ya muonekano wake? Faraha anasema kuwa jamii yake imekuwa na nafasi kubwa ya yeye kujikubali kwani wamejitahidi kumpa mzingira na upendo mwingi. Faraha amepitia matibabu mbalimbali kila wakati, mwaka wa 2018 alienda eneo la Ahmedabad India ambapo alifanyiwa upasuaji maarufu (STEM CELL TREATMENT) Matibabu haya Farah anasema kuwa yalihusisha kutolewa kwa seli kutoka mishipa ya damu yake na kisha kurejeshwa upya tena tena . Anasema matibabu haya yamemsaidia sana kwani sasa ameanza kula vizuri na pia sehemu ya utumbo wake iliyokuwa na shida ya kusaga chakula sasa imeanza kufanya kazi. Japo anasema kuwa hatua nyingine tatu kama hizo za matibabu zitahitajika kama njia ya kuimarisha afya yake katika kupigana na ugonjwa huu. Je wataaamu wanauelezea vipi ugonjwa huu wa'Scleroderma'? Scleroderma ni ugonjwa wa muda mrefu ambao huathiri ngozi ya mtu, tishu zinazohusika, na viungo vya ndani ya binadamu huathirika. Hali hii inatokea wakati mfumo wa binadamu wa kinga unasababisha mwili kutengeneza protini nyingi, katika sehemu muhimu ya ngozi yako na hali hiyo husabisha kinga ya mwili kutokuweko . Ngozi ya mtu huanza kuwa nene na ngumu mno, Scleroderma sio ugonjwa wa kuambukizwa au kuambukiza, ikimaanisha kuwa huwezi kuipata kutoka kwa watu wengine. Hakuna tiba,lakini matibabu yanaaweza kumfanyai mtu aishi maisha ya kawaida. Scleroderma husababishwa na baadhi ya matukio yakiwemo, shida za mfumo wa kinga, mfumo wa jeni na vichocheo vya mazingira. Dalili za mwanzo za ugonjwa huuwa Scleroderma ni zipi? Ngozi ya muathiriwa huwa ni ngumu huku ikionekana kuwa kavu na yenye mng'aro laini, vile vile vidole wakati mwengine huwa wakati mwengine vinaonekana kuwa nyekundu, nyeupe, au bluu. Pia , Vidonda kwenye vidole na uchungu unaotokana kuvimba kwa miguu na mikono. Farah Khalek ni mwanamke mwenye miaka 33 kutoka nchini Kenya, kama wanawake mwingine wa umri wake mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. text: Wakazi wanaoishi karibu na bandari ya Mocímboa da Praia wanaendelea kukimbia makazi yao huku mapigano yakiendelea kati ya wanajeshi wa serikali ya Msumbiji na wanamgambo wa Kiislamu. Eneo lililovamiwa liko karibu na miradi ya utafutaji wa gesi asili yenye thamani ya dola bilioni 60 na ulilengwa mara kadhaa na wanamgambo mwaka huu, kabla ya Msumbiji kutwaa tena bandari hiyo wiki iliyopita. Baadae jeshi la Msumbiji lilisisitiza kwamba limechukua udhibiti wa bandari na Rais Filipo Nyusi alizuru eneo la Cabo Delgado ambalo limekuwa likilengwa na wanamgambo tangu mwaka 2017. Laini za simu kwa ajili ya mawasiliano bado zimekatwa na miundo mbinu imeharibiwa. Rais Nyusi alisema nini? Alisema wapiganaji ambao wanahusishwa na kundi la kigaidi la Islamic State 'IS' hawajatoa tishio lolote dhidi ya jitihada za kimataifa kuharibu gesi iliyohifadhiwa. Ingawa waasi hao wanaonekana kuingia nchini humo kwa kasi na kufanya usalama wa taifa la Msumbiji kuwa mashakani. Taarifa kuhusu kile kinachoendela Mocimboa da Praia ni vigumu kubaini kwani barabara, umeme na mitambo ya simu imekatwa. Kuna ushahidi unaodai kuwa waasi hao wana silaha za uhakika na wana nia madhubuti kufanikisha lengo lao. Wanamgambo wanaofahamika kama al-Shabab, au vijana - ambao wana ajenda ya kiislamu, lakini kwa miongo wamejengwa na ukosefu wa miundo mbinu, ukosefu wa ajira, uchaguzi usio wa haki, rushwa na migogoro. Siku ya Jumatano juma lililopita Msumbiji ilisema kuwa vikosi vyake vinapigana kuchukua udhibiti wa bandari hiyo baada ya taarifa kadhaa kudai kwamba imetekwa na wanamgambo wa Islamic State Jumatano. Jeshi limesema kuwa hatua imechukuliwa kukabiliana na kundi hilo ambalo limekuwa likitumia wenyeji kama ngao yao. Hatua hiyo inafuatia mapigano ya siku kadhaa ya kutaka kuchukua bandari hiyo yenye utajiri wa gesi eneo la kaskazini. Hatua hiyo imekuja huku viongozi wa mataifa jirani wakithibitisha kujitolea kwao kusaidia Msumbiji kukabiliana na tatizo la ugaidi na mashambulizi yanayotokea nchini humo," wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Mwandishi wa BBC Africa Andrew Harding alisema kuwa kutekwa kwa bandari hiyo ni pigo kubwa kwa jeshi la Msumbiji, ambalo lina wakati mgumu kudhibiti ukuaji wa makundi ya waasi katika eneo hilo la utajiri wa mafuta la Cabo Delgado. Bandari ya Mocimboa da Praia inatumiwa kwa uwasilishaji wa mizigo kwa miradi ya eneo la pwani takribani umbali wa kilomita 60 (maili 40), ambayo inaendelezwa na kampuni kubwa za mafuta duniani ikiwemo Total. Wanamgambo - wenye kuhusishwa na kundi la Islamic State - wamekuwa wakitwaa miji kadhaa ya kaskazini katika miezi ya hivi karibuni, na kulazimisha maelfu ya watu kutoroka makazi yao. Hili lilikuwa moja ya mashambulizi kadhaa katika bandari ya Mocimboa da Praia mwaka huu. Tanzania pia imesema itafanya mashambulio dhidi ya wanamgambo wa jihadi katika misitu karibu na mpaka na Msumbiji. Mapigano yanaendelea nchini Msumbuji huku majirani wa nchi hiyo wakiahidi kutoa msaada kujinasua ya hali hiyo. text: Melfu ya watu wamejitokeza kote New York kwa maandamano yaliyoendelea usiku kucha juu ya kifo cha George Floyd Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25, mikononi mwa polisi huko Minneapolis kimesababisha maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini huko. Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali. Katika eneo la Fort Worth, Texas, inasemekana kundi dogo la watu lilisalia nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa mbili usiku. Waandamanaji katika mji wa New York pia nao walikiuka hatua ya kutoka nje iliyowekwa kuanzia saa mbili usiku. Meya wa mji alisongeza mbele muda huo kwa usiku wa pili mfululizo baada ya waandamanaji kupora eneo la kibiashara la Manhattan Jumatatu. Wanajeshi wa Marekani wakiwa mitaani kuzuwia maandamano Na katika mji wa Washington DC, kundi kubwa la watu limeendelea kukusanyika nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa moja usiku. Aidha, Takriban wanajeshi Taliban1,600 wamepelekwa katika maeneo ya mji wa Washington DC. Msemaji wa serikali amesema vikosi vilikuwa katika tahadhari ya juu. Katika jimbo la Minnesota waandamanaji wamewasilisha kesi mahakamani dhidi ya polisi kwasababu ya kifo cha Floyd. Gavana Tim Walz ameambia vyombo vya habari kwamba uchunguzi wa kifo hicho utalenga kumaliza tatizo la ubaguzi wa rangi ambalo limedhihirika kuwa sugu. Katika Los Angeles, mabango yaliyoandika Black Lives Matter - vuguvugu lililo katika maandamano ya kupinga mauaji ya polisi dhidi ya watu weusi Mwanaume mmoja na mtoto wake wa mwaka mmoja walikua miongoni mwa waandamanaji katika jiji la Californian la Pasadena Vilevile, watu wameendelea kukutana katika mji wa Floyd, Houston, Texas, na kufanya maandamano ya amani na familia ya marehemu Floyd. Watu hadi 20,000 wanatarajiwa kushiriki maandamano hayo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo. Roxie Washington, Mke wa George Floyd akizungumzia mtoto wao wa kike wa miaka sita aliyeachwa bila baba, Gianna, katika mkutano na wanahabari huko Minneapolis, "Gianna hana tena baba," alisema."Baba yake hata muona tena akikua, akihitimu shule, wala kumshika mkono siku ya harusi yake. Ikiwa ana tatizo lenye kumuhitaji baba yake, hayupo tena duniani. "Niko hapa kwa ajili ya mtoto wangu na mume wangu George kwasababu ninataka haki itendeke. Ninataka haki itendeke kwasababu alikuwa mtu mzuri haijalishi mwengine anafikiria nini." Maafisa wa usalama wakipiga goti pamoja na waandamanaji Atlanta Maafisa wa polisi na jeshi wamejitokeza katika miji tofautitofauti wakipiga goti pamoja na waandamanaji kama ishara ya kuonesha mshikamano. Katika mji wa Los Angeles, waandamanaji walikuwa wanashabikia wanajeshi pale walipopiga goti. Waandamanaji waliwataka wanajeshi kufanya maandamano nao, lakini wakasema kwamba wanahitaji kusalia sehemu moja. Mwandishi wa BBC Phoebe Frieze alikuwa katika kumbukumbu ya Lincoln Washington DC kabla tu ya kuanza kwa muda wa kutotoka nje saa moja jioni ambapo mamia ya waaandamanaji walikuwa wamepiga magoti mbele ya sanamu la Lincoln na kukaa kimya, huku vikosi vya taifa vilivyojihami vikiwa vimepanga mstari mbele vikitazama waandamanaji. Barabara nyingi zinazoelekea kwenye kumbukumbu hiyo zilikuwa zimefungwa na vizuizi vya polisi na pia helicopter inayoshika doria ilisikika kwa juu. Waandamanaji walitaja majina ya watu wengine waliokufa kwa njia tatanishi mikononi mwa polisi kama vile Tamir Rice, 12, aliyeuawa Cleveland, Ohio, 2014. Waandamanaji walitawanywa kwa gesi za kutoa machozi muda wa amri ya kutotoka nje ulipoanza Ni katika ukumbi wa Lincoln mwaka 1963 ambapo Martin Luther King Jr alitoa hotuba yake maarufu ya "I have a dream" yaani nina ndoto. Dakika 15-20 kabla ya muda wa kusalia ndani kuanza waandamanaji walianza kuondoka. Trump atoa heshima kwa mkuu wa polisi aliyepiga risasi Wakati hayo yakijiri Rais Donald Trump ametoa heshima kwa David Dorn, mkuu wa polisi mweusi aliyepigwa risasi wakati wa maandamano katika eneo la St Louis, Missouri. Dorn, 77, alipatikana amekufa mbele ya duka la moja ambalo liliporwa saa za asubuhi Jumanne. Alistaafu katika kituo cha polisi cha St. Louis, 2007, na tagu wakti huo amekuwa akihudumu kama mkuu wa polisi kwenye mji huo mdogo, kwa mujibu wa shirika la habari la ABC News. Trump alisema: "Heshima yetuni kwa familia ya David Dorn, msimamizi bora wa kituo cha polisi cha St. Louis." Rais alisema Dorn alipigwa risasi na kuuawa na waporaji hao". Hadi kufikia sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo, polisi imesema. Maandamano juu ya kifo cha raia mweusi wa Marekani George Floyd bado yanaendelea kwa usiku wa nane mfululizo. text: Mara kwa mara wahamiaji hupitia pwani ya Libya kuingia Ulaya Hatua hiyo ni kufuatia Italia kuonyesha mashaka katika jambo hilo. Macron amesema kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa ndani ya miezi miwili ijayo. Lakini Waziri mkuu wa Italia ,Paolo Gentiloni, amesema kuwa tatizo la ukimbizi haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kuwaondoa nchini humo. Macron anasema hatua hiyo itapunguza ongezeko la wahamiaji haramu Ulaya Umoja wa jumuiya ya Ulaya inapaswa kuchukua hatua ambazo zitaipatia uwezo Libya kuleta hali ya Amani. Waandamanaji wajenga ukuta kuwazuia wahamiaji Ufaransa Italia kuzuia kuingia kwa wahamiaji katika pwani zake Gentiloni pia amesema kuwa wiki ijayo wanatarajia kuwasilisha muswada bungeni utakaowapa mamlaka Italia kutumia vyombo vya majini kukabiliana na wahalifu ndani ya Libya. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametoa mapendekezo ya kuweka vituo nchini Libya ili kutekeleza mahitaji ya raia wanaomba hifadhi nje ya taifa hilo. text: Mafuta hupimwa kwa chupa kisiwani Mafia kisha kuuzwa kwa bei ya juu kuliko maeneo ya karibu kama Dar es salaam Tanzania. Mafuta hayo hupimwa kwa chupa kisha kuuzwa kwa bei ya juu kuliko maeneo ya karibu kama Dar es salaam. Wauzaji wanasema sababu kuu ya hali hiyo ni kutokua na usafiri wa kuaminika wa kuingia na kutoka kisiwani humo. Wauzaji hufunga safari kutoka Mafia hadi maeneo ya karibu kama Dar es salaam na pwani kisha hununua mafuta katika sheli za mafuta kama watu wengine wenye magari wanavyofanya, wao huweka kwenye mapipa na kusafirisha kwa mashua hadi kisiwani mafia. Wauzaji hufunga safari kwa mashua kutoka Mafia hadi maeneo ya karibu kama Dar es salaam kununua mafuta Kwa kawaida hununua mafuta kama petrol kwa dola moja ya marekani kwa lita moja kisha huongeza pesa kidogo kwa wanunuzi yanapofika mafia. Mashua hizo huweza kuchukua siku kadhaa kutokana na hali ya upepo wa bahari na wauzaji wa mafuta hayo wanasema kuna uwezekano wa mapipa kupasuka katika mashua hizo hivyo hupata hasara. Katika vibanda katika eneo hilo wauzaji wengi wamekua wakiogopa kuzungumza kutokana na kutojua hatma ya kazi yao, ingawa wamekua msaada mkubwa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri. Mmoja wa wauzaji, Abdalah Mohamed anasema kuwa gharama wanayonunua mafuta na kuuza, wanapata faida kidogo sana kutokana na gharama ya usafirishaji huo wa mafuta. Vibanda vya kuuza mafuta kama hivi vimekuwa msaada mkubwa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri ''tunayavusha katika bahari na bahari kuna wakati inakua inachafuka, vitu vinapinduka lakini sasa ndio kazi hiyo'' Anasema bwana Abdallah Wategemeaji wa mafuta kuendesha kazi zao, kama wamiliki wa taxi na bajaji, wanasema mafuta huchukua muda mrefu kufika hivyo biashara zao huweza kuathirika. Bakari ismail ni dereva wa Tax anasema kuwa amewahi kusimamisha Bashara yake kutokana uhaba wa mafuta. ''Nimewahi kupaki gari wa muda wa siku nne, wateja wananipigia simu nawaambia kuwa sina mafuta hadi nilivyopata mafuta nikaendelea na biashara'' Visiwa vya Zanzibar ambavyo havina shule za sekondari Serikali imewezaje kuruhusu mafuta kuuzwa kwa namna hii? Mkuu wa wilaya ya Mafia, Shaibu Nnondoma anasema kuwa wameruhusu wauzaji hawa wa mafuta katika vibanda kutokana na usafiri wa mashua hauwezi kuleta mafuta kwa wingi, hivyo wafanya biashara hawa wamekua na umuhimu mkubwa katika upatikanaji wa mafuta kisiwani hapa. ''Wafanyabiashara wadogo wadogo wananua kwa bei ya kawaida na wanakuja kuuza hapa, tumewaruhusu wauze kwa bei ya soko itakavyowaruhusu kwasababu akiuza bei ndogo sana hawezi kupata faida na wanasaidia sana wakazi wa hapa''amesema Nnondoma. Hata hivyo hapo awali walikua wanauza karibu na makazi ya watu , lakini uongozi wa kisiwa hiki uliwahamishia mbali na makazi ya watu. Kisiwani Mafia Tanzania, Mafuta ya petrol na dizeli huuzwa kwa reja reja katika vibanda, huku kukiwa hakuna sheli ya mafuta kwa ajili ya mahitaji ya matumizi ya watu wenye vyombo vya usafiri kisiwani humo. text: Sineenat Wongvajirapakdi, akiendesha ndege ya kivita Sineenat Wongvajirapakdi, mwenye umri wa miaka 34, anaonekana akiendesha ndege ya kivita , akiwa amevalia magwanda ya vita na kufyetua bunduki. Wadhifa wa 'consort' aliopewa Sineenat hutolewa na mfalme kwa mkewe au na Malkia kwa mumewe. Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 67, alimpa heshima hiyo Sineenat mnamo Julai, miezi miwili baada ya kumuoa Malkia Queen Suthida, mkewe wa tatu. Sineenat ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika karibu karne nzima, shirika la habari la AFP linaripoti. Sineenat Wongvajirapakdi akishiriki katika hafla ya kuteketeza mwili wa marehemu mfalme Bhumibol Adulyadej Mtandao uliokuwa na picha hizo ulikabiliwa na matatizo baadaya watu wengi kujaribu kuingia kuzitazama pica hizo kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. Wasifu wake umechapishwa karibu napicha hizo zake. Mfalme Maha Vajiralongkorn akimshikilia mbwa akiwa karibu na Sineenat Wongvajirapakdi Katika taarifa yake, Kasri la Thailand linasema mfalme "aliagiza kuundwa kwa maelezo ya maisha ya kifalme" ya Sineenat, ambaye ni rubani wa kusomea, mhudumu wa afya na mlinzi binafsi. Malkia Suthida - aliye na miaka 41- ni mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kitengo cha ulinzi wa mfalme - ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na ameonekana hadharani naye kwa miaka mingi. Alitawazwa kuwa mfalme baada ya babake kufariki mnamo 2016. Mfalme anaonekana akimwaga maji ya baraka kwenye kichwa cha Malkia Suthida Sineenat Wongvajirapakdi akilenga silaha Picha adimu za mkewe mfalme wa Thailand aliyepewa wadhifa hivi karibuni zimetolewa na kasri, na inaarifiwa kusambazwa pakubwa mitandaoni. text: Ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ambao uliifanya kenya kuwa katika picha tofauti ulichangia kujipatia alama 48. Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Dar imeshuka nafasi saba katika kipindi cha mwaka mmoja , na kupata alama 45 kwa jumla ikilinganishwa na alama 53 katika utafiti wa awali ambao ulikuwa umeiweka juu ya mataifa yote sita ya jamii ya Afrika mashariki EAC. Lakini 'Uhuru' katika ripoti hiyo ya dunia 2019 iliotolewa siku ya Ijumaa unaonyesha kwamba Kenya ilio na alama 48 ndio inayoongoza katika uhuru wa kisiasa miongoni mwa mataifa ya Afrika mashariki. Kulingana na gazeti hilo Kenya ilijipatia alama kama hizo katika ripoti iliotolewa ya 2018. Kulingana na ripoti hiyo Burundi ina alama 18 na imetajwa kuwa taifa la mwisho lenye uhuru wa kisiasa ikifuatiwa na Rwanda yenye alama 23 na Uganda ilio na alama 37. Hatahivyo licha ya tofauti hiyo ya alama , Tanzania na Kenya ni miongoni mwa mataifa yaliopo katika orodha yenye na uhuru mchache wa kisiasa katika utafiti huo. Orodha nyengine ni zile za mataifa yalio 'huru' na yale 'yasio huru' huku Uganda, Burundi na Rwanda zikiorodheshwa miongoni mwa mataifa yasio na huru kisiasa. Utafiti huo uliofanywa na shirika la Freedom House, hatahivyo umeiweka Tanzania miongoni mwa mataifa 10 inayoyaangazia mwaka 2019 . Kulingana na The Citizen Tanzania , Freedem House ni shirika huru lililo na makao yake nchini Marekani linalopigania uhuru na demokrasia duniani. Mbali na Tanzania , mataifa mengine yaliopo katika rada yake ni pamoja na Armenia, Brazil, Cambodia, Cameroon, China, Ethiopia, Iraq, Poland na Sri Lanka. Freedom House linasema kuwa mataifa yalio katika orodha hiyo ni yale ambayo yalipata maendeleo ambayo yaliathiri mwelekeo wake wa kidemokrasia. Ukamataji wa viongozi wa upinzani Tanzania Ripoti hiyo inasema kuwa kushuka kwa Tanzania kunashirikishwa na serikali yake kukamata viongozi wake wa upinzani, kuzuia maandamano dhidi ya serikali na kuweka sheria ambazo zinaimarisha nguvu za chama tawala katika siasa za mashinani 2018. Uganda ilishuka kutoka taifa lenye 'Uhuru kiasi' hadi lile lisilo na Uhuru kutokana na jaribio la rais Yoweri Museveni kuzuia uhuru wa bkujieleza , ikiwemo uchunguzi kupitia vyombo vya mawasiliano mbali na ukandamizaji kupitia kuiwekea kodi mitandao ya kijamii. Ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ambao uliifanya Kenya kuwa katika picha tofauti ulichangia kujipatia alama 48. Ripoti hiyo vilevile inaishirikisha Rwanda na ukamataji wa viongozi wa upinzani pamoja na tishio linalotolewa kwa vyama hivyo na rais Kagame. Pia inasema kuwa uongozi wa Kagame wa kiimla umeathiri vibaya demokrasia nchini humo. Nchini Burundi , inasema kuwa uongozi wa rais Pierre Nkurunziza umeendelea kuwanyamazisha wapinzani na kukiuka katiba. Tanzania imepoteza nafasi yake kama taifa lenye uhuru wa kidemokrasia katika eneo la Afrika mashariki kwa Kenya na sifa yake sasa inaonekana kwamba inashindana na maeneo yenye hatari kisiasa duniani , ripoti mpya imesema. text: Rais wa LSK Isaac Okero Rais wa LSK Isaac Okero katika taarifa siku ya Jumamosi alimkosoa rais Kenyatta kwa kumtaja jaji mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa ''wakora''. Rais Kenyatta alitoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufutilia mbali uchaguzi wake. Bwana Okero alisema: Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais Uhuru Kenyatta achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya. Amesema kuwa rais Kenyatta anapaswa kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama. Bwana Okero amesema kuwa ijapokuwa rais huyo ana haki ya kutoa maoni yake anafaa kutoa maoni yanayostahiki. ''Haki yake inafaa kuheshimu, kukubali na kulinda haki za jaji mkuu na kila jaji wa mahakama ya juu chini ya kifungu cha sheria cha 28''. ''Matamshi hayo yanakiuka na yanashutumiwa na chama cha mawakili Kenya LSK'', aliongezea. Kiongozi huyo wa LSK amesema kuwa mahakama hiyo ilifanya wajibu wake na kuwaonya viongozi wengine dhidi ya kuwatishia majaji. Mahakama ya juu inayoongozwa na jaji Maraga ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kutokana na dosari iliotekelezwa na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC. Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake. text: Ndege za Israel zashambulia kiwanda cha silaha nchini Syria Taarifa za jeshi zilisema kuwa makombora yaliyofyatuliwa kutoka anga ya Lebanon yalilenga kiwanda hicho kilicho karibu na Masyaf na kuwaua wanajeshi wawili. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kiwanda ya kutengeneza silaha za kemikali kilishambuliwa Israel yashambulia ngome ya Syria Israel: Iran inajenga kiwanda cha makombora Syria Israeli ambayo imefanya mashambulizi kadha kwenye viwanda vya silaha nchini Syria awalia haijasema lolote. Kisa hicho kinatokea siku moja baada wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kusema kuwa serikali ya Syria ilihusika na shambulizi la silaha za kemikali katika mji unaoshilkiliwa na waasi mwezi Aprili. Ndege za Israel zashambulia kiwanda cha silaha nchini Syria Takriban watu 83 waliuawa katika mji wa Khan Sheikhoun na Styria imekana kutumia silaha za kemikali. Ujasusi wa nchi za magharibi unasema kuwa Syria inandelea kuunda silaha za kemikali. Isarel inaripotiwa kuendesha mashambulizi ya ndega maeneo yanayotajwa kutumika kuunda silaha za kemikali miaka ya hivi karibuni. Hivi karibuni Isreal iliishitumu Syria kwa kuruhusu hasimu wake Iran kujenga viwanda vya makombora nchini humo na inasema inalenga kuzuia kupelekwa kwa silaha kutoka Syria hadi kwa wanamgambo wa Lebanon, Hezbolllah. Syria inasema kuwa ndege za jeshi la Israeli zimeshambulia kituo cha kijeshi magharibi mwa nchi huku ripoti zikiseka kuwa kiwanda cha silaha za kemikali zilishambuliwa. text: Tiziana alijikatisha uhai baada ya video zake za ngono kusambaa mitandaoni Mwezi Aprili mwaka 2015, mwanadada kutoka Mugnano, nje kidogo mwa Naples,alituma picha za video za ngono kupitia WhatsApp. waliopokea video hizo miongoni mwao ni rafiki yake wa kiume Sergio Di Palo, ambaye mahusiano yake naye hayakuwa mazuri. Video hizo zilimuonesha Tiziana akifanya vitendo vya ngono na wanaume kadhaa ambao hawakufahamika. ''Alikuwa mrembo lakini mwenye kuvunika oyo upesi,''alikumbuka Teresa Petrosino ambaye walikua marafiki kwa miaka 15.''Alikuwa na watu wasiofaa kwa wakati usiofaa.'' Video hizo zilisambazwa kwenye tovuti mbalimbali zinazoonyesha masuala ya ngono.Vitendo vyenyewe kwenye video hizo havikua kitu isipokua sentensi moja tu kutoka mdomoni mwa Tiziana Conte ''Unarekodi video?'' alimuuliza mwanaume aliyekuwa ameshika Kamera. ''Safiiii''. Msichana ajiua kwa sababu ya hedhi India Muuaji aliyeonekana Facebook ajiua Maneno hayo yaliashiria kuwa mwanadada huyo anapenda kupigwa picha wakati akifanya ngono.Sentensi hiyo ilifanya watazamaji waendelee kuitazama bila wasiwasi:Kama alikua anafurahia kupigwa picha, bila shaka hatachukia watu wakiitazama. Lakini waitaliano walifanya zaidi ya kutazama.Watazamaji walitumia maneno yake kwa msisitizo wakatengeneza t-shirt ambazo ziliwekwa picha yake na pia kwenye tovuti. Hakuna aliyekuwa akifikiria kuwa Tiziana asingependa, kwa kuwa alionekana kufurahia kwenye video hizo. Lakini mambo hayakua hivyo. ''Watu huchanganya kukubali jambo na jambo hilo kusambaa zaidi,'' anaeleza mtaalamu wa masuala ya mitandao Selvaggia Lucarelli. ''Unaweza kupiga picha ya video, ukawaonesha watu kadhaa,lakini kunakua na makubaliano kuwa watu hao wasisambaze zaidi.'' Mapambano ya kisheria Tiziana Cantone, aligopeshwa sana na hali hii. ''Mimi na yeye hatukuwahi kuongea kuhusu kilichomo kwenye video.'' alisema rafiki yake Teresa.''Sikuwahi kuziona, na sikutaka kuziona.Unaweza kuona alikuwa akisumbuka mno.''Lakini alikuwa na nguvu.'' Bi Cantone akaamua kupambana.Lakini hakukua na njia ya haraka ya kufanya ili kuondosha video hizo. Aliipeleka kesi mahakamani, akidai kuwa video hizo zilipelekwa kwenye mitandao bila ridhaa yake.Lakini mpaka wakati huo hakuweza kuishi maisha ya kawaida. ''Hakutaka kutoka nje akiogopa watamuona.'' Alieleza Teresa. ''Alielewa kwa kiasi fulani kuwa hali hii haiwezi kutatulika;kuwa mume wake,watoto wake wanaweza kuziona video hizo siku moja;na kuwa video hizo hazitaondoka mitandaoni.'' Mama wa Tiziana anapambana kurudisha heshima ya mtoto wake Ilimchukua wiki kadhaa Mama yake Teresa Giglio kupata nguvu kuwaambia wanahabari kuhusu maisha ya binti yake. ''Binti yangu alikua na tabia njema lakini pia alikua na mapungufu yake,'' aliiambia BBC. ''Hakua na mapenzi ya baba, tangu alipozaliwa.Hakuwahi kumuona baba yake.Hii iliathiri maisha yake.'' Mama na mwana waliishi pamoja.Katika kipindi cha furaha, Tiziana alipenda kusikiliza wanamuziki wa Italia, kusoma vitabu vya simulizi, kupiga kinanda.Lakini baada ya video kutapakaa mitandaoni hali hiyo haikuwepo tena. ''Maisha yake yaliharibika, mbele ya kila mtu,'' alisema mama yake.''Watu walimfanya kichekesho,akaitwa majina mabaya ya aibu.'' Mwezi Septemba, Mahakama ya Naples iliamuru video hizo zitolewe mitandaoni na kwenye tovuti.Lakini ilimtaka Tizianz alipe faini ya dola 21,600 za marekani, gharama za huduma za kisheria.Fedha ilikua nyingi sana. Tarehe 13 mwezi Septemba mwaka 2016, Maria Teresa Giglio alikwenda kazini, akiwa amemuacha binti yake nyumbani. Bi Giglio alipokea simu kutoka kwa wifi yake ,sauti ikiwa ya kupoa sana ikimtaka arejee nyumbani. Aliporejea alikuta Polisi, gari ya kubeba wagonjwa, ''haraka nikaelewa''alisema , huku akilia. ''Siku alipokufa maisha yangu yalikomea hapo.'' Mama wa Tiziana anataka kufahamuu ukweli kushusu sakata la kifo cha binti yake Nani aliweka video Mtandaoni? Kitendo cha Tiziana Cantone kujitoa uhai, kilifanya video hizo zifuatiliwe na watu wengi zaidi kuliko kusahaulika. Mama yake alijilazimisha azitazame video hizo. ''Nilitaka kuona kila kitu ili niweze kuuelewa ukweli.'' huyu hakua Tiziana wangu'' alishawishika kuwa binti yake alikua anatumia dawa za kulevya. Bi Giglio amemtaka mpenzi wa zamani wa binti yake, Di Pialo, kueleza hasa alishiriki vipi katika mpango wa kusambaza video zile. ''Hakunisaidia kuokoa maisha yake.Lakini labda anaweza kunisaidia kupata ukweli. Pengine haikuchukua muda mrefu kwa Tiziana Cantone kuanza mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kujikatisha uhai text: Wayne Rooney amefungia Everton mabao mawili na kusaidia ufungaji wa bao moja msimu huu Amesema mchezaji huyo "atachukuliwa hatua" kwa kufuata utaratibu wa klabu. Rooney alikamatwa muda mfupi baada ya saa nne usiku saa za Uingereza usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya polisi wa Cheshire kusimamisha gari lake aina ya VW Beetle eneo la Wilmslow. Nahodha huyo wa zamani wa England aliachiliwa huru kwa dhamana ana anatarajiwa kufika katika mahakama ya hakimu ya Stockport baadaye mwezi huu. Mchezjai huyo wa miaka 31 alistaafu soka ya kimataifa Agosti, na bado ndiye mfungaji mabao mengi zaidi katika historia England. Kikao cha kusikizwa kwa kesi yake kimepangiwa kufanyika tarehe 18 Septemba siku moja baada ya Everton kusafiri kukabiliana na Manchester United mechi ya Ligi ya Premia. Mechi hiyo itakuwa ya kwanza wka Rooney kurejea Old Trafford tangu aliporejea katika klabu yake ya utotoni, ambayo alikuwa ameihama na kujiunga na United mwaka 2002. "Tulizungumza Jumanne na mwenyekiti Bill Kenwright amezungumza naye kuhusu hali yake," Koeman amesema. "Atachukuliwa hatua kwa kufuata utaratibu wa klabu wakati ufaao." Rooney amefunga mabao mawili na kusaidia ufungaji wa bao moja mechi saba alizochezea Everton msimu huu. Uchezaji wake umemfanya meneja wa England Gareth Southgate kumtengea nafasi kikosi chake kitakachocheza dhidi ya Malta na Slovakia. Wayne Rooney alivyofunga bao dhidi ya Gor Mahia Hata hivyo, Rooney, ambaye amefungia taifa lake mabao 53 katika mechi 119, amestaafu kutoka kwenye timu ya taifa. Meneja wa klabu ya Everton Ronald Koeman amesema "amesikitishwa sana" na mashtaka ya kuendesha gari akiwa mlevi ambayo yanamkabili mchezaji wake Wayne Rooney. text: Mabinti wakiwa katika nyumba salama Sheria ya Tanzania ilieleza mwaka 1998 kuwa shughuli za ukeketaji ni uhalifu, hata hivyo vitendo hivyo bado vinafanyika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania.Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu, mwanamke mmoja kati ya kumi wenye umri kati ya miaka 15-49 wamekeketwa. Vitendo hivi ambavyo vinatishia maisha hufanyika kipindi cha mapumziko ya mwishoni mwa mwaka ambapo mamia ya wasichana hukeketwa na mara nyingi hufuatiwa na ndoa. Vitendo hivi vinafanyika hasa kutokana na imani kuwa wasichana ni lazima kukatwa sehemu zao ili kupunguza vitendo vya uzinzi.Pia wasichana waliokeketwa hutolewa gharama ya mahari mara mbili zaidi ya wasiokeketwa. Lakini jitihada za kumaliza ukeketaji nchini Tanzania zimeongezeka, waathirika wa ukeketaji wanaongoza vita dhidi ya vitendo hivi vilivyopitwa na wakati. Wasichana wanaotunzwa katika nyumba ya matumaini wanaelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji Wakitambua kuwa wazazi wao au walezi wanajiandaa kuwapeleka kukeketwa,wasichana hukimbia makazi yao kuepuka kuuzwa na kuingia kwenye ndoa za utotoni. ''Nilikimbia nyumbani kwasababu nilishapata elimu kuhusu ukeketaji lakini pia nilifahamu kuwa ukeketaji una madhara makubwa.Hivyo walipotaka kuipeleka kukatwa sikupenda.Nilijaribu kuwaeleza ni insi gani vitendo hivi vilivyo vibaya, hawakunisikiliza ndio maana nilikimbilia sehemu iliyo salama ambapo nitaweza kulindwa''Anaeleza Neema mwenye miaka 12. Nyumba salama, tumaini kwa wasichana na wanawake', ambapo Neema na maelfu ya wasichana wengine waliokimbia nyumba zao na kuelekea hapo, inasimamiwa na mwanamke aitwaye Rhobi Samwelly. Wakati wa msimu wa kukatwa, Rhobi, akishirikiana na polisi na timu yake wanapambana na ukeketaji na wakati mwingine, huwaokoa wasichana na kuwakamata wazazi na mangariba. Jamii imekuwa ikishauriwa kuwalinda wasichana dhidi ya ukeketaji ''Kilichinivutia na kuanzisha nyumba hii ni kwa sababu nilitaka wasichana kulindwa.Wakati wa msimu wa kukatwa ambapo kunakuwa na harakati nyingi kwenye jamii, wasichana wanalazimishwa kukeketwa na hakuna wa kuwasaidia.Tumewaokoa wasichana wengi.Nilianza kufanya kazi kwenye nyumba salama moja iliyokuwa chini ya kanisa,na sasa tuna nyumba mbili na tumewaokoa wasichana zaidi ya 600, ambao walilindwa wasikeketwe''.Alisema Rhobi Nyumba hizi zinatoa eliu bure kuhusu mafunzo ya ufundi, kama vile ushonaji na Kompyuta.Wasichana wanaweza kutumia ujuzi wao mpya kupata kipato na kusaidia familia zao, pia wakijiimarisha uwezo wao wa kujitegemea. Baada ya msimu wa kukata kuisha hufanyika mkutano wa mapatano ambapo wazazi huamua kama watawachukua mabinti zao na kuhakikisha kuwa hawakeketwi, huku wasichana nao wakipata nafasi ya kueleza kama wanajisikia kuwa salama endapo watarejea nyumbani kwa wazazi wao UNFPA imekuwa ikimsaidi Rhobi na timu yake kuwapatia washauri nasaha ambao wanaongeza uwezekano wa kuwashawishi wazazi kuachana na vitendo vya ukeketaji. Baada ya uzoefu huu, wasichana wengi wataweza kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya Ukeketaji, lakini pia wataweza kutembelea shule mbalimbali na jamii kutoa elimu na kufanya kampeni kumaliza vitendo vya ukeketaji. Mabinti wadogo wa umri mpaka miaka minane, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania wanaongoza operesheni dhidi ya ukeketaji kwenye jamii zao. text: Mtoto wa wiki sita amekufa kutokana baada ya kulala na mama yake kitanda kimoja Rowan Leach mwenye umri wa miaka 20, ambaye alikuwa akimlea mtoto wake peke yake alibaini kifo cha mtoto wake mara baada ya kuamka saa sita usiku kumnyonyesha mtoto huyo na kumkuta hapumui. Mama huyo aliwaelezea wapelelezi wa chanzo cha kifo cha mtoto wake wakati akisubiri huduma ya dharura ikamilike. "Kifo cha mtoto wangu kimenisikitisha sana"Bi.Leach ambaye alimpoteza mtoto wake Hadley alieleza. Licha ya kwamba mtoto huyo alikimbizwa hospitalini,wahudumu wa afya walishindwa kuokoa maisha ya mtoto huyo hivyo kufariki majira ya alfajiri mwezi septemba mwaka jana. Rowan Leach akiwa na mtoto wake Hadley wakati wa uhai wake Bi.Leach kutoka Southampton alikuwa anamlea mtoto wake kwa usaidizi wa mama yake. Alielezea hali ilivyokuwa kabla ya mtoto wake kufariki,mama huyo anasema alipitiwa na usingizi mara baada ya kumchukua mtoto wake na kumfunika kwa koti lake kwa sababu kulikuwa na baridi kali na lengo lake lilikuwa ni kumnyonyesha baada ya muda. Jane: Nina masponsa wawili na sioni tatizo "Nilishangaa kumkuta mtoto wangu yuko upande wa pili wakati alikuwa amelala upande mwingin," Bi.Leach alieleza. Mazishi ya mtoto Hadley Mchunguzi mkuu Grahame Short ambaye hakuweza kuelewa kwa haraka chanzo cha kifo cha mtoto huyo kilitokeaje lakini alisema hamlaumu mama huyo kuwa mzembe. Aliongeza kwa kudai kwamba huwa anawaonea huruma akina mama ambao wanahudumia watoto peke yao bila ya kuwa na wenza wao. Vilevile uchunguzi uliofanywa haujaleta hali yeyote iliyotiliwa mashaka maelezo ya mama huyo ya namna mtoto wake alivyokufa. Takwimu zinaonesha kwamba idadi wa watoto 133 wamefariki katika miaka mitano iliyopita kutokana na tabia ya akina mama wanaolala na watoto wao ,kwa mujibu wa data za elimu. Mama mmoja ametoa onyo kwa akina mama ambao huwa wanalala na watoto wao mara baada ya mtoto wake wa kiume mwenye wiki sita kufa na ripoti ya uchunguzi wa kifo cha mtoto wake kubainisha hivyo pia. text: Kurasa hiyo ya As Roma itakuwa ikiandika habari zake kwa lugha adhimu ya kiswahili. Ukurasa huo wa lugha ya kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanatumia lugha ya kiswahili. Mwisho wa Twitter ujumbe, 1 Akaunti hiyo ya Twitter imezinduliwa siku ya jumatano kwa video yenye maneno ya utani ya kiswahili. Akaunti hiyo imepokelewa vizuri na wasomaji wa kiswahili wa Tanzania na Kenya. Wengi wakiona kuwa ni ubunifu mzuri ambao unaonesha kuwajali mashabiki wanaoongea lugha ya Kiswahili. Idadi kubwa ya watu wameanza kufuatilia kurasa hiyo na kujibu kwa kiswahili. Rais wa klabu hiyo Jim Pallotta ametumia kurasa yake binafsi ya tweeter kuthibitisha kuwa kurasa hiyo imefunguliwa. "Tuna furaha kuzindua kurasa ya kiswahili ya AS Roma", mkuu wa mipango Paul Rogers alieleza. Uzinduzi huo umekuja mara baada ya kuzinduliwa kwa akaunti ya Pidgin Mchezaji wa As Roma, Juan Jesus Uzinduzi huu umekuja baada ya maombi ya mashabiki kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika ya kati na mataifa mengine ya mashariki na kusini mwa Afrika. Mapenzi ya soka la ulaya kutoka ukanda huu wa Afrika unastaajabisha kwa nini klabu za mpira za nje ya bara hilo kushindwa kuwasiliana kwa lugha ya kiswahili au Pidgin kabla ya mitandao ya kijamii. "Kurasa hii ya Twitter itaturahisishia mawasiliano ya moja kwa moja na mashabiki wetu kwa namna ya kwao, ni mkakati ambao tunataka kuondoa vizuizi". Akaunti mpya ya kiswahili ya AS Roma inawasiliana kwa lugha 14 tofauti katika mitandao ya kijamii. Kuna kurasa nyingine rasmi za lugha ya kiitaliano, kiingereza, kiarabu,kifaransa, kireno, kichina, lugha ya Uturuki, Bosnian, , Dutch, Farsi na Pidgin. Klabu ya mpira ya 'As Roma' nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza kutoka barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter. text: Jamii hulaumiwa kwa kuchangia kuongezeka kwa msukumo wa mabinti kuolewa Sheria hiyo ambayo inajumuisha upigaji marufuku wa ndoa za kulazimishwa, inafuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni juu ya kiwango cha udhalilishaji wanawake. Utafiti mmoja uliofanywa nchini humo, umeonesha kuwa wanawake sita kati ya 10 nchini Morocco wamepitia manyanyaso hayo. Matukio ya ubakaji ya hivi karibuni yametangazwa sana katika mitandao ya kijamiii. Mwandishi wav BBC mjini Rabat amesema sheria hiyo mpya imepokelewa vizuri lakini pia imekosolewa kwa sababu haitoi maana kamili ya unyanyasaji majumbani au marufuku katika vitendo vya ubakaji ndani ya ndoa. Kwa mujibu wa sheria hiyo, wale wote watakaotiwa hatiani kwa makosa ya kudhalilisha kingono hadharani iwe kwa kutumia maneno, ama ishara yoyote ya kudhalilisha kijinsia atakabiliwa na hukumu ya kifungo kuanzia mwezi mmoja mpaka sita gerezani na pia faini ya fedha taslimu Mashirika ya haki za binadamu yanasema kuwa wanawake wengi nchini Morocco wamekuwa ni wahanga wa matukio ya unyanyasaji kingono. Picha hii ni ya mwanamke aliyebakwa na kulazimishwa kuchorwa michoro mwilini na wabakaji Katika ripoti yake ya mwaka 2015, Shirika la Haki za Binadamu nchini humo limearifu kuwa zaidi ya asilimia 20 ya wanawake nchini Morocco wamekumbwa na matukio ya unyanyasaji wa kingono japo mara moja katika maisha yao Katika siku za hivi karibuni polisi nchini humo iliwakamata vijana 12 kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 17 na kumtesa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Duniani kote inakadiriwa kuwa wasichana milioni 51 waliyo chini ya umri wa miaka 18 wameolewa. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, ndoa za umri mdogo zimekithiri Afrika Mashariki na Asia ya Kusini . Inakadiriwa kuwa kufikia muongo mmoja ujao zaidi ya wasichana milioni 100 watakuwa wamekumbwa na ndoa za umri mdogo. Ni Sababu zipi zinazochangia ndoa za lazima? Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazochangia kuenea kwa ndoa za lazima katoka jamii. Kwa mujibu wa watetezi wa haki za binadamu ndoa za lazima ni ukiukaji wa haki za binadamu. Ndoa za aina hii kwa kawaidi huhusisha 82% ya wasichana au wanawake ambao wanalazimishwa na wazazi au familia zao kuolewa. Hali ikoje Tanzania: Kwa mujibu wa chama cha waandishi wanawake nchini Tanzania, TAMWA, taifa hilo ni moja ya nchi zilizokithiri ndoa za umri mdogo duniani. Kwa wastani, wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kutimiza miaka 18. Mnamo 2010, 37% ya wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 walioolewa kabla ya kufikia miaka 18. Hatahivyo hali hiyo imebadilika huku takwimu zinzonyesha kwamba visa vimepungua kwa 10% tangu mwaka 2004 ambapo viwango vilikuwa 41%. Betty Masanja, wakili na mwanaharakati wa masuala ya kijamii nchini Tanzania anasema ''Ndoa za lazima zipo sana miongoni mwa jamii ya watanzania. Kuna baadhi ya jamii zinahisi mtu asipoolewa anakosa heshima fulani.Sasa wazazi wanajihisi vibaya kama biti yao ametimiza umri wa kuolewa na bado yuko nyumbani''. Betty pia anasema sheria ya ndoa ya mwaka 1971 haiwalindi wasichana dhidi ya kuolewa mapema. ''Sheria hii imekuwa ikipigiwa kelele ifanyiwe marekebisho kwa mda mrefu. Sheria hii inaruhusu wasichana wenye miaka 14 kuolewa kwa ( ruhusa maalum ya wazazi), inaruhusu wasichana wenye umri kuanzia miaka 15 kuolewa iwapo umbile lao linaonekana kubwa. Hali hii ina athari kwa maendeleo ya Taifa''. Wanaharakati wa masuala ya kijamii wanasema ndoa za umri mdogo ni aina ya ubaguzi wa kijinsia ambao unawagusa wasichana wadogo na kuwafanya wasiendelee na elimu. Ubaguzi huo unawafanya wawe waathirika wa kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa urahisi wakilinganishwa na wenzao ambao hawajaolewa; na hakuna uwezekano wa wasichana hao walioolewa kupanga uzazi. Ndoa za umri mdogo ni suala la afya pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu, kwani wasichana walioolewa katika umri mdogo wana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na maradhi ya fistula na vifo vya kina mama kwani miili yao inakuwa bado haijawa na uwezo wa kuhimili mzigo wa kuzaa. Hali katika mataifa mengine Duniani Serikali ya Uingereza iliharamisha ndoa ya lazima nchini humo mnamo 2012. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kumlazimisha mtu kuoa au kuolewa bila ya hiari yao ni uhalifu Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini. Inakadiriwa kuwa kuna kati ya waathiriwa 5000 - 8000 waliolazimishwa kuoa au kuolewa nchini Uingereza. Wasichana wengi wanaolazimisha kuolewa wana umri wa chini ya miaka 21 lakini kuna ripoti kuwa wasichana wa hata umri wa miaka 15 hulazimishwa kuolewa. Familia nyingi zinazotuhumiwa kutekelaza uhalifu huo zinatoka mataifa ya bara Asia hususan taifa la Pakistan. Katika baadhi ya majimbo nchini Marekani, ndoa ya lazima ni uhalifu. Katika majimbo hayo watu wanaomlazimisha mtu kuoa au kuolewa huwa wamekiuka sheria, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji majumbani ukiwemo wa kingono, utekaji nyara na kadhalika. Nini kifanyike kupambana na ndoa za lazima Umoja wamatiafa unasisitiza umuhimu wa kuzingatia elimu endelevu kwa kutumia vyombo vya habari, utafiti, mabadiliko ya sheria na mikutano ya kijamii. Kadhalika ipo haja ya kuhamasisha viongozi wa kijamii kuhusu athari za ndoa za lazima na sheria zilizopo. Sekta ya afya inmetaja kuwa na jukumu kuu la kuwahamasisha wananchi kuhusu athari za ndoa za umri mdogo. Kuwahusisha katika mjadala huu viongozi wa dini katika kuielimisha jamii, na pia wazazi, katika kushirikiana na serikali kukomesha ndoa za aina hii. Sheria mpya ambayo inafanya unyanyasaji wa kingono na Udhalilishaji kuwa ni Uhalifu itaanza kutekelezwa nchini Morocco hivi karibuni. text: Kuna wale ambao hutumia muda mwingi kusafiri au kubisha milango ya ofisi moja hadi nyingine kutafuta kazi. Wataalamu wa masuala ya kazi wanasema mbinu hiyo ya kutafuta kazi imepitwa na wakati. Hii ni kwa sababu teknolojia mpya ya mawasiliano imebadilisha mambo mengi duniani ikiwa ni pamoja na jinsi kazi zinavyotafutwa. BBC imezungumza na Mwikali Muthiani ambaye ni mshauri wa masuala ya ajira nchini Kenya kuwapatia vidokezo vijana waliohitimu na ambao hawana kazi. Mwikali anasema kuna kazi nyingi ambazo zimeibuka kutokana na uwepo wa teknolojia ya dijitali. Kampuni nyingi zimeng'amua umuhimu wa mitandao hiyo kwa biashara zao. ''Zamani ulikuwa unaulizwa ulikuwa mzuri kwa kitu gani ulipokuwa shule na kitu hicho ndicho kilitoa mwongozo wa kile utakachosomea chuo kikuu au taasisi ya kiufundi lakini katika ulimwengu wa sasa mambo yamebadilika'' anasema Mwikali. Aidha ameongeza kuwa ni vyema kusomea kozi kwa mfano ya udaktari, uwakili, uhandisi, na uwanahabari miongoni mwa zingine lakini pia ni vyema kufahamu mazingira ya sasa ya kazi hasa za kidijitali ''Kazi hizi zinatarajiwa kuimarika na kuwa kubwa mwaka huu wa 2019. Vijana wanaotafuta kazi baada ya kuhitimu vyuo vikuu wanashauriwa kutoangazia ajira zilizo zoeleka tu kama vile uhandisi, uwakili, uwalimu au udaktari. Kwa kujiandaa vilivyo na kuwa na ujuzi wa ziada unaohitajika, unaweza kujiajiri au kujitengenezea kipato cha ziadi ikiwa umeajiriwa. Waajiri wanatafuta nini? Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa LinkedIn unaowaleta pamoja waajiri na waajiriwa hizi ndizo sifa zinazolengwa na waajiri mwaka 2019. Sifa hizi pia zikitumiwa vizuri na vijana wataalamu wa masuala ya ajira wanasema inaweza kuwasaidia kupata nafasi za ajira katika ulimwengu wa dijitali unao waleta watu pamoja kupitia mitandao ya kijamii. Usimamizi wa mitandao wa kijamii Mtandao wa kijamii wa Facebook una watumiaji bilioni 1.79, Twitter ina zaidi ya watumiaji milioni 317, Instagram ina zaidi ya watumiaji zaidi ya milioni 500 na WhatsApp ina zaidi ya watumiaji bilioni Moja. Kwa ufupi ikiwa mitandao hii ya kijamiii ingelikuwa nchi bila shaka ingelikuwa nchi iliyo na watu wengi zaidi duniani. Kwa mujibu wa Mwikali Muthiani mshauri wa masuala ya ajira, mashirika mengi yameng'amua umuhimu wa mitandao hiyo kwa biashara zao. Japo wazazi wanaweza kushangaa kwanini watatoto wao wanachukua muda mwingi kutumia mitandao ya kijamii huenda ikatoa nafasi za kazi hasaa mtumiaji akiwa makini na kuitumia kwa njia ya ubunifu. Vijana waliyohitimu wanapotafuta kazi ya uhasibu, uwakili au uhandisi pia wanashauriwa kutafuta kazi za usimamizi wa mitando ya kijamii ya makampuni na biashara kubwa ambazo zimeonekana siku hizi kukumbatia majukwaa haya kuendeleza biashara hiyo. Kazi ya kublogu. Watu wengi siku hizi wamefungua blogu zao wenyewe na kufanya kazi majumbani mwao. Ikiwa wewe ni mpenzi wa kufanya utafiti na kuandika basi huenda kazi hii ikakufaa na pia kukuletea kipato. Pia unaweza kutoa ushauri wa kile ulichosomea kwa wale waotazamia kuchukua somo hilo. Kuunda Programu Tumishi ama app Kuna App za karibu kila kitu siku hizi. Kwa mfano Google play store ina apps milioni 2.2 huku Apple app store ikiwa na apps milioni 2. Hii inaashiria kuwa apps hizi ni maarufu sana duniani na zitaendelea kuongezeka. Ukiwa na ujuzi wa kuunda app hizi bila shaka utapata nafasi ya kazi. Mchambuzi wa data Katika miaka kumi ililiopita mashirika yamekuwa mbioni kufanya utafiti wa namna ya kujiimarisha kibiashara. Baadhi ya mashirika hayo yanatafuta watu walio na ujuzi wa kuchambua data na kuwasilisha maelezo kwa ufasaha kwa ajili ya kuimarisha biashara zao. Mtaalamu wa usalama wa habari Kazi yake ni kuhakikisha anailinda usalama wa mtandao na app za makapuni na watu binafsi kuhakikisha zipo salama dhidi ya wadukuzi. Huku ulimwengu ukiendelea kupanuka kidigitali kazi za wataalamu hawa itaendela kuongezeka. Mtaalamu wa Utafutaji wa Teknolojia ya Kutafuta (SEO) Intaneti ina zaidi ya mitandao bilioni moja na mingine mingi inaendelea kubuniwa. Japo kila mtandao unawalenga watu maalum kila mmoja angelipendelea mtandao wake uonekane mtu anapotafuta kitu kinachohusiana na taaluma yake. Kuwa na mtandao uliyo na habari nzuri haitoshi unahitaji kuwekeza katika vitu ambavyo vitaufanya ukurasa wako kuwa maarufu kwa kuhakikisha Google inauorodhesha kwa kiwango cha juu. Unahitaji mtaalamu wa SEO aliye na uwezo wa kuchambua mtandao wako na kukushauri vitu vinavyohitajika kufanya ili kuimarisha mtandao wako. Mtaalamu wa kuhifadhi data mbadala. Kazi hii inahusisha kuhifadi kazi nje ya hardrive ya komputa yako ya kazi ili kuwawezesha watu wengine kuzifikia bila kutumia kompyuta. Hii ni teknolojia mpya inayoendelea kukua hasa ikizingatiwa kuwa kampuni nyingi zimeanza kutoa huduma zao nje ya mahali pao pa kazi, wafanyikazi wao wanahitaji kuwezeshwa kufikia taarifa muhimu za wakati wowote kutoka sehemu yoyote. Vijana wengi wanapohitimu wanatarajia kupata kazi ambazo wamesomea lakini kutokana na ukosefu wa ajira wanaishia kufanya kazi ambazo hawakuzitarajia. text: Paka mwenye hasira Wengi wa wale wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea wako salama zaidi, na wenye uwezo mkubwa kwenye historia ya maisha ya mwanadamu. Sasa kwanini watu wengi wanaonekana na hasira wakati wote? Madereva wenye hasira za barabarani, kutoa kauli mbaya za hasira mitandaoni, wakati mwingine . Oliver Burkeman-Mwandishi wa habari na vitabu aliyeandika jinsi ya kupata furaha Je, kwa nini tunapata hasira? mambo gani yanasababisha na muhimu zaidi, je ni jambo baya? Kwa nini tunapata hasira? Dereva mwenye hasira Ni vitu gani vilikua vikimfanya mtu awe na hasira dhidi ya mwingine? Hasira ni mfumo uliochangamana,'' anasema Aaron Sell, Profesa wa Saikolojia na mtaalamu wa masuala ya makosa ya jinai katika Chuo cha Heidelberg mjini Ohio Marekani. ''Hasira ni kitu kinachodhibitiwa akilini. Ni namna ya kuingia kwenye mawazo ya mwingine na kuyafanya yakuthamini wewe zaidi. Ni njia ya kushinda kwenye mizozo kwa kuwafanya wabadilishe akili zao.'' Profesa Sell anaeleza,wanasayansi wameweza kubainisha kuwa ''sura yenye hasira'' inarithishwa -si suala la kujifunza-kwa sababu ''Watoto wasioona wanaweza kuonyesha hasira usoni.'' Unaweza kuwachezea hawa? Unaweza kufikiri kuwa wazee wetu wa zamani hawakua na hasira wala kuwa katika ugomvi waliishi maisha marefu kuliko waliokuwa na hasira na wenye kugombana, lakini si kweli. ''Kilichokua kinatokea,'' Profesa Sell anasema ''walikua wakiyazungumza kwa namna nzuri ili kupata ufumbuzi na kwa njia hiyo waliweza kushinda''. ''Hapo zamani, watu ambao hawakua na hasira walikua wakionewa,'' anasema Profesa Sell-watu waliwaibia, waliwatishia ''matokeo yake walipoteza uvumilivu''. Kinachotokea kwenye miili yetu tunapokua na hasira Hasira hazibadili tu sura isipokua pia saikolojia yako Kuelewa suala hili la hasira tunapaswa kufikiria namna linavyoathiri kisaikolojia, namna gani linavyotufanya tutende na kufikiri au kutofikiri. Profesa Ryan Martin, mwenyekiti wa programu katika Chuo kikuu cha Wisconsin nchini Marekani, ni mtafiti wa tabia za hasira. Anasema ''Unapokua na hasira mfumo wako mzima hubadilika, Profesa Martin anasema, ''kasi ya mapigo ya moyo huongezeka, kasi ya kuhema huongezeka, unaanza kutoka jasho na mfumo wa umeng'enyaji chakula hupunguza kasi yake ya kufanya kazi.'' Mabadiliko haya ya kimwili yana nia ya kukupa nguvu kukabili hali yoyote ya uonevu unaohisi kufanyiwa. Na ubongo wako unafanya kazi hiyo pia. ''Tunafahamu pia kuwa wakati watu wakiwa katika hali hiyo watu hufikiri zaidi kujinasua wakiwa washindi au kulipa kisasi.'' Anaeleza Profesa Martin. Hutaki kuwaza vitu vingine ikiwa unajaribu kufanyia kazi uonevu uliotendewa. Kwa nini maisha ya kisasa yanachochea hasira? Unamaanisha nini ''mimi wa 15 kwenye foleni''?! Watu wengi katika nchi zilizoendelea hawana mambo mengi ya kuwafanya wawe na wasiwasi kama wazee wao wa zamani, sasa kwa nini maisha ya kisasa yana utofauti? Ni rahisi, Profesa Martin anasema: ''Watu wako na pilika nyingi, na mahitaji yameongezeka kwenye maisha yao, hivyo madhara yake yanakua makubwa kwa sasa.'' Ikiwa tutapanga mstari kupata huduma kwenye duka na kuachwa hapo muda mrefu, tunapatwa na hasira kwa urahisi-Kwa sababu hatuna muda wa kupoteza. ''Ni vitu ambavyo tungeweza kuvikwepa, vitu vyenye kutufanya tuwe na hasira, anasema Profesa Martin. Namna tunavyotenda tunapokua na hasira ''Si mara zote kunakua na matokeo mazuri katika ulimwengu wa leo.'' Je, tunaweza kudhibiti hasira kuliko tunavyofikiria? Unapokua na hasira fikiri kabla ya kutenda Ni wazi kumdhuru mtu uliye na hasira naye haisaidii wala haizai matunda- hivyo tunapaswa kutafuta namna nyingine ya kuelekeza hasira zako. Tunaweza kudhibiti hali hii kuliko tunavyofikiria anasema Maya Tamir, Profesa wa Saikolojia, Chuo cha kiebrania mjini Yerusalemu. Utafiti wake unaonyesha kuwa hasira si mara zote zinahitaji kuonyesha ukaidi. Tumia hasira kwa kutenda jambo jema Umeshawahi kutendewa isivyo haki? usipate hasira, badala yake tumia hasira yako kufanya ambo jema ili kupata matokeo chanya Hivyo hasira inaweza kuleta hasara: zinaweza kutufanya viburi kwa matendo, maneno na hata kwenye mitandao ya kijamii. Kama wale wanaotaka kulinda mamlaka zao na nafasi zao hupata hasira, inaweza kusababisha madhara makubwa sana-hata vita. Lakini wana saikolojia pia wanasema hasira zinaweza kutupa nguvu kuchukua hatua pale tunapokosewa. Lakini Mark Vernon mwanafilosofia, anaeleza namna ambavyo hasira zinaweza kukufanya kuchukua hatua chanya. ''Hasira inaweza kumfanya mtu kufanya jambo akiwa na moyo na kuwashawishi wengine kujenga hoja nzuri ili kuchukua maamuzi mazuri. Hivyo hasira si jambo baya wakati wote, tunachotakiwa kufanya ni kuzidhibiti kwa busara. Data zilizokusanywa na Umoja wa mataifa, Shirika la biashara duniani, WTO na serikali mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa katika nchi nyigi, kiwango cha umasikini kinashuka na muda wa mwanadamu kuishi unaongezeka. text: Nusrat alimwagiliwa mafuta ya taa na kuchomwa moto juu ya paa Nusrat Jahan Rafi, 19, alifariki mwezi Aprili katika mji wa Feni, uliopo kilo mita 160 nje ya mji mkuu wa Dhaka. Mwalimu mkuu aliyetuhumiwa na Nusrat kwa unyanyasaji na wanafunzi wawili wa kike ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo. Kifo chake kilishangaza nchi nzima na kusababisha msururu wa maandamano kushinikiza Nusrat apate haki. Kesi hiyo ni ya kwanza kuamuliwa haraka nchini ikilinganishwa na nyingine kama hizo ambazo huchukua miaka kadhaa kabla ya kuamuliwa. Mwendesha mashtaka Hafez Ahmed aliwaambia wanahabari kuwa "wauaji sharti wachukuliwe hatua Bangladesh". Mawakili wa washtakiwa wanasema watakata rufaa. Polisi wakishika dori nche ya mahakama Machi 24 Uchunguzi wa mauaji ya Nusrat ulionesha njama ya kutaka kumnyamazisha ambayo pia ilihusisha wanafunzi katika darasa lake pamoja na wanaume walio na ushawishi mkubwa katika jamii. Walimu watatu wakiwemo mwalimu mkuu, Siraj Ud Doula, ambaye polisi inasema alitoa amri ya kuuwa kwa mwanafunzi huyo kutoka jela, walipatikana na hatia ya mauaji siku ya Alhamisi. Wengine wawili waliopatikana na hatia ni Ruhul Amin na Maksud Alam, kiongozi wa chama tawala cha Awami League party. Maofisa kadhaa wa polisi pia walipatikana na hatia ya kushirikiana na wale waliokamatwa kueneza taarifa za uwongo kwamba Nusrat alijitoa uhai. Familia ya Nusrat, ambayo iliunga mkono hatua yake kwenda polisi mwezi machi, imepewa ulinzi, vyombo vya habari viliripoti. hukumu hiyo imepokelewa vyema na kutoa wito itekelezwe haraka iwezekanavyo. Wanawake wakiandamana nje ya mahakama siku ya Alhamisi Nini kilichomtokea Nusrat? Kwa mujibu wa taarifa ya mashtaka iliyotolewa na Nusrat, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka kwenye paa la shule, alisema mmoja wa marafiki zake alikuwa amechapwa. Wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu wanne au watano, waliokuwa wamevalia burqa, walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi dhidi ya mwalimu mkuu. Alipokataa ndipo walipommwagia mafuta ya taa na kumchoma kwa moto. Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa "walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe ". mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada baada ya kutoroka eneo la tukio. Aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa. " Mmoja wa wauaji wake alishindilia kichwa chake chini kwa kutumia mikono yake, kwa hiyo mafuta ya taa hayakumwagika pale na ndio maana kichwa chake hakikuungua ," Bwana Majumder aliiambia BBC mjini Bengali. Lakini wakati Nusrat alipopelekwa katika hospitali iliyopo karibu asilimia 80% ya mwili wake ulikuwa na majeraha. Hawakuweza kutibu vidonda , na kuamua kutuma katika hosptali ya chuo cha tiba cha Dhaka. Mashirika tofauti yameshiriki maandamano y akupinga mauaji ya Nusrat Rafi, mwanafunzi aliyechomwa moto kwa kulalamikia unyanyasaji wa kingono Unyanyasaji wa kingono ni mbaya kiasi gani Bangladesh? Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha na jamii au familia zao. Unyanyasaji wa kingono umekithiri sana nchini Bangladesh: ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na shirika misaada la ActionAid mapema mwaka huu ilibaini kuwa 80% ya wanawake wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza nguo huenda wamekumbana na visa vya unyanyasaji wakiwa kazini au kudhulumiwa kingono . Mahakama nchini Bangladesh imewahukumu kifo watu 16 waliomchoma moto hadi kufa mwanafunzi kwa kuripoti kuwa mwalimu mkuu amenyanyasa kingono. text: Lakini ukosefu wa wanawake hapa, miongoni mwa kundi la wahafidhina wa Republican wakijadili mswada wa afya na makamu wa rais, ni suala la kushangaza. Hii ni kwa sababu moja ya mambo yaliyojadiliwa ilikuwa ni ikiwa muswada huo unapaswa kuweka sharti kwamba mipango ya bima ya afya itoe "faida muhimu" zikiwemo huduma za uzazi. Mwezi Januari, Ikulu ya White House ilikabiliwa na ukosoaji mkubwa pale Rais Trump alipo saini mswada wa utoaji mimba akiwa amezingirwa na wanaume. Si ajabu kwamba wengi walianza kulalamika punde makamu wa rais Mike Pence alipotuma picha kupitia Twitter, yenye ujumbe: "Nashukuru kujiunga na @POTUS kwa mkutano na Freedom Caucus tena leo. picha hii. #PitishaMswada" Seneta wa chama cha Democratic Pat Murray alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kumjibu makamu wa rais akitoa tathmini kali juu ya picha hiyo Lakini si wanawake pekee waliokerwa na picha hiyo. Mbunge wa Congress Jim McGovern aliielezea kama ya kushangaza na kuudhi Wengine walitoa maelezo ya kuonyesha namna picha hiyo haifai kulingana na hali halisi. Rais Trump amekuwa makini sana kuwajumuisha wanawake katika picha anazopigwa wakati akisaini sheria, tangu ikulu ya White House ilipokosolewa vikali kwa kupiga picha zote peke yake akisaini sheria ya utoaji mimba, katika siku yake ya kwanza mamlakani. Chini ya wabunge watano wa Republican katika bunge la wawakilishi ni wanawake, lakini uwakilishi wa jinsia si tatizo tu la upande wa Republican - Bunge la Congress kwa ujumla bado lina wanaume wengi. Wabunge wanawake ni 20% pekee. Marekani inalinganishwa na Bangladesh inapokuja katika suala la uwakilishi wa wanawake bungeni. Nchini Sweden uwakilishi wa wanawake ni wa 44%. Kulikuwa na jumla ya wanaume 13 ( baadhi yao hawamo pichani ) ukumbini katika uzinduzi wa baraza la wasichana la Qassim nchini Saudi Arabia Marekani sio taifa pekee kuwa na picha ya wanaume pekee wakichukua maamuzi yanayowahusu wanawake na kuibua mjadala. Wiki iliyopita, uzinduzi wa baraza la wasichana katika jimbo la al-Qassim nchini Saudi Arabia ulilaaniwa wakati picha ya kwanza ilionyesha wanaume 13 wakiwa pamoja baada ya kuanzishwa kwa baraza la wasichana bila kuwemo hata mwanamke mmoja Picha kama hii si geni na inafahamikana huenda ingeweza kuchukuliwa katika vyumba mbali mbali vya mikutano katika maeneo mbali mbali duniani - wanaume wakiwa wamezunguka meza wakipanga mipango na kujadili mkataba. text: Rupali Meshram (kushoto) alichukua picha baada tu ya shambulio hilo Rupali Meshram,23, alisema alipomsikia mbuzi wake akilia ,alikimbilia nje ya nyumba yake iliyopo jimbo la Maharashtra magharibi. Alichukua fimbo na kumpiga yule chui, ambaye naye alimshambulia. Mama yake , aliyejeruhiwa pia , alimuokoa kwa kumvuta mwanae ndani ya nyumba. Wote walipatwa na majeraha madogo na wameruhusiwa kutoka hosptalini. Mbuzi hakunusurika. Bi Meshram alichukua picha ya 'selfie' baada ya tukio hilo, iliyotokea wiki iliopita lakini taarifa hizo ndo zimeanza kutoka hivi karibuni. Uso wake umefunikwa na damu. Bi Meshram alipata majeraha kwenye kichwa, miguu na mikono, lakini ameanza kupona. Nyaraka ya hospitali walivyomruhusu kumtoa ikisema ' shambulio la mnyama mwitu' "Nilidhani binti yangu angekufa," mama yake Jijabhai aliiambia idhaa ya Kihindi ya BBC, akiongozea kuwa aliogopa sana kumuona mtoto wake akiwa anavuja damu huku akimchapa viboko chui huyo. Siku kumi baada ya tukio hilo, picha hii iliochukuliwa na BBC imemunyesha Rupali bila makovu yoyote,baada ya shambulio. Rupali alifanikiaw kupona kabisa wakati Mama yake bado anauguza Wanasema walimuita mlinzi wa hifadhi ya wanyama pori, lakini alifika dakika 30 baadae na kukuta chui huyo ameshaondoka. Kijiji chao kinavamiwa na wanyama pori mara kwa mara kwa sababu kipo karibu na hifadhi ya wanyama pori. Mwanamke mmoja nchini India amenusurika kifo, madaktari wanasema,baada ya kupigania maisha yake aliposhambuliwa na chui mwenye milia aliyekuwa anataka kumla mbuzi wake. text: Twitter, Spotify, Reddit, Soundcloud na mitandao mingine yameathirika katika uvamizi wa mitandao. Kumekuwa na hofu kuhusu tishio dhidi ya usalama wa mitandao ya Marekani wakati uchaguzi mkuu ukikaribia baada ya wavamizi kufanikiwa kufikia barua pepe za chama cha Democratic na baadhi ya mashirika ya uchaguzi nchini. Mitandao hiyo ni wateja wa kampuni iitwayo Dyn ambayo inaitumia kuwasaidia wateja kupata mitandao hiyo wakiyatafuta. DynDNS imeathirika na uvamizi wa data katika kinachojulikana kama shambulio la (DDos) jambo linalofanya kuwa vigumu kwa wateja kuyapata mitandao hiyo wanapoyatafuta. Haijulikani wazi ni nani anayehusika na uvamizi huo au ni kwanini Dyn imelengwa. Katika taarifa kwenye mtandao wake, Dyn imesema uvamizi huo wa DDoS ulianza mapema Ijumaa Marekani na kuathiri kampuni zaidi mashariki mwa taifa hilo. Athari ya awali ya uvamizi huo ulisababisha baadhi ya mitandao kutopatikana wakati watu wakiyatafuta au wakati mwingine agizo linalotumwa katika mtandao kuchukua muda mrefu kabla ya kupokewa. Watu wengi waliokuwa wanatumia mitandao ya kijamii walieleza kuwa, Reddit, Twitter, Etsy, Github, Soundcloud, Spotify na mitandao mingine ilikuwa vigumu kuyafungua. Mitandao pia kama Paypal, Pinterest na Tumblr pia yanaarifiwa kuathirika. Katika ujumbe kwenye Twitter, na uliosambazwa pakubwa, Github ilisema "tukio la kimataifa" linaathiri Dyn na kufanya kuwa vigumu kuyapata mitandao yake. Athari ya uvamizi huo ulidhihirika kwa saa kadhaa na kufikia mchana Ijumaa, Dyn ilisema huduma zake zimerudi kama kawaida. Uchunguzi umeanzishwa baada ya uvamizi wa mitandao kadhaa dhidi ya kampuni ya Marekani ulioathiri huduma za baadhi ya mitandao hiyo. text: Anasema amestaafu kwa sababu mama yake ameanza kuugua kutokana na matusi aliyoyapokea. Azmoun - ambaye amepewa jina la utani 'Messi wa Iran' - alikuwa amefunga mabao 23 katika mechi 33 alizokuwa amelichezea taifa lake kabla ya michuano ya sasa. Hata hivyo, hakufanikiwa kufunga bao lolote Urusi huku vijana hao waliokuwa chini ya mkufunzi Carlos Queiroz walimaliza wa tatu katika Kundi B nyuma ya Uhispania na Ureno. Azmoun amesema uamuzi wake wa kuacha kuichezea Iran ni "mchungu". Alifunga mabao 11 katika mechi 14 alizowachezea za kufuzu kwa Kombe la Dunia na alicheza muda wote katika mechi zao tatu walizocheza katika hatua ya makundi ambapo Iran waliwashinda Morocco, wakashindwa na Uhispania na wakatoka sare na Ureno. Hata hivyo, Azmoun amesema ukosoaji ulioelekezwa kwake umemfanya mamake kuugua. "Mamangu alikuwa mgonjwa sana na alikuwa ameanza kupata nafuu na nilikuwa na furaha," anasema Azmoun anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Rubin Kazan. "Inasikitisha kwa sababu ya ukatili wa baadhi ya watu, na matusi ambayo mimi na wenzangu hatukustahili, sasa amezidiwa na ugonjwa. "Hili limeniweka katika njia panda ambapo inanilazimu kuchagua moja kati ya hayo mawili - na nimeamua kumchagua mamangu." Azmoun alianza kuchezea timu ya taifa ya Iran akiwa na miaka 19. Anashikilia nafasi ya tano katika orodha ya wafungaji mabao bora wa Iran na alikuwa anafananishwa na shujaa wa taifa hilo Ali Daei, anayeongoza akiwa na mabao 109 katika mechi 149. Mshambuliaji wa Iran ambaye amekuwa akicheza Kombe la Dunia Sardar Azmoun amestaafu kuchezea timu ya taifa akiwa na miaka 23. text: Madaktari hao 50 waliowasili Nairobi wengi wao ni wanawake. Walilakiwa na Gavana wa jimbo la Kisumu ambaye zamani alihudumu kama waziri wa afya Prof Anyang' Nyong'o na Dkt Rashid Aman, afisa mkuu msimamizi katika wizara ya afya katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Jumanne usiku. Madaktari hao kutoka Cuba wamewasili huku bado kukiwa na utata kuhusu mazingira yao yakikazi na malipo, ikiwa ni pamoja na huduma watakazopokea kutoka kwa serikali kwa mfano malazi. Chama cha madaktari nchini Kenya kimelalamika kwamba madaktari hao wanathaminiwa na kulipwa mishahara ya juu kuliko madaktari wazawa wa Kenya. Dkt Aman amesema madaktari wengine 50 watawasili nchini humo Alhamisi jioni. Wizara ya Afya imesema madaktari hao watapokea mafunzo ya kuwafahamisha zaidi na mazingira ya ya kikazi Kenya kwa wiki mbili kabla ya kutumwa kufanya kazi katika kaunti zote 47 nchini humo. "Tutawaandalia mafunzo ya kina, kuwafahamisha kuhusu Kenya, mfumo wetu na jinsi mambo huendeshwa hapa na pia kuhusu sekta ya afya humu nchini," alisema Dkt Aman. Madaktari hao wataunganishwa na madaktari wenyeji kwa matumaini kwamba wataongezana maarifa. Pacha walioshikana watenganishwa hospitali ya Kenyatta Miongoni mwa madaktari wataalamu walio kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa x-ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva. Wizara ya afya imesema madaktari 50 kutoka Kenya wanatarajiwa kwenda Cuba kwa mafunzo zaidi Septemba mwaka huu. Kundi la kwanza la madaktari kutoka Cuba ambao wameombwa na serikali ya Kenya kuanza kufanya kazi nchini humo kupunguza uhaba wa madaktari wamewasili nchini humo. text: Bendera ya Marekani Hii ni baada ya kifo cha mjumbe wa chama cha upinzani CHADEMA, Daniel John tarehe 11 Februari, ambaye mwili wake ulipatikana katika fukwe za bahari ya hindi, jijini Dar es salaam, siku moja baada ya kutekwa ukiwa na majeraha ikiwemo shingo yake kunyongwa na watu ambao hadi saa hawajajulikana. Marehemu anaripotiwa kutekwa pamoja na mwenzake, Reginald Mallya aliyenusurika na kupatikana akiwa hai akiwa na majeraha kadhaa sehemu za mkononi na kichwani. Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, akionesha picha ya marehemu Daniel John Marekani: Tunasikitishwa na vitendo vya utekaji na ukatili Tanzania Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa balozi wa Marekani, balozi wamesema "Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu." "Kuongezeka kwa makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotutia wasiwasi na kutusikitisha sana." Pamoja na hayo ubalozi umetaka "uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania." Tukio hilo limefayika ikiwa ni juma la mwisho la kampeni za uchaguzi mdogo katika majimbo mawili nchini Tanzania ambayo yalipoteza wabunge wake kwa sababu mbalimbali ikiwemo ile ya wabunge wa upinzani kujiuzulu kwa kile walichokiita kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano. Kwa upande wake, kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Murilo, amesema polisi waachwe wafanye uchunguzi kufuatia vitendo hivyo vya utekaji nyara. Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiendelea na mazoezi ya viungo huko nchini Ubelgiji. Kumekuwa na kinachoonekana kama muendelezo wa vitendo vya mashambulizi dhidi ya wanachama wa upinzani,hivi karibuni nchini Tanzania. Kikubwa kikiwa ni shambulio dhidi mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, Bw Tundu Lissu anayezidi kupata matibabu nchini Ubelgiji baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwaka uliopita. Ubalozi wa Marekani Tanzania unataka uchunguzi huru kuhusu matukio ya matumuizi ya nguvu dhidi ya harakati za kisiasa za upinzani. text: Kikosi kipya cha wanajeshi kutoka Afrika kitaweza kukabiliana na wale wanaowatishia raia Hata hivyo Bw Kiir amesema hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na hatashirikiana tena na umoja huo. Kikosi hiki cha Umoja kitakachoundwa na askari wa Afrika kitakuwa na majukumu makubwa zaidi ya askari zaidi ya 12,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wako tayari katika taifa hilo. Mapigano baina ya vikosi hasimu ya mwezi Julai yaliwauwa mamia ya watu na wengine maelfu kadhaa kuyakimbia makwao. Maelfu ya raia walilazimika kutafuta hifadhi katika ofisi za Umoja wa Mataifa wakati wa mapigano ya mwezi Julai Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinakabiliwa na kazi ngumu ya kuwalinda raia ambapo zaidi ya watu 35,000 walikimbilia kwenye makao makuu yake mjini Juba. Tofauti na kikosi cha kulinda amani kilichopo nchini humo, kikosi cha Afrika kitakachokua chini ya Umoja wa Mataifa kitaweza kukabiliana na wale watakaowatishia raia Hata hivyo haijawa wazi ikiwa kikosi hicho kitaweza kufanya kazi bila ushirikiano na Sudan kusini. Zaidi ya raia 100,000 wa Sudan kusini kwa sasa wamekimbilia katika nchi jirani kufuatia mapigano ya hivi karibuni, linasema shirika la la wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesema linajiandaa kuiwekea Sudan kusini vikwazo vya silaha, ikiwa itajaribu kuzuia kupelekwa kwa wanajeshi wa ziada wa kulinda amani nchini humo. text: Bunge chini ya Spika Job Ndugai limepitisha muswada wa vyama vya siasa mbao umekuwa ukipingwa kwa madai kuwa utaminya Demokrasia Upitishwaji wa muswada huo umepitia vigingi kadhaa, ukikosolewa vikali na vyama vya siasa vya upinzani na asasi za kiraia ambao wanadai utaminya demokrasia nchini humo. Hata hivyo wabunge wa chama tawala cha CCM ambao ni wengi Zaidi wameutetea muswada kwa kudai unaenda kusafisha siasa za vyama vingi. Baada ya kupita bungeni muswada huo unatarajiwa kusainiwa na rais Magufuli ambaye serikali yake imekuwa ikibeba lawama za kuminya upinzani na uhuru wa kujieleza. Waziri kivuli na mbunge wa Bunda, kupitia Chadema Esther Bulaya ameuita muswada huo kuwa ni 'uonevu mkubwa dhidi ya vyama upinzani.' Uonevu kwa mujibu wa Bulaya unadhihiri kwa msajili wa vyama vya siasa kupewa mamlaka ya kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili. Uonevu mwengine kwa mujibu wa upinzani ni masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kwa kuzuia vyama rafiki kutoka nje kushiriki. "Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa," amesema. Rais John Magufuli amekuwa akilalamikiwa kuminya demokrasia nchini Tanzania toka lipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alilieleza Bunge kuwakuwa muswada huo ni kiboko. Mhagama kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi ni amesema pamoja na mambo mengine muswada huo unalenga kumpa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhakiki chama cha siasa wakati wowote. "Lengo ni kuhakikisha chama cha siasa kinakuwa na sifa za usajili muda wote wa uhai wake na kueleza bayana mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa kuhakiki muda wowote utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ili kuhakikisha chama cha siasa kinazingatia na kutekeleza masharti ya usajili," amenukuliwa na Mwananchi akisema. Wakili Jebra Kambole ameiambia Dira TV ya BBC Swahili kuwa bado kuna ukakasi mkubwa hususani nguvu alizopewa msajili, "Watakaoanza kuathirika muswada ukianza kutekelezwa ni vyama vidogo (vya upinzani). Lakini pale msajili atakapotumia mamlaka yake ipasavyo vyama vingi vitaumia." Moja ya kifungu kinachopingwa ni cha Kifungu cha 19 ambacho kinasema msajili anaweza kukisimamisha usajili wa chama kwa sababu atakazozitaja na kwa muda atakaouweka mpaka ili chama hicho kiweze kujirekebisha. Maalim Seif: Yanayotokea chini ya Magufuli, hatujawahi kuyaona Tanzania Chama ambacho kimesimamishiwa usajili hakitaweza kufanya shughuli zote za kisiasa. Na iwapo msajili ataona chama hicho hakijajirekebisha anaweza kukifutia usajili. Kifungu hiki, wapinzani wanadai kinaweza kutumika kuzuia vyama kushiriki uchaguzi kwa jusimamishiwa usajili kabla yay a uchaguzi na kurudishiwa usajili baada ya uchaguzi kupita. Awali vyama vya upinzani vilionesha kufurahishwa na baadhi ya mabadiliko yaliyoyofanywa na kamati ya bunge ya sheria. Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya vyama 15 vya upinzani, Jumapili Januari 27, 2019 jijini Dar es Salaam, naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema baada ya kutoa maoni yao mbele ya kamati hiyo hivi karibuni bungeni Dodoma, hoja nyingi walizopigia kelele zimesikilizwa. "Tulipigia kelele suala la mafunzo na adhabu zake. Kamati baada ya kupitia hoja zetu, kwanza imepunguza adhabu kutoka Sh1 milioni hadi Sh500,000 na jela kutoka miezi 6 hadi mitatu," Mwalimualinukuliwa na Mwananchi. Hata hivyo, alisema bado kuna utata umebaki wa kuchanganya elimu ya uraia na kujengeana uwezo ndani ya chama. Hatimaye Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania umepitishwa na Bunge la nchi hiyo na sasa utapelewkwa kwa Rais Magufuli ili ausaini na kuwa sheria. text: Mbunge Bi van Damme ametishia kupeleka mashtaka kwa polisi Phumzile van Damme kutoka chama cha upinzani cha Democratic Alliance amesema kuwa alijipata katika mzozo na mwanamke mzungu katika mji wa V&A Waterfront uliopo Cape wakati mwanamme mzungu alipotishia kuleta ghasia na kutumia lugha chafu alipokuwa akimuongelesha akimtaja kama "wewe mweusi". Mji wa V&A Waterfront, ambao ni kitovu kikuu cha utalii, umeomba radhi kwa tukio hilo. Bi van Damme hakufurahia namna alivyotendewa na afisa wa usalama alipo ripoti kwake tukio. " Tunasikitishwa na tukio hili, ambalo hatukulishighulikia kwa malengo muhimu ,kwa heshima na huruma ," ulieleza mji wa kitalii wa V&A Waterfront kwenye ukurasa wake waTwitter. Bi van Damme amesema kuwa alikuwa amesimama kwenye mstari katika duka la bidhaa mbalimbali alipolazimika kuzoza na mwanamke ambaye anadaiwa kumwambia kuwa " atamsukuma kando". "Halafu nilipokwenda nje, alikuwa amesimama pale na familia yake katika hali ya kunitisha. Na ndipo nilipomsogelea na kumwambia, 'kwanini unaniangalia hivyo kwa kunitisha?' Halafu akasema, 'ni kwasababu wewe ni mweusi', Alisema van Damme katika video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Twitter. Alisema kuwa manamme, ambaye alikuwa na mwanamke, "alikuwa natishi kuzua ghasia, kwa hiyo katika hali ya kujilinda nilimpiga ngumi kwenye kichwa chake". Bi van Damme amesema kuwa anakubali kutoa msamaha kwa V&A Waterfront na jukumu lao la kutovumilia tabia na mienendo isiyokubalika inayofanywa na wafanyakazi wake. Amesema, hata hivyo ametishia kupeleka mashtaka kwa polisi. Visa vya ubaguzi wa rangi vimekuwa vikiendelea kugonga vichwa vya habari nchini Afrika Kusini. Matamshi na mashambulio ya mwili ni miongoni mwa matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa licha ya kipindi cha ubaguzi wa rangi kuripotiwa kumalizika baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hayati Nelson Mandela kuchukua mamlaka 1994. Mwandishi wa habari wa Afrika Kusini Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio Mwaka jana Moja ya matukio hayo ni kupigwa kwa mtangazaji wa Televisheni na redio nchini Afrika Kusini mweusi ambaye alisema kuwa alikuwa muathiriwa wa shambulio lililochochewa na ubaguzi wa rangi baada ya kusimamisha gari lake kwa ajili ya kulisaidia kundi la wazungu ambao gari lao lilikuwa limepinduka. Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio Mwaka jana. Yeye na marafiki zake wawili wa kike waliitwa "nyani", alisema. Walipoulizwa ni kwanini wanatukanwa, walipigwa hadi wakapoteza fahamu. Alisema. Taarifa juu ya shambulio hilo zilizua hasira miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Mbunge mweusi wa Afrika Kusini amejitetea kuwa alimpiga ngumi mbunge mwanamume baada ya kudaiwa kumtusi matusi ya ubaguzi wa rangi. text: Mnamo Novemba mwaka jana, zaidi ya watu 50 waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi Kampala Tabu Butariga ni mhariri wa Daily Monitor ambaye alichapisha taarifa hiyo kwenye ukurasa wa kwanza tarehe 31 mwezi Mei. Tony Glencross, Mkurugenzi mtendaji wa Nation Media Group, kampuni inayomiliki gazeti hilo, pia ameitwa na polisi kwa ajili ya mahojiano. Wakuu hao wanashukiwa kuchapisha taarifa ya uongo na ya uchochezi. Bw. Butagira ameiambia BBC kuwa shutuma hizo ''yawezekana zinachochewa kisiasa'' na kuwa mawakili wa Daily Monitor watazipinga shutuma hizo. Bwana Glencross amesema watatii wito huo, lakini kwa wakati huo alikuwa amejitenga baada ya kupata maambukizi ya Covid-19 na hataweza kufika mbele ya polisi mpaka juma lijalo. Makala ya uchunguzi ya BBC Africa Eye kuhusu mauaji ya watu watatu jijini Kampala ilitolewa tarehe 31 mwezi Mei , ilitoa ushahidi kuwa vikosi vya usalama vya Uganda vilifyatua risasi kiholela kwa watu waliokuwa wakipita kwa miguu wakati wa kudhibiti ghasia jijini Kampala mwaka jana mwezi Novemba, na kuua na kuwajeruhi watu ambao hawakuwa wamejihami wakiwemo wanawake na watoto. Daily Monitor halikuhusika kwenye uchunguzi huo.Lakini kufuatia ushahidi uliooneshwa kwenye filamu ya BBC, gazeti hilo liliripoti tarehe 18 Novemba kuhusu watuwaliokuwa na silaha kwenye gari yenye usajili namba UP5564 iliyopita katika barabara ya Kampala na kufyatua risasi za moto. Kwa muda wa dakika moja hivi, watu saba walipigwa risasi , na takribani wanne walipoteza maisha. Serikali ya Uganda iliiambia BBC kuwa vikosi vyake vya usalama vilikuwa vikidhibiti vurugu, na kuwa watu waliokuwa wamekufa katika barabara ya Kampala waliuawa kwa baada ya ''risasi kuwapata kwa bahati mbaya''. Hakuna ushahidi kuwa watu hawa saba walihusika na vurugu katika barabara hiyo. NBS ni moja kati ya mitandao ya televisheni nchini humo, ambao kawaida hurusha makala za uchunguzi za Africa Eye za BBC, lakini haikuonesha makala ya mauaji ya Kampala.Hatahivyo, makala hayo yalisambazwa kwenye mitandao ya Youtube na WhatsApp nchini Uganda tarehe 31 mwezi Mei Waganda wakitoa wito wa uwajibishwaji "Ushahidi wa kulaani [serikali] ulihitaji kuwashtaki maafisa waliowaua Waganda mnamo Novemba uko hapa," aliandika tweet Raymond Mujuni, mwandishi wa habari wa Uganda na mtangazaji wa habari. "Acha haki itawale." Akaunti nyingine ya Twitter, iliweka ushahidi uliooneshwa kwenye filamu ya BBC na kumtaka kamisaa wa polisi nchini Uganda , Asan Kasingye ''kuwataja wauaji wa watu wetu''. Jenifa Ochwo aliandika: "Maombi yangu yamekuwa kwamba angalau vitendo hivi vya kikatili vingeandikwa kwa kumbukumbu ya baadaye. Kwa ajili ya waathirika. Kwa historia. Mtawala wetu amejaribu kufuta hii au kuandika historia tena. Hatahivyo, sasa kuna rekodi. " Kuitwa kwa Bw.Butagira na Bw. Glencross kunaangazia uhasama unaozidi kuwakabili wanahabari wa Uganda, haswa wale wanaoripoti taarida za kumkosoa Rais Yoweri Museveni au kukosoa serikali yake. Chama cha waandishi wa habari wasio na mipaka wamerekodi mashambulizi 40 dhidi ya waandishi wa habari nchini Uganda kati ya mwezi Novemba mwaka 2020 na mwezi Machi mwaka 2021, yakiwemo mashambulizi ya mwili 21 na kukamatwa kwa wengine wanane. Kimeiweka Uganda nchi ya 125 kati ya 180 kwenye orodha ya nchi zenye uhuru wa habari, na kusema kuwa vitisho na unyanyasaji dhidi ya wanahabari ni ''vitendo vinavyotokea karibu kila siku Uganda''. Daily Monitor limeripoti kwa kina kuhusu mauaji ya mwezi Novemba na kuripoti kuhusu waathirika wengi wa tukio hilo. ''Azma uandishi wa habari wa Daily Monitor ni kutaka kuubainisha ukweli," Bw Butagira alieleza. "Serikali hii inajivunia kurejeshwa kwa usalama wa binadamu. Kwa hivyo, vyombo vya habari kutaka uwajibikaji kwa ajili ya raia waliopigwa risasi katika barabara za Kampala hakupaswi kuchukuliwa kama uhalifu katika jamii iliyostaarabika na ya kidemokrasia." Mhariri wa gazeti moja kubwa nchini Uganda ameitwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na polisi baada ya kuripoti matokeo ya uchunguzi uliofanywa na BBC kuhusu mauaji yaliyotekelezwa na polisi mwaka jana jijini Kampala. text: Lakini onyo hilo lililozua maswali mengi linatoka kwa Karin Michels , profesa wa tawi linalohusiana na magonjwa katika chuo kikuu cha Havard aliyetoa hotuba yake mjini Freiburg Ujerumani ambayo baadaye iliwekwa katika mtandaoi wa You Tube. Kama anavyosema profesa Michels , katika hotuba hiyo ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni moja , mafuta ya nazi ni miongoni mwa vyakula vibaya zaidi kula. Chakula kilicho na mafuta mengi kinaweza kusababisha madhara katika viungo vyako vya ndani.Sisi sio wageni wa kuambiwa kwamba chakula tunachokula kina madhara mwilini mwetu. Kumbuka tulipoambiwa kwamba nyama ya nguruwe inasababisha saratani, ama kwamba mvinyo mwekundu sio mzuri kwa afya yetu. Na wiki iliopita pekee tulipogundua kwamba , licha ya miaka kadhaa ya kuambiwa visivyo kwamba vyakula visivyo na madini ya kabohydrayte vinaweza kupunguza miaka ya maisha yako. Ni wazi kwamba Profesa Michels sio mtu wa kwanza kusema kwamba mafuta ya nazi yana mafuta mengi na ni mabaya . Mwaka 2005 - miaka 13 iliopita -shirika la afya duniani lilikuwa limeorodhesha mafuta ya nazi kuwa ,miongoni mwa vyakula ambavyo havifai kutumiwa kama chakula kama hutaki kupatwa na mshutuko wa moyo. Miaka ya 90 kulikuwa na tahadhari ya kiafya nchini Marekani wakati utafiti ulipodai kwamba 'popcorn' zinazotumika wakati watu wanapotazama filamu zina mafuta kwa sababu zilikuwa zikipikwa katika mafuta ya nazi. Wakati huohuo hatahivyo mafuta ya nazi yamekuzwa kama chakula kizuri cha kiafya. Kulingana na utafiti kutoka kwa muungano wa American Heart mwaka uliopita , takriban asilimia 72 ya raia wa Marekani wanaamini kwamba mafuta ya nazi yana afya-hata ijapokuwa katika kiwango hicho ni asilimia 37 ya wataalam wa lishe bora wanaokubali. Tofauti iliopo , wanasema inatokana na kampeni nzuri za ukuzaji kutoka kwa makampuni ya kuuza mafuta hayo ambazo zinasema kuwa yanaweza kutumika kama mbadala wa siagi na mafuta ya yanayotokana na mimea mbali na ithibati kutoka kwa watu maarufu kama Gwyneth ambaye amepiga debe kutumia kama chakula bali pia kutumia kama mafuta ya kupaka uso na nyewele. Utumizi wa mafuta ya nazi kujipaka mwilini mbali na kutia nyweleni ni mambo ya kawaida nchini India swala ambalo huenda limechangia mafuta hayo kupendwa sana kiafya. Victoria taylor afisa mwandamizi kuhusu lishe bora katika wakfu wa British Heart , aliambia BBC Three kwamba Profesa Michel yuko sawa licha ya kampeni kubwa ya kukuza mafuta hayo. Mafuta ya nazi yamejaa mafuta asilimia 86-ambayo ni thuluthi moja zaidi ya siagi , kulingana na victoria. Lakini sio kila mtu anakubaliana na matamshi ya Michel. Wengine wamesema kuwa mafuta ya nazi yametumika kama kiungo katika tamaduni nyengine hususan Afrika, Asia na kusini wa marekani kwa karne kadhaa. Iwapo umekuwa ukidurusu mitandao wiki hii , ni wazi kwamba umepata kuona kwamba mafuta ya nazi ni 'sumu halisi' na sio tiba kama ilivyodhaniwa. Inaonekana kama kutia chumvi-lakini sio chumvi mbaya hatahivyo. text: Polisi wamepakia picha za mamba huyo mtandaoni. Wakazi wa Nokomis waliwapigia simu polisi na kuomba usaidizi baada ya kumgundua mnyama huyo. Afisa wa polisi wa eneo la Sarasota alipakia mtandaoni picha ya afisa wa wanyama aliyeitwa kumnasa akiwa anamburuta mnyama huyo kutoka kwenye maji Jumamosi. Polisi wanasema mamba huyo alifanikiwa kupita kwenye uzio uliokuwepo na kuingia kwenye bwawa hilo. Mamba nchini Marekani kwa kawaida hukua hadi kuwa na futi kati ya 11 na 15 na wanaweza kuwa na uzani wa kilo 454. Mamba wa Marekani hupatikana mashariki mwa Marekani katika majimbo ya Florida na Louisiana, kila jimbo likiwa na zaidi ya mamba milioni moja. Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja. Ingawa awali walikuwa wameorodheshwa kama wanyama walio hatarini chini ya sheria za mwaka 1973, idadi yao iliongezeka sana kwa haraka na kufikia mwaka 1987 wakaondolewa kutoka kwenye orodha hiyo. Inakadiriwa kwamba kuna mamba milioni moja hivi Florida, na wengine milioni moja Louisiana. Polisi katika jimbo la Florida, Marekani wamesema mamba wa urefu wa futi 11 alipatikana kwenye bwawa la kuogelea la familia moja katika jumba hilo. text: Maelfu ya mashabiki wa Liverpool walikusanyika Anfield kusherehekea ushindi wa klabu yao baada ya miaka 30 Timu ya Jurgen Klopp ilihitaji ushindi mmoja ili kushinda ligi hiyo lakini ushindi wa Chelsea dhidi ya Manchester City una maana kwamba Liverpool haiwezi tena kufikiwa na timu yeyote ile katika jedwali. Ni kombe la 19 la Liverpool na lao la kwanza tangu msimu wa 1989-90. Licha ya kutakiwa kusalia nyumbani na meya wa mji huo kutokana na virusi vya corona , maelfu wa mashabiki walikongamana katika uwanja wa Anfiled kusheherekea ushindi huo. Wengi wa mashabiki waliokongamana katika uwanja wa klabu hiyo walivalia barakoa, huku wengine wakiwasha fataki. Baadhi ya wachezaji wa Liverpool , akiwemo kipa Alisson , beki Virgil van Dijk na kiungo wa kati Alex Oxlade Chamberlain, walisherehekea pamoja baada ya kutazama mechi hiyo ya Chelsea. Klopp ambaye alikuwa akivalia tishati ya Liverpool na aliejawa na hisia , aliambia chombo cha habri cha Sky Sports: Sina maneno ya kuelezea, siamini. Ni zaidi ya vile nilivyofikiria kwa inawezekana kuwa mabingwa na klabu hii ni jambo maridhawa. ''Sijawai kusubiri miaka 30, nimekuwa hapa kwa miaka minne na nusu, lakini ni mafanikio makubwa , hususan baada ya likizo ya miezi mitatu kwasababu hakuna mtu aliejua kwamba tutatawazwa washindi." Liverpool fans celebrate winning the Premier League for the first time at Anfield Huku mlipuko wa virusi vya corona ukiathiri maisha ya kawaida nchini England na kusababisha kusitishwa kwa muda kwa ligi ya Premia kwa miezi mitatu, mashabiki wa Red walihimili kusubiri ili kuona jinsi msimu huu utakavyokamilishwa, huku wengine wakisema huenda ukafutwa, na hivyobasi kufuta matokeo pamoja na juhudi zao katika vitabu vya rekodi. Hatahivyo hilo halikutokea kwani Ligi ya Premia ilirudi mwezi huu na hivyobasi kuwawezesha kuibuka washindi. Hatahivyo, kutoka na masharti yaliowekwa kukabiliana na virusi vya corona, The Reds hawataweza kusherehekea ushindi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wao, sio kama kawaida. Baada ya kupata ushindi mkubwa wa 4-0 dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumatano na huku wakitarajiwa kucheza dhidi ya Aston Villa siku ya Jumapili ,Julai 5 na wakisalia na mechi mbili za nyumbani - watacheza bila mashabiki. Kufikia sasa hakuna uwezekano kwamba watasherehekea na mashabiki wakiwa juu ya basi lao katika mji huo kama ilivyo kawaida. Hatahivyo mechi nyengine watakaporudi uwanjani itakuwa mechi dhidi ya wapinzani wao ManCity ambao walifanikiwa kuwashinda msimu uliopita. Kufuatia ushindi wa Chelsea, mkufunzi wa City Pep Guardiola aliwapongeza Liverpool kwa kushinda taji hilo. Watch: The moment Liverpool players found out they were champions Walivunja rekodi msimu huu Kushinda taji hilo ndio lililokuwa lengo la Liverpool ambayo ilikuwa imesubiri kwa muda mrefu ili kutawazwa mabingwa tena, baada ya kushinda taji hilo mara 11 kati ya 1973 na 1990. Lakini baada ya ufanisi huo, huenda mambo yakaimarika zaidi, na kuvunja rekodi ya pointi 100 iliowekwa na klabu ya Man City. Timu hiyo ya Klopp imefanya kampeni kali katika historia ya ligi ya Premia , kwa kujipatia pointi 86 na rekodi ya kushinda mechi 28, droo mbili na kushindwa mara moja katika mechi zao 31. Hivyo ndivyo walivyotawala, na katika wakati mmoja waliongoza jedwali la ligi wakiwa na pointi 25- uongozi uliovunja rekodi na wa pili katika historia ya ligi ya Premia. Ushindi wao wa taji hilo la ligi msimu huu ndio wa mapema katika rekodi, huku wakiwa wamesalia na mechi 7. Huo sio ushindi wa mapema kwa tarehe, ni kwasababu ya kusitishwa kwa ligi ya premia kati ya mwezi Machi na Mei kutokana na mlipiuko wa virusi vya corona. Miaka 30 ya mateso. Premier League: Mengi yametokea tangu Liverpool kushinda ligi ya Premia kwa mara ya mwisho. Ushindi huo wa liverpool unawakilisha wakati muhimu kwa mashabiki wake, waliokuwa wakizoea ushindi kati ya miaka ya 70 na 80, ikiwemo ushindi wa msimu wa 1972-73 na 1990-91 ambapo walishindwa kumaliza katika nafasi ya kwanza au ya pili katika ligi hiyo. Hatahivyo hawajakosa kushinda taji katika kipindi hicho cha miaka 30, wakishinda kombe la FA, makombe manne ya kombe la ligi, kombe la vilabu bingwa mara mbili- la mwisho wakishinda chini ya ukufunzi wa Klopp - pamoja na makombe matatu ya Super na moja la ligi ya klabu bingwa duniani. Subira vuta kheri - Subira ya liverpool ya miaka 30 ili kushinda kombe la ligi ya England imetimia baada ya klabu ya Manchester City kupoteza 2-1 dhidi ya Chelsea na hivyobasi kuwathibitisha The Reds kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo. text: Sanamu za kiafrika katika makavazi kuu ya Ubelgiji Watoto hao wanaosadikiwa kuwa karibu 20,000 walichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa mama zao waafrika na kupelelewa na kanisa katoliki na taasisi zingine zanchini Ubelgiji. Baadhi ya watoto hao ambao walizaliwa miaka ya 1940 na 1950, hawakuwahi kupewa uraia wa Ubelgiji hali iliowafanya kuishi kama watumwa.. Akilihutubia bunge la nchi hiyo,Bw. Michel alikiri kuwa Ubelgiji ilikiuka haki ya kimsingi ya watoto hao, kwa kuwachukulia kama tisho kwa mfumo wa ukoloni. Ubelgiji iliwavua uraia wao, kuwabagua na kuwatenganisha na jamaa zao. "Hatua hii itatusaidia kutambua rasmi sehemu ya historia yetu ya kitaifa,"alisema katika taarifa yake. Charles Michel, Waziri mkuu wa Ubelgiji akihutubia bunge la nchi hiyo Miaka miwili iliyopita kanisa katoliki iliomba msamaha kuhusu jukumu lake katika sakata hiyo. Na mwaka jana wabunge wa Ubelgiji walitoa wito kwa serikali kuwapa usaidizi watoto waliyoathiriwa kupata wazazi wao na pia kupewa uraia wa nchi hiyo Huku hayo yakijiri mama zao za watoto hao pia wamekuwa wakiwatafuta tangu walipochukuliwa kutoka kwao kwa lazima. Georges Kamanayo, mmoja wa watoto waliopelekwa Ubelgiji amesema hatua ya Bw. Michel ni "Utambuzi wa hakika kuwa walidhulumiwa". ''Tumejihisi kama watu duni nchini Ubelgiji kwa muda mrefu, tulijaribu kujichangaya na jamii ya wabelgiji lakini ilikuwa vigumu kwasababu tulitengwa na jamii hiyo." aliiambia gazeti la De Standaard. Ubelgiji inatajwa kuwa moja ya koloni katili zaidi enzi hizo na inakadiriwa kuwa waafrika kati ya milioni 10 na 15 waliuawa chini ya utawala wao katika Congo ya Ubeligiji ambayo sasa ni taifa la Jumhuri yaKidemokrasia ya Congo. Mwezi uliyopita , jopo la wataalamu kutoka umoja wa mataifa lililopewa jukumu la kuchunguza watu wa asili ya kiafrika wanaoishi Ubelgiji liliiambia taifa hilo kuomba msamaha kwa madhila iliyofanya enzi ya ukoloni. Ubaguzi wa rangi ulikuwa mbaya sana katika taasisi za elimu za Ubelgiji, wataalamu wa walisema katika ripoti yao. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ubelgiji Bw. Michel hata hivyo hakuzungumzia ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa. Bunge limesema kuwa hatua yake ya kuomba msamaha watu wa asili ya kiafrika waliotekwa na kupelekwa nchini humo wakiwa watoto wadogo lazima isaidie kuimarisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo. Waziri mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel, ameziomba msamaha nchi za Burundi, DR Congo na Rwanda kwa kuhusika na maelfu ya visa vya utekaji nyara wa watoto waliozaliwa na walowezi wa nchi hiyo zama za ukoloni. text: Mabaki ya ndege hiyo iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Jose Marti Wanawake watatu waliondolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo wakiwa hai, lakini taarifa zinasema wamo hali mahututi. Ndege hiyo, ambaye iliundwa karibu miaka 40 iliyopita, ilikuwa imewabeba abiria 104 na wahudumu sita wa ndege. Serikali ya Cuba imeanzisha uchunguzi, na kutangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa. Ndege hiyo Boeing 737-201 ilianguka saa sita na dakika nane mchana Ijumaa, muda mfupi baada ya kupaa kutoka Havana. Ndege hiyo ilikuwa kwenye safari ya ndani ya nchi kutoka Havana kwenda Holguin, mashariki mwa Cuba. Wahudumu wote sita wa ndege hiyo walikuwa raia wa Mexico lakini wengi wa abiria ni raia wa Cuba. Taarifa zinasema kulikuwa na abiria watano raia wa kigeni. "Kumekuwa na ajali ya ndege ya kusikitisha sana. Taarifa tulizo nazo ni za kutamausha, yamkini kuna idadi kubwa sana ya waathiriwa," Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel alisema baada ya kutembelea eneo la ajali. Ilikuwaje ndege hiyo ikaanguka? Ni mapema sana kubaini chanzo cha ajali hiyo, lakini walioshuhudia kutoka ardhini wanasema ndege hiyo ilishika moto kabla ya kuanguka katika eneo wazi lililo karibu na msitu mbogo karibu na uwanja huo wa ndege wa Havana. "Niliiona ikipaa," mfanyakazi wa duka la jumla Jose Luis aliambia shirika la habari la AFP. "Ghafla, iligeuka na kuanguka. Tulishangaa sana." "Tulisikia mlipuko mkubwa na kisha tukaona wingu la moshi ukitanda angani," Gilberto Menendez, ambaye ana mgahawa karibu na eneo la mkasa ameambia Reuters. Vifusi vya ndege hiyo vilitapakaa eneo kubwa Idara ya uchukuzi ya Mexico imesema kwenye tovuti yake kwamba "wakati wa kupaa, ndege hiyo yamkini ilipata hitilafu za kimitambo na ikaanguka." Boeing wamesema watatuma kundi la mafundi wake Cuba, "kama inavyoruhusiwa chini ya sheria za Marekani na kwa uelekezi wa Bodi ya Taifa ya Usalama katika Uchukuzi ya Marekani na maafisa wa serikali ya Cuba." Kumekuwepo na vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Cuba kwa miongo mingi. Tunafahamu nini kuhusu manusura? Watu wanne walinusurika ajali hiyo lakini mmoja alifariki akisafirishwa kupelekwa hospitalini, mkurugenzi wa hospitali ya Calixto Garcia mjini Havana, Carlos Alberto Martinez, ameambia Reuters. Manusura hao watatu wote ni wanawake, kwa mujibu wa gazeti la Chama cha Kikomunisti cha Cuba, Granma. Mmoja umri wake ni miaka 18 hadi 25, wa pili ana miaka 30 hivi na mwingine ana miaka 39. "Yuko hai lakini amechomeka sana na moto," jamaa wa mmoja wa wanawake hao aliambia Reuters katika hospitali hiyo. Wanawake watatu wamenusurika ingawa wamo hali mahututi Serikali za Argentina na Mexico zimethibitisha kwamba raia wa mataifa hayo mawili ni miongoni mwa waliofariki. Ndege hiyo ni ya aina gani? Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa kwa shirika la taifa la ndege la Cuba, Cubana de Aviación na kampuni ya uchukuzi wa ndege ya Mexico, Aerolineas Damojh. Wakazi waliojawa na simanzi walikusanyika eneo la ajali Maafisa wa Mexico wanasema ndege hiyo iliundwa mwaka 1979 na ilikaguliwa na kubainika haikuwa na kasoro yooyte Novemba mwaka jana. Mexico imesema inawatuma wataalamu wawili wa masuala ya uchukuzi wa ndege kushiriki katika uchunguzi. Aerolineas Damojh, shirika ambalo pia hufahamika kama Global Air, lina ndege tatu ambazo bado zinafanya kazi. Ajali hiyo ikoje ukilinganisha na nyingine za karibuni? Kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa sekta ya uchukuzi wa ndege, mwaka jana uliokuwa miongoni mwa miaka salama zaidi katika uchukuzi wa ndege za kubeba abiria. Lakini mwaka huu kumekuwa na ajali kadha kubwa. Ajali mbaya zaidi ya ndege Cuba ilitokea mwaka 1989, ndege iliyoundiwa Muungano wa Usovieti aina ya Ilyushin-62M ilipoanguka karibu na Havana na kuwaua watu 126 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, na wengine 24 ardhini. Watu zaidi ya 100 wamefariki dunia baada ya ndege ya kuwabeba abiria aina ya Boeing 737 kuanguka na kulipuka karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Cuba mjini Havana, katika mkasa mbaya zaidi wa ndege nchini humo katika miongo kadha. text: Wataalamu wanasema kutokea kwa ufa huo katika jimbo la Nakuru ni shughuli ya kijiolojia inayochukua muda mrefu ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda. Hilo limezua hatari ya kuanza kutokea tena kwa mitetemeko ya ardhi na milipuko ya volkano. Wanajiolojia wanasema baada ya mamilioni ya miaka, bara la Afrika litapasuka na kuwa vipande viwili. Sehemu ya mpasuko itakuwa kwenye Bonde la Ufa jambo ambalo linazua uwezekano wa Kenya na Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, kujitenga na bara la Afrika. Mwanajiolojia David Adede ameambia BBC kwamba ufa huo ni sehemu ya kutengana kwa vipande viwili vikubwa vya bara Afrika ambako kutasababisha bara Afrika kutengana na kuwa mabara mawili. Amesema shughuli hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda lakini dalili zake zilikuwa zinafichwa na majivu ya volkano ambayo polepole yamekuwa yakiziba ufa kila unapotokea. "Maji ya mvua yamesomba majivu hayo pamoja na mchanga na kuufanya ufa huo kuonekana zaidi," amesema. Ufa unaotoa dalili Tanzania na Kenya zinajitenga na Afrika Anasema vipande hivyo vimekuwa vikitengana "katika kasi ya sentimita mbili kila mwaka." Kipande kilicho na sehemu kubwa ya bara hufahamika kama Kipande cha Nubia na kipande cha pili hufahamika kama Kipande cha Somalia. Dkt James Hammond kutoka kwa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Dunia kutoka chuo cha Imperial College London alinukuliwa na jarida la mtandaoni la Mail & Guardian akisema: "Katika miaka milioni kadha ijayo, shughuli hii itakamilika na kuigawa Afrika mara mbili, na kuunda bahari mpya hapo katikati na bara jingine. Ukitumia jiografia ya sasa, bara hilo jipya litashirikisha Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania." Baadhi ya wanajiolojia wanakadiria kwamba huenda mpasuko huu ukayabeba pia mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi na maeneo ya Malawi na Msumbiji. Mwanajilojia Dereje Ayalew kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa Ethiopia aliambia jarida hilo kwamba dalili za kutokea kwa bahari zimeanza kuonekana katika maeneo ya jangwani ya Ethiopia, eneo la Afar ambalo pia linahusisha baadhi ya maeneo ya Eritrea na Djibouti. Mwaka 2005, alisema tayari nyufa nyingi zimeanza kutokea na ardhi imebonyea kwa hadi mira 100. Ufa huo ulianza kuonekana wiki moja iliyopita baada ya mvua kubwa kunyesha na barabara ya Mai Mahiu kwenda Narok ikakatika eneo lenye ufa huo. Awali, wengi waliamini ufa huo uliotokea Jumanne wiki iliyopita eneo la Karima ambalo linapatikana kilomita sita kutoka mji wa Mai Mahiu ulitokana na mvua kubwa. Ufa huo uliokuwa umeikata barabara hiyo ulikuwa umeenea umbali wa mita 700. Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara Kenya (KeNHA) wakishirikiana na mkandarasi kutoka China anayejenga reli ya kisasa, walifika eneo hilo na kuziba ufa. Baada ya uchunguzi, ilibainika kwamba ulitokana na shughuli ya kijiolojia chini ya ardhi ambayo ilihusisha mvutano wa vipande vikubwa vya ardhi. Siku chache baadaye Jumapili, ufa huo uliendelea kupanuka na kuathiri barabara hiyo tena jambo lililosababisha magari yenye kubeba mizigo mizito kutoweza kupita. Aidha, ufa huo ulianza kuathiri nyumba za wakazi. "Mkandarasi na kundi la wahandisi wamewekwa hapo kwa sasa na watasalia kuendelea kufuatilia yanayojiri kutokana na shughuli za kivolkano ambazo zilisababisha ufa huo," alisema naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa KeNHA Charles Njogu baada ya ukarabati huo mara ya kwanza. Bw Adede amesema hatua ya kuziba ufa huo kwa sasa itasaidia kwa muda mfupi tu. Ufa huo umepitia katika baadhi ya nyumba na mashamba ya watu. Bw Njoroge amelazimika kuhama kwake Mmoja wa walioathirika ni Eliud Njoroge, 77, ambaye ameambia BBC kwamba ameishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20. Anasema amelazimika kuibomoa nyumba yake na sasa analazimika kuishi kama 'mkimbizi' kwa jirani yake. Ufa umegawa shamba hili lililopandwa maharagwe mara mbili Mwandishi wa BBC aliyetembelea eneo hilo Gladys Njoroge anasema katika baadhi ya maeneo, ufa huo una upana wa mita 20 na kina cha hadi futi 50. Baadhi ya maeneo, ufa huo una kina cha zaidi ya futi 50 Wataalamu wametahadharisha kwamba nyufa zaidi zinaweza kuendelea kuonekana katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Ufa. Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi anasema viongozi wa eneo lililoathirika wamewahimiza wakazi wanaoishi karibu na maeneo yaliyotokea ufa huo kuhama, lakini baadhi kama Bw Njoroge hawawezi kuhamia mbali. Kuibuka kwa ufa mkubwa katika eneo la Suswa katika Bonde la Ufa kusini magharibi mwa Kenya kumezua wasiwasi kuhusu uthabiti wa eneo la Afrika Mashariki kijiolojia. text: Ajali ya kivuko cha MV Nyerere ambayo iliua zaidi ya watu 200 Ni janga ambalo lilisababisha idadi kubwa ya watu wapatao 1000 kupoteza maisha baada ya meli ya Mv Bukoba kuzama. Sababu ambayo ilitajwa kusababisha ajali hiyo ilikuwa idadi ya abiria kuzidi, chombo kuwa na itilafu, pamoja na vifaa vya ukozi kuwa vichache. Pamoja na ajali hiyo kubwa kuacha simanzi kwa baadhi ya familia hadi sasa, ni fundisho gani kwa kisa cha namna hiyo kutotokea tena? Lakini bado Tanzania na Afrika mashariki na kati zinaendelea kushuhudia ajali ambazo sababu ya kutokea au watu kupoteza maisha zikiwa zinafanana. Mwaka jana, Septemba 2018 jumla ya watu 224 walifariki na watu wengine 41 wakiokolewa wakiwa hai katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere. Tanzania iliweza kushuhudia pia ajali za maji ikiwemo za bahari ya hindi Mv Skagit na Mv Spice Islander nazo ziliweza kupoteza idadi kubwa ya watu. Ni wiki hii tu (Mei 20) ambapo ajali nyingine ya maji imetokea na kuua watu 16 huku wengine wakiwa hawajulikani walipo huko nchini Uganda. Boti iliyokuwa imebeba wacheza mpira 50 wakiwa na mashabiki wao huko Magharibi mwa Uganda. Huku ikikumbukwa kuwa mwaka 2016 , wachezaji 30 wakiwa na mashabiki wao walizama katika ziwa Albert na watu 20 walifariki. Mwaka 2018 nchini Uganda, watu 29 walifariki kufuatia ajali ya mashua iliyotokea ziwa Victoria. Mashua hiyo iliyokuwa na watu zaidi ya 90 waliokuwa wanaelekea sherehe, ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono. Wasanii kadhaa na watu wengine mashuhuri waliaminika kuwa kwenye mashua hiyo.. Maafisa walisema kwa mashua mbili za uvuvi ambazo ziliwasili kuokoa nazo zilifurika watu na kuzama. Mwaka 2014, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa takriban watu 98, wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Albert Magharibi mwa Uganda. Boti iliyozama ilikua imebeba zaidi ya wakimbizi 100. Aliyekuwa anaendesha boti hiyo alikamatwa na jeshi la polisi na inadaiwa kuwa alikua mlevi. Hii sio mara ya kwanza ajali ya boti kuua watu katika Ziwa Albert kutokana na kujaza abiria na mizogo kupita kiasi. Watu 50 wamefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya boti kuzama kwenye mto kaskazini mwa nchi hiyo. Mwaka 2010, ajali ya boti nchini Uganda iliuwa watu zaidi ya 70 baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa Albert nchini Uganda. Ajali hii ilitokea eneo lijulikanalo kama Kakoma katika kijiji cha Runga, Wilaya ya Hoima. Mwaka huu, Aprili 2019, takriban watu 150 wametoweka baada ya boti kuzama katika ziwa moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na watu 33 wakaokolewa katika ajali hiyo. Kulingana na Reuters mwaka uliopita , boti moja lilipinduka katika mto kaskazini mwa DR Congo , na kusababisha watu 49 kufa maji huku idadi kama hiyo ya watu wakiokolewa. Mwaka wa 2015, zaidi ya watu 100 walitoweka baada ya maboti mawili kugongana katika mto Congo nchini DR Congo kulingana na shirika la afya duniani WHO. Mnamo mwezi Julai 2011, zaidi ya watu 100 walifariki baada ya boti mbili kugongana katika mto katika eneo la mkoa wa Equateur la DR Congo. Swali kuu kutokana na visa hivi vyote kieneo ni je, funzo gani linalotokana na majanga haya majini? Ni miaka 23 tangu kisa cha ajali ambayo inatajwa kuwa mbaya zaidi katika karne kutokea barani Afrika katika ziwa victoria nchini Tanzania. text: Hali hiyo imesababisha maeneo hayo kuwa katika hatari ya kukosa kabisa uthabiti na amani na maelfu ya watu katika nchi kama vile Nigeria , Mali,Chad ,Burkina Faso na Niger wameachwa bila makao . Ufaransa ambayo imekuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi hizo kukabiliana na makundi mbali mbali ya wapiganaji pia imeonekana kushindwa katika kuleta utulivu katika eneo hilo . Hali huenda ikawa mbaya zaidi kwa sababu ya kifo cha aliyekuwa rais wa Chad Idriss Deby ambaye alikuwa mojawapo ya viongozi wanaotegemewa kupambana na kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likizihangaisha nchi za Nigeria , Chad ,Niger na Burkina faso . Mashambulizi yalianza lini? Mashambulio dhidi ya jeshi na raia katika eneo lote yanatokea kila mara na yameongezeka licha ya uwepo wa maelfu ya wanajeshi kutoka nchi zote zilizoathiriwa pamoja na Ufaransa. Mwaka wa 2019 kulikuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vya kila mwaka kutokana na mzozo wa silaha katika eneo la Sahel tangu 2012. Hali imezidi kuwa mbaya na hata kuanza kuyaathiri mataifa ya Afrika magharibi ambayo hapo awali yalionekana kuwa salama . Silaha zinatoka wapi? Kuendelea kwa mapigano nchini Libya kumesababisha kutokuwepo kwa serikali thabiti kumudu mipaka ya nchi hiyo na maeneo ya Sahel na hivyo basi silaha hatari zimezidi kupatikana katika mikono ya makundi mbalimbali ya wapiganaji . Kundi la Boko Haram limejiingiza katika ushirikiano na mitandao ya kimataifa ya ugaidi na kuendelea kufanya mashambulizi nje na ndani ya Nigeria huku serikali ya taifa hilo ikionekana kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kuwahakikishia raia wake usalama . Katika shambulizi moja lililosababisha vifo vya wanajeshi 89 wa Niger mwaka wa 2019 ,Ufaransa pia ilijipata ikisajili maafa ya wanajeshi wake baada ya helikopta ya kijeshi kuanguka nchini Mali mwezi Novemba mwaka huo . Katika maeneo ya taifa la Mauritania makundi yenye silaha kali yameendelea kufanya mshambulizi dhidi ya maafisa wa usalama na hata kushikilia miji na sehemu zenye barabara muhimu katika maeneo ya mipakani . Tatizo hilo lilianza mwaka wa 2012 wakati makundi ya wapiganaji waliokuwa na silaha walipoungana na kuchukua sehemu ya kaskazini mwa Mali na kuifanya Ufaransa kutuma vikosi vyake ili kuwazuia kufika mji mkuu Bamako . Mkataba wa amani ulitiwa saoni lakini utulivu haukurejea kabisa na makundi mengine mapya yalichipuka katika nchi jirani za Mali, Burkina Faso na Niger. Idadi ya watu wanaofariki kutokana na mashambulizi ya a makundi hayo imeongezeka mara tano tangu mwaka wa 2016 na mwaka wa 209 zaidi ya watu 4000 waliripotiwa kuawa katika ,mashambulizi ya wapiganaji wa makundi mbalimbali. Ni makundi yapi yanayotekeleza mashambulizi? Makundi yaliyojihami na mengine yanayohusishwa na Al Qaeda na Islamic State yamekuwa yakiendeleza shughuli zake katika eneo la Sahel na Afrika magharibi . Sababu za makundi hayo kufika maeneo ya nchi hizo ni pamoja na ; Kando na nchi hizo za Sahel kwa jina G5 sahel kuunda kikosi cha pamoja ili kupambana na makundi ya wapiganaji ,Ufaransa imekuwa ikivituma vikosi vyake kuvipiga jeki katika kampeni hizo lakini bila mafanikio ya kutosha . kufikia mwisho wa mwaka wa 2020 ,Ufaransa ilikuwa na takriban wanajeshi 5000 katika sehemu hiyo . Umoja wa mataifa pia una zaidi ya wanajeshi 12,000 nchini Mali ilhali Marekani ina kambi mbili za droni nchini Niger . Katika nchi za Mali na Burkina Faso makundi hayo yamehusika na mauaji ya kila mara ya raia na vikosi vya usalama . Makundi hayo huwa hayakiri kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia lakini makubwa yanayotekeleza mashambulio hayo huko Sahel ni ; Hadi kufikia sasa serikali za nchi hizo bado hazijaweza kupata suluhisho la tatizo la usalama katika mataifa hayo. Changamoto kuhusu hali ya kiuchumi na maisha katika jamii nyingi za maeneo yenye mizozo hiyo zimechanganyika na maslahi ya kidini ,kikabila na kuzua mseto wa mambo mengi ambayo hayatoweza kusuluhishwa katika siku za hivi karibuni . Iwapo hapatakuwa na serikali thabiti katika mataifa yanayohusika na mizozo kama vile Libya ambako silaha nyingi zinatokea ,itakua vigumu kumaliza kikamilifu matatizo ya ukosefu wa usalama katika eneo la Sahel na afrika magharibi . Mataifa kadhaa ya eneo la Sahel - sehemu ya mataifa kadhaa ya afrika ya kati na magharibi yaliyo jangwani yapo mashakani kwa sababu ya tishio la usalama kutoka kwa makundi mbali mbali yaliyojihami . text: Ndege hiyo ilipaa kutoka Devonport, Tasmania Rubani alikuwa peke yake kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Devonport kwenda King Island huko Tasmania tarehe 8 Novemba. Kisa hicho kwa sasa kinachunguzwa na mamlaka za usafiri nchini Astralia (ATSB). Maafisa hawajasema jinsi rubani huyo alifanikiwa kuamka na kutua salama. Ndege hiyo aina ya Piper PA-31 ya shirika la Vortex Air, ilistahili kukamilisha safari ya kilomita 240 mwenda wa saa 07:15 saa za huko. Wakati ikiwa angani rubani alilala hali iliyosababisha ndege hiyo kupita uwanja na kuendelea na safari kwa kilomita 46 zaidi. Ramani Mtaalamu wa usafiri wa ndege Neil Hansford alisema Australia ina sheria kali zinazohusu uchovu wa rubani. "Hakuna vile popote pale duniani mtu anaweza kuendesha ndege akiwa amechoka," alikiambia kituo cha habari ya serikali cha Australia. Kwenye mtandao wake, Vortex Air inasema hufanya safari za ndege kwa vikundi, makampuni na safari za starehe kote nchini Australia. ATSB ilisema itamfanyia mahojiano rubani na kuchunguza mipangilio ya huduma za shirika hilo kabla ya kutoa ripoti yake mwaka ujao. Mwaka uliopita watu watano waliuawa wakati ndege iliyokuwa safarini kwenda King Island ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Melbourne. Ndege ndogo ilipita uwanja iliostahili kutua nchini Australia kwa karibu kilomita 50 baada ya rubani kushikwa na usingizi, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa angani. text: Mshambuliaji wa klabu ya Genk na nahodha wa taifa Stars akifunga giooli dhidi ya Liverpool Akiwa na thamani ya £10m, amefunga magoli 10 msimu huu matatu katika ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool na RB Salzburg. Pia mchezaji huyo amevutia klabu kama vile Eintracht Frankfurt ya Ujerumani na Lazio ya Itali. Samatta mwenye umri wa miaka 27 alikuwa mfungaji bora katika ligi ya Ubelgiji msimu uliopita akifunga magoli 25 na kuisaidia Genk kushinda taji lao la nne la ligi katika historia yao. Samatta pia alitawazwa kuwa mshindi wa taji la Ebony Shoe mwaka uliopita ambalo hutolewa kwa mchezahi bora wa Afrika nchini Ubelgiji. Mchezaji huyo wa kimataifa awali alihusishwa na uhamisho wa klabu kadhaa za Uingereza ikiwemo Leicester, Aston Vill na Watford. Mbawana Samatta akikabwa na beki wa Liverpool Virgil van Dijk Msimu uliopita kulikuwa na tetesi kwamba nyota hyo alikuwa akinyatiwa na klabu kama vile West Ham, Everton na Burnley. Kuvuma akiwa TP Mazembe Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20. Amesalia na miezi 20 hivi kabla ya mkataba wake kumalizika. Samatta alihamia Ubelgiji mwaka mmoja baada yake kutawazwa mchezaji bora wa mwaka Mwafrika aliyekuwa anacheza ligi za barani Afrika mwaka 2015. Samatta akisherehekea goli lake dhidi ya klabu ya Sint Truidense. Alishinda vikombe sita vikuu akiwa na TP Mazembe ikiwa ni pamoja na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015 kabla ya kuondoka. Kufikia Machi mwaka huu, alikuwa ameichezea timu ya taifa ya Tanzania mechi 44 na kuwafungia mabao 16 tangu alipowachezea mara ya kwanza mwaka 2011. Samatta aliichezea Simba kabla ya kujiunga na TP Mazembe mnamo mwaka wa 2011. Ingawa Mtanzania huyo amevuma sana msimu huu, ambapo alifunga mabao manane katika mechi 11 za kwanza, msimu uliopita hakufanya vyema sana. Alifunga mabao saba katika mashindano yote akichezea klabu yake msimu wa 2017/18. Klabu za Norwich na Brighton zimeulizia kuhusu mshambuliaji wa Genk na Tanzania Mbwana Samatta. text: Mugabe alifariki mwezi mapema mwezi huu akiwa na miaka 95 na ibada ya mazishi kufanyika katika mji mkuu wa Harare. Serikali ilikua imepinga ombi la familia yake la kumzika kiongozi huyo katika eneo la Zvimba, na kushinikiza azikwe katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa. Familia yake hatimae ilikubali lakini serikali ikabadilisha msimamo huo siku ya Alhamisi. Haikubainika ni nini kilichosababisha mipango ya awali ya mazishi ya Mugabe kubadilishwa. Familia ya Mugabe ilikubali azikwe katika makaburi ya Heroes Acre baada ya makubaliano kufikiwa kuwa mnara wa makumbusho utajengwa kumuenzi kiongozi huyo wa kwanza wa Zimbabwe. Katika taarifa iliochapishwa Alhamisi, Waziri wa Mawasiliano Nick Mangwana alisema mabadiliko hayo yanazingatia sera ya "kuheshimu uamuzi wa familia ya marehemu". Mugabe alifariki Singapore alipokua anapokea matibabu yasaratani na mwili wake kusafirishwa nyumbani Zimbabwe. Baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa. Katika taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na "matakwa yake [Mugabe]". Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi atakapozikwa. Inaaminiwa kuwa Mama Taifa wa zamani Zimbabwe, Grace Mugabe, alikuwa amrithi mume wake Familia yake inasemekana kughabishwa na jinsi kiongozi huyo alivyong'olewa madarakani na mshirika wake, wa zamani Rais Mnangagwa, miaka miwili iliyopita- halia mbayo huenda imesababisha mvutano kuhusu mahali atakapozikwa. Bw. Mnangagwa alipendekeza kiongozi huyo azikwe Heroes Acre. Mugabe, alikua Rais wa kwanza wa Zimbabwe baada ya nchi hiyo kupata uhuru 1980. Miaka ya awali ya uongozi wake, alisifiwa kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu kwa waafrika walio wengi Enzi ya kisiasa ya Mugabe Lakini baadae utawala wake ulikumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukandamizaji wa wapinzani wake. Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2017 na wadhifa wake kuchukuliwa na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa. Mwili wa rais wa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe utazikwa nyumbani kwao, baada ya serikali kubadili msimamo wake wa awali kuhusu mazishi hayo. text: "Tuko nyuma. Kuna baadhi ya mambo ambayo yanamfaa yeye (Bi Clinton)," meneja wa kampeni wa Bw Trump, Kellyanne Conway amesema. Hata hivyo, ameongeza: "Hatukati tamaa. Tunajua kwamba tunaweza kushinda." Mnamo Ijumaa, Bw Trump alionekana kukiri uwezekano kwamba anaweza kushindwa. Alisema iwapo atashinda, ashindwe au atoshane nguvu na mpinzani wake, ataridhishwa na juhudi zake. Siku moja baadaye, alitangaza hatua ambazo atazichukua siku 100 akiwa uongozini iwapo atashinda. Miongoni mwa hizo ni kuweka masharti mapya kwenye mchakato wa kisiasa wa kutafuta uungwaji mkono kisiasa, mikataba ya kibiashara na mabadiliko ya tabia nchi. Kura mpya za maoni zinaonesha Bi Clinton yupo mbele sana kitaifa na katika majimbo mengi yanayoshindaniwa. Maafisa wake kampeni wa Clinton wamebashiri kwamba huu utakuwa "uchaguzi mkubwa zaidi katika historia ya Marekani". Meneja wake wa kampeni Robbie Mook aliambia Fox News Jumapili: "Watu watajitokeza kupiga kura zaidi ya wakati wowote awali." Kura za maoni katika majimbo ambayo ni ngome ya chama cha Republican kwa mfano Utah na Arizona zinaonyesha huenda majimbo kwa mara ya kwanza katika miongo mingi akaunga mkono mgombea wa Democratic. Arizona kubadilika Kura za maoni Arizona zinaweza zikawa si sahihi lakini iwapo ni sahihi, basi jimbo hilo huenda likaanzisha mtindo wa kura utakaomfaa Clinton mwaka 2016 na hapo baadaye kuwa jimbo la kushindaniwa. Sana, hilo linatokana na kuongezeka wa wapiga kura wa asili ya Kilatino (Hispania). Kwa chama cha Democratic, hizo zitakuwa habari njema sana na ambazo zitasaidia katika uchaguzi. Lakini kwa Republican, huenda ukawa mwanzo wa masaibu ya kisiasa. Zikiwa zimesalia siku 16 pekee kabla ya uchaguzi, macho ya wengi yanaelekezwa sana kwenye kashfa ambazo zimehusishwa na kampeni za Bw Trump. Jumamosi, aliapa kwamba atawashtaki wanawake waliomtuhumu kuwa aliwadhalilisha kingono. Aidha, alirejelea madai yake ya awali kwamba uchaguzi umeibwa na kwamba ulaghai wa kura unafanyika vituoni na kupitia vyombo vya habari kwenye mapendeleo. Jumapili, mwanawe Eric Trump alisema babake atakubali matokeo ikiwa tu uchaguzi utakuwa huru na wa haki. Nini kinafuata? Maafisa wa kampeni wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Donald Trump wamekiri kwamba mgombea huyo yupo nyuma ya mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democratic zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika. text: Rais Magufuli siku ya Jumatatu alimtaka Bw Makonda kuendelea kuchapa kazi Miongoni mwa mambo yaliyobainika katika ripoti hiyo iliyofanyiwa kazi siku mbili ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka yanayomkabili mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda dhidi ya vyombo vya habari. Bw Makonda anadaiwa kutotambua ukubwa wa madaraka aliyonayo na kuyatumia isivyostahili sambamba na viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana na vitendo hivyo. Kamati hiyo pia imetoa mapendekezo kadhaa ikiwemo mkuu huyo wa mkoa kuomba radhi kwa wafanyakazi wa chombo cha habari cha Clouds pamoja na wanahabari wote Tanzania. Kamati hiyo inapendekeza Bw Nauye awasilishe malalamiko ya waandishi wa habari dhidi ya mkuu huyo wa mkoa kwa Rais wa Tanzania pamoja na kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya polisi waliongia na silaha za moto kwenye chombo hicho cha utangazaji. Akipokea ripoti hiyo, Bw Nnauye pamoja na kuwataka viongozi wa umma kufanya kazi kwa uweledi, ameahidi kukabidhi taarifa hiyo kwa mamlaka za juu zaidi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kutokana na mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo Kamati iliyoundwa na waziri anayeshughulikia masuala ya habari nchini Tanzania Nape Nnauye kuchunguza uvamizi wa kituo cha habari cha Clouds, imewasilisha ripoti yake leo hii kwa waziri huyo. text: Mbunge wa makadara George Aladwa ni mwanasiasa wa tatau wa upinzani kukamtwa na maafisa wa polisi tangu kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipojiapisha Mbunge wa Makadara jijini Nairobi George Aladwa alikamatwa asubuhi ya Jumamosi nyumbani kwake na maafisa wa idara ya upelelezi na kupelekwa hadi makao makuu ya idara hiyo kwa mahojiano zaidi. Aladwa ambaye amewahi kuwa meya wa jiji la Nairobi, alikuwa katika mstari wa mbele katika mipango ya sherehe hizo ambayo haikuwa na idhini ya serikali. Aladwa sasa ni mbunge wa pili kukamatwa kuhusiana na hafla hiyo ambayo pia imeshutumiwa na jamii ya kimataifa. Mbunge mwingine wa Nairobi Tom Kajwang alikamatwa na kufikishwa mahakamani na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana. Mwanaharakati mwingine wa upinzani wakili Miguna miguna pia alikamatwa siku ya Ijumaa na angali anazuliwa na polisi licha ya mahakama kuruhusu kuachiliwa kwake kwa dhamana. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga baada ya kula kiapo cha 'kuwa rais wa watu' Bwana Aladwa alikamatwa siku ya Ijumaa usiku katika nyumba yake iliopo Buruburu kulingana na kiranja wa walio wachache bungeni Junet Mohamed. Bwana Mohammed ambaye pia mbunge wa Suna Mashariki alisema kuwa bwana Aladwa kwa sasa anazuiliwa katika makao makuu ya ujasusi. Polisi hawajatoa tamko lolote kuhusiana na kukamatwa kwa Aladwa. Mbunge mwingine nchini Kenya, amekamatwa kuhusiana na mzozo unaozunguka kujiapisha kwa aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kwa kile anachokitaja kama rais wa watu wa Kenya. text: Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga Tamko hilo limekuja mara tu baada ya kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba aachiliwe kwa dhamana . Katika maelezo yake jaji David Maraga ,amesema malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi ,na yalikuwa majukumu ya mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe. Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama. Licha ya kuwa serikali ya Kenya kupitia wizara ya mambo ya ndani kujitetea kwa ufafanuzi juu ya uraia wa wakili huyo wa upinzani Miguna Miguna,kwa msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka kusema kwamba kiongozi huyo "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wa nchi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009,wakati ambao uraia wa nchi mbili ulikuwa hauruhusiwi . Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani . text: Pesa hizo zilipatikana katika dawati la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanja wa ndege kuabiri ndege. Fedha hizo, za thamani ya jumla ya dola 150,000 za Marekani, ziligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege. Msemaji wa tume ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria Wilson Uwujaren amesema magunia hayo yalikuwa na mabunda ya noti mpya za naira 200 na 50, ambayo yalikuwa bado hayajafunguliwa kutoka kiwandani. Amesema uchunguzi unaendelea kubaini nani mwenye magunia hayo. Mabunda hayo ya noti yalikuwa yamefungwa na kuwekwa utepe kuonesha yalikuwa yametoka kwa kampuni ya kufua sarafu ya Nigeria Security and Minting Plc (NSPM). Ibrahim Bappah anayefanya kazi katika afisi ya kupambana na rushwa Kaduna alisema noti hizo mpya ziligunduliwa wakati wa ukaguzi baada ya "harufu nzuri ya kipekee" kutambuliwa. Magunia hayo yenye pesa yalikuwa yameachwa bila mtu wa kuyatunza na hayakuwa na nembo za kumtambua mwenyewe.The bags were left unattended and without tags. The EFCC is investigating whether it was an illegal attempt to move money. Maafisa wa serikali nchini Nigeria wanasema magunia matano yaliyokuwa na mabunda ya noti yamegunduliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna. text: Bodi ya mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, imetangaza kwamba chini ya makubaliano hayo, majani chai na kahawa kutoka Rwanda,tauzwa katika uwanja wa michezo viwa Paris. Kulingana na Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Rwanda (ADB) Bi Clare Akamanzi mapatano yaliyosainiwa kati ya serikali ya Rwanda na club ya Ufaransa ya Paris Saint Germain ni mapana yakihusu sekta mbali mbali : ''Ni katika kuendeleza kampeni yetu ya 'Visit Rwanda' ama tembelea Rwanda. Siyo hayo tu kwani tutatumia pia mitandao ya timu ya PSG nchini Ufaransa na kwengineko . Unajua hii ni timu ambayo ina washirika wengi katika sekta mbali mbali kama viwanda vya nguo na mitindo. Hii itatusaidia kufahamisha dunia yale ambayo na sisi tunayafanya katika sekta yetu ya utalii na mambo mengine yanayotengenezwa hapa Rwanda'', alisema Bi Kamanzi. Unaweza pia kusoma: Kwa mujibu wa mapatano hayo ya miaka 3 kwanzia mwaka ujao wa michezo mabango ya Visit Rwanda yataanza kuonekana kwenye uwanja wa timu hiyo wa Parc des Prince na kwenye fulana za timu ya wanawake. '' Zaidi ya hayo sisi pekee ndio tunaruhusiwa kuuza chai ya Rwanda na kahawa ndani ya uwanja wa PSG wakati wa mechi. Na kila mwaka tutakuwa na kampeni ya wiki nzima inayofahamika kama Rwanda week mjini Paris ni kama wiki ya maonyesho ya bidhaa na utamaduni wa Rwanda mjini Paris'' alisema Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Rwanda. Leo, ligi ya mabingwa wa Ufaransa imetuma ujumbe wa video kupitia mtandao wa Twitter, unaoonesha wachezaji kama Neymar, Kylian Mbappé, Marco Veratti na wengineo wakisifu maeneo ya kitalii ya Rwanda: Bodi ya mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, imetangaza kwamba chini ya makubaliano hayo, majani chai na kahawa kutoka Rwanda,vitauzwa katika uwanja wa michezo viwa Paris. "Bango lenye maneno 'Tembelea Rwanda' litaonyeshwa katika uwanja wa Parc des Princes, kwenye fulana za timu ya wanawake ya Paris Saint-Germain pamoja na nyuma ya nguo zao za mazoezi", tangazo hilo limesema. Hata hivyo, Rwanda na timu ya PSG hazijasema lolote kuhusu kitita cha pesa walichokubaliana katika kipindi hicho cha miaka mitatu. Baadhi ya wachezaji nyota wa PSG na baadhi ya nyota wake wa zamani watatembelea maeneo tofauti ya kitalii nchini Rwanda kama njia ya kuuvutia watu wengine duniani kuzulu pia maeneo hayo. Timu hiyo maarufu ya Ufaransa itachangia pia katika mpango wa kuinua soka ya vijana nchini Rwanda. Inasemekana kwamba mwaka 2018, Rwanda ilipata mapato ya dola milioni 380 huku mwaka huu ikipania kupata dola milioni 405. Mei mwaka jana, Rwanda ilitangaza mpango wa ushirikiano na timu ya Arsenal inayocheza ligi kuu ya England. Inasemekana makubaliano hayo yaliigarimu serikali ya Rwanda dola milioni 30. Pande zote hazijatoa maelezo yoyote juu ya gharama hiyo zote hazijazungumzia. Unaweza pia kutazama : David Luiz wa Arsenal azuru Rwanda Ushirikiano huo wa miaka 3 ulilenga kuimarisha sekta ya utalii nchini Rwanda, uwekezaji na maendeleo ya mchezo wa soka. Makubaliano kati ya Arsenal na Rwanda,yalihusu timu ya kwanza, timu ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 na timu za wanawake. Pia ilitangazwa kwamba maneno 'Tembelea Rwanda' yatakuwa yakionekana kwenye mabango maalum ya kibiasara ndani ya uwanja wa Emerates wakati wa mechi za Arsenal. Wakosoaji nchini Rwanda huistumu serikali kwa mapatano hayo wakihoji ikiwa ndiyo kipaumbele cha matatizo yanayowasumbua wananchi. Akiwajibu wakosoaji wa mpango wa kunadi utalii kwa njia ya timu kubwa, rais wa Rwanda Paul Kagame alisema wakosoaji wanapaswa kuwa na hoja za msingi wanapokosoa jambo, akisisitiza kuwa ni heri kufanya mambo ya maana kwa nchi yake kuliko kuacha kulifanya kwa kuhofia ukosoaji ambao ni lazima utakuwepo. Unaweza pia kutazama: Sherehe za kuwapatia majina sokwe zafanyika nchini Rwanda Serikali ya Rwanda na mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa wametangaza kufikia makubaliano ya kibiashara kuendeleza sekta ya utalii nchini Rwanda katika kampeni ya kuhamasisha watu kutembelea Rwanda. text: Jordan imewapokea wakimbizi wengi zaidi ya nchi nyengine yoyote duniani Nchi kumi zinzojumuisha 2.5% pekee ya pato jumla la dunia zinawahifadhi zaidi ya nusu ya wakimbizi milioni 21 duniani, inasema ripoti ya shirika hilo. Salil Shetty, katibu mkuu wa Amnesty, ameyataka mataifa tajiri kuwahifadhi wakimbizi zaidi. Shetty amesema Uingereza "mfano wa kusikitisha" kwa kushindwa kuwajibika. Uingereza imewapokea wakimbizi 8000 wa Syria tngu 2011 kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Marekani imewapokea 12,000 pekee. Na kwa mujibu wa data ya hivi karibuni ya shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, hakuna wakimbizi waliopokewa China, Uusi na katika mataifa ya kiarabu. Kwa kulinganisha, Jordan, iliyo na pato jumla la 1.2% pekee, kiwango cha Uingereza imewapokea wakimbizi 655,000 wa Syria. Uturuki imewakubali zaidi ya watu milionimbili na nusu, Pakistan milioni 1.6; na Lebanon zaidi ya milioni 1.5. "Nchi kidogo zimeachwa kuwajibika pakubwa kutokana na kuwa ni jirani tu na mataifa yanayokumbwa na mzozo," amesema Bwana Shetty. Ameongeza: "Iwapo tutagwanya jukumu hili, mfano nchi 60 kati ya 90 zikagawanya jukumu hili, tungekuwa katika hali tofauti. Ni tatizo kubwa lakini linaweza kutatulika." Matifa mengine yalio na idadi kubwa ya wakimbizi ni: Wakimbizi na wahamiaji wanaendelea kuhatarisha maisha yao wakijaribu kuingia Ulaya. Jumatatu Italia iliratibu jitihada za uokozi wa watu 2,600 kutoka pwani ya Libya. Amnesty International limeyashutumu mataifa tajiri duniani kwa kupuuza jukumu lao kwa wakimbizi likisema yanawahifadhi wakimbizi kidogo na kuwajibika kidogo. text: Jalada la kitabu cha Mein Kampf Nakala 85,000 za kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kijerumani zimeuzwa katika kipindi hicho cha mwaka mmoja. Mkuu wa Taasisi ya Historia ya Kisasa (IfZ) iliyochapisha kitabu hicho Andreas Wirsching amesema mauzo hayo yamewashangaza sana. Hata hivyo, bado hakijafikia vitabu vingine vilivyouzwa zaidi nchini Ujerumani. Nakala ya kitabu hicho huuzwa €58 (£49). Kitabu hicho kinachoangazia sera aliyoifuata Hitler kilikuwa mwongozo wa utawala wa Nazi. Hitler, kwenye kitabu hicho, alieleza wazi chuki dhidi ya Wayahudi. Kitabu hicho kilipigwa marufuku baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na serikali ya Bavaria, ambayo ilimiliki haki za kitabu hicho. Hii iliwazuia watu kuchapisha au kusambaza kitabu hicho kwa miaka 70. Kwa mujibu wa Sheria Ujerumani, hakimiliki hudumu kwa miaka 70 na baada ya kumalizika kwa kipindi hicho, IfZ ya Munich iliweza kuchapisha kitabu hicho na kuanza kukiuza Januari mwaka 2016. Tofauti na vitabu vilivyochapishwa wakati wa utawala wa Nazi, nakala za Mein Kampf za IfZ zina jalada la rangi nyeupe ambayo haina picha ya Hitler. Swastika na nembo nyingine za Nazi ni marufuku Ujerumani. Nakala za IfZ za kitabu cha Mein Kampf Bw Wirsching ameambia shirika la habari la Ujerumani DPA kwamba IfZ wanapanga kutoa nakala fupi ya lugha ya Kifaransa. Inakadiriwa kwamba nakala 4,000 za kitabu hicho ziliuzwa Ujerumani mwaka 2016. Hatua ya kuchapisha upya kitabu hicho ilishutumiwa vikali na makundi ya Wayahudi, yanayodai kazi za Sanaa za Nazi hazifai kuendelezwa. Lakini wanahistoria wanasema kitabu hicho Mein Kampf kitasaidia wasomi kufahamu yaliyotendeka wakati wa uongozi wa Nazi. Mein Kampf kilichapishwa mara ya kwanza 1925, miaka minane kabla ya Hitler kuingia mamlakani. Majeshi ya muungano yaliyoshinda vita dhidi ya Ujerumani 1945 yalikabidhi hakimiliki ya kitabu hicho kwa jimbo la Bavaria. Prof Wirsching ametetea hatua ya IfZ ya kuchapisha tena kitabu hicho Mafisa wa taasisi iliyochapisha upya kitabu cha kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler cha Mein Kampf (Mapambano au Mapigano yangu) wamesema mauzo ya kitabu hicho yaliongezeka sana tangu kuanza kuuzwa kwa kitabu hicho Januari 2016. text: Al-Shabab wapigana na vikosi vya ulinzi Kenya Vikosi tofauti vya usalama nchini Kenya vilichukua hatua za haraka kufuatia fununu kuwa eneo hilo lingeshambuliwa. Kulingana na mkuu wa polisi nchini Kenya, Joseph Boinett, shambulio hilianza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, ambapo washambulizi wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la alshabaab walivamia kituo cha polisi cha pandanguo, Lamu magharibi pwani ya Kenya. Inaarifiwa kwamba maafisa wawili wa polisi wameuwawa, na wengine saba hawajulikani waliko. Washambuliaji hao aidha waliteketeza kituo cha polisi cha pandanguo na wakaharibu mtambo wa mawasiliano katika eneo hilo usiku wa kuamkia leo. Mapigano makali yaliyodumu saa kadha yaliyotokea na mitambo ya mawasiliano ikaharibiwa, hali iliyosababisha kuwa na ugumu wa kupata habari. Wakaazi wengi wa eneo hilo la Pandanguo walitorokea msitu wa Boni na wengi wao hadi sasa hawajulikani waliko. Kulishuhudiwa ufyatulianaji mkali wa risasi majira ya asubuhi wakati maafisa wa usalama wakiwemo wanajeshi walipojibu shambulizi hilo. Alshabaab wamekiri, kupitia mitandao, kwamba ndio waliotekeleza shambulio hilo. Inaaminika kwamba wanamgambo hao huwa wanajificha kwenye msitu mkubwa wa Boni ambao uko karibu na mpaka wa Kenya na Somalia. Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab wameshambulia kituo cha polisi katika mji wa wa pwani ya kenya wa Lamu ulio karibu na mpaka wa Somalia. text: Lakini uzuri wa visiwa hivyo hauishii hapo, kwani pia vinatumika kama maabara asilia kutokana na mazingira ya kipekee ambayo yanafanyiwa utafiti wa baadhi ya magonjwa hatari ya duniani. Mkusanyiko wa visiwa 18 kutoka pwani ya Bijagos nchini Guinea-Bissau, barani Afrika Magharibi, ni makaazi ya watu 30,000 wanaotumia lugha zao na mila za pekee. Pia wanaishi karibu na wanyama pori na viboko wa kipekee wanaoishi katika wa maji ya bahari na kasa wakubwa. Lakini visiwa hivi vya kupendeza vinakabiliwa na magonjwa ya kila aina ambayo yanatishia maisha ya wenyeji. Muda wa kuishi wa watu nchini Guinea-Bissau ni miaka 60, lakini katika visiwa vya Bijagos inaaminiwa kuwa chini kidogo. Magonjwa yanayo wahangaisha watu ni pamoja na Malaria, ugonjwa wa macho unaodahamika kama trachoma, matende na minyool Hata hivyo visiwa hivyo huenda vina siri ya kukabiliana na magonjwa hayo ipasavyo. Maabara ya asilia Watafiti wa matibabu wamekuwa wakifanya kazi katika visiwa vya Bijagos kwa miaka kadhaa kubaini ikiwa wanaweza kuangamiza baadhi ya magonjwa katika visiwa hivyo. Hii ni kwa sababu visiwa hivyo vinahudumu kama maabara asilia kutokana na uhalisia wake. Japo hali hiyo inafanya maisha ya kila siku ngumu inasaidia katika juhudi za kuangamiza magonjwa. Boti kutoka bandari ya Bissau ikijiandaa kwa safari ya Bijagos Maji yanayotenganisha visiwa hivyo yanatumika kama kinga asili. Hali hiyo inasaidia kulinganisha mbinu tofauti za kudhibiti magonjwa bila hatari ya kuharibu majaribio katika maeneo mengine ya utafiti. Katika maeneo ya bara watu wanaweza kuingia na kutoka sehemu zinazofanyiwa majaribio ya tiba hali ambayo inafanya kuwa ngumu kubaini chanz na athari ya magonjwa hayo. Japo kuna visiwa vingi duniani ni vichache vinakaribiana. hii inasaidia watafiti kufanya kazi tofauti lakini vikiwa mbali mbali ni bora zaidi kwa sababu uwezekano wa majaribio ya utafiti kuharibiwa ni mdogo sana. Trachoma Watafiti kutoka chuo cha London kinachoshughulikia masuala ya usafi na tibi ya dawa za tropiki (LSHTM) awali ilikuwa inaangazi augonjwa wa macho unaofahamika kama trachoma. Ugonjwa huo unawakabili watu milioni 1.9 dunia na ni moja ya hali ambayo inasababisha upofu unaoweza kutibiwa. Trachoma unaweza kuambukizwa kupitia mikono iliyogusa macho ya mgonjwa, nguo zake au kupitia nzi aliyekalia jicho la mgonjwa. Hali hiyo huwaathiri zaidi watu wanaoishi katika mazinga machafu. Ugonjwa huo umeathiri mataifa 42 duniani. Kuna wakati mmoja kulishuhudiwa visa ambapo kila mtoto katika vijiji vya kisiwani walikabiliwa na ugonjwa huo. Dkt Anna akimhudumia mgonjwa aliye na matatizo ya macho Dkt Anna Last kutoka taasisi ya LSHTM aligundua maeneo yaliyokuwa katika hatari ya ugonjwa wa trachoma kabla ya kutibu jamii nzima kwa kutumia antibayotiki ili kukomesha mzunguko wa maambukizi. Malaria Ugonjwa wa trachoma, ambao ni chanzo cha hali inayosababisha kupofuka macho sio tatizo pekee linalo wakabili watu.katika visiwa vya Bijagos. Kuna magojwa mengine kadhaa ambayo yanashughulikiwa. Kwa sasa tunaangazia ugonjwa wa Malaria ambao unasambazwa na mbu. Dalili za awali za malaria ni kuwa na homa kali kuumwa na kichwa kabla ya hali hiyo kugeuka kuwa mbaya zaidi. Malaria huangamiza karibu watu nusu milioni duniani kila mwaka. Ukizingatia viwango vya ugonjwa wa malaria katika visiwa hivyo - ambapo mmoja kati ya kila watu wanne wanaugua Malaria , tulibaini kuwa mbu ni wazuri sana kwa kusambaza ugonjwa huo. Watafiti wa LSHTM wakiondoka kisiwa cha Rubane baada ya kufanya utafiti wa mbu Kitu cha kushangaza ni kuwa tuligundua baadhi yao hawadhuriwi na dawa ya kua wadudu. Hii inamaanisha njia maarufu zaidi ya kudhibiti malaria ambayo ni- kutumia vyandarua vya kujikinga na mbu au kupuliza dawa ya wadudu huenda hazifanyi kazi. Dawa mpya ya kukabiliana na mbu inatarajiwa kufanyiwa majaribio. Tiba zilizopita zilikuwa zinalenga kukabiliana na vimelea vya malaria ndani ya mwili wa binadamu. Lakini dawa hii mpya inalenga mbu na vimelea vya malaria ili kupunguza muda wao wa kuishi. Mwanakisiwa Ansulmani akichukua vilui lui vya mbu katika kidimbwi cha maji Katika awamu hii ya majaribio visiwa vyote vitapewa kifaa maalum cha kudhibiti viwango vya vitu kama kitanda na vyandarua vya mbu. Katika baadhi ya visiwa pia kutatolewa dawa kama njia ya ''kukabiliana'' na zingine hazitapewa dawa. Kundi la wenyeji wa kisiwani limepewa mafunzo ya kimatibabu, kama kutoa sampuli ya damu na kuchunguza kama ina viini vya malaria. Pia wamejifunza jinsi ya kubaini mbu wanaosambaza malaria kwa usaidizi wa Ba, mmoja wa maafisa wa nyanjani wakitarajia kuwa wataalamu wa kwanza wa wadudu wanaofahamika kama entomologist, katika visiwa hivyo. Ba anasomea sayansi ya entomolojia Matumaini ya siku zijazo Swali la iwapo dawa hii itakomesha malaria katika visiwa hivyo linasubiri ufumbuzi. Yote tisa kumi ni kwamba utafiti huu utawasaidi watu wanaoishi ndani na nje ya visiwa vya Bijagos. Kila utafiti unatusaidia kujifunza mengi kuhusiana na ugonjwa wenyewe na jinsi ya kuutibu, hai ambayo inaimarisha tafiti za siku zijazo. Utafiti unaofanywa visiwani unaweza kuendeshwa haraka zaidi kutokana na uwezo wa kudhibiti mazingira kwa ujumla. Tunaweza kuona kile kinacho athiri eneo maalum hali ambayo inaweza kuwanufaisha watu wote kwa njia rahisi. Mradi wa huu wa LSHTM unatarajiwa kutaendelea katika visiwa vya Bijagos kwa miaka mingine mitano. Matokeo ya tafiti zake huenda zikatumiwa kukabiliana na magonjwa hatari kama vile malaria katika maeneo mengine. Wasafiri wanaozuru visiwa vya mbali barani Afrika vinavyofahamika kama Bijagos wanatarajia kujionea mandhari ya kipekee ya fukwe za kale na misitu asilia. text: Wafugaji wa jamii ya Wamaasai kutoka Kenya wamekuwa wakivuka mpanga na kuingia Tanzania kutafuta malisho Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kupitia taarifa kwamba Tanzania ilifuata utaratibu uliopo kisheria na kwamba mataifa hayo mawili yamekuwa yakiwasiliana. Waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohamed ameilalamikia serikali ya Tanzania kufuatia hatua ya taifa hilo. ''Tulidhani kwamba mazungumzo ya kidiplomasia yangetatua mzozo huu, lakini tulishindwa kuafikia makubaliano. Ni wakati huo ambapo tuliamua kuzungumza na balozi wetu nchini humo kuwasilisha barua ya kupinga hatua ya kuwapiga mnada mifugo hao''. ''Historia ambayo tumekuwa nayo na Watanzania ni nzuri sana na kila kunapotokea tatizo tumekuwa tukitatua.Ni kwa sababu hiyo ambapo imekuwa hatua ya kushangaza miongoni mwa wafugaji wa Kenya'', waziri huyo alizungumza katika mkutano na vyombo vya habari. Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imekiri kwamba Serikali ya Kenya ilimwita balozi wa Tanzania aliyeko Nairobi kutaka maelezo zaidi. "Balozi wetu alisikiliza maelezo ya Serikali ya Kenya na akatumia fursa hiyo kuelezea masuala haya kwa Serikali ya Kenya. Vile vile Serikali imepokea barua kutoka Serikali ya Kenya kuhusu masuala haya, na Serikali itaijibu barua hiyo kutoa ufafanuzi," taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema. "Serikali inapenda kuufahamisha umma kwa ujumla kuwa uingizwaji wa mifugo na bidhaa zake nchini Tanzania huongozwa na sheria za nchi, makubaliano ya kikanda na kimataifa." Tanzania imesema kuwa ilipobainika kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya mifugo kutoka nchi za jirani wameingizwa nchini humo pasipo kufuata sheria na taratibu zilizopo, serikali iliagiza mifugo hiyo irudishwe kwenye nchi kusika. "Serikali ilitoa muda wa kutosha kwa wamiliki wa mifugo hiyo kuiondoa nchini. Tahadhari ilitolewa kwamba muda uliotengwa ukifikia ukomo, mifugo hiyo itakamatwa na kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi," taarifa hiyo imesema. Aidha, wizara hiyo imesema Waraka wa Kidiplomasia ulitumwa kwa kwa Serikali za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda, ikizihimiza kuwataka raia wao walioingiza mifugo nchini isivyo halali waiondoe. "Wamiliki wengi walitii agizo hilo la Serikali ya Tanzania na kuondoa mifugo yao nchini. "Hata hivyo, wapo wamiliki wachache kutoka nchi za jirani waliokaidi agizo hilo na hivyo ng'ombe wapatao 1113 walikamatwa katika Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro na kupigwa mnada baada ya wamiliki wake kushindwa kujitokeza." Tanzania imesema Kilimanjaro wapo ng'ombe 74 ambao wamiliki wake walijitokeza, wakalipa faini kwa amri ya mahakama na kuondoka na ng'ombe wao. Katika Mkoa wa Kigoma ng'ombe 324 ambao wamiliki wake hawajajitokeza wamekamatwa na hatua stahiki zinachukuliwa. Aidha, katika mkoa huo wa Kigoma ng'ombe 728 walikamatwa na wamiliki wao walijitokeza na kulipa faini kutokana na maamuzi ya Mahakama. Katika mkoa wa Kagera jumla ng'ombe 1,536 ambao wamiliki wake bado hawajulikani wanashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na sheria itachukua mkondo wake. "Kwa takwimu hizi ni wazi kwamba zoezi hili halijalenga nchi yeyote, kwa sababu sio nchi moja tu imeathirika," wizara hiyo ya mambo ya nje imesema. "Hili suala halipaswi kusababisha mgogoro wa kidiplomasia na nchi yeyote, labda tu mtu aamue kwa makusudi yasiyo mema kupotosha na kuchochea mgogoro." Tanzania imesema vifaranga vya kuku wa mayai 6,400 waliokamatwa Arusha kwa kuingizwa nchini bila kufuata sheria na kanuni waliteketezwa kutokana na msafirishaji wa vifaranga hivi kutokuwa na kibali cha aina yoyote kutoka mamlaka husika ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo hapa nchini humo. Wizara hiyo imesema Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania alimpigia simu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Kenya kutaka kujua kama Mamlaka za Kenya zina habari kuhusu vifaranga waliokamatwa na kama Kenya ingekubali kuruhusu vifaranga hao warudishwe Kenya. "Mkurugenzi huyu wa Kenya alisema hana taarifa kuhusu vifaranga hivyo na kwamba Kenya haiko tayari kuruhusu vifaranga hivyo kurudishwa nchini mwao kwa sababu havina nyaraka kulingana na miongozo ya kimataifa," taarifa hiyo imesema. Serikali ya Tanzania imetetea hatua yake ya kuwakamata na kuwapiga mnada mifugo pamoja na kuteketezwa kwa vifaranga kutoka nchi jirani ya Kenya. text: Picha ya Kombe la Dunia Wakati Kombe la Dunia linaanza tunajibu hayo yote na mengine mengi. 1. Nani ameshinda Kombe la Dunia? Brazil ndio wameshinda vikombe vingi zaidi vya Dunia. Kombe la mwisho lilikuwa mwaka 2002. Waliandaa kombe hilo mwaka 2014 lakini wakafungwa mabao 7-1 wakati wa nusu fainali na Ujerumani. Nani ameshinda Kombe la Dunia mara nyingi zaidi Hakuna nchi nje ya Ulaya au Amerika Kusini imeshinda Kombe la Dunia, na ushindi kwa Ujerumani, Uhispania na Italia katika fainali za mwisho tatu unamaanisha kuwa ulaya inaongoza na vikombe 11 kwa 9 vya Amerika Kusini. 2. Nani amefunga mabao mengi zaidi? Mfungaji mabao mjerumani Miroslav Klose anaongoza kwa kufunga mabao 16 kwenye mashindano manne ya Kombe la Dunia. Alistaafu mwaka 2016. MBrazil Ronaldo ni wa pili kwa mabao 15, 8 kati yao akiyafunga wakati wa kombe la Dunia la mwaka 2002. Wafungaji bora kombe la Dunia Mfaransa Fontaine anaweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye Kombe moja la Dunia. Alifunga mabao 13 kwenye mechi sita wakati wa mashindano ya mwaka 1958. 3. Vipi kuhusu wachezaji wa sasa? Kati ya wachezaji ambao wamefunga mabao 10 au zaidi wakati wa kombe la Dunia, ni Mjerumani Thomas Muller tu ambaye ataenda Urusi kama mchezaji. Kujiunga na mwenzake Klose katika orodha hiyo, Muller atahitaji kufunga mabao matano kwenye Kombe la sasa la Dunia. Mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez alishinda viatu vya dhahabu Kombe la Dunia lililolipita. Wafunga mabao mengi watakaocheza Urusi Rafael Marquez, mlinzi wa pekee aliye kwenye orodha atacheza kombe la dunia la tano kwa Mexico akiwa na rekodi sawa ya kufunga na ya Cristiano Ronaldo. 4. Timu hazipigi mikwaju jinsi zilikuwa zikifanya hapo awali. Kombe la Dunia lililopita lilikuwa na mikwaju michache zaidi tangu mwaka 1966. Licha ya hilo kulikuwa na takriban mabao 2.7 kwa kila mechi ikiwa ndiyo ya juu zaidi tangu Uhispania mwaka 1982. Yaonakana kuwepo upungufu wa mikwaju ya masafa marefu Makombora ya kulenga goli fainali kombe la Dunia 5. England inaweza kuwa na wakati mgumu lakini bado Ligi ya Primia inatawala Tangu ipate ushindi mwaka 1966, England imepita robo fanali mara moja tu. Lakini hilo halijazuia nchi zingine kujaza vikosi vyao na wachezaji kutoka ligi za Uingereza. Kuna wachezaji 130 wanaocheza Kombe la Dunia kutoka ligi kuu tatu za Uingerza ikilinganishwa na 81 kutoka Uhispania na 67 kutoka Ujerumani. Wachezaji nyota wa ligi za nyumbani 6. Nchi mwandalizi hufanya vipi? Hakuna mtu nchini Brazil atahitaji kukumbuka nyakati waliandaa Kombe la Dunia. Walipoteza kwa Uruguay mwaka 1950 na kwa Ujerumani kwa mabao 7-1 mwaka 2014. Lakini nchi zingine hufanya vyema zinapoandaa Kombe la Dunia kutokana na uungwaji mkono wa nyumbani. Urusi watakuwa na matumaini ya kufuzu kutoka kwa kundi la Uruguay, Misri na Saudi Arabia Ikiwa watafanikiwa Afrika Kusini itabaki nchi ya kwanza iliyoandaa Kombe la dunia kuweza kundolewa kwenye makundi. Timu ya nyumbani mara nyingi hupata alama nyingi 7. Penalti Hakuna mashindano ya Kombe la Dunia yamemalizika bila ya kupigwa penalti. Ni mjerumani mmoja tu ambaye amekosa penalti ya Kombe la Dunia na wameshinda penalti zote ambazo wameshiriki. Na la kushangaza England ndio wamefanya vibaya zaidi katika penalti katika historia ya Kombe la Dunia kwa kupoteza bila ya kushinda lolote. Italia iliondolewa kwa njia mbaya zaidi mara tatu ikiwemo wakati wa mechi za mwaka 1994 wakati Roberto Baggio alipoteza penalti. Nani ameshinda mechi nyingi zaidi kupitia penalti Kikosi cha Ujerumani ni kizuri kwa Penalti? Kucheza nyumbani kunasaidia kwa kiwango kipi? na ni mlinzi yupi wa Mexico aliye na rekodi sawa ya kufunga mabao na Cristiano Ronaldo? text: Manchester imeridhia kumchukua kiungo wa kati Mfaransa Adrien Rabiot, ili Juventus imchukue Paul Pogba Manchester United wanaendelea kushauriana na klabu ya China ya Shanghai Shenhua juu ya kurefushwa kwa mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo,30, hadi Januari 2021. (Goal) Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Dimitar Berbatov ametoa wito kwa klabu hiyo hiyo kutomsajili kiungo wa kati wa Brazili Philippe Coutinho, 27, msimu huu. (Mirror) Manchester United wanaendelea kushauriana na klabu ya China ya Shanghai Shenhua juu ya kurefushwa kwa mkataba wa Mnigeria Odion Ighalo Kiungo wa kati wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 24, ana 'ndoto' ya kujiunga na Boca Juniors licha ya switafahamu kuhusu hatima yake ya baadae. (Fox Sports Argentina, via Evening Standard) Inter Milan wameweka masharti 'dhidi ya-Juventus' katika mkataba wao na Paris St-Germain kumhusu mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikipewa masharti ya kulipa £13m ikiamua kumuuza kwa hasimu wao. (Goal) Manchester United wana imani kuwa watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20, nabla ya msimu ujao, licha ya juhudi za Borussia Dortmund za katakana kumpatia nota huyo mkataba mpya. (90min) Inter Milan wameweka masharti 'dhidi ya-Juventus' katika mkataba wao na Paris St-Germain kumhusu mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27 Stoke City na Preston North End wapo macho baada ya Celtic kukosa kumpatia mkataba mpya winga wa miaka 32- wa Ireland Jonny Hayes. (Mail) Middlesbrough wake tayari kumuuza beki wao wa miaka, 22- Muingereza Dael Fry, msimu huu lakini klabu hiyo inataka £20m. (90min) Tetesi bora Jumamosi tarehe 30.05.2020 Hernandez aliwahi kushinda Kombe la Dunia nchini Urusi Bayern Munich iko tayari kumtoa mchezaji wake mlinzi Lucas Hernandez, 24, kwa Manchester City wakati inapoendelea na azma yake ya kumwinda winga wa Ujerumani, 24, Leroy Sane. (TZ - via Manchest5r Evening News) Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, anatarajiwa kwamba uhamisho wake hadi Paris St-Germain utakuwa wa kudumu baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya £51.2m na Inter Milan. (Sky Sports) Aliyekuwa nahodha wa Manchester City Vincent Kompany, 34, amekataa fursa ya kurejea katika klabu hiyo kama msaidizi wa kocha Pep Guardiola muda mfupi baada ya kuondoka ili kutimiza ndoto yake ya kuwa kocha wa Anderlecht. (Sun) Kufikia mwisho wa January, Sanchez alikuwa amecheza mara saba katika timu ya Inter Milan msimu huu Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer bado anaweza kuachana na mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez msimu huu huku Inter Milan ikifikiria kuongeza mkataba wake wa makubaliano ya mkopo. (Express) AC Milan imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Burnley na Ireland Jeff Hendrick, 28, katika uhamisho usiokuwa na malipo. (Sky Sports) Ajenti wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, 21, Achraf Hakimi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Real Madrid, anasema kipaumbele kwa mchezaji huyo ni kucheza katika klabu ya Uhispania lakini anadai hakuna haraka kwa mchezaji huyo kutoka Morocco kurejea. (Evening Standard) Kristoffer Ajer (kulia) Leicester City imeimarisha nia yake ya kumsajili mlinzi wa Celtic 22 raia wa Norway Kristoffer Ajer. (Nicolo Schira, via Leicestershire Live) Kocha wa Birmingham City Pep Clotet anatarajia kwamba angalizo kwa kiungo wa kati kijana Jude Bellingham litaongezeka ikiwa ligi itarejelelewa huku Manchester United na Borussia Dortmund wakihusishwa na mchezaji huyo wa miaka, 16. (Sky Sports) Arsenal imekamilisha usajili wa winga raia mzaliwa wa Rwanda George Smith, 19, ambaye pia anaruhusiwa kuwakilisha Norway (VG - in Norwegian) Moussa Dembele ameifungia magoli kumi Lyon msimu huu wa ligi Aidha, Arsenal imeonesha tena nia kwa mchezaji wa Lyon na mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele, 23, na kuchukua hatua ya kuwasiliana na wawakilishi wake. (L'Equipe - in French) Manchester United itaongeza hamasa zaidi kwa mshambuliaji wa Lyon vilevile ambaye sasa hivi thamani yake inaweza ikapungua. (Star) Wakati huohuo, Arsenal inatarajiwa kuwafuta kazi watu 10, waliosaidia kutambua mshambuliaji Reiss Nelson, 20, na winga Bukayo Saka, 18, wakati inapoanza kutekeleza hatua za kubana matumizi kutokana na janga la corona. (Mail) Manchester United wameridhia pendekezo la kiungo wa kati Mfaransa Adrien Rabiot, 25, kujumuishwa katika mpango wa kubadilishana wachezaji, ili Juventus imchukue Paul Pogba, 27. (Calciomercato - via Express) text: Jumanne Ngoma mvumbuzi wa madini ya Tanzanite na mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Asha Mhero akimsikiliza kwa makini Mgunduzi huyo wa kwanza wa madini ya Tanzanite, aliyagundua madini ya Tanzanite mnamo mwaka 1967. Inaarifiwa kwamba, Mzee Jumanne alifariki mchana wa leo Jumatano katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili mjini Dar es Salaam. Mnamo mwaka jana 2018, Jumannne Ngoma alitambuliwa na Rais Magufuli na kumzawadia shujaa huyo milioni 100 kwa ajili ya kumsaidia kujikimu na matibabu baada ya mzee huyo kupooza sehemu ya mwili. Madini hayo ambayo ni ya kipekee kwa Tanzania, hayapatikani sehemu yeyote duniani. Mauzo ya Tanzanite duniani yanafikia takribani dola za Marekani milioni 50. Tanzanite ni jiwe lenye miaka milioni mia 6 na liligundulika Mererani, Arusha, kaskazini mwa Tanzania, mwaka 1967. Inasemekana kuwa na upekee hata zaidi ya almasi. Mwaka jana, kwa mara ya kwanza Tanzania iliadhimisha miaka 51 tangu kuvumbuliwa kwa madini hayo ya Tanzanite. Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation , iliadhimisha siku hiyo kwa kutoa taarifa na kuudhihirishia ulimwengu kuwa, madini ya Tanzanite ni fahari na urithi wetu Watanzania. Tanzania ilipoteza takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola bilioni 84 za Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya tume maalum iliyoundwa kuchunguza madini nchini Tanzania, baada ya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini uliokutikana katika makontena zaidi ya 200 katika bandari ya Dar es salaam. Mgunduzi wa madini ya Tanzanite, Mzee Jumanne Mhero Ngoma amefariki dunia. text: Alexi Sanchez Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chile, ambaye alifunga bao la ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Manchester City ana mwaka mmoja uliosalia katika kandarasi yake lakini bado hajatia saini kandarasi mpya. ''Sidhani kama unaweza kumuuza kwa klabu yoyote ya Uingereza, huo ni ukweli'', alisema Arsene Wenger. ''Lakini kama nilivyosema ,nadhani atasalia na kuweka saini kandarasi mpya''. Wenger bado hajathibitisha iwapo atasalia katika klabu hiyo ya London kaskazini, lakini anasema anafanya kazi ya kuwasajili wachezaji wapya msimu ujao. Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu na amepewa kandarasi mpya. ''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67. ''Wachezaji wanaonunuliwa ndio mpango wa kila klabu katika siku zake za usoni'' ,alisema Wenger. ''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, kilicho muhimu ni siku za usoni za klabu hii'',Wenger alisema mnamo mwezi Februari kwamba ataamua kuhusu kandarasi mpya mnamo mwezi Machi ama Aprili na baadaye kutangaza. ''Najua nitakachofanya na hivi karibuni mutajua''. Mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez hatouzwa kwa kilabu ya ligi ya Uingereza kulingana na mkufunzi Arsene Wenger. text: Awali ''wakili roboti'' iliundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondoka kwenye maeneo ya kuegesha magari ama kupata tiketi za mwendo kasi. Wakati Joshua Browder alipotengeneza DoNotPay aliita " Wakili roboti wa kwanza duniani". Ni chatbot -programu ya kompyuta inayofanya mazungumzo kwa njia ya ujumbe na maagizo ya sauti - na inatumia ujumbe wa Facebook wa Messenger kukusanya taarifa juu ya jambo na kutoa ushauri pamoja na nyaraka za kisheria. Aliyebuni programu ya DoNotPay - Joshua Browder anasema alivutiwa kubuni mfumo huo wa kisheria wa ushauri kwa wahamiaji kwasababu bibi yake alikuwa mkimbizi kutoka Austria wakati wa vita vya Holocaust Awali iliundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondoka kwenye maeneo ya kuegesha magari ama kupata tiketi za mwendo kasi. Lakini sasa Browder - Muingereza mwenye umri wa miaka 20-ambaye sasa anasoma katika chuo kikuu cha Stanford nchini Uingereza - ameweza kuwezesha roboti yake kuwasaidia wanaoomba uhamiaji. Nchini Marekani na Canada, inawasaidia wakimbizi kukamilisha maombi yao ya uhamiaji, na nchini Uingereza, inaweza kuwasaidia wanaoomba uhamiaji katika kupata usaidizi wa kifedha kutoka kwa serikali. ''Wakili roboti'' inapofahamu kwamba mtumiaji anaweza kuomba uhamiaji, huchukua mamia ya maelezo na kujaza moja kwa moja maombi ya uhamiaji. Programu ilitengeneza chatbot kwa kusaidiwa na mawakili kutoka kila moja ya nchi hizo. "hufanya kazi kwa kuuliza msururu wa maswali kubaini kama mkimbizi anapaswa kulindwa na sheria za kimataifa ,"Aliimbia BBC , "kwa mfano: 'una hofu ya kuteswa katika nchi yako unakotoka ?' "inapofahamu kwamba mtumiaji anaweza kuomba uhamiaji, huchukua mamia ya maelezo na kujaza moja kwa moja maombi ya uhamiaji. Umuhimu wake ni kwamba maswali yote ambayo roboti hiyo huuliza ni ya kiingereza kinachoeleweka na akili yake bandia hutengeneza majibu ambayo huonekana wakati wa mazungumzo." Roboti hupendekeza majibu ambayo mtumiaji anaweza kuyachagua ili kupunguza uwezekana wa maombi yake kukubaliwa, kwa mfano: " Jibu zuri kuhusu hali yako litajumuisha maelezo juu ya ni lini unyanyasaji ulianza katika nchi unakotoka." Awali teknolojia ilitumiwa kukabiliana na faini za makosa ya bara barani sasa inawasaidia wakimbizi wenye madai ya kisheria. text: China ni mteja mkubwa wa nguruwe kutoka Marekani Ametia saini hati ya maelekezo kwa maofisa juu ya namna ya kushughulikia suala la ushuru kwa bidhaa za mabilioni ya dola zinazoingizwa kutoka nchini China. Trump amesema awali aliiona China kama rafiki, lakini amebaini kuwa vikwazo vinahitajika baada ya kugundua kuwa China inaonekana kutaka kujinufaisha kijanja katika uendeshaji biashara ambao umekuwa ukiingizia Marekani hasara ya mabilioni ya dola kila mwaka. Amesisitiza kuwa China ni moja kati ya mataifa anayokusudia kuingia katika majadiliano ya kibiashara. "Ndiyo tumeanza majadiliano na umoja wa Ulaya, kwa sababu wametuwekea vikwazo, kuna mazingira ambayo yanawaruhusu kufanya biashara na sisi." "Lakini sisi hatuwezi kufanya biashara na wao. Wana vikwazo vikubwa dhidi yetu, wana ushuru wa forodha mkubwa sisi hatuna, siyo haki.Nao NAFTA wamekuwa wabaya kwetu, lakini tutajitahidi kurekebishana ama kufanya kitu cha ziada. "Mpango wa kibiashara na Korea Kusini ni wa upande mmoja, unatakiwa kufanyiwa mabadiliko. Kwa hiyo kuna mambo mengi yanayotokea, lakini kwa suala la Uchina tutatumia kifungu 301 ambacho kitahusisha dola billion 60 ambazo ni sehemu tu ya hiki tunachokizungumza," alisema Bw Trump. Hatua hii ya rais Trump dhidi ya China imekuja kufuatia uchunguzi wa mwezi Agosti kuhusiana suala la forodha ambao uliagizwa kufanyika na Trump mwenyewe. China kwa upande wake imeonya na kuongeza kuwa iko tayari kujibu mashambulizi ya kibiashara dhidi ya Marekani na imeituhumu Marekani kwa kukiuka sheria za kimataifa za kibiashara. Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mpango wa ongezeko la ushuru wa forodha kwa bidhaa za China, hali inayotarajiwa kuongeza vita vikali vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili kubwa kiuchumi duniani. text: Bob Dylan akubali kuchukua tuzo la Nobel Wanachama wa shirikisho lililotoa tuzo hiyo ya huko Sweden, wamethibitisha hilo baada ya kukutana na mwanamuziki huyo kabla ya kufanya tamasha lake la jana mjini Stockholm. Kinyume na utamaduni wa mbwembwe unaoandamana na utoaji wa tuzo kama hilo, hamna maelezo yoyote ya ziada yaliyotolewa. Bob Dylan mwenye umri wa miaka 75, hakuhudhuria sherehe rasmi za awali za tuzo hilo zilizofanyika Decemba mwaka jana. Bob Dylan mwenye umri wa miaka 75, hakuhudhuria sherehe rasmi za awali za tuzo hilo zilizofanyika Decemba mwaka jana. Sasa amepewa mda wa mpaka tarehe 10 Juni ambapo anatakiwa kutoa hotuba yake kwa mujibu wa taratibu zinazoambatana na tuzo za Nobel , la sivyo hatakabidhiwa fedha zinazoambatana na zawadi hiyo zipatazo dolla laki 9. Mwanamuziki mashuhuri Bob Dylan hatimaye amekwenda kuichukua zawadi yake ya Nobel kuhusu maswala ya fasihi, zaidi ya miezi sita tangu alipotangazwa mshindi. text: Bwa. Trump na mwenyeji wake Shinzo Abe, katika ziara yake ya kwanza nchini Japan na Bara Asia kama Rais wa Marekani Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kwamba, taifa lake litatungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini, "ikiwa hilo litahitajika". Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya Bwana Trump nchini Japan. Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan. Mbona wanamuziki wamempuuza Trump? Korea Kaskazini yaichokoza Japan Abe aishutumu Korea Kaskazini kwa kurusha kombora Trump aapa kukabiliana na Korea Kaskazini kwenye ziara yake ya Bara Asia. Alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari leo Jumatatu, Bw Trump alisema kwamba, Bwana Abe atanunua "kiasi kikubwa cha zana za kivita" kutoka Marekani. Akigusia zana hatari za kinuklea za Korea Kaskazini, Trump alisema kuwa Bw Abe "atazishambulia zikiwa bado angani" mara tu atakapokuwa amemaliza kununua silaha hizo za kijeshi, anazosema kuwa itatoa ajira ya kazi kwa Wamarekani na pia "kutoa usalama kwa Japan". Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan itatungua makombora ya Korea Kaskazini, kwa kutumia mitambo ya kijeshi iliyonunuliwa kutoka Marekani. text: Museveni anasema Bobi alikwenda Marekani na kusema kwamba watu wasije kuekeza Uganda Rais Museveni ameyasema hayo katika mahojiano na BBC. Bwana Museveni anataka kugombea muhula wa sita kama rais mnamo mwaka 2021 baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka 33. Unaweza pia kusoma: Bobi Wine, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la 'The People Power', anamshutumu rais huyo kwa kuongoza kwa mfumo wa ukandamizaji. Bwana Museveni amekataa kumueleza mwandishi wa BBC , Alan Kasujja ikiwa serikali yake ni ya ukandamizaji , lakini akasema anamshughulikia Bobi Wine kama adui. Museveni: 'Bobi Wine ni adui wa maendeleo' Rais huyo wa Uganda amemlaumu Bobi akisema kuwa alikwenda Marekani na kusema kwamba watu wasije kuwekeza Uganda: ''Unapokwenda na kuwaambia wageni kwamba hawapaswi kuja na kuwekeza katika nchi yetu, inamaanisha umeanzisha vita dhidi ya mafanikio yetu. Kwa hiyo kwa nini sasa unataka kurejea na kunufaika na mafanikio hayo?". Hii huenda ndio moja ya sababu za kufutwa kwa matamasha ya muziki ya Bobi Wine, bado sijaongea na polisi kupata taarifa zaidi, alisema. Juhudi za Bobi Wine kuhamasisha umma dhidi ya rais Yoweri Museveni zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama Rais huyo wa Uganda anasema bado ataendelea kuwepo madarakani kwa miaka mingine zaidi kukamilisha kile ambacho yeye binafsi na wapiganaji wenzake walikipanga kukifanikisha katika nchi yao na Afrika. ''Nyumba yangu inanisubiri, lakini tuna masuala kama Uganda ya kushughulikia. Ni masuala hayo ambayo yanatufanya tufanye kile tunachotaka kukifanya kisiasa pamoja na wenzetu. Kama chama tawala (NRM) kitafikiria kuwa hakihitaji mchango wa wazee basi tutaondoka madarakani kwa furaha na kufanya mambo mengine ." Museveni alimueleza mwandishi wa BBC Allan Kasujja mjini Kampala. ''Hatupo hapa kwa ajili ya maonyesho, hatuendi kwenye ukumbi wa michezo ya maigizo , sisi ni watu ambao tupo hapa kushughulikia emasuala makubwa ya Uganda na Afrika ." Alisistiza kiongozi huyo wa Uganda. Bobi Wine ameonyesha kukerwa na kauli ya Museveni kuwa yeye ni adui wa maendeleo. Kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye alikabiliwa na nguvu ya maafisa wa usalama kila alipojaribu kuonyesha upinzani dhidi ya serikali ya Museveni Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani Uganda sasa kwa zaidi ya miongo mitatu. Bwana Museveni amekuwa akikabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu hasa kutoka kwa vijana na wapinzani wake . Mpinzani wake wa muda mrefu Dkt Kizza Besigye amepitia misukosuko mingi katika harakati zake za kisiasa pamoja na Mbunge Bobi Wine ambaye juhudi zake za kutumia usanii wake wa kimuziki kuhimiza ajiuzulu zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama. Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemtaja mkosoaji wake mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa Bobi Wine, kama "adui wa mafanikio ya nchi". text: Mbwana Samatta Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaichezea klabu ya Genk na timu ya taifa ya soka nchini humo taifa Stars. Nahodha huyo wa Tanzania alishinda tuzo ya mchezaji bora wa shirikisho la soka barani Afrika Caf miongoni mwa wachezaji wanaosakata kandanda barani Afrika 2016 baada ya kuisaidia timu yake ya TP Mazembe kushinda kombe la ligi ya Afrika. Wema Sepetu ni miongoni mwa vijana walio na ushawishi mkubwa nchini Tanzania Naye mtangazaji wa habari wa BBC Swahili Salim Kikeke alikuwa wa saba katika kura hiyo akimshinda msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz. Samatta: Kupigania tuzo CAF ni heshima kwa Tanzania Matokeo ya kura hiyo nchini Ghana na Nigeria yalitolewa mapema mwaka huu. Nyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinumz Mchezaji Victor Moses alichaguliwa kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa huku wakili wa rais wa Ghana Kow Essuman akichaguliwa mtu mwenye ushawishi mkubwa nchini humo. Tazama orodha kamili ya vijana walio na ushawishi mkubwa Tanzania: Orodha ya vijana walio na ushawishi mkubwa nchini Tanzania Mchezaji wa soka kutoka Tanzania Mbwana Samatta amechaguliwa kuwa kijana mwenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania kulingana na kura ya maoni iliofanywa na chombo cha habari cha Avance media. text: Takriban watu laki nane waliuwawa ndani ya miezi mitatu. Wenyeji wanaamini kuwa maeneo hayo yana maiti ya watu takriban elfu tatu. Wakati ya mauaji wa kimbari mwaka 1994, zaidi ya watu laki nane waliuwawa ndani ya miezi mitatu. Ugunduzi huo umekuja wiki moja baada ya muda ya maombolezi rasmi ya kukumbuka maafa makubwa ya dunia nchini humo. Watu wakujitolea wamekuwa mstari wa mbele katika kuchimbua makaburi hayo, baada ya kuambiwa kuhusu makaburi hayo na mwanamke mmoja alisema kwamba aliona miili hiyo ikitupwa hapo, zaidi ya miongo miwili iliyopita. Ndugu wa walioathirika na mauaji ya kimbari wamekuwa wakutafuta ishara yoyote ya kuwabainisha kama wapendwao wao walizikwa katika eneo hilo. Lakini ugunduzi huo umezua maswali mengi miongoni ya vyombo vya habari nchini humo ,je ni kwa nini watu waliofahamu kuhusu makaburi hayo hawakujitokeza mapema. Baadhi waliohukumiwa kwa kutekeleza kimbari wamemaliza hukumu yao na kuachiliwa kutoka gerezani. Makaburi ya pamoja yamegundiliwa nchini Rwanda miaka 24 baada ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo. text: Pepe alifunga magoli 23 katika mechi 41 akiichezea Lille msimu uliopita Arsenal italipa kitita hicho kwa awamu kadhaa kulingana na bajeti yao msimu mpya. Makubaliano kati ya Arsenal na wawakilishi wake bado yanasubiri kukamilishwa. Lakini uhamisho huo unatarajiwa kukamilishwa katika kipindi cha saa 24 na 48. Klabu ya Itali Napoli pia ilikutana na Lille kuhusu bei ya mchezaji huyo lakini pendekezo lao likafutiliwa mbali na kambi ya mchezaji huyo. Pepe hupendelea kucheza upande wa kulia na kuingia katikati ya uwanja kupitia mguu wake wa kushoto , lakini pia anaweza kutumika kama mshambuliaji katika mfumo wa 4-2-2. Aliifungia Lille magoli 23 msimu uliokwisha na anaridhisha mahitaji ya Arsenal kwa mchezaji atakayecheza katika wingi kutokana na kasi yake na ufundi. Arsenal ilitoa dau la £40m kumsajili winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha mapema mwezi huu , lakini Crystal Palace inasema kwamba mchezaji huyo ana thamani ya £80m. Arsenal wameafikia makubaliano na klabu ya Ufaransa ya Lille kumsaini winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe katika makubaliano yenye thamani ya £72m. text: Chuo kikuu cha Makerere Uganda Chuo hicho ambacho kimewezaa wanasiasa kama Vile Julius Nyerere na Milton Obote kimeamua kuziangazia shahada zake ambazo zilitolewa kinyume na sheria baada ya kubaini tofauti kati ya matokeo yaliotolewa na chuo hicho na yale ya daraja la mwisho. Kulingana na gazeti hilo,chuo hicho kimesema kuwa ''waziri mmoja wa zamani pamoja na wabunge kadhaa wataathiriwa''. Gazeti hilo limewanukuu maafisa wa polisi wa Uganda wakisema kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho ambao hawakumaliza masomo walighushi vyeti bandia ambazo hutumia kama vyeti rasmi. Ufichuzi huo umesababisha kusimamishwa kazi kwa maafisa sita ambao wanawasaidia polisi kwa uchunguzi. Wiki kadhaa baada ya sherehe ya kufuzu kwa mahafala mnamo mwezi Machi , chuo hicho kilifunga mfumo wa kutoa matokeo wa mtandaoni na kusimamisha utoaji wa matokeo. Kulingana na gazeti la The Monitor, mfumo huo wa matokeo ya mtandao ulikuwa ukitumiwa kuhifadhi matokeo ya wanafunzi. ''Tumeamua kuchunguza matokeo ya miaka mitano iliopita,alisema naibu kansela wa chuo hicho Profesa Barnabas Nawangwe. Akingezea kuwa watadanya uchunguzi huo kwa kina kwa kuwa vyo vyote vimeathiriwa na kwamba wataendelea na uchunguzi huo iapo mtu yeyote atashukiwa kufanya udanganyifu''. Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kinachunguza uhakiki wa alama na viwango vya shahada zilizotolewa tangu 2011 kwa lengo la kuziangazia upya zile zilizotolewa kinyume na sheria text: Maandalizi ya mdahalo huo yanaendelea katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA). Mdahalo huo, ambao ungepeperushwa kupitia runinga, ulipangiwa kufanyika leo jioni, awamu ya kwanza ikishirikisha wagombea sita na ya pili wagombea wawili. Katika awamu ya kwanza, ni mgombea mmoja pekee aliyejitokeza, Eliud Muthiora Kariara ambaye ni mgombea mwenza wa Japheth Kaluyu. Baadhi ya wagombea wenza wa urais walikuwa wametangaza kwamba hawatashiriki katika mdahalo huo ambao ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA). Hatua ya wagombea kutojitokeza imeonekana kuwakera baadhi ya Wakenya mtandaoni, mfano Edwin Bakanja aliyeandika: "Ukikosa kufika kwa mahojiano, usisubiri upewe kazi." Miongoni mwa waliojitoa kutoka kwenye mdahalo huo ni mgombea mwenza wa chama cha Jubilee chake Rais Kenyatta, Naibu Rais William Ruto. Mgombea mwenza wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa), wake Raila Odinga, Makamu Rais wa zamani Kalonzo Muysoka pia alitangaza kwamba hapangi kuhudhuria mdahalo huo. Chama cha Jubilee kilikuwa kimedokeza kwamba kitamtuma mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa, ambaye hana mtu anayempinga uchaguzini eneo bunge lake, angemuwakilisha Bw Ruto. Kwa mujibu wa gazeti la Standard la Kenya, wagombea wenza Eliud Kariara, Emmanuel Nzai, Joseph Momanyi, Miriam Mutua, Titus N'getuny na Moses Maranga walikuwa wamemwandikia mwenyektii waandalizi wa mdahalo huo Debates Media Limited Wachira Waruru kusema hawakuwa wamepokea mawasiliano yoyote kuhusu mpangilio wa mdahalo huo. Waandalizi hata hivyo walikuwa wamesema kwamba watawakubali wagombea wenzake pekee na kwamba mdahalo huo utaendelea kama ilivyopangwa. Mdahalo wa wagombea urais umepangiwa kufanyika Jumatatu wiki ijayo. Bw Kenyatta pia ametishia kutohudhuria mdahalo huo sawa na Bw Odinga. Wawili hao walisema kuwa hawakushirikishwa wakati wa maandalizi ya mdahalo huo, na hawafurahishwi na mpangilio wake. Utata umegubika mdahalo wa moja kwa moja ambao unafaa kuwashirikisha wagombea wenza wa urais nchini Kenya. text: Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016. Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza. Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa". Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative. Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo. Miaka 3 ahudumu kama waziri baada ya kuondoka David Cameron Miaka 6 kabla ya hapo, waziri wa mambo ya ndani Ashindwakatika uchaguzi mkuu 2017 , lakini asalia waziri mkuu Asaliampiga kura katika kura ya maoni ya EU mnamo 2016 Brexit iligubika muda aliohudumu 10 Downing Street Sauti yake ilittereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: "Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maihsani mwangu kuhudumu. "Waziri mkuu mwanamke wa pili, na bila shaka sio wa mwisho. "Nachukua hatua hii bila ya uovu wowote, bali na shukrani za dhati na kubwa kutokana na kupata fursa kuitumikia nchi ninayoipenda." Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza. text: Serikali ya Zanzibar imesema si mara ya kwanza kuwa na ugeni kama huu visiwani humo Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu, na wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo. Katika mahojiano maalum na BBC naibu waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya waalimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo. Ameongeza pia wameamua kwenda mchini Nigeria kwa sababu kuna wingi wa waalimu na wenye ubora na haikuwa rahisi kuchukua kutoka nchi za karibu kwa sababu na wao pia wana tatizo la uhaba wa waalimu. ''Mchakato wa upatikanaji wa waalimu hawa hufanywa kwa kutegemea uwezo wao katika ufundishaji na pia ubora wa kazi zao.'' alisema waziri Mjengo. Serikali ya Zanzibar imesisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa ujio kama huu kwani katika miaka ya nyuma waalimu hawa wamekua wakija kwa kujitolea. Ujio wa waalimu hawa ambao watakuwepo kwa kipindi cha miaka miwili unatajwa kupunguza uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 visiwani humo. Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo. text: Bobi Wine ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulani , hivi majuzi alitangaza kwamba atamkabili bwana Museveni mwenye umri wa miaka 75 katika kinyanganyiro cha urais katika uchaguzi wa 2021. Rais huyo wa Uganda amekuwa madarakani tangu 1986. Katika ujumbe wake wa twitter Bobi Wine alimtaja rais huyo kuwa adui wa Uganda ambaye anaongoza kupitia 'mtutu wa bunduki'. Katika mahojiano hayo ya BBC , bwana Museveni alidai kwamba msanii huyo wa muziki alikuwa amesema katika ziara yake Marekani kwamba watu hawafai kwenda Uganda na kuwekeza. Lakini mgombea huyo wa urais alisema kwamba Museveni huenda amekuwa akiota ndoto kwa kuwa hajawahi kutoa matamshi kama hayo. Katika taarifa ambayo alisema huenda rais huyo alikuwa akizungumzia mnamo mwezi Septemba 2018 katika mahojiano na Al jazeera, alisema kwamba ''Wamarekani wanafaa kuwa na wasiwasi wa kumpatia Museveni ufadhili wa kijeshi kwa kuwa ufadhili huo hautumiki kuwalinda raia wa Uganda''. Bwana Museveni anataka kugombea muhula wa sita kama rais mnamo mwaka 2021 baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka 33. Bobi Wine, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la 'The People Power', anamshutumu rais huyo kwa kuongoza kwa mfumo wa ukandamizaji. Bwana Museveni amekataa kumueleza mwandishi wa BBC , Alan Kasujja ikiwa serikali yake ni ya ukandamizaji , lakini akasema anamshughulikia Bobi Wine kama adui. Museveni: 'Bobi Wine ni adui wa maendeleo' Rais huyo wa Uganda amemlaumu Bobi akisema kuwa alikwenda Marekani na kusema kwamba watu wasije kuwekeza Uganda: ''Unapokwenda na kuwaambia wageni kwamba hawapaswi kuja na kuwekeza katika nchi yetu, inamaanisha umeanzisha vita dhidi ya mafanikio yetu. Kwa hiyo kwa nini sasa unataka kurejea na kunufaika na mafanikio hayo?". Hii huenda ndio moja ya sababu za kufutwa kwa matamasha ya muziki ya Bobi Wine, bado sijaongea na polisi kupata taarifa zaidi, alisema. Juhudi za Bobi Wine kuhamasisha umma dhidi ya rais Yoweri Museveni zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama Rais huyo wa Uganda anasema bado ataendelea kuwepo madarakani kwa miaka mingine zaidi kukamilisha kile ambacho yeye binafsi na wapiganaji wenzake walikipanga kukifanikisha katika nchi yao na Afrika. ''Nyumba yangu inanisubiri, lakini tuna masuala kama Uganda ya kushughulikia. Ni masuala hayo ambayo yanatufanya tufanye kile tunachotaka kukifanya kisiasa pamoja na wenzetu. Kama chama tawala (NRM) kitafikiria kuwa hakihitaji mchango wa wazee basi tutaondoka madarakani kwa furaha na kufanya mambo mengine ." Museveni alimueleza mwandishi wa BBC Allan Kasujja mjini Kampala. ''Hatupo hapa kwa ajili ya maonyesho, hatuendi kwenye ukumbi wa michezo ya maigizo , sisi ni watu ambao tupo hapa kushughulikia emasuala makubwa ya Uganda na Afrika ." Alisistiza kiongozi huyo wa Uganda. Bobi Wine ameonyesha kukerwa na kauli ya Museveni kuwa yeye ni adui wa maendeleo. Kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye alikabiliwa na nguvu ya maafisa wa usalama kila alipojaribu kuonyesha upinzani dhidi ya serikali ya Museveni Rais Yoweri Museveni amekuwa madarakani Uganda sasa kwa zaidi ya miongo mitatu. Bwana Museveni amekuwa akikabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu hasa kutoka kwa vijana na wapinzani wake . Mpinzani wake wa muda mrefu Dkt Kizza Besigye amepitia misukosuko mingi katika harakati zake za kisiasa pamoja na Mbunge Bobi Wine ambaye juhudi zake za kutumia usanii wake wa kimuziki kuhimiza ajiuzulu zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amemjibu rais Yoweri Museveni ambaye katika mahojiano na BBC alimtaja kuwa adui wa maendeleo nchini humo. text: Tse Chi Lop alikamatwa katika uwanja wa ndege Amsterdam airport Ijumaa Tse Chi Lop - Raia wa Canada mwenye asili ya China - inasemekana kuwa yeye ndio kiongozi wa genge hilo, ambalo linamiliki karibu dola bilioni 70 la soko haramu la dawa za kulevya kote barani Asia. Akiorodheshwa kama mmoja wa watoro wanaotafutwa, Bwana Tse alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Schiphol, Amsterdam. Sasa Australia itataka ahamishwe hadi nchini humo kukabiliana na mkono wa sheria. Polisi nchini Australia inaamini kuwa kampuni ya mlanguzi huyo ambayo pia inafahamika kama Sam Gor Syndicate, ndio inayoingiza hadi asilimia 70 ya mihadarati nchini humo. Mlanguzi huyo, 56, amekuwa akilinganishwa na mlanguzi wa Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman kwasababu ya ukubwa wa biashara yake haramu anayoendesha. Polisi nchini Australia inasemekana kwamba imekuwa ikimtafuta Bwana Tse kwa zaidi ya miaka kumi kabla ya kukamatwa Ijumaa wakati akiwa anasubiri kuingia ndege ya kwenda Canada. Taarifa ya polisi ambayo haikutaja jina la Bwana Tse, ilisema kibali cha kukamatwa kwake kilitolewa 2019, huku polisi nchini Uholanzi wakifanyia kazi taarifa iliyotolewa na Interpol. "Alikuwa kwenye orodha ya wanaotafutwa na alikuwa anazuiliwa kulingana na taarifa za shirika la ujasusi," Msemaji wa polisi Uholanzi amesema Ijumaa. Shirika la habari la Reuters lilichapisha uchunguzi maalum kuhusu Bwana Tse mwaka 2019 - na kumuelezea kama "Mtu anayetafutwa zaidi Asia". Shirika hilo lilinukuu makadirio ya UN yalionesha kwamba mapato ya genge hilo kutokana na uuzaji wa dawa ya methamphetamine pekee huenda ni dola bilioni 17 mwaka 2018. Juhudi za kumkamata Bwana Tse, zilijumuisha mashirika karibu 20 ya mabara mbalimbali duniani huku lile la AFP likishika usukani, kulingana na shirika la Reuters. Ilisemekana kwamba miaka ya karibuni Bwana Tse amekuwa akiendesha shughuli zake katika miji ya Macau, Hong Kong na Taiwan. Awali, alitumikia kifungo cha miaka 9 gerezani baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Marekani miaka 1990. Vyombo vya habari vya Australia vimeelezea kukamatwa kwake kama "muhimu zaidi" kwa kikosi cha polisi nchini humo katika kipindi cha miaka 20. Polisi nchini Uholanzi wamemkamata anayesemekana kuwa kiongozi wa genge moja kubwa la ulanguzi wa mihadarati duniani, baada ya Australia kutoa kibali cha kukamatwa kwake. text: Bwana Chamisa alisema siku ya Jumatatu kwamba uchaguzi huo wa Jumamosi ulifanyiwa udanganyifu ili kumpatia rais Mnangagwa ushindi. Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung'atuliwa madarakani.Biashara zimefungwa katika mji mkuu wa Zimbabwe harare huku taifa hilo likisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yanayozozaniwa. Matumizi ya nguvu ya serikali dhidi ya upinzani nchini Zibabwe baada ya uchaguzi wa Jumatatu yameichochea jamii ya kimataifa kutoa wito wa kumaliza vurugu. Umoja wa mataifa na umoja wa ulaya kwa pamoja wamekemea juu vurugu zilizotokea na polisi kufyatua risasi kwa waandamanaji. Makundi ya waandamanaji yalikuwa katikati ya mji huo tangu alfajiri lakini habari zilipozuka kwamba Zanu PF imeshinda viti vingi katika bunge na kwamba matokeo ya urais hayakuwa tayari , hali ilibadilika. Ghasia zazuka nchini Zimbabwe Lakini upinzani wanasema kuwa ZANU PF imeingilia uchaguzi. Uchaguzi wa Jumatatu ulivutia asilimia 70 ya wapiga kura. Chombo cha habari cha ZBC kimesema kuwa Zec itatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais mwendo wa 12.30 za Zimbabwe. Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe inasema asilimia 70 ya wazimbabwe walijiandikisha kupiga kura .Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema kuwa serikali ya Zimbabwe inatakiwa kuhkikisha kuwa vurugu hizo hazitokei. Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International linaitaka serikali kufungua mashataka kwa polisi waliofyatua risasi kwa waandamanaji. ''vikosi vya usalama vinapoingilia uchaguzi ni kuwanyima haki wananchi ya kujieleza'' amesema katibu wa Amnesty. Ni matokeo gani ambayo yametangazwa hadi sasa? Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe(Zec) hadi sasa imetangaza ushindi wa viti 140 kwa chama tawala cha Zanu-PF, huku kile cha Muungano wa Upinzani MDC kikiwa na viti 58 , Kulingana na taarifa ya Shirika la Utangazaji la taifa ZBC . Kuna viti 210 Katika Bunge la Taifa la taifa. Zaidi ya watu milioni tano walijiandikisha kupiga kura, na watu wengi walijitokeza kushiriki uchaguzi kwa kiwango cha 70%. Ramani inayoonyesha chama kilichoshinda katika kila jimbo Ni nini wanachosema wakaguzi wa uchaguzi? Wanajeshi waliojihami wamepiga doria wakiwataka raia kuwa na nidhamu.Watu watatu waliuawa mjini humo siku ya Jumatano wakati wa ghasia kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani nelson Chamisa. text: Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake. Bwana Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari ama 'Correspondents diner' iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House wakati huo. Hafla hiyo ni miongoni mwa hafla maarufu sana mjini Washington. Akihutubia umati mkubwa katika jimbo la Pennsylvania, Rais Trump amelinganisha na kutofautisha, kile ametaja 'siku mia moja za wanahabari kushindwa na kazi yao', na mafanikio yake ambapo amesema amekuwa akitimiza 'ahadi zake kila siku', hususan kurejesha kazi za viwanda na kumaliza mzozo katika sekta ya makaa ya mawe. Pennsylvania ni jimbo linalotegemea uchumi wa uchimbaji madini, na lilikuwa muhimu sana katika uchaguzi wa mwaka jana. Awali maelfu ya watu waliandamana nchini Marekani dhidi ya utawala wa rais Trump na msimamo wake kuhusu mazingira. Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kutoa hotuba ya kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake. text: Alisema hayo alipohutubiwa wanahabari kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa kuwa mrithi wa Arsene Wenger. Mkufunzi huyo wa miaka 46 aliwasilishwa rasmi kwa mashabiki na wanahabari Jumatano kabla yake, akiandamana na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis kuhutubia waandishi wa habari waliokuwa wamefika kwa wingi. Alisema: "Ufanisi msimu ujao utakuwa bado tunaukuza, lakini kwa jinsi gani? Kwa kupigania kila taji. "Hilo limo ndani ya historia ya Arsenal na yangu mwenyewe." Arsenal walishindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2017 na hawatashiriki michuano hiyo msimu wa 2018-2019. Awali, walikuwa wamefuzu kila mwaka tangu 1998. Mhispania huyo Gazidis alifichua kwamba Mhispania huyo alikuwa kwenye orodha ya wakufunzi wanane ambao walikuwa wamewekwa kwenye mizani kumtafuta mtu wa kumrithi Wenger, lakini yeye ndiye aliyekuwa naatafutwa zaidi. "Wote wanane walishiriki mahojiano ya kina na hakuna hata mmoja aliyejiondoa kwenye mchakato huo," Gazidis alisema. Aliongeza kwamba kazi hiyo ni moja ya zinazotutia zaidi katika ulimwengu wa soka. "Tuna bahati sana kumpata mtu tuliyemtafuta tangu awali. "Mahojiano yetu ya kwanza tuliyafanya mnamo 25 Aprili na ya mwisho tuliyafanya 15 Mei. pendekezo la mwisho kwa bodi lilitolewa likiambatana na barua ya kurasa 100 yenye maelezo ya kina. "wanachama wote wa bodi walifurahia uamuzi wetu." Gazidis wanasema meneja huyo wa zamani wa Valencia, Sevilla na Paris St-Germain aliwapendeza sana waliokuwa wanafanya mahojiano hayo kutokanana jinsi "alivyokuwa amejiandaa". "Alifanya vyema saa na alikuwa amejiandaa tena kwa ujuzi wake kuhusu Arsenal na utathmini wa wachezaji wetu, uwezo wao na jinsi wanavyoweza kuboreshwa. "Jambo lililowatenganisha na wengine ni jinsi tulivyohusiana vyema na hisia za soka zilivyojitokeza chumbani. "Ana hisia fulani na moyo wa ushindani na ana moyo anapenda soka. Hizi pamoja na azma yake ya ushindi ndivyo vilivyotufanya kuamini kwamba anaifaa Arsenal." Emery aliwaambia wanahabari kwamba alisafiri kwenda Atlanta akiandamana na Gazidis, mkuu wa uajiri wa wafanyakazi Sven Mislintat na mkuu wa uhusiano wa soka wa klabu hiyo Raul Sanllehi ili kukutana na mwenyehisa mkuu Stan Kroenke na familia yake. "Tunataka kufanyia kazi klabu hii kwa pamoja," aliongeza. "Naijua azma yangu na kujitolea kwangu na najua ninavyotaka kukua pamoja na Arsenal. Emery alihariri maelezo yake kwenye Twitter baada ya uteuzi wake, kuonesha majukumu yake mapya "Mazungumzo yote nimekuwa nayo na klabu hii yanaonesha tuna ndoto moja kwa klabu hii." Arsenal walimaliza nafasi ya sita Ligi ya Premia msimu uliopita, nafasi yao ya chini tangu walipomaliza nafasi ya 12 msimu wa 1994-95. Mashabiki wamekuwa wakilalamikia uwezo wa wachezaji wa klabu hiyo kwa sasa. Alipoulizwa iwapo atahitaji kuajiri wachezaji zaidi majira yajayo ya joto, Emery alisema: "Ninaamini tunaweza kukua na wachezaji tulio nao. "Lengo ni kufanya kazi kwa pamoja na wachezaji hawa wenye vipaji. "Ni muhimu sana kwa klabu hii, baada ya kukaa miaka miwili nje ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, kufanya kazi kuwa klabu bora zaidi Ligi ya Premia na hata duniani." Alimsifu sana pia Wenger ambaye ameongoza klabu hiyo kwa miaka 22. "Kwa wakufunzi wote duniani, yeye ni wa kurejelewa. Tulijifunza, nilijifunza mambo yote kuhusu soka kutoka kwake. "Ni changamoto kwangu, lakini pia nimefanya miradi mingine, miradi mikubwa. kwangu, najivunia kuwa hapa na kufanya kazi baada ya Arsene Wenger." Emery ametimiza nini? Emery, 46, amejiunga na Gunners baada ya kuondoka PSG ambapo aliwaongoza kushinda ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1. Mhispania huyo pia alishinda vikombe vya ligi mara nne akiwa na miamba hao wa Ufaransa. Awali alikuwa meneja wa Sevilla ambapo aliwasaidia kushinda Europa League mara tatu mtawalia. Meneja mpya wa Arsenal Unai Emery amesema anataka klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu bora zaidi Ulaya kwa mara nyingine, na hata bora duniani. text: Sven Goran Eriksson zamani alikuwa kocha wa timu za England, Mexico na Ivory coast. Eriksson mwenye umri wa miaka , 70, raia wa Sweden alikuwa na mazungumzo mazuri na maafisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (Fecafoot) mjini Yaoundé wiki iliyopita waliokuwa wakitaka kuziba pengo lililoachwa baada ya kuondoka kwa Hugo Broos. "Baada ya kukaa saa 72, Sven-Goran Eriksson aliondoka Yaoundé Jumamosi tarehe 28 July 2018," Fecafool lilieleza kwenye ukurasa wake wa Twitter. " Meneja huyo raia wa Sweden alikuwa amekaribishwa na Cameroon kwa mazungumzo juu ya kuajiriwa kwa kocha mkuu wa timu kuu ya taifa - the Indomitable Lions. " Baada ya kumpa mtihani wa kazi Sven-Goran Eriksson na kuzingatia mapendekezo mengine yaliyopo, Fecafoot litafichua chaguo lake la kocha wa kudumu wa timu yetu ya taifa lilieleza shirikisho hilo la mpira wa miguu la Cameroon. Aliyekuwa kocha wa timu ya Indomitable Lions Hugo Broos, aliondoka mwezi Februari mwaka huu baada ya mkataba wake kuisha Eriksson, ambae alikuwa meneja wa England kati ya mwaka 2001 na 2006, na kuifikisha timu hiyo hadi michuano ya robo fainali ya Kombe la Dunia mara mbili, alikuwa mmoja wa watu 77 ambao maombi yao ya kazi yalifichuliwa mwezi Aprili. BBC inafahamu kuwa Eriksson, ambaye awali alikuwa mkufunzi wa klabu za England Manchester City na Leicester City, atalipwa CFA 50 million (€71,000) kila mwezi na atafanya kazi na kocha msaidizi raia wa Cameroon na ataishi nchini humo. Vyombo vya habari nchini Cameroon pia vimewahusisha Waholanzi Clarence Seedorf na Patrick Kluivert na kazi hiyo. Awali Eriksson alizifunza timu za Mexico na akafanikiwa kuipeleka led Ivory Coast katika Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini kabla ya kuwa meneja wa timu ya Uchina ya Guangzhou Evergrande mnamo 2013. Akiwa Uchina pia alipata fursa ya kuzifunza timu za Shanghai SIPG na Shenzhen, kabla ya kuondoka hukomwezi June 2017. Pia amekuwa akihusishwa na Iraq kama kocha. Kazi ya kocha wa timu ya Cameroon ilikuwa wazi mwezi Februari wakati aliekuwa kocha wa timu Indomitable Lions Hugo Broos, alipoondoka baada ya mkataba wake kuisha. Cameroon imethibitisha kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson kuchukua usukani wa kuifunza timu ya taifa hilo Indomitable Lions. text: Utambuzi wa virusi vya corona unaanza katika uwanja wa ndege wa Singapore Huku baadhi ya mataifa yakipata maafa mabaya zaidi kama vile China, Uhispania, Italia na Marekani , mengine yameidhinisha mikakati ambayo imezuia kusambaa zaidi kwa virusi vya corona. Na mipango hiyo iko tofauti kuanzia kuwafanyia raia wake vipimo vingi hadi kujitenga katika mikutano ya watu wengi., kusalia majumbani hadi kuchunguza maeneo ambayo raia wake wapo hatarini zaidi kuambukizwa. 1.Kwa nini Ujerumani ina vifo vichache vya coronavirus ikilinganishwa na mataifa mengine Licha ya kuwa taifa la tano lenye idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya covid 19 duniani (wagonjwa 71,808), idadi ya waathiriwa waliofariki 775 ni ndogo sana ukilinganisha na mataifa mengine ambayo yameripoti idadi inayolingana nao ya maambukizi kama vile Italia (wagonjwa 105,792 vifo 12,428), Uhispania (wagonjwa 95,923 vifo 8,464) na Uchina (wagonjwa 82,294 vifo 3,310). Hata Uingereza yenye wagonjwa 25,481 ambao ni wachache kulinganisha na Ujerumani, ina idadi ya vifo 1,793 ambayo ni zaidi ya mara mbili ya Ujerumani. Ujerumani ilisema kwamba ina uwezo wa kupima visa 160,000 kwa wiki Ipi siri ya mafanikio hayo ya kuzuia idadi ya vifo? ''Ijapokuwa hatujui sababu mwafaka, ukweli ni kwamba ...baada ya taifa hilo kugundua kuhusu hatua za dharura , lilianza kupanua vipimo vyake miongoni mwa raia ili kuzuia uwezekano wa maambukizi zaidi'', alisema Robert Koch kutoka taasisi ya masuala ya virusi akizungumza na BBCMundo. Mojawapo ya sababu muhimu ya idadi ndogo ya vifo ni jinsi taifa hilo lilivyofanikiwa kuwatambua mapema wanaobeba virusi hivyo, hatua iliozuia kuenea kwake. Mamlaka ya Ujerumani ilisema kwamba ina uwezo wa kufanya vipimo 160,000 kwa wiki. Mataifa mengine ambayo yana maambukizi chungu nzima yamekuwa yakiwafanyia vipimo waliothibitishwa kukutwa na virusi hivyo huku yakiwapuuza wale walio na dalili chache . 2.Jinsi Japani ilivyofanikiwa kudhibiti covid-19 bila kutumia karantini Huku ulimwengu ukikabiliana na mlipuko wa virusi vya corona, taifa la Japani lilpo eneo mwafaka kwa virusi hivyo kufanya madhara makubwa. Taifa hilo lipo karibu na Uchina kijografia. Pia Japani ina idadi kubwa ya watu walio na umri wa juu kuanzia miaka 65 duniani na lina kiwango kikubwa cha watu wanaotumia tumbaku suala linalofanya raia wake kuwa miongoni mwa watu walio hatarini kuambukizwa virusi vya corona. Lakini huku mataifa mengine yakichukua mbinu ya kukaa mbali na mikutano ya watu wengi ili kuzia kusambaa kwa virusi hivyo, serikali ya Japani iliamua kuendelea kuwaruhusu raia wake kukongamana. Ijapokuwa wanapendekeza watu kuwa mbalimbali , mamlaka haijawalazimu raia kuchukua hatua kama zile zilizochukuliwa na China , Uhispania na Italia katika wiki za hivi karibuni. Hakuna marufuku iliyowekwa kwa watu kutoka nje kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa. Ikilinganishwa na China na Korea, maambukizi nchini Japan na vifo viko chini sana. Japani ina wagonjwa 2,233na mpaka sasa imeripoti vifo 66. Mojawapo ya sababu ya idadi hiyo kuwa chini ni hatua ya taifa hilo kutambua maeneo ya maambukizi na kuwalinda wale walio hatarini kupata maabukizi hayo mbali na makundi ya milipuko. Hata hivyo, taifa hilo limchukua hatua za kuzuia safari za ndege baina yake na mataifa yaliyoathirika sana kama Uchina na Marekani. Pia vyombo vya habari vimeripoti wiki hii kuwa wasafiri watakaoingia nchini humo watalazimika kujiweka karantini kwa siku 14 ili kujichunguza kama wana dalili za virusi hivyo. 3. Vifaa vya kubaini Corona nchini Singapore Kufanyiwa uchunguzi na kujitenga ndio hatua muhimu za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19. Lakini Singapore ilichukua hatua zaidi: Ilitumia vifaa vya kutambua ugonjwa huo kubaini hasa uko wapi. Na hivyo ikafanikiwa kuudhibiti kutoka eneo la kitovu cha maambukizi. Singapore ina mfumo imara na thabiti wa kufuatilia mawasiliano yanayowezesha ufuatiliaji wa waliotangamana na wagonjwa kwa urahisi kutoka mtu mmoja hadi mwingine ambapo watu na jamaa zao wa karibu wanaweza kutambuliwa na kutengwa kwa wakati unaofaa. Kupitia njia hii, nchi hiyo ilifanikiwa kumaliza maambukizi katika maeneo ambayo ulikuwa umesambaa sana. Mpaka sasa nchi hiyo imeripoti wagonjwa 926 na vifo 3. Kuna programu nchini Singaore inayowatambua wale waliokaribiana na mgonjwa 4. Watu wa Italia waliofanikiwa kudhibiti kusambaa kwa virusi baada ya kupata maambukizi Si kila taarifa kutoka Italia juu ya virusi vya corona ni mbaya. Mji unaovutia eneo la Veneto unaofahamika kama Vo Euganeo ulikuwa moja ya kitovu cha ugonjwa wa covid-19 nchini humo. Eneo hilo likawa mbioni kukabiliana na jinamizi hili: Kituo cha kufanyiwa uchunguzi kikafunguliwa kwa wote wanaotaka kupimwa. Kulingana na BBC Mundo, Profesa wa magonjwa ya maambukizi na virusi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Padua, Andrea Crisanti, wakafanikiwa kupima kila mmoja katika mji huo. Na kuanzia hapo wakaamua kuanza kufanya uchunguzi wa kufuatilia virusi hivi na kufikia yafuatayo: "Kisayansi walibaini kwamba kipindi cha kirusi kuhamia ni wiki mbili na kwamba mkakati wa kudhibiti maambukizi lazima utilie maanani idadi kubwa ya watu ambao wameshaanza kuonesha dalili." Na kwa data hizi, wakafanikiwa kudhibiti mlipuko wa janga hili katika eneo husika. Ni watu 63 pekee waliofariki Korea Kusini kutokana na ugonjwa wa coronavirus 5. Mkakati uliotumiwa na Korea Kusini kunusuru maisha ya wengi Korea Kusini ilikuwa mfano duniani kwa sababu licha ya kwamba majirani zao ni China, chimbuko la ugonjwa wa Corona, idadi ya maambukizi na vifo ni ya chini. Mpaka sasa nchi hiyo imeripoti wagonjwa 9,887 na vifo 165. Kulingana na serikali ya Korea Kusini karibia watu 10,000 wanachunguzwa kila siku, na kufanya iwe rahisi kutenga wale wanaoonesha dalili, moja ya tatizo kubwa la usambazaji wa maambukizi. Aidha, matukio mengine yaliyosaidia kudhibiti janga hili Korea Kusini ni utekelezaji wa hatua ya kujitenga bila kuzembea katika maeneo ya nchi hiyo. Ingawa baadhi ya hatua za kujitenga zimekosolewa kwa kuwa kali zaidi. Wataalamu waliozungumza na BBC wamesema kwamba zilikuwa muhimu katika kuokoa maisha. Ni vigumu kupata mtu yeyote asiyetambua mlipuko wa virusi vya Coivid-19 kuwa ni janga baya zaidi duniani tangu Vita vya Pili vya Dunia. text: Hillary Clinton alitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund katika Newseum mjini Washington DC Bi Clinton, akihutubu mjini Washington DC amesema alikuwa hataki kutoka nyumbani tena. Ameambia shirika la kuwasaidia watoto wasiojiweza kwamba uchaguzi huo umewafanya Wamarekani wengi kutafakari. Bi Clinton aliongoza kwa wingi wa kura za kawaida lakini akashindwa kinyang'anyiro cha urais kupitia kura za wajumbe, ambazo ndizo huamua mshidni wa urais. "Sasa, nitakiri kwamba kuja kwangu hapa halikuwa jambo rahisi," alisema alipokuwa akitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund. "Kuna nyakati kadha wiki hiyo moja iliyopita ambapo nilitaka kujikunyata tu nikiwa na kitabu kizuri na nisiwahi kutoka nje ya nyumba tena." Aliendelea: "Ninajua wengi wengu mmevunjwa moyo sana na matokeo ya uchaguzi. Hata mimi, pia, zaidi kushinda ninavyweza kueleza. "Ninajua si jambo rahisi. Najua wiki moja iliyopita, watu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo Marekani ni nchi ambayo tumekuwa tukiamini ndiyo. "Migawanyiko iliyowekwa wazi na uchaguzi huu imekolea, lakini tafadhali nisikezi ninaposema hili. "Marekani ni ya thamani. Watoto wetu ni wa thamani. Kuweni na imani katika nchi yetu, mpiganie maadili yetu na daima, msikate tamaa." Alipokuwa anatoa hotuba ya kukubali kushindwa wiki iliyopita, Bi Clinton alsiema Bw Trump anafaa kupewa fursa ya kuongoza. Tangu wakati huo, amekuwa haonekani, ingawa siku moja alionekana akifanya matembezi porini. Bi Clinton alishinda ngome za Democratic California, Oregon, New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island, Hawaii, Washington na District of Columbia, pamoja na New Mexico na Colorado. Kwenye mawasiliano ya simu ambayo yalifichuliwa kwa wanahabari Marekani, alisikika akimlaumu mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey, aliyetangaza kuanzishwa kwa uchunguzi mpya kuhusu kashfa yake ya barua pepe zikiwa zimesalia siku 11 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika. Baadaye uchaguzi ulipokuwa umekaribia kabisa, Bw Comey alisema hakukupatikana ushahidi mpya ambao ungebadilisha uamuzi wa awali wa FBI kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumfungulia mashtaka. Mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameelezea masikitiko yake alipojitokeza hadharani mara ya kwanza tangu ashindwe kwenye uchaguzi wa rais nchini Marekani na Donald Trump wa chama cha Republican. text: Utafiti umefanyiwa wachezaji 536 kutoka timu 20 zilizokuwa kwenye ligi mwaka 2017-18 kukuwezesha kubaini ikiwa mtoto wako anaweza kufika kileleni mwa ligi ya Uingereza. Kutokana na utafiti huu unaweza kuchukua hatua hizi kumwezesha mtoto kuingia katika taaluma ya soka. Tahadhari: Kwa kutumia mbinu hizi hatuwezi kuhakikishia kuwa mtoto wako anaweza kuja kuwa mcheza soka hodari Wakati wa kumzaa mtoto wako Sasa hili litahitaji kupangwa vizuri na uhakikishe kuwa mtoto wako amezaliwa tarehe 28 Mei ambayo ni siku ya kuzaliwa ya wachezaji wengi wa Ligi ya Premia. Wanasoka watano walikuwa na bahati ya kuzaliwa tarehe hii na kama mtoto wako naye atabahatika itakuwa vyema. Hii ni kutokana na sababu watatu kati ya wachezaji hawa wako timu moja. Ikimaanisha kuwa mara moja kwa mwaka Phil Foden, John Stones na Kyle Walker watakata keki moja huko Manchester City. Kwa wale ambao hawawezani na hili basi tarehe 15 ya kila mwezi huzalisha wachezaji bora zaidi, Januari ukiwa mwezi maarufu zaidi huku Jumatano ikiwa ndiyo siku maarufu zaidi ya kuzaliwa kwa wachezaji. Kwa hivyo hii inakupa njia ya kukakisha mtoto wako ata uwezekano wa juu wa kuwa kwenye ligi ya Uingereza. Jinsi ya kumvalisha mtoto wako Ushauri mkuu: Wanunulie nguo kubwa ili wakue nazo. Wachezaji wa ligi ya Premia wana kimo cha wastani cha sentimita 182.9 karibu futi 6. Jezi nambari 7 ndiyo maarufu zaidi Lakini kimo sio kila kitu: Wanaweza kuwa wafupi hadi hata sentimita 161 (futi 5) kama Angel Gomes wa Manchester United. Pia unaweza kujaribu kuandika herufi 7 nyuma ya jezi au fulana za mtoto wako kwa kuwa ndio namba huvaliwa sana kwenye Ligi ya Premia. Sehemu ambapo utamlea mtoto wako Taarifa nzuri kwa wazazi wote wanaoishi jijini London kwa sababu hawahitaji kuhama. Huu ndio mji umezalisha wachezaji wengi zaidi katika Ligi ya Uingereza ukiwa na asilimia 2.8 ya wachezaji wanaotokea hapa. Liverpool inachukua asilimia (1.3%), Birmingham (1.3%), Manchester (1.1%) na Sheffield (0.9%), huku asilimia ndogo ikichukuliwa na Bath (0.6%), Chester (0.6%) na Stockport (0.9%) Pia kuna nchi nje ya Uingereza zinazoonekana kuwa bora kwa kuzalisha wachezaji wa Ligi wa Premia zikiweko Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani na Uhispania huku nao mji mku wa Senegal Dakar na mji wa Uholanzi Amsterdam, ikiwa miji maarufu zaidi ya kigeni kuzalisha wachezaji wa Ligi ya Kuu ya England. Jina unalompa mtoto wako Mwisho ni majina yapi unaweza kumpa mtoto ili apate kuwa na bahati ya kucheza katika Ligi ya Premia. Jina maarufu zaidi la kwanza kati Ligi ni Daniel, la kati kati ni James na jina la mwisho ni Silva ambalo mara nyingi huwa na 'da' Majina ya katikati hayana uzito sana kwa sababu wengi wa wachezaji huwa na jina moja tu. Ni wachezaji watano wana majina matatu ya kati kama vile mchezaji wa Brighton David Petrus Wenceslaus Henri Propper.. Kwa ufupi kwa kufuata takwimu hizi, ndipo uweze kuwa na mchezaji kamili unafaa kujifungua mtoto mnamo 28 Mei London na umpe jina Daniel James na Silva, kisha nguo kubwa ziwe tayari umvalishe. Kisha basi, uanze kumfundisha kucheza soka. Ligi ya Premia ni nyumbani kwa baadhi ya wachezaji maarufu zaidi duniani, na ni jambo linaonekana kuwa lisilowezekana kufikiri kuwa mtota wako anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji kama hao. Sivyo. text: Mbunge maalum Jackline Ngonyani amependekeza hatua hiyo katika hoja ya kujadili udhibiti wa maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini. Akizungumza bungeni, Mbunge huyo ameeleza bunge kwamba lengo la 90-90-90 la virusi vya ukimwi litafikiwa nchini Tanzania, pale kutakuwa na ridhaa ya watu kujipima wenyewe. Ameeleza kwamba changamoto kubwa ni kutokana na kuwa baadhi ya watu wanoana aibu kupimwa vituoni, hasaa wanaume. Suala hilo limevutia hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii kwa baadhi wakieleza kwamba kuna yalio muhimu zaidi yanayostahili kujadiliwa: Lengo 90-90-90 ni nini? Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na VVU/AIDS (UNAIDS) na washirika wake, walizindua lengo la 90-90-90 ambalo limenuia; kutambua kwa 90% watu wote walioathirika na virusi vya Ukimwi, kutoa matibabu ya dawa za kuzuia makali ya VVU kwa 90% ya waliotambuliwa, na kufanikiwa kudidimiza kusambaa kwa virusi kwa 90% kwa waliotibiwa kufikia 2020. 'Suala la mkono sweta, ni tatizo kubwa, ili kufikia 90-90-90 ni lazima tuhakikishe kwamba mikono sweta yote imeondolewa' amesema mbunge Jackline Ngonyani. Bi Ngonyani amependekeza, 'Nashauri tuanze na wabunge humu ndani ambao watabainika hawajafanya hiyo tohara ili wafanyiwe tohara mara moja'. Mbunge huyo amesisitiza kwamba wengi wanaona aibu kwenda kupima, lakini iwapo kutakuwa na utaratibu unaofuatwa wa kila mmoja kujipima mwenyewe itakuwa ni vyema na kusaidia kupunguza kusambaa kwa virusi vya ukimwi nchini. Utafiti uliofanywa kwa wingi kweli, umebaini kwamba wanaume ambao hawajatahiriwa wana nafasi ya kuambukizwa na kuenezea maambukizi mbali mbali ikiwemo ya ugonjwa wa ukimwi. Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza hatari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60. Wabunge waliopashwa tohara Africa kupunguza HIV Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe walitahiriwa katika operesheni iliyoidhinishwa nchini mnamo 2012 katika kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo Nje ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shughuli hizo za kuwapasha wabunge tohara. Nia ilikuwa ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutahiriwa kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi. Wabunge hao walijitokeza hadharani ili kupimwa hali yao ya Ukimwi. Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka 2007, shirika la WHO lilisema kuna haja kubwa ya kuanzisha harakati za kuwatahiri wanaume. Kumekuwa na mjadala nchini Tanzania na zaidi katika mitandao ya kijamii baada ya mbunge mmoja kulishauri bunge kuweka utaratibu maalum kukagua wanaume walio na 'mkono sweta' au wanaume ambao hawajatahiriwa. text: Utafiti huo, uliochapishwa kwenye jarida la Science, umetumia data kutoka Uingereza kupitia mitandao ya Biobank na 23andMe, na kugundua utofauti wa vinasaba unaohusishwa na mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja. Hata hivyo, muundo wa jeni, kwa wastani wa 25% unachangia mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja. Kundi la wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja GLAAD limesema utafiti huo umethibitisha kwa: "hakuna hitimisho la moja kwa moja juu ya ushawishi wa maumbile ama malezi katika tabia za wapenzi wa jinsia moja." Watafiti waliziangazia kwa ujumla wake mfumo mzima wa muundo wa vinasaba, kwa lugha ya kitaalamu genome - za watu 409,000 waliowafanyia utafiti. Walioshiriki utafiti huo pia waliulizwa kama wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja tu ama kama wana mahusiano na jinsia tofauti (mahusiano ya kawaida). Watafiti wmetoka katika vyuo mashuhuri vya Marekani vya Harvard and MIT na wamehitimisha kuwa vinasaba vinachangia 8-25% ya tabia ya wapenzi wa jinsia moja, baada ya kutafiti genome yote. 'Ni vigumu kubashiri' Profesa Ben Neale, mtaalamu wa vinasaba kutoka hospitali ya Massachusetts, ambaye alishiriki katika utafiti huo amesema: "Vinasaba ni chini ya nusu ya hadithi nzima ya tabia za mahusiano, lakini ni moja ya michango ya kitabia. "Hakuna hata kinasaba kimoja cha mapenzi ya jinsia moja, na kipimo cha kinasaba hakitasaidia lolote kutambua kama wewe unaweza kuwa ni mpenzi wa jinsia moja. "Ni vigumu kweli kweli kubashiri mahusiano ya kimapenzi ya mtu kwa kuangalia vinasaba vyao." Fah Sathirapongsasuti, mwanasayansi mwandamizi kutoka 23andMe, ameongeza; "Hili ni jambo la kiasili na la kawaida kwa utofauti wa maumbile yetu, na linaenda kusisitiza kuwa hakuna haja ya kujaribu kutengeneza dawa ya kutibu wapenzi wa jinsia moja." David Curtis, kutoka Chuo Kikuu cha London amesema: "Utafiti huu unaonesha dhahiri kuwa hakuna hicho kitu kinachoitwa 'kinasaba cha mapenzi ya jinsia moja'. "Hata kuwa na mapenzi ya jinsia moja hayaamuliwi kijenetiki, kama utafiti unavyoonesha, japo haimaanishi kuwa kuna mapungufu ya hapa na pale ambayo yanachangia tabia binafsi ya mtu." Zeke Stokes, mtandao wa GLAAD, amesema: "Utafiti huu unapigia mstari kile ambacho kwa muda mrefu kinajulikana kuwa hakuna hitimisho la moja kwa moja juu ya ushawishi wa maumbile ama malezi katika tabia za wapenzi wa jinsia moja." Utafiti wa vinasaba wa watu laki tano umefikia hitimisho kuwa, hakuna hata "kinasaba kimoja cha mapenzi ya jinsia moja". text: Waandamanaji wamebeba mabango kuunga mkono tume ya uchaguzi Bw Msando alitoweka Ijumaa na mwili wake ukapatikana ukiwa umetumwa viungani mwa jiji la Nairobi Jumamosi asubuhi. Mwili wake ulitambuliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City Jumatatu. George Kegoro kutoka shirika lisilo la kiserikali la Tume ya Haki za Kibinadamu Kenya (KHRC) amesema wana wasiwasi sana kwamba mauaji ya Bw Msando yatazua mtafaruku uchaguzi mkuu unapokaribia. Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango wakihimiza umuhimu wa tume ya uchaguzi IEBC, kutoingiliwa. Wamesema sababu pekee ya kumuua afisa huyo aliyekuwa akisimamia mfumo wa teknolojia wa uchaguzi katika tume hiyo ni kuingilia uchaguzi wenyewe na kwamba hilo huenda likachochea ghasia. Waandamanaji hao walikuwa wamepanga kuandamana hadi afisi za mkuu wa polisi Joseph Boinnet na makao makuu ya IEBC. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, kupitia taarifa baada ya kutambuliwa kwa mwili wa Bw Msando, alikuwa ametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha kifo chake. "Tume itamteua wakili huru wa kushirikiana na Mkuu wa Polisi katika uchunguzi. Tunataka haki kwa Chris, Haki kwa IEBC na Haki kwa Taifa." Bw Wabukati alikuwa pia amemuomba mkuu wa polisi kuimarisha ulinzi kwa makamishna na maafisa wakuu wa tume hiyo. Watetezi wa haki za kibinadamu wameandamana katika uwanja wa Uhuru Park, kushutumu kuuawa kwa afisa mmoja mkuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya Christopher Msando. text: China inasema kuwa ilihusisha ndege 40 katika zoezi la kawaida Ndege hizo zinaozodaiwa kuwa zile za kurusha mabomu,kufanya uchunguzi pamoja na ndege ya kivita ,zilipaa juu ya Miyako,kati ya Okinawa na Miyakojima. China imesema kuwa takriban ndege 40 zilihusika katika kile inachokitaja kuwa zoezi la kawaida. Ndege hizo hazikupita katika anga ya Japan,lakini hatua hiyo inaonekana kuwa maonyesho ya ubabe ya China. Ramani ya visiwa vya Japan ambapo ndege za China ziliruka juu yake Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Japan kusema itashiriki katika zoezi la pamoja na wanamaji wa Marekani katika bahari ya kusini mwa China. Msemaji mkuu wa Japan amesema kuwa taifa hilo linachunguza hatua hizo za China kwa karibu. Japan imesema kuwa ilirusha ndege zake hewani siku ya Jumapili baada ya ndege nane za China kupaa kati ya visiwa vya vyake. text: Mawaziri wa Panama na Taiwan Serikalia ya Panama ilisema inatambua kuwa kuna China moja na hivyo inatambua Tawan kuwa sehemu ya China, China inataja Taiwan kama mkoa wake ulijitenga ambao inasema unahitaji kuunganishwa nao. Serikali mjini Taipei, mji mkuu wa Taiwan, imesema imekasirishwa na hatua hiyo ya Panama kujenga uhusiano na Beijing, lakini ikasema haitashindana na China katika kile ilichokitaja kuwa mchezo wa pesa katika diplomasia. Mfereji wa Panama hutumiwa kwa wingi kwa biashara ya dunia China ambayo hutumia pakubwa mfereji wa Panama kwa safari za meli, imeongeza kiwango cha uwekezaji wake katika taifa hilo la Amerika ya kati katika miaka ya hivi karibuni. Mwezi Disemba mwaka uliopita kisiwa cha Sao Tome kilichukua hatua kama hiyo. Kwa sasa ni nchi 29 tu zimedumisha uhusiano wao na Taiwan. Kufuatia tangazo hilo la Panama, vyombo vya habari nchini China vilichapisha picha za mawaziri wa nchi za kigeni wa nchi hizo mbili wakiweka sahihi. Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China katika taarifa, ilisema kuwa serikali ya China inakaribisha hatua hiyo ya Panama. Taiwan Panama imekata uhusiano wake wa muda mrefu na Taiwana na badala yake imeboresha uhusiano na China text: Akizungumza kwa njia ya simu na kupitia runinga ya Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika makao makuu ya Chadema Lisu amesema kuwa atarudi nchini Tanzania siku hiyo ili kuadhimisha kushambuliwa kwake. ''Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo, alisema Tundu Lissu Tangazo hilo liliwafurahisha sana wanachama wa chama hicho waliokuwa katika makao makuu ya chama hicho. Mbowe amesema kuwa utaratibu wa mapokezi yake utapangwa na kutangazwa kitaifa. Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki alipokuwa nyumbani kwake. Tundu Lisu ni miongoni mwa wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Tanzania. Ametangaza kwamba yuko tayari kuwania urais 2020 iwapo vyama vya upinzani vitamridhia kufanya hivyo. Lisu adai shambulio lake lilikuwa la kisiasa Toka wakati huo, Lissu na viongozi wengine wa upinzani wamekuwa wakilihusisha shambulio hilo na kazi yake ya siasa. Wakati wa shambulio, Lissu hakuwa tu mnadhimu wa kambi rasmi bungeni Tanzania bali pia raisi wa chama cha wanasheria nchini humo. Kwa kutumia kofia zake zote mbili, mwanasiasa huyo machachari alikuwa mwiba mkali wa ukusoaji wa serikali ya Magufuli. Lissu alikuwa miongoni mwa wanansiasa wa upinzani waliopendelea kumuita Magufuli kuwa 'Dikteta Uchwara' ama kwa lugha ya kingereza'Petty Dictator'. Baada ya shambulio hilo, alikimbizwa Nairobi kwa matibabu kisha Brussels Ubelgiji toka mwezi Januari mwaka 2018. Huko kote aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya Magufuli ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake. Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha Chadema na mnadhimu mkuu wa upinzani Tanzania Tundu Lissu ametangaza kwamba atarudi nchini humo tarehe saba mwezi wa tisa ikiwa ni miaka miwili tangu aliposhambuliwa. text: Mashabiki hulalamika kwamba hakuna cha kufurahia, lakini meneja wao anaonekana kufidia hilo kwa vituko vyake. Mreno huyo alisherehekea bao la ushindi lililofungwa na kiungo wa kati Marouane Fellaini dakika ya 91 kwa kunyanyua kreti ya maji na kuiangusha chini. Kisha baadaye, alitumia kikao chake na wanahabari kutoa ujumbe kwa wanaompenda na kisha kumtawaza kipa wake "bora zaidi duniani." Manchester United walikuwa wameonekana kuelekea kuandikisha sare nyingine tasa hadi pale Fellaini alipoufikia mpira wa Romelu Lukaku eneo la hatari uliokuwa umetokana na pasi ya Luke Shaw, akafanikiwa kumzuia mkabaji Loris Benito na kisha kutumbukiza mpira kwenye kona wavuni. United wamefuzu kwa hatua ya makundi baada ya Juventus kuwalaza Valencia 1-0. Marouane Fellaini alifunga bao dakika ya 91 'Mwajua, niko sahihi' Kusherehekea. Mwanachama wa bendi ya Nirvana, Kurt Cobain, alifahamika sana kwa kukamilisha matamasha yake wakati mwingine kwa kuvunja gitaa. Mourinho alielekeza furaha yake na hisia zake kwa chupa za maji. Hakujawahi kuonekana mtu mwenye machungu hivi kwa chupa za maji Old Trafford tangu Eric Cantona alipoulizwa maoni yake kuhusu mchezaji mwenzake Didier Deschamps. Mourinho alikosolewa na Rio Ferdinand kwa kituko chake hicho kwenye BT Sport. Ferdinand, ambaye ni beki wa zamani wa Manchester United alidai kwamba Mourinho alifanya hivyo katika jaribio la kufanya kitu cha kugonga vichwa vya habari. Kama hilo lilikuwa ndilo kusudi, basi alifanikiwa. Lakini Jose hakubaliani na hilo. "Wale wanaozungumzia kandanda, si wengi wao ambao wamekuwa uwanjani kama wakufunzi," alisema baada ya mechi. "Kwa wale wanaozungumzia mtu kuonyesha masikitiko yake akiwa kwenye basi, basi ninaweza kuwaalika waje waketi nami hapo kwenye benchi kama meneja. "Pengine wanafurahia zaidi kuwa likizoni visiwa vya Barbvados na wanaweza kwenda kwenye runinga na kutumia vifaa hivyo vya kucheza kwenye skrini." "Hilo halina presha ukilinganisha na kuwa kwenye benchi. Nina uhakika asilimia mia kwamba hakuna meneja yeyote mwenye akili zake anaweza kumkosoa mwenzake kwa vituko alivyovifanya akiwa uwanjani. Kwa wale ambao wanaishi maisha mazuri yasiyo ya presha, ni tofauti." Mourinho si meneja wa kwanza kuelekeza hisia zake kwa chupa za maji. Arsene Wenger alifukuzwa uwanjani kwa kupiga teke chupa za maji alipokuwa meneja wa Arsenal walipokuwa wanacheza Old Trafford mwaka 2009. Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp naye aliomba radhi baada ya kuangusha chupa chini kwa hasira, baada ya sare ya msimu uliopita kati yao na Arsenal. Arsene Wenger alipiga chupa teke wakicheza Ligi ya Premia dhidi ya Manchester United Agosti 2009 14 kutoka kwa 14 Mourinho hakuwa tayari kuzungumzia takwimu kuhusu uchezaji wa timu yake msimu huu. United wanakaribia mkia kwenye Ligi ya Premia kuliko kileleni, na wamefungwa mabao zaidi ya mara nne ukilinganisha na wapinzani wao Manchester City na Liverpool. Walishindwa kufunga dhidi ya Crystal palace nyumbani wikendi, na mchoro huu wa Michael Caley unaonesha mambo halisi. "Muhimu zaidi kwangu ni kufuzu na kwa baadhi ya watu wanaonipenda, na wanapenda takwimu hizo, nimekuwepo Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya misimu 14 na mara 14 timu zangu zimefuzu hadi hatua ya makundi," alisema Mourinho. "Msimu ambao sikuwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, nilishinda Europa League." Mreno huyo anaonekana kufahamu vyema zaidi takwimu kuhusu ufanisi wake. 'Najua anataka kusalia' Mourinho alimsifia sana kipa wake David de Gea ambaye alitumia ustadi wa hali ya juu kuuzia United kufungwa. De Gea, 28, mkataba wake Old Trafford unadumu hadi mwisho wa msimu, lakini klabu hiyo inaweza kuuongeza hadi mwaka 2020. Fellaini amerejelea mtindo wake wa kufunga mabao muhimu mechi ikikaribia kumalizika "Ni kipa wa kiwango cha juu zaidi duniani; kipa bora zaidi duniani," alisema Mourinho. "Najua anataka kusalia na wakala wake anataka kufanya atakavyo mchezaji huyo. Bodi inamtaka asalie na tunalifanyia kazi hilo." Manchester United kwa miezi mingi sasa wamekuwa wakishutumiwa kwa kucheza mchezo usiovutia, na kwa kuandikisha matokeo yasiyo ya kuridhisha sana. text: EL Hadary alifanikiwa kuokoa mkwaju wa penalti lakini hilo halikutosha kuzuia Misri kufungwa 2-1 na Saudi Arabia ambao walikuwa wamechapwa 5-0 na Urusi mechi ya ufunguzi. El Hadary alikomboa mkwaju wa Fahad Al Muwallad kipindi cha kwanza lakini Salem Al Dawsari alifunga dhidi ya Saudi Arabia dakika za mwisho mwisho za mechi Jumatatu. Kipa huyo alicheza akiwa na miaka 45 na siku 161 na kumfanya kuwa mchezaji mkongwe zaidi kuwahi kucheza Kombe la Dunia. "Nawaomba radhi kwa watu wa Misri kwa niaba yangu, na kwa niaba ya wenzangu, baada ya kushindwa mara tatu," amesema. "Najionea fahari yale ambayo nimetimiza na ufanisi huu ni wa thamani kwa Misri. "Tulijaribu lakini bahati yetu haikusimama - hii ni soka." Katika mechi hiyo ya mwisho ya Kombe la Dunia kwa Misri, ambao walikuwa wakishiriki michuano hiyo mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 28, Misri waliongoza kupitia bao la nyota wa Liverpool Mohamed Salah dakika ya 22. Lilikuwa bao la kwanza kwa Misri kupitia uchezaji wa kawaida (si kupitia penalti) katika Kombe la Dunia tangu 1934. Lakini Salman Al Faraj aliwafungia Saudi Arabia penalti sekunde chache kabla ya muda wa mapumziko baada ya El Hadary kukomboa mkwaju wa Al Muwallad. Al Dawsari alifunga bao la ushindi sekunde chache kabla ya mechi kumalizika na kuwazawadi Saudi Arabia ushindi wao wa kwanza Kombe la Dunia tangu 1994. Kocha wa Misri Hector Cuper anasema anatumai "kila mtu Misri anafurahia" kwamba El Hadary alivunja rekodi iliyowekwa na kipa wa Colombia Faryd Mondragon, aliyekuwa na miaka 43 na siku tatu alipocheza katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil mwaka 2014. "Hakuna tofauti kubwa sana kati ya walinda lango wetu watatu lakini alifaa zaidi kucheza leo," alisema Cuper. Aidha, alipuuzilia mbali tetesi kwamba Mo Salah anafikiria kustaafu kutoka kwenye timu ya taifa kwa sababu hajafurahishwa na kutumiwa sana kwa sababu za kuitangaza timu. "Sifikiri kuna ukweli wowote hapo. Anafurahia sana fursa yoyote anayoipata ya kuichezea timu ya taifa," amesisitiza kocha huyo. Egypt walimaliza wakiwa wanashika mkia Kundi A baada ya kushinda kupata hata angalau alama moja. Walishindwa na Urusi, Uruguay na Saudi Arabia. Mlinda lango wa Misri Essam El Hadary ambaye ameweka historia ya kuwa mtu wa umri wa juu zaidi kucheza fainali za Kombe la Dunia ameomba radhi baada ya Misri kushindwa tena Kombe la Dunia. text: Rais wa Tanzania John Magufuli Ni msemo ambao hulenga kuwazungumzia wale wanasiasa waliokuwa upinzani wakahama vyama vyao na kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kwenda kuunga mkono juhudi za maendeleo za Rais John Pombe Magufuli. Wapinzani wanawatuhumu kwamba walijiunga na CCM baada ya kununuliwa, ingawa wenyewe wanaipinga tuhuma hiyo kwa nguvu zao zote. Hata viongozi wa chama walichohamia nao wanapinga madai ya kununua wanasiasa wa upinzani. Siasa za kuhama chama zilishika kasi katika awamu hii inayomaliza.Wabunge, madiwani na hata wafuasi wa kawaida kutoka vyama vikubwa vya upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) walihama kwa wingi sana. Hadi mwezi Agosti 2018 jumla ya madiwani na Wabunge wapatao 138 walijiuzulu nafasi zao na kwenda chama tawala. Kwa upande wa kundi la Wabunge hadi mwezi Februari mwaka huu Wabunge 12 walikuwa tayari wamehamia CCM kwenda kuunga mkono juhudi. Kuelekea uchaguzi mkuu wanasiasa hao wameingia katika kinyang'anyiro cha kutangaza nia na kuchukua fomu kwa tiketi ya CCM. Bahati mbaya wengi wao wameangukia pua, kwa maneno mengine wameshindwa kufua dafu katika kura za maoni za chama hicho. Ni wazi kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba ndio kilele cha maamuzi kuhusu nani atabaki na yupi atakwenda katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mintarafu hiyo kukosa kupita katika kura za maoni ni dalili kuwa ndoto yao yakuelekea Dodoma inazidi kuwa ya Alinacha. Mambo yalikuwaje majimboni? Kwanza tuiangalie hali jumla katika mchakato wa kura za maoni za mara hii ndani ya CCM katika ngazi ya Ubunge. Chama hicho kikongwe barani Afrika, kimeandika historia ya kupokeawachukua fomu wengi mno, ni zaidi ya chaguzi zilizopita. Kwa nafasi hiyo pekee wachukua fomu walifikia 10367. Katika ngazi nyengine ikiwemo udiwani na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar utitiri wa watu ulikuwa mkubwa vile vile. Ilikuwa'mpata mpatae'. Hata watu ambao hawana uzoefu na siasa wala hawajawahi kuonekana katika medani za kisiasa mwaka huu ulikuwa ni wao. Nao walikuwa ni miongoni mwa waliotangaza nia. Kulikuwa na vichekesho vikubwa katika mchakato hasa pale wachukua fomuwalipokuwa wakitangaza sera na kuomba kura. Baadhi ya sera zilizohubiriwa ziliwafanya Watanzania kuangua vicheko au kubaki midomo wazi kwa mshangao. Yote tisa, lililokuwa bora katika kinyang'anyiro hicho ni ule uwazi wakati wa kuhesabiwa kura kama alivyoagiza Mwenyekiti wa chama, Rais John Pombe Magufuli. Kura nyengine zilihesabiwa mubashara kupitia vituo vya runinga ama mitandao ya kijamii. Kwa ufupi kila mchukua fomu alivuna haki yake, hata kama ni kura sifuri. Wapo walioamini wangebebwa na umashuhuri wao kupitia mitandao ya kijamii, wengine wakiamini kuhama kwao na kutangaza utiifu kwa CCM kungewasaidia kuteleza hadi Dodoma. Lakini mambo yameenda nje ya matarajio ya wengi wao. Kipi kimewaagusha? Mchakato wa kusaka kura za maoni ili uwakilishe chama chako daima zinahitaji mizizi na ushawishi katika chama hicho. Watangaza nia waliohama upinzani na kwenda chama tawalahawakuwa na mizizi ya muda mrefu katika CCM. Na hilo ndilo rungu lililowaadhibu, wakaambulia kura chache. Ule mpango wa kuteuliwa na kupitishwa bila kupingwa walipokuwa wanagombea tena nyadhifa zao kupitia CCM baada ya kuhama vyama vyao vya upinzani, haukuwepo wakati wa kura za maoni. Kila mtangaza nia alipambana kwa nguvu zake na ushawishi alionao mbele ya wajumbe. Mchakato wa kupita bila kupingwa uliowapitisha waungaji mkono juhudi ulifanyika makusudi kwa maslahi ya kisiasa. Ilikuwa ni moja ya mbinu ya kuwavuta viongozi wengine wa upinzani wajiunge na CCM pindi watakapoona njia isiyo na vigingi ya kurudi tena Bungeni kupitia chama hicho. Muungaji mkono juhudi anapofika hatua ya kukosa nafasi kupitia CCM na hana uwezo wala nafasi ya kurudi kule upinzani alikotoka, kilichobaki ni kusubiri huruma ya Rais atakaye chaguliwa ikiwa atamteuwa katika viti maalum vya Ubunge au nyadhifa nyegine ya kiserikali. Lakini akikosa hayo yote hapo huanza kufutika polepole katika ramani ya kisiasa. Lipo swali la kisiasa linalohoji kuhusu mwanasiasa anayehama chama chake cha upinzani kwenda chama tawala kuunga mkono juhudi za Rais. Je, ikifika wakati ule upinzani unashika dola na kuongoza nchi, atahama tena kurudi chama cha zamani kwa minajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo za Rais mpya? Swali hilo ndilo linalowatia shaka wapiga kura si tu wale wanaopiga kura za maoni na hata wapiga kura katika uchaguzi mkuu, ikiwa wanasiasa wa aina hiyo ni wa kuaminika kupewa nafasi ya kwenda kuwawakilisha katika ngazi za kiuongozi. Baadhi ya vigogo wa kisiasa walioanguka katika mchakato huu wa awali ni David Silinde aliyepata kura 18 katika jimbo la Tunduma. Maulid Mtulia aliyekuwa mbunge Kinondoni,aliambulia kura 11 kati ya 403. Majina mengine makubwa yaliyokuwa katika siasa za upinzani ni Abdallah Mtolea, aliyekuwa Mbunge Temeke, Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki na Dk Vicent Mashinji, kuwataja wachache. Dk Mashinji alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema, amevunja rikodi miongoni mwa waungaji mkono juhudi kwa kuambulia kura mbili katika jimbo la Kawe. Dk Godwin Mollel jimbo la Siha na Mwita Waitara jimbo la Tarimo Vijijini ndio waunga mkono juhudi ambao wameongoza katika kura za maoni kwenye majimbo yao. Zitto aeleza makosa yaliyofanywa na muungano wa UKAWA katika uchaguzi uliopita Siasa hazitabiriki lakini anguko hili linatoa sababu ya kuamini siasa za kuhamahama zilizoshika kasi kati ya 2016 hadi 2020 huenda zitapungua au kuondoka kabisa kwa miaka kadhaa ijayo. Hesabu za wahamaji ilikuwa ni kamari ya kisiasa ambayo wengi wao wameambulia kuliwa. Mchakato huo ni wa awali, kuanzia tarehe 30 Julai CCM itakuwa na vikao vya kamati za siasa za majimbo kwa ajili kuwajadili wagombea na kufanya mapendekezo kwa kamati za siasa za mikoa. Historia inaonesha baadhi ya wagombea hukatwa, ingawa ni wa chache lakini mara hii mchakato huu umekuja na uwazi zaidi, bado ni kusubiri kuona uwazi huo utakuwa na maana gani itakapofika hatua ya mwisho ya wagombea kupitishwa. Katika siasa za Tanzania msemo huu 'waungaji mkono juhudi' umekuwa maarufu katika miaka mitatu iliyopita. text: Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi aliwakabidhi JWTZ kiwanda cha kubangua korosho cha Bucco ambacho serikali ilikirudisha mikononi mwake wiki iliyopita baada ya mwekezaji kushindwa kukiendeleza kama ilivyotakiwa wakati wa ubinafsishwaji wake. Kuanzia leo maghala yanayohifadhi zao hilo kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yapo chini ya ulinzi wa wanajeshi. Na tayari malori ya usafirishaji ya jeshi hilo yapo njiani kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa hiyo ili kuratibu uchukuzi. Rais John Magufuli juzi Jumatatu aliwakabidhi rasmi wanajeshi shughuli hiyo baada ya kuwafungia nje wafanyabiashara amabao walionekana kusuasua kununua zao hilo kwa bei elekezi ya isiyopungua Shilingi 3,000 za Tanzania kwa kilo. Awali bei ya zao hilo iliporomoka kutoka wastani wa Sh4,000 kwa kilo kwa mwaka jana mpaka wastani wa Sh1,500 na Sh2,700 kwa msimu huu. Wakulima waligomea bei hiyo na hatua hiyo iliungwa mkono na serikali. Katika kikao cha pamoja cha serikali na wafanyabiashara kilichofanyika Oktoba 28 na kuongozwa na rais Magufuli ilikubalika bei ya Sh3,300 lakini hatahivyo minada haikuendeshwa kwa kasi ambayo serikali iliitarajia. Hatua hiyo ilitafsiriwa na serikali kama mgomo baridi. Kwanza serikali iliwapa wafanyabiashara siku nne za kutaja kiwango watakachonunua lakini baadaye Magufuli alibadili maamuzi na kuipa shughuli hiyo Benki ya Maendeleo ya Kilimo na JWTZ. Leo hii mkuu wa 'operesheni korosho' Luteni Benjamin Kisinda ameimbia BBC kuwa wapo tayari kufanikisha oparesheni hiyo kwa ufanisi mkubwa. Korosho Tanzania: 'Hatima ya wafanyabiashara itajulikana baadaye' Jana waziri mpya wa kilimo nchini Tanzania Japhet Hasunga aliiambia BBC kuwa serikali itafikiria hatima ya wafanyabiashara wa korosho mara baada ya kumaliza ununuzi wa zao hilo. Hasunga aliwasili mkoani Mtwara jana mara baada ya kuapishwa na rais Magufuli juzi Ikulu jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Charles Tizeba aliyefutwa kazi kutokana na kadhia ya korosho. Korosho zaondoka na mawaziri wawili Tanzania "Hatima ya wafanyabiashara wa korosho labda wasuburi tukishanunua hizi korosho ndio tutakaa nao tuamue. Tulishakaa nao vikao vingi, tukakubaliana na bei elekezi, wao hawakutaka kuzingatia. Wanadhani serikali labda hatuwezi ndio maana tunanua wenyewe sasa, halafu ndio tufikirie sasa namna ya kushirikiana nao," amesema Hasunga na kuongeza: "Tunajua kuwa wanaumuhimu, lakini si umuhimu wa kuringa ama kutaka kununua kwa shilingi 1,500 au 2,000..." Sakata la korosho pia limesababisha aliyekuwa waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage kufutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Josephat Kakunda. Jeshi la Tanzania (JWTZ) hii leo limeanza rasmi operesheni ya kuratibu ununuzi, uhifadhi na usafirishaji wa zao la korosho kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania. text: Rais Jacob Zuma na shinikizo la kuachia madaraka Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma. Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika upinzani. Siku ya jumanne bunge la taifa hilo liliahirisha hotuba ya kitaifa iliyotarajiwa kutolewa na rais Zuma. Hata hivyo baadhi ya mitandao nchini humo imekaririwa ikisema kuwa rais Zuma anajiandaa kuachia madaraka iwapo makubaliano katiika mambo kadhaa yatafikiwa. Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC Cyril Ramaphosa. Upande wa upinzani wenyewe unashinikiza Zuma kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani,huku kikao cha kamati kuu kikidaiwa kuwa na nguvu ya kuweza kumuondoa Zuma madarakani hata bila hiari yake. Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma. text: Rais Trump na aliyekuwa mkurugenzi wa FBI,James Comey Hapo jana James Comey alihojiwa na Kamati ya Bunge la Seneti ya Usalama na kumtupia lawama Rais Trump kwa kuingilia uchuguzi unamhusu kujihusisha na Urusi. Wakili binafsi wa rais Trump,Marc Kaswitz Wakili binafsi wa rais Trump,Marc Kaswitz amepinga vikali shutuma hizo zilizotolewa na Comey na kudai kuwa huo ni uzushi. "Raisi hakuwahi kutoa maelekezo au mapendekezo kwa Comey kuacha kumchunguza wa mtu yeyote ". Rais Trump pia alitoa mustakhabali wake juu ya suala hili; "hakuna kitu chenye dhamani ambacho kinakuja kiurahisi,lakini tunajua jinsi ya kupambana vizuri zaidi mtu mwingine yeyote na hatutakata tamaa .Sisi ni washindi na tunaenda kupambana na kushinda na tutakuwa na mustakabali ambao hauelezeki kwa siku za mbeleni,na tutaenda kuwa pamoja Comey katika ushaidi alioutoa alieleza namna ambavyo alijisikia vibaya mara baada ya rais Trump kumtaka kuachana na uchunguzi huo wa mshauri wa zamani wa masuala ya usalama na juu ya urusi. Na anaona ndio sababu ilionekana haendani na majukumu ya shirika la kijasusi la FBI Donald Trump and his team have reacted furiously to allegations by the former head of the FBI that the president ordered him to drop an inquiry into links between his disgraced National Security Adviser and Rais Trump pamoja na timu yake wamejibu vikali dhidi ya tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa mkurugenzi wa FBI ,kuwa rais Trump alimtaka kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama na Urusi. text: Edward Lowassa asema kuna 'chembechembe za udikteta katika serikali ya Tanzania' Akizungumza na mwandishi wa BBC John Nene nchini Kenya, amesema kuwa alitaraji kwamba rais Magufuli angeondoa urasimu serikalini lakini "kuna mambo mengine hayajakwenda sawa ", ijapokuwa alikataa kutoa mifano alipotakiwa kufanya hivyo. Bwana Lowassa alikuwa katika chama tawala alipokuwa waziri mkuu, lakini mwaka uliopita alijiunga na upinzani wa CHADEMA ambapo alishindwa na Rais Magufuli wakati wa uchaguzi. Magufuli aliyepewa jina Tinga (Bulldozer) anajulikana kufanya maamuzi yanayopendwa tangu achukue mamlaka mwaka uliopita, kama vile kufutilia mbali sherehe za uhuru wa taifa hilo ili kuhifadhi fedha. Lakini wakosoaji wake wamemshtumu kwa kukabiliana vikali na wapinzani. Gazeti moja linalodaiwa kuwa mkosoaji mkubwa wa uongozi wake hivi majuzi lilifungwa huku mtu mmoja akikamatwa kwa madai ya kumtusi katika mitandao ya kijamii. Rais John Pombe Magufuli Serikali yake pia imepiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja ile ya faraghani ya kisiasa. Maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanywa dhidi ya serikali yaliahirishwa mwezi huu baada ya viongozi wa kidini kujitolea kuongoza mazungumzo na serikali. Bwana Lowassa amesema kuwa maandamano yalilenga kupinga ''chembechembe za udikteta katika serikali'. Aliambia wanahabari kwamba ana matumaini kuhusu mazungumzo hayo lakini hatosema kile upinzani utakachofanya iwapo yatafeli. Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa amemkosoa mpinzani wake rais John Magufuli kwa kile alichokitaja kuwa ''chembechembe za kidikteta'' nchini humo. text: Wanajeshi wa MK nje ya makao makuu ya chama cha ANC Maandamano hayo yamepangiwa kufanyika nchi nzima. Wanajeshi wa uMkhonto we Sizwe maarufu MK wametawanywa kushika doria nje ya makao makuu ya chama cha ANC mjini Johannesburg. Waziri anayeshughulika na masuala ya polisi nchini awali amewaonya wale wote watakao fanya fujo na kuharibu mali ya umma, sheria itafuata mkondo. Zuma ameponea katika siku za nyuma wito wa kumtaka ajiuzulu. Aliungwa mkono hivi juzi na kamati kuu ndani ya chama chake cha ANC. Ilikuwa inachunguza malalamiko yaliowasilishwa na baadhi ya maafisa wa juu wa chama hicho kwamba Jacob Zuma hakushauriana nao kuhusu suala la kufanyia baraza la mawaziri mageuzi. Shutuma kali zimeibuka kufuatia mageuzi hayo, zaidi kufuatia kutimuliwa kwa waziri wa fedha nchini anayeheshimika na wengi, Pravin Gordhan. Taarifa iliyotolewa na mkuu wa Jeshi la polisi nchini imeeleza kuwa maandamano hayo ya kwenda kwenye ikulu ya Rais hayana kibali, ambacho kimewaruhusu kufika huko. Maandamano ya vyama vya upinzani Afrika kusini pamoja na kundi linalo jiita Save South Africa yameanza katika kumshinikiza Rais Jacob Zuma ang'atuke madarakani. text: Bwana Kim anazuru China akiandamana na mke wake Ri Sol-ju,kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari Ripoti zinasema Bwana Kim ambaye ameandamana na mke wake Ri Sol-ju atakuwa China hadi Januari 10. Ziara hiyo inakuja wakati ambapo mikakati ya kupanga mkutano wa pili kati ya rais Kim Jong un na rais wa Marekani Donald Trump zikiendelea. Wawili hao walikutana mwezi Juni mwaka uliyopita hatua ambayo ilikuwa ni ya kwanza kwa rais wa Marekani aliye madarakani. Siku ya Jumatano kulikuwa na madai kuwa bwana Kim huenda akatumia trani yake maalum kusafiri hadi China. Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ambaye pia anaandamana na maafisa wake kadhaa, anazuru Uchina kwa mara ya nne katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja. Jumanne inaripotiwa kuwa siku ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo ambaye anasherehekea miaka 35 ya siku yake ya kuzaliwa japo tarehe ya siku hiyo haijathibitishwa na Pyongyang. China ni mshirika muhimu wa kidoplomasia wa Korea Kaskazini na moja ya vyanzo vikuu vya biashara na misaada. "[Bwana] Kim anapania kuukumbusha utawala wa Tramp kwamba taifa lake lina njia mbadala ya kujikimu kiuchumi tofauti na ile inayotolewa na Washington na Seoul," Harry J Kazianis, mkurugenzi wa taasisi ya masomo ya ulinzi aliiambia shirika la habari la Reuters. Ziara ya kwanza ya Kim nchini China ilifanyika mwezi machi mwaka jana Bwana Kim hakuwahi kukutana na Xi katika miaka sita ya kwanza ya uongozi wake nchini Korea Kaskazini. Lakini mwaka jana alizuru China mara tatu na hakuna hata ziara moja kati ya hizo zilitangazwa kabla zifanyike. Mwandishi wa BBC Laura Bicker aliyepo mjini Seoulanasema mbili kati ya ziara hizo zilifanyika kabla ya mkutano wa kihistoria kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani. Kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae-in na rais Trump, walionekana wakipanga mikakati kuelekea mkutano huo. Mkutano huu wa sasa huenda ukazua uvumi kwamba mkutano mwingine kati ya Marekai na Korea Kaskazini utafanyika hivi karibuni. Mapema wiki hii ,Bwana Trump alisema mkutano mwingine utatangazwa hivi karibuni, lakini vikwazo dhidi ya Pyongyang vitaendelea kutekelezwa. Katika hotuba yake ya mwaka mpya wiki iliyopita, bwana Kim alisema kuwa amejitolea kukabiliana na zana za nuklia, lakini akaonya kuwa huenda akabadisha msimamo ikiwa Marakani itaendelea kuiwekea nchi yake vikwazo. Hatua za kidiplomasia kati ya rais Trump na mwenzake Kim zimekwama tangu viongozi hao walipokutana nchini Singapore. Pande zote mbili wakati huo ziliafikiana kumaliza salaha za nuklia katika rasi ya Korea japo haikubainika yale yaliyokuwemo kwenya mkataba waliyotia saini. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ameanza ziara nchini China kwa mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Xi Jinping. text: Umri wa vijana kuvunja ungo au kubaleghe unalinganishwa na wakati mama zao walipo vunja ungo Akina mama ambao walivunja ungo mapema kuliko wasichana wenzao wanaishiwa kuwa na watoto wa kiume ambao wana: • wana nywele za kwapani miezi miwili na nusu mapema zaidi • wanatokwa na chunusi na sauti kubadilika miezi miwili mapema zaidi. Kwa upande mwingine mabinti zao, huota maziwa miezi sita mapema zaidi. Utafiti katika jarida la Human Reproduction umekagua data kutoka kwa akina mama 16,000 na watoto wao nchini Denmark. Taswira ambayo wataalamu Afrika mashariki wanakubaliana nayo. Umri stahiki ni upi wa vijana kubaleghe? Mmoja ya wahariri wa ripoti ya utafiti huo, Dr Nis Brix, wa chuo kikuu Aarhus nchini Denmark, anasema: "kila daktari anapokutana na mgonjwa ambaye amewahi au amechelewa kubaleghe, daktari huulizia historia ya familia kuhusu suala hilo. Umri wa wavulana na wasichana kuanza kubaleghe umekuwa ukishuka duniani kwa mujibu wa wataalamu. Unalingana kutoka mtu hadi mtu, hatahivyo, inasadikiwa kwa wastani vijana huvunja ungo katika umri wa: Wataalamu wametaja kwamba hili linatokana na kuimarika kwa afya na lishe bora katika ulimwengu wa sasa - lakini utafiti umeonyesha pia uhusiano kati ya kunenepa kupita kiasi na vijana kuvunja ungo mapema. Kuna fikra nyingi kulihusu hilo, mojawapo ikiwa ni kuongezeka kwa unene miongoni mwa watoto kunahusiana na kubaleghe mapema kwa vijana. Utafiti mnamo 2015, umebaini kwamba vijana kubaleghe mapema au kuchelewa kunahusishwa pia na hatari ya kuugua: Msichana huambiwa amevunja ungo mapema anapobaleghe kati ya miaka 8-11, na kuchelewa ni kati ya miaka 15 na 19. Kwa wavulana umri stahiki wa vijana kubaleghe ni kati ya miaka 9 na 14. Umri wa vijana kubaleghe unalinganishwa na wakati mama zao walipo vunja ungo, utafiti unaonyesha. text: Kocha wa Panama Dario Gomez (samawati) akisherehekea na Roman Torres baada ya kuwashinda Costa Rica t Juan Carlos Varela‏ aliandika katika Twitter, "Sauti za watu zimesikika...Kesho ni siku ya kitaifa." Panama ilishinda Costa Rica mabao 2-1 mjini Panama City siku ya Jumanne. Rais alisema kuwa wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya kibinafsi watapumzika na pia shule hazitafunguliwa. Watu nchini Panama walisherekea usiku kucha baada ya ushindi huo. Kulikuwa na shangwe katika mji wa Panama City Hata hivyo kumekuwa na utata ikiwa goli la kwanza la Panama lilivuka mstari wa goli. Panama imejaribu kufuzu kwa kila kombe la dunia tangu mwaka 1978 lakini haijafanikiwa hadi sasa. Nchi hiyo itashiriki katika mechi za mwaka 2018 ambazo zinaanza Urusi mwezi Juni mwaka ujao. Marekani ilikuwa katika kundi moja la kufuzu kwa nchi za kaskazini na kati mwa Marekani, lakini ikashindwa baada ya kupoteza kwa Trinidad and Tobago. Mexico na Costa Rica na walifuzu. Rais wa Panama ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku kuu baada ya nchi hiyo kufuzu kwa mechi za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanaa kabisa. text: Wachezaji wa Harambee Stars wakisherehekea kufunga bao Kasarani 14 Oktoba, 2018 Thibitisho kwamba Timu ya Taifa Harambee Stars imefuzu kwa michuano hiyo ya 2019 lilitangazwa siku ya Ijumaa baada ya kikao kisicho cha kawaida cha siku nzima cha Kamati Kuu ya Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) jijini Accra, Ghana. Kikao hicho cha Ijumaa kilithibitisha uamuzi wa kuitupa nje timu ya taifa ya Sierra Leone kutoka kwa michuano inayoendelea kwa sasa kutokana na shirikisho lao kupigwa marufuku na chama chake cha Soka kupigwa marufuku na Shirikisho la soka duniani FIFA. Sierra Leone, ambayo ilikuwa katika kundi la F la kufuzu pamoja na Kenya, Ghana na Ethiopia, sasa haitashiriki michezo yake mitatu ya mwisho. Huku ikiwa imesalia mechi moja ya makundi kukamilika, Shirikisho la CAF liliafikia uamuzi wa kufutilia mbali matokeo yote yaliyohusisha taifa hilo la Afrika Magharibi na hivyo kuliacha kundi hilo na timu tatu pekee. Sierra Leone ilikuwa imecheza tu mechi mbili katika kampeini yao na kwa sababu haikuwa imekamilisha nusu ya mechi zote za kufuzu, Shirikisho la CAF liliamua kufutilia mbali matokeo yote ya awali yaliyohusisha taifa hilo kulingana na kanuni za kufuzu. Michuano hiyo ilipangiwa kufanyika Cameroon mwaka ujao lakini taifa hilo lilipokonywa nafasi hiyo Ijumaa kutokana na kucheleweshwa kwa ujenzi wa viwanja na miundo mbinu mingine muhimu. CAF wanatarajia kuteua mwenyeji mpya kufikia mwisho wa mwezi huu. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameipongeza timu hiyo ya taifa na kusema kufuzu kwa timu ya Taifa kwa kinyanganyiro hicho barani kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 15 ni ufanisi wa kusisimua kwa wapenda soka nchini humo. Ameahidi kuiunga mkono kikamilifu timu hiyo. Sehemu ya ujumbe wa CAF ikionyesha msimamo kwenye Kundi F kwa sasa "Ufanisi wa timu yetu ya Taifa ni ishara ya mabadiliko katika michezo yetu. Tunajivunia kile vijana wetu wanafanya kuimarisha viwango vya mchezo huo nchini," amesema Rais Kenyatta. Rais Kenyatta amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo itaendelea kuiunga mkono timu ya Taifa ya Soka inapojiandaa kwa kindumbwe-ndumbwe hicho barani. "Tunajua mnaweza kushinda taji hili. Nawahakikishia usaidizi wangu na Serikali itafanikisha na kuwapa rasilimali zinazohitajika kuhakikisha mmejiandaa viivyo kwa kazi iliyo mbele yenu," Rais Kenyatta amesema. Awali, Waziri wa Michezo Rashid Echesa, kupitia akaunti yake ya Twitter Twita aliipongeza timu ya taifa kwa kufuzu. "Kinyang'anyiro hiki kimetuhepa kwa muda wa miaka 15. Nawashukuru vijana wetu kwa kupambana vilivyo dhidi ya timu zote katika kundi lao na kufuzu kuiwakilisha Kenya," Waziri alisema. Katibu katika Wizara ya Michezo, Balozi Kirimi Kaberia alisema wanamichezo wa Kenya waume kwa wanawake ni raslimali muhimu ya taifa na akaiihimiza timu ya hiyo ya Soka Harambee Stars kulenga ufanisi katika kinyanganyiro hicho. Timu ya taifa ya mpira wa miguu Kenya, Harambee Stars imefuzu kushiriki michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika (AFCON) mwaka 2019. text: Diane Rwigara baafda ya kuachiliwa Mahakama imesema kwamba imefanya uamizi huo kutokana na kwamba upande wa mashitaka haukutoa ushahidi wa kutosha. Diane Rwigara Wawili hao walishitakiwa kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. Muendesha mashtaka alikuwa ameomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela. Diane Rwigara na mamake waachiliwa huru Rwanda Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa. Marekani imeishinikiza Rwanda kuondoa mashitaka hayo, lakini Rwanda imejibu kwamba haishinikizwi na yeyote na kuomba vyombo vya sheria visiingiliwe. Mama yake Diane, Adeline Rwigara Uamuzi huo ulikuwa wa mwisho kuhusu maombi ya upande wa mashitaka ya kuwapa kifungo cha miaka 22 jela katika kikao cha mwisho mwezi uliopita, huku upande wa mawakili wao wakipinga maombi hayo na kusisitiza wateja wao kuachiwa huru mara moja. Sherehe mahakamani baada ya wawili hao kuachiliwa Waendesha mashtaka waliomba hukumu hiyo wakisema Diane Rwigara alihusika katika kughushi nyaraka wakati alipokuwa akikusanya saini za wafuasi wake wakati wa kutaka kugombea urais kama yalivyo masharti ya tume ya uchaguzi na kwamba kumekuwa na saini za wafuasi hewa baadhi wakiwa walifariki dunia na wengine wakiwa hawapo nchini. Kadhalika Diane Rwigara na Mamake walishitakiwa kuchochea chuki na kusambaza uvumi kwa lengo la kuhamasisha umma kugoma dhidi ya utawala. Uamuzi wa leo ulisubiriwa kwa hamu na gamu baada ya Diane Rwigara na mamake Adeline Mukangemanyi kukamilisha kesi hii wakiwa hawako kizuizini. Diane Rwigara akisherehekea Kwa mshangao wa wengi , mapema mwezi wa 10 mwaka huu mahakama ilichukua uamuzi wa kuwaachilia huru kwa dhamana ikisema sababu za kimsingi zilizosababisha kesi yao kusikilizwa wakiwa kizuizini hazipo tena. Wao Wanakanusha mashtaka dhidi yao wakisema yalichochewa kisiasa hasa baada ya Diane Rwigara kujitokeza katika ulingo wa kisiasa,akipinga wazi sera za chama tawala na kutaka kugombea urais katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana. Mahakama mjini kigali, Rwanda imetangaza kwamba mwanasiasa Diane Rwigara na mamake Adeline Rwigara hawana hatia na kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote. text: Bw Kenyatta na Bw Odinga waliwania tena mwaka 2013 Kwa kumtangaza aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea mwenza na makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka kuwa mgombea mwenza wake, upinzani ulikuwa umehakikisha uchaguzi wa Agosti mwaka huu utakuwa kama marudio ya uchaguzi wa mwaka 2013. Bw Odinga, akitumia muungano wa Coalition for Reform and Democracy (Cord), wakiwa na Kalonzo, walishindana uchaguzini dhidi ya muungano wa Jubilee wake Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto. Wagombea wengine ni Cyrus Jirongo wa United Democratic Party (UDP), Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance, Abduba Dida wa Alliance for Real Change (ARC), na wagombea huru Joseph Nyagah, Michael Wainaina na Japheth Kavinga. Wanachojiuliza watu ni iwapo kunafaa kutarajiwa matokeo tofauti na ya Machi mwaka 2013, Bw Kenyatta alipopata asilimia 50.7 ya kura, naye Bw Odinga akapata 43.31. Wanaoamini kwamba hakuwezi kutarajiwa matokeo tofauti, walikuwa miongoni mwa waliopinga Bw Odinga kuteuliwa kuwa mgombea wa muungano wa upinzani. Walitaka kuwe na mgombea tofauti ambaye 'angesisimua' upya hamu ya wapiga kura wenye imani na upinzani. Msimamo sawa, japo bila shaka kwa sababu tofauti, ulionekana kuwepo miongoni mwa mrengo wa serikali. Aliyeongoza ni Bw Ruto ambaye baada ya kutangazwa kwa mgombea wa upinzani, alisema: "Eti ile wametuletea ni ile ile ya 2013. Sasa, hii jameni ni utapeli wa aina gani. Sisi tulikuwa tunangojea walitwambia wako na maajabu, wako na miujiza. Tulikuwa tunafikiria wameenda kutoa mgombea nje ya nchi, kumbe ni wale wale tuliwashinda 2013. "Kama hawa, kwa sababu Raila ni yule yule, Kalonzo ni yule yule, Musalia (Mudavadi) ni yule yule .Hawa watu si tunawanyorosha asubuhi na mapema, hata kama ingewezekana tungewaambia sasa IEBC wasongeze uchaguzi ikuwe karibu," alisema akiwa mjini Thika. "Ni nini iliwazuia wangesema marudiano ya 2013 ni 2017, kivumbi tuliwaonyesha siku ile tutawaonyesha kivumbi pamoja na moshi." Walio na msimamo sawa, wanaamini safari itakuwa rahisi kwa Bw Kenyatta na wenzake kwani ukijumlisha kura alizopata Bw Odinga na zile alizopata Bw Mudavadi, ambayo sasa yumo kwenye muungano wa upinzani, hazitoshi kuwawezesha kuishinda serikali ya sasa. Bw Kenyatta alipata kura 6,173,433 naye Bw Odinga akapata 5,340,546 mwaka 2013. Bw Mudavadi alijizolea kura 483,981. Ukazijumlisha, Bw Kenyatta akiwa na 50.7, asilimia ya Bw Odinga na Bw Mudavadi kwa pamoja itakuwa ni 47.24. Lakini hali kwamba upinzani uliungana, tofauti na ilivyotarajiwa kwamba umoja wao ungesambaratika, unazua uwezekano kwamba kwa pamoja huenda wakafanya vyema kuliko awali. Wanasiasa kuhama vyama vya upinzani Bw Kenyatta ana nafuu nyingine, kwamba kuna baadhi ya magavana na wabunge walioshinda uchaguzi mwaka 2013 ambao wamehamia katika muungano wake, baadhi kutoka maeneo ambayo kura zinashindaniwa maeneo ya Pwani na Magharibi. Mfano eneo la pwani Salim Mvurya (gavana wa Kwale), Hussein Dado (gavana wa Tana River), Gideon Mung'aro (mbunge wa Kilifi Kaskazini). Manaibu gavana Kenneth Kamto (Kilifi) na Hazel Katana (Mombasa), Fatuma Amani (Kwale) pia walihamia Jubilee. Mwakilishi wa wanawake Taita Taveta Joyce Lay alihamia Jubilee na sasa anawania useneta, seneta wa jimbo hilo Dan Mwazo naye pia akahamia Jubilee na sasa anawania ugavana. Kuna wasemao hata hivyo kwamba kuhama kwa viongozi si kwamba wamehama na wafuasi wa chama na kwamba huenda wapiga kura wakawa bado walisalia katika chama chao cha asili. Samahani, kisakuzi chako hakiwezi kuonesha ramani hii Isitoshe, wapo waliokuwa upande wa serikali Pwani lakini wakashindwa na wakati huu wamehamia upinzani. Mfano ni waziri wa zamani Chirau Ali Mwakwere aliyeunga mkono Bw Kenyatta mwaka 2013 lakini akashindwa. Bw Kenyatta alimteua kuwa balozi wa Kenya nchini Tanzania. Lakini sasa mwanasiasa huyo anawania ugavana jimbo la Kwale kupitia chama cha Wiper, chake Bw Musyoka. Maeneo ya kushindaniwa Kwa kuangalia uungwaji mkono wa mirengo yote miwili kisiasa, maeneo ambayo hakuna mrengo mmoja uliopata zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa mwaka 2013, ni ishara kwamba kunaweza kukatokea mabadiliko fulani. Majimbo ambayo hakukutokea mbabe wa moja kwa moja ni pamoja na jiji kuu Nairobi, Lamu, Garissa, Wajir, Marsabit, Isiolo, Samburu, Trans Nzoia, Narok, Kajiado, Vihiga, Bungoma na wapiga kura nje ya nchi. Nini kitaamua nani atashinda? Ndipo mgombea aweze kutangazwa mshindi, mwaniaji ni lazima awe amepata kura angalau moja juu ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa. Kwa kufuata matokeo ya mwaka 2013, ambapo Rais Kenyatta alishinda kwa asilimia 50.7 kunaweza kukatokea mabadiliko kwa kutegemea idadi ya wapiga kura watakaojitokeza katika maeneo mbalimbali, ngome za kila mgombea na maeneo ya kushindaniwa. Kwa kuangalia upigaji kura wa mwaka 2013, kuna maeneo ya Pwani kwa mfamo Mombasa na Kilifi ambapo idadi ya waliojitokeza ilikuwa asilimia 66 na 65 mtawalia. Katika maeneo hayo mawili, Bw Odinga alipata asilimia 70 na asilimia 84 ya kura zilizopigwa. Hiyo inaashiria uwezekano kwamba iwapo watu wengi zaidi wangejitokeza maeneo hayo - iwapo upigaji kura ungefuata mtindo wa waliojitokeza- huenda kura zake zingeongezeka. Mtafiti mkuu katika kampuni ya Ipsos Tom Wolf, alipokuwa anatoa matokeo ya utafiti wa maoni wa kampuni hiyo 23 Julai, alidokeza kwamba kiwango cha kujitokeza kwa wapiga kura kitachangia sana kuamua nani ataibuka mshindi kati ya Bw Kenyatta na Bw Odinga. Bw Wolf anaamini mshindi atapatikana katika duru ya kwanza. Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni mbalimbali yanaonekana kutofautiana. Matokeo ya karibuni zaidi (Julai 23) ya Ipsos Kenya yasema Bw Kenyatta anaongoza akiwa na asilimia 47 naye Bw Odinga ana asilimia 43. Ipsos wanasema asilimia 5 hawajaamua watampigia nani kura. Hao wengine hawatapiga kura au watampigia wagombea hao wengine. Kwa kulinganisha na matokeo ya utafiti yaliyotolewa mwishoni mwa Juni, rais ameshuka kwa asilimia moja naye Bw Odinga akaimarika kwa asilimia moja. Matokeo ya kampuni ya Infotrak yaliyotolewa siku iyo hiyo hata hivyo yanaonesha Bw Odinga anaongoza akiwa na asilimia 47 naye Bw Kenyatta akimfuata akiwa na asilimia 46. Kwa mujibu wa Infotrak, asilimia 6 hawajaamua watamuunga nani mkono. Mkuu wa Infotrak pia anasema uwezekano wa kukosekana mshindi awamu ya kwanza ni finyu mno. Charles Hornsby mwandishi wa kitabu kwa jina Kenya: A History since Independence, (Kenya: Historia ya tangu uhuru) kwenye utathmini wake mtandaoni anasema baada ya kuzingatia idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura, asili ya wapiga kura na mtindo wa upigani kura, Bw Kenyatta ana nafasi nzuri ya kushinda katika awamu ya kwanza. Anakadiria kwamba kitaifa kiwango cha kadiri cha wapiga kura asilimia 83 watajitokeza, maeneo kama vile Kati na Nyanza yakiwa juu hadi asilimia 90 na mengine mfano Mombasa, Kilifi na Kwale yakishuhudia viwango vya chini vya wapiga kura kujitokeza vya hadi asilimia 65. Hata hivyo, mwenyewe pia anakiri kwamba ni vigumu kubashiri hasa wapiga kura watajitokeza kwa kiwango gani. Samahani, kisakuzi chako hakiwezi kuonesha ramani hii Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kila kaunti Kenya 2017 Takwimu za kufikia tarehe 31 Julai 2017. Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) ulipomtangaza mgombea wake wa urais, na mgombea mwenza katika mkutano ukumbi wa Bomas Nairobi mwezi Aprili, kinyang'anyiro cha kipekee kilianza kujisuka. text: Rais wa Marekani Donald Trump Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China ameionya Marekani kuwa ''ifuatilie masuala yayoihusu nchi yao'' kabla ya kuinyanyapaa China. Wagonjwa wa kwanza wa virusi vya corona waliripotiwa katika mji wa Wuhan nchini China mwishoni mwa mwaka 2019. Hatahivyo, wiki iliyopita msemaji wa wizara ya mambo ya nje alishutumu jeshi la Marekani kupeleka kirusi katika mji wa Wuhan. Shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo kuitaka China kuacha kusambaza ''taarifa za kupotosha'' kama ilivyojaribu '' kulaumu'' kuhusu mlipuko wa virusi. Mpaka sasa zaidi ya watu 170,000 wameambukizwa duniani, huku China ikiwa na watu 80,000 waliopata maambukizi Hatahivyo, siku ya Jumanne, Beijing ilisema ina mgonjwa mmoja tu mpya nchini China. Donald Trump amesema nini? Rais wa Marekani aliandika kwenye ukurasa wa twitter kuhusu virusi vya corona- vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 kuwa ''virusi vya China''. Shirika la afya duniani (WHO) limeonya kuhusisha virusi na eneo au kundi fulani, kutokana na hatari ya unyanyapaa. Hatahivyo maafisa wa serikali ya Marekani wameviita virusi hivyo kuwa virusi vya corona. Huku Pompeo akirejea kuita ''virusi vya Wuhan''. Kauli ya Trump imepokewaje? Geng Shuang, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, amesema kauli hiyo ni ''unyanyapaa dhidi ya China''. ''Tunaitaka Marekani kusahihisha makosa yao na kuacha kabisa kutoa shutuma zisizo na msingi dhidi ya China,'' aliongeza. Shirika la habari la Xinhua limenukuu maafisa wa China wakisema kuwa kauli ya Trump ni ya '' kibaguzi'' na kubainisha kuwa ''kutokuwajibika kwa wanasiasa'', kunakoleta athari ya hofu kuhusu virusi vya corona. Pia Trump amekosolewa ndani ya Marekani, huku Meya wa New York Bill de Blasio akisema kauli yake ''ni ya kichochezi isiyovumilika'' dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Asia. China imeghadhibishwa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuelezea virusi vya corona kuwa ni ''virusi vya China''. text: Arteta aliichezea Arsenal mara 150 kati ya 2011 na 2016 Arteta alidaiwa kuwaaga wafanyakazi wenzake katika klabu ya Man City Alhamisi asubuhi. Mawakili wa Arsenal wamekuwa wakiwasiliana na klabu ya Manchester City kuhusu Mikel Arteta kuwa mkufunzi mpya wa Arsenal. Raia huyo wa Uhispania bado yupo chini ya kandarasi ya City huku klabu hiyo ikisubiri Arsenal kuilipa fidia. Mkutano wa kaimu mkufunzi Freddie Ljungberg ulifutiliwa mbali siku ya Alhamisi.City imekasirishwa na jinsi Arsenal ilivyochukulia swala hilo tangu siku ya Jumapili. The Gunners walishindwa kusema kwamna wana hamu ya kumsajili raia huyo mwenye umri wa miaka 37 ili kuchukua mahala pake Unai Emery licha ya timu hizo mbili kukutana katika uwanja wa Emirates , lakini baadaye wakawatuma maafisa wake wao wawili kwa mkutnao wa usiku na Arteta kufuatia ushindi wa City wa 3-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates. Hatahivyo hakujakuwepo na mawasiliano yoyote ya maafisa wa kuu wa Arsenal kwa City , ambao hawamlaumu Arteta ambaye amekuwa akimpasha mkufunzi Pep Guardiola kila yanayojiri. MIkel Arteta anatarajiwa kutangazwa kuwa mkufunzi mpya wa Arsenal siku ya Ijumaa. text: Picha ya Ansbert Ngurumo akiwa Finland Ngurumo ambaye amefanya kazi na vyombo kadhaa vya habari nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na gazeti la Mwanahalisi ambalo limefungiwa hivi karibuni, anaishutumu serikali kwa kupanga njama hizo za kutoa uhai wake. Lakini Msemaji wa serikali amepuuza madai hayo ya Bwana Ngurumo na kusema Ngurumo amekimbia kwa sababu zake binafsi na kwamba uhuru wa habari na kujieleza nchini Tanzania ni wa uhakika. Aliyefanya mahojiano na wote hawa ni mwandishi wa BBC, Sammy Awami na haya ndio mazungumzo yao: Sammy: Hii ni mara ya kwanza kwa mwandishi wa habari wa Tanzania, kukimbia nchi yake na kudai kuomba hifadhi katika nchi nyingine kwa madai ya kuwa hatarini kutokana na kazi yake ya uandishi wa habari. Ngurumo: Kimsingi yaliyonikuta ni marefu sana lakini la msingi ni kuwa nimekimbia, nimejificha najihadhari na ni tofauti na wanaosema nimeikimbia nchi, mimi sijaikimbia nchi, nchi ni ya kwangu, mimi ni mtanzania na najua mambo haya yataisha na nitarudi. Lakini kitu kikubwa ni kwamba nimewakimbia wauwaji, nimekimbia watesaji , nimekimbia watu wanaowateka watu ambao wanalindwa na dola.. Sammy:Umetoa shutuma kwamba hawa watekaji, wanaoua watu, wanalindwa na dola, hizi ni shutuma nzito sana Bwana Ngurumo, una uthibitisho gani kuwa dola inawalinda hawa watu? Ngurumo: Kama hutaki kuituhumu dola katika mazingira haya, unamtuhumu nani ambaye anapaswa kushughulikia haya? Amepotezwa Azory mwandishi habari wa Mwananchi, waajiri wake na wafanyakazi wenzake wameandamana wametaka arudi. Leo ni zaidi ya siku 100 hajulikani alipo, serikali iliyohai inayofanya kazi, inayolinda uhuru wa raia, haitoi majibu nani atuhumiwe kama si wao? Ansbert Ngurumo alikuwa akiandikia gazeti la MwanaHalisi Sammy: Lakini serikali inasema inaendelea na uchunguzi wa matukio yote haya,kwa nini usiiamini? Ngurumo: Vitendo na mwenendo na tabia yake vinaifanya isiaminike, kwa sababu hatuoni ikichunguza. Kama serikali inaweza kukamata watu wanaoikosoa haraka, ikawapeleka mahakamani, inashindwa nini kukamata watu wanaowaua wanaoikosoa. "Ninaandika kwenye ukurasa wangu kwa mara ya kwanza baada ya miezi minne tangu Oktoba 2017. Ninamshukuru Mungu na Wasamaria wema kwa kunisaidia na kuiokoa maisha yangu kutoka kwa mikono ya 'watu wasiojulikana' Tanzania Sammy: Wewe ulifanya nini, ulisema nini, uliandika nini hata hawa unaowashutumu kutaka kukutoa uhai kukufuata? Ngurumo: Nimekuwa naandika kwenye magazeti kwa zaidi ya miaka 20 lakini kwa miaka kama 15, nimekuwa na makala ya maswali magumu imekuwa inawauma sana na kuwakera watawala. Utawala uliopita ulikuwa pamoja na kuchukia, ulikuwa unavumilia na wakati mwingine kufanyia kazi, lakini utawala ulioingia umekuwa hautaki kuguswa wala kukosolewa. Sammy: Lakini Bwana Ngurumo, haya unayoyasema wewe si mwandishi pekee ambaye umekosoa serikali,kuna waandishi wengi na hata viongozi wa dini na watu wengine wamekuwa wakikosoa vitendo hivi kwa nini wakufuate wewe tu? Ngurumo: Hilo swali waulize wao lakini wameshapotea wengi kabla yangu , tofauti yangu na wengine ni kuwa mimi ni mepata bahati tu ya kutonywa. Serikali yasemaje kuhusu shutma hizo? Serikali ya Tanzania nayo imekanusha madai hayo, mwandishi wetu Sammy alizungumza na Dk. Hassan Abbas ambaye ni msemaji wa serikali ya Tanzania. Haya hapa ni mazungumzo yao: Sammy :Bwana Ngurumo anaishutumu serikali kutaka kutoa uhai wake kwa sababu ya kazi yake unalizungumziaje Dk.Abbas: Mimi niseme kuwa madai yake hayana msingi na labda ana ajenda zake ambazo nafikiri tusubiri kuziona kwa sababu serikali ya Tanzania imesajili vyombo vingi vya habari na ndio inayoruhusu mwanahabari kufanya kazi zake na kila mwanahabari anatekeleza kazi zake kwa misingi ya taaluma Dk Hassan Abbas Sammy: Anatoa mifano ya watu wamepotea, kwa sababu za kisiasa, anaamini kuwa kuna watu wanakamatwa, na yeye kwa kuwa amekuwa akikosoa serikali kwa muda mrefu ndio sababu anadai serikali inataka kutoa uhai wake? Dk.Abbas: Mimi nafikiri Ngurumo tumsaidie, watu wanaodai kuwa mtu fulani amechukuliwa hatua kwa sababu ya kazi yake au kukosoa, nafikiri hawaitendei haki nchi, hakuna sheria ya nchi hii inayounda kosa la kukosoa serikali. Visa vya mauaji ya kutoweka kwa watu Tanzania Sammy:Kwa hiyo unahakikishia watu kuwa uhuru wa kujieleza na habari tanzania uko safi kabisa? Dk.Abbas:Uko salama kwa mujibu wa vigezo vya kisheria, kwamba waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa hiyo nafikiri Tanzania tuko salama tunaendelea vizuri, niwaambie wana habari watimize wajibu wao wasitengenezewe hofu isiyokuwepo lakini kikubwa tunazo sheria na taratibu za taaluma yetu. Kuhusisha suala la Azory kutekwa au kupotea na serikali; tujiulize suala moja, Azory ameandika kitu gani cha kukosoa kikaiudhi serikali? Maendeleo makubwa ambayo tunafanya kwenye nchi yetu hayawezi kuwapendeza wengi kwa hiyo tunajua wako watu watapika mambo mengi kisiasa lakini sisi tunasimama kuzingatia misingi ya sheria za nchi . Tukitoa mfano wa Sugu, alisimama mahakamani akajitetea akachukuliwa hatua, ukitoa mfano wa Azory aliandika nini na wapi dhidi ya serikali mpaka kukawa na kiashiria kama hicho? mimi nafikiri tunahusisha matukio fulani ambayo hayana uhusiano na serikali. Sammy: hili suala la uhuru wa kutoa habari, kupokea na kujieleza limezungumzwa na makundi mengi, asasi za kiraia,jumuia ya kimataifa na hivi karibuni waraka wa maaskofu imeelezwa kumekuwa na uminyaji uhuru wa kujieleza kutoa maoni yao kwa ujumla , wanauliza kwa nini Tanzania imefikia hatua hii? Dk.Abbas:Mjadala wa uhuru wa kujieleza uko sehemu zote duniani ,mjadala kuhusu weledi wa waandishi wa habari na usahihi wa habari zinazotolewa, unaposema haki ya kupata habari si habari zozote, bali habari sahihi, na kuna misingi ya kufuata. misingi yakitaaluma isipofuatwa kuna hatua za kisheria zitachukuliwa.Ukimdhalilisha mtu ukichukuliwa hatua huwezi kusema ni kukiuka uhuru wa habari .Ukiingilia usalama wa taifa nchi zote duniani zinalinda usalama wake ukiingilia unachukuliwa hatua. Mwandishi wa habari mwandamizi Ansbert Ngurumo ambaye amekimbilia ulaya nchini Finland kwa kile anachokiita kuwa ni kunusuru maisha yake, amezungumza na BBC. text: Takriban watu 40,000 wamedaiwa kudanganywa na tapeli huyo Pudit Kittithradilok ,34, alikiri kumiliki mradi mmoja wa piramidi ambao aliwaahiidi wawekezaji kupata mapato ya hali ya juu. Takriban watu 40,000 walikubali kuwekeza kiwango cha $160m katika kampuni yake. Mahakama ilisema kuwa alijihusisha na vitendo vya kutoa mikopo na makosa 2,653 ya udanganyifu. Baada ya kukiri ,mahakam hiyo ilipunguza hukumu hiyo na kumpatia kifungo cha miaka 6,637 na miezi sita. Huenda asihudumu zaidi ya miaka 20 kwa kuwa sheria ya Thai inatoa miaka 10 kwa makosa mawili aliyopatikana nayo. Waendesha mashtaka waliambia mahakama kwamba Pudit aliandaa semina ambapo waliohudhuria walishawishiwa kuwekeza katika kile alichosema ni biashara zinazohusiana na ujenzi ,urembo, uuzaji wa magari yaliotumika uuzaji wa bidhaa nje ya nchi miongoni mwa vitu nyengine. Kulingana na gazeti la Bangkok Post, wawekezaji waliahidiwa mapato makubwa na marupurupu iwapo wataleta wanachama wapya. Na kama mradi mwengine wowote wa Piramidi, wawekezaji waliowekeza fedha zao wa kwanza wanalipwa kuwalipa wanachama wao wa kwanza. Pudit alikuwa anazuiliwa katika jela ya Bangkok tangu alipokamatwa mwezi Agosti wakati aliponyimwa dhamana. Mahakama ilizipiga faini kampuni zake mbili ilio sawa na dola milioni 20 kila moja. Pudit na kampuni zake aliagizwa kulipa takriban dola milioni 17 kwa waathiriwa 2,653 pamoja na riba ya kila mwaka ya 7.5% Mahakama moja ya Thailand imemuhukumu tapeli mmoja zaidi ya kifungo cha miaka 13,000 jela. text: Maelfu ya waandamanaji walikuwa wakiimba ''utawala wa kiraia'' polisi walipowatawanya kwenye maeneo kadhaa ya mji wa Khartoum, mashuhuda wameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP. Siku ya Jumamosi, vikosi vya kijeshi vilivunja mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na waratibu wa maandamano. Jeshi nchini humo lilimuondoa madarakani rais Omar al-Bashir mwezi Aprili. Bashir aliingia madarakani kwa mapinduzi tarehe 30 mwezi Juni mwaka 1989. Wanaharakati waliitisha maandamano siku ya Jumapili, maandamano ya kwanza yaliyopangwa tangu watu kadhaa walipouawa baada ya jeshi kushambulia waandamanaji tarehe 3 mwezi Juni. Maelfu ya watu waliandamana kwenye miji mbalimbali nchini Sudani kutaka mabadiliko ya utawala na kukabidhiwa kwa raia. Jeshi lawakamata viongozi wa upinzani Sudan Omar Al Bashir ashtakiwa Mjini Khartoum, polisi waliwamwagia waandamanaji gesi ya kutoa machozi katika eneo la Bari, Mamura na Arkweit upande wa mashariki. AFP walikariri mashuhuda wa tukio hilo. Maduka yalifungwa katika maeneo ambayo maandamano yalifanyika. Vikosi vya usalama vilisambazwa katika maeneo mbalimbali kabla ya maandamano hayo. Kiongozi wa maandamano, Ahmed al-Rabie ameliambia shirika la AFP kuwa jeshi limevunja mkutano na waandishi wa habari mjini Khartoum siku ya Jumamosi. ''Kabla ya kuanza mkutano, magari matatu ya jeshi yakiwa na wanajeshi waliokuwa na silaha, walifika kwenye jengo letu.Walituambia tusifanye mkutano,'' alieleza. Kila mtu kwenye jengo alitakiwa kuondoka, alieleza bwana Rabie. Aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa uvamizi uliofanywa ni ''ukiukwaji wa uhuru, na kitendo hicho ni kibaya zaidi kuliko utawala wa rais aliyepita.'' Jeshi lilisema litawawajibisha wapinzani ikiwa kutakuwa na machafuko au vifo wakati wa maandamano. Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, ajulikanaye kwa jina la Hemeti, amewaonya ''wahalifu'' ambao watatumia vurugu hizo kutekeleza azma yao. Mazungumzo kati ya baraza la mpito la kijeshi na upinzani yalivunjika baada ya tarehe 3 mwezi Juni na hayajafanyika tena pamoja na kuwepo kwa mpatanishi kutoka umoja wa Afrika na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. Siku ya Ijumaa, kuliripotiwa kuwa viongozi wa upinzani, walikamatwa na kushikiliwa huku jumuia ya kimataifa ikiombwa kushinikiza kuachiliwa kwao. Polisi nchini Sudan wamewasambaratisha waandamanaji kwa gesi ya kutoa machozi walipoingia barabarani wakishinikiza kukoma kwa utawala wa kijeshi mjini Khartoum. text: Alex Oxlade-Chamberlain aliichezea Liverpool msimu uliopita na kufunga magoli matano Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hajacheza tangu alipopata jereha la goti wakati wa mechi ya nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Roma mnamo mwezi Aprili. Tunahisi sasa ndio wakati mwafaka kuwaambia watu kwamba Ox , msimu huu utakuwa wa kuuguza jeraha, alisema Klopp. Tulijua hili tangu alipopata jeraha hilo. OX-laide Chamberlain alikosa kombe la dunia baada ya kupata jeraha la goti wakati alipokuwa akimkabili mchezaji wa Roma Aleksandar Kolarov katika uwanja wa Anfield tarehe 24 April. Akicheza mara 32 , alihamia Liverpool kutoka Arsenal msimu uliopita kwa dau la £35m. Oxlade-Chamberlain alifanyiwa upasuaji msimu uliopita, lakini Klopp alisema kuwa mchezaji huyo hakutaka ubaya wa jeraha hilo kutajwa wakati huo kwa kuwa ungeathiri kampeni ya kutaka kushinda kombe la vilabu bingwa. Liverpool ilishindwa 3-1 katika fainali na Real Madrid. Alex Oxlade-Chamberlainalichapisha picha hii katika mtandao wake wa Instagram "Hakuna mabadiliko yoyote , kila kitu kimekwenda kulingana na wakati tulioweka'', alisema Klopp. Habari mpya ni kwamba sasa tumeanza kutoa habari kuhusu jeraha hilo hadharani. ''Hatukutaka habari hizi kuathiri mwisho wa msimu, kwa kweli tuliona ni vyema kuzungumza wakati unaofaa''. Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa kukosa kipindi kirefu cha msimu wa 2018-19 kulingana na mkufunzi Jurgen Klopp. text: Viola Davis alishinda tuzo ya mwigizaji bora msaidizi wa kike Washindi wa tuzo hizo, makala ya 74, wametangazwa kwenye hafla iliyofanyika mjini Los Angeles. Filamu ya vichekesho yenye mtungo wa muziki 'La La Land' imeshinda tuzo saba. Damien Chazelle alishinda tuzo ya mwelekezi bora wa filamu hiyo nao Ryan Gosling na Emma Stone wakishinda tuzo ya waigizaji bora wa kiume na kike mtawalia. Filamu ya Moonlight ilishinda tuzo ya filamu bora zaidi. Casey Affleck ameshinda mwigizaji bora katika vipindi vya Televisheni kwa uigizaji wake Manchester by Sea. Isabelle Huppert aliyecheza filamu ya Kifaransa ya Elle ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike. Filamu Filamu bora zaidi - Igizo Filamu bora zaidi - Ucheshi au iliyowasilishwa kwa njia ya muziki Mwigizaji bora zaidi wa kiume katika filamu - Igizo Mwigizaji bora zaidi wa kike katika filamu- Igizo Manchester by the Sea iliteuliwa kushindania tuzo tano Mwigizaji bora zaidi wa kiume katika filamu - Ucheshi au iliyowasilishwa kwa njia ya muziki Mwigizaji bora zaidi wa kike katika filamu - Ucheshi au iliyowasilishwa kwa njia ya muziki Mwigizaji msaidizi bora zaidi wa kiume Mshindi: Aaron Taylor-Johnson - Nocturnal Animals Mwigizaji msaidizi bora zaidi wa kike La La Land, ambayo waigizaji nyota ni Ryan Gosling Emma Stone, ilikuwa inashindania tuzo saba Mwelekezi bora zaidi - Filamu Mshindi: Damien Chazelle - La La Land Uigizaji bora zaidi - Filamu Filamu bora zaidi ya katuni hai Filamu bora zaidi ya lugha ya kigeni Midundo bora zaidi - filamu Wimbo bora zaidi asilia - filamu Billy Bob Thornton alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume wa filamu za televisheni wa kiume Televisheni Mwendelezo bora zaidi wa filamu za televisheni - Igizo Mwendelezo bora zaidi wa filamu za televisheni - Ucheshi au iliyowasilishwa kwa njia ya muziki Mwendelezo mdogo bora zaidi wa filamu au filamu bora zaidi za televisheni Mshindi: The People v OJ Simpson: American Crime Story Hugh Laurie na Tom Hiddleston walishinda kwa uigizaji wao The Night Manager Mwigizaji bora zaidi wa kiume katika mwendelezo wa filamu za televisheni - Igizo Mwigizaji bora zaidi wa kike katika mwendelezo wa filamu za televisheni - Igizo Mwigizaji bora zaidi wa kiume katika mwendelezo wa filamu za televisheni - Ucheshi au iliyowasilishwa kwa njia ya muziki Mwigizaji bora zaidi wa kike katika mwendelezo wa filamu za televisheni - Ucheshi au iliyowasilishwa kwa njia ya muziki Thandie Newton alishinda kupitia Westworld ya HBO Mwigizaji bora zaidi wa kiume katika mwendelezo mdogo wa filamu au filamu za televisheni Mwigizaji bora zaidi wa kike katika mwendelezo mdogo wa filamu au filamu za televisheni Mwigizaji bora wa kiume msaidizi katika mwendelezo mdogo wa filamu au filamu za televisheni Mwigizaji bora wa kike msaidizi katika mwendelezo mdogo wa filamu au filamu za televisheni Hii hapa ni orodha ya washindi na waliokuwa wanashindania tuzo kuu za filamu na televisheni nchini Marekani za Golden Globe makala ya 74. text: Barcelona yamshtaki Neymar kwa kuhamia PSG Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita cha £200m kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi Agosti baada ya kununua kandarasi yake katia klabu ya Barcelona . Barcelona sasa inamtaka kurudisha marupurupu aliyopewa baada ya kutia saini kandarasi mpya ya miaka mitano miezi tisa pekee kabla ya kulazimisha uhamisho huo. ''Klabu inataka mchezaji huyo kurudisha marupurupu aliyolipwa kwa kuwa hakumaliza kandarasi yake'', ilisema taarifa. Mbali na Yuro milioni 8.5 za marupurupu, klabu hiyo pia inataka kulipwa asilimia 10 ya fedha hizo kwa kuchelewa kulipwa. Taarifa hiyo iliendelea: Barcelona pia inaitaka PSG kuchukua jukumu la kulipa fedha hizo iwapo mchezaji huyo atashindwa kulipa. Kufuatia uhamisho huo Barcelona ilitangza kuwa inazuilia Yuro milioni 26 za marupurupu ambazo mchezaji huyo alifaa kulipwa. Barcelona imesema inamshtaki aliyekuwa mshambuliaji wake Neymar kwa kitita cha £7.8m kufuatia uhamisho wake katika klabu ya PSG nchini Ufaransa. text: Hii ni kutokana na uhasama wa kisiasa ambao umekuwa ukiendelea kati ya taifa lake la Armenia na Azerbaijan. Mkhitaryan, 29, hakuweza kusafiri pamoja na wachezaji wenzake kwenda mji mkuu wa taifa hilo, Baku, Jumatano kwa ajili ya mechi hiyo ya Alhamisi. Hakuna uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya Armenia na Azerbaijan kutokana na mzozo wa muda mrefu kuhusu eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh. "Hawezi kusafiri huko," meneja wa Arsenal Unai Emery alikiri hilo. "Tuko hapa, wachezaji wana mtazamo mwema na wamejiandaa vyema kucheza." Gunners watakutana na Qarabag katika mechi ya Kundi E saa mbili kasoro dakika tano saa za Afrika Mashariki. Uefa wameambia BBC kwamba uamuzi wa pamoja ulifanywa na Arsenal na Mkhitaryan kwamba asisafiri kwa sababu za kiusalama. Matokeo ya mechi za Jumatano Ligi ya Mabingwa UEFA Alipokuwa anawachezea Borussia Dortmund mwaka 2015, Mkhitaryan hakuweza kusafiri kwa mechi ya Europa League dhidi ya klabu ya ligi kuu ya Azerbaijan ya Gabala kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama wake. Henrikh Mkhitaryan ameanza mechi mara tano msimu huu, na kufunga bao moja Kupitia taarifa, Uefa walisema: "Ni kawaida kwa Uefa kutuma barua za kusaidia mashirika, klabu na afisi za kibalozi katika kupata viza kuwawezesha wachezaji kusafiri kwenda nchi nyingine kucheza mechi za mashindano ya Uefa." Alipoulizwa kuhusu mzozo kati ya mataifa hayo mawili, Emery alisema: "Kazi yangu ni kandanda. "Naheshimu utamaduni wa kila mtu na naliheshimu kila taifa, lakini siifahamu hali katika kila taifa. Kwangu, hawezi kucheza. "Kuna heshima kwake na heshima kwako. Tuko hapa tukiwa na fursa ya kucheza vyema." Fainali ya Europa League 2019 itachezewa mjini Baku. Alipoulizwa iwapo Mkhitaryan ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Armenia atasafiri Azerbaijan kucheza fainali iwapo Arsenal watafika hatua hiyo, Emery alisema: "Ni safari ndefu sana kwetu kufika huko fainali. "Ka sasa, tunaangazia maandalizi ya mechi zijazo." Mkufunzi mkuu wa Qarabag Gurban Gurbanov alidai Arsenal walijaribu "kumuokoa" Mkhitaryan kutoka kwa "shinikizo" za kuchezea Azerbaijan. "Sikutaka siasa ziingilie mchezo lakini hatungefanya jambo lolote zaidi kuhusu suala hilo," alisema. "Iwapo Henrikh Mkhitaryan atataka kuja Azerbaijan, haitakuwa mara ya kwanza - wachezaji wengi wa Armenia huja Azerbaijan lakini ni uamuzi wa Arsenal kwamba asije. "Arsenal huenda wana wasiwasi kwamba mbele ya mashabiki 60,000 wa Azerbaijan, Mkhitaryan atakuwa na shinikizo sana na kushindwa kucheza na ndiyo sababu hawakusafiri naye Mkhitaryan." Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan hataweza kuwachezea katika mechi yaligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya klabu ya Qarabag. text: Kombora la Korea Kaskazini Japan na Marekani zimelaani majaribio ya makombora ya masafa marefu yaliyofanywa na Korea Kaskazini katika bahari ya Japan.Rais Trump na kiongozi wa Japan, Shinzo Abe, walikuwa wanakutana mjini Florida pindi uzinduzi huo wa makomboro ulipofanyika.Bwana Abe amelielezea tukio hilo kuwa halivumiliki. Kwa upande wake, Donald Trump amesema Marekani itashirikiana na Japan kwa asilimia mia moja.aziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini nae, amesema jaribio hilo, ambalo linakiuka vikwazo vya umoja wa mataifa, linaonyesha azma ya Korea Kaskazini ya kukuza teknolojia ya makombora ya nuklia. Raia huyu katika mji mkuu wa Korea Kaskazini wa Pyongyang, wanaonyesha jinsi wanavyounga mkono mpango wa kivita wa nchi yao, nchi yetu imeonyesha msimamo wake wazi, kwamba tutaendelea kujenga uwezo wetu wa kujilinda, kwa kutumia nguvu za nuklia, na uwezo wa kushambulia, katika kipindi ambacho maadui wetu wanaendelea na vikwazo vya kutugandamiza. Tutatetea amani na usalama wa nchi yetu kwa njia yoyote, kwa jitihada zetu wenyewe, na tutachangia amani ya dunia na utulivu." Mshauri mwandamizi katika ikulu ya Marekani amesema serikali ya rais Trump ,itaimarisha ushirikiano muhimu katika eneo la pacific ili kuepusha hali ya uhasama kutoka Korea ya kaskazini. Katika mahojiano ya televisheni, Stephen Miller amesema uhusiano mkubwa baina ya nchi mbili umeonyeshwa mwishoni mwa juma ambapo ziara ya waziri mkuu wa Japan kwa marekani, ambapo amekaa katika nyumba ya rais trump mjini Florida. Marekani, Japan na Korea ya Kusini wameomba kuwepo kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ili kujadili jaribio la kombora la hivi karibuni lililofanywa na Korea ya Kaskazini katika bahari ya Japan. text: Rais Magufuli siku ya Jumatatu alimtaka Bw Makonda kuendelea kuchapa kazi Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kiongozi huyo kudaiwa kuvamia kituo cha habari cha Clouds akiwa ameambatana na askari wenye silaha ili kutoa amri ya kurushwa hewani kwa kipindi cha televisheni. Marufuku hiyo ambayo pia inaungwa mkono na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania, itaendelea mpaka pale itakapotangazwa ama kuamriwa vinginevyo, wakuu wa jukwaa hilo wamesema. Katibu wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania Nevile Meena, amesema jukwaa hilo limekerwa na hatua ya afisa huyo wa serikali kuamuru kurushwa hewani kwa kipindi cha televisheni sambamba na kutumia nguvu kupora kipindi mali ya Clouds TV. Aidha, amesema afisa huyo anadaiwa kutumia maneno ya kejeli kwa waandishi wa habari. Kando na kutangaza kwamba halitatangaza au kuandika habari zozote zinazomuhusu Makonda, jukwaa hilo pia limemtaja kama adui wa uhuru wa vyombo vya habari. Mkanda wa video za siri yaani CCTV wa usiku wa Machi 17, 2017 katika studio za Clouds unaonesha mtu anayedaiwa kuwa Bw Makonda akiingia katika ofisi za kampuni ya Utangazaji ya Clouds iliyopo Dar es salaam, akiwa ameambatana na askari polisi pamoja na maafisa wenye silaha. Mpaka sasa hajazungumza lolote kuhusu suala hilo. Rais John Magufuli alisema katika hotuba yake Jumatatu alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelee kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye rais wa nchi. Dkt Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini. Jukwaa la wahariri nchini Tanzania limeazimia kutoandika ama kutangaza habari zozote zinazomuhusisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. text: Jinsi Uturuki ilivyowasili kaskazini mwa Uturuki Mataifa ambayo yamekuwa yakiuzia silaha Uturuki ni Marekani na Ulaya, lakini hivi karibuni taifa hilo limeelekea Urusi kununua mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya angani. Hivyobasi ni mataifa gani yameipiga marufuku Uturuki na hatua hiyo inaliweka wapi taifa hilo katika ununuzi wa silaha? Ni mataifa gani yamekataa kuiuzia Uturuki silaha? Mataifa tisa ya Ulaya yameweka masharti kuhusu uuzaji wa silaha kwa Uturuki. Taifa la jamhuri ya Czech , Finland , Ufaransa, Ujerumani, Itali, Uholanzi , Uhispania, Sweden na Uingereza yote pamoja na Canada yalitangaza kwamba yanasitisha uuzaji wa silaha kwa Uturuki. Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza Dominic Raab amesema kwkamba Uingereza itaendelea kuiuzia silaha Uturuki lakini haitatoa vibali vipya vya silaha ambazo zitatumika katika operesheni ya kijeshi nchini Syria. Ujerumani na Uhispania zimesema kwamba masharti yao yanaathiri kandarasi mpya pekee. Muungano wa Ulaya haujazuia uuzaji wa silaha , ijapokuwa mawaziri wa kigeni wamekubaliana kuchukua misimamo mikali kuhusu sera yao ya uuzaji wa silaha kwa Uturuki . "Vikwazo hivyo havitarajiwi kuwa na athari kubwa , dhidi ya operesheni za Ankara iwapo vitaendelea , kulingana mchanganuzi wa maswala ya ulinzi Yvonni - Stefania Efstathiou. Lakini iwapo vikwazo hivyo vitaendelea dhidi ya silaha zinazotumika mbali na Syria, kunaweza kuwa na athari mbaya kuhusu sekta ya ulinzi ya Uturuki. Je ni mataifa gani makuu yanayoiuzia Uturuki Silaha? Katika kipindi cha mwaka 1991-2017, Uturuki ilikuwa ya tano kwa ukubwa katika ununuzi wa silaha duniani. Uturuki kihistoria ilitegemea sana washirika wake wa Nato kama vile Marekani na Ulaya kwa mahitaji yake ya ulinzi na usalama. Marekani ndio taifa ambalo limekuwa likiiuzia Uturuki silaha, ambayo ni asilimia 60 ya bidhaa za nje zilizoagizwa katika kipindi cha 2014 na 2018. Miongoni mwa mataifa ya Ulaya , Ufaransa, Uhispania na Uingereza zimekuwa zikiiuzia Uturuki silaha chungu nzima. Chini ya serikali zilizotawaliwa na serikali za Uturuki miaka ya 80 na 90, ni silaha zilizoagizwa kutoka Marekani ambazo zilikuwa nyingi. Iijipatia ndege za kijeshi , makombora , ndege aina ya helikopta, vifaru, meli na vifaa vingine ambavyo bado vinatumika na jeshi la Uturuki. Lakini Uturuki hivi majuzi ilielekea Urusi kununua mfumo wa ulinzi uliogharimu dola bilioni 2.5, uamuzi ulioshangaza washirika wake wa Nato. Wanahoji kwamba ununuzi huo wa mfumo wa S- 400 kutoka kwa adui wa Nato unaweza kuathiri usalama kwa kuwa wanajeshi wa Uturuki ni washirika wa vifaa vya Nato pamoja na mifumo ya angani ya ulinzi. Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya angani kutoka Urusi S - 400 Marekani ilijibu kupitia kuizuia Uturuki kutonunua ndege zake za kivita aina ya F-35 , zikiwa ndio ndege za kisasa zaidi duniani. Kutokana na eneo lake zuri la kimkakati, Uturuki inamiliki kambi kadhaa za kijeshi za Nato na Marekani, ikiwemo mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora unaotoa onyo mbali na operesheni za Nato mashariki mwa Uturuki. Pia inamiliki mabomu 50 ya kinyuklia ya Marekani katika kambi ya wanaanga ya Incirlik karibu na mji wa kusini wa Uturuki wa Adana. Uturuki inamiliki viwanda vya kutengenezea silaha Uturuki imetengeza kiwanda chake cha kutengeneza silaha katika muongo mmoja uliopita ikiwa na lengo la kutotegemea wauzaji wa kigeni. Waziri wa Uturuki wa maswala ya kigeni Mevlut Cavusoglu hivi majuzi alisema kwamba Uturuki kwa sasa inazalisha zaidi ya asilimia 70 ya vifaa vyake vya kijeshi na pia ni muuzaji mkubwa wa silaha. Sio rahisi kubaini jinsi viwanda hivyo vya kutengeza silaha vinaafikia mahitaji ya ulinzi ya taifa hilo, kulingana na mchanganuzi Yvonni - Stefania Efstathiou. Licha ya kwamba kile ambacho Uturuki inadai kuwa vifaa vilivyotengezwa nchini humo , ukweli ni kwamba vimenunuliwa nje. Kati ya 2014 na 2018, Uuzaji wa silaha za Uturuki uliongezeka kwa asilimia 170. Lakini 2018, likuwa taifa la 14 kwa ukubwa linalouza silaha duniani, huku Saudia , UAE na Turkimenistan wakiwa wanunuzi wake wakubwa. Mataifa mengi ya Ulaya yamesitisha uuzaji wa silha kwa Uturuki kufuatia uvamizoi wake wa kijeshi kaskaini mwa Syria. text: Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefutwa kazi baada ya kuongoza timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18. Raia huyo wa Uhispania , ambaye awali alikuwa mkufunzi wa Paris St-Germain katika ligi ya Ufaransa na kushinda mataji matatu ya Yuropa akiwa na Sevilla, aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Arsenal mwezi Mei 2018, akimrithi Arsene Wenger. Mahala pake patachukuliwa kwa muda mfupi na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Freddie Ljungberg. Arsenal inasema kwamba uamuzi huo ulichukuliwa baada ya matokeo ya timu hiyo kushindwa kufikia kiwango kilichohitajika. Arsenal haijashinda katika mechi saba na ilipoteza 2-1 nyumbani dhidi ya klabu ya Ujerumani Eitracht Frankfurt katika ligi ya Yuropa siku ya Alhamisi. Arsenal ilianza msimu huu wakirekodi misururu ya ushindi dhidi ya Newcastle na Burnley, lakini ushindi huo ulimalizwa baada ya kulazwa na Liverpool, kabla ya kurekodi sare mbili dhidi ya wapinzani wao wa London Tottenham na Watford. Ushindi wao wa mwisho katika ligi ya Uingereza ulikuwa dhidi ya Bournemouth. Freddie Ljunberg wa pili kushoto ndiye naibu wa Emery katika klabu hiyo Siku ya Jumamosi, walitoka sare ya 2-2 ikiwa ni ya sita msimu huu nyumbani dhidi ya Southampton, huku Alexander Lacazette akifunga goli la kusawazisha katika muda wa majeraha. Emery ni mkufunzi wa tatu kufutwa kazi katika ligi ya England msimu huu baada ya Javi Gracia na Mauricio Pochettino. Ushindi wa mwisho wa Arsenal ulijiri dhidi ya Vitoria Guimaraes katika ligi ya Yuropa tarehe 24 mwezi Oktoba , ambapo walihitaji mipira miwili ya adhabu kupata ushindi wa magoli 3-2. Ljungberg ameanza kuiongoza katika mazoezi timu hiyo na taarifa ya Arsenal ilisema: Tuna matumaini na Freddie Ljunberg kutuogoza. Usakaji wa kocha mpya unaendelea na tutatoa tangazo tutakapokamilisha mpango huo. Siku ya Jumatano , BBC Sport iliripoti kwamba Arsenal inamuona Mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo kama mrithi wa Emery. Majina mengine yanayohusishwa na tangazo hilo ni pamoja na mkufunzi wa zamani wa Tottenham, Pochettino naibu kocha wa Manchester City Mikel Arteta na mkufunzi wa zamani wa Juventus Massimiliano Alegri na Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe. Walianza msimu huu baada ya kugharamika zaidi ya £130m walipomsaini winga Nicolas Pepe, beki wa katikati David Luiz, Beki wa kushoto Kieran Tierney, mshambuliaji Gabriel Martinelli na beki William Saliba, ambaye atajiunga msimu ujao. Pia klabu hiyo ilimununua kwa mkopo kiungo wa kati Dani Ceballos kutoka Real Madrid. Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefutwa kazi baada ya kuongoza timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18. text: Mtoto akipewa dawa ya TB Belarus imetajwa kuwa taifa lenye viwango vya juu vya maradhi ya kifua kikuu sugu. Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani(WHO) takriban watu milioni 2.5 waliambukizwa maradhi ya TB barani Afrika mwaka 2016 hii ikiwa ni robo ya visa vipya vya ugonjwa huo kote duniani. Shirika hilo linasema mataifa saba duniani yalikadiria 64% ya visa vipya vya TB mwaka 2016, India ikiongoza kataka mataifa hayo ikifuatiwa na Indonesia, China, Philippines, Pakistan, Nigeria, na Afrika Kusini, Dr Paula Fujiwara - kutoka shirikisho la kimataifa la kukabiliana na magonjwa ya Kifua kikuu na mapafu ameiambia BBC kuwa kupatikana kwa dawa mpya ya bedaquiline ni hatua kubwa katika harakati ya kutafuta tiba ya ugonjwa wa kifua kikuu. Dawa za kifua kikuu Lakini je Kupatikana kwa dawa hii kutasaidiaje katika vita dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ama TB barani Afrika? Dr Kamene Kimenye, Mkurugenzi wa Mpango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Ugonjwa wa Kifua Kikuu Nchini Kenya anasema dawa ya bedaquiline imekuwa ikitumika kwa karibu mika mitatu sasa. Pamoja na kuwa ni dawa mpya ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu kikamilifu kwa sababu vimelea vinavyousababisha havijaizoea. Dr Kamene pia anasema, ''Kenya tumetumia dawa ya bedaquiline kwa wagonjwa 30 na mataifa mengine pia katika bara la Afrika kama vile Afrika kusini na Ethiopia zimekua zikitumia'' Hivi karibuni Viongozi wa nchi na wakuu wa serikali walipitisha azimio la kisiasa lenye lengo la kuchagiza hatua dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, au TB unaosababisha vifo vya watu milioni 1.6 kila mwaka. Azimio hilo linalofahamika kama "Ushirikiano wa kutokomeza TB: Hatua ya dharura ya kimataifa," linalenga kutafuta hatua ambayo itachangia kutokomezwa kwa ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030, ambayo pia ni ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Viongozi hao walisema kuwa wametambua changamoto zilizopo ikiwemo ukosefu wa vifaa, dawa sahihi na hata fedha, bila kusahau jinsi ambavyo TB inasababisha umaskini miongoni mwa familia, jamii na taifa. Msingi wa azimio hilo ni upi? Kwa mantiki hiyo viongozi hao wameazimia pamoja na mambo mengine kutenga fedha zaidi za utafiti na kusaka dawa sahihi sambamba na kuhakikisha hakuna mtu yeyote mwenye TB ambaye hatofikiwa na upimaji na matibabu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza hatua ya kupitishwa kwa azimio hilo lenye vipengele 53, akisema lina matarajio makubwa lakini mafanikio yake yatafikiwa iwapo jitihada za pamoja zitawekwa kwenye takwimu bora na sayansi, maamuzi sahihi, kuwezesha jamii na hatua za kimkakati na zilizofadhiliwa. Ametaja changamoto kama vile usugu wa dawa akisema kila mwaka wagonjwa 600,000 wanakabiliwa na usugu wa tiba dhidi ya TB, "tunahitaji maendeleo ya kisayansi ili kupata mbinu bora zaidi za kukabiliana na TB, sambamba na tishio la ongezeko la usugu wa dawa za kuua vijiumbe maradhi." Ladha tamu ya dawa ya TB kwa watoto inasaidia katika tiba ya ugonjwa huo kwa watoto Bwana Guterres amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kufuata mwongozo wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus na shirika lake katika kuchagiza usaidizi wa Umoja wa Mataifa kwa serikali na mashirika ya kiraia na wadau wengine ili kupata kasi inayohitajika kutokomeza TB duniani. Kwa upande wake Dkt. Ghebreyesus ametaja mambo matatu muhimu ambayo yanaweza kusaidia kufikia lengo la kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030. - Msaada usiotikisika wa wadau wote utakaofanikishwa na ungwaji mkono na viongozi wa ngazi ya juu kabisa. - Uwekezaji hasa katika sayansi na utafiti, dawa mpya, chanjo mpya na mbinu mpya za utambuzi wa TB. - Jukumu la kila mtu kumwajibisha mwenzake. Dkt. Ghebreyesus amesema "Ndio maana tunaandaa mfumo wa uwajibikaji ulio mtambuka ukiwa na misingi mikuu minne: Ahadi, hatua, ufuatiliaji na tathmini kuhakikisha kuwa kile tusemacho kinaenda sambamba na tunachotenda." Madaktari nchini Belarus wamefanikiwa kutibu zaidi ya 80% ya aina moja ya ugonjwa wa kifua kikuu sugu kwa kutumia mchanganyiko wa dawa mpya inayojulikana kama bedaquiline, pamoja na dawa zingine za antibiotiki. text: Wanawake wa Saudia husimamiwa na wanaume. Mawakili wanawake wanapendekeza kuwa hatua hiyo itamaliza kile kinachotajwa kuwa talaka za siri - ambapo wanaume hutoa talaka bila kuwaelezea wake zao. Amri hiyo itahakikisha kuwa wanawake wanajua hali ya ndoa yao na itawalinda dhidi ya masurufu. Mwaka uliopita marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa na mahakama nchini Saudia. Hatahivyo wanawake bado wako chini ya usimamizi wa wanaume. ''Sheria hiyo mpya itahakikisha kuwa wanawake wanapewa haki zao za masurufu wakati wanapopewa talaka'', alisema wakili Nisreen al-Ghamdi. Pia ina hakikisha kuwa uwezo wowote utakaotolewa na mahakama hautumiki vibaya. ''Wanawake wengi wamewasilisha malalamisihi yao katika mahakama za rufaa kwa kupewa talaka bila ya wao kujua'' , kulingana na wakili Samia al-Hindi. Hatua hiyo mpya inasemaekana kuwa miongoni mwa mabadilikio ya kiuchumi na kijamii yalioshinikizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ikiwemo kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani na kutazama mechi za kandanada mbali na kufanya kazi ambazo awali zimekuwa zikifanywa na wanaume pekee. Ni mambo gani ambayo wanawake wa Saudia hawawezi kufanya? Kuna vitu vingi ambavyo wanawake wa Saudia bado hawaruhusiwi kufanya bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa wasimamizi wao wa kiume kama vile waume zao , baba zao ndugu wa kiume ama watoto wao. Vitu hivyo ni: Hali hiyo ya kusimamiwa na wanaume imesababisha taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa ambayo usawa wa kijinsia umekandamizwa mashariki ya kati. Sheria mpya nchini Saudia inawalinda wanawake kutopewa talaka bila kujua. Kuanzia siku ya Jumapili , mahakama zitatakiwa kuwaelezea wanawake kupitia njia ya ujumbe wa simu kwamba wamepewa talaka. text: Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan Katika kipindi hicho makumi kwa maelfu ya watu walikamatwa na kushikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka chini ya agizo la Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan. Wanajeshi, Polisi, Raia, Waandishi wa Habarai na walimu ni miongoni mwa waliokamatwa. Maelfu wengine ikiwemo majaji kadhaa waliachishwa kazi zao. Reli mpya ya SGR nchini Kenya yasababisha hasara ya shilingi bilioni 10 Mfanyakazi azawadiwa gari na mwajiri wake baada ya kutembea umbali wa kilomita 32 Zawadi ya Magufuli kwa Obama na mambo mengine makuu Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari pekee hakuwezi kbadili hatua kazli za kisiasa zilizochukuliwa ambazo ziliibadili nchi hiyo na kuifanya inayokandamiza haki za binadamu. Mapema mwezi huu Rais Erdogan aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Uturuki ilimlaumu Gulen, kuhusika na jaribio la mapinduzi Wakati wa kampeni za uchaguzi, wagombea wa upinzani walisema kuwa kitu cha kwanza watakachokifanya iwapo watashinda uchaguzi ni kumaliza amri hiyo ya hali ya hatari iliyowekwa. Unamfahamu vyema Nelson Mandela? Wengi ya waliokamatwa kipindi hicho ni wale waliokuwa wakidaiwa kuwa wafuasi wa mpinzani wa Rais Erdogan anayeishi uhamishoni nchini Marekani, Fethullah Gulen, ambaye awali alikuwa mshirika wa Rais wa nchi hiyo. Uturuki ilimlaumu yeye na wafuasi wake kuwa ndio waliopanga mapinduzi ya kutaka kuiangusha serikali ya nchi hiyo. Lakini hata hivyo mwenyewe alikana taarifa hizo. Vyombo vya habari vya taifa nchini Uturuki vimetangaza kwamba serikali imeondoa hali ya hatari iliyowekwa nchini humo kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa miaka miwili iliyopita. text: Waandamana dhidi ya uongozi wa rais Jacob Zuma Wanayaita maandamano hayo #OccupyLuthuliHouse,wakitaja makao makuu ya chama hicho mjini Johannesburg,mji mkuu wa taifa hilo. Lakini waandamanaji wamepunguza kasi ya maandamano yao baada ya usalama kuimarishwa. Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko ambaye yuko katika eneo la maandamano hayo anasema kuwa yanaendelea kuwa mabaya. Ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema wanajeshi wa zamani kwa jina uMkhonto we Sizwe,wanazuia waandamanaji kuingia katika afisi ya katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe. Lakini wanajeshi hao wa zamani wamekuwa wakitumia nguvu. Kundi moja la wanachama wa ANC nchini Afrika Kusini linapinga uongozi dhidi ya Jacob Zuma. text: Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya Kaitila Murusuri ,amesema walipowakea wanafunzi 24 saa mbili asubuhi na kuwapatia huduma ya kwanza. ''Tumepokea gari ya dharura kutoka zahanati ya karibu ya mkoma ikiwa imebeba wanafunzi wa shule ya msingi wapatao 24 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajali ya kupigwa na radi , tulipowafanyia uchunguzi wengi wao walikuwa katika hali ya kawaida, tuliporidhika tuliwaruhusu lakini tulibaki na wengine watano, kikubwa ni kwamba walipata mshtuko''. Alieleza daktari Murusuri. Watu 13 wafariki kwa ajali ya basi Kenya Mabaki ya miili iliyotokana na ajali ya Ndege yapokelewa Kenya Taarifa zimesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza kwa sasa wanaendelea vizuri na tayari wengi wao wameruhusiwa kutoka hospitali. Taarida zinasema kuwa majira ya saa moja asubuhi ilipiga radi kali katika shule iliyopo maeneo ya Nzera katika halmashauri ya wilaya ya Geita, Watumishi wa afya waliwahi kuwasaidia kupata huduma ya kwanza. Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel amesema amezungumza na watoto hao wa darasa la nne. ''Ni majira ya mvua kipindi hiki radi hupiga wakati wote ukiwa barabarani radi inakufuata, ukiwa kwenye jengo lenye umeme radi inapiga, ukiwa kwenye jengo la umeme, kukiwa hakuna umeme radi inapiga kuna teknolojia inapaswa kutazamwa kuona ni namna gani tunaweza kujikinga na radi katika majengo yetu''. Amesema mkuu huyo wa mkoa. Wanafunzi 39 wa darasa la nne shule ya Msingi Ihumilo wilayani Geita wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani. text: Aliyekuwa mwanariadha wa Tanzania John Akhwari Anajulikana kwa kuwa wa mwisho kuwahi kutokea katika michezo hiyo ya Olimpiki.Alimaliza wa mwisho saa moja baada ya wanariadha wenzake kumaliza. Aliingia katika uwanja wa michezo akipepesuka huku akitokwa damu mbali na bendeji zilizokuwa katika mguu wake. Alimuambia mwandishi wa BBC Sammy Awami kwa nini hakusalimu amri katika mbio hizo. ''Taifa langu halikunituma Mexico kuanza mbio bali kumaliza.Ni kutaka kwangu na uzalendo nilionao katika maisha yangu kama mwanariadha ndio ulionifanya kumaliza mbio hizo. Licha ya kuwa nilikuwa na mauamivu mengi''. Anaelezea kuwa mataifa mengine yaliwalinda wanariadha wao lakini hakuna mtu aliyemjali kwa kuwakilisha taifa lake. Aliyekuwa mwanariadha wa Tanzania John Akhwari John sasa ni mkulima na anaangazia ushiriki wake katika michezo hiyo. ''Ni fahari kubwa kwangu kushiriki katika mbio za marathon mjini Athns,Ugiriki mwaka 1962. Nilikuwa wa pili katika mbio hizo,na shindano la pili lilikuwa lile la mwaka 1968 nchini Mexico''. Mtanzania aliyetukuka licha ya kumaliza mwisho Olimpiki Kuhusu matokeo ya Tanzania ya michezo ya Olimpiki ya Rio De Janeiro,anasema:Nahisi vibaya lakini nifanyeje.Viongozi wa michezo hawawezi kubadili matokeo hayo. ''Iwapo timu yako haikushinda katika mashindano ya mwaka huu,ni lazima utafute njia za kuimarika ili uweze kushinda mwaka ujao na kuleta heshima kwa taifa lako''. Aliyekuwa mwanariadha wa Tanzania John Stephen Akhwari anakumbukwa kwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 1968 nchini Mexico. text: Espen Egil Hansen ni mhariri wa gazeti la Aftenposten, Gazeti maarufu zaidi nchini Norway Picha hiyo inamuonyesha mtoto msichana aliyekuwa bila nguo akikimbia moto katika kijiji kimoja, katika shambulizi lililotekelezwa kwa kutumia kemikali ya napalm. Facebook ilifuta picha hiyo kwa misingi kwamba ilikuwa ya uchi. Facebook inasema imerejesha picha hiyo kutokana na umuhimu wake wa kihistoria. Gazeti moja nchini Norway, Aftenposten, liliongoza shutuma dhidi ya Facebook, baada ya kampuni hiyo kufunga akaunti ya mmoja wa wanahabari wake, aliyetumia picha hiyo. Mhariri wa gazeti la Afte-posten la Norway, amesema uamuzi wa Facebook kufuta picha hiyo inaonyesha wazi haiwezi kutofautisha kati ya picha za ponografia na zile zinazohusiana na historia ya matukio muhumu duniani. Waziri mkuu wa Norway ambaye awali alichapisha picha hiyo kwenye akaunti yake kama ishara ya maandamano, amekaribisha uamuzi wa Facebook wa kurejesha picha hiyo. Waziri mkuu wa Norway anasema uamuzi wa Facebook ulionyesha ushawishi mkubwa wa mitandao ya kijamii. "wamefanya vizuri sana, mimi ni waziri mkuu aliye na furaha, inaonyesha kwamba matumizi ya mitandao ya kijamii yanaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa, hata kwa mitandao ya kijamii yenyewe" Waziri mkuu Erna Solberg ameiambia BBC. Msichana huyo ni nani? Kim Phuc, alikuwa mwenye umri wa miaka 9 wakati picha hiyo ilipochukuliwa, akikimbia kuokoa maisha yake, baada ya shambulizi la Napalm, kaskazini mwa Saigon mwezi Juni 1972. Alikumbwa na majeraha mabaya ya moto. Mpiga picha Nick Ut na mwanahabari wa ITN Christopher Wain walimpeleka hospitalini. Waliambiwa kwamba hakukuwa na matumaini kwamba msichana huyo angeendelea kuishi. Facebook inasema imerejesha picha hii kutokana na umuhimu wake wa kihistoria. Baada ya kulazwa hospitalini kwa kipindi cha miezi 14, na kufanyiwa upasuaji mara 17 , aliruhusiwa kuenda nyumbani. Facebook imebatilisha uamuzi wake wa awali wa kufuta moja ya picha mashuhuri ya wakati wa vita vya Vietnam. text: Wanawake wawili wanajaribu kuingia hekaluni Hata hivyo hakuna mwanamke yoyote aliyeingia kwani waandamanaji wenye kuzusha wenye fujo wamezuia njia. Wanawake wawili, mwandishi Kavitha Jagdal na mwanaharakati wa masuala ya kijamii, Rehana Fathima walifanikiwa kufika katika eneo la hekalu hilo siku ya Alhamisi. Polisi zaidi ya 100 waliwalinda kuzuia mawe waliyokua wanatupiwa na waandamanaji walipokuwa wakitembea kilomita tano sawa na maili tatu kuelekea kwenye hekalu hilo. Lakini iliwalazimu kurudi baada ya kusimamishwa na wafuasi wa hekalu hilo mita chache kutoka kwenye hekalu hilo. Waandamanaji pia wamejumuisha wanawake wengi ambao wameshiriki katika migomo, kuziba barabara na kukagua magari yanayo kwenda hekaluni yakiwa yamebeba mwanamke yoyote yule aliye kati ya umri wa kupata hedhi ya kila mwezi. Wakizingatia zaidi umri wa miaka 10 mpaka 50. Hekalu hilo linavutia mamilioni ya wafuasi kutoka pembe zote za nchi ya India. Kwanini wanaandamanaji wamekasirika? Baadhi ya wanawake wanaona ni upendeleo kunyimwa kuingia hekaluni Baadhi ya wapinzani wanaopinga kwa nguvu zote maagizo ya mahakama kuu kufutilia mbali sheria ya kuzuia wanawake kuingia katika hekalu hilo, ni kwasababu waandamanaji wanaamini kuwa agizo hilo linakwenda kinyume na matakwa ya mungu Ayappa mwenyewe. Waumini wa dini ya Kihindu wanawachukulia wanawake wanaopata hedhi kuwa ni najisi na huwazuia kushiriki katika shughuli za kidini. Wakati mahekalu mengi ya Wahindu yanawaruhusu wanawake kuingia ilimradi wakiwa hawapo katika hedhi, hekalu la Sabarimala ni moja kati ya mahekalu machache ambayo huwazuia kabisa wanawake walio katika umri wa kupata hedhi kuingia hekaluni. Wafuasi wa dini ya Kihindu wanasema marufuku ya wanawake kuingia katika hekalu hilo si kwasababu ya hedhi pekee, ni kwasababu ya kutii matakwa ya Mungu wao ambaye inaaminika kuwa aliweka wazi taratibu za kufuata ili kupata baraka zake. Kuna sababu mbali mbali za kuzuia wanawake kuingia hekaluni ikiwemo hedhi Kila mwaka mamilioni ya wafuasi wa kiume wanatembea kupanda katika kilima bila kuvaa viatu mpaka juu ili kuliona kaburi. Lakini pia hufunga - funga kavu - kwa siku 41 na kuepuka kabisa kuvuta sigara, pombe, nyama, ngono na kuwasiliana na wanawake walio katika hedhi kabla ya kuanza safari. Hekaya ya mungubwana Ayappa Kila mungu katika imani ya Kihindu ana haiba yake na upekee wa visa vyake mwenyewe, na mungu Ayappa hana tofauti. Kwa mujibu wa kisa cha hekalu, mungu Ayyappa hana mahusiano kwani amechukua kiapo cha useja, yaani kutoishi na mwanamke. Kuna visa kadhaa kuhusu suala hilo, kwa mujibu wa hadithi, Ayappa alizaliwa baada ya muungano kati ya miungu wawili wa kiume ambao wamempa nguvu na uwezo wa kumshinda pepo wakike ambaye alikuwa akisumbua hadi wakati huo. Juu ya kumshinda, ilifunuliwa kwamba alikuwa ni binti mdogo ambaye alilaaniwa kuishi maisha ya pepo. Pepo hilo lilimpenda kimapenzi mungu Ayappa na kumuomba amuoe, lakini Ayappa alikataa na kusema kuwa yeye amekusudiwa kwenda msituni na kujibu maombi ya wafuasi wake. Kwa nini kutekwa kwa MO kumeacha kishindo? Pepo hilo la kike liliendelea kumbembeleza, akamjibu kuwa atamuoa siku ambayo wafuasi wapya wataacha kwenda kufuata baraka zake. Siku ambayo haija wahi kutokea. Hadithi zinasema kwamba anamsubiria katika hekalu la pili ambalo lipo njiani kuelekea kwenye kaburi kuu la Sabarimala. Wanawake hawaendi kwenye mahekalu hayo, kwa imani kwamba wakifanya hivyo watakuwa wanatukana mungu na kujitoa kwa mwanamke aliyempenda. Kwa mujibu wa hadithi nyingine, Bwana Ayappa alikuwa mwana mfalme ambaye alikomboa ufalme wake kutoka kwa mvamizi wa kiarabu aliyeitwa Vavar. Baada ya mapigano, Vavar akawa mfuasi mtiifu wa mwanamfalme. Pia kuna kaburi ambalo lina wakfu wake karibu na hekalu la Sabarimala. Inasemekana yeye huwalinda wahamiaji wanaokuja kuomba baraka zake. Katika toleo hili, bwana Ayappa hatimaye aliweka nadhiri kujibu maombi ya kila mfuasi ambaye alikuja kwake, na alijiondolea kabisa hamu yote ya kidunia ikiwa ni pamoja na mahusiano na wanawake, ambapo ndio moja ya sababu ya kwa nini wanawake hawaruhusiwi ndani ya hekalu lake. Inaweza pia kukawa na historia nyingine zinazohusiana na mungu Ayappa na kwa nini wanawake hawaruhusiwi ndani ya hekalu lake. Baadhi ya wafuasi wanasema hawatarudi kwenye hekalu hilo kama uamuzi wa mahakama utatekelezwa Waandamanaji wanasema nini? "Hakuna shangwe miongoni mwa wanawake ambao ni wafuasi wa imani ya Kihindu, kwani wamefadhaika sana," ameandika Vineetha Menon katika jarida la Organiser. Menon anajenga hoja kuwa wanawake wasiingie hekaluni ni "kutimiza nia ya mungu Bhava" Baadhi ya wafuasi wanaume wanasema kwamba hawata rudi katika hekalu hilo kama maamuzi ya mahakama yatatekelezwa. "Tumekuwa tukija katika hekalu hili kwa miaka 30 sasa. Lakini tunaweza tusirudi hapa kwasababu wanawake kuingia hekaluni ni kuharibu mfumo wa imani yetu na kanuni takatifu, Murugan, mfuasi alimwambia mwandishi wa BBC India Imram Qureshi. Hata hivyo maamuzi hayo ya mahakama yamewagawanya mahakimu waliotoa hukumu hiyo. Mgahawa ambapo wateja hulipa kwa njia ya Bitcoin Kenya Indu Malhotra, hakimu pekee wa kike alipinga hukumu iliyotolewa. "Maswala ya ndani ya kidini kwa kawaida hayatakiwi kuingiliwa na mahakama, na hata dhana ya usawa haiwezi kuibuliwa katika mambo ya kidini," alisema kwa maoni yake. Wanawake wamekuwa wakidai kuingia katika hekalu hilo kwa miongo kadhaa sasa. Lakini mwaka 2016 taarifa ya utata kutoka kwa chifu wa hekalu hilo iliibua maandamano upya. Prayar Gopalakrishnan anasema kuwa ataruhusu wanawake kuingia endapo itagundulika mashine ambayo inaweza onyesha kama mwanamke yupo kwenye hedhi au la. Saudia yabanwa mbavu mauaji ya Khashoggi Waendesha mashtaka walitumia na kunakili kauli hiyo kama mfano na kusema kuwa miongozo ya hekalu hilo ina vunja usawa ulio hakikishwa kwa wahindi wote kupitia katiba ya nchi. Waliongeza kuwa ilikuwa ni upendeleo na kuwanyima wanawake haki yao ya kuabudu. Waandishi wa habari wanasema kuwa mapigano kati ya waandamanaji na polisi yanaweza kuongezeka katika siku zijazo kwani wanawake zaidi wanatarajiwa kujaribu kuingia hekaluni. Kwa mara ya kwanza, hekalu la Sabarimala lililopo katika mji wa Kerala kusini mwa India wiki hii limefungua milango yake kwa wanawake wa kila rika baada ya uamuzi wa kihistoria wa Mahakama kuu. text: Hatua hii inafuata kusainiwa kwa makubaliano mnamo mei mwaka jana baina ya serikali ya rais Yoweri Museveni na shirika la kitaifa la nyuklia China CNNC, kulisaidia taifa hilo la Afrika mashariki kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya amani. Katika ujumbe rasmi wa wizara ya nishati Uganda, makubalinao hayo na Urusi yalisainiwa hapo jana Jumatano huko Vienna kati ya waziri Irene Muloni na naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la kitaifa la nishati ya atomiki ROSATOM, Nikolai Spasskiy. Urusi itaisaidia Uganda kujenga miundo mbinu ya nyuklia kwa matumizi katika viwanda sekta ya afya na pia ukulima. "Spasskiy ameeleza uwajibikaji na utayari wa ROSATOM kuisaidia Uganda kuidhinisha matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia hususan katika ujenzi wa kinu cha nishati ya nyuklia," taarifa imeeleza. Afrika inasonga mbele katika matumizi ya nishati ya nyuklia Kwa mujibu wa ripoti ya IAEA ya mwaka 2015, zaidi ya nchi 30 duniani, theluthi moja zikitoka Afrika zinajiandaa kuanzisha mipango ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa usaidizi wa wataalamu kutoka shirika hilo. Kampuni ya Urusi Rosatom, imeshauriana na kuingia katika mikataba ya makubaliano na serikali kadhaa barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni katika kuidhinisha matumizi ya nishati ya nyuklia. Rwanda: Mwaka jana kampuni hiyo ilitangaza kwamba imesaini makubaliano (MOU) na serikali ya Rwanda kupitia wizara yake ya miundo mbinu kushirikiana katika matumizi ya amani ya nishati ya atomiki. Makubaliano hayo yaliidhinishwa kwa misingi ya ushirikiano wa pande mbili kujenga miundo mbinu ya nyuklia Rwanda na miradi mingine inayotokana na teknolojia ya nyuklia kama ilivyo kwa Uganda hivi sasa katika sekta zikiwemo za afya na hata ukulima. Kenya: Katika nchi jirani Kenya, serikali na kampuni hiyo ya Urusi zilisaini maelewano mnamo 2016 ya matumizi ya amani ilio kutoa fursa ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili ya matumizi ya nyuklia. Katika kuhimiza ushirikiano huo, mwaka jana Rosatom ilishiriki katika warsha ya mafunzo nchini Kenya - Kenya Bureau of Standards 3rd Radiation Protection Safety and Security Training programme. Katika warsha hiyo afisa mkuu mtendaji wa Rosatom, Dmitry Shornikov alieleza kwamba mataifa mengi ya Afrika yanaelekea katika matumizi ya nishati ya nyuklia kuweka usawa wa matumizi ya nishati na kukabiliana nchangamoto katika upatikanaji wa nishati. "Nishati ya nyuklia inaweza kutegemewa, ina gharama ya kumudu na haina madhara na nishati inayotokana na chanzo kisichokuwa na athari kwa mazingira." alisema Shornikov. Kenya imesema kwamba itaendelea na mpango wake wa kuhakikisha kwamba ina kiwanda cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia kufikia 2027. Mnamo 2017, Kaimu afisa mkuu mtendaji wa kukinga dhidi ya miali nururishi nchini Kenya Joseph Maina amesema Wakenya hawafai kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia. "Kumekuwa na ajali tatu pekee kubwa za nyuklia katika historia. Kisiwa cha Three Mile Marekani, 1978; Chenorbyl nchini Ukraine, 1986 na Fukushima nchini, Japan, 2011. Usalama umeimarishwa kutokana na mafunzo kutoka kwa mikasa hiyo," amesema. Kenya imekuwa na mpango wa kuzalisha kawi ya nyuklia kwa muda. Picha ya kiwanda cha kuzalisha kawi ya nyuklia cha Cattenom mashariki mwa Ufaransa Afrika kusini Afrika kusini ina vinu viwili vya nyuklia vinavyozalisha 5% ya nishati ya umeme nchini. Kwa mujibu wa shirika la nyuklia duniani kinu cha kwanza cha nyuklia katika taifa hilo kilianza kuhudumu mnamo 1984. Kinu cha Koeberg kilijengwa na Framatome (ambao sasa inafahamika kama Areva). Kinamilikiwa na kampuni ya kusambaza umeme nchini humo Eskom. Afrika kusini iliachana na mpango uliokumbwa na mzozo - uliosainiwa chini ya utawala wa rais wa zamani Jacob Zuma - kutumia zaidi ya $76bn kwa mradi wa nishati ya nyuklia na kampunihiyo ya Urusi Rosatom. Urusi imesaini mkataba wa kujenga viwanda vya nishati ya nyuklia nchini Nigeria huku taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika likiweka mikakati ya kumaliza matatizo yake ya umeme. Nigeria Taifa lililopo Afrika magharibi Nigeria limesaini makubaliano na Urusi kuidhinisha ujenzi wa vinu vinne vya nishati ya nyuklia na taasisi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia nchini. Tume ya nishati ya atomiki nchini Nigeria (NAEC) imesaini makubaliano na kampuni hiyo ya Urusi Rosatom, mnamo 2016 kando kando mwa mkutano wa kimataifa wa atomiki, ATOMEXPO 2016 mjini Moscow. Dhamira ya kuidhinishwa makubaliano hayo ni miongoni mwa mengine, kuimarisha mfumo duni wa nishati nchini na kuweka mikakati ya kumaliza matatizo yake ya umeme. Hatahivyo tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo, kumeshuhudiwa shutuma zinazogusia zaidi na kutahadharisha kuhusu hatari za nyuklia , miongoni mwa mengine. Vinu hivyo vinavyotarajiwa kujengwa na Rosatom, vinatarajiwa kugharimu takriban $80billion, huku cha kwanza kikitarajiwa kukamilika kufikia 2025. Uganda imesaini makubaliano na Urusi kuisaidia kujenga uwezo wake wa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya kutengeneza nishati, dawa na matumizi mengine ya amani. text: CAG Prof Mussa Assad ametiwa hatiani na Bunge kwa tuhuma za kudharau chombo hicho. Akiongea na waandishi wa habari baada ya ripoti zake kuwasilishwa Bungeni, Prof Assad amesema neno hilo ni la kawaida kwenye fani ya uhasibu. "Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia," Prof Assad amesema. Hata hivyo Prof Assad hakuwepo Bungeni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mkutano wake na wanahabari umefanyika kwenye ofisi yake mjini Dodoma. "Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma," amesema Prof Assad. Mapema leo ripoti za CAG ziliwasilishwa Bungeni baada ya vuta ni kuvute toka wiki iliyopita. Hatua hiyo imeondoa wingu jeusi lililokuwa linazagaa kwa wiki mbili juu ya utata wa kikatiba kuhusiana ushirikiano wa Bunge na CAG. Wiki iliyopita, Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Bunge ni dhaifu. Mgororo uliopo ulianza Disemba 2018 baada ya CAG kuiambia Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York kuwa Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali. Lakini kwa mujibu wa Katiba, Bunge linatakiwa kupokea na kufanyia kazi ripoti ya ukaguzi wa CAG. Tayari Prof Assad alishawasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2017/18 kwa Rais John Magufuli, na matakwa ya katiba yanataka ripoti hiyo iwe imewasilishwa Bungeni ndani ya siku saba baada ya Bunge kuanza. Bunge la bajeti lilianza mwanzoni mwa wiki iliyopita. Macho na masikio ya watu nchini Tanzania yalielekezwa Bungeni iwapo ripoti hiyo ya CAG kama itawasilishwa Bungeni. Hata Hivyo, Spika wa Bunge Job Ndugai wiki iliyopita alitoa ufafanuzi kuwa, azimio lilopitishwa na Bunge ni kutofanya Profesa Mussa Assad na si ofisi yake. "Hakuna wakati wowote ambao Bunge limekataa kufanya kazi na taasisi ambayo ni ofisi ya CAG. Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Profesa Assad basi. Tusiripoti tofauti tukauchonganisha umma na kuuchanganya," alisema Ndugai. Mgogoro ulianzia mwezi Disemba ambapo Prof Assad aliiambia UN redio: "…Kama tunatoa ripoti na inaonekana kuna ubadhilifu halafu hatua hazichukuliwi huo kwangu mimi ni udhaifu kwa Bunge. Bunge linatakiwa liisimamie (serikali) na kuhakikisha kuwa pahali penye matatizo basi hatua zinachukuliwa...Sie kazi yetu ni kutoa ripoti tu na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha lakini ni jambo tunaamini muda si mrefu huenda likarekebishika. Lakini tatizo kubwa tunahisi kwamba bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa." Spika Job Ndugai aliagiza CAG ahojiwe mwezi Januari akidai kuwa amelidharau Bunge Spika Ndugai alilieleza Bunge mwezi Januari kuwa maelezo ya Assad yalioonesha dharau kubwa dhidi ya mhimili huo na kumtaka aende mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hiyari yake, ama apelekwe kwa pingu. Hata hivyo, alipohojiwa na kamati hiyo, Assad aliendeleza msimamo wake. Kumekuwa na uungwaji mkono mkubwa kwa msimamo wa Prof Assad ambapo inaarifiwa kuwa watu zaidi ya 15,000 wamesaini waraka unaolitaka Bunge kufuta azimio lake. Chama cha upinzani cha ACT kupitia umoja wake wa vijana ulipanga kufanya maandamano Jumanne lakini wakaahirisha baada ya kukatazwa na polisi. Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania Prof Mussa Assad amesisitiza kuwa ataendelea kutumia neno dhaifu. text: Manila, Ufilipino : Mvulana mdogo anaonekana akiwa amesimama katika umati wa waumini katika ibada ya Eid al-Adha Sherehe hiyo ambayo pia hufahamika kama sherehe ya kutoa kafara, ni moja kati ya sherehe kubwa za kiislam. Ni kumbu kumbu ya kujitolea kwa utashi kwa Abraham kumtoa kafara mwanae kwa Mungu na wakati wa sherehe hii waislam hutoa kafara wanyama. Katika soko la wanyama la Ashmun cattle nchini Misri, wafanyabiashara wakiuza wanyama kwa ajili ya kafara kabla ya sherehe za Eid al Adha Msicha wa kiislam katika jimbo lililojitangazia uhuru wake la Kashmir alipakwa Henna tattoo kwa ajili ya sherehe Mjini Manila, mwanamke akitazama simu yake, kabla ya kuazna kwa ibada Kondoo , waliopangwa tayari kwa kutolewa kafara, wakitazamwa na muislam mjini Beijing, Uchina Wanawake wakihudhuria ibada katika jimbo la Bandeh Aceh, Indonesia Mjini Jakarta, watu wakisubiri kuanza kwa maombi katika mtaa mmoja nje ya msikiti . Waislam kote duniani wanasherehekea sherehe za Idd al-Adha, zinazofanyika wakati wa Hija inayofanyika kila mwaka mjini Mecca. text: Boris Johnson 'aangukia pua' Bungeni Uingereza Baada ya kupiga kura, wapinzania waliibuka na ushindi wa 328 dhidi ya 301 juu ya Bunge la Commons kuchukua udhibiti wa ajenda ya kujitoa EU, maarufu kama Brexit, hali inayomaanisha kuwa wabunge wanaweza kupeleka mswada wa kuchelewesha tarehe ya Uingereza kujitoa. Waziri Mkuu Borriss Johnson amekuwa akiimarisha mipango yake ya kujitoa EU Oktoba 31, iwe kwa mkataba ama la, lakini mipango hiyo inapingwa vikali na wapinzani na baadhi ya wananchama wa chama chake cha Conservatives. Baada ya kuangushwa Bungeni, Waziri Mkuu huyo amesema atatoa hoja ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu kabla ya wakati uliopangwa. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Jeremy Corbyn amesema muswada wa kupelekwa mbele tarehe ya Brexit unapaswa kupitishwa kabla ya nchi kwenda kwenye uchaguzi. Kwa ujumla, wabunge 21 wa Conservatives, ikiwemo mawaziri wa zamani wa serikali walijiunga na vyama vya upinzani kuiangusha serikali yao. Baada ya matokeo hayo, ofisi ya Waziri Mkuu, maarufu kama 10 Downing Street, imesema kuwa wabunge wote walioasi watafukuzwa kutoka kwenye chama. Ofisi hiyo iliamini kuwa vitisho vya kuwafuta uanachama - na kufanyika uchaguzi - kungezima uasi ndani ya chama. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Jeremy Corbyn amesema muswada wa kupelekwa mbele tarehe ya Brexit unapaswa kupitishwa kabla ya uchaguzi kufanyika. Waziri Mkuu amesema muswada unaotakiwa na wa wabunge utaipa EU mamlaka ya majadiliano na hatimaye itasababisha "kutapatapa zaidi, kuchelewa zaidi na mvurugano zaidi". Johnson akaliarifu Bunge kuwa hana namna nyengine zaidi ya kuendelea na mipango ya kuitisha uchaguzi mwezi Oktoba: "Raia wa nchi hii itabidi waamue." Hii inamaana ya kuwa, wabunge sasa wana mamlaka ya kuendesha shughuli za Bunge na kuwawezesha kuandaa muswada utakaoungwa mkono na pande zote wa kumlazimisha waziri mkuu apeleke mbele tarehe ya kujitoa mpaka Januari 31, ama wabunge wakubali mkataba mpya, au wapige kura ya kuunga mkono kujitoa bila mkataba Oktoba 19. BBC inafahamu kuwa serikali inataka kuitisha uchaguzi Oktoba 15, siku mbili kabla ya Mkutano Mkuu wa EU jijini Brussels, Ubelgiji. Hata hivyo, ili hoja ya uchaguzi ipite, Bw Johnson atahitaji kuungwa mkono na cha ma kikuu cha upinzani cha Labour, sababu inabidi ipatikane theluthi mbili ya uungwaji mkono kati ya wabunge 650. Tayari Bw Corbyn ambaye ndiye kiongozi wa Labour ameshatangaza kutaka muswada wa wabunge kwanza upitishwe ndio uchaguzi ufanyike ili "kuondoa uwezekano kabisa wa kujitoa bila ya mkataba". Johnson na washauri wake wanaamini kuwa wengi miongoni mwa raia wa Uingereza wanamuunga mkono katika sera zake za Brexit, na kwenda kwenye uchaguzi kutakifanya chama chake kishinde kura na kuwa na mamlaka ya kuwasilisha matakwa ya wananchi. Wapinzania pia wanaamini wataongeza wingi wao bungeni kwa kumpiku Waziri Mkuu na hatimaye kufanikisha Brexit ya mkataba. Kuahirisha Bunge wishoni mwa mwezi uliopita, Waziri Mkuu Boris Johnson aliomba ridhaa ya Malkia na kukubaliwa kusitishwa bunge kwa muda. Hatua hiyo inatafsiriwa na wapinzani wake na wachambuzi huru kama mpango wa kulizuia bunge kuweka sauti kinzani juu ya mustakabali wa Brexit. Waandamanaji katikati mwa London wakipinga kusitishwa kwa Bunge Maandamano yameanyika kwenye pembe mabalimbali za Uingereza kupinga hatua hiyo, japo serikali inadai hatua hiyo si unyakuzi wa demokrasia. Kilichotokea Bungeni kinadhihirisha wazi nguvu ya wabunge katika kupasisha ama kutibua mipango ya serikali juu suala hilo nyeti kwenye siasa za Uingereza na Ulaya. Wabunge walioasi kutoka chama tawala cha Conservatives pamoja na wale wa vyama vya upinzani wameishinda serikali ya Uingereza katika awamu ya kwanza ya kuzuia Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (EU) bila ya mkataba. text: Kanye West atoweka katika mitandao ya kijamii Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema. Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo. Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51. Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mashabiki walipojaribu kuwasiliana na msanii huyo Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe. Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake. Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mtandaoo wa Twitter wa mkewe Kim Kardashian West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump. Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba. Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi. text: Hii ni baada ya wapiga mbizi wa jeshi la Kenya kwa ushirikiano na wapiga mbizi kutoka Afrika kusini kufanikiwa kufikia gari hilo. Miili ya mama Mariam Kighenda, 35, na mwanawe wa kike Amanda Mutheu, 4, pia imeopolewa kutoka ndani ya maji. Aliyekuwa mume wa Mariam, bwana John Wambua aliweza kutambua miili ya marehemu kabla haijaondolewa katika eneo la tukio. Vilevile ibada maalum ya kuwaombea marehemu , iliendeshwa na mchungaji mara tu baada ya miili hiyo kutolewa kwenye maji. Jitihada za kuopoa miili ya mama na mtoto wake wa kike waliokuwemo ndani ya gari hilo lililozama zilianza mnamo Septemba 29. Wakenya wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yao. Wanamaji wa Kenya walipata shinikizo kubwa la kumaliza zoezi hilo la uopoaji kabla ya Oktoba 10 - tarehe inayoadhimishwa kama sikukuu ya Mashujaa iliyopangiwa kufanyika kitaifa katika mji huo wa Pwani ya Kenya. Wakaazi walikuwa wametishia kuisusia sherehe hiyo ambayo rais Uhuru Kenyatta alitarajiwa kuhudhuria, iwapo miili hiyo haitakuwa imeopolewa. Tukio lilivyojiri: Sept 29: Gari dogo aina ya soloon lililoarifiwa kuwa na watu wawili ndani lazama katika kivuko cha Likoni Sept 30: Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ferry Bakari Gowa asema kwamba wataalam wamebaini kuwa gari hilo lilizama kima cha mita 60, hivyobasi kufanya kuwa vigumu kuliokoa. Sept 30: Shughuli za uokoaji ambazo zimejumuisha maafisa kutoka vitengo vya Kenya Navy, Kenya Ferry, na wapiga mbizi wa kibinafsi zaanza. Okt 1: Kivuko cha feri chafungwa kwa saa tatu ili kuruhusu utafutaji ulioendelea wa gari na miili ya waliokuwemo ndani. Okt 2: Familia ya waathiriwa yalalamikia kujikokota kwa operesheni ya uopoaji miili ya waathiriwa. Okt 2: Kikosi cha pamoja katika operesheni ya uopoaji kinasema kimegunuda sehemu lilipo gari. Hii ni baada ya kuyakagua maeneo kadhaa yalioshukiwa kuwepo gari hilo. Okt 3: Maafisa wanaendelea kushughulika na ukaguzi wa maeneo yalioshukiwa kuwepo gari hilo. Okt 7: Wapigambizi wa Afrika Kusini wajiunga katika operesheni hiyo ya uopoaji. Okt 8: Wapigambizi waanza kazi ya kutafuta miili na gari. Okt 9: Gari lililokuwa limezama katika kivuko cha Likoni limeonekana. Msemaji wa serikali Cyrus Oguna asema haiwezi kuthibitishwa iwapo ndilo gari lililozama Jumapili Septemba 29. Gari lililozama baharini siku 13 zilizopita katika kivuko cha Likoni feri, mjini Mombasa pwani ya Kenya hatimae limetolewa. text: Gwaride la kijeshi lililofanywa na Korea Kaskazini hivi karibuni Kombora hilo lililorushwa lilienda anagani urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri kilomita 700 kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan. Korea Kaskazini ilisema siku ya Jumatatu ni jaribio la uwezo wa kombora jipya. Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa haliweza kuthibitisha madai hayo ya Korea Kaskazini. Lakini limesema kuwa kombora hilo lilionekana kuweza kuruka angani, hatua ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa makombora ya masafa marefu kulingana na kituo cha habari cha Yonhap. Majaribio ya mara kwa mara ya makobora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani. Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne. Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema Jumatatu kwamba jaribio la kombora jipya la masafa marefu la Hwasong 12 lilifanyika kama ilivyopangwa. Limesema kuwa jaribio hilo lililenga kuonyesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa cha Nyuklia. Korea Kaskazini imedai kwamba kombora la masafara marefu ililolifanyia majaribio siku ya Jumapili ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia . text: Leo usiku timu hizo zitashuka dimbani katika mechi ya robo fainali ya pili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) jijini Cairo. Mechi ya kwanza itazikutanisha Senegal dhidi ya Benin. Japo Benin waliwatoa Morocco kwenye hatua ya mtoano kwa mikwaju ya penati, wachambuzi wengi wanaamini itakuwa ni kazi ngumu kwao kuwatoa Senegali. Hivyo ni mawazo ya wengi kuwa Senegali (ambayo imezifunga timu tatu za Afrika Mashariki) itasonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali. Upinzani mkali unatarajiwa kuwa baina ya Nigeria na Afrika Kusini. Mashabiki wa timu hizo tayari wameshabadili majina ya utani ya timu pinzani. Afrika Kusini ni maarufu kwa jina la Bafana Bafana, neno bafana kwa lugha ya Kizulu linamaanisha wavulana kwa Kiswahili, lakini mashabiki wa Nigeria wameligeuza na kuwa 'Banana Banana', banana kwa maana ya ndizi. Nigeria wao ni maarufu kwa jina la Super Eagles, lenye maana ya Tai Wakubwa, lakini mashabiki wa Bafana sasa wanawaita wapinzani wao 'Super Egos'. Ego ni neno la Kingereza lenye maana ya ubinafsi, hivyo 'Super Egos' inaweza kutafsiriwa 'wabinafsi wakubwa'. Timu zote hizo ni mabingwa wa zamani wa kombe hilo, japo Nigeria amekuwa na historia nzuri na kiwango cha juu zaidi ya Afrika Kusini. Hata hivyo timu hizo mbili zilipangwa kwenye kundi moja katika mbio za kufuzu kwenye mashindano hayo. Mechi yao ya kwanza iliisha kwa Nigeria kukubali kichapo cha 2-0 na mechi ya marudiano ikamalizika kwa sare ya 1-1. Hata hivyo, mshambuliaji kinara wa Nigeria Odion Ighalo amewaonya Afrika Kusini kuwa wasitegemee kuwa mambo yatakuwa kama kwenye mbio za kufuzu: "Tupo tayari, na tutalidhihirisha hilo kesho (leo). Mechi hii ni tofauti kabisa na zile mechi za hatua ya kufuzu. Tunajua itakuwa ni mechi ngumu, lakini tupo tayari kuwapa furaha Wanaigeria." Nigeria imetinga robo fainali baada ya kuwafunga waliokuwa mabingwa watetezi Cameroon 3-2. Afrika Kusini yenyewe iliwashangaza wengi baada ya kuwafunga wenyeji Misri goli 1-0 na kusababisha kocha wa Misri kutimuliwa na raisi wa chama cha mpira cha nchi hiyo kujiuzulu. Je nani kati yao kuibuka mbabe hii leo? Bofya hapa na ubashiri matokeo ya mchezo huo. Tayari tambo za mashabiki wa Afrika Kusini na Nigeria zimeshaanza mitandaoni, huku kila upande ukivutia upande wake na kupachika majina upande pinzani. text: Kwa upande wa mabenki, Benki Kuu imeyaagiza kufanya mjadala na wateja wao juu ya urejeshwaji wa mikopo na kutafuta namna nafuu ya urejeshaji wa mikopo hiyo "Benki Kuu itatoa unafuu kwa mabenki na taasisi za fedha zitakazotoa unafuu katika urejeshwaji wa mikopo hiyo kwa kuzingatia uwazi na bila upendeleo," imeongeza taarifa kutoka Benki ya Dunia Kwa upande wa makampuni yanayotoa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao, Benki Kuu imeagiza kuongezwa kwa kiwango cha miamala kwa siku kwa mteja kutoka TSh 3,000,000 (Milioni 3, sawa na takribani $1300) hadi Tsh 5,000,000 (Milioni 5, sawa na takribani $2,160) Maelekezo yametolewa pia juu ya kuongezwa kwa kiwango cha akiba kwa siku kwa mteja kutoka Tsh 5,000,000 (Milioni 5, sawa na takribani $2,160) Hadi Tsh. 10,000,000 (takribani $10,000,000) Benki Kuu imesema sababu ya kuchukuliwa kwa hatua hii ni kumsaidia mteja na mwananchi kwa ujumla kupunguza ulazima wa kwenda katika mabenki kupata huduma za kifedha Sera hii ya kifedha inakuja takribani miezi miwili tangu mgonjwa wa kwanza wa homa kali ya mapafu (COVID-19) kugundulika nchini. Ikilinganishwa na nchi zingine kama vile Kenya, Benki Kuu nchini humo ilitangaza hatua kama hizi katikati ya mwezi Machi, siku chache tu baada ya maambukizi kugundulika nchini humo. Taarifa hiyo kutoka Benki Kuu imesisitiza pia kwamba Tanzania bado ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kuwezesha uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi. Jinsi mataifa mengine yalivyochukua hatua za kuwapatia ahueni raia wake Ghana Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alitangaza kuwa serikali yake italipia gharama ya maji kwa kipindi cha miezi mitatu ikiwa ni jitihada za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa corona. Wafanyakazi wote wa afya hawata katwa kodi katika kipindi cha miezi hiyo mitatu. Kuosha mikono kwa sabuni na maji, Maji yanatajwa kuwa namna nzuri ya kukabiliana na maambukizi. Matenki ya maji pia yatakuepo kutoa huduma ya maji kwa wananchi wasio na uwezo. Kwa sasa wafanyakazi wa afya wanao wahudumidia wagonjwa wa Covid-19 wataongezewa mshahara kwa asilimia hamsini. DR Congo Shirika la maji na shirika la umeme nchini DR Congo yamethibitisha kufuata agizo la serikali kwa kutoa huduma ya maji ya bila malipo pamoja na umeme kwa kipindi cha miezi miwili. Mkurugenzi wa shirika la umeme bwana Jean-Bosco Kayombo, alisema kuwa watakaofaidika na huduma hiyo ya umeme na maji ya bila malipo, ni nyumba za watu na wafanyabiashara wadogo na wenye viwanda vya wastani ili kupunguza uwezekano wa maambukizi kuenea zaidi. Serikali ya Kongo imesema kuwa imeamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu watu hawaendi kazini kwa sasa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona. Kenya Gavana wa benki kuu Kenya, bwana Patrick Njoroge anasema kuwa wataweka mikakati ya kuimarisha uchumi katika kipindi hiki cha athari za kiuchumi ambazo zinawakumba wateja wao kutokana na maambukizi ya virusi vya corona. Katika harakati za kuokoa uchumi binafsi, bwana Njoroge ametaka mikopo ya ujenzi kutolewa kwa wastani. Vilevile rais pamoja na makamu wake, wametaka mishahara yao ikatwe kwa asilimia ishirini. Uganda na Rwanda wanatoa huduma ya chakula kwa raia wenye uwezo wa chini. Benki Kuu ya Tanzania imetoa maelekezo kwa mabenki na makampuni ya simu juu ya namna ya kutoa unafuu wa masuala ya kifedha kwa wateja wao text: Wanajeshi wa Urusi wamepelekwa Syria kuunga mkono serikali tangu 2015 Jeti hizo zinaunga mkono operesheni za vikosi vinavyounga mkono serikali ya Syria ili kudhibiti barabara kati ya Homs na Deir al-Zour, kwa mujibu ya waangalizi. Wanaamgambo wa IS wamefanya uvamizi na mashambulizi hivi karibuni , tukio la karibuni, siku ya Jumatani, wanajeshi tisa na wanamgambo waliuawa. Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wenye makazi yao nchini Uingereza, ambao wanafuatilia vita nchini Syria kwa kutumia vyanzo vya kimtandao , wamesema watu wengine watatu waliuawa siku ya Jumanne baada ya bomu lililotegwa ardhini na wanamgambo wa IS kulipuka katika jangwa Kusini mashariki mwa jimbo la Deir al-Zour Mashambulizi ya anga ya Urusi siku ya Jumanne yaliua wanamgambo takribani 10 mjini Deir al-Zour na katika jimbo la Hama, wakati kukiwa hakuna taarifa za madhara kutokana na mashambulizi ya Jumatano katika eneo la al-Shawla. Televisheni ya Syria, Televisheni ya upinzani, pia imesema kuwa ndege za Urusi zilikuwa zikishambulia maeneo ya wanamgambo wa IS kwenye jangwa mkoa wa Badiya. Hatahivyo, vyombo vya habari vya serikali havisema chochote kuhusu operesheni iliyoripotiwa. IS ilidhibiti eneo la kilomita za mraba 88,000 za mamlaka ya Syria umbali wa kutoka Magharibi mwa Syria kwenda Mashariki mwa Iraq na kuweka utawala wake wa kikatili kwa watu karibu milioni nane. Licha ya kushindwa kwa kundi hilo huko Iraq mnamo 2017 na Syria mnamo 2019, wataalam wa UN wanakadiria kuwa zaidi ya wanamgambo 10,000 wanaendelea kufanya kazi katika eneo hilo, wakifanya uasi wa muda mrefu. Wamejiunga makundi madogo madogo wakiwa wamejificha jangwani na vijijini, na yana uwezo wa kuvuka mipaka isiyo na ulinzi. Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na ugaidi, Vladimir Voronkov, alionya wiki iliyopita "kuwa mabaki haya makundi ni kubwa ulimwenguni''. Katika tukio tofauti siku ya Jumatano, polisi wa Uturuki walisema wamewakamata wanachama wawili waandamizi wa IS huko Ankara na kumwachilia msichana wa miaka saba kutoka jamii ya wachache ya Yazidi ya Iraq ambaye alikuwa anashikiliwa mateka. Mmoja wa washukiwa alitambuliwa kama afisa wa zamani wa jeshi la Iraq Ndege za kivita za Urusi zimefanya mashambulizi kadhaa ya anga katika maeno ya wanamgambo wa IS kwenye jangwa la Syria, wanaharakati wamesema. text: Ikiwa na soko lenye ukubwa wa takribani asilimia kumi na sita duniani, kampuni hiyo inatajwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa kubwa zaidi ya utengenezaji simu. Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hofu kutoka baadhi ya wadadisi kwamba huenda kampuni hiyo inatumiwa na Uchina kufanyia serikali za nje na pia wananchi wake ujasusi. Lakini barani Afrika, kampuni hiyo pamoja na ile ya ZTE zimehusika sana katika ujenzi wa miundo mbinu nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, miongoni mwa mataifa mengine. Nchini Nigeria kwa mfano, Huawei ilishinda kandarasi ya dola milioni themanini kutengeneza mtandao wa dijitali wa simu wa GSM mnamo mwaka 2004. Kwa kutathmini ukubwa wa uwepo wa kampuni hiyo Afrika wadadisi wanasema mzozo unaoshuhudiwa sasa inamaanisha kwamba biashara nyingi zitaathirika kutokana na changamoto ambazo Huawei inakumbana nazo. Barrack Otieno ambaye ni mtaalamu wa maswala ya sera za mtandaoni anaeleza kwamba, 'Waafrika wengi wanapokea mikopo midogo kupitia programu tumishi za simu ambazo zinatumia mfumo huo wa Android. Huenda sasa ikachangia watu wengi wakakosa mikopo na hivyo kuumia sana katika sekta za kibiashara'. Huawei pia imezindua zaidi ya mitandao hamsini ya 3G, na kutengeneza mitandao ya huduma za zaidi ya serikali thelathini. Aidha kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika teknolojia zinazokua za 4G na 5G. Je kuna namna ya kuiepuka athari? Wananchi wengi hununua simu za Huawei kwasababau ni za bei nafuu katika masoko ya simu Afrika. Wanauchumi wanaonya ikiwa simu hizo sasa zitaondolewa katika soko kutokana na athari ya yanayoshuhudiwa, ina maana itaathiri pia uchumi wa kieneo, na zaidi 'nchi ambazo hazina nguvu kiuchumi'. Serikali nyingi Afrika zinatumia teknolojia na miundo mbinu ya Huawei. Je zinapaswa kuwa na wasiwasi? Barrack Otieno anasema huenda biashara nyingi zikasambaratika kwasababu biashara nyingi zimeundwa kwa msingi wa biashara ya Huawei. 'Kusema kwamba biashara hizo zibadilishwe kwa muda mfupi kama inavyopendekeza Marekani itakuwa sio jambo la rahisi' anaeleza. Marufuku iliyoidhinishwa kwa Huawei kutotumia mfumo wa Android unagubika uzinduzi hii leo kwa simu mpya za kampuni hiyo ya China. Huawei imealikwa waandishi wa habari wa kimataifa kushuhudia uzinduzi wa simu mpya za Honor 20 Series. BBC inafahamu kwamba simu hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia kikamilifu Android. Mwaka jana, Huawei iliunda simu milioni mia mbili na nane, huku nusu ya simu hizo zikiuzwa nje ya Uchina. Julai mwaka huo huo, kampuni hiyo iliipiku mshindani wake Apple na kuchukua nafasi ya pili katika utengenezaji simu janja duniani, huku Samsung ikisalia kileleni. Lakini mpaka pale tofuai za kibiashara na Marekani zitakapotatuliwa, huenda simu zitakazo zinduliwa katika miaka ijayo zikawa na manufaa kidogo - iwapo hazitotumia mfumo huo wa Android. Na pia haijulikani wazi iwapo marufuku ya Google kwa Android ni ya muda mrefu. Bara la Afrika kuna takriban watu milioni 400 wanaotumia mtandao na kati ya hao kuna 60% wanatumia mfumo wa Android ambao ndio unatumikwa kwa simu kama za Huawei. text: Matamshi yake yanajiri baada ya rais Trump kuimuita balozi wa Uingereza nchini Marekani Kim Darroch 'mjinga' kufiatia mgogoro kuhusu barua pepe zilizofichuliwa. Aliendelea kumkosoa waziri mkuu Theresa May kuhusu Brexit , akisema kwamba alipuuzilia mbali ushauri wake na kwamba alifanya maamuzi yake ya 'kipumbavu'. Siku ya Jumapili barua pepe zilizofichuliwa zilionyesha balozi huyo aliuita utawala wa Trump usiojitambua. Wakati huohuo mkutano kati ya waziri wa maswala ya biashara za kimataifa nchini Uingereza Liam Fox na waziri wa biashara wa Marekani na Wilbur Ross ulifutiliwa mbali siku ya Jumanne. Bwana Hunt alijibu matamshi ya bwana Trump katika mtandao wa twitter: Marafiki huzungumza bila kufichana hivyobasi nitazungumza: Matamshi haya yanamkosea heshima na ni makosa kwa waziri mkuu wa taifa langu. Wakati wa mjadala uliopeperushwa hewani moja kwa moja mgombea akiye kifua mbele kumrithi waziri mkuu Theresa May Boris Johnson aliulizwa iwapo angmwacha balozi huyo kuendelea , lakini alisema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kutekeleza lolote. Bwana Johnson alisema ana uhusiano mzuri na Ikulu ya Whitehouse na kwamba ilikua muhimu kuwa na uhusiano mzuri na Marekani. Muhariri wa maswala ya kisiasa wa BBC Laura Kuenssberg alisema kuwa mgogoro huo ni ukumbusho wa ulivyo uhusiano wa Marekani na Uingereza alioutaja kuwa na hila chungu nzima mbali na changamoto inayomkuba kiongozi wa Uingereza anayekabiliana na rais ambaye hupenda kuzua migogoro. Lakini alikuwa Jeremy Hunt ambaye alionekana kuchukua tahadhari na kuzungumzia wazi na moja kwa moja na Donald Trump kuhusu swala hilo huku Boris Johnson akisema kwamba hajutii kuwa mtu wa karibu wa Ikulu ya Whitehouse. Kufuatia matamshi ya rais Trump siku ya Jumatatu kwamba Marekani haitashirikiana tena na Sir Kim , wizara ya maswala ya kigeni nchini humo imesema kuwa itaendelea kushirikiana naya hadi pale itakapopata uongozi kutoka kwa Ikulu ya Whitehgouse ama rais Trump mwenyewe. ''Tuna uhusiano maalum sana na wa kimkakati na Uingereza ambao umekuwepo kwa muda mrefu- ni kitu kikubwa zaidi ya mtu yeyote binafsi'' , wizara hiyo iliongezea. Awali serikali ya Uingereza ilisema kuwa inamuunga mkono balozi wake. Msemaji wa Theresa May alisema kuwa bwana Kim ni mchapa kazi , na afisa wa serikali anayeheshimiwa na kuthibitisha kuwa hakuna mpango kwa bi May na bwana Trump kuwasiliana kujadiliana kuhusu uhusiano wa mataifa hayo kufuatia ufichuzi huo wa barua pepe. Serikali ya Uingereza pia imethibitisha kuwa Sir Kim hatohudhuria mkutano kati ya Ivanka Trump na waziri wa bisharaza za kimataifa Liam Fox mjini Washington. Msemaji huyo alisema kuwa: hatohudhuria mkutano huo lakini anamuunga mkono Liam Fox kuhusu mambo mengine ya ziara yake. Mapema siku ya Jumanne Bwana Trump alituma ujumbe wa twitter akisema: Balozi wa Uingereza ambaye ameletwa hapa Marekani sio mtu tunayemshabikia , ni mtu 'mjinga sana'. Azungumze na taifa lake na waziri mkuu Thereza May kuhusu mazungumzo yao ya Brexit yaliofeli na sio kukasirishwa na ukosoaji wangu kuhusu vile mazungumzo hayo yalivyosimamiwa vibaya. Nilimwambia @ Theresa _ May jinsi ya kufanya makubaliano hayo , lakini alifanya uamuzi wake wa 'kipumbavu' na alishindwa . Janga. Simjui balozi huyo lakini nimeambiwa kwamba ni mpumbavu . Mwambieni Marekani ina uchumi bora zaidi na jeshi bora duniani kwa umbali na tunazidi kuimarika kwa ukubwa na uthabiti...Ahsante Bwana rais. Serikali ya Uingereza awali ilitaja ufichuzi huo kama bahati ambaya na imeanza uchunguzi ramsi . Ilisema kuwa Uingereza na Marekani bado zina uhusiano maalum na wa kudumu. Barua pepe za siri kutoka kwa balozi huyo wa Uingereza zilikuwa na msururu wa ukosoaji wa utawala wa rais Trump na kusema kuwa Ikulu ya Whitehouse ilikuwa haina utendakazi wa haja na kwamba kulikuwa na mgawanyiko mkubwa chini ya uongozi wake. Sir Kim ambaye alikuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani Januari 2016 mwaka mmoja kabla ya rais Trump kushika madaraka pia alihoji iwapo Ikulu ya Whitehouse itawahi kupata mtenda kazi , lakini pia ilionya kuwa rais huyo wa Marekani hafai kupuuziliwa mbali. Barua hizo za 2017 zilisema kuwa uvumi kuhusu mapingano na ghasia katika Ikulu ya Whitehouse yalikua ya ukweli na kwamba sera kama swala nyeti la Iran lilizua tofauti zisizo za kawaida. Donald Trump amemkosea heshima waziri mkuu wa Uingereza, waziri wa maswala ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt amesema. text: Meya Pete Buttigieg (katikati) akiwaf ungisha ndoa Mary na Gabe katika ofisi yake Pete Buttigieg, ambaye ni meya wa jimbo la South Bend, Indiana, alisema kuwa wawili hao Mary and Gabe, walimkuta ndio amewasili ofisini majira ya saa mbili unusu na wakamuomba awafungishe ndoa kabla mtoto wao hajazaliwa. Wafanyakazi wa ofisi ya Meya walikuwa ndio mashahidi na walitumia vipande vya vitambaa( riboni) kama pete kwa kuwa pete zao zilikuwa bado hazijatengenezwa Baada ya kufunga ndoa yao Mary aliweza kufika hospitalini saa tatu asubuhi kama alivyoagizwa na daktari na kujifungua salama mtoto mchanga wa kike. Mtoto Jade Katherine Jones amekuwa ''mkazi mpya kabisa'' wa South Bend ",Aliandiika Meya Buttigieg kwenye ukurasa wake wa Facebook. "Ni nyakati kama hizi ambazo nitazikosa muda wangu wa umeya utakapokwisha ," aliandika alipotuma picha ya mtoto mchanga wa kike. "Karibu Jade,katika dunia hii isiyosadikia na nzuri !" Alisema meya Buttigieg "Hongera kwa wazazi na wanandoa wapya , na karibu Jade, katika dunia hii isiyoyadikika na nzuri!" Mwezi Januari , Meya Buttigieg, mwenye umri wa miaka 37, alitangaza nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 , alipojiunga miongozi mwa wagombea wa uteuzi wa chama cha Democratic - ambao tayari idadi yao imekuwa kubwa. Ikiwa atateuliwa , Bwana Buttigieg atakuwa ni mtu wa kwanza aliyejitangaza wazi kuwa mpenzi wa jinsia moja kuwahi kuchaguliwa katika chama kikuu cha kisiasa Meya wa Marekani na mgombea wa kiti cha urais ajaye aliwafungisha ndoa wapenzi waliokuja dakika za mwisho tu kabla ya kuelekea hospitali kupata mtoto kwa njia ya upasuaji text: Panya hao hupewa mafunzo na wana uwezo wa kunusa kamasi za binaadamu na kutambua kwa haraka ugonjwa wa TB. Wana uwezo wa kutambua sampuli mia moja kwa muda usiozidi dakika 20. Tofuati na binaadamu - wataalamu wa maabara wanaotumia siku nne kuchunguza idadi hiyo ya sampuli. Tanzania sasa itawatumia panya hao katika kliniki zipatazo 60 kote nchini. Panya buku kutumika kupima TB Tanzania Mfumo huu wa kutumia panya kutambua TB ulianzishwa na shirika la misaada Ubelgiji, kama njia nyepesi na na isiyotumia fedha nyingi kutambua TB kinyume na mfumo uliozoeleka. Katika baadhi ya mataifa kusini mwa jangwa la Sahara, zaidi ya 50% ya wagonjwa wa TB hawatambuliwi au hawatibiwi na kote duniani, idadi hii ni ya juu kiasi cha milioni 4.1. Kutotambuliwa kwa wagonjwa hawa wanaojumuisha watu wasiojiweza, na wasioweza kupata matibabu - wazee kwa vijana, watu wanaoishi katika umaskini, wachimbaji migodi na hata wahamiaji. Iwapo mgonjwa hatopata matibabu, mgonjwa TB anaweza kusambaza ugonjwa huo kwa hadi watu 15 kwa mwaka. Tanzania ni mojawapo wa mataifa 30 ambako kunashuhudiwa maambukizi makubwa ya kifua kikuu, ambao ni ugonjwa mmojawapo hatari unaosambaa kwa kasi na kuua watu, lakini unaoweza kutibiwana kuzuiwa. Tanzania inaongeza maradufu idadi ya panya buku wanaotumika kuutambua ugonjwa wa kifua kikuua. text: Akizungumza na runinga ya Wasafi, afisa mkuu mtendaji wa WCB Sallam SK alias Mendez alifichua kwamba msanii huyo ameandika rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa. Sallam amesema kwamba kwa sasa moyo wa msanii huyo haupo tena na WCB na ameitisha mkutano na usimamizi wa WCB katika harakati yake ya kukubaliana na hatua hiyo. "Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi," alisema Sallam. Hatahivyo amesema kwamba muimbaji huyo wa wimbo 'My Boo' bado yupo katika mkataba wa WCB na kusisitiza kwamba ingekuwa heri iwapo Harmonise angetoka bila kuzua zahama. "Sisi kama taasisi ya WCB tuko radhi kwa kile ambacho ataamua, hatuwezi kupinga chochote. Akiamua kufuata maelezo hayo ana baraka asilimia 100 za Wasafi na akitaka kushirikiana na Wasafi wakati wowote tuko wazi. Wajua unapoondoka kwa mazingira mazuri inasaidia uhusiano usalie pale pale," alizungumza katika . Kulingana na Sallam, tangazo hilo kwamba Harmonize amejiondoa rasmi WCB litatangzwa rasmi baada ya mchakato wote huo kufuatwa na kukamilishwa "Siku ambayo atatoka kimkataba tutaangazia umma. Kwa sasa hivi ameandika barua. Nafasi yake imetoka WCB. Kufanya kazi ndani ya WCB, ndani ya moyo wake, haiko radhi tena," aliongezea Sallam. Sallam amesema katika tamasha la wasafi lililofanyika mjini Mwanza, kwamba Harmonise alitumia usafiri wa kibinafsi kufanya baadhi ya mambo yaliotoa tafsiri kwamba amejitenga. ''Alitufanyia mambo mengi ambayo hatukutarajia ikiwemo kumsimamisha msanii ambaye hana kibali chetu. Sisi hatupendi kuleta matabaka katika kundi letu lakini kama ilivyokuwa Harmonise aliingia kivyake, sio kwamba Diamond hawezi kufanya hivyo au Rayvany ni ile heshima kwamba WCB ina umoja na kwamba tunafuata sheria zilizopo''. ''Hatahivyo tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali'', amesema Sallam akinukuliwa na gazeti la Mwananchi Tanzania. Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema kwamba: Hili jambo sio sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuandamana na wasanii wenzake ambao wapo katika tamasha ni kwenda kinyume. Meneja huyo amewaomba radhi wasanii wote walioshiriki tamasha la Mwanza kutokana na Harmonise kufanya jambo hilo na kwamba uongozi wa Wasafi haukuwa na taarifa. Msanii Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize hatimaye ameandika rasmi kwa kundi la Wasafi Classic Baby WCB akitaka kandarasi yake kuvunjwa. text: Marco ameifanyia kazi klabu hiyo kwa miaka mingi, awali akiwa katika chuo cha mafunzo ya soka, na sasa akiwa mkufunzi wa Genoa. Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa akijizuia kutobubujikwa na machozi. Lakini mwishowe alilazimika ,na alikaa katika kiti chake na kutokwa na machozi ya raha. Pellegri amaye ndio msimamizi wa timu hiyo alikuwa amemuona mwanawe Pietro mwenye umri wa miaka 16 akifunga bao lake la kwanza na la pili kwa timu hiyo katika mechi ya ligi ya Serie A dhidi ya Lazio baada ya kuchukua mahala pake Ricardo Centurion katika kipindi cha kwanza. Ilikuwa ndoto iliofanikiwa kwa babake mtoto huyo, Marco ambaye alikuwa akisema kwamba iwapo nitamuona Pietro akiichezea Genoa katika uwanja wa Luigi Ferraris atafurahi. Atajihisi kana kwamba maisha yake yamekamilika. Picha za Marcos akionekana akibubujikwa na machozi ziligonga vichwa vya habari duniani na zikamfanya Pietro kushindwa kujieleza alipoonyeshwa baada ya mechi ambapo Genoa ililazwa 3-2. Na baadaye ilikuwa Pietro, saa alizokuwa ndani ya gari huku babake akimpeleka katika mechi moja hadi nyingine. Mshambuliaji huyo mchanga pia naye alijawa na hisia. Mwisho mazungumzo yalikuwa ya Petro kufunga mbele ya eneo la Gradinata Nord , eneo ambalo mashabiki wa Genoa hukongamana. Wapellegri wanatoka Genoa. Wanaishi Pegli, mji wa baharini uliopo magharibi ambapo Genoa ina uwanja wake wa soka. Marco ameifanyia kazi klabu hiyo kwa miaka mingi, awali akiwa katika chuo cha mafunzo ya soka, na sasa akiwa mkufunzi wa Genoa. Mkewe Marzia anatoka katika familia ya mashabiki wa Sampdoria. Lakini Pietro amekuwa akiwaona wale wa Genoa pekee. Wakati klabu hiyo iliposhushwa daraja hadi katika daraja la tatu kufuatia kashfa ya udanganyifu wa mechi miaka 12 iliopita ,Marco Rossi , nahodha wa klabu hiyo alikuwa akicheza playstation na mwana wa Pellegro. Rossi aliichezea Genoa mara 286 na hadi leo amekuwa mfano mkubwa katika klabu hiyo. Pietro alipenda kuishabikia klabu moja pekee, Genoa. Kitu kinachoweka historia ni kwamba licha ya kuwa kinda, klabu maarufu zimekuwa zikitaka kumsajili kwa miaka kadhaa. Beppe Marotta, mkurugenzi wa Juventus , anadai kwamba alijaribu kumsajili Pietro miaka miwili iliopita wakati ambapo hakuna aliyemjua. Msimu huu Inter Milan ilikubali kulipa Yuro milioni 60 kumsajili Pietro pamoja na kinda mwengine wa Genoa Eddie Salcedo, na ni sheria za Fifa za fair Play zilizozuia uhamisho huo. Na kufikia siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, AC Milan ilitaka kumsajili Pietro baada ya kumuuza M'baye Niang. ''Lakini mpango huo haukufaulu'', alisema afisa mkuu mtendaji Marco Fassone. Bado watajaribu tena. Wengine wanasema ni mapema mno kubaini talanta ya kinda Pietro na kwamba dunia lazima iwe makini. Marco Pellegri alipitisha mkono wake katika nywele zake na kuchukua simu yake iliokuwa katika mfuko wa ndani wa koti lake. text: Sarri amewaongoza Juventus Kutwaa taji la tisa mfululizo la ubingwa wa Ligi ya Italia Seria A, lakini vibibi vizee hao wakaondoshwa katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya kumi na Sita bora na Wafaransa Wa Lyon. Juventus Walishinda kwa goli 2-1 katika mchezo uliochezwa siku ya Ijumaa lakini Lyon walisonga mbele kwa faida ya Goli la ugenini. Sarri Mwenye miaka 61 alipewa jukumu la kuinoa Juventus kwa Miaka mitatu msimu uliopita akitokea klabu ya Chelsea ya nchini England. Sarri alichukua nafasi ya Massimilliano Allegri mwezi June 2019 Kocha wa Kikosi cha vijana na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Andrea Pirlo, anatajwa kuwa mmoja ya watu wanaopewa nafasi ya kuwa Kocha mpya wa Timu hiyo makocha wengine wanaopigiwa chapuo la kuwanoa vibibi hao wa Turin ni Zidane wa Real Madrid na Meneja wa Zaman wa Spurs Mauricio Pochettino. Miamba ya Soka ya Jiji la Turin Klabu ya Juventus imemfuta kazi meneja wake Maurizio Sarri baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu Mmoja. text: Wanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi Takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa marufuku. Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki. Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39. Sherehe hiyo ya siku ya Jumanne inayofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi inatarajiwa kuanza mwenzo wa saa nne. Waandalizi wanatarajia watu 60,000 kujaza uwanja huo huku skrini kubwa zikiwa zimewekwa nje ya uwanja huo kwa wale watakaoshindwa kuingia. Rais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hilo Baadhi ya watumbuizaji wa kabila la Maasai wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo Naibu wa rais William Ruto, pia ataapishwa. Miongoni mwa viongozi wa kigeni wanaotarajiwa ni waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, rais wa Uganda, Yoweri Museveni na rais wa Rwanda Paul Kagame. Upinzani nchini humo umewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa mwezi Agosti. Upinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8 Maafisa wapolisi wameonya upinzani huo dhidi ya kufanya mkutano huo. Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais. text: Hii ni kwa sababu ya jamaa huyo Islam Mohammed Ibrahim Battah mwenye umri wa miaka 27 kufanana sana na nyota huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 anayeichezea klabu ya Barcelona . ''Nilipoanza kuacha ndevu zangu rafiki zangu waliniambia nilikuwa nafanana na Messi . Nilipoacha zikawa ndefu hata zaidi nilifanana naye hata kabisa'' Aliliambia shirika la Habari la Reuters . Katika ziara mjini Zagazig kilomita 90 kaskazini mwa mji mkuu Cairo watoto katika hifadhi inayowapa malezi walifurahi sana . Akiwa amevalia jezi ya Barcelona Battah alicheza soka na watoto hao kwenye uwanja wa mazoezi ulio karibu ,shirika la Reauters lina furaha ya watoto hao kuona jinsi Battah anavyofanana na Messi kwa kutoweza kutofautisha ni kitu 'kisichoweza kuelezeka'. " Ukimfanya mtu afurahi ,Mungu anakuwazadi.Nilitaka wawe na furaha hii nami'' Mchoraji mmoja kutoka Misri amepata mashabiki wengi katika taifa hilo la Afrika Kaskazini hasa wapenzi wa soka wanaovutiwa na mchezo wa Nyota wa Barcelona Lionel Messi. text: Kijana mmoja wa kimasai anaripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Mamia wa watu wanaripotiwa kubaki bila makao kutokana na kuondolewa kwa jamii hii ya wafugaji. Kijana mmoja wa kimasai anaripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Hii ni sehemu ya mzozo wa muda mrefu kati ya jamii ya Maasai na mamlaka ambazo huendesha shughuli za uwindaji kwa watalii. Serikali ya Tanzania ina mipango ya kubuni eneo la ukubwa wa kilomita 1500 mraba kwenye mbuga hiyo, kwa kampuni yenye makao yake nchini Dubai ambayo hutoa huduma za uwindaji kwa watalii matajiri kutoka Milki ya nchi za kiarabu. Kijana mmoja wa kimasai anaripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Mipango hiyo itasababisha watu 30,000 kupoteza makao na matatizo mengine kwa jamii ya Masai ambayo hutegemea malisho kwa mifugo wao. Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwani Kerry Dukunyi ameambia BBC kuwa wanavijiji wamepoteza mali katika kisa hiki cha hivi punde. "Kiwango kikubwa cha chakula chetu kimeharibiwa.Tumepoteza chakula kingi," alisema "Mifugo kadhaa pia hawajulikani waliko." Zaidi ya manyatta 100 za jamii ya Maasai zinadaiwa kuchomwa moto na mamlaka za mbuga ya wanyama pori karibu na mbuga ya wanyama pori ya Serenegeti. text: Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika. Injinia ambaye ndiye fundi mkuu wa kivuko hicho kilichopinduka Mwezi wa tisa tarehe 20 mwaka wa 2018 na kuua watu zaidi ya 225, alimsimulia mwandishi wa BBC Eagan Salla mkasa mzima. 'Siku kama siku nyingine' Siku ya tukio Injinia anasema ilkuwa siku kama siku nyingine lakini kwao kwa misingi ya usafirishaji ilikuwa siku ya kazi kubwa kwani ilikuwa ni siku ya gulio eneo la Bugorora. Kawaida wakazi wa kisiwa cha Ukara hufurika gulioni kujipatia mahitaji mbalimbali na siku hiyo ilikuwa vivyo hivyo. Kabla ya safari kama kawaida alikagua chombo (MV Nyerere) zikiwemo Injini zake mbili mpya na kujiridhisha kuwa chombo kilikuwa tayari kwa safari kutoka Bugorora (Ukerewe) kueleka Bwisya (Ukara) Baada ya kuwasha Injini alimruhusu Nahodha kuianza safari ambayo kwa kawaida huchukua wastani wa dakika arobaini na tano (45) hadi saa moja. Kawaida na kwa mujibu wa mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini nchini Tanzania, Sumatra, Mtaalamu huyu ana wajibu wa kutoa mwongozo kwa nahodha kwamba chombo kiende kasi gani kutokana na hali ya Injini na mzigo kilio beba jambo ambalo injinia Cherehani siku hii alilifanya mwenyewe kutokana na msaidizi wake kutokuwa kazini. Baada kukamilisha wajibu huu wa muhimu, Injinia huyo mwenye miaka 53 mkaazi wa Magu Masanza jijini Mwanza alirejea katika chumba cha injini na kuketi katika kiti chake kuhakikisha hali ya injini zake ni shwari mpaka Mv Nyerere itakapo kita nanga. Augustine Cherehani: Injinia aliyenusurika baada ya kuzama MV Nyerere ''Ninacho kumbuka ni kwamba nilijikuta niko chini ni kama mtu kapigwa ngwara'' Mara hii MV Nyerere ilisimama bila ya kukita nanga lakini pia injini zake ambazo amekuwa akizikagua mara zote, safari hii zilikuwa juu na yeye chini jambo ambalo si la kawaida, ndipo alipogundua hali si shwari hata kujisema moyoni ''hii ya leo nayo ni kali''. Maji yaki panda kasi ya wastani tayari yalisha mvuka kiunoni lakini Injini tiifu za Mv Nyerere bado zilikuwa zikifanya kazi kabla ya kumwaga oili na kuzima. ''Injini zile zimezimika, wakati ule zimeshapata moto, na sasa zikaanza kupoozwa na maji kwa kweli ile dakika ya kwanza mpaka ya ishirini ilikuwa ni kazi kubwa sana na nilihisi naweza kufa mapema sana kwa moshi kabla ya maji''. Kiza kinene na utulivu wa mauti, Injinia huyu baba wa watoto wanne wasichana wawili na wavulana wawili aliomba kimoyo moyo na kumwambia Mungu, anajua 'yeye ni mwenye dhambi ikiwa Mungu hata ona huruma kwake basi aone huruma kwa watoto wake alio walipia kwenda kwenye makambi ya Kisabato kuutafu tafuta uso wa Mungu anaye mtumainia'. Injinia ni Cherehani ni baba wa watoto wanne wasichana wawili na wavulana wawili, ambayo walikuwa moyoni mwake wakati wote wa mkasa huo Jua linachomoza kwa walio nje ya MV Nyerere, lakini simanzi kwa wakazi wa wilaya ya Ukerewe, Tanzania inashusha bendera yake nusu mlingoti, hili si jambo la kawaida hakika taifa hili kubwa Afrika ya mashariki liko katika maombolezo. Raisi John Pombe Magufuli anatuma salamu za pole na maombolezo salamu ambazo injinia Cherehani hazipati ila kwa uzoefu na utaalamu wa kibaharia anajua taifa linalia. Kwake kiza kinaendelea na mara hii maji yanelekea kifuani, usiku wa pili usiku ambao ulikuwa na ndoto nyingi za mauti, anaposikia sauti za waokozi nje yeye anaendela kugonga akiwa na tumaini atasikika. Mtalamu huyu anagonga kitaalamu , 1 2 3 ishara za kibaharaia na mabaharia wenzake wamsikia na kumgongea 1 2 3 anashusha pumzi na kuamini huenda aka uona tena uso wa Mke wake na watoto wake wapenzi. Lakini si leo maana punde kimya kinatawala na yeye anajua sasa ni usiku umeingia, siku ya tatu bila maji wala chakula. Anaposikia sauti za waokozi anaendela kugonga, 1 2 3 kama alivyofundishwa katika mafunzo ya ubaharia na Mungu si Athuman maana safari hii anauona mwanga wa kurunzi ya mzamiaji na yeye ana mrahisishia kwa kufuta weli chafu iliyotapakaa juu ya maji. ''…namshukuru Mungu alinipa uvumilivu nikasema kwamba kama ni kifo na kinikute hapa hapa". Hakika subira huvuta kheri, mzamiaji huyu alikuja mara tatu na safari hii alimgonga begani na kumwambia ''bwana nimekuja kukuchukua lakini kabla ya hapo naomba nikupe darasa, kama utafanya mchezo nitakutoa marehemu" Baada ya dakika kadhaa za hofu na kukata tamaa ndipo kamera za waandishi wa habari zilipo mmulika, na waandishi hao kuandika: 'Injinia Mkuu wa MV Nyerere aokolewa siku tatu baada kuzama kwake akiwa amejipaka weli chafu'. Kati ya Mwaka 2009 hadi 2017 Mwezi wa tano Injinia huyu anayeliona jua baada ya siku tau alihudumu kama injinia mkuu katika vivuko vya serikali ya Tanzania kigongo ferry kabla ya kuhamishiwa Ukerewa kukihudumia kivuko cha MV Nyerere mwezi wa tano mwaka 2017 hadi siku ya mkasa huu usio sahaulika. ''Kuna namba yoyote unayo ikumbuka nikamwambia ni ya mke wangu, unaweza kunitajia nimwambie? ndipo nilipo mtajia, akanipa kuongea naye aliposikia sauti yangu akaniambia inabidi umwombe Mungu sana sisi tayari tulishaweka msiba hapa''. Baada ya kuokolewa, Injinia huyu alipatiwa huduma ya kwanza katika kituo cha afya cha Bwisya na kuchukuliwa kwa helikopta ya polisi kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando na kupatiwa matibabu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani. 'Ila mpaka sasa bado na hudhuria kliniki katika hospitali hiyo'. Jina la Injinia Augustine Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara. text: Gari la Tesla Kundi hilo kutoka kampuni ya usalama ya Keen Security Lab lilingilia programu ya breki za gari hilo wakati ilipokuwa ikiendeshwa katika umbali wa kilomita 19. Wakitumia laptopu ,wadukuzi hao pia walifanikiwa kufungua mlango wa gari hilo bila kutumia funguo. Tesla imelazimika kuimarisha programu yake ili kuzuia wadukuzi wengine kuingilia kati. Udukuzi huo ulifanyika baada ya miezi kadhaa ya utafiti na kundi hilo la Keen Security Lab lilichapisha video za juhudi zake katika mtandao wa Yutube mapema wiki hii. Wakati wa Udukuzi huo, mmoja ya wadukuzi alilidhibiti gari hilo kutoka kwa kiti cha abiria wakati ambapo dereva alikuwa akibadilisha barabara. Kampuni ya Tesla imeimarisha programu yake baada ya watafiti kutoka China kudukua mfumo wa uendeshaji wa gari hilo. text: Kiongozi wa Korea kaskazini na makamanda wake Makomboira hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido. Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara. Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake. Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa. Katika siku za hivi karibuni Pyongyang ilijaribu kombora lake lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbiili kusini mashariki mwa Japan. Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini. text: Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen iliowasili mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa sasa anawangoza raia wa taifa hilo katika sherehe ya mapokezi ya ndege hiyo. Ndege hiyo imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ikitokea mjini Seattle Marekani. Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliochapishwa awali na Mkurugenzi wa mawasiliano katika Ikulu ya rais, ndege hiyo ni ya nne kuwasili nchini humo kati ya saba zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania {ATCL} kuimarisha huduma zake. Ndege hiyo ina uwezo kubeba abiria 262. Ndege nyingine ambazo zilinunuliwa na serikali ya Tanzania ni ndege moja aina ya Bombardier Q400 Dash 8 NextGen , ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 . Mwaka 2016 Tanzania ilipokea ndege mpya ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) katika hatua ya kuimarisha safari za ndani ya nchi za shirika hilo. Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) kutoka Canada ilikotengenezewa. Rais Magufuli alikuwa ameahidi kwamba shirika hilo lingeimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani. Baadhi ya maeneo ambayo ATCL inatarajia kuongeza safari zake ni Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba na Visiwa vya Comoro. Kulingana na Boeing, 787 Dreamliner ni familia yenye teknolojia ya kisasa ,ndege zenye utendaji mzuri na vitu vipya vya kupendeza. Mbali na kuleta vigezo vya ndege kubwa katika ndege za wastani, 787 Dreamliner italipatia shirika la ndege la Air Tanzania ufanisi wa mafuta na mazingira ya utendaji, kwa kutumia chini ya asilimia 20 hadi 25 ya mafuta na asilimia 20 hadi 25 wa uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa ndege nyengine zilizotumika awali. Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imewasili nchini Tanzania text: Noura Hussein alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela Mwezi uliopita majaji walimuondolea Noura Hussein mwenye umri wa miaka 19 hukumu ya kifo na badala yake wakamhukumu miaka mitano gerezani . Majaji pia waliagiza kuwa familia ya marehemu mume Abdulrahman Mohamed Hammad ilipwe $18,600. Hukumu ya awali ya kifo ilizusha hasira kubwa, na nyota wa kimataifa kama mwanamitindo wa Marekani Naomi Campbell na muigizaji Emma Watson waliounga mkono kampeni iliyoanzishwa katika mitandao #JusticeforNoura, kutaka msichana huyo aachiwe huru. 'Tunasubiri miujiza kumuepusha mtoto wetu kunyongwa' Katika taarifa yake, Faiza Mohamed, mkurugenzi wa Afrika wa kundi la kutetea haki za wanawake Equality Now, amesema: Noura ameteseka vya kutosha! Hakuna anayestahili kuolewa akiwa mtoto, abakwe na pia atakiwe kutumikia kifungo gerezani na alipe faini juu ya hayo yote. Kwa hivyo, rufaa hii ni muhimu ili kuweza kusema - imetosha! Ukiukaji unapaswa kusita hapa na haki ni lazima itendeke." Mnamo Mei, mahakama ilimhukumu Bi Husein kifo kwa kunyongwa, kufuatia kupatikana na hatia ya kutekeleza mauaji ya kupanga ya mumewe. Bi Hussein amesema mumewe aliwaita jamaa zake wanaotuhumiwa kumshikilia kwa nguvu huku akim'baka. Na wakati alipojaribu kuregelea kitendo hicho siku ya pili, alimuua kwa kumrukia na kumchomeka kisu. Ndoa yake Noura Hussein Mnamo 2015, Noura alipokea pendekezo la kuolewa kutoka jamaa wa familia yake mwenye umri wa miaka 32, Abdulrahman Mohamed Hammad. Noura alikuwa na umri wa miaka 16. Mamake anasema kuwa Noura hakuonekana kuchukukizwa na wazo hilo, lakini aliomba aruhusiwe aendelee na masomo. Alipendekeza pia ndoa hiyo iahirishwe hadi mamake - ambaye alikuwa mja mzito wakati huo - ajifungue. Lakini shinikizo la familia zikaongezeka - zikiwemo kutoka babake-Hussein. "Wasichana wengi eneo hilo walikuwa wakipachikwa mimba na kupata watoto nje ya ndoa," anasema Hussein. Hussein anaongeza kuwa hakutaka Noura naye akutwe na hali hiyo na asalie bila mume. Hukumu ya kifo dhidi ya Noura Hussein yafutwa Sudan Je mtu tajiri zaidi barani Afrika anatafuta mke? Licha ya kushiriki kwenye sherehe ya awali ya ndoa, ilibainika wazi kuwa Noura alikuwa anapinga wazo hilo. Alitoroka hadi kwa shangaziye mji wa Sinnar, ulioko kilomita 350 na kusalia naye kwa siku mbili. Alishawishiwa arejee nyumbani akifahamu kuwa ndoa hiyo haitakamilishwa. Hata hivyo, alipofika tu, sherehe ilikuwa imekamilika. Lakini hakuhitajika kuishi na mumewe. Miaka miwili iliyofuata aliishi na familia yake. Abdulrahman alipomtembelea ,alikuwa akimueleza wazi hakutaka kufunga ndoa naye. Licha ya hayo, wazee wa familia walianza kusisitiza Noura na mumewe wahalalishe uhusiano wao na kuishi kama wanandoa. Kulingana na mila yao, sauti ya wazee zilisikika na ndio waamuzi wa masuala muhimu. Heshima na taji la familia ni mojawapo ya masuala muhimu kwenye tamaduni zao. Babake Noura, Hussein anasema hakuona sababu ya bintiye kukataa uhusiano huo. Mwanamitindo ang'atwa na papa akipiga picha naye baharini Kylie Jenner kumshinda Mark Zuckerberg kwa kasi ya utajiri Familia ilikuwa na subra kwa miaka kadhaa. Kwa lazima, Noura alikubali kuishi na Abdulrahman mwezi Aprili 2017. Kulingana na taarifa zilizotibitishwa na CNN, Noura anasema kuwa alikataa kushiriki tendo la ndoa na mumewe wiki ya kwanza. Alilia. Alikataa kula. Abdulrahman alipolala, alijaribu kuondoka chumbani, lakini ilifungwa. Siku ya tisa, Abdulrahman aliwasili chumbani pamoja na jamaa wa familia waliorarua vazi lake na kumzuia sakafuni huku mume huyo akimbaka. Siku iliyofuata, Abdulrahman alijaribu tena. Awamu hii Noura alichukua kisu alichomweleza mamake kuwa angekitumia kujiondoa uhai. Noura alikamatwa na kuhukumiwa kwa mauaji ya kupangwa. Mawakili wa msichana wa Sudan aliyemuua mume wake anayemtuhumu kumbaka, wamekata rufaa katika mahakama ya juu zaidi kutaka aachiliwe huru bila ya masharti yoyote. text: Rita Jeptoo mwanariadha mashuhuri wa Kenya alipatikana na hatia ya kutumia dawa haramu mbioni Wanariadha hao sasa wamepigwa marufuku kwa miaka miwili. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirikisho la riadha nchini humo. Wanariadha hao wawili wanawake, walipatikana na hatia ya kutumia dawa aina ya Norandrosterone. Kimetto alipatikana na hatia hio Disemba mwaka 2013, huku Kiplimo akipatikana na kosa hilo baada ya kushiriki mbio za masafa marefu mjini Yangzhou China Aprili. Shirikisho la riadha la Kenya linasema linachunguza wanariadha wengine watano wanaoshukiwa kutumia dawa hizo haramu. Kadhalika shirikisho hilo limesema kuwa wanariadha hao wametakiwa kufika katika ofisi zake siku ya Alhamisi kuzungumzia maswala kadhaa kuhusiana na utumiaji wa dawa zilizopigwa marufuku, ambazo zimetajwa na shirikisho hilo. Kimetto na Kiplimo ni wanariadha wa hivi karibuni kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, kati ya wanariadha wengine 40 katika kipindi cha miaka miwili. Bingwa wa Olimpiki, David Rudisha alisema wiki jana kwamba serikali haifanyi juhudi za kutosha kukabiliana na tatizo la utumiaji wa dawa haramu za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha. Onyo lake limetolewa takriban miaka miwili baada ya Moses Kiptanui, mmoja wa wanariadha mahiri nchini Kenya kupatikana na hatia ya kutumia dawa hizo. Bingwa huyo wa dunia mara tatu wa mbio za mita 3,000 pamoja na mkufunzi, alidai kuwa wanariadha wengi wamekuwa wakitumia dawa haramu za kusisimua misuli ili kujipatia utajiri wa haraka. Miezi miwili iliyopita,Rita Jeptoo,mshindi wa mbio za marathon za Boston na Chicago kwa miaka miwili iliyopita, aliibuka na kuwa wanariadha maarufu sana kupatikana akiwa ametumia dawa za kusisimua misuli. Wanariadha wawili wa Kenya Viola Chelangat Kimetto na Joyce Jemutai Kiplimo, wamepataikana na hatia ya kutumia dawa haramu za kusisimua misuli. text: Olomide alisafirishwa na shirika la ndege la Kenya Airways, kutoka uwanja wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa tano unusu asubuhi. Mwanamuziki huyo alikuwa amekabiliwa na shutuma baada ya kanda ya video kuenea mtandaoni ikionekana kumuonyesha akimshambulia mwanamke uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Ijumaa asubuhi, muda mfupi baada ya kuwasili. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake. Akiongea katika kituo cha televisheni ya Citizen, muda mfupi kabla ya kukamatwa, Olomide alijitetea na kusema hakukusudia kumshambulia mwanamke huyo. Alisema alikuwa ameingilia kisa ambacho aliamini ni mtu aliyetaka kumpokonya mmoja wa wachezaji densi wake pochi yake au kulikuwa na vurugu fulani. Olomide alikamatwa muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano katika kituo kimoja cha runinga jijini Nairobi. Mkuu wa polisi nchini Kenya Joseph Boinnet alikuwa ametoa taarifa na kuwaagiza polisi wachukue hatua. Mwanamuziki kutoka Jamhuri wa Demokrasi ya Congo Koffi Olomide amesafirishwa kwenda mjini kinshasa kutoka Nairobi baada ya kukamatwa Ijumaa usiku. text: Ndege hiyo yenye viti vinne aina ya Sling 4 plane ilitengenezwa na kundi la wanafunzi 20 kutoka familia tofauti. Jumla ya wanafunzi sita walishiriki katika safari hiyo kama marubani na watoa msaada wa kiufundi. Safari yao ya kilomita 12,000 ilikuwa na vituo nchini Namibia, Malawi, Tanzania (Zanzibar na Kilimanjaro), Uganda na Ethiopia. Rubani Megan Werner, msichana wa miaka 17, aliyeanzisha mradi wa U-Dream Global ambao ndio umewezesha safari hiyo amesema amefurahia mno mafanikio yao. "Nimefarijika sana kwa hiki tulichokifanya, tumeonesha utofauti ndani ya bara (Afrika) katika sehemu zote tuliposimama. "Lengo la mradi ni kuonesha Waafrika kuwa kila kitu kinawezekana kama utaweka akili yako katika kulifanikisha hilo," amesema. Huree! Wanafunzi hao walikuwa wakitoa mihadhara kwa wanafunzi wenzao kwenye kila nchi waliyosimama. Ndege nyengine aina ya Sling 4, ilikuwa ikiambatana nao na kuendeshwa na marubani wenye uzoefu ili kutoa msaada pale unapohitajika. Baba wa Megan, Bwana Des Werner ambaye ni rubani mwandamizi alikuwa ni sehemu ya timu ya msaada. Wanafunzi hao waliitengeneza ndege hiyo kwa wiki tatu kwa kuunganisha vifaa vilivyotengenezwa na kampuni moja nchini humo. Uundaji huo ulihusisha kuunganisha maelfu ya vifaa vidogo vidogo. Taarifa zaidi ya safari hiyo Hata hivyo, mafanikio hayo hayakukusa changamoto, ameeleza Megan. Wanafunzi hao walikataliwa na mamlaka za Kenya kutua jijini Nairobi na ikabidi wabadili njia. Katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, walichelewa kupata mafuta. "Baada ya kuyapata, ndege ya pili ya msaada ikaanza kuvujisha mafuta na ikashindwa kuendelea na safari nasi na ikabaki marubani wawili tu mimi na Driaan van den Heever kuendelea na safari," ameeleza Megan. "Tulikuwa na mashaka juu ya kupaa katika anga la Sudani kutokana machafuko ya kisiasa yanayoendelea." Ndege hiyo iliundwa na wanafunzi 20 kutoka familia tofauti Afrika Kusini Marubani hao sita wanafunzi walikuwa wakipokezana kurusha ndege hiyo. Hata hivyo, aina ya leseni waliyopata ambayo ni daraja la kwanza pia ikawa kikwazo. Walitakiwa kutopaa juu sana na kufikia usawa wa mawingu. Kipande cha mwisho cha safari kilikuwa ni mtihani mgumu kwa marubani hao. "Tuliendesha ndege na Driaan van den Heever kwa saa 10 bila ya ndege ya usaidizi, ilikuwa ni wanafunzi wawili angai bila usaidzi wowote," ameeleza Megan. Marubani wanafunzi (kutoka kkushoto) van den Heever, Werner na Hendrik Coetzer Marubani hao wawili wanafunzi wakapatwa na tatizo katika mifumo ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kuingia kwenye anga la Misri. Hivyo wakafanya maamuzi ya kutua kwenye uwanja wa karibu zaidi badala ya ule wa Kimataifa wa Cairo kama ilivyokuwa imepangwa awali. "Halai hiyo ilizua tafrani kidogo, lakini maamuzi yalifanyika kwa sababu za kiusalama," ameeleza Des Werner. "Mwishowe tukagundua kuwa ilikuwa nyanya moja tu imecheza na wakairekebisha mara moja, lakini kukawa na urasimu mkubwa ambao ulichukua muda mrefu na kutakiwa na mamlaka waandike ripoti." "Tulipotua Misri kwa dharura katika eneo la kwanza maafisa walitaka kutukamata, kutupokonya hati zetu za kusafiria na leseni lakini kwa bahati nzuri baada ya saa kama nne kila kitu kikawa sawa tukapata mafuta ya ziada ya kutufikisha Aswan, na kutoka hapo tukapaa mpaka hapa Cairo, lilikuwa ni jambo la furaha sana kutua Cairo," ameeleza Megan. Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi wa Afrika Kusini imetua salama Cairo, Misri wiki sita baada ya kuondoka Cape Town, Afrika Kusini. text: Tareck El Aissami{Kushoto} aliteuliwa Makamu wa Rais na Rais Nicholas Maduro wa Venezuela Pia bwenyenye maarufu wa Venezuela Samark Lopez pia amewekewa vikwazo kwa kutuhumiwa kama mshirika mkuu wa El Aissami. Tareck El Aissami aliteuliwa kama Makamu wa Rais na Rais Nicolas Maduro mwezi uliopita. Amekanusha madai ya kuhusika na visa vyovyote ya jinai. Bwana Lopez hajajibu hatua hizi za Marekani. Vikwazo hivi vinamaanisha kwamba mali yote ya Makamu wa Rais iliyoko Marekani inapigwa tanji huku akizuiwa kuingia nchini humo. Wizara ya fedha ya Marekani imesema bwana El Aissami alisimamia kuvukishwa kwa tani nyingi za mihadarati ndani ya Marekani kwa kutumia ndege au meli. Aidha imeongeza alikua kwenye orodha ya waliopokea mulungula kutoka kwa mlanguzi mkuu wa mihadarati wa Venezuela aliyeko korokoroni Walid Makled, ili kumkinga wakati akiendelea na biashara haramu. Tareck El Aissami na Rais wa Urusi Vladmir Putin Bwana El Aissami aliwahi kuwa gavana wa jimbo la Aragua na pia akawa waziri wa ndani na sheria nchini Venezuela kati ya mwaka 2008 na 2012. Taarifa zilizonadiwa na mashirika ya habari Marekani zinasema bwana El Aissami alikua akichunguzwa na Marekani kwa kushirikiana na kundi la wapiganaji la Hezbollah nchini Lebanon. Wakati akiwa waziri wa ndani imedaiwa pasipoti kadhaa za Venezuela zilipatikana zikitumiwa na wapiganaji wa Hezbollah. Mapema mwezi huu wabunge 34 wa baraza la Congress Marekani walimuandikia waraka Rais Donald Trump wakimtaka kuweka vikwazo kwa baadhi ya maafisa wa serikali ya Venezuela. Walimtaja hasa Tereck Al Aissami wakisema ana nafasi kubwa ya kuongoza nchi kama Makamu wa Rais na alistahili kuchukuliwa hatua kutokana na tuhuma zake kuhusika na ulanguzi wa mihadarati pamoja na kuwa mshirika wa kundi ambalo Marekani imeliorodhesha kama la kigaidi. Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Makamu wa Rais wa venezuela Tareck El Aissami kwa tuhuma za kuhusika na ulanguzi wa kimataifa wa mihadarati. Bwana El Aissami ameongezwa kwenye orodha ya walanguzi wakuu wanaosakwa na Marekani. text: Magufuli alipokutana na Bi Bird miaka miwili iliyopita Hata hivyo, utata bado unaendelea kuhusu msaada wa dola 50 milioni za Marekani ambazo benki hiyo ilikuwa inatarajiwa kutoa kwa taifa hilo. Taarifa iliyotumwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu baada ya mkutano huo inaeleza kuwa Rais Magufuli na Bi Bella Bird walizungumzia miradi mbalimbali ambayo imo njiani, lakini mkazo kwenye taarifa hiyo umewekwa kwenye sekya ya elimu ya awali na ya sekondari. Bi Bird amenukuliwa akisema kuwa kwa sasa wanakamilisha maandalizi ya ufadhili wa miradi mingine inayohusu sekta ya elimu hasa elimu ya awali na sekondari, itakayogharimu shilingi Trilioni 1.357, na kwamba maandalizi hayo yatakamilika mwezi ujao. Bi Bird alipokutana na Rais Magufuli katika Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Kwa jumla, miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia nchini Tanzania kwa mujibu wa Bi Bird imefikia thamani ya shilingi Trilioni 10.186. Maendeleo ya miradi hiyo ni mazuri, taarifa hiyo imemnukuu Bi Bird. "Kwa hiyo nimekutana na Mhe. Rais Magufuli kuzungumzia maendeleo ya miradi hiyo na kwa ujumla maendeleo ni mazuri," amesema Bi. Bella Bird, kwa mujibu wa benki hiyo. Taarifa kuhusu msaada Wiki iliyopita, Benki ya Dunia ilitoa taarifa ikisema imesikitishwa sana na marekebisho ya sheria yanayopendekezwa kufanywa kwenye Sheria ya Takwimu ya 2015. Benki hiyo ilisema sheria hizo haziendani na viwango vya kimataifa vilivyowekwa kuhusu takwimu. "Tumeifahamisha serikali ya Tanzania kwamba marekebisho hayo, iwapo yatatekelezwa, huenda yakaathiri sana kuandaliwa kwa takwimu rasmi na zisizo rasmi, ambazo huwa muhimu sana kwa ustawi wa taifa lolote lile," benki hiyo ilisema. "Ni muhimu sana kwa Tanzania, sawa na taifa jingine lolote, kutumia sheria za takwimu kuhakikisha takwimu rasmi ni za kiwango cha juu zaidi na za kuaminika na pia kulinda uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake, kuendeleza mjadala kwa manufaa ya raia." Kutokana na hilo, benki hiyo imesema: "Benki ya Dunia inajadiliana na serikali kuhusu utoaji wa msaada zaidi katika kujenga mifumo ya takwimu endelevu unafaa kwa wakati huu." Mkutano wa leo umefanyika kukiwa na utata kuhusu msaada wa $50m Ingawa benki hiyo ilisema mashauriano yanaendelea na kwamba wameeleza wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo ya takwimu, hawakusema wazi kwamba wamesitisha mradi huo nambari P167066. Kadhalika, kiasi hicho cha $50 milioni bado kimeorodheshwa kwenye tovuti ya benki hiyo kama msaada unaopangiwa kutolewa kwa Tanzania, ingawa mpango huo bado haujaidhinishwa, bado upo kwenye utaratibu. Benki ya Dunia ilikuwa imetumia kiasi cha $ 63.18 milioni kama msaada kuimarisha uwezo wa mfumo wa takwimu wa serikali Tanzania kufikia Juni 30,2018 chini ya mradi ambao ulikuwa umeidhinishwa mwaka 2011. Agosti, waliidhinisha kiasi kingine cha $ 8.56 milioni. Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini humo kuzungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na benki hiyo. text: Line ni mtandao unaoongoza katika mataifa kadha ya Asia Mwanamke mmoja nchini Taiwan ameruhusiwa kumpa talaka mume wake, kwa kutumia ishara kwamba ujumbe wake aliomtumia mumewe ulisomwa kama ushahidi kwamba mumewe alikuwa akimpuuza. Mtandao wa kijamii wa Line unaonesha mumewe alikuwa akifungua ujumbe huo, lakini hakujibu. Jaji amemkubalia ombi la kumtaliki mumewe. Mwanamke huyo alitumia alama za rangi ya buluu ambazo hutumiwa na mitandao kama vile Line na WhatsApp mtu anaposoma ujumbe kudai kwamba mumewe alikuwa ameupokea ujumbe. Jaji katika mahakama ya masuala ya kifamilia Hsinchu amesema hali kwamba mwanamume huyo alipuuza ujumbe huyo ni ushahidi kwamba ndoa kati ya wawili hao haiwezi 'kuokolewa' na vyombo akawaruhusu kupatiana talaka. Katika kipindi cha miezi sita hivi, mwanamke huyo ambaye jina lake la ukoo ni Lin, alimtumia mumewe ujumbe mara kadha, wakati mmoja ikiwa ni baada yake kulazwa hospitalini baada ya kuhusika katika ajali barabarani, kwa mujibu wa Jaji Kao. Katika ujumbe mmoja, alimwambia mumewe kwamba alikuwa katika chumba cha dharura hospitalini na akamwuliza ni kwa nini anasoma ujumbe wake lakini hamjibu. Ingawa mumewe alimtembelea hospitalini mara moja, mahakama ilisema kwamba hali kwamba alikuwa akipuuza ujumbe wake ni msingi tosha wa kumpa talaka. "Mshtakiwa hakumjulia hali mlalamishi, na habari aliyotumiwa na mlalamishi aliisoma lakini hakujibu," mahakama ilisema kwenye uamuzi wake. Rangi ya buluu huonesha ujumbe umesomwa na mhusika Ilikuwa ni baada ya mwezi mmoja au miwili hivi baada ya ajali hiyo ambapo mumewe alimtumia ujumbe mfupi. "Ujumbe wake ulikuwa kumhusu mbwa wao na alimfahamisha pia kwamba kulikuwa na barua iliyotumwa kwake, lakini hakuonesha ishara za kutaka kujua hali yake," Jaji Kao alisema. Wawili hao walifunga ndoa 2012. Mwanamke huyo ambaye amewahi kuolewa awali ana miaka 50 hivi na mumewe ana miaka 40 hivi. Umewahi kupuuza ujumbe wa mpenzi au mchumba wake? Tahadhari: huenda hilo likatumiwa dhidi yako kortini. text: Kufikia tarehe 7 mwezi Aprili takriban wanaume 2,232 walikuwa wamefariki kutokana na virusi hivyo mjini New York - Kitovu cha maambukizi nchini Marekani ikilinganishwa na wanawake 1,309 kulingana na idara ya afya nchii humo. Katika mahospitali kulikuwa na wagonjwa wanaume 40,000 ikilinganishwa na wanawake 34,000. Kiwango cha vifo vya Covid 19 miongoni mwa watu 100,000 mjini New York kilikuwa na wanaume 55 na chini ya wanawake 30. Wanaume wengi wamekutwa na ugonjwa huo zaidi na wanaonekana kupatwa na maafa mabaya. Mshirikishi wa Ikulu ya whitehouse kuhusu maswala ya Covid-19 Dkt Deborah Birx awali alizungumzia kuhusu suala hili linalotia wasiwasi baada ya kuchunguza takwimu nchini Itali, ambapo picha za vyumba vya wagonjwa mahututi zilionyesha wanaume wenye umri mkubwa wakipumua kwa usaidizi wa mashine. Data ya idadi ya vifo iko juu miongoni mwa wanaume Idadi ya vifo miongoni mwa wanaume inaonekana kuwa maradufu katika kila umri wa wanawake. ''Hilo ni suala ambalo linafaa kutuamsha sote ili kuendelea kuwalinda wenzetu walio katika vyumba vya uuguzi'', alisema Birx wakati alipokuwa akitoa habari kwa jopo la utawala wa Trump linalokabiliana na virusi vya corona. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa nje ya China ulibaini kwamba kiwango cha vifo miongoni mwa wanaume ni asilimia 2.8 ikilinganishwa na asilimia 1.7 ya wanawake. Uchanganuzi mwengine wa China ulibaini kwamba kati ya watu waliofariki na virusi hivyo asilimia 60 walikuwa wanaume. Wakati Itali ilivyoripoti vifo vyake hivi majuzi , asilimia 72 ya wale waliofariki walikuwa wanaume . Utafiti mwengine uliiweka idadi hiyo kuwa zaidi huku asilimia 80 wakiwa wanaume. Je ni sababu gani zinazowafanya wanaume kuwa hatarini zaidi? Wataalam wametoa sababu kadhaa ambazo zinaweza kuelezea tofauti hiyo kubwa, ikiwemo mfumo wa kinga kati ya wanaume na wanawake, tofauti ya homoni mwilini, maisha, na uwezekano wa wanaume kujiweka katika hatari nyingi. Kwa mfano , wanaume wana uwezekano wa kuvuta sigara - huku asilimia 40 wakitumia bidhaa hiyo duniani ikilinganishwa na asilimia 9 ya wanawake , kulingana na shirika la afya duniani - suala linalowaweka katika hatari kubwa ya kukutwa na magonjwa ya mapafu. Wanaume pia hunywa pombe nyingi na mara nyengine hukataa kwenda hospitali wakati wanapokuwa katika hali mbaya ya kiafya. Wakati huohuo wanawake wana uwezo mkubwa wa kukabiliana na maambukizi ya virusi ikilinganishwa na wanaume "Kuna kitu kuhusu mfumo wa kinga ya wanawake ambacho ni zaidi," Dk Janine Clayton, mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti juu ya Afya ya Wanawake katika Taasisi za Afya za kitaifa, aliambia New York Times. Wanawake pia wana nafasi nzuri ya kinga kwa kumiliki kromosomu mbili za X , ambazo zinaweza kuchangia katika kuimarisha kinga miongoni mwao wanapokabiliana na maambukizi ya virusi . "Baadhi ya sababu zizsizojulikana kwanini Covid-19 huenda ni hatari zaidi miongoni mwa wanaume zaidi ya wanawake ni kwamba ugonjwa wa moyo hupatikana sana miongoni mwa wanaume wenye umri mkubwa zaidi ya wanawake'', alisema Dkt Stephen Berger, mtaalam wa magonjwa ya maambukizi na mwanzilishi mwenza wa shirika la Global Infectious Diseases and Epidemiology Network (GIDEON). Tafiti pia zimebaini kwamba shinikizo la juu la damu na magonjwa ya ini hupatikana sana miongoni mwa wanaume suala linalochangia vifo vya Covid-19. Tatizo hilo limesababisha uzinduzi wa vipimo viwili nchini Marekani. Katika vipino hivyo , wanasayansi wanawapatia wanaume walio na COVID-19 homoni za kike ili kuona iwapo zinaweza kuwasaidia kupona Covid-19. Kitu cha kushangaza kuhusu virusi vpya vya corona ni kwamba ni hatari zaidi kwa wanaume zaidi ya wanawake. text: Takriban watu 700,000 wanahofiwa kuwa katika hatari Kimbunga hicho kilituwa siku ya Alhamisi kwa upepo mkali wenye kasi ya 220km/h (140mph) kilichoviangamiza vijiji. Takriban watu 700,000 sasa wanadhaniwa kuwa katika hatari katika eneo hilo wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha. Pemba, mji mkubwa wa jimbo la Cabo Delgado kumeshuhudiwa mvua yenye kina cha mita mbili na mafuriko. Msemaji katika ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinaadamu (Ocha) Saviano Abreu ameeleza kwamba hali ni mbaya katika miji ya Macomia na Quissanga, akiongeza kwamba kuna wasiwasi pia kwa kisiwa kisichoweza kufikiwa cha Ibo. Mawimbi ya hadi mita 4 yanatarajiwa, na mashirika ya misaada yanahofia kwamba mvua itazidi kunyesha. "Tuna wasiwasi mkubwa kwasababu, kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, mvua nzito inatarajiwa kunyesha katika siku nne zijazo," Deborah Nguyen, msemaji wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa mataifa , alieliambia shirika la habari la AFP. "Tunatarajia mvua iwe na ukubwa wa mara mbili zaidi ya ilioshuhudiwa wakati wa kimbunga Idai," ameongeza. Kimbunga Idai kilisababisha vifo vya watu 900 katika nchi tatu mnamo Machi mwaka huu. Hali ilivyo Mtwara baada ya Kimbunga Kenneth kuisha nguvu Msumbiji Ni yapi yanayojiri? Inadhaniwa kwamba watu 400,000 wanaishi Pemba , na mvua kubwa imesababisha watu wengi kuwa katika hatari. Kuna wasiwasi unaotokana na maporomoko ya ardhi katika mtaa wa Mahate mjini humo, maafisa wa Ocha katika eneo hilo wanasema, na katika mtaa wa Natite, nyumba zimeanza kuporomoka. Shirika la mpango wa chakula duniani linaarifiwa kuanza kutoa misaada kwa watu waliokwama, lakini barabara zilizoharibika zimesababisha shughuli zisitishwe katika maeneo yaliotengwa sana. Takriban watu watano wamefariki kutokana na kimbunga hicho na takriban nyumba 35000 zimeharibika vibaya au kubomoka kabisa, maafisa wa kitaifa wanasema. Maafisa wa uokozi kutoka Brazil wamewaokoa watu 350 kutoka sehemu zilizokabiliwa na mafuriko mjini siku ya Jumapili. Mafuriko yamesababisha uharibifu kwa miundo msingi na kutatiza juhudi za kuwasilisha misaada Hapo jana Jumapili msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema "amesikitishwa sana" kutokana na kimbunga Kenneth. Mashirika ya Umoja wa mataifa yanasaidia maafisa wa serikali na bwana Guterres ametoa wito wa "rasilmali za ziada" kutoka jumuiya ya kimataifa "kufadhili usaidizi wa sasa, wa siku zijazo na wa kipindi kirefu zaidi". Eneo lililoathirika liko vipi? Jimbo la Cabo Delgado halina watu wengi kama eneo lililoathirika na kimbunga Idai na inavyoonekana sehemu kubwa iko katika ardhi ya juu. Hilo kwa pamoja na tahadhari za mapema kutoka kwa maafisa husika kabla ya kutokea kimbunga hicho huenda ikasaidia kuzuia hasara ikilinganishwa na wakati wa kimbunga Idai. Lakini taarifa zinasema maelfu ya makaazi yameharibiwa kutokana na upepo mkali, na ene hilo limekabiliwa na mashambulio ya wanamgambo wenye itikadi kali za dini ya kiislamu katika miezi ya hivi karibuni, jambo ambalo linaonekana huenda likatatiza utoaji wa msaada. Tayari maelfu ya watu walikuwa wametoroka makaazi yao kutokana na ghasia kutafuta hifadhi katika kambi za kuwahifadhi watu walioachwa bila ya makaazi. Hali kaskazini mwa Msumbiji ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa, msemaji wa Umoja wa mataifa ameeleza, siku chache baada ya kimbunga Kenneth kutuwa nchini humo. text: Henry Rotich aachiliwa kwa dhamana Rotich, na mshtakiwa mwenzake katibu mkuu Kamau Thugge wameagizwa kuwasilisha pasipoti zao za usafiri kama sehemu ya masharti ya dhamana. Hakimu Douglas Ogoti amewazuia wasifike katika makao ya wizara ya fedha, na kufafanua kwamba sasa eneo hilo linachunguzwa kwa uhalifu. Mapema leo, Rotich amekanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake kuhusiana na kandarasi ya ujenzi wa mabwawa mawili siku moja tu baada ya kukamatwa na kuzuiliwa - hatua isio ya kawaida kwa waziri katika taifa hilo lenye kiwango cha juu cha ufisadi. Waziri huyo na maafisa wengine wakuu wanatuhumiwa kwa ushirikiano kuwalaghai Wakenya , miongoni mwa mashtaka mengine. Akiwa amevalia koti na tai na kusimama karibu na naibu wake katika wizara hiyo , Kamau Thugge, Rotich alikana mashtaka hayo wakati yalipokuwa yakisomwa na waendesha mashtaka katika chumba cha mahakama kilichojaa watu mjini Nairobi. Mashtaka dhidi ya Rotich yanatokana na uchunguzi wa polisi kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika miradi miwili ya mabwawa magharibi mwa taifa hilo ambayo yalikuwa yakisimamiwa na kampuni moja ya Italia kwa Jina CMC Di Ravenna. Kenya pia itaomba kurudishwa nchini kwa Paolo Porcelli, mkurugenzi wa kampuni ya CMC di Ravenna, ili kushtakiwa, nchini mkurugenzi wa mashtaka aliambia chombo cha habari cha Reuters. ''Kuna huyu raia wa Itali, hakuweza kufikishwa mahakamani hivyobasi tutaomba ahukumiwe hapa nchini , Tutahakikisha kuwa kibali cha kimataifa cha kukamatwa kwake kimetolewa'', alisema Noordin Haji. CMC di Ravenna amekana kufanya makosa. Katika taarifa siku ya Jumatatu, kampuni hiyo ilisema siku ya Jumatatu kwamba haijaelezewa kuhusu mawasiliano yoyote rasmi kutoka kwa mamlaka . Mabwawa hayo mawili yalipangiwa kugharimu dola bilioni 46 lakini wizara ya fedha ilikopesha bilioni 63 badala yake , alisema Hajj siku ya Jumatatu hivyobasi kuongeza deni kubwa la Kenya ambalo linadaiwa kufikia asilimia 55 ya mapato ya taifa hilo. Na huku hayo yakijiri mkurugenzi wa zamani wa shirika la kukabiliana na ufisadi nchini kenya John Githongo amesema kuwa raia nchini wana 'matumaini' baada ya waziri wa fedha Henry Rotich kukamatwa pamoja na viongozi wengine wakuu kuhusiana na mashtaka ya ufisadi. Bwana Githongo aliambia kipindi cha BBC News Day kwamba ni mara ya kwanza kwa taifa hili ambapo waziri na katibu wake wamekamatwa na kuwasilishwa mahakamani. Akielezea umuhimu wa kukamatwa kwake bwana Githongo amesema kuwa ni uwajibikaji ambao Wakenya hawajauzoea. Waziri wa Fedha Kenya, Henry Rotich ameachiliwa huru kwa dhamana ya $150,000 baada ya kukana zaidi ya mashtaka 10 yanayohusiana na ufisadi. text: Ugonjwa huo unafahamika kitaalamu kama mycoplasma genitalium, na ufupisho wake kwa Kiingereza ni MGen na wakati mwingine umekuwa ukifupishwa tu kama MG. Ugonjwa huo uligunduliwa miaka ya 1980 lakini ni miaka ya karibuni ambapo wanasayansi walibaini kwamba kuenea kwa ugonjwa huo kunahusiana na tendo la ndoa. Bakteria za mycoplasma genitalium huambukiza seli zilizo kwenye mfumo wa mkojo na njia ya uzazi. Hapa tumekuandaliwa mambo muhimu unayofaa kuyafahamu kuhusu ugonjwa huu kama yanavyosimuliwa na Dkt Suneeta Soni ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi nchini Uingereza na Dkt Pam Sonnenberg aliyewahi kuongoza utafiti kuhusu MGen. Je, ugonjwa huu ni wa aina gani? MGen ni ufupisho wa mycoplasma genitalium na ni ugonjwa ambao unaathiri wanaume na wanawake. Nchini Uingereza inakadiriwa kwamba asilimia moja ya watu wote wameambukizwa ugonjwa huo. Ugonjwa huo umeelezwa kama ugonjwa sugu usiosikia dawa ambao kuna hatari kwamba huenda ukafanikiwa kuhimili dawa zote na matibabu yote ambayo yapo kwa sasa. Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kinyume na Ukimwi ambao husababishwa na virusi. Bakteria za ugonjwa huu zimeonesha dalili za kuhimili antibiotiki ambazo awali zilikuwa zinatumiwa kuangamiza viini hivyo. Viini vya ugonjwa huo viligunduliwa mara ya kwanza kwenye mfumo wa kupitisha mkojo wa binadamu mwaka 1981 katika hospitali ya St Mary's, Paddington jijini London, na hatimaye vikatambuliwa kuwa vya jamii mpya ya viini ya Mycoplasma mwaka 1983. Ni ugonjwa ambao umetambuliwa kama magonjwa ambao mara nyingi unaambatana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na unaathiri pia kwa kiwango cha juu kidogo wapenzi wa jinsia moja. Wataalamu wanasema ugonjwa huo huenda ukachangia pia katika kuzuka kwa saratani ya tezi dume na saratani ya ovari katika baadhi ya watu. Wanaougua ugonjwa huo wamekuwa wakitibiwa kwa antibiotiki za familia moja ambazo zinafahamika kama Macrolide ambapo ile maarufu ni dawa ya azithromycin. Kuna pia dawa nyingine kwa jina doxycycline. Bakteria za ugonjwa huo hata hivyo zinaanza kutosikia dawa hizo. Dawa ya azithromycin hata hivyo bado inafanikiwa kuwatibu baadhi ya watu ingawa madaktari wanalazimika kuongeza kipimo cha dawa mara nyingi. Kiwango cha kutosikia dawa za Macrolide miongoni mwa bakteria za ugonjwa huo Uingereza kinakadiriwa kuwa asilimia 40 kwa sasa. Dalili zake ni gani? Dalili zake zinafanana sana na za ugonjwa mwingine unaofahamika kama chlamydia. Kwa wanaume, kuhisi maumivu wakati wa kupitisha mkojo na pia kutoa uzaha uumeni. Wanaume pia huhisi maumivu kwenye korodani Ugonjwa huo unaojulikana kama Mycoplasma genitalium (MG) hauna dalili lakini unaweza kuwa na madhara ikiwemo kusababisha utasa kwa wanawake. Kwa wanawake, ni kuhisi maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo na kwenye sehemu ya nyonga. Kadhalika, kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa na pia baadhi wanaweza wakavuja damu kwenye sehemu nyeti. Wanawake wanaweza pia kukumbwa na tatizo la mimba kukaa nje ya mji wa mimba. Idadi kubwa ya watu walioambukizwa ugonjwa huu, karibu asilimia 90, huwa hawaoneshi dalili zozote, na kuna uwezekano kwamba miili yao itafanikiwa kuangamiza viini hivyo mwilini bila tiba yoyote na hivyo kwao hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Unaweza kusababisha ugumba? Madhara ya ugonjwa huu yanakaribiana sana na ya chlamydia; ambapo mwanamume huvimba na kuambukizwa kwa mirija ya uzazi na mji wa mimba pia. Hilo linaweza kusababisha kuwepo kwa makovu na vidonda kwenye viungo hivyo jambo linaloweza kusababisha mwanamke baadaye kuwa gumba au tasa. Unawezaje kujikinga na kujiepusha na ugonjwa huu? Njia moja ni kujizuia kufanya mapenzi bila kinga. Hili litakukinga pia dhidi ya magonjwa mengine kadha ya zinaa. Dkt Sonnenberg anasisitiza umuhimu wa kupunguza idadi ya watu ambao mtu anashiriki nao tendo la ndoa. "Kadhalika, usifanye mapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja kipindi kimoja kwani hivyo ndivyo ugonjwa unavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Madaktari wanapendekeza watu watumie mipira ya kondomu wanapofanya ngono na wapenzi wengine au wanapokuwa na wapenzi wengi. Baadhi ya watu walio na dalili za ugonjwa huu wanaweza kutembelea hospitali au zahanati ambapo madaktari hawana uwezo wa kuupima ugonjwa huu. Dkt Soni anasema hapo ndipo kuna tatizo kubwa katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa sababu madaktari katika hali kama hiyo watakuwa wanatibu dalili badala ya ugonjwa wenyewe. Kutokana na hilo, watu wengi wanaishia kupewa dawa za kukabiliana na bakteria (antibiotic) ilhali ukweli ni kwamba katika kipindi hicho wanakuwa hawazihitaji. Hilo linachangia aste aste bakteria zinazosababisha MGen kuanza kuwa sugu na kuzoea dawa hizo. Dkt Peter Greenhouse, mshauri wa masuala ya ngono huko Bristol anawashauri watu kuchukua tahadhari zaidi. "Ni wakati ambapo watu wanafahamu kuhusu Mycoplasma genitalium," alisema. "Kuna sababu nzuri ya kubeba kondomu wakati wa likizo za msimu wa joto na kuzitumia. Wataalamu maeneo mbalimbali duniani, wametoa tahadhari kuhusu ugonjwa mpya wa zinaa ambao unaonesha dalili za kutosikia dawa na kuzua wasiwasi sawa na ulioibuliwa na ugonjwa wa Ukimwi. text: Shirika linalosimamiwa na rais wa Caf Ahmad limekuwa likichunguzwa katika siku za hivi karibuni Makamu huyo wa rais wa Fifa mwenye umri wa miaka 60 amedaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na wadhfa wake mbali na utumizi mbaya wa fedha. Uchunguzi kuhusu tabia ya Ahmad kutoka mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Mecca ya Umrah, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine , ilisema taarifa ya Fifa. Bwana Ahmad ambaye marufuku yake awali ilikuwa imetangazwa na BBCSport Africa , mwezi uliopita pia amepigwa faini ya $200,000. Hapo awali alikana kufanya makosa yoyote. Mwezi uliopita makamu huyo wa rais wa Fifa kutoka taifa la Madagascar alitangaza lengo lake kuwania muhula wa pili wakati uchaguzi wa Caf utakapofanyika mwezi Machi mwaka ujao. Hilo huenda lisifanyike kwasababu atalazimika kupita mtihani wa maadili ili kustahiki kusalia katika baraza la Fifa. Uwezekano wa yeye kuchaguliwa ka awamu ya pili utategemea iwapo atashinda kesi ya rufaa aliowasilisha katika mahakam ya kutatua mizozo ya michezo CAS , huku kesi hiyo akihakikisha kuwa inasikilizwa mapema ili kumruhusu kuthibitishwa kuwa mgombea. Tunaendelea kukupasha... Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika {Caf} Ahmad amepigwa marufuku ya miaka mitano na shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria kadhaa za maadili. text: Daraja hilo la kioo linapatikana katika mkoa wa Hunan Daraja hilo ndilo la juu zaidi lenye sakafu ya kioo duniani na linaunganisha milima miwili ambayo hufahamika kama Milima ya Avatar. Filamu ya Avatar iliandaliwa katika milima hiyo. Wale wenye ujasiri wataweza kutazama mandhari ya kuvutia Daraja kwa tarakimu Ujenzi ulikamilika Desemba mwaka jana. Urefu wa daraja hilo ni 430m na liligharimu $3.4m (£2.6m). Daraja hilo limewekwa 300m juu ya ardhi, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Xinhua. Sakafu yake imeundwa kwa vipande 90 vya vioo ambavyo vina tabaka tatu. Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, daraja hilo lenye upana wa mita 6, ambalo mchoro wake uliandaliwa na msanifu mijengo kutoka Israel Haim Dotan, tayari limeweka rekodi kadha za dunia katika usanifu mijengo na ujenzi. Je, na usalama wake? Hili ni suala kuu. Lakini maafisa wameandaa hafla za kudhihirisha uthabiti wake. Maafisa walituma watu wenye nyundo kujaribu kuvunja vioo. Pia magari yaliyojaa abiria yalipita juu yake mapema mwezi huu. Mwandishi wa BBC Dan Simmons ni mmoja wa walioalikwa kujaribu kubaini iwapo vioo vya daraja hilo vinaweza kuvunjika. Maafisa walituma watu na nyundo makusudi Magari yaliyojaa watu pia yalipita juu Maafisa wanasema watu 8,000 wataruhusiwa kutumia daraja hilo kila siku. Daraja refu zaidi duniani ambalo sakafu yake ni kioo limefunguliwa katika mji wa Zhangjiajie katika mkoa wa Hunan nchini China. text: Wafuasi wa upinzani wameandamana leo miji mbalimbali kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi Wawakilishi hao wa nchi 13 pamoja na Umoja wa Ulaya wamesisitiza kwamba uchaguzi mpya unafaa kuwa "bora kuliko uliofanyika awali (mwezi Agosti) - uwe huru, wa kuaminika na wa Amani". Taarifa yao ya pamoja imetolewa baada ya mkutano kati yao na maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC). Kwenye taarifa hiyo, mabalozi hao wakiwemo Robert Godec wa Marekani, Susie Kitchens wa Uingereza na Jutta Jardfelt wa Ujerumani, wametoa wito kwa wadau kuheshimu uhuru wa tume hiyo ya uchaguzi na kuiacha ifanye kazi yake bila kuingiliwa. Wafuasi wa upinzani Kenya waandamana Jaji Maraga: Hatuogopi chochote Mapema leo, wafuasi wa muungano wa upinzani National Super Alliance walitawanywa na polisi walipojaribu kuandamana nje ya afisi kuu za IEBC, Nairobi kushinikiza mabadiliko katika tume hiyo. Balozi wa Marekani nchini Kenya Bob Godec amesema juhudi za chama tawala kutaka kurekebisha sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo "zinazidisha wasiwasi na uhasama wa kisiasa". Kadhalika, ameushutumu upinzani kwa kutishia kususia uchaguzi huo. Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesisitiza kwamba "hakutakuwa na uchaguzi" iwapo maafisa ambao anadai walihusika katika kuvuruga uchaguzi uliopita hawataondolewa kwenye tume hiyo. Wafuasi wa Rais Uhuru Kenya wamekuwa wakidai mahakama iliwapokonya ushindi "Hii ni fursa kwa pande zote mbili kuonyesha sifa za uongozi bora, kuimarisha demokrasia ya Kenya na kuinua hadhi ya taifa hili kimataifa. Inasikitisha kwamba kwa sasa mambo yanaonekana kutokea kinyume," alisema Bw Godec. Majaji wa Mahakama ya Juu walipokuwa wakifuta matokeo ya uchaguzi wa awali walisema haukuwa wa wazi na kwamba ilikuwa vigumu kubaini nani alishinda kwa njia halali. Waliiamuru IEBC kuandaa uchaguzi wa marudio na kufuata kikamilifu katiba na sheria za uchaguzi. Majaji hao walisema hawatasita kufuta tena matokeo ya uchaguzi iwapo uchaguzi mpya hautaandaliwa kwa kufuata katiba na sheria za uchaguzi. Upinzani Nasa umetishia kuandaa maandamano kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza mageuzi katika IEBC. Mabalozi wa nchi za Magharibi wamewashutumu viongozi wa upinzani na viongozi wa serikali nchini Kenya huku nchi hiyo ikiendelea kujiandaa kwa maruduo ya uchaguzi wa urais baadaye mwezi huu. text: La hasha. Hapa tunaangazia baadhi ya mambo matano ambayo huenezwa sana na watu lakini si ya kweli. 1. Jua ni bonge la moto Huwa na joto la kiwango cha juu sana (nyuzi 15 milioni katika kitovu chake), lakini je huwa ni bonge moja kubwa la moto? La hasa. Huwa limeundwa kwa gesi. Kwa uzani, huwa ni haidrjeni asilimia 75 na asilimia 25 helium. Huwa kuna madini kadha ya chuma lakini huwa ni chini ya asilimia 0.1 ya uzito wake. Joto lake hutokana na shughuli ya kemikali karibu sawa na inayotumiwa kuzalisha kawi katika baadhi ya vinu vya nyuklia, kwa Kiingereza 'nuclear fusion'. Atomu za haidrojeni hugongana kwa nguvu na kasi sana na kuzalisha atomu za helium. 2. Utalipuka ukisafiri anga za juu bila vazi maalum Ni uvumi unaoenezwa, hasa kupitia filamu za kale, Kwamba naitrojeni kwenye mwili wako inaweza kupanuka na ufure kiasi kwamba mwishowe unalipuka na kufariki. Ngozi yako huwa na nguvu sana kiasi kwamba hauwezi kulipuka kutokana na hilo. Hata hivyo kuna hatari nyingine huko zikiwemo kiwango cha joto na miali nururishi hivyo ni lazima uvalie vazi kama hilo. 3. Kiumbe wa kwanza kuzuru anga za juu alikuwa mbwa Laika, mbwa koko aliyepatikana katika barabara za Moscow, alikuwa mbwa aliyependwa sana urusi baada yake kusafiri anga za juu akiwa kwenye chombo cha Sputnik mwaka 1957. Hata hivyo, hakuwa kiumbe wa kwanza kusafiri anga za juu. Mwenye rekodi hiyo ni nzi wa matunda. Nzi kadha walitumwa anga za juu na wanasayansi kutoka Marekani mwaka 1947 kuwasaidia kufahamu kuhusu athari za miali nurusishi. 4. Wana anga za juu huelewa kutokana na kuwa mbali na Dunia? Huyu ni Mae C. Jemison, aliyepigwa picha mwaka 1992 akiwa kwenye chombo cha anga za juu kwa jina Endeavour. Pengine umezitazama video za wana anga kama vile Tim Peake wakielewa angani katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS), na huenda ulifikiria kwamba hilo linatokana na hali kwamba wako mbali sana na nguvu mvuto ya Dunia. Hata hivyo, asilimia 90 ya nguvu hizo za Dunia hufika ISS. Hivyo basi mbona wanaelea? Ni kwa sababu ya jambo linalofahamika kama 'free fall'. Hii huwa na maana kwamba kwenye eneo ombwe au tupu (lisilo na chochote) vitu huanguka kwa kasi sawa, bila kujali uzito wake. Wana anga hao kwa hivyo huwa wanaanguka kuelekea kwenye Dunia kwa kasi sawa na chombo walichomo ndani yake, lakini chombo hicho huwa kinasonga hivyo wanasonga pia. Ndio maana huwa wanaonekana kama wanaelea. 5. Kuna sehemu ya Mwezi yenye giza Ni kweli, kuna sehemu ya Mwezi ambayo huwa ni giza totoro. Hata hivyo, si kweli kwamba sehemu hiyo huwa na giza wakati wote. Mwezi huwa na mchana na usiku sawa na inavyofanyika duniani kwa kila sehemu, ingawa tofauti ni kwamba mchana na usiku kwenye Mwezi huwa ni kipindi cha wiki mbili hivi. Mwana huu, China ilituma chombo cha kupeleleza yanayotoea sehemu ya mbali zaidi ya Mwezi ambayo huwa na giza. Picha za kwamba zilizoonyesha kwamba kuna sehemu ya mwezi huwa na giza zilipigwa mwaka 1959. Jua huwa na joto sana, kwa hivyo linafaa kuwa na moto mkali. Wanaosafiri anga za juu huwa wako mbali sana na Dunia, kiasi kwamba huwa hawahisi nguvu mvuto zozote. Ni kweli? text: Bw Korir amekuwa akijibu maswali kuhusu ni nani ambaye bado yuko nchini Brazil: Mkimbiaji wa mbio za Marathon, Wesley Korir, ambaye pia ni mbunge, amepakia picha za hoteli anayosema ni duni kwenye mitandao ya Twitter na Facebook akilalamika. "Timu iliyoongoza Afrika na timu ya pili dunia nzima katika riadha, na hivi ndivyo tunavyotunzwa ," ameandika. Amelinganisha mazingira ya eneo wanamoishi na mtaa wa mabanda. Wanariadha hao walilazimika kuondoka eneo la kifahari waliomoishi wanamichezo wakati wa michezo hiyo, ambalo hufahamika kama Kijiji cha Olimpiki, baada ya eneo hilo kufungwa kufuatia kumalizika kwa michezo. Wesley Korir ametoa wito ufanyike uchunguzi kuhusu utawala wa timu ya Kenya wakati wa michezo na baada ya michezo Kwenye mtandao wake wa Twitter, alisema: "Na hivi ndivyo mambo yanavyoendelea Rio #TeamKenyaa @UKenyatta haya ndiyo makazi ya timu ya kenya kwa usiku wa leo!!" Bw Korir amekuwa akijibu maswali kuhusu ni nani ambaye bado yuko nchini Brazil Alipoulizwa ni kwa nini anadhani timu ya wanariadha bado iko mjini Rio, alisema huenda wasimamizi wa Olimpiki Kenya walisubiri kuwanunulia wachezaji tiketi nafuu, na ndipo wakaamua kuwaweka muda zaidi Rio. Bw Korir kabla ya kwenda Rio Mbunge huyo wa Kenya ametoa wito uchunguzi ufanyike kuhusu usimamizi wa timu ya Kenya wakati wa michezo na baada ya michezo baada ya kutokea kwa hitilafu mbali mbali, ikiwemo kutonunuliwa kwa tiketi ya mwanamichezo maarufu mshindi wa dunia katika mchezo wa kurusha mkuki Julius Yego. Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakiishi kwenye makazi ambayo hayawafurahishi timu hiyo baada ya kumalizika kwa Michezo ya Olimpiki mjini Rio, mmoja wa wanariadha hao amelalamika. text: Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Dokta Amos Nungu amesema taarifa ya utafiti huo haikuwafikia Barua hiyo kuhusu kulitaka Twaweza litoe maelezo ndani ya siku saba kuhusu utafiti ulioifanya wa Sauti za Wananchi bila ya kibali, ambao umeonesha pia kushuka kwa uungaji mkono wa wananchi kwa wawakilishi waliowachagua. Twaweza: Umaarufu wa Rais Magufuli umeshuka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Dokta Amos Nungu amesema wameshangazwa kuona mawasiliano halali ya kiofisi yamesambazwa mitandaoni hata kabla ya kupata majibu rasmi. Matokeo hayo ya utafiti, ndiyo yaliyoifanya Tume ya Sayansi na Teknolojia, ambayo ndiyo yenye jukumu la kuratibu, kufanya tathmini na ufuatiliaji wa tafiti, kuiandikia barua taasisi hiyo ya TWAWEZA, inayoonesha pia kwamba taasisi hiyo awali iliwasilisha maombi ya vibali vya kufanya utafiti nchini, lakini utafiti huo wa Sauti ya Wananchi haukujumuishwa. Maelezo ndani ya barua hiyo imeitaka taasisi hiyo pia kutoa maelezo ndani ya ndani ya siku Saba. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti ya TWAWEZA ''Mtafiti akija kutoa matokeo ya utafiti kwenye vyombo vya habari pia tunaona kuwa utafiti ulifanyika, huu utafiti tunakiri kuwa hatuna taarifa yake sababu mtafiti anaposajiliwa mwishoni anapoondoka na taarifa zake lazima ripoti ibaki COSTECH.Tumewaomba wiki moja watupe maelezo'' Dokta Amos Nungu, Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia. Wakenya wakasirishwa na safari ya wabunge Urusi Kwa Picha: Magufuli akutana na marais wa zamani, na Lowassa Na kuhusiana na hatua gani watakazochukua juu ya mawasiliano hayo ya ndani kusambaa mitandaoni, amesema hilo ni jukumu la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. ''tume inasikitika kuwa mawasiliano halali ya kiofisi yanapelekwa mitandaoni tumeziachia mamlaka kufanya kazi yake''.Alieleza Dokta Nungu TWAWEZA imekiri kupokea barua kutoka COSTECH ''tumeipokea na tunaifanyia kazi. Twaweza haijasambaza, na haihusiki na usambazaji wa barua hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Barua yoyote inayofika Twaweza inagongwa muhuri wa kupokelewa mbele ya mjumbe aliyeleta barua hiyo. Barua inayosambaa mtandaoni hatuitambui kwa sababu haina muhuri wetu wa kuipokea Twaweza. Tunaheshimu na kuthamini sana mawasiliano yetu na wadau wetu''Alieleza Aida Eyakuze Mkurugenzi mtendaji wa TWAWEZA Hatua ya COSTECH kuhoji uhalali wa ripoti ya TWAWEZA imezua mjadala mkali mitandaoni nchini Tanzania. COSTECH pekee ndio chombo cha kutoa ushauri katika masuala yote yanayohusu sayansi, teknolojia na uvumbuzi na moja ya majukumu yake ni kusajili na kutoa vibali vya tafiti zote za muda mfupi na mrefu zinazofanywa nchini. Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania ( COSTECH) imesikitishwa na kuvuja mitandaoni kwa mawasiliano ya barua iliyoiandikia Taasisi ya utafiti isiyo ya Kiserikali ya TWAWEZA. text: Bw Trump ametoa wito wa kuimarishwa kwa ulinzi mpakani Amefanya hivyo kupitia msururu wa ujumbe kwenye Twitter. "Mtu anapoingia ndani, ni lazima mara moja, bila majaji na kesi mahakamani, tuwarejeshe walikotoka," Trump ameandika. Amesema hayo siku chache baada yake kubatilisha sera ya kuwatenganisha watoto wa wahamiaji na wazazi wao baada ya sera hiyo kushutumiwa vikali Marekani na nje ya nchi hiyo. Takwimu zinaonesha watoto 2,300 walikuwa wametenganishwa na wazazi wao kati ya Mei na Juni mwaka huu. Kuanzia mwezi Mei, wahamiaji wanaovuka mpaka wa Marekani na kuingia nchini humo kinyume cha sheria wanakabiliwa na hatari ya kufunguliwa mashtaka ya jinai chini ya sera ya Trump ya kutowavumilia wahamiaji. Rais Trump hajatofautisha kati ya wahamiaji wa kiuchumi na wale wanaotafuta hifadhi kutokana na mateso na kudhalilishwa mataifa yao. Rais huyo amekuwa akishutumiwa hata na viongozi wa chama chake cha Republican kwa lugha kali aliyoitumia kwenye Twitter. Aliposema awali kwamba wahamiaji wanatishia "kufurika na kuiambukiza nchi yetu, mbunge mwanamke wa chama cha Republican Ileana Ros-Lehtinen alimjibu kwenye Twitter akisema tamko lake halina msingi, "linakera" na linadunisha wale wanaotafuta maisha mazuri. Maafisa wa uhamiaji Marekani wanasema watoto 2,342 walitenganishwa na wazazi 2,206 kati ya 5 Mei na 9 Juni. Mnamo 20 Juni, Trump aililegeza msimamo wake wa kuunga mkono sera hiyo kali na badala yake akatia saini agizo la rais la kusitisha hatua hiyo ya kuzitenganisha familia. Bw Trump amesema sheria za uhamiaji za Marekani kwa sasa ni za "mzaha" Alisema wakati huo: "Huwa sipendi kuona au kusikia familia zikitenganishwa." Agizo la Rais Trump linaruhusu kuzuiliwa kwa muda mrefu kwa watoto wa wahamiaji (ingawa wakiwa na watoto wao), jambo ambalo wengi wanasema linaenda kinyume na sheria za taifa ambazo haziruhusu watoto kuzuiliwa kwa zaidi ya siku 20. Baada ya kuchaguliwa kwa Rais Trump mwaka 2016, idadi ya wahamiaji waliozuiliwa au kuzuiwa kuingia Marekani kwenye mipaka yake ilikuwa imeshuka pakubwa. Hata hivyo tangu Februari 2018, idadi ya wahamiaji wanaovuka mpaka kinyume cha sheria imeongezeka pakubwa. Idadi ya waliokamatwa mwezi uliopita ni zaidi ya maradufu ya idadi ya wahamiaji waliokamatwa Mei 2017. Ingawa huwa vigumu kuhesabu idadi ya wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria, idadi ya wanaokamatwa mipakani hutumiwa kama kiashiria cha idadi ya wanaovuka na kuingia Marekani kinyume cha sheria. Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa kuharakishwa kwa shughuli ya kuwatimua wahamiaji haramu nchini humo bila hata kufuata utaratibu wa mahakama. text: Viongozi wa upinzani baada ya kikao cha Azimio la Zanzibar kilichoazimia kupinga muswada huo mahakamani. Shauri hilo, lilifunguliwa na muungano wa vyama 10 vya upinzani wakidai unakiuka haki za Kikatiba za kisiasa kwa kuzifanya shughuli mbalimbali za kisiasa kuwa jinai. Wanasiasa hao wanadai muswada huo unampa mamlaka makubwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia mambo ya ndani ya vyama hivyo ikiwemo uchaguzi wa viongozi na kusimamisha uanachama kwa wanachama wa vyama hivyo. Pia walikuwa wanapinga kifungu cha 8 (3) cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi kinachozuia muswada uliowasilishwa bungeni kupingwa mahakamani. Hata hivyo, Jaji Benhajj Masoud kayika maamuzi yake leo amekubaliana na upande wa serikali walalamikaji hawakupaswa kuomba Mahakama itamke kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Haki za Msingi na Wajibu kinakiuka Katiba na kuomba mahakama itamke kuwa muswada huo unakiuka katiba. Jaji Masoud amesema kwamba shauri hilo linakiuka kifungu cha 8 (2) cha Sheria ya Haki za Msingi na Wajibu, kwani hawakufuata utaratibu unaoelekezwa katika kifungu hicho. Kifungu hicho kinaelekeza mtu yeyote anayedai haki zake zinakiuka au zinaelekea kukiukwa anapaswa kutafuta nafuu kwa kutumia njia nyingine zilizopo kwanza kabla ya kwenda mahakamani. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la Tanzania wakati wa usikilizwaji wa pingamizi hilo jopo la mawakili wa Serikali, likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Mark Mulwambo lilidai kuwa walalamikaji hawakukidhi matakwa ya kifungu hicho kwani hawakutumia njia nyinginezo zilizopo kabla ya kukimbilia mahakamani. Walibainisha kwamba mlalamikaji wa kwanza, Zitto ni mbunge tena mzoefu ambaye anazijua Kanuni za Bunge zikiwemo za mwaka 2016 ambazo zinampa nafasi kushiriki kujadili muswada wowote na kutoa maoni na mapendekezo yake kwa uhuru na zinampa kinga. Walidai kuwa pia kanuni hizo zinampa mamlaka ya kumuomba Spika aisimamishe kwa muda maalum upitishwaji wa muswaada huo ili kumpa nafasi kuwasilisha maoni yake. Hata hivyo waliiambia mahakama kuwa walalamikaji hawakutumia utaratibu huo kabla ya kwenda mahakamani. Mlalamikaji wa kwanza Zitto Kabwe baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa watarudi mahakamani kuendelea na shauri hilo. Vipengele tata Tayari mswada huo umeshawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, lakini je ni mambo gani hasa yanayolalamikiwa kwenye muswada huo? Kifungu cha 5A kinataka msajili kupewa taarifa kimaandishi na taasisi yeyote ya ndani ama ya nje ya Tanzania itakapotaka kutoa mafunzo ya kiraia ama ya kujenga uwezo kwa chama cha siasa na kutaja wahusika, malengo na nyenzo zitakazotumika katika mafunzo hayo. Msajili anayo nguvu ya kutoa kibali ama kukataa kufanyika kwa mafunzo hayo na endapo yatafanyika bila kibali taasisi hiyo inaweza kupigwa faini ya mpaka shilingi milioni 30 na watu watakaokutwa na hatia ya kwenda kinyume ni kifungu hicho wanaweza kufungwa kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja gerezani. Kifungu cha 5B cha muswada kinampa nguvu, msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania kuomba na kupewa taarifa yeyote ile ya chama chochote cha siasa. Afisaa yeyote wa chama cha siasa ambaye ataenda kinyume na takwa hilo, yaani kutokutoa taarifa husika atakuwa ametenda kosa na akikutwa na hatia atapigwa faini ya kuanzia shilingi milioni moja mpaka kumi au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi 12. Hata baada ya adhabu hiyo, afisaa huyo ama chama hicho bado kitatakiwa kutoa taarifa zilizohitajika na iwapo taarifa itaendelea kumininywa basi chama hicho kinaweza kusimamishwa ama kufutiwa usajili. Wapinzani Tanzania wanadai iwapo kifungu hicho kitapita, mipango yote ya kimkakati ya vyama vya siasa itakuwa wazi na inaweza kutumiwa na serikali katika kuwaminya. Hoja yao kuu ni kwamba msajili ni mteule wa rais, ambaye ni mwanachama pia wa chama tawala. Hivyo ofisi ya msajili inaweza kutumika dhidi yao. Kifungu cha 6 cha muswada kinamlinda msajili na wanyakazi wa ofisi yake dhidi ya kufunguliwa mashtaka: "Shauri lolote halitafunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi ama maafisa wengine chini ya Msajili kwa lolote watakalolifanya ama kutolifanya kwa nia njema chini ya sharia hii," kinasomeka kifungu hicho. Mahakama nchini Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na vyama vya upinzani nchini humo kupinga Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018. text: Mpango huo unaofanikishwa na Mradi wa wafungwa barani Afrika kwa ushirikiano na chuo kikuu cha London na unanuia kuwapa wafungwa fursa ya kushiriki kikamilifu katika taratibu za kutafuta haki. Kuhitimu kwa watatu hao kutoka Gereza Kuu la Luzira kumetazamwa kama ishara ya mwamko mpya katika mfumo wa marekebisho magerezani Uganda. Pascal Kakuru, Suzzan Kigula na Moses Ekwam walipokea shahada za digree huku wakiwa wamevalia sare nyeusi za kuhitimu. Moses Ekwam mmoja wa waliohitimu alikuwa anatumikia kifungo cha miaka mitano lakini alihudumu miaka minne baada ya kupatwa bila hatia. Kwa miaka hiyo minne alipokuwa gerezani alianza kusomea somo la sheria. Ekwam kwa hivi sasa ni mwendesha mashtaka wa jeshi la Uganda. "Mimi nilikuja hapa nikaona mimi kukaa hapa kuangalia mpira niliona shule iko ndani kwa hivyo nikaamua kujiunga na shule A level nikapita vizuri 210 hadi sasa hivi hadi sasa hivi niko wakili," aliambia BBC. Mwenzake Pascal alikuwa akitumikia kifungo kwa makosa ya uhaini na hivi sasa anaelekea kumaliza kifungo chake baada ya kupata msamaha. Anaeleza anapolenga kutumia utaalamu wake katika sheria "Ninao mpango wa kuzungumzia wale watu wanaoteseka wale watoto, kinamama, wafungwa wakimbizi ni watu hodari sana huwezi kuwaongelea wawe kama wanaharakati watu kama hao. "Kutakuwa na ulimwengu vitu kadhaa vya watu kama hao kwa hivyo nina mpango wa kuwazungumzia mahali popote wapo si kwa nchi ya Uganda peke yake bali ulimwengu mzima popote nitakapopata nafasi ya kuwasaidia watu kama hao. " Katika ripoti ya hivi karibuni Jarida la Afrika la masuala ya uhalifu na haki, idara ya magereza nchini Uganda imewekwa katika nafasi ya kwanza barani Afrika kwenye suala la mageuzi. Hata hivyo bado kuna changamoto katika kuzingatia haki za wafungwa. Owinyi Dollo ni naibu wa jaji mkuu nchini Uganda: "Unaanza kujiuliza kweli kama huku ya kifo inapaswa kuwa katika sheria zetu, unahoji kwa sababu mtu ambaye alivunja sheria jana anaweza kubadirika na kuwa mtu mwenye ushawishi mwema leo." Kwa kuhitimu wafungwa hao watatu wanafuata nyayo za rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela aliyejiimarisha kitaaluma wakati akiwa gerezani jambo linalowapa matumaini wafungwa wengi na pia kuongeza mskumo wa mageuzi zaidi magerezani. Nchini Kenya, wafungwa wamewahi kusomea sheria na kuhitimu na baadhi hata kuwasaidia wenzao kupata uhuru. Peter Ouko, mmoja wao, kwa sasa ni balozi wa shirika la Africa Prisons Project. Alikuwa amehukumiwa kifo na kuwa mfungwa kwa miaka kumi na minane kabla ya kupunguziwa kifungo na kuwa kifungo cha maisha na kisha kuachiliwa huru kwa msamaha wa rais. Alikuwa amepatikana na kosa la kumuua mkewe. Wafungwa watatu walisomea gerezani wamehitimu na shahada za digrii katika sheria, ikiwa ni mara ya kwanza kwa wafungwa nchini Uganda kufuzu na shahada ya uanasheria. text: Donald Trump (kushoto) na Benjamin Netanyahu wakiwa na wake zao uwanja wa ndege wa Tel Aviv "Iran haitaruhusiwa kamwe kumiliki silaha za nuklia," Trump aliwaambia waandishi wa habari. Alisafiri kutoka nchini Saudi Arabia, mshirika mkubwa wa Marekani ambapo alitoa hotuba kwa viongozi wa kiislamu. Bw Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina katika kipindi cha siku mbili atakazokuwa eneo hilo. Trump alizuru ukuta wa magharibi ambalo ni eneo takatifu Rais huyo amesema kupatikana kwa mkataba wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina yatakuwa mafanikio makubwa, lakini hakusema mkataba kama huo unafaa kuchukua mwelekeo gani. Amesema angependa sana pande zote mbili ziamue kuhusu mkataba huo wa amana kwa mashauriano ya moja kwa moja. Katika mkutano mkuu wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu mjini Rihadh siku ya Jumapili, Bw Trump aliwataka viongozi hao kuwa kwenye mstari wa mbele katika kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu na wapiganaji wenye itikadi kali na "kuwafurusha kutoka kwenye dunia hii." Aliitaja moja kwa moja Iran na kusema kwamba imekuwa "ikichochea mizozo ya kidini na ugaidi" katika kanda hiyo kwa miongo mingi. Bw Trump pia alikariri tena kwamba anaamini amani kati ya Waisraeli na Wapalestina inaweza kupatikana. Rais huyo wa Marekani amekuwa akichukuliwa sana kuwa muungaji mkono mkubwa wa Israel kuliko mtangulizi wake Barack Obama. Iran ikionyesha silaha zake Amechukua msimamo usio mkali kuhusu suala tata la Israel kujenga makazi ya walowezi maeneo ya Wapalestina na kudokeza kwamba upanuzi wa makao hayo na si kuwepo kwa makao yenyewe, unaweza kuwa ndio kikwazo katika kutafuta amani. Zaidi ya Wayahudi 600,000 huishi katika makao makazi 140 ya walowezi ambayo yamejengwa tangu Israel ilipotwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem mwaka 1967, maeneo ambayo Wapalestina huyachukuliwa kuwa sehemu ya "taifa litakaloundwa" la Wapalestina. Trump akihutubu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Ben Gurion eneo la Lod, nje ya mji wa Tel Aviv Makazi hayo ni haramu chini ya sheria za kimataifa, lakini Israel hupinga hilo. Rais huyo pia ametoa ishara za kukanganya kuhusu mji wa Jerusalem, na kuahidi kuhamishia ubalozi wa Israel mjini humo kutoka Tel Aviv, hatua iliyowakera Wapalestina lakini ikawafurahisha sana Waisraeli. Hata hivyo, baadaye alionekana kulegeza msimamo huo, na Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson majuzi aliambia NBC News kwamba Bw Trump bado analitafakari jambo hilo. Mzozo kuhusu Jerusalem Israel huuchukulia mji wote wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu, nao Wapalestina huchukulia maeneo ya mashariki ya mji huo kuwa makao makuu yake. Jamii ya kimataifa haijatambua umiliki wa Israel wa mji wa Jerusalem na mataifa mengi yana afisi za kibalozi mjini Tel Aviv. Kumekuwa na wasiwasi kidogo Israel kabla ya ziara ya Bw Trump kutokana na baadhi ya matamshi ya maafisa wake. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepuuzilia mbali maneno ya Bw Tillerson kwamba kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani kunaweza kuathiri shughuli ya kutafuta amani eneo hilo. Afisa wa kibalozi wa Marekani naye aliwakera Waisraeli aliposema kuwa Ukuta wa Magharibi, moja ya maeneo matakatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi haumo "katika maeneo yenu (Waisraeli) bali ni sehemu ya Ukingo wa Magharibi". White House baadaye ilisema tamko la afisa huyo wa kibalozi "hayawakilishi msimamo wa Marekani". Bw Trump na mkewe Melania walakiwa na Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud (kulia) baada ya kuwasili Saudi Arabia Ziara ya Bw Trump inajiri siku chache baada ya taarifa kusema Bw Trump alifichua taarifa za siri kwa Warusi ambazo huenda zilitoka kwa mdokezi kutoka Israel. Kisa hicho kimeibua maswali kuhusu usiri na usalama wa habari za kijasusi zinazokabidhiwa Marekani na Israel. Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea kabla ya ziara ya Bw Trump, ambaye anatarajiwa kukutana na Bw Netanyahu mjini Jerusalem Jumatatu na baadaye akutane na kiongozi wa Wapalestina Mahmoud Abbas mjini Bethlehem Jumanne Ajenda ya ziara ya Trump Bw Trump pia atazuru Brussels, Vatican, naSicily. Ziara hiyo imegubikwa na mtafaruku wa kisiasa nchini mwake, sana kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa FBI James Comey. Rais wa Marekani Donald Trump ameanza ziara yake nchini Israel kwa kuonya kuwa kuna tisho kutoka nchini Iran ikiwa itamiliki silaha za nuklia. text: Hata hivyo Achilles alitabiri sawa Iran kuishinda Morocco, Urusi kuishinda Misri na Brazil kuishinda Costa Rica. Achilles, anayeishi makavazi ya Hermitage ya mji St Petersburg, aliwekwa tayari kwa wapiga picha na kuletewa sahani mbili za chakula, moja kikiwa na bendera ya Nigeria na nyingine ya Argentina kuwekwa mebele yake. Paka huyo wa rangi nyeupe ambaye ni kiziwi, hubashiri mshindi kwa kuchagua moja kati ya bakuli mbili ambazo zimewekwa bendera za mataifa yanayocheza. Paka huyo ni miongoni mwa paka wanaofugwa kukabiliana na panya katika makumbusho ya Hermitage mjini St Petersburg, ingawa sasa ana majukumu hayo mapya. Paka huyo ni miongoni mwa paka wanaofugwa kukabiliana na panya katika makumbusho ya Hermitage mjini St Petersburg Baada ya muda mfupi Achilles alichagua sahani ya Nigeria na kwa pupa akala chakula kilichokuwa sahani ya bendera ya Nigeria, ishara kuwa Nigeria ingeishinda Argentina. Hata hivyo Achilles alitabiri sawa Iran kuishinda Morocco, Urusi kuishinda Misri na Brazil kuishinda Costa Rica. Licha ya Achilles kutabiri ushindi wa Nigeria dhidi ya Argentina, Nigeria ilibanduliwa kutoka mashindano baada ya kushindwa kwa mabao mawili kwa mamoja na Argentina. Paka huyo ni kati ya wanyama wanajaribu uwezo wao wa kutabiri matokeo ya kombe la Dunia wakiwemo wengine huko Kaliningrad, Yekaterinburg na Sochi. Wana matumaini ya kumuiga Paul the octopus ambaye alipata umarufu duniani wakati alitabiri vyema matokeo ya mechi zote za Ujerumani kwenye mechi za Kombe Dunia za mwaka 2010 na kuchagua Uhispania kama mshindi. Achilles ni kati ya wanyama wanajaribu uwezo wao wa kutabiri matokeo ya kombe la Dunia wakiwemo wengine huko Kaliningrad, Yekaterinburg na Sochi. . Paka Achilles aliyetabiri vyema matakeo ya mechi zote tatu katika mashindano ya dunia alinoa alipotabiri kuwa Nigeria ingeishinda Argentina wakati kabla ya timu hizo kukutana jana Jumanne lakini Argentina waliwashinda Nigeria kwa mabao 2-1. text: Iran releases video which it claims show its drone still flying Televisheni ya taifa imesema inaonyesha meli za kivita katika eneo hilo, na zilipigwa picha na ndege hiyo hiyo baada ya muda ambao Marekani ilitangaza kuwa ilidungua ndege hiyo. Pamoja na Iran kukana, raisi wa Marekani, Donald Trump amesema ''hakuwa na shaka'' ndege isiyo na rubani ilidunguliwa. Picha za video zinaonyesha nini? Video inaonyesha picha za rangi nyeupe na nyeusi za meli za kivita zikitembea ndani ya maji, ikionyesha muda, tarehe na eneo la kijiografia. Marekani imesema imeidungua ndege isiyo na rubani ya Iran Iran yakamata meli ya mafuta Ghuba Televisheni ya taifa ya Iran imesema kuwa picha hizo zilichukuliwa na ndege isiyo na rubani inayodaiwa kudunguliwa wakati ikiwa angani usawa wa karibu na meli ya kijeshi ya Marekani. Meli ya kijeshi ya Marekani Jeshi la Iran, ambalo lilichapisha picha za video, limesema picha hizo zilirekodiwa ''kabla na hata baada ya Marekani kutoa madai hayo'' Lakini picha hizo zina mashaka, anasema mwandishi wa masuala ya kidiplomasia Paul Adams. Anasema baadhi ya picha zinaonekana kupigwa picha na helikopta ya Iran ambayo ilikuwa pia kwenye eneo hilo. Marekani inasemaje? Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua ya ulinzi'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho. ''Ndege hiyo ilishambuliwa mara moja..baaa ya kupuuza wito wa kusimama. Iran haraka ilitupilia mbali madai ya Trump, huku afisa mmoja wa juu akisema kuwa huenda walilenga ndege yao wenyewe kimakosa. ''Nina wasiwasi kuwa Marekani iliishambulia ndege yao wenyewe kimakosa! ''Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran. Abbas Araqchi aliandika kwenye ukurasa wa tweeter siku ya Ijumaa. Iran imetoa picha kwenye vyombo vya habari ikikana madai ya Marekani kuwa imedungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la Ghuba. text: India kuwasafirisha raia wake waliokwama Qatar Shirika linalomilikiwa na serikali ya India shirika la binafsi la Jet Airways, yatafanya safari zaidi Alhamisi, kwa mujibu wa serikali. Nchi kadha za kiarabu zikiwemo Saudi Arabia na Misri zimekata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar na kuishutumu kwa kuvuruga eneo hilo. Raia wa India ndio wahamiaji wengi zaidi nchini Qatar. Hatua hiyo inakuja baada ya waziri wa usafri wa ndege nchini India Ashok Gajapathy Raju, kufanya mazungumzo na waziri wa mashauri ya kigeni Sushma Swaraj na kumhakikishia kuwa safari zitaongezwa kuwaruhusu raia wa India ambao hawajafanikiwa kupata tiketi kurudi nyumbani. Taarifa ya serikali ilisema kuwa shirika la India Air, litafanya safari zaidi kati ya mji wa kusini wa Trivandrum na Doha kutoka kuania Juni 25 na terehe 8 Julai huku shirika la Jet Airways likifanya safari kati ya Mumbai-Doha-Mumbai kati ya tarehe 22 na 23 mwezi Juni. Mashirika mawili ya ndege yataanza kufanya safari zaid kuenda mji mkuu wa Qatar Doha kuwasaidia raia wa India waliokwama nchini humo kurudi nyumbani. text: Mwenyekiti kamati ya mambo ya nje Tom Tugendhat amesema kuwa tukio la kuvuja kwa barua pepe hizo si jambo dogo, na yeyote aliyehusika lazima ashtakiwe. ''Wanadiplomasia lazima waweze kuwasiliana katika hali ya usiri'' aliiambia BBC. Ofisi ya mambo ya nje imesema kuvuja kwa barua pepe siku ya Jumapili ni jambo ''ufitini'' lakini hakukana kuhusu ukweli wa barua pepe hizo. Ikulu ya Marekani haijasema lolote kuhusu kilicho kwenye barua hizo, lakini barua hizo huenda zikaleta mushkeli kwenye mahusiano kati ya Marekani na Uingereza. Trump akutana na Kim kwenye mkutano wa kihistoria Trump adaiwa kumbaka mwandishi Katika ujumbe wa barua pepe, Balozi wa Uingereza Kim Darroch amesema Ikulu ya Marekani ''haiwezi kufanya kazi ipasavyo'' na ''imegawanyika'' chini ya utawala wa Trump. ''Hatuamini kama utawala huu utakuwa sawasawa'': ''haifanyi kazi ipasavyo; ina mgawanyiko; haina ustadi katika kushughulikia masuala kidiplomasia'', alisema. Amehoji kama kuna siku Ikulu ya Marekani ''itakuwa na uwezo''. Bwana Tugendhat ameiambia BBC kuwa kitendo cha kuvuja kwa barua pepe hizo kichunguzwe- lakini alimtetea Bwana Kim. Kazi ya balozi wa Uingereza ni kutetea maslahi na matakwa ya watu wa Uingereza'' na si masuala ya Marekani'', alisema. Ingawa Bwana Kim alisema Trump ''alishangazwa'' na ziara yake nchini Uingereza mwezi Juni, balozi alisema utawala wake utaendelea kuwa wa kujipendele wao: ''Hii ni ardhi ya Marekani kwanza''. Tofauti kati ya Marekani na Uingereza kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, uhuru wa vyombo vya habari, na hukumu ya kifo, ni vitu vitakavyojitokeza wakati nchi hizo zikitafuta kuimarisha mahusiano ya biashara baada ya Brexit, barua pepe hizo zimeeleza. Kiongozi anayeunga mkono mpango wa Brexit, Nigel Farage, amemkosoa bwana Kim kutokana na alichokiandika, akisema kuwa balozi huyo ''hafai kabisa kwa kazi hiyo'' akisema ''Ni vyema iwapo ataondoka mapema''. Hatahivyo, Waziri wa sheria David Gauke anasema ni muhimu kwa wanadiplomasia kueleza ''ukweli na kutoa ushauri wa wazi na kweli kwa nchi yao''. Alisema: ''Si jambo jema kuwa barua pepe zimevuja, lakini tutegemee mabalozi wetu kutuambia ukweli kwa namna wanavyouona.'' Mamlaka zimeanza kufanya uchunguzi kuhusu barua pepe zilizovuja zilizotoka kwa Balozi wa Uingereza mjini Washington ambayo imedai kuwa utawala wa Trump si ''stadi'' text: NTV, Citizen na KTN zilifungwa kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha matangazo ya moja kwa moja ya kuapishwa kwa Raila Odinga Lakini bado haviwezi kutazamwa na Wakenya wengi ambao hawana king'amuzi. Kupitia mtandao wao wa Twitter, NTV wamesema wamerudi hewani kwenye ving'amuzi vya "Dstv, GoTV and Zuku baada ya kufungiwa na serikali." Stesheni ya iliyokuwa mmojawapo zilizoathirika na hatua ya serikali ,Citizen TV bado haijafunguliwa. Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja matangazo sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama rais licha ya onyo kutofanya hivyo. Vituo vya habari vilifungiwa lakini wakaendelea kurusha matangazo kupitia mtandao Awali, wanaharakati waliokuwa wakiandamana kuishinikiza serikali kuvifungua vituo hivyo, walitawanywa na polisi kwa kutumia gesi ya kutoa machozi "Hii si mara ya kwanza tumiona serikali ya Jubilee ikiangamiza haki za waandishi wa wahabari. Tumeona ikifanyika kwa muda mrefu" Tom Oketch mmojawapo wa waandalizi wa maaandamano hayo ameiambia BBC . "Hawa heshimu sheria, hawa heshumi katiba, wananchi wa Kenya hawatawaruhusu kuturidisha katika enzi za Jomo Kenyatta, enzi za Moi, tutapigana nao mpaka mwisho" ameelezea Tom. Wiki iliyopita,Mahakama Kuu nchini humo iliamuru kuwashwa kwa vituo vya habari hivyo vitatu na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu. Matangazo ya vituo viwili vya televesheni Kenya, KTN na NTV yamerejea hewani baada ya kufungiwa siku 7 na serikali. text: Mkeketaji Kenya aonyesha wembe anaoutumia kuwakata wasichana Serikali inasema huu ni uwekezaji mkubwa wa kipekee kufikia leo duniani katika kusaidia kusitisha ukeketaji kufikia mwaka 2030. Ukeketaji ni utamaduni unaohusisha kukatwa kwa sehemu ndogo au nzima ya sehemu za siri za mwanamke, baadhi wakifanya kama sehemu ya utamaduni wa mtoto kuingia ukubwani. Shirika la misaada la ActionAid limekaribisha msaada huo lakini limeongeza kwamba kulenga ukeketaji pekee, "haitoshi" kusitisha ghasia dhidi ya wanawake. Mawaziri wamesema fedha hizo pia zitaifaidi Uingereza kutokana na kwamba itapunguza hatari kwa wasichana wanaosafirishwa katika nchi za nje kwenda kukeketwa. Serikali inasema kuna wasichana wanaokadiriwa 24,000 na wanawake walio katika hatari ya ueketaji Uingereza. Akitangaza msaada huo, waziri wa maendeleo ya kimataifa Uingereza Penny Mordaunt amesema ukeketaji hauwezi kumalizwa Uingereza, pasi "kuuangamiza duniani". "Wanawake wajasiri, wanaotia moyo wa Afrika wanaongoza jitihada kusitisha utamaduni huo katika nchi zao, na kwa mchango wao, jamii nyingine zimeanza kujitenga na utamaduni huo,"amesema. "Lakini hatua ipo katika kiwango muhimu, na ni lazima tushirikiane kuwalinda mamilioni ya wasichana ambao bado wamo katika hatari ya kukeketwa." Nchi zinazofaidi zaidi na msaada huu: Msaada huo utasaidia kufadhili mashirika kama vile mradi wa Saleema nchini Sudan, unaonuia kuwaonyesha wasichana kwamba wana uwezo hata wasipokatwa pamoja na kujaribu kubadili mitazamo ya wazee katika jamii. Sudan mojawapo ya nchi zenye viwango vikubwa vya ukeketaji, lakini kwa usaidizi kutoka serikali ya Uingereza, watu zaidi wanaugeuzia mgongo utamaduni huo. Katika kijiji cha Al Baseer jimboni Gazeera, kusini mwa mji mkuu Khartoum, sherehe inaendelea. Wanaume wa kati ya 30- 40 wanasimama kwenye mduara wakiimba na kucheza. Na wana kila sababu ya kusherehekea. Kijiji hiki kimeachana kabisa na ukeketaji. Inaarifiwa mara ya mwisho utamaduni huo kufanyika katika eneo hili ni katika miaka ya 90. Hakuna anayezungumzia ukeketaji. Ahmed Mohamed na mkewe Khadija Jitihada hizi zilianza mnamo 1983 wakati jamaa mmoja alipoamua kwamba imetosha kwa familia yake. Ahmed Mohamed alikuwa akifanya kazi Saudi Arabia. Aligundua kuwa ukeketaji hautekelezwi huko. 'Kuna sababu nyingi kwanini ukeketaji ni makosa. Wanawake walifariki, inawasababisha wasichana wasiwe na hamu na tendo la ndoa. Dini yetu hailikubali hilo. Wasaudi hawafanyi ukeketaji, kwahivyo ni makosa, na ndio sababu tukaamua tusilifanye tena. Mke wangu alikabiliwa na shinikizo kubwa, lakini nashukuru kwamba alikataa'. Mkewe Ahmed, Khadija, alikabiliwa na unyanyapaa na kutengwa na jirani zake. Lakini leo hali ni tofuati, anakubalika. Mwanamke anafunguka kuhusu madhila aliyoyapitia. Idadi kubwa ya wanawake na wasichana kwengineko Sudan hukeketwa 'Mimi nilikuwa miongoni mwa wasichana wa mwisho waliokeketwa katika kijiji hichi. Nilizaliwa mnamo 1989. Niliteseka sana katika maisha yangu ya kwenye ndoa na pia katika kujifungua mtoto wangu na mpaka leo naendelea kuteseka. Sitokuwa kama msichana wa kawaida ambaye hajakatwa,' anasema Rehan. Watu wengi wanatumia kigezo cha dini kutetea ukeketaji. Lakini hilo sasa linabishwa na kupingwa na viongozi wa kidini Sudan. 'Nadhani ukeketaji ni kinyume na maadili ya dini ya kiislamu na unasababisha matatizo ya ki afya kwa wasichana... tuliiomba jamii itufuate na wakafanya hivyo,' anasema Shekhe mmoja. Lakini wakunga kama Amira Abdulrahman, mama na ma bibi wanaendelea kuwa na kauli kuu katika suala hili. Amira anasema aliwakeketa wasichana wengi - wakiwemo mabinti na wajukuu zake. lakini aliachana na shughuli hiyo baada ya kisa kimoja cha msichana nusra kufariki. Amira Abdulrahman mkunga aliyekuwa akiwakeketa wasichana 'Ningependa kuwaomba radhi... watoto waliniona kama malaika wa kifo. Ilinibidi niifiche sindano nyuma yangu…. kama ningeweza kuzungumza nao, ningewaomba msamaha' anasema Amira. Wasichana wengi hukeketwa wakiwa wadogo wa umri wa kati ya miaka 7, 8 au wengine hata miaka 3. Kuna jitihada, zinazoungwa mkono na msaada wa Uingereza kuwafunza mapema kuhusu madhara ya hatari ya ukeketaji. Kwengineko nchini, idadi kubwa ya wasichana na wanawake wanakatwa. Sasa serikali ya Sudan kwa usaidizi wa msaada wa kimataifa, inatumai kuangamiza ukeketaji kitaifa kufikia mwaka 2030. Ukeketaji Chanzo: World Health Organization Uingereza itatoa msaada wa £ milioni 50 ($64m) kusaidia kusitisha ukeketaji Afrika. text: Chanchal Lahiri alifahamika kwa umaarufu kama Mandrake Chanchal Lahiri alijaribu kuiga kiini macho cha Harry Houdini - mcheza kiinimacho maarufu duniani - na alitarajiwa kujitatua na kutoroka, lakini hakuzuka kutoka kwenye mto huo uliopo katika jimbo la Bengal magharibi. Watu waliokusanyika kushuhudia kiini macho hicho wamewaarifu maafisa wa polisi , ambao wameeleza kwamba wanamtafuta sasa. Lahiri, anafahamika kwa umaarufu kama Mandrake, alitumbukizwa ndani ya mto kutoka kwenye boti. Alifungwa kwa makufuli sita na silisili au cheni wakati watu wakimtazama kutoka kwenye maboti mawili. Wengine wengi walikusanyika ufukweni katika daraja la Howrah huko Kolkata. Polisi na kikosi cha wapiga mbizi wamepiga doria katika eneo hilo lakini kufikia jana Jumapili jioni, walikuwa hawajafanikiwa kumpata jamaa huyo. Afisa mmoja amelieleza gazeti la Hindustan Times kwamba mpaka mwili wa Lahiri utakapopatikana, ndipo atakapothibitishwa kuwa amefariki. Mpiga picha wa gazeti moja katika eneo hilo, Jayant Shaw, alishuhudia mkasa huo. Ameiambia BBC kwamba alizungumza na Lahiri kabla aanze kiini macho hicho. "Nilimuuliza kwanini una hatarisha maisha yako kwa kiini macho," Shaw amesema. "Lahiri alitabasamu na kusema, 'Nikifanikiwa, ni miujiza, nisipofanikiwa basi litakuwa janga.'" Mcheza kiini macho huyo alimueleza Shaw kwamba alitaka kufanya muujiza huo ili "kufufua shauku kwa kiinimacho". Hii sio mara ya kwanza kwa Lahiri kujaribu muujiza hatari wa chini ya maji. Alitumbukizwa ndani ya mto uo huo ndani ya sanduku la kigae au glasi zaidi ya miaka 20 iliyopita lakini alifanikiwa kutoweka salama. Shaw aliwahi pia kushuhudia kiini macho hicho cha awali chake Lahiri. "Sikudhani kwamba hatofanikiwa kutoka ndani ya maji mara hii," amesema. Mcheza kiini macho nchini India aliyejaribu kuiga muujiza maarufu kwa kuruka mtoni akiwa amefungwa mikono na miguu, na kutumbukizwa kichwa chini maguu juu, anahofiwa amefariki. text: Tetemeko hilo lilifuatiwa na matetemeko mengine madogo Tetemeko la ukubwa wa 6.4 lilitokea kisiwa la Lombok siku ya Jumapili Kisiwa hicho huwavutia watalii kutoka duniani kote kutokana na fukwe zake za kuvutia na maeneo ya kutembea, eneo hilo liko umbali wa kilometa 40 mashariki mwa Bali. Zaidi ya watu 160 wamejeruhiwa na maelfu ya makazi yameharibiwa, maafisa wameeleza. Mtalii raia wa Malaysia aliyekua akitembea kuelekea mlima Rinjani ni miongoni mwa waliopoteza maisha. Utafiti wa wataalamu wa Jiolojia nchini Marekani ulisema tetemeko lilipiga umbali wa kilometa 50 Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Mataram. Kisha likafuatiwa na matetemeko madogo zaidi ya 60, kubwa likirekodiwa kuwa na ukubwa wa 5.7. Matetemeko mengine yalikaribia mji wa jirani, Bali Sutopo Purwo Nugroho, Msemaji wa taasisi ya kukabiliana na majanga, amesema kuwa madhara mengi hujitokeza pale watu wanapoangukiwa na vifuri au mawe ''Sasa tunachokitazama na kuwaokoa watu.Baadhi ya waliojeruhiwa bado wanapata matibabu kwenye vituo vya afya'', alieleza ''Tetemeko lilikuwa na nguvu....watalii waliingiwa na hofu na kuanza kuondoka hotelini'',Lalu Muhammad Iqbal afisa kutoka wizara ya mambo ya nje aliiambia BBC. ''Matetemeko yalikuwa na nguvu ''niliona mawimbi kwenye bwawa la kuogelea hotelini, tulikimbia nje ya hoteli''. ''Dakika 30 baadae kulikuwa na tetemeko la kwanza.Watu waliingiwa na hofu kwa kuwa nyumba nyingi zimetengenezwa kwa mbao na bamboo, lakini watalii walikuwa na hofu zaidi. Watalii wa UK , Katherine and Alexis Bouvier, ambao walilkuwa kwenye fungate wameiambia BBC: ''tuliamshwa na tetemeko la ardhi majira ya saa sita usiku, ilikua inaogopesha''. Nyumba nyingine zilianguka maporomoko ya ardhi yamekata mfumo wa usambazaji maji na umeme katika baadhi ya nyumba, walieleza. ''Tumepishana na magari kadhaa ya maji tulipokuwa tukielekea kusuni.Walituambia kuwa udongo wa saruji ulikuwa unadondoka kutoka sehemu ya dari na nyufa zikaanza kujitokeza kwenye majengo''. Hifadhi ya mlima Rinjani,imefungwa kutokana na maporomoko ya ardhi. Tetemeko la ardhi laua wengi Indonesia mpanda mlima Khairul Azi aliliambia gazeti la New Straits Times kuwa yeye na wenzake ''walishindwa kutoka kwenye eneo hilo kwa kuwa barabara zilikatika. ''Hali ni mbaya hapa, bado tunatafuta kuwasiliana na watembeaji wengine,'' aliongeza. Tetemeko la ukubwa wa 6.5 lilipiga pwani ya Sumatra mwaka 2016, watu kadhaa walipoteza maisha na wengine zaidi ya 40,000 waliyahama makazi yao. Watu 14 wamepoteza maisha baada ya tetemeko kupiga eneo maarufu la utalii nchini Indonesia text: Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'. Alikuwa akizungumza katika hotuba uliopeperushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini. Rais Kenyatta alisema kuwa ataiangazia idara ya mahakama ,mbali na kurejelea ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo. Wameonya kuikabili idara hiyo baada ya uchaguzi ''Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali ,sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema kuwa matokeo ya urais yaliotangazwa yalikuwa na dosari. Kivipi, kivipi? aliuliza rais Kenyatta katika ikulu ya rais alipokutana na viongozi wa chama cha Jubilee waliochaguliwa. Rais huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionya kukabiliana na majaji hao wa mahakama ya juu atakapochaguliwa. Mkutano wa wanachama wa Jubilee uliofanyika katika Ikulu ya rais ''Tuna matatizo hapa. Mwanzo ni nani aliyewachagua? tuna tatizo na lazima turekebishe'', alisema. Amesisitiza kuwa ijapokuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo ya juu na kwamba alikuwa tayari kushiriki katika uchaguzi mwengine alisema kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na makosa. ''Mahakama ya juu iliketi chini ikaamua kwamba hiyo ndio yenye nguvu zaidi ya Wakenya milioni 15 walioamka alfajiri na kupanga foleni na kumpigia mgombea wa urais waliomtaka''. Rais Uhuru Kenyatta akiwahutubia viongozi wa chama tawala ha Jubilee siku moja baada ya uchaguzi wake kubatilishwa na mahakama ''Mahakama ya juu haiwezi kufutilia mbali maono ya Wakenya.Na tutaliangazia swala hili.Niangalieni machoni na museme iwapo upendo wangu wa Wakenya kuishi kwa amani ndio unaonekana kuwa uoga, hatuogopi''. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'. text: Heroin ilipatikana ndani ya dege ya Pakistan ambaye ingesafiri kuenda London Tarehe 15 mwezi huu wa Mei, maafisa wa mipaka wa Uingereza walikamata ndege iliyokuwa ikitokea mjini Islamabad ilipowasili uwanja wa Heathrow mjini London na kuikagua kwa saa kadhaa. Shirika la kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza baadaye lilisema kuwa kiwango fulani cha heroin kilipatikana kimefichwa katika sehemu tofauti za ndege hiyo. Kuna madai kuwa utawala nchini Uingereza ulichukua hatua hiyo kutokana na taarifa ulizopokea kutoka Pakistan. Heroin ilipatikana ndani ya dege ya Pakistan ambaye ingesafiri kuenda London Hakuna mtu aliyekamatwa lakini rubani wa ndege hiyo hakuruhusiwa kurudi Pakistan siku iliyofuata. Kisa hicho kilisabisha aibu kwa shirika la ndege la Pakistan ambalo linapata nafuu baada ya ajali mbaya iliyowaua watu wengi mwezi Disemba, Tarehe 22 mwezi Mei maafisa wa Pakistan katika uwanja wa ndege wa Islamabad, walikamata zaidi ya kilo 20 za dawa ya heroin ndani ya ndege nyingine iliyokuwa isafiri kuenda Heathrow. Kwa sasa uchunguzi unafanyika kubaini ikiwa kuna ushirikiano wa kutumiwa ndega za shirika la ndege la Pakistan, kusafirisha madawa ya kulevya kuenda nchi za ng'ambo. Mimea ya kuzalisha heroin inapatikana sehemu nyingi nchini Afghanistan Shirika la ndege la serikali nchini Pakistan, linasema kuwa linachukua hatua kuhakikisha kuwa ndege zake hazitumiwi kubeba madawa ya kelevya baada ya dawa ya heroin, kupatikana kwenye ndege zake mbili zinazofanya safari kuenda mjini London text: Mwigizaji huyo akiwa na mumewe wa mwisho, Frederic von Anhalt, mwaka 1989 Mumewe wa sasa Frederic von Anhalt amesema mwigizaji huyo alifariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa amezingirwa na marafiki na jamaa. "Kila mtu alikuwa hapo. Hakufariki akiwa peke yake," Alitengeneza zaidi ya filamu sita lakini alijulikana zaidi kwa kuwa na wanaume wengi na kupenda almasi. Kwa hesabu zake mwenyewe Zsa Zsa Gabor aliwahi kuolewa mara nane na nusu, hakuchukulia ndoa yake kwa Mhispania mwaka 1983 kuwa ndoa kamili. Alikuwa maarufu kwa miongo kadhaa, kabla ya hata kuibuka kwa Paris Hilton au Kim Kardashian. Sauti yake ya kuburudisha ilikuwa pia historia. Akitoa maoni juu ya kushindwa kudumu katika ndoa Gabor alisema katika ndoa zake alifanywa kama msimamizi wa nyumba kwa sababu kila alipokuwa akipewa talaka yeye aliachiwa nyumba. Zsa Zsa Gabor alizaliwa mjini Budapest nchini Hungary tarehe 6 Februari 1917 na akahamia Marekani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Aliigiza filamu yake ya kwanza Hollywood mwaka 1952. Gabor mwaka 1954, akicheza kinanda na dada zake Eva (kushoto) na Magda Aliigiza zaidi ya filamu 70, lakini alifahamika sana kwa maisha yake ya kifahari. Aliolewa mara ya kwanza akiwa na miaka 20 na ndoa yake iliyodumu muda mrefu zaidi ilikuwa yake ya mwisho alipokuwa na miaka 70 kwa Frederic von Anhalt. Gabor alitawazwa Miss Hungary mwaka 1936, lakini baadaye akapokonywa taji hilo kwa kuhadaa kuhusu umri wake ndipo aruhusiwe kushiriki shindano hilo. Aliigiza karika filamu maarufu kama vile Moulin Rouge (1952), Lili (1953) na Queen of Outer Space (1958). Hivi karibuni, aliigiza katika filamu ya Nightmare kwenye mwendelezo wa filamu za Elm Street na pia kwenye filamu za ucheshi za Naked Gun. Mtoto wake wa pekee ni Constance Francesca Hilton, ambaye alimzaa na tajiri wa mahoteli Conrad Hilton. Alizaliwa mwaka 1947. Mamake wakati mmoja inadaiwa alimwambia: "Si lazima umuoe mwanamume yeyote unayefanya mapenzi naye." Gabor alisema alikuwa anaoa kwa sababu hakuwahi "kuacha kuwa Mkatoliki moyoni." Muigizaji maarufu Zsa Zsa Gabor enzi za uhai wake Kwenye kitabu chake kuhusu maisha yake alichokiandika mwaka 1993 kwa jina "One Lifetime is Not Enough", alidai kwamba alibikiriwa na Kemal Ataturk, mwanzilishi wa taifa la sasa la Uturuki, alipokuwa na miaka 15. Alieleza kwamba alikuwa pia na uhusiano na nyota wa filamu za James Bond Sean Connery na Frank Sinatra, kando na msururu wa wanaume alioolewa nao. Alidai kwamba aliwakataa John F. Kennedy na Elvis Presley. Gabor akiwa Beverly Hills mwaka 1989 Mwigizaji maarufu Zsa Zsa Gabor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99. text: Hili ni swali ambalo huenda la kudhalilisha- kwa mfano kabla ya tendo la ndoa ukimuuliza mpezi wako "umenawa mikono?" - lakini wataalamu wa masuala ya kujamiiana wanasisitiza umuhimu wa kuzingatia usafi katika uhusiano wa kimapenzi. Ni hatua muhimu ambayo inaweza kukuepusha kwa mfano na magonjwa yanayoathiri sehemu za siri. "Kunawa mikono na kusafisha meno ni muhimu kwasababu viungo hivyo vinatumika sana wakati wa tendo la ndoa," Thamara Martínez Farinós, mwanasaikolojia na mtaalamu wa masuala ya ngono kutoka Taasisi ya Espill Institute, mjini Valencia, Uhispania ameiambia BBC Mundo. Kando na kunawa mikono pia ni muhimu kuosha sehemu za siri kila siku. Lakini "kuosha haraka haraka" haitoshi, alifafanua mtaalamu huyo. "Usafi ni muhimu kwa sababu unasaidia kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kupitia ngono", Vicente Briet, mwanasaikolojia na mtaalamu wa saikolojia ya kujamiiana, ameiambia BBC Mundo. Mkurugenzi wa kituo cha matibabu cha Vicente Briet na mkuu wa kitengo cha saikolojia ya ngono katika Chuo Kikuu cha Alicante nchi Uhispania anasema usafi "ni chanzo kikuu cha hamasa wakati wa tendo landoa". Na kuongeza kuwa "Ukuzaji wake unaanza na umuhimu tunaopatia usafi wa miili yetu kabla na baada ya kushiriki tendo la ndoa ." Usafi huu unaweza kuzingatiwa vipi. Kwa wanaume... Mtandao wa Huduma ya Afya ya Umma ya Uingereza (NHS) unaelezea jinsi wanaume na wanawake wanavyotakiwa kusafisha maeneo yao ya siri. Madaktari wanapendekeza wanaume kuosha sehemu zao kwa kutumia maji ya uvuguvugu kila siku kwa kuangazia zaidi maeneo ambayo huenda yakachangia kukusanyika kwa bakteria, kwa kutumia sabuni ambayo inakabiliana na viini vinavyosababisha bakteria "Suluhisho la kukabiliana na bakteria wanaoshambulia maeneo ya siri kwa wanaume ni kuzingatia usafi wa mara kwa mara,"anasema Dk. Briet. Je unazingatia usafi wakati wa tendo la ndoa? "Inashangaza jinsi baadhi ya wanaume wanavyopuuza usafi wa kimwili hususani katika sehemu zao za siri. Sio tu kwamba hali hiyo huleta matatizo yanayotokana na usafi duni, lakini pia ni changamoto kwa wenzi wao, " aliandika Patrick French, mtaalamu wa afya ya uzazi katika mtandao wa NHS . "Iwe ni kutokana na kutojua, baadhi ya wanaume wanafanya kosa la kutosafisha maeneo yao ya siri, licha ya athari za kiafya ambazo huenda zikatokana na hatua hiyo kama vile: harufu mbaya na maambukizi ya magonjwa," aliamibia BBC Mundo. NHS hata hivyo inaonya wanaume kutotumia sabuni wakati wanaposafisha sehemu za siri kwani maji ya vuguvugu yanatosha kuua viini. Na ikiwa lazima watumie sabuni wataalamu wanapendekeza itumike kwa "kiwango kidogo tena isiwe na marashi ili kuzuia muwasho wa ngozi." Kwa wanawake... Wataalamu wa afya ya uzazi wanakubaliana kwamba kuna upotoshaji mwingi unaoshuhudiwa, licha ya kwamba kuna kampuni nyingi zinazojihusisha na "usafi wa sehemu za siri" za wanawake "Uke umeumbwa kwa njia ambayo inajisafisha yenyewe kiasilia. Lakini hiyo haimaanishi sehemu hiyo haihitaji kuoshwa, " Taarifa ya mtandao wa NHS inasema. "Kuna aina nyini ya bakteria ndani ya uke ambayo ipo hapo kama kinga," aliongeza mtaalamu Thamara Martínez.. Wataalamu wa saikolojia ya kujamiiana wanatahadharisha matumizi ya sabuni yenye manukato kusafisha uke kwasababu haihitajiki na pia ni hatari. "Sehemu ya nje ya uke inaweza kusafishwa kwa sabuni isiyo na manukato ama bidhaa maalum zilizotengenezwa kwa ajili ya kusafisha sehemu hiyo", anasema Thamara Martínez. "Pia inategemea ngozi ya mtu, kuna nyingine huenda zikasababisha muwasho ambao unaongeza hatari ya kupata magonjwa. Kile ninachopendekezwa ni kusafisha sehemu za siri angalau mara moja kwa siku." Baadhi ya athari za kiafya zinazosababishwa na utumiaji wa sabuni yenye manukato kuosha uke ni pamoja na : Wanaume na wanawake Kidokezo kimoja ambacho kinastahili kuzingatiwa na jinsia zote mbili kwa mujibu wa wataalamu ni kwamba wanaume na wanawake wanashauriwa kwenda haja ndogo kabla na baada ya kufanya tendo la ndoa. "Kwenda haja ndogo baada ya kufanya tendo la ndoa ni moja ya njia muhimu ya kujiepusha na magonjwa yanayosababishwa na bakteria, " anasema Martínez. "Kujisaidia haja ndogo baada ya tendo la ndoa kunasaidia kusafisha kibofu cha mkojo, hali ambayo inazuia bakteria kuathiri sehemu hiyo," anaeleza "Pia kwenda haja ndogo kabla ya tendo la ndoa ni muhimu, kwani wapenzi watakaribiana bila kuwa na hofu ." Briet anaongeza kuwa mwenendo huo "ni mzuri kwani unaweza kuzuia magonjwa yanayoathiri njia ya kupitisha mkojo kwa kiwango kikubwa hata kama sio magonjwa mengine." Wataalamu wa saikolojia ya ngono wanapendekeza wapenzi kwenda haja ndogo "punde baada ya kufanya tendo la ndoa" ili kujikinga na magonjwa na kupunguza uwezekano wa kuambukizwa magonjwa. Kulingana na wataalamu hao wanawake wako katika hatari ya kupata maabukizi ya magonjwa yanayoathiri njia ya kupitisha mkojo. Hivyo basi wanapendekeza wawe na mazoea ya kwenda haja dakika 15 kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu la ustawi wa familia(2002) unasema kuwa wanawake wenye afya ambao huenda haja dakika 15 kabla ya kujamiiana huenda wakajiepusha na hatari ya kupata maambukizi wakilinganishwa na wenzao ambao hawafanyi hivyo. Mapendekezo makuu: Chanzo: Thamara Martínez Farinós, mwanasaikolojia na mtaalamu ya masuala ya ngono katika Taasisi ya Espill. Kunawa mikono ni jambo muhimu zaidi siku hizi kuliko ilivyokuwa zamani, lakini je watu wananawa mikono kabla na baada ya kufanya tendo la ndoa? text: Mapema Jumatatu alikana mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wanne, watatu kati yao walikuwa ni watoto wakati wa uhalifu huo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 52 alionekana akiwa amevaa koti la samawati, hakuzungumza na waandishi habari aliposindikizwa kutoka gerezani na wakili wake. Alijisalimisha kwa polisi Ijumaa na alisalia gerezani wikendi nzima. Muimbaji huyo amekabiliwa na tuhuma za unyanysaji kwa miongo kadhaa pasi kushtakiwa , na amekana tuhuma zote za awali. Msemaji wa idara ya polisi Sophia Ansari amethibitisha Jumatatu kwamba R Kelly amelipa dhamana hiyo ya $100,000 ambayo ni 10% ya dhamana ya dola milioni moja iliyowekwa na jaji mwishoni mwa juma. Kufika kwake mahakamani na kukana mashtaka hayo kunajiri wiki kadhaa baada ya makala ndefu kwa jina 'Suriving R Kelly kupeperushwa. Ilituhumu unyanyasaji dhidi ya wanawake wengi, akiwemo aliyekuwa mkewe nyota huyo muimbaji. Anashtakiwa kwa unyanyasaji unoadaiwa kufanyika tangu 1998. R Kelly akitoka gerezani baada ya kulipa dhamana Alikutana na mojawapo ya wanawake hao aliyekuwa anaadhimisha miaka 16 tangu kuzaliwa katika mgahawa mmoja - na mwingine ambaye pia alikuwa na umri wa miaka 16 - aliyeomba amtilie saini nakala ya kazi yake - au autograph. Mahakama imemuagiza muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, asalimishe pasi yake ya usafiri na asiwasiliane na mtu yoyote aliye na umri wa chini ya miaka 18. Inaarifiwa kwamba alipata tabu kulpa dhamana hiyo ya $100,000 iliyohitajika kutoka katika gereza la Cook County Jail. Katika mkutano na waandishi habari baadaye, wakili maarufu Gloria Allred amesema kwamba sasa anawawakilisha wanawake sita wanaotuhumu kuwa muimbaji huyo aliwanyanyasa. Aanatarajiwa kufika mahakamani Machi 27. Nyota wa R&B R Kelly ameachiwa huru kutoka gerezani Chicago Marekani baada ya kulipa dhamana ya $100,000, msemaji wa idara ya polisi ameeleza. text: Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Farmajo Mmoja wa wabunge ambaye amechochea hoja hiyo Abdifitah Ismail Dahir ameiambia BBC wanamtuhumu Rais kwa uhaini baada ya kusaini makubaliano ya kisiasa na kiuchumi na Ethiopia na Eritrea. Amesema Rais ameshindwa kuwashirikisha taarifa wenzie kuhusiana na makubaliano yanayohusisha bandari za Somalia. Wanamlaumu pia Rais kwa madai ya kuwarejesha wahalifu isivyo halali. Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamesababisha uharibifu Somalia Wabunge wapatao 92 wanapaswa kusaini hoja hiyo ya kutokuwa na imani na Rais, kuweza kuwasilisha kwa Spika, ili aruhusu kuanza kwa mjadala. Mizozo ya kisiasa ni jambo la kawaida nchini Somalia na utata huo wa hivi karibuni umekuja wakati serikali ikikosolewa kwa kuingilia kati uchaguzi wa majimbo. Mohamed Farmajo ashinda urais Somalia Farmajo asema atalipiza kisasi kwa kundi la al-shabab Marais wa zamani waungana na Farmajo Somalia Licha ya kuchaguliwa kwa Rais Farmajo kuingia madarakani mwaka uliopita na baadhi ya watu kupata matumaini, lakini bado hali ya kisiasa nchini Somalia inaonekana haijatulia. Wabunge nchini Somalia wamewasilisha hoja bungeni ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Mohammed Abdullahi Farmajo. text: Mlipuko wa mwisho wa Ebola DR Congo ulikuwa 2017 ambapo watu 4 walifariki Kuna visa viwili vilivyothibitishwa kwa sasa, wizara ya afya ya DR Congo imethibitisha. Watu 17 walikuwa wameripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa usiojulikana, ambao unadhaniwa kuwa Ebola eneo hilo. Waziri wa Afya Kenya Bi Sicily Kariuki amesema wasafiri wote wanaofika uwanja wa ndege wa JKIA na vituo vya mpakani vya Busia na Malaba watakuwa wakipimwa viwango vyao vya joto mwilini. "Katika maeneo haya, tumeweka mtambo ya kuwatambua watu walio na kiwango cha juu cha joto kuliko kawaida," amesema. Nigeria pia imeimarisha doria mpakani. Wataalam wa maradhi ya Ebola kutoka wizara ya afya nchini DR Congo wanatarajiwa kuambatana na wale wa shirika la afya duniani WHO kwenda jimboni Equateur baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa visa hivyo. Kisa kilichotokea katika mji wa Bikoro kinajiri zaidi ya mwaka baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kusababisha vifo vya watu wanne nchini humo. Mnamo 2014 zaidi ya watu 11,000 waliuawa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia. Tangazo la kuzuka kwa visa hivyo vipya limetolewa baada ya matokeo ya uchunguzi wa maabara kuthibitisha visa viwili vya Ebola kati ya sampuli za wagonjwa watano waliokuwa wanahsukiwa, Shirika la afya duniani (WHO) limesema. Kulitokea Mlipuko wa Ebola Afrika magharibi kati ya 2014-2015 "Leng letu kuu ni kuushirikisha mji wa Bikoro na serikali,"Msemaji wa WHO Peter Salam alisema katika taarifa yake. "Kushirikiana na washirika na kukabiliana na visa mapema katika namna iliyoratibiwaitakuwa ni muhimu katika kuudhibiti ugonjwa huuu hatari." Shirika hilo la afya duniani linasema limetoa $ milioni 1 kutoka fuko la dharura na limetuma zaidi ya wataalamu 50 kufanya kazi na maafisa nchini Congo. Hii ni mara ya tisa kunazuka ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Virusi vya ugonjwa huo viligunduliwa kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Zaire, mnamo 1976 na jina lake linatokana na mto Ebola. Inadhaniwa kwamba Ebola husambazwa katika maeneo ya mbali kupitia popo na husambazwa miongoni mwa binaadamu kutokana na kula nyama za mwituni. Dalili za Ebola Njia tano za kujiepusha virusi vya Ebola Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida. Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi: 1. Sabuni na maji Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha. Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola. Unachohitaji tu ni sabuni ya kawaida. Kusalimiana kwa mikono kunafaa kuepukwa kwa ujumla, daktari Unnis Krishnan wa Plan International aliarifu BBC, kwani Ebola husambazwa haraka watu wanapowasiliana ana kwa ana na maji maji ya kimwili ya waliougua. Dalili ya ugonjwa huu huchukuwa muda kabla ya kudhihirika. Tumia njia zingine za kujuliana hali. 2. Hakuna kugusana Iwapo unashuku kuwa mtu ana Ebola, usimguse. Inaokena kuwa si maadili mema unapoona unaowapenda wakihisi uchungu na unataka kuwakumbatia na kuwahudumia, lakini maji maji ya kimwili- mkojo na kinyesi, matapishi, kamasi, mate, machozi, na mbegu za kiume na majimaji ya uke- vyote huweza kueneza Ebola. Dalili za mtu aliyeugua ni joto mwilini, maumivu kwa misuli na viungo, vidonda kooni, kuumwa na kichwa, na uchovu- kufuatiwa na kichefuchefu, kutapika, na kuharisha, ambapo mtu huweza kutoa damu pia. Tia watu hao moyo kutembelea kituo cha afya haraka iwezekanavyo. Pia ni uamuzi mzuri usiguse nguo au malaza ya waliougua Ebola- na Medecins Sans Frontieres anashauri kuwa malazi ya waliougua yanafaa kuteketezwa. 3. Epuka miili ya wafu Iwapo unadhani mtu amefariki baada ya kuugua Ebola, usiguse mwili wao, hata kama ni mila au desturi ya maziko. Baada ya mtu kufa, bado unaweza kuambukizwa Ebola kutoka kwa miili yao kwani bado inatoa maji maji ya mwili ambayo huweza kuwa hatari zaidi hata kuliko ya mtu alieugua. Fanya mipango kupata timu ya magwiji kushughulikia mwili huo haraka iwezekanavyo kwani ni hatari kuwacha mwili wa mfu kwa muda mrefu katika eneo la makazi. 4. Usile nyama ya porini Epuka kuwinda, kugusa, au kula nyama ya porini, kwa mfano popo, nyani na sokwe, kwani wanasayansi wanaamini kuwa hiyo ndiyo chanzo cha maambukizi kwa binadamu. Hata kama mnyama fulani wa porini huliwa katika eneo lenu na nyama yake ni tamu epuka myama huyo kwani nyama yake au damu yake huweza kuwa na virusi hivyo. Hakikisha vyakula vyote vinapikwa inavyostahili. 5. Usiwe na hofu Kueneza uvumi huongeza hofu. Usiogope wafanyakazi wa huduma za afya- wako hapo kukusaidia na kliniki ndipo mahali mwafaka kwa mtu kuponywa- wataongezewa maji na kutulizwa maumivu. Kuamini matibabu ya kiasili ambayo hayajathibitishwa kutoa afueni, pia huchangia ongezeko la kuenea kwa virusi vya Ebola. "Kinga ndiyo jinsi bora zaidi ya kukabiliana na Ebola, hivyo basi wacha uvumi na usiwe na hofu; inawezekana kupunguza maumivu na kuokoa maisha," daktari Krishnan asema. Serikali ya Kenya imeimarisha doria katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta na vituo vingine vya mpakani baada ya visa vya ugonjwa wa Ebola kuripotiwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. text: Makonda amesema wakati wa wanawake kutembea kifua mbele umefika na siku zote atasimama kuwatetea Bwana Makonda amesema yupo tayari kuchukiwa na wanaume wa Mkoa huo wanaokwazika na uamuzi wake wa kuwatetea wanawake. Amesema hawezi kukaa kimya kuangalia mateso ya wanawake yanayoweza kupatiwa ufumbuzi ikiwa wanaume watabadilika. Makonda alikuwa akizungumza Jumapili katika Kanisa la Inuka Uangaze la Mtume Boniface Mwamposa maarufu 'Bulldozer' lililopo Kawe, Dar es Salaam. Amesema wakati wa wanawake kutembea kifua mbele umefika na siku zote atasimama kuwatetea. "Wanawake wakati wa kutembea kifua mbele umefika, kama mlimbeba mtoto miezi tisa hakuna jambo litakalokushinda. Wanaume mjipange, siwezi kukaa kimya kwa ajili ya mama," amesema Makonda. Amesema baada ya kuwasilisha serikalini mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya ndoa, anajipanga pia kupeleka mabadiliko ya sheria ya mtoto. "Katika sheria ya mtoto tumependekeza matunzo yaanzie mimba inapoingia, mtoto atunzwe kuanzia hapo. Wasichana wengi wanatelekezwa wakipata ujauzito kwa madai mimba imeingia kwa bahati mbaya." alisema Makonda. "Wasichana wa kazi wanateseka, wanapewa mimba na mabosi zao na kufukuzwa wakiambiwa wataharibu ndoa. Kama unajijua una ndoa jisitiri na ndoa yako unahangaika ili iweje. Hadi niondoke kwenye huu mkoa kuna watu mtakuwa mmenyooka," amesema Makonda. Katika hatua nyingine iliyoibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii miongoni mwa Watanzania, Mkuu wa mkoa huyo jana Jumapili alitangaza kuwa sasa anatoa kibali kwa viongozi wa dini kwenda kuhubiri kwenye kumbi za burudani usiku ili watu wasikie neno la Mungu, wasije kusema hawakusikia. Alitoa onyo kwa kwa wamiliki wa klabu watakaozuia watumishi hao, na kwamba yeye ndiyo Mkuu wa Mkoa. Kauli hiyo ilinukuliwa na Swahili Times kwenye ukurasa wake wa Twitter. Baadhi walipinga kauli hiyo ya kupitia mitandao ya kijami mfano Tonny Adamms kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema hakuna mmiliki wa klabu atayeruhusu hilo halitafanyika: Wengine kama Mtoto wa Meko alijiuliza swali hili nae kupitia ukurasa wa Twitter: Katika hatua nyingine ya kukabiliana na mienendo ya wanaume mwanzoni mwa mwezi wa Agosti Bwana Makonda alitangaza kuwa amepanga kuzisajiri ndoa zote za mkoa huo kwa ajili ya kukabiliana na wanaume wanaowalaghai wanawake kimapenzi. Alisema kuna mpango wa kuanzisha kanzi data ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa. Kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa. Makonda amesema pamoja na kanzidata hiyo atatumia mkutano wa SADC kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo. Paul Makonda Si mara ya kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwashangaza Watanzania kwa maamuzi anayoyayachukua , Jumapili ya mwishi ya mwezi wa Agosti aliwaita. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alidai kwamba amekuwa akikutana na malalamiko mengi sana kutoka kwa wadada wa mkoa huo kwamba wamechoka kutapeliwa. Mwezi Aprili mwaka 2018, Bwn.Makonda alitoa agizo kwa wanawake wanaodai kutelekezwa na wazazi wenzao kufika katika ofisi yake ili wapate kusikilizwa Kufuatia taarifa hiyo mamia ya wanawake walijitokeza na kwenda katika ofisi yake kuelezea machungu waliyodai kupitia kutokana na kutelekezwa na wame zao. Hatua hiyo iliibua hisia tofauti miongoni mwa Watanzani hususan katika mitandao ya habari ya kijamii, baadhi wakimkosoa na baadhi wakiafiki hatua yake ya kuwasikiliza akina mama. Unaweza pia kutazama: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema yupo tayari kuchukiwa na wanaume wa Mkoa huo wanaokwazika na uamuzi wake wa kuwatetea wanawake, Limeripoti gazeti la mwananchi nchini Tanzania text: Ana Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic. Ana Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic. Kuidhinishwa kwake na bunge kutakuwa rasmi kwa kuwa chama chake na washirika wake wana wajumbe wengi. Miaka michache iliopita uteuzi wa mtu wa mapenzi ya jinsia moja usingedhaniwa. Lakini Serbia inayosubiri kujiunga na bara Ulaya imeonyesha ithibati kwamba kuna ongezeko la uvumilivu miongoni mwa raia wa eneo hilo. Hatahivyo kiongozi wa chama kidogo katika muungano wa rais huyo Dragan Markovic Palma wa muungano wa Serbia alisema kuwa bi Brnabic ''sio chagua lake la waziri wake mkuu''. Bi Brnabic atajiunga na idadi ndogo ya mawaziri wakuu ambao ni wapenzi wa jinsia moja ili kuongoza serikali barani Ulaya ikiwemo Leo Varadkar wa Jamhuri ya Ireland na Xavier Bettel wa Luxenbourg. Wadhfa wa waziri mkuu katika utawala huo utakuwa na uwezo hafifu. Rais wa Serbia amemteua mwanamke ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa waziri mkuu katika jimbo la kihafidhana la Balkan. text: Msemaji wa polisi ameambia BBC kwamba walipokea simu ya kutokea kwa mtafaruku Jumatatu adhuhuri, lakini hawakutaja jina la mwanamuziki huyo. Baadaye, mtafaruku huo ulidaiwa kuwa tukio la kimatibabu, na maafisa wa kutoa huduma ya dharura walifika eneo hilo. Msemaji wa maafisa wa huduma za dharura wa LA amesema mwanamume ambaye jina lake halikutajwa alipelekwa hospitalini "kufanyiwa uchunguzi zaidi". "Mwendo wa saa 13:20 majira ya kanda ya pasifiki, idara ya huduma za dharura ya Los Angeles ilipokea ombi la dharura la huduma ya matibabu ambalo halikuelezwa kwa kina," amsemaji huyo alisema. "Mwanamume mzima, ambaye hali yake ya afya ni thabiti, alipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi." West alifuta ziara yake ya sasa baada yake kuwafokea watu wikendi NBC news wanasema hatua ya kumlaza West imechukuliwa kwa ajili ya afya yake na usalama wake. Tovuti ya udaku ya TMZ imesema West amepelekwa hospitali kufanyiwa "uchunguzi wa kiakili" na kwamba amekuwa akitafuta matibabu "kwa sababu ya kukosa usingizi sana". Los Angeles Times imeripoti kwamba kulipigwa simu ya 911 kutoka nyumba ya Kanye West. West nawawakilishi wake hawajazungumzia tukio hilo. Mkewe, Kim Kardashian, alitarajiwa kuhudhuria hafla fulani New York Jumatatu, mara yake ya kwanza kutokea hadharani tangu avamiwe na wezi Paris mwezi Oktoba, lakini hakufika. West alikuwa amefuta tamasha zote zilizokuwa zimesalia kwenye ziara yake ya sasa ya kimuziki. Alikuwa ameondoka tamasha ya Sacramento ikiwa katikati wikendi. Alikuwa ameimba nyimbo tatu pekee Jumamosi usiku kabla ya kuanza kuwafokea watu na kushambulia Facebook, Jay Z na Hillary Clinton. Alimkosoa mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg kwa kukosa kumlipa $53m (£42.5m) alipe madeni. Alisema pia kwamba alikereka sana na hatua ya Jay Z na familia yake kutomtembelea baada ya mkewe kuporwa Paris mwezi Oktoba. Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West amelazwa hospitalini mjini Los Angeles, vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti. text: Kampuni hiyo ya Marekani imetangaza kuwa tayari imekwishafanya safari 270 za ndege ya 737 Max yenye programu iliyoboreshwa. Imeongeza kuwa itatoa taarifa kwa utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) -juu ya namna rubani anavyowasiliana na waongozaji wa ndege na hatua anazopaswa kuchukua kwa matukio mbali mbali. FAA inatarajia Boeing iwasilishe taarifa juu ya namna ilivyoboresha ndege yake kwa ajili ya kupewa idhini ya kupaa tena wiki ijayo. Ndege ya Ethiopian Airlines ilianguka mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo. Ajali hiyo ilifuatia mkasa wa Lion Air nchini Indonesia mwezi Octoba ambapo watu 189 walikufa. Ajali zote mbili ziliihusika kasoro ya mfumo wa Boeing 737 Max -ambao ulikuwa ni mpya uliolenga kuboresha udhibiti wa ndege na kuizuiwia kuelekeza uso wake juu. Boeing ilisema kuwa mara taarifa juu ya namna marubani wanavyoonyeshwa jinsi ya kutumia mfumo ulioboreshwa itakapowasilishwa kwa FAA, itashirikiana na wafuatiliaji wa usalama wa ndege kufanya majaribio ya safari za ndege na kuwasilisha hati ya mwisho. Mapema wiki hii FAA ilisema kuwa itafanya mkutano na waangalizi wa usalama wa safari za anga tarahe 23 Mei kutoka kote duniani kuwapatia taarifa za sasa juu ya tathmini ya mfumo ulioboreshwa wa Boeing na mafunzo mapya kwa marubani. Unaweza pia kutizama: Familia zaomboleza mkasa wa ajali ya ndege Ethiopia Boeing imeboresha mfumo wake ndege ya chapa -737 Max- iliyopigwa marufuku kufuatia ajali zilizosababisha vifo vya abiria wengi katika kipindi cha miezi mitano. text: Malkia wa Pembe amefikishwa katika mahakama ya Kisutu leo Bi Feng na wengine, Silvanus Matembo, na Philemon Julius Manase waliofikishwa hii leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wametiwa hatiani kwa mashtaka matatu, yanayohusu ulanguzi wa meno ya tembo ikiwemo uhujumu uchumi. Watatu hao walipandishwa kizimbani kujibu mashtaka yahusianayo na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya takriban dola milioni 6 Katika shtaka la pili la uhujumu uchumi, watatu hao wamefungwa miaka miwili ama kulipa faini ya faini ya thamani ya mara mbili ya nyara walizovuna. Jumla ya kifungo chao ni miaka 17 lakini watatumikia miaka 15 jela. Mahakama imeeleza kwamba ushahidi umetolewa na watu 11 wakiwemo wasafirishaji. Ulanguzi wa Pembe za tembo umechangia kuongezeka kwa visa vya uwindaji haramu 'Ushahidi wote unaonyesha jinsi gani nyinyi( washtakiwa) mmefahamiana kwa muda mrefu' amesema jaji Huruma Shaidi. ''Ushahidi unaonesha jinsi gani washtakiwa wote watatu walivyosaidiana kuhakikisha wanatafuta meno ya tembo sehemu mbalimbali na kuyasafirisha'' ameongeza jaji Shaidi. Waendesha mashtaka wamebaini kwamba Bi Feng aliidhinisha mtandao wa kihalifu na kufanikiwa kusafirisha meno ya tembo katika maenoe tofuati kwa kutumia mgahawa wake wa vyakula vya Kichina kujificha na hata kutishia kuwaua watu katika kuidhibiti biashara hiyo haramu. Kwa mujibu wa wanaharakati, hii ni kesi kubwa inayohusu ulanguzi wa pembe za ndovu kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Mnamo mwaka 2015, jopo maalum la maafisa wanyama pori nchini Tanzania liliwakamata Bi Feng miongoni mwa wengine walioshukiwa kusafirisha pembe za ndovu. Makundi ya kampeni dhidi ya uwindaji haramu yalieleza kuwa wale waliokamatwa ni pamoja na mwanamke aliyepewa jina la utani 'Malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan. Wahifadhi wameitaja Tanzania kama shina la uwindaji haramu wa pembe za ndovu. Feng anaonekana kama nguvu ya nyuma katika biashara hiyo haramu ya uwindaji haramu wa pembe au meno ya tembo, na magengi ya ulanguzi kwa takriban miongo miwili iliyopita. Bidhaa hizo hutolewa nchini Tanzania na kusafirishwa katika eneo la Mashariki mwa dunia. 'Malkia wa Pembe za ndovu' ni nani? Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia. Lakini tunafahamu nini kumhusu? Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14. Maafisa wa serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan kama ufanisi mkubwa. Taifa hilo la Afrika mashariki limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Raia wa China Yang Feng Glan anayefahamika kama 'Ivory queen' na washtakiwa wengine wawili wamehukumiwa miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo. text: Ukosefu wa hisia hizo husababishwa na mwanamke kutoshiriki katika vitendo vinavyoweza kuvutia hisia za ngono bila ya kuhisishwa na tatizo lolote. Kemikali kwa jina Vyleese imejaribiwa kutengeneza kile ambacho kinaweza kuitwa Viagra ya kike. Hili ni swala tata , kwa kuwa baadhi ya wataalam wanahoji asli ya tatizo la hisia za kingono na kukosoa ukosefu wa msisimko wa mapema wakati mwathiriwa anapotumia. Sindano au tembe Ikiwa imetengenezwa na kampuni ya Teknolojia ya Palatin Technologies na kuruhusiwa kuuzwa na Amag Pharmaceuticals, dawa hiyo mpya hutumika kupitia sindano ambayo husisimua njia ya akili inayotumika katika hisia za ngono na itapatikana katika baadhi ya maduka ya dawa kuanzia mwezi Septemba. Ikilinganishwa na dawa nyengine, dawa hiyo haifanyi kazi katika mfumo wa mishipa, lakini huongeza hamu ya tendo la ngono katika mfumo wa neva. Vyleesi itashindana na Addyi ya watengenezaji dawa wa Sprout, dawa ya kila siku ambapo iliidhinishwa 2015 na kwamba watumiaji hawafai kutumia pombe wakati wanapoitumia. Addyi iliidhinishwa baada ya kampeni ya kukata na shoka licha ya kukosolewa na wanasayansi wa FDA ambao wanaitambua kuwa na utendakazi wa kadri na isio salama. Jinsi waathiriwa wanavyoathirika polepole Kwa upande wake Vyleesi haizuii matumizi ya pombe na inadaiwa kutoa fursa kubwa ikilinganishwa na mshindani wake, ikiwa na athari za chini, utendakazi wa hali ya juu na sio lazima kuitumia kila siku. Athari zilizoonekana wakati wa majaribio yake ni pamoja na kichefuchefu ambacho hakikuchukua zaidi ya saa mbili na kilitokea baada ya matumizi ya dawa hizo, kulingana na kampuni hiyo ya utengenezaji wa dawa ya Amag. Asiliami 40 ya wagonjwa walihisi kichefuchefu. Dawa hiyo hutumika kupitia sindano tumboni dakika 45 kabla ya tendo la ngono. FDA inapendekeza kwamba wagonjwa hawawezi kudungwa zaidi ya dozi moja katika saa 24 na sio zaidi ya dozi 8 kwa mwezi. Wachanganuzi wanakadiria kwamba dawa ilio salama yenye uwezo wa kutibu ukosefu wa hisia inaweza kupata mapato ya hadi $ 1 billion katika soko. Baadhi ya sekta fulani katika jamii zina matatizo makubwa ya swala hilo na wengine wanakadiria kwamba mmoja kati ya wanawake 10 huathirika. Nchini Marekani , kwa mfano tatizo hilo linawaathiri wanawake milioni sita , lakini ni wachache wanaotafuta tiba kulingana na Reuters. ''Wanawake hao huathirika polepole hivyobasi hakuna soko la tayari kwa sasa'', alisema William heiden, afisa mkuu mtendaji Amag alinukuliwa na Reuters. Utata Hatahivyo shirika hilo linatambua kwamba halijui jinsi Vyleesi inavyofanya kazi akilini ili kusisimua hisia za kingono. Kuna maono tofauti kwamba dawa ndio suluhu ya tatizo hilo. Upungufu wa hisia za kingono unaweza kusababishwa na matatizo ya nje, kimaungo na kiakili, kulingana na wataalam tofauti. Utendakazi wa dawa hiyo ya Vyleesi pamoja na usalama wake ulijaribiwa katika wiki 24 ukishirikisha zaidi na wanawake 1200 ambao hawajafikia ukomo wa hedhi. Wagonjwa wengi walitumia dawa hiyo mara mbili au tatu kwa mwezi lakini sio zaidi ya mara moja ka wiki. Takriban asilimia 25 waliripoti kupanda kwa hisia za ngono ikilinganishwa na zaidi ya asilimia 17 miongoni mwa wanawake. Athari zilizorekodiwa wakati wa majaribio hayo ni pamoja na kichwa kuuma kuwa na madoa doa mekundu usoni na katika ngozi kichefuchefu. Shirika linalohusika na udhibiti wa chakula na dawa nchini Marekani FDA hivi majuzi liliidhinisha dawa mpya kutibu tatizo la ukosefu wa hisia za kingono miongoni mwa wanawake ambao hawajafikia ukomo wa hedhi. text: Korea Kaskazini na Korea Kusini wameanza mazungumzo ya Olimpiki Tangazo hilo lilijiri wakati ambapo mataifa hayo yalikutana kwa mazungumzo ya kihistoria baada ya zaidi ya miaka miwili. Ujumbe huo utashirikisha wanariadha na mashabiki miongoni mwa wengine. Korea Kusini pia ilipendekeza kukutanisha familia zilizotenganishwa na vita vya Korea wakati wa michezo hiyo ya majira ya baridi. Swala hilo lina utata mkubwa miongoni mwa mataifa hayo mawili, na Korea Kusini imekuwa ikipendekeza familia ziendelee kukutanishwa. Mpango huo wa kuzikutanisha familia unatarajiwa kufanyika wakati wa likizo ya mwaka mpya, ambayo hufanyika katikati ya michezo ya Pyeongchang. Mji wa Seoul pia uliwataka wanariadha kutoka mataifa yote ya Korea kufanya gwaride la pamoja katika sherehe ya ufunguzi ya michezo ya Olimpiki. Haijulikani ni vipi Korea Kaskazini ilijibu mapendekezo hayo. Mara ya mwisho kwa mataifa yote mawili kufanya gwaride la pamoja chini ya bendera ya rasi ya Korea ni zaidi ya miaka 10 iliopita katika michezo ya olimpiki ya 2006. Waziri wa muungano wa Korea Kusini , Cho Myoung-Gyon amesema mazungumzo hayo yanajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kuimarisha uhusiano. "Tunahudhuria mkutano huu ili kuzungumzia suala la Korea Kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatayofanyika korea kusini na kuimarisha uhusiano wan chi hizi mbili.Ninaelewa kuwa matarajio ya wengi juu ya mkutano huu ,kwanza ni kuhusu mawasiliano baina ya nchi hizi mbili ambayo yalisitishwa kwa muda.Tuna lengo la kufanya mashindano haya ya Olimpiki kuwa ya hatua ya kwanza ya kuboresha Amani baina ya nchi hizi mbili hivyo hii ni hatua nzuri na hatuna haraka."Cho Myoung-Gyon aeleza. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili uliporomoka baada ya Korea Kusini kukatisha mradi wa pamoja wa kiuchumi huko eneo la kiuchumi la Kaesong Korea Kaskazini, na kufuatiwa na majaribio ya nyuklia yaliofanywa na Korea Kaskazini. Korea Kaskazini ilikata mpaka mawasiliano ya simu na Korea Kusini Mazungumzo ya mwisho baina ya nchi hizo mbili yalifanyika Disemba mwaka 2015 huko Korea ya Kusini. Siku ya Jumatatu waziri wa muungano wa Korea Kusini alisema kuwa mazungumzo hayo yatajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa. ''wakati tunazungumzia masuala ya uhusiano wa Korea, serikali itazungumzia pia suala la matokeo ya vita na njia za kupunguza mvutano wa kijeshi'' alisema waziri Cho Myoung-gyon ambaye ataongoza mazungumzo hayo yatakayohudhuriwa na wawakilishi watano. Nayo Korea Kaskazini watatuma wawakilishi watano wakiongozwa na Ri Son-gwon ambaye ni mwenyekiti wa Idara ya serikali ya Korea ya Kaskazini mwenye dhamana ya masuala na Kusini. KWANINI MKUTANO KUFANYIKA KIJIJI CHA PANMUNJOM? Mkutano huo utafanyika katika kijiji cha Panmunjom Kijiji hicho hujulikana kama kijiji cha pande mbli, ambapo kila upande una miliki sehemu yake na katikati kuna jengo la umoja wa mataifa. Baada ya vita ya korea kuisha mwaka 1953 kijiji cha Panmunjom kiliamuriwa kuwa sehemu ya pande zote mbili, na maofisa wa pande wanaweza kukutana hapo. Korea Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul. text: Idadi kuu ya visa vya ugonjwa huu nchini China imepatikana katika mji wa Wuhan Mzee mwenye umri wa miaka 89 alikuwa mwathiriwa wa hivi majuzi wa virusi hivyo ambavyo husababisha aina moja ya homa ya mapafu. Aliishi mjini Wuhan, mji unaodaiwa kuwa chanzo cha mlipuko huo. Zaidi ya visa 200 kufikia sasa vimeripotiwa katika miji mikuu nchini China ikiwemo Beijing na Shanghai. Shirika la afya duniani WHO linafikiria kutangaza janga la dharura la kiafya kama ilivyofanya wakati wa homa ya nguruwe na Ebola. Uamuzi huo utafanywa katika mkutano siku ya Jumatano. Wahudumu 15 wa fya mjini Wuhan wameambukizwa virusi hivyo Tume ya kitaifa ya afya siku ya Jumatatu ilithibitisha kwa mara ya kwanza kwamba maambukizi hayo yanaweza kusambaa kupitia wanadamu. Ilisema kwamba watu wawili mjini Guangdong waliambukizwa kwa njia hiyo. Katika taarifa nyengine, Tume ya afya ya mjini Wuhan ilisema kwamba takriban wahudumu 15 wa afya waliambukizwa ugonjwa huo , huku mmoja wao akiwa katika hali mahututi. Wafanyakazi hao wanadaiwa kuambukizwa na virusi hivyo baada ya kugusana na wagonjwa. Wote wametengwa huku wakipata matibabu. Je ugonjwa huo umeenea maeneo gani? Ugonjwa huo mara ya kwanza uligunduliwa mjini Wuhan, mji uliopo katikati ya China ulio na idadi ya watu milioni 11 , mwaka uliopita. Kuna takriban visa 218 vya virusi nchini China kulingana na WHO. Kuna visa kadhaa ambavyo tayari vimebainika Ulaya: Viwili nchini Thailand kimoja Japan na chengine Korea Kusini. Wale walioambukzwa walikuwa wamewasili kutoka Wuhan hivi majuzi. Mamlaka katika mataifa mengi ikiwemo Australia, Singapore, Hong Kong, Taiwan na Japan zimeimarisha uchunguzi wa abiria wanaosafiri kwa ndege kutoka Wuhan. Marekani pia imetangaza mikakati kama hiyo katika viwanja vya ndege vya San Francosco , Los Angeles na New York.. Nchini Australia mtu mmoja ambaye alikuwa amesafiri kuelekea Wuhan ametengwa na anafanyiwa vipimo. China ndio taifa linalochangia watalii wengi zaidi nchini Australia , huku zaidi ya watu milioni moja wakilitembelea taifa hilo mwaka uliopita. Je virusi hivyo vinasambaa kwa kasi gani? Kuna hofu kwamba virusi hivyo vinaweza kusambaa rahisi - na katika maeneo mengine nchini huku mamlioni ya raia nchini China wakijiandaa kusafiri kuelekea nyumbani kwa siku kuu ya kusherehekea mwaka mpya nchini China wiki hii. Mamilioni ya raia wa China wanasafiri kuelekwa makwao ili kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya nchini. Mamilioni ya raia wa China wanasafiri kuelekwea makwao ili kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya nchini humo Hatua ya raia kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine inamaanisha kwamba mamlaka hazitaweza kuchunguza kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Wataalam wanasema kwamba tayari kunaweza kuwa na visa vingi vya maambukizi kutoka kwa ugonjwa huo. Ripoti ya kituo cha uchanganuzi wa magonjwa katika chuo kikuu cha Imperial mjini London kimesema kuwa kunaweza kuwa na zaidi ya maambukizi 1,700. Hatahivyo , Gabriel Leung, mkuu wa idara ya matibabu katika chuo hicho cha Hongkong anasema kwamba maambukizi hayo yanaweza kufikia watu 1,300 kufikia sasa. Mlipuko huo umesababisha virusi kwa jina Coronavirus ambavyo vimesababisha vifo vya watu 774 kati ya karibia watu 2000 nchini , wengi wakiwa barani Asia na ambapo China ilishutumiwa kwa kuficha. Rais wa China Xi Jinping ametaka juhudi kuchukuliwa ili kuzuia mlipuko huo kulingana na vyombo vya habari, ikiwemo kusambaza habari na kuchukua hatua za haraka. Je tunajua nini kuhusu virusi hivi? Sampuli ya virusi vya ugonjwa vilivyochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kuchunguzwa katika maabara na maafisa wa serikali pamoja na wale wa shirika la afya duniani WHO zimethibitisha kwamba ugonjwa huo ni ule wa Coronavirus. Virusi hivyo ni familia kubwa ya virusi sita na kirusi hicho kipya kitaongeza idadi hiyo kufikia saba ambapo ni maarufu kwa kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu. Virusi hivyo vinaweza kusababisha homa, lakini pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya wa Sars ambao uliwauwa watu 774 kati ya 8,098 walioambukizwa katika mlipuko ulioanza China 2002. Uchanganuzi wa jeni za ugonjwa huo mpya unaonyesha kuhusishwa karibu na ugonjwa wa Sars zaidi ya ugonjwa wowote wa Coronovirus. Mamlaka ya China imeripoti visa 139 vipya vya ugonjwa huo usiojulikana katika siku mbili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa maambukizi hayo kuthibitishwa nchini humo nje ya mji wa Wuhan. Mwathiriwa wa nne nchini China amefariki kutokana na virusi vipya ambavyo vimesambaa nchini humo , huku maafisa wakithibitisha kwamba vinaweza kusambazwa kupitia mtu mmoja hadi mwingine. text: Rais wa Ukrain Petro Poroshenko (wa pili kulia) akikutana na maafisa huko Donetsk mwezi Juni Kurt Volker aliiambia BBC kuwa kuihami serikali ya Ukrain itabadilisha msimamo wa Urusi. Alisema hafikirii kuwa hatua hiyo itakuwa ni uchokozi. Wiki iliyopita wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Marekani ilizitaka pande zote mbili kusitisha mapigano mashariki mwa Ukrain. "Silaha za kujilinda, zile ambazo zitaisaidia ukrain kujilinda na kuharibu vifaru kwa mafano, ambazo zitaizuia Urusi kuitisha Ukrain," bwana Volker aliiambia BBC. Eneo linalokaliwa na waasi nchini Ukrain Alisema kuwa mafanikio ya kuwepo amani mashariki mwa Ukrain yanahitaji kile alichokitaja mchakato wa mazungumzo na Urusi. Bwana Volker na mjumbe wa zamani wa Marekani kwenye Nato na aliteuliwa kwenye wadhifa huo mpya mwezi huu. Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wameuawa tangu mzozo wa Mashariki mwa Ukrain ushuke mwezi Aprili mwaka 2014 mara baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea. Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni 1.6 kuhama makwao. Mjumbe mpya wa Marekani nchini Ukrian anasema kuwa Marekani inatathmini ikiwa itatuma silaha kusaidia wale wanaopigana na waasi wanoungwa mkono na Urusi. text: Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kushoto, Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na Katibu mkuu wa chama cha KANU Nick Salat wameazimia kuungana kwa vyama vyote vya upinzani nchini Kenya Kwa mara ya kwanza, viongozi hao wameandaa hafla ya pamoja kuonyesha umoja wao na kutangaza mipangi hiyo rasmi. Aliyekuwa Waziri mkuu, na kinara wa mrengo wa upinzani, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Kiongozi wa Chama cha ANC maarufu Amani, Musalia Mudavadi, wameungana I ili kutamfuta mgombea mmoja atayewakilisha upinzani ili kukabiliana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Zaidi ya vyama kumi vimethibitisha kuungana na kutangaza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuiondoa serikali iliyo mamlakani ikiongozwa na rais Uhuru Kenyatta. Aidha, viongozi hao wameahidi lengo lao ni kuboresha hali ya taifa hilo wakidai kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu chini ya utawala wa sasa. Wanachama wa chama cha upinzani cha Wiper nje ya ukumbi wa Bomas mjini Nairobi Hata hivyo, hawakutangaza ni nani atayekuwa mgombea wao wa Urais, Uamuzi ambao unatarajiwa baada ya wiki kadhaa. Vinara wa vyama hivyo, wametoa wito wa kumuunga mkono atakayeteuliwa kuwania urais kupitia mrengo huo kwani ndio hatua pekee ya kuimarisha umoja wao. Viongozi hao wametumia mifano ya mataifa ya Afrika kama Ghana na Gambia ambapo umoja wa upinzani umeweza kuwaletea ushindi. Kuhushu sheria ya uchaguzi iliyokarabitiwa, viongozi hao wameahidi kufanya mgomo baada ya shughuli ya kuwaandikisha wapiga kura inayatorajiwa kuanza nchini humo wiki ijayo, kumalizika. Wamewahimiza wafuasi wao kujiandikisha kwa idadi kubwa ili kuzidisha nafasi zao za kupata ushindi. Baada ya uvumi kuenea kuwa upinzani ulikuwa na mikakati ya kuunda muungano mmoja, sasa viongozi hao wamethibitisha kauli hiyo leo katika ukumbi wa Bomas mjini Nairobi. text: Wakati huo alikuwa kaimu rais na alikuwa anawania urais kwa mara ya kwanza. Warusi huwa ni nadra sana kumuona rais wao akilia, ingawa kumetokea mikasa mingi sana wakati wa utawala wake wa miaka 18. Lakini ilitokea wakati mmoja, mwanzoni mwa utawala wake - mnamo 24 Februari 2000, wakati wa mazishi ya Anatoly Sobchak. Sobchak alikuwa mmoja wa watu ambao, kwa pamoja na Gorbachev na Yeltsin, walisaidia kusambaratika kwa Muungano wa Usovieti. Ndiye mwanamageuzi ambaye pia alimuinua afisa wa KGB kwa jina la Vladimir Putin ambaye alikuwa afisa wa kiwango cha wastani kutoka kutofahamika hadi kumpa kazi yake ya kwanza katika siasa. Hakuna ajuaye hasa ni nini kilimhamasisha kuchukua hatua hiyo. Lakini leo hii, mirengo ya watu wenye msimamo mkali kutoka kwa idara za usalama wakati wa Muungano wa Usovieti imechukua na kudhibiti mamlaka nchini Urusi kwa kiasi ambacho kimetishia demokrasia. Meya Anatoly Sobchak akifungua rasmi Uwanja wa Austria mjini St Petersburg mnamo Septemba 1992, akiambatana na Vladimir Putin (kushoto) Kuna wagombea wanane wa wanaowania urais uchaguzi wa sasa, lakini Putin anafahamika kuwa "mgombea mkuu" na hakuna aliye na shaka kuhusu matokeo. Mmoja wa wagombea wanaoshindana naye ameeleza uchaguzi huo kuwa "uchaguzi bandia". "Ni kama tu katika chumba cha kuchezea kamari," anasema, "ambapo mwenye chumba ndiye hushinda wakati wote, katika demokrasia ya Urusi, ushindi wakati wote huwa upande wa Putin." Jina lake mgombea huyu, usishangae, ni Ksenia Sobchak, na ni bintiye Anatoly, rafiki na mlezi wa kisiasa wa zamani wa Putin. Ksenia, kama anavyofahamika, ana miaka 36 na ni mtangazaji wa zamani wa kipindi cha uhalisia kwenye runinga ambaye amejiingiza kwenye siasa na kuwa mwanasiasa wa upinzani. Wafuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Alexei Navalny ambaye amezuiwa kuwania wanasema yeye ni kikaragosi wa ikulu ya Kremlin na rafiki wa zamani wa familia ambaye ameingizwa na Putin kwenye kinyang'anyiro cha urais kuupa uchaguzi huo hisia za uhalisia. Bila shaka, hangeweza kuwania bila idhini ya watawala. Hivyo ndivyo siasa na demokrasia Urusi hufanya kazi. Bango la kampeni: "Kura kwa Sobchak. Kura kwa ukweli. Kura kwa uhuru." Lakini wanaume wenye kuvalia nadhifu suti za rangi ya kijivu ambao huendesha mambo ikulu Urusi huenda kufikia sasa wanajutia hatua yao. Ksenia kwa sasa anatembelea studio za runinga mbalimbani na kuwafichua washirika wafisadi wa Bw Putin na pia kueleza hatua ya Urusi ya kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama iliyo haramu. Iwapo anawania, kama asemavyo, ndipo ashinde na si asikike tu, basi anavunja miiko fulani. Nini kinatendeka kweli? Tumwache binti kwa muda na tumuangazie babake. Alikuwa meya wa St Petersburg, mji wa pili kwa umuhimu baada ya Moscow. Putin alikuwa naibu wake. Wawili hao walikuwa na urafiki wa karibu sana kiasi kwamba Sobchak alipotuhumiwa kuhusika katika ulaji rushwa, Putin alimsaidia kuikimbia nchi hiyo akiwa ameabiri ndege maalum ya kukodishwa. Hayo yalitokea miaka ya 1990. Wazikumbuka siku hizo? Urusi ilikuwa kwenye vurugu. Rais wake, Boris Yeltsin, alikuwa mlevu mara kwa mara na hakuimudu kazi. Wanaume wenye suti za majivu Kremlin walifikia wamepata suluhu - mtu mwingine mwenye kuvalia suti za kijivu, asiye na doa, ambaye kutoka kwake wangeunda dawa ya kumkabili Yeltsin. Walianza kumlea Putin kama mrithi wa Boris. Kisha, ghafla, Putin alipokuwa anawania urais kwa mara ya kwanza, rafiki yake wa zamani Anatoly Sobchak, akafariki akiwa na umri wa miaka 62, akiwa chumba chake hotelini Kaliningrad. Uchunguzi wa maiti yake ulisemakwamba alifariki kutokana na mshtuko wa moyo ingawa hakukuonekana dalili zozote za mshtuko wa moyo. Mjane wa Sobchak alishuku kwamba mumewe alikuwa ameuawa na maafisa walikuwa wanaficha ukweli, na akaagiza uchunguzi huru wa maiti ufanyike. Jina lake ni Lyudmila Narusova. Nilikutana naye majuzi na kumwuliza iwapo alifikiri mumewe aliuawa. Alitulia na kunyamaza kwa muda unaotosha kusema "Ndio" mara kumi, kisha akasema: "Sijui". Ksenia Sobchak, Vladimir Putin na Lyudmila Narusova ibada ya kumkumbuka Anatoly Sobchak Baadhi wamedokeza kwamba Putin huenda alihusika katika kifo cha Sobchak. Sobchak alikuwa na siri kumhusu Putin? Narusova alipuuzilia mbali wazo hilo mara moja. Nilirudi na kuangalia kwa makini video ya mazishi ya mwanasiasa huyo. Putin anaonekana kuhuzunika sana. Macho yake mekundu, anaonekana kutatizika kumeza kitu kilichokwama kooni, huku akimkumbatia Lyudmila Narusova. Putin si mwigizaji. Aidha, si mtu ambaye watu wamemzoea kuonesha hisia zake hadharani. Hivyo, inaeleweka, kuamini kwamba anakabiliana na simanzi na majonzi halisi. Au ni kitu kingine? Dhamira yake inamhukumu? "Kulikuwa na watu waliokuwa wanamsaidia Putin kuingia madarakani," Nasurova ananiambia. Yuko sahihi. Wakati huo, Putin alikuwa chombo cha kufikia madaraka kwa baadhi ya mirengo ya watu ndani ya Kremlin. Na kwa kiasi fulani bado yeye ni chombo. Iwapo Sobchak aliuawa, aliuawa basi na moja ya mirengo hiyo iliyohofia kwamba mtu aliyemlea angechukua madaraka? Pengine. Na ikiwa ni hivyo, afisa huyo wa KGB aligundua kweli kwamba rafiki yake aliuawa akijaribu kuendeleza Mradi Putin. Ni jambo la kudhania tu, lakini naanza kufikiria hivyo. Vladimir Putin and Lyudmila Narusova revisit Sobchak's grave in 2007 Nilimwuliza Narusova kuhusu uchunguzi wa maiti uliofanywa kwa amri yake. Anasema hakutoa matokeo hayo hadharani, lakini bado ameweka stakabadhi hizo kwenye sefu katika eneo salama nje ya Urusi. Nilipomwuliza ni kwa nini, hakusema. Nilimshinikiza. Nilimwambia, "Inaonekana kana kwamba umejipatia kitu kama mpango wa bima." "Unaweza kulitazama hivyo," alijibu. "Una wasiwasi?" nilimwuliza, "kuhusu usalama wako au wa binti yako?" Anakaa kimya kidogo kisha kusema: "Unajua, kuishi katika nchi hii ni jambo la kuogofya. Hasa kwa wale ambao wana msimamo pinzani na wa serikali. Hivyo ndio, nina wasiwasi, wasiwasi ninao..." Raia wa Urusi wanapojiandaa kumchagua Vladimir Putin kuwa kiongozi wao kwa muhula wa nne mnamo 18 Machi, mwandishi wa BBC Gabriel Gatehouse ameangazia tukio la kipekee lililotokea mwanzoni mwa uongozi wa Putin ikulu. text: Baadhi yao wanasema kuwa hujificha kutoka kwa ndugu zao wa kiume ili kutoonekana ama hata kudanganya kwamba wako katika hedhi. Sophia Jamil aliambia BBC : Watu wengine hawataki kukiri tatizo hili hutokea kwa sababu huliona kama kwenda kinyume na dini ya kiislamu lakini kuna tatizo. Wakati wa Ramadhan , Waislamu hufunga wakati jua linapotoka na kufungua jua linapotoka saa za jioni bila kula chakula ama kunywa maji. Hatahivyo wakati mwanamke anapokuwa katika hedhi hawezi kufunga. Lakini licha ya hilo, wanawake wengine hawawezi kuzungumza na ndugu zao wa kiume kuhusu hedhi "Mamaangu alikuwa akiniambia , kwamba unapokuwa katika hedhi usiwaambie wanaume, ni wanawake pekee ndio wanaojua, alisema mwanablogu huyo wa urembo mwenye umri wa miaka 21. "Hivyobasi kila nilipokuwa nikinywa maji na kumuona babaangu akija nililazimika kuweka chini kikombe cha maji na kuondoka. Mamangu alikuwa akiniletea chakula chumbani kisiri na kuniambia nile kwa utulivu." Sophia ambaye anaishi mjini New York na wazazi wake wanatoka Pakistan anasema: Wakati ndugu yangu aliponishika nilikuwa na chakula mdomoni na akaniangalia vibaya. ''Ndugu zangu hupenda kutaka kunishika nikila ili kuniabisha. Natamani ningekuwa na ujasiri wa kusema kwamba ni jambo la kawaida na kwamba dini yangu inaniruhusu kutofunga kwa sababu sina usafi wa haja''. Sophia anasema kuwa hedhi ni mada ya aibu ambayo mamake hakumuelezea kwamba atakumbana nayo atakapofikisha umri wa kubalehe. ''Nadhani hedhi inafaa kuwa kitu ambacho wanawake wanamiliki , hii tabia inafaa kukomeshwa . Kunafaa kuwa na mijadala zaidi na kwamba ni jukumu la vizazi vya sasa kuleta mabadilko hayo'', anasema. Sheria ya Ramadhan Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan mtu hafai kula kunywa wala kushiriki katika tendo la ngono kutoka alfajiri hadi jioni. Lengo la kutaka kufunga ni sharti lifanyike kabla ya alfajiri. Nia hiyo inaweza kufanywa wakati wa chakula cha Suhoor ama daku. Wanawake walio katika hedhi hawawezi kufunga, kusoma kitabu kitakatifu cha Quran ama kuingia msikitini. Pia sio lazima kwa mjamzito kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhan ,wakati unapokuwa mgonjwa , unapokuwa na umri mkubwa kama vile wazee, unapokuwa na tatizo la kiakili, unapokabiliwa na njaa ama kiu kikali, unaposafiri ama hata iwapo maisha yako yatakuwa hatarini iwapo hautafungua. Rais wa muungano wa wanafunzi wa Kiislamu , Sabreen Imtair, aliambia BBC alitaka kuwasaidia watu kuzungumzia kuhusu changamoto wanazopitia wakati wa hedhi na akachapisha ujumbe katika mtandao wa Twitter ili watu kuzungumzia mitandaoni. Alisema: "Familia yangu iko wazi kuhusu maswala kama haya lakini baadhi ya wasichana hususana wakati wa Ramadhan hawawezi kula mbele ya ndugu zao wa kiume na uhisi kuwa wachafu na wenye aibu wakati wa hedhi.." "Kuna unyanyapaa mkubwa ," anasema msichana huyo mwenye umi wa miaka 18. "kuficha hedhi yako na kuhisi aibu kunawafanya watu kuona swala hilo ni la aibu zaidi. Linabadilisha vile watu wanavyofikiria kuhusu wanawake'' Uzoefu wa Sabrina upo tofauti. Anaweza kula na kunywa wakati wa Ramadhan mbele ya familia yake. ''Nilienda kununua chakula .Ndugu yangu alikuwa amefunga na akaniuliza kwa nini ninanunua chakula. Nilipomwambia kwamba niko katika hedhi aliniambia ni sawa na akakubali''. Hatahivyo, Sabreen anatambua umuhimu wa kuzungumza wazi kuhusu hedhi : Mamangu amenifunza njia za kutumia sodo na kukabiliana na damu lakini sio kuwaambia watu kuhusu changamoto hiyo, anasema. ''Sikuweza kuzungumza kuhusu swala hilo na watu hadi hivi karibuni. Ni swala nyeti sana lakini sote tuna hedhi, ni sawa tulifanye liwe swala la kawaida''. Wanawake wa kiislamu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakizungumzia changamoto wanazokumbana nazo wakati wanapokula wakati wanapokuwa katika hedhi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. text: Ingawa kuna mengi ya kujivunia katika mapambano hayo ya kutafuta usawa licha ya uwepo wa changamoto za kurudishwa nyuma.Kelvin Mwachiro ameandika. Miaka 13 iliyopita, nilikuwa sifikirii kuwa Kenya inaweza kufika hatua hii , jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja kwenda mahakamani na kupambania haki yetu. Tuna safari ndefu bado. Kizazi hiki kinia jumuiya ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ambao ni werevu na wanajaribu kuhakikisha kuwa wakenya wanajifunza kuwapenda na kuwakubali kama walivyo. Miaka 13 iliyopita, nilijiambia mwenyewe kuwa sitakubali kuishi katika jamii ambayo inawatenga watu wengine. Sitaki kuigiza kuwa mtu wa aina fulani katika mahusiano au ndoa ili niwafurahishe wazazi wangu au ndugu zangu wakati si kweli. Nilitaka kuwa na furaha mimi kama mimi kwa namna nilivyo. Baadhi ya marafiki zangu wananisifia kwa kuwa mwerevu baada ya kujitangaza hali yangu. Ilinichukua muda mrefu kuwaelewa ni nini walikuwa wanamaanisha kwa sababu nilikuwa mimi tu mwenyewe na sio kama nilikuwa mwerevu zaidi ya wengine. Nina bahati kwa kuwa ninaishi mtaa ambao watu hawajali maisha ya watu wengine. 'Kushangaliwa na Minong'ono' Nimefanya kazi katika taasisi mbalimbali ambazo wanaheshimu jinsia ya mtu. Sijawahi kubaguliwa au kunyanyasa kwa namna yeyote. Sijawahi kushindwa kupata nyumba, ajira au kukosa huduma yeyote kwa sababu mimi ninapenda mapenzi ya jinsia moja. Nina bahati kwa kweli . Lakini kuna watu wengi kama mimi ambao wamepitia kwenye manyanyaso na kubaguliwa kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Ninafahamu kuwa kuna unyanyasaji mkubwa dhidi yetu. Hivyo vitisho vipo kwangu pia. Lakini nikiwa kama mtu ambaye niko katika jumuiya hiyo ya mapenzi ya jinsia moja, tumejifunza kujitengenezea uhuru baina yetu ili kuwa sisi. Tunajivunia mapenzi yetu licha ya kuwindwa. Tuko huru lakini bado tuna hofu. Nilipokuwa kijana mdogo , ndio wakati nilipokuwa ninajificha hisia zangu za mapenzi ya jinsia moja kwa sababu nilihisi nipo peke yangu. Hakuna mtu ambaye niliweza kumkimbilia kupata msaada akanielewa jinsi ninavyojisikia. Nilikuwa mkiwa. Leo, Kuna jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja nchi nzima wanaowaunga mkono , kuwahamasisha na kupendana. Ilikuwa mwaka 2016 ambao walikuwa wanafanya kampeni ya kufungua kesi ya ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja. Miaka ya nyuma, nilikuwa naona kama ninaota nilipokuwa nasikiliza hukumu ya kesi hiyo ambayp sasa inafahamika kama kanuni ya 162. Harakati hizi zilikuwa zilikuwa zinakabiliana na sheria ambayo ilikuwepo muda mrefu uliopita. ' Mapambano ya jinsia moja' Mappambano ya wapenzi wa jinsia moja yamekoma. Mapema , mwezi Februari mwaka huu, hukumu hiyo ilihairishwa . Tulihangaika kupata waandishi wa habari kupata nafasi ya kuandikwa kwa taarifa zetu za kutetea haki ili kuhamasishana. Tumefanikiwa katika hili. Tulikuwa tunataka hukumu. Tulikuwa tunataka kushinda kwa nguvu zote, na tulikuwa na katiba nzuri ambayo iko upande wetu. Ingawa tulijua kuwa tutashindwa. Tulihudhuria mahakamani kusikiliza jinsi kesi ilivyokuwa inaendelea huku wengine wakipata taarifa kupitia vyombo vya habari. Tunamshukuru Mungu kwa teknolojia! Mgogoro ulianza pale kesi ilipohairishwa. Maumivu ya kushindwa kesi. Watu walianza kupiga kelele nje ya mahakama. Ilikuwa ni wakati ambao tulitoneshwa majeraha yetu. Lakini bado tuna nia ya kupambana juu ya jambo hili. Hata kama sio leo lakini ukweli ni kwamba katika mfumo huu inabidi twende taratibu na kutoogopa kubadilika ni ushindi pia. Miaka 13 iliyopita. Sikutarajia kuwa nitaweza kutembea katika korido za mahakama kuhamasisha utetezi wa wapenzi wa jinsia moja. Sio wengi kati yeti ambao wameweza kufanya harakati hizi. Lakini sisi tumeweza. Ubaguzi dhidi yetu utaendelea kwenye mitandao ya kijamii na sehemu za kuabudia, na unyanyasaji dhidi yetu bado utaendelea kuepo. Bado unyanyasaji wa aina mbalimbali utaendelea kuepo dhidi yetu. Lakini vilevile harakati za kupambania haki za jumuiya yetu zitaendelea nchini humu. Ninajua kuwa tutawakilisha maumivu tuliyonayo baada ya siku chache zijazo. Ninapata faraja nikiona wanaharakati wengine wakiinuka ili kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja. Nilipokuwa na miaka 16 nilijihisi kuwa niko peke yangu mwenye hisia za namna hii lakini kumbe tuko wengi: Ninataka kumwambia kijana wa miaka 16 sasa kuwa tuko kwenye mapambano hayohayo na kwa upendo , ingawa bado tupo nyuma. Angalia tu ni umbali gani tumepiga kwa miaka 13. Uamuzi uliotolewa na mahakama Kuu nchini Kenya dhidi ya wanaharakati wanaopinga mapenzi ya jinsia moja unaonekana kuwa ni mwanzo wa mapambano ya utetezi wa haki ya wanaojihusisha katika mahusiano hayo. text: Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Benki hiyo kimeambia BBC kuwa mkopo huo ambao ulikuwa unalenga kuboresha elimu nchini Tanzania hautatolewa tena. Fedha hizo zilitarajiwa kufika Tanzania mwezi uliopita, Oktoba 2018. Taarifa za kuzuiwa kwa mkopo huo awali ziliripotiwa na Shirika la Habari la CNN lenye maskani yake nchini Marekani. Chanzo hicho pia kimethibitisha kuwa moja ya sababu kuu za kuzuiliwa kwa mkopo huo ni uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua. Katika taarifa rasmi iliyotumwa kwa barua pepe na moja ya wasemaji wakuu wa benki hiyo aliyopo jijini London, Benki hiyo imesema inaendelea na majadiliano na serikali ya Tanzania juu ya suala hilo. "Benki ya Dunia inaunga mkono sera ambazo zinawatia moyo wasichana na kuwawezesha kubaki shule mpaka mwisho wa uwezo wao. Matokeo ya kiuchumi na kijamii kwa wasichana kumaliza elimu yao ni makubwa kwa kila jamii kwa vizazi vya sasa na vijavyo," sehemu ya barua pepe hiyo inasomeka na kuongeza: "Tukishirikiana na wadau wengine tutaendelea kupigania haki ya wasichana kupata elimu kwa kujadiliana na serikali ya Tanzania." Rais John Magufuli alikutana na Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Dunia Tanzania Bi Bella Bird mwezi uliopita Ikulu ya Magogoni Mwezi Juni mwaka jana, Rais Magufuli alitangaza rasmi kuwa wanafunzi watakaopata ujauzito hawataruhusiwa kuendelea na masomo katika shule za serikali. Wakati Magufuli akitoa kauli hiyo, kulikuwa na vuguvugu la wanaharakati na wanasiasa wakiwemo kutoka chama tawala cha CCM ambao walikuwa wanataka kufanyike maboresho ya sheria ili kuwaruhusu mabinti hao kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Kwa sasa hakuna takwimu rasmi inayoonyesha idadi ya wanafunzi ambao wamefukuzwa shule nchini Tanzania kutokana na ujauzito. Kwa mujibu wa chanzo chetu, sababu nyengine ya kuzuiliwa kwa mkopo huo ni maboresho ya Sheria ya Takwimu yaliyopitishwa na Bunge la Tanzania Septemba 10 ambapo pamoja na mengine, inakataza usambazaji wa takwimu zinazolenga kupinga, kupotosha au kukinzana na takwimu rasmi za serikali. Adhabu ya kufanya hivyo ni faini ya Dola 6,000 au kwenda jela miaka mitatu. Mwezo Oktoba Benki ya Dunia ilitoa taarifa rasmi ya kuonesha masikitiko yake juu ya uamuzi huo. "Tumeifahamisha serikali ya Tanzania kwamba marekebisho hayo, iwapo yatatekelezwa, huenda yakaathiri sana kuandaliwa kwa takwimu rasmi na zisizo rasmi, ambazo huwa muhimu sana kwa ustawi wa taifa lolote lile. Ni muhimu sana kwa Tanzania, sawa na taifa jingine lolote, kutumia sheria za takwimu kuhakikisha takwimu rasmi ni za kiwango cha juu zaidi na za kuaminika na pia kulinda uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake, kuendeleza mjadala kwa manufaa ya raia," ilisema taarifa hiyo. Afisa huyo wa Benki hiyo amethibitisha kuwa safari zote rasmi za wafanyakazi wa Benki ya Dunia zimesitishwa kutokana na hofu ya kukamatwa na kushtakiwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni alitangaza operesheni ya kuwakamata wapenzi wa jinsia moja lakini baadaye serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje 'ilimruka' kwa kusema uamuzi huo ni wake binafsi na si sera ya nchi. Awali BBC iliwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Tanzania Leonard Akwilapo ambaye alisema taarifa za kuzuiwa kwa mkopo huo amezisoma mtandaoni na ofisi yake haikuwa inategemea kupokea pesa yoyote kutoka Benki ya Dunia. "...hatuna taarifa rasmi na serikali haifanyi kazi kwa kusikia kwenye mitandao ya kijamii," Akwilapo ameiambia BBC. Msemaji wa serikali Dkt Hassan Abbas pia ameiambia BBC kuwa hawezi kuliongelea suala hilo sababu hana taarifa rasmi mpaka sasa. Lugola: Wapenzi wa jinsia moja wapo salama Tanzania Wakati huo huo, wanaharakati kutoka kituo cha utetezi wa haki ya uzazi kijulikanacho kama Equity Now wanasema ni wakati muafaka sasa kwa serikali ya Tanzania kuangalia upya sera yake kwasababu wasichana wanaoacha masomo kutokana na mimba ni wengi. Kwa mujibu wa kituo hicho, kwa mwaka 2013, wasichana zaidi ya 8,000 walifukuzwa au kuacha shule. "Benki ya Dunia inajaribu kuishutumu serikali kwa sababu haitendi haki kwa watoto na jukumu la Tanzania ni kuhakikisha haki za kila mtu zimetiliwa maanani," Juddy Gitau mratibu wa kituo hicho ameiambia BBC na kuongeza: "Jambo la muhimu ni kuelimisha wasichana na vijana pia ili waelewe namna ya kujikinga kuingia katika huo mtego na jamii ielewe kwa sababu mimba sio ugonjwa. Kwa mujibu wa utafiti ambao tumeufanya nchini Tanzania ,wasichana wengi wamedhulumiwa na watu wao wa karibu hivyo kuna mambo mengi ya kuangalia katika kutatua tatizo hili na sio kuwaachisha wasichana peke yao." Taarifa za Tanzania kunyimwa mkopo wa dola milioni 300 na Benki ya Dunia ni sahihi, BBC imethibitisha. text: Mkuu wa Polisi wa Galveston, Vernon Hale alisema Jumatatu mbinu hiyo ilikuwa inakubalika katika baadhi ya matukio, lakini kwamba "maafisa hawakufanya uamuzi mzuri katika tukio hili". Alisema hakuna "nia mbaya" na imebadilisha sera ya idara "kuzuia utumiaji wa mbinu hii". Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wamesema picha hii imeibua mawazo kuhusu nyakati za utumwa. Kulingana na habari iliyotolewa kutoka kwa Idara ya Polisi ya Galveston, maafisa hao wawili kwa majina P Brosch na A Smith, walimkamata Donald Neely baada ua kukiuka sheria. Polisi walifafanua kwamba hakufungwa na kamba, lakini "alikuwa amefungwa pingu mikononi na kamba ilikuwa imefungwa kwenye pingu. Idara iliongeza: "Tunaelewa maoni hasi kuhusu hatua hii na tunaamini maoni haya yanafaa kabisa kukomesha utumiaji wa mbinu hii." Bwana Hale aliomba msamaha kwa Bw Neely kwa "kudhalilishwa". Aliongeza maafisa "wangeweza kungoja usafiri katika eneo la kukamatwa". "Tumebadilisha mara moja sera ya kuzuia matumizi ya mbinu hii na tutaangalia mafunzo na taratibu zote zilizowekwa kwa njia sahihi zaidi," mkuu wa polisi alisema. Bwana Neely yuko huru kwa dhamana lakini hakuweza kupatikana kwa ajili ya kutoa maoni, Jarida la Houston liliripoti. Leon Phillips, mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Kaunti ya Galveston , aliiambia BBC picha ambayo ilisambaa mitandaoni ilipigwa na mtu ambaye hakutaka kufahamika. Bwana Phillips alisema tukio hilo ni "gumu kulizungumzia" kama mkazi wa Galveston. "Hili lilikuwa kosa la kijinga," alisema. "Ninachojua ni kwamba kama angekuwa mzungu, wasingetumia mbinu hiyo waliotumia kwa Neely. Alibainisha kuwa Bwana Neely ni mgonjwa wa akili, na maafisa walipaswa kungojea bila kujali ni muda gani gari ingechukua kufika, kwani "si kana kwamba wanalipwa na baada ya kukamata". Bwana Phillips alisema amepanga kutoa ombi la wazi katika ukumbi wa jiji ili kuangalia sera za utekelezaji wa sheria. "Mkuu wa polisi anasema hawakuvunja sera yoyote, lakini ni sera gani ya kusafirisha mfungwa? "Ninajuaje kuwa sera hiyo haikuandikwa mnamo 1875? Kuna maswali mengi ambayo hayajajibiwa." Polisi wa Texas wameomba msamaha baada ya picha ya maafisa weupe wawili wakiwa wamepanda farasi wakiongoza mtu mweusi aliyeonekana amefungwa kwa kamba hatua iliyozusha ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. text: Obama alisema kuwa alikuwa amemuounya Putin kuhusu hatua kali wakati wa mkutano wa mwezi Septemba. Akimaanisha kuwa rais wa Urusi alielewa udukuzi huo, bwana Obama alisema kuwa, si mengi yanafannyika Urusi bila Putin Kuhusika. Obama alisema kuwa alikuwa amemuounya Putin kuhusu hatua kali wakati wa mkutano wa mwezi Septemba. Mwezi mmoja baaadaye Marekani iliilaumu Urusi kwa kuingilia masuala yake ya kisiasa. Obama ameahidi kujibu vikalia udukuzi huo uliolenga chama cha Democratic na parua pepe za mwenyekiti wa kampuni ya mgombea urais Hillary Clinton. Uchaguzi Marekani: Obama ataka maswala ya udukuzi kuchunguzwa Donald Trump kuimarisha uhusiano na Urusi Rais Obama hakumlaumu mrithi wake, Donald Trump wala kumtaja jina, lakini amesrma kuwa baadhi ya warepublican wameshindwa kuona atharia za kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Marekani. Mapema wiki hii Donald Trump alikashifu madai ya mashirika ya ujasusi ya Marekani kuwa wadukuzi wa Urusi walisaidia kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Hata hivyo Urusi imekana madai hayo. Msemaji wa Putin ametaja madai hayo kuwa yasiyo ya maana Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa alimuamrisha rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha udukuzi wa mitandao kabla ya kufanyika uchaguzi nchini Marekani. text: Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika Wilaya ya Bududa ambapo wananchi hao wenye hasira inasemekana walimvamia mwananjeshi huyo kwa kisasi. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, mwanajeshi huyo mwenye miaka 32 aliyetambulika kama Fred Kimanai aliuawa wikendi na watu ambao walikuwa wanaomboleza kifo cha kijana Ivan Mukuma Wamalile. Gazeti hilo linaripoti kuwa kadhia yote ilianza baada ya wawili hao ambao wote sasa ni marehemu kugombea pombe ya kienyeji aina ya 'kiroba' inayoitwa waragi. Mwanajeshi huyo inadaiwa alichukua kisu na kumchoma mwenzake ambaye alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali. Waombolezaji wa msiba wa Mukuma walimalizia hasira zao kwa kulipa kisasi kwa kumshambulia mpaka kifo mwanajeshi huyo ambaye amerejea nchini Uganda siku si nyingi akitokea Somalia ambapo alikuwa alikinda amani. Msemaji wa polisi wa eneo hilo bwana Robert Tukei, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo mawili na kuwa uchunguzi unaendelea. "Tumepoteza wau wawili katika mkasa huo, mwanajeshi na raia. Tunachunguza matukio yote mawili," amesema. Bw Tukei ametoa onyo kali kwa raia kujichukulia hatua mikononi, na kuwa wote watakaobainika kushiriki kwenye mauaji hayo watakamatwa na kufunguliwa mashtaka. "Washukiwa watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji," amesema Bw Tukei. Pia amethibitisha kuwa marehemu hao wawili walikuwa na ugomvi uliosababishwa na pombe. Tukio hilo linatokea siku chache toka Uganda kupia marufuku utengenezwaji na usambazwaji wa pombe za waragi. Miili ya marehemu hao imehifadiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Baduda ambapo inaendelea kufanyiwa uchunguzi. Msemaji wa kikosi cha jeshi ambacho Kimanai alikuwa anahudumu wamethibitisha kifo hicho. "Tmempoteza mmoja wetu, lakini tayari tumeshatuma kikosi cha kuchunguza tukio hilo. Baada ya hapo tutajua nini cha kufanya kufuatana na ripoti tutakayopata," amesema Kapteni Abert Arinaitwe. Mwaka jana, askari wa wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Elgon iliyopo kwenye eneo hilo aliuawa na wakazi wa Baduda baada ya askari mwengine kumuua moja ya wakazi wa wilaya hilo. Mwanajeshi mmoja nchini Uganda ameuawa na wananchi wenye hasira kali nchini Uganda kwenye shambulizi linalodaiwa kuchochewa na kugombea pombe aina ya waragi. text: Kupoteza fahamu kwa muda mrefu mara nyingi huwa kunasababishwa na kuumia kwa ubongo Munira Abdulla,alipata ajali akiwa na umri wa miaka 32 na kupata jeraha katika ubongo . Munira alipa ajali kwa kugongwa na basi wakati akiwa anaelekea kumchukua mtoto wake shuleni. Mtoto wake Omar Webair, alikuwa na umri wa miaka minne wakati yeye na mama yake walipopata ajali. Katika ajali hiyo Omar ambaye alikuwa ameketi katika kiti cha nyuma hakujeruhiwa hata kidogo na alikutwa akiwa amekumbatiwa na mama yake. Bi.Abdulla alijeruhiwa vibaya lakini mwaka jana akiwa hospital moja Ujerumani alianza kurudisha fahamu. Omar ameweka wazi kuhusu ajali walioipata na kuelezea utaratibu wa matibabu ya mama yake yaliyochukua miaka mingi. 'Alinikumbatia ili nisiumie' "Sikuwahi kukata tamaa kwa sababu kila siku nilihisi kuwa kuna siku mama yangu ataweza kuamka" Omar anaeleza. Omar aliongeza kusema kuwa sababu kubwa ambayo imemfanya asimulie mkasa uliomkuta mama yangu ni kutaka kuwaambia watu kuacha kukata tamaa kwa watu wanaowapenda na mtu akifikia hatua hiyo haimaanishi kuwa amekufa. Mama mkwe wa Munira ndio alikuwa dereva " Mama yangu alikuwa amekaa na mimi katika kiti cha nyuma , na alipoona tunakaribia kupata ajali, alinikumbatia ili kuniokoa katika ajali hiyo." Katika ajali hiyo Omar hakuumia bali alibaki na jeraha dogo kichwani lakini mama yake ambaye aliumia alichelewa kupata matibabu kwa saa kadhaa. Miaka aliyotumia kupata matibabu Bi. Abdalla alifikishwa hospital baada ya muda wa saa kadhaa kupita na baadae alihamishiwa mji wa London huku walisema kuwa amepoteza fahamu lakini akiwa ana uwezo wa kuhisi maumivu. Baada ya muda lirudishwa katika mji wa Al Ain katika umoja wa falme za kiarabu ambako alikuwa akiishi na mtoto wake Omar, na kuendelea kuzunguka katika vituo mbalimbali vya afya kulingana na bima aliyokuwa nayo. Alikuwa anakula kwa mrija na kumfanya aendelee kuishi na mara kwa mara alifanyiwa mazoezi na vipimo vya viungo ili kuhakikisha kuwa misuli yake haidhoofiki kwa kuwa alikuwa atembei. Mwaka 2017, familia iliweza kupokea msaada fedha kutoka serikalini ili kumuwezesha bi.Abdulla kwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu. Alifanya upasuaji mara kadhaa ili kurekebisha mkono wake uliopunguzwa na kuweka sawa misuli ya mguu, na alipewa dawa ili kuboresha hali yake, ikiwa ni pamoja na kuamka kwake. Kelele za hospitalini Baada ya mwaka mmoja , siku moja mtoto wake alikuwa anajibizana ndani ya chumba cha mama yake hospitalini na kulichochea mama huyo kuamka. "Kulikuwa na kutoelewana katika chumba alichokuwa amelazwa na alihisi kuwa niko hatarini, jambo ambalo lilimfanya ashtuke," Omar alisema. " Alikuwa anahangaika kutoa sauti na nilikuwa nahangaika kuita madaktari ili wampime na walisema kuwa kila kitu kilikuwa sawa. Siku tatu baadae , niliamka nikasikia mtu ananiita kwa jina langu. Alikuwa ni yeye, alikuwa anaita jina langu, nilikuwa kama ninapaa kwa furaha .Kwa miaka mingi nmekuwa nikiota siku hii ifike na jina langu lilkuwa neno la kwanza kulitamka baada ya miaka 27" Omar alieleza. Na baadae akawa anaweza kuwasiliana na sasa baada ya maumivu ya muda anaweza kuzungumza. Bi. Abdalla ameweza kurudi Abu Dhabi, ambako anaendelea kupata tiba ya viungo kwa mazoezi na kupata ushauri hasa wa namna ya kukaa na kufanya misuli kuwa imara. Kesi kama ya Munira huwa inajitokeza mara chache. Bingwa wa zamani wa mashindano ya magari, Michael Schumacher aliwahi kupata koma baada ya kupata ajali mwaka 2013 Kuna kesi chache sana za watu kupona baada ya kupoteza fahamu kwa miaka mingi na kuendelea kuwa wazima kabisa. Watu ambao wanapata hali hiyo na kurudi kwenye ufahamu wao baada ya koma ya muda mrefu mara nyingi tatizo lao huwa linatokana na madhara katika ubongo. Bingwa wa zamani wa mashindano ya magari duniani, Michael Schumacher aliwahi kupata koma baada ya kupata ajali mwaka 2013 huko Ufaransa . Alipoteza fahamu kwa muda wa miez sita kabla hajarudishwa kwao Switzerland kuendelea na matibabu. Mwanamke mmoja kutoka Umoja wa falme za kiarabu(UAE) aliumia sana katika ajali ya gari ilitokea mwaka 1991 na kupoteza fahamu lakini sasa amestaajabisha wengi baada ya kuamka kutoka kwenye koma iliyomchukua miaka 27 akiwa amepona. text: Kitambaa hicho cha kuziba mdomo ambacho ni maarufu katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya kujizuia maambukizi, sasa kinatumika sana China baada ya mlipuko wa virusi vya corona ambapo watu wamepewa ushauri wa kuejiepusha na mahali palipo na msongamano wa watu. Wataalamu wa afya wameelezea namna 'mask' hizo zinavyoweza kufanya kazi ili kuzuia virusi. Kuna baadhi ya ushahidi ambao unadhania kuwa mask hizo zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi kati ya mtu na mtu. Mask ilianza kutumika kwa mara ya kwanza katika hospitali mwishoni mwa karne ya 18, lakini zilikuwa hazitumiki katika sehemu za umma mpaka mlipuko wa mafua ulipotokea Uhispania mwaka 1919 na kuuwa watu zaidi ya milioni 50. Dkt David Carrington, wa chuo kikuu cha St George, mjini London, aliiambia BBC kuwa "'mask zinazotumika wakati wa operesheni au upasuaji huwa haziwezi kufanya kazi vizuri katika maeneo ya umma kuzuia watu kupata maambukizi ya virusi vya bakteria wa hewa ambao wanaambukiza, kwa sababu zina nafasi za wazi na zinaacha macho wazi. Lakini zinaweza kupunguza maambukizi kwa kiasi fulani ya kuwakinga watu katika maambukizi ya mkono na mdomo. Utafiti uliofanywa kutoka New south Wales ulipendekeza kuwa watu huwa wanashika nyuso zao mara 23 kwa saa. Jonathan Ball, profesa wa 'molecular virology' katika chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa : "Katika tafiti moja ambayo ilifanywa hospitalini, inaonyeshha kuwa mask ya sura huwa nzuri kwa kuzuia maambukizi kama ilivyobuniwa. Wabunifu waliotengeneza mask hiyo waliitengeneza kwa namna ambayo inaweza kuzuia vimelea vya hewani. Ingawa , ukiangalia ufanisi wake kwa ujumla katika msongamano wa watu, takwimu zinaonyesha utofauti mdogo - Vilevile si rahisi kwa mtu kukaa na mask kwa muda mrefu ," Prof Ball aliongeza. Dkt Connor Bamford, wa taasisi ya afya ya Wellcome-Wolfson, iliyopo chuo kikuu cha Queen Belfast, alisema kuwa "utekelezaji wa kuweka mazingira safi ndio hatua rahisi zaidi ambayo inaweza kufanya kazi kwa uhakika". Uchina yathibitisha virusi vya corona vinaweza kusambazwa "Kuziba mdomo wakati unapiga chafya, kunawa mikono, na kujizuia kuziba midomo kwa mikono kabla ya kunawa, kunaweza kupunguza hatari ya maambukizi kupata virusi", alisema. Watu wanapaswa kuzingatia: Dkt Jake Dunning, mkuu wa masuala ya afya nchini Uingereza alisema kuwa: "Ingawa kuna watu ambao wanahisi kuvaa mask usoni kutasaidia watu kupata maambukizi, kuna ushahidi mdogo sana kuwa kitendea kazi hicho kinaweza kuwanufaisha watu wakiwa nje kwa sababu imebuniwa kwa ajili ya kufanya kazi kwenye huduma za afya. Alisema pia mask hizo hazijavaliwa vizuri, kubadilishwa kila wakati kunaweza kuwa salama haa katika mazingira ya kazi. "Utafiti unaonyesha kuwa mask hiyo ilivaliwa kwa muda mrefu huwa inapongeza nguvu ya ufanyaji kazi wake, alisema. Watu wangezingatia zaidi kufanya mazingira yao kuwa safi, kama hilo suala la usafi wangelipa kipaumbele, alisema Dkt. Dunning. Picha ya mtu aliyefunga kitambaa cha kuziba pua na mdomo ''mask'' ili kujizuia kupata virusi ni sehemu ya kinga dhidi ya maambuki ya ugonjwa. text: Man City haijamailiza chini ya nafasi nne katika misimu tisa iliopita Mabingwa hao wa ligi ya Premier pia wamepigwa faini ya £25m. Hata hivyo uamuzi huo unaweza kupingwa katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo. Manchester City imesema kwamba hatua hiyo ni jambo la kukatisha tamaa lakini halikuwashangaza na watakata rufaa. Bod ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye hesabu zake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ikionesha kwamba hawakupata hasara wala faida", na kuongeza kwamba klabu hiyo haikushirikiana na wachunguzi". Imesemekana kwamba City huenda pia ikapunguziwa pointi katika ligi ya Premier kwasababu sheria ya udhibiti wa masuala ya fedha katika ligi ya Premier kwa kiasi kikubwa inafanana na Uefa japo hazifanani moja kwa moja. Hata hivyo, adhabu hiyo haitakuwa na athari zozote kwa timu ya wanawake ya City. Kwanini Man City huenda isishiriki ligi ya mabingwa? Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manchester City: "Klabu hiyo imekuwa ikifikiria umuhimu wa kuwa na bodi huru na kufuatwa kwa mchakato usiopendelea upande wowote kuangalia ushahidi wao ulio wazi. "Disemba 2018, mchunguzi mkuu wa Uefa alisema wazi vikwazo ambavyo anataka City iwekewe hata kabla ya uchunguzi kuanza kufanywa. "Kasoro na udhaifu uliopo katika mchakato wa Uefa kwenye uchunguzi alioongoza, hakukuwa na shaka na matokeo ya uchunguzi huu. Klabu hii awali ilikuwa imewasilisha malalamiko yake kwa bodi ya nidhamu ya Uefa, ambayo yaliidhinishwa na mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo. "kwa maneno rahisi, hii ni kesi iliyowasilishwa na Uefa, ikashtakiwa na Uefa na aliyetoa uamuzi ni Uefa. Kwa mchakato wa kibaguzi aina hii ambao umemalizika, klabu hii sasa itatafuta hukumu isiyopendelea upande wowote haraka iwezekanavyo na hivyo basi, kwanza kabisa itaendelea na mchakato wake katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo bila kuchelewa." City imepangwa kucheza na Real Madrid katika timu 16 za mchujo za ligi ya mabingwa huku mchuano wa kwanza ukiwa ni Februari 16 katika uwanja wa Bernabeu. Rais wa La Liga Javier Tebas iliisifu Uefa kwa kuchukua hatua stahiki. "Kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa fedha na kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria hiyo ni jambo la msingi kwa hatma ya mpira wa kandanda," amesema. "kwa miaka mingi tumekuwa tukitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua muafaka dhidi ya Manchester City na Paris Saint-Germain, na hatimaye tumepata mfano bora na ni matumaini yetu kwamba hili litaendelezwa. Ni kheri kuchelewa kuliko kutochukuliwa kwa hatua kabisa." Na Je wachezaji Tayari tunajua kwamba kiungo wa kati wa miaka mingi David Silva atakuwa akiondoka mwisho wa msimu . Lakini idadi ya wachezaji ambao kandarasi zao zinakaribia kukamilika kabla ya City kurejea katika mechi za klabu bingwa inatia wasiwasi. Mshambuliaji Sergio Aguero yupo katika orodha hiyo. Mkataba wake unakamilika 2021 . Mkataba wa Leroy Sane nao unakamilika wakati huohuo. Kandarsi ya John Stones inakamilika mwaka huohuo. Mkataba pia utamuathiri Nicolas Otamendi. Na je hatma ya nyota ambao kandarasi zao zinakamilika mwisho wa 2022 kama vile Kevin de Bryune Ederson, Bernado Silva , Raheem Sterling na Riyadh Mahrez? iwapo Guardiola ataondoka , ni rahisi kuona idadi kubwa ya wachezaji ikiondoka, ikimaanisha kwamba huenda City ikawachwa na kibarua kikubwa cha kuanza kujijenga upya. Je hali ya kifedha ya City ikoje? Mmiliki wa klabu ya man City Sheikh mansour kushoto Hiki ndicho kitu kisichoitia kiwewe City kwa kuwa kila mtu anajua kwamba klabu hiyo ni tajiri. Kila mtu pia anajua kwamba Manchester United imekuwa ikijaribu kushiriki katika ligi ya mabingwa katika siku za hivi katribuni. Arsenal imekosa kushiriki misimu mitatu mfululizo. Chelsea ilishindwa kushiriki msimu uliopita. Liverpool ilishindwa kufuzi mwaka 2015. Ni kweli kwamba watakosa mamilioni ya fedha lakini hilo halitaiathiri sana klabu hiyo. Pengine ugumu mkubwa utakuwa kukosa fursa ya kupata alama ikimaanisha kwamba hata iwapo watarudi , klabu hiyo itakuwa klabu ya chini zaidi ya walivyotarajia kuwa na hivyobasi kupata ugumu kufika katika awamu za mwisho za mashindano hayo. Je huu ndio mwisho wa Guardiola? Pep Guradiola amekuwa akichezea Man City tangu 2016 Na Simon Stone, mwanahabari wa BBC Michezo Kwa wakati mwengine katika kipindi cha wiki chache zilizopita, mkufunzi wa City Pep Guradiolaamejibu kuhusu hatama yake kwa kuelezea malengo yake ya kuhakikisha kuwa kandarasi yake inakamilika 2021. Pia amesema kwamba anaamini uongozi wa City uliomkakikishia kwamba hakuna ukweli wowote kuhusu madai yanayochunguzw ana Uefa. Je Guardiola anahisi kusalittiwa na matokoe hayo? na anashindwa kusema. Hatahivyo ni sawa kufikiria kwamba baada ya kushinda mechi nyingi katika ligi ya Premia mbali na kuwa klabu ya kwanza kushinda mataji matatu kwa mpigo , Guradiola huenda akapoteza motisha aliokuwa nayo. Iwapo City itashinda kombe la ligi ya mabingwa, Guradiola anaweza kuondoka hatahivyo. Sasa sio rahisi kufikiria kwamba atasalia huku kukiwa na uvumi kwamba Juventus inamnyatia, ndhini kwamba uwepo wake katika klabu hiyo kutategemea iwapo rufa iliokatwa na klabu hyo itafanikiwa. Je kinyang'anyi cha timu nne bora kitakuwa cha timu tano bora? Katika mechi za wikendi hii , Chelsea ilikuwa na pointi mbili mbele ya Sheffiled katika shindano la kuwania nafasi ya nne ya ligi ya Uingereza. Hatahivyo haijulikani kile kitakachotokea iwapo City itaondolewa lakini iwapo Uefa itaamua kuchukua timu nne za England na timu iliopo katika nafsi ya tano kuchukuliwa, kutakuwa na makabiliano makali katika hatua hiyo. Kutoka Sheffiled United iliopo katika nafasi ya tano hadi Crystal Palace iliopo katika nafasi ya 14, kuna alama tisa zinazozitawanya timu 10. Kutoka kuona kwamba huenda isifuzu katika ligi ya mabingwa . Arsenal huenda ikarudi kwa goli moja. Nini ambacho City inadaiwa kufanya? Uefa ilianzisha uchunguzi baada ya gazeti la Ujerumani Der Spiegel kuchapisha nyaraka za siri zilizovuja Novemba 2018 zilizodai kwamba City iliweka kiwango kikubwa cha makubaliano ya ufadhili wao na kupotosha bodi ya soka ya Ulaya. Taarifa hiyo ilidai kwamba City - ambayo kila wakati imekuwa ikikanusha kufanya makosa - ilipotosha Uefa kwa kukusudia ili iweze kutimiza sheria ya FFP inayotaka vilabu kufikia kiwango cha fedha ambacho siyo kuwa na hasara wala faida. City ilipigwa faini ya £ milioni 49 mwaka 2014 kwasababu ya kosa la awali la kukiuka sheria. Sheria za FFP zinasemaje? Sheria ya udhibiti wa fedha ilianzishwa na Uefa kuzuia vilabu kutumia fedha nyingi kuliko uwezo wao katika msindano wanayoshiriki na kukomesha kile ambacho wakati huo rais Michel Platini alikiita udanganyifu wa kifedha ndani ya mpira wa kandakanda. Chini ya sheria hizo, uwezekano wa vilabu kupata hasara unakuwa mdogo mno na pia vinajukmu la kuhakikisha kwamba wanaweza kugharamia pesa wanazotumia wakati wa usajili wa wachezaji na kulipa wafanyakazi wao kama inavyotakikana. Vilabu vinahitajika kuwa na uwiano- wenye kuhusishwa na matumizi - usajili na mishahara - pesa wanazopata kutokana na tiketi za mechi wanazouza, pamoja na mapato mengine yanayopatikana na idara zao za biashara. Pesa zinazotumika katika viwanja, vituo vya kufanyia mazoezi, miradi ya uendelezaji wa vijana au jamii huondolewa katika hilo. Bodi ya udhibiti wa fedha iliyoanzishwa na Uefa, ina uwezo wa kupiga marufuku vilabu kushiriki mashindano ya Uefa pamoja na adhabu zingine ikiwemo kutoa onyo, kutoza faini, kuzuilia pesa zilizokuwa zitolewe kama zawadi, marufuku ya usajili, kupunguza pointi, kupiga marufuku usajili wa wachezaji wapya na masharti ya idadi ya wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa katika mashindano ya Uefa. Manchester City imepigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni. text: Angelina Jolie alivyokula buibui Cambodia Mwigizaji huyo alisema walikuwa na "ladha tamu sana". Kula wadudu ni jambo lililohusishwa kwa muda mrefu na uigizaji, katika vipindi vya runinga kama vile I'm a Celebrity... Get Me Out Of Here. Lakini je, tunafaa kuwa kama Angelina na kuanza kuwala wadudu? Kwanini tunafaa kula wadudu? Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya watu duniani itafikia bilioni tisa. Ndipo tuweze kuwalisha, itabidi uzalishaji wa chakula uongezeke maradufu. Idadi ya watu duniani inapoopanda, kuna juhudi za kutafuta njia mbadala za kupata chakula - hasa protini - badala ya vyakula vya kawaida kutoka kwa mifugo na samaki. Kula wadudu ni moja ya njia hizi mbadala. Hili linasifiwa sana kwani wataalamu wanasema ni endelevu kimazingira, wana virutubisho vingi na wanaweza kupatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na katika hali nzuri. Maanufa ya kula wadudu ni gani? Wadudu wanaweza kuliwa na vyakula vingine, mfano pizza "Wadudu ndio chakula halisi chenye virutubisho karibu vyote," anasema Shami Radia, mwanzilishi mwenza wa Grub, duka linalouza wadudu wanaoliwa. "Wana protini, madini mengi na asidi za amino na kwa hivyo ni faida sana kuwala." Wadudu pia huwa bora kwa mazingira ukilinganisha na ufugaji. Wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazochangia ongezeko la viwango vya joto duniani, hawahitaji maji mengi na huhitaji eneo kubwa la shamba kuwafuga. Wadudu pia wana kiwango cha juu sana cha kubadilisha mali ghafi kuwa kawi au chakula kwa sababu hawahitaji kudhibiti joto katika miili yao kwa kutumia damu kama wafanyavyo mifugo na wanyama wengi. Kwa kawaida, wadudu wanaweza kubadilisha kilo 2 za lishe kuwa sehemu ya mdudu. Ng'ombe atahitaji kula lishe ya kilo 8 ndipo aweze kuongeza kilo 1 katika uzani wake. Ni wadudu wa aina gani wanaoliwa? Kuna karibu wadudu aina 1,900 ambao wanaweza kuliwa duniani, kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO). Wengi wa wanaoliwa ni mende, viwavi, nyuki, nyigu, nzige, kumbikumbi, nge, vipepeo na kerengende. Licha ya kwanda wadudu hawa wanapatikana kwa wingi, ni aina chache sana ya wadudu hawa wanaoliwa na jamii Afrika Mashariki. Je, na kula buibui kama Angelina? Grub wanaamini bado itachukua muda kwa watu kukubali kuwala buibui na nge kama alivyofanya Angelina Jolie. Mwigizaji mashuhuri Angelina Jolie alizua mjadala mkali alipokuwa akivumisha filamu yake mpya nchini Cambodia alipokaanga na kuwala buibui akiwa pamoja na watoto wake. text: Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeonekana kukanusha kuwapa idhini ya kuandaa maonesho ndani na nje ya nchi hiyo, ingawa kwa njia inayokanganya. Ijumaa, Diamond na Rayvanny kupitia wa Instagram, walipakia video wakiomba radhi. Baadaye, walijitokeza eneo la Westlands jijini Nairobi nchini Kenya na kueleza kwamba walikuwa wamewasilisha barua kwa Basata kujitetea na wakapewa idhini. Lakini baraza hilo limekanusha hilo na badala yake likadai wawili hao walitoa taarifa za uongo. "Wasanii @diamondplatnumz na mwenzake Rayvanny hawajaondolewa adhabu ya kutofanya onesho ndani na nje ya nchi kufuatia kupuuza adhabu ya awali iliyowaelekeza kutoutumia wimbo wa 'Mwanza' uliofungiwa kutokana na maudhui machafu na yasiyo na staha," ujumbe wa kwanza wa Twitter uliopakiwa kwenye ukurasa rasmi wa Basata unasema. "Itakukumbukwa kwamba Wasanii hawa huku wakijua wimbo huo umefungiwa waliutumia katika moja ya onesho la Tamasha la Wasafi ambalo nalo kibali chake kimesitishwa kufuatia kukiuka kanuni ma taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa," ujumbe wa pili unasema. Diamond Platnumz aeleza yeye na Rayvanny walivyojitetea Basata, Tanzania kuhusu Mwanza Jumamosi, taarifa iliyotiwa saini na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Onesmo Kayanda, ilitolewa lakini baada ya muda inaonekana kuondolewa mitandaoni. Ujumbe huu wa Basata unaoonekana kupakiwa kwenye Instagram haufungui Lakini wa Twitter uliokuwa umeambatishwa kiunganishi cha ujumbe wa Instagram bado upo, ingawa kiunganishi hicho cha Instagram hakifungui. 'Hatua kali zaidi' Taarifa iliyotolewa na Bw Kayanda ilisema: "Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili. "Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi." Queen Darleen na Rayvanny Juhudi zetu za kutafuta ufafanuzi kutoka kwa maafisa wa Basata bado hazijafua dafu, kwani simu zao hazipokelewi. Ijumaa, baada ya kutolewa kwa taarifa ya Diamond, walikuwa wamedokeza kwamba bado kulikuwa na majadiliano zaidi yaliyokuwa yakiendelea na hawakuwa tayari kuzungumzia hilo. Baadaye, simu zao zilikuwa hazipokelewi. Diamond alikuwa amesemaje? Diamond, akiandamana na mwenzake Rayvanny na Queen Darleen, aliwaambia wanahabari Nairobi kwamba waliiandikia serikali barua kueleza kwamba walikubali walikuwa wamekosea kuucheza wimbo wa Mwanza uliofungiwa kwenye shoo yao eneo la Mwanza mwishoni mwa wiki. Kwenye barua hiyo, walijitetea kwamba awali, hawakuwa wameucheza wimbo huo kwenye shoo zao. Kinachozua utata ni iwapo barua hiyo yenyewe iliandikiwa Basata au iliandikiwa taasisi nyingine za serikali. Kwa jumla walitakiwa kulipa faini ya Tshs 9 milioni, Diamond, Rayvanny na wasafi Limited kila mmoja akilipa shilingi milioni tatu. Basata wenyewe bado hawajazungumzia hilo. Kadhalika, walieleza kwamba marufuku dhidi yao ingewaharibia sifa na pia kuwasababishia hasara kutokana na tamasha zao walizokuwa wameandaa kipindi hiki cha sikukuu. “Na tukawaambia pia kwamba tuna shoo nyingine ambazo ziko Kenya, na sehemu tofauti ambazo tayari zishalipwa (tiketi zishalipiwa),” amesema Diamond. “Kwa hivyo, tusipotumbuiza pia tutatengeneza picha mbaya, pia na hasara kwa sababu pia sisi tunafanya biashara.” Diamond, ambaye jina lake halisi ni Nasibu Abdul Juma Issaack na Rayvanny ambaye jina lake halisi ni Raymond Shaban Mwakyusa, wamepanga shoo kadha nchini Kenya chini ya Wasafi. Jumatatu 24 Desemba watakuwa mjini Embu, kisha watumbuize Mombasa tarehe 26 Desemba kabla ya kurejea Nairobi Mkesha wa Mwaka Mpya. Diamond ana shoo pia visiwani Comoro mnamo 28 Desemba. Basata ni nani hasa? Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984. Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini Tanzania. Dira yake ni Kuwa chombo chenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa huduma bora kitaifa katika maendeleo ya sanaa, na Lengo la e kuu ni Kufufua, kukuza na kuongeza maendeleo ya utengenezaji wa kazi bora za sanaa. Maadili ya msingi ya Baraza la Sanaa la Taifa, kama yalivyoelezwa kwenye tovuti yake, ni "kuhimiza na kukukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania, kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu na kuchochea ubunifu na uvumbuzi katika sanaa", na katika hili, limepania kuhimiza na kukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania, kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu na kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika sanaa. Mwenyekiti wa bodi ya BASATA ni Bw Habbi Gunze aliyeteuliwa na Rais Magufuli mnamo 1 Oktoba. Wajumbe watano wa bodi ya baraza hilo Dkt Emmanuel Mwesiga Ishengoma, Bw Hamis Mwinjuma, Dkt Saudin Jacob Mwakaje, Bw Single Mohammed Mtambalike na Dkt Asha Salim Mshana ambao wana dhamana ya kuhudumu hadi mwaka 2021. Utata umegubika kilichotokea hadi wanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny waliokuwa wamefungiwa kufanya maonesho ndani ya nje ya Tanzania wakaondoka nchini humo kwenda Kenya. text: Rais Eli Avivi, akiwa Achzivland mwaka 2006 Aliongoza taifa hilo zaidi la Achzivlabd lenye watu wawili kwa karibu nusu karne. Taifa hilo dogo lililo kaskazini mwa Israel karibu na mpaka na Lebanon, liliwavutia watu mashuhuri wakiwemo Sophia Loren. Licha ya kutotambuliwa kimataifa, lina bendera yake na wimbo wa taifa. Aviv ameacha mjane ambaye pia ndiye raia pekee wa Achzivland Rina, 71, ambaye alithibitisha kifo chake mapema Jumatano. Dada yale aliambia mtandao mmoja wa habari nchini Isreal kwa amekuwa akiugua kichomi. Eli Avivi alikuwa ni nani? Alizaliwa huko Persia na kuhamia eneo lililokuwa linatawaliwa na Uingereza la kipalesina akiwa na umri wa miaka mwili. Alijunga na jeshi na wanamaji la kiyahudi lililofahamika kama the Palyan akiwa na miaka 15 na kupigana dhidi ya jeshi la Uingereza na baadaye dhidi ya vikosi vya kiarabu wakati wa vita vya mwaka 1948. Eneo lililokuja kuwa Achzivland kilikuwa ni kijiji cha uvuvi cha kipalestina kinachofahamika kama al-Zeeb ambacho wakaazi wake walikimbia wakati kilishindwa mwaka 1948. Avivi aligundua eneo hilo miaka minne baadaye na kuishi kwenye majengo yaliyokuwa yameharibiwa akiendelea na maisha akiuza samaki. Baadaye Rina aliwasili na na Avivi akamuoa. Wawili hao waliendelea kuwa na matatizo na Israel kuanzia miaka ya sitini wakati serikali iliamua kubadili eneo hilo kuwa mbuga ya taifa na kutuma tinga tinga kubomaa majengo. Hali iligeuka kuwa mbaya wakati mamlaka ziliweka ua kulizingira eneo hilo na kumzuua Avivi kulifikia. Akipinga hilo Eli na mke wake walichana pasipoti zao na kutangaza uhuru kutoka Israel mwaka 1971. Kukamatwa kwao na kesi dhidi yao vilisababisha wapate umaarufu mkubwa pamoja na eneo la Achzivland. Wawili hao baadaye wakaafikia makubaliano na Israel kulipa kuweza kuingia eneo hilo. Wajitengenezea pasipoti zoa na wangeweza kupiga muhubi zile za wageni ambao wangezuru eneo hilo la ekari 3.5. Miaka iliyofuatia, wageni kutoka kote duniani walizuru moja ya nchi ndogo zaidi duniani isiyotambuliwa. Hatma ya Achzivland ni ipi? Haijulikani kile kitafuatia bila ya kuwepo raia wake. Wakati wa mahojiano na BBC mwaka 2015 Avivi alisema hakufikiri alikuwa na miaka zaidi ya kuishi. Alisema alitumai Rina atabaki eneo hilo lakini pia ulikuwa ni uamuzi wake. Anataka eneo hilo kuwa makumbusho kwa mumewe anayemtaja kuwa rais bora zaidi kuwai kuwepo. Ramani ya Achzivland Mmoja wa watawala wa miaka mingi zaidi huko Mashariki ya Kati amefariki dunia akiwa na miaka 88 lakini Eli Avivi hakuwa rais wa kawaida tu. text: Katika moja ya hifadhi kubwa ya wanyama pori barani Afrika Simba wameamua kuchukua fursa hiyo kujipumzisha barabarani. Msimamizi wa hifadhi ya Kruger nchini Afrika Kusini Bw. Richard Sowry siku ya Jumatano, alipokuwa katika operesheni ya kikazi alikutana na kundi kubwa la Simba waliokuwa katika usingizi mzito katikati ya barabara tofauti na hali ya kawaida ambapo watalii au wageni ndio wengi barabarani. Lakini hifadhi ya Kruger, kama ilivyo hifadhi nyingine zimefungwa tangu Machi 25, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na virusi vya corona. Walinzi wa hifadhi hiyo wanasema kwa kawaida simba huwa wanaonekana barabarani nyakati za usiku. Picha hii ilipigwa vipi? Bw Sowry alikuwa anaendelea na shughuli ulinzi kuangalia kama wawindaji pori hawavamii wanyama katika muda wakati huu wa marufuku ya kutoka nje. Simba ambaye ana umri mkubwa zaidi ni miaka 14, hivyo wamezoea kuona magari.Kwa kawaida bwana Sowry huwa anawaona simba wakiwa wamelala katika barabara za hifadhi wakati wa usiku katika majira ya baridi. Wakati alipokuwa akiendesha gari karibu na hifadhi majira ya mchana siku ya Jumatano, aliwaona samba wakiwa wamejaa barabarani wakiwa wamelala jambo ambalo si la kawaida,hivyo ilimbidi arudi nyuma kama mita tano na kuwangalia. Wakati akipiga picha kwa simu yake, Simba hao hata walikuwa hawajishughulishi kwanza wengi walikuwa katika usingizi mzito. "Simba wamezoea watu wakiwa kwenye magari," alieleza. "Wanyama wote huwa wanaogopa watu wakiwa wanatembea, hivyo kama ningetembea wasingeweza kuniruhusu." Kitu ambacho askari pori hawataki ni kuona simba kudhani kuwa barabara ziko salama kwa wao kupumzika. Marufuku dhidi ya Corona imeathiri hifadhi za wanyama kiasi gani? Nyakati hizi simba wanakuwa wanaonekana wakiwa maeneo ya wazi kama mbwa pori katika hifadhi lakini kwa upande mwingine bwana Sowry anadhani kuwa marufuku ya kuzuia watu kutoka nje haiweza kuleta mabadiliko makubwa katika tabia za wanyama pori. "Hifadhi ya Kruger ni eneo la pori sana," alisema. "Limekuwa eneo la wanyama pori na litaendelea kuwa eneo la wanyama pori." Anafurahia kuwashirikisha watu kuona picha zake kwa sababu sasa watu hawawezi kwenda kwenye mbuga za wanyama kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona. "Hii hali ni ngumu sana kwa kila mtu na lengo langu ni kuwapa watu furaha," alisema. Siku ambayo Afrika Kusini ilirikodi vifo 34 vya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na idadi ya watu wenye maambukizi kuwa 2,506 na kufanya taifa hilo kuwa ndio lililoathirika zaidi barani Afrika. Marufuku ya kutotoka nje nchini, imeongezwa kwa muda wa wiki mbili nchini Afrika Kusini. "Kila mtu ameelewa umuhimu wa marufuku hiyo na walinzi wa wanyama pori wapo kazini kufanya kazi zao za kila siku," alisema afisa wa habari Isaac Phaala. Kwa upande wao simba, aliongeza, "kawaida wapo porini kwa sababu na sasa wanafurahia maisha kwa sababu wana uhuru wote, hakuna watu wanaokuja kuwaona". Lakini katika mbuga yeyote ya wanyama, unadhani ukiuliza simba anapenda kukaa kwenye lami au kwenye nyasi? Lakini labda kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Jumanne, ndio maana waliona bora kukaa kwenye lami kwa wakati huo kwa sababu simba hawapendi unyevunyevu yaani simba hawapendi kukaa katika maji. Wakati huu ambapo baadhi ya mataifa ya Afrika yameweka marufuku ya kutotoka nje ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corano, bila shaka wanyamapori wamegundua kuwa watu wameondoka. text: Aliziambia nchi zote mbili, China na Ukraine kumchunguza bwana Biden ambaye ni kinara wa chama cha Democratic anayetaka kuwania urais, na mtoto wake. "China inapaswa kuanza kumchunguza Biden," alisema Trump. Democrats imemshutumu rais Trump kwa madai ya kutoa msaada wa kijeshi kuwa njia ya kumfanya aweze kuibua mabaya ya bwana Biden. Bwana Biden alijibu kupitia ukurasa wake wa tweeter kuwa Trump ana wazo la kumshambulia mtu yeyote mwenye msimamo ni utani. Mazungumzo ya simu kati ya rais Trump na kiongozi wa Ukraini rais Volodymyr Zelensky,Julai 25 yalipelekea wapelelezi kupeleka taarifa zinazoweza kumuondoa Trump madarakani. Ingawa siku ya alhamisi, rais Trump alidai kuwa madai hayo ni upuuzi. Katika ujumbe wake wa usiku wa manane kupitia kurasa yake ya Tweeter, Trump aliongeza kuwa yeye ana jukumu la kuchunguza kashfa za rushwa, jambo ambalo linajumuisha na kuuliza na kutoa mapendekezo kwa nchi jirani kutoa msaada. Trump anamshutumu nini Biden? Trump anamshutumu bwana Joe Biden na mtoto wake Hunter kwa kashfa za rushwa katika mikataba yao ya kibiashara na kisiasa nchini Ukraine na China , bila ya kutoa ushaidi wa kuthibitisha madai yake. Wakati ambao Hunter Biden alipoingia katika mkataba wa gesi asilia katika katika kampuni ya Burisma mwaka 2014, maswali mengi yaliibuka kuwa anaweza kuleta mgogoro kisiasa na baba yake. Ukraine ilikuwa inakabiliana na mgogoro wa kisiasa baada ya kiongozi wake kulazimishwa kuondoka madarakani, huku Biden alikuwa katika ngazi za juu za utawala wa Obama. Mwaka 2016, Joe Biden aliisukuma serikali ya Ukraini kumfukuza mwendesha mashitaka Viktor Shokin, ambaye ofisi yake ilikuwa inaichunguza kwa karibu mmiliki wa kampuni ya Burisma. Katika hotuba yake mwaka jana bwana Biden alijisifia kwa kumfukuza bwana Shokin na kutishia kutotoa mkopo wa mamilioni ya fedha kwa Ukraine. Bwana Trump na washirika wake wanamshutumu bwana Biden kwa kumlinda mwanae. Hata kama maafisa wengine wa serikali ya Ukraine pia walitaka bwana Shokin kuondoka madarakani kwa sababu ya jitihada zake za kukabiliana na rushwa. Wiki iliyopita mwendesha mashtaka nchini Ukraini ambaye alichukua wadhifa wa bwana Shokin aliiambi BBC kuwa hakuna ushaidi wa uovu alioufanya bwana Joe au Hunter Biden. Trump alijibu nini kuhusu shutuma zinazomkabili Trump alpohojiwa kuhusu mazungumzo yake ya simu na rais wa Ukraini bwana Volodymyr Zelensky alijibu kuwa jibu ni rahisi kuwa ; "Nilidhani kuwa wameanza kufanya uchunguzi tayari kama kweli walikuwa na nia njema basi wangeanza kumchunguza Biden," "Wanapaswa kumchunguza Biden" alisema Trump wakati alipohojiwa na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani. "Vilevilevile, China pia inapaswa kuanza kumchunguza Biden kwa sababu kile kilichotokea China ni sawa na kile kilichotokea Ukraine", Trump aliongeza. Trump alipendekeza tena bila kutoa ushaidi wowote dhidi ya Biden na kwa kudai uhusiano wa kibiashara kati ya Biden na mataifa hayo mawili, China na Ukraine . Mkuu wa tume ya uchaguzi aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kuhusisha madai ya nchi za kigeni katika uchaguzi wa Marekani. Biden ametoa majibu gani? Msemaji wa bwana Biden wa kampeni za mwaka 2020 amemshutumu Trump kwa kutumia vibaya televisheni ya taifa kwa taarifa za kusadikika. Naye msemaji wa Hunter Biden ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa kiwango cha dola bilioni 1.5 ni hesabu ya uongo, hawawahi kupokea fidia yoyote ya malipo ya kiwango hicho cha fedha katika kiwanda chochote China. Bidens alifanya nini China? Mwaka 2013, bwana Biden alipokuwa makamu wa rais alipofanya ziara ya kiofisi nchini China na kukutana na rais wa nchi hiyo Xi Jinping. Hunter Biden na binti yake waliongozana naye. Biden alikuwa makamu wa rais wa kwanza kuongozana na familia yake katika shughuli za kikazi. Katika ziara hiyo ya siku mbili , Hunter alikutana mfanyakazi wa benki wa nchini humo, Jonathan Li, ambaye baadae akawa mshirika wake katika biashara. Bwana Li alipata ufadhili binafsi muda mfupi tu baada ya ziara hiyo ingawa msemaji wa Hunter alikiambia chombo cha habari cha NBC News kuwa hawakujadili masuala yoyote ya kibiashara katika ziara ile na ufadhili ulikuja miezi michache baadae. Hunter amekanusha kuwa na mkutano wowote kuhusu biashara na afisa wa China. Athari za uchunguzi dhidi ya Trump Uhalifu anaoshutumiwa nao Trump unaweza kumuondoa rais madarakani, na unapitia hatua mbili za mchakato wa kisiasa. Kama kura za wawakilishi hazitatosha, basi bunge la seneti litalazimika kusimamia kesi hiyo. Kura ya seneti inahitaji walau wingi wa theluthi mbili ya wingi - na inaweza kushindwa kwa sababuchama cha Trump kina maseneta wengi zaidi. Ni marais wawili tu katika historia ya Marekani ambao ni Bill Clinton and Andrew Johnson ambao walikabiliana na kesi ya namna hiyo na hakuna kati yao ambaye alishtakiwa au kuondolewa madarakani. Rais Nixon alijiondoa madarakani kabla ya kung'olewa na bunge. Rais wa Marekani Donald Trump ambaye tayari anakabiliwa na shutuma inayoweza kumuondoa madarakani baada ya kumtaka rais wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake Joe Biden, na sasa inasemwa kuwa aliwatakata China wafanye vivyo hivyo. text: Abiria waliokuwa wakiwasili nchini Kenya kutoka China walikuwa wakipimwa mwisho wa mwezi Januari Nchini Kenya , wafanyakazi wa China wamefukuzwa kutoka vituo viwili vya ujenzi huku wengine wakitukanwa kuhusiana na virusi vya corona. Wachina ambao wamekuwa wakiendesha biashara wame torokwa na wateja hatua inayosababisha kufutwa kazi kwa baadhi ya wafanya kazi wa bishara hizo. Kanda moja ya video ambayo imekua ikisambaa nchini Kenya kuhusu raia wawili wa China wanaobaguliwa kwasababu ya hofu ya ugonjwa wa virusi vya corona katika mtaa wa mabanda imezua hisia kali katika mitandao ya kijamii. Wengine wameambia BBC kwamba hata madereva wa teksi wamekuwa wakikataa kuwabeba kwa hofu ya maambukizi ya virusi hivyo vilivyoanza mjini Wuhan huko China. Hatua hii inajiri baada ya baadhi ya raia wa China kufukuzwa katika viwanda vya ujenzi huku wiki iliopita wengine wao wakivamiwa na kutishwa kufurushwa majumbani mwao. Guu Shajar , raia wa China ambaye ameishi Kenya miaka sita alikuwa nchini China kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita lakini alipokuwa katika safari yake ya ndege kutoka Ghana amedai kwamba alibaguliwa na kunyanyaswa na maafisa katika uwanja wa ndege wa JomoKenyatta Nairobi licha ya kutimiza maagizo yote aliopewa. ''Kulikuwa na majibizano makali, mwanamke aliyekuwa katika kituo cha afya alisema hawezi kukiachilia cheti changu cha afya huku abiria wengine wakisalia katika foleni kwani waliamua kubishana badala ya kufanya kazi yake. Walinipigia kelele wakisema kwamba hii ni Kenya'', alisema. ''Najua mimi sio wa kwanza na wa mwisho kubaguliwa kwasababu raia wengi wa bara Asia wanaoishi katika mataifa ya Afrika hawapendi fujo''. Lakini maafisa katika uwanja huo wamepinga madai hayo ya ubaguzi wakisisitiza kuwa wasafiri wote huchukuliwa na kuhudumiwa sawa pamoja na kupewa heshima. Baadhi ya wakenya wakifanya kampeni kuzuia ndege kutoka China kuingia nchini mwao Vilevile migahawa na biashara zinazomilikiwa na raia wa China zimekuwa na wakati mgumu kupata wateja kutokana na hofu hatua inayowafanya watu wengi kukataa kwenda katika maeneo hayo. Huku safari zote za moja kwa moja kati ya Kenya na China zikisimamishwa , wateja wa kawaida kutoka bara Asia wamekuwa nadra kupatikana. Huwei ni mmiliki wa hoteli nchini Kenya kwa zaidi ya miaka sita na sasa anasema kwamba anatafakari iwapo anaweza kuwafuta wafanyakazi wake kutokana na biashara mbovu. ''Tumepoteza miezi miwili bila wageni kutoka bara Asia, Tumepoteza wageni kutoka Ulaya na Marekani na baada ya kuwapoteza wageni hao soko la nchini limekuwa likiyumba yumba'', aliongezea. Februari 27, ujumbe ulisambaa katika mtandao wa Facebook, ukidai kuwa mbunge mmoja wa Kenya ametaka wananchi wa jimbo lake kuepuka kuwa na muingiliano na raia wa China ambao wamerejea kutoka kwao baada ya sherehe za mwaka mpya wa China. Ujumbe huo ulionya kuwa kama serikali haitawalinda raia wake, basi watalazimika kuwaweka raia wote wa China katika karantini. Na vilevile wananchi watakuwa na ruhusa ya kumkimbiza yeyote kwa mawe katika jimbo lao. Ubalozi wa China' ulijibu madai hayo haraka kwenye kurasa ya Twitter kutaka jumuiya za watu kutoka China kulindwa na watu kuacha ubaguzi. Si Kenya peke yake ambayo ilionyesha chuki ya aina hiyo bali kuna mataifa mengine ya angwa la sahara ambayo yanahusisha wasafiri waliotoka China. Huku kukiwa hakuna unyanyapaa wa aina hiyo kwa wageni kutoka ulaya. Kabla ya Kenya haijarekodiwa kwa kesi hiyo lakini chanzo cha hayo yote ni hofu na mchanganyiko wa unyanyapaa. Huku dunia ikiendelea kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona katika mataifa tofauti, raia wa China na bara Asia wanakabiliwa na ubaguzi wa rangi. text: Chelsea 4-0 Man United The Blues ,ambao walimfuta kazi Jose Mourinho kwa mara ya pili mwaka uliopita waliongoza kunako sekunde ya 30 ya mchezo kuanza baada ya Pedro kupata mwanya katika safu ya ulinzi ya Man United. Gary Cahill alifunga bao la pili katika kipindi cha pili baada ya United kuruhusu kona iliopigwa na Eden Hazard kudunda katika eneo la hatari la man United. Chelsea ikikabiliana na Man United katika uwanja wa stamford Bridge United hawakuonyesha ishara yoyote ya kukomboa mabao hayo ,na hivyobasi wakaongezwa bao la tatu na Eden hazard baada ya mchezaji huyo kupiga mkwaju wa umbalii wa maguu 15. N'golo Kante aliimwaga safu ya ulinzi ya United na kufunga bao la nne na la mwisho na kuipatia ushindi Chelsea huku ikipanda hadi nafasi ya nne. United watasalia katika nafasi ya 7 huku pengo kati yao na viongozi wa ligi likiongezeka na kufikia pointi tano. Wakati huohuo viongozi wa Ligi Manchester City walitoka sare na Southampton katika uwanja wa Etihard. Jose Mourinho alifedheheshwa aliporudi katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya timu yake ya zamani kuicharaza Manchester United. text: Kauli ya Assad imeripotiwa kutolewa a;ipokutana na Balozi mpya wa Korea Kaskazini nchini Syria Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011 Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini. Wachunguzi wa kemikali kuruhusiwa Douma, Syria Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un." Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ulianza mwaka 1966 na kutuma vikosi na silaha wakati wa vita vya Arab na Israeli mwezi Oktoba mwaka 1973 Ripoti ya Umoja wa mataifa ilivuja mwezi Februari ikishutumu Korea Kaskazini kwa kufanya safari za meli takriban 40 kuelekea Syria kati ya mwaka 2012 na 2017, meli zinazodaiwa kubeba acid, mipira na bidhaa nyingine zinazodaiwa kuw zinaweza kutengeneza silaha za kemikali. Assad ameshutumiwa kutumia silaha za kemikali wakati wa vita vya miaka saba nchini humo lakini amekana kuwa na kemikali hizo. Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza. text: Rais Trump aliwatembelea wahanga na mamlaka waliohusika na shambulio Florida wiki iliyopita Taarifa imesema amezungumza na Seneta wa chama cha Republican John Cornyn kuhusu mswada wa vyama viwili alioiwasilisha. Mswada huo wa mwaka 2017 unalenga kuboresha vibali vya serikali ya shirikisho vitakavyopitshiwa kabla ya mtu kununua bastola. Hii inakuja baada ya mamlaka kusema kuwa mtuhumiwa katika shambulio ya shule jimboni Florida alinunua silaha ya kihalali. Shirkia la taifa la Ukaguzi wa Uhalifu kwa sasa unategemea maafisa wa jimbo na serikali kuu kuripoti mtu yeyote mwenye historia ya uhalifu au mwenye matatizo ya akili anayejaribu kununua silaha. Wanafunzi wakiokolewa Udhaifu wake uligundulika mwaka jana baada ya kikosi cha anga cha Marekani walikubali kwamba walikosa kuchukua hatua dhidi ya mshambuliaji mwenye historia ya uhalifu kabla alipowapiga risasi na kuwaua watu 27 katika kanisa la Sutherland Springs, Texas. Baada ya shambulio hilo, mswaha huo wa vyama viwili uliwasilishwa na Bw Cornyn na Senata wa Demcrats Chris Murphy. Msimamo wa Bw Trump juu ya udhibiti wa silaha umebadilika mara kwa mara, lakini aliwania rais kama mgombea anayepinga udhibiti wa silaha mwaka 2016 Mwaka jana Rais aliwaambia shirika la taifa la silaha ,NRA kwenye mkutano kuwa "hangewahi kabisa kuingilia" haki za kikatiba ya umiliki silaha. Awali alilaumu FBI na hali ya afya ya kiakili ya mshambuliaji kwa shambulio ya shule huko Florida lakini hakutoa tamko lolote kuhusu wito mpya wa wanafunzi kudhibiti silaha. Rais wa Marekani Donald Trump "anaunga mkono" jitihada za kuboresha ukaguzi wa manunuzi wa wamiliki silaha, Ikulu ya Whitehouse imesema. text: Bw Odinga na Bw Mudavadi Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga alikuwa ameahidi kwamba angetangaza ni hatua gani atachukua leo baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Ijumaa, ambapo mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi. Ajenti mkuu wa Nasa Musali Mudavadi amesema sasa muungano huo unapanga kutoa tangazo kesho Jumatano. "Tunasikitika kwamba mashauriano yanachukua muda mwingi kuliko ilivyotarajiwa na Nasa kwa hivyo hawataweza kuwahutubia Wakenya kama walivyotarajia leo." Bw Mudavadi hata hivyo amesema mashauriano "yanaendelea na yanaendelea vyema". Rais Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224. Hapo jana, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake kususia kazi kabla ya kutoa tangazo kubwa leo. Watu wengi hata hivyo walionekana kupuuza wito wa kususia kazi. Baada ya kutokea kwa maandamano katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi na mji wa Kisumu, hali ya utulivu ilianza kurejea Jumatatu. Viongozi wa muungano huo wa upinzani wanadai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na watu wenye uhusiano na serikali ya Jubilee na kwamba watu hao waliingilia na kuchakachua matokeo kumfaa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa akishindana na Bw Raila Odinga kwa mara ya pili. Tume ya uchaguzi ilisema mwanzoni ilikuwa haina taarifa kuhusu udukuzi kama huo lakini kwamba ingelifanya uchunguzi. Saa chache baadaye, tume hiyo ilisema hakuna jaribio lolote la udukuzi lililokuwa limefanyia katika sava ya matokeo ya uchaguzi. Muungano wa upinzani pia umeikosoa IEBC kwa kutoa matokeo ya urais bila kuwasilisha fomu za kutangazwa kwa matokeo katika vituo vya kupigia kura na pia katika maeneo bunge, Fomu 34A na Fomu 34B. Muungano huo umesema hautaenda kortini kupinga matokeo ya uchaguzi huo. Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) umeahirisha kikao cha kutoa tangazo kuhusu mweleko wa chama hicho kufuatia uchaguzi mkuu wa Jumanne wiki iliyopita. text: Javier Darroux Mijalchuk, kushoto, amkumbatia mjombake Roberto Javier Darroux Mijalchuk alikuwa na miezi minne wakati babake na mamake aliyekuwa mja mzito walipotoweka huko Buenos Aires. Baadaye aliasiliwa na familia ambayo haikujua kuhusu wazazi wake. Lakini miaka michache iliyopita, alianza kuingiwa na shaka kuhusu utambulisho wake asili, na akaomba usaidizi kutoka shirika la haki za binaadamu 'Grandmothers of the Plaza de Mayo'. Kundi hilo huwatafuta watoto wa vizazi vya watu waliouawa au kutoweshwa kwa lazima wakati wa utawala wa kidikteta wa kijeshi, uliodumu tangu 1976 hadi 1983, na huwakutanisha na wazazi wao. Darroux, mjombake Roberto na Estela de Carlotto, rais wa shirika la Grandmothers of Plaza de Mayo, wanashikilia picha za wazazi wake Darroux Darroux ni mtoto wa 130 ambaye shirika hilo lilifanikiwa kumtambua baada ya kufanya vipimo vya DNA. Akizungumza na waandishi habari, alimshukuru mjombake Roberto Mijalchuk, ambaye anasema alikuwa akimtafuta kwa miaka arobaini iliyopita. "Kujulikana upya kwa utambulisho wangu ni heshima kwa wazazi wangu, jambo linaloniliwaza, ni ishara ya kumbukumbu, ukweli na haki," amesema Darroux. "Ni kiashiria kwamba, kama inabidi nieleze kwa kutumia wakati, hakuna muda muhimu maishani mwangu kama nilipomkumbatia mjombangu, ambapo baada ya kunitafuta kwa miaka 40 alichoweza kuniambia ni: 'Wewe ni Javi?' na alinikumbatia kama vile ambavyo hakuna mtu amewahi na hakuna atakayewahi kunikumbatia kwa namna hiyo." Ameongeza kwamba sasa atajaribu kutafuta taarifa zaidi kuhusu wazazi wake, Juan Manuel Darroux na Elena Mijalchuk. Takriban watu 30,000 waliuawa na jeshi la junta nchini Argentina. Mwanamume ambaye wazazi wake walitekwa na majasusi mnamo 1977 amekutana na familia yake kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. text: Watu 98 wamegundulika kuwa na virusi katika nchi nyingine 18. Wote wanatoka katika familia moja na sasa wanapata matibabu. Hakuna taarifa iliyotolewa zaidi kuhusu familia hiyo na wapi wanapopatiwa matibabu. Takriban watu 213 nchini china wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo, hasa kutoka mjini Hubei, huku kukielezwa kuwa na watu 10,000 walioathirika nchi nzima. Watu 98 wamegundulika kuwa na virusi katika nchi nyingine 18. Shirika la afya duniani limetangaza mlipuko wa virusi vya corona ni janga duniani. Kwa sasa, raia 83 wa Uingereza na 27 wa mataifa ya kigeni wanarejea Uingereza kutokea Wuhan, mji ambao ni kitovu cha mlipuko nchini China. Abiria hao watawekwa karantini katika hospitali ya Arrowe Park kwa majuma mawili. Profesa Chris Whitty , afisa mkuu wa matibabu nchini England alisema: Idara ya afya nchini Uingereza imejiandaa vya kutosha na ina uzoefu wa kuzuia maambukizi na tayari tunafanya kazi mara kwa mara kutambua wale waliokaribiwa na wagonjwa ili kuzuia maambukizi zaidi. Tumejiandaa kuzuia visa vya Uingereza vya ugonjwa wa virusi vya Corona na tuna njia nyingi za dharura kukabiliana na virusi hivyo, aliongezea. Profesa Whitty alisema kwamba Uingereza inafanya kazi kwa karibu na shirika la Afya duniani WHO pamoja na jamii ya kimataifa huku mlipuko huo nchini China ukiendelea ili kuhakihs akuwa tuko tayari kwa lolote litakalotokea. WHO lilitangaza virusi hivyo kuwa janga la dharura duniani siku ya Alhamisi. Idadi ya visa vya virusi vya Corona duniani sasa imepita mlipuko wa virusi vya SARS., ambayo vilisambaa kwa zaidi ya mataifa 18 mwaka 2003. Kufikia sasa raia 83 wa Uingereza na wengine 27 raia wa kigeni wanasifiri kurudi nchini Uingereza kutoka Wuhan , mji wa China ambao ndio chanzo cha mlipuko huo. Ndege hiyo inatarajiwa kutua katika kambi ya wanahewa ya RAF Brize Norton. Abiria wa Uingereza baadaye watapelekwa hadi hospitali ya Arrowe Park na kutengwa kwa wiki mbili. Watu wawili wamegundulika kuwa na virusi vya corona nchini Uingereza, mkuu wa idara ya afya nchini humo ametangaza. text: Ndege aina ya Boeing MAX 8 ilikuwa imehudumu chini ya mwaka mmoja Ndege hiyo aina ya Boeng 737 MAX 8, ilikua mpya. Hii ni ajali ya kwanza kuhusisha ndege aina hiyo. Maelezo kuhusu nini hasa kilitokea yamekua finyu lakini chanzo cha ajali hiyo kitajulikana baaada ya uchunguzi kufanywa. Ajali ya ndege mara nyingi husababishwa na mchanganyiko wa mambo tofauti ikiwa ni pamoja na hitilafu ya kimitambo au makosa ya kibinadamu-lakini je ndege mpya inawezaje kuanguka? Ndege hiyo ya Boeng 737 MAX 8 iliyohusika katika ajali siku ya jumatatu ilikuwa imehudumu kutoka mwaka Agosti 15 mwaka 2017 Kwa mujibu wa mkuu wa tume ya kitaifa ya usalama wa uchukuzi wa angani Soerjanto Tjahjano ndege hiyo ilikua imesafiri kwa saa 800. Inasemekana rubani aliomba waelekezaji wa ndege katika uwanja wa Jakarta wamruhusu kurudi uwanjani hapo muda baada ya kupaa. Sasa imebainika ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu ya kimitambo siku ya Jumapili. Stakabadhi za kunakili hali ya kimitambo ya ndege iliyppatikana na BBC, katika uwanja wa ndege wa Denpasar mjini Bali - zinaashiria kuwa mtambo wa kudhibiti kasi ya ndege upande wa marubani ilikua ina hitilafiana. Kutokana na hilo rubani ilipeana udhibiti wa ndege hiyo kwa afisa wa kwanza na kuendelea na safari na hatimaye wakatua salama mjini Jakarta. Lion Air ahaijathibitisha ripoti hizo, lakini huenda ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu isiyojulikana ya kimitambo iliyotajwa na mkuu wa shirika hilo Edward Sirait amesema hitilafu hiyo ilitatuliwa kitaalamu kulingana na kanuni zilizowekwa. Ameongeza kuwa shirika la Lion Air lina ndege 11 za aina hiyo na kwamba hakuna mpango wa kusitisha huduma ya ndege hizo. Ni 'nadra' ndege mpya kupata ajali Mchambuzi wa masuala ya ndege Gerry Soejatman ameiambia BBC kwamba ndege zilizozeeka ndizo zilizopo katika hatari ya kupata ajali lakini pia kuna uwezekano wa ndege mpya kukumbwa na matatizo ya kiufundi. "Ikiwa ndege ni mpya kuna matatizo huchukua muda kujitokeza lakini ikitumiwa mara kwa mara matatizo hayo hugunduliwa na mara nyingi hutatuliwa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.'' Ramani ya mahali ilipoangunga ndege hiyo Mchambuzi mwingine , Jon Ostrower wa jarida la The Air Current, amesema "Kila wakati kunatokea matatizo madogo ambayo ni ya kawaida lakini si matatizo ambayo yanaweza kutishia usalama wa ndege". Ameongezea kuwa uzuri wa ndege mpya ni kuwa imekaguliwa vilivyo kwa sababu kila kitu ni kipya. Wachambuzi wote wawili wanasema ni mapemno kubaini kilichosababisha ajali ya ndege JT 610. Bwana Ostrower aliiambia BBC "Sijui ni kitu gani kitaifanya ndege mpya kama hii kuanguka," "Kuna vitu vingi vinavyoweza kuchangia ajali kama hii." Kwa upande wake Bwana Soejatman amesema anaamini huenda "chanzo cha ajali hii isiwe matatizo ya kiufundi japo ni mapema kubaini hilo". Wataalamu Iwanaamini huenda utepetevu wa usalama wa angani kama vile makosa ya kibinadamu nchini Indonesia, huenda umechangia mkasa wa siku ya Juma tatu. Shirika la Boeing limeelezea kusikitishwa kwake na kisa cha kupoteza ndege yake. Limetuma rambi rambi zake kwa jamaa za wahasiriwa wa mkasa huo na kuongeza kuwa itashirikiana katika uchunguzi wa kubaini nini hasa kilichotokea. Kwa mujibu wa shirika hilo ndege aina ya 737 MAX imekua ikinunuliwa sana katika historia yake na kwamba karibu ndege 4700 ilikua tayari imeagizwa. MAX 8 ilikuwa imeagizwa na mashirika kadhaa ya ndege ya American Airlines, United Airlines, Norway na FlyDubai. Ndege ya shirika la Lion Air iliyoanguka baharini, ikiwa na abiria karibu 190 muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu wa Jakarta nchini Indonesia imeendelea kuvutia hisia mbali mbali. text: Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao,mkuu wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na kanda ya Afrika mashariki kwa ujumla. ''Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla. Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa'' anasema Dkt. Moeti. WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona. Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya. ''Moja ya makubaliano ya wanachama ni kutoa takwimu za mwenendo wa ugonjwa, nimewakumbusha serikali ya Tanzania na ninayo kumbukumbu kwa maandishi kuwa wao ni sehemu ya wanachama hivyo wanatakiwa kuitikia wito huu. Tuna imani kuwa mawasiliano yetu kuhusu chanjo yatazingatiwa ili kukabili maambukizi ya virusi," ameongezea Dkt. Moeti. Naye katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasema anaunga mkono alichosema @MoetiTshidi, anatoa rai hatua dhabiti za kiafya kukabiliana dhidi ya corona zinapaswa kufuatwa na kujiandaa kupokea chanjo. Takwimu ni suala la muhimu pia kwa Tanzania kuzitoa , tena baada ya kesi za miongoni mwa wasafiri na wageni katika miezi ya hivi karibuni. Hatua hii ya WHO inakuja siku moja baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli kutahadharisha kuhusu chanjo ya Covid 19 ambayo imeanza kutolewa katika mataifa mbalimbali duniani. Alipozungumza katika uzinduzi wa shamba la miti huko wilayani Chato mkoani Geita, alizungumzia pia kuhusu hali ya corona nchini na kuwasihi wananchi kuendela kuomba pamoja na kujifukiza. ''Tutaendelea kuchukua tahadhari, pamoja na kujifukiza, kusali na kuswali, huku tukiendelea na shughuli zetu, ule vizuri ushibe corona ashindwe kuingia kwenye mwili wako''. Aidha kuhusu uwepo wa aina mpya ya corona Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya Watanzania walienda kupata chanjo huko nje lakini wakaletea aina mpya ya corona. ''Ninajua Kuna baadhi ya Watanzania hata wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na walivyochanjwa wakaja huku wakatuletea corona ya ajabu ajabu''. Alisema Rais Magufuli. Rais Magufuli alisisitiza juu ya madhara ya chanjo, hususani kuwa hakuna chajo za magonjwa sugu ya muda mrefu kama UKIMWI na saratani. ''Tusiwe tunakimbilia masuala chanjo chanjo, si kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima Watanzania tuwe macho, tuwe waangalifu, tutafanyiwa majaribio, tuendelee kumuomba Mungu wetu na tuendelee kuchukua tahadhari''. Tanzania haijatoa takwimu za mwenendo wa Corona tangu mwaka jana mwezi Mei. Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutaka wizara ya afya kutokimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO limeitaka nchi hiyo kujiandaa na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani. text: Burundi ni moja ya nchi maskini zaidi duniani na baadhi ya raia wanasema hawawezi kumudu gharama ya sherehe za harusi Msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani na elimu Terence Ntahiraja amesema amri hiyo itasaidia kile alichokitaja kuwa ni ongezeko la watu nchini Burundi. Amesema mahusiano yasiyo rasmi yamesababisha wasichana wengi wa shule kupata ujauzito na wanaume kupata fursa ya kuwa na mahusiano ya wanawake wengi kwa mkupuo. Rais Pierre Nkurunziza, ambaye ni muumini wa kilokole , hivi karibuni alianzisha kampeni ya kitaifa ya maadili mema . Burundi imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu mwaka 2015 Rais Nkurunziza alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula mwingine. Waziri Ntarihaja ameambia AFP kwamba ndoa zilizorasmishwa kanisani au katika afisi ya serikali ndiyo suluhu pekee kwa tatizo la ongezeko kubwa la watu nchini humo na kwamba ni jukumu la kizalendo. "Tunawataka raia wa Burundi wafahamu kwamba kila mtu anawajibikia maisha yake, na tunataka utulivu na utawala wa sheria humu nchini," alisema. "Juhudi zote zinafanywa kwa kufuata mkakati wa kuwafunza raia wawe wazalendo," alisema, akirejelea mpango huo wa kueneza uzalendo uliozinduliwa na Rais Nkurunziza. Haijabainika ni adhabu gani ambayo watapewa wale ambao hawatakuwa wamerasmisha ndoa zao kufikia mwisho wa mwaka huu. Mkulima mmoja ameambia AFP kwamba maafisa wa serikali tayari wamemtishia yeye na mpenzi wake kwamba watatozwa faini na kwamba mtoto yeyote atakayezaliwa bila wawili hao kufunga ndoa rasmi hawataruhusiwa kufaidi kutoka kwa mpango wa elimu bila malipo au huduma ya matibabu. Mkulima huyo aliyejitambulisha kwa jina moja pekee kama Pierre, alisema ameshindwa kuoa rasmi kwa sababu hangeweza kulipa mahari aliyoitishwa na familia ya mpenzi wake. Mamia ya watu walifariki tangu Bw Nkurunziza alipoanza azma yake ya kutaka kutawala kwa muhula wa tatu mwaka 2015. Lakini miezi ya karibuni, hali ya utulivu imerejea. Watu wanaoishi katika mahusiano ya mume na mke bila kufunga ndoa nchini Burundi wameamrishwa kwamba wawe wameoana rasmi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu la sivyo wataaadhibiwa vikali. text: Felix Tshisekedi (pichani) ni mwana wa waziri mkuu wa zamani na muasisi wa muungano wa upinzani wa UPDS -Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mjini Brussels mwezi wa February mwaka jana Viongozi wa vyama saba vya upinzani wanatarajia kumtangaza mwakilishi wao kufikia Novemba 15 baada ya kuafikiana kuhusu suala hilo katika kikao maalum nchini Afrika Kusini. Wachambuzi wa siasa za Kongo hata hivyo wanatilia shaka uwezekano wa upinzani kukubaliana kumteua mgombea mmoja wa uraisi atakayewaakilisha katika uchaguzi huo ambao utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya demokrasia. Rais Joseph Kabila anaelekea kuondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Chama tawala kimemteua waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary kuwa mgombe wake. Bwana Kabila alitarajiwa kuachia madaraka karibu miaka miwili iliyopita baada ya muhula wake wa pili kumalizika lakini uchaguzi mkuu ukaahirishwa hatua ambayo ilimfanya kuendelea kuwa madarakani. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila Huku hayo yakijiri mamlaka nchini DRC kwa mara ya kwanza zimeruhusu maadamano ya upinzani kufanyika katika mji mkuu wa Kinshasa, leo Ijumaa. Maandamano hayo ni ya yanashinikiza tume huru ya uchaguzi kutotumia mfumo tata wa kielektroniki wakati wa kupiga kura. Upinzani umekuwa ukihofia mfumo huo huonda ukatumiwa kuchakachua uchaguzi. Aliyekuwa mbabe wa kivita na makamu wa raisi wa zamani Jean Pierre Bemba amewasihi wafuasi wake kupinga vikali udanganyifu katika mfumo wa uchaguzi akisema mashini za kielektroniki ambazo tume ya uchaguzi inatumia hazijawahi kutumika popote duniani. Waandamanaji DRC Hata hivyo muungano mkuu wa upinzani onaoongozwa na kiongozi Felix Tshisekedi ambaye atagombea uraisi haushiriki maandamano hayo. Viongozi wawili wakuu wa upinzani, Jean Pierre Bemba na Moise Katumbi, walifungiwa nje ya kinyang'anyiro cha uchaguzi huo ujao. Katika mji wa Lubumbashi ambao ni wa pili kwa ukubwa, kiongozi wa upinzani Moise Katumbi pia alitaka wafuasi wake kuandaman akupinga mashini za kielektroniki za kupiga kura lakini polisi ilitoa onyo kali kwa yeyote atakayeshiriki maandamano hayo. Mwezi uliyopita Rais Kabila aliahidi Umoja wa Mataifa kuwa taifa hilo litafanya uchaguzi huru na wa haki. Jean Pierre Bemba kiongozi mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Hata hivyo miezi kadhaa kabla atangaze kwamba ataondoka madarakani kulishuhudiwa maandamano ya vurugu huku maafisa wa usalama wakitumia nguvu kupita kiasi kuvunja maandamano hayo. Wakosoaji wanahofia Kabila anafanya njama ya kuhakikisha mgombea ,Emmanuel Ramazani Shadary, hakabiliwi na upinzani mkali. Usiku wa Alhamisi maafisa wa usalama waliweka vizuwizi katika barabara kuu ya kuelekea mji mkuu wa Kinshasa na kuanza kufanyia ukaguzi magari Gavana wa jiji la Kinshasa aliidhinisha rasmi maandamano hayo baada ya kukutana na waandalizi wake. Seneta wa Upinzani Jacques Djoli, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waandalizi wa maandamano waliafikiana na polisi kuwa waandamanaji hawatafika wilaya ya Gombe ambao ni makao makuu ya idara nyingi za serikali, balozi za mataifa ya kigeni na biashara za hali ya juu. Mkuu wa polisi wa Kinshasa Sylvano Kasongo alitoa wito kwa waandamanaji kutozua vurugu akisema "Natutaki kuona umwagikaji wa damu wala vifo katika maandamano haya." Moise Katumbi aliondoka DRC mnamo Mei 2016, siku moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake Baada ya mazungumzo ya mjini Johannesburg, wajumbe wa upinzani uliyomeguka wametangaza kuwa watamteua mgombea wa pamoja kufikia Novemba 15. Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kukabiliana na hali ya dharura mnamo mwezi Januari mwaka huu Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuwa inakadiri wapiga kura zaidi ya milioni 46 watashiriki uchaguzi huo. Hata hivyo waandamanaji wanataka tume hiyo kuwaondoa watu zaidi ya milioni 10 katika sajili ya wapiga kura kwasababu hawajasajiliwa kwa mfumo mpya wa kidijitali. Taifa hilo kubwa katika eneo la Afrika ya Kati haijawahi kushuhudia mabadiliko ya uongozi wa amani ya nguvu tangu lijinyakulie uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka wa 1960. Vyama vikuu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vinaazimia kumteua mgombea mmoja wa kiti cha uraisi katika uchaguzi mkuu ujao utakaoandaliwa mwezi Desemba mwaka huu. text: Ni hatua kubwa kwa timu hiyo kwani mwisho walishiriki nusu-fainali mnamo 1990 - baada ya miaka 28. Hii ni baada ya kuitwanga Sweden 2-0 ugani Samara kwenye ngoma ya robo-fainali. Beki Harry Maguire aliiweka three lions kifua mbele dakika ya (30) kupitia kona kipindi cha kwanza kabla ya kiungo Dele Alli kuzidisha la pili dakika ya (58). Goli hilo la Dele Alli limemfanya kuwa Muingereza mwenye umri mdogo zaidi kuipa bao Kombe la Dunia tangu Michael Owen alipofunga akiwa na umri wa miaka (18 na siku 190) wakichuana na Romania,1998). Alli ana umri wa miaka 22 na siku 87. Mashabiki wa Uingereza Ingawa Harry Kane, anayeongoza orodha ya wafungaji Urusi akiwa na mabao 6, hakupata bao, halijamzuia kuisaidia Uingereza kwa kuwashughulisha mabeki wa Sweden, Victor Lindelöf na Andreas Granqvist. Kikosi cha Gareth Southgate kiliwanyamazisha wengi kufuatia uhodari dhidi ya Sweden ambao walikuwa wanakutana na Uingereza kwenye mechi ya tatu Kombe la Dunia. Michuano ya awali kati ya wawili hao iliishia sare ya 1-1 na 2-2 wa mwisho ukiwa 2006, nchini Ujerumani. Kipa wa Uingereza ambaye pia ndiye mchezaji bora wa mechi, Jordan Pickford, alikuwa tegemeo la timu kwa mara nyengine baada ya kupangua mipira iliyoelekea langoni na kudumisha uongozi hadi dakika ya mwisho. "Ni matokeo mazuri, tulitarajia mechi kali dhidi ya Sweden, tulijua walivyojihami, tulikabiliana nao vyema, na kwa makini. Tumejitahidi na kudhihirisha uwezo wetu na juhudi zetu mechini.'' Alisema Pickford. Imekuwa ni siku ya uchungu kwa Sweden kwani safari yao hadi robo fainali haikuwa rahisi. Ilifuzu kutoka kundi hatari lililowajumuisha Ufaransa na Uholanzi kabla kuinyima Italia katika mechi ya kumsaka mshindi. Hata baada ya kuwekwa kwenye kundi moja na Ujerumani, Mexico na Korea, katika Kundi F, Sweden ilimaliza wa kwanza. Kwa sasa Uingereza inamsubiri mshindi kati ya Croatia na Urusi kabla ya kurudisha tabasamu kwa nyuso za mashabiki wake tangu 1966 walipolitwaa Kombe la Dunia. Baada ya kujaribu kwa mara ya tisa, hatimaye timu ya taifa ya Uingereza imefuzu kwa nusu-fainali Kombe la Dunia. text: Paul Manafort amekiri kwamba alikuwa mshauri wa rais wa zamani wa Ukraine Viktor Yanukovych Mbunge wa Serhiy Leshchenko amesema ana ushahidi kwamba Bw Manafort alijaribu kuficha $750,000 (£600,800) alizolipwa na chama kinachounga mkono Urusi mwaka 2009. Msemaji wa Bw Manafort amekanusha tuhuma hizo na kusema "hazina msingi". Bw Manafort alikuwa mshauri wa rais wa zamani wa Ukraine Viktor Yanukovych. Amekanusha kupokea malipo yoyote ya kifedha. Alilazimishwa kujiuzulu kama mwenyekiti wa kampeni wa Bw Trump mwezi Agosti mwaka jana baada ya kufichuliwa kwa uhusiano kati yake na Bw Yanukovych. Bw Manafort ni mmoja wa washirika kadha wa Rais Trump ambao wanachunguzwa kuhusu uwezekano kwamba waliwasiliana na maafisa wa Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka jana. Jumatatu, mkurugenzi wa idara ya uchunguzi wa jinai Marekani (FBI) James Comey alithibitisha kwa mara ya kwanza kwamba idara hiyo inachunguza tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi huo wa Marekani. Jumanne, Bw Leshchenko, ambaye ni mwandishi mpelelezi wa zamani, alichapisha risiti ambayo inadaiwa kutiwa saini na Bw Manafort inayoonesha kwamba alipokea malipo ya $750,000 kama malipo kwa kampuni kwa jina Davis Manafort kwa uuzaji wa kompyuta. Fedha hizo zilitoka kwa kampuni iliyosajiliwa Belize, kupitia benki nyingine iliyopo Kyrgyzstan. Bw Yanukovych aliondolewa madarakani kupitia maandamano makubwa Ukraine mwaka 2014. Mwenyekiti wa zamani wa kampeni wa Rais Donald Trump Paul Manafort anakabiliwa na tuhuma mpya, kwamba alilipwa pesa kisiri kutoka Ukraine. text: Lauren alijiunga na Arsenal kutoka Mallorca mwaka 2000 na akawachezea mechi 159 ligini kwa miaka sita Arsenal watakutana na Southampton katika Ligi ya Premia Jumatano jioni na iwapo watashinda huenda wakapanda hadi nafasi ya tano. Mkataba wa Mfaransa huyo unafikia kikomo mwisho wa msimu huu na amekosolewa sana msimu huu kutokana na matokeo ya klabu hiyo. Lauren, 40, aliambia BBC Africa: "Anafahamu kukabiliana na presha, natumai kwamba mambo yatakuwa sawa hivi karibuni." Lauren alichezea Arsenal mechi 159 ligini kati ya 2000 na 2007 na alikuwa kwenye kikosi kinachosifiwa sana cha "invincibles" (Wasioshindwa) ambacho kilishinda taji la ligi mwaka 2003-2004. Beki huyo wa kulia wa zamani wa Cameroon alisema: "Sidhani (Wenger) atajiuzulu. Amekabiliwa na shinikizo kwa miaka 30-35, akisimamia klabu kubwa zinazokabiliwa na presha." Februari, Wenger alisema angeamua kuhusu mkataba mpya Machi au Aprili lakini baadaye alisema labda alifanya kosa kwa kuahidi watu kwamba angekuwa ameamua hatima yake katika kipindi hicho. Shinikizo hazitamlazimisha meneja wa muda mrefu wa Arsenal Arsene Wenger ajiuzulu, beki wa zamani wa klabu hiyo Laurena mesema. text: Noti za thamani ya rupia 1.2m (£13,300; $17,600) zilikuwa zimechanwa na kuraruliwa na panya katika benki hiyo jimbo la Assam. Polisi wanasema panya hao pengine waliiingia ndani ya mtambo huo kwa kupitia kwenye tundu lililokuwa litumiwe kuingizia nyaya, gazeti la Hindustan Times limeripoti. Picha zinazoonesha pesa zilizokuwa zimetafunwa na panya hao katika mtambo huo wa Benki ya Dola ya India katika wilaya ya Tinsukia zimesambazwa sana kwenye Twitter. Moja inaonesha mzoga wa mmoja wa panya hao kwenye mabaki ya noti hizo. Afisa wa polisi Prakash Sonowal alisema kwamba mtambo huo umekuwa haufanyi kazi kwa siku 12 hizi, gazeti la Hindustan Times limeongeza. Mafundi waliofungua mtambo huo walipata noti za rupia 2,000 na rupia 500 zikiwa zimeharibiwa. Walifanikiwa kunusuru noti za jumla ya thamani ya rupia 1.7 milioni, maafisa wanasema. Unaweza kusoma pia: Mafundi waliofika kuukarabati mtambo wa ATM ambao ulikuwa umeharibika katika jimbo moja nchini India walipigwa na butwaa walipoufungua kubaini tatizo lilikuwa wapi. text: Watoa huduma za afya kwa sasa wanawachanja watu kuzuia kusambaa ugonjwa huo Karibu watu 200 wamefariki dunia tangu Agosti, kwa mujibu wa maafisa, huku zaidi ya 300 wakithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo. Congo imekumbwa na misukosuko ya miaka mingi na jitihada za kukukabiliana ugonjwa huo zimetatizwa na mashambulizi dhidi ya watoa huduma za afya. Wakati huu visa 319 vimeandikishwa na pia vifo 198, waziri wa afya Oly Ilunga alisema. Karibu nusu ya waaathiriwa ni kutoka mji wa Beni, mji wenye wakaazi 800,000 eneo la Kivu Kaskazini, kwa mujibu wa halmashauri ya kitaifa ya afya. Beni Mlipuko wa sasa ndio wa kumi kuikumba Congo na mbaya zaidi tangu ule wa kwanza wa mwaka 1976. Mlipuko wa mwaka 1976 kwa kile kilikuwa ugonjwa usiojulikana ulizua wasi wasi mkubwa lakini ulidhibitiwa na wataalamu walioutambua kwa haraka. Ebola husambaaa kupitia maji maji ya mwila na mara nyingi huwa hatari sana kwa maisha Mlipuko wa saa wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ndio mbaya zaidi zaidi kuwai kutokea katika historia ya nchi hiyo, kwa mujibu wa wizara ya afya. text: ''Yeyote atakayefanya biashara na Iran hataruhusiwa kufanya biashara na Marekani'' , rais huyo alituma ujumbe wa twitter. Vikwazo vikali vilianza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo na vingine vikali vinavyohusiana na mafuta vitaanza mwezi Novemba. Rais wa Iran amesema kuwa hatua hizo ni vita vya kiakili ambavyo vinalenga kuleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Iran. Vikwazo hivyo vinafuatia hatua ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya kinyuklia ya Iran mapema mwaka huu. Makubaliano hayo , yalioafikiwa wakati wa utawala wa rais Barrack Obama ,yaliilazimu Iran kusitisha mpango wake wa kinyuklia huku vikwazo dhidi yake vikiondolewa. Rais Trump ameyataja makubaliano hayo 'yanayopendelea upande mmoja'' kuwa mabaya zaidi kuwahi kufanyika. Anaamini kwamba shinikizo mpya za kiuchumi zitailazimu Iran kuingia katika makubaliano mapya. Muungano wa Ulaya, ambao bado unaunga mkono makubaliano hayo ya Iran , umezungumza dhidi ya vikwazo hivyo ukiapa kulinda kampuni zinazofanya biashara halali na Iran. Ni nini chengine kilichosemwa na Trump katika ujumbe wake wa Twitter? Alivipongeza vikwazo vikali vilivyowekwa na kusema kuwa vitangozwa hadi kufikia kiwango cha juu mnamo mwezi Novemba. ''Ninaomba amani duniani, sio chengine,'' alisema. Siku ya Jumatatu alikuwa amesema kuwa Iran ilikuwa inakabiliwa la chaguo la kubadili vitisho vyake na tabia yake ya kuzua uhasama na kuingiliana na uchumi ama isalie katika njia ya vikwazo na kutengwa kiuchumi. ''Nimesalia tayari kuafikia mkataba ambao utajadili vitendo vyote vibaya vya Iran, ikiwemo mpango wake wa kutengeneza silaha za masafa marefu na kuunga mkono ugaidi'', alisema. Vikwazo hivyo ni vipi? Bwana Trump alitia saini agizo kuu ambalo lilirudisha vikwazo dhidi ya taifa hilo siku ya Jumanne. Vikwazo hivyo vinalenga: Awamu ya pili ya vikwazo hivyo vitaanza kutekelezwa mwezi Novemba ambavyo vitakuwa na athari katika sekta ya kawi na ile ya uchukuzi wa majini nchini Iran bila kusahau bishara ya mafuta, na biashara kati ya taasisi za kifedha za kigeni na benki kuu ya Iran. Hatua hiyo imesababisha hisia gani? Rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa Marekani imekataa kutumia njia ya kidiplomasia. ''Walienda kuanzisha vita vya kisaikolojia dhidi ya taifa la Iran .Majadiliano na vikwazo hayaleti maana yoyote. Kila mara tunapendelea diplomasia na mazungumzo... lakini mazungumzo pia yanahitaji uaminifu''. Mawaziri wa maswala ya nchi za kigeni , Uingereza na Ufaransa walitoa taarifa siku ya Jumatatu wakisema kwamba makubaliano hayo ya kinyuklia bado ni muhimu kwa usalama duniani. Pia walizindua sheria zao za kulinda makampuni ya Ulaya yanayofanya biashara na Iran licha ya vikwazo hivyo vibaya vya Marekani. Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa mtu yeyote anayeshirikiana kibiashara na Iran kufuatia hatua yake ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo. text: Diane Rwigara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba 2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali. Diane Rwigara alizuiwa kuwania urais mwaka uliopita na baadaye kakamatwa kwa madai ya udanganyifu na kuchochea mapinduzi ya serikali. Halmashauri ya kukusanya ushuru nchini Rwanda iliuza mashine kutoka kwa biashara ya familia ya tumbaku kwa takriban dola milioni 2 katika hatua ya kulipia kodi familia hiyo inaripotiwa kudaiwa ya dola milioni 7. Familia hiyo inasema hatua hiyo ya kuuza mali na mashtaka dhidi yake dhidi yake imechochewa kisiasa. Mauzo ya awali ya biashara za familia ya Rwigara ya tumbaku yalileta dola milioni 595. Bi Rwigara na mtetesi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati aliamua kuwania urais. Hakufaulu kuwania na alipigwa maruku baada ya uchunguzi kubaini kuwa Bi Rwigara alikuwa amekiuka sheria kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono kugombea kwake. Bi Rigwara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba 2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali. Mama yake naye anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapinduzi ya serikali. Rais Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka uliopita kwa asilimia 98.63 ya kura. Amesifiwa kwa kuleta mafanikio ya kuichumi nchini humo tangu yafanyike mauaji ya kimbari mwaka 1994. Mamlaka nchini Rwanda zimeuza mali ya familia ya mwanasiasa aliye kizuizini ambaye pia ni mkosoaji mkuwa wa Rais Paul Kagame. text: Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Maelezo zaidi kuhusu mkutano huo hayajatolewa. Hatua hiyo inajiri baada ya Israel kuwaita mabalozi wa mataifa mengine ambao waliunga mkono kura hiyo dhidi ya Israel. Netanyahu: Israel haitaheshimu azimio la UN Ban Ki-moon akosoa pendekezo la Netanyahu Israel yawashtumu mabalozi wa UK, Urusi, China na Uhispania Mkutano huo unajiri baada ya Israel kuapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi kwa kile ilichokitaja kuwa ''hatua ya aibu'' iliochukuliwa na Marekani. Hatua hiyo ambayo imekosoa ujenzi wa Israel katika eneo la West Bank na Jerusalem ilipitishwa baada ya Marekani kutoshiriki katika kura hiyo badala ya kutumia uwezo wake wa kuipinga. Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa uliokosoa mpango wa Israel kutekeleza ujenzi katika maeneo ya Palestina Israel imeishutumu Marekani ,ambaye ni mshirika wake wa karibu na mkosoaji wa ujenzi wa makaazi katika eneo la Palestina kwa kuanzisha kura hiyo -swala ambalo Marekani imekana. ''Kutokana na habari tulizonazo ,hatuna wasiwasi kwamba serikali ya Obama ilishinikiza kura hiyo ikashiriki pakubwa na kutaka ipitishwe'', alisema waziri mkuu Benjamin Netanyahu. Waziri mkuu wa Israeli amefanya kikao na balozi wa Marekani nchini humo baada ya kuamuru afike mbele yake kueleza kwa nini Marekani ilipitisha mswada wa mazungumzo katika Umoja wa Mataifa wa kuikosoa Israeli. text: Donald Trump wa Mraekani na Kim Jong-un wa raisi wa Korea ya Kaskazini Maafisa wa shirika la habari la Korea ya Kaskazini KCNA wameeleza kuwa mazoezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya "chuki" na kuyachukulia kama mazoezi ya uvamizi. Lakini pia kuna onyo lililotolewa na Marekani juu ya hatima ya mkutano wa kihistoria kati ya Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump ambao umepangwa tarehe 12 Juni. Ikumbukwe kwamba katika ya mwezi wa tatu mwaka huu, Mr Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko wa kukutana na rasi Kim, na kujinasibu kuwa "Tutajaribu kuufanya mkutano wetu kuwa wa wakati wa pekee wa Amani ya Dunia!" raisi wa Marekani aliandika haya kwenye mtandao wa Twitter wakati huo kama ilivyo kawaida yake. Idara ya Serikali ya Marekani inasema ilikuwa inaendelea kujiandaa kwa mkutano baina ya viongozi hao wawili Trump na Kim nchini Singapore na kwamba hakukuwa na taarifa zozote za kuahirishwa kwa mkutano huo kulingana na nafasi ya Korea ya Kaskazini. Huu ni kama mchezo wa bahati nasibu wa siasa za karne ya ishirini na moja Ndege za kivita zikiwa tayari kwa matumizi Tuangalie namna kiongozi wa Korea ya Kaskazini alivyoweza kusafiri, akiambatana na ndege mia moja za kivita, ikiwa ni pamoja na idadi isiyojulikana ya makombora aina ya B-52 na ndege ndogo aina ya F-15K. Korea na Amerika ya Kusini daima zimesisitiza kuwa kekee hizo ni kwa madhumuni ya ulinzi,ingawa ni kinyume na makubaliano ya utetezi wa pamoja walio tiliana saini mwaka 1953 , ingawa imejitetea kwamba mazoezi ni muhimu ili kuimarisha utayari wao ikiwa kuna mashambulizi ya nje. Mkutano huo ulipaswa kufanyika eneo la Panmunjom, kwenye eneo la kiwanja cha kijeshi katika ukanda wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili. Wawakilishi kutoka pande zote walikubaliana kujadiliana hatua za kufuatilia juu ya mikataba waliyoifanya katika mkutano wa nadra tarehe 27 Aprili. Kim Jong-un wa Korea ya Kaskazini na Mwenza wake Jae wa Korea Kusini wamekubaliana kufanya kazi ya kuondoa uhalifu wa silaha za nyuklia katika rasi zao baada ya mazungumzo hayo. Korea ya Kaskazini imesitisha mazungumzo yaliyotarajiwa kufanyika mapema wiki hii dhidi ya Korea ya Kusini kwa sababu ya kuchukizwa kwake na mazoezi ya kijeshi ya pamoja na Marekani. text: Waziri wa elimu Quebec Jean-Francois Roberge akiwa na Malala Yousafzai Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ya amani anayevaa mtandio kichwani hangeweza kutoa mafunzo katika jimbo hilo la Canada. Quebec hivi karibuni ilipitisha sheria yenye mzozo inayowazuia baadhi ya wafanyakazi wa serikali, wakiwemo walimu kutovaa mavazi yoyote ya kidini kazini. Jean-François Roberge amesema alijadiliana na Bi Malala masuala ya elimu na maendeleo ya kimataifa. Alipigwa risasi kichwani na wanamgambo wa Taliban mnamo 2012 kwa kusubutu kwenda shuleni na tangu hapo ametambuliwa kimataifa kwa kazi zake katika kampeni ya kushinikiza elimu kwa wasichana. Mnamo Juni, Quebec ilipitisha sheria inayozuia wafanyakazi wa serikali walio katika nafasi za usimamizi kutovaa mavazi ya kidini kama vile vilemba au hijab wakiwa kazini. Sheria hiyo (CAQ) inawalenga majaji, maafisa wa polisi, walimu na wafanyakazi wa umma. Mswada huo ulizusha maandamano na mjadala mkubwa katika jimbo hilo. wafuasi wanasema sheria hiyo ni hatua muhimu kuelekea kujumuishwa kutenganishwa kwa kanisa na serikali ya jimbo la Quebec. Licha ya kwamba sheria hiyo haikutaja dini yoyote maalum, wakosoaji wanalalamika kwamba inabagua na wanasema inawalenga wanawake wa kiislamu katika jimbo hilo wanaovaa hijab au vitambaa vingine vya kichwani. baadhi ywa wadadisi katika mitandao ya kijamii wamemtaja waziri huyo kuwa ni mnafiki kwa kupiga picha na Bi Yousafzai. Roberge, aliyekutana na Yousafzai akiwa Ufaransa, alitetea sheria hiyo alipoulizwa kwenye Twitter na mwandishi Salim Nadim Valji namna ambavyo angejibu iwapo Bi Yousafzai atake kuwa mwalimu Quebec. "Bila shaka ningemwambia kwamba ingekuwa heshima kubwa na kwamba hukuQuebec, kama ilivyo Ufaransa na katik amatifa mengine ya wazi yalio na waumini tofauti, walimu hawawezi kuvaa mavazi ya kidini wakati wakiwa kazini," alisema. Waziri wa elimu Quebec anashutumiwa kwa kuweka picha na mwanaharakati anayetetea elimu Malala Yousafzai. text: Chanjo ya watoto huenda ikatolewa mara moja Chanjo hiyo itakayotolewa mara moja kwa mpigo itashirikisha dawa zote katika sindano moja ambazo zitakuwa zikifanya kazi kwa muda utakaohitajika ili kumkinga mtoto na magonjwa yanayolengwa. Teknolojia hiyo imeonakana kufanya kazi miongoni mwa panya katika jarida la sayansi. Watafiti wanasema teknolojia hiyo inaweza kuwasaidia wagonjwa duniani. Chanjo ya watoto husababiha vilio na machozi na nyingi hupewa watoto kwa muda tofauti. Kundi moja la watafiti katika chuo cha kiteknolojia cha Massachusetts kimebuni chanjo ambayo inashirikisha dawa zote za chanjo anayopewa mtoto. Dawa hiyo imetengezwa katika hali ambapo chanjo zilizochanganywa hujitokeza na kuanza kufanya kazi katika muda tofauti katika kiupindi cha wiki sita licha ya kutolewa kwa pamoja. Teknolojia hiyo itawasaidia wazazi ambao hawana uwezo wa kwenda hospitalini mara kwa mara. Teknolojia ambayo huenda ikapelekea chanjo ya watoto kutolewa mara moja kwa kila mtoto imebuniwa na watafiti nchini Marekani. text: Rais wa Zambia Edgar Lungu Hii ni baada ya kuwa na maambukizi mengi, hususan miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwemnye miji ya mipaka nchini humo. Wafanyabiashara wa ngono wanasaidia kuwapata watu waliopata maambukizi mapya ya virusi vya corona e kwenye mji wa mpaka wa Nakonde, amesema waziri wa afya. Wafanyabiashara ya ngono nchini Zambia wanasaidia kuwapata watu waliopata maambukizi mapya ya virusi vya corona Chitalu Chilufya amesema 76 kati ya 85 walioripoti visa vipya katika huo wa kaskazini walikua ni wafanyabiashara wa ngo au madereva wa malori. "Makahaba wamekua wakionyesha ushijrikiano mkubwa sana na wanatupatia taarifa zote tnazozitaka kuhusu maambukizi ya corona ," Amesema Bwana Chilufya. Zambiaimethibitisha visa 267 vya maambukizi ya Covid-19, na vifo saba. Wiki iliyopita Rais Edgar Lungu alitangaza kufunguliwa tena kwa migahawa ya chakula, kumbi za kamari na za mazoezi ya mwili-(gym) baada ya nchi hiyo kuwa chini ya amari ya kutotoka nje kwa mwezi mmoja ili kutekeleza hatua za watu kutosogeleana. Zambia iliripoti wagonjwa 76 wa virusi vya corona katika mji uliopo katika mpake wake na Tanzania. Rais Edga Lungu alisemaje? Akizungumza kwa niaba ya rais wa taifa hilo, Edgar Lungu Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya alitangaza kwamba mpaka huo utafungwa kwa muda . Alisema kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa mikakati mipya ya kukabiliana na virusi hivyo kuwekwa. Katika muda huo, amesema wafanyakazi wa uhamiaji katika mpaka huo watapatiwa mafunzo mapya ya jinsi ya kuhudumia mizigo na raia wanaoingia. ''Hali kule Nakonde ni mbaya na hii leo rais Edgar Lungu ana wasiwasi , Hivyobasi ameagiza kuanzia Jumatatu tarehe 11 mwezi Mei 2020, mpaka wa Nakonde utafungwa kwa muda , hakutakuwa na usafiri ndani na nje ya mpaka huo na vilevile hakutakuwa na usafiri viungani mwa eneo hilo ili kuwezesha utekelezwaji wa mikakati inayolengwa ikiwemo kuwapa mafunzo mafisa wetu mpakani'', alisema waziri huyo wa Afya. Amesema kwamba maafisa hao vilevile watapatiwa vifaa vya kujilinda dhidi ya ugonjwa huo huku vifaa vya karantini vikiwekwa kwa lengo la kuwalinda maafisa na wakaazi wa Nakonde. Tanzania yalaumiwa kuhusu jinsi inavyokabiliana na corona Taifa la Tanzania limethibitisha wagonjwa 509 wa virusi vya corona huku wagonjwa 183 wakipona na 21 wakiripotiwa kufariki kutokana na virusi hivyo. Serikali ya Tanzania imelaumiwa katika mikakati yake ya kukabiliana na virusi hivyo huku rais John Pombe Magufuli akitilia shaka vifaa vya kuwapima wagonjwa. baadhi ya viongoxi wa kidini wamesitisha ibada, lakini wengine wengi bado wanajumuika pamoja kila Jumapili Tofauti na nchi nyingi, Tanzania haijachukua hatua kali za kupiga marufuku watu kutoka nje ijapokuwa mikusanyiko mikubwa ya watu kama misiba na harusi imepigwa marufuku. Lakini usiri wa mazishi yaliyopigwa picha unachochea hisia kuwa ukubwa haswa wa maambukizo nchini humo unafichwa. Kipaumbele kikuu cha serikali ya Tanzania ni kutoumiza uchumi wa nchi huku rais Magufuli akipinga kulifunga jiji la kibiashara la Dar es Salaam. Katika hotuba yake kwa taifa rais wa Zambia Edgar Lungu siku ya Ijumaa alitangaza kufunguliwa kwa maeneo ya kufanyia mazoezi na casino huku akitoa wito kwa wanasayansi nchini humo kutafuta suluhu ya kinyumbani katika vita dhidi ya ugonjwa huo. Hatahivyo aliamrisha kwamba klabu za burudani zitaendelea kufungwa hadi atakapotangaza tena. Zambia imechukua hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kwa kufunga mpaka wake na nchi jirani ya Tanzania kuanzia Leo Jumatatu. text: Mamilioni ya watu husafiri mpaka Makka kwa ajili ya ibada ya Hija Wizara imesema uamuzi ulifikiwa kutokana na uamuzi wa shirika la afya duniani, WHO kutangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC ni suala la dharura inayohitaji kushughulikiwa na jumuia ya kimataifa. ''Mpango wa kutoa viza kwa watu wanaoingia kutoka DRC umesimamishwa, kwa ajili ya usalama wa mahujaji,'' wizara. Saudi Arabia awali ilisema takribani watu 410 kutoka nchini DRC wanatarajia kwenda kuhiji mjini Makka baadae mwezi huu, Kiongozi wa kiislamu nchini Drc, Imamu Djuma Twaha, aliiambia BBC. ''Kuna watu walikuwa wamejiandaa kwa miaka mingi, wakati mwingine miaka kumi wakijichanga kiasi cha pauni 3,400 kwa ajili ya kufanya safari kwa ajili ya hija,'' alieleza. WHO ilitangaza hali ya dharura kutokana na mlipuko wa Ebola tarehe 17 mwezi Julai, lakini imezitaka nchi kutofunga mipaka yao dhidi ya watu wanaofanya safari au biashara. Kwa nini wanaotoroka mapigano DRC wanaathiri 'juhudi za kudhibiti Ebola' Zaidi ya watu 2,000 wameripotiwa kuugua Ebola nchini DRC Hali ni mbaya kiasi gani nchini humo? Mlipuko wa Ebola ni ugonjwa wa pili kwa ukubwa katika historia ya nchi hiyo, ulianza mwezi Agosti na inaathiri majimbo mawili nchini DRC, Kivu Kaskazini na Ituri. Zaidi ya watu 2500 wameathiriwa na ugonjwa huo na theluthi mbili kati yao wamepoteza maisha. Ilichukua siku 224 kwa idadi ya walioathirika kufika 1,000 , lakini ndani ya siku 71 zaidi idadi ilifika 2,000. Watu takribani 12 huripotiwa kupata ugonjwa huo kila siku. Mwanamke akipimwa dalili za Ebola Kwanini ugonjwa huu haujadhibitiwa? Wafanyakazi wa afya wamekua wakipata vikwazo vya kutoaminika na machafuko nchini humo. Watu wengine hawawaamini watoa huduma za afya, hivyo hufanya watu wenye dalili za ugonjwa huo kukwepa matibabu, hali hii inawia vigumu kuzuia kuenea kwa virusi vya ebola. Ingawa zaidi ya watu 1,300 wamepoteza maisha tangu mwezi Agosti, Shirika la misaada la Oxfam linasema linakutana na watu kila siku ambao hawaamini kama kuna virusi vya ebola. Tangu mwezi Januari kulikua na matukio 198 ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, na kusababisha majeruhi 58. Saudi Arabia haitatoa viza ya kusafiria kwa mahujaji kutoka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeeleza wizara ya mambo ya nje katika taarifa yake. text: Wenger amenukuliwa akisema kuwa huenda akaondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu Wenger ameifunza Arsenal tangu mwezi Oktoba 1996 na mara ya mwisho yeye kushinda taji la ligi ilikuwa mwaka 2004. Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu huu. ''Ninahisi kwamba ameamua'', mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal aliambia BBC Radio 5 live. ''Anaonekana amechoka.Unahisi kwamba anaonyesha uchovu.Nadhani atawachia mwishoni mwa msimu huu''. Matumaini ya Arsenal ya kushinda taji la ligi msimu huu yalipata pigo kubwa baada ya kushindwa 3-1 na viongozi wa ligi Chelsea kuwawacha wakiwa pointi 12 nyuma ya Chelsea. Ian Wright Wright anasema kuwa aliongea na Wenger usiku wa Alhamisi. ''Aliniambia kwamba anafikia kikomo.Sijamsikia akisema hivyo awali'',alisema Ian Wright mwenye umri wa miaka 53. ''Wachezaji wamemuangusha sana.Iwapo hataondoka mwisho wa msimu huu kutakuwa na mabadiliko makubwa mwishoni mwa msimu huu.Wanafaa kujiangalia sana.Amekuwa mwaminifu kwa timu hii''. Baadhi ya mashabiki wamemtaka Wenger kuondoka ,huku mmoja akibeba bango katika uwanja wa Stamford Bridge lililosema ''Imetosha! Ni wakati unafaa kuondoka''. Arsene Wenger amemwambia Ian Wright kwamba muda wake kama mkufunzi wa Arsenla unakaribia kikomo kulingana na mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal. text: Oscar amechezea Chelsea mechi 202 tangu ajiunge nao 2012 Inakadiriwa kwamba mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 25 atanunuliwa takriban £60m. Alijiunga na Chelsea kutoka Internacional kwa £25m mwaka 2012. Oscar alianza kwenye mechi tano za kwanza chini ya Antonio Conte lakini amechezeshwa mara nne pekee tangu Septemba. "Inategemea mambo kadha tu ya urasmi," Oscar aliambia Sportv ya Brazil. Conte hakukanusha madai ya Oscar alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake baada ya ushindi wa Chelsea wa 1-0 dhidi ya Sunderland Jumatano. Amesema hali ya Oscar itakuwa wazi zaidi siku chache zijazo. Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai. Oscar amechezea Chelsea mechi 202 na kufunga mabao 38. Ameshinda Ligi ya Premia, Europa League na Kombe la Ligi. Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar amesema ana "uhakika 90% " kwamba atahamia klabu ya Shanghai SIPG inayocheza Ligi Kuu ya China kipindi cha kuhama wachezaji Januari. text: Nahodha wa Zanzibar Suleiman Kassim Zanzibar Heroes sasa watakutana na Kenya kwenye fainali Jumapili. Zanzibar walifunga mwanzo kupitia Abdul Azizi Makame dakika ya 25 kisha Derrick Nsibambi akatuliza kimiyani bao la Uganda la kusawazisha naye Mohammed Issa Juma akapachika wavuni bao la pili la Zanzibar . Ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kufika fainali michuano hiyo tangu 1995, mwaka ambao walitwaa ubingwa. Allan Katerega wa Uganda anasema kuondolewa kwa Joseph Nsubuga kuliipunguzia nguvu timu yao. Nsubuga alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Feisal Salum Abdulla wa Zanzibar. Mchezaji wa Uganda Allan Katerega Wenyeji Kenya walifuzu baada ya kuwashinda Burundi kwa bao la muda wa ziada lililofungwa na kiungo wa kati Whyvonne Isuza. Katibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee tayari amesema: "Sasa Fifa wapende wasipende watatutambua." Bw Khamis Ali Zanzibar si wanachama wa Fifa licha ya kupigana kwa muda mrefu watambuliwe. Wanajumuishwa wote pamoja na Tanzania bara. Lakini Ali asema ndugu mkubwa hawapi fungu lao kutoka Fifa. "Nitasema hapo tumefinywa lakini tutafanikiwa siku moja." Wachezaji wa Uganda wakirejea uwanjani kwa kipindi cha pili CAF pia haitambui chama cha kandanda cha Zanzibar. Hemed: Wachezaji wa Zanzibar katika Cecafa hawana doa "Walijaribu kutuzuia CAF tusishiriki michuano hii ya Cecafa lakini ndugu mkubwa akatutetea tena tuliwaambia sisi ni baadhi ya waanzilishi miaka hiyo ikiwa Gossage Cup," asema Ali. Zanzibar wamefuzu kwa fainali ya ubingwa wa kanda ya Afrika mashariki na kati, maarufu kama Cecafa Senior Challenge baada ya kuwalaza Uganda Cranes 2-1. text: Amemshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa kura 92,153 dhidi ya 46,656. Meya huyo wa zamani wa mji wa Londona anapokea wadhifa huo kutoka kwa Theresa May kesho Jumatano. Katika hotuba yake baada ya ushindi huo, Johnson ameahidi kuwa "ataiwasilisha Brexit, kuiunganisha nchi na kumshinda Jeremy Corbyn". Akizungumza mjini London, alisema: "Tutaipa nchi nguvu. "Tutaiwasilisha Brexit kufikia Oktoba 31 na kuchukua fursa zote zitakazotokana na muamko mpya wa inawezekana. "Tutajiamini upya na tutainuka upya na kuondosha shaka na fikra za kutojiamini." Takriban wanachama 160,000 wa Conservative walikuwa na fursa ya kupiga kura na katika waliojitokeza ni 87.4%. Asilimia ya kura kwa Johnson - 66.4% - ilikuwa chini ya aliyojishindia waziri mkuu wa zamani David Cameron mnamo mwaka 2005 aliyejinyakulia 67.6%. Ushindi umepokewaje? Bi May amempongeza Johnson, na kumauhidi "ushirikiano wake kikamilifu kutoka nafasi ya nyuma". Rais wa Marekani Donald Trump pia ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akimpongeza Johnson, na kuongeza: "Atakuwa mzuri mno!" Jeremy Corbyn ralituma ujumbe kwenye twitter kwamba "ameshinda uungwaji mkono wanachama chini ya 100, 000 wasiowakilisha wa chama cha Conservative", lakini "hajashinda uungwaji mkono wa nchi yetu". "Mpango wa kupinga makubaliano ya Brexit wake Johnson utaaminisha waut kupoteza ajira, gharama kubwa madukani na kuhatarisha kuuzwa kwa huduma ya afya ya kitaifa NHS kwa mashirika ya Marekani katika makubaliano na Donald Trump," Kiongozi huyo wa Leba ameendelea kusema. "Raia wanastahili kuamua nani awe waziri mkuu katika uchaguzi mkuu," ameongeza. Familia ya Boris - Babake Stanley na dadake Rachel na mbunge mwenza wa Conservative Jo- wakati wa tangazo la ushindi Waziri wa kwanza wa Uskotchi Nicola Sturgeon amempongeza Johnson, lakini amesema "ana wasiwasi mkubwa" kuhusu Boris kuwa waziri mkuu. Changamoto inaanza wakati Johnson apata ushindi Laura Kuenssberg, Mhariri wa BBC wa kisiasa Boris Johnson atakuwa waziri mkuu mpya Uingereza. Kauli ambayo inaweza kufurahisha au kuogopesha. Kauli ambayo anaeleza kwamba miezi 12 iliyopita hata wafuasi wake sugu hawange weza kuliamini hilo. Lakini sio kauli kavu tu, pengine sio jambo la kawaida kisiasa, ambalo huenda lisikere kwa namna yoyote. Kwa vyovyote vile unvayomtazama Boris Johnson, yeye ni mwanasiasa ambaye sio rahisi kumpuuza. Huyu ni mtu ambaye hata utotoni mwake alitaka kuwa 'mfalme wa dunia'. Sasa ni mfalme wa chama ha Conservative, na wanaoipigia upatu Brexit, ndio mahakimu. Changamoto zilizoko ni za kiwango cha kihistoria. Boris anaipokea serikali ambayo haina uwingi, ilio na siasa ziliyoachanganyika na sera ambayo katika miaka mitatu ijayo Uingereza na Brussels imeshindwa kuitatua. Na yeye ni mwanasiasa, ambaye hata washirika wake wanaoshangazwa na kipaji chake wanakiri hung'ang'ana kutoa maamuzi kwa wepesi. Mojawapo ya wafuasi wake alitamka leo asubuhi pakisubiriwa tangazo la ushindi: "Changamoto inaanza sasa." Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha Conservative katika kura iliyopigwa na wanachama na atakuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza. text: Alidaiwa kupigwa risasi na watu wawili waliokuwa wakiendesha boda boda mwendo wa saa kumi na mbili na nusu siku ya Ijumaa . Mlinzi wake aliyekuwa akindamana naye pia alipigwa risasi katika gari lake. Mwisho wa Twitter ujumbe, 1 Alikuwa mmoja wa viongozi walioshinikiza kubadilishwa kwa katiba kuondoa kifungu cha 102b ili kuweza kuondoa kikomo cha umri wa rais cha miaka 75 kuondolewa. Hatahivyo hatua yake ya kutaka kikomo hicho kuondolewa ilisitishwa na kesi mahakamani baada ya kutuhumiwa kukojoa katika eneo la umma karibu na makao makuu ya wizara ya fedha mjini kampala. Abiriga baadaye alipigwa faini ya shilingi 40,000 za Uganda na mahakama ya barabarani ya Buganda kwa kuwa msumbufu wa umma. Katika eneo la Matugga, maafisa wa polisi na maafisa wengine wa usalama wamelizunguka eneo la kisa hicho ili kuhakikisha kwamba halivurugwi. Abiriga ambaye masomo yake yametiliwa shaka na wapinzani wake wa kisiasa hivi majuzi alipokea cheti cha Diploma kutoka kwa Taasisi ya Nile mjini Arua. Tayari rais wa taifa hilo Yoweri Museveni ameagiza vitengo vya usalama kuwatafuta wauaji wa kiongozi huyo . Katika mtandao wake wa Twitter Museveni alimuomboleza mbunge huyo akisema kuwa waliotekeleza kitendo hicho wana roho ngumu. ''Nimepokea habari kuhusu mauaji ya kinyama ya mbunge wa Manispaa ya Arua , mheshimiwa Ibrahim Abiriga na mlinzi wake nje ya mji wa Kampala. Nimeviagiza vitengo vya usalama kuwasaka waliotekeleza kitendo hicho na taifa litajuzwa hivi karibuni'', aliandika Museveni. Mbunge wa Manispaa ya Arua nchini Uganda (MP), Ibrahim Abiriga ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyumba yake huko Mattuga Wilaya ya Wakiso. text: Mwanamuziki ajitosa baharini kukwepa kulipa bili ya chakula Polisi walimfuata kwa kasi mwanamuziki hiyo ambaya baadaye alisema kuwa alikimbia kumsaidia rafiki yake kujifungua mtoto katika fukwe za bahari. Alikuwa na bili ya zaidi ya dola 450. Terry Peck ambaye amefunguliwa mashtaka ya wizi baadaye alidai kuwa chakula hicho hakikua kimepikwa kwa njia inayotakikana. Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 33 alifikishwa mahakani leo Jumatatu baada ya kisa hicho kilichotokea katika mgahawa wa Omeros Bros. Mwanamuziki ajitosa baharini kukwepa kulipa bili ya chakula Australia si nchi pekee ambapo kuna visa vya wateja kula kwenye mikahawa na kukosa kulipa. Mwezi uliopita polisi wa Uhispania walimkamata mtu anayeshukiwa kuwa kiongozi wa genge ambalo lilikuwa na tabia ya kula kwenye mikahawa na kisha kutoroka kaskazini mwa nchi. Kundi hilo liliwajumuisha watu 100 lilikula chakula cha thamnia ya euro 22 katika mkahawa wa Bembibre's El Carmen mwezi Machi na baadaye wote wakakimbia bila kulipa. Mwanamume mmoja raia wa Australia ambaye alikuwa na bili kubwa ya kulipa baada ya kupata mlo kwenye mkahawa mmoja aliruka na kuingia baharini ili kukwepa kulipa bili hiyo. text: Meno hayo ya bandia na chuma chake yaligundulika wiki moja bada ya upasuaji wa awali. Mgonjwa huyo mwenye miaka 72 alikuwa akilalamika kupata maumivu makali wakati wa kumeza vitu na kukohoa damu katika kipindi chote hicho. Bwana huyo, alimeza meno hayo wakati akifanyiwa upasuaji wa tumbo. Undani wa tukio hilo umechapishwa kwenye jarida la kisayansi la BMJ ambapo watunzi wake wamewataka madaktari kuhakikisha wagonjwa wao wanaondoa meno ya bandia kabla ya upasuaji. Siku sita tu baada ya upasuaji huo uliofanyika mwaka 2018, bwana huyo alienda kwa daktari na kulalamika kuwa nanashindwa kumeza vyakula vizito. Madaktari awali waliamini kuwa hiyo ni athari ya kuwekewa mpira kwenye kinywa wakati wa upasuaji, na kumpatia dawa za kukabiliana na maumivu na maambukizi ya koo. Lakini baada ya bwana huyo kurudi tena baada ya siku mbili akiwa na malalamiko zaidi, madaktari ikabidi wamfanyie uchunguzi zaidi wa koo. Vipimo vya miale ya X-Ray vikaonesha kuwa kuna meno ya bandia matatu na chuma chake cha kuyashikilia. Baada ya hapo, mzee huyo akawaambia madaktari kuwa alipoteza meno yake ya bandia katika kipindi ambacho alilazwa hospitalini kwa upasuaji wa tumbo. Ikalazimika afanyiwe upasuaji wa haraka wa koo, lakini akarudi hospitali mara nne zaidi ili kuongezewa damu. Hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget imesema imejifunza kutokana na makosa ya upasuaji huo. Watafiti wameeleza katika ripoti yao kuwa kuna zaidi ya mkasa mmoja wa watu kumeza meno ya bandia wakati wakipigwa dawa za usingizi. Uwepo wa meno bandia ama kifaa chochote cha bandia kinywani, unatakiwa uripotiwe kabla nda baada ya upasuaji, wamesisitiza kwenye ripoti ya jarida hilo. Hazel Stuart, ambaye ni mkurugenzi wa matibabu katika hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget ambapo upasuaji huo ulifanyika amesema uchunguzi wa kina ulifanyika juu ya tukio hilo. "Baada ya tukio hilo, michakato yetu imepitiwa upya, na maboresho yamefanyika katika kila eneo la mahitaji, na tuliyojifunza tumehakikisha yanawafikia wafanyaki wetu wote ili kuepuka makosa," amesema. Mgonjwa mmoja nchini Uingereza amejikuta katika maumivu makali baada ya meno yake ya bandia kunasa kooni kwa wiki moja. text: Manchester City yaikung'uta Arsenal 3-1 Bao la Kevin de Bruyne na penalti ya Sergio Aguero iliiweka Man City katika nafasi ya kushinda ligi ya tisa. Licha ya Alexandre Lacazette kuipa Arsenal bao la kuvuta machozi, Gabriel Jesus aliipa Manchester ushindi kwa kuifungia bao la tatu. Arsenal huenda wangepata kipigo zaidi isingekuwa ni jitihada za kipa Petr Cech Mafanikio ya Manchester City dhidi ya Machester United walio nafasi ya pili yatatokana na matokeo ya leo dhidi ya Chelsea. Manchester City waliwakung'uta Arsenal 3-1 na kufungua mwanya wa pointi kileleni mwa ligi ya Premier. text: Rubani Frank Njoroge (kulia) akiwa na familia yake baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi Awali waasi wa Sudani kusini waliwaachilia marubani wawili wa Kenya waliotekwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita baada ya ndege yao kupata ajali. Msemaji wa waasi alisema wakenya hao waliachiwa baada ya kampuni ya bima kulipa zaidi ya dola za marekani 100,000 kulipa fidia ya kifo cha mtu mmoja aliyepoteza maisha baada ya ndege kuanguka. Baada ya kutekwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, Kepteni Pius Frank Njoroge na msaidizi wa rubani Kennedy Shamalla wameripotiwa kuwasili salama mjini Juba. Ndege ya marubani wa Kenya ilianguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja na mifugo Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ameiambia BBC kuwa wawili hao watarejea Kenya baadae leo. Waasi waliwashikilia watu hao ndege yao ilipoanguka katika mji wa Upper Nile na kuripotiwa kumuua mwanamke mmoja na mifugo. Awali waasi walitaka zaidi ya dola 200,000 lakini walifikia makubaliano baada ya majadiliano na maafisa wa Kenya. Msemaji wa waasi amesisitiza kuwa malipo hayo sio kikombozi bali ni fidia baada ya ajali hiyo kusababisha vifo. Ilikuwa ni hali ya kusisimua na ya furaha wakali marubani waliporejea katika uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi, baada ya kutekwa nyara kwa mwezi mmoja mikononi mwa waasi wa Sudan Kusini . text: Mlango mmoja wa fahamu ulimuongoza Abdallah Nyangalio kuonesha uwezo wake jukwaani sawa na mtu mwenye viungo kamili bila kutetereka. Abdallah Nyangalio si jina geni Tanzania na Afrika mashariki, yeye ni mshonaji nguo ambaye anapima kwa kutumia viganja vya mikono yake na kushona bila kukosea. Kikubwa ni hali yake ya kuwa kipofu kutokana na maradhi lakini ameweza kupata tuzo kadhaa kwa sababu ya uweredi wa kazi yake. Fundi Nyangalio akimpima mteja Mwaka huu 2019, ameonyesha uwezo na uthubutu wa hali ya juu kwa kupanda katika jukwaa la maonyesho la mavazi katika tamasha la mavazi la stara ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo. Mwandishi wa BBC, Regina Mziwanda alifanya mazungumzo na bwana Nyangalio na kufafanua kazi hiyo aliifanyaje pamoja na changamoto alizokutana nazo wakati wa kuandaa kazi hiyo. "Zile nguo zote nimeshona mimi mwenyewe kuanzia shati mpaka magauni, na alafu nikawapa mafunzo ya namna ya kutembea jukwaani na kweli waliweza kutembea vizuri sana" Nyangalio aeleza. "Jukwaa halikuwa limetengenezwa maalum kwa watu wenye ulemavu, lakini tulipambana na lile jukwaa ingawa siku nyingine tungepewa fursa ya kutoa maoni ya namna gani ambavyo jukwaa ambalo ni rafiki kwetu walemavu". Kwa ni ni tamasha la nguo za stara mwaka huu liliamua kutumia mbunifu mlemavu wa macho "Tulitaka alete mabadiliko katika tasnia ya mitindo na ubunifu maana hiki ni kitu kipya, ni kawaida walemavu kupanda jukwaani kwa ajili ya maonyesho lakini sio wenyewe kuwa wabunifu"Asmah Makau muandaaji wa maonyesho ya stara Tanzania . Tamasha la tano la mavazi ya stara lilichukua sura mpya kwa kuwa na mavazi yenye mfanano wa wanyama pori Vazi la stara lenye muonekano wa nyoka Mavazi ya stara kwa ajili ya mwezi wa ramadhani Wabuni wengine wakongwe na mahiri katika ubunifu wa mavazi wanaona utofauti huu wa uwakilishi wa mavazi na ubunifu ni fursa kwa wengine. Fundi Nyangalio ni nani? Fundi asiyeona ,Nyangalio Ni kawaida kuwapata mafundi wa nguo wakitumia utepe wa kupimia kuwapima wateja wao kabla ya kuwashonea nguo. Lakini ukikutana na Abdallah Nyangalio, fundi hodari nchini Tanzania, mara nyingi hutampata akitumia utepe. Kwa kukugusa tu, atakuwa tayari amejua vipimo vya nguo inayokufaa, ingawa hali ikizidi hutumia utepe maalum alioukarabati ndipo kupata vipimo kwa ufasaha. Alianza kufanya hivi baada yake kupoteza uwezo wa kuona 1989, katika hali ya kusikitisha. Alipatwa na maumivu makali ya kichwa 1988 na akawa anatafuta tiba bila mafanikio. Mwaka 1989, alikutana na daktari kutoka Urusi aliyeahidi kumtibu na akamfanyia upasuaji. Lakini badala ya kumpona, alipofuka kabisa na mke wake alimtoroka. Fundi huyo wa miaka 53 ameibuka maarufu baada ya kumemshonea shati aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete. Licha ya hili, bado anaikosoa serikali kwa kutotambua vipaji vya walemavu, anaosema wengi wao huishia kuwa ombaomba barabarani. Kitu pekee anachohitaji kusaidiwa ni katika kuchagua rangi, lakini kazi hiyo nyingine atajifanyia mwenyewe. Kwa namna ya kipekee , fursa ya kuonesha nguvu ya ubunifu wa mtu mwenye ulemavu wa macho imeoneshwa katika tamasha la tano la maonesho ya mavazi la Stara. text: Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Kauli hii imekuja wakati taifa hilo likielekea kwenye uchaguzi mkuu. Serikali ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe ,ilikuwa inaunga mkono kunyang'anywa kwa mamia ya mashamba ya wazungu ambayo waliona kuwa yalikuwa yanachukuliwa bila haki. Mnangagwa ameuambia Umma mjini Harare kuwa sera hiyo ya kukanganya ni kitu kilichopita. ''Tunapaswa kuacha uzungumza kuhusu nani anamiliki shamba kwa kutazama rangi''.Alieleza. ''Ni uhalifu kuzungumza namna hiyo, Mkulima, mkulima mweusi, mkulima wa kizungu, wote ni wakulima wa Zimbabwe.'' Chamisa ni maarufu miongoni mwa vijana Hatua ya Rais Mnangagwa kushughulikia malalamiko ya wapiga kura wenye asili ya wazungu imekuja wakati ambapo kunatarajiwa kufanyika uchaguzi wa kihistoria tarehe 30 mwezi Julai. Utakuwa uchaguzi wa kwanza wa urais tangu Mugabe alipoondolewa madarakani mwezi Novemba, na kumaliza utawala wake uliodumu kwa miaka 37. Raia wa Zimbabwe wenye asili ya weupe wamekuwa wakipigia kura vyama vya upinzani kama vile Movement for Democratic Change(MDC). Rais huyo amesema kuwa serikali yake si ya kibaguzi na ameeleza jinsi mtangulizi wake alivyoshindwa kwenye suala ya mabadiliko ya sera za umiliki ardhi. kukamatwa kwa ardhi inayomilikiwa na wazungu kulisababisha kilimo kudorora na kuondoka kwa wakulima hao , pia ukosefu mkubwa wa ajira kulikowaathiri wafanyakazi wa mashambani wenye asili ya weusi. Kuna zaidi ya vyama vya siasa 120 vilivyosajiliwa wakati huu wa uchaguzi, na huenda kutakuwa na wagomea 23 wa urais. Rais huyo anapewa nafasi kubwa kushinda, lakini wachambuzi wa mambo wanasema ana maadui pia kwa pande zote mbili, kutokana na kumuangusha Mugabe. Kiongozi wa chama cha upinzani ,Nelson Chamisa, ambaye alikuwa maarufu zaidi mwezi Februari ndani ya chama cha MDC. Ni kipenzi cha vijana na wasio na ajira, atakuwa rais mdogo wa umri ambaye hajawahi kutokea nchini humo Rais wa Zimbabewe Emmerson Mnangagwa amewaambia wakulima wa asili ya kizungu kuwa ardhi zao hazitachukuliwa text: Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Uteuzi huo umefanyika baada ya waziri mkuu aliyekuwepo Bruno Tshibala, kujiuzulu. Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi wake alisema waziri huyo mkuu alielezea kipaumbele ya serikali yake itakayoundwa baadaye. ''Rais alinipokea na aliniambia ya kwamba kipaumbele cha serikali hii yetu ya muungano ni ni kuboresha maisha ya raia na kurejesha usalama'' alisema Bw. Illunga. Pia alimshukuru rais wa zamani Joseph Kabila kwa kupendekeza jina lake ali ateuliwe kuwa waziri mkuu. Raia wa Congo walikua wamesubiri zaidi ya miezi mitatu, bila ya kuwa na waziri mkuu mpya. Kuhusu ni lini serikali itaundwa amesema kwa sasa mashauriano yanaendelea kati ya vyama vyao na kwamba mashauriano hayo yatapokamilika serikali itatangazwa. Slyvestre Illunga aliwahi kutumika chini ya utawala wa Mobutu Seseko kama mshauri wake wa maswali ya uchumi. Kutokana na uzoefu wake katika masuala ya uongozi baadhi ya raia wana matumaini kuwa waziri mkuu huyo mpya ataleta mabadiliko hususan katika kupambana na rushwa ambayo imetajwa kuwa tatizo linalorudisha nyuma taifa hilo la maziwa makuu. ''Kulingana na nafasi yake ya kazi tunaamini ataongoza nchi yetu. Tunatumaini experience yake itamsaidia kung'amua wale ambao wataweka mbele maslahi ya nchi na wala sio kubomoa nchi'' alisema mmoja wa wakaazi alyezungumza na BBC. Mwanasisia huyu mwenye umri wa miaka 78 ambae pia ni miongini mwa viongizi wa chama cha Joseph Kabila, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya reli ya Congo. Tangu mwaka 2014 waziri mkuu huyu mpya alikuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya reli na wafanyi kazi wengi wa kampuni hiyo wamefanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa mishahara yao. Wakosoaji wake wanasema hiyo ni dalili mbaya ya kuonesha kwamba hatajibu haraka mahitaji yao. ''Sisi tulikua hatumjui lakini tuliposikia alikua mkurugenzi wa shirika la reli nchini tumeshangaa kwasababu hilo shirika limekufa tayari'' alisema mmoja wao. Alidai kuwa shirika hilo lilipoteza fedha nyingi nchi ya uongozi wake na mambo mwengine mengi yalifanyika hali ambaye anasema ililemaza huduma zake. ''Sasa wamemfanya kuwa waziri mkuu, je nchi nayo haitakufa?'' aliuliza. Rais Tshisekedi hata hivyo ameahidi kuwa serikali yake itakabiliana vilivyo na visa vya rushwa. Kwa mujibu wa vyama vilivyomuunga mkono Joseph Kabila kulingana na jinsi walivyo na idadi kubwa ya waakilishi katika bunge la kitaifa, lile la seneti na majimboni wana haki ya kupewa 80% ya wizara huku wakidai chama cha rais mpya kinafaa kupewa 20%. Hatua ya Rais Felix Tshisekedi kumteua Profesa Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa waziri mkuu mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imepokelewa kwa hisia mseto. text: Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanza kuweka alama za X katika nyumba 252 zilizojengwa ndani ya mpaka huo ili wahusika wazibomoe. Bw Majaliwa, aliyetembelea eneo la ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP) katika mpaka wa Tanzania na Zambia, amesema waliojenga kuanzia umbali wa mita 50 kutoka Tanzania na mita 50 kutoka Zambia wabomoe nyumba hizo kwa hiari. Kituo hicho kinajengwa na Serikali ya Tanzania na kitagharimu sh. bilioni 12 za Tanzania. "Kuna watu wamejenga ndani ya mpaka wa Tanzania na Zambia na kuendesha biashara zao jambo ambalo ni kinyume cha sheria na linazikosesha Serikali mapato," amesema. "Hatuna msamaha kwa watu waliojenga katika eneo hili kwa sababu wamesababisha tupoteze kodi nyingi, hivyo baada ya kumalizika muda huo mamlaka husika zibomoe nyumba zote zitakazosalia." Bw Majaliwa awali alikutana na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchini Zambia, Bw. Field Simwinga ambaye alisema wamekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa jambo hilo linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili. Bw Simwinga alisema tayari wameshaanza kuwaeleza wananchi wao waliojenga ndani ya mpaka huo kuanza kuondoka. Waziri mkuu wa Tanzania amesema wanataka eneo hilo liwe wazi ili iwe rahisi kuutazama mpaka huo kwa umakini. Watu waliojenga ndani ya eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia wamepewa muda wa miezi mitatu kubomoa nyumba zao na kuondoka maeneo hayo. text: 31% ya wasichana nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef Mahakama kuu ya rufaa imebatilisha uamuzi uliotolewa awali na mahakama nyingine nchini kwa misingi ya kuwa ndoa za watoto zinakiuka haki za wasichana, na nii kinyume cha sheria na katiba ya nchi hiyo. Unaweza pia kusoma: Mwanasheria mkuu wa Tanzania alikuwa amekata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama ya juu wa mwaka 2017, ambapo ilikuwa imeondoa vipengele vya sheria na kuruhusu ndoa kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 14. Msichana Initiative inasema maamuzi ya leo ni muhimu kwa wasichana wa leo na wa baadae Mahakama hii leo ilisema kuwa wasichana hawawezi kuolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, umri ambao wavulana pia wanaruhusiwa kuoa. Uamuzi huu wa mahakama ni hatua iliyopigwa katika kutetea haki za wasichana. Taarifa ya kuzuiwa ndoa za mapema kwa wasichana imepokelewa kwa hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii. Ndoa za Mapema Marufuku Tanzania Shirika la Msichana Initiative ambalo ndilo lililowasilisha kesi mahakamani kupinga sheria ya kuolewa kwa wasichana wadogo, limesema: ''Maamuzi ya leo ni maamuzi muhimu kwa wasichana wa leo na wa baadae. Kwetu sisi kama shirika na kupitia mawakili wetu, tunaona huu ni uamuzi sahihi kwasababu unaendana na kasi ya maendeleo ya taifa hili katika kuwalinda watoto wa kike'' amesema Rebecca Byumi afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo. Shirika la Gender TZ limeelezea kwamba sheria iliyokuwepo iliwanyanyasa sana vijana hasa wa vijijini: Unaweza pia kusoma: Kwa mujibu wa shrika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto Unicef, 31% ya wasichana nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, huku 5% wakiolewa kabla ya kustimiza miaka 15. Unaweza pia kutazama: Haba na Haba: Changamoto za kuwalea watoto njiti Tanzania Mahakama ya juu zaidi Tanzania imebatilisha sheria inayoruhusu familia kuwaoza wasichana wadogo wenye umri wa kuanzia miaka 14. text: Kwa zaidi ya miaka mitatu amekuwa akikwepa kukamatwa huku akiimarisha usalama wake hatua mabyo imefanya hadi kufikia sasa kuonekana mara moja , wakati alipotoa hotuba yake mjini Mosul mwaka 2014 akitangaza taifa la kidini atakalolitawala. Mpema wiki hii Bahgdad alijitokeza katika kanda ya video ya dakika 18 akiwaomba wafuasi wake kuendeleza juhudi zake lakini akashindwa kutoa ishara za maficho yake. Je yuko wapi sasa hivi, je anatafutwa vipi na ni kwa nini Marekani na washirika wake walio na vifaa vya teknolojia ya kisasa hawawezi kumpata? Ripoti zinsema kuwa mnamo mwezi Novemba tarehe 3 2016 , Baghdad alifanya makosa ambayo karibia yahatarishe maisha yake. Vita vya kupigania mji wa pili wa Iraq Mosul vilikuwa viikiendelea huku vikosi vinavyoongozwa na Marekani vikiendelea kuwasukuma wapiganaji wa Islamic State. Kutoka eneo lisilojulikana la mji huo, Baghdad alitoa wito wa dakika 45 kwa wafuasi wake kuendelea kupigana. Ujumbe huo ulishikwa na mawimbi ya ndege za kijeshi za vikosi vinavyoongozwa na Marekani , sauti inayofanana na kiongozi huyo ilibainika na kulikuwa na juhudi za kumshambulia. Lakini kufikia wakati huo kiongozi huyo wa IS alikuwa tayari ametoweka, akitoroshwa na walinzi wake huku wakimshauri kutofanya tena hivyo. Haijulikani ni wapi kiongozi huyo wa IS amejificha Ilichukua majasusi wa Marekani takriban miaka 10 kumsaka na kumuaa Osama Bin laden , kati ya siku ya shambulio la 9/11 2001 hadi alfajiri ya tarehe 2 mwezi Mei wakati ambapo wanamaji wa Marekani walivamia nyumbani kwake nchini Pakistan. Kitengo cha Ujasusi nchini Marekani NSA pamoja na kile cha Uingereza cha GCHQ vina uwezo mkubwa wa mawimbi ya kijasusi , wakichunguza na kushika kabla ya kurekodi ujumbe ulio wazi na ule uliofichwa duniani. Hapo zamani , magaidi waliokuwa katika orodha ya watu wanaosakwa mara nyengine walikuwa wanaweza kujisema waliko kupitia ujumbe wa simu za rununu ama hata kuwa mtandaoni kwa muda mrefu katika eneo moja. Bin laden alikuwa mwerevu kuhusu hilo huku naye Baghdad pia akifuata nyayo. Kiongozi huyo wa al-Qaeda hatahivyo alitafutwa na kupatikana nyumbani kwake huko Abbottabad sio kupitia mifumo ya kidijitali bali kupitia muhudumu wake ambaye alikuwa akibeba kanda zake za propaganda na ujumbe mwengine kwa mikono kutoka eneo alilokuwa akiishi hadi kule ambako kanda hizo zilikuwa zikipakuliwa katika intaneti. Hotuba ya mwisho iliotolewa na Abu Bakr al-Baghdadi ndani ya msikiti mmoja mjini Mosul 2014 Kujua ni wapi kanda hizo zinatoka ndio ujasusi ambao Marekani imekuwa ikifanya kwanza kufautia kutolewa kwa kanda za video za Baghdad, lakini kundi lake la usalama lazima linajua hilo. Ni washirika wake wa karibu sana ambao wanaandamana naye na kuna uwezekano wamekuwa wakisafiri naye mara kwa mara. Ana usalama wa hali ya juu Ni mzaliwa wa Samarra, nchini Iraq, mwaka 1971, Jina lake kamili ni Ibrahim Awad al-Badri. Akiwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu tangu akiwa mdogo, baadaye alikuwa amefungwa katika kambi moja ya Marekani kwa jina Bucca 2004 kufuatia uvamizi wa Ufaransa na Marekani. Akiwa katika kambi hiyo aliweka ushirikiano mzuri na wafungwa wengine wakiwemo maafisa wa zamani wa ujasusi nchini Iraq. Aliifunza mengi kuhusu jinsi anavyoweza kufanya operesheni zake kutoka kwa maafisa wa ujasusi wa aliyekuwa rais wa Iraq Sadaam Hussein. Usalama wake ni wa hali ya juu ,kutokana na kiwango cha juu cha wasiwasi alionao. Lakini anajificha wapi? Inadhaniwa kwamba bado yuko katika mpaka kati ya Syria na Iraq. Katika mpaka huo ni raihisi kuanzisha mitandao ya biashara za ulaghai akitumia fedha kuweza kufanya lolote miongoni mwa watu wa makabila ya eneo hilo. Alishirikiana na maafisa wa zamani wa ujasusi wa seriikali ya Iraq. Aliyekuwa rais wa Iraq Sadaam Hussein alitoroka na kwenda mafichoni kwa miezi tisa baada ya utawala wake kupinduliwa. Kitengo cha operesheni za Marekani cha Red Dawn kilimsaka na kumpata katika eneo la chini la ardhi ambalo alikuwa akilitumia kujificha karibu na eneo alikozaliwa mjini Tikrit baada ya mtoa habari mmoja kumsaliti akitarajia kupewa zawadi ya mamilioni ya madolla. Lakini kuweza kumpata mshirika kama huyo ndani ya wandani wa Baghdad ni vigumu sana. Idadi ndogo ya watu walio karibu naye huenda ni watiifu sana kuweza kuvutiwa na majaribio ya fedha. Hivyobasi iwapo mtu huyo anayetafutwa zaidi duniani anaweza kukwepa mitandao, hapigi simu kwa kutumia simu za rununu na pengine anazunguka kutoka eneo moja la maficho hadi jingine je Marekani na magharibi zina matumaini gani ya kumpata? Pengine kabla ya kupanga shambulizi jingine la IS. Hatimaye, inaweza kuwa bahati na uvumilivu: uwezekano wa kuonekana na mwanakijiji anayechunguza , au hata mwanachama wa IS aliyechoka na ambaye ameamua kuwa hatimaye wakati wa kuchukua zawadi ya pesa ili kuweza kuishi maisha yake yote, akiwa tajiri mafichoni umewadia. Ni mtu anayesakwa zaidi duniani. Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) na uongozi wake wa kidini amewekewa $25m (£19m) na serikali ya Marekani kwa mtu yeyote atakayempata text: Wahalifu wa mtandaoni wanawalenga watu binafsi pamoja na sekta mbalimbali kama usafiri, utalii,afya ,elimu, bima na shughuli nyingine. Barua pepe za ulaghai ambazo zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza, kifaransa, kiitaliano, kijapani na kituruki zimebanika. BBC imefuatilia barua hizo. 1. Kuna barua ambazo zinaelekeza wapi watu wanaweza kupata tiba ya corona Muathirika akiwa anatafuta tiba akuta taarifa zake zimeibiwa Watafiti katika makosa ya kihalifu wamethibitisha kuwa walligundua barua pepe ambayo hawakuielewa kutoka kwa wateja mwezi Februari. Ujumbe ukiwa umetoka kwa daktari anayedai kuwa kuna chanjo ambayo imebainika iliyotengenezwa na serikali ya China na Uingereza. Inawataka watu kufungua nyaraka hiyo ambayo ina maelezo kuhusu chanjo. Barua pepe zipatazo 200,000 zimetumwa kwa wakati mmoja kwa watu tofauti. "Tumeona mawasiliano mengi kwa siku kadhaa ambazo zinafanya kampeni kuhusu corona ambayo haieleweki, wengi wakiwa wanawaogopesha watu ili kuwashawishi wafungue nyaraka hiyo." alisema Sherrod DeGrippo kutoka katika kampuni ambayo inafanya utafiti wa vitisho hivyo vya mtandao. Utafiti unasema kuwa utapeli huo unafanyika kila siku. Ukweli ni kwamba kampeni hizi za uhalifu mtandaoni zinapata mapokeo yaliyogawanyika. Cha muhimu tu ni kwamba watu wasifungue nyaraka hizo ambazo zinazunguka mitandaoni kuwatapeli. 2. Kodi kwa ajili ya Covid-19 Watafiti wa makosa ya kimtandao wamewakamata baadhi ndani ya wiki kadhaa. Lakini kwa mfano asubuhi tu ya leo, zaidi ya walaghai wa mtandaoni 200 wameonekana kwa muda mfupi tu. Kama mtu akibonyeza kitufe cha nyaraka cha yeye kupata ufadhili kutoka katika serikali ya uongo na huku wakihamasisha watu kutoa kodi na kupokea taarifa za kodi. Jambo la muhimu ni kutojibu barua pepe hizo, kwa kuwa hao ni wezi. 3. Hatua ndogo za kukabiliana na corona Wahalifu wa mtandaoni wameamua kutumia jina la shirika la afya duniani Kuna wahalifu wa mtandaoni wanadai kuwa wanawakilisha shirika la afya duniani (WHO) na kueleza namna gani wanaweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo. "Ukichukua hatua hii utapona,"hayo ndio madai yao. Lakini watafiti wanasema kuwa ushauri amabao wanautoa huwa hauna msaada wowote zaidi ya kuathiri komputa yako kwa kuweka programu ijulikanayo kama 'AgentTesla Keylogger'. Rekodi hiyo inawasaidia waweze kufuatilia waathirika wao katika mtandao. Kuzuia uhalifu huu ambao unadai unatoka WHO, wakati ni feki. Ni vyema watu kutembelea tovuti rasmi ya WHO au kurasa zao za mitandao. 4. Virusi vinavyoambukizwa kwa njia ya hewa Wahalifu wngine wa mitandaoni wanadai kuwa Covid-19 ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na hivyo kufanya maambukizi kusambaa zaidi katika jumuiya . Barua hiyo imeandikwa kama vile imetoka katika kituo cha kukabiliana na magonjwa (CDC). Wahalifu wa mtandao wanadaiwa kutumia njia hiyo hili kuwatisha watu. Lakini njia nzuri ya kujilinda na barua pepe za namna hiyo ni kuhakiki. 5. Changia hapa ili kukabiliana na mapambano Hakuna ukweli kuwa kituo cha kukabiliana na magonjwa kinatafuta michango. Barua pepe feki ambazo zinawataka watu kuchangia ili chanjo iweze kutengenezwa ni utapeli tu. Zaidi ya barua pepe 513 zimeeleza kuhusu virusi vya corona vinasababisha kushambuliwa kwa komputa na malware. "Tunategemea kuwa tatizo linakuwa siku baada ya siku, wakati virusi kweli vikiendelea kusambaa lakini usalama wa mtandaoni unapaswa kuzingatiwa na kila mmoja. Wataalamu wa masuala ya usalama wamesema kuwa, mlipuko wa virusi vya corona umefanya wahalifu wa mtandaoni kutumia mwanya huu kutapeli watu pia. text: Bi Park amepelekwa kizuizini Seoul Park, 65, alisafirishwa kwa gari hadi kwenye kituo cha kuwazuilia watuhumiwa wa uhalifu kusini mwa Seoul baada ya mahakama kuidhinisha kukamatwa kwake. Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa. Bi Park amekanusha madai hayo. Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14. Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata". Walisema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ungeharibiwa iwapo Bi Park hangekamatwa. Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza. Bi Park ndiye rais wa tatu wa zamani Korea Kusini kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu, shirika la habari la Yonhap limeripoti. Mahakama ya Seoul ilitoa kibali cha kukamatwa na kuzuiliwa kwa Bi Park anapoendelea kuchunguzwa kuhusu ulaji rushwa, kutumia vibaya mamlaka, kutumia mamlaka yake kushinikiza watu na kuvujisha siri za serikali. Uamuzi wa mahakama ulitolewa baada ya kikao cha mahakama kilichodumu saa tisa Alhamisi. Bi Park alihudhuria kikao hicho. Wafuasi wa Bi Park walikusanyika nje ya nyumba yake alipokuwa mahakamani Video zilionyesha Bi Park akiwa amebebwa kwa gari jeusi aina ya sedan na kusafirishwa hadi kizuizini. Licha ya kwamba ilikuwa mapema sana asubuhi, wafuasi wake karibu 50, wakiwa na bendera za taifa hilo na wakiitisha kuachiliwa kwake, walimsubiri langoni, shirika la habari la AFP linaripoti. Bi Park anaweza kuzuiliwa kwa hadi siku 20 kabla ya kushtakiwa rasmi. Akipatikana na hatia, anaweza kufungwa kifungo cha hadi miaka 10 jela. Hwang Kyo-ahn, wambaye ni mwaminifu kwa Bi Park, kwa sasa ndiye kaimu rais. Uchaguzi utafanyika tarehe 9 Mei. Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani wiki chache zilizopita Park Geun-hye amekamatwa na kuzuiliwa kuhusiana na tuhuma za rusha ambazo zilichangia kutimuliwa kwake kutoka madarakani. text: Mara ya mwisho Italia kushindwa kufuzu kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1958 Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930. baada ya mchezo huo mlinza mlango wa muda mrefu Gianluigi Buffon ametangaza kustaafu soka la kimataifa Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro. Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani. Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao. Mara ya mwisho Sweden kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 2006 Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake. Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho. Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden. text: Wagonjwa wakipata matibabu katika hosptali za nje Maafisa wa idara ya kudhibiti majanga wanasema mamia ya watu wamejeruhiwa vibaya kwa tukio hilo lililotokea Jumapili. Tetemeko hilo lenye nguvu ya 7 kwenye vipimo vya Richter limeharibu vibaya miundombinu ya umeme na barabara sambamba na nyumba. Tetemeko hili lilisababisha watu kuchanganyikiwa Katika kisiwa jirani cha Bali picha za video zimeonyesha watu wakikimbia majumbani mwao huku wakipiga kelele za msaada. Tetemeko hili limekuja wiki moja baada ya jingingine kuipiga sehemu hiyo ya Lombok, kisiwa maarufu kwa shughuli za utalii ambapo watu 16 waliuawa. Hatari ya kuwepo kwa kwa kimbunga ilitangazwa kisiwani hapo lakini ikaondolewa saa chache baadae. Msemaji wa idara ya kudhibiti majanga ya Indonesia amesema nyumba nyingi zimeathirika vibaya, ambapo nyingi kati ya hizo zilijengwa kwa kutumia nyenzo duni. Waziri wa mambo ya ndani wa Singapore Kasiviswanathan Shanmugam alikua ziarani katika kisiwa hicho ambapo ametuma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha namna chumba chake kilivyoathirika. Muonekano wa tetemeko hilo katika picha za rada Mtu huyu ambaye hakutaja jina lake anasema alikua katika shughuli zake wakati tetemeko hilo likitokea. ''Wakati natembea nilisikia mingurumo, taratibu, taratibu, aada ikawa mikubwa na watu wakaanza kukimbia wakisema ''tetemeko'' kila mmoja wetu alichanganyikiwa na kutoka nje ya nyumba, maafisa usalama wakasema kila mtu atoke ndani.'' Daktari Ketut Sudartana, wa Hospitali ya Sanglah Mjini Bali anasema wameamua kuwatibia wagonjwa nje ili kuhakikisha usalama wao. ''Kwa wakati huu tutawatibua wagonjwa hapa nje, na kwenye sehemu ya wazi ya mazoezi. Tutaweka mahema ya dharura nje kwa msaada a BPBP ili kuwahihadhi wagonjwa wote pale, ili madaktari na manesi wetu waweze kuwahudumia vizuri zaidi.'' Mzee aliyeishi miaka 146 afariki dunia Indonesia Rais wa Indonesia Joko Widodo amesema serikali yake inafanya jitihada za kutosha kunusuru maisha ya majeruhi huku akituma salam za rambirambi kwa familia za wafiwa. Mamlaka nchini Indonesia inasema zaidi ya watu 82 wamefariki baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukipiga kisiwa cha Lombok. text: Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba ni wagombea wawili pekee, Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) wangewania kwenye uchaguzi huo. Bw Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi huo Jumanne. Dkt Aukot amesema amefurahia uamuzi huo na kwamba sasa watakuwa kwenye uchaguzi kwani mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alikuwa amejaribu kuwafungia nje Hata hivyo, amesema chama chake bado kina masuala ambayo kilitaka yashughulikiwe na tume hiyo ya uchaguzi tangu mwezi Agosti na bado hayajashughulikiwa.Mgombea mwingine aruhusiwa kuwania urais Kenya Amesema kukubaliwa kwao kuwania kutawafungulia mlango kufanya mashauriano na viongozi wa IEBC. Dkt Aukot amesema chama chake kitatoa maelezo ya kina kuhusu msimamo wao katika kipindi cha siku mbili hivi baada ya mashauriano zaidi. Maafisa wakuu wa IEBC walikutana jana kutafakari kuhusu hatua za kuchukua baada ya hatua ya Bw Odinga lakini kufikia sasa bado hawajatoa tamko. Kujumuishwa kwa mgombea huyo kuna maana kwamba IEBC haiwezi kumtangaza Bw Kenyatta kuwa mshindi wa moja kwa moja hata baada ya kujiondoa kwa Bw Kenyatta. Wafuasi wa muungano wa upinzani Nasa wamekuwa wakiandamana kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi Ekuru Aukot ni nani? Dkt Aukot ni mtaalamu wa masuala ya katiba ambaye alikuwa mkurugenzi na afisa mkuu mtendaji wa wa Kamati ya Wataalamu iliyohusika katika kuandika rasimu ya ya Katiba ya Kenya iliyoanza kutekelezwa mwaka 2010. Alikuwa amesema awali kwamba anataka kuwa rais wa taifa la Kenya kutokana na kile anachosema ni kutoheshimiwa na kuhujumiwa kwa Katiba aliyosaidia kuwepo kwake. Dkt Aukot alizaliwa miaka 45 iliyopita katika eneo la Kapedo, katika kaunti ya Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya. Alianzisha chama cha Thirdway Alliance katika juhudi za kutoa uongozi mbadala na uongozi wa mageuzi kwa Wakenya. Anaamini Wakenya hawawezi kuwategemea tena viongozi ambao wamekuwa madarakani kufikia sasa kumaliza ufisadi na ukabila. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na IEBC, Dkt Aukot alipata kura 27,311 sawa na 0.18%, nafasi ya tano kati ya wagombea wanane walioshiriki, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 August ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu. Nini kitatendeka baada ya Odinga kujiondoa? Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru mgombea urais wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti ashirikishwe kwenye uchaguzi mkuu mpya unaopangiwa kufanyika tarehe 26 Oktoba. text: 'Monty Python' alifariki wiki chache tu baada ya kugunduliwa Shirika la huduma kwa wanyama pori na bustani za wanyama Northern Territory Parks and Wildlife Service wameeleza kwamba nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa pakubwa katika mitando ya kijamii, ni wa "kustaajabisha". Amepewa jina la Monty Python, nyoka huyo aina ya chatu alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa mnamo Machi. Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake limeonekana kuwa ni mabadiliko ya asili Maafisa walimgundua nyoka huyo katika mji wa Humpty Doo, 40km kusini mashariki mwa Darwin. Ana urefu wa 15 inchi na alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake, maafisa wameiambia BBC. 'Hali' ya kawaida Shirika hilo la huduma kwa wanyama pori limesema picha za X-ray zimeonyesha kwamba hakuwa na vichwa viwili kwa pamoja. "Badala yake alionekana kuwa na fuvu moja la kichwa na jicho la ziada ukijumlisha, macho matatu yanayofanya kazi sawasawa," lilieleza kwenye Facebook. Alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake Mtaalamu wa nyoka Profesa Bryan Fry amesema mabadiliko ya maumbile ni sehemu ya kawaida ya kuumbwa. "Kila mtoto hupitia mabadiliko ya kiwango fulani - huyu alishuhudia mabadiliko yasio ya kawaida," amesema Profesa Fry, kutoka chuo kikuu cha Queensland. "Sijaona nyoka mwenye macho matatu awali, lakini tumeona chatu mwenye vichwa viwili katika maabara yetu - ni aina tofuati ya mabadiliko kama tunavyoona kwa pacha wachanga wanaozaliwa wakishikana." Ameashiria kwamba huenda jicho hilo la tatu likawa " sehemu ya mwisho ya pacha wa nyoka huyo aliyefyonzwa". Maafisa wa wanyama pori wamesambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara kaskazini mwa Auustralia. text: Kura hiyo inayotajwa kuwa "Kura yenye umuhimu" itafanyika baadaye leo wakati mjadala wa siku tano kuhusu Brexit ukikamilika. Bi May amewataka wanasiasa kuunga mkono mpango wake au kuhatarisha "kuwavunja moyo raia wa Uingereza". Lakini huku wabunge wake mwenyewe wakitarajiwa kujiunga na wa vyama vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo, inatarajiwa pakubwa kwamba mpango huo hautofaulu. Wabunge pia watapata fursa ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ambayo yanaweza kuunda upya mpango huo kabla ya kura kuanza 19:00 kwa saa ya GMT. Uingereza inajitoa katika EU mwezi Macho, na mpango wa sasa ni wa kipindi cha mpito utakaomalizika mwishoni mwa mwaka 2020 Waziri mkuu aliwahotubia wabunge wake Jumatatu jioni katika jitihada za mwisho kujaribu kupata uungwaji mkono kwa mpango wake - unaojumuisha mpango wa kujitoa kwa misingi ya ambavyo Uingereza itajitoa kwenye Muungano wa Ulaya na tangazo la kisiasa kwa uhusiano wa siku zijazo. Awali, katika bunge la wawakilishi, alisema: "Hauko imara kabisa lakini wakati historia itakapoandikwa, watu watatazama uamuzi wa bunge hili na watauliza, 'Je tuliwajibika kuhusu kura ya taifa hili kujitoa katika EU, tuliuchunga uchumi wetu, usalama na muungano au tuliwavunja moyo raia wa Uingereza?'" Bi May pia alijaribu kuwashawishi wabunge kuhusu mpango wenye mbadala wenye mzozo wa kuepuka kurudishwa kwa ukaguzi wa mipakani kati ya Uingereza na Ireland. Ametaja hakikisho jipya kutoka kwa EU kwamba mpango mbadala wa forodha unaopendekezwa utakuwa ni wa muda tu , na iwapo utaidhinishwa utadumu kwa "muda mfupi iwezekanavyo". May atalihotubia bunge Jumanne asubuhi, kabla ya mjadala kuendelea mwendo wa mchana. Lakini wabunge wengi wa Tory na wa Democratic Union wanapinga vikali mpango huo. Takriban wabunge 100 wa Conservative na 10 wa Democratic Union huenda wakajiunga na chama cha Leba na vyama vingine vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo. Mpango huo ulipata pigo kubwa katika bunge la Malodi Jumatatu usiku, wakati wabunge walipounga mkono hoja ya chama cha Leba kwa kura 321 dhidi ya 152. Hatahivyo, wabunge watano wa Conservative ambao wamekuwa wakosoaji wa mpango wa kujitoa sasa wanasema wataiunga serikali mkono , pamoja na wengine watatu wa chama cha Leba na wa kujitegemea, Frank Field. Mapendekezo kadhaa ya marekebisho yamewasilishwa na wabunge kwa mpango wa May kujaribu kuufanyia mageuzi bungeni. Nini kitakachofanyika baada ya hapa? Iwapo wabunge watapinga mpangu huu, Bi May ana vikao vya siku tatu tu kuweza kurudi bungeni na mpango mbadala. Baadhi wanasema huenda akaelekea Brussels Jumatano kujaribu kushauriana zaidi na EU kabla ya kurudi tena katika bunge la wawakilishi kutoa taarifa kuhusu mpango mpya kufikia Jumatatu. Namna Brexit utakavyoathiri soko la Kenya Hili baada ya hapo, huenda likapigiwa kura na wabunge. Iwapo hili pia halitofaulu, kuna pendekezo lililowasilishwa na wabunge wakuu wa chama cha Conservative Nick Boles, Sir Oliver Letwin na Nicky Morgan wa "Mswada wa pili wa kujitoa katika Muungano wa Ulaya". Hili litawapa mawaziri wiki tatu za ziada kuja na mpango mwingine na kuupitisha bungeni. Iwapo hili nalo bado halitofaulu, wanapendekeza kuipa kamati ya mashauriano jukumu la kuja na mpango wa kuafikiana utakaotokana na vyama vya upinzani pamoja na chama cha Conservative. Pendekezo hili pia bado litahitaji kupigiwa kura bungeni. Wabunge Uingereza wanajitayarisha kupiga kura kwa iwapo kuunga au kutounga mkono mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya. text: Mwanamke huyu alikuwa tayari amefika katika kituo cha kupiga kura Baadhi ya watu ambao hawakua na habari uchaguzi umeahirishwa walikuwa wamefika klatika vituo vyao vya kupigia kura. Musa Abubakar, ambaye alisafiri umbali wa kilomita 550 (340 miles) kutoka mji mkuu wa Abuja ili kupiga kura katika mji wa kaskazini wa Daura, ameiambia BBC "haamini" kilichotokea. Yeye ni mmoja wa raia wengi wa Nigeria waliyosafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine kushiriki zoezi la upigaji kura. "Sijui la kufanya. Sijafurahia hatua hii hata kidogo," alisema bw Abubakar. Musa Abubakar Sasa anakabiliwa na kibarua cha kuamua ikiwa atasubiri kupiga kura Daura kisha arudi kazini Abuja ama ajiandae kwa safari ya pili au kuachana kabisa na shughuli hiyo Baadhi ya watu waliamua kuangazia hasira zao katika mtando wa kijamii wa Twitter, kwa kutumia Hashtag ya "waahirishwa", "kuahirishwa" na "Inec". Bobby Ezidi, alisema tume ya uchaguzi imezembea katika kazi yake . Wengine wamekuwa wakisambaza kanda ya video inayomuonesha bw Yakubu akisisitiza kuwa kila kitu kiko shwari "uchaguzi hautaahirishwai" na kujiuliza nini kilichobadilika. Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi (INEC) ilitangaza hatua hiyo saa tano tu kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura hii leo Jumamosi. "Haiwezekani kuendelea na zoezi la uchaguzi kama ilivyopangwa," mwenyekiti wa tume hiyo Mahmood Yakubu amesema, akitaja hitilafu za kimipango. Amesema uamuzi huo mgumu umehitajika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa huru na haki. Maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema hitilafu za kimipango zimefanya kuwa vigumu kuendelea na uchaguzi Uchaguzi wa urais na ubunge umepangiwa sasa kufanyika Jumamosi ijayo Februari 23. Uchaguzi wa Ugavana, wawakilishi wa majimbo na mabaraza ya manispaa yamepangiwa kufanyika Jumamosi Machi 9. Uamuzi huo umetolewa baada ya mkutano wa dharura katika makao makuu ya tume hiyo ya uchaguzi katika mji mkuu Abuja. Atiku Abubakar (kulia) na Rais Buhari ni wagombea wakuu miongoni mwa wengine 73 katika uchaguzi wa Nigeria Ni kwanini Uchaguzi umeahirishwa? Bwana Yakubu amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya 'ukaguzi wa makini' wa 'mpango ya namna uchaguzi utakavyofanyika', akiongeza kwamba kuna 'jitihada kubwa za kuhakikisha kuna uchaguzi wa huru, haki na wa kuaminika'. Amesema ni muhimu kuchelewesha uchaguzi huo kuipa tume nafasi ya kukabiliana na masuala muhimu na pia "kusalia na hadhi katika uchaguzi", lakini hakutoa ufafanuzi zaidi. Katika wiki mbili zilizopita ofisi kadhaa za tume hiyo ya uchaguzi ziliteketezwa moto, huku maelfu ya vifaa vya kunakili kadi , na kadi za upigaji kura zikiharibiwa. Pia kumekuwa na taarifa ya uhaba wa vifaa vya upigaji kura katika baadhi ya majimbo 36 ya nchi hiyo. Nigeria imelazimika kushinikiza usalama wake kuelekea katika uchaguzi huu uliokumbwa na ghasia. Siku ya Ijumaa, maafisa katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria wamearifu kugundua miili ya watu 66, 22 kati yao ni ya watoto, na 12 ya wanawake waliouawa na 'wahalifu'. Uchumi wa Nigeria unategemea kwa kiwango kikubwa hifadhi zake za mafuta ambazo ni kubwa zaidi barani Afrika. Uchaguzi huu ni muhimu kiasi gani? Mustakabali wa taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika na lenye uchumi mkubwa, umo katika mizani. Yoyote atakayeshinda inabidi ashughulikie masuala kama uhaba wa umeme, rushwa, ukosefu wa usalama na uchumi unaojivuta. Kuna wagombea 73 waliosajiliwa katika uchaguzi wa urais, lakini kampeni zimegubikwa na Rais Muhammadu Buhari, mwenye umri wa miaka 76, na mpinzani wake mkuu, aliyekuwa makamu wa rais Atiku Abubakar, mwenye umri wa miaka 72. Buhari anasema amejenga msingi madhubuti kwa ustawi, lakini mpinzani wake anasema Nigeria mambo hayaendi sawa. Wote wanatoka eneo la kaskazini mwa nchi lenye idadi kubwa ya waislamu. Wakati wote wana umri wa miaka 70, zaidi ya nusu ya idadi jumla ya watu Nigeria, milioni 84 waliosajiliwa kupiga kura wana umri wa chini ya miaka 35. Je Nigeria imewahi kuwa na matatizo katika uchaguzi? Ndio. Sio mara ya kwanza uchaguzi umeahirishwa Nigeria - uchaguzi wa awali mnamo 2011 na 2015 ulicheleweshwa kwa siku kadhaa. Mnamo 2015, taifa hilo liliagiza kufungwa kwa mipaka yake ya nchi kavu na majini kufuatia kuwadia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa, huku kukiwepo taarifa kwamba watu wa nchi za nje wanapanga kuingia Nigeria kupiga kura. Mwaka huo huo, mojawapo ya wagombea alifariki wakati kura zinahesabiwa. Hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais na ubunge nchini Nigeria saa tano kabla ya zoezi la upigaji imezua mjadala mkali kote nchini humo. text: Jitihada za uzimaji moto zikiendelea Wafanyakazi wa dharura waliokuwa wakifanya shughuli za uokoaji wanaelezea matukio ya uharibifu uliotokana na moto huo ikiwemo kuteketea kwa msitu pamoja na magari yaliyokuwa katika maeneo hayo. Takribani watu 74 wamethibitishwa kufariki lakini idadi ya watu ambao waliopotea bado haijajulikana. Watu wakikimbilia baharini kujiokoa karibu na kijiji cha Mati Moja ya uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto huo Wakazi walitakuwa kuhama makwao Katika kisa kimoja miili 26 iligunduliwa kwa pamoja ikiwa juu ya mwamba pembezoni mwa bahari katika eneo la Mati, moja kati ya miji iliyoathirika zaidi. Wakazi wanasema walilazimika kukimbilia baharini kujiokoa walipoona wamezingirwa na moto huo. Baadhi hawakuweza kufika baharini kwa wakati. Mamlaka katika mji huo zina mashaka kuhusiana na chanzo cha moto huo na kwamba huenda umesababishwa makusudi. Waziri mkuu wa Ugiriki Alex Tsipras amesema janga hilo limeathiri nchi nzima. ''Nchi inapitia katika wakati mgumu sana. Mamia ya watu wamefariki na hili linamuumiza kila mmoja haswa kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Leo Ugiriki inaomboleza, na kwa kumbukumbu ya wale wote waliofariki tunatangaza siku tatu za maombolezo.'' Alisema Tsipras. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema ni janga la kitaifa Katika eneo la Neos Voutzas karibu na mji wa Mati, wakaazi walikua wakitizama mabaki ya nyumba zao. Theofilaktos Logothetis ni mmoja wao na anasema alikua mmoja wa wale waliokua wa mwisho kabisa kutoka nyumbani kabla ya miale ya moto kufika kwa majirani zake. Moto ukionekana kusogelea sehemu ya utalii ''Moto ni kama ulikuwa unatukimbiza, aliyekua anaweza kuondoka kabla haujafika ilikua bahati. Mtu aliyekua kulia kwangu nilipokua nikiendesha kuelekea barabara kuu aliunguzwa mpaka akawa mkaa.'' Serikali ya Ugiriki inasema kuna uwezekano mkubwa watu wengi zaidi wakawa wamefariki katika kisa hicho ambacho kimeacha simanzi kwa nchi nzima. Siku tatu za maombolezo zimetangazwa nchini humo. Jitihada za uokoaji zinaendelea huko nchini Ugiriki, ambako moto mkubwa uliwaka kuzunguka maeneo ya mji na vijiji karibu na mji mkuu Athens. text: Mwanaume akionesha sehemu ya ndege iliyopatikana katika eneo ambappo ndege iliodondoka Sikua ya Jumamosi, ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na wahudumu ilianguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa ndege mjini Moscow. Maafisa wanasema sababu zinapelekea kuwa hali ya hewa, hitilafu za kibinadamu na kiteknolojia. Tukio hili halijahusishwa kwa namna yoyote na ugaidi. Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Orsk kwenye milima ya Ural. Ilianguka karibu na kijiji cha Argunovo, kilomita 80 kusini mashariki ya Moscow. Mabaki ya ndege na miili ilisambaratika katika eneo hilo. Waokoaji na wachunguzi wakichambua mabaki ya ndege Mtoto na vijana wawili walikuwa miongoni mwa miili ya abiria iliyo patikana, kwa mujibu wa chombo cha habari cha Tass. Waokoaji walilazimika kuacha magari yao na kutembea kwa mguu hadi eneo ambalo ndege iliangukia. Msemaji wa idara ya uchunguzi Svetlana Petrenko, amesema kuwa operesheni hiyo ya kusaka eneo hilo itachukua siku moja kwa mujibu wa mtandao wa habari wa The Gazeta.ru Ndege hiyo haikupiga simu ya dharura lakini rikoda moja imepatikana. The Flightradar24 website shows the flight path Rais Vladimir Putin ametoa salaam za rambirambi kwa familia za waathirika. Nchi za Marekani na Uingereza zote zimesema kuwa "wamehuzunika sana" na tukio hilo. Hii ni mara ya kwanza ndege ya abiria inaanguka katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja- mwaka 2017 ilikuwa mwaka wa usalama zaidi katika rekodi ya usafiri wa anga. Wachunguzi nchini Urusi wanaendelea kusaka maeneo yaliofunikwa na theluji karibu na jiji la Moscow ilikupata fununu za kwanini ndege hiyo ilidondoka text: Watoto wengi walioathiriwa kwa sasa wako chini ya usimamizi wa jamaa zao. Idadi hiyo ndio imetajwa kuwa kubwa zaidi kulingana na ripoti hiyo. Watoto wengi walioathiriwa kwa sasa wako chini ya usimamizi wa jamaa zao. Vita vilizuka huko Kasai mnamo mwezi Agosti 2016 baada ya kiongozi mmoja wa kitamaduni kuuawa katika ghasia na maafisa wa usalama. Vita hivyo vimeongezeka na kuwaacha takriban watu 3000 wakiwa wameuawa. Umoja wa Mataifa umegundua makaburi mengi ya halaiki katika eneo hilo. ''Vita hivyo vimewalazimu takriban watu milioni 1.4 kutoroka makwao huku wengine 60,000 wakihamishwa mwezi Juni pekee'', alisema kaimu mkuu wa Unicef nchini DR Congo Tajudeen Oyewale. Kiongozi huyo wa kitamaduni aliyeuawa alikuwa na wadhfa wa kamuina Nsapu. Tangu kifo chake makundi tofauti ya wapiganaji wa Kamuina Nsapu yamejitokeza yakipigania malengo tofauti ,lengo lao kuu ikiwa mamalaka. Takriban watoto 850,000 wamelazimika kutoroka vita katika mkoa wa Kasai nchini DR Congo kulingana na maafisa wa Unicef. text: Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Katika taarifa yake hapo jana Jumapili , serikali ya Somalia imesema 'haina mipango wala haikuwa na mipango ya kufanya hivyo'. Taarifa hiyo ilitolewa baada ya kuwepo ripoti za kikao kilichofanyika katika mji mkuu Mogadishu cha maafisa wakuu serikalini akiwemo rais mwenyewe Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo na waziri mkuu Hassan Ali Khayre. "Somalia kwa sasa haina mpango wala haikuwa na mpango wa kunadi sehemu yoyote katika eneo linalo zozaniwa baharini hadi pale mahakama ya ICJ itakapobaini mipaka ya nchi husika," imeeleza taaifa hiyo rasmi. Imetoa ahadi kwa Kenya kuwa haitojihusisha katika shughuli zozote katika maeneo yalio kwenye mzozo hadi mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho. Somalia imeihakikishia Kenya kuwa itasubiri uamuzi wa mwisho wa mahakama ya ICJ Siku ya Jumamosi jioni, Nairobi ilitangaza kuwa inamrudisha nyumbani balozi wake aliyepo Mogadishu Luteni Jenerali mstaafu Lucas Tumbo, ikidai kuwa uamuzi wa Somalia kupiga mnada eneo moja la mafuta mjini London wiki iliopita ni sawa na uchokozi dhidi yake na mali yake asili. Vilevile Nairobi ilimrudisha nyumbani balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Nur katika kile ambacho serikali ya Kenya baadaye ilifafanuwa kwenye vyombo vya habari nchini kuwa ni kutoa fursa ya majadiliano ya kila upande katika suala hilo. ''Kwa kupuuza suluhu ya sheria za kimataifa kuhusu mipaka ama makubaliano ya kisiasa kupitia diplomasia , serikali ya Somalia imeonyesha wazi bado haijakomaa kisiasa'' , amesema katibu wa maswala ya kigeni nchini Kenya Macharia Kamau. Somalia kupitia wizara ya mambo ya nje, imeelezea masikitiko yake kufuatia hatua hiyo ya Kenya kumrudisha balozi wake pasi kuwepo mashauriano. Eneo linalozozaniwa linakakisiwa kuwa na mafuta na gesi Mambo 3 makuu yanayohatarishwa kwa mvutano huu Kumeshuhudiwa mvutano na malumbano kuhusu mipaka baina ya mataifa hayo mawili katika siku za nyuma. Baadhi ya wachambuzi wanaona kwamba hili ni jambo lisilohitajika kwa sasa. Na huenda ni jambo ambalo mataifa yote mawili yanalitambua kutokana pia na kauli ya Somalia kwenye taarifa yake jana ya kukanusha madai hayo ya kupiga mnada mafuta na gesi katika eneo hilo linalozozaniwa, kwa kukiri kwamba 'mataifa hayo "yameshikana katika namna ambayo hayawezi kuvunjika" na kuwa yana uhusiano mzito wa kihistoria na kitamaduni, ambayo Somalia haitaki kuuvunja. Kwa jumla, ni mataifa yanayotegemeana. Mchambuzi wa masuala ya Afrika, Ibrahim Aidid, anasema Kenya na Somalia ni mataifa ambayo yameweza kufanya vitu vingi kwa pamoja na kwa ushirikiano mkubwa. Mataifa hayo mawili yamekuwa yakishirikiana katika masuala ya: Usalama: Kenya inategemea ushirikiano mkubwa kutoka Somalia katika vita dhidi ya ugaidi, hususan dhidi ya kundi la wapiganaji wa Alshabaab, ambalo ni tishio sio tu kwa mataifa hayo mawili, lakini pia kieneo. Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka mataifa mengine kama Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya mwamvuli wa kikosi cha kulinda amani Amisom, wamekuwa wakiisaidia serikali ya Somalia katika vita hivyo. Wanajeshi wa Kenya waliingia Somalia mnamo mwaka 2011, kuwapiga vita wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda. Biashara: 'Kenya inapeleka biashara Somalia. Imenufaika pakubwa kifedha kwa bidhaa kwa mfano kama miraa zinazosafirishwa hadi Somalia', anasema mchambuzi wa kisiasa Ibrahim. Usafirishaji wa miraa au mirungi hadi Mogadishu, ni biashara inayokisiwa kuwa na thamani ya karibu dola nusu milioni kila siku. 'Somalia kwa upande wake, inanufaika kwa biashara ya samaki wanaoingizwa Kenya' anasema Ibrahim. Uhamiaji: Maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia wamehifadhiwa katika mojawapo ya kambi kubwa duniani ya Daadab iliopo nchini Kenya. Kambi hiyo ya Dadaab ilijengwa mnamo 1991 kuzihifadhi familia za jamii zilizokuwa zinatoroka mzozo nchini Somalia, na baadhi ya watu wamekuwa wakiishi hapo kwa zaidi ya miaka 20. Somalia inaitazama Kenya kama mshirika wake mkuu katika kufanya mageuzi ndani ya nchi hiyo. Na huenda ndiyo mambo yanayostahili kupewa uzito kwa Rais Mohammed Abdullahi Farmajo na Rais Uhuru Kenyatta wanapotathmini na kutafuta suluhu kwa mvutano uliopo sasa, anasema mchambuzi Ibrahim. Somalia imekanusha tuhuma kwamba imenadi maeneo ya mafuta yaliopo katika mpaka unaozozaniwa kati ya taifa hilo na Kenya. text: Mwanamke aliyejifunika sehemu ya uso wake na bendera ya Kenya akiandamana kupinga mauaji ya George Floyd Wiki yangu ya kwanza mji wa New York msimu uliopita, nilialikwa chakula cha jioni katika nyumba ya rafiki yangu huko Upper West Side. Nilinunua matunda ya kumpelekea na nikafika kwenye jengo analoishi nikiwa nimebeba mfuko wa plastiki. Wahudumu wa eneo hilo mlangoni wakanionesha njia ya nyuma ya jengo ambapo ni lazima upitie eneo la kutupa takataka ambalo lilikuwa chafu kupita kiasi. Baada ya kumaliza kupanda ngazi, mwenyeji wangu alifungua mlango na kuonesha kuwa mwenye aibu, uso wake ulikua umebadilika rangi. Larry Madowo anasema: ''Tukio lilinionya kabla kwamba Marekani inaweza kuwa nchi ya fursa kwa wengi, lakini inaweza bado kuishusha thamani kwa rangi yangu na kuniona kuwa asiye na thamani'' "Bawabu ni mbaguzi alifikiria kwamba wewe ni mhudumu wa kuwasilisha bidhaa na hivyo basi akakuruhusu kuingia kupitia mlango wa nyuma," akaelezea wakati anaomba msamaha. Nimefanyakazi katika nchi zenye ubaguzi wa rangi wa hali ya juu kama Afrika Kusini na Uingereza na nimesafiri maeneo mbalimbali duniani lakini bado inahuzunisha kuona kwamba Mmarekani hakufikiria kuwa mzungu kama rafiki yangu na mume wake wanaweza kuwa na miadi ya chakula cha jioni na mtu mweusi. Tukio hilo liliniandaa kwamba Marekani inaweza kuwa nchi yenye fursa kwa wengi lakini pia inaweza kunidhalilisha kiasi cha kunibagua kirangi na kuniona nisie na thamani. Haikujalisha kama ninatoka kwenye taifa ambalo wengi wao ni watu weusi, watu wanaofanana na mimi hapa, wanahitajika kufikiria mara mbili kwa utu wao dhidi ya mfumo ambao mara nyingi unawatenga, kuwaondoa na kuwaadhibu. Mwanaume huyu alichora picha ya George Floyd kutoa heshima zake kwa Floyd Nchini Kenya, naweza kutokomea kwenye kundi la watu wengi lakini Marekani, mara nyingi huwa ni mlengwa kwasababu ya rangi yangu nyeusi. Siku moja baada ya kampuni ya uwekezaji kumfuta kazi Amy Cooper kwa kuita polisi kwasababu mtu mweusi alimtaka kufuata sheria za kwenye bustani na kumfunga mbwa wake, polisi mzungu alipiga magoti juu ya shingo ya George Floyd kwa kipindi kirefu na hatimaye akasababisha kifo chake. Ilinisikitisha na kunivunja moyo mno. Kifo cha Floyd: Wamarekani weusi wasema 'hawako salama' Wakati maandamano yalipotokea kote nchini Marekani na kudai haki kwasababu ya mauaji ya Floyd, na watu wengine weusi ambao wameuawa na polisi, nilizuia pumzi kidogo, nikatafakari. Nawezaje kuanza kuomboleza mtu ambaye hata sikuwa ninamfahamu?, Naweza kuwa na machungu ambayo hata sikutarajia, kama mwafrika ambaye tu ndo nilikuwa ninaaza kuishi Marekani? Nilianza kufikiria ikiwa ningeweza kumudu kama ningekuwa raia mweusi wa Marekani katika hali hiyo. Kisha nikaona video inayoonesha waandamanaji katika ufukwe wa California, ikionesha bayana dhamira yao. "Namna nzuri ambayo raia Waafrika nchini Marekani wanaweza kuwasaidia Wamarekani wenye asili ya Afrika ni kuwaunga mkono na kuelewa kwamba sote ni sawa," alisema mmoja ambaye alikuwa ameandamana. Nilimuuliza Tom Gitaa - mwandishi ya gazeti la Mshale, ambalo linalenga wahamiaji wa Afrika eneo la Midwest Marekani - maoni yake kuhusiana na maandamano hayo, uharibu na uporaji wa mali ambao umetokea katika mji wa Minneapolis. "Wengi wetu hatukukua tukiwa na ufahamu wa masuala ya haki za kiraia barani Afrika na hivyo basi wakati mwengine ufahamu wetu huwa haupo. "Lakini kwa masuala kama mateso na unyama unaotekelezwa na polisi na unyanyapaa makazini, vinafanana na kile ambacho raia weusi wa Marekani wamekuwa wakikabiliana nacho kwa miaka kadhaa," amesema Bwana Gitaa, ambaye alihamia Marekani kutoka Afrika Mashariki miaka takriban 30 iliyopita na ambaye msichana wake, 24, raia wa Marekani amekuwa miongoni mwa wanoapaza sauti kupitia maandamano hayo barabarani. George Floyd alikufa baada ya afisa wa polisi kupiga goti kwenye shingo lake kwa zaidi ya dakika nane Kila wakati kumekuwa na wasiwasi kati ya Waafrika na raia weusi wa Marekani. Rafiki yangu Karen Attiah, na mimi tulizungumzia suala hili miaka miwili iliyopita katika gazeti la The Washington Post pale filamu inayomuangazia shujaa raia mweusi ya Black Panther ilipotoka. Ni mhariri wa makala ya Global Opinions, gazeti la The Washington Post, binti ya mhamiaji mweusi - aliyezaliwa Marekani lakini ambaye ana uhusiano wa karibu sana na bara ambalo ndo chimbuko la wazazi wake. Taarifa zaidi kuhusu kifo cha Floyd: Karen aliniamba kwamba wazazi wake kwa sasa wanajadiliana masuala la ubaguzi wa rangi hasa kwa namna ambayo yeye na ndugu zake hawakuwahi kusikia mijadala hiyo wakati wanakua. "Nafikiri tulikuwa tunahitajika kutokaribia na raia weusi wa Marekani kwasababu tulikuwa wahamiaji, tulikuwa tofauti," aliniambia wiki hii. "Lakini sasa hivi tunaelewa kwamba ikiwa polisi ataona rangi ya ngozi yako, hatauliza ikiwa wewe ni umetoka Ghana, Nigeria au Zimbambwe, au Atlanta ama kusini mwa Dallas, kwao wao wameona tu mtu mweusi." Wasani wa Afrika kama vile Lupita Nyong'o na mchekeshaji Trevor Noah wanatumia majukwaa yao yenye ushawishi kuunga mkono maandamano ya haki na kuonyesha wanafiki katika baadhi ya wanaokosoa maaandamano. Umoja wa Afrika (AU) pia nao ulitoa taarifa isiyo ya kawaida kushtumu mauaji ya Flyod na kutaka serikali ya Marekani kuhakikisha inatokomeza aina yoyote ile ya ubaguzi. Raia wa kwanza waliwasili Marekani kama watumwa - katika eneo la Virginia lililotawaliwa na Uingereza - miaka 401 iliyopita. Msanii wa Ghana Kwame Akoto-Mamfo amebuni vinyago vinavyoonyesha waliyopitia maishani mwao Mwaka jana, baadhi ya familia zao walirejea Afrika kuadhimisha "Mwaka wa Kurejea" pale ambapo mababu zao waliibwa karne nne zilizopita. Moja ya matamasha lilikuwa lile la Afrochella lililofanyika nchini Ghana Desemba mwaka jana wazo la Abdul Karim Abdullah. Nilipomuita, alikuwa ndio ana lala baada ya kutokea kwa maandamano makubwa usiku eneo analoishi la Bronx mjini New York. "Waafrika wengi wanapuuza ukweli wa kwamba hivi pia ni vita vyao," alisema. "Ukosefu wa haki kwa watu weusi popote pale ni ukosefu wa haki. Tunastahili kushirikiana na kupigana vita hii pamoja." Waafrika walio nchini Marekani pia nao wameandamana pamoja na wengine katika vuguvugu la Maisha ya Watu Weusi pia ni Muhimu, wakiunga mkono maandamano dhidi ya wazungu, wakachanga pesa kwa ajili ya kupatikana kwa haki na kuandaa matukio yao wenyewe kuonesha umoja katika jamii ya watu weusi. Waandamanaji waliokuwa wamejifunga bendera za nchi zao pia nao wametambuliwa kushiriki kwenye maandamano katika maeneo mbalimbali Marekani. "Watu wengine, hasa raia weusi ndio ambao kwa kiwango kikubwa wanateswa, hawathaminiwi na kutoeleweka katika dunia hii," Jada Walker amesema hivyo akiwa anatiririkwa na machozi mbele ya kundi la waandamanaji katika ukumbi wa Dallas, Texas. Alikuwa na wasiwasi kuhusu kile kinachomsubiri mpwa wake wa miaka miwili mwenye mahitaji maalum atakapokua. Kwasababu ya historia ya kutokea kwa ghasia ambayo imekuwa ikiendelea kati ya raia weusi na wazungu, mara myingi wazazi huwa katika njia panda. Ifrah Udgoon, mzaliwa wa Somalia mwalimu wa sayansi huko Columbus, Ohio, anaishi akiwa na hofu hiyo kwa kijana wake, 13. "Kila siku inayopita unaona ukweli wa kwamba karibu kama haijafika tayari, ataacha kuonekana kama mzuri na mtanashati na kugeuka kuwa tishio. Aliandika katika gazeti la Mail & Guardian Afrika Kusini. Bi Udgoon anakabiliana na vita kama wahamiaji wengine wengi: "Nikiwa hapa natarajiwa kuwa na shukrani. Lakini niliuza nafsi yangu kwa shetani?" Bwana Abdullah anachukulia Afrochella kama jukwaa la mtandaoni la kuunganisha Waafrika weusi wanaokabiliana na vikwazo kama hivyo. "Niliwasiliana na rafiki zangu kutoka Haiti, Benin na wale wa taifa la St Vincent and the Grenadines kwasababu ubaguzi hauna utaifa. Mfumo huu wa ubaguzi unatuathiri sote. "Kwa kipindi kirefu, sikuweza kutambua kwamba huu ni ukosefu wa haki hadi nilipoanza kuelewa lugha yenyewe. Vita hii ni vita yangu." Bwana Abdullah amesema. Sio kwamba ni vita tu ya raia weusi Marekani kama yeye, ni vita ya haki ya kuwa mweusi na salama nchini Marekani. Haya hapa tena maneno ya Karen kwasababu yalikuwa na hitimisho thabiti: "Nafikiri kile kinachoonekana sasa ni kupinga maandamano ya weusi na hilo linahamasisha ufahamu wa ushirikiano katika changamoto nyingi ingawa sio sawa lakini zote zinaendana." Wakati maandamano yanapoendelea kutanda Marekani kwasababu ya kifo cha raia mweusi wa George Floyd akiwa mikononi mwa polisi, mwanahabari wa Kenya Larry Madowo ameandika kuhusu ubaguzi ambao ameshuhudia nchini humo. text: Majina ya wachumba hao yalitanda katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter huku mashabiki wengi wakiwatakia heri njema. Waigizaji hao wamehusika katika filamu tatu pamoja, zikiwemo zilizopata umaarufu mkubwa Bajirao Mastani na Padmaavat. Jarida la Forbes linaripoti kuwa wanandoa hao wamepata faida ya $21m katika kipato cha pamoja mwaka jana. Harusi ilifanyika Jumatano, siku iliyo kumbukumbu ya walipoigiza filamu yao ya kwanza pamoja mnamo 2013 - Goliyon Ki Rasleela Ram-Leela. Licha ya kwamba waandishi hawakualikwa kwenye harusi hiyo, picha za sherehe za kabla ya harusi zilifichuka katika majarida ya burudani na magazeti. Watu wamekuwa wakizitafuta picha hizo pakubwa ambazo huenda zimesambazwa na wageni waliohudhuria sherehe katika mitandao yao ya kijamii - inaarifiwa wapenzi hao waliwapiga marufuku wageni waalikwa kuweka chochote kuhusu harusi hiyo katika mitandao. Uvumi kuhusu kuchumbiana kwa waigizaji hao nyota ulianza kusambaa miaka 6 iliyopita, lakini hawakulithibitisha hilo wazi mpaka mapema mwaka huu. Nyota wa Bollywood Deepika Padukone na Ranveer Singh wamefunga pingu za maisha katika hoteli moja ya kifahari nchini Italia. text: Watu hawa ,wengine ambao bado wapo hai ilhali wengine wamefariki wakati mmoja walionekana kuwa kileleni mwa taaluma zao za uhalifu .Ujanja wao na weledi wao kutafuta pesa na kukwepa mkono wa sheria ulionekana kama ushujaa na hadi leo katika baadhi ya nchi wangali wanachukuliwa kama 'mashujaa' . Hatahivyo walikumbana na mauti yao katika hali ambazo pesa na mali walizokuwa wametengeza hazingeweza kuwasaidia .Hawa hapa baadhi ya wahalifu sugu waliokuwa na utajiri ambao walipata kupitia uhalifu na ulaghai. Pablo Escobar Pablo Escobar alizaliwa huko Rionegro, Colombia mnamo 1949 na akaanzisha genge la kuuza dawa za kulevya huko Medellín mnamo miaka ya 1970. Wakati wa kazi yake, genge hilo lilitoa wastani wa 80% ya kokeni iliyosafirishwa kwenda Marekani Utajiri wake ulimwingiza kwenye orodha ya Forbes ya mabilionea wa ulimwengu kwa miaka saba. Baada ya Marekani kutoa amri ya kukamatwa kwake ili ashtakiwe nchini humo , Escobar alipinga kukamatwa na genge lake lililenga wanasiasa, polisi na waandishi wa habari. Baada ya kukamatwa mnamo 1991, Escobar aliwekwa ndani ya gereza la muundo wake mwenyewe, kwa jina Kanisa Kuu, ambapo aliendelea kusimamia kundi la Medellín Kwa jumla, Escobar anafikiriwa kusababisha vifo vya takriban watu 4,000. Lakini hali yake ya kuwapenda na kuwasaidia watu wake ilimfanya kuwa maarufu kati ya Wakolombia wengine ambao msaada wao aliuendeleza kwa kutoa pesa nyingi na kuwekeza katika vitongoji duni huko Medellín. Pablo Escobar, mlanguzi wa dawa za kulevya aliyefariki bado anaonekana na Wakolombia wengi kama shujaa Inasemekana kuwa wakati kilele cha nguvu zake katika biashara hiyo haramu Escobar alikuwa mtu wa saba kwa utajiri duniani huku kundi lake la Medellin likidhibiti asilimia 80 ya soko la kokeni ulimwenguni.zaidi ya miaka thelathini baada ya kifo chake ,Escobar yungali anatengeza pesa na huenda sehemu y mali yake bado ipo hadi leo Septemba mwaka wa 2020 mpwa wa Escobar alisema alipata mfuko wa plastiki na pesa zenye thamani ya $ 18m (£ 14m) zilizofichwa kwenye ukuta wa nyumba moja ya mjomba wake. Nicolás Escobar aliwaambia wanahabari wa Colombia "maono" yalimuonyesha mahali pa kutafuta pesa katika nyumba anayoishi katika jiji la Medellín. Alisema haikuwa mara ya kwanza kupata pesa mahali ambapo mjomba wake alikuwa akijificha ili kuepuka kukamatwa, kwani Escobar aliripotiwa kuficha mali ya thamani ya mamilioni ya pesa Alikufa katika ufyatulianaji wa risasi na polisi mwaka wa 1993. Nicolás Escobar alikiambia kituo cha Televisheni cha Red + Noticias cha Colombia pia alikuwa amepata mashine ya chapa , simu za setilaiti, kalamu ya dhahabu, kamera na filamu ambayo bado haijatengenezwa. Baadhi ya noti za miongo kadhaa zilikuwa zimeoza na hazitumiki tena, alisema Nicolás Escobar, ambaye amekuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mitano. Katika mahojiano hayo, alisema aliandamana na mjomba wake mara nyingi, na kwamba aliwahi kutekwa nyara na watu wanaotafuta mahali alipo Escobar Bernie Madoff Bernie Madoff, ni bwenyenye wa Wall Street aliyeaibishwa baada ya kukiri kutelekeza moja ya utapeli mkubwa katika historia ya kifedha ya Marekani na amekufa gerezani akiwa na umri wa miaka 82 wiki moja iliyopita. Kifo chake kilitangazwa na Ofisi ya Magereza. Bwana Madoff alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 150 baada ya kukiri hatia mnamo 2009 ya kuendesha mpango wa kilaghai ambao ulilipa wawekezaji pesa kutoka kwa wateja wapya badala ya faida halisi. Ulaghai wake huo wa ponzi uIlianguka wakati wa msukosuko wa kifedha wa 2008. "Bernie, hadi kifo chake, aliishi na hatia na majuto kwa uhalifu wake," wakili wake Brandon Sample alisema katika taarifa. "Ingawa uhalifu ambao Bernie alihukumiwa kufanya umefafanua ni mtu wa aina gani - pia alikuwa baba na mume. Alikuwa mzungumzaji laini na msomi. Bernie hakuwa mkamilifu. Lakini hakuna mtu aliye sawa." Taraifa hiyo iliongeza. Bwana Madoff, mtoto wa wahamiaji wa Uropa ambaye alikulia New York, alianzisha kampuni yake ya jina Bernard L Madoff Investment Securities mnamo 1960. Kampuni hiyo ikawa moja wapo ya wafanyabiashara wakubwa - wanunuzi wakiunganishwa na wauzaji wa hisa - na Bwana Madoff aliwahi kuwa mwenyekiti wa soko la hisa la Nasdaq. Kampuni hiyo ilichunguzwa mara nane na Tume ya Usalama na Ubadilishaji ya Marekani kwa sababu ilipata faida kubwa kupindukia Walimu wa shule, wakulima, fundi mitambo na wengine wengi pia walipoteza pesa. "Tulifikiri alikuwa Mungu. Tuliamini kila kitu mikononi mwake," mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Elie Wiesel, ambaye wakfu wake ulipoteza dola milioni 15.2, alisema mnamo 2009. Katika korti, Bwana Madoff alisema kwamba wakati alianza mpango huo mnamo miaka ya 1990, alitumai itakuwa kwa muda mfupi tu. Alijitengezea kiasi kikubwa cha fedha na hakujua siku moja angezipteza kwa hatua moja hadi alipkamatwa na kufungwa jela El Chapo Guzman El chapo Guzman ambaye kwa sasa anahudumia kifungo cha jela nchini Marekani alijiundia sifa kwa kutoroka gerezani Zaidi ya mara moja katika hali za kutatanisha .Hata hivo kikubwa kumhusu ni jinsi alivyotengeza kiasi kikubwa cha apesa kupitia biashara haramu za ulanguzi wa dawa za kulevya Alianza kujihusisha na uhalifu uliopangwa akiwa na umri wa miaka 15, wakati alipanda bangi katika shamba lake pamoja na binamu zake. Kisha, akachukua jina la utani "El Chapo" - jina la Mexico kumaanisha 'mtu mfupi', Lakini matamanio yake yalidhihirisha kimo chake cha kupungua (yeye ni ana kimo cha futi 5 na nchi 6 , au mita 1.64). Akiwa na umri wa miaka 20, Guzmán aliondoka La Tuna kutafuta utajiri wake katika magendo ya dawa za kulevya. "Daima alipigania maisha bora," mama yake alisema. Wazazi wake - Emilio Guzmán Bustillos na María Consuelo Loera Pérez - walipata riziki yao kwa kilimo. Baba yake alikuwa mfugaji rasmi lakini inaaminika alikuwa mkulima wa Opium , Malcolm Beith anaandika katika kitabu chake, The Last Narco. Ari ya Guzmán ya kufaulu katika biashara ilikuwa dhahiri tangu akiwa na umri mdogo. Angeweza kusaidia familia yake kwa kuuza machungwa kwa wakulima wadogo kwa pesa chache. Matamanio yake ya kutaka maisha mazuri pia yalionekana Katika jarida podcast la Vice News , dada mdogo wa Guzman Bernarda alisema angevaa vito vya dhahabu bandia wakati wa kuwatembelea watu wa familia yake. "Hata kama mtoto mdogo, alikuwa na matamanio," mama yake aliwaambia watengenezaji wa filamu mnamo 2014. Alikumbuka alikuwa na "pesa nyingi za karatasi" ambazo angehesabu na kurudia kuzihesabu . Baada ya muda, kundi la Guzmán likawa moja ya biashara kubwa za dawa za kulevya zakuingia Marekani na mnamo 2009, aliingia kwenye orodha ya Forbes ya wanaume tajiri zaidi ulimwenguni akiwa nambari 701, na wastani wa mali yenye thamani ya $ 1bn (£ 709m). Kadiri utajiri wake na himaya ilivyokua, ndivyo pia uchunguzi kutoka kwa mashirika ya sheria ya Marekani ulivyoendelea .Shirika la DEA lilikuwa likimfuata kwa miongo kadhaa . Pesa walizotengeza kupitia uhalifu ni nyingi sana na hata wakati mmoja zilizidi kiasi cha fedha katika bajeti ya baadhi ya nchi. text: Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri Waziri mkuu nchini humo Benjamin Netanyahu amesema kuwa jaribio hilo la kombora la masafa ya kadri ni ukiukaji wa sheria za Umoja wa Mataifa. Amesema kuwa atapigania Iran kuwekewa vikwazo vipya vya kimataifa wakati wa ziara yake mjini Washington mwezi ujao. Maafisa wa Marekani wamethibitisha kufanyika kwa jaribio hilo la kombora lakini wakasema kuwa haijabainika iwapo lilikiuka sheria za Umoja wa Mataifa iliopitishwa 2015 kufuatia mpango wa kimataifa kuuwekea vikwazo mpango wa Nuklia wa Iran. Hakujakuwa na tamko lolote kutoka Iran. Kabla ya kuchukua mamlaka ,rais Trump alitaja mpango huo wa Iran kuwa hatari kubwa na kusema kuwa atasitisha majaribio yake ya makombora. Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri text: Picha ya Instagram ya Beyonce Amri za Trump na mabadiliko kwa sera za Marekani vimeonekana kugubika masuala mengine yanayoibuka Marekani. Kabla ya Trump kuapishwa, mashabiki wengine walidai kuwa Beyonce angetoa albamu mpya wakati Trump akiapishwa. Hata hivyo Beyonce hakutoa albamu bali alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa angetoa vitu tofauti, Beyonce, mumewe Jay Z na binti wao Blue Ivy Ukweli ni kwamba Beyonce ana ujauzito wa mapacha. Picha ya Instagram ilimuonyesha Beyonce akiwa amepiga magoti kando na maua akionekana kuwa mjamzito. Taarifa hizo za Beyonce zilionekana kuwavutia watu kutoka mitandao mingine. Watu wengine wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu majina watakayopewa watoto wa Beyonce, wenginewakisema waitwe Yellow na Red Ivy. Binti wa umri wa miaka mitano wa Beyonce na Jay Z aliopewa jina la Blue Ivy Carter. " Chini ya wiki mbili tangu Donald Trump aapiswhe kuwa rais wa Marekani, taarifa kuu kutoka Marekani tangu wakati huo zimehusiana na siasa. text: Melania Trump Melania amesema kuwa amechagua mataifa hayo kwa sababu yamefanya kazi na shirika la misaada la Marekani USAID na washirika wake ili kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazokumba jamii. Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa unoendelea mjini New York, bi Melania amesema''Najivunia sana kufanya kazi na mataifa haya kupitia USAID na wadau wengine na nina tazamia kuendeleza mbele kampeini ya 'Be Best' katika mataifa mengine barani Afrika' Mchango wa USAID Afrika Melania ameongeza kuwa Ghana kwa mfano kwa ushirikiano na shirika la USAID inajishughulisha na masuala ya afya kwa kusaidia mikakati ya kuimarisha afya ya kinamama na watoto wachanga pamoja na kuwahamasisha kinamama hao umuhimu wa kuzingatia lishe bora. Pia ameipongeza Malawi kwa kuonyesha ishara kwamba elimu ni moja ya nguzo muhimu itakayoweza kukabiliana na umasikini na kustawisha jamii. Akizungumzia kwa kina mipango ya ziara hiyo barani Afrika , Melania amesema kuwa ziara hiyo inaandaliwa na shirika la kimataifa la misaada ya Marekani kama sehemu ya kampeini yake inayojulikana kama 'Be Best' ambayo inalenga kuboresha hali ya watoto hasa masuala ya uraibu wa mitandaoni. "Kila mmoja wetu anatokea taifa lililo na changamoto zake lakini naamini moyoni mwangu kwamba sote tuna nia ya kukuza kizazi ambacho kina furaha, afya na kuwajibika siku za usoni'' Elimu na Wanyama Pori Katika kanda ya afrika mashariki, Melania amesema kuwa atatembelea Kenya kutokana na juhudi za nchi hiyo za kuimarisha elimu na kuhifadhi wanyama pori kwa ushirikiano na shirika la USAID. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema ziara ya hivi majuzi ya kihistoria ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Mama wa Taifa Margaret Kenyatta huenda imechangia pakubwa uamuzi wa Bi Melania kuja Kenya hasa ikizingatiwa rais Kenyatta alifanya mashauri ya ana kwa ana na Rais Trump. Melania Trump na Mama wa Taifa Margaret Kenyatta walifanya mashauri ya faragha katika chumba cha masuala ya kidiplomasia katika upande wa Magharibi wa Jengo la White House. Je ziara ya rais Uhuru Marekani ilichangia zaira ya Melania Kenya? Kwa mujibu wa ikulu, ya Kenya mashauriano hayo kati ya Rais Kenyatta na Rais Trump yaliangazia zaidi nguzo nne ya ajenda kuu ya maendeleo ya Rais Kenyatta pamoja na kuimarisha vita dhidi ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi nchini humo. Viongozi hao wawili pia walijadiliana kuhusu safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York zitakazoanza mwezi Oktoba mwaka huu. Walikubaliana kwamba safari hizo za ndege zitaimarisha zaidi utalii na biashara kwa manufaa ya nchi hizi mbili. Walitoa mfano wa Mkataba wa Nafasi na Ustawi wa Afrika maarufu kama Mkataba wa AGOA kama moja wapo wa nyanja zitakazonufaika na safari hizo za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi. Bi Melania anatarajiwa kukamilisha ziara yake barani Afrika nchini Misri. Mke wa rais wa Marekani bi Melania Trump ametangaza mpango wake wa kuzuru mataifa manne ya Afrika ikiwemo Ghana, Malawi, Kenya na Misri oktoba mosi. text: Gazeti la kibinafsi la The New Times linasema operesheni hiyo ilianza wiki moja iliyopita. Kufikia sasa, makanisa 714 yamefungwa, pamoja na msikiti mmoja. Afisa wa serikali Justus Kangwagye ameambia gazeti hilo la mtandaoni kwamba makanisa hayo yamekiuka sharia za usalama. "Shughuli ya kuabudu inafaa kufanywa kwa utaratibu na kwa kutimiza masharti ya viwango vya ubora na usalama vilivyowekwa. Kutumia uhuru wako wa kuabudu hakufai kuingilia haki za watu wengine. Wametakiwa kusitisha shughuli zote hadi watimize masharti yaliyowekwa," amesema. Amesema baadhi ya makanisa haya yalikuwa yakifanya kazi bila kuwasilisha upya maombi ya leseni na kwamba maafisa wa serikali hawataruhusu makanisa hayo yafunguliwe. Taarifa zinasema baadhi ya makanisa yamekuwa yakifanya kazi kwa kutumia mahema na hayana maeneo ya kutosha ya kuegesha magari ya waumini. Baadhi ya waumini wamekuwa wakiegesha magari yao pambizoni mwa barabara na kusababisha misongamano ya magari. Wakazi wa Kigali, kwa mujibu wa gazeti hilo, wana hisia mseto kuhusu hatua hiyo. Baadhi wanaiunga mkono lakini wengine wangependa wenye makanisa hayo wamepewe muda zaidi wa kutimiza masharti hayo. Askofu Innocent Nzeyimana, rais wa Baraza la Makanisa katika wilaya ya Nyarugenge ameiomba serikali, kwa niaba ya makanisa, kuyaruhusu makanisa yaliyofungwa yaendelee kuhudumu yanapoendelea kufanya juhudi za kutimiza masharti yaliyowekwa. Serikali ya Rwanda imeyafunga makanisa zaidi ya 700 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kigali kwa kukosa kutimiza masharti yaliyowekwa ya usafi na usalama. text: Mamake Dallal, anasema kumzaa mtoto wake huyo ni 'zawadi' kutoka kwa Mungu Licha ya kuwa walikuwa wafungwa ,waliendelea kupata watoto na wake zao wambao wapo katika eneo la Wapalestina la Gaza na West Bank sehemu zinazokaliwa na waisraeli. Ripoti za mwanzo mwaka wa 2013 kwamba wafungwa walikuwa wakiweza kutoa mbegu za kiume na kuzificha kwenye kila aina ya chupa na kisha kuzitoa magerezani kisiri hadi kwa wake zao ili wapandikizwe mimba kupitia IVF zilipokelewa kwa njia ya kupuuzwa. Maafisa wa Israel wenyewe walisema kwamba haingezekana kwamba mfungwa angeachiliwa huru kisha aondoke akiwa na chupa zenye manii kuwapelekea wake za wafungwa wenzake waliobaki jela . Inavyofanyika Muhannad Ziben sasa ana umri wa miaka tisa . Alizaliwa katika hospitali Nablus's al-Arabia agosti mwaka wa 2012. Mamake Dallal anasema kumzaa mtoto wake huyo ni 'zawadi' kutoka kwa Mungu kwani babake yupo jela.Anahudumia vifungo 32 vya maisha katika gereza na Israel baada ya kushtumiwa kwa kuhusika na shambulizi la kigaidi dhidi ya Israel mwaka wa 1997 huko Jerusalem .Lakini aliwezaje kupata mimba na kumzaa Ziben? Dallal anasema aliweza kupata mimba baada ya manii ya mumewe kuletwa kimagendo kutoka gereza la Israel na kisha akatumia mbinu ya upandikizaji au IVF kuibeba mimba ile na kumzaa mtoto wake . Sio yeye pekee anayefanya hivyo kwani mamia ya wanaume wa Kipalestina anaohudumua vifungo katika jela za Israel wameendelea kuwazaa watoto na wake zao wakiwa jela kwa kutumia mbinu hiyo . Manii inavukishwa kutoka jela na kupewa mtu ambaye ameshahudumia kifungo chake anayetoka jela .Wakati mwingine jamaa wanaoruhusiwa kuwatembelea wafungwa ndio hukabidhiwa 'mali' hiyo muhimu ili kuhakikisha kwamba Waalestina wanaendeleeza vizazi vyao hata chini ya utawala wa Israel na hali ngumu ya maisha katika sehemu zao . Alipozungumza na BBC mwaka wa 2013 Dallal alisema ; "Muhannad ni zawadi kutoka kwa Mungu, Laini furaha yangu haijakamilika bila mume wake kuwa hapa na mimi' Kisa hicho cha Dallal kiliangaziwa sana na vyombo vya habari . Tangu wakati huo, BBC ilizungumza na madaktari wawili wa uzazi katika Ukingo wa Magharibi ambao wanasema sasa kuna mamia ya wanawake Kipalestina ambao wamepata ujauzito wakitumia manii iliyosafirishwa nje ya jela za Israeli. "Kwa kweli, sijui wanafanyaje na sitaki kujua jinsi wanavyofanya," alisema Dk Salem Abu Khaizaran, mmoja wa madaktari wa uzazi ambaye amekuwa akiwasaidia wanawake. "Sitaki kuingia kwenye siasa. Ninafanya hivyo kwa sababu za kibinadamu tu, kusaidia tu wanawake hawa. Kila mtu anawashughulikia sana wafungwa, lakini wanawake hawa wanateseka sana." 'Inawezekana kweli?' Huduma ya Magereza Israeli (IPS) ilitia shaka uwezekano wa mtu kupitisha manii kwa njia ya magendo. "Mtu hawezi kusema haikutokea. Walakini, ni vigumu kuamini inaweza kutokea kwa sababu ya hatua kali za usalama zinazochukuliwa wakati wa mikutano ya wafungwa na jamaa zao na kwa ujumla," msemaji wa Mamlaka ya magereza wakati huo alisema Alisema kuwa hakuna utangamano wa ana kwa ana ati ya wafungwa na familia zao, isipokuwa kwa dakika 10 za mwisho za ziara hiyo, wakati ambao watoto wa mfungwa, ikiwa ni chini ya umri wa miaka nane, wanaruhusiwa kupatana na baba yao. Tofauti na wafungwa wengine wa Israeli, Wapalestina ambao wamefungwa kwa kile Israeli inaita makosa ya usalama hawaruhusiwi ziara za ndoa ambapo wanaweza kushiriki tendo la ndoa na wake zao . IPS haikuweza kusema ikiwa Wapalestina wowote waliofungwa kwa makosa ya jinai wamewahi kupewa ziara kama hizo. "Wafungwa wa Israeli wanapata haki nyingi. Wanaruhusiwa kutoka gerezani kwa ziara za nyumbani. Wana uwezo wa kuwa na wake zao," alisema Waziri wa wakati huo wa Magereza wa Mamlaka ya Palestina Issa Qaraqa. Anaongeza kuwa Yigal Amir, mwenye msimamo mkali wa kidini na raia wa Israeli ambaye alifungwa kifungo cha maisha kwa kumuua Waziri Mkuu wa Israeli Yitzhak Rabin mnamo 1995, aliruhusiwa kuoa na kuwa na ziara za kindoa zilizosababisha kuzaliwa kwa mtoto wa kiume mnamo 2007. Dk Abu Khaizaran anaamini Wapalestina wanapaswa kupewa haki hiyo. Anasema hadi hapo itakapotokea, wafungwa wa Palestina wataendelea kujaribu kusafirisha manii nje ya jela kwa wake zao. Ni kazi ngumu kweli Daktari anasema wanawake huleta manii kwenye kliniki yake kwa chochote kutoka chupa ndogo hadi vikombe vya plastiki. Dk Abu Khaizaran anasema, katika hali nzuri, manii inaweza kuishi hadi masaa 48 kabla ya kugandishwa ili kufanya matibabu ya IVF. Kawaida anasema wanawake wanaweza kuipeleka kwa wakati mfupi kuliko huo lakini wakati mwingine mbegu za kiume hazifiki katika hali nzuri ya kutosha na wanawake wanaambiwa lazima wajaribu tena. Kliniki hiyo inasita kutoa matibabu kwa wanawake ambao tayari wana watoto wengi au ambao waume zao wanatumikia vifungo vifupi tu. Kabla ya IVF kuendelea mbele daktari anauliza kuona watu wawili wa familia za mume na mke ambao wanaweza kushuhudia kwamba manii ni ya kweli. Wanawake pia wanashauriwa kueneza habari juu ya kile wanajiandaa kufanya. "Wakati kijiji kizima kinajua mume wa mwanamke amekuwa gerezani kwa miaka 10 au 15 hatutaki atembee barabarani akiwa mjamzito," anasema Dk Abu Khaizaran. "Tunamshauri mwanamke kurudi kijijini kwake na kumwambia kila mtu kuwa ana sampuli kutoka kwa mumewe na kwamba ana mpango wa kufanya IVF katika miezi michache." Anasema kwa njia hii inaepuka uvumi ikidokeza mwanamke anaweza kuwa alikuwa akimdanganya mumewe wakati mume wake yupo gerezani Mwanzoni ungemuambia mtu kwamba jambo hili lilikuwa likitendeka basi ungekumbana na pingamizi si haba kuhusu uwezekano na hata ukweli wa kile ambaco wafungwa walikuwa wakifanya waiwa ndani ya mageeza ya Israel. text: John ambaye amepewa jina la utani la mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe aliwafurahisha maskauti katika michuano ya Afrika ya wachezaji wasiozdi umri wa miaka 17 ambalo Tanzania walikuwa mwenyeji. Kinda mwengine Claryo Boniface kutoka kikosi cha wachezaji walio chini ya umri wa miaka 20 pia ameorodheshwa katika kikosi hicho. ''Ninaamini ni wakati tuanze kujenga timu na kufikiria siku zijazo'', alisema Amunike. Tunahitaji kuanza kufikiria kuhusu vijana na kuona iwapo tunaweza kuanza kuwashirikisha katika mfumo wetu''. John alifunga katika mechi ya ufunguzi ya Tanzania wakati walipopoteza 5-4 kwa Nigeria na kupoteza tena kwa Uganda na Angola huku waandalizi hao wakishindwa kufuzu katika nusu fainali ya michuano hiyo. Amuneke pia amesema kuwa Tanzania wana mechi ya kufuzu ya CHAN dhidi ya Sudan wiki moja tu baada ya dimba hilo la mataifa ya Afrika. Mbali na vijana hao , timu hiyo pia inashirikisha wachezaji wanaosakata dimba ugenini pamoja na wale kutoka kwa ligi ya Tanzania. ''Timu hii sio tu ya Afcon bali pia ya CHAN baadaye'', alielezea. ''Hivyobasi kama timu ya kiufundi tunajiandaa vile tutakavyoingiana na CHAN baada ya Afcon''. Mkufunzi wa timu ya Taifa Stars nchini Tanzania na raia wa Nigeria Emmanuel Amuneke amemshirikisha kinda wa miaka 15 Kelvin John Pius katika kikosi chake cha watu 39 kitakachoshiriki katika Kombe la mataifa ya Afrika. text: Fabinho anatarajia kuchukua nafasi ya Emre Can ambaye anatimkia Juventus Fabinho mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye miaka 24 atajiunga na Liverpool Julai 1. Kiasi cha ziada cha ada ya uhamisho wake ambacho ni Paundi Milioni 5 kinaweza kuongezeka kutokana na mafanikio atayoipa Liverpool. Kuwasili kwake ni kwa ajili pia ya kuziba pengo la Emre Can ambaye anatarajiwa kutimkia kwa mabingwa wa Seria A Juventus muda wowote. Fabinho alijiunga na Monaco akitokea Rio Ave ya Ureno mwaka 2013 ''Hiki ni kitu ambacho sikuzote nimekuwa nikikitamani- hii ni timu kubwa, ''alisema Fabinho. ''Nimefurahishwa sana.'' Fabinho: Mwaliko wa Mourinho unaweza ''kunishawishi'' Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ''Huyu ni mchezaji ambaye ana faida sana uwanjani, anaweza kucheza nafasi nyingi, namba sita, nane ama namba mbili'. Hili ni jambo zuri sana.'' Fabinho ambaye mkataba wake unatarajiwa kuanza Julai 1 amesema Liverpool ni klabu yenye miundombinu mizuri na ya kuvutia. Liverpool imekubali kumsajili kiungo wa Monaco Fábio Henrique Tavares maarufu kama Fabinho kwa ada ya Paundi Milioni 40 ambayo inaweza kuongezeka kutokana na kiwango cha mchezaji. text: Mike Pence (kulia) ametangaza hayo baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Kuhamishwa huko kutatokea mapema kuliko ilivyotarajiwa Rais Donald Trump alipotangaza mwezi jana kwamba Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel na kuagiza maandalizi ya kuhamisha ubalozi yaanze. Bw Pence ametoa tangazo hilo akihutubia bunge la Israel. Hotuba yake ilikatishwa kwa muda na kundi la wabunge Waarabu ambao walikuwa wanalalamikia hatua hiyo ya Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hadhi ya mji wa Jerusalem imekuwa sehemu kuu ya mzozo wa Waisraeli na Wapalestina. Mwezi uliopita, Umoja wa Mataifa uliidhinisha azimio la kuitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake wa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Azimio hilo liliyataka "mataifa kujiepusha kufungua afisi za kibalozi katika Mji Mtakatifu wa Jerusalem". Kwa nini Jerusalem inazozaniwa? Mji huo una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim - Uyahudi, Ukristo na Uislamu - sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki. Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukulia mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa. Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa) na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pamoja na Wapalestina wenyewe. Kwa mujibu wa maafikiano wakati wa mazungumzo ya amani ya Wapalestina na Waisraeli ya 1993, hatima ya mji huo ilifaa kuamuliwa wakati wa hatua za mwisho za mazungumzo. Hatua ya Israel kudhibiti Jerusalem yote haijawahi kutambuliwa kimataifa na nchi zote zina afisi za kibalozi Tel Aviv. Tangu 1967, Israel imejenga makazi kadha ya Wayahudi na kuna takriban walowezi 200,000 wa Kiyahudi eneo hilo. Makazi haya yamekuwa yakishutumiwa na jamii ya kimataifa. Mataifa yalivyopiga kura kuhusu Jerusalem UN Mataifa tisa yaliyopinga azimio la Umoja wa Mataifa mwezi jana yalikuwa: Marekani, Israel, Guatemala, Honduras, visiwa vya Marshall, Micronesia, Nauru, Palau na Togo. Mataifa 35 yalisusia kura hiyo: Antigua na Barbuda, Argentina, Australia, Bahamas, Benin, Bhutan, Bosnia na Herzegovina, Cameroon, Canada, Colombia, Croatia, Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Dominika, Equatorial Guinea, Fiji, Haiti, Hungary, Jamaica, Kiribati, Latvia, Lesotho, Malawi, Mexico, Panama, Paraguay, Ufilipino, Poland, Romania, Rwanda, Visiwa vya Solomon, Sudan Kusini, Trinidad na Tobago, Tuvalu, Uganda, Vanuatu. Mataifa 128 yaliyounga mkono azimio hilo yalikuwa: Afghanistan, Albania, Algeria, Andorra, Angola, Armenia, Austria, Azerbaijan Bahrain, Bangladesh, Barbados, Belarus, Ubelgiji, Belize, Bolivia, Botswana, Brazil, Brunei, Bulgaria, Burkina Faso, Burundi Cabo Verde, Cambodia, Chad, Chile, China, Comoros, Congo, Costa Rica, Cote D'Ivoire, Cuba, Cyprus Denmark, Djibouti, Dominica Ecuador, Misri, Eritrea, Estonia, Ethiopia Finland, Ufaransa Gabon, Gambia, Ujerumani, Ghana, Greece, Grenada, Guinea, Guyana Iceland, India, Indonesia, Iran, Iraq, Ireland, Italia Japan, Jordan Kazakhstan, Kuwait, Kyrgyzstan Laos, Lebanon, Liberia, Libya, Liechtenstein, Lithuania, Luxembourg Macedonia, Madagascar, Malaysia, Maldives, Mali, Malta, Mauritania, Mauritius, Monaco, Montenegro, Morocco, Mozambique Namibia, Nepal, Netherlands, New Zealand, Nicaragua, Niger, Nigeria, North Korea, Norway Oman Pakistan, Papua New Guinea, Peru, Ureno Qatar Urusi Saint Vincent na Grenadines, Saudi Arabia, Senegal, Serbia, Ushelisheli, Singapore, Slovakia, Slovenia, Somalia, Afrika Kusini, South Korea, Uhispania, Sri Lanka, Sudan, Suriname, Sweden, Uswizi, Syria Tajikistan, Tanzania, Thailand, Tunisia, Uturuki Umoja wa Milki za Kiarabu, Uingereza, Uruguay, Uzbekistan Venezuela, Vietnam Yemen Zimbabwe Mataifa 21 hayakuwakilishwa wakati wa kupigwa kwa kura: Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, El Salvador, Georgia, Guinea-Bissau, Kenya, Mongolia, Myanmar, Jamhuri ya Moldova, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Samoa, San Marino, Sao Tome na Principe, Sierra Leone, Swaziland, Timor-Leste, Tonga, Turkmenistan, Ukraine, Zambia. Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem kabla ya mwisho wa mwaka 2019. text: Membe adai kuitwa katika kamati ya maadili ni jambo la muhimu kwake. Makada wengine wawili ni makatibu wakuu wa zamani wa chama hicho Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba. Mwezi Disemba, Halmashauri kuu ya CCM (NEC) iliagiza makada hao watatu kuhojiwa, hatua hiyo ilitimu baada ya 'vuta n'kuvute' ya muda ndani ya chama hicho. Makada wote hao, "wanakabiliwa na tuhuma za maadili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi." "Kukidhalilisha chama mbele ya Umma" Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole Disemba 13 2019, hata hivyo haikueleza bayana ni makosa gani ya kimaadili ambayo wanatuhumiwa nayo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makada wengine watatu, Januari Makamba, Nape Nnauye na William Ngeleja walisamehewa baada ya kumuomba radhi mwenyekiti wa CCM, Rais John Pombe Magufuli. Wanachama hao waliomba radhi kwake (Magufuli) baada ya "kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Wanachama hao watatu wa CCM pamoja na watatu ambao wanahojiwa hii leo wote sauti zao, wakiwa wakifanya nawasiliano kwa njia ya simu zilivujishwa kwenye mitandao nchini Tanzania wakizungumzia masuala mbalimbali kukihusu chama na mwenyekiti wake. Sehemu ya mazungumzo yaliyovuja ya Mzee Yusuf Makamba na Kinana ni pamoja na kuandaa taarifa ya malalamiko dhidi ya 'mawanaharakati' Cyprian Musiba ambaye wanamtuhumu kwa 'kuwadhalilisha' bila kuchukuliwa hatua yoyote na kuhoji analindwa na nani. Kwa upande wa Membe, licha ya kusikika kwe nye mazungumzo hayo yalivuja, amekuwa pia akituhumiwa na baadhi ya wanchama wa chama hicho kuwa najipanga 'kumhujumu' Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Kinana (kushoto) alikuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati Magufuli akiingia madarakani. Membe anahusishwa na mipango ya kutaka kugombea tiketi ya urais kupitia CCM mwaka huu, hatua ambayo baadhi wanaitafsiri kama usaliti. Japo katiba ya CCM inaruhusu hilo, imekuwa ni ada ya chama kumuachia rais aliye madarakani kupita bila kupingwa kwa awamu ya pili ya urais. Watahojiwa kwa namna gani? Wanachama hao waandamizi wanahojiwa Dodoma na kamati ya usalama na maadili ambayo ipo chini ya uenyekiti wa mwanasiasa mkongwe Philip Mangula, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Membe alikuwa wa kwanza kufika kwa mahojiano hayo Alhamisi asubuhi, na kwa mujibu wa Mangula baada yake atafuata Kinana kisha Makamba. Kila mmoja anatarajiwa kuhojiwa kwa siku moja. "Tumepanga kuwahoji kwa siku moja kila mmoja, lakini utaratibu unaweza kubadilika kulingana na maelezo atakayotoa mhusika. Kama tutaona siku moja haitoshi, atarejea tena siku inayofuatia," Mangula amenukuliwa akisema na gazeti la Uhuru. Kwa mujibu wa Mangula baada ya kuhitimisha kazi yao, vikao vya chama vitapitia maelezo ya watuhumiwa hao na kutoa maamuzi. Baada ya mahojiano ya saa tano Membe amewaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa na mkutano mzuri. "Nimepata nafasi nzuri ya kufafanua mambo kadhaa ambayo chama changu ilitaka kuyajua...Safari hii ya kuja Dodoma imekuwa na manufaa makubwa sana, sana kwangu, kwa chama na kwa taifa letu...mengine yatakuwa yanapatikana kidogo kidogo nikishiba," amesema Membe. Watapewa adhabu gani? Swali moja ambalo wengi wanajiuliza toka mwezi Disemba ni adhabu gani wanayoweza kupatiwa makada hao waandamizi endapo watakutwa na hatia. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, kanuni za uongozi na maadili za CCM toleo la 2017 zimebainisha adhabu tatu kwa wanachama wanaofika mbele ya kamati hiyo. "Katika kanuni hizo kifungu cha 5(2) kinasema; wanachama wanaovunja maadili ya chama kama yalivyoainishwa katika katiba ya CCM na kanuni za CCM wanachukuliwa hatua za kuwarekebisha na kama itashindikana kuwarekebisha ni kuwaondoa katika chama au katika uongozi," linaripoti gazeti hilo. Chama tawala nchini Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hii leo kimeanza kuwahoji makada wake watatu waandamizi akiwemo waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Bernard Membe. text: Katibu Mwenezi wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza na wanahabari Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi wa chama hicho Ado Shaibu amesema ''taratibu kila mtu, haijalishi ni wa chama au cheo gani, atafikiwa na ukandamizaji huu wa serikali''. Chama cha Upinzanzi nchini Tanzania, ACT Wazalendo, kimesema kuanza kwa kutekelezwa kwa kanuni za maudhui mtandaoni ni ishara nyingine ya jinsi ambavyo serikali nchini humo inavyoendelea kuminya uhuru wa habari na watu kujieleza. Jana mtandao maarufu wa Jamii Forums ulilazimika kufunga huduma zake baada ya kushindwa kukidhi matakwa ya kanuni hizo. Amewataka wananchi kupaza sauti kwa pamoja kuikemea serikali kwa ukandamizaji unaoendelea. Katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema, kufungwa kwa mtandao huo na mingine baada ya tarehe ya mwisho wa kujisajili kufika, ni kitendo kinachoonyesha kuwa serikali haitaki kuskiliza maoni ya wananchi kuwa kanuni hizo ni kandamizi kwa uhuru wa habari na watu kujieleza. ''Kauli yetu ni kwamba serikali ya awamu ya tano tusitarajie asilani, abadan kwamba itakoma kukandamiza haki za binaadamu.Inaonekana waziwazi serikali taratibu inaua haki moja mpaka haki nyingine kwa hiyo katika kitu tunachopoteza muda ni kudhani kuwa tukitoa rai kwa serikali basi ati watatusikiliza, imethibitika kuwa hawatusikilizai na haki nyingi zimesombwa na maji'',Alieleza Ado. Jamii Forums, mtandao ambao uliokuwa na watumiaji zaidi ya Laki 6 kila siku na wafuasi zaidi ya Milioni tatu katika mitandao yake ya Kijamii ulikuwa ni jukwaa ambalo Watanzania walilitumia kubadilishana mawazo, kutoa habari na mara nyingine kuikosoa serikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa nyeti. Wakati serikali ikiutaka mtandao huo kujisajili, Jamii Forums wenyewe wamekuwa wakisisitiza kwamba sharti hilo haliwahusu kwani wao si watoa maudhui bali ni wananchi wanaoutumia mtandao huo kwani wao ndio wanaweka humo maudhui ya mtandao huo Wanaharakati wengi wa maswala ya haki za binaadamu wamekosoa sheria na kanuni za mtandao kuwa ni kandamizi kwa uhuru wa habari na kujieleza nchini. Chama cha upinzani Tanzania ACT Wazalendo kimesema mwenendo wa serikali kudhibiti mitandao ya kijamii unaonesha nia ya kutaka kuminya haki zote za msingi za raia text: Uchukuzi wa treni ni maarufu sana Tanzania kwa safari za mbali Watu watatu wamejeruhiwa Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka, shirika la habari la kibinafsi la Azam limeripoti. Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia BBC kwamba watu watatu wamejeruhiwa. "Sababu ya ajali bado haijafahamika lakini, timu ya kutathmini ajali iko njiani kuelekea eneo la tukio," amesema. Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza. "Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa." Kubaini chanzo cha ajali Bw Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile, ndio maana ni vigumu kusema nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha ajali. Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook kwamba amezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma na kufahamishwa kwamba chanzo cha ajali ni injini kupoteza njia kufuatia mchanga uliokuwa kwenye njia ya reli. "Naomba uchunguzi ufanyike ili kuona kama mchanga ule ni sababu ya mvua kubwa zinazonyesha ama la. Treni ndio usafiri wa wanyonge wengi mkoani kwetu hivyo ajali za namna hii zinastusha na kuogopesha. Natoa pole sana kwa wana Kigoma na Watanzania wengine," amesema. Agoztimwaka jana watu watatu walifariki kwenye ajali iliyohusisha treni na gari la uchukuzi wa abiria mjini Morogoro. Mmoja wa waliofariki alikuwa mwanafunzi aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 6. Wengine wawili walipoteza maisha wakati wakipelekwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wengine 29. Treni ya kubeba abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora imepata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa Tanzania, taarifa zinasema. text: Hatua hii inajiri miezi saba baada ya Bashir kusaidia katika upatanishi na kufikiwa makubaliano ya amani kati ya Rais Kiir na kundi kuu la waasi wa upinzani Sudan kusini , uliosaidia kupata uhuru wa taifa hilo changa barani Afrika baada ya mapigano ya miongo kadhaa. "Rais amejitolea kuwa mpatanishi katika majadiliano ya makundi tofauti nchini Sudan kwa matumaini kwamba mageuzi mapya yataidhinisha siku mpya Sudan...," Reuters limenukuu taarifa ya ofisi ya rais. Mzozo wa kisiasa na wa kiaraia nchini Sudan umegubika majadaliano, lakini hali inayojiri nchini humo inatazamwa vipi kutoka Sudan Kusini? Swali kubwa ni vipi taifa hilo litakavyofanikiwa katika pendekezo hili sasa? Inafahamika kwamba Bashir alikuwa na jukumu kubwa katika kufikiwa makubaliano ya amani Sudan Kusini. Makubaliano yaliosainiwa Khartoum mnamo Juni 2018 kati ya rais Omar al-Bashir, Rais Salva Kiir Mayardit, na Riek Machar, ya kusitisha mapigano Sudan kusini Historia ya Sudan mbili Mataifa hayo mawili yana historia ndefu na huenda ndio sababu Sudan Kusini inaona ina wajibu wa kuhusika katika yanayoshuhudiwa hivi sasa Sudan. Sudan kusini ilijitenga na Sudan mnamo 2011 na miaka miwili baada ya hatua hiyo kubwa, taifa hilo changa lilitumbukia katika vita vya kiraia. Takriban watu 400,000 wameuawa na karibu thuluthi ya idadi jumla nchini imeachwa bila ya makaazi. Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar wametia saini makubaliano ya amani hivi karibuni kumaliza mzozo huo wa miaka mitano. Ni makubaliano yaliofikiwa kwa usaidizi wa Sudan, lakini jana Riek Machar alisema hayuko tayari kurudi Juba na anataka mipango ya kuunda serikali ya muungano iahirishwe mpaka masuala ya usalama yatakapo tatuliwa nchini. Siku chache zilizopita rais Salva Kiir pia amesema haoni uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano mwezi ujayo na kuongeza kwamba masuala ya usalama hayajatatuliwa. Wanaharakati mjini Juba wana wasi wasi mwingi kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano katika mzozo ambao kiini chake ni masuala ya usalama. 'Wasiwasi wa usalama utabaini amani ya kudumu Sudan kusini na tunavyozungumza muungano wa vikosi haujaidhinishwa na mpango huo bado upo katika kiwango cha awali na muda umesogea, kwahivyo hili linawatia wasiwasi wengi' anasema Sarah Nyanath, afisa katika jukwa la mashirika ya kiraia Sudan kusini. Hali Khartoum inaacha wapi mustakabali wa amani Sudan kusini? Akizungumzana BBC Bi Nyanath ameeleza kwamba hali nchini Sudan ina athari kubwa kwa mustakabali wa amani Sudan kusini. 'Ilituchukua miezi mingi katika majadiliano huko mjini Addis Ababa Ethiopia, na kilichochangia kujivuta kwa mazungumzo hayo ilikuwa ni suala la usalama. Lakini wakati mazungumzo yalipohamishwa Sudan, Na kutokana na uzoefu na uelewa wa Bashir kuhusu taifa la Sudan kusini, alisaidia sana kusukuma mazungumzo hayo na kufika mahali tulipofika. Na sasa vile kunashuhudiwa mabadiliko katika utawala wa Khartoum, hatujui ni nani anayeingia kushikilia usukani'. Nyanath anasema raia Sudan kusini wana wasiwasi zaidi kutokana na kwamba waandamanaji Khartoum wanaonekana hawana ajenda ya pamoja. 'Kwa kuangalia sababu ya kufanyika maandamano hayo ambayo awali yalikuwa ni ya kulalamikia gharama kubwa ya maisha, yakawa ya kushinikiza mageuzi ya utawala na sasa mambo mengine yanaibuka katikati ya maandamano hayo, ikiwemo baadhi wanaoshinikiza muungano wa Sudan itakayojumuisha Sudan yetu (ya kusini) ambayo tayari imejitangazia uhuru'. 'Ina tia wasiwasi, wakati waandamanaji wanaendelea kushinikiza huenda idara mbali mbali zikagawanyika au zikakataa kusikiza matakwa ya raia, na haya ni wakati tuna idadi kubwa ya wakimbizi nchini humo, na zaidi ya hayo Khartoum ikiwa ni mdhamini mkuu katika makubaliano ya amani, ikiwemo jitihada za kuundwa serikali ya muungano ambayo kufikia sasa hata haijaundwa' anaeleza Bi Nyanath. Raia katika maandamano ya amani katika siku za nyuma Sudan kusini wameelezea hasira yao na mateso yanayowakabili wanawake na watoto Juba Ameongeza kwamba haya yote yanachangia wasiwasi na maswali mengi kuhojiwa kwa sasa. Inaarifiwa kwamba serikali ya Sudan kusini imetuma ujumbe mjini, Khartoum, kwa miongini mwa mengine, kuahidi kuwajibikia uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. "Mheshimiwa rais amehakikisha kuunga mkono mageuzi ya amani yatakayo idhinisha siku mpya Sudan ambako amani, umoja na heshima ya mipaka na uhuru wa watu wa Sudan utahakikishwa." Linaripoti gazeti la South Sudan News Now kwa kunukuu ujumbe wa kutoka ikulu ya rais. Raia Khartoum wanasema watasalia katika maandamano mitaani mpaka wakati ambapo viongozi wa kijeshi ambao wanashikilia madaraka hivi sasa, watakabidhi uongozi wa nchi kwa utawala wa kiraia. Rais Salva Kiir wa Sudan kusini amejitolea kuwa mpatanishi katika kuidhinisha mageuzi ya kisiasa nchini Sudan baada ya kupinduliwa kwa kiongozi aliyekuwepo Omar al-Bashir, Reuters linaripoti. text: Mpango huo utawaruhusu wateja kuwasiliana kupitia huduma tofauti. Licha ya kwamba huduma zote tatu zitasalia kuwa programu huru zitashirikiana kupitia ujumbe utakaotumwa kutoka huduma moja hadi nyingine. Facebook imeambia BBC kwamba ndio mwanzo wa mchakato mrefu. Mpango huo kwanza uliripotiwa mjini New York na unaaminika kuwa mradi wa kibinafsi wa mwanzilishi wa facebook Mark Zuckerberg. Utakapokamilika , ushirikiano huo utamaanisha kwamba mtumiaji wa facebook anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye anamiliki akaunti ya WhatsApp. Hili haliwezekani kwa sasa kwa kuwa programu zilizopo hazina uhusiano. Hatua ya kuunganisha huduma hizo tatu umeanza , kulingana na gazeti la The new York Times na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 ama mapema mwaka ujao. Je facebook ina mpango gani? Facebook haikupendelea kuzungumzia kuhusu swala hili katikati mwa kashfa ilioikumba, lakini ililazimishwa na watu waliokuwa wakiwasiliana na New York Times. Hadi kufikia sasa , WhatsApp, Instagram na Messenger zimekuwa zikifanya kazi kivyake na kushindana kibiashara. Kuunganisha huduma hizo kwaa kutuma ujumbe kutarahisisha kazi ya facebook. Haitalazimika kuunda programu mpya kama vile stories ambapo huduma zote tatu zimeongeza katika programu yake bila mafanikio ya kufurahisha. WhatsApp, Messenger na Instagram ni bidhaa huru zinazoshindana Mawasiliano ya ujumbe kupitia huduma moja hadi nyengine yanaweza kuimarisha biashara katika huduma moja kwa kutuma ujumbe kwa huduma nyengine. Pia yatairahisishia facebook kugawana data katika huduma zote tatu ili kusaidia juhudi za matangazo yake. Hatua hiyo pia itaimarisha uwepo wa facebook na kuwa vigumu kuanguka iwapo serikali husika zitajaribu kuivunja kwa manufaa yao ya kibinafsi. Usambazaji wa data. Bwana Zuckerberg ameripotiwa kushinikiza ushirikiano huo ili kuimarisha huduma za kampuni yake kuwa muhimu na kuongeza muda wa wakati unaotumika na wateja wake katika huduma hizo. Kupitia kuunganisha wateja wake katika kundi moja kubwa, facebook itaweza kushindani vizuri na kampuni ya Google na Apple iMessage kulingana na Makena Kelly wa mtandoa wa habari wa The Verge. "Tunataka kuunda huduma bora zadi ya kutuma ujumbe ilio na ulinzi wa hali ya juu na kufanya kuwa rahisi kuwafikia marafiki na familia kupitia huduma tofauti'', aliongezea. Taarifa hiyo ilisema kuwa kulikuwa na majadiliano na mjadala kuhusu vile mfumo huo utakavyofanya kazi. Kuunganishwa kwa huduma hizo tatu kuteleta mabadiliko muhimu katika kampuni ya facebook kwa kuwa imeruhusu Instagram na WhatsApp kufanya kazi kama kampuni tofauti zilizo huru. Gazeti la the New York Times linasema kuwa hatua ya Bwana Zuckerberg kupigania mpango huo wa kuunganisha huduma hizo umesababisha mgogoro wa ndani. Inadaiwa ndio sababu ya waanzilishi wenza wa Instagram na WhatsApp kuondoka mwaka uliopita. Hatua jhiyo inajiri huku facebook ikikabiliwa na uchunguzi na kukosolewa kuhusu vile inavyotunza data za wateja wake. Facebook ina mipango ya kuunganisha huduma zake za kutuma ujumbe katika Instagram, WhatsApp na Facebook Messenger. text: Wanaharakati waandamanaji katika jiji kuu la Kenya, Nairobi Katika siku za hivi karibuni, maafisa wakuu serikalini wakiwemo makatibu, wabunge, na maafisa wanasimamia mashirika ya seiklai wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa ufisai katika mashirika wanayoyasimamia jambo ambalo limezua taharuki. Hata hivyo, kuanza kuingizwa kwa siasa katika vita hivi ndio hatua ambayo imeanza kuonekana siku za hivi karibuni na kuzua mjadala huku makundi ya kidini yakidai kuwa zaidi ya shilingi za Kenya bilioni mbili huibwa kutoka kwa serikali kila siku. Naibu Rais wa Kenya William Ruto akitoa maoni yake amekuwa akisisitiza kuwa vita dhidi ya ufisadi havifai kuingizwa siasa bali kuachiwa taasisi ambazo zimepewa jukumu hilo na katiba ya Kenya. "Kuingizwa siasa kwa uchunguzi na mashtaka kutoka kwa watu ambao si mashahidi, wachunguzi ama viongozi wa mashtaka au majaji kunahujumu vita dhidi ya ufisadi," Naibu Rais alisema. Maoni haya yemonekana na wengi nchini Kenya kuwa yenye kuwatetea maafisa wakuu kutoka jamii yake ambao wameshikwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi. Msimamo huu wa Naibu Rais wa Kenya unatokea wakati baadhi ya washirika na wandani wake wanapopinga kushikwa kwa baadhi ya wakuu wa mashirika ya serikali kwa sababu ya ufisadi katika mashirika waliokuwa wakiziongoza. Madai yamezuka sasa kwamba msukumo huo wa kuwakamata wanaoshukiwa kwa ufisadi unalenga maafisa wakuu wanaotoka kwa jamii ya Wakalenjin katika serikali. Baadhi ya viongozi kutoka bonde la ufa ambao ni washirika wa Naibu Rais William Ruto wamedai kuwa kundi linaloongoza vita dhidi ya ufisadi linatumiwa vibaya kuwalenga wataalam kutoka jamii ya Wakalenjin. Baadhi ya wachanganuzi nchini Kenya wanadai kuwa maafisa hao wakuu wamejikuta katikati ya vita vya kisiasa— kwa kuwa wao ni njia rahisi ya kumfikia kiongozi wao, Bwana Ruto. Ikikumbukwa kuwa siasa za Kenya zina msingi ya kikabila, jinsi wataalamu kutoka jamii ya Kalenjin wanaoongoza mashirika ya serikali watakavyokuwa wakishikwa ndivyo azma ya Bwana Ruto ya kuwa Rais wa Kenya itakavyokuwa inatiwa doa. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametupilia mbali madai haya ya wanasiasa wa Bonde la Ufa kuwa vita dhidi ya ufisadi vinavyoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta vinalenga watu wa jamii fulani. Bwana Odinga amesema madai hayo hayana msingi kwani vita hivyo vinalenga watu binafsi ambao ni lazima wawajibike. Alieleza kuwa watu wanapopata nafasi za kazi kwenye serikali, wanapata kama watu binafsi, na wakiiba, wanafanya hivyo kama watu binfasi. Odinga amewaonya wale wote walioiba mali ya umma kujitayarisha kwa wakati mgumu kwa kuwa vita dhidi ya ufisadi havitalegezwa hadi wezi wote wa mali ya umma watakaposhikwa na kufungwa. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewaonya viongozi kutoingiza siasa katika mapambano dhidi ya ufisadi Rais Uhuru Kenyatta naye amekuwa akisisitiza na kuwaonya viongozi kuwa vita dhidi ya ufisadi vitaendelea na havifai kuingizwa siasa. Amenukuliwa mara kadhaa akizungumzia suala hili tangu mwaka uanze na hasa baada ya kuamua kushirikiana na kiongozi wa upizani Raila Odinga. "Hivi si vita vyangu dhidi yao, hivi ni vita dhidi ya uovu huo ambao unawafanya watu wetu wakose kazi na huduma za kimsingi. Ni uovu unaofanya Kenya kutoendelea na kupanga kwa kizazi kijacho," Rais Kenyatta alieleza mnamo Novemba. "Hatutarudi nyuma katika vita dhidi ya ufisadi. Vita dhidi ya ufisadi veyenyewe havimlengi mtu ama kabila." Katika maadhimisho ya siku ya Jamhuri nchini Kenya, Rais Kenyatta aliwataka Wakenya wote kuwa macho na kuviripoti visa vyovyote vya ufisadi kwa polisi. Aliwataka wanahabari na wanaharakati wa kijamii kushirikiana katika kuvifichua visa vya ufisadi nchini kama njia ya kupigana dhidi ya ufisadi. Rais Kenyatta sasa amewataka Wakenya wote kuripoti visa vya ufisadi kwa tume ya ufisadi na maadili, vyombo vya habari, na mashirika ya kijamii . "Wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuwa mshirika katika vita hivi dhidi ya ufisadi. Ni wakati wa kusema yametosha, awe polisi wa kawaida, gavana, karani ama waziri, jaji au mwanasiasa ," Rais Uhuru alisema akiwahutubia Wakenya siku kuu ya Jamhuri. "Hakuna mtu yeyote ambaye akiwa afisni ana haki ya kuitisha hongo kutoka kwako ama kutumia vibaya kile ambacho wewe na mimi tumetoa jasho kutengeneza. Nimewaonyesha kwamba nimejitolea kwa jambo hili lakini sasa nataka kuona kujitolea kwenu.Msichoke kufanya yaliyo mema" Wanaharakati wanamtaka Rais Kenyatta achukue hatua Vita hivi vya maneno nchini Kenya kuhusu vita dhidi ya ufisadi vinakuja wakati ambapo wakuu wa mashirika mengi wanaposhukiwa kuwa na ufisadi wakishikwa na kufikishwa mahakamani. Maafisa wakuu wa mashirika ya serikali ikiwemo makatibu wa wizara mbalimbali wakuu wa mashirika ya serikali wameshikwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi. Kuna hofu kuwa vita vya maneno kuhusu ufisadi vimeanza kuchukua mkondo wa kisiasa na huenda juhudi hizo zikasabaratika kama ambavyo imekuwa ikitokea miaka ya nyuma. Katika hatamu za Rais Moi na Rais Kibaki, vita dhidi ya ufisadi vilisambaratishwa na siasa nyingi jambo ambalo lilipelekea mashirika mengine kuanguka kifedha. Katika muktadha huu, kuwepo katika nyadhifa za seikali kumechukuliwa kama njia rahisi ya kujipatia mali kwa urahisi na kuwa tajiri na kuonyesh wengine kupitia kwa magari ya kifahari, majumba makubwa ya kifahari, kutoa pesa nyingi kwenye michango na mengine ya kujitanua. Matamshi ya wanasiasa kutoka bonde la ufa kwa mfano, yanaweza kuchukuliwa kuwa ni yenye lengo la kuleta uhasama wa kikabila miongoni mwa jamii mbali mbali. Kiongozi wa mashataka ya umma, Noordin Haji na mkurugenzi wa idara ya makosa ya jinai George Kinoti, wamepongezwa pakubwa kwa mwamko mpya dhidi ya ufisadi. Bwana Haji na mwenzake sasa wanawalenga wakuu serikalini na vigogo wengine wenye uwezo nchini Kenya. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma nchini Kenya Bw Noordin Haji Viongozi hawa wawili wamevutia uungwaji mkono na Wakenya wengi na kinachosubiriwa sana ni kushtakliwa na kufgnwa kwa wakuu wa mashirika ya serikali watakaopatikana na makosa ya ufisadi. Itakumbukwa kwamba kwa muda mrefu, vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya vimekuwa vikitatizwa na siasa za ukabila wakati viongozi wa mashairika na wakuu wengine wa serikali wanapokuwa wakifuata kutaka kujibu maswali. Mara nyingi wamekuwa wakijificha chini ya mwavuli wa jamii zao na kusema kuwa jamii zao "zinalengwa" na hivyo kuwashirikisha wanajamii wao katika kujitetea. Hali hii imeifanya nchi ya Kenya kutatizwa pakubwa na ufisadi kufikia kupoteza mamilioni ya pesa kila mwaka jambo ambalo limepelekea umaskini mkubwa na matatizo mengine kama ukosefu wa ajira kwa vijana. Ukosefu huu wa ajira kwa vinana wengin wa Kenya umkuwa tatizo sugu na kusababisha ukosefu wa usalama, suala ambalo ni chamgamoto kwa nchi nzima. Takwimu zinaonyesha kuwa ripoti za mkaguzi mkuu wa matumizi ya pesa za serikali katika miaka mitano iliyopita, Wakenya hupoteza shilingi trilioni moja kila mwaka kwa ufisadi. Hii ina maana kuwa katika mika mitano iliyopita, Kenya huenda imepoteza kiasi cha trilioni 5 za Kenya kupitia kwa wafisadi, taratibu mbovu za serikali zinazovuja, na wafanyikazi wa serikali walio wafisadi. Dhahiri ni kuwa, vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya vinapaswa kuendelea bila upendeleo wowote ikiwa Kenya inategemea kupiga hatua kimandeleo. Hata hivyo, kwa kuwa siasa za Kenya zina misingi ya kikabila, itakuwa vigumu kuyatenganisha mawili haya maana wanasiasa ndio husukuma magurudumu ya ufisadi. Prof Mogambi, ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi: hmogambi@yahoo.co.uk Huku vita dhidi ya ufisadi vikichacha nchi Kenya na maafisa wakuu wa serikali wakifikishwa mahakamni kujibu mashtaka, madai kuwa vita hivyo vinachukua mwelekeo wa kikabila yamezua mjadala nchini Kenya. text: Waandamanaji jijini Washington DC wamesema hawataacha kushinikiza mabadiliko Makumi ya maelfu ya watu waliandamana mjini Washington DC ikiwa ndio maandamano makubwa kufanyika katika mji huo kufikia sasa. Makundi ya watu pia yaliandamana mjini New York, Chicago, LA na San Fransisco. Wakati huohuo , watu walitoa heshima zao kwa Floyd katika jimbo la North Carolina, ambapo alizaliwa kabla ya ibada ya kumbukumbu yake kufanywa. Bwana Floyd mtu mweusi ambaye alikuwa hana silaha , alifariki katika mikono ya polisi katika mji wa Minneapolis tarehe 25 mwezi Mei. Picha ya video ilimuonesha afisa wa polisi ambaye ni mzungu akiwa ameweka goti lake kwenye shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika tisa akiwa amekandamizwa barabarani Afisa wa polisi Derek Chauvin amefukuzwa kazi na kushtakiwa kwa kutekeleza mauaji. Maafisa wengine watatu ambao walikuwepo katika eneo hilo pia walifutwa kazi na kushitakiwa kwa kusaidia na kuunga mkono kilichokuwa kikiendelea. Sarina and Grace Lecroy ni miongoni mwa waandamanaji wanaowaunga mkono watu Wamarekani weusi Maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yalifanyika katika baadhi ya mataifa mengine. Nchini Uingereza, katika bustani ya bunge katikati ya mji wa London, kulikuwa na watu wengi licha ya wito wa serikali kutokongamana kwa hofu ya kusambaa kwa virusi vya corona. Nchini Australia , kulikuwa na maandamano makubwa katika miji ya Sidney na Melbourne na Brisbane yalioangazia jinsi raia wenye chimbuko la Australia walivyokuwa wakinyanyaswa. Pia kulikuwa na maandamano nchini Ufaransa, Ujerumani na Uhispania. Je ni nini kilichotokea katika maandamano? Maandamano makubwa zaidi yalifanyika mjini Washington DC ambapo waandamanaji waliokuwa wakibeba mabango yalioandikwa 'Black Lives Matters' - walikongamana kwa amani karibu na mji mkuu, katika eneo la kumbukumbu la Lincoln na nje ya bustani ya Lafayette , karibu na ikulu ya Whitehouse karibu na jumba jipya kwa jina Black Lives Matter Plaza. Meya Muriel Bowser aliwakaribisha waaandamanaji akisema kuwa watu hao walituma ujumbe kwa rais Trump. Siku ya Jumatatu , maafisa wa polisi walirusha vitoa machozi hewani ili kuwatawanya waandamanaji katika eneo hilo kabla ya ya rais huyo kuingia katika kanisa lililopo eneo hilo. Mjini San Francisco, waandamanaji walifunga kwa muda geti la daraja "Iwapo anaweza kuzuia chochote kufanyika Washington Dc basi anaweza kufika katika jimbo lolote na hakuna hata mmoja wetu atakayekuwa salama'', alisema. ''Wanajeshi wetu hawafai kutumiwa jinsi hii hawafai kutakiwa kuwasukuma raia wa Marekani''. Bi Bowser alikuwa ameomba kuondolea kwa maafisa wote wa polisi wa kijimbo na wale wa kitaifa katika mji huo, akisema kuwa uwepo wao hauna maana. Mtu mmoja aliyekuwa akiandamana mwenye umri wa miaka 35, Eric Wood, aliambia BBC: Niko hapa kwasababu sikuweza kukosa kuwa hapa. ''Ubaguzi umekuwa miongoni mwetu kwa muda mrefu nchini Marekani''. Crystal Ballinger , mwenye urmi wa miaka 46, alisema kwamba anahisi kuwa na matumaini kuhusu maandamano hayo wakati huu. ''Nahisi kitu tofauti kuhusu maandamano haya....nina matumaini kwamba ujumbe wa umoja na usawa unazidi kuwafikia wengi''. Mjini Chicago, baadhi ya waandamanaji walipeperusha bendera juu chini Amri ya kutotembea nje zilizokuwa zimewekwa zimeondolewa katika maeneo mengi . Ukamataji wa watu kiholela umepungua. Hatahivyo baadaye siku ya Jumamosi katika jimbo la Portland , Oregon walitangaza maandamano hayo kuwa mikutano isio halali na ukiukaji wa sheria baada ya maafisa wa polisi kushamabuliwa . Maafisa wa polisi wa Seattle pia walisema kwamba vitu vilivyokuwa vikirushwa na waandamanji viliwaathiri maafisa wa polisi. Maandamano makubwa ya amani yamefanyika kote nchini Marekani kupinga ubaguzi wa rangi na unyanyasaji unaotekelezwa na maafisa wa polisi ikiwa ni siku ya 12 ya maandamano yaliosababishwa na kifo cha George Floyd. text: Ndege ya Aseman ya ATR 72-500 Ndege hiyo ya shirika la Aseman, ilikuwa safarini kutoka mjini Tehran kwenda mji wa kusini magharibi wa Yasuf wakati ilianguka kwenye milima ya Zagros kati kati mwa Iran. Shirika la msalaba mwekundu lilituma kikisi cha uokoaji kweda eneo hilo karibu na mji wa Semirom mkoa wa Isfahan. Ndege hiyo namba 3704 iliondoka Tehran mwendo wa saa (01:30 GMT) na kutoweka kutoka kwa rada baadaye. Maafisa wanasema kuwa hali mbaya ya hewa imetatiza jitihada za uokoaji. Ndege hiyo inaaminiwa kuwa ya miaka 20 iliyotengenezewa nchini Ufaransa. Ripoti zinasema kuwa wale waliokuwa ndani ya ndege ni abiria 60, walinzi wawili, wahudumu wawili, rubani na msaidizi wake. Ramani Watu 66 wameuawa kwenye ajali ya ndege ya abiria nchini Iraan, maafisa wa kampuni wamesema. text: Raia wa Korea Kusini watazama video hiyo mjini Seol Kwenye kanda hiyo fupi mwanamume huyo anasema, "Jina langu ni Kim Han-sol, kutoka Korea Kaskazini, moja wa familia ya Kim." Anasema kuwa yuko na mama na dada yake lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu ni wapi aliko. Haya ndiyo matamshi ya kwanza kutoka kwa familia ya Kim tangu kutokea mauaji hayo. Babake aliuawa kwenye uwanja wa Kuala Lumpur tarehe 13 mwezi Februari, kwa kushambuliwa na kemikali ya VX. Maafisa wa wizara ya upatanishi nchini Korea Kusini na idara ya kitaifa ya ujasusi wanasema kuwa mtu huo ni Kim Han-sol. Video hiyo ya dakika 40 inamuonyesha mwanamume ambaye anatambuliwa kuwa Kim Han-sol, akionyesha kile kinaonekana kuwa pasipoti ya Korea Kaskazini lakini yaliyomo kwenye pasipoti hiyo hayaonekani. Tangu babake auawa tarehe 13 mwezi Februari haijabainika ni wapi na ni lini video hiyo ilirekodiwa na ni wapi Kim Han -sol alipo. Kim Han-sol alifanya mahojiano na televisheni ya Finland mwaka 2012 Kim Jong-nam aliomba msaada kwenye uwanja wa ndege muda mfupi baada ya uso wake kumwagiwa kemikali hatari ya VX Kanda moja ya video imeibuka ikimuonyesha mtoto wa kiume wa Kim Jong-nam, ndugu wa kambo aliyeuawa wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. text: Messi amempiku Christiano Ronaldo kwa Malipo bora zaidi miongoni mwa wanamichezo Mshambuliaji wa Juventus, Mreno Cristiano Ronaldo anashikilia nafasi ya pili akilipwa dola milioni 109, huku mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar ambaye ni raia wa Brazil akija katiika nafasi ya tatu kwa malipo ya dola milioni 105. Cristiano Ronaldo amechukua nafasi ya pili kwenye orodha ya Forbes akilipwa dola milioni 109 Mwaka jana mchezaji aliyelipwa kuliko wote duniani alikuwa ni mwanamasumbwi Floyd Mayweather, lakini sasa ameshuka katika orodha hiyo. Mchezaji tenesi Serena Williams ni mwanamke pekee katika watu 100 ,wanaolipwa vizuri, na kwa mujibu wa Forbes analipwa dola milioni 29.2 Serena Williams ndiye mchezaji pekee mwanamke aliyefanikiwa kuingia katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaolipwa vizuri akikadiriwa kuwa na mapato ya dola milioni 29.2 Mshindi wa mara tano wa mashindano ya dunia ya magari ya Formula 1 Lewis Hamilton na mshindi wa zamani wa masumbwi uzani wa juu Anthony Joshua ndio wanariadha wanaolipwa vizuri zaidi nchini Uingereza , wakichukua namba 13 na malipo ya dola milioni 55. Jarida hilo la Marekani lilikokotoa malipo ya wanariadha kwa kujumlisha fedha za malipo ya tuzo , mishahara na nembo walizoidhinisha kati ya Juni 2018 na Juni 2019. Miongoni mwa wanariadha wanaoshikilia nafasi za juu katika 100 kutoka nchi 25 na mapatp yao ya dola bilioni 4 yakijumlishwa yanajumuisha 5% ya kutoka mwaka jana, wakati Mayweather alipokuwa wa kwanza na malipo ya dola milioni 285. Mwaka jana mchezaji aliyelipwa kuliko wote duniani alikuwa ni mwanamasumbwi Floyd Mayweather, lakini sasa ameshuka katika orodha ya Forbes Mpambano pekee wa bondia huyo wa Marekani tangu Agosti 2017 ulikuwa baina yake na Mjapani Tenshin Nasukawa uliofanyika Disemba. Wanariadha walitakiwa kulipwa dola milioni 25 kuweza kuingia katika orodha Forbes ya mwaka huu. Messi ndie mchezaji pekee wa pili wa soka kuwa juu katika viwango baada ya Ronaldo, na ndiye mwanariadha wa nane pekee miongoni mwa wanariadha tofauti kuchukua namna moja tangu orodha hiyo ilipoanza kutolewa mnamo 1990. Ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa mpira wa miguu kuwekwa miongoni mwa watu watatu wanaolipwa vizuri kwa kucheza. Mshindi wa mara tano wa mashindano ya dunia ya magari ya Formula 1 Lewis Hamilton ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa vizuri zaidi duniani Messi ni miongoni mwa wanariadha 38 wasio Wamarekani kwenye orodha , huku wanamichezo nyota 62 wa Marekani wakishikilia nafasi za kwanza katika orodha ya watu 100. Shirikisho la mchezo wa kikapu Marekani NBA ndilo lililoongoza kwa kuwa na wachezaji wengi kwenye orodha hiyo, liliwa na wachezaji 35, huku LeBron James wa LA Lakers akiwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ambapo anashikilia nafasi ya eighth akilipwa dola 89 akija mbele ya Wachezaji wawili nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry anayeshikilia namna 9 akilipwa dola milioni 79.8 na Kevin Durant ambaye anashililia nafasi ya 10 akilipwa dola milioni 65.4 Paul Pogba ndiye anayelipwa zaidi miongoni mwa wachezaji wa Primia Ligi, kulingana na orodha ya jarida la Forbes Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika primia Ligi, na katika orodha ya Forbes anashikilia nafasi ya 44t na malipo ya dola milioni 33. (£25.9m). 10 walio juu katika Orodha ya Forbes: 1. Lionel Messi dola 127 2. Cristiano Ronaldo dola 109 3. Neymar dola milioni 105 4. Canelo Alvarez dola milioni 94 5. Roger Federer dola milioni 93.4 6. Russell Wilson dola milioni 89.5 7. Aaron Rodgers dola milioni 89.3 8. LeBron James dola milioni 89 9. Stephen Curry dola milioni 79.8 10, Kevin Durant dola milioni 65.4 Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi ndio anayelipwa malipo ya juu zaidi kuliko wachezaji wote duniani , alilipwa dola milioni 127 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes ya wachezaji 100 wanaolipwa vizuri. text: Baadhi ya kampuni China zimetishia kuadhibu wanaonunua iPhone7 Kampuni zilizotoa marufuku hiyo zinasema ni kwa sababu za kizalendo. Nyingine zimesema zinataka kuwafunza wafanyakazi wake kutopenda sana raha na anasa za dunia. Kampuni ya dawa ya Nanyang Yongkang Medicine, katika mkoa wa Henan, ni moja ya zilizoagiza wafanyakazi wake kutonunua simu za iPhone 7 au Iphone 7 Plus. "Ukivunja agizo hili, njoo moja kwa moja hadi afisini na utukabidhi barua yako ya kuacha kazi," ilani kutoka kwa kampuni hiyo iliyotumwa kwa wafanyakazi inasema. Baadhi ya wafanyakazi wanasema barua ya kampuni hiyo inakiuka haki za wafanyakazi Sera hiyo imetangazwa wakati sambamba na siku ya maadhimisho ya miaka 85 tangu wanajeshi wa Japan walipovamia maeneo ya mashariki mwa China mwaka 1931. "Septemba 18 ni siku ya kihistoria. Msisahau tulivyodhalilishwa kama taifa. Hebu tususie bidhaa kutoka nje ya nchi," ilani kutoka kwa kampuni hiyo iliongeza. Tovuti moja imemnukuu msemaji wa kampuni ya Nanyang Yongkang Medicine kwa jina Bw Liu akisema lengo la agizo hilo ni kuwahamasisha pia wafanyakazi kuangazia zaidi familia badala ya vitu vya anasa. Barua hiyo ilisambazwa sana katika mitandao ya kijamii CHina, na kitambulisha mada "Wafanyakazi watakaonunua iPhone7 kufutwa" kilivuma katika mtandao wa Weibo. Baadhi ya watu kwenye Weibo hata hivyo wameeleza kwamba kususia iPhone7 huenda kukawa kunawadhuru Wachina wenyewe kwani uzalishaji wa simu za Apple hufanywa katika viwanda vya kampuni ya Foxconn nchini Uchina. Kwenye Weibo kumesambazwa pia picha za barua ya hospitali ya Fuling Xinjiuzhou Gynecology Hospital mjini Chongqing ambayo inawaonya wafanyakazi wasinunue iPhone7. Barua hiyo inasema: "iPhone 7 imeanza kuuzwa sokoni na bei yake ni ya juu mno ukilinganisha na simu nyingine. Ili kuendeleza utamaduni kwa kutopenda matumizi ya anasa na kutumia pesa kwa busara, wasimamizi wa hospitali wamefikia uamuzi wa kuwapiga marufuku wafanyakazi wetu wasinunue simu za iPhone7." Barua hiy inaongeza kwamba wanatakaokiuka agizo hilo hawatapewa alama za juu katika utathmini wa utendaji kazi wao. Aidha, watahimizwa kurejesha simu hizo madukani. Meneja wa hospitali hiyo ameambia BBC Trending kwamba hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mfanyakazi mmoja kununua iPhone 7 ilhali inajulikana kwamba bei ya simu hiyo ni mara tatu mshahara wake. "Sipingi bidhaa kutoka nje lakini sipendi watu wakinunua simu ambazo bila shaka hawawezi kumudu kifedha. Baadhi ya watu hukopa pesa benki au kutoka kwa jamaa na marafiki, na wengine hata huuza viungo vyao kununua iPhone. Sitaki wafanyakazi wangu wafanye mambo kama hayo," amesema. Baadhi ya watu wanaotetea uzalendo wa Wachina wamekuwa pia wakipinga simu za iPhone kuonyesha kutoridhishwa kwao na uamuzi wa jopo la kimataifa uliosema China haina haki ya kumiliki visiwa ambavyo imekuwa ikidai katika bahari ya South China Sea. Rais Barack Obama aliitaka China kutii uamuzi huo. Baadhi ya watu waliharibu simu zao za iPhone kuonyesha uzalendo Video za watu wakiharibu iPhone zao kuonyesha uzalendo zimevuma sana mtandao wa Weibo. Baadhi ya maduka China pia yamekataa kuuza simu za iPhone7 kama sehemu ya kususia bidhaa kutoka Marekani. Kampuni kadha nchini Uchina zimetoa onyo kali kwa wafanyakazi wake na kuwataka wasinunue simu mpya ya kampuni ya Apple, iPhone 7. text: Rais Kiir (kulia) na Riek Machar Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar walikuwa kwenye taifa jirani la Sudan kusaini makubaliano, ambapo kiongozi wa waasi Machar anatarajiwa kurejea kama makamu wa rais wa kwanza kati ya makamu wa rais watano kwenye serikali ya umoja. Makubaliano hayo yenye lengo la kumaliza vita kwenye taifa hilo janga zaidi duniani yalitiwa sahihi mbele ya rais wa Sudan Omar al-Bashir na wenzake kutoka Kenya, Uganda na Djibouti wakiwemo pia wanadiplomasia wa kigeni. Baada ya kusainiwa mukubaliano ya mwisho, mahasimu hao watakuwa na miezi mitatu ya kuunda serikali ya mpito ambayo itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu. Vita vya karibu miaka mitano nchini Sudan Kusini vilianza wakati Kiir alimlaumu aliyekuwa makamu wake wa rais Machar kuwa alikuwa anapanga mapinduzi mwaka 2013. Vita vya Sudan Kusini vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, vikawalazimu watu milioni nne kuhama makwao Pande za Kiir na Machar tayari zimekubaliana kuondoa kabisa vikosi vyao kutoka mijini kwenye mazungumzo ya hivi majuzi yaliyoongozwa na Bashir. Mpangilio ya ugavi wa mamlaka unaeleza kuwa kutakuwa na mawaziri 35 kwenye serikali ya mpito wakiwemo washirika 20 wa Kiir na 9 wa Machar wakiwemo pia washirika wa makundi manne ya waasi. Bunge litakuwa na wabunge 550 wakimemo 332 kutoka upande wa Kiir na 128 kutoka upande wa Machar. "Makubaliano yaliyo kwenye karatasi ni makubaliano mazuri lakini utapata kuwa katika utekelezani ndio kuna changamoto na kulikuwa na makubaliano kuwa ikiwa hawangekubaliana kwenye mazungumzo hayo ilikuwa waje nchini Kenya lakini kwa wakati huu wameshakubaliana mikakati iliyopo ni kuhusu vipi yatatelezwa," kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Sudan na Sudan Kusini Mohammed Jaffar. Tayari Kiir ameonya kuwa ukubwa wa serikali itakuwa ni changamoto, "Ona ukubwa wa bunge, ona ukubwa na baraza la mawaziri. Utawalipa aje? alisema, akiongeza kuwa ana wasi wasi kuhusu ni kwa njia gani atawapa makao, maofisi na magari maafisa wapya. Hata hivyo Marekani imetilia shaka mafanikio yatakayotokana na makubaliano ya hivi punde kutokana na uhasama uliopo kati ya Kirr na Machar. Kiongozi wa waasi Riek Machar, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Sudan Omar al-Bashir na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mwezi uliopita Ikulu ya Marekani ilionya kuwa makubaliano madogo kati ya viongozi hayawezi kutatua changamoto zinazoikumba Sudan Kusini. Umoja wa Mataifa ulisema makubaliano ya ugavi wa mamlaka ni hatua kubwa. "Kwa kuweka sahihi makubaliano, bunduki ni lazima zikae kimya," alisema Nicholas Hayson mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. Vita hivyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, vikawalazimu watu milioni nne kuhama makwao na kusambaratisha uchumi wa taifa hilo lenye utajiri wa mafuta. Mahasimu nchini Sudan Kusini wameweka saini makubaliano ya kugawana madaraka huku Rais Salva Kirr akitoa wito wa kutaka kuwepo amani kwenye nchi ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha vifo vya maelfu ya watu. text: Rais Jacob Zuma inasemekana kuwa amekataa kuachia madaraka Rais huyo amekuwa anakabiliwa na shinikizo zaidi kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC siku ya Jumapili. Haijafichuliwa mazungumzo hayo yalihusu nini . Bw Zuma aliyefungwa gerezani baada ya kuhsiriki katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi anaonekana kuwa katika hatua za mwisho wa awamu wake wa pili na wa mwisho kama Rais. Julius Malema, kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mafuasi wa chama hicho cha ANC alisema kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba rais Zuma amekataa kujiuzulu. Mwisho wa Twitter ujumbe, 1 Habari ambazo hazijathibitiwa zinasema kuwa katika mkutano wa Jumapili Zuma aliomba kupata kinga dhidi ya kushtakiwa kwa yeye na familia yake. Cyril Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma, anayekabiliwa na tuhuma za rushwa. Wachambuzi wanasema wakuu wa chama hicho wanajaribu kuondoa mvutano wa kung'ang'ania madaraka ambao unaweza kukigawanya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwakani. Wanatarajiwa kuanza mchakato wa kumuondoa rais Zuma kupitia mfumo rasmi wa kumuondoa au kwa kuidhinisha hoja bungeni. Maafisa sita wakuu wa chama hicho tawala waliwasili mmoja baada ya mwingine Jumapili katika makaaziya Zuma mjini Pretoria. Walinyamaza kimya wakati mazungumzo yalipomalizika lakini wameitisha mkutano wa kamati kuu ya chama hicho Jumatatu. Zuma anastahili kusalia madarakani hadi uchaguzi mwaka ujao 2019. Hatahivyo chama hicho kimepoteza umaarufu wake katika muhula wa pili wa kiongozi huyo huku kukishuhudiwa pia kudorora kwa uchumi na tuhuma za rushwa. Kiongozi mpya wa chama cha ANC - Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu, ndani ya chama na pia serikali Mustakabali wa Zuma ni upi? Rais Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC wanaotaka kumtimua madarakani. Kwa mujibu wa taarifa rasmi, maafisa wa ngazi ya juu wa ANC wana 'jadiliana tu' na rais Zuma kuhusu "ugavi wa uongozi" ndani ya chama. Lakini nyuma ya kauli hiyo nyepesi - vita vikali vya uongozi vinajitokeza katika nchi hiyo. Rais Zuma bado yupo madarakani, lakini tangu Desemba mwaka jana, yeye sio mkuu tena wa ANC. Waendesha mashtaka wakakamavu sasa wanaonekana kushika kasi katika uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zinazomkabili bwana Zuma na baadhi ya marafaiki zake wa karibu. Wengi ndani ya ANC wanamtaka rais huyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo, ili waweze kulenga kujenga upya sifa ya chama hicho kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu nchini mwakani. Lakini kuna taarifa kwamba Zuma anajikita kisawasawa. Anatarajiwa kulihotubia bunge wiki ijayo, lakini wafuasi wa upinzani wanataka kumzuia pia, wakieleza kuwa hastahili kusalia kama rais. Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu ndani ya chama na serikali, lakini anasisitiza kuwa rais Zuma hastahili kuazirishwa. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekataa wito wa chama chake wa kujiuzulu kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. text: "Nafikiri tutamuona Rais Donald Trump akirejea kwenye mtandao wa kijamii katika kipindi cha karibu miezi miwili au mitatu," Jason Miller amezungumza na Fox News. Alisema mtandao huo "utakuwa unaovuma kati ya mitandao ya kijamii" na "utabadilisha kabisa mitandao". Bwana Trump alikatishwa kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter na Facebook baada ya kutokea kwa ghasia mbaya za mwezi Januari katika Bunge la Capitol Washington DC. Shambulio hilo lilitekelezwa Januari 6 na wafuasi wa Trump na kusababisha mauaji ya watu 5 akiwemo afisa wa polisi na kutikisa misingi ya demokrasia ya Marekani. Siku kadhaa baadaye, mtandao wa Twitter ulisema kuwa akaunti ya Bwana Trump ya - @realDonaldTrump - "imekatishwa kabisa… kwasababu ya hatari ya kusababisha ghasia zaidi. Bwana Trump alitumia mtandao wa Twitter kwa zaidi ya miaka 10 kuepuka vyombo vya habari vya zamani na aliweza kuzungumza na wapiga kura moja kwa moja. Donald Trump alikuwa na karibu wafuasi milioni 90 katika mtandao wa kijamii. Je tunajua ni mtandao gani ambao Bwana Trump atautumia? Hapana. Siyo kweli. Bwana Miller alitoa taarifa akisema kwa hilo "kila mmoja atasubiri kuona hasa ni kipi kitakachokuwa kinatekelezwa na Rais Trump". Mshauri alisema Bwana Trump alikuwa akifanya "mikutano ya ngazi ya juu" huku timu kadhaa zikifikiria mradi wake katika eneo la Mar-a-Lago fukwe ya Florida. "Kampuni kadhaa" tayari zimewasiliana na aliyekuwa rais, Bwana Miller amesema. "Mtandao huu mpya utakuwa mkubwa," aliongeza, akitabiri kuwa Bwana Trump atavutia "makumi ya mamilioni ya watu". Kwanini Trump alipigwa marufuku? Mara ya kwanza, Bwana Trump alifungiwa mtandao wa Twitter kwa saa 12 mnamo mwezi Januari baada ya kuita watu waliovamia Bunge na kusababisha "ghasia". Mamia ya wafuasi walivamia Bunge wakati linajaribu kuidhinisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa urais mwaka jana. Wakati huo, mtandao wa Twitter ulionya kuwa utamfungia Bwana Trump "kabisa" kuutumia ikiwa atakiuka tena sheria za mtandao huo. Na baada ya kuruhusiwa kuanza tena kutumia Twitter, Bwana Trump alituma ujumbe mara mbili ambazo kampuni hiyo ilisema ndio ulikuwa wa mwisho kuvumilika. Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilisema kuwa ujumbe wake huo aliotuma, zote mbili "ulikuwa sheria ya kusababisha ghasia". Akaunti za Bwana Trump katika Facebook pia zilisitishwa, mtandao wa Twitch pamoja na Snapchat. Pia unaweza kutazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani: Uchaguzi wa Marekani 2020: Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibu atarejea katika mtandao wa kijamii "mtandao wake mwenyewe", mshauri wake amesema. text: los datos recopilados por los investigadores, las personas pueden experimentar una amplia gama de síntomas diferentes. Kila moja ya aina hii inaonyesha utofauti katika makali ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona na haja ya kutumia vifaa vya usaidizi wa kupumua wakati mgonjwa anapolazwa ,kwa mujibu wa wanasayansi. "Matokeo haya ya utafiti yanamaana kubwa katika utoaji huduma na ufuatiliaji wa watu ambao wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuugua zaidi kutokana na covid-19," anasema mwandishi wa utafiti Dkt Claire Steves wa King's College London. Virusi vya corona:Shule zinafunguliwa duniani kote, Je watoto watakuwa salama? Watafiti walioongozwa na Steves walitegemea ukusanyaji wa data zilizokusanywa kutoka katika utafiti wa App ya COVID Sympston, ambayo huwawezesha watumiaji kuipakua na kuingia kupata taarifa kuhusu virusi vya corona. Ingawa kikohozi kisichokoma, homa na kukosa uwezo wa kutambua harufu kwa ujumla zinatambuliwa kama dalili kuu tatu za covid -19, data zilizokusanywa kutoka kwa watumiaji zinaonyesha kuwa watu wanaweza kupata uzoefu wa dalili tofauti , ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa kinachouma upande mmoja, maumivu ya misuli, uchovu, kuwa na mkanganyiko, kuhara, ukosefu wa hamu ya kula chakula, matatizo ya kupumua, miongoni mwa dalili nyingine. Kuongezeka kwa ugonjwa pamoja na athari zake, pia hutofautiana kwa kiwango kikubwa baina ya watu, ambapo unaweza kuanzia dalili kama ya mafua ya kawaida hadi mtu kuwa na hali mbaya na hata kifo. Los investigadores basaron sus hallazgos en información de la aplicación COVID Sympston Study App. Ili kubaini ikiwa dalili za aina fulani huwa zinajitokeza kwa pamoja na jinsi zinavyohusiana na kukua kwa ugonjwa, timu ya wanasayansi ilitumia mashine ya algorithm kuchambua data kutoka katika kundi dogo la watu wapatao 1,600 waliothibitishwa kuwa ni watumiaji wa mashine hiyo, katika nchi za Uingereza na Marekani wanaougua covid-19 ambao walikua wakisajili dalili zao katika mfumo huo kati ya mwezi Machi na Aprili. Walitegemea kanzidata huru za watumiaji 1,000 nchini Uingereza, Marekani na Sweden waliosajili dalili zao mwezi Mei. Tathmini ilibaini kuwa makundi sita ya dalili ambayo yalijitokeza kwa nyakati fulani wakati wa kukua kwa ugonjwa yaliwakilisha ''aina'' sita tofauti za Covid-19 Makundi 6 ya dalili za corona 1. "Mafua" Bila homa: Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane) , ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu, maumivu ya misuli, kikohozi, kuvimba kooni, maumivu ya kifua, bila homa. 2. "Mafua" yenye homa : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane ) ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu, kikohozi, kuvimba kooni, kupoteza sauti, homa, kukosa hamu ya chakula. 3. Maumivu ya tumbo : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane) , ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu , ukosefu wa hamu ya chakula, kuharisha, kuvimba kooni , maumifu ya kifua na kikohozi. 4.Uchovu wa mwili wa hali ya juu : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane) , ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu , kikohozi, homa, kupoteza sauti, maumivu ya kifua na uchovu wa mwili . 5.Mkanganyiko wa kiwango cha pili : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migrane), ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu , kikohozi, homa, kupoteza sauti, maumivu ya kifua na uchovu wa mwili. 6.Kiwango cha tatu cha kuugua, maumivu ya tumbo na mfumo wa kupumua : Maumivu ya kichwa upande mmoja (migraine), ukosefu wa uwezo wa kutambua harufu, ukosefu wa hamu ya chakula, kikohozi, homa, kupoteza sauti, maumivu ya kifua, uchovu, maumivu ya misuli, kushindwa kupumua vyema, kuharisha, maumivu ya tumbo. Wale wote walioripoti dalili waliugua kichwa upande mmoja(migrane) na kupoteza uwezo wa kutambua harufu, na jumla ya dalili nyingine tofauti za ziada kwa nyakati fofauti. Baadhi ya dalili hizi, kama vile kuwa na mkanganyiko, maumivu ya tumbo, kushindwa kupumua vyema, hazijafahamika bado kama dalili za covid-19. Hatahivyo zinatofautiana na zile anazopata mgonjwa mahututi. Wanasayansi tena walifanya uchunguzi juu ya ikiwa watu wanaopata aina fulani ya dalili walikua na uwezekano zaidi wa kuhitaji usaidizi wa kupumua au kuongezewa hewa ya oksijeni. Walibaini kuwa asilimia ndogo sana ya watu walikuwa katika makundi ya 1, 2, na 3 walihitaji usaidizi wa kupumua; baina ya 1.5% na 3.3%. Lakini asilimia ya wale waliokuwa na dalili za makundi ya 3, 4 na 5 walikua uwezekano wa kuhitaji usaidizi wa kupumua kwa 8.6%, 9.9% na 19.8%, kila kundi Zaidi ya hayo, takriban nusu ya wagonjwa katika kundi la 6 waliishia kulazwa hospitalini , wakilinganishwa na asilimia 16% waliokua katika kundi la 1. Kwa ujumla, wagonjwa wote walioripoti dalili kutoka makundi ya mwisho matatu walionekana kuwa wadhaifu, wakiwa na uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia, na walikua na magonjwa ya kudumu kama vile ugonjwa kisukari, au ugonjwa wa mapafu kuliko wale waliokuwa katika makundi ya 1, 2, na la 3 1 . Kwa kukusanya taarifa kuhusu dalili siku tano tu baadae baada ya mtu kupata ugonjwa na kujumuishwa na umri, jinsia, uzito wa mwili, na matatizo ya kiafya ya wagonjwa , kikosi cha wanasayansi wa King's College walitengeneza njia inayowawezesha kutambua makundi waliyomo wagonjwa na hatari zao za kulazwa na huduma ya kupumua wanayoweza kuhitaji. Kwasababu wengi miongoni mwa watu wanaohitaji huduma ya usaidizi wa kupumua huwa wanalazwa hospitalini kwa takriban siku 13 baada ya dalili za kwanza kujitokeza, siku hizo nane za mwanzo huashiria '' tahadhari ya awali '' juu ya ni nani atahitaji kuhudumiwa zaidi. "Kama unaweza kubashiri ni watu gani watakua katika siku ya tano, unaweza kuwa na muda wa kuwapatia usaidizi na kuwahudumia mapema kama vile kufuatilia kiwango cha oksijeni na viwango vya sukari mwilini, pamoja na kuhakikisha kwamba wana maji ya kutosha mwilini ,"anaeleza Dkt Steves. "Hizo ni huduma ambazo zinaweza kutolewa nyumbani, kuepuka mtu kulazwa na kuokoa maisha ," alisema.. Uchambuzi wa watafiti katika chuo cha King's College mjini London nchini Uingereza umeweza kuigawanya Covid-19 katika "aina " sita, kila aina ikitengwa kulingana na upekee wa dalili zake. text: Wayne Rooney kucheza dakika 45 dhidi ya Gor Mahia Tanzania The Toffees watakabiliana na klabu ya Kenya ya Gor Mahia katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 siku ya Alhamisi, ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18. Koeman amesema kuwa kila mchezaji wake akiwemo wayne Rooney atacheza dakika 45 dhidi ya Gor Mahia huku wakilenga kuimarisha viungo vyao. Everton wako nchini Tanzania chini ya usimamizi wa wafadhili wao wapya Sportpesa, wachezaji hao pia watatembelea jamii za taifa hilo ili kuweza kujua utamaduni wa taifa hilo la Afrika mashariki. Mpango huo utafanya ziara hiyo kuvutia zaidi na Koeman yuko tayari. ''Nimezuru mataifa kadhaa barani Afrika lakini sio Tanzania'', alisema.''Nimejiandaa vilivyo. Huwa vigumu kucheza mechi katika eneo la mbali kutokana joto na ni lazima tucheze mechi hiyo ya kirafiki.Lakini kutokana na vile tulivyojiandaa, tutaondoka siku ya Jumanne jioni na kurudi siku ya Ijumaa.Hii ni mechi yetu ya kwanza na kila mchezaji atajumuishwa kwa dakika 45.Tunacheza mechi kushinda na tutadhihirisha hilo nchini Tanzania''. Mkufunzi wa klabu ya Everton Ronald Koeman yuko tayari kuiongoza klabu yake nchini Tanzania wiki hii katika mechi ya maandalizi ya msimu ujao. text: Timothy Weekes alitoa wito kwa Bw Trump kumsaidia Mmarekani Kevin King na raia wa Australia Timothy Weekes walikuwa maprofesa katika chuo kikuu cha Wamarekani cha Afghanistan mjini Kabul. Walitekwa mwezi Agosti wakiwa kwenye magari yao nje ya chuo hicho na wapiganaji waliokuwa wamevalia sare za wanajeshi wa serikali. Baadaye mwezi huo, wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan walijaribu kuwakomboa lakini wakashindwa, Pentagon ilisema. Kwenye video hiyo ambayo inadaiwa kupigwa mnamo 1 Januari na kupakiwa mtandaoni, wanaume hao wanasema wamo buheri wa afya. Lakini wanamuomba Rais mteule wa Marekani Donald Trump kujitolea kuwabadilisha na wafungwa wa Taliban ndipo waachiliwe huru. Wanasema watauawa iwapo Marekani haitashiriki kwenye mazungumzo ya kuwaachilia huru. Kevin King pia alioneshwa Wanajeshi wa Marekani walijaribu kuwaokoa Septemba mwaka jana lakini wakafeli Wapiganaji wa Taliban wametoa kanda ya video inayowaonesha mateka wawili - Mmarekani na raia wa Australia - ambao walitekwa na wanamgambo hao nchini Afghanistan mwaka jana. text: Waziri wa mambo ya nje Adel al-Jubeir amekiambia kituo cha televisheni cha Fox News kwamba "mauaji hayo" yalikuwa 'makosa makubwa' na amekana kwamba Mwanamfalme wa Saudia aliagiza mauji hayo. Khashoggi alionekana mara ya mwisho akiingia katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul. Saudia ikiwa chini ya shinikizo kubwa kueleza aliko Khashoggi, imetoa kauli za kutofuatiana. Kauli ya Saudia ilivyobadilika Kumekuwa na maandamano sehemu mbalimbali kudai ukweji juu ya kilichompata mwandishi Jamal Khashoggi. Awali Saudia ilisema mwandishi huyo alitoka katika ubalozi huo akiwa mzima mnamo Okotoba 2 lakini siku ya Ijumaa ilikiri kwa mara ya kwanza kwamba amekufa, ikieleza kwamba aliuawa katika mapigano, kauli iliyokabiliwa na shaka kubwa. Maafisa wa UTuruki wanaamini Khashoggi, mkosoaji maarufu wa serikali ya Saudia, aliuawa na kundi la maajenti wa Saudia ndani ya jengo hil na wanasema wana ushahidi kulithibitisha hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Adel al-Jubeir amesema uchunguzi wa kina unaendelea na watatoa vielelezo vyote vinavyohitajika kwa uwazi, "ukweli ni kwamba waliofanya ukatili huu walichupa mipaka ya kazi zao. Ni Dhahiri makosa yamefanyika na makossa makubwa Zaidi ni kujaribu kuuficha ukweli." Mamlaka za Saudia zinasema awali walitangaza kuwa Khashoggi alitoka nje ya jengo lao kwa sababu taarifa waliyopata kutoka kwa wawakilishi wao ilisema hivyo, na waliibadili mara tu walipotambua kuwa haikuwa ya kweli. Mgahawa ambapo wateja hulipa kwa njia ya Bitcoin Kenya Hatahivyo, Yeni Safak, kituo cha habri kilicho na ukaribu na serikali ya Uturuki, kinasema kina taarifa zinazoonyesha kuwa ofisi ya mwanamfalme ilipokea simu nne kutoka ubalozi huo baada ya mauaji. Gazeti hilo ambalo limewahi kufichua taarifa kuhusu uchunguzi wa Uturuki kufikia sasa, limeashiria afisa wa ubalozi Maher Mutreb ametumia simu yake ya mkononi kupiga simu katika ofisi hiyo, pamoja na nambari ya Marekani inayoaminika kuwa ya kakake mdogo mwanamfalme, Khaled, aliyekuwa balozi wa Saudia kwa Marekani. Mwanamfalme Khaled bin Salman aliondoka Marekani punde baada ya kutoweka kwa Khashoggi. Mamlaka za Saudia zimekanusha Mwanamfalme Mohammed Bin Salman kuhusika katika mauaji ya Khashoggi. Wadadisi na wakosoaji wa dola hiyo wanasema Saudia inabadili maelezo yake kutokana na shutuma zinazolekezwa kwao kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa vinanukuu vyanzo kutoka ndani ya serikali ya Saudia vikisema mwanamfalme Bin Salman ameshtushwa na ukubwa wa shutuma zinaolekezwa kwa nchi yake na hakutegemea suala hilo lingelikuwa kubwa kama ilivyo kwa sasa. Shirika la habari la Reuters limeripoti jana kuwa kiongozi mmoja wa Saudia amewaambia kuwa Khashoggi aliuawa mara baada ya kukataa kurudishwa Saudia. Baada ya kuuawa, shirika hilo linaripoti kuwa, mwili wake uliviringishwa kwenye zulia na kupewa mshiriki mmoja wa tukio hilo ambaye ni raia wa Uturuki ili akauteketeze. Mmoja wa washiriki wa tukio hilo ambaye ni raia wa Saudia inadaiwa alivaa nguo za Khashoggi na kutoka nje ya ofisi hizo za ubalozi ili kupoteza ushahidi. Saudia yabanwa mbavu na mataifa yenye nguvu Nchi tatu zenye ushawishi mkubwa barani Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimelaani vikali mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi na kuitaka Saudi Arabia kutoa ufafanuzi wa kina haraka iwezekanavyo. Taarifa ya pamoja ya mataifa hayo yanaitaka Saudia kutoa vielelezo vya kina juu ya madai kuwa Khashoggi aliuawa wakati akijaribu kupigana ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki. Rais wa Marekani Donald Trump pia amebainisha kuwa "hakuridhishwa" na maelezo hayo ya Saudia. Rais wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan jana Jumapili ameahidi kudhihirisha ukweli wote juu ya tukio hilo. Erdogan amesema atatoa maelezo juu ya sakata hilo kesho Jumanne atakapolihutubia bunge la nchi hiyo. Wachunguzi wanasaka msitu wa Belgrad kutafuta mwili "Tunataka haki itendeke hapa, na juu ya jambo hili tutadhihirisha ukweli wote," Erdogan aliuambia mkutano wa hadhara jijini Istanbul. Khashoggi aliingia katika jingo la ubalozi mdogo mnamo tarehe 2 Oktoba kwa minajili ya kushughulikia karatasi zake muhimu kuhusiana masuala ya ndoa. Awali mamlaka za Saudia zilidai kuwa alitoka, lakini mamlaka za Uturuki zilikanusha vikali na kusema kuwa wanaushahidi kuwa mwanahabari huyo alizuiliwa na baadae kuuawa na kisha mwili wake kukatwa vipande vipande. Uturuki: Mwandishi 'aliuawa' ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia Khashoggi alikuwa mkosoaji kinara wa sera za Mwanamfalme Mohammed Bin Salman na alihamia Marekani mwaka 2017 akihofia usalama wake. Katika taarifa yao ya pamoja, nchi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema kuwa zimeshtushwa na mkasa huo wakiamini hakuna sababu yeyote ile ya kutetea mauaji. "Maelezo Zaidi na yenye ushahidi usiokuwa na chembe ya shaka yanahitajika… Hivyo basi, tunataka uchunguzi wa kina ufanyike na wahusika wote watambulike na hatua za kisheria zinastohili zichukuliwe kwa waliotenda unyama huu." Saudi Arabia imelaumu kuwa mwandishi habari Jamal Khashoggi aliuawa katika 'operesheni isiyo rasmi', ikitoa mtazamo mwingine wa hatua iliyochangia shutuma kubwa duniani. text: Mombasa kulikuwa ndio nyumbani kwa familia ya rubani Yared Mulugeta Gatechew Yakijulikana kama sala ya marehemu asiyekuwepo , ibada hiyo ilifanyikakatika msikiti maarufu wa Baluch katika mji wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya Jumanne jioni. Sala ya marehemu asiyekuwepo imefanyika kuashiria kwamba familia ya rubani wa ngazi ya juu Yared haina matumaini ya kuupata mwili wake, kulingana na mwandishi wa BBC Wazir Khamsin aliyepo mjini Nairobi. Mwanablogi maarufu aliyeko mjini Mombasa alituma video ya ibada ya mazishi huku rubani Capt Yared akionekana upande wa kulia kwake. Waombolezaji wakiipa pole familia ya rubani Yared Mulugeta Gatechew wakati wa sala ya kumuombea marehemu Rubani huyo wa ngazi ya juu Yared alikuwa na asili ya Ethiopia na Kenya, na baadhi ya ndugu zake wa karibu wanaishi Mombasa, ambako kunatambuliwa kama nyumbani kwa familia yake Miongoni mwa watu waliohudhuria sala ya mazishi yake ni mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu nchini Kenya Munir Mazrui na Mkurugenzi wa masuala ya utalii Mohammed Hersi. Mama yake Getachew Dr Rayan Shapi alikuwa Mkenya wa Mombasa na baba yake Dr Getachew Tessema alikuwa na asili ya Ethiopia. Wazazi wake wanaishi Nairobi. Marekani: Boeing 737 Max 8 ni salama Ethiopian Airlines: Ni nani waliopoteza maisha? Taarifa zinasema marehemu Getachew ambaye alikuwa na umri wa miaka 29 alisomea masomo ya sekondari katika shule ya sekondari ya Oshwal High mjini Nairobi. Getachew alikuwa ni rubani wa ngazi ya juu ambaye amekuwa akiiendesha ndege iliyomletea mauti tangu Novemba 2007. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ndege ya Ethiopian airlines Bwana Tewolde Gebre-Mariam, Getachew alikuwa ni rubani wa ngazi ya juu ambaye amekuwa akiiendesha ndege iliyomletea mauti tangu Novemba 2007. Ndege hiyo ilikuwana watu 157 wakiwemo wahudumu wanane waliokuwa waliokuwa wanasafiri kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi na wote walikufa. Wakenya 32 walikuwa miongoni mwao. Mamia ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya mazishi ya kiislam ya rubani mwenye umri wa miaka 29 , Yared Mulugeta Gatechew, aliyekufa katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines iliyoanguka Jumapili. text: Nchini Ghana, wenyeji wa kiasili wa Mji Mkuu wa Accra ni kabila la Ga, mwanamke anapojifungua mtoto wake wa 10 huzawadiwa kondoo mzima. Desturi hiyo hufahamika "nyongmato". Ukizunguka Jijini Accra leo, kwenye mabenki, vyombo vya usafiri, mitaani na kwengineko ni nadra kukutana na mama mwenye watoto zaidi ya wanne. Yawezekana Accra sio sehemu sahihi tena ya kutafuta familia yenye watoto 10 na kuendelea. Miezi miwili iliyopita mwandishi wa BBC nchini Ghana Elizabeth Ohene alihudhuria mazishi ya rafikiye wa toka shule ya msingi ambaye ameacha familia ya watu 44. Marehemu ameacha watoto nane,wajukuu 26 na vitukuu 8. Uzazi usiopangwa na ongezeko kubwa la watu ni moja ya sababu kuu inayotajwa kuchochea umaskini barani Afrika. Nchi ya Ghana ilikuwa na watu milioni 5 wakati ikipata uhuru mwaka 1957, miaka 60 baadae leo hii kuna watu milioni 30. Norway katika kipindi hichohicho wametoka kuwa na watu milioni 3.5 mpaka milioni 5.3. Afrika Mashariki Kwamujibu wa takwimu rasmi za serikali zilizotolewa mwezi Februari 2018, Tanzania kuna watu milioni 54, na ongezeko la watu linakadiriwa kufikia milioni 1.6 kila mwaka. Kinachoendelea Ghana kinaakisi sehemu nyengine za Afrika ikiwemo ukanda wa Afrika Mashariki. Kwamujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) idadi ya watu imeongezeka mara mbili nchini Kenya katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Idadi ya watu nchini Kenya hivi sasa inafikia milioni 50.9, na kwamujibu wa UN kama hatua stahiki hazitachukuliwa basi ongezeko hilo litapaa kwa watu milioni moja kila mwaka na nchi hiyo itafikisha idadi ya raia milioni 90 kufikia mwaka 2051. Utafiti:Hakuna pombe isiyokuwa na madhara Kama ilivyo kwa Ghana, Kenya pia inapambana na umasikini ambao unaathiri walio wengi. Takwimu zinonesha kuwa takriban 50% ya wananchi wa Kenya wanaishi katika lindi la umasikini. Ghana ilikuwa na watu milioni 5 wakati ikipata uhuru mwaka 1957, miaka 60 baadae leo hii kuna watu milioni 30. Akinadi sera ya serikali yake ya kutoa elimu bure nchini Tanzania, Rais John Magufuli alinukuliwa mara kadhaa akiwaambia wananchi wasiogope kuzaa na kutumia msemo "fyatueni tu" na serikali itawasomesha. Hatahivyo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu baadae alijitokeza na kuweka mambo sawa akisisitiza kuwa serikali bado inawaasa wananchi watumie uzazi wa mpango na kuzaa watoto ambao wataweza kuwahudumia kikamilifu. Kuhusu kauli ya Rais Magufuli, Bi Ummy alisema rais alikuwa akiwafanyia utani watania zake wa kabila la Wazaramo ambao ni wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam. Kanisa linalotukuza unywaji pombe Afrika Kusini Kwamujibu wa takwimu rasmi za serikali zilizotolewa mwezi Februari 2018, Tanzania kuna watu milioni 54, na ongezeko la watu linakadiriwa kufikia milioni 1.6 kila mwaka. Katika kupambana na ongezeko hilo kubwa la watu, Kenya wamefanikiwa kuongeza matumizi ya njia za uzazi wa mpango ambapo kwa sasa 53% ya wanandoa walikuwa wakitumia uzazi wa mpango kufikia mwaka 2014 kutoka 39% kwa mwaka 2008/2009. Serikali ya Tanzania pia imekuwa ikiwekeza katika kuchagiza matumizi ya uzazi wa mpango ambapo kwa mwaka 2018/19 imetenga shilingi bilioni 22 kwa ajili hiyo. Nchini Ghana, katika jitihada za kudhibiti ongezeko kubwa la watu Mkurugenzi wa Baraza la Idadi ya Watu Dkt Leticia Adelaide Appiah anapendekeza kuwekwa kikomo cha uzazi kwa kila mwanamke kuwa watoto watatu. Na ikitokea mtu akaongeza basi adhabu yake iwe kutopata msaada wowote kutoka serikalini. Pendekezo hilo bado halijapita lakini ni dhahiri kuwa litazua mjadala mkubwa. Katika jamii nyingi za kiafrika, kupata watoto ni jambo linalochukuliwa kama baraka. Baadhi ya jamii huchukulia kuwa na watoto wengi kama ishara ya utajiri na fahari. Ni jambo ambalo pia hupigiwa chapuo. text: Diego Mardona akifunga bao lake maarufu hand of God dhidi ya Uingereza 1996 Maradona alitumia mkono wake kufunga bao ambalo liliisaidia Argentina kuishinda Uingereza 2-1 katika robo fainali ya kombe la dunia miaka 31 iliopita. ''Kwa kweli mimi hukumbuka bao hilo kila mara ninapounga mkono utumizi wa teknolojia'' ,Maradona aliambia Fifa.com. ''Nilifikiria kuhusu bao hilo na kwa kweli bao hilo halikufaa kuidhinihswa''. Maradona anasema kuwa alifaidika kutokana na ukosefu wa teknolojia katika kombe la dunia na haikuwa mara moja bali mara mbili. ''Nitakwambia kitu chengine -katika kombe la dunia la 1990 nilitumia mkono wangu kuondoa mpira uliokuwa karibu kuingia katika goli letu dhidi ya taifa la Usovieti. ''Tulikuwa na bahati kwa sababu refa hakuona.Hakukuwepo na teknolojia wakati huo lakini sasa ni mambo mengine''. Diego Maradona ameunga mkono utumiaji wa kanda za video licha ya kukiri kwamba bao lake la ''Hand of God'' dhidi ya Uingereza 1986 halikufaa kukubalika.